Uadilifu wa maswahaba final edit.qxd
7/15/2011
12:34 PM
Page A
U A D I L I F U WA M A S A H A B A K WA M TA Z A M O WA A H L U L - B A I T
Kimeandikwa na:
Sayyid Abdur-Rahim al-Musawi
Kimetarjumiwa na:
Hemedi Lubumba Selemani
Uadilifu wa maswahaba final edit.qxd
7/15/2011
12:34 PM
Page B
ŠHaki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: 978 - 9987 - 427 - 61 - 1 Kimeandikwa na:
Sayyid Abdur-Rahim al-Musawi Kimetarjumiwa na:
Hemedi Lubumba Selemani Kimehaririwa na: Ustadh Abdallah Mohamed Kimepangwa katika Kompyuta na: Ukhti Pili Rajab Toleo la kwanza: Machi, 2008 Nakala: 1000 Kimetolewa na kuchapishwa na:
Al-Itrah Foundation P. O. Box 19701, Dar-es-Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Fax: +255 22 2127555 Email: alitrah@raha.com Website: www.alitrah.org Online: www.alitrah.info
Uadilifu wa maswahaba final edit.qxd
7/15/2011
12:34 PM
Page C
YALIYOMO Uadilifu wa masahaba kwa mtazamo wa Ahlul-Bait..................................2 Sayyid Abdul Rahm al-Musawi...................................................................2 Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul Bait (a.s).....................................................4 Nadharia ya Uadilifu wa Masahaba kwa mtazamo wa Ahlul-Bait............4 Maana ya usuhuba kwa mujibu wa lugha ya Kiarabu.................................5 Masahaba waumini wa kweli......................................................................6 Imamu Ali awasifu Masahaba waumini wa kweli.......................................8 Uchunguzi juu ya nadharia ya uadilifu wa masahaba................................11 Msimamo wa Sunna tukufu juu ya uadilifu wa kila sahaba......................11 Msimamo wa Historia juu ya uadilifu wa kila sahaba..............................15 Ili kukamilisha utafiti, Tazama baadhi ya mifano......................................19 Sababu za kuanza Nadharia hii..................................................................23 Mfumo wa Shi’a kuhusu maana ya usuhuba na sahaba............................25 Muhtasari wa Rai ya Shi’a juu ya Masahaba.............................................27
Uadilifu wa maswahaba final edit.qxd
7/15/2011
12:34 PM
Page D
NENO LA MCHAPISHAJI Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabu kwa jina la: "Adalatu'l-Sahabah" Sisi tumekiita: "Uadilifu wa Maswahaba." Kitabu hiki, "Uadilifu wa Maswahaba" ni matokea ya utafiti wa kielimu uliofanywa na Mwanachuoni wa Kiislamu, Sayyid AbdurRahim al-Musawi Sheria ya Kiislamu ni ya kipekee kwa kuwa inahusika na kila jambo huku ikiweka utatuzi wa matatizo yote yanayompata mwanadamu katika sekta zote za maisha yake. Wanachouni wa Kiislamu kama kawaida ya wanadamu wamehitilafiana katika hukumu ndogo ndogo katika matendo ya ibada, lakini kama ilivyo, tofauti ndogo kati ya wanachuo kwa wafuasi inakuwa ni mlima wa tofauti na kusababisha zongo lisilo na maana. Mambo ambayo wanachuo wetu wamehitilafiana si katika asili au misingi ya dini, na isitoshe ni mambo machache sana ukilinganisha na yale tunayokubaliana kwayo. Je, Masahaba wote ni waadilifu? Hili ni suala ambalo wanachuo wetu wamehitalifiana; ndani ya madhehebu moja na kati ya madhehebu mbalimbali. Kwa hiyo hii sio hitilafu ya madhehebu, bali ni hitilafi ya wanachuo wa madhehebu zote, wamehitilafiana juu ya suala hili. Lakini bahati mbaya Waislamu wengi hawaitambui hitilafu hii kwa usahihi na hivyo kuogelea katika dhana na kusababisha
Uadilifu wa maswahaba final edit.qxd
7/15/2011
12:34 PM
Page E
mizozo isiyokuwa na maana. Kutokana na hali hii Sheikh wetu, Sayyid Abdur-Rahim al-Musawi amelifanyia utafiti wa kina suala hili na kuweka wazi asili ya hitilafu hii, kisha akamuachia msomaji mwenyewe kutoa uamuzi. Kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote. Kutokana na ukweli huu, Taasisi yetu ya ‘Al-Itrah Foundation' imeona ikitoe kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili, kwa madhumuni yake yale yale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili, ili kuongeza ujuzi wao katika masuala ya dini na ya kijamii. Tunamshukuru ndugu yetu, Hemedi Lubumba Selemani kwa kukubali jukumu hili la kukifanyia tarjuma kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwa kitabu hiki. Mchapishaji: Al-Itrah Foundation S. L. P. 19701 Dar-es-Salaam, Tanzania.
Uadilifu wa maswahaba final edit.qxd
7/15/2011
F
12:34 PM
Page F
Uadilifu wa maswahaba final edit.qxd
7/15/2011
12:34 PM
Page 1
Uadilifu wa maswahaba final edit.qxd
7/15/2011
12:34 PM
Page 2
Uadilifu wa Masahaba kwa mtazamo wa Ahlul-Bait
UADILIFU WA MASAHABA KWA MTAZAMO WA AHLUL-BAIT SAYYID ABDUR-RAHIM AL-MUSAWI Hakika urithi wa Ahlul-Baiti ambao umetunzwa na kambi yao na wafuasi wao dhidi ya upoteaji unaonyesha kambi iliyokusanya aina mbalimbali za maarifa ya kiislamu. Kambi hii imeweza kulea nafsi mbalimbali zilizo tayari kunywa toka kwenye chemchem hiyo na kuupa umma wa kiislamu wasomi wakubwa wenye kufuata nyayo za ujumbe wa Ahlul-baiti huku wakikusanya vidodosa na maswali ya madhehebu tofauti na mitazamo tofauti ya kifikra kuanzia ndani na nje ya utamaduni wa kiislamu na wakiyatolea maswali hayo majibu na utatuzi makini ndani ya karne zote. Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-baiti imefanya hima kutetea matukufu ya risala na ukweli wake ambao umechafuliwa na makundi, madhehebu na wanaharakati mbalimbali wenye chuki na Uislamu. Jumuiya imefuata nyayo za Ahlul-baiti na wafuasi wa kambi yao bora ambayo imefanya hima kujibu madai yenye kuendelea na daima ikajaribu kubaki kwenye msitari wa mapambano kwa kiwango kinachohitajika ndani ya kila zama. Hakika uzoefu ambao umetunzwa na vitabu vya wanavyuoni wa kambi ya Ahlul-baiti katika dhamira hii ni wa aina ya pekee, kwa sababu una nguzo ya kielimu inayotegemea akili na dalili, huku ukijiepusha na matamanio na uzalendo uliokemewa, na unazungumza na wasomi pamoja na wanaharakati wenye taalumma maalumu mazungumzo ambayo yanaituliza akili na yanapokewa na maumbile salama.
