Tawhidi na shirki katika qur'ani tukufu

Page 1

Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page A

TAWHID NA SHIRKI KATIKA

QUR’AN TUKUFU Kimeandikwa na: Sheikh Ja’far Subhani

Kimetarjumiwa na: Amiri Mussa Kea


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page B

B


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page C

Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page C

©Haki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION 978 - 9987imehifadhiwa - 17 - 003 - 6 ©HakiISBN: ya kunakili na: AL-ITRAH FOUNDATION Kimeandikwa na: ISBN: 978 -Ja’far 9987 -Subhani 17 - 003 - 6 Sheikh Kimeandikwa na: Kimetarjumiwa na: Sheikh Ja’far Amiri MusaSubhani Kea Kimetarjumiwa na: na: Kimepangwa katika Kompyuta Amiri Musa Kea Al-Itrah Foundation Toleo la la kwanza: kwanza: Toleo Julai,2014 2014na: Kimepangwa katika Julai, Kompyuta Nakala: 2000 Nakala: 2000 Al-Itrah Foundation Toleo Julai,2015 2014 Toleolalakwanza: pili: Aprili, Kimetolewa na kuchapishwa na: Nakala: 2000 Nakala: 2000 Alitrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Kimetolewa kuchapishwa na: Simu: +255 22na2110640 / 2127555

Alitrahalitrah@yahoo.com Foundation Barua Pepe: S.L.P. 19701 es Salaam, Tanzania Tovuti:Dar www.ibn-tv.com Simu: 22 2110640 / 2127555 Katika+255 mtandao: www.alitrah.info Barua Pepe: alitrah@yahoo.com Tovuti: www.ibn-tv.com Katika mtandao: www.alitrah.info


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page D

Yaliyomo Neno la Mchapishaji………………………...............……....……..I Lengo la kuandika kitabu hiki………………............................…..2 Daraja za Tawhiid Tawhiid ndiyo Msingi wa Ulinganio wa Mitume..........................14 Mosi: Tawhiid katika Dhati………………........................14 Pili: Tawhiid katika Uumbaji…………..............................16 Tatu: Tawhiid katika Ulezi na Upangaji wa Mambo..........18 Nne: Tawhiid katika Utungaji Sheria…………….….....…25 Tano: Tawhiid katika Utiifu……………......................…..28 Sita: Tawhiid katika Utoaji Hukumu…………….….....…29 Saba: Tawhiid katika Ibada……………….....….…....…..30 Sehemu ya Kwanza – Tangulizi kumi za Msingi 1 – Shirki na Msingi wa Upinzani na Shabaha ya Mapambano ya Ulinganio wa Mitume………..................................................31 2 – Chanzo cha Shirki na Ibada ya Masanamu…............…......…32 3 – Tawhiid katika Ibada ya Mwenyezi Mungu…….....................36 4 – Sababu za Shirki katika Ibada…………....................…....…..37 I. Itikadi ya kuwepo waumbaji wengi…..…...............…......37 Fikra ya Kutofautiana kati ya Muumba na Muumbwa..........38 II. III. Upangaji wa Mambo Huachiwa Miungu Midogo….....…40


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page E

5 – Tafsiri ya Tawhiid katika Uungu na Ulezi…………....………45 6 – Je! Kunyenyekea na Kutukuza ni Ibada?.................................46 7 – Sio kila Unyenyekevu ni Ibada!...............................................47 8 – Upambanuzi wa maana Halisi na isiyo Halisi…………...…...52 9 – Je! Amri ya Mwenyezi Mungu hufanya Shirki isiwe Shirki?......55 10 – Maana ya Uungu na Ulezi………………………….....…….57 Je! Neno Ilahi lina maana ya Mwabudiwa?...................................62 Maana ya Rabbi (Mola Mlezi)………………………….....…..…68 Natija ya Mada Hii……………………………………….......…..78 Sehemu ya Pili – Maelezo kuhusu Maana Halisi ya Ibada.......…80 1 – Maana Tatu za Ibada………………………………….…....…81 Maana ya Kwanza……………………………………….….…..81 Swali na Jibu…………………………………………….….......86 Maana ya Pili……………………………………………......….89 Maana ya Tatu…………………………………………….....…93 2 – Nini Maana ya Tafwiidhi?........................................................96 Sura ya Kwanza………………………….................….97 Sura ya Pili…………………………….....................…99 3 – Hakuna uhusiano kati ya Uenezaji Miungu na Ukanushaji wa Mungu Mkuu.............................................................................…101 4 – Ufupisho wa Maneno…...................………………..……….103 Sisi na Mwandishi wa Kitabu cha Al-Manaar……............……..106 1. Waumini wa Sayari………….....................................…113 E


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page F

2. 3.

Waumini wa Maunbo (Vinyago)………............………114 Itikadi za Waarabu wa zama za Jahilia……........…..…114

Sehemu ya Tatu…………………….........................………..…125 1. Mawahabi na Vigezo vya Tawhiid na Shirki……...............….125 Yusuf (a.s.) na Uwezo wa Ghaibu………………….......…128 Musa (a.s.) na Utawala wa Ulimwengu…………..........…129 Watu wa Suleiman (a.s.) na Uwezo wa Ghaibu…….....…130 Suleiman (a.s.) na Uwezo Juu ya Ulimwengu…...….....…131 Isa (a.s.) na Uwezo wa Ghaib……………………...…..…132 Maelezo mengine ya Mawdudi….…………………......…138 Hitimisho…………………………………...............……..142 2. Je! Sababu ya kawaida na isiyo ya kawaida ni kigezo cha Tawhiid na Shirki?........................................................................142 Ushuhuda wa Qur’an…………….....................................….145 Kufunya Tawassuli kwa sababu zisizokuwa za Kimaumbile.....148 3. Je! Uhai na Kifo huingia katika dhana ya Tawhiid na Shirki?...........................................................................................152 4.Je! Uwezo na kutokuwa na uwezo ni vigezo vya Tawhiid na Shirki?...........................................................................................158 Mjadala kuhusu maoni haya………..................……………160 5.Je! Kuomba mambo yasiyo ya kawaida ni Shirki?...................163

F


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page G

Sehemu ya Nne – Itikadi za Mawahabi………................……167 Mchakato katika kuukubali Uislamu…………...........………167 1. Je! Kuomba ponyo kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu ni Shirki?......................................................................................177 2. Je! Kuomba Shufaa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu ni Shirki?...........................................................................................180 Mawahabi na Uombaji wa Shufaa……............……………183 3. Je! Kumwomba msaada asiyekuwa Mwenyezi Mungu ni Shirki?...........................................................................................194 Mwandishi wa Al-Manaar na maelezo yake kuhusu Uombaji Msaada….............................................................................195 Ukosoaji wa Nadharia ya Tatu…………………….....……203 4. Je! Kuwaomba watu wema ni kuwaabudu wao?......................204 Swali na Jawabu……………………..........……………….216 Muhtasari wa Mada………………………..………………217 5. Je! Kutukuza mawalii wa Mwenyezi Mungu na Kuwakumbuka wao ni Shirki?...............................................................................218 I. Kufanya sherehe za kumkumbuka Mtukufu Mtume (s) ni kumtukuza na kumnusuru…………….....………………..220 II. Kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa Mtume (s) ni kunyanyua Utajo wa Mitume…………….....………….…223 III. Kuteremshwa meza ya chakula kutoka mbinguni na siku G


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page H

hiyo kufanywa kuwa siku ya Idd……….............……..….223 6. Je! Kutabaruku kwa athari za Mtume (s) na Mawalii ni Shirki?...........................................................................................224 Kujenga Juu ya Makaburi……………....…….…….......……….226 Mawahabi na Hadithi ya Abu Hayyaj………………..…..……...230 Kuzuru Makaburi……………………………………..........……239 Kuswali Makaburini………………………………….………….245 Kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu……………....………248 1. Kiapo kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu…….……...….248 2. Viapo kwa Kiumbe au kwa Haki yake….....................…251

H


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page I

Tawhid na Shirk

NENO LA MCHAPISHAJI Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabu kiitwacho, at-Tawhid wa ‘sh-Shirk fi ‘l-Qur’ani ‘l- Karim kilichoandikwa na Sheikh Ja’far Subhani. Sisi tumekiita, Tawhid na Shirk. . Kitabu hiki kinajadili kwa mapana na marefu suala la umoja wa Waislamu na kuwakosoa wale wanaojaribu kuleta mfarakano na fitna katika dini kwa kutumia madhehebu, hususan wale wanaowashambulia Mashia katika vitabu vyao kwamba wao (Mashia) ni makafiri. Mwandishi katika kitabu hiki anaelezea imani ya Shia katika Tawhid na jinsi wanavyojiepusha na shirk nukta ambazo wapinzani wa Shia wanazitumia kuupotosha ukweli juu ya Ushia. Wapinzani hawa hawajishughulishi kusoma vitabu vya Shia wala kusoma majibu yanayotolewa juu ya vitabu vyao, bali kazi yao ni kurudiarudia tu yale yaliyotapikwa na watangulizi wao na kupotosha Umma kwa kalamu zao zenye sumu. Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote, ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni mambo ambayo hayana nafasi tena katika akili za watu. Kutokana na ukweli huo, Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili. Tunamshukuru ndugu yetu, Amiri Mussa Kea kwa kukubali jukumu hili la kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki I


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page J

Tawhid na Shirk kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake. Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa ni changamoto kubwa kwa wasomaji wetu. Mchapishaji: Al-Itrah Foundation

J


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page K

K


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 1


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 2

Tawhid na Shirk Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu

LENGO LA KUANDIKA KITABU HIKI Siku hizi Umma wa kiislamu unashuhudia mambo mengi ambayo huchochea fitina na machafuko, vile vile huleta mifarakano baina ya Waislamu na kuondoa mshikamano na umoja wao. Hushuhudia taasisi na asasi mbalimbali zikiwatuhumu na kuwasingizia Shia Imamiyyah juu ya itikadi zao madhubuti za Uislamu. Hali kadhalika wanawahujumu na kuwashambulia pamoja na kuwabebesha tuhuma nzito nzito bila ya adabu wala huruma hadi mtu anakuta kwamba yaliyosambazwa - katika kipindi cha miaka mitano ya karibuni yanazidi maradufu yaliyosambazwa katika miaka mia moja katika kushambulia kundi hili kubwa la Kiislamu ambalo ni moja ya tano ya umma wa Kiislamu, na ambalo limejulikana kwa juhudi zake kubwa za kuutumikia utamaduni na maarifa ya Kiislamu chini ya uongozi wa Maimamu wao na maualamaa wao na jumuiya zao na vipaji vyao mbalimbali. Ambapo katika kipindi cha miaka mia moja ya hivi karibuni hayajashuhudiwa mashambulizi dhidi ya itikadi ya Shia Imamiyyah isipokuwa mashambulizi sita au saba nayo ni:1. Muhadharaat fi Tarikh Umamil-Islamiya cha Khidhiri, 2. Sunnatu wa Shia cha Rashid Ridha Mwandishi wa kitabu cha Al – Manaar, 3. Swira’a (mapambano) baina Wathania wal-Islam cha Qaswiimi, 4. Fajr Islam wa Dhuhahu wa Dhuhruhu cha Ahmad Amiin, 5. Jaulat fi Rubu ‘ui sharqi Adna cha Muhammad Thabit Misrii, 6. Al-Washi’ah fi Naqdi Aqaid Shi’a cha Musa Jaarullah; 7. Al-Khututul-Ariidha cha Muhibbu Diin Khatib, 8. Tabdiid Dhulam Watanbiih Niyam cha Jabhani na vinginevyo, na hili ni jambo la kawaida kwa asiyejua itikadi na madhehebu ya ndugu yake. 2


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 3

Tawhid na Shirk Haya na kwa kuongezea kwamba mengi ya mashambulizi haya yanategemea vitabu vya mustashiriqiina na maadui wa Shia bali na Waislamu kwa ujumla, na hawa walipotambua makosa ya waliyoyaandika dhidi ya Shia Imamiyyah na itikadi zao waliomba radhi,1 walijuta na kusahihisha waliyoyasema. Wanachuoni na wasomi wa Kishia walisimama kidete kukosoa vitabu hivi na kuweka wazi itikadi sahihi za Shia Imamiyyah, misingi yake na matawi yake, hapa tunataja baadhi yake kwa mfano tu: 1. Aswilu Shi’a wa Usuuliha cha Imam Akbar Sheikh Muhammad Husein Kashif Ghitwai. 2. al-Muraajaat cha Imam Mujahhid Sayyid Sharaf Diin. 3. Tahta Ra yat Haki cha Allammah Abdullah Sabiti. 4. al-Ghadiir Juz. 3 cha Allammah Hujja Sheikh Amiini. 5. Ajwibat Musa Jaarullah cha Imam Sayyid Sharafu Diin Amili. 6. Aqaid Imamiyyah cha Allammah Hujjat Mudhafar. 7. Maa khatib fi khututil Ariidha cha Allama Sheikh Hujjat Swafi. 8. Ma’a khatib fi khututi cha Allama Sheikh Suleiman Khaqani, na vitabu vinginevyo ambavyo vimeandikwa kuhusiana na kadhia hiyo. Nasema: Hali hiyo haikushuhudiwa katika karne iliyopita isipokuwa idadi hiyo ndogo katika kujibu tuhuma ambazo zilikuwa zikizuliwa juu ya itikadi ya Shia Imamiyyah, vitabu vingi viliandikwa kwa lengo la kushambulia kundi hili la kiislamu na itikadi zake. Walifanya hivyo kutokana na chuki zao binafsi, kwa hakika ilifikia idadi kubwa ya vitabu vipatavyo arubaini baada ya mapinduzi ya Kiislamu ya Iran. 1. Kama alivyofanya hivyo Ahmad Amiin Mmisri, mwandishi wa kitabu kiitwacho Fajr Islam, Imam Akbar Sheikh Muhammad Hussein Kashif Ghatwai amesema katika kitabu Aswilu Shii'a wa Usuuliha Uk. 82 chapa ya Cairo mwaka 1377 H - 1958 A.D: Ahmad Amiin baada ya kusambaza nakala kwa watu wa sehemu mbalimbali na kuwafikia wanachuoni wa Najaf, yeye na wakufunzi wapatao thelathini, wanafunzi pamoja na watu wengine kadhaa, walihudhuria mihadhara mbali mbali na kudurusu vitabu kadhaa wakadha katika maktaba zilizosheheni maelfu ya vitabu na vingi kati ya hivyo ni vya Ahlu-Sunna katika mji wa Najaf, wakazi wake wamebobea katika elimu za aina mbalimbali, na maktaba za Cairo kubwa havina vitabu vya kishia isipokuwa vichache mno, ndiyo watu hawana elimu na Ushia wala hawajui lolote kuhusiana na Shia, na wao huandika mengi kinyume walivyo!! 3


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 4

Tawhid na Shirk Baadhi vinashambulia itikadi za kundi hilo pamoja na watu wake na vingine vinatuhumu hadithi zao na vitabu vyao vya hadithi, na vingine vinashambulia rai na maoni yao ya kifiqihi ambayo hutegemea Qur’an na Sunna, na vingine kudiriki kuwakufurisha na baadhi yake vinawatuhumu kwa umajusi na hata kuwaita washirikina n.k. Hali ya kuwa chanzo cha itikadi za kundi hili kubwa la Waislamu, fatwa zao za kifiqhi na nyinginezo ni kutoka ndani ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu (s.w.t) na Sunna sahihi za Mtume (s.a.w.w) ambazo hunakiliwa kupitia watu waaminifu na waadilifu,2. watu wetu wameshuhudia ukweli wao na umakini wao, kusihi imani yao na msimamo wao, na vinara wao ni Ahlul-Bayt Nabii watoharifu ambao wamesifiwa na waislamu wa kale kwa wingi wa fadhila, utohara, utukufu na ubora na wakaandika maelfu ya vitabu kuhusiana na hayo. Unaona mchezo gani unaochezwa hapo? au kuna njama fulani juu ya jambo hilo? Kwa nini ziwepo hujuma kubwa hizo juu ya kundi ambalo usafi na usahihi wake upo dhahiri, bila shaka hizo ni mbinu na mikakati ya mayahudi katika kuusambaratisha Uislamu, kwa kuleta chokochoko na kuchochea mifarakano, migongano na mizozo bila wao wenyewe kujua. Kwa nini watu hawajiulizi juhudi hizo zilikuwa na lengo gani kama sio kuwagawa, kuwasambaratisha na kugombanisha kati ya vikundi vya kiislamu na wanaelekea wapi? Je! Hali hiyo itawaunganisha waislamu na kuwa sababu ya kupata maendeleo katika umma wa kiislam? Kwa nini mwanya huo ulitokea katika umma wa kiislamu? Iweje waislamu wakufurishane, wawaone kuwa washirikina na kuwaita waislamu wenzao majusi? Je! Huko sio kuwatumikia watu wa nchi za Magharibi? 2. Ndio, vitabu vya kisasa vinavyozingatiwa kwa Shia kama vile Sahihi na Sunnan kwa Ahlu Sunna, ni hoja kwa yale ilivyonavyo, iwapo sanad zake ni sahihi na kutimia dalili zake ni timamu, haiwezekani kutumia hoja kwa riwaya dhaifu au zenye kupingana na akida ya watu katika vitabu hivyo na ufafanuzi wake utakaoelezwa mahala pake. 4


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 5

Tawhid na Shirk Iweje Mashia Imamiyyah watuhumiwe tuhuma nzito kama hizo pamoja na kuandaa na kuendesha makongamano mbalimbali kuhusu Ushia kwa kutolea mfano vitabu vya hadithi vya Kishia hufanyiwa kazi na hutegemea ambazo ni hadithi sahihi tu, ama zile dhaifu au zenye kupingana na itikadi sahihi huachwa na hazitendewi kazi. Na kielelezo tosha kwa kundi ambalo liko kusini mwa Lebanon ambalo linakabiliana vikali na mazayuni, hali ambayo imefanya watu watafakari Ushia na itikadi zake ambazo huwafanya wawe madhubuti na kutembea kifua mbele na kutotishika hata kidogo na mayahudi waporaji. Ikiwa watu wanadiriki kuwasingizia Mashia ni jambo la hatari sana kwani kundi hilo linaongozwa na Ahlul-Bayt ambao ni wakamilifu, waadilifu na waongofu, wamenusurika na upotovu na wako sambamba na Qur’an mpaka Siku ya Kiyama na hatimaye kuingia peponi, kama alivyosema bwana Mtume (s.a.w.w) katika hadithi ya Vizito Viwili ambayo imepokewa na Mashia na Masunni. Kundi hilo lilianzishwa na kuasisiwa na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu pale aliposema:

“Ali na wafuasi wake ndio wenye kufuzu.”3 Inakuwaje wakufurishwe mamilioni ya waislamu, wasomi, wataalamu na watu wenye kutumia akili n.k. Kundi hilo linahistoria kubwa katika kutetea Uislamu pamoja na waislamu. Nasema: Iwapo mambo hayo yamefanywa kwa ajili ya dini ingekuwa bora yaelekezwe katika mifumo ya Ujamaa na Ubepari ambayo ni hatari sana katika miji yetu katika nyanja mbalimbali za maisha, kwani kila nchi ina walinzi na wasaidizi ambao hutetea na kuhami nchi yao. 3. Tafsir Durrul-Manthur juz. 6 uk. 379 cha Suyutwi chapa ya Beirut katika mkia wa tafsiri ya maneno ya Mola aliposema: "Hakika wale walioamini na kutenda mema, hao ndio wema wa viumbe."

5


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 6

Tawhid na Shirk Je! Halikuwa ni jambo la busara kuelekeza mashambulizi katika mifumo hiyo ya kiitikadi ambayo ndio hatari kubwa zaidi inayotishia nchi za Kiislamu ndani na nje kiasi kwamba ina wafuasi na wasaidizi bali hata serikali ndani ya Ulimwengu wa Kiislamu? Je! Halikuwa jambo zuri kuelekeza mashambulizi dhidi ya kundi hili hatari la kilahidi ambalo linapinga kila kitu kuanzia na itikadi, akhlaq, amani, ukombozi na kumalizia uhuru, na wala hawaamini kila kitu kinachohusiana na dini? Je! haikuwa ni vizuri zaidi kwa wale ambao wanajidai kuwa wana uchungu na dini na kutoa mamilioni ya riali na dola katika njia ya kufarikisha baina ya makundi ya waislamu kwa njia mbalimbali kuwakusanya wanachuoni wakubwa na wasomi mashuhuri wa kiislamu na kufanya semina na makongamano mbalimbali na kujadili wanachoweza kufanya katika kukabiliana na harakati za kilahidi za Carl Marx ambazo zimeenea hadi katika miji mitakatifu ya Makka na Madina, na kuathiri vijana wake na sehemu takatifu nyinginezo? Kwa nini watu hawa hawatafakari – kama ni wa kweli – katika baadhi ya nchi za Kiislamu ambazo zinahistoria kongwe katika Uislamu lakini hivi sasa zimeshageuka na kuwa ngome za Ujamaa, baadhi yake zimeshatangaza kuwa Ujamaa ndio mfumo wa utawala wake, na nyingine zimekataza wananchi wake kufunga na nyingine zimedharau Sunna tukufu za Mtume (s.a.w.w), na mengineyo kati ya mambo yanayopinga Uislamu. Hivi sasa zipo hatari mbili ambazo huhatarisha umoja wa waislamu nazo ni: 1. Mayahudi ambao huungwa mkono na kusaidiwa kwa hali na mali na nchi za Magharibi. 2. Ujamaa ambao unapinga kuwepo mungu ambao umeathiri Mashariki, mbinu zao ambazo huzitumia ili kufikia malengo yao ni:

6


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 7

Tawhid na Shirk i. Kueneza ufisadi wa kimaadili baina ya vijana wa kiislamu. ii. Kueneza hofu na hali ya kujihisi kushindwa na kutoweza kufanya linalowezekana. iii. Kuwafanya wabaki nyuma kielimu, kitamaduni, kiuchumi n.k iv. Kuangamiza na kupotosha itikadi zao za kidini, kumwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Qiyama ambayo ndio siri ya kubakia kwao hadi hivi leo, kuvumilia kwao katika kukabiliana na mawimbi na vimbunga vikali na mengineyo. Hebu chunguza watu hao walifanya nini baada ya kudhihiri Ushia ambao ulikuwa ukiongozwa na wananchi wa kiislamu wa Iran ambao walikuwa tishio kwa Ukoloni, masilahi yake na ya vibaraka wake, na je wamefanya nini katika kukabiliana na hatari hizi mbili, na wana nguvu na uwezo ambao haujui isipokuwa Mwenyezi Mungu? Je! wamezifedhehesha nchi za Magharibi na kuzifanya kuwa adui, wamezipiga vita, na kuzitenga kama walivyozifanyia uadui nchi za Mashariki na kuzitenga kwa kiasi fulani? Je! walichukua msimamo madhubuti kuwaelekea Mayahudi ambao wamewadhalilisha Waislamu na waarabu mara kadhaa na bado wanaendelea hadi leo? walichokifanya ni kuanzisha makubaliano ya amani na Israil, wakahalalisha matendo yao na kutambua dola ya Israil katika ulimwengu wa Kiislamu, je! Hawakufanya hivyo? Kwa nini walielekeza koleo zao kubomoa itikadi sahihi za Shia ambazo asili yake ni Uislamu, zimechukuliwa kutoka kwa Ahlul-Bayt wa Mtume? Je! Sio Mashia ambao wamewafukuza wamarekani nchini Iran na kumteketeza kibaraka wao ambaye amedhalilisha waarabu na kuwanusuru Mazayuni?! Je! Sio Mashia waliowatimua Mayahudi kutoka Kusini mwa Lebanon, wakafikwa na udhalili na kupatwa na fedheha kubwa ambayo hawatoisahau kamwe? 7


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 8

Tawhid na Shirk Je! Sio msimamo na harakati za Mashia ambazo ndio zilizosababisha nchi za Magaribi na Mashariki kufanya zikose usingizi na kuwagharimu hasara kubwa na kufanya Waislamu waheshimiwe na kupata hadhi? Je! kupigwa vita Mashia leo si kwamba hakuna sababu ila ni kwa kuwa wao walizipatia nchi za Magharibi na Mashariki hasara na kushindwa kwao mara kwa mara na wamekuwa ni hatari kubwa kwa masilahi ya wageni katika nchi za kiislamu? Je! Sio Mashia ambao wamekuwa kikwazo kikubwa juu ya maslahi ya Marekani nchini Saudia, nchi za Ghuba, Misri, Lebanoni, Irak na sehemu zingine ambazo wanapatikana Mashia, au wapo wale ambao huunga mkono harakati za Mashia za mageuzi ambazo hupinga maonevu na udhalilishaji, na wakakataa serikali za vibaraka na dhalimu, na wanapinga aina zote za dhuluma huku wakibeba ujumbe usemao: “Usikubali kudhalilishwa na wala usiwategemee wale wenye kudhulumu” na “Mna nini nyinyi hampigani katika njia ya Mwenyezi Mungu na kuwatetea wanyonge” na “Kufa kishupavu ni bora kuliko kuishi katika udhalili?” Inakuwaje watu hao huchapisha kitabu na kukipa jina la (Wajaa Daurul–Majuus) yaani imefika zama za majusi waabudia moto. Hivi wanaposema waabudia moto wanawalenga watu gani? Je! Ni Wairani ambao wamejenga na kuupa nguvu Uislam na kupeperusha bendera yake, wakafasiri kitabu cha Mwenyezi Mungu, wakakusanya hadithi chungu nzima, wakatoa wasomi mashuhuri na watunzi wa vitabu sahihi sita kwa Ahlu Sunna, kama vile Imam Bukhari, Imam Muslim, Tirmidhi, Nasaai na Ibn Maaja? au wanamaanisha majusi ni wale ambao wanaomfuata Ali (a.s.) ambao kwa hakika wamefuata maneno ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) – kama alivyopokea Suyutwi katika tafsiri yake Durrul-Manthur – katika maana ya Aya hii: “Hakika wale walioamini na kutenda mema hao ndio wa bora wa viumbe” 98:7 Mtume (s.a.w.w) akasema:-

8


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 9

Tawhid na Shirk “Ewe Ali wewe na wafuasi wako ndio wa bora wa viumbe.” Je! Wanakusudiwa majusi wafuasi wa Ali ambao wamekusanya na kuandika hadithi za bwana Mtume (s.a.w.w) na Ahlul-Bayt wake watoharifu katika maelfu ya vitabu, na wakaandika na kutafsiri Qur’an tukufu, vile vile wakaandika vitabu mbalimbali vya Itikadi za kiislamu, wakamtakasa Mwenyezi Mungu kutokana na kila mapungufu, na kuwaepusha Mitume na kila aina ya aibu na wakatilia mkazo uadilifu wa Imam na Khalifa ambaye atasimamia mambo ya kiislamu kwa uaminifu na msimamo madhubuti? Ikiwa watu hao wanawatuhumu Mashia kuwa ni watu waliopotoka, na imethibiti imani yao sahihi katika makongamano mbalimbali yaliyofanywa na kushirikisha watu tofauti na kujibiwa maswali na mambo yenye utata, na hatimaye kufikia azimio la kuwa wao ni waislamu na itikadi zao ni sahihi zaidi, ni dhahiri shahiri Mashia huishi vizuri na ndugu zao waislamu kwa upendo na mahaba, husaidiana na hushirikiana katika shida na raha. Kwa nini hawa wenye kuchochea fitina na mitafaruku baina ya Shia na Sunni na kutumia fedha nyingi ili kusambaratisha umoja wa kiislamu, badala yake wasingefanya semina na warsha mbalimbali ili kuwaunganisha waislamu, kama walivyofanya majadiliano ya kielemu kati ya mwanachuoni wa kishia Imam Sharafud-Diin na Mwanachuoni wa Kisuni Imam Saliim Bushiiri Sheikh wa Azhar, wakaelimishana, wakaondoa na kuepusha mambo yenye utata na hatimaye maadui wakawa marafiki, Je! Hilo linazingatiwa? Hapana shaka wanachuoni wa Kishia wako tayari kushiriki katika makongamano kwa lengo la kuleta umoja wa kiislamu na waislamu wote kuwa kitu kimoja. Hiyo ndio kazi ya Mtume (s.a.w.w) ya kuunganisha umma, kupatanisha watu na kufanya wapendane huku akisema:

9


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 10

Tawhid na Shirk “Uwezo wa Mwenyezi Mungu upo pamoja na jumuiya.” Je! Inafaa kisheria kuwatenga watu kwa tofauti za kifiqhi na kimaoni au kutofautiana kifikra hata kama tufanye fikra hizo sio sahihi (bila shaka ni sahihi kwani zimetoka kwa Mtume (s.a.w.w) na Ahlul-Bayt wake), je! Inajuzu kuhalalisha kumwaga damu zao? Na kuhukumu kuwa madhehebu yao ni batili na kuchoma moto misikiti yao ambayo ni nyumba za Mwenyezi Mungu kama ilivyotokea Pakistani? Hali ya kuwa madhehebu manne ya Kisunni yanatofautiana mno kati yao kuliko madhehebu ya Shia Imamiyyah ukilinganisha na madhehebu mengine ya kiislamu, pamoja na hivyo hawakufurishani baina yao. Wapendwa waislamu njooni tuwe kitu kimoja, tuondokane na ujinga tuishi na wala tusifanye yale yanayowapa matumaini Mazayuni na mabwana zao Wamarekani na watu wa Magharibi na wale wanaowaunga mkono miongoni mwa Warusi na kambi ya walahidi. Njooni katika kalima moja ya Tawhiid ambayo hutukusanya pamoja wala tusifarikiane na kufarikishana. Njooni tuhukumiwe na sharia moja na tutumie akili zetu ambazo Mola Muumba ametuzawadia, tufungue mlango wa majadiliano na tuwe huru katika dini yetu, kama hatukuwa huru kifikra, kimawazo, kiutamaduni, kiuchumi na kisiasa bila shaka hiyo ni imani dhaifu, Imam Husein (a.s.) amesema:

“Hata kama mkiwa hamna dini wala hamuogopi Siku ya Kiyama basi kuweni huru katika dunia yenu”. Njooni tuwape heshima Ahlul-Bayt wa Mtume ambao Mwenyezi Mungu (s.w.t) amewatoharisha kutokana na uchafu, maasi na madhambi, tuwe pamoja nao, na tuwaheshimu wafuasi wao kwa kufuata haki, aidha tuondoe chuki, kasumba na kung’ang’ania mambo au ada za watu wa zama za ujinga. 10


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 11

Tawhid na Shirk Je! Iweje watu washambulie kundi hili na kulituhumu kwa mambo yasiyo sahihi na hata kufikia kuwatukana?! Ili kuthibitisha hayo tuliyoyaeleza ambayo yapo katika vitabu hivyo ambavyo huhujumu na kuwashambulia Mashia Imamiyyah hadi hivi leo, tunanukuu baadhi ya maneno yao ili yawe dalili na ushuhuda wa yale tuliyoyasema, tunasema: Hakika wa mwisho kati ya maadui hao wa sera ya Umoja wa Madhehebu na Ukuruba baina ya Waislamu, ni yule aliye kama mbwa mwitu mshambuliaji, yule aliyejaa kila lugha chafu, ambaye anaitwa (Ihsan ilahi Dhahir) ambaye aliazimia kuhuisha uadui baina ya Waislamu na kusambaratisha umoja wao, alijaribu kufanya kila aliwezalo ili kubatilisha itikadi sahihi za Shi’a kwa kurejea vitabu ambavyo vinawatukana na kuwakufurisha Mashia, au kuwazulia mambo ya uongo ili watu wawaone sio Waislam, na hapa tunaonyesha moja ya mambo aliyowazulia Mashia amesema: “Na ama kuhusu (Imam) wa kumi na mbili wa ndoto, yatosha kusema kwamba wao wenyewe wanasema kinaga ubaga katika vitabu vyao kwamba ’hajasisitizwa wala kupatikana, na wala kuonekana’ ijapokuwa ametafutwa sana na kuchunguzwa sana.... …”!!4 Sisi tunamuuliza muongo huyu: Maneno hayo ameyatoa wapi ni kitabu gani ambacho ametegemea madai yake hayo? Imepokewa kutoka kwa Bakra ambaye ni babu wa bwana huyo; wamekubaliana kwamba uzawa wa Imam Mahdi Al-Muntadhar Imam wa kumi na mbili ambaye habari zake zimeelezwa na bwana Mtume (s.a.w.w) amezaliwa mwezi kumi na tano Shaaban mwaka 255 A.H, wakataja majina ya wapokezi wa hadithi hiyo ambayo wamepokea kutoka kwa watu wa nyumba ya mzazi wake zama za udogoni, kisha wakataja habari na hadithi nyingi zenye kueleza habari zake na mabalozi wake katika zama za ghaibu ndogo, yaani kuanzia mwaka 260 hadi mwaka 329 A. H. kama ambavyo wameelezea nyaraka zake na barua zake na wale waliobahatika kumzuru katika vitabu vyao vilivyotungwa mahususi juu ya Mahdi, navyo ni vingi. 4. Shi'a wa Ahlul-Bayt Uk. 294 na rejea Uk. 244. . Shi'a wa Ahlul-Bayt Uk. 294 na rejea Uk. 244. 11


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 12

Tawhid na Shirk Na imani hiyo sio ya Mashia pekee (yaani imani ya kuzaliwa Imam Mahdi) bali imekubaliwa na kuaminiwa na wanachuoni wakubwa wa Ahlu Sunna wal-Jamaa na wakasema wazi kuhusiana na mazazi yake katika mwaka huo, idadi ya waandishi ambao wameandika kuhusu uzawa wake inavuka mia moja, na hivi sasa tunataja majina ya vitabu vyao kwa urefu. Habari ya Imam Mahdi ni mutawatir, zimepokewa kwa njia nyingi na sahihi, zipo katika vitabu Sahihi na Musnad, wala hakuna yeyote awezaye kukanusha tangu hapo kabla na mpaka hivi sasa hata kama zipo habari tofauti tofauti kuhusu kuzaliwa kwake. Mwandishi huyo anaandika vitu asivyovijua, kwa hakika ni mjinga wa kila kitu hata hali ya kujiona kwake yeye ni mwandishi bingwa. Ni ajabu anajifaharisha kuusingizia umma wa kiislamu mambo ambayo hayana ukweli aidha ni uzushi na udhaifu mkubwa kuzitumia hadithi dhaifu au zenye kupingana na kukinzana ndani ya vitabu vyao. Je! Inasihi na ni haki kulihusisha kundi kubwa la watu miongoni mwa Waislamu na mambo ya uzushi na potofu, kuyaandika vitabuni bila ya kuyafanyia utafiti wala kuwa na ushahidi wowote? Na lau inasihi hivyo (na haitosihi kamwe) ingesihi kuwatuhumu Ahlu Sunna kwa upotoshaji na ubadilishaji wa mambo kwa kuwepo hadithi nyingi katika vitabu vyao zenye kujulisha hayo na yanayofanana na hayo, inakutosha kurejea yale aliyoyaandika Qurtubi katika tafsiri yake kuhusiana na utafiti alioufanya katika Sura Ahzab amesema: Sura hii ilikuwa inalingana na sura Baqarah, ilikuwepo Aya ya mzinifu kupigwa mawe hadi kufa nayo ni hii: “Mtu mzima wa kiume na wa kike watakapozini wapigwe mawe mpaka wafe, ni adhabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Mwenye hekima.” Imetajwa na Abu Bakr na Ambari kutoka kwa Ubay bin Ka’b.5 Na kama ingelisihi kutolea hoja hadithi hiyo kuhusu itikadi ya watu inge12


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 13

Tawhid na Shirk tolewa hoja katika kuthibitisha mfano wa hadithi hizo katika vitabu vya hadithi na tafsiri katika kauli ya ubadilishaji wa maneno ya Mwenyezi Mungu kwa Ahlu Sunna. La hasha, sisi sio miongoni mwa wale waandishi ambao hupewa ujira fulani ili kuuza akhera yao kwa dunia yao, kwa ajili hiyo hawezi kutolea dalili mfano wa hadithi hizo potofu kwa Ahlu Sunna, bali wapo wengi wenye kubwabwaja na kusema wayapendayo bila kujali lolote. Sio jambo la uficho kwako mpendwa msomaji kwamba vitabu mfano wa hivyo vipo ambavyo Mawahabi wameviandika, na hutoa fedha nyingi ili kufikia malengo yao, huchapishwa na hutolewa bure kwa lengo la kuwagombanisha Waislamu. Vitabu vingi vya aina hiyo hutoa shutuma kali na kuwasingizia Mashia Imamiyyah kuwa ni washirikina katika ibada na kuupotosha umma wa kiislamu juu ya ukweli, hujiona kuwa wao ndio Waislamu sahihi kuliko Waislamu wengine, kwamba wao ndio wenye imani sahihi... Kwa hivyo katika kitabu hiki tumejaribu kupambanua suala la Tawhiid na Shirki, tumelitatua suala hili ambalo lilikuwa likisumbua mno umma kwa muda wa karne mbili na nusu, huenda Waislamu wakafaidika, hasa hasa wale walioathiriwa na kadhia hiyo, aidha kushughulishwa kifikra juu ya jambo hilo, hatutaki ujira kutoka kwa mtu yeyote isipokuwa kuleta wema kwa kadri itakavyowezekana, na Mwenyezi Mungu (s.w.t) ndiye mkusudiwa wa yote. 29 Shaban 1405 Hijiria.

5. Tafsir Qurtubi Juz. 14 Uk. 113 chapa ya Afsat Daru Ihyaa Turaath Arabi Beirut. (Na sisi tumeacha kunukuu hadithi zingine kutokana na mioyo kuona kinyaa). 13


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 14

Tawhid na Shirk

DARAJA ZA TAWHIID Tawhiid ndiyo Msingi wa Ulinganio wa Mitume: Tawhiid na kupinga Shirki ni miongoni mwa masuala muhimu sana ya itikadi ambayo ndiyo chimbuko la mafundisho ya dini, aidha inazingatiwa kuwa ni chanzo cha mafundisho na maarifa matukufu ya Mwenyezi Mungu, ambayo Manabii na Mitume wa Mwenyezi Mungu wamepewa katika vitabu walivyokuja navyo. Suala la Tawhiid na Shirki ni kati ya mambo ambayo Waislamu wote wamekubaliana, na wala hakuna yeyote aliyetofautiana na wenzake kuhusu asili yake, tangu zama za kale wanampwekesha Mwenyezi Mungu (s.w.t) katika dhati yake, vitendo na ibada. Waislamu wote wanaamini kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t) ni mmoja katika Dhati Yake hana mfano wala anayefanana naye, naye ndiye Mtendaji wa hakika na Muumbaji wa kila kitu, hakuna muumbaji na mtendaji kama Yeye, anafanya kila kitu na anaumba kiumbe akipendacho kwa uwezo na utashi Wake, vivyo hivyo hakuna anayestahiki kuabudiwa asiyekuwa Yeye kwa hali yoyote ile, hayo yote yanaungwa mkono na Qur’an, Sunna, Akili na Ijmau. Tawhiid ina daraja na viwango kadhaa ambavyo vimeelezwa kwa marefu na mapana na wanachuoni wa kiislamu ndani ya vitabu vyao vya itikadi na imani, katika kitabu hiki tutaeleza kwa muhtasari, aidha tutarudufu kila kigao kuhusiana na ushahidi wake kutoka katika Qur’an tukufu. Lakini tutatilia mkazo zaidi suala la (Tawhiid katika ibada) ambalo huwa ni amana kwa baadhi ya watu, tunasema Tawhiid ina daraja nyingi nazo ni: Mosi: Tawhiid katika Dhati Na makusudio yake ni kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t) hana mfano wala mwenye kufanana naye katika kila kitu, hayo yanajulishwa na maneno ya Mola Manani na dalili za kiakili pia. Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema: 14


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 15

Tawhid na Shirk

“Muumba mbingu na ardhi. Amewajaalia mke na mume katika nafsi zenu, na katika wanyama howa dume na jike, anawazidisha namna hii. Hakuna chochote kama mfano wake. Naye ni Mwenye kusikia Mwenye kuona.” (42:11) Anasema tena:

“Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa pekee. Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kukusudiwa kwa haja. Hakuzaa wala hakuzaliwa. Wala hana anayefanana naye hata mmoja.” (112: 1-4) Anasema tena:

“Yeye ni Mwenyezi Mungu mmoja, Mtenza nguvu.” (39:4) Na Aya zinginezo ambazo zinaelezea jambo hilo, ama kuhusu dalili ya kiakili katika kadhia hii ziko nyingi ambazo hubatilisha Uwili na Utatu, mwenye kupenda ufafanuzi zaidi arejee vitabu ambavyo vimeandikwa kuhusiana na kadhia hiyo.6

6. Na ufafanuzi wa malezo haya umekuja kuhusiana na aina hii ya Tawhiid na aina na daraja nyinginezo katika asili ya kitabu "Mafahiimu Qur'an fi Maalim Tawhid Uk. 274" rejea kwa kupata maelezo zaidi. 15


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 16

Tawhid na Shirk Pili: Tawhiid katika Uumbaji Makusudio yake ni kwamba hakuna chochote kilichopo isipokuwa kimeumbwa na Mwenyezi Mungu (s.w.t) kama vile bahari, madini n.k. Wala hakuna mtendaji mwenye kujitegemea mwenyewe ila Mola Muumba, na vitu vyote vilivyopo vikiwemo nyota, ardhi, milima, bahari, madini, mawingu, radi, vimbunga, Malaika, Majini ni uumbaji wake Manani. Na kila ambacho kinaitwa mtendaji au kinachotenda jambo fulani, sababu na muathiri ni Yeye Manani, yaani katika kazi hizo havijitegemei wala kujitosheleza vyenyewe, hata pale ambapo vinanasibishwa na kuitwa vitendaji, vitoaji, visababishaji n.k, vinafanya kwa msaada wa Mwenyezi Mungu (s.w.t) ambaye Yeye ndiye mwisho na hatima ya kila kitu, Yeye ndiye Msababishaji, Muunganishaji, Mtoaji na Mpaji, kwa hakika Yeye ndiye kikomo cha kila jambo. Pamoja na kuwepo dalili lukuki za kiakili, yafuatayo ni maneno ya Mola Manani anasema:

“Sema: Mwenyezi Mungu ndiye Muumba wa kila kitu na Yeye ni Mmoja, Mwenye kushinda.” (13:16) Anasema:

“Mwenyezi Mungu ndiye Muumba wa kila kitu; na Yeye Ndiye Kiongozi juu ya kila kitu.” (39:62) Anasema tena:

16


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 17

Tawhid na Shirk “Huyo Ndiye Mwenyezi Mungu Mola Wenu, Muumba wa kila kitu. Hapana mungu ila Yeye; …” (40:62) Anasema:

“Huyo ndiye Mwenyezi Mungu Mola Wenu hakuna Mola (mwingine) isipokuwa Yeye; Muumba wa kila kitu. Kwa hivyo mwabuduni Yeye...” (6:102) Anasema:

“Yeye ndiye Mwenyezi Mungu, Muumbaji, Mtengenezaji, Mtia sura, Mwenye Majina mazuri kabisa. Kinamsabihi kilicho katika mbingu na ardhi, Naye ni Mwenye nguvu, Mwenye hikima.” (59:24) Anasema:

“Inawezekanaje awe na mwana hali hana mke. Na ameumba kila kitu …” (6:101) Anasema:

“Enyi watu! Kumbukeni neema za Mwenyezi Mungu juu yenu. Je, yuko muumba mwingine asiyekuwa Mwenyezi Mungu …” (35:3) 17


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 18

Tawhid na Shirk Na anasema:

“Hakika Mola Wenu ni Mwenyezi Mungu aliyeziumba mbingu na ardhi katika siku sita; kisha akatawala kwenye Arshi. Huufunika usiku kwa mchana, ufuatiao upesi upesi. Na jua na mwezi na nyota zinatumika kwa amri Yake. Fahamuni! Kuumba na amri ni Yake. Ametukuka Mwenyezi Mungu Mola wa walimwengu wote.� (7:54). Ama dalili za kiakili kuhusu uumbaji ni wa Mwenyezi Mungu pekee ubainifu wa hilo upo katika vitabu vya itikadi. Tatu: Tawhiid Katika Ulezi na Upangaji wa Mambo:7 Makusudio yake ni kwamba ulimwengu huu una mpangaji na mwendeshaji ambaye hashirikiani katika kazi hiyo na yeyote, naye ni Mwenyezi Mungu (s.w.t), ama kazi za Malaika za kuratibu na kufanya baadhi ya mambo ni kutokana na amri na maagizo Yake kwao, na hilo linatofautina na vile wanavyoitikadi baadhi ya washirikina kuwa kila anayefungamana na Mwenyezi Mungu (s.w.t) basi ni muumbaji. Ama uendeshaji wa aina za viumbe vilivyopo ardhini huo ulitegemezwa na nyota za mbinguni, malaika, majini na viumbe visivyo na kiwiliwili ambavyo vilikuwa vikielezea ibada ya masanamu yanayoabudiwa, na kwamba Mwenyezi Mungu hahusiani na mpangilio na uendeshaji wa ulimwengu na maamuzi ya mambo 7. Waandishi wa kiwahabi wamefasiri: "Tawhiid katika Uumbaji" kuwa ni Tawhiid katika ulezi pamoja kwamba maana ya pili sio ya kwanza, hakika maana ya pili inaangazia Tawhiid katika upangaji na uendeshaji wa mambo, na ya kwanza inaangazia Tawhiid katika uumbaji na kufanya vitu viwepo, na washirikina walikuwa wenye kupwekesha katika sehemu ya kwanza yaani Tawhiid katika uumbaji, na hata kama baadhi yao walimshirikisha sehemu ya pili yaani katika Tawhiid katika upangaji na uendeshaji wa mambo. 18


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 19

Tawhid na Shirk yake. Hakika Qur’an tukufu - inaeleza bayana - kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t) ndiye Mpangaji wa mambo, Mwongozaji na Mwendeshaji, aidha inakanusha kutokuwepo mwingine mwenye kutenda hayo katika hali ya kujitegemea na bila kuhitaji msaada kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t), na kama angelikuwepo mwingine angelikuwa na taratibu zake na mipangilio yake kinyume na ilivyo sasa. Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema:

“Hakika Mola Wenu ni Mwenyezi Mungu ambaye ameumba mbingu na ardhi katika siku sita, kisha akatawala kwenye Arshi. Yeye hutengeneza mambo. Hakuna mwombezi ila baada ya idhini Yake, Huyo ndiye Mwenyezi Mungu, Mola Wenu, basi mwabuduni. Je hamkumbuki? (10:3) Na anasema:

“Mwenyezi Mungu ndiye aliyeziinua mbingu bila ya nguzo mnazoziona; kisha akatawala kwenye Arshi na amelitiisha Jua na Mwezi, kila kimoja kinaendelea mpaka muda uliotajwa…” (13:2). Kwa hivyo Mola Manani yeye ndiye pekee mpangaji wa mambo ama maana ya maneno yake (s.w.t): “Na kwa wale hupanga mambo” (79: 5) jua vilevile anasema: “Naye ndiye mwenye kushinda, (aliye) juu ya 19


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 20

Tawhid na Shirk waja na hukuleteeni (Malaika) wanao hifadhi matendo yenu…” (6:6) Kuwepo viumbe katika kupangilia baadhi ya mambo haina maana kwamba wanafanya mambo bila ya utegemezi wa Mola Manani. Kuna wakati mtu hunasibisha mambo yanayomsibu kwa nafsi yake na wakati mwingine kwa asiye kuwa yeye, hakuna mgongano kati ya hali hizo mbili, kwani Mwenyezi Mungu (s.w.t) pekee ndiye anayefanya katika hali ya kutotegemea, na viumbe wanafanya katika hali ya kutegemea, kuna wakati Mola Muumba huwaamrisha baadhi ya viumbe wake kufanya mambo fulani, kwa hivyo tunapenda kutaja hapa mifano kadhaa kuhusiana na hilo kama ifuatavyo: 1. Qur’an tukufu inaeleza katika baadhi ya Aya kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) hutoa roho pindi unapowadia muda wake anasema: “Mwenyezi Mungu hupokea roho wakati wa kufa kwao…” (34:42). Na mahala pengine anasema: “Hadi mmoja wenu anapofikiwa na mauti, basi wajumbe wetu humfisha na wao hawalegei.” (6:61) 2. Mwenyezi Mungu ndani ya Qur’an anaamrisha kuombwa msaada Yeye pekee, anasema: “Na Wewe tu tunakuomba msaada” (1:5), na mahala pengine anawaamrisha watu kusaidiana katika subira na swala anasema: “Na ombeni msaada katika Subira na Swala…” (2:45). 3. Qur’an tukufu inazingatia kwamba suala la Shufaa (uombezi) ni la Mwenyezi Mungu pekee inasema: “Sema, uombezi wote ni wa Mwenyezi Mungu” (34:44), ilihali Aya nyingine inaeleza kuwa uombezi unatolewa na asiyekuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t), kwa mfano Malaika, inasema: “Na wako Malaika wangapi mbinguni ambao uombezi wao hautafaa chochote isipokuwa baada ya Mwenyezi Mungu kutoa idhini kwa yule amtakaye na kumridhia.” (53:26). 4. Qur’an tukufu inahusisha ujuzi wa elimu ya ghaib kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) tu inasema: “Sema, hakuna aliyoko katika mbingu na 20


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 21

Tawhid na Shirk ardhi ajuaye yasiyoonekana ila Mwenyezi Mungu tu, nao hawajui ni lini watafufuliwa.” (27:65), na sehemu nyingine inaeleza kuwa Mola Manani huwateua baadhi ya waja na huwafunulia elimu ya mambo yasiyoonekana, inasema: “Wala hakuwa Mwenyezi Mungu mwenye kuwajulisheni mambo ya ghaibu, lakini Mwenyezi Mungu humchagua katika mitume yake amtakaye” (3:179). 5. Qur’an tukufu inanukuu maneno ya Ibrahim (a.s.) kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t) humponya yeye pindi anapoumwa, inasema: “Na ninapougua basi yeye ndiye anayeniponya” (26:80) Dhahiri ya Aya hiyo inahusisha uponyaji wa maradhi kwa Mwenyezi Mungu pekee, hali ya kuwa mahala pengine inaeleza kuwa asali ni tiba na ponyo, inasema: “…..Kinatoka katika matumbo yao kinywaji chenye rangi mbali mbali, ndani yake kina matibabu kwa watu …” (16:69), inasema: “Na tunateremsha Qur’an ambayo ni ponyo …” (17:82). 6. Kwa mtazamo wa Qur’an tukufu Mwenyezi Mungu (s.w.t) ndiye mtoaji pekee wa riziki inasema: “Kwa hakika Mwenyezi Mungu ndiye mtoaji wa riziki, Mwenye nguvu madhubuti.” (51:58), hali ya kuwa tunakuta Qur’an inawaamrisha wale wenye uwezo wa mali wawapatie wenye kuhitaji na wasiojiweza inasema: “Na walisheni katika hayo na muwavishe” (4:5) 7. Hakika mkulima halisi na wa hakika kwa mujibu wa Qur’an ni Mwenyezi Mungu (s.w.t) inasema: “Je! mimea mnayoilima? Je! nyinyi mmeiotesha au tumeiotesha Sisi?” (56:63-64), Ilihali katika Aya nyingine inawaachia kabisa sifa hiyo ya ukulima watu, na kueleza kuwa wao ndio wakulima inasema: “Ukawafurahisha walio upanda …” (48:29). 8. Hakika Mwenyezi Mungu (s.w.t) Yeye ndiye mwandishi wa matendo ya waja wake anasema: “Na Mwenyezi Mungu huyaandika wanayoshauriana usiku basi waache.” (4:81), na katika Aya nyingine inaeleza kwamba malaika ndiyo ambao wameamrishwa kuandika matendo ya waja, ina21


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 22

Tawhid na Shirk sema: ”Au wanadhani kuwa hatusikii siri zao na minong’ono yao? Naam, na Wajumbe wetu wako karibu yao wanayaandika.” (43:80). 9. Na ipo Aya katika Qur’an tukufu inayonasibisha upangaji wa matendo ya makafiri kwa Mola Manani, inasema: “Hakika wale wasioamini Akhera tumewapambia vitendo vyao ….” (27:4) na katika Aya nyingine kazi hiyo huinasibisha na kuihusisha na Shetani inasema: “Na kumbuka pindi shetani alipowapambia vitendo vyao …” (8:48) na katika Aya nyingine huinasibisha kwa wengine, inasema: “Na tutawawekea makafiri waliowapambia yale yaliyo mbele yao na nyuma yao…” (41:25). 10. Imetangulia hapo kabla kwamba upangaji wa mambo ni kazi ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) pekee, hata washirikina watakapoulizwa nani mpangaji wa mambo husema: Ni Yeye Mwenyezi Mungu pekee, maneno hayo yapo katika Sura ya 10 Aya ya 31, Qur’an inasema: “Na ni nani atengenezaye mambo yote? Basi watasema: Ni Mwenyezi Mungu.” hali ya kuwa mahala pengine Qur’an inasema wazi katika Aya zingine kwamba kazi ya upangaji wa mambo inafanywa na asiyekuwa Mola Manani, inasema: “Na kwa wale wenye kupanga mambo” (79:5). Kwa hakika wale ambao hawana maarifa ya kutosha juu ya Qur’an hushindwa kuelewa bali huchanganyikiwa kwani hukumbana na mgongano na mkang’anyiko wa mambo, ama wale wenye maarifa ya kutosha juu ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu wanadiriki uhakika wa mambo hayo, (ninamaanisha suala la kutoa riziki na kuponya) hayo na yanayofanana na hayo humhusu Mwenyezi Mungu pekee sio katika hali ya kushirikiana na kiumbe bali hufanya bila kumtegemea yeye, asili ya kuwepo kwake na vitendo vyake, ama asiyekuwa Mwenyezi Mungu hufanya mambo katika hali ya kufuatiza akisaidiwa kiuwezo na Mola Manani, na kwa kuwa ulimwengu huu ni wa sababu na msababishaji. Ni dhahiri kwamba kila jambo hapana budi lifuate kanuni na utaratibu maalum ambao uko katika nidhamu na mpangilio makhsusi, Qur’an tukufu inanasibisha matokeo yake na sababu ya maumbile pasi na kuzuia uum22


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 23

Tawhid na Shirk baji wa Mwenyezi Mungu, kwa hivyo inakuwa kama ilivyokwishatangulia hapo juu kwamba Mwenyezi Mungu anafanya kwa kujitegemea, ama asiyekuwa Yeye ni tegemezi tu yaani hufanya jambo kwa msaada na kwa uwezo aliopewa na Mola Muumba. Kwa ibara fupi tunasema asiyekuwa Mwenyezi Mungu hufanya moja kwa moja, na Mola Muweza uhusiano wake katika hayo ni usababishaji (Tasbiibu), na Qur’an tukufu inatoa ishara kuhusu nisba au uhusiano wa pande hizo mbili, Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema: “Na hukutupa wakati ulipotupa, lakini Mwenyezi Mungu ndiye aliyetupa ….” 8:17 Na kwa upande mwingine anaelezwa Mtume (s.a.w.w) kuwa ndiye mtupaji inasema: “Wakati ulipotupa” na tunakuta upande mmoja inaeleza Mwenyezi Mungu ndiye mtupaji na upande mwingine ni Mtume (s.a.w.w), na linalothibiti hapa kuwa mtupaji wa hakika ni Mwenyezi Mungu (s.w.t) ni kwamba Mtume (s.a.w.w) alipofanya tendo la utupaji ni kutokana na uwezo aliyopewa na Mwenyezi Mungu (s.w.t) ambao aliutumia kufanya hivyo, kwa hivyo kiumbe anafanya jambo kwa utashi wake kwa uwezo au nguvu aliyopewa na Mola Muweza, kwa mantiki hiyo Mwenyezi Mungu (s.w.t) anashiriki katika tendo la mtu kwa kumpatia uwezo na nguvu ya kutenda tendo husika, kwani mambo ya utangulizi au vitu ambavyo binadamu hufanya vimeumbwa na kukadiriwa na Mola Manani, lakini mtu hutenda kwa utashi na hiari yake, ndio maana ataulizwa kutokana na vitendo vyake. Na sisi tumetilia mkazo zaidi katika kitabu hiki masuala ya Tawhiid na Shirki kwa mtazamo wa Qur’an tukufu, lakini tumeacha kutaja dalili za kiakili kuhusiana na Tawhiid, pamoja na hivyo inatoa ishara kuhusiana na mambo hayo mawili kwa kutoa dalili zenye kutosheleza na kukinaisha, kwa maelezo zaidi na kwa ujumla tunasema: Hakika Qur’an tukufu inathibitisha kwa kutumia nguvu ya hoja kuwa mpangaji wa mambo ya ulimwengu ni Mwenyezi Mungu pekee, hayo yameelezwa katika Aya mbili zifuatazo:

23


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 24

Tawhid na Shirk

“Lau wangelikuwako humo (mbinguni na ardhini) waungu wengine asiyekuwa Mwenyezi Mungu, lazima zingeharibika…” (21:22), Na Aya nyingine inasema:

“Mwenyezi Mungu hakujifanyia mwana, wala hanaye mungu mwingine. Ingelikuwa hivyo basi kila Mungu angelichukua alivyoviumba. Na baadhi yao wangeliwashinda wengine.” (23:91). Angalia dalili hizo ni zenye kupambanua: Iwapo itadhaniwa kuwa yupo mwendeshaji mwingine wa ulimwengu huu hali ingekuwa kama ifuatavyo: 1. Kwa hakika kila mmoja angelifanya kinyume na mwingine kwa kujitegemea bila kuingiliwa na mwenziwe. Kwa mtindo huo ingelilazimu ulimwengu kuwa na mipango mingi na taratibu mbalimbali zenye kutofautiana, na hali hiyo ingelisababisha kupatikana uovu na ufisadi mkubwa ulimwenguni na kuvurugika mfumo na utaratibu huu uliyopo, kama Qur’an tukufu, inavyoashiria hilo, Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema: “Lau wangelikuwepo humo (mbinguni na ardhini) waungu wengine asiyekuwa Mwenyezi Mungu, lazima zingeharibika…” (21:22). 2. Ama kila mmoja angelipanga na kuongoza sehemu fulani, basi inalazimu kila mahala au upande kuwa na utaratibu wake maalum tofauti na mahala pengine, aidha kusingelikuwa na mafungamano na mahusiano yoyote kati ya pande hizo husika, na hivyo ingelilazimu kukatika mafungamano ya ulimwengu, ilhali tunaona ulimwengu huu una nidhamu na 24


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 25

Tawhid na Shirk upangiliaji mmoja, na mambo yote yanakwenda sawa bila migongano, hii ni dalili tosha kwamba mpangaji na muongozoji wake ni mmoja, naye si mwingine bali ni Mwenyezi Mungu aliyetukuka, na hayo yanaungwa mkono na maneno ya Mwenyezi Mungu (s.w.t), anasema: “Ingelikuwa hivyo basi kila Mungu angelichukua alivyoviumba. Na baadhi yao wangeliwashinda wengine..” (23:91). 3. Mmoja wa Miungu hiyo angelikuwa mtawala kwa Miungu wengine, na kwa hivyo yangelikuwapo mafungamano na maelewano kati yao, na hivyo huyu Mungu mtawala ndio atakuwa Mungu wa kweli bila ya Miungu mingine, na hilo linatolewa ishara na Qur’an tukufu inasema: “Baadhi yao wangelikuwa juu ya wengine.” (23:91). Kwa ufupi Aya zote zinaeleza juu ya hoja moja kwamba ulimwengu huu una Mola na mpangaji Mmoja. Nne: Tawhiid Katika Utungaji Sheria Hakuna shaka kila mwenye akili timamu huamini kwamba maisha ya binadamu ya kijamii yanahitaji sheria na kanuni madhubuti zenye kupangilia maisha ya jamii ya kibinadamu na hali zao, na kuwaongoza kwenye ukamilifu ambao wameumbwa kwa ajili yake, (na kila mmoja anakwenda kulingana na maumbile aliyoumbiwa), isipokuwa ni kwamba Qur’an tukufu haikukiri kwamba wanadamu wamepewa jukumu la kutunga sheria, bali inaona jukumu hilo ni la Mwenyezi Mungu (s.w.t.), Yeye ndiye mtungaji wa kanuni na mwekaji sheria kwa wanadamu. Na zipo Aya chungu nzima kuhusiana na kadhia hiyo hapa tunataja baadhi ya hizo; Mwenyezi Mungu anasema:

25


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 26

Tawhid na Shirk

“Hamwabudu badala Yake ila majina matupu mliyoyapanga wenyewe na baba zenu. Mwenyezi Mungu hakuyateremshia dalili yoyote. Hapana hukumu isipokuwa ya Mwenyezi Mungu tu. Ameamrisha msimwabudu yoyote isipokuwa Yeye tu. Hiyo ndiyo dini iliyonyooka, lakini watu wengi hawajui” (12:40). Mradi wa utoaji hukumu ni kwamba yeye Mola Manani ndiye mhusika pekee wa kuwatungia watu sheria, na sio binadamu ampangie binadamu mwenzake sheria, la hasha, jukumu hilo ni la Mola Muumba tu, ni haramu mtu kuamuru na kukataza, kuharamisha na kuhalalisha isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kuhusu hilo Mwenyezi Mungu anasema: “Hakuna hukumu isipokuwa ya Mwenyezi Mungu”, Mola Manani anasema: “Ameamrisha asiabudiwe yeyote ila Yeye tu” na iwapo mtu atauliza: ikiwa Mwenyezi Mungu ndiye mhusika pekee inakuwaje awaamrishe waja wake katika baadhi ya sehemu kufanya hivyo? Tunajibu kwa haraka na bila kuchelewa kama ifuatavyo: Mwenyezi Mungu anasema:

“Ameamuru asiabudiwe isipokuwa Yeye tu.” Na amesema (s.w.t.): “Je, wanataka hukumu za kijahiliya? Na ni nani aliye mzuri zaidi kwa hukumu kuliko Mwenyezi Mungu kwa watu wenye yakini?” (5:50). 26


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 27

Tawhid na Shirk Hakika Aya hii inagawa kanuni ambazo zinahukumu viumbe katika makundi mawili, hukumu ya Mwenyezi Mungu na za viumbe yaani (za kijahilia), ni dhahiri kwamba hukumu isiyokuwa ya Mwenyezi Mungu ni hukumu ya kijahilia. Mwenyezi Mungu anasema:

“Na wasiohukumu kwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio Makafiri” (5:44), Na

“Na wasiohukumu kwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio madhalimu” (5:45). Na

“Na wasiohukumu kwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio mafasiki” (5:47). Aya hizo zinaelezea kwamba wapo watu wenye kuhukumu kwa asiyoyateremsha Mwenyezi Mungu ambao wana sifa kuu tatu nazo ni: ukafiri, udhalimu na uovu (ufasiki), na hakika lengo la kuwekwa sheria ni ili zitekelezwe na kutendewa kazi na watu wenye akili. Aina tatu hizo ni marufuku kuweka au kutunga sheria kwani sheria hizo zitakwenda kinyume na sheria zilizowekwa na Mwenyezi Mungu, kwa hivyo uwekaji sheria na utoaji hukumu ni kazi makhususi ya Mwenyezi 27


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 28

Tawhid na Shirk Mungu na jukumu hilo hakumpatia kiumbe yeyote. Watu ambao huhukumu kwa yale asiyoyateremsha Mola Manani hao ni makafiri, kwani huenda kinyume na hukanusha sheria za Mwenyezi Mungu. Aina ya pili ni madhalimu ambao hujipa jukumu la utungaji sheria ambalo ni la Mola Manani. Aina ya tatu ni waovu (mafasiki), kundi hili limetoka nje ya utiifu wa Mwenyezi Mungu, ama wayafanyayo wanachuoni na mafaqihi wa kiislamu ni kufafanua na kubainisha yale ambayo jamii ya kiislamu inayahitaji, ili kutekeleza ipasavyo sheria za Mwenyezi Mungu, kwa hivyo hawaanzishi kanuni na sheria zao binafsi. Tano: Tawhiid Katika Utiifu: Makusudio yake ni kwamba hakuna apasaye kutiiwa kwa dhati ila Mwenyezi Mungu aliyetukuka, inawajibika Yeye pekee kutiiwa na amri zake zitekelezwe, ama kumtii mwingine asiyekuwa Yeye itakuwa wajibu iwapo ataamrisha Mwenyezi Mungu mja wake kufanya hilo, na kama sio hivyo itakuwa ni haramu na Shirki. Kwa ajili hiyo tunakuta Qur’an tukufu inaeleza kinaga ubaga suala hilo la kumtii Mwenyezi Mungu pekee, inasema:

“Basi mcheni Mwenyezi Mungu vile muwezavyo, na sikieni, na toeni, itakuwa heri kwa nafsi zenu …” (64:16). Kisha Qur’an inaeleza wazi kwamba Mtume hatiiwi isipokuwa kwa idhini ya Mola Manani, inasema: “Na hatukumpeleka mtume yeyote ila apate kutiiwa kwa amri ya Mwenyezi Mungu …” (4:64). Kwa mantiki hiyo itatulazimu kuwatii wale ambao Mwenyezi Mungu ametuamrisha kuwatii, kwa hivyo kumtii mtume, wale waliopewa madaraka na Mwenyezi Mungu, wazazi wawili na wengineo hufanyiwa hivyo kwa ruhusa ya Mola Muweza na sio vinginevyo, bila hivyo isingewajibika hata kidogo kuwatii na kutekeleza amri zao pamoja na maagizo yao. 28


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 29

Tawhid na Shirk Kwa ujumla kufanya hivyo ni kumtii Mwenyezi Mungu, kwa sababu Yeye ndiye aliyeamrisha hivyo, ama sababu ya kuhusisha utiifu Kwake na sio kwa mwingine maelezo zaidi utayapata katika vitabu vya itikadi (Aqaid). Sita: Tawhiid Katika Utoaji Hukumu: Hakuna shaka kwa yeyote mwenye akili kuwa hudiriki kwamba kuwepo sheria ni jambo la dharura na la kimaumbile, kwani linahifadhi na kuweka nidhamu katika jamii, huboresha utamaduni na maendeleo ya miji na wanajamii pia, wadhifa wao na haki zao. Ni dhahiri shahiri kuwa matendo ya serikali na utawala wa sheria hulazimu matumizi ya nafsi na mali, na hulinda uhuru na mipaka yake, kwa hivyo kuna haja ya kuwepo wasimamizi na waangalizi. Na watu wote ni sawa mbele ya sheria na mbele ya Mwenyezi Mungu, naye habagui wala hampendelei kiumbe yeyote, au kuwapa baadhi madaraka ya kuwakandamiza binadamu na viumbe vingine ulimwenguni, bali utawala na madaraka yote ni ya Mwenyezi Mungu tu, Yeye ndiye aliyemzawadia kiumbe uhai, kuwepo kwake na mahitaji yake yote, haifai kwa yeyote kuwatawala waja isipokuwa kwa idhini ya Mola Muumba, kwa mantiki hiyo Mitume, wanachuoni na waumini wamepewa na Mwenyezi Mungu idhini ya kutiiwa na madaraka ya kuongoza watu, kwani madaraka na serikali ya haki ni ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu anasema:

“Hapana hukumu isipokuwa ya Mwenyezi Mungu tu. Ameamrisha msimwabudu yoyote isipokuwa Yeye tu. Hiyo ndio dini iliyonyooka, lakini watu wengi hawajui� (12:40). Hukumu ina maana pana sana katika wigo wa kanuni na sheria, na hayo yanawekwa bayana kutokana na maneno ya Mwenyezi Mungu, anasema: 29


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 30

Tawhid na Shirk “Hakuna hukumu ila ya Mwenyezi Mungu, anaeleza haki naye ndiye mbora wa kupambanua” (6:57), na anasema: “Ala, hukumu ni Yake naye ni Mbora wa wenye kuhesabu” (6:62). Inafaa ieleweke kwamba Mwenyezi Mungu huhusika moja kwa moja na mja, bali makusudio yake ni kuwa yeyote atakayetawala ni lazima apewe idhini ya kutawala na kuongoza mambo ya umma na kusimamia majukumu ya watu na mali zao. Ndio maana tunaona ndani ya Qur’an Mwenyezi Mungu anawapa baadhi ya Mitume madaraka ya kuongoza umma, anasema:

“Ewe Daud! Hakika Sisi tumekufanya uwe Khalifa ardhini. Basi wahukumu watu kwa haki, wala usifuate matamanio, yakakupoteza Njia ya Mwenyezi Mungu” (38:26). Kwa ajili hiyo serikali na tawala mbalimbali katika jamii ya kiislamu zinatokana na Mwenyezi Mungu, aidha kupitishwa na Yeye, na kama si hivyo utakuwa ni utawala wa kibeberu ambao umekemewa na Qur’an katika Aya chungu nzima. Saba: Tawhiid Katika Ibada Makusudio yake ni kwamba hapaswi kuabudiwa yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu, hilo wamewafikiana Waislamu wote wala hakuna ikhtilafu kati yao tangu zama hizo hadi hivi sasa, kila Mwislamu anakiri hilo. Pamoja na kutofautiana katika baadhi ya vipengeke kuhusiana na kuwafanyia watu jambo hilo kwa lengo la kuwatukuza na kuwaheshimu. Kwa ujumla neno ibada lina wigo mpana sana, zipo ibada makhususi ambazo hufanyiwa Mwenyezi Mungu pekee, ama kuwaheshimu wanachuoni wakubwa au sehemu takatifu n.k hilo ni jambo ambalo maelekezo yake 30


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 31

Tawhid na Shirk yametoka kwa Mwenyezi Mungu kupitia wajumbe wake, hilo wala sio Shirki. Lakini Mawahabi huzingatia kufanya hivyo ni (Shirki katika ibada) na huwakufurisha Waislamu na kuwafanya wao ni kitu kimoja na wale wenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu katika ibada. Kwa ajili hiyo tumeona ni lazima kumaizi na kupambanua mafuhumu ya ibada kwa mtazamo wa Qur’an tukufu na Sunna sahihi za bwana Mtume (s.a.w.w), ili watu waweze kuelewa na wapate faida kutokana na mada hii, na hatimaye utata utatoweka, ubishi pamoja na mizozo isiyo ya lazima, na hilo ndilo ambalo waandishi wengi wa kiwahabi wameghafilika nalo, ambao wamepoteza muda wao mwingi kuwakufurisha Waislamu na kuwaambia wanafanya Shirki katika ibada bila kuzingatia mafundisho ya Qur’an tukufu na maelekezo yake ambayo yanathibitisha suala hilo, lakini kabla ya kufafanua hayo tunaeleza mambo kadhaa nayo ni: Sehemu ya kwanza: Tangulizi kumi za msingi: Shirki ni msingi wa upinzani na shabaha ya mapambano ya ulinganio wa Mitume. Jambo ambalo lilikuwa shabaha ya mapambano ya ulinganio wa Mitume katika zama zao ni kukabiliana na kupinga Shirki kwa nguvu zote na kuwaita viumbe katika ibada ya Mwenyezi Mungu Mmoja na kujiepusha na kumwabudu mwingine asiyekuwa Yeye. Tawhiid katika ibada, kupiga vita ushirikina na kuabudu masanamu, ndio lengo kuu la mapambano ya ujumbe wa Mitume (a.s.), kwa hakika Mitume wote wamelingania suala la Tawhiid na kupiga vita ushirikina. Qur’an tukufu inabainisha kinaga ubaga jambo hilo inasema: “Na kwa hakika tulimtuma Mtume kwa kila umma kwamba mwabuduni Mwenyezi Mungu na mumwepuke taghuti.…” (16:36), anasema tena Mwenyezi Mungu:

31


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 32

Tawhid na Shirk “Na hatukutuma kabla yako Mtume yeyote ila tulimfunulia ya kwamba hakuna Mola abudiwaye ila Mimi tu basi, niabuduni” (21:25). Kisha mahala pengine Qur’an tukufu inaeleza Tawhiid katika ibada kwamba katika asili inashirikiana kati ya sheria za kiungu inasema: “Sema, Enyi watu wa Kitabu, njooni katika neno lililo sawa baina yetu na yenu, tusimuabudu ila Mwenyezi Mungu tu, wala tusimshirikishe na chochoite …” (3:64). Na iwapo utataka kujua vipi Qur’an tukufu inazungumzia (Shirki) katika ibada, au vigawo vyake vyote, na jinsi ilivyotoa taswira halisi ya jinsi Washirikina walivyokikosa kile ambacho wao hukitegemea katika uhai wao, Qur’an inasema:

“Na anayemshirikisha Mwenyezi Mungu ni kama kwamba ameporomoka kutoka mbinguni, kisha ndege wakamnyakua au upepo ukampeleka mahala mbali.” (22:31 ). Aya hiyo inaeleza bayana hasara atakayoipata mshirikina pamoja na matendo yake kupotea bure katika maisha haya na ya hapo baadaye. 2. Chanzo cha Shirki na Ibada ya Masanamu Hakika fikra na mawazo potofu ni chanzo cha upotofu wa itikadi ambao uliwaathiri mno wanadamu, kwani maudhui ya ibada ya masanamu haikuwa kwa kaumu moja wala mbili au aina moja wala mbili, bali ilikuwa ina wigo mkubwa ambao unahitaji utafiti wa kina zaidi juu ya chanzo chake. 32


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 33

Tawhid na Shirk Kwa mfano ibada ya masanamu kwa (waarabu) hutofautiana na (Barahimat), kwa hakika itikadi zao zinatofautiana kati ya moja na nyingine kuhusiana na ushirikina.8 Ama waarabu wa zama za kale kama vile Adi na Thamud umma wa Nabii Huud na Swaleh, wakazi wa Madiyana na Sabai, umma wa Shuaib na Suleiman walikuwa waabudu masanamu na jua,9 itikadi zao na jinsi ya kufikiri kwao kumetajwa ndani ya Qur’an tukufu. Walikuwa waarabu wa zama za ujahilia miongoni mwa watoto wa Ismail wakimpwekesha Mwenyezi Mungu kwa muda fulani, walikuwa wakifuata mafundisho ya Nabii Ibrahim (a.s.) na mwanawe Ismail (a.s.), lakini zama zilivyozidi kwenda ikiwa ni pamoja na kuchanganyikana na waabudu masanamu, wakaathiriwa na ibada ya masanamu na hatimaye ikachukua mahala pa Tawhiid katika jamii ya kiarabu ya kijahilia.10 Hivyo ndivyo ilivyokuwa hali ya waarabu na vitongoji vyake hapo kabla. Ama umma ulioishi Makka na viunga vyake zama za karibu na kuja Mtume (s.a.w.w), wanahistoria wameeleza kwamba mtu wa mwazo kuingiza ibada ya masanamu Makka na vitongoji vyake alijulikana kwa jina la (Amru bin Hayy), ibada hiyo alijifunza wakati alipofunga safari kwenda Sham (Syria na Palestina) akawaona watu wanaabudu masanamu, alipowauliza: kwa nini wanaabudu masanamu? Wakajibu: “Masanamu haya tunayaabudu kwa sababu pindi tunapoyaomba mvua hunyesha na tunapoyaomba nusra tunapata.” Akawaambia: “Je! mnaweza kunipatia baadhi 8. Imeshereheshwa na kuchambuliwa na vitengo vya Maarifa hususan kitengo cha Maarifa cha Bustani na kwamba itikadi hizo ni za watu ambao sehemu kubwa wanaishi Bara la Asia. 9. Mwenyezi Mungu anasema: "Nimemkuta yeye na watu wake wakilisujudia jua badala ya Mwenyezi Mungu." (27:24) 10. Hii inafanya ibada ya masanamu iendelee misingi yake katika jamii ya kiarabu ya zama za ujinga hadi zama za mbali, hata ikiwa uingiaji wake Makka na vitongoji vyake ulikuwa sio kwa umbali huo kulingana na yale yaliyonakiliwa na Ibn Hisham na wanahistoria wengine. 33


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 34

Tawhid na Shirk nami niende nayo Uarabuni na ili wayaabudu?” hivyo ndivyo alivyoleta sanamu kubwa Makka na wakalipa jina la Hubal, wakaliweka juu ya Ka’ba tukufu kisha akawalingania watu waliabudu.11 Siku ya Suluhu ya Hudaybiya ilinyesha mvua usiku wake ambapo ndala zao hazikuloa, mtu mmoja akamwita Mtume (s.a.w.w): “Hamswali juu ya vikalio vya wanyama wenu,” wakaswali na walipomaliza kuswali Mtume (s.a.w.w) akasema: “Je! Mnajua aliyosema Mola wenu?” Wakajibu: “Mwenyezi Mungu na Mtume ndio wanaojua,” hapo akasema: Mwenyezi Mungu anasema: ???? ?? ????? ???? ?? ????? ???? ?? ???: ????? ????? ???? ????? ??? ???? ? “Leo miongoni mwa waja wangu yupo aliyeamka akiniamini na akinikufuru mimi, na ama mwenye kusema tumepata mvua kwa baraka za Mwenyezi Mungu na kwa fadhila zake basi huyo ni muumini wa Mwenyezi Mungu, na mwenye kukufuru nyota, na ama mwenye kusema nyota fulani imetupa mvua na kadhaa wa kadha” na katika riwaya nyingine imekuja: “Na watoto wake kadhaa wa kadha, basi huyo ni muumini wa nyota na amenikanusha mimi”12 Kutokana na maelezo hayo inathibiti kwamba waarabu wa zama za ujahilia baadhi yao au wote walikuwa washirikina, na wengine walikuwa wakiamini kuwa masanamu yanaleta mvua pindi wanapoyaomba, hilo lishike kuhusiana na mambo yatakayokuja hapo baadaye. Wapo baadhi ya watafiti wanaona kuwa (ibada ya masanamu) chanzo chake kilikuwa ni utukuzaji wa watu mashuhuri na udumishaji wa kumbukumbu zao, na alipokufa mmoja kati ya watu hao mashuhuri walitengeneza sanamu linalofanana naye ili kuhuisha utajo wake, lakini baada ya kupita zama nyingi na vizazi baada ya vizazi vikawa vinaabudu masanamu hayo na haukupita muda mrefu itikadi hiyo ikaenea na kushamiri. 11. Siirat Ibn Hisham Juz. 1 Uk. 79. 12. Siirat Ibn Halabiyya Juz. 3 Uk. 29.

