Tabaruku

Page 1

Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page A

TABARUKU KWA MUJIBU WA AHLUL-BAYT

Kimeandikwa na:

Ustadh Sabah Ali al-Bayati

Kimetarjumiwa na: Ustadh Hemedi Lubumba Selemani


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page B

Haki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION

ISBN: 978 - 9987 - 512 - 42 - 3 Kimeandikwa na: Ustadh Sabah Ali al-Bayati Kimetafsiriwa na: Ustadh Hemedi Lubumba Selemani

Kupangwa katika Kompyuta na: Hajat Pili Rajab Toleo la kwanza: Desemba, 2008 Nakala: 1000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Nukushi: +255 22 2127555 Barua Pepe: alitrah@raha.com Tovuti: www.alitrah.org Katika mtandao: www.alitrah.info B


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page C

YALIYOMO Kutafuta Tabaruku.............................................................................2 Baraka ndani ya Qur’an Tukufu........................................................4 Kutafuta baraka ndani ya Historia.....................................................8 Kutafuta baraka ndani ya nyumati zilizotangulia..............................9 Jinsi walivyotafuta baraka kupitia mwili wa Mtukufu Mtume.......14 Jinsi walivyotafuta baraka kupitia nywele za Mtukufu Mtume......15 Jinsi walivyotafuta baraka kupitia jasho la Mtukufu Mtume...........16 Jinsi walivyotafuta baraka kupitia Maji ya udhu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w)..........................................................................................17 Jinsi walivyotafuta baraka kupitia kunywea bilauri ya Mtukufu Mtume.............................................................................................22 Jinsi walivyotafuta baraka kupitia fimbo ya Mtukufu Mtume, Mavazi na Pete yake.......................................................................24 Jinsi walivyotafuta baraka kupitia mimbari ya Mtukufu Mtume...28 Jinsi walivyotafuta baraka kupitia kaburi la Mtukufu Mtume .......29 Hoja ya utata ya Aliyani...................................................................33 C


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page D

Jinsi masahaba walivyotafuta baraka kupitia maeneo aliyosalia Mtukufu Mtume...............................................................................35 Jinsi sahaba walivyotafuta baraka kupitia sahaba na waja wema...42 Kutafuta baraka kupitia Makaburi ya waja wema na kupitia athari zao...................................................................................................52 Kujigusisha kwenye kitu cha kutafutia baraka................................57 Kutafuta baraka kwa upande wa Ahlul - Bayt.................................62 Walivyotafuta baraka kupitia kaburi la Mtukufu Mtume................63 Walivyotafuta baraka kupitia athari za baadhi yao..........................64 Walivyotafuta baraka kupitia udongo wa Husein............................65 Kutafuta baraka kupitia shuka la Ka’aba.........................................70 Kutafuta baraka kupitia mabaki ya maji ya muumini na masalio ya Udhuu wake.....................................................................................71 Kutafuta baraka kupitia maji ya mto Furati....................................73 Rai za baadhi ya wanachuoni kuhusu kutafuta baraka..................76

D


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page E

‘KUTAFUTA BARAKA’ (TABARRUKU) KWA MUJIBU WA AHLUL-BAYT. NENO LA JUMUIYA Hakika mirathi ya Ahlul-Bayt ambayo imehifadhiwa na kambi yao na wafuasi wao dhidi ya upotovu inaonyesha kambi iliyokusanya aina mbalimbali za taaluma za kiislamu. Kambi hii imeweza kulea nafsi mbalimbali zilizo tayari kunywa kutoka kwenye chemchemu hiyo, na kuupa umma wa kiislamu Wanachuoni wakubwa wenye kufuata nyayo za ujumbe wa Ahlul-Bayt. Wanachuoni waliyokusanya vidodosa na maswali mbalimbali ya madhehebu na mitazamo tofauti ya kifikira kuanzia ndani ya desturi ya kiislamu hadi nje ya desturi hiyo, huku wao wakitoa majibu na utatuzi makini juu ya maswali hayo ndani ya karne zote. Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bayt imefanya hima kutetea tukufu za ujumbe wa Uislamu na ukweli wake ambao umechafuliwa na makundi, madhehebu na wanaharakati mbalimbali wenye chuki na Uislamu. Jumuiya imefuata nyayo za Ahlul-Bayt na za wafuasi wa kambi yao njema ambayo imefanya hima kujibu madai yenye kuendelea na daima ikajaribu kubaki ndani ya msitari wa mapambano kwa kiwango kinachohitajika ndani ya kila zama. Hakika uzoefu ambao umehifadhiwa ndani ya vitabu vya Wanachuoni wa


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page F

kambi ya Ahlul-Bayt katika dhamira hii ni wa aina ya pekee, kwa sababu una hazina ya kielimu inayotegemea akili na hoja, huku ukijiepusha na matamanio na upendeleo uliokatazwa. Unazungumza na wasomi na wanafikra wenye fani maalum, mazungumzo ambayo yanakubalika kiakili na yanapokewa na maumbile yaliyo salama. Jaribio hili la Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bayt limekuja kuwapa watafuta ukweli hatua mpya ya uzoefu wa thamani katika ulingo wa mazungumzo na maswali na kujibu hoja za utata zilizotolewa zama zilizopita au zinazotolewa leo kwa njia ya Tovuti, na hasa kwa kupewa nguvu na baadhi ya duru zenye chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu. Ikijiepusha na uchochezi uliokatazwa, na ni yenye kuhangaikia kuzishauri akili zenye kufikiria na nafsi zenye kutafuta haki, ili ziweze kufikia kwenye haki ambayo inatolewa na kambi ya Ahlul-Bayti ulimwengu mzima, ndani ya zama ambazo akili inaerevuka na nafsi na roho zinaboreka kwa kasi ya pekee. Ni lazima tugusie kuwa mfululizo huu wa tafiti hizi umeandaliwa na Kamati maalum toka jopo la Wanachuoni watukufu, hivyo tunatoa shukurani njema kwa hawa wote na kwa wasomi na wahakiki kwa kila mmoja miongoni mwao kupitia sehemu ya tafiti hizi na kutoa mchango wao wa thamani kuhusu tafiti hizi. Na sote tunategemea na kutaraji kuwa tutakuwa tumetoa kile tulichokiweza katika juhudi za kutekeleza baadhi ya wajibu tulionao mbele ya ujumbe wa Mtukufu Mola Wetu Mlezi ambaye alimtumma Mtume Wake na uongofu na dini ya haki ili aipe ushindi dhidi ya dini zote. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa shahidi. Jumuiya ya kimataifa ya Ahlu-Bayt Kitengo cha utamaduni


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page G

‘KUTAFUTA BARAKA’ (TABARRUK) KUPITIA MAWALII,WATU WEMA NA MAKABURI MATUKUFU UTANGULIZI Kila sifa ni za Mwenyezi Mungu Mola wa viumbe. Rehma na amani zimfikie Muhammad na Kizazi Chake kitakatifu. Miongoni mwa mambo ambayo uchunguzi wake unajirudia mara kwa mara na kwa mifumo mbalimbali ni suala la ‘’Kutafuta Baraka’’ kupitia Mawalii na watu wema ndani ya umma na maeneo na Makaburi yaliyo matukufu kwa Waislam. Ni kutokana na udadisi au utata unaozuka tena au kujirudia juu ya suala hilo na hadi mara nyingi kufikia kiwango kibaya, huku mara nyingine ukipelekea kuigawa jamii iliyoshikamana pamoja huku ukileta mgawanyiko ndani ya wanajamii. Hivyo je; ‘’Kutafuta Baraka’’ ni Sunna au ni Bidaa? Je, suala hilo limetajwa ndani ya Qur’ani au Sunna? Je, lina historia yoyote kati ya waislamu na hasa ndani ya karne za mwanzo? Je, lina Sheria na kanuni? Hayo yote yatazungumziwa na Uchunguzi huu kwa muhtasari unaonasibiana na kwa kiwango kinachotosha kutuwafikisha. Tunamwomba Mwenyezi Mungu awe pamoja na makusudio na Yeye ndiye Mwenye Taufiki.

G


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page H

Neno la Mchapishaji Kitabu kilichoko mikononi mwako, ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabu kwa jina la: "At-Tabarruku" Sisi tumekiita: “Tabaruku" Kitabu hiki, "Tabaruku" ni matokea ya utafiti wa kielimu uliofanywa na Mwanachuoni huyu wa Kiislamu, Sheria ya Kiislamu ni ya kipekee kwa kuwa inahusika na kila jambo huku ikiweka utatuzi wa matatizo yote yanayompata mwanadamu katika sekta zote za maisha yake. Wanachouni wa Kiislamu kama kawaida ya wanadamu wamehitilafiana katika hukumu ndogo ndogo katika matendo ya ibada, lakini kama ilivyo, tofauti ndogo kati ya wanachuo kwa wafuasi inakuwa ni mlima wa tofauti na kusababisha zongo lisilo na maana. Mambo ambayo wanachuo wetu wamehitilafiana si katika asili au misingi ya dini, na isitoshe ni mambo machache sana ukilinganisha na yale tunayokubaliana nayo. Tabaruku ni suala ambalo wanachuo wetu wamehitalifiana; ndani ya madhehebu moja na kati ya madhehebu. Kwa hiyo hii sio hitilafu ya madhehebu, bali ni hitilafi ya wanachuo wa madhehebu zote wamehitilafiana juu ya suala hili. Lakini bahati mbaya Waislamu wengi hawaitambui hitilafu hii kwa usahihi na hivyo kuongelea katika dhana na kusababisha mizozo isiyokuwa na maana. Kutokana na hali hii Sheikh wetu,amelifanyia utafiti wa kina suala hili na kuweka wazi asaili ya hitilafu hii, kisha akamuachia msomaji mwenyewe kutoa uamuzi.

H


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page I

Kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote. Kutokana na ukweli huu, Taasisi yetu ya 'Al-Itrah Foundation' imeona ikitoe kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili, kwa madhumuni yake yale yale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili, ili kuongeza ujuzi wao katika masuala ya dini na ya kijamii. Tunamshukuru ndugu yetu, Hemedi Lubumba Selemani kwa kukubali jukumu hili la kukifanyia tarjuma kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwa kitabu hiki.

Mchapishaji: Al-Itrah Foundation S. L. P. 19701 Dar-es-Salaam, Tanzania.

I


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

J

Page J


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 1


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 2

Tabaruku

‘KUTAFUTA BARAKA’ Maana ya Baraka Baraka ndani ya lugha ya kiarabu ni: Mafanikio na ustawi.1 Al-Farau amesema kuhusu kauli ya Mwenyezi Mungu: “Rehema za Mwenyezi Mungu na baraka Zake ziwe juu yenu Kizazi cha Mtume.2” Baraka ni Fanaka.3 Baada ya kaleta kauli hii Abu Mansuri Al-Az’hariyu amesema: Na pia kauli yake ndani ya At-Tashahudi: “Amani iwe juu yako ewe Mtume na rehema za Mwenyezi Mungu na baraka Zake” kwa sababu atakayepewa fanaka na Mwenyezi Mungu kama fanaka aliyompa Mtume basi amepata mafanikio yaliyobarikiwa daima.4 Kuomba Baraka: Ni kumwombea Baraka mwanadamu na kitu kingine. Husemwa: Nilimbariki Baraka. Maana yake nilisema: Mwenyezi Mungu akubariki.5 Ibnu Athir amesema: Ndani ya Hadithi ya Ummu Sulaymu “Na akamlambisha asali na kumbariki.” Maana yake alimwombea Baraka.6 1 -Hilo limesemwa na Al-Khalilu Af-Farahidiyu 5: 368, Neno Alibariki. Tazama Lisanul-Arabi 10: 390. As-Swahahu cha Al-Jawhariyu 4: 1075. Mu’jamulMaqayisi Lughati cha Ibnu Farisi 1: 230. Al-Muf’radati cha Ar-Raghibu AlIsbihani: 44. An-Nihayatu cha Ibnu Athir 1:120. 2 Hud: 73 3 Ma’aanil-Qur’anii 2: 23. 4 Tahdhibil-Lughati 10: 232. 5 Tahdhibil-Lughati cha Al-Az’Hariyu 10: 132 6 An-Nihayah 1: 120. 2


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 3

Tabaruku

Al-Jauhariyu amesema: “Husemwa: Mwenyezi Mungu abariki kwa ajili yako, kwako na juu yako na akubariki.”7

Mwenyezi Mungu amesema: Amebarikiwa aliyomo katika Moto. (AnNaml : 8.) Ibnu Mandhur amesema: “Mwenyezi Mungu amebariki kitu, amebariki ndani yake na juu yake: Amekiwekea Baraka, na chakula chenye Baraka ni kama kwamba kimebarikiwa.”8 Al-Fuyumiyu amesema: “Mwenyezi Mungu amebariki ndani yake na hivyo ni chenye kubarikiwa, na asili ni: Kilichobarikiwa ndani.” 9 ‘Kutafuta Baraka’ ni: Kuomba Baraka, nayo ni ustawi au fanaka. Na ‘’Kutafuta Baraka’’ kupitia kitu: Ni kuomba baraka kupitia njia yake. Ibnu Mandhuri amesema: “Nimetafuta Baraka kwacho: Maana yake nimestawika kwacho.”10 Ibnu Athir amesema: “Ustawi: Baraka. Na fulani amestawika juu ya kaumu yake, hivyo yeye amefanikiwa kwani amekuwa mbarikiwa juu yao. Na amestawika kwacho: Maana yake amebarikika.”11 ‘Kutafuta Baraka’: Kiistilahi hummaanisha kuomba baraka kupitia vitu au maana alizoziteua Mwenyezi Mungu kwa kuzipa vyeo na heshima maalum 7 As-Swahahu 4:1575. 8 Lisanul-A’rabi 10:390. 9 Al-Mis’bahul-Muniru 1: 45. 10 Lisanul-Arabi 13: 408. 11 An-Nihayah 5: 302. 3


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 4

Tabaruku

na kuzihusisha na Baraka huku akizipa kipaumbele kwa msaada Wake juu ya nyingine. Kama ilivyo katika kugusa mkono wa Mtume kwa ajili ya kustawika kupitia baraka yake. Au kugusa baadhi ya athari zake tukufu baada ya kifo chake. Na huu ndio muradi wa ‘Kutafuta Baraka’ ambayo ndio kiini cha uchunguzi. Vyovyote itakavyokuwa ni kuwa hakika chanzo chake ni Baraka ambayo Mwenyezi Mungu ameifanya muhtasi kwa vitu au watu fulani tu bila kuhusisha wengine.

BARAKA NDANI YA QUR’ANII TUKUFU Ndani ya Qur’ani Tukufu neno Baraka limekuja mara nyingi ili kuonyesha jinsi watu maalum, sehemu na nyakati maalum zilivyo mahususi kwa Baraka ambayo Mwenyezi Mungu ameiweka humo kutokana na sababu zilizopelekea hekima ya Mwenyezi Mungu kufanya hivyo. Miongoni mwa watu waliojumuishwa na neno Baraka ndani ya Qur’ani Tukufu ni: Nabii Nuhu (a.s.) na aliyekuwa pamoja naye. Hilo ni katika Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Shuka kwa salama itokayo kwetu na baraka nyingi juu yako na juu ya watu walio pamoja nawe….” (Hudi: 48.) Nabii Isa (a.s.) katika kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na amenifanya mbarikiwa popote nilipo, na ameniusia Swala na Zaka….” (Mariamu: 31.) 4


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 5

Tabaruku

Nabii Ibrahim na mwanae Nabii Is’haka katika kauli ya Mwenyezi Mungu: “Basi alipoufikia ikanadiwa kuwa: Amebarikiwa aliyemo katika Moto na aliyeko pembeni mwake….” (An-Namlu: 8.) Na kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na tukambarikia yeye na Is’haka….” (As-Swafat: 113.) Kizazi cha Mtume au kizazi cha Ibrahim (a.s.) kwa mujibu wa baadhi ya kauli, hilo ni katika kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Rehema ya Mwenyezi Mungu na Baraka Zake ziko juu yenu enyi watu wa nyumba hii. Hakika Yeye ndiye Mwenye Kusifiwa Mwenye Kutukuzwa.” (Hudi: 73.) Kama lilivyokuja neno Baraka na lile lenye maana yake ndani ya Qur’ani Tukufu yakiwa muhtasi kwa ajili ya maeneo, ardhi na viunga maalum kwa kuwa yanahusika na utakaso maalum. Miongoni mwake ni: 1- Nyumba Tukufu huko Makka Tukufu, kwa kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Hakika nyumba ya kwanza waliyowekewa watu ni ile iliyoko Makka yenye kubarikiwa na Mwongozo kwa Viumbe.” (Aali Imrani: 96.) 2- Ardhi kwa ujumla wake ameiwekea Baraka kwenye pande zake mbalimbali, hilo ni kwa kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na akaweka humo milima juu yake na akabarikia humo na akapima humo chakula chake….” (Fuswilati: 10.)

5


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 6

Tabaruku

Maana yake aliweka humo heri nyingi ambayo vilivyopo juu ya ardhi kuanzia mimea, mnyama na binadamu atavitumia kwa manufaa mbalimbali katika maisha yake.12 Ar-Razi amesema: “Na Baraka ni ongezeko la heri, na heri nyingi zipatikanazo toka aridhini.”13 3- Msikiti wa Mbali na vilivyomo pembezoni mwa Nyumba Tukufu katika ardhi ya Palestina, kwa Kauli ya Mwenyezi Mungu: “….Mpaka Msikiti wa Mbali ambao tumevibariki vilivyoko pembezoni mwake…..” (Al-Isra’a: 1.). Na pia katika kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na tukawarithisha watu waliokuwa wanaonekana dhaifu Mashariki ya ardhi na Magharibi yake ambayo tuliitia Baraka….” (Al-Aa’araf: 13.) Na kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na tulimwokoa yeye na Lut katika ardhi tuliyoibariki kwa ajili ya walimwengu wote.” (Al-Ambiyau: 71.) 4- Yemen: Kwa kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na baina yao na baina ya miji tuliyoibariki tukaweka miji iliyo dhahiri….” (Saba’: 18.) 5- Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na useme: Mola Wangu Mlezi uniteremshe mteremsho wenye Baraka, maana wewe ni mbora wa wateremshaji.” (Al-Muuminuna: 29.)

12 Tafsiril-Mizani ya At-Tabatabai 17: 363, 385. 13 At-Tafsiri Al-Kabir ya Ar-Razi 27: 402, Tafsiri ya Aya (Tukaweka humo milima…) 6


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 7

Tabaruku

Pia ndani ya Qur’ani Tukufu imepatikana maana ya Baraka ikiwa ni sifa ya Kitabu Kitukufu. Hilo ni katika kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na hiki ni Kitabu tulichokiteremsha, kilichobarikiwa, chenye kuhakikisha yaliyotangulia.” (Al-An-aam: 92.)

“Na hii Qur’ani ni Kitabu tulichokiteremsha, kilichobarikiwa, basi kifuateni na muwe Wachamungu ili mrehemewe.” (Al- An’aam: 155.)

“Na haya ni makumbusho yaliyobarikiwa tuliyoyateremsha, je ninyi mtayakataa?” (Al-Anbiyau: 50.)

“Kitabu tumekiteremsha kwako chenye Baraka ili wapate kuzifikiri Aya Zake….” (Surat As-Swadi: 29.) Imepatikana maana ya Baraka ikionyesha kuwa baadhi ya viumbe vya Mwenyezi Mungu kuanzia mimea na vinginevyo vina Baraka, kama ilivyo katika kauli ya Mwenyezi Mungu: “Kama nyota ing’aayo inayowashwa katika mti uliobarikiwa wa mzaituni…..” (An-Nuru: 35.)

“Basi alipofika aliitwa kutoka upande wa kulia wa bonde, katika kiwanja kilichobarikiwa, kutoka mtini….” (Al-Qaswas: 30.) 7


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 8

Tabaruku

“Na tumeyateremsha kutoka mawinguni maji yaliyobarikiwa na kwa hayo tukameesha mabustani na nafaka zivunwazo.” (Suratu Qafu: 9.) Kama Mwenyezi Mungu alivyofanya baadhi ya nyakati kuwa muhtasi kwa Baraka, kama ilivyo katika kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Kwa hakika tumeiteremsha katika usiku uliobarikiwa, bila shaka Sisi ni waonyaji.” (Ad-Dukhan: 3.) Hizi ni baadhi ya maana za Baraka na matumizi yake ndani ya Qur’ani Tukufu. Ama Sunna Tukufu ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ni kuwa Hadithi ambazo zinabeba madhumuni ya Baraka na matumizi yake ni nyingi sana, na baadhi yake zitakujia ndani ya vipengele vya uchunguzi ujao ili kuonyesha kuwa Baraka na ‘Kutafuta Baraka’ ni jambo lililothibiti ndani ya Sheria. Iliyo mashuhuri mno ni ile iliyothibiti toka kwake (s.a.w.w.) katika namna ya kumtakia rehema: “Ewe Mwenyezi Mungu mfikishie rehema Muhammad na ndugu wa Muhammad kama ulivyomfikishia rehema Ibrahim na ndugu wa Ibrahim. Na mbariki Muhammad na ndugu wa Muhammad kama ulivyombariki Ibrahim na ndugu wa Ibrahim. Hakika wewe ni Mwenye Kusifiwa Mwenye Kutukuzwa.”

‘KUTAFUTA BARAKA’ NDANI YA HISTORIA. Je, kitendo cha ‘Kutafuta Baraka’ kwa namna ya kiistilahi kina tukio lolote la kihistoria lililotokea kwenye nyumati zilizopewa Sheria ili ndani ya mwenendo wao na Hadithi zao tuweze kugundua aina hii ya mwenendo walioujua, na mara nyingi kuutenda kama Mwenendo wa Kisheria? 8


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 9

Tabaruku

Tufuatilie jibu la swali hili katika hatua mbili za msingi: Moja inahusu historia ya nyumati zilizotangulia, na ya pili inazungumzia ‘’Kutafuta Baraka’’ ndani ya mwenendo wa waislamu na maarifa yao tangu zama za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kufuatia zama za karibu na Mtume. Na hatua hii ndiyo yenye uchambuzi mwingi.

