TAQIYYA KWA MUJIBU WA SHERIA YA KIISLAMU
Kimeandikwa na: Shaikh Abdul-Karim al-Bahbahani
Kimetarjumiwa na: Hemedi Lubumba Selemani
ترجمة
التقية
تأليف الشيخ عبد الكريم البهبهاني
من اللغة العربية الى اللغة السوا حلية
© Haki ya kunakili imehifadhiwa na: Al-Itrah Foundation ISBN No: 978 – 9987 – 17 – 087 – 6 Kimeandikwa na: Shaikh Abdul-Karim al-Bahbahani Kimetarjumiwa na: Hemedi Lubumba Selemani Kimehaririwa na: Ustadh Abdalla Mohamed Kimepitiwa na: Ramadhani S. K. Shemahimbo Na Mubarak Ali Tila Kimepangwa katika Kompyuta na: Al-Itrah Foundation Toleo la kwanza Octoba 2014 – Nakala 1000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. - 19701, Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 / 2127555 Barua Pepe: alitrah@yahoo.com Tovuti: www.ibn-tv-com Katika mtandao: www.alitrah.info
Yaliyomo Neno la Mchapishaji........................................................................1 Neno la Jumuiya..............................................................................3 Taqiyya kwa Mujibu wa Sheria ya Kiislam.....................................5 Sahaba na Wanafunzi wao walifanya Taqiyya.................................9 Msingi wa Sheria ya Taqiyya kwa Shia Imamiya..........................16 Kwa nini Taqiyya ni Mashuhuri kwa Mashia, na si kwa Waislamu wengine?.......................................................18 Vigawanyo vya Taqiyya.................................................................23
1- Taqiyya dhidi ya kafiri:........................................................23
2- Taqiyya dhidi ya mwislamu:................................................23
3- Taqiyya katika ibada:...........................................................25
4- Taqiyya katika fatwa:...........................................................26
5- Taqiyya katika siasa:............................................................27
Matokeo ya Uchambuzi.................................................................29
v
TAQIYYA
بسم اهلل الرحمن الرحيم NENO LA MCHAPISHAJI
K
itabu ulichonacho mikononi mwako asili yake ni cha lugha ya Kiarabu kwa jina la, at-Taqiyyah, kilichoandikwa na Sheikh Abdul-Karim al-Bahbahani. Sisi tumekiita, Taqiyya kwa Mujibu wa Sheria ya Kiislamu. Kuna tofauti ya maoni kuhusu suala hili la taqiyya, hususan kati ya Shia na Sunni, bali kuna makundi mengine katika Uislamu wanaiona taqiyya kama ni unafiki. Mwandishi katika kitabu hiki anathibitisha bila ya shaka yoyote kwamba taqiyya ni suala ambalo limeruhusiwa kisheria katika Qur’ani na Sunna. Na uthibitisho huo ndio ambao msomaji ataukuta ndani ya kitabu hiki. Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa makubwa, hususan wakati huu wa sayansi na teknolojia kubwa ambapo ngano, hadithi za kale na upotoshaji wa historia ni vitu ambavyo havina nafasi kwa watu wa sasa. Kutoka na ukweli huu, taasisi yetu ya Al-Itrah imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili. Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa ni chenye manufaa makubwa kwao. Tunamshukuru ndugu yetu al-Haj Ustadh Hemedi Lubumba Selemani kwa kufanikisha tarjuma ya kitabu hiki katika lugha ya Kiswahili, pia na wale wote waliosaidia kwa njia moja au nyingine 1
TAQIYYA
hadi kufanikisha kuchapishwa kwake na kuwa mikononi mwa wasomaji. Allah awalipe wote malipo mema hapa duniani na kesho Akhera pia. Amin! Mchapishaji: Al-Itrah Foundation
2
TAQIYYA
بسم اهلل الرحمن الرحيم NENO LA JUMUIYA
H
akika mirathi ya Ahlul-Bait ambayo imehifadhiwa na kambi yao na wafuasi wao dhidi ya upotovu inaonyesha kambi iliyokusanya aina mbalimbali za taaluma za kiislamu. Kambi hii imeweza kulea nafsi mbalimbali zilizo tayari kunywa kutoka kwenye chemchemu hiyo, na kuupa umma wa kiislamu wanachuoni wakubwa wenye kufuata nyayo za ujumbe wa AhlulBait.Wanachuoni waliokusanya vidodosa na maswali mbalimbali ya madhehebu na mitazamo tofauti ya kifikira kuanzia ndani ya desturi ya kiislamu hadi nje ya desturi hiyo, huku wao wakitoa majibu na utatuzi makini juu ya maswali hayo ndani ya karne zote. Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bait imefanya hima kutetea utukufu wa ujumbe wa Uislamu na ukweli wake ambao umechafuliwa na makundi, madhehebu na wanaharakati mbalimbali wenye chuki na Uislamu. Jumuiya imefuata nyayo za Ahlul-Bait na za wafuasi wa kambi yao njema ambayo imefanya hima kujibu madai yenye kuendelea na daima ikajaribu kubaki ndani ya msitari wa mapambano kwa kiwango kinachohitajika ndani ya kila Zama. Hakika uzoefu ambao umehifadhiwa ndani ya vitabu vya wanachuoni wa kambi ya AhlulBait katika dhamira hii ni wa aina ya pekee, kwa sababu una akiba ya kielimu inayotegemea akili na hoja, huku ukijiepusha na matamanio na upendeleo uliokatazwa. Unazungumza na wasomi na wanafikra wenye fani maalumu, mazungumzo ambayo yanakubalika kiakili na yanapokewa na maumbile yaliyo salama. 3
TAQIYYA
Jaribio hili la Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bait limekuja kuwapa watafuta ukweli hatua mpya ya uzoefu wa thamani katika ulingo wa mazungumzo na maswali na kujibu hoja za utata zilizotolewa zama zilizopita au zinazotolewa leo kwa njia ya Tovuti, na hasa kwa kupewa nguvu na baadhi ya duru zenye chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu. Ikijiepusha na uchochezi uliyokatazwa, na ni yenye kuhangaikia kuzishauri akili zenye kufikiria na nafsi zenye kutafuta haki, ili ziweze kufikia kwenye haki ambayo inatolewa na Kambi ya AhlulBayt ulimwengu mzima, ndani ya zama ambazo akili inaerevuka na nafsi na roho zinaboreka kwa kasi ya pekee. Ni lazima tugusie kuwa mfululizo huu wa tafiti hizi umeandaliwa na Kamati maalumu toka jopo la wanachuoni watukufu, hivyo tunatoa shukurani njema kwa hawa wote na kwa wasomi na wahakiki kwa kila mmoja miongoni mwao kwa kupitia sehemu ya tafiti hizi na kutoa mchango wao wa thamani kuhusu tafiti hizi. Na sote tunategemea na kutaraji kuwa tutakuwa tumetoa kile tulichokiweza katika juhudi za kutekeleza baadhi ya wajibu tulionao mbele ya ujumbe wa Mtukufu Mola Wetu Mlezi ambaye alimtuma Mtume Wake na uongofu na dini ya haki ili aipe ushindi dhidi ya dini zote. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa shahidi. Jumuiya ya kimataifa ya Ahlu-Bait (as). Kitengo cha utamaduni
4
TAQIYYA
بسم اهلل الرحمن الرحيم TAQIYYA KWA MUJIBU WA SHERIA YA KIISLAM
T
aqiyya huchukuliwa kuwa ni miongoni mwa kanuni za msingi za kimatendo zilizotolewa na Qur’ani Tukufu, na bila shaka imetoa maelezo ya ruhusa yake ndani ya kauli ya Allah:
َ َ ون ْال َكا ِفر ْ ون ْالم ْ اَل َيتَّ ِخ ِذ ْالم َ ُؤ ِم ِن َ ُُؤ ِمن ين ِ ين أ ْولَِيا َء ِم ْن ُد ِ ْس ِم َن اللهَِّ ِفي َش ْي ٍء إِ اَّل أَ ْن َتتَّ ُقوا َ َو َم ْن َي ْف َع ْل َذٰلِ َك َفلَي ير ُ ص َ ِم ْن ُه ْم تُ َقا ًة َوي ِ ُح ِّذ ُر ُك ُم اللهَُّ َن ْف َس ُه َوإِلَى اللهَِّ ْال َم “Wenye kuamini wasiwafanye makafiri kuwa viongozi badala ya wenye kuamini, na atakayefanya hivyo, basi hana chochote kwa Mwenyezi Mungu, ila mtakapojilinda nao kwa kujihifadhi. Na Mwenyezi Mungu anawatahadharisha na Nafsi yake, na kwa Mwenyezi Mungu ndio marejeo.” (Sura ali Imran: 28).
