Takwa

Page 1

ǶƎ ȈĉƷǂċ dzơ ǺƎ º Ù Ǹă Ʒą ǂċ dzơ Ǿĉ ºōǴdzơ ǶƎ Lją ƥƎ

TAKWA

Mwandishi: Ustadh Murtadha Mutahhari

Kimetarjumiwa na: Salman Shou

Mhariri: Al-Haj Ramadhani S. K. Shemahimbo


ƨŦǂƫ

ȃȂǬƬdzơ

ǦȈdz Ƙƫ ȅǂĈȀǘǷ ȄǔƫǂǷ ƾȈȀnjdzơ

ƨȈǴƷ ơȂLjdzơ ƨǤǴdzơ ńơ ƨȇDŽȈǴųȍơ ƨǤǴdzơ ǺǷ


ŠHaki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION

ISBN: 978 - 9987 - 512 - 62 - 1

Kimeandikwa na: Ustadh Murtadha Mutahhari

Kimetarjumiwa na: Salman Shou

Kimepangwa katika Kompyuta na: Al-Itrah Foundation

Toleo la kwanza: Julai, 2013 Nakala: 1000

Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. - 19701, Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 / 2127555 Barua Pepe: alitrah@raha.com Tovuti: www.ibn-tv-com Katika mtandao: w.w.w.alitrah.info


YALIYOMO Neno la Mchapishaji………………………………. ..........................................v SEHEMU YA KWANZA ............................................................ 06

Neno Takwa……………………………………… ............................................. 07 Kumuogopa Mungu……………………………… .......................................... 10 Maana ya Takwa…………………………………. ........................................... 12 Utekelezaji Kivitendo……………………………. .......................................... 15 Takwa katika Nahjul-Balaghah……………………....................................... 16 Takwa: Uhuru au Kizuizi?..................................... .................................. 20 Mtu kulinda takwa yake…………………………. ......................................... 22 Thamani na athari ya Takwa…………………….. ....................................... 25 Takwa na Afya…………………………………… ............................................ 29 Takwa na Utambuzi……………………………… .......................................... 30 Takwa na Wokovu……………………………….. ........................................... 30

SEHEMU YA PILI .................................................................... 32

Uhusiano baina ya takwa na utambuzi…………… ................................... 33 Takwa na hekima ya kivitendo……………………...................................... 33 Takwa husaidia akili……………………………… ......................................... 35 Athari za takwa kwenye utambuzi wa mtu……….. ................................. 37 Tofauti baina ya akili na uwezo wa kutumia akili… ............................... 42 Takwa na utakaso wa hisia na mhemuko…………................................... 44 Takwa na Kushinda Matatizo…………………….. ....................................... 45 Aina Mbili za Matatizo…………………………… ......................................... 46

iv


NENO LA MCHAPISHAJI

K

itabu ulichonacho mikononi mwako ni mkusanyiko wa makala zilizochukuliwa kutoka jarida la Message of Thaqalayn ambalo lilifululiza makala yenye mada ya Takwa kutoka kitabu kiitwacho Dah Goftaar kilichoandikwa kwa lugha ya Kifarsi na Ustadh Shahid Murtadha Mutahhari. Maudhui makubwa ya kitabu hiki ni takwa. Takwa maana yake ni pana sana kama utakavyoona katika kitabu hiki, lakini kwa ufupi maana yake ni uchamungu. Takwa ndio lengo kubwa la muumin ili kupata maendeleo ya kweli ya kiroho. Ustadh Shahid Murtadha Mutahhari alikuwa mwanachuoni mkubwa, mwanamapinduzi na mwanafalsafa mchamungu. Katika kitabu hiki anafafunua takwa ni nini na jinsi ya kuifikia ili kupata maendeleo ya kiroho. Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote, ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni vitu ambavyo havina nafasi tena katika akili za watu. Kutokana na ukweli huu, Taasisi yetu ya Al-Itrah imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumini yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili. Tunamshukuru ndugu yetu Salman Shou kwa kazi kubwa aliyofanya ya kukitarjumi kitabu hiki kutoka lugha ya Kiingereza. Pia na wale wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake. Allah awalipe wote malipo mema hapa duniani na kesho Akhera – Amin. Mchapishaji Al-Itrah Foundation v


TAKWA

SEHEMU YA KWANZA ϡ˴ ΃ ˲ Ϯ˸ ο˶έ˴ ή˸ ϴ˴Χ ˳ϥ΍˴ ϭ ˶ Ϫ˰͉ Ϡϟ΍ ˴ Ϧ˶ϣ ̆ϯ˴ Ϯ˸ ϘΗ˴ ̆ϰ˴ Ϡ˴ϋ Ϫ ϴ˸ ϨΑ˵ ˴β͉γ˴ ΃ ˸ Ϧ˴ Ϥ˴ ϓ˴ ΃ ˵ϧ˴Ύ˴ ˴ ˴˴ϋ Ϫ ϴ˸ ή˵Ο Ύ˴ ϔ˴η ̆ϰϠ ϧ ϲ˶ ϓ ˶ Ϫ˶ Α ˴ έΎϬ ϓ ˳έΎϫ ϨΑ˵ ˴β͉γ΃ ˸ Ϧϣ ˴ϧ˸Ύ˴ ˴ ˳ϑ˵ ͉ ˶έΎ˴ ˵ϧ˴Ύ˴ ‫ك‬ ˶Ύ͉ψϟ΍ ˴ Ϧϴ˶Ϥϟ ϡ˸ Ϯ˴ Ϙϟ΍ ΪϬ ϳ ϻ Ϫ ˰͉ Ϡ ϟ΍ ੱ Ϣ Ϩ Ϭ Ο ϭ ˸ ϱ˶ ˴ ˴ ͉ ˴ ˴ ˴˴ ˸˴ ˵ “Je, aliyeweka msingi wa jengo lake kwa kumcha Mwenyezi Mungu na radhi (yake) ni bora au aliyeweka msingi wa jengo lake juu ya ukingo wa shimo linalomomonyoka, na likamomonyoka likaanguka pamoja naye katika Moto wa Jahannam? Na mwenyezi Mungu hawaongozi watu madhalimu.” [9:109]

NENO TAKWA

T

akwa ni dhana ya Kiislamu ya kuwa na hali ya kujitawala au kujizuia. Neno hili limetumika mara 251 ndani ya Qur`ani ama kama nomino au kitenzi. Neno takwa asili yake ni neno la Kiarabu “wa-qa-ya” ambalo maana yake ni “ulinzi” au “msaada.” Takwa haikuwa imaanishe “hofu” au “uepukaji,” lakini kwa sababu kuwa na hofu ni sharti la kujilinda na jambo fulani na kuliepuka, wakati mwingine inaweza kurejelea kuwa na hofu. Pia, kwa kuwa kujilinda kutokana na kitu fulani kunahitaji kuandamana na hisia za hofu, wakati mwingine kisitiari inaweza kurejelea maana ya “uepukaji” 6


TAKWA

au “hofu.” Maana zote ni sahihi ingawaje hakuna ushahidi wa kuthibitisha kwamba hili kisitiari maana yake ni “hofu” au “kujizuia.” Wakati ambapo inaaminika sana kwamba amri isemayo ittaqu`llah maana yake ni “muogope Allah” na “ittaqunnar” maana yake ni “ogopa moto,” kwa kweli amri hizi zinazungumzia mtu kujilinda kutokana na adhabu ya Mwenyezi Mungu na madhara ya moto. Zaidi ya hayo, wale watu wanaojidhibiti kwa kujizuia kutenda kulingana na tamaa zao ambako kunahitaji subira msimamo madhubuti wanaitwa “muttaqiin,” ambalo ni neno la Kiarabu linalomaanisha “wale wanaotekeleza takwa kivitendo.” Ni muhimu kutambua kwamba takwa sio kutekeleza mambo ya faradhi ya kidini tu kama vile kuswali na kufunga saumu: ni kuhusu kuishi maisha ya ucha-Mungu. Mtu mwenye takwa hujitenga na kuishi maisha ya kinyama na uovu, kisha yeye akachagua kuishi maisha ya uadilifu. Ingawaje kuna fasili zingine za neno hili, kama vile takwa ya kijamii na kisiasa, takwa ya kidini ina hadhi bora na ya hali ya juu zaidi. Ni katika msingi wa dini tu ambamo mtu anaweza kutengeneza takwa yenye msingi madhubuti ndani mwake. Kama Qur`ani inavyosema: ϡ˴ ΃ ˲ ή˸ ϴ˴Χ ˳ϥ΍˴ Ϯ˸ ο˶έ˴ ϭ ˶ Ϫ˰͉ Ϡϟ΍ ˴ Ϧ˶ϣ ̆ϯ˴ Ϯ˸ ϘΗ˴ ̆ϰ˴ Ϡ˴ϋ Ϫ ϴ˸ ϨΑ˵ ˴β͉γ˴ ΃ ˸ Ϧ˴ Ϥ˴ ϓ˴ ΃ ˵ϧ˴Ύ˴ ˴ ˴ ˶ ˶ ˳ ϴ έ Ύ˴ ϧ ϲ˶ ϓ Ϫ Α έ Ύ Ϭ ϧ Ύ˴ ϓ έ Ύ ϫ ϑ Ϩ Α β γ ΃ Ϧ ϣ ή Ο Ύ ϔ η ϰ Ϡ ϋ Ϫ ϧ ˴ Ύ ˸ ˴ ˸ ˴ ˴ ͉ ˶ ˳ ˴ ˵˵ ˴ ̆ ˴ ˵ ˴˸ ˵ ˴͉ ˶Ύ͉ψϟ΍ ˴ Ϧϴ˶Ϥϟ ϡ˸ Ϯ˴ Ϙϟ΍ ΪϬ Ϡϟ΍˴ ੱ ˴ Ϣ͉ ϨϬ ϭ ‫ك‬ ˸ ϱ˶ ˴ ˴˴Ο ˸ϳ˴ ϻ˴ Ϫ ˵˰͉ “Je, aliyeweka msingi wa jengo lake kwa kumcha Mwenyezi Mungu na radhi (yake) ni bora au aliyeweka msingi wa jengo lake juu ya ukingo wa shimo linalomomonyoka, na likamomonyoka likaanguka pamoja naye katika Moto wa 7


TAKWA

Jahannam? Na mwenyezi Mungu hawaongozi watu madhalimu.� [9:109]

Raghib anasema katika kitabu chake kiitwacho Al-Mufradat fi Gharib al-Qur`an kwamba maana ya neno ‘wa-qa-ya’ ni kulinda kitu dhidi ya kila kitu kinachoweza kukiharibu kitu hicho, na takwa maana yake ni kuiweka nafsi chini ya ulinzi dhidi ya chochote kinachoitishia nafsi hiyo. Hata hivyo, wakati mwingine kufuatana na kanuni ya kutumia kisababishi badala ya athari na kinyume chake, maneno hofu na takwa hutumika kwa kubadilishana. Katika sheria ya dini, takwa maana yake ni kuiweka nafsi mbali na chochote kinachoweza kumwelekeza mtu afanye dhambi ili aweze kujizuia kujiingiza kwenye vitendo vilivyo haramishwa. Kwa wazi kabisa Raghib anasema kwamba takwa maana yake ni mtu kujilinda mwenyewe. Pia anasema kwamba neno hili linaweza kutafsiriwa kama hofu na halimaanishi kwamba katika mfano wa ittaqu`llah maana ya kisitiari ndiyo inayokusudiwa. Na kama tulivyosema, hakuna sababu ya kuthibitisha kwamba katika sentensi za aina hiyo sitiari yoyote imetumika. Jambo la kushangaza ni kwamba neno hili linatafsiriwa kama kujizuia (parhizkari) katika lugha ya Kiajemi. Kamwe haijaonekana kwamba bingwa yeyote wa lugha amejitokeza na kudai kwamba neno hili limetumika katika maana hii. Kama ambavyo tumesema kabla ya hapa, Raghib ametafsiri neno hili kama hofu lakini hakulitumia kama kizuizi. Hakuna uhakika wapi, lini, na kwa nini neno hili likatafsiriwa kama ucha-Mungu katika lugha ya Kiajemi. Nadhani ni watu wanaozungumza lugha ya Kiajemi tu ndio wanaopata maana ya kujizuia kutokana na neno takwa. Hakuna mtu anayezungumza Kiarabu anayelielewa neno hili kwa njia hii. 8


TAKWA

Hapana shaka kwamba katika matumizi, sharti la kuwa na takwa na kujilinda dhidi ya kitu fulani ni kukiepuka, lakini haimaanishi kwamba neno “takwa� lina maana hii.