1- ‘KUTAFUTA BARAKA’ NDANI YA NYUMATI ZILIZOTANGULIA Hamna shaka kuwa tukio la ‘’Kutafuta Baraka’’ kupitia athari za Manabii ni maarufu mno hata kwa nyumati zilizotangulia kabla ya Uislamu na ambalo limehusisha ‘Kutafuta Baraka’ kupitia nguo za hao Manabii na masazo yao. Miongoni mwa mifano ya ‘Kutafuta Baraka’ kwa upande wa nyumati zilizotangulia ni: Nabii Yakub, yeye alitafuta Baraka kupitia kanzu ya mwanae Nabii Yusuf. Mwenyezi Mungu amesema:

“Nendeni na kanzu yangu hii na mumwekee baba yangu usoni, atakuwa mwenye kuona.” (Yusuf: 93) Ndugu wa Yusuf walitimiza amri yake na wakaja na kanzu yake na kuiweka usoni kwa baba yake ambaye alipofuka kwa ajili ya huzuni ya kutengana na mwanae Yusuf. Hivyo Mwenyezi Mungu akaifanya kanzu ya Yusuf kuwa sababu ya baba yake Yakub kuona, na hilo lilitokana na uwezo wa Mwenyezi Mungu na Baraka ya kanzu hiyo. Inajulikana kuwa Mwenyezi Mungu anao uwezo wa kurudisha kuona kwa Yakub bila kuhitajia kumuwekea kanzu hiyo usoni, lakini Mwenyezi Mungu ana hekima maalum katika kuvifanya baadhi ya vitu vilivyobariki9


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 10

Tabaruku

wa kuwa sababu ya kutimia malengo. Na bila shaka malengo ni kukifanya kitendo hicho kiwe mwenendo watakaoufata viumbe na wajue kuwa kuna vitu, maeneo, nyakati na watu walio na vyeo kwa Mwenyezi Mungu, hivyo akaviwekea Baraka itakayowezesha kumponya mgonjwa au kujibiwa dua au ombi la kufutiwa dhambi, na mfano wa hayo. Az-Zamakhshari amesema: Imesemekana kuwa: Ni kanzu ya urithi ambayo ilikuwa katika kinga ya Yusuf na ilitoka Peponi, Jibril aliamrishwa amletee, na hakika ilikuwa na harufu ya Peponi, hawekewi mwenye matatizo wala mgonjwa ila ni lazima atapona.14 Miongoni mwa mifano ni: Wana wa Israeli, wao waliomba Baraka kupitia Sanduku ambalo lilikuwa na athari za watu wa Musa na watu wa Haruna na ndilo alilolitaja Mwenyezi Mungu alipokuwa akisimulia kuhusu Nabii wa Wana wa Israeli ambaye aliwabashiria ujio wa Twaluti atakayekuwa Mfalme juu yao:

“Hakika alama ya ufalme wake ni kuwafikieni Sanduku lenye matummaini yatokayo kwa Mola wenu Mlezi na masazo ya yale waliyoyaacha watu wa Musa na watu wa Haruna likichukuliwa na Malaika.� (Al-Baqaratu: 248.) Lilikuwa sanduku ambalo Mwenyezi Mungu alimteremshia Musa, na mama yake akamuweka humo na kisha kumtupia mtoni. Lilikuwa liki14 Al-Kashafu 2: 503. 10


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 11

Tabaruku

heshimiwa mno na Wana wa Israili na wakitafuta Baraka kupitia Sanduku hilo. Hivyo Musa alipokaribiwa na kifo aliweka humo Ubao, Deraya yake na Alama za unabii alizokuwa nazo akamuwekea Wasii wake Yoshua. Waliendelea kuwa na Sanduku hilo mpaka wakaja kulidharau na watoto wadogo wakawa wakilichezea mitaani. Wana wa Israili waliendelea kuwa katika heshima na starehe kipindi chote walichokuwa na Sanduku, basi walipotenda maasi na kulidharau Sanduku ndipo Mwenyezi Mungu alipoliondoa kwao. Na walipomwomba Nabii wao; Mwenyezi Mungu aliwatumia Twaluti awe Mfalme juu yao apigane pamoja nao na akawarudishia Sanduku. Al-Zamakh’shari amesema: Tabuti ni Sanduku la Taurati, na Musa alipokuwa akipigana alikuwa akilitanguliza na hapo nafsi za Wana wa Israili hupata matummaini na wala hazidhoofiki……..Na kauli Yake: “Na masazo ya yale waliyoyaacha watu wa Musa na watu wa Haruna.” Ni vijipande vya ubao, fimbo ya Musa, nguo yake na sehemu ya Taurati.15 Tunawakuta Wana wa Israili kwa amri ya Nabii wao wanahifadhi aliyoyaacha Musa na Haruna na nafsi zao zinapata matummaini kutokana na Baraka aliyowahadithisha, ambayo Mwenyezi Mungu ameifanya muhtasi kwa Sanduku kwa kuwa linatokana na athari za Nabii wao, mpaka walipozidharau athari hizi zilizobarikiwa ndipo Mwenyezi Mungu akawaadhibu na kuwanyima Baraka zake, jambo linaloonyesha utukufu wa athari hizi na Baraka iliyomo humo kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.

15 Al-Kashafu 1: 293. 11


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 12

Tabaruku

2- SERA YA WAISLAMU KATIKA ‘’KUTAFUTA BARAKA’’ KWANZA: Mwenendo wa Sahaba katika kuomba Baraka kupitia Mtume zama za uhai wake Muhammad Twahiru Al-Makkiyyu amesema: “Bila shaka ‘Kutafuta Baraka’ kupitia athari zake ulikuwa ni mwenendo wa Sahaba, Mwenyezi Mungu awe radhi nao. Na athari zao katika hilo zikafatwa na wale waliyopita njia yao kuanzia Tabiina na waumini wema. Na zama zake ilitokea ‘Kutafuta Baraka’ kupitia baadhi ya athari zake (s.a.w.w.) na akaridhia na wala hakukanusha, hivyo kitendo hicho kikawa dalili yakinifu juu ya kuruhusiwa kisheria. Na laiti isingekuwa ni ruhusa kisheria basi (s.a.w.w.) angekataza na kuhadharisha. Pia Hadithi Sahihi na Kongamano la Sahaba vinaonyesha ruhusa yake kisheria. Mwenendo huo unaonyesha nguvu ya Imani ya Sahaba, mapenzi yao Makali, kumtawalisha kwao na kumfata kwao Mtukufu Mtume mpaka kiwango cha kauli ya Mshairi: Ninapita kwenye Majumba, majumba ya Salma Nakibusu chenye ukuta na chenye ukuta Si kuzipenda nyumba ndiko kulikoukonga moyo wangu Lakini ni kumpenda aliyeishi nyumba hizo.16 Hivyo Sahaba walikuwa wakitafuta Baraka kupitia Mtume zama za uhai wake kwa kugusa mwili wake Mtukufu na kubusu mkono wake na kunywa masalia ya ndani ya chombo chake na kwa maji ya udhu wake na kohozi lake na nywele zake na mengineyo. Na wanapozaliwa watoto wao 16 Tabaruk As-Swahabati biathari Ar-Rasuli: 7. 12


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 13

Tabaruku

huwaleta ili Mtume awalambishe asali na kuwabariki na kuwaombea dua. Miongoni mwa hayo ni riwaya aliyoitoa Muslim ndani ya Sahih yake kuwa Mtume alikuwa akiletewa watoto anawabariki na kuwarambisha asali.17 Ibnu Hajar amesema: “Kila mtoto aliyezaliwa zama za uhai wa Mtume huhukumiwa kuwa alimuona Mtume, hii ni kwa sababu Ansari wote walikuwa wakiwaleta watoto wao kwa Mtume kwa ajili ya kuwarambisha asali na kuwabariki, kiasi kwamba imesemwa kuwa: Wakati Makka ilipokombolewa watu wa Makka wakawa wanakwenda kwa Mtume wakiwa na watoto wao ili awaguse vichwa vyao na awaombee Baraka.”18 Zimepokewa Hadithi Nyingi kuhusu hilo na sisi tunatoa baadhi yake: 1- Imepokewa kutoka kwa Ummu Kaysi kuwa alisema: Alimletea Mtume wa Mwenyezi Mungu mtoto wake mdogo ambaye bado hajaanza kula chakula basi akamkalisha mapajani mwake, mara akakojolea nguo zake. Mtume akaomba maji na kurashia nguo zake na wala hakuziosha.19 Ibnu Hajar amesema: “Ndani ya Hadithi hii mna faida nyingi ikiwemo kuhimiza uhusiano mwema, unyenyekevu, huruma kwa wadogo, kumrambisha asali mtoto aliyezaliwa na ‘Kutafuta Baraka’ kupitia watu wa kheri na kuwabeba watoto wachanga wakati wa kuzaliwa na baada yake.20 17 Sahih Muslim 1: 164, Mlango wa hukumu ya mkojo wa mtoto anyonyaye, na 6: 176, Mlango wa ni Sunna kumrambisha mtoto asali. 18 Al-Isabah 3: 638, Herufi wawu Sehemu ya Kwanza. Mlango Wawu na Kafu, Wasifu wa Walidu bin Aqabatu, namba 9147. 19 Sahih Bukhari 1: 62, Mlango wa kuosha. Sunan An-Nasai 1: 93, Mlango wa mkojo wa mtoto ambaye bado hajaanza kula chakula. Sunan At-Tirmidhiyu 1: 104. Sunan Abu Daud 1: 93, Mlango wa mkojo wa mtoto unaoipata nguo. Sunan Ibnu Majah 1: 174. 20 Fat’hul-Bari 1: 326 Kitabu cha Udhu, Mlango wa 59 mlango wa mkojo wa mtoto, hadithi ya 223. 13


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 14

Tabaruku

Imepokewa toka kwa Aisha: Mtume alikuwa akiletewa watoto wadogo anawarambisha asali na kuwabariki.21 Toka kwa Abdur-Rahmani bin Aufi amesema: “Hakuzaliwa mtoto yeyote wa mtu ila aliletwa kwa Mtume na kumwombea.”22 Toka kwa Muhammad bin Abdur-Rahman mtumwa wa Abu Twalha toka kwa Dhiiri Muhammad bin Twalha amesema: Muhammad bin Twalha aliletwa kwa Mtume ili amrambishe asali na amwombee na hivyo ndivyo alivyokuwa akiwafanyia watoto wadogo.23 Mwenendo wa Sahaba wema ulikuwa ni ‘’Kutafuta Baraka’’ kupitia Mtume na athari zake zama za uhai wake na baada ya kifo chake. Hadithi kuhusu hilo haziwezi kuhesabika isipokuwa sisi tutatoa baadhi ya mifano michache kuhusu Sahaba ‘’Kutafuta Baraka’’ kupitia Mtume na athari zake ili kuonyesha ‘’Kutafuta Baraka’’ kulivyoruhusiwa kisheria.

JINSI WALIVYOTAFUTA BARAKA KUPITIA MWILI WA MTUKUFU MTUME Imepokewa kuwa Mtume (s.a.w.w.) alikwenda sokoni akamkuta Zuhayr amesimama wima akiuza bidhaa, basi akaja kutokea mgongoni mwake na kumkumbatia kwenye kifua chake kwa mkono wake. Hapo Zuhayr akihisi kuwa ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Anasema: Nikawa nikigusisha mgongo wangu kwenye kifua chake nikitaraji kupata baraka.24 21 Musnad Ahmad 7: 303, hadithi ya 25243. Al-Isabah 1: 5 toka kwa Muslim Hotuba ya Kitabu, sehemu ya pili 22 Al-Mustadraku 4: 479. Al-Isabah 1: 5 Hotuba ya Kitabu, sehemu ya pili 23 Al-Isabah 1: 5 Hotuba ya Kitabu, sehemu ya pili. 24 Siratu Dahlani 2: 267. Al-Bidayatu Wan-Nihayatu 6: 47 amesema kuwa ni Sahih na wapokezi wake ni waaminifu. Musnad Ahmad 3: 938, hadithi ya 12237, kuomba kwao baraka kwa nywele za (s.a.w.w.) 14


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 15

Tabaruku

JINSI WALIVYOTAFUTA BARAKA KUPITIA NYWELE ZA MTUKUFU MTUME Imepokewa kutoka kwa Anas amesema: “Nilimwona Mtume wa Mwenyezi Mungu huku kinyozi akimnyoa na Sahaba zake wamemzunguka wakiwa hawataki unywele udondoke isipokuwa udondokee kwenye mkono wa mtu.”25 Kutoka kwa Abdullah bin Zaid amesema: “…….Basi Mtume wa Mwenyezi Mungu akanyolea kichwa chake ndani ya nguo yake na kisha akampa na zikagaiwa kwa Sahaba. Akakata kucha zake na kisha akampa Sahaba wake. Amesema: Zenyewe ziko kwetu tunazipaka hina: Yaani nywele zake.”26 Mtume wa Mwenyezi Mungu alipochinja Sadaka alimwita kinyozi na wakahudhuria waislamu wakiomba nywele za Mtume wa Mwenyezi Mungu, ndipo akampa kinyozi upande wa kulia wa kichwa chake kisha akampa nywele hizo Abu Twalha Al-Ansariyu. Na Khalid bin Walid akamwomba za utosini kwake pindi ziliponyolewa, basi akampa na akawa akiziweka mbele ya kofia yake. Hivyo akawa hakutani na kundi lolote ila hulisambaratisha.27 Imepokewa toka kwa Abu Bakar kuwa alikuwa akisema: “Hakukuwa na ukombozi mkubwa kama wa Hudaibiya, lakini siku hiyo rai zao haziku25 Sahih Muslim: Ufafanuzi wa An-Nawawiyu 15: 83. Aruwaul-Ghalili 4: 288. Musnad Ahmad 3: 591. Musnadati Ibnu Malik hadithi ya 11955. As-SunanlKubra cha Al-Bayhaqiyu 7:68. As-Siratu Al-Halbiyatu 3: 303. Al-Bidayatu WanNihayatu 5: 189. 26 As-Sunanl-Kubra cha Al-Bayhaqiyu 1:25. Mlango wa nywele za Mtume. Musnadi Ahmad 4: 630, hadithi ya 16039. Maj’mau Zawaidi 4: 19. 27 Maghazil-Waqidiyu: 3: 1108. 15


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 16

Tabaruku

fikia yaliyokuwepo kati ya Muhammad na Mola Wake………Nilimwona Suhaylu bin Amru kwenye Hija ya kuaga akiwa amesimama wima kwenye Machinjio akimsogezea Mtume mnyama na Mtume akimchinja kwa mkono Wake. Akamwita kinyozi akanyoa kichwa chake huku nikimwona Suhaylu akiokota nywele zake na ninamwona akiziweka juu ya macho yake huku nikikumbuka jinsi alivyogoma isiandikwe Bismillahi Rahmani Rahimi Siku ya Hudaibiya.28

JINSI WALIVYOTAFUTA BARAKA KUPITIA JASHO LA MTUKUFU MTUME Imepokewa kutoka kwa Anas bin Malik kuwa amesema: Hakika Ummu Sulaymu alikuwa akimtandikia Mtume mkeka wa ngozi na akijipumzisha kwa kulala juu ya mkeka huo wa ngozi. Amesema: Mtume akishalala huchukua jasho lake na nywele zake na kuzikusanya ndani ya chupa kisha huzikusanya ndani ya manukato.”29 Katika kufafanua Hadithi hii, Ibnu Hajar amesema: “Kutajwa nywele ndani ya kisa hiki kunashangaza (Kunatia wasi wasi). Baadhi yao wameitafsiri kuwa ni zile nywele za Mtume (s.a.w.w.) zilizokuwa zikiruka pindi anapozichana kwa kuzinyoosha. Kisha ndani ya riwaya ya Muhammad bin Saad nikaona jambo linaloondoa utata, kwani yeye ametoa kwa njia sahihi toka kwa Thabiti toka kwa Anas kuwa Mtume aliponyoa nywele zake huko Mina, Abu Twalha alichukua nywele na kumletea Ummu Sulaymu akaziweka ndani ya manukato yake. Ummu Sulaymu amesema: Alikuwa akija na kujipumzisha kwangu juu ya mkeka wa ngozi na nikawa nakusanya jasho.”30 28 -Kanzul-Ummali 10: 472. Hadithi ya 30136. 29 Sahih Bukhari 7: 140, Kitabu cha kuomba idhini. 30 Fat’hul-Bari 11:95. At-Tabakatul-Kubra 8: 313. 16


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 17

Tabaruku

JINSI WALIVYOTAFUTA BARAKA KUPITIA MAJI YA UDHU WA MTUKUFU MTUME (S.A.W.W.) Kutoka kwa Abu Juhayfa amesema: “Nilikwenda kwa Mtume akiwa Kuba Hamrau kwa mbele nikamwona Bilal amechukua maji ya udhu wa Mtume na huku watu wakikimbilia maji ya udhu wake anayeupata anajipaka na asiyeyapata anachukua toka kwenye unyevunyevu wa mkono wa mwenzake.” Katika tamko lingine: Mtume alitoka siku yenye joto kali akaletewa maji ya udhu basi watu wakawa wanachukua maji aliyofanyia udhu huku wakijipaka maji hayo.31 Kutoka kwa Ibnu Shihabi amesema: Mahmud bin Ar-Rabiu alinipa Hadithi. Amesema: Na yeye ndiye ambaye Mtume alimtemea usoni maji toka kisimani mwao akiwa bado mdogo. Na Urwatu amesema toka kwa Al-Masuri na mwenzake – Kila mmoja akithibitisha ukweli wa mwenzake: Mtume anapotawadha walikuwa wakikaribia kuuwana kwa kugombania maji ya udhu wake.32 Katika ufafanuzi wake Ibnu Hajar amesema: “Kitendo cha Mtume kumfanyia Mahmud imma ni kwa ajili ya kumfanyia mzaha au kwa ajili ya kumbariki kama ilivyokuwa kawaida yake kuwabariki watoto wa Sahaba.”33 31 Sahih Bukhari 1: 55, Kitabu cha udhu Mlango wa kutumia masazo ya udhu wa watu wengine. Musnad Ahmad 5: 398, hadithi ya 18269. Sunanl-Kubra cha AlBayhaqiyu 1: 395. Dalailu An-Nubuwati cha Al-Bayhaqiyu 1: 183. Sahih Muslim 1: 360. Sunan An-Nasai 1: 87. 32 Sahih Bukhari 1: 55, Kitabu cha udhu Mlango wa kutumia masazo ya udhu wa watu wengine. Musnad Ahmad 6: 594, hadithi ya 2310. Sunani Ibnu Majah 1:246. 33 Fat’hul-Bari 1: 157, Mlango wa ni wakati gani inasihi kumsikiliza mtoto. 17


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 18

Tabaruku

Kama wasimulizi na wanahadithi walivyotoa kisa cha kuja Urwatu bin Masuudi At-Thaqafiyu kwa makurayshi kabla ya Suluhu ya Hudaibiya, kwani kitendo cha Sahaba pamoja na Mtume kilimshitua, akasema: - Akisimulia aliyoyaona - Hatawadhi udhu wowote ila waliukimbilia na wala hatemi mate yoyote ila waliyakimbilia wala hauanguki unywele wowote kati ya nywele zake ila waliuchukua. Na katika riwaya nyingine: Naapa kwa Mwenyezi Mungu, Mtume wa Mwenyezi Mungu hakutoa kohozi lolote ila liliangukia kiganjani mwa mtu miongoni mwao na kuupaka uso wake na ngozi yake, na anapowaamuru huharakisha kutekeleza amri yake na anapotawadha hukaribia kuuwana kwa kugombania maji ya udhu wake.34 Kutoka kwa Saad amesema: “Niliwasikia baadhi ya Sahaba wa Mtume akiwemo Abu Usayd na Abu Hamid na Abu Sahli ibnu Saad wakisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu alikwenda kisima cha Bidhaa akatawadha ndani ya ndoo na kuirudisha kisimani na mara nyingine akatemea ndani ya ndoo na kutemea mate kisimani na akanywa maji toka humo. Basi ikawa anapougua mgonjwa zama zake husema: Mwogesheni maji ya kisima cha Bidhaa. Hapo huogeshwa na ndipo mgonjwa huwa kana kwamba kafunguliwa kamba.”35 Kutoka kwa Jabir bin Abdullah Al-Ansari, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, amesema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu alikuja kunitembelea ili34 Musnadi Ahmad 5:423 hadithi ndefu 18431. Sunanl-Kubra cha Al-Bayhaqiyu 9: 219, Mlango wa suluhu kwa mtazamo wa waislamu. Bukhari 1: 66, Kitabu cha udhu, 3:180 Kitabu cha usia. Siratul-Halbiyatu 3: 18. Siratu Ibnu Hishami 3:328. Al-Mghazi cha Al-Waqidiyu 2:598. Tarikhul-Khamisi 2: 19. 35 Siratu Ibnu Dahlani 2: 225. At-Tabakatu Al-Kubra 1-2 : 184.

