TALAKA TATU ًالطالق ثالثا
Kimeandikwa na: Sheikh Ja’far Subhani
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 1
11/25/2014 4:30:32 PM
ترجمة
اإلشهاد على الطالق و الطالق ثالثاً
تأليف ّ المحقق جعفر السبحاني الفقيه
من اللغة العربية إلى اللغة السواحلية
11/25/2014 4:30:32 PM
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 2
©Haki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: 978 - 9987 - 17 - 097 - 5 Kimeandikwa na: Sheikh Ja’far Subhani Kimetarjumiwa na: Alhaj Hemedi Lubumba Kimehaririwa na: Alhaj Ramadhani S. K. Shemahimbo Kimepitiwa na: Mubarak A. Nkanatilla Kimepangwa katika Kompyuta na: Al-Itrah Foundation Toleo la kwanza: Mei, 2015 Nakala: 2000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. - 19701, Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 / 2127555 Barua Pepe: alitrah@yahoo.com Tovuti: www.ibn-tv-com Katika mtandao: w.w.w.alitrah.info
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 3
11/25/2014 4:30:32 PM
Yaliyomo Neno la Mchapishaji........................................................................ 1 Utangulizi......................................................................................... 3 Kuweka Mashahidi Wakati waKutaliki........................................... 5 Talaka Tatu kwa Tamko moja au Kutamka Mara Tatu Katika Kikao Kimoja............................................................. 20 Uchambuzi wa Aya Zinazozungumzia Maudhui hii...................... 26 Tafsiri ya Kauli ya Mwenyezi Mungu: Au kuachana kwa Hisani..................................................................................... 30 Dalili kwa Njia ya Kitabu Kupitia Hoja Mbambali....................... 36 Dalili kwa Njia ya Sunna............................................................... 47 Dalili za Mwenye kusema Kuwa Talaka Tatu za Mpigo ni Sahihi ........................................................................................ 50 Dalili Zao kwa Njia ya Sunna........................................................ 52 Ddalili Zao kwa Njia ya Sunna Ijmai............................................ 56 Rai Binafsi Mkabala na Maandiko................................................ 58 Mambo Yenye Kuhalalisha Hukumu ya Khalifa........................... 63 Malipo ya Kuchepuka Njia Kuu.................................................... 80
iv
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 4
11/25/2014 4:30:32 PM
TALAKA TATU
بسم اهلل الرحمن الرحيم NENO LA MCHAPISHAJI
K
itabu ulichonacho mikononi mwako kimetarjumiwa kutoka kitabu cha Kiarabu kwa jina la, at-Talaqu Thalatha, kilichoandikwa na Sheikh Ja’far Subhani. Sisi tumekiita, Talaka Tatu. Moja ya sababu ambazo Waislamu wanadai kurejeshwa kwa Mahakama ya Kadhi hapa Tanzania Bara ni kuhusu utekelezaji na hukumu za ndoa na talaka ambavyo vyote vimeanishwa katika Qur’ani Tukufu. Kwa Waislamu, jambo lolote linapotajwa katika Qur’ani Tukufu huwa ni amri (imperative) na kwa hivyo lazima litiiwe, lifuatwe na litekelezwe vilivyo. Hii ndio maana ya kuitwa “Uislamu ni dini na ni mfumo wa maisha”, kwa maana kwamba Uislamu huhudumia roho na mwili au kwa lugha nyingine, huhudumia roho na kusimamia mambo yote yanayohusu maisha ya watu. Na huu ndio umuhimu wa Mahakama ya Kadhi kwa Wailslamu sio suala la kupuuzia kwao. Mwandishi anazungumzia utekelezaji wa talaka, inavyopaswa kutolewa na wakati gani. Shia na Sunni wanahitilafiana juu ya utoaji wa talaka tatu kwa mpigo mmoja. Sunni wanasema talaka tatu kwa mpigo mmoja zinasihi, ambapo Shia wanasema haisihi na itokeapo mtu akatoa talaka tatu kwa mpigo mmoja, hiyo huisabiwa kuwa ni moja tu. Dalili na hoja za kielimu utazipata katika kitabu hiki Hii ni moja kati ya kazi kubwa zinazofanywa na Taasisi ya AlItrah katika kuwahudumia kielimu wasomaji wake wazungumzaji 1
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 1
11/25/2014 4:30:32 PM
TALAKA TATU
wa Kiswahili. Na kwa maana hiyohiyo, imeona ikichapishe kitabu hiki chenye hazina kubwa kwa lugha ya Kiswahili kwa lengo lake lilelile la kuwahudumia Waislamu, hususan wanaozungumza Kiswahili. Hivyo, ni matumaini yetu kwamba wasomaji wetu watanufaika vya kutosha kutokana na kitabu hiki, kwani tumekiona ni chenye manufaa sana hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni vitu ambavyo havina nafasi tena katika akili za watu. Tunamshukuru mwandishi wa kitabu hiki, Sheikh Ja’far Subhani kwa kazi kubwa aliyoifanya kwa ajili ya Umma huu wa Waislamu, Allah ‘Azza wa Jallah amlipe kila kheri na amuingize Peponi kwa salama na amani insha’Allah. Halikadhalika tunamshukuru Alhaj Hemedi Lubumba kwa kukitarjumi kwa Kiswahili kitabu hiki, insha’Allah na yeye Allah Mwenye kujazi amlipe kila kheri hapa duniani na Akhera pia, bila kuwasahau na wale wote waliochangia kwa namna mmoja au nyingine mpaka kufanikisha kuchapishwa kwa kitabu hiki. Allah awalipe wote malipo mema hapa duniani na kesho Akhera pia. Mchapishaji Al-Itrah Foundation
2
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 2
11/25/2014 4:30:32 PM
TALAKA TATU
بسم اهلل الرحمن الرحيم UTANGULIZI
َّب ْسم الله يم ح الر ٰن م ح الر َّ َّ ْ ِ ِ َ ِ ِ ِ ِ
K
Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu
ila sifa njema ni ya Mwenyezi Mungu, Mola wa walimwengu. Swala na salamu zimfikie mbora wa viumbe na hitimisho la Mitume Wake, Muhammad (saww), pia kizazi chake kitakatifu ambacho ndio hifadhi ya elimu yake na hazina ya mafunzo yake. Ama baad; Hakika Uislamu ni imani na sheria. Imani ni kuamini Mwenyezi Mungu, Mitume Wake na Siku ya Mwisho. Na sheria ni hukumu za Mwenyezi Mungu ambazo zina dhamana ya kumpa mwanadamu maisha bora na kumhakikishia saada ya dunia na Akhera. Sharia ya Kiislamu ni ya kipekee kwa kuwa inahusika na kila jambo huku ikiweka utatuzi wa matatizo yote yanayompata mwanadamu katika maeneo yote ya maisha yake, Mwenyezi Mungu anasema:
ُ ْال َي ْو َم أَ ْك َم ْل ُت لَ ُك ْم ِدي َن ُك ْم َوأَ ْت َم ْم ُت َعلَي ْك ْم ِن ْع َم ِتي ُ ض يت لَ ُك ُم الإْ ِ ْسلاَ َم ِدي ًنا ِ َو َر
“Leo nimewakamilishia dini yenu na kuwatimizia neema Yangu na nimewapendelea Uislamu kuwa dini.” (Surat Al-Maidah 5:3). 3
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 3
11/25/2014 4:30:32 PM
TALAKA TATU
Isipokuwa kuna masuala madogo madogo ambayo wanazuoni wa sharia wametofautiana kwa sababu ya kuhitilafiana kwao kuhusu riwaya zilizopokewa kutoka kwa Mtume (saww), jambo ambalo limewapelekea kutofautiana hata kuhusu masuala madogo madogo ya sharia. Kwa kuwa ukweli hutokana na utafiti, basi hakika katika mtiririko wa masomo haya tumejaribu kuliweka suala hili juu ya meza ya utafiti, kwani huenda ikawa ndio njia ya kuunganisha mtazamo na kusogeza hatua katika uwanja huu, kwani tofauti iliyopo si katika asili na misingi ya dini hata ipelekee kuwa na uadui na chuki, bali tofauti iliyopo ni kuhusu riwaya zilizonasibishwa na Mtume (saww), nalo ni jambo dogo ukilinganisha na mambo mengi ambayo madhehebu za Kiislamu zinaafikiana kati yao. Na mwongozo wetu katika njia hii ni kauli ya Mwenyezi Mungu:
ْ َو ْل اللهَِّ َج ِميعًا َو اَل َت َف َّر ُقوا َو ْاذ ُك ُروا ِ اع َت ِ ص ُموا ِب َحب ُْن ُقل َّْك ْم إ ْذ ُك ْنتُ ْم أَ ْع َدا ًء َفأَل ُ َ َّلله َ َ وب ُك ْم ي ب ف َ ِ ِ ِن ْع َم َت ا ِ َعلي ص َب ْحتُ ْم ِب ِن ْع َم ِت ِه إِ ْخ َوا ًنا ْ ََفأ “Na Shikamaneni na kamba ya Mwenyezi Mungu nyote wala msifarikiane; na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu juu yenu mlipokuwa maadui, naye akaziunganisha nyoyo zenu; hivyo kwa neema Yake mkawa ndugu; « (Surat Aal-Imran 3:103).
Ja’far Subhani, Taasisi ya Imam as-Sadiq (as). Qum – Iran.
4
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 4
11/25/2014 4:30:32 PM
TALAKA TATU
بسم اهلل الرحمن الرحيم KUWEKA MASHAHIDI WAKATI WA KUTALIKI
M
iongoni mwa mambo ambayo yanaitofautisha madhehebu ya Shia Imamiyyah na madhehebu nyingine ni kauli yao kwamba: Hakika ushahidi wa waadilifu wawili ni sharti katika kusihi kwa talaka, na iwapo utakosekana basi talaka haitasihi. Lakini wanazuoni wa madhehebu nyingine wametofautiana nao katika hilo.1 Sheikh Tusi amesema: “Kila talaka ambayo haikuhudhuriwa na mashahidi wawili Waislamu waadilifu, hata kama itakuwa imetimiza masharti mengine, talaka hiyo si sahihi. Wanazuoni wote wa madhehebu nyingine wamekhalifu hilo na hakuna hata mmoja kati yao aliyezingatia ushahidi kuwa ni moja kati ya masharti ya talaka.”2
Sayyid Sayiq amesema: “Wanazuoni wa Kisunni kuanzia wa mwanzo mpaka waliofuatia, wote wanaona kwamba talaka inasihi hata bila kuweka mashahidi, kwa sababu talaka ni haki ya mwanamume na wala hahitaji ushahidi wa waadilifu wawili ili kutumia haki yake, wala hakijapokewa chochote kutoka kwa Mtume (saww) wala kutoka kwa Maswahaba kinachoonesha sharia ya kuweka mashahidi. Na wanazuoni wa Shia Imamiyyah wamekhalifu hilo…. Na miongoni mwa Maswahaba wanaoona wajibu wa kuweka mashahidi na kufanya ni sharti la kusihi kwake (talaka) ni Amirul-Muuminina Ali bin Abu Talib na Imran bin Haswin (ra), na miongoni mwa Tabiina ni Imam Muhammad al-Baqir, Imam Ja’far as-Sadiq, watoto wao 1 2
Al-Intiswar Uk. 127 – 128. Al-Khilaf, Juz. 2, Fasili ya Talaka, Mas’ala ya 5. 5
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 5
11/25/2014 4:30:32 PM
TALAKA TATU
Maimamu wa Ahlul-Bayti (ra), na kadhalika Atau, Ibn Jurih na Ibn Sirin.”3 Hakika mgongano uliopo katika maneno yake uko wazi, iko wapi kauli yake: “Wala hakijapokewa chochote kutoka kwa Mtume (saww) wala kutoka kwa Maswahaba kinachoonesha sharia ya kuweka mashahidi.” Mbele ya kauli yake: “Na miongoni mwa Maswahaba wanaoona wajibu wa kuweka mashahidi na kufanya ni sharti la kusihi kwake (talaka) ni Amirul-Muuminina Ali bin Abu Talib na Imran bin Haswin (ra)”, au hawa wawili si miongoni mwa Maswahaba waadilifu?! Wala katika vitabu vya Fiqhi vya Masunni hatujapata anwani ya maudhui husika bali rai yao tunaikuta ndani ya vitabu vya tafsiri wakati wa kutafsiri kauli ya Mwenyezi Mungu:
َّ َفإِ َذا َبلَ ْغ َن أَ َجلَه ُ ُن َفأَ ْم ِس ُك وف أَ ْو ُ وه َّن ِب َمع ٍ ْر َ ُ ار ُق وف َوأَ ْش ِه ُدوا َذ َو ْي َع ْد ٍل ِم ْن ُك ْم ُ وه َّن ِب َمع ٍ ْر ِف َّ َوأَ ِقي ُموا َِّالش َها َد َة للِه “Basi wanapofikia muda wao, muwashike kwa wema, au farakianeni nao kwa wema. Na mshuhudishe mashahidi wawili waadilifu miongoni mwenu. Na simamisheni ushahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.” (Surat At-Talaq 65:2).
Na kati yao yupo anayeifanya kuwa ni sharti la talaka na rejea, na yupo anayeifanya kuwa ni sharti makhususi kwa ajili ya rejea tu inayotokana na kauli ya Mwenyezi Mungu: “Muwashike kwa wema.” Tabari amepokea kutoka kwa asSadiy kwamba alifasiri kauli ya Mwenyezi Mungu: “Muwashike 3
Fiqhis-Sunnah, Juz. 2, Uk. 230. 6
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 6
11/25/2014 4:30:32 PM
TALAKA TATU
kwa wema.” Mara kwa maana ya rejea na akasema: “Wekeni mashahidi wakati wa kuwashika iwapo mtawashika, na hiyo ndiyo rejea.” Na mara nyingine kwa maana ya talaka na akasema: “Wakati wa talaka na wakati wa kumrejea.” Na akanukuu kutoka kwa Ibn Abbas kwamba yeye aliitafsiri kwa maana ya talaka na rejea.4 Suyutiy amesema: “Ameandika Abdulrazaq kutoka kwa Atau kuwa alisema: ‘Ndoa ni kwa mashahidi, talaka ni kwa mashahidi, na kumrejea ni kwa mashahidi.’ Na aliulizwa Imran bin Haswin kuhusu mwanamume aliyetaliki bila kuweka mashahidi na akamrejea mke bila kuweka mashahidi, nini hukumu yake? Akasema: ‘Ni jambo baya sana alilotenda, ametaliki kwa bidaa na amemrejea pasi na Sunna. Aweke mashahidi wakati wa talaka yake na wakati wa kumrejea kwake, na amuombe Mwenyezi Mungu maghofira.’”5 Qurtubiy amesema: “Kauli ya Mwenyezi Mungu: ‘Na mshuhudishe’, imetuamuru kuweka mashahidi wakati wa talaka. Na inasemekana: Wakati wa kumrejea. Na dhahiri ni kwamba (ibara hii) inarejea kwenye rejea na si kwenye talaka. Kisha kuweka mashahidi ni sunna kwa Abu Hanifa kama ilivyo katika kauli ya Mwenyezi Mungu: ‘Na wekeni mashahidi mnapouziana’, na kwa Shafiy ni wajibu wakati wa kumrejea.”6 Alusiy amesema: “Na mshuhudishe mashahidi wawili waadilifu miongoni mwenu, wakati wa kurejea iwapo mtachagua kumrejea, au wakati wa kutengana iwapo mtachagua kutengana, ili kujiepusha na tuhuma.”7 Jamiul-Bayan, Juz.28, Uk. 88. Ad-Durul-Manthur, Juz. 6, Uk. 232. Imran bin Huswin Min Kibari As’habi Imam Ali (as). 6 Al-Jamiu Liahkamil-Qur’an, Juz. 18, Uk. 157. 7 Ruhul-Maaniy, Juz. 28, Uk. 134. 4 5
7
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 7
11/25/2014 4:30:32 PM
TALAKA TATU
Aya inaonesha kwa uwazi ulazima wa kuweka mashahidi ili talaka iwe sahihi, na muundo wa dalili ni kwamba kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na mshuhudishe mashahidi wawili waadilifu miongoni mwenu”, ima iwe inarejelea kwenye talaka kana kwamba amesema: “Mtakapowataliki wanawake basi watalikini katika eda yao na muweke mashahidi”. Au iwe inarejelea kwenye mtengano: “Au farakianeni nao kwa wema.”, au kwenye rejea ambayo Mwenyezi Mungu ameielezea kwa neno ‘kushika’, akasema: ‘Muwashike kwa wema’, na hairuhusiwi kurejelea kwenye mtengano (uwezekano wa pili) kwa sababu wenyewe hapa si kitu chenye kutendeka na kufanyika, bali ni ile hali ya kutokumrejea hivyo hufarakiana naye kwa kutomrejea, na mwanamke hutengana naye kwa talaka iliyotangulia. Zaidi ya hapo ni kwamba hakuna yeyote anayewajibisha kuweka mashahidi katika mtengano huu, wakati dhahiri ya tamko la amri inahitaji wajibu. Na wala amri hiyo ya kuweka mashahidi hairuhusiwi kurejelea kwenye rejea kwa sababu hakuna yeyote anayewajibisha kuweka mashahidi wakati wa rejea bali ni mustahabu kufanya hivyo, hivyo inathibiti kuwa amri ya kuweka mashahidi inarejelea kwenye talaka.8 Na mengine mengi yaliyosemwa katika tafsiri ya Aya hii. Na miongoni mwa waliotangaza ukweli ni wanazuoni wawili wakubwa, nao ni: Ahmadi Muhammad Shakir, Kadhi wa Misri, na Sheikh Abu Zahrah. Baada ya kunukuu Aya mbili za mwanzo wa Sura Talaq, amesema wa kwanza: “Dhahiri ya mtiririko wa Aya mbili hizi ni kwamba kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na mshuhudishe mashahidi” inarejelea kwenye yote mawili, kwenye talaka na kwenye rejea, na amri ni ya wajibu, kwa sababu wajibu ndio maana yake halisi (kirejelewa) na wala haielekei kwenye maana nyingine isiyokuwa wajibu isipokuwa kwa dalili na 8
Al-Intiswar, Uk. 300. 8
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 8
11/25/2014 4:30:32 PM
TALAKA TATU
wala hapa hakuna dalili inayoitoa kwenye wajibu, bali inazidi kusisitiza maana ya wajibu.” Aliendelea kueleza mpaka aliposema: “Atakayeweka mashahidi wakati wa talaka yake atakuwa ametoa talaka kwa namna iliyoamrishwa, na kadhalika yule atakayeweka mashahidi wakati wa rejea. Na ambaye hatofanya hivyo atakuwa amevuka mipaka ya Mwenyezi Mungu ambaye alimwekea mipaka hiyo na hivyo amali yake itakuwa batili na haitakuwa na tija yoyote (ya kisharia).” Aliendelea kueleza kuwa: “Shia wanaona kuwa ni wajibu kuweka mashahidi katika talaka na kwamba ni moja ya nguzo zake, na wala hawajafanya kuwa ni wajibu wakati wa rejea, na kutofautisha baina ya hali hizo mbili ni jambo geni lisilo na dalili.”9 Abu Zahrah amesema: “Wanazuoni wa Shia Imamiyyah Ithnaashariyyah na wa Ismailiyyah wamesema: ‘Hakika talaka haisihi bila kuweka mashahidi wawili waadilifu, kwa mujibu wa kauli ya Mwenyezi Mungu – kuhusu hukumu za talaka na uanzishwaji wake katika Sura at-Talaq:-
َّ َفإِ َذا َبلَ ْغ َن أَ َجلَه ُ ُن َفأَ ْم ِس ُك وف أَ ْو ُ وه َّن ِب َمع ٍ ْر َ ُ ار ُق وف َوأَ ْش ِه ُدوا َذ َو ْي َع ْد ٍل ِم ْن ُك ْم ُ وه َّن ِب َمع ٍ ْر ِف َّ َوأَ ِقي ُموا ْ ان ي َ ُوع ُظ ِب ِه َم ْن َك ُؤ ِم ُن َ الش َها َد َة للِهَِّ َ ٰذلِ ُك ْم ي ِباللهَِّ َو ْال َي ْو ِم آْال ِخ ِر َو َم ْن َيتَّ ِق اللهََّ َي ْج َع ْل لَ ُه َم ْخ َر ًجا
“Basi wanapofikia muda wao, muwashike kwa wema, au farakianeni nao kwa wema. Na mshuhudishe mashahidi wawili waadilifu miongoni mwenu. Na simamisheni ushahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Hivyo ndivyo anavyoagizwa anayemwamini Mwenyezi 9
Nidhamut-Talaq Fil-Islami, Uk. 118 – 119. 9
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 9
11/25/2014 4:30:32 PM
TALAKA TATU
Mungu na Siku ya Mwisho. Na anayemcha Mwenyezi Mungu, Yeye humtengezea njia ya kutokea.” (Surat At-Talaq 65:2),
Amri hii ya kuweka mashahidi imekuja baada ya tamko la kuianzisha talaka na kuruhusu rejea, hivyo ilifaa irejelee kwenye talaka, na hakika kutaja sababu ya kuweka mashahidi kuwa ni ili kumpa mawaidha anayemwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, kunaunga mkono hilo na kulitia nguvu, kwani hakika mashahidi waadilifu watakaohudhuria hawatakosa mawaidha mazuri watakayoyatoa kwa mke na mume, na hivyo yatakuwa ni njia ya kutokea ya kuachana na talaka ambayo ndio halali ichukiwayo zaidi na Mwenyezi Mungu Mtukufu. “Na laiti tungekuwa tuna mamlaka ya kuchagua rai ya kufanyiwa kazi katika Misri basi tungechagua rai hii, kwani ili talaka isihi ni sharti wahudhurie mashahidi wawili waadilifu.”10 Maelezo haya yanaonesha kuwa baina ya jamaa (Masunni) yupo anayesema kuwa amri ya kuweka mashahidi inarejelea kwenye rejea peke yake, na yupo anayesema kuwa inarejelea kwenye rejea na kwenye talaka. Na hakuna yeyote katika Masunni aliyesema kuwa inarejelea kwenye talaka peke yake isipokuwa yale uliyoyatambua kutoka kwenye maneno ya Abu Zuhrah. Na kwa ajili hiyo baada ya kunukuu maelezo ni wajibu kwetu kutafakari na kufuata Kitabu cha Mwenyezi Mungu na hukumu yake. Mwenyezi Mungu amesema:
ُ َيا أَُّي َها النَّ ِب ُّي إِ َذا َطلَّ ْقتُ ُم النِّ َسا َء َف َطلُِّق وه َّن لِ ِع َّد ِت ِه َّن ُ صوا ْال ِع َّد َة َواتَّ ُقوا اللهََّ َرب ُ َّك ْم اَل تُ ْخ ِر ُج وه َّن ِم ْن ُ َوأَ ْح 10
Al-Ahwalu as-Shakhsiyyah, Uk. 365, kama ilivyo katika al-Fiqhi Alal-Madhahibi alKhamsah, Uk. 131. 10
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 10
11/25/2014 4:30:33 PM
TALAKA TATU
َ بُيُو ِت ِه َّن َو اَل َي ْخ ُر ْج َن إِ اَّل أَ ْن َي ْأ ِت اح َش ٍة ُم َبيِّ َن ٍة ِ ين ِب َف َو ِت ْل َك ُح ُدو ُد اللهَِّ َو َم ْن َي َت َع َّد ُح ُدو َد اللهَِّ َف َق ْد َظلَ َم َن ْف َس ُه ُح ِد ُث َب ْع َد َ ٰذلِ َك أَ ْم ًرا ْ اَل َت ْد ِري لَ َع َّل اللهََّ ي َّ َفإِ َذا َبلَ ْغ َن أَ َجلَه ُ ُن َفأَ ْم ِس ُك وف أَ ْو ُ وه َّن ِب َمع ٍ ْر َ ُ ار ُق وف َوأَ ْش ِه ُدوا َذ َو ْي َع ْد ٍل ِم ْن ُك ْم ُ وه َّن ِب َمع ٍ ْر ِف َّ َوأَ ِقي ُموا ْ ان ي َ ُوع ُظ ِب ِه َم ْن َك ُؤ ِم ُن َ الش َها َد َة للِهَِّ َ ٰذلِ ُك ْم ي ِباللهَِّ َو ْال َي ْو ِم آْال ِخ ِر َو َم ْن َيتَّ ِق اللهََّ َي ْج َع ْل لَ ُه َم ْخ َر ًجا “Ewe Nabii! Mtakapowataliki wanawake, basi wapeni talaka wakati wa eda zao, na fanyeni hisabu ya eda, na mcheni Mwenyezi Mungu, Mola Wenu. Msiwatoe katika nyumba zao, wala wasitoke wenyewe, ila wakifanya uchafu ulio wazi. Hiyo ndiyo mipaka ya Mwenyezi Mungu msiikiuke; na mwenye kuikiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu, amejidhulumu nafsi yake, hujui pengine Mwenyezi Mungu ataleta jambo jingine baada ya haya. Basi wanapofikia muda wao, muwashike kwa wema, au farakianeni nao kwa wema. Na mshuhudishe mashahidi wawili waadilifu miongoni mwenu. Na simamisheni ushahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Hivyo ndivyo anavyoagizwa anayemwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Na anayemcha Mwenyezi Mungu, Yeye humtengezea njia ya kutokea.” (Surat At-Talaq 65:1-2).