Na ndani ya kauli:
ْ َم ْن َك َف َر باللهَِّ ِم ْن َب ْع ِد إي َما ِن ِه إ اَّل َم ْن أُ ْكر َه َو َق ْلبُ ُه م ُط َم ِئ ٌّن ِ ِ ِ ِ ْ ْإ َ َ ْه ْم َغ ض ٌب ٰ َ ان َو َ ل ِك ْن َم ْن َش َر َح ِبال ُك ْف ِر ِ ص ْد ًرا َف َعلي ِ الي َم ِ ِب ٌ ِم َن اللهَِّ َولَ ُه ْم َع َذ اب َع ِظي ٌم 5
TAQIYYA
“Anayemkataa Mwenyezi Mungu baada ya imani yake isipokuwa yule aliyelazimishwa hali moyo wake unatulia kwa imani, lakini anayefungua kifua kwa kufru, basi ghadhabu ya Mwenyezi Mungu iko juu yao, na watapata adhabu kubwa.” (Sura Nahli: 106).
Aya hizi zimeelezea Taqiyya na kutoa maana yake, hiyo ni kwa sababu imani ina nguzo tatu, nazo ni: Kuitakidi kwa moyo, kutamka kwa ulimi na kutenda kwa viungo. Hivi ndivyo ilivyo imani katika mazingira ya kawaida. Na kwa kuwa Uislamu ni sheria ya matendo inayotizama uhalisia wa kitu na kutatua matatizo yake yote, basi ni lazima iwawekee wazi mukalafu namna ya kuamiliana na matukio katika mazingira ya kawaida na yale yasiyo ya kawaida, kama pale binaadamu atakapokuwa analazimika kuchagua baina ya kifo au matatizo makali na kati ya kuachana na matokeo ya imani au baadhi ya sifa zake. Ndipo ikaja Aya hii Tukufu ili iweke wazi kuwa, nguzo ya awali ambayo ni kuitakidi kwa moyo haiwezekani kuachana nayo kwa hali yoyote ile. Kwa sababu yenyewe ndio nguzo ya imani na jauhari yake, nayo kikawaida ndio nguzo ya siri. Ama nguzo ya pili na ya tatu, zenyewe Aya imewaruhusu waumini kutoudhihirisha Uislamu kwa muda maalumu ikiwa tu kufanya hivyo kutawaondolea kifo au matatizo makubwa, na ikawa pia hailazimu kubomoa dini na kuidhoofisha. Aya imepatikana katika kadhia ya Ammar bin Yasir pindi washirikina walipomwamuru kumtukana Mtume (s.a.w.w.) na ayatukuze masanamu, akafanya hivyo chini ya mkandamizo wa mateso makali. Alipomjia Mtume (s.a.w.w.) akamwambia: “Nyuma yako kuna nini?” Akasema: “Shari ewe Mtume wa Allah, sikuachiwa mpaka nilipokutusi na kuitaja miungu yao kwa kheri.” Akamuuliza: 6
TAQIYYA
“Uliuonaje moyo wako?” Akajibu: “Umetulia kwa imani.” Mtume akasema: “Wakirudia na wewe rudia.”1 Ulamaa wa kiislamu wamethibitisha sheria ya Taqiyya kupitia Aya hizo mbili zilizotajwa hapo kabla. Na Al-Maraghiy katika tafsiri yake ameonyesha kuwa miongoni mwa matendo ya Taqiyya ni, kuwapumbaza makafiri, madhalimu na mafasiki, na pia kuwa na kauli laini kwao, kutabasamu mbele yao na kuwapa mali ili kuzuia udhia wao na kulinda heshima dhidi yao. Tabraniy ameandika kauli ya Mtume (s.a.w.w.): “Chochote anachokitumia muumini kulinda heshima yake ni sadaka.”2 Na wala haya si unafiki, ambao Qur’ani Tukufu imeuzingatia kuwa ni kitu duni na kibaya zaidi kuliko ukafiri, kwani hakika unafiki ni kuficha ukafiri au uadui na kudhihirisha imani au mapenzi. Ilihali Taqiyya ni kuficha imani na kudhihirisha kinyume chake, na laiti kama Taqiyya ingekuwa ni miongoni mwa mifano halisi ya unafiki, basi ni kwa nini Allah ameihalalisha kwa maelezo ya Aya? Na kisha ikamsifu muumini wa ali Firaun, ikamtaja kwa sifa njema: “Na akasema mtu muumini aliyekuwa mmoja wa watu wa Firaun anayeficha imani yake…” (Sura Ghafir: 28) Na katika Aya mbili za kitabu chake ikamsifu mke wa Firaun na kumfanya mfano wa kuigwa kwa waumini, naye bila shaka aliishi na Firaun kwa Taqiyya. Pia Taqiyya inatofautiana kabisa na kitendo cha kukiri na kujisalimisha katika jambo la dini, kwani kwa hakika kukiri na kujisalimisha ni kuamini madai ya upande wa pili huku ukiacha na kutupilia mbali itikadi uliyokuwa nayo. Ilihali Taqiyya ni kuendelea Al-Mustadrakul-Hakim Juz. 2, Uk. 357. Pia rejea Sunan Ibnu Majah Juz. 1, Uk. 150, mlango wa 11. Tafsirul-Mawaridiy Juz. 3, Uk. 192, chapa ya Beirut. Tafsirur-Razi Juz. 20 Uk. 121, na tafsiri nyinginezo. 2 Tafsirul-Maraghiy Juz. 3, Uk. 136, chapa ya Misri. 1
7
TAQIYYA
kukataa na kutokudhihirisha mkatao huo kwa muda maalumu, huku ukidhihirisha hali ya kuafikiana na adui mpaka pale kipindi cha udhaifu kitakapokwisha, pale itakapotimu fursa ya kuandaa nguvu. Hivyo Taqiyya ni mbinu ya kiakili yenye lengo la kumzuia muumini asiangukie ndani ya shimo la kukiri na kujisalimisha, na badala ya hayo inamvisha nguzo za uimara wa kiroho na kisaikolojia ili asiteleze na kuanguka mbele ya migandamizo ya kiadui, na ili ahifadhi kiwango cha chini kabisa cha imani, nayo inaangalia kwa umakini matarajio ya mustakbali huku ikisubiri kupata fursa stahili kwa ajili ya mabadiliko. Ilihali kujisalimisha kunamwepusha mtu na sifa za uimara na matarajio na fikra ya mabadiliko, mwanzoni tu mwa fursa iwezekanayo. Na kwa usemi mwingine ni kuwa Taqiyya inamaanisha kuishinda ile hali ya kujisalimisha, kukata tamaa, kukiri na nyinginezo miongoni mwa hali za udhaifu na kushindwa, ambazo adui hujaribu kuzilazimisha juu ya muumini. Hivyo kumjibu adui kwa Taqiyya kunamaanisha kuzitupia hali hizi ndani ya nafsi yake, kwani pindi adui anapojua fika kuwa muumini katika kukabiliana naye hushikamana na Taqiyya, na kuwa hii Taqiyya inamfanya awe mwanaadamu imara, asiyetambua kusalimu amri wala kushindwa, basi adui huangukia ndani ya shimo la kukata tamaa dhidi ya malengo yake.
