Tiba ya maasumina

Page 1

TIBA YA MAASUMINA Bwana Mtume (saww) na Ahlul Bait Wake (as)

Kimeandikwa na: Dkt. Labib Baydhun

Kimetarjumiwa na: Ustadh Amir Mussa

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 1

8/10/2017 1:21:55 PM


‫طب املعصومين‬

‫الرسول وأهل بيته (ع)‬

‫تأليف‬

‫الدكتور لبيب بيضون‬

‫من اللغة العربية إلى اللغة السواحلية‬

‫‪8/10/2017 1:21:55 PM‬‬

‫‪04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 2‬‬


©Haki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: 978 - 9987 – 17 – 010 – 4 Kimeandikwa na: Dkt. Labibu Baydhun Kimetarjumiwa na: Ustadh Amiri Mussa Kea Kimehaririwa na: Al Haji Hemedi Lubumba Selemani Kimepitiwa na: Al Haji Mujahid Rashid Kimepangwa katika Kompyuta na: Al-Itrah Foundation Toleo la kwanza: Novemba, 2017 Nakala: 1000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. - 19701, Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 / 2127555 Barua Pepe: alitrah@yahoo.com Tovuti: www.alitrah.info

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 3

8/10/2017 1:21:55 PM


YALIYOMO Dibaji................................................................................................ 1 Neno la Mchapishaji........................................................................ 2 Utangulizi......................................................................................... 4 Sababu za Kusigana kwa Hadithi.................................................... 8 Kutoka katika Wahyi wa Qur’ani tukufu....................................... 14 Tiba katika Uislamu....................................................................... 23 Vipimo vya Tiba za Kale................................................................ 24 Furungu.......................................................................................... 25 Wanja wa Antimoni........................................................................ 27 Peasi............................................................................................... 28 Sikio............................................................................................... 30 Mchele............................................................................................ 31 Mkate wa mchele........................................................................... 32 Kuhara............................................................................................ 33 Ulaji wa Wastani............................................................................ 34 Adabu za kula................................................................................ 39 Kusema Bismillah kabla ya kula.................................................... 41 Kula punje zilizodondoka chini..................................................... 42 Kula chakula kichache................................................................... 44 Kula sana na kuvimbiwa................................................................ 45 Ufuatanishaji wa Chakula juu ya Chakula..................................... 48 Bilinganya...................................................................................... 50 Nguvu za Kiume na Harufu Mbaya ya Kinywa............................. 52 Maradhi ya Uvimbe wa Utando wa Mapafu (Pleurisy)................. 53 Ukoma............................................................................................ 54

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 4

8/10/2017 1:21:55 PM


Baraka............................................................................................ 55 Tende Mbichi................................................................................. 57 Ngozi.............................................................................................. 57 Macho............................................................................................ 58 Kitunguu maji................................................................................ 60 Maumivu ya Tumbo na Ugonjwa wa Tumbo................................ 63 Tikitimaji........................................................................................ 65 Mboga ya Bibi Fatima................................................................... 68 Mbogamboga................................................................................. 70 Kulia............................................................................................... 72 Kikohozi......................................................................................... 72 Kubaleghe...................................................................................... 76 Balungi........................................................................................... 76 Bahaqu........................................................................................... 79 Bawasiri......................................................................................... 80 Haja ndogo..................................................................................... 83 Mayai............................................................................................. 85 Kusaidiana kwa mada na athari zake............................................. 87 Kusigana kwa viasili vya Vyakula................................................. 88 Kupiga miayo................................................................................. 89 Uchokoaji wa Meno....................................................................... 89 Tufaha............................................................................................ 91 Tende.............................................................................................. 94 Tini............................................................................................... 101 Kitungu Saumu............................................................................ 103 Jibini............................................................................................. 105 Ukoma.......................................................................................... 107 Karoti........................................................................................... 109 v

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 5

8/10/2017 1:21:56 PM


Ngozi............................................................................................ 110 Kujamiana.................................................................................... 110 Janaba........................................................................................... 119 Uwendawazimu............................................................................ 120 Jozi............................................................................................... 120 Njaa na Shibe............................................................................... 121 Habasoda...................................................................................... 122 Ndumiko / Kuumika.................................................................... 126 Joto na baridi................................................................................ 129 Harmala........................................................................................ 131 Kwikwi......................................................................................... 133 Vijiwe katika kende...................................................................... 134 Hifidhi na Ukumbukaji................................................................ 135 Uingizaji wa bomba Sehemu ya Haja Kubwa............................. 140 Uwatu........................................................................................... 140 Unyoaji wa nywele...................................................................... 141 Haluwa......................................................................................... 143 Homa............................................................................................ 143 Humswi Chickpea........................................................................ 148 Bafu.............................................................................................. 149 Mlo kamili.................................................................................... 149 Hina.............................................................................................. 151 Handhala / Aina ya Tango............................................................ 153 Uhai na maisha marefu................................................................ 154 Hedhi na Kumwingilia Mwanamke............................................. 155 Mkate........................................................................................... 156 Jando............................................................................................ 158 Saladi............................................................................................ 159 vi

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 6

8/10/2017 1:21:56 PM


Upakaji wa hina........................................................................... 160 Siki............................................................................................... 162 Siki ya tufaha............................................................................... 164 Tabia............................................................................................. 165 Pombe na vilevi............................................................................ 166 Nguruwe na nyama yake.............................................................. 170 Khulunjani.................................................................................... 170 Khayriyyu na mafuta yake........................................................... 171 Ugonjwa na dawa......................................................................... 172 Dawa Mujumuiko........................................................................ 183 Kwale........................................................................................... 185 Damu............................................................................................ 186. Ubongo ........................................................................................ 186 Mafuta ya Mimea na Upakaji wa mafuta..................................... 187 Wadudu........................................................................................ 188 Jogoo............................................................................................ 189 Inzi............................................................................................... 190 Kiungo cha Uzazi cha Mwanaume.............................................. 190 Kichwa......................................................................................... 190 Raha............................................................................................. 191 Pumu............................................................................................ 191 Unyonyeshaji............................................................................... 191 Utokaji wa Damu Puani............................................................... 193 Komamanga................................................................................. 193 Ugonjwa wa macho...................................................................... 198 Roho............................................................................................. 199 Upepo wa Tumboni na Riyahi..................................................... 200 Harufu Nzuri................................................................................ 203 vii

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 7

8/10/2017 1:21:56 PM


Ua Zuri la Jabalini........................................................................ 204 Mtindi........................................................................................... 207 Zabibu.......................................................................................... 208 Zahiir (Kite)................................................................................. 209 Za’tar (Su’tar).............................................................................. 210 Mafua........................................................................................... 211 Zinaa............................................................................................ 213 Zanbaq.......................................................................................... 215 Ndoa............................................................................................. 218 Mafuta ya Kula (na Zaytuni)........................................................ 218 Mkunazi....................................................................................... 221 Sadhabu........................................................................................ 222 Kikohozi....................................................................................... 223 Su’d.............................................................................................. 224 Su’twi (Nushuuqu)....................................................................... 226 Pera.............................................................................................. 227 Sukari ya mawe............................................................................ 231 Mua.............................................................................................. 233 Mchadi......................................................................................... 233 Sumu............................................................................................ 235 Ulezi ............................................................................................ 235 Usikivu......................................................................................... 236 Samaki.......................................................................................... 236 Samli............................................................................................ 238 Jino na meno................................................................................ 238 Sanamaki ya Makka..................................................................... 240 Usafishaji Meno kwa Mswaki...................................................... 242 Sawiiq.......................................................................................... 245 viii

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 8

8/10/2017 1:21:56 PM


Nywele......................................................................................... 248 Mkate wa shairi............................................................................ 249 Maji ya shairi............................................................................... 251 Kipandauso.................................................................................. 251 Sharmari (Mbegu za Raaziyanji)................................................. 252 Nuru ya jua................................................................................... 253 Hamu na Kutamani...................................................................... 254 Mvi............................................................................................... 255 Sabiru........................................................................................... 256 Afya ya mwili.............................................................................. 257 Maumivu ya kichwa..................................................................... 261 Kifua............................................................................................ 264 Su’tur............................................................................................ 265 Funga........................................................................................... 266 Elimu ya tiba................................................................................ 267 Wosia wa Matibabu...................................................................... 269 Mtabibu wa kiarabu Harith bin Kaladat Thaqafi......................... 270 Mazungumzo Thabiti juu ya Tiba................................................ 271 Maumbile manne......................................................................... 274 Maunbile ya Mwili....................................................................... 274 Elimu ya Maamuni na wingi wa Maarifa yake............................ 277 Chakula........................................................................................ 280 Manukato..................................................................................... 282 Udongo......................................................................................... 283 Kucha........................................................................................... 285 Adesi............................................................................................ 287 Maambukizo................................................................................ 289 Jasho............................................................................................. 290 ix

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 9

8/10/2017 1:21:56 PM


Asali............................................................................................. 291 Mishipa........................................................................................ 298 Uboho (Urojo wa Mfupa)............................................................ 299 Kujistahi (Mwanamke kujizuia na Zinaa).................................... 300 Akili............................................................................................. 301 Uvaaji wa pete ya Akiki............................................................... 303 Akika............................................................................................ 306 Zabibu.......................................................................................... 307 Jicho............................................................................................ .309 Ghubayraa.................................................................................... 313 Kuoga........................................................................................... 314 Tunda........................................................................................... 316 Kiharusi........................................................................................ 318 Figili............................................................................................. 319 Kinywa......................................................................................... 320 Maharage...................................................................................... 320 Quthau na Tango.......................................................................... 322 Kujitibu kwa Qur’ani................................................................... 323 Mung’unya................................................................................... 325 Karafuu........................................................................................ 326 Qust.............................................................................................. 328 Moyo............................................................................................ 329 Ngano........................................................................................... 332 Misokoto ya Tumbo..................................................................... 333 Utapikaji....................................................................................... 334 Ini ................................................................................................ 335 Wanja na upakaji wa Wanja......................................................... 335 Liki............................................................................................... 337 x

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 10

8/10/2017 1:21:56 PM


Figili............................................................................................. 339 Kazbara........................................................................................ 340 Figo.............................................................................................. 341 Kamaa.......................................................................................... 342 Kisibiti......................................................................................... 343 Peasi, Ubani Kundur na Tiba ya Uchomaji.................................. 345 Ubani (Bukhuri) na Kunduru....................................................... 346 Maziwa......................................................................................... 352 Ufizi............................................................................................. 356 Nyama.......................................................................................... 356 Kung’atwa na Nge....................................................................... 365 Tanipu.......................................................................................... 366 Maji (na unywaji)......................................................................... 367 Maji ya mwanaume...................................................................... 375 Choroko (Mashi).......................................................................... 377 Kibofu cha mkojo........................................................................ 377 Sababu ambayo imefanya yameharamishwa Bandamaa, Tupu mbili na Uti wa Mgongo..................................................... 380 Mihadarati.................................................................................... 381 Nyongo nyeusi............................................................................. 382 Supu............................................................................................. 384 Chanuo na Kuchana..................................................................... 384 Utumbo........................................................................................ 385 Chumvi......................................................................................... 388 Mzoga.......................................................................................... 391 Nasisa........................................................................................... 391 Wanawake (Mwanamke).............................................................. 392 Usafi............................................................................................. 394 Nafsi............................................................................................. 395 xi

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 11

8/10/2017 1:21:56 PM


Jongo............................................................................................ 396 Sisimizi........................................................................................ 397 Usingizi........................................................................................ 399 Uzee............................................................................................. 401 Haluwa......................................................................................... 402 Mmeng’enyo wa chakula............................................................. 403 Badamu........................................................................................ 404 Hindubaau.................................................................................... 405 Waridi na (Maji Waridi)............................................................... 409 Mtoto............................................................................................ 410

xii

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 12

8/10/2017 1:21:56 PM


TIBA YA MAASUMINA

‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬

DIBAJI

K

itabu hiki ni toleo la Kiswahili la taasisi ya Al Itrah Foundation. Chapisho lake limelenga kukidhi mahitaji ya kiroho ya zama hizi pamoja na Ubongo na fikra zinazokuwa za Muislam. Jitihada kubwa zimefanywa na Taasisi kuweka chapisho hili la Kiswahili katika msingi wa haki na wenye kukubalika katika Uislam. Unaombwa kwa Taadhima ukisome kitabu hiki katika malengo yaliyokusudiwa. Pia Unaombwa kuwasilisha kwetu maoni yako huru juu ya chapisho letu hili, jambo ambalo tutashukuru sana. Kutangaza ujumbe wa Uislam ni kazi ambayo inahitaji ushirikiano wetu sote. Taasisi inakuomba kuungana na kushirikiana kama ilivyoagizwa katika aya ya Qur’an: (Surat Saba’ 34:46). Na rehma za Allah ziwe juu yako. Wako katika Uislam Al Itrah Foundation Barua Pepe: alitrah@yahoo.com SMS: +255 778 300 140

1

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 1

8/10/2017 1:21:56 PM


TIBA YA MAASUMINA

‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬

NENO LA MCHAPISHAJI

K

itabu ulichonacho mikononi mwako kimetarjumiwa kutoka kitabu cha Kiarabu kwa jina la, Tibbu ‘l-Ma’sumin: al-Rasul wa Ahlu ‘l-Bayt kilichoandikwa na Dkt. Labib Baydhun. Sisi tumekiita, Tiba ya Maasumina: Bwana Mtume (saww) na Ahlul Bait Wake (as) Kitabu kimeshughulika sana katika kuelezea tiba mbadala au tiba Asilia. Waraabu walikuwa mbele sana katika nyanja hii, na alipokuja Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliitumia tiba hii na kuiongezea nguvu, hivyo, ikawa maarufu na bora zaidi. Walipokuja Maimamu wa Ahlul Bait (a.s.) waliiboresha zaidi na wao wenyewe wakawa mabingwa wa tiba hii. Tiba hii hutumia madawa ya asili yasiyo na kemikali za maabara, kama vile, majani ya miti, mizizi, matunda, maua, madini na mazao mengine yanayotokana na miti. Pia katika tiba hii kuna ushauri wa kutumia vyakula maalumu kwa magonjwa maalumu au kuuweka mwili katika siha nzuri na kinga ya magonjwa mengi. Hii ni moja kati ya kazi kubwa zinazofanywa na Taasisi ya Al-Itrah katika kuwahudumia kielimu wasomaji wake wazungumzaji wa Kiswahili. Na kwa maana hiyohiyo, imeamua kukkichapisha kitabu hiki chenye manufaa makubwa kwa lugha ya Kiswahili kwa lengo lake lilelile la kuwahudumia Waislamu, hususan wanaozungumza Kiswahili. Hivyo, ni matumaini yetu kwamba wasomaji wetu watanufaika vya kutosha kutokana na kitabu hiki, kwani tumekiona ni ­chenye 2

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 2

8/10/2017 1:21:56 PM


TIBA YA MAASUMINA

manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote ambapo magonjwa yamekuwa ni mengi na sugu kiasi kwamba tiba ya kisasa wakati mwingine inakwama kuyatibu na badala yake madaktari wanashauri tiba mbadala itumike kutibu magonjwa hayo. Tunamshukuru mwandishi wa kitabu hiki, Dkt. Labib Baydhun, kwa kazi kubwa aliyoifanya kwa ajili ya Umma huu wa Waislamu na kwa wanadamu wote kwa ujumla, Allah Azza wa Jallah amlipe kila kheri na amuingize Peponi kwa salama na amani insha’Allah. Halikadhalika tunamshukuru ndugu yetu Sheikh Amiri Mussa kwa kukitarjumi kwa Kiswahili kitabu hiki, insha’Allah na Yeye Allah Azza wa Jallah amlipe kila kheri hapa duniani na huko Akhera pia, bila kuwasahau na wale wote waliochangia kwa namna mmoja au nyingine mpaka kufanikisha kuchapishwa kwa kitabu kwake. Allah Mwenye kujazi awalipe wote malipo mema hapa duniani na Akhera pia. Mchapishaji Al-Itrah Foundation

3

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 3

8/10/2017 1:21:56 PM


TIBA YA MAASUMINA

‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬

UTANGULIZI

W

aarabu wametoa mchango mkubwa katika uwekaji misingi ya tiba za kale na kubobea katika suala hilo. Na Mtume (s.a.w.w) pamoja na Ahlulbayt wake (a.s) walikuwa ni mabingwa katika nyanja hii ya kielimu, kwa kuzingatia kwamba wao walikuwa kwa upande mmoja ni matabibu wa binadamu kwa upande wa tiba ya miili, na kwa upande mwingine ni matabibu wa binadamu kwa tiba ya roho. Na ilikuwa tiba ya maasumu hawa (a.s) ikihusika katika mambo mawili; tiba ya kinga na tiba ya madawa. Na kuhusiana na tiba ya kinga imetegemea misingi mbalimbali, ikiwemo kuwa na wastani katika kila kitu, sawa katika ulaji wa vyakula au matumizi ya dawa au katika kujipatia ladha mbalimbali. Basi imekatazwa kuvimbiwa, na imekatazwa utumiaji wa dawa ila wakati wa haja, na imekatazwa kula, kulala na kufanya tendo la ndoa ila pale ambapo yanakuwepo matamanio na hamu ya kufanya hivyo… na kwa hivyo ipo kauli ya Imam Ali bin Abu Twalib (a.s) kwa mwanawe Hasan (a.s) alipomwambia: “Ewe mwanangu! Je, nikujuze kuhusiana na mambo manne ambayo yatakutosheleza na tiba?” Akasema: Ndio, ewe Amirul-Muuminina. Akasema: “Usikae kula chakula ila ukiwa mwenye njaa. Acha kula hali ya kuwa una hamu nacho. Tafuna vizuri, na unapotaka kulala basi nenda msalani. Na utakapofanya hivyo hautaugua.” Na ama katika upande wa matibabu ya dawa hakika amebainisha bwana Mtume (s.a.w.w) na Maimamu (a.s) hususan suala la chakula na vinywaji, na namna ya kujipatia hayo. Basi wakaweka misingi 4

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 4

8/10/2017 1:21:56 PM


TIBA YA MAASUMINA

endelevu katika utumiaji wa vyakula mbalimbali, basi wakabainisha vyakula ambavyo husigana, kama vile walivyobainisha vyakula ambavyo vinaafikiana. Aina ya kwanza: Ni samaki na maziwa, na samaki na mayai. Na aina ya pili: Ni siagi na karanga na tende na tango, na tikitimaji na tende. Na ama kuhusiana na siha ya mwili, hakika tiba ya kale ilikuwa inategemea juu ya mambo mengi ya kimatibabu, lengo lake ni kurejesha wastani katika mpangilio wa mwili, kwa kuzingatia kwamba umejengwa katika tabia nne, nazo ni: Damu, kikohozi, nyongo ya manjano na nyongo nyeusi. Hivyo basi, maradhi ni hali ya moja ya tabia hizi kuwa na nguvu zaidi kushinda nyingine. Kwa hivyo siha ya mwili inategemea juu ya kuondoa sehemu iliyofurutu na kuirejesha katika wastani wake. Na hapa ndipo wakasema: Hakika tiba ina njia saba, kati ya hizo ni; utoaji damu, ufyonzaji wa damu mwilini, unyoaji wa nywele sehemu za siri, uingizaji wa bomba la maji sehemu za haja kubwa na utapikaji. Na ni kama walivyozingatia baadhi ya vitu kuwa ni chanzo cha siha ya mwili na kinga ya maradhi, na miongoni mwa vitu muhimu ni: Asali na habasoda. Na elimu zote hizi zilizopokewa kutoka kwa Ahlulbayt maasum (a.s) sasa zimeungwa mkono na tafiti mbalimbali za tiba. Nazo kwa ujumla wake ni sahihi na zina faida, lakini hilo halikanushi uwezekano wa kuwepo nyongeza kidogo iliyoingizwa, na ni upuuzi kuacha faida hizo na kuzitelekeza eti kwa sababu ya nyongeza hiyo, basi lile lisilowezekana lote haliachwi lote. Na tunapopitia tiba ya Ahlulbayti (a.s) tunakuta kwamba, baada ya Mtume (s.a.w.w) maimamu waliojitokeza zaidi na ambao walitilia umuhimu zaidi suala la tiba ni; Imam Ali (a.s), kisha ni maimamu wawili al-Baqir (a.s) na as-Sadiq (a.s). Kisha ni Imam Ridha (a.s) ambapo suala la tiba katika zama zake lilikuwa zaidi, jambo ambalo lilimfanya Maamuni amwite Imam (a.s) na kumuomba amwandikie 5

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 5

8/10/2017 1:21:56 PM


TIBA YA MAASUMINA

insha inayohusu tiba atakayoifanya dira katika maisha yake. Imam (a.s) akamwandikia insha iliyojulikana kwa jina la Insha ya Dhahabu. Maamuni alipopelekewa insha hiyo, aliisoma na akatambua thamani yake, akasema: “Ni lazima iandikwe kwa wino wa dhahabu.” Basi kuanzia hapo ndipo ikaitwa kwa jina hilo la Insha ya Dhahabu. Imam (a.s) aliiandika kwa muda wa juma moja, nayo ilikusanya kila kitu anachokihitaji binadamu maishani mwake katika maarifa ya tiba, kama ilivyokusanya ufafanuzi wa vyakula ambavyo huliwa kila mwezi katika miezi ya mwaka, vile vinavyoleta manufaa na vinavyodhuru. Na hili ni la upeo wa juu katika misingi ya tiba, ambapo inazingatiwa kuwa kila maada inayoathiri mwili ina mafungamano na hali ya mtu, kwa kuzingatia zama, mahali na wakati na mwitikio wa mwili wake. Hivyo kila mwezi mwili unahitaji vyakula maalum, na watu wa sehemu ya baridi wanahitaji vyakula ambavyo huenda vikawadhuru watu wa sehemu ya joto. Na kila dawa na chakula hutofautiana uathiri wake kwa binadamu, kulingana na mwili wake na mazoea yake. Na Imam Ridha (a.s) amejali dawa mchanganyiko ambazo huitwa (Aqrabadhin) na akabainisha matumizi ya kazi yake. Na kati ya yale aliyovumbua ni dawa mchanganyiko ambayo inafaa kutibu maradhi mengi. Na tunakuta katika vitabu wasifu wa dawa hii, kama vile tunavyokuta dawa nyingine yenye kunasibishwa kwa Mtume (s.a.w.w) na huitwa ponyo. Na mazingatio yetu katika kitabu hiki yamejikita upande wa kimaada katika suala la tiba, na haikujikita maudhui yetu katika tiba ya kiroho, na wala lile ambalo lina mafungamano na dua na Aya za Qur’anii Tukufu. Bali maudhui yetu imehusika zaidi katika nyanja zifuatazo:

6

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 6

8/10/2017 1:21:56 PM


TIBA YA MAASUMINA

1.

Mwili wa binadamu na viungo vyake.

2.

Mimea na mata za kitiba.

3.

Maradhi na dawa.

Na hakika mpangilio wa mata za tiba katika kitabu hiki zipo kwa mpangilio wa herufi za kiarabu, na ni kwa ajili hiyo kitabu hiki kikaitwa ‘Utaratibu wa maudhui wa tiba ya Ahlulbayt (a.s)’ au ‘Tiba ya Maasumu’. Na kitabu hiki kinajumuisha maudhui 220, na hakika yametimia maelezo ya jumla ya baadhi ya mada kabla ya utajo wa hadithi zenye mafungamano nayo. Na ama kwa upande wa vyanzo na vitabu rejea, hakika mchakato wa somo letu umetegemea marejeo ya msingi katika maudhui hii, nayo yamethibitishwa katika kurasa zifuatazo, na idadi yake inafikia rejea thelathini. Na limeshiriki kundi la vijana wenye upeo wa kuona mbali katika ufanikishaji wa kazi hii, ambao wanaamini kazi ni mfumo wa kielimu wenye ujumbe na malengo, hivyo basi wakathibitisha kwamba kazi ya pamoja huleta matunda zaidi. Na hao ni mabwana Raafat Fayadh, Abbas Liham, Ibrahim Zulzilat, Abdu Khidhr, Muhammad Ali Sayis na Muhammad Zakiy Diruwan. Na tunamuomba Mwenyezi Mungu atuwezeshe na kutuwafikisha katika kuhifidhi urithi wetu wenye thamani kubwa, na kufaidika kutokana na elimu ya Maimamu watoharifu, na tuongoke kwa nuru za waongofu wema. Hakika Yeye ni Msikivu Mwenye kuitikia maombi. 1 / 1 / 1993 Damascus. Syria Labibu Baydhun. 7

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 7

8/10/2017 1:21:56 PM


TIBA YA MAASUMINA

‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬

SABABU ZA KUSIGANA KWA ­HADITHI

T

unapozikuta baadhi ya hadithi zinasigana na nyingine, hilo halina maana kwamba moja kwa moja hadithi hizo sio sahihi. Bila shaka ziko sababu ambazo zinapelekea uwepo wa msigano, na hapa tunaziashiria baadhi yake kama ifuatavyo: Saduq katika kitabu chake Iitiqadaat amesema: Hakika habari zilizopokewa kuhusiana na tiba zipo katika mitazamo ifuatayo: Kati ya mitazamo hiyo ni: Zile hadithi zilizosema kuhusiana na hali ya hewa ya Makka na Madina, hizo hazifai kutumiwa katika hali ya hewa nyingine. Kati ya mitazamo hiyo ni: Yale aliyoyaeleza msomi (yaani Imam) kwa kuzingatia hali ya mazingira ya muulizaji, hayakuvuka mazingira ya muulizaji. - Kati ya mitazamo hiyo ni: Yale ambayo wahalifu wameyaingiza na kuyachakachua katika vitabu kwa kuchafua sura ya madhehebu mbele ya watu. - Kati ya mitazamo hiyo ni: Yale ambayo ndani yake umo usahaulifu kutoka kwa mnukuu wake. - Kati ya mitazamo hiyo ni: Yale yaliyohifadhiwa baadhi yake na kusahauliwa baadhi nyingine. Kama ilivyopokewa katika suala la kustanji kwa maji ya baridi kwa yule mwenye maradhi ya bawasiri; hakika hilo ni ikiwa bawasiri yake inatokana na joto. Na yale yaliyopokewa kuhusiana na bilinganya na ponyo, kwani hilo huwa wakati tende zinapoiva na si nyakati nyingine…hadi mwisho.1

Na amezungumza Allamah Majlisi katika kitabu chake BiharulAnwaar kuhusiana na sababu ya kupingana kwa baadhi ya hadithi, 1

Biharul-An’war, Juz. 62, uk. 29. 8

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 8

8/10/2017 1:21:57 PM


TIBA YA MAASUMINA

akasema: Hutba za Mtume (s.a.w.w) ziko za aina mbili; Ya ujumla kwa watu wa ardhini, na mahsusi kwa baadhi yao, ya kwanza ni kama vile ujumla wa hutba zake, na ya pili ni kama vile kauli ya Mtume (s.a.w.w) inayosema: “Msielekee Qibla wakati mnapojisaidia haja kubwa na ndogo wala msikipe mgongo Qibla, lakini elekeeni mashariki au magharibi, na hili sio kwa kuwazungumzia watu wa mashariki wala wa magharibi wala wa Iraq, lakini kwa watu wa Madina na mfano wake kama vile wa Sham na wengineo.2

VITABU REJEA: TIBA YA AHLUL-BAYT (A.S):

• • • • • •

2

Qur’ani tukufu. Nahjul-Balaghah, ni maneno ya yaliyokusanywa na Sharifu Ridhawi.

Imam Ali

(a.s)

Mustadraku Nahjul-Balaghah cha Sayyid Hadi Kashif Ghatwai, kimechapishwa na maktaba ya Andolus ya Beirut. Fiqhu yenye kunasibishwa na Imam Ridha (a.s), ni mashuhuri kwa jina la Fiqhur-Ridha, kimehakikiwa na taasisi ya Aalul-Bayt Li Ihyaai Turathi, kimepigwa chapa mwaka 1986. Sahifat cha Imam Ridha (a.s), kimehakikiwa na Muhammad Mahdi Najaf, Mashhad mwaka 1986. Aqdul-Farid, Juz. 7, uk. 263 – 272, na Juz. 8, Uk. 1 – 80 cha Ibn Abdu Rabbih (amekufa mwaka 328 AH), kimehakikiwa na Muhammad Said Uryaan, Maktabat Tujariyat Kubra, chapa ya pili mwaka 1953.

Biharul-An’war, Juz. 62, uk. 28. 9

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 9

8/10/2017 1:21:57 PM


TIBA YA MAASUMINA

• • • • • •

• • •

Twibbun-Nabawiy cha Abu Abbas Ja’far bin Muhammad Mustaghfiri (amekufa mwaka 432 AH) ni kitabu kidogo kimechapishwa Qum. Twibbun-Nabawiy cha Dhahabi (amekufa mwaka 748 AH). Twibbun-Nabawiy cha Shamsu Diin Muhammad bin Abi Bakri bin Ayub Zarii Damishqi, mashuhuri kwa jina la Ibn Qayyim Joziyyat (amekufa mwaka 751 AH) kimehakikiwa na Abdul-Ghaniy Abdil-Khaliq, Misri mwaka 1957. Twibbu fi Qur’ani cha Mahmud Nasiimi kutoka Halabi, anajibu kitabu kilichotangulia. Twibbun-Nabawiy cha Mahmud Nasiimiy kina juzuu tatu. Ajaibul-Makhluqaat wa Gharaaibul-Maujudaat cha Zakariyya bin Muhammad Qazwini (amekufa mwaka 682 AH), mwishoni mwa juzuu ya pili kutoka kitabu HayaatuHayawaani-Kubra cha Damiiry, chapa ya nne maktaba ya Mustafa Albabi, Halabi, Misri mwaka 1970, Faslul-Nabaat, uk. 162 – 198. Al-Mahasin cha Ibn Ja’far Ahmad bin Muhammad Kuufi Barqi (amekufa mwaka 280 AH). Qurbul-Isnaad cha Abdullah bin Ja’far bin Husein bin Malik bin Jaamiul-Humeiry (ni miongoni mwa watu wa karne mbili ya tatu na nne), chapa ya Haydariyyat Najaf. Twibbul-Aimmat (a.s) kwa mujibu wa hadithi ya Abdillah na Husein, ni watoto wawili wa Bastwam Naysaburayn (karne ya nne Hijiria), Daarul-Kitaab-Islamiy Beyrut mwaka 1385 AH. 10

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 10

8/10/2017 1:21:57 PM


TIBA YA MAASUMINA

• • • • • • • •

Tuhaful-Uquul an Aali Rasuul (s.a.w.w) cha Ibn Shuubat Harrani kutoka kwa ulamaa wa karne ya 4 A.H, kimechapishwa na taasisi ya Aalami Beyrut, chapa ya 5 mwaka wa 1974. Uyuunu-Akhbar Ridha (a.s) cha Sheikh Saduuq, kimehakikiwa na Sayyid Mahdi Huseini – Ajuurudiy. Khiswal cha Sheikh Saduuq, maktaba Saduuq chapa ya Tehran 1389. Ilalul-Sharaai cha Sheikh Saduuq, chapa ya Haydariya, Najaf, mwaka 1966. Kitabul-Qanuun fi kitabu Twibbi cha ibn Sina (Avicena) – kutoka chapa ya Ruumiyya Italia mwaka 1593 AD, kimefafanuliwa na kupangiliwa na Jiraan Jabuur, chapa ya pili maktaba ya Maarifa, Beirut, mwaka 1980. Makarimul-Akhlaq cha Abu Nasr Hasan bin Fadhl Twabarasi (amekufa mwaka 548 AH), naye ni Ibn Allamah mtunzi wa Tafsir Majmaul-Bayaan, uk. 134 - 195, kimechapishwa na taasisi ya Aalami ya Beirut, chapa ya pili, mwaka 1972. Saluut Haziin, uk. 137 – 162 kinajulikana kama kitabu Daa’wat cha Qutbu Diin Raawandi (amekufa mwaka 573 AH), kimesambazwa na Madrasat Imam Mahadi (a.s) Qum. Wasailu-Shi’a ila Tahswiil Masaail Shariiat, Juz. 16, uk. 405 – 543 na Juz. 17, uk. 1 - 221 cha Muhammad bin Hasan Hurru Aamiliy (amekufa mwaka 104 A.H), kimehakikiwa na Sheikh Abdul-Rahiim Rabbani Shirazi, kimepigwa chapa na Daarul-Ihyaai Turaathi-Ilmiiy ya Beirut.

11

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 11

8/10/2017 1:21:57 PM


TIBA YA MAASUMINA

• • • • • • •

Biharul-An’war, Juz. 62 cha Allamah Muhammad Baqir Majlisi (amekufa mwaka 111 A.H), kimepigwa chapa na Daarul-Kutubil-Islamiyyat ya Tehran. Safinatul-Bihar cha Sheikh Abbas Qummi, kimechapishwa na maktaba Ilmiyya ya Najaf, mwaka 1355 AH, chapa ya Hajar. Tuhfatul-Ridhawiyyat fi Mujarrabaat Imamiyyat, uk. 57 – 80 cha Muhammad bin Ridhawy Kashmiiry Najafii, chapa ya tatu, Tehran mwaka 1982. Ramzul-Sihat fi Twibbin-Nabiyyi wal-Aimmat (a.s) cha Mahmuud bin Musawy Aldihi Salkhi Isfahaniy, chapa ya pili mwaka 1983. Twibbul-Aimmat (a.s) cha Allamah Sayyid Abdullah Shubbar, kimesambazwa na Iitiswaam ya Kuwait mwaka 1990 A.D. Twibbu Imam as-Sadiq (a.s) cha Muhammad Khalili, kimesambazwa na Daarul-kitabul-islamiyy ya Beirut mwaka 1979. Majmuat Athar Imam Ridha (a.s), mijaladi miwili, kimesambazwa na Muutamar Aalamiy Awwali wa Thaani LiImam Ridha (a.s), Mashhad mwaka 1986 na 1988. Na mwishoni mwa juzuu ya kwanza ipo Insha ya Dhahabu ya Imam Ridha (a.s), kimehakikiwa na Muhammad Mahdi Najaf. Mandhumat cha Sheikh Muhammad Husein Aaswim kinahusu vyakula na viywaji, kimesahihishwa na MajmaulBuhuuthil-Islamiyyat, Mashhad, mwaka 1410 A.H. 12

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 12

8/10/2017 1:21:57 PM


TIBA YA MAASUMINA

• • • • • •

Jamiu Limufradaat Aduwiyyat wal-Aghadhiyyat cha Abdullah bin Ahmad bin Baytwar, kimepigwa chapa na Bulaaq. Tadhkiratu Uulul-Albaab wal-Jaamiu lil-Ajabil-Ajaaib, kimeandikwa na Daud bin Umar Antwaki (amekufa mwaka 100 A.H.), Maktabat Thaqafiyyat ya Beirut. Nabataatu Twibbiyyat wa Isti’malaatiha cha Dr. Muhammad Audaat Jorg Liham, Ahaaly, kimechapishwa na kusambazwa Damascus, ina juzuu mbili, chapa ya kwanza mwaka 1987. Nabataatu Twibbiyyat wal-Uturiyyat wa Saamat filwatwan Arabiy, Jaamiat Duwalil-Arabiyyat, Munadhamat Arabiyyat lil-Tanmiyat Ziraaiyyat ya Khartuum mwaka 1988. Tadaawi bil-Aashaab cha Dr. Amiin Rawayhat, kimechapishwa na Daarul-Qalam ya Beirut, chapa ya nne. Mufradaatu Nabataat Twibbiyat, kimaendikwa na Ahmad Saleh Dahaymash, kimepichapishwa Damascus mwaka 1998.

13

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 13

8/10/2017 1:21:57 PM


TIBA YA MAASUMINA

KUTOKA KATIKA WAHYI WA QUR’ANI ­TUKUFU Mwenyezi Mungu anasema:

‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬ Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu:

َ ْ ُ ُ ُ َ َ َّ َ ُّ َ َ َّ ُ ُ ْ ُ ْ َ ّ ‫ات َما َر َزق َناك ْم َواشك ُروا ِلل ِه ِإ ْن ك ْن ُت ْم ِإ َّي ُاه‬ ‫ي‬ ‫ط‬ ‫ب‬ ِ ِ ‫يا أيها ال ِذين آمنوا كلوا ِمن‬ َ ‫ت ْع ُب ُدو َن‬ ُ َ َّ َ َ َ ْ َ ْ‫َّ َ َ َّ َ َ َ ْ ُ ُ م‬ ُ ْ َ َّ َ ْ ْ ‫اضط َّر‬ ‫الد َم َول ْح َم ال ِخن ِز ِير َو َما أ ِه َّل ِب ِه ِلغ ْي ِر الل ِه ۖ ف َم ِن‬ ‫ِإنما حرم عليكم اليتة و‬ َّ َّ ْ َ َ َ ْ َ‫َ ْ َ َ َ اَ َ َ ا‬ ٌ ‫ور َر ِح‬ ٌ ‫الل َه َغ ُف‬ ‫يم‬ ‫غير ب ٍاغ ول ع ٍاد فل ِإثم علي ِه ۚ ِإن‬ Enyi mlioamini! Kuleni vizuri tulivyowaruzuku, na mumshukuru Mwenyezi Mungu ikiwa mnamwabudu Yeye tu. Hakika amewaharamishia mzoga,na damu, na nyama ya nguruwe,na kilichochinjiwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Basi aliyefikwa na dharura (akala) bila kutamani wala kupita kiasi, yeye hana dhambi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghufira. Mwenye ­kurehemu.3

3

َ‫ا‬ َ ْ‫ُ ْ ُ َ َ ً َ ْ َ ُ ّ َ َ م‬ َ ْ‫َ َ ْ َ ُ َ َ َ م‬ ‫يض ۖ َول‬ ‫ح‬ ‫ال‬ ‫ي‬ ‫ف‬ ‫اء‬ ‫س‬ ‫الن‬ ‫وا‬ ‫ل‬ ‫ز‬ ‫ت‬ ‫اع‬ ‫ف‬ ‫ى‬ ‫ذ‬ ‫أ‬ ‫و‬ ‫ه‬ ‫ل‬ ‫ق‬ ۖ ‫يض‬ ‫ح‬ ‫ال‬ ‫ويسألونك ع ِن‬ ِ ِ ِ ِ ِ ِ ِ َ ْ َ ْ َّ َّ ُ ُ ُ ‫وه َّن َح َّت ٰى َيط ُه ْر َن ۖ َفإ َذا َتط َّه ْر َن َفأ ُت‬ ُ ‫َت ْق َرُب‬ ‫وه َّن ِم ْن َح ْيث أ َم َرك ُم الل ُه ۚ ِإ َّن الل َه‬ ِ َّ ‫ُيح ُّب‬ َ ‫الت َّواب َين َو ُيح ُّب مْالُ َت َط ّهر‬ ‫ين‬ ِ ِ ِ ِ ِ

Sura 2, aya 172-173.

14

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 14

8/10/2017 1:21:57 PM


TIBA YA MAASUMINA

“Na wanakuuliza kuhusu hedhi. Waambie: Ni udhia, basi jitengeni na wanawake wakati wa hedhi. Wala msiwakurubie mpaka watwaharike. Wakisha twaharika, basi waendeeni pale alipowaamrisha Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanaotubia na huwapenda wanaojitwaharisha.”4

َ َ َ َّ َّ ُ ْ َ َ َ َ ْ َ ْ َ َ ْ َ ْ َ َّ ُ َ َ‫َ ْ َ َ ُ ُ ْ ْ َ َ ْ ا‬ ‫اعة‬ ‫والو ِالدات ير ِضعن أولدهن حولي ِن ك ِاملي ِن ۖ مِلن أراد أن ي ِتم الرض‬ “Na wazazi wa kike wawanyonyeshe watoto wao miaka miwili kamili kwa anayetaka kukamilisha kunyonyesha.”5

َ َ َ َْ َ َ َّ َ ‫َم َث ُل َّالذ‬ ‫ين ُي ْن ِف ُقو َن أ ْم َوال ُه ْم ِفي َس ِب ِيل الل ِه ك َمث ِل َح َّب ٍة أن َبت ْت َس ْب َع َس َن ِاب َل ِفي‬ ِ َ ُ َّ َّ َ ُ َ َ ُ ُ َ ُ َ َّ َ ُْ ُ ّ ُ ٌ ‫اعف ل ْن َيش ُاء ۗ َوالله َو ِاس ٌع َع ِل‬ ‫يم‬ ِ‫ك ِل سنبل ٍة ِمائة حب ٍة ۗ والله يض ِ م‬ “Mfano wa wale wanaotoa mali zao katika njia ya Mwenyezi Mungu, ni kama vile mfano wa punje moja itoayo mashuke saba, katika kila shuke punje mia. Na Mwenyezi Mungu humzidishia amtakaye na Mwenyezi Mungu ni mwenye wasaa, mwenye kujua.”6

َ ْ‫َ َ ُّ َ َّ َ َ ُ َّ َ ْ َ ْ ُ َ مْ َ ْ ُ َ أْ َ ْ َ ُ َ أ‬ ٌ ‫ال ْ اَزل ُم ر ْج‬ ‫س ِم ْن َع َم ِل‬ ‫يا أيها ال ِذين آمنوا ِإنما الخمر والي ِسر والنصاب و‬ ِ ُ َّ َ ُ ُ َ ْ َ َ ْ َّ ‫وه ل َعلك ْم ُت ْف ِل ُحو َن‬ ‫الشيط ِان فاجت ِنب‬ “Enyi mlioamini! Hakika pombe na kamari na mizimu na mburuga ni uchafu katika kazi ya shetani. Basi jiepusheni nayo ili mpate kufaulu.”7

ْ َ َ َ ّ ُ َ َ َ َ ْ َ ْ َ َ ً َ َ َّ َ ‫َ ُ َ َّ َ ْ َ َل‬ ‫�ش ْي ٍء فأخ َر ْج َنا ِم ْن ُه‬ ‫وهو ال ِذي أنز ِمن السم ِاء ماء فأخرجنا ِب ِه نبات ك ِل‬ ْ َ ْ ْ َّ َ َ َ ُْ َ ْ ُ َّ َ ٌ َ ٌ ْ ‫ات ِم ْن‬ ٍ ‫خ ِض ًرا نخ ِر ُج ِمنه ح ًّبا ُمت َر ِاك ًبا َو ِمن النخ ِل ِمن طل ِع َها ِقن َوان دا ِن َية َوجن‬   Sura 2, aya 222.   Sura 2 aya 233. 6   Sura 2 uk. 261. 7   Sura 5 aya 90. 4 5

15

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 15

8/10/2017 1:21:57 PM


TIBA YA MAASUMINA

َ َ ُ ْ َْ َ َ َ َ ْ َ َّ ُّ َ ‫َ ْ َ َ َّ ْ ُ َن‬ ‫ان ُمش َت ِب ًها َوغ ْي َر ُمتش ِاب ٍه ۗ انظ ُروا ِإل ٰى ث َم ِر ِه ِإذا أث َم َر َو َي ْن ِع ِه‬ ‫اب والزيتو والرم‬ ٍ ‫أعن‬ َ‫َّ َٰ ُ آ‬ ‫ات ِل َق ْو ٍم ُي ْؤ ِم ُنو َن‬ ٍ ‫ۚ ِإن ِفي ذ ِلك ْم ل َي‬ “Naye ndiye aliyeteremsha maji kutoka mbinguni, na kwayo tunatoa mimea ya kila kitu. Kisha tukatoa kutokana nayo kijani; tukatoa ndani yake punje zilizopandana. Na katika mitende yakatoka kwenye makole yake mashada yaliyo karibu, na bustani za mizabibu na mizaituni na makomamanga, yanayofanana, na yasiyofanana. Angalieni matunda yake yanapozaa na kuiva kwake. Hakika katika hayo kuna ishara kwa watu wanaoamini.”8

َ‫ا‬ ُ​ُ ُ ُ َ ُ ُ ُ ُ َ‫ا‬ ْ ‫َيا َب ِني َآد َم خذوا ِزين َتك ْم ِع ْن َد ك ِ ّل َم ْس ِج ٍد َوكلوا َواش َرُبوا َول ت ْس ِرفوا ۚ ِإ َّن ُه ل‬ ُ ْ‫م‬ ‫ُي ِح ُّب ال ْس ِر ِف َين‬ “Enyi wanadamu! Chukueni, mapambo yenu katika kila msikiti, na kuleni na kunyweni wala msifanye ufujaji (israaf), hakika Yeye hawapendi wafanyao ufujaji.”9

َ َ َ َ َ َ​َ ُ َ ًَ ْ ‫فل َّما َس ِم َع ْت ِب َمك ِر ِه َّن أ ْر َسل ْت ِإل ْي ِه َّن َوأ ْع َت َد ْت ل ُه َّن ُم َّتكأ َوآت ْت ك َّل َو ِاح َد ٍة ِم ْن ُه َّن‬ َ ّ ْ َ َ ‫ِس ِك ًينا َوقال ِت اخ ُر ْج َعل ْي ِه َّن‬ “Basi (mkewe mheshimiwa) aliposikia vitimbi vyao, akawaita na akawafanyia karamu na akawapa kila mmoja wao kisu na akasema (Yusuf) tokeza mbele yao.”10

ً‫ْ اَّ َ ا‬ ُ ‫ص ْد ُت ْم َف َذ ُر‬ َ ‫ال َت ْز َر ُعو َن َس ْب َع سن َين َد َأ ًبا َف َما َح‬ َ ‫َق‬ ‫وه ِفي ُسن ُب ِل ِه ِإل ق ِليل ِم َّما‬ ِ ِ ُ​ُْ ‫َتأكلو َن‬   Sura 6 aya 99.   Sura 7 aya 31. 10   Sura 12 aya 31. 8 9

16

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 16

8/10/2017 1:21:57 PM


TIBA YA MAASUMINA

“Akasema: Mtalima miaka saba mfululizo. Mtakachovuna kiwacheni katika mashuke yake, isipokuwa kidogo mtakachokula.”11

َّ ‫ُه َو َّال ِذي َأ ْن َز َل م َن‬ ٌ ‫الس َم ِاء َم ًاء ۖ َل ُك ْم ِم ْن ُه َش َر‬ ‫اب َو ِم ْن ُه َش َج ٌر ِف ِيه ُت ِس ُيمو َن‬ ِ َُ َّ ّ ُ ْ َ َ َ ْ َ ْ‫َّ ْر َ َ َّ ْ ُ َن َ َّ َ َ أ‬ َ‫الث َم َرات ۗ إ َّن في َٰذلك‬ ‫ُي ْن ِب ُت لك ْم ِب ِه الز ع والزيتو والن ِخيل والعناب و ِمن ك ِل‬ ِ ِ ِ ِ َ ‫آَل َي ًة ل َق ْوم َي َت َف َّك ُر‬ ‫ون‬ ٍ ِ “Yeye ndiye aliyewateremshia maji kutoka mbinguni. Katika hayo nyinyi mnapata ya kunywa, na miti ya kulishia. Kwayo anazalisha mimea kwa ajili yenu na mizaituni na mitende na mizabibu na kila matunda. Hakika katika hayo zipo ishara kwa watu wanaofikiri.”12

َ َ ْ ُ​ُْ َّ ‫َو ُه َو ال ِذي َس َّخ َر ال َب ْح َر ِل َتأكلوا ِم ْن ُه ل ْح ًما ط ِرًّيا‬ “Na yeye ndiye aliyeitiisha bahari iwatumikie ili kutoka humo mpate kula nyama freshi…..”13

َ َّ َ َ ُّ َ ٰ َ ْ َ َ َّ َ َ ً ُ ُ َ ْ َ ‫الش َج ِر َو ِم َّما َي ْع ِر ُشو َن‬ ‫وأوحى ربك ِإلى‬ ‫الن ْح ِل أ ِن َّات ِخ ِذي ِمن ال ِجب ِال بيوتا و ِمن‬ ُ ُ ً‫ا‬ ُ ُ َّ ُ ْ ْ ‫ات َف‬ ٌ ‫اس ُل ِكي ُس ُب َل َرّب ِك ُذلل ۚ َي ْخ ُر ُج ِم ْن ُبط ِون َها َش َر‬ ‫اب‬ ِ ‫ث َّم ك ِلي ِمن ك ِ ّل الث َم َر‬ ِ ٌ َْ ُ َ ‫ف َأ ْل َو ُان ُه فيه ش َف ٌاء ل َّلناس ۗ إ َّن في َٰذل َك آَل َي ًة ل َق ْوم َي َت َف َّك ُر‬ ‫ون‬ ‫مخت ِل‬ ِ ِ ِ ِ ِ ِ ِ ِ ٍ ِ “Na Mola Wako akampa wahyi nyuki kwamba, tengeneza nyumba katika milima, na katika miti, na katika wanayoyajenga (watu). Kisha kula katika kila matunda, na ufuate katika njia za Mola Wako mlezi zilizo dhalili nyepesi. Na katika matumbo yao kinatoka kinywaji chenye rangi mbali mbali, ndani yake kina   Sura 12 aya 47.   Sura 16 aya 10 -11. 13   Sura 16 aya 14. 11

12

17

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 17

8/10/2017 1:21:57 PM


TIBA YA MAASUMINA

matibabu kwa watu. Hakika katika haya kuna ishara kwa watu wanaofikiri.”14

َّ َ َّ ‫الل ُه َأ ْخ َر َج ُك ْم م ْن ُب ُطون ُأ َّم َها ِت ُك ْم اَل َت ْع َل ُمو َن َش ْي ًئا َو َج َع َل َل ُك ُم‬ ‫الس ْم َع‬ ‫و‬ ِ ِ َ ْ‫َ أْ َ ْ َ َ َ أ‬ َ ‫ال ْفئ َد َة ۙ َل َع َّل ُك ْم َت ْش ُك ُر‬ ‫ون‬ ِ ‫والبصار و‬ “Na Mwenyezi Mungu amewatoeni matumboni mwa mama zenu hamjui kitu, na amewajaalieni usikivu na uoni na nyoyo ili mpate kushukuru.”15

ْ َُ ْ ْ ٌ َ ‫َونن ّ ِز ُل ِم َن ال ُق ْر ِآن َما ُه َو ِشف ٌاء َو َر ْح َمة ِلل ُمؤ ِم ِن َين‬ “Na tunateremsha katika Qur’ani ambayo ni ponyo na rehema kwa wenye kuamini…..”16

َ َ َ ْ َ َُ ُ َ ْ َّ ْ ْ ‫النخل ِة ت َسا ِقط َعل ْي ِك ُرط ًبا َج ِن ًّيا فك ِلي َواش َرِبي َوق ّ ِري َع ْي ًنا‬ ‫َو ُه ّ ِزي ِإل ْي ِك ِب ِجذ ِع‬ “Na litikise kwako shina la mtende, utakuangushia tende nzuri zilizoiva. Basi kula na kunywa na uburudishe jicho…..”17

َ ْ‫َ َ ْ َ ْ َ َ َّ َ َ ً َ َ َ َ ْ َ َّ ُ أ‬ َ ‫ال ْ ض ۖ َوإ َّنا َع َل ٰى َذ َهاب به َل َقاد ُر‬ ‫ون‬ ِ ِ​ِ ٍ ِ ِ ‫وأنزلنا ِمن السم ِاء ماء ِبقد ٍر فأسكناه ِفي ر‬ ُ​ُْ َ َ ُ َ َْ َ​َ ُ َ َْ َ َْ​َ َ ْ َّ َ ‫اب لك ْم ِف َيها ف َو ِاك ُه ك ِث َير ٌة َو ِم ْن َها َتأكلو َن‬ ٍ ‫فأنشأنا لك ْم ِب ِه جن‬ ٍ ‫ات ِمن ن ِخ ٍيل وأعن‬ ْ‫آ‬ ُّ ‫َو َش َج َر ًة َت ْخ ُر ُج م ْن ُطور َس ْي َن َاء َت ْن ُب ُت ب‬ ‫الد ْه ِن َو ِص ْب ٍغ ِلل ِك ِل َين‬ ِ ِ ِ ُ َُ ُ َُ ُ ً َ ْ َ ْ‫أ‬ ٌ َ ‫َوِإ َّن لك ْم ِفي الن َع ِام ل ِع ْب َرة ۖ ن ْس ِقيك ْم ِم َّما ِفي ُبط ِون َها َولك ْم ِف َيها َم َنا ِف ُع ك ِث َيرة َو ِم ْن َها‬ ُ​ُْ ‫َتأكلو َن‬

Sura 16 aya 68-69.   Sura 16 aya 78. 16   Sura 17 aya 82. 17   Sura 19 aya 25-26 14 15

18

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 18

8/10/2017 1:21:57 PM


TIBA YA MAASUMINA

“Na tumewateremshia kutoka mbinguni maji kwa kiasi, na tukayatuliza ardhini, na hakika Sisi ni wenye uwezo wa kuyaondoa. Basi kwa maji hayo tukawafanyia bustani za mitende na mizabibu, mnapata humo matunda mengi, na katika hayo mnakula. Na mti utokao katika mlima wa Sinai, unaotoa mafuta na kitoweo kwa walaji. Na hakika katika wanyama howa mna mazingatio (makubwa). Tunawanywesheni ninyi katika vile vilivyomo matumboni mwao, na mnapata katika hao manufaa mengi, na katika hao mnawala.”18

َ ْ‫َّ ُ ُ ُ َّ َ َ َ أ‬ ُ ‫ص َب‬ ْ ‫اح ۖ مْ ِال‬ ٌ ‫ص َب‬ ْ ‫ال ْرض ۚ َم َث ُل ُنوره َكم ْش َكاة ف َيها م‬ ‫اح ِفي‬ ِ ‫الله نور السماو‬ ِ ِ ٍ ِ ِ​ِ ِ ‫ات و‬ َ َ َ َ َ ُ َ َ ُّ َ َ َ‫َ ا‬ َ َ ‫ُز َج‬ ‫اجة كأ َّن َها ك ْوك ٌب ُد ّ ِر ٌّي ُيوق ُد ِم ْن ش َج َر ٍة ُم َب َارك ٍة َزْي ُتون ٍة ل ش ْر ِق َّي ٍة‬ ‫اج ٍة ۖ الزج‬ َ َ َ َ ُ ‫َواَل َغ ْرب َّية َي َك ُاد َزْي ُت َها‬ ‫�ض ُيء َول ْو ل ْم ت ْم َس ْس ُه ن ٌار‬ ‫ي‬ ٍ ِ ِ “Mwenyezi Mungu ni Nuru ya mbingu na ardhi, mfano wa nuru yake ni kama shubaka ndani yake mna taa. Taa hiyo imo katika tungi, tungi hilo ni kama nyota inayomeremeta, inayowashwa kwa mafuta yanayotokana na mti uliyobarikiwa, mzaituni. Si wa mashariki wala magharibi. Yanakaribia mafuta yake kun’gaa ingawa haujayagusa na moto…..”19

َّ َّ ُ ُ َ َ َ َ َّ ‫اسا َو‬ َّ ‫الن ْو َم ُس َب ًاتا َو َج َع َل‬ ً ‫الل ْي َل ل َب‬ ً ‫الن َه َار ُن ُش‬ ‫َو ُه َو ال ِذي جعل لكم‬ ‫ورا‬ ِ “Na Yeye ndiye aliyewafanyieni usiku kuwa ni vazi na usingizi kuwa ni mapumziko, na akaufanya mchana kuwa ni wa matawanyiko.”20

ً ٌ ‫َو ُه َو َّالذي َم َر َج ْال َب ْح َرْين َٰه َذا َع ْذ ٌب ُف َر‬ ٌ ‫ات َو َٰه َذا م ْل ٌح ُأ َج‬ ‫اج َو َج َع َل َب ْي َن ُه َما َب ْر َزخا‬ ِ ِ ِ ً ‫َو ِح ْج ًرا َم ْح ُج‬ ‫ورا‬   Sura 23 aya 18-21.   Sura 24 aya 35. 20   Sura 25 aya 47. 18 19

19

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 19

8/10/2017 1:21:57 PM


TIBA YA MAASUMINA

َ َ ‫َو ُه َو َّالذي َخ َل َق م َن مْالَاء َب َش ًرا َف َج َع َل ُه َن َس ًبا َوص ْه ًرا ۗ َو َك‬ ‫ان َرُّب َك ق ِد ًيرا‬ ِ ِ ِ ِ “Na yeye ndiye aliyezichanganya bahari mbili, hii ni tamu mno, na hii ni chumvi sana, na akaweka kinga kati yake na kizuizi kizuiacho. Na Ndiye aliyemuumba mwanadamu kutokana na maji, na akamjaalia kuwa na nasaba na ukwe. Na Mola Wako ni Mwenye uwezo.”21

َّ ُ َّ ُ ً ُ ْ َ ْ َ ْ َ َ َ َّ ُ ْ َ ْ ْ ُ َ َ َ ‫ف ق َّوة ث َّم َج َع َل ِم ْن َب ْع ِد‬ ٍ ‫ف ثم جعل ِمن بع ِد ضع‬ ٍ ‫الله ال ِذي خلقكم ِمن ضع‬ َ ْ ُ َ ْ َ ُ َ ُ َ َ َ ُ ُ ْ َ ً َ ْ َ َ ً ْ َ َّ ُ ‫يم الق ِد ُير‬ ‫قو ٍة ضعفا وشيبة ۚ يخلق ما يشاء ۖ وهو الع ِل‬ “Mwenyezi Mungu Ndiye ambaye amewaumbeni katika udhaifu, akajaalia nguvu baada ya udhaifu, kisha akajaalia udhaifu baada ya nguvu na uzee; anaumba atakavyo; Naye Ndiye Mjuzi Mwenye uweza.”22

ٌ ‫َف َن َب ْذ َن ُاه ب ْال َع َر ِاء َو ُه َو َس ِق‬ ‫يم‬ ِ ًَ َ َ َْ​َ َََْْ​َ ْ ْ َ ‫وأنبتنا علي ِه شجرة ِمن يق ِط ٍين‬ “Kisha tulimtupa ufukweni patupu hali ya kuwa mgonjwa. Na tukamuoteshea mmea wa mung’unye.”23

َ َ ‫َوأ ْم َد ْد َن ُاه ْم ِب َف ِاك َه ٍة َول ْح ٍم ِم َّما َي ْش َت ُهو َن‬ ٌ ‫َي َت َنا َز ُعو َن ِف َيها َك ْأ ًسا اَل َل ْغ ٌو ِف َيها َواَل َت ْأ ِث‬ ‫يم‬ “Na tutawapa matunda na nyama katika vile watakavyopenda. Watapeana humo gilasi (za vinywaji) kisicholeta upuuzi wala dhambi.”24   Sura 25 aya 53-54.   Sura 30, aya 54. 23   Sura 37, aya 145-146. 24   Sura 52 aya 22-23. 21 22

20

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 20

8/10/2017 1:21:58 PM


TIBA YA MAASUMINA

َ ْ‫َ أ‬ َ َ ْ‫أ‬ َ ‫ض َو‬ َ ‫ال ْر‬ ‫و‬ ‫ض َع َها ِللن ِام‬ ْ َ ْ‫َ َ َ ٌ َ َّ ْ ُ َ ُ أ‬ ‫ات الك َم ِام‬ ‫ِفيها ف ِاكهة والنخل ذ‬ ُ ‫الرْي َح‬ ْ َْ ُ َ ْ َ َّ ‫ف َو‬ ‫ان‬ ِ ‫والح ُّب ذو العص‬ “Na ardhi ameiweka kwa ajili ya viumbe. Humo yamo matunda na mitende yenye mafumba. Na nafaka zenye makapi na mrehani.25

ٌ ‫فيه َما َفاك َه ٌة َو َن ْخ ٌل َو ُر َّم‬ ‫ان‬ ِ ِ​ِ َ َ‫ا‬ َ ّ َُ ُ ‫ف ِبأ ّ ِي آل ِء َرِّبك َما تك ِذ َب ِان‬ “Mna matunda na mitende na komamanga. Basi ni ipi katika neema ya Mola Wenu mnayoikanusha nyinyi wawili?”26

َ ‫َو َفاك َهة م َّما َي َت َخ َّي ُر‬ ‫ون‬ ِ ٍ ِ َ َ ‫َول ْح ِم ط ْي ٍر ِم َّما َي ْش َت ُهو َن‬ ٌ ‫َو ُح‬ ‫ور ِع ٌين‬ َ​َ ْ َ ْ‫ُّ ُ م‬ ‫كأ ْم َث ِال الل ْؤل ِؤ الك ُنو ِن‬ “Na matunda wayapendayo. Na nyama ya ndege kama wavyotamani. Na mahurulain. Walio kama mfano wa lulu zilizohifadhiwa.”27

ْ ُ َ ْ َ َ ْ ُ َ ْ َ​َ ‫اب ال َي ِم ِين‬ ‫اب ال َي ِم ِين ما أصح‬ ‫وأصح‬ ُ ْ ْ ‫ود‬ ٍ ‫ِفي ِسد ٍر َمخض‬   Sura 55 aya 10-12.   Sura 55 aya 68-69. 27   Sura 56 aya 20-23. 25 26

21

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 21

8/10/2017 1:21:58 PM


TIBA YA MAASUMINA

ُ ْ َْ َ ‫ود‬ ٍ ‫وطل ٍح َمنض‬ ‫َو ِظ ٍ ّل َم ْم ُد ٍود‬ ُ ْ َ َ​َ ‫وب‬ ٍ ‫وم ٍاء مسك‬ َ َ ‫َوف ِاك َه ٍة ك ِث َير ٍة‬ َ ‫وعة َواَل َم ْم ُن‬ َ ُ ْ َ‫ا‬ ‫وع ٍة‬ ٍ ‫ل َمقط‬ “Na wa kuume; je, ni yapi ya wa kuume? Katika mikunazi isiyo na miiba. Na migomba iliyopangiliwa, na kivuli kilichotanda, na maji yanayomiminika. na matunda mengi (ya kila aina). Hayakatiki wala hayakatazwi.”28

َ َ ُ َ ْ ْ‫َ ْ َ ْ ُ إ‬ ‫ان ِإل ٰى ط َع ِام ِه‬ ‫النس‬ ِ ‫فلينظ ِر‬ َ ‫ص َب ْب َنا مْالَ َاء‬ َ ‫َأ َّنا‬ ‫ص ًّبا‬ َ َ ْ َ ْ‫ُ َّ َ َ ْ َ أ‬ ‫ض ش ًّقا‬ ‫ثم شققنا الر‬ ْ َْ​َ ‫فأن َبت َنا ِف َيها َح ًّبا‬ ْ ‫َوع َن ًبا َو َق‬ ‫ض ًبا‬ ِ ْ َ َ ً ُ ْ ‫َ َز‬ ‫و يتونا ونخل‬ ُْ ‫َو َح َدا ِئ َق غل ًبا‬ ُْ ‫َو َح َدا ِئ َق غل ًبا‬ ُ َْ ُ َ ً َ َ ‫مت‬ ‫اعا لك ْم َوأِلن َع ِامك ْم‬ “Hebu na atazame mtu chakula chake. Hakika tumeyamimina maji mmiminiko. Kisha tukaipasua ardhi mpasuko. Tukaotesha humo na28

Sura 56 aya 27-33. 22

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 22

8/10/2017 1:21:58 PM


TIBA YA MAASUMINA

faka. Na zabibu na mboga. Na mizaituni na mitende. Na mabustani yenye miti mingi. Na matunda na ndisho. Kwa ajili ya manufaa yenu na ya wanyama wenu.”29

ّ َ َّ ‫التين َو‬ ‫الزْي ُتو ِن‬ ِ ِ ‫و‬ ُ َ ‫ور ِسي ِن َين‬ ‫ط‬ ِ ‫و‬ َ ْ‫َ َٰ َ ْ َ َ أ‬ ‫وهذا البل ِد ال ِم ِين‬ “Naapa kwa Tiini na Zaituni. Na kwa mlima Sinai. Na kwa mji huu wenye amani.”30

ُ ُ ‫َف ْل َي ْن ُظر إْال ْن َس‬ ‫ان ِم َّم خ ِل َق‬ ِ ِ ُ ‫خ ِل َق ِم ْن َم ٍاء َدا ِف ٍق‬ ْ ُّ َّ ْ ‫الصل ِب َوالت َرا ِئ ِب‬ ‫َيخ ُر ُج ِم ْن َب ْي ِن‬ “Basi naatazame mtu ameumbwa kwa kitu gani. Ameumbwa kwa maji yanayotoka kwa kuchupa. Yanayotoka baina ya uti wa mgongo na kifua.”31

TIBA KATIKA UISLAMU Katika kitabu Ayatul-Ahkam cha Jazairiy kuna maelezo kwamba: Imeelezwa kwamba Rashid alikuwa ana mganga nguli Mnaswara, ndipo siku moja akamwambia Ali bin Husein bin Waqid: “Hakuna chochote ndani ya kitabu chenu kinachohusiana na elimu   Sura 80 aya 24-32.   Sura 95 aya 1-3. 31   Sura 86 aya 5-7. 29 30

23

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 23

8/10/2017 1:21:58 PM


TIBA YA MAASUMINA

ya tiba! Na hakika elimu zipo za aina mbili: Elimu za dini na elimu za miili!” Ali akamwambia yeye: “Hakika Mwenyezi Mungu amekusanya tiba zote katika nusu ya Aya kutoka ndani ya Kitabu Chake, anasema: ‘Na kuleni (vizuri) na kunyweni (vizuri) na wala msipite kiasi.’32 Na akaikusanya Nabii wetu Muhammad (s.a.w.w) katika maneno yake pale aliposema: ‘Mfuko wa chakula ni nyumba ya ugonjwa, lishe kamili ni kichwa cha kila dawa, na upe mwili kile ulichokizoea.’” Basi hapo yule mganga akasema: “Hakika kitabu chenu na Nabii wenu hawajamuachia chochote Galenos katika tiba.”

VIPIMO VYA TIBA ZA KALE Gramu: Rita 408 ni sawa na wakia 12. 10.

Wakia 34 ni sawa na mithqal saba, ambazo ni sawa na Dirham Mithqal 4.8 ni sawa na karati 24. Dirham 3.4 ni sawa na Mithqal 7/10. Karati za Kiarabu 0.2 ni sawa na punje nne za ngano. Punje 0,50 ni sawa na gramu 1/20.

Rejea: Jarida la Majmaul-Lughatil-Arabiyyat, Damascus – mjaladi wa 61, Juz. 1, uk. 3 – vipimo vya tiba kwa kalamu ya Dr. Mukhtar Hashim.

32

Sura 7, aya 31. 24

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 24

8/10/2017 1:21:58 PM


TIBA YA MAASUMINA

FURUNGU Maelezo yake: Nalo ni tunda linalofanana na chungwa. Hakika umepokewa utajo wake ndani ya Qur’ani kwa jina la ‘matakia’ katika Sura Yusuf (a.s):

َ َ َ َ َ َ​َ ُ َ ًَ ْ ‫فل َّما َس ِم َع ْت ِب َمك ِر ِه َّن أ ْر َسل ْت ِإل ْي ِه َّن َوأ ْع َت َد ْت ل ُه َّن ُم َّتكأ َوآت ْت ك َّل َو ِاح َد ٍة ِم ْن ُه َّن‬ َّ َ َ َ ْ ُ َ َّ ُ َ ْ َ َ ْ َّ َ َ ُ َ ْ َ ْ َ ُ َ ْ َ َ َّ َ َ َّ ْ َ َ ْ ُ ْ َ َ َ ً ّ ‫اش ِلل ِه‬ ‫ِس ِكينا وقال ِت اخرج علي ِهن ۖ فلما رأينه أكبرنه وقطعن أي ِديهن وقلن ح‬ ٌ ‫َما َٰه َذا َب َش ًرا إ ْن َٰه َذا إ اَّل َم َل ٌك َكر‬ ‫يم‬ ِ ِ ِ “Aliposikia vitimbi vyao. Aliwaita na akawawekea matakia, na akampa kila mmoja wao kisu. Akasema: Tokeza mbele yao. Walipomuona wakaona ni kitu kikubwa na wakakata mikono yao. Na wakasema: Hasha lillahi! Huyu si mtu, hakuwa huyu ila ni Malaika mtukufu.”33

Na mshairi mmoja kuhusu hilo amesema: Kana kwamba nyinyi ni mfurungu, ni mzuri kwa kubeba na kwa maua. Na ni mzuri kwa matawi na majani. Na zimepokewa hadithi mbalimbali kwamba tunda hilo huliwa kabla na baada ya chakula, lakini kula baada ya chakula kuna manufaa zaidi.

33

Sura 12, aya 31. 25

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 25

8/10/2017 1:21:58 PM


TIBA YA MAASUMINA

Hadithi: Mtume (s.a.w.w) amesema: “Mfano wa muumini ambaye anasoma Qur’ani ni kama vile furungu, ladha yake ni nzuri na harufu yake ni nzuri.”34 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Ni juu yenu kula tunda la furungu, kwani hilo linatia nuru vifua, na huzidisha nguvu katika ubongo.”35 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Kuleni furungu kabla na baada ya chalula, hakika Aali Muhammad (s.a.w.w) wanafanya hivyo.”36 Imepokewa kutoka kwa Imam al-Baqir (a.s) kuwa amesema: “Hakika furungu ni zito, basi likiliwa ni mkate ndio utakaoliyayusha katika mfuko wa chakula [yaani mtu akila furungu na likamdhiki kutokana na wingi wake, basi ale kipande cha mkate mkavu.]”37 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kwamba aliwaambia wafuasi wake: “Ni kitu gani ambacho wanakuamrisheni waganga wenu kuhusiana na furungu?” Wakasema: Wanatuamrisha kula kabla ya chakula. Akasema (as): “Hakuna kitu ambacho ni kizuri kama vile kulila kabla ya chakula, na hakuna kitu chenye manufaa zaidi kama vile kulila baada ya chakula. Basi ni juu yenu kulila, hakika lina harufu nzuri ndani yake kama vile harufu ya miski.”38 Imepokewa kutoka kwa Ibrahim bin Umar Samnani, amesema: Nilisema kumwambia Abu Abdillah as-Sadiq (a.s): Hakika watu wanadai kuwa ulaji wa furungu kabla ya kula kitu chochote ni mzuri   Twibbu Nabawy cha ibn Qaym Jawziyyat, uk. 218.   Biharul-Anwar, Juz. 62, uk. 297 kutokana na tiba ya Mtume (s.a.w.w) cha Allamah Majlisi. 36   Wasaail Shi’ah, Juz. 17, uk. 136 kutoka kitabu Furuu Kaafi wal-Mahaasin cha Barqi. 37   Wasaail Shi’ah, Juz. 17, uk. 20 cha Hurr Aamiliy. 38   Twibbul-Aimmat, uk. 135 cha Ibnay Bisatwam Naysabuurayn. 34 35

26

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 26

8/10/2017 1:21:58 PM


TIBA YA MAASUMINA

zaidi. Basi akasema (a.s): “Ikiwa litaliwa kabla ya chakula ni bora, na baada ya chakula ni bora zaidi.”39 Imepokewa kutoka kwa Ja’fari kutoka kwa Imam Kadhim (a.s), alisema: “Ni kitu gani ambacho wanaamrisha waganga wenu kuhusiana na furungu?” Nikasema: Wanatuamrisha sisi kula kabla ya chakula. Akasema: “Lakini ninawaamrisheni kulila baada ya chakula.”40 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kuwa alisema: “Hakika Mtume (s.a.w.w) alikuwa akipenda zaidi kuangalia tunda la furungu la rangi ya kijani, pia tufaha la rangi nyekundu.”41

WANJA WA ANTIMONI Maelezo yake: Nalo ni jiwe jeusi la wanja, hupatikana katika mji wa Isfahan, Iran. Na lililo zuri zaidi ni lile lililo jepesi zaidi kuvunjika, ambalo humeremeta kutokana na uvunjikaji wake, na linang’aa zaidi ndani bila kuwa na uchafu. Sifa zake ni mchanganyiko wenye baridi kavu. Faida yake: Unalisaidia jicho na kulitia nguvu na kuimarisha mishipa yake na kuhifadhi afya yake. Husafisha uchafu wa jicho na kuliweka katika hali nzuri zaidi. Huondoa maumivu ya kichwa pindi mtu anapojipaka wanja huo kwa kuchanganya na asali nyepesi ya majimaji (nyuki wadodo).   al-Kaafi cha Allamah Kulayni…   Wasaail Shi’ah, Juz. 17, uk. 136 kutoka kwa kitabu Furuu Kaafi na Mahasin cha Barqi. 41   Wasaail Shi’ah, Juz. 17, uk. 136 kutoka katika kitabu Furuu Kaafi na Mahasin cha Barqi. 39 40

27

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 27

8/10/2017 1:21:58 PM


TIBA YA MAASUMINA

Hadithi: Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Ni juu yenu kujipaka wanja kwani huleta harufu nzuri ya kinywa, na ni juu yenu kupiga mswaki kwani kufanya hivyo kunaimarisha nguvu ya macho.” Mpokezi wa hadithi hii anasema: Nikasema: Inakuwaje hili? Akasema (as): “Mtu anapopiga mswaki kikohozi huteremka na hivyo huimarisha nguvu ya macho. Na anapojipaka wanja kikohozi huondoka na hivyo husafisha kinywa.”42 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kuwa alisema: “Ni juu yako kujipaka wanja, kwani unang’arisha macho, na unaotesha taraza, na unaongeza nguvu wakati wa tendo la ndoa.”43

PEASI Faida zake: Ni miongoni mwa matunda maarufu. Na tunda hili hutumiwa katika tiba ili kuponya shinikizo la damu litokanalo na umri mkubwa (50 -60), au litokanalo na yabisi ya mishipa inayopokea damu, au litokanalo na maradhi ya figo.44 Hadithi: Mtume (s.a.w.w) amesema: “Zabibu inaondoa homa, na peasi linasafisha moyo.”45 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Peasi linasafisha moyo, na linatuliza maumivu ya tumbo kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (a.s).”46   Makarimul-Akhlaq, uk. 47.   Makarimul-Akhlaq, uk. 46. 44   Tadaawy bil-Aashaab, uk. 260 cha Dr. Amiin Rawayhat. 45   Ramzu Swihhat, uk. 15 cha Dahsarkhiy. 46   Makarimul-Akhlaq, uk.175 cha Twabarsi. 42 43

28

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 28

8/10/2017 1:21:58 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Jabir amesema: Mtu mmoja alimlalamikia Abu Ja’far Imam al-Baqir (a.s) maumivu yaliyomshika kiasi cha kutaka kuchanganyikiwa. Basi akamwambia (a.s): “Yatulize kwa peasi.”47 Imepokewa kutoka kwa Azraq bin Sulaiman, amesema: Nilimuuliza Abu Abdillah as-Sadiq (a.s) kuhusiana na peasi, Akasema (a.s): “Ni lenye kufaa kwa nyongo, na hulainisha sehemu za maungio. Basi usizidishe, utapatwa na upepo katika maungio.”48 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Kitu cha kwanza alichokula Nabii Adam pindi aliposhuka ardhini ni peasi.”49 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Peasi linalainisha mfuko wa chakula, na linautia nguvu, nalo pamoja na pera la rangi nyeusi ni sawa sawa. Nalo likiliwa baada ya kushiba lina manufaa zaidi kuliko asubuhi kabla ya kula chochote.”50 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Kula Peasi kabla ya kula chochote kunatuliza nyongo, isipokuwa ni kwamba kufanya hivyo kunachochea riahi.”51 Imepokewa kutoka kwa Ziyad Qundi, amesema: Niliingia kwa Imam Ridha (a.s) wakati mbele yake kulikuwa na chombo kidogo, na ndani yake kuna peasi jeusi, akasema: “Hakika hilo linachochea joto, na ninaona peasi linapunguza joto, na linatuliza manjano. Na hakika yabisi itokayo humo inaiweka barabara damu, na inaondoa ugonjwa angamizi kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.”52   Twibbul-Aimmat, uk. 136.   Twibbul-Aimmat, uk. 136. 49   Ranzul-Swihat, uk. 15, cha Duhsarkhi. 50   Wasail Shii’a, Juz. 17, uk. 134. 51   Twibbul-Aimmat, uk. 136. 52   Wasail Shii’a, Juz. 17, uk. 137, kutoka katika kitabu Furuu Kaafi. 47 48

29

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 29

8/10/2017 1:21:58 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwao (a.s) kuwa walisema: “Ni juu yenu kula peasi la kale, hakika manufaa ya ukongwe yangalipo na madhara yake yametoweka. Kuleni likiwa limemenywa maganda yake, kwani lina manufaa kwa kila nyongo na joto na moto unaojitokeza mwilini.”53

SIKIO Mtume (s.a.w.w) amesema: “Sadhabu (ni aina ya mtishamba) ni nzuri kwa ugonjwa wa sikio.”54 Dawa ya maumivu ya sikio: Itachukuliwa gao moja la ulezi usiokobolewa, na gao moja la khardali, zinasagwa kila moja pekee, kisha vinachanganywa pamoja, na yanatolewa mafuta yake na kuwekwa ndani ya chupa ya kioo, na hufunikwa kwa kizibo cha chuma. Unapotaka kutumia basi utadondoshea sikioni matone mawili, na ziba kwa pamba kwa muda wa siku tatu, kwani litapona kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (s.w.t). Mtu mmoja miongoni mwa mawalii alimlalamikia mmoja wa maasumu (a.s) maumivu ya sikio na utokaji usaha na damu, akamwambia: “Chukua jibini ya kale, isage vizuri mpaka ilainike, kisha ichanganye kwa maziwa ya mwanamke, na ichemshe kwa moto hafifu, kisha dondoshea matone katika sikio ambalo linatoa damu, kwani hilo hupona kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (s.w.t).”55 Dawa ya sikio utakapoitwanga: Utachukua Sadhabu na kuipika kwa mafuta ya kula, na dondoshea ndani yake matone kadhaa, kwani hiyo hutuliza maumivu kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (s.w.t).56   Twibbul-Aimmat, uk. 136.   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 144, kutoka katika kitabu Mahasin. 55   Twibbul-Aimmat, uk. 72. 56   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 145, kutoka katika kitabu Twibbul-Aimmat. 53 54

30

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 30

8/10/2017 1:21:58 PM


TIBA YA MAASUMINA

MCHELE Mtume (s.a.w.w) amesema: “Bwana wa chakula cha duniani na akhera ni nyama, na kisha mchele.” Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Chakula bora ni wali, na sisi tunautumia huo kwa wagonjwa wetu.” Imepokewa kutoka kwa Zurarat amesema: Abu Abdillah (a.s) alisema: “Chakula bora ni wali, hupanua utumbo na hukata bawasiri. Na hakika sisi tunaomba tuwe kama watu wa Iraq kwa kula kwao wali na tende inayokaribia kuiva, hakika hivyo viwili vinapanua utumbo, na hukata bawasiri.”57 Imepokewa kutoka kwa Yunus bin Yakub amesema: Abu Abdillah (a.s) alisema: “Hakitujii sisi kitu kutoka kwenu kilicho bora zaidi kuliko mchele na urujuani. Hakika mimi nilisumbuliwa na maumivu makali basi nikapata ilhamu ya kula mchele, nikaamrisha uletwe, basi ukaoshwa na kukaushwa kisha ukakaangwa na kusagwa, basi nikatengenezewa chakula cha unga huo kwa mafuta ya kula, pamoja na supu, basi Mwenyezi Mungu akaniondolea maumivu.”58 Imepokewa kutoka kwa Mufadhal bin Umar, amesema: Niliingia wakati wa chakula cha mchana kwa Imam as-Sadiq (a.s), naye alikuwa katika meza ya chakula, basi akasema: “Ewe Mufadhal njoo tule.” Nikasema: Ewe bwana wangu! Hakika nimeshakula chakula cha mchana. Imam (as) akasema: “Fahamu hakika huu ni wali.” Nikasema: Ewe bwana wangu hakika nimeshakula. Basi akasema (a.s): “Njoo nikusimulie wewe hadithi.” Nikakaribia kwake na nikaketi, basi akasema (a.s): “Amenisimulia baba yangu kutoka kwa baba zake, imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Punje ya kwanza ambayo ilikiri upweke wa Mwenyezi Mungu kwa 57 58

Wasail Shii’a, Juz. 17, uk. 95, kutoka kitabu Furuu Kaafi na Mahasin cha Barqi.   Wasail Shii’a, Juz. 17, uk. 95, kutoka katika kitabu Furuu Kaafi na Mahasin cha Barqi. 31

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 31

8/10/2017 1:21:58 PM


TIBA YA MAASUMINA

Mwenyezi Mungu (s.w.t), na ilikiri utume kwangu mimi, na ilikiri uwasii kwa ndugu yangu Ali, na ilikiri pepo kwa umma wangu, ni mchele.” Kisha akasema: “Endelea kula ili nikuongezee elimu.” Basi nikaendelea kula, akasema (a.s): “Amenihadithia baba yangu kutoka kwa baba zake kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Kila kitu kitokacho ardhini ni ugonjwa na ponyo, ila mchele kwani ni ponyo wala hauna ugonjwa ndani yake.” Kisha akasema (a.s): “Endelea kula ili nikuongezee elimu.” Nikaendelea kula, akasema: “Amenisimulia baba yangu kutoka kwa baba zake kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: ‘Lau kama mchele ungelikuwa ni mtu basi angelikuwa ni mpole mno.’” Kisha akasema (a.s): “Endelea kula ili nikuongezee elimu.” Nikaendelea kula, akasema: “Amenisimulia baba yangu kutoka kwa baba zake kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: ‘Wali humshibisha mwenye njaa na kumpa raha mwenye shibe.’”59 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Dawa bora ni wali, ni baridi sahihi, ni salama kutokana na kila ugonjwa.”60

MKATE WA MCHELE Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Walisheni wenye maumivu ya tumbo mkate wa mchele, hakuna kitu chenye manufaa zaidi tumboni mwa mwenye kichochokojo au kuhara kushinda chakula hicho. Hulainisha mfuko wa chakula, na huondosha ugonjwa kabisa.”61   Biharul-Anwaar, Juz. 66, uk. 261.   Makarimul-Akhlaq, uk. 155. 61   Wasail Shii’a, Juz. 17, uk. 5. 59 60

32

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 32

8/10/2017 1:21:58 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kuwa alisema: “Hakuna kitu chenye kubakia tumboni kuanzia mchana mpaka usiku, ila mkate wa mchele.”62 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kuwa alisema: “Hakijaingia ndani ya tumbo la mwenye kuhara kitu chenye manufaa zaidi kuliko mkate wa mchele.”63

KUHARA Imepokewa kutoka kwa Ibn Kathir kuwa alisema: Tumbo langu lilinisumbua kwa kuhara, basi Imam as-Sadiq (a.s) akaniamrisha ninywe uji wa shairi kwa maji ya komoni.” Basi nikafanya hivyo ukazuia tumbo langu na nikapona.”64

ISHNAAN HYSSOPUS Maelezo yake: Ni mmea mdogo wa kichakani ambao huota katika ardhi ya mchanga. Faida zake: Mmea huu au majivu yake hutumiwa katika kufulia nguo au kuoshea mikono.65 Na hakika ametaja mmoja wao kwamba mwanamke mmoja katika mji wa Rahibat alikunywa mmea huu ili kuharibu mimba, basi ukaanguka ujauzito wake. Na huenda hili lilitokana na yale   Wasail Shii’a, Juz. 17, uk. 5, kutoka katika kitabu Furuu Kaafi Juz. 6, uk. 305.   Wasail Shii’a, Juz. 17, uk. 5. 64   Wasail Shii’a, Juz. 17, uk. 101, kutoka katika kitabu Furuu Kaafi. 65  Muujamul-Wasiit. 62 63

33

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 33

8/10/2017 1:21:58 PM


TIBA YA MAASUMINA

y­ aliyoelezwa na hadithi ifuatayo ambapo inasema: “Huharibu maji ya mgongo.” Basi Ishnaan (Hyssopus) huharibu maji ya mwanaume na maji ya mwanamke katika hali sawa, na huharibu ujauzito. Hadithi: Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Kula Ishnaan hudhoofisha magoti na huharibu maji ya mgongo.”66

ULAJI WA WASTANI Baadhi ya wenye busara wamesema: Haimpasi mtu mwenye akili kuiacha bure nafsi yake bila mambo matatu katika hali ya kutokupitisha kiwango: Kula na kutembea na kufanya tendo la ndoa. Ama kula, hakila mfuko wa chakula hubana kwa kuacha kula. Na ama kutembea, hakika asiyejizoeza kutembea utafika wakati atataka kutembea lakini hatoweza. Na ama tendo la ndoa, ni kama vile kisima, kadiri uchotavyo ndivyo maji yake huongezeka, na akiacha maji yake huwa mazito. Na haki ya haya yote ni kuyafanya kwa wastani bila kufurutu.67 Wosia unaohusu afya: Ibn Sina (Avisena) (na inasemekana ni Abu Muayyad Jazri) alisema: “Sikilizeni nyote wosia wangu na utendeeni kazi. Tiba imekusanyika katika mpangilio wa maneno yangu. Punguza kufanya tendo la ndoa kadiri utakavyoweza, hakika hayo ni maji ya uhai ambayo humwagiwa kwenye mfuko wa uzazi. Na fanya chakula chako kila siku ni mara moja, na jihadhari kula chakula kabla ya mmeng’enyo wa chakula. Usidharua maradhi madogo kwani hayo ni kama vile moto mdogo, huwa mkubwa na wenye kuchoma.” 66 67

Khaswail, Juz. 1, uk. 63 cha Saduuq.   Aqdul-Fariid cha ibn Umar Ahmad bin Muhammad bin Abdu Rabbih Andolusi amekufa mwaka 328 H, amekifanyia uhakiki Muhammad bin Said Uryan, maktabatu Tijariyyatulkubra, chapa ya pili, mwaka 1953 juz.7 uk. 263. 34

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 34

8/10/2017 1:21:58 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Isa bin Maryam (a.s) kwamba, siku moja alisimama akahutubia, akasema: “Enyi wana wa Israil, msile mpaka muwe na njaa, mnapokuwa na njaa kuleni wala msishibe. Hakika nyinyi mkishiba zitanenepa shingo zenu na mbavu zenu, na mtamsahau Mola Wenu Mlezi.”68 Mtume (s.a.w.w) amesema: “Usile ambacho umejua madhara yake, wala usitangulize matamanio yako juu ya raha ya mwili wako. Na lishe kamili ni kuwa na wastani katika kila kitu. Na asili ya tiba ya pumu ni kuthibiti midomo miwili kwa mikono miwili. Na ugonjwa wenye kuangamiza ni kuongeza chakula juu ya chakula. Jiepushe na dawa unapokuwa na afya njema, na unapohisi uwepo wa ugonjwa basi uangamize kwa yale ambayo yatauzuia kabla ya kutumia dawa.”69 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Sisi ni watu ambao hatuli mpaka tuwe na njaa, na tukila hatushibi [yaani tunainuka na kuacha kula kabla hatujashiba].” Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Kunyweni na kuleni kwa wastani wa matumbo yenu, kwani kufanya hivyo ni sehemu ya unabii.”70 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Binadamu hakujaza chombo shari kushinda anavyojaza tumbo lake. Yamtosha binadamu matonge yanayoimarisha mgongo wake, na ikiwa atalazimika kula; basi theluthi yake iwe ni chakula, na theluthi nyingine kinywaji chake, na theluthi nyingine pumzi yake.”71   Wasail Shii’a, Juz. 16, uk. 410.   Biharul-Anwaar, Juz. 59, uk. 269. 70   Jaamiul-Saadat, Juz. 2, uk. 7. 71   Twibbu Nabawiy, uk. 12 cha ibn Qaym Jawziyyat. 68 69

35

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 35

8/10/2017 1:21:58 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Yule anayeshiba hujiadhibu adhabu tatu; huweka kifuniko juu ya moyo wake, kusinzia kwa macho yake na uvivu juu ya mwili wake.”72 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Kukithirisha kula kunaua moyo, kama vile ukithirishaji wa maji unavyoua mazao.”73 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Yule anayekula chakula safi, na akatafuna chakula vizuri, na akaacha chakula ilhali anakitamani, na hakuzuia haja kubwa ikimjia, hatougua ila maradhi ya kifo.”74 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Usiutafute uhai ili ule, bali tafuta kula ili uishi.”75 Asbagh bin Nabat amesema: Nilimsikia Amirul-Muuminina (a.s) akimwambia mwanawe Hasan (a.s): “Ewe mwanangu! Je, nikujuze maneno manne ambayo utatosheka nayo bila kuhitajia matibabu?” Basi akasema: Ndiyo, ewe kiongozi wa waumini. Akasema (a.s): “Usikae kwenye meza ya chakula ila ukiwa na njaa. Acha kula ilhali wewe unakitamani, na tafuna vizuri, na kabla ya kulala nenda msalani; basi ukifanya haya hutahitajia matibabu.”76 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa amesema: “Usiinue mkono wako kutoka kwenye chakula ila wewe ukiwa unakitamani, na ukifanya hivyo unakiwezesha kisagike vizuri.”77 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Watu wanazidhuru nafsi zao kwa vitu vitatu; kuzidisha kula kwa kutegemea   Hikmat no. 674, Sharh Nahajul-Balaghah cha ibn Hadiid.   Hikmat no. 723, Sharh Nahajul-Balaghah cha ibn Hadiid. 74   Makarimul-Akhlaq, uk. 146. 75   Hikmat no. 824, Sharh Nahajul-Balaghah cha ibn Hadiid. 76   Khiswaal, Juz. 1, uk. 269 cha Saduuq. 77   Biharul-Anwaar, Juz. 77, uk. 268. 72 73

36

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 36

8/10/2017 1:21:59 PM


TIBA YA MAASUMINA

afya. Na kujikalifisha kubeba zaidi ya uwezo wao kwa kutegemea nguvu. Na kuzidisha kufanya amali fulani kwa kutegemea uwezo wao.”78 Na imepokewa kutoka kwake (a.s) kuwa alisema: “Yule anayetaka kubakia wala hakuna ubakiaji kama huo; basi na ale chakula cha mchana mapema, na acheleweshe kula chakula cha usiku (na katika hadithi nyingine: Na avae viatu vizuri) na apunguze kufanya tendo la ndoa, na afanye tahfifu kuchukua deni.”79 Imepokewa kutoka kwa Imam al-Baqir (a.s) kuwa alisema: “Yule anayetaka asidhurike na chakula, asile isipokuwa awapo na njaa na uwapo safi mfuko wake wa chakula; basi akila aseme Bismillah, na atafune vizuri, na aache kula ilihali anakitamani chakula hicho.”80 Imepokewa kwamba siku moja mganga mmoja mnaswara aliingia kwa Imam as-Sadiq (a.s), akamwambia: Ewe mtoto wa Mtume (s.a.w.w) je, ipo tiba katika kitabu cha Mola wenu mlezi au katika sunna ya Nabii wenu? Akasema: “Ndiyo, ama ndani ya kitabu cha Mola wetu Mlezi ni kauli yake (s.w.t): ‘Kuleni na kunyweni wala msipitishe kiasi.’ Na ama katika sunna ya Nabii wetu amesema: ‘Wastani katika kula ni chanzo cha kila dawa, na upitaji kiasi katika kula ni kiini cha kila ugonjwa.” Basi akasimama yule mnaswara huku akisema: “Naapa kwa Mwenyezi Mungu hakikuacha kitu kitabu chenu wala sunna ya Nabii wenu katika tiba ya Galenosi.”81 Na imeelezwa kwamba Rashid alikuwa na mganga nguli wa kinaswara. Siku moja akamwambia Ali bin Husein bin Waqid: “Hakuna ndani ya kitabu chenu chochote kuhusiana na suala la tiba, na elimu ni mbili; elimu ya dini na elimu ya miili.” Basi Ali akamwam  Hikmat no. 70, Sharh Nahajul-Balaghah cha ibn Hadiid.   Biharul-Anwaar, Juz. 59 uk. 267, kutoka katika maombi ya Qutbu Diin Raawandiy. 80   Wasaail Shi’ah juz. 16 uk. 540, kutoka kitabu Twibbul-Aimmat. 81   Al-Anwaarul-Nuumaniyat, Juz. 4, uk. 163 cha Neematullah Jazaairy, Taasisi ya Aalamy. 78 79

37

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 37

8/10/2017 1:21:59 PM


TIBA YA MAASUMINA

bia yeye: “Hakika Mwenyezi Mungu amekusanya tiba yote katika nusu aya ndani ya Kitabu chake, nayo ni kauli yake (s.w.t) inayosema: ‘Na kuleni na kunyweni wala msipitilize kiasi.’ Na Nabii wetu amekusanya katika kauli yake pale aliposema: ‘Mfuko wa chakula ni nyumba ya ugonjwa, na wastani katika chakula ni chanzo cha kila tiba, na upe mwili kile ulichozoea.’” Basi mganga akasema: “Hakikuacha kitu Kitabu chenu wala sunna ya Nabii wenu katika tiba ya Galenosi.”82 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema kuwa: “Hapana budi kwa binadamu kula chakula kinachoimarisha uti wake wa mgongo, na anapokula mmoja wenu chakula, basi aache theluthi ya tumbo lake kwa ajili ya chakula, na theluthi ya tumbo lake ni kwa ajili ya maji na theluthi ya tumbo lake ni kwa ajili ya kupumua. Wala msinenepe unenepaji wa nguruwe kwa ajili ya kuchinjwa.”83 Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Lau watu watakuwa na wastani katika kula, basi miili yenu ingelikuwa sawa sawa.”84 Imam Kadhim (a.s) kuhusiana na matumizi ya dawa amesema: “Hakuna dawa yoyote ila inachochea ugonjwa, na hakuna kitu chenye manufaa zaidi na mwili kuliko kuwa na wastani katika chakula, asile ila pale ambapo ana haja nacho.”85 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Hakuna kitu kinachomchukiza zaidi Mwenyezi Mungu kuliko tumbo lililojaa.”86 Imam Ridha (a.s) katika barua yake ya dhahabu aliyomwandikia Maamuni alisema: “Na yule ambaye atakula chakula zaidi hakitom  Aayatul-Ahkaam cha Jazairy.   Wasail Shii’a, Juz. 16, uk. 406, kutoka katika kitabu Mahasin cha Barqi. 84   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 266. 85   Rawdhatul-Kaafi, uk. 273 cha Kulayni. 86   Sahifatul-Ridha (a.s) uk. 54. 82 83

38

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 38

8/10/2017 1:21:59 PM


TIBA YA MAASUMINA

nufaisha yeye bali kitamdhuru, na atakayekula kwa wastani si kwa kuzidisha wala kupunguza katika chakula chake, basi kitamnufaisha. Vivyo hivyo katika maji, chukua chakula kile kinachokutosha kwa siku zako, na ondoa mkono wako ilhali una hamu na unakitamani chakula, na wewe unavutiwa nacho, kwani hilo lina maslahi zaidi kwa mfuko wa chakula na mwili wako, na ni usafi zaidi wa akili yako, na wepesi mno wa kiwiliwili chako.”87 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Usiliache tumbo lako bila chakula, na punguza unywaji wa maji, wala usijamiiane ila unapokuwa na hamu na tendo hilo, na mboga bora ni mchadi.”88 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa amesema: “Chakula cha usiku cha Manabii ni baada ya giza, wala msiache chakula cha usiku, ikiwa utakiacha huharibu mwili.”89

ADABU ZA KULA: Mtume (s.a.w.w) amesema: “Yule anayekuta tonge na akaliokota na akalifuta vizuri, na akaliosha hilo vizuri, halitatulia tumboni mwake mpaka Mwenyezi Mungu amwache huru yeye na moto.”90 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa amesema: “Ewe Ali hakika kutia wudhuu kabla na baada ya kula, ni ponyo katika mwili, na huongeza riziki.”91 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa amesema: “Kula sokoni ni kujishusha hadhi.”92   Baharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 311.   Makarimul-Akhlaq, uk. 181. 89   Tuhful-Uquul, uk. 78. 90   Biharul-Anwaar, Juz. 66, uk. 431. 91   Wasail-Shii’a, Juz. 16, uk. 472. 92   Makarimul-Akhlaq uk. 149. 87 88

39

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 39

8/10/2017 1:21:59 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa amesema: “Baraka ipo katikati ya chakula, basi kuleni pembezoni mwake, wala msile katikati yake.”93 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (as) kuwa amesema: “Kuosha mikono miwili kabla na baada ya kula, huongeza riziki, na husafisha macho, na huondoa ufukara.”94 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa amesema: “Yule anayeosha mkono wake kabla na baada ya kula, atabarikiwa yeye mwanzo wa kula na mwisho wake, na ataishi katika hali ya wasaa, na ataponywa kutokana na balaa mwilini mwake.”95 Imepokewa kutoka kwa Imam Hasan (a.s) kuwa alisema: “Katika meza ya chakula kuna mambo kumi na mbili ambayo ni wajibu kwa mwislamu kuyajua; manne ni ya faradhi, na manne ni ya sunna, na manne ni ya adabu… na ama ya adabu ni: Kula mbele yako, kumega tonge dogo, kutafuna vizuri na kupunguza kuangalia watu usoni.”96 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa amesema: “Usile hali ya kuwa wewe unatembea, ila ukidharurika kufanya hivyo.”97 Imepokewa kutoka kwa Umar bin Abi Shuubat kuwa amesema: “Sikuwahi kumuona Abu Abdillah (a.s) akila hali ya kuwa ameegemea kitu.” Kisha akamtaja Mtume (s.a.w.w) akasema: “Asilani Mtume hakuwahi kula hali ya kuwa ameegemea kitu mpaka amefariki.”98   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 291.   Khiswalu, Juz. 1, uk. 612 cha Saduuq. 95   Biharul-Anwaar, Juz. 66, uk. 364. 96   Makarimul-Akhlaq, uk. 141, kutoka katika kitabu Man la Yahdhuruhu Faqiih. 97   Biharul-Anwaar, Juz. 66, uk. 388, kutoka kitabu Al-Uyuunu wal-Mahasin, Juz. 2, uk. 459. 98   Makarimul Akhlaq, uk. 146. 93 94

40

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 40

8/10/2017 1:21:59 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa amesema: “Usile ukiwa umeegemea kitu fulani, na ukiwa katika hali ya kifudifudi basi hali hiyo ni mbaya zaidi kuliko kuegemea kitu.”99 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa amesema: “Refusheni kukaa katika meza (sehemu) za chakula, kwani huo ni muda ambao hauhesabiwi katika umri wenu.”100 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kuwa amesema: “Unapokula basi egemea ubavu wako wa kushoto, ukiweka mguu wako wa kulia juu ya mguu wako wa kushoto.”101 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) katika barua yake ya dhahabu kwenda kwa Maamuni, kuwa alisema: “Na anza na chakula kile kilicho chepesi zaidi ambacho mwili wako utakula utakiweza, kwa kiwango cha kawaida yako, na kulingana na uwezo wako na uchangamfu wako na wakati wako.”102