2
Uadilifu wa maswahaba final edit.qxd
7/15/2011
12:34 PM
Page 3
Uadilifu wa Masahaba kwa mtazamo wa Ahlul-Bait Jaribio hili la Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-baiti limekuja kuwapa watafuta ukweli hatua mpya ya uzoefu huo wa thamani katika ulingo wa mazungumzo, maswali na majibu ya hoja za utata zilizotolewa zama zilizopita au zinazotolewa leo kwa njia ya tovuti (Internet), na hasa kwa kupewa nguvu na baadhi ya nchi zenye chuki na Uislamu na Waislamu. Jumuiya imejiepusha na udadisi uliokemewa pia ni yenye kwenda hima kuzidadisi akili zenye kufikiria na nafsi zenye kutafuta haki ili ziweze kufungukia kwenye haki itolewayo na kambi ya Ahlul-baiti ulimwengu mzima, ndani ya zama ambazo akili zinapevuka na nafsi zinaboreka kwa kasi ya kipekee. Ni lazima tugusie kuwa mfululizo huu wa tafiti hizi umeandaliwa na kamati maalumu kutoka kwenye jopo la waheshimiwa wanavyuoni, hivyo tunatoa shukrani za dhati kwa hawa wote na kwa wasomi na wachunguzi kwa kila mmoja miongoni mwao, kwa kupitia baadhi ya tafiti hizi na kutoa mawazo yao ya thamani kuhusu tafiti hizi. Tunategemea na kutaraji kuwa tutakuwa tumetoa kile tunachoweza katika juhudi za kutekeleza baadhi ya wajibu tulionao mbele ya ujumbe wa Mola wetu Mtukufu ambaye alimtuma Mtume Wake na uongofu na dini ya haki ili aidhihirishe juu ya dini zote. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa shahidi.
3
Uadilifu wa maswahaba final edit.qxd
7/15/2011
12:34 PM
Page 4
Uadilifu wa Masahaba kwa mtazamo wa Ahlul-Bait JUMUIYA YA KIMATAIFA YA AHLUL-BAITI (A.S.) IDARA YA ELIMU NADHARIA YA UADILIFU WA MASAHABA KWA MTAZAMO WA AHLUL-BAITI Nadharia ya uadilifu wa maswahaba: Inamaanisha kuwa kila aliyemsuhubu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) angalau hata kwa kipindi kifupi mno basi yeye ni mwadilifu, hasemi uongo wala hakosei kwa makusudi, bali inasihi kumfuata kwenye yale ayasemayo au kuyapokea au ayatendayo na yeye huchukuliwa kuwa ni hoja dhidi ya mwingine. Nadharia hii ilianza ndani ya mazingira ya siasa mahususi na malengo maalumu ya kisiasa, ambayo kwa ufupi ni kuimarisha utawala wa Bani Umaiyya na kuhalalisha vitendo vyao na kuvipaka aina fulani ya rangi ya kisheria. Baadhi ya wapinzani wameendeleza nadharia hii na kuitumia kwa kuieneza miongoni mwa umma wa kiislamu na kuifanya njia mbadala na ruhusa ya kuukana msimamo wa Ahlul-baiti ambao Kitabu kimeelezea utakaso wao kwa Mwenyezi Mungu kuwaondolea uchafu na kuwatakasa kabisa. Japokuwa makada wa nadharia hii walijaribu kushikilia dalili fulani ili kuipa nadharia nguvu na kuiwekea chapa fulani ya kielimu, lakini kundi dogo la wanavyuoni wa kiislamu limeikanusha nadharia hii na kuhoji dalili zake, na wala halijayapokea matokeo yake kama ilivyo kwa makada wenyewe wa nadharia hii, kwani hawajayakubali matokeo yake pale walipoanza kutetea vitendo vya makhalifa na watawala wao dhidi ya baadhi ya maswahaba ambao waliukosoa utawala wao. Ili tuweze kujua msimamo wa kambi ya Ahlul-baiti kuhusu nadharia ya uadilifu wa maswahaba na usahihi wake, itatulazimu kuanzia kwenye maana ya usuhuba kilugha (Kiarabu) kisha tuonyeshe msimamo wa 4
Uadilifu wa maswahaba final edit.qxd
7/15/2011
12:34 PM
Page 5
Uadilifu wa Masahaba kwa mtazamo wa Ahlul-Bait Qur’ani kisha tutoe maelezo ya Ahlul-baiti na kisha tuonyeshe dalili za nadharia hii na kuzijadili kwa maelezo ya Kitabu na Sunna ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kisha tutaashiria sababu zilizopelekea kuanza nadharia hii. MAANA YA USUHUBA KWA MUJIBU WA LUGHA YA KIARABU Al-Raghibu Al-Isfahani amesema: “Sahibu ni mwenye kushikamana na kitu….wala hakuna tofauti kati ya mshikamano wake kuwa kimwili na ndio asili na mara nyingi, au kimsaada na kujali. Mmiliki wa kitu huambiwa: Yeye ni mwenye kushikamana nacho, pia ndivyo huambiwa mwenye matumizi nacho. Na neno usahibu na usuhuba ni fasaha mno kuliko neno ujamaa, kwa sababu usuhuba unahitaji kuishi naye muda mrefu hivyo kila usuhuba ni ujamaa na wala si kila ujamaa ni usuhuba.”1 Ndani ya Qur’ani kumepatikana maneno yanayounga mkono maana hii ambayo imetajwa na kamusi za lugha ya Kiarabu. Maana hiyo imo ndani ya matamshi mbalimbali, yote yakishirikiana katika maana zinazokaribiana, nazo ni: Kuishi pamoja na mshikamano upatikanao kwa ujamaa, kukutana na kuishi pamoja bila kujali muungano wa imani au wa mwenendo. Hivyo Qur’ani imetumia neno hili (usuhuba) katika maisha ya pamoja tu. Na anayefuatilia maneno: “Unifanye sahibu” “Kaa nao kwa wema” “Sahibu wake” “Na mke wake” “Na watu wa” “Na maswahibu wao” atayakuta yamerudiwa mara tisini na saba ndani ya Qur’ani tukufu kwa maana hii hii isiyo na mipaka. Hivyo hakuna tofauti kati ya maana ya kilugha ambayo imetajwa na watu wa lugha na maana ya usuhuba iliyomo ndani ya Qur’ani tukufu. 