Tujifunze misingi ya dini

Page 1

Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:14 PM

TUJIFUNZE MISINGI YA DINI

Kimeandikwa na: Sheikh Nassir Makarim Shirazi

Kimetarjumiwa na: Ustadh Abdallah Mohamed

Page A


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:14 PM

ŠHaki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: 978 - 9987 - 427 - 62 - 2 Kimeandikwa na: Sheikh Nassir Makarim Shirazi Kimetarjumiwa na: Ustadh A. Mohamed Kimehaririwa na: Ramadhani Kanju Shemahimbo Kimepangwa katika Kompyuta na: Ukhti Pili Rajab Toleo la kwanza: 1989 Imechapishwa na ADHIM Abu dhar Islamic Mission Dar es Salaam Toleo la Pili: Nakala 1000, Novemba 2008 Kimetolewa na kuchapishwa na:

Al-Itrah Foundation S.L.P. - 19701, Dar-es-Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Nukushi: +255 22 2127555 Barua Pepe: alitrah@raha.com Tovuti: www.alitrah.org Katika mtandao: www.alitrah.info

Page B


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:14 PM

Page C

YALIYOMO TUMJUE MUNGU (1) Somo la kwanza: Kumjua Mwenyeezi Mungu ............................................................3 Kutoa Shukrani..................................................................................4 Kuwapo pamoja na mambo yenye faida na yasiyo na faida katika utafiti huu.......................................................................................... 4

Somo la Pili: Ishara ya Mwenyeezi Mungu katika maisha yetu ya kila siku.........6 Kumjua Mwenyezi mungu na maendeleo ya kielimu....................... Kumjua Mwenyeezi Mungu, Juhudi na matumaini...........................7 Kumjua Mwenyeezi Mungu na majukumu yake..............................8 Kumjua Mwenyeezi Mungu na utulivu............................................8

Somo la Tatu: Njia mbili za kumjua Mwenyeezi Mungu .......................................9 Njia ya ndani....................................................................................10 Huu ndio mwito mtakatifu wa kimaumbile ya binadamu...............10

Somo la Nne: Jibu la swali hilo muhimu...............................................................12


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:14 PM

Page D

Tujifunze Misingi ya Dini

Somo la Tano: Kisa cha kweli...................................................................................

Somo la Sita: Njia ya pili ya kumjua Mwenyeezi Mungu......................................17 Sababu zifuatazo zinafafanua na kuondosha mashaka....................18 Uhusiano katika utaratibu na akili...................................................19

Somo la Saba: Mifano itokanayo na kuumba...................................................................20

Somo la Nane: Ulimwengu wa maajbu kwenye ndege mdogo................................23

Somo la Tisa: Marafiki wawili wa kale..................................................................26 Maelezo ya mwisho ya somo la kumi utukufu ulioje wa sifa za Mwenyeezi Mungu..........................................................................33 Sifa za Uukufu na uzuri ..................................................................34

TUUJUE UADILIFU (2) Somo la Kwanza Uadilifu ni nini?.........................................................................................39

Somo la Pili Dalili za uadilifu wa Mwenyeezi Mungu..................................................44 D


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:14 PM

Page E

Somo la Tatu Heima ya Mungu ya kuleta maafa ............................................................48

Somo la Nne Hekima na misukosuko katika maisha......................................................52

Somo la Tano Maelezo mengine ya hekima ya maafa....................................................54

Somo la Sita Kutenzwa nguvu na kuachiliwa................................................................58

Somo la Saba Hoja za wazi kuhusu Hiyari......................................................................63

Somo la Nane Maana ya njia ya kati.................................................................................66

Somo la Tisa Ufafanuzi juu ya uongofu na upotovu.......................................................70

Somo la Kumi Uadilifu wa Mwenyeezi Mungu na suala la milele....................................75

E


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:14 PM

Page F

TUUJUE UTUME (3) Somo la Kwanza Haja ya kuwa na viongozi kutoka kwa Mungu..........................................80

Somo la Pili Haja ya mitume kuleta sheria za Mwenyeezi Mungu................................85 Uhusiano kati aya upweke wa Mwenyeezi Mungu....................................89

Somo la Tatu Kwa nini Mitume Hawatendi dhambi.......................................................90

Somo la Nne Njia nzuri za kuwajua Mitume...................................................................93

Somo la Tano Muujiza mkuu wa Mtume Muhammad.....................................................98 Kisa cha Walid bin Mughira....................................................................100

Somo la Sita Tutazame muujiza wa Qur’an.................................................................103

Somo la Saba Mtazamo wa Qur’an kwenye ulimwengu................................................106

Somo la Nane Qur’an Tukufu na ugunduzi wa kisasa wa Ki-sayansi..........................111 Uvumbuzi wa dunia kuzunguka jua.........................................................133 F


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:14 PM

Page G

Somo la Tisa Hoja nyingine ya kuthibitisha ukweli wa Mtume wa dini ya kiislamu.....115

Somo la Kumi Mtume wa Uislmu ndiye muhuri wa unabii...........................................119

TUUJUE UIMAMU (4) Somo la Kwanza Uimamu ulianza lini?...............................................................................126

Somo la Pili Hekima ya kuwepo Imam.......................................................................130

Somo la Tatu Masharti ya sifa maalum za Imam..........................................................134

Somo la Nne Ni nani mwenye jukumu la kumteua Imam...........................................138

Somo la Tano Qur’an na Uimamu..................................................................................143

Somo la Sita Uimamu katika Hadithi za Mtume (s.a.w.w.)..........................................149

Somo la Saba Hadithi ya ‘Manzila’ na Yaumud-Daari..................................................153 G


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:14 PM

Page H

Somo la Nane Hadith ‘Thaqalaini na ya Safina tun -Nuh..............................................157 Hadithi ya (Safinatun -Nuh-....................................................................160

Somo la Tisa Maimamu kumi na wawili.......................................................................161

Somo la Kumi Imamu Mah’di (a.s) Msuluhishaji wa ulimwengu...................................166

TUYAJUE MAREJEO (5) Somo la Kwanza Je kifo ni mwanzo au ni mwisho.............................................................175

Somo la Pili Kuamini ‘Ufufuo’ Hufanya maisha yawe na maana................................179

Somo la Tatu Mifano ya mahakama ya kiyama iko ndani yetu.....................................184

Somo la Nane Ufufuo na ufunuo wa kimaumbile...........................................................188

Somo la Tano Ufufuo na mizani ya uadilifu...................................................................191 H


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:14 PM

Page I

Somo la Sita Ushahdi wa ufuo hapa duniani................................................................195

Somo la Saba Ufufuo na hekima ya kuumbwa...............................................................198

Somo la Nane Kubaki roho ni dalili ya ‘ufufuo’.............................................................201

Somo la Tisa Ufufuo wa ‘Kimwili’ na wa ‘Kiroho’......................................................206

Somo la Kumi Pepo, Moto na kujiunda matendo yetu...................................................211

I


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:14 PM

Page J

NENO LA MCHAPISHAJI Kitabu kilichoko mikononi mwako, ni tarjuma ya mfululizo wa vijitabu vitanao vilivyoandikwa na Sheikh Nassir Makarim Shirazi: (1) Maarifatul llah (Tumjue Mungu) (2) Maarifatul Adl (Tuujue Uadilifu) (3) Maarifatul Nubuwah (Tuujue Utume) (4) Maarifatul Imamah (Tuujue Uimamu) (5) Maarifatul Maad (Tuyajue Marejeo). Katika toleo hili la pili ambalo ni chapisho la Taasisi ya Al-Itrah tumevikusanya vijitabu hivyo pamoja katika kijitabu kimoja kwa jina la "Tujifunze Misingi ya Dini.", kwa vilie hii ndio misingi mikuu ya Dini ya Uislamu. Kama lilivyo jina la kijitabu hiki, mwandishi ameelezea kwa ufupi lakini katika lugha pana misingi hii mikubwa ya Uislamu ambayo ndiyo inayowaunganisaha Waislamu wote, pamoja na hitilafu ndogo katika misingi miwili: Adl (Uadilifu) na Imamah (Uimamu). Hata hivyo, hitilafu hizo ni ndogo sana kiasi kwamba haziwezi kuleta mgongano baina ya madhehebu zetu za Kiislamu. Kwa hiyo maudhui yaliomo katika kitabu hiki ni yenye kufaa kwa Waislamu wote wa madhehebu zote. Kutokana na umuhimu wa maudhui haya ambapo kwa uchahce kila Mwislamu anatakiwa aijue misingi hii, tumeona tuyatoe masomo haya katika lugha ya Kiswahili ili wasomaji wetu wa Kiswahili wapate kufaidika na yaliomo katika safu hii ya masomo na kuongeza ujuzi wao katika masuala ya dini na ya kijamii. Tunamshukuru ndugu yetu, Ustadh Abdallah Mohamed kwa kukubali jukumu hili la kukifanyia tarjuma kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapish-


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

wa kwa kitabu hiki. Mchapishaji: Al-Itrah Foundation S. L. P. 19701 Dar-es-Salaam, Tanzania.

9/5/2008

10:14 PM

Page K


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

L

9/5/2008

10:14 PM

Page L


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:14 PM

Page 1


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:14 PM

Page 2

Tujifunze Misingi ya Dini

TUMJUE MUNGU (1)

2


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:14 PM

Page 3

Tujifunze Misingi ya Dini

Kwa jina la Allah, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.

SOMO LA KWANZA KUMJUA MWENYEZI MUNGU Kwa nini tuwaze na tufanye utafiti wa kumjua Muumba wa ulimwengu? 1. Sote tunapenda kudadisi mengi kuhusu ulimwengu tunaoishi. Tunapenda kujua ukweli wa mambo yalivyo: Je hii mbingu iliyo juu na nyota zake zenye kupendeza, hii ardhi pana yenye mandhari ya kuvutia, hivi viumbe mbalimbali, ndege wazuri, samaki wa kila aina walioko baharini, maua yaliyochanua na kustawi vizuri, na miti mirefu, je hivi vyote vimejileta vyenyewe hapa duniani? Au ni usanii uliofanywa na msanii hodari anaeelewa vyema kazi yake? Tukiachilia mbali hayo, swali la kwanza tunalojiuliza akilini mwetu ni: Sisi tumetoka wapi? Tuko wapi, na tunaelekea wapi? Bila shaka tungelikuwa na furaha isiyo na kifani kama tungelijua majibu ya maswali haya, yaani tujue maisha yetu yalianzaje, yataishia vipi na tunawajibika tufanye nini hivi sasa. Kupenda kwetu kutambua kunatulazimisha tusijikalie tu bila ya kutafuta majibu ya maswali haya. Hutokea mara kwa mara kwamba mtu apatwapo na ajali ya gari na kupoteza fahamu, hupelekwa hospitalini kwa matibabu. Anaporudiwa na fahamu na kupata afuweni jambo la kwanza atakalowauliza walio karibu 3


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:14 PM

Page 4

Tujifunze Misingi ya Dini ni,’ je niko wapi? Kwa nini nimeletwa hapa? Na lini nitatoka? Haya yote yanaonyesha vile ambavyo binadamu hawezi kunyamaa pasi na kuyauliza. Hivyo basi, kitu cha kwanza kinachofuata tutake kumjua Mwenyezi Mungu na viumbe vilivyomo ulimwenguni, ni ile kiu yetu ya kufanya utafiti juu ya hayo.

2. Kutoa shukrani Hebu fanya kama ulialikwa katika hafla muhimu, ukakaribishwa na kuandaliwa vyema kwa sababu ulialikwa kupitia kwa ndugu yako, hukuweza kumtambua vizuri mwalishi wako. Hivyo basi, jambo la kwanza utakalofanya ni kumtafuta ili umpe shukrani. Kadhalika tukiangalia upana wa dunia tunayoishi na neema mbalimbali tulizopewa kama: macho yaonayo, masikio yasikiayo, akili timamu, nguvu mbali mbali za kimwili na roho, na njia tofauti za kujitafutia riziki; bila shaka moja kwa moja tutaanza kuwaza jinsi ya kujaribu kumtambua aliyetuneemesha yote haya ili tupate kumshukuru japo yeye hana haja na shukrani zetu lakini tusipofanya hivyo hatutakuwa na furaha tunajisikia kuwa hatujatimiza wajibu wetu. Hii ni sababu nyingine inayotupelekea kufanya utafiti juu ya kumtambua Mwenyezi Mungu.

3. Kuwapo pamoja na mambo yenye faida na yasiyo na faida katika utafiti huu Hebu tufanye kama tuko safarini na katika safari yetu tukawa tumefika kwenye njia panda yenye rabsha za watu, kila mmoja miongoni mwao akituonya tusimame hapo kutokana na hatari nyingi zilizopo. Ili tusiingie hatarini, kila kikundi kinatutaka tufuate njia yake. Kimoja kinasema, njia nzuri ni inayoelekea upande wa mashariki. Kingine kinadai, fuateni njia 4


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:14 PM

Page 5

Tujifunze Misingi ya Dini inayoelekea Magharibi. Wakati huo huo kingine kinasema tushike njia iliyo kati ya njia mbili hizo kikisema, ‘shikeni njia hii kwani ndiyo njia pekee ya kujiokoa na kufika salama mwendako, na ndio njia pekee itakayowafikisha kwenye furaha na usalama.’ Je hapo tutachagua kufuata njia yoyote bila ya kuchunguza? Au akili zetu zitaridhika kubaki papo hapo (hatarini) bila ya kuchagua njia yoyote? Bila shaka jibu ni hapana. Bila shaka akili zetu zitatuambia tuanze kufanya uchunguzi mara moja kwa kusikiliza na hatimaye kukubali upande ulio na maelezo sahihi ya kweli na yenye sababu za kutosha ili tufuate njia yake. Na mara tu tutakapojihakikishia njia iliyo sawa, ndipo tutaifuata. Hivyo hivyo katika ulimwengu huu tuna hali kama hiyo. Kuna dini na madhehebu mbalimbali vinavyotaka tufuate njia zao lakini kama ilivyo furaha zetu na misiba yetu, kuendelea kwetu na kubaki nyuma kwetu kunategemea sana uchunguzi wetu na jinsi ya kujichagulia yafaayo. Hivyo basi tunalazimika kufikiria juu ya hili ili tujilinde kutokana na kuanguka kwenye majanga machafu na migogoro, na hii ndiyo sababu nyingine inayotupeleka kwenye utafiti juu ya Muumba wa ulimwengu. Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amesema:

“Wape biashara waja (wangu) wanaosikiliza maneno na kuyafuata yaliyo mazuri zaidi.”(39:18).

5


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:14 PM

Page 6

Tujifunze Misingi ya Dini

SOMO LA PILI ISHARA YA MWENYEZI MUNGU KATIKA MAISHA YETU YA KILA SIKU

1. Kumjua Mwenyezi Mungu na maendeleo ya kielimu Hebu chukua mfano rafiki yako ametoka safarini akakuletea zawadi ya kitabu na ukakisifia kuwa ni kitabu kizuri mno kilichoandikwa na msomi barabara, bingwa na mahiri katika kazi yake. Bila shaka hutakisoma juu juu bali utazingatia kila ibara na hata mpangilio wa maneno yake. Endapo patakuwa na ibara ambayo hukuielewa huenda ukatumia masaa au masiku kadhaa kadri utakavyoweza kuichungua mpaka utakapoelewa maana yake hasa. Kwa nini? Kwa sababu mtunzi wa kitabu hicho si wa kawaida, bali ni msomi barabara anaezingatia kila neno analoliandika. Lakini ikiwa kinyume na hivyo, ukaambiwa, “japokuwa kitabu hiki ni kizuri ukikitazama kwa nje, lakini mtunzi wake hakuelimika na hana misingi ya kutegemewa kieleimu,” ni wazi kwamba utakiangalia juu juu tu na endapo utakuta jumla usiyoielewa, utasema hii ni kwa sababu mtunzi hana elimu ya kutosha, tena kukisoma ni kupoteza wakati bure.” Hivyo hivyo huu ulimwengu ni kama kitabu kikubwa ambacho kila kiumbe kilichomo ni kama neno au sentensi. Kwa maoni ya mtu anayeamini Mwenyezi Mungu, kila chembe iliyomo duniani ina mafunzo. Muumini hasa mwenye kumuabudu Mwenyezi Mungu atafanya utafiti wa ndani wa kujua siri ya kuumbwa kwake viumbe – na sababu hii ndio inayosaidia elimu ya binadamu kuendelea – kwa sababu yeye hupata kujua ya kwamba Muumbaji wa ulimwengu huu anaelimu na uwezo usio na mwisho, na kila alifanyalo lina hekima na falsafa. Hivyo basi wakati binadamu anapofanya uchunguzi wake, huwa mdadisi sana ili apate kuzijuwa vizuri siri za 6


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:14 PM

Page 7

Tujifunze Misingi ya Dini uumbaji. Lakini mtu wa kiyakinifu (asiyeamini Mwenyezi Mungu) hana sababu itakayomfanya kutafiti siri za uumbaji, kwa sababu anaamini kuwa viumbe vyote vimeumbwa na “utaratibu wa nguvu asili” (Nature). Hata hivyo tukiangalia uvumbuzi na utaalamu wa kimaada, hatutofautiani na fikra za wasioamini Mungu kwani yeye hakubali kuwepo kwa Mwenyezi Mungu, isipokuwa humwita “utaratibu wa nguvu asili” (Nature). Kwa sababu anakubali mpango na utaratibu uliopo wa kimaumbile duniani. Hivyo basi, kumuabudu Mwenyezi Mungu ni mojawapo ya njia za maendeleo kielimu.

2. Kumjua Mwenyezi Mungu, juhudi na matumaini Mwanadamu anapokabiliwa na matatizo katika maisha yake na milango ya kuelekea kwenye kuyatatua inapofungwa, hujihisi mnyonge, asiye na matumaini na mpweke, hapo hukimbila kumwamini Mwenyezi Mungu na kumuomba msaada, naye hupatiwa. Mtu mwenye kumwamini Mwenyezi Mungu kamwe hahisi upweke au unyonge, wala hakati tamaa kwa sababu anaamini kwamba Mungu ndiye Mshindi wa matatizo yote na hakuna jambo zito kwake. Akiwa na matarajio ya kupata msaada na urahimu wa Mwenyezi Mungu, muumini hutumia nguvu zake zote katika kukabiliana na matatizo. Kwa kumpenda Mwenyezi Mungu na kumtumainia, hupata msukosuko wa kuongeza bidii na juhudi na hatimaye huyashinda matatizo. Ndiyo! Kumwamini Mwenyezi Mungu ndiyo mategemeo makubwa ya mwanaadamu. Ndiko kunakoleta uthabiti na kunafufua matumaini ya daima nyoyoni.

7


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:14 PM

Page 8

Tujifunze Misingi ya Dini Kwa sababu hii muumini hathubutu hata kidogo kujiua kwa sababu kujiua kunasababishwa na kujikatia tamaa, kukosa matumaini na kujihisi kushindwa, muumini hakati tamaa wala hahisi kushindwa.

3. Kumjua Mwenyezi Mungu na majukumu yake Kuna madaktari ambao wakiendewa na wagonjwa masikini, huwatibu na kuwapatia pesa za madawa, badala ya wao kuwadai malipo ya matibabu. Isitoshe atakesha nyumbani kwa mgonjwa pindi anapohisi hatari juu ya mgonjwa huyo. Watu kama hawa ndio wanaoamini na kumuabudu Mwemyezi Mungu. Na bila shaka tumeshapata kumuona daktari ambaye hayuko tayari hata kuanza hatua ya kwanza kumtibu mgonjwa mpaka alipwe malipo ya matibabu kwanza, na hivyo ni kwa sababu imani yake ni dhaifu. Mtu mwenye imani, kazi yoyote aifanyayo hujuhisi kuwa na majukumu, hutambua wajibu wake, hufanya mema, msamehevu na daima huhisi ya kwamba ndani ya moyo wake kuna askari anayeviangalia vitendo vyake. Lakini wakosefu wa imani ni wachoyo, ni watu hatari na ambao hawajioni kuwa na majukumu. Ukandamizaji, uonevu na dhulma juu ya haki za watu, ni kazi rahisi sana kwao, na hawako tayari kufanya wema.

4. Kumjua Mwenyezi Mungu na utulivu Wanasaikolojia wanasema kwamba maradhi ya moyo ni mengi katika zama hizi kuliko ilivyokuwa katika siku zilizopita. Wanasema kwamba sababu zinazosababisha ni kuwa na mashaka juu ya mustakabali wa hali ya maisha, vifo, vita na kuwa na wasiwasi juu ya kutofaulu katika shughuli kadha wa kadha. Na wakaongeza kuwa miongoni mwa mambo yanayoweza kuondoa mashaka katika nafsi ya mtu ni kumuamini Mwenyezi Mungu, kwa sababu 8


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:14 PM

Page 9

Tujifunze Misingi ya Dini mashaka yanapotaka kuingia katika nafsi ya mtu huondoshwa na imani ya kumuamini Mwenyezi Mungu aliye Mwema, Mwenye kuruzuku, ajuaye hali za waja wake, na anayewasaidia kila wanaporejea kwake na kutaka msaada na ambaye humuondolea mashaka. Kwa sababu hii ndipo tunaona mwenye imani hasa daima ana hisia za amani moyoni na hana wasiwasi wowote ndani ya nafsi yake. Chochote akifanyacho hukifanya kwa kumuelekea Mwenyezi Mungu ili amfariji. Mtu kama huyo hata anapoingia katika medani ya vita, huingia na huku akitabasamu. Mwenyezi Mungu amesema katika Qur’ani:

“Wale walioamini na hawakuchanganya imani yao na dhuluma; hao ndio watakaopata amani.” (6:82).

SOMO LA TATU NJIA MBILI ZA KUMJUA MWENYEZI MUNGU Tangu zamani hadi leo, vitabu vingi vimetungwa vikielezea juu ya kumjua Mwenyezi Mungu, na mengi yamezungumzwa na wasomi na wasiokuwa wasomi kuhusiana na suala hilo. Kila mmoja kati yao amechagua njia ya kufikia kulielewa suala hili, lakini miongoni mwa njia zote kuna njia mbili bora za haraka kutufikisha kwenye misingi ya kumjua Mwenyezi Mungu (s.w.t.). Ya kwanza ni njia ya ndani iliyo karibu zaidi, na ya pili ni njia ya nje (iliyo wazi zaidi). Kwa kutumia njia ya kwanza tuliyopata kujua kwa kutumia undani wa nyoyo zetu tunaposikia mwito wa Tawhid (Upweke wa Mwenyezi Mungu s.w.t.

9


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:14 PM

Page 10

Tujifunze Misingi ya Dini Kwa kutumia njia ya pili tunatafiti katika uvumbuzi wa viumbe vilivyomo ulimwenguni, na tunaona alama za Mwenyezi Mungu katika viumbe vyote na katika kiini cha kila chembe. Kila moja kati ya njia hizi inahitaji ufafanuzi wa hali ya juu, lakini tutajaribu kwa kifupi kuzifanyia utafiti.

Njia ya ndani Hebu tuziweke fikra zetu katika maudhui yafuatayo: 1- Wasomi wanasema kwamba binadamu yeyote mwenye akili timamu, wa taifa ama tabaka yoyote, hata kama ataishi peke yake bila kupata taaluma yoyote na bila kusikia maoni ya wanaoamini Mwenyezi Mungu au wasioamini, atatambua kuwa kuna nguvu iliyo juu ya Nguvu-asili (Nature). Nguvu inayotawala dunia nzima, aidha atahisi kuwa mna mwito ndani ya nafsi yake uliojaa wema, mwito ambao uko wazi na wenye nguvu ambao unamlingania aelekee kwa mwanzilishi mkuu wa ulimwengu Ambaye atamwita Allah (Mwenyezi Mungu).

Huu ndio mwito mtakatifu wa kimaumbile ya binadamu. 2. Naam, hutokea kwamba mtu huwa ameshughulishwa na ghasia za ulimwengu wa kimaada (wa dhahiri) na harakati za maisha ya kila siku yaliojaa anasa, na hivyo umfanye apuuze kusikia mwito huu kwa muda kidogo; anapokumbwa na mabalaa yanayoikumba dunia kama mafuriko, tetemeko la ardhi au tufani, katika wakati ambao mbinu zake zote na uwezo wa kidunia zimeshindwa, na hana pa kukimbilia; ndipo mwito huu wa ndani unapopata nguvu, na huhisi ndani ya nafsi yake mna nguvu inayomwita, nguvu iliyo juu ya nguvu zote, nguvu iliyofichika ambayo kwa kutumia nguvu hiyo, matatizo yote huwa mepesi. Ni mara chache sana kupata mtu asiyekuwa katika hali kama hiyo. Wakati anapopata misukosuko. Hii ndiyo dalili inayoonesha jinsi wanadamu tulivyo karibu Naye, na Yeye alivyo karibu nasi. Yeye yomo ndani ya nafsi na roho zetu. 10


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:14 PM

Page 11

Tujifunze Misingi ya Dini Naam, bila shaka mwito wa kiasili umo ndani yetu lakini wakati wa matatizo hupata nguvu zaidi. 3. Historia inatueleza kwamba, hata wafalme wakubwa ambao hawataki hata kutaja jina la Mungu wakati wa amani na utulivu, pia nao humkumbuka Mungu na kuusikia mwito wake wa asili, mara wanapoona misingi ya uwezo wao inaanza kuyumba, na kwamba watapoteza mamlaka yao. Historia inatueleza kwamba wakati Firaun alipoona kwamba anakufa maji katika mawimbi ya bahari alisema: “Nakiri kuwa hakuna Mungu mwingine ila Mungu wa Musa.� Mwito huu ulikuja kutoka ndani ya nafsi yake. Si Firaun pekee, bali watu wote wanaokuwa katika hali kama hiyo, huwa kama yeye. 4. Ukichunguza sababu hasa za jambo hili utakubali kuwa kuna nuru iliyo ndani ya nafsi yako inayoongoza na kukulingania uelekee kwa Mwenyezi Mungu, huenda imeshakutokea kwa baadhi ya nyakati ambazo umekabiliwa na matatizo, na kutumia kila mbinu za kuyatatua bila mafanikio, hapa bila shaka uliona kuwa pana nguvu ulimwenguni inayoweza kukupatia ufumbuzi wa matatizo hayo. Wakati huo tumaini lenye upendo litajaa moyoni mwako na kuondosha mawingu ya kiza kutoka katika nafsi.

Naam, Hii ndiyo njia ya karibu zaidi mtu unaweza kuifuata kumfikia Mwenyezi Mungu swt. Swali moja tu: Yawezekana mmoja wenu kujiuliza maswali yafuatayo: Je uwezekano wa kuwepo kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu si unatokana na jinsi tulivyokulia katika mazingira haya (ya imani) au jinsi tulivy11


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:14 PM

Page 12

Tujifunze Misingi ya Dini ofundishwa na wazazi ndipo katika hali ya shida tufikirie kumuomba Mwenyezi Mungu? Tunafahamu kwamba una haki ya kujiuliza swali hili, nasi tuna majibu yake kutoka katika somo litakalofuata. Mwenyezi Mungu anasema katika Qur’ani:

“Na wanapopanda vyomboni (wakapatwa na misukosuko), humuomba Mwenyezi Mungu, na hali ya kuwa wanamtakasishia utii. Lakini anapowafikisha salama barani, mara wanamshirikisha.” ( 29:65).

SOMO LA NNE Jibu la swali hilo muhimu:Swali: Katika somo lililopita tumeona kwamba daima sisi huusikia mwito wa upweke wa Mwenyezizi Mungu (Tawhid) ndani ya nafsi zetu, na hasa tunapokabiliwa na matatizo ndipo tunapousikia wazi wazi na kwa nguvu zaidi, na mara huanza kufikiri juu ya Mwenyezi Mungu swt. na kuomba msaada Wake. Hapa inawezekana kuwe na swali kwamba, hii sauti ya ndani tunayoiita “nguvu za asili” ya Mwenyezi Mungu (Fitrah) si inatokana na mambo tuyasikiayo katika mazingira yetu au kwa wazazi wetu au shuleni, na hivyo imekuwa ni jambo la kawaida tulilolizoea?

12


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:14 PM

Page 13

Tujifunze Misingi ya Dini Jibu: Jibu la swali hili linahitaji maelezo kidogo. Kwa kawaida mila hubadilika. Hatuwezi kupata katika historia ya nchi zote mila ambazo hazikubadilika, mila za leo zinaweza kubadilika kesho, kama ambavyo mila na desturi za watu haziwezi kuwa kwa watu wengine. Hivyo basi tunapoona kwamba mila zilizomo katika mataifa yote zimekuwako wakati wote na katika zama zote bila hitilafu, ni lazima tutambue kwamba hakika yake inatokana na Fitrah iliyofumwa ndani ya roho na nafsi ya mwanaadamu. Tuchukue mfano wa penzi la mama kwa mtoto wake, hili kwa vyovyote haliwezi kusemekana kuwa linasababishwa na propaganda, ada au mila, sababu hakuna kabila, taifa au wakati wowote unaoweza kuona mama akimchukia mwanawe. Ndiyo, inawezekana mama kumchukia mwanawe, aidha kutokana na kuwa na akili taahira, au baba alikuwa akiishi zama za “Ujahiliya�(Kabla ya Mtume kuutangaza Uislamu) aliweza kumzika mtoto wake wa kike angali hai, kutokana fikra potofu za kishirikina, lakini hata hivyo, mambo kama haya ni nadra kutokea. Baada ya maelezo haya tuangalie jinsi watu wa zamani na wa sasa wanavyomuabudu Mwenyezi Mungu, (kwa kuwa somo hili ni gumu kidogo, tafadhali jaribu kuwa mwangalifu). 1. Wanasisitiza wataalamu wa elimu ya jamii na wanahistoria kwamba hapajatokea wakati wowote ambao watu hawajakuwa na imani na Mwenyezi Mungu au ya kitu chochote, isitoshe dini zimeendelea kuwepo katika kila zama, na hii ni dalili za wazi kwamba kumuabudu Mwenyezi Mungu kunatoka ndani ya roho, na msingi wake ni Fitrah ya binadamu, na si mila. Kwa sababu lau kama ingelikuwa misingi yake ni ada na mila kusingelienea na kudumu duniani.

13


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:14 PM

Page 14

Tujifunze Misingi ya Dini Tuna ushaidi unaoonesha kwamba kabla ya kuanza kuandikwa historia, kulikuwa na aina mbalimbali za dini. Bila shaka watu wa kale hawakuweza kumuelewa Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo walijaribu kumtafuta miongoni mwa viumbe, wakijitengenezea masanamu na vitu vilivyoumbwa, lakini kutokana na kukua kwa akili waliweza kidogo kidogo kujua ukweli ulipo, wakaacha kuabudu masanamu ambayo ni viumbe vya ki-maada, na kukubalina na Mwenyezi Mungu Mmoja. 2. Baadhi ya wanasaikolojia mashuhuri wanaeleza wazi wazi kwamba nafsi au roho ya binadamu ina hisia nne: Ya kwanza: Hisia ya maarifa, inayomfanya atafute elimu, na awe na kiu ya kutaka kujua, ni mamoja iwe na manufaa kwake ya kimaada au haina. Ya pili: Hisia ya maadili mema ambayo ndiyo msingi wa tabia na maadili mema ya binadamu. Ya Tatu: Hisia ya uzuri ambao ndio msingi wa ushairi, fasihi na usanii wenye maana za ndani sana. Ya nne: Ni hisia ya imani inayomlingania binadamu kumjua Mwenyezi Mungu na kutii amri zake. Kwa hiyo twaona kwamba hisia za imani zina mizizi mikubwa yenye kina kirefu ndani ya nafsi ya mtu. Kwa maneno mengine, hapana utengano kabisa kati ya binadamu na imani. 3. Katika masomo yetu yatakayofuata, tutaona jinsi wengi miongoni mwa watu wa kiyakinifu na wasioamini Mwenyezi Mungu wanavyokiri kuwepo kwa Mwenyezi Mungu, japo hawalitaji jina lake wazi wazi na badala yake humwiita ‘Nguvu-asili’ (Nature) au humbandika majina mengine lakini sifa wanazoipa hiyo nguvu ya asili kwa kweli ni sifa za Mwenyezi Mungu kabisa. Kwa mfano, kwamba nguvu hiyo imempa mwandamu figo mbili kwa 14


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:15 PM

Page 15

Tujifunze Misingi ya Dini sababu ilijua kwamba endapo mojawapo kati ya hizo itashindwa kufanya kazi sawa sawa, nyingine itaendeleza utendaji wake wa kazi, n.k. Swali ni, je maelezo hayo yanafafanua juu ya ‘Nguvu-asili’ iliyopo na Isiyo na fahamu? Au yanafafanua juu ya Mwenyezi Mungu mwenye ujuzi wa mambo yote na yasiyokwisha, ila tu wanamwita ‘Nguvu za asili’? Katika utafiti huu uliopita tunapata mambo haya: - Upendo wa Mwenyezi Mungu daima upo nasi, na utaendelea kuwapo - Imani juu ya Mwenyezi Mungu ni mwali (mwako) wa milele unaotia vuguvugu nyoyo na roho zetu. - ili tumjue Mwenyezi Mungu hatulazimiki kufuata njia ndefu, bali inatupasa kuangalia undani wetu na ndipo tutakuwa na imani naye. Qur’ani Tukufu inasema: “….nasi tu karibu zaidi na mwanadamu kuliko mshipa wa shingo yake.” (50:16).

SOMO LA TANO Kisa cha kweli Tumeshasema kuwa hapo awali wapinzani hukanusha kuwepo kwa Mwenyezi Mungu kwa ndimi zao tu, lakini wana imani nyoyoni mwao. Hapana shaka kuwa ushindi na ufanisi - hasa kwa baadhi ya wenye uwezo - huleta majivuno ambayo humfanya ajisahau kiasi kwamba hata yeye mwenyewe husahau maoni yake. Lakini anapopata mikasa ya kilimwengu, na kuvamiwa na upepo wa matatizo kutoka pande zote, ndipo pazia za majivuno na inda zinapofunguka mbele yao na nguvu za asili za Mwenyezi Mungu (Fitrah) na Tawhid (imani ya Mwenyezi Mungu mmoja) inapojitokeza. Historia inapiga mifano mingi ya watu kama hawa ambao maisha yalijaa ghiliba: 15


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:15 PM

Page 16

Tujifunze Misingi ya Dini Palikuwa na Waziri aliyekuwa na nguvu na uwezo mkumba katika enzi zake. Alikuwa na mamlaka yote na hakuna aliyempinga. Siku moja aliingia ndani ya mkutano uliokuwa umejaa wanavyuoni, aliwageukia Akasema: “Mpaka lini mtaendelea kudai kuwa Mwenyezi Mungu yupo, mimi nina dalili elfu za kupinga hayo.” Alisema na huku akijitapa sana, lakini wanavyuoni waliohudhuria hapo walitambua kwamba yeye si mtu wa hoja na mantiki, na kwamba uwezo na mamlaka aliyo nayo tu ndiyo yalimfanya ajione, kiasi ambacho hawezi kuathirika na ukweli wowote; Hivyo waliamua kunyamaza. Baada ya kupita siku kadhaa, waziri huyo alimfanyia ufidhuli bwana mmoja, hivyo mfalme aliyekuwa akitawala wakati ule aliamuru akamatwe na kufungwa gerezani. Mmoja kati ya wanavyuoni walikuwepo katika mkutano wa siku ile, aliona sasa umefika wakati wa kumzindusha waziri huyo, kwani alikuwa amekwishateremka juu ya farasi wa kifahari, pia hisia za kuukubali ukweli zimeamka ndani ya nafsi yake. Mwanachuoni huyo aliona kwamba iwapo atawasiliana naye na kumnasihi huenda akanufaika kwa nasaha zake. Hivyo aliomba idhini na akaruhusiwa kwenda kuonana naye. Alipoingia gerezani, alimkuta peke yake akizunguka mle ndani na kusoma beti za mashairi yenye maana ifatayo: “Sisi sote ni kama michoro ya simba iliyochorwa kwenye kitambaa cha bendera.Uvumapo upepo nayo hutingishika na hata kuonyesha kama inayoshambulia, lakini kwa kweli haina ifanyalo kwani ni upepo ndio unaotingisha. Halikadhalika sisi tunapokuwa na nguvu Mwenyezi Mungu ndiye anayetupa na atakapo hutunyang’anya.” Hapo yule mwanachuoni akagundua kwamba, katika hali hiyo, si kwamba waziri hakanushi kuwapo kwa mwenyezi Mungu tu, bali anamjua Mwenyezi Mungu vilivyo. Baada ya kusalimiana akamwambia: “Je 16


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:15 PM

Page 17

Tujifunze Misingi ya Dini unakumbuka siku ile uliposema kwamba una hoja elfu za kuthibitisha kutokuwepo kwa Mwenyezi Mungu? Kwa hiyo nimekuja kukujibu hoja zako nyingi kwa hoja moja tu, “Mwenyezi Mungu ndiye aliyekuvua madaraka yako uliyokuwa nayo.” Waziri akainamisha kichwa, akashindwa kujibu kwa sababu alikiri makosa yake baada ya kuhisi nuru ya Mwenyezi Mungu ndani ya nafsi yake. Allah swt. anasema katika Qur’ani:

“Hata kulipomfikia Firaun kuzama alisema: ‘Naamini kwamba hapana aabudiwaye kwa haki ila yule wanayemuamini wana wa Israil.’” (10:90).

SOMO LA SITA NJIA YA PILI YA KUMJUA MWENYEZI MUNGU

Njia ya nje: Kwa haraka haraka tunapotazama ulimwengu huu tunaoishi tutaona kwamba haukuumbwa shalabela au ovyo ovyo tu, aidha mambo yote yanakwenda sambamba kulingana na mielekeo yake sahihi kama ilivyopangwa. Mambo yote yaliyomo duniani ni kama jeshi kubwa lililogawanywa katika vikosi vilivyopagwa barabara na viendavyo sawa sawa kuelekea upande maalum.

17


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:15 PM

Page 18

Tujifunze Misingi ya Dini Sababu zifuatazo zinafafanua na kuondosha mashaka: 1. Ili kila kiumbe kidhihiri na kuendelea kuishi hapa ulimwenguni, ni lazima kuwepo na mpangilio wenye utaratibu wake maalum. Kwa mfano, ili upatikane mti ni lazima kuwe na maji, ardhi ifaayo na hali ya hewa inayolingana, kwa ajili ya kuupanda na kuunyunyuzia maji ili kila mbegu ipate kumea, kustawi na kukua vyema. Kwa hivyo ni lazima pawe na utaratibu huu, vinginevyo, hapatakuwa na tija nzuri ya kumea na kukua. Maandalizi ya taratibu hizi na uhakika wa mahitaji muhimu ya mwanzo, unahitaji akili na maarifa. 2. Kila kiumbe kina mambo yake maalum yanayokihusu pekee. Mathalan, moto na maji, kila kimojawapo kina mambo yake maalum yasiyoweza kutengana nacho, na hufuata utaratibu rasmi wa daima uliopangwa. 3. Viungo vyote vya viumbe hai vinafanya kazi pamoja kwa ulingano na ushirikiano. Kwa mfano, viungo vya mwili wa binadamu ambao wenyewe ni kama dunia, hufanya kazi pamoja kwa uwiyano maalum, inapotokea hatari itakayoudhuru mwili huo, viungo vyote huwa tayari kuuhami. Kwa hivyo uhusiano na ushirikiano huu ni dalili nyingine ya kuwapo kwa utaratibu maalum ulimwenguni. 4. Tazamo moja katika mandhari ya dunia linatosha kukudhihirishia kwamba, si viungo vya kiumbe hai ndivyo vinavyoshirikiana tu, bali hata viumbe vingine tofauti ulimwenguni hushirikiana. Kwa mfano ili kuvifanya viumbe vingine viendelee kuishi, jua huleta mwangaza, mawingu huleta mvua, na ardhi na mali asili zake pia hutoa mchango wake. Hayo yote ni dalili za wazi ya kuthibitisha kuwapo kwa utaratibu maalum ulimwenguni.

18


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:15 PM

Page 19

Tujifunze Misingi ya Dini Uhusiano katika utaratibu na akili Ukweli uko wazi katika akili ya kila mtu kwamba popote unapodhihiri utaratibu, ni dalili ya kuonyesha kwamba nyuma yake kuna akili, fikra, mpango na lengo. Kwa sababu binadamu anapoona utaratibu, kanuni maalum na mpangilio wa kimahesabu unavyokwenda sawa sawa atatambua kwamba kuwapo kwa yote kunategemea elimu na uwezo. Naye wala hahitaji hoja ya kuyajua haya (yako wazi). Binadamu anajua wazi kwamba kipofu au mtu asiyejua kuandika hawezi kuchapa insha ya kuvutia ya fasihi au kuandika maswala yanayohusiana na mambo ya jamii; pia mtoto mwenye umri wa miaka miwili hawezi kuchora picha nzuri ya thamani kwa kujichorea mistari tu juu ya karatasi. Hivyo, tunapoona insha au makala nzuri, moja kwa moja tunafahamu kwamba imendikwa na msomi, au tunapoona michoro mizuri bila shaka tutafahamu kuwa mchoroji hodari ndiye aliyechora, japo hatujakutana naye. Hivyo basi, popote penye utaratibu ulinaolingana, pana akili iliyo pamoja nao, na kadri utaratibu huo unavyokuwa mkubwa, sahihi na kuvutia, ndivyo elimu iliyouleta inavyokua zaidi. Wakati mwingine kanuni maalum katika fani ya hesabu za hali ya juu iitwayo “kanuni ya uwezakano” (Law of probabilities) hutumika, ili kuthibitisha usemi huu usemao kwamba kila utaratibu unahitaji kuwa na msingi wa elimu. Mathalan, iwapo mtu asiyejua kusoma anataka kuchapa au (kuandika) makala, insha, au shahiri kwa kubahatisha tu, kwa kubonyeza vidole vya taipureta atachukua mamilioni ya miaka kufikia lengo lake, muda ambao umri wa binadamu hauwezi kufikia. Mwenyezi Mungu amesema katika Qur’ani: “Tutawaonesha alama zetu katika pambizo na katika nafsi zao wenyewe mpaka iwabainikie 19


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:15 PM

Page 20

Tujifunze Misingi ya Dini kwamba haya ni ya kweli. Je haikutoshi kwa Mola wako kuwa yeye ni Mjuzi wa kila kitu?�

SOMO LA SABA MIFANO ITOKANAYO NA KUUMBA Utaratibu, lengo na mpango ni mambo yaliyo dhahiri ulimwenguni kote. Hivyo basi uwe mwangalifu wakati tukijaribu kuchimbua mifano yake. Tutakupigia mifano mikubwa na midogo: Kwa bahati nzuri, hivi maendeleo makubwa yaliyopatikana katika sayansi ya mali asili uvumbuzi wa siri na maajabu ya asili ya dunia, mizungu ya kuumbwa binadamu, wanyama na mimea, ya chembe-hai na utaratibu wa sayari; yote yametufungulia milango ya kumjua Mwenyenzi Mungu, kwa jinsi vinavyohusiana na upweke wa Mwenyezi Mungu, kwa jinsi vinavyofundisha kuhusiana na uumbaji mkuu, na hivyo kuondosha pazia inavyofahamika kutambulika kwa utaratibu wa viumbe vya dunia hii na vinaonyesha mkuu wa ulimwengu huu.

Makao makuu ya utawala wa mwili wako Mafuvu yetu yamejazwa kitu chenye rangi ya kijivu kitwacho ubongo. Ubongo unaunda taratibu sahihi katika miili yetu, kwa sababu unatawala nguvu zote za miili yetu na kusimamia vyombo vyote vya mpangilio wa miili yetu. Ili waweze kuelewa makao makuu haya, ni vizuri tukisimulia tukio lifuatalo: Magazeti yalichapisha habari kuwa mwanafunzi mmoja wa Shiraz aliyekuwa Khuzistan alipatwa na ajali ya gari na kuharibika ubongo wake, Hata hivyo baadaye alikuwa kama vile ambaye hakupatwa na lolote. Viungo vyake vyote vilikuwa timamu na vyenye nguvu, lakini jambo la kushangaza ni kwamba alisahau mambo yote aliyoyafanya katika siku zili20


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:15 PM

Page 21

Tujifunze Misingi ya Dini zopita. Akili yake ilifanya kazi barabara. Aliweza kusoma sawasawa, lakini kila alipowaona wazazi wake hakuweza kuwatambua. Alikuwa akishangaa sana aonyeshwapo mama yake. Baadaye walimchukua na kumpeleka kwao mjini Shiraz. Walimuonyesha kazi zake za usanii alizofanya na kuziangika kwenye kiambaza chumbani kwake, lakini alizitazama kwa mshangao na kudai kwamba ni mara ya kwanza kuziona. Katika uharibifu wa ubongo alioupata, ni dhahri kwamba zile chembe hai zinazounganisha mawazo na kumbukumbu kichwani, hazikuweza kufanya kazi tena, au kama fyuzi iliyokatika na kukata umeme ndivyo zilivyokatika kumbukumbu zake. Pengine kijifyuzi hicho kilichoacha kufanya kazi katika ubungo wake ukubwa wake haufikii hata ncha ya sindano, lakini athari kiliyoiacha katika maisha yake ni kubwa. Hapa inadhihiri jinsi ubongo wetu ulivyo muhimu. Bongo zetu zimegawanyika katika sehemu mbili: Ya kwanza ni sehemu inayotawala vitendo vyetu tuvifanyavyo kwa hiari kama kutembea kutazama, kusema, n.k. Ya pili ni ya vitendo visivyo vya hiyari ambavyo vinatawala harakati za moyo, tumbo, n.k. Endapo sehemu moja tu katika sehemu ya ubongo itaacha kufanya kazi, moyo au kiungo kingine pia kitasimama.

Moja kati ya viungo vya ajabu vya ubongo, ‘Cerebrum’ Kiini cha ubongo (Cerebrum) ndiyo makao ya matakwa, utambuzi na kumbukumbu. Kwa maneno mengine, ni vitendo vingi nyenye hisia katika ubongo, na vitendo vingine vyenye hisia za ndani vinavyofungamana nacho kama hasira, hofu na n.k. Kama tutakitoa kiini hicho kutoka kwa mnyama na tukaviacha viungo vingine kama vilivyo, atabaki hai lakini 21


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:15 PM

Page 22

Tujifunze Misingi ya Dini atakosa uwezo wake wa kufahamu. Kuna watu walifanya majaribio kama hayo, walikiondoa kiini hicho katika njiwa, basi alikuwa hai kwa muda, lakini hakuweza kula punje alizopatiwa japokuwa alikuwa na njaa. Aliporuhusiwa kuruka, aliruka mpaka akagonga nguzo na kuanguka.

Kumbukumbu ya ajabu Sehemu nyingine ya ajabu ya ubongo ni hisia za kumbukumbu. Je umepata kufikiri jinsi hisia zetu za kumbukumbu zilivyo? Je umeweza kufikiri jinsi hali yetu itakavyokuwa ngumu iwapo hisia yetu ya kumbukumbu itatolewa kutoka vichwani mwetu japo kwa muda wa saa moja tu? Kitu cha kumbukumbu kinachounda sehemu ndogo katika akili zetu ndipo pale kumbukumbu za maisha yetu yote zinazohifadhiwa. Mambo yote yanayohusiana na mtu tumjuaye kama ukubwa wa umbo, rangi, mavazi na tabia; yamefadhiwa katika sehemu zake maalum na kupangiwa jalada (faili) maalum, hivyo tunapokutana na mtu huyo, akili zetu humtafuta mara moja kutoka kwanye jalada lake na kupata kumbukumbu yote kumhusu, kisha akili yetu hutuamuru jinsi ya kukabiliana naye. Akiwa rafiki tutamheshimu, akiwa adui tutamchukia. Yote haya hufanyika kwa haraka mno kiasi kwamba haupiti muda. Maajabu zaidi ni pale tunapotaka kukumbuka kila tulichohifadhi na kukichora, kukiandika au kukirekodi katika kinasa-sauti (Tepu), bila shaka zitahitajika karatasi na tepu nyingi zinazoweza kujaa ghalani. Tunapotafuta mchoro au mkanda mmojawapo miongoni mwa wingi huo, tutahitajia makarani na wafanyakazi wengi, hisia zetu za kumbukumbu (kichwani) hufanya kazi zote hizo kiurahisi na kwa haraka zaidi.

22


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:15 PM

Page 23

Tujifunze Misingi ya Dini Vipi ‘Nguvu-asili’ isiyo na akili iumbe yenye akili? Vitabu vingi vimetungwa kuelezea juu ya maajabu ya ubongo wa mwanadamu. Je waweza kusadiki kwamba utaratibu huo sahihi, wa kiajabu, wenye kushangaza uwe umeumbwa na nguvu isiyo na akili? Mwenyezi Mungu anasema katika Qur’ani:

“Na katika ardhi kuna ishara (nyingi za kuonyesha kuwepo kwa Mungu) kwa wenye yakini. Na katika nafsi zenu pia (pia zimo) je hamuoni?” (51:20-21).