8
TAQIYYA
SAHABA NA WANAFUNZI WAO WALIFANYA TAQIYYA
T
utakapoachana na Kitabu cha Allah na Sunna ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na tukahamia kwenye matendo ya sahaba na wanafunzi wao na wanachuoni wa fiqhi wa zama za mwanzo, tutakuta historia inatuonyesha kuwa wao walikuwa wakifanya Taqiyya kila inapowalazimu kufanya hivyo. Na wao wana visa maarufu katika hilo, na kwa mfano tu ni Abdullah ibn Mas’ud, Abu Dardai, Abu Musa Al-Ash’ariy, Abu Hurayra, Ibnu Abbas, Said bin Jubair, Rajau bin Haywah, Waswil bin Atau, Amru bin Ubaydu Al-Muutazaliy na Abu Hanifa. Imepokewa kutoka kwa Al-Harith bin Suwayd, amesema: “Nilimsikia Abdullah ibn Mas’ud akisema: ‘Hakuna mtawala yeyote atakayetaka kunilazimisha maneno yatakayoniondolea mjeledi au mijeledi miwili, ila ni lazima nitayatamka.”’ Hayo ameyaandika Ibnu Hazmi ndani ya kitabu Al-Muhala, na amesema: “Na hajulikani yeyote aliyekhalifu miongoni mwa sahaba.”3
Bukhari ameandika ndani ya Sahih yake kwa njia yake, kutoka kwa Abu Dardai kuwa alikuwa akisema: “Sisi hukenua mbele ya nyuso za kaumu na huku, kwa hakika, nyoyo zetu zikiwalaani.”4 Kauli hii pia imenasibishwa na Abu Musa Al-Ash’ariy,5 na pia jemedari wa waumini (a.s.).6 Al-Muhal cha Ibnu Hazmi Juz. 8, Uk. 336, mas’ala ya 1409, chapa ya Darul-Afaqi AlJadid Bairut. 4 Sahih Bukhari Juz. 8, Uk. 37, kitabu cha adabu, mlango wa kuishi vizuri na watu. 5 Al-Furuuq cha Al-Qaradhiy Al-Malikiy, tofauti ya mia mbili sitini na nne. 6 Mustadrakul-Wasail Juz. 12 Uk. 261, mlango wa 27 kati ya milango ya kuamrisha mema na kukataza maovu, Hadithi ya 2. 3
9
TAQIYYA
Bukhari ameandika kwa njia yake, kutoka kwa Abu Huraira kuwa alisema: “Nimehifadhi makapu mawili kutoka kwa Mtume wa Allah (s.a.w.w.), ama moja tayari nimeshalisambaza na ama lingine laiti kama ningelisambaza basi bulghamu yangu hii ingekatwa.”7 Ibnu Hajar ndani ya kitabu Fat’hul-Bariy ametamka wazi kuwa: “Ulamaa wametafsiri kapu ambalo hajalisambaza kuwa ni zile hadithi ambazo zinataja wazi wazi majina ya watawala waovu na hali zao. Na kuwa alikuwa akiwataja baadhi yao kwa mafumbo, hawataji waziwazi akihofia nafsi yake dhidi yao, kama aliposema: ‘Najikinga kwa Allah dhidi ya mwanzo wa sitini na utawala wa mtoto mdogo.’ Akikusudia utawala wa Yazid bin Muawiya, kwa sababu wenyewe ulianza mwaka wa sitini Hijiriya.”’8 At-Tahawiy ameandika kwa njia yake kutoka kwa Atau kuwa alisema: “Mtu mmoja alimwambia Ibnu Abbas: ‘Je una chochote kuhusu Muawiya kusali witri kwa rakaa moja?’9 Ibnu Abbas akajibu: ‘Muawiya amepatia.”’ Wakati huohuo At-Tahawiy amebainisha maelezo mengine yanayoonyesha Ibnu Abbas alikanusha usahihi wa Sala ya Muawiya. Ameandika kwa njia yake kutoka kwa Akrimah, amesema: “Nilikuwa na Ibnu Abbas kwa Muawiya tukizungumza mpaka nusu ya usiku ilipoondoka, ndipo Muawiya akasimama kusali, akarukuu rakaa moja, Ibnu Abbas akasema: ‘Iko wapi witri? Ameichukua punda?”’ Baada ya maelezo hayo At-Tahawiy amesema: “Na inawezekana ikawa kauli ya Ibnu Abbas: ‘Muawiya amepatia.’ Ni Taqiyya.” Kisha akaandika kutoka kwa Ibnu Abbas kuwa witri ni rakaa tatu.10 Sahih Bukhar Juz. 1, Uk. 41, kitabu cha elimu, mlango wa kuhifadhi elimu. Fat’hul-Bariy cha Ibnu Hajar Al-Asqalaniy Juz. 1, Uk. 173. 9 Lengo la muulizaji ni kumwaibisha Muawiya. 10 Sharhul-Maanil-Athar cha At-Tahawiy Juz. 1 Uk. 389, mlango wa wtri, chapa ya pili, ya Darul-Kutub Al-Ilmiyah, Beirut 1407 A.H. 7 8
10
TAQIYYA
Abu Ubaydah Al-Qasim bin Salama ameandika kutoka kwa Hasan bin Abu Yahya Al-Kindiy, amesema: “Nilimuuliza Said bin Jubayri kuhusu Zaka, akasema wape watawala.” Amesema: “Said aliponyanyuka nilimfuata nikamwambia: ‘Wewe umeniamuru niwape watawala hali wao wanazitumia kufanyia kadha wa kadha?’ Akasema: ‘Iweke kama alivyokuamuru Allah, uliuliza mbele ya watu hivyo sikuwa na jinsi ya kukupa habari – kama ilivyo.’’11 Na pia ameandika kutoka kwa Qatadah kuwa yeye alimuuliza Said bin Al-Musayyab swali hilo hilo, Ibnu Al-Musayyab akakaa kimya wala hakumjibu. Al-Alama Al-Amin ameandika Taqiyya ya Said bin Al-Musayyab toka kwa Saad bin Abu Waqqas, alipomuuliza kuhusu hadithi ya Ghadiri. Kwa ufafanuzi zaidi rejea huko.12 Al-Qurtubi Al-Malikiy amesema: “Idirisa Ibnu Yahya amesema: ‘Al-Walid bin Abdul-Malik alikuwa akiwaamuru majasusi wawapeleleze viumbe na kumletea habari, basi mtu mmoja akahudhuria kipindi cha Rajau bin Haywatu, akasikia baadhi yao wakimtia dosari Al-Walid, ndipo akaenda kumpa habari. Al-Walid akasema: ‘Ewe Rajau hivi unaacha natajwa kwa ubaya kwenye kikao chako na wala hubadili?!!’ Akajibu: ‘Haikuwa hivyo ewe kiongozi wa waumini.’ Al-Walid akamwambia: ‘Sema: Allah ni yule ambaye hapana Mola wa haki ila Yeye.’ Akasema: ‘Allah ni yule ambaye hapana Mola wa haki ila Yeye.’ Al-Walid akawaamuru majasusi wakampiga mijeledi sabini, ndipo akawa akutanapo na Rajau husema: ‘Ewe Rajau kupitia kwako mvua huombwa kunyesha, na mijeledi sabini ipo juu ya mgongo wangu.’ Na Rajau itabul-Am’wali, Abu Ubaydah Al-Qasim bin Salaam 567: 1813, uhakiki wa Dk. K Muhammad Khalil Haras, chapa ya kwanza, ya Darul-Kutub Al-Ilmiyah, Beirut 1406 A.H. 12 Al-Ghadir cha Al-Alama Al-Amin Juz. 1, Uk. 380, chapa ya tano , ya Darul-Kutub AlArabiy, Beirut 1403 A.H. 11
11
TAQIYYA
husema: ‘Mijeledi sabini mgongoni kwako ni bora kuliko mwislamu kuuawa.’”’13 Taqiyya kama hii ilimpata Saad bin Ashras – Rafiki wa Malik bin Anas - dhidi ya mtawala wa Tunisia, pindi alipokuwa amemuhifadhi mtu aliyekuwa akitafutwa na mtawala, alipopelekwa mbele yake alikanusha na akaapa kuwa hakumuhifadhi na wala hajui sehemu yoyote alipo.14 Ibnu Al-Jawziy Al-Hambaliy amesema: “Waswil bin Atau alitoka kwa nia ya kusafiri akiwa na kundi, ndipo kundi la jeshi miongoni mwa khawariji likamzuia. Waswil akasema: ‘Yeyote miongoni mwenu asitamke chochote niacheni mimi nao.’ Ndipo Waswil akawakusudia, walipokaribia khawariji wakaanza kuwashambulia ili wawauwe. Waswil akasema: ‘Vipi mnahalalisha haya ilihali hamjui sisi ni akina nani, na tumekuja kwa lengo gani?’ Wakasema: ‘Ndio, ninyi ni akina nani?’ Akasema: ‘Ni kundi miongoni mwa mushrikina tumekuja ili tusikie maneno ya Allah.’ Ndipo wakaacha na mtu miongoni mwao akaanza kusoma Qur’ani, alipomaliza Waswil akasema: ‘Tayari tumesikia maneno ya Allah, hivyo tupeni hifadhi ili tujifikirie ni jinsi gani tutakavyoingia ndani ya dini.’ Wakasema: ‘Hili ni wajibu, endeleeni na safari.’” Amesema: “Tukaendelea kwenda, na makhawariji walikuwa pamoja nasi wakitulinda njia nzima mpaka tulipokaribia mji wasio na utawala nao, ndipo wakaondoka wakarudi.”15 Na katika habari za mapinduzi ya Ibrahim bin Abdullah na kaka yake Muhammad Dhin-Nafsi Zakiyyah dhidi ya Al-Mansur AlAbbasiy, ambayo yaliishia kwa wao kuuwawa, ni kuwa siku moja Al-Jamiu Liahkamil-Qur’ani cha Al-Qurtubiy Juz. 10, Uk. 124. Al-Jamiu Liahkamil-Qur’ani cha Al-Qurtubiy Juz. 10, Uk. 124. 15 Kitabul-Adhkiyai cha Ibnu Al-Jawziy: 136, chapa ya kwanza, ya Darul-Kutub Al-Ilmiyah, Beirut 1405 A.H. 13 14