9


TAKWA

KUMUOGOPA MUNGU

N

i muhimu kuelewa kwamba haitarajiwi mtu kuwa na mawazo hasi kuhusu Mungu wakati wa kumuogopa Yeye. Mwenyezi Mungu sio wa kuonekana kama kitu cha kuchukiza sana au kinachoogopesha sana. Kwa usahihi zaidi, Mungu ni ukamilifu wa kipekee na chanzo kizuri zaidi kwa binadamu kupenda. Dhana ya binadamu kupaswa kumuogopa Mungu kwa hakika inarejelea kuogopa uadilifu wa Mungu. Dhana hii inaonekana kwenye dua ifuatayo:

ϪϟΪϋ ϻ· ˷ ϑΎΨϳ ϻϭ ˬ ϪϠπϓ ϻ˷· ϰΟήϳ ϻ Ϧϣ Ύϳ “Ee Ambaye hutumainiwi ila kwa fadhila Zake, na haogopewi ila uadilifu Wake.”1

Dhana ya kuogopa uadilifu Wake inaonekana kwenye dua nyingine:

ϰΟήϳ ϥ΃ ϭ ˬ ϝΪόϟ΍ ϻ· ˷ ϚϨϣ ϑΎΨϳ ϥ΃ ΖϠϠΟ Ϟπϔϟ΍ ϭ ϥΎδΣϻ΍ ϻ· ˷ ϚϨϣ “Wewe ni mkubwa mno kuogopewa kwa uadilifu Wako, na kutumainiwa isipokuwa kwa ukarimu na fadhila Zako.”2

Uadilifu wenyewe ulivyo si kitu cha kuchukiza. Kuogopa uadilifu kwa uhakika kunagusia mtu kujiogopa mwenyewe 1

Biharul-Anwar, Jz. 92, uk. 439

2

Ibid, Jz. 99, uk. 55

10


TAKWA

kwa sababu ya matendo yake ya nyuma au mtu huogopa kwamba anaweza kuvuka mpaka na kukiuka haki za wengine siku za usoni. Kuhusu suala la woga na matumaini ambapo muumini wakati wote lazima awe na matarajio na mategemeo mema ambapo wakati huo huo huwa na hofu na wasiwasi, maana yake ni kwamba wakati wote lazima awe mwenye hofu ya kuvuka mpaka katika kufuata matamanio yake yasiotulizika ili kwamba kamwe yasichukue hatamu ya kuongoza mambo yake kutoka akilini mwake na imani yake, ambapo wakati huo huo lazima awe na matarajio na matumaini kwa Mungu, na kumtegemea Mungu ambaye wakati wote atamsaidia yeye. Imam Ali bin Husayn (a.s.) amesema kwenye du’a maarufu; Du’a ya Abu Hamzah Thumali: ΖόϤσ Ϛϣήϛ Ζϳ΃έ ΍Ϋ·ϭ Ζϋΰϓ ϲΑϮϧΫ ϱϻϮϣ Ζϳ΃έ ΍Ϋ· “Ee Mola Wangu! Ninapoangalia dhambi ambazo nimezitenda, huingiwa na hofu na ninapoangalia ukarimu Wako, ninakuwa na matumaini.”3

3

Al-Misbah cha al-Kaf ‘ami, uk. 588.

11


TAKWA

MAANA YA TAKWA

T

akwa ni sharti kwa mtu anayetaka kuishi maisha kwa kufuata kanuni fulani, ama ziwe za kidini au la, na anatakiwa kuwa na mwelekeo ulio wazi ili aweze kwenda kwenye lengo mahususi. Katika kufanya hivyo, anatakiwa ajilinde dhidi ya matamanio ya kupita ambayo hayaendani na malengo na kanuni zake. Kwa hiyo, katika maana iliyo pana zaidi, takwa ni sharti la kila mtu anayetaka kuwa binadamu wa kweli, aishi chini ya udhibiti wa akili, na afuate kanuni fulani. Katika mazingira ya kidini, takwa ni sifa ya wale wanaojilinda kutokana na yote yale yanayoďŹ kiriwa na dini kuwa ni upotofu na dhambi. Katika kulieleza hili, zipo aina mbili za takwa: Aina ya kwanza ni kule tu kuepuka kukabiliana na mazingira, ambamo humo dhambi zinaweza kuchukua nafasi na kufanyika, na hii ni sifa ya watu dhaifu na huwaelekeza kwenye upweke na kujitenga, ambapo aina ya pili ni kukabiliana na changamoto na kukataa kubadili msimamo, na hii ni sifa ya wale ambao ni imara katika imani yao na wanaweza kutoa mchango mkubwa katika jamii. Kufuatana na ile aina ya kwanza, mtu hujilinda kutokana na dhambi kwa kuepuka mazingira yenye mwelekeo wa kutenda dhambi. Hii ni sawa na mtu ambaye anaepuka sehemu yenye ugonjwa ambukizi kwa lengo la kulinda afya yake. Kufuatana na aina ya pili, mtu hutengeneza hali na uwezo ndani ya nafsi yake ambao humpa usalama wa kiroho na kimaadili. Ni kwamba, endapo mtu huyo anajikuta katika mazingira ambamo njia na visababishi vya kufanya dhambi vimemzunguka, ile hali ya kiroho humlinda yeye na hum12


TAKWA

zuia asitende dhambi. Hii ni sawa na mtu ambaye hutengeneza kinga ya kiafya mwilini mwake hivyo kwamba vijiumbe maradhi havitaathiri afya yake. Sasa, watu wa kawaida hufikiria takwa ni ile ya aina ya kwanza. Kwa wale ambao wanasemekana kuwa na takwa, kwa kawaida ina maana kwamba ni mtu ambaye wakati wote hujipwekesha na kujitenga kwenye kona na kujizuia kutokana na visababishi vya dhambi. Imeeleweka hivi kwa sababu neno takwa kila wakati limekuwa likitafsiriwa kwetu kuwa ni kujihini. Zaidi ya hayo, kujizuia kufanya dhambi siku zote kumetafsiriwa pole pole kuwa ni kuepuka chimbuko la dhambi; baadaye maana ilibadilika na kuwa kujipwekesha na kuepuka jamii. Hivyo, neno hili linaposikika kwenye mazungumzo ya kawaida, aina fulani ya hali ya kuepuka na kukalifu huja akilini. Ingawaje sharti la kuendesha maisha ya maana ni kufuata kanuni fulani mahususi, si busara kuepuka maisha ya kijamii katika kufanya hivyo. Ufunguo wa kuishi maisha yaliyo sahihi ni kutengeneza hali ya kinga ndani ya nafsi yetu ambayo hatimae hutulinda. Kwenye kitabu chake maarufu cha mashairi kiitwacho Gulistan, Sa`di anasema: “Nilimuona mtu adhimu kwenye eneo la milimani. Ambaye kwa kuridhika ameiacha dunia na kuishi pangoni. Kwa nini, niliuliza, wewe huji mjini Japo mara moja ili ulegeze vifungo vya moyo wako? Akajibu: Huko kuna wanamwari wenye sura nzuri. Maiti zitakapokuwa tele, tembo watajikwaa.”4 4

Gulistan ya Sa’di, Sura ya 5, Hadithi ya 17 iliyotafsiriwa na Sir Edwin Arnold.

13


TAKWA

Kwenye shairi hilo hapo juu, mtu ambaye alijipwekesha huko milimani anajizuia kurudi mjini kwa sababu ya “wanamwari wenye sura nzuri” ambao hatimae wangeweza kusababisha “ajikwae.” Hii ni aina ya kwanza ya “takwa.” Hata hivyo, sio kwa manufaa mtu kujiweka mbali na sehemu yenye utelezi ili kujizuia asiteleze. Kilicho bora zaidi ya hicho ni mtu kujua namna ya kutembea juu yake bila kuyumba na kupoteza mwelekeo sawa. Baba Tahir anasema: “Chini ya udhalimu wa macho na moyo mimi ninalia, Kwani macho yote yale yanaona, na moyo unahifadhi: Nitajitengenezea upanga wa chuma cha pua wenye ncha kali, Niyachomoe macho yangu hivyo niuweke huru moyo wangu.”

Bila shaka, mioyo yetu itatekwa na kila kitu ambacho macho yetu yanakiona. Hata hivyo, kujipofusha wenyewe si tu ndiyo chaguo pekee. Njia iliyo bora zaidi ni kutengeneza uwezo ndani ya nafsi zetu ili kwamba macho yetu yasiziteke nyara nafsi zetu. Kama tunataka kutengeneza sime yenye ncha ya chuma kwa lengo la kuokoa nyoyo zetu kutokana na macho, tunahitaji sime nyingine kwa ajili ya masikio yetu kwani kila kitu kinachosikiwa na sikio, moyo hukigeukia. Hali ni ile ile kwa milango yote ya fahamu yaani; kuonja, kugusa, na kunusa. Katika hali hii, binadamu anakuwa kama simba asiye na mkia. tumbo, na kichwa ambaye Maulawi (Jalal al-Din Rumi) alimuelezea kwenye simulizi yake katika Mathnawi.

14


TAKWA

UTEKELEZAJI KIVITENDO

K

wenye baadhi ya vitabu vinavyozungumzia mambo ya kiroho, marejeo yanafanywa kwa baadhi ya watu ambao walitumia mbinu za kivitendo kujilazimisha kushikamana na sheria ya dini. Mathalan, walikuwa wakiweka changarawe midomoni mwao kwa lengo la kudhibiti ndimi zao kutokana na kuongea sana au kujiingiza kwenye mazungumzo ya porojo au yaliyo haramishwa. Kwa kawaida njia ya aina hii inachukuliwa kama mfano kamili wa kuwakilisha uchaji-Mungu. Hata hivyo, mtu kujiwekea majukumu ya kivitendo ili kuepuka kutenda dhambi, si lazima iwe na maana kwamba mtu huyo amejikamilisha. Kama tukifaulu kufanya hivyo na kujizuia kufanya dhambi, ni kweli tutakuwa tumejizuia kutenda dhambi, lakini nafsi zetu zitakuwa bado hazijabadilika. Ni kwamba nafsi zetu zimetulia tu kwa sababu hazina njia ya kutenda dhambi. Hivyo, ukamilifu wa kweli umo kwenye uhuru wa mtu wa kuweza kutenda dhambi lakini bado anachagua kujizuia kukosea bila kutumia aina yoyote ya kujilazimisha. Aina hizi za uzuiaji zinaweza kuchukuliwa kama ni ukamilifu pale tu ambapo zinaonekana kama hatua za mwanzo za kuelekea kwenye hatua kubwa za kutengeneza sifa ya ucha-Mungu. Hii ni kwa sababu ucha-Mungu unaweza kutengenezwa baada ya mlolongo wa mazoezi pinzani dhidi ya vitendo viovu. Lakini nguvu halisi ya ucha-Mungu ipo mbali sana na vitendo hivi. Ni hali takatifu na nguvu kuu ya nafsi inayowasaidia na kulinda wanadamu. Mtu lazima apambane ili aweze kupata ile nguvu halisi ya ucha-Mungu. 15


TAKWA

TAKWA KATIKA NAHJULBALAGHAH

N

eno “Takwa” limesisitizwa kwenye mkusanyo wa hotuba na semi za Imam Ali (a.s.) ambao kwa pamoja unaitwa Nahjul-Balaghah, na kila mara limetumika kumaanisha tabia ya kuiimarisha na kuilea nafsi yenye kutamani maovu na matamanio yake yasiyotulizika. Kwenye kitabu hiki, Imam Ali (a.s.) amenukuliwa kuwahi kusema:

ƩƘǸǛƗ ȁ ǶȀȈdzƢȈdz ƩǂȀLJƗ ŕƷ ǾƬǧƢű ǶđȂǴǫ ƪǷDŽdzƗ ȁ ǾǷǁƢŰ ƅơ ƔƢȈdzȁƗ ƪŧ ƅơ ȃȂǬƫ ǹƐ ƛ ǶǿǂƳơȂǿ “Kwa hakika kumuogopa Allah kumewaokoa wapenzi wa Allah kutokana na yaliyo haramu na kumeweka hofu Yake kwenye nyoyo zao hivyo kwamba wanapitisha nyakati za usiku wakikesha na kupitisha michana yao kwa kiu ya maji.”5

Kwenye nukulu hiyo hapo juu Imam Ali (a.s.) kwa wazi kabisa anaelezea maana ya “Takwa” kama hali ya kiroho ambayo huwaokoa watu kutokana na kutenda dhambi na anachukulia kumuogopa Mungu kuwa ni mojawapo ya matokeo yake. Kwa hiyo, Takwa haimaanishi “kuogopa” bali mojawapo ya matokeo yake ni kuzifanya nyoyo kumuogopa Allah. Kama ilivyotamkwa huko mwanzoni, “ittaqu`llah” haimaanishi amri ya “kumuogopa Mungu.” Katika hadith nyingine, Imam Ali (a.s.) anasema: 5