SOMO LA NANE ULIMWENGU WA MAAJABU KWENYE NDEGE MDOGO Katika somo hili tungelipenda utoke katika ulimwengu wa mwili wa mwanadamu ambao tumeugusia kidogo tu na utazame maajabu ya mpangilio wa maisha ya wanyama wengine. Hebu tutupe macho yetu angani katika giza la usiku, tutamuona ndege wa kipekee akitumia uwezo wake wote katika kujitafutia chakula, ndege huyu ni popo. Kwa hakika ulimwenguni kuna maajabu mengi, lakini kuruka wakati wa usiku ni miongoni mwa maajabu zaidi. Urukaji wa kasi wa popo gizani bila ya kugonga kitu chochote ni jambo lishangazalo mno kiasi ambacho mtu anapozidi kufanya utafiti ndivyo anavyozidi kila siku kugundua siri zingine. 23


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:15 PM

Page 24

Tujifunze Misingi ya Dini Popo huruka kwa mwendo wa kasi na uhodari zaidi ya njiwa anavyoruka wakati wa mchana. Hapana shaka kwamba kuna kitu kinachotambulisha vizuwizi katika mwendo wake. Kama si hivyo, ingelikuwa uzito wa kuruka kwa wepesi. Endapo atakuwa akirukaruka na kugeukageuka ndani ya shimo jembamba lenye giza na lililojaa moshi, basi ataweza kurukaruka humo bila ya kugonga viambaza vya shimo hilo, na bila ya kupatikana japo kiasi kidogo cha moshi juu mbawa zake. Uwezo huu wa ajabu unatokana na nguvu inayofanana na nguvu za ‘Rada.’ Kwa hivyo basi, si vibaya tujue ‘Rada’ ni nini, ili tuweze kuitambua jinsi ilivyo kwa mnyama huyu mdogo. Upande wa elimu ya Fizikia, katika maelezo ya aina mbalimbali za sauti, kuna mawimbi ya sauti ambayo yapo juu ya mawimbi ya sauti ya kawaida. Mawimbi haya ni yale ambayo masafa yake na frikwensi zake ni za hali ya juu sana kiasi ambacho masikio ya mwanadamu hayawezi kuyasikia ndipo yakaitwa mawimbi ya ‘Meta-sound.’ Mawimbi haya yanapofunguliwa kwa kutumia ‘Transimita’ yenye nguvu sana husafiri, na yanapokutana na kizuizi chochote mbele (kama ndege ya adui n.k.) hugonga na kurudi, kama vile mpira unapogonga ukuta na kurudi au kama sauti zetu tunaposema mbele ya mlima au ukuta mrefu, na kwa kutumia vipimo vya kujua muda gani sauti zetu zimechukua hadi kuturudia, ndipo tutaweza kupima masafa sahihi ya pale inapogonga. Kutokana na utaratibu kama huo ndege na meli huongozwa kwa kutumia ‘Rada’ na huzipeleka popote zinapotaka kwenda. Aidha hutumika kwa kutambua pale mahali meli ama ndege ya adui ilipo. Wataalamu wa Sayansi wanasema kwamba kiumbe hiki kidogo (popo) kina kitu kinachofanana na ‘Rada,’ wanatoa dalili kwamba endapo atawekwa ndani ya chumba kilichowekwa kipaza sauti cha kubadilisha mawibbi ya sauti yasiyo ya kawaida ‘Meta–sound waves’ na kufanya yawe ya kawaida yasiosikika basi kila sekunde (mara 30 hadi 60) mawimbi hayo ya 24


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:15 PM

Page 25

Tujifunze Misingi ya Dini sauti isiyo ya kawaida (Meta-sound) yatasikika. Sasa swali ni hili: ni chombo gani kwa popo kinachotoa mawimbi? Au ni chombo gani haswa kinachomwezesha popo kutoa na kupokea mawimbi? Katika kufafanua majibu ya swala hili, wataalamu wanasema, mawimbi haya hutoka kwenye mishipa ya koromeo yenye nguvu na kutolewa na miale ya pua yake. Na masikio yake nayo yanapokea sauti inaporudi. Hivyo basi, popo hutegemea zaidi masikio yake anaposafiri usiku. Mtaalamu mmoja wa kirusi anayeitwa Zurin amethibitisha – kupitia majaribio – kwamba, akiyaondoa masikio ya popo hatoweza kuruka na kukwepa vitu, lakini akiyaondoa macho yake, ataweza kuruka. Yaani popo haoni kwa macho, huona kwa masikio! Haya ni maajabu makubwa! Hebu fikiria, ni nani aliyeumba viungo hivi viwili vya shani ndani ya mwili wa mnyama huyu mdogo? Alimfundisha vipi jinsi ya kuvitumia? Na vipi anavyoweza kuepuka hatari zilizopo usiku anaporuka? Muumba ni nani? Je ni nguvu-asili? (Nature) inaweza kufanya (kuumba) hivi? Je, inaweza kutengeneza vifaa hivi viwili ambavyo wanasayansi watoa juhudi na gharama nyingi kuvitengeneza? Akimtaja popo Imam Ali (a.s) anasema katika Nahjul-balagha: “Kiza cha usiku hakiwezi kumzuia popo asitembee, utukufu wote ni wa Mwenyezi Mungu aliyeumba kila kitu bila kuiga mfano wa kitu kingine.’’(Khutba no.155).

25


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:15 PM

Page 26

Tujifunze Misingi ya Dini

SOMO LA TISA MARAFIKI WAWILI WA KALE Hebu fanya siku moja – katika majira yanapokaribia kiangazi – utembelee mbugani au shambani utaona aina mbalimbali za wadudu kama nyuki, nzi, vipepeo na mbu wanaoruka kimya kimya kutoka katika ua moja hadi jingine katika tawi hili na lile. Katika hali hiyo, huwa wanashughulika sana, kiasi ambacho mtu anaweza kudhani kwamba kuna mwajiri anayeangalia utendaji wao wa kazi na kuwatuma mfululizo. Huku miguu yao ikiwa imefunikwa na mbelewele (unga unga) za maua, zikiwafanya waonekana kama wafanyakazi waliovalia magwanda ya kazi, na kwa mapenzi na kutilia maanani, wanaendelea na kazi yao. Kwa kweli wadudu wana kazi muhimu na kubwa sana, ndipo Profesa Leon Briton akasema, “Si watu wengi wanaotambua kwamba, kama si kazi inayofanywa na wadudu, vikapu vyetu vya matunda vingelikuwa vitupu.” Nasi twaongeza, “Pia mabustani na mashamba yetu yangalikosekana.” Hivyo basi, wadudu, bila shaka, ndio wakuzaji wakubwa wa matunda na watayarishaji wa mbegu za maua. Huenda ukataka kujua sababu. Sababu ni kwamba kazi muhimu ya uhai wa maua hufanywa kwa msaada wa wadudu. Pengine umepata kusikia kwamba, maua ni kama baadhi ya wanyama ambayo yana pande mbili, ya kiume na ya kike, na tija inayopatikana kutokana na uhusiano huo, ndipo hutupatia mbegu na matunda. Hata hivyo, je umeshawaza jinsi pande mbili za maua zinavyovutiana? Kwa kawaida kazi hii hufanywa na wadudu, baina kwa upande mwingine pia ni 26


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:15 PM

Page 27

Tujifunze Misingi ya Dini kazi ya upepo, hata hivyo, hii si kazi rahisi kama tunavyodhani. Ndoa hii muhimu ya baraka ambayo wadudu hujihusisha kwa kuiunganisha, ina masimulizi na maelezo marefu ambayo tutayataja hapa kwa kifupi.

Marafiki vipenzi wa kale Wataalamu wa elimu ya sayansi na mali-asili baada ya utafiti wao walisema kwamba maua na mimea ilidhihiri katika awamu ya pili katika enzi za kuumbwa dunia, jambo la kushangaza ni kwamba, wadudu pia walidhihiri katika enzi hizo hizo. Viumbe hivi viwili daima vimekuwa marafiki, wenye kuaminiana na kukidhiana mahitaji. Maua huhifadhi majimaji matamu ili kuuvutia na kuzidisha uhusiano. Wanapoingia ndani ya maua kwa ajili ya kuhamisha mbegu za kiume na kutayarisha ndoa na utungaji mimba; nayo maua, kwa makusudi, hutoa utamu wake kwao, utamu huo wa sukari wenye thamani una ladha nzuri sana kwa wadudu, hivyo huwafanya wavutike nao. Baadhi ya wataalamu wa maua wanaamini kwamba rangi na harufu nzuri ya manukato ya maua pia vina umuhimu mkubwa katika kuwavutia wadudu. Majaribio mbalimbali yaliyofanyiwa nyuki, yamethibitisha kwamba wana uwezo wa kutofautisha rangi na harufu za maua. Kwa kweli, hayo maua huwa na harufu nzuri kwa ajili ya kuwavutia vipepeo na nyuki. Wadudu huukubali mwaliko huo na kwa haraka sana huanza matayarisho ya harusi (kuoanisha mbegu) na kula chakula cha harusi. Utamu huu wa chakula cha harusi ni wa aina ya sukari inayochukuliwa kuwa ndiyo chakula kipendwacho sana na wadudu, hasa nyuki, unapohifadhiwa mahali pamoja, hugeuka kuwa asali. Basi wadudu wanapohud27


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:15 PM

Page 28

Tujifunze Misingi ya Dini huria harusi na kula chakula cha harusi, na chengine huchukua nyumbani kuweka akiba na kuhifadhi kwenye masega yao. Huu ndio uhusiano wa urafiki na mapenzi ambao msingi wake ni faida ya vyote viwili, uhusiano ambao daima utaendelea kuwapo baina ya wadudu na maua.

Somo linalohusiana na Upweke (Tawhid) Mwanaadamu anapofanya utafiti juu ya vifungu vya maajabu katika maisha ya wadudu na maua, atajiuliza, ²Nani aliyeanzisha uhusiano huo wa mapenzi na urafiki kati ya wadudu na maua? Ni nani aliyeyapa maua rangi hizi za kupendeza, uzuri na harufu inukiayo vizuri? Ni nani aliyefanya wadudu wayafuate? Ni nani aliyewapa wadudu miili mikubwa na midogo wadudu, vipepeo na nyuki ili wajitayarishe na kazi ya kuziunganisha mbelewele za maua?” Kwa nini maisha ya maua na ya wadudu yameanza wakati mmoja duniani? Hivi mtu yeyote hata awe mshindani yapo bila ya utaratibu wowote? Na kanuni ya “Nguvu-asili” isiyo na akili ilete mandhari haya ya ajabu? Kamwe haiwezekani, Mwenyezi Mungu swt. anasema:

“Na Mola wako akamfahamisha nyuki ya kwamba, jitengenezee majumba yako mlimani na mitini na katika yale (majumba) wanayojenga (watu).’ Kisha kula katika matunda, na upite katika njia za Mola wako zilizofanywa nyepesi (kuzipita).” (16:68-69).

28


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:15 PM

Page 29

Tujifunze Misingi ya Dini

SOMO LA KUMI ULIMWENGU WA VITU VIDOGO Kwa sababu tunaishi katika ulimwengu wa maajabu wa viumbe na tumevizoea, si rahisi kwetu kufahamu umuhimu wa maajabu yake mengi kama vile: 1. Wadudu na vijinyama vidogo vidogo tunavyoishi navyo ambavyo lau vitapimwa havitafika hata milimita mbili, lakini maumbile yao ni kama wanyama; vina mikono, miguu, macho, masikio, pia vina hata ubongo, mishipa ya fahamu na matumbo ya kusagia chakula! Tukiweka ubongo wa mdudu chungu kwenye darubini maalum ya kutazamia vitu vidogo, na kuchunguza kwa makini umbo lake la ajabu, tutaona jinsi alivyo na kijimwili cha ajabu na cha kuvutia. Ubongo huo una sehemu mbalimbali ambazo zimepangwa moja baada ya nyingine, kila sehemu mojawapo inaamuru kiungo fulani katika kijimwili cha mdudu huyo, na endapo patatokea mabadiliko kidogo tu katika sehemu hizi, basi yatapoozesha sehemu ya kijimwili chake. La kushangaza zaidi ni ubongo wake ulio mdogo zaidi kuliko ncha ya pini, ambapo hapo ndipo penye ulimwengu uliyokusanya utambuzi, busara, hisia ya ladha na usanii. Ndipo kikundi cha wataalamu hupoteza miaka mingi katika maisha yao wakichunguza vijinyama hivi, na hatimaye huandika maelezo yanayovutia katika vitabu vyao. Je aliyeumba utambuzu wote huu busara na ladha kwa kujinyima kidogo, anaweza kuwa ni nguvu-asili ambayo yenyewe haina hata kiasi cha ujuzi na busara cha ukubwa ncha ya sindano?

29


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:15 PM

Page 30

Tujifunze Misingi ya Dini Tukiangalia katika ulimwengu wa vitu vya ajabu, tutaona kwamba kiumbe kidogo zaidi kinachotambulika ulimwenguni hivi sasa ni ‘chembe’ ndogo sana ya tonoradi ijulikanayo kwa lugha ya kigeni kama ‘Atom.’ Ni kitu kidogo mno, hata darubini kali iwezayo kukigeuza kipande kidogo sana kionekane kikubwa kama mlima, haiwezi kuionyesha ‘Atom.’ Ukitaka kujua udongo wa ‘Atom’ ulivyo, ni kwamba tone moja la maji lina ‘Atom’ nyingi kuliko idadi ya watu wote wanaoishi duniani. Ikiwa tunataka kuzihesabu ‘Proton’ zilizomo katika sentimita moja tu ya waya mwembamba na kuna watu elfu moja wa kutusaidia, na kufanya kila sekunde moja tutoe ‘proton’ moja tu yaani kwa sekunde moja, watu elfu moja tutakuwa tumetoa ‘proton’ elfu moja. Hata hivyo ingelituchukua miaka mia tatu zaidi, usiku na mchana kuzihesabu (na hii itategemea na idadi ya ‘ Atoms’ zilizomo). Sasa bila shaka umeshafahamu kwamba, sentimita moja ya waya mwembamba ina ‘Atom’ nyingi sana. Hivyo basi, Hebu fikiria kuna ‘Atom’ ngapi zilizopo mbinguni, duniani, angani, kwenye nyota, sayari na kwenye jamii ya nyota?

‘Atom’ (chembe za tonoradi) zinazotufundisha Tawhid Tunaposoma habari za ‘Atom’ ambayo ni mjadala muhimu sana wa kisayansi siku hizi, hutupa somo zuri za kufaa katika ‘Tawhd,’ kwa sababu ulimwengu wa ‘Atom’unatufanya tuzielekeze fikra zetu katika mambo manne:

Mpangilio usio wa kawaida Mpaka sasa (tunapondika kitabu hiki) katika elimu ya fizikia kuna ‘Element’( maada za kifizikia zinazogawanyika) zipatazo zaidi ya mia moja zilizogunduliwa ambazo zilianza kujitokeza kidogo kidogo kutoka kwenye ‘Electron’ moja na kuzaana hata kufika mia moja. Mpangilio huu 30


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:15 PM

Page 31

Tujifunze Misingi ya Dini wa ajabu kamwe hauwezi kuletwa na kitu kisicho na akili.

Nguvu ya uwiyano Tunafahamu kwamba nguvu mbili za umeme zinavutana. Hivyo basi, Electroni ambazo ni ‘Negative’ huwa zinavutana na ‘Nucleus’ ambazo ni ‘Positive.’ Kwa kuongezea ni kwamba ule mzunguko ‘Encirclement’ kwa ‘Electron’ unazunguka ‘Nucleus’ husababisha nguvu ya msukumo iitwayo ‘ Repulsive’. Kwa hiyo nguvu hii inapovuta, inafanya ‘Electron’ zikatike kutoka kwenye mazingira ya Ki-atom (yaani hazishikani) kwa sababu hiyo, ‘Atom’ hutengwa na nguvu yake hutoka kuzivuta ‘Electron’ na kuziharibu. Hapa ndipo mtu huona jinsi ‘Nguvu ya msukumo’ na ‘nguvu ya mvutano’ zilivyopangwa kwa njia sahihi kwenye ‘Atom’ kiasi kwamba, ‘Electron’ hazikimbii (kusukumwa) wala hazivutiki bali siku zote ziko sawa tu, zikiendelea na nyendo zake. Je inawezekana “Nguvu–asili” kiziwi au pofu kufanya uwiyano huu uwepo?

Kila moja ina njia yake Tumeshasema hapo awali kwamba ‘Atom’ zina ‘Electron’ zote hazizunguki kwenye mzunguko (circuit) mmoja (kama inavyoonyesha kwenye picha maalum ya X-ray wakati wa somo la fizikia). Umbali wake uko katika mizunguko mingi, na kila ‘Electron’ ina umbali wake, kila moja iko kwenye eneo lake na mwendo wa kasi maalum. Huenda kwa mamilioni ya miaka pasi na kupingana. Je ni kazi rahisi kuweka vitu vyote hivi kwa mzunguko, mwendo wake maalum na utaratibu huo wa ajabu?

31


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:15 PM

Page 32

Tujifunze Misingi ya Dini Nguvu kubwa ya ’Atom’ Ili kufahamu nguvu kubwa ya ‘Atom’ hebu tazama mfano huu: Mnamo mwaka 1945 bomu la majaribio la ‘Atomic’ lililipuka katika jangwa la Mexico ambalo halikuwa na maji wala mimea. Bomu hilo lililokuwa limewekwa juu ya nguzo ya chuma, lilisababisha kuyeyuka kwa nguzo hiyo, mlipuko na umeme mkubwa uliambatana na sauti ya kutisha. Wataalamu walipokwenda kulitafuta muda mfupi baadae hawakupata kitu chochote. Katika mwaka huo huo wamarekani walilipua mabomu kama hayo nchini Japan katika miji ya Nagasaki na Hiroshima. Mjini Nagasaki, watu elfu thelathini waliuwawa na wengine wengi kujeruhiwa, na hivyo kuifanya Japan kusalimu amri bila masharti yoyote katika vita hivyo. Je kwa kuichunguza ‘Atom’ hakutoshi kumfanya mwanadamu kujua ukuu wa Muumba wa ulimwengu? Inawezekana kusema kwamba kama ulivyo uwingi wa ‘Atom’ zilizomo duniani, pia kuna sababu nyingi za kuthibitisha kuwapo kwa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu anasema:

“Na lau kama miti yote iliyo ardhini ingelikuwa kalamu, na bahari hii (ikafanywa wino), na kusaidiwa na (kuongezwa maji) na bahari nyingine saba, ingekwisha bahari, maneno ya Mwenyezi Mungu yasingelikwisha…”(31:27). (Mifano hii hueleweka zaidi na mtu alisoma elimu ya Fizikia).

32


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:15 PM

Page 33

Tujifunze Misingi ya Dini

MAELEZO YA MWISHO YA SOMO LA KUMI UTUKUFU ULIOJE WA SIFA ZA MWENYEZI MUNGU Sifa zake Elewa ya kwamba kwa kiasi, kufahamu kuwapo kwa Mwenyezi Mungu kupitia kwa siri za ulimwengu ni jambo sahali, lakini ni vigumu sana kuzisoma sifa zake, na kunahitaji uangalifu mkubwa. Huenda ukashagaa na kutaka kujua kwa nini iwe hivyo. Sababu iko wazi, ni kwamba Mwenyezi Mungu hafanani na kitu chochote tulichopata kukiona ama kukisikia. Hivyo basi, sharti la kwanza la kumjua ni kumtenganisha na kiumbe chochote cha ulimwengu wa ki-maada. Hapa ndipo inakuwa vigumu kufahamu, kwa sababu tumekulia ndani ya ‘asili’ hii. Tumehusika na kuzoeana nayo kila siku, hivyo basi, daima tunaelekea kukilinganisha na kila tukionacho. Yaani chochote tukionacho kina umbo la kimaada. Yaani viumbe vyenye muda na mahali maalum. Kwa sababu hii, inakuwa na vigumu sana kumfahamu Mwenyezi Mungu asiye na macho, muda na mahali: na wakati huo huo yuko mahali pote, nyakati zote na asiye na mipaka. Hivyo basi, hili ni jambo linalohitaji uangalifu mkubwa. Lakini ni muhimu tujikumbushe kwamba hatutaweza kujua asili hasa ya Mwenyezi Mungu, na tusitegemee kwamba tutaweza kufanya hivyo, kwani matarajio hayo ni sawa na kutarajia kuijaza bahari na bilauri, au kutegemea mtoto aliye tumboni ajue mambo yote yaliyoko ulimwengu ulio nje ya tumbo la mama yake. Je yawezekana haya?

33


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:15 PM

Page 34

Tujifunze Misingi ya Dini

SIFA ZA UTUKUFU NA UZURI Kwa kawaida tunazigawanya sifa za Mwenyezi Mungu katika mafungu mawili: Sifa alizo nazo na sifa asizokuwa nazo? Hapa pana swali, je sifa ngapi za dhati alizo nazo? Jibu ni kwamba, kwa upande mwingine, zinaweza kujumuishwa katika sifa moja kwa sababu zinaweza kufupishwa kama ifuatavyo: Dhati ya Mwenyezi Mungu ni dhati isiyo na mwisho kwa pande zote, na ni yenye ukamimilifu wote. Kwa upande wa sifa asizokuwa nazo zinafupishwa hivi: Dhati ya Mwenyezi Mungu ni dhati isiyo na upungufu kwa vyovyote. Lakini pia kwa kuwa ukamilifu na upungufu una viwango vyake, yaani tunaweza kusema kwamba, Mwenyezi Mungu ana sifa za ukamilifu zisizokwisha na pia sifa zisizomstahiki hazina mwisho, kwa sababu ukamilifu wowote utakaofikiria, yeye anao. Na upungufu wowote utakaouwaza, yeye hana. Kwa hivyo, sifa zinazomstahiki na zisizomstahiki hazina kikomo. Sifa mashuhuri za Mwenyezi Mungu Sifa mashuhuri za Mwenyezi Mungu ni hizi: Mjuzi ‘Alim’: Yeye ni mjuzi wa kila jambo. Muweza ‘Qadir’: Ni Muweza wa mambo yote. Mwenyezi Mungu ni ‘Hai’: kwani kila aliye hai ana utambuzi na uwezo, na kwa kuwa Mwenyezi Mungu ana sifa hizo mbili basi yeye ni Hai. Mwenye matakwa ‘Murid’: Yaani ana hiari na halazimishwi kufanya jambo, na lolote alifanyalo lina lengo na busara, hata jambo dogo lililopo duniani lina hekima na lengo. Mtambuzi ‘Mudrik’: Yaani Mwenyezi Mungu hutambua mambo yote. 34


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:15 PM

Page 35

Tujifunze Misingi ya Dini Huona kila kitu husikia kila kitu na hujua yote. Asiye na mwanzo na wa milele ‘Qadim na Azal’: Maana yake ni kuwa, daima alikuwapo, na kuwapo kwake hakuna mwanzo kwani kunatokana na Dhati Yake, kwa sababu hii yeye ni mwanzo na wa milele kwa kuwa mwenye kupatikana kwa dhati yake hawezi kutokuwepo na kutoweka. Msemaji ‘Mutakallim’: Maana yake ni kwamba anaweza kuunda mawimbi ya sauti hewani yakazumgumza na Mtume wake. Hii haina maana kwamba Mwenyezi Mungu ana ulimi, mdomo na koo. Mkweli ‘Swadiq’: yaani lolote asemalo ni kweli, kwani uongo husababishwa na ujinga, udhaifu, ama kutokuwa na uwezo. Na ni muhali kwa Mungu aliye Mjuzi, Mwenye uwezo kusema uongo.

Na sifa ‘ zisizomtashiki’ ni: 1. Kuwa mwenye tabaka; hakutengeneza kwa mchanganyiko wa nyenzo, kwani kama ingelikuwa hivyo, angelihitaji nyenzo zingine, ambapo yeye si mhitaji. 2. Mwenyezi Mungu si mwili, kwani kila mwili una mipaka yake, una mabadiliko na hutoweka. Mwenyezi Mungu haonekani, kwa maana hiyo, lau angelionekana, angelikuwa na mwili, muda maalum na angelitoweka. Hana makazi, kwani yeye si mwili hata ahitajie makazi. Hana mshirika, kama angelikuwa naye, angelikuwa ni kiumbe chenye kikomo, kwani viumbe viwili visivyo na kikomo haviwezi kuwepo, isitoshe umoja wa kanuni za kidunia unathibitisha upweke wake. Hana umaana; yaani sifa zake ndiyo dhati yake. 35


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:15 PM

Page 36

Tujifunze Misingi ya Dini Mwenyezi Mungu si muhitaji bali mwenye kujitosheleza. Ni tajiri na ana kila kitu, elimu isiyokwisha, uwezo wa vitu vyote havipungui. Anasema katika Qur’an: “Hana mfano wa chohote.” (42:11).

36


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:15 PM

Page 37

Tujifunze Misingi ya Dini

TUUJUE UADILIFU (2)

37


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:15 PM

Page 38

Tujifunze Misingi ya Dini

SOMO LA KWANZA UADILIFU NINI? Kwa nini sifa ya Uadilifu wa Mwenyezi Mungu ambayo ni moja kati ya sifa zake, inazingatiwa kuwa ni sehemu ya misingi ya dini? Ni nini tofauti kati ya ‘Uadilifu’ na ‘usawa’? 1. Kwa nini uadilifu umechaguliwa pekee miongoni mwa sifa zingine za Mwenyezi Mungu? Kabla ya kuzama katika upekuzi huu ni lazima tufahamu kwa nini wanavyuoni wameichukulia sifa ya uadilifu, ambayo ni moja kati ya sifa za Mwenyezi Mungu, kuwa ni msingi miongoni mwa misingi mitano ya dini. Mwenyezi Mungu ana sifa nyingi, miongoni mwazo ni: Mjuzi, Mwenye nguvu, Mwadilifu, Mwenye hekima, Mwingi wa Rehma, Mwenye kurehemu, wa kale, wa milele, Muumba na Mwenye kuruzuku: lakini kwa nini uchaguliwe uadilifu miongoni mwa sifa hizi na kuwa ni moja kati ya misingi mitano ya dini? Kwa kujibu swali hili muhimu, hapana budi tuzielewe baadhi ya sababu: Ya kwanza: Uadilifu ni sifa muhimu miongoni mwa sifa za Mwenyezi Mungu kiasi ambacho sifa zake nyingi zarejea kwenye sifa hizi, kwa sababu uadilifu, kwa ujumla una maana ya kuweka mambo mahali pake, Mtoaji riziki, Mwingi wa rehema na nyingine kama hizo, hutegemea sifa 38


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:15 PM

Page 39

Tujifunze Misingi ya Dini ya uadilifu. Ya pili: Kama vile ambavyo kufufuliwa kunategemea (ni kwa ajili ya) ‘Uadilifu’ wa Mwenyezi Mungu, pia ujumbe wa Mwenyezi Mungu na majukumu waliyopewa maimamu yanategemea Uadilifu wake. Ya tatu: Mwanzoni mwa Uislamu palitokea tofauti ya maoni kuhusiana na suala la uadilifu wa Mwenyezi Mungu nayo ni: Kikundi kimoja cha Waislam cha ‘Ash’ari’ kilikataa kata kata uadilifu wa Mwenyezi Mungu na kusema kuwa ‘Uadilifu’ na ‘Uonevu’ havina maana yoyote kuhusiana na Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye Mtawala wa viumbe vyote vya duniani, ni vyake na kila alifanyalo hulifanya kwa uadilifu. Kikundi cha Ash’ari hakikuamini hata wema na uovu unaotambuliwa kiakili. Wanasema: “Akili zetu pekee haziwezi kupambanua kati ya ubaya na, hata uzuri wa kufanya jambo zuri na ubaya wa kufanya baya…” na makosa mengi mengine kama haya. Kuna wengine katika masunni waitwao ‘Mu’tazila’ wao pamoja na Mashi’a wanaamini Uadilifu wa Mwenyezi Mungu kuwa ni katika misingi ya dini na wanaamini kuwa Mwenyezi Mungu hafanyi dhuluma. Ili kuweza kuyatofautisha makundi haya mawili, kundi la pili pia liliitwa ‘Adiliyah’ kwa vile ‘Uadilfu’ (adl) waliuzingatia kuwa ni mojawapo ya misingi ya dini. Kundi la kwanza liliitwa ‘Ghair Adiliyah’ (Kinyume cha hilo la kwanza). Mashi’a ndio hilo kundi la pili (Adiliyah) ili Mashi’a wajitofautishe na ‘(Adiliyah) wengine, walizingatia Uimamu kuwa ni moja kati ya misingi ya dini, kwa hivyo panapokuwa na mjadala kuhusu ‘uadilifu’ na ‘Uimamu’ marejeo yake ni madhehebu ya Shi’a Imamiyya.

Ya nne: Kwa kuwa matawi ya dini ni miale tu ya misingi ya dini na kwam39


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:15 PM

Page 40

Tujifunze Misingi ya Dini ba mwale wa Uadilifu wa Mwenyezi Mungu una athari kubwa katika jamii ya watu, basi uadilifu umekuwa ni msingi muhimu katika jamii. Kuchaguliwa ‘Uadilifu’ kuwa ni mojawapo ya misingi ya dini kunakusudiwa kuimarisha uadilifu katika jamii ya watu na kupambana na aina yoyote ya dhuluma. Kama ilivyokuwa umoja wa dhati ya Mwenyezi Mungu, sifa zake na kumwabudu ni nuru Iliyolingania kwenye umoja kwa watu ili wawe sawa, pia uongozi wa Mitume na Maimamu umekuwa ni kielelezo cha uongozi wa kweli katika jamii ya watu. Kwa hivyo basi, msingi wa Uadilifu wa Mwenyezi Mungu ulimwenguni pote ni dalili ya haja ya kuwapo kwa uadilifu katika maeneo yote ya wanaadamu. Asili ya uumbaji wa ulimwengu ni uadilifu wa Mwenyezi Mungu, kwani jamii ya wanadamu haiwezi kuwapo bila ya Uadilifu.

1. Uadilifu ni nini? Uadilifu una maana mbili tofauti: Kwanza: Maana pana ya neno hili - kama tulivyosema hapo awali - ni ‘kuweka kila kitu mahali pake inavyostahili’. Yaani kuweka sawa sawa kwa uwiano. Maana hii ndiyo inatawala ulimwenguni kote kama vile kwenye mkusanyiko wa nyota, kwenye chembe za ‘Atom’ kwenye umbo la mwanadamu, mimea pamoja na wanyama wote, na hii ndio maana iliyokuja katika maneno ya Mtume Muhammad (s.a.w.w.) aliposema: “Kwa maana halisi ya Uadilifu ndipo mbingu na ardhi zikawapo.”

Mathalan, lau kama ‘nguvu ya mvutano’ (Attraction) na ‘nguvu ya msuku40


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:15 PM

Page 41

Tujifunze Misingi ya Dini mo’ (Repulsion) zilizoko duniani zitakosa kulingana na mojawapo kati ya hizo itaondolewa ama kuharibiwa, dunia ingevutwa upande wa jua na kuteketea, au ingeacha mzunguko wake na kuzunguka katika pambizo za ulimwengu zisizo na mwisho, na hatimaye kuharibika kabisa. Ikiwa utaumwagilia maji mti wa waridi na miti ya matunda, basi utakuwa umeyaweka maji mahali pake; na huo ni uadilifu. Lakini ukimwagila maji miba na magugu utakuwa umemwaga mahali ambapo si pake; na huo ni udhalimu. Pili: Maana nyingine ya ‘uadilifu’ ni kuchunga haki za watu, na kinyume chake ni ‘udhalimu’ na upendeleo kwa maana ya kuchukua haki za watu wengine na kuwapa wengine, au watu wengine kupewa haki zao na wengine kunyimwa. Ni wazi kwamba maana hii ya pili tuliyoitaja ni maana ‘mahsusi’ na ile ya kwanza ni ya ‘ujumla’. Vilevile ni lazima ifahamike kwamba maana zote hizo mbili zasadikisha ukweli wa Mwenyezi Mungu, hata hivyo, maana hiyo ya pili ndiyo tutakayoizungumzia zaidi hapa. Maana ya ‘Uadilifu’ wa Mwenyezi Mungu ni kuwa hanyang’anyi haki za mtu, hachukui haki za mtu na kumpa mwingine, wala hapendelei. Yeye ni mwadilifu, kwa maana yote ya neno lenyewe. Hoja za kuthibitisha uadilifu wake tutazitaja katika somo lijalo. Mwenyezi Mungu ametakasika na (hawezi kufanya) dhulma iwe ni kwa kunyang’anya haki za mtu, kumpokonya zake na kumpa mwingine au kwa kwa kubagua. Hamwadhibu mtenda mema, wala hamlipi mema mkosefu, na hamtii makosani mtu yeyote kwa makosa yaliyofanywa na mwengine. Vile vile hauchomi (mti) mbichi na mkavu pamoja.

Hata kama jamii yote ya watu itatenda madhambi ila mtu mmoja tu, basi 41


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:15 PM

Page 42

Tujifunze Misingi ya Dini Mwenyezi Mungu atamtenganisha kutokana na hesabu ya wengine wote, na hatamwadhibu kama atakavyowaadhibu hao wengine. Ama wanavyosema ‘Maash’ari’ kwamba, “Hata kama Mwenyezi Mungu atawatia motoni Mitume na kuwatia peponi waovu huo si uonevu” ni maneno ya upotofu, machafu na yasiyo na misingi, na kila mwenye akili anafahamu upotofu huo.

3. Tofauti iliyopo kati ya ‘Uadilifu’ na ‘Usawa’ Jambo jingine muhimu kufahamika katika somo hili ni kwamba, kuna wakati ambapo maana hukanganya kati ya ‘Uadilifu’ na ‘usawa’ ambapo makusudio yake si hivyo. ‘Uadilifu’ siyo sharti la kupatikana ‘usawa’, bali uadilifu katika kuchunga haki, na kupewa nafasi ya kwanza lazima kuangaliwe sana. Kwa mfano, Uadilifu darasani kati ya mwanafunzi, hauna maana kwamba wote wapate alama sawa, au uadilifu kati ya wafanyakazi wawili, sio kwamba wapate mishahara sawa, bali uadilifu hapa ni kuwa kila mwanafunzi apate alama kulingana na fahamu na uwezo wake kimasomo, aidha kila mfanyakazi alipwe mshahara wake kulingana na juhudi na utendaji wake wa kazi. Kadhalika, katika ulimwengu uadilifu una maana pana kama ulivyo. Mathalan, ikiwa moyo wa nyangumi wenye uzito wa tani moja uwe sawa na moyo wa ndenge ambao pengine hauzidi hata gramu moja, bila shaka hapatakuwa na uadilifu, au mizizi ya mti mkubwa ilingane na mizizi ya mti mdogo huo si uadilifu bali ni uonevu. Hivyo basi, uadilifu ni kuwa, kila kiumbe kipate haki yake kulingana na uwezo wake.

42


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:15 PM

Page 43

Tujifunze Misingi ya Dini

SOMO LA PILI DALILI ZA UADILIFU WA MWENYEZI MUNGU Wema na uovu Tumeshaona kuwa suala hili ni muhimu kwamba akili zetu zitofautishe baina wema na uovu kwa kiasi kikubwa. Hivi ndivyo wanavyuoni wanavyoeleza kulingana na istilahi ya ‘uzuri na uovu wa kiakili.’ Mfano, twajua kwamba uadilifu na wema ni mambo mazuri, na dhulma na ubahili ni mambo mabaya, tulifahamu ilivyo hata kabla dini haijasema, hata hivyo kuna mambo mengine yaliyopo ambayo akili zetu haziwezi kufahamu, hivyo yatupasa tuhitaji msaada wa uongozi utokao kwa Mwenyezi Mungu na Mitume. Kwa hivyo, ikiwa kikundi cha waislamu cha Ash’ar kinakanusha wema na uovu unaotambuliwa kiakili kutofautisha mambo mawili hayo na kudhani kwamba dini ilileta suala la uadilifu na udhalimu, basi kikundi hicho kimekosa kabisa, kwa sababu, ikiwa akili zetu haziwezi kuchagua baya (tukaliepuka) na zuri (tukalifanya) tutajuaje kama Mwenyezi Mungu angetuma au asingetuma ujumbe wake wa Manabii waongo? Lakini tunaposema kuwa kusema uongo ni kosa, basi haiwezekani Mwenyezi Mungu aseme uongo. Tunajua pia kuwa ahadi za Mwenyezi Mungu daima ni za kweli, na kwamba yeye ni mkweli, kwa hivyo hawezi kuunga mkono uongo na hawezi kumpa mtu mwongo uwezo wa kufanya miujiza. Hapa ndipo tunategemea vile dini na sharia ya Mwenyezi Mungu inavyosema. Na tunajumuisha kwamba kuamini kuwa wema na uovu unatambuliwa kiakili ni jambo la 43


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:15 PM

Page 44

Tujifunze Misingi ya Dini kidini. Hebu turudi kwenye dalili za uadilifu wa Mwenyezi Mungu. Ili tuweze kufahamu, yatupasa tujue mambo yafuatayo:

2. Nini chimbuko la udhalimu? Chimbuko la udhalimu ni moja kati ya mambo haya yafuatayo: Kwanza: Kutojua, wakati mwingine utokea kwamba dhalimu huwa hajui hasa alifanyalo, hajui kama anaharibu haki za wengine. Pili: Kuhitaji, mara nyingi mtu hutamani kitu cha mtu mwingine hapo hushawishiwa na shetani, ambapo kama asingekuwa muhitaji, asingedhulumu. Tatu: Uchoyo, chuki na kulipiza kisasi, hutokea mara nyingine kuwa huenda dhuluma isisababishwe na sababu tulizozitaja hapo juu, ila ni kwa sababu ya uchoyo, kutaka kulipiza kisasi, na chuki ndiyo iliyomfanya mtu adhulumu haki za wengine, au pia mtu kupenda kumiliki peke yake husababisha dhuluma kwa wengine. Nne: Kushindwa kujizuia: Wakati wingine mtu hataki kupunja haki za wengine, lakini kwa kuwa hawezi kujizuia, kufanya hivyo ndipo hudhulumu. Lakini waelewa ya kwamba Mwenyezi Mungu hana sifa mbaya kama hizi, kwa sababu yeye ni Mjuzi wa mambo yote, hana haja na chochote, mwenye uwezo juu ya kila kitu na ni mwema kwa viumbe vyote, kwa ajili hiyo hawezi kutenda dhuluma. Mwenyezi Mungu ambaye daima yuko, hana mwisho, ukamilifu wake hauna mpaka, tunachotaraji kutoka kwake ni wema, uadilifu na huruma.

44


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:15 PM

Page 45

Tujifunze Misingi ya Dini Atakapowaadhibu watenda madhambi, basi ni kwa ajili ya makosa yao, kama ambavyo mtu hupatwa na maradhi na hufa kwa kutumia madawa ya kulevya na pombe. Qur’ani yasema: “Hamtalipwa ila kwa yale mliyokuwa mkiyachuma.”

Qur’ani na Uadilifu wa Mwenyezi Mungu Ni muhimu kufahamu kwamba Qur’ani inahimiza sana suala hili, ikisema:

“Hakika Mwenyezi Mungu hawadhulumu watu chochote lakini watu wanajidhulumu (wenyewe) nafsi zao.” (10:44). Qur’ani inasema tena:

“Hakika Mwenyezi Mungu hawadhulumu (viumbe vyake) hata kitu kilicho sawa na uzito wa mdudu chungu…”(4:40). Katika Aya nyingine anasema:

“Nasi tuweke mizani ya uadilifu Siku ya Kiyama, na haitadhulumiwa nafsi ya yoyote hata kidogo…” (21:47).

45


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:15 PM

Page 46

Tujifunze Misingi ya Dini (Elewa kwamba maana ya ‘mizani’ hapa ni njia fulani ya kupima mambo mema na mabaya, na si mizani hii ya duniani tunayoijua).

Mwito wa kulingania kwenye Uadilifu Tumeshasema hapo awali kwamba sifa za binadamu ni lazima ziwe ni kama mwanga wa sifa za Mwenyezi Mungu, na zienee katika jamii ya binadamu. Kwa msingi huo, Qur’ani tukufu kwa kadri ya kusisitiza uadilifu wa Mwenyezi Mungu, pia imesisitiza kuwe na uadilifu katika jamii na kwa mtu mmoja mmoja. Qur’ani inasema kwamba uonevu na dhuluma vikiendelea, vitaharibu jamii na kwamba madhalimu hawana mwisho mwema. Qur’ani, kwa kuongezea, imetaja mwisho mbaya wa makabila (dhalimu) yaliyopita, na imekariri kutaja ukweli huu ili watu waone matokeo ya dhuluma na ufisadi na adhabu iliyowapata watu hao ili nao wasije wakawa na mwisho mbaya katika maisha yao kama zama zilizopita. Qur’ani inataja waziwazi kwa kusema:

“Kwa hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha uadilifu, na kufanya hisani, kuwapa jamaa (na wengineo) na anakataza uchafu na uovu, na dhuluma…” (16:90). Ni lazima ifahamike kwamba kufanya dhuluma ni kitendo kibaya, pia kukubali dhuluma na kuinyenyekea ni makosa kulingana na uislamu na Qur’ani tukufu, kama ilivyosema Qur’ani:

“Msidhulumu wala msidhulumiwe…” (2:279). 46


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:15 PM

Page 47

Tujifunze Misingi ya Dini Kwa ujumla, kuridhia dhulma ni kuunga mkono uonevu kukubali na kuwasaidia wadhalimu.

SOMO LA TATU HEKIMA YA MUNGU YA KULETA MAAFA Toka zamani hadi sasa, kuna watu wengine wasiojua, wanaopinga uadilifu wa Mwenyezi Mungu, ama si hivyo tu hata kusema hakuna Mwenyezi Mungu, kwa kutoa dalili za maafa yanayotokea kama tufani, mitetemeko ya ardhi, na mengineyo, Pia kuzidiana ubora kati ya watu na watu, na hata misiba mingine duniani inayowasibu watu, mimea na wanyama. Hapa tunarejea katika maudhui ya kumjua Mungu kwa wale wampingao. Ili tukufahamishe upeo wa fikra hizi ni lazima tuziangalie kwa undani kama ifuatavyo:

Hukmu zinazohusiana na kikomo cha ujuzi wetu Kwa kawaida sote tunapohukumu mambo na kuyathibitisha, tunalinganisha na jinsi tunavyohusiana nayo, mathalani tunasema kitu fulani kiko karibu, au kiko mbali kwa kulingana nasi, au tunaweza kusema fulani ana nguvu, na fulani ni mnyonge kwa kulinganisha na uwezo wetu wa kimwili na kiroho. Halikadhalika huwa hivyo hivyo kwetu katika mambo yanayohusu uovu, wema, misiba na maafa ya kilimwengu. Kwa mfano, mvua ikinyesha katika sehemu fulani ambayo athari yake haituhusu, ila tunaangalia mazingira yetu au nyumba na mashamba yetu tu. Ikiwa mvua haikuleta maafa, tutasema: “Ni neema ya Mwenyezi Mungu”, vinginevyo tunasema “Hii ni balaa.” 47


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:16 PM

Page 48

Tujifunze Misingi ya Dini Au tukiona watu wanashughulika kubomoa jumba kwa ajili ya kujenga jingine jipya, nasi tusiwe na fungu lolote hapo isipokuwa mchanga tu utakaotuingia puani tupitapo hapo, tutadai kuwa halina maana yoyote, japokuwa twajua wazi kuwa baadaye litakuwa ni jengo la hospitali itakayotufaa sote. Mfano huo uliotangulia; hata kama mvua iliyoleta maafa italeta mazao sehemu nyingine, bado tutaishutumu (kwa sababu tu, ilitudhuru sisi). Nyoka mathalani, tunapohukumu kwa kumtazama kijuu juu, tutachukulia kwamba kuumwa na mdudu huyo ni balaa (upande wetu) lakini hapo hapo tunasahau kwamba kuuma kwake huko na sumu ndiyo njia anayoitumia kwa kujihami; aidha tunasahau kwamba wakati mwingine madawa muhimu yanayookoa maisha ya maelfu ya watu hutengenezwa kutokana na sumu hiyo hiyo. Kwa hiyo basi, ili tusiingie makosani, ni lazima tunapohukumu tusijiangalie sisi na mambo yanayotuhusu, bali tuangalie pande zote ili maamuzi yetu yahusike kila sehemu. Kimsingi, matukio duniani yanaungana kama mkufu. Kimbunga kinachopiga mjini kwetu hivi leo na mvua kubwa inayosababisha mafuriko, ni mojawapo ya mambo yanayolingana na yanayohusiana na matukio yaliyotokea zamani na yakayotokea baadaye. Kwa hivyo mtu kujiamulia jambo kwa kuonyesha kidole tu, ni kutotumia akili. Kila wanayostahili viumbe ni mema, lakini ikiwa jambo ni baya, basi upande mwingine ni zuri, kama upasuaji ni maumivu lakini kwa upande mwingine kuna faida kwa hivyo huzingatiwa kuwa kwa upande mwingine kuna faida, kwa hiyo huzingatiwa kuwa ni kuzuri. Kwa maelezo zaidi, hebu tuangalie tukio la tetemeko la ardhi. Ni kweli kwamba tetemeko husababisha maangamizi lakini tukilihusisha na mambo mengine tutaona kuwa lina faida na hapo tutabadili maoni yetu. 48


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:16 PM

Page 49

Tujifunze Misingi ya Dini Je tetemeko la ardhi linahusiana na msongo wa joto uliyomo chini ya ardhi? Au linahusiana na mvutano wa mwezi unaovuta vilivyomo ardhini? Au linahusiana na yote na yote? Hapo wanasayansi wametofauiana. Lakini yovyote itakuwa, lazima tuangalie athari zinazopatikana. Mathalani, lazima tufahamu kwamba joto lililoko chini ya ardhi husababisha kupatikana mafuta ambayo ni nishati muhimu siku hizi, isitoshe pia husababisha kupatikana makaa ya mawe na vinginevyo, kwa hivyo uzuri wa joto hapo unahusika. Vilevile kupwa na kujaa kwa maji ya bahari kunatokana na mvuto wa mwezi na kuwepo kwa bahari na viumbe vyake. Huu pia ni uhusiano mzuri. Kutokea hapo ndipo tunapotambua kwamba maamuzi yanayohusina nasi na uchache wa ujuzi wetu tulionao ndio unaotufanya tuyaone matukio haya kama nguvu za giza tu. Kadri tunavyoangalia zaidi uhusiano uliopo baina ya matukio ndivyo tunavyozidi kufahamu umuhimu wake. Qur’ani yatuambia hivi:

“Nanyi hamkupewa katika elimu ujuzi ila kidogo tu.” (17:85).

Mambo yasiyopendeza na maonyo Bila shaka tumeshaona wakati wa utulivu katika bahari ya maisha ya watu ambao wanapozama katika hali hii husahau wajibu na mambo ya muhimu. Vile vile tumeshaona wakati wa ulitulivu katika bahari ya maisha ya mtu jinsi anavyojisahau, ambapo hali hiyo ikiendelea mwishowe humletea balaa kubwa mtu huyo. Kwa hivyo bila shaka mabalaa yanampata katika maisha yake yana lengo la kumwondolea ujuba na kumwamsha kutoka 49


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:16 PM

Page 50

Tujifunze Misingi ya Dini usingizini na kujisahau. Bila shaka umepata kusikia madereva hodari wanavyolalamika kuhusu barabara ya tambarare isiyo na konakona na vibonde, na kwamba barabra kama hizo ni hatari, kwa kuwa humfanya dereva alale, na hapo ndipo ajali hutokea. Ndipo tunaona kuna baadhi ya nchi zilizotengeneza vibonde na vishimo vya bandia njiani ili kukinga hatari kama hizo. Halikadhalika njia ya maisha ya binadamu iko hivyo hivyo, kama maisha hayatakuwa na misukosuko na mabalaa atamsahau Mwenyezi Mungu na kughafilika, na hayo yatamzuia asitimize wajibu wake kama ipasavyo. Kwa kusema hivi hatukusudii kwamba mtu ajiingize kwenye mabalaa au kuwacha masaibu yampate, kwani siku zote misiba iko na itaendelea kuwepo: bali tunachosema ni kuwa yampasa mtu awe macho na kuitambua hekima hii ambayo lengo lake ni kumfanya mtu asiwe na kiburi na asijisahau, kwani mambo hayo ndio maadui wakubwa wa ufanisi wake. Tunarudia tena kusema kuwa, hii ni hekima ihusiayo baadhi tu ya misukosuko impatayo mwanadamu, si yote. Kwani kuna mengine ambayo tutayataja baadaye. Qur’ani inasema

“… kisha tukazitia katika dhiki na mashaka ili zipate kunyenyekea (baada ya kufanya ukaidi). “(6:42).

50


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:16 PM

Page 51

Tujifunze Misingi ya Dini

SOMO LA NNE HEKIMA NA MISUKOSUKO KATIKA MAISHA Tumeshasema hapo mwanzoni kuwa kikundi cha walahidi walipatiliza suala hili la kutokea maafa na misukosuko inayompata mwanadamu na kulifanya kuwa ni sababu ya kuwapo Uadilifu wa Mwenyezi Mungu, si hivyo tu, hata kutokuwapo Mwenyezi Mungu mwenyewe. Katika somo lilopita tumeeleza falsafa mbili na sasa tunaendelea. Mwanadamu hukua katika hali ya kukabiliana na matatizo Tunakiri kusema kuwa haipasi tujiingize kwenye matatizo sisi wenyewe, Bali matatizo hutuongezea nguvu ya matakwa yetu, mithili ya chuma kinachowekwa motoni ili kizidi kuwa madhubuti. Nasi pia tunazidi kuwa na uzoefu na uimara tunapopatwa na matatizo. Mapambano kwa kawaida si mazuri lakini mara nyingine mapambano ya muda mrefu huleta ustawi na umoja. Mwanahistoria mmoja mashuhuri anasema: “Ustawi wa kimaendeleo katika sehemu nyingi duniani umepatikana baada ya nchi nyingi kuingiliwa na mataifa ya nje, wakaamka na kujiandaa.� Ndiyo, bila shaka athari za matatizo si sawa baina ya watu na jamii zote. Kuna wengine watakata tamaa, watadhoofu na watakuwa wameathirika kinyume na faida. Lakini wengine hujiandaa vyema wanapokabiliana na matatizo hayo na kutiwa hamasa nayo na kuanza kuyashughulikia huku wamejawa na hamasa na mwisho hufanikiwa kuyatatua. Lakini katika hali kama hizo, watu wengi huamua tu, kutokana na wanavy51


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:16 PM

Page 52

Tujifunze Misingi ya Dini oona juu juu, wanachokiona ni taabu na matatizo tu na wanasahau na kupuuza faida zinazopatikana kwenye matatizo hayo. Hata hivyo hatusemi kwamba matatizo na misukosuko yote ina faida hizo kwa mwanadamu bali kwa watu wengine huwa hivyo. Ukisoma habari za maisha ya wajuzi wa ulimwengu utaona kwamba wengi wao walipambana na matatizo na masaibu makubwa. Ni wachache sana waliokulia katika maisha ya raha na kufikia daraja za juu. Kamanda mzuri wa jeshi ni yule aliyepambana na taabu na vita vya muda mrefu. Mabingwa wa uchumi ni wale waliopata taabu sana katika uchumi. Wanasiasa wakuu ni wale waliopitia mapambano magumu ya kisiasa. Kwa kifupi tunaweza kusema kuwa matatizo na machungu anayoyapata mtu ndiyo yanayomkomaza. Qur’ani yasema:

“Huenda mkakichukia kitu na Mwenyezi Mungu ametia kheri nyingi ndani yake.� (4:19).

Matatizo humfanya mtu arejee kwa Mwenyezi Mungu Katika maelezo yaliyopita, tumeona kwamba kila sehemu kati ya viungo vya maumbo yetu ina lengo na sababu. Macho yetu, masikio, nyoyo, akili pamoja na mishipa yetu ya fahamu; vyote vimeumbwa kwa sababu, hata ncha za vidole vyetu zina hekima yake. Hivyo basi, itawezekanaje kuumbwa kwetu kwa ujumla kusiwe na lengo? Vilevile tumesoma huku nyuma kuwa lengo la yote hayo ni kufikia kwenye ukamilifu kwa mwanaadamu, na bila shaka kufikia kwenye ukamilifu huu 52


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:16 PM

Page 53

Tujifunze Misingi ya Dini kunahitaji ratiba ya mafunzo na malezi ya kutosha, ndipo Mwenyezi Mungu akampelekea Mitume na vitabu ili kumuongoza mwanadamu huyo, licha ya kumpa fikra ya Tawhid. Kwa kukamilisha kazi hii yapasa madhambi ya mtu na uasi wake uonyeshwe kwa misiba. Katika kupambana na shida, wakati wa kufuata amri za Mwenyezi Mungu mtu atajua ubaya wake, hivyo atarejea kwa Mwenyezi Mungu. Hapa ndipo matatizo na matukio ya ghafla huwa ni rehema itokanayo na Mwenyezi Mungu. Qur’ani yasema:

“Uharibifu umedhihiri barani na baharini kwa sababu ya yale yaliyofanywa na mikono ya watu, ili awaonyeshe (adhabu ya) baadhi ya mambo waliyoyafanya, huenda wakarudi (wakatubia).” (30:41). Tukiangalia kwa makini haya tuliyosoma, na mtazamo wetu ukizingatia kuwa matukio haya ni balaa, na kwamba yanapingana na Uadilifu wa Mwenyezi Mungu; basi utakuwa ni mtazamo usiokubaliana na mantiki na hoja za kiakili, kwani kadri tunavyoingia ndani ya maudhui haya, ndivyo tunavyozidi kupata upana na hekima mbalimbali zilizomo.