KUSEMA BISMILLAHI KABLA YA KULA Mtume (s.a.w.w) amesema: “Semeni Bismillahi mnapoanza kula, na shukuruni pale mnapomaliza kula.”103 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa amesema: “Pambeni meza ya chakula kwa mbogamboga pamoja na kusema Bismillahi, kwani kusema hayo kunafukuza mashetani.”104 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Sijawahi katu kulinenepesha tumbo langu.” Akaulizwa; Kwa nini? Akasema:   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 388.   Makarimul-Akhlaq, uk. 141. 101   Makarimul-Akhlaq, uk. 147. 102   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 311. 103   Aqdul-Fariid, Juz. 8, uk. 8. 104   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 300. 99

100

41

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 41

8/10/2017 1:21:59 PM


TIBA YA MAASUMINA

“Sijawahi kuinua mkono wangu kumega tonge ila nilisema Bismillah kabla.”105 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Ewe Kumail! Unapokula chakula basi sema Bismillahi, kwa jina la Mwenyezi Mungu ambaye kwa jina hilo hakuna maradhi yanayodhuru, na ndani yake ipo tiba ya kila maradhi.”106 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Mimi ni mdhamini wake, yule ambaye anasema Bismillahi katika chakula chake, kwamba kwa hakika hatosumbuliwa na lolote.” Ibn Kuwaa alisema kumwambia yeye: “Ewe Amirul-Muuminina, jana nilipokula chakula nilisema Bismillahi na kikanipa maudhi.” Akasema (a.s): “Huenda ulikula aina mbalimbali ya vyakula, basi ukasema Bismillahi juu ya baadhi na hukusema juu ya vingine, ewe mpumbavu.”107 Na katika hadithi nyingine imekuja: Basi yule mtu akacheka na akasema: Umesema kweli ewe Amirul-Muuminina. Basi akasema (as): “Hakika hilo ni kutokana na kutosema Bismillahi ewe mpumbavu.”108

KULA PUNJE ZILIZODONDOKA CHINI Mtume (s.a.w.w) alimuona Abu Ayub Answariy (r.a) akiokota punje zilizodondoka juu ya meza ya chakula. Akasema (s.a.w.w): “Umebarikiwa wewe, umebarikiwa juu yako, na umebarikiwa ndani yako…” kisha akasema: “Yule atakayefanya hivyo Mwenyezi Mun  Safinatul-Bihar, Juz. 1, uk. 25.   Tuhful-Uquul cha ibn Shu’ba Harrani. 107   Mustadrak uk. 170. 108   Twibbul-Aimmat, uk. 60. 105 106

42

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 42

8/10/2017 1:21:59 PM


TIBA YA MAASUMINA

gu atamkinga na uwendawazimu, ukoma, mbalanga, manjano na upumbavu.”109 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kwamba alimwambia Ali (a.s): “Kula kilichodondoka chini ya meza yako ya chakula, hakika hilo linakuepusha wewe na ufukara, nayo ni mahari ya Hurulaini, na yule atakayekula utaingia moyo wake elimu, upole, imani na nuru.”110 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Utukuzeni mkate, hakika Mwenyezi Mungu alizitiisha mbingu na ardhi kwake, na kuleni kilichodondoka mezani.”111 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Yule anayekula kilichodondoka mezani ataishi maisha mazuri yenye riziki pana, na ataepushwa na haramu mtoto wake na mtoto wa mtoto wake, na imekuja katika hadithi nyingine: Ataponywa kutokana na ukoma.”112 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Kula kila kinachodondoka mezani, kwani ni ponyo la kila ugonjwa kwa yule anayetaka kuponywa.”113 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Kula kinachodondoka mezani huzidisha riziki.”114 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Kula kinachodondoka mezani, kwani ni ponyo ya kila ugonjwa, na imepokewa kuwa hilo huepusha ufukara, na huongeza watoto, na humchangamsha mwenye janaba.”115   Biharul-Anwaar, Juz. 66, uk. 431 na Makarimul-Akhlaq, uk. 145 cha Twabarasi.   Biharul-Anwaar, Juz. 66, uk. 431. 111   Aqdul-Fariid, Juz. 8, uk. 4. 112   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 292, na kutoka Firdausi. 113   Makarimul-Akhlaq, uk. 146. 114   Twibbul-Aimmat, uk. 147 cha Shubbar, kutoka katika Bihar. 115   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 280. 109 110

43

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 43

8/10/2017 1:21:59 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Abdillah bin Saleh Khushiami amesema: Nilimlalamikia Abu Abdillah (a.s) maumivu ya kitovuni, akasema: “Ni juu yako kula punje zidondokazo mezani.” Basi nikafanya hivyo maumivu yakaniondokea.116 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kuwa alisema: “Vile vinavyodondoka mezani ni mahari ya Hurulaini, basi kuleni.”117

KULA CHAKULA KICHACHE Aliulizwa mwenye hekima: Vipi unapata hekima? Akasema: Kwa kula chakula kichache. Na akaulizwa mfanya ibada: Ni upi uso wa ibada? Akasema: Kula chakula kichache. Akaulizwa yule mwenye kujinyima dunia: Vipi unaweza kujinyima? Akasema: Kwa kula chakula kichache. Akaulizwa msomi: Vipi unapata elimu? Akasema: Kwa kula chakula kichache. Akaulizwa mmoja wa wafalme: Kitu gani kinamfanya mfalme kuwa na adabu? Akasema: Kula chakula kichache. Akaulizwa mmoja wa madaktari: Vipi unapata afya? Akasema: Kwa kula chakula kichache. Luqman alimwambia mwanawe: Ewe mwanangu! Shibe inakuzuia wewe kuwa na mtazamo wa mbali na uzingatiaji, na inazuia ulimi wako kuwa na hekima, na inakutia uzito wa kufanya ibada.”118 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Vaeni, kuleni, na kunyweni kwa wastani wa matumbo yenu, kufanya hivyo ni sehemu ya unabii.”119   Kaafi, Juz. 6, uk. 300.   Sahifatul-Ridha (a.s), uk. 50. 118   Adabul-Nafsi, Juz. 1 uk. 189 cha Sayyid Muhammad Aynathiy. 119   Tanbihul-Khawatir, uk. 81. 116 117

44

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 44

8/10/2017 1:21:59 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Hakuna kitu kilichompendeza zaidi Mtume (s.a.w.w) kuliko hali ya kushinda na njaa akiwa mwenye hofu ya Mwenyezi Mungu.”120

KULA SANA NA KUVIMBIWA Wamesema: Ujaaji wa tumbo huondoa uerevu.121 Luqman alimwambia mwanawe: “Utakapojaza mfuko wa chakula fikra italala, hekima itakosekana na viungo vitabweteka na kuacha ibada.”122 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Yule anayejizoesha kukithirisha kula na kunywa, basi moyo wake huwa mgumu.”123 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Ole wenu na ufedhuli wa kula, kwani hutia sumu moyo kwa kusaza chakula, na huzuia polepole viungo kumtii Mwenyezi Mungu, na huzuia masikio kusikiliza mawaidha.”124 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Moyo huwa na uwezo wa kubeba hekima pindi tumbo linapokuwa tupu, na moyo hupoteza hekima pale ambapo tumbo linapokuwa limejaa.”125 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Yule anayekula kidogo mwili wake huwa na afya, na husafika moyo wake, na yule ambaye anakula zaidi mwili wake huugua, na moyo wake huwa mgumu.”126   Wasail-Shii’a, Juz. 16, uk. 408.   Aqdul-Fariid, Juz. 8, uk. 9. 122   Jaamius-Saadat, Juz. 2, uk. 5 cha Naraaqi. 123   Ramzul-Swihhat, uk. 9. 124   Biharul-Anwaar, Juz. 72, uk. 99. 125   Tanbiihul-Khawatir, Juz. 2, uk. 118. 126   Biharul-Anwar, Juz. 59, uk. 268. 120 121

45

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 45

8/10/2017 1:21:59 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Msiue mioyo yenu kwa kuzidisha kula na kunywa, hakika mioyo inakufa kama vile inavyokufa mimea pindi inapomwagiwa maji mengi.”127 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Binadamu hakujaza chombo shari kushinda anavyojaza tumbo lake. Yamtosha binadamu matonge yanayoimarisha mgongo wake, na ikiwa atalazimika kula; basi theluthi yake iwe ni chakula, na theluthi nyingine kinywaji chake, na theluthi nyingine pumzi yake.”128 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Ole wenu na vitambi, kwani huharibu mwili na huleta magonjwa, na huleta uvivu katika kutekeleza ibada.”129 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Mambo matano husababisha ukoma: … kula wakati bado una shibe.”130 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Hakuna afya pamoja na kuvimbiwa….”131 Imepokewa pia kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Kuzidisha kula na kulala vinaharibu nafsi, na vinaleta madhara.”132 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Yule anayekula sana afya yake huwa ndogo, na huzidi uzito juu ya nafsi yake katika mahitaji yake.”133 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Ole wako na ujazaji tumbo, basi yule anayelijaza huzidi magonjwa yake.”134   Makarimul-Akhlaq, uk. 150 cha Twabarasi.   Twibbu Nabawy, uk. 12 cha Ibn Qaym Jawziyat, kutoka kitabu Musnad Ahmad bin Hanbali, Sahihi Tarmidhi, Ibn Maaja na Hakim. 129   Biharul-Anwaar, Juz. 59, uk. 266. 130   Khiswalu, Juz. 1, uk. 270 cha Saduuq. 131   Biharul-Anwaar, Juz. 59, uk. 268. 132   Mustadrakul-Wasaail, Juz. 3, uk. 81. 133   Mustadrakul-Wasaail, Juz. 3, uk. 81. 134   Ghurarul-Hikam cha Amadiy. 127 128

46

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 46

8/10/2017 1:21:59 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Tumbo linapojaa kwa kitu cha halali moyo hupofuka kwa kutoyaona mema.”135 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Udumishaji wa shibe husababisha aina nyingi za magonjwa.”136 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Ole wenu na udumishaji wa shibe, kwani huchochea magonjwa na huamsha magonjwa.”137 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Hakuna uerevu hali ya kuwa tumbo limejaa.”138 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Ni mara ngapi vyakula vichache huzuia vyakula vingi.”139 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Sijaumbwa mimi ili kushughulishwa na vizuri, kama vile wanyama wafugwao ambao lengo lao ni nyasi, au kama wanyama huru ambao hima yao ni nyasi, na kufanya upuuzi kwa kucheza huku na kule……Na kana kwamba mimi nipo mbele ya msemaji wenu anayesema: Ikiwa hiki ndicho chakula cha Ali bin Abu Twalib, basi udhaifu utamzuia kupigana na wapinzani, na kupambana na mashujaa. Ee hakika mti wa bara ni mgumu zaidi, na kijani kibichi ni chepesi zaidi, na mimea ya vijijini ni yenye kuwaka kwa nguvu zaidi na si rahisi kuzimika.”140 Imepokewa kutoka kwa Imam al-Baqir (a.s) kuwa alisema: “Tumbo linaposhiba mtu hupituka mipaka.”141   Ghurarul-Hikam cha Amady.   Ghurarul-Hikam cha Amady. 137   Mustadrakul-Wasaail, Juz. 3, uk. 82. 138   Ghurarul-Hikam cha Amady. 139   Nahjul-Balaghah: 173. 140   Nahjul-Balaghah, kitabu na: 45. 141   Wasaail Shi’ah, Juz. 16, uk. 408 na Makarimul-Akhlaq, uk. 143. 135 136

47

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 47

8/10/2017 1:21:59 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Kula wakati bado una shibe kunasababisha ukoma.”142 Imepokewa pia kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Hakika Mwenyezi Mungu anachukia kula mno.”143 Imepokewa kutoka kwa Harith bin Mughira kuwa alisema: Nilimlalamikia Imam as-Sadiq (a.s) uzito ninaojikuta nao kifuani kwangu, na tumbo kuwa kubwa kutokana na chakula changu, akasema: “Kula komamanga hili tamu na mafuta yake, kwani hulainisha mfuko wa chakula, na linaponyesha kitambi, na linameng’enya chakula, na hufanya tasbihi tumboni.”144 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kuwa alisema: “Hakuna kitu kinachomchukiza mno Mwenyezi Mungu (a.j) kama vile tumbo lililojaa.”145 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Hakuna kitu chenye madhara zaidi katika moyo wa muumini kuliko uzidishaji wa chakula, nao unasababisha vitu viwili; moyo kuwa mgumu na matamanio ya kupituka.”146

UFUATANISHAJI WA CHAKULA JUU YA CHAKULA Maamuni Kanani alikuwa rais wa kitengo cha Fizikia katika chuo kikuu cha Damascus, alikuwa hafatanishi milo, na alikuwa akisema sentensi yake iliyo mashuhuri: Uingizaji wa chakula juu ya chakula ni madhara makuu.   Aamaliy uk. 436 cha Saduuq.   Mahasin cha Barqi. 144   Twibbul-Aimmat, uk. 134. 145   Sahifat Imam Ridha (a.s), uk. 54. 146   Mustadrakul-Wasaail, Juz. 3, uk. 80. 142 143

48

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 48

8/10/2017 1:21:59 PM


TIBA YA MAASUMINA

Mganga mmoja wa kiarabu aitwaye (Harth bin Kaladat) alimtembelea Kisra Anusharawan, na pindi alipomuuliza yeye; Ni upi ugojwa mbaya zaidi? Harth alisema: Kufuatanisha chakula juu ya chakula, nacho ndicho kilichowaangamiza watu wa nchi kavu na kuua wanyama wakali katika bara. Na alipoulizwa Galenos: Kwa nini hupatwi na maradhi? Alisema: Hakika mimi sijakusanya pamoja baina ya vyakula viwili vibaya, na wala sijafuatanisha chakula juu ya chakula kingine, na sijazuia ndani ya mfuko wangu wa chakula kilichonipa maudhi.147 Hadithi: Mtume (s.a.w.w) amesema: “Ugonjwa uangamizao ni ufatanishaji wa chakula juu ya chakula.”148 Mtu mmoja alimlalamikia Abu Abdillah (a.s) yale anayokutana nayo kutokana na maumivu na kitambi, basi akasema (a.s): “Kula chakula cha mchana na kula chakula cha usiku, na wala usile chochote baina ya milo hiyo, kwani kufanya hivyo (kula baina ya milo hiyo) ni kuharibu mwili. Hivi hujamsikia Mwenyezi Mungu (a.j) anasema: “Na wao wana riziki humo asubuhi na jioni.”149 Mshairi amesema: “Mambo matatu yanachangia kifo na husababisha siha kugeuka maradhi: Kudumu katika chakula, kuendekeza kujamiiana, na kufuatanisha chakula juu ya chakula.” Sufiyan bin Uyyayna amesema: “Wameafikiana waganga wa kiajemi kwamba ugonjwa ni kufuatanisha chakula juu ya chakula.”150   Twibbu Nabawi, uk. 321 cha ibn Qaym Jawziyyat.   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 26. 149   Twibbul-Aimmat, uk. 59. 150   Mustatrifu, Juz. 2 uk. 350 cha Abushiihi. 147 148

49

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 49

8/10/2017 1:21:59 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imam Ali (a.s) ana mashairi kadhaa, amesema: “Siku zote jizuie kufuatanisha chakula juu ya chakula kabla ya mmeng’enyo. Na kila chakula ambacho jino limeshindwa kukitafuna usikikaribie, kwani hicho ni chakula kibaya zaidi.”151 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Mfuko wa chakula ni nyumba ya ugonjwa, wastani katika kula ni kiini cha dawa, na asili ya kila ugonjwa ni ubaridi.” (Na makusudio ya ubaridi: kufuatanisha chakula juu ya chakula katika mfuko wa chakula kabla ya kutimia mmeng’enyo wa kwanza).152 Bilinganya: Mtume (s.a.w.w) amesema: “Kuleni bilinganya kwani hilo ni mti niliouona peponi…basi atakayekula akiamini kuwa ni ugonjwa basi utakuwa ugonjwa, na atayekula akiamini kuwa ni dawa basi utakuwa ni dawa.”153 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Kuleni bilinganya na kithirisheni kuula, kwani ni mti wa kwanza uliomwamini Mwenyezi Mungu (a.j).154 Mtume (s.a.w.w) alipokuwa katika nyumba ya Jabir bin Abdillah Answari (r.a) alipewa bilinganya, Mtume (s.a.w.w) akawa anakula. Jabir akasema: Hakika ndani yake kuna joto, hapo Mtume (s.a.w.w) akasema: “Ewe Jabir nyamaza, hakika huu ni mti wa kwanza kumwamini Mwenyezi Mungu, kaangeni na liivisheni, na litieni mafuta na maziwa, kwani huzidisha hekima.”155   Mustatrifu, Juz. 2, uk. 349 cha Abushiihiy.   Mugaddimatu, uk. 415 cha ibn Khaldun chapa ya nne. 153   Makarimul-Akhlaq, uk. 184, kutoka Firdaus. 154   Makarimul-Akhlaq, uk.184 cha Twabarasi. 155   Biharul-Anwaar, Juz. 66, uk. 224. 151 152

50

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 50

8/10/2017 1:22:00 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam Zaynul-Abidiina (a.s) kuwa alisema: “Bilinganya ni mafuta ya ardhi, nalo ni zuri kwa kila kitu kinachoangukia ndani yake.”156 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Kuleni bilinganya, kwani ni zuri kwa nyongo nyeusi, wala halidhuru manjano.”157 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Kuleni bilinganya kwani linaondosha ugonjwa wala hakuna ugonjwa ndani yake.”158 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Ukitumia tende na zabibu iliyoiva, huondoa madhara ya bilinganya.”159 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Zidisheni kula bilinganya wakati wa uchumaji wa tende, kwani ni tiba ya kila ugonjwa, linaongeza mng’ao wa uso na linajaza mishipa damu, na linaongeza maji ya mgongo.”160 Imepokewa kutoka kwa Imam Hadi (a.s) kuwa alisema: “Wanasema baadhi ya waaminifu wakweli: Zidisheni kuleta kwetu bilinganya, kwani ni joto wakati wa baridi, na ubaridi wakati wa joto, na ni hali ya kati na kati nyakati zote, ni zuri kwa hali zote.”161 Imepokewa kutoka kwa Abdul-Rahman Hashimi kuwa alisema: Imam Hadi (a.s) aliwaambia watumishi wake: “Punguzeni zaidi kwetu vitunguu maji na zidisheni kwetu bilinganya.” Mmoja wa watumishi akashangaa na kuuliza: Bilinganya? Imam akasema: “Ndio, ni bilinganya, ni kusanyiko la ladha na ondosho la ugonjwa. Ni zuri   Firdaus….   Twibbul-Aimmat (a.s) uk. 139 na yale yanayoshabihiana nayo. 158   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 166, kutoka kitabu Furuu na Mahasin. 159   Wasaail-Shii’ah, Juz. 17, uk. 167 na Safinat Bihar, Juz. 1, uk. 66. 160   Makarimul-Akhlaq, uk. 184 cha Twabarasi. 161   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 139. 156 157

51

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 51

8/10/2017 1:22:00 PM


TIBA YA MAASUMINA

kwa maumbile, ni lenye insafu kwa hali zake, ni zuri kwa mtu mzima na kijana, ni la wastani katika joto lake na ubaridi wake, ni joto sehemu ya baridi, na ubaridi sehemu ya joto.”162

NGUVU ZA KIUME NA HARUFU MBAYA YA KINYWA Hadithi: Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuhusiana na komamanga na mafuta yake, amesema: “Hakika linaondoa vitobo na harufu mbaya na linafanya mdomo kuwa na harufu nzuri.”163 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Hakika tunda la Tini linaondosha harufu mbaya ya kinywa.”164 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Suutar-Thaimu - thaimu na chumvi vinafukuza harufu mbaya vifuani… na vinaondosha harufu mbaya kinywani, na vinafanya kiungo cha uzazi cha mwanaume kuwa na nguvu.”165 Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) kwamba mmoja wa masahaba wake alimwandikia yeye akimlalamikia harufu mbaya kinywani, basi akasema: “Kula tende.”166

MAFUSHO Mtume (s.a.w.w) amesema: “Faidikeni na ubaridi wa kipupwe, kwani huo unafanya miili yenu kama vile inavyofanya kwa miti yenu, na   Wasaail Shi’ahh, Juz. 67, uk. 167, kutoka Furuu Kaafi, Juz. 6, uk. 373.   Wasaail Shi’ahh, Juz. 17, uk. 123, kutoka Mahasin cha Barqi. 164   Wasaail Shi’ah, Juz. 17, uk. 133. 165   Makarimul-Akhlaq, uk. 191. 166   Wasaail Shi’ah, Juz. 17, uk. 107. 162 163

52

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 52

8/10/2017 1:22:00 PM


TIBA YA MAASUMINA

jiepusheni na baridi la vuli, kwani linafanya miili yenu kama vile linavyofanya kwa miti yenu.”167 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: Jikingeni na baridi mwanzo wake na mkutane nayo mwisho wake, kwani inafanya katika miili yenu kama vile inavyofanya katika miti: mwanzo wake inaunguza na mwisho wake inatoa majani.”168 Imepokewa kutoka kwa Aamir Sha’abi, kwamba Zarri bin Habesh alisema: “Amirul-Muuminina (a.s) alisema maneno manne katika tiba, kama angeliyasema hayo Baqraat au Galenos basi angeletewa mbele yake majani mia (yaani yangeliwekwa majani mia moja mbele yake ili kuyatukuza maneno hayo) kisha angeyapamba kwa maneno hayo, nayo ni kauli yake (a.s): ‘Jikingeni na baridi …… mwisho wake unatoa majani.’”169

MARADHI YA UVIMBE WA UTANDO WA MAPAFU (PLEURISY) Maelezo yake: Ni ugonjwa unaotokana na kuvimba kwa utando uliopo baina ya ini na moyo, nao husababisha kupayuka. Hadithi: Imepokewa kutoka kwa Seif Timar kuwa alisema: Mmoja wa marafiki zetu aliugua huko Makka maradhi ya uvimbe wa utando wa mapafu (pleurisy). Nikaingia kwa Imam as-Sadiq (a.s) nikamweleza   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 271.   Nahjul-Balaghah, hekima ya 128. 169   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 271, kutoka kitabu Daa’wat cha Qutbu Diin Raawandiy. 167 168

53

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 53

8/10/2017 1:22:00 PM


TIBA YA MAASUMINA

hilo, akaniambia: “Mnywesheni uji wa shairi, kwani huponya kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu, nacho ni chakula ndani ya tumbo la mgonjwa.” Tukamnywesha uji siku mbili au mara mbili, basi rafiki yetu akapona.170 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Yule anayeumwa homa akinywa usiku huo kiasi cha dirhamu mbili mbegu za katani au tatu, basi atasalimika na uvimbe wa utando wa mapafu katika ugonjwa huo.”171 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Hakika mchadi unaondoa mbalanga, na haiingii dawa iliyo bora tumboni mwa mwenye maradhi ya uvimbe wa utando wa mapafu kushinda majani ya mchadi.”172

UKOMA Imepokewa kutoka kwa Ibn Abbas kuwa alisema: Mtume (s.a.w.w) amesema: “Mambo matano yanasababisha ukoma; uondoaji wa nywele za mwilini katika siku ya Ijumaa na siku ya Jumatano, kutia wudhuu na kuoga kwa kutumia maji yaliyochemshwa na jua, kula hali ya kuwa na janaba, kujamiiana na mwanamke katika siku za hedhi, na kula wakati bado una shibe.”173 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Siku moja wana wa Israeli walipatwa na ukoma, basi Mwenyezi Mungu akamfunulia Nabii Musa (a.s) awaamrishe hao kula nyama ya ng’ombe iliyochanganywa na mchadi.”174   Wasaail Shi’ah, Juz. 17, uk. 10.   Makarimul-Akhlaq, uk. 215 cha Twabarasi. 172   Kaafi cha Kulayni…… 173   Khiswalu, Juz. 1, uk. 270. 174   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 211, na kutoka kitabu Mahasin uk. 519. 170 171

54

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 54

8/10/2017 1:22:00 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuhusiana na sanamaki kuwa alisema: “Hakika jani hilo ni amani kutokana na ukoma, mbalanga, uwendawazimu, kiharusi na ukosefu wa nguvu…”175 Imepokewa pia kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Sawiiq kavu inaondoa ukoma.”176 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Kula wakati bado una shibe kunasababisha ukoma.”177 Imepokewa pia kutoka kwa Imam as-Sadiq a.s) kuwa alisema: “Figili huleta kumbukumbu, na inasafisha moyo, na inaondoa uwendawazimu, mbalanga na ukoma.”178 Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) kuwa alisema: “Yule atakayekunywa supu ya nyama ya ng’ombe, Mwenyezi Mungu atamwondoshea yeye maradhi ya ukoma na mbalanga.”179 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kuwa alisema: “Ni juu yenu kulamba chumvi, kwani ni ponyo ya magonjwa sabini, kati ya hayo ni mbalanga, ukoma na uwendawazimu.”180 BARAKA Mtume (s.a.w.w) alisema: “Fanyeni vipande vidogo vidogo vya mikate yenu, hakika kila kipande cha mkate kina baraka.”181 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Hakuna maziwa anayonyonya mtoto mchanga yaliyo na baraka zaidi kwake kushinda maziwa ya mama yake.”182   Makarimul-Akhlaq, uk. 188.   Wasaail Shi’ah, Juz. 17, uk. 8, kutoka Furuu wal-Mahasin. 177   Makarimul-Akhlaq, uk. 147. 178   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 284. 179   Biharul-Anwaar, Juz. 62 uk. 212, kutoka kitabu Twibbu Aimmat (a.s), uk. 104. 180   Sahifat Ridha (a.s), uk. 78. 181   Biharul-Anwaar, Juz. 66, uk. 272 na Wasaail Shi’ah, Juz. 16, uk. 513. 182   Mustadrakul-Nahj, uk. 171. 175 176

55

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 55

8/10/2017 1:22:00 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Kuleni tikitimaji, kwani ni tunda la peponi, na ndani yake kuna baraka elfu na rehema elfu, na kula hilo ni tiba ya kila ugonjwa.”183 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Mkila tango kuleni kuanzia chini, kwani sehemu hiyo ina baraka kubwa mno.”184 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kuwa alisema: “Hakika Mwenyezi Mungu (s.w.t) amejaalia baraka ndani ya asali, na ndani yake ipo tiba ya magonjwa, na imebarikiwa na Manabii sabini.”185 Imepokewa pia kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kuwa alisema: “Ni juu yenu kula adesi, kwani imebarikiwa na imetukuka, na hiyo inafanya moyo kuwa laini, na inazidisha machozi, na hiyo imebarikiwa na Manabii sabini na wa mwisho wao ni Nabii Isa bin Maryam (a.s).”186 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Kiacheni chakula chenye joto mpaka kipoe, hakika Mtume (s.a.w.w) alipelekewa chakula, akasema: ‘Kiacheni mpaka kipoe na kiwezekane kuliwa. Na Mwenyezi Mungu hakuwa Mwenye kutulisha sisi chakula moto, na baraka ipo katika chakula baridi.” Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Mmoja wenu akila chakula, basi afyonze vidole vyake ambavyo amevitumia katika kula, Mwenyezi Mungu (a.j) anasema: Mwenyezi Mungu ametia baraka ndani yako.”187

Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 296.   Wasaail Shi’ah, Juz. 17, uk. 166, kutoka kitabu Furuu wal-Mahasin. 185   Sahifat Ridha (a.s), uk. 90. 186   Sahifat Ridha (a.s), uk. 75. 187   Khiswalu juz. 2 uk. 613. 183 184

56

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 56

8/10/2017 1:22:00 PM


TIBA YA MAASUMINA

TENDE MBICHI Hadithi: Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Vitu vinne vinafanya ulinganifu wa maumbile; komamanga la Suurani, tende iliyopikwa, urujuani na hindubaau (Chickory).”188 Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) kuwa alisema: “Chakula bora ni wali, hupanua utumbo, na hukata bawasiri, na mimi ninapendelea niwe kama watu wa Iraq kwa kula kwao wali na tende mbichi, hakika hivyo viwili vinapanua utumbo na vinakata bawasiri.”189 Ngozi Imam Ali (a.s) kuhusu mafuta ya kujipaka amesema: “Hulainisha ngozi, huongeza akili na ubongo, na hurahisisha mapito ya maji.”190 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Yule atakayeonja chumvi kabla ya tonge la kwanza la chakula basi huondokana na mikunjo ya uso.”191 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Kunywa sawiiq kwa mafuta ya kula, huotesha nyama na hukaza mishipa, hulainisha ngozi na huongeza maji ya uzazi.”192 Imepokewa vilevile kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Kitunguu maji huleta uzuri wa kinywa, na hukaza mgongo na hulainisha ngozi [yaani hufanya ngozi kuwa nyororo na rangi safi.]”193   Khiswal, Juz. 1, uk. 249.   Wasaail Shi’ah, Juz. 17, uk. 95. 190   Khiswal cha Saduuq…. 191   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 377 cha Abdullah bin Shubbar. 192   Mahasin cha Barqi. 193   Makarimul-Akhlaq, uk. 182. 188 189

57

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 57

8/10/2017 1:22:00 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kuwa alisema: “Ni juu yenu kushikamana na upakaji hina, kwani unapendezesha ngozi, na unazidisha nguvu katika tendo la kujamiana.”194

MACHO Mtume (s.a.w.w) amesema: “Kuleni pera mtaoneana upole kati yenu, kwani linasafisha macho, na linaotesha upendo moyoni…”195 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) pia kuwa alisema: “Mtapoingia mji wa jamii fulani na mkahofia mabalaa yake, basi ni juu yenu kula vitunguu maji vya sehemu hiyo kwani husafisha macho.”196 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Tende… inaongeza usikivu na uonaji….”197 Imepokewa pia kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Katika upakaji wa hina kuna mambo kumi na nne; ….unaondoa harufu ya masikio, na unasafisha uonaji wa macho.”198 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Pakeni ndevu zenu hina, kwani inasafisha macho, inaotesha nywele, inaleta harufu nzuri na inamtuliza mke.”199 Imepokewa kutoka kwa Abu Khaswib kuwa alisema: jicho langu lilikuwa jeupe, na sikuwa naweza kuona chochote, basi nikamuona Amirul-Muuminina Ali (a.s) usingizini, nikamwambia: Ewe bwana wangu jicho langu limepatwa na tatizo kama unavyoona! Akasema: “Chukua zabibu zisage na upake nyusi zako zabibu hizo” basi nikachukua zabibu nikasaga kokwa zake. Na hapo nikapaka nyusi zangu,   Sahifat Ridha (a.s), uk. 90.   Makariml-Akhlaq uk. 171. 196   Ramzul-Sihat uk. 144, kutoka kitabu Firdausi. 197   Makarimul-Akhlaq, uk. 169. 198   Twibbul-Aimmat uk.349 cha Abdullah bin Shubbar. 199   Twibbul-Aimmat (a.s) uk. 350 cha Abdullah bin Shubbar. 194 195

58

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 58

8/10/2017 1:22:00 PM


TIBA YA MAASUMINA

basi likaondoka giza kwenye macho yangu, na nikaliangalia nikalikuta likiwa sahihi.”200 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Vitu vinne vinatia nguvu macho; maji yenye kutiririka, kumwangalia mwanamke mrembo, kukaa mbele ya watu wa kheri, na kujipaka wanja wakati wa kulala. Na vitu vinne vinadhoofiha macho; kujamiiana na ajuza, kumwangalia anayesulubiwa, kuangalia kiini cha jua na kula hali ungali na shibe.”201 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Upakaji wanja unaotesha nywele, na unaimarisha macho, na unasaidia kusujudu kwa muda mrefu.”202 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Wanja unafanya macho kuona vizuri, unaotesha nywele, na unaondoa chozi.”203 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Upigaji mswaki una mambo kumi, na akayataja: …. unasafisha jicho, na unaondoa kikohozi.”204 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Vitu vinne vinasafisha macho, vinayanufaisha wala haviyadhuru.” Akaulizwa juu ya hivyo, ni vitu gani hivyo? Akasema: “Suutar Thaimu na chumvi vikichanganywa pamoja, na kisibiti na karanga vikichanganywa pamoja.”205 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuhusiana na nyama amesema: “Hakika hiyo inaongeza usikivu na uonaji.”206   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 354 cha Abdullah bin Shubbar.   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 358 cha Abdullah bin Shubbar. 202   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 350 cha Abdullah bin Shubbar. 203   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 350 cha Abdullah bin Shubbar. 204   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 350 cha Abdullah bin Shubbar. 205   Makarimul-Akhlaq, uk. 191. 206   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 280. 200 201

59

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 59

8/10/2017 1:22:00 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kuwa alisema: “Msiwakaribie wanawake mwanzo wa usiku… akishika ujauzito atajifungua mwenye matatizo ya ufahamu mzuri na kiharusi… au mwenye udhaifu wa kuona.”207 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kuwa alisema: “Msichukie vitu vinne kwa sababu ya manufaa manne; msichukie ugonjwa wa macho kwani hukata mizizi ya upofu…..”208 Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) kuwa alisema: “Vitu vitatu huvuta uonaji; kuangalia kijanikibichi, kuangalia maji yenye kutiririka na kuangalia uso mzuri.”209

KITUNGUU MAJI Faida zake: Ibn Sina (Avicenna) amesema: Kitunguu maji kinafanya ngozi kuwa nyekundu na kinavuta damu hadi nje, na kina mambo mahsusi katika kuzuia madhara ya hewa yenye sumu. Na juisi yake inasaidia kutokana na maji yanayoteremka kutoka jichoni na kinasafisha macho.210 Na juisi ya vitunguu inatumika kama njia ya kufukuza vijidudu mwilini, na inatumika pia katika maradhi ya mfuko wa chakula na utumbo na uvimbe wa lozi mbili. Kama vile juisi yake iliyochanganywa na asali inavyotumika kwa ajili ya kuzuia ongezeko la ukungu wa jicho. Na juisi yake inasaidia kwa mgonjwa wa kisukari na mara  Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 327 cha Allama Majlisi.   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 350 cha Abdullah bin Shubbar. 209   Rawdhatul-Waidhiina, uk. 308 cha Ibn Fital Naysabuuriy. 210   Ajaaibul-Makhluqaat cha Qazwiini, mwishoni mwa kitabu Hayaat Hayawaan Kubra, Juz. 2 uk. 182 cha Damiriy. 207 208

60

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 60

8/10/2017 1:22:00 PM


TIBA YA MAASUMINA

dhi ya kukauka kwa mshipa upelekao damu moyoni na kuipeleka kwenye tishu, na hususan mshipa upokeao damu kutoka moyoni na kuipeleka kwenye ubongo. Na aidha juisi yake safi hutumika katika kutibu vidonda na uondoaji wa mikunjo, na katika kutia nguvu nywele na kuondoa mikunjo ya uso.”211 Na kitunguu kina mada (Firumanat) nayo inafanya kazi ya umeng’enyaji wa chakula katika urojorojo wa mfuko wa chakula na utumbo. Kama vile kina mada (kokeni) ambayo ina nguvu ya insulini kwa ajili ya kazi ya uunguzaji wa maada (chembe chembe) za sukari na kuziangamiza, na kwa hivyo inatibu maradhi ya kisukari ya haja ndogo. Na juisi ya vitunguu maji ina mafuta mazuri, yenye nguvu na kuua virusi (vijidudu) vibaya vya aina mbalimbali, na virusi vya taifodi mbaya na majipu. Kama ambavyo kitunguu kina chumvi inayotia nguvu misuli na kuvuta usingizi, na ndani ya kitunguu kuna mada nyingine zinazokinga mshipa upokeao damu moyoni na kuipeleka kwenye tishu kutokana na kushupaa (maji ya mgongo), na mrundikano wa mada za kaboneti ya kalisi ya kiasili katika umri wa utuuzima, hufanya mzunguko wa damu kuwa mzuri……. Faida zote hizi zipo katika kitunguu kimoja, je, inawezekana kwa dawa ya kulevya ya mkemia mmoja imiliki faida zote hizi zilizokusanyika pamoja, na iwe rahisi kwa kiwango hiki?!212 Hadithi: Mtume (s.a.w.w) amesema: “Mtakapoingia katika mji, basi kuleni mbogamboga zake na vitunguu vyake, kinawafukuzia nyinyi magonjwa yake, kinaondoa uchovu, kinakaza mishipa ya fahamu, kinaongeza maji ya uzazi, na kinaondoa homa.”213   Nabaatati Twayyibat wa Isti’imaaluha, Juz. 1, uk. 182 cha Dr. Muhammad Awdaat mwaka 1987. 212   Majallat Ahraam Riyaadhi, uk. 77 idadi 100 tarehe TASHRIIN THAANI mwaka 1991. 213   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 300. 211

61

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 61

8/10/2017 1:22:01 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Mtakapoingia mji ambao una ugonjwa wa homa, na nyinyi mnahofia homa yake, basi ni juu yenu kula vitunguu vyake, kwani vinasafisha macho na vinang’arisha nywele, vinaongeza maji ya uzazi ya mwanaume, na vinazidisha nguvu ya kutembea, vinaondoa weusi usoni na pia uchovu.”214 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kwamba kilitajwa mbele yake kitunguu, akasema: “Kinaondoa harufu mbaya ya kinywa, kinaondoa kikohozi, na kinaongeza nguvu katika tendo la ndoa.”215 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Kuleni kitunguu kwani ndani yake kuna mambo matatu; kinaondoa harufu mbaya ya kinywa, kinaimarisha ufizi na kinaongeza maji na nguvu ya tendo la ndoa.”216 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Kitunguu kinaondoa uchovu, kinakaza mgongo, kinaongeza maji na nguvu ya kutembea na kinaondoa homa.”217 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Kitunguu kinasafisha kinywa, kinakaza mgongo na kinafanya ngozi kuwa nyororo.”218 Imepokewa pia kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: Mtume (s.a.w.w) amesema: “Mtakapoingia mji kuleni kitunguu chake, kwani kinawaepusha nyinyi na homa yake.”219 Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) kwamba siku moja aliulizwa na ndugu yake Ali, kuhusiana na kitunguu saumu na ki  Ramzul-Sihat, uk. 144, kutoka kitabu Firdausi.   Wasaail Shi’ah, Juz. 17, uk. 118 kutoka Furuu na Mahasin cha Barqi. 216   Khiswal, Juz. 1, uk. 158 cha Saduq. 217   Khiswal, Juz. 1, uk. 158 cha Saduq. 218   Wasaail Shi’ah, Juz. 17, uk. 168, kutoka Furuu wal-Mahasin. 219   Wasaail Shi’ah, Juz. 17, uk. 169, kutoka kitabu Furuu wal-Mahasin. 214 215

62

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 62

8/10/2017 1:22:01 PM


TIBA YA MAASUMINA

tunguu maji, kinaweza kuwekwa ndani ya dawa kabla ya kupikwa? Akasema: “Hakuna tatizo.” Na akamuuliza kuhusiana na kula kitunguu saumu na kitunguu maji kwa siki? Akasema: “Hakuna tatizo.”220

MAUMIVU YA TUMBO NA UGONJWA WA TUMBO Imepokewa kutoka kwa Hamran, kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: Mtu mmoja alimlalamikia Amirul-Muuminina Ali (a.s) kuhusu maumivu ya tumbo, Ali (as) akamwambia: “Mwombe mkeo dirhamu moja kutokana na mahari yake, nunua kwa dirhamu hiyo asali na kunywa kwa maji ya mvua.” Alifanya alivyoamrishwa, na hatimaye akapona. Akamuuliza Amirul-Muuminina (a.s) kuhusu hilo, je, kuna kitu ulichokisikia kutoka kwa Mtume (s.a.w.w)? Akasema: “Hapana, lakini nimemsikia Mwenyezi Mungu ndani ya Kitabu Chake akisema: ‘Lakini wakikupeni chochote kwa radhi ya nafsi katika hayo, basi kileni kiwashuke kwa raha.’221 na amesema: ‘Kinatoka katika matumbo yao kinywaji chenye rangi mbalimbali ndani yake kina matibabu kwa watu…’222 na amesema: ‘Na tumeyateremsha kutoka mawinguni maji yaliyobarikiwa.’223 Hivyo umekusanyika uzuri, raha, baraka na ponyo, basi ndipo nikakuta ponyo katika mchanganyiko huo.”224 Imepokewa kutoka kwa Dhurih kuwa alisema: Nilimwambia Imam as-Sadiq (a.s): Hakika mimi ninakuta tumboni mwangu ngurumo na maumivu. Akasema (a.s): “Ni kitu gani kinakuzuia kutumia habasoda, kwani ndani yake kuna ponyo la kila ugonjwa ila sumu.”225   Wasaail Shi’ah, Juz. 17, uk. 171 , kutoka kitabu Qurbul-Isnaad uk. 116.   Surat 4 aya 4. 222   Sura 16 aya 69. 223   Sura 50 aya 9. 224   Tafsirul-Ayaashi, Juz. 1, uk. 219 na Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 270. 225   Makarimul-Akhlaq, uk. 186 na yanayoshabihiana nayo. 220 221

63

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 63

8/10/2017 1:22:01 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Hakika habasoda ni tiba ya kila ugonjwa, mimi natumia nikiwa na homa, maumivu ya kichwa, ugonjwa wa macho, maumivu ya tumbo na kila maumivu yanayonisumbua, na Mwenyezi Mungu (a.j) huniponya kwayo.”226 Imepokewa kutoka kwa Hamran kuwa alisema: Imam as-Sadiq (a.s) alikuwa akiamrisha apikiwe wali wenye kuchanganywa na sumaq Sumac anapopatwa na maumivu ya tumbo, na alikuwa akipona anapokula chakula hicho.”227 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Nilipatwa na ugonjwa wa tumbo, nikakonda, na nikadhoofika sana, ikanijia kichwani mwangu kwamba, nichukue mchele niuoshe, kisha niukaange na niusage, kisha nipike uji, basi mwili wangu ukarudi tena, na mishipa yangu ikawa na nguvu.”228 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Nilipatwa na maumivu ya tumbo, mmoja akaniambia: Chukua mchele, uoshe kisha uanike kivulini, kisha usage hadi uwe laini, na kula gao moja kila asubuhi.”229 Imepokewa kutoka kwa Muhammad bin Ghaydh kuwa alisema: Nilikuwa kwa Abu Abdillah Imam as-Sadiq (a.s), ghafla akaja mtu akamwambia: Hakika binti yangu amenyong’onyea na anaumwa tumbo, akasema: “Ni kitu gani kinakuzuia kutumia mchele na mafuta? Chukua mawe manne au matano yaweke juu ya moto, na tia mchele ndani ya chungu (sufuria) na upike mpaka uive, na chukua mafuta safi mimina ndani ya wali na weka mafuta juu ya chombo pamoja na mawe, na weka juu yake chombo kingine, kisha koroga   Makarimul-Akhlaq, uk. 186.   Kaafi, Juz. 6, uk. 342. 228   Biharul-Anwaar, Juz. 59, uk. 172, kutoka kitabu Mahasin uk. 503. 229   Biharul-Anwaar, Juz. 59, uk. 172, kutoka kitabu Mahasin uk. 503. 226 227

64

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 64

8/10/2017 1:22:01 PM


TIBA YA MAASUMINA

sana, na dhibiti usitoke mvuke wake, na mafuta yatakapoyeyuka basi changanya na wali, kisha kula.”230 Mtu mmoja alimlalamikia Imam Ridha (a.s) kuwa anakaribia kufa kutokana na msokoto wa tumbo, akasema (a.s): “Ikiwa jambo litazidi na ukazidiwa na maumivu, basi chukua karanga isiyomenywa na iweke juu ya moto mpaka ujue kuwa imeungua hadi ndani na imekolea moto vizuri, menya maganda yake yote, hakika hiyo inatuliza muda huo huo.” Akasema: Naapa kwa Mwenyezi Mungu sikufanya ila ni mara moja tu, yakatulia maumivu yangu yenye kusumbua, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (a.j).231 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kuwa alisema: “Hakuna kitu kinachomchukiza zaidi Mwenyezi Mungu (a.j) kama vile tumbo kujaa chakula.”232 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kuwa alisema: “Kuleni tende kabla hamjala chochote, kwani hiyo inaua vijidudu tumboni.”233 Niliwasikia wazee wetu wakisema: Maziwa ya ngamia ni tiba ya kila ugonjwa na maradhi ya mimea, na kwa yule mwenye maumivu ya tumbo atumie mkojo wake.”234

TIKITIMAJI Mtume (s.a.w.w) amesema: “Vuli ya umma wangu ni kipindi cha zabibu na matikitimaji.” Na akasema: “Ng’ata tikitimaji wala usilikate vipande, kwani hilo ni tunda lenye baraka na zuri, linatohari  Biharul-Anwaar, Juz. 59, uk. 172, kutoka kitabu Mahasin uk. 503.   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 101. 232   Sahifat Ridha (a.s), uk. 54. 233   Sahifat Ridha (a.s), uk. 51. 234   Kaafi cha Kulayni. 230 231

65

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 65

8/10/2017 1:22:01 PM


TIBA YA MAASUMINA

sha kinywa, ni utukufu wa moyo, linang’arisha meno, linamridhisha Rahmani, harufu yake ni nzuri kuliko ambari, na maji yake ni mazuri kuliko kawthari…”235 Imepokewa kwamba Mtume (s.a.w.w) alipelekewa zawadi ya tikitimaji kutoka Twaif, basi akalinusa na kulibusu kisha akasema: “Ling’ate tikitimaji kwani hilo linatokana na mapambo ya ardhi, maji yake yanatokana na rehema na utamu wake unatoka peponi.”236 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Kula tikitimaji kabla ya chakula linaosha tumbo na linaondoa mizizi ya ugonjwa.”237 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Vuli ya umma wangu ni wakati wa zabibu na matikitimaji.”238 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Kuleni tunda la tikitimaji, kwani hilo ni tunda la peponi, na ndani yake kuna baraka elfu na rehema elfu, na ulaji wa hilo ni ponyo la kila ugonjwa.”239 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Hakuna mwanamke mjamzito atakayekula tikitimaji kwa jibini ila mtoto atakayemzaa atakuwa mwenye sura nzuri na umbo zuri.”240 Imepokewa pia kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Kuleni tunda la tikitimaji, hakika maji yake ni rehema, na utamu wake unatokana na utamu wa peponi.”241   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 296.   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 298. 237   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 299. 238   Makarimul-Akhlaq, uk. 174. 239   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 296. 240   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 299. 241   Makarimul-Akhlaq, uk. 184, na kutoka kitabu Firdausi. 235 236

66

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 66

8/10/2017 1:22:01 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Tarmidhi kuwa alisema: Mtume (s.a.w.w) alikuwa akila tikitimaji kwa tende na akisema: “Joto hili linaisukuma baridi hii.”242 Imepokewa kutoka kwa Ibn Abbas kuwa alisema: Mtume (s.a.w.w) amesema: “Ni juu yenu kula tikitimaji hakika ndani yake kuna mambo kumi; nalo ni chakula na kinywaji, linaosha kinywa, meno na tumbo, kama vile mrehani unavyosafisha vyombo. Aidha linaosha njia za viungo vya uzazi na kuosha tumbo, na linaongeza maji ya mgongo na nguvu katika kujamiiana, linakata ubaridi na linang’arisha ngozi.”243 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Tikitimaji ni mafuta ya ardhi, halina ugonjwa wala madhara ndani yake.”244 Imepokewa vilevile kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Ndani ya tikitimaji kuna vitu kumi; ni chakula, kinywaji, tunda, harufu nzuri, afya, utamu, linasafisha kinywa na tumbo, ni mboga na dawa.”245 Na hakika amekusanya Imam Ridha (a.s) maana hizi katika beti zifuatazo, kutoka katika kitabu Rawdha: “Siku moja tulipewa zawadi ya tikitimaji kutoka katika mapambo ya ardhi na nyumba ya usalama. Limekusanya sifa mbalimbali adhimu ambazo hakika nimezihisabu, nalo linasifika kwa mpangilio. Vivyo hivyo amesema mteule Muhammad babu yangu rehema na amani ziwe juu yake: Maji na utamu na harufu nzuri. Ni tunda, kiongeza hamu, chakula na mchuzi. Linasafisha kibofu cha mkojo, linafanya nyuso ziwe safi, linasafisha kinywa, na mambo kumi yametimia.”   Twibuun- Nabawwi, uk. 221 cha ibn Qaym Jawziyyat.   Ramzul-Sihat, uk. 14 cha Dahsurkhiy. 244   Makarimul-Akhlaq, uk. 185. 245   Makarimul-Akhlaq, uk. 185. 242 243

67

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 67

8/10/2017 1:22:01 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Kuleni tikitimaji hakika ndani yake kuna mambo kumi yenye kukusanyika pamoja: Nalo ni mafuta ya ardhini, halina ugonjwa ndani yake wala madhara, nalo ni chakula, kinywaji, tunda, harufu nzuri na linasafisha kinywa, meno na ni mchuzi, na linaongeza maji ya uzazi ya mwanaume, linaosha kibofu cha mkojo, (na katika hadithi nyingine) na linayeyusha mbegu za kende mbili.”246 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kuwa alisema: Siku moja Mtume (s.a.w.w) aliletewa tikitimaji na tende, basi akala vyote viwili, akasema: “Hivi viwili ni vizuri viwili.”247 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kuwa alisema: “Ulaji wa tikitimaji asubuhi kabla ya chochote husababisha kiharusi.”248

MBOGA YA BIBI FATIMA (RIJLAT – FARFUKH) PURSLANE Ibn Baytwar amesema: Nayo ni mboga yenye baraka na ni mboga safi. Galenos amesema: “Mboga hii ni baridi yenye mchanganyiko wa majimaji, na ndani yake kuna ushikaji na uachiaji.” Imepokewa kwamba Fatima Zahra (a.s) alikuwa akiipenda mboga hii basi ikanasibishwa kwake, na ikasemwa: Ni mboga ya Fatima, kisha ukaja ukoo wa Umayya wakaibadilisha jina hilo na wakaiita: Mboga pumbavu. Daud Antwaki katika kitabu chake Tadhkirat amesema: Iliitwa ya wapumbavu kwa kujiotea kwake yenyewe njiani, nao ni mmea   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 139 na Makarimul-Akhlaq uk. 185.   Sahifat-Ridha (a.s), uk. 78. 248   Mahasin, uk. 557. 246 247

68

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 68

8/10/2017 1:22:01 PM


TIBA YA MAASUMINA

wenye unene sawa na unene wa vidole, hurefuka lakini huwa haufikii dhiraa, na unatambaa ardhini, na unatoa maua mengi meupe, na unaacha mbegu ndogo ndogo, na unadiriki vuli na kiangazi, nao ni baridi na unyevunyevu.249 Faida zake: Nao ni tajiri kwa mada za madini kama vile potasiamu na chuma, na hutumiwa ili kuponya kuhara na magonjwa ya kuambukiza na bawasiri na dhidi ya uvujaji damu kutoka kwenye mfuko wa chakula, unasafisha haja ndogo na kufukuza vijidudu.250 Sifa zake na matumiza yake: Ni mboga yenye kuburudisha, ladha yake kwa ndani ni ya chumvi. Mahali pake pa asili ni Asia ndogo, inapikwa kwa mapishi mbalimbali. Na majani yake safi yanatumiwa katika kachumbali. Na mboga hii huleta uchachu ndani ya mfuko wa chakula.251 Hadithi: Mtume (saww) alikuwa anapohisi joto, hung’ata rijlat na hapo hupata raha kwayo, akasema: “Ewe Mwenyezi Mungu ibariki ndani yake, hakika ndani yake kuna ponyo ya magonjwa tisini na tisa. Iotesheni popote mtakapo.”252 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Ni juu yenu kula Farfukh, nayo ni akili, na ikiwa kuna kitu kinaongeza akili basi ni hiyo.”253   Al-Jaamiu Li Mufradaat Adawiwwa wa-Aghdhiyat, Juz. 4, uk. 198 cha ibn Baytwar.   Nabataat Twayyibat wal-Atriyat fi watan Arabi, uk. 244 Khartum mwaka 1988. 251   Tadaawi bil-Aashab, uk. 336 cha Dr. Amiin Ruwayhat chapa ya nne Daaruul-Qalam Beirut. 252   Ramzu Sihat uk. 192. 253   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17 uk. 154 kutoka kitabu Mahasin. 249 250

69

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 69

8/10/2017 1:22:01 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kwamba Fatima (a.s) alikuwa akiipenda mboga hii basi ikanasibishwa kwake, ikaitwa: Mboga ya Zahra, kama walivyosema: Ni aina ya mti wenye maua ya rangi zing’arazo na wenye majani yaliyoachana. Kisha ukaja ukoo wa Umayya wakaibadilisha na wakaiita: Mboga pumbavu.254 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Hakuna juu ya ardhi mboga iliyo bora zaidi wala yenye manufaa zaidi kuliko Farfukh, nayo ni mboga ya Fatima (a.s).” Kisha akasema: “Mwenyezi Mungu awalaani Bani Umayya, wao ndio walioiita hiyo mboga kwa jina pumbavu, kutokana na chuki waliyonayo kwetu na uadui wao kwa Fatima (a.s).”255 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Siku moja Mtume (s.a.w.w) alikanyaga changarawe za moto basi zikamuunguza, na akaukanyaga mmea wa Rijlat, nao ni mboga mboga pumbafu, basi likapungua joto la changarawe, na akaiombea hiyo na alikuwa akiipenda. (Na hadithi iliyopo katika kitabu al-Kaafi inasema): Hakuna mboga yenye baraka zaidi yake!”256 MBOGAMBOGA Mtume (s.a.w.w) amesema: “Mtakapoingia kwenye mji kuleni mbogamboga na vitunguu vyake, vinafukuza ugonjwa wake, huondoa uchovu, vinakaza mishipa ya fahamu, vinaongeza maji ya uzazi, na vinaondoa homa.”257 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema; ‘Kila kitu kina pambo, na pambo la meza ya chakula ni mbogamboga.”258   Biharul-Anwaar, Juz. 66, uk. 235.   Wasaail Shi’ah, Juz. 17 uk. 154 kutoka Mahasin. 256   Wasaail Shi’ah, Juz. 17 uk. 154 kutoka Furuu wal-Mahasin. 257   Biharul-Anwaar, Juz. 62 uk. 300. 258   Makarimul-Akhlaq, uk. 176. 254 255

70

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 70

8/10/2017 1:22:01 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa pia kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Pambeni meza zenu za chakula kwa mbogamboga, kwani hizo zinamfukuza shetani zinapoliwa kwa Bismillah.”259 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Ilitajwa mbogamboga mbele ya Mtume (s.a.w.w) akasema: ‘Kuleni liki, hakika hakuna mfano wake katika mbogamboga, ni kama vile mkate katika vyakula vingine.”260 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Mboga ya Mtume (s.a.w.w) ilikuwa ni hindubaau Chickory, na mboga ya Amirul-Muuminina (a.s) ilikuwa ni bilinganya, na mboga ya Fatima (a.s) ilikuwa ni farfukh.”261 Imepokewa kutoka kwa Muwafaq Madiniy kutoka kwa baba yake kutoka kwa babu yake, amesema: Alinituma mimi aliyepita hapo kabla (yaani Imam Kadhim), siku moja akanizuia ili nile chakula, na pindi walipokuja kwenye meza ya chakula hakukuwa na mboga yoyote, basi akazuia mkono wake, kisha akasema kumwambia kijana: “Hivi hujui kuwa mimi sili juu ya meza ya chakula ikiwa hakuna mboga? Basi niletee mboga.” Basi yule kijana akaenda akaleta mboga na akaiweka juu ya meza, basi hapo akanyoosha mkono wake na akala.”262 Imepokewa: Kula tunda unapoingia mji wake, na bora zaidi ni komamanga na balungi, kuhusiana na harufu mbili ni ya waridi na balungi, na kuhusiana na mboga ni hindubaau Chickory na saladi.263 Nabii Musa (a.s) katika Talmud alisema:   Biharul-Anwaar, Juz. 62 uk. 300.   Makarimul-Akhlaq, uk. 178. 261   Biharul-Anwaar, Juz. 17, uk. 90. 262   Wasaail Shi’ah, Juz. 16 uk. 531 kutoka kitabu Mahasin Barqi. 263   Mustadrakul-Wasaail, Juz. 3, uk. 119. 259 260

71

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 71

8/10/2017 1:22:01 PM


TIBA YA MAASUMINA

“…Wale ambao meza zao hazijakosa saladi, tango na figili, wakati wa kiangazi au masika.” Na akasema mwalimu (yaani Musa): “Figili inasaga chakula katika mfuko wa chakula, na saladi inakigeuza, na tango linanyoosha tumbo.” Kisha anasema: “Lakini je, hakuwafundisha Ismail wanafunzi wake kwamba tango linadhuru mfuko wa chakula kama vile panga? Hakuna katika hili tatizo lolote, kwani mmoja wao anazungumzia tango kubwa, na mwngine tango dogo.”264 KULIA Imam as-Sadiq (a.s) alisema kumwambia Mufadhal bin Umar: “Elewa ewe Mufadhal kilio cha watoto kina manufaa, na jua kwamba katika ubongo wa watoto kuna unyevunyevu, ikiwa utabakia ndani yake utazusha kwao matukio makubwa, na maradhi mengi ikiwemo kuondoka nguvu ya uonaji na mengineyo. Basi kulia kunaondoa unyevunyevu huo kutoka vichwani mwao, na kuwaletea wao afya katika miili yao, na usalama katika macho yao. Je, huoni kwamba kulia kunawafaa watoto ijapokuwa wazazi wake hawalijui hilo?!”265 KIKOHOZI Mtume (s.a.w.w) amesema: “Dawa ya kikohozi ni bafu.”266 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Ni juu yenu kula zabibu, kwani hiyo inafichua kibofunyongo, na inaondoa kikohozi.”267   Tarjumat Arabiyyat, uk. 45 cha Tilmuud Baabali Fayadh Daarul-Ghadiir Damascus chapa ya kwanza mwaka 1991. 265   Tawhidul-Mufadhal, uk. 47. 266   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 386 cha Abdullah Shubbar. 267   Khiswal, Juz. 1, uk. 344 cha Saduq. 264

72

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 72

8/10/2017 1:22:01 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Mambo matano yanaondoa usahaulifu na yanaongeza nguvu ya kumbukumbu, na yanaondoa kikohozi: Kupiga mswaki, funga, usomaji wa Qur’ani, asali na ubani (yaani kundur).”268 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Kutafuna ubani kunakaza magego, na kunaondoa kikohozi.”269 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Asali ni tiba ya kila ugonjwa, wala haina ugonjwa ndani yake, pia inapunguza kikohozi na inasafisha moyo.”270 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “… Na punguzeni kula samaki, hakika nyama yake inafanya mwili kusinyaa, na inazidisha kukohoa na inafanya nafsi kuwa nzito.”271 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Ni juu yenu kutumia mafuta ya kula, kwani yanafichua kibofunyongo, yanaondoa kikohozi na yanakaza mishipa ya fahamu…”272 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Usomaji wa Qur’ani, upigaji mswaki na ubani husafisha kikohozi.”273 Imepokewa kutoka kwa Imam al-Baqir (a.s) kuwa alisema: “Ole wako ewe Zurara, hawakughafilika watu kuhusiana na fadhila ya sukari ya mawe, nayo inafaa kwa magonjwa sabini, nayo inaondoa kikohozi, ulaji mkubwa na inang’oa mizizi yake.”274 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Mambo matatu ni raha tupu; sawiiq kavu kabla ya kula kitu, ina  Makarimul-Akhlaq, uk. 166 kutoka kitabu Firdausi.   Twibbul-Aimmat (a.s), uk.386 cha Abdullah Shubbar. 270   Makarimul-Akhlaq, uk. 166. 271   Wasaail Shi’ah, Juz. 17 uk. 18 na mfano wake. 272   Mustadrakul-Nahj, uk. 168. 273   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 66. 274   Twibbul-Aimmat, uk. 67. 268 269

73

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 73

8/10/2017 1:22:01 PM


TIBA YA MAASUMINA

safisha kibofunyongo na kikohozi.” Mpaka ikasemwa: Ataendelea kuacha kingine chochote.275 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Suutar Thaimu na chumvi vinafukuza upepo kutoka kifuani, vinafungua kizuizi na vinaunguza kikohozi.”276 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Sawiiq inang’oa kibofunyongo na kikohozi kutoka kwenye mfuko wa akiba wa chakula, na inakinga aina sabini ya mabalaa.”277 Imam as-Sadiq (a.s) aliisifu dawa ya kikihozi akasema: “Chukua sehemu ya ubani wa Roma, na sehemu ya kundur, na sehemu ya komoni muluuki, na sehemu ya habasoda, vyote viwe sawa sawa, vinasagwa kila kimoja peke yake mpaka vinakuwa laini, kisha vinachanganywa vinakandwa hadi vichanganyike pamoja, kisha ichanganywe pamoja na asali, na ale kila siku mchana na usiku wakati wa kulala, hakika hiyo inafaa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (s.w.t).”278 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Kula figili, hakika ndani yake kuna mambo matatu; … na mizizi yake inakata kikohozi.”279 Imepokewa vilevile kutoka kwa Imam asSadiq (a.s) kuwa alisema: “Ubora wa tende yenu ni Barni inaondoa kila ugonjwa wala haina ndani yake ugonjwa, na inaondoa uchovu na inashibisha, na inaondoa kikohozi, pamoja na kila tembe ya tende kuna wema.”280 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Nabii Musa alilalamika kwa Mola Wake Mlezi kuhusu kikohozi,   Wasaail Shi’ah, Juz. 17 uk. 8 kutoka kitabu Furuu, Juz. 6 uk. 306.   Makarimul-Akhlaq, uk. 191. 277   Wasaail Shi’ah, Juz. 17 uk. 6. 278   Twibbul-Aimmat, uk. 19. 279   Kaafi cha Allama Kulayni. 280   Wasaail Shi’ah, Juz. 17 uk. 105 kutoka kitabu Furuu. 275 276

74

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 74

8/10/2017 1:22:01 PM


TIBA YA MAASUMINA

basi Mwenyezi Mungu akamfunulia yeye, achukue Haliylij Tropical Almond, Baliylij Terminalia bellerica, na ablij kiasi sawa, akikaange kwa mafuta ya samli, na achanganye na asali.” Na akasema (a.s): “Hiyo inaitwa Twarifal ndogo, ndani yake kuna ponyo la kila ugonjwa ila sumu.”281 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa kilitajwa mbele yake kitunguu basi akasema: “Kinaondoa harufu ya kinywa, kinaondoa kikohozi na kinaongeza nguvu wakati wa kujamiiana.”282 Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) kuwa alisema: “Tufaha ni ponyo ya sumu, uchawi na uwendawazimu mwepesi ambao unawapata watu wa ardhini, na kikohozi kilichoshindikana, na hakuna kitu kinachoharakisha zaidi manufaa kuliko hilo.”283 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kuwa alisema: “Vitu vitatu vinazidisha kumbukumbu na vinaondoa kikohozi; usomaji wa Qur’ani, asali na ubani (kundur).”284 Vilevile imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kuwa alisema: “Ndani ya asali ipo ponyo ya kila ugonjwa. Kulamba asali kabla ya kula chochote kunakata kikohozi na kunaondoa manjano na kunazuia kibofunyongo cheusi.”285 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kuwa katika barua yake ya dhahabu aliandika: “Na anayetaka aondokane na kikohozi mwilini mwake au kukipunguza, basi naale kila siku asubuhi kiasi fulani cha jawaarish (yaani vitu ambavyo vina ladha ya ukali kama vile pilipili), kwani kufanya hivyo kunazidisha uhitaji wa kuingia bafuni, hamu ya kukutana kimwili na kukaa juani. Na ajiepushe na kula vyakula vyenye ubaridi, kwani kufanya hivyo kunaondosha   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 386 cha Abdullah Shubbar.   Wasaail Shi’ah, Juz. 17 uk. 168 kutoka kitabu Furuu wal-Mahasin. 283   Wasaail Shi’ah, Juz. 17, uk. 125. 284   Sahifat Ridha (a.s), uk. 68 na Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 66. 285   Sahifat Ridha (a.s), uk. 346.

281 282

75

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 75

8/10/2017 1:22:01 PM


TIBA YA MAASUMINA

kikohozi na kunakichoma.”286 Hadi pale aliposema: “Na anayetaka aondokewe na kikohozi basi ale kila siku asubuhi atrifal Menyanthes Trifoliata ndogo gramu moja.”287 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kuwa alisema: “Kikohozi huondolewa kwa Haliylij Tropical Almond, ya manjano gramu moja, na gramu ya khardali, na gramu ya Aaqir Qarha Anacyclus pyrethrum, basi inasagwa usagaji mzuri na kuwa laini, na kupiga mswaki kwayo kabla ya kula chochote, kwani inaponya kikohozi na huleta harufu nzuri ya kinywa.”288

KUBALEGHE Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Umri wa kubaleghe wa mwanamke ni miaka tisa.”289 Imepokewa kutoka kwa Imam al-Baqir (a.s) kuwa alisema: “Kijana haifai kununua na kuuza, wala hatoki katika uyatima, mpaka afikie miaka kumi na tano, au ajiotee au ziote nywele ngumu sehemu za siri.”290

BALUNGI Faida zake: Balungi linaota katika sehemu zenye kivuli kizuri. Mtu akinywa maua yake kwa maji ya uvuguvugu yatamfaa kwa dondakoo na Ummu Subiyani.   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 325.   Biharul-A nwaar, Juz. 62 UK. 325. 288   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 387 cha Abdullah Shubbar. 289   Biharul-Anwaar, Juz. 103, uk. 162. 290   Wasaail Shi’ah, Juz. 13, uk. 143. 286 287

76

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 76

8/10/2017 1:22:01 PM


TIBA YA MAASUMINA

Ibn Sina (Avicenna) amesema: Linatuliza maumivu ya kichwa yatokanayo na damu, kwa kunusa na kujipaka, na linafaa kwa ugonjwa wa macho utokanao na joto.”291 Na majani yake hutumiwa kama vile mada tawanyishi yenye kuamsha na kutoa jasho, na inabandikwa katika uvimbe uchungu wa njia ya upumuaji, kama ambavyo inafaa pia kwa maumivu ya maungio ya viungo na mishipa ya fahamu.”292 Na kunywa majani ya balungi yaliyochemshwa kunaponya kikohozi na uvujaji wa damu, na huondoa mikunjo na hupunguza nguvu ya kisukari. Na ama mafuta ya balungi yanaponya maumivu ya kichwa cha moto, na yanawafanya walale wale wakeshaji, na yanafanya ubongo kuwa safi, na yanafaa kwa kipanda uso, kuzidi kwa yabisi na ukavu. Atapaka mafuta hayo kwa kuondoa maradhi ya ngozi na mwasho yabisi. Na yanalainisha sehemu za muunganiko, na yanawaweka vizuri watu wenye kuathiriwa na joto katika zama za kiangazi. – Na miongoni mwa maajabu ya mafuta haya ni kuwa yanatia joto katika masika na ubaridi katika kiangazi, kama Imam Ali (a.s) alivyoelezea. Mtume (s.a.w.w) amesema: “Ubora wetu Ahlul-Bayt kwa watu wengine ni kama vile mafuta ya balungi mbele ya mafuta mengine.”293 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Peaneni balungi kwani Mtume (s.a.w.w) amesema: Kama watu wangelijua yaliyomo ndani ya balungi wangelilishupalia mno.”294   Ajaaibul-Makhluqaat cha Qazwiini, mwishoni mwa kitabu Hayaatul-Hayawan kubra, Juz. 2 uk. 182 cha Dumiriy. 292   Nabataat Twayyibat wa isti’malaatiha, uk. 170 cha Dr. Muhammad Awdaat mwaka 1987. 293   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 221 kutoka kwa kitabu Nawadir Rawandiy. 294   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 221. 291

77

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 77

8/10/2017 1:22:02 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Jipakeni mafuta ya balungi, kwani hayo ni baridi wakati wa kiangazi na yana joto wakati wa masika.”295 Imepokewa pia kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Liondoeni joto la homa kwa balungi na maji baridi, hakika joto lake linatoka katika mdomo wa Jahannam.”296 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Fadhila ya balungi mbele ya mafuta mengine ni kama vile fadhila ya Uislamu mbele ya dini nyingine. Mafuta bora ni mafuta ya balungi, kwani yanaondoa ugonjwa kutoka kichwani na jichoni, basi jipakeni hayo.”297 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Hakika balungi ni baridi wakati wa kiangazi na ya joto wakati wa masika, ni laini kwa wafuasi wetu, yabisi kwa maadui zetu, lau wangelijua watu yaliyomo katika balungi wangelithaminisha kwa kipimo cha wakia ya dinari.”298 Imepokewa kutoka kwake (a.s) kuwa alisema: “Mafuta ya balungi ni baridi wakati wa kiangazi, laini na joto wakati wa masika.”299 Imepokewa kutoka kwa Ayub bin Yakub kuwa alisema: Imam as-Sadiq (a.s) alisema: “Hakitujii kitu kutoka pande zenu kinachotupendeza ziadi sisi kuliko mchele na balungi.”300 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Mafuta ya balungi yanalegeza ubongo au yanaufanya kuwa wenye nguvu.”301   Biharul-Anwaar, Juz. 66, uk. 145.   Khaswal, uk. 117 cha Saduq. 297   Kaafi, Juz. 6 uk. 521 298   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 93. 299   Kaafi, Juz. 6, uk. 521 cha Kulayni. 300   Kaafi, Juz. 6, uk. 521. 301   Kaafi, Juz. 6, uk. 522. 295 296

78

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 78

8/10/2017 1:22:02 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Pakeni nyusi zenu balungi, kwani inaondosha maumivu ya kichwa.”302 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Vitu vinne vinaleta ulinganifu wa maumbile; komamanga la surani, tende iliyopikwa, balungi na hindubaau Chickory.”303 Imepokewa kutoka kwake pia kuwa alisema: “Balungi ni bwana wa mafuta.”304 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Mfano wa balungi mbele ya mafuta ni kama vile muumini kwa watu wengine.” Kisha akasema: “Hakika hilo ni joto wakati wa masika na baridi wakati wa kiangazi, na hakuna mafuta mengine yenye ubora zaidi ya haya.”305

BAHAQU /POLIOSIS Ni ugonjwa ambao huondoa rangi ya ngozi na kusababisha mabaka meupe. Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuhusiana na sanamaki, kuwa alisema: “Ama huo ni amani kutokana na bahaqu, ukoma mbalanga, uwendawazimu, kiharusi na ukosefu wa nguvu…”306 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alilalamikiwa na mtu mmoja kuhusu bahaqu, akasema: “Ingia bafuni na changanya hina na maua, na ujipake kwa hivyo viwili, hakika wewe hakitokusumbua chochote baada ya kufanya hivyo.” Akasema yule mtu: Naapa kwa Mwenyezi Mungu nilifanya mara moja tu Mwenyezi Mungu akaniponyesha ugonjwa huo, na haukurudia tena.307   Kaafi, Juz. 6, uk. 522.   Khiswal, Juz. 1, uk. 249 cha Saduq chapa ya zamani 117. 304   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 93 305   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 93. 306   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 218 307   Twibbul-Aimmat (a.s) 302 303

79

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 79

8/10/2017 1:22:02 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kuwa aliulizwa na mmoja wa masahaba wake kuhusu bahaqu. Muulizaji anasimulia kwamba: “Basi akaniamrisha mimi nipike maashi Lathyrus sativus, Indian pea, (punje za kijani za duara dogo kuliko uwatu) na kuzifanya chakula changu, basi nikafanya hivyo siku kadhaa na hatimaye nikapona.”308 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kuwa alisema: “Chukua maashi Lathyrus sativus, Indian pea, zilizoiva katika siku zake na zisage pamoja na majani yake, na kamua maji na kunywa kabla ya kula kitu, na jipake kabla ya kula kitu juu ya bahaqu.” Basi nikafanya hivyo nikapona.309

BAWASIRI Mtume (s.a.w.w) kuhusu Tini amesema: “Hakika hiyo inakata bawasiri na inafaa katika maunganiko ya nyayo na zaidi katika dole gumba.”310 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Kustanji kwa maji ya baridi ni salama kwa bawasiri.”311 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Kustanji kwa maji ya baridi kunakata bawasiri.”312 Imepokewa kutoka kwa Is’haq Jariri kuwa alisema: Imam alBaqir (a.s) amesema: “Ewe Jariri! Naona rangi yako imekuwa safi, je, una bawasiri?” Nikasema: “Ndiyo ewe mtoto wa Mtume, na ninamuomba Mwenyezi Mungu (a.j) asininyime mimi ujira.” Akas  Makarimul-Akhlaq, uk. 187.   Makarimul-Akhlaq, uk. 187. 310   Makarimul-Akhlaq, uk. 173. 311   Mustatraf, Juz. 2, uk. 349. 312   Tuhful-Uquul, uK. 73. 308 309

80

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 80

8/10/2017 1:22:02 PM


TIBA YA MAASUMINA

ema: “Je, nikuongezee dawa?” Nikasema: Ewe mtoto wa Mtume hakika nimejitibu zaidi ya dawa elfu wala hazikunifaa chochote, na hakika bawasiri inapunguza damu!” …. Akasema (as): “Ole wako ewe Jariri, hakika mimi ni mganga wa waganga, na kichwa cha wasomi, na rais wa wenye hekima, na madini ya wanazuoni, na bwana wa watoto wa Mitume juu ya uso wa ardhi.” Nikasema: “Vivyo hivyo ewe bwana wangu.” Akasema (as): “Ikiwa bawasiri yako ni ya kike basi inapunguza damu.” Nikasema: “Umesema kweli ewe mtoto wa Mtume (s.a.w.w).” Akasema: “Ni juu yako kuchukua mshumaa na mafuta ya yasimini na maziwa, asali na sumaq/Sumac na surukatani, ikusanye katika upawa juu ya moto, na ikishachanganyika, chukua kiasi kidogo bandika kwenye makalio yako, utapona kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (a.j).” “Naapa kwa Mwenyezi Mungu ambaye hapana mungu ila Yeye, sikufanya ila mara moja tu hadi nilipopona, na sikuhisi baada ya hivyo damu wala maumivu.”313 Imepokewa kutoka kwa Abu Abdillah (a.s) kutoka kwa babu yake kutoka kwa baba yake (a.s), amesema: Amirul-Muuminina Ali (a.s) amesema: “Kurefusha ukaaji msalani kunasababisha bawasiri.”314 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa aliulizwa kuhusiana na liki akasema: “Kula, hakika ndani yake kuna mambo manne; unasafisha kinywa, unafukuza harufu mbaya, unakata bawasiri, nao ni kinga ya mbalanga kwa yule anayedumu katika ulaji wake.”315 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Karoti ni kinga ya maradhi ya uvimbe wa utumbo mpana (coli  Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 81.   Khiswal, Juz. 1, uk. 18 cha Saduq. 315   Khiswal, Juz. 1, uk. 250 cha Saduq. 313 314

81

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 81

8/10/2017 1:22:02 PM


TIBA YA MAASUMINA

tis), na inafaa kwa bawasiri, na inasaidia katika tendo la ndoa.”316 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) pia kuwa alisema: “Komoni muluki na karanga zinachoma bawasiri na zinafukuza hurufu mbaya…”317 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuhusiana na ghubayraa Rowan – sorbus, kuwa alisema: “Hakika nyama yake huotesha nyama…nayo ni kinga ya bawasiri na utokaji wa matone ya haja ndogo.”318 Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) kuwa alisema: “Chakula bora ni wali, unapanua utumbo na unakata bawasiri, na sisi tunapenda kuwa kama vile watu wa Iraq kwa kula kwao wali na tende, kwani hivyo viwili vinapanua utumbo na vinakata bawasiri.”319 Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) kuwa alisema: “Sioni kula nyama ya hubari Houbara bustard (ni mojawapo ya aina za tandawala) kuwa ni tatizo, kwani ni nzuri kwa bawasiri, na maumivu ya tumbo, nayo ni miongoni mwa yale yanayosaidia kuzidisha ngvu wakati wa tendo la ndoa.”320 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kuwa baada ya kueleza dawa ya bawasiri alisema: “Azimia kula samaki, siki na mbogamboga.”321 Vilevile imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) katika barua yake ya dhahabu kwenda kwa Maamuni alisema: “Na yule anayetaka amani kutokana na maumivu ya chini ya kitovu na maumivu ya bawasiri, basi ale kila usiku tende saba za barani kwa mafuta ya samli, na ajipake baina ya sehemu zake za siri kwa mafuta halisi ya yungiyungi.”322   Fusuul Muhimmat cha Hurru Aamiliy na Makarimul-Akhlaq, uk. 184 .   Makarimul-Akhlaq, uk. 191. 318   Makarimu-Akhlaq, uk. 176. 319   Mahasin, uk. 504. 320   Makarimul-Akhlaq, uk. 161. 321   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 102. 322   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 324. 316 317

82

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 82

8/10/2017 1:22:02 PM


TIBA YA MAASUMINA

HAJA NDOGO Katika wosia wa Mtume (s.a.w.w) kwa Ali (a.s) alisema: “Ewe Ali, vitu tisa vinasababisha usahaulifu…. kujisaidia haja ndogo kwenye maji yaliyotuama.”323 Mtume (s.a.w.w) amesema: “Yule anayeacha kujisaidia haja ndogo hufuatiwa na janaba, na ninachelea kutokuwa na uhakika wa kubakia maji katika mwili wake, pia inamsababishia ugonjwa ambao hauna dawa.”324 Imepokewa kutoka kwa Ali (a.s) kuwa alisema: “Mzizi wa figili unakata kikohozi na unameng’enya chakula, na majani yake yanasaidia utokaji wa haja ndogo.”325 Omar Afraq alilalamika kwa Imam al-Baqir (a.s) kuhusu utokaji wa matone ya haja ndogo, Imam (as) akasema: “Chukua harmala Peganum na ioshe kwa maji baridi mara sita, na kwa maji ya moto mara moja, kisha ikaushe kivulini, kisha mwagia juu yake mafuta halisi ya rozi, kisha kunywa asubuhi kabla ya kula chochote, hakika utakatika utokaji matone kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu.”326 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Kula figili, hakika ndani yake ina vitu vitatu; jani lake linafukuza harufu mbaya, moyo wake unarahisisha haja ndogo na mmeng’enyo wa chakula, na mzizi wake unakata kikohozi.”327 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuhusu ghubayraa Rowan – sorbus, amesema: “Hakika nyama yake huotesha nyama … nayo ni kinga ya bawasiri na utokaji wa matone wa haja ndogo...”328   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 28 kutoka kitabu Man la yahdhuruhul-Faqiih na Khiswal, Juz. 2, uk. 47 chapa ya kwanza. 324   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 312 cha Abdullah Shubbar. 325   Makarimul-Akhlaq, uk. 182. 326   Twibbul-Aimmat (as), uk. 68. 327   Kaafi cha Allama Kulayni. 328   Makarimul-Akhlaq, uk. 176. 323

83

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 83

8/10/2017 1:22:02 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Mufadhal amesema: Nilimlalamikia Imam as-Sadiq (a.s) kuwa mimi ninajisaidia haja ndogo kwa shida, basi akaniambia: Chukua habasoda na tumia kila usiku.”329 Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) kuwa alisema: “Mkojo wa ngamia ni bora kuliko maziwa yake, Mwenyezi Mungu amejaalia ponyo katika maziwa yake.”330 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kuwa alisema: “Ukiwa na njaa kula, na ukiwa na kiu kunjwa, na unapobanwa na haja ndogo basi jisaidie…”331 Katika barua ya dhahabu Imam Ridha (a.s) amesema: “Na yule anayetaka asilalamikie kibofu chake cha mkojo basi asizuie haja ndogo, hata kama akiwa juu ya myama.”332 Imepokewa kutoka kwa Musa bin Abdullah bin Hasan kuwa alisema: Niliwasikia wazee wetu wakisema: “Maziwa ya ngamia ni tiba ya kila ugonjwa na maradhi ya mimea, na mtu mwenye pumu inamfaa mikojo yake. (na katika hadithi nyingine): Na mwenye tumbo kubwa inamfaa mikojo yake.”333 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Asijisaidie mmoja wenu njiani, wala juu ya dari katika anga, wala katika maji yanayotiririka; basi atakayefanya hivyo na akapatwa na chochote asimlaumu yeyote ila nafsi yake, kwani maji yana wenyewe na pia anga lina wenyewe. Atakapojisaidia mmoja wenu asiuinue juu wala asiuelekezee upepo.”334   Makarimul-Akhlaq, uk. 176.   Makarimul-Akhlaq, uk. 194. 331   Fiqhu Ridha (a.s), uk. 340. 332   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 323. 333   Kaafi cha Allama Kulayni. 334   Tuhful-Uquul, uk. 73. 329 330

84

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 84

8/10/2017 1:22:02 PM


TIBA YA MAASUMINA

MAYAI Miongoni wa wosia wa Mtume (s.a.w.w) kwa Ali (a.s) ni kuwa alisema: “Ewe Ali, kula mayai ambayo yamehitilafiana ncha zake, na miongoni mwa samaki wale wenye magamba, na miongoni mwa ndege wale wenye kupiga mbawa, na acha nisiyokueleza, na miongoni mwa ndege ni wale wenye kidole gumba kwa nyuma na kibofu cha kooni.”335 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Hakika Nabii mmoja alilalamika kwa Mwenyezi Mungu (a.j) uchache wa vizazi kwa umma wake, basi akamwamrisha awaamrishe kula mayai. Basi wakafanya hivyo na vikakithiri vizazi vyao.”336 Imepokewa kutoka Imam al-Baqir (a.s) kuwa aliulizwa uwepo wa mayai mengi kisiwani, akasema: “Kula yale ambayo yametofautiana ncha zake mbili (yaani uwe upande wake mmoja umeinama zaidi kuliko mwingine), na wala usile yale ambayo ncha zake mbili ziko sawa sawa.”337 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Mmoja wa Manabii wa Mwenyezi Mungu alilalamika kwa Mwenyezi Mungu uchache wa kizazi, basi akamwambia: Kula nyama kwa mayai.”338 Lilitajwa yai mbele ya Imam as-Sadiq (a.s), akasema: “Hakika hilo ni hafifu, nyama yake haina madhara.”339 Imepokewa kutoka kwa Hamran bin Aayun amesema: Nilimwambia Abu Abdillah as-Sadiq (a.s): Hakika watu wanadhani   Makarimul-Akhlaq, uk. 441.   Wasaail Shi’ah, Juz. 17, uk. 58. 337   Ramzu Sihat, uk. 144, Wasaail Shi’ah, Juz. 17, uk. 62 na Makarimul-Akhlaq uk.164. 338   Wasaail Shi’ah, Juz. 17, uk. 57. 339   Wasaail Shi’ah, Juz. 17, uk. 57. 335 336

85

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 85

8/10/2017 1:22:02 PM


TIBA YA MAASUMINA

kwamba unjano wa yai ni mwepesi zaidi kuliko weupe, akasema (a.s): “Ndiyo wanaamini hivyo?” Nikasema: Wanadhani manyoya yanatokana na weupe na mshipa wa fahamu unatokana na unjano. Akasema: Basi manyoya ni mepesi zaidi.” (Kwa hivyo Imam (a.s) anakiri kuwa weupe ni mwepesi zaidi kuliko unjano, na hili limethibiti kielimu). Imepokewa kutoka kwa Muhammad bin Umar bin Abi Hasanat Jammal, amesema: Nilimlalamikia Imam Kadhim (a.s) kuhusu uchache wa watoto, akasema: “Muombe msamaha Mwenyezi Mungu na kula yai kwa kitunguu maji.”340 Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) kuwa alisema: “Zidisheni kula mayai kwani yanaongeza upatikanaji wa watoto.”341 Mshairi mmoja amesema: “Na imekuja kutoka kwao katika hadithi kwamba, kuzidisha kula mayai kunaongeza upatikanaji wa watoto.” Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) katika barua yake ya dhahabu kwenda kwa Maamuni: “Udumishaji wa kula mayai unadhihirisha vichunusi usoni… na kuzidisha kula mayai na kuendelea kula kunazalisha takataka za chini na upepo ndani ya mfuko wa chakula, 342 na ujazaji wa mayai yaliyolowekwa yanasababisha pumu na ukatikaji wa pumzi.”343

Wasaail Shi’ah, Juz. 17, uk. 58.   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 58 kutoka kitabu Furuu wal-Mahasin. 342   Amesema Ibn Baytwar: Na inampasa ajiepushe na mayai yaliyolowekwa ndani ya maji kwa yule anayesumbuliwa na kubirukwa na tumbo. 343   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 321. 340 341

86

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 86

8/10/2017 1:22:02 PM


TIBA YA MAASUMINA

KUSAIDIANA KWA MADA NA ATHARI ZAKE Hadithi: Imepokewa kutoka kwa Abdullah bin Ja’far amesema: “Nilimuona Mtume (s.a.w.w) usingizini akiwa na tango, na kushotoni kwake tende, naye akila huku na huku.”344 Na imenukuliwa kutoka kwa Qurtubi amesema: Inachukuliwa kuwa inafaa kuchanganya sifa za vyakula na maumbile yake, na matumizi yake kwa kufuata kanuni za tiba, kwa sababu katika tende kuna joto, na katika tango kuna baridi, na akila pamoja huwa inapatikana hali ya kati na kati. Na hii ni asili kubwa katika muunganiko wa madawa.345 Alikuwa Mtume (s.a.w.w) akila tango kwa chumvi, na akila tikitimaji kwa jibini346 …. Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Jibini na karanga katika kila moja wapo kuna ponyo, na vikitofautiana ­itakuwa kila moja kati ya hizo mbili ni ugonjwa.”347 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “­ Jibini na karanga kila moja kati ya hizo mbili ni ponyo, na ikiwa zitatofautiana itakuwa kila moja kati ya hizo ni ugonjwa.”348 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Yule atakayelala hali ya kuwa tumboni mwake kuna samaki, hakufatilizia kwa tende au asali, mishipa ya kiharusi itaendelea kugonga mpaka atakapoamka asubuhi.”349   Ramzu-Sihat, uk. 236.   Ramzu-Sihat, uk. 236. 346   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 299. 347   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 281. 348   Makarimul-Akhlaq, uk. 189. 349   Wasaail Shi’ah, Juz. 17, uk. 54. 344 345

87

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 87

8/10/2017 1:22:02 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Vitu vinne vinasafisha macho, vinanufaisha wala havidhuru” basi akaulizwa kuhusiana na hivyo, akasema: “Suutar/Thaimu na chumvi inapokusanyika pamoja, na komoni muluki na karanga ikikusanyika pamoja.” Ikaulizwa: Na kwa kitu gani vinafaa hivi vinne pindi vinapokusanyika pamoja? Akasema: “Komoni muluki na karanga zinaunguza bawasiri na zinafukuza upepo na vinapendezesha ngozi, na vinafanya kuwa mgumu mfuko wa chakula, na vinachemsha kiungulia. Na Suutar/Thaimu na chumvi vinafukuza upepo kutoka kifuani, na vinafungua vizuizi, vinaunguza kikohozi, na vinazungusha maji, na vinaleta harufu nzuri, na vinalainisha mfuko wa chakula, na vinaondoa harufu mbaya kinywani na vinaimarisha dhakari.”350

KUSIGANA KWA VIASILI VYA VYAKULA Mtume (s.a.w.w) alikuwa hakusanyi katu kati ya maziwa na samaki, wala kati ya maziwa na limao.351 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) katika kitabu RisalatulDhahabiyah, katika barua aliyomwandikia Maamuni kuwa alisema: “Na jihadhari ewe Kiongozi kukusanya baina ya yai na samaki katika mfuko wa chakula wakati mmoja, kwani hivyo viwili wakati vinapokusanyika pamoja tumboni mwa mtu vinazalisha uvimbe katika maungio, ugonjwa wa mingurumo ya tumbo, bawasiri na maumivu ya magego. Na maziwa na pombe ambayo wanakunywa watu wake, pindi vikikusanyika pamoja huzalisha uvimbe katika maungio na ukoma.”352   Makarimul-Akhlaq, uk. 191.   Twibbul-Nabawiy, uk. 173 cha ibn Qaym Jawziyyat. 352   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 321. 350 351

88

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 88

8/10/2017 1:22:02 PM


TIBA YA MAASUMINA

KUPIGA MIAYO Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Kupiga miayo ni neena miongoni mwa neema za Mwenyezi Mungu, na pindi akipiga miayo mmoja wenu basi amshukuru Mwenyezi Mungu, wala asinyanyue upigaji wa miayo wake.353 Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) kuhusiana na mrehani wa milimani, amesema: “Na unaondoa uzito na unafanya uzuri upigaji miayo pia tendo la ndoa.”354 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kuwa alisema: “Hapigi mtu miayo ila husagika chakula chake. Na wala hapigi miayo ila hulainisha mapito ya chakula.”355 UCHOKOAJI WA MENO Uchokoaji ni kitendo cha kutoa mabaki ya chakula kwenye meno. Hadithi: Mtume (s.a.w.w) amesema: “Chokoeni mabaki ya chakula na sukutueni kwa maji, kwani kufanya hivyo kunayafanya meno kuwa na afya na imara.”356 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: Mtume (s.a.w.w) amesema: “Chokoeni meno, kwani kufanya hivyo kuna maslahi kwa ufidhi na kunaleta uimara.”357 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Msichokoe meno kwa mua, wala kwa Aasi wala kwa komamanga.”   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 57.   Makarimul-Akhlaq, uk. 179. 355   Al-Fiqhu al-Mansuub li imam Ridha (a.s), uk. 391. 356   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 291. 357   Kaafi cha Kulayni. 353 354

89

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 89

8/10/2017 1:22:02 PM


TIBA YA MAASUMINA

Na akasema: (s.a.w.w): “Hakika mimea hiyo hutikisa mishipa ya meno.”358 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: Mtume (s.a.w.w) alimpatia Ja’far bin Abi Twalib kichokoa meno, akasema: “Ewe Ja’far, chokoa meno, kwani kufanya hivyo kuna maslahi kwa kinywa (au amesema: Maslahi ya ufidhi) na huleta riziki.”359 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Chokoeni meno yenu, kwani kufanya hivyo ni usafi, na usafi unatokana na imani, pia mhusika wake ataingia peponi.”360 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Yule anayetumia miti miwili (yaani vichokoa meno na mswaki) atasalimika na maumivu ya koleo la kung’olea meno (yaani hatahitaji koleo kung’olea meno kinywani mwake).”361 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Jibrail aliteremka kwa Mtume (s.a.w.w) akiwa na mswaki na vichokoa meno na kinyonya damu chafu.”362 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Msichokoe meno yenu kwa kijiti cha mrehani, wala kigogo cha mkomamanga, kwani hivyo viwili vinachochea mbalanga.”363 Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) kuwa alisema: “Miongoni mwa haki ya kuchokoa meno ni uuzungushe ulimi kinywani mwako, kile kitakachokukubalia kimeze, na kile kitakachokukatalia kichokoe, kisha kiteme.”364   Wasaail Shi’ah, Juz. 16, uk. 434.   Wasaail Shi’ah, Juz. 16, uk. 532. 360   Ramzul-Sihat, uk. 5 cha Dahsurkhi. 361   Ramzul-Sihat, uk. 5 cha Dahsurkhi. 362   Mahasin, uk. 558 cha Barqi. 363   Khiswal, Juz. 1, uk. 63 cha Saduq. 364   Makarimul-Akhlaq, uk. 145. 358 359

90

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 90

8/10/2017 1:22:02 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kuwa alisema: “Amenihadithia mimi baba yangu kutoka kwa Husein bin Ali (a.s), amesema: Alikuwa Amirul-Muuminina Ali (a.s) akituamrisha sisi kuchokoa meno yetu (yaani kutoa mabaki ya chakula kati ya meno yetu), hatukunywa maji isipokuwa tulisukutua mara tatu.”365

TUFAHA Faida zake: Tufaha ni tunda tajiri kwa chumvi, mfano wa kalisiamu, semitali ambayo huwaka haraka, chuma na potasiamu, na vitamini lukuki, mfano vitamini B na C. Na kutoka hapa zikaja faida zenye kumaizi na kuchanganua ili kulitofautisha tufaha hili lenye faida nyingi na matunda mengine.366 Mtume (s.a.w.w) amesema: “Kuleni tufaha kabla hamjala kitu, kwani hilo linaosha na linasafisha mfuko wa chakula.”367 Katika wosia wa Mtume (s.a.w.w) kwa Ali (a.s) amesema: “Ewe Ali. Vitu tisa vinasababisha usahaulifu; ulaji wa tufaha chachu, na ulaji wa kazbara na jibini.”368 Imekuja katika hadithi: “Hakika tufaha linasababisha usahaulifu, kwani hilo huleta kizazi ndani ya mfuko wa chakula wa mke.”369 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Ni juu yenu kula tufaha, kwani linasafisha na kutia harufu nzuri mfuko wa chakula.”370   Sahifat Ridha (a.s), uk. 89.   Angalia namna ya utengezaji wa siki ya tufaha katika maada: Siki. 367   Ramzul-Sihat, uk. 155. 368   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 128. 369   Makarimul-Akhlaq, uk. 173. 370   Ramzul-Sihat, uk. 155. 365 366

91

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 91

8/10/2017 1:22:02 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Kuleni tufaha, kwani linalainisha mfuko wa chakula.”371 Imepokewa kutoka kwa Imam al-Baqir (a.s) kuwa alisema: “Unapotaka kula tufaha linuse kisha lile. Jua kwamba ukifanya hivyo linatoa kutoka mwilini mwako kila aina ya ugonjwa na madhara, na linatuliza yale ambayo yanapatikana kutokana na harufu zote.”372 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Lau watu wangelijua yaliyomo ndani ya tufaha wasingeliwatibu wagonjwa wao kwa dawa nyingine ila kwalo, kwani lina manufaa zaidi na hususan katika vifua, hakika hilo linamletea mtu furaha.”373 Imepokewa kutoka kwake (a.s) kuwa alisema: “Walisheni wagonjwa wenu wa homa tufaha, hakuna kitu chenye faida zaidi kuliko tufaha.”374 Imepokewa kutoka kwa Abu Yusuf Qindiy amesema: Watu walipatwa na homa wakati tukiwa Makka, nami pia ikanipata, basi nikamwandikia barua Imam Abu Hasan Kadhim (a.s), yeye akaniandikia: “Kula tufaha,” nikala basi nikapona.375 Imepokewa kutoka kwa Abu Yusuf Qindiy amesema: Niliingia Madina nikiwa pamoja na ndugu yangu Saif, basi watu wakapatwa na ugonjwa wa utokaji wa damu puani, na alikuwa mtu akitokwa na damu puani kwa muda wa siku mbili anakufa. Nikarejea nyumbani kwangu ghafla nikamkuta Saif akitokwa na damu puani kwa wingi, nikaingia kwa Abu Abdillah (a.s), akasema: “Ewe Ziyad, mlishe Saif tufaha”. Basi nikarejea na nikamlisha yeye na akapona.376   Kafii cha Kulayni.   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 135. 373   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 135 na Kaafi cha Kulayni. 374   Ramzul-Sihat, uk. 33. 375   Wasaail Shi’ah, Juz. 17, uk. 127 kutoka Furuu Kaafi na Mahasin cha Barqi. 376   Wasaail Shi’ah, Juz. 17, uk. 126. 371 372

92

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 92

8/10/2017 1:22:02 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Kula tufaha kwani hilo linazima joto na linatia baridi tumbo na linaondoa homa.”377 Imepokewa vilevile kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kwamba alitajiwa suala la homa, akasema: “Hakika sisi watu wa nyumba ya Mtume hatutibiani ila kwa maji ya baridi ambayo humwagiwa juu yetu, na kwa ulaji wa tufaha.”378 Imepokewa kutoka kwa Muhammad bin Faydh amesema: Nilimwambia (As-Sadiq) nafsi yangu nimeitoa fidia kwako, tuna mgonjwa anaumwa, basi waganga wanamuamrisha kutumia lishe kamili? Akasema (a.s): “Hapana, lakini sisi Ahlul-Bayt hatutumii lishe kamili ila tende. Ndiyo, tunajitibu kwa tufaha na maji ya baridi.”379 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kwamba alipomuona mmoja wa masahaba zake akila tufaha alimwambia: “Je, unakula hili hali ya kuwa watu wanalichukia?” Akasema: “Imenipata mimi homa usiku huu ndipo nikatuma na nikaletewa, nalo linaondoa homa pia linatuliza joto.”380 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Hakuna dawa inayojulikana zaidi kwa utoaji wa sumu na yenye manufaa zaidi kuliko sawiiq ya tufaha.”381 Imepokewa pia kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Kula tufaha kwani linatuliza joto, na linatia ubaridi tumbo na linaondoa homa.”382 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Matano ni matunda ya peponi lakini yapo duniani; komamanga la Malasi, tufaha la Isfahani, pera, zabibu na tende ya Mashani.”383   Wasaail Shi’ah, Juz. 3, uk. 30 cha Hurru Aamiliy.   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 93 na Mahasin cha Barqi. 379   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 140. 380   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 93. 381   Kaafi cha Kulayni. 382   Wasaail Shi’ah, Juz. 17, uk. 125 kutoka kitabu Mahasin uk. 551. 383   Mahasin na Khiswal, Juz. 1, uk. 289. 377 378

93

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 93

8/10/2017 1:22:03 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Abu Bakiir amesema: Nilitokwa na damu, basi akaulizwa Imam as-Sadiq (a.s) kuhusu hilo, akasema: “Mnywesheni sawiiq ya tufaha” basi ukakatika utokaji wa damu puani.384 Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) kuwa alisema: “Katika tufaha kuna ponyo ya mambo kadhaa, ikiwemo ponyo ya sumu, uchawi na uchizi, na kikohozi sugu. Na hakuna kitu kinacho harakisha manufaa zaidi kuliko hilo.”385 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kuwa alisema: “Hakika alikuwa Mtume (s.a.w.w) akipendezwa na uangaliaji wa furungu la rangi ya kijani na tufaha jekundu.”386 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Kula tufaha kunasafisha mfuko wa chakula.” [basi ulaji wa tufaha unaondoa uchafu kutoka kwenye mfuko wa chakula na kuusafisha kabisa].387

TENDE Tende kimsingi ina sukari asilimia 64 na protini asilimia 20. Na baadhi ya chumvi mfano wa kalisiamu na chuma. Na ina kiasi kikubwa cha vitamin, mfano wa vitamin A, na vitamin hivi vinatia nguvu misuli na hulainisha mishipa ya damu, kama vile inavyotia unyevunyevu utumbo na kuulinda kutokana na uvimbe na uchungu na udhaifu. Kwa hivyo tende ina neema nyingi ya sukari, na hasa hasa sukari ya matunda na sukari ya zabibu (glukosi), kazi yake ni sawa na kazi ya asali. Na kipambanuzi cha sukari hizi ni kwamba hiyo inaharakisha ufyonzaji, na ni rahisi kufanana na hali ya mwili, na inakwen  Makarimul-Akhlaq, uk. 193.   Makarimul-Akhlaq, uk. 173. 386   Wasaail Shi’ah, Juz. 17, uk. 136. 387   Khiswal, Juz. 2, uk. 212. 384 385

94

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 94

8/10/2017 1:22:03 PM


TIBA YA MAASUMINA

da moja kwa moja kwenye damu, na hutia nguvu viungo na kuleta uchangamfu, kwa hivyo ni mustahabu kula tende kwa wafungaji, ili kuongeza sukari mwilini kwa dakika chache. Faida zake: Na sukari iliyomo ndani ya tende faida zake haiishii tu katika kutia joto na nguvu na uchangamfu, bali inafanya kazi ya uoshaji wa kibofu cha mkojo na husafisha ini, na kwa hivyo tende ni bora zaidi kuliko chakula ambacho hupewa mgonjwa ambaye ini na nyongo na moyo vimeshindwa kufanya kazi kabisa, na maradhi yote mengine ambayo hulazimika kujiepusha nayo kutokana na protini nyingi na mafuta, na inahitaji harara ya hali ya juu ili kufunika haja za mwili. Na kuongezea katika hayo ni kwamba, tende inaupa mwili baadhi ya chumvi nyingi, mfano wa mpangiko wa magnesi na shaba na kibiriti na chuma na kalisiamu na potasiamu. Pia ina mada za florini, ambazo zinazuia uozaji wa meno, achilia mbali kalisiamu na semitali ambazo huchangia katika suala la ujenzi wa meno. Si hayo tu, bali inaelezwa kuwa tende ni kama vile mada ya msingi ya vyakula kwa mjamzito kulingana na majaribio mbalimbali ya elimu za kisasa, na kwa hivyo inasaidia kuwa na sukari na vitamin lukuki na idadi kubwa ya madini ya chuma kwa mwanamke na mtoto wake. Na kwa hivyo ulaji wa tende pamoja wa maziwa huzingatiwa kuwa ni mlo kamili wa mtu. Ni kama ilivyothibiti kielimu kuwa viambata vya tende, na hasa hasa uchachu ambao upo ndani yake, unasaidia kuangamiza idadi kubwa ya vijidudu mwilini. Zaidi ya hayo ni kwamba, tende inasaidia kuondoa kikohozi kutoka katika mfumo wa upumuaji. Na kwa ujumla faida hizi zinatokana na wosia wa Mtume (s.a.w.w) na Maimamu watoharifu (a.s) waliosisitiza ulaji wa tende, 95

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 95

8/10/2017 1:22:03 PM


TIBA YA MAASUMINA

na hasa hasa kabla ya kula chochote, na wakataja katika hadithi zao faida zaidi ya hizo tulizotajwa.388 Na hakika masomo mbali mbali ya kisasa yamebainisha manufaa yake lukuki ya kitiba, ikiwa ni pamoja na kuwa kinga dhidi ya maradhi ya saratani, hiyo ni kutokana na kuwa na mada ya maginiziamu ambayo ina uhusiano mkubwa na saratani, na hakika imethibiti katika tafiti kwamba ardhi ambazo hulimwa mitende kwa wingi ni nadra mno watu wake kupatwa na maradhi hayo.389 Na tende inalainisha maumbile, na inaongeza manii, na inapoliwa pamoja na tango na saladi huwa ina manufaa zaidi. Ama tende ikitafunwa baada ya kula kitunguu saumu hakika hiyo inakata harufu yake. Hadithi: Mtume (s.a.w.w) amesema: “Hakika miongoni mwa miti upo ambao majani yake hayadondoki, nao ni mfano wa Mwislamu, nijuzeni ni upi huo?” Basi watu wakawa watajata miti ya shamba. Kisha wakasema: Ewe Mtume(s.a.w.w) tujuze ni upi huo? Akasema: “Ni mtende. Hakika mtende tangu unapoota hadi kukua na kuwa yabisi huliwa kwa aina tofauti ya mazao yake, na kisha mazao yake yote huleta manufaa mengi. Vivyo hivyo ndivyo ilivyo baraka ya Mwislamu kwa ujumla katika hali zake zote, na manufaa yake ni yenye kuendelea kwake mwenyewe na kwa asiyekuwa yeye.”390 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema “Kuleni tende kabla ya kula chochote, kwani inaua vijidudu tumboni.”391   Majmuatul-Aathar, Juz. 2, uk. 327 cha imam Ridha (a.s).   Ajaaibul-Makhluqaat, Juz. 2, uk. 178 cha Quzwayni. 390   Tafsiri Jalaleni, surat Raad tafsiri ya aya ya 5. 391   Sahifat Ridha (a.s), uk. 51. 388 389

96

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 96

8/10/2017 1:22:03 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Yule anayepata tende basi afuturu kwayo, na yule asiyepata basi afuturu kwa maji kwani hayo ni tohara.”392 Mtume (s.a.w.w) aliletewa zawadi ya tende barni miongoni mwa tende za Yemani, akasema: “Tuleteeni zaidi tende hizi. “Basi hapo akashuka Jibrail akasema: “Tende barni inashibisha, inaongeza furaha na inaleta murua, nayo ni dawa wala hakuna ugonjwa ndani yake, na kila tende ina wema, na inamridhisha Rahmani, na inamchukiza shetani, na inazidisha katika maji ya uti wa mgongo.”393 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Hakika Mtume (s.a.w.w) aliletewa zawadi ya tende, akasema: ‘Ni ipi tende yenu hii?’ Wakasema: Barni Ewe Mtume(s.a.w.w). Akasema: ‘Huyu hapa Jibrail ananipa habari kuwa ndani ya tende yenu hii kuna mambo tisa; inamfadhaisha shetani, inatia nguvu mgongo, inaongeza nguvu katika tendo la ndoa, inazidisha usikivu, na uonaji, na inafanya kuwa karibu na Mwenyezi Mungu, inamkimbiza shetani, inameng’enya chakula, inaondoa ugonjwa na inaondoa harufu mbaya ya kinywa.”394 Imepokewa kutoka kwa Muhammad bin Faydh amesema: Nilisema kumwambia Imam as-Sadiq: Nafsi yangu nimeitoa fidia kwako, kuna mgonjwa anaumwa miongoni mwetu basi waganga wanamwamrisha kutumia lishe kamili? Akasema: “Hapana, lakini sisi Ahlul-Bayt hatutumii lishe kamili ya tende, tunajitibu kwa tufaha na maji baridi.”395 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Mwanamke akijifungua chakula chake cha awali kiwe ni tende mbichi   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 296.   Wasaail Shi’ah, Juz. 17, uk. 108. 394   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 107 na kitabu Mahasin cha Burqi. 395   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 140. 392 393

97

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 97

8/10/2017 1:22:03 PM


TIBA YA MAASUMINA

tamu au tende mbivu, kwani lau kama kungekuwa kuna kitu bora zaidi kuliko hizo Mwenyezi Mungu angelimlisha Maryam pindi alipojifungua Isa (a.s).”396 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Hali mjamzito chochote, wala hajitibu kwa kitu bora zaidi kuliko tende. Mwenyezi Mungu (a.j) amesema: ‘Na litikise kwako shina la mtende, litakuangushia tende nzuri, zilizoiva, basi ule na unywe na uburudishe macho.’”397 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Tende zenu bora ni barni, basi walisheni wanawake zenu wakati wa nifasi zao, watawazalia nyinyi wasichana warembo (na katika hadithi nyingine): Watawazalia nyinyi watoto wazuri.”398 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Walambisheni watoto wenu wadogo tende, hivyo ndivyo alivyofanya Mtume (s.a.w.w) kwa Hasan na Husein (a.s).”399 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Tofautianeni na walevi, kuleni tende, hakika ndani yake kuna ponyo la kila ugonjwa.”400 Imepokewa kutoka kwa Imam Hasan (a.s) kuwa alisema: “Hakika Mtume (s.a.w.w) alikuwa kitu cha mwanzo alichofuturu katika msimu wa tende mbivu ni tende mbivu, na katika msimu wa tende kavu ni tende kavu.”401 Imepokewa kutoka kwa Imam al-Baqir (a.s) au Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema kuhusiana na kauli ya Mwenyezi Mungu: “Basi   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 296.   Sura 19 aya 25 – 26. 398   Makarimu-Akhlaq, uk. 169. 399   Wasaail Shi’ah, Juz. 17, uk. 18 kutoka kitabu Khiswal. 400   Wasaail juz. 17 uk. 104. 401   Ramzul-Sihat, uk. 157,cha Dahsurkh 396 397

98

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 98

8/10/2017 1:22:03 PM


TIBA YA MAASUMINA

mtu aangalie chakula chake.”402 akasema: “Chakula kizuri zaidi ni tende.”403 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Hawakujitibia wanawake kwa kitu bora mfano wa tende mbivu, hakika Mwenyezi Mungu alimlisha Maryam (a.s) katika nifasi yake.”404 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Matano ni matunda ya peponi yapo hapa duniani; komamanga Malasi, tufaha la Isfahani, pera, zabibu na tende la Mashani.”405 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Yule anayekula kila siku tende saba zilizosindikwa kabla ya kula kitu kutokana na tende ya hali ya juu (sehemu ya mashariki ya Madina) haitomdhuru yeye sumu, wala uchawi wa shetani.”406 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Yule aliyelala ndani ya tumbo lake kuna samaki, na hakufuatilizia kwa tende au asali, itaendelea mizizi ya kiharusi ikipiga juu yake mpaka anapoamka asubuhi.”407 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Walisheni wanawake wenu tende barni katika nifasi zao, itawafanya wawe wazuri watoto wenu.”408 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Hakuletewa Mtume (s.a.w.w) chakula ikiwepo na tende, basi yeye alianza kula tende.”409   Sura 80 aya 24.   Wasaail Shi’ah, Juz. 17 uk. 103 kutoka kitabu Furuu Kaafi na Mahasin. 404   Ramzul-Sihat, uk. 156 cha Dahsurkh. 405   Mahasin na Khiswal, Juz. 1, uk. 289 cha Saduq. 406   Kaafi cha Kulayni. 407   Wasaail Shi’ah, Juz. 17, uk. 54. 408   Makarimul-Akhlaq, uk. 169. 409   Ramzul-Sihat, uk. 157 cha Dahsurkh. 402 403

99

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 99

8/10/2017 1:22:03 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Alikuwa Mtume (s.a.w.w) akipendezwa na utamu wa tende.”410 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Tende yenu bora ni barni (asili yake ni barniik kutoka Magharibi mwa Iran, na maana yake ni ubebaji mzuri) inaondoa kila aina ya maradhi na haina ndani yake ugonjwa, na inaondoa uchovu, na inashibisha, na inaondoa kikohozi, na kila tende ina wema, na inatia utamu.”411 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuhusiana na tende kuwa alisema: “Hakika ndani yake kuna ponyo ya sumu, kwani haina ugonjwa ndani yake wala madhara, na hakika ulaji wa tende saba zilizosindikwa wakati wa kulala inaua vijidudu tumboni.”412 Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) kuwa alisema: “Aliandikia mmoja wa masahaba wake kwamba akimlalamikia harufu mbaya kinywani, akasema: Kula tende barni.”413 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kuwa alisema: “Hakika Mtume (s.a.w.w) aliletewa tikitimaji na tende mbivu, basi akala vyote viwili, akasema: ‘Hivi viwili ni vizuri zaidi.’”414 Kutoka katika hadithi ya Abdullah bin Ja’far amesema: “Nilimuona Mtume (s.a.w.w) akila tende mbivu kwa tango.”415 Bibi Aisha alisema: Walinilisha kwa kila kitu sikunenepa, basi wakanilisha kwa tango na tende mbivu basi nikanenepa.”416   Wasaail Shi’ah, Juz. 17, uk. 103.   Mahasin, uk. 633 cha Barqi. 412   Furuu Kaafi, Juz. 6, uk. 349 cha Kulayni na kitabu Mahasin uk. 532. 413   Wasail Shi’ah, Juz. 17, uk. 107. 414   Sahifat Ridha (a.s), uk. 78. 415   Twibbul-Aimmat, uk. 80 cha ibn Qaym Zawziyyat kutoka kitabu Tirmidhi na vinginevyo. 416   Twibbun-Nabawiy, uk. 81 cha ibn Qaym Jawziyyat. 410 411

100

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 100

8/10/2017 1:22:03 PM


TIBA YA MAASUMINA

TINI Faida zake: Imethibiti hadithi kwamba tini ni ponyo na kinga ya saratani, kutokana na uwepo wa maada ifanyayo kazi ya kukinga, nayo ni mafuta ya lozi chungu, na ulaji wa tini unapunguza ukuaji na ongezeko la saratani kwa kiwango cha uzito wa asilimia 40. Na tini hutumiwa kwa kupunguza uvimbe uchungu na husaidia kusitisha utokaji wa damu, na hupunguza upandaji wa joto, na husaidia mmeng’enyo wa chakula. Na ni kwa jumla ya faida hizo Mola Manani ameapa kwa tini katika Surat Tini kwa kauli yake: “Naapa kwa Tini na Zaituni, na kwa Mlima Sinai, na huu mji wa amani.”417 Na tini kama ilivyo dhahiri zaidi ni tunda na chakula iwapo litaliwa wakati wa njaa bila kufuatiliziwa na kitu kingine. Na mtu akidumu katika kula tunda hilo asubuhi kwa muda wa siku arobaini pamoja na mmea wa binzari nyembamba, basi atanenepa unenepaji ambao haufanani na kitu chochote. Na Tini inafungua mirija ya utumbo na inatia nguvu ini na inasaidia katika ugonjwa wa bawasiri, na inaondoa maradhi ya bandama, bawasiri, ubanaji wa haja ndogo na kusinyaa kwa kende na mpapatiko wa moyo na kubana kwa upumuaji na kikohozi na maumivu ya kifua. Na akila pamoja na rozi atakuwa mwenye amani kutokana na sumu yenye kuua. Na akila pamoja na lozi na karanga (njugu) hufaa kwa miili miembamba, na inaongeza akili na ubongo. Na inafaa kwa maradhi ya kukakamaa, kiharusi na maradhi ya rutuba, na tini mbichi ni bora kuliko kavu katika yote hayo. Na maziwa ya tini ya bara hukaushwa na kutengenezwa jibini mfano wa figo.   Chimbuko: Toleo lenye anuwani: Tiini kama kitenda kazi katika kuzuiwa AWRAAN, imeandaliwa na Muhammad Usama Qawtali na Dr. Dhahir Atwar – Damascus.