34


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 35

Tawhid na Shirk Na wakati mwingine alikuwa kiongozi wa familia akitukuzwa na kuheshimiwa mno wakati akiwa hai, anapokufa watu hutengeneza sanamu linalofanana naye kisha huliabudu. Na Wagiriki na Warumi wa kale, ada yao ilikuwa kwamba anapofariki baba wa familia au mkuu wa ukoo, familia au ukoo husika hutengeneza sanamu lake kisha huliabudu. Mpaka hivi sasa unakuta katika nyumba za makumbusho za kilimwengu yapo masanamu ya watu wa dini, viongozi na watu mashuhuri ambao hutukuzwa kama walivyokuwa watu wa zamani wakiyaabudu. Ama jaribio la Nabii Ibrahim (a.s.) la kukabiliana na kiongozi wa kaumu yake (Namrud), tunafaidika kwamba Namrud alikuwa akiabudiwa na watu wake, kama vile alivyokuwa Firaun katika zama za Musa (a.s.), pamoja na kuwa akiabudiwa na watu wake, naye pia alikuwa akiabudia masanamu, kwa sababu alikuwa na hadhi kubwa kama wale waliomtangulia katika Mafirauni (Mafarao), Qur’an tukufu inasema:

“Na wakasema wakuu wa kaumu ya Firaun: Je, utamwacha Musa na watu wake walete uharibifu katika nchi na kukuacha wewe na waungu wako?� (7:127). Kwa ufupi ni kwamba hakika masanamu na vinyago vilitengenezwa kwa lengo la kuweka kumbukumbu ya viongozi wao mashuhuri, lakini baada ya kupita muda mrefu na vizazi na vizazi kupita, na lengo la asili la kutengenezwa kutoweka, lengo hilo likabadilika na wakawa wanaabudu masanamu na vinyago vile.

35


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 36

Tawhid na Shirk 3. Tawhiid Katika Ibada ya Mwenyezi Mungu Makusudio ya aina hii ya Tawhiid ni kwamba: Hii ni ibara ya kumpwekesha, kumwamini na kumwabudu Muumba wa ulimwengu Yeye pekee, na kujiepusha kabisa kumwabudu asiyekuwa Yeye, jambo hili linapingana na kukabiliana na Shirki katika ibada, ambayo ni binadamu kumwabudu kiumbe na kumuacha Mola Muumba wa ulimwengu kutokana na sababu fulani. Mawahabi hilo huliita Tawhiid katika Uungu kama vile huiita Tawhiid katika Dhati na Tawhiid katika Ulezi, na istilahi zote mbili ni batili kama utakavyoelewa maana ya uungu ambayo haina maana ya mwenye kuabudiwa, bali neno ilahu na Allah maana yake ni moja kulingana na chimbuko na mafuhumu yake, isipokuwa neno la kwanza lina maana pana zaidi, ama neno la pili linaingia katika maana ya kwanza. Ama Ulezi maana yake ni upangaji wa mambo na uendeshaji wa ulimwengu sio Uumbaji hata kama kulingana na dalili za kifalsafa zinaonyesha kuwa upangaji wa mambo hautengani na uumbaji. Ni dhahiri kwamba Tawhiid katika dhati na Tawhiid katika uungu hapana shaka makusudio yake ni mamoja na yanamhusu Mwenyezi Mungu (s.w.t), hakuna mungu zaidi ya Allah (s.w.t), ama miungu midogo ambayo haimiliki chochote ila iko chini ya miliki ya Mola aliyetukuka, Yeye ndiye mtoaji Shufaa (uombezi), msamaha na mengineyo, hayo na yanayofanana na hayo ni katika vitendo na kazi za Mola Muumba kama walivyokuwa waarabu wa zama za ujahilia wakiamini. Vile vile Tawhiid katika Uumbaji (khaaliqiya) hutofautiana na Tawhiid katika Ulezi (Rubuubiya), kama inavyofahamika neno Rabbu (mlezi) halina maana ya Khaaliq (Muumba), lakini hayatofautiani hakika na dhahiri kwa mujibu wa dalili za kiakili.

36


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 37

Tawhid na Shirk Kama ambavyo linalofaa ni kuimaanisha Tawhiid katika ibada kwa kutumia lafudhi hiyo hiyo, na si kwa kutumia lafudhi ya ’Tawhiid katika uungu’, kwani kama ilivyokwisha tangulia hapo kabla kuwa neno ilahu (Mungu) halina maana ya ma’abuudu (Muabudiwa). Kwa hivyo natija inayopatikana hapa kuhusiana na maelezo ya Shirki ni: Kuwepo miungu mingi na sio kuamini kuwa ulimwengu huu una muumba asiyekuwa Mwenyezi Mungu mmoja wa pekee ambaye ameumba ulimwengu huu, na kuamini kuwepo miungu mingine huenda ikasababisha kuacha kumwabudu Mola Muumba na hatimaye kumwabudu mwingine asiyekuwa Yeye. Kuabudu viumbe au masanamu, ibada hiyo ilifanywa na umma na kaumu zilizotangulia hapo zama za kale, huenda sababu yake ikawa ndogo na wakati mwingine huchochewa na msukumo wa maneno ya kifalsafa, na muda sio mrefu tutaweka bayana sababu kubwa za ushirikina. 4 - Sababu za Shirki Katika Ibada Hapa tunataja sababu tatu kati ya sababu nyingi zinazohusu jambo hilo nazo ni kama ifuatavyo: I. Itikadi ya kuwepo waumbaji wengi: Waabudu masanamu walikuwa pamoja na wale wenye itikadi ya utatu ambayo imesababisha kuabudu miungu zaidi ya mmoja. Mabudha wao wanaamini miungu mitatu au dhahiri ya majina matatu nayo ni: i. Barahima (Mungu mwenye kufanya vitu vitokee) ii. Siifa (Mungu mwenye kufanya vitu vitoweke) iii. Shiishnu (Mungu mhifadhi na mkingaji), ama wakristo wao huamini na kuabudu majina matatu: i. Mungu Baba. ii. Mungu Mwana. iii. Mungu Roho Mtakatifu.

37


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 38

Tawhid na Shirk Na miongoni mwa Mazaradoshti huamini (Ehura na Mazda) nayo ni ibara ya miungu miwili ambayo ni: i. Yazdan. ii. Ehriman.13 Iwapo imani ya Mazaradoshti ingelikuwa sahihi kuhusiana na miungu hiyo miwili ingelituchanganya na kutufanya kuwa katika mkanganyiko. Kwa hivyo imani ya kuwepo miungu mingi kwa hakika ilikuwa moja ya sababu ya kuabududiwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu na kwamba ndiyo sababu ya watu kufanya Shirki katika ibada, na hakika Qur’an tukufu imebatilisha dalili zote ambazo huwa ni msingi wa itikadi hiyo potofu, kwa hivyo hoja na dalili zinazohusu jambo hilo zimeshaelezwa hapo kabla katika suala la Tawhiid katika upangaji wa mambo na ulezi. II. Fikra ya Kutofautiana kati ya Muumba na Muumbwa: Sababu ya pili iliyofanya watu waabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu ni kule kumuweka Mwenyezi Mungu mbali na kiumbe, hii inamaanisha kwamba watu hao walikuwa wakidhani kuwa Mwenyezi Mungu yuko mbali na viumbe, hakuna uhusiano wowote kati yao, maombi na dua zao, na kudhani kuwa hazimfikii Yeye, kwa hivyo wakachagua njia au vitu ambavyo walidhani kwamba vitakuwa sababu au nyenzo za kufikisha dua zao Kwake, wakawa wanawaabudu makasisi, malaika, majini na vitu vinginevyo ili wafikishe maombi yao kwa Mola Mlezi. Kwa hakika Qur’an tukufu imebatilisha mawazo, fikira na imani hizo kwa nguvu ya hoja kwa kusema: “Mwenyezi Mungu yu karibu zaidi na viumbe kuliko vitu vyote.” Hakika Mwenyezi Mungu aliyetukuka husikia siri zao, maombi yao na mambo wayafanyayo dhahiri. Mwenyezi Mungu huzingira vitu vyote na hubaini yale yote wayafichayo na wayadhihirishayo. 13. Na kwa tafsiri hii Majusi huwa ni miongoni mwa waabudu masanamu au wenye imani ya utatu, basi zingatia. 38


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 39

Tawhid na Shirk Kwa hivyo hakuna haja ya kuvifanya viumbe kuwa miungu, na vilevile haifai kuviabudu, na ikiwa sababu ya kuviabudu hivyo vitu ni ili vifikishe maombi, dua na haja zao kwa Mola Muumba, basi Yeye anajua mambo yote hafichwi wala kupitwa na kitu. Na zipo Aya nyingi ndani ya kitabu cha Mwenyezi Mungu zinazoashiria na kuweka bayana suala hilo:

“Na hakika tumemuumba mtu, na tunayajua yanayoitia wasiwasi nafsi yake. Na Sisi tuko karibu naye kuliko mshipa wa shingo.” (50:16)

“Je! Mwenyezi Mungu hamtoshei mja wake ?”14 ( 39:36)

“Niombeni nitawajibu” (40:60)

“Sema: kama mkificha yaliyomo vifuani mwenu au kuyadhihirisha Mwenyezi Mungu anayajua” (3:29)

14. Ndio, Aya mbili hizo haziko wazi katika yale sisi tuliyo na shaka nayo, kwa mfano wa Aya iliyokwisha tangulia basi chunguza. 39


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 40

Tawhid na Shirk “Hawashauriani kwa siri watatu ila Yeye ni wanne wao, wala watano ila Yeye ni wa sita wao, wala wachache kuliko hao…wala zaidi ila Yeye huwa pamoja nao popote walipo …” (58:7) Kwa mujibu wa Aya hizo za Qur’an, zinapinga katakata ibada ya masanamu pamoja na Shirki … III. Upangaji wa Mambo Huachiwa Miungu Midogo: Kila binadamu anahisi ndani ya nafsi yake kuwepo nguvu ya hali ya juu, na anaona nafsi yake si chochote kuelekea nguvu hiyo, hisia hiyo ni ya kimaumbile hata kama haidhihiri ulimini na katika viungo vingine, lakini hali hiyo inapatikana katika dhamira yake, nayo ni hali ya kujihisi unyenyekevu kuelekea nguvu hiyo kwa upande mmoja, na kwa upande mwingine huwa ni ada na desturi ya kujihisi vizuri, kuhurumia viumbe....... Kwa msingi huo mshirikina hupeleka na huihusisha nguvu hiyo ya ghaib (isiyoonekana) katika vitu vyenye kuonekana, maumbo au masanamu yenye maumbo mbalimbali, na kuongeza kuwa hufikiri na huamini kila jambo na tukio linalotokea ulimwenguni husababishwa na nguvu kuu, nayo imeumbwa na Mwenyezi Mungu, kama vile mungu wa bahari, mungu wa vita, mungu wa amani n.k na utawala wa ulimwengu unafanana na utawala wa ardhi ambao kutekeleza kila nyanja ya maisha kunaelekea kwa mmoja, kila mmoja ana uwezo na vitendo maalum. Watu walioishi kando kando mwa bahari waliabudu (mungu wa bahari) kwa sababu walipata mahitaji yao kutokana na bahari na kukingwa na maafa na vimbunga, ama wale wakazi wa bara na majangwani walikuwa wakiabudu (mungu wa bara) kwa sababu waliamini mungu huyo akiwaletea manufaa na mahitaji yao, aidha akiwakinga na madhara ya ardhini kama vile matetemeko ya ardhi na maafa mengine pamoja na majanga mbalimbali ya majangwani, lakini hawakuwa na uwezo wa kuiona kwani imani yao ilitokana na mawazo yao wenyewe waliyoyabuni, fikra zao zilisababisha kutengeneza vinyago na masanamu, na hatimaye wakawa 40


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 41

Tawhid na Shirk wanayaabudu badala ya nguvu isiyoonekana kama walivyokuwa wakidhani. Kutokana na sababu hiyo kundi la waarabu wa zama za ujahilia wakawa wanaabudu malaika na kundi lingine likawa linaabudu nyota zenye kung’ara mbinguni na kutembea, lingine likiabudu majini, lingine likiabudu nyota zilizo madhubuti, na lengo la kufanya hivyo ni kwamba vitu hivyo vinawaletea manufaa na heri, vilevile huwakinga na madhara na shari zake. Wakawa wanatengeneza vinyago na masanamu kulingana na upeo wa kufikiri kwa nafsi zao, na kwa hivyo kila mmoja alikuwa na sanamu la aina yake na umbile ambalo aliwazalo. Kwa hakika walifanya hivyo kutokana na ile nguvu ya hisia isiyoonekana, ambayo ilisababisha na kuwafanya watengeneze miungu midogo ambayo kwa dhati yake haikuwa na hisia yoyote, wakawa wanaamini hivyo kuwa ni vitu ambavyo vinawanufaisha dhahiri, ndio maana wakaamua waviabudu. Kwa hakika Qur’an tukufu ilikabiliana vikali na imani na fikra hiyo potofu na kuikemea na kushadidia katika sehemu nyingi kwamba Mwenyezi Mungu pekee ndiye mpangaji na mwendeshaji wa ulimwengu pamoja na mambo yake, inasema:

“Hakika Mola wenu ni Mwenyezi Mungu ambaye ameziumba mbingu na ardhi katika nyakati sita, kisha ukakamilika (uumbaji wake) katika Arshi, anaendesha (kila) jambo …”15 (10:3). 15. Sura 13 aya 2 na Sura 32 aya 5. 41


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 42

Tawhid na Shirk Hakika Qur’an katika Aya nyingi zinaelezea uumbaji, kuhuisha, kufisha, mfumo wa nyota, jua, mwezi na utoaji riziki kwamba ni kazi za Mwenyezi Mungu pekee,16 na kupinga vikali fikra na imani ya ushirikina na kuwepo ushirikiano kati ya kiumbe na Mola Manani, na kusema kuwa: Fikra ya kuwa viumbe wameachiwa kufanya kila kitu kwa kujitegemea pasi na kuhusika Mwenyezi Mungu hata kidogo katika kuendesha ulimwengu na vilivyopo sio sahihi. Zipo Aya nyingi za Qur’an ambazo huelezea kadhia hiyo, lakini hapa tunataja kwa muhtasari kwa kuchelea mada kuwa ndefu. Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema:

“Hakika Mola wenu ni Mwenyezi Mungu aliyeziumba mbingu na ardhi katika nyakati sita, kisha ukakamilika (uumbaji wake) katika Arshi, huufunika usiku kwa mchana uufuatiao upesi, na jua na mwezi na nyota vimetiishwa kwa amri yake, fahamuni kuumba na amri zote ni zake, ametukuka Mwenyezi Mungu Mola wa walimwengu wote” (7:54) Anasema: 16. Mambo hayo hufanywa na Mwenyezi Mungu tu, haizuii kuingia katikati sababu ambazo hufanya kwa amri ya Mwenyezi Mungu na kwa utashi Wake, na kwa hivyo nguvu yake inakuwa katika mlolongo wa nguvu za kiungu, ni dhahiri kwamba uletaji wa mambo hayo kwa njia ya sababu haimaanishi mambo yote kuachiwa ulimwengu, kwa maelezo zaidi rejea kitabu cha mwandishi kilichotajwa hapo kabla sehemu ya nane, yaani Tawhiid katika Ulezi na Upangaji wa Mambo. 42


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 43

Tawhid na Shirk

“Sema; ni nani anayekuruzukuni kutoka mbinguni na ardhini? Au ni nani anayemiliki kusikia na kuona? Na ni nani anayemtoa hai kutoka maiti, na akamtoa mfu katika uzima? Na ni nani atengenezaye mambo yote? Basi watasema: ni Mwenyezi Mungu, basi waambie: Je! Hamumwogopi Mwenyezi Mungu. Basi huyo ndiye Mwenyezi Mungu, Mola wenu wa haki.� (10 : 31-32). Mpaka hapa tumeshabainisha misukumo mitatu ambayo husababisha kwa namna moja au nyingine watu wamshirikishe Mwenyezi Mungu katika ibada, na hatusemi ni sababu hizo tatu pekee zinazowafanya watu wamshirikishe Mola Manani, la hasha, bali zipo nyingi sana ndani ya Qur’an tukufu zinazoelezea asili na mwanzo wake na namna ilivyoenea ulimwenguni. Mwislamu anaitakidi kwamba Mola wa ulimwengu ni mmoja, yupo kila mahala, yupo karibu zaidi na viumbe wake, yeye ndiye Muumba, Mmiliki wa viumbe wote, Mpangaji na Mwendeshaji wa ulimwengu na jukumu hilo hajampatia yeyote. Mwislamu kulingana na itikadi yake asilani hawezi kumwabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu, bali humwabudu Yeye tu, na hatosheki na hivyo, bali huipiga vita itikadi ya Shirki na ibada ya masanamu kwa hali yoyote ile, aidha anahakikisha hakuna anayethubutu kuvuka mipaka ya Tawhiid hata kidogo. Na kuhusu msukumo na sababu ya tatu tunapenda kutaja hapa jambo muhi43


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 44

Tawhid na Shirk mu nalo ni: Huenda mtu akaamini kwamba jukumu la kuongoza na kuendesha ulimwengu ni la Mwenyezi Mungu pekee, na hajampatia yeyote kazi hiyo, lakini ana itikadi mambo yasiyo ya kimada (kuonekana) ambayo hufungamana na matendo ya waja kama vile uombezi (Shufaa), kusamehe (maghfira) ni miongoni mwa mambo ambayo yanamuhusu Mwenyezi Mungu, lakini inawezekana majukumu hayo akawapa baadhi ya waja wake, na hiyo ni kati ya sababu ya kuabudiwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t), lakini Qur’an tukufu inaeleza bayana kwamba Shufaa (uombezi) ni haki makhsusi ya Mola Muumba, na mwingine hafanyi hivyo isipokuwa kwa idhini yake, inaeleza: “Sema: uombezi wote ni wa Mwenyezi Mungu.” (39:44). Kama alivyoifanya kazi ya kusamehe dhambi za waja wake ni Yake yeye pekee, hashirikiani na yeyote, na mwenye kuamini msamaha ni haki ya mwingine kwa hakika atakuwa amemshirikisha Mwenyezi Mungu (s.w.t). Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema:

“Na wale ambao wanapofanya uchafu au wanapodhulumu nafsi zao humkumbuka Mwenyezi Mungu wakaomba msamaha wa madhambi yao, na ni nani anayesamehe madhambi isipokuwa Mwenyezi Mungu, na hawaendelei na (maovu) waliyoyafanya hali wanajua.” (3:135). Kundi la waabudu masanamu wakati wa zama za Mtume (s.a.w.w) lilikuwa likiabudu masanamu ambayo liliyatengeneza kwa mikono yao, wakawa wanaamini kuwa masanamu hayo yanawasaidia kupeleka mambo yao kwa Mwenyezi Mungu, na kwamba suala la uombezi na kusamehe limetegemezwa kwao. Na katika somo litakalofuata tutaelezea aina hii ya Shirki ambayo ni dhai44


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 45

Tawhid na Shirk fu mno, na yatakapobainika malengo, misukumo na sababu za ushirikina, hapo itabainika kwetu namna Qur’an tukufu inavyokosoa itikadi hizo potofu, na inatulazimu kuchunguza yale yanayoelezwa na waandishi wa kiwahabi katika vitabu vyao. 5. Tafsiri ya Tawhiid Katika Uungu na Ulezi: Waandishi wa kiwahabi bado wanaitakidi kuwepo aina mbili za Tawhiid, aina ya kwanza huita ’Tawhiid katika Ulezi’, na aina ya pili ’Tawhiid katika Uuungu’, kisha wanasema hivi Tawhiid katika Ulezi ni kuitakidi upweke wa Muumbaji, na haitoshi kuamini Yeye ni mmoja kama walivyoeleza Manabii na Mitume watukufu ambayo hayo waliyaeleza na kuyaeneza katika jamii ya wanadamu, bali pamoja na hivyo kwa mujibu wa ’Tawhiid katika Ulezi’ ni wajibu kumwabudu Yeye pekee na kutomshirikisha na chochote katika ibada, kwani washirikina wa kiarabu pamoja na kumwamini muumba mmoja wa ulimwengu, lakini bado Qur’an ilikuwa ikiwaona ni washirikina, inasema: “Na wengi wao hawaamini Mwenyezi Mungu isipokuwa wao ni washirikina tu.” (12:106).17 Hakuna maneno kuhusiana na maudhui hiyo na Tawhiid ya Ulezi, nayo ina hatua nne hata kama Mawahabi wameshika mbili za mwanzo na kuacha mbili za mwisho, kila namna watu wote wanaafikiana juu ya suala hilo wala hawatofautiani, wote wanakubaliana juu ya wajibu wa kujiepusha na ibada isiyokuwa ya Mwenyezi Mungu, lakini la kushangaza ni kauli yao ya kuwa kutukuza Mitume na Mawalii ni ibada, hali ya kuwa kutukuza na kuabudu kwa nadharia ya watu wengine ni mambo mawili tofauti. 17. Fat'hul-Majiid Uk. 12 na 20 kimeandikwa na Sheikh Abdul-Rahman bin Hasan bin Muhammad bin Abdillah bin Abdul-Wahab aliyekufa mwaka 1285, na jambo hili hupotoshwa hivi sasa katika Muhtasari wa mosomo kwao, na hutilia mkazo aina mbili hizi kutokana na Tawhiid kisha huwatuhumu Waislamu kwamba wao ni wapwekeshaji wa ulezi na sio uungu. Na imeeleweka katika yale yaliyotangulia kwamba kuiita Tawhiid katika uumbaji kuwa ni Tawhiid katika Ulezi, na kuiita Tawhiid katika Ibada kuwa ni Tawhiid katika Uungu, ni makosa kilugha na kwa istilahi ya Qur'an. 45


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 46

Tawhid na Shirk Kwa ibara nyingine hakuna tofauti baina ya Waislamu kuhusiana na jambo hilo, kwani wote huamini kuwa haifai kamwe kumwabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t), isipokuwa tofauti inapatikana katika baadhi ya matendo na amali kama ni ibada, ilhali kwa mtazamo wa wengine matendo hayo sio ibada. Kwa ibara nyingi za kitaalamu hapana budi kusema: Kwa ujumla hakuna tofauti, bali tofauti inakuwepo katika kuainisha mfano halisi (misdaq ). Ili kutatua mushkeli huu hapana budi - kwanza – kujua mafuhumu ya hakika ya ibada ili tuweze kumaizi ibada isiyokuwa ya Mwenyezi Mungu. Vivyo hivyo inawezekana kueleza kwamba maudhui ya ziara (kufanya ziyara) kuwa ni miongoni mwa mambo ambayo kwa itikadi ya Mawahabi huzingatia kuwa ni Shirki, kufanya Tawassuli kwa Mawalii wa Mwenyezi Mungu na kuwaomba haja, na hilo wanatofautiana na Waislamu wengine, kwani wao huruhusu Tawassuli na huizingatia kuwa ni aina ya kushikamana na sababu ambayo imeelezwa na sheria takatifu. 6. Je! Kunyenyekea na Kutukuza ni Ibada? Wataalamu wa lugha ya kiarabu katika kamusi za lugha wameeleza maana mbalimbali za lafudhi ya ibada, wao wanafasiri neno ibada kuwa ni unyenyekevu na kujidhalilisha, yafuatayo ni baadhi ya maneno waliyoyaeleza: Ibn Manduur katika kitabu chake - Lisaanul-A’rab anasema: “Asili ya ibada ni unyenyekevu na kujidhalilisha.” Raaghib katika kitabu chake - Mufradaat anasema: “Ibada ni kudhihirisha udhalili, na ibada ina maana pana zaidi, kwani ni kikomo cha kujidhalilisha, na hali hiyo hapaswi kufanyiwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu aliyetukuka. Kwa mantiki hiyo anasema: “Msimwabudu ila yeye tu.” Feiruuz Abadi katika kitabu chake - Qaamuus Muhiit amesema: “Ibada ni utiifu.” 46


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 47

Tawhid na Shirk Ibn Faris katika kitabu chake - Maqaayiis anasema: “Neno ibada lina asili mbili zenye kupingana, moja inajulisha ulaini na udhalili, na la pili lina maana ya neno la kwanza, akaongeza kusema: Awali ni ngamia aliyefundishwa, pili ni njia inayopitwa kwa udhalili. 7. Sio Kila Unyenyekevu ni Ibada! Pamoja na kwamba ibada hata kama wameifasiri kuwa ni utiifu, unyenyekevu na kudhihirisha upeo wa juu wa udhalili, isipokuwa ni kwamba tafsiri zote hizi si kingine ila ni aina za tafsiri za jumla tu, kwani utiifu, unyenyekevu na kudhihirisha udhalili sio maana pekee ya ibada, kwa sababu unyenyekuvu wa mtoto kwa baba yake, au mwanafunzi kwa mwalimu wake na askari mbele ya mkuu wake hauhesabiwi kuwa ni ibada hata kama unyenyekevu na kujidhalilisha kuwe ni kwa hali ya juu, hayo yanaelezwa na Aya nyingi, zifuatazo ni baadhi ya Aya ambazo zinazoelezea suala hilo: Kitendo cha Malaika kumsujudia Adam ni jambo linalodhihirisha kilele cha unyenyekevu, Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema: “Na pindi tulipowaambia Malaika; msujudieni Adam, wakanyenyekea isipokuwa Ibilis alikataa na akajivuna…” (2:34) Aya hiyo inajulisha kwamba Adam alisujudiwa na Malaika na kitendo hicho hakikuhesabiwa wala kuzingatiwa kuwa ni Shirki, au kwamba hiyo ni ibada ambayo amefanyiwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu, na Malaika hawakuona tendo hilo kuwa ni Shirki wala kumwabudu asiyekuwa Mola Muumba, bali tendo lao hilo lilikuwa ni kumwadhimisha na kumtukuza Adam, hii ni dalili tosha kwamba kumtukuza asiyekuwa Mwenyezi Mungu sio kumwabudu muhusika, na ibara “Msujudieni Adam” hata kama inaungana na ibara “Msujudieni Mwenyezi Mungu” ila ni kwamba ibara ya kwanza haichukuliwi kuwa ni amri ya kuwabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu, na ibara ya pili huhesabiwa ni amri ya kumwabudu Mwenyezi Mungu.”18 18. Na hilo linajulisha kwamba linalozingatiwa ni nia na makusudio yaliyomo katika dhamiri na sio mawazo ya dhahiri. 47


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 48

Tawhid na Shirk Na huenda ikadhaniwa kwamba maana ya kumsujudia Adam katika Aya hiyo ni kumnyenyekea Adam na si kusujudu kwa maana yake halisi, na yajulikana wazi kwamba unyenyekevu pekee sio ibada, bali (kilele cha unyenyekevu) ambacho ni sajda (sujuud) ndio ibada. Na huenda ikadhaniwa pia kuwa makusudio ya Adam kusujudiwa (au sajda aliyofanyiwa) ni kule kumfanya Qibla, na si kumsujudia sajda ya hakika na halisi. Lakini dhana zote mbili ni batili. Ama kuhusu dhana ya kwanza, ni kwamba kutafsiri sajda iliyozungumziwa katika Aya kwamba ni unyenyekevu, tafsiri hiyo inatofautiana na dhahiri ya neno, ufahamu wa wanalugha na mazoea ya watu, kwani maana ya awali na ya haraka inayomjia mtu toka katika neno hilo ni sajda hii ya kawaida inayoeleweka na kujulikana, na sio unyenyekevu, kama ambavyo dhana ya pili nayo ni batili, kwa sababu maelekezo yake hayana chimbuko, rejea wala dalili. Na katika kuongezea hilo ni kwamba Adam (a.s.) lau angelikuwa Qibla cha Malaika isingelikuwa na upinzani na Shetani pale aliposema: “Je! Nimsujudie yule ambaye umemuumba kwa udongo.” (17:61). Sio lazima Qibla kiwe ni bora zaidi kushinda mwenye kusujudu hadi kiwe chanzo cha upinzani, bali cha lazima ni kwamba mwenye kusujudiwa awe ni bora kushinda mwenye kusujudu, wakati ambapo Adam hakuwa bora zaidi kwa mtazamo wa Ibilisi, na hiyo inajulisha kuwa sajda ilifanywa mbele ya msujudiwa. Jaswas anasema: “Wapo miongoni mwa watu wanaosema kuwa: Sajda alifanyiwa Mwenyezi Mungu, ama Adam alikuwa ni mahala pa Qibla chao, na hilo sio lolote, kwani hilo linasabibisha kutokuwa na hadhi na utukuzwaji na kukirimiwa Adam, bila shaka hilo linajulisha kwamba amri ya kusujudu lengo lake lilikuwa ni kumtukuza Adam na kumfadhilisha yeye, kama anavyoeleza Mola Manani maneno ya Ibilis:

48


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 49

Tawhid na Shirk

“Na (kumbuka) tulipowaambia Malaika; msujudieni Adam, basi wakamsujudia isipokuwa Iblis, akasema; Je! nimsujudie yule uliyemuumba kwa udongo? akasema: Unaonaje, huyu ndiye umempa heshima zaidi kuliko mimi?...” (17 : 61-62). Ibilis akaeleza sababu ya kukataa kwake kusujudu, aliona kuwa haipasi Mwenyezi Mungu kumwamrisha amsujudie na kumtukuza asiyestahiki, na kama ingelikuwa amri ya kusujudu ni mfano wa Qibla kwa wale wenye kusujudu pasi na utukuzaji na ufadhilishaji, wala Adam asingelikuwa na fadhila yoyote hata ipelekee kuonewa husda na Shetani.19 Na hakika mafuhumu ya Aya yanakuwa hivi, malaika walimsujudia Adam kwa kutekeleza amri ya Mwenyezi Mungu (s.w.t), na hapa inadhihirika namna Malaika walivyonyenyekea kikomo cha unyenyekevu mbele ya Adam, lakini pamoja na hivyo wao hawakuwa wenye kumwabudu yeye. Na huenda mmoja akawaza kwamba sajda ya Malaika ingelikuwa haikuamrishwa na Mwenyezi Mungu ingelisihi kauli ya kuwa walimsujudia Adam, lakini walifanya hivyo kutekeleza amri ya Mola Manani, na hilo ni jawabu tosha la kuwajibu Mawahabi. 2- Qur’an tukufu inasema kinaga ubaga kwamba wazazi wa Yusuf walimfanyia yeye hivyo: “Na wote wakaporomoka kumsujudia (Mwenyezi Mungu) akasema: Ewe baba yangu hii ndio tafsiri ya ndoto yangu ya zamani” (12:100), na ndoto ambayo aliyoiona, Qur’an inaeleza katika Aya ifuatayo. Inasema. “Yusuf alipomwambia baba yake: “Ewe baba yangu, hakika mimi nimeona (katika ndoto) nyota kumi na moja na jua na mwezi, nimeviona vikinisujudia” (12:4), na ndoto hiyo ilitimia 19. Ahkamul-Qur'an Juz. 1 Uk. 302. 49


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 50

Tawhid na Shirk baada ya kupita miaka mingi, na Qur’an tukufu inaeleza wazi kwamba walimsujudia Yusuf. Kwa ubainifu huo inaeleweka kwamba sajda aliyofanyiwa Yusuf lengo lake sio kumwabudu yeye, bali ni kuonyesha unyenyekevu. Ama wale ambao hufasiri sajda kwa maana ya ibada, bila shaka Aya hiyo na ile inayoelezea kusujudiwa Adam ni dalili tosha kwao, ambayo ilikuwa kwa amri ya Mwenyezi Mungu, kwa hivyo inatoka nje ya mada yetu inayohusu: “Je! amri ya Mwenyezi Mungu inafanya jambo la Shirki lisiwe Shirki? “Zingatia. 3- Mwenyezi Mungu (a.j) anawaamrisha watu wawanyenyekee wazazi wawili na kutowakorofisha, anasema: “Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa huruma…” (17:24). Pamoja na hivyo unyenyekevu huo sio ibada. 4- Waislamu wote hutufu - miongoni mwa amali na matendo ya Hija – nyumba ambayo imejengwa kwa mawe na udongo, na kuzunguka baina ya Swafa na Marwa, na hayo yameamrishwa na Mwenyezi Mungu (a.j) anasema: “Na waizunguke nyumba ya kale.” (22:29). Vile vile anasema:

“Hakika Swafa na Marwa ni katika alama za (dini) ya Mwenyezi Mungu, basi mwenye kuikusudia Al-Ka’ba, au kuizuru, si vibaya kuizunguka …” (2:158). Je! huoni kuzunguka mchanga, mawe na mlima ni ibada? na kama ungekuwa kila unyenyekevu ni ibada ingelilazimu matendo hayo yawe ni Shirki ambayo imeruhusiwa na Mola Manani, na hakika Mwenyezi Mungu ame50


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 51

Tawhid na Shirk tukuka kutokana na hayo. Wakiwa Waislamu wote hugusa jiwe jeusi wakiwa katika Hijja – na ugusaji jiwe ni miongoni mwa matendo ya Sunna ya Hijja, kwa dhahiri matendo hayo yanashabihiana na matendo ya Washirikina wanapoelekea masanamu, na amali hiyo huhesabiwa ni Shirki, ama wafanyavyo Waislamu ni ibada na hulipwa thawabu na Mwenyezi Mungu (s.w.t) na wala haihesabiwi kuwa ni Shirki, na dhahiri ya matendo hayo ni moja wala haitofautiani na matendo ya waabudu masanamu. 5. Hakika Qur’an tukufu inaamrisha kufanya sehemu za ibada kuwa mahala pa kuswalia inasema: “Na mpafanye mahala aliposimama Ibrahim pawe pa kuswalia” (2:125 ) Na hakuna shaka Swala inayoswaliwa sehemu hiyo ni ya Mwenyezi Mungu, lakini kuitekeleza mahala hapo ambapo ipo athari ya nyayo za Ibrahim ni aina ya kumtukuza Nabii Ibrahim, na tendo hilo halihesabiwi kuwa ni kumwabudu Ibrahim. 6- Waumini hunyenyekeana kati yao na huwa shupavu kwa makafiri, Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anasema:

“Enyi Mlioamini! Atakayeiacha miongoni mwenu dini yake basi hivi karibuni Mwenyezi Mungu ataleta watu (ambao) atawapenda nao watampenda, wanyenyekevu kwa Waislamu na wenye nguvu juu ya makafiri” (5:54). Hakika Aya hizo zote na matendo hayo ya Hijja hujulisha kwamba unyenyekevu, kujidhalilisha na utukuzaji sio ibada, na tumeona maelezo ya wataalamu wa lugha ya kiarabu wamefasiri ibada kwamba ni unyenyekevu na kujidhalilisha, maana hiyo ni pana zaidi, yaani wamekusudia ile maana pana, ili hali ibada ni aina maalumu ya unyenyekevu kama tutaka51


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 52

Tawhid na Shirk vyotaja muda mfupi ujao. Kwa ubainifu huo tunafaidika kwamba kuheshimu na kutukuza pekee sio ibada, kwa sababu kama si hivyo tutawaona Waislamu wote hata Mitume ni washirikina, kwani walikuwa wakimheshimu yule ambaye imelazimu kumheshimu. Na hilo ameashiria marehemu Sheikh Ja’far Kashiful-Ghatwai (yeye ni mtu wa mwanzo kudiriki - katika zama zake – itikadi za Mawahabi na athari zao), amelitolea ishara kwa kusema: “Hapana shaka kwamba (Tafsiri ya wataalamu wa lugha kwamba sajda maana yake ni ibada) haikusudii ibada hii ambayo haipasi ila kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, ambayo mwenye kuifanya kwa ajili ya asiyekuwa Mwenyezi Mungu atakuwa amekufuru, ambayo ni unyenyekevu wa moja kwa moja, kama inavyodhihirika katika maneno ya wataalamu wa lugha, la sivyo italazimu kuwakufurisha watumwa, waajiriwa na wafanyakazi wa watawala, bali kuwakufurisha Mitume kwa kule kuwa kwao wanyenyekevu kwa wazazi wao.”20 8 -Upambanuzi wa maana Halisi na isiyo Halisi: Huenda lafudhi ya neno ibada na maneno yanayotokana na neno hilo katika mazoea ya watu na lugha yakatumika kwa maana fulani, lakini kutumia neno fulani katika maana nyingine sio dalili kuwa ndio maana halisi ya neno hilo, bali huenda ikawa katika lengo la kushabihisha matuminizi hayo na maana halisi kutokana na kule kuwepo mnasaba kati ya maana mbili za neno hilo, angalia vidokezo vifuatavyo: 1- Mwenye kupenda hudhihirisha kikomo cha unyenyekevu kwa mpenzi wake, huvumilia matatizo na hutekeleza kila alitakalo, pamoja na hivyo unyenyekevu huu hauitwi kuwa ni (ibada), ijapokuwa husemwa kwa maana isiyo halisi kwamba ”ana mwabudu mwanamke”. 20. Minhaju Rashaad Uk. 24 chapa ya 1343H mwandishi Sheikh Akbar marhumu Sheikh Ja'far Kashif Ghitwai aliyefariki mwaka 1228, na aliandika kitabu hicho ili kujibu barua ya mmoja wa viongozi wa Saudia ambao walikuwa ni vibaraka wa Mawahabi tangu siku ya mwanzo hadi hivi leo. 52


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 53

Tawhid na Shirk 2- Watu ambao huchukuliwa mateka na matamanio yao – huwa na nafsi ya kuamrisha maovu – hufuata matamanio yao na huyanyenyekea, lakini hatuwezi kusema kwa hakika ni waabudu matamanio, wala hawahisabiwi ni washirikina kama vile waabudu masanamu, hata kama itasemwa ”anaabudu matamanio yake”, hiyo ni aina ya kushabihiana na kueleza kwa maana isiyo halisi na hakika, pamoja na kuwa Qur’an inasema matamanio ni mungu, kwa hivyo inalazimu kwamba kunyenyekea matamanio ni ibada, lakini kwa njia ya majazi na sio halisi, inasema: “Je! Umemuona yule aliyefanya matamanio yake kuwa mungu wake? …” (25:43). Vivyo hivyo neno mungu limetumika kwa maana ya matamanio, lakini ni kwa njia ya majazi na si halisi, vilevile kutumia neno ibada katika kufuata matamanio ni kwa lengo la majazi. 3- Wapo baadhi ya watu hujitolea kila kitu ili wafikie malengo yao kama vile cheo, madaraka n.k. hadi hufikia watu kusema hao wanaabudu cheo na madaraka, lakini wao hawahisabiwi kwamba kwa hakika wanaabudu cheo na wala hawazingatiwi kuwa washirikina. 4- Hakika wapo watu katika zama hizi – kama vile Mayahudi – husifika kwa ubinafsi, hutuhumiwa kuweka mbele ulaji na unywaji, ijapokuwa huambiwa kuwa ni waabudu zama, starehe, nafsi na shetani, lakini ukweli unaonyesha kazi yao hio sio ibada, kwani kumfuata shetani ni jambo moja na kumwaabudu yeye ni kitu kingine, na pindi tunapoona Qur’an inasema kumtii shetani kwamba ni ibada, basi itakuwa ni sehemu ya kushabihisha, na lengo lake ni kuonesha na kubainisha kuwa jambo hilo ni baya sana, inasema:

“Je! Sikukuagizeni enyi wanadamu msimwabudu shetani, hakika yeye ni adui aliye dhahiri kwenu, na kwamba mniabudu Mimi, hii ndio njia iliyonyooka.” (36 : 61 – 62). 53


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 54

Tawhid na Shirk Na Aya mbili zifuatazo:

i. “Ewe baba yangu usimwabudu shetani, hakika Shetani ni muasi kwa Rahmani.” (19 : 44)

ii. “Na wakasema: Je! Tuwaamini watu wawili walio mfano wetu na watu wao ni watumwa wetu.” (23 : 47) Hapana shaka kwamba Bani Israil hawakuwa wanamwabudu Firauni na wasaidizi wake isipokuwa kujidhalilisha kwao kwake kulipofikia kiwango cha juu zaidi, ikasihi kutumia neno ibada kwa njia ya majazi na sio katika maana halisi ya neno. Na hata kama Qur’an imetumia neno ibada katika sehemu hizo kadhaa, lakini haina maana imewafanya watu hao kuwa washirikina, kwani haipasi kusadikisha kwamba kila unyenyekevu, utiifu, utukuzaji na kuheshimu ni ibada, na hapo itampambanukia mpendwa msomaji kwamba matumizi ya neno hilo katika sehemu mbalimbali yanatokana na aina maalum na uhusiano wa maana isiyo halisi. Kwa ibara nyingine waabudu matamanio, wafu, nafsi na cheo hata kama wao huzingatiwa ni watenda dhambi bila shaka adhabu kali inawangojea, lakini hawahisabiwi kuwa ni washirikina katika ibada, na wao wana hukumu yao makhsusi katika sheria za kiislamu. Na kwa nini isiwe hivyo, ilhali tunasoma katika hadithi ya Mtume (s.a.w.w) amesema: “Mwenye kumsikiliza msemaji amemwabudu na ikiwa msemaji anatamka maneno ya Mwenyezi Mungu atakuwa amemwabudu Mwenyezi Mungu na ikiwa anatamka yasiyokuwa ya

54


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 55

Tawhid na Shirk Mwenyezi atakuwa amemwabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu�21 Leo watu wanasikiliza vyombo mbalimbali vya habari, husikiliza mazungumzo ya watu tofauti, watangazaji wa redio na televisheni, na aghlabu ya watu hao huzungumza yasiyokuwa ya Mwenyezi Mungu, je! inafaa kusema wote wanaosikiliza mazungumzo yao wame waabudu watu hao? Bali sahihi ni kwamba lafudhi ya neno ibada huzingatiwa mfano wa sehemu ambazo ni aina ya majazi (kutumia neno katika maana isiyowekewa) kwa kuwepo mnasaba kati ya maana halisi na ile isiyo halisi (majazi). Watu wengi husema: Fulani anaabudu tumbo au wale waabudu tumbo, je! kwa hakika watu hao wanaabudu tumbo na matamanio, au unyenyekevu ambao unatokana na nguvu ya matamanio ya nafsi hufanana na unyenyekevu ambao hufanyiwa Mwenyezi Mungu muumba wa ulimwengu? na hivyo katika mchakato huu unyenyekevu huo umewasilishwa kwa neno ibada. 9- Je! Amri ya Mwenyezi Mungu hufanya Shirki isiwe Shirki? Huenda ikaelezwa kwamba sajda ya Malaika kwa Adam, kugusa jiwe jeusi na yale yenye kufanana na matendo hayo, kwa kuwa yameamrishwa na Mola Manani hayawi Shirki, wala mwenye kufanya hivyo hahisabiwi kuwa mshirikina,22 na kwa ibara nyingine; ingawa ibada halisi na ya hakika ni pamoja na unyenyekevu na heshima lakini iwapo matendo hayo yote yakitekelezwa kwa amri ya Mwenyezi Mungu huhesabiwa kuwa ni ibada, na kama sio hivyo, bali hutokana na mtu mwenyewe na si amri ya Mwenyezi Mungu hiyo huwa ni Shirki.

21. Safinatul-Bihar Juz. 2 mada Abdu. 22. Na msemaji wa hayo ni Sheikh Abdul-Azizi Imam wa msikiti wa Mtume (s.a.w.w) katika majadiliano yake na baadhi ya waheshimiwa. 55


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 56

Tawhid na Shirk Lakini hao wenye kusema hivyo wanaghafilika na jambo muhimu ambalo ni: Mafungamano ya Hukumu na maudhui fulani hayabadilishi kabisa uhakika wa maudhui husika, na wala mafungamano ya amri ya Mwenyezi Mungu na maudhui hiyo hayabadili hali yake. Hakika akili iliyosalimika huhukumu kuwa mwenye kumtukana mtu mwingine amemdhalilisha, na muktadha wa jambo hilo ni maumbile ya mtukanaji na maneno machafu, hivyo hata kama Mwenyezi Mungu atawajibisha kumtukana yeyote bado amri yake haitobadilisha hali halisia itokanayo na kashfa. Kama vile ambavyo kukirimu wageni kimaumbile ni kuwaheshimu wageni, hivyo lau kutaharamishwa uharamisho huo hautaondoa uhalisia wa uzuri wa kukirimu, namaanisha kwamba kule kukirimu hakutabadilika na kuwa udhalilishaji pale kutakapoharamishwa, bali ukweli ni kwamba kule kukirimu kutaendelea kuwa na hali yake ileile hata kama kutakuwa kunafungamana na agizo la uharamishwaji, hivyo mambo mengine kama vile kusujudu, kugusa jiwe jeusi na yanayofanana na hayo yakiwa kidhati ni ibada, basi amri ya Mwenyezi Mungu haitayabadilisha katika dhati na uhalisia wake, na matendo hayo hayatokuwa ni kumwabudu Adam (a.s.) au Yusuf au jiwe jeusi. Na kauli ya kwamba kufanya hivyo ni kuviabudu vitu hivyo lakini kwa kuwa umefanya kutokana na amri ya Mola Muumba basi hapo Shirki imeondoka, kauli hiyo inalazimu aina hiyo ya matendo kuwa Shirki iliyoruhusiwa, na maneno hayo hawezi kuyakubali binadamu yeyote. Muhtasari wa suala hili ni kwamba ima tuzungatie kwambamatendo hayo sio Shirki hata kidogo na kiasili hayaingii chini ya dhana ya Shirki, au kwamba ni katika aina ya Shirki katika ibada, lakini ni Shirki iliyoruhusiwa na Mwenyezi Mungu. Uchaguzi ni kwamba kauli ya pili ni batili mno, yeyote hawezi kudhania 56


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 57

Tawhid na Shirk hilo seuze kuamini hivyo. Bila shaka yakutosha kutambua kwamba baadhi ya matendo kwa kigezo fulani yanaweza kuwa ni kuadhimisha na kutukuza kwa upande mmoja, na kwa kigezo kingine yakawa ni Shirki, kwa mfano lau kama Malaika wangelimsujudia Adam kwa itikadi kuwa ni Mungu, jambo hilo lingekuwa ni Shirki, na bila shaka asingeliamuru Mwenyezi Mungu– kama tutajaalia hivyo–. Na ama ikiwa wangemsujudia bila itikadi hiyo basi halingekuwa Shirki hata kama Mola Manani hajaamrisha hilo. Hakika Sheikh Abdul-Azizi Imam wa msikiti wa Mtume (s.a.w.w) ametoa maelezo kwa kusema inaruhusiwa kisheria uadhimishaji huo kwakuwa ipo amri ya Mwenyezi Mungu (a.j) juu ya jambo hilo, aidha anatoa ushuhuda kupitia yale aliyoyasema Umar bin Khattab kuhusu kubusu jiwe jeusi: “Mimi najua, wewe hunufaishi wala hudhuru, na lau kama nisingelimuona Mtume (s.a.w.w) akikubusu nisingelikubusu.”23 Na tumeshamwambia Sheikh: Tunayoyapata kutokana na maneno yake ni kuwa matendo hayo ni katika Shirki iliyoruhusiwa. Sasa tuiangalie Aya ifuatayo katika kukabiliana na mtazamo wa Sheikh, inasema:

“Sema hakika Mwenyezi Mungu haamrishi mambo mabaya, Je! mnasema juu ya Mwenyezi Mungu msiyoyajua?” (7:28) Kama ingelikuwa sajda (kumsujudia) Adam (a.s.) na kugusa jiwe jeusi ni katika kumwabudu Adam na jiwe na ni Shirki, basi abadan Mwenyezi Mungu (a.j) asingeliamrisha mambo hayo.

10. MAANA YA UUNGU NA ULEZI Kuhusu neno Uungu sidhani mpendwa msomaji anahitaji kujua maana ya 23. Sahihi Bukhari Juz. 3 Uk. 149 Kitabul-Hajji chapa ya Uthman Khalifa. 57


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 58

Tawhid na Shirk Ilahi kwani lafudhi yake na neno Allah chimbuko lake ni moja, pamoja na kuwa yanatofautiana katika hali halisi ya nje, tofauti ya umoja na wingi. Lakini neno Allah ni lafudhi iliyotukuka kinyume na neno Ilahi, kwani Allah, yaani Mwenyezi Mungu ni Mmoja wa pekee hakuna mwingine, ama neno Ilahi yaani mungu haizuii kuwa zaidi ya mmoja, kwa hivyo kuna ikhtilafu kati ya hayo mawili, kama vile neno Zayd na binadamu au mtu. Ukipenda sema: Hapa tuna neno ambalo linahusu zaidi ya mungu mmoja, nalo ni Ilahi, nalo ni umoja wa neno Aalihatu yaani miungu, ama neno Allah yaani Mwenyezi Mungu ni neno makhususi Kwake Yeye tu na wala hahusiki nalo yeyote mwingine abadan. Jina hilo linafanana na neno Khudaa katika lugha ya Kiajemi, yaani mungu, hilo halimhusu mungu mmoja, ama neno Khudavand linamhusu Mwenyezi Mungu tu, aidha neno god katika lugha ya Kiingereza halimhusu mungu mmoja, ama likikusudiwa maalum huwa God kuanza na herufi kubwa. Huenda neno Allah kutumika makhususi kwa Mola Muumba wa ulimwengu katika lugha ya Kiarabu, ilikuwa hivi: Waarabu katika mazungumzo yao walipokuwa wanataka kumaanisha Muumba walikuwa wakimwasilisha kwa neno Ilahi, yaani Muumba, neno hilo likazoeleka katika ndimi zao kwa kumaanisha Muumba, na baada ya muda mrefu likaongezwa Alifu (a) na laam (L) likawa Allah, kisha likawa makhususi kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) Muumba wa ulimwengu aliyetukuka.24 Zamakhshari anaashiria hilo katika kitabu chake Kashaf, anasema: Neno Allah asili yake ni Ilah, mshairi amesema: Tunajilinda kusema mungu ni kama vile mbuzi aliyekosa mwelekeo wala hana mchungaji.25 Mfano wake ni sawa na neno: Naas (watu), asili yake ni Unaas, ikaondolewa herufi Hamza (A) na ikabadilishwa kuwa Laam (L), kwa hivyo 24. Kwa ukaribu huu kuhusiana na nadharia zingine kwa kupata maarifa zaidi rejea kitabu Taajuk-Aruus Juz. 9 neno (Ilah). 25. Mshairi amejilinda kwa Mwenyezi Mungu kutokana na kumfananisha Yeye na mpendwa wake kwa swala au sanamu au mnyama pori aliyechinjwa

58


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 59

Tawhid na Shirk husemwa katika kumuita Mwenyezi Mungu: Ya Ilah (Ewe Mwenyezi Mungu), aidha husemwa: Ya Allah, na neno Ilah (mungu) ni miongoni mwa majina ya jinasi (yaani jumuishi) kama vile Rajulu (mwanaume) na Farasu (Farasi) (ambapo hayo yanakusanya wanaume na farasi mbalimbali bila kikomo).26 Allama Tabarasi katika kitabu chake cha Tafsiri ananukuu kutoka kwa Siibaway kwamba neno Allah asili yake ni Ilahi katika mzani wa Fiaal,27 ikafutwa herufi ya mwanzo ya nomino nayo ni Hamza (A) badala yake ikafanywa Alifu na Laam ikawa (AL),.......28 Raaghibu katika kitabu chake, Mufradaat amesema: Neno Allah asili yake ni Ilahi, ikafutwa Hamza (I) ikabakia (lahi), hapo ikaingizwa Alifu na Laam (AL) likawa Allah, jina hilo likawa makhsusi kwa Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu (a.j) anasema: “Je! Unajua jina lake.�29 Kwa ubainifu huo hakuna haja ya kutafsri neno Ilahi kwa kitu kingine kwani hilo liko bayana, na limekuwa maalum kwa dhati ya Mwenyezi Mungu (a.j) Mkamilifu wa kila sifa njema na Muumbaji wa vitu vyote, na hizo ni sifa makhsusi za Mwenyezi Mungu wala sio sifa za mungu mwingine asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Na huenda likatumika neno Allah mahala pa neno Ilahi,30 yaani kwa hali ya ujumla na sio sifa maalum kwa mungu mmoja, kwa hivyo inasihi jina moja kutumia mahala pa jina ligine, kama asemavyo Mwenyezi Mungu (s.w.t.):

26. Al-Kashif Juz. 1 uk. 30 katika tafsiri ya Bismillah. 27. Kwa maelezo zaidi rejea sarufi ya kiarabu. 28. Majmaul-Bayan Juz. 1 Uk. 19 chapa ya Swayda. 29. Mufradaat Raaghib Uk. 31 neno Ilahi. 30. Limetumika katika maana isiyo kuwa ya kawaida. 59


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 60

Tawhid na Shirk

“Na yeye ndiye Mwenyezi Mungu katika mbingu na Ardhi, anajua ndani yenu na nje yenu na anajua yale mnayoyachuma.” (6 : 3). Na mzani wa Aya hizo unalingana na Aya hii:

“Na Yeye ndiye anayeabudiwa mbinguni na anayeabudiwa ardhini, naye ni Mwenye hekima, Mwenye elimu” (43 : 84). Anasema:

“Wala msiseme watatu, wacheni (itikadi hiyo) ni bora kwenu, hakika Mwenyezi Mungu ni mmoja tu, ameepukana na kuwa na mtoto” (4 : 171). Na anasema:

“Yeye ndiye Mwenyezi Mungu ambaye hapana aabudiwaye isipokuwa Yeye tu, Mfalme Mtakatifu, Mwenye salama, Mtoaji wa amani, Mwangaliaji, Mwenye nguvu, Jabbari, Mkubwa, Mwenyezi Mungu yu mbali na hao wanaomshirikisha” (59 : 23).

60


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 61

Tawhid na Shirk Na anasema: “Yeye ndiye Mwenyezi Mungu, Muumbaji, Mtengenezaji, Mfanyaji wa sura, Mwenye majina mazuri …” (59:24). Bila shaka neno Allah katika Aya hizo na zinazofanana na hizo kwa ujumla huradifiana, yaani ni mungu ambaye ana sifa kadhaa wa kadha. Kutokana na hilo Aya ya kwanza inakaribiana na Aya hii ifuatayo, Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema:

“Sema: Muombeni Mwenyezi Mungu au muombeni Rahmani kwa jina lolote mnalomwita, kwani ana majina mazuri …” (17 : 110). Hakika lafudhi ya neno Allah ukilihesabu kama majina mengine na ukatumia kumwita Allah, huenda likaamsha hisia ya kuwekwa kando maana ya usomi, na likachukua maana ya sifa iliyopo katika neno Ilahi na mengineyo, mfano maneno ya Mwenyezi Mungu (s.w.t):

“Yeye ndiye Mwenyezi Mungu ambaye hapana aabudiwaye isipokuwa Yeye tu, Mfalme Mtakatifu, Mwenye salama Mtoaji wa amani, Mwangaliaji, Mwenye nguvu, Jabbari, Mkubwa, Mwenyezi Mungu yu mbali na hao wanao mshirikisha, Yeye ndiye Mwenyezi Mungu, Muumbaji, Mtengenezaji, Mfanyaji wa sura, Mwenye majina mazuri …” (59 : 23–24).

61


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 62

Tawhid na Shirk Katika Aya mbili hizo jina la Mwenyezi Mungu limetumika kwa maana ya jumla isiyo makhsusi na ya kitaalamu kama lilivyodhihiri hilo kwa mwenye kuchunguza kwa undani. Tunakubali kwamba jina takatifu Allah linatokana na Ilahi lenye maana ya mja au kutahayari, pindi mja anapotafakari juu ya jambo fulani hutahayari, au neno Ilahi ambalo lina maana ya fadhaa, kwani viumbe hupata fadhaa kwake katika haja zao, au linatokana na lahi lenye maana ya utulivu, kwa hakika viumbe wanapata utulivu pindi wanapolitaja jina lake, au limechukuliwa kutokana na neno Lah lenye maana ya kufichikana, kwa hakika Mwenyezi Mungu amefichika kutokana na mawazo au mambo mengineyo waliyotaja,31 lakini hizo ni dhana tu ambazo hazina dalili wala ushahidi wowote, na hata kama tujaalie ni sahihi au baadhi yake ni sahihi bado hazitofidisha chochote zaidi ya uhusiano huo tu. Ama dai la kwamba kubakia uhusiano huo mpaka wakati wa kuteremshwa Qur’an na kisha Qur’an ikaja kutumia uhusiano huo ilikuwa ni katika kulinda na kuhifadhi mahusiano hayo, kwa hakika jambo hilo halina dalili yoyote. Ni dhahiri kwamba maana hizo zinatokana na maana ya neno Ilahi na athari zake, kwani mwenye kumfanya mtu kuwa mungu wake humwabudu kwa lazima, na humkimbilia wakati wa shida na matatizo, moyo wake hutulia pindi anapomtaja, na yasiyo kuwa hayo miongoni mwa athari zinazopatikana na zitokanazo na sifa za kiungu, na lau mpendwa msomaji atachunguza kwa makini Aya ambazo ndani yake lipo jina Ilahi, na akachunguza vielelezo vya fuo na mtiririko wa maneno pindi linapotajwa jina hilo, ataona linamaanisha ileile maana ipatikanayo kwenye jina Allah, isipokuwa tu ni kwamba neno la kwanza (Ilahi) sio makhususi, ama neno la pili (Allah) ni makhususi.