Nahjul-Balaghah, Semi ya 114

16


TAKWA

ƩȐưŭơ ǺǷ Ǿȇƾȇ śƥ ƢǸǟ ŐǠdzơ Ǿdz ƪƷǂǏ ǺǷ ǹơ .ǶȈǟǃ Ǿƥ ƢǻƗ ȁ ǾǼȈǿǁ DZȂǫƗ ƢŠ ŕǷƿ ȁ ƢȀǴǿƗ ƢȀȈǴǟ Dzŧ džſ DzȈƻ ƢȇƢǘŬơ ǹơ ȁ ȏƗ...ƩƢȀƦnjdzơ ǶƸǬƫ Ǻǟ ȃȂǬƬdzơ ǾƫDŽƴƷ ơȂǘǟơ ȁ ƢȀǴǿƗ ƢȀȈǴǟ Dzŧ Dzdzƿ ƢȇƢǘǷ ȃȂǬƬdzơ ǹơ ȁ ȏƗ .ǁƢǼdzơ ľ Ƕđ ƪǸƸǬƬǧ ƢȀǸŪ ƪǠǴƻ .ƨǼŪơ ǶēƽǁȁƢǧ ƢȀƬǷǃƗ “Wajibu wa yale ninayoyasema umehakikishwa na mimi ninawajibika kwa ajili ya hayo. Yeye ambaye kwake uzoefu umeonyesha dhahiri adhabu za mfano zilizopita zamani [walizoadhibiwa watu na Allah] anazuiwa na ucha-Mungu kutokana na kuangaukia kwenye shaka….. Zingatia kwamba dhambi ni sawa na farasi wakaidi ambao juu yake wamewekwa wapandaji wake hatamu zao zimelegezwa na kwa hiyo wanaweza kuruka nao ndani ya Jahannam. Tambua kwamba ucha-Mungu ni sawa na farasi waliopata mafunzo ambao wapanda farasi wao wamewekwa juu yao na hatamu zao mikononi mwao hivyo kwamba wanaweza kuwafikisha wapandaji wao Peponi.”6

Kwenye hotuba hii, maana ya takwa ni kudhibiti au kutawala nafsi. Mtu ambaye si imara vya kutosha kuweza kukataa kutii matamanio yake na anasalimisha udhibiti wake kwa nafsi yake anafananishwa na mpanda farasi asiye stadi aliyempanda farasi mkaidi asiye na dhamira. Sharti la takwa na kujidhibiti ni kuongeza nguvu ya dhamira ya mtu na kuwa na shaksia ya kiroho na kiuwiano, kama mpanda farasi mwenye busara ambaye anampanda farasi wake kwa ustadi, na farasi wake naye, kwa haraka sana akamtii. Mtu anayempanda farasi mkaidi wa matamanio, anasa, ulafi wa mali na tamaa ya makuu ni tegemezi wa uovu huu na akiachia 6

Nahjul-Balaghah, Semi ya 16

17


TAKWA

hatamu ya dhamira yake huponyoka mikononi mwake, basi hawezi kudhibitiwa na hekima na utambuzi. Na kwa yule ambaye hutegemea takwa, ni kana kwamba amepanda farasi wa udhibiti wa nafsi na anashikilia hatamu za dhamira. Anajiongoza mwenyewe katika mielekeo yote. Kuhusu hili, Imam Ali (a.s.) anasema:

ƨǼĈƴdzƊơ ńƛ Ǫȇǂǘdzơ ƾǣ ľ ȁ ƨǼĈŪƌ ơ ȁ ǃǂūơ ǵȂȈdzơ ľ ȃȂǬƬdzơ ǹƢǧ “Kwa hakika, kwa leo ucha-Mungu ni ulinzi na ngao, na kwa kesho (Siku ya Hukumu) ni njia ya kuelekea Peponi.”7

Imam (a.s.) anaendelea kufafanua zaidi juu ya ucha-Mungu kwa kutoa mfano wenye mguso sana:

ǾȈdzƛ ƢŪ ǺǷ ǃǂŹ ȏ ȁ ǾǴǿƗ ǞǼŻ ȏ DzȈdzƿ ǺǐƷ ǁơƽ ǁȂƴǨdzơ ȁ DŽȇDŽǟ ǺǐƷ ǁơƽ ȃȂǬƬdzơ ǹơ “Jueni, Enyi viumbe wa Allah, kwamba ucha Mungu ni nyumba imara ya ulinzi ambapo kutomcha Mungu ni nyumba dhaifu ambayo haiwezi kulinda watu wake, na haiwezi kumpa usalama yule anayechukua hifadhi humo.”8

Hapa, ucha Mungu (Takwa) umefananishwa na nyumba madhubuti ya ulinzi. Na bado kwenye hotuba nyingine ijulikanayo sana iitwayo “Wachaji Mungu” (al-Muttaqin), Imam Ali (a.s.) anajibu ombi la Hammam bin Shuray ambaye alimuomba aeleze wacha Mungu ni watu gani ili aweze kuwaelewa zaidi. Mwanzoni Imam Ali (a.s.) alitoa jibu fupi, lakini hata hivyo, Hammam 7

Nahjul-Balaghah, Semi ya 189

8

Nahjul-Balaghah, Semi ya 155

18


TAKWA

hakutosheka na alisisitiza Imam (a.s.) atoe maelezo kwa upana zaidi. Hivyo, Imam (a.s.) alijibu kwa kutoa sifa zaidi ya mia moja za kiroho, kiakili, kimaadili za wacha-Mungu. Kwa mujibu wa wanahistoria, mara baada ya Imam (a.s.) alipomaliza kutoa hotuba yake, Hammam alivutiwa sana na majibu hivyo kwamba alilia sana na akafariki dunia. Hivyo, ni dhahiri kwamba takwa ni hali ya kiroho ambayo ni kama ngome, hirizi, au farasi aliyefundishwa kwa ajili ya nafsi. Kwa ufupi, takwa ni nguvu ya kiroho.

19


TAKWA

TAKWA: UHURU AU KIZUIZI?

T

akwa si kizuizi; ni ulinzi. Hata kama tukiita takwa ni kizuizi, basi kizuizi hiki kwa kweli ni ulinzi. Kama vile ilivyo kimakosa kuiita nyumba kizuizi pamoja na kwamba imejengwa kwa kuta, vyumba, milango migumu na madirisha ili kuwaweka wakazi wake katika hali ya usalama kutokana na hali ya hewa yenye madhara na kuziweka samani na vitu vingine kwenye sehemu za usalama, takwa, kama ilivyo nyumba, ni ulinzi. Tunaweza kukiita kitu kuwa ni kizuizi pale kinapotunyang`anya zawadi au furaha, lakini kitu kinachozuia hatari isitupate na kutulinda ni usalama, si kizuizi. Kwenye Qur`ani, takwa imefafanuliwa kama vazi kwa vile huulinda mwili dhidi ya baridi kali na joto kali kama vile nyumba inavyowalinda watu. Ndani ya Qur`ani baada ya kutaja vazi kwa ajili ya mwili, inatamkwa: ˴˴ϋ Ύ˴ ˶ ˸ Ύ˱θϳ˶ έ˴ ϭ ˸ Ϣ˵ Ϝ˶ Η΁˸ Ϯ˴γ ϱ˶ έ΍˴ Ϯϳ˵ Ύ˱γΎ˴ Βϟ Ϣ˵ Ϝ˸ ϴϠ Ϩϟ˴ ΃ Ϊ ϗ ˴ ϡΩ ϨΑ˴ Ύϳ˴ ˸ΰϧ˴ ˴΁ ϲ˶ ˸˴ ̆ ˴ ͉˴ ˶˴ ͉ϳ˴ ˸ Ϋ ̆ϯ˴ Ϯ˸ Ϙ͉ Θϟ΍ ˵αΎ˴ Βϟ ϭ ϥ Ϋ ੱ‫˲ ن‬ ή˸ ϴ˴Χ ˴Ϛ˶ ϟ̆ ή͉ ϛά ϢϬ όϟ˴ ˶ Ϫ˰͉ Ϡϟ΍ ˶ΕΎϳ˴΁ ˸ Ϧ˶ ϣ ˴Ϛ˶ ϟ˴ ˴ϭ˵ ˵Ϡ ‫ق‬ ੱ

“Enyi wanadamu! Hakika tumewateremshia vazi lifichalo tupu zetu na vazi la pambo. Na vazi la taqqwa ndio bora. Hayo ni katika ishara za Mwenyezi Mungu ili wapate kukumbuka.”[7:26]

Katika kutoa muongozo wa kuwa na takwa, Imam Ali (a.s.) anasema katika moja ya hotuba zake:

ƢđơȂǻȂǐƫ ȁ ƢǿȂǻȂǐǧ ȏơ 20


TAKWA

“…..mnatakiwa kuichunga na nyinyi mjichunge wenyewe kupitia hiyo …..”9 Zaidi ya hayo, Imam Ali (a.s.) anashikilia kwamba ucha Mungu ni sababu kubwa ya uhuru. Anasema:

Ƣđ ƨǰǴǿ Dzǯ ǺǷ ƧƢų ȁ ƨǰǴǷ Dzǯ ǺǷ ǪƬǟ ȁ ƽƢǠǷ ǽŚƻƿ ȁ ƽơƾLJ ƵƢƬǨǷ ƅơ ȃȂǬƫ ǹƜǧ .ƤƟƢǣǂdzơ DZƢǼƫ ȁ ƣǁƢŮơ ȂƴǼȇ ȁ ƤdzƢǘdzơ ƶƴǼȇ “Hakika, ucha Mungu ni ufunguo wa kuelekea kwenye muongozo, mahitaji ya Akhera, ni uhuru kutokana na aina zote za utumwa, na ukombozi wa kututoa kwenye maangamizi. Kwa msaada wake mtafutaji hufaulu na yule anayetafuta salama huepuka na kupata malengo yake.”10

Takwa humsaidia mhusika kufikia malengo yake na humlinda dhidi ya maadui zake. Kwanza kabisa, takwa huwapa wanadamu uhuru katika masuala ya kiroho na kimaadili, humfungulia minyororo ya utumwa ya matamanio ya muda mrefu, na humpa yeye ahueni ya mateso ya ulafi, wivu, ashiki na hasira. Kwa njia isiyo ya moja kwa moja, pia humpa mhusika uhuru wa kijamii. Utumwa na utwana katika jamii ni matokeo ya utumwa wa kiroho. Mtu ambaye ni mtumwa na anautii ukwasi na mamlaka hawezi kuishi kwa uhuru kijamii. Kwa hiyo, ni kweli kusema kwamba takwa huwapa binadamu “uhuru kutokana na utumwa wa kila aina.” Hivyo, si tu kwamba takwa haina mnyororo au kizuizi, lakini kwa kweli takwa yenyewe ndiyo uhuru. 9 10

Nahjul-Balaghah, Semi ya 233 Nahjul-Balaghah, Semi ya 228

21


TAKWA

MTU KULINDA TAKWA YAKE

K

ufikiria takwa kuwa ngome na mlinzi inaweza kuwafanya baadhi ya watu kuwa na majivuno na kuwa wajinga na wanaweza kudhani kwamba mtu mwenye takwa hawezi kufanya makosa. Hii inaweza kuwa na matokeo ya kutokuweza kabisa kutambua hatari kubwa ya takwa. Lakini ukweli ni kwamba, ingawaje takwa ni hali iliyo kamilika, pia inahusisha hatari fulani pia. Sio kwamba haiwezekani kwa mtu kuishi chini ya ulinzi wa takwa, na yeye akailinda takwa pia. Imam Ali (a.s.) amerejelea aina zote za ulinzi katika kauli ifuatayo: “Mnatakiwa kuichunga na ninyi wenyewe mjichunge kupitia hiyo!” Hivyo, lazima tuichunge takwa na yenyewe ituchunge sisi. Pia, lazima tutafute ukaribu kwa Mungu kupitia takwa na pia tumuombe Mwenyezi Mungu atujaalie na takwa. Pia Imam Ali (a.s.) alisema:

ơȂǼȈǠƬLjƫ ǹơ ȁ ǶǰǬƷ ƅơ ȄǴǟ ƨƦƳȂŭơ ȁ ǶǰȈǴǟ ƅơ ǪƷ ƢĔƜǧ ƅơ ȃȂǬƬƥ ƅơƽƢƦǟ ǶǰȈǏ ȁơ .ƅơ ȄǴǟ Ƣđ ơȂǼȈǠƬLjƫ ȁ ƅƢƥ ƢȀȈǴǟ “Ninawashaurini Enyi viumbe wa Mwenyezi Mungu, kwamba mnapaswa kumcha Allah kwa sababu ni haki Yake juu yenu na hutengeneza haki yenu juu ya Allah, na kwamba mnapaswa kuomba msaada wa Allah kutoka humo, na msaada wake katika kukutana na Allah.”11 Hata hivyo, hatari zinazodhoofisha takwa lazima zifikiriwe. Inaonekana katika hukmu za kidini kwamba takwa inaju11