18


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 19

Tabaruku

hali mimi ni mgonjwa sijitambui. Akatawadha na kunimwagia maji ya udhu wake na ndipo nikajitambua.”36 Pia imepokewa toka kwake amesema: “Hakika Mtume alitawadhia ndani ya beseni nikalichukua na kumwagia ndani ya kisima chetu.”37 Kutoka kwa Abu Musa amesema: “Mtume aliomba chombo chenye maji akanawia humo mikono yake na uso wake na kutemea mate kisha akawaambia: Yanyweni na mwagieni juu ya nyuso zenu na shingo zenu.38 Ibnu Hajar amesema: Lengo la kutemea mate ni kuiweka Baraka humo.”39 Kutoka kwa Mama Haniu: Mtume aliingia kwake Siku ya Ukombozi akamletea kinywaji akanywa na yakasalia mabaki, basi Mtume akampa akanywa kisha akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu nimefanya kitu ambacho sijui utaafikiana nacho au hapana. Akasema: “Ni kitu gani hicho ewe Mama Haniu?” Akasema: “Nilikuwa ni mwenye Saumu na sikupendezwa kukataa mabaki yako hivyo nikanywa.” Katika riwaya nyingine: “Nimekunywa ilihali ni mwenye Swaumu.” Akasema: “Kitu gani kimekupelekea kufanya hivyo?” Akasema: Kwa ajili ya mabaki yako sikuwa na sababu ya kuyaacha, sikuwa na uwezo wa kuyapata na ndipo nilipoyapata nikanywa.40 Hadithi hizi zimetolewa na Maimamu na Wanahadithi ili zijulishe mwenendo wa Sahaba Wema katika ‘’Kutafuta Baraka’’ kupitia Mtume zama za 36 Sahih Bukhari 1: 60, 7: 185, 9: 124. Sahih Bukhari 3: 1235. 37 Kanzul-Ummali 12: 422, hadithi ya 35473. 38 Sahih Bukhari 1: 55, Kitabu cha udhu Mlango wa kutumia masazo ya udhu wa watu wengine 39 Fat’hul-Bari 1: 236, Kitabu cha udhu, Mlango wa kutumia masazo ya udhu wa watu wengine 8: 37, Mlango wa Vita vya Taifu. 40 Musnadi Ahmad 7:575, hadithi ya 26838. At-Tabakatu Al-Kubra 8:109. 19


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 20

Tabaruku

uhai wake. Mwenendo huu uliendelea kwao baada ya kifo chake kiasi kwamba Sahaba walikuwa wakitafuta Baraka kupitia athari zake. Hivyo wakawa wanakunywa katika visima ambavyo Mtume alikunywa toka humo au alitemea mate. Wakawa wanaomba Baraka kupitia masazo ya nywele zake, mimbari yake, pete yake, fimbo yake, bilauri yake, kaburi lake tukufu, mavazi yake, viatu vyake na kila alichokiacha Mtume baada ya kifo chake. Tabiina waliwafuata katika hili na mwenendo wa waislamu ukaendelea katika ‘’Kutafuta Baraka’’ kupitia athari za Mtume mpaka leo hii. Hadithi kuhusu hilo ni nyingi mno na hapa tutazitaja baadhi yake: PILI: Sahaba na Tabiina wakitafuta Baraka kupitia athari za Mtukufu Mtume baada ya kifo chake Bukhari ametenga mlango kuhusu: Yaliyotajwa kuhusu deraya ya Mtume, fimbo yake, upanga wake, bilauri yake, pete yake na vitu walivyotumia Makhalifa baada yake, miongoni mwa hivyo ambavyo mgao wake haujatajwa. Na nywele zake, viatu vyake na vyombo vyake, miongoni mwa vitu walivyotumia Sahaba zake na wengine kutafutia Baraka baada ya kifo chake.41 Kutoka kwa Abdullah bin Mawhabi amesema: “Mke wangu alinituma kwa Ummu Salama bilauri ya maji yenye nywele za Mtume, na ilikuwa mtu apatwapo na kijicho au kitu humpelekea kipakia rangi chake, basi nikachungulia ndani ya chupa ya rangi nikaona nywele nyingi nyekundu.”42 41 Sahih Bukhari 4: 46, Mlango wa yaliyotajwa kuhusu fimbo ya Mtume na upanga wake…. 42 Sahih Bukhari 7: 207. 20


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 21

Tabaruku

Pindi Muawiya alipokaribiwa na kifo aliusia azikwe ndani ya kanzu ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, joho lake na shuka lake na baadhi ya nywele zake.43 Umar bin Abdul-Aziz alipofikiwa na kifo aliomba nywele miongoni mwa nywele za Mtume na kucha miongoni mwa kucha zake kisha akasema: Nikifariki chukueni nywele na kucha muweke ndani ya sanda yangu.44 Ndani ya hunuti ya Anas bin Malik mliwekwa miski na nywele miongoni mwa nywele za Mtume.45 Mtoto wa Fadhil bin Ar-Rabiu walimpa Abu Abdullah – Yaani Ahmad bin Hambali- nywele tatu alipokuwa gerezani akamwambia: Hizi ni nywele za Mtume, basi Abu Abdullah akausia kuwa atakapofariki juu ya kila jicho uwekwe unywele mmoja na juu ya ulimi wake unywele mmoja.46 Kutoka kwa Ibnu Sirini amesema: Nilimwambia Ubayda: Tuna nywele za Mtume tulizipata kutoka kwa Anas au toka kwa ndugu wa Anas. Akasema: Kuwa na unywele wake mmoja kwangu ni jambo nilipendalo mno kuliko kuwa na dunia na yote yaliyomo ndani yake.47 Al-Waqidiyu ametaja kuwa Aisha Mama wa Waumini aliulizwa: Mmetoa wapi nywele hizi zilizopo kwenu? Akasema: “Hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu aliponyoa kichwa chake katika Hija yake aligawa nywele zake kwa watu, hivyo tukapata zile walizozipata watu.”48 43 As-Siratu Al-Halbiyatu 3: 109. Al-Isabah 3: 400. Tarikhu Damishki 59: 229. 44 At-Tabaqati 5: 406. Wasifu wa Umar bin Abdul-Aziz. 45 At-Tabaqati 7: 25, Wasifu wa Anas bin Malik. 46 Swifatu As-Swafuwatu 2: 357. 47 Sahih Bukhari 1: 51, Kitabu cha udhu , Mlango wa maji ambayo huoshewa nywele za mwanadamu. 48 Al-Mahgaziyu 3: 110. 21


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 22

Tabaruku

JINSI WALIVYOTAFUTA BARAKA KUPITIA KUNYWEA BILAURI YA MTUKUFU MTUME Kutoka kwa Sahl bin Saad ndani ya Hadithi amesema: “Siku hiyo akaja Mtume na kuketi ndani ya ukumbi wa Saqifa wa kizazi cha Saad akiwa yeye na Sahaba zake kisha akasema: ‘Tunyweshe ewe Sahlu.’ Nikawatolea bilauri hii na kuwanyweshea.” Mpokezi amesema: Sahlu akatutolea bilauri hiyo na tukanywea. Akasema: Kisha baada ya hapo Umar bin AbdulAziz akaiomba apewe kama zawadi na ndipo akapewa.”49 Kutoka kwa Anas: “Bilauri ya Mtume ilivunjika hivyo vipande vilivyokuwa vimesambaa akavitengenezea cheni ya fedha. Asimu amesema: Bilauri hiyo niliiona na nilinywea.”50 Abu Bardatu amesema: Abdullah bin Salami aliniambia kuwa: Nakunywesha ndani ya bilauri aliyonywea Mtume.51 Kutoka kwa Swafiyyah binti Bahratu amesema: “Ami yangu Faris aliomba zawadi ya bakuli kutoka kwa Mtume alilomwona Mtume akinywea, basi akampa bakuli hilo. Amesema: Alipokuwa Umar akituijia husema: “Nitoleeni bakuli la Mtume wa Mwenyezi Mungu.” Tunamtolea na analijaza maji ya Zamzam na kunywea na kumwagia juu ya uso wake.”52 49 Sahih Bukhari 6: 352 Kitabu cha vinywaji. Sahih Muslim 6: 103, Mlango wa Ruhusa ya Nabidhi ambayo haijanunuliwa na wala haijabadilika na kuwa kilevi. 50 Sahih Bukhari 4: 47, Mlango wa mwanzo wa uumbaji. 51 Sahih Bukhari 6: 352 Kiatabu cha vinywaji. 52 Al-Isabah 3:202, Herufi Al-Fau, sehemu ya kwanza, Wasifu wa Firasu namba 6971. Usudul-Ghaaba 4: 352, Herufi Al-Fau, Firasu ami wa Swafiyatu, namba 4202. Kanzul-Ummal 14: 264. 22


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 23

Tabaruku

JINSI WALIVYOTAFUTA BARAKA KUPITIA SEHEMU ALIYOWEKA MTUKUFU MTUME MKONO WAKE NA MDOMO WAKE Katika kisa cha Mtume kufikia nyumbani kwa Abu Ayyub Al-Ansari pindi alipohama na kufika Madina, Abu Ayyub amesema: “Tulikuwa tukimwekea chakula cha usiku kisha tunampelekea na anapoturudishia mabaki yake mimi na mama Ayyub hukusudia eneo aliloweka mkono wake, na huwa tunakula eneo hilo tukitafuta Baraka kupitia kitendo hicho. Mpaka usiku mmoja tukampelekea chakula chake cha usiku tukiwa tumemuwekea kitunguu maji na kitunguu Swaumu, basi Mtume wa Mwenyezi Mungu akakirudisha na wala sikuona athari ya mkono wake ndani yake, ndipo nilipomjia nikihofu na kumwambia: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, kwa haki ya baba yangu na mama yangu umerudisha chakula chako na wala sijaona ndani yake sehemu uliyoweka mkono wako? Akasema: “Hakika nimekuta humo harufu ya mti huu, na mimi ni mtu mwenye kuongea na Mwenyezi Mungu, ama ninyi kuleni bila shaka…..”53 Kutoka kwa Anas: Mtume aliingia nyumbani kwa Ummu Sulaymu, na ndani ya nyumba kulikuwa na kiriba kilichotungikwa chenye maji, ndipo akakichukua na kunywa kupitia mdomo wake ilihali kasimama. Basi Ummu Sulaymu akakichukua na kuukata mdomo wake kisha akauweka kwake.54 53 Dalailun-Nubuwat cha Al-Bayhaqiyu 2: 510. Siratu Ibnu Hisham 2: 144. AlBidayatu Wan-Nihayah 3: 201. 54 Musnad Ahmad 7: 520 hadithi ya 26574. At-Tabaqati 8: 313. 23


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 24

Tabaruku

Kutoka kwa Ummu Amiru - Jina lake ni Fakihatu au Asmaa - binti Yazid bin As-Sakanu, amesema: “Nilimwona Mtume wa Mwenyezi Mungu ameswali Magharibi msikitini kwetu nikaenda nyumbani kwangu nikamletea nyama na vipande vya mkate, kisha nikamwambia: Kula chakula cha usiku. Akawaambia Sahaba zake: Kuleni, basi akala yeye na Sahaba zake ambao walikuja……..” Amesema: Na akanywa kwangu kutumia mfuniko wa chupa, ndipo nikauchukua nikaupaka mafuta na kuuficha, na tulikuwa tukimnyweshea mgonjwa na baadhi ya wakati tukinywea tukitaraji kupata Baraka.”55 Kutoka kwa Abdur-Rahmani bin Abu Amratu kutoka kwa bibi yake Kulthum amesema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu aliingia kwetu na sisi tukiwa na kiriba kilichotungikwa basi akanywea maji, ndipo nilipoukata mdomo wa kiriba na nikakiondoa tukitafuta Baraka kupitia sehemu ulipokaa mdomo wa Mtume wa Mwenyezi Mungu.”56

JINSI WALIVYOTAFUTA BARAKA KUPITIA FIMBO YA MTUKUFU MTUME, MAVAZI NA PETE YAKE Kutoka kwa Muhammad bin Sirini kutoka kwa Anas bin Malik kuwa: “Alikuwa ana fimbo ya Mtume na alipokufa akazikwa pamoja nayo kati ya mbavu yake na kanzu yake.”57 55 Al-Isabah 4: 471, Herufi Al-Aynu, sehemu ya kwanza, Wasifu wa mama Amiru, namba 1374. At-Tabaqati 8: 234. 56 Usudul-Ghaaba 5: 539, Herufi Ak-Kafu, Wasifu wa Kulthamu namba 7243. Sunan Ibnu Majah 2: 1132. 57 Al-Bidayatu Wan-Nihaya 6:6. 24


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 25

Tabaruku

Kutoka kwa Ibnu Umar kuwa Mtume alitengeneza pete ya dhahabu au ya fedha na akaweka jiwe lake eneo la baada ya kitanga chake na kuliwekea nakshi ya: “Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu.” Basi watu wakatengeneza mfano wake. Alipowaona wameitengeneza akaiacha na kusema: “Sivai tena milele.” Kisha akatengeneza pete ya fedha na watu wakatengeneza pete za fedha. Ibnu Umar amesema: “Pete hiyo baada ya Mtume akaivaa Abu Bakr kisha Umar kisha Uthuman mpaka ilipodondokea ndani ya kisima cha Urisu toka kwa Uthumani.”58 Kutoka kwa Sahlu bin Saad amesema: “Mwanamke mmoja alikuja na shuka…… Akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, hakika mimi nimefuma shuka hii kwa mkono wangu ili nikufunike kwayo, basi Mtume akaichukua akiwa anaihitaji, ndipo alipotutokea huku ikiwa imemfunika, basi mtu mmoja katika kundi akaichunguza kwa mkono na kusema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu utanifunika hilo? Akasema: Ndiyo.” Akawa kwenye kikao muda, na kisha akarejea akalikunja na kumtumia. Ndipo watu wakamwambia mtu yule: Hukufanya vizuri umemwomba hilo shuka ilihali unajua kuwa huwa hamnyimi mwombaji. Yule mtu akasema: “Naapa kwa Mwenyezi Mungu, sikuomba ila liwe sanda yangu siku nitakayokufa.” Sahlu amesema: Na likawa sanda yake.59 Ibnu Hajar amesema: Na katika riwaya ya Abu Ghasan ni kuwa alisema: Nilitaraji Baraka zake pindi Mtume alipojifunika….. 58 Sahih Bukhari 7: 55 Kitabu cha vazi, Mlango wa pete ya fedha. Al-Istiab kwenye maelezo ya ziada ya Al-Isabah 2: 494, Wasifu wa Amru bin Saidi bin Al-Aswi. Sahih Muslim 3: 1656. An-Nasai 8: 196. Abu Daud 4: 88. Musnad Ahmad 2: 96 hadithi ya 4720. 59 Sahih Bukhari 7: 189, 2: 98, 3: 80, 8: 16. Musnad Ahmad 6:456, hadithi ya 22318. Sunan Ibnu Majah 2: 1177. 25


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 26

Tabaruku

Katika ufafanuzi wake akasema: “Faida inayopatikana ndani ya Hadithi hii: Mna ‘’Kutafuta Baraka’’ kupitia athari za waja wema.” Akasema: Al-Muhibu At-Tabari ndani ya Al-Ahkamu yake amefidisha kuwa: “Ni Abdur-Rahmani bin Aufi na akamnasibisha na AtTabarani.” Na wala sijamwona ndani ya Al-Muujamu Al-Kabir, si kwenye orodha ya hadithi za Sahlu wala za Abdur-Rahmani. Na Shekhe wetu Ibnu Al-Mulkinu amemnukuu toka kwa Al-Muhibu ndani ya Shar’hul-Umdati. Pia Shekhe wetu Al-Hafidhu Abul-Hasan Al-Haythamiyu ametuambia kuwa alimfatilia lakini hakupata alipo. Na Shekhe wetu Ibnu AlMulakinu ndani ya Shar’hu tam’mbihi amefikia kuwa ni Sahlu bin Saadu, na huko ni kujichanganya. Kisha akanukuu toka kwa At-Tabarani kuwa ni Saad bin Abu Waqqas. Na ndani ya riwaya nyingine imetoka kwake kuwa ni Bedui.60 Muawiya bin Abu Sufiyan alitaka kununua toka kwa Kaabi bin Zuhayri shuka la Mtume kwa thamani ya dirhamu elfu kumi ambalo alimvisha baada ya yeye kusilimu, lakini Kaabi akakataa na kusema: Siwezi kumtanguliza mtu yeyote kwa nguo ya Mtume wa Mwenyezi Mungu. Alipofariki Muawiya alituma dirhamu elfu ishirini kwa warithi wake na akalichukua toka kwao. Nalo ndilo shuka lilikuwepo kwa watawala na ndilo ambalo Makhalifa hulivaa kwenye sikukuu.61 Kutoka kwa Ummu Atwiyatu Al-Ansari. Radhi za Mwenyezi Mungu zimwendee. Amesema: Mtume aliingia kwetu pindi binti yake alipofariki 60 Fat’hul-Bari 3: 144, 28. Mlango wa aliyejiandaa na sanda zama za Mtume (s.a.w.w.) na hakumkataza, mwishoni mwa hadithi ya 1277. 61 Tabarruku As-Swahabati: 17. Tarikhul-Islami cha Ad-Dhahabiyu 2: 412. AsSiratu Al-Halbiyatu 3: 242. Tarikhul-Khulafai cha As-Suyuti: 19. 26


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 27

Tabaruku

akasema: “Mwosheni mara tatu au tano au zaidi mkitaka. Kwa maji na mkunazi na wekeni karafuu maiti katika josho la mwisho au sehemu ndogo ya karafuu maiti na mtakapomaliza niruhusuni. Tulipomaliza tulimruhusu na akatupa shuka na kusema: “Mfunikeni.” Yaani shuka lake.62 Kutoka kwa Muhammad bin Jabir amesema: “Nimemsikia baba yangu akitaja toka kwa babu yangu kuwa yeye ni mjumbe wa kwanza aliyekwenda kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kutoka kwa kizazi cha Hunayfa, alimkuta akiosha kichwa chake ndipo akasema: “Kaa ewe kaka wa jamaa wa Yamama na uoshe kichwa chako.” Nikaosha kichwa changu kutumia mabaki ya josho la Mtume wa Mwenyezi Mungu…… Nikamwambia: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu nipe kipande cha kanzu yako kinitulize moyo wangu. Akanipa. Muhammad bin Jabir amesema: Babu yangu akanisimulia kuwa kipande hicho kilikuwepo kwetu tukimwoshea mgonjwa na tukipona kwacho.63 Kutoka kwa Isa bin Tahmani amesema: Anas aliamuru na mimi nikiwa kwake akatoa viatu vikiwa na kamba mbili ndipo nikamsikia Thabiti AlBananiyu akisema: Hivi ni viatu vya Mtume.”64 62 Sahih Bukhari 2: 74, Kitabu cha jeneza, Mlango karafuu maiti huwekwa mwishoni. Sahih Muslim 2: 647. Musnad Ahmad 7: 556 hadithi ya 26752. AsSunan Al-Kubra cha Al-Bayhaqiyu 3:547, Mlango wa 34 hadithi ya 6634, 4: 6 Mlango wa 72 hadithi ya 6764. Sunann-Nasai 4: 31. 63 Al-Isabah 2: 102, Herufu As-Sinu sehemu ya kwanza Wasifu wa Sayawisi Huria wa Al-Yamaniyu, namba 3626. 64 Sahih Bukhari 7: 199, 4: 101. Al-Bidayatu Wan-Nihaya 6:6. At-Tabaqatu cha Ibnu Saad 1: 478. 27


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 28

Tabaruku

JINSI WALIVYOTAFUTA BARAKA KUPITIA MIMBARI YA MTUKUFU MTUME Mtume ameubainishia umma wake kuwa mimbari yake ina utukufu maalum haipasi kuvuka mipaka ukiwa juu yake, hivyo aliweka kanuni ya kuharamisha Kiapo cha Uongo juu ya mimbari yake akasema: “Atakayeapa juu ya mimbari akiwa mwongo angalau juu ya kijiti cha Araki basi ayaandae makalio yake kwa moto.”65 Kutoka kwa Jabir: Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema: Mtu yeyote miongoni mwa waislamu atakayeapa kwenye mimbari yangu ili kuchukua haki ya mwislamu mwingine kupitia kiapo hicho basi Mwenyezi Mungu atamwingiza motoni hata kama itakuwa ni juu ya kijiti kijani.66 Sahaba walilijua hilo na ndio maana tunamkuta Zaid bin Thabit anakataa kuapa juu ya mimbari pindi Marwan alipomuhukumu kufanya hivyo, akasema: “Apa badala yangu kwa ajili yake.” Zaid akaanza kuapa na akakataa kuapa juu ya mimbari na huku Marwan anamshangaa.67 Hivyo tunawakuta waheshimiwa Sahaba wanajua utukufu wa mimbari hii na Baraka zake ndio maana tunawakuta wanaendelea kugusisha mikono yao kwenye eneo lake la kati na kwenye makalio ya Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenye mimbari hiyo na wanaiweka sehemu hiyo ya kati juu ya nyuso zao ili wapate Baraka kupitia mimbari hiyo. Imepokewa kutoka kwa Ibrahim bin Abdur-Rahmani bin Abdul-Kari: Kuwa alimwona Ibnu Umar ameuweka mkono wake juu ya makalio ya 65 Musnad Ahmad 4: 357 hadithi ya 14606. Fat’hul-Bari 5: 210. At-Tabaqatu 1: 1/10. 66 Kanzul-Ummal 16: 697 hadithi ya 46389, na imo itokayo kwa Abu Huraira 67 Sahih Bukhari 3: 134. 28


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 29

Tabaruku

mimbari ya Mtume, kisha akauweka juu ya uso wake.68 Kutoka kwa Yazidi bin Abdullah bin Kusaytu amesema: Niliwaona watu miongoni mwa Sahaba wa Mtume wanapotoka Msikitini huweka mikono yao kwenye eneo la kati la mimbari ing’arayo ambayo iko karibu na kaburi kuliani kwao, kisha huelekea Kibla na kuomba dua.69

JINSI WALIVYOTAFUTA BARAKA KUPITIA KABURI LA MTUKUFU MTUME Sera ya Waislam tangu kufa kwa Mtume zama zote mpaka leo hii ni ‘Kutafuta Baraka’ kupitia kaburi la Mtume, kuomba mvua kupitia kaburi hilo na kuomba kupona kupitia udongo wake. Waislamu wote wameafikiana juu ya hilo bila kujali makundi yao kizazi baada ya kizazi na wala hakuna aliyekwenda kinyume nao ila Makada wa njia ya Salfaiya. Wa kwanza wao ni Ibnu Taymiya Al-Haraniyu ambaye alidai kuwa wema waliotangulia hawakulijua hilo na wala hawakulikubali. Isipokuwa vitendo vya waislamu wakiwemo Sahaba Wakubwa na Tabiina miongoni mwa Wanachuoni wao mabingwa na wasimulizi wao tena kwa idadi isiyodharaulika, vinapingana na madai hayo ya Ibnu Taymiya na kuyabatilisha, hivyo miongoni mwa ushahidi wa sera ya waislamu wakiwemo Sahaba Wema juu ya ‘Kutafuta Baraka’ kupitia kaburi la Mtume ni: Kutoka kwa Daud bin Salihu amesema: “Siku moja Marwan alikuja akamkuta mtu ameweka uso wake juu ya kaburi akamwambia: Je, unafahamu unachokifanya? Akamgeukia kumbe ni Abu Ayyub Al-Ansari akamjibu: Ndiyo, mimi nimemjia Mtume wa Mwenyezi Mungu na wala sikulijia jiwe, nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu akisema: Msiililie 68 At-Tabaqatul-Kubra 1: 254, Kutaja mimbari ya Mtume. At-Thuqati cha Ibnu Habani:9 69 At-Tabaqatul-Kubra 1: 254, Kutaja mimbari ya Mtume. 29


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 30

Tabaruku

dini kama mtawala wake ni mtu anayestahili lakini ililieni dini kama mtawala wake ni mtu asiyestahili.70 Kutoka kwa Ali (a.s.) amesema: Kuna bedui alikuja kwetu baada ya kuwa zimepita siku tatu tangu tumemzika Mtume wa Mwenyezi Mungu, akajitupa kwenye kaburi la Mtume, akajipaka kichwani udongo wa kaburi lake na akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ulisema tukasikia usemi wako na uliyapokea toka kwa Mwenyezi Mungu nasi tulipokea toka kwako, na miongoni mwa yale uliyoteremshiwa ni “Na lau wangelikujia walipojidhulumu nafsi zao…….” Na mimi nimejidhulumu na nimekujia uniombee msamaha. Basi ikanadiwa kutoka Kaburini: Hakika Mwenyezi Mungu amekusamehe.71 Al-Hafidh bin Al-Asakir ametoa ndani ya At-Tuhufa kwa njia ya Twahiru bin Yahya Al-Husayn amesema: “Baba yangu amenisimulia kutoka kwa babu yangu kutoka kwa Jafari bin Muhammad kutoka kwa baba yake kutoka kwa Ali (a.s.) amesema: Alipozikwa Mtume wa Mwenyezi Mungu Fatima alikuja na akasimama juu ya kaburi lake, akachukua gao la udongo wa kaburi na kuuweka juu ya macho yake huku akilia na akaanza kusema: Mtu aliyenusa udongo wa Kaburi la Ahmad halaumiwi iwapo milele hatonusa manukato mazuri. Yamenipata masaibu ambayo laiti yangeliupa-