JE! NENO ILAHI LINA MAANA YA MWABUDIWA? Hilo ndilo linalodhihiri kwa wafasiri wengi kwamba neno Ilahi lina maana ya mja, hilo linashuhudiwa na usomaji usio mashuhuri katika maneno ya Mola Manani, Mwenyezi Mungu (a.j) anasema: 31. Majmaul-Bayan Juz. 9 Uk. 19. 62


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 63

Tawhid na Shirk “Je! Utamwacha Musa na watu wake walete uharibifu katika nchi na kukuacha wewe na miungu (Ilahi ) wako…?” (7:127) Imesomwa Ilahi kuwa yamaanisha ibada zako, na huenda dhana hiyo imetokana na kwamba mungu wa hakika au mungu wa kutengenezwa daima huwa shabaha la ibada kwa watu wote na wa mataifa yote, kwa ajili hiyo limefasiriwa neno Ilahi kwa maana ya mwabudiwa, la sivyo ni kwamba kuabudiwa ni sifa mwambata ya Ilahi na wala si maana yake ngeni. Na linalojulisha hapa kwamba neno Ilahi halina maana ya mwabudiwa, ni lile Neno la Ikhlasi: “la ilaha illa llah”, kama ingelikuwa makusudio ya neno Ilahi ni mwabudiwa, basi sentensi hiyo ingelikuwa ya uongo, kwani ni dhahiri shahiri kwamba kuna maelfu ya waabudiwa katika hii dunia, nao si Mwenyezi Mungu (s.w.t), katika hali hiyo inawezekana vipi kukanusha mwabudiwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t), kwa ajili hiyo ndio maana yule mwenye kusema kuwa neno Ilahi (mungu) lina maana ya mwabudiwa akalazimika kukadiria uwepo wa neno haki baada ya neno Ilahi na sentensi kuwa hivi: “la ilaha (bihaqi) illa llah” maana yake ni ”hakuna apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t),” hiyo ni ili kujiepusha na mushkeli huu. Lakini hapa haihitaji kukadiria neno haki, kwani hutofautiana na dhahiri ya sentensi, kwani lengo la Neno la Ikhlasi (kumpwekesha mungu) ni kukanusha hakuna Ilahi (mungu) ulimwenguni isipokuwa Allah, na kwamba dhana hiyo haina mfano halisi ila Yeye Allah pekee, na hayo hayaafikiani na kauli inayodai kwamba Ilahi maana yake ni mwabudiwa, kwani vipo vingi vinavyoabudiwa ulimwenguni hata kama vimetengenezwa. Ama kutumiwa neno hilo katika Aya hiyo si sababu ya kwamba linamaanisha mwabudiwa, bali ni kutokana na itakadi ya waarabu kuwa wana miungu asiyekuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t), kwa mantiki hiyo Mola Manani anasema: “Je! Wanao miungu wanaowalinda badala yetu …?” (21:43).

63


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 64

Tawhid na Shirk Na ukipenda ufafanuzi zaidi ya yale tunayoyafafanua katika tafsiri ya lafudhi ya neno Ilahi (mungu) rejea mambo ambayo huzingatiwa na watu kwamba ni miongoni mwa mamlaka ya kiungu, mwenye kusimamia yote hayo au baadhi yake naye ni Ilahi, kwa hivyo uumbaji, upangaji wa mambo, uendeshaji wa mambo, kuhuisha, kufisha, uwekaji sheria, msamaha na utoaji Shufaa, hayo ni mambo yanayomuhusu Mwenyezi Mungu Muumba Mola wa haki wala hana mwingine. Zifuatazo ni Aya ambazo zinajulisha kwamba Ilahi (mungu) haimaanishi kuwa ni mwabudiwa, bali maana yake ni mpangaji na mwendeshaji wa mambo, au majukumu ya mambo yote yako kwake, baadhi ya Aya hizo ni zile zifuatazo: 1 - Qur’an tukufu inasema: “Lau kama wangelikuwako humo (mbinguni na ardhini) waungu wengine isipokuwa Mwenyezi Mungu, lazima zingeharibika …” 2 : 22 Hoja ya kukanusha kuwako waungu wengi ambao wanaongoza ulimwengu au wenye majukumu ya mambo yote itatimu pale tu iwapo neno Ilahi (mungu) katika Aya hii litakuwa na maana ya mpangaji na mwendeshaji wa mambo, au ambaye majukumu ya mambo yote yako kwake, lakini kama tutajaalia Ilahi (mungu) kwa maana ya mwabudiwa basi dalili hiyo na hoja yake vitakuwa batili, kwani ni wazi kwamba vipo vitu vingi katika ulimwengu huu ambavyo huabudiwa na bado mpangilio wa ulimwengu haujafisidika na kuharibika, kwani wakati wa kuteremshwa aya hizi yalikuwapo masanamu mengi Hijaz (Saudia) yakiitwa Ilahi (miungu), na bado nidhamu na mpangilio wa ulimwengu ulikuwa ni mmoja wala haukuharibika wala haujafisidika mpaka leo. Na yule ambaye anafanya neno Ilahi (mungu) kwa maana ya mwabudiwa hulazimika kuongeza neno ”kwa haki’, yaani lau kama kungelikuwa na waabudiwa wengi wa haki ulimwenguni basi ungeharibika. Lakini hiyo ni kulazimisha mambo. 64


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 65

Tawhid na Shirk 2 - Qur’an tukufu inasema:

“Mwenyezi Mungu hakujifanyia mtoto wala hakuwa pamoja naye Ilahi (mungu) – mwingine- hapo kila Ilahi (mungu) angeliwachukua aliowaumba, na baadhi yao wangeliwashinda wengine” (23 : 91). Dalili hiyo inatimia iwapo tu tutafasiri neno Ilahi (mungu) kama tulivyosema hapo kabla kuwa ni jinasi ambayo huwasilishwa kwa kutumia jina takatifu la Mola Manani (Allah), ukipenda sema hivi: Hapo imetumika kama kinaya ya Muumba au Mpangaji na Mwongoza ulimwengu au Mwenye kufanya mambo yote, na linalonasibiana na maudhui hii ni Muumbaji, na kitendo cha kuwepo waumbaji wengi kingelazimu kila mungu kuwachukuwa wale aliowaumba na baadhi yao wangeliwashinda wengine. Hivyo lau tutajaalia neno hilo Ilahi (mungu) liwe na maana ya mwabudiwa basi dalili na hoja yake vitabatilika, kwani japo vipo vingi vinavyoabudiwa lakini bado ulimwengu haujavurugika katika nidhamu yake na mpangilio wake, na dalili imejulisha hivyo, kwani katika Ka’ba kulikuwako waungu (Ilahi) wengi mia tatu na sitini, wala haukutokea mgongano, mtafaruku, ufisadi wala uharibifu wowote ule ulimwenguni katika nidhamu yake. Kwa hivyo inamlazimu mfasiri wa neno Ilahi (mungu) kuwa ni mwabudiwa ajikalifishe juu ya yale tuliyoyaeleza kuhusiana na Aya iliyokwisha tangulia. 3 - Qur’an tukufu inasema:

65


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 66

Tawhid na Shirk “Sema: lau wangelikuwa pamoja naye waungu (wengine) kama wasemavyo, hapo bila shaka wangelitafuta njia ya kufikia kwa Mwenye Arshi” (17 : 42). Hakika kutafuta njia ya kufikia kwa Mwenye Arshi ambaye ni Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ni matokeo mwambata ya kuwapo waumbaji wengi au wapangaji wa mambo ya ulimwengu tofauti, au wale wenye kushika hatamu ya ulimwengu au mengine miongoni mwa mambo ambayo yanasawiri akilini mwetu maana ya uungu. Na si matokeo mwambata ya uwepo wa waabudiwa wengi. 4 - Qur’an tukufu inasema:

“Hakika nyinyi na wale mnaowaabudu kinyume cha Mwenyezi Mungu, ni kuni za Jahannam mtaifikia, lau hawa wangelikuwa miungu wasingeliingia humo (Jahannam) na wote watakaa humo milele.” (21 : 98-99). Aya hiyo inajulisha kuingia motoni kwa masanamu na waabudu masanamu, hiyo inaonyesha kuwa hao sio mungu kwani wangekuwa mungu wasingeliingia motoni. Na hoja hiyo inatimu iwapo tu tutafasiri neno Ilahi (mungu) kwa maana tuliyoisema huko nyuma, kwani yule aliye Muumba wa ulimwengu na mwenye kuuendesha, au yule ambaye kazi hizo za Mwenyezi Mungu amekabidhiwa yeye haiwezekani ahukumiwe kuingia motoni na awe kuni za moto huo. Hali hiyo itakuwa tafauti lau kama itafasiriwa neno Ilahi (mungu) kuwa ni mwabudiwa, kwani dalili hiyo haitotimia kutokana na ukweli kwamba vilikuwako vitu vingi vikiabudiwa na vimefanywa kuwa ni kuni za Jahannam. Na lau kama utazama kwa makini katika Aya zilizokuja na neno 66


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 67

Tawhid na Shirk Ilahi au Aliha ambayo ni wingi wa Ilahi, bila shaka mwishoni utalipata lile tulilochagua, na kati ya hizo ni Aya:

“Basi mungu wenu ni Mungu Mmoja kwa hiyo nyenyekeeni kwake, na wabashirie habari njema wanyenyekevu” (22:34). Lau itafasiriwa neno Ilahi (mungu) lililopo katika Aya hiyo kuwa ni mwabudiwa, ingelilazimu kuwa uongo, kwani kuna waabudiwa wengi katika jamii ya wanadamu, na kwa ajili hiyo huenda ikalazimu kuongeza neno ”kwa haki”, yaani mwabudiwa kwa haki ni yeye mungu mmoja. Na iwapo tutafasiri kwa maana nyepesi ambayo ina athiri ulimwenguni kwa kupanga na kuendesha mambo, kuleta manufaa na kukinga madhara katika hali ya kujitegemea, wala sio kwa usaidizi wa mwengine, hakutakuwa na haja ya kukadiria neno lenye kubainisha (kwa haki), kwani ni jambo linaloeleweka kwamba katika maisha ya kiumbe na jamii ya watu hakuna mungu mwenye kusifika na sifa hizo. Hatutaki kusema kwamba: Neno Ilahi (mungu) lina maana ya muumbaji, mpangaji, mfishaji na msamehevu, kwani maana inayomjia mtu toka katika neno hilo ni moja isiyo na mpandano, bali ni kwamba hizi sifa ni anwani zinazoashiria ile maana iliyowekwa ya asili ya neno Ilahi (mungu), na yajulikana wazi kwamba sifa hizi kuwa anwani zenye kuashiria ile maana ya asili ya neno hilo, haimaanishi kwamba sifa hizo ndio maana yenyewe ya asili ya neno hilo, kama ambavyo Mwenyezi Mungu kuwa na mamlaka juu ya ulimwengu wote ni sifa inayoashiria ile maana nyepesi ya neno Ilahi (mungu), lakini sio maana yenyewe ya neno hilo. Mpaka hapa mpendwa msomaji umefahamu kuwa neno Ilahi (mungu) na uungu hayana maana ya mwabudiwa, bali makusudio yake ni Allah yaani Mwenyezi Mungu, na si kingine, isipokuwa neno moja ni makhususi na lingine sio makhususi. 67


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 68

Tawhid na Shirk Jambo lililobakia hapa ni kuelezea maana ya neno Rabbi (mola) na Rubuubiyya (ulezi) ambayo hupatikana zaidi katika maneno ya Mawahabi, tunasema:

MAANA YA RABBI (MOLA MLEZI) Neno Rabbi katika Kiarabu ni, mmiliki, mfalme, muumba na mwenyewe, au mwenye kukifanyia islahi kitu, husemwa: Rabbi fulani anashughulikia mambo fulani, pale anapokuwa analifanyia jambo fulani islahi, na Mwenyezi Mungu aliyetukuka ndiye Rabbi kwani hushughulikia na kuboresha mambo ya viumbe, neno Rabbu huwa na maana ya mwenye kusimamia mambo ya mlelewa.32 Feiruz Abaad anasema: Rabbi (Mlezi) wa kila kitu; maana yake ni mmiliki wake, mstahiki na msimamizi wa hayo‌ Rabbi (Mlezi) wa jambo fulani; yaani mwenye kushughulikia na kuboresha.33 Na katika kitabu kamusi ya kiarabu ipo ibara: Rabbi (Mlezi) ni mmiliki, mboreshaji na bwana.34 Maana hii ipo katika vitabu vya Lugha na kamusi mbalimbali.

JE! NENO RABBI (MLEZI) LINA MAANA TOFAUTI? Kazi ya vitabu vya Lugha na kamusi miongoni mwa kazi zake ni kudhibiti maeneo ya matumizi ya maneno na lafudhi mbalimbali, bila kujali je hutumiwa katika maana iliyowekewa au hapana. Ama kazi ya kuainisha hali, kumaizi pamoja na kupambanua hakika na kinaya, hayo yako nje ya utaratibu na matumizi ya vitabu vya lugha. 32. Maqayiis Lugha Juz. 2 uk. 381. 33. Qamus Lugha mada ya Rabbu. 34. Munjid mada ya Rababa. 68


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 69

Tawhid na Shirk Na hiyo ni kasoro na mapungufu yanayopatikana katika vitabu vya lugha na kamusi, kwani mtu hukumbana na maana tofauti zenye kutofautiana lakini ni za lafudhi moja, hali ambayo humsababishia kujiuliza je mwanzilishi wa kiarabu ameweka lafudhi moja kuwa na maana kumi, lakini baada ya kufanywa utafiti wa kina inabainika sivyo hivyo bali ni maana moja, ama maana zingine zilizobakia zinatokana na maana ya asili. Na hilo ndio lilitokea kwa mwandishi aliyejulikana kwa jina la Maududi, yeye alifikiri neno Rabbi (mlezi) lina maana tano katika asili, na akaitolea kila maana ushahidi wa Qur’an tukufu. Na hakuna shaka kwamba neno Rabbi (mlezi) limetumiwa na Qur’an na lugha ya kiarabu kwa maana moja katika sehemu zifuatazo ambazo ni sura pana na mifano halisia tofauti, baadhi ya sehemu hizo ni: 1- Malezi: Mfano malezi kwa mtoto. 2- Kuchunga: Mfano wa mchungaji wa mifugo. 3- Serikali na Siasa: Mfano fulani anaongoza watu wake, au anawatawala na kuwaongoza. 4- Mmiliki: Kama ilivyopokewa habari kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Je! ni bwana wa mifugo au bwana wa ngamia?” 5- Mwenyewe mwenye kitu: mfano wa mwenye nyumba, kama inavyosema Qur’an tukufu: “Basi wamuabudu Mola wa Nyumba hii” (106:3). Hapana shaka lafudhi hii imetumiwa katika nyanja mbalimbali katika hayo na yanayofanana na hayo, lakini maana zote zinarejea katika maana moja ya asili, na maana hizo nyingine zote ni sura tofauti na mifano tofauiti ya maana ya asili, na ni mifano aina tafauti ya kimatendo ya ile dhana moja ya asili, naamisha yule ambaye aliyeachiwa jukumu lote la malezi ya kitu na yote yanayohusu shughuli za kimalezi. Hivyo iwapo itasemwa mwenye shamba amelishughulikia shamba lake na kuliboresha, hiyo ni kwa sababu jukumu la kushughulikia shamba lina muhusu yeye na liko chini yake. Na tukisema kiongozi wa watu fulani ni 69


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:23 PM Page 70

Tawhid na Shirk Rabbi (mlezi) hiyo ni kwa sababu hatima ya mambo ya watu hao huwa mikononi mwake, naye ndiye kiongozi wao, mwenye kupanga na kuratibu mambo yao. Na iwapo mwenye nyumba tukimwita Rabbi (mlezi), basi hiyo ni kwa sababu madaraka ya nyumba hiyo yamo mikononi mwake, yeye ndiye mwenye kuiendesha atakavyo. Kwa mtindo huo bwana, kiongozi, mmiliki, mwenyewe na mfano wa hao, ni mifano tu miongoni mwa mifano halisi ya maana moja ya asili ambayo hupatikana katika mifano yote hiyo, na hivyo haipasi kuichukulia mifano hiyo kuwa ni maana nyingine ngeni ya neno Rabbi, bali maana halisi iliyowekewa hilo neno ni: Mwenye mamlaka ya kupanga mambo ya kitu fulani na kuyaendesha, na hiyo ni dhana jumuishi ambayo inajumuisha mifano yote hiyo mitano iliyotajwa, yaani kulea, kuchunga, kumiliki, kuongoza na muhusika wa kitu. Hivyo Nabii Yusuf (a.s.) anapotumia neno Rabbi kwa Mfalme wa Misri pale anaposema: “Bila shaka yeye (mumeo) ni Rabbi wangu ametengeneza makazi yangu vizuri…” (12:23) ni kwa sababu Yusuf (a.s.) alilelewa katika nyumba ya Mfalme wa Misri, aliyekuwa msimamizi wa malezi yake na kushughulikia mambo yake. Tunapomkuta Yusuf anamsifu Mfalme wa Misri kwamba yeye ni Rabbi wa mfungwa aliyekuwa na Yusuf korokoroni, pale aliposema: “Enyi wafungwa wenzangu wawili! ama mmoja wenu atamnywesha Rabbi wake pombe...” (12:41) ni kwa sababu Mfalme wa Misri ni kiongozi, mtawala na mwenye kuongoza mambo ya Misri. Qur’an inaeleza kwamba Mayahudi na Wakristo wamewafanya viongozi wao kuwa Marabi, inasema: “Wamewafanya Makasisi wao na watawala wao kuwa ni marabi badala ya Mwenyezi Mungu…” (9:31), ni kwa sababu wao waliwapa hao madaraka ya utawala ambayo kwa hakika yanamhusu Mwenyezi Mungu pekee. Mwenyezi Mungu (s.w.t) Yeye mwenyewe anajisifu kuwa ni Rabbi wa 70


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 71

Tawhid na Shirk nyumba, kwani Yeye ndiye anayemiliki mambo ya nyumba hiyo, mambo yenye kuonekana na mambo yasiyoonekana, na hakuna yeyote mwenye jukumu hilo. Qur’an tukufu inasema: “Rabbi wa mbingu na ardhi na yaliyomo kati yake, na ni nani Rabbi wa mashariki zote. (na magharibi zote.)” (37:5) Inasema tena: “Na kwamba Yeye ndiye Rabbi wa (nyota) na shiiraa.” (53:49), ni kwa sababu Yeye ndiye mwenye madaraka ya kuongoza na kuendesha mambo yote. Kwa ubainifu huo tutakuwa tayari tumeondoa giza na tumepambanua maana halisi ya neno Rabbi, ambalo linapatikana katika Aya nyingi ndani ya Qur’an tukufu. Ni jambo lililozagaa baina ya Mawahabi kwamba Tawhiid imegawanyika katika sehemu kuu mbili: 1. Tawhiid katika Ulezi 2. Tawhiid katika Uungu. Wamesema kwamba: Hakika Tawhiid katika ulezi hii ina maana ya kuamini kwamba muumba wa ulimwengu huu ni mmoja, hata washirikina wa enzi za Mtume (s.a.w.w) walikuwa wakilitambua hilo, ama Tawhiid katika uungu ni kumpwekesha Mwenyezi Mungu (s.w.t) katika ibada, yaani kutomwabudu mwingine asiyekuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t), na Mtume (s.a.w.w) alifanya juhudi kubwa juu ya jambo hilo. Na ukweli ni kwamba suala la washirikina zama za Mtume (s.a.w.w) kukubaliana juu ya Muumba halina shaka, lakini kosa lililofanyika ni kuiita Tawhiid ya uumbaji kuwa ni Tawhiid katika ulezi. Hilo ni kosa kwa sababu maana ya Ulezi haina maana ya Uumbaji, bali maana yake ni kama vile tulivyokwisha bainisha hapo kabla, ambayo ni 71


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 72

Tawhid na Shirk kupanga na kuendesha mambo ya ulimwengu, na hilo la kupanga mambo na kuendesha sio jambo waliloafikiana baina ya washirikina na waabudu masanamu katika zama za Mtume (s.a.w.w) kama kundi hilo lilivyodai. Tunakubali kwamba walikuwako watu katika zama za ujinga (jahilia) wakiitakidi kwamba hakuna mpangaji na mwendeshaji wa ulimwengu ila Mwenyezi Mungu pekee, lakini walipata upinzani mkubwa kutoka kwa kundi kubwa la wale ambao waliokuwa wakiitakidi kuwapo waendeshaji wengi wa ulimwengu, kadhia hiyo tunaipata kutoka katika Aya mbalimbali za Qur’an tukufu na vitabu vya rejea. Hapa tunawatupia macho Mawahabi ambao huita Tawhiid katika Ibada kuwa ndiyo Tawhiid katika Ulezi, tunawaelekeza katika Aya zifuatazo ili iwe bayana kwao kwamba kulingania Tawhiid katika Ulezi si kulingania Tawhiid katika uumbaji, bali huko ni kulingania Tawhiid katika Upangaji na uendeshaji wa mambo. Katika zama za ujinga Washirikina walipotoka kuhusiana na kumpwekesha Mwenyezi Mungu (s.w.t) katika ulezi, na wakawa wanaamini kuwako wapangaji na waendeshaji wengi wa ulimwengu, ijapokuwa walikuwa wakiamini kwamba Muumba wa ulimwengu ni mmoja, hivyo kamwe hatuwezi kufasiri neno Rabbi katika Aya zifuatazo kwa maana ya Muumba, hebu zingatia Aya hizi: i- “Akasema: Bali Rabbi wenu ndiye Rabbi wa mbingu na ardhi ambaye aliziumba.” (21:56) Na lau ingelikuwa makusudio ya Rabbi hapa kwamba ni muumbaji basi sentensi hii: “Ambaye aliziumba” ingekuwa ni nyongeza isiyohitajika (na isiyo na maana), dalili juu ya hilo ni kwamba lau sisi tutaweka lafudhi au neno muumba mahala pa Rabbi katika Aya hii, tutakuwa muda huo hatuna haja ya sentensi “Ambaye aliziumba”, (kwani itasomeka “Akasema: Bali Muumba (Rabbi) wenu ndiye Muumba (Rabbi) wa mbingu na ardhi ambaye aliziumba.”). hiyo ni tofauti na pale litakapofasiriwa nena Rabbi kuwa ni mpangaji wa mambo na mwendeshaji wake, katika sura hii sen72


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 73

Tawhid na Shirk tensi ya mwisho “Ambaye aliziumba” ni muhimu, kwa sababu ibara hiyo ni sababu ya sentensi ya kwanza, inamaanisha itakuwa hivi: hakika muumba wa ulimwengu ndiye mwenye kuupangilia, kuumiliki na mwenye kuendesha mambo yake yote. ii- “Enyi watu! Mwabuduni Rabbi wenu aliyewaumba…” (2:21). Hakika neno Rabbi katika Aya hii halina maana ya muumbaji kama tulivyoeleza, kwa sababu kama kweli ingelikuwa neno hilo linamaana ya muumbaji basi sentensi hii “ambaye amekuumbeni” isingetajwa hapa, na hiyo ni tofauti na pale tutakaposema neno Rabbi linamaanisha mpangaji na mwendeshaji wa mambo, kwani hapo sentensi “ambaye amekuumbeni” inakuwa sababu ya Tawhiid katika Ulezi, kwani maana itakuwa: Hakika ambaye amekuumbeni ndiye mpangaji na mwendeshaji wa mambo yenu. iii- “Sema: je! Nishike Rabbi mwengine asiyekuwa Mwenyezi Mungu, na hali yeye ndiye Rabbi wa kila kitu!” (6:164). Aya hii inaelezea hali ya Washirikina wa zama za Mtume (s.a.w.w). Walikuwa wakitofautiana na Mtume (s.a.w.w) katika suala la Ulezi. Mtume (s.a.w.w) alipinga itikadi zao na aliwakataza kumfanya mwingine asiyekuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) kwamba ni Rabbi, na ni maarufu kwamba tofauti iliyokuwepo kati ya Mtume na washirikina, haikuwa katika suala la Tawhiid katika Uumbaji, ushuhuda wa hilo ni Aya zilizokwishatangulia, ambazo zinathibitisha kwamba walikuwa wakikiri kwamba hapana muumba asiyekuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t). Kwa hivyo hatuna sababu ya kudai kulikuwako tofauti baina ya waislamu na washirikina katika suala la muumba, bali tofauti ilikuwapo kuhusiana na mpangaji wa mambo ya ulimwengu na mwendeshaji wake. iv- “Na (kumbuka) Rabbi wako alipowaleta katika wanaadamu kutoka miongoni mwao kizazi chao, akawashuhudisha juu ya nafsi zao: Je! Mimi siye Rabbi wenu? Wakasema: Ndiye, tunashuhudia (kuwa wewe 73


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 74

Tawhid na Shirk ndiye Rabbi wetu) msije mkasema Siku ya Kiyama, hakika sisi tulikuwa tumeghafilika nayo.” (7:172). Hakika Mwenyezi Mungu (s.w.t) katika Aya hiyo ameeleza kwamba viumbe wote wamekiri kuhusu Tawhiid katika Ulezi (rububiyya), na sababu katika hilo ni kwamba atatumia ahadi hiyo Siku ya Qiyama kuwahojia waja wake, anasema:

“Au mkasema; baba zetu ndio walioshirikisha zamani, nasi tulikuwa kizazi nyuma yao, je! Utatuangamiza kwa sababu ya yale waliyoyafanya wapotovu?” (7 : 173). Ikiwa hilo limebainika basi tunasema: Aya hiyo ambayo imeteremshwa katika jamii ya Washirikina ni dalili tosha ya kuwepo kundi fulani ambalo lilikuwa likienda kinyume na ahadi hiyo, na kama ingelikuwa ulezi una maana ya uumbaji ingelazimu katika jamii ile kuwepo watu wenye kumkhalifu Mtume (s.a.w.w) kuhusiana na Tawhiid katika Uumbaji, lakini lilo la Washirikina kutofautiana na Mtume katika suala la kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika uumbaji halikuwapo katika zama za Mtume (s.a.w.w), hata tuwazingatie kuwa ndio wenye kukhalifu ahadi hiyo iliyotajwa, hivyo bila shaka tofauti ilikuwepo katika suala la upangaji wa mambo na uendeshaji wa ulimwengu. Kwa ubainifu huo inabainika kwamba maana ya Rabbi ni mwendeshaji wa ulimwengu. v- “Je! Mtamuua mtu kwa sababu anasema Rabbi wangu ni Mwenyezi Mungu? Na kwa hakika yeye amekuleteeni dalili za wazi wazi zitokazo kwa Rabbi wenu.” (40 : 28). Aya hii inafungamana na muumini wa familia ya Firaun ambaye alikuwa akimtetea Nabii Musa (a.s.) mbele ya watu wa karibu wa Firaun; 74


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 75

Tawhid na Shirk aliyekuwa akimuhami Mtume huyu adhimu asifikwe na hatari. Ama dalili ya neno Rabbi kuwa lina maana ya mpangaji wa mambo ipo wazi, kwa sababu Firaun hakudai kuwa yeye ni muumba wa mbingu na ardhi wala kuwa mshirika wa Mwenyezi Mungu (s.w.t) katika kuumba ulimwengu na mwenye kufanya vitu viwepo. Vile vile uhakika huo unabainishwa na historia ya Mafiraun (mafarao), kwa mtazamo huo lazima makusudio ya ulinganio wa Nabii Musa (a.s.) aliposema: “Rabbi wangu ni Mwenyezi Mungu” yawe ni kuhusisha kwa Mwenyezi Mungu upangaji wa mambo ya ulimwengu na uwendeshaji wake, yaani hiyo ni kazi ya Mwenyezi Mungu tu, na wala makusudio si uumbaji, kwani ingelikuwa makusudio ni mambo ya uumbaji basi kusingekuwako mzozo na tafauti kati yake na Firaun, kwani Firaun alikuwa anakiri kuwepo muumba ambaye ni Mwenyezi Mungu kama tulivyoeleza huko nyuma, na zaidi ya hapo ni kwamba Mwenyezi Mungu katika Aya ifuatayo anasema: vi- “Na akasema Firaun, niacheni nimuue Musa, naye amwite Rabbi wake! Hakika ninachelea asije kuiharibu dini yenu au kuleta matata katika nchi.” (40 : 26). Hakika kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika uumbaji hakukuwa na sababu ya kutofautiana wala mzozo hadi iwe chanzo cha ulinganio wa Nabii Musa (a.s.) kwa wana wa Israeli ili kuwabadilisha, kwa ufafanuzi huo yanaeleweka maneno ya Firaun pale aliposema: “Mimi ndiye Rabbi wenu mkubwa.” (79 : 24) vii- “Wakasema: Rabbi wetu ni Rabbi wa mbingu na ardhi, hatumuombi Mungu yeyote ila Yeye.” (18 : 14). Hakika vijana ambao walikimbia uovu wa beberu mkubwa wa zama zile walikuwa wakiishi katika jamii ya watu wanaoabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t), lakini uovu wa wakati ule haukuwa ni ile aina ya watu kuamini kuwa hiyo miungu yao ni waumbaji wa ulimwengu, na hasa kwamba tukio la watu wa pangoni (As’haabul-Kahf) lilitokea baada 75


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 76

Tawhid na Shirk ya kuzaliwa Nabii Isa (a.s.), muda ambao akili za viumbe na fikra zao vilikuwa vimeelimika zaidi katika suala la Tawhiid, akili za watu wa jamii ile hazikuwa zinakanusha uumbaji wa Mwenyezi Mungu, isipokuwa Shirki yao ilikuwa kutokana na itikadi ya kuwepo wapangaji na waendeshaji wengi wa mambo. viii- Hakika dalili iliyo wazi kabisa kuhusiana na kwamba ulezi ndiyo upangaji na uendeshaji wa mambo, na sio uumbaji kama inavyodhaniwa, ni Aya ifuatayo inayopatikana katika Sura Rahman ambayo imejirudufu humo: “Basi nyinyi wawili mtakataa mema ya Rabbi wenu?” (55 : 13). Aya hiyo imerudufu mara 31 na neno Rabbi limefuatana hatua kwa hatua na neno Neema, ni jambo lisilo na kificho kwamba kutaja kadhia ya neema sambamba na kutaja suala la ulezi wa Mwenyezi Mungu katika maisha ya viumbe na kuhifadhi vizazi vyao dhidi ya kutoweka, ni jambo lenye uwiano na kuoana vizuri zaidi, kwani kutaja neema ambazo ni sehemu ya ulezi wa Mwenyezi Mungu autoao kwa viumbe, ni jambo linalolingana na kuwiana na maudhui ya ulezi na upangaji wa mambo ambayo yanaambatana na udumishaji wa utoaji wa neema. ix- Suala la kushukuru limeambatanishwa na neno Rabbi ndani ya Qur’an tukufu katika sehemu tano, na shukrani huenda sanjari na neema ambayo ndiyo sababu ya kubakia uhai wa mwanadamu, kuuhifadhi, kuudumisha, kuukinga na kuuepusha na maharibiko, na kwa hakika kumwendesha mwanadamu si jambo jingine ila ni kule kudumisha uhai wake na kuuhifadhi usiharibike wala kutoweka, hebu angalia Aya hizi:

“Na (kumbukeni) alipotangaza Rabbi Wenu, kama mkishukuru bila shaka nitakuzidishieni, na iwapo mtakufuru basi adhabu yangu ni kali sana.” (14:7)

76


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 77

Tawhid na Shirk

“Na akasema: Ewe Rabbi wangu! Nipe nguvu nishukuru neema Yako uliyonineemesha mimi na wazazi wangu…” (27 : 19)

“Akasema: haya ni kwa fadhila za Rabbi wangu, ili anijaribu nitashukuru au nitakufuru? Basi anayeshukuru ni kwa ajili ya nafsi yake…” (27 : 40)

“Akasema: Ee Rabbi wangu! Niwezeshe nishukuru neema Zako ulizonineemesha mimi na wazazi wangu…” (46 : 15)

“Kuleni katika riziki ya Rabbi wenu na mumshukuru, na Rabbi ni mwingi wa kusamehe” (34 : 15) x- Na miongoni mwa yale yanayojulisha tuliyoyasema ni maneno ya Mola Manani:

“Nikawaambia; ombeni msamaha kwa Rabbi wenu, hakika Yeye ni mwingi wa kusamehe, atakuleteeni mawingu yanyeshayo mvua nyingi na atakupeni mali na watoto, na atakupeni mabustani, na ataku77


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 78

Tawhid na Shirk fanyieni mito.” (71 : 10-12). Vile vile huelezwa mfano wa hayo katika Sura Hud: 52, hivyo ndivyo mpendwa msomaji unavyoelewa kuwa ni vipi uendeshaji wa mambo ya ulimwengu, na kazi hiyo ndio tafsiri ya neno Rabbi, yeye ndiye ambaye huleta mvua, huongeza mali na watoto, naye hufanya mabustani na mito, na mambo yote hayo yanahusiana na upangaji na uendeshaji wa mambo.

NATIJA YA MADA HII Kutokana na utafiti wa kina kuhusiana na mada hii tunafaidika na mambo mawili: 1. Hakika ulezi wa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ni ibara ya uendeshaji wa mambo ya ulimwengu na sio uumbaji wake. Aya nyingi zilizotangulia zimejulisha kwamba hakukuwepo na makubaliano juu ya suala la “Tawhiid katika upangaji na uendeshaji wa mambo”, kinyume na suala la “Tawhiid katika uumbaji”, na ni kwamba katika historia kwa hakika kulikuwepo na kundi kubwa ambalo lilikuwa likiitakidi kwamba upangaji na uendeshaji wa mambo yote au baadhi ya mambo ya ulimwenguni unafanywa na asiyekuwa Mwenyezi Mungu (azza wa jal), na walikuwa wakiwanyenyekea na kuwaamini marabi hao. Ulezi katika Sheria sio Ulezi katika Uumbaji, na huenda baadhi ya vikundi vikampwekesha Mwenyezi Mungu (s.w.t) katika Uumbaji lakini vikamshirikisha katika Sheria. Mayahudi na Manaswara walijiingiza katika Shirki ya Ulezi katika Sheria, kwani wao wanawapa hatamu ya uongozi, upangaji mambo na utungaji sheria Makasisi wao, watawa na wakuu wao wa kanisa, na wakawafanya kuwa marabi wao, na hali kwa hakika upangaji na uendeshaji wa mambo hayo ikiwemo utungaji wa sheria ni wa Mola Manani. Qur’an tukufu inasema: “Wamewafanya Makasisi wao na Watawa wao kuwa ni Marabi badala ya Mwenyezi Mungu…” (9 : 31) 78


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 79

Tawhid na Shirk Vile vile inasema: “Wala baadhi yenu wasiwafanye baadhi kuwa Marabi badala ya Mwenyezi Mungu…” (3 : 64) Ilhali kwamba makundi mengine Shirki katika Ulezi kwao wao haikukomea katika wigo huu tu bali ilishamiri mpaka katika sekta nyingine zinazohusu ulimwengu, na hivyo kunasibisha uendeshaji wa ulimwengu kwa malaika, majini, roho takatifu, nyota na sayari. Hata kama hawakunasibisha mambo yote ya uendeshaji wa mambo kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu (azza wa jal), lakini suala la ushirikina katika ulezi huhusisha zaidi utelekezaji wa baadhi ya mambo ya ulimwengu kwa baadhi ya watu, waja wema na viumbe wengine. . Kwa hakika Aya zilizotangulia zinajulisha faida hii, kwa kweli tulitaka kueleza mengi hapa, lakini tutatosheka na hayo tuliyoyaeleza kutokana na Aya mbalimbali. Tunamwachia mpendwa msomaji mtafiti achunguze na kuzingatia kwa makini Aya hizo za Qur’an tukufu. Ewe Mpendwa msomaji baada ya kujua kwa undani tangulizi hizo kumi sasa umewadia wakati wa kujikita katika kufafanua maana ya ibada, asili na uhakika wake, kwani ndio jambo muhimu sana katika mada husika, kwani kwa kubainisha maana halisi ya ibada ndipo tutajua Tawhiid ni nini na Shirki ni nini, na ndipo tutapambanua Mwanatauhidi katika ibada ni yupi na mshirikina katika ibada ni yupi. Na hilo litakuwa kigezo na dira ya kupembua na kupambanua matendo mengi ambayo hujiri katika sira na ada za Waislamu, mambo ambayo huyatenda maishani mwao tangu enzi za Mtume hadi hivi leo.

79


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 80

Tawhid na Shirk

SEHEMU YA PILI: MAELEZO KUHUSU MAANA HALISI YA IBADA Ibada ni unyenyekevu ambao unatokana na ile hali ya kuitikadi uungu wa mwabudiwa, ulezi wake na utendaji wake wa mambo kwa kujitosheleza na kujitegemea. Neno ibada ni dhana kama dhana nyingine za wazi, ni kama vile maji au ardhi, ijapokuwa kidhihinia na kidhana ni jambo linalojulikana lakini ni vigumu kulieleza kwa kina hata kama linafahamika katika akili za watu. Na ibada kama ambavyo ni jambo linalojulikana kidhihinia na kidhana pia linajulikana kimfano na kimatendo, kiasi kwamba ni jambo jepesi kumaizi baina ya kitendo kinachomwadhimisha mtu na kumtukuza, na kile kingine kisichofanya hivyo. Kwa hivyo mtu kumkumbatia mpenzi wake, kumbusu, kuhifadhi nguo yake kwa shauku, au kubusu kaburi lake baada ya kufariki kwake, hayo hayanasibishwi wala kuhesabiwa kuwa ni ibada ambayo anamfanyia mpenzi au mpendwa wake. Kwa mfano watu wanapokwenda kuzuru makaburi ya watu watukufu na waheshimiwa, husimama mbele ya makaburi yao kwa heshima, huadhimisha na kuwatukuza watu hao, na matendo yao abadan hayahesabiwi kuwa ni ibada, hata kama matendo hayo wakati fulani hufikia unyenyekevu wa hali ya juu, kwa hivyo dhamira ndiyo hakimu mwadilifu awezaye kutofautisha kati ya uadhimishaji au utukuzaji na ibada, na wala hakuna haja ya kujikalifisha, lakini tukitaka tuelewe vizuri neno ibada kwa maelezo maalum tunalitolea maelezo kwa maana tatu nazo ni:

80


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 81

Tawhid na Shirk 1. MAANA TATU ZA IBADA: Maana ya kwanza: Ibada ni unyenyekevu wa maneno au wa vitendo, ambao chanzo chake ni kule kuamini Uungu (Uluhiyya)wa mwenye kunyenyekewa. Zipo Aya chungu nzima zinazotoa ishara kuhusiana na tafsiri hiyo, kwa hakika zitakapochunguzwa kwa makini na undani bila shaka yatabainika mambo mawili: Jambo la kwanza: Waarabu wa zama za ujinga (jahiliya) ambao Qur’an imeteremshwa katika jamii zao walikuwa wakiitakidi yale waliyokuwa wakiyaabudu kuwa ni miungu. Jambo la pili: Hakika ibada ni ibara ya kauli na matendo na chanzo chake ni kule kuitikadi uungu wa mwabudiwa, na kwamba kauli na matendo yasipotokana na itikadi hiyo basi unyenyekevu huo au utukuzaji na heshima hiyo havitokuwa ibada. Hapa yapo madai mawili: Dai la kwanza: Waarabu wa zama za ujinga bali waabudu Masanamu, waabudu Jua, Nyota na Majini walikuwa wakiitakidi kwamba vile vinavyoabudiwa kuwa ni miungu, na vitu hivyo huvifanya miungu wadogo na juu yao yupo mungu mkuu ambaye tunamwita Allah, yaani (Mwenyezi Mungu). Dai la pili: Hakika dhahiri ya Aya ni kwamba ibada ni ibara ya unyenyekevu ambao hujieleza kwa maneno na matendo yatokanayo na ile imani ya kuamini uungu, sawa iwe uungu mdogo au mkubwa. Ama kuhusu dai la kwanza, kwa hakika zipo Aya kadhaa zinazojulisha hilo na hapa tunataja baadhi ya Aya hizo, Mwenyezi Mungu anasema:

81


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 82

Tawhid na Shirk

“Ambao wanafanya kuwa pamoja na Mwenyezi Mungu, mungu mwingine basi karibuni watajua” (15:96)

“Na wale ambao hawamuombi mungu mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu…” (25:68)

“Na walifanya waungu badala ya Mwenyezi Mungu ili wawe nguvu kwao.” (19:81)

“Je! Nyinyi mnashuhudia kwao wao waungu wengine pamoja na Mwenyezi Mungu?” (6:19)

“Na (kumbukeni) Ibrahim alipomwambia baba yake Azar; Je! Unawafanya masanamu kuwa Miungu?” (6:74) Aya hizo zinashuhudia kwamba ulinganio wa Washirikina ulikuwa unakwenda pamoja na imani ya kuwa masanamu ni miungu, aidha neno Shirki limefasiriwa katika baadhi ya Aya kuwa ni kuyafanya masanamu kuwa waungu pamoja na Mwenyezi Mungu (s.w.t), na hayo ni kwa mujibu wa maneno ya Mola Manani anaposema:

82


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 83

Tawhid na Shirk “Tangaza unaloamrishwa na ujitenge mbali na washirikina. Hakika sisi tunakutosha kwa (shari ya) wafanyao dhihaka. Ambao wanaofanya kuwa pamoja na Mwenyezi Mungu mungu mwingine, basi karibuni watajua” (15:94-96) Kwa hivyo Qur’an inafasiri uhalisia wa Shirki kwamba ni kule kuitakidi kwao uungu wa vile wanavyoviabudu, hiyo ni pale Mwenyezi Mungu aliposema: “Au yuko kwao anayeabudiwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu? Mwenyezi Mungu ametakasika na hao wanaomshirikisha naye.” (52:43) Kwa hivyo katika Aya hiyo imefanywa kule kuitakidi kwao uungu wa asiyekuwa Mwenyezi Mungu kuwa ndiyo kigezo cha Shirki, na makusudio ya Shirki hapa ni Shirki katika Ibada. Kwa kuzirejea Aya hizo na zile zinazofanana na hizo ambazo zimeeleza maudhui ya Shirki hususan mada ya ushirikina wa waabudu masanamu hudhihiri uhalisia huu waziwazi kabisa, kwamba ibada zao zilikuwa zikiambatana na itikadi ya kuwa hiyo ni miungu, bali inawezekana ikadhihirika kwamba ushirikina wao ulitokana na kule kuitakidi kwao uungu wa vile walivyokuwa wakiviabudu, na kwa ajili ya itikadi hiyo wakawa wanayaabudu hayo na wakawa wanayawekea nadhiri na kuchinja mifugo kwa ajili yake, na mengineyo ambayo yanayofungamana na taratibu na mambo ya ibada. Na kwa kuwa Tawhiid inapiga vita itikadi yao ya uungu wa asiyekuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t), ndio maana walikuwa wakijiona na kutakabari wakati walipokuwa wakisikia neno la Tawhiid, kama Mola Muumba anavyosema: “Hakika wao walipokuwa wakiambiwa; hakuna anayepaswa kuabudiwa isipokuwa Mwenyezi Mungu tu hujivuna.” (37:35) Hii ina maana kwamba watu hao walikataa katu katu maneno hayo, kwani walikuwa wakiitakidi masanamu waliyokuwa wakiyaabudu kuwa ni miun83


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 84

Tawhid na Shirk gu, na wakiyaabudu kwa kuwa ni Miungu - kulingana na mawazo yao –, kutokana na itikadi hiyo potovu walikuwa wakilinganiwa katika kumwamini Mwenyezi Mungu Mmoja, walimkanusha na kumkufuru Yeye, kwa sababu wao hawakuutambua Uungu Wake pekee, na iwapo mlinganiaji atamletea Allah mshirika katika uungu basi watamwamini na kuungana naye katika mawazo na fikira hiyo, Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema:

“Hayo ni kwa sababu ya kuwa alipoombwa Mwenyezi Mungu peke yake mlikataa, na aliposhirikishwa mkaamini, basi hukumu ni yake Mwenyezi Mungu, Mtukufu, Mkuu.” (40:12). Mpaka hapa imedhihirika wazi dai la kwanza, ama dai la pili linabainishwa na Aya zifuatazo ambazo zinaamuru aabudiwe Mwenyezi Mungu (s.w.t), na zinakataza kuabudiwa mwingine, na kutoa ushuhuda kuwa hapana mungu anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t), Allah anasema: “Enyi watu wangu nyinyi hamna mungu ila Yeye” (7:59) Na maana ya Aya hiyo ni kwamba anayestahiki kuabudiwa ni yule aliye mungu, naye ni mwingine ila Allah, vipi basi mnamwabudu asiyekuwa Yeye ambaye hana sifa ya Uungu, na inakuwaje mnamwabudu mwingine na kumuacha Mwenyezi Mungu ambaye ndiye inalazimu kuabudiwa? Madhumuni ya Aya hiyo yameelezwa katika sehemu l0 au zaidi ndani ya Qur’an tukufu, mpendwa msomaji unaweza kurejea kama ifuatavyo:

1. “Enyi kaumu yangu! Mwabuduni Mwenyezi Mungu, nyinyi hamna Mungu ila Yeye tu, basi hamuogopi?” (7: 65) 84


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 85

Tawhid na Shirk

2. “Enyi watu wangu! Mwabuduni Mwenyezi Mungu, nyinyi hamna Mungu ila Yeye.” (7:73)

3. “Enyi kaumu yangu! Mwabuduni Mwenyezi Mungu hamna mungu ila Yeye.” (7: 85)

4. “Enyi watu wangu! Mwabuduni Mwenyezi Mungu, nyinyi hamna mungu isipokuwa Yeye tu.” (11:50)

5. “Enyi watu wangu! Mwabuduni Mwenyezi Mungu, nyinyi hamna mungu ila Yeye tu.” (11:61)

6. “Akasema: Enyi watu wangu! Mwabuduni Mwenyezi Mungu nyinyi hamna mungu ila Yeye tu.” (11:84)

7. “Na hatukumtuma kabla yako Mtume yeyote ila tulimfunulia ya kwamba hakuna anayeabudiwa ila Mimi tu, basi niabuduni.” (21:25)

8. “Enyi watu wangu! Mwabuduni Mwenyezi Mungu hamna Mungu 85


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 86

Tawhid na Shirk isipokuwa Yeye…” (23:23)

9. “Na tunawapelekea Mtume kutoka miongoni mwao, (akawaambia); mwabuduni Mwenyezi Mungu hamna Mungu isipokuwa Yeye…” (23:32)

10. “Kwa hakika mimi ndiye Mwenyezi Mungu hakuna anayeabudiwa ila mimi tu…” (20:14). Maelezo hayo yanaleta faida kwamba ibada ni ibara ya unyenyekevu na kujidhalilisha kutokanako na ile imani ya Uungu wa ya mwabudiwa, kwani tunapochunguza na kujiuliza hivi inakuwaje Qur’an inakanusha ibada ya washirikina ambayo hufanyiwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t)? ni kwa sababu wanavyoviabudu sio Miungu, na ibada ina sifa zake ambazo ni ibara ya kuamini uungu wa yule mwabudiwa, (itakapopatikana sifa hiyo ya Uungu) hapo hufaa kumwabudu na kumfanya mwabudiwa, na kwa kuwa sifa hiyo haipatikani isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) hivyo inapasa kuabudiwa Yeye tu.

SWALI NA JIBU Swali: Hapana shaka kwamba dai la kwanza limethibiti nalo ni kwamba Washirikina walikuwa wakiamini masanamu kuwa ni miungu, na hayo yamethibiti kutokana na aya kadhaa zinazothibitisha hilo, isipokuwa ni kwamba dai la pili halijathibiti, na kwa ufupi faida inayopatikana kutokana na Aya zilizotangulia hapo kabla ni kwamba ibada zao zilianza kutokana na itikadi ya Uungu, na hilo halijulishi kwamba dhana ya Uungu imo ndani ya dhana ya ibada kama inavyodaiwa. Kwa ujumla ni kwamba Aya hizo hazijulishi zaidi ya kwamba ibada yao ya Masanamu iliambatana na imani hii au chanzo chake kilikuwa ni hicho.

86


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 87

Ama ibada kuwa maana yake ni unyenyekevu utokanao na ile itikadi ya Uungu kiasi kwamba chanzo cha itikadi hiyo kinakuwa ni sehemu ya maana ya Ibada, kwa hakika Aya hizo hazileti maana hiyo. Ama kuhusu jawabu la swali hilo tunasema: Mushkeli huo utakuwepo lau tu tutasema kwamba itikadi ya uungu ipo ndani ya dhana ya Ibada, hata isemwe kuwa Aya hizo hazielezi zaidi ya kwamba Ibada ni mambo makhususi ya Uungu, na kwa kweli hatusemi dhana ya Uungu imo ndani ya dhana ya Ibada, bali makusudio ni kwamba si kila unyenyekevu na kujidhalilisha ni Ibada, bali Ibada ni jambo finyu kuliko hivyo, na hili ndilo analolitambua kila mtu kimaumbile, isipokuwa ni kwamba sisi tunaashiria sifa yake mahususi na tunapambanua ufinyu huu kwa kusema: Ni unyenyekevu ’utokanao na ile hali ya kuamini Uungu au Ulezi’, kama utakavyotambua hilo katika taarifa ya pili, la hasha! hakika sentensi hii ’utokanao na ile hali ya kuamini Uungu au Ulezi’, haiingii kwa vipengele vyake vyote katika dhana ya Ibada na maana yake. Na kwa ibara nyingine ni kuwa binadamu huenda asiweze kukieleza kwa uasilia wake, au mnyumbuliko wake ili akili yake iweze kuweka mipaka yake na kueleza maana sahihi na iliyokamilika, lakini yeye katika nafsi yake huvikuta vitu vinavyounda hilo, na jambo ambalo sisi tunalizungumzia liko hivyo, kwani tunakuta kuadhimisha, kunyenyekea na kujidhalilisha na yanayofanana nayo ni mambo yanayopatikana katika Ibada na nje ya Ibada, hivyo hudhani kwamba hilo (kunyenyekea na kujidhalilisha) ndio inayokusanya Ibada na lililo nje ya Ibada, na anakuta kwamba Ibada ina sifa mahusui inayojitofautisha na lili lililo nje ya Ibada, lakini hawezi kuelezea wasifu wa sifa hiyo kwa neno moja, hivyo analazimika kuleta sentensi nzima badala ya neno moja, nayo ni kama ile tuliyosema ’utokanao na ile hali ya kuamini Uungu au Ulezi’. Na kwa ibara ya tatu ni kwamba: Hakika binadamu anakuta kwamba Ibada sio kila kutukuza na kujidhalilisha, bali yenyewe ni miongoni mwa sifa zinazomuhusu yule ambaye mambo yote ya wanadamu yamo mikononi 87


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 88

Tawhid na Shirk mwake, au yote yanayohusiana na maisha ya binadamu ya sasa au ya baadaye, kama vile kifo, uhai, uumbaji, riziki, wema, ubaya, utoaji msamaha na uombezi, vyote vimo mikononi mwake, hivyo yeye ndiye huendesha mambo yake na kupanga mustakabali wake kama inavyopasa. Ila ni kwamba sentensi hizo hazimo ndani ya dhana ya Ibada, lakini zenyewe huashiria ile sifa makhususi iliyomo humo. Kwa hivyo inasihi kueleza kuwa: Ibada ni kigao makhsusi cha unyenyekevu na heshima kimaneno na kimatendo, (ambayo hufanywa na mja kwa lengo la kumtukuza yule anayemwamini kuwa ni mungu), na maelezo yaliyomo ndani ya mabano, ijapokuwa yapo nje ya dhana ya ibada, isipokuwa ni kwamba yenyewe hubainisha makusudio ya kigao maalum na makhususi cha unyenyekevu mwanzoni mwa ibara........ Hakika wataalamu wa lugha wanafasiri neno swahiyl kuwa ni sauti ya farasi na zaqazaqah kuwa ni sauti ya ndege, lakini ndege na farasi hawaingii katika dhana na dhihinia ya sauti hizo, isipokuwa ni katika kuweka upambanuzi makhsusi na ni katika mfumo wa utoaji ishara ya kuainisha sauti. Mpaka hapa imeeleweka kwamba ukweli katika utoaji maana au maelezo ya Ibada ni kusema: Ibada ni unyenyekevu utokanao na ile hali ya kuamini Uungu wa yule mwabudiwa. Na anaashiria hilo Ayatullah Marhuum Sheikh Muhammad Jawad katika kitabu chake Aalau Rahmani pale anapoelezea na kuchambua uhakika na uhalisia wa Ibada, anasema: “Ibada ni ile hali ambayo inaleta hisia ya kumnyenyekea yule ambaye huzingatiwa na mwenye kunyenyekea kuwa ni mungu, ili amtekelezee lile analoona kuwa ni haki inayomkhusu yeye kutokana na ule Uungu.”35 Hakika Allamah Sheikh Balaghi ameeleza yale anayoitakidi au ukweli anaouhisi kimaumbile kuhusu Ibada, amefanya hivyo kupitia lafudhi mbalimbali na maneno pamoja na ubainifu, hali kadhalika Aya za Qur’an, yote 35. Aalau Rahman Uk. 57 chapa ya Swayda, na ilichapishwa katika tafsiri hii juzuu mbili pekee. 88


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 89

Tawhid na Shirk hayo yakiunga mkono maana hii ya Ibada tuliyoielezea.

MAANA YA PILI Ibada ni kunyenyekea mbele ya yule ambaye unaitakidi kuwa ndiye anayemiliki jambo miongoni mwa mambo ya kuwepo kwako na maisha yako, ya sasa na yajayo. Kwa ufafanuzi zaidi, kuabudu ni kati ya mambo ya mmilikiwa na wadhifa wake, na pindi mtumwa anapohisi katika nafsi yake aina fulani ya kumilikiwa na kwa upande mwingine kumhisi mmiliki, hisia hiyo huidhihirisha kupitia maneno na matendo kwa aina maalum, na hapo maneno na matendo yake huwa udhihirisho wa hisia hizo, na kila kitendo au kauli yenye kudhihirisha hisia hizo za kina ni Ibada. Hapana shaka makusudio ya kumilikiwa sio kila kumilikiwa, kwa hivyo itikadi ya kumilikiwa kwa mujibu wa kanuni (kama ile ya mwajiriwa kuwa chini ya milki ya mwajiri wake, au mtoto kuwa chini ya milki ya baba, au mke kuwa chini ya milki ya mume), abadani katika umilikiwaji wa namna hiyo haina maana kwamba unyenyekevu utokanao na hisia za umilikiwaji huo ni Ibada, kwani katika zama za utumwa wa mtu mmoja mmoja, na vivyo hivyo katika zama za utumwa wa watu wengi, watu kutekeleza amri za mabwana (mabosi wao) zao hakuzingatiwi kuwa ni Ibada. Hivyo hapana budi makusudio ya kumilikiwa hapa yamesimama katika msingi wa uumbaji na kuumba na kwamba mambo ya maisha yako yapo katika mamlaka yake. Yafuatayo ni maelezo bainifu ya chanzo cha aina za umilikiwaji wa hakika: 1 - Husemwa ni mmiliki kwa kuwa ni Muumbaji, hivyo Mwenyezi Mungu (swt) huwa ni mmiliki halisi wa mwanadamu kwa sababu ndio muumba wake na mwenye kumpa uhai, kwa hivyo tunaona Qur’an tukufu inawazingatia viumbe wote ni watumwa (waja) wa Mwenyezi Mungu, na inae89


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 90

Tawhid na Shirk leza kwamba Allah (s.w.t) ndio mmiliki halisi, na hiyo ni kwa sababu Yeye ndiye aliyemuumba. Mwenyezi Mungu anasema:

“Hakika kila kilichopo mbinguni na ardhini kitamjia Mwenyezi Mungu hali ya kuwa ni dhalili.” (19:93). Tunamkuta Mwenyezi Mungu anawaamrisha watu wamwabudu Yeye kwa kutoa sababu kwamba Yeye ndiye Mola wao ambaye amewaumba na sio mwingine, anasema:

“Enyi watu! Mwabuduni Mola Wenu aliyewaumba nyinyi na waliokuwa kabla yenu, ili mpate kuokoka” (2:21)

“Huyo ndiye Mwenyezi Mungu Mola Wenu, hakuna anayeabudiwa ila Yeye tu, Muumba wa kila kitu basi mwabuduni, naye ni mlinzi wa kila kitu.” (6:102). - Kwa hakika inaelezwa kwamba Yeye ndiye Mmiliki halisi kwani yeye ndiye Mtoaji riziki, Mwenye kuhuisha na kufisha, kwa hivyo humfanya kila kiumbe mwenye maumbile yaliyo sahihi ajihisi kuwa yeye ni katika milki ya Mwenyezi Mungu (s.w.t), kwa sababu Yeye ndiye Mmiliki wa uhai na mauti wake pamoja na riziki yake, kwa ajili hiyo Qur’an tukufu inamzingatia binadamu kuwa ni milki ya Mwenyezi Mungu, kwani Yeye ndiye anayemruzuku binadamu, anayemfisha na kumhuisha, anafanya hayo ili amzindue kuwa Mwenyezi Mungu pekee ndiye anayestahiki kuabudiwa, anasema:

90


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 91

Tawhid na Shirk

“Mwenyezi Mungu ndiye aliyekuumbeni kisha akakupeni riziki kisha atakufisheni, kisha atakufufueni.” (30:40)

“Je! Miongoni mwa washirika wenu yuko awezae kufanya lolote katika hayo?” (30:40) “Yeye anahuisha na kufisha” (10: 56) -Na huelezewa kwamba ni Mmiliki kwa kuwa Shafaa, na maghfira vimo mikononi mwake, ambapo Yeye (a.j) ndio mmiliki wa Shafaa: “Sema: Shafaa yote ni ya Mwenyezi Mungu.” (39:44). Na katika maghfira: “Ni nani anayesamehe dhambi zote?” (3:135). Kwa hakika hamiliki Shafaa yeyote miongoni mwa waja isipokuwa kwa idhini Yake (s.w.t), hali ambayo binadamu wa kawaida anahisi katika dhamira yake kuwa Mwenyezi Mungu (a.j) ni mmiliki wa maisha yake ya wema wa akhera, na atakapohisi binadamu kumilikiwa kwa namna hii na namna ile, ndipo huidhihirisha hisia hii kupitia maneno na matendo, na hapo huwa mwenye kumwabudu bila wasi wasi wowote. Kwa hivyo hayo hurejea kwenye ile tafsiri ya ibada kuwa ni unyenyekevu kwa yule ambaye anaitakidi Urabi (Ulezi) wake, hivyo iwapo unyenyekevu wake wa kauli na kivitendo kwa yeyote unatokana na kule kuamini Urabi (Ulezi) wake, basi katika upande huu, huyu mtu huwa ni mwenye kumwabudu mtu huyo. Na makusudio ya lafudhi Rabbi (Mlezi) katika maelezo haya huwa ni mmiliki wa mambo ya mhusika na ni mpangaji na mwendeshaji wa mambo yake. 91


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 92

Tawhid na Shirk Na kwa hivyo neno kuabudiwa linakuwa mkabala na neno kulelewa, yaani mmiliki na mlezi wa kitu na mwendeshaji wake, na mpangaji wa hatima yake ya sasa na ya baadaye, na hilo linajulishwa na baadhi ya Aya za Qur’an tukufu ambazo zinatoa sababu kwamba jambo la kuabudiwa linamhusu Mwenyezi Mungu pekee kwa kuwa Yeye ndiye Rabbi (Mlezi) na si mwingine, kama vile baadhi ya Aya zifuatazo zinavyoeleza:

“Bila shaka wamekufuru wale wanaosema, Mwenyezi Mungu ni Masihi bin Mariam, na Masihi alisema: Enyi wana wa Israeli, mwabuduni Mwenyezi Mungu Rabbi (Mlezi) Wangu na Rabbi (Mlezi) Wenu…” (5:72)

”Kwa hakika huu Umma wenu ni Umma mmoja, na mimi ni Rabbi (Mlezi) wenu, kwa hiyo niabuduni.” (21:92)

“Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Rabbi (Mlezi) Wangu na ni Rabbi (Mlezi) Wenu, basi mwabuduni, hii ndio njia iliyonyooka.” (3:51). Na madhumuni ya Aya hizo zilizotangulia ya kwamba Ibada inatokana na Ulezi, pia yanapatikana katika Aya zifuatazo:

“Huyo ndiye Mwenyezi Mungu Rabbi (Mlezi) wenu, basi mwabuduni …” (10:3)

92


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 93

Tawhid na Shirk

“Na umwabudu Rabbi (Mlezi) Wako …” (15:99)

“Na hakika Mwenyezi Mungu ni Rabbi (Mlezi) Wangu na Rabbi (Mlezi) Wenu basi mwabuduni, hii ni njia iliyonyooka.” (19:36)

“Rabbi (Mlezi) wa mbingu na ardhi na vilivyomo kati yake, basi mwabudu Yeye na udumu katika ibada Yake …” (19:65)

“Kwa hakika Mwenyezi Mungu ndiye Rabbi (Mlezi) Wangu na Rabbi (Mlezi) Wenu, basi mwabuduni, hii ndio njia iliyonyooka…” (43:64) Na kwa hali yoyote ile ni kwamba dalili ya wazi juu ya tafsiri ya neno Ibada ni Aya hizo zilizokwishatangulia hapo kabla.

MAANA YA TATU: Ibada tunaweza kuieleza kwa ibara ya tatu kama ifuatavyo: Ibada ni unyenyekevu wa yule ambaye anajiona kuwa tegemezi katika kuwepo kwake na katika vitendo vyake, unyenyekevu aufanyao mbele ya yule ambaye sio tegemezi katika mambo yote na hali zote. Mwenyezi Mungu (a.j) Yeye mwenyewe amejieleza katika sehemu nyingi ndani ya Kitabu chake kitakatifu kwamba Yeye ndiye pekee mwenye kujitosheleza kwa kila kitu, anasema:

“Mwenyezi Mungu hakuna anayeabudiwa isipokuwa Yeye tu, Mzima wa milele, Mwenye kusimamia mambo…” (2:255 ) 93


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 94

Tawhid na Shirk Vivyo hivyo anasema:

“Mwenyezi Mungu, hakuna anayeabudiwa isipokuwa Yeye tu, Mzima wa milele, Mwenye kusimamia mambo ya viumbe” (3:2), Anasema tena:

“Na nyuso zitadhalilika mbele ya (Mwenyezi Mungu) aliye hai wa milele…” (20:111). Na makusudio yake ni kwamba Yeye yupo bila utegemezi kwa yeyote, wala hakuna Aya inayoeleza kwamba Yeye ni fakiri na mhitaji kutoka kwa asiyekuwa Yeye, bali kila kilichopo humtegemea Yeye. Na kwa ibara nyingine: Ibada ni kule kumwomba Mwenyezi Mungu (s.w.t) na kumnyenyekea na kumpelekea Yeye haja zetu za duniani na akhera, naye ndiye anafanya lolote kwa hiari na utashi Wake, ndiye Mmiliki halisi wa mambo yote ya duniani na akhera, na iwapo mtu atampa mwingine sifa hizo au baadhi ya hizo atakuwa amefanya Shirki, na mtu huyo akiitwa mshirikina ni mahala pake. Na kwa hivyo lau mmoja wetu atamnyenyekea kiumbe kwa kuitakidi kuwa kiumbe huyo si mhitaji na anajitegemea kwa kila hali katika dhati yake au vitendo vyake, basi unyenyekevu huo ni Ibada. Bali hata kama atampa majukumu ya Mwenyezi Mungu yule asiyekuwa Yeye, au akafanya maombi yake kwake na huku akiamini yeye ndiye pekee atakayempatia au kumkidhia hilo, kinyume na Mwenyezi Mungu (s.w.t), kwa hakika maombi yake hayo yatakuwa ni Ibada na hiyo ni Shirki, kwani kuomba katika namna hiyo kunaambatana na unyenyekevu. La msingi tunalotaka kulitilia mkazo hapa ni kwamba yampasa mtu ajue matendo na kazi za Mwenyezi Mungu (s.w.t) na kuzimaizi na matendo ya wengine ili asikumbwe na kunasa katika Shirki pindi anapoomba kitu kutoka kwa Mitume, Mawalii 94


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 95

Tawhid na Shirk na watu wengineo. Tunasema: Miongoni mwa vigawo vya Shirki ni kuihusisha kazi ya Mwenyezi Mungu kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu, na jambo linaloeleweka ni kwamba kazi ya Mwenyezi Mungu sio tu uumbaji, uendeshaji wa mambo na utoaji wa riziki bila kuzingatia kwamba katenda Yeye Mwenyewe moja kwa moja au kwa idhini Yake, kwa sababu Yeye (s.w.t) baadhi ya kazi amezikabidhi kwa wengine kwa mujibu wa Qur’an tukufu, bali msingi ni kutenda kwa kujitegemea mwenyewe, hivyo iwapo mtu atanyenyekea mbele ya kiumbe mwenzake kwa kuitakidi kwamba kiumbe huyo hujitegemea katika vitendo vyake, hiyo ni kumwabudu kiumbe huyo, sawa iwe ni katika vitendo vya kawaida kama vile kutembea na kuzungumza, au mambo yasiyokuwa ya kawaida kwa mfano miujiza ambayo Nabii Isa (a.s.) alikuwa akiifanya.36 Kwa ufafanuzi zaidi tunasema: Hakika Mwenyezi Mungu (a.j) ni Mwenye kujitosheleza katika vitendo vyake, kama vile kujitosheleza katika dhati Yake. Yeye huumba, hutoa riziki, hufisha na huhuisha bila kumtegemea yeyote,37 na haombi wala kuhitaji usaidizi wowote kutoka kwa viumbe, lakini Yeye ndiye muumba wa vitu vyote, na anafanya hivyo bila usaidizi wa yeyote, anaumba na kukipa kitu sura na umbile alipendalo wala hashi36. Kama katika Sura 3 aya 49 inasema: "Mimi nitakufanyieni katika udongo kama namna ya ndege, kisha napulizia ndani yake (awe) ni ndege kwa idhini ya mwenyezi Mungu. Na niwaponye vipofu na wenye mbalanga, niwafufue watu kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na niwape habari ya mnavyokula na mnavyo viweka akiba katika nyumba zenu." 37. Ndio, imekwishatangulia kuhusiana na somo la tawhid katika ulezi kwamba Mwenyezi Mungu si mwenye kuhitajia kutoka kwa yeyote yule katika vitendo vyake, hailazimu afanye mwenyewe mambo yote, na kwamba dhati yake ndiyo chimbuko la uumbaji, utoaji riziki, uhuishaji, ufishaji pasi na kuwepo sababu yoyote kwa hayo, bali maana yake ni kwamba awepo mwingine katika vitendo vyake anayefanya moja kwa moja au anayesababisha - sawa katika vitendo vyake mwenye kujitosheleza na hamhitajii mwingine, hata ikiwa vitendo vyake vikipita katika kanuni na nidhamu ya sababu na visababishaji, rejea kitabu cha mwandishi Almausum kilichotajwa hapo kabla - sehemu ya nane. 95


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 96

Tawhid na Shirk rikiani na yeyote. Hivyo tukiitakidi kwamba kuna kiumbe ambaye hutenda hutenda katika hali na sifa kama hiyo, sawa katika viyendo vya kawaida au vya kimuujiza, bila shaka tutakuwa tumemfanya mshirika wa Mwenyezi Mungu na mwenza wake, na hiyo ni Shirki. Kwa muhtasari ni kwamba kigezo cha msingi kuhusiana na mchakato huu wa kuelezea maana halisi ya jambo hili ni: ’Kutotegemea na kutegemea kwa mtendaji katika utendaji wake’. Kwa hakika Tawhiid katika maana hiyo hushirikiana baina ya msomi na asiyekuwa msomi, kwani lile analolitambua na kuligundua mwanatawhiidi kupitia dalili za akili na Aya, ambalo ni kwamba mwabudiwa hujitegemea na mwenye kuabudu hutegemea, ndilo hilo hilo hulitambua na kuligundua kwa maumbile yake yule asiyekuwa mwanatawhiidi. Hivyo utambuzi huo na ugunduzi huo wa kwamba mwabudiwa sio tegemezi wala hahitaji usaidizi kutoka kwa yeyote, bali mwenye kuabudu ndiye tegemezi ni jambo ambalo hushirikina kati ya mjuzi na asiyekuwa mjuzi, mkamilifu na asiye mkamilifu, isipokuwa kila mtu ana kiwango chake cha ufahamu na uwezo aliopewa wa kudiriki mambo. Mwenyezi Mungu (a.j) anasema: “Ameteremsha maji kutoka mawinguni na mabonde yakapitisha maji kwa kadiri yake…” (13:17) Isipokuwa linalozungumzwa midomoni mwa wanaoitakidi Tafwiidhi (watu ambao huamini mwanadamu kaachiwa mambo yote wala Mwenyezi Mungu hahusiki na lolote katika mambo yake) wanaeleza kwa mapana na marefu makusudio yao.

2. NINI MAANA YA TAFWIIDHI? Wanatawhiid wameafikiana kwamba itikadi ya Tafwiidhi hulazimu ushirikina, na unyenyekevu utokanao na imani hiyo huhesabiwa ni ibada kwa mnyenyekewa, na Tafwiidhi inadhaniwa katika sura mbili: I- Mwenyezi Mungu ameachia mamlaka ya upangaji na uendeshaji wa ulimwengu mikononi mwa waja wema miongoni mwa Malaika, Manabii na Mawalii, na hiyo huitwa Tafwiidhi ya kimaumbile. 96


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 97

Tawhid na Shirk II- Mwenyezi Mungu ameachia mambo ya kiungu mikononi mwa waja wake: Kama vile uwekaji Sheria, utoaji wa msamaha na Shufaa, ambayo huhesabiwa ni katika mambo ya Mwenyezi Mungu (a.j), na hiyo huitwa Tafwiidhi katika Sheria.