Nahjul-Balaghah, Semi ya 190

22


TAKWA

likana kama ulinzi wenye uhakika na kinga dhidi ya dhambi nyingi, lakini ipo mipaka kwa ajili ya dhambi zingine zenye kuvutia zaidi. Mathalani, haijatamkwa katika hukumu za kidini kwamba mtu kukaa peke yake mahali ambapo kipo kitendea kazi kinachotumiwa kwa kazi ya wizi wa kunyang`anya, kunywa mvinyo, uuaji wa binadamu, kuakatazwa. Au haikuharamishwa mtu kuwa peke yake ndani ya nyumba usiku, ambamo hakuna vizuizi juu ya mtu kama akitaka kunywa mvinyo. Imani na takwa vitamhakikishia ulinzi. Lakini kuhusu silika ya ngono ambayo ina nguvu na ushawishi zaidi, takwa haimhakikishii mtu huyo ulinzi na inakatazwa mtu kuwa peke yake na mtu wa jinsia nyingine kwa sababu silika ya ngono ni hatari na inaweza kuharibu takwa hata kama takwa ikiwa na nguvu zaidi. Kuna beti moja kwenye shairi mashuhuri la Hafiz ambayo kwamba wakati wowote ninapoikuta, suala ambalo nimelitaja hunijia akilini mwangu, kana kwamba Hafiz alitaka kueleza ukweli huu wa kiroho kwa njia tamu sana ya namna yake mwenyewe. “Kwa sarafu, hivi ni kwamba wanachukua mtihani ili kwamba baada ya kazi zao, wote wenye matao wachukue? Katika uoni wangu, ushauri ni kwamba wote wanafanya kazi, marafiki Unapaswa kuachia waende, na chukua mpotano wa miti ya rafiki Ncha ya msuko wa Saki, marafiki kwa furaha wachukua. Kama anga ikiwaruhusu, mapumziko kidogo wanachukua.”12 12

ya Hafidh Shirazi. Tafsiri ya awali na Henry Wilberforce Clarke (1840-1905) Jz. 2, uk.387, Ghazil ya 209 (253), 1891. Sehemu ya 2 (makala 1.03) iliyokusanywa na kusahihishwa na Dk. Behrouz Homayoun Far, Ghazal na. 185, uk. 172. Makala ya kwenye mtandao inaweza kupatikana: http//www2enel ucalgary.ca/People/Far/hobbie/iran/hafiz.html

23


TAKWA

Halafu anasema: “Kwa wale walio wazuri sana, msijivunie sana mkono wenu wenye nguvu ya usahili,”13 “Kwani, miongoni mwa kabila hili, wakiwa na mmoja aliye kipandoni, ngome wanaichukua.”14

Kwenye beti ya hapo juu, takwa imefananishwa na uzio, kama vile Imam Ali (a.s.) alivyoeleza. Halafu, imesemwa kwamba uwezo wa “wale wazuri” ni mkubwa zaidi ya ule wa ngome hii na hapana yeyote miongoni mwao anayeweza kukata kwa meno. Katika kundi hili hata mpanda farasi mmoja anaweza kuvunja uzio, na wala hapahitajiki shambulizi la pamoja.

13

Hafidh anatumia neno “parhiz” ambalo hapa lina maana ya taqwa.

14

Ibid

24


TAKWA

THAMANI NA ATHARI YA TAKWA

Z

aidi ya athari za kuvutia za takwa za baada ya maisha haya na ukweli kwamba ndio njia pekee ya ukombozi wa binadamu kutoka kwenye unyonge wa daima milele, takwa ina thamani zingine na athari nyingi katika maisha haya ya kidunia. Imam Ali (a.s.), ambaye alisisitiza takwa katika maelekezo yake na aliwasihi watu waielekee kwa namna ya kujipambanua kabisa, amerejelea matokeo mengi ya takwa. Mathalani, alisema:

ƨǰǴǿ Dzǯ ǺǷ ƧƢų ȁ ƨǰǴǷ Dzǯ ǺǷ ǪƬǟ “Uhuru kutokana na aina zote za utumwa na ukombozi kutokana maangamizi yote.”15

Au mahali pengine alisema:

ĄƵȐƊ Ǐ ă ȁă Ƕą ǯƌ ƽĉ ƢăLjƳą ƗƊ Ǒ Ǝ ǂă Ƿă ƔÉ ƢƊǨNjĉ ȁă Ƕą ƌǰƫĉƾă Ơĉǧƒ ƗƊ ȄăǸǟă Ąǂǐ ă ƥă ȁă Ƕą ǰƌ ƥƎȂƌǴǫƌ ƔÊ ơăƽ ƔÉ ơăȁƽă ƅơ ȃăȂǬƒ ƫă ǹō ƜƊǧ ȁă Ƕą ǰƌ Njĉ Ƣƒ Ƴă ǝƎ DŽă ǧƊ ĄǺǷą ƗƊ ȁă Ƕą ǯƌ ǁƎ ƢăǐƥąƗƊ Ƣănjǟă ÉƔȐƊ ƳƎ ȁă Ƕą ƌǰLjÊ ƌǨǻąƗƊ dž Ǝ ǻăƽă ǁĄ ȂĄȀǗƌ ȁă Ƕą ǯƌ ǁƎ ȁƾĄǏ ƽĉ ƢăLjǧƊ Ƕą ƌǰƬĉǸă Ǵƒ ƌǛ ƽĉ ơăȂLJă ƔÉ ƢăȈǓ ĉ “Kwa hakika , kumuogopa Allah [Takwa] ni dawa ya nyoyo zenu, uwezo wa kuona kwa roho zenu, tiba ya maradhi ya miili yenu, mrekebishaji wa uovu ndani ya vifua vyenu, mtakasaji wa uchafu ndani ya akili zenu, nuru ya giza la macho yenu, mtulizaji wa hofu ya nyoyo zenu na mng’aro juu ya utusitusi wa ujinga wenu.” 16 15

Hafidh; Semi ya 228

16

Hafidh; Semi ya197

25


TAKWA

Kwa kweli, Imam Ali (a.s.) anashikilia kwamba takwa inayo manufaa kwa matatizo na dhiki zote za binadamu. Kwa kweli, kama hatuďŹ kii tu mwelekeo hasi wa takwa na tukaiďŹ kiria kama Imam Ali (a.s.) alivyoiďŹ kiria, lazima tukubali kwamba takwa ni mojawapo ya nguzo za maisha ya binadamu, ama katika maisha binafsi au ya kijamii, na kwamba msingi wa maisha haungekuwa imara bila takwa. Thamani ya kitu huwa dhahiri zaidi baada ya kitu hicho kujulikana iwapo kama kinaweza ama hakiwezi kubadilishwa na kitu kingine. Takwa ni mojawapo ya vijenzi ama sehemu muhimu ya maisha, kwa sababu hapana kitu kingine iwe ama ni mamlaka, fedha, au kutunga sheria kinachoweza kushika nafasi yake. Miongoni mwa matatizo yetu ya kila siku ni kuwepo kwa hukumu na kanuni nyingi sana ambazo hubadilika kwa mfululizo. Sheria na kanuni hutengenezwa kwa ajili ya mambo mahususi halafu baadaye hubadilishwa na huanzishwa zingine mpya. Hata hivyo, sheria hazitoshi kuirekebisha jamii. Kwa kweli, hapana shaka kwamba sheria yenyewe nayo pia ni jambo la maisha. Licha ya kuwepo kwa sheria za jumla za dini, watu wanahitaji mlolongo wa sheria za kiraia. Lakini jamii hazirekebishwi zote na sheria hizo. Mipaka inaazishwa na sheria; kwa hiyo, watu wanatakiwa kuwa na namna fulani ya uwezo wa kuona thamani ya mipaka hii na kuikubali. Nguvu hii huitwa takwa. Inasemekana kwamba sheria lazima iheshimiwe. Hii ni kweli, lakini kama kanuni za takwa hazikutumika, hivi bado tunaweza kutegemea watu kuzingatia sheria zote na kanuni wakati wote? Mathalani, yapo baadhi ya matatizo katika maisha yetu ambayo huzungumziwa rasmi na kwenye vyombo vya habari watu huombwa kupendekeza ufumbuzi wa matatizo hayo. Kuongezeka kwa idadi ya watu 26


TAKWA

wanaotalikiana, mapitio ya mfumo wa uchaguzi na taratibu za matumizi ya barabara ni baadhi ya hayo. Ingawa siwezi kujua sababu zote za ongezeko la idadi ya talaka, ninaelewa kwamba kupungua kwa takwa ndiyo sababu kubwa. Kama watu wasingepoteza takwa na hawakuwa walioachwa huru sana, tusingekuwa na idadi kubwa ya watu wanaotalikiana. Siku za nyuma, watu walikuwa na matatizo na mahitaji mengi zaidi katika maisha yao, lakini kwa sababu ya kukubali wajibu wao wa kidini na kimaadili, palikuwepo na kesi chache za kutalikiana. Hakika, matatizo tunayoyaona leo katika maisha ya familia ni mengi kuliko ilivyokuwa zamani. Takwa na imani zinaweza kuyatatua mengi katika hayo. Leo hii tumepoteza sifa hizo na pamoja na kwamba leo hii uwezo wetu ni bora zaidi kuliko siku za nyuma, tunakabiliwa na matatizo mengi zaidi. TukiďŹ kiria kupanda kwa kiwango cha talaka, tunaweza kujaribu kukipunguza kwa kutumia nguvu ya kuongeza masharti ya sheria kwa wanamume na wanawake, kwa kutumia nguvu ya taratibu, usimamiaji wa uadilifu, mamlaka makuu kwa serikali, na kwa kubadilisha kanuni na sheria. Hata hivyo, yote hayo hayataweza kutatua tatizo kuu la msingi. Kuhusu suala la uchaguzi, tunaona baadhi ya watu wanasisitiza juu ya maoni kwamba matatizo katika uchaguzi yameibuka kutokana na dosari zilizomo katika sheria za uchaguzi zilizoanzishwa miaka hamsini iliyopita na haziendani na mahitaji ya leo. Si lengo langu kuitetea sheria ya uchaguzi ya sasa. Kwa hakika inayo mapungufu. Lakini, hivi watu wanatenda kufuatana na hata hii sheria iliyopo? Hivi sheria iliyopo sasa ndio sababu ya uďŹ sadi? Au uďŹ sadi unatokea kwa sababu watu hawafuati hata isemavyo hii sheria iliyopo, na 27


TAKWA

hakuna anayefikiria mipaka yake au kuwapa wengine haki yoyote. Hivi sheria iliyopo ingeweza kumruhusu mtu yeyote kuingia mjini na kuwaambia watu: “Mimi ni mwakilishi wenu mpende au msipende?” Ambapo watu wa mji huo hawajawahi kumuona au kusikia jina lake kabla ya hapo? Uovu wa aina hiyo hauwezi kusitishwa kwa kuendeleza au kubadilisha sheria tu. Inawezekana tu pale ambapo inakuwapo aina fulani ya utambuzi, imani, na takwa miongoni mwa watu. Mwisho, kuhusu kukosekana kwa uwajibikaji juu ya sheria za barabarani na kuendesha kwa kasi sana, hivi tatizo hilo linakuwapo kwa sababu ya kanuni zilizopo au kuna sababu nyingine? Siku hizi, mara kwa mara tunakabiliwa na masuala mengi ya kijamii. Watu wanauliza kwa nini kiwango cha talaka kinaongezeka na kwa nini watu wanafanya uhalifu kama vile unyang`anyi na mauaji. Kwa nini udanganyifu umekuwa kitu cha kawaida? Kwa nini uasherati umekuwa kitu cha kawaida? Ni udhaifu wa imani na kubomoka kwa ngome ya takwa ambako kunakosababisha ufisadi kama huu. Ni jambo la kushangaza sana kwamba wapo watu wanaozungumza na kuandika kuhusu mambo haya mara kwa mara, lakini wao wenyewe hukata mizizi ya masuala haya kwenye nafsi za watu na kuwaelekeza watu kwenye machafuko ya kimaadili, kwenye ubomoaji wa misingi ya takwa, na kwenye kudhoofisha kinga ya takwa kwa sababu kimsingi hawaamini katika hilo. Kama hakuna imani na takwa - tunaomba hifadhi kwa Mwenyezi Mungu - watu wanakuwa rahisi kudhuriwa na wanaweza hata kufikiria kwamba kuiba, kudanganya, na kutenda uovu kama vitendo vinavyokubalika.

28


TAKWA

TAKWA NA AFYA

K

ama ilivyoelezwa hapo juu, Imam Ali (a.s.) amesema kuhusu takwa:

“Kwa hakika kumuogopa Allah (Takwa) ndio …. tiba kwa maradhi ya miili yenu….”17 Mtu anaweza kuuliza kuna uhusiano gani kati ya takwa (jambo la kiroho) na afya ya kimwili? Kama mambo yalivyo, takwa si kidonge na sio dawa, lakini kama takwa haipo, tabibu hatakuwa na uwezo wa kutibu maradhi ya mtu anayehitaji takwa. Mtu mwenye takwa ametosheka na mipaka yake na haki zake, anajihisi kutulia na anajiamini, na anayo amani ndani mwake. Hii husababisha matokeo ya moyo wenye afya njema; wasiwasi hautamfanya augue vidonda vya tumbo na maumivu mengine kwenye utumbo. Hatakuwa dhaifu na mnyonge kwa sababu ya kuwa huru katika uhusiano wa kijinsia. Ustawi wa mwili wake, maisha yake ya kijamii, na kiroho yote yanategemea takwa.