SOMO LA TANO MAELEZO MENGINE YA HEKIMA YA MAAFA Kutokana na ugumu na mkanganyo katika maelezo yanayohusu maafa, matukio ya ghafla na misiba inayozungumza Zaidi katika somo la kumjua 53


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:16 PM

Page 54

Tujifunze Misingi ya Dini Mwenyezi Mungu na Tawhid; basi hapa na tuendelee kueleza hekima ya baadhi ya maafa na misiba.

Matatizo na kuwa na hali mbaya na nzuri huyapa uhai maisha Huenda ikawa ni vigumu kwa watu wengine kufahamu kwamba, kama maisha yangekuwa ni raha tupu, yasingelikuwa na thamani. Imethibitishwa kitaalamu kwa siku hizi kwamba, tukiweka kitu kama kioo katikati ya chumba kisha tukimulike kwa taa za aina moja kutoka kila pembe ya chumba; hatutaweza kukiona kitu hicho kwa sababu kivuli kinapokuwa nyuma ya mwangaza, ndipo umbo la kitu linapodhiri, na kivuli hupambanua kati ya kitu na mwanga, ndipo tunaweza kukiona kitu hicho. Vile ambavyo ile thamani ya tunu ya maisha hatuwezi kuiona bila ya vivuli vinene au vyembamba vya matatizo ya ugonjwa, thamani ya afya isingelijulikana. Mathalan, baada ya kushikwa na homa kali usiku na tunapopata nafuu asubuhi yake, huhisi raha na kutambua thamani ya afya na hasa pale tunapoukumbuka usiku huo uliopita wa homa na maumivu. Kwa ujumla maisha ya aina moja tu, hata yawe ya raha kiasi gani yanachosha, hayana maana, na ni kama kifo. Mara nyingi imetokea kwamba kuna baadhi ya watu wanaochoshwa na maisha hata kutaka kujiua na hulalamika kila siku juu ya maisha yao, kwa sababu ya maisha ya raha yasiyo na taabu yoyote. Vilevile huwezi kupata mjenzi hodari atakayejenga chumba kikubwa na kikawa hakina hitilafu, bali hutia nakshi na huwa na vijishimo kwenye viwambaza vyake. 54


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:16 PM

Page 55

Tujifunze Misingi ya Dini Kwa nini ulimwengu ukapendeza? Kwa nini mandhari ya mapori yenye milima na mikondo ya mito yenye konakona kati ya miti mikubwa na midogo ikawa ni ya kuvutia? Sababu ni kwamba vyote hivyo havikufanana wala kulingana. Utaratibu wa kuwapo mwanga wa giza, kuja na kuondoka mchana na usiku, kunakoelezwa katika Aya kadha wa kadhaa za Qur’ani, una umuhimu mkubwa katika kufanya wanaadamu wasichoke na maisha. Kwa nini? Kwa sababu, ikiwa jua daima litasimama mahali pamoja na kumulika ardhi bila ya kubadilisha mahali na kusiwe na usiku, kwa kipindi kifupi tu binadamu wote wangelichoka. Ni kwa sababu hii ndipo inatubidi tukubali kwamba matatizo yanayotupata yanatokana na matukio ya ghafla, huyapa thamani maisha na kuyafanya yawe mazuri na yanayoweza kuvumiliwa. Yanadhihirisha thamani na neema yake na humpa mwanaadamu fursa ya kufaidika na mambo yale aliyopewa na Mwenyezi Mungu kwa kadri ya uwezo wake. Matatizo ya kujitakia Jambo jingine ambalo ni muhimu kulitaja mwishoni mwa mjadala huu ni kwamba, watu wengi wanaelewa kimakosa sababu za matukio haya yasiyotazamiwa, wanaichukulia dhulma inayofanywa na madhalimu kuwa ni kukosekana Uadilifu wa Mwenyezi Mungu. Mathalan, mara kwa mara watu hao husema,�kwa nini kuna mawe mengi katika njia anayopita kiwete?� Kwa nini mitetemeko ya ardhi inayoikumba miji haileti madhara makubwa mijini kuliko mashambani ambako watu wengi hupoteza maisha yao na kukosa mahali pa kuishi? Uadilifu gani huu? Ikiwa kama majanga yanayowapata watu hugawanywa, kwa nini yasigawanywe kwa usawa? Kwa nini majanga hayo yawapate wanyonge siku 55


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:16 PM

Page 56

Tujifunze Misingi ya Dini zote? Na kwa nini maradhi ya kuambukiza huwakumba wao zaidi?’ (yote haya ni kumtia dosari Mwenyezi Mungu Muumba). Hao hawafahamu mambo haya hayahusiani na utaratibu wa uumbaji wa Mwenyezi Mungu, bali yanasababishwa na uonevu, ukoloni na unyanyasaji wanaofanyiana wanaadamu. Lau kama si kuwa watu hao wamedharauliwa na kupatwa na umaskini kwa sababu ya uonevu wa watu wa mijini, na lau wangeweza kujijengea nyumba bora na imara kama za mijini, mitetemeko isingeliwadhuru kiasi hicho. Lakini ikiwa nyumba zao hujengwa kwa udongo au mbao, na kutiwa saruji kidogo tu, tena kwa ujenzi hafifu wa kubambanya tu, ni rahisi kwao kuathirika hata kwa upepo au tetemeko hafifu. Kwa hivyo tusitegemee kuwa hali yao itakuwa nzuri zaidi ya hii. Je haya yanahusiana vipi na Uadilifu wa Mwenyezi Mungu? Haifai tukae tukilalama tu kuwa Mwenyezi Mungu ndiye aliyewatajirisha wengine na kuwafukarisha wengine, yatupasa kujitahidi kuuondoa umasikini na kuwapatia haki wanyonge ili kusiwe na hali kama hiyo. Lawama zote zitupiwe hali yenyewe isiyo ya usawa na mfumo wa kimakosa wa jamii. Ni lazima tuzinduke na tumalize uonevu huu katika jamii. Tupambane na unyanyasaji na umaskini, na tupewe wanyonge haki zao ili yasitokee mambo kama hayo. Lau kama jamii yote itapata chakula, na matibabu ya kutosha, bila shaka itaweza kukabiliana na maradhi. Lakini yakifanyika makosa katika utaratibu wa jamii kwa mtu mmoja kujikusanyia mambo mengi, ambapo mbwa wake na paka wake wanaishi vizuri na kupata matibabu na huku binadamu wengine hawapati mahitaji ya kutosha katika maisha; badala ya kumlaumu Mwenyezi Mungu katika hali kama hizo yatupasa tujilaumu wenyewe.

56


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:16 PM

Page 57

Tujifunze Misingi ya Dini Watu wote wapate angalau huduma za afya, chakula cha kutosha, makazi na nafasi za elimu na utamaduni wetu. Kifupi, tusilaumu kuumbwa kwetu kutokana na madhambi yetu wenyewe. Mwenyezi Mungu alituwekea lini utaratibu huu? Alipendekeza wapi? Bila shaka Mwenyezi Mungu alituumba huru, kwa sababu kuwa huru ndiyo asili ya maendeleo, lakini sisi ndiyo tunaotumia vibaya uhuru wetu kwa kuoneana, na ndipo matokeo yake ni kuleta uharibifu katika jamii. Kwa bahati mbaya, kosa hili hufanywa na watu wengi. Qur’ani yasema:

“Hakika Mwenyezi Mungu hawadhulumu watu chochote: Lakini watu wanajidhulumu (wenyewe) nafsi zao” (10:44). Mpaka hapa tunakamilisha maelezo yetu kuhusu matukio na maafa, japokuwa kuna maelezo mengi kuhusu maudhui haya, lakini haya machache yanatosha kwa somo hli fupi.

SOMO LA SITA ‘KUTENZWA NGUVU’ NA ‘KUACHILIWA’ Miongoni mwa masuala yanayohusiana moja kwa moja na suala la Uadilifu wa Mwenyezi Mungu ni suala la ‘kutenzwa nguvu’ na ‘kuachiliwa.’ Kuna kikundi kiitwacho ‘Mujabbira’ kinachoamini kwamba mwanaadamu hana hiari ya kufanya jambo lolote, na kwamba mwenendo, maneno na viungo vyake ni kama vinavyoendeshwa na mtam57


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:16 PM

Page 58

Tujifunze Misingi ya Dini bo wa Mwenyezi Mungu (hutenzwa nguvu). Sasa hapa swali hujitokeza, vipi fikra hii ihusiane na uadilifu wa Mwenyezi Mungu? Pengine kwa sababu hii ndipo Maash’ari - kikundi tulichokitaja hapo awali kinachokanusha wema na uovu unaotambuliwa kiakili - wanakubaliana na fikra hiyo ya Mujabbira (ya Mwenyezi Mungu kulazimisha kwa nguvu) uadilifu wa Mwenyezi Mungu hautakuwa na maana kwake. Kwa ufafanuzi zaidi twapaswa kufanya upekuzi kwa uangalifu katika maudhui yafuatayo: Msingi wa imani hii Watu wote katika nafsi zao wanajihisi kwamba wana uhuru wa kufanya watakavyo. Mathalan, mtu ana uhuru akitaka kumkopesha rafiki yake fulani au asimkopeshe, au anapowekewa bilauri ya maji anapokuwa na kiu, ni hiyari yake anywe au asinywe, au na hiyari ya kusamehe anapofanyiwa kosa na mtu mwingine au asimsamehe; pia kila mtu anaweza kutambua tofauti kati ya mkono unaotingishika (bila ya hiari) kwa sababu ya uzee au ugonjwa, na mkono unaotingishwa kwa makusudi. Licha ya ukweli juu ya suala la hiari katika hisia za mwanaadamu, kwa nini baadhi ya watu wanafuata fikra za Mujabbira? Bila shaka kuna sababu nyingi, hapa tutataja moja: Mwanaadamu huona kwamba mazingira huathiri fikra na nafsi ya mtu kwa kiasi fulani yakichangiwa na elimu, propaganda na mila. Vilevile hali za kiuchumi humfanya mwanaadamu awe na mwendo fulani, na hakuna anayekataa ukweli huu.

58


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:16 PM

Page 59

Tujifunze Misingi ya Dini Mkusanyiko wa mambo yote haya ndiyo unaomfanya mtu adhani kwamba hana hiari bali visababishi vya ndani na nje ndivyo husaidia kutulazimisha kuamua mambo fulani ambayo lau si hivyo tusingelipatwa na matatizo haya. Mambo yote haya yanawezwa kuitwa ‘vilazimishi vya mazingira’ ‘vilazimishi vya uchumi’ na ‘vilazimishi vya elimu,’ navyo huchukuliwa kuwa ni muhimu kwa kikundi cha Mujabbira. Kosa kubwa la ‘Mujabbira’ Wale wenye fikra wamesahau jambo muhimu kwamba majadilianao hayahusu visababishi vyenye upungufu, bali yanahusu sababu yenyewe. Kwa msemo mwingine ni kwamba, hapana akataaye athari inayosababishwa na mazingira, mila na uchumi katika fikra na vitendo vya mwanadamu, bali ni kwamba pamoja na kuwapo visababishi vyote hivi, uamuzi wa mwisho (kwa hiari) tunao sisi wenyewe. Kwa sababu tunafahamu vizuri kwamba hata tukiwa chini ya utawala mbaya unaomuasi Mwenyezi Mungu, ambao una kila aina ya upotofu, hatulazimiki kupotoka (kwa ajili ya mazingira hayo) na kuzama kwenye ufisadi. Kwa hiyo yampasa mtu atofautishe kati ya visababishi na msingi wenyewe, kwa sababu hii, ndipo twaona watu wengi waliokulia katika maisha mazuri, au waliokulia katika mila potofu, au waliorithishwa na mambo yasiyofaa; wamebadilika na kufuata njia za wengine na kuacha mwenendo wa mazingira yao waliyokulia. Kama kila binadamu angelihitajika kufuta mazingira na mila za wakati wake tu, kusingelikuwa na mabadiliko yoyote duniani, kila mmoja angebaki na mfumo wake, asingejenga mfumo mpya. Visababishi vyote vilivyotajwa havisabishi mtu kuwa katika hali fulani, ni njia tu, sababu kubwa ni mtu kufanya jambo kwa hiari yake. 59


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:16 PM

Page 60

Tujifunze Misingi ya Dini Mfano wake ni kama tunapoamua kufunga wakati wa joto kali la kiangazi; mwili wetu unahitaji maji, lakini kwa ajili ya kutii amri ya Mwenyezi Mungu hatujali yote hayo na twaendelea kufunga, ambapo wengine hawafungi. Kwa ufupi ni kwamba nyuma ya visababishi vyote na misukomo yote kuna kitu kinachoitwa uhuru wa mtu wa kujiamulia mambo yake. Kwa hivyo, visababishi vinavyompeleka mtu kufanya mambo viko chini ya hiari ya binadamu mwenyewe. Visababisha vya kijamii na kisiasa katika madhehebu ya ‘Mujabbira’ Ukweli ni kwamba suala la ‘kutenzwa nguvu’ na kuachiliwa’ limetumiwa vibaya. Mfululizo wa visababishi vya majaaliwa umezidisha imani ya kuamini kuwa binadamu amelazimishwa na Mwenyezi Mungu kufanya kila jambo, na umekanusha kuwa binadamu ana hiari ya kufanya mambo, miongoni mwa visababishi hivyo ni: a) Visababishi vya kisiasa Wanasiasa wengi madhalimu, wachoyo, ambo kwa ajili ya kutaka kuzima moto wa mapinduzi ya wanyonge, na kwa ajili ya kuendekeza utawala wao; wanajaribu kila wawezavyo kuwasadikisha watu kwamba, wao (watu wanyonge) hawana hiari, majaaliwa ya kihistoria ndiyo yaliyowafanya wao watawale; na ikiwa watu fulani ni watawala na wengine ni watawaliwa hayo ni majaaliwa ya kihistoria tu? Hapa twaona wazi jinsi fikra hii inavyowapumbaza watu na kusaidia kuendeleza siasa za kikoloni, ambapo yote tuyafanyayo, kiakili na kisheria, yako mikononi mwetu; na hakuna ‘hukmu na qadar,’ kwa maana ya majaaliwa. ‘Hukmu na qadar’ ni kwa mjibu wa harakati zetu, matamanio, matakwa, imani na juhudi tuzifanyazo. 60


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:16 PM

Page 61

Tujifunze Misingi ya Dini b) Visababishi vya kisaikolojia Watu wavivu na wazembe ambao mara kwa mara hushindwa kupata ufanisi huu kwamba uzembe na makosa na makosa yao ndiyo yanayosababisha kushindwa kwao, hivyo basi, ili kujitakasa na kuonekana ni watu wa maana, ndipo tutegemee itikadi hiyo ya ‘kulazimishwa’ na Mwenyezi Mungu, kwa njia hii wanapata utetezi wa uongo. Hulalamika wakisema: Tufanyeje? Bahati zetu tayari zimeshafanywa nyeusi, haziwezi kugeuzwa ziwe nyeupe hata kwa maji ya ‘Zamzam’ au ya ‘Kawthar,’ kwa hakika tuna vipaji na bidii lakini hatuna bahati!” c) Visababishi vya kijamii Kuna baadhi ya watu wanaotaka kuwa huru kufuata matamanio yao ya kimwili, na kutenda madhambi wayatakayo, na wakati huo huo kujisadikisha kuwa wao si watenda dhambi na kuwahadaa watu kwamba wao hawana makosa! Hapa ndipo wanageukia imani ya ‘majaaliwa’ ili kukidhi matamanio yao kwa kudai kuwa binadamu hatuna hiari ya kuacha madhambi. Lakini tunajua vyema kwamba hayo wayasemayo yote ni ya uongo, hata hao wanaodai hivyo wanatambua kuwa madai yao hayana msingi, lakini matamanio na njozi zao huwafanya wasikubali ukweli. Kwa hivyo, ili tujenge jamii imara, ni lazima tukubaliane ipasavyo na fikra hii ya hawa Mujabbira kwani huko kuamini ‘majaaliwa’ ni fikra inayotumiwa na waonevu na ndiko kunakosababisha ufisadi katika maendeleo ya kijamii.

61


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:16 PM

Page 62

Tujifunze Misingi ya Dini

SOMO LA SABA HOJA ZA WAZI KUHUSU HIYARI Dhamira za wanaadamu hazikubaliani na fikra ya ‘majaaliwa’ Pamoja na kuwa wanafalsafa na wanavyuoni wanatoa hoja zinazotofautiana juu ya suala la hiyari ya mwanadamu, hapa tunajaribu kwa kifupi kutoa hoja iliyo wazi inayotolewa na wanaounga mkono suala hilo, nayo ni dhamira ya pamoja ya mwanaadamu. Hata tukikanusha, hatuwezi kukanusha ukweli kwamba jamii zote za wanaadamu, zinakubali kuwa lazima wao wafuate sheria, vinginevyo, zinapaswa kuadhibiwa; ama ziwe jamii hizo ni za wanaoabudu Mwenyezi Mungu au za walahidi, za mashariki au za magharibi, za kale au za kisasa, zilizoendelea au zisizoendelea; ama ziwe zi katika mila zozote. Kwa maneno mengine, sheria na majukumu ya watu kuhusiana nazo na kuadhibiwa wavunjaji sheria, ni mambo ambayo wenye akili wote wanakubaliana nayo isipokuwa makabila mashenzi na yasiyostarabika tu, ndiyo hayakubali rasmi mambo haya matatu. Ukweli huu tunaoueleza ambao ndiyo dhamiri ya mwanaadamu ni ushahidi wa wazi kuthibitisha kuwepo kwa hiyari na uhuru wa kujichagulia kwa mwanaadamu. Itakubalika vipi mtu alazimishwe kutenda mambo bila ya hiari na hapo hapo awe chini ya sheria? Aidha avunjapo sheria ahukumiwe kisha aambiwe kwa nini alifanya hivi au kwa nini hakufanya? Kisha ikithibitishwa kuwa alikosa apelekwe gerezani au auwawe kulingana na makosa hayo. Bila shaka haya yote 62


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:16 PM

Page 63

Tujifunze Misingi ya Dini hayakubaliki. Mfano huu ni kama mfano wa mawe yaliyowaangukia watu kutoka mlimani na kusababisha vifo; kisha tuyafungulie mashtaka! Bila shaka ni kweli kwamba binadamu si sawa na mawe lakini ikiwa twakanusha kuwapo kwa hiyari ya kuchagua kufanya mambo kwa binadamu, basi tofauti iliyopo kati ya binadamu na mawe haitakuwa na maana, na wote hao watakuwa chini ya nguvu ya kujaaliwa kufanya jambo. Jiwe linalazimishwa na nguvu iitwayo ‘ya mvutano’ (Force of gravity), ili liangike, na binadamu avutwe na nguvu nyingine iitwayo “Mujabbira” yanaonekana hapana tofauti kutokana na matokeo ya vitu viwili hivyo, kwani kila kimoja hakikufanya hivyo kwa hiyari yake; kama ni hivyo kwa nini basi kimoja kihukumiwe na kingine kiachwe? Ama sisi tuko kwenye njia panda (katikati), aidha tupinge kuwapo kwa dhamira ya wanadamu wote na tuzingatie kuwa mahakama na adhabu kwa kuvunja sheria (vyote) ni upuuzi mtupu na uonevu: au tupinge imani ya Mujabbira. Hapo bila shaka maoni ya pili ndiyo ya sawa. Jambo la kushangaza ni kwamba hao wanaofuata imani ya ‘Mujabbira’ (ya kuwa kila kitu ni majaliwa) na kutoa hoja za kutetea imani zao, wanapokumbwa na mikasa ya kidunia, hukimbilia kwenye imani ya hiyari! Mathalan, wakidhulumiwa au wakidhuriwa na mtu, humpeleka mahakamani na hawapumziki mpaka waone mtu huyo ameadhibiwa. Basi ikiwa mtu hana hiyari kwa jambo alifanyalo na hafanyi kwa kupenda, kuna haja gani basi kupelekana mahakamani, na kuwa na mizozo ya kushtakiana? 63


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:16 PM

Page 64

Tujifunze Misingi ya Dini Kwa hiyo vyovyote iwavyo, dhamira hii ya watu wenye akili ni hoja ya wazi ya kuonyesha kuwa wanaadamu wanakubali kuwa mwanaadamu ana hiari ya kufanya jambo, na siku zote ataishi hivyo na hawezi kuishi kinyume na hivyo hata siku moja, na kwamba gurudumu la uhai wake hulisukuma kwa kuamini hivyo hivyo. Mwanafalsafa mkuu wa kiislamu, Khawja Nasir din Tusi, anajadili kuhusu suala la majaaliwa katika kitabu chake ‘Tajribatul-aqaid’ akisema: “Dhamira zetu zatwambia kuwa sisi ndio dhamana ya vitendo vyetu vyote.” Mgongano kati ya mantiki ya majaaliwa na mantiki ya dini Hapo awali tulipozungumzia migongano iliyopo kati ya fikra ya ‘majaaliwa’ na dhamira ya pamoja ya ulimwengu, kutoka kwenye maoni ya pande zote, wanaounga mkono dini na wapinzani wa dini. Lakini katika upande wa maoni ya Mujabbira. Imani ya kidini kwanza haikubaliani na maoni hayo, kwani kukubaliana nayo kutageuza imani yote hiyo. Vipi tutazungumzia fikra ya Uadilifu wa Mwenyezi Mungu – tuliuthibitiha katika somo lililopita – kisha tuupatanishe na fikra ya Mujabbira na kusema kuwa hazigongani? Mwenyezi Mungu ataweza kumlazimisha mtu atende dhambi kisha amuadhibu kwa kulitenda hili halikubaliani na akili hivyo basi, tukikubaliana na fikra hiyo, basi thawabu, adhabu, Pepo na Moto vitakuwa havina maana yoyote; kadhalika, Daftari la vitendo, kuulizwa, hesabu ya Mwenyezi Mungu, kuwakemea watenda dhambi, kuwapa moyo watenda mema, haya yote hayatakuwa na maana, kwa sababu kulingana na fikra hii, watenda mema na watenda maovu wote hawana hiyari.

64


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:16 PM

Page 65

Tujifunze Misingi ya Dini Tukiongeza ni kwamba, tunapambana na moja kati ya suala la mwanzo ambalo ni ‘wajibu’ lakini mambo haya yana maana gani ikiwa mtu hana hiari? Je twaweza kumkataza mtu ambaye mikono yake hutetemeka kwa ugonjwa bila ya hiyari, asifanye hivyo; twawezaje kumzua mtu anayebingiria akianguka kutoka mlimani asifanye hivyo, na badala yake ajizuie? Ndipo Imam Ali (a.s.) akasema: “Hayo maneno ya Mujabbira ni maneno ya wanaoabudu masanamu, wanachama wa chama cha Iblis, na ni maadui wa Mwenyezi Mungu.” (Usulul-Kafi, kitabu 1. uk. 119).

SOMO LA NANE MAANA YA NJIA YA KATI Tukiacha imani ya Mujabbira (ya kutenzwa nguvu) ambayo ni yenye kuruka mpaka, kuna imani nyingine ya ‘kuachiliwa’ (Tafwidhi) ambayo ni ya kurusha mpaka. Wanaokubali imani hii (Mufawwidha) wanaaamini kwamba Mwenyezi Mungu ametuumba na akutuachia kila jambo, na kwamba yeye hahusiki na chochote tukifanyacho, kwa hivyo tuna uhuru (kupita kiasi) na kuchagua la kufanya. Bila shaka imani hii haikubaliani na Tawhid (kuamini kuwa Mwenyezi Mungu ni mmoja) kwa sababu Tawhid imetufundisha kuwa Mwenyezi Mungu anatawala ulimwengu mzima hakuna kinachozidi uwezo wake, wala hiari zetu haziwezi kuzidi uwezo wake, wala hiyari zetu haziwezi kuzidi uwezo wake, vinginevyo tukiamini kinyume na hivyo, itakuwa ni shirk. 65


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:16 PM

Page 66

Tujifunze Misingi ya Dini Au kwa ufafanuzi zaidi wa maneno haya ni kuwa, hatuwezi kuamini kuwapo kwa miungu wawili, mmoja awe ni Mungu mkubwa Muumba wa ulimwengu na wa pili awe ni Mungu mdogo, yaani awe ni mwanadamu aliye huru kufanya alitakalo, anayejitegemea, kiasi kwamba hata Mwenyezi Mungu ashindwe la kufanya kutokana na vitendo vya mwanaadamu huyo. Twarudia tena kusema, hii ni shirk, tena ni kuwafanya Miungu ni wawili. La muhimu kwetu ni kujua kuwa wanaadamu wana uhuru, wana hiari na wakati huo huo Mwenyezi Mungu ndiye hakimu juu ya watu wote na vitendo vyao. 2. Fikra ya kati Jambo muhimu hapa kufahamu ni kuwa tusidhani kuwa mambo mawili haya yana mgongano. Ukweli ni kwamba tunaamini Uadilifu wa Mwenyezi Mungu na pia tuamini hiyari na wajibu wa wanaadamu. Vile vile tunaamini umoja wake Mungu na utawala wake juu ya ulimwengu mzima, na hii ndiyo iitwayo ‘Njia ya kati’ (ilivyo katika imani mbili zilizozidi mpaka). Hebu na tufafanue jambo hili kwa kutoa mifano, kwani ni jambo linalotatiza mno: Hebu tuchukulie kuwa wewe ni dereva wa treni ya umeme, kwenye njia ya treni hiyo lazima kuweko na waya mgumu ulioungwa na gari hiyo na kuifanya iende, na kila dakika umeme hupita hadi kwenye injini kwa kutumia waya huo kiasi ambacho lau umeme utakata na kuacha kwenda kwenye injini kwa kitambo kidogo tu basi treni yote itasimama. Hapo bila shaka twaona kwamba, ukiwa dereva una hiyari na uwezo wa kusimama popote utakapo au unaweza kwenda mwendo wa kasi uutakao. Lakini pamoja na hiyari uliyonayo ya kufanya hivyo, bado kuna msimamizi anayefanya kazi katika idara yako inayotoa umeme 66


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:16 PM

Page 67

Tujifunze Misingi ya Dini anayeweza akafanya treni yako isimame kwa sababu tegemeo lote katika uendeshaji wako ni umeme ambao yeye ndiye msimamizi. Tukiangalia mfano huu kwa makini tutaona kwamba japo mtu ana hiari na jukumu, pia bado yuko chini ya uwezo wa mwingine, na wakati huo huo mambo haya mawili hayapingani. Mfano mwingine: Hebu chukulia kuwa mishipa ya mtu haifanyi kazi sawa kutokana na ugonjwa au ajali akawa hana uwezo wa kufanya mkono wake ufanye kazi, lakini tukiunganisha – kitaalamu - na umeme kidogo, mishipa hiyo itapashwa moto na kuweza kufanya kazi. Kwa hivyo endapo mtu huyo atatenda maovu kwa kutumia mkono huo kama kupiga mtu kofi, au kumdunga kisu, bila shaka yeye ndiye atakayekuwa muhusika wa makosa hayo kwa sababu ana mambo yote, ana uwezo na hiyari ya kufanya hivyo, na mtu mwenye uwezo na hiari ndiye anayehusika na vitendo vyake mwenyewe. Wakati huo mtu huyo anayeupa mkono (uliofanya makosa, umeme na kuupa uwezo na nguvu ya kutenda, ni msimamizi tu, lakini aliyetenda maovu ndiye mwenye hiari ya kutenda hivyo. Bada ya kutoa mifano hii, turudi kwenye maudhui yetu, Mwenyezi Mungu ametupa nguvu za kimwili au uwezo na kila mara huendelea, na endapo vitakatika japo kwa dakika moja tu, uhusiano wetu na Mwenyezi Mungu pia utakatika na hivyo tutaangamia. Tunapoweza kufanya jambo, basi ni kwa sababu ya uwezo tuliopewa na Mwenyezi Mungu unaeendelea mara kwa mara hata hiyari na matakwa yetu yanatokana na yeye - yaani yeye ametaka tuwe na hiyari, mtu aweze kujifikisha kwenye ukamilifu.

67


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:16 PM

Page 68

Tujifunze Misingi ya Dini Kwa hivyo wakati tuna hiyari na matakwa, pia tuko chini ya mamlaka yake na hatuwezi kuwa juu ya uwezo wake. Wakati ambapo tuna uwezo na nguvu, pia tunamtegemea yeye na bila ya yeye tutaangamia, na hii ndiyo maana ya jambo katika njia mbili kwani katika imani hii, hatumtambui kiumbe mwingine atakayelingana na Mwenyezi Mungu na kuwa mshirika wake, wala hatuamini kwamba viumbe wamelazimishwa kutenda wanayoyatenda tunasema kwamba wamedhulumiwa. Tumefundishwa somo hili na Maimamu wetu watukufu (a.s.) kwamba, kila walipoulizwa, je kuna njia iliyo kati ya imani ya ‘Mujabbira’ na ya ‘Mufawwidha’? Hujibu “Ndiyo, iko njia pana kuliko upana ulioko kati ya mbingu na ardhi.” (Usuulul-Kafi, kitabu 1, uk. 121). Qur’ani na suala ‘kulazimishwa’ na ‘kuachiliwa’ Qur’ani tukufu imeeleza suala hili waziwazi na ikathibitisha hiari ya mwanaadamu; kuna Aya nyingi zinazozungumzia hilo. Hebu tuangalie hoja zifuatavyo: a) Aya zote zinazohusu kuamrisha mema na kukataza maovu ni ushahidi wa uhuru wa kuchagua mwenyewe binadamu analolitaka kufanya, kwani kama mtu atalazimishwa kufanya vitendo vyake, kuamrisha mema na kukataza maovu kusingelikuwa na maana. b) Aya zote zinazowasifu watenda mema ni ushahidi tosha wa kuthibitisha kuwa mwanadamu ana hiyari, kwani mtu akilazimishwa jambo lolote lawama au sifa hizo hazitakuwa na maana yoyote. c) Aya zote zinazozungumzia juu ya kuulizwa siku ya Kiyama, kuhukumiwa watu, kisha adhabu na malipo mema, yaani Moto na Pepo, ni ushahidi pia wa kuonyesha mwanaadamu ana hiyari kwa 68


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:16 PM

Page 69

Tujifunze Misingi ya Dini afanyayo, kwani ikiwa mtu atachukulia kwamba amelazimishwa, basi kuulizwa, kuhukumiwa malipo mema na adhabu zitakuwa ni uonevu. d) Kuna Aya zinathibitisha kuwa mwanadamu ndiye mdhamini wa vitendo vyake nazo ni: “Kila nafsi itafungika (motoni) kwa amali mbovu ilizozichuma.” (74:38). Nyingine ni: “Kila mtu atalipwa kwa kile alichokichuma.”(52:21). Nyingine inasema: “Hakika sisi tumemuongoa (tumembainishia) njia (mbili hizi: hii ya kheri na hii ni ya shari). Basi (mwenyewe tena) atakuwa ni mwenye shukrani au mwenye kukufuru (kukanusha).” (76:3).

SOMO LA TISA UFAFANUZI JUU YA UONGOFU NA UPOTOVU Aina za uongofu na upotovu Hebu tuangalie mfano huu: Imetokea kwamba msafiri amekutana nawe na huku akiwa na anuani mkononi mwake, kisha akakuomba umsaidie kufika pale anapokwenda, hapo utachagua kufanya jambo moja kati ya wawili, aidha utafuatane naye mpaka anapokusudia kwenda kisha muagane, au umuonyeshe tu kwa kumuelekeza pale anapotaka kwenda. Ni dhahiri kwamba katika njia zote hizo utakuwa umemsaidia kufika pale aendapo, hata hivyo pana tofauti kati ya njia hizo: Ya kwanza ilikuwa ni kumchukua na kumfikisha, na ya pili ilikuwa ni kuelekeza tu, Qur’ani tukufu na Hadith zimeteja kuhusu njia zote hizo. 69


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:16 PM

Page 70

Tujifunze Misingi ya Dini Wakati mwingine uongofu huwa ni kwa upande wa sharia na kanuni na wakati mwingine kwa upande wa uumbaji. Kama Mwenyezi Mungu anavyoiongoza mbegu (manii) hadi kufikia kupatikana mwanadamu kamili; na njia zote mbili hizi zimetajwa katika Qur’ani na Hadith. Kwa ufafanuzi zaidi wa maana za uongofu (na kinyume chake, upotofu) hebu turejee nyuma katika mjadala wetu: Tunasoma katika Aya nyingi za Qur’ani tukufu kwamba, uongofu na upotovu ni kazi ya Mwenyezi Mungu. Bila shaka ‘kuonyesha njia’ kunatokana na Mwenyezi Mungu. Kwa nini? Kwa sababu ameleta Mitume na Vitabu vitakatifu ili kuonyesha njia watu. Lakini ‘kufika kwenye lengo’ (la kuongoka) kwa kulazimishwa naye, hakukubaliani na hiari ya kujichagulia, lakini kwa sababu uwezo na nguvu za kutuwezesha kuongoka, tumepewa na Mwenyezi Mungu, na yeye ndiye anayetufikisha katika njia hii, kwa maana hiyo basi uongofu pia unatoka kwake. Yaani kuandaa nyenzo na vitangulizi na kuweka chini ya mwanaadamu. Swali muhimu Hapa pana swali muhimu nalo ni kuwa, tunasoma katika Aya za Qur’ani tukufu kwamba:

“Kisha Mwenyezi Mungu anamuacha kupotea amtakaye, na anamuongoza amtakaye.” (14: 4). Kuna watu ambao, huzisoma bila ya mazingatio aya za Qur’ani na mfungamano wa tafsiri na baadhi ya Aya na nyinginezo, anaposoma Aya hiyo hapo juu, kwa haraka husema: “Ikiwa Mwenyezi Mungu 70


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:16 PM

Page 71

Tujifunze Misingi ya Dini humuongoza amtakaye na humpoteza amtakaye, basi tunakosa gani?” Jambo la muhimu ni kwamba ili tuzifahamu vizuri Aya za Qur’ani, ni lazima siku zote tuzisome kwa makini tukiangalia jinsi zinavyofungamana. Hapo tutataja baadhi ya Aya kuhusu uongofu na uotovu ili uweze kuzisoma uone jinsi zinavyofungamana na Aya hiyo tuliyoitaja hapo juu. “Mwenyezi Mungu huwathubutisha wale walioamini kwa kauli thabiti, katika maisha ya dunia na katika akhera.”

UFAFANUZI JUU YA UONGOFU WA UPOTEVU

“Na Mwenyezi Mungu huwaacha kupotea hao wenye kudhulumu (nafsi zao). Na Mwenyezi Mungu hufanya apendavyo.” (14:27). Katika Aya nyingine: “Kama hivyo, Mwenyezi Mungu humuacha kupotea yule anayepindukia mipaka katika maasia, anayojitia shaka.” (40:34). Na katika Aya nyingine:

“Na wale wanaojitahidi kwa ajili yetu, kwa yakini tutawaongoza katika njia zetu. Na bila shaka Mwenyezi Mungu yu pamoja na wafanyo mema.” 29:69).

71


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:16 PM

Page 72

Tujifunze Misingi ya Dini Kama tunavyoona, matakwa ya Mwenyezi Mungu si kuwa hayana hesabu (yaani yawe hivi hivi) yeye hawafikishi mtu kuongoka (asiyetaka) au amzuie asiyeongoka (anayetaka). Wale wanaopigana katika njia ya Mwenyezi Mungu, kupambana na matatizo ya nafsi zao na kuonyesha uthabiti, wameahidiwa uongofu, na huu ndio uadilifu hasa. Ama wale wanaodumisha dhulma na ukandamizaji, na wale wasioelekea kwenye uadilifu, shaka na vishawishika; Mwenyezi Mungu naye huwakosesha tawfiki ya kuongoka, na matokeo yake ni nyoyo kuwa nyeusi na hawataweza kufikia daraja ya kufaulu. Na hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu alivyotuachia vitendo vyetu na huu ndio Uadilifu. Elimu ya kale (ya Mwenyezi Mungu) ndiyo sababu ya kuasi? Hoja ya mwisho ambayo ni vyema tuitaje hapa katika mjadala huu wa ‘kulazimishwa na kuachiliwa’ ni kuhusu udhuru unaotolewa na baadhi ya ‘Mujabbira’ ambao ni elimu ya kale ya Mwenyezi Mungu. Wanauliza: “Je Mwenyezi Mungu hujua kama mtu fulani ataua au atalewa saa fulani au siku fulani?” Hapa tukijibu: “Hajui,” tutakuwa tumekanusha ujuzi wa Mwenyezi Mungu. Na tukikubali kuwa mwenyezi Mungu anajua kama mtu atafanya kosa hilo, basi itabidi mtu huyo afanye kosa hilo (kwani kujua kwa Mwenyezi Mungu huwajibisha jambo litokee) ama sivyo, ujuzi wake utakuwa na upungufu. Na hivyo, ili ujuzi wa Mwenyezi Mungu uhifadhike, itamlazimu atende dhambi kwa kufanya atakavyo Mwenyezi Mungu. Lakini ukweli ni kwamba, udhuru huu unatolewa na watu hao ili 72


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:16 PM

Page 73

Tujifunze Misingi ya Dini kuficha madhambi yao wanayotaka kuyatenda, lakini wamesahau kuwa tumeshasema kwamba Mwenyezi Mungu tayari alikwishajua tangu zamani kwamba tutaelekea kwenye hiyari ya matakwa yetu katika kufanya mema na maovu, yaani hiyari na matakwa yetu yanajulikana na Mwenyezi Mungu. Na hii ina maana kwamba endapo tutalazimishwa basi ujuzi wa Mwenyezi Mungu utakuwa haufai. (Angalia kwa makini hapa). Hebu tuongeze maswali katika maudhui haya. Chukua mfano wa mwalimu anayejua kuwa mwanafunzi mvivu ndiye atakayefeli katika muhula wa mwisho, na mwalimu huyo ana uhakika wa jambo hilo kutokana na uzoefu wa miaka mingi katika kazi ya ualimu. Sasa endapo mwanafunzi huyo atafeli, je ataweza kumlaumu mwalimu na kumwambia, kujua kwako kuwa nitafeli ndiko kulikonifanya nifeli? Hebu tupige mfano mwingine. Kuna mtu ambaye hatendi dhambi, akawa anafahamu kuwa kuna mauaji yatakayotokea siku fulani, kisha akaingilia kati kuyazuia yasitokee, je kujua huko kwake kutaondoa jukumu kwa mhalifu na kutamlazimisha atende maovu? Au tuchukulie kumeundwa chombo kipya kinachoweza kutabiri mambo yanayotokea kabla ya masaa machache, kitaweza kusema kuna mtu fulani atafanya jambo fulani saa fulani na wakati fulani. Je kutabiri huko kutamlazimisha mtu huyo kufanya hayo? Kwa ufupi elimu ya Mwenyezi Mungu hailazimishi mtu kutenda jambo.

73


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:16 PM

Page 74

Tujifunze Misingi ya Dini

SOMO LA KUMI UADILIFU WA MWENYEZI MUNGU NA SUALA LA MILELE Tunaelewa kwamba Qur’ani tukufu inataja waziwazi juu ya adhabu ya milele watakayopewa wanafiki, makafiri na watenda dhambi. Inasema: “Mwenyezi Mungu amewaahidi wanafiki wanaume na wanafiki wanawake na makafiri, moto wa jahanam kukaa humo daima. Huo unawatosha (kuwaadhibu); na Mwenyezi Mungu amewalaani; nao wana adhabu itakayodumu.” (9:68). Hivyo hivyo katika Aya inayofuata Mwenyezi Mungu amewaahidi waumini wanaume na waumini wanawake kukaa ndani ya mabustani ya Peponi daima, ikasema: “Mwenyezi Mungu amewaahidi waumini wanaume na waumini wanawake, mabustani (Pepo) yapitayo mito mbele yake - kukaa humo daima - na makazi mazuri katika mabustani hayo yenye kudumu. Na radhi za Mwenyezi Mungu ndizo kubwa zaidi. Huko ndiko kufuzu kukubwa.: (9: 72). Hapa kuna swali hujitokeza nalo ni kwamba, vipi itafaa mtu atende madhambi katika maisha yake ambayo ni miaka thamanini au mia moj na kisha aadhibiwe milele? Jibu: Ili kupata jibu sahihi katika maelezo haya, kuna kwanza; adhabu za Siku ya Kiyama hazifanani na mateso ya kidunia. Mathalan, mtu akipatikana na hatia hutiwa gerezani kwa kipindi maalumu, lakini adhabu za Siku ya Kiyama hutegemea athari za vitendo vya mtenda dhambi mwenyewe.

74


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:16 PM

Page 75

Tujifunze Misingi ya Dini Kwa lugha nyepesi ni kuwa, mateso atakayoyapata mtu akhera yatatokana na athari ya vitendo vyake. Qur’ani yasema;

“Basi leo nafsi yoyote haitadhulumiwa chochote kile wala hamtalipwa ila kwa yale mliyokuwa mkiyatenda.” (36:54). Tutatoa mfano mmoja mwepesi ili tuufahamu uhakika wa jambo hili: Kuna mtu anayetumia madawa ya kulevya na pombe, na kila anapoambiwa aache kutumia vitu hivyo vitakudhuru afya, moyo na mishipa yake ya fahamu, hakubaliani na nasaha hizo, bali kwa majuma na miezi kadhaa huzama katika vileo hivyo, hatimaye huanza kidogo kidogo kupata ugonjwa wa vidonda tumboni, maradhi ya moyo na maradhi ya mishipa ya fahamu na baadaye kwa miaka mingi, mpaka mwisho wa maisha yake husumbuliwa na maradhi haya na kulalama usiku na mchana. Je kutokana na mfano huu mtu atashindana kuhusu sababu zinazomfanya mtu aliyetenda dhambi kwa kipindi kifupi ateseke kwa kipindi kirefu? Tumeshaeleza tayari kujibu kwamba haya yote ni kwa sababu ya vitendo vyake mwenyewe, hata kama ataishi umri mrefu kuliko alioishi Nabii Nuh, nasi tumuone akiendelea kuishi katika hali hiyo hiyo ya maumivu, tutasema kwamba hayo amejitakia mwenyewe. Basi adhabu ya Siku ya Kiyama nayo iko hivyo hivyo, kwa hivyo hapana mtu atakayepinga Uadilifu hapo katika hali hii. Pili, ni makosa watu wengine kudhani kwamba muda wa adhabu ulingane na muda wa madhambi, kwa sababu ulingano kati ya madhambi na adhabu si ulingano wa muda (yaani hauangaliwi muda uliotenda madhambi), bali adhabu hutegemea aina ya madhambi yenyenye 75


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:16 PM

Page 76

Tujifunze Misingi ya Dini na athari zake. Kwa mfano, mtu amemuua mtu mwingine asiye na hatia kwa muda mfupi wa sekunde moja tu, kisha kulingana na sheria za baadhi ya nchi afungwe maisha. Hapa twaona kuwa kitendo chake cha kuua kilifanyika kwa sekunde moja tu lakini akahukumiwa kufungwa miaka chungu nzima, na hakuna mtu atakayeona kuwa huyu muuwaji ameonewa. Kwa nini? Kwa sababu hukumu hapa haiangalii muda wa siku, wiki, miezi au miaka aliyofanya kosa hilo, bali huangalia uzito wa kosa lenyewe. Tatu, kukaa milele motoni na adhabu za milele zitawapata wale tu waliojifungia milango yote ya uongofu na kujilazimisha kwenye ufisadi, upotovu, ukafiri na unafifiki kiasi ambacho kiza cha madhambi hufunika ubinadamu wao wote matokeo yake watu hao huwa ni sehemu ya madhambi na ukafiri. Qur’ani yasema:

“Naam, wanaochuma ubaya - na makosa yao yakawazunguka - hao ndio watu wa motoni; humo watakaa milele.” (2:81). Hawa ndio watu waliokataa kabisa uhusiano na Mwenyezi Mungu na wakajifungia milango yote ya uokovu na kufaulu. Ni kama ndege ambaye, kwa makusudi amevunja mbawa zake na kujinyoa manyoya yake akalazimika kutembea chini daima na asiweze kuruka tena angani. Tukiyaangalia kwa makini mambo haya matatu tuliyoyataja, tutafahamu waziwazi kuwa hukumu ya kukaa milele motoni kwa wanafiki na makafiri haipingani na Uadilifu wa Mwenyezi Mungu; hukumu 76


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:16 PM

Page 77

Tujifunze Misingi ya Dini hiyo ni matokeo mabaya ya vitendo vyao wenyewe, kwani walikuwa tayari wameshaonywa na Mitume kuhusu matokeo hayo mabaya. Basi hapana shaka kwamba wale watu ambao ujumbe wa Mitume wa Mwenyezi Mungu haukuwafikia na wakafanya makosa kwa kutojua, hawataadhibiwa vikali kiasi hicho. Ni muhimu pia kueleza kwamba, Aya za Qur’ani tukufu na Hadith za kiislamu zimefafanua kuwa bahari ya rehema za Mwenyezi Mungu ni pana kiasi kwamba mawimbi yake huosha madhambi ya wakosefu wengi. Baadhi yao kwa kuombewa, baadhi yao kwa msamaha, wengine kwa vitendo vyema vidogo walivyotenda, Lakini kwa utukufu wake huwapa thawabu nyingi; na wengineo watatakaswa na kuingizwa katika rehema yake baada ya kuteswa motoni kwa muda fulani. Watakaobaki motoni milele ni wale tu wenye kung’ang’ania kufanya uadui dhidi ya ukweli wa Mwenyezi Mungu, kufanya udhalimu, ufisadi na unafiki mpaka wakafanikiwa ndani ya kiza cha udhalimu ukafiri na kutokuwa na imani.

77


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:16 PM

Page 78

Tujifunze Misingi ya Dini

TUUJUE UTUME (3)

78


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:16 PM

Page 79

Tujifunze Misingi ya Dini

Kwa jina la Allah, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu

SOMO LA KWANZA HAJA YA KUWA NA VIONGOZI KUTOKA KWA MUNGU

Uchache wa elimu yetu Huenda baadhi ya watu wakataka kujua kama pana umuhimu wowote wa Mwenyezi Mungu kuwatuma mitume ili waongoze watu. Je akili zetu hazitoshi kuutambua ukweli? Je maendeleo ya kielimi hayatoshi kuvumbua siri zote na kuufunua ukweli? Aidha, chochote tutakachoambiwa na mitume lazima kitakuwa kati ya njia mbili, ama akili zetu zitafahamu vyema ama hazitafahamu. Katika hali ya kwanza hatuhitaji mitume, na katika hali ya pili, hatuwezi kukubaliana na jambo linalopingana na akili na hekima zetu. Tukiachana na hayo, je ni sawa kwa mwanaadamu kuwekwa mikononi mwa wengine, na kukubali atakachoambiwa bila ya kuuliza? Je mitume si wanaadamu kama sisi? Vipi tutajiweka chini na kumsikiliza tu mwanaadamu kama sisi vyovyote atakavyosema? Majibu ya maswali haya ni kama iafuatavyo: Kwa kuzingatia hoja zifuatazo tutaelewa waziwazi daraja ya mitume katika maisha ya mwanaadamu.

79


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:16 PM

Page 80

Tujifunze Misingi ya Dini 1. Ni lazima tutambue kwamba ujuzi tulionao ni mchache. Pamoja na maendeleo yote tuliyoyafikia wanaadamu katika sayansi na teknolojia, ukilinganisha kile tunachokijua na tusichokijua; ni kama kulinganisha tone moja la maji na habari (tusiyoyajua ni mengi) kama walivyosema baadhi ya wasomi wakuu kwamba, ujuzi wote tulionao hivi sasa unaweza kuwa ni ‘abc’(alfabeti tu za kitabu kikuu cha ulimwengu). Kwa maelezo mengine upeo na ufahamu wa akili yetu ni mdogo sana unaong’arishwa na elimu zetu. Ni kweli kwamba akili zetu ni kama taa yenye mwanga mkali, lakini wahyi wanaokuja nao mitume kutoka kwa Mwenyezi Mungu ni kama jua ling’aalo duniani. Je mtu si anaweza kusema, “maadamu nina taa yenye mwanga mkali, basi sina haja ya jua?” Isitoshe kuna mfano ulio dhahiri: Mambo ya kimaisha yamegawanyika katika mafungu matatu: ‘Yanayozingatia akilini,’ yasiyoingilika akilini,’ na ‘yasiyojulikana.’ Mitume kamwe hawawezi kusema ‘upuuzi’ yaani kusema jambo litakalopingana na akili au hekima, na endapo watafanya hivyo, basi hao sio mitume. Aidha, wao hutusaidia kufahamu mambo yasiyojulikana, na hili ni jambo muhimu sana kwetu. Hivyo basi, wale waliosema zamani kwamba ikiwa mtu ana akili ya kutosha hahitaji mitume, (mfano taifa la Barham la huko India na kwingineko) au hawa wanaodai siku hizi kwamba elimu za kutosha alizonazo mwanaadamu hahitaji mitume na mafunzo yao; hawa hawajatambua mipaka ya elimu ya mwanaadamu wala maana ya ujumbe wa mitume. Mtu huyu aliyesoma abc (alfabeti) katika darasa la kwanza kisha akasema, “kwa hakika nimekwishajua kila kitu, hivyo sihitaji mwalimu.” Je haya si maneno ya kipuuzi? Mitume si waalimu tu, bali ni viongozi, na habari zinazohusu uongozi wao zinahitaji majadiliano ya pekee, ambayo tutayafafanua katika masommo 80


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:16 PM

Page 81

Tujifunze Misingi ya Dini yajayo. 2. Hakuna aliyesema ati wanaadamu lazima wawe chini ya mtu. Tulichosema ni kwamba mitume - kama tutakavyothibitisha huko mbele wameambatana na wahyi wa Mwenyezi Mungu, yaani elimu isiyokwisha ya Mwenyezi Mungu, na ndipo tu ujumbe wa Mwenyezi Mungu utakapokubaliwa, na ndipo tutakapokubali mafunzo yao ya kweli kwa nyoyo zetu zote. Chukua mfano: Endapo nitafuata ushauri wa daktari hodari, je nitakuwa nimefanya makosa? Bila shaka sikufanya, ikiwa ni hivyo, basi mitume ni madaktari wakuu wa roho. Ikiwa nitakubali masomo niliyofunzwa na mwalimu yanayowiana na akili, je nitakuwa nimekosa? Ikiwa ni hivyo, basi mitume ndio walimu wakuu wa wanaadamu. Lililo muhimu zaidi kwetu, ni kujaribu kuzichunguza kwa makini sana sababu za msingi za Mwenyezi Mungu, nazo ni:

Haja ya kujifunza: Tuchukue mfano, lau tutapanda farasi (kwa bandia tu) aliyetengenezwa kwa umeme (uendao kwa kasi sana) na kila sekunde moja tusafiri kilometa laki tatu katika uwanja usio na mwisho, bila shaka tutahitaji tuishi maelfu ya miaka kama ya nabii, Ili tuweze kuona japo sehemu ndogo tu ya dunia hii pana. Ni dhahiri kwamba dunia hii, pamoja na upana wake haikuumbwa kiholela, na kama tulivyosoma katika somo la kumjua Mwenyezi Mungu, kwamba kuubwa kwa ulimwengu huu hakumnufaishi chochote Mwenyezi Mungu, kwa sababu yeye ni mkamilifu asiyehitaji chochote, asiye na mwisho wala upungufu ambao atautosheleza kwa kuumba dunia na watu. 81


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:17 PM

Page 82

Tujifunze Misingi ya Dini Hivyo basi, kwa kuongeza ni kwamba, lengo lake ni kuwahurumia viumbe na kuwasaidia kufikia ukamilifu. Kama mfano wa jua linalotuangazia bila ya kuhitajia chochote kutoka kwetu. Mwanga na joto tulipatalo kutokana na jua ni kwa manufaa yetu tu. Na kama si hivyo, tutalilipa nini? Kwa upande mwingine, tusema akili na elimu zetu zinatosha kutupeleka kwenye njia sahihi na kutufikisha kwenye utu kamili? Je ni ngapi za ulimwengu tunazozijua? Ni upi kweli wa maisha? Dunia iliumbwa lini? Bila shaka hakuna ajuaye majibu ya maswali haya. Au dunia itabaki hadi lini? Hili pia hakuna alijuaye. Kila msomi wa kibinadamu ana maoni ya kijamii na kiuchumi tu. Mathalani, wasomi fulani wanapendekeza ifuatwe siasa ya ubepari, na wengine wanaonelea kwamba ukomunisti ndiyo nadharia bora, wengine hawaungi mkono upande wowote na kuziachilia mbali nadharia zote hizo. Katika masuala mengine ya kimaisha, pia kuna tofauti za maoni miongoni mwa wasomi, kiasi cha kumfanya mtu apigwe na butwaa, asijue pa kufuata. Hapa ndio lazima tukubali kwamba, ili tuweze kufikia shabaha ya msingi ya kuumbwa, yaani ukamilifu na ustawi wa mwanaadamu katika pande zote, tunahitaji kupata mfululizo wa mafunzo sahihi yasiyo na makosa, yenye mategemeo ya ukweli wa maisha, na yanayoweza kutusaidia kupita katika njia hii ndefu na kufikia kwenye shabaha kuu. Na hili halipatikani ila kupitia kwenye elimu ya Mwenyezi Mungu yaani, wahyi wa Mwenyezi Mungu kupitia kwa mitume. Kwa sababu hii, Yeye aliyetuumba ili tuifuate njia hii ni lazima aweke elimu chini yetu.