1. Mufradati Al-Fadhil-Qur’ani Al-Karimi cha Al-Raghibi Al-Isfahaniy: 275. 5
Uadilifu wa maswahaba final edit.qxd
7/15/2011
12:34 PM
Page 6
Uadilifu wa Masahaba kwa mtazamo wa Ahlul-Bait Sunna tukufu imetumia tamko sahaba juu ya kila aliyesuhubiana na Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) miongoni mwa waislamu, sawa awe amemwamini kweli kiundani au kimuonekano tu, hivyo matamshi ya riwaya tutakazozitaja kuhusu sahaba yakawa yanamjumuisha Muislamu muumini wa kweli na Muislamu mnafiki. Na pindi Umar bin Al-Khattab alipomuomba Mtume (s.a.w.w.) ruhusa amuuwe Abdallah bin Ubayy ibnu Abi Saluli - aliyekuwa mnafiki mashuhuri - Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Ewe Umar, itakuwaje pindi watu watakapoanza kuzungumza kuwa Muhammad anawaua sahaba zake?2 Na pindi Abdallah bin Abdallah bin Ubayy alipomuomba ruhusa Mtume (s.a.w.w.) amuuwe mzazi wake, Mtume alimjibu: “Bali tunamhurumia na kusuhubiana naye kwa wema madamu yuko nasi.”3 Muhtasari wa maneno ni kuwa: Sunna imetumia tamko ‘Sahaba’ ili limjumuishe hata yule aliyekuwa mashuhuri kwa unafiki wake, kama vile Abdallah bin Ubayy ibnu Abi Saluli, ukiachia mbali kutumia tamko sahaba kwa wale ambao unafiki wao umejificha, kwani Mtume amesema: “Hakika miongoni mwa sahaba wangu kuna wanafiki.”4 MASAHABA WAUMINI WA KWELI Hakika maswahaba wa Mtume waliokuwa waumini wa kweli ni wale waislamu wa mwanzo ambao walimwona Mtume na wakapata sharafu kwa usuhuba bora, wakabeba jukumu muhimu katika kueneza wito wa Uislamu, kama pia wachache miongoni mwao walivyojitolea nafsi na mali 2. As-Siratun-Nabawiyah cha Ibnu Hisham: 3:303, na As-Siratu An-Nabawiya cha Ibnu Kathir; 3:299, na As’babun-Nuzuli cha Al-Wahidiyu: 452. 3. As-Siratu Al-Nabawiyah cha Ibnu Hisham 3:2-5, na As-Siratun-Nabawiya cha Ibnu Kathir 3:301. 4. Musnad Ahmad 5:40, na Tafsiril-Qur’ani Al-Adhimi cha Ibnu Kathir 2:399. 6
Uadilifu wa maswahaba final edit.qxd
7/15/2011
12:34 PM
Page 7
Uadilifu wa Masahaba kwa mtazamo wa Ahlul-Bait zao kwa ajili ya imani yao kwa Mtume na utume wake mpaka Uislamu ukaenea dunia nzima na laiti kama si jasho la panga zao, nguvu za miundi yao na subira zao basi Uislamu usingesimama hata nguzo moja. Anayefuatilia Qur’ani na Sunna tukufu atakuta zinawapa hadhi sahaba waumini wa kweli kwa kuwasifu na kuwakirimu. Mwenyezi Mungu anasema: “Muhammad Mtume wa Mwenyezi Mungu, na walio pamoja naye ni imara mbele ya makafiri na wenye kuhurumiana wao kwa wao, utawaona wakiinama na wakisujudu wakitafuta fadhila za Mwenyezi Mungu na radhi yake. Alama zao ni katika nyuso zao kwa athari ya kusujudu, huo ndio mfano wao katika Taurati na mfano wao katika Injili. Kama mmea uliotoa matawi yake kisha yakautia nguvu ukawa mnene ukasimama sawasawa juu ya shina lake ukawafurahisha walioupanda ili awakasirishe makafiri. Kwa ajili yake Mwenyezi Mungu amewaahidi walioamini na kutenda mema katika wao msamaha na malipo makubwa.”5 Na hao ndio wale waliomnusuru Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na wakahuisha dini yake wakasimamisha nguzo za dola ya kiislamu na kutokomeza ujahiliya. Na kuna Aya nyingi zinazowasifu maswahaba kwa kuwapa sifa kubwa mno, hivyo anayesoma Aya zilizoteremka kuwasifu Muhajirina na Ansari na wale waliowafuata kwa wema basi hutamani nafasi yao na cheo chao cha juu. Na anayesikia Aya zilizoteremka kuhusu haki ya sahaba ambao walimpa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) kiapo cha utii chini ya mti basi moyo wake husisimka kwa kulitamani hilo kundi dogo lenye imani ambalo lilitekeleza yale liliyomuahidi Mwenyezi Mungu.