12
TAQIYYA
Al-Mansur alimwambia Amru bin Ubaydu: “Zimenifikia habari kuwa Muhammad bin Abdullah bin Al-Hasan alikuandikia barua.” Amru akasema: “Ilinifikia barua inayotaka kufanana na barua yake.” Akamuuliza: “Ulimjibu nini?” Akasema: “Si unajua mtazamo wangu katika upanga pindi ulipokuwa ukija kwangu, kwa hakika simuoni tena.” Al-Mansur akasema: “Sawa, lakini je utaniapia ili moyo wangu utulie?” Amru Akasema: “Kama nitakuongopea kwa kufanya Taqiyya, bila shaka nitakuapia kwa kufanya Taqiyya.” Al-Mansur akasema: “Wallahi Wallahi wewe ni mkweli uliye mwema.”16 Al-Khatib Al-Baghdadiy ameandika ndani ya Tarikh yake kwa njia yake kutoka kwa Sufiyan bin Wakiu, amesema: “Amru bin Hammad Ibnu Abu Hanifa alikuja akaketi kwetu, akasema: Nimemsikia baba Abu Hammad akisema: Alitumwa Ibnu Abu Layla kwa Abu Hanifa, naye akamuuliza kuhusu Qur’ani, akajibu ni kiumbe, akasema: ‘Tubu, la sivyo nitakushambulia.’ Amesema: “Ndipo akamfuata na akasema: ‘Qur’ani ni maneno ya Allah.’” Amesema: “Akamzungusha kwa watu huku akiwapa habari kuwa ameshatubu dhidi ya kauli yake ya kuwa Qur’ani ni kiumbe. Baba yangu akasema: Nikamwambia Abu Hanifa: ‘Imekuwaje umekubali hili na kumfuata?’ Akasema: ‘Ewe mwanangu mpendwa!! Nilichelea kunishambulia, hivyo nikampa kwa kufanya Taqiyya.”’17 Hii ni jumla ya mifano ya kivitendo iliyothibiti kivitendo katika suala la Taqiyya katika uhai wa ulamaa maarufu miongoni mwa sahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na wanafunzi wao na wanazuoni. Na pia kuna mifano mingine kedekede tumeacha kuitaja ili tusije arikh Baghdad cha Al-Khatib Al-Baghdadiy Juz. 12 Uk. 168 – 169, katika wasifu wa T Amru bin Ubaydu Al-Muutazaliy. 17 Tarikh Baghdad cha Al-Khatib Al-Baghdadiy Juz. 13 Uk. 379 - 380, katika wasifu wa Abu Hanifa, chini ya anwani: Kutaja riwaya za anayeelezea kuhusu Abu Hanifa, kauli ya kuumbwa kwa Qur’ani.. 16
13
TAQIYYA
tukarefusha, nayo imepokewa ndani ya vitabu vya Sunni, na jambo lenyewe hili limekuwa mashuhuri na limeenea mno katika matendo ya wale wenye kuifanyia kazi sheria ya bwana na mbora wa mitume (s.a.w.w.) kila pale mazingira yanapowakimbizia kwenye Taqiyya, mpaka jambo hili limekuwa dhahiri katika historia ya uislamu, ambalo kila mtafuta haki na ukweli ameliona kwa macho yake, hali ambayo ilimfanya Jamalud-Din Al-Qasimiy agusie yale aliyoyataja Sheikh Murtaza Al-Yamaniy kuhusu sababu zinazopelekea haki kufichika na ukweli kufunikwa katika hali nyingi, kwani amenukuu kuwa: “Na kinachozidisha utata na mficho kwenye haki ni mambo mawili: La kwanza: Ni ile khofu ya wajuzi walio wachache dhidi ya ulamaa waovu, watawala wajeuri na viumbe waovu, huku Taqiyya ikiwa imeruhusiwa katika hali kama hiyo kwa mujibu wa maelezo ya Qur’ani na ijmai ya waislamu. Na bado khofu inaendelea kuwa kizuizi dhidi ya kudhihirisha haki, na mwenye haki hajaacha kuwa adui wa wengi miongoni mwa viumbe.”18 Na kutokana na nafasi kubwa ya Taqiyya ambayo haiwezekani kwa muumini kutokuijua, ndio maana tunaikuta sheria ya kiislamu katika milango yake mbalimbali imejaa maeneo yake, kiasi kwamba mukalafu anakuta humo suala la kisheria linalohusu ibada maalumu au muamala maalumu lina hukmu ya kisheria ya pale mukalafu awapo katika hali ya kawaida, na lina hukmu nyingine ya pindi awapo katika mazingira ya dharura, anayolazimishwa kuchagua jambo kwa udhalimu na uadui. Na mlango huu ni mpana zaidi unahusu milango yote ya fiqhi na vitabu vyake, kuanzia mambo ya ibada mpaka ya muamala, na hakuna anayekanusha kuwepo hukmu za dharura ndani ya fiqhi ya kisunni, zilizo maalumu kwa yule anayelazimishwa kufanya jambo 18
Mahasinut-Taawil Juz. 4 Uk. 82, chapa ya pili ya Darul-Fikri. 14
TAQIYYA
fulani kwa dhulma na ujeuri, na hukmu hizo si chochote bali ni sehemu ya mifano halisi ya Taqiyya na maeneo inapopatikana.19
19
azama maeneo ya hukmu hizi ndani ya fiqhi ya kisunni ndani ya kitabu WaqiutT Taqiyya I’ndal-Madhahibi-Islamiyyah min ghairis-Shiatil-Imamiyah, cha Sayyid Thamir Al-Amidiy. 15
TAQIYYA
MSINGI WA SHERIA YA TAQIYYA KWA SHIA IMAMIYA
U
lamaa wa kishia, ukiachilia mbali Aya mbili zilizotajwa huko nyuma, pia wamethibitisha ruhusa ya Taqiyya, bali wajibu wake katika baadhi ya hali, kwa kutumia riwaya nyingi zilizofikia kiwango cha Istifadha.20 Na yenyewe ina mlango maalumu wa riwaya katika kitabu Wasailus-Shia, katika sura inayozungumzia kuamrisha mema na kukataza maovu. Zifuatazo ni baadhi tu: 1. Kutoka kwa Ibnu Abu Yaafur, kutoka kwa Abu Abdullah, amesema: “Taqiyya ni ngao ya muumini na Taqiyya ni kinga ya muumini.”21 2. Kutoka kwa Imam al-Sadiq (a.s.) kuwa alimwambia AlMufadhal: “Utakapofanya Taqiyya hawatokuweza katika hilo kwa ujanja wowote ule, nayo ni ngome imara, na kati yako na maadui zako kutakuwa na kinga imara ambayo hawawezi kuitoboa.”22 3. Kutoka kwa Ali Jemedari wa waumini amesema: “Taqiyya ni kati ya matendo bora ya muumini anajikinga kwayo nafsi yake na ndugu zake dhidi ya waovu.”23 i msamiati unaotumika katika taaluma ya Hadithi, ukimaanisha kiwango fulani cha N wingi wa hadithi zenye maana na maudhui moja. 21 Usulul-Kafiy Juz. 2, Uk. 221, mlango wa Taqiyya. 22 Wasailus-Shia Juz. 16, Uk. 213, mlango wa 24. 23 Tafsirul-Imam Al-Hasan Al-Askariy (a.s.): 320. 20
16
TAQIYYA
4. Abu Jafar Al-Baqir (a.s.) amesema: “Taqiyya ni sehemu ya dini yangu na dini ya baba zangu.”24 5. Kutoka kwa Imam al-Sadiq (a.s.) amesema: “Ilindeni dini yenu, ikingeni kwa kufanya Taqiyya…..”25
24 25
Usulul-Kafiy Juz. 2, Uk. 219, mlango wa Taqiyya. Usulul-Kafiy Juz. 2 Uk. 219, mlango wa Taqiyya. 17
TAQIYYA
KWA NINI TAQIYYA NI MASHUHURI KWA MASHIA, NA SI KWA WAISLAMU WENGINE?