417

101

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 101

8/10/2017 1:22:03 PM


TIBA YA MAASUMINA

Hadithi: Mtume (s.a.w.w) amesema: “Ulaji wa tini ni amani kutokana na mingurumo ya tumbo…”418Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Kuleni tini mbivu na yabisi, kwani inaongeza nguvu katika kujamiiana, na inakata bawasiri, na inasaidia katika maradhi ya jongo, na ubaridi ambao unalipata tumbo.”419 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Kuleni tini, hakika kila upande una Bismillah yenye nguvu.”420 - Imekuja katika hadithi: “Yule anayetaka moyo wake uwe mwepesi, basi adumishe ulaji wa tini.” 421 Imepokewa kutoka kwa Abu Dharri kuwa alisema: Mtume (s.a.w.w) alipelekewa zawadi sahani iliyo na tini, akasema kuwaambia masahaba wake: “Kuleni, kama utauliza ni tunda lipi limeteremka kutoka peponi, nitasema: Hili. Kwani hili ni tunda lisilo na kokwa, kuleni hili kwani linakata bawasiri, na linasaidia kwa mwenye maradhi ya jongo.”422 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Ulaji wa tini hulainisha ufungaji, nalo linasaidia kwa mwenye maradhi ya kungurumwa na tumbo. Basi zidisheni kulila mchana, na kuleni hilo usiku bila kuzidisha.”423 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Ni juu yenu kula tini, kwani hilo linasaidia kwa mwenye ugonjwa wa kubirukwa na tumbo.”424   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 296.   Makarimul-Akhlaq, uk. 174. 420   Ramzul-Sihat, uk. 164 cha Dahsurkh. 421   Makarimul-Akhlaq, uk. 174. 422   Makarimul-Akhlaq, uk. 173. 423   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 137. 424   Twibbul-Aimmat (a.s), uk.137. 418 419

102

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 102

8/10/2017 1:22:03 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Hakika tini inaondosha harufu mbaya ya kinywa, na inakaza mifupa, na inaotesha nywele, na inaondoa ugonjwa, wala haihitajiki dawa.”425 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kuwa alisema: “Tini ndio inayofanana zaidi na mimea ya peponi, nayo inaondoa harufu mbaya ya mdomo.”426 Na katika hilo mshairi Ibn Aasam katika utenzi wake amesema: “Na Tini kwa yale ambayo yaliyokuja ndani yake katika sunna, ndilo linaloshabihiana zaidi na mimea ya peponi. Linaondoa bawasiri na kila ugonjwa, ukiwa nalo hauhitajii dawa. Mwenyezi Mungu alimfunulia (Sha’ya) kuponya vidonda vya ugoko kwa maji ya Tini.”427

KITUNGUU SAUMU Faida zake: Kitunguu ni antibayotiki inayokaribiana sana na Penicillin na Streptomycin, na inazuia ukuaji wa virusi. Na kitunguu saumu kimesheheni elementi ya njano na ndimu vinavyoupa uchangamfu mwili, nacho ni kichocheo chenye nguvu katika kutia hamu na kusaidia mmeng’enyo mzuri. Na kinatumiwa katika maradhi ya kimada na kiroho, na katika hali ya kupanda kwa mgandamizo wa damu, na wakati unaposinyaa mshipa upokeao damu moyoni na kuipeleka kwenye tishu, na   Wasaail Shi’ah, Juz. 17, uk. 133 kutoka kwa kitabu Furuu Kaafi na Mahasin cha Barqi.   Wasaail Shi’ah, Juz. 17, uk. 133. 427   Biharul-Anwaar, Juz. 14, uk. 162. 425 426

103

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 103

8/10/2017 1:22:03 PM


TIBA YA MAASUMINA

wakati wa uvimbe mchungu wa utumbo mkubwa na uuguaji wa muda mrefu, na katika kuponya uozaji wa mirija ya utumbo mwembamba na kuondoa mmeng’enyo mbaya, pumu na uvimbe mchungu wa mapafu na homa ya mafua. Pia kitunguu saumu husaidia pindi mtu anapogongwa na nyoka, ambapo hubandikwa juu ya sehemu iliyogongwa. Na baadhi ya vyanzo vinaeleza kwamba kitunguu saumu hupunguza uwezo wa ukuaji wa vimelea vya saratani.428 Na mapishi ya kitunguu saumu na uchomaji wake hutuliza maumivu ya meno, na kusukutua mapishi yake husaidia pia kutuliza maumivu ya meno, na hususan kikichanganywa na ubani kundur.429 Na kinachojulikana ni kwamba kitunguu saumu kinapunguza mgandamizo wa damu kwa wagonjwa. Hadithi: Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Kuleni kitunguu saumu na mjitibie kwacho kwani ndani yake kuna ponyo ya magonjwa sabini.”430 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Haifai kula kitunguu saumu ila kilichopikwa.”431 Imepokewa kutoka kwa Abu Baswiir kuwa alisema: Aliulizwa Imam as-Sadiq (a.s) kuhusu kula kitunguu saumu, kitunguu maji na liki? Akasema: “Hakuna tatizo kwa kula kilichochomwa na kilichopikwa. Wala hakuna tatizo kujitibu kwa kitunguu saumu, na lakini akila hicho asitoke mmoja wenu kuelekea msikitini.”432   Nabataat Twibat wa Isti’imalaatiha, Juz. 1, uk. 39 cha Dr. Muhammad Awdaat 1987.   Qanun, uk. 50 cha ibn Siina. 430   Makarimul-Akhlaq, uk. 182. Kutoka kwa Firdausi. 431   Firdausi. 432   Wasaail Shi’ah, Juz. 17, uk. 170. 428 429

104

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 104

8/10/2017 1:22:03 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) kuwa alipoulizwa na ndugu yake kuhusiana na ulaji wa kitunguu saumu, kitunguu maji na siki, alisema: “Hakuna tatizo.”433 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) katika barua yake ya dhahabu kuwa alisema: “Na yule ambaye hataki kupatwa na hurufu ya mwilini kwake basi na ale kitunguu saumu mara moja katika kila siku saba.”434

JIBINI Madhara yake: Zimepokewa baadhi ya hadithi zenye kulaumu ulaji wa jibini kwani inadhoofisha mwili na inazidisha usahaulifu na usingizi. Na inaondoa madhara ya jibini akila pamoja na jozi. Na imepokewa kwamba madhara ya jibini yako katika ganda lake, kwani linadhuru likiliwa asubuhi na linanufaisha likiliwa usiku. Hadithi: Mtume (s.a.w.w) amesema: “Hakuna mwanamke mjamzito atakayekula tikitimaji kwa jibini ila kichanga chake kitakuwa na sura na umbo zuri.”435 Alikuwa Mtume (s.a.w.w) akila tango kwa chumvi, akila tikitimaji kwa jibini.”436 Katika wosia wa Mtume (s.a.w.w) aliomuusia Ali (a.s), alisema: “Ewe Ali vitu tisa vinasababisha usahaulifu: Ulaji wa tufaha chachu, kula kuzbara na jibini…”437   Wasaail Shi’ah, Juz. 17, uk. 171 kutoka kitabu Qurbul-Isnaad, uk. 116.   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 325. 435   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 299. 436   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 299. 437   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 128. 433 434

105

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 105

8/10/2017 1:22:03 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Kuleni jibini, kwani inasababisha usinziaji, na inasaidia mmeng’enyo wa chakula.”438 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Hakika jibini na jozi vikikusanywa pamoja huwa ni dawa, na vikiachanishwa huwa ni ugonjwa.”439 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Jibini inaleta mmeng’enyo wa chakula cha kabla yake, na inaleta hamu ya kula baada yake.”440 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) pia kuwa alisema: “Tonge bora ni jibini, inaondoa harufu mbaya ya kinywa, inalainisha mmeng’enyo wa chakula cha kabla yake, na inakipa ladha kile cha baada yake.”441 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Tonge bora ni jibini, inakipa utamu kinywa, inaondoa harufu mbaya ya kinywa, inasaidia mmeng’enyo wa chakula kile cha kabla yake na inaleta hamu ya chakula, na yule anayetegemea ulaji wake mwanzo wa mwezi inakaribia kutorudishiwa haja yake.”442 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuhusiana na jibini kuwa alisema: “Hiyo ni yenye kudhuru ikiliwa asubuhi, na yenye manufaa ikiliwa usiku, na inaongeza maji ya mgongo.”443 Imepokewa pia kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Jibini na lozi kila moja wapo kati ya hizo mbili ni tiba, na vikitenganishwa kila kimoja kinakuwa ni ugonjwa.”444   Ramzul-Sihat, uk. 18 cha Dahsurkhi.   Wasaail Shi’ah, Juz. 17, uk. 93. 440   Wasaail Shi’ah, Juz. 17, uk. 93. 441   Daa’waat Raawadhiy, na Biharul-Anwaar, Juz. 66, uk. 105. 442   Waasail Shi’ah, Juz. 17, uk. 94 443   Wasaail Shi’ah, Juz. 17, uk. 92. 444   Makarimul-Akhlaq, uk. 189. 438 439

106

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 106

8/10/2017 1:22:03 PM


TIBA YA MAASUMINA

UKOMA Mtume (s.a.w.w) amesema: “Ole wenu na ulaji wa nyama kavu kwani inachochea ukoma.” Na amesema (s.a.w.w): “Waliponywa Mayahudi kwa kuacha kwao kula nyama kavu.”445 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Ukimbie ugonjwa wa ukoma kama unavyomkimbia simba (huenda kwa sababu simba hupatwa zaidi na maradhi haya kuliko mnyama mwingine).”446 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Yule atakayekula girigirani usiku, atapatwa na ukoma kutoka puani kwake, na atalala akitokwa na damu puani.” Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Upunguzaji wa masharubu kutoka Ijumaa moja mpaka Ijumaa nyingine, ni kinga ya ukoma, na nywele ya puani ni kinga yake pia.447”448 Imepokwa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Mtu asimsemeshe mwenye ukoma ila uwepo kati yao hao wawili umbali wa dhiraa moja, (na katika hadithi nyingine) umbali wa utupaji mshale.”449 Imepokewa vilevile kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuhusiana na ghubayraa Rowan – sorbus kuwa alisema: “….inakomesha vimelea vya ukoma kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (a.j).”450 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kwamba aliulizwa kuhusiana na liki, akasema: “Lile, hakika ndani yake kuna mambo manne; linafanya uzuri tendo la ndoa, linafukuza harufu mbaya na   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 105.   Twibbul-Swadiq, uk. 35. 447   Mahasin, cha Barqi. 448   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 106. 449   Twibbul-Swadiq (a.s), uk. 35. 450   Makarimul-Akhlaq, uk. 176. 445 446

107

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 107

8/10/2017 1:22:03 PM


TIBA YA MAASUMINA

linakata bawasiri, nalo ni kinga ya ukoma kwa yule anayedumu katika ulaji wake.”451 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Figili linasababisha hifidhi, linasafisha moyo, na linaepusha uwendawazimu, mbalanga na ukoma.”452 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Hakika Mwenyezi Mungu aliwaondolea Mayahudi ukoma, kwa ulaji wao wa mchadi na ung’oaji wao wa mishipa (yaani ukataji wa mishipa kutoka kwa mnyama na kuitupa).”453 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuhusu sanamaki amesema: “Ama huo ni kinga ya bahaq POLIOSIS, ukoma, mbalanga, uwendawazimu, kiharusi na ukosefu wa nguvu….”454 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuhusu Harmala amesema: “Nayo ni ponyo ya magonjwa sabini na ugonjwa mdogo zaidi ni ukoma.”455 Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) kuwa alisema: “Yule anayekunywa supu ya nyama ya ng’ombe, Mwenyezi Mungu atamuondolea yeye ukoma na mbalanga.”456 Imepokewa kutoka kwa Ali bin Musayyib kuwa alisema: Mja mwema alisema: “Ni juu yako kula kabichi, kwani hakuna yeyote ila ana mirija ya ukoma, na hakika inayeyuka kwa ulaji wa kabichi.” Nikasema: Lililokaangwa au lililopikwa? Akasema: “Kwa hali zote mbili.”457   Khiswal, Juz. 1, uk. 250 cha Saduuq.   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 284. 453   Mahasin, uk. 519. 454   Makarimul-Akhlaq, uk. 188. 455   Makarimul-Akhlaq, uk. 186. 456   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 212 kutoka kitabu Twibbul-Aimmat (a.s) uk. 104. 457   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 212 kutoka kitabu Twibbul-Aimmat (a.s) uk. 105. 451 452

108

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 108

8/10/2017 1:22:03 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kuwa alisema: “Hina baada ya unyoaji wa nywele ni kinga ya mbalanga na ukoma.”458 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kuwa alisema: “Ni juu yenu kuramba chumvi kwani ni ponyo ya magonjwa sabini, kati ya hayo ni mbalanga, ukoma na uwendawazimu.”459

KAROTI Faida zake: Inapikwa kwa asali na inaliwa kila siku kwa kiasi cha dirham tano, kwani inazidisha maji ya mwanaume kwa kiwango kikubwa mno, na inatia nguvu kende.”460 Na murabi yake ni rahisi zaidi kuitafuna, na inamfaa mweye upungufu wa maji na inatuliza matatizo ya mingurumo ya tumbo na hasa hasa mbegu zake. Hivyo hivyo majani yake yanachochea hamu ya kufanya tendo la ndoa na yanazungusha damu na haja ndogo.461 Hadithi: Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Karoti ni kinga ya mingurumo ya tumbo, na inasaidia kwa mwenye maradhi ya bawasari, na inasaidia katika tendo la ndoa.”462 Imepokewa kutoka kwa Daud bin Farqad kuwa alisema: Nilimsikia Imam Kadhim (a.s) akisema: “Ulaji wa karoti unachemsha korodani mbili na unasimamisha uume.” Nikasema: Nafsi yangu   Sahifat Ridha (a.s), uk. 76.   Sahifat Ridha (a.s), uk. 78. 460   Ajaaibul-Makhluqaat mwishoni mwa kitabu Hayaatul-Hayawaan Kubra, Juz. 2 uk. 184. 461   Qanun uk. 59 cha Ibn Sinaa. 462   Makarimul-Akhlaq na Wasaail Shi’ah, Juz. 17, uk. 164. 458 459

109

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 109

8/10/2017 1:22:04 PM


TIBA YA MAASUMINA

nimeitoa fidia kwako vipi nitaila hali mimi sina meno? Akasema: “Mwamrishe kijakazi wako ailoweke na uile.”463 NGOZI Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuhusiana na ghubayraa Rowan – sorbus, amesema: “Hakika nyama yake inaotesha nyama, na mfupa wake unaotesha mfupa, na ngozi yake inaotesha ngozi….”464 KUJAMIIANA Ndege wengi hupandana sana, wakati mwingine hupandana mara mia moja ndani ya saa moja, na kwa hivyo umri wao hupungua, kwani hawaishi zaidi ya mwaka. Na inaelezwa kuwa Abu Muslim Khurasani alikuwa ni mtu mwenye wivu mno, na alikuwa hamwendei mkewe katika mwaka ila mara moja, na alikuwa akisema: “Tendo la ndoa ni uwendawazimu, na inamtosha mtu kuwa mwendawazimu mara moja kwa mwaka.”465 Na baadhi ya watu wamedai kwamba umri wao unarefuka kwa kuacha kujamiiana, kama unavyokuwa umri wa nyumbu. Na wamesema: Hakika kupungua kwa umri wa ndege ni kutokana na kuzidisha tendo la kujamiiana. Wamesema: Na ndege wanajamiiana mno, na tembo anafanya tendo la kujamiiana mara chache.466 Na miongoni mwa viashiria ambavyo hutuliza hamu ya kushiriki tendo la ndoa na vinapunguza ndoto za kufanya mapenzi ni Kafur, shairi, hindi, pumba, mtama (ulezi), maji ya adesi, Sadhabu Rue, yasimini iliyochemshwa, pera, mboga pumbavu na saladi.   Wasaail Shi’ah, Juz. 17, uk. 164 kutoka kitabu Furuu Kaafi na Mahasin cha Barqi.   Makarimul-Akhlaq, uk. 176. 465   Kunaya wal-Alqaab, Juz. 1 uk. 157. 466   Aqdul-Fariid, Juz. 7, uk. 231 cha ibn Abdullah Rabbih. 463 464

110

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 110

8/10/2017 1:22:04 PM


TIBA YA MAASUMINA

Hadithi: Inachukiza kujamiiana siku ya kupatwa kwa jua na kupatwa kwa mwezi, au linapotokea ndani yake tetemeko, na upepo mweusi na upepo mwekundu na wa manjano. Mtume (s.a.w.w) amesema: “Usijamiiane na mwanamke mwanzo wa mwezi na katikati yake, na mwisho wake, kwani uwendawazimu na kuchanganikiwa unakwenda haraka hadi kwa mtoto wake.”467 Imepokewa pia kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Yule anayejamiiana na mwanamke wake naye akiwa katika hedhi, na akatoka mtoto mwenye mbalanga basi asimlaumu yeyote ila nafsi yake.”468 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Naapa kwa yule ambaye nafsi yangu iko mikoni Mwake, kama mtu atamwingilia mkewe, na katika nyumba yupo mtoto aliye macho, anawaona na anasikia maneno yao na upumuaji wao, hatofaulu kamwe. Akiwa wa kiume basi atakuwa mzinifu, na akiwa wa kike atakuwa malaya.”469 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Hakika harufu nzuri inakaza moyo na inazidisha hamu ya kujamiiana.”470 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Kuleni tini iliyoiva na kavu, kwani inaongeza nguvu wakati wa kujamiiana.”471 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Yule anayekula mung’unya kwa adesi, moyo wake utakuwa   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 409 cha Abdullah Shubbar.   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 392. 469   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 440. 470   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 443. 471   Makarimul-Akhlaq, uk. 174. 467 468

111

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 111

8/10/2017 1:22:04 PM


TIBA YA MAASUMINA

mwepesi mbele ya Mwenyezi Mungu, na litamuongezea nguvu ya kujamiiana.”472 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Hina ni pambo la Uislamu, inaongeza katika kazi ya muumini, na inaondoa maumivu ya kichwa, na inasafisha uonaji, na inaongeza nguvu katika kujamiiana, nayo ni bwana wa maua mazuri ya duniani na Akhera.”473 Mtume (s.a.w.w) amekataza mtu kuzidisha maneno wakati wa kujamiiana, akasema: “Hakika hilo linasababisha mtoto kuwa kiziwi.”474 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Yule anayezidisha kujamiiana atakumbwa na fedheha.”475 Imepokewa pia kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa aliulizwa kuhusiana na suala la kujamiiana: Akasema: “Haya inaondoka, tupu zinakusanyika pamoja, inafanana na hali ya uwendawazimu. Kuzidisha mno kunaleta uzee, na kuzinduka kutokana na hilo ni majuto. Na tunda la halali yake ni mtoto, akiishi huwa ni mtihani na akifa huwa ni huzuni.”476 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Yule anayetaka kubakia na hakuna ubakiaji kama huu, basi awahi mapema kula kifungua kinywa, na apunguze kula chakula cha usiku na apunguze kujamiiana na wanawake.”477 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Kula pera kunaongeza nguvu ya mwanaume na kunaondoa udhaifu wake.”478   Makarimul-Akhlaq, uk. 177.   Biharul-Anwaar, Juz. 59, uk. 299. 474   Makarimul-Akhlaq, uk. 425. 475   Ghurarul-Hikam. 476   Ghurarul-Hikam cha Aamadiy. 477   Biharul-Anwaar, Juz. 59, uk. 267. 478   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 136. 472 473

112

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 112

8/10/2017 1:22:04 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam Zaynul-Abidina (a.s) kuwa alisema: “Mambo manne yanazeesha kabla ya umri wa uzee: Kula nyama kavu, kukaa juu ya unyevunyevu, kupanda juu ya ukingo na kujamiana na bibi kizee.”479 Imepokewa kutoka kwa Imam al-Baqir (a.s) kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa amesema: “Mmoja wenu akiwa na maumivu katika mwili wake ilihali limemzidi joto, basi ni juu yake kulichukua godoro.” Imam al-Baqir (a.s) akaulizwa: Ewe mtoto wa Mtume (s.a.w.w) ni nini maana ya godoro? Akaesema: “Kujamiiana na wanawake, kwani hulituliza na hulizima.”480 Imepokewa kutoka kwa Imam al-Baqir (a.s) kuwa alisema: “Na jua kwamba yule anayejiepusha na upuuzi na ladha wakati zinapodhihiri aya mbalimbali, anakuwa miongoni mwa wale wanaozichukulia aya za Mwenyezi Mungu kuwa ni upuuzi.”481 Imepokewa kutoka kwa Jabir kuwa amesema: Aliniambia mimi Imam al-Baqir (a.s): “Jihadhari kufanya tendo la ndoa hali ya kuwa mtoto mdogo anakuona, atafanya uzuri kuelezea hali yako…”482 Imepokewa kutoka kwa Imam al-Baqir (a.s) kuwa alisema: “Usijamiiane na mwanamke huru mbele ya mwanamke huru, ama kijakazi mbele ya kijakazi hakuna tatizo.”483 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Wanja unaongeza kujamiiana, pia hina inaongeza hilo.”484   Tuhful-Uquul, uk. 315 cha Ibn Shuu’ba Harani.   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 94. 481   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 131. 482   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 133. 483   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 133. 484   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 130. 479 480

113

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 113

8/10/2017 1:22:04 PM


TIBA YA MAASUMINA

Aliulizwa Imam as-Sadiq (a.s) kuhusiana na ulemavu katika maumbile yao? Akasema: “Hao ni wale ambao baba zao wanawaendea wanawake wao katika hedhi.”485 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Maziwa ni yenye kunufaisha kwa yule ambaye yamepungua maji yake ya mgongo.”486 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Ni juu yako kula hindubaau Chickory, kwani linaongeza maji na linapendezesha ngozi, nalo ni la joto na laini, linaongeza watoto wa kiume.”487 Imepokewa kutoka kwa Abu Baswir kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Jihadhari kujamiiana na mke wako na mtoto akikuangalia, hakika Mtume (s.a.w.w) alikuwa akilichukia hilo mno.”488 Mtu mmoja alimwambia Imam as-Sadiq (a.s): Hakika mimi ninanunua vijakazi, na ninapenda unifundishe kitu kitakachonifanya niwe na nguvu zaidi juu yao. Akasema: “Chukua kitunguu maji kikate vipande vidogo vidogo na vikaange kwa mafuta, kisha vunjia mayai na changanya na nyunyuzia chumvi kidogo, kisha changanya katika vitunguu, na kaanga kisha kula.” Yule mtu akasema: Basi nikafanya hivyo nikawa sitaki chochote kutoka kwao ila ninakipata.”489 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Kuleni kitunguu, hakika kina mambo matatu; kinafanya uzuri tendo la ndoa, kinakaza ufizi na kinazidisha maji na kujamiiana.”490   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 392.   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 130. 487   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 130. 488   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 133. 489   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 130. 490   Fusuulul-Muhimmat, uk. 137 cha Hurru Aamili. 485 486

114

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 114

8/10/2017 1:22:04 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kwamba kilitajwa mbele yake kitunguu, akasema: “Kinafanya uzuri tendo la ndoa, kinaondoa kikohozi na kinaongeza tendo la kukutana kimwili.”491 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Karoti ni kinga ya mingurumo ya tumbo, ni yenye manufaa kwa bawasiri, na ni yenye kusaidia juu ya tendo la ndoa.”492 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Unywaji wa sawiiq kwa mafuta unaotesha nyama, unakaza mifupa, na unafanya ngozi kuwa nyororo, na unaongeza suala la kujamiiana.”493 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Hakika mmoja wa Manabii alimlalamikia Mwenyezi Mungu udhaifu na upungufu katika tendo la ndoa, basi akamwamrisha ale Harissa (nayo ni punje ya maharisi pamoja na nyama).”494 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Chukueni katika meno yenu Suud Flat sedge, kwani inapendezesha kinywa, na inaongeza nguvu katika tendo la ndoa.”495 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Kuleni tikitimaji, hakika ndani yake yamekusanyika mambo kumi; … na linaongeza nguvu katika tendo la ndoa.”496 Aliulizwa Imam as-Sadiq (a.s): Ni kitu gani kina ladha zaidi? Akasema: “Kitu chenye ladha zaidi ni kujamiiana na wanawake.”497   Makarimul-Akhlaq, uk. 183 na mfano wake.   Fusuul-Muhimmat, cha Hurru Aamili. 493   Mahasin cha Barqi. 494   Wasaail Shi’ah, Juz. 17, uk. 49 kutoka kitabu Furuu Kaafi. 495   Khiswal, Juz. 1, uk. 63 na Kaafi Juz. 6, uk. 379. 496   Makarimul-Akhlaq, uk. 185. 497   Wasaail Shi’ah, Juz. 14, uk. 10. 491 492

115

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 115

8/10/2017 1:22:04 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Watu hawajapata ladha iliyo nzuri zaidi duniani na akhera kuliko ladha ya kujamiiana na wanawake.”498 Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) amesema: “Sio vibaya kujitenga na mambo sita; mwanamke ambaye ana yakini kuwa hazai, mzee, mwanamke fedhuli, muovu, na mwanamke ambaye hamnyonyeshi mwanawe, na kijakazi.”499 Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) kuwa alisema: “Sioni vibaya kula nyama ya ndege hubari - Houbara bustard (ni mojawapo ya aina za tandawala), kwani ni nzuri kwa bawasiri, na maumivu ya mgongo, nayo ni miongoni mwa yale yanayosaidia katika tendo la ndoa.”500 Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) kuwa alisema: “Mambo manne ni mambo ya Mitume; kujinukisha manukato mazuri, kujisafisha, unyoaji wa nywele mwilini, na kuzidisha kujamiiana.”501 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Tumbo lako lisikae tupu bila chakula, na upunguzaji wa kunywa maji, wala usijamiiane ila ukiwa na hamu, na mboga bora ni mchadi.”502 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kwamba alimwambia Maamuni katika barua yake ya dhahabu: “Na kukutana na mwanamke mwenye hedhi kunasababisha mbalanga kwa mwanawe, na kufanya tendo la ndoa bila kutoa maji kunawajibisha vijimawe, na tendo la ndoa baada ya kujamiiana bila ya kupitisha kati yake kuoga kunasababisha uwendawazimu kwa mtoto.”503   Wasaail Shi’ah, Juz. 14, uk. 10.   Khiswal, Juz. 1, uk. 329. 500   Makarimul-Akhlaq, uk. 161. 501   Makarimul-Akhlaq, uk. 40. 502   Makarimul-Akhlaq, uk. 181. 503   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 321. 498 499

116

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 116

8/10/2017 1:22:04 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kuwa alisema: “Usimkaribie mwanamke mwanzo wa usiku msimu wa kiangazi wala masika, kwa sababu mfuko wa chakula na mirija hujaa, nalo sio jambo zuri na lenye kusifiwa, ikiwa atazaliwa mtoto atapatwa na ugonjwa wa kukakamaa, kiharusi, ukosefu wa nguvu, maradhi ya jongo, vijimawe, na utokaji matone wa haja ndogo, mpasuko, na uoni dhaifu. Na unapotaka hilo basi iwe mwisho wa usiku, kwani linafanya vizuri mwili, na linaleta mtoto, na linamfanya mtoto watakayempata awe na akili. “Wala usifanye tendo la ndoa na mwanamke hadi umchezee kwanza, na zidisha kumchezea, na kumtomasa matiti yake, hakika wewe ukifanya hilo matamanio yake yatashinda na hukusanyika maji yake, kwani maji yake yanatoka matitini mwake, na hamu inadhihiri usoni mwake na machoni mwake, na atatamani kutoka kwako lile ambalo unalitamani kutoka kwake.” Wala usijamiiane na mwanawake ila awapo tohara. Na ukifanya hivyo wala usisimame, wala usikae, lakini egemea ubavu wako wa kulia. Kisha kajisaidie haja ndogo ukimaliza tendo lako hilo, hakika wewe utapata amani ya vijiwe kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (a.j). Kisha oga, na kunywa dawa ya nguvu muda huo huo iliyochangwa na asali, au asali iliyochujwa, kwani hurejesha maji ambayo yametoka kwako.”504 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kuwa alisema: “Yule anayetaka asipatwe na vijiwe basi asibane haja ndogo wala asizuie manii wakati wa kushuka shahawa zake, wala asirefushe kukaa juu ya mwanawake.”505 Imepokewa kutoka kwa Ahmad bin Is-haq kuwa alisema: Nilimwandikia barua Abu Muhammad Askari (a.s) nikamuuliza kuhusi  Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 327aw.   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 449 cha Abdullah Shubbar.

504 505

117

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 117

8/10/2017 1:22:04 PM


TIBA YA MAASUMINA

ana na Isqanqur Scincus, je anaingia katika dawa za tendo la ndoa, yeye ana makucha na mkia. Je, anafaa kuliwa? Akasema: “Ikiwa ana magamba basi hakuna tatizo.”506 Sayyid Abdulla Bushahri ametaja Khawlanjaan Alpinia, akasema: ikichukuliwa kiasi cha dirham ikasagwa na ikachujwa, na akamwagia ndani yake kiasi cha nusu lita ya maziwa ya ng’ombe, na akanywa kabla ya kula chochote, huwa ni kiboko katika kuongeza nguvu za kiume. 507 Wamesema baadhi ya wahenga: Inamfaa mtu aiahidi nafsi yake mambo matatu: Inampasa asiache kabisa kutembea kwa miguu, hivyo ikiwa atahitaji siku moja kutembea kwa mguu ataweza kutembea. Na yampasa asiache kula, lasivyo utumbo wake utabana. Na yampasa asiache tendo la ndoa, hakika kisima ikiwa hakitasafishwa basi maji yatatoweka.508 Shaafi amesema: “Mambo manne yanaongeza nguvu za kiume: Kula ndege jamii ya korobindo, atrafar Menyanthes, njugu na mbegu za mkaruba.”509 Qazwiini amesema: Kwale ni ndege mwenye baraka… nyama yake inaliwa na supu yake inanywewa, kwani inaongeza nguvu katika tendo la ndoa, na inaongeza shahawa na matamanio, na kudumu katika kula nyama yake kunaongeza ubongo na ufahamu… na manii.”510 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Ni mustahabu kwa mwislamu amwendee mkewe mwanzo wa usiku wa mwezi wa Ramadhani, kwa mujibu wa kauli ya Mwenyezi Mungu (a.j) anas  Makarimul-Akhlaq, uk. 162.   Tuhfatul-Ridhawiya fi Mujarabat Imamiyyat, uk. 74 kutoka kitabu Sahabu Laali. 508   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 194. 509   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 320. 510   Ajaaibu Makhluqaat mwishoni mwa kitabu Hayaatul-Hayawaan kubra, Juz. 2, uk. 275. 506 507

118

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 118

8/10/2017 1:22:04 PM


TIBA YA MAASUMINA

ema: ‘Mmehalalishiwa nyinyi usiku wa funga kujamiiana na wanawake wenu.’511 Na neno rafath lina maana ya kufanya tendo la ndoa.”512 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Mmoja wenu anapotaka kukutana na mkewe asifanye haraka, hakika wanawake wana haja nyingi.”513 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Mtu akivutiwa na mwanamke basi amwendee mkewe, hakika kwa mkewe kuna mfano wa yale aliyoyaona.”514 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Mtu akimwangalia mwanamke aliyemvutia basi amshike na kumtomasa mkewe, kwani yeye ni mwanamke kama yule mwanamke.”515 JANABA Mtume (s.a.w.w) amesema: “Mambo matano husababisha ukoma; ….na kula wakati una janaba na kumwingilia mwanamke katika hedhi yake…”516 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Mtume (s.a.w.w) alikataza kula hali ya kuwa una janaba, na akasema: Hakika hilo linasababisha ufukara.”517 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Mwislamu asilale na janaba, wala asilale ila akiwa na tohara, na kama hakupata maji basi afanye tayamamu kwa mchanga.”518   Sura 2 aya 187.   Khiswal, Juz. 2, uk. 612. 513   Khiswal, Juz. 2, uk. 637. 514   Khiswal, Juz. 2, uk. 637. 515   Nahjul-Balaaghah, hekima: 430. 516   Khiswal, Juz. 1, uk. 270. 517   Makarimul-Akhlaq, uk. 424. 518   Wasaail Shi’ah, Juz. 1, uk. 501. 511

512

119

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 119

8/10/2017 1:22:04 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam al-Baqir (a.s) kuwa alisema: “Mwenye janaba akitaka kula na kunywa aoshe mkono wake, asukutue maji na aoshe uso wake, na ale na anywe.”519 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kuwa alisema: “Hakika chini ya kila unywele kuna janaba.”520 UWENDAWAZIMU Mtume (s.a.w.w) amesema: “Ewe Ali, mambo matatu huleta uwendawazimu; kujisaidia haja kubwa makaburini, kutembea na kiatu kimoja, na mtu kulala peke yake.”521 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Figili husababisha hifidhi, hutakasa moyo na huepusha uwendawazimu, mbalanga na ukoma.”522 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kuwa alisema: “Ni juu yenu kulamba chumvi, kwani ni ponyo ya magonjwa sabini, miongoni mwa hayo ni mbalanga, ukoma na uwendawazimu.”523 JOZI Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Kula jozi wakati wa joto kunachochea joto, na vidonda mwilini, na kula wakati wa baridi kunachemsha kende mbili na hukinga baridi.”524 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Hakika jibini na jozi vikikusanyika pamoja huwa ni dawa, na ikiwa vitatengana huwa ni ugonjwa.”525   Wasaail Shi’ah, Juz. 1, uk. 495.   Fiqhu Ridha (a.s), uk. 83. 521   Biharul-Anwaar, Juz. 76, uk. 319 kutoka kitabu Khiswal, Juz. 1, uk. 126 cha Suduuq. 522   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 78. 523   Sahifat Ridha (a.s), uk. 78. 524   Wasaail Shi’ah, Juz. 17, uk. 94 kutoka kitabu Furuu Kaafi na Mahasin cha Baeqi. 525   Wasail Shi’ah, Juz. 17, uk. 93 kutoka kitabu Furuu Kaafi na Mahasin. 519 520

120

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 120

8/10/2017 1:22:04 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Vitu vitatu haviliwi lakini hunenepesha, na vitu vitatu vinaliwa lakini hukondesha. Ama ambavyo huliwa lakini hukondesha ni; chavuo, matunda na jozi, na ama vile ambavyo haviliwi lakini hunenepesha ni; unyoaji wa nywele, kujipaka manukato na kuvaa nguo ya katani.”526 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Vitu vinne vinasafisha macho na vinanufaisha wala havidhuru.” Basi akaulizwa ni vipi hivyo? Akasema: “Suutar Thaimu pamoja na chumvi vikikusanyika pamoja, na komoni muluki na jozi vikikusanyika pamoja. Akaulizwa: Na vinafanyaje uzuri hivi vinne vinapokusanyika pamoja? Akasema: “Komoni muluki na jozi vinaunguza bawasiri, vinafukuza harufu mbaya, vinafanya ngozi kuwa nzuri na vinaufanya mgumu mfuko wa chakula, na vinachemsha kende. Na Suutar Thaimu na chumvi vinafukuza harufu kutoka moyoni, na vinafungua vizuizi, na vinaunguza kikohozi na vinazungusha maji, na vinafanya uzuri tendo la ndoa, na vinalainisha mfuko wa chakula, na vinaondoa harufu mbaya kinywani na vinaongeza nguvu katika kiungo cha uzazi cha mwanaume.”527 NJAA NA SHIBE Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: Nuru ya hekima ni njaa, na shibe ndio kuwa mbali na Mwenyezi Mungu… wala msishibe mtazima nuru ya maarifa kutoka nyoyoni mwenu.”528 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Asifanye tendo la jimai, yule mwenye njaa na mgonjwa.”529   Wasaail Shi’ah, Juz. 16, uk. 541.   MakarimulAkhlaq, uk. 191. 528   Biharul-Anwaar, juz. 70, uk. 71. 529   Mustadrakul-Wasaail, Juz. 3, uk. 82. 526 527

121

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 121

8/10/2017 1:22:04 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Salmani Farsi (r.a) kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Watu wengi wenye kushiba duniani ndio hao watakuwa na njaa akhera. Ewe Salmani hakika dunia ni jela ya muumini na pepo ya kafiri.”530 Imepokewa kutoka kwa Imam Hadi (a.s) kuwa alisema: “Ukeshaji una ladha zaidi ya usingizi, na njaa inaongeza utamu wa chakula.”531 HABASODA Nayo ni majani yanayonasibishwa na kijakazi mweusi aliyekuwa mhudumu wa Bwana Mtume (s.a.w.w) na jina lake ni Barkat. Na mimea hii ina majani yenye kufungamana yenye kuwa katika vifungu vidogo vyepesi, hubeba matunda, maganda na mbegu nyeusi. Na Ibn Baytwar ameuita: Komoni nyeusi. Faida zake: Habasoda ni wenye kutia nguvu, wenye kuhadhari, wenye kushurutisha, wenye kufukuza harufu, una cortisone ya asili. Huwekwa katika bendeji, huponya maumivu ya kichwa, huchanganya haja ndogo, humsaidia mwenye kikohozi, kupendezesha na kuleta huba kwa vijana. Kuutumia zaidi kunadhuru. Hakika kawaida ya habasoda ni joto yabisi, nayo ni yenye kuondoa masaibu, inasaidia kwa mwenye homa ya kipanda uso na kikohozi, inafungua kizuizi na harufu. Ikitwangwa na kuchanganywa na asali na akanywa kwa maji moto itayeyusha vijimawe na itazungusha haja ndogo na hedhi, inasafisha na kukata matone ya haja ndogo. Na ikisagwa na kufungwa kwa kitambaa cha katani na mtu akadumu   Ramzul-Sihat, uk. 220 cha Dahsurkhi.   Biharul-Anwaar, Juz. 78, uk. 369.

530 531

122

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 122

8/10/2017 1:22:04 PM


TIBA YA MAASUMINA

katika kuinusa husaidia kwa mwenye mafua ya baridi. Na ikiwa zitalowekwa punje saba kwenye maziwa ya mwanamke, na akanusa kama ugoro yule mwenye homa ya manjano humsaidia, na akinywa hayo kwa kiwango cha mithqaal kwa maji basi humsaidia mwenye pumu, na bendeji yake husaidia maumivu ya kichwa baridi.532 Hakika habasoda chungu inakata kikohozi, inaondosha hurufu na masaibu, na ina usafishaji wa hali ya juu. Inakata maradhi ya Warts na bahaq POLIOSIS na ukoma. Huwekwa pamoja na siki juu ya chunusi na hufungua kikohozi. Na inasaidia kwa mafua. Na huwekwa kitovuni pamoja na katani, na hupakwa juu ya paji la uso kutokana na maumivu ya kichwa yatokanayo na baridi. Na kuipika pamoja na siki husaidia kwa mwenye maumivu ya meno pindi anaposukutua. Inaua vijidudu… na inazungusha hedhi ikiwa itatumiwa siku kadhaa. Na kuinywa kwa asali na maji moto humsaidia mwenye vijiwe ndani ya kibofu cha mkojo na kende mbili.533 Matumizi ya mafuta: Mafuta ya habasoda yanatumiwa dhidi ya kikohozi na maradhi ya kifua, na hiyo ni kwa kuongezea matone matano ya mafuta haya kwenye kahawa na chai. Na mafuta hutuliza vidonda vya tumbo na hufukuza gesi na huzungusha hedhi na udenda.534 Hadithi: Saad amesema: Mtume (s.a.w.w) alisema: “Hakika punje hii ndani yake kuna ponyo ya kila ugonjwa ila sumu.” Nikasema: Ni sumu gani? Akasema: “Kifo.” Nikasema: Ni ipi hiyo habasoda? Akasema: “Shuuziiz” Nikasema: Nitatengeneza vipi? Akasema: “Unachukua punje 21 unazifunga katika kitambaa, na unaziloweka ndani ya maji   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 230.   Qanun, uk. 288 cha ibn Sinaa. 534   Nabataat Twibbiyat wal-Utriyyat fil-Watwan Arabiy, uk. 123, 1988. 532 533

123

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 123

8/10/2017 1:22:04 PM


TIBA YA MAASUMINA

usiku, na unadondoshea matone mawili katika tundu la pua la kulia, na katika tundu la kushoto tone moja, na utakapoamka utadondoshea tone moja moja katika pua zote mbili. Katika siku ya pili utadondoshea tone mbili katika pua ya kulia, na tone moja pua ya kushoto. Ama katika siku ya tatu utondoshea tone moja katika tundu la pua la kulia, na matone mawili katika tundu la kushoto, utatofautisha baina ya matundu hayo katika siku tatu.” Saad amesema: Na hulijadidisha penzi kila siku.535 Mtu mmoja alilalamika kwa Mtume (s.a.w.w) kuhusiana na anayoyapata tumboni mwake, Mtume akasema: “Chukua kinywaji cha asali na tia ndani yake punje tatu za habasoda, au tano au saba, na kunywa, utapona kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.” Basi yule mtu akafanya hivyo na akapona.536 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kwamba aliitisha komoni muluki na Suutar Thaimu na habasoda, hivyo akawa akidharau alapo mayai na chakula chenye gesi…”537 Mtume (s.a.w.w) amesema: “Katika usiku ambao nilipelekwa mbinguni sikuona kongamano la malaika ila walisema: Ewe Muhammad uamrishe umma wako kutumia ndumiko, dawa bora kabisa kati ya hizo mnazozitumia ni kujiumika na habasoda na udi wa kihindi.”538 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Katika habasoda na asali kuna ponyo ya kila ugonjwa ila sumu. Ikaulizwa: Ewe Mtume(s.a.w.w) ni ipi hiyo sumu? Akasema: “Kifo.” Akasema: “Hivi viwili havijazi joto na baridi, hakika hivyo viwili ni ponyo popote vitakapoangukia.”539   Makarimul-Akhlaq, uk. 211.  Biharul-Anwaar, Juz. 62 uk. 72 kutoka kitabu Daaimul-Islam. 537   Makarimul-Akhlaq, uk. 187. 538   Ramzul-Sihat, uk. 19 cha Dahsurkhi. 539   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 68. 535 536

124

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 124

8/10/2017 1:22:05 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam al-Baqir (a.s) kwamba aliulizwa kuhusiana na homa ya vipindi (inakuja leo na kupotea siku nyingine) akasema: “Achukue asali na habasoda na alambe mara tatu, hakika itakatika, hakika hivyo viwili ni vyenye baraka, amesema (s.w.t) kuhusu asali: “Kinatoka katika matumbo yao kinywaji chenye rangi mbali mbali ndani yake kina matibabu kwa watu.540”541 Imepokewa kutoka kwa Dhurayh kuwa alisema: Nilimwambia Imam as-Sadiq (a.s): Hakika ninakuta tumboni mwangu maumivu katika utumbo. Akasema: “Kipi kinakuzuia wewe kutumia habasoda? Hakika ndani yake kuna ponyo ya kila dawa, ila sumu.”542 Imepokewa kutoka kwa Mufadhal amesema: Nilimlalamikia Imam as-Sadiq (a.s) kwamba ninajisaidia haja ndogo kwa shida, akasema: “Chukua habasoda katika mwisho wa usiku.”543 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Hakika ndani ya habasoda kuna ponyo ya kila ugonjwa, na mimi ninaitumia kwa ajili ya homa na maumivu ya kichwa na ugonjwa wa macho na maumivu ya tumbo, na kila linalonitokea mimi kuhusiana na maumivu basi Mwenyezi Mungu (a.j) ananitibu kwayo.”544 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kuwa alisema: “Hakika habasoda ni yenye baraka, inatoa ugonjwa uliyojificha kutoka mwilini.”545 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kuwa alisema: “Hakika habasoda ni ponyo ya kila ugonjwa ila sumu.”546   Surat 16 aya 69.   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 51. 542   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 68. 543   Makarimul-akhlaq, uk. 212. 544   Makarimul-Akhlaq, uk. 212. 545   Fiqhul-Ridha (a.s), uk. 346. 546   Fiqhu-Ridha (a.s), uk. 346. 540 541

125

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 125

8/10/2017 1:22:05 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kuwa alisema: “Ni juu yenu kutumia asali na habasoda.”547 NDUMIKO/ KUUMIKA Kuumika kunamaanisha ufyonzaji wa damu mwilini. Na kitendo hicho kimeitwa kwa jina hilo kwa sababu ufyonzaji wa damu ni sharti la kitendo. Hadithi: Mtume (s.a.w.w) amesema: “Hakika dawa bora kabisa kati ya zile mnazojitibia ni ndumiko na udi wa kihindi.”548 Imepokewa pia katika sunna ya Mtume (s.a.w.w) kwamba alikuwa akijitibu kwa kuumika katikati ya kichwa chake anapopatwa na kipanda uso.”549 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Hakika ufyonzaji wa damu ni afya ya mwili na unaimarisha akili.”550 Imepokewa kwamba hakuna mtu aliyemlalamikia Mtume (s.a.w.w) kuhusiana na maumivu ya kichwa ila alimwambia: “Tumia ndumiko.” Wala hakuna mtu aliyemlalamikia yeye maumivu ya miguu yake ila alimwambia: “Zipake ndevu zako hina.”551 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Damu ya mtu itakapochafuka basi atumie njia ya ufyonzaji wa damu.”552 Imepokewa pia kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Ikiwa ndani ya kitu kuna ponyo basi ni sharti mtu atumie njia ya ufyonzaji wa damu, au unywaji wa asali.”553   Fiqhul-Ridha (a.s), uk. 346.   Sahihi Bukhari na Muslim. 549   Sahihi Bukhari, Muslim na Nasaai. 550   Ramzul-Sihat, uk. 37 cha Dahsurkhi. 551   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 69. 552   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 118 kutoka kitabu Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 69. 553   Mahasin, Juz. 2, uk. 35 cha Barqi. 547 548

126

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 126

8/10/2017 1:22:05 PM


TIBA YA MAASUMINA

Mtume (s.a.w.w) amesema: “Katika usiku ambao nilipelekwa mbinguni sikuona kongamano la malaika ila walisema: Ewe Muhammad uamrishe umma wako kutumia ndumiko, dawa bora kabisa kati ya hizo mnazozitumia ni kujiumika na habasoda na udi wa kihindi.”554 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kutoka kwa baba yake kuwa alisema: “Mtume (s.a.w.w) alitumia njia ya ufyonzaji wa damu kichwani kwake, mabegani kwake na mgongoni kwake mara tatu, akiita moja ni yenye manufaa, na nyingine ni yenye kutoa msaada na ya tatu ni yenye kuokoa.”555 Imepokewa kutoka kwa Abu Baswiir kuwa alisema: Abu Ja’far al-Baqir (a.s) alisema: “Ni kitu gani mnakula baada ya kujiumika? Nikasema: Hindubaau Chickory na siki. Akasema: “Hakuna tatizo katika hayo.”556 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Dawa zipo nne; Ufyonzaji wa damu, unyoaji wa nywele, utapishaji na kupiga bomba.”557 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Tiba bora kati ya yale ambayo mnayojitibia nyinyi ni ufyonzaji wa damu na unusaji, bafu na uingizaji wa bomba sehemu ya haja kubwa.”558 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Aliteremka Jibrail kwa Mtume (s.a.w.w) akiwa na mswaki, vichokoa meno na ndumiko.”559   Ramzul-Sihat, uk. 19 cha Dahsurkhi.   Ramzul-Sihat, uk. 37 cha Dahsurkhi kutoka kitabu Ma’anil-Akhbar. 556   Ramzul-Sihat, uk. 40. 557   Fusuulul-Muhimmat, cha Hurru Aamiliy na Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 55. 558   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 54. 559   Wasaail Shi’ah, Juz. 16, uk. 532. 554 555

127

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 127

8/10/2017 1:22:05 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Jihadhari kutumia ndumiko kabla ya kula chochote.” Na akasema: “Wala usijiumike mpaka ule chochote, kwani kitendo hicho huzungusha mishipa na kumaliza nguvu za mwili.”560 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Kuumika kunaongeza akili na kunazidisha hifidhi kwa mhifidhi.”561 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Kuumika kwenye kichwa kunasaidia, kunanufaisha kutokana na kila ugonjwa ila sumu (yaani kifo).” Kisha akaweka shibiri kati ya nyusi mbili hadi ukubwa wa dole gumba, kisha akasema: “Hapa.”562 Imepokewa pia kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Ufyonzaji wa damu kichwani unaondoa usinziaji, na maumivu ya magego.”563 Imepokewa kutoka kwa msomi (yaani Imam Kadhim) kuwa alisema: “Ufyonzaji wa damu ufanyike baada ya kula, kwani mtu akishiba kisha akafanya ufyonzaji wa damu kunakusanya damu na kutoa maradhi, na akifanya ufyonzaji wa damu kabla ya kula itatoka damu bila ugonjwa.”564 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) katika barua yake ya dhahabu kwenda kwa Maamuni kuwa alisema: “Ikiwa utataka kufanya ufyonzaji wa damu basi iwe katika usiku wa mwezi kumi na mbili (12) wa mwezi mwandamo hadi usiku wa mwezi kumi na tano (15), kwani kufanya hivyo kunasaidia afya zaidi ya mwili. Ukiisha mwezi usifanye ufyonzaji wa damu, ila utakapokuwa mwenye kud  Ramzul-Sihat, uk. 40 Cha Dahsurkhi.   Ramzul-Sihat, uk. 41 cga Dahsurkhi. 562   Ramzul-Sihat, uk. 41 cha Dahsurkhi. 563   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 361 cha Abdullah Shubbar. 564   Ramzul-Sihat, uk. 40 cha Dahsurkhi. 560 561

128

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 128

8/10/2017 1:22:05 PM


TIBA YA MAASUMINA

harurika kwa hilo, kwani damu hupungua kadiri mwezi mwandamo unavyopungua, na inaongezeka kadiri unavyokua.” Na uwe ufyonzaji wa damu kwa kiwango cha miaka: Na kila mtu wa miaka 20 afanye mara moja ndani ya kila siku 20, na mtu wa miaka 30 afanye mara moja ndani ya kila siku 30. Na vivyo hivyo yule anayefikia umri wa miaka 40 atafanya ufyonzaji wa damu kila baada ya siku 40, na anayezidi basi yamtosha hilo la umri wa miaka 40. Na jua ewe Amirul-Muminina hakika kuumika ni kuchukua damu kutoka kwenye mishipa midogo iliyoenea katika nyama, na ushahidi wa hilo ninalolitaja ni kwamba hakudhoofishi nguvu, kama vile udhaifu unaopatikana wakati wa kupasua mshipa mkubwa.”565 JOTO NA BARIDI Mtume (s.a.w.w) amesema: “Wapeni bishara njema kuwa wana umri mrefu wale wenye kujipaka mafuta.”566 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Asili ya kila ugonjwa ni ubaridi.”567 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Kuleni tini mbivu yabisi, kwani hiyo inaongeza nguvu katika suala la kujamiiana, na inataka bawasiri, na inasaidia katika maradhi ya jongo, na ubaridi ambao unalisibu tumbo.”568 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Kula lozi wakati wa joto kunachochea joto, na kunachochea vidonda mwilini,   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 318.   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 290. 567   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 29o. 568   Makarimul-Akhlaq, uk. 74. 565 566

129

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 129

8/10/2017 1:22:05 PM


TIBA YA MAASUMINA

na kula lozi katika kipindi cha baridi kunachemsha kende mbili, na kunazuia ubaridi.”569 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuhusiana na asali na habasoda kuwa alisema: “Hivi viwili havielemei upande wa joto wala ubaridi, hakika hivyo viwili ni ponyo popote viangukiapo.”570 Imepokewa pia kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema kuhusu tufaha: “Nalo linang’oa homa na linatuliza joto.”571 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Mtu anapokanyaga mchanga wenye joto humuunguza, basi akikanyaga juu mboga pumbavu itatuliza joto liunguzalo.”572 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Hakika sawiiq kavu ikiwa itachukuliwa kabla ya kula chochote, inazima joto na inatuliza kibofunyongo.”573 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Sawiiq ya adesi inakata kiu, inatia nguvu mfuko wa chakula, na ndani yake kuna ponyo ya magonjwa sabini, na inazima manjano, na inatia baridi tumbo.” Na alikuwa (a.s) anaposafiri haachani nayo. Na alikuwa mmoja wa waheshimiwa anapopatwa na shinikizo la damu, huambiwa: “Kunywa sawiiq ya adesi, kwani hiyo inachochea damu, na inazima joto.”574 Imepokewa kutoka kwa as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Kula tufaha, kwani hilo linazima joto, na linatia ubaridi tumbo, na linaondoa homa.”575   Wasaail Shi’ah, Juz. 17, uk. 94 kutoka kitabu Furuu Kaafi na Mahasin cha Barqi.   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 51 na 68. 571   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 93. 572   Wasaail Shi’ah, Juz. 17, uk. 154. 573   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 67. 574   Makarimul-Akhlaq, Juz. 193. 575   Wasaail Shi’ah, Juz. 3, uk. 30 cha Hurru Aamiliy. 569 570

130

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 130

8/10/2017 1:22:05 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa pia kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Dawa bora ni mchele, ni baridi sahihi, ni salama ya kila ugonjwa.”576 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kuwa alisema: “Jipakeni mafuta ya balungi, kwani hiyo ni baridi wakati wa kiangazi, na joto wakati wa masika.”577 Imepokewa pia kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kuhusiana na maji baridi kuwa alisema: “Kwani hayo yanazima joto na yanatuliza manjano, na yanaleta mmeng’enyo wa chakula na yanaondoa mabaki ambayo yako juu ya kichwa cha mfuko wa chakula, na yanaondoa homa.”578 Imepokewa kutoka kwa Imam Hadi (a.s) kuwa aliwaambia baadhi ya masahaba wake: “Zidisheni kwetu sisi bilinganya, kwani hilo ni joto wakati wa joto, na baridi wakati wa baridi, linaleta ulinganifu katika nyakati zote, ni zuri kwa hali zote.”579 HARMALA Peganum Maana yake: Ni mmea wa majani, unaota Kaskazini mwa Afrika, kama unavyoota Iraq na Kuwait na Jordani na Penisula ya Uarabu. Majani yake yanatambaa na yenye kuvuma, maua yake ni meupe yenye muundo wa nyota, na matunda yake yanafanana na mafigo, na rangi yake ni buni iliyokoza. Ni mimea yenye harufu ichukizayo. Na sehemu ya tiba ni majani yake, mbegu na mizizi. Na kwa hivyo mmea huu una umuhimu katika kutibu ugonjwa wa kupooza na kudhoofu mwili (Barkinusium), nao unapunguza mkandamizo wa damu, na upanukaji wa utumbo. Na uliolowekwa   Makarimul-Akhlaq, uk. 155.   Sahifat Ridha (a.s), uk. 52. 578   Fiqhul-Ridha (a.s), uk. 346. 579   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 139. 576 577

131

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 131

8/10/2017 1:22:05 PM


TIBA YA MAASUMINA

au uliochemshwa hutumiwa wakati wa hali ya uvimbe uchungu wa koo na koromelo. Faida zake: Tangu zamani mbegu za Harmala hutumiwa kama muhadarati na kifukuzaji wadudu kwenye mshipa upelekao damu moyoni na kuipeleka kwenye tishu, kwa kuwa Harmala ina Alkaloid. Na huliwa kidogo mbegu zake ili kuponya ugonjwa wa kifua. Na mbegu zake hutengenezwa mafuta kwa ajili ya macho. Vivyo hivyo maradhi ya ngozi. Kama ambavyo unga wa mbegu zake hutumiwa ili kuchochea utokaji wa maziwa ya wanyonyeshaji, na katika utiaji nguvu kwa wanaume wakati wa tendo la ndoa.580 Ibn Sina (Avicena) amesema: “Hakika ni nzuri kwa maumivu ya sehemu za maungo, na inasaidia kwa ugonjwa wa kukakamaa, kwa kunywa na kwa kujipaka.”581 Hadithi: Mtume (s.a.w.w) amesema: “Yule atakayekunywa Harmala asubuhi arobaini, kila siku uzito wa gramu moja, ili kupata nuru ya hekima moyoni mwake, ataponywa magonjwa 72 lililo dogo zaidi ni ugonjwa wa mbalanga.”582 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Hauoti mmea wa Harmala ila kuna malaika aliyewakilishwa katika mti huo, hadi unapomfikia utakayemfikia. Na hakika katika mzizi wake na matawi yake ipo kinga ya yale yachukizayo. Na katika punje yake   Nabataat Twibbiyat al-Uturiyat fil-Watanil-Arabiyyat, uk. 57, Khartuum 1988.   Ajaaibul-Makhluqaat mkiani mwa kitabu Hayaatul-Hayawaanil-Kubra, Juz. 2, uk. 184. 582   Biharul-Anwaar, Juz. 59, uk. 235 kutoka kitabu Firdausi. 580 581

132

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 132

8/10/2017 1:22:05 PM


TIBA YA MAASUMINA

kuna ponyo ya magonjwa 72, basi jitibieni kwa mmea huo na kwa kundur.”583 Imepokewa kutoka kwa Muhammad bin Hakam kuwa alisema: Imam as-Sadiq (a.s) alisema: “Nabii alilalamika kwa Mwenyezi Mungu (a.j) kuhusu uoga wa umma wake, basi Mwenyezi Mungu akamfunulia yeye: ‘Uamrishe umma wako kula Harmala, kwani unazidisha ushujaa.”’584 Imam as-Sadiq (a.s) aliulizwa kuhusiana na Harmala na ubani, akasema: “Ama Harmala, haukosi mizizi ardhini, wala halinyanyuki tawi lake hadi mbinguni, ila Mwenyezi Mungu huliwekea malaika hadi unapokuwa vipande, au unapomfikia yule utakayemfikia. Hakika shetani hutoboa nyumba 70 ila nyumba ambayo humo kuna Harmala, nao ni ponyo ya magonjwa 70, dhaifu zaidi kati ya magonjwa hayo ni mbalanga, wala usiwapite mmea huo.”585 “Na ama ubani (yaani kunduru) nalo ni chaguo la Mitume (a.s) wa kabla yangu, nao Maryam (a.s) alikuwa akiutumia kuomba msaada. Na hakuna moshi unaopanda juu mbinguni kwa haraka zaidi kuushinda wenyewe, nao humfukuzisha shetani, na hukinga wadudu waharibifu. Wala nao usiwapite.”586 KWIKWI Ametaja Allamah Amin (r.a) kwamba hakika miongoni mwa mambo yaliyojaribiwa na kusihi katika kutibu kwikwi, ni anywe maji kidogo, katika misukumo mingi, au aweke maji mdomoni mwake wala asipumue.587   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 67.   Makarimul-Akhlaq, uk. 212. 585   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 68 inafanana nao. 586   Makarimul-Akhlaq, uk. 212 cha Twabarasi. 587   Maadinul-Jawaahir, Juz. 1. 583 584

133

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 133

8/10/2017 1:22:05 PM


TIBA YA MAASUMINA

VIJIWE KATIKA KENDE Imeandikwa katika barua ya dhahabu ya Imam Ridha (a.s) kwamba: “Usimkaribie mwanamke mwanzo wa usiku msimu wa kiangazi wala masika, kwa sababu mfuko wa chakula na mirija hujaa, nalo sio jambo zuri na lenye kusifiwa. Ikiwa atazaliwa mtoto atapatwa na ugonjwa wa kukakamaa, kiharusi, ukosefu wa nguvu, maradhi ya jongo, vijimawe, na utokaji matone wa haja ndogo, mpasuko, na uoni dhaifu. Na unapotaka tendo hilo basi iwe mwisho wa usiku, kwani linafanya vizuri mwili, na linaleta mtoto, na linamfanya mtoto watakayempata awe na akili. Wala usifanye tendo la ndoa na mwanamke hadi umchezee kwanza, na zidisha kumchezea, na kumtomasa matiti yake, hakika wewe ukifanya hilo matamanio yake yatashinda na hukusanyika maji yake, kwani maji yake yanatoka matitini mwake, na hamu inadhihiri usoni mwake na machoni mwake, na atatamani kutoka kwako lile ambalo unalitamani kutoka kwake.” Wala usijamiiane na mwanawake ila awapo tohara. Na ukifanya hivyo wala usisimame, wala usikae, lakini egemea ubavu wako wa kulia. Kisha kajisaidie haja ndogo ukimaliza tendo lako hilo, hakika wewe utapata amani ya vijiwe kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (a.j). Kisha oga, na kunywa dawa ya nguvu muda huo huo iliyochanganywa na asali, au asali iliyochujwa, kwani hurejesha maji ambayo yametoka kwako.”588 Katika barua ya dhahabu ya Imam Ridha (a.s) amesema: “Na yule ambaye anataka asipate vijiwe na kubanwa na haja ndogo, basi asizuie manii wakati wa kuteremka shahawa, wala asirefushe ukaaji juu ya mwanamke.”589   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 327aw.   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 324.

588 589

134

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 134

8/10/2017 1:22:05 PM


TIBA YA MAASUMINA

HIFIDHI NA UKUMBUKAJI Mtume (s.a.w.w) amesema: “Mfano wa yule ambaye anajifundisha udogoni ni kama vile anayeweka nakshi juu ya jiwe, na mfano wa yule ambaye anajifundisha ukubwani ni kama vile anayeandika juu ya maji.”590 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Yule anayetaka kuhifadhi basi ale asali.”591 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Kuleni figili, kwani linasababisha hifidhi, nalo ni chakula cha Khidhri (a.s).”592 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Ewe Ali, mambo matatu huongeza hifidhi, na yanaondoa ugonjwa; Ubani, kupiga mswaki na usomaji wa Qur’ani.”593 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Mambo matano huondoa usahaulifu na huzidisha hifidhi, pia huondoa kikohozi: upigaji wa mswaki, funga, usomaji wa Qur’ani, asali na ubani (yaani kundur).”594 Miongoni mwa wosia wa Mtume (s.a.w.w) kwa Ali (a.s) ni: “Ewe Ali vitu tisa vinasababisha usahaulifu; ulaji tufaha la ugwadu, kula kazbara, jibini na maji aliyokunywa panya, usomaji wa maandishi ya makaburini, kutembea baina ya wanawake wawili, kutupa chawa hai, ufyonzaji wa damu mwilini na kujisaidia haja ndogo katika maji yaliyotuama.”595   Kanzul-Ummal, hadithi 29336.   Makarimul-Akhlaq, uk. 165. 592   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 388 cha Shubbar. 593   Khiswal, Juz. 1, uk. 126. 594   Makarimul-Akhlaq, uk. 166, kutoka kitabu Firdausi. 595   Biharul-Anwaar, Juz. 66, uk. 245, kutoka kitabu Khiswal, Juz. 2, uk. 423 cha Saduuq. 590 591

135

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 135

8/10/2017 1:22:05 PM


TIBA YA MAASUMINA

Na Sakhawi ameyatungia beti mambo ambayo yanaathari katika usahaulifu, akasema: “Jikinge mambo kwa kuhofia usahaulifu: usomaji maandishi yaliyoandikwa katika makaburini ya kale. Na ulaji wako wa tunda maadamu ni chachu. Na kazbara la kijani ndani yake kuna sumu yake. Vivyo hivyo utembeaji baina ya wanawake wawili na kufanya ufyonzaji wa damu mgongoni. Na kati ya hayo kuna majonzi nayo ni makubwa zaidi. Na kutokana na ujisaidiaji wa haja ndogo katika maji yaliyotuama. Na unywaji wako wa mabaki ya maji aliyokunywa panya na hilo ndilo hitimisho lake.”596 Kaf’amiy katika kitabu al-Jannah amesema: Miongoni mwa dawa na mitishamba ambayo inasaidia hifidhi na kukumbuka ni yale aliyoyapokea Ibn Masuud kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuhusiana na hifidhi ya Qur’ani, yale yanayokata kikohozi na haja ndogo, na hutia nguvu mgongo: “Huchukuliwa dirham 10 ya karafuu, vivyo hivyo Harmala, na kundur nyeupe, na sukari nyeupe, husagwa vyote na huchanganywa pamoja ila Harmala, yenyewe itafinyangwa mkononi, na huliwa asubuhi kwa kipimo cha dirham na vivyo hivyo wakati wa kulala.”597 Kaf’amiy amesema: Na nililiona hili kama lilivyo katika kitabu (Luqatul-Fawaid) na ndani yake pia kuna: Hakika yule anayetaka kuzidisha uwezo wa hifidhi yake na kupunguza usahaulifu wake basi ale kila siku gramu tano za tangawizi murabbi. Na mtunzi wa kitabu Luqatul-Fawaidi amesema: Miongoni mwa yale yaliyojaribiwa kwa ajili ya hifidhi ni achukue zabibu nyekun  Misbaahu, uk. 267 cha Kafia’mi.   Biharul-Anwaar, Juz. 59, uk. 271 kutoka kitabu Jannat cha Kafia’mi.

596 597

136

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 136

8/10/2017 1:22:05 PM


TIBA YA MAASUMINA

du iliyo safi pukupuku kiasi cha dirhamu ishirini, na achukue Suud Flatsedge ya Mji wa Kufa kiasi cha gramu tano, na achukue ubani dhakar kiasi cha dirham mbili, na achukue zafarani kiasi cha nusu dirham, visagwe hivyo na kuchanganywa kwa maji ya shamari, na atumie asubuhi kabla ya kula chochote kila siku kwa kiasi cha dirham moja. Akasema: Na yule anayedumisha kula zabibu kabla ya kula chochote ataruzikiwa ufahamu na hifidhi na ubongo, na atapunguza kikohozi (dirham ni sawa na gram tatu ya nne). Na miongoni mwa dawa za uletaji hifidhi, imepokewa kutoka kwa Abu Baswiir kuwa alisema: Nilisema kumwambia Imam asSadiq (a.s): Vipi tunaweza kuidhibiti elimu hii mliyoigawanya matawi mbalimbali kwetu? Akasema: “Chukua kipimo cha dirham 10 ya karafuu, na mfano wake kundur dhakar, zisagwe hadi ziwe laini kisha tumia kidogo asubuhi kabla ya kula kitu.” Na miongoni mwa dawa hizi kwa yule anayekuwa mbali na ubongo na anahifidhi ndogo, basi achukue Sina ya Makka, na Suud Flatsedge ya kihindi, na pilipili nyeupe, na kundur dhakar, na zafarani halisi, viungo sawa, na visagwe na vichanganywe na asali, na anywe hiyo kipimo cha gramu tano kila siku, kwa muda wa siku saba mfululizo, hakika akifanya kitendo hicho kwa siku 14, nachelea ataambiwa kuwa ni mchawi kutokana na ukali wa hifidhi.598 Na miongoni mwa hayo ni yale yaliyopokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Yule atakayechukua sehemu ya zafarani halisi na sehemu ya Suud Flatsedge, na akachanga hivyo viwili na asali, na akanywa kiasi cha mithqal mbili kila siku, nachelea ataitwa mchawi kutokana na ukali wa hifidhi.”   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 272.

598

137

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 137

8/10/2017 1:22:05 PM


TIBA YA MAASUMINA

Na miongoni mwa yale yaliyokutwa kwa hati ya Sheikh Ahmad bin Fahad, ni maelezo ya dawa ya hifidhi, nimeshuhudia usahihi wake kwa vitendo, nayo ni: achukue kwa kiwango sawa Kundur na Suud Flatsedge na Sukar Twabrizad, na visagwe hivyo hadi viwe laini, kisha atumie kiasi cha dirham tano asubuhi kabla ya kula kitu, kwa muda wa siku tatu, kisha akae siku tano bila kutumia, kisha atumie tena kwa muda wa siku tatu, kisha akae siku tano bila kutumia, aendelee kwa utaratibu huo.599 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Ufyonzaji wa damu mwilini unaongeza akili na unamzidishia mwenye kuhifadhi hifidhi.”600 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Figili inasababisha hifidhi na inatakasa moyo na inaepusha uwendawazimu, mbalanga na ukoma.”601 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Na neema kubwa mno juu ya mtu ni hifidhi, na pia usahaulifu, kwani lau kama si usahaulifu basi mtu asingejiliwaza wakati wa msiba.”602 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kuwa alisema: “Mambo matatu husababisha hifidhi na huongeza balgham; usomaji wa Qur’ani, asali na ubani (kundur).”603 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kuwa alisema: “Ndani ya asali ipo tiba ya kila ugonjwa. Na yule atakayelamba asali kabla ya kula chochote itakata kikohozi na itaondoa manjano na itazuia kibofunyongo cheusi, na itasfisha ubongo na itaifanya hifidhi kuwa   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 273, kutoka kitabu Luqatul-Fafiid.   Makarimul-Akhlaq, uk. 76. 601   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 284. 602   Biharul-Anwaar, Juz. 3, uk. 81. 603   Sahifat Ridha (a.s), uk. 68. 599 600

138

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 138

8/10/2017 1:22:05 PM


TIBA YA MAASUMINA

nzuri, ikiwa itatumiwa pamoja na ubani dhakar (nao ni gundi litokalo kwenye mti wa kundur).604 Katika Barua ya dhahabu ya Imam Ridha (a.s) amesema: “Na yule ambaye anataka kuongeza hifidhi yake basi ale mithqal saba za zabibu asubuhi kabla ya kula chochote, na yule anayetaka kupunguza usahaulifu wake na kuwa mwenye kuhifadhi, basi ale kila siku vipande vitatu vya tangawizi murabbi kwa asali, na apake khardali kwenye chakula chake kila siku. Na yule anayetaka kuzidisha akili yake basi naale kila siku halilijat tatu kwa sukari ya Abliji.”605 Imepokewa kwamba tufaha linasababisha usahaulifu, na hiyo ni kwa sababu linasaidia kizazi katika mfuko wa chakula cha mwanamke.”606 Ametaja Sheihk Muhammad bin Husein Jundaqi: Hakika wakati mzuri zaidi kwa ajili ya kuhifadhi ni usiku wa manane, na kwa ajili ya utafiti ni mapema mno asubuhi, na kwa uandishi ni katikati ya mchana, na kwa ajili ya kurudia na kujikumbusha masomo ni usiku na sio mchana, na wakati wa njaa ni bora kuliko wakati wa shibe, na sehemu iliyo mbali na burudani ni bora.607 Wale madaktari waliofuatia wamesema: Unusaji wa nywele za mtu mchana na usiku huondoa maradhi ya usahaulifu kabisa. Kwa hakika hilo ni jambo mujarabu.608 Nasru-Diini Tuusi katika Aadabul-Mutaa’llimiina amesema: “Na sababu yenye nguvu zaidi katika hifidhi ni: Juhudi na kudumu katika suala hilo, na upunguzaji wa chakula, na swala ya usiku kwa unyenyekevu na khushui, na usomaji wa Qur’ani. Na pia mion  Fiqhul-Ridha (a.s), uk. 346.   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 324. 606   Makarimul-Akhlaq, uk. 173. 607   Tuhfatul-Ridhawiyya fi Mujarrabaat Imamiyyat, uk. 79. 608   Tuhfatul-Ridhawiyya fi Mujarrabaat Imamiyyat, uk. 79. 604 605

139

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 139

8/10/2017 1:22:06 PM


TIBA YA MAASUMINA

goni mwa sababu zinazopelekea hifidhi… ni kukithirisha kumswalia Mtume (s.a.w.w), kupiga mswaki, kula asali, kula kundur pamoja na asali, na kula punje 21 za zabibu nyekundu kila siku asubuhi kabla ya kula kitu, yote hayo yanasaidia hifidhi, na yanaponya maradhi na magonywa mengi. Na kila ambalo linapunguza kikohozi na unyevunyevu linaongeza hifidhi, na kila ambalo linaongeza kikohozi husababisha usahaulifu. Na ama yale ambayo yanasababisha usahaulifu, ni maasi mengi, na wingi wa majonzi na huzuni… na ulaji wa kuzbara na tufaha la uchachu, kumwangalia anayesulubiwa, na usomaji wa maandishi ya makaburini, na upitaji katika njia za ngamia, na utupaji wa taka hai juu ya ardhi, na ufyonzaji wa damu mwilini, yote hayo husababisha usahaulifu.”609 UINGIZAJI WA BOMBA SEHEMU YA HAJA KUBWA Mtume (s.a.w.w) amesema: “Hakuna tatizo kuingiza bomba sehemu za haja kubwa, na kama si hivyo tumbo litavimba.”610 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Uingizaji wa bomba sehemu ya haja kubwa ni dawa.”611 Imepokewa pia kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Dawa ni nne; ufyonzaji wa damu mwilini, upakaji, utapishaji na uingizaji wa bomba sehemu ya haja kubwa.”612 UWATU Ni mmea wa pembezoni una maua meupe, unafanana na mmea wa Alfalfa, na kiungo chenye kufanya kazi, una mbegu zilizoiva na umesheheni koloidi nyingi, miongoni mwa hizo ni kolini.   Nuswusul-Dirasiyyat fil-Hawzat Ilmiyyat Qum, uk. 18 kimehakikiwa na Muhammad bin Husein Jalali. 610   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 134, kutoka kitabu Dawaaim. 611   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 54. 612   Khiswal, Juz. 1, uk. 249, kutoka kitabu Twibbul-Aimmat, uk. 55. 609

140

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 140

8/10/2017 1:22:06 PM


TIBA YA MAASUMINA

Faida zake: Vitabu vya tiba vya kale vinasifia Uwatu kwamba unatia nguvu mfuko wa chakula, unasababisha uwepo wa mada ya kibofunyongo, na kwamba unasafisha damu ikiwa mtu ataunywa asubuhi kabla ya kula kitu chochote, na ukichemshwa unafanya maziwa ya mama anayenyonyesha yatoke kwa wingi. Na uwatu uliyochemshwa unatumiwa hivi leo kwa kunywa ili kuongeza uzito, kama vile unavyowasaidia wagonjwa wa kutokwa na haja ndogo, na kwa wenye kisukari ili kuponya vidonda, na unatumiwa kutibu uvimbe mchungu kwenye mapafu na uchafu wa utumbo, na unazuia bawasiri. Pia uliochemshwa unatumiwa katika hali za uvimbe wa lozi mbili, na ugonjwa wa dondakoo.613 Hadithi: Mtume (s.a.w.w) amesema: “Jitibuni kwa Uwatu, lau umma wangu ungelijua yale yaliyomo katika Uwatu wangelijitibu kwawo hata kama wangelipa thamani yake kwa dhahabu.614 UNYOAJI WA NYWELE Mtume (s.a.w.w) amesema: “Yule ambaye anamwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho basi asiache kinena chake siku 40 bila kunyoa, wala sio halali kwa mwanamke anayemwamini Mwenyezi Mungu kuacha kinena chake zaidi ya siku 20 bila kunyoa.”615 Imepokewa kutoka kwa Anas kuwa alisema: “Mtume (s.a.w.w) alituwekea wakati sisi wa mtu kunyoa nywele za kinena chake, ni   Nabataat Twibbiyyat wal-Aturiyat fil-watan Arabi, uk. 69 mwaka 1988.   Makarimul-Akhlaq, uk. 213, Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 233, na kutoka kitabu Daa’im uk. 274. 615   Makarimul-Akhlaq, uk. 59. 613 614

141

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 141

8/10/2017 1:22:06 PM


TIBA YA MAASUMINA

ndani ya kila siku 40, na anyoe kikwapa chake kila zinapojitokeza, wala asiache masharubu yake yarefuke, na akate kucha zake siku ya Ijumaa hadi Ijumaa nyingine.”616 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Yule ambaye anamwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho asiache kunyoa nywele za kinena chake zaidi ya wiki moja, wala asiache kuondoa nywele za mwili zaidi ya mwezi.”617 Alikuwa Imam as-Sadiq (a.s) akizipunguza nywele za kwapa zake bafuni na akisema: “Unyofoaji wa nywele za kwapani unadhoofisha mabega mawili na unadhoofisha uonaji.” Imepokewa pia kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Unyoaji ni bora zaidi kuliko unyofoaji, na utoaji kwa upakaji ni bora zaidi kuliko unyoaji wake.”618 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kuwa alisema: “Mambo manne ni tabia ya Mitume; Kujipaka manukato, kujisafisha kwa wembe, kunyoa nywele za mwili na kuzidisha kujamiiana.”619 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Unyofoaji wa nywele za kwapani unaondoa harufu ichukizayo, nayo ni tohara na sunna.”620 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Upunguzaji wa masharubu ni usafi, nayo ni miongoni mwa sunna.”621 Mambo matano hufanywa katika kichwa: Utindaji wa masharubu, usukutuaji wa maji, upandishaji wa maji puani, upigaji mswaki na utenganishaji wa nywele za kichwa.   Tafsiru Durru Manthuur, Juz. 1, uk. 113 cha Suyuuti.   Makarimul-Akhlaq, uk. 59. 618   Makarimul-Akhlaq uk. 60. 619   Makarimul-Akhlaq uk. 63. 620   Tuhfatul-Uquul uk. 72. 621   Tuhfatul-Uquul, uk. 72. 616 617

142

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 142

8/10/2017 1:22:06 PM


TIBA YA MAASUMINA

Na matano hufanywa katika mwili: Ukataji wa kucha, unyoaji wa nywele za kinena, jando na upunguzaji wa nywele za kwapa na kuosha athari ya haja kubwa.”622 HALUWA Mtume (s.a.w.w) amesema: ‘Muumini ni mtamu anapenda utamu, na muumini haluwa anapenda haluwa.’623 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Kila mwenye kuwa na huba zaidi na sisi, huzidi huba yake kwa wanawake na haluwa.”624 Imam Kadhim (a.s) amesema: “Hakika sisi na wafuasi wetu tumeumbwa kutokana na utamu, basi sisi tunapenda haluwa.”625 HOMA Mtume (s.a.w.w) amesema: “Homa inapukutisha madhambi kama vile mti unavyopukutisha majani.”626 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Mwenye homa atumie kipimo cha dirham 10 cha sukari kwa maji ya waridi asubuhi kabla ya kula kitu (dirham inalingana na robo tatu ya gram).”627 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Asali ni ponyo inayofukuza harufu ya homa.”628 Imepokewa pia kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Homa inatokana na uchemkaji wa jahannam basi izimeni kwa maji ya baridi.”629   Kamil, Juz. 1, uk. 113 cha ibn Athiir.   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 218, kutoka kitabu Mahasin cha Barqi. 624   Ramzul-Sihat, uk. 178. 625   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 52, kutoka kitabu Furuu Kaafi, Juz. 6, uk. 321. 626   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 301. 627   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 50. 628   Ramzul-Sihat, uk. 299. 629   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 49. 622 623

143

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 143

8/10/2017 1:22:06 PM


TIBA YA MAASUMINA

Mtume s.a.w.w) aliingia kwa Ali (a.s) naye akiwa na homa, basi akamwamrisha yeye kula ghubayraa Rowan – sorbus.630 Imepokewa kwamba: Homa ni kifo kilicholala, na homa inatokana na mdomo wa Jahannam, na homa ina kinga ya kila muumini kutokana na moto.631 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Homa ni kifo kilichotulia, nayo ni jela la Mwenyezi Mungu ardhini, nayo inapukutisha madhambi kama vile manyoya yanavyopukutika kutoka kwenye nundu la nyumbu.”632 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Liondoeni joto la homa kwa balungi.”633 Imepokewa pia kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Zabibu inaondoa homa.”634 Vilevile imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Hakuna ugonjwa ila unatoka ndani ya tumbo isipokuwa jeraha na homa, kwani hayo mawili yanapatikana uwepo wake. Liondoeni joto la homa kwa balungi na maji ya baridi, hakika joto lake linatokana na mdomo wa Jahannam.”635 Imepokewa kutoka kwa Imam Zaynul-Abidiina (a.s) kuwa alisema: “Lowesheni tumbo la mwenye homa kwa sawiiq na asali mara tatu, na ibadilishe kutoka kwenye chombo cha kwanza kisha anywe mwenye homa, kwani inaondoa homa ya joto, na hakika imefanyiwa kazi kwa ufunuo.”636 Imepokewa kutoka kwa Imam al-Baqir (a.s) kuwa alisema: “Utoaji wa homa upo katika vitu vitatu; katika utapikaji, utoaji wa damu kutoka katika mishipa na muharo wa tumbo.”637   Uyuun, Juz. 2, uk. 43, na Makarimul-Akhlaq, uk. 176.   Dhawhu-Shub-haat. 632   Mustadrakul-Nahj, uk. 161. 633   Mustadrakul-Nahj, uk. 170. 634   Makarimul-Akhlaq, uk. 175. 635   Khiswal, uk. 161 cha Saduuq. 636   Makarimul-Akhlaq, uk. 192. 637   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 50. 630 631

144

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 144

8/10/2017 1:22:06 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Kila ugonjwa unatokana na mmeng’enyo mbaya, ila homa hakika, hiyo huja yenyewe.”638 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Yule anayeumwa homa anywe usiku huo kiwango cha dirham mbili za mbegu za katani au tatu, atapata amani kutokana na bawasiri katika ugonjwa huo.”639 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Kitunguu kinaondosha uchovu, na kinakaza mishipa ya fahamu, na kinaongeza katika upigaji hatua na kinazidisha maji, na kinaondoa homa.”640 Imepokewa kutoka kwa Ibrahim Ju’afi kutoka kwa baba yake amesema: Niliingia kwa Abu Abdillah as-Sadiq (a.s), akaniambia: “Mbona sikuoni mwenye uso wenye kuchangamka?” Nikasema: Hakika mimi nina homa ya nne641 ewe bwana wangu, akasema (a.s): “Uko wapi wewe na mti wenye baraka wenye harufu nzuri, saga sukari kisha chukua kwa maji na kunywa asubuhi kabla ya kula kitu, fuatilizia maji kama kuna haja ya kunywa maji.”642 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Kula tufaha, kwani linazima joto, na linaleta ubaridi tumboni, na linaondoa homa.”643 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kwamba lilitajwa kwake suala la homa, akasema: “Hakika sisi Ahlul-Bayt hatujitibu ila kwa kujimwagia maji ya baridi ambayo huwa tunamwagiwa juu yetu, na kwa ulaji wa tufaha.”644   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 80.   Makarimul-Akhlaq, uk. 215. 640   Fusuulul-Muhimmat, uk. 137 cha Hurru Aamili. 641   Homa ya robo ni ile ambayo inajitokeza siku na inaacha siku mbili na inakuja siku ya nne. 642   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 56. 643   Wasaail- Shi’ah, Juz. 3, uk. 30 cha Hurri Aamili. 644   Mahasin, uk. 551. 638 639

145

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 145

8/10/2017 1:22:06 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Walisheni wagonjwa wenu wa homa tufaha, hakuna kitu chenye manufaa zaidi kuliko tufaha.”645 Imepokewa vilevile kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuhusiana na tufaha kuwa alisema: “Nalo linang’oa homa na linatuliza joto.”646 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Uchanaji wa nywele unaondoa homa, na uchanaji wa ndevu unakaza magego.”647 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Hakika ndani ya habasoda kuna ponyo la kila ugonjwa, na mimi ninaitumia kwa ajili ya homa, maumivu ya kichwa na ugonjwa wa macho…”648 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Kababu inaondoa homa.”649 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Kitunguu maji kinaondoa homa.”650 Imepokewa kutoka kwa Imam asSadiq (a.s) kuwa alisema: “Sijakuta kinachoondoa homa mfano wa maji ya baridi, na maombi.”651 Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) kuwa alisema: “Sawiiq ikioshwa mara saba na ikageuzwa kutoka chombo hadi kingine basi inaondoa homa, na inateremsha nguvu kwenye ngoko mbili na miguu miwili.”652   Mahasin, uk. 551 na Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 63.   Biharul-Anwaar, Juz. 62 uk. 93. 647   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 33 cha Shubbar. 648   Makarimul-Akhlaq, uk. 186. 649   Mahasin, uk. 468. 650   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 99. Na Mahasin uk. 522. 651   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 50. 652   Wasaail-Shi’ah, Juz.. 17 uk. 8 kutoka kitabu Furuu na Mahasin. 645 646

146

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 146

8/10/2017 1:22:06 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) kwamba aliulizwa kuhusu homa yenye kuja na kupotea, akasema: “Inachukuliwa asali na habasoda na anatumia vijiko vitatu, hakika inaondoa. Na hivyo viwili ni vyenye baraka, hakika Mwenyezi Mungu aliyetukuka anasema: “Inatoka matumboni mwao…” na Mtume (s.a.w.w) amesema: “Ndani ya habasoda kuna ponyo la kila tiba ila sumu. Ikaulizwa: Ewe Mtume, ni sumu ipi hiyo? Akasema: Kifo.” Akasema: Hivi viwili haviegemei katika ujoto wala ubaridi, wala katika maumbile, hakika hivi viwili ni ponyo vitakapopatikana pamoja.”653 Kutoka kwa Imam Ridha (a.s): Kutoka kwa Muhammad bin Sinan amesema: Nilimsikia Imam Musa bin Ja’far (a.s) alipolalamika kuwa ana homa, wakamjia wataalamu wa tiba (yaani waganga) wakawa wanamwelezea yeye maajabu mbalimbali. Akasema: Wapi inawapelekeni nyinyi? Kuweni na dawa hizi tu, haliji, shamari na sukari. Mwanzo wa kiangazi zitumieni katika miezi mitatu, na katika kila mwezi mara tatu. Na mwanzo wa masika zitumieni miezi mitatu, katika kila mwezi siku tatu.”654 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kuwa alisema: “Hakika hindubaau Chickory.” ni ponyo la magonjwa elfu, hakuna ugonjwa ndani ya mwili wa mtu ila huondolewa na hindubaau Chickory.”655 Na siku moja akaagiza (a.s) hindubaau Chickory kwa ajili ya mfuasi wake, alikuwa akisumbuliwa na homa na maumivu ya kichwa, basi akaamrisha isagwe kisha ifungwe kwenye karatasi, na atie juu yake mafuta ya balungi, na aiweke juu ya kichwa chake, kisha akasema: “Ama hii inakomesha homa na inaondoa maumivu ya kichwa.”656   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 51.   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 50. 655   Khiswal, Juz. 1, uk. 249. 656   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 144, kutoka kitabu Furuu Kaafi. 653 654