70 Al-Mu’jamul-Awsatu 1:94. Al-Jamius-Swaghiru cha As-Suyuti: 728. KanzulUmmal 6: 88 hadithi ya 14967. Talkhisu Maj’mauz-Zawaidi cha Ad-Dhahabi :4 22. Wafaul-Wafa cha As-Samuhudiyu 2: 410. Shafaul-Asiqami cha As-Sabkiyu: 152. 71 Ar-Raudhu Al-Faiqu: 380. Al-Mawahibul laduniyya cha Al-Qastalani 4: 583. Mashariqul-Anwari 1: 121. Wafaul-Wafa 4: 1399. Kanzul-Ummai 2: 386 hadithi ya 4322 na 4: 259 hadithi ya 10422. 30


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 31

Tabaruku

ta Mchana basi ungeligeuka na kuwa Usiku.72 Al-Khatibu bin Jamaatu amesema kuwa Abdullah bin Umar alikuwa akiweka mkono wake wa kulia juu ya Kaburi Tukufu, na kuwa pia Bilali aliweka shavu lake juu yake. Na nimeona ndani ya Kitabu As-Suulati cha Abdullah bin Imamu Ahmad - Ameitaja Hadithi iliyotangulia kutoka kwa Ibnu Jamaatu - Kisha akasema: Bila shaka kuzama ndani ya mapenzi kunapelekea kuruhusu hilo, na makusudio ya hayo yote ni kumuheshimu na kumtukuza. Watu wametofautiana viwango katika hilo kama vilivyokuwa vimepishana zama za uhai wake, hivyo wapo watu wanapomwona walikuwa hawazimiliki nafsi zao na wanaharakisha kwake. Na baadhi ya watu miongoni mwao ni wazito wanachelewa, na wote wako sehemu ya kheri.73 Kutoka kwa Abu Darda amesema: “Bilali mwadhini wa Mtume siku moja alimuona Mtume wa Mwenyezi Mungu ndotoni akimwambia: Ewe Bilali mbona umenitupa kiasi hiki? Je, haujakufikia wakati wa kunizuru ewe Bilali? Basi Bilali akazindukana usingizini akiwa na huzuni na hofu nyingi. Akapanda kipando chake kuelekea Madina na akafika kwenye Kaburi la Mtume na akawa analia pale kaburini huku anausugua uso wake kwenye Kaburi. Mara Hasan na Husein wakafika na hapo akawakumbatia na

72 Imepokewa na Ibnu Al-Jawzi ndani ya Al-Wafaul-Wafa fi Fadhailil-Mustafa: 819 hadithi ya 1538. Na Ibnu Sayidin-Nasi fi As-Sirati An-Nabawiyati 2: 432. Na imepokewa kwa ufupi na Al-Qastalani ndani ya Al-Mawahibu Ad-Duniyatu 4: 563. Na Al-Qariu ndani ya Shar’hus-Shamaili 2:210. Na As-Shabrawayi ndani ya Al-Itihafi: 330. Na As-Samuhudi ndani ya Wafaul-Wafa 4: 1405. Siratu AalamunNublai 2: 134 na wengineo. 73 Wafaul-Wafa cha As-Samuhudi 4: 1405. 31


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 32

Tabaruku

kuwabusu.74 As-Samuhudi amesema: “Walikuwa wakichukua udongo wa Kaburi ndipo Aisha alipoamuru ukawekwa ukuta kuwazuia, na kwenye ukuta kulikuwa na dirisha, hivyo wakawa wanauchukua kupitia dirisha hilo, ndipo alipoamuru kuziba dirisha na likazibwa.�75 As-Samuhudi amesema kuwa watu walikuwa wakitafuta Baraka kwa kuswali kwenye Kaburi.76 Akasema: Imepokewa kutoka kwa Hishamu bin Urwa amesema: Baba yangu alinipa Hadithi akasema: Watu walikuwa wakisali kwenye Kaburi ndipo Umar bin Abdul-Aziz akaamuru ujengwe ukuta basi ukuta ukainuliwa ili mtu asisalie hapo.77 Ibnu Munkadiru - mmoja wa Wanachuoni wakubwa wa Tabiina - alikuwa akiketi pamoja na Sahaba zake, amesema: Alikuwa akipatwa na ukimya basi ananyanyuka kama alivyo na kuweka shavu lake juu ya kaburi la Mtume kisha anarejea. Basi akaulizwa kuhusu hilo, akasema: Hunisibu ukimya ghafla, na nikipatwa na hali hiyo huomba kupona kupitia kaburi la Mtume. Na alikuwa anakuja eneo maalumu la Msikiti la katikati na kujisugua hapo na kujilaza. Akaulizwa kuhusu hilo, akasema: Hakika mimi nilimwona Mtume akiwa sehemu hii. Yaani usingizini.78 Ibnu Qadama Al-Hambali ndani ya Al-Mughuniyu amesema: Ni Sunna 74 Tarikh Damashki cha Ibnu Asakir 7: 137. Muhtadharu Tarikh Damashki 4: 118, 5: 265. Tahdhibul-Kamali 4: 289. Usudul-Ghaaba 1: 244. Wafaul-Wafa cha As-Samuhudi 4: 1356. Shifaus-Saqami: 53. Mashariqul-Anwari 1: 121. 75 Wafaul-Wafa 1: 544. 76 Yaani Kaburi la Mtume 77 Wafaul-Wafa 2: 547. 78 Al-Waful-Wafa 2: 444 Kutoka kwa Abu Khaythamu Zuhayru bin Harbi amesema: Ametusimulia Masuabu bin Abdallah, ametusimulia Ismaili bin Yakub AtTaymiyu. 32


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 33

Tabaruku

kuzika ndani ya eneo la makaburi ambamo wamezikwa mawalii wengi na mashahidi ili apate Baraka zao, na pia kwenye viunga vitukufu. Huu ndio mwenendo walioufata Sahaba na Tabiina katika kutaka Baraka kupitia kaburi la Mtukufu Mtume na kutafuta kupona kupitia udongo wake na hakuna yeyote aliyewakhalifu ila Watawala wa Kizazi cha Umayyah, mfano wa Marwan bin Al-Hakam aliyefukuzwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu, ambaye Mwenyezi Mungu alimlani tangu akiwa kwenye mifupa ya mgongo wa baba yake. Kama alivyotoa Hadithi hiyo Aisha na Abdullah bin Zubair.79

HOJA YA UTATA YA ALIYANI Ali bin Nafiy Aliyani amesema: “Na kuhusu hili ni kuwa hali ya watu wa zama za Ujahiliya ni kama hali ya mwanadamu mwingine yeyote, wanatamani mafanikio na ustawi katika mali zao, miili yao, makkabila yao, watoto wao na kila wanachokihitaji ndani ya uhai huu wa dunia. Mafanikio haya na ustawi huu ambao ndio Baraka yenyewe; huutafuta kutoka kwenye masanamu yao kwa kuamini kwao kuwa haya masanamu huleta heri nyingi na kuwa yenyewe yamebarikiwa. Na hata wanaonasibisha kitendo hiki kwa Mwenyezi Mungu na wao wanaamini kuwa haya masanamu na roho zinazokaa humo vina mchango mkubwa katika kumuathiri Mwenyezi Mungu ili awatimizie wanayoyataka. Na hii ndio maana ya usemi wao: “Na wala hatuwaabudu ila ili watukurubishe kwa Mwenyezi Mungu.” Kwa ajili hiyo ‘’Kutafuta Baraka’’ ulikuwa ni mfano halisi miongoni mwa mifano ya Uabudu Masanamu zama za 79 Maj’mauz-Zawaidi 5: 241. Al-Istiab 3: 425. Wasifu wa Marwan bin Al-Hakami na Wasifu wake ndani ya Usudul-Ghaba 5: 144, namba 4841, As-Sunan al-Kubra cha An-Nasai 6: 485 33


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 34

Tabaruku

Ujahiliya wa mwanzo.”80 Hakika maneno haya yako mbali na mantiki kwani anataka kulinganisha kati ya niya na matendo ya Waislamu na yale matendo mukabala ya washirikina. Na yeye anatoa hoja kutumia kauli ya Mwenyezi Mungu katika Aya aliyoitoa huku akijisahaulisha kuwa muundo mzima wa Aya unaongea kwa ulimi wa washirikina kuwa: “Hatuwaabudu” na wala haujasema: “Hatutafuti Baraka kwao.” Hivyo washirikina wa zama za ujahiliya walikuwa wakiviomba vitu alivyovitaja Aliyani kwa kuamini kuwa Miungu hii inadhuru na inanufaisha bila uwezo wa Mwenyezi Mungu. Hivyo mshirikina hakuwa anaamini Ufufuo na Mtawanyiko, Thawabu na Adhabu, kwa ajili hiyo alikuwa akiyaabudu masanamu haya kwa imani kuwa yenyewe yanaweza kumletea madhara ya kimaada hapa duniani, kama vile kuteketeza wanyama wake, mazao yake au kumpa ugonjwa angamizi na mengineyo, na wakati huo huo alikuwa anaamini kuwa yana uwezo wa kumpa heri anayoihitaji. Ni wapi yanafanana matendo haya ya mushirikina na matendo ya Waislamu Wanatauhidi ambao wanaamini kuwa heri yote inatoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na kuwa Baraka zake huteremka kwa idhini yake yeye, huku akiwa amehadithisha ndani ya Kitabu chake Kitukufu kuhusu kuwepo viumbe vyake alivyoviwekea sifa ya ziada na kuvifanya vibarikiwa na kwa kuwa Mwenyezi Mungu anavipenda viumbe hivi vilivyobarikiwa basi amevikirimu kwa kuvifanya sababu ya kujibiwa dua za viumbe kwa wao kutawasali kupitia viumbe hivyo kutokana na hadhi yao mbele ya Mwenyezi Mungu. Huenda kauli bora inayowakilisha imani ya waislamu katika ‘’Kutafuta Baraka’’ ni kauli ya Khalifa wa kizazi cha Abbas Al-Maamun akimwambia Kadhi Yahya bin Akthamu: Bila shaka mtu atakaponiletea kipande cha kiji80 At-Tabaruku Al-Mash’ruu 53. 34


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 35

Tabaruku

ti au ubao au kitu ambacho huenda thamani yake haiwi ila dirhamu moja au mfano wake kisha aseme: Hiki kilikuwa cha Mtume au aliweka mkono wake juu yake au chini yake au alikigusa, ilihali kwangu yeye si mwaminifu na wala sina dalili juu ya ukweli wa mtu huyo, basi mimi kwa niya na mapenzi ya dhati nakubali hilo na kukinunua kwa thamani ya dinari elfu moja na zaidi au chini kidogo, kisha nakiweka juu ya uso wangu na macho yangu na ‘’Kutafuta Baraka’’ kwa kukitazama na kukigusa. Na nitaombea kupona wakati wa ugonjwa utakaonisibu au kumsibu ninayemjali na nitamkinga kama ninavyojikinga mwenyewe, ilihali si chochote bali ni kijiti tu ambacho yeye hajakifanya chochote wala hakina sifa yoyote inayolazimu mapenzi ila ni kule tu kusema kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu alikigusa.81 Hivyo Al-Maamun anajua kuwa kijiti hiki chenyewe kama kijiti hakinufaishi wala hakidhuru lakini anakiheshimu kwa ajili ya kumuheshimu Mtume na hiyo ndio imani ya waislamu. Hapo iko wapi imani ya Mushirikina?!

JINSI MASAHABA WALIVYOTAFUTA BARAKA KUPITIA MAENEO ALIYOSALIA MTUKUFU MTUME Hili ni jambo lingine ambalo Salafiya na Mawahabi wameikhalifu jamuhuri nzima ya Waislam, kwani sera ya Waislam kwa ujumla wao na zama zote ni ‘’Kutafuta Baraka’’ kupitia kila eneo alilofika Mtume wa Mwenyezi Mungu na hulichukulia kuwa ni eneo lenye Baraka na hasa maeneo ambayo alikuwa akiketi mara kwa mara, kama vile kuketi juu ya Mimbari yake na Pango la Hira na Nyumbani kwake na maeneo mengine kwa kuzingatia kuwa ni maeneo yaliyochukua Baraka kutoka kwenye mwili wa Mtume Mtakasifu. 81 Tarikh Baghdadi cha Ibnu Twayfuri 45. 35


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 36

Tabaruku

Kama Sahaba walivyokuwa wakitafuta Baraka kwa kutumia kuugusa mwili wake mtukufu. Bila shaka Waislam wote wakiwemo Sahaba wema pia walikuwa wakitafuta Baraka kutumia maeneo ambayo yaliguswa na mwili wake mtukufu. Wala hakuna asiyekuwa Wahabi anayewakhalifu Waislam katika hilo, hivyo wao huzuia ‘’Kutafuta Baraka’’ kwenye maeneo yaliyobarikiwa au maeneo ambayo alisalia Mtume wa Mwenyezi Mungu huku wakitoa dalili mbovu kama vile kauli ya Nasiri bin Abdur-Rahmani bin Muhammad AlJadiu aliyetoa dalili mbili: Moja wapo ni: Hakuna dalili kutoka kwenye maelezo ya kisheria (Aya na Hadithi.) yanayoonyesha ruhusa ya kitendo hicho au usunna wake. Ya pili ni: Sahaba kwa umoja wao hawajanukuu kutoka kwa yeyote miongoni mwao kuwa yupo aliyetafuta Baraka kupitia eneo lolote kati ya maeneo ambayo aliketi Mtume wa Mwenyezi Mungu au kiunga alichosalia humo Mtume rehema na amani ziwe juu yake. Huku wao ndio umma wenye shauku mno ya Kuomba Baraka kupitia Mtume na wanayajua maeneo hayo na wana mapenzi mno kwa Mtume na wakimuheshimu ilihali wakifuata Sunna zake.82 Hizi ndio dalili mbili ambazo anazitoa Al-Jadiu akiamini kuwa ameshinda ushindi mkubwa katika suala hili, ilihali kwa hakika zenyewe ni mbovu mno kuliko utando wa buibui, kwani ikiwa hakuna dalili ya Maelezo ya Kisheria inayoruhusu hilo au kulifanya Sunna, basi pia upande wa pili hakuna dalili ya Maelezo ya Kisheria inayoonyesha kuwa hilo haliruhusiwi au kuwa ni Karaha. Hivyo kanuni ni kuwa inapokosekana dalili ya kuharamisha basi 82 At-Tabaruku Anuwaihi Waahkamihi: 243 – 244. 36


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 37

Tabaruku

kukosenekana huko huonyesha uhalali wake. Ama usemi kuwa haijanukuliwa kutoka kwa Sahaba yeyote kuwa yupo aliyetafuta Baraka kupitia eneo lolote, hoja hiyo ni mbovu zaidi kuliko hoja yake ya kwanza, kwani wasimulizi wa hadithi wametoa hadithi zinazotengua dai hilo na tayari hadithi nyingi zimeshatangulia. Na pia tunasema: Imepokewa kutoka kwa Musa bin Akaba amesema: Nilimwona Salimu bin Abdullah akitafuta maeneo maalumu njiani kisha anaswali humo huku akisimulia kuwa baba yake alikuwa akisalia humo na kuwa alimwona Mtume akisali kwenye maeneo hayo. Na Nafiu alinisimulia kutoka kwa Ibnu Umar kuwa alikuwa akisalia kwenye maeneo hayo, na nilimuuliza Salim, hivyo hakuna eneo alilolijua isipokuwa aliafikiana na Nafiu katika maeneo yote, ila wao walitofautiana kuhusu eneo la Msikiti karibu na Ar-Rahau.83 Ibnu Hajar katika kufafanua Hadithi hii amesema: Kutokana na kitendo cha Ibnu Umar imejulikana kuwa ni Sunna kufuatilia athari za Mtume na ‘’Kutafuta Baraka’’ kupitia athari hizo.84 Ibnu Abdul-Bari amesema: Ibnu Umar alikuwa mwingi wa kufatilia athari za Mtume…….na alikuwa akitangulia kusimama maeneo aliyosimama Mtume huko Arafa na maeneo mengine ambayo Mtume alisimama hapo.85 Ibnu Athir amesema: Hakika Abdullah bin Umar alikuwa mwingi wa 83 Sahih Bukhari 1: 130. Kanzul-Ummali 6: 247. Al-Isabah 2: 349 Herufi AlAynu, sehemu ya kwanza, wasifu wa Abdullah bin Umar, namba 4834. AlBidayatu Wan-Nihayatu 5: 149. 84 Fat’hul-Bari 1: 469. Asw-Swarimu: 108 kutoka kwa Imamu Malik kuwa ni Sunna kuswalia maeneo aliyosalia Mtume (s.a.w.w.) 85 Al-Istiab 2: 342, kwenye maelezo ya Al-Isabah, wasifu wa Abdullah bin Umar. 37


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 38

Tabaruku

kufatilia athari za Mtume wa Mwenyezi Mungu mpaka akawa anafikia alipofikia Mtume na kuswalia kila eneo alilosalia Mtume. Na Mtume alifikia chini ya Mti hivyo Ibnu Umar akachukua dhamana ya kuumwagilia maji ili usikauke.86 Kutoka kwa Nafiu: Hakika Abdullah bin Umar alikuwa akifikia eneo la Makka lililopo Dhul-Halifa ambalo Mtume wa Mwenyezi Mungu alikuwa akifikia hapo na kuswalia hapo.87 Al-Waqidi amesema: Na kutoka kwa Aflahu bin Hamid kutoka kwa baba yake amesema: Ibnu Umar alikuwa akitupa Hadithii kuwa Mtume alikaa chini ya Mti wa Summaratu, na Ibnu Umar alikuwa akimwagia vitu chini yake kwenye shina la mti akitaka uendelee kubaki.88 Hivyo vitendo vya Ibnu Umar vingekuwa haviruhusiwi basi Sahaba wangempinga na kumkataza. Al-Aliyani amesema - Kuhusu kuzuwiliwa ‘’Kutafuta Baraka’’ kupitia maeneo na viumbe visivyo hai - “Wala hilo halichafuliwi na riwaya aliyoipokea Bukhari ndani ya Sahih yake kuwa: Ut’banu bin Malik - ambaye ni mmoja wa Sahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu na miongoni mwa Ansari aliyeshuhudia Badri - kuwa alimjia Mtume wa Mwenyezi Mungu na kumwambia: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu macho yangu hayaoni na mimi huwaswalisha jamaa zangu na inaponyesha mvua bonde lililopo kati yangu na wao hufurika maji na huwa siwezi kwenda kuwaswalisha msikitini kwao. Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu nimependelea wewe uje kwangu na usali nyumbani kwangu ili nipafanye sehemu ya kuswalia.” Mtume wa Mwenyezi Mungu akamwambia: “Nitafanya hivyo Mola 86 Usudul-Ghaaba 3: 34, wasifu wa Abdullah bin Umar, namba 3080. 87 Musnad Ahmad 2: 269, hadithi ya 5968. Sahih Bukhari 3:140. Sahih Muslim 2: 1981. 88 Maghazi Al-Waqidi 2: 1096, Mlango wa Hija ya kuaga. 38


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 39

Tabaruku

akipenda.” Ut’banu amesema: Ndipo Mtume wa Mwenyezi Mungu na Abu Bakar wakaja Asubuhi pindi Mchana ulipoinuka, hapo Mtume akaomba ruhusa na nikamruhusu. Alipoingia ndani hakukaa sana akawa amesema: Ni eneo lipi la nyumba yako unapenda nisalie? Amesema: Nikamwashiria upande mmoja wa nyumba. Hapo Mtume wa Mwenyezi Mungu akasimama na kutoa Takbira nasi tukasimama na kupanga safu, akaswali rakaa mbili kisha akatoa salamu.89 Kwa sababu lengo la Ut’banu si ‘’Kutafuta Baraka’’ kupitia eneo alilosalia Mtume bali lengo lake ni Mtume aridhie Sala ya Jamaa nyumbani kwake pindi anapokuwa hana uwezo wa kuhudhuria Jamaa pindi bonde linapofurika maji, hivyo akataka Mtume amfungulie Msikiti ndani ya nyumba yake, na kwa ajili hii ndio maana Bukhari ameweka mlango ndani ya Sahih yake kwa anuani ya: Mlango wa misikiti ya majumbani. Na Al-Barau bin Azib alisali Jamaa ndani ya msikiti wake nyumbani kwake – na hili linatokana na elimu yake. Mwenyezi Mungu amrehemu Hivyo lengo ni Mtume amfungulie sheria ya kuswali Sala ya Jamaa ndani ya nyumba yake wakati wa haja kama ilivyokuwa kwa Sahaba mwingine Al-Barau bin Azib aliyeweka Jamaa ndani ya msikiti wake ndani ya nyumba yake na wala hakuzuiliwa ilihali yeye akiishi zama za kuwekwa Sheria. Na inawezeka malengo ya Ut’bani ni kuipata Qibla yenyewe halisi, kwani Mtume wa Mwenyezi Mungu haridhii makosa laiti akisali kwa kuelekea upande usio Qibla.90” Nasema: Bila shaka hamu ya Sahaba Ut’bani kutekeleza Sala ya Jamaa ndani ya nyumba yake ni moja ya sababu za hilo, lakini si zote. Kwani hamu yake katika ‘Kutafuta Baraka’ kupitia eneo alililosalia Mtume iko 89 Sahih Bukhari 1: 115, 170, 175. Sahih Muslim 1: 445, 61, 62. 90 At-Tabaruku Al-Mash’ruu: 68 – 69. 39