17

Hafidh; Semi ya197

29


TAKWA

TAKWA NA UTAMBUZI

T

akwa huongoza kwenye utambuzi ulio wazi zaidi na umaizi kama ilivyotamkwa kwenye Qur`ani:

.....Ύ˱ ϧΎ˴ ϗ˸ ή˵ ϓ ˸ Ϣ˵ Ϝϟ͉ Ϟ˴ ό˸ Πϳ˴ Ϫ Ϡϟ΍ ΍Ϯ˵ Ϙ͉ ΘΗ˴ ϥ˶ · ΍Ϯ˵ Ϩϣ Ϧϳ˶ άϟ΍ ͉ ΎϬ ΃ Ύϳ˴ ˴˰͉ ˴΁ ˴ ˴ϳ͊˴

“Enyi mlioamini! Mkimcha Mwenyezi Mungu atawapeni kipambanuzi ………………”[8:29]

Aya hii inaonyesha kwamba utambuzi ni miongoni mwa athari muhimu za takwa na tunaweza kusema kwamba hii imesafisha njia ya safari hii inayotatiza.

TAKWA NA WOKOVU

A

thari nyingine ya takwa ni kwamba mtu aliyenayo anaweza kujiokoa kutoka kwenye hatari na matatizo. Qur`ani inasema:

ΐ˶ δ˴ Θ˸ Τϳ˴ ϻ˴ ˵ Κ˸ ϴ˴Σ ˸ Ϧ˶ ϣ Ϫ ϗ˵ ί˸ ήϳ˴˴ ϭΎ˱Ο˴ ή˸Ψϣ ό˸ Πϳ˴ Ϫ Ϡϟ΍ ˶ ϖ͉ Θϳ˴ Ϧϣ ϭ...." ˴ Ϫ ˴˰͉ ˴˴ ˵ ˵˸ ˵ϟ͉ Ϟ˴ ˶ΎΑ˴ Ϫ Ϊ ϗ ੱ‫˶ ن‬ ϩ˶ ήϣ ΃ ˵ώϟ Ϡϟ΍ ϥ · ੱ‫ ن‬Ϫ Β˸δ˴Σ ˴ ϮϬ ϓ ˶ Ϫ˰͉ Ϡϟ΍ ϰ˴ Ϡ˴ϋ ˸ Ϟ͉ ϛ˴ Ϯ˴ Θϳ˴ Ϧϣ ϭ ͉˶ ˸˴ ˴˰͉ ˴˴ ˸˴ ˵˵ ˵˴ ˳˸ϲ˴η ͋ ˶ Ϫ "΍˱ έΪ ϗ ˯ Ϟ˵ Ϝϟ Ϡϟ΍ ˴ Ϟ˴ ό˴Ο ˸˴ ˵˰͉ ‫ن‬ ੱ

30


TAKWA

“…..Na anayemuogopa Mwenyezi Mungu na siku ya Mwisho, (Mwenyezi Mungu) humtengenezea njia ya kuokoka. Na humpa riziki kwa mahala asipopatazamia, na anayemtegemea Mwenyezi Mungu basi naye humtosheleza, kwa hakika Mwenyezi Mungu anatimiza kusudio lake, hakika Mwenyezi Mungu amekwisha kukiwekea kila kitu kipimo.”[65:2-3]

31


TAKWA

SEHEMU YA PILI

18

K

wa ufupi: Kwenye sehemu ya kwanza ya makala hii, Ayatullah Mutahhari alifafanua kwa undani fasili, maana, thamani na athari za Takwa, au kumuogopa Mwenyezi Mungu, na mtu kujizuia mwenyewe, kama ilivyosisitizwa ndani ya Qur`ani na Nahj al-Balaghah. Alionyesha kwamba: Kumuogopa Mungu kwa hakika ni kuogopa uadilifu Wake, ucha Mungu ni zaidi ya kutekeleza masuala ya wajibati za kidini, takwa ni uhuru na si mpaka, na ukamilifu wa kweli umo kwenye uhuru wa mtu wa kutenda kosa na bado akajizuia kufanya hivyo. Kwenye makala hii, Mutahhari anatoa nyongeza ya maana ya takwa: ni kile kitu kinachompa mtu utambuzi, au uwezo wa kufanya maamuzi yaliyo sahihi, na nguvu ya kushinda matatizo. Ili mtu aweze kuzipata sifa hizi, lazima yeye mwenyewe aondokane na matamanio mabaya yasiyo na maana ambayo huzuia uwezo wake wa kufikiri vizuri na hatimaye kufikia kwenye hali ya uadilifu. Kama ilivyoelezwa kwenye sehemu ya kwanza ya makala hii, neno takwa linarejelea kumuogopa Mungu na kujizuia binafsi. Kama ambavyo neno “muttaqi” kwa kawaida hueleweka kama ni mtu ambaye “anamuogopa Mungu,” ni muhimu kuelewa kwamba woga huu unatafsiriwa kama woga unaomaanisha kuogopa adhabu ya Mwenyezi Mungu kuliko kuogopa sifa Zake. Athari mbili za takwa zilizotajwa kwenye Qur`ani ni kumpatia mtu utambuzi na kumpa mtu nguvu ya kuyashinda matatizo. 18

Makala hii inatokana na mhadhara uliotolewa na Ayatollah Mutahhari tarehe 21, Oktoba,1960 kwa lugha ya Kiajemi, na kuchapishwa huko Dah Goftar.

32


TAKWA

UHUSIANO BAINA YA TAKWA NA UTAMBUZI

I

li kuweza kuelewa uhusiano baina ya takwa na utambuzi, ni muhimu kulielezea jambo hili katika mtazamo wa kisayansi na kifalsafa. Swali linalojitokeza ni inawezekanaje takwa ambayo ni sifa ya kimaadili inayohusiana na tabia ya mtu kuwa na athari kwenye hekima, mantiki, na uamuzi wake. Pamekuwepo na kutokuelewana iwapo kama kuwa na takwa ndiyo njia pekee ya kupata kiwango cha juu cha hekima.

TAKWA NA HEKIMA YA KIVITENDO

K

wa sehemu kubwa, wanafalsafa wa Kiislamu, pamoja na wanafalsafa wa Kigiriki wa zamani kabla yao, wamekubaliana kwamba sehemu ya kimantiki ya binadamu imegawanywa mara mbili; ya kivitendo na kinadharia. Yaani, uwazaji wa kimantiki huzalisha hizi aina mbili za uzalishaji wa ďŹ kra ambazo hutofautiana kabisa. Hekima inayozalishwa na takwa ni ya kivitendo, sio ya kinadharia. Fikra ya kinadharia ndiyo inayosababisha utambuzi wa mitazamo ya milele ya ulimwengu. Huu ndiyo msingi wa sayansi ya kimaumbile na kimahesabu, na falsafa ya dini. Mchango wa akili kwenye sayansi zilizotajwa, ni kuamua au kuhukumu mambo. Kukusanya jambo, sehemu ya taarifa hukusanywa na kufanyiwa 33


TAKWA

uamuzi kwa kuzingatia misingi ya uhakika wake. Hata hivyo, akili ya kivitendo ni uwezo wa mtu kufanya maamuzi, yaani ni kitu gani sahihi cha kufanya. Akili ya kivitendo ndiyo msingi wa sayansi za maisha na kanuni za kimaadili. Kufuatana na wanachuoni wa zamani, akili ya kivitendo ni msingi wa maadili, usimamizi wa familia na siasa za miji. Hata hivyo, akili ya kivitendo pia ni msingi wa sayansi za maisha na kanuni za kimaadili. Akili ya kivitendo ni uwezo wa mtu wa kufanya maamuzi. Akili ya kivitendo ndiyo inayotengeneza dhana za wema na ubaya, uadilifu na uovu, cha muhimu na kisicho cha muhimu na kanuni na taratibu. Njia ambayo binadamu hutumia kufanya uchaguzi katika maisha yake inahusiana na jinsi anavyofanya kazi na kufanya maamuzi. Takwa humfanya mtu atumie akili yake kikamilifu ambapo huleta hekima. Mtu kuwa na takwa anaweza kutambua tatizo vizuri zaidi na ufumbuzi wake; mtu huyu anakuwa na uwezo mzuri zaidi wa kufanya maamuzi mazuri ya kimaisha. Takwa haina uhusiano wowote na akili ya kinadharia wala haiathiri akili ya kinadharia ya mtu. Kwa maneno mengine, takwa haiboreshi ustadi wa kimahesabu au kipaji kwa ajili ya sayansi za kimaumbile. Hii pia inatumika katika falsafa ya kidini, kama ikiwa na mtazamo wa kifalsafa na kuendelea na mantiki na hekima ya kuandaa vigezo na kuďŹ kia hitimisho. Takwa, utakaso, na jitihada za kiroho (jihad) zina athari kwenye aina nyingine ya sayansi za kidini ambamo humo akili ya kinadharia, falsafa, mantiki, na ďŹ kra hazimo na mpangilio wa vigezo na namna ya kuďŹ kiri sio kutoka kwenye matokeo kwenda kwenye vigezo na si kutoka kwenye vigezo kwenda kwenye matokeo. Wazo la kwamba Takwa inaleta 34


TAKWA

matokeo kwenye hekima na utambuzi halihusiani na akili ya kinadharia. Labda sababu inayowafanya baadhi ya wanachuoni kutokukubaliana na jambo hili ni kwamba wanalihusisha jambo hili na akili ya kinadharia. Lakini hili hutumika kwenye akili ya kivitendo, na inaweza kutamkwa kwamba kabla ya tafakari yoyote, uzoefu unalithibitisha jambo hili. Kwa kweli, Takwa huathiri utambuzi na akili; haimaanishi kwamba akili ni kama mwanga wa taa na Takwa ni mafuta yake au mfumo wa akili ni kama mtambo wa kuzalisha umeme ambao wakati mwingine huzalisha kiasi fulani cha kilowati za umeme na inapoingia Takwa, inaongeza kilowati kadhaa zinazozalishwa na mtambo huo.

35


TAKWA

TAKWA HUSAIDIA AKILI

K

una aina nyingi tofauti za marafiki na maadui. Imam Ali (a.s.) anasema: “Marafiki zako ni watatu na maadui zako vilevile ni watatu. Marafiki zako ni hawa: rafiki yako, na rafiki ya rafiki yako, na adui wa maadui zako ni hawa: adui yako, na adui ya rafiki yako, na rafiki ya adui yako.”19

Ni kwa njia ile ile kwamba katika mapambano ya kivita, adui ya adui hufanya vitendo katika hali ya kama rafiki kwa kuwa anamzuia adui wa adui na kumshughulisha na kwa hiyo hawezi kupanga au kuleta madhara makubwa sana, katika vita ya kiroho ndani mwetu, takwa inahudumia akili kwa kupigana dhidi ya maadui wa akili. Nguvu za kiroho za mtu huathiriana zenyewe kwa zenyewe. Wakati mwingine zinaweza kudhoofisha au kuzimua athari za kila mojawapo na wakati mwingine zinaweza kuimarishana. Huko zamani na sasa uzingativu umeelekezwa kwenye ulinganivu uliopo baina ya nguvu mbali mbali za binadamu.

19

Nahj al-Balaghah, Semi Na: 295

36


TAKWA

ATHARI ZA TAKWA KWENYE UTAMBUZI WA MTU

M

atamanio yaliyovuka kiwango na hisia za chuki na ukaidi ni hali ya kiroho ambayo ina athari hasi kwenye akili ya kivitendo ya mtu. Kwa sababu uwanja au umiliki wa akili ya kivitendo unahusiana na vitendo vyake mtu, ni umiliki huohuo wa hisia, mielekeo na tamaa. Kama masuala haya yakizidi kiwango cha kawaida na mtu akadhibitiwa nayo badala ya kuyatawala, yataamuru dhidi ya akili, yatapiga kelele dhidi ya wito wa dhamira. Kwa wale wanaodharau wito huu, hawatasikia wito wa akili na watapulizia vumbi na moshi mzito dhidi ya nuru yake, na kuifanya nuru isiweze kunururisha. Mathalani, tupo tumekaa hapa, tunazungumza, tunasikia na tunaona, hali ambayo mtu mmoja akizungumza wengine wapo kimya; ni sawa na kama nuru inaangaza na angahewa inakuwa angavu. Lakini kama kila mtu angekua azungumze kwa sauti kubwa wakati mzungumzaji anaongea, ni wazi kwamba hata mzungumzaji mwenyewe asingeweza kusikia sauti yake mwenyewe. Na kama sehemu hii ingekuwa ijazwe vumbi na moshi, haingekuwa rahisi kwa wale waliomo humu ndani kuonana wao kwa wao. Jambo hili limeelezewa kwenye mashairi kadhaa. Mathalani, kwenye kitabu chake “Bustaan” Sa`di anaandika: “Ukweli ni nyumba isiyokuwa na doa Hawaa na tamaa, vumbi lililopulizwa Hivi huoni vumbi lilikopuliziwa? Hakuna anayeweza kuona, ingawa ana uono mzuri.” 37


TAKWA

Hafiz anasema: “Sio pazia au kiwambo cha nguo chenye urembo wa kweli. Lakini weka pembeni vumbi la njia (la uhai wako) ambalo huzuia usiweze kuona kitu.”