5. Al-Fat’hu:29 7
Uadilifu wa maswahaba final edit.qxd
7/15/2011
12:34 PM
Page 8
Uadilifu wa Masahaba kwa mtazamo wa Ahlul-Bait
Imamu Ali awasifu Masahaba waumini wa kweli Amesema (a.s.): “Hakika tulikuwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) tukiwaua baba zetu, watoto zetu, ndugu zetu na ami zetu na hilo halituzidishii chochote isipokuwa imani, kujisalimisha, kupita katika njia bora, subira dhidi ya maumivu ya uchungu na juhudi katika jihadi dhidi ya adui. Hivyo Mwenyezi Mungu alipoona ukweli wetu alimteremshia udhalili adui yetu na akateremsha ushindi juu yetu mpaka Uislamu ukatulia huku ukiimarika na miji yake ikikalika. Naapa, laiti kama tungekuwa tunaleta mliyoyaleta basi isingesimama nguzo yoyote ya dini wala lisingechanua tawi lolote la imani.”6 Pia (a.s.) akawasifu na kuukumbuka ukubwa wa nafasi zao huku akihuzunika kwa kuwakosa, akasema: “Hakika niliwaona sahaba wa Mtume (s.a.w.w.) na sioni yeyote miongoni mwenu anayefanana nao. Hakika walikuwa wakiamka kama mtawanyiko wa vumbi huku wakiwa wamekesha katika hali ya kusujudu na kusimama wakijishughulisha kati ya vipaji vya nyuso zao na mashavu yao na wakisimama juu ya mfano wa moto kutokana na kukumbuka marejeo yao.”7 Na (a.s.) akasema huku akiwa anaumia kutokana na kuwa na shauku nao: “Wako wapi ndugu zangu ambao waliipanda njia na wakapita juu ya haki? Yuko wapi Ammar? Yuko wapi mwana wa At-Tayhani? Yuko wapi mwenye shahada mbili? Wako wapi mfano wao miongoni mwa ndugu zao ambao waliisoma Qur’ani na kuifahamu vilivyo, wakazingatia faradhi na wakazisimamisha, wakahuisha Sunna tukufu na wakaangamiza bidaa, wakaitwa kwenye jihadi wakaenda na wakamwamini kiongozi na kumfuata.”8 6. Nahjul-Balagha; uhakiki wa Subuhiy-swalih: 91-92. 7. Nahjul-Balagha; uhakiki wa Subuhiy-swalih: 97-143 8. Nahjul-Balagha; uhakiki wa Subuhiy-swailh: 182-264. 8
Uadilifu wa maswahaba final edit.qxd
7/15/2011
12:34 PM
Page 9
Uadilifu wa Masahaba kwa mtazamo wa Ahlul-Bait
Imam Ali
Bin Husein (a.s.) awaombea kheri masahaba waumini wa kweli
Imamu Zainul-Abidin amewaombea maswahaba wa Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Ewe Mwenyezi Mungu! Ee Mola na maswahaba wa Muhammad hasa, ambao waliandamana naye kwa wema na ambao walipigana kishujaa katika kumnusuru, wakamsaidia na kuharakisha katika kuunga mkono ujumbe wake na kuitikia mwito wake, waliomwitikia mara tu alipowasikilizisha hoja za ujumbe wake, wakajitenga na wake zao na watoto wao katika kulidhihirisha neno lake, wakapigana na baba zao na watoto wao katika kuthibitisha utume wake na wakanusurika kwaye….”9 Abdallah bin Abbas awasifu masahaba waumini wa kweli Siku moja Muawiya alimuuliza Ibnu Abbas kuhusu baadhi ya mambo, akamuuliza kuhusu maswahaba na Ibnu Abbas akasema: “Walisimamisha mafunzo ya dini na kunasihi juhudi kwa waislamu mpaka zikastaarabika njia zake na kuimarika nguzo zake huku zikidhihirika neema za Mwenyezi Mungu, ikatulia dini yake na minara yake ikawa wazi. Kupitia wao akauangusha ushirikina na kuwang’oa viongozi wake na kuyafutilia mbali mafunzo yake na neno la Mwenyezi Mungu likawa ndilo la juu na neno la waliokufuru likawa chini.”10 Nadharia ya uadilifu wa kila sahaba Wamesema: “Bila shaka sahaba ni kila aliyekutana na Mtume (s.a.w.w.) angalau muda mfupi na kumwamini na akafa katika Uislamu, hivyo maswahaba wote ni waadilifu, haiwapati dosari, na atakayemtia dosari yeyote miongoni mwao basi yeye ni mzandiki.11 9. Sahifatu Sajadiyya cha Imam As-Sajjad Ali bin Husein…Bado wafuasi wa Ahlul-baiti wanasoma du’a zake nyakati za maombi. 10. Muruju Dhahabi Lil-Mas’udi 3:66, 425, 426. 11. Al-Iswabatu fi tamyizis-Swahabata cha Al-Asqalaniy 1:11. 9
Uadilifu wa maswahaba final edit.qxd
7/15/2011
12:34 PM
Page 10
Uadilifu wa Masahaba kwa mtazamo wa Ahlul-Bait Nadharia hii inalazimu kusihi kila anachopokea kila sahaba na wala hairuhusu kumtia dosari sahaba yeyote. Masunni wameafikiana kuwa maswahaba wote ni waadilifu na hakuna aliyepinga nadharia hii miongoni mwao ila wachache, Al-Khatibu ndani ya Al-Kifaya amesema: “Wao wote ni bora kuliko wote waliokhalifu baada yao na walio sawa ambao wanakuja baada yao.” Abu Muhammad bin Hazmi amesema: “Maswahaba wote wataingia peponi bila shaka, na wala haingii motoni yeyote miongoni mwao kwa sababu wao wametajwa na kauli ya Mwenyezi Mungu: “Hakika ambao wema toka kwetu umetangulia kwa ajili yao hao wametengwa nao (moto).”12 Nadharia hii inaona kuwa wote ni watu wa tabaka la kwanza kuanzia Bani Umayya mfano wa Abu Sufiyani na wanawe na wana wote wa Marwan na hata yule aliyefukuzwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu na watoto wake, wote ni maswahaba waadilifu. Dalili za nadharia ya uadilifu wa kila sahaba Kwanza: Makada wa nadharia hii wametoa dalili kutumia baadhi ya Aya na miongoni mwazo ni kauli ya Mwenyezi Mungu: “Ninyi ni kundi bora mliotolewa kwa ajili ya watu.”13 Na kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na hivyo tumekufanyeni umma bora.”14 Na kauli ya Mwenyezi Mungu: “Kwa hakika Mwenyezi Mungu amewapa radhi waumini walipofungamana nawe chini ya mti na alijua yaliyomo nyoyoni mwao.”15 12. Al-Iswabatu fi tamyizis-Swahabata cha Al-Asqalaniy 1:10. Na Al-Jarhu wa Taadili cha Ar-Razi: 7-9. 13. Aali-Imrani:110. 14. Al-Baqara:143. 15. Al-Fat’hu:18.
10
Uadilifu wa maswahaba final edit.qxd
7/15/2011
12:34 PM
Page 11
Uadilifu wa Masahaba kwa mtazamo wa Ahlul-Bait Na kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na wale waliotangulia wakawa wa kwanza katika Muhajirina na Ansari na wale waliowafuata kwa mwendo mzuri, Mwenyezi Mungu amewaridhia nao wamemridhia.”16 Pili: Wametoa dalili kutumia Sunna tukufu ya Mtume (s.a.w.w.), kwani maelezo mengi yanafidisha uadilifu wa kila sahaba, wala hadithi hazijamvua yeyote miongoni mwao. Imepokewa toka kwa Mtume (s.a.w.w.) kuwa amesema: “Maswahaba zangu ni kama nyota, yeyote mtakayemfuata mtaongoka.” “Karne bora ni karne yangu, kisha watakaowafuatia, kisha watakaofata.” “Nilindieni heshima kwa maswahaba zangu.” “Msiwatusi maswahaba zangu.”17.