SURA YA KWANZA: Hapana shaka kwamba maelezo hayo yanasababisha na kulazimu kuwapo Shirki, kwani iwapo mtu ataitakidi kwamba mambo yote ya ulimwengu, upangaji wa mambo ya ulimwengu na uendeshaji, kama vile kuumba, kutoa riziki, kufisha na kuteremsha mvua na mengineyo miongoni mwa matukio ya ulimwenguni, Mwenyezi Mungu (s.w.t) ameyaacha mikononi mwa Malaika au waja wema, kwa hakika mtu huyo atakuwa amemwekea Mola Muumba kikomo na kumpunguzia utawala, na viumbe hao watakuwa ni wenza wa Mwenyezi Mungu, kwani Tafwiidhi hapo si kingine bali ni kule kuamini kwamba viumbe hao hawahitaji usaidizi wala msaada wowote katika matendo yao, hawana mahusiano yoyote na Allah katika yale wanayoyatenda na wanayoyakusudia katika baadhi ya mambo. Na kwa muhtasari ni kwamba uendeshaji kuwa mikononi mwa viumbe ni kumpa kiumbe hali ya kujitegemea katika vitendo na kazi zake, sawa iwe ni katika vitendo ambavyo vinamrejea mwenyewe kwa mfano kutembea, kuzungumza n.k, au vile vinavyohusu kuendesha ulimwengu na matukio yake, isipokuwa ni tu kwamba kwa sababu dai la kujitegemea katika matendo ya kawaida ya wanadamu lina uhusiano wa moja kwa moja na falsafa ndio maana Washirikina wa kiarabu hawakulielekea, na hivyo wakajikita katika dai la kujitegemea katika uendeshaji wa ulimwengu, ijapokuwa hata dai la kwanza lilikuja kuwa chanzo cha migongano na majadiliano katika ulimwengu wa kiislamu katika zama za mwanzo, kiasi kwamba dai hilo liliwagawa wachambuzi katika mafungu mawili: Wafuasi wa Jaaza (Jabru) na wale wa Tafwiidhi. Kwa ufupi tunasema: Jambo hilo linazunguka kati ya ima mja hufanya mambo kwa kujitegemea bila kupata msaada kutoka kwa yeyote hata Mwenyezi Mungu, au mja hufanya kwa idhini na utashi wa Mola Manani, 97


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 98

Tawhid na Shirk na kwa kweli Tafwiidhi si suala la tatu, bali yenyewe ndie sura ya kwanza. Ama kuamini kwamba watakatifu miongoni mwa malaika, majini, manabii na mawalii wanadabiri ulimwengu kwa idhini na utashi Wake, amri na uwezo Wake bila ya kujitegemea, hiyo haihesabiwi kuwa ni Shirki, bali jambo hilo ima liwe ni sahihi lenye ukweli wa kivitendo kama vile kunasibisha hilo kwa malaika, na ima ni makosa na ni kinyume na ukweli kama vile kunasibisha hilo kwa Nabii au Walii, kwani Mitume na Mawalii hawako katika chani ya visababisho na sababu za matukio ya mpangilio wa maumbile ya kiulimwengu, bali wao ni kama vile watu wengine ambao hufaidika na mpangilio wa maumbile, kiasi kwamba huvurugika utaratibu wa maisha yao pindi unapotokea mvurugiko wa mpangilio huo wa maumbile. Na ni dhahiri shahiri kwamba si kila kilicho kinyume na uhalisia au ukweli ni ushirikina, kwani makosa yaliyopo hapo ni kule kumweka Walii nafasi ya sababu za kimaumbile na mpangilio wa kiulimwengu, na wala itakidi ya aina hiyo ya kumweka Walii nafasi ya sababu za kimaumbile na mpangilio wa kiulimwengu au sehemu ya mpangilio wa kimaada si Shirki. Linalopaswa kusemwa hapa ni kwamba Washirikina wa zama za Mtume (s.a.w.w) walikuwa wakiamini kuwa miungu yao inayo aina fulani ya kujitegemea katika vitendo vyao na walikuwa wakiielekea miungu hiyo, kama ilivyokwisha tangulia hapo kabla kwamba Amru bin Ubay wakati alipokwenda miji ya Sham aliwaona watu wakiabudu masanamu, akawauliza sababu ya kuyaabudu wakamwambia: “Masanamu haya tunayoyaabudu tunapoyaomba mvua yanatuletea mvua, na tunapoyaomba yatunusuru yanatupa nusura�38 Kulikuwa na kundi la Wanafalsafa wakiamini kwamba kila moja kati ya hayo mawili lina mola wake ambaye ameachiwa aina fulani ya uendeshaji 38. Siirat Ibn Hisham Juz. 1 Uk. 79, na ufafanuzi wa kisa hiki umekwisha angukia hapo kabla, na yale aliyosema bwana Mtume (s.a.w.w) katika Hudaybiya kuhusiana na uombaji wa mvua kwa aina ambayo ilienea kwa watu zama za ujahilia, na yale tulioyanukuu kutokana na Siirat Halabiyya Juz. 3 Uk. 29 katika utangulizi nambari ya 2 katika kitabu hiki basi rejea Uk. 33. 98


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 99

Tawhid na Shirk wa mambo; amekabidhiwa uongozi wa ulimwengu ambao ni miongoni mwa kazi za Mwenyezi Mungu, kama walivyokuwa Waarabu wa zama za ujinga wakiabudu malaika na sayari – zinazozunguka na zisizo zunguka – wakiabudu kwa imani kuwa vimekabidhiwa majukumu ya kuongoza na kuendesha mambo ya ulimwengu – kama walivyodhani – na hakika Mwenyezi Mungu amejiuzulu katika majukumu hayo, hivyo vyenyewe ni vimiliki halisi vya kazi hizo na sio Mwenyezi Mungu, kwa hivyo unyenyekevu wao uliotokana na hisia hii ulizingatiwa ni Ibada, na bila shaka baadaye utaelewa itikadi za Waarabu wa zama za ujinga kuhusiana na vile walivyokuwa wakiviabudu.

SURA YA PILI YA TAFWIIDHI Tukiamini kwamba Mwenyezi Mungu (a.j) amempa mmoja wa viumbe wake majukumu ya kutunga Sheria, Shufaa na utoaji msamaha hakika tutakuwa tumemshirikisha Mwenyezi Mungu na mwingine, na hapo tumemfanya kuwa na mipaka, kama Qur’an tukufu inavyosema:

“Na miongoni mwa watu wako ambao hufanya miungu wasiokuwa Mwenyezi Mungu kuwa ni washirika wakiwapenda kama kumpenda Mwenyezi Mungu.” (2:165) Na hapana shaka kwamba kiumbe hawezi kuwa na ushirikiano na Mola Muumba isipokuwa pale atakapokuwa anatenda kwa kujitegemea jambo au kitendo miongoni mwa vitendo makhususi vya Mwenyezi Mungu, na si pale atendapo kwa idhini na amri ya Mola aliyetukuka, kwani iwapo ni kwa idhini ya Mola Manani hatakuwa mwenza wala mshirika wa Mwenyezi Mungu (s.w.t), bali hapo anakuwa mja mtiifu na mtumwa Wake na ni mwenye kutekeleza amri na matakwa ya Mwenyezi Mungu (s.w.t).

99


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 100

Tawhid na Shirk Aidha Shirki ya chini kabisa waliyokuwa nayo Mayahudi, Wakristo na Waarabu wa zama za ujahilia ilikuwa ni kundi miongoni mwao kuamini kuwa Mwenyezi Mungu amewapa makasisi na makadinari jukumu la utungaji sheria, Qur’an tukufu inasema: “Wamewafanya makasisi wao na watawa wao kuwa ni badala ya Mwenyezi Mungu …” (9:31). Na kwamba hakika Mwenyezi Mungu ameyapa masanamu na viabudiwa haki ya Shufaa na msamaha ambapo mambo hayo ni katika haki mahsusi za Mwenyezi Mungu, na kwamba masanamu na viabudiwa hivi hayategemei msaada wowote katika utekelezaji wa mambo hayo, kwa ajili hiyo wakawa wanayaabudu, kwa imani kuwa ni waombezi wao kwa Mwenyezi Mungu, na ni yenye kumiliki uombezi, Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema kuhusiana na hilo:

“Nao wanaabudu kinyume cha Mwenyezi Mungu wasiowadhuru wala kuwanufaisha, na wanasema; hawa ndio waombezi wetu mbele ya Mwenyezi Mungu …” (10:18). Hivyo ndivyo Aya za Qur’an zinavyosisitiza na kusema kuwa majukumu ya kufanya hayo ni ya Mwenyezi Mungu au kwa yule aliyempa idhini ya kufanya hivyo, na lau kama wangelikuwa Washirikina wanaitakidi kwamba yale wanayoyaabudu huwa yanawapa Shufaa kwa idhini ya Mola Muumba basi kusingekuwa na haja ya kusisitiza suala hilo ambalo Washirikina wameafikiana baina yao. Baadhi ya Waarabu wa zama za ujinga walikuwa wakiyaabudu masanamu, walifanya hivyo kwa imani kuwa yanamiliki Shufaa (uombezi) na sio waumbaji au waendeshaji wa mambo ya ulimwengu, na kwa msingi huo wa mawazo potofu na batili walikuwa wakiyaabudu na huku wakiitakidi au kudhani kuwa kuyaabudu hayo ni sababu inayopelekea kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu, Qur’an inasema:

100


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 101

Tawhid na Shirk “Lakini wale wanaowafanya wengine kuwa waungu badala yake (husema) Sisi hatuwaabudu hawa ila wapate kutufikisha karibu kabisa na Mwenyezi Mungu” (39:3) 3. HAKUNA UHUSIANO KATI YA UENEZAJI MIUNGU NA UKANUSHAJI WA MUNGU MKUU Hakika ugawaji na uenezaji wa sifa ya uungu katika miungu wadogo ambao hawastahiki kupewa sifa hiyo ni batili kutokana na dalili za kiakili na maandiko, hatuna haja ya kurefusha maneno kwa kutumia dalili za kiakili achilia mbali dalili lukuki zilizotolewa na Aya za Qur’an tukufu. Ugawaji wa mambo ya kiungu – kama ilivyokuwa dhana ya Waarabu wa zama za ujinga – hakulazimu ukanushaji wa mungu mkuu mtenza nguvu, bali walikuwa watu wa zama zile wakiamini mungu mkuu pamoja na hivyo wakiabudu masanamu na kuamini kwamba yanayo sifa ya uungu. Lakini Mwalimu Maududi39 amebatilisha fikira ya uenezaji wa sifa ya uungu kwa kutoa sababu kwamba ugawaji huu hauambatani na imani ya kuwepo mungu mkuu, amesema: “Hakika watu wa zama za ujinga hawakuwa wanaitakidi kuhusiana na miungu yao kuwa sifa ya uungu imegawanywa kati yao, na hakuna juu yao mungu mkuu zaidi ya mtenza nguvu, bali walikuwa na taswira ya kwamba wanaye mungu ambaye walimzingatia katika lugha yao kwa neno Allah.”40 Maelezo hayo yanahitaji tafakari, kwani kuziweka pamoja kauli: “Hakika uungu umegawanywa kati yao” na kauli: “Hakuna juu yao mungu mtenza nguvu” inaleta dhana kwamba uenezaji wa uungu unapelekea kukanusha uwepo wa mungu ambaye yu zaidi ya wote, lakini ukweli sivyo hivyo, kwani Swaabiat ambao wametajwa ndani ya Qur’an wameamini uungu wa jua na uendeshaji wake wa mambo, lakini pamoja na hayo waliamini kwamba yupo mungu mtenza nguvu, wakasema: Hakika jua ni malaika 39. Bihar Anwar Juz. 25 Uk. 320-350. 40. Mustwalahat Arba'at Uk. 19. 101


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 102

Tawhid na Shirk kati ya malaika, lina akili na nafsi, aidha lina nuru ya nyota na huangaza ulimwengu, na viumbe ambavyo vina daraja la chini vinastahiki kuliadhimisha, kulitukuza, kuliomba na kulisujudia.41 Miongoni mwa Swaabiat wapo wanaosema: “Hakika mwezi ni malaika miongoni mwa malaika kwa hivyo unastahili kuabudiwa, kwani hupanga na kuendesha mambo ya ulimwengu huu ya ngazi za chini na vipengele vingine vidogo vidogo, na kwa hilo huivisha vitu na huvifikisha katika ukamilifu wake”42 Na haifai kwa yeyote kutafsiri kauli yao hiyo kuwa wanamaanisha kwamba jua na mwezi kwa mujibu wa itikadi yao vilikuwa vinachukua mahala pa sababu za kimaumbile, na kwamba hivyo viwili vilikuwa vikifanya kazi za sababu za kimaumbile na wala si vinginevyo, kwani wao walivifanya vitu hivyo kuwa ni miongoni mwa Malaika na kwamba vina akili, nafsi, upangaji na uendeshaji utokanao na akili, na bila shaka sifa hizi zinanasibiana na Uungu, na ni waungu wawili, na wala sio sababu za kimaumbile, kwani laiti hivyo viwili vingelikuwa ni sababu za kimaumbile basi wasingeliviabudu namna hiyo. Kwa mantiki hiyo hakuna kizuizi kizuiacho Washirikina pindi wanapogawa uungu kwa waungu wadogo, hapo hapo kuamini uwepo wa mungu mkuu mtenza nguvu, naye ndiye aliyewagawia uungu. Kwa hivyo Waarabu wa zama za ujinga walikuwa wakiamini kwamba masanamu yameachiwa utoaji Shufaa na msamaha na hapo hapo wakiamini kuwepo kwa mungu mkuu mtenza nguvu, na msamaha na uombezi ni miongoni mwa mambo ya kiungu, na dalili juu ya hilo la kwamba walikuwa wakiamini kuwa masanamu yameachiwa majukumu yote ya ulimwengu, ni ule msisitizo wa Qur’an tukufu kwamba kazi ya Shufaa si ya mwingine ila ni ya Mwenyezi Mungu (a.j) tu, inasema: “Ni nani awezaye kuombea mbele yake bila ya idhini yake?” (2:255) “Na ni nani 41. Milal wa Nihal Uk. 265-266 cha Shahristan. 42. Milal wa Nihal Uk. 265-266 cha Shahristan. 102


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 103

Tawhid na Shirk anayesamehe madhambi isipokuwa Mwenyezi Mungu” (3:135) Nadhani – na huenda ni dhana sahihi – kwamba hakika Ustadh nyuma ya maneno haya “Ugawaji wa uungu unakanusha itikadi ya kuwepo mungu mwingine” ana lengo na kusudio lingine, nalo ni kuthibitisha kuwa kwa mujibu wa Qur’an neno mungu lina maana ya mwabudiwa, na hiyo ni kufuata nyayo za Sheikh wake Ibn Taimiyyah, kwa maana kwamba kilichopelekea masanamu yasifike kwa Uungu ni kile kitendo cha kuabudiwa, na si kwa sababu ni waungu wadogo na Mwenyezi Mungu (s.w.t) ndiye mungu mkubwa wao. Ustadh pamoja na wanafunzi wa madrasa yake wamewatakasa Washirikina dhidi ya kauli yao ya uungu wa masanamu, eti wao walikuwa wakiyaabudu pasi na kuyafanya waungu wadogo mkabala na mungu mtenza nguvu. Katika kuongezea hayo tunasema: Kwa hakika wao wamechafua sifa nzuri ya Waislamu pale walipofasiri zile Aya zinazokataza kufanya vitu vingine kuwa miungu, kuwa maana yake ni kukataza kuviabudu vitu hivyo, kwa sababu mungu kwa mtazamo wao ana maana ya mwabudiwa. Kisha wakaziambatanisha Aya hizo juu tawassuli za Waislamu na kuzuru makaburi ya Mawalii wao. Kwa kweli kutafsiri Aya hizo zinazokataza kujifanyia miungu kuwa zinakataza kufanyia mwabudiwa, hilo ni kosa, na hata kama tutajaalia ni tafsiri sahihi lakini bado kuziambatanisha na tawassuli za Waislamu pamoja na kuzuru kwao makaburi ya Mawalii wao ni kosa lingine.

4. UFUPISHO WA MANENO Ufupisho wa maneno yanayohusiana na mada hii ni kwamba kila kazi inayoibuka kutokana na imani hii ya kuamini kwamba kiumbe huyu ni mungu wa ulimwengu au mlezi wake au mwenye kujitosheleza katika kazi zake, au yeye ndiye chimbuko la matendo ya uungu, basi unyenyekevu wowote utokanao na imani hiyo ni Ibada, na mwenye kufanya hivyo 103


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 104

Tawhid na Shirk huzingatiwa ni mshirikina kwa kumfanyia Mwenyezi Mungu (s.w.t) mwenza. Mkabala na imani hiyo ni ile kauli au kitendo au unyenyekevu ambao hautokani na itikadi hii. Hivyo kiumbe kunyenyekea kwa kupindukia mbele ya kiumbe mwenza na bila unyenyekevu huo kutokana na ile imani ya Uungu wa kiumbe huyo, hali hiyo si Shirki na wala si kumwabudu kiumbe huyu, ijapokuwa huenda ikawa ni haramu kufanya hivyo, kwa mfano mtu kumsujudia mpenzi wake, au mke kumsujudia mumewe, hata kama ni haramu katika sheria ya kiislam lakini kufanya hivyo sio Ibada, kitu kuwa haramu haimaanishi kuwa ni Ibada, kwani uharamu wa kusujudu mbele ya binadamu pasi na kuamini kuwa yeye ni mungu, mlezi na mola, unatokana na sababu nyingine. Kwa ubainifu huo hapa linadhihiri jawabu la swali ambalo huenda likajitokeza kuhusiana na maudhui hii, nalo ni: ikiwa kuamini Uungu au Ulezi au Tafwiidhi ni sharti katika kuthibiti Ibada, basi je inafaa mtu kumsujudia mwingine nje ya nia hiyo? Swali hilo hujibiwa hivi: Hakika sajda au kusujudu ni nyenzo kuu ya Ibada, na kwa kuwa kitendo hicho hutumiwa na mataifa mbalimbali na makabila tofauti kumwabudia Mwenyezi Mungu (s.w.t), kiasi kwamba kwa kitendo hicho huwa hapo halikusudiwi jingine ila Ibada, ndio maana Uislamu haujaruhusu kutumiwa nyenzo hiyo ya kimataifa katika sehemu ambazo sio Ibada. Na utukuzaji huo ni makhsusi katika Uislamu tu kwani hapo kabla haikuwa haramu kutumia nyenzo hiyo katika mambo yasiyokuwa Ibada, la sivyo Nabii Yakub (a.s.) na wanawe wasingelimsujudia Nabii Yusufu (a.s.), Qur’an tukufu inasema:

“Na akawanyanyua wazazi wake na kuwaweka katika kiti chake na wote wakaporomoka kumsujudia (Mwenyezi Mungu)” (12:100). 104


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 105

Tawhid na Shirk Jaswas amesema: Hakika sajda iliruhusiwa kufanyiwa viumbe katika sheria za Nabii Adam (a.s.), na hii ilibakia hadi katika zama za Nabii Yusufu (a.s.), ilikuwa ikistahiki kufanyiana kati yao na ikawa ni aina ya kutukuzana na kuheshimiana, kama vile kukumbatiana na kupeana mikono na kubusiana mikono. Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) ruhusa ya kubusiana mikono, na imeelezwa kwamba ni makuruhu, isipokuwa kumsujudia asiyekuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) kwa nia ya kuheshimiana na kusalimiana bila shaka imefutwa kwa mujibu wa maneno ya bwana Mtume (s.a.w.w) yaliyopokewa na Bi Aisha, Jaabir na Anas, Mtume (s.a.w.w) amesema: “Haifai mtu kumsujudia mtu mwingine, na lau ingelifaa hilo ningeliamrisha mwanamke amsujudie mumewe kutokana na haki adhimu aliyonayo juu yake”43 Mpaka hapa tumeweza kujua maana halisi ya Ibada na Shirki, na faida tunazozipata kutokana na utafiti huu tunasema: Mtu atakapowanyenyekea wengine na kuwaheshimu pasi na imani ya kuwa wao ni waungu au marabi, au chanzo cha matendo na mambo ya kiungu, bali unyenyekevu wake kwao ni kwa ajili ya kuwatukuza kwa sababu wao ni “Waja watukufu na waheshimiwa, na hao wanafanya mambo kwa idhini na amri ya Mwenyezi Mungu” (21:26-27) Hakika unyenyekevu na utukuzaji huu asilan sio Ibada. Mwenyezi Mungu (s.w.t) amewasifu baadhi ya waja wake kuwa wanastahiki kutukuzwa pale aliposema: “Hakika Mwenyezi Mungu amemchagua Adam na Nuh na watoto wa Ibrahim na watoto wa Imran juu ya walimwengu” (3:33), na mahala pengine katika Qur’an anasema: “Akasema: Hakika mimi nitakufanya Imam wa watu (Ibrahim).” (2:124). Sifa zote hizo tukufu ambazo Mwenyezi Mungu (s.w.t) amemsifu Nabii Nuhu, Ibrahim, Suleiman, Musa, Isa na Muhammad (s.a.w.w) ni mambo 43. Ahkamul-Qur'an Juz. 1 Uk. 32 cha Abu Bakr Ahmad bin Ali Raazi maarufu kwa jina la Jaswas aliyefariki mwaka 370. 105


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 106

Tawhid na Shirk ambayo yanalazimu kuyaingiza mioyoni na vifuani, na inawajibisha kuwapenda na kuwaheshimu wenye nayo, na baadhi yao tunalazimishwa kuwapenda kwa ushuhuda wa maandiko ya Aya za Qur’an tukufu.44 Tutakapomheshimu mmoja kati ya waheshimiwa hao maishani mwao na baada ya kufariki kwao basi si kwa jambo lingine, bali ni kwa kuwa wao ni waja wa Mwenyezi Mungu (s.w.t) ambao wametukuzwa na ni Mawalii watukufu, na si kwa kuitakidi kuwa wao ni Miungu, au Marabi, au ni vianzo vya mambo ya kiungu. Kuwatukuza hao hakuhisabiwi kuwa ni ibada, wala mtendaji wa hayo hahesabiwi kuwa ni mshirikina abadan, kwa hivyo kubusu mkono wa Mtume (s.a.w.w), Imam, Walimu, Wazazi wawili, Qur’an, vitabu vya dini, sehemu takatifu au majengo walimozikwa mawalii wa Mwenyezi Mungu (s.w.t) ni kwa lengo la kutukuzwa na sio Ibada.

SISI NA MWANDISHI WA KITABU CHA AL-MANAAR Na katika kuhitimisha mada hii ni vizuri tumkumbushe mpendwa msomaji kundi lingine la maana za Ibada, tunataja baadhi ya hizo: 1. Mwandishi wa kitabu cha Al-Manaar anaandika hivi: “Ibada ni aina ya unyenyekevu na kikomo chake ni kujihisi kimoyo moyo utukufu wa mwabudiwa, hajui chanzo chake wala hadiriki dhati yake ilivyo.”45 Na maana hiyo ina mapungufu, kwani baadhi ya Ibada hazina unyenyekevu wa hali ya juu, kama vile katika baadhi ya swala zilizokosa unyenyekevu, kisha huenda ukawapo unyenyekevu kutoka kwa mpenzi kumfanyia mpendwa wake, askari kwa mkuu wake, unyenyekevu wa hali ya juu kabi44. "Sema, siombi malipo yoyote kutoka kwenu isipokuwa kuwapenda ndugu zangu wa karibu" 42:23 45. Al-Manaar Juz. 1 Uk. 57. 106


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 107

Tawhid na Shirk sa kushinda ule wa muumini anaomfanyia Mwenyezi Mungu (s.w.t) pindi anapomuomba na kuswali, pamoja na hivyo unyenyekevu huo hauhesabiwi kuwa ni Ibada, ilhali unyenyekevu wa waumini kwa Mola Manani huwa ni ibada hata kama ukiwa unyenyekevu huo ni mdogo kuliko wa awali. Ndio, hakika mwandishi huyo ametaja katika maelezo yake maana halisi na sahihi ya Ibada inayoafikiana na ile tuliyoeleza, anasema kwamba: “Ibada zipo za aina nyingi katika kila dini miongoni mwa dini, zimeanzishwa ili kumkumbusha binadamu ile hisia ya Uungu mkuu, hisia ambazo ndio roho na mhimili wa Ibada na siri yake.”46. Ibara: “Hisia ya Uungu mkuu” inaeleza hali ya mwenye kuabudu kuwa anaamini Uungu wa mwabudiwa, kwa hivyo matendo yake hapo huwa ni Ibada, ama yale yasiyokuwa na sifa hiyo hayawi Ibada. 2. Katika maelezo ya Sheikh wa zamani wa Azhar, Sheikh Muhammad Shaltut, kuhusiana na maana ya ibada yanaafikiana kimaana na yale aliyoyaeleza mwandishi wa kitabu cha Al-Manaar na yanatofautiana kimatamshi, amesema: “Ibada ni unyenyekevu ambao hauna mpaka wala kiwango cha ukubwa wake.”47 Kwa hivyo maelezo hayo yanaambatana, chunguza maelezo yaliyoko katika Tafsiri Al-Manaar ambayo yanahusiana kwa namna fulani, anasema: “Ibada chanzo chake ni ile hali ya moyo kuhisi utukufu ambao chanzo chake hakijulikani.”, Ilihali ukweli ni kwamba mwenye kuabudu anajua sababu ya utukufu huo kuwa ni “Ukuu wa Uungu” ambao ndio Uungu wa mwabudiwa, na anauhitajia sana utukufu huo, na anajua kwamba mikononi mwa utukufu huo ndimo imo hatima ya yeye mwenye kuabudu, sasa basi iweje asijue chanzo chake.48 Maana yenye mushkeli sana ni ile maana iliyoelezwa na Ibn Taimiyyah, 46. Al-Manaar Juz. 1 Uk. 57. 47. Tafsir Qur'an Kariim Uk. 37. 48. Aalau Rahman uk. 59. 107


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 108

Tawhid na Shirk amesema: “Ibada ni neno lenye mkusanyiko wa kila analolipenda Mwenyezi Mungu (s.w.t) na analoliridhia miongoni mwa maneno na vitendo vya batini na vya dhahiri, kama vile Swala, Zaka, Swaumu, Hija, kusema kweli, kutekeleza amana, kuwatendea wema wazazi wawili na kuunganisha udugu”.49 Mwandishi huyu hakufarikisha baina ya Ibada na kujikurubisha, na kutawasaru kwamba kila lenye kumkurubisha mtu kwa Mwenyezi Mungu ni Ibada, ilihali ukweli si hivyo, kwani yapo mambo yanayomridhisha Mwenyezi Mungu na ambayo yanawajibisha kulipwa thawabu, na hayo huenda ikawa ni Ibada kwa mfano Swala, Swaumu, Hija, na mengine huenda yakawa ni kujikurubisha kwake tu bila ya kuwa ni Ibada, kama vile kuwafanyia wema wazazi wawili, kutoa zaka na khumsi, haya yote ya mwisho huwajibisha kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) ilhali sio Ibada, hata kama ikiitwa katika istilahi ya wanahadithi ni Ibada, huwa inakusudiwa kuwa yanafanana na Ibada katika upatikanaji wa thawabu kutokana nayo. Na kwa ibara nyingine: Hakika utekelezwaji wa matendo hayo huhesabiwa ni kumtii Mwenyezi Mungu (s.w.t), lakini sio kila utiifu ni Ibada. Ukipenda sema hivi: Yapo mambo ya kiibada na mambo ya kujikurubisha, kila Ibada ni kujikurubisha na sio kila kujikurubisha ni Ibada, mathalan kumpa fakiri chakula na kuwahudumia watoto yatima yanawajibisha kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) lakini sio Ibada, kwa maana ya kwamba mwenye kufanya hayo awe ni mwenye kumwabudu Mwenyezi Mungu (s.w.t) kupitia matendo hayo. Bila shaka ndugu yangu mpendwa msomaji, mpaka hapa umekwishaelewa maana halisi ya Ibada na dhana yake na uhakika wake kwa mujibu wa Qur’an na Sunna za bwana Mtume (s.a.w.w), hakuna utata wowote kwako kuhusiana na maana ya Ibada na uhalisia wake. Na sasa baada ya kujua 49. Majallat Buhuuth Islamiya, toleo la 2 Uk. 187 imenakiliwa kutoka kitabu "Al-Ubudiyya uk. 38." 108


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 109

Tawhid na Shirk kigezo cha msingi katika Ibada, ni juu yako ulinganishe matendo mengi ambayo hufanywa na Waislamu tangu zama za Mtume (s.a.w.w) hadi zama zetu hizi je! yanapingana na Tawhiid na kuafikiana na Shirki? Au yanaafikiana na Tawhiid na kupingana na Shirki na wala ndani yake hakuna hata chembe ya ushirikina abadan. Na kwa ajili hiyo tutaendelea kwenda pamoja na wewe katika njia hii ya kuhakiki mas’ala ya Ibada, tunasema: “Hakika matendo ambayo Mawahabi huyakanusha juu ya Waislamu” ni: 1 - Kufanya tawassuli kwa Mitume na mawalii katika kukidhiwa haja na kuhakikisha maombi yao yanajibiwa, je! hiyo ni Shirki au hapana? Ni lazima ndugu yangu mpendwa kwamba kabla ya kujibu swali hili kwanza uelewe kigezo cha msingi kilichopita katika kutoa maana halisi ya Ibada na dhana yake, je! Mwislamu anayefanya tawassuli kwa Mitume na Mawalii anaitakidi Uungu wao au Urabi wao, angalau hata kwa daraja la chini? Au wanaamini kuwa hao ni waja watukufu mbele ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) aliyetukuka na dua zao hujibiwa kupitia kwao? Majibu ya maswali hayo yanajibiwa na Qur’an tukufu. Lau mtu atafanya tawassuli kwa Mitume kwa maana ya kwanza (Yaani kwa kuamini Uungu wao) basi atakuwa amefanya Shirki na mtu huyo atakuwa ametoka katika Uislamu. Na ama akifanya hayo, ikawa sio kwa maana ya kwanza bali kwa maana ya pili (Yaani kwa kuamini kuwa hao ni waja watukufu mbele ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) aliyetukuka) hatokuwa amefanya Shirki. Ama suala la je tawasuli hiyo ina manufaa yoyote kwake au la, na je nje ya Shirki tawassuli hiyo ni haram au ni halali, mazungumzo kuhusu hayo yako nje ya mada yetu ambayo inahusu Tawhiid na Shirki ambayo inalenga kubainisha Shirki ni nini na ni kipi sio Shirki? 2 - Kuomba Shufaa Kutoka kwa Watu Wema ambao Qur’an Tukufu 109


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 110

Tawhid na Shirk na Sunna Sahihi zimethibitisha Shufaa Zao. Kwa hakika kuomba Shufaa kutoka kwa watu hao kana kwamba wao ndio wamiliki wa hilo, na kwamba hiyo ni haki ya msingi na ina wahusu wao tu, au wameachiwa wao cheo hicho, bila shaka hiyo ni Shirki na huko ni kwenda kombo na Tawhiid, na ni kukiri Uungu kwa mmiliki wa Shufaa (uombezi) na kuwa yeye ndiye Rabbi, mola na mlezi, kwa hivyo kuwaomba watu Shufaa kwa maana hiyo ni Shirki ya dhahiri. Ama kuwaomba Shufaa watu wema, kwa kuwa wao ni waja ambao wameamrishwa na Mwenyezi Mungu kufanya hivyo, au wameruhusiwa na kupewa idhini juu ya hilo, na kuwa hivyo ni makhsusi na ni haki ya Mwenyezi Mungu (s.w.t), Naye ndiye huwapatia waja wake ruhusa hiyo, waja ambao ni mawalii na watukufu, maana hiyo ya Shufaa haipingani na Tawhiid, na wala haihusiani kabisa na Shirki, ambayo ni kuomba kitu kutoka kwake (walii) pamoja na kuitakidi kuwa ni Mungu na kumwabudu yeye na kutekeleza amri zake. Ama suala la je ombi hilo lina manufaa kwake au halina, au je nje ya Shirki ombi hilo ni halali au haramu, suala hilo liko nje ya mada hii, kwani ni kama tulivyotangulia kusema kwamba mada yetu inahusu kupambunua kati ya Tawhiid na Shirki katika Ibada. 3 – Kuadhimisha na kuwakumbuka Mawalii wa Mwenyezi Mungu na kuyatukuza makaburi yao. Je! Amali hiyo inakubaliana na misingi ya Tawhiid au inaafikiana na misingi ya Shirki? Jawabu ni hili: Hakika amali hiyo huenda ikaafikiana na Tawhiid kwa upande mmoja na huenda ikaafikiana na Shirki kwa upande mwingine, ikiwa uadhimishaji na utukuzaji – kwa aina yoyote itakavyokuwa – kama watu wamefanya kuwa Mawalii hao ni waja wema, waliyapitisha maisha yao katika ulinganio wa Mwenyezi Mungu (s.w.t), waka110


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 111

Tawhid na Shirk jitolea nafsi zao, ndugu zao, na waliwatumikia watu kwa hali na mali, basi mfano wa uadhimishaji huo unaafikiana na Tawhiid, kwani kumtukuza mja miongoni mwa waja wa Mwenyezi Mungu (s.w.t) kwa aliyoyafanya katika kudumisha dini ya Mwenyezi Mungu (s.w.t), pamoja na kuamini kwamba yote aliyonayo amepewa na Mola Manani, naye hana uwezo wowote isipokuwa atakapowezeshwa na Mwenyezi Mungu (s.w.t), basi hakika uadhimishaji huo hautofautiani na misingi ya Tawhiid, na hilo halina shaka. Ama akiadhimishwa na kutukuzwa walii – akiwa hai au amekufa – kwa imani kuwa ni mmiliki halisi wa uungu au daraja la kiungu, au ana sifa ya Rabbi au daraja miongoni mwa madaraja yake, kwa hakika hakuna shaka hiyo ni Shirki na mtu huyo atakuwa ametoka katika Uislamu na mipaka ya Tawhiid. Na ama suala la je uadhimishaji huo una manufaa kwake au hauna, au je nje ya Shirki uadhimishaji huo ni halali au haramu, suala hilo liko nje ya mada hii, kwani ni kama tulivyotangulia kusema kwamba mada yetu inahusu kupambanua kati ya Tawhiid na Shirki katika Ibada. 4. Kuomba msaada kwa Mawalii Je! hilo linaafikiana na Tawhiid au na Shirki? Jibu: Hakika jibu la swali hilo litabainika baada ya kuupima uombaji huo juu ya mizani tuliyopewa na Qur’an tukufu. Lau mtu ataomba msaada kwa mmoja miongoni mwa Mawalii akiwa hai au amekufa, amsaidie kutimiza jambo la ada au lisilokuwa la ada, kama vile kugeuza fimbo nyoka au maiti awe hai, kwa imani kwamba huyo anayeombwa msaada ni mungu, au rabbi, au ni aliyeachiwa baadhi ya majukumu ya kuendesha ulimwengu, basi uombaji wa namna hiyo ni Shirki bila mjadala. Na ama akimuomba huku akiitikadi kuwa ni kiumbe na hana uwezo wa 111


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 112

Tawhid na Shirk lolote lile ila yale aliyokadiriwa na kupewa na Mwenyezi Mungu (s.w.t), na kuwa hafanyi lolote isipokuwa kwa idhini ya Mola Manani na utashi Wake, basi kumuomba yeye msaada katika hali hiyo ni sehemu ya Tawhiid na pasi na kutofautisha je Walii huyo yu hai au amekufa, na je jambo hilo ni la kawaida au si la kawaida. Ama kuhusu je muombwa ana uwezo wa kutekeleza aliloombwa au hapana? au uombaji huo ni katika kitu cha halali au haramu? Hayo yako nje na mazungumzo yetu na wala hayahusiani na mada yetu. 5 Kuomba ponyo kupitia Mawalii wa Mwenyezi Mungu: Je! hilo linaafikiana na misingi ya Tawhiid au hapana? Lau mtu atamuomba ponyo mmoja wa Mawalii wa Mwenyezi Mungu (s.w.t) kwa kuamini kuwa asili ya jukumu au kazi hiyo ni ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) yeye ndiye mponyaji wa hakika, lakini wakati fulani huzifikisha rehema Zake kwa waja Wake kupitia sababu za kimaumbile na zisizo za kimaumbile, basi ombi hilo linaafikiana na Tawhiid na si vingine, kwa sababu anayeombwa hafanyi isipokuwa kwa amri ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) na utashi wake. Ama muombaji atakapoitakidi kuwa muombwa anajitegemea katika utoaji ponyo, naye ndiye mmiliki wa ponyo au ameachiwa jambo hilo bila kuingiliwa na yeyote, bila shaka atakuwa amefanya Shirki, na kutoka nje ya wigo wa Tawhiid. Ama suala la je kuomba ponyo toka kwa Mawilii kuna faida au hapana, au je wao wana uwezo wa kutoa ponyo au laa, au je nje ya Shirki kazi hiyo inajuzu kisheria au haijuzu, hayoyote yako nje ya mada yetu ambayo inahusu kupambunua kati ya Tawhiid na Shirki katika Ibada. Tumeleta mifano hiyo ili uwe mwangaza na dira atakayoifuata msomaji mpendwa katika kudurusu mambo yaliyobakia ambayo Mawahabi huya112


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 113

Tawhid na Shirk kanusha bali huyachukia mno, hatuwezi kuyataja yote kuchelea mada hii kuwa ndefu. Kwa kuwa Mawahabi hukosea, hufanya makosa na hufahamu kimakosa maana ya Uungu na Ulezi, vivyo hivyo katika kueleza vigezo vya Tawhiid na Shirki, sisi tunarudufu mada hii kwa lengo la kusahihisha mawazo yao potovu na ukoseaji wao juu ya maana halisi ya Tawhiid na Shirki, ambapo yameelezwa katika vitabu vyao vingi kutoka kwa wanafikra wao na waandishi wao. Kabla hatujaingia katika mada na kuchambua kwa kina suala hili tunahitimisha mada hii kwa kutaja itikadi za waabudu masanamu katika zama za ujinga na namna walivyokuwa wakiyaomba masanamu, kwani kueleza jambo hilo kutasaidia sana kujua Aya nyingi ambazo Mawahabi wamezitumia katika kufikia malengo yao ya kupinga dua nyingi na tawassauli nyingi kwa kudai kuwa ni Shirki . 6 - Itikadi za Waarabu wa zama za jahilia na waabudu Masanamu: Hakika waabudu Masanamu katika wakati huo walikuwa katika makundi mbalimbali kama vile waumini wa Sayari, Viumbe na Dahari, na na ufuatao ni ufafanuzi wa itikadi za baadhi ya vikundi hivyo: I. WAUMINI WA SAYARI Walikuwa wakisema: Hakika binadamu hana kiwango na upeo wa kumwabudu Mwenyezi Mungu (s.w.t) na kuwa na mahusiano naye moja kwa moja, bali hapana budi kuwepo wa kiungo baina yake na Mungu, ili huyo kiungo awaweke karibu, na kwa kuwa maruhani hayakuwa mikononi mwao basi wakakimbilia kwenye Sayari saba, walikuwa wakijikurubisha kwenye Sayari hizo ili ziwakurubishe kwa maruhani, na hayo maruhani yawakurubishe kwa mola muumba, na kwamba hizo Sayari ni viwiliwili vya Maruhani. Walikuwa wakifanya sherehe maalum wakati wa kuabudu Sayari hizo, na 113


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 114

Tawhid na Shirk walikuwa wakitengeneza pete na vinyago vyenye sura zake, wakawa wanavaa mavazi mahususi katika saa maalum katika siku maalum, aidha walifukiza kwa mafusho maalum kwa ajili ya kila Sayari kisha wakiziomba haja zao, vilevile walikuwa wakiziita kwa jina la Arbaabu yaani miungu, na Mwenyezi Mungu (s.w.t) nndiye Mungu wa waungu naye ndiye Mungu Mkuu.50 II. WAUMINI WA MAUMBO (VINYAGO) Washirikina hawa hawana tofauti na kundi lililotangulia katika baadhi ya itikadi, isipokuwa wao walikuwa wakiabudu maumbo au vinyago vya Sayari badala ya Sayari zenyewe, kwa sababu Sayari zilichomoza usiku na mchana hazikuonekana, kwa hivyo wakatengeneza vinyago vyenye sura zinazofanana nazo wakisema: Tunaomba na kujikurubisha kwa vinyago, navyo hujikurubisha kwa Sayari hizo za kiruhani, nazo hujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t), na tunayaabudu hayo kwa ajili ya kutufanya tuwe karibu mno na Mwenyezi Mungu.51 III. ITIKADI ZA WAARABU WA ZAMA ZA JAHILIA Walikuwepo Waarabu wachache ambao walikuwa wakifuata dini ya Dahari wakisema kuwa maumbile ndio huleta uhai, na Dahari ni yenye kuondoa uhai huo, na maisha kwa mtazamo wao huwa ni muunganiko wa maumbile, viasilia na viumbe wenye hisia katika ulimwengu wa hali ya chini, vitu vyote vinaletwa na maumbile na vinaangamia na kutoweka na kazi hiyo inafanywa na Dahari. Lakini wengi wao walikuwa wakikiri kuwepo muumbaji na kuumbwa kwa viumbe, lakini walikanusha kufufuliwa na kurudi tena na uletwaji wa mitume toka kwa Mwenyezi Mungu.52 Na miongoni mwao walikuwa wakiabudu malaika na majini, wakiamini 50. Milal wa Nihal Juz. 2 Uk. 244. 51. Milal wa Nihal Juz. 2 Uk. 244. 52. Milal wa Nihal Juz. 2 Uk. 244. 114


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 115

Tawhid na Shirk kuwa ni wasichana wa Mwenyezi Mungu (s.w.t). Na wengineo walikuwa wakiitwa Swabiaat ambao wakiabudu nyota. Na wengine walikanusha kuwepo muumbaji, na kusema kuwa vitu vyote vimezuka vyenyewe, aidha walikanusha kuwepo Mitume na Kiyama, lakini watu wa vikundi vyote viwili walikuwa wakiabudu masanamu na kuzingatia ni wamiliki wa Shufaa mbele ya Mwenyezi Mungu (s.w.t). Na walikuwako miongoni mwa Waarabu wakiitakidi na kufuata dini ya Mayahudi au Wanaswara (wakristo) kwani walikuwa wakiishi katika kitongoji kimoja cha mji wa Madina na sehemu ya Najran kwa upande mwingine. Ama makundi matatu ya Wakristo ambayo yalikuwa yakitofautiana kati yao kuhusu Mungu baba, Mwana na Roho mtakatifu yalikuwa yakiitwa Maikaniya, Nasturiya na Yaakubiya. Makundi hayo pamoja na tofauti zao lakini yaliafikiana katika kumwabudu Masihi (Isa) ambaye hakuwa ila mtume. Na katika Aya zinazoelezea hoja za Ibrahim (a.s.) zinatoa ishara ya itikadi za waabudu Nyota na Sayari zilizopo mbinguni, hali kadhalika zipo Aya ambazo zinabainisha itikadi za Wakristo. Vile vile zipo Aya ndani ya Qur’an tukufu ambazo zinawakemea vikali waabudu masanamu zikiwahusisha Waarabu wa zama za ujinga ambapo walikuwa wakiamini itikadi za kijinga za kiajabu ajabu, wengi wao walikuwa wakiabudu masanamu na kuyaona yanatoa Shufaa au ni waungu wadogo, na mfano wa Aya hizo ni:

“Na wanapokuona wale waliokufuru hawakufanyii chochote ila mzaha (wakisema) Je! huyu ndiye anayewataja waungu wenu? Na hao ndio wakataao mawaidha ya Mwingi wa rehema.” (21:36) 115


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 116

Tawhid na Shirk

“Je! wanao miungu wanaowalinda badala yetu? Hawawezi kujisaidia wenyewe wala hawatahifadhiwa nasi.” (21:43)

“Na wakamfanyia Mwenyezi Mungu, majini kuwa washirika, hali amewaumba na wanaomsingizia kuwa ana watoto wa kiume na wa kike pasipo kujua ...” (6:100)

“Je! Mmeona Lata na Uzza? na Manata, mwingine wa tatu?” (53:1920) AYA HIZO ZINAASHIRIA KITU GANI? Hakika lengo la msingi katika Aya hizo ni: Kukataza ile imani ya makundi ya waabudu masanamu, ambao walikuwa wakiyafanya masanamu kuwa washirika wa Mwenyezi Mungu (s.w.t) katika baadhi ya uendeshaji wa mambo au wamiliki wa Shufaa na wakawa wakiyanyenyekea, kuyaomba msaada na ponyo kwa imani ya kuwa ni miungu wadogo ambao wameachiwa mambo ya ulimwengu na kutenda wapendavyo duniani na akhera. Kwa hivyo kuna uhusiano gani kati ya Aya hizi na kitendo cha kuiomba msaada roho tukufu ikiwa muombaji msaada haamini uungu wa roho hiyo bali anaamini huyo mwenye roho ni miongoni mwa waja wema wa Mwenyezi Mungu (s.w.t.)? Basi makusudio ya maneno ya Mola Manani aliyetukuka: “Na hakika misikiti ni ya Mwenyezi Mungu basi msimuombe yeyote pamoja na 116


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 117

Tawhid na Shirk Mwenyezi Mungu.” Na yale yanayofanana na hayo yamekwishatangulia hapo mwanzoni, nayo ni kukataza ile ibada ambayo washirikina walikuwa wakiifanya mbele ya Lata, Uzza na Manata au Nyota, Sayari zilizopo mbinguni, Malaika na Majini, kana kwamba Aya inataka kusema: “Wala msimwabudu mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu.” Na ikiwa Qur’an tukufu imekataza ushirikishwaji kati ya Mwenyezi Mungu na asiyekuwa Yeye katika ibada, basi kuna mafungamano gani katika suala hili na suala la maombi kwa watu wema, na kuwaomba haja hao miongoni mwa yale wayatendayo kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) na ukadiriaji Wake, Qur’an tukufu inasema:

“Kwake ndiyo maombi ya haki, na wale wanaowaomba badala Yake hawawajibu chochote.” (13:14)

“Na wale mnaowaabudu badala yake hawana uwezo wa kukunusuruni wala wa kujinusuru wenyewe.” (7:197)

“Hakika wale mnaowaabudu badala ya Mwenyezi Mungu ni waja kama nyinyi…” (7:194)

“Na wale mnaowaabudu kinyume chake, wao hawamiliki hata utando wa kokwa ya tende” (35:13

117


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 118

Tawhid na Shirk

“Sema: je! tumuombe asiyekuwa Mwenyezi Mungu ambaye hatupi faida wala hawezi kutudhuru …” (6:71)

“Wala msiabudu badala ya Mwenyezi Mungu ambao hawakunufaisheni wala hawakudhuruni …” (10:106) Na Aya zinginezo ambazo zimejaa ndani ya Qur’an, Aya zote hizo zinafungamana na maombi ambayo yanahusu ibada ya Masanamu, Nyota, Sayari, Malaika na Majini, kwa imani kuwa ni waungu wadogo na kuona kuwa wanastahiki kuabudiwa, kupanga na kuendesha mambo ya ulimwengu na kwamba wao wanatoa Shufaa kwa ukamilifu. Ama kuhusu watu wema na kuwaomba wao Shufaa kwa kuamini hawana uwezo wowote na hawafanyi lolote bila idhini ya Mwenyezi Mungu (s.w.t), je! inafaa kulinganisha kati ya maombi hayo na maombi ya Masanamu? Bila shaka hayo yanatofautiana kabisa! Ni dhahiri kwamba dalili ipo wazi ya kutofautiana kati ya maombi hayo mawili, lakini Mawahabi wanaitakidi kwa mfano kwamba, kuwaomba Mitume watakatifu ni Shirki na haramu baada ya kufariki kwao, bali inafaa wakati wa uhai wao, na tumethibitisha - hapo kabla – kwamba kifo na uhai haviathiri chochote katika uasilia wa tendo au amali fulani, kutokana na kufaa na kutofaa kwake. Kwa hakika imebainika hapo kabla yale yaliyomo katika kitabu Fat’hul Majiid pale aliposema: “Na kauli yake: ’Au amuombe mwingine’: Jua kwamba dua zipo za aina mbili: dua ambayo ni ibada na dua ambayo ni maombi, na katika Qur’an wakati fulani inakusudia hili na wakati mwingine inakusudia lile, na muda mwingine inakusudia yote mawili kwa pamoja. 118


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 119

Tawhid na Shirk Dua ya maombi ni yale maombi ambayo humfaa muombaji ama kupata manufaa au kumuepusha na madhara, na hilo limekanushwa vikali na Mwenyezi Mungu (s.w.t) kumuomba mwingine asiyekuwa Yeye, ambaye hana uwezo wa kumiliki madhara na kuleta manufaa kama anavyosema (s.w.t):

“Sema: Je! Mnamwabudu badala ya Mwenyezi Mungu ambaye hawezi kuwadhuruni wala kukunufaisheni? na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua.” (5:76) Allah (s.w.t.) na anasema tena:

“Sema: Je! Tumuombe asiyekuwa Mwenyezi Mungu ambaye hatupi faida wala hawezi kutudhuru, na turudishwe nyuma baada ya Mwenyezi Mungu kutuongoza, sawa na yule ambaye mashetani yamempoteza akiwayawaya katika ardhi? Anao marafiki wanaomwita kwenye muongozo hasa ni muongozo wa Mwenyezi Mungu na tumeamrishwa tumnyenyekee Mola wa walimwengu wote.” (6:71)

119


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 120

Tawhid na Shirk

“Wala usiabudu badala ya Mwenyezi Mungu ambao hawakunufaishi wala hawakudhuru, na ukifanya hivyo, basi hakika utakuwa miongoni mwa madhalimu.” (10:106) Sheikhul-Islam, Ibn Taimiyyah amesema: Kila dua ni ibada, sawa iwe dua ya ibada au dua ya maombi, kwani dua ya maombi hufungamana na ibada, Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema:

“Muombeni Mola wenu kwa unyenyekevu na kwa siri, hakika Yeye hawapendi warukao mipaka” (7:55)

“Sema: mnaonaje kama ikiwafikieni adhabu ya Mwenyezi Mungu au kiwafikieni Kiyama, je! mtamwita asiyekuwa Mwenyezi Mungu ikiwa nyinyi ni wa kweli? Bali yeye ndiye mtamwita, naye atakuondoleeni mnayomuomba akipenda, na mtasahau mnaowashirikisha.” (6:40-41)

“Na kwa hakika misikiti yote ni ya Mwenyezi Mungu basi msimuombe mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu” (72:18)

120


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 121

Tawhid na Shirk

“Kwake ndiyo maombi ya haki, na wale wanaowaomba badala yake hawawajibu chochote, isipokuwa kama yule anyooshaye mikono yake miwili kwenye maji ili yafikie kinywani mwake, lakini hayafikii, na hayako maombi ya makafiri ila katika upotovu.” (13:14) Mfano wa maombi yote hayo yanafungamana na maombi ambayo ni ibada, kwa sababu muombaji amefanya ikhlas kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) katika maombi yake na hiyo ni miongoni mwa ibada bora. Vivyo hivyo mwenye kumtaja Mwenyezi Mungu na kufuata kitabu chake na anayefanya mfano wa hayo anakuwa ni mwombaji na mfanya ibada. Kwa hakika yamedhihirika maneno ya Sheikhul-Islam kwamba dua ambayo ni ibada hulazimu dua ambayo ni maombi kama ambavyo ndani ya dua ambayo ni maombi mna ibada.53 Kwa utafiti huo unaohusiana na dua aina mbili, moja ikiwa ni ibada na ya pili ikiwa si ibada, tunapata mambo yafuatayo: Mosi: Ni vipi Ibn Taimiyyah alivyofaidika kutokana na Aya hii: “Muombeni Mola wenu kwa unyenyekevu na siri” na Aya: “Kwa hakika misikiti ni ya Mwenyezi Mungu wala msimuombe mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu” kwamba hakika kumuomba mtu haja ni kumwabudu muombwa.

53. Fat'hul-Majiid Uk. 166. 121


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 122

Tawhid na Shirk Ikiwa neno ni “Muombeni” katika Aya hii: “Muombeni Mola wenu kwa unyenyekevu” na neno “Msimuombe” katika Aya hii: “Wala msimuombe mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu” yana maana ya kuomba iweje maombi ya kutaka kitu kwa fulani yawe ni kumwabudu muombwa. Hakika aya mbili hizo hazijulishi kitu zaidi ya kukataza kumuomba asiyekuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t), ama eti maombi hayo ni ibada, dhahiri ya Aya haionyeshi hivyo abadan, kwani kukataza jambo sio dalili ya kilichokatazwa kuwa ni ibada. Pili: Hakika dua ya maombi ya jambo itakuwa ni ibada iwapo muombaji ataitakidi kwamba muombwa ni mungu kwa moja ya daraja za uungu, katika hali kama hiyo maombi yatakuwa ni ibada na dua hiyo itakuwa ni ibada, na hakika hayo huwa maombi ya kiibada, lakini endapo mtu atakapomuomba mwingine bila kuitakidi hivyo, maombi yake hayatakuwa ni ibada au anamuabudu muombwa. Tatu: Ni jambo la kushangaza sana kuona inafaa kumuomba aliye hai na jambo hilo kuruhusiwa kisheria moja kwa moja, na kughafilika kuwa lau ingekuwa kuomba msaada vyovyote vile kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu (hata kama haiambatani na itikadi ya uungu au umiliki wa maombi) ni Shirki kusingekuwa na hadithi yoyote katika sehemu hii kwa maiti anayeombwa au mtu aliye hai. Hebu tuangalie yale yaliyopokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w), amesema: “Dua ni kiini cha ibada” makusudio yake ni maombi mahsusi ambayo huambatana na itikadi ya kuwa muombwa ni Mungu. Kwa ibara nyingine hakika makusudio ya dua katika hadithi iliyotangulia ni kumuomba Mwenyezi Mungu (s.w.t) ambapo ndio kiini cha ibada. Kuna uhusiano gani kati ya hadithi hiyo na kuwaomba watu wema pale ambapo hakuna itikadi ya Uuungu wa muombwa!!

122


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 123

Tawhid na Shirk Hapa kuna swali, nalo ni kwamba kumuomba mwingine hata kama sio ibada au kumwabudu yeye kama tulivyoeleza huko nyuma, lakini kwa mujibu wa Aya hizo ni jambo la haramu kuwaomba watu wema waliokufa, kwa sababu anaombwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t), na maombi yaliyokatazwa ni yale ambayo muombwa sio Mola muumba. Ndio Aya hizo hazihusiani kabisa na kuwaomba watu hai kwani ni jambo lililoruhusiwa kisheria, kwa hivyo basi natija inayopatikana ni haramu kuwaomba watu wema waliopita (wafu) hata kama si Shirki. Jawabu la swali hilo liko wazi baada ya kueleweka vizuri yale tuliyoyataja kwamba Aya hizo zinahusu maombi maalum yanayofanywa na washirikina kwa yale waliodhani kuwa ni waungu wao na mabwana wao, na katazo hilo la maombi mahsusi halifanyi maombi yote kuwa haramu ikiwa hayafanani na hayo. Na dalili iliyo dhahiri kutokana na yale tuliyosema ni kule kukiri kwa muulizaji swali, ambapo amekiri kwamba Aya hizo hazimjumuishi muombwaji aliye hai, hivyo tunasema hakika mwombwaji huyo si kwamba kuvuliwa hukmu ya Aya hizo bali ni kwamba tangu mwanzo yeye si maudhui ya hukmu hiyo na wala ahusiani na Aya hizo, kama tulivyokwishasema kwamba Aya hizo zinaangalia na kuangazia maombi ya washirikina ambao hupitisha maisha yao yote kuomba masanamu na kuyafanya kuwa ni miungu, aidha yana uwezo wa kuwanufaisha, kudhuru, uombezi na msamaha, na vigezo hivyo havipo katika kuwaomba watu wema. Kuhusu imani hiyo juu ya miungu Mwenyezi Mungu (s.w.t) ananukuu maneno ya Saamiry kuhusu yule mungu aliyemtengeneza Saamiry, anasema:

123


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 124

Tawhid na Shirk

“Na akawatolea ndama kiwiliwili chenye sauti, na akasema: Huyu ndiye mungu wenu na mungu wa Musa, lakini alisahau. Je! Hawakuona ya kuwa (ndama huyo) hakuwarudishia neno wala hakuweza kuwadhuru wala kuwafaa?” (20:88–89) Na miongoni mwa yale yanayojulisha tuliyoyasema ni kurudufu neno “kinyume na yeye” katika Aya hizo, hakika halijulishi maombi yote ambayo huelekezwa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) hadi tuhitaji kutoa baadhi ya vigawo, yaani kuwaomba haja watu hai, au kuwaomba wafu kwa kutawassuli, bali limekuja kubainisha sifa maalumu ya maombi haya, nayo ni kumwomba asiyekuwa Mwenyezi Mungu kwa kuzingatia kuwa wanajitegemea katika mambo bila ya Mwenyezi Mungu (s.w.t), kama wanavyoitakidi washirikina kwa miungu yao. Ama kuhusu muombaji kumuomba haja mtu fulani ambaye kwa itikadi ya muombaji hana uwezo wa kufanikisha jambo hilo isipokuwa kwa amri ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) na kwa utashi wake, hakika maombi hayo hayako nje ya mtiririko ule ule wa kumuomba Mwenyezi Mngu (s.w.t), kwa hivyo maombi hayo si mfano halisi wa maneno ya Mola Subhaanah:

“Kwake ndiyo maombi ya haki na wale wanaowaomba badala yake hawawajibu chochote.” (13:14)

124


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 125

Tawhid na Shirk

SEHEMU YA TATU 1. MAWAHABI NA VIGEZO VYA TAWHIID NA SHIRKI Je! Itikadi ya nguvu ya ghaibu kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) ni kipimo cha Tawhiid na Shirki? Hapana shaka kwamba kumuomba haja yeyote inasihi iwapo muombaji ataitakidi kuwa muombwa ni muweza na atamtimizia haja yake. Na uwezo huenda ukawa wa dhahiri au kimaada kama vile tunapomuomba mtu maji ili ayaweke chini ya matumizi yetu, na huenda uwezo ukawa ni ule usioonekana, ukawa upo nje ya utaratibu wa kimaumbile na kanuni za kimaada, kwa mfano vile atakapoitakidi mmoja wetu kuwa Imam Ali (a.s.) aling’oa mlango wa Khaybar kwa uwezo wa ghaib (usioonekana) kama ilivyoelezwa katika hadithi. Au Isa (a.s.) alikuwa anafanya mambo kwa uwezo wa ghaibu, kuponyesha wagonjwa ambao magonjwa yao yalishindikana kupona bila ya kutumia dawa wala kufanyiwa upasuaji. Na kuamini mfano wa uwezo huu wa ghaibu (usioonekana) hata kama utahusishwa na idhini ya Mwenyzi Mungu (s.w.t) na kuwa uwezo huo amepewa na Mola Manani, katika hali hiyo hautafautiani na uwezo wa kimaada wa kidhahiri, bali wenyewe ni sawa na uwezo wa kimaada ambao kuuamini si Shirki, kwa sababu Mwenyezi Mungu (s.w.t) aliyempatia mtu huyo uwezo wa kimaada, ndiye aliyempatia mwingine uwezo usioonekana, pasi na kiumbe huyo kuhesabiwa na kuzingatiwa kuwa ni muumbaji, na bila mtu kudhani kuwa kiumbe huyo hamhitajii Mwenyezi Mungu (s.w.t). Lau mtu atamtibu mgonjwa kwa njia ya uwezo wa ghaib atakuwa amefanya kwa amri, idhini na utashi wa Mwenyezi Mungu (s.w.t), na kwa mfano huo haihesabiwi kuwa amefanya Shirki. Na kumaizi na kuchanganua kati 125


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 126

Tawhid na Shirk ya uwezo ambao huegemezwa na kuhusishwa na Mwenyezi Mungu (s.w.t) na uwezo wenye kujitegemea, ndio kigezo cha msingi cha kupambanua kati ya Tawhiid na Shirki, na hapo ndipo hudhihiri makosa mengi kwa wale ambao hawatofautishi baina ya uwezo wa ghaibu tegemezi na uwezo wa ghaib usio tegemezi. Wakasema: Lau mtu atamuomba mtu mwema – akiwa hai au amekufa – ili amponyeshe ugonjwa wake, kurudishwa mifugo yake au aweze kulipa deni lake, hayo yanahitaji kuamini uwezo wa ghaib kwa yule mtu mwema, na kwamba ana uwezo katika taratibu za kimaumbile zenye kutawala ulimwengu, hali ambayo inamfanya awe na uwezo wa kufanya mambo yasiyo ya kawaida, na kuamini uwezo huo kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu huko ni kuamini kuwa muombwa ni mungu, hakika uombaji huo wa haja kwa hali hiyo unakuwa ni Shirki. Na lau mtu mwenye kiu atamuomba mtumishi wake maji, hakika amefuata utaratibu wa kimaumbile ili kupata anachokitaka. Ama atakapomuomba Imam au Nabii maji kutoka ardhini kwa kuwa anaishi sehemu ya ukame, hakika ombi hilo linafungamana na hulazimu itikadi ya uwezo wa ghaib, kwa hivyo akiitakidi kwamba Nabii au Imam ana uwezo kama wa Mwenyezi Mungu (s.w.t), mfano wa itikadi hiyo ni kuamini kuwa muombwa ni mungu!! Miongoni mwa watu walioeleza kinaga ubaga maneno hayo ni mwandishi Abu Aala Mawdudi anasema: “Kwa ufupi kitu ambacho kinachomfanya binadamu kumuomba msaada Mwenyezi Mungu (s.w.t), na kumnyenyekea Yeye ni kutokana na kufikiri kwamba ni Mmiliki Mwenye mamlaka wa kanuni za maumbile, na ni uwezo uliyo nje ya mzunguko wa utekelezaji wa kanuni za kimaumbile”54 Maneno hayo yako wazi kwani huifanya itikadi ya kuwepo uwezo na nguvu yenye mamlaka ni kigezo cha imani ya Uungu. Na ameeleza wazi 54. Muswtalahat Arba'at Uk. 17. 126


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 127

Tawhid na Shirk katika sehemu nyingi ndani ya kitabu chake jinsi alivyojaalia kigezo cha jambo hilo katika mlango wa Uungu kuwa ni kuitikadi na kuamini kwamba muombwa ni muweza wa kunufaisha na kudhuru ambako kuko nje ya mfumo wa kanuni na taratibu za kimaumbile zilizowekwa, anasema: Mwenye kukifanya kiumbe chochote kuwa msaidizi wake, chenye kumnusuru, utatuzi wa matatizo, chenye kukidhi haja zake, chenye kujibu maombi yake na kina uwezo wa kumpa manufaa, hayo yote kwa msaada ulio nje ya taratibu za kimaumbile, basi sababu ya kuamini hivyo huwa ni kule kudhani kwamba kiumbe hicho kina moja ya nguvu zinazoongoza ulimwengu huu, na ni vivyo hivyo mwenye kumuogopa mtu na anayeona hasira ya mtu huyo itamsababishia kupata madhara, na kwamba ridhaa yake itamsababishia apate manufaa, hali hiyo haitokani ila kule kuamini kwamba mtu huyo ana nguvu na uwezo unaotawala na kuendesha ulimwengu huu. Na yule mwenye kumuomba asiyekuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) haja na tatizo lake baada ya kuwa amemwamini Mwenyezi Mungu aliyetukuka, haimsukumi kufanya hivyo ila kule kuamini kwake kwamba huyo asiyekuwa Mwenyezi Mungu ni mshirikina wa Mwenyezi Mungu katika nguvu na uwezo wa kiungu.�55 Uwazi na ubainifu wa maneno hayo unaonyesha kwamba kuna uwiano baina ya uwezo wa kunufaisha na kudhuru sanjari na imani ya uwezo wa kiungu, na kila uwezo katika utoaji manufaa na kudhuru usiopitia njia za kimaumbile unabeba Uungu. Na hilo ni jambo la kushangaza kutoka kwa Mawdudi. Zaidi ya hapo ni kwamba kuitakidi Uungu hakulazimu kuitakidi mamlaka ya upande mwingine, bali yatosha kuamini kuwa yeye ni mmiliki wa Shufaa na maghfira, kama vile kundi moja miongoni mwa waarabu wa zama za ujinga walivyokuwa wakiamini kuwa Masanamu yao ni miungu, kwa sababu yalikuwa yanamiliki uombezi wao na msamaha wao. Na inajulikana wazi 55. Muswtalahat Arba'at Uk. 23, na katika sehemu nyingine amesema wazi ulazima huu katika Uk. 30 aliposema: "Hakika uwezo wa aina zote mbili hulazimu mwingine." 127


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 128

Tawhid na Shirk kwamba kuamini umiliki wa uombezi si kuamini uwepo wa nguvu inayokusudiwa: mamlaka katika ulimwengu wa kimaumbile. Hakika itikadi ya uwepo wa uwezo wa ghaib ulio nje ya mfumo na taratibu za kimaumbile haiwajibishi itikadi ya Uungu. Hakika kuwa na uwezo juu ya ulimwengu kwa ujumla wake ikiwa ni kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu (s.w.t) na kwa idhini yake hali hiyo si Uungu. Kama ambavyo Mwenyezi Mungu (s.w.t) alivyowapatia baadhi ya watu uwezo maalum katika mambo yao ya kawaida, na kuwafadhilisha baadhi yao kushinda wengine katika uwezo huo, vivyo hivyo haizuiliki kupewa mmoja kati ya waja wake wema uwezo kamili juu ya ulimwengu wote, sawa iwe katika mambo ya kawaida au yasiyokuwa ya kawaida, na hilo pekee halilazimu Uungu. Na ambalo linaweza kuzungumziwa hapa ni je kiumbe huyo ana nguvu hizo na kwamba je Mwenyezi Mungu (s.w.t) amempa nguvu hizo. Qur’an tukufu inaeleza kinaga ubaga mahala pengi, kama vile maelezo yaliyokuja katika kadhia ya Yusuf (a.s.).

YUSUF (A.S.) NA UWEZO WA GHAIBU Yusuf (a.s.) aliwaamuru ndugu zake wachukue kanzu yake na waipeleke kwa baba yake na kisha waiweke juu ya macho yake ili apate kuona, Qur’an tukufu inasema: “Nendeni na kanzu yangu hii na mumwekee usoni baba yangu, atakuwa mwenye kuona.”56 “Basi alipofika mtoaji wa habari njema akaiweka (kanzu ya Yusuf) mbele ya uso wake mara akaona …” 57 Hakika dhahiri ya Aya za Qur’an ni kwamba kurejea uoni kwa Nabii Yakub (a.s.) kulikuwa kwa utashi wa Yusuf (a.s.) na jambo hilo halikufanywa moja kwa moja na Mwenyezi Mungu (s.w.t) hakika lilifanywa hilo na Nabii Yusuf (a.s.) kwa uwezo aliopewa na Mwenyezi Mungu (s.w.t). 56. Sura 12 aya 93. 57. Sura 12 aya 96. 128


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 129

Tawhid na Shirk Na lau kama tiba ya Nabii Yakub (a.s.) ingefanywa moja kwa moja na Mwenyezi Mungu (s.w.t) bila Nabii Yusuf (a.s.) kuhusika asingeliwaamrisha ndugu zake kuweka kanzu yake juu ya uso wa baba yao, bali ingetosha kumuombea dua kule mbali aliko, je! hiyo sio kazi au matumizi ya Walii wa Mwenyezi Mungu (s.w.t) katika ulimwengu kwa idhini ya Mola Manani aliyetukuka?