Rumi pia alieleza: “Wakati maslahi binafsi yanapotokeza, uadilifu hufichika: mapazia mia moja huibuka kutoka kwenye moyo na jicho.”20

Sa`di, Hafiz, na Rumi wote wanaonyesha hawaa, tamaa na maslahi binafsi kama kipingamizi hatari kwa uwezo wa mtu kuweza kupata hali ya uadilifu na kuona uzuri wa Allah. Kwenye mfano mwingine, mfikirie kijana mwanafunzi anayerudi kutoka shule akifikiria ni muhimu afanye kazi ya nyumbani aliyopewa na mwalimu wake. Ili aweze kufanya kazi hiyo, anapaswa kutumia muda wa saa kadhaa kusoma, kuandika, na kufikiria huku akijua kwamba matokeo ya kutozingatia na kuwa mvivu ni kufeli mtihani, na kuwa mtu asiye na elimu, na sababu ya mabalaa mengine mengi. Tunaelewa kwamba kufanya kwake bidii ni matokeo ya wito wa akili yake. Inawezekana pakawepo na wito wa tamaa dhidi ya wito wa akili, ile hali ya kutazama kwa matamanio na ufisadi ndani ya moyo wake ambao humzuia asiwe na utulivu. Endapo wito huu ukiongezeka, kijana huyu hawezi tena 20

Mathnawi ya Rumi, iliyotafsiriwa na R.A.Nicholson, Kitabu cha Kwanza, Hadithi ya 111. Mfalme wa ki-Dewish, Waziri wake, na Wakristo.[1930]

38


TAKWA

kuusikia wito wa akili yake na kumzuia asiizingatie nuru ya asili yake kama atakavyokuwa anajisemea mwenyewe: “Ngoja tujipatie muda wa starehe sasa na baadaye nitafikiria nini cha kufuatia.” Kwa hiyo, kama matamanio ya aina hiyo yanakuwepo ndani ya akili na moyo wa mtu, yatadhoofisha na kutangua athari ya akili yake na kwa maneno mengine, matamanio haya hugeuka kuwa adui ya akili ya binadamu. Washairi walioathiriwa na Ma’sumin (a.s.), na hao Ma’sumin wenyewe, wote wamewaonya watu dhidi ya wito huu. Imam Ali (a.s.) anaeleza kuhusu majivuno na kujiona sana: “Majivuno yake mtu ni adui ya akili yake mwenyewe.”21

Imam (a.s.) pia anasema: “Mapungufu mengi ya akili hutokea kwa sababu ya kuingiwa ghafla na ulafi.”22

Imam as-Sadiq (a.s.) anasema: “Matamanio yasiyofaa ni adui ya akili.”23

Sa`di pia anasema kuhusu hili: “Ulafi wa mali huziba uoni wa mwenye akili Uroho hukitega kila kiumbe chenye uhai.”24

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema: “Adui yako mkubwa sana ni nafsi yako yenye kushawishi tamaa zisizokidhika ambazo zipo karibu sana na wewe [kuliko kitu chochote] na zimewekwa baina ya pande zako mbili.”25 21

Nahj al-Balaghah, Semi ya. 212.

22

Nahj al-Balaghah, Semi ya. 219.

23

Misbah al-Shari`a, Sura ya 38, uk. 223.

24

Sa`di, Gulstaan.

25

Bihar al-Anwar

39


TAKWA

‘Nafsi tamanishi na matamanio yasiyokidhika’ ndio maadui wakubwa wa binadamu kwa sababu ni maadui wa akili yake. Mtume (s.a.w.w.) anaichukulia nafsi tamanishi na matamanio yake yasiyozimika kama maadui kwa sababu “rafiki halisi wa kila mtu ni akili yake.”26 Tunaweza kujilinda wenyewe kutokana na kila adui kwa kutumia nguvu ya akili; hata hivyo, kama adui anaweza kuiba akili ya mtu, hiyo itakuwa ni hatari zaidi. Akitumia hadith iliyotajwa hapo juu kwenye shairi lake, Sa`ib Tabrizi anasema, “Tunawezaje kutandika kitanda cha kujiliwazia kwa usingizi mnono ambapo tunaye adui kama moyo ulivyo pembezoni mwetu.?” Kwa hiyo, hali ya kiroho na nguvu za mtu zina athari mbaya juu ya kila mojawapo kati yao kwa sababu ya tofauti zilizopo baina yao. Karibu kila moja inatangua athari za nyingine; kwa maneno mengine, matamanio na akili zinaoneana wivu. Kwa hiyo, athari ya takwa katika kuimarisha akili na kuongeza utambuzi inakuwa wazi. Bila shaka, tabia bainifu kama hasira, ashiki, uroho, wivu, kiburi, umimi, ubinafsi na mengine yafananayo na hayo humfanya mtu kuwa kiziwi na kipofu. Mtu ambaye ana matamanio yasiyotoshelezeka ni kipofu na kiziwi. Hivi inawezekana kuwa na shaka kuhusu jambo hili kwamba mojawapo ya hali ya kiasili ya binadamu ni kwamba haoni mapungufu yake mwenyewe ila huyaona mapungufu ya wenzake ambapo yeye ameathirika zaidi kuliko wengine? Hivi sababu ya upofu huu wa mtu kutokuona mapungufu yake ni nyingine kuliko ubinafsi? Hivi kuna shaka yoyote kwamba wacha Mungu, ambao hujitahidi kimaadili na hushinda ubinafsi na ulafi na maovu mengine yatokanayo na nafsi ya mtu mwenyewe, 26

Bihar al-Anwar

40


TAKWA

wanaweza kuelewa mapungufu yao vizuri zaidi? Na kuna elimu yoyote ya binadamu ambayo ina manufaa zaidi kuzidi ile ya kujitambua mwenyewe, mapungufu yake, na namna ya kuyasahihisha? Kama tunaweza kufaulu kuidhibiti nafsi yenye kushawishi basi tunaweza kupata njia ya kujikomboa. Tungeweza kupata utambuzi ulio dhahiri kama matokeo ya kuwa na akili ambayo inaweza kudhihirisha maadili na dosari zetu. Pia tungeweza kutatua vizuri matatizo yetu kwa urahisi, tukielewa kwamba kipingamizi kwenye wito wa akili zetu ni matamanio yetu yasiyo na mipaka. Kwa hiyo, tungeweza kuelewa vizuri zaidi, tungeweza kuona vizuri zaidi, na akili zetu zingeweza kutudhihirishia mambo vizuri zaidi.

41


TAKWA

TOFAUTI BAINA YA AKILI NA UWEZO WA KUTUMIA AKILI

W

apo wale ambao ni stadi na wenye akili katika masuala ya kisayansi ingawaje hawawezi kujua kwa usahihi jinsi ya kuendesha maisha yao. Kwa upande mwingine wale wenye uwezo wa akili wa wastani wanaweza kujua namna ya kufanya uchaguzi unaofaa zaidi. Kwa hiyo, watu wana aina mbili za uwezo wa kiakili: akili na uwezo wa kutumia akili (ujuzi). Watu wengine ni werevu zaidi; wengine ni wajanja zaidi. Lakini ukweli ni kwamba hakuna uwezo wa aina mbili: akili na ujuzi wa kutumia akili. Wapo watu ambao ni werevu sana ambao wamechanganyikiwa katika mambo ya kivitendo kwa sababu ya maadui zao wa akili wamekuwa hawana mpaka kabisa. Watu kama hao wana nafsi zilizochanganyikiwa, ingawaje hawana mapungufu yoyote katika akili zao. Mwanzoni, nilitamka kwamba takwa, jitihada za kimaadili na usafi wa nafsi - havina athari za moja kwa moja kwa kile ambacho akili ya kinadharia inahusika nacho. Hata teosofia ya kifalsafa haihusiani na dhana hizi za kimaadili. Pia nilitamka kwamba takwa na jitihada za kimaadili zina athari katika kupata elimu ya dini kwa namna nyingine. Imam Ali (a.s.) anaelezea hali ya muumini anayejitahidi kupambana na matamanio yake mwenyewe: “Yeye [muumini] aliiweka akili yake kwenye uhai na aliyaua [matamanio ya] moyo wake hadi mwili wake ukakonda, uzito wake ukapungua, na mng`ao wa mwanga mkali uliwaka kwa ajili yake. Mwanga huo ulimmulikia 42


TAKWA

njia na kumpeleka kwenye njia iliyo [sahihi]. Milango mbali mbali ilimwelekeza kwenye mlango wa salama na sehemu ya makazi yake ya [daima milele]. Miguu yake, ikauweka mwili wake sawa, ikagandamizwa hapo mahali pa salama na starehe, kwa sababu aliuweka moyo wake [katika matendo mema] na akamridhisha Allah.”27

Allah [SWT] huwaongoza wale ambao hujitahidi katika kutafuta radhi Yake:

Ϧϣ ή˸Ψϳ˵˴ ϭ ˶ ϡϼ˴͉δϟ΍ ˴ Ϟ˵ Β˵γ Ϫ Ϯ˸ ο˶ έ ˴ϊ˴ ΒΗ͉΍ ˶Ϧϣ Ϡϟ΍ ˶ Ϫ˶ Α ϱ˶ ΪϬ ˴ ˴ Ϫ ͋ ϢϬ ˵˵Ο˶ ˵ϧ˴΍˴ ˵˰͉ ˸ϳ˴ ˵͊ψϟ΍ έϮ͊ Ϩϟ΍ ϰϟ˴˶ · ˶ΕΎ˴ ϤϠ Ϣϴ˶ Ϙ˴ Θ˸δϣ ρ΍˴ ή˶ λ ̆ϰϟ˴˶ · ˸ Ϣ˶ Ϭϳ˶ ΪϬ ϭ ˶ Ϫ˶ ϧ˸ ΫΈ Α ˶ ˴˴ ͊ ˳ ˸ϳ ˶˶ ˳

“Kwa [kitabu] hicho Mwenyezi Mungu humuongoza mwenye kutafuta radhi Yake katika njia za salama na huwatoa katika giza kuwapeleka kwenye nuru kwa amri yake na kuwaongoza kwenye njia iliyonyooka.” [5:16]

27

Nahj al-Balaghah hotuba na. 218

43


TAKWA

TAKWA NA UTAKASO WA HISIA NA MHEMUKO

T

akwa huathiri hisia na mhemuko wa mtu. Huzifanya hisia kuwa laini zaidi. Sio jambo lisilowezekana kabisa kwa mtu mcha Mungu kuwa na hisia kama za mtu aliyezama katika matendo machafu na maovu. Mcha Mungu ambaye anajizuia na machafu, matendo maovu, unafiki na udanganyifu, na badala yake akaiweka nafsi yake kuwa safi ili kulinda heshima yake na fikra pevu na yeye huyazingatia tu yale mambo halisi yaliyopo na si miundo, kwa hakika mtu huyo atakuwa na akili zaidi na hisia nyeti zaidi na atakuwa na muathiriko mzuri zaidi na mambo mazuri ya kiroho. Mtu huyu huiona dunia kwa utambuzi tofauti na huhisi vizuri zaidi uzuri wa akili hapa duniani. Wakati mwingine tunakutana na swali kwamba kwa nini hakuna washairi wakubwa mashuhuri kama wale wa zamani. Na kwa nini hakuna mfanano wa ulaini katika maneno ya washairi wa leo na yale ya Sa`di na Hafidh? Hali ambayo ni kinyume na ukweli kwamba mambo yote kama sayansi na fikra na dunia vimeendelea katika nyanja zote. Ni matumaini yangu kwamba washairi wa zama za leo hawatahisi kuumizwa na maneno yangu. Haya ni maoni yangu tu na mengi mengineyo. Sababu ipo kwenye ukweli kwamba kwa nyongeza kwenye vipaji vya kimaumbile na ubunifu angalifu, washairi pia wanahitaji aina maalum ya ulaini na kiwango cha hisia ndani ya nafsi zao, hali ambazo hupatikana zaidi pale mtu anapozingatia zaidi takwa, yaani, anakuwa na dhamira ya makusudi na fikra pana zaidi na hawi mateka wa matamanio na hasira. Lakini kama baa44


TAKWA

dhi ya watu wanasisitiza kuwajulisha washairi wa zamani, ambao wana dhamira safi, kuwa ni kama watu waovu kama wao wenyewe, hilo ni suala lingine. Kwa vyovyote vile, mtu muovu mwenye moyo uliojaa uchafu hawezi kuelewa rehema ya Mungu, hata kama ana kiwango cha juu cha akili, hataweza kutengeneza maana zenye neema nzuri na ulaini sawa na zile zilizomo kwenye maneno ya watu wengine.