S
i siri kuwa Shia Imamiya waliishi ndani ya mazingira magumu ya kisiasa muda wote wa utawala wa Bani Umayya na dola ya Bani Abbas, ambayo ilidumu mpaka baada ya ghaibu ya Imam wa kumi na mbili. Katika karne hizi kulipita vipindi ambavyo ilikuwa ni nafuu kwa mtu kuitwa ‘mzandiki’ kuliko kuitwa ‘Shia’, hiyo ni kutokana na mbinyo, unyimwaji wa haki za msingi, na kufukuzwa kulikokuwa kukiwapata mashia, achilia mbali kule kusingiziwa uongo na kutuhumiwa kwa bidaa na upotovu, hali ambayo inaweza kuwa nzito mno kwao kuliko kule kuuawa kulikowasibu bila huruma. Hivyo ni lazima mazingira haya yaliyodumu kwa muda mrefu yalazimishe njia maalumu ya maisha itakayoifanya Taqiyya kuwa mbinu ya lazima ili kuzihifadhi nafsi, watoto na mali, na bila shaka hali kama hii itasaidia sana kuenea hadithi maalumu zinazohusu Taqiyya kati ya watu wa kundi hili, mpaka Taqiyya imekuwa sifa ya pekee kwao inayowatofautisha na wengine waliokuwa wamestarehe ndani ya amani angalau hata kama ni kwa kiwango fulani. Kisha baada ya hapo vikaja vishawishi vya ugomvi kwa baadhi ya watu ili kubadili msingi wa Taqiyya, wakienda huku na huko ili kuwatia doa na ubaya wafuasi wa madhehebu ya Ahlul-Bait, wakijisahaulisha kuwa asili ya msingi wa Taqiyya ni miongoni mwa mambo yanayokubalika na Kitabu, na ni miongoni mwa dharura za sheria, ambazo waislamu wote wa mwanzo hadi wa sasa wamekubaliana juu yake. 18
TAQIYYA
Pia adui hao wameghafilika dhidi ya wajibu wao uliyobakia katika kutokomeza dhulma na ugandamizaji ambao umeteketeza kundi kubwa la waislamu hadi ikapelekea Taqiyya kudumu karibuni karne tatu zenye kufuatana. Hivyo badala ya kutokomeza dhulma, ujeuri na uvunjaji wa haki za watu na umwagaji wa damu zao, wao wamekuwa wakimshambulia na kumtokomeza yule aliyedhulumiwa na aliyegandamizwa pindi anapokimbilia kwenye mbinu ya kisiasa ili kuihami nafsi yake, dini yake na mali yake, nayo ni mbinu ambayo sheria imeiridhia kwa wafuasi wake wawapo katika hali kama hii, kama ilivyotangulia, bila kuwepo tofauti yoyote baina ya waislamu katika hilo. Hakika ubaya huu na hali hii inayowakabili wafuasi wa AhlulBait inatupa sura halisi ya yale mazingira ya kihistoria yaliyo magumu ambayo hawa walikuwa wakiishi katika zama za utawala wa Bani Umayya, Bani Abbas na dola ya Uthmaniyya, bila shaka yenyewe ni mabaki ya mazingira yale magumu na ni urithi wa zama zile zilizopita, ambazo waliishi baadhi ya wafuasi wa Ali (a.s.) huku wakificha ushia wao hata kwa wake zao, siku ambayo ukituhumiwa kwa ushia basi ni adhabu kali mno kuliko ya tuhuma yoyote ile. Ibnu Abu Hadid amepokea kutoka kwa Al-Madainiy, Naftawih na Imam Muhammad al-Baqir (a.s.), maneno ambayo muhtasari wake ni: “Siku moja Muawiya bin Abu Sufiyan aliwaandikia magavana wake kuwa: ‘Mimi sina dhima na yeyote anayepokea chochote kile kuhusu fadhila za Abu Turab (Ali bin Abu Talib ) na watu wa nyumba yake.’ Ndipo wakasimama makhatibu katika kila kizingiti na juu ya kila mimbari wakimlaani Ali na kujitenga naye, huku wakimtusi yeye na watu wa nyumba yake. Na watu waliokuwa na balaa kubwa zama hizo ni wakazi wa mji wa Kufa, kutokana na mji huo kuwa na wafuasi wengi wa Ali (a.s.), hivyo akampa ugavana wa mji huo Ziyad bin Sumaiyya, na 19
TAQIYYA
akamwongezea mamlaka ya mji wa Basra katika ugavana wake, hivyo akawa akiwafuata mashia, naye alikuwa akiwatambua kwa sababu alikuwa miongoni mwao zama za Ali. Akawa akiwauwa chini ya kila jiwe kubwa na dogo. Akawafukuza na kuwatoa Iraq, na hatimaye humo hakubakia shia yeyote maarufu. Kama ambavyo Muawiya alivyowaandikia magavana wake pande zote wasiruhusu ushahidi wa yeyote aliye mfuasi wa Ali (a.s.) na watu wa nyumba yake. Na akaandika barua nyingine akisema: “Chunguzeni yeyote ambaye ushahidi umethibitisha kuwa anampenda Ali (a.s.) na watu wa nyumbani kwake, basi mumfute kwenye diwani na mumfutie kipawa chake na riziki yake.” Na katika barua nyingine aliandika akisema: “Yeyote mtakayemtuhumu kuwa anawatawalisha watu hawa, basi mteseni na bomoeni nyumba yake.” Mambo yaliendelea kuwa hivyo mpaka alipofariki Hasan bin Ali (a.s.) na hapo ndipo balaa na mtihani vikazidi, hakubaki yeyote wa namna hii ila alihofia damu yake au kufukuzwa. Kisha mambo yakazidi uzito baada ya kuuwawa Husein (a.s.) na Abdul-Malik bin Marwan akatawala, hapo hali ikawa mbaya zaidi kwa mashia, akawawekea Al-Hajjaj bin Yusuf awatawale, ndipo watu wa dini, wema na ibada wakajikurubisha kwake kwa kumchukia Ali (a.s.) na kuwapenda maadui zake na kuwapenda watu wanaodai kuwa ni maadui zake… Wakakithirisha kumtia dosari Ali (a.s.), aibu, doa na ubaya mpaka ikafikia mtu mmoja26 akasimama mbele ya Hajjaj na kupiga kelele: “Ewe kiongozi! Hakika ndugu zangu walininyima haki yangu wakanipa jina la Ali, nami ni fukara mkata, nami nahitaji uhusiano na kiongozi.” Hajjaji akajichekesha kwake na kusema: “Kwa uzuri wa wasila uliopitia ninakufanya mtawala wa eneo kadha.”27 26 27
Inasemekana ni babu wa Abdul-Malik bin Qarib. Sharhu Nahjul-Balaghah Juz. 11: 44 – 46. 20
TAQIYYA
Na yale yaliyowapata mashia zama za Bani Abbas hayakuwa madogo kuliko haya, huyu hapa Ibnu Sikiti mmoja wa ulamaa wa fasihi wa zama za Al-Mutawakil, khalifa alimteua awe mwalimu wa wanawe, basi siku moja akamuuliza ni akina nani uwapendao sana, je ni wanangu hawa wawili au Hasan na Husein? Ibnu Sikiti akajibu: “Wallahi Qambar mhudumu wa Ali ni bora kuliko wewe na kuliko wanao hao wawili.” Al-Mutawakil akasema: “Ng’oeni ulimi wake kinywani mwake.” Wakafanya hivyo na hatimaye akafariki. Hakika baadhi ya watu walikumbana na aina hii ya ugandamizaji na udhoofishwaji muda wa karne nyingi, hivyo ni kawaida kabisa wachague njia ya kati, baina ya kushindwa na kujisalimisha mbele ya adui, na kutokomea na kutoweka kabisa, ili wabaki wakiendelea kupinga dhulma na upotovu kwa upande mmoja. Na kwa upande mwingine wakiwa si wenye kuzipeleka nafsi zao kwenye hali ya kutokomea, kutoweka na kuisha kabisa. Huu ndio msingi wa Taqiyya, hivyo yale aliyosema Ibnu Taymiya kuwa: “Taqiyya ni uongo na unafiki.”28 Hayana mwelekeo wowote na wala hayakubaliki na akili, kama ambavyo hayaungwi mkono na nukuu za wazi za Kitabu na Sunna kwa pamoja. Kwani yenyewe imeletwa na Qur’ani kama tulivyotanguliza, na ikaridhiwa na Sunna, na hatimaye sahaba wakubwa na wanafunzi wao wakaifanyia kazi, na ikajaa tele ndani ya enklopedia za fiqhi ya kisunni, tena katika milango mbalimbali, kama tulivyogusia baadhi yake. Zaidi ya hapo ni kuwa Taqiyya haikuwa ndio njia pekee iliyokita katika maisha ya mashia muda wote wa karne hizi, bali waliishi pia kwa roho ya mapinduzi ambayo yalijaa historia kwa sura yake ya kuvutia zaidi, ikiwa ni kuondoa dhulma na ufisadi wa kisiasa, kiidara na kiuchumi, na upotovu wa kidini kwa watawala waovu waliofuatana katika utawala. 28
Minhajus-Sunnah Juz. 1Uk. 68, uhakiki wa Dk. Muhammad Rishad Salim. 21
TAQIYYA
Ndio, mashia waliamini kuwa uislamu ndio dini yenye kutawala maisha yao na wala haipasi kwenda kinyume nayo au kufuata nyingine, na kwa ajili yake wakatoa kila cha thamani na ghali, na katika njia yake zikamwagwa damu za nafsi tukufu mno ulimwenguni. Na mapinduzi ya Husein bin Ali (a.s.) hayakuwa kingine bali ni katika njia ya dini hii na kwa ajili ya kuilinda dhidi ya mmong’onyoko na kuchezewa baada ya mikono ya Bani Umayya kuichezea hadi kukaribia kuitokomeza na kutoweka mafunzo yake. Kisha baada ya mapinduzi ya Husein (a.s.) yalifuata mapinduzi mengine ya kiislamu, yote yakilenga kuhifadhi na kuilinda dini hii, na hakika Shia walipita ndani ya msafara huo wa jihadi kuu huku wakitoa kila walichonacho na wanachokimiliki katika njia ya uislamu. Na lau kama unafiki ungekuwa unatembea ndani ya nyoyo za mashia basi yasingepatikana mauaji kama hayo kwa mashia wa Ali (a.s.). Na lau kama shia angekuwa anahadaa katika dini yake au kufanya unafiki basi mijeledi ya watawala na panga zao visingeupata hata unywele wao mmoja. Lakini kwa kuwa walikuwa wazi katika lile wanaloamini na kudhihirisha lile wanaloitakidi, ndio maana ladha ya upanga ilikuwa tamu kwao kuliko hadaa, au kuliko ria ambayo waliitumia wasiokuwa wao ili kuafikiana na watawala waovu na viongozi wapotovu.