MUSA (A.S.) NA UTAWALA WA ULIMWENGU Mfano kama huo tunaukuta aidha kwa Mitume wengine kama vile Nabii Musa (a.s.) alipoambiwa: “Tukasema: Lipige jiwe kwa fimbo yako, mara zikabubujika humo chemchem…” (2:60), kama isingelikuwa upigaji wa jiwe kwa fimbo uliofanywa kwa utashi wake ni sababu ya jiwe kupasuka na kutoka maji basi Allah asingeamuru lipigwe. Huenda ikaonekana kuwa Musa (a.s.) amepiga jiwe kwa fimbo yake lakini Mwenyezi Mungu (s.w.t) ndiye aliyepasua na kutoa mito, na hivyo haijulishi nguvu na uwezo wa ghaib aliokuwa nao Musa (a.s.), kwani mwisho wa mambo ni Mwenyezi Mungu (s.w.t) kutoa mito kwa pigo la Musa (a.s.). Bila shaka wazo hilo ni duni, hujibiwa katika lugha na lafudhi ya amri ya kupiga kwa fimbo. Hakika kupiga kwa fimbo sio sawa na dua hadi isemwe kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) anatakabali maombi yake. Kwa ujumla haiwezekani kukanusha kuwepo uhusiano wa upigaji wa fimbo yake na utashi wake katika tendo lile la ububujikaji wa mito ya maji ijapokuwa ni kwa idhini na utashi wa Mwenyezi Mungu (s.w.t), na aya hiyo haijulishi zaidi ya hilo. Na mfano mwingine wa maneno ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema: “Mara tulimpelekea wahyi Musa: Piga bahari kwa fimbo yako, mara ikatengana, na kila sehemu ikawa kama mwamba” (26:63) na Aya hiyo haitofautiani na Aya iliyokwishatangulia.

129


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 130

Tawhid na Shirk WATU WA SULEIMAN (a.s.) NA UWEZO WA GHAIBU Uwezo wa ghaib haukuishia tu katika mifano tuliyoitaja hapo kabla, bali Qur’an tukufu inauthibitisha kwa watu wa Nabii Suleiman (a.s.) kwa mfano uletaji wa kiti cha mfalme wa Sabai kabla Nabii Suleiman (a.s.) hajasimama mahala pake inasema: “(Suleiman) akasema: Enyi wakuu wa baraza! Ni nani atakayeniletea kiti chake cha enzi kabla hawajafika kwangu hali ya kuwa wamekwisha kusilimu? Akasema Afriti katika majini: “Mimi nitakuletea hicho kabla hujasimama kutoka mahala pako, na mimi bila shaka ninazo nguvu za hayo (na) ni mwaminifu”58 bali mwingine akasema: Mimi nitakuletea kabla hujapepesa jicho, iliposema: “Akasema yule aliyekuwa na elimu ya kitabu: “Mimi nitakuletea hicho kabla ya kupepesa jicho lako, basi alipokiona kimewekwa mbele yake akasema! Haya ni kwa fadhila za Mola wangu”59 mpaka sasa haijabainika ni elimu gani hiyo, au upi mradi wa elimu aliyokuwa nayo hadi kufikia kusema: “Mimi nitakuletea kabla hujapepesa macho yako”60 Jawabu: Mradi wa elimu hiyo ni elimu mahsusi ya vitu vya ajabu na namna ya uletaji wa kiti cha mfalme kutoka mbali kwa muda mchache zaidi na usiofikia upepesaji wa jicho, au mradi wake ulikuwa mwingine sio huo, kwa vyovyote itakavyo kuwa na itakavyokadiriwa, elimu hiyo sio miongoni mwa elimu za kifikira ambazo huchumwa na kujifundisha, na jambo hilo si la kawaida na lenye kufuata nidhamu na taratibu za kimaumbile zilizo bayana na kueleweka, na huenda ikadhaniwa kwamba tendo hilo lilifanywa kwa njia za ajabu katika mambo ya ajabu yaliyojificha kwa watu, lakini ni katika mambo ya kawaida, ingawa inahesabiwa kuwa ni katika elimu za ajabu na huenda alikuwa na elimu mahsusi, pamoja na hivyo - ni jambo ambalo halina dalili - lakini haiepukani kitendo cha mten58. Sura 27 aya 38-39. 59. Sura 27 aya 40. 60. Wafasiri wengi wameeleza kauli mbali mbali na mielekeo tofauti tofauti, rejea Miizan Juz. 15 Uk. 363. 130


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 131

Tawhid na Shirk daji kuwa kwake ni katika aina za muujiza na mfano wa karama ambayo hawayawezi isipokuwa Mawalii wa Mwenyezi Mungu (s.w.t). Na baadhi wakadhani kwamba kitendo cha mletaji ni Miujiza unaotokana na elimu yake ya kujua kanuni za kawaida ambazo watu wengine hawazijui hivyo akazitumia kanuni hizo zisizojulikana kwa wengine kutokana na jinsi alivyokuwa akizijua, na hiyo sio elimu ya kifikra ambayo huchumwa na kujifunza, na hiyo yatosha kuihesabu kuwa ni Muujiza au karama.

SULEIMAN (A.S.) NA UWEZO JUU YA ULIMWENGU Qur’an inaeleza waziwazi kwamba Nabii Suleiman (a.s.) alikuwa na mamlaka ya ajabu katika Sura mbali mbali za Qur’an: Alikuwa na mamlaka juu ya majini na ndege hadi wakawa ni miongoni mwa jeshi lake:

“Na alikusanyiwa Suleiman majeshi yake kutoka katika majini na watu na ndege, nao wakiwekwa makundi makundi” (27:17) Alipewa uwezo wa kuzungumza na wanyama, ndege na vijidudu na akawa anazungumza nao, na akiwaamrisha na wakitekeleza amri zake:

“Na akawakagua ndege na akasema: “Imekuwaje mbona simuoni Hudihudi au amekuwa miongoni mwa wasiokuwako? lazima nitamuadhibu adhabu kali au nitamchinja, au ataniletea hoja iliyo wazi.” (27:20-21) 131


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 132

Tawhid na Shirk 3. Alikuwa akiwatawala majini na wakawa wanatekeleza amri zake na utashi wake: “Na kwa Suleiman (tukautiisha) upepo wa nguvu uendao kwa amri yake kwenye ardhi…” (21:81) Na makadirio hayo hakuna uwezo mkubwa zaidi kuliko uwezo huo juu ya ulimwengu wa maumbile ambao alikuwa nao Nabii Suleiman (a.s.), jambo la msingi hapa ni kwamba zipo baadhi ya Aya ambazo zimeeleza kinaga ubaga kwamba yapo mambo yasiyo ya kawaida yakitendeka kwa amri yake.

ISA (A.S.) NA UWEZO WA GHAIB Mfano wa yale tuliyoyaeleza hapo kabla ambayo yamefanywa na watukufu hao, aidha yametendwa na Nabii Isa (a.s.) hudhihirisha kwamba naye anao uwezo usiokuwa wa kawaida, anaumba umbo la ndege kutokana na udongo kisha anampulizia na anakuwa ndege, au anaponya magonjwa yaliyoshindikana wala hayana dawa, bila ya kutumia dawa, Qur’an tukufu inasema:

“Mimi nitakufanyieni katika udongo kama namna ya ndege, kisha napulizia ndani yake (awe) ni ndege kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na niwaponye vipofu na wenye mbalanga, niwafufue wafu kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na niwape habari na mnavyokula na mnavyoviweka akiba katika nyumba zenu, hakika katika hayo mna dalili kwenu ikiwa nyinyi ni wenye kuamini.” (3:49) La muhimu kueleza ni kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t) anaeleza wazi katika Aya nyingine kuwa kazi hizo zilifanywa na Isa mwenyewe, hata 132


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 133

Tawhid na Shirk kama aliupata uwezo huo kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) pale anaposema:

“Na ulipotengeneza udongo katika sura ya ndege kwa idhini Yangu, na ulipowaponyesha vipofu na wakoma kwa idhini Yangu, na ulipowafufua wafu kwa idhini Yangu…” (5:110) Aya hiyo imebainisha kwamba vitendo na kazi hizo zilifanywa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) wala Nabii Isa (a.s.) hakufanya hayo kwa kujitegemea, lakini watu hupotoka kwa kuamini kwamba yeye ni mungu kutokana na kufanya hayo, kwa maana hiyo ikawa kila Aya inayoelezea suala la kufufua, kuumba, kuponya n.k inamalizikia kwa ibara “kwa idhini ya Mwenyezi Mungu”, kisha ikahitimisha kadhia hiyo katika Aya nyingine kwa kusema: “Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mola wangu na ni Mola wenu, basi muabuduni hii ndiyo njia iliyonyooka” (3:51) Na linalodhihirika katika maneno yake “Hakika mimi nakuumbieni” ni kitendo kutoka kwake na lengo lake halikuwa kutoa hoja na kuwaeleza kuwa hakuna kati yao awezaye kufanya hivyo, na kama mradi wake ungelikuwa ni huo ingebidi kusema: mkiuliza na mkitaka. Kulingana na yale atakayoyasema Mwenyezi Mungu (s.w.t) na kumwambia yeye Siku ya Kiyama, inajulisha kwamba yaliyoelezwa na Aya hizo ni dalili iliyotimia, anasema: “Na ulipotengeneza udongo katika sura ya ndege kwa idhini yangu, na ulipowaponyesha vipofu na wenye ukoma kwa idhini yangu, na ulipowafufua wafu kwa idhini yangu…” (5:110)

133


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 134

Tawhid na Shirk Na hapo linabainika swali hili: Ikiwa kutoa habari za ghaib ni dalili miongoni mwa dalili za Muujiza, kwa nini hazikuwekewa sharti la “kwa idhini ya Mwenyezi Mungu” kama ilivyoelezwa katika Aya zingine kwa sharti hilo, pamoja na kuwa mambo yote yanayothibitisha dalili ya utume yanaambatana na idhini ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) kama anavyosema: “Na haikuwa kwa mtume yeyote kuleta Muujiza wowote ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu…” (40:78) Katika kujibu swali hilo tunasema: Hakika kueleza wanayokula watu na wanayoyahifadhi katika nyumba zao si kama vile kuumba, kufufua maiti na kuwa hai, kuponyesha ukoma na kufanya vipofu waone, kwani nyoyo zenye ufahamu mdogo hufikiria mtu mwenye kufanya hayo ni mungu, ambapo ni kinyume na yule mwenye kueleza mambo ya ghaib, kwani nyoyo hizo hazioni kuwa kueleza mambo ya ghaibu ni sula makhsusi linalomuhusu Mwenyezi Mungu (s.w.t) tu, bali zinaona kwama kila aliyeridhiwa au kohani hueleza mambo ya ghaibu, kwa ajili hiyo hakuona haja ya kuongeza ibara “kwa idhini ya Allah”.61 Swali lingine: Hakika maneno ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) yanasema: “Hakika mimi nakuumbieni udongo kama namna ya ndege …” (3:49) Hujumuisha mambo kadhaa wa kadha, nayo ni: 1- Kuumba umbile la ndege kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (s.w.t). 2- Kuumba umbile la ndege kutokana na udongo. 3- Kupulizia umbile lile. La kwanza na la pili ni katika vitendo vya Isa (a.s.), ama kitendo cha tatu kiko nje ya kitendo chake bali ni katika vitendo na kazi ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) kutokana na fuo la maneno “kwa idhini Yake” tofauti na cha kwanza na cha pili. 61. Miizan Juz. 3 Uk. 218. 134


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 135

Tawhid na Shirk

Kwa ujumla neno uumbaji lina maana mbili: i- Kukifanya kitu kiwepo kutokana na kutokuwepo. ii- Ukadiriaji. Linalochaguliwa hapa ni maana ya pili, kwani kukifanya kitu kiwepo kutokana na kutokuwepo ni iwapo tu hakuna mada yenye kubadilika, na lililothibiti ni kwamba kulikuwako na udongo, na alichokifanya Nabii Isa (a.s.) ni kukadiria udongo umbo la ndege, na jambo lililobakia ni kuligeuza lile umbile kuwa ndege, hakika kazi hiyo ni ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) iliyotimia kwa idhini yake. Hivyo mpaka hapa hakuna tendo lisilo la kawaida alilolifanya Isa (a.s.) yeye mwenyewe. Ama jawabu la swali hilo tunasema: Kwanza sisi hatukubali kuwa neno ”kwa idhini ya Allah” linarejea katika jambo la tatu, bali hutegemewa sana kuwa linarejea kwenye mambo yote matatu, na ushahidi wa hilo ni kwamba jambo la kwanza limewekewa sharti hilo katika Sura ya 6, pale Mwenyezi Mungu (s.w.t) aliposema: “Na unatengeneza kutokana na udongo umbile la ndege kwa idhini Yangu …” (5:110), na kwa hivyo haijulishi ibara ”kwa idhini yangu” kuwa mambo mawili ya kwanza ni kitendo cha Isa, na jambo la kwanza ni kitendo cha Mwenyezi Mungu, bali ni kwamba yote kwa upande mmoja ameyafanya yeye Isa na kwa upande mwingine kayafanya Mola Manani. Pili: Lau tutakubali hilo la uumbaji wa ndege, tutasema nini katika uponyaji ukoma na ufufuaji maiti ambayo ni miongoni mwa kazi za Mwenyezi Mungu (s.w.t) kama ilivyo kuufanya udongo ndege, kwani navyo Mwenyezi Mungu amevihusisha na Isa, akasema: “Naponya vipofu na ukoma na nafufua maiti kwa idhini ya Mola wangu” (3:49) Na mahala pengine ananasibisha vitendo hivyo kwa Isa (a.s.) kwa kumwambia: “Na unaponya vipofu na ukoma kwa idhini Yangu na 135


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 136

Tawhid na Shirk unapofufua maiti kwa idhini Yangu” (5:110) na wakati mwingine Mwenyezi Mungu (s.w.t) anaeleza kwamba miongoni mwa malaika kawapa uwezo huo, kuhusiana na Jibril (a.s.) anasema: “Mwenye nguvu sana” (62:5), yaani nguvu yake ya kielimu ni kubwa zaidi ya zote, hivyo anajua na anatenda62 na vipi asiwe mwenye nguvu ilihali kwa hakika aling’oa kijiji cha watu wa Lut akakinyanyua juu ya mbingu na kisha akakigeuza. Na miongoni mwa nguvu zake nyingi, ni ukelele wake kwa watu wa Thamud hadi walipoangamia.63 Na lau ikiwa mradi wa mwenye nguvu kubwa ni Jibril (a.s.), basi amesifiwa mahala pengine na Mwenyezi Mungu (s.w.t): “Mwenye nguvu, mwenye cheo na heshima …” (81:20) na hayo yote yamefanywa kutokana na nguvu na uwezo wa ghaib kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) juu ya ulimwengu. Na je! iko nguvu na uwezo wa ghaib zaidi ya huo ambao unathibitishwa na Qur’an tukufu kwa baadhi ya waja wa Mwenyezi Mungu (s.w.t) na Mawalii wake? Na ikiwa itikadi ya uwezo wa ghaib kwa kiumbe hulazimu kuitikadi kuwa ni mungu ingelilazimu wote hao kuwa miungu kwa mujibu wa Qur’an, bali hapana budi kusema kwamba hakika upatikanaji wa nguvu na uwezo huo wa ghaib ni jambo linalowezekana kwa watu – hata kwa wasio kuwa Mitume – kwa njia ya ibada. Ibada ambayo aghlabu ya watu hufikiria kwamba athari na matokeo yake huleta ridhaa ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) na kukinga ghadhabu zake tu, huipa roho uwezo mkubwa na upeo wa kina zaidi kushinda hilo, kwa hivyo ibada ina athari kubwa sana kiundani na kiroho. Kuachana na mambo ya haramu na yale ya makruhu kwa upande mmoja, na kujituma kuyatekeleza mambo ya wajibu na ya mustahabu kwa upande mwingine, kwa ikhlas kabisa, bila shaka kufanya hivyo kuna athari kubwa sana, aidha huikomaza roho na kuiandaa kuwa na uwezo makhsusi kuhusiana na yale yaliyo nje ya kanuni na mipango ya kimaumbile, kiasi kwam62. Majmaul-Bayan Juz. 5 Uk. 173. 63. Mafatihu-Ghaib Juz. 7 Uk. 702 cha Razi. 136


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 137

Tawhid na Shirk ba roho inakuwa chanzo cha matokeo yaliyo nje ya ada na kanuni. Na hilo ndilo lililoashiriwa na hadithi sahihi, kati ya hizo ni: Imepokewa katika hadithi Qudus Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema: “Hakuna kitu ambacho humkurubisha mja Kwangu kuliko yale niliyofaradhisha juu yake, hakika yeye anajiweka karibu Yangu kwa sunna mpaka nampenda, na ninapompenda nitakuwa masikio yake ambayo anasikilizia, macho yake ambayo huona kwayo, ulimi wake ambao hutamkia na mkono wake ambao hushikia.”64 Ukweli ni kwamba: Hakika nguvu na uwezo wa ghaib ambao Mwenyezi Mungu (s.w.t) amewapatia miongoni mwa waja wake wema ili kuendesha na kuutumia katika ulimwengu kwa idhini Yake na wafanye mambo kinyume na kawaida katika nyanja mbalimbali, uwezo huo haulazimu kuitakidi Uungu, na mwenye kuwa nao si mshirika wa Mwenyezi Mungu (s.w.t). Ni dhahiri shahiri kwamba kuitakidi kuwepo nguvu na uwezo wa ghaib (unaojitegemea) bila kupata usaidizi wowote kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t), inalazimu kuamini Uungu wa mwenye nao, na kuhusu jambo hilo Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema: “Na haiyumkini kwa 64. Usuul-Kafi Juz. 1 Uk. 302 amepokea hadithi hii kwa isnad sahihi na dhahiri ya hadithi kuhusiana na ibada huiumbia nafsi uwezo usiokuwa wa kawaida miongoni mwa yale yasiokanushwa, na muelekeo ni kwamba makusudio yake ni kwamba kitendo cha mja kinakuwa ni chenye kuhifadhika kwa ridhaa ya Mwenyezi Mungu, naye hafanyi wala haachi isipokuwa yale aliyoyaridhia, ni muelekeo wenye nguvu sana, kwa hakika mwendo kulingana na ridhaa yake huwa ni katika uhai wote, hadithi hii makhsusi kwa ajili ya kitendo cha kuswali swala za faradhi na sunna zake, bali hiyo ni kabla ya kila kitu, ni hadithi ya kuamini Mwenyezi Mungu, thawabu zake na adhabu zake, na sio kuzikabili faradhi na sunna zake, na ikiwa vitendo hivi vitakuwa na athari katika mwendo huo, basi vilevile iwe kwa funga, hija na jihadi, lakini ni kwa nini hakuitaja. Jua kwamba hakika swala ya faradhi na sunna yake zina athari katika kutia nguvu nafsi na roho na kuinyanyua hadi binadamu huweza kwazo kuwa dhihirisho la Mwenyezi Mungu katika uonaji wake na usikiaji wake, nguvu yake na uzungumzaji wake, basi huona kwa uoni wake na husikia kwa usikiaji wake, ambalo halioni wala halisikii mwingine. 137


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 138

Tawhid na Shirk mtume kuleta muujiza isipokuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu …” (13:38).

MAELEZO MENGINE YA MAWDUDI: Mawdudi katika kueleza itikadi za Waarabu wa zama za ujinga anasema: “Itikadi zao kuhusu miungu yao zilikuwa kwamba hiyo miungu ina uwezo na mafungamano ya kufanya mambo ya kiungu na Mungu aliyetukuka, na maombi yao yanakubaliwa, aidha mambo yao hayamfikii Mungu aliyetukuka isipokuwa hupitia kwao, huwanufaisha na kuwaepusha na madhara kwa kuwaomba hao.”65 Na kuhusu ibara hii: “Miungu yao ina uwezo na maingiliano na Mungu wa juu aliyetukuka” inahitaji ufafanuzi, kwani kitendo cha mtu mwingine kuingilia katika mambo ya Mola Subhanahu wa Ta’ala kina aina mbili: Mosi: Iwe hiyo miungu inafanya vitendo vyao na amali zao katika hali ya kujitegemea, na hilo hulazimu Shirki na mwenye kuingilia hujifanya mungu na kumwelekea mtu huyo ni kumwabudu. Pili: Uingiliaji kati na utekelezaji kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) pamoja na amri yake, uingiliaji huo hatukubali ubatili wake na itikadi hiyo sio Shirki pia uombaji huo si ibada, vipi iwe ni Shirki ilihali Qur’an inaeleza kinaga ubaga kwamba Malaika (a.s.) hupanga mambo ya ulimwengu, inasema: “Na wale wenye kupanga mambo” (79:5) Na hakika hao hutoa roho na waliangamiza nyumati zilizotangulia, pale Qur’an inaponukuu maneno ya Malaika (a.s.): “Hakika sisi tumetumwa kwa watu wa Lut …” (11:70) “Na amri yetu ilipofika tukapindua chini juu na tukawapelekea mvua ya mawe …” (11:82) 65. Muswtalahat Arba'at Uk. 19. 138


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 139

Tawhid na Shirk Sisi tunazingatia na kuamini kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t) Yeye ndiye mtendaji, lakini wanaotekeleza moja kwa moja uangamizaji ni Malaika (a.s.), kwa hivyo hakuna kigezo na sababu ya kupelekea kubadili neno uingiliaji na kuweka neno Taf’wiidhi na mengineyo ambayo kwa njia moja au nyingine humaanisha kutenda kwa kujitegemea na bila idhini na msaada wa Mwenyezi Mungu. Ama kuhusu yale yaliyonakiliwa kutoka kwao kwamba wanaitakidi kuhusu miungu yao kwamba ”mambo yao hutimia kupitia kwao, huwapa manufaa na huwakinga na madhara pindi wanapoiomba hiyo”, ibara hiyo ina mapungufu mengi.66 Kwa hakika wakiwa wanakusudia kunufaishwa akhera na kukingwa na adhabu ya akhera, jua haifai kumuomba asiyekuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t), na huo unakuwa mfano wa waabudu masanamu wa zama za ujinga, kwani Qur’an inaeleza bayana, hapana shaka dua ya Mtume (s.a.w.w) kwa mtekelezaji wa zaka hulazimu kupatikana utulivu kwao, na huondoa hali yao ya hofu na wasiwasi, Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema: “Hakika maombi yako ni utulivu kwao…” (9:103), kama ilivyo istighfari ya Mtume (s.a.w.w) husababisha watu kusamehewa dhambi zao, Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema: 66. Kuongezea hayo: Hakika Waarabu wa jahilia walikuwa wakiyaomba masanamu yao manufaa na kinga ya madhara na kuamini kuwa ni miungu, na hayo yalitokana na chimbuko la kauli ya kuamini uungu wao, na kwa ajili hiyo yakahesabika matendo yao kuwa ni shirki, kuna tofauti kubwa kati ya kuomba kinga ya madhara na kuomba shufaa kutoka kwa yale ambaye ni mja mwenye karama anayetoa shufaa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na baina ya yule anayezingatiwa kuwa yeye ni mungu mwabudiwa na anayejitegemea katika kitendo chake, na kwa hivyo hakuna tofauti sawa iwe madhara ya kidunia au ya akhera, ni kwamba hilo linafaa kwa yule wa kwanza, na halifai kwa huyu wa pili. Ilipasa Ustadh ajikite katika utafiti wa je juu ya itikadi ya muombaji juu ya mwenye kumuomba amletee manufaa na amkinge na madhara, je! anaitakidi uungu wa muombwaji na kujitegemea kwake katika kuleta manufaa na kukinga madhara? au anaitakidi uumbe wake na kwamba yeye haleti manufaa wala hakingi madhara isipokuwa kwa idhini ya Allah, inampasa kujikita juu ya hili na sio katika utofautishaji baina ya madhara ya kidunia na ya akhera. 139


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 140

Tawhid na Shirk

“Na lau wao walipodhulumu nafsi zao wakakujia wakamuomba msamaha Mwenyezi Mungu na Mtume akawaombea msamaha wangelimkuta Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe Mwenye huruma.” (4:64) Kama ilivyokuwa dua ya Nabii Yakub (a.s.) ni sababu ya kusamehewa dhambi za wanawe waliposema: “Ewe baba yetu tusamehe dhambi zetu” Nabii Yakub (a.s.) akawajibu: “Nitakuombeeni msamaha kwa Mwenyezi Mungu.” (12:98) Na hiyo inabainisha faida ya uombaji wake wa msamaha, bila hivyo isingelifaa na asingwaahidi kuwaombea. Na hivyo inajuzu kumuomba Mtume du, na msamaha, nayo ni kumwomba manufaa ya Akhera. Ni manufaa gani unayoyaona yanafaa zaidi kuliko ya Akhera, na ukingaji madhara gani unaoshinda dua ya Mtume (s.a.w.w) kuepusha adhabu ya Mwenyezi Mungu? na lau mtu atamuomba Mtume (s.a.w.w) amuombee dua na msamaha ili apate manufaa na aepukane na madhara, kisha Mtume (s.a.w.w) akafanya hivyo, hiyo sio Shirki na wala si kumwabudu Mtume (s.a.w.w). Je! baada ya mifano hiyo ya wazi yupo anayeamini kwamba kuamini kwamba dua ya Mtume (s.a.w.w) na Walii ina athari katika kuleta manufaa na kukinga madhara ya akhera ni Shirki, ilihali Qur’an inaeleza hilo kinaga ubaga juu ya mashahidi. Na hakika ikiwa makusudio ya kunufaisha na kudhuru – katika maneno yake – ni manufaa na madhara ya kidunia, na kwamba kuwaomba hao inalazimu Shirki, hiyo si kweli kwani Qur’an imekiri kutokea kwa hilo sembuse kuwezekana kwake! 140


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 141

Tawhid na Shirk Hakika watu wa Nabii Musa (a.s.) – walimuomba mvua – na wao bila shaka walimuomba yeye manufaa ya kidunia na wala Nabii Musa (a.s.) hakuwakemea kwa hilo, bali aliwaombea mvua kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) na mvua ikanyesha wakati huo huo. Qur’an tukufu inatoa ishara juu ya jambo hilo inasema: “Kumbuka watu wa Musa walipomuomba mvua” (2:60), kama vile walivyomuomba yeye awaletee neema za mbinguni na hakuwakemea kuhusiana na hilo bali aliwaombea. Na hakika watu wa Firaun walimuomba Nabii Musa (a.s.) awaondolee adhabu ya dunia iliyotajwa kabla na Aya ifuatayo: “Na ilipowaangukia adhabu, wakasema: Ewe Musa! Tuombee kwa Mola wako yale aliyokuahidi …” (7:134) Yote hayo yanajulisha kwamba kumuomba asiyekuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) manufaa na kukingwa na madhara ya kidunia ni jambo linalofaa, na kama isingelikuwa hivyo bila shaka Mtume angewakemea katika mambo yote hayo, na kuwaeleza kwamba wamuelekee Mwenyezi Mungu (s.w.t) na wamuombe Yeye moja kwa moja wala wasimuombe yeye, kwani yeye ni kiumbe miongoni mwa viumbe wa Mwenyezi Mungu (s.w.t) na mja katika waja wake. Na hapana shaka Nabii Musa (a.s.) alihusika katika upatikanaji wa manufaa ya kidunia, vivyo hivyo katika ukingaji wa madhara. Basi ni wajibu kwa Ustaadh ayawekee sharti maneno yake wala asiyaache hivi hivi katika suala la kuzuia manufaa na kukinga madhara, angesema: ”Kwa kujitegemea kiasi kwamba muombwa anakuwa ni mwenye kujitegemea katika hilo”. Na katika kufupisha maneno tunasema: Yafaa ieleweke kwamba utatuzi wa mas’ala haya ni kufarikisha baina ya uwezo wenye kutegemea utashi wa Mwenyezi Mungu (s.w.t) pamoja na idhini Yake, na uwezo wenye kujitegemea, wala tusichanganye kati ya hayo mawili.

141


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 142

Tawhid na Shirk HITIMISHO Hakika zipo nadharia mbalimbali kuhusiana na chimbuko la Miujiza kutoka kwa waja wema wa Mwenyezi Mungu (s.w.t) katika kauli nne: Yale wanayoamini Maghulat na Mufawidha kwamba hao wanajitegemea katika uumbaji na kuleta uhai (kuhuisha) na kifo (kufisha). Hakika Mwenyezi Mungu (s.w.t) ndiye ambaye huleta mambo hayo kwa utashi wao. Tuliyoyadhihirisha kutokana na Aya mbalimbali kwamba kitendo kinahusishwa na wao kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) na ukadiriaji wake. Nadharia ya ufanyaji wa vitu, zimepokewa hadithi chungu nzima achilia mbali zile tulizozieleza na kuzitolea ishara juu ya hilo, wala hakuna mgongano kati ya nadharia tatu za mwisho, kwani haishindikani kuzikusanya na kuwa kitu kimoja. Nadharia ya mwisho imejengwa juu ya hisia na utambuzi katika viumbe wote, na hilo tumelibainisha kwa dalili zake katika somo la tatu. Na vilivyomo ulimwenguni hufuata amri ya Mtume (s.a.w.w) anapoamrisha kitu fulani, na hilo linaungwa mkono na Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema: “Basi tukautiisha upepo ukaenda pole pole kwa amri yake anakotaka kufika.� (38:36). 2. JE! SABABU YA KAWAIDA NA ISIYO YA KAWAIDA NI KIGEZO CHA TAWHIID NA SHIRKI? Masufi na Madaruweshi katika kuwasifu Masheikh wao pamoja na taratibu zao hufikia kiwango cha Shirki kama hilo lilivyo dhahiri, na kwa hivyo hupituka mipaka ya Tawhiid na kuingia katika Shirki, na hilo limedhihiri142


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 143

Tawhid na Shirk ka kutokana na beti ambazo zinawasifu Masheikh wao hali ya kuvuka mipaka na kuwa na harufu ya Shirki ya waziwazi achilia mbali ile ya ndani. Beti hizo zinapingana kabisa na misingi ya Tawhiid iliyoelezwa na Qur’an, hata kama baadhi yao wanajaribu kuziepusha na Shirki, lakini ukweli ni kwamba mwenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu (s.w.t) haifai kuzikumbatia beti hizo na maneno yao, bali hairuhusiwi kisheria kutamka na wala mtu kupitiwa ulimini mwake maneno ambayo yanapingana na Tawhiid ya kiislamu ambayo huambatana na Qur’an tukufu. Hakika kundi hili lilikuwa na mtazamo maalum kuhusiana na dhana ya Shirki na fikra potovu, kwani zipo aina nyingi za Shirki wao huziona ndiyo Tawhiid halisi!! Na kwa hivyo wakalifanya suala la Shirki kuwa dogo na kulibana mno!! Na kinachoshabihiana na kikundi hicho ni kikundi cha Mawahabi, wao wamepanua zaidi wigo na uhakika wa Shirki, hadi kujumuisha kila harakati na shughuli na kila jambo linalotoka kwa wanatawhiid na Mawalii wa Mwenyezi Mungu (s.w.t) kwa lengo la kuwaheshimu, Mawahabi huona ni Shirki, na mtendaji wa hayo humwita ni mshirikina, hata kunifanya mimi nikutane na kamati ya kuamrisha mema ndani ya msikiti mtukufu wa Makka (Masjidul – Haram) na mimi niliinamisha kidogo kichwa changu – wakati wa kukutana – ghafla mtu mmoja kwa hali ya kuudhika akasema: Usifanye hivyo … ni Shirki, akimaanisha kwamba usiinamishe kichwa chako, jambo hilo ni Shirki!! na ukweli ulivyo ni kwamba lau ingelikuwa maana ya Shirki na Tawhiid ni kama waonavyo Mawahabi na wasemavyo, isingewezekana kumruhusu yeyote ulimwenguni mwenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu (s.w.t) kamwe kuwa na sifa hiyo ya Tawhiid. Mmoja kati ya rafiki zangu ambaye ni mwaminifu amenieleza kwamba Imam wa msikiti wa Mtume (s.a.w.w) na khatibu wake sheikh Abdul- Aziz alikuwa anasema kuhusu maana ya Shirki: “Hakika kila jambo lisilomhusu Mwenyezi Mungu (s.w.t) ni Shirki!”

143


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 144

Tawhid na Shirk Nasema: Lau ingelikuwa maana ya Shirki ni kama wasemavyo Mawahabi hapana budi kuwaona watu wote hapa duniani ni washirikina, bila kuwatoa baadhi hata Mawahabi wenyewe, kwa sababu wao huomba na mambo yao hupita kwa tawassuli na kupitia sababu fulani, na hatuwezi kusema hizo sababu ndiye Mwenyezi Mungu (s.w.t), bali hizo si Mwenyezi Mungu (s.w.t). Na kwa hivyo tunafaidika kwamba mambo na mahitaji yao yanafungamana na asiyekuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t), pamoja na hivyo mambo hayo na sababu hizo na zinazofanana na hizo sio tu kwamba sio Shirki, bali vilevile huhesabiwa kuwa ndio Tawhiid, kwani uhai wa mwanadamu hapa duniani hufungamana na sababu mbali mbali. Hatima ya mambo hayo mawili ni kutoitakidi kuwa sababu hizo zinajitegemea na wala hazina uhusiano wowote, utashi wowote na matakwa ya Mwenyezi Mungu (s.w.t), bali hana budi kuamini vina athari kutokana na utashi wa Mwenyezi Mungu (s.w.t). Ndio, mafungamano kati ya sababu na dhahiri ya mambo ya kimada huenda ikawa ni Tawhiid halisi kwa upande mwingine, na ni Shirki kwa upande mwingine, kwani wakati ambapo hatuamini kuwa sababu hizi zinajitegemea, pale ambapo hatuamini kwamba kuna kitu kinaathiri pasipo na utashi wa Mwenyezi Mungu (s.w.t), bali tunaitakidi kwamba vitu hupatikana katika mlolongo ambao huishia kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t), hapo huwa hatujatoka nje ya wigo wa Tawhiid, aidha sio katika fikra ya Tawhiid kuepukana na kigezo hicho, bali inabidi kuamini mfano wa kigezo hicho. Ama tutakapoona sababu hizi zinajitegemea, na kuaamini kwamba uwezo wa kuathiri kwake hauna uhusiano na Mwenyezi Mungu hapo tutakuwa tumetoka nje ya Tawhiidi kwa kuamini waumbaji wawili. Kwa hivyo mwenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu (s.w.t) ni lazima aihifadhi Tawhiidi yake kwa kubeba kigezo hicho, kwamba sababu zote hazijitegemei zenyewe katika kusababisha bali upatikanaji wake, uwepo wake na usababishaji wake vyote vinatokana na utashi wa Mwenyezi Mungu na Yeye ndio kikomo na chanzo cha sababu hizo. Mwanatawhiid 144


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 145

Tawhid na Shirk ijapokuwa kwamba anajua maisha haya, na anaamiliana nayo kwa msingi ya kwamba yako chini ya nidhamu ya sababu na msababishaji isipokuwa anatazama sababu hizi kwa msingi wa kwamba kuwepo kwake, kubakia kwake na athari yake ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t). Kwa mantiki hiyo sababu ya kwanza ni Mwenyezi Mungu (s.w.t), ama sababu zingine nazo zimeumbwa na Yeye, zinafuata utashi Wake unaotokana na matakwa Yake kwa marefu yake na wala sio kwa mapana yake. Hakika tofauti kubwa ya msingi kati ya Mwanatawhiid na mtu wa mada inatokana na jambo hili. Pili: Mshirikina anaamini asili ya sababu za kimaada na kujitegemea kwake katika kuathiri, wakati ambapo Mwanatawhiid hutegemeza na kuhusisha kila kitu kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) Mola muumba, pamoja na kukiri kwamba kanuni za sababu (sababu na kinachosababisha) hutawala ulimwengu huu.

USHUHUDA WA QUR’AN Hakika kadhia ya kujitegemea au kutojitegemea kwa sababu za kimaumbile ya kimaada hiyo ndiyo tofauti ya msingi kati ya Tawhiid na Shirki. Katika kulibainisha hilo, Qur’an tukufu imetoa ishara juu ya hilo katika Aya nyingi sana. Wapo baadhi ya watu ambao wanapokumbwa na matatizo magumu huchukua njia ya kumuelekea Mwenyezi Mungu (s.w.t) na kumuomba, na wanapookolewa hurejea tena katika ushirikina wao. Hiyo ni hali ya baadhi ya watu ambayo yaelezwa na baadhi ya Aya za Qur’an, na sisi tunazitaja baadhi ya Aya hizo, lakini la msingi kwetu ni kujua makusudio ya Shirki kama ifuatavyo:

145


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 146

Tawhid na Shirk “Watu wakipatwa na madhara humuomba Mola wao kwa kunyenyekea kisha anapowaonjesha rehema yake hapo baadhi yao mara humshirikisha Mola wao.” (30:33)

“Na wanapopanda katika Jahazi, humuomba Mwenyezi Mungu wakimtakasia utii, lakini anapowafikisha salama bara (nchi kavu), mara wanamshirikisha.” (29:65)

“Sema Mwenyezi Mungu hukuokoeni katika hayo na katika kila mashaka, kisha nyinyi mnamshirikisha.” (6:64)

“Kisha anapowaondoleeni dhara, mara kundi moja miongoni mwenu linamshirikisha Mola wao.” (16:54) Hizo ni baadhi ya Aya kuhusiana na kadhia hii na lililo la msingi ni kuzingatia kwa makini ibara isemayo “Pindi wao wanapofanya ushirikina”. Hakika inakusudiwa Shirki katika Aya hizo, sio tu wanapookolewa na kufika bara huendelea na ibada yao ya masanamu, bali makusudio makubwa zaidi ya hayo Ni kwamba wanapookolewa kutoka katika matatizo hurejea katika hali yao ya kabla wakazikumbatia sababu za kimaada wakidhani kuwa sababu hizo hujitegemea katika kurefusha uhai wao bila kupata msaada wowote kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t), na kuziona hizo ni sababu zenye kujitegemea na hazihitaji chochote kutoka kwa Mwenyezi 146


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 147

Tawhid na Shirk Mungu (s.w.t), bila shaka uangaliaji huo ni Shirki ambapo wanapaswa kuepukana nao, na huo ndio mhimili wa tofauti baina ya wenye imani ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) na wale wenye imani ya kimaada, na lau ungezama ndani ya Aya hizo zinazofungamana na suala la Shirki na Tawhiid bila shaka ungeona ni jinsi gani Qur’an tukufu imejikita zaidi katika kusisitiza kuwa katika ulimwengu huu hakuna uwezo sambamba na uwezo wa Mwenyezi Mungu (s.w.t) na wala hakuna utashi mkabala na utashi Wake. Qur’an inakuongoza katika hilo kwani inaitakidi kuwa Mola Manani (s.w.t) ndiye muongozaji katika giza la bara na baharini. Yeye hutuma upepo kama bishara njema toka kwake Yeye kwa rehema Zake, na huteremsha mvua, anasema:

“Au ni nani anayekuongozeni katika giza la bara na bahari, na ni nani azipelekaye pepo kutoa khabari njema kabla ya rehema zake? Je yuko mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Mwenyezi Mungu ametukuka juu ya wale wanaowashirikisha.” (27:63) Pamoja na kuwa kiumbe alikuwa hapo kabla na bado angali anaendelea kufaidika kwa baadhi za sababu na miundombinu ya kimaumbile kama vile nyota na sayari mbalimbali, aidha hupata uongofu au kuongoka na nyenzo zingine katika safari ya bara na baharini, hayo yote si kwa lolole isipokuwa kwa ajili ya msababishaji wa sababu hizo, naye si mwingine bali ni Mwenyezi Mungu (s.w.t). Kama vile upepo na mvua katika maumbile haya chanzo chake ni msururu mrefu wa sababu za kimaumbile ambazo husababisha kuwepo upepo au mvua, pamoja na hivyo Qur’an inasema: “Na yeye ndiye apelekaye pepo kuwa khabari njema kabla ya kufika rehema yake (mvua)...” (7:57) 147


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 148

Tawhid na Shirk aidha inasema: “Naye ndiye anayeteremsha mvua baada ya wao kukata tamaa, na kueneza rehema yake...” (42:28) Hiyo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu yuko nyuma ya sababu hizo, ambazo zinafanya kazi kwa amri Yake na kwa uwezo Wake. Kwa maneno mengine, hakika sababu hizo sio zenye kujitegemea, sio katika kuwepo kwake wala katika kuathiri kwake, bali vyote vimeumbwa, na kupatikana kwake kote na kuathiri kwake ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo Qur’an tukufu inaonesha kinaga ubaga kwamba Mola muumba ndiye mwongozaji katika giza la bara na baharini huleta Upepo na kuteremsha mvua baada ya kukata tamaa. Na hayo ndiyo ambayo yamewekwa bayana na Aya za Surat Waaqiati. Hilo linamaanisha kuwa si kwamba Qur’an tukufu inakanusha kuwepo kwa sababu za kimaumbile na kukanusha uingiliaji wake na kutupilia mbali mchango wake, bali ni kwamba sababu hizo hazina uwezo binafsi na kujitegemea zenyewe na kutohusika Mwenyezi Mungu (s.w.t) na chochote katika kazi zake, nafasi yake ilivyo ni kama vile maana ya herufi katika sentensi, kwani herufi haina maana ila itakapokuwa katika sentensi, na hilo limepelekea kwa upande mmoja kunasibisha dhahiri ya matukio ya kiulimwengu kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) na kwa upande mwingine kwa sababu, na upande wa tatu kwa vyote viwili, Mwenyezi Mungu (s.w.t) na sababu, Allah anasema: “Na hukutupa wakati ulipotupa lakini Mwenyezi Mungu ndiye aliyetupa.” (8:17) KUFANYA TAWASSULI KWA SABABU ZISIZOKUWA ZA KIMAUMBILE Mpaka hapa imebainika kwamba nadharia ya sababu za kimaumbile kwa kuzingatia kuwa sababu hizo sio zenye kujitegemea, bila shaka hiyo ni Tawhiid halisi, na kuzingatia kuwa zinajitegemea ni Shirki hasa. Na ama zisizo za kimaumbile miongoni mwa sababu hukumu yake ni ile ya 148


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 149

Tawhid na Shirk kimaumbile, kwani tawassuli inakuwa haifai iwapo itazingatiwa kwa kigezo cha mfano wa pili na hiyo ni Shirki halisi, ama kwa kigezo cha mfano wa kwanza hiyo ni Tawhiid halisi. Lakini Mawahabi wameifanya tawassuli iliyo nje ya sababu za kimaumbile kwamba imechanganyika pamoja na Shirki. Kuhusu hilo Mawdudi anasema: “Mathalani mtu anapopatwa na kiu akamwita mtumishi wake akamwamrisha amletee maji kitendo hicho hakiitwi dua wala hakimfanyi yule mtu kuwa ni Mungu wake. Na yote aliyoyafanya mtu huyo yako katika kanuni za sababu. Lakini atakapomuomba Walii katika hali hiyo, hapana shaka kumuomba yeye amuondolee matatizo yake kwa hakika amemfanya Mungu, kana kwamba amemuona msikivu na muoni na anadhani ana uwezo fulani kuwa ni muweza wa kumletea maji au ponyo kutokana na maradhi yake.” ”Kwa muhtasari hakika dhana ambayo inamfanya mtu amuombe Mungu msaada na kumnyenyekea, ni kule kumfanya Yeye ndiye mmiliki wa uwezo na mamlaka katika kanuni za kimaumbile, na ana nguvu zilizo nje ya wigo wa kanuni za kawaida.” Hakika mazungumzo kuhusiana na mada hii yako katika mambo mawili: La kwanza: Iwapo mtu anaitakidi kwamba dhahiri ya mambo fulani inasababu mbili, ya kimaumbile na isiyokuwa ya kimaumbile, anapokata tamaa na sababu ya kwanza na kuifuata ya pili je! hilo huhesabiwa ni Shirki au hapana? La pili: Iwapo ataitakidi kwamba mtu fulani ana uwezo wa ghaib katika ulimwengu huu na anafanya kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) je! itikadi hiyo huhesabiwa kuwa ni kuamini kuwa yeye ni mungu? Tumeshachunguza kauli inayohusu jambo la pili, na sasa tunatilia mkazo katika jambo la kwanza, tunasema: Mtu atakapoitakidi kuwa kuponya maradhi yake kuna njia mbili moja ni ya kawaida na nyingine isiyo ya kawaida, akatumia njia ya kwanza lakini hukufikia lengo lake, ama akaa149


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 150

Tawhid na Shirk mua (kutumia) kuchukua njia ya pili kama vile Nabii Isa (a.s.) kumpangusa kwa mkono wake je! itikadi hiyo humfanya awe mshirikina na kutoka katika mpaka wa Tawhiid au hapana? Na wewe utakapochunguza vigezo ambavyo unavifahamu katika kupambanua Shirki na lisilokuwa Shirki, utapata jibu kwamba hilo halipingani na Tawhiid bali linaambatana nayo, na yeye anaamini kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t) ndiye aliyeipa dawa athari ya kuponya, ndiye aliyeifanya asali iwe ni ponyo na ndiye aliyempa Isa (a.s.) uwezo wa kuponya wagonjwa kwa idhini yake (s.w.t) vipi (iwaje) itikadi hiyo ihesabiwe ni Shirki? Na kwa maneno mengine: Hakika Shirki ni kuamini kwamba kitu hiki kinajitegemea katika kuathiri, yaani athari yake inatokana nacho na wala sio kutoka kwa muumba wake, na ukweli wa hilo ni kinyume chake, sasa iweje iwe ni ushirikina? Na kutofautisha kati ya tawassuli ya kupitia sababu za kawaida na zisizokuwa za kawaida kwa kulifanya jambo la kwanza liafikiane na Tawhiidi bila ya la pili, ni tofauti isiyokuwa na mwelekeo wala kigezo, kwani kuinasibisha athari kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) katika hali ya kuathiri kwake kwa idhini ya Mola Subhaanah ni sawa sawa. Ndio, inawezekana mtu akamkosoa anayesema kuhusiana na sababu ya jambo, na akasema kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t) hakumpatia Walii uwezo maalum wa kuponya na kwamba hawezi kuponya, lakini hilo liko nje ya mada yetu. Hakika mada yetu imejikita katika kumaizi na kupambanua kati ya Shirki na lisilokuwa Shirki, sio kuthibitisha uwezo wa mtu na kutokuwa na uwezo. Nadhani wenye kusema kuwa itikadi hiyo na uombaji huo ni Shirki lau wangelizingatia kwa undani mada na mchakato wa upambanuzi na upembuzi yakinifu kuhusu vigezo vya Shirki na lisilokuwa Shirki, ingekuwa rahisi kwao kupambanua haki na isiyokuwa haki. Hivi kuna tofauti gani kati ya kuitakidi kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) ndiye aliyelifanya jua liangaze na moto uunguze, na akafanya asali iponye, na kwamba yeye ndiye aliyempatia Isa (a.s.) uwezo wa kuponya, au amezipatia roho takatifu za Mawalii wake uwezo wa kufanya baadhi ya mambo 150


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 151

Tawhid na Shirk hapa ulimwenguni, na ipo ndani ya Qur’an tukufu mifano hai kuhusu kupewa athari maalum kwa sababu zisizo za kawaida au za kimaumbile kama tulivyoeleza hapo kabla, na ufuatao ni ubainifu wake:1. Hakika Qur’an inaeleza ndama wa Samiriyi kwa kauli yake: “Akawatolea ndama kiwiliwili chenye sauti, na wakasema huyu ndiye Mungu wenu na Mungu wa Musa lakini alisahau.” (20:88) Baada ya Musa kurejea kutoka kwa Mola wake na akaona hali hiyo akamuuliza Samiriyi (Msamaria) juu ya amali yake hiyo, vipi aliweza kufanya kazi hiyo na nia yake ilikuwa nini? akajibu: “Akasema: Niliona wasiyoyaona na nikashika sehemu chache ya mwendo wa Mtume, kisha nikautupa, na hivyo ndivyo ilinielekeza nafsi yangu” (20:96), na akatoa sababu kuhusiana na amali yake hiyo kwamba alichukua sehemu ya athari ya Mtume akatumia kufanikisha yale aliyeomba, basi akawa ndama mwenye kutoa sauti. Na hilo linajulisha kuwa udongo uliochukuliwa kutoka katika athari ya Mtume ulikuwa na athari makhsusi na Saamiri alifanya tawassali kwayo. 2. Hakika Qur’an inaeleza namna alivyopona Nabii Yakub (a.s.) kutokana na matatizo ya macho yake, ikinukuu maneno ya Yusufu (a.s.) inasema:

“Nendeni na kanzu yangu hii na mumwekee usoni baba yangu, atakuwa mwenye kuona, na mniletee watu wenu wote wa nyumbani” (12: 93), na

151


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 152

Tawhid na Shirk

“Basi alipofika mtoaji wa habari njema, akaiweka (kanzu ya Yusuf) mbele ya uso wake mara aliona, akasema: Je! Sikuwaambieni, hakika mimi najua kwa Mwenyezi Mungu msiyoyajua” (12:96) Iwapo mtu ataitakidi kwamba aliyetengeneza kutokana na udongo uliyochukuliwa kutoka katika athari ya Mtume athari maalumu yenye kutoa sauti, au aliyeipa kanzu ya Yusufu (a.s.) athari ya ajabu ndiye aliyezipa sababu zingine zisizo za kimaumbile athari makhususi ambazo binadamu huzitumia na kufaidika kwazo katika mazingira maalum, Je! inajuzu kwetu kumtuhumu mwenye kuitakidi hivyo kuwa ni mshirikina? Na kuna tofauti gani kati ya alichokichukua Saamiry kutoka katika athari ya Mtume au kanzu ya Yusufu (a.s.) na sababu zinginezo pamoja na kwamba sababu zote si zilizozoweleka? Hakika kufanya tawassuli kwa roho takatifu na kutaka msaada kwa nafsi takatifu zilizo hai mbele ya Mwenyezi Mungu ni aina ya kushikamana na kufuata sababu, Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema: “Enyi mloamini! mcheni Mwenyezi Mungu na tafuteni njia ya kumfikia...” (5:35) Na ama utafiti kuhusu je roho na nafsi hizo zina uwezo wa kutoa msaada kwa mwombaji au hapana? hilo liko nje na maudhui yetu 3. JE! UHAI NA KIFO HUINGIA KATIKA DHANA YA TAWHIID NA SHIRKI? Hapana shaka kushirikiana na kupingana kati ya wanadamu ni jambo la kawaida katika maisha, na haikuwa historia ya binadamu isipokuwa ni matokeo ya juhudi za wanadamu wenyewe ambazo zimevumbua mahusiano na kusaidiana, maingiliano na jukumu la kubadilishana uzoefu na 152


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 153

Tawhid na Shirk kunufaika na uwezo walio nao. Qur’an tukufu inaeleza mifano mingi kuhusiana na kufaidishana kati ya binadamu, inasema:

“Na aliingia mjini wakati wenyeji wake walikuwa katika ghafla, na akakuta humo watu wawili wakipigana, huyu katika jamaa zake na huyu katika adui zake. ndipo Musa akampiga ngumi na akammaliza, akasema: “Hiki ni kitendo cha shetani yeye ni adui mpotezaji wa dhahiri.” (28:15) Kwa hiyo suala la binadamu kusaidiana kati yao ni jambo ambalo lenye kutokea maishani mwao, na inafaa kwa nyakati zote isipokuwa Mawahabi wana maelezo marefu kuhusu kikomo cha maumbile baina ya Tawhiid na Shirki, wanasema: Hakika kufanya tawassuli kwa Mtume na Mawalii ni jambo linalowahusu wakiwa hai na hairuhusiwi wanapofariki. Muhammad bin Abdul-Wahab anasema: “Na hilo linajuzu kuhusu jambo la dunia na akhera, kwenda kwa mtu mwema na kumwambia: Niombee mimi kwa Mwenyezi Mungu kama walivyokuwa masahaba wa Mtume (s.a.w.w) wakimuomba wakati wa uhai wake. Na ama baada ya kufariki haifai na hawakufanya hivyo, bali walimkemea aliyekusudia kumuomba Mwenyezi Mungu (s.w.t) katika kaburi lake sembuse kumuomba yeye mwenyewe.”67

67. Kashfu Irtiyaab Uk. 271 imenukuliwa kutoka kitabu Kashfu Shubuhat Uk. 70 chapa ya Misri mwandishi Muhammad bin Abdul-Wahab. 153


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 154

Tawhid na Shirk Hakika Tawhiid na Shirki huwa na vigezo mahsusi ambavyo hutofautiana kimoja na kingine, na Uislamu haukuacha kutuelezea vigezo na mipaka maalum ya kila kimoja. Na tumebainisha hayo huko nyuma na hatukuona kuwa miongoni mwa vigezo hivyo uhai na kifo kuwa ndio mipaka ya Tawhiid na Shirki, kwani kumuomba aliye hai pamoja na itikadi ya kwamba anajitegemea katika utoaji au kuathiri ni Shirki, na kuenea baina ya watu wenye akili kile kitendo cha kuwaomba walio hai si dalili ya usahihi wake iwapo tu uwombaji huo huambatana na itikadi ya kujitegemea kwa huyo anayeombwa. Kwa hivyo ombi la mfuasi wa Nabii Musa (a.s.) liliambatana na Tawhiid isipokuwa katika aina moja nayo ni: Iwapo ataitakidi kwamba Musa (a.s.) ni mwenye kujitegemea katika kuathiri hilo, na litafaa iwapo ataamini uwezo wa kuathiri wa Musa (a.s.) wakati wote una mafungamano na Mwenyezi Mungu (s.w.t). Hakika hali hiyo ndiyo iliyotumika katika kuziomba msaada roho takatifu kulingana na maelezo ya Qur’an na kama inavyoungwa mkono na elimu za kisasa, na iwapo mfuasi wa Musa (a.s.) atamuomba Nabii Musa (a.s.) msaada baada ya kutoka roho yake kwa itikadi hiyo hatokuwa amefanya Shirki, na wala hatokuwa amemfanya Musa (a.s.) kuwa mshirika wa Mwenyezi Mungu (s.w.t) katika dhati yake, sifa zake, vitendo vyake na katika ibada, na kwa uombaji huo hatakuwa amemwabudu Musa (a.s.). Na ama lau angelimuomba huku akiitakidi anajitegemea katika hilo na kwamba yeye ana uwezo wa kufanya hilo bila msaada wowote kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t), bila shaka atahesabiwa amefanya Shirki, na kulingana na itikadi hiyo atakuwa ameamini kuwa Musa (a.s.) ni mungu. Na ama uhai wa muombwaji na kifo chake kuathiri katika jambo hilo ni pale tu iwapo mwombaji atafanya hilo kwa kukusudia na sio kwa mzaha, na hilo halihusiani na mada yetu ya kuainisha ni ipi Tawhiid na ni ipi Shirki, na mada inayohusu kukusudia au mzaha haihusiani kabisa na maudhui yetu. 154


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 155

Tawhid na Shirk Na la kushangaza ni kule kuzingatia kuwa kuomba kupitia aliye hai na kuhitaji uombezi wake ni katika kumpwekesha Mwenyezi Mungu (s.w.t) na ni Tawhiid halisi, lakini kufanya hivyo akiwa mwombwaji ni mfu eti ni Shirki, na mfanyaji wa hilo ni wajibu atubishwe na kuuawa. Hakika Mawahabi wanakubali kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t) amewaruhusu waovu waende kwa Mtume (s.a.w.) na wamuombe ili awaombee msamaha kwa Mola Muweza, wanasema hilo kwa dhahiri ya Aya:

“Na hatukumpeleka mtume yeyote ila apate kutiiwa kwa amri ya Mwenyezi Mungu, na lau wangelikujia walipojidhulumu nafsi zao wakaomba msamaha kwa Mwenyezi Mungu, na mtume akawaombea msamaha, bila shaka wangelimkuta Mwenyezi Mungu, ni mwenye kupokea toba, mwenye kurehemu.” (4:64) Kama vile wanavyokubali kwamba watoto wa Nabii Yakub (a.s.) walimuomba baba yao awaombee msamaha kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t), wakasema:

“Wakasema: Ewe baba yetu! tuombee msamaha kwa dhambi zetu, hakika sisi tulikuwa wenye makosa akasema: Nitakuombeeni msamaha kwa Mola Wangu, kwani Yeye ndiye Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu” (12:97-98)

155


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 156

Tawhid na Shirk Lakini sehemu hizo mbili ni katika Tawhiid kwani walimuomba akiwa hai na ama kumuomba hilo baada ya kufariki kwake ni Shirki. Lakini mpendwa msomaji anajua kuwa ni hali moja mtu akiwa hai au amekufa, na kama ingelikuwa kufanya tawassuli wakiwa wamekufa haifai ingelifarikisha na kupambanua wakiwa hai tu sio baada ya kufariki kwao, na iwapo mtu atapinga dhana ya kumuomba maiti kwamba ni tendo la kipuuzi, na vile vile ni bidaa wala halijaelezwa katika sheria, tunajibu kwa kusema: Kwanza: Hakika tendo hilo litakuwa bidaa iwapo muombaji atalileta kwa anwani ya kuwa jambo limeelezwa na sheria, ama lau atalileta yeye mwenyewe bila kulinasibisha na sehemu basi halitahisabiwa kuwa ni bidaa au ni jambo ambalo limezushwa katika dini, kwani bidaa ni kuingiza jambo ambalo halina asili katika dini na kulifanya ni katika dini. Pili! Hakika mada yetu inahusiana na uchunguzi yakinifu baina ya Tawhiid na Shirki, na sio kwamba tendo hili lina faida au hapana, au ni bidaa au sio bidaa, yote hayo yako nje ya mada yetu. Aidha napenda kuongezea zaidi suala hilo hakika imethibiti kisheria kwamba kufanya tawassuli kupitia roho takatifu inafaa kwa dalili na akili zilizo wazi.68 Kwa hali yoyote ile haiwezekani kuzingatia kwamba kumuomba maiti ni Shirki, iweje Shirki ilhali haamini kuwa muombwa ana itegemea katika dhati yake, sifa zake na vitendo vyake, bali huhesabiwa ni kukiri kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t) ndiye anayestahili kuabudiwa, na kumwelekea Mtume au Walii ni katika kumtukuza na kumuheshimu tu, na sio lingine, na lau tutajisahaulisha kanuni hiyo basi kamwe asingelipatikana ardhini mwanatawhiid. Mpendwa msomaji, na yatakayofuata ni maelezo ya mwanafunzi wa Ibn Taimiyyah kuhusiana na maudhui hii, naye ni Ibnul-Qaim anasema: “Na miongoni mwa aina za Shirki ni kuomba wafu haja mbali mbali na kuwaelekea wao, na huo ni msingi wa Shirki ya ulimwengu, hakika maiti amali 68. Kashfu Irtiyaab Uk. 301 kwa kupata dalili zaidi. 156


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 157

Tawhid na Shirk zake zimeshakoma, hana uwezo wa kujipa manufaa na kujikinga na madhara.”69 Na dalili aliyoitaja haithibitishi kabisa madai yake kwani kauli yake: “Hakika maiti amali zake zimeshakoma” ni dalili ya kutofaidika kwa kumuomba maiti, na sio dalili kwamba kufanya jambo hilo ni Shirki au sio Shirki, naye hakutofautisha kati ya mambo mawili. Na la kushangaza katika maneno yake: “Wala hamiliki kujinufaisha kwa ajili ya nafsi yake wala kujikinga na madhara” wala hakuna tofauti kati ya aliye hai na aliye kufa, na mtu hamiliki kwa nafsi yake kujinufaisha na kujikinga na madhara bila idhini ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) na utashi wake, sawa yuko hai au amekufa, na kwa idhini na utashi wa Mwenyezi Mungu (s.w.t) maiti au mtu hai anamiliki kunufaisha na kudhuru. Na kutokana na hilo unabainika udhaifu wa yale aliyoyaeleza Ibnu Taimiyyah pale aliposema: ‘’Kila aliyempa Mtume sifa asiyostahiki au akamfanya mtu mwema kuwa ni mungu, kwa mfano mtu atakaposema: Ewe bwana wangu fulani ninusuru na nisaidie … huo ni upotovu na Shirki, na kwamba muombaji anatakiwa atubu, na asipotubu auawe.”70 Ikiwa kuziomba nafsi au roho takatifu au maiti kama wasemavyo Mawahabi inalazimu kuitakidi aina fulani ya uungu kwa roho hizo takatifu na wafu (maiti), kwa mantiki hiyo itawalazimu kuwa uombaji huo kwa mtu yeyote yule awe hai au mfu kwa kukusudia au kwa mzaha sio aina ya Tawhiid bali ni Shirki ya wazi. Wakati ambapo watu kuombana wao kwa wao au kumuomba mtu hai ni miongoni mwa mambo ya dharura na ya msingi katika maisha ya jamii ya wanadamu. Na ifuatayo ni mifano mingine kutokana na maneno ya Ibnu Taimiyyah kuhusiana na suala hili anasema: “Na wale ambao wanamuomba 69. Fat'hul-Majiid Uk. 68 chapa ya sita. 70. Fat'hul-Majiid Uk. 167. 157


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 158

Tawhid na Shirk Mwenyezi Mungu (s.w.t) pamoja na miungu mingine mfano wa Masihi, Malaika na Masanamu hawakuwa na itakidi kuwa ni waumbaji viumbe, au wanateremsha mvua isipokuwa walikuwa wakiabudu makaburi yao, au wakiabudu vinyago vinavyofanana na sura zao huku wakisema tunafanya hivi ili yatukurubishe kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) na hawa ndio waombezi wetu.71 Hakika kiyasi (ulinganishaji) wa kuwaomba Mawalii wa Mwenyezi Mungu (s.w.t) na yale waliyokuwa wakiyafanya Wakristo na waabudu masanamu ni kujiweka mbali na maudhui husika, kwani wakristo walikuwa wakiitakidi kuwa Isa (a.s.) ni mungu, na waabudu masanamu wakiamini masanamu yao yanamiliki uombezi, bali baadhi yao kama alivyonukuu Ibnu Hisham walikuwa wakiamini masanamu hayo yana uwezo wa kufanya mambo fulani katika ulimwengu na waletaji wa mvua, na kwa ajili ya itikadi hiyo maombi yao kwa Isa (a.s.) na masanamu ilikuwa ni ibada na kuwaabudu. Kwa hali hiyo ikawa uombaji umeambatana na itikadi ya kiungu wa mwombwaji bila shaka itakuwa ni Shirki, na ama uombaji kwa mtu hai au mfu ukiwa umeepukana na itikadi hiyo hautakuwa Shirki wala ibada, bali kutaka msaada kwa mja ni kwa kuwa tunajua kwamba mja hafanyi lolote isipokuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (s.w.t). Ndio, ni wajibu katika kutaka msaada kwa maiti (wafu) tujadili je kuna manufaa katika uombaji huu au hakuna manufaa, na sio kujadili je uombaji huo ni Shirki na ibada kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t), na mazungumzo yetu kwa sasa ni juu ya suala la pili na sio la kwanza. 4. JE! UWEZO NA KUTOKUWA NA UWEZO NI VIGEZO VYA TAWHIID NA SHIRKI? Huenda maneno ya Mawahabi yakaleta maana kuwa kipo kigezo kingine cha Shirki katika ibada nacho ni: “Uwezo wa muombwa katika kukidhi 71. Fat'hul-Majiid Uk. 167. 158


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 159

Tawhid na Shirk haja na kushindwa kwake.” Mtu atakapomuomba mwenziwe haja ambayo hana uwezo nayo isipokuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) jambo hilo na ombi hilo litahesabiwa kuwa ni ibada na Shirki. Kuhusiana na hilo Ibnu Taimiyyah anasema: “Yeyote atakayekwenda katika kaburi la Nabii au la mtu mwema na akamuomba haja yake, kwa mfano akamuomba amuondolee maradhi, amlipie deni lake au yanayofanana na hayo miongoni mwa mambo ambayo hana uwezo nayo ila Mwenyezi Mungu (s.w.t), hilo ni Shirki ya wazi ambayo inapaswa mtu ajiepushe nayo na atubishwe na asipotubu auawe.”72 Hakika katika ibara hii amefanya Shirki kuwa na kigezo kingine nacho ni uwezo wa muombwaji na kutoweza kwake kutekeleza ombi la muombaji, na kama kipimo kingekuwa ni hiki ingelipasa Ibnu Taimiyyah aongeze baada ya maneno yake: “Kaburi la Nabii au mtu mwema” sentensi nyingine nayo: ”au walii aliye hai,” ili ibainike kwamba kigezo ambacho amekitegemea hapa sio kifo au uhai wa muombwaji, bali ni uwezo wake wa kukidhi haja kama alivyofanya Swana’aniy ambaye ni mmoja wa watunzi wa kiwahabi aliposema: “Miongoni mwa wafu na watu hai,” na yafuatayo ni maneno ya Swana’aniy: “Kuwaomba viumbe hai msaada katika yale ambayo wana uwezo nayo ni jambo ambalo halikanushwi na yeyote; ama mazungumzo ni kuhusiana na wafu na wengineo miongoni mwa Mawalii, na kuwaomba wao haja katika mambo ambayo hawana uwezo nayo isipokuwa Mwenyezi Mungu aliyetukuka ikiwa ni pamoja na kumpa afya mgonjwa na mengineyo. Ummu Salama alisema: ’Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu muombee Anasi mtumishi wako kwa Mwenyezi Mungu.’ Na Masahaba walikuwa wakimuomba Mtume (s.a.w.w) awaombee dua na hali akiwa hai, na jambo hili halina utata kwa yeyote na limeruhusiwa pia, na utata ni kuhusu kuwaomba wafu wa makaburini au walio hai ili wawaponye wagonjwa wao na kurejesha walio mbali na yanayofanana na hayo miongoni mwa maombi ambayo 72. Ziyaratu-Qubuur wal-Istighathat bil-Qubuur Uk. 156 Wasail Sunna Uk. 40 na Kashfu Irtiyaab. 159


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 160

Tawhid na Shirk hayawezi kuyatekeleza yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t).”73 Hivyo ndivyo tunavyojua kigezo cha jambo hilo sasa ni tofauti na kile kilichotangulia. Katika maudhui iliyokwishatangulia kigezo kilikuwa ni uhai na kifo kwa muombwa wala haikuwa kumuomba aliye hai ni Shirki, bali kumuomba mfu ndio ilikuwa Shirki. Ama katika maudhui hii ya sasa imefanywa au imejaaliwa kwamba uwezo wa muombaji katika kukidhi haja aliyoombwa, au kutoweza kwake kufanya hivyo kuwa ni mzani na kigezo cha Tawhiid na Shirki, na lau mtu ataomba haja kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) na haja hiyo ni katika mambo ambayo yako nje ya uwezo wa muombwa ambaye si Mwenyezi Mungu (s.w.t), hakika hilo huzingatiwa ni Shirki bila kujali yu hai au mfu, kwa hivyo hakuna tofauti ya muombwaji aliye hai na mfu.