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 40

Tabaruku

wazi, na Mtume alifahamu hamu hii ya Ut’bani ndio maana akaharakisha kumuuliza kuhusu eneo ambalo anapenda aswalie kwa ajili yake ndani ya nyumba yake. Na laiti jambo hilo lingelikuwa kama anavyosema Aliyani basi Mtume angelisalia eneo lolote la nyumba hiyo linalofaa kwa sala. Upande wa pili ni kuwa: Dai la Aliyani kuwa hamu ya Sahaba Ut’bani ni kuipata Qibla yenyewe halisi, dai hilo halina hoja kwani mkewe au Sahaba mwingine alikuwa ana uwezo wa kumjulisha Qibla hiyo na wala jambo hilo lisingelihitaji Mtume aswali rakaa mbili eneo hilo, jambo linalojulisha kuwa haikuwa sala ya faradhi. Ilikuwa inatosha aashirie upande wa Qibla ili Sahaba huyo afanye ni dalili juu ya Qibla. Na wala sidhani kwamba Aliyani alikuwa na uwezo wa ufahamu kuliko Allamatu Ibnu Hajar Al-Askalani ambaye katika kufafanua hadithi hii amesema: “Na hakika Mtume aliomba ruhusa kwa sababu aliitwa aswali ili mwenye nyumba apate Baraka kupitia eneo alilosalia Mtume, hivyo akamwomba aswalie eneo ambalo ni lazima kulitenga kwa ajili ya hilo.”91 Na pia akasema: Na katika hadithi ya Ut’bani na ombi lake kwa Mtume ili aje aswali ndani ya nyumba yake ili eneo hilo alifanye sehemu ya kuswalia na kule Mtume kukubali ombi hilo, vyote ni dalili ya kuruhusu ‘Kutafuta Baraka’ kutumia athari za waja wema.92 Ikiwa ombi la Ut’banu kwa Mtume ili aje aswali ndani ya nyumba yake ni kwa sababu ambazo kazidai, basi tutasema nini kuhusu ombi la Ummu Sulaymu na Sahaba wengine waliyomwomba aswalie ndani ya nyumba zao, kama ilivyo katika simulizi walizotoa wanahadithi na kama ifuatavyo: Kutoka kwa Anas bin Malik kuwa: Ummu Sulaymu alimwomba Mtume 91 Fat’hul-Bari 1: 433. 92 Fat’hul-Bari 1:469. 40


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 41

Tabaruku

aende kwake na aswali ndani ya nyumba yake ili aifanye sehemu ya kuswalia, basi akaenda kwake. Akamtandikia mkeka na kuunyunyuzia maji na ndipo Mtume akaswali na wakaswali pamoja nae.93 Pia imepokewa kutoka kwake amesema: “Ami yangu alitengeneza chakula na akamwambia Mtume: ‘Hakika mimi napenda ule nyumbani kwangu na usalie kwangu.’ Amesema: Akaenda kwake ilihali nyumbani kwake kukiwa na dume kati ya madume haya, basi akaamuru upande mmoja ufagiliwe, ukafagiliwa na kunyunyuziwa maji kisha akaswali na tukaswali pamoja naye.”94 Pia imepokewa kutoka kwake kuwa: “Amesema: Kuna mtu mnene alikuwa hawezi kuswali pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu, basi akamwambia Mtume: Mimi siwezi kuswali pamoja na wewe hivyo natamani ungekuja nyumbani kwangu ili nikufate katika Swala. Basi mtu yule akatengeneza chakula kisha akamwita Mtume, akanyunyuzia maji upande mmoja wa mkeka wao na ndipo Mtume akaswali rakaa mbili.95 Je, pindi Ummu Sulaymu alipomwomba Mtume aswali ndani ya nyumba yake lengo lake alikuwa anataka awe Imamu wa Waislam nyumbani kwake kama Ut’bani? Au yeye alimwomba ili apate Baraka kwa kuswalia eneo ambalo ataswalia Mtume wa Mwenyezi Mungu? Na je, ami wa Anas na mtu mwingine ambaye jina lake halijatajwa nao ni vipofu, hivyo Mtume akaja ili awalengee Qibla halisi? Na kama malengo ya mtu huyo si kutaka Baraka, kwani haikuwa inatosha kumwomba Mtume 93 Sunanin-Nasai 1: 268 Kitabu cha misikiti, mlango wa Sala juu ya mkeka, hadithi ya 816. 94 Sunan Ibnu Majah 1: 249, Kitabu cha Misikiti. Mlango wa Misikiti majumbani, hadithi ya 756. Musnad Ahmad 3: 13 kwa njia mbili. Musnad Anas bin Malik hadithi ya 11920. 95 Musnad Al-Imamu Ahmad 3: 586, Hadithi ya 11920, chapa ya Taasisi ya Historia ya Uarabu. 41


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 42

Tabaruku

ruhusa ya kutokuhudhuria sala msikitini kutokana na kuwa vigumu juu yake. Hivi hilo halikutosha bila haja ya kumwomba Mtume ahudhurie nyumbani kwake ili aswali ndani ya nyumba yake.

JINSI SAHABA WALIVYOTAFUTA BARAKA KUPITIA SAHABA NA WAJA WEMA Kutokana na maelezo yaliyotangulia imebainika kuwa hakuna tofauti kati ya makundi ya Waislam katika ruhusa ya ‘Kutafuta Baraka’ kupitia Mtume zama za uhai wake na kwa athari zake baada ya kifo chake. Na kuwa baadhi ya dalili walizozitoa baadhi ya wapingaji hazikubaliki na zinabatilishwa na vitendo vya Sahaba wenyewe. Isipokuwa tofauti ni je, inaruhusiwa ‘Kutafuta Baraka’ kwa kutumia asiye kuwa Mtume (s.a.w.w.) kuanzia Sahaba, Tabiina na Waja Wema? Au hairuhusiwi? Baadhi ya wanazuoni wa kiislamu wameruhusu hilo na wengine wamezuia hilo. Miongoni mwa waliozuia hilo ni As-Shatwabiyu amesema: “Sahaba, radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, hata mmoja miongoni mwao, baada ya kifo cha Mtukufu Mtume hakufanya hilo kupitia yule aliyeachwa na Mtume, kwani Mtume hakumwacha aliye bora baada yake ndani ya umma kuliko Abu Bakr, kwani yeye alikuwa ndiye Khalifa wake na wala hakijafanywa chochote kwake kuhusiana na hilo. Wala kwa Umar na yeye ndiye aliyekuwa mbora ndani ya umma baada yake, kisha vilevile kwa Uthmani, kisha kwa Ali, kisha kwa Sahaba wengine ambao hakuna yeyote ndani ya umma huu aliye mbora kuliko wao.

Kisha haijamthibitikia mtu yeyote miongoni mwao kwa njia sahihi iliyo 42


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 43

Tabaruku

maarufu kuwa mwenye ‘Kutafuta Baraka’ alitafuta Baraka kupitia Sahaba kwa kutumia moja kati ya nyuso hizo au mfano wake. Bali waliishia kufuatana kwenye vitendo, kauli na mwenendo ambao walimfuata Mtume, hivyo hiyo ni Ijimai kutoka kwao juu ya kuacha mambo hayo.”96 Pia akasema: “Haisihi mtu aliyekuja baada yake (ya Sahaba) kumfuata katika kitendo cha ‘Kutafuta Baraka’ kutumia nyuso hizo au nyingine, na atakayemfata basi huku kufuata kwake kutakuwa ni bidaa.”97 Na miongoni mwa wanaozuia ni Ibnu Rajabu aliposema: “Pia ‘Kutafuta Baraka’ kutumia athari, hakika hilo walikuwa wakilifanya Sahaba kupitia Mtume na walikuwa hawalifanyi kupitia baadhi yao…. Na Tabiina hawalifanyi kupitia Sahaba japokuwa hadhi yao ni ya juu, hivyo hilo likaonyesha kuwa hiki (kitendo cha ‘Kutafuta Baraka’) hakifanywi ila kwa kupitia Mtume, kama vile ‘Kutafuta Baraka’ kutumia udhu wake, masaze yake na nywele zake, pia kunywa mabaki ya kinywaji chake na ya chakula chake.”98 Hivyo dai la wenye kuzuia limesimamia msingi wa kuwa Sahaba hawajatafuta Baraka kupitia baadhi yao wala Tabiina hawajatafuta Baraka kupitia wao Sahaba, hivyo huku kuacha kwao kukaonyesha kuwa hairuhusiwi ‘Kutafuta Baraka’. Isipokuwa ni kuwa dai la kuwa Sahaba hawakuwahi ‘Kutafuta Baraka’ kupitia baadhi yao na pia kuwa hawakutafuta Baraka kupitia Kizazi cha Mtume, dai hilo si sahihi. Kwani kuna ushahidi sahihi juu ya kutokea hilo, na baadhi ya wanazuoni wakubwa wa kiislamu wametumia ushahidi huo ‘Kutafuta Baraka’, si kwa kutumia Sahaba na Tabiina tu bali hata kwa kutumia kila mwenye kheri na wema. Miongoni mwa walioruhusu wakisema hilo ni Imamu An-Nawawi ambaye 96 Al-I’itiswamu 2: 8. 97 Al-I’itiswamu 2: 10. 98 Al-Hukmu Al-Jadiratu Bil-Idhaatu: 55. 43


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 44

Tabaruku

ametumia baadhi ya riwaya sahihi zinazoelezea kisa cha Umar bin AlKhattabi alivyoomba mvua kupitia Abbas na jinsi baadhi ya Sahaba walivyoomba mvua kupitia wale walio wema miongoni mwao. Amesema: “Inaruhusiwa kuomba mvua kupitia walio wema katika ndugu wa karibu wa Mtume kwa sababu Umar aliomba mvua kupitia Abbas akasema: “Ewe Mwenyezi Mungu bila shaka tulikuwa tunapopatwa na ukame tunaomba kwako kupitia Mtume wetu na ukitupa mvua, basi sasa tunakuomba kupitia kwa ami ya Mtume wetu basi tupe mvua.” Basi hupewa mvua. Na mvua huombwa kupitia watu wema kutokana na riwaya iliyopokewa kuwa Muawiya aliomba mvua kupitia Yazid bin Al-Aswad akasema: “Ewe Mwenyezi Mungu sisi tunakuomba mvua kupitia aliye mbora wetu na mwenye kheri zaidi yetu, ewe Mwenyezi Mungu sisi tunakuomba mvua kupitia Yazid bin Al-Aswad. Ewe Yazid inua mikono yako kwa Mwenyezi Mungu. Basi akainua mikono yake na watu wakainua mikono yao, ndipo mawingu yakatembea kutoka magharibi na upepo ukayapiga na hapo wakapata mvua kiasi kwamba ikabakia kidogo watu washindwe kuyafikia majumba yao.”99 Ibnu Hajar ametumia tukio la Umar kuomba mvua kupitia Abbas kuthibitisha ruhusa ya ‘Kutafuta Baraka’ na ‘Kuomba Shifaa’ kupitia baadhi ya watu wema akisema: Kutokana na kisa cha Abbas tunapata kuwa ni Sunna kuomba Shifaa kupitia watu wema wenye kheri na Watu wa

99 Al-Maj’mua Shar’hul-Muhadhabi cha Imamu An-Nawawi 5: 68, Kitabu cha Sala, mlango wa Sala ya kuomba mvua, na Ibnu Hajar amesema: Abuz-Zur’atu Ad-Damashiqiyu ameitoa kwa njia Sahih ndani ya kitabu chake cha historia. Na ameipokea Abul-Qasim Al-Kalalikaiyu ndani ya As-Sunatu kwenye Karama za mawalii. 44


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 45

Tabaruku

Nyumba ya Mtume.100 Na ifuatayo ni baadhi ya mifano ya Sahaba wakitafuta Baraka kupitia baadhi yao na Tabiina wakitafuta kupitia Sahaba: Abdullah bin Mas’ud amepokea kuwa Umar bin Al-Khattab alitoka na kuomba mvua kupitia Abbas akasema: “Ewe Mwenyezi Mungu hakika sisi tunajikurubisha kwako kupitia ami ya Mtume wako na wa mwisho kati ya baba zake na mkumbwa kati ya wanaume wa familia yake, kwani bila shaka umesema na usemi wako ni haki: “Na ama ukuta basi ulikuwa wa watoto wawili mayatima mjini….” Basi ukawahifadhi kwa ajili ya wema wa baba yao, basi ewe Mwenyezi Mungu muhifadhi Mtume wako kupitia ami yake, na hakika tunatawaswali kwako kupitia kwake huku tukiomba Shifaa na huku tukiomba msamaha….101 Na katika tamko lingine: Tumepokea kutoka kwa baadhi ya watu kutoka kwa Umar kuwa alitoka kuomba mvua na akatoka pamoja na Abbas akasema: ‘Ewe Mwenyezi Mungu hakika sisi tunajikurubisha kwako kupitia ami ya Mtume wako na tunaomba kupitia kwake, basi muhifadhi kwa ajili ya Mtume wako kama ulivyowahifadhi watoto wawili kwa ajili ya wema wa baba yao, na tumekujia huku tukiomba msamaha na huku tukiomba Shifaa.’ Kisha akawaelekea watu na kuwaambia: ‘Mwombeni msamaha Mola wenu Mlezi hakika yeye ni msamehevu’ - Mpaka akasema: Matone ya mvua yakaanza kutoka mawinguni basi watu wakasema: ‘Mnaona, mnaona.’ Kisha yakajaa na kutimia na yakapigwa na 100 Fat’hul-Bari 2: 399. 101 Sharhu Nahjul-Balagha cha Ibnu Abil-Hadidi 7: 274, ufafanuzi wa hotuba ya 114, mlango wa habari na hadithi za kuomba mvua. Iqtidhau Asw-SwiratulMustaqimi cha Ibnu Taymiyya: 338. 45


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 46

Tabaruku

upepo, kisha yakatikisika na kunyesha. Naapa kwa Mwenyezi Mungu hawakuondoka hapo ila walikimbilia kwenye kuta na wakajaza maji vihifadhio, na watu wakamzunguka Abbas huku wakijipangusa kwenye viungo vyake na wakisema: Hongera ewe Mnyweshaji wa maeneo mawili matakatifu (Makka na Madina). Ndani ya tamko la Ibnu Athir: Na baada ya watu kupata mvua wakawa wanajipangusa kwa Abbas na kumwambia: Hongera ewe uliyeyanywesha maeneo mawili Matakatifu (Makka na Madina) na Sahaba walikuwa wanajua ubora wa Abbas wakimtanguliza na kumtaka ushauri.102 Al-Hasan Al-Basri ambaye Umar alimrambisha asali kwa mkono wake, mama yake alikuwa mtumishi wa Ummu Salama mke wa Mtume, hivyo baadhi ya nyakati mama yake alikuwa akiondoka na hivyo Ummu Salama humpa chuchu lake na kumbembeleza kwalo mpaka mama yake anaporudi, na ndipo humpa chuchu lake na kuanza kunyonya, hivyo watu walikuwa wakisema ufasaha wake unatokana na Baraka za kitendo hicho.103 As-Samuhudiyu anapoelezea Muhimili wa Al-Mahrasu amesema: “Ali bin Abi Talib alikuwa akiketi kwenye bapa lake ambalo linagusa Kaburi karibu na mlango wa Mtume huku akiwa ameelekea mlango mdogo ambao Mtume alikuwa akitumia kuingilia msikitini kwa ajili ya Swala atokeapo nyumba ya Aisha. Nayo ni nguzo husalia hapo Kiongozi wa Madina kwa kuuweka nyuma ya 102 Usudul-Ghaaba 3: 167, wasifu wa Abbas bin Abdul-Mutwalibi, namba 2797. 103 Swifatu Asw-Swafuwatu 3: 47. 46


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 47

Tabaruku

mgongo wake, kwa ajili hiyo Al-Akishahariyu amesema: Bila shaka nguzo iliyokuwa ndio eneo la kuswalia Ali, leo ni mashuhuri mno kiasi kwamba haifichiki kwa watu wa eneo Takatifu (Madina) na bado mpaka leo viongozi wanaketi na kuswalia hapo. Na akasema kuwa inaitwa: makao ya viongozi, hiyo ni kwa sababu ya sharafu ya yule aliyekuwa akiketi hapo.104 Imenukuliwa kutoka kwa Muslim bin Abu Mariyam na wengineo kuwa mlango wa nyumba ya Fatima binti wa Mtume ulikuwa kwenye mraba uliyoko kwenye Kaburi. Sulaymani amesema: Muslimu aliniambia: Usisahau fungu lako kwa kuswali kwenye mraba huo kwani wenyewe ni mlango wa Fatima, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, ambao Ali alikuwa akiutumia kuingilia kwake atokeapo kwenye Kaburi.105 Na anapozungumzia nguzo ya Tahajjudi amesema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu alikuwa akitoa mkeka kila usiku pindi watu wanapoacha kuja (Msikitini) kisha anautandika nyuma ya nyumba ya Ali na kuswali Sala ya Usiku……” Na Said bin Abdullah bin Fadhlu amenisimulia akasema: ‘Muhammad bin Al-Hanafiya alipita kwangu ilihali nikiwa naswali eneo hilo akaniambia: Nakuona huachani na nguzo hii, je, una Hadithi yoyote iliyokujia?’ Nikasema: Hapana. Akasema: ‘Usiachane nayo kwani bila shaka ilikuwa ndio eneo la Sala ya Mtume wa Mwenyezi Mungu Usiku.’ Ibnu Hajar amesema: “Kutokana na hili ni kuwa ni Sunna kuswalia kwenye nguzo zote za Msikiti wa Mtume kwa sababu ni lazima Sahaba wakubwa walisalia hapo.”106 Kama ilivyopokewa kutoka kwa baadhi kuwa: Umar bin Al-Khattab 104 Wafaul-Wafa: 2: 448. 105 Wafaul-Wafa: 2:450. 106 Wafaul-Wafa: 452. 47


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 48

Tabaruku

alipomchumbia Ummu Kulthum binti wa Kiongozi wa Waumini Ali bin Abi Talib alisema: ‘Hakika mimi napenda niwe na kiungo kutoka kwenye viungo vya Mtume wa Mwenyezi Mungu.’107 Husein bin Ali alipotoka Madina kuelekea Makka alipita kwa Ibnu Mutwiu akamkuta akichimba kisima chake basi akamwambia: ‘Nimekufidia baba yangu na mama yangu, unaelekea wapi?’ Akasema: ‘Naelekea Makka – Akamwambia wafuasi wake wa huko Kufa wamemwandikia barua. – Ibnu Mutwiu akamwambia: ‘Nimekufidia baba yangu na mama yangu, tustareheshe kwa nafsi yako na wala usiende kwao.’ Husein akakataa. Ibnu Mutwiu akamwambia: Hiki hapa kisima changu nimeshatoboa maji yake na leo mpaka sasa hatujapata maji yoyote ndani ya ndoo, tunaomba utuombee Baraka. Akasema: ‘Lete maji yake.’ Basi akaletewa maji yake akanywa kisha akasukutua na kuyarudisha ndani ya kisima, ndipo maji yakaongezeka na kuwa matamu.108 Imam Ali bin Musa Ar-Ridhaa (a.s.) alipofika Nisaburi watu walikusanyika na kumzunguka mnyama wake, akatoa kichwa chake toka kwenye riksho lake na kushuhudiwa na watu wote, basi yupo aliyekuwa akitoa ukulele na yupo aliyekuwa akilia na yupo aliyekuwa akichana nguo yake na yupo aliyekuwa akisugua uso wake udongoni huku mwingine akibusu kwato za nyumbu wake au akibusu hatamu ya nyumbu wake….109 Bali bila shaka Mtume alitafuta Baraka kupitia udhu wa Waislam. Kama ilivyopokewa hivyo ndani ya Hadithi Sahihi: Imepokewa kutoka kwa Ibnu Umar amesema: Nilimwambia Mtume wa Mwenyezi 107 Dhakhairul-Uqba: 169, sehemu ya nane kwenye kumtaja Ummu Kulthum binti wa Fatimah na Ali (a.s.) 108 At-Tabaqatul-Kubra 5: 107. 109 As-Sawa’iqul-Muhriqa: 310, sehemu ya tatu kwenye hadithi zilizopokewa kuhusu kuwachukua Kizazi cha Mtume. Nurul-Absari cha Ash-Shablanjiyu: 168, sehemu ya fadhila za bwana Ali Ar-Ridhaa bin Musa Al-Kadhimu. 48


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 49

Tabaruku

Mungu: Ni lipi likupendezalo mno kati ya mimi kutawadha kwa kutumia jagi la shaba jipya lililobadilishwa au kutumia chombo maalum cha kuchukulia tohara? Akasema: “Kwa kutumia chombo maalum cha kuchukulia tohara, kwani Dini ya Mwenyezi Mungu imerahisisha matendo yake mepesi. Amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu alikuwa akituma aletewe maji kutoka kwenye chombo maalum cha kuchukulia tohara kisha huyanywa maji hayo akitaraji kupata Baraka za mikono ya Waislam.110 Hizi ni baadhi tu ya Hadithi miongoni mwa Hadithi zinazothibitisha kuwa Sahaba na Tabiina na wale waliyokuwa ndani ya karne tatu za mwanzo walikuwa wakitafuta Baraka kupitia baadhi yao. Kinyume na wanavyodai baadhi ya watu mfano wa Al-Jadiu aliposema: Ukweli ni kuwa haijapokewa athari yoyote kutoka kwa Mtume kuwa aliamrisha ‘Kutafuta Baraka’ kupitia yeyote asiyekuwa yeye, kuanzia Sahaba mpaka wengineo, sawa iwe ‘Kutafuta Baraka’ kupitia wao wenyewe au athari zao au kuwa aliwaelekeza hilo. Amesema: “Pia hakuna nukuu iliyopatikana kuhusu aina hii ya Sahaba (r.a.) ‘Kutafuta Baraka’ kupitia asiyekuwa Mtume, si zama za uhai wake wala baada ya kifo chake…..111 Akasema kuhusu sababu ya kutokufanya hivyo: “Bila shaka sababu ya msingi ya Sahaba radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao kuacha ‘Kutafuta Baraka’ kupitia baadhi yao ni kule kuamini kuwa ‘Kutafuta 110 Majma’uz-Zawaidi 1: 214 na akasema: At-Tabrani ameipokea ndani ya AlAwsat na wapokezi wake ni waaminifu. Kanzul-Ummali 7: 112, hadithi ya 18231. 111 At-Tabaruku Anuwaihi wa Ahkamihi: 261. 49


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 50

Tabaruku

Baraka’ ni jambo muhtasi kwa kupitia Mtume tu na si mwingine isipokuwa Manabii wengine……” Na akasema akiwa amenukuu kutoka kwa Ash-Shatibiyu: Kwa mujibu huu haisihi mtu aliyekuja baada yake kumfuata Sahaba katika kitendo cha ‘Kutafuta Baraka’ kupitia nyuso hizo au nyingine, na atakayemfuata basi ufuataji wake huu utakuwa ni Bidaa, kama ilivyokuwa kumfuata Sahaba katika kuzidisha wanawake wanne ni Bidaa.112 Nasema: Baada ya kuthibitisha jinsi Sahaba na Tabiina walivyotafuta Baraka kupitia baadhi yao na kupitia waja wema ndani ya umma, basi kitendo cha Mtume kutoamrisha ‘Kutafuta Baraka’ kupitia asiyekuwa yeye ni mkabala na kitendo cha yeye (s.a.w.w.) kutokukataza, kwani laiti jambo hili lingekuwa na kiwango kama hiki cha hatari dhidi ya imani za Waislam basi Mtume asingeghafilika na jambo hili na angelikataza kwa nguvu zake zote. Hilo liko wazi ndani ya kauli ya Mtume iliyotoka kwa Amr bin Al-Aas kuwa Mtume alisema: Bila shaka hakuna Nabii kabla yangu ila alikuwa na wajibu wa kuuonyesha umma wake heri yao anayoijua na kuwaonya dhidi ya shari yao anayoijua……113 Je, Mtume anajipinga mwenyewe? Na je, analificha jambo hili ambalo lina uharibifu kwa umma bila kuwabainishia wana-umma?!!! Kamwe haiwezekani. Ama kusema haisihi kumfuata mwingine katika kitendo cha ‘Kutafuta Baraka’, eti kwa kulinganisha na kitendo cha kutokusihi kuoa wanawake zaidi ya wanne, kipimo hicho ni batili kwani Mtume ameshaufundisha 112 At-Tabaruku Anuwaihi wa Ahkamihi: 264 amenukuu toka kwenye AlI’itiswamu 2: 9. 113 Sahih Muslim 3: 1472, Kitabu cha dalili, mlango wa wajibu wa kutekeleza kiapo cha utii wa Makhalifa wa kwanza ni wa mwanzo. 50