22
TAQIYYA
VIGAWANYO VYA TAQIYYA
I
nafaa baada ya duru hii sasa tubainishe vigawanyo vya Taqiyya na muhtasari wa kauli za ulamaa wa fiqhi ya kiislamu juu ya kila kigawanyo. Na hakika Taqiyya kulingana na vigezo vya mgawanyo imegawanyika katika vigawanyo mbalimbali. Kwa kigezo cha anayehofiwa, tunaweza kugawa: Taqiyya dhidi ya kafiri na Taqiyya dhidi ya mwislamu. Kwa kigezo cha amali, tunaweza kugawa: Taqiyya katika ibada, Taqiyya katika fatwa na Taqiyya katika siasa. Na kwa kigezo cha hukmu tano za kisheria, tunaweza kugawa: Taqiyya ya hiari, Taqiyya ya wajibu na Taqiyya ya haramu. 1.
Taqiyya dhidi ya kafiri:
Waislamu wote wameafikiana juu ya Taqiyya hiyo, nayo ndio iliyotamkwa na Qur’ani katika sehemu zile mbili zilizopita. 2.
Taqiyya dhidi ya mwislamu:
Uchambuzi wake kati ya ulamaa wa kiislamu unahusu kuruhusiwa na kutoruhusiwa, na wale ambao wameona kuwa hairuhusiwi wametumia dalili kuwa Qur’ani Tukufu imetamka wazi Taqiyya ya mwislamu dhidi ya mshirikina, na wala haijatamka mwingine. Ulamaa wa Imamiya na baadhi ya wanazuoni wa fiqhi ya kisunni wameona Taqiyya hii imeruhusiwa, na kwamba dalili juu ya hilo ni Qur’ani Tukufu katika Aya zake mbili zilizotajwa huko nyuma, kwani kwa hakika Aya mbili japokuwa zilipatikana katika Taqiyya ya dhidi ya mshirikina, lakini kanuni inayofuatwa na wanachuoni wa 23
TAQIYYA
elimu ya misingi ya sheria (Usuulul fiq’hi) ni kuwa: ‘Sababu haizuii hukumu isienee.’ Na kanuni inayofuatwa na ulamaa wa tafsiri ni kuwa: ‘Kigezo ni ujumuishi wa tamko na si sababu.’ Hivyo ni lazima iwe wazi kwanza: Je Qur’ani katika Aya hizi mbili imetizama hali ya mwislamu au hali ya mshirikina? Ikiwa Taqiyya imemtizama mshirikina basi Taqiyya inayoruhusiwa itakuwa ni ile iliyo dhidi ya mshirikina, na si ile iliyo dhidi ya mwislamu. Na ikiwa Qur’ani imetizama hali ya mwislamu na ikawa Taqiyya imekuja kwa lengo la kumuhifadhi basi inathibiti kwetu kuwa Taqiyya inaruhusiwa dhidi ya kila dhalimu hata kama ni mwislamu. Na maana ya pili ndio iliyo dhahiri toka ndani ya Qur’ani Tukufu, kwani kwa hakika Taqiyya imekuja kwa lengo la kumlinda mwislamu dhidi ya hatari na kumuhifadhi dhidi ya maadui, na sababu hii ipo kwenye Taqiyya dhidi ya mwislamu kama ilivyo kwenye Taqiyya dhidi ya mshirikina. Na katika hili aligusia mmoja wa ulamaa wakubwa wa kisunni pale aliposema: “Hukmu ya nne: Dhahiri ya Aya inaonyesha kuwa Taqiyya inaruhusiwa dhidi ya makafiri walioshinda, isipokuwa madhehebu ya Shafi yanaona kuwa, hali kati ya waislamu ikiwa kama ile iliyopo baina ya mwislamu na mshirikina, basi Taqiyya huchukua nafasi ili kuzihami nafsi.”29 Zaidi ya hapo ni kuwa Taqiyya ni mwenendo wa kiakili ulio jumuishi, na wala hakuna maana yoyote kuuhusisha na baadhi ya madhalimu na kuwaacha wengine, na huenda siri ya wapingaji kupinga Taqiyya ya mwislamu dhidi ya mwislamu ni ile hali ya mapenzi binfasi. Kwani hakika wafuasi wa madhehebu ya kisunni walipoona sheria za utawala wa kibani Umayya na Abbasiya zinahukumu 29
At-Tafsiirul-Kabiir Juz. 1, Uk. 20 na 120. 24
TAQIYYA
wajibu wa kumtii kila mtawala, sawa awe muovu au mwema, ikawa ni kawaida kuona harakati zozote zile zinazopingana na tawala hizi mbili ni harakati zisizo za kisheria, na hatimaye Taqiyya aliyokuwa akiifanya Shia ikawa inamaanisha mwenendo usio wa kisheria kwa upande huu, na si kwa upande ule wa kuwa Taqiyya ya mwislamu dhidi ya mwislamu si Taqiyya ya kisheria, na hapo upembuzi unatoka nje ya ulingo wa Taqiyya, vigawanyo vyake na dalili zake. La sivyo, ni kuwa Taqiyya ni jambo la kiakili na ulamaa wengi wa madhehebu ya kiislamu waliifanya kama ulivyojua. Huyu hapa Abu Huraira anasema: “Nimehifadhi makapu mawili kutoka kwa Mtume wa Allah (s.a.w.w.), ama moja tayari nimeshalisambaza na ama lingine laiti kama ningelisambaza basi bulghamu yangu hii ingekatwa.”30 Je hii sio Taqiyya ya mwislamu dhidi ya mwislamu? Na je mamia ya mifano ikiwemo mingine iliyotangulia sio katika namna hii (ya Taqiyya ya mwislamu dhidi ya mwislamu?). 3.