MJADALA KUHUSU MAONI HAYA Na ukweli ni kwamba maoni haya ni dhaifu sana wala hayahitaji kujadiliwa na kukosolewa, ni kwa sababu uwezo wa muombwaji au kutokuwa na uwezo huwa ni kigezo cha je jambo hilo la kumwomba asiye na uwezo wa kukidhi maombi linaingia akilini au haliingii akilini, wala sio kigezo cha kutenganisha Tawhiid na Shirki. Kwa mfano aliyetumbukia kisimani lau ataomba au kutafuta msaada kwa mawe na majabali yaliyozunguka kisimani, hilo kwa mtazamo wa wenye akili huhesabiwa ni upuuzi kwa nadharia. Ama lau ataomba msaada kwa mtu aliyesimama kandokando mwa kisima mwenye uwezo wa kumuokoa yeye, ombi lake hilo litakuwa ni tendo linaloingia akilini. Na dhana yenye nguvu ni kwamba makusudio ya Mawahabi katika maneno yao: “Miongoni mwa mambo ambayo hawezi yeyote kuyafanya isipokuwa Mwenyezi Mungu aliyetukuka’’ sio kutofautisha baina ya muweza na asiyeweza, na kwamba kumuomba haja asiyeweza kukidhi ni Shirki ama kumwomba anayeweza si Shirki, ijapokuwa hayo ndio yanayodhihiri katika maneno yao, bali makusudio ya sentensi zao ni kutofautisha kati ya 73. Kashif Irtiyab Uk. 272. 160


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 161

Tawhid na Shirk kuomba yale ambayo ni katika matendo ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) na yale ambayo hayako katika vitendo vya Mwenyezi Mungu (s.w.t), hivyo matokeo ni kwamba iwapo mtu atamuomba asiyekuwa Mwenyezi Mungu yale ambayo ni katika matendo ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) anakuwa amefanya Shirki. Hayo ni kulingana na ibara ya Ibnu Taimiyyah pale aliposema: “Anamuomba amuondolee maradhi yake, amkidhie deni lake na mfano wa hayo, ni miongoni mwa mambo ambayo hana uwezo nayo isipokuwa Mwenyezi Mungu.” Na mfano wa hayo ni ibara ya Swana’aniy aliposema: “Ikiwa ni pamoja na mgonjwa kupata afya na mengineyo …” Na hapana shaka kumwomba mwingine yale ambayo yanatokana na kitendo cha Mwenyezi Mungu (s.w.t) hiyo ni aina ya Shirki, na muombaji huhesabiwa amemwabudu yeye, na tendo lake hilo huwa ni ibada, na ubainifu wa aina hiyo ya Shirki umeshakwisha kutangulia huko nyuma katika maelezo yanayohusu maana ya tatu ya ibada. Sisi pamoja na waislamu wote tunakubaliana nao katika msingi huo, isipokuwa maelezo yote yanahusu uchanganuaji wa je ni yapi yale ambayo huhesabiwa kuwa ni katika vitendo vya Mwenyezi Mungu (s.w.t), na ni yapi yale ambayo huhesabiwa kuwa ni katika vitendo vya mwingine asiyekuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t), na hakika Ibnu Taimiyyah amekubali na kukiri kwamba kumponya mgonjwa, kumkidhia haja, na kumlipia deni mtu kwa ujumla ni katika matendo ya Mola manani (s.w.t), na hayo haifai kabisa kumuomba mwingine (yeyote) asiyekuwa Mwenyezi Mungu aliyetukuka. Lakini ukweli ni kwamba hakika mambo hayo yote siyo katika vitendo vya Mwenyezi Mungu (s.w.t) moja kwa moja, bali kuna baadhi ya vitendo mahsusi huhesabiwa ni vya Mola Manani pekee, kama vile kukidhi haja ya mwombaji moja kwa moja kwa kujitegemea na bila kumtumia yeyote. Ama sehemu ambazo yule asiyekuwa Yeye anafanya kwa idhini Yake na ukadiriaji Wake hapo haihesabiwi kuwa ni vitendo Vyake mahsusi. Kwa ajili hiyo lau mtu atamuomba baadhi ya mambo mwingine asiyekuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) huku akiamini kuwa muombwaji hufanya hayo kwa kutegemea uwezo wa Mwenyezi Mungu (s.w.t) na kwa idhini na ruhu161


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 162

Tawhid na Shirk sa Yake haitokuwa Shirki. Vipi isiwe hivyo, ilihali hakika Qur’an tukufu imenasibisha uponyaji wagonjwa, vipofu na wenye ukoma kwa Nabii Isa (a.s.) kwa idhini ya Mola Manani pale aliposema: “Na ulipowaponyesha vipofu na wenye ukoma kwa idhini Yangu” (5:110) Kama vile Qur’an ilivyonasibisha uumbaji, uendeshaji ulimwengu, kuhuisha, kufisha na kutoa riziki kwa waja wake wengi, pamoja na hivyo wala hapana shaka ni miongoni mwa vitendo vya dhahiri vya Mwenyezi Mungu (s.w.t). Hivyo ni wajibu kwa Ibnu Taimiyyah na wafuasi wake kudurusu vyema vitendo vya Mwenyezi Mungu na kuvipambanua na vitendo vya wengine kwanza, kwani ndio utatuzi wa matatizo haya, bali ndio ufunguo na njia ya kutatua hitilafu zote katika dhahiri za Aya ambazo dhahiri zinaonekana zinapingana na Aya zingine katika kunasibisha vitendo hivyo kwa Mwenyezi Mungu. Na kwa hiyo kuomba kuondolewa maradhi, kumrejesha aliyepotea na yanayofanana na hayo huwa katika aina mbili: Ya kwanza: Inamhusu Mola Manani pekee na haifai kumuomba asiyekuwa Yeye, la sivyo muombaji atahesabiwa kuwa mshirikina na mwenye kumwabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t). Ya pili: Inafaa kumuomba asiyekuwa Yeye (s.w.t) na mwombaji hahesabiwi kuwa ni mshirikina, na maombi yake hayazingatiwi kuwa ni katika kumwabudu asiyekuwa Mola Muumba. Na ama je mwenye kuombwa na kutakiwa msaada ana uwezo wa kutekeleza na kukidhi haja au hapana? Na je! Mwenyezi Mungu (s.w.t) amemwezesha juu ya hilo au la? Hayo yako nje ya maudhui yetu.

162


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 163

Tawhid na Shirk 5. JE! KUOMBA MAMBO YASIYO YA KAWAIDA NI SHIRKI? Hapana shaka kwamba kila jambo lililopo lina kanuni na sababu yake kwani bila sababu jambo haliwezi kutokea, na kila jambo au kitu kina mafungamano na kitu kingine, na kila tukio lina chanzo chake na kitu kilichosababisha kitokee. Vivyo hivyo; miujiza ya Mitume na karama za Mawalii haziko nje na utaratibu huu, hayawezi kutokea bila sababu, lakini sababu yake sio ya kawaida na ya kimaumbile, na hiyo haina maana kwamba hutokea bila sababu yeyote. Inapobadilika fimbo ya Musa (a.s.) na kuwa nyoka anayetembea huku na kule na kumeza vijinyoka vidogo, inaporudi roho katika kiwiliwili kilicho maiti katika muujiza wa Nabii Isa (a.s.), na unapopasuka mwenzi pande mbili katika muujiza wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), au kuzungumza na fimbo yake na mengineyo, haina maana kwamba matukio hayo hayana sababu kama matukio mengine ya kiulimwengu, bali hufungamana na sababu mahsusi zisizo za maumbile na zisizo za kawaida na zisizozoeleka. Na lau binadamu atamuomba haja binadamu mwingine kulingana na sababu za kawaida atakuwa amefuata kanuni iliyozoeleka kwa watu wenye akili, hivyo hakika mjadala ni kuhusiana na kuomba kukidhiwa haja kwa njia za ghaib na sababu zisizo za kawaida, hilo ndilo ambalo hudhaniwa kuwa ni Shirki, na kwa hilo Mawdudi amesema: �Lau mtu ataomba haja au jambo fulani kisha akapatiwa au kukidhiwa haja yake bila kupitia sababu za kawaida ambazo ziko nje ya taratibu na mipangilio ya kilimwengu atakuwa amefanya Shirki na hilo hulazimu kuitakidi kwamba muombwaji ni mungu.�74 Isipokuwa ni kwamba ufafanuzi hatuwezi kuutegemea kwani ni ada iliyozoeleka kupitia nyendo za wenye akili kwamba wao huomba waletewe muujiza na mambo ambayo sio ya kawaida toka kwa yule anayedai unabii, 74. Muswtalahat Arba'at Uk. 14. 163


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 164

Tawhid na Shirk ili muujiza huo wautumie kuthibitisha unabii wake. Qur’an imenukuu nyendo za wenye akili kutoka kwa wale ambao waliishi katika zama za Mitume bila kuleta upinzani wowote na wala Mwenyezi Mungu (s.w.t) kulikosoa hilo, anasema: “Akasema kama umekuja na hoja basi ilete ukiwa ni miongoni mwa wasemao kweli” (7:106) Na walikuwa Mitume wakiwaita watu ili washuhudie yale waliyokuwa wakiyafanya ambayo sio ya kawaida, kwa hivyo iwapo mtu atamuomba Mtume amletee muujiza ili amkubali na asadikishe madai yake ya utume kwa kuponywa maradhi yake, au upofu na ukoma kama walivyomuomba Nabii Isa (a.s.) awaponye kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (s.w.t),75 kwa hakika mtu mwenye kufanya hivyo hawi mshirikina, na vivyo hivyo atakapomuomba baada ya kunyanyuliwa na Mwenyezi Mungu (s.w.t). Wala hatuwezi kutenganisha kati ya sura mbili kwa kuizingatia sura ya kwanza kuwa ni Tawhiid na ya pili kuwa ni kitendo chenye Shirki. Napenda kuongezea kwamba Wana wa Israil walimuomba Musa (a.s.) maji na mvua ili awaokoe kutokana na kiu chao, Qur’an tukufu inasema:

“Tukampa ufunuo Musa, walipomuomba maji watu wake kuwa; piga jiwe kwa fimbo yako, mara zikabubujika chemchem kumi na mbili, na kila watu wakajua mahala pao pa kunywea, na tukawafunika kivuli kwa mawingu na tukawateremshia manna na salwa; kuleni katika vitu vizuri tulivyokupeni, wala hawakutudhulumu sisi, bali walikuwa 75. Kwa kupata miujiza zaidi rejea Sura 3 aya 249 na Sura 5 aya 110. 164


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 165

Tawhid na Shirk wamejidhulumu wenyewe.” (7:160) Na Nabii Suleimani (a.s.) aliomba atakayemletea kiti cha Mfalme wa Sabai ambaye alikuwa mwanamke akiwaongoza watu wake, Mwenyezi Mungu (s.w.t) anaelezea hilo kwa kusema:

“(Suleiman) akasema: Enyi wakuu wa baraza! ni nani atakayeniletea kiti chake cha enzi kabla hawajafika kwangu, hali ya kuwa wamekwisha kusilimu? Akasema Ifriti katika majini: Mimi nitakuletea hicho kabla hujasimama kutoka mahala pako, na mimi bila shaka ninazo nguvu za hayo na mwaminifu.” (27:38–39) Na lau ingelikuwa kuomba mambo ambayo sio ya kawaida kwa mwingine asiyekuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) kuwa ni Shirki iweje Wana wa Israil wamuombe Nabii wao Musa (a.s.), vivyo hivyo Nabii Suleimani (a.s.) kuomba aletewe kiti cha Mfalme kilichopo mbali? Yote hayo yanatoa taswira na kuashiria kuomba kitu au jambo ambalo sio la kawaida na lililo nje ya njia na kanuni za kimaumbile sio kigezo cha Shirki, kama vile ambavyo uhai na kifo sio kigezo cha Shirki. Haiwezekani kusemwa kwamba kuomba jambo au kitu ambacho kisicho cha kawaida imeruhusiwa kwa aliye hai tu na sio kwa mfu, na kwa ajili hiyo tulitilia mkazo zaidi katika kigezo cha Tawhiid na Shirki. Na kufikiri kuwa kuomba mambo ambayo sio ya kawaida hulazimu kuitakidi kwamba mhusika ana uwezo wa ghaib, na mwenye uwezo wa ghaibu ni Mwenyezi Mungu (s.w.t) tu! jawabu la hilo umeshakwishalipata katika maudhui inayohusiana na jambo hilo. 165


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 166

Tawhid na Shirk Na wazo la kwamba mtu kuomba ponyo na kuomba deni lake litatuliwe ni kumwomba asiyekuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) atende kitendo makhsusi cha Mwenyezi Mungu (s.w.t), hilo limeshakwisha kujibiwa huko nyuma pale ulipofahamishwa kwamba kigezo cha kumaizi kitendo cha Mwenyezi Mungu (s.w.t) na kile kisichokuwa Chake si kitendo kuwa nje ya mipaka, kanuni na taratibu za kawaida za ulimwenguni, hata iwe kuomba kitendo mfano wa hicho toka kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) ni kumwomba asiyekuwa Mwenyezi Mungu kazi ya Mwenyezi Mungu (s.w.t). Bali kigezo katika kazi na matendo ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) ni mtendaji kujitegemea katika uumbaji na uletaji wa vitu, na asipate msaada wowote ule kutoka kwa asiyekuwa Yeye, sawa jambo hilo liwe ni la kawaida au sio la kawaida. Ni wajibu kwa kila mtafuta haki na ukweli asome kwa makini vitendo vya Mwenyezi Mungu (s.w.t) na vitendo vya wengine kwa undani kulingana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu (s.w.t), Sunna na akili sahihi. Na kwa maneno mengine: Sio kila kitendo kisicho cha kawaida sio cha binadamu, na kila kitendo kinachotokea kisicho cha kawaida ni cha Mwenyezi Mungu (s.w.t), bali viko baadhi huhesabiwa ni vya Mwenyezi Mungu (s.w.t) hivyo haifai kuombwa mwingine; liwe ni jambo la kawaida au lisilo la kawaida, na vingine huhesabiwa ni kitendo kisicho cha Mwenyezi Mungu (s.w.t), na inafaa kumuomba mwingine, kiwe cha kawaida au kisicho cha kawaida. Inafaa ifahamike kwamba aina tuliyoieleza na kuibainisha hapo kabla haiendi kinyume wala kupingana na misingi ya Tawhiid.

166


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 167

Tawhid na Shirk

SEHEMU YA NNE: ITIKADI ZA MAWAHABI Hakika mwenye kusoma na kudurusu vitabu vya Mawahabi na aliyeishi nao, bila shaka ameona kwamba tuhuma za Shirki ni kitu kikubwa zaidi ambacho hurudufu mara kwa mara katika vitabu vyao na ndimi zao, hageuki kulia wala kushoto isipokuwa husema hiki ni Shirki au huyu ni mshirikina, au acha bidaa, wewe mtu wa bidaa na mengineyo. Hali ikiwa kipimo ni yale wayasemayo katika vitabu vyao, basi mtu atawaona Waislamu wengi hawampwekeshi Mwenyezi Mungu (s.w.t) hata kidogo. Unaona ufinyu ulioje ambao Mawahabi wanakabiliana nao katika umma wa kiislamu, na je! huo ndio ukweli wa mambo? Na je hufanya hivyo kwa msukumo wa kutaka kumpambanua kati ya mwenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu (s.w.t) na mshirikina, au hayo ni mambo ya kisiasa, na ni mambo na mbinu ambazo wakoloni huzitumia kwa lengo la kugawa na kuwasambaratisha Waislamu na kuvunja umoja wao? Kwa hakika Mwenyezi Mungu (s.w.t) pekee ndiye ajuae zaidi. Hapa tunataka tuliweke jambo hilo mbele ya Qur’an, Sunna ya Mtume (s.a.w.w) na nyendo za Makhalifa wake, ili tuone je! katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu (s.w.t), Sera ya Mtume (s.a.w.w) na Makhalifa wake limeelezwa hivyo? Bila shaka jawabu lake sio hivyo kama utakavyoona‌

MCHAKATO KATIKA KUUKUBALI UISLAMU Hakika mwenye kuchunguza zama za Mtume (s.a.w.w) na zama zilizofuata za mabadiliko ya kiitikadi na kifikra, atakuta umma na jamii mbalimbali zilizokuwa na desturi tofauti ziliupokea Uislamu, na wengi wao walishikamana na dini hii, na atakuta Mtume (s.a.w.w) na Waislamu kwa jumla waliukubali Uislamu wao na wakitosheka na Shahada mbili toka kwao bila kujali desturi zao za kijamii, na hali yao katika desturi mpya inatofautiana 167


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 168

Tawhid na Shirk kabisa na desturi na ada zao za zamani, kitendo cha watu kuwaheshimu wazee wao na kuwatukuza, kuzuru makaburi yao na kudhihirisha mapenzi yao kwao na uhusiano wao kwao ilikuwa ni desturi ya kijamii iliyoenea. Na hadi leo tunaona mataifa mbalimbali - ya Mashariki na Magharibi – wakiadhimisha na kudumisha utajo wa watukufu wao, huzuru makaburi yao na kufanya vikao vya maombolezo, hulia na hutokwa na machozi‌ Yote hayo huhesabiwa ni katika aina za kuheshimu na kuwatukuza, ambapo hali hiyo chanzo chake ni upendo na hisia za ndani ya dhamira zao. Kwa ufupi ni kwamba hakika sisi hatujapata sehemu hata moja ambayo Mtume (s.a.w.w) ili kukubali Uislamu wa watu hao aliweka sharti kwamba waachane na ada na desturi zao za kale na baada ya kuzifanyia uchunguzi itikadi zao, bali tunamkuta Mtume (s.a.w.w) anatosheka na Shahada mbili tu na kuyatupilia mbali masanamu. Na ikiwa ada na desturi hizi ni Shirki ingelilazimu Mtume (s.a.w.w) kuzikataza na kutokukubali kusilimu kwa hao Waislamu au kwa mtu mmoja mmoja ila baada ya kuwa wamemwahidi kwamba wataachana na ada na desturi zao za kale na hawatorudia tena kutenda ya hapo kabla. Faida inayopatikana hapa ni kwamba kuacha kufanya tawassuli (kupitia) kwa mawalii, na kutabaruku kwa athari zao na kuzuru makaburi yao kungelikuwa ni sharti la kupatikana imani iliyo mkabala na Shirki angeliwajibika kwa Mtume (s.a.w.w) kufanya hilo kuwa sharti la kusilimu pindi alipokuwa akijiwa na ujumbe wa makabila kadhaa kwa lengo la kusilimu, ni ingemlazimu kutangaza sharti hilo dhahiri kinaga ubaga mimbarini na mbele ya watu wote, na lau angelisema sharti hilo wazi wazi basi lingelijulikana kwa Waislamu. Kwa hivyo yote hayo yanajulisha kwamba kuacha mambo hayo haikuwa ni sharti la kuwa mwislamu wala haikuwa ni sharti la kuwa na imani, na wala mtendaji wa hayo hakuzingatiwa kuwa ni mshirikina na ni aliye nje ya Uislamu. Na lau kutawassali na kutabaruku na kuzuru makaburi kungekuwa ni kuitakidi Uungu (wa anayefanyiwa hayo) basi hilo lingewekwa wazi na Mtume 168


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 169

Tawhid na Shirk kwa Waislamu ambao mwenendo wao wa kawaida wa kivitendo ulikuwa ni kufanya hayo, kwani la sivyo kitendo chao kingekuwa kinapingana na imani ya mungu mmoja. Na zimepokewa hadithi chungu nzima kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) na Ahlul-Bayt kwamba Uislamu unalinda na kukinga umwagaji wa damu, kumkosea adabu, heshima na kumwaibisha mwislamu, uporaji wa mali zake, na unahimiza kutekeleza amana na mengineyo miongoni mwa hukumu za kiislamu. Mpendwa msomaji yanakutosha yale aliyoyaeleza Bukhari kutoka kwa Ibnu Abbas kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kwamba bwana Mtume (s.a.w.w) alimwambia Ma’adhi bin Jabal pindi alipomtuma Yemen: ???? ????? ???? ??? ???? ???? ????? ?????? ??? ?? ?????? ?? ?? ??? ???? ???? ???? ?????? ???? ???? ???? ?? ?????? ?? ???? ??????? ?? ???? ??? ????? ??? ????? ?? ??? ??? ????? ??? ?? ?????? ?? ???? ??????? ??? ???? ?? ??? ????? ???? ???? ?? ???????? ???? ??? ??????? ??? ?? ?????? ?? ???? ????? ?????? ??????? “Hakika wewe utawaendea watu waliopewa kitabu, na utapofika kwao walinganie washuhudie kwamba hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) na Muhammad ni mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.w.t), watakapo kubali na kutii waeleze kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t) amefaradhisha kwao Swala tano kila (siku) mchana na usiku, wakikutii waeleze kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t) amefaradhisha kwao Sadaka (zaka) huchukuliwa kutoka kwa matajiri wao na kupewa mafakiri wao, wakikutii ole wako kuwakosea adabu, heshima na utu wao pamoja na kuchukua mali zao.” Na ameeleza Bukhari na Muslim katika mlango wa Fadhila za Imam Ali (a.s.) kwamba Mtume (s.a.w.w) katika vita vya Hunayni amesema:

169


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 170

Tawhid na Shirk

“Kesho nitampa bendera mtu ambaye anampenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake, naye anapendwa na Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hakika Mwenyezi Mungu ataleta ukombozi kupitia kwake.” Umar bin Khattab akasema: “Sikupenda utawala, ila siku hiyo.” akaongeza kusema: ”Nilikuwa natamani niitwe mimi, hatimaye Mtume (s.a.w.w) akamwita Ali bin Abi Talib akamkabidhi bendera, na hapo akasema: ??? ??? ????? ??? ???? ???? ???? “Nenda wala usirudi nyuma mpaka Mwenyezi Mungu (s.w.t) alete ukombozi kupitia kwako,” basi akaenda wala hakugeuka nyuma, akauliza: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, kwa sharti ganii tunapigana na watu? Mtume (s.a.w.w) akasema: ?????? ??? ?????? ?? ?? ??? ???? ???? ???? ?????? ???? ???? ???? ????? ??? ??? ????? ??? ?????? ???????? ??? ?????? ??????? ??? ???? “Pigana nao mpaka washuhudie kwamba hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) na Muhammad (s.a.w.w) ni Mjumbe Wake, watakapofanya hivyo usimwage damu zao na haifai kuchukua mali zao isipokuwa kwa haki na hisabu yao ni kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t).”76 Na Bukhari, Muslim, Tirmidhi na Nasaai wamepokea kutoka kwa Abdullah bin Umar amesema: Mtume (s.a.w.w) amesema: ??????? ?????? ???? ?????. “Uislamu umejengwa juu ya mambo matano: Kushuhudia kwamba hapana mungu apasaye kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu

76. Sahih Muslim Juz. 6 mlango Fadhila za Ali bin Abi Twalib. 170


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 171

Tawhid na Shirk (s.w.t) na Muhammad ni Mjumbe Wake, kusimamisha Swala, kutoa Zaka, kuhiji na kufunga Ramadhani.”77 Pia Bukhari amepokea kutoka kwa mtoto wa Umar kwamba Mtume (s.a.w.w) amesema: ???? ?? ????? ?????? ???? ?????? ?? ?? ??? ???? ???? ???? ?????? ???? ???? ??????? ??????? ?????? ??????? ??? ????? ??? ????? ???? ?????? ???????? ???? ???? ??????? ??????? ??? ???? “Nimeamrishwa nipigane na watu mpaka washuhudie kwamba hakuna mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu na Muhammad ni Mjumbe Wake, wasimamishe Swala na watoe Zaka, na watakapofanya hivyo ni haramu kumwaga damu zao na kuchukua mali zao isipokuwa kwa haki ya Uislamu na hisabu zao ni kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t).”78 Na hadithi nyinginezo za Bwana Mtume (s.a.w.w) ambazo zinapatikana katika vitabu mbali mbali kama vile katika mlango wa Iman katika vitabu sahihi vya kisuni na Sunani. Na ama kwa yale yaliyopokewa na Maimamu wa Ahlul-Bayt (a.s.) yakutosha yale aliyopokea Samaat kutoka kwa Imam Swadiq (a.s.) amesema: ???????: ????? ?? ?? ??? ???? ???? ????????? ????? ???? ?? ???? ??????? ???? ??????? ????????? “Uislamu ni kushuhudia hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu (s.w.t) na kumswadikisha Mtume Wake. Itakuwa ni haramu kumwaga damu zao, inaruhusiwa kuoleana na kurithiana.”79 77. Taaj Jaamiu lil Usuul fi Ahadiith Rasuul Juz. 1 Uk. 20 cha Sheikh Mansur Ali Naswif. 78. Sahih Bukhari Juz. 1 Kitabul-Imani mlango "Iwapo watatubia na wakasi mamisha swala;" na Sahih Ibn Maja Juz. 2 Uk. 457 mlango kujizuia kwa yule mwenye kusema: "La ilaha illa llah". 79. Al-Kaafi Juz. 2 Uk. 25 chapa ya haditha mlango Imani Yashariku Islam wal Islam la yushariku Iman, zipo hadithi nyingi zinazoeleza kinaga ubaga kuhusiana na hayo, Taaj Juz. 1 Uk. 20 - 34 kitabul-Islam wal-Imani. 171


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 172

Tawhid na Shirk Na hadithi zote hizo zinaeleza kinaga ubaga kwamba haifai kumwagwa damu ya mtu ambaye ameingia katika Uislamu na kustahiki yale wanayostahiki Waislamu wengine, nayo ni kutokana na itikadi ya Tawhiid na kumpwekesha Mola Manani aliyetukuka, aidha kuamini na kuukubali utume wa Mjumbe Wake. Na ilijiri Sunna ya Mtume (s.a.w.w) katika hili, na kwa hivyo alitosheka mtu kudhihirisha utamkaji wa Shahada mbili, na wala hakuwatuhumu hata kidogo wala kuwahoji wale waliokuwa wakija kusilimu: Je wao hufanya tawassuli kwa Mitume, Mawalii na Watakatifu au hapana? Je! wao wanatabaruku kwa athari zao au hapana? Je! wao huzuru makaburi ya Mitume au la? ili awape sharti la kuacha kufanya tawassuli, kutabaruku na kuzuru. Kwa mantiki hiyo, hayo yote yanajulisha kwamba Uislamu unakataza umwagaji damu, kuvunja heshima na kuchukua mali za watu ambao wametamka Shahada mbili na kuzidhihirisha tu, ama kinyume na hivyo hakuna uhusiano kabisa na mambo hayo. Ndio maana Mwenyezi Mungu (s.w.t) amefaradhisha kwa Waislamu wanapozozana na kutofautiana katika jambo fulani basi warudi kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) na Mtume (s.a.w.w), Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema:

“Enyi Mlioamini! Mtiini Mwenyezi Mungu na mtiini Mtume na wenye mamlaka katika nyinyi, na kama mkigombana katika jambo lolote basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume ikiwa mnamwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, hilo ni bora zaidi na ni lenye mwisho mzuri zaidi.� (4:59) Na anasema: 172


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 173

Tawhid na Shirk

“Na linapowafikia jambo lolote la amani au la khofu hulitangaza, (hivyo msifanye) na kama wangelipeleka kwa Mtume na kwa wenye mamlaka katika wao, bila shaka wangelijua wale wanaochunguza katika wao, na kama isingelikuwa fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema Yake mngelimfuata shetani isipokuwa wachache.” (4:83) Na kwa hivyo haifai muislam yeyote kulitukana kundi miongoni mwa vikundi vya kiislamu sembuse kuwatuhumu kwa ukafiri au ulahidi, maadamu wanatamka na kushuhudia Shahada mbili, wanasimamisha swala na wanatoa zaka, tuhuma zote hizo wanazotuhumiwa ni kwa ajili ya kufanya kwao tawassuli kwa Mitume au kutabaruku na athari zao, au makundi mengine ya kifikra ambayo yanatofautiana kimaoni na kinadharia na wanachuoni wao. Hakika mwenye kuwatuhumu hao, kuwaita washirikina na ametoka katika mfumo wa kiislamu ambao Mwenyezi Mungu (s.w.t) amewapangia Waislamu, anasema:

“Hakika wale waliofarikisha dini yao na wakawa makundi makundi huna uhusiano wowote nao, bila shaka shauri lao ni kwa Mwenyezi Mungu, kisha atawaambia yale waliyokuwa wakiyatenda.” (6:159) 173


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 174

Tawhid na Shirk Anasema tena:

“Enyi mlioamini; mtakaposafiri katika njia ya Mwenyezi Mungu basi pelelezeni, wala msimwambie mwenye kuwapa salamu; wewe si muumini, mnataka mafao ya dunia na kwa Mwenyezi Mungu kuna neema nyingi, hivyo ndivyo mlivyokuwa zamani, na Mwenyezi Mungu amewafanyieni hisani, basi chunguzeni, hakika Mwenyezi Mungu ni mjuzi wa yale mnayoyatenda.” (4:94) Anasema tena:

“Enyi Mlioamini! Mcheni Mwenyezi Mungu ipasavyo kumcha wala msife ila na nyinyi muwe ni waislamu.” (3:102) Anasema tena:

174


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 175

Tawhid na Shirk “Na shikamaneni na kamba ya Mwenyezi Mungu nyote wala msifarakane, na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu mlipokuwa maadui na akaziunganisha nyoyo zenu, hivyo kwa neema Yake mkawa ndugu na mlikuwa ukingoni mwa shimo la Moto naye akawaokoeni nalo, hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu anavyokubainishieni dalili zake ili mpate kuongoka.” (3:103) Na makusudio ya kamba ya Mwenyezi Mungu ambayo ni wajibu kushikamana nayo ni dini ya kiislamu kama anavyosema Mwenyezi Mungu (s.w.t):

“Hakika dini mbele ya Mwenyezi Mungu ni Uislamu, na waliopewa kitabu hawakuhitilafiana ila baada ya kuwajia elimu, kwa sababu ya hasadi baina yao, na anayezikataa Aya za Mwenyezi Mungu, basi hakika Mwenyezi Mungu ni mwepesi wa kuhesabu”. (3:19) Na Uislamu ni kudhihirisha Shahada mbili na hakuna kikundi katika vikundi vya Waislamu kisichotamka hizo, isipokuwa wale ambao imekubalika kwamba wametoka katika Uislamu kama vile Makhawariji na Nawasibu, na mwenye kurejea Qur’an na Sunna anakuta kwamba vinatilia mkazo zaidi ulinganio wake juu ya Waislamu kupendana wasitofautiane wala kuchukiana, wasiitane makafiri, wasitukanane, wasipigane na kuuana. Bukhari ameeleza kwa njia na wapokezi tofauti kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) katika hija ya kuaga amesema:

175


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 176

Tawhid na Shirk ??????? ??? ?????? ???? ?????? ???? ????? ???? ???

“Angalieni msirudi katika ukafiri baada yangu kwa baadhi yenu kuuawa baadhi yao.�80 Inakuwaje Mawahabi wanakuwa na ujasiri wa kuwatuhumu Waislamu wenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu (s.w.t) kuwa ni washirikina kwa kutokana na (kudhihirisha kwao) upendo kutokana na waliyoyapata kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kwa kubusu mahala alipozikwa na kwa kumtukuza. Pamoja na hayo yote sisi tunazipima itikadi za Mawahabi katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna kwa bayana mpaka haki idhihirike dhahiri shahiri. Kwa muhtasari mada hii itahusu kuyajadili kwa kina mambo yafuatayo: Je! kuomba ponyo kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu ni Shirki? Je! kuomba Shufaa kwa waja wa Mwenyezi Mungu ni Shirki? Je! kuomba msaada kwa Mawalii wa Mwenyezi Mungu ni Shirki? Je! kuwaomba watu wema ni Shirki? Je! Kuwakumbuka na kuwatukuza Mawalii ni Shirki? Je! Kutabaruku kwa athari ya Mtume (s.a.w.w) na Mawalii ni Shirki? Je! Kujenga juu ya makaburi ni Shirki? Je! Kuzuru makaburi ni Shirki? Je! Kuswali pembezoni mwa makaburi ya watu wema ni Shirki? Je! Kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu ni Shirki? Na iwapo itakadiriwa kwamba mambo hayo sio Shirki je! Hayo yanafaa au hapana? kwa hakika utafiti wetu unajikita na kutuama juu ya kwamba je! 80. Sahih Bukhari Juz. 9 kitabu Fitan mlango wa saba hadithi ya kwanza na ya pili, aidha ameipokea katika vitabu vyake tofauti, vile vile ameipokea Ibn Maja Juz. 2 Uk. 462 mlango wa "Kumtukana muislamu ni ufasiki" chapa ya Misri. 176


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 177

Tawhid na Shirk jambo hilo ni Shirki au sio Shirki na sio kuhusiana na kufaa au kutofaa, kwa ujumla maudhui hii itajikita na kutuama katika mchanganuo na upembuzi yakinifu katika kubainisha vigezo vya Tawhiid na Shirki pamoja na mipaka yake, sio kujuzu au kutojuzu kwake. 1. JE! KUOMBA PONYO KWA ASIYEKUWA MWENYEZI MUNGU NI SHIRKI? Hapana shaka katika ulimwengu huu, ulimwengu wa nidhamu na mpangilio, mambo yote yaliyoko ulimwenguni huwa na chanzo chake, na kwamba sababu ambazo zinahusiana nazo zimeumbwa na Mwenyezi Mungu (s.w.t). Na kwa kuwa sababu hizo hazina uwezo wa kujitegemea, yaani ukamilifu wa kidhati, bali zimepatikana kwa utashi wa Mola Muumba, na zikawa na athari na kuathiri vitu vingine kwa matakwa ya Mwenyezi Mungu (s.w.t), ndio maana imesihi Mwenyezi Mungu kunasibisha athari za sababu hizo Kwake mwenyewe Mwenyezi Mungu, kama ambavyo inasihi kuzinasibisha athari hizo kwa sababu hizo. Na hayo ndio tuliyoyabainisha vizuri huko nyuma, hivyo inadhihiri kwamba ponyo mara hunasibishwa kwa Mwenyezi Mungu na mara hunasibishwa kwa sababu za athari hizo na hivyo hakuna ukinzani kati ya Aya zinazonasibisha athari mara kwa sababu na mara kwa Mwenyezi Mungu, kwani sababu hazitendi kwa kujitegemea bali ni kwa idhini na utashi na uwezo wa Mwenyezi Mungu. Qur’an tukufu inasema: “Na ninapougua, basi Yeye ananiponya”. (26:80) Yeye ndiye ambaye aliyewapa Mitume Wake na Mawalii Wake uwezo wa kuponya, kutibu na kufanya vipofu waone, Naye ndiye aliyewapa idhini wautumie uwezo na vipaji alivyowapa kwa masharti maalum. Qur’an inaeleza kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t) ndiye mponyaji wa hakika kama ilivyokuja katika sura 26 aya 80, na inaeleza asali pia inaponya inasema: “Kisha kula katika kila matunda, na upite katika njia za Mola Wako zilizofanywa nyepesi, kinatoka katika matumbo yao kiny177


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 178

Tawhid na Shirk waji chenye rangi mbali mbali, ndani yake kina matibabu kwa watu, hakika katika hayo mna mazingatio kwa watu wanaofikiri.” (16:69) Aidha inahusisha uponyaji kwa Qur’an tukufu inasema: “Na tunateremsha Qur’an ambayo ni ponyo na rehema kwa wenye kuamini, wala hayawazidishii madhalimu ila hasara tu.” (17:82) Na njia ya kukusanya pamoja yale ambayo tuliyoyataja na kuyaeleza huko nyuma, vivyo hivyo na yanayojiri hapa katika maada hii, tunasema: Hakika uponyeshaji katika hali ya kujitegemea ni katika kazi ya Mwenyezi Mungu na sio mwingine, na kwa kufuata na kutokuwa na hali ya kujitegemea ndio kazi ya vitu hivi, na sababu hizi Yeye ndiye aliyeziumba na kisha akazipatia athari na uwezo, kwa hivyo vinafanya kwa idhini Yake na utashi Wake. Kwa aina hii atakapoomba mtu ponyo kwa Mawalii kwa kuangalia asili hii81. basi jambo hili linafaa na limeruhusiwa kisheria na linaafikiana na Tawhiid mia kwa mia, kwa sababu lengo la kuomba Shufaa kwa Mawalii ni kama lile lile la kutafuta ponyo kutoka katika asali, vidonge na matunda, ijapokuwa vitu hivyo hutoa athari zake bila utashi na kudiriki ilihali Mitume na Mawalii hutenda kwa kwa utashi na hiyari, hivyo lengo la Walii kuombwa ponyo si jingine ila ni kumuomba autumie uwezo aliyozawadiwa ili amponye mgonjwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (s.w.t), kama alivyokuwa anafanya Nabii Isa (a.s.) pindi alipokuwa anaponya magonjwa wale wenye magonjwa sugu ambayo yaliyoshindikana kutibika. Akafanya hivyo kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) kwa kutumia uwezo aliopewa na Mola Muumba, kwa hivyo jambo hilo limeruhusiwa kisheria na halipingani hata kidogo na misingi ya Tawhiid. Na ni dhahiri shahiri kwamba mfano wa kazi hizi na zinazofanana na hizi hazihesabiwi kuwa ni Shirki, kwani hata kidogo hazihusiani kabisa wala kuwa na mafungamano ya aina yoyote na vigezo na misingi ya Shirki. Kwa hivyo tunaweza kuanzisha mjadala kwamba je! wao wanaweza kufanya hayo au la? na je! wamepewa uwezo huo au hapana? lakini maudhui 81. Yaani wao wanaponya na kuathiri kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, uwezo wake na utashi wake na sio wao kama wao. 178


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 179

Tawhid na Shirk yetu haihusiani na hayo, bali inahusu kama uombaji unaafikiana na Tawhiid au hauafikiani na Tawhiid. Na linalofafanua hilo ni kwamba Mafirauni walikuwa wakimuomba Musa (a.s.) awaondolee matatizo kama ilivyokuja katika maneno ya Mola Subhaanahu wa Taala, Qur’an inasema: “Na ilipowaangukia adhabu, wakasema: Ewe Musa! Tuombee kwa Mola Wako yale aliyokuahidi, kama ukituondolea adhabu, bila shaka tutakuamini na kwa hakika tutawapeleka Wana wa Israeli pamoja nawe.” (7:134) Wala hatutaki kuthibitisha usahihi wake kupitia ombi la Firaun au jamaa zake bali hoja na dalili ni kile kitendo cha Musa (a.s.) kunyamaza mbele ya maombi mfano wa hayo, na hiyo ni dalili tosha juu ya kusihi hilo. Kwa ujumla lau mtu atamwomba Nabii Isa (a.s.) na akamwambia ”Wewe unasema: “Na ninawaponya vipofu na wenye mbalanga, ninawafufua wafu kwa idhini ya Mwenyezi Mungu...” (3:49) basi huyu hapa mwanangu amepatwa na maradhi ya ukoma na imeshindikana tiba yake, mponyeshe kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (s.w.t), na huyu hapa ndugu yangu amekufa nakuomba umfufue na baada ya hivyo mimi pamoja na familia yangu tutaamini utume wako.” Je! Unaona Nabii Isa (a.s.) atanasibisha maombi hayo kuwa ni Shirki na kumhesabu muombaji huyo kuwa mshirikina? Unadhani atamwambia: Hakika kuponya na kufufua ni vitendo vya Mwenyezi Mungu? Au ni kwamba huyu mtu aliyetahayari yuko katika njia ya haki na anatafuta uongofu? Bila shaka uponyaji na uhuishaji huhesabiwa ni katika kazi za Mwenyezi Mungu (s.w.t) tu iwapo ni kwa kujitegemea, na hivyo kumuomba hilo mtu katika hali ya kujitegemea na kuamini kwamba mwenye kutenda hayo ana uwezo wa kujitegemea ni kuamini Uungu wake na uombaji huo ni kumwabudu mtu huyo. Na ama akiamini kwamba yule mwenye kuponya na kufufua uwezo wake wa kufanya hayo amepewa na Mwenyezi Mungu (s.w.t) na kwamba ameruhusiwa na Mola Manani, huhesabiwa mponyaji na mfufuaji kuwa ni 179


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 180

Tawhid na Shirk nyenzo na sababu za kutekeleza utashi wa Muumba, itikadi kama hiyo si kuamini Uungu wa mtu huyo, na ni dhahiri kwamba uombaji huo sio ibada. 2. JE! KUOMBA SHUFAA KWA ASIYEKUWA MWENYEZI MUNGU NI SHIRKI? Hakuna kipingamizi kwamba Shufaa ni haki mahususi ya Mwenyezi Mungu (s.w.t), Aya za Qur’an na dalili za kiakili zote kwa pamoja hujulisha hilo, mfano Aya hii: “Sema: uombezi wote ni wa Mwenyezi Mungu, ufalme wa mbingu na ardhi ni Wake, kisha mtarejeshwa Kwake.” (36:44) Isipokuwa zipo baadhi ya Aya zinazojulisha kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t) ametoa idhini kwa kundi miongoni mwa waja waitumie haki hiyo, wanatoa Shufaa kwa mazingira na masharti maalum, hadi baadhi ya Aya hizo zimeeleza kinaga ubaga majina kadhaa ya watoaji Shufaa, Qur’an tukufu inasema: “Na wako Malaika wangapi mbinguni ambao uombezi wao hautafaa chochote isipokuwa baada ya Mwenyezi Mungu kutoa idhini kwa amtakaye na kumridhia.” (53:26) Vile vile Qur’an imethibitisha kwamba Mtume Muhammad (s.a.w.w) ana mahala maalum na mwenye kutukuzwa, inasema: “Na katika usiku amka kwa (kusoma) hiyo Qur’an ni (ibada) zaidi kwako huenda Mola wako akakuinua cheo kinachosifika.” (17:79) Na wafasiri wa Qur’an wamesema kwamba makusudio ya ibara “ cheo kinachosifika” ni cheo cha kutoa Shufaa kulingana na hadithi mbalimbali ambazo zimepokewa kuhusiana na jambo hilo. Yote hayo ni katika mambo ambayo Waislamu wote wamekubaliana, lakini mjadala ni kuhusu je kuomba Shufaa toka kwa anayefaa kuombwa Shufaa ni Shirki au la? kwa mfano mtu akisema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu tupe Shufaa” Je! hiyo ni Shirki au hapana? Na mada yetu haihusu je! Muombaji anakusudia kwa hilo au anafanya mzaha na anatania? Bali mjadala wetu ni je! hiyo ni ibada au hapana? 180


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 181

Tawhid na Shirk Tunasema: Jibu limedhihirika kutokana na yale tuliyoyaeleza huko nyuma katika maudhui zilizotangulia, lau tutaitakidi kwamba hao tunaowaomba Shufaa na wao wanajitegemea katika hilo pasi na kupata ruhusa na idhini ya Mola Manani wala hawana haja Naye katika hilo, bila shaka kufanya hivyo ni ibada na muombaji atakuwa mshirikina na ametoka katika wigo wa Tawhiid, kwa sababu ameomba kitendo cha Mwenyezi Mungu (s.w.t) kwa asiyekuwa Yeye. Na ama lau tutamuomba Shufaa mmoja wa watoaji Shufaa na hali ya kuwa sisi tunaitakidi kuwa hao ni viumbe ambao wameumbwa na Mwenyezi Mungu (s.w.t) na hawawezi kutoa Shufaa kwa yeyote isipokuwa kwa idhini yake Subhanahu wa Taala, jambo hilo ni la kawaida, na mtu mwenye kutenda hilo hajatoka katika mipaka ya Tawhiid. Na iwapo mtu atafikiri kwamba tendo hilo (yaani la kuomba Shufaa kwa Mawalii) kidhahiri linashabihiana na matendo ya Washirikina walipokuwa wanayaomba masanamu yao Shufaa, huo ni ufikiriaji batili na uko mbali na ukweli. Kwani kushabihiana na kufanana kidhahiri sio kigezo cha hukumu, bali kigezo cha hakika cha hukumu ni nia na makusudio ya muombaji na itikadi yake kwa muombwa. Na jambo lililodhahiri ni kwamba kigezo cha amali yoyote ile ni nia na dhamiri ya mhusika, sio umbo na dhahiri ya mambo, zaidi ya hapo ni kwamba kuna tafauti kubwa kati ya amali mbili, nayo inabainika kwa mitazamo ifuatayo: Mosi: Kwa hakika kuna tafauti kubwa mno kati ya itikadi ya mwanatawhiid kuhusiana na haki ya Mawalii na itikadi ya mshirikina kuhusiana na masanamu, bali kuna tafauti kubwa sana baina ya imani hizo mbili; ya Mpwekeshaji Mwenyezi Mungu na mshirikina. Kwani masanamu kwa mujibu wa itikadi ya washirikina yalikuwa ni miungu midogo ambao walikuwa wakimiliki jambo kati ya mambo ya kiungu kama vile kutoa Shufaa na msamaha, tofauti na wanatawhiid, kwani wao wanaitakidi na kuwaona wale ambao wawaombao Shufaa kuwa ni waja watukufu, hawamuasi Mwenyezi Mungu (s.w.t), ni wachamungu na wao wanatekeleza amri za Mola Muumba, na kwamba wao hawamiliki chochote kuhusiana na Shufaa bali wanatoa Shufaa kwa idhini ya Mwenyezi 181


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 182

Tawhid na Shirk Mungu (s.w.t) na kwa ajili ya kuridhiwa kwao na Mwenyezi Mungu (s.w.t), na hakuna afanyaye hilo isipokuwa yule aliyeridhiwa kufanya hivyo. Kwa mantiki hiyo ili Shufaa ipatikane na ithibiti kwa yeyote yahitajika yatimie mambo mawili nayo ni: 1. Mtoaji Shufaa anatakiwa aruhusiwe na Mwenyezi Mungu (s.w.t) kufanya hivyo. 2. Muombewa (anayeombewa) anatakiwa awe mwenye kuridhiwa na Mola Manani. Na lau Mwislamu atamwambia mmoja kati ya watu wema: “Niombee Shufaa kwa Mwenyezi Mungu,” yeye hatafanya hivyo ila baada ya kutimia masharti mawili yaliyotangulia. Pili: Hakika washirikina walikuwa wakiyaabudu masanamu pamoja na kuyaomba Shufaa, huku wakiona uombaji wao wa Shufaa na kujibiwa maombi yao ni fidia ya zile ibada walizokuwa wakiyafanyia masanamu hayo, ambapo hali hiyo ni tafauti na ile ya watu wa Tawhiid, wao hawamwabudu hata chembe mwingine asiyekuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t). Uombaji wao wa Shufaa toka kwao haumaanishi chochote isipokuwa ni kutaka kufaidika na cheo chake au mahala pake patukufu (Maqaamu Mahmuud) ambapo Mwenyezi Mungu (s.w.t) amempatia Mjumbe wake na hufanya hivyo kwa idhini yake, kwa hivyo ulinganishaji kati ya uombaji Shufaa wa Waumini na ule wa washirikina ni uchanganyaji na uvurugaji wa mambo, bali una lengo la kuleta utata na mkanganyiko baina ya watu. Aidha imeshaelezwa hapo kabla na kurudiwa mara kadhaa wa kadhaa kwamba lau kama kingelikuwa kigezo ni ufananaji wa dhahiri katika mambo basi ingelilazimu kuzingatia Uzungukaji wa Ka’ba tukufu, kugusa Jiwe jeusi na kutembea kati ya Swafa na Marwa kuwa ni Shirki na ni kuabudu masanamu. 182


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 183

Tawhid na Shirk

MAWAHABI NA UOMBAJI WA SHUFAA Hakika Mawahabi huzingatia kwamba kuomba Shufaa ni Shirki na ni kuwaabudu hao wanaowombwa, na wanadhani kwamba Qur’an imewaeleza waabudu masanamu kuwa ni washirikina sio kwa jambo lingine, isipokuwa ni kwa sababu ya uombaji wao wa Shufaa kwa Masanamu yao, Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema: “Nao wanaabudu kinyume cha Mwenyezi Mungu wasiowadhuru wala kuwanufaisha, na wanasema hawa ndio waombezi wetu mbele ya Mwenyezi Mungu, sema: Je! Mtamwambia Mwenyezi Mungu asiyoyajua katika mbigu wala katika ardhi? Ameepukana na upungufu na ametukuka na hao wanaowashirikisha.” (10:18) Kwa hivyo basi Shufaa hii hata kama imethibiti kwa watoaji Shufaa isipokuwa haifai kuwaomba wao kwa sababu kufanya hivyo ni kuwaabudu hao, Muhammad bin Abdul –Wahab amesema: “Watu wema hawana chochote, lakini nawakusudia na natarajia kutoka kwa Mwenyezi Mungu Shufaa zao, Jawabu ni kwamba hayo ni maneno ya makafiri na hakuna tofauti kati yao, na hapo nitawasomea maneno ya Mwenyezi Mungu (s.w.t):

“Sikilizeni: Utii halisi ni haki ya Mwenyezi Mungu, lakini wale wanaowafanya wengine kuwa waungu badala yake (husema): Sisi hatuwaabudu hawa ila wapate kutufikisha karibu kabisa na Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu atahukumu baina yao katika yale wanayohitilafiana, bila shaka Mwenyezi Mungu hamuongozi aliye muongo aliye kafiri.” (39:3) 183


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 184

Tawhid na Shirk Na amesema:

Nao wanaabudu kinyume cha Mwenyezi Mungu wasiowadhuru wala kuwanufaisha, na wanasema hawa ndio waombezi wetu mbele ya Mwenyezi Mungu, sema: Je! Mtamwambia Mwenyezi Mungu asiyoyajua katika mbingu wala katika ardhi? Ameepukana na upungufu na ametukuka na hao wanaowashirikisha.” (10:18)82 Na iwapo atasema: Hakika Mtume (s.a.w.w) amepewa haki ya Shufaa na mimi naiomba kutoka kwa aliyepewa na Mwenyezi Mungu (s.w.t), jibu: hakika Mwenyezi Mungu amempa yeye haki ya Shufaa na amekukataza kumuomba yeye, anasema:

“Na kwa hakika Misikiti yote ni ya Mwenyezi Mungu basi msimuombe mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu.” (72:18). Vile vile hakika Shufaa wamepewa wengine wasiokuwa Mitume, na sahihi kwamba Malaika wanatoa Shufaa na Mawalii wanatoa Shufaa pia, aidha imekubalika kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t) amewapa hilo, sasa kufanya hivyo ni kuwaabudu watu wema kutokana na ibara ambayo Mwenyezi Mungu (s.w.t) ameitumia ndani ya kitabu chake”83 Mtoto wa Abdul-Wahabi ametumia Aya tatu kama dalili ya kuharamisha ombi la Shufaa, nazo ni: 82. Kashfu Shubhat Uk. 7 - 9 chapa ya Cairo. 83. Kashfu Shubhat Uk. 7 - 9 chapa ya Cairo. 184


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 185

Tawhid na Shirk

Ya kwanza: “Na wanaabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu ambayo hayawanufaishi wala kuwadhuru mbele ya Mwenyezi Mungu.” (10:18) Muhammad bin Abdul-Wahabi amesema: “Ibada ya washirikina kwa masanamu ilithibiti kutokana na kuwaomba hayo Shufaa na sio kwa jambo lingine.”

Ya pili: “Sikilizeni! Utii halisi ni haki ya Mwenyezi Mungu, lakini wale wanaowafanya wengine kuwa waungu badala yake (husema): Sisi hatuwaabudu hawa ila wapate kutufikisha karibu kabisa na Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu atahukumu baina yao katika yale wanayohitilafiana, bila shaka Mwenyezi Mungu hamuongozi aliye muongo aliye kafiri.” (39:3) Amesema: ‘’Hakika washirikina waliyaabudu Masanamu na ikawa sababu ya kuyaomba hayo Shufaa.” Ya tatu: “Na kwa hakika Misikiti yote ni ya Mwenyezi Mungu basi msimuombe mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu”. (72:18) Hapana budi kutoa maelezo ya kina kuhusiana na Aya alizozitumia kama dalili kudai kwamba kumwomba Shufaa yule mwenye haki ya kutoa Shufaa ni kumwabudu yeye, tunasema: Ama jibu kuhusu Aya ya kwanza, jibu lake lipo katika mitazamo miwili: 185


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 186

Tawhid na Shirk 1. Maneno ya Mwenyezi Mungu (s.w.t): “Na wanaabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu, hawawadhuru wala kuwanufaisha..…” hayajulishi wala kumaanisha makusudio yao, tunapoona Qur’an inawaeleza watu hao kuwa washirikina sio kwa sababu walikuwa wanayaomba Masanamu Shufaa, bali ni kwa sababu wao walikuwa wanayaabudu. Na kwa kuwa Masanamu hayo hayakuwa na uwezo wa kuitikia na kukidhi haja za waabudu Masanamu, basi matendo yao pia yakawa ni ya kipuuzi upande huu na sio Shirki kama upande wa kwanza (Hivyo yalikuwa ni Shirki na ni Upuuzi kwa vigezo viwili tofauti vilivyojikusanya pamoja). Ikichunguzwa kwa kina maana ya Aya pamoja na kuzingatia kuwa watu hawa washirikina walikuwa wakifanya amali mbili: Ibada na kuomba Shufaa kama yanavyojulisha maneno ya Mwenyezi Mungu (s.w.t): “Na wanaabudu na wanasema” huvumbua sababu ya wao kuitwa washirikina na kustahili kwao sifa hiyo, nayo ni kwa sababu ya ibada yao kwa Masanamu na sio kwa sababu ya kuyaomba Shufaa. Na lau ingelikuwa kuyaomba Masanamu Shufaa ni kuyaabudu na ni ibada basi kusingelikuwa na haja ya kuleta sentensi nyingine: “Wanasema hawa ndio waombezi wetu” baada ya kauli yake: “Na wanaabudu” bila shaka huko kungelikuwa ni kurudia sentensi bila faida. Hakika kuunga sentensi ya pili katika sentensi ya kwanza inajulisha kwamba kuna tofauti kati ya hizo mbili, aidha Aya haijulishi kwamba kuyaomba masanamu Shufaa ilikuwa ni ibada, seuze kuwaomba Shufaa Mawalii wachaji Mungu. Ndio kuyaomba masanamu Shufaa kulikuwa ni kuyaabudu hayo kwa dalili zingine. 2. Hakika kuna tofauti kati ya aina mbili za uombaji Shufaa wa waabudu Masanamu ambapo walikuwa wakiamini kwamba sanamu ndio Mola wao mmiliki wa Shufaa, ana uwezo wa kutoa Shufaa kwa yeyote na kwa namna apendavyo, na uombaji Shufaa kwa itikadi hii ni Shirki, na kwa ajili hiyo Mwenyezi Mungu katika kukosoa itikadi hiyo anasema: “Sema: Uombezi wote ni kwa Mwenyezi Mungu...” (39:44) 186


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 187

Tawhid na Shirk Na hali ya kuwa Waislamu hawaitakidi kwamba Mawalii wao wanamiliki sifa hiyo, kwani wao husoma usiku na mchana maneno ya Mola Manani: “Ni nani awezaye kuombea mbele yake bila ya idhini yake?” (2:255) Pamoja na tofauti hiyo ya dhahiri kabisa, na hilo liko wazi wazi vipi usihi ulinganishaji huo? Na dalili inayojulisha kwamba washirikina walikuwa wakiamini kuwa Masanamu yao yanamiliki Shufaa kuna mambo mawili: La kwanza: Qur’an imetilia mkazo katika Aya hizo kwamba utoaji Shufaa kwa mhusika una sharti la kupata idhini ya Mwenyezi Mungu na kuridhiwa hilo. Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema: “Ni nani awezaye kuombea mbele yake bila ya idhini yake?” (2:255) Anasema:

“Hakika Mola wenu ni Mwenyezi Mungu ambaye ameziumba mbingu na ardhi katika nyakati sita, kisha ukakamilika (uumbaji wake) katika Arshi, anaendesha (kila) jambo, hakuna muombezi ila baada ya idhini Yake, huyo ndiye Mwenyezi Mungu Mola wenu, basi mwabuduni, Je hamkumbuki?” (10:3) Na anasema:

''Siku hiyo uombezi hautafaa ila wa aliyemruhusu Mwingi wa rehema na akamridhia kusema'' (20:109) Na anasema: “Na wako Malaika wangapi mbinguni ambao uombezi 187


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 188

Tawhid na Shirk wao hautafaa chochote isipokuwa baada ya Mwenyezi Mungu kumpa amtakaye na kumridhia.” (53:26) Anasema: “Anajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao na hawamuombei yeyote ila yule anayemridhia, nao kwa kumuogopa Yeye wananyenyekea” (21:28) La pili: Qur’an inatilia mkazo kwamba Masanamu hayamiliki Shufaa bali hiyo ni haki kwa aliyepewa. Mwenyezi Mungu anasema: “Wala hawana uwezo wa uombezi wale wanaowaabudu badala Yake, ila anayeishuhudia haki, nao wanajua” (43:86) Anasema: “Hawatakuwa na mamlaka ya kufanya uombezi ila yule aliyeshika ahadi kwa Rahmani.” (19:87) Kwa hakika Shufaa halisi ni haki kwa mmiliki wake, na sio mwingine isipokuwa Mwenyezi Mungu, kama Aya za Qur’an zilivyoeleza kinaga ubaga kuhusu hilo, na ama washirikina wao walikuwa wakiitakidi kuwa Masanamu yao yanamiliki uhai wao, na kwa ajili hiyo basi wakawa wanayaabudu. Na pili wakawa wanayaomba yawaombee Shufaa kwa Mwenyezi Mungu. Kweli dhahiri ya maneno ya Mwenyezi Mungu: “Hawatakuwa na mamlaka ya kufanya uombezi ila yule aliyeshika ahadi kwa Rahmani.” (19:87) Na: “Wala hawana uwezo wa uombezi wale wanaowaabudu badala Yake, ila anayeishuhudia haki, nao wanajua.” (43:86) ni kwamba watu ambao wamechukua ahadi na kushuhudiliwa kwa haki wanamiliki haki ya Shufaa. Lakini makusudio ya umiliki katika Aya mbili hizo ni upewaji idhini kulingana na fuo la maneno la Aya zilizotangulia, sio umiliki wa kujitege188


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 189

Tawhid na Shirk mea na kuachiwa kabisa bila Mwenyezi Mungu kuhusika, yaani Tafwiidhi, la sivyo ingelilazimu kuwepo tofauti na ukinzani baina ya maana za Aya. Ama yale yaliyopokewa na kuelezwa katika sira na historia kwamba washirikina walikuwa katika kuhirimia na kutufu wakisema: “Huna mshirika, yote ni yako unammiliki na anayomiliki.”84 hudhaniwa mambo mawili: Kwa hiyo unadhihirika udhaifu wa utoaji dalili kwa kutumia Aya ya pili nayo: “Hatuyaabudu isipokuwa yatukurubishe kwa Mwenyezi Mungu” kwani Muhammad bin Abdul-Wahab amechukulia maana ya maneno ya Mwenyezi Mungu: “Hatuyaabudu hayo” ni kuyaomba Shufaa, ilihali ni kwamba Aya iliyotangulia inaeleza wazi hakuna uhusiano kabisa kati ya ibada na kuomba Shufaa. Ndio inawezekana ikawa ni ibada iwapo muombaji atamfanya muombwa kuwa ni mungu au mungu mdogo kama ilivyokwishatangulia. Ama yale aliyokiri Muhammad bin Abdul-Wahab katika maneno yake kwamba Mwenyezi Mungu amempa Nabii wake Shufaa lakini amewakataza watu kuomba toka kwake, ni jambo la kushangaza sana kwamba hakuna hata Aya moja wala Sunna ya Mtume (s.a.w.w) inayojulisha juu ya kukatazwa huko, ni jambo la kustaajabisha hata kwa mujibu wa akili, mfano apewe maji mgawaji maji kisha wakatazwe watu kumuomba yeye hayo maji, au ampe Mtume wake hodhi ya maji kisha awakataze watu au umma wake kumuomba. Na maneno yake (s.w.t): “Basi usimuombe pamoja na Mwenyezi Mungu yeyote” ambayo ni Aya ya tatu katika hoja za Muhammad bin Abdul-Wahab ambazo amezitoa utapata faida yake na maana yake muda mfupi ujao, na tutabainisha kwamba makusudio ya ulinganio na wito katika Aya iliyotangulia ni ibada, hivyo maana ya: “Msimuombe yeye” ina84. Milal wa Nihal Juz. 2 Uk. 255. 189


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:24 PM Page 190

Tawhid na Shirk kuwa ni ”msimwabudu pamoja na Mwenyezi Mungu mwingine”, hivyo uharamu ambao ameukataza ni kumwabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu, na si kila kumuomba asiyekuwa Mwenyezi Mungu, na kuomba Shufaa sio jambo lingine bali ni kumwomba asiyekuwa Mwenyezi Mungu, na tofauti kati ya mambo mawili haya ni kama vile mbingu na ardhi. Na kwa hivyo unadhihiri udhaifu wa hoja na dalili ya nne ya Muhammad bin Abdul-Wahab katika upambanuzi wa utata na mkanganyiko, na yaliyopatikana katika hoja zake ni: “Hakika kumuomba Shufaa muombezi hupingana na ikhlasi katika wajibu wa kumpwekesha Mwenyezi Mungu (Tawhiidul-wajib) uliyopo katika maneno yake: “Wenye kumtakasa yeye na dini.”85 Jibu ni kwamba: Hakika kumuomba Shufaa mtu aliyeidhinishwa na kuridhiwa na Mwenyezi Mungu sio kumuabudu muombwa mpaka kupingane na Tawhiid katika ibada ya Mwenyezi Mungu, bali ni maombi kama maombi mengine kwake. Kwa hakika ikhlasi ni sharti katika ibada, na si katika kuomba kitu toka kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t), kama ambavyo pia haipingani na kitendo cha kumwomba Mwenyezi Mungu, kwani kumuomba Shufaa mtoaji Shufaa ni kumuomba Mwenyezi Mungu (s.w.t), na si kumuomba zaidi ya Mwenyezi Mungu …hivi kuna tatizo gani kwa mpendwa msomaji? Ni jambo la ajabu kutafsiri kwamba kuomba Shufaa kutoka kwa Mtume au mwingine ni kumuomba Mtume pamoja na Mwenyezi Mungu kama ilivyokuja katika maswali ya Sheikh Ibnu Balhiji ambaye ni Kadhi Mkuu miongoni mwa wanachuoni wa Madina, anasema: “Na ambayo hufanywa na wajinga katika kaburi kwa kugusa na kumuomba pamoja na Mwenyezi Mungu.” Ni dhahiri katika maneno yake kuna udhaifu mkubwa. Kwanza: Ama watu ambao wanafanya tawassuli katika makaburi ya 85. Limenukuu Jarida Ummul-Qura toleo la 69 tarehe 17 mfungo mosi mwaka 1344 kuna maswali na majibu. 190


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 191

Tawhid na Shirk wachamungu hawamshirikishi mwingine katika dua (ambayo ndio kiini cha ibada), na hawamuombi mwingine ila Mwenyezi Mungu mmoja Mtenza nguvu. Wao huwaomba Mawalii wao waunganishe dua zao pamoja na dua za wafanya tawassuli, kwa hivyo wao hushirikiana nao katika kumuomba Mwenyezi Mungu ili haja zao zikubaliwe, na lau kama si hivyo uombaji Shufaa usingelikuwa na maana. Kwa hakika Shufaa imechukuliwa kutokana na neno Shufu’a kama tulivyosema - ambayo kinyume chake ni witri, kwa hivyo mtu humuomba Walii achanganye dua hiyo pamoja na dua yake na ajumuike naye katika amali yake, sasa ipo wapi hali ya kumshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu kingine katika dua? Pili: Hakika Waislamu hawayaombi makaburi, bali wanamuomba aliye kaburini, aliyopo kaburini hushirikiana nao katika dua, kwani ana hadhi na heshima kubwa mbele ya Mola wake na anaruzukiwa kwa mujibu wa Aya za Qur’an hata kama ni maiti, na kwamba wao hawarudishi maombi na dua zao. Mwenyezi Mungu kwa daraja alilonalo Mtume (s.a.w.w) anasema:

“Na hatukumpeleka Mtume yeyote ila apate kutiiwa kwa amri ya Mwenyezi Mungu, na lau wangelikujia walipodhulumu nafsi zao wakaomba msamaha kwa Mwenyezi Mungu, na Mtume akawaombea msamaha, bila shaka wangemkuta Mwenyezi Mungu ni Mwenye kupokea toba na ni Mwenye huruma” (4:64) Anasema tena:

191


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 192

Tawhid na Shirk “Chukua sadaka katika mali zao, uwasafishe na uwatakase kwa hizo (sadaka zao) na uwaombee, hakika dua yako ni utulivu kwao, na Mwenyezi Mungu ndiye Asikiaye, Ajuaye” (9:103) Kisha inadhihiri kutoka kwa Ibnu Taimiyyah katika baadhi ya barua zake86 na kutoka kwa mwanafunzi wake Muhammad bin Abdul-Wahab katika risala yake aliyoipa jina Arbaa Qawaaid “kanuni nne.”87 Kwamba hao wawili wamejaribu kuthibitisha uharamu wa kuomba Shufaa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu kwa kutumia maneno ya Mola Manani: “Sema: Uombezi wote ni wa Mwenyezi Mungu, ufalme wa mbingu na ardhi ni Wake, kisha mtarejeshwa kwake.” (39:44); kana kwamba uthibitishaji wa hoja umejengeka kwa maana ya Aya nao ni: ”Allah ndiye apasaye kuombwa Shufaa pekeyake”. Lakini huko ni kutafsiri Aya kinyume na dhahiri yake, kwani Aya haimaanishi Mwenyezi Mungu ndiye pekee ambaye anaombea na hapana mwingine anayeombea, kwa sababu Mola manani aliyetukuka haombei kwa yeyote (bali Yeye ndiye anayeombwa), kisha ni kwamba imethibiti kuwa Mtume, watu wema na malaika wanaomba Shufaa Kwake. Kama vile ambavyo si maana yake kwamba haifai kuomba Shufaa isipokuwa kwa Mola aliyetukuka, bali maana yake ni kwamba hakika Mwenyezi Mungu ndiye mmiliki wa jambo hilo na hawezi yeyote kutoa Shufaa isipokuwa kwa idhini Yake. Mwenyezi Mungu anasema: “Ni nani ambaye anatoa Shufaa kwake yeye isipokuwa kwa idhini Yake” na akasema: “Wala hawatoi Shufaa ila mwenye kumridhia” na inabainika kutokana na hayo tuliyoyasema kwamba pindi tutakapochunguza mwanzo wa Aya ifuatayo: “Au wamejifanyia waombezi kinyume cha Mwenyezi Mungu? Sema: Ingawa haw86. Risalat "Ziyaratul-Qubuur Wal-Istighathat Bil-Qubuur Uk. 156". 87. Kashfu Irtiyab Uk. 240-241 na Kashfu Shubuhat Uk. 8 cha Muhammad bin Abdul-Wahab. 192


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 193

Tawhid na Shirk ana mamlaka juu ya kitu chochote wala hawatambui? Sema Uombezi wote ni kwa Mwenyezi Mungu, ufalme wa mbingu na ardhi ni Wake, kisha mtarejeshwa kwake” (39:43-44); tutakuta sehemu ya mwisho ya Aya inahusu kuwakanya wale wenye kuyafanya masanamu na mawe kuwa waombezi kwa Mwenyezi Mungu na wakasema: Hawa ndio waombezi wetu kwa Mwenyezi Mungu pamoja na kuwa hayakuwa yanamiliki chochote, na vipi yawe yanamiliki Shufaa ilhali hayana akili hadi yatoe Shufaa!! Zamakhshari katika kitabu chake Kashafu anasema: “Asiyekuwa Mwenyezi Mungu” yaani bila idhini Yake: “Sema Shufaa yote ni ya Mwenyezi Mungu” yaani mmiliki wake, hivyo yeyote hatoombea ila kwa masharti mawili:- Mwenye kuombewa awe ameridhiwa, na mwenye kuomba Shufaa awe ameruhusiwa, na hapa masharti yote mawili hayapo.”88 Na aliyoyaamini Muhammad bin Abdul-Wahab na Mwalimu wake Ibnu Taimiyyah aliyemtangulia pamoja na wafuasi wao pia, kwamba Aya hiyo inajulisha juu ya maombi ya Shufaa kwamba hafanyiwi yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu pekee, pasi na kuiomba kwa viumbe wake hata kama ana haki ya Shufaa, hilo halijasemwa na mfasiri yeyote. Kisha vipi inawezekana kutofautisha kati ya maombi ya Shufaa kutoka kwa aliye hai na maombi ya Shufaa kwa maiti (mfu), la kwanza lijuzu kwa maneno ya Mola Muweza: “Na lau wangelikujia walipojidhulumu nafsi zao wakaomba msamaha kwa Mwenyezi Mungu, na Mtume akawaombea msamaha, bila shaka wangemkuta Mwenyezi Mungu, Mwenye kupokea toba, Mwenye kurehemu” (4:64) Na kwa dalili ya ombi la watoto wakubwa wa Nabii Yaqub (a.s.) kwa baba yao kuhusu Shufaa: “Wakasema: Ewe baba yetu tuombee msamaha kwa dhambi zetu, hakika sisi tulikuwa wenye makosa.” (12:97); na 88. Tafsirul-Kashaf Juz. 3 Uk. 34. 193