147

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 147

8/10/2017 1:22:06 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kuhusu maji ya waridi kuwa alisema: “Hakika hayo yanazima joto, na yanatuliza manjano, na yanalainisha chakula, na yanaondoa mabaki ambayo yako juu ya kichwa cha mfuko wa chakula, na yanaondoa homa.”657 Imepokewa kutoka kwa Imam Hadi (a.s) kuwa alisema: “Vitu bora zaidi kwa homa ya nne, ni kula siku husika Faludhaji (ni haluwa inayotengenezwa kutokana na unga, maji na asali) na iliyotengenezwa kwa asali, na azidishe zafarani yake, wala asile kingine katika siku yake husika.”658

HUMSWI CHICKPEA Faida zake: HUMSWI/CHICKPEA inasaidia kwa aina mbali mbali za maumivu ya kichwa baridi hususan kipanda uso, na inasafisha sauti na inaondoa uvimbe kooni, kifuani na kikohozi. Na ikiwa ataendelea kula ikiwa imekaangwa pamoja na lozi kidogo itamnenepesha yeye unenepaji wa kupindukia, na inamsaidia yule ambaye amepoteza matamanio yake ya jinsia.659 Hadithi: Imepokewa kutoka kwa Bazantwi kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kuwa alisema: “Humswi/Chickpea ni nzuri kwa maumivu ya mgongo, na alikuwa akiitisha hiyo kabla na baada ya kula.”660   Fiqhul-Ridha (a.s), uk. 346.   Rumzul-Sihat, uk. 33 cha Dahsurkhi, kutoka kitabu Twibbul-Aimmat (a.s). 659   Rumzul-Sihat, uk. 33 cha Dahsurkhi, kutoka kitabu Twibbul-Aimmat (a.s). 660   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 97 kutoka kitabu Furuu Kaafi na Mahasin. 657 658

148

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 148

8/10/2017 1:22:06 PM


TIBA YA MAASUMINA

BAFU Mtume (s.a.w.w) amesema: “Yule aliyemwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho wala asifanye upuuzi na mkewe hadi bafuni.”661 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Nyumba bora ni bafu, inakumbusha moto na inaondoa taka.”662 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Usiingie bafuni ila tumboni mwako kuna kitu ambacho kitazima joto ya mfuko wa chakula, nalo linatia nguvu zaidi za mwili. Wala usiingie na wewe ukiwa umeshiba sana chakula.”663 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Yule anayeingia bafuni asubuhi kabla ya kula kitu ni safisho la balgham, na akiingia baada ya kula ni safisho zaidi la kibofunyongo, na ikiwa unataka uongeze nyama yako basi ingia bafuni ukiwa umeshiba, na ikiwa unataka ipungue nyama yako basi ingia kabla ya kula chochote.”664 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Na mwagia maji ya baridi juu ya nyayo zako utakapotoka (bafuni) kwani hilo linaondoa ugonjwa kutoka mwilini kwako.”665 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Mambo mtatu yanaangamiza mwili na huenda yakaua; kula nyama kavu, kuingia bafuni hali tumbo limejaa na kumwingilia ajuza.”666 Ali bin Yaqtwin alimuuliza Imam Kadhim (a.s): Ninasoma (sehemu yoyote ya Qur’ani) bafuni na ninapokutana kimwili” akasema: “Hakuna tatizo.”667   Makarimul-Akhlaq, uk. 53.   Mustdrakul-Nahj, uk. 165. 663   Biharul-Anwaar, Juz. 76, uk. 77, Fusuulul-Muhimmat cha Hurri Aamili na Twibbu Imam Swadiq uk. 81. 664   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 66. 665   Makarimul-Akhlaq ,uk. 52, kutoka kitabu Man la yahdhurhul-Faqiih cha sheikh saduuq. 666   Buharul-Anwaar, Juz. 63 uk. 76. 667   Makarimul-Akhlaq, uk. 53. 661 662

149

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 149

8/10/2017 1:22:06 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) kuwa alisema: ­“Kuingia bafuni ni siku moja na siku nyingine hapana, kwani hilo linazidisha nyama, kwani kudumisha kuingia kila siku kunayeyusha mafuta ya kende mbili.”668 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kwamba alimwambia Maamuni katika barua yake ya dhahabu: “Na jua ewe AmirulMuuminina hakika bafu la sokoni limepangwa juu ya mpangilio wa mwili; bafu lina vyumba vinne; mfano wa tabia za kimaumbile nne za mwili; ya kwanza baridi yabisi, ya pili baridi na unyevunyevu, ya tatu joto na unyevunyevu, na ya nne joto na yabisi. Na manufaa ya bafu ni makubwa, linapelekea ulinganifu, linaondoa taka, linalainisha ghadhabu na mishipa, na linatia nguvu viungo vya wale wenye umri mkubwa, linayeyusha mabaki na linaondoa kuchakaa.”669 MLO KAMILI Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Haifai mlo kamili baada ya siku saba.”670 Imepokewa kutoka kwa Muhammad bin Faydh kuwa amesema: Nilimuuliza Imam as-Sadiq (a.s): Nafsi yangu nimeitoa fidia kwako, anaumwa miongoni wetu mgonjwa basi waganga wanamwamrisha kutumia mlo kamili? Akasema: “Hapana, lakini sisi Ahlul-Bayt hatufanyi mlo kamili ila kutokana na tende, na tunajitibu kwa tufaha, na maji ya baridi.” Nikasema: Kwa nini mnafanya mlo kamili kwa tende? Akasema: Hakika Mtume (s.a.w.w) alimwandalia mlo kamili Ali (a.s) kwa hayo katika maradhi yake.”671   Makarimul-Akhlaq, uk. 53.   Biharul-Anwaar, Juz. 59, uk. 322 cha Sheikh Majlisi. 670   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 59. 671   Ilalu-Sharaai, Juz. 2, uk. 149 cha Saduuq na Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 59. 668 669

150

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 150

8/10/2017 1:22:06 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) kuwa alisema: “Sio mlo kamili kuacha kula kitu kabisa, lakini mlo kamili ni kula kitu kwa tahfifu.”672 Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) kuwa alisema: “Hakuna kitu katika mwili chenye manufaa zaidi kuliko kuuzuia mkono ila kwa kile ambacho unakihitajia hicho.”673 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kuwa alisema: “Lau kama watu wangelipunguza ulaji wa chakula miili yao ingelisimama sawa sawa.”674 Imepokewa pia kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kuwa alisema: “Mlo kamili ni chanzo cha kila dawa, na mfuko wa chakula ni nyumba ya kila ugonjwa, na izoesheni miili yenu yale iliyoyazoea.”675 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kuwa alisema: “Chanzo cha mlo kamili ni kuafikiana na mwili.”676 Imepokewa pia kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kuwa alisema: “Hakika mlo kamili wa mbali zaidi ni siku 14, na hakika huko si kuacha kula kitu, lakini ni kuacha kuzidisha chakula.”677

HINA Faida zake: Hina ni miongoni mwa mimea ambayo inapatikana juu ya Arshi nzuri, hutumiwa sana katika kijipaka na kujirembesha tangu hapo zama za kale. Nao ni mmea tajiri kwa mada ya kushika na kusokota.   Rawdhutul-Kaafi, uk. 291.   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 68. 674   Makarimul-Akhlaq, uk. 419. 675   Fiqhul-Ridha, uk. 340. 676   Fiqhul-Ridha, uk. 340. 677   Fiqhul-Ridha, uk. 347. 672 673

151

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 151

8/10/2017 1:22:06 PM


TIBA YA MAASUMINA

Na hakika aliutumia Bwana Mtume (s.a.w.w) pale alipopatwa na maumivu ya kichwa, kwani unafaidisha katika kuua vidudu hatarishi. Na alikuwa (s.a.w.w) akiwaamrisha masahaba wake kuitumia katika hali ya maumivu ya nyayo, na kutokwa na jasho mno na pia vidonda.678 Hadithi: Mtume (s.a.w.w) amesema: “Hina ni bwana wa manukato mazuri ya watu wa peponi…”679 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Hina ni pako la Uislamu, inaongeza kwa muumini amali yake, na inaondoa maumivu ya kichwa, na inanyoosha macho, na inazidisha tendo la kujamiiana, nayo ni bwana wa manukato ya duniani na akhera.”680 Imepokewa kutoka kwa mtumishi wa Mtume (s.a.w.w) kwamba yeye (s.a.w.w) alisema: “Ni juu yenu kujipaka hina, hakika hiyo inazidisha nguvu wakati wa kukutana kimwili, na inapendezesha ngozi.”681 Imepokewa kwamba, hakuna mtu aliyemlalamikia Mtume (s.a.w.w) kuhusiana na maumivu ya kichwa ila alimwambia: “Tumia ndumiko.” Wala hakuna mtu aliyemlalamikia yeye maumivu ya miguu yake ila alimwambia: “Zipake ndevu zako hina.”682 Imepokewa kutoka kwa mtumishi wa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Mtume (s.a.w.w) alikuwa hayamsibu majeraha wala miiba ila aliweka juu yake hina.”683   Majallatul-Ahraam Riyaadhi, uk. 77 toleo la 100 tashriin THANI mwaka 1991.   Makarimul-Akhlaq, uk. 82 kutoka kitabu Firdausi. 680   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 299. 681   Makarimul-Akhlaq, uk. 12. 682   Twibbul-Nabawi, uk. 69 cha Ibn Qaym, na kutoka kitabu Bukhari uk. 69 kutoka kitabu katika Tarikh Bukhari yake. 683   Twibuun-Nabii cha Ibn Qaym Zayziyyat kutoka kwa Tirmidhi. 678 679

152

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 152

8/10/2017 1:22:06 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa alisema: “Jipakeni hina, kwani hiyo inasafisha macho, inapendezesha nywele, inaleta harufu nzuri na inamtuliza mke.”684 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Mambo manne ni miongoni mwa sunna za Mitume, usafishaji meno, kujipaka hina, kujipaka manukato mazuri na wanawake.”685 Imepokewa kutoka Imam Ridha (a.s) kuwa alisema: “Upakaji hina baada ya unyoaji wa nywele ni kinga ya mbalanga na ukoma.”686 HANDHALA / AINA YA TANGO Katika Handhala huchukuliwa lile lenye weupe uliyokoza na laini, na yapaswa lisichumwe likiwa halijafikia katika rangi ya manjano, na halijageuka kuwa rangi ya kijani kibichi kwa ukamilifu. Faida zake: Nalo ni la joto yabisi, lenye kusaidia kwa maumivu ya mishipa ya fahamu na muunganiko, na mishipa ya wanawake na jongo ya baridi. Linasafisha ubongo, na mizizi yake inapikwa pamoja na siki, na kusukutua kwa yule mwenye ugonjwa wa meno… na ikiwa litapikwa kutoa mafuta, basi mafuta hayo yatakuwa matone mepesi na yatafaa kwa maumivu ya sikio na yatarahisisha ung’oaji wa meno.687 Hadithi: Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) kuwa alisema: “Dawa ya gego, utachukua Handhala utaimenya kisha utatoa mafuta yake,   Twibbul-Aimmat (a.s) uk. 309 cha Abdullah bin Shubbar.   Makarimul-Akhlaq, uk. 41. 686   Sahifat Ridha (a.s), uk. 76. 687   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 163 kutoka kitabu Kaafi. 684 685

153

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 153

8/10/2017 1:22:06 PM


TIBA YA MAASUMINA

ikiwa gego limetoboka basi dondoshea ndani yake matone, na unafanya hivyo kwa pamba ndogo kwa kuweka ndani ya gego, na utalala chali, utatumia dawa hiyo kwa muda wa mikesha matatu. Na ikiwa gego halina tundu lakini lina harufu, utadondoshea matone katika sikio lililopo upande wa gego, utafanya hivyo kwa muda wa mikesha mitatu, kila usiku matone mawili au matone matatu, litapona kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.”688 UHAI NA MAISHA MAREFU Bazru Jamhar amesema: “Mambo manne yanaangamiza umri na huenda yakaua; kuingia bafuni hali ya kuwa tumbo limejaa, na kushiriki tendo la ndoa wakati tumbo limejaa, na ulaji wa nyama kavu, na unywaji wa maji baridi kabla ya kula chochote.”689 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Yule anayetaka kubakia na hakuna ubakiaji kama huo, basi mtu awahi mapema kifungua kinywa, na acheleweshe chakula cha usiku, na afanye tahfifu kuchukua madeni, na apunguze kukutana kimwili na wanawake.” Ikaulizwa: Na ipi tahfifu ya madeni? Akasema: Ukopaji na uchukuaji wa madeni.”690 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuwa alisema: “Tunda la uhai mrefu ni ugonjwa na uzee.”691 Imepokewa kutoka kwa Abu Abdillah Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Mihimili ya mtu na ubakiaji wake ni katika mambo manne; moto, nuru, upepo na maji. Kwa moto anakula na anakunywa. Kwa nuru anaona na kutia akilini. Kwa upepo anasikia na kunusa. Na kwa maji anapata ladha ya chakula na kinywaji. Na kama si kuwe  Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 163 kutoka kitabu Kaafi.   Aqdul-Fariid, Juz. 8, uk. 17. 690   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 267 na Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 29 na inafanana nacho. 691   Ghurarul-Hikam. 688 689

154

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 154

8/10/2017 1:22:07 PM


TIBA YA MAASUMINA

po na moto katika mfuko wa chakula chake basi usingelipatikana mmeng’enyo wa chakula na kinywaji. Na kama si nuru katika uoni wake usingelikuwepo uoni wala akili. Na kama si upepo usingelichochea moto wa mfuko wa chakula. Na kama si maji isingelipatikana ladha ya chakula na kinywaji.”692

HEDHI NA KUMWINGILIA MWANAMKE Mtume (s.a.w.w) amesema: “Mambo matano yanasababisha ukoma: …. Na kukutana kimwili na wanawake katika siku za hedhi….”693 Imepokewa kutoka kwa Ali bin Mihziyaar kuwa alisema: Hakika kijakazi (binti mdogo) wetu, alipatwa na hedhi, na ikawa haikatiki, mpaka akakaribia kufa. Basi akaamrisha Imam al-Baqir (a.s) akasema: “Anywe uji wa adesi.” Basi akanywa na ikakatika na akapona.694 Imepokewa kutoka kwa Ismail bin Yushaa kuwa alisema: Nilimwambia Imam Ridha (a.s): Hakika msichana umeondoka ugonjwa wake. Akasema: “Kipake kichwa chake hina, hakika hedhi itarejea kwake”. Nikafanya hilo, basi ikarejea hedhi yake.695 Mwanamke mmoja aliandika barua kwenda kwa Imam Ridha (a.s) akimlalamikia yeye utokaji wa damu yake bila kukatika, basi akamwandikia yeye: “Mwenyezi Mungu akipenda yatosha kutumia kazbara, na mfano wa sumaku, basi iweke hiyo usiku chini ya nyota, kisha ichemshe kwa moto kwenye chungu, basi kunywa hiyo kiwango cha sukarjat, itakatika damu yako, ila katika nyakati za hedhi.696   Khiswal, Juz. 1, uk. 227.   Khiswal, Juz. 1, uk. 270. 694   Makarimul-Akhlaq, uk. 193. 696   Makarimul-Akhlaq, uk. 81. 696   Fiqhul-Aimmat (a.s), uk. 64 kutoka kitabu cha Masuudiy. 692 693

155

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 155

8/10/2017 1:22:07 PM


TIBA YA MAASUMINA

MKATE Mtume (s.a.w.w) amesema: “Ewe Mwenyezi Mungu tubariki katika mkate, wala usifarikishe baina yetu na yake, na lau kama sio mkate tusingelifunga wala tusingeswali, wala tusingelitekeleza faradhi za Mola Wetu Mlezi.”697 Na katika hilo amesema mshairi ibn A’asim katika utenzi wake: “Fadhila ya mkate ambao lau usingelikuwa huo – asingeliweza mja siku kumwabudu Mungu Wake. Hakika imepokewa kuwa lau sio huo tusingelitekeleza – madeni yetu wala tusingelifunga wala tusingeliswali.” Mtume (s.a.w.w) amesema: “Kateni vipande vidogo vidogo mikate yenu, kwani kila kipande cha mkate kina baraka.”698 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Mtakapoletewa mkate na nyama, basi anzeni kula mkate na ondoeni njaa, kisha kuleni nyama.”699 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Utukuzeni mkate kwani umefanya yale ambayo yapo baina ya arshi mpaka ardhini, na ndani yake ni miongoni mwa viumbe wake.” (anakusudia malaika). Kisha akasema kuwaambia wale waliomzunguka: “Je, nikuhadithieni?” Wakasema: Ndio, ewe Mtume, baba zetu na mama zetu wawe fidia kwako. Basi akasema: “Hakika alikuwepo Nabii kabla yenu aliyeitwa Daniel, yeye alimpa mtu wa kivuko kipande cha mkate ili avuke nacho, basi akakitupa yule mvukaji kile kipande cha mkate na akasema: ‘Nitafanya nini na mkate. Mkate huu kwetu ni wa kukanyagwa na miguu.’ Na pindi Daniel alipoliona hilo, aliinua mkono wake mbinguni, kisha akasema: ‘Ewe Mwenyezi Mungu   Makarimul-Akhlaq, uk. 15.   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 279. 699   Wasaail-Shi’ah, Juz.. 16, uk. 512. 697 698

156

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 156

8/10/2017 1:22:07 PM


TIBA YA MAASUMINA

utukuze mkate, kwa hakika ewe Mola Wangu Mlezi umeona alivyofanya mja huyu na alichosema.’ Mwenyezi Mungu akaipa Wahyi mbingu izuie mvua, na akaipa Wahyi ardhi iwe ngumu isioteshe chochote. Basi haikunyesha mvua hata tone moja, mpaka ikafikia hali baadhi yao kuwala wengine.”700 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Utukuzeni mkate, hakika Mwenyezi Mungu (a.j) aliuteremsha kwa baraka za mbingu, na akaufanya kuwa miongoni mwa baraka za ardhi.” Ikaulizwa: Na upi utukuzaji wake? Akasema: “Usikatwe hovyo wala usikanyagwe.”701 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Utukuzeni mkate, kwani umefanya yale yaliyopo baina ya arshi hadi ardhini na yaliyopo katikati yake.”702 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Hakika mwili umejengwa juu ya mkate.”703 Imepokewa kutoka kwa Abu Baswiir kuwa alisema: “Hakika Imam as-Sadiq alikuwa anachukia kuwekwa kipande cha mkate chini ya mfereji na alikataza hilo.”704 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa alisema: “Hakika watu wa kijiji miongoni mwa wale waliokuwa kabla yenu, Mwenyezi Mungu aliwapanulia riziki hadi walipopituka mipaka, wakasema baadhi yao kuwaambia wengine: “Mnaonaje kama tutakitegemea kitu hiki katika kujisafishia?” basi wakawa wanatumia kustanjia. Ulikuwa ni laini zaidi kuliko mawe. Na pindi walipofanya hivyo Mwenyezi Mungu akawatuma juu ya ardhi yao wadudu   Wasaail-Shi’ah, Juz. 16, uk. 505 kutoka kitabu Furuu Kaafi, Juz. 1, uk. 165.   Makarimul-Akhlaq, uk. 154. 702   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 279. 703   Makarimul-Akhlaq. uk. 154. 704   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 279. 700 701

157

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 157

8/10/2017 1:22:07 PM


TIBA YA MAASUMINA

wadogo mno kuliko nzige, hawakuacha chochote ila walikula, basi wakaendelea kula mpaka wakawapata wale waliokuwa wakitumia mkate kustanjia, nacho ni kijiji ambacho Mwenyezi Mungu amesema ndani ya Qur’ani: “Na akapiga mfano…”705 JANDO Mtume (s.a.w.w) amesema: “Mambo matano yanatokana na maumbile; jando, istihdaad, kunyofoa nywele za kwapa, ukataji wa kucha na upunguzaji wa masharubu.”706 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Jando ni sunna ya wanaume, ni utukufu kwa wanawake.”707 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Watieni jando watoto wenu siku ya saba, kwani hiyo ni tohara na inakuza haraka nyama.”708 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Watieni jando watoto wenu wala asiwazuie nyinyi aliyehuru wala asiyehuru, kwani hiyo ni tohara ya mwili. Na hakika ardhi inapiga ukelele kwa Mwenyezi Mungu kutokana na mkojo wa mwenye govi (asiyetiwa janjo).”709 UVAAJI WA PETE Hadithi: Imepokewa kutoka kwa Anas bin Malik amesema: Hakika Mtume (s.a.w.w) alikuwa akivaa pete mkono wake wa kulia.”710   Surat Nahli; aya 112.   Sahihi Bukhari, Juz. 7, uk. 137 Maktabat Nahdhat Hadiitha Makka tukufu mwaka 1376. 707   Makarimul-Akhlaq, uk. 238. 708   Sahifatul-Ridha (a.s), uk. 41. 709   Tuhfal-Uquul, uk. 88. 710   Rawdhatul-Waidhiina, uk. 309 cha ibn Fataal Naysabuuri. 705 706

158

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 158

8/10/2017 1:22:07 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Msivae pete isiyokuwa ya fedha, hakika Mtume (s.a.w.w) amesema: ‘Hakutoharisha Mwenyezi Mungu mkono ambao ndani yake kuna pete ya chuma’.”711 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Yule anayetia nakshi juu ya pete yake miongoni mwa majina ya Mwenyezi Mungu, basi augeuze mkono ambao anautumia kustanjia.”712

SALADI Faida zake: Saladi huvuta usingizi, inakinga kiu na inakata hamu ya kufanya tendo la ndoa, hivyo huliwa na wanaume wenye nguvu zaidi ya wanawake, na huliwa pia na wanawake ambao wanaume wao hawapo ili kukata hamu ya tendo la ndoa. Mbegu zake zikitafunwa, huzuia kujiotea na utokaji wa manii.713 Hakika saladi ni tajiri kwa aina mbalimbali ya vitamin, na ndani yake kuna kiwango kikubwa cha madini chumvi mfano wa chuma. Na mkemia (Nuyuman) amesema: Saladi imesheheni utajiri wa chuma, inaongeza chembechembe za damu nyekundu, inaongeza wekundu katika midomo, na hutuliza uchofu na inasaidia kwa usingizi. Saladi inachukua nafasi ya juu katika uvutaji wa hewa miongoni mwa mbogamboga, nayo ni tajiri kwa vitamin lukuki na chumvi, basi majani yake ni tajiri kwa vitamini A kama vile ilivyo na vitamini B na vitamini C.   Tuhfal-Uquul, uk. 73.   Tuhfal-Uquul, uk. 73. 713   Tuhful-Uquul, uk. 73. 711

712

159

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 159

8/10/2017 1:22:07 PM


TIBA YA MAASUMINA

Na inayo baadhi ya madini mfano wa kalisiam, elementi ya njano na chuma. Na saladi ni tajiri kwa viasilia vya sulfati ambavyo vinasaidia katika kupambana na uzuiaji wa haja wa muda mrefu. Vivyo hivyo hakika saladi inasaidia katika kuupa mwili rutuba na kulainisha haja ndogo, khususan kwa wale waliopatwa na jongo na vimawe katika kibofu cha mkojo. Na saladi inasaidia katika mishipa ya fahamu na inasaidia kuleta usingizi kutokana na kuwa na maada ya (Taraliyars 7) ambayo inamiliki vishawishi vya usingizi na vitulizo vya mishipa ya fahamu. Na saladi inatia nguvu uoni na mishipa kwa sababu ya utajiri wake wa vitamini A. HADITHI: Imepokewa kutoka kwa Nabii Musa (a.s) katika Telmuud, akasema mwalimu: “Figili inasaga chakula katika mfuko wa chakula, na saladi inabadilisha hayo, na tango linanyoosha tumbo.”714 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Kula saladi, kwani inasababisha usingizi na mmeng’enyo wa chakula.”715 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Ni juu yenu kutumia saladi, kwani hiyo inasafisha damu (katika hadithi nyingine) inazima damu.”716 Na imepokewa pia kutoka kwa Imam asSadiq (a.s) amesema: “Ni juu yako kutumia saladi, kwani inakata damu.”717 UPAKAJI WA HINA Mtume (s.a.w.w) amesema: “Badilisheni uzee (yaani pakeni nywele zenu kwa hina) wala msijifananishe na Mayahudi.”718 Vilevile im  Temuud Babali, uk. 45 tarjumat ya Nabiil Fayadh.   Makarimul-Akhlaq, uk. 183. 716   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 285. 717   Makarimul-Akhlaq, uk. 183. 718   Nahjul-Balaghah, Juz. 2, uk. 497. 714 715

160

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 160

8/10/2017 1:22:07 PM


TIBA YA MAASUMINA

epokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Dirham moja inayotumiwa katika upakaji wa hina ni bora zaidi kuliko utoaji wa dirham katika njia ya Mwenyezi Mungu, na ndani yake kuna mambo kumi; inafukuza harufu ya masikioni, inasafisha katika kifuniko cha jicho, na inalainisha pua na inafanya uzuri tendo la ndoa, na inakaza fizi, na inaondoa uchovu, na inapunguza wasiwasi wa shetani, na inafurahisha malaika, na inatoa bishara njema kwa muumini, na inamfanya ashindwe kafiri, nayo ni pambo na inaleta harufu nzuri, na inaleta haya kwa Munkari na Nakiir.”719 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Ni juu yenu kutumia hina, kwani inafanya ngozi kuwa nzuri na inaongeza nguvu katika kujamiiana.”720 KHATMI (AU KHATMIYYAT) Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Uoshaji wa kichwa kwa khatmi unaondoa taka na uchafu.”721 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Uoshaji wa kichwa kwa khatmi ni kinga ya maumivu ya kichwa, na ni uwekwaji mbali na ufukara, na ni tohara ya kichwa, na ni kuepukana na mapunye.” (Na katika hadithi): kunaundoa ufukara, kunaongeza riziki, nayo ni ushangamfu.”722 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Uoshaji wa kichwa kwa khatmi katika kila siku ya Ijumaa ni kinga ya ukoma na uwendawazimu.”

Khiswal, Juz. 2, uk. 497.   Sahifat Ridha (a.s), uk. 72. 721   Tuhful-Uquul, uk. 72. 722   Makarimul-Akhlaq. 719 720

161

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 161

8/10/2017 1:22:07 PM


TIBA YA MAASUMINA

SIKI Uandaaji wake: Siki ya pombe ni maji ya zabibu ambayo ndani yake kuna kiwango cha siki, na inawekwa juani hadi iwe siki. Faida zake: Siki ya zabibu inasaidia mfuko wa chakula wenye uvimbe mchungu, na inakomesha manjano, na inakinga madhara ya madawa yenye kuua, na inachuja maziwa na damu vikiganda tumboni. Na inasaidia bandama, na inalainisha mfuko wa chakula, na inafunga tumbo, na kukata kiu. Na inazuia uvimbe na inasaidia mmeng’enyo wa chakula, na inakabiliana na kikohozi, na inafanya wepesi chakula kizito na inafanya damu kuwa nyepesi. Na ikiwa itasukutuliwa ikiwa imechemshwa inasaidia maumivu ya meno, na inatia nguvu ufizi.723 Hadithi: Mtume (s.a.w.w) amesema: “Mchuzi bora ni mchuzi wa siki, ewe Mwenyezi Mungu tubariki katika siki, kwani ni mchuzi wa Manabii wa kabla yangu.”724 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Hakika Mwenyezi Mungu na malaika Wake wanaiteremshia neema meza ambayo juu yake kuna siki na chumvi.”725 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Siki ya pombe inakaza ufizi, na inaua vijidudu vya tumboni, na inakomaza   Twibbu Nabawiy, uk. 236 cha ibn Qaym Jawziyyat.   Makarimul-Akhlaq, uk. 190. 725   Biharul-Anwaar, Juz. 66, uk. 304. 723 724

162

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 162

8/10/2017 1:22:07 PM


TIBA YA MAASUMINA

akili.”726Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) vilevie kwamba amesema: “Siki inatuliza nyongo, inahuisha moyo, inaua vidudu vya tumboni na inakaza kinywa.”727 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Mchuzi bora ni siki, inakata kibofunyongo, inahuisha moyo, inakaza ufizi na inaua vidudu vya tumboni.”728 Imepokewa kutoka kwa Imam asSadiq (a.s) amesema: “Upakaji wa siki unaondosha (katika hadithi nyingine: Unakata) hamu ya zinaa.”729 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Siki na mafuta ni miongoni mwa vyakula vya Mitume.”730 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Alikuwa Amirul-Muuminina Ali (a.s) akifanana mno na Mtume (s.a.w.w) katika chakula chake, alikuwa akila mkate na siki na mafuta, na akiwalisha watu mkate na nyama.”731 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Mtume (s.a.w.w) aliingia kwa Ummi Salama, basi akamkaribisha yeye kipande cha mkate. Akamuuliza: Je, unao mchuzi? Akajibu: Hapana, Ewe Mtume(s.a.w.w) sina chochote ila siki, basi akasema: Mchuzi bora ni siki, na wala haiwi fukura nyumba ambayo ndani yake kuna siki.”732 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Siki inakaza akili.”733 Imepokewa pia kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s)   Wasail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 69.   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 275. 728   Biharul-Anwaar, Juz. 66, uk. 304. 729   Biharul-Anwaar, Juz. 66, uk. 304. 730   Biharul-Anwaar, Juz. 66, uk. 304. 731   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 64 kutoka kitabu Furuu, Juz. 6, uk. 328 na kitabu Mahasin, uk. 483 cha Barqi. 732   Wasaail-Shi’ah, Juz.. 17, uk. 66. 733   Wasail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 65. 726 727

163

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 163

8/10/2017 1:22:07 PM


TIBA YA MAASUMINA

amesema: “Hakika sisi tunaanza kwa siki, kama vile nyinyi mnavyoanza kwa chumvi, hakika siki inaimarisha akili.”734 Imepokewa pia kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kwamba ilitajwa mbele yake siki ya pombe, akasema: “Inaua vidudu vya tumboni na inakaza kinywa.”735 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Hakika siki inakaza ubongo na inaongeza katika akili.”736 Imepokewa vilevile kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Mchuzi bora ni siki, na kamwe hawatokuwa mafukara watu wa nyumba ambamo kuna siki.”737 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Kuleni siki ya pombe iliyoharibika yenyewe, wala msile ile mliyoiharibu nyinyi.”738

SIKI YA TUFAHA Utatengenezaje siki ya tufaha: Linaoshwa tufaha vizuri, na unaondoa viungo vilivyochoka. Linakamuliwa tufaha au linasagwa kwa mashine ya kusaga (blenda) lote pamoja na moyo na maganda yake. Inaongezwa katika juisi hiyo maji ya uvuguvugu baada ya kuchemka kwake, kiasi cha lita moja ya maji kwa kila kilogram moja inayotokana na juisi ya tufaha. Kisha inaongezwa gram mia moja ya sukari, na gram 10 ya unga wa mkate, na hivyo ni ili kuharakisha katika kazi ya utengezaji wa pombe, unakihifadhi chombo kilicho wazi katika joto la daraja 20 – 30) na kukiweka mbali na mionzi ya jua na mwanga, kwani hiyo   Wasaail-Shi’ah, juz. 16 uk. 522, kutoka kitabu Mahasin cha Barqi.   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 67. 736   Wasaail-Shi’ah, Juz. 16, uk. 523. 737   Sahifat Ridha (a.s), uk. 50. 738   Sahifat Ridha (a.s), uk. 74. 734 735

164

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 164

8/10/2017 1:22:07 PM


TIBA YA MAASUMINA

husimamisha kazi ya utengezaji wa pombe, wala hakuna tatizo kuuweka mchanganiko huo kwenye chombo cha kioo. Hatua ya kwanza: Unaachwa mchanganyiko ili kutengeneza pombe kwa muda wa siku 10 (kuwa pombe ya Alkoholi). Na hivyo kwa kuihifadhi hiyo sehemu yenye ujoto. Na unakorogwa mchanganyiko huo kwa kijiko cha ubao mara tatu kila siku, kisha unamiminwa katika chujio lenye nyuzi nyepesi na unakamuliwa (ili kuisafisha) kisha unawekwa ndani ya chombo chenye uwazi mpana. Hatua ya pili: Unafunikwa mdomo wa chombo kwa mfuko wa nyuzi na kukazwa vizuri na kuhifadhiwa mahali pa ujotojoto ili kukamilisha kazi ya utengezaji wa pombe. Muda wa uandaaji wa siki ya tufaha ni kuanzia (siku 40 hadi 60) kulingana na joto. Kisha unasafishwa mchanganyiko na unawekwa ndani ya chupa za kioo zilizofungwa vizuri (ili kuondoa mgandamizo) na unahifadhiwa katika mahali pa baridi wakati wa matumizi yake.739 TABIA Mtume (s.a.w.w) amesema: “Tabia mbaya inaharibu amali, kama vile siki inavyoharibu asali.”740Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kwamba alisema kumwambia Ali (a.s): “Kula mung’unya, kwani anayekula hilo inakuwa nzuri tabia yake, na linang’arisha uso wake, nacho ni chakula changu na chakula cha Manabii wa kabla yangu.”741 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Ni juu yenu kula mafuta, kwani yanafichua kibofunyongo.. na yanafanya tabia kuwa nzuri, yanapendezesha kinywa na yanaondoa kikohozi.”742   Twibbul-Sha’abi kwa ufupi.   Sahifat Ridha (a.s), Uk. 65. 741   Biharul-Anwaar, Juz. 17, uk. 25. 742   Makarimul-Akhlaq, Uk. 190. 739 740

165

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 165

8/10/2017 1:22:07 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Husein bin Khalid amesema: Nilimwambia Abu Hasan Imam Kadhim (a.s) hakika watu wanasema: Asiyekula nyama siku tatu tabia yake inakuwa mbaya, ni kweli? Akasema: “Wamedanganya, lakini yule anayekula nyama kwa siku 40 inabadilika tabia yake na mwili wake, vivyo hivyo katika uhamaji wa tone la maji ya uzazi kwa idadi ya siku 40.”743 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Ni juu yenu kula nyama, kwani inaotesha nyama, na yule anayeacha kula nyama kwa muda wa siku 40 inakuwa mbaya tabia yake.”744 POMBE (VILEVI AU URAHIBU) Yule aliyeiharamishia nafsi yake pombe katika zama za ujinga: Imeelezwa kuwa hakika Abdullah bin Judh-a’ni Taymi alikuwa ni miongoni mwa wale ambao waliojiharamishia pombe katika zama za ujinga baada ya kuwa mwenye mapenzi nayo. Siku moja alilewa usiku, akawa ananyoosha mkono wake ili kuukamata mwanga wa mwezi ili auchukue, basi wakacheka wale waliokaa naye, na akapewa habari juu ya hilo pindi hali yake iliporudi na kuwa ya kawaida, basi hapo akaapa kuwa hatokunywa tena abadani.745 Hadithi: Aliulizwa bedui: Una nini wewe hunywi pombe? Akasema: Kwa ajili ya mambo matatu iliyonayo; inapoteza mali, inaondoa akili na inaondoa murua. Qusway bin Kilabu aliwausia wanawe kwa kusema: “Enyi wanangu! Ole wenu na unywaji wa pombe, kwani ukiwa unafaa kwa miili basi unaharibu ubongo.”746   Wasaail-Shi’ah, Juz.. 17, Uk. 25.   Sahifatul-Ridha (a.s), Uk. 74. 745   Kunay wal-Alqaab, Juz. 1, Uk. 238 cha Sheikh Abbas Qummi. 746   Aamaal, Uk. 13 cha Saduuq ni machapisho ya taasisi ya Aalamiy. 743 744

166

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 166

8/10/2017 1:22:07 PM


TIBA YA MAASUMINA

Mtume (s.a.w.w) amesema: “Yule anayekunywa pombe haikubaliwi swala yake kwa muda wa siku 40.” (Kwani athari ya pombe inabakia tumboni mwa mja na mishipani mwake na viungoni mwake kwa siku 40).747 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuwa amesema: “Hakika Ibilisi aliwazungumzisha mashetani wenzake: Ni juu yenu kula nyama, ulevi na wanawake, hakika mimi sikuti mkusanyiko wa shari ila katika hayo.”748 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kwamba amesema: “Pombe ni kusanyiko la kila dhambi, na mama wa kila uchafu na ufunguo wa kila shari.”749 Miongoni mwa wosia wa Mtume (s.a.w.w) kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Mnywaji pombe ni kama vile mwabudu masanamu, ewe Ali, Mwenyezi Mungu hazikubali swala za mnywaji pombe kwa muda wa siku 40, na iwapo atakufa katika siku 40 hizo basi atakufa hali ya kuwa ni kafiri. Ewe Ali! Yamefanywa madhambi yote katika nyumba, na umefanywa ufunguo wake ni unywaji pombe. Ewe Ali! Utafika muda mnywaji pombe hamjui ndani yake Mola Wake mlezi (a.j). Ewe Ali! Kila kilevi (uraibu) ni haramu, na kunywa zaidi yake basi ni ujasiri kwayo ni haramu.”750 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Mwenyezi Mungu ameilaani pombe, mkamuaji wake, muoteshaji wake, mnywaji wake, mnyweshaji wake muuzaji wake mnunuzi wake, mlaji wa thamani yake, mbebaji wake na kilichobebewa kwacho.”751   Twibbu Nabawi, Uk. 24 cha Ibn Qaym Jawziyyat.   Biharul-Anwaar, Juz. 62, Uk. 293. 749   Biharul-Anwaar, Juz. 79, Uk. 149. 750   Makarimul-Akhlaq, uk. 433 na 434. 751   Biharul-Anwaar, Juz. 79, uk. 126. 747 748

167

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 167

8/10/2017 1:22:07 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Haikusanyiki pombe na imani tumboni au moyo wa mtu abadani.”752 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuhusiana na nyama amesema: “Hakika nyama inayo ada kama vile ada ya pombe.”753 Imepokewa kutoka kwa Imam al-Baqir (a.s) kuhusiana na sababu ya uharamisho wa pombe amesema: “Na ama pombe hakika ni haramu kwa ajili ya kitendo chake na uovu wake.” Kisha akasema: “Hakika mnywaji mno wa pombe ni kama vile mwabudu masanamu, inasababisha utetemekaji wa mwili, inaharibu murua wake, inamchukua yeye juu ya ujasiri wa kufanya haramu, umwagaji wa damu, na kufanya zinaa, mpaka asiamini anapolewa kufanya (kuchupia) haramu, naye haitikii akili, na pombe haimuongezei mnywaji wake ila kila shari.”754 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Mwenye kudharurika asinywe pombe, kwani hiyo haimuongezei yeye ila shari, na hakika hiyo anayeinywa humuua, wala asinywe hata tone moja.”755 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Bia ni haramu, na sisi Ahlul-Bayt hatunywi haramu.”756 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Hakumtuma Mwenyezi Mungu Nabii yeyote katu ila alimfundisha kwamba ikiwa dini yake itakamilika itakuwa katika uharamisho wa pombe, na bado inaendelea pombe kuwa haramu. Hakika dini inabadilika kutoka jambo moja mpaka lingine, na lau ingeliruhusiwa hiyo basi kwa ujumla watu wangelishika hiyo na kuacha dini.”757   Biharul-Anwaar, Juz. 79, uk. 152.   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 32. 754   Aamaal, uk. 529 cha Suduq, Chapa ya tano. 755   Ilalu-Sharaai, Juz. 2, uk. 164. 756   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 62. 757   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 237. 752 753

168

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 168

8/10/2017 1:22:07 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Saif bin Umairat, kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Tulikuwa mbele yake basi mzee mmoja akasema: ‘Hakika mimi nina maumivu, na mimi ninakunywa bia.’ Akasema (a.s): “Ni kitu gani kinachokuzuia kunywa maji ambayo Mwenyezi Mungu amefanya kila kitu kuwa hai kwayo?” Akasema: Hayaafikiani nami. Akasema (as): “Ni kipi kinakuzuia wewe kutumia asali? Hakika Mwenyezi Mungu anasema: ‘Ndani yake ipo ponyo kwa watu’”? Akasema: Siipati. Akasema (as): “Ni kipi kinakuzuia wewe kunywa maziwa ambayo yameotesha nyama yako na kuimarisha mifupa yako?” Akasema: Hayaafikiani nami. Akasema Imam as-Sadiq (a.s): “Je, unataka nikuamrishe kunywa pombe? Hapana naapa kwa Mwenyezi Mungu siwezi kukutaka uniamrisha hilo.”758 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema kumwambia Maamuni: “Miongoni mwa dini ya Ahlul-Bayt (a.s) ni mwenye kudharurika asinywe pombe kwani inaua.”759 Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) amesema: “Hakika Mwenyezi Mungu (a.j) hakuharamisha pombe kwa jina lake bali ameiharamisha kwa matokeo yake, na kile chenye matokeo sawa na pombe basi hicho ni pombe.”760 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Wala msikae juu ya meza ambayo inanywewa juu yake pombe, hakika mja hajui muda gani itatolewa roho yake.”761 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Yule anayekunywa pombe hali ya kuwa yeye anajua ni haramu basi Mwenyezi Mungu atamnywesha yeye udongo wa ro  Tafsirul-Ayaashi, Juz. 2, uk. 264.   Mahasin, Juz. 2, uk. 126. 760   Wasail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 273. 761   Tuhful-Uquul, uk. 78. 758 759

169

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 169

8/10/2017 1:22:07 PM


TIBA YA MAASUMINA

jorojo ya watu wa motoni, na hata kama atakuwa ni mwenye kusamehewa.”762 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Mnywaji mno wa pombe wakati atakapokutana na Mwenyezi Mungu (a.j) atakutana Naye kama vile mwabudu masanamu.” Akasema Hujru bin Uday: ‘Ewe Amirul-Muuminina ni nani mdumishaji wa pombe?’ Akasema (a.s): “Ni yule ambaye akiipata basi huinywa.’”763 NGURUWE NA NYAMA YAKE Imam al-Baqir (a.s) kuhusiana na sababu ya uharamisho wa ulaji wa nyama ya nguruwe amesema: “Na ama nyama ya nguruwe, hakika Mwenyezi Mungu (a.j) aliwafanya watu kuwa wanyama katika sura mbalimbali, mfano wa nguruwe, ngedere na dubu, kisha akakataza kula mfano wa nyama zao ili wasinufaike nao wala kupunguziwa adhabu zao…”764 KHULUNJANI ALPINIA OFFICINARUM Faida zake: Sayyid Abdullah Abu Shahri ameitaja khulunjani na baadhi ya mambo yake mahsusi, akasema: Ikiwa itachukuliwa hiyo dirham moja na ikasagwa na kuchujwa, ikachanganywa na kiasi kidogo cha nusu lita ya maziwa ya ng’ombe, na akanywa kabla ya kula chochote, ni kiboko (mwisho) katika masuala ya unyumba. Na hili ni mujarabu kama walivyonukuu hilo baadhi ya waganga.765   Tuhful-Uquul, uk. 78.   Tuhful-Uquul, uk. 86. 764   Aamaal, uk. 529 cha saduuq chapa ya tano. 765   Tuhfatul-Ridhawiyyat fi Mujarrabaat Imamiyyat, uk. 75 kutoka kitabu Sahabu Alaaiy. 762 763

170

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 170

8/10/2017 1:22:07 PM


TIBA YA MAASUMINA

Na khulunjani inasaidia kwa mwenye uvimbe katika kibofu cha mkojo na inapunguza mgandamizo na mkanganyiko na kutotulia kinafsi. KHAYRIYYU (NA MAFUTA YAKE) GILLYFLOWER Ibn Baytwar amesema: Khayriyyu ni mmea maarufu, una maua mbalimbali: Baadhi yake meupe, na mengine ya manjano. Na ya manjano yana manufaa zaidi katika kazi za tiba. Galenos amesema: Uzuri wa mmea huu ni kwamba una nguvu ya usafishaji, nao ni mzuri wa majimaji, na nguvu nyingi inayopatikana ni kutokana na majani yake. Faida zake: Ibn Baytwar kuhusiana na mufuta ya khayriyyu gillyflower amesema: Tamimi amesema: Ni mazuri mepesi, ni rafiki na yanaafikiana na majeraha, na hususan yale yanayotokana na maua ya njano, nayo ni mazuri sana kwa kuondoa uvimbe sehemu ya uzazi, na uvimbe uliopo katika maunganiko, na uvimbe na mafundo yanayojitokeza katika mishipa ya fahamu. Na kazi yake katika kutibu matatizo hayo ni nzuri zaidi kushinda mafuta yote yenye kutokana na maua mengine. Na hakika hutia nguvu nywele za kichwa na huzifanya kuwa nyingi, na mafuta haya ni sehemu ya dawa zinazotegemewa kwa ajili ya vidonda.766 Hadithi: Miongoni mwa yale yaliyopokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) imesemwa: Yalitajwa mafuta ya balungi basi akayatakasa, kisha akasema: “Na hakika mafuta ya khayriyyu gillyflower ni mazuri.”767   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 226.   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 223, kutoka kitabu Kaafi.

766 767

171

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 171

8/10/2017 1:22:07 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Hasan bin Juham amesema: Nilimuona Abu Hasan Imam Kadhim (a.s) akijipaka mafuta ya khayriyyu gillyflower basi akaniambia mimi: “Jipake.” Nikasema: Upo wapi wewe na mafuta ya ua la urujuani (Banafsanji Wild Viola), na hakika yamepokewa maelezo mengi kulihusu kutoka kwa Abu Abdillah as-Sadiq (a.s). Akasema: “Ninachukia harufu yake.” Nikamwambia: Na hakika hata mimi ninachukia harufu yake, na nilikuwa naogopa kukwambia wewe hilo kutokana na maelezo yaliyopokewa kutoka kwa Abu Abdillah (a.s). Basi akasema: “Hakuna tatizo.” *Na makusudio ya: Hakuna tatizo, ni kwamba hakika ubaya wa harufu yake hausigani na fadhila na manufaa ya ua hilo.768 UGONJWA NA DAWA (PONYO) Qur’ani tukufu imekariri chanzo cha matibabu kwa kutizama pande zake mbili: Upande wa Ndani (unywaji wa dawa), na Upande wa Nje (mafuta na asali). Na hilo linadhihiri kutokana na kauli yake (s.w.t) kwa Nabii Ayub (a.s) pindi alipopatwa na majaribu ya maradhi ya ngozi, akasema kumwambia yeye: “Sugua kwa miguu yako… na kinywaji”769 yaani sugua ardhi kwa miguu yako, na itabubujika kwako chemchem ya kwanza, basi osha kwa chemchem hiyo. Kisha itabubujika kwako chemchem nyingine, basi kunywa kwayo, utapona kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Hizi chemchem mbili ndani yake kuna mawadi (viasili) ya tiba kutokana na aina mbili zenye kutofautiana: Ya kwanza inaponya maradhi ya ngozi ya nje kama vile marhamu, na ya pili ndani yake ina antibayotiki, basi unywaji wake kwa mgonjwa unaponya maradhi yaliyopo ndani ya mwili. Na aya   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 223, kutoka kitabu Kaafi, Juz. 6, uk. 522.   Surat Swaad, aya 42.

768 769

172

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 172

8/10/2017 1:22:08 PM


TIBA YA MAASUMINA

imekusanya aina mbili zenye kukamilika kwa matibabu, basi Nabii Ayub (a.s) akapona kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu. Dawa ambayo haina ugonjwa ndani yake: Imesemwa: Walikusanyika kwa mfalme Kisra wenye hekima wanne; Mwirak, Mroma, Mhindi na Mweusi. Kisra akawaambia: Kila mmoja miongoni mwenu anielezee dawa ambayo haina ugonjwa ndani yake! Basi Mwirak akasema: “Dawa ambayo haina ugonjwa ndani yake ni kunywa kila siku mikupuo mitatu ya maji moto kabla ya kula kitu.” Na Mrumi akasema: “Dawa ambayo haina ugonjwa ndani yake ni kumeza kila siku punje kidogo za habasoda.” – Na Mhindi akasema: “Dawa ambayo haina ugonjwa ndani yake ni kula kila siku punje za Haliylij nyeusi Tropical Almond.” – Na mtu mweusi akanyamaza, na alikuwa ni mtaalamu zaidi yao. Basi Mfalme Kisra akamwambia: Kwa nini wewe huzungumzi? Akasema: “Ewe maulana wetu, maji moto yanayeyusha mafuta ya ini na yanalegeza mfuko wa chakula, na punje za habasoda zinachochea manjano, na haliylij nyeusi inachochea weusi. Akasema: Na kipi unakisema wewe? Akasema: Ewe maulana wetu, dawa ambayo haina ugonjwa ndani yake ni usile ila unapokuwa na njaa, na unapokula inua mkono wako kabla hujashiba, kwani wewe hautaugua ila ugonjwa wa kifo.” *Na hilo linakaribiana zaidi na kauli ya Imam Ali (a.s) pale alipomwambia mwanawe Hasan: “Ewe mwanangu, je, nikujuze mambo manne yatakayokutosha ambayo yatakufanya usihitajie tiba? Akasema Hasan (a.s): Ndio, akasema: Usikae ili kula hali ya kuwa wewe umeshiba, acha kula hali ya kuwa wewe una hamu nacho, na 173

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 173

8/10/2017 1:22:08 PM


TIBA YA MAASUMINA

kabla ya kulala nenda msalani. Ikiwa utafanya hivyo basi hautohitajia tiba!770 Hadithi: Mtume (s.a.w.w) amesema: “Mwenyezi Mungu hakuteremsha ugonjwa ila aliteremsha dawa yake, akamfundisha yule aliyemfundisha na hakuijua yule asiyeijua.”771 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Msichukie manne kwani hayo yana manne, msichukie mafua kwani ni amani ya mbalagha, na msichukie majipu kwani hayo ni amani ya ukoma, wala msichukie ugonjwa wa macho kwani huo ni amani ya upofu, wala msichukie kukohoa kwani hali hiyo ni amani ya kiharusi.”772 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kwamba amesema: “Ugonjwa ambao Mwenyezi Mungu ameuteremsha basi ameteremsha ponyo lake.”773 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Yule mwenye kuitegemea rai yake hajitibu, basi dawa itasababisha ugonjwa.”774 Imepokewa kutoka kwa Abu Dardaa amesema: Mtume (s.a.w.w) amesema: “Hakika Mwenyezi Mungu ameteremsha ugonjwa na dawa yake, na akafanya kila ugonjwa na dawa yake, basi jitibieni wala msijitibie kwa haramu.”775 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Magonjwa yapo matatu na dawa zipo za aina tatu, basi ugonjwa ni wa kibofunyongo, kikohozi na damu, na dawa ya damu ni ufyonzaji wa damu mwilini, na dawa ya kobofunyongo ni utembeaji na dawa ya kikohozi ni bafu.”776   Shajaratu Tuuba, Juz. 2, uk. 368 cha Mazandaraani, kutoka kitabu Khiswal cha Saduuq.   Iqdul-Fariid, Juz. 7, uk. 264. 772   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 184, kutoka kitabu Khiswal, Juz. 2, uk. 99 cha Saduuq. 773   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 29. 774   Al-Iqdul-Fariid, Juz. 7, uk. 263. 775   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 76. 776   Makarimul-Akhlaq, uk. 76. 770 771

174

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 174

8/10/2017 1:22:08 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Hakika yule ambaye ameumba dawa na akajaalia ugonjwa wake, na hakika dawa nzuri zaidi ni ufyonzaji wa damu mwilini, utoaji wa damu, na punje nyeusi.” 777 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Hakuteremsha Mwenyezi Mungu ugonjwa ila aliteremsha dawa yake.”778 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Hakuteremsha Mwenyezi Mungu ugonjwa ila aliteremsha ponyo lake.”779 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Hakuumba Mwenyezi Mungu ugonjwa ila aliumba dawa yake, isipokuwa sumu (kifo).”780 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Jitibieni; Mwenyezi Mungu hakuteremsha ugonjwa ila aliteremsha dawa, isipokuwa sumu (yaani kifo), kwani haina dawa.”781 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Jiepusheni na dawa ambayo inategemewa mwili wako kuwa na ugonjwa, ikiwa ugonjwa hautodhaniwa basi ni dawa.”782 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Jiepusheni na dawa ambayo haitokufanya kuwa na afya, na ukihisi baraka basi iunguze na itupilie mbali kabla ya kuitumia.”783 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Mtakapoingia kwenye mji na mkahofia ugonjwa wake basi ni juu yenu kula vitunguu vyake…”784   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 73.   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 70, kutoka kitabu Dhaw-u l-Shahaab wa Da’awaat cha Rawandiy. 779   Biharul-Anwaar, Juz. 59, uk. 68. 780   Twibbu Nabiy (s.a.w.w), uk. 19. 781   Biharul-Anwaar, Juz. 59, uk. 65, kutoka kitabu Saraair cha ibn Idriis. 782   Makarimul-Akhlaq, uk. 418. 783   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 269. 784   Ramzul-Sihat, uk. 144, kutoka kitabu Firdausi. 777 778

175

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 175

8/10/2017 1:22:08 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Hakika habasoda ni ponyo ya kila ugonjwa ila sumu (kifo).”785 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kwamba ilitajwa mbele yake nyama na mafuta basi akasema: “Hakuna kipande cha hivyo viwili kitakachoingia ndani ya mfuko wa chakula, ila kitaotesha mahala pake ponyo, na kuondoa ugonjwa.”786 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Yule ambaye Alhamdu haitomponyesha basi Mwenyezi Mungu hatomponya.”787 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Huenda dawa ikawa ni ugonjwa, na ugonjwa ukawa ni dawa.”788 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Unywaji wa dawa kwa ajili ya mwili ni kama vile sabuni kwa ajili ya nguo, na inaisafisha lakini inaidhoofisha.”789 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Nyama ya ng’ombe ni ugonjwa, na maziwa yake ni dawa, na samli yake ni ponyo.”790 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Mwislamu hajitibu mpaka maradhi yake yashinde afya yake.”791 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Tembea na ugonjwa wako kama vile ulivyotembea kwako.”792Imepokewa vilevile kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Mwisho wa dawa ni kutapisha.”793   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 68.   Sahifat Ridha (a.s), uk. 68. 787   Biharul-Anwaar, Juz. 59, uk. 75. 788   Nahjul-Balaghah, kitabu: 31. 789   Mwisho wa Sharhu Nahjul-Balaghah hekima: 422 cha ibn Abu Hadidi. 790   Mustadrakul-Nahju, uk. 162, na Makarimul-Akhlaq uk. 159. 791   Khiswal, uk. 161 cha Saduuq. 792   Nahjul-Balaghah, hekima: 26.H 793   Nahjul-Balaaghah, Hutba 166. 785 786

176

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 176

8/10/2017 1:22:08 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Salio la maji ya muumini ni ponyo” (salio la maji: Ni yale yaliyobakia kwenye chombo baada ya kunywa).794 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Hakuna ugonjwa ila huo unatoka ndani ya tumbo lake mtu isipokuwa jeraha na homa.”795Vilevile imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) katika mazungumzo yake pamoja na Habbabat Waalibiya, hakika alitaka kumlisha kaka yake nyama ya samaki mweusi (kambare) basi akasema: “Ewe Habbabat, hakika Mwenyezi Mungu hakujaalia ponyo kwa yale ambayo yameharamishwa…”796 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Asali ni ponyo la kila ugonjwa wala hakuna ugonjwa ndani yake, inapunguza kukohoa, na inasafisha moyo.”797 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Yule anayefikia umri wa miaka 40 atapatwa na maumivu bila ya ugonjwa.”798 Imepokewa pia kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Tikitimaji ni mafuta ya ardhi, hayana ugonjwa ndani yake wala madhara.”799 Imepokewa kutoka kwa Imam Zaynul-Abidiina (a.s) amesema: “Afya ni mfalme aliyejificha.”800 Imepokewa kutoka kwa mmoja wa masahaba wetu kwamba alisema: mwanamke mmoja alinikabidhi ghazali, akasema: “Mswage mpaka Makka ili akashone nguo ya Kaaba.” Basi nikachukia kumswaga hadi kwa Hujibat kwani watu hao nilikuwa nawafahamu vizuri. Nilipofika Madina niliingia kwa Abu Ja’far al-Baqir (a.s) na   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 208, kutoka kitabu Khiswal 400.   Khiswal, uk. 161 cha Saduuq. 796   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 86. 797   Makarimul-Akhlaq, uk. 166. 798   Mustadrakul-Nahju, uk. 188. 799   Makarimul-Akhlaq, uk. 185. 800   Sahifat Ridha (a.s), uk. 86. 794 795

177

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 177

8/10/2017 1:22:08 PM


TIBA YA MAASUMINA

nikamwelezea yeye hilo basi akasema: “Nunua kwayo asali na Zafarani, na chukua udongo wa kaburi la Husein (a.s) na uchanganye hayo kwa maji ya mvua na ingiza ndani yake kitu kutokana na asali na zafarani, na gawa kwa wafuasi, ili wajitibu kwavyo wagonjwa wao.”801 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kwamba alimwambia Bashir Nabil, akasema: “Ni kitu gani mnawatibia wagonjwa wenu?” akasema: Kwa dawa hizi chungu. Akasema: “Hapana, akiumwa mmoja wenu basi chukua sukari nyeupe na isage, kisha mimina juu yake maji ya baridi na kisha umnyweshe, hakika ambaye amejaalia ponyo katika uchungu ameweka pia katika utamu.”802 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Hakika Nabii mmoja aliugua, basi akasema: Hapana, sijitibu mpaka awe yule ambaye aliyenipa ugonjwa ndiye ambaye ataniponya, basi Mwenyezi Mungu aliyetukuka akamfunulia yeye: ‘Sikuponyi wewe hadi ujitibu, hakika ponyo ni kutoka Kwangu Mimi (na dawa kutoka kwangu).’ Basi akawa anajitibu na ndipo akapelekewa ponyo.”803 Katika hadithi ya Imam as-Sadiq (a.s) kutokana na yule aliyemuuliza kuhusu kutumia ulevi kwa ajili ya bawasiri, alisema: “Hakika Mwenyezi Mungu (a.j) hakujaalia dawa katika kitu chochote katika yale aliyoyaharamisha, si dawa wala si ponyo.”804 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuhusiana na dawa yenye kuchanganywa na pombe? akasema: “Sipendi kuiangalia wala   Wasaail-Shi’ah, Juz.. 17, uk. 75, kutoka kitabu Mahasin cha Barqi.   Mahasin, uk. 501. 803   Makarimul-Akhlaq, uk. 362. 804   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 362. 801 802

178

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 178

8/10/2017 1:22:08 PM


TIBA YA MAASUMINA

siwezi kuinusa, basi vipi nitajitibia kwayo?!”805 Katika hadithi ya Imam as-Sadiq (a.s) aliulizwa kuhusiana na mtu anayetibiwa na Yahudi na Mnaswara, akasema: “Hakuna tabu hakika ponyo iko mbele ya Mwenyezi Mungu.”806 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuwa aliulizwa kuhusiana na mwanamke anayepatwa na magonjwa mwilini kwake, je, inafaa kutibiwa na mwanaume? Akasema: “Ikiwa atadharurika kwa hilo hakuna tatizo.”807 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Udhihirishaji wa jambo kabla halijatimia, ni wenye kuharibu jambo.”808 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s): Muhammad bin Khalid Amir wa Madina alimlalamikia yeye maumivu anayoyapata tumboni mwake, basi akasema: “Amenihadithia mimi baba yangu kutoka kwa babu yake kutoka kwa Ali (a.s) kwamba mtu mmoja alimlalamikia Mtume (s.a.w.w) maumivu anayoyapata tumboni mwake, akasema: Chukua kinywaji cha asali na ingiza ndani yake punje tatu za habasoda au tano au saba, na kunywa hiyo utapona kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Basi yule mtu akafanya hivyo akapona. Basi chukua wewe hilo.”809 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Yule anayepatwa na udhaifu katika moyo wake au mwili wake, basi ale nyama ya mbuzi kwa maziwa, kwani hiyo inaondoa kwa asili yake kila ugonjwa na madhara, inatia nguvu mwili wake na inakaza mgongo wake.”810   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 90, kutoka kitabu Kaafi, Juz. 6, uk. 414.   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 74. 807   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 74. 808   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 97 cha Shubbar. 809   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 72, kutoka kitabu Da’aimul-Islam. 810   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 64.

805

806

179

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 179

8/10/2017 1:22:08 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Yule ambaye imedhihirika afya yake (yaani imekuwa ya juu zaidi) juu ya ugonjwa wake, basi akaitibu nafsi yake na akafa, kwa hakika atakuwa ameisaidia nafsi yake katika kuiangamiza.”811 (Na katika hadithi nyingine): “Basi mimi mbele ya Mwenyezi Mungu nipo mbali naye.”812 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Mwenyezi Mungu ameteremsha ugonjwa na akateremsha ponyo lake, na wala Mwenyezi Mungu hajaumba ugonjwa ila alijaalia dawa yake, basi kunywa na taja jina la Mwenyezi Mungu aliyetukuka.”813 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Jiepushe na dawa ikiwa unategemea mwili wako kupatwa na ugonjwa.”814 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Lau watu wangelijua yaliyomo ndani ya tufaha, wasingeliwatibu wagonjwa wao ila kwalo.”815 Imepokewa pia kutoka kwa Imam asSadiq (a.s) amesema: “Hakika Tini inaondosha hurufu ya kinywa, na inakaza mifupa, na inaotesha nywele, na inaondoa ugonjwa wala haihitaji dawa yoyote.”816 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Kila kitu kitokacho ardhini kina ugonjwa na ponyo, ila mchele kwani una ponyo na hauna ndani yake ugonjwa.”817 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Maharagwe yanaondoa ugonjwa na hayana ugonjwa ndani yake.”818   Twibbul-Aimmat, (a.s), uk. 61.   Khiswal, Juz. 1, uk. 26 cha Saduq. 813   Twibbul-Aimmat, (a.s), uk. 63. 814   Fusuulul-Muhimmat cha Hurru Aamili. 815   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 93. 816   Wasaail-Shi’ah, Juz.. 17, uk. 133, kutoka kitabu Furuu na Mahasin. 817   Biharul-Anwaar, Juz. 66, uk. 261. 818   Makarimul-Akhlaq, uk. 183. 811

812

180

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 180

8/10/2017 1:22:08 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Tende zenu bora ni za Barni zinaondoa ugonjwa na hazina ugonjwa ndani yake….”819 Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) katika nasaha zake kuhusu upunguzaji wa ulaji dawa amesema: “Hakuna dawa ila inachochea ugonjwa, na hakuna chochote mwilini chenye manufaa zaidi kuliko kuuzuia mkono (yaani upunguzaji wa kula chakula) ila kwa kadiri ya anachokihitajia.”820 Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) amesema: “Zuieni matibabu ya waganga wenu kadiri mnavyoweza, kwani ni kama ujengaji, uchache huzaa wingi.”821 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Yule anayechukua sukari mbili (vipande viwiwli vya sukari ya mawe) wakati wa kulala, itakuwa ni ponyo ya kila ugonjwa ila sumu (kifo).”822 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Ndani ya asali kuna ponyo la kila ugonjwa….”823 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Hakika tunda lililoiva lina ponyo ndani yake kwa kauli yake (s.w.t): “Kuleni kutokana na tunda lake linapoiva.824”825 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Ikiwa ndani ya kitu kuna ponyo, basi ni sharti kuwe na ufyonzaji wa damu mwilini au unywaji wa asali.”826   Mahasin, uk. 533 cha Barqi.   Rawdhatul-Kaafi, uk. 273. 821   Ramzul-Sihat, uk. 23 cha Dahsurkhi, kutoka kitabu Twibbul-Aimmat. 822   Ramzul-Sihat, uk. 210. 823   Fiqhul-Ridha (a.s), uk. 346. 824   Surat An-aam, aya 141. 825   Fiqhul-Ridha (a.s), uk. 347. 826   Sahifatul-Ridha (a.s), uk. 53. 819 820

181

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 181

8/10/2017 1:22:08 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Hakika Mwenyezi Mungu (a.j) amejaalia baraka katika asali, na ndani yake kuna ponyo la maumivu, na hakika imebarikiwa na Manabii sabini.”827 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) alimwambia mmoja wa masahaba wake: “Basi ni juu yako kutumia mchadi, kwani huo unaota juu ya ufukwe wa mto wa Firdausi, na ndani yake kuna ponyo ya magonjwa, nao unafanya mifupa kuwa mikubwa, na unaotesha nyama.”828 Imepokewa pia kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Walisheni wagonjwa wenu mchadi, (yaani majani yake) hakika ndani yake kuna ponyo, wala hauna maradhi wala madhara …”829 Imepokewa kutoka kwa Kaamil amesema: Nilimsikia Musa bin Abdillah bin Hasan anasema: Niliwasikia wazee wetu wakisema: Ubani Liqaah (yaani ngamia) ni ponyo la kila ugonjwa na vijidudu mwilini.”830Na imepokewa kutoka kwa baadhi ya Ahlulbayt (a.s) kwamba Nabii (s.a.w.w) hakika alikuwa yeye unapompata ugonjwa, anakusanya baina ya maji ya Zamzam na asali, na kuomba chochote kutoka katika zawadi ya mahari ya watu wake. Na alikuwa akisema: Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema: “Na tumeteremsha kutoka mbinguni maji yenye baraka.”831 Na akasema: “Ndani yake kuna ponyo kwa watu”832 na akasema (a.s): “Maji ya Zamzam pindi alipoyanywa” na akasema (s.w.t): “Lakini wakikupeni chochote kwa radhi ya nasfi katika hayo basi kileni kiwashuke kwa raha.”833 basi   Sahafatl-Ridha (a.s), uk. 90.   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 159. 829   Makarimul-Akhlaq, uk. 181. 830   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 102. 831   Surat Qaaf, aya 9. 832   Surat Nahl, aya 69. 833   Surat Nisa’ aya 4. 827 828

182

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 182

8/10/2017 1:22:08 PM


TIBA YA MAASUMINA

akakusanya kati ya vile ambavyo vimebarikiwa, na kati ya vile ambavyo ndani yake vina ponyo, na vizuri kwenu na starehe, hivyo vinakaribia kuleta afya.834

DAWA MJUMUIKO Nayo ni dawa iliyojumuisha maada mbalimbali zinazotibu ugonjwa zaidi ya mmoja kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (s.w.t), miongoni mwa zilizo mashuhuri ni: Dawa ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) nayo ni dawa yenye kuponya, na dawa mjumuiko ya Imam Ridha (a.s). Hadithi: Imepokewa kutoka kwa Mufadhal bin Umar kutoka kwa Imam asSadiq (a.s) alisema: “Dawa hii ni dawa ya Muhammad (s.a.w.w), nayo inafanana na dawa ambayo Jibrail (a.s) alimzawadia Musa bin Imran (a.s). Hakika Firaun alimwalika Musa na kaumu yake kwenye meza ya chakula, na alitaka awape sumu wana wa Israil. Basi akawafanyia wao sikukuu siku ya Jumapili, na akaweka sumu katika vyakula. Musa (a.s) alikwenda na wana wa Israil na wao walikuwa 600000, na kabla ya kula akawanywesha dawa hii, alimnywesha kila mtu kiwango kidogo sawa na kichwa cha sindano. Na pindi walipokula haikuwadhuru wao sumu na wakaokoka. Kisha Mwenyezi Mungu akateremsha juu ya Mtume wake (s.a.w.w) dawa hiyo kwa njia ya Jibrail.” Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Nayo ni dawa ambayo haitumiwi ila humnufaisha mtumiaji wake, nayo pindi hunywewa kwa ajili ya magonjwa, maradhi na maumivu yote….Na huu hapa ni mpangilio wake: Utachukua vipande vya vitunguu saumu vilivyo  Mustatrafu, uk. 348 cha Aabashiihi.

834

183

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 183

8/10/2017 1:22:08 PM


TIBA YA MAASUMINA

menywa, kisha utaviponda kidogo wala usivilainishe sana katika usagaji wake, na utaviweka katika sufuria au chungu au chombo kile utakachokuwa nacho, kisha utawasha moto hafifu chini yake, kisha utamimina juu yake samli ya ng’ombe kiasi cha kuweza kuvifunika vile vitunguu, na utaipika kwa moto hafifu mpaka ikauke ile samli. Kisha utaongeza samli mara nyingine na uipike mpaka ikauke. Kisha utaongeza samli mara nyingine na uipike mpaka kitunguu saumu kisiweze kuvyonza tena ile samli. Kisha utamimina juu yake maziwa, na utawasha moto hafifu chini yake, na utafanya hivyo kama ulivyofanya kwenye samli, na maziwa hayo yawe maziwa ya ng’ombe aliyezaa hivi karibuni, yatachemka mpaka kitunguu saumu kisiweze kuvyonza tena yale maziwa. Kisha utamimina asali mbichi na utaikamua kutoka katika masega yake, na utaichemsha juu ya moto mkali, wala masega yasiwe na kitu chochote, kisha utamimina juu ya vitunguu saumu, na utawasha moto hafifu chini yake, kama ulivyofanya kwenye samli na maziwa. Kisha utamimina dirham 10 ya hababarakati na utazisaga hadi zilainike, na utaisafisha wala hutaichuja, na utachukua kiwango cha dirham 5 cha pilipili na marzanjushi utazisaga, kisha utamwagia ndani yake, na utaifanya hivyo mfano wa khabiswu juu ya moto. Kisha utaiweka ndani ya chombo ambacho hakiwezi kuingiza vumbi wala upepo, na utamimina ndani ya chombo kiasi kidogo cha samli ya ng’ombe na chombo hicho kiwe kimepakwa mafuta, kisha itazikwa ndani ya shairi au vumbi kwa muda wa siku 40, na kila anapoiacha huru basi ndiyo inakuwa ni nzuri zaidi. - Na atatumia mwenye ugonjwa kila anapopatwa na maumivu.”835 * Dawa mkusanyiko ya Imam Ridha (a.s) amesema: “Chukua sunbul, na zafarani na qaaqirat, a’qir qarha, kharbaq nyeupe, banju   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 252.

835

184

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 184

8/10/2017 1:22:08 PM


TIBA YA MAASUMINA

na pilipili nyeupe, vipimo sawa, na abrifyun juzuu mbili, vitasagwa vyote mpaka viwe laini na kuchujwa, na inachanganywa kwa nyongeza ya asali mbichi, na atakunywa mgonywa, hakika atapona muda huo huo kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.”836 *Imepokewa kutoka kwa Ahmad na Husein watoto wa Bastwam katika kitabu (Twibbul-Aimmat) wamesema: “Alitutajia Ahmad bin Riyah dawa hizi, na alisema kwamba alizieleza kwa Imam naye akaziridhia, na akasema: Hakika hizo zinatibu kwa idhini ya Mwenyezi Mungu… KWALE Ni ndege mwenye baraka, ni mwingi wa kuzalisha, ni mwenye mgongo ulioinama, mbashiri wa kipupwe. Nyama yake huliwa na hunywewa supu yake, kwani inaongeza nguvu katika tendo la ndoa, na inatia nguvu shahawa. Na kudumisha kula nyama yake kunaimarisha ubongo, ufahamu na manii.837 Hadithi: Mtume (s.a.w.w) amesema: “Yule anayependa aiue au aidhibiti ghadhabu yake, basi ale kwale (yaani kumla kunaondoa ghadhabu).838Imepokewa pia kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Yule anayehisi maumivu kifuani kwake na kuzidi hasira zake, basi ale kwale.”839 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Mmoja wenu akipandwa na hasira au kupatwa na tatizo, na hajui sababu yake, basi ale nyama ya kwale, kwani inatuliza kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu.”840   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 245 na 247 hadithi zote mbili.   Ajaaibul-Makhluqaat, cha Qazwiini. 838   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 107, na kinachofanana na hicho. 839   Twibbul-Aimma (a.s), uk. 107. 840   Makarimul-Akhlaq. 836 837

185

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 185

8/10/2017 1:22:08 PM


TIBA YA MAASUMINA

DAMU Imepokewa kutoka kwa Imam al-Baqir (a.s) kuhusiana na sababu ya uharamisho wa kula damu amesema: “Na ama damu, hakika ulaji wake unasababisha maji ya manjano, na unasababisha kichaa cha mbwa, moyo mgumu, na upungufu wa upole na huruma, kisha hamwamini mpenzi wake, wala hamwamini yule anayeongozana naye.”841 Imepokewa pia kutoka kwa Imam asSadiq (a.s) amesema: “Hakika damu inapozidi zipo alama tatu; vipele mwilini, mwasho na utembeaji wa mdudu. (yaani kujihisi kutokwa na vipele).”842 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuhusiana na uji wa dengu amesema: “….Na alikuwa inapopanda damu ya yeyote kwa heshima yake atasema: Kunywa uji wa adesi (dengu), kwani unatuliza upandaji wa damu na unazima joto.”843 Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) amesema: “Damu ina alama nne; muwasho, kutokwa vipele, usinziaji na kizunguzungu.”844 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kuhusiana na mchadi amesema: “Unaimarisha akili na unasafisha damu.”845 UBONGO Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Mung’unya linaongeza akili na ubongo, nalo ni zuri kwa maumivu ya ugonjwa wa kukakamaa.”846   Aamali, uk. 529 cha Saduuq chapa ya tano.   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 55. 843   Makarimul-Akhlaq, uk. 193. 844   Khiswal, Juz. 1, uk. 250 cha Saduuq. 845   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 159. 846   Kashful-Akhtar, cha Shamu-Diin bin Muhammad Huseiniy – Makhtut. 841 842

186

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 186

8/10/2017 1:22:08 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Ulaji wa Baqila (Aina ya maharagwe) unaimarisha ngoko mbili, na unaongeza nguvu katika ubongo, na unazalisha damu safi.”847 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Mafuta ya balungi yanaufanya ubongo kuwa makini.”848 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Ni juu yenu kutumia mung’unya, kwani linaimarisha ubongo (yaani katika uchangamfu wake).”849

MAFUTA YA MIMEA NA UPAKAJI WA ­MAFUTA Imepokewa kutoka kwa Ibn Abbas kwamba Mtume (s.a.w.w) alisema: “Hakuna kitu cha kheri kwa mwili kuliko Raaziq.” Nikauliza: Ni nini Raaziqi? Akasema: “Yasimini.”850 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kwamba amesema: “Ni juu yako kutumia mafuta ya mimea, kula na jipake, hakika yule anayelala na kujipaka hatokaribiwa na shetani kwa muda wa siku 40.”851 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kwamba amesema: “Jipakeni mafuta ya mimea siku moja na acheni siku inayofuata, na jipakeni wanja kila baada ya siku mbili mara moja, na chaneni nywele kwa marefu na kuzitenga, na safisheni meno kwa mswaki daima.”852   Twabari – Makarimul-Akhlaq, uk. 183.   Kaafi, Juz. 6, uk. 522. 849   Sahifatul-Ridha (a.s), uk. 76. 850   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 76. 851   Wasail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 71 na kinachafanana nacho. 852   Fiqhul-Ridha (a.s), uk. 407. 847 848

187

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 187

8/10/2017 1:22:08 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Jipakeni mafuta ya mimea na endeleeni kufanya hivyo, kwani ni mafuta ya watu wema ni mchuzi wa wateule…”853 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Hayakuwa mafuta ya wa mwanzo ila mafuta ya kula.”854 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Yasimini ni mafuta bora zaidi kuliko yale yote mnayojipaka katika miili yenu.”855 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Mafuta ya mimea yanalainisha ngozi, na yanaimarisha ubongo na akili, na yanarahisisha tohara (na katika kitabu Khiswal: yanarahisisha mapito ya maji) na yanaondoa woga, na yanasafisha rangi.”856 WADUDU Mtume (s.a.w.w) amesema: “Kuleni tende kabla ya kula chochote, kwani inaua wadudu tumboni.” Saduq amesema: Yaani kila tende ila Barni, hakika kuila kabla ya kula chochote inasababisha kiharusi.”857 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Yule anayekula tembe nne za tende zilizosindikwa wakati wa kulala basi huua wadudu wa tumboni mwake.”858 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Siki ya pombe inakaza ufizi na inaua wadudu wa tumboni na inaimarisha akili.”859   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 71.   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 72. 855   Twibbul-Aimmat, uk.76. 856   Tuhful-Uquul, uk. 72. 857   Wasaail-Shi’ah, Juz. 62, uk. 165, kutoka kitabu Uyuun Juz. 2, uk. 40. 858   Kaafi cha Kulayni – na Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 65. 859   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 69. 853 854

188

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 188

8/10/2017 1:22:09 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Sufyani bin Samtwi kwamba Imam as-Sadiq (a.s) alisema: “Ni juu yako kula siki ya pombe, basi piga mbizi ndani yake, kwani hatabakia ndani ya tumbo lako mdudu ila itamuua.”860 Imepatikana katika baadhi ya vitabu vya marafiki zetu kwamba: Hakika uwatu ukilowekwa ndani ya siki usiku, na ukaliwa asubuhi kabla ya kula chochote, bila ya kula kitu katika siku hiyo, ni mzuri kwa kuuwa wadudu.”861 JOGOO Mtume (s.a.w.w) amesema: “Msimtukane jogoo, kwani yeye anajulisha juu ya nyakati za swala.”862 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Uwikaji wa jogoo ni swala yake, na upigaji wa mabawa yake ni rukuu yake na sajda yake.”863 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Jogoo mweupe ni rafiki yangu na ni rafiki wa kila muumini.”864 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Jogoo mweupe ana mambo matano miongoni mwa mambo ya manabii; Kujua nyakati za swala, wivu, ukwasi, ushujaa na kuzidisha kufanya tendo la ndoa.”865

Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 69.   Tuhfatul-Ridhawiyyat min Majarribaat Imamiyyat, uk. 65. 862   Makarimul-Akhlaq, uk. 130. 863   Ramzul-Sihat, uk. cha Dahsurkhi. 864   Makarimul-Akhlaq, uk. 130 na kinachoshabihiana nacho. 865   Khiswal, Juz. 1, uk. 298 cha Saduuq. 860 861

189

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 189

8/10/2017 1:22:09 PM


TIBA YA MAASUMINA

INZI Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Lau sio inzi ambaye anatua juu ya vyakula vya watu kwa namna ambayo hawajui, basi wangepatwa haraka na ugonjwa wa mbalanga.”866 Ahmad bin Umar bin Miqdad Raazi amesema: “Inzi alitua juu ya Mansur akamfukuza, basi akarudia akamfukuza hadi akahamaki. Basi hapo akaingia kwake Imam Ja’far as-Sadiq (a.s), Mansur akamwambia: Ewe Abu Abdillah, kwa nini Mwenyezi Mungu kaumba inzi? Akasema: “Ili awadhalilishe mabeberu.”867 KIUNGO CHA UZAZI CHA MWANAUME Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Na sa’tar na chumvi (kwa pamoja) vinafukuza harufu ya vifua… na vinaimarisha kiungo cha uzazi cha mwanaume (dhakari).”868 Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) amesema: “Ulaji wa karoti unachemsha kende mbili na unasimamisha kiungo cha uzazi cha mwanaume...”869 KICHWA Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) amesema: “Mambo matano ni miongoni mwa sunna za kichwani, na matano mwilini. Ama yale ya kichwani ni usafishaji wa meno, upunguzaji wa masharubu, ufarikishaji wa nywele, usukutuaji na upandishaji wa maji puani. Na ama ambayo ni ya mwilini ni jando, unyoaji wa kinena, kutoa nywele za kwapani, ukataji wa kucha na kustanji.”870   Twibbul-Aimmat, uk. 109 na Makarimul-Akhlaq, uk. 152.   Kashful-Ghummat fi Maa’rifatil-Aimmat, Juz. 2, uk. 370 cha Ali bin Isa bin Fat-hi Urbili, Daarul-Adhuai Beirut. 868   Makarimul-Akhlaq, uk. 191. 869   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17 uk. 164, kutoka kitabu Furuu na Mahasin. 870   Khiswal, Juz. 1, uk. 271. 866 867

190

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 190

8/10/2017 1:22:09 PM


TIBA YA MAASUMINA

RAHA Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Mke muafaka ni moja ya raha mbili.”871 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Yule anayepunguza kwa kutosheka, hakika atakuwa katika raha na atakuwa amejipunguzia maumivu.”872 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Usingizi ni raha ya mwili, na utamkaji ni raha ya roho na unyamazaji ni raha ya akili.”873 PUMU Imepokewa kutoka kwa Mufadhal bin Umar amesema: Nilimuuliza Imam as-Sadiq (a.s) nikasema: Ewe mtoto wa Mtume, ninapatwa na pumu kali ikiwa nitatembea, mpaka wakati mwingine ninakaa chini mara mbili katika masafa ya umbali uliyopo kati ya nyumba yangu na nyumba yako. Akasema: “Ewe Mufadhal kunywa mikojo ya ngamia jike.” Basi nikanywa huo basi Mwenyezi Mungu akaniponya ugonjwa wangu.874 Ninasema: Inatilia mkazo hili maana ya kauli ya Imam Kadhim (a.s) juu ya ngamia jike: “Mikojo ya ngamia ni bora kuliko maziwa yake, na Mwenyezi Mungu anajaalia ponyo katika maziwa yake.”875 UNYONYESHAJI Mtume (s.a.w.w) amesema: “Wakingeni watoto wenu na maziwa ya Malaya na mwendawazimu, hakika maziwa yanaambukiza.”876   Ghurarul-Hikam.   Nahju hikma: 371. 873   Majalis cha Saduuq. 874   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 17, uk. 87. 875   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17. uk. 87. 876   Biharul-Anwaar, Juz. 103, uk. 323. 871 872

191

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 191

8/10/2017 1:22:09 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Msiwaombe awanyonyeshee watoto wenu mpumbavu wala mlemavu wa macho, hakika maziwa yanaambukiza.”877 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Mtoto hana maziwa bora zaidi kuliko maziwa ya mama yake.”878 Miongoni mwa wosia wa Mtume (s.a.w.w) kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Hakuna unyonyeshaji baada ya kuacha kunyonya, wala hawi yatima baada ya kujiotea.”879 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Hakuna maziwa ambayo yenye baraka zaidi kwa mtoto kuliko maziwa ya mama yake.”880 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Angalieni ni nani anayenyonyesha watoto wenu, hakika mtoto anakua kwa maziwa yake.”881 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Msiwape awanyonyeshee watoto wenu mpumbavu, hakika maziwa yanashinda maumbile.”882 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Wachagueni kwa unyonyeshaji kama vile mnavyochagua wale mnaowaoa.”883 Imepokewa kutoka kwa Imam al-Baqir (a.s) amesema: “Mnyonyeshe mtoto wako maziwa ya wanawake wazuri, na jiepushe na wale wenye maumbile mabaya, hakika maziwa yanaambukiza.”884   Biharul-Anwaar, Juz. 103, uk. 323.   Biharul-Anwaar, Juz. 103, uk. 323. 879   Makarimul-Akhlaq, uk. 437. 880   Mustadrakul-Nahj, uk. 171. 881   Wasaail-Shi’ah, Juz. 15 uk. 188, na Mustadrakul-Nahju, uk. 170. 882   Biharul-Anwaar, Juz. 103, uk. 324. 883   Biharul-Anwaar, Juz. 103, uk. 323. 884   Wasaail-Shi’ah, Juz.. 15, uk. 189. 877 878

192

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 192

8/10/2017 1:22:09 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Maziwa ya myahudi, mnaswara na mmajusi ni bora kuliko maziwa ya mtoto wa zinaa.”885 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Msimpe mmajusi kumnyonyesha mtoto, na atamnyonyesha myahudi na mnaswara. Wala wasinywe pombe kwani hilo linawazuia kunyonyesha.”886 UTOKAJI WA DAMU PUANI Imepokewa kutoka kwa Ibn Bakiir amesema: Nilitokwa na damu puani, basi nikamuuliza Imam as-Sadiq (a.s) kuhusiana na hilo, akasema: “Kunywa sawiiq ya tufaha” basi ukakatika utokaji huo wa damu.887 KOMAMANGA Faida zake: Lina faida katika punje zake na ganda lake na mizizi yake. Na miongoni mwa faida muhimu zaidi za juisi ya komamanga ni kwamba ina maada mmeng’enyo ambayo ni mahsusi kwa kuzalisha mafuta ya kujipaka. Na ama maganda na mizizi yake hutumiwa kwa ufukuzaji wa wadudu. Ama ganda la tunda hutumiwa kwa kuchemsha wakati wa maradhi ya tumbo la siki, kuhara na mvurugiko wa tumbo.888 Ama kifuniko chepesi ambacho kipo kati ya punje za komamanga, chenyewe hulainisha mfuko wa chakula na kuutia nguvu, nacho   Wasaail-Shi’ah, Juz. 15 uk. 185.   Wasaail-Shi’ah, Juz. 15 uk. 185. 887   Makarimul-Akhlaq, uk. 193. 888   Nabataat Twayyibat wa Isti’imalatiha, Juz. 1, uk. 144 cha Dr. Muhammad Uwdaat. 885 886

193

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 193

8/10/2017 1:22:09 PM


TIBA YA MAASUMINA

ndio makusudio yaliyopo katika hadithi lukuki zisemazo: “Kuleni komamanga kwa mafuta yake, kwani hilo ni lainisho la mfuko wa chakula.” Angalizo: Komamanga Maliyasi ni komamanga ambalo rangi ya punje zake huwa za kijani na mbegu zake ni punje ndogo, nayo ndio aina bora zaidi kati ya aina za komamanga. Wakati ambapo komamanga lekundu mbegu zake huwa zinakuwa kubwa. Hadithi: Imepokewa kutoka kwa Abdullah bin Abbas kwamba alikuwa akisema: Hakika Mtume (s.a.w.w) alikuwa akila komamanga hakuwa anashirikiana na yeyote kwalo, anasema: “Katika kila komamanga kuna punje miongoni mwa punje za peponi.”889 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Kuleni komamanga mazzu kwa mafuta yake, kwani ni sagio la mfuko wa chakula, na uhai wa moyo, na linaondoa wasiwasi wa shetani.”890 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Walisheni watoto wenu wadogo komamanga, kwani linaharakisha ndimi zao.”891 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Kuleni komamanga kwa mafuta yake na nyama yake, basi hilo ni sagio la mfuko wa chakula.” Imepokewa kutoka kwa Yahud kwamba alimwambia Ali (a.s): Hakika Muhammad alisema: “Hakika katika kila komamanga   Ramzul-Sihat, uk. 193.   Tuhful-Uquul, uk. 88. 891   Makarimul-Akhlaq, uk. 171. 889 890

194

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 194

8/10/2017 1:22:09 PM


TIBA YA MAASUMINA

kuna punje ya peponi, na mimi nililivunja moja na nikala lote.” Ali (a.s): akasema: “Amesema kweli Mtume (s.a.w.w),” kisha Imam (as) akazipiga ndefu za Yahudi Yule, ikaanguka punje ya komamanga, hapo Imam (a.s) akaichukua na kuila, na akasema: “Punje hiyo haili kafiri, na sifa njema zote zinamstahiki Mwenyezi Mungu.”892 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Alikuwa Amirul-Muuminina (a.s) anapokula komamanga hulikunjua chini yake kwa duara, ndipo akaulizwa kuhusu hilo? Akasema: “Hakika ndani yake ipo punje kutoka peponi.” Akaulizwa: Hakika Yahudi na Mnaswara na wasiokuwa hao wanakula tunda hilo! Akasema: “Inapokuwa hivyo, Mwenyezi Mungu humtuma kwake malaika ambaye humnyang’anya punje hiyo ili asiile.”893 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kutoka kwa baba zake (a.s) kutoka kwa Amirul-Muuminina (a.s) amesema: “Kula komamanga kwa mafuta yake kwani hilo ni sagio la mfuko wa chakula, na kila punje katika hizo ikiwa itatulia ndani ya mfuko wa chakula huupa uhai moyo na hung’arisha nafsi na kuondoa wasiwasi wa shetani kwa muda wa siku 40, na komamanga linatokana na matunda ya peponi, Mwenyezi Mungu amesema: “Mna matunda na mitende na makomamanga.894”895 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuhusu komamanga na mafuta yake kwamba alisema: “Kwani hilo linaondoa maradhi ya meno ambayo yanasababisha kudondoka, na harufu mbaya ya mdomoni na linaimarisha kinywa.”896   Kharayij wal-Jarayih, cha Qutbu Diin Raawandi.   Wasaail-Shi’ah, Juz. 16, uk. 526. 894   Sura 55 aya 68. 895   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 134. 896   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17 uk. 123, kutoka kitabu Mahasin cha Barqi. 892 893

195

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 195

8/10/2017 1:22:09 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam Zaynul-Abidiina (a.s) amesema: “Vitu viwili ni vizuri lakini vikiingia tumboni huliharibu, na vitu viwili ni vibaya lakini vikiingia tumboni hulifanya liwe zuri. Ama ambavyo vinalifanya tumbo la binadamu liwe zuri ni komamanga na maji ya uvuguvugu. Na ama ambavyo vinaliharibu ni jibini na nyama kavu.”897 Imepokewa kutoka kwa Imam al-Baqir (a.s) amesema: “Matunda yako ya aina 120, na bwana wa hayo ni komamanga.”898 Na katika hilo mshairi ibn A’asim katika utenzi wake amesema: “Na bwana wa matunda ni komamanga – analila hilo mwenye njaa na mwenye shibe. Linatia nuru moyo wa watu wa dini – na linaondoa wasiwasi wa mlaaniwa.” Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Lau ningelikuwa Iraq ningelikula kila siku komamanga la suraniyya, na ningepiga mbizi kwenye mto furati.”899 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Walisheni watoto wenu komamanga, kwani linaharakisha ukuaji kwa vijana wao” (yaani vijana wao wanakuwa haraka na kufikia umri wa ujana)900.Imepokewa pia kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kwamba lilitajwa komamanga mbele yake, akasema: “Mazzu ni zuri tumboni.”901   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 280, na Wasaail Shi’ah, Juz. 17, uk. 38 na kinachofanana nacho. 898   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 119, kutokana na Furuu na Mahasin. 899   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 119, kutoka Furuu na Mahasin. 900   Wasaail-Shi’ah, Juz. Cha Hurri Aamili na Twibbu Imam Swadiq, uk. 72 cha Muhammad Khalili. 901   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 122. 897

196

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 196

8/10/2017 1:22:09 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Harith bin Mughira amesema: Nililalamikia kwa Imam as-Sadiq (a.s) uzito ninaopata kifuani kwangu na kuvimba tumbo kutokana na chakula changu, akasema: “Chukua komamanga tamu hili na lile kwa mafuta yake, kwani linalainisha mfuko wa chakula, na linaponya kutokana na uvimbaji wa tumbo, na linameng’enya chakula na linafanya tasbihi tumboni.”902 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Yule ambaye anakula komamanga asubuhi kabla ya kula chochote, linatia nuru moyo wake, na linafukuza wasiwasi wa shetani kwa siku 40.”903 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Vinne vinaleta ulinganifu wa maumbile; komamanga la surani (suriy ni sehemu iliyoko Iraq, linanasibishwa huko) na tende yenye kupikwa, balungi na hindubaau.”904 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Yule mwenye kula komamanga wakati wa kulala, basi atakuwa mwenye amani nafsini mwake hadi anapoamka.” Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Matano ni miongoni mwa matunda ya peponi hapa duniani, komamanga Amliisi” (yaani ambalo halina mbegu…).905 Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) amesema: “Moshi wa mti wa mkomamanga unafukuza wadudu watambaao.”906 Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) amesema: “Miongoni mwa yale ambayo Nabii Adam (a.s) alimuusia Hibatullah ni: “Ni juu yako kula komamanga hakika wewe ukilila na wewe   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 134.   Wasaail-Shi’ah, Juz. 16, uk. 530. 904   Khiswal, Juz. 1, uk. 249. 905   Khiswal, Juz. 1, uk. 289. 906   Kaafi cha Kulayni. 902 903

197

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 197

8/10/2017 1:22:09 PM


TIBA YA MAASUMINA

una njaa litakutosha, na ikiwa utalila na wewe umeshiba utakuwa vizuri.”907 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Kuleni komamanga, basi hakuna punje itaingia kwenye mfuko wa chakula ila itautia nuru moyo, na itamtia uziwi shetani kwa muda wa siku 40.”908 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Kuni za mkomamanga zinafukuza wadudu watambaao.”909 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Ulaji wa komamanga tamu unaongeza nguvu katika maji ya mwanaume na unafanya mtoto kuwa mzuri.”910 Imepokewa kutoka kwa Abdullah bin Hasan (a.s) amesema: “Kuleni komamanga kwani linasafisha vinywa vyenu.”911 UGONJWA WA MACHO Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Msichukie vinne; Ugonjwa wa macho kwani unakata mirija ya upofu, mafua kwani yanakata mizizi ya mbalanga, kikohozi kwani kinakata mirija ya kiharusi, na majipu kwani yanakata mirija ya ukoma.”912 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Macho ya Salmani na Abu Dharr (r.a) yalipatwa na maumivu, Mtume (s.a.w.w) akawatembelea hao wawili, na pindi alipowaangalia akamwambia kila mmoja wao: Usilalie upande wa kushoto maadam una maumivu ya macho yako, wala usiikaribie tende hadi akuponye Mwenyezi Mungu (a.j).”913   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 119, kutoka kitabu Furuu na Mahasin.   Sahifat Ridha (a.s), uk. 53. 909   Safinatul-Bihar, Juz. 1, uk. 536. 910   Waaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 121 na 122. 911   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 121. 912   Biharul-Anwaar, Juz. 59, uk. 301. 913   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 85. 907 908

198

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 198

8/10/2017 1:22:09 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Hakika katika habasoda kuna ponyo la kila ugonjwa, na mimi ninaitumia kwa ajili ya homa, maumivu ya kichwa, ugonjwa wa macho, ugonjwa wa tumbo na kila maumivu yanayonitokea mimi, na Mwenyezi Mungu (a.j) huniponya.”914 ROHO Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “…Hakika roho ya muumini inapaa hadi kwa Mwenyezi Mungu (a.j) [inakusudiwa wakati akiwa amelala] anaibusu na anaibariki; na ukiwa wakati wake umefika anaijaalia katika hazina za rehema Zake (na katika kitabu Tuhaful-Uquul: Anaijaalia katika sura nzuri), na ikiwa muda wake haujafika basi anaipeleka pamoja na waaminifu Wake miongoni mwa malaika Wake basi wanairudisha kwenye mwili wake.”915 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Hakika Mwenyezi Mungu aliyetukuka ameiumba roho, na akaiwekea sultani, na sultani wake ni nafsi. Na mja akilala roho inatoka na anabakia sultani wake.”916 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Kutamka ni raha ya roho, na kunyamaza ni raha ya akili.”917 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Mwili umejengwa juu ya mambo manne; juu ya roho na akili, na damu na nafsi. Na pindi roho ikitoka akili huifuata, na roho inapoona kitu akili hukihifadhi kitu hicho, na hubakia damu na nafsi.”918   Makarimul-Akhlaq, uk. 212.   Khiswal, Juz. 2, uk. 613. 916   Manaqib ibn Sharashuub – Qiswat As-ilat Nasw-raniyyiin. 917   Majalis cha Saduuq. 918   Khiswal, Juz. 1, uk. 226. 914 915

199

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 199

8/10/2017 1:22:09 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuhusiana na wale waliotangulia amesema: “Hao ni Mitume wa Mwenyezi Mungu, na walio mahsusi kwa Mwenyezi Mungu miongoni mwa viumbe Wake. Amejaalia ndani yao roho tano; amewaunga wao mkono kwa Roho mtakatifu, na kwa roho huyo wamejua vitu. Na amewaunga mkono kwa Roho wa imani, na kwa roho huyo wamemuogopa Mwenyezi Mungu (a.j). Na amewaunga mkono wao kwa Roho wa nguvu, na kwa roho huyo wakaweza kumtii Mwenyezi Mungu. Na amewaunga mkono wao kwa Roho wa matamanio, kwa roho huyo wakatamani kumtii Mwenyezi Mungu na wakachukia maasi. Na ameweka ndani yao Roho mudrij, ambaye kwa roho huyo watu wanakwenda na wanakuja.”919 UPEPO WA TUMBONI NA RIYAHI Miongoni mwa VIPENGELE vyenye riha na unenepeshaji ni punje za nafaka kwa aina zake zote, mfano wa uwatu, na maharagwe na hasa hasa yakipikwa na majani yake, na maharage na mashi, na adesi na shairi ikiwa kama haikuwa laini upikaji wake. Na miongoni mwa viasili vyenye kuleta harufu; komoni na mtishamba, anisiumu na kasham. Na sifa za kinywaji cha kuundosha gesi za tumboni: Unachukua mimea sita ifuatayo:

• • • •

Mbegu za komoni (vijiko viwili vya chai). Punje za Yanisun (nusu kijiko cha chai). Maryamat (kijiko kikubwa). Mbegu za khuwlanji.

Kaafi, Juz. 1, uk. 272 cha Kulaini.

919

200

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 200

8/10/2017 1:22:09 PM


TIBA YA MAASUMINA

• •

Shummar (nusu kijiko cha chai). Na’nai (kulingana na utashi).