UCHUNGUZI JUU YA NADHARIA YA UADILIFU WA MASAHABA a: Msimamo wa Qur’ani juu ya uadilifu wa kila sahaba Tunasisitiza kuwa lile linalojengwa na nadharia ya uadilifu wa kila sahaba halikubaliani na semi za Qur’ani tukufu, kwa sababu ndani ya Qur’ani maswahaba wapo katika makundi tofauti, na hivyo haiwezekani kuwafanya kundi moja, nalo ni wawe wote waadilifu, ni kwa sababu miongoni mwao wamo waliotangulia wakawa wa kwanza, na wamo waliofungamana naye chini ya mti na Muhajirina na watu wa ushindi. 16. Al-Isaba fi Tamyizis-Sahaba cha Al-Asqalani: 9-10, na Tafsiril-Qur’anil-Adhimu cha Ibnu Kathir 1:399, na Durul-Manthuri cha As-Suyutiy 2:293. 17. Sunnani Tirmidhiy: hadith ya 2302, 2303, Fat’hul-Bari cha Ibnu Hajar 7:6 na 13: 21, It’haful-Sadati al-Mut’qinu cha Az-Zabidiy 2: 223, Talkhisil-Habiri cha Ibnu Hajar 4:204, Al-Bidayatu wan-Nihaya cha Ibnu Kathir 7: 493, Tarikh Baghdadi cha Al-Khatibu AlBaghdadiy 2:53.
11
Uadilifu wa maswahaba final edit.qxd
7/15/2011
12:34 PM
Page 12
Uadilifu wa Masahaba kwa mtazamo wa Ahlul-Bait Kama pia Qur’ani inavyotaja aina nyingine mukabala na hao, mfano wanafiki,18 na wanafiki waliyojificha ambao Mtume hawafahamu,19 madhaifu wa imani na wenye magonjwa ya moyo,20 na wanaowasikiliza wafitini,21 waliochanganya matendo mema na mengine maovu,22 wanaokaribia kuritadi pale mambo yanapokuwa magumu,23 mafasiki ambao vitendo vyao havioani na kauli zao,24 waislamu ambao imani bado haijaingia ndani ya nyoyo zao,25 ambao wanadhihirisha Uislamu na kutiwa nguvu kwa kupewa fungu la sadaka kutokana na udhaifu wa yakini yao,26 na wenye kukimbia vitani mbele ya makafiri.27 Hivyo hawa maswahaba japo wametofautiana na kupishana misimamo lakini Qur’ani imewachukulia kama maswahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na kuna mifano halisi ya baadhi ya maswahaba ambao Qur’ani imeteremka kuwakemea na kuashiria uovu wao na kuwa wao ni watu wa motoni na miongoni mwao wamo waliomzushia uongo Mwenyezi Mungu na kujaribu kupindisha Qur’ani. Na miongoni mwa Aya hizo ni: “Je, muumini anaweza kuwa sawa na yule aliye muovu? Hawawi sawa. Ama wale walioamini na wakafanya vitendo vizuri, basi watakuwa nazo bustani za makazi ndio mafikio kwa waliyokuwa wakiyatenda. Lakini wale waliyofanya uovu basi makazi yao ni 18. Al-Munafiquna: 10.
19. At-Tawba: 101. 20. Al-Ahzab: 11. 21. At-Tawba: 45-47. 22. At- Tawba: 102. 23. Ali-Imrani: 154. 24. Al-Hujirati: 6 na Al-Sajdatu: 18 25. Al-Hujirati:14. 26. At- Tawba: 60. 27. Al-Anfalu:15-16. 12
Uadilifu wa maswahaba final edit.qxd
7/15/2011
12:34 PM
Page 13
Uadilifu wa Masahaba kwa mtazamo wa Ahlul-Bait motoni, watakapotaka kutoka humo watarudishwa humo na wataambiwa onjeni adhabu ya moto ambayo mlikuwa mkikadhibisha.”28 Tunaporejea tafsiri na vitabu vya historia tunakuta kuwa Aya zinaashiria kuwa muumini hapa ni Ali bin Abi Talib, na muovu hapa ni Al-Walidi bin Aqaba, na yeye alikuwa gavana wa Uthman huko Kufa, na gavana wa Muawiya na mwanaye Yazidi huko Madina.29 “Na ni nani dhalimu mkubwa kuliko yule amzuliaye uongo Mwenyezi Mungu au mwenye kusema: Nimefunuliwa wahyi na hali hakufunuliwa chochote….”30 Aya hii ilishuka ikimuhusu Abdallah bin Abu Sarhu, na yeye alikuwa ni gavana wa Uthman huko Misri, kwani yeye ndiye aliyemzushia Mwenyezi Mungu uongo, na Mtume akahalalisha damu yake hata kama atakumbatia Al-Kaaba. Na siku ya ukombozi wa Makka, Uthman alikwenda naye akimuombea amani na alipokuwa hakuuwawa ndipo alipompa amani, 28. Al-Sajdatu:18-20. 29. Shawahidut-Tanzili cha Al-Hakim Al-Haskaniy Al-Hanafiy hadith ya 445 na 453. Na angalia kitabu: Aliyyu bin Abi Talib cha Ibnu Al-Maghaziliy As-Shafiiy: hadith ya 324 na 370 na 371, na Tafsiri Tabariy 21:107, Al-Kashaf cha Zamakhshariy 3:514, Fat’hul-Qadir cha As-Shaukaniy: 200, Asbabun-Nuzuli cha As-Suyutiy kilichochapwa pembezoni mwa Tafsirul-Jalalayni: 550, Ah’kamul-Qur’ani cha Ibnu Arabiy 3:1489. Na rejea kitabu: Sharhu Nahjul-Balagha cha Ibn Abil-Hadid 4:80 na 6:292. Na rejea kitabu: Kifayatu-Talibi cha Al-Kanjiy As-Shafiiy: 140, Ad-Durul-Manthuri cha As-Suyutiy 5:178, DhakhairulUq’ba cha At-Tabariy As-Shafiiy: 88, Al-Manaqib cha Al-Khawarazimiy Al-Hanafiy: 197, Nadh’mu Durari simtiini cha Az-Zarandiy Al-Hanafiy 92, Tadh’kiratul-Khawasiy cha Sibt Al-Jawziy Al-Hanafiy: 207, Matalib Al-suuli cha Ibnu Tal’fatu Al-Hambaliy 6:340, Ansabul-Ash’raf cha Al-Baladhariy 2:148, hadith ya 150, Tafsir Al-Khazinu 3:470 na 5:187, Maalimu Tanzili cha Al-Baghawiy As-Shafiiy pembezoni mwa Al-Khazinu 5:187, SiratulHalabiyya cha Al-Hal’biyi As-Shafiiy 2:85, Takhri Al-Kashafu cha Ibnu Hajari AlAsqalaniy kilichochapwa mwishoni mwa Al-Kashafu 3:514, Al-Intisafu fi ma tudhaminuhu Al-Kashaf mwishoni mwa Al-Kashaf, 3:244. 30. Al-An’am: 93