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 194

Tawhid na Shirk Nabii Yaqub (a.s.) akawaahidi hayo kwa kuwaombea, lakini la la pili, yaani kumuomba hilo maiti lisijuzu? Je! Inawezekana uhai na kifo vikaathiri asili ya kitendo? Ilihali imeshatangulia hapo kabla kuwa uhai na kifo sio kigezo cha Tawhiid na Shirki, na si kigezo cha kuruhusiwa au kutoruhusiwa. Na utakapochunguza vitabu vya Mawahabi utaona ambacho kimewafanya wawe katika makosa na mgawanyiko ni kushabihisha amali ya wanatawhiid katika kuomba Shufaa na kuwaomba msaada na kufanya tawassuli kwao, na ile amali ya washirikina kwa masanamu yao, na hilo limewafika kwa kuangalia dhahiri ya mambo na kughafilika na nia na yaliyo katika dhamira. Na wewe mpendwa msomaji lau utachunguza kwa makini yale yaliyomo katika maudhui hizi utaona tofauti kati ya amali hizo mbili kwa vidokezo mbalimbali baadhi ya hivyo ni: i. Hakika Washirikina walikuwa wakisema kwamba masanamu ni miungu kwa maana ambayo imeshatajwa hapo kabla, tofauti na wanatawhiid (wenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu). ii. Hakika masanamu hayakuwa na uwezo wa kuitikia maombi yao, na hilo linatofautiana na roho takatifu, hakika uhai wake umeelezwa na kitabu kitukufu cha Mwenyezi Mungu na zina uwezo wa kuitikia maombi yao. iii. Hakika masanamu hayajaidhinishwa na kuruhusiwa na Mwenyezi Mungu, tofauti na Mtume (s.a.w.w), yeye ameidhinishwa kwa Aya za Qur’an tukufu. Mwenyezi Mungu anasema: “Na katika usiku amka kwa (kusoma) Qur’an ni (ibada) zaidi kwako huenda Mola Wako akakuinua cheo kinachosifika.” (17:79) na mahala patukufu kwa itifaki ya wafasiri ni kupewa cheo cha kutoa Shufaa. 3. JE! KUMWOMBA MSAADA ASIYEKUWA MWENYEZI MUNGU NI SHIRKI? Hakika kumuomba msaada asiyekuwa Mola Manani huenda kukapatikana katika aina mbili nazo ni: 194


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 195

Tawhid na Shirk I. Tumuombe mtendaji – sawa awe ni wa kawaida au sio wa kawaida huku tukiitikadi kwamba amali yake hutegemea Mwenyezi Mungu, hii ina maana kwamba yeye ana uwezo wa kuwasaidia waja na kuondoa matatizo yao kwa uwezo ambao alioupata kutoka kwa Mola Muweza na kwa idhini Yake. Na aina hii ya uombaji msaada kwa hakika inafungamana na kumuomba Mwenyezi Mungu kwa dhati yake, kwani inaambatana na imani ya kwamba uwezo huo amepewa na Yeye, na wakati wowote akipenda huuchukua, na mkulima anapotenda kwa msaada wa pembejeo na nyenzo zingine za kimaumbile kama vile jua, maji na ulimaji wa ardhi kwa hakika anakuwa amemuomba Mola Manani kwa sababu Yeye ndiye aliyempatia nyenzo hizo katika uoteshaji wa mimea, ukuaji wa mche na utoaji mazao. II. Na atakapotumia binaadamu nyenzo au hali ya kimaumbile ya kawaida au isiyokuwa ya kawaida huku akiitakidi kwamba nyenzo hizo zinajitegemea katika kuwepo kwake au katika utendaji kazi wake, hapana shaka itikadi yake hiyo itakuwa ni Shirki na uombaji huo utakuwa ni Shirki, aidha uombaji huo utakuwa ni ibada. Na iwapo mkulima atakapotenda kutumia nyenzo na pembejeo zilizotajwa hali ya kuwa anaamini zinajitegemea katika utendaji na utoaji athari wake au zinajitegemea katika kuwepo kwake, kwa hakika atakuwa amefanya Shirki na maombi yake yatakuwa ni ibada. MWANDISHI WA AL-MANAAR NA MAELEZO YAKE KUHUSU UOMBAJI MSAADA Hakika mwandishi wa Tafsiri Al-Manaar amefikiri kwamba maana ya Tawhiid ni: Tutumie nguvu yetu na tusaidiane kati yetu katika daraja la kwanza, kisha mambo yote tumwachie Mwenyezi Mungu Muweza wa kila kitu, na tumuombe Yeye tu na sio mwingine, kuhusu hayo anasema: “Ni wajibu kwetu kufanya yale tunayoweza kwa umakini zaidi na kwa ufanisi mkubwa, tusaidiane baina yetu na tumkabidhi Mola Muweza wa kila kitu yale ambayo hayapo katika uwezo wetu na tuombe msaada katika vitendo 195


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 196

Tawhid na Shirk ambavyo athari yake ni kutoka kwa Mola Subhaanahu Wataala na sio mwingine.”89 Hivi! ni sahihi kwamba ni lazima kwetu tufaidike tu na uwezo wetu au nyenzo na uwezo wa kimaumbile. Kuna mlolongo wa sababu zisizo za kawaida ambazo zote hizo hutoka kwa waja wema wa Mwenyezi Mungu ambao wana uwezo wa kuwasaidia wale wenye kuwaomba msaada 90 kwa masharti maalum na kwa idhini ya Mwenyezi Mungu pasi na hao kuwa ni wenye kujitegemea katika kuwepo kwao na mambo yao, kwa hivyo mtu huyo atakapoutumia uwezo huo usio wa kawaida pamoja na itikadi iliyotajwa hapo kabla, utumiaji wake hautokuwa ila ni amali sahihi bali ni katika kumtegemea na kumuomba msaada Mwenyezi Mungu. Vivyo hivyo katika aina mbili hizo za uombaji msaada ”utumiaji wa nyenzo za kawaida na kuwatumia waja wema wa Mwenyezi Mungu” hakuna tofauti hata kidogo. Ikiwa utumiaji wa nyenzo za waja wema kwa aina tuliyotaja – utakuwa ni Shirki basi ingelilazimu utumiaji nyenzo wa aina ya kwanza kuwa Shirki pia, na kutofautisha kati ya utumiaji wa nyenzo za kawaida na zisizo za kawaida itakapokuwa kipimo ni kimoja na muelekeo ni mmoja nao ni ule wa kutegemea uwezo wa Mwenyezi Mungu kwa idhini Yake na utashi Wake, kwa kudai kwamba utumiaji wa kwanza ni Tawhiid na wa pili si Tawhiid, ni utofautishaji usio na dalili. Kwa ubainifu huo bila shaka limebainika lengo la makundi mawili ya Aya kuhusiana na suala la uombaji msaada kama ifuatavyo: Kundi la kwanza: Linabainisha kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t) pekee ndiye anayestahiki kuombwa msaada, na linamzingatia kuwa ndiye nyenzo na msaada pekee na sio mwingine. 89. Al-Manaar Juz. 1 uk. 59. 90. Utafiti umejikita katika suala la kuomba msaada katika hali hii je ni Shirki? Ama suala la je! Wamepewa uwezo wa kutoa msaada au hapana, hilo liko nje ya maudhui yetu. 196


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 197

Tawhid na Shirk Kundi la pili: Linatuelekeza tufuate mlolongo wa mambo maalum yasiyokuwa Mwenyezi Mungu, na linayazingatia mambo hayo kuwa ni nyenzo na msaada sambamba na Mwenyezi Mungu (s.w.t). Nasema: Kutokana na ubainifu uliopita imeeleweka mtazamo wa kijumla kati ya aina mbili za Aya. Unabainisha kwamba hakuna kabisa msigano na mgongano baina ya makundi hayo mawili, isipokuwa kuna kundi la watu linashikamana na fungu la kwanza la Aya, na hapo hukosoa uombaji msaada kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu, kisha wao hudharurika kutumia zile Aya ambazo zinazungumzia kuomba usaidizi kwa Mwenyezi Mungu, kukiengua kile �kitendo cha uombaji msaada kupitia uwezo wa kibinadamu na sababu za kimada�. Kwa maana nyingine ni kwamba wao wanasema: Hakika kutumia au kutaka usaidizi toka kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu haijuzu na haifai isipokuwa katika mazingira ambayo Mwenyezi Mungu ametoa idhini kufanya hivyo, kwa maana hiyo kuomba usaidizi toka kwenye uwezo wa kibinadamu na ule wa nyenzo za kawaida ijapokuwa ni kuomba usaidizi toka kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu, lakini kwa hapo imeruhusiwa kisheria kwa aina ya umakhsusi. Kwa kweli jambo hilo halimridhishi mwanatawhiid, kwani lengo la Aya hizo sio hivyo kabisa, kwani Aya hizo zinalingania jambo moja, nalo ni kutoomba usaidizi toka kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu, na hivyo uombaji usaidizi toka kwenye nyenzo nyingine ni lazima uwe haupingani na uombaji usaidizi toka kwa Mwenyezi Mungu, bali inabidi iwe katika namna ambayo uombaji usaidizi toka kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu uwe ndio uombaji usaidizi toka kwa Mola Mwenyezi na sio toka kwa mwingine. Na kwa ibara nyingine: Hakika Aya hizo zinataka kusema: Msaidizi na msaada wa pekee ambao kila msaidizi na msaada umeegemea Kwake ni uwezo Wake Mwenyezi Mungu na athiri Yake, lakini pamoja na hivyo 197


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 198

Tawhid na Shirk Mwenyezi Mungu ameusimamisha ulimwengu huu katika mfumo wa sababu mbalimbali ambazo hufanya kazi kwa uwezo na amri Yake Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo uombaji usaidizi na msaada toka kwenye sababu hizo unakuwa ni kuomba usaidizi na msaada toka kwa Mwenyezi Mungu, kwani kuomba usaidizi toka kwenye tawi ni kuomba usaidizi toka kwenye asili yake na shina lake. Na zifuatazo ni baadhi ya Aya zinazotoa ishara kuhusiana na makundi hayo mawili, nazo ni:

“Na Mwenyezi Mungu hakufanya ila ni bishara kwenu, na zipate tumaini nyoyo zenu, na msaada hautoki (popote) isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Mwenye hekima.” (3:126) Na akaendelea kusema: “Wewe tu tunakuabudu, na kwako tu tunataka msaada.” (1: 5) Akasema tena: “Na Mwenyezi Mungu hakufanya haya ila iwe habari ya furaha na ili nyoyo zenu zitue kwayo, na hakuna ushindi ila utokao kwa Mwenyezi Mungu tu, hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye nguvu, mwenye hekima.” (8:10) Aya hizo zinahusiana na mifano ya kundi la kwanza, na zifuatazo zinahusu kundi la pili ambalo hutulingania sisi kutafuta usaidizi kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) miongoni mwa nyenzo na sababu kadhaa, Qur’an tukufu inasema: “Na ombeni msaada kwa subira na Swala na kwa hakika jambo hilo ni gumu isipokuwa kwa wanyenyekevu” (2:45) Inasema tena: “Na saidianeni katika mema na takwa wala msisaidiane 198


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 199

Tawhid na Shirk katika dhambi na uadui...” (5:2) Na inasema: ”Akasema: Yale ambayo Mola wangu amenimakinishia ni bora, lakini nisaidieni kwa nguvu, nitaweka boma baina yenu na wao.” (18:95) Ikasema tena: “Na kama wakiomba msaada kwenu katika dini, basi ni juu yenu kuwasaidia, isipokuwa juu ya watu ambao yapo mapatano kati yenu na wao na Mwenyezi Mungu anayaona mnayoyatenda” (8:72) Na ufunguo wa ufumbuzi na utatuzi wa ukinzani wa makundi hayo ya Aya ni maelezo tuliyoyaeleza huko nyuma na huu ni muhtasari wake: Hakika katika ulimwengu yupo muathiri kamili na mkuu, mwenye kujitegemea wa pekee wala sio wengi, ni mwenye kujitegemea katika kuwepo kwake na katika vitendo vyake, naye sio mwingine bali ni Mwenyezi Mungu (s.w.t). Na ama nyenzo nyingine zote zahitajia na ni tegemezi katika kuwepo kwake na katika vitendo vyake, zinahitajia toka kwa Mola. Zinafanya mambo kwa idhini Yake, utashi Wake na uweza Wake. Na lau zisingelipatiwa uwezo huo zisingeliweza kufanya lolote lile. Kwa hivyo usaidizi wa hakika katika kila hatua mbalimbali kwa ukamilifu ni wa Mwenyezi Mungu, na haifai kupata usaidizi kwa yeyote na kumuona ni nyenzo yenye kujitegemea. Kwa mtazamo huo ndiyo maana ukahusishwa uombaji huo na Mola Muweza pekee. Lakini hilo halizuii kabisa kuomba usaidizi kutoka kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu kwa kuzingatia kwamba ni tegemezi, yaani anatoa usaidizi au anafanya jambo fulani kwa kutegemea uwezo wa Mwenyezi Mungu, na lililo dhahiri ni kwamba uombaji usaidizi kama huu hautofautiani na uombaji usaidizi toka kwa Mwenyezi Mungu, na hiyo ni kwa sababu mbili: 199


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 200

Tawhid na Shirk Ya kwanza: Uombaji usaidizi toka kwenye nyenzo nyingine sio kuingilia uombaji usaidizi ulio makhsusi kwa Mwenyezi Mungu, kwani uombaji usaidizi ulio makhsusi kwa Mwenyezi Mungu ni: “pale tunapoomba huku tukiitakidi kwamba hicho tunachokiomba msaada ni muweza kwa dhati yake na hakitegemei kwa mwingine.” Wakati usahihi ni kwamba sisi tunapoomba usaidizi toka kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu huwa tunaitikidi kwamba msaidizi ni muweza, lakini anategemea uwezo toka kwa Mwenyezi Mungu, wala hajitegemei kidhati. Na kwa kweli hiyo ni aina nyingine ya uombaji usaidizi. Hii ina maana kwamba, ikiwa uombaji usaidizi wa aina ya kwanza ni maalum na makhsusi kwa Mwenyezi Mungu, hiyo haijulishi kwamba uombaji usaidizi wa aina ya pili ni makhsusi kwake Yeye pia. Ya pili: Hakika uombaji usaidizi kama huu hautofautiani na uombaji usaidizi toka kwa Mwenyezi Mungu, bali huo ni uleule uombaji usaidizi toka kwa Mwenyezi Mungu, na wala si kitendo kilicho nje ya mtazamo wa mwanatawhiid ambaye anaona ulimwengu wote huu ni katika kazi za Mwenyezi Mungu. Kutokana na maelezo yaliyotangulia imebainika kwako mpendwa msomaji jibu la mushkeli uliyopo katika maneno ya Ibn Taimiyyah pale aliposema: “Ama mwenye kukiri yaliyothibiti katika Qur’an, Sunna na Ij’maa (mkusanyiko wa rai za wanazuoni) kuhusiana na Shufaa yake, na tuwassuli yake na yanayofanana na hayo. Lakini akasema: Hamuombi ila Mwenyezi Mungu, na kwamba mambo ambayo hayawezi mwingine isipokuwa Yeye hamuombi mwingine ila Yeye, kwa mfano kusamehe dhambi, kuongoza nyoyo, kuteremsha mvua au kutoleta mvua, kuotesha mimea na yanayofanana na hayo, hilo ni sawa, bali halina mzozo baina ya waislamu pia. Mwenyezi Mungu anasema: “Ni nani anayesamehe dhambi ila Mwenyezi Mungu,” Na anasema: “Hakika wewe humuongozi umpendaye lakini Mwenyezi Mungu humuongoza amtakaye,” 200


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 201

Tawhid na Shirk Na anasema: “Enyi watu kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu kwenu je! yupo muumbaji asiyekuwa Mwenyezi Mungu? Anakuruzukuni katika mbingu na ardhi.” Na “Wala Mwenyezi Mungu hakujaalia ila bishara kwenu na ili nyoyo zenu zipate utulivu, na hakuna ushindi isipokuwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu,” Na anasema: “Msipomnusuru yeye, ameshakwisha kumnusuru Mwenyezi Mungu walipomtoa wale waliokufuru, wakiwa wawili katika pango pindi aliposema kumwambia rafiki yake: usihuzunike, hakika Mwenyezi Mungu yupo pamoja nasi.”91 Ibn Taimiyyah ameghafilika na baadhi ya mambo hayo; kwani inawezekana kumuomba asiyekuwa Mola Manani huku ukiitakidi kwamba huyo unayemuomba hajitegemei katika kufanikisha hilo, na hili halipingani na kitendo cha kumuomba Mwenyezi Mungu huku ukiamini kwamba Yeye ndiye anayejitegemea na kujitosheleza katika ufanikishaji. Ndio, uombaji huo wa usaidizi hautokuwa wenye kutoa faida isipokuwa pale tu itakapothibiti uwezo wa huyo asiyekuwa Mwenyezi Mungu katika ufanikishaji maombi. Lakini hilo liko nje ya mada yetu, kwani kiini cha maudhui yetu ni je kutaka msaada toka kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu ni Shirki au hapana, ama kuhusu je muombwa ni muweza wa hilo au hapana, hilo liko nje ya mada yetu. Na huenda ikadhaniwa kwamba hata kama ana uwezo lakini hanufaishi isipokuwa kwa kuidhinishwa na Mola Manani aliyetukuka, kama ambavyo hata kama uombaji msaada huo si Shirki lakini inahitajika pia ipatikane idhini ya kumuomba msaada utokanao na uwezo huo. Tunasema: Hilo halikubaliki, hakika kitendo cha kupewa uwezo ni dalili ya 91. Majmu'at Rasail Kubra Uk. 382 cha Ibn Taimiyyah barua ya 12. 201


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 202

Tawhid na Shirk kuidhinishwa katika matendo yake kwa ujumla, kwani hakuna maana kiakili Mwenyezi Mungu ampe uwezo mhusika na kisha amzuie kabisa kufaidika nao na kufaidisha wengine. Na inatosha kuthibitisha ufaaji wa jambo hilo, kwamba vitendo vya viumbe kiasili huwa vimeruhusiwa kisheria, hadi pale inapopatikana moja kati ya anwani mbili: haramu au hairuhusiwi. Mwisho tunamkumbusha mpendwa msomaji kuwa mtunzi wa kitabu cha Al Manaar vyovyote itakavyokuwa hakufikiri juu ya uombaji msaada toka kwenye roho takatifu ila sura moja, na kwa sura hiyo akazingatia kuwa kufanya hivyo ni Shirki, akasema: “Na hadi hapa mnajua kwamba wale ambao wanawaomba watu wa makaburini ili wawakidhie haja zao, kuwafanyia wepesi mambo yao, kuponya maradhi yao, kustawisha mazao na mashamba yao, kuangamiza maadui na mengineyo miongoni mwa mambo yenye maslahi, huko ni kutoka nje ya mipaka ya Tawhiid na kukengeuka utajo wa Mwenyezi Mungu.�92 Ni wazi maelezo hayo si sahihi, kwani utakaji msaada toka kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu una namna mbili: Moja ni Tawhiid halisi na nyingine ni Shirki. Moja inakurubisha na kutukumbusha Mwenyezi Mungu, hii ni ile aina ya kwanza, na nyingine hutuweka mbali na Mwenyezi Mungu, na hii ni ile aina ya pili. Hakika kigezo na kipimo na kitenganishi cha Tawhiid na Shirki si kule kuwa ni sababu za dhahiri au kutokuwa ni sababu za kidhahiri, bali hakika kigezo, kipimo na kitenganishi ni kujitegemea na kutojitegemea, ni kujitosheleza na kuhitajia, ni asili na kutokuwa asili. Hakika kuziomba msaada nyenzo zisizojitegemea bali hizo humtegemea Mwenyezi Mungu, hazifanyi wala kuathiri lolote isipokuwa kwa idhini Yake (s.w.t) sio kwamba kunasababisha kughafilika na Mwenyezi Mungu, 92. Al-Manaar Juz. 1 Uk. 59. 202


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 203

Tawhid na Shirk bali hilo ni jambo la heri ambalo huleta kumkumbuka Mola Manani, hii ina maanisha kwamba sababu zote na vyanzo vyote huishia Kwake. Pamoja na hayo, iweje mwandishi wa kitabu cha Al-Manaar aseme: “Hao wameghafilika na Mwenyezi Mungu,” na lau kutaka msaada kwa namna hiyo kungelazimu kughafilika na kumsahau Mwenyezi Mungu basi ingelazimu kwamba kutumia sababu za kimaada za kawaida nako kusababishe kumsahau Yeye. Na lakushangaza zaidi kuhusu hilo ni maneno ya Sheikh wa Azhar Sheikh Mahmud Shaltut ambaye amenukuu - kuhusiana na kadhia hii – maneno ya Abdih bila kuongeza wala kupunguza na akahitimisha suala hilo kwa maneno hayo, akachukua dhahiri ya takhsisi iliyopo kwenye ibara: “Kwako wewe tu tunakuomba msaada,” akighafilika uhakika wa Aya nyingine zenye kuelezea wazi suala la uombaji msaada.93

UKOSOAJI WA NADHARIA YA TATU Ipo rai nyingine ambayo huwa kati ya rai mbili nayo ni kwamba inaruhusiwa kisheria kuomba mahitaji ya kibinadamu kupitia sababu za kawaida, na wala haifai kuomba kupitia sababu zisizo za kawaida, isipokuwa kwa njia ya tawassuli na Shufaa kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t). Na kauli hii hata kama ina haki na ukweli lakini ina kasoro, kwa nini izuiliwe kuomba kupitia sababu zisizo za kawaida? Ikiwa ni kwa sababu inalazimu Shirki kauli hiyo si sahihi, kwani muombaji anapoomba huitakidi kwamba uwezo alionao muombwa amepatiwa na Mwenyezi Mungu (s.w.t), naye anafanya kwa idhini na utashi wa Mola, na uombaji msaada wa aina hii haupelekei Shirki. Na hata kama ikajaaliwa hivyo kwamba ni Shirki, kuna tofauti gani baina ya uombaji msaada uliokatazwa ambao ni kutotumia sababu zisizokuwa za kawaida na ule ulioruhusiwa ambao ni 93. Tafsir Shartut Uk. 36-39. 203


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 204

Tawhid na Shirk Tawassuli na Shufaa? Na ikiwa inazuiwa kufanya hivyo kwa ajili ya wahusika kutokuwa na uwezo wa kusaidia, huo ni mjadala mwingine ambao uko nje ya maudhui yetu, kwani mada inahusiana na kujaalia wahusika wana uwezo wa hayo. Na lau uzuiaji ungelikuwa ni kwa ajili ya maneno ya Mwenyezi Mungu (s.w.t): “Na kwako wewe tu tunaomba msaada” ambayo yanaelekeza kuomba msaada Kwake kama tulivyoliweka wazi hilo hapo kabla, basi haiwezekani kuhusisha tawassuli na uombaji Shufaa, kwa sababu ulimi wake unakataa kulihusisha hilo. Lakini ukweli ni kama tulivyofafanua hilo huko nyuma. 4. JE! KUWAOMBA WATU WEMA NI KUWAAABUDU WAO? Katika maudhui zilizotangulia imebainika kwamba uombaji haja toka kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu na kuitakidi kuwa hamiliki chochote katika mambo ya kiungu, aidha hakuachiwa afanye lolote atakavyo, bali hatendi jambo lolote isipokuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (s.w.t), uombaji huo si Shirki. Na katika kadhia hii yapo maelezo mengine nayo ni: Hakika Qur’an tukufu imekataza – katika sehemu mbali mbali – kumuomba asiyekuwa Mwenyezi Mungu, lakini Mawahabi huona Aya hizi zinasababisha maombi kuwa ibada. Na zifuatazo ni Aya zinazohusiana na madhumuni hayo, bali zinaeleza kinaga ubaga nazo ni:

“Na kwa hakika misikiti yote ni ya Mwenyezi Mungu basi msimuombe mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu” (72:18) 204


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 205

Tawhid na Shirk

“Kwake ndiyo maombi ya haki, na wale wanaowaomba badala yake hawawajibu chochote, isipokuwa kama yule anyooshae mikono yake miwili kwenye maji ili yafikie kinywani mwake, lakini hayakifikii, na hayako maombi ya makafiri ila katika upotovu” (13:14)

“Na wale mnaowaomba badala yake hawana uwezo wa kukunusuruni wala wa kujinusuru wao wenyewe” (7:197)

“Hakika wale mnaowaomba badala ya Mwenyezi Mungu ni waja kama nyinyi, basi waiteni nao wawaitikieni ikiwa nyinyi mnasema kweli” (7:194)

“Huingiza usiku katika mchana na huingiza mchana katika usiku na amevitiisha jua na mwezi, vyote vinapita mpaka muda maalum, huyo ndiye Mwenyezi Mungu, Mola wenu, Mwenye ufalme na wale mnaowaomba kinyume chake wao hawamiliki hata utando wa kokwa ya tende!”(35:13) 205


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 206

Tawhid na Shirk

“Sema waiteni wale mnaodai (kuwa ni waungu) badala Yake, kisha hawataweza kukuondoleeni dhara wala kubadilisha” (17:56)

“Wala usimwite badala ya Mwenyezi Mungu ambaye hakufai wala hakudhuru, na ukifanya (hivyo), basi hakika utakuwa miongoni mwa madhalimu” (10:106)

“Kama mkiwaomba (masanamu) hao hawasikii maombi yenu, na kama wakisikia hawatakujibuni, na Siku ya Kiyama watakataa Shirki yenu, wala hatakuambia (yeyote) kama (Mwenyezi Mungu) Mwenye habari” (35:14)

“Na mpotevu mkubwa ni nani kuliko yule anayemuomba asiyekuwa Mwenyezi Mungu ambaye hatamjibu mpaka Siku ya Qiyama, na hao hawatambui dua zao!” (46:5)

206


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 207

Tawhid na Shirk Hakika amefanya kumuomba mwingine katika Aya hizi sawa sawa na kumuomba Mwenyezi Mungu (s.w.t), na matokeo ni kwamba kumuomba mwingine ni kumuabudu yeye, na kutokana na Aya hizo Mawahabi wanazitumia kukataza kuwaomba Mawalii na watu wema baada ya kufa kwao, na huona huko ni kumwabudu muombwa. Na katika kufupisha maneno wao humuona mfanya tawassuli pindi anaposema: “Ewe Muhammad,” basi ombi lake hilo ni kumwabudu muombwa. Kuhusiana na kadhia hiyo Swana’aniy anasema: ”Hakika Mwenyezi Mungu huzingatia maombi hayo kuwa ni ibada pale aliposema: “Niombeni nitawajibu, hakika wale ambao wanatakabari kutokana na ibada yangu …” Na mwenye kuomba kitu kwa kutumia jina la Mtume au mtu mwema au akasema: ’Niombeeni Shufaa kwa Mwenyezi Mungu katika haja yangu, au namuomba Mwenyezi Mungu kupitia kwako kuhusu shida yangu’ au mfano wa hayo, au akasema: ’Nikidhie deni langu au niponyeshe maradhi yangu’ au yanayofanana na hayo, kwa hakika kumuomba hivyo maombi hayo Nabii au mtu mwema itakuwa ni ibada, bali hakuna shaka anakuwa amemwabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) na kwa hivyo atakuwa mshirikina. Kwani haitotimia Tawhiid isipokuwa kwa kumpwekesha Mwenyezi Mungu (s.w.t) katika uungu kwa kuamini hakuna muumbaji wala mtoaji riziki mwingine asiyekuwa Yeye, na katika ibada pia kwa kutomwabudu asiyekuwa Yeye, na waabudu masanamu walikuwa wanafanya Shirki kutokana na kutompwekesha Mwenyezi Mungu (s.w.t) katika ibada.”94 Bila shaka katika Kiarabu kuomba ni kutafuta haja, hivyo dhana ya maombi haitimii isipokuwa katika kuomba haja, na lau neno ombi litatumiwa kwa maana ya wito tu bila kuambatana na haja, basi huwa ni kwakuwa muombaji humtaka muombwa amwelekee. Ama neno ibada lenyewe lina maana nyingine, nayo ni: unyenyekevu ambao chanzo chake ni itikadi ya Uungu na Urabbi wa yule anayenyenyekewa, kama yalivyotangulia mae94. Tanziihu Itikad cha Swana'ani kama ilivyokuwepo katika Kashfu Irtiyab Uk. 272-274. 207


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 208

Tawhid na Shirk lezo yake hapo kabla. Na wala haiwezekani kuzingatia kuwa ombi na ibada ni lafudhi mbili zenye kufanana na zenye kushirikiana katika maana, iwe maombi maana yake ni ibada, haiwezekani hilo kwa sababu zifuatazo, nazo ni: Ya kwanza: Hakika Qur’an tukufu inatumia lafudhi ya ombi na dua katika sehemu kadhaa ambazo haiwezekani kuwa mradi wake ni ibada, mathalan: “Akasema: Ee Mola wangu! kwa hakika nimewaita watu wangu usiku na mchana.” (71:5) Je! Inawezekana tuseme kuwa makusudio ya Nabii Nuhu (a.s.) yalikuwa kuabudu watu wake usiku na mchana?!!! Vile vile mfano wa maneno ya (s.w.t) akinukuu maneno ya Shetani amesema:

“Na shetani atasema itakapokatwa hukumu, hakika Mwenyezi Mungu alikuahidini ahadi ya kweli, nami nilikuahidini, lakini sikukutimizieni, wala sikuwa na mamlaka juu yenu isipokuwa nilikuiteni nanyi mkaitikia, basi msinilaumu bali jilaumuni wenyewe, siwezi kukusaidieni, wala nyinyi hamuwezi kunisaidia, hakika mimi nilikataa kunishirikisha kwenu toka zamani, hakika madhalimu watakuwa na adhabu yenye kuumiza.” (14:22) Je! Inafikiriwa kwamba makusudio ya Shetani ni kuabudu wafuasi wake, 208


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 209

Tawhid na Shirk ilhali ibada - lau itasihi– basi si vingine bali inakuwa ni kutoka kwa wafuasi wake kumuelekea yeye na wala sio yeye kuwaelekea wafuasi wake, na mfano wa Aya hizo mbili ni hizi zifuatazo:

“Na enyi watu wangu! Mimi nina nini nakuiteni kwenye uongofu, nanyi mnaniita kwenye Moto! “ (40:41)

”Na kama mkiwaita kwenye muongozo hawatawafuateni...” (7:193)

“Na kama mkiwaita katika uongofu hawasikii...” (7:198)

“Na kwa hakika wewe unawaita kwenye njia iliyonyooka” (23:73)

“Na atakayebishana nawe katika hili baada ya ujuzi uliokujia, basi waambie, njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wanawake wetu na wanawake wenu, na nafsi zetu na nafsi zenu, kisha tuombe kwa unyenyekevu na tuiweke laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie wenye kusema uongo.” (3:61) Katika Aya hizo zinazofanana na zote zimetumia neno dua na maombi sio kwa maana ya ibada, na kwa hivyo hatuwezi kuyazingatia hayo maneno 209


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 210

Tawhid na Shirk mawili ni yenye kuradifiana na kufanana, kwa hivyo lau mtu atamuomba Nabii, Walii au mtu mwema kwa hakika tendo na amali yake hiyo haitokuwa ni ibada kwake, kwani maombi yana maana pana zaidi ya ibada na mengineyo. Ya pili: Hakika makusudio ya maombi katika Aya hizo (zilizotajwa mwanzoni mwa mada hii) si kila maombi wala kila wito, bali ni ombi maalum ambalo huenda likawa linaradifu lafudhi ya ibada. Kwa sababu Aya zote hizo zinahusiana na waabudu masanamu ambao walikuwa wakifikiria kuwa masanamu yao ni miungu wadogo ambayo imepewa madaraka katika baadhi ya mambo ya kiungu, wakiamini kwamba inajitegemea katika utendaji wa mambo. Na lililo dhahiri ni kwamba unyenyekevu na kujidhalilisha na aina yoyote ya usemaji au utendaji jambo mbele ya kiumbe kwa kuamini kuwa ni mhusika, ni mlezi au mmiliki wa baadhi ya mambo ya kiungu itakuwa ni ibada. Hapana shaka unyenyekevu wa waabudu masanamu, uombaji wao na utakaji wao mahitaji kwa masanamu yao ulikuwa una sifa ya kuyaona masanamu yale ni miungu, walezi, wamiliki halisi wa Shufaa na kuamini kwamba ni miungu yenye kujitegemea katika utendaji kazi katika mambo ya dunia na akhera, na dhahiri shahiri kwamba ombi lolote lile kulielekeza kwa vitu hivyo na vinavyofanana na hivyo kwa sharti hilo ni ibada wala hakuna kipingamizi. Fungu lingine la Aya linaonyesha kwamba maombi ya waabudu masanamu yalikuwa yakiambatana na itikadi kuwa masanamu hayo ni miungu au wamiliki halisi wa Shufaa, utoaji msamaha na mengineyo, baadhi ya Aya hizo ni:

210


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 211

Tawhid na Shirk “Nasi hatukuwadhulumu lakini wao wamejidhulumu wenyewe na waungu wao waliokuwa wakiwaomba badala ya Mwenyezi Mungu, hawakuwafaa kitu ilipofika amri ya Mola Wako na hawakuwazidishia ila maangamizo.” (11:101) Katika Aya hiyo inabainika kwamba wao walikuwa wakiyaabudu masanamu, walikuwa na itikadi wakidhani na kuamini kuwa masanamu hayo yatawatosheleza kwa kitu kama hali ilivyo kwa Mungu halisi mtendaji wa hayo.

“Wala hawana uwezo wa uombezi wale wanaowaomba badala yake ila anayeishuhudia haki nao wanajua” (43:86)

“Na wale wanaowaomba kinyume chake, wao hawamiliki hata utando wa kokwa la tende!” (35:13)

Sema waiteni wale mnaodai (kuwa ni waungu) badala yake kisha hawataweza kukuondoleeni dhara wala kubadilisha.”( 17:56) Basi Aya zilizotajwa (mwanzoni kabisa wa maudhui hii) hazifungamani kabisa na mada yetu, kwani maudhui ni maombi bila itikadi ya kiungu, bila umilikaji wa kitu na bila kujitosheleza, na bila kujitegemea katika utendaji wa mambo ya dunia na akhera, bali ni kwa ajili ya kwamba muombwa 211


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 212

Tawhid na Shirk ni mja miongoni mwa waja wema wa Mwenyezi Mungu (s.w.t), naye ana daraja tukufu la kiroho na anastahiki cheo cha Unabii na Uimamu, na kwamba wameahidiwa wafanya tawassuli kutakabaliwa dua zao na maombi yao ikiwa atakusudiwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) katika njia na taratibu zake, kama ilivyoolezwa kuhusiana na haki ya Bwana Mtume (s.a.w.w):

“Na hatukumpeleka mtume yeyote ila apate kutiiwa kwa amri ya Mwenyezi Mungu, na lau wangelikujia walipojidhulumu nafsi zao wakaomba msamaha kwa Mwenyezi Mungu, na Mtume akawaombea msamaha, bila shaka wangemkuta Mwenyezi Mungu, Mwenye kupokea toba, Mwenye kurehemu” (4:64) Ya tatu: Huenda ikasemwa kwamba makusudio ya maombi katika Aya hizi ni aina mahususi ya maombi, inamaanisha ni ile aina inayoenda sambamba na ibada, na wala si kwamba maombi maana yake halisi na hakika ni ibada, bali ni kwamba maombi yana maana yake halisi lakini kwa kuwa yalipozungumziwa katika Aya mbalimbali yaliambatana na itikadi ya Uungu wa waombwaji ndio maana ingekuwa kwamba aina iliyokatazwa katika Aya hizo ni ile aina makhsusi yenye kuambatana na itikadi ya Uungu wa wale waombwaji, na si kila maombi, hivyo imani ya waombaji juu ya waombwaji ni kielelezo hisishi, ambacho kinaashiria kwamba kilichokatazwa si kila maombi bali ni yale yanayoambatana na itikadi hiyo, na hayo ndio mfano miongoni mwa mifano halisi ya ibada. Na dalili ya kwamba makusudio ya maombi katika Aya hizo ni yale yenye kulazimu ibada, ni kwamba huenda ikapatikana katika moja ya Aya mbili madhumuni moja kupitia lafudhi maombi na katika Aya nyingine kupitia lafudhi kuabudu, mfano wa maneno ya Mola Manani: “Sema Je! Mnamwabudu badala ya Mwenyezi Mungu ambae hawezi kuwadhuruni wala kukunufaisheni? na Mwenyezi Mungu ni Mwenye 212


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 213

Tawhid na Shirk kusikia Mwenye kujua.” (5:76) Na katika aya nyingine anasema:

“Sema je! tumuombe asiyekuwa Mwenyezi Mungu ambaye hatupi faida wala hawezi kutudhuru, na turudishwe nyuma baada ya Mwenyezi Mungu kutuongoza sawa na yule ambaye mashetani yamempoteza akiwayawaya katika ardhi? Anao marafiki wanaomwita kwenye mwongozo hasa ni muongozo wa Mwenyezi Mungu na tumeamrishwa tumnyenyekee Mola wa walimwengu wote.” (6:71) Vilevile katika Aya nyingine anasema:

“Na bahari mbili haziwi sawa, hii ni tamu yenye ladha, kinywaji chake kinateremka uzuri, na hii (nyingine) ni chumvi yenye uchungu ila katika zote mnakula nyama mbichi na mnatoa mapambo mnayoyavaa na ndani yake unaziona jahazi zikikata (maji) ili mpate fadhila yake na ili mpate kushukuru.” (35:12) Katika Aya hiyo na zilizotangulia hapo kabla imetumika lafudhi ”mnamu213


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 214

Tawhid na Shirk omba na tunamuomba” katika hali nyingine imetumiwa katika Aya ya kwanza kwa lafudhi ”mnaabudu”. Mfano wa hayo ni yale yaliyotangulia katika kauli Yake (s.w.t):

“Hakika nyinyi mnayaabudu masanamu kinyume cha Mwenyezi Mungu, na mnatengeneza uongo, bila shaka wale mnaowaabudu kinyume cha Mwenyezi Mungu wao hawakushikieni riziki, kwa hiyo tafuteni riziki kwa Mwenyezi Mungu, na mwabuduni na mshukuruni, Kwake mtarudishwa.” (29:17) Lafudhi zote mbili zimepatikana katika Aya moja, na zimetumika katika maana moja, nayo ni:

“Sema: Hakika nimekatazwa kuwaabudu wale mnaowaabudu kinyume cha Mwenyezi Mungu, sema sifuati matamanio yenu, maana hapo nitapotea na sitokuwa miongoni mwa walioongoka” (6:56)

“Na Mola wenu husema: Niombeni nitakujibuni kwa hakika wale wajivunao kufanya ibada Yangu, wataingia Jahannam wakifedheheka.” (40:60) 214


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 215

Tawhid na Shirk Aya hiyo na zilizokwishatangulia zinadhihirisha makusudio ya maombi kuwa ni ibada na sio uhitaji na kuhitaji, na hilo sio kwa maana ya matumizi ya neno maombi kwa maana ya ibada mpaka iwe ni matumizi ya kikinaya, bali ni kwamba neno maombi limetumiwa katika maana yake halisi lililowekewa, lakini kwa kuwa maombi haya yaliambatana na kitendo cha muombaji kuamini Uungu wa muombwaji ndio maana imekuwa muradi wa maombi hapo ni ibada. Na hayo yanaungwa mkono na yale maelezo yaliyomo katika dua ya kiongozi wa wenye kusujudu akiashiria faida ya Aya iliyotangulia, anasema: “Kukuomba wewe umekuita ni ibada na kuacha kufanya hivyo ni kufanya kiburi, na mwenye kuacha kufanya hivyo ameahidiwa kuingia motoni.”95 Kwa hivyo tunamuomba mpendwa msomaji arejee mwenyewe mada ya maombi katika kitabu kiitwacho Mu’ujamul-Mufaharis ataona kuwepo madhumuni mamoja kuhusiana na lafudhi ya ibada na kwa upande mwingine kwa lafudhi ya dua na maombi. Na hilo ni dalili iliyo wazi kwamba makusudio ya maombi katika Aya zilizotajwa mwanzoni mwa mada hii ni ibada na sio maombi yoyote yale. Mpendwa msomaji utakapodurusu mjumuiko wa Aya ambazo zimeelezea lafudhi ya maombi na ikakusudiwa kigao chenye kuleta ulazima wa ibada ataona kwamba Aya hizo ima zinaelezea kuhusiana na muumbaji wa ulimwengu ambaye wanatawhiid wote wanakiri Uungu Wake, Ulezi Wake na umiliki Wake, au zinaelezea waabudu masanamu ambao walikuwa wakifikiria kuwa masanamu hayo ni miungu na kwamba yanamiliki utoaji Shufaa, na katika hali kama hii ni ajabu sana na ni jambo la kushangaza kuzitumia Aya hizo kama dalili juu ya maudhui yetu ambayo ni yale maombi yasiyoambatana na itikadi ya kuamini Uungu wa muombwaji.

95. Sahifar Sajjadiyya dua ya 49. 215


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 216

Tawhid na Shirk

SWALI NA JAWABU Mpaka hapa imebainika kwamba kuwaomba waja wema kwa vyovyote itakavyokuwa, sawa iwe kwa ajili ya kufanya tawassuli na uombaji Shufaa au kwa ajili ya kuomba haja na utekelezaji, hilo sio ibada wala halijumuishwi katu na Aya zenye kukataza maombi, isipokuwa hapa linajengeka swali, nalo ni: Iwapo atakuwa mwingine asiyekuwa Mola Manani hamiliki hata chembe wala hamiliki (yaani hana uwezo wa) kujiepusha na madhara na kuyageuza, ni ipi faida ya maombi hayo? kwani (s.w.t) amesema:

“Sema: waiteni wale mnaodai (kuwa ni waungu) badala yake kisha hawataweza kukuondoleeni madhara wala kubadilisha.” (17:56)

“Huingiza usiku katika mchana na huingiza mchana katika usiku na amevitiisha jua na mwezi, vyote vinapita mpaka muda maalum, huyo ndiye Mwenyezi Mungu Mola wenu, mwenye ufalme na wale mnaowaabudu kinyume chake, wao hawamiliki hata utando wa kokwa ya tende.” (35:13) Jawabu: Hakika utafiti kuhusiana na somo hili umehusishwa katika kumaizi na kuchanganua maana ya ibada na isiyokuwa ibada, ama maombi hayo yana faida au hapana, hilo liko nje ya maudhui yetu, zaidi ya hayo 216


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 217

Tawhid na Shirk ni kwamba Aya kadhaa ambazo amezitumia katika suali zinajulisha maudhui nyingine ambayo haifungamani kabisa na mada hii. Muhtasari wa Mada: Hakika Aya hizi zinahusiana na suala la masanamu ya mbao ya Waarabu, ya madini na mawe, na hilo inabainika kutokana na fuo la Aya kadhaa, hilo ni la kwanza, la pili hakika lengo la ukanushaji wa umiliki kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) sio kabisa kabisa bali mradi wa umiliki ni ule wenye kunasibiana na cheo cha Mola (s.w.t), yaani Yeye ndiye mmilikaji wa kujitegemea, na ukanushaji wa umilikaji huu kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu haijulishi kutokuwepo yale yanayopatikana kutoka kwa Mwenyezi Mungu kupitia kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu, na hilo linaungwa mkono na maneno ya Allah (s.w.t), anasema: “Enyi watu! Hakika nyinyi ni mafukara kwa Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu ndiye tajiri msifika. “ Na makusudio ya ufakiri (uhitajio) hapa ni ufakiri wa dhati wala haikanushi uwezo wa kiumbe ambao amepatiwa na Mwenyezi Mungu (s.w.t), aidha ana utumia uwezo huo kwa idhini Yake. Ama kuhusu dalili inayoonyesha kwamba Waarabu walikuwa wakiitakidi masanamu yao kuwa yana uwezo aidha yanajitegemea ni kwa mujibu wa maneno ya Mwenyezi Mungu (s.w.t):

“Sema: je! mnamwabudu badala ya Mwenyezi Mungu ambaye hawezi kuwadhuruni wala kukunufaisheni? na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua.” (5:76) “Na wanawaabudu kinyume na Mwenyezi Mungu wasiowamilikishia 217


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 218

Tawhid na Shirk riziki (hata kidogo) kutoka mbinguni na ardhini, wala hawana uwezo (wowote).” (16:73) Na kwa hivyo lau Mwenyezi Mungu atasema kuwa bila Yeye hawamiliki wala hawana uwezo wa kuondoa madhara na wala kubadilisha, basi makusudio yake ni kukanusha umilikaji maalum na sio wowote ule. 5. JE! KUTUKUZA MAWALII WA MWENYEZI MUNGU NA KUWAKUMBUKA WAO NI SHIRKI? Mawahabi huchukizwa mno kutokana na kitendo cha kutukuzwa Mawalii wa Mwenyezi Mungu na kuwakumbuka pia, aidha uwekaji wa vikao vya kuadhimisha siku za kuzaliwa kwao na kuomboleza siku za kufa kwao. Wao huzingatia kuwa watu ambao hukusanyika katika vikao hivyo ni Shirki na upotovu. Kwa kadhia hiyo Muhammad Hamid Faqii Rais wa Jumuiya ya Answari Sunna katika mstari wa pambizo katika kitabu Fat’hul Majiid anasema: “Maadhimisho ya kumbukumbu ambayo yameenea katika miji mbalimbali kwa jina la Mawalii ni aina ya kuwatukuza hao na kuwaabudu” Hakika watu hawa hawajaainisha wigo na mipaka ya Tawhiid na Shirki na hasa hasa suala la ibada, wao huona kila tendo lina harufu ya Shirki, kwa hivyo kumtuhumu mtendaji kuwa ni mshirikina, wao hufikiri kwamba kila aina ya uadhimishaji ni ibada na Shirki. Kwa hivyo mwandishi huyo amefanya kuadhimisha ni ibada na akafikiria kwamba hayo maneno mawili yana maana moja, na katika mambo ambayo hayana shaka ndani yake ni kwamba Qur’an inaadhimisha Manabii na Mawalii kwa ibara za waziwazi, kuhusiana na Zakaria na Yahya (a.s.) inasema: “Basi tukampokelea na tukampa Yahya na tukamponyeshea mkewe, hakika wao walikuwa wepesi kufanya wema na wakituomba kwa shauku na hofu, nao walikuwa wakitunyenyekea” (21:90) Na lau mtu atafanya kikao pembezoni mwa makaburi ya wale ambao 218


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 219

Tawhid na Shirk wametajwa ndani ya Qur’an kwa majina yao katika Aya hiyo, pia katika kikao hicho akasoma Aya hiyo kwa ajili ya kuwatukuza hao je! atakuwa amefuata isiyokuwa Qur’an? Vilevile Qur’an tukufu kuhusiana na Ahlul–Bayti Rasuli inasema: “Na huwalisha chakula masikini na yatima na mfungwa hali ya kuwa wanakipenda” (76:8) Je! iwapo watu watakusanyika siku ya kuzaliwa Ali bin Abi Talib – yeye ni mmoja wa ndugu wa karibu wa mtume – kisha wakasema: Hakika Ali (a.s.) alikuwa akiwapa chakula Masikini, Yatima na Mateka je! watakuwa washirikina? Je! utamuona kuwa ni mshirikina yule ambaye atasoma Aya ya kumsifu bwana Mtume (s.a.w.w) katika sherehe za kukumbuka kuzaliwa kwake? Mfano wa Aya zifuatazo:

“Na bila shaka una tabia njema” (68:4)

“Ewe nabii kwa hakika sisi tumekutuma (ili uwe) shahidi na mtoaji wa habari njema na muonyaji, na muitaji (wa watu) kwa Mwenyezi Mungu kwa idhini Yake, na (uwe) taa itoayo nuru.” (33:45-46)

“Bila shaka amekujieni mtume kutoka miongoni mwenu, yanamhuzu219


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 220

Tawhid na Shirk nisha yanayokuhuzunisheni, ana kuhangaikieni, kwa waumini ni mpole, mwenye kurehemu.” (9:128) Na

“Hakika Mwenyezi Mungu na Malaika wake humsalia mtume, enyi mlioamini! msalieni (mtume) na muombeeni amani” (33:56) Na lau mtu atasoma Aya hizo mbele ya Mtume (s.a.w.w) au akasoma tarjuma yake kwa lugha nyingine, au mtu huyo mwenye mapenzi na Mtume (s.a.w.w) akaamua kutunga shairi na kisha akasoma katika hafla au katika kikao hicho atakuwa amefanya Shirki na kuwa mshirikina? Kwa hakika kutokuwepo sherehe hizi zama za Mtume (s.a.w.w) sio dalili ya kumfanya mtendaji awe mshirikina, bali huenda ikasemwa ni bidaa na sio Shirki, na wala si kumuabudu binadamu mwema. Ni dhahiri jambo hilo halihesabiwi kuwa ni bidaa, kwani iwapo zitafanywa sherehe na hafla au vikawekwa vikao vya maombolezo na vikanasibishwa kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t), au ikadaiwa kwamba vimeamrishwa na Mola manani, hapo italazimu ufanyike uchunguzi na utafiti juu ya usahihi wa unasibishaji huo na ukweli wa madai hayo, na sio kusema tu kwamba kufanya hivyo ni Shirki. Na hata kama itafanywa hivyo bila kuhusishwa na Mwenyezi Mungu (s.w.t) au kudai imeamrishwa na Yeye, kabisa haiwi bidaa! Hakika Aya za Qur’an zinajulisha kufaa kufanya vikao hivyo na kwa anwani maalum, hapa tunazitolea ishara anwani hizo: I. KUFANYA SHEREHE ZA KUMKUMBUKA MTUKUFU MTUME (S.A.W.W) NI KUMTUKUZA NA KUMNUSURU: 220


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 221

Tawhid na Shirk Kwa nini isiwe hivyo, ilhali Qur’an tukufu inawasifu watu ambao humtukuza Mtume (s.a.w.w) inasema:

“Basi ambao waliomuamini yeye na kumtukuza na kumsaidia na wakafuata nuru iliyoteremshwa pamoja naye hao ndio wenye kufaulu” (7:157) Sifa ambazo zimeelezwa katika Aya hiyo na Mola Muweza ni: 1. Wamemwamini yeye 2. Wamemtukuza yeye 3. Wamemnusuru yeye 4. Wakafuata nuru ambayo imeteremshwa pamoja naye. Je! yupo anayedhani kuwa sentensi hizo tatu: Wakamwamini, wakamtukuza, wakamnusuru, na wakamfuata zilihusu zama za Mtume (s.a.w.w) tu? Jawabu ni hapana. Hakika Aya haimaanishi wale waliokuwepo zama za Mtume (s.a.w.w) tu. Kwa hivyo ni dhahiri ibara ya: “Wakamtukuza” haiwahusu wao tu, na katika kuongezea maelezo hayo tunasema: kwa hakika inalazimu kwa kiongozi adhimu kuheshimiwa na kutukuzwa katika kila zama, je! kuweka vikao vya kuhuisha kumbukumbu za viongozi kama vile siku ambayo alianza rasmi Mtume (s.a.w.w) kulingania Uislam au siku ya kuzaliwa kwake, hapo zikatolewa hutuba na mihadhara mbalimbali pamoja na kasida je! Kitendo hicho sio mfano halisi wa maneno ya Mola (s.w.t): “Na wakamtukuza” ambayo yanamaanisha kumuadhimisha, kumkumbuka, kumsifu na kumtukuza? Ajabu iliyoje Mawahabi huwatukuza viongozi wao wa siasa za kidunia na huwaheshimu kupita kiasi kuliko wafanyavyo wengine kwa 221


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 222

Tawhid na Shirk Mawalii wa Mwenyezi Mungu, na hilo haliwi Shirki, ama akifanya mwingine kidogo yale wayafanyayo wao husema ni Shirki?!! Kwa hakika katazo la kuwatukuza Manabii na Mawalii – wakiwa hai au wamekufa – huchafua sura ya Uislamu mbele ya maadui, kwamba ni dini iliyokosa muelekeo, na haina hata chembe ya upendo kwa binadamu, isiyoafikiana na maumbile ya kibinadamu, na ni dini isiyo na mvuto unaotakiwa, aidha hatimaye ni kupoteza uwezo wa kuwavutia watu wa mataifa mengine na kuukubali. Wanasemaje! kuhusiana na kisa cha Nabii Yakub (a.s.) wale ambao wanapinga kufanya vikao vya maombolezo kuwakumbuka wale waliokufa shahidi katika njia ya Mwenyezi Mungu (s.w.t)? Na wanasema nini kuhusu yeye hali ya kuwa alimlilia mwanawe Yusufu (a.s.), alikuwa akiuliza ambaye amekutana na mwanawe mpaka macho yake yakapoteza nguvu ya kuona? Mola manani anasema: “Na macho yake yakawa meupe kwa huzuni …” (12:84) Vipi hilo likubalike hali ya kuwa mtoto (Yusuf) yuko hai, aidha liende sanjari na misingi ya Tawhiid na akiwa amekufa iwe ni Shirki? Iwapo mtu atafuata njia ya Nabii Yakub (a.s.) akalia kwa kufarikiana na Mawalii wa Mwenyezi Mungu (s.w.t) na vipenzi wake siku ambayo wamekufa shahidi, kwa nini haihesabiwi amali yao ni kufuata nyayo za Nabii Yakub (a.s.)? Hapana shaka kwamba kuwapenda ndugu wa karibu wa Mtume (s.a.w.w) ni moja ya faradhi za dini ya kiislamu ambayo imeelezwa kinaga ubaga. Ikiwa mtu ataamua kutekeleza faradhi hii baada ya kupita karne kumi na nne na ana uwezo wa kufanya hivyo, je! Afanyeje ili afikie hilo? Je, yeye hapaswi kufurahi kwa furaha zao na kuhuzunika kwa huzuni zao? Na ikiwa mtu katika kudhihirisha furaha yake akaweka kikao cha kukumbuka maisha yao namna walivyojitolea na kubainisha masaibu waliyoyapata, je kitendo chake hicho cha kudhihirisha upendo ambao umeelezwa ndani ya Qur’an tukufu ni kosa?

222


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 223

Tawhid na Shirk Na mtu atakapozuru makaburi ya ndugu wa karibu wa Mtume (s.a.w.w) ili kudhihirisha mapenzi na upendo zaidi, kwa hivyo akaamua kuweka vikao hivyo pembezoni mwa makaburi yao je! hilo kiakili halikubaliki? Naye hafanyi kwa lengo lingine isipokuwa ni kudhihirisha upendo. II - KUADHIMISHA KUMBUKUMBU YA KUZALIWA MTUME (S.A.W.W) NI KUNYANYUA UTAJO WA MTUME: Hakika Qur’an tukufu inaeleza kinagaubaga kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t) amemneemesha Mjumbe Wake kwa kumpanulia kifua chake, kumuondolea mizigo na kulitukuza jina lake kwa ibara ifuatayo: “Je! hatukukupanulia kifua chako, na tukakuondolea mizigo yako ambayo imeelemea mgongo wako na akaunyanyua utajo wako? …” (94:1-4) Basi Mwenyezi Mungu (s.w.t) ameinua jina lake na kumfanya mashuhuri ulimwenguni kwa lengo la kumtukuza yeye, kwa hivyo sherehe hizo ambazo zina lengo na madhumuni ya kudumisha utajo na kumbukumbu za Mtume (s.a.w.w), ikiwa Qur’an tukufu ni kigezo chema kwetu basi kwa nini hatuifuati Qur’an na kwa nini tusimkumbuke Mtume (s.a.w.w) na tulitaje jina lake?! III - KUTEREMSHWA MEZA YA CHAKULA KUTOKA MBINGUNI NA SIKU HIYO KUFANYWA KUWA SIKU YA IDD Hakika Nabii Isa (a.s.) alimuomba Mola wake (s.w.t) amteremshie meza ya chakula. Mwenyezi Mungu (s.w.t) ananukuu maneno yake: “Akasema Isa bin Mariam: “Ee Mwenyezi Mungu, Mola wetu tuteremshie chakula kutoka mbinguni ili iwe sikukuu kwa wa mwanzo wetu na wa mwisho wetu.” (5:114) Kwa hiyo Nabii Isa (a.s.) alifanya siku ambayo imeteremshwa meza ya chakula na baraka ya Mungu kuwa ni siku ya sikukuu kwa sababu (s.w.t) alimtukuza yeye pamoja na wanafunzi wake kwa meza hiyo, kuteremshwa 223


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 224

Tawhid na Shirk meza ya mbinguni ikawa sababu ya kuifanya siku hiyo kuwa ni sikukuu! Kwa nini tusifanye siku ambayo Mtume (s.a.w.w) ameanza rasmi kazi ya utume ambayo ni siku ya baraka kama vile siku ya kuteremshwa meza ya kiroho kuwa ni Idd? Je! Mtu anaweza kudai kwamba utukufu wa Mtume (s.a.w.w) na aliyokuja nayo miongoni mwa sheria takatifu yenye kudumu, ina baraka chache kuliko meza ya kiroho ambayo imeteremshwa kwa Nabii Isa (a.s.) na wanafunzi wake? 6 - JE! KUTABARUKU KWA ATHARI ZA MTUME (S.A.W.W) NA MAWALII NI SHIRKI? Hakika imepita sunna ya watu wema wa hapo kabla ambapo walitabaruku na athari ya Mtume (s.a.w.w) na Aali zake (a.s.), na kuwa ni sunna ambayo haina shaka kwa kila mwenye kujua historia ya waislamu. Kwa hilo Sheikh Muhammad Tahil Makki Muaswi ameandika kitabu kuhusiana na hilo na akakipa jina la “Tabarruku Sahaaba biathari Rasulillah.� Humo amenukuu ushahidi mwingi wa kihistoria yakinifu kuhusiana na kutabaruku kwao na vilevile kizazi kilichokuja baada ya masahaba, na kitabu hicho kimepigwa chapa mwaka 1385 A.H. na chapa ya pili mwaka 1394 A.H. Pamoja na hivyo Mawahabi wamekanusha vikali hilo na kulihesabu kuwa ni Shirki hata kama ikiwa ni kwa lengo la kutetea mahaba kwa Mtume na kizazi chake na kuwapenda wao. Tunauliza je anayefanya tabaruku kwa kutegemea kitendo cha Nabii Yakub (a.s.) pale alipoweka kanzu ya Yusufu (a.s.) juu ya macho yake na papo hapo akaona, je! inafaa kwetu sisi kumwita mtu huyo mshirikina (kumtuhumu kwa ushirikina), kuna tofauti kati ya kutabaruku kupitia athari za Mtume (s.a.w.w) na athari za mawalii, na tabaruku ya Nabii Yakub (a.s.) kwa kanzu ya Nabii Yusufu (a.s.)? Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema: 224


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 225

Tawhid na Shirk “Basi alipofika mtoaji wa khabari njema, akaiweka (kanzu yaYusuf) mbele ya uso wake mara akaona…” (12:96) Na sisi tunaona Nabii Yakub (a.s.) ametabaruku kupitia kanzu ya Yusuf (a.s.), na Qur’an imetaja hilo kama pia ilivyoeleza kwamba alirudishiwa uoni kupitia kanzu hiyo na tabaruku hiyo. Hivyo lau tendo hilo lingekuwa linalazimu ushirikina asingelifanya Nabii mtukufu, aidha Qur’an tukufu isingelitaja na wala lisingelikuwa na athari. Kuna tofauti gani kati ya kanzu iliyoshonwa kwa nyuzi za pamba na jengo la kaburi lililotengenezwa kwa chuma! Na iweje tendo la awali liwe ni Tawhiid na lipelekee kurejesha uonaji? na la pili ambalo ni kubusu mahala tohara alipozikwa Mtume (s.a.w.w) liwe ni Shirki na limfanye mtu kuwa nje ya wigo wa Tawhiid! Kwa nini uletwe utofautishaji huu ambao husababishwa na Mawahabi, hayo ndiyo ambayo yanahusu somo letu katika kitabu hiki. Tumeeleza kwa ufupi juu ya mambo ambayo Mawahabi huyakanusha kwa kutumia Qur’an tukufu na sisi tunatosheka na kiwango hicho cha maelezo. Na kama si hivyo, sunna na historia vina ushuhuda mwingi kuhusiana na upatikanaji wa tabaruku, huku ikiwa masahaba na kizazi kilichokuja baada yao walikuwa wakitabaruku kupitia athari za Mtume (s.a.w.w) na za Mawalii, nini kosa sisi kufanya hayo! Kwa hakika hayo yamo katika vitabu Sahihi vya Ahlul-Sunna na vinginevyo miongoni mwa vitabu vya hadithi, Sira, historia; na kuna hadithi chungu nzima zinazoeleza bayana namna masahaba na taabiina walivyokuwa wakitabaruku kwa athari za Mtume (s.a.w.w), hapa tunataja baadhi ya hizo: Katika Sahih Bukhari mlango wa vita vya Taifu, imepokewa kutoka kwa Abu Musa amesema: Nilikuwa kwa Mtume (s.a.w.w) naye akiteremka mahala panapoitwa Jaaranat kati ya Makka na Madina akiwa pamoja na Bilal, hapo akajiwa na Mwarabu wa jangwani akasema: “Je! Unaweza kunipatia uliyoniahidi?’’ Akamwambia: “Nakubashiria kheri.” Akasema: “Umekithirisha kunibashiria,” akamwelekea Abu Musa na Bilal kwa hali ya kughadhibika akasema: “Ubashiri umerudishwa basi kubalini nyinyi.” 225


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 226

Tawhid na Shirk Wakasema: “Tumekubali,” kisha akaomba aletewe chombo chenye maji akaosha mikono yake na uso wake kisha akasema kunyweni mengine osheni nyuso zenu, basi wakachukua chombo, Ummu Salama akaita nyuma ya pazia nibakishieni mabaki, wakambakishia kiasi. Na katika Sahih Bukhari katika kitabu cha Vazi mlango wa Quba jekundu, imepokewa kutoka kwa Ibnu Abu Juhaifa, kutoka kwa baba yake amesema: “Nilimjia Mtume (s.a.w.w) naye akiwa katika Quba jekundu, nilimuona Bilal akichukua mabaki ya maji aliyotawadhia Mtume (s.a.w.w) na watu wanayagombania mwenye kubahatika kuchukua kiasi anajipangusa nayo na mwenye kukosa anachukua unyevunyevu kutoka kwa wenziwe.” Na katika Sahih Muslim kitabu cha Fadhila mlango wa Mtume (s.a.w.w) kukaribiana na watu, na watu kutabaruku naye, kutoka kwa Anas bin Malik amesema: “Mtume (s.a.w.w) alikuwa akiswali Swala ya mchana huja watumishi wa Madina na vyombo vyao vikiwa na maji ambapo bwana Mtume (s.a.w.w) akiingiza mkono wake humo wakati huo.” Na katika Sahih Bukhari katika kitabu cha Adabu mlango wa Tabia nzuri na Ukwasi, kutoka kwa Sahil bin Sa’ad amesema: “Mwanamke mmoja alikwenda kwa Mtume (s.a.w.w) akampatia Burdat (nguo), Sahil akasema kuwaambia watu: “Je mnajua Burdat?” Wakasema: “Ni Shumlat.” Suhal akasema ni Shumlat iliyosukwa pembeni mwake, yule mwanamke akasema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, nakuvika hii. “ Mtume (s.a.w.w) akaichukua, ghafla mtu mmoja kati ya masahaba akamwambia: “Ewe Mtume, uzuri ulioje vazi hilo, akasema: “Ndio,” Na Mtume (s.a.w.w) alipoondoka masahaba wake wakasema: “Hukufanya vizuri ulipomuona Mtume amelichukua kwa kulihitajia, kisha ukamuomba hali unajua akiombwa kitu hakatai.” Akasema: “Nilitaraji baraka zake alipolivaa Nabii (s.a.w.w) ili nikafiniwe nayo.”

KUJENGA JUU YA MAKABURI 226


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 227

Tawhid na Shirk Hakika kujenga juu ya makaburi ya Mitume na Mawalii ni miongoni mwa mambo ambavyo yamefanywa na wafuasi wa Mtume na kuruhusiwa na sheria za mbinguni kabla ya Uislamu na baada ya Uislamu. Walikuwa wakijenga majengo juu ya makaburi ya Mitume na Mawalii na bado majengo hayo yamesimama mpaka hivi sasa huko Iraq, Palestina na Sham, isipokuwa Mawahabi hudhani hiyo ni Shirki au bidaa, kwa hivyo wakakusanya nguvu zao na kuyabomoa majengo hayo. Ibnu Qaim katika kitabu chake Zaadul-Maad Fi Huda Khayril Ibad anasema: “Ni wajibu kubomoa majengo ya Mashahidi ambayo yamejengwa juu ya makaburi na haifai kuyaacha kamwe baada ya kuwepo uwezo wa kuyateketeza na kuyaangamiza kabisa.”96 Na kwa sunna au mwenendo huo mbaya Mawahabi wameshikamana nao na kuwa ndio dira yao, kwani walipotwaa madaraka katika Hijaz (Makka), wanachuoni wao wa Madina wakatoa fatwa ya kubomoa majengo hayo na makaburi wakitaja katika fatwa zao hukumu kuhusu suala hilo, na jawabu ambalo huwajibika kujibu wanazuoni wa Madina. Ibnu Talhid –siku hizo– aliuliza swali kama ifuatavyo: “Miongoni mwa maneno ya wanazuoni wa Madina Munawwara, Mwenyezi Mungu awazidishie ufahamu na elimu, ni kuhusu majengo yaliyopo juu ya makaburi na kuyafanya misikiti, je hilo linafaa au hapana? Na ikiwa haifai bali ni marufuku, limekatazwa na kukemewa vikali97 je! ni wajibu kuyabomoa aidha je imekatazwa kuswali hapo?”98 Na kwa kuwa mada hii kitivo chake na mhimili wa utafiti wake ni kutafiti masuala hayo kwa mwangaza wa Qur’an tukufu, sisi tunalielekeza suala hili mbele ya Kitabu kitukufu cha Mwenyezi Mungu (s.w.t) na humo ndimo limo jawabu sahihi. Tunayojifunza kutoka katika Qur’ani tukufu kuhusiana na kadhia hiyo ni: 96. Zaadul-Maad Uk. 661. 97. Hebu angalia jibu lifuatalo kuhusu fatwa za wanazuoni wa dini ambao walitoa fat'wa sanjari na hilo!! 98. Jariidat Ummul-Quraa toleo la 17 kutoka Iilaam 14. 227


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 228

Tawhid na Shirk 1. Ni dhahiri katika baadhi ya Aya zinaeleza kwamba watu wafuatao sheria za mbinguni walikuwa wakijenga misikiti juu ya makaburi ya Mawalii wao, kwa ajili hiyo ukazuka mzozo kuhusiana na watu wa pango (As’haabul-kahf) miongoni mwa washirikina wakasema: “Jengeni juu yao majengo kwani Mola wao ni mjuzi zaidi yao.” Wakasema wengine nao ni Waislamu: “Hakika tutajenga jengo juu yao, msikiti.” (18:21) Zamakhshari katika kutafsiri maneno ya Mola Manani: “Jengeni juu yao” akasema: “yaani jengeni katika mlango wa pango lao ili watu wasije wakachukua udongo wao na uhifadhike, kama ulivyohifadhika udongo uliopo katika kaburi la bwana Mtume (s.a.w.w).” Na akasema katika kutafsiri maneno ya Mola (s.w.t): “Wakasema walioshinda katika jambo lao: tutajenga juu yao msikiti.” “Yaani Waislamu ambao walikuwa na haki ya kujenga juu yao wakasema: Tutafanya katika mlango wa pango Msikiti wataswali hapo Waislamu, watatabaruku sehemu yao.”99 Na katika tafsiri Jalaleni amesema: “Basi watasema - yaani makafiri – “Jengeni juu yao” yaani pembezoni mwao jengo ambalo litawastiri wao, “Mola wao ni mjuzi zaidi yao wakasema wale ambao wameshinda juu ya jambo lao” suala la vijana nao ni waumini, wakasema: “Tujenge juu yao”, yaani pembezoni mwao msikiti ambao utaswaliwa.100 Kwa ujumla wafasiri wote wameafikiana kwamba waliosema kuhusu kujenga msikiti juu ya makaburi ya Mawalii walikuwa Waislamu safi, na lengo la Qur’an kunukuu maneno hayo ambayo yametokana na wao ni ishara tosha kwamba tuwafuate na tuchukue kutoka kwao kigezo chema. Na lau ingelikuwa kujenga msikiti juu ya makaburi yao na katika makaburi ya Mawalii wengine ni jambo la haramu, bila shaka Qur’an ingeliitupitilia mbali kauli hiyo, kuikosoa na kuikemea vikali ili mjinga asipotee. Na ama yale yaliyopokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kwamba amesema: 99. Kashafu Juz. 2 Uk. 254. 100. Tafsir Jalalain Juz. 2 Uk. 3. 101. Sahih Bukhari Juz. 2 Uk. 111 kitabu Janaiz. 228


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 229

Tawhid na Shirk

“Mwenyezi Mungu amewalaani Mayahudi na Wanaswara kwa kufanya makaburi ya Manabii wao kuwa ni misikiti,” makusudio yake ni kufanya makaburi ya Manabii101 na mengineyo kuwa Kibla chao katika swala, na kwa hakika Waislamu wameepukana na hayo,” Qastwalaani ameliweka wazi suala hilo katika kitabu chake Irshad Saari Fi Sharh Sahih Bukhari. Hakika makaburi ya Mitume yameenea pembezoni mwa msikiti wa Baytul-Muqadas kama vile kaburi la Nabii Daud (a.s.) ambalo lipo katika Qudus, na kaburi la Ibrahim na mwanae Is’haaq na Yusuf (a.s.) ambalo Nabii Musa (a.s.) alilihamisha kutoka Misri hadi Baytul Muqadas katika mji wa Khalili, majengo yote hayo yamejengwa kwa mawe makubwa ya kawaida katika miji ya kiislamu hadi hivi leo, isipokuwa Ibnu Taimiyyah aliomba udhuru kutokana na hilo katika kitabu chake Siraatul Mustaqiim, amesema: “Hakika jengo ambalo lilikuwepo katika kaburi la Nabii Ibrahim (a.s.) lilikuwepo tangu wakati wa ukombozi na zama za Masahaba, isipokuwa mlango wa jengo lake ulikuwa umefungwa mpaka mwaka 400 A.H.” Lakini maneno haya hayafaidishi katu wala hayatudhuru, kwa sababu Umar aliikomboa Baytul Muqadas aliliona jengo hilo pamoja na hivyo hakulibomoa, sawa iwe imesihi kauli ya Ibnu Taimiyyah kwamba lilikuwa limefungwa hadi mwaka wa 400 A.H au haikusihi, bado inajulisha kwamba sio haramu kujenga juu ya makaburi, na jengo hilo lilidumu karne na karne chini ya dola mbalimbali za kiislamu, na wala haikusikika toka kwa yeyote miongoni mwa wanazuoni, watu wema, wanadini na wasiokuwa hao kabla ya Mawahabi kupinga hilo, na sio kupinga tu na hadi kufikia kuamrisha yabomolewe au kuharamisha kujengewa au kuwakemea wafanya ziara kutoka vitongoji mbalimbali duniani. Na katika kuongezea hilo tuseme kwa hakika alizikwa Mtume chumbani mwake, aidha walizikwa humo sahaba (rafiki) zake wawili na hakuna tofauti kati ya jengo la 229


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 230

Tawhid na Shirk kabla na la baada, na hakuna aliyenukuu kwamba ipo tofauti kati ya jengo la zamani na la sasa. Na kwa faida zaidi rejea historia ya kujengewa eneo la kaburi Mtume (s.a.w.w), basi zingatia.