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 51

Tabaruku

umma wake hukmu ya kisheria kuhusu hilo na hakuna mwislamu yeyote ardhini tokea zama za Mtume mpaka leo isipokuwa ni lazima atakuwa anajua uharamu huo kwa asiyekuwa Mtume (s.a.w.w.). Na hii ni dalili kubwa juu ya usahihi wa tunayosema na ni uduni wa dalili ya Ash-Shatibiyu, kwani laiti ‘Kutafuta Baraka’ kupitia asiyekuwa Nabii kungekuwa ni jambo lililoharamishwa basi angelibainisha kwa umma wake kama alivyobainisha uharamu wa kuoa zaidi ya wanawake wanne. Miongoni mwa hoja nyingine duni ambazo Al-Jadiu ametumia kuthibitisha kutoruhusiwa ‘Kutafuta Baraka’ kupitia asiyekuwa Nabii ni kule kudai kuwa kufanya hivyo ni kuziba uwezekano wa kumshirikisha Mwenyezi Mungu, kwa sababu ‘Kutafuta Baraka’ kupitia athari za waja wema kunasababisha kuwapenda kupita kiasi na kuwaabudu kinyume na Mwenyezi Mungu, hivyo ikawajibika kuzuia hilo….. Na hivyo imebainika kutoruhusiwa kuwalinganisha waja wema na Mtume, na kwa ajili hiyo hairuhusiwi ‘Kutafuta Baraka’ kupitia waja wema wenyewe au athari zao sembuse wasio wao, na hakika kukitukuza kitu na ‘Kutafuta Baraka’ kupitia kitu hicho hairuhusiwi ila kwa dalili ya kisheria.114 Nasema: Tumethibitisha kuwa haipasi Mtume auache umma wake bila kuuzindua dhidi ya hatari ya jambo hili, kwa sababu kufanya hivyo atakuwa hajatimiza jukumu la kutekeleza ujumbe wake, na kuucha umma wake katika hali hiyo kunaupeleka kwenye shimo la upotovu na umma unakuwa umeangukia ndani ya shimo la Shirki, na hilo ni jambo lisiloruhusiwa kiakili wala kisheria. Hivi hilo linalingana na kauli ya Mtume: Nimekuacheni kwenye jambo la wazi?!!! 114 At-Tabaruku Anuwaihi wa Ahkamihi: 268. 51


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 52

Tabaruku

‘KUTAFUTA BARAKA’ KUPITIA MAKABURI YA WAJA WEMA NA KUPITIA ATHARI ZAO Waislam hawakuishia ‘Kutafuta Baraka’ kupitia kaburi la Mtume na athari zake tu baada ya kifo chake, bali pia mwenendo wao ulikuwa ni ‘Kutafuta Baraka’ kupitia Makaburi ya Sahaba, Tabiina na waja wema ndani ya umma na kupitia athari zao huku wakiomba Shifaa na mvua kupitia athari hizo. Miongoni mwao ni: Bilal Al-Habashiyyu: Mwadhini wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, kaburi lake liko Damascas na kwenye kichwa cha kaburi hilo lililobarikiwa kuna historia yenye jina lake (a.s.). Na Du’a inayoombwa eneo hili lililobarikiwa huwa ni yenye kujibiwa. Mawalii wengi na waja wema wenye kheri wamejaribu hilo na wakabarikiwa kwa ziara zao.115 Abu Ayyub Al-Ansari: Al-Hakimu amesema: “Wanaliendea kaburi lake mara kwa mara na wanalizuru na kuomba mvua kupitia kaburi hilo pindi wanapopatwa na ukame.”116 As-Suhaybu Ar-Rumi: As-Samuhudiyu amesema: “Hakika wao waliujaribu udongo wa kaburi la As-Suhaybu kwa mwenye homa na ukaonekana unakidhi.” Hamza bin Abdul-Mutwalib: As-Samuhudiyu amenukuu kauli ya AzZamakhshari akasema: “Kisha udongo wa Hamza umeondolewa kwenye hukmu ya kutokuruhusiwa kubeba udongo wa Madina na kuupeleka mji mwingine, kwa sababu watu wamekubaliana juu ya kuuchukua kwa ajili ya dawa.” Kisha akasema: Al-Burhani bin Farahani amesimulia kutoka kwa 115 Rihlatu Ibnu Jubayri: 251. 116 Al-Mustadrak 3: 518 Na Ibnul-Jawzi ndani ya Swifatu Asw-Swafuwatu 1: 407. 52


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 53

Tabaruku

Imamu msomi Abu Muhammad Abdus-Salami bin Ibrahim bin Maswali bin Al-Hahani amesema: Nimenukuu kutoka ndani ya kitabu cha Sheikh Msomi Abu Muhammad Swalihu Al-Harmaziyu amesema: Amesema Swalihu bin Abdul-Halimu: Nilimsikia Abdus-Salami bin Yazid As-Sanahaji akisema: Nilimuuliza Ibnu Bakuni kuhusu udongo wa Makaburi ambayo watu walikuwa wakiubeba kwa ajili ya ‘Kutafuta Baraka’, je, inaruhusiwa au imekatazwa? Akasema: “Inaruhusiwa na bado watu wanaendelea ‘Kutafuta Baraka’ kupitia Makaburi ya wanachuoni, mashahidi na waja wema, na hapo zamani watu walikuwa wakibeba udongo wa kaburi la Bwana wetu Hamza bin Abdul-Mutwalib.”117 5- Al-Husein bin Ali: Ash-Shabrawiyu ameweka mlango mkubwa kwenye kaburi la kichwa cha Husein bin Ali ukizungumzia Ziara yake na baadhi ya karama zake na kuhuisha siku ya Jummanne kwa kumzuru, akasema: Na Baraka za kaburi hili zinaonekana kwa macho na zawadi zinazomrudia mwenye kumzuru hazijifichi nazo zinatokana na Du’a Sahihi muda wote na matendo kwa nia njema. Na Abul-Khitabi bin Dahyatu ana utenzi mzuri juzuu moja kuhusu hilo. Na Al-Kadhi Zakiyud-Dini Abdul-Adhimu ametoa tamko kuhusu hilo akasema: Hii ni sehemu tukufu na Baraka zake ni dhahiri na kukusanyika hapo ni kheri na amani. Umuhimu ulioje wa Jengo hili sharifu na Kaburi lenye nuru tukufu kwa kauli ya Msemaji: Nafsi yangu ni fidia kwa ajili ya Kaburi ambalo bila siri zake heshima ya Nabii ingekanyagwa. Na ni sitara ya heshima ambayo yumo humo Mtukufu. 117 Wafaul-Wafa 1: 69

53


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 54

Tabaruku

Kiwanja ambacho akili zimeendelea kustaajabishwa na kubabaishwa. Paji lake linawapa watazamaji haiba yake huku mwenye kukodoa macho akibetua jicho lake. Nyota zimehusudu nafasi yake hivyo nyota ikashinda kutwa ikitamani lau ingekuwa jirani naye. Mdomo umepata heshima ya juu mno kwa kubusu udongo wake hivyo akawa wanambusu kwa vipaji vyao. 6- Umar bin Abdul-Aziz Khalifa kutoka kizazi cha Umayya aliyefariki Mwaka 101 A.H.: Adh-Dhahabi amesema: Kaburi lake liko Dayrus-Samuani hutembelewa.118 7- Ali bin Musa Ar-Ridhaa (a.s.): Abu Bakri bin Al-Muumilu amesema: “Tulitoka tukiwa pamoja na Imamu wa watu wa hadithi Abu Bakri bin Khuzayma na mwenza wake Abu Ali At-Thaqafi pamoja na kundi miongoni mwa mashekhe wetu wakati huo wakiwa katika msafara wa kuelekea kumzuru Ali bin Musa Ar-Ridhaa huko At-Tusi. Amesema: Nikaona njinsi anavyokitukuza- Yani Ibnu Khuzaymatu- kitalu hicho na akinyenyekea kwa ajili yake na akitoa heshima yake pale kwa kiwango kilichotuduwaza.119 Pia Al-Khatibu Al-Baghdadi ametoa kwa njia yake kutoka kwa Ahmad bin Jafari bin Hamdani Al-Katiiyu amesema: “Nilimsikia Al-Hasan bin Ibrahim Baba Ali Al-Khalalu Sheikh wa Mahambali zama zake akisema: ‘Sikutatizwa na jambo lolote na nikaenda 118 Tadhkiratul-Hufadhi 1: 121. 119 Tahdhibut-Tahdhibu 7: 339. 54


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 55

Tabaruku

kwenye kaburi la Musa bin Jafari na nikatawaswali kupitia yeye isipokuwa lazima Mwenyezi Mungu alinirahisishia nilipendalo.’120 8- Al-Allamatu Ahmad bin Muhammad Al-Makkariyu Al-Malikiyyu aliyefariki mwaka 1041 A.H. amesema ndani ya kitabu Fat’hulMutaali Bisifatil-Niali akiwa amenukuu kutoka kwa Waliyud-Dini Al-Arakiyu kuwa: Al-Hafidhu Abu Said bin Al-Ala alitoa Hadithi akisema: Nimeona kwenye maneno ya Ahmad bin Hambali ndani ya jalada la zamani likiwa na hati ya Ibnu Nasiri121 na wanakumbukumbu wengine kuwa: Imamu Ahmad aliulizwa kuhusu kubusu kaburi la Mtume na kubusu Mimbari yake akasema: Si vibaya kufanya hivyo. Amesema: “Tukamwonyesha mchaji Ibnu Taymiyya basi akawa anastaajabu hilo na kusema: Nimestaajabishwa na Ahmad, kwangu ni mwenye hadhi!! Hivi haya ni maneno yake au maana ya maneno yake. Na akasema: “Kuna ajabu gani kuhusu hilo ilihali tumepokea kutoka kwa Imamu Ahmad kuwa alifua kanzu ya Shafi na akanywa maji aliyofulia.”122 Ikiwa huku ndio kuwaheshimu wasomi itakuwaje kiwango cha Sahaba na vipi kuhusu athari za Manabii (a.s.). Ni uzuri ulioje wa kauli ya aliyechanganikiwa kwa ajili ya Layla: Napita kwenye majumba majumba ya Layla 120 Tarikhu Baghdadi 1: 120. 121 Ni Al-Hafidhu Muhammad bin Nasiri Abul-Fadhlu Al-Baghdadiyu - aliyefariki mwaka 505 hijiriya. Ibnu Al-Jawzi ndani ya Al-Muntadhimu 17: 103 namba 4210 amesema: Alikuwa mwenye kuhifadhi makini mwaminifu. 122 Manaqib Ahmad cha Ibnu Al-Jawzi: 609. Al-Bidayatu Wan-Nihaya cha Ibnu Kathir 10: 365, matukio ya mwaka 241 hijiriya. 55


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 56

Tabaruku

Nakibusu chenye ukuta na chenye ukuta. Si kuzipenda nyumba ndiko kulikokonga moyo wangu Lakini ni kumpenda aliyeishi nyumba hizo123 Al-Kadhi Iyadhu Al-Malikiyyu amesema ndani ya kitabu Ash-Shafa: “Maeneo yaliyoishi kwa Ufunuo na Mteremsho. Jibril na Mikail wakayazunguka mara kwa mara. Malaika na Roho wakapanda kutokea hapo. Viwanja vyake vikalia kwa kutakasa na kufanya Tasbihi. Udongo wake ukajumuisha mwili wa mbora wa wanadamu. “Kutokea hapo dini ya Mwenyezi Mungu na Sunna za Mtume wake zikaenea kwa wingi. Maeneo ya Mafunzo na Aya, masujudio na Swala. Vituo vya fadhila na kheri. Vyuo vya dalili na miujiza na ibada za dini. Maeneo ya ibada za Waislam, misimamo ya Bwana wa Mitume na Makazi ya Hitimisho la Manabii. Kiasi kwamba hapo pakachomoza utume na chemchemu ikamwaga mafuriko yake. Eneo la mashukio ya utume na ardhi ya kwanza udongo wake kugusa ngozi ya Mteule ni lazima viwanja vyake vitukuzwe, pumzi yake ivutwe na jengo na kuta zake zibusiwe……..”124 Huu ndio mwenendo wa Waislam wa sasa wakirithi kutoka kwa waliotangulia, na huu ndio msimamo wa Sheikh wa ki-Hambali kuhusu ‘Kutafuta Baraka’ kupitia athari za waja wema na mawalii. Sheikh ambaye Ibnu Taymiya na wafuasi wake wanadai kuwa wao ni wanafunzi wake. Wala hawana hoja ithibitishayo ila ni ile kauli yao kuwa huko ‘Kutafuta Baraka’ huenda kukampelekea kwenye Shirki na kumwabudu mtu atakayekuwa njia ya Kutafutia Baraka.

123 Fat’hul-Mutaali: 329. 124 Ash-Shifau Bitaarifi Huququl-Mustwafa 2: 131. 56


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 57

Tabaruku

KUJIGUSISHA KWENYE KITU CHA KUTAFUTIA BARAKA Mwisho napenda kuhitimisha utafiti huu kwa kugusia maudhui ambayo baadhi huitolea hoja za utata wakilenga kuwapotosha Waislam kupitia hoja hizo, na kuwapeleka nje ya msitari sahihi kwa kuzua shaka ndani ya nafsi zao kwa lengo la kuweza kuzichezea itikadi zao na kuwapeleka kwenye semi zao ambazo nje zinang’ara mno lakini ndani zimefifia haziwezi kumkinaisha mwanadamu aliyetimia akili. Nayo ni maudhui ya kugusa na kujipaka miili ya watu au vitu unavyotafuta Baraka kupitia kwavyo. Baada ya Al-Aliyani kufululiza maneno kuhusu ubora wa baadhi ya maeneo akasema: Atakayeishi Makka au Madina au Shamu kwa lengo la ‘Kutafuta Baraka’ za Mwenyezi Mungu ndani ya vitalu hivyo, sawa iwe kwa kutaka kuzidishiwa riziki au kuondolewa fitina basi amepata kheri nyingi. Ama mja akivuka zaidi ya hapo katika ‘Kutafuta Baraka’ kama vile ajipake udongo wake, mawe yake na miti yake au aweke udongo wake ndani ya maji ili ajitibu kwa maji hayo na mfano wa hayo basi yeye atasaidiwa na hatolipwa. Kwa sababu katika ‘Kutafuta Baraka’ yeye amepita mapito ambayo hajayapita Mtume wa Mwenyezi Mungu na wala halijayapita kundi la mwanzo.125 Akasema: Wema waliotangulia walikuwa wakikataza kuwatukuza mno, kama vile Anas, At-Thawriyu na Ahmad, na Ahmad alikuwa akisema: “Mimi ni nani mpaka mnakuja kwangu!! Nendeni mkaandike hadithi.” Na alikuwa aulizwapo kitu husema: Waulizeni wasomi. Na akiulizwa kitu kuhusu Uchamungu husema: Mimi sistahiki kuzungumzia Uchamungu, laiti kama Bashru angekuwa hai angezungumzia hili. 125 At-Tabaruku Al-Mashuruu: 42.

57


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 58

Tabaruku

Na mara nyingine akaulizwa kuhusu Ikhlasi akasema: “Nendeni kwa watawa sisi tuna nini mpaka mnakuja kwetu? Akaja mtu mmoja kwake kisha akapitisha mkono wake juu ya nguo yake na kuupaka uso wake, basi Imamu Ahmad akachukia na kukataza hilo kwa nguvu zote na kusema: Jambo hilo mmelichukua kutoka kwa nani?126 Kwanza hapa: Ni kuwa Al-Aliyani amefahamu mambo kinyume na ilivyo, kwa sababu vitendo vya Maimamu hao na kuwakataza watu wasiombe Baraka kupitia kwao haikuwa kwa sababu ya kukataza ‘Kutafuta Baraka’ yenyewe kama Baraka, bali ilikuwa kwa lengo la unyenyekevu ambao ndio sera ya wanazuoni na waja wema. Na Imamu Ahmad hakumtuhumu mtu aliyetafuta Baraka kupitia kwake kama wanavyofanya wanaodai kuwa wanamfuata Imamu huyu katika kuwakufurisha Waislam na kuwatuhumu kwa ushirikina. Kwa sababu hawa Wanachuoni walikuwa wanajua vizuri kuwa kufanya hivyo si shirki na si upotovu kwa dalili ambayo ni: Wao wenyewe walikuwa wanatafuta Baraka kupitia wanazuoni wengine na Maimamu Wema bali mpaka walikuwa wakitafuta Baraka kupitia Makaburi yao kama ilivyotangulia katika hadithi iliyotangulia, wakiwemo Maimamu wa Watu wa Hadithi. Wala hatujui ni dalili ipi wanaitumia hawa wajinga kuthibitisha kutokuruhusiwa kisheria kujipaka mwili wa yule unayetafuta Baraka kupitia kwake. Hawana Hadithi wala athari yoyote wanayoitegemea kuthibitisha usahihi wa madai yao yasiyo na hoja, ilihali athari zote zinaonyesha ubatili wa rai zao.

Imetangulia mwanzo kuwa Sahaba walikuwa wakigusa kwa mikono yao ya kulia eneo la kati la mimbari ya Mtume kisha wanaomba du’a. Sahaba 126 At-Tabaruku Al-Mashuruu: 86. 58


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 59

Tabaruku

Ibnu Umar alikuwa akipitisha mkono wake juu ya eneo alilokuwa akiketi Mtume katika mimbari kisha anapitisha mkono wake juu ya uso wake. Pia imetangulia kuwa Mtume alikuwa akipitisha mkono juu ya vichwa au viwiliwili vya watu na kuwaombea, jambo linaloonyesha sifa maalum ya kupitisha, kwa sababu du’a ya Mtume inatosha kuleta jibu. Riwaya zilizokuja zikiwa zimebeba maana hii ni nyingi sana na sisi hapa tutakomea kugusia baadhi tu ili kubainisha lengo na umuhimu wa kufanya hivyo yaani kupitisha mkono juu ya mwili. Imepokewa kutoka kwa Aisha kuwa: Mtume alikuwa akiwakinga baadhi ya wakeze basi anapaka kwa mkono wake wa kulia huku akisema: ‘Ewe Mwenyezi Mungu, Mola wa watu, ondoa ugonjwa na mponye, Wewe ni Mwenye kuponya hakuna tiba ila tiba Yako, tiba ambayo haiachi ugonjwa……’127 Pia imepokewa kutoka kwake kuwa Mtume alikuwa akimsomea mgonjwa: Kwa jina la Mwenyezi Mungu, udongo wa ardhi yetu, kwa ute wa baadhi yetu, anapona mgonjwa wetu, kwa idhini ya Mola wetu Mlezi.128 As-Samuhudiyu amesema: “Ilikuwa mtu amlalamikiapo ugonjwa Mtume au awapo na kidonda au jeraha basi Mtume alikuwa akisema hivi kwa kidole chake - Akaweka kidole Shahada aridhini, kisha akakiinua na kusema: - Kwa jina la Mwenyezi Mungu, udongo wa ardhi yetu, kwa ute wa baadhi yetu, anapona mgonjwa wetu kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.”129

127 Sahih Bukhari 7: 172. 128 Sahih Bukhari 7: 172. 129 Wafaul-Wafa 1: 69 59


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 60

Tabaruku

Imepokewa kutoka kwa Abu Hazimu kuwa Sahlu bin Saad alisema kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu alisema Siku ya Khaybari: “Bila shaka kesho nitampa bendera hii mtu ambaye Mwenyezi Mungu atashinda kupitia mikono yake, yeye anampenda mno Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na Mwenyezi Mungu na Mtume Wake wanampenda mno.” Akasema: Basi watu wakalala huku wakiukaba usiku wao kuwa atampa nani? Walipofika asubuhi watu waliamkia mapema kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kila mmoja akitaraji kuwa atapewa yeye. Mtume akasema: Yuko wapi Ali bin Abi Talib? Wakasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu analalamikia macho yake. Akasema: ‘Mtumieni mjumbe aje.’ Basi akaletwa na ndipo Mtume wa Mwenyezi Mungu akamtemea mate ndani ya macho yake na akamwombea, basi akapona kama kwamba hakuwa na ugonjwa na hapo akampa bendera…..130 Hakika hili linaweka wazi baadhi ya mambo na miongoni mwa hayo ni: Mtume alikuwa hatosheki na du’a tu bali pia alikuwa anapitisha mkono juu ya kiungo chenye ugonjwa ikiwa ni du’a ya kumwombea uponaji. Na inapokuwa ni du’a ya kuomba Baraka alikuwa anapitisha mkono wake juu ya kichwa. Hivyo lazima kupitisha mkono kutakuwa na maana maalum. Pia miongoni mwa hayo ni: Bila shaka sisi tumekuta ndani ya riwaya kuwa Mtume alikuwa akiomba du’a ya tiba kupitia udongo. Pia katika Hadithi hizi zipo zinazoonyesha kuwa aliamrisha kuchanganya udongo na ute ili Baraka na tiba vitimie kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Jambo linaloonyesha hadhi maalum ya udongo wa Madina yenye Nuru, kwa kuifanya sababu ya kupona kwa idhini ya Mwenyezi Mungu kutokana na Baraka zilizomo humo ambazo Mwenyezi Mungu amezifanya muhtasi kwa udongo huo. 130 Musnad Ahmad 5: 333. Sahih Bukhari 4: 30 na 207. Majma’uz-Zawaidi 6: 150, Mlango wa vita vya Khaybari. Kitabus-Sunnati cha Abu Asimu: 594. AsSunan Al-Kubra cha An-Nasai 5: 46 na 108, Kitabu cha fadhila, fadhila za Ali bin Abi Talib. Musnad Abu Yaala 1: 291. Al-Mu’jamu Al-Kabir cha At-Tabarani 6: 152. 60