13
Uadilifu wa maswahaba final edit.qxd
7/15/2011
12:34 PM
Page 14
Uadilifu wa Masahaba kwa mtazamo wa Ahlul-Bait hivyo yeye ndiye aliyejaribu kupotosha Kitabu na ndiye kiumbe dhalimu mno.31 “Enyi mlioamini, mmekuwaje mnapoambiwa: Nendeni kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu mnajitia uzito katika ardhi? Je mmekuwa radhi na maisha ya dunia kuliko ya akhera? Lakini starehe za maisha ya dunia kwa akhera ni kidogo. Mkikosa kwenda atakuadhibuni kwa adhabu iumizayo na atawaleta watu wengine badala yenu, wala hamtamdhuru chochote, na Mwenyezi Mungu ni Muweza juu ya kila kitu.”32 Aya hii pia imetamka wazi kuwa kuna baadhi ya maswahaba walijitia uzito kwenda kwenye jihadi wakachagua kukimbilia maisha ya dunia huku wakijua kuwa ni starehe ya muda tu, mpaka wakawajibika kukemewa na Mwenyezi Mungu na kutishwa kwa adhabu iumizayo na kuwabadili wao kwa kuleta waumini wa kweli. Kama vilivyo vitisho vya kubadili katika Aya nyingine, kitendo kinachoonyesha wazi kuwa ni mara nyingi walijitia uzito dhidi ya jihadi. Mwenyezi Mungu amesema: “Na kama mkirudi nyuma basi Mwenyezi Mungu ataleta watu wengine badala yenu, nao hawatakuwa mfano wenu.”33 Aya hii na mfano wake zinaashiria msimamo wa makosa ambao waliuchukua baadhi ya maswahaba na wakastahili kemeo kutokana na msimamo huo. Pia zinatilia mkazo kushindwa kuoana nadharia ya uadilifu wa kila sahaba na kile kinachofahamika toka ndani ya Qur’ani kwa mujibu wa aya zilizoteremka na suala hili. 31. Siratul-Halabiyya 3:81 mlango wa ukombozi wa Makka, Al-Jamiu liah’kamil-Qur’ani cha Al-Qur’tubiy 7:39, Al-Kamilu fi Tarikh cha Ibnu Athiri 2: 249 ukombozi wa Makka.
32. At-Tawba: 38-39 33. Muhammad: 38 14
Uadilifu wa maswahaba final edit.qxd
7/15/2011
12:35 PM
Page 15
Uadilifu wa Masahaba kwa mtazamo wa Ahlul-Bait b: Msimamo wa Sunna Tukufu juu ya Uadilifu wa kila Sahaba Tutakapoiuliza Sunna tukufu juu ya ufahamu wake wa sahaba tutakuta yenyewe inaweka wazi kwa kutumia neno hili sahaba juu ya mkweli na asiye mkweli miongoni mwao. Zimekuja riwaya mbalimbali zikiwasifu kwa uzuri na wakati huo huo zimekuja nyingine zikiwatuhumu baadhi yao. Miongoni mwa riwaya zinazowasifu kwa mazuri ni kauli ya (s.a.w.w.): “Ewe Mwenyezi Mungu endeleza uhamaji wao kwa maswahaba zangu na wala usiwarudishe nyuma kwa visigino vyao.”34 Na kauli yake (s.a.w.w.): “Ewe Mwenyezi Mungu iwapo leo litahiliki kundi hili basi hutoabudiwa.” Na kauli yake (s.a.w.w.): “Aliye imara mno kwenye njia ni yule mwenye mapenzi mno kwa kizazi changu na maswahaba zangu.”35 Ama riwaya zinazowalaumu ni: “Msinizushie uongo, kwa hakika yule atakayenizushia uongo basi ataingia motoni.”36 Akasema (s.a.w.w.): “Mimi sihofii juu yenu kuja kumshirikisha Mwenyezi Mungu baada yangu lakini nahofia juu yenu dunia; kwani mtaigombania na kuuwa kisha mtaangamia kama walivyoangamia waliyokuwepo kabla yenu.”37 Akasema (s.a.w.w.): “Bila shaka mimi nitawatangulieni kwenye hodhi, na nitawaona watu (wakipelekwa motoni) na kuwafahamu kisha nitasema: Ewe Mola Wangu! maswahaba zangu, maswahaba zangu, nitaambiwa: 34. Sahihi Bukhari; 5:87-88. 35. As-Siratun-Nabawiyya cha Ibnu Hisham 2:279. 36. Sahih Bukhar 1:38 na Sahih Muslim 1:9. 37. Sahih Muslim 7:68 kitabu cha ubora, mlango wa kuthibitisha hodhi na sifa za Mtume wetu {s.a.w.w.}, As-Sunanil-Kubra cha Al-Bayhaqiy 4:14 mlango wa kutaja riwaya. 15
Uadilifu wa maswahaba final edit.qxd
7/15/2011
12:35 PM
Page 16