Hakika makusudio ya “Basi wanapofikia muda wao” ni kukaribia kufika mwisho wa kipindi cha eda. Na makusudio ya “Muwashike” ni kuwarejea, na hii ni istiara. Kama ambavyo makusudio ya “Farakianeni nao” ni kuwaacha watoke kwenye eda na kuten11
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 11
11/25/2014 4:30:33 PM
TALAKA TATU
gana. Na hapana shaka kwamba kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na mshuhudishe mashahidi wawili waadilifu” dhahiri inarejelea kwenye wajibu kama zilivyo amri nyingine zilizopatikana katika sharia na wala hazielekei kwenye maana nyingine isiyo wajibu isipokuwa kwa dalili, hivyo mzozo upo kwenye kirejelewa, hivyo hapa kuna uwezekano wa namna tatu: 1.
Ima iwe ni sharti la kauli ya Mwenyezi Mungu: “Basi wapeni talaka wakati wa eda zao.”
2.
Na ima iwe ni sharti la kauli ya Mwenyezi Mungu: “Muwashike kwa wema.”
3.
Na ima iwe ni sharti la kauli ya Mwenyezi Mungu: “Au farakianeni nao kwa wema.”
Na hajasema yeyote kuwa sharti linarejelea kwenye uwezekano wa mwisho, hivyo jambo lipo baina ya ima uwezekano wa kwanza au wa pili, na dhahiri ni kwamba inarejelea kwenye uwezekano wa kwanza, na hiyo ni kwa kuwa Sura ipo katika nafasi ya kubainisha hukumu za talaka, na imeanza kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Ewe Nabii! Mtakapowataliki wanawake”, ikataja kuwa talaka ina hukumu kadhaa: 1.
Talaka iwe ndani ya eda zao.
2.
Kufanya hesabu ya eda.
3.
Kutokuwatoa katika nyumba zao.
4.
Mume ana hiyari ima ya kushika au kufarakiana wakati eda yao inapokaribia kuisha.
12
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 12
11/25/2014 4:30:33 PM
TALAKA TATU
5.
Kuweka mashahidi wawili waadilifu kutoka miongoni mwenu.
6.
Eda ya mwanamke asiyepatwa na hedhi licha ya kuwa katika umri wa kupatwa na hedhi.
7.
Eda ya wajawazito.
Na ukizichunguza Aya za Sura hii kuanzia ya kwanza hadi ya saba utazikuta zipo katika kubainisha hukumu za talaka, kwa sababu ndio makusudio ya asili na wala si rejea inayotokana na kauli ya Mwenyezi Mungu: “Muwashike kwa wema” iliyotajwa kwa kufuata asili. Na hili ndilo lililopokewa kutoka kwa Maimamu wetu (as), Muhammad bin Muslim amesema: “Mtu mmoja alikuja kwa Amirul-Muuminina (as) huko Kufa, akasema: ‘Hakika mimi nimemtaliki mke wangu baada ya kutoharika na hedhi yake kabla sijamwingilia.’ Amirul-Muuminina (as) akasema: ‘Je uliweka mashahidi wawili waadilifu kama alivyokuamuru Mwenyezi Mungu?’ Akasema: ‘Hapana.’ Amirul-Muuminina (as) akasema: ‘Nenda zako hakika talaka yako si chochote.’”11 Na amepokea Bikir bin Aayun kutoka kwa Imam Muhammad alBaqir na Imam Ja’far as-Sadiq (as) kwamba walisema: “Na kama atamtaliki mwanzoni mwa eda yake akiwa katika twahara na bila kumwingilia, lakini bila talaka hiyo kushuhudiwa na wanaume wawili waadilifu, basi talaka yake hiyo aliyomtaliki si talaka (sahihi).”12 Na Masahaba wema wa Imam al-Baqir na Imam as-Sadiq (as) kama vile Zurarah, Muhammad bin Muslim, Buraydi na Fudhayli wamepokea kutoka kwao hao wawili kwamba walisema: “Na kama atamtaliki mwanzoni mwa eda yake akiwa katika twahara na bila Al-Wasail, Juz. 15, Mlango wa 10 katika milango ya vitangulizi vya talaka, Hadithi ya 3 na 7, tazama pia hadithi nyingine za mlango huu. 12 Al-Wasail, Juz. 15, Mlango wa 10 katika milango ya vitangulizi vya talaka, Hadithi ya 3 na 7, tazama pia hadithi nyingine za mlango huu. 11
13
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 13
11/25/2014 4:30:33 PM
TALAKA TATU
kumwingilia, lakini bila talaka hiyo kushuhudiwa na wanaume wawili waadilifu, basi talaka yake hiyo aliyomtaliki si talaka (sahihi).”13 Na amepokea Muhammad bin Fudhayli kutoka kwa Abul-Hasan (as) kwamba alimwambia Abu Yusuf: “Hakika dini si kwa ulinganisho kama ulinganisho wako na ulinganisho wa jamaa zako. Hakika Mwenyezi Mungu ameamrisha talaka ndani ya Kitabu chake na akasisitiza kuweka mashahidi wawili na hakuwaridhia isipokuwa waadilifu. Na ameamrisha ndoa ndani ya Kitabu chake na akaiacha bila mashahidi, lakini nyinyi mmeweka mashahidi wawili pale ambapo Mwenyezi Mungu hakuwaweka, na mmewaondoa mashahidi wawili pale aliposisitiza Mwenyezi Mungu wawepo. Na mmeruhusu talaka ya mwendawazimu na mlevi.” Kisha akataja hukumu ya kujiweka kivulini kwa mtu aliye katika ihramu.14 Twabarasiy amesema: “Wafasiri wamesema: ‘Wameamrishwa kuweka mashahidi wawili waadilifu wakati wa talaka na wakati wa rejea ili mwanamke asikanushe kurejewa kwake baada ya eda kumalizika, na wala mwanamume asiikane talaka. Na imesemekana kuwa: Maana yake ni: Wekeni mashahidi wakati wa talaka ili kulinda dini yenu, na ndio maana iliyopokewa kutoka kwa Maimamu wetu (as), na hii ndio inayolingana zaidi na dhahiri, kwa sababu kama tutaifungamanisha na talaka itakuwa ni amri inayohitaji wajibu na iliyo miongoni mwa masharti ya talaka. Na mwenye kusema kuwa inarejelea kwenye rejea ameitafsiri kwa maana ya pendekezo (mustahabu).15 Na miongoni mwa ajabu ni kuitafsiri amri ya kuweka mashahidi iliyo katika Aya hii kuwa ina maana ya pendekezo (mustaha Al-Wasail, Juz. 15, Mlango wa 10 katika milango ya vitangulizi vya talaka na masharti yake, Hadithi ya 3. 14 Al-Wasail, Juz. 15, Mlango wa 10 katika milango ya vitangulizi vya talaka, Hadithi ya 12, tizama pia hadithi nyingine za mlango huu. 15 Majmaul-Bayan, Juz.5, Uk. 306. 13
14
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 14
11/25/2014 4:30:33 PM
TALAKA TATU
bu). Alusiy amesema: “Wekeni mashahidi wawili waadilifu kutoka miongoni mwenu wakati wa rejea kama itakuwa mmechagua rejea, au wakati wa kufarakiana ‘Au farakianeni nao kwa wema’ kama itakuwa mmechagua kufarakiana, hiyo ni ili kujitakasa na tuhuma na kukata mzozo. Na hii ni amri ya pendekezo (mustahabu) kama ilivyo kwenye kauli ya Mwenyezi Mungu: ‘Na wekeni mashahidi mnapouziana’. Na Shafiy amesema katika kitabu al-Qadim: ‘Hakika yenyewe ni ya wajibu wakati wa rejea.’”16 Anajibiwa kuwa: Hakika kiashiriwa 17 kinachotokana na tamko la amri ni wajibu, na tumesema mahali pake kuwa: Hakika kanuni inayofuatwa na wenye akili timamu, kanuni ambayo imekubaliwa na mwekasharia (Mwenyezi Mungu na Mtume) ni kwamba ‘Amri ya Bwana haiachwi bila jawabu’, na jawabu ni ima kuitekeleza amri au kupatikane dalili nyingine inayoonesha kuwa ni amri ya pendekezo (mustahabu), na kwa msingi huo ni kwamba hakika amri iliyopo hapa ni ya wajibu na hasa ukizingatia hekima ya kuwekwa sheria hii (ya kuweka mashahidi), hekima aliyoitaja yeye mwenyewe, aliposema: ‘Hiyo ni ili kujitakasa na tuhuma na kukata mzozo.’ Ama kauli ya Mwenyezi Mungu: ‘Na wekeni mashahidi mnapouziana’, umma wote umekubaliana kuwa amri ya kuweka mashahidi wakati wa kuuziana ni ya pendekezo (mustahabu). Kisha ni kwamba Sheikh Ahmad Muhammad Shakir, ambaye ni Kadhi halali wa Misri, aliandika kitabu kuhusu ‘Utaratibu wa Talaka Katika Uislamu’ na akampa Allamah Sheikh Muhammad Husain Kashifu al-Ghatau zawadi nakala moja ya kitabu hicho kikiwa kimeambatana na barua yake, na akamwandikia kuwa: “Hakika mimi ninaamini ni sharti wawepo mashahidi wawili wakati wa talaka. Na kwamba 16 17
Ruhul-Maaniy, Juz. 28, Uk. 134. Kiashiriwa: Istilahi hii katika fasihi ya Kiswahili hutumiwa kuelezea wazo linalomjia mtu akilini baada ya neno fulani kutajwa au kutumiwa – Mtarjumi. 15
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 15
11/25/2014 4:30:33 PM
TALAKA TATU
kama itapatikana talaka pasipo na kuwepo mashahidi wawili haitakuwa talaka (sahihi) na hatakaa eda kwa talaka hiyo. Na kauli hii hata kama ni kinyume na madhehebu manne maarufu isipokuwa ni kwamba inaungwa mkono na dalili na inaafikiana na madhehebu ya Maimamu wa Ahlul-Bayt na Shia Imamiyyah. Na ninaamini pia kuwa ni sharti wawepo mashahidi wawili wakati wa rejea, nayo ni kauli inayoafikiana na moja kati ya kauli mbili za Imam Shafiy na inakwenda kinyume na madhehebu ya Ahlul-Bayt na Shia, na nimeshangazwa na kauli yao (hao Mashia) ya kutenganisha baina ya talaka na rejea katika hilo wakati dalili yake ni moja ‘Na mshuhudishe mashahidi wawili waadilifu.’” Allamah Sheikh Kashifu al-Ghatau akamtumia barua ya kumjibu akibainisha humo sababu ya kutenganisha baina ya talaka na rejea katika hilo, na yafuatayo ni maelezo husika kutoka kwenye barua hiyo, baada ya maneno yake alisema: “Ni kana kwamba - Mwenyezi Mungu atie nuru hoja yako –hujachunguza kwa undani hapa katika Aya tukufu kama ulivyochunguza kwa undani kama kawaida yako katika sehemu nyingine isiyokuwa hii, la sivyo isingefichikana kwako kwamba Sura Tukufu imekuja kubainisha sifa za talaka na hukumu zake mpaka ikawa imepewa jina la Surat Talaq, na mwanzo ikaanza mazungumzo kwa kauli ya Mwenyezi Mungu: “Mtakapowataliki wanawake”, kisha ikataja ulazima wa talaka kutolewa mwanzoni mwa eda, yaani isiwe ni katika tohara aliyoingiliwa wala katika hedhi, kisha ikataja ulazima wa kuhesabu eda na kutokuwatoa majumbani. Kisha akarukia kutaja rejea wakati wa kubainisha hukumu za talaka, ambapo Mwenyezi Mungu akasema: ‘Basi wanapofikia muda wao, muwashike kwa wema’, yaani watakapokaribia kutoka kwenye eda 16
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 16
11/25/2014 4:30:33 PM
TALAKA TATU
mna hiyari ya kuendelea kuishi nao kwa rejea au kuwaacha kwa kufarakiana nao na kutengana nao. Kisha ikarudi kukamilisha hukumu za talaka, ikasema: ‘Na mshuhudishe mashahidi wawili waadilifu miongoni mwenu’ yaani katika talaka ambayo muktadha wa maneno yote ni kubainisha hukumu zake, na inatia ukakasi kurudi kwenye rejea ambayo haijatajwa isipokuwa kwa kufuata asili, hivi huoni kwamba kama msemaji atasema: ‘Atakapokujia aalimu ni wajibu kwako kumheshimu na kumkirimu na umpokee, sawa awe amekuja peke yake au pamoja na mtumishi wake au rafiki yake, na ni wajibu kumsindikiza na kumuaga vizuri.’ Hutafahamu kutoka kwenye maneno haya isipokuwa wajibu wa kumsindikiza na kumuaga aalimu huyo na si mtumishi wake na rafiki yake, hata kama watakuja baada yake. Na Wallahi kulingana na kanuni za Kiarabu na ladha nzuri bayana na iliyo wazi, kama si kughafilika (na kwa kughafilika hujitokeza wasiwasi) basi hili lisingefichikana kwako ilihali wewe ni bingwa wa Kiarabu. Huu ni upande wa tamko la dalili na muktadha wa Aya Tukufu. “Na kuna jambo nyeti zaidi na lenye haki zaidi ya kuzingatiwa upande wa hekima ya sharia, falsafa ya Uislamu, utukufu wake na mtazamo wake wa mbali kuhusu hukumu zake, nalo ni kwamba inajulikana wazi kuwa hakuna halali inayochukiwa sana na Mwenyezi Mungu kushinda talaka, na dini ya Uislamu kama mnavyojua - ni ya jumuiya ya kijamii – haipendelei aina yoyote ile ya mfarakano na hasa katika familia, na hususan katika ndoa baada ya kila mmoja kumfunulia mwenzake kile alichomfunulia. Hivyo kwa hekima yake ya hali ya juu Muwekasheria anataka 17
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 17
11/25/2014 4:30:33 PM
TALAKA TATU
kupunguza utokeaji wa talaka na mfarakano (katika jamii), hivyo akakithirisha miko na masharti yake kwa msingi wa kanuni maarufu isemayo kwamba jambo linapokuwa na masharti mengi ni vigumu na mara chache kutokea. Hivyo akaweka sharti la kuweka mashahidi wawili kwanza ili kudhibiti (utokeaji wa talaka), na pili ili kuchelewesha na kusubirisha. Na huenda mpaka watakapofika mashahidi wawili au mpaka watakapofika mke na mume au mmoja wao, watakuwa wamejutia azma yao na wamerudi kwenye mshikamano kama ilivyoashiriwa hali hiyo na kauli ya Mwenyezi Mungu: ‘Hujui pengine Mwenyezi Mungu ataleta jambo jingine baada ya haya,’ na hekima hii ya kina ya kuweka mashahidi wawili bila shaka imezingatiwa na Muwekasheria Mwingi wa hekima, ukiongezea pia faida nyingine, na yote haya ni kinyume na rejea, kwani hakika Muwekasheria anataka ifanyike haraka kwani kuichelewesha huenda kukasababisha madhara, hivyo hakuwajibisha sharti lolote katika rejea. “Kwetu sisi Shia Imamiyyah rejea inasihi kwa kauli au kitendo au ishara itakayojulisha kuwa amemrejea na wala si sharti ifanyike kwa tamko makhususi kama ilivyo katika talaka, yote hayo ni ili kurahisisha utokeaji wa jambo hili linalopendwa na Muwekasheria Mwingi wa huruma kwa waja Wake na mwenye shauku kubwa ya kuona wanashikamana bila kufarakana. Na vipi isitoshe katika rejea ishara, kumgusa na kuweka mkono wake juu yake kwa kusudio la kumrejea ilihali – mtalaka yeyote wa talaka rejea – kwetu sisi Imamiyyah bado angali ni mke mpaka atakapotoka kwenye eda, na kwa ajili hiyo ndio maana anarithi kutoka kwa mumewe na anarithiwa na mumewe, 18
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 18
11/25/2014 4:30:33 PM
TALAKA TATU
anamuosha mumewe na anaoshwa na mumewe, na ni wajibu kwa mume kumpa matumizi na wala si ruhusa kwa mume kumuoa dada yake au mke wa tano, na mengineyo mengi miongoni mwa hukumu za ndoa.”18
18
Aslus-Shia Wa Usuliha, Uk. 163 – 165, Chapa ya Pili. 19
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 19
11/25/2014 4:30:33 PM
TALAKA TATU
TALAKA TATU KWA TAMKO MOJA AU KUTAMKA MARA TATU KATIKA KIKAO KIMOJA
M
iongoni mwa mas’ala ambayo yamepelekea ugumu na vurugu katika maisha, na kupelekea kuvunjika kwa familia na kukatika mahusiano ya wanandugu katika nchi nyingi, ni mas’ala ya kuona kuwa talaka tatu kwa mpigo ni sahihi, kwa mfano aseme mara tatu: ‘Nimekutaliki talaka tatu.’ Au arudie mara tatu kwa kusema katika kikao kimoja: ‘Nimekutaliki. Nimekutaliki. Nimekutaliki.’ Ambapo huhesabika kuwa ni talaka tatu za kweli na mtalikiwa huwa ni haramu kwa mume wake mpaka aolewe na mume mwingine. Hakika talaka kwa Masunni wengi haina masharti yenye kuzuia uharakishaji wa kutoa talaka, kama vile sharti la kutokuwa katika hedhi au la kutokuwa katika tohara aliyoingiliwa au sharti la ulazima wa kuwepo waadilifu wawili. Kwani huenda mume akazidiwa na hasira na kumilikiwa na ghadhabu na hatimaye akamtaliki talaka tatu kwa mpigo katika kikao kimoja, kisha baadaye akajutia kitendo chake na hivyo akataka kujinasua na athari yake mbaya, lakini hatapata njia ya kujinasua na athari hiyo, si kwa Maimamu wa Madhehebu nne (za Kisunni) wala si kwa walinganiaji wa madhehebu hizo, hivyo atabaki akiwa ni mwenye kujikunyata mwenye kulaumiwa, na maswali na udadisi wa kutafuta njia hiyo hayatamzidishia isipokuwa hali ya kuikimbia fiqhi na fatwa. Hakika kuziba na kuufunga mlango wa ijtihadi mbele ya umma na kuwazuia wanafikra kung’amua hukumu kutoka kwenye Kitabu na Sunna bila kulazimika kufuata rai ya Imamu makhususi, kumezua matatizo mengi katika mas’ala yenye uhusianao na familia, mwandi20
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 20
11/25/2014 4:30:33 PM
TALAKA TATU
shi Muhammad Hamidu al-Faqiy, kiongozi wa kundi la AnswarusSunnat al-Muhammadiyyah anasema: “Hakika taasisi ya familia ambayo Mwenyezi Mungu ameiunganisha kwa nguzo ya ndoa imetetereka na inakaribia kusambaratika, bali katika matabaka mengi tayari imesambaratika, na chanzo cha hilo ni mienendo mibaya waliyoiweka watu katika ndoa na mbinyo waliouweka mafaqihi wa zamani na wa sasa katika talaka kiasi cha kuifanya ishabihiane na upuuzi na mchezo au minyororo na pingu, na mara nyingi nimekutana na mashaka mengi katika maisha yangu ya uhubiri, kutoka kwa waume ambao kutokuwa na bahati kumewatia katika tatizo miongoni mwa matatizo ya talaka, na wanapotafuta utatuzi kutoka kwa mmoja kati ya hao mahafidhina huwa hauwazidishii utafutaji huo isipokuwa mkanganyiko zaidi.”19 Na si al-Faqiy peke yake ndiye ambaye mwenye kulalamikia kitendo cha kufungwa mlango wa ijtihadi na kufuata utaratibu wa Madhehebu nne, bali yeye ni mmoja kati ya wale waliounganisha sauti zao kwenye sauti ya Ahmad Muhammad Shakir, mjumbe wa Mahakama Kuu ya Kisharia, ambaye naye aliona hatari ya msimamo huu, hatari ambayo imesababisha kanuni za kibinadamu kuchukua nafasi ya hukumu za Kiislamu. Anasema: “Mzazi wangu Sheikh Muhammadi Shakir alikuwa ni mwandishi wa fatwa kwa Sheikh wake Sheikh Muhammad al-Abbas al-Mahdiy, Mufti wa Misri – Mwenyezi Mungu amrehemu - siku moja alikuja mwanamke kijana ambaye mume wake alikuwa amehukumiwa kifungo cha muda mrefu, na mwanamke huyo alikuwa anahofia majaribu hivyo alitaka kuwasilisha jambo lake kwa Mufti ili aone kama inawezekana kupata talaka kutoka kwa mumewe ili aolewe na mume mwingine. Katika madhehebu ya Abu Hanifa hakuna suluhisho la tatizo kama hili isipokuwa ni kufanya subira na kungojea, hivyo mzazi 19
Utangulizi wa Kitabu Nidhamut-Talaq Fil-Islam, Uk. 6. 21
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 21
11/25/2014 4:30:33 PM
TALAKA TATU
wangu alimrudisha huku akimuomba samahani na akisikitika na kuumia. Kisha aliwasilisha suala husika kwa Sheikh wake Mufti wa Misri na kumuomba kwamba katika matatizo kama hayo achukue baadhi ya hukumu kutoka kwa Imamu Malik, lakini Sheikh alikataa kabisa na kupinga kabisa rai hii. Na kulitokea baina ya mwalimu na mwanafunzi wake mjadala mkali kuhusu suala hili na hata hivyo haukuathiri upendo na mapenzi yaliyokuwepo baina yao wao wawili, na mzazi wangu – Mwenyezi Mungu amhifadhi - aliendelea kushikilia rai yake akiitakidi usahihi wake na faida yake kwa watu.”20 Na laiti mzazi wa Sheikh Ahmad (Muhammad Shakir) angekuwa anaijua fiqhi ya Maimamu wa Ahlul-Bayt (as) na kwamba katika tatizo hili gumu wao wana suluhisho bayana kutoka kwenye Kitabu na Sunna angemuomba mwalimu wake arejee kwenye fiqhi hiyo. Na kwa nini isiwe hivyo wakati Imam Ja’far as-Sadiq (as) ndiye baba wa mafaqihi, na Maimamu wanne wamejifunza mikononi mwake ima moja kwa moja au kwa kupitia kwa mwanafunzi wake. Hakika matatizo mengi aliyokutana nayo Sheikh katika mahakama yalikuwa ni udikteta wa mume, kumdhuru kwake mke, kuwa naye mbali kwa muda mrefu na mfano wa hayo, na hakukuwa na suluhisho la matatizo hayo katika fiqhi ya Imamu Abu Hanifa, wakati ambapo matatizo haya yametatuliwa katika fiqhi ya Imamiyyah kwa njia bayana. Na ilikuwa ni bora zaidi kwa Sheikh kutoa rai ya kuvunja kizuizi cha taklidi na kurejea kwenye Kitabu na Sunna ili kung’amua hukumu za kisharia bila kulazimika kufuata rai ya Imamu makhususi, na hili ndio jiwe la msingi la kutatua matatizo haya, na fiqhi ya Imamiyyah haijaacha kulingania msingi huu katika karne zote. Sisi tunajua kwa yakini kwamba Uislamu ni dini nyepesi na rahisi isiyo na uzito, na hali hii inawasukuma walinganiaji wenye niya njema kuyasoma upya mas’ala mapya kwa uhuru kinyume na 20
Nidhamut-Talaq Fil-Islam, Uk. 9 - 10. 22
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 22
11/25/2014 4:30:33 PM
TALAKA TATU