Anachemsha maji katika birika kubwa la chai kiwango cha lita na nusu na vinaongezwa kwayo viwango vilivyotangulia, kisha anaiacha kwa muda wa robo saa baada ya kuifunga kwa kitambaa cha kuchuja mawaad, kisha anakunywa nayo ikiwa imechemshwa pamoja na sukari kama vile chai. Kwa matumizi na faida ya dawa hizi hapana budi kudumisha kuinywa kwa mwezi mara tatu kila siku, kila mara kikombe kikubwa baada ya chakula, kwani hiyo inaondoa harufu na gesi na maumivu ya tumbo na uvimbe wa koloni kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Hadithi: Mtume (s.a.w.w) amesema: “Asali ni ponyo inafukuza harufu na homa.”920 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Maharage yanafukuza upepo wa tumboni.”921 Alilalamika Dhariih bin Muharibi maumivu ya tumboni mwake kwa Imam as-Sadiq (a.s) akasema: Je, unapata maumivu? Akasema: Ndio. Akasema: Ni kipi kinakuzuia kutumia habasoda na asali kwa hilo.”922 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s), aliulizwa kuhusiana na karath, akasema: “Ile” hakika ndani yake kuna mambo manne, inafanya uzuri tendo la ndoa, na inafukuza harufu na inakata   Ramzul-Sihat, uk. 229.   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 101. 922   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 100. 920 921

201

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 201

8/10/2017 1:22:09 PM


TIBA YA MAASUMINA

bawasiri, nayo ni amani ya mbalanga kwa yule ambaye amedumisha juu yake.”923 Imepokewa kutoka kwa Is-haq bin Ammar, akasema: Nikasema kumwambia Imam as-Sadiq (a.s): “Wanasema mafuta ya kula yanachochea harufu, akasema: Hakika zaituni inafukuza harufu.”924 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Kula figili, hakika ndani yake kuna mambo matatu; na majani yake yanafukuza harufu, na moyo wake unarahisisha haja ndogo na mmeng’enyo, na mizizi yake inakata kikohozi.”925 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Komoni Malaki na jozi, vinachoma bawasiri, na vinafukuza harufu, na vinafanya rangi kuwa nzuri, na vinafanya ugumu mfuko wa chakula, na vinachemsha kende. Na sa’tar na chumvi vinafukuza harufu kifuani, na vinaondoa harufu mbaya kinywani, na vinafanya kiungo cha uzazi cha mwanaume kuwa kigumu .”926 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Hakika harufu zote zinatokana na kibofunyongo yenye kushinda, au damu yenye kuungua, au kikohozi yenye kushinda, basi ajishughulishe mtu kwa uchungaji wa nafsi yake kabla haijamshinda juu yake kutokana na maumbile basi inaiangamiza.”927 Jabir bin Hassan Swafi aliandika kwa baba wa Abdillah Imam as-Sadiq (a.s) akasema: “Ewe mtoto wa Mtume, imenizuia mimi harufu tatanishi imeweka nyavu kuanzia utosini hadi nyayoni mwangu basi niombee kwa Mwenyezi Mungu, basi akamuombea yeye na   Khiswal, Juz. 1, uk. 250 cha Saduuq.   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 72. 925   Furuul Kaafi, Juz. 6, uk. 371 na Khiswal, Juz. 1, uk. 144. 926   Makarimul-Akhlaq, uk. 191. 927   Twibbu Imam Swadiq (a.s), uk. 80, na kutoka kitabu Biharul-Anwaar, Juz. 14, uk. 546. 923 924

202

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 202

8/10/2017 1:22:09 PM


TIBA YA MAASUMINA

akamwandikia yeye; Ni juu yako kwa unusaji ya ambari na yasimini, utapona kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu.”928 Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) amesema: “Harufu inatatanisha, kinga na sindano katika maungo, unachukua gau la uwatu na gao la tiini yabisi, unazizamisha ndani ya maji na unazipika ndani ya chungu kisafi, kisha unazisafisha kisha zinapoa, kisha unainywa siku moja na unaacha siku nyingine mpaka utainywa hiyo yote siku zako kiwango cha kikombe.”929 Barua ya dhahabu ya Imam Ridha (a.s): “Na yule anayetaka asipatwe na harufu mwilini kwake, basi na ale kitunguu saumu mara moja kwa siku saba.”930 HARUFU NZURI Imepokewa kutoka kwa Imam Hasan (a.s) amesema: “Mtume (s.a.w.w) alinipatia kwa mikono yake miwili ua la waridi, akasema: Hili ni bwana wa maua mazuri la watu wa dunia na akhera.”931 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Akija mmoja wenu na ua zuri basi alibusu na aliweke juu ya macho yake, kwani hilo linatoka peponi.”932 Imepokewa kutoka kwa mfalme wa Juhani amesema: Nilimpelekea baba wa Abdillah ua zuri, basi akalichukua na akalibusa na akaliweka juu ya macho yake kisha akasema: “Yule ambaye atachukua ua zuri na akalibusu na akaliweka juu ya macho yake, kisha akasema: Allahumma swalli a’la Muhammad wa Aali Muhammad, halitoanguka ardhini mpaka asamehewe yeye.”933   Twibbu Imam Swadiq (a.s), uk. 55.   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 175, kutoka kitabu Rawdhat Kaafi, Juz. 8, uk. 191. 930   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 325. 931   Makarimul-Akhlaq, uk. 45. 932   Makarimul-Akhlaq, uk. 41. 933   Makarimul-Akhlaq, uk. 42, kutoka kitabu Rawdhatul-Kaafi. 928 929

203

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 203

8/10/2017 1:22:10 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kwamba: Kula tunda wakati utapoingia kwenye mji husika, na bora zaidi ni komamanga na Furungu, na kutokana na maua mazuri ni waridi na banafsaji, na kutokana na mboga mboga ya hindubaau na khissi.”934 Galenos amesema: Yule ambaye ana vipande viwili vya mkate, basi ajaalie kimojawapo thamani ya Nasisai, hakika mkate ni chakula cha mwili, na Nasisai ni chakula cha roho.935 Ua zuri la jabalini: (Badharuuji au HUUK) Maana yake: Ni mmea wa jabalini miongoni mwa mboga mboga, na linaitwa katika lugha nabtwiyyat (Balungi) na katika ibriyat (Huuk). Na kati ya hizo ni aina ambayo majani yake yanakuwa madogo na mengi yanaitwa Rayhanul-Farsi au (Hubuk), na asili yake katika kifarsi (Badurnak), nalo linalimwa majumbaji. Faida zake: Rayhanu linaondoa gesi na ubanaji wa haja ndogo na uponyaji wa Rheumatism, nalo linatia nguvu moyo vizuri, na linapunguza pafu na kifua, na linafanya maziwa yatoke kwa wingi. Na wafursi wanakula hilo kama vile na’naa na legevu, na inaingia katika utengenezaji wa uturi. Kisa kutokana na Rayhan: Katika kitabu (Maajabu ya viumbe) cha Qazwiini: Hakika Rayhan ya kifarsi haikuwa kabla ya Kisra Anushiiruwaan, na hakika imepatikana katika zama zake.   Mustadarkul-Wasaail, Juz. 3 uk. 119.   Ajaaibul-Makhluqaat cha Qazwiini mwishoni mwa kitabu Hayaatul-SahabaJuz. 2 uk. 197 cha Damiiri.

934 935

204

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 204

8/10/2017 1:22:10 PM


TIBA YA MAASUMINA

Na sababu yake ni kwamba siku moja alikuwa amekaa mbele ya watu wenye malalamiko ya kufanyiwa dhulma, ghafla akaja nyoka mkubwa akitambaa chini ya kitanda cha ufalme wake, basi walinzi wakaazimia kumuua, Kisra akasema: “Mwacheni huyo hakika mimi ninadhani huyo ni mdhulumiwa.” basi akapita akitambaa, basi Kisra akamfuata na baadhi ya washauri wake. Akaendelea mpaka alipoteremka juu ya mdomo wa kisima. Basi nyoka yule akateremka ndani yake, kisha akawa anachungulia. Mtu mmoja alipochungulia akaona ndani ya kina kirefu cha kisima kuna joka lililouawa na pembeni yake kuna nge mweusi, basi mtu yule akageuzia mshale wake kwa nge na hatimaye akamuua. akarudi kwa Mfalme na kumfahamisha hali ya nyoka. Na pindi ulipofika mwaka uliofuatia nyoka yule alikuja tena katika siku ambayo Kisra alikuwa amekaa kusikiliza malalamiko ya waliodhulumiwa, na akawa akitambaa hadi akasimama mbele yake, akatoa kutoka kinywani mwake mbegu nyeusi. Mfalme akaamuru mbegu zile zipandwe, zikapandwa na hatimaye zikaota mmea wa Rayhan… na Mfalme alikuwa mwingi wa mafua na maumivu ya ubongo, basi akautumia mmea huo na hatimaye ukamsaidia vizuri.936 Hadithi: Mtume (s.a.w.w) amesema: “Huuk ni mboga nzuri kana kwamba mimi ninaona inaota peponi, na girigirani ni mboga khabithi kana kwamba ninaiona inaota motoni.”937 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: Mtume (s.a.w.w) alitajiwa Huuk nayo ni Balungi, akasema: “Ni mboga yangu na mboga ya manabii wa kabla yangu, hakika mimi ninaipenda na ninaila, hakika mimi ninaangalia mti wake unaota peponi.”938   Kunay wal-Alqaab, Juz. 1, uk. 79 cha Sheikh Abbas Qumi.   Makarimul-Akhlaq, uk. 179. 938   Makarimul-Akhlaq, uk. 179. 936 937

205

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 205

8/10/2017 1:22:10 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Shaiiri amesema: Mboga ambayo ilikuwa ikimpendeza zaidi Mtume (s.a.w.w) ni Badharuuj.”939 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Alikuwa Amirul-Muuminina (a.s) likimpendeza Balungi.”940 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Huuk ni mboga ya manabii (a.s). Na hakika ndani yake kuna mambo nane; inafanya chakula kiwe kizuri na inafungua kizuizi, na inapendezesha kubeua, inafanya uzuri tendo la ndoa, na inaleta hamu ya chakula, na inarahisisha mzunguko wa damu, nayo ni amani ya mbalanga, na ikiwa itatulia tumboni mwa mtu inaondoa magonjwa yote.”941 Kisha akasema: “Hakika hilo linapamba kwayo meza za watu wa peponi.”942 Aliulizwa Imam as-Sadiq (a.s) kuhusu mboga, akasema: “Hindubaau na badharuuj kwetu, na girigirani ni la bani Umayya.”943 Imam Kadhim (a.s) kuhusiana na Balungi amesema: “Hakika mimi ninapenda nifungue chakula changu kwayo, kwani hiyo inafungua kizuizi, inatia hamu ya chakula, na inaondoa dhana mbaya. Na sijali ninapofungua kwayo, sili baada yake chakula, hakika mimi siogopi ugonjwa wala madhara… kisha akasema: Malizia kwayo chakula chako kwani hiyo inafanya kizuri kile cha kabla na inatia hamu kile cha baada, na inaondoa uzito, na inapendezesha kubeua na tendo la ndoa, (jushaau: yaani kubeua).944 Mtindi   Ramzul-Sihat uk. 139.   Kaafi cha Kulayni. 941   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 147. 942   Makarimul-Akhlaq, uk. 179. 943   Wasaal-Shi’ah, Juz. 17, uk. 156, Twibbul-Aimmat (a.s) uk. 139 na kinachofanana nacho. 944   Makarimul-Akhlaq, uk. 179. 939 940

206

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 206

8/10/2017 1:22:10 PM


TIBA YA MAASUMINA

Faida zake: Mtindi wa moto na tende, ndani yake kuna faida nyingi, miongoni mwa hizo ni; uivishaji na uyeyushaji. Na unaponya mavimbe ambayo yanakuwa upande wa masikio mawili na vifereji viwili katika figo, ambavyo hupitisha mkojo na kuishia kibofuni, na uvimbe wa kinywani, na mavimbe mengine ambayo yanajitokeza mwilini mwa mwanamke na watoto, ikiwa itatumiwa peke yake. Na ikilambwa kwayo inamfaidisha yule anayetokwa na damu a­ mbayo inakuwa kutokana na pafu, na huivisha uvimbe wenye kujitokeza ndani yake. Nayo inalainisha maumbile na mishipa na uvimbe mgumu ­wenye kujitokeza kutokana na kibofunyongo cheusi na kukohoa, inanufaisha kutokana na kufanya kuwa yabisi yenye kujitokeza mwilini. Na ikiwa itapakwa juu ya maoteo ya meno ya watoto, inakuwa yenye kusaidia juu ya uotai wake na uchomozaji wake. Nayo ni yenye manufaa ya ukohoa ambao unatokana na ubaridi na uyabisi, na inaondoa ugonjwa ambao unatoa magamba mwilini, nao ni hadhaarat na ugumu wa mwilini, na inalainisha maumbile. Na inaondosha hamu ya chakula, na inaondoa uzito wa utamu wa asali na tende. Vivyo hivyo alikuwa Mtume (s.a.w.w) akikusanya hiyo na tende, kwa hekima kubwa nayo ni ulinganifu wa baadhi yake na nyingine. Hadithi: Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: ‘alitutembelea Mtume (s.a.w.w) na akatuzawadia sisi Ummu Ayman maziwa na mtindi na tende, basi Mtume akala pamoja hayo.”945 Imepokewa kutoka kwa watoto wawili wa Yasri Salmiyyina wakasema: Mtume (s.a.w.w) aliingia kwetu basi tukampatia mtindi   Ramzul-Sihat, uk. 199 cha Dahsurkhi.

945

207

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 207

8/10/2017 1:22:10 PM


TIBA YA MAASUMINA

na tende basi akala. Na alikuwa akipenda mtindi na tende.”946 ZABIBU Mpangiko wake: Nayo ni zabibu kavu, ina kiwango cha sukari cha zabibu, na pili yenye umbo la koni ya potasiamu. Na aina ya wekundu kwayo ni tajiri ya sukari ya zabibu, ambayo ni chakula cha msingi kwa viungo na sehemu tupu za ubongo. Na uzuri zaidi ina wingi wa mafuta, ganda jepesi, mbegu ndogo maarufu kwa jina la Darbaliy, na inafuatiwa na weusi unaopiga ladha yale kuelekea katika uchachu, na zinafuatiwa hizo mbili na wekundu ukweli wa utamu.947 Faida zake: Zabibu inapoza kidogo, na inaua wadudu ikiwa italiwa asubuhi kabla ya kula chochote. Nayo inachangamsha mwaka na inafanya ulaini na inapingana na Antibiotiki na lishe (Nourishing). Hadithi: Mtume (s.a.w.w) amesema: “Ni juu yenu kula zabibu, kwani inazima Murrat, na inakula kikohozi, na inafanya mwili kuwa na afya, na inafanya tabia kuwa nzuri, na inakaza mishipa, na inaondoa maradhi na maumivu ya muda mrefu.948 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Ni juu yenu kula zabibu, kwani inafichua kibofunyongo, na inaondoa balgham, na inakaza mishipa, na inaondoa uchovu, na inapendezesha tabia, na inapendezesha mdomo, na inaondoa majonzi” (hizo ndizo   Ramzul-Sihat, uk. 199.   Mufradaat Nabataat Twibbiyat, uk. 316. 948   Makarimul-Akhlaq, uk. 175. 946 947

208

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 208

8/10/2017 1:22:10 PM


TIBA YA MAASUMINA

sifa za zabibu).949 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Lau watu watajua yale yaliyomo katika sanamaki wangelifikia (wangelikabili) kila mithqal kwayo mithqal mbili ya dhahabu… na inachukuliwa pamoja zabibu nyekundu ambayo haina kokwa, na inafanywa pamoja nayo haliyliji ya Kabul ya rangi ya manjano na nyeusi viungo sawa, inatumiwa asubuhi kabla ya kula chochote, kiwango cha dirham tatu, na utakapokwenda kitandani kwako mfano wake, nayo ni bwana wa madawa.”950 [Dirham: ni sawa na gram 3 ya 4]. Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Yule anayekula zabibu nyekundu 21 kabla ya kula chochote, hatokuta mwilini kwake kitu kinachomtia karaha. (na katika hadithi nyingine) hatoumwa ila maradhi ya kifo.”951 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Zabibu inakaza moyo, inaondoa maradhi, inazima joto na inapendezesha kinywa.”952 Kaa’fai amesema: Yule anayedumisha ulaji wa zabibu asubuhi kabla ya kitu chochote ataruzukiwa ufahamu na hifidhi na ubongo na kupunguza kikohozi.”953 Zahiir (kite) Imepokewa kutoka kwa Imam Baqir (a.s) amesema: “Hakika mtu mmoja alimlalamikia yeye juu ya kite, basi akamwambia: Chukua udongo wa armani na ugeuze geuze katika moto hafifu, na itumie hakika hiyo itakutuliza wewe.”954   Khiswal, Juz. 1, uk. 344.   Makarimul-Akhlaq, uk. 188. 951   Sahifat Imam Ridha (a.s), uk. 79. 952   Makarimul-Akhlaq, uk. 175. 953   Safinatul-Bihar, Juz. 1, uk. 542. 954   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 65. 949 950

209

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 209

8/10/2017 1:22:10 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam Baqir (a.s) kuhusu Zahiir amesema: Unachukua juzuu kutokana na kharbaq (hellebore) nyeupe, na juzuu kutokana na mbegu za katani na juzuu kutokana na kundi la kiarabu, na juzuu kutokana na udongo wa Armani, unakaanga katika moto hafifu na itumie hiyo.”955 Imepokewa kutoka kwa Yunus bin Yakub amesema: Nilikuwa nikimhudumia Imam as-Sadiq (a.s) wakati wa ugonjwa wake – nao ni kaswende – akasema: “Ole wako ewe Yunus, je, hujui mimi nimepewa ilhamu katika maradhi yangu kuwa nile wali. Niliamrisha (yaani Imam) na hatimaye mchele ukaoshwa kisha ukakaushwa, kisha ukakaangwa, kisha ukawekwa ndani ya chombo na ukapikwa, basi nikaula kwa mafuta yake (mafuta safi), basi Mwenyezi Mungu ameondoa ugonjwa huo kutoka kwangu mimi.”956 ZA’TAR (SU’TAR) Faida zake: Za’tar ni ya joto yabisi, inapendezesha na inafukuza harufu na uvimbaji wa tumbo, na inafanya mmeng’enyo wa chakula kizito, na inakausha mfuko wa chakula na inazungusha haja ndogo na hedhi, inatia nguvu uonaji wa macho dhaifu. Hadithi: Imepokewa kutoka kwake Mtume (s.a.w.w) kwamba amesema: yeye aliitisha komoni muluki, su’tar na habasoda, basi akawa akaitumia akila mayai na chakula chake hakuna madhara…..957 Imepokewa kwamba hakika su’tar inalainisha mfuko wa chakula.958   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 174, kutoka kitabu Twibbul-Aimmat uk. 65.   Twibbul-Aimmat, uk. 100. 957   Makarimul-Akhlaq, uk. 187. 958   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 173, kutoka kitabu Mahasin cha Barqi. 955 956

210

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 210

8/10/2017 1:22:10 PM


TIBA YA MAASUMINA

Na katika hadithi nyingine imekuja hivi: Hakika su’tar inaotesha zi’bar ya mfuko wa chakula (yaani kidole tumbo).959 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Na su’tar na chumvi vinafukuza harufu ya kifuani…”960 Na imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: Ilikuwa dawa ya Amirul-Muuminina Ali (a.s) ni Saa’tar, na alikuwa akisema: Hakika hiyo inafanya mfuko wa chakula kufumba, kama vile ufumbaji wa Qatifa.”961 Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) amesema: “Alimlalamikia mmoja wao kuhusu umaji maji, basi akamwamrisha atumie su’tar kabla hajala kitu chochote.”962 Mafua Wasifu wake: Unatumiwa wasifu huu tangu yalipojitokeza mafua kwa mara ya kwanza. Unaweka baadhi ya vijiti vya qirfat na magome ya mkarafuu katika bilauri maji, kisha unachemsha kwa muda wa dakika tatu. Na inaachwa kwenye maji kwa muda wa dakika 20 na inasafishwa na kuichemsha, na inaongezwa kwayo juisi ya limao chachu nusu, na kijiko kikubwa cha asali… na unakunywa kabla ya kulala.963 Hadithi: Mtume (s.a.w.w) amesema: “Msichukie manne; ugonjwa wa macho kwani unakata mizizi ya homa, mafua kwani yanakata mizizi ya mbalanga…”964   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 173, kutoka kitabu Mahasin cha Barqi.   Makarimul-Akhlaq, uk. 191. 961   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 172. Kutoka kitabu Furuu Kaafi na Mahasin cha Barqi. 962   Wasaail- Shi’ah, Juz. 17, uk. 172. 963   Dalail Jadiid li swihhat, uk. 174 cha Kuluud Gharihi. 964   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 301. 959 960

211

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 211

8/10/2017 1:22:10 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Hakuna yeyoye miongoni mwa wanadamu ila ndani yake kuna mishipa miwili: Mshipa uliopo kichwani ambao huchochea mbalanga, na mshipa uliopo mwilini ambao huchochea ukoma, na unapovimba mshipa uliopo kichwani Mwenyezi Mungu huleta mafua ili kuondoa uchafu uliyomo ndani ya mshipa husika. Na unapovimba mshipa uliyomo mwilini Mwenyezi Mungu huleta majipu ili kuondoa uchafu uliyomo ndani ya mshipa husika. Hivyo basi, yeyote miongoni mwenu akipatwa na mafua na majipu amhimidi Mwenyezi Mungu (a.j) kwa kumpa afya njema.” – Na akasema: “Mafua ni mabaki ya uchafu wa kichwani.”965 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) walimlalamikia baadhi ya masahaba wake kuhusu mafua, akasema (a.s): “Ni kitu kilichotengenezwa na Mwenyezi Mungu, na jeshi miongoni mwa majeshi ambayo ameyatuma kwa ugonjwa wako ili yauondoe, na yanapouondoa basi ni juu yako kutumia kipimo cha daniq cha habasoda na nusu daniq ya kundus, inasagwa na inapuliziwa puani kwani inaondosha mafua, na ukiweza usiyatibu kwa chochote basi yaache usifanye chochote, kwa hakika ndani yake kuna manufaa mengi.”966 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Unachukua mafuta ya kujipaka ya banafsaji katika pamba, basi ibebe katika suflatika wakati wa kulala, kwani inafaa kwa mafua kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu.”967 Imepokewa kuoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Alikuwa Mtume (s.a.w.w) hajitibu mafua na akisema: “Hakuna yeyote ila kwake upo mzizi wa mbalanga, na yakimsibu mafua huondoa.”968 Barua ya dhahabu ya Imam Ridha (a.s): “Na yule anayataka   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 184.   Twibbul-Aimmat, uk. 64 na Twibbul-Imam Swadiq (a.s) uk. 54. 967   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 84, kutoka kitabu Makarimul-Akhlaq, uk. 377. 968   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 183, kutoka kitabu Rawdhat, Juz. 8, uk. 382. 965 966

212

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 212

8/10/2017 1:22:10 PM


TIBA YA MAASUMINA

kukinga mafua katika siku za masika, basi naale kila siku matonge matatu ya mshumaa wa asali.”969 Na miongoni mwa hizo ni: Wala asicheleweshe kunusa Nasisa, kwani linazuia mafua katika nyakati za masika, vivyo hivyo habasoda, na akihofia mtu mafua katika zama za kiangazi basi naale kila siku matango na ajihadhari kukaa juani.970 Zinaa Rejea (kujihifadhi na maasi). Jibrail aliteremka hadi kwa nabii Musa (a.s) akamwambia: “Ewe Musa yule anayezini anaziniwa (kwa mkewe), jihifadhini watajihifadhi wake zenu.”971 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Mwenyezi Mungu alimfunulia nabii Musa (a.s): “Hakika mimi ninawalipa wanadamu kwa kazi za mababa, hakika kheri kwa kheri na shari kwa shari. Msizini wataziniwa wake zenu. Yule anayemwingilia mwanamke wa mwislamu ataingiliwa mkewe. Kama ufanyavyo utafanyiwa.”972 Imepokewa kutoka kwa Masiih (a.s) amesema: “Mwanamke yeyote atakayejipaka manukato na akatoka ikipatikana harufu yake basi yeye ni mzinifu, na kila jicho linazini.”973 Imepokewa kutoka kwa Masiih (a.s) amesema: “Msiangalie kwa jicho kali kwa yale ambayo sio yenu, kwani hauzini utupu wako ikiwa utahifadhi jicho lako, na ukiweza usiangalie katika nyumba ya mwanamke ambaye sio halali kwako, basi fanya hivyo.”974   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 324.   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 324. 971   Twibbul-Aimmat, uk. 441 cha Shubbar. 972   Twibbul-Aimmat, uk. 440 cha Shubbar. 973   Tanbiihul-Khawaatir, uk. 23. 974   Tanbiihul-Khawaatir, uk. 50. 969 970

213

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 213

8/10/2017 1:22:10 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) alimwambia Ali (a.s): Ewe Ali, zinaa ina mambo sita; matatu duniani na matatu akhera” Ama ambayo ni ya duniani inaondoa haiba, inaharakisha kifo, na inakata riziki. Na ama yale ambayo ni ya akhera, hesabu mbaya, kukasirikiwa na Rahmani na kuishi motoni melele.”975 Mtume (s.a.w.w) amesema: “Laana ya Mwenyezi Mungu na ya malaika Wake na watu wote… iko juu ya yule anayefanya punyeto, na juu ya yule anayewaingilia watoto wa kiume kutokana na walimwengu.”976 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Laana ya Mwenyezi Mungu na malaika Wake na watu wote… iko juu ya yule anayemwingilia mnyama, na juu ya yule anayefanya punyeto.”977 Imepokewa kutoka kwa Imam Baqir (a.s) amesema: Nimekuta ndani ya kitabu cha Ali (a.s) amesema: “Mtume (s.a.w.w) amesema: “Zinaa ikizidi baada yangu, vitazidi vifo vya ghafla.”978 Aliulizwa Imam Baqir (a.s) kuhusiana na mwanaume mmoja aliyembaka mwanamke, akasema (a.s): “Anauawa, akiwa mwenye mke au hana mke (na adhaku ya haddi isiyokuwa ya kupaka, akiwa mzinifu ni kapela anapigwa mijeledi, na akiwa mwenye ndoa anapigwa mawe hadi kufa, na katika hali ya kubaka anauliwa sawa ameoa au kapela.)”979 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Mwanaume aliyejifanya mbabe kwa mwanamke juu ya nafsi yake (kumwingilia kinguvu), atapigwa kwa upanga pigo moja, atakufa kwalo au ataishi.”980   Mkarimul-Akhlaq, uk. 441.   Kanzul-Ummal, hadithi 44057. 977   Kanzul-Ummal, hadithi 44057. 978   Biharul-Anwaar, Juz. 79, uk. 27. 979   Wasaail-Shi’ah, Juz. 18, uk. 381. 980   Wasaail-Shi’ah, Juz. 18, uk. 382. 975 976

214

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 214

8/10/2017 1:22:10 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Upakaji wa siki unaondoa hamu ya zinaa.”981 Imepokewa pia kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Zinaa zitapozidi basi yatadhihiri matetemeko ya ardhi.”982

ZANBAQ Maana yake: Na katika kamusi: Zanbaq ni mafuta ya yasimini na wariid. Ibn Baytwar amesema: Raaziqi nayo ni suuzan nyeupe, na mafuta yake nayo ni mafuta ya Raaziqi. Hadithi: Imepokewa kutoka kwa ibn Abbas amesema: Mtume (s.a.w.w) amesema: “Hakuna kitu cha kheri kwa mwili kuliko Raaziqi” nikasema: ni nini huyo Raziqi? Akasema (s.a.w.w): “Zanbaq (yasimini).”983 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Hakuna mafuta yanayofaa vizuri zaidi mwili kuliko mafuta ya zanbaq. Hakika ndani yake kuna manufaa mengi na ponyo ya magonjwa sabini.”984 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Raziqu ni bora zaidi ya yale mnayojipaka kwayo mwili.”985 Ali bin Yaqtwin amesema: Nilimwandikia Imam Ridha (a.s): “Hakika mimi ninakuta kichwanii kwangu baridi kali hadi unapovuma upepo nilikaribia kuzimia.” Basi akaniandikia: “Ni juu yako kutumia kunusa ambari na zanbaq (yasimini) baada ya chakula, utapona ugongwa huo kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (a.j).”986   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 282.   Biharul-Anwaar, Juz. 79 uk. 21. 983   Twibbul-Aimmat, uk. 86. 984   Twibbul-Aimmat, uk. 94. 985   Twibbul-Aimmat, uk. 86. 986   Twibbul-Aimmat, uk. 87. 981 982

215

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 215

8/10/2017 1:22:10 PM


TIBA YA MAASUMINA

NDOA Mtume (s.a.w.w) amesema: “Enyi kongamano la vijana, yule anayeweza miongoni mwenu kufanya tendo la ndoa basi naaoe kwani ndoa inainamisha macho, na inahifadhi tupu. Na yule ambaye hatoweza basi afunge kwani huko kunakata matamanio.”987 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: Yule ambaye mwanawe amefikia umri wa kuoa, na anacho cha kumuozea mke na hakumuozea, kisha akafanya jambo basi dhambi ni juu yake.”988 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Ndoa ni katika sunna yangu, basi yule ambaye asiyeitendea kazi sunna yangu hayuko nami, basi oeni hakika mimi ni mwenye kujifaharisha nanyi kwa umma mbali mbali.”989 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Mja anapooa kwa hakika anakuwa amekamilisha nusu ya dini yake, basi amche Mwenyezi Mungu katika nusu iliyobaki.”990 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Chagueni kwa ajili ya maji ya uzazi, hakika wanawake wanazaa wanaofanana na kaka zao na dada zao.”991 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Ole wenu kuoa wapumbavu, hakika kuongozana nao ni balaa, na watoto wao ni wapotevu.”992 Imepokewa kutoka kwa Abu Said Khudri amesema: Mtume (s.a.w.w) alimuusia Ali bin Abi Twalib (a.s) akasema: “Ewe Ali… mzuie bibi harusi katika saba yake ya kwanza kutokana na vitu hivi   Twibbu Nabawi, uk. 195 cha Ibn Qaym Jawziyyat.   Kanzul-Ummal, hadithi 44403. 989   Kanzul-Ummal, hadithi 44408. 990   Kanzul-Ummal, hadithi 44403. 991   Kanzul-Ummal, hadithi 44557. 992   Biharul-Anwaar, Juz. 103 uk. 237. 987 988

216

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 216

8/10/2017 1:22:11 PM


TIBA YA MAASUMINA

vinne: kutokana na kula ubani, siki, Kuzbara na tufaha chachu. Ali (a.s) akasema: Ewe Mtume, kwa ajili gani nimzuie yeye hivi vitu vinne? Akasema: Hakika mfuko wa uzazi unakuwa tasa na unakuwa baridi kwa vitu hivi kutokana na utungaji wa uzauzito…” *Ali (a.s) akasema: “Ewe Mtume (s.a.w.w) siki inazuia nini? Akasema: Akiwa na hedhi juu ya siki hatotoharika Abadani kwa ukamilifu, kuzbar inatia nuru hedhi tumboni mwake na inakaza juu yake uzazi, na tufaha la ugwadu linakata hedhi yake na hilo linakuwa ni ugonjwa kwake.”993 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Rakaa mbili anazoziswali mtu aliyeoa ni bora zaidi kuliko rakaa sabini anazoziswali asiyeoa.”994 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Jibrail aliteremka kwa Mtume (s.a.w.w) akasema: “Ewe Muhammad, hakika Mola Wako anakusalimia na anasema: Hakika mabikira miongoni mwa wanawake ni kama vile tunda juu ya mti, likiiva basi hakuna dawa ila ni kuchumwa, na kama si hivyo litaharibiwa na jua na kubadilishwa na upepo, na hakika mabikira wanapofikia yale wanayofikia wanawake, hakuna dawa ila wanaume…”995

MAFUTA YA KULA (NA ZAYTUNI) Faida zake: Yanazingatiwa mafuta ya zaituni kuwa na maada ya shahamu ya chakula, na yanatumiwa kwa baadhi ya magonjwa ya mfumo wa mmeng’enyo wa chakula. Vivyo hivyo yanazingatiwa ni miongoni   Ikhtiswaswi, uk. 132 cha Mufiid.   Biharul-Anwaar, Juz. 103 uk. 219. 995   Biharul-Anwaar, Juz. 16, uk. 223. 993 994

217

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 217

8/10/2017 1:22:11 PM


TIBA YA MAASUMINA

mwa mamilioni kwa ajili ya utumbo wa mwili wa binadamu. Na huzingatiwa mafuta haya ni dawa muhimu kwa yule ambaye figo zake hazifanyi kazi vizuri. Vivyo hivyo yanatumiwa mafuta ya zaituni kama vile mafuta ya nje kwa ajili ya mwili, namna ambayo inaelezwa kutibu kwamba ni yenye kutuliza vigao mbali mbali vyenye uvimbaji wa ngozi, na katika maradhi ya Eczema na mengineyo, kwani ni mazuri na yenye kuneemesha ngozi.996 Na uondoaji wa vijiwe ambavyo vipo katika figo au nyongo, na yanachukuliwa mafuta ya zaituni pamoja na juisi ya limao kila siku kabla ya kula chochote, basi mafuta yanalainisha vijiwe na Himswu inavipondaponda na kuviyeyusha. Na hakika nimeona pindi nilipokuwa mwalimu katika (Tolkilakh) mtu mwenye umri mkubwa alikuwa akija kila siku na kikombe kidogo cha kahawa, akijaza nusu yake mafuta, kisha inakamuliwa juu yake limao, na anaitingisha kisha anakunywa hiyo kabla ya kula kitu. Na alikuwa mtu huyu pamoja na wembamba wa mwili wake lakini ni mwenye nguvu zaidi kuliko vijana, miongoni mwa yale yanayojulisha juu ya dawa hii ni kimaumbile nayo ni kubwa zaidi ya nyenzo zenye kuchangamsha mwili na kuutia nguvu. Hadithi: Mtume (s.a.w.w) amesema: “Ni juu yenu kula miti ambayo Mwenyezi Mungu ameizungumza kwayo Musa bin Imran, mafuta ya zaituni basi jipakeni kwayo, hakika ndani yake kuna ponyo la bawasiri.” Na akasema: Kuhusiana na zaituni Mwemyezi Mungu (a.j) anasema: “Na mti unatoka…kwa walaji.” (mafuta ni ya zayt).997 Ime  Majmu’atul-Athaar, Juz. 2, uk. 333 cha Imam Ridha (a.s).   Aqdul-Fariid, Juz. 7, uk. 265.

996 997

218

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 218

8/10/2017 1:22:11 PM


TIBA YA MAASUMINA

pokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Zaituni yanafukuza harufu na yanaongeza maji.”998 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Jipakeni mafuta, na yafanyeni mchuzi na chakula, kwani ni mafuta ya watu wema na mchuzi wa wateule. Imefutwa kwa baraka katika sehemu mbili kutokana na Qur’ani, imebarikiwa mbele, na nyuma. Na hayadhuru pamona nayo ugonjwa.999”1000 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Ni juu yenu mafuta, kwani yanafichufua kibofunyongo na yanaondoa balungi na yanakaza mishipa na yanaondoa machovu na kufanya vizuri tabia na yanapendezesha kinywa na yanaondoa majonzi.”1001 Aliulizwa Imam as-Sadiq (a.s) kuhusiana na mtu ambaye amevunjika mikono yake na miguu yake, je, ajitibu? Akasema: “Ndio, kwa samli na mafuta.”1002 Imepokewa kutoka kwa Muhammad bin Muslim kutoka kwa Imam Baqir au As-Sadiq (a.s) amesema; Nilimuuliza kuhusu mahramu amevunjika mikono yake? Akasema: ‘Aipake kwa mafuta au samli au kwa haalat.”1003 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Hayakuwa mafuta ya kujipaka kwa wa mwanzo ila zayt.”1004 - Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Alikuwa Amirul-Muuminina Ali (a.s) akifanana na Mtume (s.a.w.w) kuliko watu   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 282.   Umepatikana utajo wa mti wa mzaituni kwa utohara na baraka na utakatifu katika sehemu nne katika Qur’ani nazo ni: Katika Surat An-aam aya 99, Surat Nuru aya 35, Surat Abasa aya 29 na aya ya kwanza ya Surat Tiin. 1000   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 71. 1001   Biharul-Anwaar, Juz. 66, uk. 179, kutoka kitabu Sahifatul-Ridha uk. 57. 1002   Twibbul-Aimmat, uk. 75 cha Abdullah Shubbar. 1003   Twibbul-Aimmat, uk. 75 cha Abdullah Shubbar. 1004   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 72. 998 999

219

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 219

8/10/2017 1:22:11 PM


TIBA YA MAASUMINA

wote kwa chakula chake. Alikuwa akila mkate na siki na mafuta, na akiwalisha wanawake mkate na nyama.”1005 Imepokewa kutoka kwa Is-haq bin Ammar amesema: Nilimwambia Imam as-Sadiq, wanasema: Zaituni inachochea harufu! Basi akasema: Hakika zaituni inafukuza harufu.”1006 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Zaituni inaongeza katika maji ya mgongo ya mwanaume, yaani manii.”1007 Imepokewa pia kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Siki na zayti ni miongoni mwa chakula cha Waislamu (na katika hadithi: Mitume.)”1008- Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Sio fukara nyumba ambayo kuna siki na zayt.”1009 Imepokewa kutoka kwa Khalid bin Najiih amesema: Nilikuwa ninafuturu pamoja na Maimamu wawili As-Sadiq na Kadhim (a.s) katika mwezi wa Ramadhani, kilikuwa kitu cha kwanza kikiletwa kwake ni chungu kilichowekwa ndani yake siki na zayt, na kilikuwa kidogo alichokuwa akila ni matonge matatu, kisha akiletewa jufnat.”1010 Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) amesema: “Yalikuwa kati ya ambayo nabii Adam (a.s) alimuusia Hibatullah (a.s): Kula zaituni, kwani hilo ni miongoni mwa miti na yenye baraka.”1011 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Mtume (s.a.w.w) alisema kumwambia Ali (a.s) katika wosia wake kwake:   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 64 kutoka kitabu Furuu al-Kaafi, Juz. 6, uk. 328.   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 72 kutoka kitabu Furuu al-Kaafi na Mahasin. 1007   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 73. 1008   Biharul-Anwaar, Juz. 66, uk. 304. 1009   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 65. 1010   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 63. 1011   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 72 kutoka kitabu Furuu al-Kaafi na Mahasin. 1005 1006

220

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 220

8/10/2017 1:22:11 PM


TIBA YA MAASUMINA

“Ewe Ali, juu yako zayt, yale na jipake kwayo, hakika yule anayekula na kujipaka hayo hatomkaribia shetani kwa muda wa siku 40.”1012 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Neema ya chakula ni zayt, inafanya uzuri tendo la ndoa, na inaondoa kikohozi, na inasafisha rangi, na inakaza mishipa na inaondoa maumivu, na inazima ghadhabu.”1013 Mkunazi Imepokewa kutoka kwa Imam Sadiq (a.s) amesema: “Osheni vichwa vyenu kwa maji ya mkunazi, kwani ameyatukuza kila malaika mkaribu na kila Nabii Mtume, na yule atakayeosha kichwa chake kwa majani ya mkunazi Mwenyezi Mungu atamuondolea yeye wasi wasi wa shetani siku sabini, na yule ambaye Mwenyezi Mungu atamuondolea yeye wasi wasi wa shetani kwa siku sabini hatakuwa muasi, na yule ambaye hatomuasi ataingia peponi.”1014

Sahifatul-Ridha (a.s), uk. 78.   Makarimul-Akhlaq, uk. 190. 1014   Rawdhatul-Waidhiina, uk. 308 cha Ibn Naysabuuri. 1012 1013

221

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 221

8/10/2017 1:22:11 PM


TIBA YA MAASUMINA

SADHABU Wasifu wake: Huo ni mmea unakaribiana na mti wa mkomamanga, na majani yake yanakaribiana na majani ya su’tar, nayo ladha yake ni ya uchungu kweli, na harufu yake inachukiza. Faida zake: Faida za sadhabu ni nyingi zenye kustaajabisha: Ulaji wake unaongeza katika nguvu ya tendo la ndoa, na harufu yake inamnufaisha aliyepandwa na jini na maumivu ya kichwa katika hali hiyo, hasa hasa ikiwa ya rutwab.1015 Na Ibn Sina katika kitabu chake Qanun amesema: Sadhabu rutwab ya moto yabisa, na juisi yake iliyochemshwa katika majani ya komamanga ikidondoshewa matone yake sikioni basi inalisafisha, na yanatuliza maumivu na ugongaji na duwiy, inaua wadudu, na inapakwa juu ya vidonda vya kichwani, na inafanya macho yawe makali, hasa hasa juisi yake pamoja na juisi ya raaziyanji (shummar) na asali, kujipaka kama wanja na pia kwa kula.1016 Na inatumiwa sadhabu ili kutia nguvu ukuta wa mshipa wa damu mwepesi, kama vile maada za kiharusi na baridi yabisi (Rheumatism), na ukosefu wa hamu ya kula. Hadithi: Mtume (s.a.w.w) amesema: “Yule anayekula sadhabu na akalala juu yake, atalala mwenye amani kutokana na ugonjwa, na dabiila, na mwenye janaba.”1017   Ajaaibul-Makhluqaatm, mwishoni mwa kitabu Hayaatul-Hayawaan, Juz. 3, uk. 189.   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 189 cha Majlisi. 1017   Firdausi. 1015 1016

222

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 222

8/10/2017 1:22:11 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Sadhaabu ni nzuri kwa ugonjwa wa sikio.”1018 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Yule anayekula sadhabu na akalala juu yake atapata amani kutokana na kizunguzungu.”1019 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Sadhabu inaongeza katika akili, isipokuwa inaharibu maji ya mgongo.”1020 Watoto wawili wa Bastwam wamesema: Kwa maumivu ya sikio inachukuliwa sadhabu, inapikwa kwa mafuta ya kula, na inadondoshwa matone ndani yake, hakika maumivu yatatulia kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.1021

KIKOHOZI Rejea mada ya Shummar: (Raaziyanji) Mtume (s.a.w.w) amesema: “Msichukie manne; Ugonjwa wa macho kwani unakata mizizi ya upofu, mafua kwani yanakata mizizi ya mbalanga, sua’li kwani inakata mizizi ya kiharusi na majibu kwani yanakata mizizi ya ukoma.”1022 Maamuni alihutubia katika msikiti wa Marwan, basi akawakuta zaidi ya watu wa msikiti wanasumbuliwa na kikohozi. Akasema mwisho wa hutuba yake: Yule ambaye anasumbuliwa na kikohozi, basi ajitibie kwa siki, basi wakafanya hivyo Mwenyezi Mungu akawaponya.1023   Makarimul-Akhlaq, uk. 180.   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 300. 1020   Makarimul-Akhlaq, uk. 180. 1021   Twibbul-Aimmat, uk. 73. 1022   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 301. 1023   Mustatrifu, Juz. 2, uk. 349 cha Abshiihay. 1018 1019

223

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 223

8/10/2017 1:22:11 PM


TIBA YA MAASUMINA

Su’d Wasifu wake: Ni mmea maarufu, iko mingi Misri, na inaoteshwa majumbaji na huitwa Rayhan Qiswar, nao una majani mapana mazghab, wenye matawi membamba, ni kiungo chenye kutumika kwayo mizizi yake wenye kifua kikuu. Na katika kitabu Tadhkirat: Su’d kwa irabu ya [U] maarufu, nao kwa asili unafanana na Karaath, ila huo ni mwembamba zaidi na mrefu zaidi. Na ndani yake una manufaa mengi katika vidonda ambavyo vimekuwa ni vigumu uponaji wake. Na kwa kikohozi ni mmea mzuri, una mzizi chini ya ardhi mweusi na wenye harufu nzuri. Faida zake: Ni aina ya kihindi kwa huo unakausha uvimbe na vipele, na unafaa kutokana na uchafu wa pua na mdomo na ung’oaji na unaongeza katika hifidhi sana, na unanufaisha vidonda vya mdomo wa vilaji. Unaonda vimawe na kuvizungusha, na unanufaisha kutokana na utokaji matone wa haja ndogo na udhaifu kibofu cha mkojo sana… nao ni wenye kunufaisha sana kutokana na kuumwa kwa nge na wadudu wengine. Hadithi: Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Ichukueni Su’d kuwa ni dawa ya meno yenu, kwani inafanya kinywa kuwa kizuri, na inaongeza katika kujamiana.”1024   Khiswal, Juz. 1, uk. 63 na Kaafi, Juz. 6, uk. 379.

1024

224

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 224

8/10/2017 1:22:11 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) amesema: “Yule anayetumia Su’d kustanjia baada ya kujisaidia haja kubwa, na akaosha kwayo mdomo wake baada ya kula, hautomsibu ugonjwa wa mdomo, na hatohofia chochote kutokana na harufu za bawasiri.”1025 Imepokewa kutoka kwa Abu Wilaad amesema: Nilimuona baba Hasan wa kwanza Imam Musa Kadhim (a.s) katika jiwe, na akiwa wamekaa pamoja naye watu wa nyumbani kwake kadhaa, basi nikamsikia akisema: Meno yangu yaliuma basi nikatumia suu’d na nikafikisha kwenye meno yangu, basi ikanifaa hiyo na yakatulia maumivu yangu.”1026 Imepokewa kutoka kwa Ibrahim bin Nidham (au Bastam), akasema: Walinichukua mimi wezi, na wakaweka mdomoni mwangu kiharusi ya moto hadi ilipoiva, kisha baada ya hivyo wakanikusanyia barafu, yakadondoka meno yangu na magego yangu. Basi nikamuona Imam Ridha (a.s) msingizini, nikamlalamikia yeye hilo, akasema: “Tumia su’d, kwani yataota meno yako.” Na pindi nilipobebwa na kupelekwa Khurasani basi ikanifikia habari kwamba yeye anapita kwetu, basi nikaenda kumpokea na nikamsalimia, na nikamwelezea hali yangu, kwamba mimi nilimuona usingizini, na akaniamrisha kutumia su’d, akasema: Mimi ninakuamrisha katika hali ya kuwa upo macho. Basi nikaitumia, basi yakarejea meno yangu na magego yangu kama yalivyokuwa.1027 Imepokewa kutoka kwa Ibrahim bin Bastam kuwa meno yake yalianguka, basi akamuamrisha yeye Imam Ridha (a.s) atumie su’d, akaitumia hiyo basi yakareja meno yake na magego yake kama yalivyokuwa hapo kabla.1028   Kaafi, Juz. 6, uk. 378 cha Kulaini.   Kaafi cha Kulaini. 1027   Twibbul-Aimmat, uk. 363 cha Abdullah Shubbar. 1028   Makarimul-Akhlaq, uk. 218. 1025 1026

225

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 225

8/10/2017 1:22:11 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Ibrahim bin Bilaad amesema: Alinichukua Abbas bin Musa akaamrisha kutokana na maumivu ya magego yangu basi yakatetemeka meno yangu, wala sikuweza kutafuna chakula. Basi akamuona usingizini baba wa Shaybat Khurasani, akamwambia yeye: Yakaze kwa su’d, basi nikasukutua kwa su’d, basi yakatulia meno yangu.1029 SU’TWI (NUSHUUQU) Imepokewa kutoka kwa Imam Baqir (a.s) amesema: “Kitu bora ambacho mnajitibia kwacho ni uingizaji wa bomba la maji sehemu za haja kubwa na ufyonzaji wa damu mwilini na bafu.”1030 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Miongoni mwa dawa za manabii ni; Ufyonzaji wa damu mwilini, unyoaji wa nywele na unusaji.”1031 Imepokewa kutoka kwa Ali bin Yaqtwin amesema: Nilimwandikia Imam Ridha (a.s): hakika mimi ninakuta baridi kali kichwani kwangu, hadi ukivuma upepo nilikaribia kuzimia, basi akaniandikia: “Ni juu yako kutumia unusaji wa ambari na yasimini baada ya chakula, utapona ugonjwa huo kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (a.j).”1032 Su’twi inaleta afya ya kichwa, na ni ponyo ya mwili na maumivu mengine ya kichwa.1033

Kaafi, Juz. 6, uk. 379 cha Kulaini.   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 57. 1031   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 57. 1032   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 87. 1033   Tuhfu uk. 72. 1029 1030

226

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 226

8/10/2017 1:22:11 PM


TIBA YA MAASUMINA

PERA Khawasi zake: Pera ni baridi yabisi, linatofautiana katika hilo kwa utofauti wa ladha yake. Na ulaji wa hilo baridi lenye kushika, ni zuri kwa mfuko wa chakula. Na ni tamu hilo lenye baridi kidogo na yabisi, na linaegemea kwenye ulinganifu. Na la ugwadu linashika zaidi na yabisi na baridi. Faida zake: Linatuliza kiu na utapikaji, linazungusha haja ndogo, linatia akili ya maumbile, na linaharakisha katika upunguzaji wa uzito, na kuunguza matawi yake na majani yake yenye kuoshwa, kama vile madini meupe katika kitendo chake.1034 Hadithi: Imepokewa kutoka kwa Zubeir kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Kula pera, kwani ndani yake kuna mambo matatu. Akasema: Ni yapi hiyo Ewe Mtume(s.a.w.w)? Akasema: Inakusanya kifua, mtu bakhili anakuwa mtoaji, na muoga anakuwa shujaa.”1035 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Ni juu yenu kula pera, kwani hilo linaongeza mafuta na linaondoa maumivu makali ya kifua na linamfanya mtoto kuwa mzuri.”1036 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Kuleni pera na linaleta upole baina yenu, kwani linasafisha macho, na linaotesha   Twibbu Nabawiy, uk. 247 cha Ibn Jawziyyat.   Khiswal, Juz. 1, uk. 157 cha Saduuq. 1036   Makarimul-Akhlaq, uk. 172. 1034 1035

227

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 227

8/10/2017 1:22:11 PM


TIBA YA MAASUMINA

mapenzi moyoni. Na walisheni wake zenu wajawazito kwani hilo linafanya watoto kuwa wazuri. (na katika hadithi) linafanya tabia za watoto wenu kuwa nzuri.”1037 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Ulaji wa pera unaondoa giza la macho.”1038 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Harufu za mitume (a.s) ni harufu za pera, na harufu za Hurul-Aini ni harufu ya Aasi, na harufu za malaika ni harufu za waridi, na harufu ya binti yangu Fatuma Zahraa (a.s) ni harufu ya pera, Aasi na waridi, wala hakumtuma Mwenyezi Mungu nabii wala wasii ila alikutwa akiwa na harufu ya pera, basi kuleni hilo na walisheni wajawazito wenu kwani linawafanya watoto wenu kuwa wazuri.”1039 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Ulaji wa pera unaongeza nguvu kwa mwanaume na kunaondoa udhaifu.”1040 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Harufu ya pera ni harufu ya Mitume.”1041 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Niliingia siku moja kwa Mtume (s.a.w.w) na mkononi kwake akiwa na pera, na akawa anakula na ananilisha mimi, na huku akisema: Kula ewe Ali, kwani hilo ni zawadi ya Mola muumba kwangu na kwako, akasema: Bali nikakuta ndani yake kila ladha. Akasema kuniambia mimi: Ewe Ali, ulaji wa pera kwa muda wa siku tatu kabla ya kula chochote unasafisha ubongo na unajaza tumbo upole na elimu, na unakinga wigo na Ibilisi na jeshi lake.”1042   Biharul-Anwaar, Juz. 66, uk. 177, na Makarimul-Akhlaq, uk. 172.   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 296. 1039   Makarimul-Akhlaq, uk. 172. 1040   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 136. 1041   Makarimul-Akhlaq, uk. 172. 1042   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 132, kutoka kitabu Uyuun Juz. 2, uk. 73 chapa ya Qum. 1037 1038

228

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 228

8/10/2017 1:22:11 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Ulaji wa pera unatia nguvu moyo uliyodhoofika, na unafanya vizuri mfuko wa chakula, na unaleta uerevu wa moyo, unamfanya muoga kuwa shujaa na unafanya mtoto kuwa mzuri.”1043 Na kuhusiana na hilo amesema mshairi Ibn Aasim katika utenzi wake: Na katika pera imepokewa hadithi – wanakula hilo wajawazito basi mtoto anakuwa mzuri Na ulaji wake unamtia ushujaa muoga – kama vile unatia nguvu moyo na upole Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Ulaji wa pera unatia nguvu moyo, uerevu wa moyo na unamtia ushujaa muoga.”1044 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Ulaji wa pera kabla ya kula chochote yatakuwa mazuri maji yake na kufanya mtoto kuwa mzuri.”1045 Imepokewa pia kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Yule anayekula pera Mwenyezi Mungu atamtamkisha yeye hekima juu ya ulimi wake kwa siku 40.”1046 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Pera linaondoa majonzi ya mwenye huzuni, kama vile mkono unavyofuta jasho la paji la uso.”1047 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Juu yenu kula pera, kwani linaongeza katika akili na murua.”1048   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17 uk. 129, kutoka kitabu Furuu na Mahasin.   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 131. 1045   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 131 cha Hurru Aamili. 1046   Wasaail- Shi’ah, Juz. 17, uk. 126 , kutoka kitabu Furuu na Mahasin. 1047   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 131, kutoka kitabu Furuul-Kaafi. 1048   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17 uk. 131, kutoka kitabu Mahasin cha Barqi. 1043 1044

229

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 229

8/10/2017 1:22:11 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: ‘Matunda matano ya peponi yapo hapa duniani; komamanga malaysi, tufaha shashaai, pera, zabibu na tende mashan.”1049 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Peasi linalainisha mfuko wa chakula, na linautia nguvu, na pera pia.”1050 Imepokewa kutoka kwa Twalha bin Zayd kutoka kwa Imam asSadiq (a.s) amesema: “Hakika pera lina mambo sita katika matunda mengine! Nikasema: Ni yapi hayo Ewe Mtume (s.a.w.w)? akasema: Linamfanya muoga kuwa shujaa. Na naapa kwa Mwenyezi Mungu hili linatokana na elimu ya manabii (a.s).”1051 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Pera linapendezesha uso na linakusanya kifua.”1052 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Ni juu yako ulaji wa pera tamu pamoja na punje zake, kwani linamtia nguvu mdhaifu, linafanya mfuko wa chakula kuwa mzuri na linatakasa moyo.”1053 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Alikuwa Ja’far bin Abi Twalib (a.s) mbele ya Mtume (s.a.w.w), basi akampa zawadi Mtume (s.a.w.w) ya pera, akakata hilo Mtume (s.a.w.w) kipande na akampatia Ja’far, basi akakataa kula. Mtume (s.a.w.w) akasema: “kula kwani hilo linatakasa moyo na linamtia ushujaa muoga. (Na katika hadithi): “Kula kwani hilo linasafisha ngozi na linafanya mtoto kuwa mzuri.”1054   Khiswal, Juz. 1, uk. 289.   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 134. 1051   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 136. 1052   Wasaail-Shi’ah, uk. 301. 1053   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 136. 1054   Kaafi, Juz. 5, mlango wa kuchagua mke. 1049 1050

230

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 230

8/10/2017 1:22:12 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kwamba siku moja alimwangalia kijana mzuri akasema: “Inapaswa kuwa baba yake huyu kijana amekula pera.”1055

SUKARI (ya mawe) Maana yake: Inadhihiri katika baadhi ya maneno yao kwamba sukari ya mawe ni maarufu kama sukari ya mimea. Na kwa mujibu wa hadithi mbali mbali ni kuwa hiyo ni Qinde (sukari ya mawe), nayo ni sukari ya miwa ambayo tunaitumia kwa chai. Na inaitwa twabazaz – nalo ni neno la kifarsi lenye irabu – kanbisat kwa twabari nalo ni shoka, kana kwamba nyuso zake zenye kung’ara kwa hakika ni kama zimepondwa kwa shoka (kamusi Muhiit). Hadithi: *Alikuwa Ali Amirul-Muuminina (a.s) akitumia kwa homa kiwango cha dirham ya sukari kwa maji ya baridi kabla ya kula chochote.1056 Imepokewa kutoka kwa Zurara kutoka kwa Imam Baqir (a.s) amesema: “Ole wako ewe Zurara, hawajaghafilika watu kutokana na fadhila ya sukari ya mawe, nayo inanufaisha magonjwa sabini, nayo inakula kikohozi kabisa, na inaking’oa kwa mizizi yake.”1057 Alikuwa Imam as-Sadiq (a.s) akitoa sadaka ya sukari, akaulizwa yeye kuhusu hilo? Akasema: “Hakuna kitu kutokana na chakula kinachonipendeza mimi kuliko hiyo, na mimi ninapenda nitoe sadaka vitu ambavyo navipenda zaidi.”1058   Kaafi, Juz. 6, mlango wa yale ambao ni mustahabu kumlisha mjamzito.   Safinatul-Bihar, Juz. 1, uk. 636. 1057   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 67. 1058   Ramzul-Sihat, uk. 209 cha Dahsurkhi. 1055 1056

231

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 231

8/10/2017 1:22:12 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Ibn Abi Umeir, imenyanyuliwa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Mtu mmoja alimlalamikia kuhusu homa, akamwambia: Na upo wapi wewe na kizuri chenye baraka! Ni kipi hicho kizuri chenye baraka? Akasema: Sulaimani wenu huyu, akasema Imam as-Sadiq (a.s): Hakika ni wa kwanza aliyechukua sukari ya Sulaiman bin Daud (a.s).1059 Imepokewa kutoka kwa Ibn Asbaat kutoka kwa Yahya bin Bashir Nabal, amesema Abu Abdillah as-Sadiq (a.s): “Ewe Bashir ni kitu gani mnatumia kutibu wagonjwa wenu? Akasema: Hizi dawa za uchungu. Akasema: Hapana, akiumwa mmoja wenu basi chukua sukari nyeupe na isage kisha itie ndani ya maji baridi na mnyweshe huyo, hakika ambaye amefanya ponyo katika vichungu ni muweza alifanye katika vitamu.”1060 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: ‘Ikiwa jibini inadhuru kula kitu, wala hainufaishi chochote, basi hakika sukari inanufaisha kila kitu wala haidhuru kitu.”1061 Imepokewa kutoka kwa Ali bin Nuuman kutoka kwa baadhi ya masahaba wetu amesema: Nilimlalamikia baba wa Abdillah asSadiq (a.s) maumivu, akasema: “Unapotaka kulala basi kula sukari mbili” akasema: Basi nikafanya hivyo nikapona, na nikawapa habari hiyo baadhi ya waganga, na alikuwa ni mmoja wa waganga bingwa katika mji wetu. Akasema: Abu Abdillah (a.s) amejua kutoa wapi hili. Hili linatoka katika hazina ya elimu yetu? Ama hakika yeye mtunzi wa vitabu inapasa kuwa alilipata hilo katika baadhi ya vitabu vyake.1062   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 80 na kinachofanana nacho.   Ramzul-Sihat, uk. 32 kutoka kitabu Mahasin. 1061   Wasaail-Sh’ah, Juz. 17, uk. 76. 1062   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 79. 1059 1060

232

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 232

8/10/2017 1:22:12 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) amesema: “Yule anayechukua sukari mbili wakati wa kulala, itakuwa ni ponyo kwake la kila ugonjwa ila sumu (kifo).”1063 Mua Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) amesema: “Vitu vitatu havidhuru; zabibu raazaqi, mua na tufaha la Lebanoni.”1064 Imepokewa pia kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) amesema: “Mua unafungu kizibo,1065 wala hakuna ugonjwa ndani yake wala madhara.”1066

MCHADI Faida zake: Ibn Sina amesema: Juisi ya mchadi inaondoa (wart) na inaua chawa, na inaosha kwayo kichwa basi inaondosha kumvi (utando kama ukoko kichwani) na ueneaji wa nywele. Hadithi: Imepokewa kutoka Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Hakika Mwenyezi Mungu aliwaondolea mayahudi mbalanga, kwa ulaji wao wa mchadi, na ukataji wa mizizi yake kutokana na nyama na kutokuila.”1067   Makarimul-Akhlaq, uk. 168.   Khiswal, Juz. 1, uk. 144 cha Saduuq. 1065   Amesema katika kitabu Bahrul-Jawahir: SADAD katika lugha: takayuri ya jicho. Na katika matibabu ni hali ya kubakia mtu pamoja na utokeaji wake ghafla anakuta katika kichwa chake uzito mkubwa, na katika macho yake giza, na huenda mlio wa sauti sikioni kwake, na huenda ikaondoka pamoja nayo akili yake. Na akasema: Sadaa kwa wake na uzito inabana katika mapito na misuli yenye kubana, na hubakia ndani yake, inazuia chakula na uchafu wa vyakula kupenya ndani yake. 1066   Makarimul-Akhlaq, uk. 168. 1067   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 158. 1063 1064

233

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 233

8/10/2017 1:22:12 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Hakika watu miongoni mwa wana wa Israili walipatwa na weupe, basi Mwenyezi Mungu akamfunulia Musa (a.s) kwamba waamrishe wao kula nyama ya ng’ombe kwa mchadi.”1068 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kwamba alisema kumwambia mmoja wa masahaba wake: “Ni juu yako kutumia mchadi, kwani unaota juu ya ufukwe wa Firdausi, na ndani yake kuna matibabu kutokana na madawa, nao unanenepesha mifupa na unaiotesha nyama. Na lau usingeliguswa na mikono ya waovu lingelikuwa jani linalositiri wanaume.”1069 Na katika hadithi nyingine amesema (a.s): “Inakata akili na inasafisha damu.”1070 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Msiache tumbo lako tupu bila chakula, na uchache kutokana na unywaji wa maji wala halikusanyiki ila kutokana na hamu ya tendo hilo, na neema ya mboga mboga ni mchadi.”1071 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Walisheni wagonjwa wenu mchadi – yaani majani yake – hakika ndani yake kuna matibabu, wala hakuna ugonjwa wala madhara kwake, na unatuliza usingizi wa mgonjwa. Na jiepusheni mzizi wake kwani unachochea weusi.”1072 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Hakika mchadi unakata mirija ya mbalanga, na hakijaingia tumboni mfano wa mubarsim mfano wa jani la mchadi.”1073

Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 158.   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 159. 1070   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 159. 1071   Makarimul-Akhlaq, uk. 181. 1072   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 157, kutoka kitabu Furuu Kaafi. 1073   Kaafi cha Kulauni. 1068 1069

234

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 234

8/10/2017 1:22:12 PM


TIBA YA MAASUMINA

SUMU Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuhusiana na tende amesema: “Hakika ndani yake kuna matibabu ya sumu, kwani hiyo haina ugonjwa ndani yake wala madhara.”1074 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Tende Ujwat inatoka peponi, na ndani yake kuna matibabu ya sumu.”1075 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Tende Ujwat Barni inatoka peponi, nayo ni matibabu ya sumu.”1076

ULEZI Faida zake: Ibn Sina amesema: Majani yake na juisi ya mti wake unarefusha nywele, nayo inanufaisha kutokana na kipanda uso, kunywa na kujipaka, na inanenepesha mno. Na ule uliyolowekwa unakoroga hedhi. Na uliokaangwa unaongeza katika nguvu ya tendo la ndoa na chembe chembe asili ya manii.1077 Hadithi: Alikuwa Mtume (s.a.w.w) akinusa mafuta ya ulezi pindi kikiuma kichwa chake. Ibn Baytwar amesema: Juljulaan ni ulezi, nao uko wa aina mbili nyeupe na nyeusi.1078   Furuul-Kaafi juz. 6 uk. 349, kitabu Mahasin uk. 532 cha Barqi.   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 109. 1076   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 195. 1077   Ajaaibul-Makhluqaat cha Qazwiini, mwishoni mwa kitabu Hayaatul-Sahaba, Juz. 2, uk. 189. 1078   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 143, kutoka kitabu Qurbul-Isnaad. 1074 1075

235

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 235

8/10/2017 1:22:12 PM


TIBA YA MAASUMINA

USIKIVU Rejea (sikio) Mtume (s.a.w.w) amesema: “Tende… inaongeza katika usikivu na uonaji.”1079 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuhusiana na nyama amesema: “Hakika hiyo inaongeza katika usikivu na uonaji.”1080 SAMAKI Mtume (s.a.w.w) amesema: “Msile kilichowindwa cha majusi ila samaki.”1081 Alikuwa Mtume (s.a.w.w) hakusanyi pamoja baina ya maziwa na samaki.1082 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Punguzeni ulaji wa samaki, hakika nyama yake inafanya mwili kusinyaa, inazidisha balgham na inafanya nafsi kuwa ngumu.”1083 Imepokewa vilevile kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Samaki aliyepakwa mafuta anayeyusha nyama.”1084 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Msidumishe ulaji wa nyama, kwani hiyo inayeyusha mwili.”1085 Imepokewa pia kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Punguzeni ulaji wa nyama ya samaki, kwani hiyo inayeyusha mwili, inazidisha kikohozi na inafanya nafsi kuwa ngumu.”1086   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 107.   Biharul-Anwaar, Juz. 62 uk. 280. 1081   Ramzu Sihat, uk. 10. 1082   Twibbu Nabawiy, uk. 173 cha ibn Qaym Jawziyyat. 1083   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 18 na kinachofanana nacho. 1084   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 56. 1085   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 56. 1086   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 56. 1079 1080

236

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 236

8/10/2017 1:22:12 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema AmirulMuuminina Ali (a.s): “Utakapompata samaki, haujui ni mzuri zaidi au sio mzuri (hapa inakusudiwa amechinjwa kisheria au hapana, na uchinjaji wake ni kumtoa majini akiwa hai na anakufa kwenye hewa) basi mtumbukize majini, akielea juu ya maji hali amelala chali juu ya mgongo wake basi huyo sio mzuri, na akilalia juu ya uso wake basi huyo mzuri.”1087 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Ukila samaki basi kunywa juu yake maji.”1088 Na imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Yule anayelala hali ya kuwa tumboni mwake mna samaki, na hakufuatilizia kwa kula tende au asali litaendelea jasho la kiharusi likipiga juu yake mpaka anapoamka asubuhi.”1089 Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) amesema: “Nyama inaotesha nyama, na samaki anayeyusha mwili.”1090 Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) amesema: “Samaki aliyepakwa mafuta anayeyusha mwili.”1091 Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) amesema: “Samaki aliyepakwa mafuta anayeyusha mafuta ya macho mawili.”1092 Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) amesema: “Ni juu yenu ulaji wa samaki, hakika ulaji wake bila ya mkate unakutosha, na ikiwa utamla kwa mkate ni mzuri zaidi.”1093   Wasaail-Shi’ah, Juz. 16, uk. 341.   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 54. 1089   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 54. 1090   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 57. 1091   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 54. 1092   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 54. 1093   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 54, kutoka kitabu Furuu, Juz. 6, uk. 323 na Mahasin uk. 475. 1087 1088

237

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 237

8/10/2017 1:22:12 PM


TIBA YA MAASUMINA

SAMLI Mtume (s.a.w.w) amesema: “Nyama ya ng’ombe ni ugonjwa, samli yake ni ponyo, na maziwa yake ni dawa, na hakijaingia kitu tumboni kama vile samli.”1094 Na imepokewa pia kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuhusiana na hadithi ya Suhayb amesema: “Ni juu yako kutumia maziwa ya ng’ombe kwani hayo ni ponyo, na samli yake ni dawa na nyama yake ni ugonjwa.”1095 Imepokewa kutoka kwa Amirul-Muminina Ali (a.s) amesema: “Nyama ya ng’ombe ni ugonjwa, maziwa yake ni dawa na samli yake ni ponyo.”1096 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Mtu akifikia umri wa miaka 50 wala asilale hali ya kuwa tumboni mwake kuna kitu kutokana na samli (yaani asile kabla ya kulala chakula ambacho ndani yake kuna samli.”1097 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Neema ya mchuzi ni samli, na hakika mimi ninaichukia hiyo kwa mzee, akasema: Nayo katika kiangazi ni bora kuliko katika masika.”1098

JINO NA MENO Rejea (KHALAL) na (usafishaji wa meno kwa mswaki). Mtume (s.a.w.w) amesema: “Ufyonzaji wa damu kichwani unaondoa usinziaji, na maumivu ya magego.”1099 Na imekuja katika hadithi: “Hakika ulaji barafu unaondoa utafunwaji wa meno.”1100   Ramzul-Sihat, uk. 214 Dahsurkhi.   Twibbu Nabawiy, uk. 250 cha Ibn Qaym Jawziyyat. 1096   Mustadrakul-Nahj, uk. 162. 1097   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 82. 1098   Biharul-Anwaar, Juz. 66, uk. 88. 1099   Biharul-Anwaar, Juz. 66, uk. 88. 1100   TTwibbul-Aimmat (a.s), uk. 361 cha Abdullah Shubbar. 1094 1095

238

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 238

8/10/2017 1:22:12 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa: Hakika ulaji wa komamanga unaomdoa harufu ya kinywa na tundu la jino, hasa hasa pamoja na mafuta yake.1101 Imepokewa kutoka Muhammad bin Muslimu amesema: Nilimuona baba wa Ja’far Imam Baqir (a.s) akitafuna ubani, basi akasema: Ewe Muhammad! Umevunjika mshipa wa magego yangu, na nikatafuna ubani huu ili niyakaze. Imepokewa kutoka kwa Ja’fari amesema: Nilimsikia baba wa Hasan Musa Kadhim (a.s) akisema: Dawa ya gego: Unachukua hindhala utaimenya hiyo, kisha utatoa mafuta, hakika likiwa gego lenye kuliwa limetoboka, atadondoshea ndani yake matone, na inafanywa kwayo katika pamba ndogo, na anafanya katika tumbo la gego, na analala chali mhusika, na anachukua kwa mausiku matatu.” *Katika barua ya dhahabu ya Imam Ridha (a.s): Hakika nzuri zaidi istakta kwayo ili nikuone, kwani hiyo inafanya meno kuwa mazuri, na inafanya uzuri tendo la ndoa na inakaza ufidhi na inakuza hilo, nayo ni yenye kunufaisha kutokana na kuchimbika ikiwa katika hali ua ulingano, na uzidishaji wa hiyo unaupa wepesi meno na unatikisa hilo na unadhoofisha mizizi yake. *Katika barua ya dhahabu ya Imam Ridha (a.s) imekuja: “Na yule anayetaka meno yake yawe meupe basi achukue sehemu kidogo ya chumvi ya Unduraani, na mfano wake takataka za bahari, basi aisage hadi iwe laini, na inanenepesha hiyo. *Na amesema (a.s): “Na yule anayetaka yasiharibike meno yake, basi asile utamu ila baada ya uvunjaji wa mkate.”1102 - Na upikaji wa kitunguu saumu na uchomaji wake unatuliza maumivu ya meno, na usukutuaji kwa kile kilichopikwa unafaa pia maumivu ya jino, na hasa hasa kikichanganywa na ubani.1103   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 363 cha Abdullah Shubbar.   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 368 cha Abdullah Shubbar. 1104   Qanun, uk. 50 cha Ibn Sinaa. 1101 1102

239

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 239

8/10/2017 1:22:12 PM


TIBA YA MAASUMINA

SANAMAKI (MAKIY) Maana yake: Sanamaki ni mmea wa mti unaotokana na conea, ua la manjano, na punje zake muflathu nyepesi, umbo lake ni la kuluwisi. Majani yake na maua yake yanatumika kwa kujitibia. Na mzuri zaidi ni wa Saudia, na Unajulikana kwa jina la Sanamaki Makkiy. Nayo iko ya aina mbili: Sanamaki ya Iskandari, nayo ina jani la kasiya, rahmiyat na nyeupe, na Sanamaki ya India, nayo ni kisiya mstatiri. Na jani la Sanamaki la rangi ya kijani ni nzuri zaidi na lina harufu hafifu na ladha ya utamu. Na inawezekana kutoa ule ukhususia wa Sanamaki kwa utumiaji wa maji baridi au ya moto. Na inazingira juu ya mfanyaji wepesi, inatengana juu ya umbo la maada nyekundu na manjano iliyokoza fuwele, na juu kidogo kutokana na mafuta ya ndege. Faida zake: Umayya bin Abi Swilt amesema: Sanamaki ni la ujoto yabisi katika daraja la kwanza, linafanya wepesi kibofunyongo manjano na kibofunyongo nyeusi, na kikohozi, na linazamisha ndani kabisa ya viungo, na kwa hivyo linanufaisha munqarisina, na jasho la wanawake, na maumivu ya sehemu za muunganiko wenye kuzuka kutokana na mchanganyiko wa kibofunyongo ya manjano na kikohozi. Khawasi zake (mambo yake mahasusi): Sanamaki mushilu inaongeza harakati za kidudu kwenye utumbo, na inaongeza uchafu wa utumbo kidogo, na inafanya kazi katika utumbo mwembamba zaidi kuliko mnene. Na hakika inaleta ugonjwa wa ghafla na kukakamaa na inapangilia Sanamaki mara nyingi pamoja 240

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 240

8/10/2017 1:22:12 PM


TIBA YA MAASUMINA

na chumvi yenye kufanya wepesi mengine, mfano wa chumvi ya Uingereza na twaratwat ya potasiamu. Na inatoa Sanamaki katika hali za mapigo ya moyo na maradhi mengine ya kuogofya. Wala haifai utoaji wake ikiwa njia ya umeng’enyaji ni mbaya. Uandaaji wake: Mchanganyiko wa Sanamaki (nyeusi) unapangika kutokana na: Sanamaki iliyosagwa (7) na kuzbara iliyosagwa (3) na Tiini (12) na tende ya India (9) na Lubbu Kisiya: tango shunbar (9) na Khukh kavu (6) na Rubbu Suus (2 ya 4) na sukari (30) na maji muqtwir (24) na unywaji wake ni gram 4 na kuendelea. Hadithi: Mtume (s.a.w.w) amesema: “Lau kutakuwa katika kitu matibabu basi yangekuwa katika Sanamaki.”1104 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Jitibieni kwa Sanamaki kwani ingelikuwa kitu kinarudisha kifo basi Sanamaki kingelirudisha.”1105 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) alimwambia Asmaa bint Umais: “Kwa kitu gani ulikuwa ukijitibia kutokana na unywaji wa Mus-hil katika zama za ujinga?” Akasema: Kwa shubrum. (istimshaau: Unywaji wa mus-il). Akasema: Ni ya joto ya joto (au ya joto Yaar). Kisha akasema: Tulikuwa tunatumia kwa Sanamaki. Akasema: Lau hakika kama kuna kitu kinachorudisha Qadar basi ni Sanamaki.”1106 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Lau watu watajua yale yaliyomo ndani ya Sanamaki wangelifikia mith  Ramzul-Sihat, uk. 18. ,   Qurbul-Isnaad, uk. 70. 1106   Aqdul-Fafiid, Juz. 6, uk. 272 cha Ibn Abdu Rabbih, na Juz. 7, uk. 264. 1104 1105

241

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 241

8/10/2017 1:22:12 PM


TIBA YA MAASUMINA

qal kwayo mithqal mbili ya dhahabu. Ama hakika hiyo ni amani ya bahaq, ukoma, mabalagha, wendawazimu, kiharusi na ukosefu wa nguvu, na inachukuliwa pamoja zabibu nyekundu ambayo haina kokwa, na inafanya pamoja nayo Halaylij ya Kaabul ya manjano na nyeusi viungo sawa, na inatumiwa asubuhi kabla ya kula chochote dirham tatu, na pindi unapotaka kulala mfano wake, nayo ni bwana wa madawa.”1107

Usafishaji meno kwa mswaki Maelezo yake: Unafanya meno kuwa meupe ukitumiwa mswaki ukiweka juu ya yasimini iliyosagwa, na zu’tar iliyosagwa iliyochanganywa kwa mkaa wa Huru nyeusi. Au usugue meno kwa juisi ya limao usugue meno hayo kwa kipande cha mlimao. Hadithi: Mtume (s.a.w.w) amesema: “Matano yanaondoa usahaulifu na yanaongeza katika hifidhi, na yanaondoa kikohozi: Usafishaji meno, funga, usomaji wa Qur’ani, asali na ubani (yaani kundur).1108 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Ewe Ali katika usafishaji meno kuna mambo 12 nayo ni; sunna, unatoharisha kinywa, unasafisha macho, unamridhisha Mola Mlezi aliyetukuka, na unamuumiza shetani, na unatia hamu chakula, na unaondoa kikohozi na unazidisha katika hifidhi, na unaongeza mema na unawafurahisha malaika.”1109   Makarimul-Akhlaq, uk. 214 cha Twabarasi.   Makarimul-Akhlaq, uk. 166 kutoka kitabu Firdausi. 1109   Biharul-Anwaar, Juz. 76, uk. 129, kutoka kitabu Khiswal, Juz. 2 uk. 481 cha Saduuq. 1107 1108

242

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 242

8/10/2017 1:22:12 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Safisheni njia ya Qur’ani, ikaulizwa: Kwa kitu gani” akasema: kwa usafishaji meno.”1110 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Safisheni meno kwa mswaki kwa njia ya mapana na sio kwa marefu.”1111 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Usafishaji meno ni sehemu ya imani.”1112 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Usafishaji meno una mambo 10; Unatoharisha kinywa, unamridhisha Mola Mlezi, unaongeza mema mara sabini, nayo ni sunna na unaziba matobo, unafanya meno kuwa meupe, unakaza ufidhi, unakata kikohozi, unaondoa kizibo cha macho na unatia hamu ya kula.”1113 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesma: “Neema ya usafishaji meno ni kwa mti wa mzaituni wenye baraka, unaondoa matobo juu ya meno nao ni usafishaji meno wangu na usafishaji wa manabii wa kabla yangu.”1114 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) katika wosia wake kwa Ali (a.s) amesema: “Ewe Ali ni juu yako usafishaji wa meno kila unapotia wudhuu.”1115 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Aliendelea Jibrail akiniusia usafishaji meno, mpaka nikadhani anafanya hilo kuwa ni faradhi.”1116   Biharul-Anwaar, Juz. 76, uk. 130.   Biharul-Anwaar, Juz. 76, uk. 139. 1112   Makarimul-Akhlaq, uk. 49. 1113   Khiswal, Juz. 2, uk. 449. 1114   Makarimul-Akhlaq, uk. 49. 1115   Makarimul-Akhlaq, uk. 49. 1116   Biharul-Anwaar, Juz. 76, uk. 126. 1110 1111

243

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 243

8/10/2017 1:22:12 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Jibrail (a.s) aliteremka kwa Mtume (s.a.w.w) akiwa na mswaki, kichokoa meno na njia ya ufyonzaji damu mwilini.”1117 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Manne ni moingoni mwa sunna za Mitume ni; Usafishaji meno, upakaji hina, manukato na wanawake.”1118 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema; “Kila kitu kina tohara, na tohara ya kinywa ni usafishaji meno.”1119 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: Hakika Mtume (s.a.w.w) amesema: “Lau sio kutowafanyia uzito umma wangu ningeliwajibisha usafishaji meno kila wakati wa swala.”1120 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Usafishaji meno unasafisha uonaji wa macho, unaotesha nywele na unaondoa machozi.”1121 Imam Ridha (a.s) akimwandikia Maamuni katika barua ya dhahabu alisema: “Na jua ewe Amirul-Muuminina hakika linalokufaa zaidi ni Liif Arak, kwani hiyo inapendezesha meno, inaleta harufu nzuri ya kinywa, na inakaza ufizi. Nayo ina manufaa zaidi katika kuzuia utobokaji wa meno ikiwa itatumiwa kwa ulinganifu. Na kuzidisha matumizi yake kunadhoofisha meno na kuyatingisha pamoja na fizi zake, na yule anayetaka meno yake yawe meupe basi achukue sehemu ya chumvi andarani, na sehemu ya zubadulbahari, basi azisage hizo mbili hadi zilainike, na apige mswaki kwazo.”1122   Wasaail-Shi’ah, Juz. 16, uk. 532.   Makarimul-Akhlaq, uk. 41. 1119   Makarimul-Akhlaq, uk. 49. 1120   Fiqhul-Ridha (a.s), uk. 137. 1121   Makarimul-Akhlaq, uk. 50, nakutoka kitabu Twibbul-Aimmat (a.s). 1122   Biharul-Anwaar, Juz. 32, uk. 317. 1117 1118

244

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 244

8/10/2017 1:22:12 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Jipakeni ghibba… na pigeni mswaki kwa mapana.”1123 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Upigaji wa mswaki unamridhisha Mola mlezi, na unafanya mdomo uwe mzuri, nayo ni miongoni mwa sunna.”1124

SAWIIQ Maana yake: Ni chakula kinachotengenezwa kutokana na ngano iliyosagwa na shairi, imeitwa kwa jina hilo kutokana na inavyopita kooni, na inawezekana kutengenezwa kwa vitu saba; ngano, shairi, nabaq (tunda la mti wa mkunazi) na tufaha na qur’u, punje za komamanga na ghubayraa. HADITHI: Imepokewa kutoka kwa Imam Zaynul-Abidina (a.s) amesema: “Lowesheni tumbo la mwenye homa kwa sawiiq na asali mara tatu, na unaigeuza chupa moja hadi nyingine na ananyweshwa mwenye homa, kwani inaondoa homa ya joto, na imefanywa kwa ufunuo.”1125 Imepokewa kutoka kwa Imam Baqir (a.s) amesema: “Hakuna kitu chenye baraka zaidi kama sawiiq, mtu akiinywa juu ya shibe inafanya uzuri mmeng’enyo wa chakula, na mtu akiinywa akiwa na njaa basi atashiba, na neema ya masurufu ya safarini na hali sio ya safari ni: Sawiiq.”1126   Fiqhul-Ridha (a.s), uk. 407.   Tuhful Uquul, uk. 72. 1125   Makarimul-Akhlaq, uk. 192. 1126   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 67. 1123 1124

245

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 245

8/10/2017 1:22:12 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Sawiiq kavu inaondoa weupe (yaani ukoma na weupe wa jicho).1127 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Unywaji wa sawiiq kwa mafuta huotesha nyama na unakaza mifupa, na unafanya ngozi kuwa nyororo na unaongeza nguvu katika tendo la ndoa.”1128 Imepokewa kutoka kwa Imam Sadiq (a.s) amesema: “Hakika sawiiq kavu ikitumiwa asubuhi kabla ya kula kitu huzima joto, na hutuliza kibofunyongo, na ikichanganywa pamoja na maji kidogo au mafuta au samli kisha akanywa haifanyi hivyo.”1129 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Sawiiq inaondoa kibofunyongo na kikohozi kutoka kwenye mfuko wa chakula, na inakinga aina sabini za mabalaa.”1130 Imepokewa kutoka kwa Ibn Abi Kathir amesema: Tumbo langu lilikuwa na maradhi ya kuharisha basi Imam as-Sadiq (a.s) akaniamrisha mimi nichukue sawiiq Jawurus (nayo ni dukhun na kutokana na sifa zake kuwa ni kali na yenye kushika) kwa maji ya komoni. Nikasema: Basi tumbo langu likashika na nikapona.1131 Imepokewa kutoka kwa Khidhri amesema: “Nilikuwa kwa Imam as-Sadiq (a.s) akajiwa na mtu miongoni mwa masahaba wetu, basi akamwambia: Anazaliwa kwetu mtoto basi anakuwa na ugonjwa na udhaifu, akasema (a.s): “Kipi kinachokuzuia kutumia sawiiq, kwani hiyo inakaza mifupa na inaotesha nyama.”1132   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 67.   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 9. 1129   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 67. 1130   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 6. 1131   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 101, kutoka kitabu Furuu Kaafi. 1132   Wasaail-Shi’ah, Juz.7, uk. 7. 1127 1128

246

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 246

8/10/2017 1:22:12 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Wanywesheni watoto wenu sawiiq udogoni mwao, hakika hilo linaotesha nyama na linakaza mifupa, na yule atakayekunywa sawiiq kwa siku 40 asubuhi yatajaa nguvu mabega yake.”1133 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Matatu ni raha (yaani kamshaat) sawiiq kavu kabla ya kula kitu, inasafisha kibofunyongo na kikohozi, mpaka isikaribie kuacha kitu.”1134 Imetajwa sawiiq kwa Imam as-Sadiq (a.s), akasema: “Hakika imefanywiwa kazi na ufunuo.”1135 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Sawiiq ni chakula cha mitume (au alisema) chakula cha manabii (a.s).”1136 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Sawiiq ikinywewa basi inanufaisha ugonjwa wowote na kwa manufaa yaliyokusudiwa kwayo.”1137 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Neema ya chukula ni sawiiq, ikiwa unanjaa utashiba, na ukiwa umeshiba kitaleta mmeng’enyo wa chakula chako.”1138 Ilitajwa nyama na mafuta mbele ya Mtume (s.a.w.w) akasema: “Hakuna kati ya hivyo viwili sehemu inaingia katika mfuko wa chakula, ila itaotesha mahali pake ponyo, na itaondoa kutoka sehemu yake ugonjwa.”1139   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 7.   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 8, kutoka kitabu Furuu, Juz. 6, uk. 306. 1135   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 6. 1136   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 6. 1137   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 7. 1138   Kaafi, cha Kulayni. 1139   Sahifatul-Ridha (a.s), uk. 75, na kitabu Da’awat Raawandiy. 1133 1134

247

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 247

8/10/2017 1:22:13 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuhusiana na mafuta ya kujipaka amesema: “Hulainisha ngozi, yanaongeza katika akili na ubongo, na yanafanya wepesi njia ya maji, na yanaondosha ukungu, na yanang’arisha rangi.”1140 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Yule anayekula tonge la mafuta, litateremka mfano wake ugonjwa.”1141 Imepokewa kutoka kwa Zurara: “Nikasema kumwambia Imam as-Sadiq (a.s): Nafsi yangu nimeitoa fidia kwako, mafuta yapi ambayo hutumiwa kwa ajili ya dawa? Akasema: Hiyo ni shahmat ya ng’ombe. Ewe Zurara hajaniuliza yeyote hilo kabla yako.”1142 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuhusiana na ng’ombe amesema: “Maziwa yake ni dawa, na mafuta yake ni ponyo na nyama yake ni ugonjwa.”1143 Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) amesema: “Nyama inaotesha nyama, na yule ambaye anaingiza tumboni mwake tonge la mafuta linatoa mfano wake miomgoni mwa magonjwa.”1144

NYWELE Rejea (unyoaji wa nywele) na (uchanaji ­nywele) Mtume (s.a.w.w) amesema: “Matano ni katika maumbile; Jando, unyoaji wa nywele za kinenani, na utoaji wa nywele za kwapani, ukataji wa kucha na upunguzaji wa masharubu.”1145   Khisal, Juz. 610 cha Saduq.   Makarimul-Akhlaq, uk. 159. 1142   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 29. 1143   Ramzul-Sihat, uk. 221, kutoka kitabu Makarimul-Akhlaq. 1144   Makarimul-Akhlaq, uk. 159, na Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 29. 1145   Sahihi Bukhari, Juz. 7, uk. 137 Maktabat Nahdhat Hadithi Makka mwaka 1376. 1140 1141

248

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 248

8/10/2017 1:22:13 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Mtakapoingia mji na jamii husika na mkahofia homa yake, basi ni juu yenu kula kitunguu chake, kwani hicho kinasafisha uonaji na kinasafisha nywele.”1146 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Punguzeni masharubu na ziacheni ndevu wala msijifananishe na mayahudi.”1147 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Jipakeni hina, kwani inasafisha uonaji, inaotesha nywele, inaleta harufu nzuri na inamtuliza mke.”1148 Imepokewa kutoka kwa Sulaiman bin Khalid amesema: Nilimwambia Imam as-Sadiq (a.s): Mwanamke anajaalia kichwani kwake nywele bandia? Akasema: “Inaruhusiwa za sufi, na zinazotokana na mwanamke mwenyewe. Na ni karaha kuunganisha mwanamke nywele zingine (na katika hadithi nyingine): Hakika nywele zake ni maiti.”1149 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Hakika chini ya kila unywele kuna janaba.”1150 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Tiini inaondosha harufu ya kinywani, inakaza mifupa na inaotesha nywele…”1151

[MKATE] WA SHAIRI Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Mtume (s.a.w.w) hakula mkate burri katu, wala hakushiba kutokana na mkate wa shairi katu.”1152   Ramzul-Sihat, uk. 144, kutoka kitabu Firdausi.   Makarimul-Akhlaq, uk. 67. 1148   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 309 cha Abdullah Shubbar. 1149   Makarimul-Akhlaq, uk. 84. 1150   Fiqhul-Ridha (a.s), uk. 83. 1151   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 133. 1152   Wasaail-Shi’ah, Juz. 16, uk. 409. 1146 1147

249

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 249

8/10/2017 1:22:13 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Lau Mwenyezi Mungu angeliiona katika kitu kingine ponyo kuliko shairi basi asingelifanya kuwa chakula cha manabii (a.s).”1153 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Iliendelea shairi kuwa chakula cha Mtume (s.a.w.w) mpaka Mwenyezi Mungu alipoichukua roho yake.”1154 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Kilikuwa chakula cha Mtume (s.a.w.w) ni shairi na haluwa ya tende na mchuzi wake ni mafuta ya kula.”1155 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Fadhila ya mkate wa shairi juu ya ngano ni kama vile fadhila yetu kwa watu, na hakuna nabii ila alimuombea mlaji wa shairi na akaibariki juu yake, na haikuingia tumboni ila inaondoa kila ugonjwa ndani yake, nayo ni chakula cha manabii na chakula cha watu wema, Mwenyezi Mungu aliyetukuka amekataa kujaalia chakula cha manabii ila shairi.”1156 Na katika hilo mshairi Ibn Aasim katika utenzi wake amesema: Kilicho bora zaidi yake ni mkate wa shairi – basi huo ni chakula cha fukara mwenye kukinai Haujaingia tumboni katu ila huondoa – kutokana na kila ugonjwa nao ni chakula cha manabii Kwake juu ya ngano ni bora katika nafaka – kama vile watu wa nyumba ya Mtume katika watu wengine

Makarimul-Akhlaq, uk. 154.   Ramzul-Sihat, uk. 223 cha Dahsurkhi. 1155   Makarimul-Akhlaq, uk. 154 1156   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 4, na Makarimul-Akhlaq, uk. 154. 1153 1154

250

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 250

8/10/2017 1:22:13 PM


TIBA YA MAASUMINA

MAJI YA SHAIRI Maana yake: Yanatengenezwa kutokana na shairi nzuri iliyopondwa (mardhudhu), na maji safi matamu mara tano ya kiwango cha shairi, na inawekwa katika chombo kisafi, na inapikwa kwenye moto wa kawaida, hadi ibakie moja ya tano, na isafishwe na itumiwe kwa kwa kadiri ya mahitaji. Faida zake: Maji ya shairi yananufaisha kwa ugonjwa wa kikohozi na ugumu wa koo, yanafungua njia za haja ndogo, yanasafisha mfuko wa chakula, yanakata kiu, yanazima joto. Yanaimarisha nguvu na kuchangamsha.1157 Hadithi: Imepokewa kutoka kwa Aisha amesema: Alikuwa Mtume (s.a.w.w) mmoja wa watu wa familia yake anapopatwa na joto kali, anaamrisha kuletewa maji ya shairi basi na kutengeneza, kisha anawaamrisha wanaitumia dawa hiyo. Kisha akasema: “Hakika dawa hiyo inatia nguvu kifua cha mwenye huzuni, na inafichua maradhi ya kifua cha mgonjwa, kama anavyodhihirisha mmoja wenu uchafu kwa maji kutoka kwenye uso wake.”1158 Kipandauso Imepokewa katika sunna kwamba Mtume (s.a.w.w) aikuwa akijitibu kwa ufyonzaji wa damu katikati ya kichwa chake kutokana na kipandauso kilichompata.1159   Twibbu Nabawiy, uk. 254 cha Ibn Qaym Jawziyyat.   Twibbu Nabawiy, uk. 254 cha Ibn Qaym Jawziyyat. 1159   Sahihi Bukhari, Muslim na Nasaai. 1157 1158

251

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 251

8/10/2017 1:22:13 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Osheni mikono yenu baada ya kutoka kwenu bafuni (huenda yeye anakusudia kwa maji ya baridi) kwani hayo yanaondoa kipandauso…”1160 Imam Ridha (a.s) katika barua yake ya dhahabu kwa Maamuni amesema: “Na unapotaka kuingia bafuni, na usipate kichwani kwako yale yanayokuudhi basi anza kabla ya kuingia huko kwa magao matano ya maji ya uvuguvugu, hakika wewe utasalimika kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu na maumivu ya kichwa na kipandauso. Na inasemekana: ni magao matano ya maji ya uvuguvugu unamwagia kichwani kwako wakati wa kuingia bafuni.”1161 Na imekuja ndani yake: “Na yule anayehofia kipandauso na shuswa (ugonjwa wa njia ya hewa), wala asicheleweshe ulaji wa samaki safi kiangazi au masika.1162

SHAMARI (MBEGU ZA RAAZIYANJI) Faida zake: Inafaidisha shamari kwa mwenye kifua na pumu na ubanaji wa punzi, na inafungua na kuondoa maumivu ya upande na mfuko wa chakula, na inatibua haja ndogo na hedhi, na inasafisha kibofu cha mkojo na maumivu ya kichwa, na inateketeza vijiwe vya kende. Ibn Sina katika Qanun kitabu cha tatu amesema: Na ama vitu ambavyo vinanufaisha utumiaji wake kwa jicho na vinahifadhi nguvu zake, basi vitu vyenye kuchukuliwa wanja na aina ya madini nyeupe murabba kwa njia ya marzunjushi na maji ya   Makarimul-Akhlaq, uk. 55.   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 322. 1162   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 324. 1160 1161

252

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 252

8/10/2017 1:22:13 PM


TIBA YA MAASUMINA

raaziyanji. Na upakaji nyusi kila wakati kwa maji ya raaziyanji kwa hakika kuna ajabu kubwa na yenye kunufaisha.1163 Hadithi: Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) amesema: “… toshekeni na bwana huyu wa madawa; Haliyliji, raaziyanji na sukari” (rejea homa).1164 Imepokewa kutoka kwa Muhammad bin Abdul-Salam akasema kumwambia Imam Ridha (a.s) amesema: Ninakulalamikia kikohozi kikali, basi akasema: “Je, mpya au ya kale?” nikasema yote mawili. Akasema: “Chukua pilipili nyeupe juzuu, abrifium juzuu mbili, kharbaqa nyeupe juzu moja, na kutokana na bangi juzuu, na utachunga kwa kitambaa na unachanganywa kwa asali mbichi mfano wa kipimo chake, na inatumiwa kwa ajili ya kikohozi cha hapo kabla na cha sasa kwayo punje moja kwa maji ya raaziyanji wakati wa kulala, na yawe maji ya uvuguvugu sio ya baridi, kwani inaing’oa kutoka katika mizizi yake.”1165 NURU YA JUA Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: Mtume (s.a.w.w) amesema: “Juani kuna mambo manne; linabadilisha rangi, harufu mbaya, linakausha nguo na linasababisha ugonjwa.”1166 Imepokewa kutoka kwa Amirul-Muminina Ali (a.s) amesema: “Msilielekee jua kwani hilo linaleta harufu mbaya kinywani, kufifia ngozi, linaozesha nguo na linadhihirisha ugonjwa uliyojificha.”1167   Ramzul-Sihat, uk. 51 cha Dahsurkhi.  Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 99. 1165   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 86. 1166   Khiswal, Juz. 1, uk. 249. 1167   Khiswal, Juz. 1, uk. 97. 1163 1164

253

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 253

8/10/2017 1:22:13 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Mmoja wenu akikaa juani basi alielekezee mgongo wake. Kwani hilo linadhihirisha ugonjwa uliyojificha.”1168 Imam Ali (a.s) alimuona mtu mmoja amekaa juani, akasema: “Simama toka juani” kwani hilo linasababisha harufu mbaya kinywani, linatoa harufu mbaya, na linaozesha nguo, na linadhihirisha ugonjwa uliyojificha [yaani jua linadhihirisha ugonjwa uliojificha mwilini, ambao umetweza maumbile.]1169” HAMU NA KUTAMANI Imepokewa kutoka kwa Ibn Abbas kwamba Mtume (s.a.w.w) alimtembelea mwanaume mmoja akamwambia: “Unatamani nini? Akasema: Ninatamani mkate wa Burri. Mtume (s.a.w.w) akasema: Yule aliyenao mkate wa burri basi ampelekee nduguye. Kisha akasema: Mmoja wenu atakapokuwa na hamu ya kitu fulani basi mpatieni ale.”1170 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Kula unapokuwa wewe na hamu, na acha kula unapokuwa na hamu.”1171 Imepokewa pia kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Muumini anakula kwa hamu ya familia yake, na mnafiki familia yake wanakula kwa hamu yake.”1172 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Hazijazidi nywele za mwanaume katu, ila inapungua akili yake.”1173 Wamedhani: Hakika yule anayekata mtazamo wake juu ya nasisa wakati   Tuhful-Uquul, uk. 76.   Dastuur Maalimlil-Hikam, uk. 102 cha Qadhaiy. 1170   Twibbu Nabawiy, uk. 84 cha Ibn Qaym Jawziyyat. 1171   Ramzul-Sihat, uk. 4 cha Dahsurkhi. 1172   Ramzul-Sihat, uk. 5 cha Dahsurkhi. 1173   TwibbulAimmat (a.s), uk. 443. 1168 1169

254

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 254

8/10/2017 1:22:13 PM


TIBA YA MAASUMINA

wa kufanya tendo la ndoa hukata matamanio yake kabisa wala hayatoki.”1174 Mvi Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Watu walikuwa hawazeeki, basi akaonekana nabii Ibrahim (a.s) na mvi katika ndevu zake, akasema: Ewe Mola Wangu mlezi ni kitu gani hiki? Akasema: Hii ni heshima. Akasema: Ee Mola Wangu mlezi niongezee heshima.”1175 Mtume (s.a.w.w) amesema: “Mvi mbele ya kichwa ni zawadi, na katika mapanda uso ni ukwasi, na kati kati ya kichwa ni ushujaa na kisogoni ni mkosi.”1176 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Mvi ni nuru wala msizinyofoe.”1177 Alikuja mtu mmoja kwa Mtume (s.a.w.w) basi akamwangalia katika ndevu zake, Mtume (s.a.w.w) akasema: “Yule anayekuwa na mvi katika Uislamu basi itakuwa ni nuru kwake siku ya Kiyama.”1178 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Msizinyofoe ndevu kwani ni nuru ya Mwislamu, na yule ambaye atakuwa na mvi katika Uislamu basi itakuwa nuru kwake siku ya Kiyama.”1179 Imepokewa kutoka kwa Amirul-Muminina Ali (a.s) amesema: “Hakika yeye alikuwa haoni tabu kulinda mvi, na akichukia kuzinyofoa.”1180   Ajaaibul-Makhluqaat, mwishoni mwa kitabu Hayaatul-Hayawan, Juz. 2 uk. 197.   Biharul-Anwaar, Juz. 12, uk. 8 1176   Khiswal, Juz. 1, uk. 235. 1177   Makarimul-Akhlaq, uk. 66. 1178   Makarimul-Akhlaq, uk. 66. 1179   Khiswal, Juz. 2, uk. 612. 1180   Makarimul-Akhlaq, uk. 69. 1174 1175

255

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 255

8/10/2017 1:22:13 PM


TIBA YA MAASUMINA

Sabiru Maana yake: Sabiru ni miongoni mwa dawa mashuhuri ya jicho kwa waganga, ulaji wake na kujipaka kwake kwenye nyuso. Faida zake: Ibn Sina katika kitabu chake Qanun amesema: Sabiru inaondoa mabaki ya ugonjwa ambao upo kichwani, na inamnufaisha kutokana na vidonda vya jicho na udhaifu wake na magonjwa yake, na kutokana na maradhi ya upele sehemu ya siri na inakausha unyevunyevu wake.”1181 Hadithi: Imam Kadhim (a.s) amesema kwamba mmoja wa masahaba wake analalamika kuhusu jicho lake akamwambia: “Ni kipi kinakuzuia wewe kujipaka wanja wa Abu Ja’far (a.s): akasema: kipimo kidogo cha Kafuri rabahi, na kipimo kidogo cha mpungate usqutury, vinasagwa vyote na vinachungwa kwa kwa Hariri, anajipaka nyusi kwayo kama vile anavyojipaka wanja…”1182 *Mtu mmoja aliingia kwa Imam as-Sadiq (a.s) naye akilalamika kuhusiana na jicho lake, basi akamwambia: “Uko wapi wewe kuvitumia viungo hivi vitatu; Sabiru, kafuuri na ukakasi? Basi yule mtu akafanya hivyo, na ugonjwa wake ukamuondokea.”1183

Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 148.   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 150, kutoka kitabu Kaafi, Juz. 8, uk. 384. 1183   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 148, kutoka kitabu al-Kaafi, na Twibbul-Aimmat (a.s) uk. 83. 1181 1182

256

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 256

8/10/2017 1:22:13 PM


TIBA YA MAASUMINA

Afya ya mwili Katika wosia wa Mtume (s.a.w.w) kwa Abu Dharri amesema: “Neema mbili ni hasara ndani ya hizo mbili kwa watu wengi; afya na faragha.”1184 (Na katika hadithi nyingine): “Matatu yanafurahisha kwayo mwili na huufanya kuwa mzuri; kujipaka mafuta, mavazi laini na unywaji wa asali.”1185 Imepokewa kutoka kwa Usbugh bin Nubatat amesema: Nilimsikia Amirul-Muuminina Ali (a.s) akisema kumwambia mwanawe Hasan (a.s): Ewe mwanangu je, nikujulishe mambo manne ambayo utatosheka kwayo na matibabu? Akasema: Ndio, ewe AmirulMuminina. Akasema: Usikae ili kula hali ya kuwa wewe umeshiba, na simama hali ya kuwa wewe unakitamani, na tafuna vizuri na nenda msalani kabla ya kulala, na ukifanya haya hautohitajia matibabu.” Na akasema: “Hakika ndani ya Qur’ani ipo aya inakusanya yote inasema: “Na kuleni (vizuri) na kunyweni (vizuri) wala msipite kiasi.”1186, 1187 Imepokewa kutoka kwa Amirul-Miminina Ali (a.s) amesema: “Mimi ninamdhamini yule ambaye anayesema Bismillah juu ya chakula chake, hatosumbuliwa na chochote.” Ibnul-Kuwa1188 akamwambia: Ewe Amirul-Muuminina, hakika nimekula jana chakula nikasema Bismillah na kikaniletea maudhi. Akasema: “Huenda wewe umekula aina mbali mbali, na ukasema Bismillah kwa baadhi na haukusema kwa vingine, ewe mpumbavu.1189   Makarimul-Akhlaq, uk. 459.  Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 295. 1186   Sura 7 aya 31. 1187   Khiswal cha Saduq na kitabu Mustadrakul-Nahj, uk. 162. 1188   Naye ni Abdillah bin al-Kuwa, ni mtu aliyejitoa aliyelaaniwa. 1189   Makarimul-Akhlaq, uk. 143. 1184 1185

257

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 257

8/10/2017 1:22:13 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Amirul-Muminina Ali (a.s) amesema: “Jikingeni na ubaridi mwanzoni mwake na ipokeeni mwishoni mwake, kwani inafanya katika miili kama vile inavyofanya katika miti, mwanzo wake inaunguza na mwisho wake inatoa majani.”1190 Imepokewa kutoka kwa Amirul-Muminina Ali (a.s) amesema: “Afya ya mwili ni kutokana na uchache wa husda.”1191 Imepokewa kutoka kwa Amirul-Muminina Ali (a.s) katika tafsiri ya kauli yake (s.w.t) inayosema: “Kisha utaulizwa siku hiyo neema zote.”1192 akasema: “Ni neema ya amani, afya na uzima.”1193 Imepokewa kutoka kw a Amirul-Muminina Ali (a.s) amesema: “Ninashangaa mghafiliko wa mahasidi kutokana na usalama wa miili.”1194 Imepokewa kuwa Imam Ali (a.s) amesema: “Anayetaka kuwa na afya nzuri, atafune vizuri chakula, ale juu ya usafi, anywe maji akiwa na kiu, apunguze unywaji wa maji, arefushe kikao baada ya kula, na atembee kidogo baada ya kula chakula cha usiku, wala asilale ila baada ya kwenda msalani, na ajihadhari kuingia bafuni baada ya kujaa tumbo, na kibofunyongo wakati wa kiangazi ni bora mara kumi kuliko wakati wa masika, na ulaji wa nyama kavu (yaani nyama iliyo kaushwa) usiku inasaidia kuisha, na kufanya tendo la ndoa na ajuza linazeesha umri wa waliohai, na hufanya wenye afya kuwa wagonjwa.”1195 Pindi alipokaribia kufariki baba wa matibabu kwa waarabu Harith bin Kaladat, basi wakakusanyika kwake watu, wakasema:   Nahjul-Balaaghah, hekima 128.   Nahjul-Balaaghah, hekima 258. 1192   Sura 102 aya 8. 1193   Adabul-Nafsi, Juz. 1, uk. 216 cha Ayshaani. 1194   Twibbu Nabawiy, uk. 319 cha Ibn Qaym Jawziyyat. 1195   Ghurarul-Hikam. 1190 1191

258

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 258

8/10/2017 1:22:13 PM


TIBA YA MAASUMINA

Tuamrishe jambo ambalo tutaishia kwalo baada yako. Akasema: Msioe wanawake ila msichana, wala msile tunda ila linapoiva, wala asijitibu mmoja wenu kwa lile ambalo unategemewa mwili kupatwa ugonjwa, na juu yenu kwa unyoaji wa nywele katika kila mwezi, kwani ni yenye kuyeyusha kikohozi, ni yenye kuangamiza nyongo, ni yenye kuotesha nyama. Na atakapokula mmoja wenu chakula cha mchana basi apumzike saa moja, na akila chakula cha usiku basi atembee hatua 40.1196 Sheikh Abbas Qummi amesema: Haya ni katika yale ambayo niliyoyadondoa kutokana na wosia wa Amirul-Muminina Ali (a.s).1197 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Lau watu watakuwa na matumizi mazuri ya chakula, miili yao ingelisimama vizuri.”1198 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Vitatu haviliwi lakini vinanenepesha, na vitatu vinaliwa lakini vinakondesha. Ama ambayo vinaliwa lakini vinakondesha ni; tende isiyoiva, kasabu na jozi. Na ama ambayo haviliwi lakini vinanenepesha ni; unyoaji wa nywele, kujipaka manukato na kuvaa nguo ya katani.” - Na katika kuhitimisha hadithi: Na viwili vinanufaisha kwa kila kitu wala havidhuru chochote, na hivyo viwili ni sukari na komamanga.1199 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Vitatu vinanenepesha na vitatu vinakondesha. Ama ambavyo vinanenepesha ni; kudumisha kwenda bafuni, kunusa harufu nzuri na kuvaa nguo laini. Na ama ambavyo vinakondesha ni; kudumisha ulaji wa mayai, samaki na ujazaji tumbo kwa chakula.”1200   Twibbu Nabawiy, uk. 319 cha Ibn Qaym Jawziyyat   Twibbu Nabawiy, uk. 319 cha Ibn Qaym Jawziyyat. 1198   Fusuulul-Muhimmat, cha Hurru Aamili. 1199   Wasaail-Shi’ah, Juz. 16, uk. 541, na Makarimul-Akhlaq, uk. 195. 1200   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 4. 1196 1197

259

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 259

8/10/2017 1:22:13 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Unywaji wa maji kwa kusimama mchana ni kunatia nguvu zaidi na kuna afya zaidi kwa mwili (na katika hadithi nyingine): “Kunazungusha jasho na kunatia nguvu zaidi mwili.”1201 Imam as-Sadiq (a.s) alimwambia Anuani Baswari: “Ole wako kula chakula hali ya kuwa huna hamu nacho, kwani kunasababisha upumbavu na ufahamu mdogo, wala usile ila ukiwa na njaa. Na ukila kula cha halali, na sema Bismillah.”1202 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Vitatu vinazeesha mwili na huenda vikaua; ulaji wa nyama yabisi yenye kutoa harufu mbaya, na kuingia bafuni ukiwa umeshiba mno na kukutana kumwili na ajuza.” (Na akaongeza ndani yake Abu Is-haq Nahawandiy: Na kukutana kimwili na wanawake hali ya kuwa tumbo limejaa.)1203 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema; “Afya ni neema iliyojificha, ikipatikana inasahaulika, na inapokosekana inakumbukwa.”1204 Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) amesema: “Matano ni miongoni mwa sunna ya kichwa, na matano ya mwili, na ama ambayo ni ya kichwani; ni upigaji wa mswaki, kukata masharubu, utenganishaji wa nywele, usukutuaji na upandishaji wa maji puani. Na ama ambayo ya mwilini; jando, unyoaji wa nywele za kinenani, unyofuaji wa nywele za kwapani, ukataji wa kucha na kustanji.”1205 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Unapoumwa na njaa basi kula, na utakapokuwa na kiu basi kunywa, na   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 192.   Twibbu Imam Swadiq (a.s), uk. 80 cha Muhammad Khalily. 1203   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 38, kutoka kitabu al-Furuu na Mahasin 1204   Biharul-Anwaar, Juz. 74, uk. 243. 1205   Khiswal, Juz. 1, uk. 271. 1201 1202

260

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 260

8/10/2017 1:22:13 PM


TIBA YA MAASUMINA

ukibanwa na haja ndogo basi jisaidie, wala usifanye tendo la ndoa ila ukiwa na haja, na ukisinzia basi lala, kwani hilo lina maslahi kwa mwili.”1206 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Kichwa cha hekima ni kuendana na mwili.”1207 Imepokewa pia kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “… na uzoeshe mwili wako yale uliyozoea.”1208

MAUMIVU YA KICHWA Aina za maumivu ya kichwa na matibabu yake: Muhammad bin Zakaria katika kitabu (Bardul-Sa’at) amesema: Ikiwa maumivu ya mbele ya kichwa na sehemu inayofuata ya paji la uso, hakika hilo ni kutokana na wingi wa damu. Na matibabu yake atoe kiasi cha damu kwa ufyonzaji wa damu au kupiga chuku, kwani hilo linatuliza mahali hapo, au unanusa kiasi cha Afiun ya Misri nzuri, na aweke puani mwake na shavuni kwake, au achukue kiasi fulani cha zabibu na kinywaji chake, au ale mchuzi wa adesi, au ale kazbara yabisi kidogo, kwani hiyo inatuliza mahali hapo. Na maumivu ya kichwa yanaweza kuwa katikati ya kichwa, na dalili ya hilo ni joto, na tiba yake ni kulowesha kitambaa cha katani kwa mafuta na siki ya pombe, na akiweke juu ya kichwa. Au aloweshe kwa mafuta ya waridi na maziwa ya kijakazi, hakika hilo linatuliza mahali husika. Au anuse naylafar, au ale kiini cha tango ambacho amekiweka katika siki chachu mno, au ale kiasi fulani cha mbegu chachu ambazo zina kawaida ya kuzima umanjano,   Fiqhul-Ridha (a.s), uk. 340.   Fiqhul-Rdha (a.s), uk. 340. 1208   Fiqhu-Ridha (a.s), uk. 340. 1206 1207

261

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 261

8/10/2017 1:22:13 PM


TIBA YA MAASUMINA

kwani kufanya hivyo kunatuliza wakati huo. Au apake chini ya miguu yake mafuta ya banafsaji na chumvi, kwani hiyo inatuliza mahali husika. Kisa kutoka kwa Hajjaj: Miongoni mwa matabibu bingwa na mahiri ni Tayazuq. Hakika Hajjaj alipata kichwani kwake maumivu, basi akatuma aletwe, akamleta kwake, Tayazuq akamwambia Hajjaj: “Osha miguu yako kwa maji ya moto na ipake mafuta.” Wakati huo mmoja wa walinzi wa Hajjaj alikuwa amesimama kichwani kwake, basi akisikia maneno yake, akasema: “Naapa kwa Mwenyezi Mungu sijamuona mtabibu mwenye maarifa kidogo ya tiba kuliko wewe. Kiongozi analalamika kuwa ana maumivu ya kichwa, halafu wewe unamwelekeza dawa ya kuweka katika miguu yake?” Tayazuq akamjibu: “Hakika ishara ya usahihi wa lile nililolisema iko dhahiri ndani yako!” Mlinzi akasema: “Ni ipi hiyo?” Akasema Tayazuq: “Zimeondolewa kende zako mbili basi zikaondoka nywele za ndevu zako.”1209 Hadithi: Mtume (s.a.w.w) amesema: “Hina ni pako la Uislamu, inaongeza kwa muumini amali yake, inaondosha maumivu ya kichwa, na inafanya macho yaone vizuri, na inaongeza katika kujamiana, nayo ni bwana wa harufu nzuri duniani na akhera.”1210 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Hakika Mwenyezi Mungu anapompenda mja anamwangalia, na akimwangalia anampa moja ya mambo matatu; homa, maumivu ya jicho na maumivu ya kichwa.”1211   Majallatul-Irfan, uk. 535 toleo la NIISAAN mwaka 1930.   Ramzul-Sihat, uk. 17. 1211   Makarimul-Akhlaq, uk. 358. 1209 1210

262

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 262

8/10/2017 1:22:13 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Jipakeni nyusi zenu kwa balunji, kwani hiyo inaondoa maumivu ya kichwa.”1212 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Hakika katika habasoda kuna matibabu ya kila ugonjwa, na mimi ninaitumia kwa homa, maumivu ya kichwa, ugonjwa wa macho, ugonjwa wa tumbo, na kila ambalo linanitokea mimi kutokana na maumivu, na Mwenyezi Mungu ananiponya.”1213 Imepokewa kutoka kwa Imam Swadiq (a.s) amesema: “Alikuwa Mtume (s.a.w.w) akinusa mafuta ya ulezi pindi alipougua maumivu ya kichwa.”1214 Alikuja mtu wa Khurasani kwa Imam as-Sadiq (a.s) akamwambia: Ewe mtoto wa Mtume (s.a.w.w) bado ninaendelea kusumbuliwa na maumivu ya kichwa tangu nitoke nyumbani kwangu. Akamwambia: “Simama saa yako hii na ingia bafuni, usianze na kitu mpaka umwagie juu ya kichwa chako magao saba ya maji ya moto, na sema Bismillah aliyetukuka katika kila mara, hakika wewe hautosumbuliwa tena baada ya kufanya hivyo kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu.”1215 Imepokewa kutoka kwa Imam Sadiq (a.s) amesema: “Osha kichwa chako kwa khutwami, ni amani ya maumivu ya kichwa.”1216 Imepokewa kutoka kwa Imam Baqir na as-Sadiq (a.s) kwamba hao wawili walitoka bafuni wakiwa wamevaa vilemba wakati wa masika au kiangazi, na wakawa wanasema: “Hiyo ni amani ya maumivu ya kichwa.”1217   Kaafi, Juz. 6, uk. 522.   Makarimul-Akhlaq, uk. 212. 1214   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 143, kutoka kitabu Qurbul-Isnaad uk. 71. 1215   Twibbul-Aimmat (a.s) uk. 71. 1216   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 333 cha Abdullah Shubbar. 1217   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 334 cha Abdullah Shubbar. 1212 1213

263

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 263

8/10/2017 1:22:13 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Umar bin Ibrahim amesema: Nilimlalamikia Imam Ridha (a.s) kuhusu kibofunyongo nilichokuwa ninakipata, hadi kufikia hali inayofanana na uwenda wazimu na maumivu makubwa ya kichwa. Akasema: “Ni juu yako mboga mboga hii ambapo unayakunja majani yake, basi yaweke hayo juu ya kichwa chako, na waamrishe waweke hayo juu ya vichwa vya watoto wao, kwani hiyo ina manufaa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Akasema: Basi nikafanya hivyo, maumivu yakatulia” na (mboga mboga hiyo ni balaab).1218 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kwamba siku moja aliitisha aletewe hindubaau kwa baadhi ya wenye heshima, na hakika alikuwa akitumia kwa homa na maumivu ya kichwa, basi akaamrisha aisage, kisha aifunge kwenye karatasi, na amwagie juu yake mafuta ya balungi, na aweke hiyo juu ya kichwa chake, kisha akasema: “Ama hakika hiyo inakata homa na inaondoa maumivu ya kichwa.”1219 Na katika kitabu cha Furju bin Salaam: Ikiwa utaingia bafuni basi piga juu ya kichwa chako kwa maji yaliyochemshwa mara saba, kwani kwa hilo utadhihiri usalama kutokana na maumivu ya kichwa kwa uwezo wa Al-Jabbar.

KIFUA: (KILE KITOKACHO KIFUANI) Mtume (s.a.w.w) amesema: “Neema ya kinywaji ni asali, inachunga moyo na inaondoa ubaridi kifuani.”1220 Ibn Sina katika dawa ya kile kiteremkacho kifuani amesema:   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 338 cha Abdullah Shubbar.   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 144, kutoka kitabu Furuul-Kaafi. 1220   Makarimul-Akhlaq, uk. 165. 1218 1219

264

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 264

8/10/2017 1:22:14 PM


TIBA YA MAASUMINA

“Katika mwanzo wa kuteremka damu, na katika – mwisho wa uteremkaji bafuni Baina ya hivyo viwili maji ya shairi kwayo – kuna afya kutokana na kile kiteremkacho mwilini.

Su’tur Rejea (Za’tar) Nyongo ya manjano: Imepokewa kutoka kwa Amirul-Muminina Ali (a.s) amesema: “Juu yenu kutumia nyongo kwa vidonda vya tumbo na inaondoa kikohozi…”1221 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Kuleni bilinganya, kwani ni zuri kwa nyongo nyeusi, wala halidhuru umanjano.”1222 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Sawiiq ya adesi inakata kiu, na inatia nguvu mfuko wa chakula, ndani yake kuna ponyo la magonjwa sabini, na inazima umanjano na inatia ubaridi tumbo…”1223 Imam Ridha (a.s) kuhusiana na maji ya baridi amesema: “Hakika hayo yanazima joto, yanatuliza umanjano na yanafanya mmeng’enyo wa chakula.”1224 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Katika asali kuna ponyo la kila ugonywa. Yule anayelamba asali kabla ya   Sahifatul-Ridha (a.s), uk. 57.   Kashful-Akhtar, cha Shamsu Diin bin Muhammad Huseini – Mahtut. 1223   Makarimul-Akhlaq, uk. 193. 1224   Fiqhul-Ridha (a.s), uk. 346. 1221 1222

265

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 265

8/10/2017 1:22:14 PM


TIBA YA MAASUMINA

kula kitu, inakata kikohozi, inaondoa umanjano na inazuia nyongo nyeusi.”1225 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) katika barua ya dhahabu amesema: “Na yule anayetaka azime mwale wa umanjano, basi ale kila siku kiasi cha rutwab ya baridi, na aupe raha mwili kwa wali, apunguze mishughuliko na azidishe kumwangalia yule ampendaye.”1226

FUNGA Mtume (s.a.w.w) amesema: “Fungeni mpate afya.”1227 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Matani yanaondoa usahaulifu, yanaongeza hifidhi na yanaondoa kikohozi; upigaji mswaki, funga, usomaji wa Qur’ani, asali na ubani (yaani kundur).1228 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Enyi kongamano la vijana, yule anayeweza miongoni mwenu kufanya tendo la ndoa basi aoe, kwani linainamisha macho na linahifadhi zaidi tupu. Na yule asiyeweza basi ni juu yake kufunga, kwani hiyo kwake inakata matamanio.”1229 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Ni juu yenu kufunga, kwani hiyo kunakata jasho na kwenye kuondoa majigambo.”1230 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Funga ya siku tatu kwa kila mwezi; jumatano baina ya Alkhamisi mbili, na   Fiqhul-Ridha (a.s), uk. 346.   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 325 cha Allama Majlisi. 1227   Biharul-Anwaar, Juz. 96, uk. 255. 1228   Makarimul-Akhlaq, uk. 164, kutoka kitabu Firdausi. 1229   Twibbu Nabiwi, uk. 195 cha Ibn Qaym Jawziyyat. 1230   Kanzul-Ummal, hadithi 2361. 1225 1226

266

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 266

8/10/2017 1:22:14 PM


TIBA YA MAASUMINA

funga ya shaabani; zinaondoa wasi wasi wa kifua na balabili ya moyo.”1231 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Alikuwa Mtume (s.a.w.w) akifuturu anaanza kufuturu kwa kitu kitamu, na kama hakupata basi anafuturu kwa maji ya uvuguvugu, na alikuwa akisema: Husafisha mfuko wa chakula na ini, na kunapendezesha tendo la ndoa kinywa, na hutia nguvu mtoto wa jicho na inapendezesha uangaliaji, na kunaosha madhambi, na kunatuliza jasho lanalotiririka kwa wingi, na nyongo yenye kushinda, kunakata kikohozi, kunazima joto na kunaondoa maumivu ya kichwa.”1232 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Hakika mfungaji akifunga huondoka macho yake, na akifuturu kwa haluwa yanarejea sehemu yake.”1233 Elimu ya tiba Uingiaji: Imam Ali (a.s) amesema: “Elimu ni elimu mbili; elimu ya dini na elimu ya miili.” Na akasema (a.s): “Elimu zipo za aina nne; Fiqhu kwa dini, na tiba kwa miili, na nahawu kwa ulimi, na nyota kwa kujua zama, na walikuwa Maimamu (a.s) ni matabibu wa nyoyo na matabibu ya miili, kwa hilo amesema Imam Ali (a.s) akiisifu nafsi yake: “Ni tabibu mwenye kuzunguka na dawa zake, aliyeandaa marhamu, na anayajua maeneo yake. Anaiweka hiyo mahala inapohitajika, katika nyoyo zilizopofuka, na masikio yaliyokufa, na ndimi za ma  Khiswal, Juz. 2, uk. 612.   Minhaj Da’awat, Juz. 2, uk. 49 cha Sheikh Husein Ma’tuq. 1233   Minhaj Da’awat, Juz. 2, uk. 50. 1231 1232

267

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 267

8/10/2017 1:22:14 PM


TIBA YA MAASUMINA

bubu. Mwenye kufuatilia kwa dawa zake sehemu za mghafiliko, na mahali penye mashaka.”1234 Hadithi: Imepokewa kutoka kwa Asbugh bin Nubatat amesema: “AmirulMuminina Ali bin Abi Twalib (a.s) alimwambia mwanawe Hasan (a.s): “Ewe mwanangu, je nikujuze mambo manne ambayo yatakutosheleza wewe na matibabu? Akasema: Ndio, ewe Amirul-Muminina. Akasema: Usikae juu ya meza ya chakula ila ukiwa wewe una njaa, na simama hali ya kuwa unakitamani hicho, na tafuna vuzuri na unapotaka kulala basi nenda msalani kajisaidie, hayo yatakutosheleza kuhusiana na matibabu.”1235 Na akasema (a.s): “Hakika ndani ya Qur’ani ipo aya inayokusanya matibabu yote, nayo ni: “Na kuleni na kunyweni wala msipitilize kiasi.”1236 Imepokewa kutoka kwa Imam Baqir (a.s) amesema: “Tiba ya waarabu ipo katika mambo matatu; kujishurtisha kwa ufyonzaji wa damu, uingizaji wa bomba la maji katika sehemu ya haja kubwa na dawa ya utapishaji.”1237 Imepokewa kutoka kwa Imam Baqir (a.s) amesema: “Tiba ya waarabu ipo katika sehemu saba; kujishurtisha na ufyonzaji wa damu, uingizaji wa bomba la maji katika sehemu ya haja kubwa, bafu, unusaji, utapikaji, kujishurtisha ulaji wa asali, na mwisho wa dawa ni utapishaji. Na huenda ikaongezwa unyoaji wa nywele kwayo.”1238 Siku moja Imam as-Sadiq (a.s) alihudhuria kwenye kikao cha   Nahjul-Balaghah; hutba no. 106.   Khiswal, Juz. 1, uk. 229. 1236   Surat Aaraf, aya 29. 1237   Twibbul-aimmat (a.s), uk. 55. 1238   Twibbul-Aimmat, uk. 55. 1234 1235

268

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 268

8/10/2017 1:22:14 PM


TIBA YA MAASUMINA

Maamuni na akiwa na mtu kutoka India akisoma vitabu vya tiba, basi akawa Imam as-Sadiq (a.s) akisikiliza usomaji wake. Na pindi alipomaliza yule mhindi akamwambia: Ewe baba wa Abdullah je, unataka chochote kati ya yale niliyonayo? Akasema: “Hapana, mimi ninazo zilizo bora zaidi ya ulizonazo wewe. Akasema: Ni zipi hizo? Akasema: Ninatibu joto kwa baridi, na baridi kwa joto, laini kwa yabisi, na yabisi kwa laini, na nanirejesha mambo yote kwa Mwenyezi Mungu (a.s), na ninatumia yale ambayo amesema Mtume (s.a.w.w). na jua kwamba hakika mfuko wa chakula ni nyumba ya magonjwa, na lishe kamili nayo ni dawa, na ninauzoesha mwili yale ambayo umeyayozoea. Akasema mhindi: Na je, tiba ila ni hii? Akasema: “Unanizulia kwamba nimechukua kutoka katika vitabu vya tiba?: Akasema: Ndio. Akasema: “Naapa kwa Mwenyezi Mungu sijachukua ila kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t)…”1239 Wosia wa matibabu Abu Bakar Raazi katika kitabu chake kiitwacho (Yule asiyehudhuria kwa mganga) amesema: Ukiweza kupata matibabu kwa njia ya vyakula wala usijitibie kwa madawa mengine. *Na inakaribia kwalo kauli ya Harith bin Kildat ambaye alisilimu kwa Mtume (s.a.w.w) akasema: Acha dawa ambayo umeikuta achana nayo, wala usiinywe ila kwa dharura, kwani hiyo haifai chochote ila huharibu. Na hili linafanana na kauli ya Imam Ali (a.s) pale aliposema: “Unywaji wa dawa kwa mwili ni kama vile sabuni kwa nguo inaisafisha lakini inaifanya ichakae.1240   Khiswal, Juz. 2, uk. 512.   Hikmat: 422, mwisho wa kitabu Sharhu Nahjul-Balaghah cha Ibn Abi Hadid.

1239 1240

269

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 269

8/10/2017 1:22:14 PM


TIBA YA MAASUMINA

Mtabibu wa kiarabu Harith bin Kaladat Thaqafi Aliwasili Harith bin Kaladat Thaqafi1241 kwa Kasri Anusharwan, basi akampa idhini ya kuingia kwake. Na pindi aliposimama mbele yake akamwambia: Ni nani wewe? Akasema: Mimi ni Harith bin Kaladat Thaqafi. Akasema: Ni ipi shughuli yako? Akasema: Tiba. Akasema: Wewe ni mwarabu? Akasema: Ndio, mimi ni Mwarabu kindakindaki. Akasema: Ni kitu gani wanafanya waarabu kwa tiba pamoja na ujinga wao, na udhaifu wa akili zao, na ubaya wa chakula chao? Akasema: Ewe mfalme, ikiwa hizo ndizo sifa zao zitakuwa zenye hoja zaidi kwa yule anayefanya vizuri kwa ujinga wao, na anayenyoosha upindaji wao, na anayeongoza miili yao, na anayefanya uadilifu michanganyiko yao, hakika mwenye akili anajulikana kwalo kutoka katika nafsi yake‌ Kisha Kasri akasema: Kwa kitu gani unasifu kutokana na tabia zao, na inakushangaza wewe kutokana na madhehebu yao na huluka zao? Akasema Harith: Ewe mfalme, wao wana nafsi za ukwasi, na nyoyo safi, na lugha fasaha, na ndimi zenye balagha, na nasaba sahihi, na makoo matukufu, yanatoka kutoka vifuani mwao maneno makali kama vile sumu inayotokana na aina fulani ya mti, na matamu zaidi kuliko hewa ya kipupwe, na laini kutokana na salsabili isaidiayo. Mahala pa chakula katika yabisi, na wenye kupiga mshale vitani. Wala hauna mfano utukufu wao, wala kudhuru jirani yao, wala hawahalalishi kuzuia utukufu wao, wala hadhalilishwi mkarimu wao. Wala hawakiri kwa fadhila za wanadamu, ila kwa mfalme mkusudiwa, ambaye hana mfano wake na yeyote, wala hapimwi na yeyote katika uwezo na ufalme wake!   Alikuwa Harith bin Kaladat anatoka Taifu, naye ni mtabibu wa kiarabu katika zama zake. Alisafiri hadi Iran na akijua tiba, na akajua ugonjwa na dawa. Na akabakia masiku ya Mtume (s.a.w.w) na zama za makhalifa wanne. Akafa yapata mwaka wa 50 H.

1241

270

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 270

8/10/2017 1:22:14 PM


TIBA YA MAASUMINA

Basi akatulia Kisra kwenye kiti chake, na akafurahi kwa yale aliyosikia katika maneno yake ya sawa, akasema kuwaambia wale waliokaa naye: Hakika mimi nitakuta hayo ni yenye uzito zaidi, na kaumu yake ni watu wenye sifa, na kwa fadhila zao zinatamka, na kwa yale ambayo yanapatikana kutokana na lafudhi zake ya ukweli; na vivyo hivyo mwenye akili ambaye uzoefu mbali mbali umemfanya awe na hekima! Kisha akamwamrisha yeye kukaa na akakaa. Akamwambia: Vipi mtazamo wako kuhusiana na matibabu? Akasema: Achana nayo!

MAZUNGUMZO THABITI JUU YA TIBA: Kasri akasema: Ni ipi asili ya tiba? Akasema: Kuthibiti midomo miwili, na urahisi wa mikono miwili. Akasema: Umepatia! Ni upi ugonjwa uangamizao? Akasema: Uingizaji wa chakula juu ya chakula, na hilo linawafanya watu watoweke, na kuangamiza wanyama wakali porini. Akasema: Ni nini kaa lipi ambalo hukoleza moto wa maradhi? Akasema: Kuvimbiwa, ikiwa kutabakia tumboni kunaua, na kikisambaa kinakuachia maradhi. Akasema: Umesema kweli‌ Akasema: basi unasemaje kuhusu suala la uingiaji wa bafuni? Akasema: Usiingie ukiwa umeshiba, wala usilale usiku bila ya nguo, wala usikae kwenye chakula hali umekasirika; na itulize nafsi utaipa raha akili yako, na punguza kula chakula chako, usingizi wako utakuwa mnono. Akasema: Unasemaje kuhusiana na dawa? Akasema: ‘Kile ambacho kinakulazimu wewe afya yako jiepushe nacho, ikiwa ugonjwa utajitokeza basi udhibiti kwa kwa kinachoufaa kabla haujakomaa, hakika mwili ni kama vile ardhi; ukiitengeneza vizuri itaimarika na ikiwa utaiacha itaharibika. 271

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 271

8/10/2017 1:22:14 PM


TIBA YA MAASUMINA

Akasema: Ni nyama mbili zipi ni bora? Akasema: Ya mbuzi kijana. Na nyama kavu ya chumvi inamwangamiza mlaji; na jiepushe na nyama ya ng’ombe. Akasema: Unasemaje kuhusu matunda? Akasema: Kula yote katika upatikanaji wake na wakati wa kuiva kwake, na yaache yanapokuwa hayajaiva na kupitwa zama zake. Na bora zaidi ni tunda la komamanga na Furungu, na bora zaidi ya maua mazuri ni waridi na banafsaji na bora zaidi ya mboga mboga ni hindubaau na khissi. Akasema: Unasemaje kuhusiana na unywaji wa maji? Akasema: Nayo ni uhai wa mwili na kwake ndiyo kusimama kwake. Hukunufaisha kile unachokunywa kwa kiwango cha haja, na kunywa baada ya usingizi ni madhara. Na bora zaidi uzuri wake, na mepesi zaidi ni yaliyosafi zaidi. Akasema: Ni upi utamu wake? Akasema: Kitu hakiwezi kusifiwa. Akasema: Na ipi rangi yake? Kukosea juu ya macho ya rangi yake, kwani inaelezwa rangi ya kila kitu inakuwa ndani yake. Maumbile manne: Kisra akasema: Basi ni juu ya mafinyango mangapi ya maumbile ya mwili? Akasema: Juu ya maumbile manne; kibofunyongo cheusi, nayo ni baridi yabisi. Na nyongo ya manjano, nayo ni ya joto yabisi. Na damu nayo ni ya joto na rutwab, kikohozi nayo ni baridi rutwab‌ Akasema: Je, unaamrisha bomba la maji kupitia sehemu za siri? Akasema: Ndio, nimesoma katika baadhi ya vitabu vya wenye hekima kwamba uingizaji wa bomba sehemu za siri unasafisha tumbo, na hupunguza sana nguvu ya dawa kwayo. Na la kushangaza ni yule ambaye aliyepenyezewa bomba vipi azeeke, au akose mtoto! Na hakika mjinga ni yule anayekula kile ambacho anajua madhara yake, na humuathiri matamanio yake juu ya mwili wake. 272

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 272

8/10/2017 1:22:14 PM


TIBA YA MAASUMINA

Akasema: Ni nini lishe kamili? Akasema: Ni kuwa na matumizi mazuri katika kila kitu; hakika kula kupita kiwango hubana roho katika uwanja wake, na hufunga matumizi yake…. Kisha akasema Kisra: Naapa kwa Mwenyezi Mungu nyumba yako wewe inatokana na bedui! Hakika umepewa elimu, na umekuwa mahsusi uerevu na ufahamu.. na muunganiko wake mzuri, na akaamrisha kutibu kwa yale ambayo aliyoyatamka kwayo.1242 *Na pindi alipohudhuria Harith bin Kaladat wakakusanyika watu kwake, wakasema: Tuamrishe jambo ambalo tunamalizia kwalo baada yako. Akasema: Msioe miongoni mwa wanawake ila msichana, wala msile matunda ila katika zama za kuiva kwake, wala asimtibu yeyote miongoni mwenu kwa yale yanayotegemewa kwayo mwili wake ugonjwa, na juu yenu kwa unyoaji wa nywele za mwili kila mwezi kwani hilo linayeyusha kikohozi, lenye kuangamiza nyongo ni lenye kuotesha nyama, na ikiwa atakula mmoja wenu chakula cha mchana basi alale juu ya athari ya chakula chake, na ikiwa atakula chakula cha usiku basi atembee hatua 40. *Na miongoni mwa wosia wa mtabibu (Tiyadhuuq) kwa Hajjaj unaofanana na hayo akasema: Usile nyama ila ya mnyama ya ndama, wala usioe ila msichana, wala usinywe dawa ila kutokana na ugonjwa, wala usile tunda ila linapoiva, na tafuna chakula vizuri, na ikiwa utakula mchana sio vibaya kulala kidogo, na ukila chakula cha usiku usilale mpaka utembee hatua 50, wala usizuie haja ndogo, na chukua bafu kabla haijajichukua kutoka kwako. Na hakika amechukua baadhi ya maana yake kutokana na maneno ya Imam Ali (a.s) aliposema: “Asijitibie Mwislamu mpaka pale ambapo maradhi yake yanashinda afya yake.   Quswasul-Arabi, Juz. 1, uk. 132 cha Jaadi Maula na Jabawi na Abu Fadhl Ibrahim, kutoka kitabu Buruughul-Arb, Juz. 3, uk. 328 na Aqdul-Fariid, Juz. 4, uk. 341.

1242

273

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 273

8/10/2017 1:22:14 PM


TIBA YA MAASUMINA

Uondoe ugonjwa wako kama vile ambavyo umeingia kwako.” Isipokuwa kutokana na wosia wake (a.s) kwa mwanawe Hasan (a.s) nao ni maneno manne ambayo humtosheleza yeye kwayo kuhusiana na matibabu. Miongoni mwa nasaha za bwana wetu Ali (a.s) amesema: Yule anayeanza chakula chake cha mchana kwa chumvi Mwenyezi Mungu humuondolea yeye kila ugonjwa, na yule anayekula zabibu punje 21 kila siku hatoona tumboni mwake kitu kinachomkera, na nyama inaotesha nyama, na chakula cha kiarabu, na nyama ya ng’ombe ni ugonjwa na maziwa yake ni dawa, na samli yake ni ponyo, na mafuta yake yanaondoa mfano wake miongoni mwa ugonjwa, na yanakausha wanawake kwa kitu bora zaidi kuliko rutwab, na upigaji mswaki na usomaji wa Qur’ani kunaondoa kikohozi, na yule anayetaka kubakia (na hakuna abakiaye ila Mwenyezi Mungu) basi ale mapema chakula cha mchana, na apunguze kuchukua madeni, na apunguze kukutana kimwili na wanawake. MAUMBILE YA MWILI Tiba ya Galenos: Alikuwa Galenos (129 – 201 AD) akifuata athari ya mwanafalsafa wa kiyunani Ibuqrat, na kwa hili hakika alikuwa akiitakidi kwamba mwili wa kiumbe unazingira juu ya mchanganyiko huu:1243i) Damu ii) kikohozi iii) Nyongo nyeusi iv) Nyongo ya manjano. 1243  Maumbile manne nayo ni: Damu, kikohozi, umanjano na weusi, na ama damu inashamiri moyo na mishipa na vinavyofuatia. Na ama kikohozi hukusanya chombo cha upumuaji kwa njia zake na mishipa miwili na mrija wa hewa na vinavyofuatia. Na ama umanjano unashamili chombo cha mmeng’enyo wa chakula, ini, nyongo, mapafu bankurias na vinavyofuatia. Na ama weusi inashamili yote pamoja na njia ya haja ndogo na kiungo cha uzazi na rahmi na vinavyofuata hiyo. (Majmu’atul-Aathar, uk. 414 cha Imam Ridha (a.s). 274

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 274

8/10/2017 1:22:14 PM


TIBA YA MAASUMINA

Na ukipatikana mchanganyiko huu wote kulingana na muambatano, itakuwa ni tija ya ulingano wa maumbile ya mtu na tabia yake. Ama ikiwa mtu mmoja atazidisha mchanganyiko huu wa wastani, hakika maumbile ya mtu huyo hutofautiana, na yanakuwa ima ya damu au ya maji (baridi), au ya moto, au yenye kujificha (nyeusi). Ila hakika Galenos hakuwa anapambana na maradhi kuelekea mvurugano wa mchanganyiko kama alivyosema Ibqarat, lakini yeye akipambana nao kwa kuelekea mapungufu ya viungo, nayo ni nadharia imethibitika usahihi wake na inayo umuhimu mkubwa.1244 Maumbile manne katika mtazamo wa Imam Ja’far As-Sadiq (a.s): Abu Hafan amesema: Nilimwambia mtabibu Ibn Masuwayh amesema: Hakika Ja’far bin Muhammad (s.a) amesema: Maumbile yapo ya aina nne: Damu: Nayo ni mja, na huenda mja akamuua bwana wake. Harufu: Naye ni adui, ukimfungulia yeye mlango basi anakujia kutoka katika mlango mwingine. kikohozi: Naye ni mfalme anayezunguka. Nyongo: Nayo ni maradhi, ikitetemeka hutetemeka kwa yule aliye juu yake. Basi ibn Masuwayh akasema: Rudia tena, naapa kwa Mwenyezi Mungu yule ayafanyaye vizuri Galenos aelezee wasifu huu. Na hakika ameainisha elimu ya tiba ya kisasa kwamba nyongo (au umanjano) nayo ni awriy au haja ndogo, na kikohozi (au weusi) nayo ni bwana zaidi wa awriya yako au tone la haja ndogo.1245   Kitabul-Ma’arafatuk. 800 – herufu T – toleo la tano.   Madrasatu-Ahlul-Bayt (a.s), minhaj wa Uluum uk. 48 cha Hassan Abu Saleh.

1244 1245

275

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 275

8/10/2017 1:22:14 PM


TIBA YA MAASUMINA

Hadithi: Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Mwili umejengwa juu ya vitu vinne; juu ya roho na akili, na damu na nafsi. Na pindi roho itakapotoka akili humfuata, na roho itakapoona kitu akili hukihifadhi juu yake, na hubakia damu na nafsi.”1246 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Hakika maradhi yote yanatokana na nyongo yenye kushinda au damu yenye kuungua au kikohozi chenye kushinda, basi mwanaume ajishughulishe kwa uchungaji wa nafsi yake kabla hakijamshinda yeye kitu kutokana na maumbile haya na anakiangamiza.”1247 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Vinne vinaleta ulinganifu wa maumbile; komamanga suraani, tende yenye kupikwa, balungi na hindubaau.”1248 Hadithi ya Yohana bin Masuwayh mtabibu mashuhuri wa kinaswara: Hakika Ja’far bin Muhammad (a.s) akasema: Maumbile ni manne; damu nayo ni mtumwa, na huenda mtumwa akamuua bwana wake. Na harufu nayo ni adui, ukimfanyia wema mlango mmoja basi anakujia kwa mlango mwingine. Na kikohozi ni mfalme anayezunguka. Na nyongo nayo ni maradhi, ikiwa itatetemeka atatetemeka yule aliye juu yake. Ibn Masuwayh akasema: Rudia tena, naapa kwa Mwenyezi Mungu yale ayafanyayo vizuri Galenos anaeleza kwa wasifu huu.1249 Imepokeawa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Maarifa ya mtu thamani yake aijue kwa maumbile manne, na misukumo minne, na nguzo nne. Basi maumbile yake ni; damu, nyongo, harufu   Khiswal, Juz. 1, uk. 226.   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 264. 1248   Khiswal, Juz. 1, uk. 119 cha Saduuq chapa ya kwanza. 1249   Twibbul-Aimmat, uk. 4. 1246 1247

276

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 276

8/10/2017 1:22:14 PM


TIBA YA MAASUMINA

na kikohozi. Na misukumo yake ni; akili (na kutokana na akili ni uerevu) na ufahamu na hifidhi na elimu. Na nguzo zake ni; nuru, moto, harufu na maji. Basi akamuonesha na akasikia na akatia akili kwa nuru, na akala na akanywa kwa moto, na akafanya tendo la ndoa na akafanya harakati kwa roho, na akakuta utamu wa uonjaji na utamu wa maji. Na taasisi hii ni picha yake.”1250 Elimu ya Maamuni na wingi wa maarifa yake Ja’far bin Muhammad Anmatwiy amesema: Pindi alipoingia Maamuni Baghdad na akakaa huko ukaaji wake, akaamrisha waingie kwake miongoni mwa wanazuoni, wanaitikadi na watu wa elimu, na jumuiya ya wale aliowachagua kwa waliojikusanya kwake na kuzungumza naye. Na wakati wa mchana wa masika alikuwa anakaa juu ya tandiko la sufu, na wakati wa kiangazi juu ya mkeka wake, hakukuwa na chochote kinachotokana na magodoro mengine. Na akikaa ukumbini kila Ijumaa mara mbili, na hakimzuii chochote kufanya hivyo. Na wakachukuliwa kwake miongoni mwa wanazuoni kwa wale anaokaa nao wanaume mia moja, na akaendelea akiwachagua hao tabaka baada ya tabaka, hadi wakafikia kumi, na alikuwa miongoni mwao Ahmad bin Abi Daud, Bishru Mariisi, na mimi nilikuwa kati yao. Elimu ya Maamuni kwa matibabu: Siku moja tulikula chakula cha mchana kwake, basi ninadhani viliwekwa juu ya meza ya chakula zaidi ya aina mia tatu ya vyakula; basi kila kilipowekwa aina fulani ya chakula alikiangalia akasema:   Twibbul-Aimmat, uk. 62 cha Abdullah Shubbar.

1250

277

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 277

8/10/2017 1:22:14 PM


TIBA YA MAASUMINA

Hiki kinafaa kwa jambo hili, na hiki kinanufaisha hiki, basi yule ambaye miongoni mwenu ana kikohozi ajiepushe na hiki, na yule mwenye umanjano basi ale hiki, na yule aliyezidiwa juu yake na weusi basi ale hiki, na yule anayependa nyongeza katika nyama zake basi ale hiki, na yule anayekusudia kupunguza ulaji basi atoshoke na hiki. Naapa kwa Mwenyezi Mungu iliendelea katika hali hiyo kila alipoletewa chakula, mpaka ikaondolewa meza ya chakula. Yahya bin Akthum akamwambia: Ewe Amirul-Muminina, ikiwa tutakuhusisha na tiba basi umekuwa Galenos katika maarifa yake! Au katika nyota umekuwa Harmas katika hesabu yake! Au fiqhi (elimu ya sharia) umekuwa Ali bin Abi Twalib katika elimu yake! Au tukiwataja wakwasi basi wewe umekuwa ni kilele katika utoaji wake! Au tukitaja ukweli wa mazungumzo umekuwa wewe Abu Dharr katika ukweli wa maneno yake! Au tukitaja ukarimu umekuwa Kaab bin Maamat katika kuwapendelea wengine kuliko nafsi yake! Basi akafurahi Maamuni kwa maneno hayo, akasema: Ewe baba wa Muhammad; hakika mtu hufadhilishwa juu ya mwingine juu ya watu wa kawaida kwa kitendo chake na akili yake, na umaizi wake (uchanganuaji wake wa mambo), na lau sio hivyo isingelikuwa nyama ni nzuri zaidi kuliko nyama, wala damu ni nzuri zaidi kuliko damu!1251 Na hakika Maamuni alichukua mambo mengi kutokana na elimu ya tiba kutoka kwa Imam Ridha (a.s), na kwa hivyo walikusanyika kwake Naysabuuri, basi Maamuni akamuomba Imam Ridha (a.s) amwandikie yeye barua katika matibabu, basi haukupita muda alipokwenda Maamuni Balhk na aliporudi Naysabuuri, basi Imam (a.s) akampatia yeye barua ya muhtasari katika misingi ya matibabu. Na pindi Maamuni alipoisoma akatambua ukubwa wake na akakiri   Asrul-Maamun, Juz. 1, uk. 360 cha Dr. Fariid Rifaai.

1251

278

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 278

8/10/2017 1:22:14 PM


TIBA YA MAASUMINA

thamani yake akasema: Iandikwe kwa maji ya dhahabu, basi kuanzia hapo ikaitwa “barua ya dhahabu.” Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) alimwambia Maamuni katika kitabu (Risaalatul-Madhhabiyat): “Hakika Mwenyezi Mungu (s.w.t) ameijenga miili juu ya maumbile manne, nayo mawili ni (umanjano na weusi) na damu na kikohozi. Basi viwili ni joto na viwili vingine ni baridi, na hakika vimetofautiana kati ya hivyo viwili, basi akafanya vya moto viwili ulaini na yabisi na vivyo hivyo vya baridi mbili unyevunyevu na yabisi. Kisha akatenganisha hilo juu ya viungo vinne vya mwili; juu ya kichwa, kifua, sharasiif na chini ya tumbo. Na jua ewe Amirul-Muminina hakika kichwa na masikio mawili na macho mawili na mdomo na pua vinatokana na damu, na hakika kifua kinatokana na kikohozi na upepo, na sharasiif inatokana na nyongo ya manjano, na hakika chini ya tumbo inatokana na nyongo nyeusi.”1252 *Mpaka alipomwambia Maamuni katika barua ya dhahabu: “Na jua ewe Amirul-Muminina hakika hali za mtu ambazo Mwenyezi Mungu amezijenga na akazifanya zenye kutumika kwake, ni hali nne; hali ya kwanza kwa miaka kumi na tano, na ndani yake kuna ujana wake, uzuri wake na upendezaji wake, na sultani wa damu katika mwili wake. Na hali ya pili kutoka miaka kumi na tano hadi miaka thelathini na tano, na ndani yake kuna sultani wa nyongo ya manjano, na nguvu inayomshinda mtu nayo ina nguvu zaidi ambayo inakua, na inaendelea hivyo mpaka unakwisha muda uliotajwa nao ni mwaka wa 35. Kisha anaingia kwenye hali ya tatu hadi anapofikia umri wa miaka 60, na anakuwa sultani nyongo nyeusi, nao ni umri wa hekima, mawaidha, maarifa, elimu na mpangilio wa mambo, na   Biharul-Anwaar, Juz. 59, uk. 316.

1252

279

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 279

8/10/2017 1:22:14 PM


TIBA YA MAASUMINA

usahihi wa mtazamo katika mwisho wa mambo, na ukweli wa rai na maoni, na uthabiti wa kuchanganikiwa katika matumizi mbali mbali. Kisha anaingia hali ya nne, nayo ni hali ambayo hayabadiliki kwayo yaliyobakia, ila uzee, ugumu wa maisha, na usinyaaji na upungufu katika nguvu na uharibifu katika utengenezaji wake, na anakanusha kila kitu kilichopo anajua kutokana na nafsi yake, hadi analala akiwa na watu anakesha wakati wa kulala, na anakumbuka yale ambayo aliyoyatanguliza na anasahau yanayotokea nyakati hizo, na husinyaa ada yake, hubadilika yale anayoyaahidi, na hukauka maji yenye ubora yenye hadhi, na unapungua uotaji wa nywele zake na kucha zake, na unaendelea mwili wake katika kwenda kinyume na kurudi nyuma ambayo aliyoishi, kwani yeye yuko katika sultani wa kikohozi, naye ni baridi ngumu, basi kwa kuwa ngumu na kuwa kwake baridi ndivyo mwili unavyokwisha na unatawala juu yake kwa mwingine nguvu ya kikohozi.”1253

CHAKULA Rejea (ulaji) Ilielezwa kwa Mtume (s.a.w.w): Ewe Mtume (s.a.w.w) hakika wewe unapunguza unywaji wa maji. Akasema: “Hilo ni zuri zaidi katika chakula changu.”1254 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Msiache kula chakula cha usiku hata kidogo. Hakika mimi ninachelea juu ya umma wangu kuacha chakula cha usiku kuzeeka, hakika chakula cha usiku ni nguvu ya mzee na kijana.”1255   Biharul-Anwaar, Juz. 59, uk. 317 cha Allamah Majlisi.   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 19. 1255   Wasaail-Shi’ah, Juz. 16, uk. 467. 1253 1254

280

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 280

8/10/2017 1:22:14 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Chakula cha mtoaji ni dawa, na chakula cha bakhili ni ugonjwa.”1256 Imepokewa kutoka kwa Amirul-Muminina Ali (a.s) amesema: “Yule anayetaka kubakia na hakuna ubakiaji kama huo, basi ale mapema chakula cha mchana…”1257 Imepokewa kutoka kwa Amirul-Muminina Ali (a.s) amesema: “Chakula cha usiku cha manabii kilikuwa baada ya kuingia giza, wala msiache kula chakula cha usiku, hakika kuacha kula chakula cha usiku huharibu mwili.”1258 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Yampasa mzee asilale hali ya kuwa tumbo lake limejaa chakula, kwani hilo (la kutojaa tumbo) hutuliza usingizi wake na zuri kwa tendo lake la ndoa.”1259 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema; “Kitu cha kwanza kinachoharibu mwili ni kuacha kula chakula cha usiku.”1260 Imepokewa kutoka kwa Marazim amesema: Alituletea sisi baba wa Abdillah (a.s) chakula cha joto, akasema: “Kuleni kabla hakijapoa, kwani kufanya hivyo ni vizuri zaidi.”1261 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Utakaposwali swala ya alfajiri basi kula kila kipande cha mkate, kunafanya uzuri kwayo tendo lako la ndoa, na kunazima kwayo joto lake, na kunasimamisha magego yako, na kunakaza ufidhi wako. Na kunavuta riziki yako na kunafanya vizuri tabia yako.”1262   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 291.   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 267. 1258   Wasaail-Shi’ah, Juz. 16, uk. 468. 1259   Wasaail-Shi’ah, Juz. 16, uk. 470. 1260   Wasaail-Shi’ah, Juz. 16, uk. 466. 1261   Wasaail-Shi’ah, Juz. 16, uk. 518, kutoka kitabu Mahasin cha Barqi. 1262   Biharul-Anwaar, Juz. 66, uk. 345. 1256 1257

281

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 281

8/10/2017 1:22:14 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Msiache kula chakula cha usiku hata kwa matonge matatu, na yule anayeacha kula chakula cha usiku hufa jasho la mwili wake na haiwi hai abadani.”1263 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Unywaji wa maji kwa kusimama mchana unarahisisha mmeng’enyo wa chakula na kuwa laini.”1264 Imepokewa kutoka kwa Ja’far amesema: Alikuwa Imam Kadhim (a.s) haachi kula chakula cha usiku hata kwa biskuti, na alikuwa akisema: “Hakika hicho ni nguvu ya mwili, na hufanya uzuri tendo la ndoa.”1265 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Msiliache tupu tumbo bila chakula, na punguzeni unywaji wa maji, wala usifanye tendo la ndoa ila ukiwa na hamu nalo…”1266 Waganga wanasema: Kikitoka chakula kabla ya masaa sita ya kula kingine basi inadhuru, na kikisimama tumboni zaidi ya masaa 24 basi nayo ni madhara.”1267 Manukato Mtume (s.a.w.w) amesema: “Harufu nzuri inakaza moyo.”1268 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kwamba amesema: “Nimependezwa mimi kutokana na dunia yenu matatu; wanawake, manukato na swala imefanywa kwangu ni tulizo la jicho.”1269   Safinatul-Bihar, Juz. 2, uk. 199.   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 191. 1265   Wasaail-Shi’ah, Juz. 16, uk. 467, kutoka kitabu Mahasin cha Barqi. 1266   Makarimul-Akhlaq, uk. 181. 1267   Aqdul-Fariid, Juz. 7, uk. 261. 1268   Makarimul-Akhlaq, uk. 41. 1269   Twibbu Nabiwi, uk. 260 cha Ibn Qaym Jawziyyat. 1263 1264

282

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 282

8/10/2017 1:22:14 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Amirul-Muminina Ali (a.s) amesema: “Manukato yaliyo mazuri zaidi ni miski, na uchukuaji wake ni mwepesi, uturi wake ni mzuri.”1270 Imepokewa kutoka kwa Amirul-Muminina Ali (a.s) amesema: “Manukato ni rukiya, asali ni rukiya na upandaji ni rukiya na uangaliaji wa kijani kibichi ni rukiya.1271, 1272 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Alikuwa bwana Mtume (s.a.w.w) akitumia zaidi katika manukato kuliko anavyotumia katika chakula.”1273 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Harufu nzuri inakaza akili na inazidisha katika tendo la ndoa.”1274 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Manne ni miongoni mwa sunna ya mitume; upigaji mswaki, upakaji wa hina, kujipaka manukato na wanawake.”1275 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Yule ambaye anajipaka manukato asubuhi akili yake itaendelea kuwa pamoja naye mpaka usiku.”1276

UDONGO Mtume (s.a.w.w) amesema: “Ulaji wa udongo ni haramu juu ya kila mwislamu.”1277   Nahjul-Balaagha, hikma 397.   Nushrat ni rukiya inayotumika kutibu mgonjwa kwayo (kujilinda). 1272   Nahjul-Balaagha , hikma 400. 1273   Furuu al-Kaafi Juz. 6 uk. 512. 1274   Biharul-Anwaar juz. 62 uk. 275. 1275   Makarimul-Akhlaq, uk. 41. 1276   Furru al-Kaafi, Juz. 6, uk. 510. 1277   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 300. 1270 1271

283

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 283

8/10/2017 1:22:15 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Msile udongo hakika ndani yake kuna mambo matatu; unasababisha ugonjwa, unatunisha tumbo na unafanya rangi ya ngozi kuwa ya manjano.”1278 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kwamba aliulizwa kuhusu mtoto kula udongo na mkaa, akasema: “Yule anayekula udongo hakika unamsaidia juu ya nafsi yake, na yule atakayekula na akafa basi haswaliwi. Na ulaji wa udongo unasababisha unafiki.”1279 Imepokewa kutoka kwa Imam Baqir (a.s) amesema: “Udongo uliopo kwenye kaburi la Husein (a.s) ni ponyo la kila ugonjwa, na amani ya kila hofu nao ni yale yaliyochukuliwa kwake.”1280 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Udongo uliopo kwenye kaburi la Husein (a.s) ni ponyo la kila maradhi, nao ni dawa kubwa zaidi.”1281 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Hakika udongo uliyopo kwenye kaburi la Husein (a.s) ni miski yenye baraka, yule atakayeula miongoni mwa wafuasi wetu utakuwa ni ponyo kwake la kila ugonjwa, na yule atakayekula miongoni mwa maadui zetu basi utayeyuka kama vile inavyoyeyuka ilyat.”1282 Mtu mmoja alimlalamikia Imam as-Sadiq (a.s) kuhusiana na ukoma; basi akamwamrisha achukue udongo kwenye kaburi la Imam Husein (a.s) atumie kwa maji ya mvua, basi akafanya hivyo akapona.”1283   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 300.   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 275. 1280   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 52. 1281   Makarimul-Akhlaq, uk. 167. 1282   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 166. 1283   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 398 cha Abdullah Shubbar. 1278 1279

284

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 284

8/10/2017 1:22:15 PM


TIBA YA MAASUMINA

Aliulizwa Imam as-Sadiq (a.s) kuhusiana na udongo wa Armani, unachukuliwa kutoka kwake aliyevunjika na kuvimba tumbo, je, ni halali kuuchukua na kuutumia huo? Akasema (a.s): “Hakuna tatizo. Ama hakika huo unatokana na udongo wa kaburi la Dhu Qarnayni, na udongo wa kaburi la Husein (a.s) ni bora kuliko huo.”1284 Kucha Kinachojulikana: Kucha inakua kila wiki milamu 2, na inahitajika kubadilishwa kucha zote kwa miezi minne. Hadithi: Mtume (s.a.w.w) amesema: “Matano yanatokana na maumbile; Jando, msiba, unyofoaji wa nywele za kwapani, ukataji wa kucha na utindaji wa masharubu.”1285 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Yule anayetaka aepukane na ufukara, maumivu ya jicho, ukoma na uwenda wazimu basi akate kucha zake siku ya Alkhamisi baada ya alasiri, na aanze kidole kidogo cha mkono wa kushoto.”1286 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Yule anayekata kucha zake siku ya Ijumaa, Mwenyezi Mungu atamuondolea mizizi ya ugonjwa, na ataingiza ndani yake ponyo.”1287 Imepokewa kutoka kwa Anas bin Malik amesema: Mtume (s.a.w.w) alituelezea wakati wa mtu kunyoa nywele zake za kinenani   Makarimul-Akhlaq, uk. 167.   Sahihi Bukhari, Juz. 7, uk. 137 Makatab Nahdhat Hadith Makka Mukarrama mwaka 1376 H. 1286   Makarimul-Akhlaq, uk. 66, kutoka kitabu Firdausi. 1287   Makarimul-Akhlaq, uk. 64. 1284 1285

285

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 285

8/10/2017 1:22:15 PM


TIBA YA MAASUMINA

ni kila baada ya siku 40, na unyofoaji wa nywele za kwapani kila zinapochomoza, wala asiache masharubu yake yawe marefu, na akate kacha zake siku ya Ijumaa mpaka Ijumaa nyingine.”1288 Imepokewa kutoka kwa Amirul-Muminina Ali (a.s) amesema: “Ukataji wa kucha siku ya Ijumaa kabla ya swala unazuia ugonjwa mkubwa. Na akasema (a.s): Ukataji wa kucha siku ya Ijumaa unazuia kila ugonjwa, na ukataji wake siku ya Alkhamisi unazungusha riziki uzungushaji.”1289 Imepokewa kutoka kwa Imam Baqir (a.s) amesema: “Hakika ukataji wa kucha zake mtu ni siku ya Ijumaa, na aanze kwa kidole chake kidogo cha mkono wake wa kushoto, na amalizie kwa kidole kidogo cha mkono wake wa kulia.”1290 Imepokewa kutoka kwa Imam Baqir (a.s) amesema: “Hakika sio vingine kateni kucha kwani hilo ni semeo la shetani, na kwazo kunaleta usahaulifu.”1291 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Yule anayekata kucha zake kila Alkhamisi hayatougua macho yake.”1292 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Ukataji wa kucha na upunguzaji wa masharubu siku ya Ijumaa mpaka Ijumaa nyingine, ni amani ya mbalanga.”1293 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Udumishaji wa unyoaji wa nywele na ukataji wa kucha zake, akifanya hivyo, nayo ni sunna. Na katika kitabu Mahasin: Nayo ni sunna ya   Tafsiru Durrul-Manthuur, Juz. 1, uk. 113 cha Suyuutwi.   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 138. 1290   Makarimul-Akhlaq, uk. 66. 1291   Wasaail-Shi’ah, Juz. 1, uk. 433. 1292   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 84. 1293   Makarimul-Akhlaq, uk. 64. 1288 1289

286

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 286

8/10/2017 1:22:15 PM


TIBA YA MAASUMINA

wajibu. Na imepokewa kwamba hakika miongoni mwa sunna ni; zizikwe nywele, kucha na damu.”1294 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) katika barua ya dhahabu amesema: “Na yule anayetaka kucha zake zisivunjike wala asiegemee kwa unjano wala kuharibu kuhusiana na kucha zake, wala hakati kucha zake ila siku ya Alkhamisi.”1295 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Ukataji wa kucha unazuia ugonjwa mkubwa, na unavuta riziki na kuizungusha.”1296 Adesi Viungo vyake vya asili vitenda kazi: Adesi inafaidisha mno, na ndani yake kuna maada zenye kusheheni protini pungufu na wanga na madini ya chumvi, mfano magneziam, potasiamu, elementi ya njano, chuma, kalisiamu, na vitamini B na C. Faida zake: Inatumiwa katika hali mbali mbali kama vile katika ukosefu wa damu, na kama vile chakula cha watu, na mzunguko wa maziwa, na kwa udhaifu wa misuli na ubadilishaji wa juhudi. Na ikipikwa bila maganda yake hufunga tumbo kutokana na kuhara.1297 Mtume (s.a.w.w) amesema: “Mtume mmoja alilalamika kwa Mwenyezi Mungu (a.j) ugumu wa mioyo ya watu wake, basi akamfunulia Mwenyezi Mungu naye katika mswala wake, waamrishe   Makarimul-Akhlaq, uk. 66.   Biharul-Anwar, Juz. 62, uk. 324 cha Allama Majlisi. 1296   Tuhful-Uquul, uk. 72. 1297   Mufradaat Nabataat Twibbiyat, uk. 394 kimeandaliwa na Ahmad Saleh Damiscus. 1294 1295

287

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 287

8/10/2017 1:22:15 PM


TIBA YA MAASUMINA

watu wako wale adesi, kwani hiyo inafanya moyo kuwa laini na hutoa machozi, na inaondoa kiburi na makuu, nacho ni chakula cha watu wema.”1298 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Yule anayekula mung’unya kwa adesi, unalainika moyo wake katika utajo wa Mwenyezi Mungu, na unaongeza katika tendo la ndoa (na katika hadithi nyingine: Ubongo wake.)”1299 Imepokewa kutoka kwa Ali bin Mihziyar amesema: Hakika kijakazi wetu alipatwa na hedhi na ikawa haukatiki utokaji wake, mpaka akakaribia kufa, basi akamwamrisha Imam Baqir (a.s) anywe sawiiq ya adesi, basi akanywa na ikakatika hiyo na akapona.”1300 Imepokewa kutoka kwa Musa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Sawiiq ya adesi inakata kiu, inatia nguvu mfuko wa chakula, na ndani yake kuna ponyo ya magonjwa sabini, inazima umanjano, inatia tumbo ubaridi. Na alikuwa akisafiri (a.s) haachani nayo. Na mtu alipopatwa na shinikizo la damu, basi kwa heshima yake atamwambia: Kunywa sawiiq ya adesi, kwani hiyo inatuliza shinikizo la damu, na inazima joto.”1301 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Ni juu yenu kutumia adesi, kwani hiyo ni yenye baraka na takatifu, na hakika hiyo inalainisha moyo, na inazidisha machozi, na hakika hiyo imebarikiwa ndani yake na manabii sabini (mmoja wao) nabii Isa bin Maryam (a.s) [yaani yeye aliiombea ibarikiwe].1302   Makarimul-Akhlaq, uk. 188, kutoka kitabu cha Firdausi.   Makarimul-Akhlaq, uk. 179. 1300   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 10, kutoka kitabu Furuu al-Kaafi, Juz. 6, uk. 307. 1301   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 10. 1302   Sahifatul-Ridha (a.s), uk. 75. 1298 1299

288

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 288

8/10/2017 1:22:15 PM


TIBA YA MAASUMINA

Maambukizo Melezo yake: Hakika Mtume (s.a.w.w) amesema: “Hakuna maambukizo katika Uislamu” haina maana kuwa inakanushwa fikra ya uambukizaji na hakika maradhi huambukiza kutoka kwa mgonjwa hadi kwa mtu mzima, na hakika lengo la kauli yake ni kwamba hakika Uislamu umetilia mkazo juu ya usafi na juu ya kinga ya maradhi, na kutokana na kuwa hali hii inaondoa katika mjumuiko wake maradhi na inasafisha maambukizo. Au hakika maana ya hadithi ni katazo kutokana na kutokufuata sababu moja kwa moja ambazo zinapelekea uambukizaji wa magonjwa hadi kwa wengine, na mfano wa kauli yake (s.a.w.w) amesema: “Hakuna twayrat (yaani msiwe na fikira za kuamini mikosi), mfano wa kauli yake (s.a.w.w) amesema: “Hakuna madhara wala kujidhuru katika Uislamu, yaani ni katazo kutokana na kudhuru mwingine.” Na hakika ameweza mmoja wa matabibu wa kiislamu nchini Marekani kuunga mkono usahihi wa kauli ya Mtume (s.a.w.w) inayosema: “Hakuna maambukizi katika Uislamu” basi akagundua kwamba mtu anayemiliki utashi wa nguvu kama vile waumini wenye kumwamini Mwenyezi Mungu, anamiliki mionzi miekundu inayotoka ndani ya ngozi yake, ambayo huteketeza bakteria wanaomkaribia yeye. Ama mtu mwenye utashi mdogo yeye hutoa mionzi ya bluu ambayo huwa haiwezi kufanya chochote.

289

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 289

8/10/2017 1:22:15 PM


TIBA YA MAASUMINA

Hadithi: Mtume (s.a.w.w) amesema: “Msimweke mgonjwa juu ya mwenye afya.”1303 Na katika hadithi nyingine amesema (s.a.w.w): “Mgonjwa asiwe pamoja na mwenye afya.”1304 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Hakuna maambukizi katika Uislamu.” Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Ukimbieni ugonjwa wa mbalanga kama vile mnavyomkimbia simba.” Imepokewa kutoka kwa Ibrahim bin Sa’ad amesema: Nilimsikia Usama bin Zayd akimhadithia Sa’ad kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Mtakaposikia ugonjwa wa tauni katika ardhi fulani basi msiingie huko, na ikiwa utatokea na nyinyi mko huko basi msitoke huko” [hadi uenee ugonjwa]. Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Maambukizo sio haki.”1305 JASHO Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Unywaji wa maji kwa kusimama mchana, unasukuma jasho, na kuutia nguvu zaidi mwili.”1306 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Hakika Mwenyezi Mungu aliwaondolea mayahudi mbalanga kwa kula kwao mchadi, na kukata mishipa kutoka kwenye nyama.”1307   Sahihi Bukhari, Juz. 7, uk. 120 uhakiki wa Muhammad Abu Fadhl na marafiki waki wawili, Maktabat Nahdhat Hadiithat Makka mwaka 1376 H. 1304   Ameipokea Muslim katika salamu, Bukhari katika Tiba, Abu Daud na Ahmad katika Musnad wake. 1305   Nahjul-Balaagha, hikma 400. 1306   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 192, kutoka kitabu Man la yahdhuruhul-Faqiih, Juz. 3, uk. 23. 1307   Mahasin, uk. 519. 1303

290

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 290

8/10/2017 1:22:15 PM


TIBA YA MAASUMINA

ASALI Mambo yake mahsusi: Asali ni kimiminika chenye rangi ya manjano, na aina nzuri ni ile ambayo inamiminika kutokana na mashudu bila kuchemshwa au mgandamizo. Na harufu yake ni nzito hasa, na ladha yake ni tamu sana. Na uzito wake ni 1.34, ina sukari nyingi, na harufu yake nzuri inatofautiana kulingana na tofauti ya maua ambayo imetengenezwa kwayo, na mara nyingi hughushiwa na wasio na ujuzi nayo, na ili kufichua hilo huwekwa kwenye maji ya moto, na pindi yanapopoa huongezwa elementi ya lodini na ikipatikana rangi ya bluu inajulisha juu ya uhalisia wake.

VIAMBATA VYA ASALI Asali ni maada ya kale zaidi miongoni mwa mada tamu alizozijua mwanadamu, na inarudi historia yake nyuma hadi miaka 5500 kabla ya kuzaliwa kwa Masihi Isa, Yesi mwana wa Mariamu, ambapo ilijugundulika huko Misri. Nayo ni mada kali mahsusi aitoayo nyuki. Na asali ziko za aina mbali mbali kulingana na aina ya nyuki na aina ya maua ambayo aliyofyonza. Na aina bora zaidi ya asali ni ile ambayo aliyovyonza kutokana na idadi kubwa ya maua. Na asali inakuwa ya kipekee kwani inahifadhika kutokana na kuharibika kwa muda mrefu hadi kufikia miaka miwili, kwa sharti ihifadhiwe mbali na unyevunyevu. Na sababu katika hilo ni kuzingira kwake juu ya kiua vijasumu (antibiotic) na tutakapoweka ndani yake kipande cha nyama hakika hakitoharibika, na inahifadhi uasili (freshness) wake kwa miezi mitatu. Na kwa hivyo inawezekana kui291

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 291

8/10/2017 1:22:15 PM


TIBA YA MAASUMINA

hifadhi ndani yake aina yoyote ya mbegu miaka 10 bila kuharibika. Na kwa sababu hii inatumika katika utengenezaji wa aina nyingi za madawa ya tiba, kwa kule kutoharibika kwake. Na katika uchanganuaji wa asali imepatikana ndani yake zaidi ya maada tofauti sabini, zilizo muhimu zaidi ni: 1.

Aina mbalimbali za sukari; wamegundua wasomi aina zisizopunga 15 za sukari katika asali, zilizo muhimu zaidi ni: Sukari ya matunda (fruktosi) asilimia 40% sukari ya zabibu (glukosi) asilimia 30%. Na ya kwanza ni lishe ya msingi kwa ajili ya ubongo, na ya pili ni nzuri mno kwa watoto kwani inanyonywa katika miili yao kichwani wala haihitajiki uchanganuzi.

2.

Kimeng’enya (cha hamira): Nayo ni ya dharura kwa mtu kwa ajili ya kumeng’enya mada (viasili) mbali mbali, mfano hamira ya shairi ambayo hugeuza wanga hadi kuwa sukari, na kimeng’enya cha lipase kinachoyeyusha mafuta.

3.

Aina mbali mbali za vitamini: Asali ina idadi kubwa ya vitamini kwa mwili, miongoni mwa vitamini hizo ni: vitamini A na vitamini B6, B5, B3, B1, B, na vitamini C na vitamini E na vitamini K.

4.

Baadhi ya asidi amino na protini nyingi; mfano asidi fomi, na vichangamsha mwili, na harufu nzuri.

5.

Madini chumvi: Mfano wa chumvi ya kalisiamu, potasiamu, sodiamu na magnesi na chuma na iodini.

6.

Kiua vijasumu (antibiotic) dhidi ya ukuaji wa vijidudu maradhi (bakteria).

7.

Homoni ya jinsia itokanayo na estrojeni. 292

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 292

8/10/2017 1:22:15 PM


TIBA YA MAASUMINA

Faida za asali: Hakika imethibitika kielimu kwamba asali inafaidisha uponyaji mkubwa wa maradhi miongoni mwa hayo ni: maradhi ya pua, sikio na koo, na maradhi ya upumuaji na mirija miwili, na maradhi ya mfumo wa ulainishaji, maradhi ya ngozi, maradhi ya macho, maradhi ya kike, maradhi ya chombo cha mishipa ya fahamu, kinga kutokana na kuharibika kwa meno, kinga ya watoto, maradhi ya saratani na mionzi. Na hakika ametaja Imam Ali Ridha (a.s) baadhi ya matumizi haya ya asali, na miongoni mwa hayo matumizi ni uponyeshaji wa maradhi ya pua, sikio na koo, na maradhi ya mfumo wa mmeng’enyo wa chakula. Hakika imebainika kuwa ulaji wa asali pamoja na maziwa ya moto au chai, baada ya kuichanganya asali na juisi ya limao, kwa muda wa kuanzia siku tatu hadi saba unapunguza kupatwa na mafua na fluu. Na vivyo hivyo hakika utumiaji wa asali unapunguza maumivu yafuatayo: maumivu ya uvimbe wa katikati ya mfupa unaowasiliana na katikati ya sikio unapooshwa kwa asali, maumivu ya kinywa baada ya kun’goa jino, maumivu ya koo maumivu ya pua. Na kwa upande wa maradhi ya mfumo wa umeng’enyaji chakula, hakika imethibitika faida ya asali katika kupambana na maradhi ya manjano na ini, na inasaidia umeng’enyaji wa chakula, kwa tindikali yake, na inatumika katika kupunguza tindikali katika mfuko wa chakula kwa ajili ya uponyaji wa vidonda vya tumbo, kama vile inavyotumika katika uponyaji wa maradhi ya kuhara na hasa hasa kwa watoto. Ukiachilia mbali mchango wa asali katika ziada ya hifidhi na kumbukumbu, na hiyo kwa sababu inachangamsha ubongo na inaupatia lishe na nguvu inayohitajika. Na Mwenyezi Mungu amesadikisha pale aliposema: 293

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 293

8/10/2017 1:22:15 PM


TIBA YA MAASUMINA

َ َّ َ َ ُّ َ ٰ َ ْ َ َ َّ َ َ ً ُ ُ َ ْ َ ‫الش َج ِر َو ِم َّما َي ْع ِر ُشو َن‬ ‫الن ْح ِل أ ِن َّات ِخ ِذي ِمن ال ِجب ِال بيوتا و ِمن‬ ‫وأوحى ربك ِإلى‬ ُ َّ ُ َّ ّ ُ ْ ْ ‫ات َف‬ ٌ ‫اس ُل ِكي ُس ُب َل َرّب ِك ُذ ُل اًل ۚ َي ْخ ُر ُج ِم ْن ُب ُط ِون َها َش َر‬ َ ‫الث َم‬ ‫اب‬ ‫ر‬ ‫ل‬ ‫ك‬ ‫ن‬ ‫م‬ ‫ي‬ ‫ل‬ ‫ك‬ ‫ثم‬ ِ ِ ِ ِ ِ َ ٰ ٌ َْ ُ َ ‫ف أ ْل َو ُان ُه فيه ش َف ٌاء ل َّلناس ۗ إ َّن في َذل َك آَل َي ًة ل َق ْوم َي َت َف َّك ُر‬ ‫ون‬ ‫مخت ِل‬ ِ ِ ِ ِ ِ ِ ِ ِ ٍ ِ “Na Mola Wako akampa wahyi nyuki kwamba, tengeneza nyumba katika milima, na katika miti na katika wanayoyajenga. Kisha kula katika kila matunda, na ufuate njia za Mola Wako zilizo dhalili. Na katika matumbo yao kinatoka kinywaji chenye rangi mbalimbali, ndani yake kina matibabu kwa watu. Hakika katika haya kuna ishara kwa watu wanaofikiri.”1308

Hadithi: Mtume (s.a.w.w) amesema: “Ni juu yenu kutumia asali, naapa kwa Yule ambaye nafsi yangu iko mikoni Mwake hakuna nyumba ambayo ndani yake ipo asali ila malaika wanaiombea msamaha nyumba hiyo, ikiwa mtu atakunywa zitaingia tumboni mwake dawa elfu moja itaondoa magonjwa elfu.”1309 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Yule anayekunywa asali kila mwezi mara moja, inaponywa magonjwa sabini.”1310 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Neema ya kinywaji ni asali, inachunga moyo na inaondoa baridi kifuani.”1311 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Yule anayetaka hifidhi basi ale asali.”1312   Sura 16 aya 68 na 69.   Ramzul-Sihat, uk. 11 cha Dahsurkhi. 1310   Makarimul-Akhlaq, uk. 165. 1311   Makarimul-Akhlaq, uk. 165. 1312   Makarimul-Akhlaq, uk. 165. 1308 1309

294

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 294

8/10/2017 1:22:15 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Vitano vinaondoa usahaulifu na vinazidisha hifidhi, na vinaondoa balgham ni; upigaji mswaki, funga, usomaji wa Qur’ani, asali na ubani (yaani kundur).1313 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Manukato yanaondoa majonzi, asali inazuia hasira kupanda, huondoa majonzi, na uangaliaji kijani kibichi unaondoa majonzi.”1314 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) mtu mmoja alimlalamikia Mtume (s.a.w.w) kuhisiana na maumivu anayoyakuta tumboni mwake, akasema: “Chukua kinywaji cha asali, na ingiza humo punje tatu za habasoda au tano au saba, na kunywa utapona kwa idhini ya Mwenyezi Mungu,” basi akafanya hivyo na akapona.”1315 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Asali ni ponyo inafukuza harufu na homa.”1316 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Msiache kunywa asali kwa yule anayekuleteeni.”1317 Mtu mmoja alimwambia Amirul-Muminina Ali (a.s): Hakika mimi ninakuta maumivu tumboni mwangu, akasema (a.s): “Je, una mke? Akasema: Ndio. Akasema: Chukua kutoka kwake kiasi kidogo cha mali yake iliyokuwa kwa kipendacho nafsi yake, kisha nunua asali kwayo, kisha mwagia ndani maji ya mvua, kisha kunywa, hakika mimi nimemsikia Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema: “Na tukateremsha kutoka mbinguni maji yenye baraka.”1318   Makarimul-Akhlaq, uk. 164, kutoka kitabu Firdausi.   Nahjul-Balaghah, hikma 400. 1315   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 72, kutoka kitabu Daaimul-Islam. 1316   Ramzul-Sihat, uk. 229. 1317   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 296. 1318   Surat Qaaf aya 9. 1313 1314

295

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 295

8/10/2017 1:22:15 PM


TIBA YA MAASUMINA

Na akasema: “Kinatoka katika matumbo yao kinywaji chenye rangi mbali mbali ndani yake kina matibabu kwa watu.”1319 Na akasema: “Lakini wakikupeni chochote kwa radhi ya nafsi katika hayo basi kileni kiwashuke kwa raha.”1320 na ikikusanyika baraka na ponyo na uzuri utaponya kwa utashi wa Mwenyezi Mungu.”1321 Imepokewa kutoka kwa Amirul-Muminina Ali (a.s) amesema: “Asali ni ponyo la kila ugonjwa wala hakuna ugonjwa ndani yake, inapunguza kikohozi na inasafisha moyo.”1322 Imepokewa kutoka kwa Imam Zaynul Abidina (a.s) amesema: “Lipozeni tumbo la mwenye homa kwa sawiiq (uji wa nafaka) na asali mara tatu, na unaigeuza chombo kimoja hadi kingine na utamnywesha mwenye homa, hakika hiyo inaondosha homa ya joto. Na hakika imefanywa kwa ufunuo.”1323 Imam Baqir (a.s) alimwambia mmoja wa masahaba wake: “Chukua udongo kutoka kwenye kaburi la Husein (a.s) na uuchanganye na maji ya mvua, na mwagia kiasi kidogo cha asali na zafarani, na isambaze kwa wafuasi wetu ili wawatibie wagonjwa wao.”1324 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Yule anayelala na tumboni mwake kuna samaki, na hakufuatilia kwa kula tende au asali, litaendelea kutoka jasho la kiharusi likipiga juu yake mpaka asubuhi.”1325 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Ni juu yenu kwa ponyo mbili, kutokana na asali na Qur’ani.”1326   Sura 16 aya 69.   Sura 4 aya 4. 1321   Majmau kutoka kwa Ayaashi. 1322   Makarimul-Akhlaq, uk. 166. 1323   Makarimul-Akhlaq, uk. 192. 1324   Mahasin cha Barqi. 1325   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 54. 1326   Makarimul-Akhlaq, uk. 165. 1319 1320

296

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 296

8/10/2017 1:22:15 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Yule anayetaka hifidhi basi na ale asali.”1327 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) katika barua ya dhahabu kwa Maamuni amesema: “Na jua ewe Amirul-Muminina hakika asali ina dalili inayotofautisha baina ya yenye manufaa kutokana na yenye madhara, hiyo ni kwa sababu ipo ambayo kama mtu atainusa atapiga chafya. Na ipo ambayo inalewesha na ni yenye uchachu mkali, hizi ni aina za asali zenye kuua.”1328 Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) amesema: “Yule ambaye yamebadilika maji yake ya mgongo, yatamnufaisha yeye maziwa na asali.”1329 Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) amesema; “Asali ni ponyo ya kila ugonjwa, ukiichukua kutoka kwenye masega yake. [umeichukua kutoka kwenye masega yake sasa hivi].1330 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Hakika Mwenyezi Mungu (s.w.t) amejaalia baraka kwenye asali, ndani yake kuna ponyo ya magonjwa, na hakika wameibariki hiyo manabii sabini.”1331 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Ni juu yenu kutumia asali na habasoda.”1332 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Katika asali kuna ponyo ya kila ugonjwa, na yule anayelamba asali kabla hajala kitu inakata balaghamu na inakata umanjano na inazuia nyongo nyeusi, na inasafisha ubongo, na inafanya uzuri hifidhi, ikiwa   Makarimul-Akhlaq, uk. 165.   Risaalat Dhahabiya, uk. 37 kimehakikiwa na Muhammad Mahdi Najaf. 1329   Makarimul-Akhlaq, uk. 165. 1330   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 74. 1331   Sahifatul-Ridha (a.s), uk. 90. 1332   Fiqhul-Ridha (a.s), uk. 346. 1327 1328

297

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 297

8/10/2017 1:22:15 PM


TIBA YA MAASUMINA

pamoja na ubani dhakar” [nao ni gundi ambalo linatokana na mti wa kundur].1333 Imepokewa kutoka ka Imam Ridha (a.s) amesema: “Ikiwa katika kitu kuna ponyo basi ni katika ufyonzaji damu na unywaji wa asali.”1334 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Vitatu vinazidisha hifidhi na vinaondoa kikohozi; usomaji wa Qur’ani, asali na ubani [kundur].”1335 Imepokewa kutoka kwa Imam Hadi (a.s) amesema: “Ulaji wa asali unasababisha kuwa na hekima.”1336 Mishipa Mtume (s.a.w.w) amsema: “Ni juu yenu kula zabibu, kwani inafichua nyongo, inaondoa kikohozi na inakaza mishipa…”1337 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Ni juu yenu kula zabibu, kwani inazima nyongo, inakula kikohozi na inakaza mishipa…”1338 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Kitunguu maji kinaondoa uchovu na kinakaza mishipa…”1339 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Zabibu inakaza mishipa, inaondoa uchovu na inafanya nafsi kuwa nzuri.”1340   Fiqhul-Rdha (a.s), uk. 346.   Sahifatul-Ridha (a.s), uk. 53. 1335   Sahifatul-Ridha (a.s), uk. 68. 1336   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 75. 1337   Khiswal, Juz. 1, uk. 344. 1338   Makarimul-Akhlaq, uk. 175. 1339   Khiswal, Juz. 1, uk. 158. 1340   Kashfuul-Akhtar cha Shamsu Diid bin Muhammad Huseini – mahtut. 1333 1334

298

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 298

8/10/2017 1:22:15 PM


TIBA YA MAASUMINA

Upigaji chafya Imam Ridha (a.s) amesema: “Hajapiga mpigaji chafya ila hulainika chakula chake, au kupiga miayo chakula chake huwa kizuri.”1341 MFUPA Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Sawiiq inaotesha nyama na inakaza mifupa.”1342 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuhusiana na ghubayraa amesema: “Hakika tunda lake linaotesha nyama, na kokwa yake inaotesha mfupa na ganda lake linaotesha ngozi…”1343 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Hakika Tiini inaondoa harufu ya kinywa na inakaza mifupa…”1344 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) alimwambia mmoja wa masahaba wake: “Basi ni juu yako kula mchadi, kwani huo unaota ufukweni mwa Firdausi, na ndani yake kuna ponyo la maradhi, nayo inaimarisha mifupa na inaotesha nyama.”1345 UBOHO ( UROJO WA MFUPA) Mtume (s.a.w.w) amesema: “Waovu wa umma wangu ni ni wale ambao wanakula uboho wa mifupa.”1346 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Ulaji wa maharagwe unazidisha uboho katika ugoko basi itakuwa ni saba  Fiqhul-Ridha (a.s), uk. 391.   Makarimul-Akhlaq, uk. 192. 1343   Makarimul-Akhlaq, uk. 176. 1344   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 133, kutoka kitabu Furuu Kaafi na Mahasin cha Barqi. 1345   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 159, kutoka kitabu Mahasin, na katika Makarimul-Akhlaq, uk. 181 na kinachofanana nacho. 1346   Ramzu-Sihat, uk. 9. 1341 1342

299

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 299

8/10/2017 1:22:15 PM


TIBA YA MAASUMINA

bu ya kuimarika kwake. Na pia huongeza uboho na kuzalisha damu safi.”1347 Kujistahi (mwanamke kujizuia na zinaa): Mtume (s.a.w.w) amesema: ‘Yule atakaye na uwezo wa kumtendea mwanamke au kijakazi (msichana) tendo la haramu, lakini akaacha kulitenda kwa kumuogopa Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu atamharamishia yeye moto, na atampa amani kutokana na hofu kubwa na atamuingiza peponi.”1348 Mtume (s.a.w.w) amesema: “Mtu hatakuwa na uwezo wa kutenda haramu, kisha akaiacha kwa sababu tu ya kumuogopa Mwenyezi Mungu, isipokuwa Mwenyezi Mungu atambadilishia yeye hapa duniani kabla ya akhera lile lililo bora kuliko haramu aliyotaka kuitenda.”1349 Mtume (s.a.w.w) amesema: “Watu saba watafunikwa kwenye kivuli cha Mwenyezi Mungu siku ambayo hakuna kivuli ila kivuli chake; … na mtu aliyeitwa na mwanamke mwenye cheo na uzuri, akasema hakika mimi ninamuogopa Mwenyezi Mungu Mola mlezi wa walimwengu.”1350 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Waheshimuni wanawake wa wengine, wataheshimiwa wanawake wenu.”1351 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Zaka ya uzuri ni kujizuia na maasi.”1352   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 100, kutoka kitabu Furuu al-Kaafi na Mahasin cha Barqi.   Wasaail-Shi’ah, Juz. 11, uk. 199. 1349   Kanzul-Ummal, hadithi no. 43113. 1350   Khiswal, Juz. 2, uk. 333. 1351   Biharul-Anwaar, Juz. 73, uk. 19. 1352   Ghurarul-Hikam. 1347 1348

300

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 300

8/10/2017 1:22:16 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam Baqir (a.s) amesema: “Hajaabudiwa Mwenyezi Mungu kwa kitu bora zaidi kuliko uzuiaji wa tumbo na tupu.”1353 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Kuvumilia dhidi ya matamanio ni kujistahi…”1354 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: ‘Astaha inadhoofisha matamanio.”1355 AKILI Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Mung’unya linaongeza akili na ubongo, nalo ni zuri kwa maumivu ya ugonjwa wa kukakamaa.”1356 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Mafuta ya balungi yanaufanya ubongo kuwa makini.”1357 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Ni juu yenu kutumia mung’unya, kwani linaimarisha ubongo (yaani katika uchangamfu wake).”1358 Mtume (s.a.w.w) amesema: “Ni juu yenu kula kursuf, kwani ikiwa kuna kitu kinachozidisha akili basi ni hicho.”1359 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Usingizi ni raha ya mwili, uzungumzaji ni raha ya roho na unyamazaji ni raha ya akili.”1360   Kaafi, Juz. 2, uk. 76 cha Kulaini.   Ghurarul-Hikam. 1355   Ghurarul-Hikam. 1356   Kashful-Akhtar, cha Shamu-Diin bin Muhammad Huseiniy – Makhtut. 1357   Kaafi, Juz. 6, uk. 522. 1358   Sahifatul-Ridha (a.s), uk. 76. 1359   Ramzu-Sihat, uk. 18 cha Dahsurkhi. 1360   Majalis, cha Sheikh Suduuq. 1353 1354

301

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 301

8/10/2017 1:22:16 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Mung’unya) linazidisha akili na ubongo, nalo ni zuri kwa ugonjwa wa kukakamaa kwa mwili.”1361 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Siki inaimaraisha akili.”1362 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Ni juu yenu kula pera, kwani linazidisha katika akili na murua.”1363 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Nyama inaotesha nyama na inaongeza akili, na yule ambaye atakayeiacha masiku kadhaa itaharibika akili yake.”1364 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Mwili umejengewa juu ya mambo manne; juu ya roho na akili, na damu na nafsi. Basi roho ikitoka akili inamfuata, na roho itakapoona kitu akili inakihifadhi juu yake, na inabakia damu na nafsi.”1365 Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) amesema: “Hakuna tatizo kwa utumiaji wa maji, kwani unapangilia chakula katika mfuko wa chakula, yanatuliza ghadhabu, yanazidisha uelewa, na yanazima nyongo.”1366 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) katika barua ya dhahabu amesema: “Na yule anayetaka aongeze akili yake basi ale kila siku halaylij tatu kwa sukari ya mimea (abliju).”1367   Kashful-Akhtar, cha Shamsu Diin bin Muhammad Huseini – mahtut.   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 65. 1363   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 131, kutoka kitabu Mahasin. 1364   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 139. 1365   Khiswal, Juz. 1, uk. 229. 1366   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 189, kutoka kitabu Furuu na Mahasin. 1367   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 324. 1361 1362

302

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 302

8/10/2017 1:22:16 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Hakika siki inaimarisha ubongo na inakuza akili.”1368 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kuhusiana na mchadi amesema: “Unaimarisha akili na unasafisha damu.”1369 Dr. Muhmuud Bastani anasema: Katika upande wa kiakili tunakuta nasaha juu ya utumiaji wa kila kinachotokana na: 1.

Siki: Kwa sifa yake inaimarisha akili.

2.

Pera: Kwa sifa yake linakuza akili.

3.

Mchadi: Kwa sifa yake unaimarisha akili.

4.

Mtishamba (ruta): Kwa sifa yake unakuza akili.

5.

Komamanga: Kwa sifa yake linaimarisha ubongo.

6.

Mung’unya: Kwa sifa yake linaimarisha ubongo na akili.

7.

Baaqila: Kwa sifa yake inaimarisha ubongo.

8.