Uadilifu wa Masahaba kwa mtazamo wa Ahlul-Bait Bila shaka wewe hujui waliyoyazua baada yako.”38 Hivyo miongoni mwa maswahaba wapo wanaomzulia Mtume uongo na wapo waliokuwa wakimwaga damu kwa ajili ya dunia na wapo walioritadi baada ya kifo cha Mtume wa Mwenyezi Mungu, basi itawezekanaje hawa wote wawe waadilifu? Pia ilihali Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amewahabarisha maswahaba zake kuwa wao watapupia utawala, akasema: “Hakika ninyi mtapupia utawala kisha siku ya Kiyama mtapata majuto na majonzi, basi ni muovu mno mnyonyeshaji ziwa na ni mwema mno muachishaji ziwa.”39 Na hivyo ndivyo ilivyokuwa. Amesema kweli Mtume wa Mwenyezi Mungu. Hali halisi ni kuwa matokeo ya nadharia hii ni kuhalalisha vitendo na mambo yanayokhalifu amri za Mwenyezi Mungu yaliyotendwa na baadhi ya maswahaba. Nadharia hii iliwafanya watu waovu waliochukua utawala baadae wawe kama waaminifu wa kweli ambao sheria za Mwenyezi Mungu huchukuliwa kupitia kwao, na utawala wao ukakubalika japo baadhi yao walimwaga damu kwa dhuluma au kunywa pombe au kula mali za waislamu. Zaidi ya hapo ni kuwa riwaya walizotumia kuthibitisha nadharia ya uadilifu wa maswahaba, nyingi ni dhaifu upande wa njia ya upokezi, kwa mfano riwaya ya “Maswahaba zangu ni kama nyota…”40 ni dhaifu upande wa njia yake ya upokezi. Al-Isfahaniy na Abu Hayana Al-Undulusiy na mwanafunzi wake TajudDin wote wameona riwaya hii kuwa ni ya kuzushwa. 38. Musnad Ahmad 2:35. 39. Musnad Ahmad 3:199. 40. Mizanul-Itidali cha Ad-Dhahabiy 1:413. 16
Uadilifu wa maswahaba final edit.qxd
7/15/2011
12:35 PM
Page 17
Uadilifu wa Masahaba kwa mtazamo wa Ahlul-Bait Ama riwaya isemayo: “Hakika Mwenyezi Mungu kaniteua mimi na akateua maswahaba zangu, basi akawafanya wakwe zangu na akawafanya wasaidizi wangu na watakuja watu mwisho wa zama na kuwatia dosari. Basi msiwaozeshe na wala msiowe kwao, basi msiunge nao undugu wala msiunge undugu juu yao, laana imekaa juu yao.”41 Katika njia yake ya upokezi yumo Bashir bin Ubaydullah na yeye ni mtu asiyejulikana. Bali Ibnu Habani amesema: “Hadithi hii ni batili haina asili.”42 Dr. Atwiyya ibnu Atiqi Az-Zahraniy amesema: “Hadithi hii haisihi.”43 Ama riwaya isemayo: “Karne bora ni karne yangu,” nayo haijatimia upande wa njia yake ya upokezi kama walivyothibitisha hilo wasomi wengi akiwemo mwandishi wa Al-Kifaya44. Ama maana yake ya kuwa kila kilichotokea karne aliyotumwa Mtume ni haki na sahihi na kinakubalika hata kama kinavunja heshima ya Uislamu, mfano kumuuwa kiongozi wa waumini Ali bin Abu Talib, au kuwaua wajukuu wawili wa Mtume Hasan na Husein au kuwafanya mateka watu wa nyumba ya Mtume kama ilivyotokea kwenye tukio la mauwaji ya Karbala lenye kuumiza, au kuruhusu uovu kwenye mji wa Mtume Madina kama ilivyotokea kwenye tukio la uvamizi wa Madina, tukio ambalo zilivunjwa heshima za waislamu, yakapasuliwa matumbo ya waja wazito na kuuawa maswahaba na tabiina wema,45 hakika maana hiyo hairidhii mwenye akili sembuse msomi. Itakuwaje isihi kunasibisha hayo kwa Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu?!
41. Sahih Muslim 4:1873, na Sunnan Tirmidhiy 5:662, na Musnad ya Ahmad 3:14. 42. Mukhalafatus-Sahabiy Lil-hadithin-Nabawiy cha Abdil-Karimi An-Namla: 83 43. As-Sunnat cha Abu Bakr Al-Khilali 1:483. 44. Al-Kifayatu fi ilmid-Diraya: 47. 45. Tarikh Yaaqubiy 2:250, na Al-Kamilu fi Tarikhi cha Ibnu Athir 4:111-119, na Taajilil-man’faatu cha Al-Asqalaniy: 453 wasifu wa Yazidi bin Muawiya. 17
Uadilifu wa maswahaba final edit.qxd
7/15/2011
12:35 PM
Page 18
Uadilifu wa Masahaba kwa mtazamo wa Ahlul-Bait C: Msimamo wa Historia juu ya Uadilifu wa kila Sahaba Historia imethibitisha uendaji kinyume na uhalifu ambao ulitendwa na baadhi ya maswahaba dhidi ya amri za Mwenyezi Mungu na Mtume Wake kipindi cha uhai wake hadi baada ya kifo chake. Kwa mfano, tunakuta baadhi yao wamekimbia kwenye vita vya Uhud, wakashindwa kuinuka kwenye (vita vya) Handaki na wakamkhalifu Mtume wa Mwenyezi Mungu. Pia tunawakuta wengi miongoni mwa Muhajirina na Ansari wamekhalifu amri ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) ya kuelekea kwenye vita dhidi ya Roma chini ya uongozi wa Usama bin Zayd.46 Wanahistoria wametaja matukio ya kuhuzunisha yaliyotokea baada ya kifo cha Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) yakitendwa na baadhi ya maswahaba ambao baadae walikuwa viongozi wa waumini. Kuanzia pale walipowabeba watu kwa nguvu, vitisho na kipigo na kuvamia nyumba ya bi. Fatima (a.s.) binti wa Mtume ili aende kutoa kiapo cha utii na kuishia kumnyang’anya haki yake ya zawadi na urithi na fungu lake la jamaa wa karibu mpaka akafariki akiwa amewaghadhibikia. Pia kumtoa na kumfukuza Abu Dharr kutoka mji wa Mtume wa Mwenyezi Mungu na kumpeleka Ar-Rabadha. Pia kumpiga Ammar bin Yasir, kumpiga Abdallah bin Mas’udi mpaka kumvunja mbavu zake. Na kuwavua vyeo maswahaba wema na kuwavisha vyeo watawala waovu. Kumtukana kiongozi wa waumini Ali bin Abu Talib na kutoka kwenda kumpiga vita kwenye vita vya Jamal, Siffin na Nahrwan.