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 61

Tabaruku

Hadithi za Mtume zinazoonyesha hilo ni nyingi, na sisi tutataja baadhi tu ya kauli zake (s.a.w.w.): Vumbi la Mji wa Madina ni tiba ya ukoma.131 Vumbi la Mji wa Madina huponya ukoma. Vumbi la Mji wa Madina huzima ukoma. Bila shaka ndani ya vumbi lake mna tiba ya kila ugonjwa. Naapa kwa yule ambaye nafsi yangu imo mikononi mwake kuwa udongo wake una Imani na bila shaka wenyewe ni tiba ya ukoma.132 Hivi hilo halionyeshi hadhi maalum aliyoiweka Mwenyezi Mungu ndani ya baadhi ya maeneo mpaka udongo wake na vumbi lake kwa idhini ya Mwenyezi Mungu vikawa tiba ya magonjwa hatari. Basi ikiwa kuchanganya udongo na ute na kujitibu kwavyo ni amri kutoka kwa Mtume, vipi tena iwe hairuhusiwi ‘Kutafuta Baraka’ kupitia udongo huu mtukufu. Ni ipi hadhi ya Jiwe Jeusi na baadhi ya nguzo za Kaaba mpaka mamilioni ya Waislam waanguke na kufariki kwa kutaka kuligusa wakiwa wanamfuata Mtukufu Mtume, kwa nini wasitosheke na kuizuru tu Nyumba Tukufu bila kugusa chochote katika Nyumba hiyo ikiwa kweli madai ya hawa ni sahihi? Hivi huoni maana ya yote haya ni ile hali ya baadhi ya maeneo kuwa na utukufu maalum ambao Mwenyezi Mungu ameuweka humo na Baraka imo ndani ya udongo wake na vumbi lake. Basi kwa nini isiruhusiwe kujipaka udongo huo na kuubusu kwa ajili ya ‘Kutafuta Baraka’?!!! Kutokana na hayo yote inabainika kuwa ‘Kutafuta Baraka’ ni jambo lililoruhusiwa na Mweka Sheria (Mwenyezi Mungu) Mtukufu, na Manabii 131 Kanzul-Ummali 13: 205. Wafaul-Wafa 1: 67. 132 Kanzul-Ummali 13: 205. Wafaul-Wafa 1: 67. 61


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 62

Tabaruku

wakalitenda akiwemo Mtume wetu, amani na rehema ziwe juu yake na juu ya kizazi chake. Katu hakuna athari yoyote iliyotujia inayothibitisha kuwa Mwenyezi Mungu au Mtume wake wamekataza chochote katika hilo. Hivyo Waislam waliendeleza sera yao ya ‘Kutafuta Baraka’ kupitia Mtume tokea zama za uhai wake na ‘Kutafuta Baraka’ kupitia athari zake baada ya kifo chake, na Sahaba wakatafuta Baraka kupitia baadhi yao na wakaswalia kwenye maeneo aliyosalia Mtume wakitafuta Baraka za maeneo hayo. Mwenendo huo wa Waislam ukaendelea kizazi baada ya kizazi wakipata mafuriko ya Baraka za Mwenyezi Mungu bila Itikadi zao kuzimwa na shirki wala upotovu na bila ya yeyote kukusudia kumfanya mtu kuwa Mungu au kitu chochote anachotafutia Baraka. Bali ndani ya karne zote waliendelea kuwa wanatauhidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, wakiamini kuwa Yeye pekee ndiye mwenye uwezo juu ya kila kitu na uwezo wa kuteremsha Baraka. Na kuwa ‘Kutafuta Baraka’ kupitia viumbe Vyake si chochote isipokuwa ni kwa ajili ya kumpenda Mwenyezi Mungu na kuwapenda anaowapenda na wanaompenda. Na wala si chochote kingine miongoni mwa hayo wanayodai wajinga.

‘KUTAFUTA BARAKA’ KWA UPANDE WA AHLUL-BAYT Tumethibitisha ruhusa ya kisheria juu ya ‘Kutafuta Baraka’ ndani ya maudhui zilizotangulia kwa mujibu wa makundi yote ya kiisilamu na kuwa Mtume alipitisha hilo. Na tumebatilisha hoja za wasemao kuwa ‘Kutafuta Baraka’ ni muhtasi kwa Mtume tu na hakumuhusu mwingine yeyote ndani ya umma huu. Na tumethibitisha kuwa sera ya Sahaba na Tabiina Wema ilikuwa ni kuendelea na mfumo huu wa ‘Kutafuta Baraka’ kupitia athari za 62


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 63

Tabaruku

Mtume na Kizazi chake na hata kupitia waja wema ndani ya umma huu. Baada ya hayo yote ni lazima tulete baadhi ya Hadithi kuhusu ‘Kutafuta Baraka’ kwa upande wa Ahlul-Bayt wa Mtume na jinsi walivyohimiza na kuwatamanisha watu ‘Kutafuta Baraka’.

WALIVYOTAFUTA BARAKA KUPITIA KABURI LA MTUKUFU MTUME Pindi ulipofika muda wa kifo cha Imam Hasan bin Ali alimuusia ndugu yake Husein, na miongoni mwa aliyomuusia yalikuwa ni kumwambia: Nikitimiza kipindi changu basi unifumbe macho, unioshe, univike sanda na uniingize kwenye jeneza langu na unipeleke kwenye Kaburi la babu yangu Mtume wa Mwenyezi Mungu ili nikajadidishe ahadi. Kisha unirudishe kwenye Kaburi la bibi yangu Fatima (Binti Asadi) radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na unizike huko.133 Kutoka kwa Muhammad bin Mas’ud amesema: Nilimwona Abu Abdullah (As-Sadiq) yuko kwenye Kaburi la Mtume na akaweka mkono wake juu yake.134 Kutoka kwa Ibnu Fadhali amesema: Nilimwona Abul-Hasan anatoka kuaga ili atoke kwenda Umra, basi baada ya Magharibi akaja kwenye Kaburi eneo la kichwa cha Mtume wa Mwenyezi Mungu kisha akamtolea salamu Mtume na kulikumbatia Kaburi.135

133 Biharul-Anwar 44: 156. 134 Biharul-Anwar 100: 154. 135 Biharul-Anwar 100: 157. 63


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 64

Tabaruku

Pindi Imamu alipoazimia kutoka Makka baada ya kifo cha Muawiya, usiku ule alitoka nyumbani kwake na akaelekea Kaburini kwa babu yake akasema: Amani iwe juu yako ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu. Mimi ni Husein bin Fatima kifaranga chako na mwana wa kifaranga chako. Kisha akaketi na kuanza kulia Kaburini mpaka ilipokaribia Asubuhi, ndipo akaweka kichwa chake juu ya Kaburi akalala kidogo‌..136 Kutoka kwa Ar-Ridhaa (a.s.) amesema: Nilipotaka kutoka Madina kwenda Khurasani nilikusanya familia yangu na nikawaamrisha wanililie ili nisikie kilio chao, kisha nikawagawia dinari elfu kumi na mbili, kisha nikawaambia: Bila shaka kamwe mimi sirejei kwenye familia yangu. Kisha nikamchukua Abu Jafari nikamwingiza Msikitini na nikaweka mkono wake juu ya mzunguko wa Kaburi na nikamgusisha Kaburi na nikamuhifadhi kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu.137

WALIVYOTAFUTA BARAKA KUPITIA ATHARI ZA BAADHI YAO Imepokewa kutoka kwa Sulaymani bin Khalid na Muhammad bin Muslim, wamesema: Tulipita Al-Hiyrati tukaomba idhini na tukaingia kwa Abu Abdullah tukakaa kwake na tukamuuliza kuhusu Kiongozi wa Waumini, akasema: Mtakapotoka na mkavuka At-Thawiyatu na Al-Kaimu na mkafika umbali wa mtupo wa mshale au mishale miwili kutokea Najaf mtaona nguzo nyeupe katikati yake kuna kaburi limeliwa na mapito ya maji, basi hilo ndilo Kaburi la Kiongozi wa Waumini. Basi asubuhi iliyofuata tukaondoka tukavuka At-Thawiyatu na AlKaimu, ghafla tukaona nguzo nyeupe basi tukaziendea na tukaliona Kaburi kama alivyolielezea likiwa limeliwa na mapito 136 - Biharul-Anwari 44: 328. Al-Futuhu cha Ibnu Aathamu 5: 26. 137 -Al-Anuwaru Al-Bahiyatu: 110. 64


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 65

Tabaruku

ya maji, basi tukashuka tukatoa salamu na kuswali hapo kisha tukaondoka. Kesho yake tulikwenda asubuhi kwa Abu Abdullah tukamweleza, akasema: Mmepatia, Mwenyezi Mungu amewapa uongofu.138 Kutoka kwa Abani bin Taghlabu amesema: Nilikuwa pamoja na Abu Abdullah akapita nyuma ya kaburi akashuka kisha akaswali rakaa mbili, kisha akasogea mbele kidogo akaswali rakaa mbili, kisha akatembea kidogo akashuka na kuswali rakaa mbili, kisha akasema: Hili ni eneo la Kaburi la Kiongozi wa Waumini. Nikasema: Mimi ni fidia kwako, vipi kuhusu maeneo mawili ambayo umesali ndani yake? Akasema: Eneo la Kichwa cha Husein na eneo la Mimbari ya Al-Kaimu (Al-Mahdi).139 3- Ahlul-Bayti walikuwa wakitafuta Baraka kupitia jiwe la nyumbani kwa Fatimah (a.s.). Imepokewa kutoka kwa Ali bin Musa Ar-Ridhaa (a.s.) amesema kuwa: Fatimah alijifungua Hasan na Husein juu ya jiwe hilo, au Fatimah alikuwa akisalia juu ya jiwe hilo.140

WALIVYOTAFUTA BARAKA KUPITIA UDONGO WA HUSEIN Imepokewa kutoka kwa Abul-Yasaa amesema: Kuna mtu alimuuliza Abu Abdullah huku nikimsikia. Alimuuliza kuhusu kuoga pindi anapokwenda kwenye Kaburi la Husein, akasema: Je, ninaposali niliweke upande wa Kibla? Akasema: Nenda kidogo pembeni. Akasema: je, nichukue udongo wa Kaburi lake niuweke kwangu ili niwe natafuta Baraka zake? Akasema: Ndiyo. Au akasema: Si vibaya kufanya hivyo.141 138 - Biharul-Anwari 100: 237. 139 - Biharul-Anwari 100: 241. 140 -Wafaul-Wafa cha As-Samuhudiyu 1: 572. 141 Biharul-Anwari 83: 320. 65


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 66

Tabaruku

Kutoka kwa Abu Yaafuri amesema: Nilimwambia Abu Abdullah: Mtu kachukua udongo wa Kaburi la Husein na akanufaika nao, na mwingine akauchukua na akawa hakunufaika nao. Akasema: Naapa kwa Mwenyezi Mungu haiwezekani. Hauchukui yeyote huku akiona kuwa Mwenyezi Mungu atamnufaisha nao isipokuwa ni lazima atamnufaisha nao.142 Kutoka kwa As-Sadiq (a.s.): Hakika Mwenyezi Mungu ameufanya udongo wa Husein tiba ya kila ugonjwa na amani ya kila hofu, hivyo iwapo mmoja wenu atauchukua basi aubusu na auweke juu ya jicho lake na aupitishe juu ya mwili wake.143 Kutoka kwa Al-Yakitiniyu amesema: Abul-Hasan Ar-Ridhaa (a.s.) alinitumia furushi la nguo na kijana - Mpaka akasema: - Nilipotaka kupokea nguo niliona udongo katikati ya nguo, hivyo nikamuuliza mjumbe, ni kitu gani hiki? Akasema: “Si kuipa bidhaa sura fulani ila ameweka humo udongo kutoka Kaburi la Husein “ Kisha mjumbe akasema: ‘Abul-Hasan amesema: ‘’Wenyewe ni amani kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.’’144 Mtu mmoja alimuuliza Abu Abdullah, akasema: ‘’Je, nichukue udongo wa Kaburi la Husein niwe nikitafutia Baraka?’’ Akasema: ‘’Si vibaya kufanya hivyo.’’145 As-Sadiqi aliugua, hivyo akawaamuru waliokuwepo kwake wamkodie mtu atakayemwombea du’a kwenye Kaburi la Husein, basi wakampata mtu na wakamwambia hayo. Akasema mimi nitakwenda lakini Husein ni Imamu tuliyelazimishwa kumtii na yeye (As-Sadiqi) pia ni Imamu tuliyelazimishwa kumtii!! Basi wakarejea kwa As-Sadiqi (a.s.) wakamweleza Hadithi. Akasema: ‘’Ndivyo kama alivyosema, lakini hakujua kuwa Mwenyezi 142 Biharul-Anwari 101: 119. Al-Wasa’ilu 10: 409. 143 Biharul-Anwari 101: 119. Al-Wasa’ilu 10: 409. 144 Biharul-Anwari 101: 119. Al-Wasa’ilu 10: 409. 145 Al-Wasa’ilu 10: 415. Al-Bihar 101: 125. 66


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 67

Tabaruku

Mungu ana viwanja ambavyo ndani yake du’a hujibiwa, hivyo kiwanja kile (cha Husein) ni miongoni mwa viwanja hivyo.’’146 Kutoka kwa Abul-Hasan amesema: ‘’Ni juu ya mmoja wenu atakapomzika maiti na akamwekea mto kwa udongo aweke kipande cha udongo wa Husein mukabala na uso wake na wala asiuweke chini ya kichwa chake.’’147 Abu Abdullah As-Swadiq alikuwa na mkebe wa mfuko wa kitambaa cha njano, ndani yake mlikuwa na udongo wa Abu Abdullah Husein, hivyo ilikuwa sala ifikapo huumwagia juu ya busati na kusujudu juu yake. Kisha akasema: Kusujudu juu ya udongo wa Husein kunaondoa vizuizi saba.148 Imepokewa kutoka kwa As-Swadiqi Jafar bin Muhammad amesema: “Hakika Tasbihi ya Fatimah binti Muhammad ilikuwa inatokana na uzi wa sufi iliyochambuliwa uliofungwa mafundo kwa idadi ya Takbira. Na yeye (a.s.) alikuwa akiizungusha kwa mkono wake, akikuza na kutukuza mpaka alipouwawa Hamza bin Abdul-Muttwalib ndipo akatumia udongo wake, hivyo akatengeneza Tasbihi na watu wakazitumia. Alipouwawa Husein (rehma za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake), jambo likahamishiwa kwake, hivyo wakatumia udongo wake kutokana na ubora na sifa ulionayo.149 10- Abu Abdullah aliulizwa kuhusu kutumia udongo wa Kaburi la Hamza na Kaburi la Husein na ubora kati ya udongo wa hayo mawili. Akasema: “Tasbihi ambayo yenyewe inatokana na udongo wa Kaburi la Husein hutukuza kwa mkono wa mtu bila ya yeye kutukuza.”150

146 Al-Wasa’ilu 10: 421 -422. 147 Biharul-Anwari 101: 136. 148 Biharul-Anwari 101: 135. 149 Biharul-Anwari 101: 133. 150 Biharul-Anwari 101: 133. 67


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 68

Tabaruku

11- Imepokewa kutoka kwa As-Swadiqi (a.s.) kuwa: “Atakayezungusha vijipande vya udongo wa Husein na akaomba maghfira mara moja basi Mwenyezi Mungu atamwandikia mara sabini. Na iwapo atashika Tasbihi bila ya kumtukuza kwayo basi katika kila punje moja ya Tasbihi atamwandikia mara saba.”151 12- Kutoka kwa Muhammad bin Muslim amesema: “Niliwasikia Abu Jafar na Jafar bin Muhammad (a.s.) wakisema: ‘Hakika Mwenyezi Mungu amempa Husein kitu mbadala kutokana na kuuwawa kwake, nacho ni Uimamu kuwa katika kizazi chake, tiba kwenye udongo wake na kujibiwa dua kwenye kaburi lake.’’152 13- Kutoka kwa Ibnu Abbas kutoka kwa Mtume kuwa alimpa Hadithi za kuuwawa Husein mpaka akasema: Bila shaka hakika kujibiwa kuko chini ya kuba lake na tiba iko kwenye udongo wake na Maimamu wanatokana na kizazi chake.153 14- Kutoka kwa Harith bin Al-Mughira amesema: “Nilimwambia Abu Abdulla: Hakika mimi ni mtu mwenye magonjwa na maradhi mengi na hakuna dawa yoyote niliyoacha kujitibu kwayo. Akaniambia: Uko wapi wewe na udongo wa Kaburi la Husein bin Ali, hakika wenyewe una tiba ya kila ugonjwa na amani ya kila hofu, hivyo utakapouchukua sema maneno haya: Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi nakuomba kupitia haki ya udongo huu na haki ya Malaika ambaye aliuchukua na haki ya Mtume ambaye aliushika na haki ya Wasii ambaye alifika hapo. Mrehemu Muhammad na Kizazi cha Muhammad Watu wa Nyumba yake na unifanyie hivi na hivi.”154 151 Biharul-Anwari 101: 136. 152 Al-Wasa’ilu 10: 329. 153 Al-Wasa’ilu 10: 352. Kifayatul-Athari cha Al-Khazazi: 290. 154 Biharul-Anwari 101: 118. 68


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 69

Tabaruku

15- Kutoka kwa Muhammad bin Muslim: Yeye alikuwa mgonjwa basi Abu Abdullah akamtumia kinywaji na akanywa. Basi ndipo alipokuwa kama aliyefunguliwa kutoka kwenye kitanzi. Kisha akaingia kwake, akamuuliza: ‘Umeonaje kinywaji?’ Akasema: ‘Bila shaka nilikuwa nimekata tamaa juu ya nafsi yangu, basi nikanywa na nimekuja kwako kama vile nimefunguliwa kutoka kwenye kitanzi.’ Basi Imamu akasema: ‘Ewe Muhammad, hakika kinywaji ulichokunywa ndani yake kilikuwa na udongo wa Makaburi ya wazee wangu na ndio tiba bora tunayojitibia, hivyo usijitenge nayo kwani hakika sisi huwanywesha watoto zetu na wanawake wetu na huwa tunaona kila kheri kutoka humo.”155 16- Kutoka kwa As-Swadiqi (a.s.) amesema: “Warambisheni watoto wenu udongo wa Husein hakika udongo wenyewe ni amani.”156 17- Kutoka kwa As-Swadiqi (a.s.) amesema: ‘’Ndani ya udongo wa Kaburi la Husein mna tiba ya kila ugonjwa na wenyewe ni dawa kubwa.’’157 18- Kutoka kwa Abu Abdullah amesema: ‘’Atakayepatwa na ugonjwa kisha akaanza kutumia udongo wa Kaburi la Husein basi Mwenyezi Mungu atamponya dhidi ya ugonjwa huo isipokuwa ugonjwa huo utakapokuwa unatokana na sumu.”158 19- Kutoka kwa Abul-Hasan Ar-Ridhaa (a.s.) amesema: “Kila udongo ni haramu kama mzoga na damu na kilichochinjwa kwa ajili ya asiyekuwa Mwenyezi Mungu isipokuwa udongo wa Kaburi la Husein, hakika wenyewe una tiba ya kila ugonjwa.”159 155 Biharul-Anwari 101: 118. 156 Biharul-Anwari 101: 118. 157 Biharul-Anwari 101: 118. 158 Biharul-Anwari 101: 118. 159 Biharul-Anwari 101: 120. Al-Wasailu 10: 415. Amalish-Shaykhi: 202. 69


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 70

Tabaruku

20- Kutoka kwa Abu Abdullah amesema: “Kila udongo ni haramu kwa wanadamu ila udongo wa Kaburi la Husein, basi atakayeula kutokana na maumivu basi Mwenyezi Mungu atamponya.”160 21- Kutoka kwa Abu Jafar Al-Baqir amesema: “Udongo wa Kaburi la Husein ni tiba ya kila ugonjwa na amani ya kila hofu na wenyewe ni kwa ajili ya shabaha aliyouchukulia.”161

‘KUTAFUTA BARAKA’ KUPITIA SHUKA LA KA’ABA 1- Kutoka kwa Utubah bin Abdullah amesema: Nilimuuliza Abu Abdullah kuhusu nguo ya Kaaba inayotufikia, je inafaa sisi tuvae chochote kutoka kwenye nguo hiyo? Akasema: Inafaa kwa watoto, misahafu na mto wa kulalia akiwa anatafuta Baraka kupitia nguo hiyo, Mwenyezi Mungu akipenda.162 2- Kutoka kwa Marwani bin Abdul-Malik amesema: “Nilimuuliza Abul-Hasan kuhusu mtu aliyenunua kipande cha shuka la Kaaba, hivyo kipande akakidhia haja zake na kingine kikabaki mikononi mwake, je inafaa akiuze? Akasema: Auze kiasi anachotaka na anufaike nacho na aombee Baraka zake….”163

160 Biharul-Anwari 101: 130. 161 Biharul-Anwari 101: 132. 162 Al-Kafi. Al-Furuu 1: 228. At-Tahdhibu 1: 5757. Man la Yahdhuruhu AlFaqihu 1: 91. Al-Wasa’ilu 9: 359, Mlango wa hukumu ya kunafaika na shuka la Kaaba. 163 Al-Wasa’ilu 9: 360. 70


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 71

Tabaruku

‘KUTAFUTA BARAKA’ KUPITIA MABAKI YA MAJI YA MUUMINI NA MASALIO YA UDHU WAKE. Kutoka kwa Muhammad bin Ismail ameivusha akasema: “Atakayekunywa mabaki ya muumini kwa ajili ya ‘Kutafuta Baraka’ kupitia mabaki hayo basi Mwenyezi Mungu ataumba Malaika kati ya hao wawili atakayewaombea maghfira mpaka Kiyama kitakaposimama.”164 Kutoka kwa Abdullah bin Sanani amesema: Abu Abdullah alisema: Ndani ya mabaki ya muumini mna tiba ya magonjwa sabini.165 Kutoka kwa Ali – Ndani ya Hadithi Mia Nne - amesema: Mabaki ya muumini ni tiba.166 Kunywa maswalio ya udhu wa muumini ni tiba dhidi ya magonjwa sabini, dogo mno kati ya hayo ni maumivu ya moyoni.167

‘KUTAFUTA BARAKA’ KUPITIA KUNYWA MAJI YA MBINGUNI 1- Kutoka kwa Hamrani kutoka kwa Abu Abdullah amesema: “Mtu mmoja alimlalamikia Kiongozi wa Waumini, ndipo akamwambia: Mwombe mkeo dirhamu moja kutoka kwenye mahari yake na ununulie asali kisha uinywe kwa kutumia maji ya mvua. Basi akafanya alivyoamrishwa na akapona. 164 Al-Wasa’ilu 17: 208, hadithi ya 2. Thawabul-Aamali: 83. 165 Al-Wasa’ilu 17: 208, hadithi ya 2. Thawabul-Aamali: 83. 166 Al-Wasa’ilu 17: 208. Al-Khisal 2: 157. 167 Kanzul-Ummali 9: 189. 71