TAKWA NA KUSHINDA MATATIZO

S

wali linalojitokeza hapa ni: Kuna uhusiano gani baina ya takwa, ambayo ni tabia ya kiroho na kimaadili, na kushinda matatizo? Hii inahusisha athari nyingine ya takwa ambayo imetamkwa ndani ya Qur`ani:

Ύ˱Ο˴ ό˸ Πϳ˴ Ϫ Ϡϟ΍ ˶ϖ͉ Θϳ˴ Ϧϣ ϭ ή˸Ψϣ ˴˰͉ ˴˴ ˴ Ϫ ˵ϟ͉ Ϟ˴ “…………. na anayemcha Mwenyezi Mungu, Yeye humtengenezea njia ya kutokea.”[65:2]

Na:

΍˱ ή˸δϳ˵ ˶ ϩ˶ήϣ ΃ ˸ Ϧ˶ϣ Ϫ ό˸ Πϳ˴ Ϫ Ϡϟ΍ ˶ϖ͉ Θϳ˴ Ϧϣ ϭ ˴˰͉ ˴˴ ˸˴ ˵ϟ͉ Ϟ˴ “……..na anayemcha Mwenyezi Mungu, Yeye Mwenyezi Mungu humfanyia mambo yake kuwa mepesi.”[65:4]

45


TAKWA

Imam Ali (a.s.) anasema: “Kwa hiyo, yeyote anayemogopa Allah, matatizo huwa mbali naye, baada ya kuwa karibu naye hapo kabla, mambo yake hugeuka kuwa matamu baada ya kuwa machungu; mawimbi [ya matatizo] hupungua baada ya kumzunguka kwa wingi, matatizo yanakuwa rahisi baada ya kumtokea.28

AINA MBILI ZA MATATIZO

K

ama utangulizi, lazima itamkwe kwamba yapo matatizo ya aina mbili ambayo humkabili binadamu. Aina ya kwanza ni matatizo yale ambayo yapo nje ya uwezo wa mtu kuyadhibiti, yaani, yale yanayosababishwa na majanga ya kimaumbile. Aina ya pili ni ile ambayo mtu anaweza kuyadhibiti. Haya ni matatizo ya kijamii na kimaadili. Kuhusu aina ya kwanza, siwezi kusema kama Qur`ani inasema lolote kuhusu kuwaokoa binadamu kutokana na matatizo haya au la. Hata hivyo, hakuna tatizo la kuwepo kwa sheria ya aina hiyo kama dhamana ya dini hapa duniani, kama kuitikia kwenye swala. Lakini kuhusu aina ya pili, ipo kauli ndani ya Nahj al-Balaghah ambayo tunaweza kuichukulia kama tafsiri ya jambo hili. Imam Ali (a.s.) anasema:

28

Nahj al-Balaghah hotuba na. 198

46


TAKWA

“Mnapaswa kujua kwamba yeyote anayemcha Mungu, Yeye atamtengenezea njia ya kuondokana na matatizo na atamjaalia nuru ya kumsaidia aondoke gizani.”29

Majonzi ni matatizo ya kimaadili na kijamii. Matatizo yanayosababishwa na majanga ya kimaumbile sio mengi kuliko yale yanayosababishwa na matatizo ya kimaadili na kijamii. Matatizo mengi zaidi yanayowapata watu husababishwa na matendo maovu ambayo huyafanya maisha ya mtu kuwa machungu na yaliyojaa dhiki, na yanamnyang`anya furaha ya aina yoyote hapa duniani na Akhera. Tukifikiria kwamba sababu kuu ya matatizo ya mtu ni kutokana na vitendo vyake mwenyewe na kwamba kila mmoja hutengeneza hatima yake yeye mwenyewe kupitia maamuzi yake, Sa`di anasema: “Hapana ambaye angemfanyia adui yake Kile ambacho mpumbavu, kwa ajili ya matamanio yake, hujifanyia yeye mwenyewe.”30

Kupitia uzoefu wangu mwenyewe, na kudadisi ule wa wengine, nimefika kwenye hitimisho kwamba matatizo mengi tunayopata hutengenezwa na sisi wenyewe, si watu wengine. Kuwa na takwa huleta kinga dhidi ya matatizo ya kimaadili na kijamii. Mwenyezi Mungu anawapa wale wacha-Mungu utambuzi wa kipekee:

29

Nahj al-Balaghah hotuba na. 183

30

Sa`di, Ushauri, Ghazals No. 33.

47


TAKWA

Ϧϣ ΋Ύ˴σ ˸ ϢϬ Ϋ˶ · ΍˸ Ϯ˴ ϘΗ͉΍ ˴ Ϧϳ˶ άϟ΍ ͉ ϥ · ˴ ͉˶ ˴ ΍˴ ͋ ˲ϒ˶ ˵͉δϣ ˴Η˴ ˶ϥΎ˴τ˸ ϥ ή˶μ˸ Βϣ ΫΈ ϓ ΍ϭ˵ ή͉ ϛά ϴ͉θϟ΍ ˴ϭ˵ ͊ Ϣϫ ˶˴ ˵ ΍˴ “Hakika wale wenye takua, zinapowagusa pepesi za shetani huzinduka.” [7:201]

Kwa sababu takwa huongeza utambuzi, pia itazalisha ile athari ya pili vilevile ambayo ni kuwaokoa watu kutoka kwenye hali za hatari na matatizo. Matatizo hutokeza kwenye giza cha dhambi na matamanio. Nuru ya takwa inapohisiwa, mtu anaweza kutofautisha kati ya mema na maovu, na kumzuia asiingie kwenye matatizo. Kama mtu akihusika na tatizo, anaweza kupata njia nzuri zaidi ya kutatua matatizo hayo kupitia nuru ya takwa. Kwa nyongeza ya athari hizi, takwa humzuia mtu kupoteza nguvu zake kwenye mambo yaliyoharamishwa na pia upotovu. Ni wazi kwamba mtu imara na mwenye kudhamiria anaweza kufanya maamuzi na akajiokoa mwenyewe vizuri zaidi kuliko wengine. Nguvu na nuru husaidia katika kukombolewa. Kuelekea mwisho wa Sura Yusuf ndani ya Qur`ani, baada ya Yusuf kuwa mtawala wa Misri na ndugu zake walipokwenda Misri kutoka Canaan kuchukua nafaka wakati wa njaa hawakumtambua Yusuf. Hata hivyo, Yusuf alikuwa anawajua wao walikuwa ni akina nani pamoja na kwamba hakujitambulisha kwao. Ndugu zake Yusuf walipofika Misri kwa mara ya kwanza, Yusuf alitumia hila ya udhuru kwa lengo la kumzuia mdogo wake wa damu kamili, Benjamin abakie naye. Mara ya pili ndugu zake walifika Misri, walimwomba na kumsihi sana Yusuf awape nafaka. Qur`ani Tukufu inaonyesha hali yao ya kusikitisha kwenye aya ifuatayo: 48


TAKWA

˴ϫ ˴˴ϋ ΍Ϯ˵ ˴˴ ή͊πϟ΍ Ύ˴ ϨϠ ΃˴ ϭ Ύ˴ Ϩ͉δϣ ΰϳ˶ ΰ˴ όϟ΍ ΃ Ύϳ˴ ΍ϮϟΎ˴ Ϫ˸ ϴϠ Ϡ˴ ΧΩ ϤϠ ϓ ˸ ΎϬ ˵ ϗ ˶ ˴ Ύ͉ ˴ ˵ ˴ϳ͊˴ ͊ ˸˴ ˴˴ϋ ˸ Ϫ Ϡϟ΍ ϥ · ੱ‫ ق‬Ύ˴ Ϟ˸ ϴ˴ Ϝϟ΍ Ϩϟ˴ ˶ϑ˸ ϭ˴ ΄˴ ϓ ˳ ΓΎ˴Ο˸ ΰϣ Δ˴ϋΎ˴π˶Β˶ Α Ύ˴ Ϩ˸ Ό˶Ο˴ ϭ Ϩ˸ ϴϠ ϕΪ ϭ ˴ ˸ Ύ˴ ͉˶ ͉˴μΗ˴˴ ˴˰͉ ͊ ˳ Ϧϴ˶ ϗΪ Θ˵ Ϥϟ΍ ΰ˸ Πϳ˴ ˸ ϱ˶ ˴ ͋˴μ˴

“Basi walipoingia kwa Yusuf walisema: Ewe mheshimiwa! Imetupata shida sisi na watu wetu, na tumeleta mali kidogo, basi tupimie kipimo na fanya kama unatupa sadaka.Hakika Mwenyezi Mungu huwalipa wanaotoa sadaka.”[12:88]

Kwa hiyo, Yusuf aliamua kujitambulisha mwenyewe kwao: ˸˴ ϥ Ϡ˶ ϫΎ˴Ο ˸ Ϣ˵ Θϧ˴ ΃ ˸ Ϋ˶ · ˶ Ϫϴ˶Χ˴ ΃˴ ϭ ˴ϒ˵γϮ˵ ϴ˶ Α Ϣ˵ ΘϠ ό˴ ϓ Ύϣ Θ˸ Ϥ˶ Ϡ˴ϋ ˸ Ϟϫ ϗ ˴Ϯ˵ ˴Ύ˴ ˴ ϝ ͉ Ϣ˵

“Akasema je, mnajua mliyomfanyia Yusuf na ndugu yake mlipokuwa wajinga?” [12:89]

Yeye aliwauliza kama wanaweza kukumbuka yale waliyomfanyia Yusuf na nduguye. Swali hili liliwashangaza: Ζϧ˴Ϸ˴ ˴Ϛ͉ ϧ˶ ·˴ ΃ ΍ϮϟΎ˴ Ϧϣ ϗ ੱ‫ ق‬ϲ˶Χ˴ ΃ ΍˴ ά̆ ˰ϫ ϭ ˵ϒ˵γϮϳ˵ Ύ˴ ϧ˴ ΃ ϝ ϗ ੱ‫˵ ق‬ϒ˵γϮϳ˵ ˴ ˵ ϗ ͉ ˴Ύ˴ ˸˴ ˴ Ϊ ˴˴ ˴ ˴ ‫ق‬ Ύ Ϩ ϴ Ϡ ϋ Ϫ ˰͉ Ϡ ή Ο ΃ ϊ ϴ˶ π ϳ ϻ Ϫ ˰͉ Ϡ ϟ΍ ϥ Έ ϓ ή Β μ ϳ ϭ ϖ Θ ϳ Ϧ ϣ Ϫ ϧ · ੱ ͉ ˴ ˴ ͉ ˴˸ ˴ ˵ ϟ΍ ˴˸ ˵ ˵ ˴ ˶ ˸˶˸ ˴˴ ˶͉ ˴ ˴ ˵ ˶ Ϧϴ˶ Ϩ˶ δ˸ Τ˵ Ϥϟ΍ ˸ ˴

“Wakasema: Je, wewe ni Yusuf? Akasema:Mimi ni Yusuf na huyu ni ndugu yangu! Mwenyezi Mungu ametuneemesha. Hakika mwenye takua na akasubiri, basi Mwenyezi Mungu haupotezi ujira wa wafanyao mazuri.” [12:90]

Haya ni matunda ya takwa na utakaso. Yusuf alikuwa mtumwa lakini alidumisha takwa. Mmojawapo wa wanawake 49


TAKWA

maarufu na wazuri sana kwa sura wa Misri alifanya jaribio la kumtongoza Yusuf, kijana asiyejulikana, pamoja na kwamba alijiweka chini ya ulinzi wa takwa aliposema:

ϲ˶ Ϩϧ˴Ϯ˵ϋΪ Ϥ˶ϣ ͉ϲϟ˴˶ · ͊ ΐ˴Σ˴ ΃ ˵ Ϧ˸ Π͋δϟ΍ ͋ Ώ˴ έ ϝ ϗ ˴Ύ˴ ˸ϳ˴ Ύ͉ ‫˶ ق‬ ੱ Ϫ˸ ϴϟ˴˶ · “….. Ee Mola wangu! Gereza linapendeza zaidi kwangu kuliko haya wanayoniitia,…..”[12:33]

Takwa aliyoiweka Yusuf katika hali ile, ilimfanya kuwa mtawala wa Misri. takwa, subira, na ucha Mungu ni vitu ambavyo havitapotea hapa duniani; huwanyanyua watu kutoka kwenye kiwango cha chini sana na kumfikisha kwenye kiwango cha juu sana cha heshima na hadhi kama ilivyotamkwa kwenye Qur`ani:

Ϧϴ˶ Ϩ˶δ˸ Τ˵ Ϥϟ΍ ή˸ Ο˴ ΃ ˵ϊϴ˶πϳ˵ ϻ˴ Ϫ Ϡϟ΍ ϥ ϓ ˸ ˴ ˴ ͉Έ ˴˰͉ ˶˴ “Hakika mwenye takua na akasubiri, basi Mwenyezi Mungu haupotezi ujira wa wafanyao mazuri.” [12:90]

Hii inaonyesha kama vile Qur`ani Tukufu inafupisha matokeo ya kisa cha Yusuf katika sentensi moja: Takwa ni tunda la kuvumilia ambalo linawaokoa watu kutokana na matatizo na kuwachukua kutoka kwenye kiwango cha chini hadi cha juu kabisa cha hadhi, kama ilivyoelezwa na Qur’ani Tukufu:

50


TAKWA

Ύ˱Ο˴ ή˸Ψϣ ό˸ Πϳ˴ Ϫ Ϡϟ΍ ˶ϖ͉ Θϳ˴ Ϧϣ ϭ ˴ Ϫ ˴˰͉ ˴˴ ˵ϟ͉ Ϟ˴ “………… na anayemcha Mwenyezi Mungu, Yeye humtengenezea njia ya kutokea.”[65:2] Wacha Mungu ambao wakati wote hujilinda hawashindwi na kitu. Mtu hawezi kuvumilia isipokuwa kuyapenda maneno ya Imam Husayn (a.s.) alipokuwa akiwahutubia watu wa familia yake adhimu na akiwathibitishia kwa imani kamili na kujiamini. Mungu wangu! Ni kiwango gani cha moyo, imani, na kujiamini alichokuwa nacho, na alipata wapi uhakika kama huo? Kulingana na baadhi ya vyanzo vya kihistoria, Imam Husayn (a.s.) aliposema kwa heri kwa familia yake kwa mara ya pili aliwahutubia: “Lazima muwe tayari kuvumilia matatizo na kutambua kwamba Mwenyezi Mungu anawalinda na kuwasaidieni nyinyi, na Yeye atawaokoa na kuwapeni mwisho mwema, na kuwapa adhabu mbali mbali maadui zenu na kuwatunukieni rehema na neema kwa ajili ya uvumilivu wenu kwenye matatizo haya. Kamwe msilalamike na kutamka yale ambayo yanaweza kupunguza thamani yenu.”