MAWAHABI NA HADITHI YA ABU HAYYAJ Katika kuhitimisha maudhi hii tunatoa kigezo walichoking’ang’ania Mawahabi katika ubomoaji wa makaburi. Amepokea Muslim katika Sahihi yake amesema: “Ametuhadithia Yahya bin Yahya, Abu Bakr bin Abu Shaiba na Zuheir bin Harb Yahya amesema: Ametupa habari na mwingine akasema: Ametusimulia Waqii bin Sufiyan kutoka kwa Habibu bin Abu Thabit kutoka kwa Abu Wail kutoka kwa Abu Hayyaj Asadi amesema: Ali bin Abi Talib aliniambia, je nikutume kama alivyonituma Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kwamba usiache sanamu isipokuwa umelivunja na wala kaburi isipokuwa umelisawazisha.”102. Mawahabi katika ulazima wa kubomoa makaburi na kuyasawazisha yawe sawa na ardhi wametolea dalili kulingana na maneno ya Mtume (s.a.w.w):

“Wala kaburi lililoinuka isipokuwa umelisawazisha”. Hakika uthibitishaji wa hadithi hiyo iliyotajwa hujikita katika mambo mawili: Sanad (mtiririko wa wapokezi) ya hadithi iwe sahihi na wapokezi wake wawe waaminifu. Dalili ya hadithi ijulishe makusudio yake. Lakini hadithi hiyo ina mapungufu katika pande zote mbili: ama upande 102. Sahihi Muslim Juz. 3 Uk. 61 kitabu Janaiz; Sunan Tirmidhi Juz. 2 Uk. 256 mlango yaliyokuja katika kulisawazisha kaburi na Sunan Nasai Juz. 4. Uk. 88 mlango wa kulisazisha kaburi. 230


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 231

Tawhid na Shirk wa sanadi wapo watu ambao haifai kutolewa hoja kutokana na hadithi wazipokeazo, hao ni: 1. 2. 3. 4.

Wakii Sufiyan Thauri Habibu bin Abu Thabit Waili Asadi.

Na ama kuhusu Wakii, Imam Ahmad bin Hanbali amesema: “Amekosea katika hadithi mia tano.”103 Kama ilivyonukuliwa kutoka kwa Muhamad bin Murwazi kwamba (Wakii) alikuwa akisimulia hadithi kwa maana yake na hakuwa miongoni mwa wanahadithi, yaani hayumo miongoni mwa wasimulizi wa hadithi, na hakupokea hadithi kwa matini yake na lafudhi yake, aidha hakuwa mjuzi wa lugha ya kiarabu.104 Ama Sufiyan Thauri hakika amemnukuu Ibnu Mubaraka amesema: “Sufiyan alisimulia hadithi nikaenda basi nikamkuta akitia maneno yake, na aliponiona mimi akaona haya.105 Na imenakiliwa katika wasifu wa Yahya bin Qatwan, kuwa imepokewa kutoka kwake amesema: “Sufiyan alikuwa akijaribu asiyekuwa mwaminifu kwangu kumfanya awe mwaminifu, lakini hakuweza.”106 Ama kuhusu Habib bin Abu Thabit imenakiliwa kutoka kwa Abu Hibban amesema: “Alikuwa mpotoshaji wa hadithi “anaongeza kitu katika hadithi na anapunguza”107 103. 104. 105. 106. 107.

Tahadhib Tahadhib Juz. 11 Uk. 125. Tahadhib Tahadhib Juz. 11 Uk. 130. Tahadhib Tahadhib Juz. 4 Uk. 115. Tahadhib Tahadhib Juz. 11 Uk. 218. Tahadhib Tahadhib Juz. 3 Uk. 179. 231


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 232

Tawhid na Shirk Vivyo hivyo imenukuliwa kutoka kwa A’twa kuhusu yeye amesema: “Maneno yake hayafuatwi na hakuwa na uwezo wa kuhifadhi.”108 Na ama Wail huelezwa kwamba alikuwa ni mtu ambaye ana chuki na Imam Ali bin Abi Talib (a.s.), hayo yanahusu sanadi (mtiririko wa wapokezi wa hadithi). Na ama kuhusu jambo la pili “yaani dalili ya hadithi” Hapana budi kuzingatia kwa makini katika lafudhi mbili zilizopatikana ndani yake nazo ni: “lililoinuka” na “utalisawazisha kabisa”. Ama kuhusu ibara “kuinuka” makusudio yake ni sehemu ya juu au kichuguu.109 Na imekuja ibara katika kamusi: “Sharafa Muharrakata” ni muinuko, na juu ya ngamia ni nundu lake.110 Ama kuweka sawa sawa mradi wake ni kuweka sawa kisichonyooka, husemwa: ameweka kitu sawa: Yaani amekifanya sawa sawa, na husemwa: nimekiweka kitu sawa: Yaani nimekifanya sawa sawa, na husemwa: amekiweka kilicho panda sawa yaani amekitengeneza sawa sawa, katika Qur’an tukufu imekuja: “Ambaye ameumba akakamilisha.” (87:2) Na kwa hivyo maana ya karibu inayoeleweka kuwa nimeliweka kaburi sawa yaani nimeliondoa nundu lake, na sio maana yake kulibomoa chini yake, na hayo ndiyo Madhehebu ya jamaa, miongoni mwao ni Mashafi, kwani imekuja katika kitabu kiitwacho Al Fiqhu Ala Madhahibul-Arba’ah: “Na inasuniwa kunyanyua mchanga juu ya kaburi kwa kadiri ya shubiri moja.”111 Aidha imekuja: Na hufanywa kama nundu la ngamia, na Shafii akasema: 108. Sharhul-Hadiidi. 109. Manjid mada ya Sharafu. 110. Qamus Mada ya Sharafu. 111. Fiqhu ala Madhahib Arbaat Juz. 1 Uk. 420. 232


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 233

Tawhid na Shirk ”Kufanya mchanga sawa sawa ni bora zaidi ya kuweka nundu juu yake.”112 Hadithi hiyo inaungwa mkono na Madhehebu ya Shaafi na imani hiyo ndiyo ya Mashia Imamia. Na la msingi na la kuzingatiwa ni kwamba Muslim ambaye ni mtunzi wa kitabu Sahih Muslim ameiandika hadithi hiyo chini ya anwani: “Mlango wa kusawazisha kaburi” sio chini ya anwani “Amri ya kuharibu makaburi na kuyabomoa.”113 Na katika kuunga mkono hayo Muslim amenukuu katika Sahihi yake ambayo huungwa mkono na yale tuliyoyaeleza katika hadithi iliyotajwa kutokana na maana hiyo, baada ya kutaja wapokezi lukuki akasema: “Thamamat bin Shufaya amesema: Tulikuwa pamoja na Fudhalat bin Abiid katika ardhi ya Roma akaamrisha lisawazishwe kaburi lake kisha akasema: “Nilimsikia Mjumbe wa Mwenyezi Mungu akiamrisha liwekwe sawa sawa.” Na hapana shaka hakika mradi wa kaliweka sawa sawa sio kulifanya hilo sawa sawa na ardhi, kwa sababu hilo linakwenda kinyume na Sunna sahihi ambayo ina hukumu kunyanyuliwa ardhi shubri moja, hivyo kusudio linakuwa ni kulisawazisha nundu lake, na hilo limekuja katika ibara ya Nawawi alipofasiri hadithi iliyotajwa katika Sahih Muslim, amesema: “Wala haliwekwi nundu, bali hunyanyuliwa mfano wa shubiri moja na huwekwa sawa sawa. “114 Na hii si tafsiri yetu sisi tu juu ya hadithi hii, bali ameeleza hilo Ibnu Hajar Qastwalani katika kitabu chake Irshad Saari fi Sherh Sahih Bukhari115 aliposema baada ya kutaja kwamba Sunna ni kusawazisha kaburi na kwamba haifai kuacha kulisawazisha eti ili tu kutofautiana na Mashia: ”Kwani haikukusudiwa kulisafisha na kulisawazisha sawa na ardhi, bali ni kuliondolea nundu....”. 112. Fiqhu ala Madhahub Arbaat Juz. 1 Uk. 420 113. Sahih Muslim Juz. 3 Uk. 61 kitabu Janaiz. 114. Sherh Sahihi Muslim cha Nawawi. 115. Irshad Saari Juz. 2 Uk. 468. 233


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 234

Tawhid na Shirk Na mwisho ni kwamba haikupatikana katika hadithi ya Mtume (s.a.w.w) kwamba amesema: “Wala kaburi isipokuwa umelisawazisha, wala jengo lililojengwa juu ya kaburi wala Qubba isipokuwa lisawazishe” kwa hivyo mradi wake sio mwingine ila yale tuliyoyaeleza hapo kabla, nayo ni kutoweka nundu juu ya kaburi, ama kujenga juu au pembezoni mwa kaburi sio makusudio yake, na hakuna dalili wala hadithi inayojulisha kutofaa kujenga juu ya makaburi, bali nyendo, tabia na matendo ya Waislamu ni kinyume na hivyo, kama ulivyokwishaelewa hapo kabla. Na hata tukijaalia mradi wa kuweka sawa sawa ni kuharibu Qubba na majengo yaliyopo juu ya makaburi, basi linalotegemewa sana mradi wake ni makaburi ya washirikina waliotukuzwa wakati huu na waabudu masanamu na washirikina, kwani makaburi hayo baada ya kuja Uislamu yaliachwa katika hali yake na kama yalivyo, hilo linaungwa mkono na ile hali ya kwamba bwana Mtume (s.a.w.w) alimtuma Ali (a.s.) kubomoa vinyago vilivyokuwepo katika vitongoji vya mji wa Madina, na vinyago hivyo na picha hazikuwa ila ni Masanamu ambayo yalikuwa yakiabudiwa hata baada ya kuja Uislamu. Kwa hivyo kuna mafungamano gani kati ya hadithi hiyo na makaburi ya Mitume na watu wema? 1. Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema: “Katika nyumba alizoruhusu Mwenyezi Mungu litukuzwe na litajwe humo jina lake…” (24:36); “watu ambao biashara wala kuuza hakuwashughulishi na kumkumbuka Mwenyezimungu..” (24:37) Hoja ya Aya hizo juu ya kujuzu kujenga juu ya makaburi, inajikita juu ya mambo mawili: 1. Ni upi mradi wa nyumba hizo? 2. Na upi mradi wa kunyanyuliwa? Ama jambo la kwanza hakika imepokewa hadithi kutoka kwa Ibnu Abbasi kwamba mradi wa hizo ni Misikiti kutukuzwa na kuzuiwa kufanya upuuzi ndani yake, na kutajwa humo jina la Mwenyezi Mungu (s.w.t). 234


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 235

Tawhid na Shirk Bila shaka ni wajibu kwetu katika mchakato huu kuchunguza tafsiri hii, kwani ni dhahiri shahiri kwamba tafsiri ya Ibnu Abbasi ya “nyumba” kuwa ni Misikiti ni moja miongoni mwa mifano halisi ya nyumba hizo, na sio kuwa ndio mfano halisi pekee, bali tafsiri kama hizo za kutaja mfano mmoja bila kutaja yote ni nyingi sana, wala sio katika kadhia hiyo pekee. Bali inawezekana ikasemwa: “nyumba” sio Msikiti, kwani msikiti ni Sunna usiwe umefunikwa paa, na mfano bora ni Msikiti mtukufu wa Makka, tunaona kwa hisia dhahiri umejengwa ukiwa wazi bila paa, na kwa kweli katika Kiarabu jengo lisilo na paa haliitwi nyumba bali ni lile lenye kuta na paa, Mola manani anasema: “Bila shaka tungelifanya dari za nyumba za watu wanaomkufuru Rahmani kuwa paa la fedha.” (45:33) “Wala sio wema kuyaendea majumba yenu kwa nyuma yake.” (2:189) Na hilo ni dhahiri na liko wazi kwa mazingatio na mazoea ya watu, wao hutumia neno nyumba kumaanisha nyumba za waarabu na mahema yao yaliyoko shamba, na si kwa kumaanisha vijiji kwa kuwa vyenyewe viko wazi bila paa, hiyo ni tofauti na mahema, kwani yenyewe hufunikwa paa, na kwa ajili ya hayo tuliyoyataja huwezi kupata ndani ya Qur’an tukufu mahala ambapo pametaja nyumba kuwa ni msikiti, ila ilipotajwa Ka’ba, kwa kuwa yenyewe ina paa ndio maana imeitwa nyumba ndani ya Qur’an katika mahala mbalimbali. Mwenyezi Mungu anasema:

“Muitakase nyumba yangu kwa ajili ya wenye kutufu (kuzunguka) na kwa wenye kukaa na wenye kuinama na kusujudu.” (2:125) na akasema:

235


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 236

Tawhid na Shirk “Mwenyezi Mungu akajaalia Kaaba tukufu kuwa ni kisimamo cha watu.” (5:97) na akasema:

“Katika hayo yamo manufaa kwa ajili yenu mpaka muda maalum, kisha mahala pa kuchinjiwa kwake ni kwenye nyumba ya kale.” (22:33) kutokana na maelezo hayo ni kwamba makusudio ya Aya hiyo “Katika nyumba alizoruhusu Mwenyezi Mungu litukuzwe na litajwe humo jina lake…” sio misikiti bali nyumba takatifu ambazo Mwenyezi Mungu ameidhinisha litajwe humo jina lake, na nyumba za Manabii na Mawalii hasa hasa ndio mifano halisi ya nyumba hizo, kutokana na yale ambayo Mwenyezi Mungu ameyahusisha katika nyumba hizo na watu wake ambayo ni wingi wa utukufu na sharafu. Mwenyezi Mungu kuhusu nyumba ya Mtume (s.a.w.w) na ndugu zake wa karibu anasema: “Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu watu wa nyumba (ya Mtume) na (anataka) kukutakaseni sana sana” (33:33) Na nyumba hizo zinafanana na nyumba ya Ibrahim (a.s.) kama vile Malaika walivyosema kuhusiana na shani yake kwa mke wa Nabii Ibrahim, Mwenyezi Mungu anasema:

“Wakasema: Unastaajabu amri ya Mwenyezi Mungu? Rehema za Mwenyezi Mungu na baraka zake iko juu yenu enyi watu wa nyumba hii, hakika yeye ndiye msifiwa, mwenye kutukuzwa.” (11:73) 236


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 237

Tawhid na Shirk Kwa ajili hiyo tunamuona Al-Allama Suyutwi baada ya kunukuu kauli ya Ibnu Abbas akanukuu kutoka kwa Mujahidi pale aliposema: “Hakika mradi wake ni nyumba za Mtume (s.a.w.w).” Na ameeleza Ibnu Murduway kutoka kwa Anas bin Malik na Buraida, anasema: “Mtume (s.a.w.w) alisoma Aya hiyo, mtu mmoja akasimama na kuuliza: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ni nyumba gani hizo? Akasema: “Nyumba za Manabii wa Mwenyezi Mungu” Abu Bakr akasimama akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu miongoni mwa nyumba hizo ni nyumba hii (yaani nyumba ya Ali na Fatima)? Akasema: “Ndio, nayo ndiyo bora zaidi ya hizo.”116 Hilo linahusiana na jambo la kwanza, na ama mradi wa kunyanyuliwa, nalo ndilo jambo la pili, huzingatiwa moja kati ya maana mbili: 1. Mwenyezi Mungu ameidhinisha nyumba hizo ziinuliwe kwa majengo ili ziwe mahala pa ibada ambayo imeelezwa ndani ya Aya hiyo, ambayo ni kutajwa jina lake tukufu na kumsabihi ndani yake asubuhi na jioni. Na hilo linajulishwa na maneno ya Mola (s.w.t):

“Na (kumbukeni) Ibrahim na Isma’il walipoinua misingi ya nyumba (wakaomba) Ewe Mola wetu utukubalie, hakika wewe ndiye Mwenye kusikia, Mwenye kujua.” (2:127) Na lililo dhahiri hapa ni kwamba mradi wa “kuinuliwa” katika sehemu zote mbili ni kuzijenga na kuziimarisha “nyumba” na kuziinua juu. 2. Hakika mradi wa kunyanyua ni kuzitukuza na kuziheshimu hizo. 116. Durrul-Manthuur fi Tafsir bil Maathuur Juz. 5 Uk. 50. 237


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 238

Tawhid na Shirk Na lau yatakuwa makusudio yake ni ya kwanza basi itakuwa ni tamko la wazi linaloelekeza kujenga juu ya makaburi ambayo yamo majumbani mwao. Na kama makusudio ni ya pili basi itakuwa ni tamko la wazi linaloelekeza kuheshimu, kuzitukuza na kuziadhimisha nyumba hizo. Na ni jambo lajulikana wazi kwamba kuliendeleza jengo na kulilinda dhidi ya kuharibika na kulikarabati upya, aidha kutandika mikeka na majamvi ndani yake na kuipamba kwa yasiyokatazwa na Mwenyezi Mungu na kulilinda kutokana na uharibifu na kubomoka, ni kuliheshimu na kulitukuza, kama ambavyo kuisitiri Ka’ba tukufu kwa sitara za thamani ni kuitukuza kama ilivyozoeleka. Yote hayo ni kumtukuza Mtume (s.a.w.w) ili yatimie malengo yaliyotajwa na Aya ”kutajwa jina la Mwenyezi Mungu na kumtakasa Yeye asubuhi na jioni”. 3. Kujenga juu ya makaburi ni katika kuadhimisha alama za dini ya Mwenyezi Mungu, anasema: “Hivyo ndivyo anayeziheshimu alama za Mwenyezi Mungu basi hayo ni katika unyenyekevu wa nyoyo.” (22:32) na neno “Shaa’ira” ni wingi wa neno “Shaii’rat” lenye maana ya alama, sio makusudio yake alama na dalili za kuwepo Mwenyezi Mungu, kwani ulimwengu umefunika dalili za kuwepo Kwake bali, ni alama za dini Yake. Kwa ajili hiyo wafasiri wa Qur’an wakafasiri kuwa ni alama za dini ya Mwenyezi Mungu. Allah amesifu na kueleza “Swafa na Marwa” kuwa hiyo milima miwili ni miongoni mwa alama za Mwenyezi Mungu, anasema:

“Hakika Swafa na Marwa ni katika alama za (dini) ya Mwenyezi Mungu” (2:158) Na anasema:

“Na ngamia (wa sadaka) tumekufanyieni kuwa katika alama za Mwenyezi Mungu juu yao …” (22:36) 238


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 239

Tawhid na Shirk Na anasema:

“Enyi mlioamini msivunje heshima ya alama za Mwenyezi Mungu …” (5:2) Na mradi wake sio kitu kingine isipokuwa ni alama za dini yake, kwa hivyo ikiwajibika kutukuza alama za Mwenyezi Mungu kwa kuelezwa na Qur’an kinagaubaga na kutaja sababu ya kufanya hivyo kwamba ni kwa ajili ya uchamungu wa nyoyo, basi itafaa pia kuwatukuza Manabii na Mawalii kwa kuwazingatia kuwa wao ni alama kubwa zaidi za Mwenyezi Mungu na ni wenye kufaa kuadhimishwa na kutukuzwa zaidi. Wao ndiyo watu ambao wamefanya juhudi na kazi kubwa ya kufikisha dini ya Mwenyezi Mungu kwa viumbe, kwa hivyo kuhifadhi makaburi yao, majengo na athari zao ni bora zaidi. Na ukipenda sema: Hakika kutukuza kitu ni kulingana na hadhi yake na mtindo wake, basi kuitukuza Ka’ba ni kuisitiri kwa sitara mbalimbali, na kutukuza ngamia ambaye ni miongoni mwa alama za Mwenyezi Mungu kuwa ni kule kuendeleza kumpeleka kwenye chinjo lake, kuacha kumpanda na kumpa malisho, na kuwatukuza Manabii na Mawalii katika uhai wao Ni kwa mtindo mbali tofauti na ule wa kuwatukuza baada ya kufariki kwao. Hivyo kila linalohesabiwa kuwa ni kuadhimisha na kutukuza inafaa, katika uhai wao ni kwa njia moja, na baada ya kufariki kwao ni kwa njia nyingine, hivyo yote yanazingatiwa kuwa ni kutukuza na kuadhimisha, na kufuatana na Aya hii ni jambo lisilo shaka wala utata kwamba inajuzu.

8. KUZURU MAKABURI Waislamu wote wameafikiana kuhusiana na kuruhusiwa kisheria kuzuru makaburi, na hilo linadhihirika kwa yule atakayerejea vitabu vya kifiqihi 239


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 240

Tawhid na Shirk na hadithi, wala haturefushi maelezo kuhusiana na mchakato wa kujuzu kuzuru makaburi kwa kutaja hadithi kadhaa wa kadhaa zinazo husiana na kadhia hii, na yatosha kuhusu hilo ile fat’wa iliyotolewa na Maimamu wa Madhehebu manne kama ilivyokuja katika kitabu (Fiqh Ala Madhahib alArbaat) kama ifuatavyo: “Kuzuru makaburi ni jambo la Sunna, ni kwa lengo la kuwaidhika na kujikumbusha akhera, na inatiliwa mkazo zaidi siku ya Ijumaa, siku ya kabla yake na baada yake. Yampasa mwenye kuzuru kujishughulisha kwa dua, kuwa na unyenyekevu na kuzingatia kifo, aidha kusoma Qur’an kwa ajili ya maiti, kwa hakika hilo hunufaisha maisha.” Aliendelea hadi aliposema: “Hakuna tofauti katika kuyazuru makaburi baina ya makaburi ya karibu na yale ya mbali, bali ni Sunna kufunga safari kwa lengo la kwenda kuzuru maiti hasa hasa makaburi ya watu wema. Ama kuzuru kaburi la bwana Mtume (s.a.w.w) kuna fadhila kubwa zaidi, nalo ni miongoni mwa makaburi yaliyo adhimu zaidi kwa ajili ya kujikurubisha.” 117 Na mwenye kutaka kuzitambua hadithi zinazoelezea suala hilo basi arejee vitabu vya hadithi miongoni mwa vitabu Sahihi na Sunani. Na kati ya hadithi hizo ni zile zilizopokewa kutoka kwa bwana Mtume (s.a.w.w) amesema:

“Nilikuwa nimekukatazeni kuzuru makaburi, hakika Muhammad ameruhusiwa kuzuru kaburi la mama yake, basi zuruni makaburi kwani huwakumbusha akhera.” Imepokewa hadithi hiyo na waandishi watano wa Sahih isipokuwa 117. Fiqhu ala Madhahib Arbaat Juz. 1 Uk. 424-425 mwisho wa kitabu swalat. 240


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 241

Tawhid na Shirk Bukhari, na nukuu hiyo ni kwa mujibu wa lafudhi ya Tarmidhi. Riwaya juu ya kadhia hii si hiyo tu bali zipo hadithi nyingi sana ambazo amezikusanya mwanachuoni mkubwa anayeitwa Al-Allama Samuhud katika kitabu chake kiitwacho Wafaaul-Wafa. 118 Isipokuwa sisi tunataka hapa tuthibitishe kujuzu na kuruhusiwa kwa tendo na amali hiyo katika Kitabu kitakatifu, tunasema: Hakika Mwenyezi Mungu amemkataza Nabii Wake kusimama juu ya makaburi ya washirikina na kuwaswalia hao, anasema: “Wala usimswalie yeyote miongoni mwao akifa wala usisimame kaburini pake...”(9:84) Aya tukufu inakataza kusimama juu ya kaburi la Mnafiki na Mshirikina na kumswalia kama inavyojulisha kwa njia ya mafuhumu, na hiyo ni kwamba kusimama juu ya makaburi ya Waumini, kuwaombea dua na kuwaswalia ilikuwa ni sira na mwenendo wa Mtume (s.a.w.w). Na muradi au makusudio ya kusimama si mahsusi wakati wa kuzika tu hadi tuseme kwamba haijumuishi kisimamo kile cha kuzuru makaburi. Hiyo ni kwa sababu imekosekana dalili inayotenga hilo, bali lafudhi: ”Usisimame juu ya kaburi lake abadan” yaani ni katika zama zote, na hivyo inajumuisha baada ya kuzika pia. Na huenda hayo tuliyoyaeleza ndio aliyoyafasiri mwandishi wa Jalaleni katika kitabu chake aliposema: ”kwa kuzika au kwa kuzuru.” Na makusudio ya Swala si swala ya maiti tu, kwani lau ingekuwa makusudio ni Swala ya maiti tu basi asingelisema ”abadan”, kwa sababu swala ya maiti huwa wajibu mara moja, na wala haijikariri hata asema “Abadan.” Na wala makusudio si kujumuisha mifano yote halisi ya washirikina na kuonyesha kwamba hukumu hiyo inawahusu wote, kwani tayari hilo ameshalibainisha mwanzo aliposema: ”yeyote miongoni mwao”, na pia lafudhi “Abadan” hubainisha kuendelea kwa hukumu katika zama zote na 118. Wafaul-Wafa Juz. 2Uk. 3903-3904. 241


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 242

Tawhid na Shirk sio ueneaji kwa wahusika, Mwenyezi Mungu anasema: “Wala msioe wake zake baada yake abadan...” (33:53) Hii inamaanisha hata baada ya miaka 10 au 20 mpaka mwisho wa zama. Hivyo inajulisha kwamba makusudio Swala hapo ni kitendo chochote cha kuomba rehema ambacho kinajirudia maishani, na sio Swala ya maiti tu. Ndiyo, na yenyewe Swala ya maiti ni moja ya sehemu za kitendo cha kuomba rehema hivyo nayo inaingia chini ya makusudio, lakini si yenyewe pekee. Ikiwa kitendo hicho ni katika mwenendo wa Mtume (s.a.w.w) basi ni kwa dalili gani ya Qur’an kiwe leo ni bidaa? Bali ni lazima kiwe ni Sunna isiyo na shaka, Mwenyezi Mungu anasema:

“Bila shaka mnao mfano mwema kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, kwa mwenye kumuogopa Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho na kumtaja Mwenyezi Mungu sana.” (33:21) Amesema tena: “Sema: ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu, basi nifuateni, Mwenyezi Mungu, atawapenda na atawasamehe madhambi yenu na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa msamaha, Mwenye kurehemu” (3:31) Ikiwa ni Sunna kuzuru kaburi la Muumini, namaanisha kusimama mbele ya kaburi la muumini, na ni mwenendo wa Mtume (s.a.w.w), basi ni vipi isiwe Sunna kusimama kwenye kaburi la Mtume (s.a.w.w) na makaburi ya Maimamu (a.s.), ilihali wao ndiyo nguzo za dini na viongozi wa waumini, na ndiyo wakamilifu zaidi wenye fadhila zaidi na wabora kuliko wengine wote.

242


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 243

Tawhid na Shirk Na katika kuhitimisha maudhui hii hapa tunaashiria yale ambayo Mawahabi wameshikamana nayo katika kuzuia kufunga safari kwa lengo la kuzuru makaburi. Wametolea dalili kupitia yale aliyoyapokea Bukhari kutoka kwa Abu Huraira kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kwamba amesema:

“Haifungwi safari ila kwa lengo la kwenda misikiti mitatu, msikiti wa Makka (Masjidul–Haraam), Msikiti wa Mtume na msikiti wa Qudus (Palestina).”119. Abdullah bin Muhammad bin Abdul-Wahab amesema: “Husuniwa kumzuru Mtume (s.a.w.w) na isifungwe safari isipokuwa kuzuru msikiti na kuswali humo, na itakapokusudiwa hayo pamoja na kulizuru kaburi (msikiti na kuzuru kaburi) si vibaya.”120 Na hakika ni kwamba hadithi hii ambayo wameshikamana nayo Mawahabi haijulishi uharamisho wa kufunga safari kwenda kuzuru makaburi na sehemu takatifu.....121 (hiyo ni kwa mujibu wa kanuni za lugha ya Kiarabu kwa mujibu wa muundo wa sentensi hiyo.) Naongezea katika hilo kwamba hakika dharura inahukumu kuruhusiwa kufunga safari kwa lengo la kufanya biashara, kutafuta elimu, kupigana jihadi, kuwatembelea wanazuoni, watu wema na matembezi, na kwamba Waislamu katika msimu wa Hijja hufunga safari kwenda Arafa, Muzdalifa na Mina na sehemu nyingi nyinginezo. Pamoja na hivyo vipi iwezekane kusema kuwa makusudio yake ni “Haifungwi safari kwenda sehemu yoyote miongoni mwa sehemu isipokuwa katika sehemu hizo tatu.” 119. Risalat Thaniya min Rasail Maasuumat Bi "Hadiyyat Saniyyat". 120. Risalat Thaniya min Rasail Maasuumat Bi "Hadiyyat Suniyyat". 121. Tumeondoa ufafanuzi wa mwandishi unaohusu kanuni za lugha ya kiarabu na ufafanuzi wa Hadithi hiyo kwa mujibu wa kanuni hizo, kwa kuzingatia kwamba usingeeleweka ila kwa yule ajuaye vyema kanuni, fasaha na balagha ya lugha adhimu ya Kiarabu - Mhariri wa toleo la Kiswahili. 243


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 244

Tawhid na Shirk Na natija ipatikanayo hapa ni kwamba hapatwi na shaka yule ambaye ana maarifa kidogo ya lugha ya kiarabu na mpangilio wake kwamba makusudio ya maneno yake: “Haifungwi safari” yaani haimpasi mtu kusafiri kwa lengo la kwenda kwenye msikiti nje ya misikiti hii, na sio kusafiri mahala pengine popote pasipokuwa misikiti hiyo mitatu. Haya ndio madhumuni ya hadithi na maana yake, pamoja na hivyo bado haifahamiki katika hadithi hiyo na inayofanana na hiyo ule uharamu wa kusafiri kwenda misikiti iliyobakia, bali dhahiri ya hadithi hiyo ni kuonyesha fadhila kubwa za misikiti hiyo kushinda ile isiyokuwa hiyo, na kuna fadhila kubwa mno kufunga safari kwa lengo la kwenda kwenye misikiti hiyo na kuswali ndani yake. Ama misikiti mingine haina hadhi hiyo, kwani thawabu hutarajiwa kwa kila mwenye kuelekea msikiti wowote ule, na misikiti isiyokuwa hiyo kama vile msikiti wa jumuiya au msikiti wa sokoni au msikiti wa kitongoji, yote hiyo ipo katika mji wa mhusika, haimpasi kufunga safari kwenda miji mingine madamu misikiti hiyo ipo kila mji na inalingana kifadhila na ubora. Ndio, yale yanayotegemewa kupatikana katika kufunga safari kwenda misikiti misikiti mitatu huzidi mno kuliko yale yanayotokana na misikiti mingine. Hivyo muhtasari wa mchakato huu ni kwamba maana ya hadithi ni kutofunga safari kwenda kwenye misikiti miongoni mwa misikiti na sio kutokwenda sehemu miongoni mwa sehemu, hilo la kwanza. La pili: Hakika ukatazo wa kufunga safari kwenda misikiti mingine isiyokuwa hiyo mitatu sio katazo la lazima kuachwa, bali ni mwongozo uelekezao kwamba kule kuelekea misikiti mingine isiyokuwa hiyo mitatu hakuna thawabu nyingi mno. Na dalili juu ya hilo ni kwamba Mtume (s.a.w.w) alikuwa akifunga safari kwenda misikiti mingine isiyokuwa hiyo mitatu iliyotajwa katika hadithi, kama ilivyokuja katika Sahih Bukhari: “Katika mlango wa kwenda msikiti wa Qubaa kwa kipando na kwa miguu, imepokewa kutoka kwa Ibnu Umar amesema: ”Mtume (s.a.w.w) alikuwa akienda Quba akiwa katika kipando na akitembea kwa miguu.”122 122. Sahih Bukhari Juz. 2 Uk. 61. 244


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 245

Tawhid na Shirk Na katika mlango wa mwenye kwenda katika msikiti wa Quba kila Jumamosi, imepokewa kutoka kwa mtoto wa Umar amesema: ”Kila Jumamosi alikuwa Mtume (s.a.w.w) akienda msikiti wa Qubaa kwa miguu na akiwa juu ya kipando.” Na alikuwa Abdallah (mtoto wa Umar) akifanya hivyo.123 Na katika mlango wa msikiti wa Qubaa imepokewa kutoka kwa mtoto wa Umar alikuwa akihadithia kwamba Mjumbe wa Mwenyezi Mungu alikuwa akizuru msikiti huo akiwa juu ya kipando na akitembea kwa miguu.124 Huyo ndiye Imam Bukhari, amepokea hadithi na kutusimulia sisi kwamba bwana Mtume (s.a.w.w) alikuwa akifunga safari kwenda msikiti wa (Qubaa), je! hiyo sio dalili ya kufaa kufunga safari kwenda misikiti na sehemu nyingine isiyokuwa misikiti hiyo mitatu? Je! Si Sahihi Bukhari ndicho kitabu sahihi zaidi na kinachokubalika mno kati ya vitabu vinavyotegemewa kwa Ahlu Sunna? Na iko wapi kauli ya Allama Suyutwi kuhusiana nayo, hivi ndivyo asemavyo: ”Hakika hakuna kitabu sahihi kingine kama vile Sahihi Bukhari, kimekusanya yasiyo na mithili, na hakuna Musnad kama vile Musad Ahmad.” Basi kwa nini wamekiacha na kukiweka nyuma ya migongo yao, wakaamini baadhi yaliyomo na kuacha na kuyaweka kando mengine!

9. KUSWALI MAKABURINI Ibnu Taimiyyah katika barua yake Ziyaratul-Qubuuri (kuzuru makaburi) anasema: “Hajasema yeyote miongoni mwa Maimamu waliotangulia kwamba kuswali makaburini na katika sehemu walizozikwa Mashahidi ni Sunna, na wala kwamba kuswali na kuomba dua maeneo hayo ni bora na kuna fadhila zaidi kuliko sehemu nyingine, bali wao wote wamekubaliana kwamba kuswalia ndani ya misikiti na majumbani ni bora kushinda kuswalia katika makaburi ya Mitume!!”125 123. Sahih Bukhari Juz. 2 Uk. 61. 124. Ziyaratul- Qubuur Uk. 159-160. 125. Ziyaratul-Qubuur Uk. 159-160. 245


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 246

Tawhid na Shirk Maneno hayo ni ya Ibnu Taimiyyah, na mwenye kufuata nyayo zake, miongoni mwa Mawahabi, tunasema: “Hakika lile linalojulisha ruhusa ya kuswalia na kuomba dua kila mahala, linajulisha pia ruhusa ya kuswali na kuomba dua mbele ya kaburi la Mtume (s.a.w.w), makaburi ya Mitume wengine na watu wema pia. Na mtu yeyote mwenye maarifa kidogo juu ya Kitabu cha (Qur’an) na Sunna hawezi kutilia shaka ruhusa hiyo. Bali mjadala ni kuhusu je kufanya hayo katika makaburi yao ni bora zaidi au la. Kuhusiana na hilo tunasema: “Hakika kusimamisha swala katika makaburi hayo ni kwa ajili ya kutabaruku kwa wale waliozikwa humo na sehemu hizo, na wao ndio waliozozifanya ziwe tukufu. Na kwa hakika hapo sio kumswalia aliyopo kaburini, la hasha, bali ni kuswali kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kama vile kuswali misikitini ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu pia na mtu huchuma fadhila zaidi kutokana na kitendo cha kuisimamisha swala katika sehemu hiyo tukufu ambayo ni msikiti, na wala si kwa lengo la kuabudu msikiti. Waislamu huswali makaburini kutokana na utukufu alionao aliyezikwa mahala hapo kwa lengo la kupata baraka ya wale ambao wamejaaliwa na Mwenyezi Mungu kuwa wenye baraka, kama wanavyoswali sehemu ambayo lipo jiwe lililopata utukufu kwa ajili ya kukanyagwa na nyayo za Nabii Ibrahim (a.s.), Mwenyezi Mungu anasema:

“Na (kumbukeni) tulipoifanya nyumba kuwa ni marejeo ya watu na (mahala pa) amani na mpafanye mahala aliposimama Ibrahim pawe pa kuswali...” (2:125) Na hakuna sababu ya kufanya mahala pa Ibrahim kuwa ni sehemu ya kuswalia ila ni kwa sababu ya kupata baraka za Ibrahim (a.s.) aliyesimama hapo, na wao wanamuomba Mwenyezi Mungu makaburini kwa ajili ya utukufu wa aliyezikwa mahala hapo, basi dua yao katika sehemu hizo hujibiwa na kukubalika haraka, kama vile dua iombwayo msikitini au ndani ya 246


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 247

Tawhid na Shirk Ka’ba au katika moja ya sehemu au zama ambazo Mwenyezi Mungu amezitukuza. Na tija ya yote ni kwamba dalili tosha katika kuruhusiwa kuswalia sehemu hizo moja kwa moja ni hadithi ya Mtume (s.a.w.w) inayojulisha kwamba ardhi imefanywa msikiti na tohara kwa ajili ya Umma wa Muhammad. Kwa kutilia uzito ni kwamba kitendo cha kutabaruku kwa sehemu aliyozikwa Nabii au Walii mwenye cheo na daraja mbele ya Mwenyezi Mungu ni kama vile kutabaruku mahala pa Ibrahim (a.s.), Je! Mahala ambopo umelala mwili wa Nabii mtukufu sio mahala ambapo pamebarikiwa? Sio mahala ambapo ni Sunna kufanyia ibada ikiwepo kuswali? Na la kushangaza ni kwamba Ibnu Qaim ameeleza katika kitabu chake kiitwacho (Zaadul-Maad) yale yanayokwenda kinyume na itikadi yake, na itikadi ya mwalimu wake Ibnu Taimiyyah pale aliposema: “Hakika matokeo ya subira ya bi Hajir na mwanae juu ya ugeni na kukubali kuchinjwa mtoto, ni miongoni mwa mambo yaliyopelekea athari zao hao wawili na mahala palipokanyagwa na nyayo zao ziwe ni matendo miongoni mwa matendo ya ibada za waumini, na maeneo ya ibada ambayo hutekelezwa hadi siku ya Qiyama, na huu ndio utaratibu wa Mwenyezi Mungu kwa yule atakaye kumnyanyua na kumtukuza miongoni mwa viumbe wake.”126 Ikiwa athari za Ismail na za bi Hajir zitokanazo na yale yaliyowasibu miongoni mwa matatizo yamepelekea kustahiki na kufanywa ni sehemu takatifu za ibada na matendo ya kiibada, je, athari za Mtume (s.a.w.w) aliye bora kushinda wote, alisema:

“Hakuudhiwa Nabii yeyote kama nilivyoudhiwa mimi.” Hazifai kufanywa matendo ya kiibada? Je! Mahala alipozikwa yeye hapastahili kuabudiwa Mwenyezi Mungu! Na ikawa anayeabudiwa ni Mwenyezi Mungu? je! Kutabaruku kupitia sehemu hizo ni Shirki na Ukafiri? 126. Zaadul-Maad fi hadyi khayril-Ibaad chapa ya Babi Halabi Misri rejea ya Twaha Abdul-Rauf chapa ya mwaka 1390 H 1970 A.D. 247


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 248

Tawhid na Shirk Vipi isifae kufanyia ibada sehemu hizo ilihali Bi Aisha alikuwa akiishi katika chumba ambacho amezikwa humo bwana Mtume (s.a.w.w), aidha pembeni mwake alizikwa sahaba wake, naye Aisha aliendelea kuishi nyumbani humo na alikuwa akiswali nyumbani humo, je tendo lake hilo lilikuwa ni kumwabudu aliyopo ndani ya kaburi? 10. KUAPA KWA ASIYEKUWA MWENYEZI MUNGU Mawahabi wamezuia kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu na wakahesabu hiyo kuwa ni Shirki bila kipingamizi, vivyo hivyo wakasema kuhusu yale yote yanayonasibishwa na viapo vya Mwenyezi Mungu kwa kiumbe miongoni mwa waja wake. Na yafuatayo ni maelezo yanayohusu masuala yote mawili: I- KIAPO KWA ASIYEKUWA MWENYEZI MUNGU (S.W.T) Kabla hatujaeleza matini za hadithi zenye kujulisha ruhusa ya kufanya jambo hilo hapana budi suala hili tulipime katika Qur’an ili tuone je! Mwenyezi Mungu ameapa kwa viumbe wake au hapana? Hakika zikirejewa Aya tukufu zinaleta faida kwamba Mwenyezi Mungu ameapa kwa viumbe wake katika sehemu nyingi na hufikia Aya arubaini. Akaapa kwa malaika katika sura zifuatazo: Swafat, Mursalaat, Naziaat na Dhariyaat, na akaapa kwa Mtume (s.a.w.w), anasema: “Naapa kwa maisha yako, hakika wao walevi wanahangaika” (15:72.) Vile vile katika Surat Buruuj aya 3 anasema: “Na kwa shahidi na kwa anayeshuudiwa” na katika Surat Balad anasema: “Naapa kwa Mji huu” (90:1) Na akaapa kwa Qur’an katika Surat Yasiin aya 1 - 3 na katika Surat Dukhan aya 1 - 3, katika Surat Qaaf aya 1-3, katika Surat Zukhruf aya 41 na katika Surat Swaad aya 1. 248


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 249

Tawhid na Shirk Na akaapa kwa nafsi ya binadamu katika Surat Shams aya 7-10 na katika Surat Qiyama aya 2, na akaapa kwa kidau cha wino na kalamu katika Surat Qalam aya 1. Na akaapa kwa kitabu katika Surat Tuur aya 2 - 3 na akaapa kwa farasi katika Surat Aadiyat aya 2, na akaapa kwa Mzazi na mwanawe katika Surat Balad aya 3, na akaapa kwa Jua na Mwanga wake katika Surat Shams aya 1, na akaapa kwa Mbingu katika Surat Dhariyaat aya 7 na katika Surat Buruuj aya 1, katika Surat Twariq aya 11, na akaapa kwa Asubuhi katika Surat Mudathir aya 34, katika Surat Takwiir aya 18 na katika Surat Fajr aya 1, na kisha akaapa kwa wakati wa mchana Adhuhuri na Alasiri na wakati wa kuzama jua, Usiku, Nyota, Ardhi, Mwezi, Upepo, Mawingu, Bahari, Meli, Tiin, Zaytun, Shufaa, Witri na vingine vilivyopo ulimwenguni. Hivyo hivyo unabainika uhakika wa hilo katika aya zingine za Qur’an zilizopo katika sura mbalimbali iwapo zitarejewa, kwani tumeacha kuzitaja zote kuchelea kurefuka mada hii na inatosha mifano tuliyoitaja. Je! Inawezekana kuapa kwa asiyekuwa Mola kukawa ni Shirki na ni jambo baya na kisha hilo litendwe na Mwenyezi Mungu!? Je! Inawezekana kupatikana kitendo hicho wingi huu katika Kitabu kitukufu na bado kiwe ni haramu kwa mwingine? Bila Mwenyezi Mungu kutaja uharamu wa hilo katika kitabu chake kitukufu? Je! ni sahihi kwetu kusema: Hakika kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu ni Shirki iwapo kiapo hicho ni kutoka kwa kiumbe na sio Shirki ikiwa ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu muumba? Huo ni mkanganyiko wa maneno, kwa sababu tendo ni moja lenye asili moja na dhati moja, na kwamba dhati moja haitoi hali mbili na zenye kusigana. Kwa ujumla ikiwa Qur’an ni kigezo chema, na kila lililokuja humo miongoni mwa kauli au kitendo ni dira ya Waislamu wote, na vipi iwezekane kufikiri viapo hivi vitoke kwa Mwenyezi Mungu na ifae kwake na isifae 249


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 250

Tawhid na Shirk kwa asiyekuwa Yeye? Iwe kwa upande mmoja ni Tawhiid halisi na ni Shirki kwa upande mwingine, ilhali kitendo ni kimoja na asili yake ni moja, hilo ni kuhusu Kitabu kitukufu. Ama kuhusu Sunna tukufu ya Mtume (s.a.w.w). Amepokea Muslim katika kitabu chake Sahih amesema: Mtu mmoja alikwenda kwa Mtume (s.a.w.w) akasema: “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni sadaka gani ambayo ina ujira mkubwa mno?” Akasema: “Naapa kwa mama na baba yako, utoe sadaka na hali ya kuwa wewe una haja nayo na unahofia ufakiri.”127 Na hakika Mtume (s.a.w.w) ameapa kwa mama na baba wa muulizaji kwa kusema “Naapa kwa baba yako.” Na vilevile imepokewa kwamba siku moja mtu mmoja miongoni mwa watu wa Najdi alikwenda kwa Mtume (s.a.w.w) akamuuliza kuhusu Uislamu, Mtume (s.a.w.w) akasema: “Kuswali swala tano mchana na usiku.” Akauliza: Je! Nalazimika jambo lingine lisilokuwa hilo? Akasema: “Hapana, isipokuwa ukipenda kuswali Sunna, kisha kufunga mwezi wa Ramadhani.” Akauliza: Je! Nawajibika kwa lingine? Akasema: “Hapana, ila kufunga sunna.” Hapo yule mtu akakengeuka (akampa kisogo) huku akisema: Naapa kwa Mwenyezi Mungu sizidishi katika hayo wala sipunguzi chochote, Mtume (s.a.w.w) akasema: “Amefaulu yeye pamoja na baba yake ikiwa amesema ukweli, au ataingia peponi na baba yake iwapo atakuwa amesadiki (amesema kweli)” 128 127. Sahih Muslim Juz. 3 Uk. 94. 128. Sahih Muslim Juz. 1 Uk. 31-32 mlango ni nini Uislam na ubainfu wa mambo yake. 250


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 251

Tawhid na Shirk Na katika hadithi nyingine kwa sanadi (mlolongo wa wapokezi) ya Ahmad bin Hanbali hakika Mtume (s.a.w.w) amesema: “Naapa kwa umri wangu hakika kuzungumza katika kuamrisha mema na kukataza mabaya ni bora kuliko kunyamaza.”129 Na hakika wametoa fat’wa baadhi ya viongozi wa Madhehebu manne kuwa hilo linajuzu, pia imekuja katika kitabu (Fiqh Ala MadhahabilArbaat) kama ifuatavyo: Mahanafi wamesema: Kuapa kwa mfano: kwa baba yako na umri wako, na mfano wa hayo inajuzu lakini ni makuruhu. Mashafii wamesema: “Ni makuruhu kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu, ikiwa hakitakusudiwa chochote kati ya yale yaliyotajwa juu ya Sahifa” (yaani kamshirikisha Mwenyezi Mungu …) Maliki amesema: Kuapa kwa vitu ambavyo vimeadhimishwa kisheria kama vile Mtume, Ka’ba na yanayofanana na hayo zipo kauli mbili; ni haramu na makuruhu, na kauli iliyo mashuhuri ni haramu. Mahambali wamesema: “Ni haramu kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) kwa sifa Zake, na hata kwa Nabii au Walii.”130 Vyovyote itakavyokadiriwa, ni sawa kuruhusu kiapo kwa asiyekuwa Mola Manani au hapana? haisababishi kuwa ni Shirki, wala muapaji (mtoaji kiapo) si mshirikina, kwani kuapa kwa kitu haijulishi kwamba mtoaji kiapo anaitakidi kuwa kitu hicho ni Mungu na Rabbi Mlezi, na linalojulikana ni utukuzaji na uadhimishaji, na mtoaji fatwa anajua kwamba suala hilo lina ikhitalfu ndani yake, sasa je! inafaa kumtuhumu Mwislamu na kumhusisha na ushirikina kwa tendo ambalo fatwa zimegongana kuhusiana na hilo? 129. Musnad Ahmad bin Hambali Juz. 5 Uk. 225, Musnad Ahmad Juz. 5 Uk. 212 na Sunan Ibn Maja Juz. 4 Uk. 995 na Juz. 1 Uk. 225. 130. Fiqhu ala Madhahib Arbaat Juz. 2 Uk. 75. 251


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 252

Tawhid na Shirk Ndiyo, hakuna shaka kiapo kinachomuhusu asiyekuwa Mwenyezi Mungu hakitimii, na katika mahkama ya kiislamu hawakikubali isipokuwa kile kinachofungamana na Mola Manani (s.w.t), na hilo halijulishi kuwa kiapo kinachotolewa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) ni Shirki au haramu.

II. VIAPO KWA KIUMBE AU KWA HAKI YAKE Hakika Mawahabi wamezuia viapo vinavyotolewa kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) kupitia kiumbe miongoni mwa viumbe wake, kwa mfano iwapo muombaji atasema: Naapa juu ya fulani, au kwa haki ya fulani au nakuomba wewe kwa ajili ya fulani au kwa haki yake, nayo katika nadharia yao ni miongoni mwa aina za tawassuli. Kwa hivyo njoo uwe nami tulitathmini katazo hili je! linaafikiana na mwenendo na taratibu za matendo ya Waislamu au hapana? na kabla ya yote tunasema: Hakika viapo kwa asiyekuwa Mola muumba havihesabiwi kuwa ni Shirki kwa mwenye kuapa, hiyo ni kutokana na yale uliyoyajua kuhusu kigezo na kipimo na kitenganishi cha Shirki na Tawhiid. Bali mjadala ni kuhusu je kiapo hicho kinaruhusiwa kisheria au hakiruhusiwi. Tunasema: Hapana shaka kwamba hakika Mwenyezi Mungu (s.w.t) amewasifu watu kadhaa anasema: “Wafanyao subira na wasemao kweli, na watii, na watu watoao (sadaka) na waombao msamaha (nyakati za) karibu ya alfajiri” (3:17) Lau mtu atasema katika dua na maombi yake: “Ewe Mola wangu, hakika nakuomba kwa haki ya wenye kukuomba msamaha usiku wa manane nisamehe dhambi zangu.” Je! atakuwa amefanya Shirki? Na kwa nini tendo lake hilo liwe ni Shirki? Na hapo kabla umeshajua kigezo cha Shirki kwamba inathibiti iwapo muombaji ataitakidi Uungu na Urabbi kwa muombwa, je! katika mfano 252


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 253

Tawhid na Shirk huu tuliotoa mzungumzaji anaitikadi kinyume na yale aliyoeleza Mwenyezi Mungu? Je! Mwenyezi Mungu (s.w.t) hakuwasifu na kuwaeleza pale anaposema: “Wenye kuomba msamaha usiku wa manane”? Hakika Shirki na Tawhiid hazijaachwa chini ya matamanio yetu kwamba tuseme tutakavyo huyu ni mshirikina na yule ni mwanatawhiid, na bila shaka Qur’an tukufu imefahamisha mzani halisi wa Shirki na Tawhiid katika sehemu mbalimbali, na mshirikina ni yule aliyeelezwa na Mwenyezi Mungu (s.w.t) kuwa: “Na anapotajwa Mwenyezi Mungu peke yake nyoyo za wale wasioamini akhera huchukia, na wanapotajwa wale walio kinyume naye, mara wanafurahi.” (39:45) Vilevile mshirikina anaelezwa na Qur’an, inasema: “Hakika wao walikuwa wakiambiwa hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu tu hufanya kiburi na husema haiwezekani tuache miungu yetu ili tumfuate mshairi mwendawazimu”131 je! inafaa kwetu kuwazingatia wale wenye kuapa kupitia viumbe wema na bora wa Mwenyezi Mungu kuwa ni washirikina? na kuwafanya ni miongoni mwa wale waovu walioelezwa na Aya lukuki za Qur’an? Na baada ya kubainika kwamba viapo kwa asiyekuwa Mola manani sio Shirki kwa mujibu wa Qur’an tukufu, sasa tuweke bayana suala hili kulingana na hadithi tukufu. Hakika imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kwamba alimfundisha kipofu aseme:

“Ewe Mola wangu kwa baraka ya Mtume wako Muhammad Nabii mwenye rehema nakuomba jambo kadhaa.”132 131. Sura 37 aya 35-36. 132. Sunan Ibn Maja Juz. 1 Uk. 441 na Musnad Ahmad Juz. 4 Uk. 138 na vinginevyo. 253


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 254

Tawhid na Shirk Vilevile amepokea Abu Khudri kutoka kwa Bwana Mtume (s.a.w.w) alikuwa akisema:

“Ewe Mola Wangu mimi nakuomba kwa haki ya wenye kukuomba, aidha nakuomba kwa haki ya umpendaye.”133 Kinachobakia hapa ni sisi kujua kwamba wao wanapinga jambo hili kwa kudai kwamba yeyote yule hana haki kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t), wanasema: Hakika suala hili la kuomba kwa haki ya kiumbe haliruhusiwi kisheria kwa sababu kiumbe hana haki kwa Mola Muumba. Na jawabu ni kwamba hilo ni sahihi, isipokuwa pale tu Muumba atakapompa kiumbe haki juu Yake, na hilo Mwenyezi Mungu amelifanya pale anaposema:

“Na kwa hakika tuliwatuma Mitume kwa watu wao na wakawafikia kwa miujiza wazi wazi kisha tukawaadhibu wale waliokosa, na ilikuwa haki juu yetu kuwasaidia Waumini.” (30:47) Na anasema:

“Hakika ni ahadi iliyo haki kuwanusuru waumini katika taurati na injili…” (9:111) 133. Sunan Ibn Majaa juz. 1 Uk. 261 na 262 na Musnad Ahmad Juz. 3 hadithi ya 21. 254


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 255

Tawhid na Shirk Na anasema:

“Vivyo hivyo ni haki yetu kuwaokoa waumini …” (10:103) Anasema:

“Hakika toba inayopokelewa (yenye haki ya kupokelewa) na Mwenyezi Mungu ni ya wale tu wanaofanya uovu kwa ujinga kisha wakatubia kwa haraka, basi hao ndio Mwenyezi Mungu huipokea toba yao, Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mwenye hekima” (4:17) Aidha imekuja katika hadithi kama ifuatavyo: Mtume (s.a.w.w.) amesema:

“Ni haki juu ya Mwenyezi Mungu kumsaidia ambaye ameoa kwa kutaka kujizuia na yale yaliyoharamishwa na Mwenyezi Mungu.”134 Mtume (s.a.w.w.) amesema:

“Mambo matatu ni haki ya Mwenyezi Mungu kumsaidia mpiganaji katika njia ya Mwenyezi Mungu …”135 Mtume (s.a.w.w) amesema: 134. Jamiu Swaghiir Juz. 2 Uk. 33 cha Suyutwi. 135. Sunan Ibn Maja Juz. 2 Uk. 841. 255


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 256

Tawhid na Shirk

“Je! Unajua haki ya waja kwa Mwenyezi Mungu…”136 Kutokana na mada hiyo imebainika kwamba kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) si Shirki, bali haitoki nje ya wigo wa utukuzaji, na hasa ukizingatia kwamba kumtukuza aliyetukuzwa na Mwenyezi Mungu (s.w.t) si Shirki, na hadithi nyingi hujulisha kinyume na hivyo, bali huruhusu na hujuzisha hilo, hakika hakuna baada ya haki isipokuwa ni upotovu. Huu ndio mwisho wa yale tuliotaka kuyaeleza katika risala hii yanayohusiana na suala la Tawhiid na Shirki katika Qur’an tukufu, hali ya kutaraji kuwa Mwenyezi Mungu atawanufaisha Waislamu kupitia risala hii, na kwamba iwe ndio hatua ya umoja wao na mshikamano baina ya makundi ya kiislamu. Na tunahitimisha maelezo yetu kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu Mola Muumba wa walimwengu.

136. Sunan Ibn Maja Juz. 2 Uk. 841. 256


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 257

Tawhid na Shirk

ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION 1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9. 10. 11. 12. 13. 14. 15. 16. 17. 18. 19. 20. 21. 22. 23. 24. 25. 26.

Qur'an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Thalathini Uharamisho wa Riba Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili Hekaya za Bahlul Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.) Hijab vazi Bora Ukweli wa Shia Ithnaashari Madhambi Makuu Mbingu imenikirimu Abdallah Ibn Saba Khadijatul Kubra Utumwa Umakini katika Swala Misingi ya Maarifa Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia Bilal wa Afrika Abudharr Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu Salman Farsi Ammar Yasir Qur'an na Hadithi Elimu ya Nafsi Yajue Madhehebu ya Shia Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur'an Tukufu 257


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 258

Tawhid na Shirk 27. 28. 29. 30. 31. 32. 33. 34. 35. 36. 37. 38. 39 40. 41. 42. 43. 44. 45. 46. 47. 48. 49. 50. 51. 52. 53. 54. 55. 56. 57.

Al-Wahda Ponyo kutoka katika Qur'an Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii Mashukio ya Akhera Al Amali Dua Indal Ahlul Bayt Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna. Haki za wanawake katika Uislamu Mwenyezi Mungu na sifa zake Kumswalia Mtume (s) Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) Adhana Upendo katika Ukristo na Uislamu Tiba ya Maradhi ya Kimaadili Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu Kupaka juu ya khofu Kukusanya swala mbili Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Kusujudu juu ya udongo Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s) Tarawehe Malumbano baina ya Sunni na Shia Kupunguza Swala safarini Kufungua safarini Umaasumu wa Manabii Qur’an inatoa changamoto as-Salaatu Khayrun Mina -'n Nawm Uadilifu wa Masahaba Dua e Kumayl Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu 258


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 259

Tawhid na Shirk 58. 59. 60. 61. 62. 63. 64. 65. 66. 67. 68. 69. 70. 71. 72. 73. 74. 75. 76. 77. 78. 79. 80. 81. 82. 83. 84. 85. 86. 87.

Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mtume Muhammad (s) Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili Kuzuru Makaburi Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita Tujifunze Misingi Ya Dini Sala ni Nguzo ya Dini Mikesha Ya Peshawar Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu Ubora wa Imam 'Ali Juu ya Maswahaba Na Ushia ndio njia iliy onyooka Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake Liqaa-u-llaah Muhammad (s) Mtume wa Allah Amani na Jihadi Katika Uislamu Uislamu Ulienea Vipi? Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) Urejeo (al-Raja’a ) Mazingira Utokezo (al - Badau) Hukumu ya kujenga juu ya makaburi Swala ya maiti na kumlilia maiti Uislamu na Uwingi wa Dini 259


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 260

Tawhid na Shirk 88. 89. 90. 91. 92. 93. 94. 95. 96. 97. 98. 99. 100. 101. 102 103. 104. 105. 106. 107. 108. 109. 110. 111. 112. 113. 114. 115. 116. 117. 118.

Mtoto mwema Adabu za Sokoni Johari za hekima kwa vijana Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu Tawasali Imam Mahdi katika Usunni na Ushia Hukumu za Mgonjwa Sadaka yenye kuendelea Msahafu wa Imam Ali Ngano ya kwamba Qur’ani imebadilishwa Idil Ghadiri Kusoma sura zenye Sijda ya wajibu Hukumu zinazomuhusu mkuu wa kazi na Mfanyakazi Huduma ya Afya katika Uislamu Sunan an-Nabii Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza) Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili) Shahiid Mfiadini Kumsalia Nabii (s.a.w) Ujumbe -Sehemu ya Kwanza Ujumbe - Sehemu ya Pili Ujumbe - Sehemu ya Tatu Ujumbe - Sehemu ya Nne Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu Hadithi ya Thaqalain Ndoa ya Mutaa Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza Ukweli uliopotea sehemu ya Pili Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu 260


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 261

Tawhid na Shirk 119. 120. 121. 122. 123. 124. 125. 126. 127. 128. 129. 130. 131. 132. 133. 134. 135. 136. 137. 138. 139. 140. 141. 142. 143. 144. 145. 146. 147.

Ukweli uliopotea sehemu ya Nne Ukweli uliopotea sehemu ya Tano Mkutano wa Maulamaa wa Baghdad Safari ya kuifuata Nuru Fatima al-Zahra Myahudi wa Kimataifa Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi Visa vya kweli sehemu ya Kwanza Visa vya kweli sehemu ya Pili Elimu ya Ghaibu ya Maimamu Mwanadamu na Mustakabali wake Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Kwanza) Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Pili) Khairul Bariyyah Uislamu na mafunzo ya kimalezi Vijana ni Hazina ya Uislamu Yafaayo kijamii Tabaruku Taqiyya Vikao vya furaha Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje? Visa vya wachamungu Falsafa ya Dini Azadari-Kuhuzunika na Kuomboleza Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah Mtazamo Mpya - Wanawake katika Uislamu Kuonekana kwa Allah Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza) Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili) 261


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 262

Tawhid na Shirk 148. 149. 150. 151. 152. 153 154. 155. 156. 157. 158. 159. 160. 161. 162. 163. 164. 165. 166. 167. 168. 169. 170. 171. 172. 173. 174. 175. 176. 177. 178.

Ndugu na Jirani Ushia ndani ya Usunni Maswali na Majibu Mafunzo ya hukmu za ibada Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 1 Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 2 Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 3 Abu Huraira Vipengee kadhaa katika Swala ya Jamaa na Msikiti. Mazingatio kutoka katika Qur’an - Sehemu ya Kwanza Mazingatio kutoka kaitka Qur’an - Sehemu ya Pili Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya kwanza Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya Pili Qur’ani Tukufu – Pamoja na Tarjuma ya Kiswahili Falsafa ya Mageuzi ya Imam Husein (a.s) Amali za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani Elimu ya Tiba za Kiislamu - Matibabu ya Maimamu Uislamu Safi Majlisi za Imam Husein Majumbani Je, Kufunga Mikono Uislam wa Shia Amali za Makka Amali za Madina Asili ya Madhehebu katika Uislamu Sira ya Imam Ali kuhusu Waasi Ukweli uliofichika katika neno la Allah Uislamu na Mifumo ya Uchumi Umoja wa Kiislamu na Furaha Mas’ala ya Kifiqhi Jifunze kusoma Qur’ani As-Sahifatul Kamilah as-Sajjadiyyah 262


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 263

Tawhid na Shirk 179. 180. 181. 182. 183. 184. 185. 186. 187. 188. 189. 190. 191. 192. 193. 194. 195. 196. 197. 198. 199. 200. 201. 202. 203. 204. 205. 206. 207. 208.

Hayya ‘Alaa Khayri’l-’Amal Katika Adhana Ukweli kuhusu Funga ya Siku ya Ashura Dua za Miezi Mitatu Mitukufu (Rajabu, Shaabani na Ramadhani) Uadilifu katika Uislamu Mahdi katika Sunna Maswali Ya Uchunguzi Kuhusu Uislam Kazi na Bidii ni njia ya maendeleo Abu Talib – Jabali Imara la Imani Ujenzi na Utakaso wa Nafsi Vijana na Matarajio ya Baadaye Usalafi – Historia yake, maana yake na lengo lake Ushia – Hoja na Majibu Mateso ya Dhuria wa Mtume (saww) Maombolezo – Msiba wa Bwana wa Mashahidi (a.s.) Shahidi kwa Ajili ya Ubinadamu Takwa Mwonekano wa Upotoshaji katika Hazina ya Kiislamu Amirul Muuminina (‘as) na Makhalifa Uongozi na Utawala katika Mwenendo wa Imam ‘Ali (‘a) Kuvunja hoja iliyotumika kutetea Uimamu wa AbuBakr Adabu za vikao na mazungumzo Hija ya Kuaga Uwazi baina ya Maslahi na Vikwazo Fadhila za watukufu watano katika Sahih Sita Mdahalo baina ya Mwanachuoni wa Kisunni na Mwanachuoni wa Kishia (Al- Muraja’aat) Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (as) Upotoshaji dhahiri katika Turathi (Hazina) ya Kiislamu Mtazamo kuhusu msuguano wa Kimadhehebu Nchi na Uraia – Haki na wajibu kwa Taifa Mtazamo wa Ibn Taymiyyah juu ya Imam Ali (as) 263


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 264

Tawhid na Shirk 209. 210. 211. 212. 213. 214. 215. 216. 217. 218. 219. 220. 221. 222. 223. 224.

Uongozi wa Kidini – Maelekezo na Utekelezaji wa Kijamii Maadili ya Ashura Mshumaa – Shahidi na Kifo cha Kishahidi Mizani ya Hekima – Hadithi za Ahlul Bait (as) (Sehemu ya Kwanza) Imam Ali na Mambo ya Umma Imam Ali na Mfumo wa Usawa Kuvunja Hoja Iliyotumika Kutetea Uimamu wa Abu Bakr Mfumo wa Wilaya Vipi Tutaishinda Hofu? Kumswalia Mtume ni Ufunguo wa Utatuzi wa Matatizo Maeneo ya Umma na Mali Zake Nahjul-Balagha – Majmua ya Khutba, Amri, Barua, Risala, Mawaidha na Semi za Amirul-Muuminin Ali bin Abu Talib (a.s.) Mukhtar – Shujaa aliyelipiza kisasi dhidi ya wauaji wa Imam Husein (as) hapo Karbala Uimamu na Tamko la Kutawazwa Imam Husain ni Mfumo wa Marekebisho na Mageuzi Mjadala wa Kiitikadi KOPI NNE ZIFUATAZO ZIMETAFSIRIWA KWA LUGHA KINYARWANDA

1. 2. 3. 4.

Amateka Na Aba'Khalifa Nyuma yaho naje kuyoboka Amavu n’amavuko by’ubushiya Shiya na Hadithi ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION KWA LUGHA YA KIFARANSA

1.

Livre Islamique 264


Tawhid na shirik FINAL 22.01.2014:Tawhid na shirik FINAL1.qxd 1/23/2014 3:25 PM Page 265

Tawhid na Shirk

BACK COVER Kitabu hiki kinajadili kwa mapana na marefu suala la umoja wa Waislamu na kuwakosoa wale wanaojaribu kuleta mfarakano na fitna katika dini kwa kutumia madhehebu, hususan wale wanaowashambulia Mashia katika vitabu vyao kwamba wao (Mashia) ni makafiri. Mwandishi katika kitabu hiki anaelezea imani ya Shia katika Tawhid na jinsi wanavyojiepusha na shirk nukta ambazo wapinzani wa Shia wanazitumia kuupotosha ukweli juu ya Ushia. Wapinzani hawa hawajishughulishi kusoma vitabu vya Shia wala kusoma majibu yanayotolewa juu ya vitabu vyao, bali kazi yao ni kurudiarudia tu yale yaliyotapikwa na watangulizi wao na kupotosha Umma kwa kalamu zao zenye sumu. Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote, ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni mambo ambayo hayana nafasi tena katika akili za watu. Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 / 2127555 Barua Pepe: alitrah@yahoo.com Tovuti: www.ibn-tv.com Katika mtandao: www.alitrah.info

265


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.