Haja ya uongozi katika jamii na tabia Kama tujuavyo, pamoja na elimu na akili tulizonazo pia tuna silika ndani ya maumbile yetu. Silika ya kujipenda, ghadhabu, ukali, tamaa na nyingine 82


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:17 PM

Page 83

Tujifunze Misingi ya Dini nyingi. Tusipoweza kuzimiliki vyema silika zetu, hapana shaka zitatutawala na kuzifunga elimu na akili zetu. Wanaadamu - kama walivyo - madhalimu katika historia mara hubadilika na kuwa hatari hata kushinda mbwa mwitu. ( wanapotawaliwa na silika hizo). Hivyo basi; twahitaji mwalimu wa elimu ya maadili. Twahitaji kielelezo kizuri ambapo tutajifunza kutoka kwake kulingana na kanuni za ufundishaji anazofunza, na wanafunzi walio tayari kumuiga. Hivyo, anahitajika mtu mwenye nidhamu, aliyekamilika ili kutuongoza katika njia hii iliyobeta na yenye kombokombo, atakayeweza kuziokoa silika zetu zisipotoke, na kuweka misingi ya maadili na vitendo vyema ndani ya nyota zetu. Pia aweze kutupa uthabiti, ujasiri, uhusiano mwema na viumbe, udugu, usemehevu, uaminifu, ukweli na usafi katika nafsi zetu. Je ni nani huyo zaidi ya mtume asiyetenda dhambi, mtakatifu, angeliweza kuteuliwa kwa kazi hii ya kuwa mwalimu wa kiongozi? Kwa sababu hii, ni muhali kwa Mwenyezi Mungu Mwenye huruma nasi asituletee viongozi na waalimu kama hao. (Maelezo zaidi ya somo hili yataendelea katika somo lijalo).

83


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:17 PM

Page 84

Tujifunze Misingi ya Dini

SOMO LA PILI HAJA YA MITUME KULETA SHERIA ZA MWENYEZI MUNGU Katika somo lililopita tumejua haja ya kuwapo kwa mitume katika sehemu mbili, ya malezi na ya mafunzo. Sasa tumefikia mahali ambapo tunahitaji kujua kuhusu kanuni za kijamii na wajibu muhimu wa mitume katika sehemu hii. Tanajua kwamba sehemu muhimu ya maisha ya mwanaadamu ambayo ndiyo sababu ya maendeleo yake katika nyanja mbali mbali, ni maisha ya kijamii. Ni kweli kabisa kwamba, lau wanaadamu watatengana kila mtu kuishi peke yake, maisha yao yangelikuwa hayatofautiani na ya watu walioishi katika ‘Enzi ya mawe’ (Stone –age). Naam, ushirikiano na juhudi za pamoja ndizo zilizowasha taa ya ustaarabu na maendeleo. Na ni kwa kupitia kwenye ushirikiano huo tu ndipo uvumbuzi wote wa kisayansi ulipoanzia. Mathalan, tukiangalia safari ya kwenda mwezini, utaona kwamba, kufanikiwa huko si kwa ajili ya tija ya kazi ya wanasayansi kadhaa, tu bali ni tija ya juhudi iliyofanywa na kutokana na uzoefu walioupata kwa kuishi pamoja, ndipo ujuzi huu ukafikia pale ulipo leo. Ikiwa daktari wa kisasa aliyehitimu anaweza kufanya upasuaji wa moyo kwa kuutoa kutoka kwa maiti na kuweka kwa mtu mwingine hai na hivyo kuyaokoa maisha yake, basi kazi hiyo isingefaulu ila kwa kuwa ni tija ya uzoefu wa miaka mingi wa madaktari waliowapokeza wanafunzi wao.

84


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:17 PM

Page 85

Tujifunze Misingi ya Dini Lakini maisha ya kijamii, kwa upande mwingine, huwa na matatizo kutokana na kuhitilafiana kwa haki na hivyo kuyakoa maisha yake, basi kazi hiyo isingefaulu ila kwa kuwa ni tija ya uzoefu wa miaka mingi wa madaktari waliopokeza wanafunzi wao. Lakini maisha ya kijamii, kwa upande mwingine, huwa na matatizo kutokana na kuhitilafiana kwa haki na manufaa ya wanaadamu kati yao, jambo linalosababisha mizozo na hata vita. Ndipo kukawa na haja ya kuwa na sheria yenye mpangilio mzuri na masharti yaliyo wazi. Sheria zitakazoweza kutanzua matatizo mkubwa matatu: Kufafanua jukumu la mmoja kwenye jamii. Wajibu wa jamii nao ubainishwe na vipaji vitumike kwa uwiano ili vilete ustawi kwa binadamu. Kutengeneza njia zifaazo kufuatwa ili kila mmoja aweze kutimiza wajibu wake ipasavyo. Kuzuia watu kutoingilia katika haki zao, hivyo kuzuia machafuko na mizozo itakayojitokeza miongoni mwao, na kuwaadhibu wachokozi inapobidi.

Ni nani mletaji sheria? Sasa tuangalie anayefaa kuleta sheria hizi zitakazokidhi mahitaji ya mwanaadamu katika hali ambayo masharti yote matatu yaliyotangulia yaweza kupatikana yaani kufafanua mipaka, majukumu na haki za kila mtu katika jamii ili utaratibu ufaao ufuatwe na uadui uzuiwe. Hebu tukupigie mfano: Jamii ya watu inaweza kufananishwa na treni kubwa, na viongozi ndiyo injini yake inayofanya hii jamii ya watu kuelekea pale inapokusudia. Sheria ni kama reli au njia zinazofanya treni kufuata na kufika pale inapokwenda, ikipita kwenye njia zenye konakona. 85


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:17 PM

Page 86

Tujifunze Misingi ya Dini Ni dhahiri kwamba treni nzuri ni lazima ifuate masharti yafuatayo: a) Ardhi inapopita treni nzuri ni lazima iwe na nguvu za kutosha kuweza kuhimili kulemea kwake. b) Ni lazima umbali uliopo baina ya reli mbili uwe sawa sawa na magurudumu na kuta za mashimo ya reli; na urefu wa mashimo ya reli ulingane na treni ipitayo. c) Miinuko wa mabonde yasizidi auwezo wa nguvu za breki ya treni. d) Ni lazima ichunguzwe kwa makini kama pana uwezekano wa kuwapo maporomoko ya ardhi au mafuriko katika njia ifuatayo treni, ili kupita bila ya taabu yoyote. Baada ya mifano hii, naturudi katika jamii ya mwanaadamu. Mletetaji sheria ambaye anapenda kuwapa wanaadamu sheria bora, ni lazima awe na sifa zifuatazo: Ayajue vizuri mazingira ya wanaadamu kwa kuzijua silika, hisia, mahitaji na matatizo yao. Sifa zote nzuri na vipaji vya wanaadamu zitiliwe maanani na sheria zitumike kwa manufaa na ustawi wao. Awe na uwezo wa kuotea matukio katika jamii kabla ya kutokea na hivyo hadhari zifaazo zichukuliwe. Asiwe ni mwenye kujivutia maslahi yake katika jamii kama vile wakati wa kuleta sharia asifikirie maslahi yake, ya familia yake au ya watu wanaomhusu.

86


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:17 PM

Page 87

Tujifunze Misingi ya Dini Awe anajua hatua ya mendeleo anayopiga mwanaadamu na kujua kushindwa kwake. Awe na daraja ya mwisho kabisa ya kutofanya makosa na kughafilika. Awe na sifa ya mwisho ya mletaji sharia huyo, ni kuwa na nguvu kuu kiasi cha kutotishwa na nguvu yoyote na kutomwogopa yeyote. Na wakati huo huo awe na kiwango kikubwa cha upole na mwenye huruma na mapenzi. Hebu niambie, ni nani aliyekusanya sifa zote hizi? Je mwanaadamu anaweza kuwa ndiye mletaji sharia aliye bora? Na je kuna mtu yeyote aliyepata kumwelewa mwanaadamu vilivyo hadi sasa? Ndipo msomi mmoja maarufu wa kisasa akaandika kitabu alichokiita ‘Mwanaadamu, kiumbe asiyejulikana.� Je roho, silika na hisia za mwanaadamu zinajulikana vilivyo mpaka leo hii (sio juu juu tu?). Je kunaweza kupatikana mtu miongoni mwa watu wa kawaida ambaye hana maslahi ya kibinafsi? Je wamjua yeyote miongoni mwa watu wa kawaida asiyetenda dhambi au kufanya makosa na ambaye anajua matatizo yote ya jamii na ya watu. Hivyo basi hakuwezi kupatikana mtu wa kawaida atakayekuwa na sharti zinazohitajika, isipokuwa Mwenyezi Mungu ambaye anampa wahyi yule anayemuona kuwa anafaa kuleta sharia. Hiyo ni kusema: Hakuwezi kuwa na mletaji sheria mkamilifu kuliko Mwenyezi Mungu na mitume waliopokea ufunuo kutoka kwake. Kwa hali hiyo, tunaongeza kusema kwamba, Mwenyezi Mungu aliyemuumba Mwanaadamu ili afikie ukamilifu, ni lazima awapelekee mtu ambaye ni kiongozi wa kuwaletea sharia zake. 87


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:17 PM

Page 88

Tujifunze Misingi ya Dini Ni dhahiri kwamba watu watakapojua ya kuwa sharia hizo ni za Mwenyezi Mungu watazifuata kama inavyostahili na kwa yakini kabisa. Kwa maneno mengine, kujua huku ndiko dhamana kubwa ya kufuata sharia hizo za ukamilifu.

Uhusiano kati ya Upweke wa Mwenyezi Mungu (Tawhid) na utume Hapa ni muhimu tuiangalie hoja ifuatayo, nayo ni utaratibu wa kuumbwa, ambao wenyewe ni ushahidi tosha wa kuwepo kwa mitume na ujumbe wa Mwenyezi Mungu. Sababu ni kwamba, tukitupa jicho kwenye utaratibu wa ajabu wa uumbaji wa Mwenyezi Mungu; tutaona kwamba kutokana na huruma yake, hakuacha chochote katika kukidhi mahitaji ya viumbe, mathalan, alipotupa macho ili tuone, pia aliyapa kope na kingo ili kuyakinga na mwanga uingiapo na hivyo kuyafanya yasidhurike. Zaidi ya hayo ametengeneza kitu katika kingo za jicho kinachotoa machozi yanayolifanya jicho lisiwe kavu. Kisha akatengeneza tundu ndogo ya kutolea machozi yaliyozidi mpaka kwenye pua, lau si tundu hiyo basi nyuso zetu zingejaa machozi. Na pambizoni mwa jicho kuna mishipa mbalimbali inayowezasha macho kuwa na uwezo wa kuzunguka na kuweza kuona sehemu mbalimbali bila ya mtu kugeuza kichwa. Je inawezakana Mwenyezi Mungu aliyekidhi mahitaji yote ya mwaadamu asimletee kiongozi mtakatifu na mkweli wa kuleta ufunuo wake? Mwanafalsafa mashuhuri Ibn Sina ameandika katika kitabu chake kiitwacho Ash-Shifaa’ amesema: “Haja ya kuletwa mitume kwa wanaadamu, kwa ajili ya wokovu na ukamilifu wao, ni kubwa zaidi, kuliko haja ya kuwa na nyusi na kope. Je inawezekana Mwenyezi Mungu awajibishe kupatikana kwa hivyo vingine vidogo na aache haya?” 88


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:17 PM

Page 89

Tujifunze Misingi ya Dini

SOMO LA TATU KWA NINI MITUME HAWATENDI DHAMBI? Jambo la muhimu zaidi kwa mitume ni lazima wawe waaminifu kwa watu wote kiasi kwamba maneno yale yasiwe na uongo au makosa; vinginevyo uongozi wao utayumba. Endapo mitume hawakuhifadhiwa na madhambi, kwa udhuru kwamba walifanya makosa, bila shaka watu wanaotafuta ukweli kutoka kwenye mahubiri yao wataushuku mwito wao, na kwa vyovyote maneno yao hayatakubaliwa kwa dhati. Na uaminifu ndiyo sababu kubwa ya kuwa mitume wamehifadhiwa na madhambi (hawatendi dhambi). Kwa maneno mengine, itakuaje Mwenyezi Mungu awape watu maamrisho yake kupitia kwa mtu asiye mwaminifu, awezaye kukosa au kutenda dhambi? Bila shaka watu wasingelimfuata. Kwani kama wangelifuata nao wangelikosa, na kama wasingelimfuata, cheo chake acha uongozi kisingelikuwa na maana na hasa kwa vile nafasi ya uongozi wa mitume inatofautiana kabisa na ya uongozi wa watu wengine, wanaopokea utaratibu wao wa kiitikadi kutoka kwa mitume. Ndipo tunaona wafasiri wakuu wakifasiri Aya hii:

“….Mtiini Mwenyezi Mungu na mtiini Mtume na wenye mamlaka juu yenu..” (4:59).

89


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:17 PM

Page 90

Tujifunze Misingi ya Dini Wamesema kwamba amri hiyo ya kutii ni kwa sababu mtume na ‘mwenye mamlaka’ wote wamehifadhiwa na madhambi. Na viongozi watakatifu walio kama mitume ndiyo wajulikanao kama ‘wenye mamlaka.’ Kinyume na hivyo, Mwenyezi Mungu asingeliamuru kuwatii inavyopasa. Njia nyingine ya kuthibitisha kutakasika kwa mitume ni kuwa hana vivutio katika nafsi yake, vyenye kumfanya atende dhambi. Sisi wenyewe tukijiangalia tutaona kwamba sisi pia (tukiwa na akili timamu) tunakurubia kuwa ni wenye kuhifadhiwa na kutenda makosa fulani. Hebu tazama mifano ifuatayo: Je waweza kupata mtu mwenye akili akiwaza kula moto, takataka au uchafu? Je waweza kumwona mtu mwenye akili timamu kutembea uchi barabarani na madukani? Bila shaka hayo hayawezekani. Tutakapomuona akifanya vitendo hivyo, tutatambua kwamba mtu huyo ni punguani, kwani mwenye akili timamu hawezi kuyatenda haya. Tukiufafanua zaidi mwendo huo, tutaona ubaya wa vitendo hivyo uko waziwazi kiasi ambacho mwenye akili hawezi kufikiria kufanya hivyo. Hapo ndipo tunapoweza kuelewa maana ya ibara hii fupi isemayo kwamba kila mwenye akili na afya hawezi kufanya vitendo hivyo, na akitenda, tutatambua kwamba mtu huyo ni punguani, kwani mwenye akili timamu hawezi kuyatenda hayo. Kutoka daraja hii, tunapiga hatua moja mbele. Tunaona kuna baadhi ya watu ambao hawatendi kabisa vitendo vibaya (ambavyo watu wengine wa kawaida huvitenda). Kwa mfano, daktari anayejua vizuri aina mbalimbali za viini vya maradhi, hawezi kunywa maji machafu yanayotokana na nguo chafu ya mgonjwa anayeugua maradhi hatari yaambukizayo; wakati ambapo mtu asiyejua 90


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:17 PM

Page 91

Tujifunze Misingi ya Dini chochote anaweza kunywa. Tukiongeza mfano zaidi, tumefikia kwamba kadri daraja ya mtu inavyopanda katika kujua ubaya wa vitendo viovu, ndivyo kujizuia kwake kufanya maovu kunavyozidi. Tukiangalia zaidi, tumefika kwamba ikiwa imani ya mtu kujichunga kwake na kukubali uadilifu wa Mwenyezi Mungu, huko juu kiasi ambacho huwa kama unavyoyaona yote hayo kwa macho yake, mtu kama huyo hawezi kutenda dhambi na kila kitendo kibaya unachokiona huwa ni kama sisi unavyomuona mtu akitembea vibaya barabarani. Kwa mtu huyu mali ya haramu ni sawa na makaa ya moto. Ni kama sisi vile hatuwezi kuweka kaa la moto vinywani mwetu, yeye pia hawezi kuweka kitu cha haramu mdomoni mwake. Mwisho tunajumuisha maelezo haya kwa kusema kwamba mitume kwa sababu ya elimu, utakatifu na imani isiyo ya kawaida waliyokuwa nayo imeweza kuondosha vivutio vya dhambi, na mambo yanayoghuri hayawezi kushinda akili na imani walizonazo mitume. Ndipo tukasema kwamba mitume ni watakatifu na wamehifadhiwa na madhambi (maasum). Vipi utakatifu (kutotenda dhambi) uwe ni fahari? Baadhi ya watu wasiofahamu maana ya utakatifu na kuhifadhiwa na madhambi wanakanusha sifa ya utakatifu kwa kudai kwamba ikiwa Mwenyezi Mungu ndiye anayeweka kizuizi ili mtu madhambi basi hilo si jambo la fahari kwa mtu huyo, kwa sababu kuhifadhiwa kwake ni kwa kulazimishwa. Lakini suala la majadiliano juu ya jambo hili, liko wazi. Kuhifadhiwa mitume kutokana na madhambi si jambo la kushurutishwa, bali ni jambo 91


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:17 PM

Page 92

Tujifunze Misingi ya Dini lililotokana na imani zao thabiti, akili na elimu zao zisizo na kifani, na hii ni fahari kubwa mno kwao. Mathalani, iwapo daktari atakuwa mwangalifu wakati wa kumtibu mtu mwenye ugonjwa hatari, je kufanya hivyo kunaonyesha kwamba yeye anashurutishwa? Au mtu akifuata kanuni za afya inavyopasa, je hii ni fadhila (aliyopewa na Mwenyezi Mungu)? Iwapo wakili atajaribu kutetea kosa, je hii ni fadhila pia? Kwa maana hiyo, kutofanya dhambi kwa mitume ni kwa hiari yao na pia ni fahari kubwa kwao.

SOMO LA NNE NJIA NZURI ZA KUWAJUA MITUME Bila shaka haiingii akilini kusadiki madai ya kila anayedai Utume. Yawezekana madai ya Utume ni ya kweli, lakini pana uwezekano pia mzushi kujidai kuwa yeye ni Mtume. Kwa hiyo ni lazima pawe na kipimo maalumu cha kupitia madai ya utume na uhusiano wao na Mwenyezi Mungu. Pana njia nyingi zilizoko mpaka kufika shabaha hiyo. Njia hizi mbili zifuatazo ni za muhimu: Kuchunguza kwa makini yaliyomo katika mahubiri yake, na mkusanyiko wa sheria na dalili. Kuwa na miujiza inayozidi mwanaadamu wa kawaida.

92


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:17 PM

Page 93

Tujifunze Misingi ya Dini Hebu kwanza tuzungumze juu ya miujiza. Kuna baadhi ya watu wanaoshangazwa na neno ‘miujiza’ au hulichukua kama ngano na masimulizi tu, lakini tukitazama kwa makini maana ya ‘miujiza’ tutapata picha sahihi kabisa ya neno hili. Muujiza si jambo lisilowezekana au lisilo na sababu, au kwa maelezo mepesi, ni jambo lisilo la kawaida. Ni kitendo kilicho zaidi ya uwezo wa mwanaadamu wa kawaida, ambacho hufanyika kwa msaada unaotokana na uwezo ulio juu ya ‘nguvu- asili’ (Nature). Kwa hiyo, Miujiza ina masharti yafuatayo: Liwe ni jambo linalowezekana na kukubaliwa. Watu wa kawaida hata wawe mabingwa washindwe kufanya miujiza kwa kutumia uwezo wa kibinadamu tu. Anayefanya miujiza ni lazima awe na uhakika wa anachokifanya, kiasi ambacho awe tayari kuwaita wengi na kuwataka wafanye kama alivyofanya. Kuwe hapana mtu mwingine awezaye kufanya miujiza na hivyo kila mtu kukubali kushindwa mbele ya miujiza. Miujiza ni lazima ihusiane na madai ya utume au uimamu (hivyo basi, kitendo chochote cha ajabu kitakachofanywa na asiyekuwa mtume au imam mtakatifu si muujiza bali ni ‘karama’). Baadhi ya mifano iliyo dhahiri: Watu wengi wanafahamu miujiza iliyokuwa ikifanywa na nabii Issa (a.s.) aliyekuwa akifufua maiti na kuponya wagonjwa wasiotibika.

93


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:17 PM

Page 94

Tujifunze Misingi ya Dini Je kuna hoja yoyote ya kiakili, inayoweza kuthibitisha kwa nini mwanaadamu aliyekufa hawezi kuwa hai? Je kuna kuthibitisha kwa nini mgonjwa mwenye maradhi sugu kabisa hayawezi kuponywa? Bila shaka uwezo alionao mwanaadamu kwa wakati huu hauwezi kufufua maiti au kutibu baadhi ya maradhi, hata kama iwe madaktari wa dunia nzima watashirikiana kubadilishana uzoefu na ujuzi. Lakini ni kitu gani kitakachoweza kumzuia mtu aliyepewa uwezo na Mwenyezi Mungu, kutoka kwenye bahari ya elimu ya Mwenyezi Mungu isiyokwisha, kuweza kufufua maiti na kuponya wenye ugonjwa usiotibika? Sayansi inasema, “Sijui na siwezi.” Lakini haikusema kwamba hilo haliwezekani. Mfano mwingine: Ni muhali kwa mwanaadamu kwenda mwezini bila kutumia chombo, lakini wakati huohuo hakuna kinachoweza kuzuia nguvu ya hali ya juu na farasi mwenye nguvu kuliko farasi wa kawaida awe chini ya mtu na aweza kupaa naye hadi mwezini au juu ya sayari zilizo juu ya mwezi. (Mtume Muhammad alifanya hivyo, soma kisa cha Mir’aj). Kwa hivyo basi, ikiwa mwaadamu anaweza kufanya jambo la ajabu kisha akadai utume na kuwataka wenzake wafanye hivyo hivyo, nao wakashindwa kufanya hivyo, hapo tutajua kwamba kitendo hicho ni cha muujiza unaotoka kwa Mwenyezi Mungu, kwa sababu Mwenyezi Mungu hawezi kumpa uwezo wote huo mtu mzushi atayewapoteza viumbe wake (soma kwa uangalifu maelezo haya).

Miujiza sio mazingaombwe Kuwepo kwa siasa kali zenye mrengo wa kulia na kushoto daima kumekuwa ndio chimbuko la ufisadi na kuficha ukweli. Hata kuhusu miujiza pia jambo hili linadhihiri, ambapo kuna baadhi ya wasomi bandia wanokanusha miujiza. Wengine wanajaribu kutia chumvi kwa kuzichukua 94


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:17 PM

Page 95

Tujifunze Misingi ya Dini ‘Hadith’1* dhaifu na hekaya za kishirikina ambazo, kwa msaada wa maadui, huzichanganya na miujiza ya mitume ya kielimu na kuficha kwa hekaya za uongo ili miujiza hasa isijulikane. Kwa sababu hii ndipo wanavyuoni wa kiislamu daima huwa waangalifu sana kwa kuepuka makosa yanayopatikna katika Hadithi zinazohusiana na miujiza. Na kwa sababu hii hii ndipo ikaanzishwa elimu ya ‘maisha ya wapokezi wa Hadithi’. Ili mfumo wa upokezi wa Hadith ujulikane, na Hadith ‘sahih’ (ya kweli) na ‘Dhaif’ (isiyo na uhakika) zitofautishwe. Na isiyofaa isichanganywe na inayofaa. Mbinu zinazotumiwa siku hizi na wakoloni na walahidi, ni kujaribu kuchanganya itikadi nzuri na mbaya ili kuzifanya nzuri zionekane kuwa hazina maana. Kwa hiyo ni lazima tuwe macho na njama hizi za maadui. Kuna tofauti gani ya miujiza na vitendo vingine visivyo vya kawaida? Tumepata kusikia mara nyingi habari za mawalii2 wanaoweza kufanya mambo ya ajabu (karama). Na ni watu wengi walioyashuhudia hayo, si riwaya tu. Tofauti za miujiza na maajabu mengine: Hapo ndipo twajiuliza, pana tofauti gani kati ya karama na miujiza ya mitume? Na tutumie kipimo gani ili tuweze kutofautisha? Swali hili lina majibu mengi, na yaliyo wazi ni haya mawili: Daima walii huonyesha maajabu yenye kipimo. Yaani hakuna walii awezaye kufanya shani kama anavyotaka. Yeye huweza kufanya ile aliyojizoeza tu kuifanya na kujifunza jinsi ya kufanya vizuri na ile aijuayo vyema. *Hadithi”: Ni maneno ya Mtume Muhammad yaliyopokewa na kuhifadhiwa 2. Mawalii: Ni watu waliofikia daraja ya juu ya kumcha Mungu kiasi cha kuweza kuonyesha karama. 95


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:17 PM

Page 96

Tujifunze Misingi ya Dini Na sababu ya hivyo iko wazi; ni kuwa uwezo wa kila mwanaadamu una mipaka, tena katika baadhi ya mambo tu anayoyajua. Lakini maajabu ya mitume hayana kikomo, hapana masharti ya kufanya, wanaweza kufanya muujiza wowote wanaotakiwa kuufanya, kwa sababu wanapata uwezo unaotokana na uwezo wa Mwenyezi Mungu usiokwisha, kama tunavyojua kwamba uwezo Wake hauna kikomo, kinyume na uwezo wa mwanaadamu. Jambo linalofanywa na walii, pia linaweza kufanywa na walii mwingine kama alivyofanya, yaani hauzidi uwezo wa mwanaadamu. Kwa hiyo, aonyeshaye karama hawaiti wengine kufanya hivyo na hashindani nao, kwa sababu anajua kwamba kuna watu walioko mjini hapo au jirani wawezao kufanya vivyo hivyo. Lakini mitume, huku wakiwa na hakika, huwaita wengine na kushindana nao katika jambo hilo wakisema, “Hata kama mtawakusanya wafanye miujiza kama tunavyofanya hawataweza kufanya.” Tofauti hii iko kati ya miujiza na ‘uchawi’ inarejea katika tofauti mbili, kama tulivyoeleza zinavyotofautisha miujiza na ‘uchawi’. (kwa hiyo unaposoma uwe muangalifu).

96


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:17 PM

Page 97

Tujifunze Misingi ya Dini

SOMO LA TANO MUUJIZA MKUU WA MTUME MUHAMMAD Wanavyuoni wote wa kiislamu wanaamini kwamba Qur’ani ndiyo muujiza mkuu wa Mtume Muhammad. Tunasoma kuwa Qur’ani ndicho Kitabu kikuu kupita vyote, ni kwa sababu: Kwanza, Qur’ani si muujiza wa kiakili tu, bali pia inafungamana na nafsi za watu. Pili, ni muujiza wa milele. Tatu: Ni muujiza uliosikika kwa zaidi ya karne kumi na nne ukisema: ‘Ikiwa hamuamini kama hiki ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu, basi leteni kitabu kama hiki.’ Mwito huu wa kutaka wapinzani walete kitabu kilicho sawa na Qur’ani au mfano wake umekuja mara nyingi katika Qur’ani. Kuna Aya isemayo:

“Sema, hata wakikusanyika watu (wote) na majini ili kuleta mfano wa hii Qur’ani basi hawangaliweza kuleta mfano wake, hata kama watasaidiana wao kwa wao.” (17:88). Katika Aya nyingine imerahisisha sana masharti ya kuleta kitabu kilichofanana nayo, imesema: “Ndiyo kweli wasema kuwa: ‘Amekitunga 97


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:17 PM

Page 98

Tujifunze Misingi ya Dini mwenyewe (Muhammad kitabu hiki)’ Sema: Basi leteni sura kumi za uongo zilizotungwa mfano wa hii, na waiteni muwawezao (kuwaita) badala ya Mwenyezi Mungu (waje wakusaidieni kutunga hivyo) ikiwa mnasema kweli.’” (11:13). “Na kama hakukuitikieni, basi jueni ya kwamba kimeteremshwa kwa elimu ya Mwenyezi Mungu.” (11:14).

“Na kama mna shaka na hayo tuliyoyamteremshia Mtume Wetu, basi leteni Sura moja iliyofanywa na mtu aliye mfano wake, na muwaite waungu wenu waisokuwa Mwenyezi Mungu (wawasaidieni); ikiwa mnasema kweli.” (2:23). Katika Aya inayofuatia inasema waziwazi:

“Na msipofanya - na hakika hamtafanya kamwe - basi uogopeni moto.” (2:24). Mwito huu uliokuwa mara kwa mara ukiwataka wapinzani wajitokeze katika ushindani na Qur’ani, unaonyesha kwamba Mtume Muhammad alitilia mkazo sana kwenye muujiza huu wa Qur’ani, japokuwa alikuwa na miujiza mingine mingi iliyotajwa katika vitabu vya historia ya kiislamu. Kwa kuwa Qur’ani tukufu ndiyo muujiza wa milele, nasi tutaipa uzito zaidi katika maelezo haya. Jinsi wapinzani walivyoshindwa kukabiliana na Qur’ani

Ni vizuri kufahamu kwamba Qur’ani iliwachagiza wapinzani wahud98


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:17 PM

Page 99

Tujifunze Misingi ya Dini hurie kwenye uwanja wa mapambano ili kusiwe na udhuru kwa yoyote. Walishindwa Maneno: “Ikiwa wasema kweli.” “Wala hamtaweza kufanya, “hata kama mtasaidiana,” “leteni Sura moja tu kama hii.” Zote hizi ni ibara za kuchochea na kuhimiza, ili kusiwe na udhuru wowote. Upande mwingine mapambano kati ya Mtume na wapinzani hayakuwa rahisi, kwani Uislamu haukutishia dini yao tu, bali pia maslahi yao ya kiuchumi, kisiasa na hata maisha yao kwa ujumla. Kwa maneno mengine, maendeleo ya Uislamu yalisababisha maisha yao kuwa shelabela. Hivyo basi walilazimika kupambana nao kwa uwezo wao na nguvu zao zote. Ili kumpokonya Mtume Silaha yake hiyo kubwa, iliyopasa walete aya kama ya Qur’ani tukufu, kwa vyovyote itakavyokuwa, ili Waislamu wasiitegemee tena kuwa kama muujiza wao, na kila anayeiamini ashindwe, na hiyo Aya yao (wapinzani) iwe ndiyo ushahidi wa kuthibitisha ukweli wao. Wapinzani hao walijaribu sana kuwaalika mabingwa wa lunga ya kiarabu ili kushindana na Qur’ani, lakini kila walipofanya hivyo, walishindwa na kukimbia. Visa hivi vimeelezwa kwa kirefu katika vitabu vya historia.

KISA CHA WALID BIN MUGHIRA Miongoni mwa waliokuwa katika mashindano hayo, alikuwa ni Walid bin Mughira wa kabila la Bani la Makhzum. Walid alikuwa maarufu sana kwa fikra zake zinazolenga na jinsi anavyofikiria mambo vizuri miongoni mwa waarabu wakati huo. 99


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:17 PM

Page 100

Tujifunze Misingi ya Dini Walimwomba ajiunge na kutoa maoni yake kuhusu na Aya za Qur’ani na mvuto wake wa ajabu. Alikwenda moja kwa moja hadi kwa mtume Muhammad na kumuomba amsomee Aya ya Qur’ani naye akamsomea baadhi ya Aya zilizomo katika “Surat Hamim- Sajdah.” Alipozisikia aliathirika sana, na bila ya kujijua, alikwenda moja kwa moja hadi kwenye baraza waliyokuwa wameketi watu wa kabila lake na kuwaambia, “Naapa! Nimesikia maneno ambayo si ya binadamu wala si ya malaika. Ni matamu na yenye uzuri wa aina yake, tena ni kama tawi la mti lililobeba matunda maridhawa aidha, hayashindiki.” Makuraishi3 waliposikia maneno haya kutoka kwa Walid, walinong’onezana huku wakisema: “Walid amepotezwa na Muhammad.” Akiwa amerukwa na akili, Abu Jahl alikwenda na kumtaka Walid aende akakutane nao. Alipohudhuria kwenye kikao chao aliwauliza: “Je mwadhani Muhammad ni mwendawazimu?” Waliohudhuria wakamjibu, “La.” Akaendelea: “Mwadhani ni mwongo? Je si yeye aliyekuwa akisifika kwa ukweli na uaminifu wake? Au si ndio mliomwita mkweli na muaminifu?” Baadhi yao wakaulizana: “Sasa tumwiteje?” Walid aliwaza kidogo, kisha akasema, “Mwiteni Mchawi.” Wakajaribu sana kuwatenga watu na Qur’ani iliyowavutia sana kwa kutumia neno ‘uchawi’, ambalo leyewe lilikuwa ni ushahidi tosha wa kuonyesha mvuto wa ajabu uliomo ndani ya Qur’ani, na ndipo wakauita ‘ulozi’ wakati ambapo yenyewe haihusiani chochote na uchawi. Kwa sababu hiyo ndipo Maquraishi wakaeneza uvumi kila mahali ya kwamba Muhammad ni mchawi, watu wajiepushe naye na wasimsikilize atakalosema. 3.Maquraishi ni kabila la wenyeji wa Makka, na ni kabila la Mtume. 100


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:17 PM

Page 101

Tujifunze Misingi ya Dini Lakini pamoja na bidii na juhudi zao zote mpango wao huo haukufaulu. Waliokuwa na kiu ya Qur’ani walikuwa ni wengi na walionea kila mahali, walikuwa na nyoyo safi. Makundi kwa makundi walijiunga na Qur’ani wakanywa maji safi ya ujumbe wa Mwenyezi Mungu; na maadui wakashindwa na kurudi nyuma. Hadi leo Qur’ani inawaita watu wa dunia nzima – wakiweza - kuja kushindana nayo ikisema: “Enyi wanavyuoni, wana falsafa, mafasihi na waandishi popote mlipo, mkiwa na shaka na ukweli wa Aya hizi na mkadhani kuwa ni fikra za mwanaadamu, basi leteni zenu zinazofanana na hizo.” Pia twajua kwamba maadui wa Uislamu, hasa mapadri wanaojua kwamba Uislamu ni shule ya kimapinduzi, iliyojaa maana zote, mshindani imara na hatari, hutumia mamilioni ya pesa kila mwaka ili kusambaza propaganda dhidi ya Uislamu. Wamejiingiza katika nchi za kiislamu wakisingizia kwamba wanashughulika na elimu, sayansi na afya. Je nini kinachowazuia wasijumuike na wasomi waarabu-wakristo, washairi, waandishi na wanafalsafa ili waandike Aya kama za Qur’ani kwa ajili ya kuwanyamazisha waislamu? Kwa hiyo ni dhahiri kwamba kama wangeliweza kufanya hivyo kwa gharama yoyote basi wangelifanya. Lakini ni kweli kabisa hawawezi, na hiyo ndiyo hoja ya ushindi mbele ya wapinzani, na ndiyo ushahidi wa miujiza ya Qur’ani.

101


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:17 PM

Page 102

Tujifunze Misingi ya Dini

SOMO LA SITA TUTAZAME MUUJIZA WA QU’RANI Herufi (za mkato) zilizoko mwanzoni mwa baadhi ya Sura zina maana gani? Tunaposoma Qur’ani, mara nyingi twaona mwanzoni mwa Sura nyingi kuna herufi kama ‘Alif, laam miim raa’ na Yasin.’ Jinsi Qur’ani inavyoweza kutumia herufi hizo ndogo zinaunda maneno makubwa kushinda herufi zenyewe ambazo hata mtoto yeyote anaweza kuzisoma. Kwa hivyo hutokea kwa jambo hili kubwa kwenye herufi kama hizo, ni muujiza wa aina yake. Hapa utajiuliza: Kwa maoni gani tutasema kuwa Qur’ani ni muujiza? Je ni sababu ya fasihi yake au ni kwa sababu ya utamu wa ibara zake, bayana ya melezo yake na ufasaha wake wa ajabu, au sababu ya kitu kingine? Ukweli ni kwamba, tunapoangalia Qur’ani tukufu kwa maoni mbali mbali, kila mojawapo utapata sababu za miujiza yake kama: Ufasaha: Ina utamu na mvuto wa kipekee wenye maneno na ufahamu wa ajabu. Imekusanya mambo yenye maana kubwa, hasa imani zisizokuwa na ushirikina. Ina miujiza ya kielimu. Kwani inavumbua mambo ambayo mwanaadamu hakuyajua wakati huo. Inajua kimbele na inasema waziwazi na kwa usahihi kuhusu mambo 102


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:17 PM

Page 103

Tujifunze Misingi ya Dini yatakayotokea baadaye na mambo ya ghaibu. Haina mgongano wala hitilafu; imepangwa vizuri. Maelezo yanayohusiana na kila moja kati ya mambo haya matano ni mapana mno, hata hivyo, tutajaribu kuyazungumzia baadhi. Ufasaha: Kama tujuavyo kwamba katika kila maneno kuna sehemu mbili: matamshi na maana. Matamshi na maneno mazuri yanapokusanya mfumo mzuri na yakawa si magumu kufahamika, pia ibara zake zikiwa zinavutia kuzisikiliza na kuuvuta moyo, husemwa kuwa huo ndio ‘ufasaha.’ Qur’ani ina sifa zote hizi kwa kiasi kikubwa kabisa, kiasi ambacho hadi sasa hapana hata mtu mmoja aliyeweza kuleta Aya na Sura zenye kuvutia, na utamu kama wa Qur’ani. Tumeona katika somo lililopita jinsi msanii hodari Walid bin Mughira alivyosomewa Qur’ani akashindwa jinsi ya kutafuta namna ya kumfanya Mtume adharaulike mbele ya watu, hatimaye akaamua kutumia neno ‘uchawi’, na kumwita Mtume Muhammad ‘mchawi.’ Hivyo ndivyo walivyomwita Mtume wa dini ya Kiislamu, walijaribu kumshutumu lakini kwa kweli hawakuweza. Ikawa kule kumwita ‘mchawi’, ni kukiri maajabu yaliyomo katika Qur’ani: kwa maana ya kwamba haiwezi kufafanuliwa kirahisi na ieleweke kuwa ni muujiza. Lakini badala ya kuukubali ukweli na kuwa ni muujiza ili waumini, waliuchukulia kuwa ni ngano na hekaya tu. Walipotea kudai kuwa Qur’ani ni uchawi. Kama inavyoeleza Historia ya kiislamu kwamba, mara nyingi watu wakali 103


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:17 PM

Page 104

Tujifunze Misingi ya Dini walipokwenda kumwona Mtume, au waliposikia aya za Qur’ani zikisomwa, walibadili mienendo yao na kukubali mwanga wa Qur’ani uwaongoze. Huu ni uthibitisho tosha wa kuonyesha kwamba mvuto wa ufasaha wa Qur’ani ni muujiza. Kabla hatujakwenda mbali, tunaweza kuona kwamba watu wanaojua barabara lugha ya kiarabu wanaposoma Qur’ani na kuikariri hupendezwa nayo na hawachoki kuisoma. Maneno ya Qur’ani ni sahihi, yana mpangilio mzuri wa maelezo, na wakati huo huo yako wazi na ni makali sana inapobidi. Ni vizuri ifahamike pia kwamba waarabu walikuwa wamefika kiwango cha juu sana cha usanii wa fani ya mashairi katika enzi hizo. Na ilikuwa ni kawaida ya wasanii kukutana kila mwaka, na kila mmoja huleta tungo zake katika kituo cha biashara ya fasihi katika soko la ‘Ukaadh’. Hapo huchaguliwa shairi bora la mwaka na kuwekwa ndani ya Al-Ka’aba. Mtume alipotangaza ujumbe wa Mwenyezi Mungu, kulikuwa na mashairi saba yaliyowekwa katika Al-Ka’aba yaliyojulikana kama ‘Mu’alaqaat Sab’a.’ Lakini mara baada ya kutereshwa Qur’ani hayakuweza kulinganishwa na ufasaha wa Qur’ani na hivyo yaliondolewa moja baada ya jingine na kusahaulika kabisa katika historia. Wafasiri wametoa juhudi zao zote katika kueleza undani wa Aya za Qur’ani, ili kurahisisha kuzifahamu kwa anayetaka kuzisoma. Maarifa yaliyomo katika Qur’ani yanaonyesha kwamba Mtume hakuongeza sifa aliposema: “Udhahiri wa Qur’ani ni mzuri mno, ina undani sana, maajabu yake hayahesabiki, na sifa zake hazichakai.” Amirul-muminin Ali (a.s.) mwanafunzi mkuu wa Qur’ani pia amesema katika kitabu ‘Nahjul-Balgha’: “Chemchemi za nyoyo na chimbuko la elimu vimo ndani ya Qur’ani, na hakuna cha kusafisha kutu za moyo ila Qur’ani.” 104


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:17 PM

Page 105

Tujifunze Misingi ya Dini

SOMO LA SABA MTAZAMO WA QUR’ANI KWENYE ULIMWENGU Kabla ya kueleza chochote, yatupasa tujue kuhusu mazingira ya kifikra na ya kistaarabu yalimoshukia Qur’ani. Kulingana na maelezo ya wanahistoria, nchi ya Hijaz (Saudi Arabia ya sasa) ilikuwa ni nchi iliyokuwa nyuma sana kimaendeleo. Katika wakati uliokuwa kabla ya kuja uislamu, watu wa nchi hiyo walijulikana kama washenzi. Kiitikadi walipenda sana kuabudu masanamu yaliyochongwa kutokana na mawe na mbao. Maendeleo yao yoyote yalifunikwa na kivuli kiovu cha masanamu haya, na yanasemekana pia waliyatengeneza kutokana na tende na kuyapigia magoti, lakini waliposhikwa na njaa waliyala. Ingawaje walichukia sana kupata watoto wa kike, kiasi kwamba kila walipowapata watoto hao waliwazika wangali hai lakini pia malaika watukufu waliwaita, “mabinti wa Mwenyezi Mungu” ni kama wanadamu. Walishangaa sana kusikia kwamba, yampasa kila mtu kumwabudu Mwenyezi Mungu mmoja tu. Ndipo Mtume alipowataka wafanye hivyo, kwa mshangao mkubwa walisema,

“Oh! Amewafanya Miungu (wote) kuwa Mungu mmoja tu! Bila shaka hili ni jambo la ajabu.” (38:5). Na yeyote aliyepinga imani potofu, walimwita muongo na mwendawazimu, walikuwa wakitawaliwa na mfumo wa kikabila. Mizozo nayo ilienea sana kati ya makabila na kuweza kusababisha vita vilivyosababisha 105


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:17 PM

Page 106

Tujifunze Misingi ya Dini madimbwi ya damu katika maeneo yao. Watu waliojua kusoma na kuandika walikuwa ni wachache mno. Pia ilikuwa ni nadra sana kumpata mtaalamu. Naam, katika mazingira hayo ndipo alitokea mtu (Mtume Muhammad (s.a.w.w.) ambaye hakupata kuhudhuria masomo kwa waalimu, akaleta Kitabu kilichojaa mkusanyiko wa mambo na maana ambayo hadi karne ya kumi na nne wanavyuoni wangali wanayafafanua, na kadri miaka inavyosonga mbele ndivyo wanavyopata ukweli mpya kutoka kwenye Kitabu hicho. Qur’ani inatoa picha sahihi ya ulimwengu. Inaueleza umoja (tawhid) wa Mwenyezi Mungu kwa vizuri zaidi. Inafafanua Siri za kuumbwa ardhi na mbingu, usiku na mchana, jua na mwezi, mimea na watu, kila kimoja kati ya hivi ni dalili ya kuwepo kwa Mwenyezi Mungu mmoja. Wakati mwingine Qur’ani inazama katika kueleza undani wa mwanaadamu, imani na asili ya maumbile ya kibinadamu, inasema:

“Na wanapopanda katika vyombo (wakafikiwa na misukosuko), humuomba Mwenyezi Mungu, na hali ya kuwa wanamtakasishia utii. Lakini anapowafikisha salama, mara wanamshirikisha.” (29:65). Wakati mwingine hutoa sababu za kiakili kuhusu umoja wa Mwenyezi Mungu ikitegemea maelezo ya safari za angani na yanayohusu nafsi za watu: siri za uumbaji wa ardhi na mbingu, wanyama, milima, bahari, mvua, upepo na mwili pamoja na roho ya binadamu. Inasema:

106


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:17 PM

Page 107

Tujifunze Misingi ya Dini

“Tutawaonyesha alama zetu katika nchi za mbali na katka nafsi zao.” (41:53). Ina maelezo mazuri na ya ndani sana inapotaja sifa za Mwenyezi Mungu, inasema:

“Hakuna chochote mfano wake….”(42:11). Katika Aya nyingine:

“Yeye ndiye Mwenyezi Mungu Ambaye hakuna aabudiwaye kwa haki isipokuwa yeye tu. Anayejua yaliyofichikana na haki isipokuwa yeye tu. Anayejua yaliyofichikana na yaliyo dhairi, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu. Yeye ndiye Mwenyezi Mungu ambaye hakuna aabudiwaye kwa haki isipokuwa Yeye tu, Mfalme mtakatifu, Mwenye salama, mtoaji wa amani, Mwenye kuyaendesha mwenyewe mambo yake, Mwenye shani, Anayefanya analolitaka, Mkubwa, Mwenyezi 107


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:17 PM

Page 108

Tujifunze Misingi ya Dini Mungu yu mbali na hao wanaomshirikisha naye. Yeye ndiye Mwenyezi Mungu, Muumbaji, Mtengenezaji mfanyaji wa sura (za namza namna za viumbe): Mwenye majina (sifa) mazuri. Kinamtukuza kila kilichomo mbinguni na ardhini. Naye ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima.” (59:22-24). Katika kueleza ujuzi wa Mwenyezi Mungu usiokwisha, inasema hivi:

“Na lau kama miti yote iliyomo katika ardhi ingelikuwa kalamu, na bahari hii (ikafanywa wino). Na ikasadiwa na kuongezwa maji) na bahari nyingine saba; maneno ya Mwenyezi Mungu yasingelikwisha.” (31:27). Inapoeleza kuwapo Mwenyezi Mungu mahali popote inasema:

“Na Mashariki na Magharibi ni za Mwenyewe Mungu. Basi mahala pote mgeukipo (alikokuamrisheni Mwenyezi Mungu) mtazikuta huko radhi za Mwenyezi Mungu…” 2:115). Wakati inapozungumziwa siku ya ufufuo huwakemea wanaomshirikisha Mungu inasema:

108


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:17 PM

Page 109

Tujifunze Misingi ya Dini

“Na akatupigia mfano, na akasahau kuumbwa kwake (kwa manii) akasema: “Nani atakayeifufua mifupa na hali imesagika?” Sema: ‘Ataifufua aliyeiumba mara ya kwanza, naye ni Mjuzi wa kila (namna ya) kuumba.” Ambaye amekufanyieni moto katika mti mbichi, mkawa nanyi kwa (mti) huo mnawasha. Je yule aliyeziumba mbingu na ardhi (mnaona) hana uwezo wa kuumba (mara ya pili) mfano wao (wanaadamu)? Kwa nini? Nawe ni Muumbaji mkuu, Mjuzi (wa kila jambo). Hakika amri yake anapotaka chochote (kile kitokee) ni kukiambia: “kuwa”, basi huwa.” (36: 78-82). Katika kueleza itakavyokuwa siku hiyo, Qur’ani inasema:

“Siku hiyo (ardhi) itatoa habari zake (zote.)” (99:4). “Na wao waziambie (hizi) ngozi zao ‘mbona mnatushuhudilia?’ Nazo ziwaambie: ‘Mwenyezi Mungu aliyekitamkisha kila kitu ndiye aliyetutamkisha, naye ndiye aliyekuumbeni mara ya kwanza. Na kwake (hivi sasa) mnarudishwa.” “ (41:21). 109


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:17 PM

Page 110

Tujifunze Misingi ya Dini Katika kuzungumzia ushahidi wa viungo inasema:

“Siku hiyo tutaviziba vinywa vyao, ituzungumzie mikono yao na itoe ushahidi miguu yao kwa yale waliyokuwa wakiyachuma.” (36:65). Thamani ya Qur’ani tukufu, mkusanyiko wake na kutakata kwake na mageuzo hufahamika waziwazi inapolinganishwa na Injili na Tawrat inavyosema kuhusu kuumbwa kwa mwanaadamuu na jinsi Qur’ani tukifu inavyosema. Utaona jinsi Tawrat na Injili zinavyosema kuhusu mitume, na jinsi Qur’ani tukufu inavyosema. Vipi Injili na Torati vinavyomuelezea Mwenyezi Mungu, na jinsi Qur’ani inavyomueleza. Hapo ndipo utakapoona tofauti dhahiri iliyopo kati a vitabu hivi.