usomaji wa mahafidhina ambao wamefunga mbele yao mlango wa kufanya ijtihadi katika hukumu za kisharia, na kinyume na usomaji wa wafuata matamanio waharibifu ambao wanataka kuuachanisha umma na Uislamu. Wao walinganiaji wenye niya njema huchunguza mas’ala na kutafuta hukumu yake kutoka kwenye Kitabu na Sunna huku wakijiepusha na kila rai iliyopo tangu mwanzo wakitaraji kwamba huenda baada ya hapo Mwenyezi Mungu ataibua jambo, na huenda tatizo litafumbuka na Mufti atapata njia ya kujinasua na tatizo hili lililosababishwa na taklidi ya madhehebu. Na tunakunukulia baadhi ya kauli: Sheikh Tusiy amesema: “Iwapo atamtaliki talaka tatu kwa tamko moja atakuwa ameleta bidaa, na itasihi moja iwapo masharti mengine yatatimia, hiyo ndio rai ya jamaa zetu wengi, na miongoni mwao yumo anayesema: ‘Haisihi kabisa hata moja, na ndivyo alivyosema Ali (as) na watu wa dhahiri.’ Twahawi amesimulia kutoka kwa Muhammad bin Is’haqa kwamba itasihi moja kama tulivyosema, na imepokewa kwamba Ibn Abbas na Tawusi walikuwa wanafuata rai ya Imamiyyah.” Shafiy amesema: “Iwapo atamtaliki talaka mbili au tatu kwa mpigo au kwa kutenganisha wakati akiwa katika tohara ambayo hajamwingilia, itakuwa ni talaka halali na isiyo na kizuizi na itasihi. Na katika Maswahaba ndio kauli ya Abdurahman bin Awfi, na wameipokea kauli hiyo kutoka kwa Hasan bin Ali (as), na katika Matabiina ndio kauli ya Ibn Sirin, na katika Mafaqihi ndio kauli ya Ahmad na Is’haqa na Abu Thawri.” Na jamaa wengine wamesema: “Iwapo atamtaliki katika tohara moja talaka mbili au tatu kwa mpigo au kwa kutenganisha atakuwa ametenda haramu, ameasi na kupata dhambi. Katika Maswahaba kauli hiyo ni ya Ali (as), Umar, Ibn Umar, Ibn Masuud na Ibn Abbas. Na katika Mafaqihi ni kauli ya Abu Hanifa, wafuasi wake na 23
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 23
11/25/2014 4:30:33 PM
TALAKA TATU
Maliki, wao wamesema: ‘Isipokuwa ni kwamba itakuwa imesihi.’”21 Ibn Rushdi amesema: “Mafaqihi wengi wa miji wanaona kwamba talaka ya kutamkwa mara tatu hukumu yake ni sawa na hukumu ya talaka tatu. Na watu wa dhahiri na jamaa wengine wamesema: ‘Hukumu yake ni hukumu ya talaka moja wala tamko halina athari yoyote katika hilo.’”22 Abdurahman al-Jaziriy amesema: “Mwanaume huru anamiliki talaka tatu, hivyo iwapo mwanaume atamtaliki mke wake talaka tatu kwa mpigo mmoja, kwa mfano aseme mara tatu: ‘Nimekutaliki’, kwa mujibu wa Madhehebu manne itamlazimu ile idadi aliyoitamka, na hiyo ndio rai ya mafaqihi wengi, lakini baadhi ya mujitahidina wamewakhalifu katika hilo, kama vile Tusiy, Ikrimah, Ibn Is’haqa na wa kwanza wao ni Ibn Abbasi – Mwenyezi Mungu awe radhi naye.”23 Faqihi wa zama hizi Wahbah az-Zuhayliy amebainisha fatwa za jamhuri ya wanazuoni wa Kisunni, amesema: “Wameafikiana Mafaqihi wa Madhehebu manne na madhehebu ya Dhahiriyyah kwamba iwapo mwanamume atamwambia mara tatu mwanamke ambaye hajaingiliwa: ‘Nimekutaliki’ zitakuwa ni talaka tatu sahihi, kwa sababu zote zimepatikana ndani ya ndoa, hivyo zote zimesihi, na pia kama atamwambia hivyo mwanamke aliyeingiliwa. Na wameafikiana pia kwamba kama mume atamwambia mke wake: ‘Nimekutaliki. Nimekutaliki. Nimekutaliki.’ na kukawepo na kitenganishi baina ya matamko hayo, zitakuwa ni talaka tatu sahihi, sawa awe amekusudia kusisitiza au la, kwa sababu ni kinyume na dhahiri. Na akisema: Nimekusudia kusisitiza basi kiapo chake kitakubalika na Al-Khilaf, Juz. 2, Faslu ya Talaka, Mas’ala ya 3. Na kwa mujibu wa aliyoyataja ni kwamba amenukuu kutoka kwa Imam Ali (a.s.) rai mbili zenye kupingana: Haisihi na inasihi japo atakuwa ametenda dhambi. 22 Bidayatul-Mujtahidi, Juz. 2, Uk. 61, Chapa ya Beirut. 23 Al-Fiqhi Alal-Madh’hab al-Ar’baat, Juz. 4, Uk. 341. 21
24
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 24
11/25/2014 4:30:33 PM
TALAKA TATU
hatalazimishwa. Na kama hakutakuwa na kitenganishi basi kama amekusudia kusisitiza talaka ya kwanza kwa talaka mbili za mwisho, talaka moja itakuwa sahihi, kwa sababu kuweka msisitizo katika maneno ni jambo linalokubalika kilugha na kisharia. Na kama (kwa kurudia huko mara tatu) amekusudia kuanza tamko upya au hakuwa ni mwenye kukusudia lolote (si msisitizo wala kuanza tamko upya) basi talaka zote tatu zitakuwa sahihi kwa kufuata dhahiri ya tamko. Na hivyo hivyo huwa ni talaka tatu iwapo atasema: ‘Nimekutaliki. Kisha nimekutaliki. Kisha nimekutaliki.’ Au iwapo ataunganisha matamko hayo kwa Waw au Fau.”24 Hii ndio rai ya jamhuri ya wanazuoni wa fiqhi wa Kisunni, na kuna Maswahaba na Tabiina zaidi ya mmoja waliowakhalifu katika hilo ambao Shawkaniy amewataja majina yao katika kitabu Naylul-Awtari, amesema: ‘Kundi miongoni mwa wanazuoni linaona kwamba talaka haifuatilizwi na talaka hivyo ni moja tu ndio husishi. Ameeleza hayo mwandishi wa al-Bahri kutoka kwa Abu Musa, na riwaya ni kutoka kwa Ali (as), Ibn Abbas, Tawus, Atau, Jabir bin Zaydi, al-Hadi, al-Qasim, al-Baqir, an-Nasir, Ahmad bin Isa na Abdullah bin Musa bin Abdullah. Na riwaya nyingine ni kutoka kwa Zaydi bin Ali na ndio iliyofuatwa na baadhi ya jamaa waliokuja baadaye akiwemo Ibn Taymiyyah, Ibn al-Qayyim, na baadhi ya jamaa miongoni mwa wahakiki. Ameinukuu Ibn Mughith katika kitabu alWathaiq kutoka kwa Muhammad bin Wadhah, na imenukuliwa fatwa kwa mujibu wa kauli hiyo kutoka kwa baadhi ya jamaa miongoni mwa Masheikh wakubwa kama vile Muhammad bin Baqiy, Muhammad bin Abdus-Salami na wengineo. Na ameinukuu Ibn al-Mundhir kutoka kwa watu wa Ibn Abbas kama vile Atau, Tawus na Umar bin Dinar, na pia ameisimulia Ibn Mughith katika kitabu hicho kutoka kwa Ali (as), Ibn Masuud, Abdurahman bin Awfi na Zubayri.”25 24 25
Al-Fiqhi al-Islamiy Waadilatihi, Juz. 7, Uk. 391 – 392. Naylul-Awtar, Juz. 6, Uk. 231. 25
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 25
11/25/2014 4:30:33 PM
TALAKA TATU
Na mengineyo mengi miongoni mwa maneno yenye kuonesha jinsi jamhuri ya mafaqihi wa kisunni waliokuja baada ya kipindi cha Tabiina wanavyoafikiana katika kukubali talaka hiyo wakitumia hoja ulizosikia, na mwongozo wao katika kukubali kwao talaka ya namna hiyo ni Umari bin Khattabi ambaye alikubali talaka ya namna hiyo mbele ya macho na masikio ya Maswahaba. Lakini kama tukigundua kuwa Qur’ani na Sunna vinaonyesha kinyume chake basi wajibu ni kuchukua kile kilichoelezwa na Qur’ani na Sunna. Na tutabainisha haki kupitia mambo yafuatayo: Uchambuzi wa Aya zinazozungumzia maudhui hii: Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema:
ُ َو ْال ُم َطلََّق َّص َن ِبأَ ْن ُف ِس ِه َّن َثلاَ َث َة ُق ُرو ٍء َو اَل ْ ات َي َت َرب َّ َي ِح ُّل لَه ُن أَ ْن َي ْكتُ ْم َن َما َخلَ َق اللهَُّ ِفي أَ ْر َحا ِم ِه َّن ْ إِ ْن ُك َّن ي َّ ُؤ ِم َّن ِباللهَِّ َو ْال َي ْوم آْال ِخ ِر َوبُعُولَتُه ُن أَ َح ُّق ِ َ ُُن ِم ْثل َّ صلاَ ًحا َولَه ْ ِِب َر ِّد ِه َّن ِفي َ ٰذلِ َك إِ ْن أ َرا ُدوا إ َّ َ ِ لر َج َ ْه َّن َد َر َج ٌة ِّ ِوف َول ُ ْه َّن ِب ْال َمع ِ ْر ِ ال َعلي ِ ال ِذي َعلي ٌ َواللهَُّ َعز يز َح ِكي ٌم ِ “Na wanawake waliopewa talaka watangoja twahara tatu. Wala si halali kwao kuficha alichokiumba Mwenyezi Mungu katika matumbo yao, ikiwa wanamwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Na waume zao wana haki zaidi ya kuwarudia katika muda huo, kama wakitaka kufanya suluhu. Nao (wanawake) wanayo haki sawa na ile iliyo juu yao kwa sharia. Na wanaume wana daraja juu yao. Na 26
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 26
11/25/2014 4:30:33 PM
TALAKA TATU
Mwenyezi Mungu ana nguvu, Mwenye hekima.” (Surat al-Baqarah 2:228).
Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Nao (wanawake) wanayo haki sawa na ile iliyo juu yao kwa sharia.” Ni neno la haki na tamko la wazi kwamba baina yao wao wawili (mume na mke) kuna haki za kupeana, hakuna kitendo ambacho mke atamfanyia mume isipokuwa na yeye kuna kitendo anachopaswa kumtendea, hivyo wao wako sawa katika haki na matendo na wala maisha hayawi mazuri isipokuwa kwa kila mmoja kati ya wanandoa kuheshimu na kuchunga haki ya mwenzake na kila mmoja kutekeleza wajibu wake, hivyo ni wajibu kwa mwanamke kuratibu na kutekeleza kazi za nyumbani, na ni wajibu kwa mwanamume kujituma na kutafuta chumo nje ya nyumba. Hii ndio kanuni ya asili iliyo thabiti katika maisha ya ndoa na inayokubalika na maumbile, na Mtume (saww) aligawa kazi baina ya binti yake Fatima (as) na mume wake Ali (as) kwa namna hiyo tuliyoitaja.
َّ ٌ الطلاَ ُق َم َّر َتان َفإ ْم َس يح ُ اك ِب َمع ٌ وف أَ ْو َت ْس ِر ٍ ْر ِ ِ ُ ان َو اَل َي ِح ُّل لَ ُك ْم أَ ْن َت ْأ ُخ ُذوا ِم َّما آ َتيْتُ ُم وه َّن ٍ ِبإِ ْح َس َشي ًْئا إِ اَّل أَ ْن َي َخ َافا أَ اَّل يُ ِقي َما ُح ُدو َد اللهَِّ َفإِ ْن ِخ ْفتُ ْم أَ اَّل َ َ يُ ِقي َما ُح ُدو َد اللهَِّ فَلاَ ُج َن ْه َما ِفي َما ْاف َت َد ْت ِب ِه ِ اح َعلي َ ِت ْل َك ُح ُدو ُد اللهَِّ فَلاَ َت ْع َت ُد َِّوها َو َم ْن َي َت َع َّد ُح ُدو َد الله َّ ولٰ ِئ َك ُه ُم َ َُفأ َ الظالِ ُم ون 27
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 27
11/25/2014 4:30:33 PM
TALAKA TATU
“Talaka ni mara mbili; basi ni kushikamana kwa wema au kuachana kwa hisani. Wala si halali kwenu kuchukua chochote katika mlichowapa, isipokuwa wakiogopa (wote wawili) kwamba hawataweza kusimamisha mipaka ya Mwenyezi Mungu. Basi mkiogopa kwamba hawataweza kusimamisha mipaka ya Mwenyezi Mungu, itakuwa hapana ubaya kwao kupokea ajikomboleacho mke. Hii ndiyo mipaka ya Mwenyezi Mungu; basi msiipetuke. Na watakaoipetuka mipaka ya Mwenyezi Mungu, basi hao ndio madhalimu.” (Surat al-Baqarah 2:229).
Wakati wa Ujahiliyya Waarabu walikuwa na talaka na eda ya kukadiria kwa ajili ya mtalikiwa, na walikuwa pia na rejea iliyokuwa inafanywa ndani ya eda, lakini talaka yao haikuwa na idadi maalumu. Wakati mwingine mwanamume aliweza kumtaliki mke wake mara mia moja kwa kumrejea, na wakati huo mwanamke anakuwa kikaragosi mikononi mwa mwanamume, anamdhuru kwa talaka na anamrejea wakati wowote atakao. Na imekuja katika baadhi ya riwaya kwamba mwanamume mmoja alimwambia mke wake: “Sintakukaribia kamwe lakini bado utaendelea kubaki katika himaya yangu na wala huwezi kuolewa na mwingine.” Mwanamke akauliza: “Ni vipi?” Akasema: “Nakutaliki na utakapokaribia muda wa eda kumalizika nakurejea, kisha nakutaliki tena, nitafanya hivyo milele.” Ndipo mwanamke akaenda kumshitakia hilo Mtukufu Mtume (saww) na ndipo Mwenyezi Mungu akateremsha: “Talaka ni mara mbili”, 26 yaani talaka ambayo Mwenyezi Mungu ameiwekea sharia ya rejea ni talaka ya kwanza na ya pili tu, ama baada ya talaka ya tatu si halali kumrejea mpaka aolewe na mume mwingine, basi wakati huo kama huyo mume mwingine atamtaliki itakuwa ni halali kwa mtalaka wake wa kwanza kumuoa, hii ndio maana ya Aya: 26
Majmaul-Bayan, Juz.1, Uk. 328. Tafsirul-Baghawi, Juz. 1, Uk. 304. Ruhul-Maaniy, Juz. 2, Uk. 135. Al-Kashif, Juz. 1, Uk. 346. 28
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 28
11/25/2014 4:30:33 PM
TALAKA TATU
َفإِ ْن َطلََّق َها فَلاَ َت ِح ُّل لَ ُه ِم ْن َب ْع ُد َحتَّىٰ َت ْن ِك َح َز ْو ًجا َ َ ْر ُه َفإ ْن َطلََّق َها فَلاَ ُج َن اج َعا إِ ْن َ ْه َما أَ ْن َي َت َر ِ اح َعلي ِ َ َغي َظنَّا أَ ْن يُ ِقي َما ُح ُدو َد اللهَِّ َو ِت ْل َك ُح ُدو ُد اللهَِّ يُ َبيِّنُ َها لِ َق ْو ٍم َ َيعْلَ ُم ون َّ َوإِ َذا َطلَّ ْقتُ ُم النِّ َسا َء َف َبلَ ْغ َن أَ َجلَه ُ ُن َفأَ ْم ِس ُك وه َّن ُ وف َو اَل تُ ْم ِس ُك ُ وف أَ ْو َس ِّر ُح وه َّن ُ وه َّن ِب َمع ُ ِب َمع ٍ ْر ٍ ْر ارا لَِت ْع َت ُدوا ً ض َر ِ “Na kama amempa talaka (ya tatu) basi si halali kwake baada ya hapo mpaka aolewe na mume mwingine. Na (mume wa pili) akimwacha, basi hapo si vibaya kwao kurejeana wakiona kuwa watasimamisha mipaka ya Mwenyezi Mungu. Na hii ni mipaka ya Mwenyezi Mungu anayoibainisha kwa watu wajuao. Na mtakapowapa wanawake talaka, wakafikia muda wao, basi washikeni kwa wema au waacheni kwa wema. Wala msiwaweke kwa kudhuriana mkafanya uadui.” (Surat al-Baqarah 2:230 - 231).
Tumeleta Aya nne - ijapokuwa Aya inayohusika kama dalili ya maudhui husika ni Aya ya pili – ili tuzitumie kama ushahidi ndani ya uchunguzi wetu, na kabla ya kuanza kutoa dalili tunaashiria nukta kadhaa katika Aya hizi: Marat (mara): Maana yake ni kuonesha mpigo mmoja katika kitendo. Imsak (Kushika): Ni kinyume cha kuacha huru. 29
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 29
11/25/2014 4:30:34 PM
TALAKA TATU
Tasrih (Kuacha) iliyopo katika “au kuachana kwa hisani”: Ni kuacha huru, husemwa: Sarraha al-Mashiyatu Fil-Mar’a (Amewaachia wanyama malishoni), pindi anapowaacha huru. Na makusudio ya Imsak (Kushika) ni kumrejesha kwenye dhima ya ndoa. Tafsiri ya kauli ya Mwenyezi Mungu: “Au kuachana kwa hisani”: Hakika makusudio ya ‘kuachana’ kwanza ni kutomzuia kuendelea na eda katika kila talaka ili eda yake iishe. Pili ni talaka ya tatu ambayo nayo pia ni aina mojawapo ya kuachana. Hiyo ni kwa sababu ‘kuachana’ ambako ni kinyume cha ‘kushikamana’ kunakubali kuoana na mambo mawili: Kwanza: Kutomzuia kuendelea na eda mpaka eda yake iishe. Pili: Amrejee kisha amtaliki talaka ya tatu. Na kwa msingi huo, wafasiri wana rai mbili katika kutafsiri kauli ya Mwenyezi Mungu: “Au kuachana kwa hisani”: Ya kwanza: Inakusudia kutomzuia kuendelea na eda mpaka eda yake iishe. Kauli hii unaweza kuitetea kwa hoja zifuatazo: a. Hakika kuachana kwa hisani kulikotajwa katika Aya ya 231 kumekusudiwa kutokumrejea, Mwenyezi Mungu anasema: “Na mtakapowapa wanawake talaka, wakafikia muda wao, basi washikeni kwa wema au waacheni kwa wema.” Hivyo ni awla pia kuitafsiri Aya ya pili kwa maana ya kutokumrejea ijapokuwa zimetofautiana katika ibara, ambapo katika Aya tunayoizungumzia imetumika: “Au kuachana kwa hisani” lakini katika Aya nyingine imetumika: “Au waacheni kwa wema”, na huwenda maneno ‘wema’ na ‘hisani’ yana maana moja, kama pia alivyo30
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 30
11/25/2014 4:30:34 PM
TALAKA TATU
tumia lafudhi ‘Au farakianeni nao kwa wema’ kuelezea kitendo cha kuacha kumrejea, hivyo ni awla kutafsiri ibara zote kwa maana ya kuacha kumrejea. b. Hakika talaka ya tatu imetajwa baada ya ibara hii “Au kuachana kwa hisani”, ambapo Mwenyezi Mungu amesema: “Na kama amempa talaka (ya tatu) basi si halali kwake baada ya hapo mpaka aolewe na mume mwingine.” Hivyo ni lazima kuitafsiri ibara hii kwa maana ya kuacha kumrejea ili isilazimike kujirudia. c. Si ruhusa kuitafsiri kauli ya Mwenyezi Mungu: “Au kuachana kwa hisani” kwa maana ya talaka ya tatu, kwani la sivyo italazimika kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na kama amempa talaka (ya tatu) basi si halali kwake baada ya hapo mpaka aolewe na mume mwingine” iwe ni talaka ya nne, wakati hakuna talaka ya nne katika Uislamu.27 Ya pili: Makusudio ya “Au kuachana kwa hisani” ni talaka ya tatu na si kuacha kumrejea baada ya talaka ya pili, hivyo maana ya Aya ni kwamba baada ya mume kumtaliki mke wake mara mbili ni wajibu kwake kutafakari zaidi jambo la mke wake mpaka atambue kwamba hana la kufanya baada ya talaka mbili isipokuwa moja kati ya mambo mawili: Ima amshike kwa wema na kuendelea kuishi naye, au amwache kwa hisani kwa kumtaliki talaka ya tatu ambayo kamwe haina rejea isipokuwa katika mazingira makhususi ambayo yametajwa na Aya ifuatayo kwa kusema: “Na kama amempa talaka (ya tatu) basi si halali kwake baada ya hapo mpaka aolewe na mume mwingine.” Hivyo hapo kauli ya Mwenyezi Mungu: “Au kuachana kwa hisani” inakuwa ni ishara inayoashiria talaka ya tatu ambayo haina rejea, hivyo kwa mujibu wa kauli hii ibara “kuachana” inayozungumziwa hapa inatimia katika 27
Hoja hizi kazitaja al-Jaswasw katika Tafsiir yake, Juz. 1, Uk. 389. 31
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 31
11/25/2014 4:30:34 PM
TALAKA TATU
talaka ya tatu, na si kuacha kumrejea kama ilivyo kwa mujibu wa kauli nyingine. Haya tuliyoyataja ndio muhtasari wa kauli mbili na ya kila msemaji wa maudhui hii. Ama kuhusu hoja zilizotolewa kuunga mkono kauli ya kwanza, kwa kweli ya pili na ya tatu zinaweza kujibiwa. Ama kuhusu ya pili ni kwa sababu hakuna kizuizi kinachozuia kukitaja kitu muhtasari kwanza “Au kuachana kwa hisani” kisha kukitaja tena kwa ufafanuzi kwa kauli yake: “Na kama amempa talaka (ya tatu) basi si halali kwake baada ya hapo mpaka aolewe na mume mwingine,” hivyo haya ni maelezo ya ufafanuzi ya kuachana baada ya kuwa ameyaeleza kwa muhtasari, na ufafanuzi unajumuisha maelezo ambayo hayamo kwenye muhtasari ambayo ni mwanamke huyo kuwa haramu kwake baada ya hapo mpaka aolewe na mume mwingine, na iwapo mume wa pili atamtaliki kwa hiyari yake basi hapo si vibaya kwao kurejeana wakiona kuwa watasimamisha mipaka ya Mwenyezi Mungu. Wapi na wapi baina ya ufafanuzi huu na kauli yake Mtukufu: “Au kuachana kwa hisani”?! Na kwa maelezo hayo linajulikana jibu la hoja ya tatu, kwa sababu kuitafsiri kauli yake Mtukufu: “Au kuachana kwa hisani” kuwa ni talaka ya tatu hakulazimu kauli ya Mtukufu “Na kama amempa talaka (ya tatu) basi si halali kwake baada ya hapo mpaka aolewe na mume mwingine” kuwa ni talaka ya nne, bali ni ufafanuzi wake. Zaidi ya hapo ni kwamba riwaya za makundi yote mawili (Sunni na Shia) zinaunga mkono maana ya pili. Abu Razin amepokea kwamba mtu mmoja alikuja kwa Mtukufu Mtume (saww), akamwambia: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Kauli ya Mwenyezi Mungu inasema: ‘Talaka ni mara mbili; basi ni kushikamana kwa wema au kuachana kwa hisani’ iko wapi basi talaka ya tatu?” Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) akasema: “Basi ni kushikamana kwa wema au kuachana kwa hisani.” Na ny32
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 32
11/25/2014 4:30:34 PM
TALAKA TATU
ingine mfano wa hiyo ameipokea Thawri na wengineo kutoka kwa Ismail bin Samiu kutoka kwa Abu Razin.28 Tabarasiy ameiegemeza kauli ya kwanza kwa Abu Ja’far na Abu Abdillah (as) ijapokuwa Sayyid Bahraniy amepokea katika Tafsiir al-Burhani riwaya sita kutoka kwa Maimamu wa Ahlul-Bayt (as) zikiunga mkono rai ya pili. Vyovyote iwavyo ni kwamba hoja ya pili na ya tatu zinaweza kujibiwa, ama hoja ya kwanza yenyewe jibu lake liko wazi, hiyo ni kwa sababu neno ‘tasrihi’ lililopo sehemu zote tatu lina maana ya ‘kuacha huru’ isipokuwa tofauti inapatikana katika mfano wake halisi wa nje (namna ya kuacha huru), hivyo hakuna kizuizi kinachozuia mfano wake halisi wa nje (namna ya kuacha huru) katika Aya hii kuwa ni talaka, na mfano wake halisi wa nje (namna ya kuacha huru) katika Aya mbili kuwa ni kuacha kumrejea, na kuwepo tofauti katika mfano wake halisi wa nje (namna ya kuacha huru) hakuwajibishi kuwepo tofauti katika maana halisi. Mpaka hapa imekamilika tafsiri ya kauli ya Mwenyezi Mungu: “Talaka ni mara mbili; basi ni kushikamana kwa wema au kuachana kwa hisani.” Na ifuatayo ni tafsiri ya sehemu iliyobaki ya Aya, yaani kauli ya Mwenyezi Mungu:
َّ ٌ الطلاَ ُق َم َّر َتان َفإ ْم َس يح ُ اك ِب َمع ٌ وف أَ ْو َت ْس ِر ٍ ْر ِ ِ ْ َ ُ ُ ان َو اَل َي ِح ُّل لَ ُك ْم أ ْن َتأ ُخذوا ِم َّما آ َتيْتُ ُم وه َّن ٍ ِبإِ ْح َس َشي ًْئا إِ اَّل أَ ْن َي َخ َافا أَ اَّل يُ ِقي َما ُح ُدو َد اللهَِّ َفإِ ْن ِخ ْفتُ ْم أَ اَّل َ َ يُ ِقي َما ُح ُدو َد اللهَِّ فَلاَ ُج َن ْه َما ِفي َما ْاف َت َد ْت ِب ِه ِ اح َعلي 28
Tafsir Qurtubiy, Juz. 3, Uk. 128. 33
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 33
11/25/2014 4:30:34 PM
TALAKA TATU
َ ِت ْل َك ُح ُدو ُد اللهَِّ فَلاَ َت ْع َت ُد َِّوها َو َم ْن َي َت َع َّد ُح ُدو َد الله َّ ولٰ ِئ َك ُه ُم َ َُفأ َ الظالِ ُم ون “Wala si halali kwenu kuchukua chochote katika mlichowapa, isipokuwa wakiogopa (wote wawili) kwamba hawataweza kusimamisha mipaka ya Mwenyezi Mungu. Basi mkiogopa kwamba hawataweza kusimamisha mipaka ya Mwenyezi Mungu, itakuwa hapana ubaya kwao kupokea ajikomboleacho mke. Hii ndiyo mipaka ya Mwenyezi Mungu; basi msiipetuke. Na watakaoipetuka mipaka ya Mwenyezi Mungu, basi hao ndio madhalimu.” (Surat al-Baqarah 2:229).