Asali: Kwa sifa yake inaimarisha hifidhi.1370

UVAAJI WA PETE (AQIIQ) Mtume (s.a.w.w) amesema: “Vaeni pete ya Aqiiq, kwani hapatwi mmoja wenu na majonzi maadamu ameivaa.”1371 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Amenihadithia mimi Mtume (s.a.w.w) akasema: “Alinijia mimi Jibrail kabla   Wasaail-Shi’ah, Juz. 16, uk. 523.   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 159. 1370   Diraasat fi ilmi-Nafsi Islamiy, Juz. 2, uk. 240, chapa ya pili. 1371   Makarimul-Akhlaq, uk. 87. 1368 1369

303

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 303

8/10/2017 1:22:16 PM


TIBA YA MAASUMINA

akasema: Vaeni aqiiq, kwani hilo ni jiwe la mwanzo lililomshuhudia Mwenyezi Mungu kwa upweke Wake, na mimi kwa utume, na Ali kwa uwasii, na watoto wake kwa uimamu na kwa wafuasi wake pepo.”1372 Imepokewa kutoka kwa Salmani Farsi kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) alimwambia Ali (a.s): “Vaa pete ya Yemeni utakuwa miongoni mwa wakurubishwa. Akasema: Ewe Mtume ni nani wakurubishwa: Akasema: Jibrail na Mikail. Akasema: Ewe Mtume nitavaa pete gani? Akasema: “Aqiiq nyekundu, kwani hiyo ni jabali ambalo lilikiri upweke wa Mwenyezi Mungu, na utume wangu, na uwasii wako, na uimamu wa watoto wako, kwa wenye kukupenda wewe pepo na kwa wafuasi wako na watoto wako pepo ya Firdausi.”1373 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kutoka kwa baba zake (a.s) amesema: “Mtu mmoja alimlalamikia Mtume (s.a.w.w) kuwa amezuiwa njiani, akamwambia: Je, unavaa Aqiiq? Kwani hiyo inakulinda kutokana na kila ubaya.”1374 Imepokewa kutoka kwa Amirul-Muminina Ali (a.s) amesema: “Vaeni jiwe au kito” kwani hiyo inazuia vitimbi vya mashetani.”1375 Imepokewa kwamba alikuwa Amirul-Muminina Ali (a.s) ana pete nne; pete yenye kito cha yaquut nyekundu akivaa hiyo kwa utukufu wake na fadhila zake, na pete yenye kito cha Aqiiq nyekundu akivaa hiyo ili kujikinga na waovu, na pete yenye kito ya Feiruz akivaa hiyo ili kuwashinda maadui zake, na pete kito chake ni chuma cha china akivaa hiyo kwa nguvu zake. Na akawakataza wafuasi wake kuvaa pete ya chuma.”1376   Hadaiqul-Wardiyat, uk. 7.   Fadhail Amirul-Muminin cha Khawarzimi. 1374   Makarimul-Akhlaq, uk. 88. 1375   Makarimul-Akhlaq, uk. 89. 1376   Makarimul-Akhlaq, uk. 87. 1372 1373

304

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 304

8/10/2017 1:22:16 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Amirul-Muminina Ali (a.s) amesema: “Yule ambaye anavaa pete ya Aqiiq Mwenyezi Mungu atamvisha yeye amani na imani.”1377 Imepokewa kutoka kwa Amirul-Muminina Ali (a.s) amesema: “Vaeni pete ya Aqiiq mtabarikiwa, na mtakuwa katika amani kutokana na mabalaa.”1378 Imepokewa kutoka kwa Imam Baqir (a.s) amesema: “Yule anayevaa Aqiiq ataendelea kuangaliwa kwa wema maadamu ipo mkononi mwake, na ataendelea kuwa na kinga ya Mwenyezi Mungu juu yake.”1379 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Vaeni pete ya Aqiiq… na mwenye kuvaa pete hiyo akiswali swala yake inakuwa na daraja 40 zaidi kuliko ya yule aliyevaa pete a kito kingine.”1380 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Yule ambaye anavaa pete ya fedha yenye kito cha Aqiiq, hatokuwa fukura na hatopata ila lile lililo zuri zaidi.”1381 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Hakijainuliwa kiganja kuelekea kwa Mwenyezi Mungu kinachopendeza zaidi kwake ila kile ambacho kina Aqiiq.”1382 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Aqiiq ni hirizi ya safarini.”1383   Makarimul-Akhlaq, uk. 87.   Makarimul-Akhlaq, uk. 88. 1379   Makarimul-Akhlaq, uk. 88. 1380   Makarimul-Akhlaq, uk. 87. 1381   Makarimu-Akhlaq, uk. 88. 1382   Minhajul-Baraa’at, Juz. 3 uk. 451 kilicho hakikiwa na Kuhkumriy. 1383   Minhajul-Baraa’at, Juz. 3, uk. 451 kilicho hakikiwa na Kuhkumriy. 1377 1378

305

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 305

8/10/2017 1:22:16 PM


TIBA YA MAASUMINA

Mtu mmoja kati ya watu wa familia ya Abi Twalib alipita kwa Imam as-Sadiq (a.s) akiwa anapelekwa kwa mtawala, Imam akasema mpelekeeni pete ya Aqiiq, wakampelekea pete ya Aqiiq na hatimae hakupatwa na madhara yoyote.”1384 Na imepokewa kwamba: Rakaa mbili anazoziswali mtu akiwa amevaa Aqiiq ni bora zaidi kwake kuliko rakaa elfu moja bila ya kuvaa Aqiiq.”1385 AKIKA Akika ni mustahabu katika siku ya saba ya mtoto tangu azaliwe, nayo achinyiwe kondoo na nyama yake igaiwe mafukara, na hiyo inaitwa Akika. Kama vile ni mustahabu kumnyoa kichanga nywele za kichwa na kuzitolea sadaka ya hela kulingana na uzito wake, ni kufuata nyayo za bwana Mtume (s.a.w.w) kwani alifanya hinyo pindi walipozaliwa wajukuu zake Hasan na Husein (a.s). Imepokewa kwamba Mtume (s.a.w.w) wakati alipozaliwa Hasan (a.s) alimfanyia Akika ya kondoo na akamnyoa nywele za kichwa na akaamrisha itolewe sadaka ya hela kulingana na uzito wake. Na hakika alifanya vivyo hivyo wakati alipozaliwa Husein (a.s).1386 Na imepokewa katika hadithi nyingine kwamba Mtume (s.a.w.w) alitoa sababu ya kumnyoa nywele kichanga katika siku ya saba, kuwa nywele hizi ni nywele najisi, kwani zimeota katika mfuko wa uzazi baina ya uchafu, na akinyolewa zitaota sehemu yake nywele mpya tohara. Na sisi tunajua kutokana na tiba kwamba upunguzaji wa nywele unastawisha nywele na kuziimarisha, na hasa hasa nywele za kichanga.   . Minhajul-Baraa’at juz. 3 uk. 451 kilicho hakikiwa na Kuhkumriy.   Biharul-Anwaar, Juz. 44, uk. 136. 1386   Biharul-Anwaar, Juz. 44 uk. 136. 1384 1385

306

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 306

8/10/2017 1:22:16 PM


TIBA YA MAASUMINA

HADITHI Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Wanyoeni nywele watoto wachanga siku ya saba, na toeni sadaka ya hela mtakapowanyoa vichwa vyao kulingana na uzito wa nywele zao, kwani ni wajibu juu ya kila mwislamu. Vivyo hivyo amefanya bwana Mtume (s.a.w.w) kwa Hasan na Husein (a.s).1387 ZABIBU Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Pindi maji yalipokauka na mifupa ya wafu ikaonekana, nabii Nuh (a.s) alihuzunika sana na akapatwa na majonzi kwa hilo, basi Mwenyezi Mungu akamfunulia nabii Nuh (a.s): “Kula zabibu nyeusi ili yakuondokee majonzi yako.”1388 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Chakula chenu bora ni mkate, na matunda yenu bora ni zabibu.”1389 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Vuli la umma wangu ni zabibu na tikitimaji.”1390 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Kuleni zabibu punje baada ya punje, kwani ni tamu na zuri zaidi”1391 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Zabibu ni idaam na tunda na chakula na haluwa.”1392 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Zabibu inaimarisha mishipa, inaondoa uchovu na inapendezesha nafsi.”1393   Tuhful-Uquul, uk. 77.   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 118, kutoka kitabu Mahasin. 1389   Makarimul-Akhlaq, uk. 174. 1390   Makarimul-Akhlaq, uk. 174. 1391   Biharul-Anwaar, Juz. 66, uk. 174, na Sahifat Ridha (a.s), uk. 53. 1392   Makarimul-Akhlaq, uk. 174. 1393   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 70 cha Muhammad Khalili. 1387 1388

307

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 307

8/10/2017 1:22:16 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Mtume mmoja alilalamika kwa Mwenyezi Mungu kuhusiana na majonzi (naye nabii Nuh) basi akamwamrisha ale zabibu.”1394 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Matunda matano ya peponi yapo hapa duniani; komamanga malasiy, tufaha shamshani, pera, zabibu na tende mashan.”1395 Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) amesema: “Vitu vitatu havidhuru; zabibu Raaziqi, mua na tufaha la Lebanoni.”1396 ZABIBU Imepokewa kutoka kwa Amirul-Muminina Ali (a.s) amesema: “Zabibu inaondoa homa.”1397 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Fadhila ya zabibu kwa matunda, ni kama vile fadhila yetu kwa watu.”1398 Imepokewa kutoka kwa Ibn Abi Haswiin amesema: Macho yangu yalipatwa na weupe na nikawa sioni chochote kwayo, basi nikamuona Amirul-Muminina usingizini, basi nikasema: Ewe bwana wangu macho yangu, hakika unaniona kile kilichonisibu, akasema: “Chukua zabibu zisage na jipake kwenye nyusi. Basi nikachukua zabibu nikasaga kokwa zake na nikajipaka kwenye nyusi kwayo, basi likaniondokea giza machoni mwangu, na nimeliangalia mimi hilo basi likawa ni sahihi.”1399

Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 117.   Uyuun na Mahasin na Khiswal, Juz. 1, uk. 289 cha Saduuq. 1396   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 114, kutoka kitabu Khiswal, uk. 70. 1397   Makarimul-Akhlaq, uk. 199 cha Twabarasi. 1398   Makarimul-Akhlaq, uk. 176. 1399   Makarimul-Akhlaq, uk. 199 cha Twabarasi. 1394 1395

308

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 308

8/10/2017 1:22:16 PM


TIBA YA MAASUMINA

JICHO Rejea (uonaji) na (upakaji wanja): Mtume (s.a.w.w) amesema: “Hakuna ugonjwa ila ugonjwa wa jicho, wala majonzi ila majonzi ya dini.”1400 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Kam-at inatokana na neema ambayo Mwenyezi Mungu ameiteremsha juu ya wana wa Israil, nayo ni ponyo la jicho.”1401 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Kam-at ni miongoni mwa mimea ya peponi, maji yake ni yenye kunufaisha kutokana na ugonjwa wa jicho.”1402 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Kam-at ni miongoni mwa neema, na maji yake ni ponyo la jicho.” Imam Zaynul Abidiin (a.s) amesema: “Maelezo ya hilo ni kwamba achukue kam-ata na aioshe mpaka isafike, kisha aikamue na achuje kwa kitambaa, na achukue maji yake na ayaweke juu ya moto mpaka yakauke, kisha adondoshee humo matone ya miski, kisha aiweke hiyo ndani ya chupa, na ajipake kama vile wanja kutokana na maumivu yote ya jicho.”1403 Imepokewa kutoka kwa Amirul-Muminina Ali (a.s) amesema: “Jicho la Salman na la Abu Dharr (r.a) yalipatwa na maumivu basi wakaenda kwa Mtume (s.a.w.w) wakakutana naye akiwa anakwenda kuwajulia hali hao wawili, na alipowaangalia hao wawili akasema kumwambia kila mmoja wao: Usilalie upande wa kushoto maadamu yanakuuma macho yako, wala usikaribie tende mpaka Mwenyezi Mungu (a.j) akuponye.”1404   Biharul-Anwaar, Juz. 63, uk. 301.   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17 uk. 132. 1402   Mahasin, uk. 256. 1403   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 151 cha Allama Majlisi. 1404   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 85. 1400 1401

309

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 309

8/10/2017 1:22:16 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam Baqir (a.s) amesema: “Hakika samaki ni mbaya kwa kifuniko cha jicho.”1405 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s), kwamba alijiwa na mtu mmoja akisumbuliwa na jicho akamwambia: “Uko wapi wewe kutokana na viungo hivi vitatu; swabiru, kaafur na nyongo? Basi yule mtu akafanya hilo, na yakamuondokea maumivu.”1406 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Samaki anayeyusha mafuta ya jicho.”1407 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Mswaki unaondoa machozi na unapendezesha uonaji.”1408 Mtu mmoja alimlalamikia baba wa Abdillah (a.s) kuhusiana na weupe jichoni mwake, basi akamwamrisha achukue pilipili nyeupe na daru filfili,1409 kila moja kipimo cha dirham mbili, na amonia safi nzuri kipimo cha dirham, basi azisage zote, kisha achunge na apake kwenye nyusi zake, kwa kila jicho lenye kuhadaa, na asubiri katika hilo saa, kwani hiyo inakata weupe, na inasafisha nyama ya jicho, na inatuliza maumivu ya kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (s.w.t), kisha ataosha macho yake kwa maji ya baridi, kisha atafuatilia kwa wanja kwa kupaka kwenye nyusi zake.”1410 Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) amesema: “Matatu yanavuta uonaji; kuangalia kijani kibichi, kuangalia maji yatiririkayo na kuangalia uso mzuri.”1411   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 84.   Kaafi, Juz. 8, uk. 383. 1407   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 84. 1408   Mahasin, uk. 563. 1409   Daaru Filfil: ni mti wa pilipili wa mwanzo ambao hutoa matunda. 1410   Twibbul-Swadiq (a.s), uk. 54. 1411   Khiswal, uk. 44 cha Saduuq. 1405 1406

310

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 310

8/10/2017 1:22:16 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Salim huria wa Ali bin Yaqtiin, kwamba alikuwa akipata maumivu machoni mwake, basi Imam Kadhim (a.s) akamwandikia barua kwamba: “Kipi kinachokuzuia wewe kupaka wanja wa Abu Ja’far (a.s): Sehemu ya kafuur Riyahi, na sehemu ya swabiru isqartwarii, vinasagwa vyote na kuchungwa kwa kitambaa cha Hariri, anapaka kama anavyopaka wanja wa kawaida. Kujipaka wanja kwa mwezi mara moja kunakusanya maradhi ya kichwani na kuyatoa mwilini. Akasema: Na alikuwa akijipaka wanja huo (wa Abu Ja’far), na hakuwahi kulalamikia maradhi ya jicho lake mpaka alipokufa.”1412 Ibn Sina amesema: Na ama vitu ambavyo vinanufaisha matumizi yake kwa jicho na vinahifadhi nguvu yake, basi ni vitu vyenye kuchukuliwa kutokana na wanja na zinki pembe nne kwa maji ya marzanjushi na maji ya raaziyanji…1413 KUPATWA NA JICHO LA HUSDA Katika tafsiri ya Majmaul-Bayaan cha Twabarasi kuhusiana na kauli ya Mola Subhaana katika Surat Yusuf: “Enyi wanangu msiingie… tofauti”1414 Yaquub alihofia juu yao jicho la husda kwani wao walikuwa wazuri wenye haiba na ukamilifu. *Mtume (s.a.w.w) amesema: “Hakika jicho ni haki, na jicho linamteremsha mtu kutoka juu ya jabali.1415 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Hakika jicho la husda linamuingiza mtu kaburini na uzuri usio na kifani.”1416   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 150, kutoka kitabu Kaafi, Juz. 8, uk. 384.   Qanuun: kitabu cha tatu. 1414   Surat Yusuf, aya 67. 1415   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 319 cha Abdullah Shubbar. 1416   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 320 cha Shubbar. 1412 1413

311

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 311

8/10/2017 1:22:16 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa katika habari kwamba Mtume (s.a.w.w) alikuwa akiwalinda Hasan na Husein (a.s) akisema: “Ninakulindeni nyinyi wawili kwa maneno ya Mwenyezi Mungu yaliyokamilika. Kutokana na kila shetani na matatizo, pia kutokana na kila jicho baya la lawama.” Na sura mbili hizi za muawadhatain zilikuwa ni kinga ya Mtume (s.a.w.w) na Hasan na Husein dhidi ya kijicho, na maradhi mengine.”1417 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Yule anayeona kitu kinachomshangaza na akasema: Allah, Allah, Maashaallah, la haula wala Quwwata ila billah, hakitomdhuru chochote.”1418 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Lau ingelikuwa kitu kinatangulia Qadar, lingelitangulia jicho, na kutokana na kumsibu yeye jicho anasoma Surat Fatiha.”1419 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Jicho ni haki, wala usiliamini juu ya nafsi yako, wala juu ya mwingine, ukihofia kitu kutokana nalo, sema mara tatu; Maa shaallah la hawla wala Quwwata ila billahil-a’liyyil-Adhiim.”1420 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuhusu jicho amesema: “Audhu nafsi wa dhurriyati wa ahli bayti, bikalimaatillah taammat, min sharri kulli shaytwani wa haammat, wamin kulli sharri ayni laammat.”1421 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Lau mngelifukuliwa makaburi mngeliona zaidi ya wafu wenu kwa macho, kwa sababu jicho ni haki, hakika Mtume (s.a.w.w) amesema:   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 320.   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 320. 1419   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 320. 1420   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 320 1421   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 320. 1417 1418

312

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 312

8/10/2017 1:22:16 PM


TIBA YA MAASUMINA

“Jicho ni haki, basi yule anayevutiwa na kitu kutoka kwa ndugu yake basi amtaje Mwenyezi Mungu katika hilo, na akimtaja Mwenyezi Mungu hatomdhuru yeye.”1422 GHUBAYRAA Maana yake: Ni mmea unaotokana na mche wa waridi, ndani yake kuna aina za harajiyay, tunda lake linashabihiana na zabibu. Khususia zake: Maua yake akinusa mwanamke inasisimka haja ya matamanio ya tendo la ndoa, mpaka anatupilia mbali haya na hali yake ya kujilinda nyuma ya mgongo wake.1423 Faida zake: Ghubayraa inaondoa umanjano wenye kumwagiwa kwenda viungo vya tumbo, na inakata kuvuja, na inazuia kikohozi, na inazuia utapikaji, inafunga choo, na inasaidia kwa mtu mwenye tatizo kwenda haja ndogo mara kwa mara. Hadithi: Imepokewa kutoka Imam Ridha (a.s) amesema: “Aliingia Mtume (s.a.w.w) kwa Ali bin Abi Twalib (a.s) naye akiwa mwenye homa, basi akamwamrisha yeye kula Ghubayraa.”1424 Imepokewa kutoka kwa Ibn Bakiir amesema: Nilimsikia Imam as-Sadiq (a.s) akisema kuhusiana na Ghubayraa: “Hakika   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 320.   Ajaaibul-Makhluqaat, cha Qazwiini, mwishoni mwa kitabu Hayatul-Hayawan Juz. 2, uk. 171. 1424   Sahifatu-Ridha (a.s), uk. 80. 1422 1423

313

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 313

8/10/2017 1:22:16 PM


TIBA YA MAASUMINA

tundaa lake linaotesha nyama, na kokwa yake inaotesha mfupa, na ganda lake linaotesha ngozi. Na pamoja na hivyo hakika inachemsha figo, na inalainisha mfuko wa chakula, nayo ni amani ya bawasiri na utokaji matone wa haja ndogo, na inatia nguvu ngoko mbili, na inakata mizizi ya mbalanga kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.”1425 KUOGA Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Kuoga kwa ajili ya Eid ni tohara kwa yule ambaye anayetaka kuomba haja mbele ya Mwenyezi Mungu (a.j) na ni ufuataji wa Sunnah.”1426 Ufuaji wa nguo unaondoa majonzi na ni tohara ya swala.”1427 Majonzi Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: Mwenyezi Mungu alimfunulia Nabii Nuhu (a.s) baada ya kuona mfupa wa mfu baada ya tufani: Kula zabibu nyeusi yataondoka majonzi yako.”1428 Imepokewa kutoka kwa Masiih Nabii Isa (a.s) amesema: “Yule ambaye yamezidi majonzi yake huumwa mwili wake.”1429 Mtume (s.a.w.w) amesema: “Ni juu yenu kula zabibu, kwani hiyo inaondoa uchungu… inapendezesha nafsi, na inaondoa majonzi.”1430 Imepokewa kutoka kwa Amirul-Muminina Ali (a.s) amesema: “Ni juu yenu kutumia mafuta, kwani yanaondoa muwasho, yanaondoa kikohozi, yanaimarisha mishipa na yanaondoa uchovu, na   Makarimul-Akhlaq, uk. 176.   Tuhful-Uquul, uk. 72. 1427   Tuhful-Uquul, uk. 73. 1428   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 118, kutoka kitabu Furuu al-Kaafi. 1429   Biharul-Anwaar, Juz. 72, uk. 260. 1430   Khiswal, Juz. 1, uk. 344 cha Saduuq. 1425 1426

314

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 314

8/10/2017 1:22:16 PM


TIBA YA MAASUMINA

yanamfanya mtu awe na tabia nzuri, na yanapendezesha nafsi na yanaondoa majonzi.”1431 Imepokewa kutoka kwa Amirul-Muminina Ali (a.s) amesema: “Yule aliyelalamikia kifua chake na kuzidi majonzi yake, basi ale kwale (naye ni ndege anayefanana na sikipi ni mkubwa zaidi yake.)”1432 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Majonzi yanakondesha mwili.”1433 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Huzuni inadhoofisha mwili.”1434 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Majonzi yanaleta maradhi ya nafsi.”1435 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Yule anayepata majonzi bila kujua sababu yake, basi aoshe kichwa chake.”1436 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Mmoja wa manabii miongoni mwa manabii alilalamika kwa Mwenyezi Mungu kuhusiana na majonzi, basi akamwamrisha kula zabibu.”1437 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Zabibu inaimarisha mishipa, inaondoa uchovu, na inapendezesha nafsi.”1438   Makarimul-Akhlaq, uk. 190.   Makarimul-Akhlaq, uk. 161. 1433  Ghurarul-Hikam. 1434   Ghurarul-Hikam. 1435   Ghurarul-Hikam. 1436   Biharul-Anwaar, Juz. 76, uk. 323. 1437   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 117. 1438   Twibbu Swadiq (a.s), uk. 70, Kashful-Akhtar cha Shamsu Din bin Muhammad Huseini, Mahtut. 1431 1432

315

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 315

8/10/2017 1:22:16 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Pera linaondoa majonzi ya mwenye huzuni, kama vile mkono unavyoondoa jasho ya paji la uso.”1439 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Mkipika chakula basi zidisheni mung’unya, kwani hilo linaleta wepesi wa moyo wa mwenye huzuni.”1440 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Vaeni pete ya Aqiiq, kwani hiyo haimpatii yeyote miongoni mwenu majonzi maadamu ameivaa.”1441 TUNDA Mtume (s.a.w.w) amesema: “Ni juu yenu kula matunda pindi unapowadia wakati wake, kwani hayo yanaleta afya kwa miili, yanaondoa huzuni, na yatupeni pindi unapopita muda wake kwani yanaleta ugonjwa kwenye miili.”1442 Imepokewa kuwa: Kula tunda lile unalolikuta katika mji wake, na bora zaidi ni komamanga na furungu, na kuhusiana na manukato ni waridi na balungi, na kuhusiana na mboga mboga ni hindubaau na khissi, na bora zaidi ya maji ni maji ya mito mikubwa, na yaliyobaridi zaidi na safi zaidi.”1443 Impokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Alikuwa Mtume (s.a.w.w) anapoliona tunda jipya hulibusu na huliweka juu ya macho yake na mdomo wake, kisha anasema: Ee Mwenyezi Mungu kama ulivyotuonesha mwanzo wake katika afya, basi tuoneshe mwisho wake katika afya.”1444   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 130, kutoka kitabu Furuu Kaafi.   Sahifatul-Ridha (a.s), uk. 54. 1441   Sahifatul-Ridha (a.s), uk. 62. 1442   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 296. 1443   Mustdrak, Juz. 3, uk. 199. 1444   Makarimul-Akhlaq, uk. 146, kutoka kitabu Aamali cha sheikh Saduuq. 1439 1440

316

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 316

8/10/2017 1:22:16 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Hakika kila tunda lina sumu (huenda inakusudiwa sumu ya vijidudu vidogo ambavyo viko juu yake) basi mtakapolipata liosheni kwa maji.”1445 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Pindi Mwenyezi Mungu alipomteremsha Adam (a.s) kutoka peponi, alimteremsha akiwa pamoja na matunda 120; 40 kati ya hayo yanaliwa ndani yake na nje yake, na 40 kati ya hayo yanaliwa nje yake na yanatupwa ndani yake, na lipo ambalo lina mbegu ya kila kitu.”1446 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kwamba: “Alikuwa yeye akichukia umenyaji wa tunda.”1447 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Matunda matano ni ya peponi na yapo hapa duniani; komamanga malasi, tufaha la isfahani, pera, unay na tende mashani.”1448 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Hakika matunda yakiiva ndani yake kuna ponyo, kwa mujibu wa kauli ya Mwenyezi Mungu (a.j) anasema: “Angalieni matunda yake yanapopamba na kuiva kwake.1449”1450 Faliji/Kiharusi Maana yake: Ugonjwa wa kupooza upande mmoja wa mwili, basi unabatilisha hisia zake na harakati zake, na huenda ukawa katika kipanda uso, na unazuka ghafla.1451   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 115, kutoka kitabu Furuu na Mahasin.   Khiswal, Juz. 2, uk. 601. 1447   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 115. 1448   Mahasin na Khiswal, Juz. 1, uk. 289. 1449   Sura 6 aya 99. 1450   Fiqhul-Ridha (a.s), uk. 347. 1451   Safinatul-Bihar, Juz. 2, uk. 384 cha Sheikh Abbas Qummi. 1445 1446

317

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 317

8/10/2017 1:22:16 PM


TIBA YA MAASUMINA

Hadithi: Mtume (s.a.w.w) amesema: “Miongoni mwa alama za Kiyama ni kudhihirika kiharusi na vifo vya ghafla.”1452 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Ulaji wa tikitimaji kabla ya kula chochote unasababisha kiharusi.”1453 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Yule anayelala tumboni mwake kuna samaki, na hakufuatilizia kula tende au asali, mshipa wa kiharusi utaendelea kumgonga mpaka anapoamka asubuhi.”1454 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuhusiana na sanamaki amesema: “Ama hilo ni amani ya bahaqi, ukoma na mbalanga, uwenda wazimu, kiharusi na ukosefu wa nguvu.”1455 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Msiwakaribie wanawake mwanzo wa usiku… kwani ikitunga mimba mtoto atakayezaliwa atakuwa na mingurumo ya tumbo na kiharusi…”1456 FIGILI Faida zake: Ikiliwa figili baada ya kitunguu saumu inakata harufu ya kitunguu saumu. Na udumishaji wa ulaji wake unasafisha mfuko wa chakula. Na ikiwa atakula mwanamke aliyejifungua basi huzidi maziwa yake, na ikiwa watakula wanaume huimarisha katika nguvu ya ufahamu wao.   Biharul-Anwaar, cha Allama Majlisi.   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 139. 1454   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 54. 1455   Makarimul-Akhlaq, uk. 188. 1456   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 327 cha Allama Majlisi. 1452 1453

318

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 318

8/10/2017 1:22:17 PM


TIBA YA MAASUMINA

Mbegu zake zinachochea tendo la ndoa ikiwa zitaliwa, na zinafaidisha uondoaji wa sumu. Na majani yake yanafanya uonaji wa macho kuwa mkali, na huongeza maziwa.1457 Hadithi: Nabii Musa (a.s) katika kitabu Telmud amesema: Na akasema mwalimu: “Figili inasaga chakula ndani ya mfuko wa chakula, na khissi inakigeuza na tango linanyoosha tumbo.”1458 Imepokewa kutoka kwa Amirul-Muminina Ali (a.s) amesema: “Mzizi wa figili unakata kikohozi, unameng’nya chakula, na majani yake yanapunguza haja ndogo.”1459 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Mizizi ya figili inakata kikohozi, moyo wake unameng’enya chakula, na majani yake yanapunguza haja ndogo kabisa.”1460 Na imekuja katika hadithi kwamba: “Majani yake yanarahisisha mmeng’enyo wa chakula.”1461 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Kula figili hakika ndani yake kuna mambo matatu; majani yake yanaondoa harufu mbaya, moyo wake unapunguza haja ndogo (na mmeng’enyo wa chakula) na mizizi yake inakata kikohozi.”1462 Kinywa Imepokewa kutoka kwa Abdullah bin Hasan (a.s) amesema: “Kuleni komamanga kwani linasafisha vinywa vyenu.”1463   Ajaaibul-Makhluqaat, cha Qazwiini, mwishoni mwa kitabu Hayatul-Hayawan, Juz. 2, uk. 192. 1458   Telmud ya Baabaly tarjuma ya Nabiil Fayadh uk. 45. 1459   Makarimul-Akhlaq, uk. 182. 1460   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 163, kutoka kitabu Furuu Kaafi. 1461   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 163, kutoka kitabu Furuu na Mahasin. 1462   Furuu Kaafi, Juz. 6, uk. 371 na kitabu Khiswal, Juz. 1, uk. 144. 1463   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 121. 1457

319

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 319

8/10/2017 1:22:17 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Kitunguu maji kinapendezesha kinywa, kinaimarisha mgongo na kinafanya ngozi kuwa nyororo.”1464 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Vinywa vyenu ni njia miongoni mwa njia za Mola Wenu, basi visafisheni kwa kupiga mswaki.”1465 Maharage Virutubisho vyake: Ina protini nyingi na mamia ya kaboni, na madini ya chumvi mfano wa kibiriti, kalisiamu, elementi ya njano na chuma, na vitamini lukuki kama vile vitamini E, K, A, B1 na PP na vitamini C. Faida zake: Yakisagwa na kuwa laini yana manufaa makubwa kwa mwenye uvimbe wenye maumivu, kama vile katika matiti na tupu mbili. Vivyo hivyo kinena cha mtoto kikifungwa bendeji kwa unga wa maharagwe kwa muda mrefu hakitaota nywele. Na maharage ni mazuri kwa mwenye kikohozi, na yananenepesha mwili.1466 Hadithi: Mtume (s.a.w.w) amesema: “Kilikuwa chakula cha Nabii Isa (a.s) ni maharage hadi aliponyanyuliwa, na Isa (a.s) hakula chochote kilichobadilishwa na moto mpaka aliponyanyuliwa.”1467   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 168, kutoka kitabu Furuu na Mahasin.   Sahifatul-Ridha (a.s), uk. 54. 1466   Mufradaat Nabataat Twayyibat, uk. 445 kimeandikwa na Ahmad Saleh Damiscus. 1467   Makarimul-Akhlaq, uk. 183. 1464 1465

320

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 320

8/10/2017 1:22:17 PM


TIBA YA MAASUMINA

Mtume (s.a.w.w) amesema: “Yule anayekula maharage na ganda lake, Mwenyezi Mungu (a.j) atamuondolea yeye ugonjwa mfano wake.”1468 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Ulaji wa maharage unaimarisha ngoko mbili, na unaimarisha ubongo na unaongeza damu.”1469 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Kuleni maharagwe na maganda yake, kwani hilo linalainisha mfuko wa chakula.”1470 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “maharage yanaondoa ugonjwa na wala hana maradhi.”1471 Quthau na Tango Maana yake: Morocco: Tango ndilo hutumiaka kama Quthau, na hilo limeelezwa wazi wazi na Jawhari. Na inadhihiri kutokana na baadhi ya matabibu kwamba Quthau ni refu lenye kupinda. Manufaa ya tango: Tunda lake lina manufaa kutokana na homa zemye joto kali, na husukuma haja ndogo, kwa wakati huohuo linaleta kiu kwa sababu ya kutokukubaali kubadilika kuwa umanjano. Manufaa ya Quthau: Ama Quthau, hakika tunda lake linatuliza kiu, linatia nguvu ufizi, linaondoa joto kwa mtu mwenye kuzimia.1472   Makarimul-Akhlaq, uk. 183.   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 100, kutoka kitabu Furuu Kaafi na Mahasin. 1470   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 101, kutoka kitabu Mahasin cha Barqi. 1471   Makarimul-Akhlaq uk. 183. 1472   Ajaaibul-Makhluqaat cha Qazwiini, mwishoni mwa kitabu Hayatul-Hayawan, Juz. 2, uk. 193. 1468 1469

321

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 321

8/10/2017 1:22:17 PM


TIBA YA MAASUMINA

Na kuhusu hilo mshairi mmoja amesema: Liangalie hilo ni kama chupa – iliyovishwa zamaradi ya kijani isiyo na majani Ukiligeuza jina lake litabainika mng’ao wake – kuakisi kwake ni ujumbe usemao; hakika mimi ninawaamini. Hadithi: Nabii Musa (a.s) katika Telmud amesema: “Na akasema mwalimu: “Figili inasaga chakula katika mfuko wa chakula, na khissi inakigeuza na tango linanyoosha tumbo.” Kisha akasema: “Lakini Ismail hakuwafundisha wanafunzi wake kwamba tango linadhuru mfuko wa chakula kama upanga? hakuna tatizo lolote katika hilo, kwa sababu mmoja anazungumzia tango kubwa (lenye faida) na mwingine anazungumzia dogo (lenye kudhuru”.”1473 Alikuwa Mtume (s.a.w.w) akila tango kwa chumvi, na akila tikitimaji kwa jibini…”1474 Amesema bibi Aisha: Ninenepesheni kwa kila kitu wala sinenepi, na ninenepesheni kwa tango na tende, basi nitanenepa.”1475 Kutokana na hadithi ya Abdullah bin Ja’far amesema: Nilimuona Mtume (s.a.w.w) akiwa anakula tende na tango.”1476 Imepokewa kutoka kwa A’mmat kutoka kwa Abdullah bin Ja’far kwamba amesema: Nilimuona Mtume (s.a.w.w) katika mkono wake wa kulia akiwa na quthau na katika mkono wake wa kushoto akiwa na tende, naye mara akila hili na mara akili hili.”1477   Telmud Baabaly, tarjuma ya Nabiil Fayadh uk. 45.   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 299. 1475   Twibbu Nabiy, uk. 81 cha Ibn Qaym Jawziyyat. 1476   Twibbu Nabii, uk. 80 cha Ibn Qaym Jawziyyat. 1477   Ramzu Sihat, uk. 236 cha Dahasurkhi. 1473 1474

322

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 322

8/10/2017 1:22:17 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: ‘Mtakapokula qithau basi kuleni kuanzia chini yake, kwani kufanya hivyo kuna baraka kubwa mno.”1478

KUJITIBU KWA QUR’ANI Mtume (s.a.w.w) amesema: ‘Matano yanaondoa usahaulifu, yanaongeza hifidhi, na yanaondoa balgham; upigaji mswaki, funga, usomaji wa Qur’ani, asali na ubani (kundur).”1479 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Yule asiyetaka kujitibu kwa Qur’ani Mwenyezi Mungu hamtibii.”1480 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Hasan (a.s) alipatwa na ugonjwa na hatimae ukamzidia, Fatimah (a.s) akamchukua na kumpeleka kwa Mtume (s.a.w.w) akimuomba msaada akamwambia: Ewe Mtume muombe Mwenyezi Mungu ili amponye mwanao huyu, na akamweka mbele yake, basi Mtume (s.a.w.w) akasimama hadi alipokaa mbele ya kichwa chake, kisha akasema: Ewe Fatimah ewe binti yangu hakika Mwenyezi Mungu Yeye ndiye aliyekuzawadia wewe huyu, naye ni mwenye uwezo wa kumtibu yeye. Basi hapo akateremka Jibrail (a.s) akasema: Ewe Muhammad, hakika Mwenyezi Mungu (a.j) hakuteremsha kwako Sura miongoni mwa sura za Qur’ani ila ndani yake ipo herufi Fau, na kila Fau inatokana na maafa (madhara), isipokuwa Surat al-hamdu, kwani hiyo hakuna ndani yake Fau, itisha chombo cha maji uyasomee Surat Alhamdu mara 40, kisha mmwagie, hakika Mwenyezi Mungu atamponya. Basi akafanya hivyo, akachangamka akawa kana kwamba ni mtu aliyeachiwa huru.”1481   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 166, kutoka kitabu Furuu Kaafi na Mahasin.   Makarimul-Akhlaq, uk. 164, kutoka kitabu Firdausi. 1480   Makarimul-Akhlaq, uk. 363. 1481   Ramzu-Sihat, uk. 33 cha Dahsurkhi. 1478 1479

323

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 323

8/10/2017 1:22:17 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) amesema: “Ndani ya Qur’ani kuna ponyo la kila ugonjwa.”1482 Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) amesema: “Yule atakayetaka kujitosheleza kwa aya za Qur’ani kutoka mashariki na magharibi zitamtosheleza, ikiwa ni kwa yakini.”1483 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Matatu yanaongeza hifidhi na yanaondoa kikohozi; usomaji wa Qur’ani, asali na ubani” (kundur).1484

Mung’unya Faida zake: Inatajwa kwamba Mtume (s.a.w.w) alikuwa akipenda kula mung’unya, na aina ya tango kwa sababu ya ubaridi wake linapokuwa tumboni. Na mung’unya linalainisha ubongo, na ni lenye kuondoa vizuizi, linasukuma haja ndogo, linalainisha mfuko wa chakula, na lenye kumsaidia mwenye homa ya manjano na homa kali. Na linatumiwa kwa wingi na wale ambao wenye kutokwa zaidi na jasho. Na ama wale ambao imepungua nguvu na akili zao kutokana na utu uzima ni juu yao kuzidisha kula mung’unya, kwani ndani yake kuna faida mahsusi yenye kuongeza chembechembe hai na nguvu. Na Qar’u inaua minyoo ya tumbo na tegu. Na linaondoa kuvimbiwa na ni kiuavijasumu cha vijidudu vya maradhi ya kufunga haja ndogo. Hadithi: *Mtume (s.a.w.w) alimwambia Ali (a.s): “Kula Yaqtwiin (mung’unya), kwani mwenye kula hilo tabia yake inakuwa nzuri,   Makarimul-Akhlaq, uk. 363.   Makarimul-Akhlaq, uk. 363. 1484   Sahifatul-Ridha (a.s), uk. 68. 1482 1483

324

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 324

8/10/2017 1:22:17 PM


TIBA YA MAASUMINA

unang’ara uso wake, nacho ni chakula changu na chakula cha manabii wa kabla yangu.”1485 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Ikiwa mmoja wenu atachukua mchuzi, basi azidishe ndani yake mung’unya, kwani linaimarisha ubongo na akili.”1486 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Yule anayekula mung’unya kwa adesi, moyo wake utakuwa mwepesi mbele ya Mwenyezi Mungu, na anaongeza hamu ya tendo la ndoa.”1487 Imepokewa kutoka kwa Amirul-Muminina Ali (a.s) amesema: “Mmea wa Yaqtwiin nao ni dubbau, nalo ni Qar’u (mung’unya).”1488 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s), Amirul-Muminina Ali (a.s) amesema: “Kuleni mung’unya, na sisi watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w) tunalipenda hilo.”1489 Imepokewa kutoka kwa Dharih amesema: Nilimuuliza Imam asSadiq (a.s): Hadithi iliyopokewa kutoka kwa Amirul-Muminina (a.s) kuhusiana na mung’unya, kwamba amesema: “Kuleni mung’unya, kwani linaimarisha ubongo. Basi Imam as-Sadiq (a.s) akasema: Ndio, na mimi ninasema: Hakika hilo ni zuri kwa maumivu ya ugonjwa wa kukakamaa.”1490 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Mtakapopika chakula basi zidisheni mung’unya, kwani linafurahisha moyo wa mwenye huzuni.”1491   Biharul-Anwaar, Juz. 66, uk. 229.   Ramzu-Sihat, uk. 15. 1487   Makarimul-Akhlaq, uk. 177. 1488   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 172, kutoka kitabu Mahasin cha Barqi. 1489   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 138. 1490   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 138. 1491   Sahifatul-Ridha (a.s), uk. 54. 1485 1486

325

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 325

8/10/2017 1:22:17 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Juu yenu kula mung’unya kwani hilo linaimarisha ubongo” (yaani linatia nguvu ya kufikiri).1492

KARAFUU Maana yake: Nayo ni chipukizi (bira’m) la karafuu yenye harufu ya uturi kabla ya kuchanua, na inaletwa hiyo kutoka visiwa vya India ya mashariki. Umbo lake ni kama vile umbo la msumari, nayo ina kichwa chenye meno manne, yaliyo juu yake, ni yenye kujifumba sio yenye kufunguka, na rangi yake ni kahawiya yenye kuiva, na ladha yake ni yenye kuwasha. Na ikikandamizwa kwa kucha inatoa mafuta yenye rangi ya manjano yenye kuiva mwanzoni, kisha yanabadilika na kuwa kahawia. Na uzito wake ni 1,055. Na karafuu ina utomvu na msokoto. FAIDA ZAKE: Karafuu inazindua ina harufu nzuri na inaondoa harufu mbaya, inatumiwa ili kutuliza utapikaji kwa wajawazito, na ili kukabiliana na upepo katika mfumo wa mmeng’enyo. Na mafuta yake huongezwa kwenye vilainishi. Na inawekwa katika dawa za meno ili kupunguza maumivu yake. Ibn Siina amesema: “Tunda la karafuu linaimarisha tendo la ndoa, linasafisha macho kuondoa ukungu. Mwingine amesema: Linaondoa kichefuchefu, na harufu yake inatia nguvu ubongo baridi ambao umezidiwa na weusi, na inautia nguvu moyo na kuufurahisha.1493   Sahifatul-Ridha (a.s), uk. 76.   Ajaaibul-Makhluqaat cha Qazwiini, mwishoni mwa kitabu Hayatul-Hayawan Juz. 2, uk. 172.

1492 1493

326

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 326

8/10/2017 1:22:17 PM


TIBA YA MAASUMINA

Hadithi: Miongoni mwa madawa na miti shamba ambayo inasababisha hifidhi ni ile aliyoipokea Ibn Masuod kutoka kwa Mtume (s.a.w.w), pia inakata balgham na haja ndogo, na inatia nguvu mgongo: inachukuliwa uzito wa dirham 10 ya karafuu, na uzito wa dirham 10 za harmala, na sehemu ya kundur nyeupe, na sukari nyeupe, zinasagwa zote na kuchanganywa… na inaliwa hiyo asubuhi kwa uzito wa dirham, na wakati wa kulala.1494 Na miongoni mwa madawa ya hifidhi, imepokewa kutoka kwa Abi Baswiir amesema: Nilimuuliza Imam as-Sadiq (a.s): Vipi tunaweza kuitekeleza elimu hii ambayo umetupatia? Akasema: “Chukua kipimo cha uzito wa dirham 10 za karafuu, na kundur dhakar mfano wake, isage iwe laini kisha itumie kidogo kabla ya kula kitu kila siku” (dirham – ni sawa ¾ ya gram).1495

QUST (UDI WA KIHINDI NA KIARABU) Qust: Udi wa kihindi na kiarabu, unaimarisha na kunufaisha mno ini, na inaondoa minyoo na homa ya vipindi kwa kunywa, na mafua na uchafu wa kooni kwa kufukiza, na ukurutu na mabaka ya ngozi hasa kwa wanawake wajawazito kwa kupaka. Na Qust iko ya aina mbili: Mojawapo ni nyeupe ambayo inaitwa ya bahari. Na nyingine ya kihindi, nayo ni yenye joto zaidi, na nyeupe ni laini zaidi. Na manufaa ya zote mbili ni mengi zaidi, na hizo aina mbili ni za joto yabisi, zinaondoa kikohozi, zinakata mafua. Na mtu akinywa hizo mbili hunufaisha kutokana na udhaifu wa ini na mfuko wa chakula na kutokana na ubaridi wake, na kutokana na homa ya kizunguzungu na ya vipindi. Na zinaondoa maumivu ya   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 271, kutoka Jannat cha Kafu’amiy.   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 272.

1494 1495

327

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 327

8/10/2017 1:22:17 PM


TIBA YA MAASUMINA

mbavu na sumu. Na unga wake ukichanganywa na asali na maji na akatumia kujipaka usoni husaidia kuondoa mabaka. HADITHI: Mtume (s.a.w.w) amesema: “Kitu bora kati ya vile mnanyojitibu nanyo ni ufyonzaji damu na udi wa qust bahari.”1496 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Ni juu yenu kutumia huu udi wa kihindi, hakika ndani yake kuna maponyo saba, miongoni mwa hayo ni kwa mwenye janaba.”1497 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Kitu bora kati ya vile mnavyojitibia navyo ni; ufyonzaji wa damu, habasoda na qust.”1498 MOYO Mtume (s.a.w.w) amesema: “Yule anayetaka ulainike moyo wake, basi adumishe ulaji wa Tiini.”1499 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Vitatu vinafanya moyo kuwa mgumu; kusikiliza upuuzi, kupenda uwindaji na kwenda kwenye mlango wa sultan.”1500 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Manne vinaua moyo; dhambi juu ya dhambi, kuzidisha kujadiliana na wanawake (kuzungumza nao), kubishana na mpumbavu, ambaye unasema naye anasema wala harejei kwenye kheri, na kukaa na wafu. Ikaulizwa: Ewe Mtume! Ni nani hao wafu? Akasema: Kila tajiri mfujaji.”1501   Ramzu-Sihat, uk. 19, cha Dahsurkhi, kutoka kitabu cha Twibbu Nabawy.   Ramzu-Sihat, uk. 19, cha Dahsurkhi. 1498   Ramzu-Sihat, uk. 19 cha Dahsurkhi 1499   Makarimul-Akhlaq, uk. 173. 1500   Biharul-Anwaar, Juz. 75, uk. 370. 1501   Biharul-Anwaar, Juz. 73, uk. 349. 1496 1497

328

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 328

8/10/2017 1:22:17 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Kinywaji bora ni asali, inalainisha moyo, inaondoa ubaridi wa kifua.”1502 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Ndani ya mtu kuna sagio linaposalimika na kuwa na afya utasalimika mwili wote, basi likiugua unaugua mwili wote na kuharibika, nalo ni moyo. Na akasema (s.a.w.w): “Moyo wa mtu unapokuwa salama na mwili wake unasalimika, na moyo unapoharibika na mwili wote unaharibika.”1503 Imepokewa kutoka kwa Amirul-Muminina Ali (a.s) amesema: “Kukithirisha chakula kunaua moyo, kama wingi wa maji unavyoua mazao.”1504 Imepokewa kutoka kwa Amirul-Muminina Ali (a.s) amesema: “Ulaji wa pera unatia nguvu ya moyo dhaifu, unaimarisha mfuko wa chakula, unasafisha kifua, unamtia ushujaa muoga na unamfanya mtoto kuwa mzuri.”1505 Imepokewa kutoka kwa Amirul-Muminina Ali (a.s) amesema: “Asali ni ponyo la kila ugonjwa, na wala haina ugonjwa ndani yake, inapunguza kikohozi na inasafisha moyo.”1506 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Ulaji wa pera unatia nguvu moyo, uwerevu wa kifua na unatia ushujaa kwa muoga.”1507 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Lau watu wangelijua yale yaliyomo katika tufaha, wasingeliwatibia wagonjwa ila kwalo, kwani ndio kitu chenye manufaa ya haraka na kifua, kwakuwa hiyo linafurahisha.”1508   Makarimul-Akhlaq, uk. 165.   Khiswal, Juz. 1 uk. 31 cha Saduuq. 1504   Hikamat: 723 Sherh ya Ibn Abil Hadid. 1505   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 129. 1506   Makarimul-Akhlaq, uk. 166. 1507   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 131. 1508   al-Kaafi cha Kulayni, na Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 127 mwanzo wake, na Twibbul1502 1503

329

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 329

8/10/2017 1:22:17 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Sehemu ya akili ni ubongo, na ugumu na wepesi ni moyoni.”1509 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Hakika nguvu ya muumini ipo moyoni mwake, je, hamuoni hakika nyinyi kuna mtu dhaifu wa mwili mwenye mwili wa kukonda, lakini anasimama usiku na anafunga mchana.”1510 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Na Sa’atar na chumvi, zinaondoa harufu itokayo kifuani…”1511 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Siki inatia nuru moyo (na katika hadithi nyingine) inahuisha moyo.”1512 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Figili inasababisha hifidhi, inaleta uwerevu wa moyo na inaondoa uwenda wazimu, mbalanga na ukoma.”1513 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Pera linasafisha moyo na linatuliza maumivu ya tumbo kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (a.j).”1514 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kwamba alimwambia mtu aliyemlalamikia maumivu anayoyakuta moyoni mwake na uzito anaoupata, akamwambia: Kula pera.”1515 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Ni juu yenu kula adesi, kwani ni yenye baraka na takatifu, kwani inafanya moyo kuwa mwepesi na inazidisha machozi…”1516 Aimmat (a.s), uk. 135 na kinacho shabihiana nacho.   Biharul-Anwaar, Juz. 78, uk. 254. 1510   Man la Yahdhurhul-Faqiih, Juz. 3, uk. 365 cha Saduuq. 1511   Makarimul-Akhlaq, uk. 191. 1512   Biharul-Anwaar, Juz. 66, uk. 304. 1513   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 284. 1514   Makarimul-Akhlaq, uk. 175. 1515   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 135. 1516   Sahifatul-Ridha (a.s), uk. 75. 1509

330

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 330

8/10/2017 1:22:17 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Mtakapopika chakula basi zidisheni qar’u, linafurahisha moyo wa mwenye huzuni.”1517 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Kuleni komamanga, hakuna ndani yake punje inayoanguka kwenye mfuko wa chakula, ila itatia nuru moyo, na kumfanya shetani kuwa bubu kwa siku 40.”1518

NGANO Rejea mkate na Halua Ngano ni lishe kamili, ina wanga na protini lukuki na chumvi. Ama ganda lake limesheheni vitamini nyingi, na ndani yake kuna usafi na ulainishaji na usafishaji mwingi. Vikitolewa viasili vya wanga tunapata wanga wenyewe. Na ngano inasafisha uso. Na vinatengenezwa kutokana na ngano iliyokandwa vipande vidogovidogo vinavyomezwa kila siku kabla ya kula kitu kwa ajili ya usafishaji wa damu. Na ngano ikisagwa na kupikwa pamoja na nyama tunapata halua, nayo ni lishe. Majani ya kijani ya ngano: Rafiki yangu aliyeko Lebanoni amenieleza mimi kwamba amesoma katika tiba ya kichina kwamba majani ya ngano yana faida kubwa katika uchangamshaji wa mwili. Tunapopanda kiwango kikubwa cha punje za ngano katika kitalu huchipua na kutoa majani ya kijani iliyokolea ambayo huwa yamejaa kiambato cha chanikiwiti ambacho kinaweza kuliwa ili kuupa mwili uchangamfu na uhai.   Sahifatul-Ridha (a.s), uk. 54.   Sahifatul-Ridha (a.s), uk. 53.

1517 1518

331

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 331

8/10/2017 1:22:17 PM


TIBA YA MAASUMINA

Na hakika rafiki yangu amenieleza mimi kwamba yeye huchuma majani hayo ya kijani na kuyaweka katikati ya kurasa za daftari, kila siku anakula majani kadhaa, kila saa jani moja kati ya hayo, basi anapata uchangamfu mkubwa mwilini kwake na kufanya kazi kwa nguvu, na yeye anakaribia umri wa miaka 50. Kiambata cha chanikiwiti: Nacho ni kiambata cha kijani kibichi katika mimea, na hakika imethibiti kwamba ni dawa safi ya kusafishia vidonda vichafu. Kama ilivyothibiti kwamba majani yake makavu yanarudisha upya ujana wa mwili wote, kama yanavyoponya upungufu wa damu na udhaifu wa moyo, na yanapunguza ongezeko la shinikizo la damu na uyabisi wa mishipa ya damu, na yanatuliza hasira, na inapangilia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula, na kazi ya uandaaji wa lishe.1519 MISOKOTO ya tumbo Maana yake: Qawlanji: Ni maradhi ya tumbo yenye kuleta maumivu yanayosababisha ugumu wa haja na riahi (upepo), na sababu zake ni uvimbe wa utumbo mkubwa. Na sababu ya uvimbe wa utumbo mkubwa ni aina mbili: kwanza, upindukiaji katika matumizi ya vichangamsho na viungo. Pili matatizo ya kisaikolojia na kinafsi kwa mtu, jambo ambalo husababisha uvimbe wa utumbo na maumivu na kukosa hamu ya chakula. Na ulaji wa mkate wa makapi baada ya kuondoa viungo na vichangamsho unasidia kutibu hayo maradhi ya mingurumo.

  Kujitibu kwa miti shamba, uk. 337 cha Dr. Amiin Ruwayhat.

1519

332

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 332

8/10/2017 1:22:17 PM


TIBA YA MAASUMINA

Hadithi: Imepokewa kutoka kwa Amirul-Muminina Ali (a.s) amesema: “Ni juu yenu kula Tini, kwani hiyo ina manufaa kwa ugonjwa wa mingurumo ya tumbo.”1520 Imepokewa kutoka kwa Amirul-Muminina Ali (a.s) amesema: “Ulaji wa Tini unaondoa vizuizi, na unasaidia kwa mtu mwenye riahi na mingurumo ya tumbo.”1521 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Yule anayelala tumboni mwake kuna majani ya hindubaau, atapata amani ya mingurumo ya tumbo katika usiku wake huo.”1522 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Karoti ni amani ya mingurumo ya tumbo, inafaidisha bawasiri, na inasaidia katika kujamiana.”1523 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Mung’unya linaongeza akili na ubongo, nalo ni zuri kwa maumivu ya mingurumo ya tumbo.”1524 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: ‘Msiwakaribie wanawake mwanzo wa usiku, kiangazi au masika, na hilo ni kwa sababu utumbo na mishipa inakuwa imejaa, nalo sio lenye zuri, kwani inazalisha mingurumo ya tumbo na kiharusi…”1525 Na miongoni mwa yale yanayonasibishwa kwa Ibn Sina ni kauli yake: Meza kutokana na sabuni kipimo cha dirham – unanusurika kutokana na kubirukwa na tumbo lisilo kali.   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 137.   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 137. 1522   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 144. 1523   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 164. 1524   Kashful-Akhtar, cha shamsu Diin bin Muhammad Huseini – Mahtut. 1525   Biharul-Anwaar, Juz. 62 uk. 327. 1520 1521

333

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 333

8/10/2017 1:22:17 PM


TIBA YA MAASUMINA

UTAPIKAJI Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Yule anayetapika bila ya kujitapisha inakuwa ni bora zaidi ya magonjwa sabini, na matapishi kwa njia hii yanatoa kila ugonjwa na tatizo.”1526 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Dawa ziko aina nne; ufyonzaji wa damu mwilini, upakaji, utapishaji na kupiga bomba.”1527 Ini Rejea (nyongo) ya manjano – herufi SWAD Ukaaji mrefu msalani hutia maumivu ya ini.1528 Ini la Nabii Ezekieli (Hizqiil a.s) lilipatwa na kidonda, basi Mwenyezi Mungu akamfunulia achukue maziwa ya Tini, ajipake juu ya kifua chake. Basi akafanya hivyo na yakatulia maumivu.1529 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Yanyonye maji, wala usiyamimine kwa kuyagugumia, kwani hilo linasababisha maradhi katika ini.”1530 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) katika ugawaji wake wa nafsi katika aina nne, amesema: “Ipo yenye ukuaji wa mmea, hii ina nguvu tano; kuvuta, kushika, kusaga, kukinga na kulea. Na ina sifa mbili mahsusi ambazo ni ziada na pungufu, na chimbuko lake ni kutoka kwenye ini.”1531   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 67.   Fusuul-Muhimmat, cha Hurru Aamili na Khiswal uk. 117 cha Saduuq. 1528   Biharul-Anwaar, Juz. 80, uk. 184. 1529   Biharul-Anwaar, Juz. 13, uk. 383. 1530   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 188, kutoka kitabu Firuu Kaafi na Mahasin. 1531   Mustadrakul-Nahjul-Balaagha, uk. 159. 1526 1527

334

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 334

8/10/2017 1:22:17 PM


TIBA YA MAASUMINA

Muhsin Washa amesema: Nilimlalamikia baba Abdillah (a.s) kuhusu maumivu ya ini, basi akaitisha kitoa damu akanitoa damu kutoka nyayoni kwangu.1532 Wanja na upakaji wa wanja: Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kwamba: “Alikuwa anakataza kujipaka wanja ila witiri, na akaamrisha upakaji wa wanja wakati wa usiku, na akaamrisha upakaji wanja kwenye nyusi, na akasema: Ni juu yenu upakaji huo, kwani unaondoa uchafu wa jicho na unaimarisha uonaji.”1533 Bedui mmoja alikwenda kwa Mtume (s.a.w.w) na alikuwa na unyevunyevu machoni mwake, Mtume (s.a.w.w) akamwambia: Ninaona macho yako mawili yana unyevunyevu! Akasema: Ndio, Ewe Mtume hayo mawili kama unavyoona ni madhaifu. Akasema: Ni juu yako kutumia wanja kwani huo ni taa ya jicho.”1534 Imepokewa kutoka kwa Imam Husein (a.s) amesema: “Lau watu wangelijua yaliyomo ndani ya haliylij ya manjano wangeliinunua kwa kipimo cha dhahabu. Akasema kumwambia mtu miongoni mwa masahaba wake: Chukua haliylij ya manjano, na punje saba za pilipili zisage na zichunge kisha zipake nyusi zako kwayo.”1535 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Wanja unaimarisha tendo la ndoa na hina inazidisha ndani yake.”1536Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Wanja unaotesha nywele, unapunguza machozi, una unaondoa riiqu, na unasafisha uonaji.”1537   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 127.   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 151. 1534   Makarimul-Akhlaq, uk. 46. 1535   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 86. 1536   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 130. 1537   Khiswal, Juz. 1 uk. 18. 1532 1533

335

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 335

8/10/2017 1:22:17 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kwamba mmoja wa masahaba wake alipomlalamikia kuhusu binti yake mwenye udhaifu wa macho, alimwambia: “Ajipake nyusi zake nyongo na sabiru na kafuur, viwango sawa.”1538 Imepokewa kutoka kwa Salim huria wa Ali bin Yaqtiin, kwamba alikuwa akipata maumivu machoni mwake, basi Imam Kadhim (a.s) akamwandikia barua kwamba: “Kipi kinachokuzuia wewe kupaka wanja wa Abu Ja’far (a.s): Sehemu ya kafuur Riyahi, na sehemu ya swabiru isqartwarii, vinasagwa vyote na kuchungwa kwa kitambaa cha Hariri, anapaka kama anavyopaka wanja wa kawaida. Kujipaka wanja kwa mwezi mara moja kunakusanya maradhi ya kichwani na kuyatoa mwilini. Akasema: Na alikuwa akijipaka wanja huo (wa Abu Ja’far), na hakuwahi kulalamikia maradhi ya jicho lake mpaka alipokufa.”1539 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Jipakeni mafuta kwa kadiri ya mahitaji, na pakeni wanja mara tatu.”1540 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Yule anayejipaka wanja uliyochanganyika na kilevi, wanja wake huo utamsababisha Mwenyezi Mungu amuingize motoni.”1541

LIKI Faida zake: Miongoni mwake kuna aina mbili: Wa Sham na Nabtwi. Na ulio mkubwa kati ya hizo ni ule unaofanana na kitunguu nao ni wa Sham, majani yake ni mepesi yanafanana na kitunguu saumu nao ni Nabt  Twibbul-Swadiq (a.s), uk. 54.   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 150, kutoka kitabu Kaafi, Juz. 8, uk. 384. 1540   Fiqhul-Ridha (a.s), uk. 407. 1541   Biharul-Anwaar, Juz. 62 uk. 90. 1538 1539

336

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 336

8/10/2017 1:22:18 PM


TIBA YA MAASUMINA

wi, na unaotumiwa kati yao ni vichwa vya vitunguu vyake virefu vyeupe. Ibn Sina amesema: Liki ya Sham inaondoa sugu na vichunusi, na ulaji wake unaharibu ufidhi na meno, na unadhuru macho, na liki ya Uarabuni inaondoa bawasiri, na iliyolowekwa inaliwa na kubandikwa kama bendeji, na inachochea tendo la ndoa, na inawekwa juu ya majeraha yenye kutoa damu inakata damu. Na watu wa kughani wanaitumia ili kusafisha sauti zao.1542 HADITHI: Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: Ilitajwa mbele ya Mtume (s.a.w.w) mboga, basi akasema: “Kuleni Karath, hakika hilo mfano wake katika mboga, ni kama vile mkate katika vyakula vingine.”1543 Imepokewa kutoka kwa mwana habari wa Kuufa kwa isnadi yake kutoka kwa Musa bin Ja’far kutoka kwa As-Sadiq kutoka kwa Baqir (a.s) amesema: Mtu mmoja miongoni mwa vipenzi vyake alimlalamikia maumivu ya mapafu, na alitibiwa tiba zote hali ilizidi kuwa mbaya mpaka alikaribia kuangamia. Akasema (a.s): Nunua kwa pesa kipande cha kurath na kikaange vizuri kwa samli ya kiarabu, na mlishe yule mwenye maumivu kwa siku tatu, kwani akifanya hivyo atapona kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu (s.w.t).1544 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Kila kitu kina bwana, na bwana wa mboga ni Karath.”1545 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) aliulizwa kuhusiana na Liki, na akasema: “Kula hiyo, hakika ndani yake kuna mambo   Ajaaibul-Mkhluqaat cha Qazwiini, mwishoni mwa kitabu Hayatul-Hayawan, Juz. 2, uk. 194. 1543   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 151, kutoka kitabu Furuu Kaafi na Mahasin cha Barqi. 1544   Ramzu-Sihat, uk. 65 cha Dahsurkhi, kutoka kitabu Twibbul-Aimmat (a.s). 1545   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 151. 1542

337

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 337

8/10/2017 1:22:18 PM


TIBA YA MAASUMINA

matano; inaimarisha tendo ndoa, inaondoa harufu mbaya ya kinywa, inakata bawasiri, nayo ni kinga ya mbalanga kwa yule atakayedumisha kuila.”1546 Imepokewa kutoka kwa Hannan bin Sadiir alisema: Nilikuwa pamoja na Imam as-Sadiq (a.s) juu ya meza ya chakula iliyopambwa kwa hindubaau. Akaniambia: “Ewe Hannan kwa nini huli liki? Nikasema: Kutokana na yaliyokuja kutoka kwenu kuhusiana na Hindubaau (chickory). Akasema: Ni kipi ambacho kimekuja kutoka kwetu sisi kuhusu hiyo hindubaau? Nikasema: Hakika hiyo inadomdokewa kila siku na tone moja kutoka peponi. Akaniambia: Basi liki ina matone saba. Nikasema: Niile vipi? Akasema: Kata mizizi yake na tupa vichwa vyake.”1547 Imepokewa kutoka kwa Yunus bin Yakub amesema: Nilimuona baba Hasan Kadhim (a.s) akikata liki kwa mizizi yake na akiiosha kwa maji na akiila.”1548

FIGILI FAIDA ZAKE: Figili inaimarisha tendo la ndoa, na inaongeza shahawa ya tendo la ndoa kwa wanaume na wanawake, na inapowekwa juu ya kiungo chenye kutetemeka basi kinatulia. Na inatibu tatizo la haja ndogo kwa mgonjwa wa kisukari, na inatoa kondo ya nyuma, na inajaza unyevunyevu kwenye mfuko wa uzazi iwapo utadumishwa ulaji wake. Inatibu matatizo ya haja ndogo ya mwenye kisukari, na upungufu wa damu. Kama inavyoliwa ili kutibu maumivu ya baridi yabisi (Rheumatism) na ugonjwa wa jongo, na inaondoa tatizo la kubanwa na punzi, na udhaifu wa mishipa ya viungo vya jinsia.   Khiswal, Juz. 1 uk. 250.   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 151, kutoka kitabu Furuu Kaafi. 1548   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 153. 1546 1547

338

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 338

8/10/2017 1:22:18 PM


TIBA YA MAASUMINA

Hadithi: Mtume (s.a.w.w) amesema: “ Figili ni mboga ya manabii.”1549 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Ni juu yenu kula Figili, kwani hiyo ni chakula cha Nabii Iliyas, Yasaa na Yushaa bin Nuun.”1550 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Figili inasababisha hifidhi na inatakasa moyo na inaondoa uwenda wazimu, mbalanga na ukoma.”1551 KAZBARA Kazbara ina faida nyingi kwa kunywa na kubandika kama bendeji, lakini wametaja matabibu kwamba udumishaji wake na uzidishaji wake unachanganya ubongo, na unatia jicho giza, unafanya hafifu manii, na inatuliza nguvu za tendo la ndoa, na inasababisha usahaulifu. Nao ni mmea wenye kufaidisha mfuko wa chakula kwani unazindua mahitaji yake, inaondoa gesi, na inazuia kiu, na inaukinga moyo na maradhi ya mzunguko wa damu, na inalinda mapigo ya moyo na kizunguzungu. Daud Antokia anasema: Kazbara inazuia kutapika, kiu na vidonda na mwasho, na upele, inatumika kwa kula na kupaka. Na maji yake yakichanganywa na sukari yanaleta hamu ya chakula na yanazuia kuvimbiwa na unatia nguvu moyo na inalinda mapigo ya moyo. Na yakichanganywa na thaimu (za’tar) na sukari yanazuia kuharisha, na yakichanganywa na udi wa sandali na yansun yanatia nguvu mfuko wa chakula na yanaua vijidudu.1552   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 153.   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 153. 1551   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 284. 1552   Nabataat Twibbiyat wal-Uturiyat fil-Watwan Arabiy uk. 251 Khartum mwaka 1988. 1549 1550

339

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 339

8/10/2017 1:22:18 PM


TIBA YA MAASUMINA

Hadithi: Katika wosia wa Mtume (s.a.w.w) kwa Ali (a.s) amesema: “Ewe Ali, vitu tisa vinasababisha usahaulifu; ulaji wa tufaha la ugwadu, ulaji wa kazbara, jibini, mabaki ya maji aliyokunywa panya, usomaji wa maandiko makaburini, kutembea baina ya wanawake wawili, utupaji wa chawa hai, ufyonzaji wa damu mwilini katika jongo, na kujisaidia haja ndogo kwenye maji yaliyotuama.”1553 FIGO Imepokewa kutoka kwa Amirul-Muminina Ali (a.s) amesema: “Ulaji wa jozi katika joto kali unachochea joto na vidonda mwilini, ulaji wake katika masika unaongeza joto kwenye figo mbili na unaondoa baridi.”1554 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Kisibiti na jozi, zinatibu bawasiri, na zinaondoa harufu mbaya kinywani, zinafanya rangi kuwa nzuri, zinafanya mfuko wa chakula kuwa mgumu, zinaongeza joto kwenye figo…”1555 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuhusiana na ghubayraa amesema: “Hakika nyama yake inaotesha nyama, na kokwa yake inaotesha mfupa na ngozi yake inaotesha ngozi, pamoja na hivyo hakika hilo linaongeza joto kwenye figo na kulainisha mfuko wa chakula…”1556 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Alikuwa Mtume (s.a.w.w) hali figo – pasi na kuziharamisha – kwa ukaribu wake na haja ndogo.”1557   Khiswal, Juz. 1, uk. 422.   Wasaail-Shi’ah, Juz 17, uk.93, kutoka kitabu Furuu na Mahasin. 1555   Makarimul-Akhlaq, uk. 191. 1556   Makarimul-Akhlaq, uk. 176. 1557   Sahifatul-Ridha (a.s), uk. 64. 1553 1554

340

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 340

8/10/2017 1:22:18 PM


TIBA YA MAASUMINA

KAMAA (Terfeziaceae/Truffles) Maana yake: Ni mmea unaoota chini ya ardhi, hauna mbegu wala mzizi, lakini huo unachipuka kama vile johari katika vina virefu vya ardhi. Na hakika Mtume (s.a.w.w) aliufananisha na manna pale aliposema: “Hakika kamaa ni sehemu ya manna� kwani huo unaota ardhini bila taabu, kama vile manna (yenye asili ya sukari) inadondoka kutoka angani pasi na taabu. Na katika kitabu Qanun cha ibn Sina amesema: Ni aina ya uyoga inayotokana na fungi, inakithiri katika mwaka wa mvua na radi, nayo inazalika ardhini bila majani wala maua. Na ina hujulikana kuwepo kwake ardhini kwa alama ya mpasuko wa ardhi. Nao umesheheni protini ambazo unazifyonza kutoka kwenye Aazutiya (azotobacter) inayozalishwa angani wakati wa radi, na ambao huteremka pamoja na mvua inayonyesha sehemu husika. Ni kama naitrojeni na chumvi ya ammonia (ammonium nitrate). Faida zake: Ni lishe nzito nyeusi isiyo kifani, na kinywaji chake ni kiuasumu, lakini inahofiwa kusababisha kiharusi na kuzimia. Na ni ngumu kuyeyuka kwake na ni nzito kwa mfuko wa chakula, inasababisha mingurumo ya tumbo na haja ndogo. Ikikamuliwa hakika maji yake yanasafisha jicho, kama ilivyopokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w).

341

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 341

8/10/2017 1:22:18 PM


TIBA YA MAASUMINA

Hadithi: Mtume (s.a.w.w) amesema: “Kamaa ni sehemu ya manna aliyoiteremsha Mwenyezi Mungu kwa wana wa Israel, nayo ni ponyo la jicho.”1558 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Kumaa’ inatokana na manna, na manna inatoka peponi, na maji yake ni ponyo kwa jicho.”1559 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Kamaa inatokana na mmea wa peponi, na maji yake yanaponyesha maumivu ya jicho.”1560 Akaongeza Zaid bin Ali bin Husein (a.s) kutokana na dawa inayoponyesha jicho: “Maelezo juu ya hilo ni kwamba achukue kamaa aioshe mpaka isafike, kisha aikamue kwa kitambaa na achukue maji yake, basi aiweke juu ya moto mpaka ikauke, kisha amwagie ndani yake kipimo cha gram 0,2 za miski, kisha aiweke hiyo katika chupa na ajipake hiyo kwa ajili ya maumivu yote ya jicho. Na ikikauka jichoni basi aifute kwa maji ya mvua au mengine kisha ajipake kama vile wanja.”1561 KISIBITI Manufaa yake: Ibn Sina amesema: Ukiosha uso kwa maji ya kisibiti unakuwa safi, na ikisagwa kwa siki na kuwekwa kwenye jeraha hukata utokaji wa damu, na juisi yake inang’arisha macho.   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 132.   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 159, kutoka kitabu Furuu Kaafi. 1560   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17 uk. 159, kutoka kitabu Mahasin cha Barqi. 1561   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 151, kutoka kitabu Daa’im. 1558 1559

342

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 342

8/10/2017 1:22:18 PM


TIBA YA MAASUMINA

Na moja ya sifa zake ni kwamba sisimizi hukimbia kutokana na hurufu yake.1562 Na hakika uwepo wake katika chakula kunachangamsha utumbo na kunasaidia kuondoa riahi (gesi), na pia inatumiwa kama kitulizo cha maumivu ya vidonda vya tumbo. Na Daud Antoki amesema: Kisibiti kinajulikana kwa harufu yake nzuri, nacho kinaondoa riahi na ubaridi, na kinaondoa uvimbe na kinaondoa sumu na matatizo ya mmeng’enyo na kinaondoa ubanaji wa pumzi na yabisi kali kinapotumiwa kwa njia ya kunywa baada ya kukichanganya na siki na maji. Na kikichanganywa na thaimu (za’tar) na kikaumuka kwa kupikwa hutuliza maumivu ya meno na utokaji wa damu.1563 (Na kisibiti): Ni mmea ambao una punje za rangi ya manjano zenye harufu nzuri huwekwa wakati mwingine juu ya mkate, nayo ni komani muluki. Na imesemwa kwamba hakika kisibiti kina aina tatu; cheusi nacho ni chenye asili ya Kerman Iran, na cha manjano nacho ni cha asili ya Uajemi na ndicho huitwa komoni muluki, na cheupe kinaitwa komoni ya kawaida. Na kizuri zaidi ya vyote ni chenye asili ya Kerman nacho ni cha nchi kavu, na mbaya zaidi ni cheupe cha bustani. Na nguvu yake hudumu kwa miaka tisa. Hadithi: Mtume (s.a.w.w) amesema: “Thufaau (nao ni kisibiti au hardali au hubbu Rashaad) ni dawa ya kila ugonjwa, na hakuna dawa mfano wake katika kutibu uvimbe na maumivu.”1564   Ajaaibul-Makhluqaat, cha Qazwiini, mwishoni mwa kitabu Hayatul-Hayawan, Juz. 2, uk. 195. 1563   Nabataat Twayyibat wal-Uturiyat fil-Watwan Arabiy, uk. 252 Khartum mwaka 1988. 1564   Makarimul-Akhlaq, uk. 191. 1562

343

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 343

8/10/2017 1:22:18 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kwamba aliitisha kisibiti na thaimu na habasoda, na alikuwa akiitumia kavu anapokula samaki na chakula anachohofia madhara yake. Na alikuwa akikichanganya pamoja na chumvi ya mawe, na anafungulia chakula, na alikuwa akisema: Maadamu nimekula kisibiti basi sijali madhara ya chakula chochote kile. Na pia alikuwa akisema: Kinaimarisha mfuko wa chakula, na kinakata balgham, nayo ni kinga ya nusu kiharusi cha uso.”1565 Imepokewa kutoka kwa Ibn Kathir amesema; tumbo langu lilipatwa na kuharisha, basi Imam as-Sadiq (a.s) akaniamrisha nitengeneze uji mzito wa ulezi kwa maji ya kisibiti. Basi nikafanya hivyo na tumbo langu likatulia basi nikapona.1566 Na kutoka kwenye kitabu cha Farju bin Salam: Katika Thufaau kuna dawa sabini, na katika kisibiti kuna dawa sitini kama ilivyosemwa. Ameyasema hayo Hermes katika vitabu vyake hivyo usiache thufaau na kisibiti.

PEASI, UBANI KUNDUR NA TIBA YA ­UCHOMAJI Imepokewa kutoka kwa Imam Baqir (a.s) amesema: “Tiba ya kiarabu iko katika aina tatu; kuumika, kupiga bomba, na nyingine ni tiba ya uchomaji ili kuondoa sumu.”1567 Imepokewa kutoka kwa Muhammad bin Muslim amesema: Nilimuuliza Abu Ja’far Baqir (a.s) je, inawezekana kutumia tiba ya uchomaji? Akasema: “Ndio, hakika Mwenyezi Mungu (a.j) ame  Makarimul-Akhlaq, uk. 187.   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 101, kutoka kitabu Furuu Kaafi. 1567   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 55. 1565 1566

344

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 344

8/10/2017 1:22:18 PM


TIBA YA MAASUMINA

jaalia katika dawa baraka, ponyo na kheri nyingi, na si vibaya mwanaume kujitibu kwa tiba hiyo.”1568 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Tiba ya waarabu ipo katika mambo matano; kuumika, kupiga bomba, kunusa, kutapika, na kuoga na tiba ya mwisho ni uchomaji ili kuondoa sumu mwilini.”1569 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kwamba aliruhusu tiba ya uchomaji ili kuondoa sumu mwilimi ikiwa tu hakuna hofu ya kuangamia wala madhara.1570 Ubani (bukhuri) na kunduru Maana yake: Katika kitabu Tadhkirat cha Umar Antoki: Kunduru ni ubani, unaitwa bastaju, nao ni utomvu wa mti wenye miba ambao majani yake ni kama vile Aasi (myrtus communis), huchumwa katika mwezi wa oktoba. Wala haupatikani ila eneo la Shahr (eneo huko Omani) na jabali la Yemeni. Na kunduru dhakar ni ya mviringo, ngumu yenye kuelekea kwenye wekundu, na ya untha ni nyeupe na kavu. Na nguvu hudumu kwa miaka 20. Ibn Sina amesema: Kunduru inaitwa iliki ya Roma, nayo ni aina miongoni mwa aina a iliki yenye kutibu kikohozi zaidi.1571 Na katika kitabu Lisanul-Arab: Hakika kunduru ni aina ya ubani, na inapatikana katika mji wa Ugiriki, na pia inapatikana katika miji ya India, na rangi yake inaelekea kama ya yakuti, na ipo inayoelekea kwenye rangi ya bilinganya.   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 54, na Biharul-Anwaar, Juz. 62 uk. 64.   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 55. 1570   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 74. 1571   Qanun, uk. 145. 1568 1569

345

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 345

8/10/2017 1:22:18 PM


TIBA YA MAASUMINA

Nayo ni ngumu haivunjiki kirahisi, na ikivunjwa ndani hupatikana vipande vinavyoweza kuunganishwa. Na ikisuguliwa hutoa harufu ya utomvu wa mustaki, nayo ni rahisi kukauka kuliko kundur. Na inawezekana kughushi kundur kwa gundi ya kiarabu na gundi ya msonobari. Na kugundua kughushi kwake ni jambo liko wazi, na hiyo ni kwa sababu gundi la kiarabu halilipuki moto, na gundi la msonobari linatoa moshi, na kunduru inatoa mwale wa moto. Na pia harufu mahsusi ya kundur inajulisha hadaa. Na mti wa ubani ni wenye miiba haukui zaidi ya dhiraa mbili, nao unaota katika majabali ya Shahr huko Omani, na majani yake kama vile majani ya Aasi. Gundi lake nalo ni (kundur), huchuruzika kutoka kwenye mti baada ya sehemu ya mti huo kupasuliwa kwa shoka. Yule anayedumisha kuutafuna moyo wake utatakasika na kutamsaidia kukumbuka vitu alivyovisahau.1572

MJUMUIKO WAKE: Kundur ni gundi la utomvu lina harufu ya Uturi, na ladha yake ni chungu, na mjumuiko wake ni asilimia 60 ya utomvu, na asilimia 30 ya gundi, na asilimia 8 ya mafuta ya mimea.1573 Na kuna aina mbili za ubani: Aina inayopatikana kwenye kingo za mto Naili ya bluu katika Afrika, na nyingine inapatina kwenye kingo za kusini za Saudia. Lakini sehemu kubwa zaidi inapatikana kutoka Afrika. Ili kuupata ubani tunapasua magogo ya mti wa kunduru, basi unachuruzika utomvu mweupe wenye kumeremeta na ulio safi. Inawezekana kufanyiwa majaribio ili kuchanganua aina mbili za ubani; bukhuri ya India, na bukhuri ya Afrika. Na aina ya Afrika ina   Nabataat Twayyibat wal-Uturiyat fil-Watwan Arabiy, uk. 176 Khartum mwaka 1988.   Ajaaibul-Makhlauqaat cha Qazwiini, mwishoni mwa kitabu Hayatul-Hayawan, Juz. 2, uk. 175.

1572 1573

346

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 346

8/10/2017 1:22:18 PM


TIBA YA MAASUMINA

mng’ao zaidi kuliki ya India. Huletwa bukhuri ya India kutoka Kolkata, nayo ni ya manjano yenye mng’ao kidogo, ina harufu na ladha kali zenye kushabihiana kwa ukaribu na harufu na ladha ya utomvu wa msonobari. Na aina hii ya India ndio inayopatika zaidi sokoni. Ubani dhakar: Kwa watu wengi jina la “ubani dhakar” hutumika kumaanisha aina moja ya ubani. Inaitwa dhakar kutokana na njia ya ugandaji, na katika aina hii vipande vya ubani hugandana katika umbo la uume. Ibn Sina katika kitabu Qanun amesema: Iliyo nzuri zaidi ni dhakar nyeupe yenye kubilingika kiungo cha ndani. Nayo inayeyuka ndani ya maji na ndani alkoholi kwa umbo la vipande vipande, na ni ngumu kuyeyuka katika joto, inawaka kwa mwale mweupe na utaupa moshi mzito na harufu nzuri. Nalo ni gundi ya utomvu; inatengezwa kutokana na tindikali ya Buzuwiylian, na utomvu wa bukhuri, na mafuta ya mimea na gundi. Matumizi ya ubani ni ya tangu zamani, hakika ameueleza Abu Qiraat (Hippokrates) katika vitabu vyake vya tiba, na jina lake limetokana na asili ya ugiriki. Na unatumiwa ubani kama vile mafusho ya moshi (bukhuri) wakati wa baridi yabisi (Rheumatism) na kama kiuasumu, na kama gundi, na pia hutumiwa dhidi ya maumivu ya kichwa.1574 Faida zake: Katika kitabu (Tuhfatul-Radhawiyat fil-Mujarribaat Imamiyyat) ametaja Sayyid Mubiidi katika kitabu chake Kashkuuli amesema: Na maelezo yaliyokuja katika matibabu na habari nyingi ni kwamba ubani unasaidia kuondoa udhaifu katika tendo la ndoa kwa kula   Utafiti uliyotarjumiwa kutoka kitabu Firdausi cha matibabu cha kifaransa.

1574

347

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 347

8/10/2017 1:22:18 PM


TIBA YA MAASUMINA

pamoja na yai lililochemshwa kidogo, tiba hii ni mujarabu. Na ikiwa sehemu ndogo ya ubani italowekwa katika maji, na akanywa maji hayo kila siku kabla ya kula chochote, inasaidia kuondoa balgham na usahaulifu, tiba hii ni mujarabu. Kisha aliendelea kuelezea faida zake lukuki, na akataja kwamba inaongeza hifidhi. Na katika kitabu Bihar imekuja: Ibn Baytway amesema: Ubani huo ni kundur, nao unaunguza damu na kikohozi, na unakausha unyevunyevu wa kifuani, na unatia nguvu mfuko wa chakula uliyodhaifu, na unatia joto ini likiwa la baridi. Na ukisafishwa kidogo na kulowekwa katika maji na akanywa kila siku husaidia kuondoa kikohozi na unaongeza hifidhi na ubongo unakuwa safi na unaondoa usahaulifu, isipokuwa ni kwamba humsababishia mnywaji wake maumivu ya kichwa iwapo atakithirisha, nao unasaga chakula na kuondoa riyahi. Na Galenos (Galenos) amesema: Ukipakwa kwenye nyusi ya jicho ambalo ndani yake ipo damu iliyoganda basi husaidia kuondoa tatizo hilo. Kisha akataja kuwa una sifa chungu tele.1575 Hadithi: Imepokewa kutoka kwa Imam Hasan (a.s) kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Walisheni wajawazito wenu ubani, hakika mtoto aliyopo tumboni mwa mama yake akila ubani basi akili yake itakuwa kali zaidi.”1576 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Walisheni wanawake wenu wajawazito ubani, kwani unaongeza nguvu ya akili ya mtoto.”1577   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 235 cha Allama Majlisi.   Wasaail-Shi’ah, mlango wa 34, hadithi ya kwanza, hukumu za watoto. 1577   Makarimul-Akhlaq, uk. 194, kutoka kitabu Firdausi. 1575 1576

348

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 348

8/10/2017 1:22:18 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Walisheni wajawazito wenu ubani, hakika mtoto akila tumboni mwa mama yake ubani, moyo wake utakuwa madhubuti zaidi na utaongeza nguvu katika akili yake.”1578 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Fukizeni majumba yenu ubani na thaimu (su’tar).”1579 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Matano yanaondoa usahaulifu na yanazidisha hifidhi, na yanaondoa kikohozi; upigaji mswaki, funga, usomaji wa Qur’ani, asali na ubani.” (yaani kundur).1580 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Ni juu yenu kutumia ubani, kwani unaondoa joto kutoka moyoni kama vile kidole kinavyofuta jasho kutoka katika paji la uso, na unaimarisha mgongo, unaongeza akili, unatakasa ubongo, unang’arisha uonaji na unaondoa usahaulifu.”1581 Imepokewa kutoka kwa Amirul-Muminina Ali (a.s) amesema: “Usomaji wa Qur’ani, upigaji mswaki na utafunaji ubani unaondoa kikohozi.”1582 Imepokewa kutoka kwa Amirul-Muminina Ali (a.s) amesema: “Utafunaji wa ubani unakaza magego, unaondoa balgham na unakata hurufu mbaya ya kinywa.”1583 Imepokewa kutoka kwa Amirul-Muminina Ali (a.s) amesema: “Ni juu yako kutumia ubani, kwani huo unatia ushujaa moyo, na unaondoa usahaulifu.”1584   Kaafi, Juz. 6 mlango wa yale yaliyokuja katika kumlisha mjamzito.   Twibbu-Nabawi, uk. 301 cha Ibn Qaym Jawziyyat. 1580   Makarimul-Akhlaq, uk. 164, kutoka kitabu Firdausi. 1581   Biharul-Anwar, Juz. 62, uk. 294. 1582   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 66. 1583   Mkarimul-Akhlaq, uk. 194. 1584   Twibbu-Nabawi, uk. 301 cha Ibn Qaym Jawziyyat. 1578 1579

349

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 349

8/10/2017 1:22:18 PM


TIBA YA MAASUMINA

Na imetajwa kutoka kwa Ibn Abbas (r.a) amesema: Kutafuna ubani pamoja na sukari kabla ya kula chochote ni vizuri kwa mwenye matatizo ya haja ndogo na usahaulifu.”1585 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Alikuwa Mtume (s.a.w.w) akila asali, na akasema: Usomaji Aya za Qur’ani na utafunaji wa ubani kunaondoa kikohozi.”1586 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Hakuna moshi unaopanda hadi mbinguni ila ubani, na hakuna watu wa nyumba ambamo ndani yake kuna ubani ila huondolewa kwao maifriit miongoni mwa majini.”1587 Aliulizwa Imam as-Sadiq (a.s) kuhusiana na harmala na ubani, akasema: “Ama Harmala… na ama ubani (kunduru) nao ni chaguo la manabii (a.s) kabla yangu, na alikuwa Maryam (a.s) anautumia huo, na hakuna moshi unaopanda mbinguni haraka zaidi kuliko huo, nao unafukuza mashetani, na ni kinga dhidi ya wadudu wenye kung’ata, basi usiwapite huo.”1588 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kuhusiana na asali amesema: “Inasafisha ubongo, inafanya akili iwe nzuri ikiwa pamoja na ubani dhakar.”1589 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: ‘Vitatu vinazidisha hifidhi, vinaondoa kukohoa: usomaji wa Qur’ani, asali na ubani (kundur).1590 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Zidisheni utumiaji ubani, utafuneni, na ni linalopendeza zaidi hilo kwangu,   Twibbu-Nabiy, uk. 301 cha Ibn Qaym Jawziyyat.   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 73, kutoka kitabu Furuu na Mahasin. 1587   Makarimul-Akhlaq, uk. 194. 1588   Makarimul-Akhlaq, uk. 212. 1589   Fiqhul-Ridha (a.s), uk. 346. 1590   Sahifatul-Ridha (a.s), uk. 68. 1585 1586

350

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 350

8/10/2017 1:22:18 PM


TIBA YA MAASUMINA

kwani linaondoa balgham ya utumbo na linausafisha, kunaimarisha akili na kunafanya chakula kishuke vizuri kooni.”1591 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Walisheni wajawazito wenu ubani, hakika mtoto aliyopo tumboni mwa mama yake kama atazaliwa wa kiume atakuwa mwenye moyo safi… shujaa. Na kama akiwa wa kike atakuwa mwenye umbo zuri na tabia nzuri.”1592 Imepokewa kutoka kwa Riyan bin Silt amesema: Nilimsikia Ridha (a.s) akisema: “Mwenyezi Mungu hakutuma nabii ila alimharamishia pombe, na kwamba akiri kuwa hakika Mwenyezi Mungu anafanya ayatakayo, na iwe katika urithi wake kundur.”1593

MAZIWA Maelezo: Waarabu hapo zamani walikuwa wakiyaita maziwa mabichi kuwa (laban), ama maziwa ya mgando walikuwa wakiyaita (laban Raaib) kwani yalikuwa yakiongezwa kichocheo (Ruubat) ambacho kiliyabadilisha kutoka katika ubichi na kuwa mgando. Hadithi: Mtume (s.a.w.w) amesema: “Hakuna kinachotosheleza mahali pa chakula na kinywaji kisichokuwa maziwa.”1594 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Nyama ya ng’ombe ni ugonjwa, samli yake ni ponyo na maziwa yake ni dawa.”1595   Makarimul-Akhlaq, uk. 194 cha Twabarasi.   Wasaail-Shi’ah, Juz. 34 hadithi ua pili, hukumu za watoto. 1593   Biharul-Anwaar, Juz. 4, uk. 97. 1594   Ramzu-Sihat, uk. 11. 1595   Ramzu-Sihat, uk. 214 cha Dahsurkhi. 1591 1592

351

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 351

8/10/2017 1:22:18 PM


TIBA YA MAASUMINA

Mtume (s.a.w.w) alimuona mtu mnene, akamuuliza: Unakula nini? Akajibu: Katika ardhi yetu hakuna nafaka, hakika mimi ninakula nyama na maziwa, akasema (s.a.w.w): “Umekusanya nyama mbili.”1596 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Ni juu yenu kutumia maziwa ya ng’ombe, kwani yanatengenezwa kutokana na kila mti.”1597 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Hakuna yeyote anayechukizwa na unywaji wa maziwa, hakika Mwenyezi Mungu aliyetukuka anasema: “Maziwa safi ni mazuri kwa wanywao.1598”1599 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Wanywesheni wanawake wenu wajawazito maziwa (na katika hadithi nyingine ubani) kwani hayo yanazidisha uimara katika akili ya mtoto.”1600 Alikuwa Mtume (s.a.w.w) hakusanyi pamoja kati ya maziwa na samaki, wala kati ya maziwa na ugwadu (huenda maziwa yanayokusudiwa hapa ni mabichi, kwani yanaathiriwa na ugwadu).1601 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Nabii Nuhu (a.s) alimlalamikia Mola Wake (a.j) kutokana na udhaifu wa mwili wake, basi Mwenyezi Mungu akamfunulia kwamba, pika nyama kwa maziwa na ule, hakika Mimi nimetia nguvu na baraka ndani ya hivyo viwili.”1602   Biharul-Anwaar, Juz. 66, uk. 75.   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 176, na linachoshabihiana nacho kutoka kitabu QurbulIsnaad uk. 52. 1598   Sura 16 aya 66. 1599   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 84. 1600   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 294. 1601   Twibbu-Nabawi, uk. 173 cha Ibn Qaym Jawziyyat. 1602   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 64. 1596 1597

352

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 352

8/10/2017 1:22:18 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Amirul-Muminina Ali (a.s) amesema: “Kunyweni maziwa kidogo kidogo ni ponyo kutokana na kila ugonjwa ila kifo.”1603 Aliulizwa Imam as-Sadiq (a.s) kuhusiana na maziwa ya punda; je ni dawa anayoweza kunywa mtu? Akasema: “Hakuna tatizo katika hayo.”1604 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Maziwa ni chakula cha Mitume.”1605 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kwamba ametaja kuwa hakika Imam Ali (a.s) alikuwa akipendelea kufuturu maziwa.1606 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kwamba aliambiwa na mtu mmoja: “Nafsi nimeitoa fidia kwako, hakika mimi ninakuta udhaifu mwilini mwangu,’ basi akasema: “Ni juu yako kunywa maziwa, kwani yanaotesha nyama na yanaimarisha mifupa.”1607 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Yule anayepata udhaifu moyoni mwake au mwilini mwake, basi na ale nyama ya mbuzi kwa maziwa, kwani kunang’oa mizizi ya kila ugonjwa na madhara, na yanatia nguvu mwili na yanaimarisha mgongo wake.”1608 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kutoka kwa baba zake (a.s) amesema: “Alikuwa Mtume (s.a.w.w) akipenda kunywa maziwa.”1609   Ramzu-Sihat, uk. 284 cha Dahsurkhi.   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 63. 1605   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 84. 1606   Ramzu-Sihat, uk. 250. 1607   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 84, kutoka kitabu Furuu na Mahasin. 1608   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 64. 1609   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 216. 1603 1604

353

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 353

8/10/2017 1:22:18 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Abdullah bin Sinan, kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Nabii mmoja alimlalamikia Mwenyezi Mungu udhaifu, akamwambia: Pika nyama kwa maziwa, na akasema: Hakika hivyo viwili vinaimarisha mwili. Nikasema (bin Sinan): Je, hayo ni yenye kudhuru? Akasema: Hapana, lakini nyama kwa maziwa.” (huenda makusudio ya maziwa ni yale ya mbuzi yaliyokamuliwa wakati huohuo).1610 Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) kwamba amesema: “Nyama kwa maziwa ni supu ya Manabii.”1611 Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) amesema: “Yule ambaye maji yake ya mgongo yamebadilika, basi yanamfaa yeye maziwa na asali.”1612 Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) amesema: “Mkojo wa ngamia ni bora kuliko maziwa yake, na Mwenyezi Mungu anajaalia ponyo katika maziwa yake.”1613 Imepokewa kutoka kwa Kaamil amesema: Nilimsikia Musa bin Abdillah bin Hasan akisema: Niliwasikia wazee wetu wakisema: Maziwa ya ngamia ni ponyo ya kila ugonjwa na kupooza kwa mwili, nayo yanasafisha mwili na yanaondoa uchafu wake na yanaosha kabisa.”1614 UFIZI Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Kuleni kitunguu maji, hakika ndani yake kuna mambo matatu; kinafanya chakula kishuke vizuri kooni, kinaimarisha ufizi na kinaongeza maji na nguvu ya kujamiana.”1615   Biharul-Anwaar, Juz. 66, uk. 68.   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 40, kutoka kitabu Furuu na Mahasin. 1612   Rawdhatul-Kaafi, uk. 191. 1613   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 87, kutoka kitabu Furuu na Tahdhiib. 1614   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 102. 1615   Fusuulul-Muhimmat, uk. 137 cha Hurru Aaamili. 1610 1611

354

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 354

8/10/2017 1:22:19 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Siki ya pombe inaimarisha ufizi, inaua wadudu wa tumboni na inaimarisha akili.”1616 NYAMA Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema:

َ َ ‫َوأ ْم َد ْد َن ُاه ْم ِب َف ِاك َه ٍة َول ْح ٍم ِم َّما َي ْش َت ُهو َن‬

“Na tutawapa matunda na nyama kama watakavyopenda.”1617

Na anasema (s.w.t):

َ ‫َو َفاك َهة م َّما َي َت َخ َّي ُر‬ ‫ون‬ ِ ٍ ِ َ َ ‫َول ْح ِم ط ْي ٍر ِم َّما َي ْش َت ُهو َن‬

“Na matunda wayapendayo. Na nyama ya ndege kama wanayotamani.”1618

Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Nabii Nuhu (a.s) alimlalamikia Mola Wake (a.j) kuhusu udhaifu wa mwili wake, basi Mwenyezi Mungu aliyetukuka akamfunulia; ‘kula nyama kwa maziwa, hakika mimi nimejaalia nguvu na baraka ndani yake.”1619 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Bwana wa chakula cha duniani na akhera ni nyama, na bwana wa vinywaji vya duniani na akhera ni maji.”1620   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 69.   Sura 52 aya 22. 1618   Sura 56 aya 20 – 21. 1619   Twibbul-Aimmat, (a.s), uk. 62. 1620   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 27, kutoka kitabu Qurbul-Isnaad. 1616 1617

355

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 355

8/10/2017 1:22:19 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Nyama inaotesha nyama, na mwenye kuiacha hiyo siku 40 kunasababisha tabia yake kuwa mbaya, na yule ambaye tabia yake itakuwa mbaya basi muadhinieni sikioni mwake.’”1621 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Nyama ya ng’ombe ni ugonjwa (huenda ni kwa sababu ya uwepo vijidudu) na maziwa yake ni dawa, na nyama ya mbuzi ni dawa na maziwa yake ni ugonjwa.”1622 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Alikuwa Mtume (s.a.w.w) akila nyama, na akipenda nyama.”1623 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Hakika sisi makuraishi ni watu tunaokula nyama.”1624 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Yule ambaye zimepita kwake siku 40 hajala nyama basi akope kwa dhamana ya Mwenyezi Mungu, na ale.”1625 Alikuwa Mtume (s.a.w.w) akipenda dhiraa na bega, na akichukia paja kwa ukaribu wake na sehemu ya mikojo.”1626 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kwamba alimwambia Ali (a.s): “Usikate nyama kwa kisu juu ya meza, kwani hicho ni kitendo cha wasio waarabu, na kuikata kwa njia nzuri ni utulivu zaidi na vizuri zaidi.”1627 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Ni juu yenu kula nyama ya ngamia, kwani haili hiyo isipokuwa muumini   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 293.   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 296. 1623   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 23. 1624   Wasail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 23. 1625   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 26, kutoka kitabu Firuu na Mahasin. 1626   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 40, kutoka kitabu Furuu na Baswair Darajaat. 1627   Biharul-Anwaar, Juz. 26, uk. 427. 1621 1622

356

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 356

8/10/2017 1:22:19 PM


TIBA YA MAASUMINA

mwenye kwenda kinyume na mayahudi ambao ni maadui wa Mwenyezi Mungu.”1628 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Katika ukamilifu wa Uislamu ni kupenda nyama ya ngamia ndama.”1629 Imepokewa kutoka kwa Jabir bin Abdillah Answari kwamba amesema: Mtume (s.a.w.w) aliwaamrisha matajiri kula mbuzi na kondoo na mafukara kula kuku.”1630 Imepokewa kutoka kwa Amirul-Muminina Ali (a.s) amesema: “Ni juu yenu kula nyama, hakika nyama inatokana na nyama, na nyama inaotesha nyama.”1631 Imepokewa kutoka kwa Amirul-Muminina Ali (a.s) amesema: “Punguzeni ulaji wa nyama ya nyangumi, kwani hiyo inayeyusha mwili, na inazidisha balgham na inatia nafsi uzito.”1632 Imepokewa kutoka kwa Amirul-Muminina Ali (a.s) kwamba ilitajwa mbele yake nyama ya ndege akasema: “Nyama nzuri zaidi ni nyama ya kinda…”1633 Imepokewa kutoka kwa Amirul-Muuminna Ali (a.s) amesema: “Hakika nyama nzuri zaidi ni nyama ya kinda la njiwa pori, ambaye ameanza kuruka au anakaribia kuruka.”1634 Imepokewa kutoka kwa Amirul-Muminina Ali (a.s) amesema: “Msiyafanye matumbo yenu kuwa ni makaburi ya wanyama.”1635   Makarimul-Akhlaq, uk. 160.   Makarimul-Akhlaq, uk. 160. 1630   Makarimul-Akhlaq, uk. 160. 1631   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 27. 1632   Khiswal, cha sheikh Saduuq. 1633   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 31. 1634   Biharul-Anwaar, Juz. 66, uk. 75. 1635   Sharhul-Nahjul-Balaaghah, Juz. 1 uk. 26 cha Ibn Abi Hadid. 1628 1629

357

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 357

8/10/2017 1:22:19 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Alikuwa Isa (a.s) akichukia udumishaji wa kula nyama, na akisema: Hakika ina madhara kama vile madhara ya pombe.”1636 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Nyama kwa maziwa ni supu ya Manabii.”1637 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuhusiana na kware amesema: “Hakika nyama yake inaotesha nyama, mfupa wake unaotesha mfupa na ngozi yake inaotesha ngozi…”1638 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Yule anayepatwa na udhaifu moyoni mwake au mwilini mwake, basi naale nyama ya mbuzi kwa maziwa, kwani inatoa ugonjwa na madhara kwenye mishipa yake, na inatia mwili nguvu na inamarisha mgongo wake.”1639 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Hakika watu miongoni mwa wana wa Israeli walipatwa na mbalanga, basi Mwenyezi Mungu akamfunulia Nabii Musa (a.s) awaamrishe hao kula nyama ya ng’ombe kwa mchadi.”1640 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Uji unaotesha nyama na unaimarisha mifupa.”1641 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Wanywesheni watoto wenu uji udogoni mwao, kwani huo unaotesha nyama na unamarisha mifupa, na yule atakayekunywa uji asubuhi kwa muda wa siku 40 utajaza nguvu mabega yake.”1642   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 32.   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 40. 1638   Makarimul-Akhlaq, uk. 176. 1639   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 64. 1640   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 158. 1641   Makarimul-Akhlaq, uk. 192. 1642   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 7. 1636 1637

358

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 358

8/10/2017 1:22:19 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Nyama kavu ni nyama mbaya, kwani haina nguvu kwenye mfuko wa chakula, inachochea ugonjwa na haina manufaa yoyote bali inaudhuru.”1643 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Nyama inaotesha nyama, na inaongeza akili, na yule anayeiacha kwa siku nyingi inaharibika akili yake.”1644 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Alikuwa Amirul-Muminina Ali (a.s) akishabihiana mno na Mtume (s.a.w.w) katika chakula, na alikuwa akila mkate, siki na mafuta, na akiwalisha watu mkate na nyama.”1645 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Yule anayeacha kula nyama siku arobaini, tabia yake itakuwa mbaya na itaharibika akili yake, na yule ambaye tabia yake inaharibika basi mwadhinieni sikioni mwake.”1646 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kwamba mtu mmoja alimwambia: Ewe mtoto wa Mtume (s.a.w.w), hakika watu miongoni mwa wanazuoni wa Ahli Sunna wanapokea kuwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Hakika Mwenyezi Mungu anawachukia wale ambao wanazidisha mno ulaji wa nyama, na anawachukia watu wa nyumba ambayo inaliwa nyama kila siku! Akasema: “Wamekosea kosa la wazi kabisa, na hakika Mtume (s.a.w.w) amesema: Hakika Mwenyezi Mungu anachukia watu wanaokula majumbani mwao nyama za watu, yaani wanawasengenya watu, wana nini hao?! Mwenyezi Mungu asiwarehemu, wameielekea halali basi wakaiharamisha kwa kukithiri hadithi zao.”1647   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 38, kutoka kitabu Furuu al-Kaafi, Juz. 6, uk. 314.   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 139. 1645   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 64, kutoka kitabu Furuu, Juz. 6, uk. 328 na Mahasin cha Barqi. 1646   Twibbul-Aimmat (a.s), 139. 1647   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 138. 1643 1644

359

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 359

8/10/2017 1:22:19 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) aliambiwa na mtu mmoja: Nafsi yangu nimeitoa fidia kwako, hakika mimi ninakuta udhaifu mwilini mwangu, basi akamwambia: Ni juu yako kunywa maziwa, kwani yanaotesha nyama na yanaimarisha mifupa.”1648 Imepokewa kutoka kwa Abdullah bin Sinan amesema: Nilimuuliza Imam as-Sadiq (a.s) kuhusiana na bwana wa mchuzi duniani na akhera? Akasema: “Nyama, ama hujasikia kauli ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) inasema: “Na nyama ya ndege kwa yale wanayokuwa na hamu nayo.”1649 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Iliingizwa nyama nyumbani kwa Mtume (s.a.w.w) akasema: “Kateni vipande vidogo vidogo sana, na zidisheni mchuzi, na wagawieni majirani, kwani kunaharakisha uivaji wake, na kuna baraka zaidi.”1650 Imepokewa kutoka kwa Darasti kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: Tulitaja vichwa vya mbuzi, basi akasema: “Kichwa ni mahali pa uelewa, na karibu zaidi na upataji wa chakula, na mbali zaidi na madhara.”1651 Imepokewa kutoka kwa Hasan bin Khalid amesema: Nikamwambia Abu Hasan Kadhim (a.s): Hakika watu wanasema: Hakika yule ambaye hali nyama kwa siku tatu tabia yake itakuwa mbaya, akasema: Wamekadhibisha, lakini yule ambaye hajala nyama kwa muda wa siku 40, hubadilika tabia yake na mwili wake, na hilo ni kwa sababu tone la manii hutembea kwa muda wa siku 40.”1652   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 84, kutoka kitabu Furuu na Mahasin.   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 19. 1650   Biharul-Anwaar, Juz. 66, uk. 75. 1651   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 49, kutoka kitabu Furuu na Mahasin. 1652   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 25. 1648 1649

360

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 360

8/10/2017 1:22:19 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) amesema: “Si vibaya kula nyama ya nyati, na kunywa maziwa yake, na kula samli yake.”1653 Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) amesema: “Nyama inaotesha nyama, na yule ambaye ameingiza tumboni mwake kipande cha nyama, basi ametoa ugonjwa mfano wake.”1654 Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) amesema: “Sioni tatizo ulaji wa nyama ya korongo, kwani hiyo ni nzuri kwa bawasiri, na maumivu ya mgongo, nayo ni miongoni mwa zinazosaidia katika kujamiana.”1655 Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) kwamba aliletewa ndege firigogo taji, basi akasema: “Hakika nyama hiyo ina baraka.” Na ilikuwa ikimpendeza, na alikuwa akisema: Mlisheni mwenye homa ya manjano ile iliyochomwa.”1656 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Hakika ulaji wa nyama unaongeza usikivu na uonaji, na ulaji wa mayai unaimarisha nguvu za kiume.”1657 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kwamba alimwambia Maamuni katika barua ya dhahabu: “Na uzidishaji wa ulaji wa nyama pori na ng’ombe, unasababisha ubadilikaji wa akili na ufahamu, unalaza ubongo, na unazidisha usahaulifu.”1658 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Tununulie sisi nyama ya sehemu ya juu wala usitununulie nyama ya sehemu ya   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 35, kutoka kitabu Furuu.   Makarimul-Akhlaq, uk. 159 na Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 29. 1655   Makarimul-Akhlaq, uk. 161. 1656   Makarimul-Akhlaq, uk. 161. 1657   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 280. 1658   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 322. 1653 1654

361

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 361

8/10/2017 1:22:19 PM


TIBA YA MAASUMINA

chini, hakika ya juu ni karibu zaidi na njia ya chakula na mbali zaidi na maradhi.”1659 Imepokewa kutoka kwa Sa’ad bin Sa’ad Ashi’ath amesema: Nilimwambia Imam Ridha (a.s): “Hakika watu wa nyumbani kwangu hawali nyama ya kondoo! Akasema: Kwa nini? Nikasema: Wanasema hakika hiyo inachochea nyongo ya manjano, na maumivu ya kichwa na maumivu mengine. Basi akasema: Ewe Sa’ad, lau angelijua Mwenyezi Mungu kitu kitukufu zaidi kuliko kondoo asingelimtoa huyo fidia kwa Ismail.”1660 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) alimwambia mmoja wa masahaba wake: “Basi ni juu yako kutumia mchadi, kwani unaoteshwa juu ya ufukwe wa Firdausi, na ndani yake kuna ponyo ya maradhi, nayo inakomaza mifupa na inaotesha nyama.”1661 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Bwana wa chakula duniani na akhera ni nyama, kisha mchele.”1662 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Ilitajwa mbele ya Mtume (s.a.w.w) nyama na mafuta yake akasema: Hakuna katika hivyo kipande kitakachoanguka ndani ya mfuko wa chakula ila kitaotesha ponyo sehemu yake ponyo, na kitaondoa ugonjwa kutoka sehemu hiyo.”1663 Imepokewa kutoka kwa Imam Hadi (a.s) amesema: “Sikula chakula chenye kubakia zaidi wala chenye kuchochea zaidi ugonjwa kuliko nyama yabisi (yaani kavu).”1664   Biharul-Anwaar, Juz. 66, uk. 75.   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 27, kutoka kitabu Furuu na Mahasin. 1661   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 159, kutoka kitabu Mahasin cha Barqi. 1662   Sahifatul-Ridha (a.s), uk. 52. 1663   Sahifatul-Ridha (a.s), uk. 75. 1664   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 38, kutoka kitabu Furuu al-Kaafi, Juz. 6, uk. 314. 1659 1660

362

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 362

8/10/2017 1:22:19 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kwamba: “Ulaji wa nyama ya ndama ya mbuzi iliyoiva unanenepesha, na sio nyama kavu, wala sio ya ndama wa ngamia wala wa ng’ombe.”1665 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Mwislamu akidhoofika basi naale nyama kwa maziwa, hakika Mwenyezi Mungu amejaalia nguvu katika hivyo viwili.”1666 Mshikaki Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Mshikaki unaondoa homa.”1667 Imepokewa kutoka kwa Musa bin Bakir amesema: Aliniambia Imam Kadhim (a.s): “Kwa nini ninakuona wa manjano? Nikasema: Imenipata homa nyepesi. Akasema: Kula nyama, basi nikala. Kisha akaniona baada ya juma moja mimi nikiwa na hali ile ile ya umanjano. Akasema: Je, sikukuamrisha kula nyama? Nikasema: Sijakula kitu kingine tangu uliponiamrisha. Akasema: Umekulaje? Nikasema: Iliyopikwa. Akasema: Hapana, kula mshikaki, basi nikala. Kisha akanitumia mjumbe na akaniita baada ya wiki, basi damu ikarejea usoni kwangu. Akasema: Hivi sasa barabara.”1668 Pia imepokewa kutoka kwake amesema: Nilisumbuliwa Madina na udhaifu, nikaenda kwa Abul Hasan Imam Musa (a.s), akaniambia: Ninakuona mdhaifu. Nikasema: Ndio. Akaniambia: Kula mshikaki, basi nikala nikapona.”1669

Mustadrak, Juz. 3, uk. 105.   Tuhful-Uquul, uk. 76. 1667   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 49. 1668   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17 uk. 48. 1669   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 48. 1665 1666

363

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 363

8/10/2017 1:22:19 PM


TIBA YA MAASUMINA

KUNG’ATWA NA NGE Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Mtume (s.a.w.w) aling’atwa na nge, basi akamtemea mate, na akasema: Mwenyezi Mungu akulaani wewe, hasalamiki na wewe muumini wala kafiri. Kisha akaitisha chumvi akaiweka juu ya mahali alipong’atwa, kisha akakamua kwa dole gumba lake mpaka pakayeyuka. Kisha akasema: Lau watu wangelijua yale yaliyomo kwenye chumvi wasingelihitajia dawa ya kijiuasumu.”1670 Mmoja wa masahaba wa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Tulikuwa pale mmoja wetu anapogongwa na nyoka au nge, husema (a.s): Mnywesheni uji wa tufaha.”1671 Imepokewa kutoka kwa Abdul-Rahman bin Hajjaj amesema: Mtu mmoja alimuuliza Abu Hasan Imam Kadhim (a.s) kuhusiana na dawa inayokinga madhara ya sumu? Akasema: “Haina madhara. Akasema: Ewe mtoto wa Mtume, hakika huwekwa ndani yake nyama za njoka! Akasema: Usiifanye ni uchafu.”1672

Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 407.   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 128, kutoka Furuu Kaafi. 1672   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 63. 1670 1671

364

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 364

8/10/2017 1:22:19 PM


TIBA YA MAASUMINA

Maelezo: Taryaq (kijiuasumu) ni dawa yenye mchanganyiko maalum wenye kumsaidia aliyegongwa na wadudu aina saba wenye sumu kali; na moja ya mchanganyiko wake ni nyama za nyoka. Na kauli yake: “Usiifanye ni uchafu” yaani msiifanye haramu juu yetu. Ibn Bastam amesema: Amenihadithia baba mzazi akasema: Miongoni mwa yale yaliyojaribiwa kwa ajili ya tiba ya aliyeng’atwa na nge ni kuivunja kokwa ya ukwaju nusu mbili, unaweka nusu ya sehemu ya ndani mahali alipogongwa na nge, na unakaza hadi inanasa sehemu husika, kwani hiyo ni yenye manufaa mujarabu.1673 Na akasema: Amenisimulia mmoja wa wenye fadhila akasema: Miongoni mwa yale yaliyojaribiwa kuhusu hilo ni kisagwe kitunguu maji na kichanganywe na chumvi laini, na iwekwe juu ya sehemu iliyogongwa na nge mara mbili au tatu, atapona ndani ya wakati.1674 TANIPU Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Hakuna yeyote ila anacho chanzo cha mbalanga, basi kuleni tanipu katika wakati wake litawaondosheeni chanzo hicho.”1675 Na imekuja katika hadithi nyingine: “Hakuna yeyote ila anacho chanzo cha mbalanga, hakika tanipu linaondoa chanzo hicho, basi kuleni katika wakati wake, linawaondoshea nyinyi kila aina ya ugonjwa.”1676 Imepokewa kutoka kwa Ali bin Musayyib amesema: Alisema mja mwema (a.s): “Ni juu yako kula tanipu, kwani hakuna yeyote   Tuhfatul-Ridhawiyyat fil-Mujarrabaat Imamiyyat, uk. 75.   Tuhfatul-Ridhawiyyat fil-Mujarrabaat Imamiyyat, uk. 75. 1675   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 165, kutoka kitabu Mahasin cha Barqi. 1676   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 165, kutoka kitabu Mahasin cha Barqi. 1673 1674

365

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 365

8/10/2017 1:22:19 PM


TIBA YA MAASUMINA

ila anacho chanzo cha mbalanga, na hakika ulaji wa tanipu unaondoa chanzo hicho. Nikasema: Bichi au la kupikwa? Akasema: hali zote mbili.�1677 Maji (na unywaji) Faida yake: Zimepatikana hadithi mbali mbali zenye kusigana katika dhahiri, baadhi yake zinalingania unywaji wa maji, na nyingine zinakataza na kulaumu hilo. Na uhakika ni kwamba unywaji wa maji una madhara baada ya chakula, wala hakuna tatizo katikati yake kwa ulinganifu. Ama kabla ya kula chochote na baina ya milo basi ni yenye kufaidisha, hakika upungufu wa maji mwilini unasababisha maradhi mengi ya hatari, na unachangia katika utengenezaji wa vijiwe katika figo. Usafishaji wa maji safarini: Ibn Sina katika kitabu (Qanun) katika sehemu ya kumkinga msafiri na madhara ya unywaji maji tofauti amesema: Hakika tofauti ya maji inaweza kumtia msafiri katika maradhi mbalimbali, basi inawajibika kuchunga suala la maji, na kujikinga na madhara yake, na moja ya njia za kujikinga na madhara yake ni kuyasafisha. Akasema: Na miongoni mwa yale yanayoondoa uharibifu wa maji tofauti ni: Kitunguu maji, hasa hasa pamoja na siki na kitunguu saumu, kwani hilo ni dawa (kijiuasumu) inayozuia madhara ya sumu. Na miongoni mwa miongoni mwa mambo yanayoondoa madhara ya maji mazito ni kuyatia kitunguu saumu, kwani hiyo ni kijiuasumu.   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 214, kutoka kitabu Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 105.