SOMO LA NANE QUR’ANI TUKUFU NA UGUNDUZI WA KISASA WA KI- SAYANSI Inatulazimu tutafute humo mwangaza wa imani na uongofu, ucha Mungu, utu na tabia njema; pamoja na sharia. Nayo inakusanyika mambo yote haya. Lakini ili Qur’ani kufikia lengo lake hili, inadokeza baadhi ya elimu na siri za kuubwa, na hasa katika maelezo yanayohusu (Mwenyezi Mungu). Inaondoa pazia za siri zilizomo ulimwenguni, na inafunua mambo ambayo hayakujulikana na wasomi wa wakati ule. 110


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:17 PM

Page 111

Tujifunze Misingi ya Dini Ufafanuzi huu uliomo katika Qur’ani twauita miujiza ya kielimu ya Qur’ani. Tutataja hapa baadhi tu miujiza hiyo kwa kifupi: Qur’ani tukufu na kanuni ya nguvu ya mvutano (Law of attraction) Kabla ya kuja mtaalamu Isaac Newton hapana mtu aliyekuwa amegundua kanuni za ‘nguvu ya mvutano.’ Ilitokea kwamba siku moja Newton alipokuwa ameketi chini ya mti. Akaangukiwa na tunda la tofaa, akawaza sababu ya kuanguka kwa tunda hilo akijisemea moyoni ‘ni nguvu gani hii inayolivuta tofaa chini? Kwa nini lisipande juu, lakini baada ya miaka mingi ya kufanya utafiti, akagundua kanuni ya ‘nguvu ya mvutano’. Ilipogunduliwa kanuni hii ndipo ukathibitishwa utaratibu wa sayari, sababu ya dunia kulizunguka jua na kwa nini sayari haziangukiani; na nguvu gani zinazozifanya zibaki kwenye mzunguko wake maalum (Orbit) zisipotoke na kwenda huko na huko. Naam, Newton aligundua harakati za kitu za ndani ambazo husababisha kitu hicho kitoke (kisukumwe) kutoka mahali pake na nguvu ya mvutano hukivuta mahali pake, na nguvu hizi mbili zitakapolingana, yaani ya kusukuma kutoka mahali pake na ya kuvuta, husababisha kitu hicho kuzunguka kuwa Qur’ani imeeleza jambo hili kabla ya miaka elfu moja katika Aya ifuatayo:

“Mwenyezi Mungu ndiye aliyeziinua mbingu bila ya nguzo mnaziona hivi. Kisha akatawala juu ya Arshi (yake). Na akalitiisha (kwenu) jua 111


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:17 PM

Page 112

Tujifunze Misingi ya Dini na mwezi (akavifanya vitii). Kila kimoja kinaendelea mpaka muda uliowekwa. Yeye ndiye anayeliendesha kila jambo. Anazipambanua Aya hivi ili mpate yakini ya kukutana na Mola wenu.” (13:2). Katika kufafanua Aya hii Imam Ridha (a.s.) amesema kumwambia mpokezi, “Je Mwenyezi Mungu siye aliyesema kwamba ameziinua mbingu bila ya nguzo mnazoweza kuziona?” Mpokezi akasema “Ndio.” Imam akamwambia: “Basi nguzo hizo zipo lakini huwezi kuziona.” Je kuna ufafanuzi mwepesi, zaidi ya huu, wa kuwafahamisha waarabu wa kawaida? Naye Imam Ali (a.s.) amesema: “Hizi nyota zilizoko mbinguni ni kama miji iliyoko duniani na kila mji umeungana na mwingine kwa miale ya mwanga.” Wasomi wa kisasa wa elimu, “Pia wanaamini kwamba kuna mamilioni ya nyota ambazo viumbe hai vinaishi humo, japokuwa bado havijagunduliwa hadi sasa.”

Uvumbuzi wa dunia kuzunguka jua Historia yatueleza kwamba mtu wa kwanza kuvumbua jambo hilo alikuwa ni Mtaliano mmoja aitwaye Galileo aliyeishi yapata karne nne nyuma kabla ya msomi wa kimisri, Ptolemy hajasema nadharia yake ya kwamba, dunia ndiyo kitovu cha ulimwengu na vitu vyote huizunguka. Galileo alikemewa sana na kanisa kwa uvumbuzi wake; na ili kuyaokoa maisha yake, ilimbidi aukane uvumbuzi wake huu, hata hivyo wasomi waliifuatilia na kutilia mkazo nadharia yake, na wakaendelea hivyo, hatimaye leo imekuwa ndiyo inayotegemewa kisayansi na imethibitishwa na vifaa vya angani. Kwa Muhtasari, fikra ya kusema kwamba dunia ndiyo kitovu imekosewa, 112


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:18 PM

Page 113

Tujifunze Misingi ya Dini na ni wazi kwamba hili ni kosa la mawazo yetu, kwa sababu unachanganyika kati ya mwendo wa nyota na sayari, na mwendo wa dunia. Tunadhani kuwa hizo ziko mwendoni, lakini sisi ndiyo tuko mwendoni. Nadharia hii ya Ptolemy ilidumu kwa muda wa miaka elfu moja na mia tano na kuathiri sana fikra za wasomi wa wakati ule, na wakati iliposhuka Qur’ani tukufu hapakuwa na yeyote aliyethubutu kusema kinyume na hivyo. Lakini tukirudi kwenye Qur’ani yatuambia:

“Na unaiona milima unaidhania imetulia, nayo inakwenda kama mawingu (yanavyokwenda), ndiyo sanaa ya Mwenyezi Mungu (matengenezo yake) aliyekitengeneza kila kitu; bila shaka Yeye anazo habari za yote mnayoyatenda.” (27:88). Qur’ani inaeleza waziwazi kuhusu mwendo wa milima ambapo sisi tunaiona haiendi, na mlingano wa mwendo wa milima na mawingi unaonyesha kutulia. Tukiangalia hapa kwenye Aya, twaona kwamba badala ya kutajwa mwendo wa dunia, ujulikane, kwa sababu milima bila ya kuwapo dunia ardhi haiwezi kwenda, na kwenda kwa milima ndiko kwenda (kuzunguka) kwa hiyo dunia, ni sawa, iwe ni kuzunguka yenyewe, kulizunguka jua, ama vyote viwili. Hebu fikiria, wakati wasomi wote ulimwenguni na watu wa kawaida walipokuwa wakidhani kuwa dunia haizunguki, na kuwa nyota pamoja na sayari ndivyo vinavyozunguka, bila shaka upizani wa kinadharia uliokwenda kinyume na mawazo yao, ulikuwa ni muujiza wa kielimu! Tena aliyeyasema hayo (Muhammad) ni mtu ambaye hakusoma na alikulia katika sehemu ambayo haikuwa ya waalimu na na ilikuwa nyuma kielimu na kimaendeleo. Je hii si hoja tosha ya kuthibitisha ukweli wa Kitabu hiki? 113


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:18 PM

Page 114

Tujifunze Misingi ya Dini

SOMO LA TISA HOJA NYINGINE YA KUTHIBISHA UKWELI WA MTUME WA DINI YA KIISLAMU Ili kuelewa ukweli wa mwito wa anayedai utume, kuuelewa ukweli na uongo wake, zipo njia nyingine ambazo si miujiza zinazothibitisha na kueleza kufikia kwenye ukweli, nazo ni: Tabia yake na historia ya maisha yake. Hali za eneo la mwito huo. Wakati. Yaliyomo katika mwito. Mipango na njia kufika kwenye lengo. Athari zilizopatikana katika eneo lililofikiwa na mwito huo. Imani, na kujitolea kwa anayedai utume. Kutopatana na mapendekezo yenye kupotosha ya wapinzani. Kasi ya athari za mwito wake kwenye maoni ya watu. Kuwaelewa waumini na kujua ni watu wa tabaka gani. Tukiweza kuyazingatia mambo haya kumi na kuyahusiha na kila anayedai utume; na kuyapanga katika jalada maalumu, itakuwa ni rahisi kwetu kuutambua ukweli. Sasa basi, baada ya kuyatazama kwa makini yaliyotajwa hapo juu, hebu sasa na tuchunguze na mambo hayo kisha tuyalinganishe na tabia ya Mtume mtukufu Muhamadi (s.a.w.w.) japokuwa kila jambo litahitaji utafiti wake pekee: Miongoni mwa sifa za kimaadili zinazohusiana na Mtume Muhammad ambazo zimeandikwa na wanahistoria; alikuwa mtakatifu tena mtu barabara, mpaka akapewa jina la ‘mwaminifu’ katika enzi hizo ambazo watu walikuwa wajinga. Historia inaeleza: “Alipotakiwa kuhama kutoka 114


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:18 PM

Page 115

Tujifunze Misingi ya Dini Makka kwenda Madina, alimwachia Ali (a.s.) amana zote za watu alizokuwa nazo ili awarudishie wenyewe.” Ushujaa wake, uthabiti, tabia nzuri, utu, kusamehe vitani na kupenda amani kwake, kunajulikana, na hasa pale alipowasamehe watu wa Makka baada ya ushindi katika mji huo na kusalimu amri wakatili wa Makka mbele yake, haya yote ni ushahidi wazi wa tabia zake njema. 2. Sote twafahamu kwamba watu wa kawaida na mabingwa katika nyanja mbali mbali wanafuata mila zinapolingana na mazingaira wanayoishi, wapende ama wasipende kwao ni lazima, japokuwa watatofautiana kwa uchache ama wingi wa kufuata mila hizo. Sasa hebu fikiria, mtu aliyeishi miaka arobaini katika mazingira ya enzi za mfumo shirki na imani potofu na kisha vipi inawezekana watu wakafuata Tawhid na kupambana na aina zote za ushirikina? Na vipi elimu ya hali ya juu ijitokeze na ustawi katika mazingira hayo ya ujinga? Je kuna mtu anayeweza kuamini kwamba maajabu hayo yote yangelitokea bila ya kuungwa mkono na Mwenyezi Mungu? 3. Ni lazima ifahamike kwamba enzi alizokuja Mtume zilikuwa ni enzi za katikati, ulikuwa ni wakati wa dhulma, ubaguzi, ukandamizaji, na ubwana. Hebu tusome kabla na baada ya kutokea Uislamu, akisema: “Mwenyezi Mungu alimpeleka Mtume Wake katika wakati ambapo watu walikuwa wamepotea, wasomi wao walikuwa wametawaliwa na tamaa, walipotea kati ya upumbavu na fadhaa.” (Nahjul-Balaghah). Hebu fikiri juu ya dini hii ambayo mwito wake ni kutaka kuwe na usawa miongoni mwa wanaadamu na kupinga ubaguzi, jinsi inavyolingana na hali ya wakati huo. Mwenyezi Mungu anasema katika Qur’ani: “Kwa hakika waumini wote ni ndugu..”(49:10). 4. Mwito wa Mtume ulete umoja kila mahali uondoshe kabisa uonevu, ukandamizaji, uunde utawala wa watu wote duniani uwatetee wanyonge na 115


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:18 PM

Page 116

Tujifunze Misingi ya Dini kuamini kuwa ucha Mungu na uaminifu ndivyo vipimo vya thamani ya utu. 5. Ama kuhusu mipango iliyopangwa kupitishwa, haikuruhusiwa kufanya tu ili kufikia lengo, bali ni lazima zifuatwe njia za sawa kama inavyosema Qur’ani,

“…Wala kuchukiana na watu kusikupelekeeni kutowafanyia insafu (uadilifu)..” (5:8). Hata vitani Mtume ameamrisha watu kudumisha tabia njema, kwa kutowashambulia raia, kutokata miti na mitende, kutochafua maji ya kunywa ya maadui na kuwatendea mema mateka; haya yote n uthibitisho wa ukweli huu. Athari ya mwito wake ilikuwa kubwa katika mazingira yake, hata maadui waliogopa watu wasiende karibu naye kwani wangevutiwa na mvuto wake wa ajabu. Wakati mwingine walipiga mayowe alipokuwa akizungumza ili watu wasisikie analolisema, ili kuyazuia maneno yake yasiingie ndani ya nyoyo zao zenye kiu. Kwa ajili hii ya kufunika ukweli wa mambo alikuwa akiyasema, walimwita ‘mchawi’ na maneno yake wakayaita ‘uchawi.’ Huko kufanya hivyo, ni kukubali athari ya ajabu iliyomo katika mwito wa mtume mtukufu. Kujitolea kwake wakati wa mwito wake kunaonyesha jinsi alivyokuwa na imani thabiti juu ya dini aliyoileta. Alisimama imara ambapo wale waliokuwa wapya katika Uislamu walikimbia. Hakuwajali maadui ambao mara kwa mara walimtisha kila walivyoweza. Alihifadhi imani yake na hakuonyesha udhaifu wala shaka. Mara nyingi walijaribu kumuua wakidai kwamba alikuwa amepotoka, lakini hakusalimu amri, alisema: “Hata mkiweka jua, mwezi na sayari zote 116


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:18 PM

Page 117

Tujifunze Misingi ya Dini mikononi mwangu, sitaacha jambo hili.� Kuathiri kwa mwito wake kulishangaza na kuenea kwa kasi kwa mwito huo kulishangaza zaidi. Wale waliopata kusoma vitabu vilivyoandikwa na waandishi wa ki-magharibi juu ya Uislamu, wataona kwamba waandishi wote hao wameshangazwa na kasi ya kuenea kwa Uislamu. Miongoni mwa walioandika kuhusu historia ya maendeleo ya Waarabu na chimbuko la Mashariki, wanakubaliana na juhudi zilizofanywa katika kutafiti, jambo ambalo bado halijajulikana hadi leo, ni jinsi Uislamu ulivyoenea kwa kasi zaidi kwa kipindi kisichozidi karne moja. Ndiyo, bila shaka ni kitendawili kisichoteguka kwamba Uislamu umeweza kupenya kwa haraka ndani ya nyoyo za mamilioni ya watu, kwa kuweza kuziondosha desturi zingine na kuleta ustaarabu mpya. 10. Mwisho hebu tutazame maadui zake ambao walikuwa ni viongozi makafiri, wadhalimu, na matajiri wenye kujipenda, wakati ambapo wenye imani safi walikuwa ni vijana duni waliokuwa na hamu ya kutaka kujua ukweli, ambao baadhi yao walikuwa ni watumwa wasio na rasimali yoyote zaidi ya nyoyo zao safi na walikuwa na kiu ya kutaka kufuata ukweli. Katika mkusanyiko wa upekuzi huu mrefu, tutaona kwamba mwito wa Mtume Muhammad ulikuwa ni wa Mwenyezi Mungu, uliokuwa na nguvu isiyo ya kawaida, unaotoka kwa Muumba; ili kuwaokoa wanaadamu kutokana na ufisadi, ujinga, kumshirikisha Mwenyezi Mungu, uonevu na dhuluma.

117


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:18 PM

Page 118

Tujifunze Misingi ya Dini

SOMO LA KUMI MTUME WA UISLAMU NDIYE MUHURI WA UNABII

Maana halisi ya ‘Muhuri’ Mtume wa dini ya kiislamu ndiye Mtume wa mwisho wa Mwenyezi Mungu na daraja zote za Utume zaishia kwake. Jambo hili ni moja katika mafundisho muhimu ya kiislamu. Maana ya umuhimu hapa ni kwamba yeyote atayejinga na waislamu ni lazima hapa ni kwamba yeyote atayejiunga na Waislamu ni lazima aelewe ya kwamba waislamu wote wanaamini hivi na kwamba hiyo ndiyo moja kati ya imani hasa. Yaani wale wanaoshirikiana na waislamu wanajua kwamba waislamu wanasisitiza msingi wa Tawhid (Umoja wa Mwenyezi Mungu) na ni lazima watambue pia kwamba waislamu wote wanakubaliana juu ya suala la kuwa Mtume Muhammad ndiye muhuri (mwisho) wa Utume mwingine. Ilivyo ni kwamba mwanaadamu anapita mienendo mingi kufikia ukamiliifu ikiwa ni pamoja na kuletwa mitume mpaka wakafikia hali ya kuweza kujitegemea, yaani wanaweza kutatua matatizo yao kwa kufuata mafunzo ya kiislamu. Pia twaweza kusema kwamba Uislamu ndio sharia ya mwisho iliyokusanya kila kitu katika enzi za kukomaa kwa ubinadamu. Kiimani, dini ya kiislamu ina mkusanyiko uliokamilika wa ufahamu wa kidini. Kivitendo, ina mfumo unaowiana na kila enzi na kila kizazi.

Dalili za kuwa Muhammad ni Mtume wa mwisho Tuna sababu za kutosha za kuthibitisha jambo hili, za muhimu ni hizi: 118


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:18 PM

Page 119

Tujifunze Misingi ya Dini Umuhimu wa suala lenyewe. Tumeshaeleza kwamba, yeyote anayeshirikiana na waislamu mahali popote duniani atagundua kwamba wanaamini ya kuwa Mtume wao (Muhammad) ndiye wa mwisho, na mtu atakapokubali Uislamu kwa hoja zenye kumtosheleza, basi hana budi kukubali kuwa Mtume Muhammad ndiye wa mwisho. Na kama tulivyotoa hoja za kutosha katia somo lililopita, ni lazima tukubaliane na wazo hili ambalo ni moja kati ya mambo ya lazima ya dini hii. Ushahidi wa Aya za Qur’ani pia uko wazi juu ya jambo hili. Qur’ani inasema:

“Muhammad si baba wa yeyote katika wanaume wenu, bali yeye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na mwisho wa mitume..” (33:40). Aya hii ilishuka wakati ambapo ada ya kuchukua ‘watoto wa kulea’ ilikuwa imeenea miongoni mwa waarabu. Walikuwa wakifanya watoto wa baba na mama mwingine kama watoto wao hasa. Mtoto huyo huwa ‘Mahram’4 na aliweza kurithi wanapofuka. Lakini Uislamu ulipokuja uliondoa ada hizi za kijahiliya na kuamuru kwamba watoto wa kulea hawafai kuwa kama watoto wa kuzaa katika masuala ya kisheria. Miongoni mwa watoto kama hao alikuwa ni Zayd, mtoto aliyekuwa akilelewa na kuchukuliwa kama mtoto wa Mtume Muhammad (s.a.w.w.), ndipo ikashuka Aya inayowataka Waislamu wamwite Mtume kwa sifa zake hasa ambazo ni: Mtume wa Mwenyezi Mungu na mwisho: badala ya 4. Mahram:Watu wasioweza kuoana 119


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:18 PM

Page 120

Tujifunze Misingi ya Dini kumwita kwa jina la baba wa mmoja wao. (Alikuwa akiitwa ‘baba wa Zayd’). Jambo hili linaonyesha kwamba sifa ya Utume wa mwisho ni ya wazi miongoni mwa Waislamu, la kudumu, na ndio uamuzi wa mwisho kama ulivyo utume wenyewe. Swali lililobaki hapa ni: Ni nini hasa maana ya neno khatm? Khatm ina maana ya kufika mwisho wa jambo, mathalan muhuri hupigwa mwisho wa jambo, mathalan mwishoni mwa kuandika barua, na wakati mwingine tunaona pete huitwa ‘khatm’ (hii ni kwa mujibu wa lugha ya kiarabu) hiyo ni kwa sababu katika enzi za Mtume pete ilitumika kama muhuri wa jina la mwandishi wa barua, kwani jina lake lilikuwa likichongwa kwenye kito cha pete na anapomaliza kuandika barua, huipiga muhuri kwa kutumia pete hiyo ambapo kila pete ilikuwa na alama inayomhusu mtu maalum tu. Tunasoma katika mapokezi ya kiislamu kwamba, “Mtume Muhammad (s.a.w.w.) alipotaka kuwaandikia barua wafalme au viongozi wa wakati huo ili kuwaita katika Uislamu, aliambiwa kuwa wafalme hawangekubali barua ambayo haikupigwa muhuri, ndipo akaamuru pete yake ichapwe maneno haya: Hapana mola isipokuwa Allah, na Muhammad ni Mtume Wake. Kuanzia hapo akaamuru barua zake ziwe zikipigwa muhuri huo. Kwa hivyo mpaka kufikia hapa maana halisi ya pete/muhuri imefahamika. Tuna Hadithi nyingi zinazothibitisha kuwa Mtume Muhammad ni wa mwisho, miongoni mwazo ni: Iliyopokelewa na Jabir bin Abdillahi AlAnsari, alimsikia Mtume akisema: “Mfano wangu na mitume wengine ni kama mfano wa nyumba iliyojengwa yote ikabaki tofali moja tu ndipo ikamilike, kila aingiaye hupendezwa nayo ila sehemu ile iliyo wazi tu, basi mimi ndiye hilo tofali, na utume wa mitume wote utaishia kwangu.” (Tafsir Majmaul-Bayan). 120


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:18 PM

Page 121

Tujifunze Misingi ya Dini Imam Sadiq naye amesema, “Halali ya Muhammad (iliyohalalishwa naye) ni halali hadi siku ya Kiyama; na haramu yake ni haramu hadi siku ya Kiyama.” Na katika Hadithi mashuhuri wanayokubaliana Mashi’a na Masunni ni ile ambayo Mtume alimwambia Ali: “Wewe kwangu ni kama alivyokuwa Haruni kwa Musa isipokuwa hapana Mtume baada yangu.” Si hizo tu, bali kuna Hadithi nyingi juu ya suala hilo.

* * * * * Kuna maswali kadhaa yaliyojitokeza kuhusiana na maudhui haya ya kwisha utume, ambayo yatapasa tuyafahamu: Kuna baadhi ya watu husema kwama ikiwa Mwenyezi Mungu aliwapeleka mitume kwa ajili ya huruma aliyonayo, kwa nini basi watu wa wakati huu (wa sasa) wanyimwe huruma hiyo? Na kwa nini kusiwe na njia nyingine mpya ya kuwaongoza watu wa wakati huu? Hao wasemao hivyo wamesahau jambo moja muhimu kwamba kutoletewa mtume wakati wetu si kwa sababu fikra za kibinadamu zimefika upeo, na kwa kuyaelewa mafunzo ya Mtume wa Uislamu wanaweza kuyafuata mafunzo hayo. Ni vyema tutoa mfano hapa: Mitume walioleta sharia ama vitabu ni watano: Nuh, Ibrahim, Musa, Isa na Muhammad (amani ziwashukie wote) walifanya bidii kuwaongoza na kuwaweka watu katika ukamilifu kwenye maeneo maalum kufikia kwenye mkondo mahususi. Ni kama mfano wa mihula mitano ya masomo ambayo yampasa mwanafunzi aimalize. Akishamaliza mihula hiyo haina maana kuwa hakitajii kusoma; bali ni kwamba sasa anaweza kujiendeleza mwenyewe bila ya kuhitaji mwalimu. Mihula hiyo ni shule ya msingi, ya 121


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:18 PM

Page 122

Tujifunze Misingi ya Dini kati (Middle school), ya upili (Secondary), ya chuo kukuu na phd. Kwa hiyo mwenye phd haina maana kuwa hafai kusoma, bali kwamba ana uwezo wa kumwezesha kutatua matatizo yake ya kielimu na kujiendeleza. Swali jingine ni hili: Ikiwa jamii ya binadamu inaendelea na kugeuka tutawezaje kukidhi mahitaji yake kwa kutumia sharia za kudumu za kiislamu zisizogeuka? Kwa kujibu tunasema: Uislamu una aina mbili za sheria: Ya kwanza, ni mfululizo wa sharia zinazolingana na sifa za kudumu za mwanaadamu kama wajibu wa kuamini Tawhid (Mwenyezi Mungu ni Mmoja, huku hakubadiliki) kudumisha usawa na kupambana na udhalimu wa aina yoyote. Ama ya pili ile ambayo inakubaliana na mabadiliko kulingana na hali zake kiasi ambacho zitaendelea kukidhi mahitaji ya kila siku. Kwa mfano, mafunzo ya msingi ya kiislamu yanasema, heshimu mkataba uliowekwa na uwe mwaminifu. Bila shaka kadri wakati unavyobadilika ndiyo unavyoundwa uhusiano mpya wa kijamii, kibiashara na kisiasa ambapo mtu anaweza kuweka mkataba kwa kuangalia misingi ya kanuni. Kuna kanuni iitwayo “La dharaar’, yaani sharia yoyote itakayowadhuru watu au mtu lazima iwe na mipaka. Hapa unaweza kuona jinsi kanuni hizi za kiislamu zinavyotatua matatizo, na sharia kama hizi ni nyingi katika Uislamu. Hapana shaka Uislamu unahitaji uongozi baada kukosekana mitume na kughibu kwa naibu wake kwa sababu ya hukumu ya kwisha Utume, hatutazamii kuja Mtume mwingine. Je hili halitawaathiri Waislamu? Kwa kujibu swali hili twasema: Katika enzi hii mambo muhimu ya kiislamu yanapitia kwenye uongozi wa 122


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:18 PM

Page 123

Tujifunze Misingi ya Dini mwanachuoni wa kidini aliyekusanya masharti ya elimu, ucha Mungu na uongozi; na njia za kumtambua kiongozi kama huyo pia zimeelezwa waziwazi katika Uislamu, hapana haja ya kubabaika juu ya jambo hili. Hivyo basi, ‘Uongozi wa wanachuoni’ ndiyo uendelezaji wa mfuatano wa kazi za mitume. Na uongozi huo wa mtu aliyekusanya masharti yanayomwezesha kuwa hivyo ni dalili ya kuonyesha kwamba jamii ya kiislamu haikuachwa hivi hivi bila ya uongozi.

123


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:18 PM

Page 124

Tujifunze Misingi ya Dini

TUUJUE UIMAM (4)

124


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:18 PM

Page 125

Tujifunze Misingi ya Dini

Kwa jina la Allah, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu

SOMO LA KWANZA UIMAMU ULIANZA LINI? Baada ya kufariki Mtume Muhammad (s.a.w.w.) waislamu waligawanyika makundi mawili, moja lilisema kuwa Mtume (s.a.w.w.) hakubaini atakayeshika wadhifa wa ukhalifa baada ya kufa kwake, na kwamba kazi hiyo aliwaachia waislamu wenyewe wajichagulie kiongozi wao; hili ni kundi la ‘Ahlu-Sunna’ (MaSunni). Kundi jingine likasema kuwa khalifa wa Mtume (s.a.w.w.) lazima awe amehifadhiwa na madhambi na makosa, awe mjuzi, awezaye kuongoza umma kiroho na kidunia, na aweze kuhifadhi na kudumisha misingi ya dini ya kiislamu. Linasema kuwa khalifa huyo ni lazima awe amechaguliwa na Mwenyezi Mungu kupitia kwa Mtume wake, na wanasema kuwa Mtume alifanya hivyo kwa kumchagua Ali (a.s.) kuwa khalifa wake, kundi hili ni Imamiyyah au Shi’a. Lengo letu katika upekuzi huu ni kufuatilia suala hilo kwa kutegemea hoja za kiakili, kihistoria, Aya za Qur’ani na Hadithi za Mtume (s.a.w.w.). Lakini kabla hatujaingia kwenye maudhui yenyewe yatupasa tutaje mambo yafuatayo: Je kufanya upekuzi katika maudhui haya kutasabaisha kutoelewana? 125


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:18 PM

Page 126

Tujifunze Misingi ya Dini Yanapozungumzwa mambo yanayohusu uimamu, kuna baadhi ya watu hudakia na kusema: “Huu si wakati wa kuzungumzia hayo bali ni wakati wa kuzungumzia umoja baina ya waislamu, kuzungumzia mambo ya ukhalifa kutazusha kutoelewana na utengano. Isitoshe tuna maadui wakubwa wanaoshirikiana wa kizayuni, wakoloni wa kimashariki na kimagharibi wanaotupiga vita ambao inatupasa tupambane nao, badala ya kuzungumzia mambo yatakayotutenganisha.” Lakini fikra hizi si sahihi kwa sababu zifuatazo: Kwanza, yanayosababisha mizozo na utengano ni yale mazungumzo ya chuki, kuropokwa na kukasirikiana, lakini mazungumzo ya kiakili yenye hoja yasiyo na mizozo, tena yanayofaywa kwa njia ya kirafiki, si kwamba hayatasababisha kutoelewana tu, bali pia yataondoa utengano uliopo kati ya makundi haya mawili na kuimarisha ushirikiano. Katika safari nilizopata kuzuru nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu huko Makka na kuzungumza na wanavyuoni wa kiSunni, nilihisi kama wao, ya kwamba licha ya kuwa upekuzi huu hauna athari mbaya yoyote pia husaidia kuelewana, kudhaniana vizuri na kuondosha chuki nyoyoni. Jambo muhimu katika masomo haya ni kwamba, tuna mambo mengi yanayolingana katika madhehebu haya mawili yatakayotusaidia katika kupambana na maadui zetu wanaoshirikiana. MaSunni wamegawanyika katika madhehebu manne: Hanafi, Hanbali, Shafi’i, na Maliki; hata hivyo kugawanyika huku hakukusababisha utengano kati yao na watakapoyakubali madhehebu ya Shi’a kama madhehebu ya tano, tofauti nyingi kati yao zitaondoshwa, kama ilivyotokea wakati Mufti mkuu wa chuo kikuu cha Al-Azhar (nchini Misri) Sheikh mSunni Mahmud Shaltut alipochukua hatua muhimu ya kutangaza kuwa madhehebu ya Shi’ah kuwa ni madhehebu ya kiislamu pamoja na madhehebu ya Sunni. Hii ilikuwa ni hatua nzuri ya kuleta maelewano mazuri ya kiislamu na uhusiano mwema kati yake na mwanachuoni mkubwa wa ki126


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:18 PM

Page 127

Tujifunze Misingi ya Dini Shi’ah marehemu Burujerdi. Jambo la pili, tunaamini kwamba Uislam ndio Ushi’ah, na wakati ambapo tunaheshimu madhehebu zote za kiislamu, tunaamini kwamba madhehebu ya Shi’ah yana uwezo wa kueleza vizuri zaidi Uislam kwa mwelekeo wake na kutatua matatizo yote yanayohusiana na uongozi katika jamii ya kiislamu. Kwa nini basi tusiwafundishe watoto wetu madhehebu haya na hoja na mantiki, ambapo tusipofanya hivyo tutakuwa tumewafanyia hiyana. Tuna uhakika kuwa Mtume (s.a.w.w.) alimchagua khalifa wake, sasa kuna makosa gani kuyafuatilia maudhui hayo kwa kufuata uongofu wa hoja na akili? Tunapofanya upekuzi katika maudhui haya, tunalazimika kuwa waangalifu ili tusizitweze hisia za kimadhehebu za watu wengine. Jambo la tatu, ili maadui wawagombanishe na kuwatenganisha waislamu, huzusha madai mengi ya uongo kati ya Sunni na Shi’ah na kuwachochea kiasi cha kuwafanya watengane. Na katika nchi nyingi wamefanikiwa kufanya hivyo. Tunapozungumzia suala la uimamu kwa kutumia njia zilizotajwa hapo awali, na tunapotaja dalili wanazozitegemea Shi’ah kwa kutumia ushahidi uliyomo katika vitabu vya Sunni tutaona dhahiri kuwa propaganda za uongo zilitumiwa na maadui; na kwamba adui alijaribu kuyatia sumu mazingira ya uelewano baina ya Sunni na Shi’ah. Mathalan, moja katika safari zangu katika nchi ya Hijaz (Saudia), nilipata kukutana na mwanachuoni mmoja mkubwa wa ki-Sunni akaniambia: “Nimesikia kuwa Shi’ah wana Qur’ani yao tofauti na hii.” Nikwamwambia, si hivyo hata kidogo, na kwa kuthibitisha hilo nakualika ufuatane na mimi twende kwetu baada ya kumaliza Umra, aidha wewe au 127


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:18 PM

Page 128

Tujifunze Misingi ya Dini mwakilishi wako, hapo utaona Qur’ani zimetapakaa kila mahali, mitaani madukani, misikitini, na majumbani, kisha tuziangalie Qur’ani humo, bila shaka utagundua kuwa hazina tofauti zozote na zenu. Isitoshe, Qur’ani nyingi tuzitumiazo zimechapishwa nchini hapa, Misri au katika nchi nyingine za kiislamu. Hapa bila shaka utaona kuwa maneno haya ya kirafiki na ya kidugu kati yangu na mwanachuoni huyo yaliondosha sumu iliyokuwa imetiwa ndani ya akili ya wanachuoni huyo mkubwa. Kwa hiyo, majadiliano kuhusu uimamu kwa njia hii yanaimarisha umoja katika jamii ya kiislamu, yanasaidia kuueleza ukweli na kupunguza tofauti za maoni zilizopo.

Uimamu ni nini? Imam kama lilivyo tamko lenyewe, ni kiongozi wa kiislamu. Kwa misingi ya itikadi ya Shi’ah, imam ‘ma’sum’ (mwenye kuhifadhiwa na dhambi), ni mrithi wa Mtume (s.a.w.w.) katika mambo yote, tofauti tu ni kuwa mtume ni muazilishi wa dini na imam ni mlinzi na mhifadhi wa dini hiyo. Tofauti nyingine ni kuwa, wahyi uliteremshwa kwa mitume, wa sharia, bali wao wamejifunza kutoka kwa Mtume, si kwa maimam wa kawaida, bali wao wamejifunza kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) na wakawa na elimu ya kutosha. Kulingana na itikadi ya ki-Shi’ah, maimamu ma’sum si viongozi wa sharia za kiislamu tu, bali pia ni viongozi wa kiroho, kimaada, kindani na kidhahiri. Yaani wao wana jukumu la uongozi katika mambo yote, katika kulinda na kuhifadhi imani ya kiislamu bila ya kufanya makosa yoyote; na wao ni wateule wa Mwenyezi Mungu. Lakini masuni wanaelewa kimakosa uima128


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:18 PM

Page 129

Tujifunze Misingi ya Dini mu, wanachukulia kuwa ni kiongozi wa serikali ya kiislamu, yaani viongozi wa kila zama ni makhalifa wa Mtume na ni maimamu wa waislamu. Katika masomo yajayo tutaona uthibitisho kwamba katika kila zama, lazima kuwe na mwakilishi wa Mwenyezi Mungu, awe ni Mtume au Imam, awepo duniani kwa ajili ya kulinda dini ya Mwenyezi Mungu na kuwaongoza wale wanaotaka kufuata ukweli, na atakapoghibu machoni kwa watu, basi ni lazima kuwa na mtu atakayekuwa akihifadhi maagizo na kupanga muongozo wa kiislamu.

SOMO LA PILI HEKIMA YA KUWEPO IMAM Utafiti tuliofanya ulithibitisha haja ya kuletwa kwa mtume duniani, pia unathibitisha kwa kiasi kikubwa haja ya kuwapo kwa maimamu baada yake, kwani mambo haya mawili yanahusiana katika mambo mengi ya muhimu isipokuwa suala la uimamu lahitaji maelezo zaidi:

Ukamilifu wa Kiroho na uongozi wa Mwenyezi Mungu Kabla ya jambo lolote, hebu tuangalie lengo la kuumbwa mwanadamu kuwa kiumbe wa hali ya juu kuliko chochote duniani. Anapofuata njia ndefu yenye konakona nyingi kuelekea kwa Mwenyezi Mungu kwenye ukamilifu wowote, bila shaka hawezi kufikia lengo lake hilo bila ya kuongozwa na kiongozi ma’sum, kiongozi wa ki-Mungu. Kwa sababu hii ni njia yenye giza na hatari za kupotea. Ni kweli kwamba Mwenyezi Mungu alimuumba mwanadamu akampa hiyari, akili, kitabu chenye mafunzo ya dini na akamletea mitume, lakini pamoja na hayo yote, anaweza kupotea njia. Kwa hivyo, kuwapo kwa 129


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:18 PM

Page 130

Tujifunze Misingi ya Dini kiongozi ma’sum kutamsaidia kumzuia mwanadamu kuepukana na hatari ya kupotoka na kupotea. Kwa njia hii, kuwapo kwa imam ni muhimu kwa ajili ya kukamilisha lengo la kuubwa mwanadamu. Hii ndiyo hutwa ‘Kanuni ya huruma’ maana yake ni kuwa Mwenyezi Mungu ni mwenye hekima ambaye amemsaidia mwanadamu kwa mambo yote muhimu yatakayomfikisha kwenye lengo la kuumbwa kwake, miongoni mwa mambo hayo ni: Kuleta mitume na kuteua maimam ma’sum, bila ya kufanya hivyo lengo hilo lisingetimia (soma kwa uangalifu).

Ulinzi wa sheria za Mwenyezi Mungu Dini ya Mwenyezi Mungu inapowashukia mitume huwa kama matone safi ya maji ya mvua yaletayo uhai yastawishayo, lakini mara tu yanapoingiana na kuchanganyikana na mazingira yaliyochafuliwa, na akili dhaifu huanza kidogo kidogo kuchafuka, kadhalika imani potofu za kishirikina huongezwa (katika dini hiyo) kiasi cha kuifanya ipoteze utakatifu wake iliyokuja nao, na hapo huwa haivutii, na mafunzo yake hukosa maana, vile vile haikati kiu wala haistawishi. Hapo ndipo inaonekana kuwa pana umuhimu wa kuwapo imam ma’sum, awe ni mlinzi wa kuhifadhi asili ya dini na utaratibu wake, aweze kulinda kutokana na upotofu, kuongezewa mambo, fikra potofu na uzushi; kwani endapo mafundisho ya dini yatakosa kiongozi kama huyo, kwa kipindi kifupi tu yatapoteza asili na ukweli wake. Ndipo Imam Ali (a.s.) akasema: “Bila shaka kwa vyovyote vile, ulimwengu daima haukosi anayesimama kulinda hoja za dini ya Mwenyezi Mungu ili zisiharibiwe; aidha msimamizi huyo aonekane wazi wazi au awe ameghibu.”(Nahjul-Balaghah: 147).

130


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:18 PM

Page 131

Tujifunze Misingi ya Dini Kwa kweli, moyo wa imani ni kama kasha la kuwekea nyaraka muhimu ili zihifadhike kutokana na wevi na ajali nyinginezo. Hii ni sababu nyingine ya kuwepo Imam.

Uongozi wa umma kisiasa na kijamii Bila shaka jamii haiwezi kudumu bila ya kuongozwa na kiongozi imara. Kwa sababu hii, ndio makabila na mataifa yote tangu zamani hadi sasa huchagua kiongozi atakayeweza kuwa mzuri, lakini mara nyingi sana hutokea kuwa mbaya. Mara nyingi kwa kuitumia fursa hii ya umma kuhitaji uongozi, ndipo hujitokeza mpenda makuu na uongozi akajitwalia madaraka, matokeo yake umma hupata kiongozi dhalimu. Huu ni upande mmoja. Kwa upande mwingine ili mwanadamu afikie lengo lake la kiroho, ni lazima afuate njia hii, na si mmoja pekee bali kwa pamoja, kwani nguvu ya mtu mmoja kiroho, kiakili, na kimwili ni dhaifu, si kama ya wengi. Jamii inayofaa, ni ile inayofuata utaratibu mzuri na kuvitumia vizuri vipaji vyake kuupinga upotofu, na kulinda haki za watu wote kama inavyostahiki ili kufikia lengo kuu. Ni kweli kwamba mwanadamu hutenda dhambi ndipo; siku zote tunashuhudia upotofu ulimwenguni, hivyo basi, pana umuhimu wa kuwapo kiongozi ma’sum wa kusimamia dini ya Mwenyezi Mungu na kutumia uwezo wa watu na fikra za wanavyuoni kwa ajili ya kuzuia upotofu huo. Na hii ni hoja kati ya hekima za kuwapo Imam ma’sum, na ni moja kati ya kanuni za Mwenyezi Mungu. Umuhimu wa kukamilisha hoja Kuwapo kwa Imam si kwa ajili ya kuziongoza nyoyo za watu tu, bali pia 131


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:18 PM

Page 132

Tujifunze Misingi ya Dini ni hoja kwa wale wakosao kwa makusudi na kujipoteza; ni hoja juu yao watakapoadhibiwa, wasije wakadai kuwa wameadhibiwa pasina sababu au hawakupata mwongozo ndipo wakapotea. Kwa maneno mengine, kuwapo kwa imam ni kufunga nyudhuru kwa ubainifu wa kwamba hoja zimetolewa kwa kiasi cha kutosha, na wasiofahamu wamefahamishwa vya kutosha na kuwapa nguvu katika matakwa yao wao wanaofahamu.

Imam ni wasita mkuu wa rehma za Mwenyezi Mungu Wengi miongoni mwa wanavyuoni – kwa kutegemea Hadithi za kiislamu - wanalinganisha kuwapo kwa maimamu katika jamii ya wanaadamu, ni kama ulivyo moyo katika mwili wa mtu, kwani moyo unapopiga hupeleka damu kwenye sehemu zote za mwili na kuzalisha chembechembe zote zilizomo. Kwa kuwa Imam ma’sum ni mwanadamu kamili na ni kiongozi wa jamii ya mwanaadamu, na ndiyo sababu ya kumshukia rehema za Mwenyezi Mungu kila anayefungamana naye au mtume; basi ni lazima tuseme kwamba kama vile moyo ulivyo wasita wa maisha ya mwanadamu, mitume na maimam pia ni wasita wa kuzifikisha rehma za Mwenyezi Mungu kwao (soma kwa makini). Hapa isieleweke vibaya, ukweli ni kwamba mitume na maimam hawana uwezo wa kuwapa watu wengine, bali kila uwezo walionao unatokana na Mwenyezi Mungu, isipokuwa tu wao ni kama jinsi ulivyo wasita wa kuzilepeleka rehma za Mwenyezi Mungu kwa mwili, wao ni wasita wa kuzipeleka rehma hizo kwa watu wa aina mbalimbali.

132


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:18 PM

Page 133

Tujifunze Misingi ya Dini

SOMO LA TATU MASHARTI YA SIFA MAALUM ZA IMAM Kabla ya jambo lolote, katika suala hii ni vizuri tufahamu kwamba cheo cha uimamu ni kikubwa anachoweza kufika mwanaadamu; katika kisa cha nabii Ibrahim (a.s.), aliyevunja masanamu, tunasoma:

“Na (kumbukeni) Mola wake alipomfanyia mtihani (nabii) Ibrahim kwa amri nyingi; naye akatimiza. Akamwambia: “Hakika mimi nitakufanya kiongozi (imam) wa watu.” (Ibrahim akasema): “Je na katika kizazi changu pia?” Akasema: “(Ndiyo, lakini) ahadi yangu haitawafikia (waovu) madhalimu wa nafsi zao.” (2:124). Yaani baada ya kupita daraja ya utume na kufaulu mitihani mingi ya Mwenyezi Mungu, akafikia daraja kubwa ya uongozi wa kidhahiria, kindani, kimaada na kiroho katika kuwaongoza watu. Vile vile Mtume Muhammad (s.a.w.w.) pamoja na cheo cha utume pia alikuwa na cheo cha uongozi wa juu. Pia kuna baadhi ya mitume waliofika daraja hii. Huo ni upande mmoja, upande mwingine tunafahamu kwamba masharti na sifa maalum zinazotakiwa awe nazo zichukuane na 133


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:18 PM

Page 134

Tujifunze Misingi ya Dini majukumu atayohitajika kuyabeba, yaani kadri cheo kinavyokuwa cha juu zaidi, ndivyo masharti na sifa zinazolazimu awe nazo zinavyozidi kuwa muhimu na nzito zaidi. Mathalani, ni sharti kwa mtu anayekuwa na jukumu la uhakimu, ushahidi au imamu anayeswalishaSwala ya jamaa na kusoma Sura za Qur’ani, sharti awe mwadilifu, basi itakuwaje kwa mtu atakayechukua jukumu la uimamu? Kwa ujumla ni lazima imam atimize masharti yafuatayo: 1. Kuhifadhiwa na kutotenda dhambi (isma) Imam ni lazima awe amehifadhiwa na madhambi au makosa, kama Mtume, vinginevyo hawezi kuwa kiongozi, hawezi pia kuwa mfano bora kwa watu na mwenye kuaminika. Imam ni lazima azitawale nyoyo za watu, na amri zake zikubaliwe bila kipingamizi. Mtenda dhambi hawezi kuaminiwa kiasi hicho. Vipi mtu afanyaye makosa katika maisha yake ya kila siku, mwongozo wake utegemewe katika kazi za jamii na ufuatwe bila kipingamizi? Hivyo basi, bila shaka Mtume ni lazima awe hatendi dhambi wala hafanyi makosa, vilevile imam ni lazima awe na sifa hii kama tulivyotaja hapo awali. Maelezo haya yanaweza pia kuthibitishwa kwa njia nyingine, nayo ni ‘Kanuni ya huruma’ ya Mwenyezi Mungu ambayo inawajibisha kuwepo kwa Mtume na Imam, kwani lengo la kuwepo wawili hao halitimii bila ya kuwa na sifa hii ya kuhifadhiwa na madhambi, vinginevyo tuliyoyataja kutoka somo lililopita juu ya hekima ya kuwapo wawili hao hayatakuwa na maana kamili.

134


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:18 PM

Page 135

Tujifunze Misingi ya Dini Elimu ya kutosha Imam, kama alivyo Mtume, yeye hutegemewa na watu katika maswala ya kielimu. Ni lazima ajue barabara misingi na matawi yote ya dini, udhahiri wa Qur’ani na undani wake, ajue vizuri sana Sunna za Mtume (s.a.w.w.) na mambo yote yanayohusiana na dini ya kiislamu, kwani ndiye mlinzi na mhifadhi wa sheria za kiislamu; vilevile ni mwongozo na mkuu wa watu. Wale wanaokwama pindi wanapokabiliwa na maswala magumu, au kutegemea kuuliza wengine kwa sababu ya uchache wa elimu zao ambazo haziwezi kujibu maswali yanayohusu jamii ya kiislamu; hawawezi kubeba jukumu la uimam na uongozi wa umma wa kiislamu. Kwa mukhtasri, imam ni lazima awe mjuzi sana na anayefahamu vilivyo mambo yote yanayohusu dini ya Mwenyezi Mungu. Vile Vile azibe nafasi iliyoachwa na Mtume haraka iwezekanavyo, ili dini ya kiislamu iendelee kwa kufuata njia zake sahihi bila ya kupotoka. Ujasiri Imam ni lazima awe jasiri sana, kwani kiongozi lazima awe jasiri, aweze kukabiliana na masaibu magumu ya kimaisha, na aweze kusimama imara dhidi ya madhalimu wenye nguvu na maadui wa ndani na nje.

Kuchukia anasa za dunia Tunafahamu kwamba wale wanaovutiwa na mapambo na anasa za dunia ni rahisi kuhadaika na kupotoka na hivyo huacha njia ya haki na uadilifu, ama 135


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:18 PM

Page 136

Tujifunze Misingi ya Dini kwa tamaa au kwa kutishwa. Mtu kama huyu ni mateka wa dunia, lakini imam ni lazima awe mshindi juu ya anasa na mapambo ya dunia. Asitawaliwe na mapenzi ya nafsi yake na tamaa ya utajiri na cheo, ili asihadaiwe na kuathiriwa na yoyote na hivyo kumfanya asalimu amri na kusikilizana naye. Mvutano wa kitabia Qur’ani inasema hivi kumhusu Mtume Mtukufu:

“Basi kwa sababu ya rehma itokayo kwa Mwenyezi Mungu umekuwa laini kwao (ewe Muhammad). Na kama ungekuwa mkali na mwenye moyo mgumu bila shaka wangalikukimbia…”(3:159). Si Mtume pekee anayepaswa kuwa na tabia ya hali ya juu kiasi hicho, bali hata Imam ni lazima awe na sifa nzuri ili watu wavutiwe naye, kama chuma kinavyovutwa na sumaku. Bila shaka ukali na tabia mbaya humfanya mtu aepukwe na watu na hilo ni aibu kubwa kwa mtume au imam, ndipo mitume na maimam wakahifadhiwa na aibu hii, kwani kama isingealikuwa hivyo hekima ya kwapo kwao isingealikuwa na maana. Haya ndiyo masharti muhimu waliyoyataja wanavyuoni ambayo inabidi imam ayatimize. Vilevile, kuna sifa zingine mbali na hizi tano tulizozitaja anazopaswa kuwa nazo, isipokuwa hizi ni muhimu zaidi.

136


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:18 PM

Page 137

Tujifunze Misingi ya Dini

SOMO LA NNE NI NANI MWENYE JUKUMU LA KUMTEUA IMAM? Baadhi ya waislamu wa madhehebu ya Sunni wanaamini kwamba, Mtume Muhammad (s.a.w.w.) alifariki bila ya kumteua atakayeshikilia wadhifa wa ukhalifa baada yake. Wanaamini pia kwamba jukumu hilo ni la waislamu wenyewe, ni juu yao wao kwa makubaliano yao wote ya pamoja ambayo wanayachukulia kuwa ni moja ya hoja ya kidini. Wanaongeza kusema kwamba, na hilo ndilo lililotokea kwa mara ya kwanza pale khalifa wa kwanza alipochaguliwa makubaliano ya umma wa kiislamu. Huyo khalifa wa kwanza naye akamteua khalifa wa pili kushika wadhifa huo baada yake. Khalifa wa pili kwa upande wake naye akachagua baraza la ushauri la watu sita limchague atakayeshika nafasi hiyo baada yake, nalo lilikuwa na watu wafuatao: Ali, Uthman, Abdul-Rahman Bin Awf, Twalha, Zubeir na Sa’ad bin Abi Waqas. Katika maagizo yake, khalifa wa pili aliagiza kwamba endapo baraza hilo litagawanyika katika makundi matatu, basi liwe kundi litakalokuwa na Abdul-Rahman bin Awf (mkwewe Uthman) ndilo litakalomchagua khalifa; na hivyo ndivyo ilivyotokea kwani kundi la watu watatu: Sa’ad bin Abi Waqas, Twalha na Abdu-Rahman Bin Awf lilimchagua Uthman kushika nafasi hiyo. Mwishoni mwa utawala wake Uthman, watu walikabiliana na Ali na kumchagua awe khalifa wao atakayeshika mahali pa Mtume (s.a.w.w.); isipokuwa Muawiya alikuwa wakati huo ni liwali wa Uthman nchini Sham (Syria), ambaye aliona kwamba hangemwacha Ali aendelee kushika cheo hicho. Hivyo akaanzisha upinzani mkali dhidi ya Imam Ali; ukawa ndio mwanzo wa fedheha kubwa katika his137


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:18 PM

Page 138

Tujifunze Misingi ya Dini toria ya kiislamu, iliyosababisha umwagikaji wa damu nyingi ya watu wasio na hatia. Hapa pana maswali ambayo hapana budi tuyataje, ili kutoa mwanga zaidi katika utafiti wa kielimu na kihistoria, nayo ni: Je umma una haki ya kumchagua khalifa wa Mtume? Jibu la swali hili ni rahisi: Tukizingatia uimamu kwa maana ya uimam wa kidhahiri kwa umma wa kiislamu, hapo yawezekana imam achaguliwe na watu. Ama tukizingatia kwa maana tuliyoieleza hapo awali kutokana na maelezo ya Qur’ani; bila shaka hapana mwingine afaaye kumteua khalifa isipokuwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na kwa amri itokayo Kwake, kwani kulingana na maelezo haya, miongoni mwa masharti ya uimamu ni kuwa na ujuzi wa kutosha juu ya misingi na matawi ya dini, ujuzi unaotoka kwa Mwenyezi Mungu na kutegemewa elimu ya Mtume (s.a.w.w.), ili aweze kulinda na kuhifadhi sheria za dini ya kiislamu. Sharti jingine kwa imam, ni lazima awe amehifadhiwa na Mwenyezi Mungu kwa kutotenda dhambi au kosa ili aweze kubeba jukumu la wadhifa wa uimamu, na kuongoza umma kimaana, kidhahiri na kindani. Vile vile awe na sifa za kutopenda mambo ya dunia, awe mcha-Mungu na awe shujaa, sifa ambazo ni muhimu kwa anayeshikilia wadhifa huo. Kuweza kupambanua sifa hizi, ni jambo gumu isipokuwa kwa wasita wa Mtume (s.a.w.w.) kutoka kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, kwani yeye (Mwenyezi Mungu) Ndiye ajuaye kiwango cha hali ya juu 138


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:18 PM

Page 139

Tujifunze Misingi ya Dini cha elimu, ucha-Mungu, utawa, na ushujaa mambo ambayo ni lazima kwa anayefaa kushika nafasi ya uimamu. Ama wale waliowapa watu uwezo wa kumchagua imam na khalifa, kwa hakika wamebadili maana ya uimam kama inavyotaka Qur’ani na kufanya iwe na maana ya uongozi wa kidunia, viginevyo (na ndivyo inavyotakiwa) masharti ya kuwa imam mkamilifu, mwenye sifa zote njema, hapana ajuaye ila Mwenyezi Mungu tu. Suala hili ni sawa na swala la uteuzi wa Mtume, kwani mtume hawezi kuchaguliwa kwa kura za watu, bali huteuliwa na Mwenyezi Mungu; na watu humtambua kutokana na miujiza yake, na hapana azijuaye sifa za kuwa mtume ila Mwenyezi Mungu.