Taqiyya katika ibada:
Nayo inamaanisha kuleta ibada katika namna ambayo inakhalifu usahihi ambao mwislamu mhusika anaamini kulingana na madhehebu yake, afanye hivyo ili kujikinga na hatari ya dhulma dhidi yake au kwa lengo la kuyavutia pamoja madhehebu mengine ya kiislamu. Na katika hilo Imam Khomeini amesema: “Hakika Taqiyya inaweza kuja kwa ajili ya kuondoa hatari inayotarajiwa juu ya jamii ya waislamu, pale atakapohofia kusambaratika umoja wa waislamu kwa sababu ya kuiacha. Au anahofia jamii ya waislamu kudhurika kupitia kitendo cha umoja wa waislamu kuvunjika, na mengineyo. Na muradi wa Taqiyya ya kuyavuta (makundi mengine ya kiislamu) 30 S ahih Bukhari Juz. 1, Uk. 41, kitabu cha elimu, mlango wa kuhifadhi elimu. MahasinutTaawil cha Al-Qasimiy Juz. 4, Uk. 82, chapa ya Misri. 25
TAQIYYA
ni kuwa kinachotafutwa iwe ni kulekule kuleta umoja kwa kuwapendezesha walio kinyume, na kuvuta mapenzi yao bila hofu.”31 Imepokewa toka kwa Imam Sadiq (a.s.) kuwa alimwambia Hisham bin Al-Hakam: “Unganisha udugu katika familia zao, watembelee wagonjwa wao, na hudhuria majeneza yao… Wallahi Allah hakuabudiwa kwa kitu akipendacho zaidi kama mficho.” Nikamwambia: “Mficho ni nini?” Akasema: “Taqiyya.”32 4.
Taqiyya katika fatwa:
Nayo ni mwanachuoni wa sheria ya kiislamu atoe fatwa juu ya jambo fulani kinyume na usahihi anaouamini yeye. Hii yenyewe inatofautiana kulingana na tofauti za hali na sura. Hivyo inaweza kuwa haramu na inaweza kuwa jaizi, na inaweza kuwa wajibu pia, (yote ni kulingana na hali husika.). Sayyid Hasan Al-Bajanuridiy amesema: “Katika hali kama hii ni wajibu kukimbia na kujiepusha kutoa fatwa kwa namna yoyote iwezekanavyo, na pia iwapo fatwa italazimu kuharibu nafsi au kuvunja heshima za wake. Hivyo katika la kwanza (kuharibu nafsi) haruhusiwi kutoa fatwa hata kama kutotoa fatwa kutalazimu kumwangamiza na kuuwawa kwake. “Ama maimamu maasumina japo katika baadhi ya nyakati walikuwa wakitoa fatwa kinyume na hukumu yenyewe halisi ya mwanzo, lakini wao baada ya hapo walikuwa wakiwatanabahisha watu kuwa fatwa ile ilikuwa kinyume na uhalisia wa hukumu yenyewe, ima kwa ajili ya kuhifadhi nafsi yake mwenyewe (a.s.) au kwa ajili ya kuhifadhi nafsi za wale walioomba fatwa…. 31 32
Ar-Rasailu: 174. Wasailus-Shia kitabu cha kuamuru mema na kukataza maovu, mlango wa 26, hadithi ya 2. 26
TAQIYYA
“Matokeo ni kuwa hakika kutoa fatwa iliyo kinyume na yale aliyoteremsha Allah, eti kwa lengo la kufanya Taqiyya, ni jambo lenye utata, na kuna tofauti sana kulingana na Mufti na jinsi rai yake inavyokubalika na isivyokubalika kwa watu wa kawaida….”33 5.
Taqiyya katika siasa:
Yenyewe iko wazi mno na Taqiyya nyingi ni za namna hii, na tayari imeshakuwa wazi kuwa Taqiyya si jaizi muda wote daima, na si wajibu daima, bali inaweza ikawa haramu katika baadhi ya mazingira. Imam Khomeini amezungumzia Taqiyya iliyo haramu, amesema: “Miongoni mwake ni baadhi ya mambo ya haramu na ya wajibu ambayo kwa mtazamo wa sheria yana umuhimu mkubwa mno, mfano kubomoa Al-Kaaba na makaburi matukufu…Na mfano kuupinga uislamu, Qur’ani na tafsiri kwa namna ambayo inaharibu madhehebu na kuafikiana na ukafiri…. Na katika mlango huu ni pale mwenye kufanya Taqiyya atakapokuwa na nafasi na umuhimu mkubwa katika mtazamo wa viumbe kiasi kwamba inakuwa kutenda kwake baadhi ya mambo ya haramu kwa kufanya Taqiya, au kuacha baadhi ya wajibu, kutapelekea kuonekana ni mwenye kuyadhalilisha madhehebu na ni mwenye kuyavunjia heshima yake…..Na lililo aula kuliko yote hayo katika kutoruhusiwa kufanya Taqiyya ni pale iwapo msingi wowote miongoni mwa misingi ya kiislamu au madhehebu, au dharura miongoni mwa dharura za dini vitakapokuwa katika hatari ya kutoweka, kubomoka na kubadilishwa, kama pale waovu wapotovu watakapotaka kubadili kanuni za urithi na talaka……”34 Al-Alama Al-Mudhaffar amesema: “Taqiyya ina hukumu tofauti huenda ikawa wajibu na au isiwe wajibu, kulingana na tofauti za 33 34
Al-Qawaidu Al-Fiqhiyah Juz. 5 Uk. 68. Ar-Rasailu: 177 - 178. 27
TAQIYYA
maeneo ya khofu na madhara yaliyotajwa kwenye milango yake ndani ya vitabu vya ulamaa wa fiqhi. Na wala yenyewe si wajibu katika kila hali, bali inaweza kuwa ruhusa ya hiari au ikawajibika kutenda kinyume chake katika baadhi ya hali, kama pale itakapokuwa kuidhihirisha haki na kujipamba nayo ndio kuinusuru dini na kuutumikia uislamu na jihadi katika njia yake, basi katika hali hiyo mali huwa hazina thamani wala nafsi huwa hazina uzito….”35
35
A’qaidul-Imamiya: 85. 28
TAQIYYA
MATOKEO YA UCHAMBUZI
H
akika Taqiyya ni sheria ya asili ya Uislamu iliyo jumuishi, Allah ameiweka ndani ya Qur’ani Tukufu na ikathibitishwa na maelezo ya Sunna Tukufu. Kama ilivyothibitishwa na maelezo mengi kutoka kwa maimamu wa Ahlul-Bait, na hatimaye sahaba na ulamaa wakawa wameifanyia kazi, na wanafiqhi wa kiislamu wa pande zote mbili wakawa wametoa fatwa kuihusu katika sehemu mbalimbali, nayo ni msingi wa kudumu mpaka siku ya Kiyama, kama alivyotamka hilo Razi ndani ya Tafsiir yake, na wala hakuna nafasi ya kulikanusha kwa hali yoyote ile. Na mwisho wa dua yetu ni kumshukuru Allah Mola Mlezi wa viumbe.