Kifungu hiki cha Aya kimekuja kubainisha mambo mawili: Jambo la kwanza: Pindi mume akitaka kumtaliki mke wake si halali kwake kuchukua chochote kutoka kwa mke katika vile vitu alivyompa, Mwenyezi Muungu amesema: “Wala si halali kwenu kuchukua chochote katika mlichowapa.” Na katika Aya nyingine amesema: “Na mtakapotaka kubadilisha mke mahali pa mke, na mkawa mumempa mmoja wao rundo la mali, basi msichukue katika mlichowapa. Je, mnakichukua kwa dhulma na kwa makosa yaliyo wazi?”29 Jambo la pili: Katika hukumu ya kutoruhusiwa mume kuchukua kitu Mwenyezi Mungu ameengua sura makhususi, nayo ni pale mke anapokuwa amemchukia mume na hawezi kuendelea kuishi naye kiasi kwamba kumchukia kwake kutampelekea kumuasi Mwenyezi Mungu kwa kutotekeleza haki za mume, na mume naye pia huenda akahofia kumkabili kwa ubaya zaidi kuliko inavyostahili, katika hali hii inaruhusiwa kwa mke kuomba talaka kwa mume kwa fidia atakayoiridhia mume, kama ambavyo pia anaruhusiwa mume 29
Sura an-Nisai: 20. 34
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 34
11/25/2014 4:30:34 PM
TALAKA TATU
kuchukua fidia atakayojikombolea mke, na hukumu hiyo ndio inayoashiriwa na kauli ya Mwenyezi Mungu: “Basi mkiogopa kwamba hawataweza kusimamisha mipaka ya Mwenyezi Mungu, itakuwa hapana ubaya kwao kupokea ajikomboleacho mke.” Mpaka hapa imekamilika tafsiri ya Aya ya 229, na ifuatayo sasa ni tafsiri ya Aya ya 230. Mwenyezi Mungu amesema:
َفإِ ْن َطلََّق َها فَلاَ َت ِح ُّل لَ ُه ِم ْن َب ْع ُد َحتَّىٰ َت ْن ِك َح َز ْو ًجا َ َ ْر ُه َفإ ْن َطلََّق َها فَلاَ ُج َن اج َعا إِ ْن َ ْه َما أَ ْن َي َت َر ِ اح َعلي ِ َ َغي َظنَّا أَ ْن يُ ِقي َما ُح ُدو َد اللهَِّ َو ِت ْل َك ُح ُدو ُد اللهَِّ يُ َبيِّنُ َها لِ َق ْو ٍم َ َيعْلَ ُم ون “Na kama amempa talaka (ya tatu) basi si halali kwake baada ya hapo mpaka aolewe na mume mwingine. Na (mume wa pili) akimwacha, basi hapo si vibaya kwao kurejeana wakiona kuwa watasimamisha mipaka ya Mwenyezi Mungu. Na hii ni mipaka ya Mwenyezi Mungu anayoibainisha kwa watu wajuao.” (Surat al-Baqarah 2:230).
Madhumuni ya Aya ni kwamba atakayemtaliki mke wake mara tatu, mke huyo si halali kwake tena baada ya hapo mpaka aolewe na mume mwingine kwa ndoa sahihi, kisha iwapo mume huyo atatengana naye kwa kifo au talaka na eda yake ikamalizika hapo anaruhusiwa mume wa kwanza kumuoa tena mara ya pili. Na ni kwamba huyu mume mwenye kuhalalisha ndoa ya mara ya pili ni lazima atimize masharti ambayo yametajwa katika vitabu vya fiqhi. 35
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 35
11/25/2014 4:30:34 PM
TALAKA TATU
Ama Aya ya nne, yaani kauli ya Mwenyezi Mungu, hakika maana yake iko wazi:
َّ َوإِ َذا َطلَّ ْقتُ ُم النِّ َسا َء َف َبلَ ْغ َن أَ َجلَه ُ ُن َفأَ ْم ِس ُك وه َّن ُ وف أَ ْو َس ِّر ُح وف ُ وه َّن ِب َمع ُ ِب َمع ٍ ْر ٍ ْر “Na mtakapowapa wanawake talaka, wakafikia muda wao, basi washikeni kwa wema au waacheni kwa wema.” (Surat al-Baqarah 2:231).
Haya ndio tuliyopenda kuyataja kuhusu tafsiri ya Aya hizi, na sasa hebu turejee kwenye mada husika, nayo ni hukumu ya talaka tatu, tunasema: Kama umetambua maana ya Aya basi tambua kuwa Kitabu na Sunna vinajulisha ubatilifu wa talaka tatu za mpigo, na kwamba ni wajibu kwamba talaka iwe moja baada ya nyingine kwa kutenganishwa ima na rejea au ndoa. Hivyo kama mume atamtaliki mke wake talaka tatu mara moja kwa mpigo au atarudia tamko la talaka, hapo talaka tatu hazitasihi. Ama kuhusu kuhesabu hizo tatu kuwa ni talaka moja, hata kama suala hilo ni haki lakini liko nje ya maudhui tunayoichunguza hapa, na hivyo zifuatazo ni dalili za Kitabu kwanza, kisha za Sunna:
Kwanza: Dalili kwa njia ya Kitabu kupitia hoja MBALIMBALI: 1.
Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Talaka ni mara mbili:”
Hakika kauli ya Mwenyezi Mungu: “Talaka ni mara mbili” inaonesha kuwa: 36
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 36
11/25/2014 4:30:34 PM
TALAKA TATU
30
a.
Hakika hukumu hii inajumuisha vigawanyo vyote vya talaka na kwamba hakika kutenganisha baina ya talaka hakutokani na sifa makhususi ya kipekee iliyopo katika talaka fulani na haipo katika talaka nyingine, bali ni kwamba tabia asili ya talaka haiachani na kila talaka, kwa sababu Alifu na Lam (katika lugha ya Kiarabu) inapokuwa si ya jambo linalojulikana hujulisha mjumuisho, hivyo makadirio ya Aya ni: Kila talaka ni mara mbili, na mara ya tatu, na kama angesema hivyo basi ingejulisha kuwa talaka iliyowekwa kisharia ni ya kutenganisha, kwa sababu mara haipatikani isipokuwa baada ya kutenganisha.30
b.
Hakika kauli yake: Mara mbili inaonesha ulazima wa kutokea kwa talaka mara moja baada ya nyingine na si mara moja kwa mpigo, la sivyo itakuwa ni mara moja na kwa mpigo, na kwa ajili hiyo ndio maana Mwenyezi Mungu ameelezea hilo kwa neno ‘mara’ ili lioneshe namna ya kitendo na kwamba ni kitendo kimoja, kama ambavyo maneno Daf’atu, Kurrat na Nazlat, yalivyo sawa na Marat (mara) katika mizani, maana na mazingatio. Na kwa mujibu wa hayo tuliyoyataja ikiwa mwenye kutaliki atasema: “Nimekutaliki talaka tatu” atakuwa hajamtaliki mke wake mara moja baada ya nyingine, na pia atakuwa hajamtaliki mara mbili, bali ni talaka moja, na wala kauli yake ‘talaka tatu’ haiwi ni kurudia kitendo. Na hilo linathibitishwa na vipengele vingine vya kifiqhi ambavyo hakuna mwanafiqhi hata mmoja aliyesema kuwa kuongeza idadi zaidi ya moja wakati wa kutekeleza vipengele hivyo ni kurudia. Kwa mfano katika yamini ya kujiombea
At-Tafsirul-Kabir, Juz.6, Uk. 103. 37
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 37
11/25/2014 4:30:34 PM
TALAKA TATU
laana31 ni sharti kuapa mara nne, na haisihi kuapa kiapo kimoja chenye kufuatiwa na kauli ‘mara nne’. Na pia katika vipengele vya Adhana ambavyo inapasa kurudiwa mara mbili, havisomwi mara moja na kufuatilizwa na kauli ‘mara mbili’. Na pia katika kiapo kama mtu atasema; “Naapa kwa Mwenyezi Mungu viapo hamsini kwamba huyu ndiye aliyemuua” hiki kitakuwa ni kiapo kimoja. Na hata akisema mwenye kukiri kuwa kafanya zinaa: “Mimi nakiri mara nne kuwa nimefanya zinaa” atakuwa amekiri mara moja tu na atahitajika kukiri tena mara tatu. Na ni hivyo hivyo katika maeneo mengine ambayo idadi haichukui nafasi ya kitendo cha kurudia. Hiki ndio kipimo cha jumla katika kila eneo ambalo inahitajika idadi, kama katika kurusha vijiwe vidogo (changarawe) saba, haisihi kurusha kijiwe kimoja. Na katika kutoa takbira tano za Swala ya Iddi au saba zenye kufuatana – kama ilivyo kwa Masunni – kabla ya kisomo, mwenye kuswali haleti takbira moja na kuifuatanisha na kauli ‘mara tano au mara saba.’ Au katika Swala ya Tasbihi 32 ambayo ina sharti la kusoma tasbihi mara kumi au mara kumi na tano, haisihi tasbihi moja kuwa badala ya idadi husika kwa kufuatilizwa na kauli ‘mara kumi au mara kumi na tano.’ Haya yote ni mambo yasiyo na tofauti. Na sijamuona yeyote aliyesitasita katika hayo isipokuwa Ibn Hazmi, akadai kuwa neno mara linaweza kutumika kwa maana nyingine, akasema: “Ama kauli yao kuwa: ‘Maana ya kauli ya Mwe Hii ni yamini maalumu ambayo hufanyika baina ya wanandoa ili mume kuthibitisha madai yake dhidi ya mke, na ili mke kukanusha madai hayo, na kila mmoja hujiombea laana iwapo anayoyasema ni uwongo. Athari ya yamini hii ya kujiombea laana ni kuondoa adhabu (hadi) kwa mwanamke mtuhumiwa au mume kumkataa mtoto, hivyo yamini hii ya kujiombea laana hufanyika linapotokea moja kati ya mambo mawili: Kwanza mume anapomtuhumu mke wake kwa uzinzi. Pili ni pindi mume anapomkataa mtoto aliyezaliwa ndani ya ndoa yake ilihali dhahiri ya mazingira inaonesha kuwa ni mwanawe – Mtarjumi. 32 Makusudio ni Swala ya Ja’far Twayyar. 31
38
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 38
11/25/2014 4:30:34 PM
TALAKA TATU
nyezi Mungu: Talaka ni mara mbili, kuwa ni mara moja baada ya mara nyingine, ina makosa, bali Aya hii ni sawa na kauli ya Mwenyezi Mungu: Tutampa ujira wake mara mbili, yaani maradufu pamoja, na Aya hii pia ni mafunzo kuhusu talaka ambazo huwa kabla ya talaka ya tatu.”33 Anajibiwa kwa hayo aliyoyataja, kwamba kutumika neno ‘mara mbili’ katika Aya hii kwa maana ya maradufu ni kwa ajili ya kuwepo dalili, na laiti isingekuwepo dalili hiyo basi ingetafsiriwa kwa maana yake halisi, hiyo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu anawaambia wake wa Mtukufu Mtume (saww) kwa kauli mbili: Ya kwanza:
ْ اح َش ٍة ُم َبيِّ َن ٍة ِ َيا ِن َسا َء النَّ ِب ِّي َم ْن َيأ ِت ِم ْن ُك َّن ِب َف َي َ ْن َو َك ُ اع ْف لَ َها ْال َع َذ َ ُض َِّان َ ٰذلِ َك َعلَى الله ِ اب ِ ض ْع َفي يرا ً َي ِس “Enyi wake wa Mtume! Yeyote kati yenu atakayefanya uchafu dhahiri, atazidishiwa adhabu mara mbili. Na hilo kwa Mwenyezi Mungu ni jepesi.” (Surat Al-Ahzab 33:30).
Ya pili:
صالِ ًحا نُ ْؤ ِت َها َ َو َم ْن َي ْقنُ ْت ِم ْن ُك َّن للِهَِّ َو َر ُسولِ ِه َو َت ْع َم ْل َأ َ َ ْن َوأَ ْع َت ْد َنا لَ َها ِر ْز ًقا َك ِري ًما ي ت ر م ا ه ر ج َّ ْ َ َ ِ 33
Al-Muhalliy, Juz. 10, Uk. 168. 39
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 39
11/25/2014 4:30:34 PM
TALAKA TATU
“Na yeyote katika nyinyi atakayemtii Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na akatenda wema, tutampa malipo yake mara mbili, na tutamwandalia riziki yenye heshima.” (Surat Al-Ahzab 33:31).
Kauli yake katika Aya ya kwanza: “Atazidishiwa adhabu mara mbili” ni dalili inayoonesha kwamba makusudio ya kauli ya Mwenyezi Mungu: “Tutampa malipo yake mara mbili” ni kumpa malipo maradufu na si malipo baada ya malipo, hivyo kutumika neno ‘mara mbili’ katika sehemu ya ‘maradufu’ haiwi ni dalili ya kuwa imetumika hivyo katika sehemu nyingine zote. Al-Jaswasw amesema: “Na dalili ya kwamba makusudio ya kauli ya Mwenyezi Mungu: ‘Talaka ni mara mbili’ kuwa ni amri ya kutenganisha talaka na ni kubainisha hukumu ya namna ya kutoa talaka rejea ambazo huwa kabla ya talaka ya tatu, ni kule kusema kwake: ‘Talaka ni mara mbili’, hakuna jinsi kuwa hiyo inalazimu kutenganisha, kwa sababu kama atamtaliki talaka mbili pamoja haitasihi kusema: ‘Amempa mara mbili’, mpaka atenganishe utoaji ndipo itasihi kusemwa hivyo, na ikiwa hivi ndivyo basi ikiwa hukumu iliyokusudiwa na tamko ni ile inayohusu talaka mbili, ambayo ni kuwepo nafasi ya rejea, hiyo itapelekea kutokuwepo faida ya kutajwa neno ‘mara mbili’, kwani hukumu hii (kuwepo nafasi ya rejea) ni thabiti ipo hata atakapomtaliki talaka mbili kwa mara moja kwa mpigo, hivyo inathibiti kuwa kutajwa ‘mara mbili’ ni amri inayotaka talaka itolewe mara mbili na inakataza kuzikusanya zote mbili mara moja kwa mpigo.”34 Mtume (saww) amesema: “Hakuna talaka isipokuwa baada ya ndoa.” Na amesema: “Hakuna talaka kabla ya ndoa.” Na amesema: “Hana talaka asiyemiliki.”35 Hivyo hakuna ndoa baada ya tamko la kwanza mpaka atalikiwe. 34 35
Ahkamul-Qur’an, Juz. 1, Uk. 378 – 379. As-Sunanul-Kubra, Juz. 7, Uk. 318 – 321. Al-Mustadrak cha Hakim, Juz. 2, Uk. 24. 40
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 40
11/25/2014 4:30:34 PM
TALAKA TATU
Haya yote ni kama atatoa talaka tatu kwa tamko moja, ama akirudia tamko, huenda asiye mwerevu akadanganyika na akadai kuwa kurudia tamko kunaoana na Aya husika, lakini nalo hili linakataliwa kwa njia nyingine, nayo ni: Hakika tamko la pili na la tatu linakuwa batili kwa sababu ya kutokuwepo sababu ya msingi ya hukumu, kwani talaka ni kwa ajili ya kukata uhusiano wa ndoa, na hakuna uhusiano wa ndoa baada ya tamko la kwanza hata uhitaji kukatwa, wala hakuna mafungamano ya kikanuni hata yatenguliwe. Ndiyo, huenda mtu akasema kuwa: Mtalikiwa bado angali katika himaya ya mume na hukumu yake ni hukumu ya mke, hivyo tamko la pili na la tatu linakuwa na athari kutokana na kizuizi hiki. Anajibiwa kuwa: Anakusudia nini anaposema: ‘Hukumu yake ni hukumu ya mke’? Kama anakusudia kuwa mume ana haki ya kumrejea, jambo hilo ni sahihi na kwa ajili hiyo ndio maana husemwa: ‘Mtalikiwa wa talaka rejea ana hukumu ya mke, au ni mke’, kwa kuzingatia kuwa mume ana haki ya kurudia kujenga jengo alilolibomoa kwa talaka, hakuna haja ya ndoa mpya. Lakini hili silo linalodaiwa. Na akikusudia kuwa yeye ni mke kwa maana ya kwamba tamko la talaka halijaathiri chochote na wala halijabomoa jengo la ndoa, na kwamba hali ya mwanamke kabla ya talaka ni ileile kama iliyonayo baada ya talaka, dai hilo ni kinyume na misingi sahihi. Vipi hali yake kabla ya talaka itakuwa sawa na ile ya baada ya talaka, ilihali kama ataachwa mpaka eda yake iishe atakuwa ni mwanamke ajinabi kwake na mtu kambo kabisa. Na uwezekano wa yeye kupewa talaka ya pili - kabla ya rejea – umejengwa juu ya dhana ya pili ambayo tayari umeshajua kuwa inapingana na misingi, na wala haujajengwa juu ya dhana ya kwanza. 41
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 41
11/25/2014 4:30:34 PM
TALAKA TATU
Na kwa ibara iliyo wazi zaidi: Ni kwamba talaka ni mume kukata uhusiano wa ndoa uliyopo baina yake na mke wake na kumwacha huru, nalo ni jambo ambalo halitimii bila kuwepo kwanza huo uhusiano wa kidhihinia wa kijamii, na ni jambo linalojulikana kuwa mtalikiwa hatalikiwi, na aliye huru haachwi huru. Zaidi ya hapo ni kwamba kuna utata unaojitokeza katika sura hii ya kutoa talaka tatu bila kurudia tamko. Muundo wa utata huo ni kwamba, hakika talaka ni jambo la dhihinia ambalo linapatikana kupitia kauli ya mtaliki, na haina uhalisia nje ya fikra, kinyume na jambo la kimaumbile ambalo lina uhalisia nje ya dhana na fikra. Hivyo kama kauli ni moja basi hivyo hivyo kizalishwa chake ni kimoja, hivyo wingi wa talaka unategemea wingi wa kauli, wakati kwa mujibu wa sura hii kauli ni moja. Ndiyo, utata huu haupatikani iwapo tamko la ndoa litarudiwa, kama atasema: “Nimekutaliki. Nimekutaliki. Nimekutaliki.” Hitimisho ni kuwa kutaliki talaka tatu kwa namna hii hakutimizi idadi mahususi ambayo ndio maudhui ya Aya ifuatayo, yaani kauli ya Mwenyezi Mungu:
َفإِ ْن َطلََّق َها فَلاَ َت ِح ُّل لَ ُه ِم ْن َب ْع ُد َحتَّىٰ َت ْن ِك َح َز ْو ًجا ْر ُه َ َغي “Na kama amempa talaka (ya tatu) basi si halali kwake baada ya hapo mpaka aolewe na mume mwingine.” (Surat al-Baqarah 2:230).
Kwa sababu wingi wa talaka unategemea uwepo wa ndoa baina ya talaka mbili, angalau kwa rejea, na kama hazitatenganishwa na ndoa basi kuongea huko itakuwa ni sawa na kuongea maneno ya upuuzi. 42
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 42
11/25/2014 4:30:34 PM
TALAKA TATU
Samaki amesema: “Hakika ndoa ni fundo linalofungwa, na hufunguliwa kwa talaka, na vipi itawezekana kufungua fundo kabla halijafungwa?!36 Hitimisho ni kwamba iwapo atasema: “Nimekutaliki” ni kama amesema: “Nimefungua fundo lililokuwepo baina yangu na wewe, nimevunja mkataba huu, nimekata kiunganishi hiki ambacho kinamuunganisha kila mmoja wetu na mwenzake, hivyo ukivunjwa mkataba uliokuwepo baina yao, au likifunguliwa fundo au kukatwa kamba ni wapi tena mume atamiliki uwezo wa kuvunja mkataba au kufungua fundo au kukata kamba tena mara nyingine au mara ya tatu? Na ni katika mkataba upi kati ya mikataba ya sharia hii takatifu au sharia nyingine na kanuni nyingine, mtu anaweza kuuvunja mkataba mmoja mara mbili au mara tatu ilihali mkataba ni mmoja. Labda kama mkataba utarudiwa upya ndipo anaweza tena kuuvunja, na hapo inakuwa ni kuvunja mkataba mwingine.37 2.
Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Basi ni kushikamana kwa wema au kuachana kwa hisani.” Imeshatangulia kwamba katika tafsiri ya kifungu hiki cha Aya kuna kauli mbili zenye kutofautiana, na katika wafasiri wapo wanaokihusisha na kifungu kilichotangulia, yaani kauli ya Mwenyezi Mungu: ‘Talaka ni mara mbili’, na wapo wanaokihusisha na talaka ya tatu ambayo imekuja katika Aya iliyofuata. Na bila shaka umeshajua haki ni ipi, kwani kifungu hiki kinaonesha ubatilifu wa talaka tatu za mpigo kwa dhana zote. Ama kwa mujibu wa dhana ya kwanza: Ubatilifu wake uko wazi, kwa sababu maana ya kifungu hiki ni kuwa kila mara talaka inapoto36 37
As-Sunanul-Kubra, Juz. 7, Uk. 321. Nidhamut-Talaq Fil-Islam, Uk. 72. 43
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 43
11/25/2014 4:30:34 PM
TALAKA TATU
ka katika mara hizo mbili ni wajibu ifuatiwe na moja kati ya mambo mawili: Kushikamana kwa wema au kuachana kwa hisani. Ibn Kathir amesema: “Yaani utakapomtaliki talaka moja au mbili, maadamu tu eda yake ingalipo, wewe una hiyari wakati huo ima kumrejesha kwako kwa niya ya kutengeneza na kufanya hisani, na ima umuache mpaka amalize eda yake na hatimaye atengane na wewe na umwache huru huku ukimtendea hisani bila kudhulumu haki yake yoyote wala kumdhuru.”38 Wapi na wapi hili na talaka tatu za mpigo ambazo hazitenganishwi na moja kati ya mambo mawili -Kushikamana kwa wema au kumuacha mpaka amalize eda yake, sawa amtaliki kwa tamko la ‘Nimekutaliki talaka tatu’ au ‘Nimekutaliki. Nimekutaliki. Nimekutaliki.’?! Shawkaniy amesema: “Ili talaka ya tatu isihi ni sharti kwamba mwanamke awe katika hali ambayo inasihi kwa mume kumzuia (kuendelea kuishi naye) – kabla ya talaka ya tatu, na kama haisihi kumzuia (kuendelea kuishi naye) isipokuwa baada ya kumrejea hapo talaka ya tatu haisihi isipokuwa baada ya kufanya hivyo, na kama inalazimika kufanya hivyo katika talaka ya tatu basi inalazimika pia katika talaka ya pili.39 Ama kwa mujibu wa dhana ya pili: Hakika hata kama kifungu hiki kinazungumzia hali ya talaka ya tatu na kimenyamazia hali ya talaka mbili za mwanzo, lakini tunasema: Hakika baadhi ya Aya zinajulisha kwamba madhumuni yake ni sehemu ya sifa za asili za talaka zote bila kutofautisha baina ya mbili za mwanzo na ya tatu, hivyo ni wajibu talaka ilivyo kama talaka ifuatiwe na moja kati ya mambo mawili: Mwenyezi Mungu amesema: “Na mtakapowapa 38 39
Tafsir Ibn Kathir, Juz. 1, Uk. 53. Naylul-Awtar, Juz. 6, Uk. 234. 44
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 44
11/25/2014 4:30:34 PM
TALAKA TATU
wanawake talaka, wakafikia muda wao, basi washikeni kwa wema au waacheni kwa wema.”40 Kwanza: Kuwashika kwa wema. Pili: Kuwaacha kwa wema. Hivyo hitimisho la mjumuiko wa Aya hizi ni kwamba talaka kufuatiwa na moja kati ya mambo mawili ni miongoni mwa sifa za lazima zisizoachana na tabia asili ya talaka ambayo inasihi kumrejea mke. Na hilo linadhihiri kwa uwazi pale tutakapotambua kuwa kauli ya Mwenyezi Mungu: “Wakafikia muda wao” ni miongoni mwa masharti yaliyofuata aghlabu, kwani lililo wajibu tangu mtu amtaliki mke wake ni kufanya moja kati ya mambo mawili, lakini kuyahusisha mambo hayo na muda makhususi ambao ni ‘wakafikia muda wao’ ni kwa sababu mtaliki ambaye kazidiwa na ghadhabu na hasira, ghadhabu yake huwa haitulii haraka mpaka kipite kiasi fulani cha muda ambacho ndani yake anaweza kutafakari kuhusu jambo la mke wake na atamke moja kati ya mambo mawili. Hivyo “Basi washikeni kwa wema au waacheni kwa wema” inapasa kuwa ni hukumu yenye kujumuisha muda wote kuanzia alipotamka tamko la talaka mpaka sekunde ya mwisho inayomalizika pamoja na eda. Hivyo kwa mujibu wa hayo tuliyotaja, kifungu hiki kinajulisha ubatilifu wa mtindo wa talaka tatu na kwamba unakhalifu namna ya kisharia ya utoaji talaka, isipokuwa dalili ya ubatilifu wake kwa mujibu wa kauli ya kwanza ni Aya yenyewe, na kwa mujibu wa kauli ya pili ni kwa msaada wa Aya nyingine. 3. 40
Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Basi wapeni talaka wakati wa eda zao.”