Je hakuchagua atakayeshikia wadhifa huo? Bila shaka dini ya kislamu ni dini ya ulimwengu mzima na ya milele, na wala si ya muda na mahali maalumu. Hilo limeelezwa na Qur’ani tukufu. Na bila shaka yafahamika kwamba wakati alipofariki Mtume (s.a.w.w) mafundisho ya kiislamu yalikuwa hayajaenea hadi nje ya Bara Arabu. Kwa upande mwingine tunaona kwamba Mtume Muhammad alitumia miaka kumi na mitatu ya umri wake katika kupambana na shirk na ibada ya masanamu; kisha miaka kumi ya mafanikio iliyofuatia baada ya kuhama kwake kutoka Makka na kwenda Madina, aliitumia zaidi katika kuzima mizozo na vita vilivyolazimishwa na maadui zake. Licha ya kuwa Mtume (s.a.w.w.) hakuacha hata dakika moja ipite katika umri wake bila ya kuitumia katika kueneza mafunzo ya kiislamu; hata hivyo, kazi ya kutatua matatizo mengi ya kiislamu ilihitaji muda mrefu. Hivyo basi kulikuwa na haja ya kuwapo mtu mwenye sifa kama zake atakayeweza kuendeleza kazi hiyo baada ya kufa kwake. Isitoshe, kupanga mustakabali wa umma na kuandaa mambo yatakayoendeleza kudumu kwa amani ni katika mambo muhimu ambayo kila kiongozi 139


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:18 PM

Page 140

Tujifunze Misingi ya Dini anapaswa kuyafikiria na kutoyasahau kamwe. Tukiachana na yote hayo, hapa tunaona kuwa mara kwa mara Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akitoa mafunzo mahsusi katika mambo mengi madogo yanayohusiana na maisha ya kila siku, sasa iweje apuuze jambo muhimu la ukhalifa, uongozi na uimamu, na asiliwekee utaratibu maalum? Njia hizi tatu tulizozifafanua ni dalili za wazi za kuonyesha kwamba Mtume (s.a.w.w.) hawezi kupuuza suala la kumuainisha khalifa atakayekuwa baada yake. Tutataja mapokezi yanayotegemewa ili kutoa mwanga zaidi kwenye maudhui haya katika masomo yajayo, Insha’llah. Imethibiti kwamba Mtume (s.a.w.w.) hakughafilika na jambo hilo katika maisha yake yote licha ya matukio ya kisiasa yaliyozushwa baada ya kufariki kwake ili ionekane kwamba Mtume hakumuainisha atakayeshika ukhalifa. Je mtu anaweza kusadiki kwamba Mtume hakuacha mji wa Madina bila ya kuwepo kiongozi katika siku chache za safari yake ya vitani (k.v. vita vya Tabuk?) Itakuaje basi asiache kiongozi baada ya kuondoka duniani? Auache umma wa kiislamu katika mizozo na machafuko bila ya kuukabidhi mikononi mwa kiongozi anayetegemewa? Bila shaka kukosa kuainishwa khalifa kungeleta hatari kubwa kwa Uislam uliokuwa ukiinukia, hapa ndipo akili na mantiki zinaamua kuwa haiwezekani Mtume (s.a.w.w.) afanye hivyo. Na wale wanaodai kwamba Mtume (s.a.w.w.) aliwaachia umma jukumu hilo, nawalete hoja zao za kuthibitisha kama Mtume (s.a.w.w.) alitangaza hilo hadharani. Lakini hata hivyo hakuna hoja zozote zinazotolewa kuhusu jambo hilo.

140


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:18 PM

Page 141

Tujifunze Misingi ya Dini Makubaliano na baraza la ushauri Hebu tumchukulie kuwa Mtume (s.a.w.w.) alipuuza jambo hilo muhimu na kuwaachia waislamu wenyewe wachague khalifa kwa njia ya ‘makubaliano’.. lakini tunavyofahamu, ‘makubaliano’ maana yake ni maafikiano ya waislamu wote na tunajua kwamba maafikiano hayo hayakufanyika alipochaguliwa khalifa wa kwanza ambapo waislamu wengi walikuwa nje ya Madina hawakushirikishwa kwenye jambo hilo wala kwenye kutoa maoni yao; licha ya hao hata wengi wao waliokuwepo mjini humo pia hawakuwepo, kama Imam Ali na ukoo wa Bani Hashim. Kwa hivyo basi, makubaliano kama hayo hayakubaliki. Aidha, ikiwa huu ndiyo mfumo sahihi unaofaa kufuatwa, kwa nini khalifa wa kwanza asiufuate katika uteuzi wake wa kumteua khalifa wa pili? Kwa nini alijiteulia mtu amtakaye? Na kama pana mtu anayefaa kumteua khalifa basi Mtume anafaa zaidi kuliko mtu mwingine yeyote. Licha ya hayo, pana tatizo la tatu linalojitokeza kuhusiana na khalifa wa tatu: Kwa nini khalifa wa pili hakutumia utaratibu alioutumia khalifa wa kwanza katika uteuzi wake wa khalifa wa pili; akawa hakufuata makubaliano wala hakuteua, bali aliteua baraza la ushauri lifanye kazi hiyo? Ikiwa fikra ya kushauriana ni sahihi, kwa nini wawe ni watu sita pekee? Na kwa nini kati ya hao sita, watu watatu kati yao watosheleze kwa rai yao? Maswali haya ni lazima yampitie mtu kichwani; msomaji yeyote wa historia ya kiislamu, na kukosekana majibu yake kunadhihirisha kwamba kati ya njia zote hizi hakuna hata moja ifaayo kumchagua Imam.

4. Imam Ali (a.s.) ndiye aliyefaa kwa wadhifa huo Hebu tuchukulie kuwa Mtume (s.a.w.w.) hakumuainisha yeyote 141


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:18 PM

Page 142

Tujifunze Misingi ya Dini atakayeshika ukhalifa baada yake, na kwamba jambo hilo aliuacha umma wa kiislamu, je wakati tunapochagua yafaa tumuache aliye mjuzi zaidi kuliko wengine wote kisha tuwachague aliowashinda? Wanavyuoni wengi wa kiislamu wakiwemo wa madhehebu ya Sunni wameeleza waziwazi kwamba Ali (a.s.) alikuwa mjuzi zaidi wa dini ya kiislamu, na mafunzo mengi aliyowaachia umma wa kiislamu yanathibitisha hilo. Historia ya kiislamu yatuambia kuwa yeye ndiye aliyekuwa tegemeo la umma katika masuala magumu ya kielimu, hata makhalifa waliomtangulia mara kwa mara walirejea kwake walipokabiliwa na maswala magumu ya kidini. Vile vile alikuwa na daraja kubwa sana ya ushujaa, uchamungu, kutopenda mambo ya kidunia na sifa nyinginezo. Kwa hivyo tunapochulia kwamba kuchaguliwa kwa khalifa wameachiwa watu, basi Ali (a.s.) alifaa zaidi kuliko wengine. (Maelezo haya ni mapana na yana ushahidi wa kutosha ambao hautoshi kueleza hapa, rejea vitabu vinavyohusika).

SOMO LA TANO QUR’ANI NA UIMAMU Kitabu kitakatifu cha Qur’ani ndicho kiongozi chema katika mambo yote, hata suala la imam limegusiwa humo: Qur’ani yasema kuwa ni uteuzi wa Mwenyezi Mungu. Katika masomo yaliyopita, tumesoma kisa cha Nabii Ibrahim (a.s.) aliyevunja masanamu, na tukaona kwamba Qur’ani inazingatia kuwa wadhifa wa uimamu na uongozi uliopita baada ya kupata utume na ujumbe na kufaulu majaribu mengi, inasema: 142


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:18 PM

Page 143

Tujifunze Misingi ya Dini

“Na (kumbukeni) Mola Wake alipomfanyia mtihani (nabii) Ibrahim kwa amri nyingi naye akazitimiza. Akamwambia, hakika mimi nitakufanya kiongozi (imam) wa watu.” (2:124). Kuna dalili nyingi za Qur’ani na za kihistoria zinazoonyesha kuwa alipata daraja hii baada ya kupambana na waabudu masanamu wa nchi ya Babel (Babylon, Iraq ya sasa) na kuhama kwenda nchi ya Sham (Syria), kisha kwenda kujenga Al-Ka’aba huko Makka na kumchukua mwanawe Ismail (a.s.) hadi kwenye mahali pa kumtoa kafara. Ikiwa utume na ujumbe ni mambo yanayotoka kwa Mwenyezi Mungu, basi hapana budi uteuzi wa uimamu - ambao ni uongozi mkubwa – pia utoke kwa Mwenyezi Mungu, hayo ni mambo ambayo hayapaswi kuachiwa watu, ndipo Mwenyezi Mungu akasema akimwambia Ibrahim (a.s.) kuwa “… hakika mimi nitakufanya kiongozi (imam) wa watu…” (2:124). Aidha Qur’ani inatoa maelezo ikizungumzia mitume Ibrahim, Lut, Is’haq na Yaqub kwa kusema: “Na tukawajaalia kuwa maimam, wanaongoza kwa amri yetu.” (21:73). Kuna Aya zingine katika Qur’ani zinazofanana na hizi, zote zinaonyesha kuwa huu ni wadhifa unaotoka kwa Mwenyezi Mungu na ni Yeye ndiye mteuzi wa anayetaka kumpatia wadhifa huu. Kama tuonavyo katika Aya hiyo hiyo inayozungumza uimamu wa Ibrahim (a.s.) kuwa yeye aliwaombea dhuria wake wapate daraja hiyo, lakini Mwenyzi Mungu akamjibu: “…Ahadi yangu haitawafikia (waovu) madhalimu wa nafsi zao.” (2:124).

143


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:18 PM

Page 144

Tujifunze Misingi ya Dini Yaani maombi yamejibiwa, lakini wale waovu katika dhuria wako hawatafikia daraja hii kubwa. Tukiangalia kwa makini ufafanuzi wa neno “dhalimu” kilugha kwa ujumla, na kilugha ya Qur’ani, tutaona kuwa limekusanya maana kubwa, ikiwa ni pamoja na madhambi kama vile shirki ya waziwazi na ya kisiri, na watu kujidhulumu wenyewe au kuwadhulumu wengine. Haya yote hakuna ayajuaye kiuhakika ila Mwenyezi Mungu, kwani Yeye ndiye pekee anayejua yaliyomo ndani ya nyoyo za watu, kwa hivyo hapa twaona ni dhahiri kwamba ni Mwenyezi Mungu tu peke yake ndiye awezaye kumteua imamu kwa minajili ya kushika wadhifa huo. Kufikisha ujumbe Mwenyezi Mungu amesema:

“Ewe Mtume! fikisha uliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wako; na kama hutafanya, basi ni kama haukufikisha ujumbe wake. Na Mwenyezi Mungu atakulinda na watu. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongozi watu wanokufuru.” (5:67). Aya hii inaonyesha kuwa Mtume (s.a.w.w.) alipewa jukumu kubwa lenye kuwakera baadhi ya watu na pengine kusababisha upinzani kutoka kwao, kwa hivyo akampoza kwa kusema, “Na Mwenyezi Mungu atakulinda na watu.” Vile vile suala hili halikuhusu mambo ya tawhidi na shirk au kupambana na maadui wa kiyahudi, wanafiki, n.k. kwa kuwa mambo hayo yote tayari yalikwishatengenezwa kabla ya kushuka Aya hii. 144


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:18 PM

Page 145

Tujifunze Misingi ya Dini Isitoshe, kuletwa mafunzo ya kiislamu (hapo mwanzoni) hakukufuatana hatari hizi, na kulingana na inavyodhihiri katika Aya hii ni kwamba ilikuwa ni amri yenye uzito, kama wa ujumbe wenyewe, kiasi ambacho kama asingeufikisha ujumbe huo, angelikuwa kama ambaye hakutimiza ujumbe wenyewe hasa. Je amri hii si suala la ukhalifa? Hasa tukiangalia kwamba Aya imeshuka mwisho wa umri wa Mtume, yaani wakati unaofaa kumtaja atakayekuwa khalifa wa Mtume. Aidha, kuna mapokezi mengi kutoka kwa maswahaba wakubwa wa Mtume kama akina Zaid bin Al-Arqam, Abu Said el- Khudri, Ibnu Abbas, Jabir Bin Abdillah Al-Ansari, Abu Huraira, Hudhaifa na Ibn Mas’ud. Mapokezi haya yamepokelewa kwa njia kumi na moja, ambazo nyingi zimepokelewa na wafasiri, wapokezi na wanahistoria wa ki-Sunni. Riwaya zote hizo zinasema kuwa Aya hii imeshuka kwa sababu ya Ali (a.s.) siku ya Ghadir. Ama sisi tunatosheka kwamba Aya hii yadhihirisha ya kuwa Mwenyezi Mungu alimuamuru Mtume wake, alipokuwa akirejea kutoka kwenye Hijja yake ya mwisho, amtangaze rasmi Ali (a.s.) kuwa khalifa baada yake mbele ya kadamnasi ya waislamu.

Aya ya kuwatii wenye mamlaka Mwenyezi Mungu amesema: “Enyi mlioamini! Mtiini Mwenyezi Mungu na mtiini Mtume na wenye mamlaka juu yenu …’(4:59). Hapa tunaona kuwa, kuwatii mweye mamlaka kumetajwa baada ya kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume Wake bila ya sharti lolote. Je hawa ‘wenye mamlaka’ wanakusudiwa viongozi wa wakati wowote au mahali popote? Mathalan, waislamu wa miji mbalimbali wa wakati huu wawatii watawala wao tu vivi hivi? (kama baadhi ya Sunni wanavyosema). Maelezo haya hayaingii akilini, kwani watawala wengi, katika nyakati mbalimbali ni wapotofu, waasi na madhalimu. 145


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:19 PM

Page 146

Tujifunze Misingi ya Dini Je makusudio yake ni kuwatii watawala kwa sharti kwamba hawatayapinga mafundisho ya kiislamu? Haya pia hayachukuani na maelezo ya Aya hii. Au makusudio yake ni maswahaba wa Mtume? Haya pia hayachukuani na ufahamu wa Aya kutokana na tofauti za zama (zama hizi za sasa hakuna maswahaba). Kwa hiyo basi, ni wazi kwamba makusudio ya ‘wenye mamlaka’ ni kiongozi aliyehifadhiwa na madhambi aliyeko kila zama za wakati, ambaye yapasa afuatwe bila sharti lolote, na amri yake yapasa kutekelezwa kama ilivyo amri ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Mapokezi mengi yanahusu suala hili, ambayo yanafafanua kuwa ‘wenye mamlaka’ ni Imam Ali na Maimamu watakatifu ni dalili nyingine ya kutilia mkazo suala hili. Aya ya uongozi (Wilaya) Mwenyezi Mungu amesema:

“Hakika viongozi wenu (hasa) ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na walioamini ambao husimamisha Swala na kutoa Zaka na huku wamerukuu.” (5:55). Katika sarufi ya lugha ya Kiarabu (Nahw), inapotumika herufi ‘innamaa’ inakusudia kudhibiti kimipaka, hapa Qur’ani inadhibiti mipaka ya uongozi kwa watatu pekee, Mwenyezi Mungu, Mtume wake na wale walioamini, wanotoa Zaka huku wamerukuu. Bila shaka neno ‘wilaya’ halimaanishi mapenzi baina ya waislamu, kwani 146


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:19 PM

Page 147

Tujifunze Misingi ya Dini mapenzi baina yao wote hayahitaji masharti yote haya. Na hupendana hata kama hawakutoa Zaka wakati wakirukuu, kwa hivyo neno ‘wilaya hapa limaanisha uongozi na uimam wa kimaada na wa kiroho na hasa neno hilo lilivyoambatanishwa na uongozi wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Vile vile Aya yenyewe inaeleza waziwazi mtu maalum aliyetoa sadaka na huku akiwa amrukuu, kwani si kama hivyo, hakuna kitakachomfanya mtu atoe sadaka akiwa kakika hali ya kurukuu anaposwali. Hii ni sifa maalum, si ya wote. Aya hiyo iliyotangulia inaeleza kisa cha Imam Ali (a.s.). Siku moja alikuwa akiswali, alipokuwa katika hali ya kurukuu, alimsikia masikini akiomba apatiwe sadaka, hata hivyo hakuna yeyote aliyemshughulikia, ndipo akamnyooshea kidole chake cha mkono wa kulia kilichokwa na pete ya thamani ili aichukue. Yule masikini akaitwaa pete hiyo akaenda zake. Mtume (s.a.w.w.) alishuhudia yote hayo, alipomaliza kuswali, aliinua kichwa chake na kusoma: “Ewe Mola wangu! Ndugu yangu Musa (a.s.) alikuomba akasema: “Ee Mola Wangu, nikunjue kifua changu, unifanyie sahali kazi zangu, ufungue fundo lililo katika ulimi wangu, wapate fahamu maneno yangu, unifanyie msaidizi katika jamaa zangu, ndugu yangu Harun, nitie nguvu kwa ndugu yangu huyu na umshirikishe katika kazi yangu hii.” Kisha akamwambia: ‘Tutautia nguvu mkono wako kwa ndugu yako na tutakupeni na ushindi hata hawatowafikieni, kwa sababu ya ishara zetu, nyinyi na watakaokufuateni watashinda.’ Ee Mola! Na mimi Muhammad ni nabii Wako, nikinjue kifua changu, unisahilishie kazi yangu na unifanyie msaidizi katika jamaa zangu unitie nguvu kwa Ali…” Kabla Mtume hajamaliza dua yake hii, akaja Malaika Jibril (a.s.) akamsomea Aya tuliyoitaja hapo mwanzoni. Ni vizuri kufahamu kwamba, wafasiri wengi wa ki-Sunni, wapokezi 147


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:19 PM

Page 148

Tujifunze Misingi ya Dini wa Hadithi na wanahistoria wao wanasema kuwa Aya hiyo imeshuka kumhusu Imam Ali (a.s.). Aidha kuna maswahaba wapatao kumi waliopokea Hadithi hiyo kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.). Kuna Aya nyingi zinatoa maelezo juu ya jambo hili la ‘wilaya’ lakini tumetosheka na hizo nne tu katika somo hili.

SOMO LA SITA UIMAMU KATIKA HADITHI ZA MTUME (S.A.W.W.) Mtu anaposoma vitabu maalum vya Hadithi za kiislamu, na hasa vitabu vya madhehebu ya Sunni, ataona kuwa kuna Hadithi nyingi mno zinazothibitisha uimam na ukhalifa wa Ali (a.s.). Kisha mtu huyo hushangazwa kwa nini wamechagua njia nyingine isiyokuwa ya Ahlu Bait licha ya Hadithi nyingi hizo ambazo zinaondoa shaka zote juu ya suala hili. Hadithi hizi ni kwa mamia (kama Hadithi ya Ghadir) na zinaungwa mkono na nyingine nyingi na ziko waziwazi ndani ya vitabu mashuhuri ya kiislamu, kiasi ambacho lau tutaacha maneno yasiyo na uhakiki na kufuata tu, jambo hili lingekuwa liko wazi kabisa hata tusingelihitaji hoja zozote, hapa tunataja baadhi ya Hadithi mashuhuri, tukiwataka wale wale wanaotaka kuzisoma, warejee kwenye vitabu tutakavyovitaja. Hadithi ya Ghadir Wanahistoria wengi wa kiislamu wanasema kwamba Mtume (s.a.w.w.) alipotekeleza faradhi ya Hijja, iliyokuwa ya mwisho katika maisha yake, alirejea akiwa amefuatana na sahaba zake wapya na wa zamani, na waislamu wengine walikuwa wamekusanyika ili waungane naye katika kutekeleza faradhi ya Hijja. 148


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:19 PM

Page 149

Tujifunze Misingi ya Dini Walipofika katikati ya Makka na Madina mahali paitwapo Juhfa, Mtume alikwenda hadi mahali paitwapo Ghadir Khum, mahali ambapo mahujaji hutawanyika na kila mmoja kushika njia yake. Mtume (s.a.w.w.) akaamuru watu wasiondoke na warejee wale ambo tayari walikuwa wameshaanza kuondoka. Hali ya hewa ya mahali hapo ilikuwa ni ya joto kali mno, na hapakuwa na mahali pa kuziba jua. Waliswali Swala ya adhuhuri pamoja na Mtume (s.a.w.w.), na baada ya kumaliza Swala akawaamuru wabaki hapo ili wasikilize jambo muhimu litokalo kwa Mwenyezi Mungu. Akatengeneza mimbari ili awahutubie watu. Akasimama, akamhimidi Mwenyezi Mungu na kuanza kuhutubu. Katika mambo aliyoyasema ni: “…Enyi watu!Sikilizeni kwa hakika mimi sijui kama nitakutana nanyi tena baada ya mwaka huu, mimi nina majukumu nanyi pia mnayo. Je mwanishuhudilia vipi?” Watu wakapaza sauti zao wakisema: “Twashuhudia ya kwamba umefikisha ujumbe, umeonya, na umejitolea kwa juhudi zako zote, Mwenyezi Mungu akulipe kheri.” Akaendelea: “Je mwakiri kwamba hapana Mola apasaye kuabudiwa isipokuwa Mwenyezi Mungu na kwamba Muhammad ni Mtume wake, na Mwenyezi Mungu atawafufua wafu siku ya Kiyama?” Wote wakajibu: “Ndiyo tunakiri yote hayo.” Akasema: “Ee Mola shuhudia.” Kisha akawauliza: “Mwanisikia?” Wakajibu” “Ndiyo.” Watu wote wakanyamaza kimya isipokuwa sauti ya upepo iliyosikika ikivuma. Akaendelea: “Hebu niambieni mtavifanyia nini vizito hivi viwili nitakavyowaachia baada ya kuondoka kwangu?” Akasimama mtu mmoja miongoni mwa waliohudhuria, akauliza “Ni vipi hivyo?” Mtume (s.a.w.w.) akajibu: “Kizito cha kwanza ni kikubwa, nacho ni Qur’ani, Kitabu cha Mwenyezi Mungu ambacho mkishikamana nacho hamtapotea; na cha pili ni Ahlul-Bait wangu, Mwenyezi Mungu aliye na huruma na Mjuzi ameniambia kuwa vitu viwili hivyo havitatengana mpaka vinirudie kwenye ‘Hawdh’ Siku ya Kiyama. Mkivipita mtaangamia na mkivikhalifu 149


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:19 PM

Page 150

Tujifunze Misingi ya Dini mtaangamia.” Kisha Mtume(s.a.w.w.) akawa akitazama huku na huko kama aliyekuwa akitafuta mtu. alipomuona Ali (a.s.) alimwiinua juu mkono wake mpaka weupe wa makwapa ukionekana, watu wote wakamtambua. Akauliza: “Ni nani bwana aliye bora zaidi kwa waumini?” Wakajibu: “Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndiyo wajuao zaidi.”Akaongeza: “Mwenyezi Mungu ni bwana wangu nami ni bwana wa waumini na ni mbora wao; basi yeyote ambaye mimi ni bwana wake, basi na Ali pia ni bwana wake.” alikariri maneno haya mara tatu au mara nne (kulingana na mapokezi mengine). Mtume (s.a.w.w.) akainua kichwa chake akakielekeza mbinguni akasema: “Ee Mola! Mpende anayempenda Ali, na mchukie amchuikiaye. Mnusuru anayemnusuru Ali, na umwepuke amwepukaye; na iweke haki pamoja naye popote awapo.” Kisha akasema: “Je nimefikisha ujumbe?” Akajibiwa, “Ndio.” Akaongeza: “Basi aliyeko hapa amweleze asiyekuwepo.” alishuka Jibril (a.s.) akamsomea Mtume haya yafuatayo:

“…Leo nimekukamilishieni dini yenu, na kukutimizieni neema yangu na nimekupendeleeni Uislam uwe dini yenu…” (5.3). Kisha Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Allahu Akbar, Allahu Akbar, (Mungu ni mkubwa, Mungu ni mkubwa) namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kukamilsha dini, kutimiza neema, kuridhia ujumbe wangu na kumtangazia uongozi Ali baada yangu.” Watu wakasongamana kumpongeza Ali (a.s.), miongoni mwao walikuwa ni Abu Bakr na Umar ambao walimfuata na kila mmoja akimwambia: “Pongezi! Ee mwana wa Abu Twalib, umekuwa bwana wangu na bwana 150


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:19 PM

Page 151

Tujifunze Misingi ya Dini wa kila muumini.” Hadithi hii imetajwa na wanavyuoni wengi wa kiislamu katika vitabu vyao, wengine wameitaja kwa kirefu na wengine wameitaja kwa kifupi mno na kutia tofauti ndogo ndogo katika maneno. Hadithi hii huzingatiwa kuwa ni moja kati ya Hadithi zisizotiliwa shaka, hata mwanachoni Al-Amin katika kitabu chake Al-Ghadir ametaja majina ya maswahaba 110 waliotaja Hadithi hii na pia vitabu 360 ambavyo imetajwa Hadithi hiyo, miongoni mwa hivyo ni vitabu vya ki-Sunni vya tafsiri, historia na Hadithi. Vile vile wanavyuoni wengi wakubwa wa kiislamu wametunga vitabu maalum juu ya tukio hili. Kama kitabu cha Al-Ghadir cha Shekh Al-Amin ambamo ametaja humo wanavyuoni wapatao ishirini na sita waliotunga vitabu maalum juu ya tukio hilo la Ghadir. Watu wengi ambao wameona kwamba Hadithi hii haiwezi kukanushwa, wamejaribu kuikanusha kwenye suala la uimamu na ukhalifa. Wakasema neno “maula” (bwana) lina maana ya rafiki; ambao lau mtu ataichunguza kwa makini Hadithi yenyewe na mfumo wakati na mahali, ataona kwamba shabaha yake ni suala la uimamu yaani uongozi kwa maana zote sababu zifuatazo: Aya ya tabligh tuliyoitaja hapo awali na iliyoshuka kabla ya tukio la Ghadir inaonyesha wazi kwamba basi kusingekuwa na haja ya kutiliwa umuhimu na kuhimizwa kiasi hicho. Vile vile Aya maalum inayotaja ‘kukamilishwa dini’ ambayo ilishuka baadaye inatoa hoja wa wazi kuonyesha kuwa jambo hilo lina umuhimu mkubwa wa uongozi na ukhalifa baada ya Mtume (s.a.w.w.). Jinsi ilivyoelezwa Hadithi yenyewe, kama vile jangwa lenye joto palipotolewa hotuba, na watu kuchukua kiapo juu ya imani zao mahali hapo, yote 151


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:19 PM

Page 152

Tujifunze Misingi ya Dini yanathibitisha umuhimu wa madai hayo tuyasemayo. Pongezi alizozipata Ali (a.s.) kutoka tabaka za watu mbalimbali waliohudhuria hapo, na mashairi yaliyoimbwa kwa kuadhimisha siku hiyo; yote haya yanaonyesha kuhusika kwa Imamu Ali (a.s.) kupewa uongozi wa uimam.

SOMO LA SABA HADITHI YA ‘MANZILA’ NA ‘YAUMUD-DAARI” Wafasiri wengi wa ki-Sunni na ki-Shi’ah wameelezea Hadithi ya Manzila pale wanapozifasiri aya ya 142 katika Sura ya 7 ambayo inafungamana na Nabii Musa (a.s.) pale alipokwenda kukutana na Mwenyezi Mungu kwa muda wa siku 40, akamwacha ndugu yake Harun awe naibu wake. Hadithi ya ‘Manzila” ni hii: Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa akienda kupigana vita huko Tabuk (Tabuk ni mji ulioko kaskazini mwa Bara Arabu upande uliopakana na mashariki mwa utawala wa warumi), alipashwa habari kwamba mtawala wa kirumi wa upande wa mashariki ametuma jeshi ili kuyazuia mapinduzi ya kiislamu kabla hayajafikia kwenye mpango wake kwa wanaadamu. Mtume (s.a.w.w.) akafunga safari kwenda huko akimwacha Ali (a.s.) kushika mahali pake. Imam Ali (a.s.) akasema: “Je waniacha nibaki na wanawake na watoto? Kwa nini usiniruhusu niungane nawe vitani?” Mtume (s.a.w.w.) akamwambia: “Je huridhiki uwe na daraja kwangu kama aliyokuwa nayo Harun kwa Musa (a.s.) isipokuwa tu kwamba hakuna mtume mwingine baada yangu?” Ibara hii imetajwa katika vitabu mashuhuri vya ki-Sunni, kama vile Sahih 152


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:19 PM

Page 153

Tujifunze Misingi ya Dini Bukhari na Sahih Muslim, tofauti tu kuwa Sahih Bukhari imetaja Hadithi yote, lakini katika Sahihi Muslim Hadithi yote imekuja mara moja, na sehemu nyingine imekuja sentensi moja tu, “Wewe una daraja kwangu kama Harun aliyokuwa nayo kwa Musa (a.s.).” Vilevile Hadithi hii ya manzila imetajwa katika vitabu vikubwa vikubwa vya ki-Sunni kama: Sunan cha Ibn Maja, Sunan Tirmidhi, Musnad ya Ahmad, na vinginevyo. Na maswahaba waliopokea Hadithi hiyo ni zaidi ya ishirini, miongoni mwao ni Jabir bin Abdillah al-Ansari, Abu Said El-Khidri, Abdallah bin Mas’ud na Muawiya. Abu Bakr Baghdad mwenye kitabu Tarikh Baghdad, amenukuu kutoka kwa Umar bin Al-Khattab: Kwamba alimwona mtu akimtukana Ali (a.s.), Umar akamwambia: “Mimi naona wewe ni mnafiki, kwani nimemsikia Mtume akisema, ‘Ali ana daraja kwangu kama aliyokuwa nayo Harun kwa Musa (a.s.) isipokuwa tu hakuna mtume baada yangu.”

Jambo muhimu la kuangalia katika vitabu muhimu vya Hadithi ni kwamba Mtume (s.a.w.w.) hakusema maneno haya wakati akienda Tabuk tu, bali ameyakariri mara saba katika sehemu mbambali, nazo ni: 1. Siku Mtume (s.a.w.w.) alipojenga udugu kwa mara ya kwanza baina ya waislamu wa huko Makka, wakati waislamu walipochukua ahadi na kuunganishwa udugu wa kiislamu. Yeye alimchagua Ali (a.s.) alitaja ibara hii pia. Siku ya kuungana udugu mara ya pili huko Madina, kati ya Muhajirina na Ansar. Mtume aliikariri tena ibara hii. Siku Mtume (s.a.w.w.) alipoamuru kufungwa milango yote ya nyumba inayofunguliwa kuelekea kwenye msikiti wa Mtume, na kuachwa wazi mlango wa Ali (a.s.) pekee; pia alikariri ibara hii. 153


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:19 PM

Page 154

Tujifunze Misingi ya Dini Katika vita vya Tabuk, kama tulivyokwishaeleza. Vile vile katika sehemu tatu zingine ambazo zimetajwa katika vitabu vya Sunni. Kwa hivyo basi, hapana sababu ya kutia shaka juu ya usahihi wa Hadithi ya ‘Manzila’ si kwa upande wa mapokezi, wala si kwa maana yake kwa ujumla. Yaliyo katika Hadithi ya ‘Manzila’ Tukiangalia kwa makini Hadithi hii, na tukiachilia mbali maamuzi yetu tuliyoyataja hapo nyuma, tutaona kwamba vyeo vyote alivyokuwa navyo Harun kwa Waisrail - ukitoa utume - pia Ali (a.s.) alikuwa navyo, kwa sababu hayakutajwa katika Hadithi hii masharti mengine. Kwa hivyo utaona: 1. Ali (a.s.) alikuwa na sifa bora zaidi baada ya Mtume (s.a.w.w) kama alivyokuwa, na vile alivyokuwa Harun (a.s.) kwa Waisraeli. 2. Ali (a.s.) alikuwa ni msaidizi maalum wa Mtume (s.a.w.w.) na mshirika wake katika kuuongoza umma. (Angalia Sura ya 20, Aya ya 29-32). 3. Alikuwa ni khalifa wa Mtume (s.a.w.w.) hata kabla hajafariki, na kama nafasi aliyokuwa nayo Harun kwa Musa (a.s.).

Hadithi ya ‘Yawmud-Dari’ Vitabu vya historia vinaeleza kwamba mnamo mwaka wa tatu wa utume, Mtume (s.a.w.w.) aliamrishwa kutangaza dini ambayo ilikuwa siri mpaka muda huo, kama inavyoeleza Aya ifuatayo: “Na waonye jamaa zako wa karibu.” (26:214). Mtume alipopata maagizo hayo; aliwaalika chakula jamaa zake kwenye 154


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:19 PM

Page 155

Tujifunze Misingi ya Dini nyumba ya ami yake Abu Twalib. Walipomaliza kula, alisimama akasema: “Enyi wana wa Abdul Muttalib, kwa hakika mimi ni muonyaji na mtoaji bishara kutoka kwa Mwenyezi Mungu, basi kubalini na mnisikilize ili mpate kuongoka.” Kisha akaendelea: “Je ni nani kati yenu atakayeungana nami, ni nani atakayenisaidia na kuwa khalifa wangu baada yangu?” Watu wote wakanyamaza, alikariri mara tatu maneno haya lakini hata mara moja hakuna aliyemjibu isipokuwa Ali (a.s.) ambaye alijibu: “Ni mimi, ewe Mtume wa Allah.” Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Basi ni wewe” (unafaa kusikilizwa). Watu wote wakainuka na kutawanyika na huku wakimdhihaki Abu Twalib wakimwambia: “Angalia, umeamrishwa kumtii mtoto wako mwenyewe!” Katika mapokezi mengine Abu Rafi’i anasema: “Mtume (s.a.w.w.) aliwakusanya wana wa Abdul-Mutwalib katika nyumba ya Abu Twalib akawatayarishi paja la mbuzi, wakala mpaka wakashiba, kisha akawaletea asali, wakainywa hadi wakatosheka, akasimama kawaambia: “Hakika Mwenyezi Mungu amaeniamrisha niwaonye jamaa zangu wa karibu, na nyinyi ndio jamaa zangu, na Mwenyezi Mungu hakumtimizia Mtume kwa watu isipokuwa humjaalia kutokana na watu wake, ndugu, waziri wake, mrithi, wasii na khalifa wake. Ni yupi kati yenu atakayeniunga mkono awe ni ndugu yangu, mrithi, waziri, wasii, na awe na daraja kama aliyokuwa nayo Harun kwa Musa; ila tu kwamba hakuna Mtume baada yangu?” Wote wakanyamza. Akasema: “Na asimame mmoja wenu ama sivyo mtajuta.” alikariri maneno haya mara tatu. Mwishowe Ali (a.s.) alisimama akamuunga mkono. Mtume (s.a.w.w.) akamwambia: “Sogea karibu nami.” Ali akasogea, akafungua mdomo wake, Mtume (s.a.w.w.) akamtufia,5 kisha akamtufia kati ya mabega yake na kifua chake. Abu Lahb alipoyaona hayo akasema “We Muhammad! kwa nini wamtemea mate binamu yako?” Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Nimemjaza hekima na elimu.” 5. Kutemea mate kwa uchache. 155


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:19 PM

Page 156

Tujifunze Misingi ya Dini Hadithi hii inaitwa ‘Hadith ad-Daari’ ambayo dalili zake ziko wazi. Ama kuhusu isnadi6 ya Hadithi yenyewe, imetajwa na wanavyuoni wengi wa Sunni kama Ibn Jarir, Ibn Abu Hatim, Ibn Murdawayh, Abu Nu’aim, Al-Bayhaqi, Tha’labi, Tabari, Ibn Athir, Abul-Fidaa na wengineo. Hata tukiangalia kijuu juu tu Hadithi hii, ukhalifa na uongozi wa Ali (a.s.) utatudhihirikia waziwazi.

SOMO LA NANE HADITH YA ‘THAQLAIN’ NA YA ‘SAFIINATUN-NUH’ Isnad ya Hadithi ya ‘Thaqalain.’ Hii ni Hadithi mashuhuri sana kwa wanavyuoni wa Sunni na wa Shi’ah. Hadithi hii imepokewa na idadi kubwa ya maswahaba, moja kwa moja kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.), hata baadhi ya wanavyuoni wasema kwamba, imepokewa na wapokezi wasiopungua 30 katika maswahaba wa Mtume (s.a.w.w.); vile vile imetajwa na wafasiri na wapokezi wengi katika vitabu vyao, kiasi cha kuifanya isitiliwe shaka kuwa miongoni mwa ‘Hadith mutawaatir.’ Mwanachuoni mkubwa, Sayyid Hashim Bahrani ametaja katika kitabu chake Ghaayatul-Maraam na ameisanidisha na isnadi 39 kutoka kwa wanavyuoni wa Sunni, na 80 kutoka kwa wanavyuoni wa Shi’ah. Ama Mir Hamid Hasan, mwanachuoni mkubwa wa kihindi, amezama katika ufuatiliaji wa Hadithi hii akaipata imetajwa na wanavyuoni 200 wa Sunni, na akakusanya mijadalada sita mikubwa ya upekuzi wake kuhusu 6. Isnadi: mfululizo wa majina ya waliopokea Hadithi ya Mtume (s.a.w.w) 156


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:19 PM

Page 157

Tujifunze Misingi ya Dini Hadithi hii. Miongoni mwa maswahaba mashuhuri waliotaja Hadithi hii ni: Abu Sa’id El-Ghaffari, Zaid bin Arqam, Zaid bin Thabit, Abu Rafi’i, Jubair, Bin Mu’tim, Hudhaifu, Dhumratul-Aslami, Jabir bin Abdillah Al-Ansari, Ummu Salama na wengineo. Na Hadithi yenyewe hasa (asili) kama ilivyopokelewa na Abu Dharr, ni kama ifuatavyo: “Mtume (s.a.w.w.) alipotoka Hijja ya kuaga (ya mwisho) alisimama juu ya mimbari akasema: “Enyi watu! Mimi nina jukumu, nanyi pia mnalo… Mimi nawaachia vizito viwili, Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Ahlu Bait wangu, na kwa hakika vitu viwili hivyo havitaachana, mpaka vinirudie katika birika (la Kawthar).” Hadithi hii imepokewa na vitabu vya ki-Sunni vinavyotegemewa, kama vile Sunan Tirmidhi, Nasai, Musnad Ahmad, Kanzul-Ummal, Mustadrakil Hakim na vinginevyo. Katika baadhi ya mapokezi imekuja ibara ‘thaqalaini’ na baadhi nyingine kwa ibara ‘khalifataini’ hata hivyo hapana tofauti kubwa kati ya maana ya ibara hizi mbili. Mwenye kuangalia kwa makini, atagundua kwamba mapokezi mengi ya Hadithi za Mtume (s.a.w.w.) yanaonyesha kwamba yalikariri kwa watu mara nyingi maneno hayo. Hadithi iliyopokelewa na Jabir bin Abdillah Al-Ansari inasema kuwa Mtume (s.a.w.w.) alisema maneno haya siku ya Arafa katika siku za Hijja. Naye mpokezi mwingine Abdullah bin Hantab amesema: “Kwamba Mtume aliyasema hayo mahali paitwapo Juhfa, hapo ni katikati ya Makka 157


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:19 PM

Page 158

Tujifunze Misingi ya Dini na Madina wanapohirimia mahujaji. Ummu Salama naye katika mapokezi yake anasema kuwa Mtume aliyasema hayo huko Ghadir Khum. Vile vile yamekuja mapokezi mengine yanayosema kwamba maneno hayo yalisemwa na Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa kitandani hajiwezi, katika siku za mwisho za uhai wake wenye kubarikiwa. Mapokezi mengine yanasema kwamba maneno hayo aliyasema huko Madina akiwa juu ya mimbari. Katika kitabu As-sawaiqul-Muhriqa cha mwanachuoni mkubwa wa kiSunni, Ibn Hajar, imeandikwa: “Mtume (s.a.w.w.) aliushika mkono wa Ali bin Abi Twalib, akauinua juu, akasema: “Ali yuko pamoja na Qur’ani, na Qur’ani iko pamoja naye, na hawatatengana mpaka wanirudie katika birika (la Kawthar).” Hivi ndivyo ilivyodhihiri kwamba Mtume (s.a.w.w.) amesisitiza mara nyingi ufahamu huu akiuzingatia kuwa ndio msingi, kwani alikuwa kila anapopata fursa, huitumia kwa kuufafanua kweli huu ili usije ukasahaulika.

Yaliyomo katika Hadithi ya “Thaqalain” Hapa hebu tuangalie mambo yaliyomo katika Hadithi hiyo: Kutajwa Qur’ani na kizazi cha Mtume kuwa ni vizito viwili ni kuwataka waislamu waendelee kushikamana navyo daima na hasa tukiangalia kwa makini Hadithi yenyewe inavyosema: “Mkishikamana navyo hamtapotea kamwe baada yangu.” Qur’ani kuwekwa pamoja na Ahlu Bait ni dalili ya kuonyesha kwamba kadri ambavyo Qur’ani haitapotoshwa na daima itahifadhiwa, pia Ahlu Bait wa Mtume watahifadhiwa. Yamekuja mapokezi yasemayo kwamba Mwenyezi Mungu atawauliza 158


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:19 PM

Page 159

Tujifunze Misingi ya Dini watu jinsi walivyofungamana na viwili hivyo. Vyovyote tutakavyofungamana na Ahlu Bait wa Mtume (s.a.w.w.), Ali ndiye uthibitisho wa hayo, kwani amesema katika Hadithi nyngi kwamba, yeye hakutengana na Qur’ani, nayo haikutengana naye. Isitoshe kuna mapokezi yasemayo kwamba, iliposhuka Aya ya ‘mubahala’ Mtume (s.a.w.w.) alimwita Ali, Fatima, Hasan na Husein (a.s.) akisema: “Hawa ndiyo Ahlu Bait wangu.” Pamoja na kuwa habari za siku ya Kiyama hatuzijui sisi tunaoishi duniani, lakini kulingana na mapokezi, zinatuambia kuwa ‘birika la Kawthar’ ni mto maalum ulioko Peponi, ambao ni mahususi kwa waumini, wakweli, Mtume Mtukufu, Maimamu na wafuasi wao. Mpaka kufikia hapa tumefahamu kuwa kiongozi na marejeo ya umma baada ya Mtume ni Ali (a.s.) na Maimam wa Ahlu Bait (a.s.).

HADITH YA ‘SAFINATUN-NUH’ Hadithi ya kuzingatiwa sana aliyokuja katika vitabu vya Sunni na vya Shi’ah ni ni Hadithi mashuhuri ya ‘Safinatun-Nuh’ (Jahazi la Nuh). Amesema Abu Dharr kwamba: “Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Mfano wa Ahlu Bait wangu ni kama jahazi la Nuh (a.s.) wenye kulipanda huokoka: na mwenye kulikhalifu huzama.” Hii ni miongoni mwa Hadithi mashuhuri ambazo zinawajibisha watu kumfuata Ali na Ahlu Bait wa Mtume (s.a.w.w.) kwa kuwa twafahamu kwamba jahazi la Nabii Nuh (a.s.) lilikuwa ndilo tegemeo la kuokoka kutokana na gharika iliyoukumba ulimwengu siku zile, ndipo tufahamu ukweli huu, yaani tutakapokumbwa na tofani baada ya Mtume (s.a.w.w.) ni juu yetu kushikana na Ahlu Bait, kwani hakuna njia nyingine ya kuokoka zaidi ya hiyo. 159


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:19 PM

Page 160

Tujifunze Misingi ya Dini

SOMO LA TISA MAIMAMU KUMI NA WAWILI Hadithi kuhusu Maimam kumi na wawili Baada ya kuthibitisha uimamu na ukhalifa wa Imam Ali (a.s.), hebu tuzungumzie juu ya maimamu wengine: Kwanza, hivi leo tuna vitabu vingi vya ki-Sunni na vya ki-Shi’ah vilivyonukuu mapokezi yanayotaja waziwazi ukhalifa wa maimam na makhalifa kumi na wawili. Hadithi hizi zimo katika vitabu vikubwa vya Sunni kama Sahih Bukhari, Sunan Tirmidhi, Musnad Ahmad na vinginevyo. Katika kitabu kiitwacho Munakhibul-Athar kuna Hadithi 271 zinazozungumzia jambo hili. Nyingi kati ya hizo zimenukuliwa kutoka katika vitabu vya ki-Sunni na vingine vya ki-Shi’ah. Kwa mfano, tunasoma katika Sahih Bukhari ambacho ni mashuhuri sana katika vitabu vya Sunni: “Kutakuwa na viongozi kumi na wawili.” Anaendelea Jabir: “Kisha alisema neno ambalo sikulisikia, kisha baba yangu akaniambia, alisema: “Wote watakuwa ni Maquraish.”

160


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:19 PM

Page 161

Tujifunze Misingi ya Dini Katika Sahihi Muslim Hadithi hii imeelezwa hivi: Jabir amesema: “Uislam utaendelea kuwa mtukufu mpaka watimie makhalifa kumi na wawili.” Anaendelea Jabiri: “Kisha Mtume (s.a.w.w.) alisema jambo ambalo sikulifahamu, nikamuuliza baba yangu, Mtume alisema nini? Akasema: “Wote hao watakuwa ni Maquraishi.” Vile vile katika Musnad ya Ahmad imepokewa kutoka kwa Abdallah bin Mas’ud (swahaba maarufu) amesema: “Mtume (s.a.w.w.) aliulizwa kuhusu makhalifa, akajibu: “Ni kumi na wawili kama walivyokuwa wakuu wa makabila kumi na mawili ya kiisraeli.” Maana ya Hadithi hizi Baadhi wanaonelea kuwa utukufu wa waislamu umefungamana na makhalifa hao kumi na wawili, na wengine wanoonelea kwamba uhai na kudumu kwa dini hii mpaka Siku ya Kiyama kumekabidhiwa wao, nao wote ni Maquraishi. Kwingine imeelezwa - wote ni katika ukoo wa Bani Hashim. Lakini hii hufungamana na madhehebu ya Shi’ah pekee, ambapo maelezo yake ni mepesi kufahamika; wakati ambapo wanavyuoni wa kiSunni wanajaribu kutafuta wajihi wa kuielezea. Je, Hadithi hii inakusudia makhalifa wanne wa mwanzo pamoja na waliofuta wa kibani Umayya na kibani Abbas? Ama sisi tunafahamu kwamba makhalifa wa mwanzo hawakuwa kumi na wawili na hata tukiongezea na wa kibani Umaya na kibani Abbas hawakufika idadi hiyo. Hapo idadi ya kumi na wawili haiingii. Isitoshe katika makhalifa wa kibani Umayya, kuna makhalifa kama kina Yazid; na katika Bani Abbas kuna kina Mansur Dawaniqi na Harun Rashid, ambao hakuna anayetia shaka kuwa wamefanya dhulma na matendo mengi maovu. Kwa hivyo haiyumkini kuwazingatia kuwa wao ni makhalifa wa Mtume (s.a.w.w.), vyovyote vile tutakavyojaribu kuyafanya matendo yao yaonekane si mabaya sana. 161


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:19 PM

Page 162

Tujifunze Misingi ya Dini Tukiachana na yote hayo, twaona kwamba hatuwezi kupata idadi ya makhalifa kumi na wawili inayoingia hapa isipokuwa ya Maimamu kumi na wawili wa ki-Shi’ah. Hebu hapa tumuachie mwanachuoni mashuhuri wa ki-Sunni, Suleiman bin Ibrahim Qanduzi Hanafi atufafanulie: Mwanachuoni huyo amesema katika kitabu chake, Yanabiul-Mawadda kwamba: “Baadhi ya wahakiki wa Hadithi wamesema kwamba Hadithi zinazojulisha kuwa makhalifa watakaokuja baada ya Mtume (s.a.w.w) ni kumi na wawili, zimetangaa kwa njia nyingi, na kwa ufafanuzi wa wakati na mahali yaonyesha kuwa, makusudio ya Mtume (s.a.w.w.) katika Hadithi yake hii ni Maimam kumi na wawili watokanao na Ahlu Bait wake na kizazi chake, kwani makusudio yake hayawezi kuwa ni maswahaba wake kwa sababu hawakutimia kumi na wawili. Vile vile makusudio yake si watawala wa kibani Umayya, kwani wao walizidi idadi hiyo, na walifanya dhuluma sana – isipokuwa Umar Bin Abdul Aziz pekee - isitoshe, wao hawakuwa katika ukoo wa Bani Hashim, ambapo Mtume (s.a.w.w) alisema kuwa ‘wote ni katika Bani Hashim.’ Katika Hadithi iliyopokewa na Abdul Malik kutoka kwa Jabir na alivyosema kwa sauti ya chini Mtume (s.a.w.w.) inatilia nguvu Hadithi hii kwamba wao hawafai ukhalifa ambao umewahusu Bani Hashim. Aidha makusudio ya makhalifa hao si watawala wa kibani Abbas, kwani idadi yao ilizidi kumi na wawili, pia hawakutilia maanani Aya inayowataka watu wawapende Ahlu Bait, na waliipuuza Hadithi ya ‘Kisa’a.’ Kwa hivyo, makusudio ya Hadithi hii bila shaka ni Maimamu kumi na wawili wanaotokana na kizazi cha Mtume (s.a.w.w), kwani wao walikuwa ni wajuzi zaidi wa zama zao, walikuwa ni watukufu, wachaMungu, wenye nasaba bora wenye hadhi na watukufu zaidi mbele za Mwenyezi Mungu. Elimu zao walizopokea kwa baba zao zilifungamana na babu yao Mtume 162


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:19 PM

Page 163

Tujifunze Misingi ya Dini Muhammad (s.a.w.w.). Pia wajuzi, wahakiki waliwatambua maimamu kwa elimu zao za kurithi zinazotoka kwa Mwenyezi Mungu. Jambo hilo pia linatiliwa nguvu na Hadithi ya ‘Thaqalain’ na nyinginezo zilizotajwa katika kitabu hiki.” Ni vizuri nitaje hapa kwamba, nilipotembelea Hijaz (Saudia) nilipata kusikia wanavyuoni wakitoa maelezo mengine ya Hadithi hii. Mmoja wao alisema: “Huenda ikawa makusudio ya makhalifa kumi na wawili, ni wale wanne waliotangulia kwanza na wengine watakuja siku za baadaye.” Hapo wanasahau mfuatano uliotajwa katika Hadithi hiyo, sisi twasema: Kuna haja gani ya kuacha kufuata maelezo yaliyo waziwazi, kama inavyoonyesha Hadithi yenyewe, na kupitia kwenye maelezo yenye kutatanisha yasiyo msingi?