Imani ya Imam Husayn (a.s.) juu ya ushindi wa mwisho ambao kwamba aliwatia moyo familia yake chimbuko lake ni kwenye Qur`ani: “…Na anayemcha Mwenyezi Mungu, Yeye humtengenezea njia ya kuokoka.” [65:2]. Aina hii ya kujiamini na imani ilikuwa sawa na ile ya Yusuf mchaMungu ambaye alisema kwa furaha na kuridhika: “Hakika mwenye takua na akasubiri, basi Mwenyezi Mungu haupotezi ujira wa wafanyao mazuri.” [12:90] na baadaye 51


TAKWA

alivuna matunda ya takwa. Lakini Imam Husayn (a.s.) alijua matokeo kabla ya kadhia hiyo kufikia mwisho. Maneno yaliyoeleweka wazi ya Imam Husayn (a.s.) yalikita kwenye nyoyo za watu wa familia yake kama mkuki. Walivumilia matatizo kama yale ya kuchukuliwa mateka, lakini chini ya ulinzi wa subira na takwa, matokeo ya matendo yao yalikuwa ni yale ambayo Imam Husayn (a.s.) alikwisha kuwaahidi na Mwenyezi Mungu alikwisha kuithibitisha ndani ya Qur`ani. Baada ya Imam Husayn (a.s.) kupata Shahada, Bibi Zainab (s.a.) aliyarudia maneno ya kaka yake mbele ya adui yao katili: “Tumia kila hila unayotaka na ufanye bidii sana lakini ninaapa Wallahi kwamba hutaweza kuyatelekeza majina yetu, hutasababisha umashuhuri wetu kupungua na kuacha kutuheshimu na kuvuruga wahyi wa Mwenyezi Mungu katika familia yetu. Aibu, fedheha na kashfa ndivyo vitu pekee utakavyobaki navyo hapa duniani.”

Kwa kweli, wakati wa msiba wa Karbala, Imam Husayn (a.s.) na Bibi Zainab (a.s.) walionyesha ukamilifu wao katika ucha-Mungu, na tabia hii bainifu iliwaongoza katika kuvumilia mateso na maumivu ya kupoteza wapendwa wao na haki zao kuvyogwa. Wale wanaoishi maisha yaliyoongozwa na misingi madhubuti huongeza uwezo wa dhamira yao na huwa na shaksia ya kiroho na kibusara. Kuwa na takwa au kuepuka yale ambayo yanaweza kukutumbukiza kwenye kutenda dhambi wakati ukiwa mcha-Mungu, huwasaidia kufika kwenye malengo hayo. Humpa mtu hisia ya uadilifu wa kiwango 52


TAKWA

cha juu, kumpa uhuru kutokana na utumwa wa aina zote, iwe ni mawazo yake mwenyewe yenye ushawishi muovu au utumwa katika kijamii. Pia huwaongoza kuwa wenye kutosheka, kujiamini, na utambuzi ulio wazi na utulivu. Si tu kwamba humsaidia mtu binafsi lakini husaidia jamii kwa ujumla, kwani uharibifu wa takwa ndiyo chanzo cha matatizo ya kijamii. Kwa hiyo, takwa inachukuliwa kama mojawapo ya nguzo za maisha ya mtu, binafsi au kijamii, ambayo bila kuwa nayo mtu huwa kigeugeu.

53


TAKWA

ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION 1.

Qur’an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Thalathini

2.

Uharamisho wa Riba

3.

Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza

4.

Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili

5.

Hekaya za Bahlul

6.

Muhanga wa Imamu Husein (A.S.)

7.

Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.)

8.

Hijab vazi Bora

9.

Ukweli wa Shia Ithnaashari

10.

Madhambi Makuu

11.

Mbingu imenikirimu

12. Abdallah Ibn Saba 13. Khadijatul Kubra 14. Utumwa 15. Umakini katika Swala 16. Misingi ya Maarifa 17. Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia 18. Bilal wa Afrika 54


TAKWA

19. Abudharr 20. Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu 21.

Salman Farsi

22. Ammar Yasir 23. Qur’an na Hadithi 24. Elimu ya Nafsi 25. Yajue Madhehebu ya Shia 26. Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur’an Tukufu 27. Al-Wahda 28. Ponyo kutoka katika Qur’an. 29. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii 30. Mashukio ya Akhera 31.

Al Amali

32. Dua Indal Ahlul Bayt 33. Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna. 34. Haki za wanawake katika Uislamu 35. Mwenyeezi Mungu na sifa zake 36. Kumswalia Mtume (s) 37. Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) 38. Adhana. 39

Upendo katika Ukristo na Uislamu

40. Tiba ya Maradhi ya Kimaadili 41.

Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu

42. Kupaka juu ya khofu

55


TAKWA

43. Kukusanya swala mbili 44. Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara 45. Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya 46. Kusujudu juu ya udongo 47. Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s) 48. Tarawehe 49. Malumbano baina ya Sunni na Shia 50. Kupunguza Swala safarini 51.

Kufungua safarini

52. Umaasumu wa Manabii 53. Qur’an inatoa changamoto 54. as-Salaatu Khayrun Mina -’n Nawm 55. Uadilifu wa Masahaba 56. Dua e Kumayl 57. Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu 58. Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake 59. Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata 60. Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mitume Muhammad (s) 61.

Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza

62. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili 63. Kuzuru Makaburi 64. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza 65. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili 56


TAKWA

66. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu 67. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne 68. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano 69. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita 70.

Tujifunze Misingi Ya Dini

71.

Sala ni Nguzo ya Dini

72. Mikesha Ya Peshawar 73. Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu 74. Ubora wa Imam ‘Ali Juu ya Maswahaba Na Ushia ndio njia iliyonyooka 75. Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake 76. Liqaa-u-llaah 77. Muhammad (s) Mtume wa Allah 78. Amani na Jihadi Katika Uislamu 79. Uislamu Ulienea Vipi? 80. Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) 81.

Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s)

82. Urejeo (al-Raja’a ) 83. Mazingira 84. Utokezo (al - Badau) 85. Hukumu ya kujenga juu ya makaburi 86. Swala ya maiti na kumlilia maiti 87. Uislamu na Uwingi wa Dini 88. Mtoto mwema 89. Adabu za Sokoni 57


TAKWA

90. Johari za hekima kwa vijana 91.

Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza

92. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili 93. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu 94. Tawasali 95. Imam Mahdi katika Usunni na Ushia 96. Hukumu za Mgonjwa 97. Sadaka yenye kuendelea 98. Msahafu wa Imam Ali 99. Ngano ya kwamba Qur’ani imebadilishwa 100. Idil Ghadiri 101. Kusoma sura zenye Sijda ya wajibu 102 Hukumu zinazomuhusu mkuu wa kazi na Mfanyakazi 103. Huduma ya Afya katika Uislamu 104. Sunan an-Nabii 105. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza) 106. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili) 107. Shahiid MďŹ adini 108. Kusalia Nabii (s.a.w) 109. Ujumbe -Sehemu ya Kwanza 110. Ujumbe - Sehemu ya Pili 111. Ujumbe - Sehemu ya Tatu 112. Ujumbe - Sehemu ya Nne 58


TAKWA

113. Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu 114. Hadithi ya Thaqalain 115. Maarifa ya Kiislamu 116. Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza 117. Ukweli uliopotea sehemu ya Pili 118. Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu 119. Ukweli uliopotea sehmu ya Nne 120. Ukweli uliopotea sehmu ya Tano 121. Johari zenye hekima kwa vijana 122. Safari ya kuifuata Nuru 123. Fatima al-Zahra 124. Myahudi wa Kimataifa 125. Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi 126. Visa vya kweli sehemu ya Kwanza 127. Visa vya kweli sehemu ya Pili 128. Muhadhara wa Maulamaa 129. Mwanadamu na Mustakabali wake 130. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Kwanza) 131. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Pili) 132. Khairul Bariyyah 133. Uislamu na mafunzo ya kimalezi 134. Vijana ni Hazina ya Uislamu. 135. Yafaayo kijamii 59


TAKWA

136. Tabaruku 137. Taqiyya 138. Vikao vya furaha 139. Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje? 140. Visa vya wachamungu 141. Falsafa ya Dini 142. Azadari-Kuhuzunika na Kuomboleza 143. Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah 144. Mtazamo Mpya - Wanawake katika Uislamu 145. Kuonekana kwa Allah 146. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza) 147. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili) 148. Ndugu na Jirani 149. Ushia ndani ya Usunni 150. Maswali na Majibu 151. Mafunzo ya hukmu za ibada 152. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisusunni No 1 153 Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisusunni No 2 154. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisusunni No 3 155. Abu Huraira 156. Vipengee kadhaa katika Swala ya Jamaa na Msikiti. 157. Mazingatio kutoka katika Qur’an - Sehemu ya Kwanza 60


TAKWA

158. Mazingatio kutoka kaitka Qur’an - Sehemu ya Pili 159. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya kwanza 160. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya Pili 161. Qur’ani Tukufu – Pamoja na Tarjuma ya Kiswahili 162. Falsafa ya Mageuzi ya Imam Husein (a.s) 163. Amali za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani 164. Elimu ya Tiba za Kiislamu - Matibabu ya Maimamu 165. Uislamu Safi 166. Majlisi za Imam Husein Majumbani 167. Mshumaa. 168. Uislam wa Shia 169. Amali za Makka 170. Amali za Madina 171. Asili ya Madhehebu katika Uislamu 172. Sira ya Imam Ali kuhusu Waasi 173. Ukweli uliofichika katika neno la Allah 174. Uislamu na Mifumo ya Uchumi 175. Umoja wa Kiislamu na Furaha 176. Mas’ala ya Kifiqhi 177. Jifunze kusoma Qur’ani 178. As-Sahifatul Kamilah as-Sajjadiyyah 179. Hayya ‘Alaa Khayri’l-’Amal Katika Adhana 180. Ukweli kuhusu Funga ya Siku ya Ashura 61


TAKWA

181. Dua za Miezi Mitatu Mitukufu (Rajabu, Shaabani na Ramadhani) 182. Uadilifu katika Uislamu 183. Mahdi katika Sunna 184. Jihadi ya Imam Hussein (‘as) 185. Kazi na kujituma ni njia ya maendeleo 186. Abu Talib – Jabali Imara la Imani 187. Ujenzi na Utakaso wa Nafsi 188. Vijana na Weledi juu ya Mustakabali 189. Usalafi – Historia yake, maana yake na lengo lake 190. Ushia – Hoja na Majibu 191. Mateso ya Dhuria wa Mtume (saww) 192. Maombolezo – Msiba wa Bwana wa Mashahidi (a.s.) 193. Shahidi kwa Ajili ya Ubinadamu 194. Takwa 195. Mwonekano wa Upotoshaji katika Hazina ya Kiislamu 196. Amirul Muuminina (‘as) na Makhalifa

62


TAKWA

KOPI NNE ZIFUATAZO ZIMETAFSIRIWA KWA LUGHA KINYARWANDA 1.

Amateka Na Aba’Khalifa

2.

Nyuma yaho naje kuyoboka

3.

Amavu n’amavuko by’ubushiya

4.

Shiya na Hadithi

63


MUHTASARI


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.