Sura al-Baqarah: 231. 45
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 45
11/25/2014 4:30:34 PM
TALAKA TATU
Hakika kauli ya Mwenyezi Mungu: ‘Talaka ni mara mbili’, inazungumzia talaka ambayo inaruhusiwa kumrejea mwanamke, na kwa upande mwingine kauli ya Mwenyezi Mungu: “Mtakapowataliki wanawake, basi wapeni talaka wakati wa eda zao, na fanyeni hisabu ya eda”41 inajulisha kuwa lililo wajibu katika haki ya hawa ni kukaa eda na kufanya hisabu ya eda, sawa tuseme kwamba ‘eda zao’ ni kwa maana ya wakati, yaani ‘Wakati wa eda zao’, au ni kwa maana ya lengo, na makusudio ni kwa lengo la kukaa eda, kwani vyovyote vile inaonesha kuwa miongoni mwa sifa za talaka ambayo inaruhusiwa kumrejea mke ni kukaa eda na kufanya hisabu ya eda. Na jambo hilo halipatikani isipokuwa kwa kutenganisha baina ya talaka ya kwanza na ya pili, la sivyo talaka ya kwanza haitakuwa na eda na wala haitafanyiwa hisabu ya eda iwapo atamtaliki talaka mbili mara moja kwa mpigo. Na kama akimtaliki tatu kwa mpigo basi talaka ya kwanza na ya pili zitakuwa na kasoro hizo. Baadhi ya Maimamu wa Ahlul-Bayt (as) wametumia Aya hii kuthibitisha ubatilifu wa talaka tatu za mpigo. Amepokea Swaf’wan al-Jammal kutoka kwa Abu Abdillah (as) kwamba mtu mmoja alimwambia: “Mimi nimemtaliki mke wangu talaka tatu katika kikao kimoja.” Imam akasema: “Si chochote, hivi hujasoma Kitabu cha Mwenyezi Mungu: ‘Ewe Nabii! Mtakapowataliki wanawake, basi wapeni talaka wakati wa eda zao, na fanyeni hisabu ya eda, na mcheni Mwenyezi Mungu, Mola Wenu. Msiwatoe katika nyumba zao, wala wasitoke wenyewe, ila wakifanya uchafu ulio wazi. Hiyo ndiyo mipaka ya Mwenyezi Mungu msiikiuke; na mwenye kuikiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu, amejidhulumu nafsi yake, hujui pengine Mwenyezi Mungu ataleta jambo jingine baada ya haya.’” Kisha Imam akasema: “Kila kinachokhalifu Kita41
Sura Talaq: 1. 46
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 46
11/25/2014 4:30:34 PM
TALAKA TATU
bu cha Mwenyezi Mungu na Sunna hurudishwa kwenye Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna.”42 4.
Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Hujui pengine Mwenyezi Mungu ataleta jambo jingine baada ya haya.”
Hakika kama talaka tatu za mpigo zitasihi basi kauli ya Mwenyezi Mungu: “Hujui pengine Mwenyezi Mungu ataleta jambo jingine baada ya haya” haitakuwa na faida, kwa sababu watakuwa wametengana na mwisho wa jambo hautakuwa mzuri na hakutakuwa na ufumbuzi isipokuwa kwa mwanamke kuolewa na mume mwingine na kutalikiwa, wakati dhahiri ya kifungu hiki ni kwamba tatizo litafumbuliwa kwa njia ya rejea au ya kufunga ndoa ndani ya eda. Pili: Dalili kwa njia ya Sunna: Umeshajua hukumu ya Kitabu kuhusu mas’ala hii, ama hukumu ya Sunna yenyewe inaeleza kwamba Mtukufu Mtume (saww) alikuwa anaona talaka kama hii ni kukifanyia mchezo Kitabu Kitukufu. 1.
Ameandika an-Nasaiy kutoka kwa Mahmudu bin Lubaydi kuwa alisema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) alipewa habari za mwanamume aliyemtaliki mke wake talaka tatu pamoja kwa mpigo, Mtume akasimama kwa ghadhabu kisha akasema: ‘Hivi anachezea Kitabu cha Mwenyezi Mungu na mimi ningali baina yenu?!’ akasimama mtu mmoja na kusema: ‘Niende nikamuuwe ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?’”43
Mahmud bin Lubaydi ni sahaba mdogo na ana hadithi alizosikia, amepokea Ahmad kwa sanadi sahihi kutoka kwake, Qarbul-Isnad, Uk. 30. Wasailus-Shiah, Juz. 15, Mlango wa 29 kati ya milango ya utangulizi wa talaka, Hadithi ya 25. 43 Sunanun-Nasaiy, Juz. 6, Uk. 142. Ad-Durul-Manthur, Juz. 1, Uk. 283. 42
47
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 47
11/25/2014 4:30:34 PM
TALAKA TATU
amesema: “Alitujia Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) akatusalisha Maghribi katika msikiti wetu, baada ya kutoa salamu akasema: ‘Rukuuni rakaa hizi mbili majumbani kwenu, kwa ajili ya kusabihi baada ya Maghribi.”’44 Na hii ni dalili kwamba ana hadithi alizosikia moja kwa moja kutoka kwa Mtukufu Mtume (saww), na al-Hafidh Ibn Hajar amemnukuu katika kitabu alIswabah.45 Na huenda mwanaume huyu aliyemtaliki mke wake talaka tatu za pamoja kwa mpigo ni Rakanah ambaye tutamzungumzia katika hadithi ya pili. Kisha tunaona Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anaisifu aina hii ya talaka kuwa ni kukichezea Kitabu cha Mwenyezi Mungu, na kisha zinaonekana usoni kwake athari za ghadhabu. Je inawezekana kweli kusema aina hii ya talaka ni sahihi wakati hii ndio hadhi yake?! Na hata kama tukikubali kuwa Ibn Lubaydi hakuwahi kusikia hadithi moja kwa moja kutoka kwa Mtume (saww) kama anavyodai Ibn Hajar katika kitabu Fat’hul-Bariy46 lakini yeye bado ni Swahaba, na hakuna ubishi kuwa hadithi mursalu za Maswahaba ni hoja kwa Mafaqihi (wa Kisunni) kwa kufuata kanuni ya kwamba Maswahaba wote ni waadilifu. 2.
Ibn Is’haqa amepokea kutoka kwa Ikrimah, kutoka kwa Ibn Abbas kuwa alisema: “Rakanah alimtaliki mke wake talaka tatu katika kikao kimoja, kisha akahuzunika sana kwa kitendo hicho, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) akamuuliza: ‘Ulimtaliki vipi?’ akasema: ‘Nilimtaliki talaka
Musnad Ahmad, Juz. 5, Uk. 427. Tazama Juz. 6, Uk. 67. 46 Fat’hul-Bariy, Juz. 9, Uk. 315, pamoja na hayo kasema wapokezi wake ni waaminifu, na amesema katika kitabu chake kingine Bulughul-Marami, Uk. 224, wapokezi wake ni watu waaminifu. Na Shawkaniy amenukuu katika Naylul-Awtari, Juz. 6, Uk. 227, kutoka kwa Ibn Kathir kwamba amesema: Sanadi yake ni nzuri. 44 45
48
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 48
11/25/2014 4:30:34 PM
TALAKA TATU
tatu katika kikao kimoja.’ Mtume akasema: ‘Hakika hiyo ni talaka moja, mrejee.’”47 Na muulizaji ni Rakanah bin Abdu Yazid, Imam Ahmad amepokea kwa sanadi sahihi kutoka kwa Ibn Abbas kuwa alisema: “Rakanah bin Abdi Yazid ndugu wa Bani Mutwalib alimtaliki mke wake talaka tatu katika kikao kimoja, kisha akahuzunika sana kwa kitendo hicho, ndipo Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) akamuuliza: ‘Ulimtaliki vipi?’ Akasema: ‘Nilimtaliki talaka tatu.’ Akamuuliza: ‘Katika kikao kimoja?’ Akasema: ‘Ndiyo.’ Akasema: ‘Hakika hiyo ni talaka moja hivyo mrejee kama unataka.’ Akamrejea.” Hivyo Ibn Abbas alikuwa anaona kuwa talaka ni wakati wa kila twahara.48
Bidayatul-Mujtahid, Juz. 2, Uk. 61. Na wameipokea wengine kama vile Ibn Qayyim katika kitabu Ighathatul-Lahfani, Uk. 156. Na Suyutiy katika ad-Durul-Manthur, Juz. 1, Uk. 279, na wengineo. 48 Musnad Ahmad, Juz. 1, Uk. 265. 47
49
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 49
11/25/2014 4:30:34 PM
TALAKA TATU
DALILI ZA MWENYE KUSEMA KUWA TALAKA TATU ZA MPIGO NI SAHIHI
M
wenye kusema kuwa inaruhusiwa kutoa talaka tatu pamoja kwa mpigo au kwa kutenganisha katika kikao kimoja, anatumia Kitabu, na mara nyingine Sunna na Ijmai kama dalili ya kutetea hilo. Ama kuhusu Kitabu anatumia Aya zifuatazo: 1.
Kwamba kauli ya Mwenyezi Mungu: “Au kuachana kwa hisani” (Surat al-Baqarah 2:229), inajumuisha talaka tatu zinazotolewa pamoja kwa mpigo.
2.
Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na kama mkiwapa talaka kabla ya kuwagusa.” (Surat al-Baqarah 2:237).
3.
Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Si vibaya kwenu kama mkiwapa wake talaka ambao hamjawagusa.” (Surat al-Baqarah 2:236).
4.
Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na wanawake waliopewa talaka wapewe cha kuwaliwaza kulingana na desturi; hiyo ni haki kwa wenye takua.” (Surat al-Baqarah 2:241), Aya hizi hazijatenganisha baina ya kutolewa talaka moja au mbili kwa pamoja au tatu kwa pamoja.
Na hoja za dalili hizi zimejibiwa kwamba mjumuisho huu uliopo kwenye hizi Aya umetenguliwa na kuzuiwa na dalili nyingine ambazo zinazuia kutolewa talaka zaidi ya moja wakati mmoja.49 Na ni bora ijibiwe kuwa, ili kushikamana na kauli jumuishi ni sharti kwamba mzungumzaji awe katika nafasi ya kufafanua na si katika 49
Naylul-Awtari, Juz. 6, Uk. 232. 50
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 50
11/25/2014 4:30:35 PM
TALAKA TATU
nafasi ya kutoa muhtasari, kwa mfano, kama mzungumzaji atakuwa katika nafasi ya kubainisha hukumu ya tabia asili ya kitu na akasema kwa mfano: ‘Kondoo ni halali na nguruwe ni haramu’, haiwezekani kutumia kauli hii kuhalalisha kondoo hata kama ni kondoo mla kinyesi au wa kuporwa, eti kwa kushikamana na mjumuisho uliopo kwenye kauli. Na imekubaliwa katika elimu ya Misingi ya Sharia kwamba kushikamana na kauli jumuishi inategemea masharti matatu: La kwanza: Mzungumzaji awe katika nafasi ya kubainisha namna ya jambo ambalo sisi tunataka kulitolea hukumu yake, hivyo kama atanyamaza (bila kuweka sharti) hapo inasihi kushikamana na mjumuisho, ama akiwa hayupo katika nafasi ya kubainisha namna hiyo husika, haisihi kushikamana na mjumuisho huo. Na Aya hizi ni miongoni mwa aina hii, kwani hakika zenyewe zipo katika nafasi ya kubainisha mambo mengine, ya kwanza ipo katika nafasi ya kubainisha kwamba mtalikiwa huwa ni haramu mpaka aolewe na mume mwingine. Ya pili ipo katika nafasi ya kubainisha hukumu ya mtalikiwa mwenye kutalikiwa kabla ya kuingiliwa. Na ya tatu na ya nne nazo zipo katika nafasi ya kubainisha kwamba mtalikiwa ana haki maalumu inayojulikana kwa jina la ‘kiliwazo’. Wapi na wapi baina ya maudhui hizi na ruhusa ya kutaliki talaka tatu kwa mpigo?! Na haki ni kwamba kufungwa kwa mlango wa Ijtihadi kuanzia katikati ya karne ya saba mpaka leo hii ndio sababu ya kudhoofika kwa ung’amuzi wa sharia kutoka kwenye vyanzo vyake vya kisharia, la sivyo hauwezi kujificha udhaifu wa aina hii ya dalili kwa mng’amuzi mjuzi wa Misingi ya Sharia.
51
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 51
11/25/2014 4:30:35 PM
TALAKA TATU
DALILI ZAO KWA NJIA YA SUNNA
M yake: 1.
wenye kusema kuwa zinasihi talaka tatu za pamoja zinazotolewa katika kikao kimoja, pia hutumia Sunna kutetea kauli
Habari ya Fatima binti ya Qays: Amepokea Ibn Hazmi kupitia njia ya Yahya bin Abi Kathir kwamba: Abu Salamah bin Abdurahman alinipa habari kwamba Fatima binti ya Qays alimpa habari kwamba mume wake mtoto wa Hafsu bin al-Mughirah al-Makhzumiy alimtaliki talaka tatu za pamoja kwa mpigo kisha akaenda zake Yemen, Khalid bin Walid akiwa na kundi la watu walikwenda kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) katika nyumba ya Maimuna Mama wa Waumini, wakasema: ‘Hakika mtoto wa Hafsu amemtaliki mke wake talaka tatu za pamoja kwa mpigo je ana haki ya kupewa matumizi?’ Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) akasema: ‘Hana haki ya kupata matumizi, na ni wajibu wake kukaa eda.’”50 Hivyo kama ingekuwa talaka tatu za pamoja za mpigo ni jambo lisilokubalika kisharia Mtume (saww) angelikataa.
Anajibiwa kuwa: Hakika Ibn Hazmi amenukuu riwaya hii kinyume na ilivyo. Ahmad amepokea ndani ya Musnad yake kutoka kwa Fatima binti ya Qaysi, kuwa alisema: “Nilikuwa kwa Abu Amru mtoto wa Hafsu bin al-Mughirah na alikuwa amenitaliki mara mbili, kisha yeye alikwenda pamoja na Ali (as) Yemen pindi alipotumwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww), ndipo akanitumia talaka ya tatu.”51 50 51
Al-Muhaliy, Juz. 10, Uk. 172. Musnad Ahmad, Juz. 7, Uk. 563, Hadithi ya 26789. 52
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 52
11/25/2014 4:30:35 PM
TALAKA TATU
Na katika Sunanud-Daruqutniy amepokea kwa njia yake kutoka kwa Abu Salmah bin Abdurahman kutoka kwa Fatima binti ya Qaysi kwamba alimpa habari kuwa yeye alikuwa kwa Abu Amru mtoto wa Hafsu bin al-Mughirah, ndipo akamtaliki talaka ya mwisho kati ya talaka tatu, akadai kuwa yeye (Fatima binti ya Qaysi) alikwenda kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) kumuuliza hukumu ya yeye kutoka nyumbani kwake.52 Maelezo waliyoyanukuu wanahadithi wawili ni dalili kwamba talaka hizi zilikuwa za kutenganisha si za pamoja kwa mpigo, isipokuwa ni kwamba Ibn Hazmi alighafilika kutaja maelezo ya hadithi. 2.
Hadithi ya Aisha: Ibn Hazmi amepokea kwa njia ya Bukhari kutoka kwa Aisha Mama wa Waumini kuwa alisema: “Hakika mwanaume mmoja alimtaliki mke wake talaka tatu kisha akaolewa na kutalikiwa tena (na mume wa pili), Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) akaulizwa je mwanamke huyu ni halali kwa mume wa kwanza? Akasema: ‘Hapana, mpaka aonje asali yake kama alivyoonja mume wa kwanza.’” Mtume (saww) hakukataa swali hili na laiti ingekuwa hairuhusiwi Mtume angeeleza.53
Anajibiwa kuwa: Hakika riwaya hii haioneshi kuwa talaka hizi tatu zilikuwa za pamoja kwa mpigo bali dhahiri ni kwamba zilikuwa ni za kutenganisha, kwa ushahidi kwamba talaka hizo zilitolewa wakati wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww), na talaka tatu za pamoja katika zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww), zama za Abu Bakri na katika miaka miwili ya mwanzo ya ukhalifa wa Umar zilikuwa zinahesabika kuwa ni talaka moja.54 Sunanud-Daruqutniy, Juz. 4, Uk. 29, Faslu ya Talaka, Hadithi ya 80. Al-Muhaliy, Juz. 10, Uk. 171. 54 Sahih Muslim, Juz. 2, Mlango wa talaka tatu, Hadithi ya 15. 52 53
53
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 53
11/25/2014 4:30:35 PM
TALAKA TATU
3.
Hadithi ya Sahli: Sahli bin Saad as-Saidiy amesema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) aliwaapisha yamini ya kujiombea laana Zubeir al-Ajlaniy na mke wake, walipojiombea laana mume alisema: ‘Nikiendelea kuishi naye nitakuwa nimemsingizia uwongo, hivyo nimemtaliki talaka tatu.’ Mtume (saww) akasema: ‘Huna njia juu yake.’”55 Hoja za dalili hii: Hakika al-Ajlaniy alikuwa amemtaliki mke wake ndani ya wakati ambao hakuwa na haki ya kutaliki humo, alimtaliki talaka tatu za pamoja kwa mpigo, na Mtukufu Mtume (saww) akambainishia hukumu ya wakati na kwamba hana haki ya kumtaliki ndani ya wakati huo, lakini hakumbainishia hukumu ya idadi ya talaka, na laiti idadi hiyo ingekuwa ni haramu na bidaa basi angembainishia. Anajibiwa kuwa: Hii ni miongoni mwa dalili za ajabu, kwani hakika mume anapoapizana na mke wake kwa kuombeana laana anakuwa ni haramu kwake milele.56 Hivyo hakuna nafasi ya ndoa wala talaka, lakini kwa kuwa mtu huyo alikuwa hajui hukumu ya Uislamu na kwamba mke wake ametengana na yeye kwa yamini ya kujiombea laana bila haja ya kutoa talaka, hivyo alimtaliki talaka tatu za pamoja kwa mpigo kwa kudai kuwa ni mke wake kwa mujibu wa sharia ya zama za ujahiliya. Ama kuhusu Mtukufu Mtume (saww) ni kwamba katika maneno yake hakuna kiashiria kinachoonesha kuwa aliikubali na kuridhia kauli ya al-Ajlaniy – aliyoisema baada ya yamini - ya kwamba amemtaliki talaka tatu, bali yeye (saww) aliashiria uharamu wa milele na kwamba mwanamke huyo 55 56
Sunanul-Bayhaqiy, Juz. 7, Uk. 328. Mafaqihi wa Madhehebu manne wamekubaliana kuwa yamini ya kujiombea laana inaharamisha milele mahusiano ya ndoa (baina ya mume na mke), hivyo mwanamke anakuwa si halali kwake milele hata kama mume atakiri baadaye kuwa alisema uongo. Ndiyo, Mahanafi wamesema anakuwa ni Haramu kwake milele isipokuwa kama mwanamume atakiri baadaye kuwa alisema uwongo. (al-Fiqhi al-Islamiy Waasilatihi, Juz. 7, Uk. 177.). 54
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 54
11/25/2014 4:30:35 PM
TALAKA TATU
amekuwa haramu kwa mume wake, na akasema: ‘Huna njia juu yake.’ Wapi na wapi kauli hii na Mtume kukubali na kuridhia hukumu ya idadi.
55
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 55
11/25/2014 4:30:35 PM
TALAKA TATU
DALILI ZAO KWA NJIA YA IJMAI
W
enye kusema kuwa zinasihi talaka tatu za pamoja zinazotolewa katika kikao kimoja, pia hutumia Ijmai kutetea kauli yao, kwa kudai kuwa talaka iliyozungumziwa ndani ya Kitabu ilifutwa, al-Ayniy amesema ndani ya Umdatul-Qarii: “Ukisema: ‘Ni upi usahihi wa ufutaji huu wakati Umar hana mamlaka ya kufuta? Na inawezekana vipi kupatikana ufutwaji wa hukumu baada ya Mtukufu Mtume (saww)?’ Nitasema: Umar aliwahutubia Maswahaba kwa kuwaambia hilo na hakuna ukanushaji uliyotokea na hivyo ikawa ni Ijmai, na ufutwaji hukumu kupitia Ijmai umeruhusiwa na baadhi ya masheikh zetu kwa njia ya kwamba Ijmai inapelekea kuwa na yakini kama yalivyo maandiko (Kitabu na Sunna), hivyo inasihi kuthibitisha ufutwaji wa hukumu kupitia Ijmai, na ni kwa kuwa Ijmai ni hoja yenye nguvu zaidi kushinda riwaya ambayo ni habari mashuhuri, hivyo ikiwa ufutwaji wa hukumu unaruhusiwa kwa riwaya ambayo ni habari mashuhuri basi ni bora zaidi uruhusiwe kwa Ijmai. Ukisema: ‘Ijmai hii ya kufutwa hukumu ni kutoka ndani ya nafsi zao wenyewe na wao hawana haki ya kufanya hivyo.’ Nitasema: Inategemewa kuwa kuna andiko lililodhihiri kwao na ndilo lililowajibisha kufutwa hukumu, lakini andiko hilo halijatufikia.”57 Anajibiwa kuwa: Inakuwaje anadai uwepo wa Ijmai wakati kuna andiko mutawatiri kuwa katika zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww), zama za Abu Bakri na katika miaka miwili ya mwanzo ya ukhalifa wa Umar talaka tatu za pamoja kwa mpigo zilikuwa zinahesabika kuwa ni talaka moja. Pamoja na hayo inakuwaje anadai uwepo wa Ijmai wakati kuna tofauti kuhusu mas’ala hii na wengi miongoni mwa Maswahaba na Tabiina wanaona kuwa talaka tatu za pamoja kwa mpigo si sahihi?! 57
Umdatul-Qarii, Juz. 20, Uk. 222. 56
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 56
11/25/2014 4:30:35 PM
TALAKA TATU
Ama kushikilia kunyamaza kwa watu (pindi Umar alipotoa tamko lake) hakuoneshi na si dalili kuwa kuna andiko linaloonesha kuwa hukumu imefutwa, kwani kama lingekuwepo andiko wangelidhihirisha na bila shaka lingekifikia kizazi kilichofuata kutoka kizazi kilichopita, kwa sababu mas’ala hii ni miongoni mwa mas’ala yenye kuwatokea watu katika maisha ya kawaida. Na hata tukijaalia kuwa andiko lipo ilikuwaje lisijulikane na lifichikane katika zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww), zama za Abu Bakr na katika sehemu ya kipindi cha ukhalifa wa Khalifa wa pili?!