Kutajwa maimamu kwa Majina Ni muhimu tufahamu kuwa baadhi ya Hadithi za Mtume zilizopokelewa na ambazo zimetufikia kutoka kwa wanavyuoni wa ki-Sunni zinatawala Maimam hao kumi na wawili kwa majina na kuzibainisha sifa na fadhila zao. Mwanachuoni mashuhuri, Sheikh Suleiman Al-Qanduzi anasema katika kitabu chake hicho hicho Yanabiul-Mawadda kuwa: “Myahudi mmoja aitwaye Na’athal alikwenda kwa Mtume (s.a.w.w.) na kumuuliza maswali mbalimbali, na miongoni mwayo alitaka kujua kuhusu mawasii na makhalifa wa Mtume baada yake. Mtume akajibu: “Hakika wasii wangu ni Ali Abi Twalibu, baada yake ni wajukuu zangu wawili Hasan na Husein, baadaye watafuata Maimamu tisa kutokana na kizazi chake (Husein). Baada ya Husein atafuata mwanawe Ali baada ya Ali, atafuata mwanawe Muhammad. Baada ya Muhammad atafuata mwanawe Jafar, ambaye naye atafuatiwa na mwanawe Musa. Atakayechukua wadhifa huo baada ya Musa ni mwanawe Ali, atakayefuatiwa na mwanawe Muhammad. Naye 163


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:19 PM

Page 164

Tujifunze Misingi ya Dini atafuatiwa na mwanawe Ali. Atakayeshika uimamu baada ya Ali ni Hasan, kisha baada yake ni mwanawe, Hujja Muhammad al-Mahdi. Hao ndio Maimamu kumi na wawili.”

Afaye bila ya kumjua Imam wake ….. Katika vitabu vya Kisunni kuna Hadithi isemayo: Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Mwenye kufa bila ya kumjua Imam wake, basi amekufa kifo cha kijahiliya.” Hadithi hii imepokewa katika vitabu vya ki-Shi’ah kwa namna hii: “Mwenye kufa wala asimjue Imam wake, basi amekufa kifo cha kijahiliya.” Hadithi hii ni dalili wazi kuwa katika kila zama na kila wakati kuna Imam aliyehifadhiwa na madhambi, na ni wajibu kwa kila mtu amjue, na kwamba asiyemjua ni kama mtu aliyeishi katika zama za ukafiri na ujahiliya. Sasa je, makusudio ya Maimamu katika Hadithi hii ni watawala kama akina Ghengis Khan, Harun Rashid na vibaraka vyao? Bila shaka hapa jibu litakuwa ni la! Kwa sababu wengi wao kati ya viongozi hawa ni wafisadi na madhalimu, na mara nyingi hutegemea maagizo kutoka nchi za kimashariki na kimagharibi ili kuendeleza ubeberu wao. Bila shaka kuwatambua na kuwakabali kuwa ni maimam, humpeleka mtu mahali pabaya. Kwa hivyo, mpaka hapa yaeleweka kwamba katika kila zama na kila wakati kuna Imam aliyehifadhiwa na madhambi ambaye ni wajibu watu wamtambue na kumkubali kuwa kiongozi wao. Kama tulivyosema kwamba uthibitisho wa Imam hutimu kwa mapokezi kutoka kwa Imam aliyetangulia.

164


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:19 PM

Page 165

Tujifunze Misingi ya Dini

SOMO LA KUMI IMAM MAHDI (A.S.) MSULUHISHAJI WA ULIMWENGU 1. Mwisho wa usiku wa giza Tunapoangalia hali yetu ya sasa na kuona ongezeko la vitendo vya uhalifu, mauaji, vita, umwagaji damu, mizozo miongoni mwa mataifa mbalimbali na ufisadi; tunajiuliza: Je hali hii itaendelea kuwa hivi hivi? Je uhalifu na uharibifu utaenea kiasi cha kumpeleka mwanadamu kwenye vita visivyokwisha? Je upotofu wa kiitikadi na ubaradhuli utamdidimiza mwanaadamu kama yanavyodidimiza matope? Au pana mategemeo yoyote ya kuokoka na kutengenea kwa mwanadamu? Hapa pana majibu mawili, la kwanza ni lile wanalosema watu wa kimaada na wale waaminio kuwa kila kitu ni kiovu, kwamba mustakbali wa ulimwengu ni kiza tu na kwamba kila wakati kuna hatari tupu. Jibu la pili ni wanaomuamini Mungu, hasa waislamu, na hasa Shi’ah, wanasema: “Kwa hakika nyuma ya usiku huu mweusi wenye kiza, kuna asubuhi yenye matumaini. Mawingu yenye kiza na mafuriko yaangamizayo, hatimaye yatatoweka na jua liangazalo litachomoka mbinguni na kusafisha anga. Ulimwengu unasubiri msuluhishaji mkuu atakayekuja kuugeuza ulimwengu uwe ni wa haki na uadilifu.” Kwa kweli wafuasi wa dini mbalimbali wamempa jina maalum msuluhishaji huyu. Kama asemavyo mshairi:

165


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:19 PM

Page 166

Tujifunze Misingi ya Dini Kwa kweli uzuri wako ni mmoja twaushufu Zingawa mtawanyiko sifa tunazokusifu Hatuna mbali twendako wasifu tunaposifu Sote tupo kwenye safu kusifu jamali yako

Maumbile na kudhahiri msuluhishaji mkuu Ilhamu zetu za ndani ambazo mara nyingi huwa na nguvu kuliko fahamu zetu, hazitufahamishi kuwapo kwa Mungu tu, bali pia zinaweza kufanya dalili katika itikadi zetu zote za kidini ambazo mojawapo ni suala hili tunalolizungumzia hapa, na kuthibitisha hilo hebu tuangalie sababu zifuatazo: Kwanza kupenda uadilifu uwepo kwa ujumla. Watu wote duniani, pamoja na tofauti zao, wanapenda amani na uadilifu. Sote tunalilia na kupigania uadilifu na amani kwa watu wote. Isitoshe, hakuna dalili iliyo bora zaidi kama kumngojea msulihishaji mkuu huyu, hilo ni jambo la kimaumbile, na hiyo ni kwa sababu matakwa yoyote yanayotakiwa na watu wote, ni dalili ya kuwa ni ya kimaumbile yao. (Soma kwa uangalifu kifungu hiki). Kila penzi la kiasili la kimaumbile linaonyesha kuwapo mpenzi aliye dhahiri; itawawezekanaje Mwenyezi Mungu aumbe kiu ndani ya mwili wa mwanadamu bila kuumba chemchem ya maji ndani ya mwili huo itakayoondoa kiu hiyo? Nasi ndipo tukasema kwamba maumbile ya mwanadamu yanafuata uadilifu yanapaaza sauti kusema kuwa iko siku ambayo Uislam na uadilifu utatawala ulimwengu mzima, na dhulma, jeuri na ubinafsi utatoweka. Wanaadamu wataungana pamoja na kuishi chini ya bendera moja ya maelewano na maisha mema.

166


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:19 PM

Page 167

Tujifunze Misingi ya Dini Pili: Dini na madhehebu zote zinasubiri kuja kwa msulihishaji mkuu wa ulimwengu. Mara nyingi katika dini zote utakuta ibara inayoeleza imani ya kuja mwokozi mkuu, atakayekuja kutibu jeraha chungu la wanadamu. Imani hii sio ya Waislam pekee, bali kuna dalili zinazothibitisha kuwepo kwake zamani katika dini za watu wa kimashariki na kimagharibi; lakini kwa kuwa dini ya kiislamu ni dini iliyokamilika ndipo inatilia mkazo sana jambo hili. Katika kitabu kiitacho Zand cha dini ya Wazoroaster (dini ya waajemi) kinataja mgongano uliopo daima kati ya wafuasi wa dini ya Mwenyezi Mungu na wafuasi wa dini ya shetani, kisha kinaendelea: “…Baadaye watu wa Mungu watashinda watu wa shetani ambao wataangamia… na ulimwengu utapata ufanisi wake wa mwanzo, na binadamu ataketi katika kiti cha hadhi…” Katika kitabu kilichoandikwa na Zaroaster kiitwacho Jamasab Nomah imeandikwa: “Katika nchi ya Tazyin (Uarabuni) atakuja mtu mwenye kichwa kikubwa, mwili na miguu mikubwa, mtu huyo atafuata dini ya baba yake, atakuwa na jeshi kubwa…… na atajaza uadilifu ulimwenguni.” Katika kitabu Washan Jok miongoni mwa vitabu vya Indo-China, imeandikwa: “Mwishowe dunia itarejea kwa mtu anayempenda Mungu, mtu huyo ni miongoni mwa waja wake wenye ikhlasi.” Kitabu kingine cha wahindi, Basic, tunasoma hivi: “Mzunguko wa ulimwengu utakomea kwa mfalme mwadilifu siku za mwishoni, atakuwa ni kiongozi wa malaika, majini na binadamu; haki itakuwa pamoja naye, na atamiliki hazina zote zilizomo baharini, ardhini na milimani; ataelezea mambo yote yaliyomo mbinguni na ardhini na wala hapatakuwa na mtu mtukufu zaidi yake.”

167


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:19 PM

Page 168

Tujifunze Misingi ya Dini Kutoka katika Agano la Kale (Tawrat na vinavyofungamana navyo) tunasoma hivi: “Atakata mizizi ya waovu, na wenye kumtegemea Mungu ndio watakaorithi ardhi. Wakweli ndiyo wakatakorithi ardhi na wataishi humo milele.” Kuna maneno kama haya pia katika kitabu cha Isaya katika Tawrat. Katika Sura ya 24 katika Injili ya Mathayo inasema: “Kama umeme utokao upande wa mashariki ukadhihiri mpaka upande wa magharibi, ndivyo mwanadamu atakavyokuwa.” Katika Injili ya Luka Sura 12 inasema: “Fungeni mikanda yenu, washeni taa zenu, na muwe kama mtu anayemngoja bwana wake, wakati wowote atakapokuja na kugonga mlango mfanye haraka kumfungulia.” Katika kitabu Alaimu-Dhuhur imeelezwa: “Katika vitabu vya kale vya wachina, katika itikadi za wahindi, watu wa Scandinavia, wamisri wa kale na hata wamexico na wengineo, wanaamini kwamba atakuja msulihishaji wa ulimwengu.”

3. Dalili za kiakili a) Kutokana na utaratibu za uumbaji tuanapata funzo kwamba wanaadamu, mwishowe ni lazima watawaliwe na uadilifu na wabaki katika utaratibu huo chini ya msingi wa utawala wa amani. Kwa sababu, jinsi tuunavyo, ulimwengu ni mkusanyiko wa utaratibu maalum. Kuwapo kwa kanuni zilizopangwa zinazotawala ulimwengu ni dalili za kuonyesha muungano uliopo kata ya ulimwengu na utaratibu huu wa kuumbwa. Suala la kuwepo kanuni, utaratibu na mipango, ni suala muhimu kuhusu ulimwengu huu, kuanzia utaratibu wa jua kubwa hadi chembe ndogo za tonoradi (Atom) ambazo zinaweza kuwekwa hata mamilioni kwenye ncha 168


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:19 PM

Page 169

Tujifunze Misingi ya Dini ya sindano tu (jinsi zilivyo ndogo) lakini vyote hivyo vinaendeshwa chini ya utaratibu maalum wa hali ya juu kabisa. Vile vile ukiangala katika mwili wa binadamu, kuanzia chembe hai (Cell) na jinsi mishipa ya fahamu ilivyopangwa hadi kufikia kwenye ubongo, moyo na mapafu, vyote vinafanya kazi kwa mpango kama vyombo vya saa. Je katika ulimwengu kama huu, yawezekana mwanaadamu – ambaye ni sehemu ya ulimwengu huo – aishi kinyume na utaratibu huo, kwa vita, kumwaga damu na dhuluma? Je yawezekana katika hali hiyo ya dhuluma, kuharibu tabia na jamii ambako ni kinyume na utaratibu kuendelea kuwapo? Matokeo ni kwamba, mambo tunayoshuhudia ulimwenguni yanatufanya tutambue kwamba mwishowe jamii ya binadamu itakubali kufuata utaratibu na uadilifu, na kurudia kwenye asili yake iliyoumbiwa.

b) Kuendelea kwa jamii: Hii ni dalili nyingine ya kuonyesha hali ya baadaye mwanaadamu, kwani ni jambo lisilopingika kwamba jamii ya mwanadamu, tangu ilipojitambua, haikubaki katika hali moja tu, bali siku zote ilibadilika na kupiga hatua. Tukiangalia upande wa makazi, mavazi, chakula usafiri na mawasiliano, tutaona kuwa mwanaadamu hapo mwanzoni aliishi maisha duni sana, lakini hivi leo amefikia hali inayoshangaza akili na kuzubaisha macho, na bila shaka hali hii itaendelea kukua. Ama kwa upande wa elimu na utamaduni, mwanaadamu amepiga hatua kubwa, kwani kila siku kuvumbua vitu vipya na kupata habari ngeni.

169


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:19 PM

Page 170

Tujifunze Misingi ya Dini Kanuni hii ya mabadiliko ya ukamilifu, mwishowe itaingia kwenye upande wa kijamii na kitabia, itamwongoza mwanaadamu kuelekea kwenye uadilifu, amani na mwenendo mwema. Huu upotofu wa kitabia, tunaushuhudia hivi leo, ni njia tu ya kufikia kwenye ukamilifu. Tunaposema hivi, hatuamaanishi kuwa tunaupa nguvu uovu, la, tunachosema ni kwamba uovu utakapopita mipaka, mwishowe utaelekea kwenye mapinduzi ya tabia njema. Mwanadamu anapofikia ukingoni kutokana na madhambi yake, kichwa chake kigonge jiwe na kufikia mwisho wake, hapo, japo kwa uchache atajiandaa kukubali misingi atakayoletewa na kiongozi atokaye kwa Mwenyezi Mungu.

Qur’ani na kudhihiri kwa Imam Mahdi (a.s.) Katika Kitabu kitukufu cha Mwenyezi Mungu, Qur’ani, kuna Aya nyingi zinazotoa habari njema ya kudhihiri kwake. Hebu tutazame Aya moja tu ifuatayo: “Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walioamini miongoni mwenu na kufanya vitendo vizuri, kuwa atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyowafanya makhalifa wake waliokuwako kabla yao…” (24:55). Aya hii yaeleza wazi kwamba, hatimae utawala utawatoka madhalimu na kuwaendea waumini… Kisha Mwenyezi Mungu anatoa ahadi tatu, mbele ya Aya hiyo hiyo: “… Na kwa yakini atawasimamishia dini yao aliyowapendelea na atawabadilishia amani baada ya hofu yao. Wawe wananiabudu, hawanishirikisha na chochote…”(4:55). Katika kuieleza Aya hii, Imam Ali bin Husein (a.s.) alisema: “Wallahi! Hao ni wafuasi wetu, na Mwenyezi Mungu atawafanyia hayo kupitia kwa mikono ya mtu atakayetokana na sisi, naye ni Mahdi wa umma huu.” 170


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:19 PM

Page 171

Tujifunze Misingi ya Dini Imam Mahdi katika vitabu vya Hadithi Hadithi zinazosema kwamba utawala wa ulimwengu, wenye uadilifu na amani utakaoanzishwa na mmoja katika watu wa Ahlu Bait aitwaye Mahdi, ni nyingi. Zimetajwa katika vitabu vya ki-Sunni na ki-Shi’ah. Ama zinazotaja kuwa yeye ni Imam wa kumi na mbili: Khalifa wa Mtume (s.a.w.w.); wa tisa katika kizazi cha Imam Husein; na kuwa yeye ni mtoto wa Imam Hasan Al-Askary, ni nyingi na hupatikana katika vitabu vya kiShi’ah. Kuhusu kifungu cha kwanza tulichokitaja, yaani kuhusu mapokezi ya upande wa ki-Sunni kuhusu kudhihiri kwa Imam Mahdi, wanavyuoni wa madhehebu hayo wanataja jambo hilo waziwazi, kama tunavyosoma katika risala iliyotolewa hivi karibuni na jumuiya ya Rabitwa yenye makao makuu yake nchini Saudi Arabia: “Yeye ni mwisho wa Makhalifa kumi na wawili waliotajwa na Mtume (s.a.w.w.) katika Hadithi sahih; na Hadithi hizo zimenukuliwa na maswahaba wengi kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.)…” Baada ya kutaja majina ya maswahaba ishirini waliopokea Hadithi hiyo, risala hiyo inaendelea: “….. Kuna wengine walionukuu Hadithi hizi: na baadhi ya wanavyuoni wa Sunni wametunga vitabu maalum kuhusu Hadithi zinazomhusu Mahdi. Miongoni mwao ni: Abu Nuaim Al-Asfahani, Ibn Hajar Al- Haithami, Shawkani, Idris Al-Maghribi na Abu Abbas bin Abdul Mumini.” Kisha inaongeza “… Kuna kikundi cha wanavyuoni wa zamani wa Kisunni, na wapokezi wa Hadithi, ambao wanasema waziwazi kwamba Hadithi zinazomhusu Mahdi ni ‘Mutawaatir.’” Baada ya kutaja idadi ya majina yao risala inaendelea kusema wapokezi wa Hadithi wametangaza kuwa katika Hadithi zinazohusu Mahdi, nyingine ni ‘Sahih’ nyingine ni ‘Hasan’ nazo kwa pamoja ni mutawaatir; na imani juu ya Mahdi ni sahih na wajibu, nayo ni katika imani za Ahlu-Sunna wal-Jamaa: na wenye kukanusha ni mjinga na mzushi.” 171


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:19 PM

Page 172

Tujifunze Misingi ya Dini Kwa upande wa Hadithi za Shi’ah Yatosha kujua kwamba kuna mamia ya Hadithi zilizopokelewa na wapokezi mbalimbali kuhusu jambo hili, kutoka kwa Mtume na Maimam (a.s.) kufikia daraja ya ‘Mutawaatir’ kwa Shi’ah, Suala hili ni muhimu sana (dharuriyat) kiasi ambacho mtu hawezi kuwa katika madhehebu haya, na asikubali kudhiri kwa Imam Mahdi, mambo yanayohusu yeye tu, alama za kuja kwake, jinsi ya uongozi na mipango yake mbalimbali. Wanavyuoni wakubwa wa ki-Shi’ah, tokea karne za mwanzo hadi hivi leo, wameandika na wanaendelea kuandika vitabu vingi na kukusanya Hadithi zinamhusu Imam Mahdi. Hapa tutataja baadhi tu ya Hadithi, tukitoa mfano, na kwa wale wanaotaka maelezo zaidi tunawashauri wasome vitabu vilivyotungwa mahsusi juu ya jambo hili, kama kitabu kiitwacho “Al-Mahdi” kilichoandikwa na mwanachuoni mkubwa Seyyid Sadrudin As-Sadr. Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Lau kama itabakia siku moja tu ya ulimwengu, basi Mwenyezi Mungu atairefusha siku hiyo mpaka alete mtu kutoka Ahlu Bait wangu ambaye atakuja kuujaza ulimwengu usawa na uadilifu, utakapokuwa umejaa dhuluma na uonevu.” Kutoka kwa Imam Sadiq amesema: “Atakaposimama mwenye kusimama (Mahdi) kutahukumiwa kwa uadilifu, uonevu utaondoka; katika siku hizo, njia zitakuwa na amani, ardhi itatoa baraka zake na kila mtu atarudishiwa haki yake ….. Watu watahukumiwa kwa hukumu za Daudi na Muhammad (a.s.); na hapo ndipo ardhi itakapotoa hazina zake na kuzionyesha baraka zake; na hatapata yeyote kati yenu mahali pa kutoa sadaka yake au pa kutendea wema wake kwa sababu ya kuenea utajiri kwa waumini wote.” Mwisho: Tunajua kwamba katika zama za kughibu Imam, wadhifa huo huendelea kwa unaibu wa utawala wa faqihi.

172


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:19 PM

Page 173

Tujifunze Misingi ya Dini

T U YA J U E M A R E J E O (5)

173


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:19 PM

Page 174

Tujifunze Misingi ya Dini

Kwa jina la Allah, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu

SOMO LA KWANZA JE KIFO NI MWANZO AU NI MWISHO? Watu wengi huogopa kifo kwa nini? Kila mara mwanadamu anapofikiria kifo, hukiona kuwa ni chenye kumtisha na kumpokonya utamu wa maisha mithili ya tonge lililo mdomoni mwake. Si kifo tu, mwanadamu huogopa hata kutaja makaburi ndipo hufanya kila awezalo kuyapamba na kuyatia nakshi ili angalau apate kusahau undani na ukweli wake. Tukirejea kuangalia katika mataifa mbalimbali tutaona waziwazi jinsi kifo kinavyoogopewa kwa kuitwa ‘maangamivu,’ ‘ajali’ n.k. Wanapotaja kifo, kwa haraka sana husema ‘Mungu atuepushie!’ Au ‘Mungu akuweke!’ n.k. Kwa hivyo yatupasa tufahamu ni jambo gani linalowafanya wanadamu daima wakiogope. Kisha tufahamu kwa nini kuna wengine ambao – kinyume na hivyo – wao hawaogopi kifo bali hukipokea kwa tabasamu la furaha, na kukikongowea. Historia yatuambia kwamba kulikuwa na watu waliokuwa wakitafuta maji 174


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:19 PM

Page 175

Tujifunze Misingi ya Dini ya uhai na dawa ya ujana ili wapate kuishi; na wakati huo huo kulikuwa na wengine waliokuwa wakiharakisha kwenda kupigana katika vita vya jihadi kwa kupenda kwao, na kukielekea kifo na huku wakiwa na furaha, hawakupendelea kuishi maisha marefu kwa sababu ya hamu kubwa waliokuwa nayo ya kutaka kukutana na mpenzi wao, Allah. Na haya ndiyo tunayoyashuhudia leo katika nyuso za haki zinazopinga batili, kwani watu hao hujitoa mhanga wakiwa na roho mikononi.

Kwa nini watu huogopa kifo Tukichunguza kwa undani tunaona kuwa pana sababu mbili:

Kwanza: Kufa ni kutoweka. Ni maumbile ya mwanadamu kujiepusha na hali ijulikanayo kama ‘kukosekana’. Mwanadamu hujiepusha na maradhi kwa sababu yanasababisha kukosekana afya. Hujiepusha na giza kwani husababisha kukosekana mwanga. Hujiepusha na ufakiri kwani hufanya utajiri ukosekane. Isitoshe mwanaadamu mara nyingine hukimbia hata nyumba iliyo pweke au upweke wa jangwani, kwa sababu ya kukosa mwenzake. La ajabu zaidi ni kuwa yeye huogopa hata maiti yenyewe! Mathalan, atakapoambiwa alale chumba kimoja na maiti ambaye alikuwa hamuogopi kabla ya kufa kwake, hapo huogopa! Je, wadhani ni sababu gani inafanya mwanaadamu kuogopa huko ‘kukosekana’? Bila shaka sababu yake iko wazi, ‘kuwepo’ hufungamana na kupatikana; haiwezekani ‘kuwepo’ kufungamana na ‘kukosekana’, kwa sababu hiyo ndipo ikatokea sisi wanaadamu tuogope ‘kukosekana.’ Tunaposema kuwa kufa ndiyo mwisho wa kila jambo, na kwamba kifo ndicho hufikisha kila jambo kwenye hatima yake, bila shaka hapo itatupasa tukiogope na tuliogope hata jina lake pia, kwa sababu kifo hutupokonya 175


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:19 PM

Page 176

Tujifunze Misingi ya Dini kila kitu. Lakini tukizingatia kwamba kifo ni mwanzo tu wa maisha mapya, maisha ya milele na ni upenyo unaotupeleka kwenye ulimwengu mkuu, hapo bila shaka hatutakiogopa, bali tutazidi kuwapongeza watakatifu wanaopiga hatua kukielekea kwa uthabiti na kujiamini.

Sababu ya pili, ni kuwa na ‘vitabu vyeusi’ Tunafahamu kwamba kuna watu wanaoonelea kuwa kifo si kutoweka na kukosekana tu, kwa sababu wanaamini kuwa kuna maisha baada ya kufa, lakini licha ya hivyo bado wanaogopa kifo kwa sababu, vitabu vya matendo yao vimekuwa vyeusi mno kiasi cha kuwafanya waogope adhabu kali zitakazowapata baada ya kufa. Watu hao wana haki ya kuogopa kifo, kwa sababu wao ni kama wahalifu hatari wanaoogopa kutolewa gerezani, wakijua kwamba kutolewa kwao humo kutawapelekea kwenye kunyongwa, kwa hivyo wanapendelea kubaki gerezani, si kwa sababu hawapendi kuwa huru, la, ni kwa sababu kuwa huru huko kutawapeleka kwenye kitanzi! Hiyo ndiyo hali ya watenda maovu, wao wanaonelea kwamba kutoka roho (kufa) kwenye jela hii finyu (dunia) kutawapeleka kwenye kila aina za adhabu kutokana na maovu, dhuluma na ufisadi walioutenda, ndipo wakaogopa kufa. Lakini hilo ni kinyume na wale ambao wanaonelea kuwa kifo si kutoweka, wala vitabu vyao vya matendo si vyeusi. Ni kipi kitakachowafanya waogope kufa? Kwa kweli wao hupenda maisha haya ya dunia ili wayatumie kwa kujijengea maisha mapya baada ya kufa, na hujiandaa kuyapokea mauti kwa njia yenye kumridhisha Mwenyezi Mungu. Hilo ndilo lengo tukufu na la kujivunia.

176


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:19 PM

Page 177

Tujifunze Misingi ya Dini Maoni mawili tofauti Tumeshasema hapo awali kwamba watu wamegawanyika katika makundi mawili. Kundi la kwanza - ambalo lina watu wengi - ni kundi linaloogopa kifo. Kundi la pili ni lile ambalo liko tayari kukipokea kifo chenye kuelekea kwenye lengo kubwa, kama kufa katika njia ya Mwenyezi Mungu, au wanapohisi kuwa kifo kinawakaribia hawapatwi na majonzi wala simanzi. Sababu hasa ya kuwepo makundi haya mawili ni kutofautiana katika maoni. Kundi la kwanza, ama litakuwa ni miongoni mwa wale wasioamini mambo ya akhera, ama wasioamini kila usadikisho, hivyo kundi hilo huona wakati wa kufa ni kama wakati wa kufarikiana na kila kitu, kwani kufarikiana na kila na kutoka kwenye mwanga, na kuingia gizani ni jambo zito lenye uchungu mwingi, kama hali ya mtu anayetolewa rumande ili apelekwa mahakamani akashtakiwe kwa kosa ambalo anajua kuwa litamthibitikia, bila shaka hali hiyo huwa ni ya kutisha. Ama kundi la pili, hukiona kifo ni kama kuzaliwa upya na kutoka kwenye mazingira ya dunia finyu yenye kiza na kuingia kwenye ulimwengu mpana wenye kung’ara. Naam, bila shaka ni kujikwamua kutoka kwenye tundu dogo na kuruka juu ya anga pana; kutoka kwenye mazingira yaliyojaa uhasama, vita, kiza na chuki, na kuingia ndani ya ulimwengu uliotakasika na machafu yote haya, huwafanya watu wa kundi hili la pili wapende kifo na wasikiogope. Imam Ali (a.s.) amesema: “Wallahi! mwana wa Abu Twalib huburudika na kifo kuliko mtoto mchanga anavyoburudika na chuchu ya mama yake.� Kama alivyosema mshairi

177


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:19 PM

Page 178

Tujifunze Misingi ya Dini Kama mauti ni mti Mimi siyahofu katu

yaambie yanijie tayabana yasikie

Ashaddi ya kuyabana Mimi ninayo hakika Njema ninayoitaka

ya kupata roho ile inayodumu milele

Mzoga yaambulie Kwa hivyo, si ajabu katika historia kuwepo na watu waliojitolea mhanga kama Imam Husein (a.s.) na wafuasi wake, kila wakati kifo kinapowakaribia ndivyo furaha na shauku ya kutaka kukutana na mpenzi wao inavyokuwa kubwa, na pia nyuso zao hutoa nuru wanapokaribia kukutana naye (Mwenyezi Mungu). Na hivi ndivyo tunavyosoma hata katika historia ya maisha matukufu ya Imam Ali (a.s.) wakati alipopigwa dharba ya upanga wa yule muuaji wake mwovu alisema: “Naapa kwa Mola wa Al-Ka’aba, mimi nimefaulu!” Kimsingi, maneno haya hayamaanisha kuwa watu wanahimizwa wajitupe kwenye maangamivu na kutovitumia vipaji walivyopewa na Mwenyezi Mungu, bali makusudio yake ni kuwataka waishi maisha salama yasiyozungukwa na kuogopa mwisho wake na hasa yakiwa ni maisha yenye lengo kuu na tukufu.

SOMO LA PILI KUAMINI ‘UFUFUO’ HUFANYA MAISHA YAWE NA MAANA Tukichukulia kwamba hakuna ulimwengu mwingine zaidi ya huu tutaona kwamba ni upuuzi na hauna maana yoyote, ni kama kufananisha maisha ya kilenge (kitoto kilichomo tumboni mwa mama yake) ambacho hakitarajii kutoka kwenye maisha hayo na kuja kwenye maisha haya duniani. Lau 178


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:19 PM

Page 179

Tujifunze Misingi ya Dini kitoto hicho kinachokaa gerezani (tumboni) humo kwa miezi kadhaa kitapewa akili ya kufikiri juu ya kuwapo kwake humo, kingelishangaa sana. Kwa nini nimefungwa ndani ya jela hii yenye kiza? Kwa nini basi niogelee ndani ya maji maji na damu. Natija yake ni nini? Ni nani aliyeniweka hapa, na kwa nini? Lakini akiambiwa kuwa, utakaa hapa kwa muda maalum ili viungo vyako vijengeke, viimarike ili viweze kufanya kazi na kushughulika, kisha utaingia katika ulimwengu mwingine mkubwa, na kwamba muda wa kukaa humo ni miezi tisa, kasha utaingia kwenye ulimwengu wenye jua lenye kuangaza na mwezi ung’arao, miti ya kijani kibichi, mito na neema maridhawa, hapo kitoto hicho bila shaka kingelifurahi na kusema: ‘Sasa nimejua hekima ya kuwekwa ndani ya jela hii!’ Dunia hii ni mwanzo tu, ni shule inayomuandaa mtu kuingia chuo kikuu. Ama ukiondoa uhusiano uliopo (tulioutaja) wa maisha ya hicho kitoto na maisha ya dunia hii, kila kitu kitakuwa ndani ya kiza tororo kuwa ni upuuzi mtupu; na ingelikuwa hiyo jela ni yenye kutisha, na mustakabali wake pia ungelikuwa mchungu zaidi.

Basi hivyo hivyo ndivyo ulivyo uhusiano baina ya maisha ya hapa duniani na akhera. Ni kitu gani kinachofanya tuishi hapa duniani kwa kipindi kisichopungua au kinachozidi miaka sabini huku tukivumila shida, na tukiutumia muda mchache kwa mafunzo hadi tukue, kisha tusome hadi tuelimike na mwishowe tujikute theluji ya uzee (mvi) imefunika vichwa vyetu? Lengo la yote haya ni nini? Je, lengo lake ni kula, kulala, kuvaa na kuhesabu miaka tu? Je mbingu hii angavu, ardhi pana, masomo, majaribio, walimu, na walezi, wote hawa wapo duniani kwa ajili ya kunywa, kula na kuvaa tu? Hapa kwa wale wasioamini akhera, ndipo maisha huonekana ni upuuzi na 179


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:19 PM

Page 180

Tujifunze Misingi ya Dini hayana maana yoyote, kwa sababu hawawezi kuyasawirisha mambo haya kuwa ndiyo lengo la maisha ya wakati huo huo hawaamini kama kuna maisha baada ya kufa hata hilo liwe ndilo lengo. Kwa sababu hiyo, ndipo mara nyingi watu hao hujiua ili kuepukana na maisha yasiyo na lengo wala maana. Lakini tukisadiki kuwa maisha ya dunia ni mavuno ya akhera na pia kwamba yatupasa tupande mbegu hapa ili tupate mavuno kwa ajili ya maisha ya milele; aidha tutakapojua kuwa dunia hii ni chuo kikuu, basi itatupasa tuchukue mafunzo ili tujiandae na maisha ya milele. Isitoshe dunia hii ni ya daraja tu la kuvuka ili tuelekee pale tunapokusudia; wakati huo dunia hii itakuwa ni yenye maana na si ya upuuzi, pia tutaona kuwa maisha yake yalikuwa ni kipindi cha maandalizi tu kwa ajili ya maisha ya milele, ambapo inastahiki tujifanyie mema zaidi ya haya. Kwa hivyo, imani juu ya marejeo inayafanya maisha yawe na maana, yasiwe na machafuko, simanzi na yasionekane kuwa ni upuuzi. Imani ya ufufuo hufunza Katika kuamini kuwapo kwa mahakama kuu ya uadilifu ya Mwenyezi Mungu siku ya mwisho, kuna athari kubwa katika maisha, tukiongezea kama tulivyoeleza hapo awali. Hebu chukua mfano kuwa imetangazwa nchini kwamba watu watendapo makosa katika siku fulani, mwaka Fulani, hawataadhibiwa na wasiwe na wasiwasi kwani maaskari na mahakama zitakuwa mapumzikoni; na kesho yake hali itaporejea ya kawaida, maovu mengi yaliyotendwa yasahaulike. Hebu fikiria hali ya watu itakuwaje siku hiyo! Kwa hakika imani ya Siku ya Kiyama ni imani ya kuamini nyumba yenye uadilifu mkubwa usiolingana na mahakama hizi za dunia. Mambo maalumu yaliyoko kwenye mahakama ya uadulifu wa Mwenyezi Mungu ni kama ifuatavyo: 180


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:19 PM

Page 181

Tujifunze Misingi ya Dini Mahakama ya Mwenyezi Mungu haitumii wasita, wala upendeleo, wala hakimu wake hadanganywi na hoja potofu. Haihitaji hati ya mapatano ya muda fulani kama ilivyo katika mahakama za dunia, kwa hivyo hukumu hazicheleweshwi wala kuahirishwa, bali hutolewa mara moja kwa haraka kama umeme, na hutolewa kwa usahihi kabisa. Ni mahakama inayotegemea amali za mtu mwenyewe, yaani amali zitakuwapo na kumthibitishia mtendaji aliyoyafanya kwa kiasi ambacho hatoweza kuyakana. Viungo ndivyo vitakavyotoa ushahidi kwa mtuhumiwa. Mikono yake, masiko, macho, miguu, masikio, macho, ulimi, ngozi, na hata kiwanja cha nyumba yake, milango na kuta, vitashuhudia pale alipotenda maasi au alipotelekeza jambo la wajibu katika kumtii Mwenyezi Mungu. Mashahidi hao wote ni vigumu kuwakana kama zilivyo athari za vitendo vyake mtu. Hakimu wa mahakama hiyo ni Mwenyezi Mungu, ajuaye kila jambo, aliyetosheka na kila kitu, na ni Muadilifu asiyelingana na yeyote. Mwisho, maamuzi ya mahakama haya hayakupangwa kabla, bali yamepangwa na amali zetu wenyewe. Matendo yetu ndiyo yatakayotuadhibu au kutustarehesha katika neema ya Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo kuamini kuwepo kwa mahakama hiyo humfanya mtu akariri yale aliyoyasema Imam Ali (a.s.): “Wallahi! Ni kheri nilale juu ya mti wa miba au nikokotwe huku nimefungwa minyororo, kuliko kukutana na Mwenyezi Mungu na Mtume Wake Siku ya Kiyama na huku nikiwa nimedhulumu waja Wake au kunyang’anya kitu miongoni mwa ghasia za kilimwengu…” Imani hiyo hiyo ndiyo iliyomfanya amchome na chuma cha moto nduguye aliyeomba pesa za hazina ya Waislamu. Alipokuwa akilalama 181


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:20 PM

Page 182

Tujifunze Misingi ya Dini kwa maumivu alimwambia, ‘Kufa! Ee Aqil! Walalama kwa machungu ya chuma kilichokolezwa na moto wa mwanaadamu kama mchezo wake, na hali wanipeleka mimi kwenye moto uliokokwa na Mwenyezi Mungu kwa hasira Zake…” (Nahjul-Balaghah: Khutba Na. 224).

Hebu angalia kisa hiki, je mtu mwenye imani kama hii anaweza kuhadaiwa? Je hongo inaweza kuinunua dhamira yake? Je, ahadi na vitisho vinaweza kumpotosha kutoka kwenye njia ya haki na kuelekea kwenye njia ya batili? Qur’ani tukufu inasema:

“Na madaftari yatawekwa (mbele yao). Utawaona wabaya wanavyoogopa kwa sababu ya yale yaliyomo (madftarini): na watasema: “Ole wetu! namna gani kitabu hiki! hakiachi dogo wala kubwa ila kimeyadhibiti (yameandikwa)…” (18:49). Hivi ndivyo roho ya mwanadamu inavyochimbuka kuwa na hisia za kuwa na majukumu katika kila amali zake, inayomfanya asipotoke na kuelekea kwenye dhuluma na uadui.

182


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:20 PM

Page 183

Tujifunze Misingi ya Dini

SOMO LA TATU MIFANO YA MAHAKAMA YA KIYAMA IKO NDANI YETU Kwa maswala ya maisha baada ya kufa na mahakama ya Siku ya Kiyama yanaonekana ni mapya kwa binadamu anayeishi katika dunia hii finyu, ndipo Mwenyezi Mungu akatuwekea mfano mdogo wa mahakama hiyo hapa duniani, nayo ni mahakama ya ‘dhamira.’ Hebu tufafanue maudhui haya: Mambo mengi ayafanyayo mwanadamu huhukumiwa katika mahakama mbali mbali, ya kwanza ni mahakama za kawaida za kibinaadamu ambazo zimejaa udhaifu, upungufu na makosa. Pamoja na kwamba mahakama hizi husaidia kupunguza utendaji maovu, lakini misingi yeke si yote yenye uadilifu kamili. Kanuni zilizotungwa, mahakimu waovu, hongo, upendeleo wa kujuana au wa kidugu, mbinu za kisiasa, na mengi mengineyo yanayodharaulisha mahakama kiasi ambacho kutokuwepo kwake ni bora kuliko kuwepo kwake ambako kunasaidia kutekeleza matakwa ya watu wenye sauti. Hata kama mahakama hizi zingekuwa na kanuni zenye usawa na mahakimu wachamungu na wakweli, bado kuna wahalifu wengi ambao wangeweza kuficha habari za maovu yao, au ni mahodari wanaoweza kuzipotosha hoja zitakazotolewa dhidi yao na hivyo kumfanya hakimu ashindwe kuwahukumu kwa haki. Mahakama ya pili kwa mwanaadamu ni ‘matokeo ya vitendo vyake.’ Vitendo vyetu vina athari na matokeo yanayotupata, iwe ni baada ya muda mfupi au mrefu, ikiwa hukumu hiyo haikuenea kwa watu wote lakini 183


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:20 PM

Page 184

Tujifunze Misingi ya Dini husadikishwa kwa uchache kulingana na watu wengi wanoathirika. Tumeshapata kuona serikali nyingi dhalimu zilizotenda kila aina ya maovu, lakini mwishowe zikajikuta zikiangukia kwenye mtego uliyojitegea zenyewe, zikajikuta zimenaswa ndani ya nyavu zilizozisuka zenyewe, zikapigwa radda zikavunjika na kutoweka kabisa. Kwa kuwa matokeo ya vitendo ndiyo uhusiano kati ya sababu na aliyesababishwa, basi ni vigumu sana kwa mtu kuweza kujiokoa kutokana na makucha yake kwa kubuni (kughushi) uongofu, kama inavyofanywa katika mahakama za kawaida. Mahakama hizi hazikukusanya mambo yote yanayotakikana, kwa hivyo haziwezi kutufanya tusitegemee mahakama ya Siku ya Kiyama. Mahakama ya tatu ni mahakama ya dhamiri, ambayo ni ya undani zaidi kuliko hii ya pili. Kama ilivyo kwamba, utaratibu wa mzunguko wa ajabu wa jua unalingana na ule uliomo kwenye tonoradi (Atom); basi yawezekana kusema kuwa mahakama (kuu) ya Siku ya Kiyama inajilinganisha ndani ya dhamira zetu (ndogo). Mwanandamu ana kitu kilichomo ndani yake ambacho wanafalsafa hukiita ‘akili ya vitendo.’ Qur’ani hukiita ‘nafsi yenye kujilaumu.’ Watu wa kisasa hukiita ‘dhamira.’ Mtu hafanyi jambo lolote lile, liwe la kheri au la shari isipokuwa mahakama ya dhamiri huweka kikao cha dharura chenye muafaka, kisicho na mizozo: kisha hutoa hukumu aidha ya malipo mema au mabaya, hupitisha hukumu hiyo kwa umbo la athari za kiroho. Wakosefu mara nyingi malipo yao mabaya huwa ni kupata shida kiasi kwamba hutamani kifo, hukikongowea na hukiona ni bora kuliko maisha; na huandika katika usia wake baada ya kujiua: “Nimejiua ili kuepukana na mateso ya dhamiri!”

184


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:20 PM

Page 185

Tujifunze Misingi ya Dini Mara nyingine thawabu za amali ya kheri huwa nyingi kiasi cha kumfurahisha mwenye kutenda, na humletea utulivu wa kiroho kiasi cha kushindwa kuelezea utamu uliomo. Mahakama hii ina mambo maaulum nayo: Ina hakimu wake, shahidi wake, afisa mwendesha mashtaka mmoja, naye ni dhamiri, ambayo ndiyo inayotoa ushahidi, kisha kwa bidii yake yote inatoa hukumu. Kinyume na mahakama za kawaida ambazo zina rabsha nyingi, na mara nyingine kesi moja inachukua miaka mingi, lakini mahakama hiyo huamua kwa haraka sana kama umeme, isipokuwa tu kesi yenyewe itakapokuwa na utatanishi unaohitaji wakati wa kuchunguza hoja na kuondosha pazia la kughafilika moyoni, hata hivyo ikithibitishwa, hukumu yake huwa ni ya uhakika. Uamuzi utolewao na mahakama hii ni wa aina moja tu, hakuna kukata rufani kwani uamuzi wake huwa ni wa mwisho kabisa. Mahakama hii haitoi hukumu ya adhabu tu, pia hutoa hukumu ya malipo mema na thawabu; hii ni kusema kwamba mahakama hii huangalia pande zote kwa kuwaadhibu wakosaji na kuwalipa mema waadilifu. Adhabu zitolewazo nayo hazifanani na za mahakama ya kawaida, kwani kwenye mahakama hizi hakuna jela hasa, viboko wala vitanzi vya kunyongea, bali adhabu zake ni kali na jela yake ni mbaya sana kwa anayeadhibiwa, kiasi kwamba dunia hii pana huwa finyu mno kwake kama ilivyo jela ndogo ya mtu mmoja tu. Isitoshe, mahakama hii haifanani na yoyote miongoni mwa hizi mahakama za kawaida, bali ni aina ya mahakama za Siku ya Kiyama. Ni kuu mno hata Qur’ani imeapa kwayo, kama ilivyoapa kwa mahakama ya Siku ya Kiyama, Mwenyezi Mungu amesema katika Qur’ani: 185


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:20 PM

Page 186

Tujifunze Misingi ya Dini

“Naapa kwa Siku ya Kiyama. Tena naapa kwa nafsi inayojilaumu. Anadhani mtu kuwa sisi hatutaikusanya mifupa yake? Kwa nini! Sisi tunaweza (hata) kuzisawazisha ncha za vidole vyake�. (75:1-4). Kimsingi, kwa kuwa mahakama hii ya dhamiri ni ya kidunia, basi kwa vyovyote vile itakuwa na udhaifu wake, hivyo basi itatufanya tutegemee mahakama ya Siku ya Kiyama. Udhaifu huo ni: Ukanda wake unayo nafasi ndogo ambayo haiwezi kuhifadhi mambo yote, bali inalingana na fikra na utambuzi tu wa wanaadamu. Kuna watu ambao ni walaghai mno kiasi cha kuweza kuzihadaa hata dhamiri zao wenyewe. Wakati mwingine mwito wa dhamiri huwa ni dhaifu sana hata hauwezi kufika kwenye masikio ya waovu. Kwa hivyo, ndipo inatudhihirikia kwamba hapana budi kuwe na mahakama ya nne ambayo ni mahakama ya Siku ya Kiyama.

186


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:20 PM

Page 187

Tujifunze Misingi ya Dini

SOMO LA NNE UFUFUO NA UFUNUO WA KIMAUMBILE Wasomi wanasema kwamba maarifa ya nafsi ya kumjua Mungu hutokana na maumbile ya mtu; na tunapoangalia dhamiri ya mtu mwenye mwamko na asiye na mwamko inatudhihirikia imani yake ya asili ya kuumbwa kwake inayomfanya aone kuwa aliyeumba ulimwengu huu ni Muumbaji Mjuzi, aliyeumba kwa utaratibu maalum na kwa lengo maalum. Kwa hivyo fikra hii haiepukani na ‘Tawhid na kumjua Mungu,’ pia mizizi yote ya dini pamoja na matawi yake lazima yawe kwenye fitra hiyo, vinginenevyo itakuwa kule ‘kuweka sharia’ kwa Mwenyezi Mungu na ‘kuumba’ hakuna maana (soma kwa makini hapa!). Tunapochunguza undani zaidi ya nyoyo zetu, tutasikia sauti ikituambia: ‘Maisha hayaishi kwa sababu ya kifo, bali kifo ni njia tu ya kwenda kwenye ulimwengu wa milele.’ Ili tuufahamu ukweli huu, yatupasa tuzinduke na kuangalia mambo yafuatayo: Kupenda kudumu Kama ingelikuwa mwanaadamu ameumbwa ili afe na kutoweka, bila shaka angelikupenda huko kutoweka kwa sababu ingelikuwa ndio lengo la kuumbwa kwake; na angelifurahia kifo, lakini haijatokea hata siku moja mtu kufurahishwa na kifo, bali hujaribu kukiepuka kwa kadri ya uwezo wake, hilo linathibitishwa na juhudi zake azifanyazo katika kujaribu kurefusha umri wake, kutafuta dawa ya 187


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:20 PM

Page 188

Tujifunze Misingi ya Dini kurudi ujanani na kutafuta maji ya uhai! Hivyo basi, uhusiano huu wa mwanadamu, wa kupenda kuishi (kudumu) ni dalili ya wazi ya kuonyesha kwamba sisi wanaadamu tumeumbwa ili tuishi (tudumu) hatukuubwa ili tufe; kwani kama tungeumbwa ili tufe, tusingelipenda kuishi kiasi hiki. Kwa mapenzi yote yaliyo ndani ya nafsi zetu, lengo lake ni kutufikisha kwenye ukamilifu, miongoni mwayo ni penzi la kupenda kudumu ambalo linakamilisha sababu ya kuumbwa kwetu. Ndugu msomaji, usisahau kwamba bado tunaendelea na upekuzi katika somo la ‘ufufuo’ baada ya kukubali kuwapo kwa Mwenyezi Mungu, Mjuzi na Mwenye hekima. Bila shaka tunaamini kwamba kila alichotuumbia Mwenyezi Mungu kina hekima na uthibiti, kwa hivyo bila shaka kuna hekima ya penzi hili alilotupa la kupenda kudumu; na hekima hiyo ni kuwapo ulimwengu mwingine baada ya ulimwengu huu. Siku ya Kiyama na watu wa kale Historia inayotueleza kuhusu kuwapo kwa dini mbali mbali katika enzi mbali mbali, pia inatufunulia kwamba mwanaadamu aliyeishi zamani alikuwa akiamini kuwa kuna ‘maisha baada ya kufa.’ Kumbukumbu zilizosalia za watu wa kale, na hasa waliokuwako kabla ya kuandikwa historia, kama vile sanaa za nakshi kwenye makaburi na jinsi walivyokuwa wakizika, yote haya yanaonyesha jinsi walivyokuwa wakiamini kuwako kwa maisha mengine baada ya kufa. Kwa hivyo basi, imani hii iliyoota mizizi katika historia ya maisha ya mwanadamu isichukuliwe kuwa ni imani duni au ni desturi tu. Isitoshe, kila tukiisadifisha imani iliyoota mizizi na yenye kudumu katika historia ya mwanadamu, tutaona kuwa ni imani ya asili ya 188


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:20 PM

Page 189

Tujifunze Misingi ya Dini kimaumbile, kwani ni hiyo pekee ndiyo inayoweza kuendela kuhifadhika kutokana na kupita nyakati na mabadiliko ya kijamii na kifikra, na hubaki katika hali yake hiyo hiyo. Lakini ada na desturi hubadilika na kusahaulika kadri siku zinavyopita. Mathalan, kuvaa mtindo fulani wa mavazi, kuwe kwa desturi au kwa ada ambayo baadaye hubadilika kutokana na mabadiliko ya nyakati. Lakini penzi la mama kwa mwanawe ni maumbile yaliyomo ndani ya mama, kwa hiyo hayawezi kubadilika kwa wakati au hali yoyoye, miale ya penzi hilo haidhoofishwi na mazingira wala rangi ya pendo hilo haiwezi kubadilika kutokana na vumbi la kusahau. Na kila mvuto unaotokana ndani ya mwanaadamu ni maumbile yake aliyoumbiwa na ataendelea kuwa nayo. Wataalamu wanasema: “Utafiti wa hali ya juu uliofanywa umethibitisha kuwa watu wa kale walikuwa wanaamini aina fulani za dini, kwani walikuwa wakizika maiti zao kwa aina maalumu, wakiwazika pamoja na vitu vyao pia, hili linathibitisha kwamba wao walikuwa wakiamini kuwapo kwa ulimwengu mwingine.” Hapa tunafahamu kwamba watu hao walikubaliana na fikra ya kuwepo ulimwengu mwingine baada ya kufa, japo walikosea kwa kudhani ulimwengu huo mwingine hautofautiani kabisa na huu, na kwamba vitu alivyokuwa akivitumia marehemu hapa ulimwenguni huenda vikamfaa baadaye katika huo ulimwengu mwingine. 3. Kuwapo kwa mahakana ya ‘dhamiri’ ni dalili nyingine ya kuonyesha kuwa fikra ya marejeo ni ya kiasili. Tumeshasema mwanzoni, kwamba sote tunahisi kuwa ndani ya nafsi zetu kuna mahakama inayoangalia vitendo na maneno yetu, hisia ambayo hutulipa wema tuufanyao, tukahisi raha, utulivu wa kiroho, 189


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:20 PM

Page 190

Tujifunze Misingi ya Dini furaha na uchangamfu kwa namna isiyoweza kuelezeka. Vile vile mahakama hiyo hutuadhibu kwa maovu tuyafanyayo, na hasa madhambi makubwa ambayo mateso yake huwa makali kiasi cha kufanya yawe machungu kama shubili. Mara kwa mara hutokea kwamba wahalifu, baada ya kutenda kosa kama kuua, hutoroka na baadaye, kwa hiyari yao wenyewe hujisalimisha kwenye kitanzi cha mahakama, na huku wakisema kwamba wamefanya hivyo ili kuepukana na mateso ya dhamiri. Mtu anapowaza juu ya mahakama hii ya ndani hustaajabu: ‘Kwa nini ndani ya nafsi yangu kuwe na mahakama kama hii ilhali ya kwamba mimi ni kiumbe mdogo, na isiwepo kwenye ulimwengu huu mkubwa mahakama inayolingana nayo?’ Kutokana na maelezo hayo yote yaliyotutangulia, tunaweza kuthibitisha njia tatu za itikadi ya kiasili kuhusu ‘ufufuo’ nazo ni: Kupenda kuendelea kuwako Kihistoria, ambayo inathibitisha imani hiyo iliyokuwapo kwa mwanaadamu toka enzi za kale. Mfano mdogo uliomo ndani ya nafsi ya mwanaadamu.