29
TAQIYYA
ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION 1. i) Qur’ani Tukufu – Pamoja na Tarjuma ya Kiswahili ii) Qur’an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Thelathini 2. Uharamisho wa Riba 3. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza 4. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili 5. Hekaya za Bahlul 6. Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) 7. Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.) 8. Hijab vazi Bora 9. Ukweli wa Shia Ithnaashari 10. Madhambi Makuu 11. Mbingu imenikirimu 12. Abdallah Ibn Saba 13. Khadijatul Kubra 14. Utumwa 15. Umakini katika Swala 16. Misingi ya Maarifa 17. Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia 18. Bilal wa Afrika 19. Abudhar 20. Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu 21. Salman Farsi 22. Ammar Yasir 23. Qur’an na Hadithi 24. Elimu ya Nafsi 25. Yajue Madhehebu ya Shia 26. Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur’an Tukufu 27. Al-Wahda 28. Ponyo kutoka katika Qur’an 29. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii 30. Mashukio ya Akhera 31. Al Amali 32. Dua kwa Mujibu wa Ahlulbayt (a.s) 33. Udhuu kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna 34. Haki za wanawake katika Uislamu 35. Mwenyezi Mungu na sifa zake 36. Kumswalia Mtume (s) 30
TAQIYYA
37. Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) 38. Adhana 39. Upendo katika Ukristo na Uislamu 40. Qur’ani na Kuhifadhiwa Kwake 41. Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu 42. Kupaka juu ya khofu 43. Kukusanya Sala Mbili 44. Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara 45. Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya 46. Kusujudu juu ya udongo 47. Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s) 48. Tarawehe 49. Malumbano baina ya Sunni na Shia 50. Kupunguza Swala safarini 51. Kufungua safarini 52. Umaasumu wa Manabii 53. Qur’an Yatoa Changamoto 54. as-Salaatu Khayrun Mina -’n Nawm 55. Uadilifu wa Masahaba 56. Dua e Kumayl 57. Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu 58. Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake 59. Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata 60. Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mtume Muhammad (s) 61. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza 62. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili 63. Kuzuru Makaburi 64. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza 65. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili 66. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu 67. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne 68. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano 69. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita 70. Tujifunze Misingi Ya Dini 71. Sala ni Nguzo ya Dini 72. Mikesha Ya Peshawar 73. Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu 74. Ubora wa Imam ‘Ali na Ushia ndio njia iliyonyooka 75. Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake 76. Liqaa-u-llaah 77. Muhammad (s) Mtume wa Allah 78. Amani na Jihadi Katika Uislamu 31
TAQIYYA
79. Uislamu Ulienea Vipi? 80. Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) 81. Dhana ya Ndoa ya Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) 82. Urejeo (al-Raj’ah) 83. Mazingira 84. Utokezo (al - Badau) 85. Hukumu ya kujenga juu ya makaburi 86. Swala ya maiti na kumlilia maiti 87. Uislamu na Uwingi wa Dini 88. Mtoto mwema 89. Adabu za Sokoni Na Njiani 90. Johari za hekima kwa vijana 91. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza 92. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili 93. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu 94. Tawasali (AT- TAWASSUL) 95. Imam Mahdi katika Usunni na Ushia 96. Hukumu za Mgonjwa 97. Sadaka yenye kuendelea 98. Msahafu wa Imam Ali 99. Maimamu wa Ahlul Bait – Ujumbe na Jihadi 100. Idi Al-Ghadir 101. Kusoma sura zenye Sijda ya wajibu 102. Hukumu zinazomuhusu mkuu wa kazi na Mfanyakazi 103. Huduma ya Afya katika Uislamu 104. Sunna za Nabii Muhammad (saww) 105. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza) 106. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili) 107. Shahiid Mfiadini 108. Mwanamke Na Sharia 109. Ujumbe -Sehemu ya Kwanza 110. Ujumbe - Sehemu ya Pili 111. Ujumbe - Sehemu ya Tatu 112. Ujumbe - Sehemu ya Nne 113. Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu 114. Hadithi ya Thaqalain 115. Ndoa ya Mutaa 116. Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza 117. Ukweli uliopotea sehemu ya Pili 118. Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu 119. Ukweli uliopotea sehemu ya Nne 120. Ukweli uliopotea sehemu ya Tano 32
TAQIYYA
121. Mkutano wa Maulamaa wa Baghdad 122. Safari ya kuifuata Nuru 123. Fatima al-Zahra 124. Myahudi wa Kimataifa 125. Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi 126. Visa vya kweli sehemu ya Kwanza 127. Visa vya kweli sehemu ya Pili 128. Elimu ya Ghaibu ya Maimamu 129. Mwanadamu na Mustakabali wake 130. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Kwanza) 131. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Pili) 132. Khairul l’Bariyyah 133. Uislamu na mafunzo ya kimalezi 134. Vijana ni Hazina ya Uislamu 135. Adhana ni Ndoto au ni Wahyi? 136. Tabaruku 137. Saada Kamili – Kitabu cha Kiada cha Maadili 138. Vikao vya furaha 139. Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje? 140. Visa vya wachamungu 141. Falsafa ya Dini 142. Kuhuzunika na Kuomboleza 143. Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah 144. Mjadala wa Kiitikadi 145. Kuonekana kwa Allah 146. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza) 147. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili) 148. Ndugu na Jirani 149. Ushia ndani ya Usunni 150. Maswali na Majibu 151. Mafunzo ya hukmu za ibada 152. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 1 153. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 2 154. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 3 155. Abu Huraira 156. Vipengee kadhaa katika Swala ya Jamaa na Msikiti. 157. Mazingatio kutoka katika Qur’an - Sehemu ya Kwanza 158. Mazingatio kutoka kaitka Qur’an - Sehemu ya Pili 159. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya kwanza 160. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya Pili 161. Shia na Qur’ani – Majibu na Maelezo 162. Falsafa ya Mageuzi ya Imam Husein (a.s) 33
TAQIYYA
163. Amali za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani 164. Elimu ya Tiba za Kiislamu - Matibabu ya Maimamu 165. Uislamu Safi 166. Majlisi za Imam Husein Majumbani 167. Je, Kufunga Mikono 168. Uislam wa Shia 169. Amali za Makka 170. Amali za Madina 171. Asili ya Madhehebu katika Uislamu 172. Sira ya Imam Ali kuhusu Waasi 173. Ukweli uliofichika katika neno la Allah 174. Uislamu na Mifumo ya Uchumi 175. Umoja wa Kiislamu na Furaha 176. Mas’ala ya Kifiqhi 177. Jifunze kusoma Qur’ani 178. as-Sahifatul Kamilah as-Sajjadiyyah 179. Hayya ‘Alaa Khayri’l-’Amal Katika Adhana 180. Ukweli kuhusu Funga ya Siku ya Ashura 181. Dua za Miezi Mitatu Mitukufu (Rajabu, Shaabani na Ramadhani) 182. Uadilifu katika Uislamu 183. Mahdi katika Sunna 184. Maswali Ya Uchunguzi Kuhusu Uislam 185. Kazi na Bidii ni njia ya maendeleo 186. Abu Talib – Jabali Imara la Imani 187. Ujenzi na Utakaso wa Nafsi 188. Vijana na Matarajio ya Baadaye 189. Historia maana na lengo la Usalafi 190. Ushia – Hoja na Majibu 191. Mateso ya Dhuria wa Mtume (saww) 192. Maombolezo – Msiba wa Bwana wa Mashahidi (a.s.) 193. Shahidi kwa Ajili ya Ubinadamu 194. Takwa 195. Upotoshaji Dhahiri katika (Turathi) Hazina ya Kiislamu 196. Amirul Muuminina (‘as) na Makhalifa 197. Tawheed Na Shirki 198. Kuvunja hoja iliyotumika kutetea Uimamu wa AbuBakr 199. Adabu za vikao na mazungumzo 200. Hija ya Kuaga 201. Uwazi baina ya Maslahi na Vikwazo 202. Fadhila za watukufu watano katika Sahih Sita 203. Mdahalo baina ya Mwanachuoni wa Kisunni na Kishia (Al- Muraja’aat) 34
TAQIYYA
204. Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (as) 205. Imam Husain ni Mfumo wa Marekebisho na Mageuzi 206. Mtazamo kuhusu msuguano wa Kimadhehebu 207. Nchi na Uraia – Haki na wajibu kwa Taifa 208. Mtazamo wa Ibn Taymiyyah juu ya Imam Ali (as) 209. Uongozi wa Kidini – Maelekezo na Utekelezaji wa Kijamii 210. Maadili ya Ashura 211. Mshumaa – Shahidi na Kifo cha Kishahidi 212. Mizani ya Hekima – Hadithi za Ahlul Bait (as) – Sehemu ya Kwanza 213. Imam Ali na Mambo ya Umma 214. Imam Ali na Mfumo wa Usawa 215. Uimamu na Tamko la Kutawazwa 216. Mfumo wa Wilaya 217. Vipi Tutaishinda Hofu? 218. Kumswalia Mtume ni Ufunguo wa Utatuzi wa Matatizo 219. Maeneo ya Umma na Mali Zake 220. Nahju ‘L-Balagha – Majmua ya Khutba, Amri, Barua, Risala, Mawaidha na Semi za Amirul-Muuminin Ali bin Abu Talib (a.s.) 221. Mukhtar – Shujaa aliyelipiza kisasi dhidi ya wauaji wa Imam Husein (as) hapo Karbala 222. Mazingatio Katika Swala 223. Imam Hasan na Mfumo wa Kujenga Jamii 224. Vyakula Na Vinywaji 225. Kuelewa Rehema ya Mwenyezi Mungu 226. Tiba ya Maradhi ya Kimaadili 227. Yafaayo kijamii 228. Shia Na Hadith - Majibu na Maelezo 229. Mkakati wa Kupambanana Ufakiri 230. Mtazamo Mpya - Mwanamke katika Uislamu 231. Taqiyya Kwa Mujibu Wa Sheria Ya Kiislamu 232. Imam Mahdi Na Bishara Ya Matumaini 233. Jihadi 234. Majanga Na Jukumu La Jamii 235. Muhadhara wa Maulamaa 236. Mashairi ya Kijamii 237. Ngano ya kwamba Qur’ani imebadilishwa 238. Mwanamke Katika Harakati Za Mageuzi 239. Shia Na Sahaba - Majibu na Maelezo 240. Yusuf Mkweli 241. Hotuba Za Kiislamu Juu ya Haki Za Binadamu 242. Ugaidi wa Kifikra katika Medani ya Kidini
35
TAQIYYA
KOPI NNE ZIFUATAZO ZIMETAFSIRIWA KWA LUGHA KINYARWANDA 1. 2. 3. 4.
Amateka Ya Muhammadi (s.a.w.w) Na Aba’ Khalifa Nyuma yaho naje kuyoboka Amavu n’amavuko by’ubushiya Shiya na Hadithi
ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION KWA LUGHA YA KIFARANSA 1.
Livre Islamique
36