57
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 57
11/25/2014 4:30:35 PM
TALAKA TATU
RAI BINAFSI MKABALA NA MAANDIKO
M
tukufu Mtume (saww) aliaga dunia ikiwa tayari imechomoza mielekeo miwili yenye kutofautiana na fikra mbili zenye kupingana, Ali (as) na waliomfuata na Maimamu wengine wa AhlulBayt walikuwa wanazitambua hukumu za kisharia kupitia maandiko ya kisharia, ambayo ni ima Aya au Hadithi, na kamwe hawatendi kwa rai zao binafsi. Mkabala na wao kulikuwa na kundi dogo la Maswahaba waliokuwa wakitumia rai binafsi ili kuifikia hukumu ya kisharia kwa njia ya kujua maslahi na hivyo wakiweka hukumu kulingana na mahitaji ya maslahi husika. Hakika kutumia rai binafsi katika jambo lisilo na maandiko, na kuweka hukumu kulingana na maslahi ni jambo linalokubali kujadiliwa na kuchunguzwa, na hakika mazungumzo ni kuhusu kutumia rai binafsi katika jambo ambalo maandiko yake yapo. Kundi la pili lilikuwa likitumia rai yake binafsi mkabala na maandiko, si katika jambo ambalo halina maandiko kutoka katika Kitabu au Sunna, bali hata katika jambo ambalo lina maandiko na dalili ya kisharia. Ahmad Amini al-Misriy anasema: “Imenidhihirikia kuwa Umar bin Khattab alikuwa akitumia rai binafsi katika maana pana zaidi kushinda hii tuliyoitaja, na hiyo ni kwa sababu tulilotaja ni kutumia rai binafsi mahali ambapo hakuna maandiko kutoka katika Kitabu wala Sunna, lakini sisi tunamuona Khalifa (Umar) akienda mbali zaidi ya hapo. Alikuwa akitumia rai binafsi katika kujua maslahi ambayo kwa ajili yake Aya iliteremka au hadithi imepatikana, kisha anatumia maslahi hayo kutoa hukumu zake, na huo ni mtindo ulio 58
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 58
11/25/2014 4:30:35 PM
TALAKA TATU
karibu zaidi na ule unaojulikana sasa kama mtindo wa Kuongozwa na Roho ya Sharia badala ya ibara yake.58 Hakika mtindo wa Kuongozwa na Roho ya Sharia badala ya ibara yake uliyoashiriwa na Ahmad Amini ni jambo jingine na kutupilia mbali maandiko na kufuata rai binafsi ni jambo jingine mbali, lakini kundi la pili lilikuwa likitupilia mbali maandiko na kufanyia kazi rai yao binafsi. Na yale yaliyopokelewa kutoka kwa Khalifa kuhusu mas’ala hii ni miongoni mwa namna hii ya mambo, na kama una shaka na hilo basi tunakusomea yale tuliyoyapata: 1.
Muslim amepokea kutoka kwa Twawus kutoka kwa Ibn Abbas kuwa alisema: “Katika zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww), zama za Abu Bakr na katika miaka miwili ya ukhalifa wa Umar talaka tatu za pamoja kwa mpigo zilikuwa ni talaka moja, Umar bin Khattab akasema: ‘Hakika watu wamefanya haraka katika jambo ambalo walikuwa na ustahimilivu nalo hivyo si ni vizuri tukawaridhia?’ Ndipo akawaridhia.”59
2.
Muslim amepokea kutoka kwa Ibn Twawus kutoka kwa baba yake kwamba hakika Abu Swahbau alimwambia Ibn Abbas: “Hivi unajua kwamba talaka tatu za pamoja kwa mpigo katika zama za Mtukufu Mtume (saww) na zama za Abu Bakr na miaka mitatu ya mwanzo ya ukhalifa wa Umar zilikuwa zinafanywa kuwa ni talaka moja?” Akasema: “Ndiyo.”60
3.
Na pia Muslim amepokea kutoka kwa Twawus kwamba Abu Swahbau alimwambia Ibn Abbas: “Leta habari zako za kushangaza, hivi katika zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) na zama za Abu Bakr talaka tatu hazikuwa talaka
Fajrul-Islam, Uk. 238, kilichochapishwa na Darul-Kutubi. Sahih Muslim, Juz. 4, Uk. 184, Mlango wa talaka tatu, Hadithi ya 1. 60 Sahih Muslim, Juz. 4, Uk. 184, Mlango wa talaka tatu, Hadithi ya 2. 58 59
59
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 59
11/25/2014 4:30:35 PM
TALAKA TATU
moja?” Akasema: “Ndiyo ilikuwa hivyo lakini ilipofika zama za Umar ilijitokeza tabia ya watu kufuatanisha katika talaka ndipo akairidhia dhidi yao.”61 Na inaweza kusemwa kuwa riwaya hii inakhalifu maelezo yaliyopokewa kutoka kwa Ibn Abbas kwamba yeye alitoa fatwa ya kusihi talaka tatu za pamoja kwa mpigo. Ahmad bin Hanbal amesema: “Watu wote wa Ibn Abbas wamepokea kutoka kwake maelezo yaliyo kinyume na yale aliyoyapokea Twawus katika mas’ala hii, nawakusudia Said bin Jubayri, Mujahidi na Nafiu. Abu Dawud amesema ndani ya Sunan yake: Imekuwa ndio kauli ya Ibn Abbas katika riwaya aliyotusimulia Ahmad bin Swalih, amesema: “Alitusimulia Abdul-razaq kutoka kwa Ma’amar kutoka kwa Zah’riy kutoka kwa Abu Salmah bin Abdulrahman na Muhammad bin Abdulrahman bin Thawban, kutoka kwa Muhammad bin Iyasi kwamba Ibn Abbas na Abu Huraira na Abdullah bin Amru bin al-Aswi waliulizwa kuhusu bikira ambaye mume wake kamtaliki talaka tatu za pamoja kwa mpigo, wote wakasema: ‘Si halali kwake mpaka aolewe na mume mwingine.’”62 Anajibiwa kuwa: Kinachozingatiwa ni riwaya ya Ibn Abbas, nayo ni yenye kubatilisha talaka tatu za pamoja kwa mpigo. Ama kuhusu rai iliyonukuliwa kutoka kwake ambayo ni hoja kwake yeye mwenyewe na si kwa mtu mwingine, hata kama ikisihi kuwa alitoa fatwa kinyume na riwaya yake hiyo haiwi dalili ya kwamba riwaya ni dhaifu, kwa sababu mambo yanayoweza kusababisha yeye kuacha riwaya na kwenda kwenye rai ni mengi na miongoni mwayo ni kusahau na mfano wake. Kisha hakika Shawkaniy baada ya kutaja jibu hili amesema: “Hakika wenye kusema kuwa zinasihi talaka tatu za pamoja za 61 62
Sahih Muslim, Juz. 4, Uk. 184, Mlango wa talaka tatu, Hadithi ya 3. Naylul-Awtar, Juz. 6, Uk. 233. 60
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 60
11/25/2014 4:30:36 PM
TALAKA TATU
mpigo wametoa majibu mengi kuhusu hadithi ya Ibn Abbas na yote hayako nje ya duara la hoja ya nguvu, na haki ndiyo yenye haki ya kufuatwa.63 1.
Al-Bayhaqiy amepokea kwa kusema: Abu Swahbau alikuwa ni mwingi wa maswali kwa Ibn Abbas, amesema: “Hivi unajua kwamba katika zama za Mtukufu Mtume (saww), zama za Abu Bakr na mwanzoni mwa utawala wa Umar (r.a.) ilikuwa mume akimtaliki mke wake talaka tatu za pamoja kwa mpigo kabla hajamwingilia zinafanywa ni moja, lakini Umar alipoona kuwa watu wamefuatana katika suala la talaka ndipo akasema: ‘Naruhusu dhidi yao talaka tatu za pamoja kwa mpigo.’”64
2.
Ameandika Twahawiy kutoka katika njia ya Ibn Abbas kwamba alisema: “Kilipofika kipindi cha Umar (r.a.) alisema: ‘Enyi watu! Hakika mlikuwa na ustahmilivu katika talaka, na hakika yeyote atakayefanya haraka katika talaka badala ya ustahmilivu wa Mwenyezi Mungu tutamlazimisha (kutenda kwa mujibu wa) talaka hiyo.”65
3.
Kutoka kwa Twawus amesema: Umar bin Khattab alisema: “Hakika mlikuwa na ustahmilivu katika talaka lakini nyinyi mmefanya haraka badala ya kustahmili, nasi tumeruhusu kwenu lile mlilolifanyia haraka.”66
4.
Kutoka kwa Hasan amesema: “Hakika Umar bin Khattab alimwandikia barua Abu Musa al-Ash’ariy: “Nilikusudia kufanya kwamba mtu akimtaliki mke wake talaka tatu katika kikao kimoja ihasabike kuwa ni talaka moja, lakini watu wamejiwekea
Naylul-Awtar, Juz. 6, Uk. 234. Sunanul-Bayhaqiy, Juz. 7, Uk. 339. Ad-Durul-Manthur, Juz. 1, Uk. 289. 65 Umdatul-Qarii, Juz. 9, Uk. 537, na amesema: Sanadi yake ni sahihi. 66 Kanzul-Ummal, Juz. 9, Uk. 676, Hadithi namba 27943. 63 64
61
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 61
11/25/2014 4:30:36 PM
TALAKA TATU
hivyo (talaka tu za mpigo), basi nami nailazimisha kila nafsi kile ilichojilazimisha yenyewe. Yeyote atakayemwambia mke wake: ‘Wewe ni haramu kwangu’ basi anakuwa ni haramu kwake. Na yeyote atakayemwambia mke wake: ‘Nimetengana na wewe, basi anakuwa katengana naye. Na yeyote atakayemwambia mke wake: ‘Nimekutaliki talaka tatu’ zitakuwa ni talaka tatu kweli.”67 Maandiko haya yanajulisha kwamba kitendo cha Khalifa hakikutokana na kufanya Ijtihadi katika jambo ambalo halina maandiko, wala si kwa kufuata mtindo wa Kuongozwa na Roho ya Sharia badala ya ibara yake ambao ni kuieneza hukumu ya kisharia mpaka kwenye maeneo ambayo yanakutana na maandiko katika mas’ala moja, kama pale atakaposema: ‘Pombe ni haramu’, hukumu hii (uharamu) inaenea hadi kwenye kila kileo kwa kufuata Roho ya Sharia, nayo ni ile sababu iliyopelekea uharamu huo, ambayo ni ulevi uliomo ndani ya kile kilichotamkwa na maandiko (pombe) na ndani ya kile ambacho hakikutamkwa na maandiko (vileo vingine). Bali hakika kitendo cha Khalifa kilitokana na jambo jingine la tatu nalo ni kutumia rai binafsi mkabala na maandiko na kuitupilia mbali dalili ya kisharia na kufuata rai yake na fikra yake binafsi. Ndiyo wamejaribu kutaja mambo kadhaa ya kuhalalisha hukumu hii ya Khalifa, nasi tunayataja hapa moja baada ya jingine:
67
Kanzul-Ummal, Juz. 9, Uk. 676, Hadithi namba 27943. 62
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 62
11/25/2014 4:30:36 PM
TALAKA TATU
MAMBO YANAYODAIWA KUHALALISHA HUKUMU YA KHALIFA
B
aada ya hukumu iliyotolewa na Khalifa kuwa ni yenye kukhalifu maandiko ya Qur’ani au dhahiri yake, baadhi ya wahakiki wamejaribu kuhalalisha kitendo hiki cha Khalifa kwa baadhi ya hoja ili tu wahalalishe hukumu yake na kuifanya sahihi na kuitoa kwenye wigo wa kutumia rai binafsi mkabala na maandiko, bali kwa kufanya hivyo itakuwa ni hukumu iliyotokana na dalili ya kisharia. Ufuatao ni ufafanuzi wake: 1. M aandiko ya Kitabu yamefutwa kwa Ijmai yenye kufichua uwepo wa maandiko (yenye kufuta maandiko ya kwanza): Hakika talaka iliyozungumziwa ndani ya Kitabu imefutwa, ukisema: ‘Ni upi usahihi wa ufutaji huu wakati Umar hana mamlaka ya kufuta? Na inawezekana vipi kupatikana ufutwaji wa hukumu baada ya Mtukufu Mtume (saww)?’ Nitasema: Umar aliwahutubia Maswahaba kwa kuwaambia hilo na hakuna ukanushaji uliyotokea na hivyo ikawa ni Ijmai, na ufutwaji hukumu kupitia Ijmai umeruhusiwa na baadhi ya masheikh zetu kwa njia ya kwamba Ijmai inapelekea kuwa na yakini kama yalivyo maandiko (Kitabu na Sunna), hivyo inasihi kuthibitisha ufutwaji wa hukumu kupitia Ijmai, na ni kwa kuwa Ijmai ni hoja yenye nguvu zaidi kushinda riwaya ambayo ni habari mashuhuri. Ukisema: ‘Ijmai hii ya kufutwa hukumu ni kutoka ndani ya nafsi zao wenyewe na wao hawana haki ya kufanya hivyo.’ Nitasema: Inategemewa kuwa kuna maandiko yaliyodhihiri kwao na ndiyo yaliyowajibisha kufutwa hukumu, lakini maandiko hayo hayajatufikia.”68
68
Umdatul-Qarii, Juz. 9, Uk. 537. 63
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 63
11/25/2014 4:30:36 PM
TALAKA TATU
Anajibiwa kuwa: Kwanza hakika mas’ala hii ilikuwa na kauli mbili baina ya Maswahaba siku ambayo aliitolea fatwa Khalifa, vipi sasa ilipatikana hali ya kukongamana katika kauli moja?! Bila shaka umeshazijua kauli mbalimbali mwanzoni mwa mas’ala hii. Na kwa ajili hiyo ndio maana tunaona wengine wakikataa kabisa uwepo wa hali ya kukongamana (Ijmai) na wanasema: “Mpaka mwaka wa pili wa ukhalifa wa Umar Maswahaba walikuwa bado wamekongamana kwamba talaka tatu za tamko moja ni talaka moja, na kongamano hili halikutenguliwa na kinyume chake, bali ni kwamba bado wapo katika umma huu karne baada ya karne mpaka leo hii, watu wanaotoa fatwa kwa mujibu wa kongamano hili.”69 Pili: Maelezo haya yanapingana na maelezo aliyoyatoa Khalifa kuhalalisha kitendo chake pale aliposema: ‘’Hakika watu wamefanya haraka katika jambo ambalo walikuwa na ustahmilivu nalo hivyo si ni vizuri tukawaridhia?’’ Ndipo akawaridhia, kama kungekuwa kuna maandiko kwa Khalifa angepaswa kuhalalisha kwa kupitia maandiko husika. Mwishoni tunasema: Wapi na wapi maneno aliyoyataja mwandishi wa Umdatul-Qarii na maneno aliyoyataja Sheikh Swalih bin Muhammad al-Amriy (aliyetawafu mwaka 1298A.H.) ambapo amesema: “Hakika lililo maarufu kwa Maswahaba na waliowafuata kwa wema mpaka siku ya malipo, na kwa wanazuoni wengi wa Kiislamu, ni kwamba hukumu ya mtawala Mujtahid ikikhalifu maandiko ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu au Sunna ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) ni wajibu kuitengua na kuzuia utekelezwaji wake. Wala maandiko ya Kitabu na Sunna hayapingwi kwa dhana za kiakili na mawazo ya kinafsi na ushabiki wa kishetani kwa kusema: Huenda Mujtahidi huyu alipata maandiko lakini akayaacha kwa sababu ya udhuru uliomdhihirikia, au kwa sababu alipata dalili ny69
Taysiirul-Wusul, Juz. 3, Uk. 162. 64
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 64
11/25/2014 4:30:36 PM
TALAKA TATU
ingine, na mfano wa hayo miongoni mwa mambo yaliyotamkwa na kundi la Mafaqihi wenye ushabiki na kutekelezwa na wajinga wenye kukalidi.”70 2. Kuwaadhibu kwa kuvuka kwao mipaka ya Mwenyezi Mungu: Lengo la kupitisha talaka tatu za pamoja zinazotolewa katika kikao kimoja haikuwa isipokuwa ni ili kuwaadhibu kutokana na tendo lao, na kuwaadhibu kwa kule kuvuka kwao mipaka ya Mwenyezi Mungu, hivyo akawaomba ushauri wenye rai na wenye mamlaka na akasema: ‘Hakika watu wamefanya haraka katika jambo ambalo walikuwa na ustahmilivu nalo hivyo si ni vizuri tukawaridhia?’ walipomuwafiki katika lile aliloazimia akawaridhia na kusema: ‘‘Enyi watu! Hakika mlikuwa na ustahmilivu katika talaka, na hakika yeyote atakayefanya haraka badala ya ustahmilivu wa Mwenyezi Mungu tutamlazimisha (kutenda kwa mujibu wa) talaka hiyo.”71 Katika utafiti wangu sijapata maandiko yakionesha Umar akiwataka ushauri wenye rai na mamlaka zaidi ya barua aliyomwandikia Abu Musa al-Ash’ariy kwa kusema: “Nilikusudia kufanya kwamba mtu akimtaliki mke wake talaka tatu katika kikao kimoja ihesabike kuwa ni talaka moja....”72 nayo inafichua azma yake na kusudio lake na si kutaka ushauri, na kama angekuwa anataka ushauri ilikuwa ni bora awatake ushauri Muhajirina na Ansari miongoni mwa Maswahaba waliokuwa wakiishi Madina na wa kwanza wao ni Ali bin Abu Talib, ambaye alikuwa akimtaka ushauri katika matukio mengi nyeti na akiifanyia kazi rai yake. Na wala haraka ya watu haiwi ni kigezo halali cha kukhalifu Kitabu na Sunna, bali ilikuwa ni wajibu kwake kuwazuia watu kwa nguvu wasiendelee na kitendo Iyqadhu Himamu Uwlil-Abswar, Uk. 9. Musnad Ahmad, Juz. 1, Uk. 314, Hadithi ya 2877. 72 Kanzul-Ummal, Juz. 9, Uk. 676, Hadithi ya 27944. 70 71
65
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 65
11/25/2014 4:30:36 PM
TALAKA TATU
chao hicho. Inasihi vipi yeye kuwaadhibu kwa kitendo chao kupitia kitendo ambacho Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) alikiita kuwa ni kukifanyia mchezo Kitabu cha Mwenyezi Mungu?!73 Kisha ni kwamba Ahmad Muhammad Shakir mtunzi wa Nidhamut-Twalaq Fil-Islam ijapokuwa amedhihirisha ushujaa katika mas’ala hii na akatoa fatwa ya kubatilika kabisa kwa talaka tatu zinazotolewa kwa pamoja kwa mpigo na akaweza kung’amua hukumu ya mas’ala hii kutoka kwenye Kitabu na Sunna kwa hoja inayofaa kutiliwa umuhimu, lakini yeye amehalalisha kitendo cha Khalifa kwa hoja ya nguvu, amesema: “Ulazimishaji huu kutoka kwa Umar haukuwa ni kubadilisha hukumu iliyo dhahiri kutoka ndani ya Qur’ani na iliyothibiti kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) ambayo ni kwamba talaka haifuatilizwi na talaka, na kwamba baada ya talaka ya kwanza mwenye kutaliki hana isipokuwa ima kumrejea mke au kutengana naye. Na kadhalika ndivyo ilivyo katika talaka ya pili baada ya kumrejea au kumuoa upya, bali ilikuwa ni lazima inayotokana na hukumu ya kisiasa ya kisharia kwa kutizama maslahi, kutokana na mamlaka aliyowapa Mwenyezi Mungu watawala baada ya kushauriana na wenye mamlaka ambao ni maulamaa, viongozi wa watu na watawa wao. Umar na Maswahaba walitaka kuwazuia watu kutoa talaka holela na kuharakisha kutengana hivyo wakamlazimisha mwenye kutaliki mara tatu katika eda moja aendelee na dhana yake ya kwamba mke wake ametengana naye kwa ile talaka moja (yaani zile tatu za mpigo ni sawa na moja), hivyo wakamzuia kumrejea kwa utashi wake na kumuoa upya mpaka aolewe na mume mwingine, na kwa ajili hiyo Umar alisema: ‘Na hakika yeyote atakayefanya haraka badala ya ustahmilivu wa Mwenyezi Mungu tutamlazimisha (kutenda kwa mujibu wa) talaka hiyo.’ Hivyo akaifanya ni amri ya lazima kutoka kwa Imamu na kutoka kwa wenye mamlaka, na wala hakuifanya kuwa ni hukumu ya kusihi talaka am73
Ad-Durul-Manthur, Juz. 1, Uk. 283. 66
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 66
11/25/2014 4:30:36 PM
TALAKA TATU
bayo haijasihi, kwa sababu hukumu zilizothibiti kwa Kitabu na Sunna ziko wazi na hamiliki yeyote yule haki ya kuzibadilisha au kuwa na hiyari ya kuzifuata hizo au nyinginezo, sawa awe ni mtu binafsi au ni umma uliokongamana.”74 Anajibiwa kuwa: Kwanza mtawala ana wajibu wa kufuata siasa inayofaa kwa ajili ya kuipeleka jamii kwenye lile lenye saada yake na wema wake na kuizuia na uharibifu. Na hivyo adhabu nyingi ndogo ndogo (zisizokuwa Hadi) nyingi zinatokana na mlango huu na ni sharti kabla ya kila kitu jambo hilo liwe ni halali na si haramu. Hivyo haisihi kuwaadhibu watu kwa jambo ambalo halijahalalishwa na sharia. Kutokana na maelezo hayo haiwezekani kitendo cha Umar kuridhia na kupitisha talaka tatu za pamoja kwa mpigo kuhesabika kuwa ni siasa ya kisharia, kwa sababu hii ni moja ya kuwasukuma watu kutenda jambo ambalo wamekatazwa, na Mtume (saww) amewahadharisha nalo na amelihesabu kuwa ni kukichezea Kitabu cha Mwenyezi Mungu pale aliposema tena kwa ghadhabu: “Hivi anachezea Kitabu cha Mwenyezi Mungu na mimi ningali baina yenu?!’ Pili: Kitendo hicho alichofanya Khalifa, kilipokewa na Maswahaba na Tabbiina na waliokuja baada yao kama sharia na si kama hukumu ya adhabu, na kwa ajili hiyo walikichukua ndani ya karne zote mpaka leo hii na hawakukikhalifu isipokuwa wachache miongoni mwa Masunni, kama vile Ibn Taymiyyah katika al-Fatawa alKubra, Ibn al-Qayyim ndani ya Iilamul-Muwaqiin na katika Ighathatul-Luhfani. Ni haki kusemwa: Hakika Khalifa kupitisha na kuridhia aina hii ya talaka kwa sababu yoyote ile iwayo, kumeleta matatizo na madhara katika familia, kwani imekuwa ni sababu ya ndoa kuvunjika katika familia nyingi. 74
Nidhamut-Twalaq Fil-Islam, Uk. 80. 67
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 67
11/25/2014 4:30:36 PM
TALAKA TATU
Na kutokana na hayo tuliyoyataja unadhihirika udhaifu wa sababu aliyoitoa Ibn al-Qayyim al-Jawziyyah katika kuhalalisha kitendo cha Khalifa kwa kusema: “Hakika kauli hii imethibitishwa na Kitabu, Sunna, Qiyas, na Ijmai ya zamani na wala haijakuja baada yake Ijmai nyingine yenye kuibatilisha, lakini Kiongozi wa Waumini Umar (r.a.) aliona kwamba watu wanadharau suala la talaka na wamekithirisha kuitoa kwa tamko moja hivyo akaona ni maslahi kuwaadhibu kwa kuiridhia na kuipitisha dhidi yao ili watambue kwamba ikiwa mmoja wao ataitoa kwa tamko moja mwanamke atatengana naye na atakuwa ni haramu kwake mpaka aolewe na mume mwingine kwa ndoa ya hiyari ya kudumu na si ya kuhalalisha. Hivyo watakapotambua hilo watajizuia kutoa talaka iliyoharamishwa. Hivyo Umar aliona jambo hili lina maslahi kwao katika zama zake, na aliona kwamba utaratibu waliokuwa nao zama za Mtukufu Mtume (saww) na zama za Abu Bakr na mwanzoni mwa ukhalifa wake ulikuwa unafaa zaidi kwao kwa sababu walikuwa hawatoi talaka kiholela na walikuwa wakimcha Mwenyezi Mungu katika talaka, na Mwenyezi Mungu amemuwekea suluhisho kila mwenye kumcha, lakini walipoacha kumcha Mwenyezi Mungu na wakaanza kukichezea Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kutoa talaka kinyume na sharia aliyoiweka Mwenyezi Mungu aliwalazimisha lile walilojilazimisha ili iwe adhabu kwao, kwani hakika Mwenyezi Mungu ameweka talaka mara moja baada ya mara nyingine na wala hajaweka zote kwa pamoja mara moja.”75 Na kutokana na tuliyoyataja unajulikana udhaifu wa maneno ya Ahmad bin Muhammad Shakir hivyo hatutarudia. 3. Talaka tatu zilipitishwa ili kutoa adhabu (hadi) kutokana na uwongo: 75
Iilamul-Muwaqiin, Juz. 3, Uk. 36. 68
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 68