SOMO LA TANO UFUFUO NA MIZANI YA UADILIFU Tukitupa jicho kwenye utaratibu wa ulimwengu na mpangilio wa uumbaji, tutaona kwamba kuna kanuni inayotawala na kukiweka kila kitu mahali pake panapostahili. Tukiangalia kwenye mwili wa mwanadamu, mathalani, tutaona jinsi ulivyopangiliwa kwa uangalifu 190


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:20 PM

Page 191

Tujifunze Misingi ya Dini wa hali ya juu sana kiasi kwamba ikhtilafu ndogo tu katika mwili huo huweza kusababisha maradhi na hata kifo. Hebu tazama jinsi moyo, jicho au ubongo ulivyopangiliwa, utaona kwamba kila kitu kimewekwa mahali pake maalum, tena kwa ustadi kabisa na kwa kiwango maalum tena kwa ustadi kabisa na kwa kiwango chake mahsusi. Mpangilio huu hauko kwa mwanadamu pekee, bali hata katika ulimwengu mzima, kwani: “Mbingu na ardhi zimedumu kwa ulinganifu.� Chembe ya tonaradi (Atom) ndogo sana kiasi ambacho unaweza kuziweka milioni juu ya ncha ya sindano, angalia jinsi zilivyo na utaratibu mzuri kiasi cha kuweza kudumu kwa mamilioni ya miaka, hii inatokana na mpangilio ulio sahihi wa kimahesabu wa Elektroni na Protoni ambazo hazitoki nje ya mpangilio wake. Je, mwanadamu ni kiumbe wa kipekee? Au ni doa jeusi kwenye ulimwengu huu mkubwa mweupe? Kwa hivyo yu huru afanye atakavyo kama vile dhulma na uonevu? Au kuna siri iliyofichika hapa? Uhuru wa kujiamulia Ukweli ni kwamba mwanaadamu ana tofauti za kimsingi na viumbe wengine duniani. Yeye ana uhuru wa kujiamulia. Kwa nini aliumbwa na kupewa uhuru huo? Na kwa nini akapewa uwezo wa kuamua kufanya atakavyo? Sababu ni kwamba kama asingepewa uhuru, ukamilifu wake usingelitimia. Tofauti hii kubwa kati yake na viumbe wengine ndiyo inayodhamini ukamilifu wake wa kitabia na kiroho.

191


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:20 PM

Page 192

Tujifunze Misingi ya Dini Mathalani, lau mtu atalazimishwa kuwasaidia wanyonge au kufanya kazi nyinginezo zenye manufaa katika jamii; zote hizo zitahesabiwa kuwa ni kazi njema lakini hazitamvuta mtu huyo kwenye ukamilifu wa kitabia na kiutu; lakinii atakapojitolea yeye mwenyewe kufanya kazi hizo za kheri, kwa hiyari yake, atakuwa amejivuta kuelekea kwenye ukamilifu wa kiroho na kitabia. Kwa kuongeza ni kwamba, sharti la kwanza la ukamilifu wa mwanadamu kitabia na roho, ni kuwa na hiari na kuweza kujiamulia kufanya mambo kwa namna atakavyo na kwa mapenzi yake, si kwa kulazimishwa, na Mwenyezi Mungu alimpa kipawa hiki mwanadamu kwa lengo hili tu. Lakini kipawa hiki kikubwa alichopewa mwanaadamu ni kama mfano wa ua la waridi lililozungukwa na miiba, nako ni kutumia vibaya nafasi hii ya uhuru kunakofanywa na baadhi ya watu kwa kufanya uonevu na ufisadi. Kimsingi ni kuwa, si kazi ngumu kwa Mwenyezi Mungu kumwadhibu mara moja mtu dhalimu adhabu kali itakayomfanya hata asiwaze kutenda maovu tena, kama kupoozesha mkono, kumpofusha au kumfanya asiweze kusema na hivyo asithubutu kuutumia vibaya uhuru aliopewa na amche Mungu; lakini uchaji Mungu wa aina hii utakuwa ni wa kulazimishwa na hautakuwa na fahari kwa mtu huyo, bali utakuwa ni kwa ajili ya kuogopa adhabu ya papo kwa papo tu. Kwa hivyo basi, ni lazima mwanadamu awe na uhuru wa kujiamulia, apasi mitihani atakayowekewa na Mwenyezi Mungu na asiadhibiwe ghafla ila katika hali zisizo za kawaida, ili aweze kuonyesha thamani ya utu wake. Lakini hali kama itabaki hivyo hivyo tu, na kila mtu kuchagua njia yake, kanuni ya uadilifu wa Mwenyezi Mungu inayotawala dunia ingelikuwa na kasoro. Na kuanzia hapa ndipo inabainika kwamba kuna mahakama na nyumba ya uadilifu iliyowekewa watu na kwam192


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:20 PM

Page 193

Tujifunze Misingi ya Dini ba wote watafika hapo bila ya kubaguliwa na kupewa adhabu ama malipo mema kwa mujibu wa uadilifu wa Mwenyezi Mungu. Je inawezekana watu kama Namrud, Firaun, Jangiz Khan na Qarun ambao maisha yao yote walidhulumu na kufanya maovu, waachwe tu hivi hivi bila ya kuadhibiwa? Je inawezekana watu wema na maovu wawe sawa mbele ya Mwenyezi Mungu? Mwenyezi Mungu amesema: “Je tuwafanye wanaotii sawa na waasi? Mmekuwaje? Mnahukumu namna gani?” (68: 35-36). Katika Aya nyingine: “…. Au tuwajaalie watawa (wacha Mungu) kuwa sawa na waovu?” (38:28). Ndiyo, ni kweli kwamba kuna baadhi ya watenda maovu huadhibiwa hapa hapa duniani au hupata nusu ya adhabu; ni kweli kwamba mahakama ya dhamiri ni swala la muhimu; na ni kweli pia kwamba matokeo ya dhuluma na madhambi ayafanyayo mtu mara nyingine humrudia mwenyewe, lakini tukiyaangalia kwa makini mambo haya matatu tutaona kwamba hayatokei kwa kila dhalimu au mwovu, kuweza kupata adhabu sahihi ya maovu aliyoyafanya. Kuna wengi miongoni mwao wanaookoka na adhabu ya mahakama ya dhamiri au matokeo ya vitendo vyao, au wanaopata adhabu kwa uchache tu. Kwa ajili ya watu kama hawa, ndipo Mwenyezi Mungu akaweka huko akhera mahakama kuu ya uadilifu ya kuwahukumu na kupima vitendo vyao, viwe ni vyema au viovu, hata kama vina uzito wa ncha ya sindano; vinginevyo asili ya uadilifu wa Mwenyezi Mungu itakuwa haina maana. Kwa hiyo basi mtu atakapokubali kuwapo kwa Mwenyezi Mungu na uadilifu wake, itambidi akubali ufufuo na mahakama ya Siku ya Kiyama, haiwezekani kutofautisha kati ya mambo haya mawili.

193


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:20 PM

Page 194

Tujifunze Misingi ya Dini

SOMO LA SITA USHAHIDI WA UFUFUO HAPA DUNIANI Aya tukufu za Qur’ani zinaonyesha wazi kwamba si makafiri na waabudu masanamu tu waliokuwa wakati wa Mtume ndiyo waliokuwa wakipinga ufufuo na suala la maisha baada ya kufa, bali hata umma zilizopita pia zilikuwa na msimamo huo huo. Walikuwa wakiwaita Mitume kuwa ni wendawazimu: “Na waliokufuru walisema (kuambiana wenyewe kwa wenyewe kwa stihizai): ‘Je! Tukijulisheni mtu anayekuambieni ya kwamba mtakapochambuliwa vipande (makaburini baada ya kufa kwenu) kuwa (mtafufuliwa na) mtakuwa katika umbo jipya?’” (Mwenyezi Mungu anasema): “Je! (wanamuona) amezua uwongo juu ya Mwenyezi Mungu au amepata wazimu?”…(34:7-8). Naam, kwa kuwa watu katika enzi hizo walikuwa na mawazo mafupi, ilikuwa ni rahisi kwao kumdhania mtu anayeamini mambo ya akhera kuwa ni mwendawazimu; au walichukulia kuwa ni kumtukana Mungu na huku wakisema kwamba madai ya mwili uliokwisha kufa kupatiwa uhai ni ya kiwazimu. Lakini ni jambo lenye kuvutia kuona jinsi Qur’ani tukufu inavyozipinga fikra zao hizo kwa kutoa hoja mbali mbali ambazo ni rahisi kufahamika kwa mtu wa kawaida na kwa mtu aliyeelimika, kila mmoja kulingana na uwezo wake wa kufahamu. Japokuwa ufafanuzi wa hoja za Qur’ani juu ya jambo hili ni mrefu unaohitaji kitabu kizima, hapa tutataja kwa mukhtasari tu baadhi yake: 194


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:20 PM

Page 195

Tujifunze Misingi ya Dini Moja katika Aya za Qur’ani tukufu inasema: “Na Mwenyezi Mungu ndiye anayepeleka pepo zikaharakisha mawingu na tutayafikisha katika nchi iliyokufa, na kwayo, tukaihuisha ardhi baada ya kufa kwake. Kama hivyo ndivyo (kutakavyokuwa) kufufuliwa.” (35:9). Tunapotembea mbugani wakati wa kipupwe tutaona ishara na harufu ya kifo imeenea kila mahali. Miti haina majani wala matunda, magogo hukauka, na hapana ua linalotabasamu wala kustawi. Yanapokuja majira ya mvua, anga husafika, mvua ikaanza kunyesha na kuleta uhai, mara utaona harakati za uhai katika kila kitu, mimea hustawi, mti hukua mara vikonyo vyake hujitokeza na ndege huanza kujenga viota vyao matawini na hivyo kufanya hali kuwa ni ya kuvutia. Lau kama maisha baada ya kufa hayana maana tusingeona mandhari haya kila mwaka, au kama yasingelikuwapo na ingechukuliwa kuwa ni maneno ya kipuuzi tu, tusingeliweza kuyaona na kuyahisi mandhari haya kila mwaka. Na hapana tofauti kati ya kufufuliwa ardhi iliyokufa (kama tuonvyo katika majira ya kuchipua ya kila mwaka) na kufufuliwa mwanaadamu aliyekufa. Mahali pengine Qur’ani huwachukua watu na kuwapeleka kwenye asili ya kuumbwa. Inataja habari ya Bedui aliyekwenda kwa Mtume (s.a.w.w.) na huku ameshika mfupa uliyooza akamwambia: “Ee Muhammad! Nani atakayeihuisha mifupa na hali imesagika?” Mwenyezi Mungu akamwamuru Mtume Wake amjibu: “Sema: ‘Ataihusisha yule alieiumba mara ya kwanza…’ ” (36: 78-79). Hakuna tofauti yoyote kati ya kuumba kwa mara ya kwanza na kuumba upya, ndipo Aya nyingine inasema: “…Kama tulivyoanza umbo la awali tutalirudisha tena.” (21:104). Wakati mwingine Qur’ani huashiria uwezo mkuu alionao Mwenyezi Mungu kwa kuwataka watu waangalie ulimwengu huu mpana wenye 195


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:20 PM

Page 196

Tujifunze Misingi ya Dini mbingu na ardhi, yasema: “Je yule aliyeziumba mbingu na ardhi (mnaona) hana uwezo wa kuumba (mara ya pili) mfano wao (wanadamu)? Kwa nini? Naye ni Muumbaji mkuu, Mjuzi (wa kila jambo). Hakika amri yake anapotaka chochote (kile kitokee) ni kukimbia: ‘kuwa,’ basi mara huwa.” (36:81-82). Waliokuwa hawaamini jambo hili, walikuwa na mawazo mafupi sana, hawakuweza hata kuona nje ya nyumba zao, lakini ingelikuwa kinyume na hivyo wangegundua kwamba kuumbwa tena mara ya pili ni jambo sahali kuliko mara ya kuanza, na kwamba kurudishiwa uhai maiti si jambo gumu kwa Mwenyezi Mungu aliyeumba mbingu na ardhi kabla ya hapo. 4. Wakati mwingine Qur’ani hutaja nishati za ufufuo ikisema: “Ambaye amekufanyieni moto katika mti mbichi, mkawa nanyi kwa (mti) huo mnauwasha.” (36:80). Tunapochunguza maelezo haya ya ajabu ya Qur’ani, kwa msaada wa kisayansi, tutaona kuwa sayansi inasema: Miti ya kijani kibichi huhifadhi nishati inayotokana na mwanga wa jua na tunawapowasha kipande cha kuni ule moto unaotoka hapo ni nishati ya joto iliyohifadhiwa kutokana na mwanga wa jua kwa muda mrefu, nasi hudhania kuwa imekufa na kuharibika, lakini mara tu tunaona hivi leo ikiwa na maisha mapya. Kwa hivyo basi ikiwa Mwenyezi Mungu ana uwezo wa kuweza kuihifadhi nishati ya jua ibaki ndani ya gogo la mti kwa miaka mingi na kuitoa mara moja, atashindwaje kufufua waliokufa? Hivi ndivyo tunavyoona jinsi Qur’ani kwa dalili na kimantiki inavyowajibu na kuwaziba midomo wale wanaotilia shaka ‘ufufuo’ ikiwathibitishia uwezekano wa ufufuo kwa kutegemea dalili hizo tulizozitaja. 196


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:20 PM

Page 197

Tujifunze Misingi ya Dini

SOMO LA SABA UFUFUO NA HEKIMA YA KUUMBWA Watu wengi hujiuliza: ‘Kwa nini tumeumbwa na Mwenyezi Mungu?’ Wengine huuliza zaidi: “Nini hekima ya kuumbwa ulimwengu huu mkubwa?” Mlimaji bustani huwa na haja ya mazao, ndipo hupanda kwa ajili ya kupata matunda, hulima, akapanda mbegu kwa ajili ya kuvuna. Kwa nini muumbaji mkuu wa bustani akatuumba? Je kulikuwa na upungufu uliomfanya hata atuumbe ili akamilike? Na ikiwa ni hivi, basi atakuwa ni muhitaji ambapo sifa hiyo ni muhali kwake Yeye Muumbaji na asiye na mwisho. Kwa kujibu haya, kuna maneno mengi yaliyosemwa, lakini hapa tutajaribu kuyafupisha: Ni kosa kubwa kulinganisha sifa za Mwenyezi Mungu na zetu, kwa sababu vitendo vyetu vina mipaka, sisi hushughulika ili kukidhi mahitaji yetu tu, mathalani tunasoma ili tupunguze ujinga, tunafanya kazi ili tupate pesa na tunahangaika mahospitalini kutafuta matibabu ili tuzilinde afya zetu. Lakini kwa upande wa Mwenyezi Mungu wa milele, yatupasa tuangalie malengo ya vitendo vyake nje ya Dhati Yake. Mwenyezi Mungu haumbi kwa ajili ya kupata manufaa au kujitimizia haja, bali lengo lake ni kueneza rehema na ukarimu Wake kwa waja Wake. Ni kama jua liangazalo daima bila ya kutarajia chochote, bali huneemesha watu wote kwa mwanga na ukarimu wake. Katika mahukumilio ya dhati yake ni kuwachukua waja Wake na kuwapele197


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:20 PM

Page 198

Tujifunze Misingi ya Dini ka kwenye ukamilifu. Kuumbwa kwetu baada ya kutokuwapo hapa duniani, kutuletea mitume na kututeremshia vitabu, ni kaida ya kufikia kwenye ukamilifu. “Ulimwenguni huu ni kama chuo kikuu, nasi tu wasomi wake, ulimwengu huu ni kama shamba nasi tu wakulima wake, ulimwengu huu ni duka la mawalii wa Mungu.” (Nahjul Balagha). Kwa hivyo basi, itawezekanaje tuseme kwamba kuubwa hakuna lengo? Na hali ya kuwa tukiangalia na kuchunguza vitu vyote tutakuta kwamba kila kitu kina lengo. Kwa mfano, tukiangalia viungo vya miili yetu, hatuwezi kupata kiungo kisichokuwa na lengo, hata kope na mashimo ya nyayo zetu yana lengo. Itawezekanaje viungo vya miili yetu viwe na lengo na miili yenyewe isiwe na lengo? Vile vile tukiachana miili yetu na kuangalia ulimwengu, tutaona kuwa kila kitu kina lengo: Kuchomoza jua kuna lengo, kunyesha mvua na kuvuma upepo pia kuna lengo. Je yawezekanaje ulimwengu mzima usiwe na lengo? Ukweli ni kwamba ndani ya ulimwengu huu ulimwengu mpana yaonekana pana picha zinazoonyesha lengo lake mwishoni, lengo ambalo hatuwezi kulitambua kabla, nalo ni ‘elimu na ukamilifu.’ Baada ya kufahamu kiujumla lengo la kuumbwa, sasa tuangalie kama lengo la kuumbwa kwetu na kuishi siku chache ni kwa ajili ya shida na misiba au ni kwa nini? Hebu tuchukue mfano, mimi nitaishi duniani hapa kwa muda wa miaka sitini, na kila siku nitakwenda kazini asubuhi na kurudi jioni 198


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:20 PM

Page 199

Tujifunze Misingi ya Dini kwa ajili ya kujitafutia riziki, na hurudi nyumbani nikiwa nimechoka. Matokeo yake nitakula tani kadhaa za maji na chakula katika muda wa maisha yangu hayo, kisha nitasumbuka nijenge nyumba na baadaye nife na kutoka ulimwenguni hapa. Je wafikiri lengo hili ndilo litanifanya niishi duniani nikikumbwa na shida zote hizi? Bila shaka sote tutastaajabu, kwani mapumziko ya mpita njia wa saa moja tu, ndiyo yamsababishie mjenzi taabu zote hizo?! Kwa hivyo, ndipo wale wasioamini ufufuo na maisha baada ya kufa wanaona kuwa dunia hii haina lengo na ni upuuzi tu, na mara nyingi madai haya tunayapata katika vitabu vya watu na kimaada (wasioamini Mungu) ambao wanaamini kuwa maisha duniani hayana lengo na hivyo huwapelekea kujiua kwa sababu ya kuchoka na maisha yasiyokuwa na lengo. Kwa kweli jambo linalofanya dunia hii iwe na lengo na kuyafanya maisha yawe na maana, ni kuzingatia kuwa dunia hii ni njia tu ya mwanzo, ya kuelekea kwenye ulimwengu mwingine, na matatizo anayokabiliwa nayo mwanadamu ni maandalizi ya kutengeneza njia ielekeayo kwenye maisha ya milele. Tumeshatoa mfano hapo awali juu ya jambo hili tukasema kuwa, iwapo mtoto aliye tumboni mwa mama yake atapewa akili ya kufahamu, kisha aambiwe kuwa maisha haya unayoyapitisha humu, mwishowe hayana manufaa yoyote, bila shaka angesema kuwa, basi hakuna maana nifungiwe mahali hapa penye dhiki na giza kisha kusiwe chochote. Lakini akihakikishiwa kwamba miezi hii michache anayokaa humo ni njia tu anayopitia kuelekea kwenye ulimwengu mpya mwenye maisha marefu na mwenye nafasi, mwanga na neema maridhawa, bila shaka mtoto huyo aliyemo tumboni, ataridhika na kuona kuwa muda 199


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:20 PM

Page 200

Tujifunze Misingi ya Dini anaoupitisha humo tumboni una lengo na hivyo anaweza kuvumilia. Qur’ani tukufu yasema: “Na bila shaka nyinyi mnajua umbo la kwanza (hili walilonalo viumbe wote kuwa tumelifanya sisi): kwa nini hamkumbuki (kuwa sisi ni waweza vile vile na hilo umbo la pili).”(56:62). Kwa muhtasari ni kwamba ulimwengu huu bila shaka unasema waziwazi kwamba kuna ulimwengu mwingine baada yake, na kama si hivyo, basi ulimwengu huu ungelikuwa hauna maana yyoyote. Qur’a tukufu yasema: “Je mlidhani kwamba tumekuumbeni bure na ya kwamba nyinyi kwetu hamtarudishwa.” (23:115). Yaani kama si marejeo kwa Mwenyezi Mungu, kama ilivyotajwa katika Qur’ani, kuumbwa kwa mwaadamu kusingelikuwa na maana. Twarudia tena kusema kuwa, hekima ya kuumbwa yasema, ni lazima kuwe na ulimwengu mwingine baada ya huu.

SOMO LA NANE KUBAKI ROHO NI DALILI YA ‘UFUFUO’ Haijajulikana mwanadamu alianza lini kufikiria juu ya kuwepo kwa roho. Tunaweza kusema kuwa tokea mwanzo mwanadamu alitambua tofauti iliyoko kati yake na viumbe vingine vya ulimwenguni kama vile mawe, mbao, milima, majangwa na wanyama. Mwanadamu ameshapitiwa na usingizi na kifo, na ameona kwamba hutokea mabadiliko makubwa ya hali yake anapolala au anapokufa, bila ya kubadilika kitu katika mwili na umbo lake. Kuanzia hapo 200


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:20 PM

Page 201

Tujifunze Misingi ya Dini ndipo akagundua kuwa pana kitu kingine kisichokuwa mwili. Kisha akajiona kuwa yu tofauti na wanyama wengine kwa sababu yeye anaweza kupanga jambo na kulifanya atakavyo, ambapo wanyama huongozwa na hisia zao zinazotawala vitendo vyao tu. Zaidi ya haya mwanadamu huona mambo fulani usingizini wakati baadhi ya viungo vya mwili wake vinapumzika akiwa amejitupa. Hapo ndipo alipogundua kuwa kuna nguvu ya ndani sana iliyofichikana, akaiita ‘roho’. Wanafalsafa walipoanza kuzungumzia utu, waliifanya roho kuwa ni swala kubwa la muhimu na wakataka kujua uhakika wa ‘roho’. Nadharia na maoni yao juu ya roho yakafikia zaidi ya elfu kulingana na kauli ya wanafalsafa wa kiislamu. Mengi yamezungumzwa juu ya jambo hili, lakini ya muhimu kuyajua, ni majibu yanayohusika na maswali yafuatayo: Je, roho ni kitu gani? Je, iko pekee au inategemeea ubongo na mishipa? Baadhi ya wanafalsafa wa kimaada wanashikilia kusema kuwa roho na mambo yake ya kidhahiri, ni kama chembechembe za ubongo, mtu anapokufa nazo pia hufa, kama vile saa ikivunjwa vunjwa huacha kufanya kazi. Upande mwingie kuna wanafalsafa wanaomwamini Mungu na baadhi ya wanafalsafa wa kimaada, wanaoamini asili ya roho na kwamba roho inaendelea kubaki hata kama mwanadamu atakufa. Kwa kuthibitisha hilo wanatoa sababu nyingi ambazo hazitoshi kuzitaja hapa, hata hivyo tutataja baadi ya zile zilizo wazi na kwa njia nyepesi: 201


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:20 PM

Page 202

Tujifunze Misingi ya Dini Ulimwengu mkubwa hauwezi kuingizwa kwenye ulimwengu mdogo Hebu chukua mfano kuwa umekaa ufukoni mwa bahari na nyuma yako pana milima mirefu inayofika mawinguni, wakati huo mawimbi makali yanapiga na kurudi baharini, na juu ya jabali kuna makelele ya upepo na mawingu, kisha uyaangalie madhari haya kwa mara moja tu, halafu ufumbe macho yako, bila shaka yale mandhari uliyoyaona utayaona tena katika bongo lako, kama ulivyoona pamoja na ukubwa wake. Bila shaka ramani hii ya kwenye ubongo inahitaji ipate mahali panapotosha ukubwa wake. Hii inaonyesha kwamba kuna ‘kitu’ kingine mbali na chembe chembe za ubongo, kinachoweza kuhifadhi picha na mandhari uliyoyaona kwa ukubwa na umbo lake; na lazima kitu hiki kisiwe ni katika vitu vyenye kugusika (kimaada) kwa sababu katika vitu vya aina hiyo hakuna mfano wake. Mambo maalumu ya kidhahiri ya roho Tuna vitu vingi vinavyofanya kazi kikemia na kifizikia ndani ya miili yetu, mathalani, kazi inayofanywa na moyo ni ya kifizikia au kazi ya kusagwa na kuyeyushwa chakula ndani ya miili yetu ifanywayo na matumbo ni kikemia na mifano mingi mingineyo. Ikiwa roho na fikra zetu ni za kifizikia na kikemia mbona zinatofautiana na mambo yanayohusiana na mwili? Kusema kweli, roho na fikra zetu zinatuwasilisha na kutupasha habari za ulimwengu ulio nje ya miili yetu, lakini vitu mahususi, kama kemia ya tumbo au harakati za macho, moyo na ulimi haviwezi kufanya hivyo. Yaani, sisi tunahisi kabisa kwamba tunafungamana na ulimwengu uliyo nje ya miili yetu, na tunajua mengi kuuhusu. Je ina maana kuwa ulimwengu wetu wa nje umeingia ndani ya miili yetu? Bila shaka 202


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:20 PM

Page 203

Tujifunze Misingi ya Dini hapana, na kama ni hivyo, je tusemeje? Bila shaka tunaona ramani ya ulimwengu na bila shaka mambo ya dhahiri ya kiroho ndiyo yanayotufanya tuutambue ulimwengu ulio nje yetu; ambapo mambo haya hatuwezi kuyajua kwa hali za kifizikia au kikemia zulizomo kwenye miili yetu (soma kwa uangalifu sehemu hii). Hii inaonyesha kwamba kuna kazi nyingine ambazo hufanywa na roho tu. Dalili za kimajaribio za asili na kuwapo pekee kwa roho Kwa bahati nzuri, wataalamu leo wameweza kisayansi kuthibitisha asili ya kujitenga kwa roho, na hivyo wamefanikiwa kuwanyamazisha kabisa wale wanaopinga uasili wa roho na wanaodai kwamba roho ni kitu. Kwa mfano kuna jambo liitwalo ‘kuzuga au kwa lugha ya kiingereza ‘Hypnotism’, yaani kumweka mtu chini ya uwezo wako na kumtuia utakavyo, bila yeye mwenyewe kujijua. Watu wengi wamepata kuishuhudia, ama wale ambao hawajashuhudia hebu tuwape maelezo yake kidogo: Kuna watu wanaoweza kumlaza mtu kwa kumuangalia kwa macho makali na mengineyo, lakini usingizi usio wa kawaida, kwani huwa amesimama lakini wakati huo hajijui kisha huzungumza naye, naye humjibu na kusema maneno ya ajabu ambayo alikuwa hayajui, mathalani anaweza kuzungumza lugha asiyoijua kabisa, anaweza kujibu maswali magumu ya hesabu, au anaweza kuyanakili mambo juu ya karatasi yaliyomo ndani ya sanduku lililofungwa, bila ya kulifungua, na mengineyo mengi. Jambo lingine linalothibitsha kuwa roho haipo pamoja na mwili ni ile shughuli kuzihudhurisha roho au kuwasiliana na roho za maiti (Spiritualism) na kuzihudhurisha kwenye mikutano ya roho. Kuna jumuiya nyingi zinazoshughulika na mambo hayo zilizotapakaa dunia 203


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:20 PM

Page 204

Tujifunze Misingi ya Dini nzima na zinatoa zaidi ya magazeti mia tatu – kama anavyosema mwanachuoni wa Kimisri Farid Wajdi – ambapo jumuiya hizo hukutana kwenye vikao vyao na kuzihidhurisha roho za watu mashuhuri ya kufanya mambo ya kimaajabu. Licha ya kuwa kuna watu wadanganayifu wanaojihusha na shughuli hiyo na kuiba mali za watu, lakini wanavyuoni wanakubaliana kuwapo kwa mambo haya. Haya yote ni dalili ya kuonyesha kuwa roho iko pekee na itababaki baada ya mtu kufariki, na hii ni hatua kubwa juu ya suala tunalolizungumzia la majereo na kuwapo uhai baada ya kufa. 3. Vile vie ndoto tuziotazo tunapokuwa usingizini, ambapo mara nyingine mtu huona mambo yatakayotukia baadaye na pengine huvumbua mambo yaliyojificha kiasi ambacho tunaamini wazi kwamba ni mambo ya kweli si ya kibahati tu. Hii pia ni dalili ya kuonyesha kuwa roho iko pekee. Na bila shaka watu wengi wamewahi kupitiwa na ndoto za kweli kama hizo katika umri wao, au kusikia kutoka kwa marafiki zao kwamba baadhi ya mambo waliyoyaona ndotoni yalitokea kuwa kweli baadye. Haya yote yanaonyesha kuwa mtu alalapo roho yake huwasiliana na ulimwengu mwingine na kuona baadhi ya matukio yatakayotukia baadaye. Mambo yote haya yanaonyesha kuwa roho sio ‘kitu’ na wala sio kazi inayofanywa na ubongo wa binadamu, bali ni ukweli usio wa kawaida, ulio nyuma ya maumbile, na kwamba roho haifi kama unavyokufa mwili wake bali hujiaandaa kwa siku ya ufufuo.

204


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:20 PM

Page 205

Tujifunze Misingi ya Dini

SOMO LA TISA UFUFUO WA ‘KIMWILI’ NA WA ‘KIROHO’ Miongoni mwa maswali muhimu yayojijitokeza katika maudhui ya ufufuo, ni swali kwamba, je, kufufuliwa kutakuwa ni kwa ‘kiroho’ pekee au kutakuwa ni kwa ‘kiroho na kimwili’? Na kwamba je, mtu atakuwa na daraja kubwa zaidi na kuendelea na maisha mapya? Baadhi ya wanafalsafa wa kale walikuwa wakiamini kuwa wafu watafufuliwa kiroho tu, kwani wao walikuwa wakiamini kwamba mwili ni kitu kinachohusiana na maisha ya kidunia tu, na hivyo mwanadamu hauhitaji huko akhera; na kwamba roho yake inapotokea tu, kwa haraka sana hukimbilia kwenye ulimwengu wa kiroho. Lakini wanavyuoni wanafalsafa wakubwa wa kiislamu wanaamini kwamba mwanaadamu atafufuliwa akiwa na roho na mwili wake pamoja. Ndiyo, ni kweli kwamba mwili wa mwanaadamu hugeuka mchanga baada ya muda anapozikwa na kwamba mchanga huu hutapanyika ardhini, lakini Mwenyezi Mungu ni Muweza wa wa kuvikusanya vyote hivi siku ya ufufuo na kuvipa nguo mpya ya uhai. Hili ndilo wanavyuoni hao huliita ufufuo wa ‘kimwili’ kwa sababu kufufuliwa roho ni jambo lisilo na shaka, na kwa kuwa mjadala unahusu juu ya kufufuliwa ‘kimwili’ ndipo wakauita hivyo. Vyovyote iwavyo, Aya za Qur’ani zilizoshuka juu ya jambo hilo ni nyingi, kama tutakavyoona: Qur’ani na ufufuo wa ‘kiroho’: Tumeshasoma hapo awali kisa cha Bedui aliyekwenda kwa Mtume (s.a.w.w.) akiwa ameshika kipande cha mfupa uliooza, akamuuliza Mtume: “Nani atakayehuisha mifupa na hali imesagika?” Akajibiwa, 205


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:20 PM

Page 206

Tujifunze Misingi ya Dini kwa kwa amri ya Mwenyezi Mungu:

“Sema, ‘ataihuisha yule aliyeiumba mara kwa kwanza, naye ni Mjuzi wa kila (namna ya) kuumba. Ambaye amekufanyieni moto katika mti mbichi, mkawa nanyi kwa mti huo mnauwasha.’” (36:78-80).

Mahali pengine Qur’ani inasema:

“Na kisha tutapiga baragumu (la kufufuliwa), tahamaki hao wanatoka makaburini kwenda mbio mbio kwa Mola wao.” (36:51). Katika Aya nyingine:

“Macho yao yatainama chini, wanatoka katika makaburi kama kwamba ni nzige waliotawanyika.” (54:7). Kama tujuavyo, makaburini ni mahali panapozikwa miili ya watu na si roho zao, kwa hivyo Aya hizo zilizotangulia zinaonyesha dhamiri ufufuo wa kimwili. Wapinzani wengi wa ufufuo walipinga kwa sababu walikuwa wakishangazwa na jinsi mchanga uliotapanyika na kupotea ardhini utakavyoweza kukusanyika na mtu kurudia uhai tena: Amesema Mola (s.w.t.):

206


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:20 PM

Page 207

Tujifunze Misingi ya Dini

“Na huusema (kwa maskhara): ‘Je, tutakapopotea katika ardhi, (tukageuka mchanga) ndio tutarudishwa katika umbo jipya?’” (32:10). Mwenyezi Mungu naye anawajibu:

“Je, hawaoni Mwenyezi Mungu jinsi aanzishavyo viumbe kisha atavirudisha (mara ya pili). Hakika hayo kwa Mwenyezi Mungu ni sahali.” (29:19). Waarabu katika enzi ya ujahiliya walikuwa wakisema:

“Je, anakuahidini ya kwamba mtakapokufa na mkawa udongo na mifupa, kuwa mtatolewa (mtafufuliwa)?” (23:35). Aya hizi za Qur’ani na nyinginezo zinaonyesha dhahiri kwamba Mtume (s.a.w.w.) alizungumzia ufufuo wa ‘kimwili,’ kwani hata kwa waabudu masanamu pia kuko upande huu wa ufufuo wa ‘kimwili’, ndipo Qur’ani nayo ikatoa mifano ya ufufuo huo kwenye mimea na vitu avionavyo mwanaadamu kwa macho yake, kama mifano ya kuumba kwa mwazo na uwezo wa Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo, haiwezekani kwa mwislamu ambaye ni msomaji Qur’ani akanushe ufufuo wa ‘kimwili’ kwani, kulingana na Qur’ani kuukanusha ufufuo huo wa ‘kimwili’ ndiko kukanusha ufufuo 207


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:20 PM

Page 208

Tujifunze Misingi ya Dini wenyewe. Hoja za kiakili Tukiachana na Qur’ani, hata akili pia yatwambia kuwa roho na mwili ni vitu visivyotengana, pamoja na kila kimoja kujitegemea, lakini bado vinaungana. Vinakua na kufikia ukamilifu pamoja, na bila shaka vinahitajiana ili kuendeleza maisha ya kudumu. Japokuwa viwili hivi hutengana wakati wa ‘Barzakh’ (katikati ya maisha ya dunia na ya akehra, mtu anapokufa) lakini kutengana huko hakuwi kwa daima, kwani mwili bila ya roho huwa na upungufu na vilevile roho huwa na upungufu bila ya mwili. Roho ndiyo iamrishayo, na mwili ndio unaotii amri na kuitekeleza, kwa hivyo haiwezekani kuwe na muamrishaji bila ya muamrishwaji na kinyume chake, na kwa kuwa roho itakuwa na daraja ya juu Siku ya Kiyama, bila shaka mwili pia kwa upande wake ni lazima uwe hivyo hivyo, yaani siku hiyo mwili hautakuwa na upungufu kama ulivyokuwa nao duniani. Basi vyovyote iwavyo, roho na mwili vimezaliwa pamoja na na kukamilika pamoja, kwa hivyo ufufuo pia hautakuwa wa ‘kimwili’ au wa ‘kiroho’ pekee; yaani somo hili laonyesha uhusiano uliopo baina ya roho na mwili na jinsi zitakavyofufuliwa pamoja. Tukisonga mbele zaidi tutaona kanuni ya uadilifu wa Mwenyezi Mungu kwa upande mwingine, yasema: Ni lazima vitu viwili hivyo vifufuliwe pamoja, kwa sababu mwanaadamu alipofanya mema au alipotenda madhambi duniani, aliyatenda akiwa na vyote viwili roho na mwili. Kwa maana hiyo, vyote viwili vilipwe pamoja, iwe ni thawabu au adhabu. Kwani kama ingelikuwa ni kimojawapo tu kati ya hivyo ndicho kinachoadhibiwa, kusingelifanyika uadilifu. Maswali kuhusu ufufuo wa ‘kimwili’

208


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:20 PM

Page 209

Tujifunze Misingi ya Dini Wasomi wametoa maswali mengi kuhusu jambo hili nasi tutataja baadhi ya maswali hayo: Majaribio yaliyofanywa na wanasayansi wa elimu ya viumbe yanaonyesha kwamba mwili wa binadamu hubadilika kila baada ya miaka saba na huendelea hivyo maisha yake yote. Sasa swali ni, je! siku ya ufufuo mwanaadamu atakuwa katika umbo gani miongoni mwa mabadiliko hayo? Nasi kwa kujibu twasema kuwa mwanaadamu atafufuliwa katika umbo lake la mwisho; kama Aya zilizopita zinavyosema kwamba Mwenyezi Mungu atamfufua mwanadamu kwa mifupa na mchanga na mwili wake aliozikwa. Hapa yamaanisha kwamba katika umbo alilokufia mtu ndilo atakalofufuliwa kwalo. Kama Aya hii inavyosema: “… Kwa hakika Mwenyezi Mungu atawafufua walio makaburini.” (22:7). Ufafanuzi wa Aya hii ni kuwa, mwanaadamu atafufuliwa akiwa na mwili wake ule ule aliyozikwa nao; lakini mwili huo utakuwa umekusanya sifa zote za mwili mzima ulio kamili, alizokuwa nazo katika mabadiliko ya maisha yake; utakuwa una sifa zote hizo na hivyo utastahiki kufanyiwa uadilifu, kwa kulipwa mema au kuadhibiwa. Wengine husema hivi: Tunapokufa na kugeuka kuwa mchanga, chembechembe za miili yetu pia huwa mchanga na hapo huwa ni chakula cha miti na mimea, kisha huingia kwenye matunda ambayo baadaye huliwa na mwanadamu wengine, sasa vipi miili hiyo itarejeshwa tena Siku ya Kiyama na hali imeshachanganyika na mingine? Jibu la swali hili ni refu mno, lakini tutajaribu kulijibu kwa kifupi tutakavyoweza: Hapana shaka juu ya chembechembe za mwili wa mtu zilizoinga kwa mtu mwingine kurudi kwa mwenyewe wa kwanza. Hili limeelezwa wazi wazi katika Aya zilizopita.

209


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:20 PM

Page 210

Tujifunze Misingi ya Dini Tatizo linajitokeza hapa ni kuhusu upungufu wa mwili wa mtu huyo; lakini ukweli ni kwamba hautakuwa na upungufu wowote bali utakuwa mdogo; kwani chembechembe hizo zitakuwa zimeenea mwili mzima, zinaporudishwa kwake huwa ndogo. Miili ya mtu wa kwanza na wa pili haitatoweka ila tu huo mwingine wa pili utakuwa mdogo, na hili si tatizo kwani tunafahamu kwamba miili midogo na yenye kasoro itafufuliwa kamili kabisa.

SOMO LA KUMI PEPO, MOTO NA KUJIUNDA MATENDO YETU Mara nyingi watu hujiuliza: Je, akhera inafanana na dunia hii, ama zinatofautiana? Je, malipo mema, adhabu na kanuni zinazotawala ni kama hizi za ulimwengu huu? Nasi kwa kujibu twasema: Kuna ushahidi mwingi unaoonyesha tofauti zilizopo kati ya ulimwengu huu na wa akhera, na kwamba kile tukijuacho kuhusu akhera ni kama mangati yanayoonekana kwa mbali, kama maji. Ni vizuri turejee kwenye mfano tulioupiga mwanzo wa kilenge kilichomo tumboni na ulimwengu huu ndiyo tofauti iliyoko baina yaulimwengu huu na akhera au hii ni kubwa zaidi. Lau kilenge hicho kilichomo tumboni kitakuwa na fahamu na kikataka kipate picha sahihi akilini mwake ya ulimwengu wa nje ya mbingu, ardhi, jua, mwezi, nyota, milima, mapori, na bahari, basi kisingeliweza, kwani kamusi yake ya maneno bado ni ndogo mno, ili kwamba lau atasemeshwa na mtu aliye nje ya tumbo la mama yake hatafahamu 210


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:20 PM

Page 211

Tujifunze Misingi ya Dini chochote. Kwa hivyo tofauti iliyoko kati ya ulimwengu huu tuishio wenye kikomo na ulimwengu mpana wa akhera ni kama hii au zaidi yake, na hivyo hatuwezi kupata picha (ndani ya fikra zetu) ya neema, adhabu, Pepo na moto iliyoko akhera. Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Hakuna jicho lililopata kuona wala sikio lililosikia wala moyo wa mwanadamu uliopitiwa na mawazo ya neema zilizomo Peponi.” Qur’ani tukufu nayo inasema:

“Nafsi yoyote haijui waliyofichiwa katika hayo yanayofurahisha macho huko peponi: ni malipo ya yote waliyokuwa wakiyafanya.” (32:17). Uwezo na mfumo wa utawala pia unatofautiana kati ya ulimwengu huu na akhera. Mathalani, katika kutoa hukumu Siku ya Kiyama, ushahidi wa vitendo alivyovitenda mtu utatolewa na mikono yake, miguu, ngozi na hata ardhi ya pale alipofanyia vitendo hivyo. Qur’ani tukufu yasema:

“Siku hiyo tutaviziba vinywa vyao, itazungumza mikono yao na itoe ushahidi miguu yao kwa yale waliyokuwa wakiyachuma.” (36:65).

211


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:21 PM

Page 212

Tujifunze Misingi ya Dini Aya nyingine yasema:

“Na wao waziambie (hizi) ngozi zao, ‘mbona mnatushuhudilia?’ Nazo ziwaambie, ‘Mwenyezi Mungu aliyekitamkisha kila kitu ndiye aliyemtutamkisha, Naye ndiye aliyekuumbeni mara ya kwanza. Na kwake (hivi sasa) mnarudishwa.” (41:21). Hapo zamani ilikuwa ni vigumu watu kuamini kwamba viungo vitazungumza, lakini baada ya mwanadamu kupiga hatua ya kisayansi na kuweza kurekodi sauti ya picha (k.m. video, sinema, n.k), imekuwa si jambo la ajabu tena. Naam, pamoja na kuwa hatuna uwezo wa kufahamu mambo ya akhera ila ni kama mangati tu kwetu, lakini tunachofahamu, ni kwamba adhabu na malipo mema huko akhera yatakuwa ni ya kiroho na kimwili, kwa sababu ufufuo pia utakuwa ni wa kiroho na kimwili. Qur’ani inasema:

“Na wabashirie walioamini na kufanya vitendo vizuri, kwamba watapata mabustani yapitayo mito mbele yake; na humo watapata wake waliotakasika (na kila mabaya na machafu); na watakaa milele humo.” (2:25). 212


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:21 PM

Page 213

Tujifunze Misingi ya Dini Aya nyingine yasema: “… Na radhi za Mwenyez Mungu ndizo kubwa zaidi.” (9:72). Ndiyo, kutambua kwa watu watakaokwenda Peponi kuwa wameridhiwa na Mola wao, kutawafanya wahisi furaha isiyo na kifani. Vile vile watu watakaoingia motoni, pamoja na adhabu ya kimwili watakayoipata humo, pia watahisi kughadhibikiwa na Mwenyezi Mungu ambayo hiyo ndiyo adhabu mbaya zaidi kupita zote. Kujiunda vitendo Aya nyingi za Qur’ani zinaeleza jinsi vitendo vyetu vitakavyojiunda katika mambo mbalimbali hapo siku ya Kiyama. Dhuluma itakuja kwa sura ya wingu jeusi litakalomzunguka dhalimu, kama isemavyo Hadith: “Dhuluma ni giza Siku ya Kiyama.” Nayo Qur’ani tukufu yasema:

“Hakika wale ambao wanakula mali za mayatima kwa dhuluma, bila ya shaka wanakula moto matumboni mwao, na wataungua katika moto (wa Jahannam) uwakao.” (4:10). Aya nyingine yasema:

“Siku utakapowaona Waislamu wanaume na Waislamu wanawake, nuru zao zinakwenda mbele yao…” (57:12).

213


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:21 PM

Page 214

Tujifunze Misingi ya Dini Miongoni mwa Aya hizo ni: “Wale wanaokula riba, hawasimami (kuendesha yao) ila kama anavyosimama yule ambaye shetani amemzuga kwa wazimu…” (2:275). Miongoni mwazo ni ile isemayo: “Wala wasione wale ambao wanafanya ubakhili katika yale aliyowapa Mwenyezi Mungu katika fadhila zake kuwa ni bora kwao (kufanya ubakhili huko). La, ni vibaya kwao. Watafungwa kongwa (madude ya kunasa shingoni ) za yale waliyofanyia ubakhili - Siku ya Kiyama…” (3:180). Hii ni baadhi tu ya mifano iliyomo katika Qur’ani ikionyesha jinsi vitendo vyetu vitakavyojiunda Siku ya Kiyama. Sote tunafahamu kwamba sayansi inasema kuwa hakuna kitu kitakachotoweka kabisa bali hubadilika na kuwa katika umbo jingine kwa hivyo basi, hata vitendo vyetu havitatoweka bali vitabaki milele, kulingana na kanuni hii. Katika Qur’ani kuna kipande cha Aya kuhusu Kiyama ambacho kinaweza kumtingisha mtu, kinasema: “…Na watakuta yote waliyoyafanya yamehudhuria hapo …” (18:49). Ni dhahiri kwamba kila yanayowapata wanaadamu ni matokeo ya vitendo vyao wenyewe, ndipo Mwenyezi Mungu akaongeza katika Aya hiyo hiyo: “…Na Mola wako hamdhululumu yoyote.” (18:49). Tukiendelea zaidi juu ya suala hili tunakuta sehemu nyingine katika Qur’ani tukufu ikisema: “Siku hiyo watu watatoka (makaburini) vikundi vikundi ili waonyeshe vitendo vyao. Basi anayefanya wema (hata) wa kiasi cha uzito wa mdudu chungu ataona jaza yake. Na anayefanya maovu (hata) kiasi cha uzito wa mdudu chungu ataona jaza yake.” (99:6-8)

214


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:21 PM

Page 215

Tujifunze Misingi ya Dini Ukichunguza Aya hizi utaona kuwa zinazungumzia ‘kuona’ mtu vitendo vyake. Kwani amali zetu zote duniani zitahifadhiwa na hazitatoweka, ziwe ndogo ama kubwa, mbaya ama nzuri, bila shaka hilo ni onyo kwetu ili tuweze kujiepusha na vitendo viovu na tufanye mema kwa wingi. Tukiendelea na maudhui haya, hivi leo hapa hapa duniani kuna vyombo vilivyogunduliwa vinavyoweza kuhifadhi vitendo vyetu. Wataalamu wanasema: “Sayansi imeweza kuyarudisha na kuyafanya yasikike mawimbi ya sauti yaliyozungumzwa na wafinyanzi wa kiMisri zaidi ya miaka elfu mbili iliyopita.” Katika vyombo vya kaure vilivyoko katika jumba la makumbusho nchini Misri, kuna vyombo vya kaure vilivyofanyiwa ufundi wa kuweza kutoa sauti za wafinyazi walipokuwa wakifinyanga, sauti hizo zilinaswa na vyombo hivyo na zinaweza kusikika hivi leo kwa masikio yetu. Kwa hivyo basi, vyovyote iwavyo, maswali mengi yahusuyo ufufuo, kuishi milele, adhabu kwa watenda maovu na kulipwa mema kwa watu wema yaliyomo katika Qur’ani tukufu, yanaweza kujibiwa kwa kuzingatia ‘kujiunda amali,’ kwani amali, iwe ni nzuri au mbaya, huacha athari yake rohoni mwetu, na Athari hiyo hubaki nasi.

215


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:21 PM

Page 216

Tujifunze Misingi ya Dini

ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION: 1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9. 10. 11. 12. 13. 14. 15. 16. 17. 18. 19. 20. 21. 22. 23. 24. 25. 26. 27.

Qur'an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Ishirini. Uharamisho wa Riba Uharamisho wa uwongo Juzuu ya kwanza Uharamisho wa uwongo Juzuu ya pili Hekaya za Bahlul Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.) Hijab vazi Bora Ukweli wa Shia Ithnaashari Madhambi Makuu Mbingu imenikirimu Abdallah Ibn Saba Khadijatul Kubra Utumwa Umakini katika Swala Misingi ya Maarifa Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia Bilal wa Afrika Abudharr Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu Salman Farsi Ammar Yasir Qur'an na Hadithi Elimu ya Nafsi Yajue Madhehebu ya Shia Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur'an Tukufu Al-Wahda 216


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:21 PM

Page 217

Tujifunze Misingi ya Dini 28. 29. 30. 31. 32. 33. 34. 35. 36. 37. 38. 39 40. 41. 42. 43. 44. 45. 46. 47. 48. 49. 50. 51. 52. 53. 54. 55. 56. 57. 58. 59. 60.

Ponyo kutoka katika Qur'an. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii Mashukio ya Akhera Al Amali Dua Indal Ahlul Bayt Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna. Haki za wanawake katika Uislamu Mwenyeezi Mungu na sifa zake Amateka Na Aba'Khalifa Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) Adhana. Upendo katika Ukristo na Uislamu Nyuma yaho naje kuyoboka Amavu n’amavuko by’ubushiya Kupaka juu ya khofu Kukusanya swala mbili Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Kusujudu juu ya udongo Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s) Tarawehe Malumbano baina ya Sunni na Shia Kupunguza Swala safarini Kufungua safarini Umaasumu wa Manabii Qur’an inatoa changamoto as-Salaatu Khayrun Mina -'n Nawm Uadilifu wa Masahaba Dua e Kumayl Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mitume Muhammad (s) 217


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:21 PM

Page 218

Tujifunze Misingi ya Dini 61. 62. 63. 64. 65. 66. 67. 68. 69. 70. 71. 72. 73. 74. 75. 76. 77. 78.

Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili Kuzuru Makaburi Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu Tujifunze Misingi Ya Dini Sala ni Nguzo ya Dini Mikesha Ya Peshawar Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu Ubora wa Imam 'Ali Juu ya Maswahaba Na Ushia ndio njia iliy onyooka Shia asema haya, Sunni asema haya, Wewe wasemaje? Liqaa-u-llaah Muhammad (s) Mtume wa Allah Amani na Jihadi Katika Uislamu Uislamu Ulienea Vipi? Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s)

218


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

10:21 PM

Page 219

Tujifunze Misingi ya Dini

BACK COVER Kama jina la kitabu hiki linavyojieleza - Tujifunze Misingi ya Dini mwandishi ameelezea kwa ufupi lakini katika lugha pana, misingi hii mikubwa ya Uislamu ambayo ndiyo inayowaunganisha Waislamu wote licha ya kuwepo hitilafu ndogo katika misingi miwili mingine, yaani Uadilifu ('Adl) na Uimamu (Imaamah). Hata hivyo, hitilafu hizo ni ndogo kiasi kwamba haziwezi kuleta mgongano baina ya madhehebu zetu za Kiislamu. Kwa hivyo, maudhui yaliyomo katika kitabu hiki ni yenye kuwafaa Waislamu wote wa madhehebu zote. Kutokana na umuhimu wa maudhui haya ambayo kwa uchache kila Mwislamu anatakiwa aijue misingi hii, tumeona tuyatoe masomo haya katika lugha ya Kiswahili ili wasomaji wetu wa Kiswahili wapate kufaidika na yaliyomo katika safu hii ya masomo na kuongeza ujuzi wao katika masuala ya kidini na kijamii.

Kimetolewa na kuchapishwa na:

Al-Itrah Foundation S.L.P - 19701, Dar-es-Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Nukushi: +255 22 2127555 Barua Pepe: alitrah@raha.com Tovuti: www.alitrah.org Katika mtandao: www.alitrah.info

219


Tujifunze misingi ya dini EDITED 28 Aug 2008.qxd

9/5/2008

Tujifunze Misingi ya Dini

220

10:21 PM

Page 220


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.