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 72

Tabaruku

Kiongozi wa Waumini akaulizwa kuhusu hilo: Je, ni kitu ulichokisikia kutoka kwa Mtume?” Akasema: “Hapana, lakini nilimsikia Mwenyezi Mungu akisema ndani ya Kitabu chake: “Lakini wakikupeni chochote kwa radhi ya nafsi katika hayo, basi kileni kiwashuke kwa raha.” Na akasema: “Na tumeyateremsha kutoka mawinguni maji yaliyobarikiwa.” Hivyo vikakusanyika utulivu na raha na baraka na tiba basi nikataraji wema kutokana na hayo.”168 2- Kutoka kwa Muhammad bin Muslim amesema: “Nilimsikia Abu Jafari akisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema ndani ya kauli yake: “Na tumeyateremsha kutoka mawinginu maji yaliyobarikiwa.” Akasema: “Hakuna maji yoyote yaliyomo ardhini isipokuwa yamechanganyikana na maji ya mvua.”169 3- Kutoka kwa Abu Abdullah amesema: Kiongozi wa Waumini amesema: Kunyweni maji ya mvua hakika yenyewe hutoharisha mwili na huondoa magonjwa. Mwenyezi Mungu amesema: “Na akakuteremshieni maji mawinguni ili kukutakaseni kwayo na kukuondoleeni uchafu wa Shetani na kuzipa nguvu nyoyo zenu na kuitia imara miguu.”170 164 Al-Wasa’ilu 17: 208, hadithi ya 2. Thawabul-Aamali: 83. 165 Al-Wasa’ilu 17: 208, hadithi ya 2. Thawabul-Aamali: 83. 166 Al-Wasa’ilu 17: 208. Al-Khisal 2: 157. 167 Kanzul-Ummali 9: 189. 168 Tafsirul-Iyashiyu 1: 218. Aya ni kipande cha Aya ya 4 ya Surati An-Nisai. 169 Al-Kafi 6: 387, hadithi ya 2. Aya ni ya 9 ya Surati Qaf. ni kipande cha Aya ya 4 ya Surati An-Nisai. 170 Al-Wasa’ilu 17: 210 – 211, Furuul-Kafi 6: 287. Al-Mahasinu: 574. Aya ni ya 11 ya Surat Al-Anfal. 72


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 73

Tabaruku

‘KUTAFUTA BARAKA’ KUPITIA MAJI YA MTO FURATI Kutoka kwa Abu Abdullah amesema: Nadhani hakuna yeyote anayerambishwa utotoni maji ya Mto Furati isipokuwa ni lazima atatupenda AhlulBayti…..171 Kutoka kwa Ali bin Al-Husein ameivusha akasema: Abu Abdullah amesema: “Kuna umbali gani kati yenu na Mto Furati? Nikampa Hadithi. Akasema: Natamani laiti umbali huo ungekuwa kwetu, kwani ningeuendea Asubuhi na Mchana.”172 Kutoka kwa Saidi bin Jubayr amesema: “Nilimsikia Ali bin Husein akisema: “Malaika kutoka mbinguni hushuka kila usiku akiwa na gramu tatu za manukato ya peponi na kuyamwagia ndani ya Mto Furati. Hakuna mto wowote Mashariki ya ardhi na Magharibi yake wenye Baraka kuliko huo.”173

‘KUTAFUTA BARAKA’ KUPITIA UDONGO Kutoka kwa Abul-Hasan Ar-Ridhaa (a.s.) kuwa alikuwa akiipakaza barua udongo na akasema: “Si vibaya.”174 Kutoka kwa Ali bin Atwiyatu amesema kuwa yeye aliona barua ya AbulHasan ikiwa imepakazwa udongo.175 171 Al-Wasa’ilu 17: 211. 172 Al-Wasa’ilu 17: 212. Al-Furuu 6: 288. 173 Al-Wasa’ilu 17: 212. Al-Furuu 6: 288. 174 Al-Wasa’ilu 8: 497, Mlango wa Sunna kuipakaza barua udongo. 175 Al-Wasa’ilu 8: 497, Mlango wa Sunna kuipakaza barua udongo. 73


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 74

Tabaruku

Kutoka kwa Ar-Ridhaa (a.s.) amesema: Abul-Hasan alikuwa akipakaza barua yake udongo.176 Kutoka kwa Ar-Ridhaa kutoka kwa wazazi wake kutoka kwa Mtume, amesema: “Ombeni haja zenu mapema hakika zenyewe ni nyepesi, na ipakazeni udongo barua hakika wenyewe hufaulisha haja na ombeni kheri kwenye nyuso njema.”177 Ndani ya vitabu vya hadithi vya Masuni mmepokewa Hadithi kuhusu hilo, na kati ya hizo ni: Atakapoandika mmoja wenu basi aipakaze barua udongo kwani hakika huo hufaulisha haja.178 Zipakazeni udongo barua zenu hakika wenyewe hufaulisha, na hakika udongo umebarikiwa.179 Hakika Mtume alituma barua mbili kwenda vijiji viwili akiwaita kwenye Uislamu, basi barua moja akaipakaza udongo na nyingine hakuipakaza udongo, ndipo watu wa kijiji alichopakaza barua yao udongo wakasilimu.180 Mmoja wenu atakapoandika basi apakaze barua yake udongo kwani wenyewe unafaulisha.181 176 Al-Wasa’ilu 8: 497, Mlango wa Sunna kuipakaza barua udongo. 177 Al-Wasa’ilu 8: 497, Mlango wa Sunna kuipakaza barua udongo. 178 Jaamiu At-Tirmidhiyu 5: 66. Kanzul-Ummali 6: 289. 179 Sunan Ibnu Majah 2: 1240, Mlango wa kuipakaza barua udongo, hadithi ya 3774. Kanzul-Ummali 6: 517 Hadithi ya 16799. 180 Al-Isabah 2: 304. Herufi Al-Aynu, sehemu ya kwanza, wasifu wa Abdullah bin Rabiu An-Nummayriyu, namba 4669. 181 Kanzul-Ummali 10: 245. 74


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 75

Tabaruku

Mmoja wenu atakapoandika barua, basi aipakaze udongo, kwani hakika udongo umebarikiwa na wenyewe hufaulisha haja.182 Utakapoandika barua basi ipakaze udongo, kwani hakika wenyewe hufaulisha haja na udongo umebarikiwa.183 Pakazeni barua udongo na ipake udongo tokea chini, kwani hakika wenyewe hufaulisha haja.184 Pakazeni barua udongo, kwani hakika wenyewe una Baraka Kubwa na hufaulisha haja.185 Pakazeni barua udongo, kwani hakika wenyewe hufaulisha haja.186 Ndiyo haya, na kuna nyingi zimepokewa na kufurika kuhusu ‘Kutafuta Baraka’ kupitia Qur’ani, Mwezi wa Ramadhani, Daku, Udongo wa Madina na Tende zake, Maji ya Zamzamu, Mlima wa Uhudi na mengineyo mengi. Jambo linaloonyesha Umuhimu wa maudhui ya ‘Kutafuta Baraka’, hivyo tunawakuta Waislam bila kujali tofauti zao wanaharakisha kwenda ‘Kutafuta Baraka’ kupitia kila wanachokijua kuwa chenyewe kina Baraka. Wanafanya hivyo wakitafuta kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na kutii amri ya Mtukufu Mtume na wala hakuna wazo linalogusa moyo wa yeyote kuwa anafanya hivyo kwa ajili ya kujikurubisha kwa mtu au kitu anachotafutia Baraka, au kuwa yeye anaona kitendo chake hiki ni kumwabudu mtu huyu au kitu hiki anachotafutia Baraka. 182 Kanzul-Ummali 10: 245 Hadithi ya 29306 183 Kanzul-Ummali Hadithi ya 29307. 184 Kanzul-Ummali Hadithi ya 29309. 185 Kanzul-Ummali 10: 246, hadithi ya 29310. 186 Kanzul-Ummali 10: 246, hadithi ya 29310. 75


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 76

Tabaruku

Bali wao wote wameungana mkono juu ya ‘Kutafuta Baraka’ kuwa kwenyewe ni miongoni mwa matendo ambayo kwayo radhi za Mwenyezi Mungu zinatafutwa na wala si kitu kingine. Kutokana na hili ndio maana tokea zama za Mtukufu Mtume mpaka leo hii, huo umekuwa ndio mwenendo wa Waislam na hakuna jamuhuri ya Waislam iliyokhalifu isipokuwa watu wachache ambao hawana maarifa na Kitabu cha Mwenyezi Mungu. Hivyo wanachukua Aya zenye kufichikana na wanapindisha maneno kutoka kwenye maana yake ili wawapoteze Waislam huku wakiwashutumu kwa Shirki na Bidaa. Isipokuwa ni kuwa Waislam wanajua vizuri uchafu wa njia hizi na lengo lake la upotovu, kwa ajili hiyo wanachuoni wakubwa kutoka makundi yote mawili (Shia na Sunni) wamesimama kidete ili kuzuia uzushi wa kundi hili dogo potovu na wakabatilisha hoja zao kwa kutumia dalili nzito na wakarudisha vitimbi vyao shingoni mwao. Na wa kwanza aliyeziba nafasi za Wema Waliotangulia ni Sheikh Sulaymani bin Abdul-Wahabi, yeye ni ndugu mwenza wa Muhammad bin Abdul-Wahabi ambaye ni mbebaji wa bendera ya Bidaa hii, hivyo akamjibu kwa kitabu chake: Vimondo Vya kimungu katika kuwajibu Mawahabi. Kisha kwa ajili ya masilahi ya Uislamu wakamfuatia wanachuoni wengine katika kujibu na kuvunja hoja za kundi hili.

RAI ZA BAADHI YA WANACHUONI KUHUSU ‘KUTAFUTA BARAKA’ Tunapenda kuhitimisha Uchunguzi wetu huu kwa kutoa rai za baadhi ya wanachuoni wa Shia Imamiya kutoka miongoni mwa wale waliozungumzia mada hii ili tubainishe rai zao juu ya hilo. Na miongoni mwao ni: 1- Sheikh Jafar bin Sheikh Khadharu Al-Jananiyu An-Najafiyu (1156 – 1228 A.H.) amesema: Hakika unyenyekevu na ‘Kutafuta Baraka’ na kuheshimu yaliyo matukufu kwa Mwenyezi Mungu ni kumtukuza 76


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 77

Tabaruku

Mwenyezi Mungu. Kama pia ilivyo kuiheshimu Qur’ani Yake, Nyumba Yake na Msikiti Wake kwa sababu ya kunasibishwa Kwake ni kumheshimu Yeye Mtukufu. Basi atakayemheshimu Isa na Mariyam na Uzeyr kwa sababu ya utumwa wao na ukuruba wa nafasi yao nako ni kumtukuza kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Kama pia atakayeheshimu nyumba ya sultani, mtumwa wake, kijana wake na wafuasi wake kwa kuwa tu wako chini yake (ya sultani) basi anakuwa amemheshimu sultani. Ama yule atakayevikuta vinafaa kuheshimiwa na vina sifa hiyo kutokana na dhati yake kwa ajili ya utumwa na ufuasi, japokuwa lengo lake ni kujikurubisha mno, bila shaka atakuwa amavitukuza. Na hakika mimi tokea miaka thelathini iliyopita bado nachunguza misingi ya makundi ya Waislam kuanzia yale ya haki mpaka ya batili bado sijamkuta mtu yeyote anaheshimu Kitabu au Mtume fulani au eneo au mja mwema bila kukusudia kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu au kunasibisha kitendo hicho Kwake. Imedhihiri kuwa haya yote ni kwa ajili ya kumtii Mwenyezi Mungu na kumtukuza. Ama waabudu masanamu na waabudu waja wema, bila shaka wao huwa wanaviabudu hivyo ukweli wa ibada. Kwani walikuwa wakisali na kufunga kwa ajili ya hivyo. wanafanya hivyo kwa sababu ndani ya nafsi zao vina haki ya Umola Mlezi kwao au ili viwakurubishe kwa Mwenyezi Mungu, hivyo yenyewe ni ibada halisi kutokana na sababu hizo mbili……187 2- As-Sayyidu Muhsinu Al-Amini Al-Amiliyu amesema: Laiti ingekuwa kuheshimu Makaburi ya Manabii na Waja Wema ni 187 Manhaju Ar-Rashadi: 152, Sehemu ya tatu kuhusu ‘Kutafuta Baraka’ kupitia Makaburi. 77


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 78

Tabaruku

kuyaabudu na ni Shirki, basi ingekuwa kuheshimu Ka’aba Tukufu na kule Kuitufu, Jiwe Jeusi na kule kulibusu Jiwe hilo, Eneo la kisimamo, Msikiti, Maeneo Matukufu, Wazazi Wawili na kule kuwatii na kuwanyenyekea, Kupunguza sauti mbele ya Mtume na yeye kuwa mpole mbele ya waumini wanaomfuata. Na Malaika kumsujudia Adam, na ndugu wa Yusuf na baba yake kumsujudia, Askari kuwakweza viongozi wao na Sahaba wa Mtume, Makhalifa na Manabii kuwakweza wazazi wao na kule kuwasimamia na kuwanyenyekea na Mawahabi kumkweza mfalme Ibnu Su’ud na mengine kama hayo yote ni kumwabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu na ni Shirki, na ikiwa Nabii hajasalimika na Shirki itakuwaje hali ya asiyekuwa Nabii. Huwezi kusema kuwa hatuna matatizo na kule kuheshimu ambako Sheria imekuelezea na ikaamuru. Lakini maneno ni kuhusu kule kuheshimu ambako Sheria haijakuelezea. Tunasema huwezi kusema hivyo kwa sababu: Ikifanywa kuwa kila kuheshimu ni ibada na kila ibada isiyokuwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ni Shirki, basi Mwenyezi Mungu anakuwa kaamuru Shirki na kairidhia na kaipenda. Na dai hilo ni batili…..188 3- Ash-Sheikh Muhammad Jawadi Al-Balaghiyyu amesema: Jua kuwa miongoni mwa mambo ya dharura ndani ya Dini na yaliyokubalika na tabaka zote za Waislam, bali ni miongoni mwa nguzo kubwa za misingi ya Dini ni kule Ibada kuwa muhtasi kwa ajili ya Mola Mlezi wa walimwengu. Hivyo haistahiki mwingine na wala hairuhusiwi kuitenda kwa ajili ya mwingine, na atakayemwabudu mwingine basi yeye ni kafiri mshirikina, sawa aabudu masanamu au aabudu Malaika Mtukufu au kiumbe bora, na jambo hili hana shaka nalo yeyote yule miongoni mwa wanaoijua Dini ya Uislamu. Itakuwaje ashakie ilihali yeye kila siku anasoma mara kumi: “Wewe tu tunakuabudu na wewe tu tunakuomba msaada.” (Al-Fatiha: 5.) 188 Kashful-Irtiyabi: 431. 78


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 79

Tabaruku

Baada ya kuleta Aya zenye maana hii anasema: Lakini Ibada kama ilivyoelezwa na wafasiri na waarabu na wanachuoni wa kiislamu ni kilele cha unyenyekevu, kama kusujudu, kurukuu na kuweka shavu juu ya udongo na majivu kwa ajili ya kunyenyekea, na yanayofanana na hayo kama wanavyofanya waabudu masanamu kwa ajili ya masanamu yao. Ama kuzuru makaburi na kujipitisha mwili kwenye kaburi na kulibusu na ‘Kutafuta Baraka’ kwalo si chochote katika hilo (la kumnyenyekea asiyekuwa Mwenyezi Mungu) kama ilivyo wazi. Bali katika hayo hamna unyenyekevu wowote ukiachia mbali kilele cha unyenyekevu. Pia unyenyekevu tu si Ibada, kwani ingekuwa hivyo basi watu wote wangekuwa Washirikina na hata Mawahabi wenyewe, kwani wao huwanyenyekea maraisi, viongozi na wakubwa wao kwa kutumia baadhi ya unyenyekevu. Na watoto wao huwanyenyekea baba zao na watumishi huwanyenyekea waajiri wao na watumwa huwanyenyekea mabwana zao na kila tabaka la watu hulinyenyekea tabaka la juu yake, hivyo huwanyenyekea baadhi ya unyenyekevu na hujinyenyekeza kwao baadhi ya unyenyekevu……189 Al-Allama Al-Amini ndani ya: At-Tabaruku bil-Qabri Ash-Sharifi amesema: “Katika mada hii hatujakuta kauli iharamishayo kutoka kwa mwanachuoni yeyote miongoni mwa Wanachuoni wa Madhehebu manne ambayo yana rai yenye hadhi ndani ya jamii. Bali anayesema kuwa imekatazwa ni yule atokaye kwa wale wanaoona ‘Kutafuta Baraka’ ni kwa ajili ya kutukuza na si kwa ajili ya heshima. Na anasema kuwa ni Karaha kwa kutegemea dai la kuwa kukaribia kaburi tukufu kunaenda kinyume na adabu njema na anaona kwamba kuwa mbali nalo ni bora zaidi. 189 As-Sawaiqu Al-Ilahiyatu fi Radi Alal-Wahabiyati: 47 – 56. 79


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 80

Tabaruku

Haifai kwa mwanachuoni wa Sheria aliyeelimika atoe fat’wa ndani ya dini ya Mwenyezi Mungu kwa kutegemea mitazamo kama hii ambayo haina msingi wowote na inatofautiana kutokana na tofauti za rai na mitazamo. Ndiyo, wapo waliokwenda kinyume na Sheria ya kweli na wakahukumu kuwa ni haramu, kauli bila dalili na kulazimisha bila dalili na rai bila hoja, na wao wanajulikana kwa kwenda kinyume ndani ya jamii, hivyo hawatiliwi umuhimu, kuanzia wao hadi rai zao.190

190 Al-Ghadir 5: 146, Mlango wa ‘Kutafuta Baraka’ kupitia Kaburi tukufu 80


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 81

Tabaruku

ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL - ITRAH FOUNDATION: 1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9. 10. 11. 12. 13. 14. 15. 16. 17. 18. 19. 20. 21. 22. 23.

Qur'an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Ishirini Uharamisho wa Riba Uharamisho wa uwongo - Juzuu ya kwanza Uharamisho wa uwongo - Juzuu ya pili Hekaya za Bahlul Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.) Hijab vazi Bora Ukweli wa Shia Ithnaashari Madhambi Makuu Mbingu imenikirimu Abdallah Ibn Saba Khadijatul Kubra Utumwa Umakini katika Swala Misingi ya Maarifa Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia Bilal wa Afrika Abudharr Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu Salman Farsi Ammar Yasir Qur'an na Hadithi 81


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 82

Tabaruku

24. 25. 26. 27. 28. 29. 30. 31. 32. 33. 34. 35. 36. 37. 38. 39 40. 41. 42. 43. 44. 45. 46. 47. 48. 49. 50. 51. 52. 53. 54.

Elimu ya Nafsi Yajue Madhehebu ya Shia Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur'an Tukufu Al-Wahda Ponyo kutoka katika Qur'an. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii Mashukio ya Akhera Al Amali Dua Indal Ahlul Bayt Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna. Haki za wanawake katika Uislamu Mwenyezi Mungu na sifa zake Amateka Na Aba'Khalifa - Kinyarwanda Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) Adhana. Upendo katika Ukristo na Uislamu Nyuma yaho naje kuyoboka - Kinyarwanda Amavu n’amavuko by’ubushiya - Kinyarwanda Kupaka juu ya khofu Kukusanya swala mbili Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Kusujudu juu ya udongo Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s) Tarawehe Malumbano baina ya Sunni na Shia Kupunguza Swala safarini Kufungua safarini Umaasumu wa Manabii Qur’ani inatoa changamoto as-Salaatu Khayrun Mina'n-Nawm 82


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 83

Tabaruku

55. 56. 57. 58. 59. 60. 61. 62. 63. 64. 65. 66. 67. 68. 69. 70. 71. 72. 73. 74. 75. 76. 77. 78. 79.

Uadilifu wa Masahaba Dua e Kumayl Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mitume Muhammad (s) Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili Kuzuru Makaburi Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu Tujifunze Misingi Ya Dini Sala ni Nguzo ya Dini Mikesha Ya Peshawar Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu Ubora wa Imam 'Ali Juu ya Maswahaba Na Ushia ndio njia iliy onyooka Shia asema haya, Sunni asema haya, Wewe wasemaje? Liqaa-u-llaah Muhammad (s) Mtume wa Allah Amani na Jihadi Katika Uislamu Uislamu Ulienea Vipi? Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) Amali za Ramadhani

82.

Ujumbe Sehemu ya Kwanza

83.

Ujumbe sehemu ya Tatu

84.

Swala ya Maiti na Kumlilia Maiti 83


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 84

Tabaruku

85.

Amali za Ramadhani

86.

Ujumbe sehemu ya Pili

87.

Al-Mahdi katika Sunna

88.

Sunnani-Nabii

89.

Ukweli wa Shia

90.

Mariam, Yesu na Ukristo kwa Mtazamo wa Kiislamu

91.

Amali za Ramadhani

92.

Hadithi Thaqalain

84


Tabaruku D.Kanju Final.qxd

7/15/2011

12:17 PM

Page 85

Tabaruku

Back Cover Miongoni mwa mambo ambayo uchunguzi wake unajirudia mara kwa mara na kwa mifumo mbalimbali ni suala la ‘’Kutafuta Baraka’’ kupitia Mawalii na watu wema ndani ya umma na maeneo na Makaburi yaliyo matukufu kwa Waislam. Ni kutokana na udadisi au utata unaozuka tena au kujirudia juu ya suala hilo na hadi mara nyingi kufikia kiwango kibaya, huku mara nyingine ukipelekea kuigawa jamii iliyoshikamana pamoja huku ukileta mgawanyiko ndani ya wanajamii. Hivyo je; ‘’Kutafuta Baraka’’ ni Sunna au ni Bidaa? Je, suala hilo limetajwa ndani ya Qur’ani au Sunna? Je, lina historia yoyote kati ya waislamu na hasa ndani ya karne za mwanzo? Je, lina Sheria na kanuni? Hayo yote yatazungumziwa na Uchunguzi huu kwa muhtasari unaonasibiana na kwa kiwango kinachotosha kutuwafikisha. Tunamwomba Mwenyezi Mungu awe pamoja na makusudio na Yeye ndiye Mwenye Taufiki. Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Nukushi: +255 22 2127555 Barua Pepe: alitrah@raha.com Tovuti: www.alitrah.org Katika mtandao: www.alitrah.info

85


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.