11/25/2014 4:30:36 PM
TALAKA TATU
Na huenda katika kuhalalisha kitendo cha Khalifa wa pili ikasemwa kuwa kuna tofauti baina ya zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) na zama za Khalifa. Katika zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) watu walikuwa katika wema na mafanikio na wanaposema: “Kauli yetu: ‘Nimekutaliki. Nimekutaliki. Nimekutaliki.’ Tulikusudia msisitizo” kauli yao inakubalika, ambapo ni kinyume na zama za Khalifa. Katika zama zake ulienea uharibifu na uwongo hivyo walikuwa wakitumia udhuru ule ule waliokuwa wakiutumia Maswahaba, wakati ambapo sehemu kubwa kati yao walikuwa ni waongo katika kauli yao, hivyo Khalifa hakuwa na budi isipokuwa kuchukua dhahiri ya maneno yao nayo ni talaka tatu za pamoja kwa mpigo. Hoja hii kainukuu Shawkaniy, amesema: “Katika zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) na zama za Abu Bakri watu walikuwa katika ukweli wao na usalama wao na kusudio lao katika tabia na chaguo zuri. Haukudhihiri udanganyifu na uwongo kati yao, na walikuwa wakisema kweli katika kukusudia msisitizo. Katika zama zake Umar alipoona mambo yamedhihiri na hali zimebadilika na imeenea tabia ya kutoa talaka tatu kwa tamko moja lisilokubali tafsiri nyingine aliwalazimisha kufuata talaka tatu katika sura ya msisitizo, kwani (talaka tatu) iligeuka na kuwa kusudio lao, na ameashiria hilo kwa kauli yake: ‘Hakika watu wamefanya haraka katika jambo ambalo walikuwa na ustahmilivu nalo.’” Kisha baada ya kunukuu hoja hii Shawkaniy ameijibu kwa kusema: “Jibu hili kalikubali al-Qurtubiy, na Nawawi amesema: ‘Ni jibu sahihi zaidi kuliko majibu yote, na haifichikani kwamba atakayekuja na tamko linalokubali kuwa la msisitizo kisha akadai kuwa alikusudia msisitizo, dai lake linakubaliwa hata kama ni mwisho wa dahari, itakuwaje katika zama ambazo ndio karne bora na katika zama zinazofuatia?! Na atakapokuja na tamko ambalo halikubali kuwa 69
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 69
11/25/2014 4:30:36 PM
TALAKA TATU
la msisitizo hatakubaliwa dai lake bila kutofautisha baina ya zama moja na nyingine.’”76 Nasema: Hakika utetezi huu – ukiachilia mbali aliyoyataja Shawkani – ni sawa na kuondoa uharibifu kwa kutumia kilicho kiharibifu zaidi, na hakika ameyaongezea maji matope, ambapo mwenye kujibu amejaribu kuhalalisha kitendo cha Khalifa na kumsafisha na makosa hata kama itakuwa ni kwa thamani ya kuvunja heshima ya baadhi ya Maswahaba na Tabiina, ambapo wengi kati yao walikuwa wakirejea kwa Khalifa, inakuwaje anawatuhumu kwa uwongo na udanganyifu?! Na mwishoni tunaleta maneno ya thamani ya Shawkaniy, yeye baada ya kutaja dalili za wenye kusema kuwa talaka tatu za pamoja zinasihi na walivyoitafsiri vingine riwaya ya Ibn Abbas na kutetea kitendo cha Khalifa, amesema: “Ikiwa kufanya hivyo ni kwa ajili ya kwenda sawia na madhehebu ya waliotangulia basi hilo ni jambo duni na dogo mno ambalo halipaswi kutangulizwa mbele ya Sunna tukufu. Na ikiwa ni kwa ajili ya Umar bin Khattab basi ni wapi anakaa masikini huyu mbele ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, ni mwislamu yupi miongoni mwa Waislamu ambaye akili yake na elimu yake inaona ni vizuri kuitanguliza kauli ya Swahaba juu ya kauli ya al-Mustwafa?!”77 Ndiyo, baadhi ya maulamaa wa Kisunni katika zama zetu hizi wameipuuza aina hii ya talaka na kwa ajili hiyo ilibadilika kanuni ya Mahakama Kuu ya Misri ya Kisharia na ikaikhalifu madhehebu ya Hanafi baada ya kupata uhuru kutoka kwa utawala wa Dola ya Uthmaniya. Kama pia ambavyo mamufti kadhaa wa Sunni wameipuuza aina hii ya talaka, katika hili anasema mtunzi wa al-Manari baada ya uchunguzi safi kuhusu mas’ala hii: “Makusudio si kuwajadili waka76 77
Naylul-Awtar, Juz. 6, Uk. 233. Naylul-Awtar, Juz. 6, Uk. 234. 70
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 70
11/25/2014 4:30:36 PM
TALAKA TATU
lidi au kuwazuia makadhi na mamufti kufuata madhehebu zao, hakika wengi wao huyaona maandiko haya katika vitabu vya hadithi na vinginevyo lakini hawayajali, kwa sababu wao hutenda kwa mujibu wa kauli za vitabu vyao na si kwa mujibu wa Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna ya Mtume wake (saww).”78 4. Hukumu hubadilishwa kwa sababu ya maslahi: Ibn al-Qayyim al-Jawziyyah ana maneno marefu katika kuhalalisha kitendo cha Umar kupitisha talaka tatu za pamoja kwa mpigo, katika hilo anategemea ubadilishwaji wa hukumu kwa sababu ya maslahi, na anachanganya mbivu na mbichi, nzima na mbovu, na ufuatao ni muhtasari wa maneno yake, amesema: “Hukumu zina aina mbili: Aina ya kwanza ni ile ambayo haibadiliki kutoka kwenye hali moja iliyonayo, si kwa kulingana na wakati wala sehemu wala Ijtihadi ya Maimamu, kama vile wajibu wa mambo yaliyo wajibu, uharamu wa mambo yaliyo haramu, adhabu kubwa (hadi) iliyowekewa kiwango na sharia kulingana na makosa. Aina ya pili ni ile inayobadilika kulingana na maslahi yanayotokana na wakati, sehemu na hali, kama vile viwango vya adhabu ndogo ndogo, aina ya adhabu hizo na sifa za adhabu hizo – alipofika hapa akaleta mifano mingi kuhusu adhabu ndogo ndogo na akasema -: Na kutokana na hali hiyo yeye Mwenyezi Mungu awe radhi naye – Umar bin Khattab – alipoona watu wamekithirisha idadi katika talaka aliona kuwa wao hawataacha jambo hilo isipokuwa kwa adhabu hivyo akaona ni bora kuwalazimisha kufuata talaka hiyo ili kuwaadhibu na kuwazuia kufanya hivyo, na hiyo ni: Ima ni miongoni mwa adhabu inayojitokeza ambayo hutolewa wakati inapohitajika kufanya hivyo kama alivyokuwa akichapa viboko themanini na kunyoa nywele za kichwa katika unywaji pombe. 78
Tafsirul-Manar, Juz. 2, Uk. 386, Chapa ya tatu, 1376A.H. 71
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 71
11/25/2014 4:30:36 PM
TALAKA TATU
Na ima ni kwa dhana ya kwamba kuzihesabu talaka tatu za pamoja kwa mpigo kuwa ni talaka moja ilifanywa hivyo kisharia kwa sharti lililokuwepo na sasa limeondoka. Na ima ni kwa sababu ya kizuizi kilichojitokeza katika zama zake kilichozuia kuzifanya talaka tatu za pamoja kwa mpigo kuwa talaka moja. – Aliendelea kueleza mpaka akasema:- Kiongozi wa Waumini (Umar) alipoona kwamba Mwenyezi Mungu amemwadhibu aliyetaliki talaka tatu, kwa kuweka kizuizi baina yake na mke wake na akamharamisha mwanamke huyo kwake mpaka aolewe na mume mwingine, (Umar) alijua kuwa adhabu hiyo ni kwa sababu ya kuichukia kwake (Mwenyezi Mungu) talaka iliyoharamishwa, hivyo yeye Kiongozi wa Waumini (Umar) akamuwafiki katika adhabu yake kwa mwenye kutaliki talaka tatu za pamoja kwa mpigo kwa kuzipitisha talaka hizo na kumlazimisha kuzifuata. Ikisemwa: ‘lililokuwa rahisi zaidi ni yeye kuwazuia watu kutoa talaka tatu za pamoja kwa mpigo na awaharamishie jambo hilo na amwadhibu mtendaji wake kwa kumpiga na kumwadabisha ili kwamba kusipatikane athari mbaya zitokanazo na jambo hilo.’ Itasemwa: Ndiyo, Wallahi alikuwa anaweza kufanya hivyo na ndio maana alijutia hilo siku zake za mwisho na akatamani kwamba angefanya hivyo. al-Hafidh Abu Bakri Ismailiy amesema katika Musnad Umar: ‘Alitupa habari Abu Ya’la kuwa: Alitusimulia Swalih bin Malik: Alitusimulia Khalid bin Yazid bin Abu Malik kutoka kwa baba yake, alisema: Umar bin Khattab alisema: ‘Sijawahi kujutia kitu kama ninavyojutia mambo matatu: Kutoharamisha talaka, kutokuwaozesha watumwa na kutowauwa wanawake wenye kuililia maiti kwa sauti.’ Na talaka aliyokusudia kuiharamisha si talaka rejea ambayo Mwenyezi Mungu ameihalalisha na ukajulikana uhalali wake kutoka kwenye dini ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, na wala si talaka ili72
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 72
11/25/2014 4:30:36 PM
TALAKA TATU
yoharamishwa ambayo Waislamu wamekongamana juu ya uharamu wake kama vile talaka inayotolewa wakati wa hedhi na katika tohara aliyoingiliwa, wala si talaka inayotolewa kabla ya kumwingilia, hivyo inabainika kwa yakini kwamba talaka aliyotaka kuiharamisha ni talaka tatu za pamoja zinazotolewa kwa mpigo. – Aliendelea kueleza mpaka akasema:- Na Umar aliona kwamba uharibifu utaondoka kwa kuwalazimisha kutenda kwa mujibu wa talaka ya tatu, lakini ilipobainika kuwa uharibifu haujaondoka kwa kitendo hicho na kwamba jambo hilo halijazidisha isipokuwa shida alieleza kwamba ilikuwa ni bora kuhamia kwenye kuharamisha talaka tatu za pamoja, kuharamisha ambako kutaondoa uharibifu kuanzia kwenye chimbuko lake, na kuondoka kwa uharibifu huu ni kwa jambo kuwa kama lilivyokuwa katika zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww), zama za Abu Bakr na mwanzoni mwa ukhalifa wa Umari.”79 Anajibiwa kuwa: Ama alilosema kuwa hukumu zinagawanyika katika aina mbili hilo ni sahihi, lakini ni wapi amejua kwamba hukumu ya talaka tatu ni katika aina ya pili, kuna tofauti gani baina ya hukumu ya mambo ya wajibu na mambo ya haramu na kauli ya Mwenyezi Mungu: “Talaka ni mara mbili”, na inakuwaje inabadilika hukumu ambayo Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) aliita kuwa ni kuichezea dini? Ama kuhusu dhana tatu alizozitaja ni kwamba dhana ya kwanza ndiyo iliyochukuliwa na ndiyo inayoafikiana na maneno ya Khalifa mwenyewe. Ama dhana mbili za mwisho, yaani kuzihesabu talaka tatu za pamoja kwa mpigo kuwa ni talaka moja ilifanywa hivyo kisharia kwa sharti lililokuwepo na sasa limeondoka, au kwa sababu kilijitokeza kizuizi kilichozuia kuzifanya talaka tatu za pamoja kwa 79
Iilamul-Muwaqiin, Juz.3, Uk. 36, na ameashiria hilo tena katika kitabu chake IghathatulLahfan Min Maswayidis-Shaytan, Juz. 1, Uk. 336. 73
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 73
11/25/2014 4:30:36 PM
TALAKA TATU
mpigo kuwa talaka moja, hazitegemewi na inaonekana sababu iliyosukuma kutasawari dhana hizi mbili ni kule kunyenyekea kwenye mapenzi na kukihalalisha kitendo cha Khalifa kwa namna yoyote ile. 5. Kubadilika hukumu kulingana na mahitaji ya wakati: Hakika hukumu ambazo hubadilika kulingana na kubadilika kwa wakati na mazingira ni zile hukumu ambazo kiini chake kimeainishwa kwa kuzingatia maslahi, na sifa zake na namna yake vimeachwa mikononi mwa mtawala wa Kiislamu. Aina hii ya hukumu hupatwa na mabadiliko, na si zile hukumu ambazo Mwekasharia ameainisha kiini chake, namna yake na (kayfa) yake na hajaacha nafasi ya mtawala wa Kiislamu kuingilia kati. Na hukumu zilizopatikana kuhusu hali za watu ni katika aina hii ya hukumu, hivyo mtawala hana haki ya kuingilia katika hukumu za nasaba, ukwe, kunyonya na idadi. Hana haki ya kuharamisha lile alilohalalisha Mwenyezi Mungu au kinyume chake eti kwa kumwadhibu mkosefu, bali hizo ni hukumu zilizothibiti, hazikubali rai ya mtawala au mwingine yeyote. Ama zile hukumu ambazo inaruhusiwa kwa mtawala kuingilia kati ni zile ambazo sifa zake na namna yake vimeachwa mikononi mwa mtawala ili alinde maslahi ya Uislamu na Waislamu kulingana na mazingira yaliyopo yanavyohitaji, na ifuatayo ni idadi ndogo ya mifano yake ili zisichanganyikane: a.
Katika upande wa mahusiano ya kidiplomasia kati ya nchi na nchi ni wajibu kwa dola ya Kiislamu kuchunga maslahi ya Uislamu na Waislamu, huu ni msingi uliothibiti na ni kanuni kuu. Ama namna ya kuchunga maslahi hayo inatofautiana kulingana na mazingira ya wakati na sehemu. Kuna mara maslahi yanahitaji amani na muwafaka na kufanya sulhu na adui, na mara nyingine yanahitaji jambo 74
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 74
11/25/2014 4:30:36 PM
TALAKA TATU
dhidi ya hayo. Na ni hivyo yanatofautiana maamuzi na hukumu makhususi katika upande huu kulingana na kutofautiana mazingira, lakini hukumu hizo hazitoki nje ya duara la kanuni kuu ambayo ni kuchunga maslahi ya Uislamu na Waislamu kama kauli ya Mwenyezi Mungu isemavyo: “Na Mwenyezi Mungu hatawafanyia makafiri njia ya kuwashinda waumini.”80 “Mwenyezi Mungu hawakatazi kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakuwapiga vita, wala hawakuwatoa makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu. Hakika Mwenyezi Mungu anawakataza kufanya urafiki na wale tu waliowapiga vita, na wakawatoa makwenu, na wakasaidia katika kufukuzwa kwenu. Na wanaowafanya hao marafiki basi hao ndio madhalimu.” (Surat Al-Mumtahana 60: 8 – 9).
80
b.
Mahusiano ya kibiashara baina ya nchi na nchi: Masilahi yanaweza kuhitaji kuweka makubaliano ya kiuchumi na kuanzisha mashirika ya kibiashara au taasisi za viwanda kwa kushirikiana baina ya Waislamu na wasiokuwa wao. Na pia maslahi yanaweza kuhitaji jambo kinyume na hayo. Na kutokana na mlango huu mwanafiqhi na Imam, Mwenyezi Mungu amsamehe, Sayyid Shirazi alitoa fatwa ya kuharamisha uvutaji wa sigara ili kuzuia utekelezwaji wa makubaliano ya kiuchumi ambayo yalifikiwa katika zama zake baina ya Iran na Uingereza, kwa kuwa makubaliano hayo yalikuwa yanadhulumu haki za umma wa Kiislamu wa Wairan, kwa sababu yaliipa Uingereza haki ya kulimbikiza tumbaku ya Iran.
c.
Kutetea hadhi ya Uislamu na kulinda uhuru wa nchi na mipaka yake dhidi ya maadui, ni kanuni iliyothibiti
Sura Nisai: 141. 75
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 75
11/25/2014 4:30:36 PM
TALAKA TATU
isiyobadilika, makusudio ya juu kabisa ya Mwekasharia ya Uislamu ni kulinda utukufu dhidi ya hatari ya maadui na madhara yao, na kwa ajili hiyo akawajibisha kutafuta nguvu ya mapambano na kuandaa jeshi imara lisilorudi nyuma, kama anavyosema Mwenyezi Mungu: “Na waandalieni nguvu kama vile muwezavyo na kwa farasi waliofungwa, ili mumtishe adui wa Mwenyezi Mungu na adui yenu, na wengineo msiowajua nyinyi, Mwenyezi Mungu anawajua. Na chochote mtakachotoa katika njia ya Mwenyezi Mungu, mtarudishiwa, wala nyinyi hamtadhulumiwa.� (Surat Al-Anfal 8:60). Huu ndio msingi uliothibiti katika Uislamu ambao unaungwa mkono na akili na maumbile. Ama namna ya kujitetea na mbinu zake na aina ya silaha au ulazima wa kutumikia jeshi au kutotumikia, hayo yote yameachwa kwenye mazingira ya wakati, hivyo yanabadilika kulingana na kubadilika kwa mazingira hayo. Lakini ni ndani ya kanuni kuu, katika Uislamu hakuna msingi uliothibiti hata wa mas’ala moja unaolazimisha uaskari wa lazima wa kujitolea, ambao umekuwa ni miongoni mwa mambo ya asili katika nchi nyingi. Na tunaloliona katika vitabu vya fiqhi la kutenga milango au kuweka faslu makhususi za hukumu za mashindano ya mbio au ya kurusha mishale na mingineyo miongoni mwa aina za ushujaa ambazo zilikuwa zinajulikana katika zama zilizopita, ikiwa ni pamoja na kunukuliwa hadithi kutoka kwa Mtukufu Mtume (saww) na Maimamu (as) katika milango hiyo, yote hayo hukumu zake si za asili zilizothibiti katika Uislamu ambazo sharia imeziweka kwa sura ya msingi usiobadilika bali ilikuwa ni aina mojawapo ya kutabakisha hukumu hiyo (ya kutetea hadhi ya Uislamu na kulinda uhuru wa nchi na mipaka yake dhidi ya maadui). Lengo lilikuwa ni kukusanya 76
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 76
11/25/2014 4:30:36 PM
TALAKA TATU
nguvu za kutosha dhidi ya adui katika zama hizo. Ama hukumu zinazopasa kutabikishwa katika zama hizi zenyewe zinapasa kulingana na mazingira ya wakati husika.81 Hivyo ni wajibu kwa mtawala wa Kiislamu kulipa nguvu jeshi lake na vikosi vyake vya usalama kwa njia ambazo kwazo litaweza kulinda Uislamu na Waislamu dhidi ya hatari, na litaweza kulingana na mahitaji ya wakati kuzuia kila aina ya njama zinazofanywa na maadui dhidi yake. Na Mwekasharia ambaye anataka kanuni Yake idumu na nidhamu aliyokuja nayo iendelee hapaswi kugusia vipengele vya mambo na matawi yake bali anapaswa kuweka misingi na kanuni kuu ili kanuni zake zikusanye zama zote kwa sura na nmna zake tofauti, na kama atapita njia isiyokuwa hii basi kudumu kwake ni kudogo sana. d.
81
Kueneza elimu na maarifa na kukamilisha maarifa ambayo yatatoa dhamana ya jamii kutukuka kimada na kiroho inazingatiwa kuwa ni miongoni mwa faradhi za Uislamu. Ama kutimiza hilo na kuiainisha aina yake na aina ya nyenzo zake ni jambo lisilofungwa na mpaka maalumu, bali jambo hilo linaachwa kwenye mtazamo wa mtawala wa Kiislamu. Na maamuzi yamo mikononi mwake kulingana na uwezo uliopo na kwa mwangaza wa kanuni zilizothibiti. Na kwa muhtasari ni kwamba Uislamu umewalazimisha wasimamizi wa Waislamu na wenye madaraka kueneza elimu baina ya wanadamu na kung’olea mbali ujinga baina yao na kupambana na kila aina ya umbumbumbu. Ama kuhusu aina ya elimu na sifa zake hayo yote yameachwa kwenye mtazamo wa mtawala wa Kiislamu na yeye ndiye atakayejua mahitaji
  Muhaqiq amesema katika kitabu Ashara’iu, uk. 152, Faida ya mashindano ya kukimbia na kutupa mishale ni kuipa nafsi maandalizi ya kupigana na kupata uwezo wa kulenga shabaha, jambo hilo ni muamala sahihi. 77
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 77
11/25/2014 4:30:36 PM
TALAKA TATU
ya zama zake. Huenda sayansi haikuwa lazima katika zama zilizopita kwa kutokuwa na haja nayo, lakini hivi leo imekuwa ni ya kwanza katika elimu za lazima zenye wema wa jamii kama vile uchumi na siasa. e.
Kulinda nidhamu na usalama na kunadhimu mambo ya ndani na kuinua kiwango cha uchumi n.k. ni miongoni mwa mambo ya dharura, hayo na mfano wake yote yanafuata mazingira na mahitaji na Uislamu hauna hukumu makhususi isiyobadilika inayofuatwa katika hayo, bali unalolitaka Uislamu ni kufika kwenye malengo haya na kuyatimiza kwa nyenzo zinazowezekana bila kuiainisha aina ya nyenzo hizi bali hilo limeachwa kwenye uwezo wa wakati ambao humo anaishi mwanadamu, na yote hayo ni chini ya mwangaza wa kanuni kuu.
f.
Uislamu umekuja na kanuni thabiti isiyobadilika katika medani ya mali, nayo ni kauli ya Mwenyezi Mungu:
“Wala msile mali zenu baina yenu kwa batili na kuzipeleka kwa mahakimu ili mpate kula sehemu ya mali ya watu kwa dhambi, na hali mnajua.” (Sura al-Baqarah: 188). Na kwa msingi wa kanuni hii mafaqihi wameng’amua sharti la kusihi kwa makubaliano ya kuuza au muamala, wakasema: ‘Ili muamala usihi ni sharti kuwepo na faida inayokubalika kisharia, la sivyo muamala huo hausihi.’ Na kuanzia hapa ndipo wakaharamisha kuuza damu na kuinunua. Isipokuwa ni kwamba hukumu ya kuuza damu na kuinunua katika Uislamu si hukumu thabiti isiyobadilika bali uharamu wake ulitokana na kwamba katika zama zilizopita uuzaji wake ulikuwa na sura ile iliyozungumziwa na Aya wa kuharamisha kula mali kwa batili. Na ilikuwa kuuza damu katika zama hizo ni mfano halisi wa kitendo hicho cha kula mali kwa batili, hivyo hukumu inataza78
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 78
11/25/2014 4:30:36 PM
TALAKA TATU
ma uwepo wa faida ambayo itautoa muamala huo kutoka kwenye kuwa ni kula mali kwa batili, na kutopatikana faida ambayo itautoa muamala huo kutoka kwenye kuwa ni kula mali kwa batili, hivyo kama itapatikana faida inayokubalika kiakili katika kuuza damu na kuinunua basi hukumu ya uharamu itabadilika na kuwa halali, na hukumu thabiti hapa ni kauli ya Mwenyezi Mungu: “Wala msile mali zenu baina yenu kwa batili” (ambayo ndio kanuni kuu). Na kwa madhumuni haya imepokewa kwamba Ali (as) aliulizwa kuhusu kauli ya Mtukufu Mtume (saww): “Zigeuzeni mvi wala msijifananishe na Mayahudi.” Akasema (as): “Hakika kweli alisema hayo wakati ambao Dini ilikuwa na watu wachache, ama hivi sasa, imepanuka na kuenea na kuwa na nguvu, basi mtu ana hiyari.”82 Basi kwa kuwa hukumu ya kusihi kwa talaka tatu za pamoja zinazotolewa kwa mpigo ni yenye kuleta uharibifu muda wote wa historia, Ibn al-Qayyim pamoja na kuhalalisha kitendo cha Khalifa kwa aliyoyataja lakini amebainisha athari mbaya iliyotokana na hukumu hiyo na ilivyowafurahisha maadui wa dini, nasi hapa tunakunukulia maelezo ya maneno yake.