1677

366

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 366

8/10/2017 1:22:19 PM


TIBA YA MAASUMINA

Na miongoni mwa yale yaliyokuja kutokana na tadaburi nzuri kwa yule ambaye anakunywa maji tofauti atembee na maji ya mji wake, basi ayachanganye na maji ya mji aliofikia, na achukue maji ya mji huo aliofikia hadi kwenye mji mwingine unaofuata, achanganye na maji yake, na ataendelea hivyo mpaka afikie alikokusudia. Na awe na udongo wa mji wake na auchanganye na wa mji aliofikia, kisha auchanganye na maji mpaka uchanganyike, kisha ayaache mpaka yasafike, anywe baada ya kuchujwa kwa kitambaa.1678 Hadithi: Mtume (s.a.w.w) amesema: “Sadaka bora zaidi ni ya maji.”1679 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kwamba amesema: “Mnapokunywa maji yanyonyeni, wala msinywe kwa kugugumia, kwani hilo linasababisha maradhi katika ini.”1680 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Yule ambaye anakunywa maji hali amesimama na akapatwa na kitu miongoni mwa maradhi hatopona abadani.”1681 Na miongoni mwa sunna ni: Mtu apumue mara tatu kati kati ya kunywa maji, na ataanza kwa kumtaja Mwenyezi Mungu, na atamalizia kwa kumhimidi Mwenyezi Mungu, wala asipumulie chomboni.”1682 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Unywaji wa maji kwa kutumia kikombe cha wengi ni kinga dhidi ya ukoma na mbalanga.”1683   Itihaafu bihibbil-Ashraaf, uk. 48 cha Shabrawiy.   Ramzu-Sihat, uk. 8 cha Dahsurkhi. 1680   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 188, kutoka kitabu Furuu na Mahasin. 1681   Biharul-Anwaar, Juz. 66 uk. 472. 1682   Biharul-Anwaar, Juz. 66 uk. 472. 1683   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 269. 1678 1679

367

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 367

8/10/2017 1:22:19 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Miongoni mwa unyenyekevu ni mtu kunywa maji yaliyobakishwa na ndugu yake muumini.”1684 Imepokewa kutoka kwa Amirul-Muminina Ali (a.s) amesema: “Maji ni bwana wa vinywaji duniani na akhera.”1685 Imepokewa kutoka kwa Amirul-Muminina Ali (a.s) amesema: “Hayakuonekana maji kwa mwenye akili na akakataa.”1686 Imepokewa kutoka kwa Ibn Abbas (r.a) amesema: “Hakika Mwenyezi Mungu atayaondoa maji matamu kabla ya siku ya Kiyama, isipokuwa ya Zamzam, na hakika maji yake yanaondoa homa, na maumivu ya kichwa, na kuchungulia ndani yake kunasafisha macho, na yule atakayekunywa kwa tiba Mwenyezi Mungu atamponya, na yule atakayekunywa hali ya kuwa na njaa basi Mwenyezi Mungu atamshibisha.”1687 Imepokewa kutoka kwa Sulaiman bin Khalid akasema: Nilimuuliza Abu Abdillah (a.s) kuhusiana na mtu anayekunywa kwa punzi moja. Akasema hilo ni baya, na ni unywaji wa Haim. Nikasema: Ni nini Haim? Akasema: Ni ngamia.”1688 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Mmoja wenu atapokunywa maji akasema: Bismillah, kisha akakata hiyo akasema: Al-hamdulillahi. Kisha akanywa akasema: Bismillah, kisha akaikata, akasema: Al-hamdulillah (akafanya hivyo mara tatu) maji hayo yatafanya tasbihi kwa niaba yake maadamu yangali tumboni mwake hadi yatakapotoka.”1689   Ramzu-Sihat, uk. 6.   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17 uk. 186, kutoka kitabu Furuu Kaafi. 1686   Kauli iliyo mashuhuri. 1687   Biharul-Anwaar, Juz. 66, uk. 451. 1688   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17 uk. 190, kutoka kitabu Tahdhiib cha Twabarasi na Mahasin cha Barqi. 1689   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 199, kutoka kitabu Furuu al-Kaafi na Mahasin. 1684 1685

368

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 368

8/10/2017 1:22:19 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Mtume (s.a.w.w) alipita kwa watu wakinywa maji kwa vinywa vyao katika vita vya Tabuuk, Mtume (s.a.w.w) akasema: “Kunyweni kwa mikono yenu kwani yenyewe ndio vyombo bora mlivyonavyo.”1690 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Salio la maji ya muumini ni ponyo katika magonjwa sabini.”1691 Mtu mmoja alimuuliza Imam as-Sadiq (a.s) kutokana na ladha ya maji, akasema: “Uliza kwa kutaka kujua wala usiulize kwa ubishi, ladha ya maji ni ladha ya uhai.”1692 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Maji ya Zamzam ni ponyo la kila ugonjwa.” Na ninadhani alisema: “Vyovyote yatakavyokuwa kwa sababu Mtume (s.a.w.w) alisema: Maji ya Zamzam ni kwa nia utakayoinywea.”1693 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Msizidishe unywaji wa maji, kwani hayo ni chanzo cha kila ugonywa.”1694 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Asinywe mmoja wenu maji mpaka awe na kiu nayo, na akiyatamani basi apunguze unywaji wake.”1695 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Lau watu watapunguza unywaji wa maji basi itasimama sawasawa miili yao.”1696 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Alikuwa Mtume (s.a.w.w) akila shahamu kupunguzaunywaji wa maji.   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 206, kutoka kitabu Furuu al-Kaafi na Mahasin cha Barqi.   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 208, kutoka kitabu Twawabul-Aamal, uk. 83 cha Saduuq. 1692   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17 uk. 187, kutoka kitabu Furuu al-Kaafi. 1693   Twibbul-Aimmat (a.s), 52. 1694   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 190, kutoka kitabu Furuu al-Kaafi na Mahasin. 1695   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 190, kutoka kitabu Mahasin cha Barqi. 1696   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 190, kutoka kitabu Mahasin cha Barqi. 1690 1691

369

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 369

8/10/2017 1:22:20 PM


TIBA YA MAASUMINA

Akaulizwa: Ewe Mtume (s.a.w.w) hakika wewe unapunguza unywaji wa maji! Akasema: Nao ni mzuri zaidi kwa chakula changu.”1697 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Ukila samaki shushia kwa maji.”1698 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Kunyweni maji ya mvua, kwani ni tohara kwa mwili na yanakinga magonjwa, Mwenyezi Mungu (s.w.t) amesema: “Na anakuteremshieni maji mawinguni ili kukutakaseni nayo. 1699, 1700 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Unywaji maji mchana kwa kusimama kunafanya chakula kishuke vizuri, na unywaji maji usiku kwa kusimama kunasababisha maji ya manjano.”1701 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Mmoja wenu asinywe maji akiwa mwenye kusimama, kwani yanasababisha ugonjwa ambao hauna dawa, ila Mwenyezi Mungu amponye.”1702 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Unywaji wa maji mchana kwa kusimama kunatoa jasho na kunatia nguvu mwili.”1703 Na amekusanya Sheikh Muhammad Husein Aasim sifa zote hizi za maji katika utenzi wake kuhusiana na adabu za kula chakula na kunywa kinywaji amesema:   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 190, kutoka kitabu Mahasin cha Barqi.   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 54. 1699   Surat Anfaal, aya 11 1700   Khiswal, uk. 171 cha Saduuq. 1701   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 191, kutoka kitabu Furuu na Mahasin. 1702   Tuhful-Uquul, uk. 80. 1703   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 192, kutoka kitabu Man la yahdhuruhul-Faqiih, Juz. 3, uk. 223. 1697 1698

370

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 370

8/10/2017 1:22:20 PM


TIBA YA MAASUMINA

Bwana wa vimiminika ni maji – ambayo hujitosheleza yenyewe bila kuhitajia kingine chochote Hivi huoni wahyi ulioteremshwa kwa Mtume – kutokana nayo tumefanya kila kitu kuwa hai Na inakatazwa ukithirishaji wake kwa uwepo wa andiko – na pia kuyanywa bila kunyonya Unywaji huo ni kuyadhuru maini – yaani maumivu ya ini Utayanywa usiku kwa kukaa - kwa mujibu wa walivyopokea na utayanywa mchana kwa kusimama. Imepokewa kutoka kwa Muhammad bin Faydh amesema: Nilimwambia Imam as-Sadiq (a.s): Nafsi yangu nimeitoa fidia kwako, anaumwa mmoja miongoni mwetu, basi waganga wanamwamrisha kutumia lishe kamili! Akasema: “Hapana, lakini sisi Ahlul-bayt hatutumii lishe kamili ila kutokana na tende, na tunajitibu kwa tufaha, na maji ya baridi.”1704 Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) amesema: “Namshangaa mtu aliyekula mfano wa kiganja (akiashiria kwa kiganja chake cha mkono) na hakunywa juu yake ila maji, vipi usipasuke mfuko wake wa chakula.”1705 Imepokewa kutoka kwa Ibn Abi Tayfur Mutabibu amesema: “Niliingia kwa Imam Kadhim (a.s) nikamuliza kuhusiana na unywaji wa maji. Akasema: Hakuna tabu kwa maji, nayo yanazungusha chakula katika mfuko wa chakula, na yanatuliza ghadhabu, yanakuza akili na yanazima nyongo.”1706   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 59, na Ilalu-Sharaai, Juz. 2, uk. 149 cha Saduuq.   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 189, kutoka kitabu Furuul-Kaafi. 1706   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 189, kutoka kitabu Furuul-Kaafi na Mahasin. 1704 1705

371

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 371

8/10/2017 1:22:20 PM


TIBA YA MAASUMINA

Barua ya dhahabu ya Imam Ridha (a.s): “Na yule anayetaka asiudhiwe na mfuko wake wa chakula, asinywe maji baina ya chakula chake mpaka akimaliza. Na yule atakayefanya hivyo (yaani akanywa maji kati kati ya chakula) mwili wake utakuwa na unyevunyevu na utakuwa dhaifu mfuko wake wa chakula, na haitopata nguvu mishipa ya chakula, kwani chakula kinakuwa kama kisichoiva, yakimwagwa maji juu ya chakula kwanza ni bora zaidi.”1707 Barua ya dhahabu ya Imam Ridha (a.s): “Na ama wema wa msafiri na kukinga maudhi safarini, nayo ni kwamba asinywe maji kila nyumba anayofikia ila baada ya kuyachanganya na maji ya nyumba ya kabla yake, au awe na maji aina mmoja anayoyachanganya na maji anayokutaka nayo. Na la wajibu msafiri ajiandalie masurufu kutokana na udongo wa mji wake, na kila ambapo atafika kwenye nyumba atatia kwenye chombo ambacho atakitumia kunywea udongo kidogo ambao amesafiri nao kutoka katika mji wake, na hapo atatia maji na udongo ndani ya chombo atatingisha, na acheleweshe kunywa mpaka yasafike vizuri sana. Na maji mazuri zaidi kunywa kwa yule mkazi au msafiri ni maji ya chemchem ya upande wa mashariki kutokana na wepesi weupe wake. Na maji bora zaidi ni yale yanayotokea mawio ya jua wakati wa kiangazi, na yenye afya nzuri zaidi na bora zaidi ni yale yenye kusifika kwa sifa ya chemchem na yakawa na njia yake katika milima ya udongo, hilo ni kwa sababu hayo maji wakati wa masika ynakuwa ya baridi, na wakati wa kiangazi ni yenye kulainisha tumbo, yenye manufaa kwa watu wenye kuathiriwa na joto. Na ama maji ya chumvi na maji mazito hakika hayo yanafanya tumbo kuwa yabisi. Na maji ya barafu ni mabaya kwa miili mingine, na ni yenye madhara mengi zaidi. Na ama maji ya mvua hakika hayo   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 323.

1707

372

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 372

8/10/2017 1:22:20 PM


TIBA YA MAASUMINA

ni mepesi, matamu, safi na yenye manufaa kwa mwili, ikiwa hayatuama na kuhifadhika ardhini. Na ama maji ya kisima hakika hayo ni matamu, safi na yenye manufaa, ikiwa yatadumu kutembea bila kutuama ardhini.”1708 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Tumbo lako usiliache tupu bila ya chakula, na unywe maji kidogo, wala usifanye tendo la ndoa ila ukiwa na hamu…”1709 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Bwana wa chakula cha duniani na akhera ni nyama, na bwana wa kinywaji duniani na akhera ni maji.”1710 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kuhusiana na maji baridi amesema: “Hakika hayo yanazima joto, yanatuliza umanjano, na yanarahisisha mmeng’enyo wa chakula, na yanayeyusha mabaki ambayo yako juu ya kichwa cha mfuko wa chakula, yanaondoa homa.”1711 Imepokewa kutoka kwa mmoja wa masahaba wetu ameirufaisha kwa kusema: Unywaji wa maji baada ya chenye mafuta ya mnyama unachochea ugonjwa.”1712

Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 326.   Makarimul-Akhlaq, uk. 181. 1710   Sahifatul-Ridha (a.s), uk. 54. 1711   Fiqhul-Ridha (a.s), uk. 346. 1712   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 190, kutoka kitabu Mahasin cha Barqi. 1708 1709

373

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 373

8/10/2017 1:22:20 PM


TIBA YA MAASUMINA

MAJI YA MWANAUME Maana yake: Makusudio ni maji ya mgongo, au maji ya uti wa mgongo au maji ya mwanaume yaani manii. Hadithi: Amepokea Mtume (s.a.w.w) kutoka kwa Jibrail (a.s) amesema: “Tende barni inashibisha na inapendezesha na inatia uzuri, nayo ni dawa wala hakuna ugonjwa ndani yake, na kila tunda ni zuri, na linamridhisha Al-Rahma, na linamchukiza Shetani, na linaongeza maji ya mgongo.”1713 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Zidisheni ulaji wa bilinganyi wakati wa uvunaji wake, kwani ni ponyo la kila ugonjwa, linaongeza ung’aavu wa uso, na linaimarisha mishipa, na linaongeza maji ya uti wa mgongo.”1714 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuhusiana na jibini amesema: “Nayo asubuhi ni yenye kudhuru, inanufaisha usiku, na inaongeza maji ya mgongo.”1715 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Kuleni kitunguu maji, hakika hicho kina mambo matatu; kinaboresha tendo la ndoa, kinaimarisha ufidhi na kinaongeza maji ya tendo la kujamiana.”1716 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Kitunguu maji kinaondoa uchovu, kinaimarisha mishipa ya fahamu, na kinaongeza upigaji hatua, kinaongeza maji na kinaondoa homa.”1717   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 108.   Makarimul-Akhlaq, uk. 184. 1715   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 92. 1716   Fusuulul-Muhimmat, uk. 137 cha Hurru Aamili. 1717   Fusuulul-Muhimmat, uk. 137 cha Hurru Aamili. 1713 1714

374

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 374

8/10/2017 1:22:20 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Yule anayekula pera kabla ya kula chochote maji yake yatakuwa mazuri na mtoto wake atakuwa mzuri (na katika hadithi nyingine) utakuwa mzuri uso wake.”1718 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Na Sa’atar na chumvi vinaondoa harufu kutoka kifuani, na vinafungua vizuizi, vinaunguza kikohozi na vinazungusha maji…”1719 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Na Sa’atar na chumvi, zinaondoa harufu itokayo kifuani…”1720 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Ulaji wa ashnaan unadhoofisha magoti mawili na unaharibu maji ya mgongo.”1721 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Maziwa ni yenye manufaa kwa yule ambaye maji yake ya mgongo yamebadilika.”1722 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Ni juu yako kula hindubaau, kwani linaongeza maji na linafanya rangi kuwa nzuri, nalo ni laini linaongeza katika upatikanaji wa watoto wa kiume.”1723 Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) amesema: “Yule ambaye yamebadilika maji yake ya kutengeneza mtoto yanamfaa yeye maziwa na asali.”1724   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 131.   Makarimul-Akhlaq, uk. 191. 1720   Makarimul-Akhlaq, uk. 191. 1721   Khiswal, Juz. 1, uk. 63 cha Saduuq. 1722   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 130. 1723   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 130 1724   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 266. 1718 1719

375

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 375

8/10/2017 1:22:20 PM


TIBA YA MAASUMINA

Barua ya dhahabu ya Imam Ridha (a.s): “Na yule anayetaka asipatwe na vijiwe na kubanwa na haja ndogo, asizuie manii wakati wa uteremkaji wa shahawa, wala asirefushe ukaaji juu ya wanawake.”1725

CHOROKO (MASHI) Maana yake: Ni miongoni mwa mimea yenye kutambaa na punje duara za kijani, ndogo kuliko za uwatu, unapatikana Sham na wa India. Hadithi: Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) aliulizwa na mmoja wa masahaba wake kuhusu mabaka?1726 muulizaji anasema: “Basi akaniamrisha nipike choroko (mashi) nizikaushe na kuziweka ndani ya chakula changu, basi nikafanya hivyo siku kadhaa na nikapona.”1727 Na imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Chukua choroko mbichi katika siku zake na isage hiyo na majani yake, na kamua maji na kuyanywa kabla ya kula kitu, na jipake juu ya mabaka, basi nikafanya hivyo na nikapona.”1728

KIBOFU CHA MKOJO Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Kuleni tikitimaji, kwani ndani yake kuna mambo 10 yenye kukusanyika;… na linaosha kibofu cha mkojo na linaleta haja ndogo. Na katika hadithi nyingine: na linayeyusha vijiwe katika kibofu cha mkojo.”1729   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 324.   Ni weupe mwilini hautokani na ukoma. 1727   Makarimul-Akhlaq, uk. 187. 1728   Makarimul-Akhlaq, uk. 187. 1729   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 139, na Makarimil-Akhlaq uk. 185. 1725 1726

376

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 376

8/10/2017 1:22:20 PM


TIBA YA MAASUMINA

Mambo ya haramu na ya makuruhu Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema:

ُ َ َّ َ َ َ ْ َ ْ‫َّ َ َ َّ َ َ َ ْ ُ ُ م‬ َّ َ ْ ْ ۖ ‫الد َم َول ْح َم ال ِخن ِز ِير َو َما أ ِه َّل ِب ِه ِلغ ْي ِر الل ِه‬ ‫ِإنما حرم عليكم اليتة و‬ “Hakika amekuharamishieni mzoga na damu, na nyama ya ­nguruwe, na mwenye kuchinjwa kwa jina lisilokuwa la Mwenyezi Mungu…..”1730

Imepokewa kutoka kwa Amirul-Muminina Ali (a.s) amesema: “Hakika Mtume (s.a.w.w) alikuwa akichukia ulaji wa vitu vitano; bandama, uume, masikio, uuke, na atiria (vishimo viwili vya mishipa ya moyo).”1731 Imepokewa kutoka kwa Amirul-Muminina Ali (a.s) amesema: Siku moja alipita kwa wauza nyama, basi akawakataza kuuza vitu saba vinavyotokana na mbuzi, akawakaza kuuza damu, tezi, atiria, bandama, mapupu na uume. Mtu mmoja miongoni mwa wauza nyama akamwambia: Ewe Amirul-Muminina ini na bandama ni sawa. Akamwambia: “Umesema uongo ewe mpumbavu, niletee maji yenye tindikali ya amino nitakuletea tofauti iliyopo baina ya hivyo viwili. Basi akaletewa ini na bandama na maji yenye tindikali. Akasema: Zamisha kila moja kati ya hivyo viwili ndani ya chombo chake, basi akavizamisha kama alivyomwamrisha, ini likakunjamana na halikutoa chochote, lakini bandama haikukunjamana na ikatoa yote iliyokuwa nayo na yote yakawa ni damu na haikubakia ila ngozi na mishipa yake. Basi akasema: Hii ndiyo tofauti kati ya hivi viwili, na hii ni nyama na hii ni damu.1732   Sura 2 aya ya 173.   Khiswal, Juz. 1, uk. 284 cha Saduuq. 1732   Khiswal, Juz. 2, uk. 341. 1730 1731

377

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 377

8/10/2017 1:22:20 PM


TIBA YA MAASUMINA

Amirul-Muminina Ali (a.s) amesema: “Mmoja wenu akinunua nyama basi atoe humo tezi, kwani hiyo inachochea vyanzo vya mbalanga.”1733 Imepokewa kutoka kwa Muhammad bin Adhafir kutoka kwa baba yake amesema: Nilimuuliza Abu Ja’far Muhammad bin Ali Baqir (a.s) kwa kusema: Kwa nini Mwenyezi Mungu ameharamisha mzoga, damu, nguruwe na pombe? Akasema: “Si kwa kupendelea aliyoyahalalisha na wala si kwa kuchoshwa na aliyoharamisha ndio Mwenyezi Mungu (s.w.t) akaharamisha hayo kwa waja wake na akahalalisha visivyokuwa hivyo. Lakini ni kwamba Yeye (a.j) ameumba viumbe na akajua yale yanayoimarisha miili yao, na yanayowafaa, basi akawahalalishia hivyo na kuwapa ruhusa, na akajua yale yanayowadhuru wao basi akawakataza hayo. Kisha akamhalalishia yule aliyedharurika wakati ambao hauimariki mwili ila kwalo, basi akamhalalishia kwa kiwango cha kukidhi haja yake na sio kinyume na hivyo. Kisha akasema: Ama mzoga hakuna atayeutumia ispokuwa utadhoofisha mwili wake, utapunguza nguvu zake, na utakata kizazi chake. Na mla mzoga hafi ila kwa ghafla. Na ama kuhusu damu inamsababishia mlaji maji ya manjano, na inasababisha kichaa na moyo mgumu na ukosefu wa upendo na huruma, kisha hamwamini kipenzi chake wala hamwamini rafiki yake. Na ama nyama ya nguruwe, hakika Mwenyezi Mungu (s.w.t) aliwafanya watu kuwa sura mbali mbali mfano wa nguruwe, ngedere na dubu, kisha akakataza kula mfano wake ili wasifaidike hao wala wasipate tahfifu adhabu zao. Na ama pombe hakika Yeye ameiharamisha hiyo kwa vitendo vyake na uovu wake. Kisha (a.s) akasema: Hakika mwenye kudum  Ilalul-Sharaai, uk. 561 cha Sheikh Saduuq (amekufa mwaka 380) kimechapishwa na Daaru Ihyaai Turaath Arabi Beirut.

1733

378

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 378

8/10/2017 1:22:20 PM


TIBA YA MAASUMINA

isha unywaji wa pombe ni kama vile mwabudu sanamu, inamsababishia yeye kutetemeka na inaondoa murua wake, na inamfanya awe jasiri kutenda mambo ya haramu, kutokana na umwagaji wa damu na kufanya zinaa, mpaka haaminiki akilewa kutenda jambo la haramu bila kujua, na pombe haimuongezei mnywaji wake ila kila shari.”1734 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kutoka kwa baba yake kutoka kwa babu yake, kutoka kwa Ali bin Abi Twalib (a.s) kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) katika wosia wake kwake amesema: “Ewe Ali vimeharamishwa kutokana na mbuzi vitu saba; Damu, uume, kibofu cha mkojo, uti wa mgongo, tezi, bandama na nyongo.”1735

SABABU AMBAYO IMEFANYA ­YAMEHARAMISHWA BANDAMAA, TUPU MBILI NA UTI WA MGONGO: Imepokewa kutoka kwa Abu Abdillah (a.s) aliulizwa: “Vipi imekuwa bandama ni haramu nayo inatokana na kilichochinywa? Akasema: “Hakika Nabii Ibrahim (a.s) alipoteremshiwa kondoo kutoka Thabiir nalo ni jabali la Makka ili amchinje, alimjia ibilisi akamwambia: Nipe fungu langu kutokana na kondoo. Akasema: Ni lipi fungu lako na hii ni kafara ya Mola Wangu na fidia badala ya mwanangu? Basi hapo Mwenyezi Mungu akamfunulia yeye kuwa yeye ana fungu humo, nalo ni bandama, kwani hiyo ni kusanyiko la damu, na akaharamisha tupu mbili kwani hizo ni sehemu ya tendo la kujamiana na njia ya maji ya uzazi. Basi Ibrahim akampatia yeye bandama, tupu mbili nazo ni korodani mbili.” Basi nikamwambia: Vipi ameharami  Aamali, uk. 529 cha Saduuq, kimechapishwa na taasisi ya Aalami chapa ya tano.   Khiswal, Juz. 2, uk. 341.

1734 1735

379

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 379

8/10/2017 1:22:20 PM


TIBA YA MAASUMINA

sha uti wa mgongo? Akasema: “Kwa sababu ni mahali pa maji panapo sukuma maji ya dume na jike, nao ni ute mrefu ambao unakuwa katika uti wa mgongo.”1736 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Mwenyezi Mungu amehalalisha ng’ombe, mbuzi, kondoo na ngamia kwa wingi wake na uwezekano wa upatikanaji wake, na uhalali wa ng’ombe pori na wengineo ni miongoni mwa wanyama pori walio halali kuliwa, kwa sababu chakula chake sio makruhu wala haramu wala sio chenye kuwadhuru wao wenyewe wala si chenye kudhuru watu wala hakina uharibifu.”1737 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Jiepusheni kula ndege ambaye hana kidole gumba wala kifuko cha chakula shingoni.”1738 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Jizuieni kula wale wanyama wakali wenye meno ya kuwindia, na kila mwenye makucha miongoni mwa ndege. Wala msile bandama, kwani imeota kutokana na damu chafu.”1739 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Jiepusheni na kula tezi, kwani hiyo inachochea mishipa ya mbalanga.”1740 MIHADARATI Mtume (s.a.w.w) amesema: “Itakuja zama umma wangu watavuta kitu ambacho jina lake ni bangi, na mimi nipo mbali nao, na wao watakuwa mbali nami.”1741   Ilalul-Sharaai, uk. 562 cha Saduuq.   Ilalul-Sharaai, uk. 561 cha Saduuq. 1738   Tuhfal-Uquul, uk. 75. 1739   Tuhful-Uquul, uk. 75. 1740   Tuhfal-Uquul, uk. 75. 1741   Mustadrakul-Wasail, Juz. 3, uk. 145. 1736 1737

380

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 380

8/10/2017 1:22:20 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Wasalimieni mayahudi na manaswara, wala msimsalimie mvutaji wa bangi.”1742 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Yule ambaye anadharau dhambi ya bangi hakika amekufuru.”1743 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Yule anayevuta bangi, ni kama vile amevunja Kaaba mara 70, na kana kwamba ameua malaika wa karibu 70, na kama vile ameua manabii 70, na kama vile ameunguza misahafu 70, na kama vile amemrushia Mwenyezi Mungu mawe 70, naye yuko mbali zaidi na rehema ya Mwenyezi Mungu kuliko mnywaji pombe, mlaji riba, mzinifu na msengenyaji.”1744 Nyongo nyeusi Mtume (s.a.w.w) amesema: “Ni juu yenu kutumia zabibu, kwani inafichua nyongo, inaondoa kikohozi na inakaza mishipa ya fahamu… ”1745 Mtu mmoja alimlalamikia Imam Baqir (a.s) kwamba mara nyingi alipatwa na matamanio, mpaka alikaribia kuchanganikiwa, akamwambia: “Yatulize kwa kula peasi.”1746 Imepokewa kutoka kwa Azraq bin Sulaiman, alimuuliza Imam as-Sadiq (a.s) kuhusiana na peasi akasema: “Ni lenye kuondoa nyongo, na linalainisha maungo, wala usizidishe kula hilo itajaza hewa katika maunganio yako.”1747   Mustadrakul-Wasail, Juz. 3, uk. 145.   Mustadrakul-Wasail, Juz. 3 uk. 145. 1744   Mustadrakul-Wasail, Juz. 3, uk. 145. 1745   Khiswal, Juz. 1, uk. 344 cha Saduuq. 1746   Twibbul-Aimamat (a.s), uk. 136. 1747   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 136. 1742 1743

381

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 381

8/10/2017 1:22:20 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Kula peasi kabla ya chakula chochote hutuliza nyongo, ila hakika hilo (ukizidisha kula) huchochea riyahi.”1748 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Kuleni bilinganya, kwani hilo ni zuri kwa nyongo nyeusi, wala haidhuru umanjano.”1749 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Ndio, mchuzi wa siki, unavunja nyongo na unahuisha moyo...”1750 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Hakika sawiiq kavu ikiliwa kabla ya kula chochote, inazima joto na kutuliza kibofunyongo...”1751 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Vitatu ni raha nyingi; sawiiq kabla ya kula chochote, inafuta nyongo na kikohozi, mpaka akasema: Inakaribia kutokuacha kitu.”1752 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Sawiiq inafuta nyongo na kikohozi na balgham na inakinga aina sabini ya mabalaa.”1753 Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) amesema: “Hakuna tatizo katika maji, nayo yanapangilia chakula katika mfuko wa chakula, na yanatuliza ghadhabu, yanaimarisha akili na yanazima nyongo.”1754 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Walisheni wagonjwa wenu mchadi (majani yake) na jiepusheni na mzizi wake kwani unachochea weusi.”1755   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 136.   Kashful-Akhtwar, cha Shamsu Diin bin Muhammad Huseini – Mahtut. 1750   Biharul-Anwaar, Juz. 66, uk. 304. 1751   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 67. 1752   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 8, kutoka kitabu Furuu. 1753   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 6. 1754   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 189, kutoka kitabu Furuu na Mahasin. 1755   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 157. 1748 1749

382

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 382

8/10/2017 1:22:20 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Katika asali kuna ponyo la kila ugonjwa, yule anayelamba asali kabla ya kula chochote inakata kikohozi na inakata umanjano na inazuia nyongo nyeusi…”1756 SUPU Mtume (s.a.w.w) amesema: “Ewe Ali! Ukipika kitu pamoja na nyama basi zidisha mchuzi, kwani hilo ni moja ya nyama mbili, na wagawieni majirani, hakika kama hawatapata nyama watapata mchuzi.”1757 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Nyama ilipokuwa ikiingizwa kwenye nyumba ya Mtume (s.a.w.w) alikuwa akisema: “Kateni vipande vidogo vidogo, na zidisheni mchuzi, na wagawieni majirani, kwani inaharakisha uivaji wake, na ina baraka kubwa.”1758 Chanuo na Kuchana Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Uchanaji wa nywele unaondoa homa na uchanaji wa ndevu unaimarisha magego.”1759 Imepokewa kutoka kwa Abu Abdillah (a.s) kuhusiana na kauli ya Mwenyezi Mungu (a.j) inayosema: “Chukueni mapambo yenu… ”1760 akasema: “Uchanaji nywele, kwani uchanaji nywele unavuta riziki, na unapendezesha nywele, unakidhi haja, na unaongeza maji ya mgongo, unakata kikohozi, na alikuwa Mtume (s.a.w.w)   Fiqhul-Ridha (a.s), uk. 346.   Makarimul-Akhlaq, uk. 158. 1758   Biharul-Anwaar, Juz. 66, uk. 75. 1759   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 330 cha Abdullah Shubbar. 1760   Surat Aaraf aya ya 31. 1756 1757

383

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 383

8/10/2017 1:22:21 PM


TIBA YA MAASUMINA

akichana chini ya ndevu zake mara 40, na juu yake mara saba, na anasema: Hakika hilo linaongeza nguvu katika ubongo na linakata kikohozi.”1761 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Jipakeni mafuta kwa kadiri ya mahitaji, na pakeni nyusi zenu wanja kwa mfululizo, na chaneni kwa kuziachanisha kwa marefu, na pigeni mswaki kwa mapana.”1762 Utumbo Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) amesema: “Chakula bora ni mchele, unapanua utumbo na unakata bawasiri, na hakika sisi tunapenda tuwe kama vile watu wa Iraq kwa kula kwao wali na tende, hakika hivyo viwili vinapanua utumbo na vinakata bawasiri.”1763 Mtume (s.a.w.w) amesema: “Tumbo ni nyumba ya ugonjwa, na lishe kamili ni kichwa cha kila dawa, na upe mwili kile ulichokizoea.” Mtume (s.a.w.w) amesema: “Hakika huyu Jibrail (a.s) ananijuza kwamba hakika katika tende kuna mambo tisa; inaboresha tendo la ndoa, inatibu tumbo na inameng’enya chakula…”1764 Ilitajwa nyama na mafuta yake mbele ya Mtume (s.a.w.w) akasema: “Hakuna kipande kutokana na hivyo viwili kinachoingia ndani ya tumbo, ila kinaotesha mahali pake ponyo, na kitaondoa sehemu yake ugonjwa.”1765   Khiswal, Juz. 1, uk. 268.   Fiqhul-Imam Ridha (a.s), uk. 407. 1763   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 95, kutoka kitabu Furuu na Mahasin. 1764   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 107 kutoka kitabu Mahasin. 1765   Sahifatul-Ridha (a.s), uk. 75. 1761 1762

384

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 384

8/10/2017 1:22:21 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Amirul-Muminina (a.s) amesema: “Kuleni komamanga na vijingozi vya utando wake, kwani hulainisha tumbo.”1766 Imepokewa kutoka kwa Amirul-Muminina Ali (a.s) amesema: “Ni juu yenu kula tufaha, kwani linaimarisha tumbo.”1767 Imepokewa kutoka kwa Muhammad bin Amru bin Ibrahim amesema: Nilimuuliza Abu Ja’far Imam Baqir (a.s) na nikamlalamikia yeye udhaifu wa tumbo langu, akasema: “Kunywa hazaa kwa maji baridi, (Hazaa ni mmea pori ambao unafanana na figili).1768 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Sawiiq ya dengu inakata kiu, inatia nguvu tumbo na ndani yake kuna ponyo la kila ugonjwa.”1769 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Kisibiti (komoni muluk) na jozi vinaunguza bawasiri, vinaondoa harufu, vinafanya rangi kuwa nzuri, vinaimarisha tumbo vinachemsha figo. Na thaimu (su’tar) na chumvi vinaondoa riyahi kifuani, vinafungua kizuizi, vinaunguza kikohozi, vinazungusha maji, vinaboresha tendo la ndoa, vinalainisha tumbo, vinaondoa harufu mbaya kinywani na vinaimarisha kiungo cha uzazi cha mwanaume.”1770 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuhusiana na ghubayraa amesema: “Hakika nyama yake inaotesha nyama… na pamoja na hivyo linachemsha figo na linalainisha tumbo…”1771 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Usiingie bafuni ila tumboni mwako kuwe na kitu kinachozima joto, hilo   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 134.   Ramzul-Sihat, uk. 155. 1768   Ramzul-Sihat, uk. 69. 1769   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 459 cha Abdullah Shubbar. 1770   Makarimul-Akhlaq, uk. 191. 1771   Makarimul-Akhlaq, uk. 176. 1766 1767

385

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 385

8/10/2017 1:22:21 PM


TIBA YA MAASUMINA

ni lenye nguvu zaidi kwa ajiali ya mwili. Wala usiingie hali tumbo lako limejaa chakula.”1772 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Kuleni maharagwe na maganda yake, kwani hayo yanalainisha tumbo.”1773 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Peasi linalainisha tumbo na linatia nguvu, hilo na pera pia.”1774 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Ni juu yako kula pera tamu pamoja na punje zake, kwani linaondoa udhaifu, linapendezesha tumbo na linatakasa kifua.”1775 Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) amesema: “Na hakuna tatizo kwa maji, nayo yanazungusha chakula ndani ya tumbo …”1776 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kuhusiana na maji baridi amesema: “Hakika hayo yanazima joto, yanatuliza umanjano, yanasaidia mmeng’enyo wa chakula, yanaondoa mabaki kwenye mlago wa utumbo na yanaondoa homa.”1777 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Kuleni komamanga, hakuna ndani yake punje inayoangukia tumboni ila hunawirisha moyo na inamfunga kinywa shetani kwa muda wa siku 40.”1778 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Lishe kamili ni kichwa cha kila dawa, na tumbo ni nyumba ya kila ugonjwa, na uzoeshe mwili kile ulichozoea.”1779   Fusuulul-Muhimmat, cha Hurru Aamili.   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 101. 1774   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 134. 1775   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 136. 1776   Wasaail=Shi’ah, Juz. 17, uk. 189, kutoka kitabu Furuu na Makasin. 1777   Fiqhul-Ridha, uk. 346. 1778   Sahifatul-Ridha (a.s), uk. 53. 1779   Fiqhul-Ridha, uk. 340. 1772 1773

386

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 386

8/10/2017 1:22:21 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kuhusiana na utafunaji wa ubani amesema: “Hakika huo unaondoa tumboni na kulisafisha, unaimarisha akili na unaleta hamu ya chakula.”1780 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) katika barua ya dhahabu amesema: “Yule anayetaka tumbo lake lisipate madhara basi asinywe maji wakaati wa kula mpaka amalize, na yule atayefanya hivyo (yaani atayekunywa maji kati kati ya kula chakula) mwili wake utakuwa na unyevunyevu, na litadhoofika tumbo lake, na utakuwa dhaifu mfuko wake wa chakula, na haitopata nguvu mishipa ya chakula, kwani chakula kinakuwa kama kisichoiva, yakimwagwa maji juu ya chakula kwanza ni bora zaidi.”1781 CHUMVI Mtume (s.a.w.w) amesema: “Ewe Ali, fungua chakula chako kwa chumvi, hakika hiyo ndani yake kuna ponyo ya magonjwa sabini kati ya hayo ni uwendawazimu, mbalanga, ukoma, maumivu ya koo, magego na maumivu ya tumbo.”1782 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Ewe Ali, fungua chakula kwa chumvi, na hitimisha kwa chumvi, hakika ndani yake kuna ponyo ya magonjwa sabini na mbili.”1783 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Hakika Mwenyezi Mungu na malaika Wake wanawateremshia rehema juu ya meza ya chakula ikiwa juu yake ipo chumvi na siki.”1784 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Kiamsha hamu chenu bora kwa chakula ni chumvi.”1785   Twibbul-Aimmat, uk. 460 cha Abdullah Shubbar.   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 323. 1782   Wasaail-Shi’ah, Juz. 16, uk. 522. 1783   Biharul-Anwaar, Juz. 66, uk. 398, na Wasaail-Shi’ah, Juz. 16, uk. 521. 1784   Biharul-Anwaar, Juz. 66, uk. 304. 1785   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 293. 1780 1781

387

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 387

8/10/2017 1:22:21 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Nyinyi mnakaribia kuwa kama chumvi katika chakula, wala hakiwi chakula hakifai ila kwa chumvi.”1786 Imepokewa kutoka kwa Amirul-Muminina Ali (a.s) amesema: “Anzeni kwa chumvi mwanzoni mwa kula chakula chenu, na lau watu wangelijua yale yaliyomo ndani ya chumvi wangeichagua kabla ya kijiuasumu.”1787 Imepokewa kutoka kwa Imam Baqir (a.s) amesema: “Mwenyezi Mungu alimfunulia Musa bin Imran (a.s): Waamrishe watu wako waanze kula kwa kulamba chumvi na wahitimishe kwayo, na wasipofanya hivyo basi wasimlaumu yeyote ila nafsi zao.”1788 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Hakika katika chumvi kuna ponyo la aina sabini ya magonjwa kisha akasema (a.s): Lau watu wangelijua yale yaliyomo ndani ya chumvi wasingelijitibia ila kwayo.”1789 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Mtume (s.a.w.w) aling’atwa na nge, basi akamtemea mate, na akasema: Mwenyezi Mungu akulaani wewe, hasalamiki na wewe muumini wala kafiri. Kisha akaitisha chumvi akaiweka juu ya mahali alipong’atwa, kisha akakamua kwa dole gumba lake mpaka pakayeyuka. Kisha akasema: Lau watu wangelijua yale yaliyomo kwenye chumvi wasingelihitajia dawa ya kijiuasumu.1790 Ninasema: Katika kuongezea hayo ni kwamba chumvi ni maada yenye uyabisi na huenda inaungana na sumu ya nge, kwani uwekaji wa chumvi   Twibbu-Nabawi, uk. 309 cha ibnQaym Jawziyyat.   Wasaail-Shi’ah, Juz. 16, uk. 520. 1788   Wasaail-Shi’ah, Juz. 16, uk. 520. 1789   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 60. 1790   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 60. 1786 1787

388

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 388

8/10/2017 1:22:21 PM


TIBA YA MAASUMINA

juu ya mahali aligonga nge hilo linasaidia juu ya uondoaji wa sumu kutoka kwenye jeraha hadi nje kulingana na umakhsusi wa mgandamizo wa pembezoni kwa kufunika, na hili linasimama kisimamo cha uvyonzaji wa jeraha ili kutoa sumu kabla ya kuchanganyika mwilini. Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Yule anayeweka chumvi juu ya tonge la kwanza la chakula chake, ­kunamuondolea yeye mikunjo ya uso.”1791 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Yule anayeanza kulamba chumvi kabla ya kuanza kula, hakika Mwenyezi Mungu atamuondolea magonjwa sabini, la kwanza kati ya hayo ni mbalanga.”1792 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Ni juu yenu ulambaji wa chumvi kabla ya kula, kwani hiyo ni ponyo ya magonjwa sabini, miongoni mwa hayo ni mbalanga, ukoma na uwendawazimu.”1793 Imam Ridha (a.s) aliwauliza masahaba wake: “Ni kiamsha hamu gani kizuri zaidi? (na katika hadithi nyingine: kitamu zaidi). Wakasema baadhi yao: Nyama, baadhi yao wakasema: Samli, na wengine wakasema: Mafuta. Yeye akasema: “Hapana, ni chumvi, tumetoka kwenda matembezini basi kijana akasahau chumvi ­(walituchinjia mbuzi aliyenona mno) basi hakikutufaa kitu hadi tulipokwenda zetu.”1794 Mtume (s.a.w.w) alimwambia mwanamke mmoja miongoni mwa ukoo wa Ghaffar pindi alipopatwa na hedhi na damu yake ikakipata   Kaafi, Juz. 6, uk. 326.   Sahifatul-Ridha (a.s), 78. 1793   Sahifatul-Ridha (a.s) uk. 78. 1794   Makarimul-Akhlaq, uk. 189, na Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 60 na kinacho shabihiana nacho. 1791 1792

389

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 389

8/10/2017 1:22:21 PM


TIBA YA MAASUMINA

kipando chake: “Chukua chombo chenye maji na tia chumvi ndani yake, kisha osha sehemu iliyoangukia damu.”1795 MZOGA Imam al-Baqir alisema kuhusiana na sababu za kuharimshwa ­mzoga: Ama mzoga hakuna atayeutumia ispokuwa utadhoofisha mwili wake, utapunguza nguvu zake, na utakata kizazi chake. Na mla mzoga hafi ila kwa ghafla. NASISA (NARJIS) Galenos amesema: Yule ambaye ana vipande viwili vya mkate, basi ajaalie kimojawapo katika thamani ya nasisa, hakika mkate ni chakula cha mwili, na nasisa ni chakula cha roho.”1796 Wamedai kwamba: Hakika kuacha uangaliaji wa nasisa wakati wa kufanya tendo la ndoa, kunafunga matamanio bila kuyaachia.1797 Mtume (s.a.w.w) amesema: “Nuseni nasisa, hakuna miongoni mwenu ila yule ambaye ana baina ya kifua na moyo sehemu ya ukoma au uwendawazimu au mbalanga, hautoki ila kwa unusaji wa nasisa.”1798 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Nuseni nasisa lau kwa siku mara moja, lau kwa wiki mara moja, lau kwa mwezi mara moja, lau kwa mwaka mara moja, lau kwa dahari mara moja, hakika moyoni kuna punje ya uwendawazimu, mbalanga na ukoma, na kulinusa hilo kunaitoa.”1799   Siirat Ibn Hisham, Juz. 3, uk. 357.   Ajaaibul-Makhluqaat, cha Qazwiini, mwishoni mwa kitabu Hayatul-Hayawan kubra, Juz. 2 uk. 197 cha Damiiri. 1797   Ajaaibul-Makhluqaat cha Qazwiini, mwishoni mwa kitabu Hayatul-Hayawan Kubra, Juz. 2, uk. 197 cha Damiiri. 1798   Ajaaibul-Makhluqaat, cha Qazwiini, mwishoni mwa kitabu Hayatul-Hayawan Kubra, Juz. 2, uk. 197 cha Damiiri. 1799   Biharul-Anwar, Juz. 62, uk. 299. 1795 1796

390

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 390

8/10/2017 1:22:21 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Mnusishane nasisa lau mara moja kwa mwaka, hakika ndani ya moyo wa mtu kuna hali ambayo haiondoki ila kwa nasisa.” WANAWAKE (MWANAMKE) Mtume (s.a.w.w) amesema: “Hakika ibilisi anawahutubia mashetani wenzake akiwaambia: Ni juu yenu nyama, pombe na wanawake, hakika mimi sioni mkusanyiko wa shari ila ndani ya hayo.”1800 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Yamenipendeza mimi katika dunia yenu matatu; wanawake, manukato na imefanywa swala kwangu ni tulizo la jicho langu.”1801 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Yule anayepeana mikono na mwanamke anakuwa haramu juu yake, kwa hakika amestahiki ghadhabu ya Mwenyezi Mungu (a.j).”1802 Miongoni mwa wosia wa Mtume (s.a.w.w) kwa Ali (a.s) amesema: “Yule anayemtii mke wake, Mwenyezi Mungu atauchoma moto uso wake. Ali (a.s) akasema: Ni utiifu gani huo? Akasema: Anamruhusu mkewe kwenda katika bafu, maharusini, sherehe na uvaaji wa nguo nyepesi.”1803 Imepokewa kutoka kwa Amirul-Muminina Ali (a.s) amesema: “Mtume (s.a.w.w) alikataza utokaji wa mwanamke kutoka nyumbani kwake bila idhini ya mumewe, ikiwa atatoka hulaaniwa na kila malaika wa mbinguni na kila kitu ambapo anapita kwacho miongoni mwa majini na watu, mpaka anarejea nyumbani kwake.” Na amekataza Mtume (s.a.w.w) kujipamba kwa asiyekuwa mumewe, na   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 293.   Twibbu-Nabawi. uk. 260 cha ibn Qaym Jawziyyat. 1802   Makarimul-Akhlaq, uk. 430. 1803   Makarimul-Akhlaq, uk. 438. 1800 1801

391

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 391

8/10/2017 1:22:21 PM


TIBA YA MAASUMINA

akifanya hivyo itakuwa haki kwa Mwenyezi Mungu (a.j) amuunguze yeye motoni.” Na amekataza suala la mwanamke kuzungumza na asiyekuwa mumewe pia asiyekuwa mahrimu wake, na kama hapana budi kwake kuongea basi yasizidi maneno matano.”1804 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Kila aliye na upendo zaidi kwetu, huzidi kupenda wanawake na vitu vitamu.”1805 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Manne ni miongoni mwa Sunna ya Mitume; Upigaji mswaki, hina, manukato na wanawake.”1806 WANAWAKE WAJA WAZITO Mtume (s.a.w.w) amesema: “Hakuna mwanamke mja mzito atakayela tikitimaji ila atakayemzaa atakuwa mwenye sura nzuri na tabia njema.”1807 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Walisheni wanawake wenu waja wazito ubani kwani unaongeza akili ya mtoto.”1808 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Walisheni wanawake wenu pera kwani linafanya tabia za watoto wenu kuwa nzuri.”1809   Makarimul-Akhlaq, uk. 425 cha Twabarasi.   Ramzu-Sihat, uk. 178 cha Dahsurkhi. 1806   Makarimul-Akhlaq, uk. 41. 1807   Safinatul-Bihar, Juz. 1, uk. 341. 1808   Safinatul-Bihar, Juz. 1, uk. 341. 1809   Safinatul-Bihar, Juz. 1, uk. 341. 1804 1805

392

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 392

8/10/2017 1:22:21 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Walisheni wanawake wenu waja wazito ubani, akiwa tumboni mwake kijana basi atatoka akiwa mwerevu wa moyo, mjuzi na shujaa, na akiwa wa kike atakuwa mwenye tabia nzuri na umbo zuri.”1810 USAFI Mtume (s.a.w.w) amesema: “Mja mbaya ni yule mchafu.”1811 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Jisafisheni kadiri muwezavyo, hakika Mwenyezi Mungu ameujenga Uislamu juu ya usafi, na kamwe hatoingia peponi ila kila msafi.”1812 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Hakika Uislamu ni usafi basi jisafisheni, kwani hatoingia peponi ila msafi.”1813 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Ingieni msalani kwani huo ni usafi, na usafi unatokana na imani, imani pamoja na sahiba wake wote wanaingia peponi.”1814 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Jisafisheni kwa maji kutokana na harufu mbaya, na ziahidini nafsi zenu, hakika Mwenyezi Mungu anamchukia mja wake mchafu, anahisi kinyaa yule ambaye anayekaa karibu yake.”1815 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Uoshaji wa chombo na ufagiaji uchafu kunavuta riziki.”1816   Safinatul-Bihar, Juz. 1 uk. 341.   Furuu Kaafi, Juz. 6, uk. 439. 1812   Kanzul-Ummal, hadithi 26002. 1813   Kanzul-Ummal, hadithi 26007. 1814   Ramzul-Sihat, uk. 5. 1815   Tuhfal-Uquul, uk. 78. 1816   Wasaail-Shi’ah, Juz. 3, uk. 571. 1810 1811

393

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 393

8/10/2017 1:22:21 PM


TIBA YA MAASUMINA

NAFSI Mtume (s.a.w.w) amesema: “Ni juu yenu kula zabibu, kwani hiyo inaondoa nyongo, inaondoa kikohozi, inaimarisha mishipa ya fahamu, inaondoa uchovu, inapendezesha umbo, inatengeneza nafsi, na inaondoa majonzi.”1817 Ninasema: Sifa zote hizi zilizotajwa zinapatikana katika mafuta ya zabibu kavu na zabibu mbichi. Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Kuzidisha kula na kulala kunaharibu nafsi, kunavuta madhara.”1818 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Ni juu yenu kula mafuta, kwani yanaondoa nyongo…na yanafanya tabia kuwa nzuri, yanapendezesha nafsi na yanaondoa majonzi.”1819 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Mwili umejengewa juu ya vitu vinne; juu ya roho, akili, damu na nafsi, na roho inapotoka akili huifuata, na roho inapoona kitu huhifadhi juu yake akili, na hubakia damu na nafsi.”1820 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Zabibu inaimarisha mishipa ya fahamu, inaondoa ghadhabu na inafanya nafsi kuwa nzuri.”1821 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Zabibu inakaza moyo, inaondoa maradhi, inazima joto na inafanya uzuri nafsi.”1822   Khiswal, Juz. 1, uk. 344.   Mustadrakul-Wasail, Juz. 3, uk. 81. 1819   Makarimul-Akhlaq, uk. 190. 1820   Khiswal, Juz. 1, uk. 226 cha Saduuq. 1821   Twibbul-Swadiq (a.s), uk. 70. 1822   Makarimul-Akhlaq, uk. 175. 1817 1818

394

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 394

8/10/2017 1:22:21 PM


TIBA YA MAASUMINA

Msomi (yaani Imam Kadhim) kuhusiana na maumbile ya mtu amesema: “… Na alimuumba kwa nafsi, mwili na roho; basi roho yake haimuachi ila kwa kufarikiana na dunia, na nafsi yake ambayo anaona kwayo ndoto na vyeo mbali mbali, na mwili wake ambao utatoweka na kurejea kwenye udongo.”1823 Sifa za mwili zinavyoathiri sifa za nafsi: Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Mtu mzito wa kusikia huambatana na ukarimu, na pupa huambatana na urefu, na uerevu huambatana na ufupi, na heshima huambatana na kimo cha kati kwa kati, na tabia njema huambatana na kengeza, na kuburi huambatana na chongo, na mshangao huambatana na, na uerevu huambatan na ububu.”1824 JONGO Maana yake: Ni ugonjwa unaowapata wanaume, nao ni uvimbe unaotokea katika muunganiko wa nyayo, na katika dole gumba lake zaidi. Na katika kitabu Qamuus: Jongo ni ugonjwa wa uvimbe katika maunganiko ya vifundo viwili na vidole vya miguu. Hadithi: Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuhusiana na Tini amesema: “Hakika hiyo inakata bawasiri, na inasaidia kuondoa jongo.”1825 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Msiwakaribie wanawake mwanzo wa usiku… kwani kunazalisha mingurumo ya tumbo, kiharusi, ukosefu wa nguvu, jongo na vijiwe.”1826   Khaswais, uk. 143, kutoka kitabu Bihar, Juz. 14, uk. 461.   Hikmat 469, katika mwisho wa Sharhul-Nahjul Balaaghah cha ibn Abi Hadid. 1825   Makarimul-Akhlaq, uk. 173. 1826   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 327. 1823 1824

395

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 395

8/10/2017 1:22:21 PM


TIBA YA MAASUMINA

SISIMIZI (MDUDU CHUNGU) Ili kuwafukuza sisimizi saga kisibiti na mwagia hiyo katika shimo la sisimizi.1827 Qazwiini katika kitabu chake Ajaaibul-Makhluqaat amesema: Miongoni mwa sifa za kisibiti ni kwamba sisimizi wanakimbia kutokana na harufu yake. Dawa ya kuondoa visiki vya nywele: Namna ya kutengeneza Dawa ya kuondoa visiki vya nywele Dawa ya kuondoa visiki vya nywele hutengenezwa bafuni ili kuondoa nywele za mwili. Inachukuliwa ndimu vipande viwili, na asenia kidogo (aina ya kemikali nyeupe ya sumu inayotumika katika dawa nyingine kuulia panya), vinachanganywa kwa maji na vinaachwa bafuni kwa kiasi cha kuweza kupata mchanganyiko mzuri na kushikana. Kisha atajipaka mwilini, na itabaki mwilini kwa muda kiasi mpaka zitakapoonekana athari yake, katika muda huo asiiondoe dawa hiyo kwa maji. Kisha baadae ataosha na kuiondoa pamoja na nywele, na anapaka mahali pake hina ili kuondoa joto lake. Na alikuwa Mtume (s.a.w.w) anapojipaka huanza kwa sehemu zake za viungo vya uzazi, kisha sehemu nyingine ya mwili wake.1828 Hadithi: Hakika wa kwanza aliyeingia bafuni na akatengenezewa dawa ya kuondoa nywele zake za mwilini ni Nabii Sulaiman bin Daud (a.s).”1829   Twibbul-Aimmat (a.s) uk. 140.   Twibbu-Nabawi, uk. 312 na 313 cha Ibn Qaym Jawziyyat. 1829   Twibbu-Nabawi, uk. 312 cha Ibn Qaym Jawziyyat. 1827 1828

396

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 396

8/10/2017 1:22:21 PM


TIBA YA MAASUMINA

Mtu mmoja alikuja kwa Mtume (s.a.w.w) akimlalamikia suala la kuzidisha kujamiana, basi akamwamrisha yeye aoe mwanamke wa pili, lakini hata hivyo haikumsaidia, akasema (s.a.w.w): Huenda wewe unazidisha upakaji wa dawa ya kuondoa nywele za mwilini? Akasema: Ndio. akasema (saww): “Punguza upakaji wako utapunguza kujamiana kwako.”1830 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Inapendeza kwa muumini ajipambe katika kila siku 15 mara moja kwa kunyoa nywele za mwilini.”1831 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Unyoaji wa nywele za mwilini unaimarisha mwili, na unatoharisha mwili.”1832 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Yule anayemwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho asiache kunyoa kinena chake kwa zaidi ya siku 40, na ikiwa hajapata cha kunyolea basi afanye baada ya siku ya 40 na asicheleweshe.”1833 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Ni sunna kunyoa nywele za sehemu za siri katika kila siku 15, basi akipitisha siku 20 basi amkope Mwenyezi Mungu (s.w.t) ili anyoe nywele zake hizo. Na yule ambaye akipitisha siku 40 na hakunyoa nywele zake hizo sio muumini wala muislamu wala mwenye karama.”1834 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Vitatu haviliwi na vinanenepesha, na vitatu vinaliwa na vinakondesha. Ama ambavyo haviliwi na vinanenepesha, ni unyoaji wa nywele na manukato na uvaaji wa katani…”1835   Iqdul-Fariid, Juz. 7 uk. 272.   Tuhfal-Uquul, uk. 88. 1832   Tuhfal-Uquul, uk. 72. 1833   Rawdhatul-Waidhiina, uk. 309 cha ibn Fataal Naysabuuri. 1834   Rawdhatul-Waidhiina, uk. 309 cha ibn Fataal Naysabuuri. 1835   Wasaail-Shi’ah, Juz. 16, uk. 541. 1830 1831

397

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 397

8/10/2017 1:22:21 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) amesema: “Vinne vinatokana na tabia ya Mitume; Kujipaka manukato, kujisafisha na unyoaji wa nywele za mwili na kuzidisha kujamiana.”1836 USINGIZI Faida zake: Yule anayehofia kutokwa jasho basi ale vijiko viwili vya asali pamoja na siki ya tufaha, kwani hiyo inasaidia kupata usingizi. Na mchanganyiko wa asali na siki pamoja na maji na sukari unafanya kuwa kinywaji, nacho kinaitwa (Sakanjabiin) nacho kinachemsha mwili kwa ujumla. Baadhi ya wataalamu wamesema: Walikusanya rai na maoni ya marafiki sabini, kwamba kuzidi kwa usingizi kunatokana na unywaji maji kwa wingi.1837 Mtu mmoja alikwenda kwa Mtume (s.a.w.w) akasema: Ewe Mtume, hakika katika zama za ujinga mimi nilikuwa mtu mwerevu na mwenye ubongo wa kuelewa, lakini sasa katika uislamu siioni nafsi yangu! Akamwambia: “Je, ulikuwa ukilala kailula (kulala baada ya kula chakula cha mchana)? Akasema: Ndio. akasema: Rudia ulivyokuwa ukilala kailula (kulala baada ya kula chakula cha mchana).”1838 Miongoni mwa wosia wa Mtume (s.a.w.w) kwa Ali (a.s) alimwambia: “Ewe Ali, usingizi upo wa aina nne; Mitume wanalalia migongo yao yaani chali… na muumini analalia ubavu wake wa kulia akielekea Qibla, na wafalme na watoto wao wanalalia ubavu   Makarimul-Akhlaq, uk. 40.   Adabul-Nafsi, uk. 190 cha Aynaai. 1838   Iqdul-Fariid, Juz. 6, uk. 274. 1836 1837

398

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 398

8/10/2017 1:22:21 PM


TIBA YA MAASUMINA

wao wa kushoto ili wapate raha kwa vile wanavyokula, na ibilisi na ndugu zake … wanalala kifudifudi wakilalia matumbo.”1839 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Mwanaume asilalie uso wake, na yule mnayemuona analalia uso wake basi mzindueni wala msimwache.”1840 Imepokewa kutoka kwa Imam Baqir (a.s) amesema: “Usingizi wa mwanzo wa mchana ni upumbavu, na mwenye kulala baada ya adhuhuri ni neema, na usingizi baada ya alasiri ni upumbavu, na usingizi baina ya magharibi na isha unakimbiza riziki.”1841 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Yule anayejitoharisha kisha akaenda kitandani kwake na akalala basi godoro lake ni kama vile msikiti wake, na ikiwa atakumbuka hana wudhuu basi afanye tayamamu kutokana na shuka lake vyovyote liwavyo, na iwapo atafanya hilo ataendelea kuwa katika swala na kumtaja Mwenyezi Mungu (a.j).”1842 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Usingizi ni raha ya mwili…”1843 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Ulalaji chali baada ya kushiba unanenepesha mwili, na unatuliza chakula, na unaondoa ugonjwa.”1844 Imepokewa kutoka kwa Abal- Hasan Imam Kadhim (a.s) amesema: “Hakika mtu anapolala roho ya unyama inabaki mwilini, na ambayo humtoka ni roho ya akili.”1845   Biharul-Anwaar, Juz. 76, uk. 186.   Khiswal, Juz. 2 uk. 613. 1841   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 377 cha Abdullah Shubbar. 1842   Biharul-Anwaar, Juz. 76, uk. 182. 1843   Majalis cha Sheikh Saduuq. 1844   Biharul-Anwaar, cha Allama Majlisi na Twibbul-Sawdiq (a.s), uk. 81. 1845   Biharul-Anwaar, Juz. 61, uk. 43. 1839 1840

399

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 399

8/10/2017 1:22:21 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Walisheni wagonjwa wenu mchadi (yaani majani yake) hakika ndani yake kuna ponyo, wala hakuna ugonjwa ndani yake wala madhara, hutuliza usingizi wa mgonjwa…”1846 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema katika barua ya dhahabu kwa Maamuni: “Na jua ewe Amirul-Muminina kwamba usingizi ni sultani wa ubongo, nao ndiyo unaimarisha mwili na nguvu zake, utakapotaka kulala basi uwe ulalaji wako kwanza kwa ubavu wa kulia, kisha geuka ubavu wa kushoto. Na vivyo hivyo simama kutoka sehemu ya kulala kwa upande wa ubavu wako wa kulia kama ulivyofanya wakati wa kulala.”1847 Na ndani yake yapo: Na yule anayetaka mmeng’enyo wake wa chakula uwe mzuri basi aegemee ubavu wake wa kulia baada ya kula, kisha ageuke baada ya hivyo juu ya ubavu wake wa kushoto, mpaka alale.”1848 Uzee Imepokewa kutoka kwa Usamat bin Shirik amesema: Nilikuwa kwa Mtume (s.a.w.w) wakaja mabedui wakasema: Ewe Mtume, je, tunaruhusiwa kujitibu? Akasema: Ndio, enyi waja wa Mwenyezi Mungu, jitibieni, hakika Mwenyezi Mungu (a.j) hakuweka ugonjwa ila aliweka dawa yake, isipokuwa ugonjwa mmoja. Wakasema: Ni upi huo? Akasema: Uzee.”1849 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Majonzi ni nusu ya uzee.”1850   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 157, kutoka kitabu Furuul-Kaafi.   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 316. 1848   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 325. 1849   Musnad Ahmad bin Hanbal. 1850   Biharul-Anwaar, Juz. 78, uk. 53. 1846 1847

400

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 400

8/10/2017 1:22:22 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Majonzi ni moja ya uzee kati ya aina mbili za uzee.”1851 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Manne yanazeesha; Ulaji wa nyama kavu, ukaaji juu ya unyevunyevu, upandaji wa ngazi na kufanya tendo la ndoa na ajuza.”1852 HALUWA Maana yake: Ni ngano iliyopikwa pamoja na nyama, na imeitwa haluwa kwa sababu punje zinazotumika ndani yake zinazama kabla ya kupikwa. Hadithi: Mtume (s.a.w.w) amesema: “Alinijia Jibrail na akaniamrisha kula Haluwa, ili uimarishe mgongo wangu, na ili niwe na nguvu ya kufanya ibada za Mola Wangu mlezi.”1853 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Nilipata udhaifu katika swala na tendo la ndoa, basi kikateremka kwangu chungu kutoka mbinguni basi nikala kile kilichomo, zikazidi nguvu zangu zaidi ya nguvu za watu 40, kwa nguvu na tendo la ndoa, nacho ni haluwa.”1854 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Hakika nabii miongoni mwa manabii alimlalamikia Mwenyezi Mungu udhaifu na upungufu wa tendo la ndoa, basi akamwamrisha ale haluwa.”1855   Ghurarul-Hikam cha Aamadi.   Biharul-Anwaar, Juz. 78, uk. 230. 1853   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 50. 1854   Uyuunul-Akhbar Ridha (a.s), Juz. 2, uk. 36. 1855   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 49. 1851 1852

401

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 401

8/10/2017 1:22:22 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kwamba Mtume (s.a.w.w) alimlalamikia Mola Wake kuhusu maumivu ya mgongo, basi akamwamrisha yeye kula punje za haluwa pamoja na nyama.”1856 MMENG’ENYO WA CHAKULA Mtume (s.a.w.w) amesema: “Hakika Jibril (a.s) huyu hapa ananipa habari kwamba katika tende kuna mambo tisa; inafanya uzuri tendo la ndoa, inafanya mfuko wa chakula kuwa mzuri na inafanya mmeng’enyo wa chakula…”1857 Imepokewa kutoka kwa Imam Baqir (a.s) amesema: “Hakuna chenye baraka zaidi ya uji, mtu akiunywa wakati ameshiba unashuka vizuri zaidi, unafanya uzuri mmeng’enyo wa chakula, na akiunywa akiwa na njaa unamshibisha. Na masurufu bora ya safari na nyumbani ni uji.”1858 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Mzizi wa figili unakata kikohozi, na moyo wake unasaga chakula, na majani yake yanaleta haja ndogo.”1859 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Ulaji wa figili ndani yake yapo mambo matatu; majani yake yanaondoa harufu, moyo wake unarahisisha utokaji wa haja ndogo na mmeng’enyo wa chakula, na mizizi yake inakata kikohozi.”1860 Imepokewa kutoka kwa Imam Ali Ridha (a.s) kuhusiana na maji ya baridi amesema: “Hakika hayo yanazima joto, yanatuliza umanjano na yanasaga chakula.”1861   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 50.   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 107 kutoka kitabu Mahasin cha Barqi. 1858   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 68. 1859   Makarimul-Akhlaq, uk. 182. 1860   Furuu Kaafi, Juz. 6, uk. 371. 1861   Fiqhul-Ridha (a.s), uk. 346. 1856 1857

402

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 402

8/10/2017 1:22:22 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Hapigi chafya mpigaji chafya ila huwa kinasagika chakula chake, au hacheui ila chakula chake hushuka vizuri.”1862 BADAMU Maana yake: Ni mti unaoota India na Kabul na China, tunda lake linafanana na umbo la punje ya msonobari mkubwa, na kwa ajili hiyo umbo la badamu limekuja katika umbo la yai. Nayo ina aina nyingi, kati ya hizo ni ya manjano, kijani kibichi, na kati ya hizo ni nyeusi ya India, nayo ni ya kukoza katika uivaji na nene zaidi. Na kati ya hizo ni ya Kabul nayo ni kubwa kuliko zote, na kati ya hizo ni ya Uchina, nayo ni nyembamba nyepesi. Na nzuri zaidi ni ya manjano iliyokoza unjano wake na kuelekea kijani kibichi, ngumu. Faida zake: Ibn Sina amesema: Aina zake zote zinazima joto la kibofunyongo, zinasaidia kuondoa mbalanga, na ya Kabul inaimarisha hisia, na inazidisha hifidhi na akili, na inaondoa maumivu ya kichwa.1863 Na Razi katika kitabu chake kiitwacho Haawi amesema: Inatia nguvu hisia, inazidisha hifidhi na kuimarisha ubongo.”1864 Hadithi: Mtume (s.a.w.w) amesema: “Ni juu yenu kutumia badamu nyeusi kwani ni miongoni mwa miti ya peponi, na ladha yake ni ya uchungu na ndani yake kuna ponyo la kila ugonjwa.”1865   Fiqhul-Ridha (a.s), 391.   Qanun, uk. 65 cha Ibn Sina. 1864   Majuuatul-Aathar, Juz. 1, uk. 407 cha Imam Ridha (a.s). 1865   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 300. 1862 1863

403

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 403

8/10/2017 1:22:22 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam Hasan (a.s) amesema: “Lau watu wangelijua yaliyomo ndani ya badamu ya manjano wangeliinunua hata kwa thamani ya dhahabu.” Na akasema (a.s) kumwambia mtu mmoja miongoni mwa masahaba wake: “Chukua badamu ya manjano na punje saba za pilipili, zisage na zichange kisha jipake kwenye nyusi zako kama wanja.”1866 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) kuhusiana na Sanamaki amesema: “Utaichukuwa pamoja na zabibu nyekundu ambayo haina kokwa, utachanga pamoja na badamu ya Kabul ya manjano na nyeusi, vipimo sawa. (rejea Sanamaki).1867 Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) amesema: “Zinamtosha bwana huyu (inakusudiwa homa) dawa hizi: Badamu, raziyanji na sukari ya mimea.”1868 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) katika barua ya dhahabu amesema: “Na yule anayetaka kuongeza akili yake, basi naale kila siku badamu tatu kwa sukari ya mimea.”1869 HINDUBAAU (Chickory) Maana yake: Ni mboga mboga inayolimwa pembezoni, vipande vyenye kufungamana, majani yake hupikwa, au hutengenezwa kama saladi. Nayo ipo ya aina mbili; ya kujiotea na ya bastani, yenye majani mapana na yenye majani mepesi.

Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 86.   Makarimul-Akhlaq, uk. 214. 1868   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 50. 1869   Biharul-Anwaar juz. 62 uk. 324 cha Allama Majlisi. 1866 1867

404

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 404

8/10/2017 1:22:22 PM


TIBA YA MAASUMINA

Faida zake: Hindubaau inatumiwa kama maada inayofungua hamu ya kula kwa sababu ya yale iliyonayo miongoni mwa virutubisho na uchungu, kama ilivyo kawaida kwamba mmea wenye uchungu huzaa sumu yenye kuua vijidudu na virutubisho vyenye kutia nguvu mfuko wa chakula. Na Hindubaau inatumiwa mara nyingi kama vile kichangamshaji na kichocheo cha usagaji wa chakula na utoaji wa umanjano, na katika hali mbalimbali za uzuiaji wa muda mrefu, na inasaidia katika hali ya upungufu wa damu, na mvurugiko wa tumbo, na inatia nguvu ini. Na inatumika kikamilifu katika tiba ya kichina katika utoaji wa athari za sumu, na kuongeza mzunguko wa maziwa, kama vile inavyotumiwa juisi ya majani yake katika maradhi ya ngozi, na huchemshwa wakati wa uandaaji. Na inanasihiwa kutumia Hindubaau mara moja katika chakula (lishe), hususani ukizingatia kwamba hakika ina mkusanyiko wa vitamini B na protini zenye kurahisisha mmeng’enyo wa chakula, achilia mbali yale iliyonayo miongoni mwa uchungu na madini chumvi na elementi ya njano na kalisiumu, mambo ambayo huongeza thamani ya lishe ya hali ya juu. Kama vile hutumiwa kwa kuchanganywa na kahawa – au mbadala wa kahawa – ili kuondokana na athari za pembeniz kafeini.1870 Hadithi: Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Kuleni Hindubaau au kisibiti (komon muluk), kwani hakuna siku miongoni mwa masiku ila hudondokewa na matone kutoka peponi.”1871   Nabataat Twibbiyyat wal-Istiimalaatiha, Juz. 1, uk. 68 na 166 cha Dr. Muhammad Awdaat mwaka 1987. 1871   Biharul-Anwaar, Juz. 66, uk. 320 kutoka kitabu Firdausi. 1870

405

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 405

8/10/2017 1:22:22 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Ulaji wa hindubaau ni ponyo la kila ugonjwa, na hakuna ugonjwa tumboni mwa binadamu ila hung’olewa na Hindubaau.”1872 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Ni juu yako kula Hindubaau, kwani inaongeza maji na inapendezesha mtoto, nayo ni ya joto laini inaongeza katika upatikanaji wa watoto wa kiume.”1873 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Mboga ya Mtume (s.a.w.w) ilikuwa hindubaau, na mboga ya AmirulMuminina Ali (a.s) ilikuwa Badharuuj nalo ni (Huuk), na mboga ya Fatmah (a.s) ni Farfukh (nayo ni Rijlat).1874 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Yule atakayelala hali ya kuwa tumboni mwake kuna nguvu kutokana na hindubaau, atapata amani kutokana na ugonjwa wa msokoto wa tumbo usiku wake, Mwenyezi Mungu akipenda.”1875 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Vinne vinaleta ulinganifu wa maumbile; komamanga surani, tende iliyopikwa, balungi na hindubaau.”1876 Imepokewa kutoka kwa Hanan bin Sadiir amesema: “Nilikuwa pamoja na Abu Abdillah (a.s) juu ya meza ya chakula, basi nikapenda Hindubaau. Akaniambia: “Ewe Hanan kwa nini huli Karaath? Nikasema: Kutokana na yale yaliyokuja katika hadithi kuhusu Hindubaau. Akasema: Ni yapi yale yaliyokuja kutoka kwetu kuihusu? Basi nikasema: Kwani hiyo kila siku inadondokewa na matone kutoka peponi…”1877   Kaafi, Juz. 6 uk. 363.   Biharul-Anwar, Juz. 62 uk. 215, kutoka kitabu Kaafi, Juz. 6, uk. 363. 1874   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 142, kutoka kitabu Furuu Kaafi na Mahasin cha Barqi. 1875   Biharul-Anwaar, Juz. 62, uk. 215, kutoka kitabu Kaafi, Juz. 6, uk. 362. 1876   Khiswal, Juz. 1, uk. 249 cha Saduuq. 1877   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 151, kutoka kitabu Furuu na Mahasin. 1872 1873

406

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 406

8/10/2017 1:22:22 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Muhammad bin Faydh amesema: Nilikula pamoja na Imam as-Sadiq (a.s) na mezani kuna mboga, na alikuwa pamoja nasi mzee, basi akawa anaisogeza hindubau, Imam (a.s) akamwambia: “Ama mnadhani kuwa hiyo ni baridi, sio hivyo, na hakika hiyo ni linganifu (kati kwa kati) na ubora wake juu ya mboga ni kama vile ubora wetu sisi kwa watu.”1878 Imepokewa kutoka kwa Muhammad bin Abi Baswiir kutoka kwa baba yake kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Nilimlalamikia yeye maumivu kichwani kwangu na kwenye magego yangu, na mapigo katika jicho langu mpaka ukaumuka uso wangu, akasema: ‘Ni juu yako hii hindubaau, ikamue na chukua maji yake, na tia juu yake sukari ya mawe, na zidisha hiyo, kwani hiyo inatuliza na inakinga madhara yake.’ Basi nikaondoka nyumbani kwangu, basi nikajitibu usiku huo kabla sijalala na nikanywa na kisha nikalala, basi nikaamka asubuhi nimeshapona kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu na neema zake.”1879 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Ni juu yenu kula mboga ya Hindubaau, kwani hiyo inaongeza mali na watoto, na yule anayependa izidi mali yake na watoto wake wa kiume basi adumishe ulaji wa hindubaau.”1880 Imepokewa kutoka kwa Muhammad bin Ismail amesema: Nilimsikia Imam Ridha (a.s) akisema: “Hakika katika hindubaau kuna ponyo la magonjwa elfu, na hakuna ugonjwa tumboni mwa mtu ila unaondolewa na hindubaau.” Akasema: Na wakaliitisha hilo siku moja kwa baadhi ya wenye heshima, na hakika alikuwa akiitumia hiyo kwa homa na maumivu ya kichwa, basi akaamrisha isagwe kisha ifungwe kwenye karatasi, na imwagiwe juu yake mafuta ya balungi, na iwekwe juu ya kichwa   Kaafi, Juz. 6 uk. 363.   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 138. 1880   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 142, kutoka kitabu Mahasin cha Barqi. 1878 1879

407

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 407

8/10/2017 1:22:22 PM


TIBA YA MAASUMINA

chake, kisha akasema: “Ama hiyo inakata homa na inaondoa maumivu ya kichwa.”1881 Imepokewa kutoka kwa mmoja wa watu wema amesema: Iliniwia ugumu mimi kuhuisha kisimamo cha swala ya usiku, na ilikuwa imenichukua sana hali hiyo, basi nikamuona Imam wa zama usingizini, akaniambia: ‘Ni juu yako kunywa maji ya hindubaau, hakika Mwenyezi Mungu atakufanyia wepesi hilo!’ Basi nikazidisha kuinywa, nikapata wepesi juu ya hilo.”1882 Waridi na (maji waridi) Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) amesema: “Hakika maji ya waridi yanaongeza haya za uso na yanaondoa ufukara.”1883 Imepokewa kutoka kwa Imam Hasan (a.s) amesema: “Mtume (s.a.w.w) alinipatia waridi kwa mikono yake miwili, akasema: Hili ni bwana wa maua yenye harufu nzuri duniani na akhera.”1884 Imepokewa kutoka kwa Hasan bin Mundhir kwa kuirufaisha amesema: Yule anayetaka kunusa harufu ya Mtume (s.a.w.w) basi anuse waridi.”1885

MTOTO Maelezo: Makusudio ni uzuri wa mtoto katika hadithi mbali mbali, ili mtoto umbo lake liwe zuri na tabia yake pia.   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 144, kutoka kitabu Fruul-Kaafi.   Daawaat cha Qutbu Diin Raawandi. 1883   Makarimul-Akhlaq, uk. 44. 1884   Makarimul-Akhlaq, uk. 45. 1885   Makarimul-Akhlaq, uk. 45, kutoka kitabu Twibbul-Aimmat (a.s). 1881 1882

408

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 408

8/10/2017 1:22:22 PM


TIBA YA MAASUMINA

Hadithi: Mtume (s.a.w.w) amesema: “Watoto wetu ni maini yetu, wadogo wao ni viongozi wetu, wakubwa wao ni maadui zetu, ikiwa wataishi watatutia katika mtihani, na wakifa watatuhuzunisha.”1886 Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Kuleni pera na peaneni zawadi… na walisheni hilo wake zenu waja wazito, kwani hilo linafanya watoto wenu kuwa wazuri (na katika hadithi nyingine) linafanya tabia za watoto wenu kuwa nzuri.”1887 Imepokewa kutoka kwa Amirul-Muminina Ali (a.s) amesema: “Ulaji wa pera unatia nguvu moyo wa dhaifu… na unafanya mtoto kuwa mzuri.”1888 Imepokewa kutoka kwa Amirul-Muminina Ali (a.s) amesema: “Walisheni watoto wenu wadogo komamanga, kwani hilo linaharakisha kuongea kwao.”1889 Imepokewa kutoka kwa Imam Baqir (a.s) amesema: “Yule aliyekosa mtoto basi ale mayai na azidishe kuyala, kwani huzidisha kizazi.”1890 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Ni juu yako kula hindubaau, kwani hilo linaongeza maji, linafanya mtoto awe mzuri, nalo lina joto na ni laini, linazidisha upatikanaji wa watoto wa kiume.”1891 Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Yule anayekula pera kabla ya kula chochote, maji yake ya uzazi yatakuwa mazuri na mtoto wake atakuwa mzuri.”1892   Biharul-Anwaar, Juz. 104, uk. 97.   Makarimul-Akhlaq, uk. 171, na 172. 1888   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 129, kutoka kitabu Furuu na Mahasin. 1889   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 412 cha Abdullah Shubbar. 1890   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 130 cha Abdullah Shubbar. 1891   Twibbul-Aimmat (a.s), uk. 130 cha Abdullah Shubbar. 1892   Wasaail-Shi’ah, uk. 301 cha Hurru Aamili. 1886 1887

409

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 409

8/10/2017 1:22:22 PM


TIBA YA MAASUMINA

Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: “Hamu inapelekea tendo la ndoa ambalo ndani yake kuna kudumu kwa kizazi na ubakiaji wake…kama mtu angelikuwa anajamiiana kwa ajili ya kutaka mtoto, basi ingekuwa ni rahisi kwake kunyong’onyea na kizazi chake kupungua au kukatika kabisa. Hakika miongoni mwa watu yupo asiyependa kupata mtoto wala halitilii umuhimu hilo.”1893 Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) amesema: “Mtume (s.a.w.w) alivunja pera na akamlisha Ja’far bin Abi Twalib (a.s), akamwambia: “Kula, kwani hili linang’arisha rangi, na linafanya mtoto kuwa mzuri.”1894 Imepokewa kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) amesema: “Ulaji wa mayai kwa wingi unaongeza watoto.”1895 Imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) amesema: “Ni juu yenu kula mboga ya hindubaau, kwani hiyo inaongeza mali na watoto, na yule anayependelea zaidi izidi mali yake na watoto wake basi adumishe ulaji wa hindubaau.”1896

Dirasaat fi ilmil-nafsi, Juz. 2, uk. 245 cha Dr. Mahmuud Bastaani, chapa ya pili, kutoka kitabu Bihar. 1894   Wasaail-Shi’ah, Juz. 17, uk. 131. 1895   Biharul-Anwaar, Juz. 62 uk. 58, kutoka kitabu Furuu na Mahasin. 1896   Wasaali-Shi’ah, Juz. 17, uk. 142, kutoka kitabu Mahasin cha Barqi 1893

410

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 410

8/10/2017 1:22:22 PM


TIBA YA MAASUMINA

Orodha Ya Vitabu Vilivyo ­Chapishwa Na Al-Itrah Foundation 1. i) Qur’ani Tukufu – Pamoja na Tarjuma ya Kiswahili ii) Qur’an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Thelathini 2. Uharamisho wa Riba 3. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza 4. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili 5. Hekaya za Bahlul 6. Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) 7. Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (a.s.) 8. Hijab vazi Bora 9. Ukweli wa Shia Ithnaashari 10. Madhambi Makuu 11. Mbingu imenikirimu 12. Abdallah Ibn Saba 13. Khadijatul Kubra 14. Utumwa 15. Umakini katika Swala 16. Misingi ya Maarifa 17. Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia 18. Bilal wa Afrika 19. Abudhar 20. Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu 21. Salman Farsi 22. Ammar Yasir 23. Qur’an na Hadithi 24. Elimu ya Nafsi 25. Yajue Madhehebu ya Shia

411

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 411

8/10/2017 1:22:22 PM


TIBA YA MAASUMINA

26. Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur’an Tukufu 27. Al-Wahda 28. Ponyo kutoka katika Qur’an 29. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii 30. Mashukio ya Akhera 31. Al Amali 32. Dua kwa Mujibu wa Ahlulbayt (a.s) 33. Udhuu kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna 34. Haki za wanawake katika Uislamu 35. Mwenyezi Mungu na sifa zake 36. Kumswalia Mtume (s) 37. Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) 38. Adhana 39. Upendo katika Ukristo na Uislamu 40. Qur’ani na Kuhifadhiwa Kwake 41. Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu 42. Kupaka juu ya khofu 43. Kukusanya Sala Mbili 44. Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara 45. Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya 46. Kusujudu juu ya udongo 47. Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s) 48. Tarawehe 49. Malumbano baina ya Sunni na Shia 50. Kupunguza Swala safarini 51. Kufungua safarini 52. Umaasumu wa Manabii 53. Qur’an Yatoa Changamoto 54. as-Salaatu Khayrun Mina -’n Nawm 55. Uadilifu wa Masahaba 56. Dua e Kumayl 412

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 412

8/10/2017 1:22:22 PM


TIBA YA MAASUMINA

57. Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu 58. Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake 59. Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata 60. Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mtume Muhammad (s) 61. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza 62. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili 63. Kuzuru Makaburi 64. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza 65. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili 66. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu 67. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne 68. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano 69. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita 70. Tujifunze Misingi Ya Dini 71. Sala ni Nguzo ya Dini 72. Mikesha Ya Peshawar 73. Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu 74. Ubora wa Imam ‘Ali na Ushia ndio njia iliyonyooka 75. Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake 76. Liqaa-u-llaah 77. Muhammad (s) Mtume wa Allah 78. Amani na Jihadi Katika Uislamu 79. Uislamu Ulienea Vipi? 80. Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) 81. Dhana ya Ndoa ya Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) 82. Urejeo (al-Raj’ah) 83. Mazingira 84. Utokezo (al - Badau) 85. Hukumu ya kujenga juu ya makaburi 86. Swala ya maiti na kumlilia maiti 87. Uislamu na Uwingi wa Dini 413

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 413

8/10/2017 1:22:22 PM


TIBA YA MAASUMINA

88. 89. 90. 91. 92. 93. 94. 95. 96. 97. 98. 99. 100. 101. 102. 103. 104. 105. 106. 107. 108. 109. 110. 111. 112. 113. 114. 115. 116. 117. 118.

Mtoto mwema Adabu za Sokoni Na Njiani Johari za hekima kwa vijana Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu Tawasali (AT- TAWASSUL) Imam Mahdi katika Usunni na Ushia Hukumu za Mgonjwa Sadaka yenye kuendelea Msahafu wa Imam Ali Maimamu wa Ahlul Bait – Ujumbe na Jihadi Idi Al-Ghadir Kusoma sura zenye Sijda ya wajibu Hukumu zinazomuhusu mkuu wa kazi na Mfanyakazi Huduma ya Afya katika Uislamu Sunna za Nabii Muhammad (saww) Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza) Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili) Shahiid Mfiadini Mwanamke Na Sharia Ujumbe -Sehemu ya Kwanza Ujumbe - Sehemu ya Pili Ujumbe - Sehemu ya Tatu Ujumbe - Sehemu ya Nne Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu Hadithi ya Thaqalain Ndoa ya Mutaa Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza Ukweli uliopotea sehemu ya Pili Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu 414

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 414

8/10/2017 1:22:22 PM


TIBA YA MAASUMINA

119. Ukweli uliopotea sehemu ya Nne 120. Ukweli uliopotea sehemu ya Tano 121. Mkutano wa Maulamaa wa Baghdad 122. Safari ya kuifuata Nuru 123. Fatima al-Zahra 124. Myahudi wa Kimataifa 125. Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi 126. Visa vya kweli sehemu ya Kwanza 127. Visa vya kweli sehemu ya Pili 128. Elimu ya Ghaibu ya Maimamu 129. Mwanadamu na Mustakabali wake 130. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Kwanza) 131. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Pili) 132. Khairul l’Bariyyah 133. Uislamu na mafunzo ya kimalezi 134. Vijana ni Hazina ya Uislamu 135. Adhana ni Ndoto au ni Wahyi? 136. Tabaruku 137. Saada Kamili – Kitabu cha Kiada cha Maadili 138. Vikao vya furaha 139. Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje? 140. Visa vya wachamungu 141. Falsafa ya Dini 142. Kuhuzunika na Kuomboleza 143. Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah 144. Mjadala wa Kiitikadi 145. Kuonekana kwa Allah 146. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza) 147. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili) 148. Ndugu na Jirani 149. Ushia ndani ya Usunni 415

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 415

8/10/2017 1:22:22 PM


TIBA YA MAASUMINA

150. 151. 152. 153. 154. 155. 156. 157. 158. 159. 160. 161. 162. 163. 164. 165. 166. 167. 168. 169. 170. 171. 172. 173. 174. 175. 176. 177. 178. 179. 180.

Maswali na Majibu Mafunzo ya hukmu za ibada Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 1 Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 2 Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 3 Abu Huraira Vipengee kadhaa katika Swala ya Jamaa na Msikiti. Mazingatio kutoka katika Qur’an - Sehemu ya Kwanza Mazingatio kutoka kaitka Qur’an - Sehemu ya Pili Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya kwanza Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya Pili Shia na Qur’ani – Majibu na Maelezo Falsafa ya Mageuzi ya Imam Husein (a.s) Amali za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani Elimu ya Tiba za Kiislamu - Matibabu ya Maimamu Uislamu Safi Majlisi za Imam Husein Majumbani Je, Kufunga Mikono Uislam wa Shia Amali za Makka Amali za Madina Asili ya Madhehebu katika Uislamu Sira ya Imam Ali kuhusu Waasi Ukweli uliofichika katika neno la Allah Uislamu na Mifumo ya Uchumi Umoja wa Kiislamu na Furaha Mas’ala ya Kifiqhi Jifunze kusoma Qur’ani as-Sahifatul Kamilah as-Sajjadiyyah Hayya ‘Alaa Khayri’l-’Amal Katika Adhana Ukweli kuhusu Funga ya Siku ya Ashura 416

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 416

8/10/2017 1:22:22 PM


TIBA YA MAASUMINA

181. Dua za Miezi Mitatu Mitukufu (Rajabu, Shaabani na Ramadhani) 182. Uadilifu katika Uislamu 183. Mahdi katika Sunna 184. Maswali Ya Uchunguzi Kuhusu Uislam 185. Kazi na Bidii ni njia ya maendeleo 186. Abu Talib – Jabali Imara la Imani 187. Ujenzi na Utakaso wa Nafsi 188. Vijana na Matarajio ya Baadaye 189. Historia maana na lengo la Usalafi 190. Ushia – Hoja na Majibu 191. Mateso ya Dhuria wa Mtume (saww) 192. Maombolezo – Msiba wa Bwana wa Mashahidi (a.s.) 193. Shahidi kwa Ajili ya Ubinadamu 194. Takwa 195. Upotoshaji Dhahiri katika (Turathi) Hazina ya Kiislamu 196. Amirul Muuminina (as) na Makhalifa 197. Tawheed Na Shirki 198. Kuvunja hoja iliyotumika kutetea Uimamu wa AbuBakr 199. Adabu za vikao na mazungumzo 200. Hija ya Kuaga 201. Uwazi baina ya Maslahi na Vikwazo 202. Fadhila za watukufu watano katika Sahih Sita 203. Mdahalo baina ya Mwanachuoni waKisunni na Kishia (Al- Muraja’aat) 204. Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (as) 205. Imam Husain ni Mfumo wa Marekebisho na Mageuzi 206. Mtazamo kuhusu msuguano wa Kimadhehebu 207. Nchi na Uraia – Haki na wajibu kwa Taifa 208. Mtazamo wa Ibn Taymiyyah juu ya Imam Ali (as) 209. Uongozi wa Kidini – Maelekezo na Utekelezaji wa Kijamii 210. Maadili ya Ashura 211. Mshumaa – Shahidi na Kifo cha Kishahidi 417

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 417

8/10/2017 1:22:22 PM


TIBA YA MAASUMINA

212. Mizani ya Hekima – Hadithi za Ahlul Bait (as) – Sehemu ya Kwanza 213. Imam Ali na Mambo ya Umma 214. Imam Ali na Mfumo wa Usawa 215. Uimamu na Tamko la Kutawazwa 216. Mfumo wa Wilaya 217. Vipi Tutaishinda Hofu? 218. Kumswalia Mtume ni Ufunguo wa Utatuzi wa Matatizo 219. Maeneo ya Umma na Mali Zake 220. Nahju ‘L-Balagha– Majmua ya Khutba, Amri, Barua, Risala, Mawaidha na Semi za Amirul-Muuminin Ali bin Abu Talib (a.s.) 221. Mukhtar – Shujaa aliyelipiza kisasi dhidi ya wauaji wa Imam Husein (as) hapo Karbala 222. Mazingatio Katika Swala 223. Imam Hasan na Mfumo wa Kujenga Jamii 224. Vyakula Na Vinywaji 225. Kuelewa Rehema ya Mwenyezi Mungu 226. Imam Mahdi na Bishara ya Matumaini 227. Mtazamo Mpya - Wanawake katika Uislamu 228. Shia Na Sahaba - Majibu na Maelezo 229. Majanga Na Jukumu la Jamii 230. Shia Na Hadith - Majibu na Maelezo 231. Upotofu Ndani ya Kitabu cha Mitaala kwa Shule za Sekondari 232. Ugaidi Wa Kifikra Katika Medani Ya Kidini 233. Yafaayo kijamii 234. Uswalihina Dhahiri Na Batini Yake 235. Mkakati wa Kupambana na Ufakiri 236. Mwanamke Katika Harakati Za Mageuzi 237. Jihadi 238. Hija Katika Maneno Na Ujumbe Wa Imam Khomeini (R.A) 239. Tiba Ya Maradhi Ya Kimaadili 240. Yusuf Mkweli

418

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 418

8/10/2017 1:22:23 PM


TIBA YA MAASUMINA

241. Taqiyya Kwa Mujibu Wa Sheria Ya KIISLAMU 242. Imam Mahdi (A.S) Imam Wa Zama Hizi Na Kiongozi Wa Dunia 243. Talaka Tatu 244. Safari Ya Kuelekea Kwa Mwenyezi Mungu 245. Hotuba Za Kiislamu Juu Ya Haki Za Binadamu 246. Mashairi Ya Kijamii 247. Ngano Ya Kwamba Qur’ani Imebadilishwa 248. Wito Kwa Waumini: “Enyi Mlioamini” 249. Imam Husain (a.s) ni Utu na Kadhia 250. Imam Husain ni Kielelezo cha Kujitoa Muhanga na Fidia 251. Imam Mahdi ni Tumaini la Mataifa 252. Kuchagua Mchumba 253. Mazungumzo ya Umoja – Ukosoaji na Usahihishaji 254. Utamaduni wa Mwamko wa Kijamii 255. Hekima za kina za Swala 256. Kanuni za Sharia za Kiislamu 257. Utamaduni kufuatana na Qur’ani na Utekelezaji wa Kivitendo (Sehemu ya Kwanza) 258. Kauli sahihi zaidi katika kufafanua Hadithi

KOPI ZIFUATAZO ZIMETAFSIRIWA KWA LUGHA KINYARWANDA 1.

Amateka Na Aba’ Khalifa

2.

Nyuma yaho naje kuyoboka

3.

Amavu n;amavuko by;ubushiya

4.

Shiya na Hadithi 419

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 419

8/10/2017 1:22:23 PM


TIBA YA MAASUMINA

5.

Kor’ani Nziranenge

6.

Kwigisha Mu Buryo Bw’incamake Uka Salat Ikotwa

7.

Iduwa ya Kumayili

ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION KWA LUGHA YA KIFARANSA 1.

Livre Islamique

420

04_17_TIBA YA MAASUMINA_10_August_2017.indd 420

8/10/2017 1:22:23 PM


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.