82
Nahjul-Balaghah, Hekima ya 16. Tazama kitabu chetu Mafahimul-Qur’an, Juz. 3, Uk. 265 – 275. 79
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 79
11/25/2014 4:30:37 PM
TALAKA TATU
MALIPO YA KUCHEPUKA NJIA KUU
H
akika Ibn al-Qayyim – kama ulivyojua – alikuwa miongoni mwa watetezi wakubwa wa fatwa za Khalifa na amehalalisha hukumu yake kwa kudai kuwa maslahi ya wakati huo yalikuwa yanahitaji kuchukua lile alilojilazimisha mwenyewe mwenye kutaliki. Na bila shaka umeshajua udhaifu wa utetezi wake na udhaifu wa maneno yake lakini yeye mwishoni mwa maneno yake ametaja kwamba maslahi yaliyopo katika zama zetu hizi ni kinyume na ilivyokuwa katika zama za Khalifa, na kwamba kukubali usahihi wa talaka tatu za pamoja kwa mpigo kunaleta matatizo kwa Waislamu katika mazingira yetu na sehemu zetu, na imekuwa ni sababu ya maadui kuidhihaki dini na wanadini, na kwamba ni wajibu katika zama zetu hizi kuchukua uchungu wa Kitabu na Sunna, nao ni kwamba haisihi isipokuwa talaka moja. Lakini ameghafilika na lile ambalo ndio haki katika mada hii na kwamba maslahi katika zama zote yalikuwa katika namna moja na kwamba mipaka aliyoiweka Mwenyezi Mungu ndio inayolingana na maslahi ya waja na hatima yao, na kwamba ubaya na dhihaka aliyoitaja Ibn al-Qayyim al-Jawziyyah mambo hayo yametokana na kitendo cha kuchepuka njia kuu na kufanya Ijtihadi mkabala na maandiko bila kuwepo dharura inayolazimu kuhama na bila kuwepo matatizo au shida, na kwa ajili hiyo tunaleta maneno yake ili yawe mazingatio kwa yule anayetaka kuchezea hukumu za kisharia kwa madai ya hoja hizi katika zama zetu hizi. Yafuatayo ni maelezo ya maneno yake: “Mas’ala hii ni miongoni mwa mas’ala ambazo fatwa zake zilibadilika kulingana na wakati, ama katika zama zetu hizi ambazo ndoa 80
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 80
11/25/2014 4:30:37 PM
TALAKA TATU
zimeshtaki kwa Mola Wake kutokana na madhara ya kuhalalisha na ubaya unaotendwa na wenye kuhalalisha, jambo ambalo ni matongotongo bali ni upofu katika jicho la dini na ni mfupa katika koo za Waumini, kutokana na mabaya yake yenye kuwafurahisha maadui wa dini na yenye kuwazuia wengi wenye kutaka kuingia katika dini, ambapo ulimi hauwezi kueleza kwa undani wala kitabu hakiwezi kuudhibiti, hakika (katika zama zetu hizi) waumini wote wanaiona mas’ala hii kuwa ni katika mambo mabaya zaidi na wanaihesabu kuwa ni miongoni mwa fedheha kubwa, ambapo imebadili sura ya dini na jina lake, na beberu la kuazima83 limemnenepesha mtalikiwa kwa najisi ya kuhalalisha, huku likidai kuwa limemsafisha kwa ajili ya halali. Oh ajabu iliyoje! Ni usafi gani aliourudisha huyu beberu maluuni?! Na ni maslahi yapi aliyomtimizia yeye na mtaliki wake (mume wa kwanza) kupitia kitendo hiki duni?! “Unamuona mume mtaliki au walii amesimama mlangoni huku beberu maluuni likiwa limemvua (mwanamke) nguo zake na kuondoa nikabu yake na kumfanya sehemu ya starehe, na mume au walii anaita: ‘Chakula hiki hujapewa ili ushibe, hakika wewe, mke, sisi, mashahidi, waliohudhuria, malaika waandishi na Mola wa walimwengu, sote tunajua fika kwamba hakika wewe si miongoni mwa waume, wala mwanamke au walii wake hawana radhi wala furaha na wewe, bali wewe ni sawa na beberu la kuazima kwa ajili ya kupanda, ambapo kama isengekuwa balaa hili tusingekuridhia kusimama mlangoni.’ 83
Mwanamume anayemuoa mwanamke aliyetalikiwa talaka tatu za kisharia kwa lengo na dhamira ya kuhalalisha mwanamke huyo kuolewa na mume wake wa kwanza, mwanamume wa namna hiyo ameitwa na Mtume (saww) kuwa ni BEBERU LA KUAZIMA, kama ilivyokuja katika hadithi kadhaa. Na sababu ya kuitwa hivyo ni kwamba mmiliki wa mbuzi huazima beberu si kwa lengo la kummiliki bali ni ili awapande mbuzi wake, kadhalika mwanaume mwenye kuhalalisha humuoa mwanamke husika si kwa kumpenda na kwa kutaka kuishi naye bali yeye huazimwa na ndugu wa mke ili ampande binti yao kwa dhamira ya kumhalalishia mume wa kwanza – Mtarjumi. 81
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 81
11/25/2014 4:30:37 PM
TALAKA TATU
“Watu huidhihirisha ndoa na huitangaza kwa furaha na nderemo lakini sisi tunausiana kuficha gonjwa lisilopona na tunalifanya ni jambo la kufunikwa bila kaswida wala dufu, bila ndugu wala tangazo, bali tunausiana ufichaji na usiri. Na ijapokuwa mwanamke huolewa kwa dini yake, nasaba yake, mali yake na uzuri wake lakini beberu la kuazima haliulizi chochote kuhusu hayo, kwa sababu hatoishi naye bali amekuja kumhalalisha. Mwenyezi Mungu amemfanya kila mmoja kati ya mume na mke kuwa tulizo kwa mwenzake na ameweka baina yao mapenzi na huruma ili kwa njia hiyo yapatikane makusudio ya mkataba huu adhimu, na kwa njia hiyo yatimie maslahi ambayo kwa ajili yake Mtukufu Mwenye hekima ameweka sharia ya ndoa. Hebu sasa liulize beberu la kuazima: ‘Je lina fungu lolote katika hayo? Na je hekima ya mkataba huu, makusudio yake na maslahi yake ni yeye kuwa ajnabi wa kambo?!’ Na liulize: ‘Je amemfanya mwanamke huyu kuwa ni halali kwake na kitanda cha kulalia? Na je mwanamke amemridhia kuwa mume wake na tegemeo lake wakati wa matatizo yake?’ “Na waulize watambuzi wa mambo na wenye akili: ‘Je fulani kaolewa na fulani?! Na je katika sharia, kiakili na kwa maumbile ya mwanadamu, jambo hili huhesabika kuwa ni ndoa? Na inakuwaje Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) amlaani mtu kutoka katika umma wake ikiwa kafunga ndoa sahihi kisharia na hajatenda jambo lolote la haramu wala baya katika ufungaji wa ndoa yake?! Na itakuwaje amshabihishe na beberu la kuazima ilihali yeye ni miongoni mwa watu wema?! Na imekuwaje ndoa hiyo imekuwa ni aibu kwa mwanamke baina ya ndugu zake na jirani zake katika kipindi chote cha maisha yake kiasi cha kuinamisha kichwa chake pindi linapotajwa beberu hilo baina ya wanawake?!’ 82
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 82
11/25/2014 4:30:37 PM
TALAKA TATU
“Na liulize beberu la kuazima: ‘Je lilifikiria wakati wa ndoa hii ambayo ni ndugu wa unafiki, kuhusu matunzo, au mavazi au kiwango cha mahari?! Na je mwanamke huyo alitamani chochote kati ya hayo, au je alitafakari chochote kuhusu hayo?! Na je aliomba kutoka kwake mtoto mwema na kumfanya familia na kipenzi?!’ Na ziulize akili za walimwengu na maumbile yao: ‘Walio bora katika umma huu ni wale wengi wa kuhalalisha? Na je mhalalishaji ambaye amelaaniwa na Mwenyezi Mungu na Mtume Wake ndiye mwongofu zaidi?’ Na liulize beberu la kuazima: ‘Je kuna yeyote kati yao wawili aliyejipamba kwa ajili ya mwenzake kama wanavyojipamba wanaume kwa ajili ya wanawake na wanawake kwa ajili ya wanaume? Au je kuna yeyote kati yao mwenye kuvutiwa na mwenzake kwa sababu ya nasaba au mali au uzuri?’ Na muulize mwanamke: ‘Je anachukia kuolewa na beberu hili la kuazima au anafurahia? Au je anachukia kuona kuna mwanamke mwingine anakuwa chini ya beberu hili? Au kuona mwanamke huyo analiuliza kuhusu mali yake, kazi yake, maisha yake na uwezo wa kuhudumia kwake?!’ “Na liulize beberu la kuazima: ‘Je liliulizia yale ambayo huulizia mwenye kukusudia kweli kuoa au lilipitia njia ya mashemeji kwa zawadi na hadaya na njia ya pesa ambayo huitumia mchumba mdanganyifu?’ Na muulize: ‘Je yeye ni baba mchukuaji au ni baba mtoaji? Na je kauli yake wakati wa kusoma abjedi za mkataba huu huwa ni chukua matumizi ya harusi hii au acha?’ Na liulize: ‘Je kauli: Chukua matumizi ya harusi hii au acha imebeba mzigo wa ndoa hii?’ Na muulize kuhusu walima wa harusi yake: ‘Je amefanya walima angalau hata kwa mbuzi? Na je amemwalika yeyote kati ya maswahiba zake na akamtimizia haki yake na kumpa?’ Na muulize: ‘Je amevumilia kutokana na mzigo wa ndoa hii yale ambayo huvumilia wenye kuoa, au wamemjia maswahiba na watoa pongezi? Na je aliambiwa: Mwenyezi Mungu awabariki ninyi wawili na awakusanye katika kheri na afya? Au Mwenyezi Mungu 83
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 83
11/25/2014 4:30:37 PM
TALAKA TATU
amemlaani mwenye kuhalalisha na mwenye kuhalalishiwa laana kamilifu?’”84 Anajibiwa kuwa: Hakika aibu ambayo – Ibn al-Qayyim anadai kuwa – imeufika Uislamu, imetokana na kitendo cha kukubali talaka tatu za pamoja kwa mpigo na kuihesabu talaka moja kuwa ni talaka tatu. Ama kanuni iliyowekwa na sharia ya usahihi wa ndoa baada ya talaka ya tatu kutegemea mhalalishaji yenyewe ni miongoni mwa kanuni zake tukufu na bora, imara na makini haina aibu juu ya Uislamu kamwe, hiyo ni kwa sababu: Kwanza: Inamzuia mume kutoa talaka ya tatu kwa kuwa anajua kwamba baada ya talaka hiyo kumuoa kwake mwanamke huyo kunategemea uhalalishaji ambao hauvumiliwi na wanaume wengi. Pili: Hafanyi hivyo isipokuwa anapokata tamaa ya kuoa mke mpya, kwa sababu uzoefu wenye kujirudia umethibitisha kuwa wanandoa hawako katika namna moja upande wa maadili na mambo ya kiroho, hivyo mtu hamuoi tena mtalaka wake (aliyemtaliki talaka tatu za kisharia) isipokuwa baada ya kukata tamaa ya kuoa mke mpya, na ni mara chache sana kama si nadra kabisa kutokea mtu kuanza maisha upya na mke ambaye alimtaliki talaka tatu za kisharia, hivyo kwa mazingira hayo haja ya kuhitaji mhalalishaji inapungua sana, na hii ni kinyume na pindi talaka moja inapokubaliwa kuwa ni talaka tatu sahihi. Mara nyingi katika hali hii mume hujutia talaka na hutaka kujenga upya nyumba ambayo aliibomoa kwa talaka na kama ilivyo hutegemea mhalalishaji ambaye huwaletea aibu na kupatwa na yale aliyoyataja Ibn al-Qayyim al-Jawziyyah katika maneno yake marefu. Na katika maneno yake kuna maeneo mengine yanahitaji maelezo tumeyaacha hasa katika taswira yake ya kwamba mha84
Iilamul-Muwaqiin, Juz.3, Uk. 41 - 43, na tazama Ighathatul-Luhfan, Juz. 1, Uk. 312. 84
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 84
11/25/2014 4:30:37 PM
TALAKA TATU
lalishaji ni kama mwajiriwa kwa ajili ya kuhalalisha na kwamba anaoa kwa lengo hilo, nayo ni taswira ya kimakosa sana, bali yeye anaoa kwa lengo lilelile analoolea wanawake wengine, isipokuwa ni kwamba kama atamtaliki mke wake kwa hiyari yake atakuwa ni halali kwa mume wake wa kwanza, wapi na wapi hilo na lililokuja katika maneno yake?!
85
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 85
11/25/2014 4:30:37 PM
TALAKA TATU
ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION 1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9. 10. 11. 12. 13. 14. 15. 16. 17. 18. 19. 20. 21. 22. 23. 24. 25. 26. 27.
i) Qur’ani Tukufu – Pamoja na Tarjuma ya Kiswahili ii) Qur’an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Thelathini Uharamisho wa Riba Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili Hekaya za Bahlul Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.) Hijab vazi Bora Ukweli wa Shia Ithnaashari Madhambi Makuu Mbingu imenikirimu Abdallah Ibn Saba Khadijatul Kubra Utumwa Umakini katika Swala Misingi ya Maarifa Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia Bilal wa Afrika Abudhar Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu Salman Farsi Ammar Yasir Qur’an na Hadithi Elimu ya Nafsi Yajue Madhehebu ya Shia Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur’an Tukufu Al-Wahda 86
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 86
11/25/2014 4:30:37 PM
TALAKA TATU
28. 29. 30. 31. 32. 33. 34. 35. 36. 37. 38. 39. 40. 41. 42. 43. 44. 45. 46. 47. 48. 49. 50. 51. 52. 53. 54. 55. 56. 57. 58. 59. 60.
Ponyo kutoka katika Qur’an Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii Mashukio ya Akhera Al Amali Dua kwa Mujibu wa Ahlulbayt (a.s) Udhuu kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna Haki za wanawake katika Uislamu Mwenyezi Mungu na sifa zake Kumswalia Mtume (s) Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) Adhana Upendo katika Ukristo na Uislamu Qur’ani na Kuhifadhiwa Kwake Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu Kupaka juu ya khofu Kukusanya Sala Mbili Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Kusujudu juu ya udongo Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s) Tarawehe Malumbano baina ya Sunni na Shia Kupunguza Swala safarini Kufungua safarini Umaasumu wa Manabii Qur’an Yatoa Changamoto as-Salaatu Khayrun Mina -’n Nawm Uadilifu wa Masahaba Dua e Kumayl Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mtume Muhammad (s) 87
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 87
11/25/2014 4:30:37 PM
TALAKA TATU
61. 62. 63. 64. 65. 66. 67. 68. 69. 70. 71. 72. 73. 74. 75. 76. 77. 78. 79. 80. 81. 82. 83. 84. 85. 86. 87. 88. 89. 90. 91. 92. 93.
Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili Kuzuru Makaburi Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita Tujifunze Misingi Ya Dini Sala ni Nguzo ya Dini Mikesha Ya Peshawar Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu Ubora wa Imam ‘Ali na Ushia ndio njia iliyonyooka Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake Liqaa-u-llaah Muhammad (s) Mtume wa Allah Amani na Jihadi Katika Uislamu Uislamu Ulienea Vipi? Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) Dhana ya Ndoa ya Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) Urejeo (al-Raj’ah) Mazingira Utokezo (al - Badau) Hukumu ya kujenga juu ya makaburi Swala ya maiti na kumlilia maiti Uislamu na Uwingi wa Dini Mtoto mwema Adabu za Sokoni Na Njiani Johari za hekima kwa vijana Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu 88
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 88
11/25/2014 4:30:37 PM
TALAKA TATU
94. 95. 96. 97. 98. 99. 100. 101. 102. 103. 104. 105. 106. 107. 108. 109. 110. 111. 112. 113. 114. 115. 116. 117. 118. 119. 120. 121. 122. 123. 124. 125. 126.
Tawasali (AT- TAWASSUL) Imam Mahdi katika Usunni na Ushia Hukumu za Mgonjwa Sadaka yenye kuendelea Msahafu wa Imam Ali (as) Maimamu wa Ahlul Bait – Ujumbe na Jihadi Idi Al-Ghadir Kusoma sura zenye Sijda ya wajibu Hukumu zinazomuhusu mkuu wa kazi na Mfanyakazi Huduma ya Afya katika Uislamu Sunna za Nabii Muhammad (saww) Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza) Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili) Shahiid Mfiadini Mwanamke Na Sharia Ujumbe -Sehemu ya Kwanza Ujumbe - Sehemu ya Pili Ujumbe - Sehemu ya Tatu Ujumbe - Sehemu ya Nne Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu Hadithi ya Thaqalain Ndoa ya Mutaa Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza Ukweli uliopotea sehemu ya Pili Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu Ukweli uliopotea sehemu ya Nne Ukweli uliopotea sehemu ya Tano Mkutano wa Maulamaa wa Baghdad Safari ya kuifuata Nuru Fatima al-Zahra Myahudi wa Kimataifa Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi Visa vya kweli sehemu ya Kwanza 89
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 89
11/25/2014 4:30:37 PM
TALAKA TATU
127. 128. 129. 130. 131. 132. 133. 134. 135. 136. 137. 138. 139. 140. 141. 142. 143. 144. 145. 146. 147. 148. 149. 150. 151. 152. 153. 154. 155. 156. 157. 158. 159.
Visa vya kweli sehemu ya Pili Elimu ya Ghaibu ya Maimamu Mwanadamu na Mustakabali wake Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Kwanza) Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Pili) Khairul l’Bariyyah Uislamu na mafunzo ya kimalezi Vijana ni Hazina ya Uislamu Adhana ni Ndoto au ni Wahyi? Tabaruku Saada Kamili – Kitabu cha Kiada cha Maadili Vikao vya furaha Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje? Visa vya wachamungu Falsafa ya Dini Kuhuzunika na Kuomboleza Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah Mjadala wa Kiitikadi Kuonekana kwa Allah Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza) Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili) Ndugu na Jirani Ushia ndani ya Usunni Maswali na Majibu Mafunzo ya hukmu za ibada Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 1 Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 2 Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 3 Abu Huraira Vipengee kadhaa katika Swala ya Jamaa na Msikiti. Mazingatio kutoka katika Qur’an - Sehemu ya Kwanza Mazingatio kutoka kaitka Qur’an - Sehemu ya Pili Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya kwanza 90
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 90
11/25/2014 4:30:37 PM
TALAKA TATU
160. 161. 162. 163. 164. 165. 166. 167. 168. 169. 170. 171. 172. 173. 174. 175. 176. 177. 178. 179. 180. 181. 182. 183. 184. 185. 186. 187. 188. 189. 190. 191. 192.
Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya Pili Shia na Qur’ani – Majibu na Maelezo Falsafa ya Mageuzi ya Imam Husein (a.s) Amali za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani Elimu ya Tiba za Kiislamu - Matibabu ya Maimamu Uislamu Safi Majlisi za Imam Husein Majumbani Je, Kufunga Mikono Uislam wa Shia Amali za Makka Amali za Madina Asili ya Madhehebu katika Uislamu Sira ya Imam Ali kuhusu Waasi Ukweli uliofichika katika neno la Allah Uislamu na Mifumo ya Uchumi Umoja wa Kiislamu na Furaha Mas’ala ya Kifiqhi Jifunze kusoma Qur’ani as-Sahifatul Kamilah as-Sajjadiyyah Hayya ‘Alaa Khayri’l-’Amal Katika Adhana Ukweli kuhusu Funga ya Siku ya Ashura Dua za Miezi Mitatu Mitukufu (Rajabu, Shaabani na Ramadhani) Uadilifu katika Uislamu Mahdi katika Sunna Maswali Ya Uchunguzi Kuhusu Uislam Kazi na Bidii ni njia ya maendeleo Abu Talib – Jabali Imara la Imani Ujenzi na Utakaso wa Nafsi Vijana na Matarajio ya Baadaye Historia maana na lengo la Usalafi Ushia – Hoja na Majibu Mateso ya Dhuria wa Mtume (saww) Maombolezo – Msiba wa Bwana wa Mashahidi (a.s.) 91
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 91
11/25/2014 4:30:37 PM
TALAKA TATU
193. 194. 195. 196. 197. 198. 199. 200. 201. 202. 203. 204. 205. 206. 207. 208. 209. 210. 211. 212. 213. 214. 215. 216. 217. 218. 219. 220.
Shahidi kwa Ajili ya Ubinadamu Takwa Upotoshaji Dhahiri katika (Turathi) Hazina ya Kiislamu Amirul Muuminina (‘as) na Makhalifa Tawhiid Na Shirki katika Qur’ani Tukufu Kuvunja hoja iliyotumika kutetea Uimamu wa AbuBakr Adabu za vikao na mazungumzo Hija ya Kuaga Uwazi baina ya Maslahi na Vikwazo Fadhila za watukufu watano katika Sahih Sita Mdahalo baina ya Mwanachuoni wa Kisunni na Kishia (Al- Muraja’aat) Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (as) Imam Husain ni Mfumo wa Marekebisho na Mageuzi Mtazamo kuhusu msuguano wa Kimadhehebu Nchi na Uraia – Haki na wajibu kwa Taifa Mtazamo wa Ibn Taymiyyah juu ya Imam Ali (as) Uongozi wa Kidini – Maelekezo na Utekelezaji wa Kijamii Maadili ya Ashura Mshumaa – Shahidi na Kifo cha Kishahidi Mizani ya Hekima – Hadithi za Ahlul Bait (as) – Sehemu ya Kwanza Imam Ali (as) na Mambo ya Umma Imam Ali (as) na Mfumo wa Usawa Uimamu na Tamko la Kutawazwa Mfumo wa Wilaya Vipi Tutaishinda Hofu? Kumswalia Mtume ni Ufunguo wa Utatuzi wa Matatizo Maeneo ya Umma na Mali Zake Nahju ‘L-Balagha – Majmua ya Khutba, Amri, Barua, Risala, Mawaidha na Semi za Amirul-Muuminin Ali bin Abu Talib (a.s.) 221. Mukhtar – Shujaa aliyelipiza kisasi dhidi ya wauaji wa Imam Husein (as) hapo Karbala 222. Mazingatio Katika Swala 223. Imam Hasan na Mfumo wa Kujenga Jamii 92
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 92
11/25/2014 4:30:37 PM
TALAKA TATU
224. Vyakula Na Vinywaji 225. Kuelewa Rehema ya Mwenyezi Mungu 226. Tiba ya Maradhi ya Kimaadili 227. Yafaayo kijamii 228. Shia Na Hadith - Majibu na Maelezo 229. Mkakati wa Kupambana na Ufakiri 230. Mtazamo Mpya - Wanawake katika Uislamu 231. Taqiyya Kwa Mujibu Wa Sheria Ya Kiislamu 232. Imam Mahdi Na Bishara Ya Matumaini 233. Jihadi 234. Majanga Na Jukumu La Jamii 235. Muhadhara wa Maulamaa 236. Mashairi ya Kijamii 237. Ngano ya kwamba Qur’ani imebadilishwa 238. Mwanamke Katika Harakati za Mageuzi 239. Shia Na Sahaba - Majibu na Maelezo 240. Yusuf Mkweli 241. Hotuba Za Kiislamu na Haki Za Binadamu 242. Ugaidi wa Kifikra katika Medani ya Kidini 243. Imam Mahdi (as) – Imam wa zama hizi na Kiongozi wa Dunia 244. Imam Mahdi (as) ni Tumaini la Mataifa 245. Imam Husein (as) ni Utu na Kadhia 246. Talaka Tatu 247. Uswalihina Dhahiri na Batini yake 248. Upotofu ndani ya kitabu cha mitaala kwa Shule za Sekondari juu ya Uislamu 249. Imam Husein (as) ni Kielelezo cha kujitoa Muhanga na Fidia 250. Uislamu wa Shia
93
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 93
11/25/2014 4:30:37 PM
TALAKA TATU
KOPI NNE ZIFUATAZO ZIMETAFSIRIWA KWA LUGHA KINYARWANDA 1. 2. 3. 4.
Amateka Ya Muhammadi (s.a.w.w) Na Aba’ Khalifa Nyuma yaho naje kuyoboka Amavu n’amavuko by’ubushiya Shiya na Hadithi
ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION KWA LUGHA YA KIFARANSA 1.
Livre Islamique
94
42_14_TALAKA_25_Nov_2014.indd 94
11/25/2014 4:30:37 PM