46. Al-Kamilu fi Tarikh cha Ibnu Athir 3:317. 18
Uadilifu wa maswahaba final edit.qxd
7/15/2011
12:35 PM
Page 19
Uadilifu wa Masahaba kwa mtazamo wa Ahlul-Bait Pia kumuua bwana wa vijana wa peponi Imam Husein na yaliyotokea kwenye tukio la uvamizi wa Madina kiasi kwamba idadi ya watu waliouawa kwenye tukio hilo ikafika elfu kumi, wakiwemo maswahaba themanini. Na katika tukio hili ndipo walipofariki maswahaba wote waliopigana vita vya Badri, hivyo baada yake hakubaki mpiganaji yeyote wa vita vya Badri47 ILI KUKAMILISHA UTAFITI, TAZAMA BAADHI YA MIFANO: Mtu mmoja alikuwa akimwandikia Mtume (s.a.w.w.) na alikuwa ameshawahi kusoma Suratil Baqara na Aali-Imran, basi Mtume akawa akimsomea: ‘Ghafuuran rahiimaa’ yeye anaandika ‘a’liiman hakiimaa’. Mtume akamwambia: Andika hili na hili. Akasema: Naandika nitakavyo. Akawa anamsomea: ‘a’liiman hakiimaa’ yeye anaandika: ‘samiia’n baswiiiraa.’ Huku akisema: “Mimi namjua mno Muhammad kuliko ninyi.” Basi alipofariki mtu yule, Mtume akasema: “Ardhi haitomkubali.” Anas amesema: “Abu Talha amenisimulia kuwa alikwenda kwenye ardhi ya eneo alilofia mtu huyo na akamkuta ametelekezwa, Abu Talha akasema: “Vipi mtu huyu?” Wakasema: “Tumemzika mara nyingi lakini ardhi haimkubali.” Ibnu Athir amesema: “Riwaya hii ni sahihi kwa kanuni za mashekhe wawili (Bukhari na Muslim) lakini hawajaitoa.48 Huyu hapa mwingine, Al-Walid bin Aqaba bin Abu Muitu ambaye aliitwa fasiki na Mwenyezi Mungu pale alipotumwa na Mtume (s.a.w.w.) kuhusu sadaka za Bani Al-Mustalaq akarudi na kumwambia Mtume kuwa wao wametoka kuja kumvamia kivita, hivyo Mtume akataka kuwaandalia jeshi na ndipo Mwenyezi Mungu akateremsha : “Enyi mlioamini, kama fasiki 47. Al-Imamatu Wasiyasatu cha Ibnu Qutaybatu Al-Daynuriy 1:215-216, na AlMuntadhamu cha Ibnu Al-Jawziy 6:16. 48. Tarikh ibnu Kathir 6:170. 19
Uadilifu wa maswahaba final edit.qxd
7/15/2011
12:35 PM
Page 20
Uadilifu wa Masahaba kwa mtazamo wa Ahlul-Bait akikujieni na habari yoyote basi pelelezeni, msije mkawadhuru watu kwa ujahili….” Huyu alikuwa miongoni mwa maswahaba hivyo uko wapi uadilifu toka kwa mtu fasiki?49 Huyu hapa Al-Jaddu bin Qays mmoja wa Bani Salama, kwa ajili yake iliteremka Aya: “Na miongoni mwao yuko anayesema: ‘Niruhusu wala usinitie katika fitna.’ Hakika wameanguka katika fitna na Jahanamu ndiyo iwazungukayo makafiri.”50 Huu hapa msikiti wa udhia na kufuru. Ni upi huo msikiti wa udhia? Ulijengwa na kundi la watu wenye alama za uswahaba wakijionyesha humo kwa kutekeleza Swala nyakati ambazo hawawezi kufika kwa Mtume (s.a.w.w.), lakini Mwenyezi Mungu alifichua siri yao na jambo lao likabainika na kuwa wao ni wanafiki. Mwenyezi Mungu akawateremshia: “Na wale waliojenga msikiti wa udhia na kufuru na kuwafarakisha waumini na kuufanya mahala pa kuvizia kwa waliompiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume wake zamani. Na bila shaka wataapa: ‘Hatukukusudia ila wema,’ na Mwenyezi Mungu anashuhudia kwamba wao ni waongo.”51 Walikuwa ni wanafiki wanaume kumi na wawili, miongoni mwao ni Khadhamu bin Khalid bin Ubayd na eneo la nyumba yake ndipo ulipopatikana msikiti. Na Muatabu bin Qushairi na Abu Habiba bin Abi AlAza’ru na wengineo.52 Huyu hapa Tha’laba bin Hatibu bin Umar bin Umayya ambaye ni miongoni mwa watu waliyoshuhudia vita vya Badr na Uhud, alizuwia Zaka ya mali yake ndipo Mwenyezi Mungu akateremsha: “Na miongoni mwao wako waliomwahidi Mwenyezi Mungu; akitupa katika fadhila Zake 49. Tafsir ibn Kathir 4:212. 50. Siratu ibnu Hishamu 2:332. 51. At-Tawba: 108. 52. Siratu ibnu Hishamu 1:341. Na Tafsir ibnu Kathir 2:388. 20
Uadilifu wa maswahaba final edit.qxd
7/15/2011
12:35 PM
Page 21
Uadilifu wa Masahaba kwa mtazamo wa Ahlul-Bait lazima tutatoa sadaka na bila shaka tutakuwa miongoni mwa watendao mema. Lakini alipowapa katika fadhila Zake wakazifanyia ubahili na wakageuka na huku wakipuuza.”53 Huyu Thaalaba alikuwa sahaba mshika Swala mwenye kutekeleza Swala ndani ya wakati wake na alikuwa ni fukara asiye na kitu, ndipo akamwambia Mtume: ‘Niombee dua kwa Mwenyezi Mungu aniruzuku mali.’ Mtume akamwambia: ‘Ole wako Tha’laba, kichache unachoshukuru ni bora kuliko kingi usichokiweza.’ Tha’laba akasema: ‘Naapa kwa yule aliyekupa unabii kwa haki, iwapo utamuomba Mwenyezi Mungu na akaniruzuku mali basi bila shaka nitampa kila mwenye haki haki yake.’ Hapo Mtume (s.a.w.w.) akasema: ‘Ewe Mwenyezi Mungu mruzuku Thaalaba mali.’ Ndipo mapato yake yalipoongezeka na akakataa kutoa Zaka yake, basi ndipo unafiki ulipompata mpaka siku atakayokutana na yale aliyoshindwa kuyatekeleza na akawa miongoni mwa waongo. Huyu hapa Dhuu Thudayya alikuwa miongoni mwa maswahaba, tena mchaji mwenye kufanya ibada kiasi kwamba kuabudu kwake na juhudi zake vilikuwa vinawastaajabisha watu, lakini Mtume akaamrisha auwawe. Mtume alikuwa akisema: “Hakika yeye ni mtu mwenye doa jeusi usoni mwake toka kwa shetani.” Akamtuma Abu Bakr ili akamuuwe lakini alipomuona anaswali akarejea. Akamtuma Umar naye hakumuuwa, kisha akamtumma Ali lakini hakumkuta.54 Na yeye ndiye aliyekuwa kiongozi wa waasi (Khawariji) na aliuliwa na Imam Ali (a.s.) siku ya Nahrwani. Hawa hapa watu waliopata alama za uswahaba ambao walikuwa wakikusanyika ndani ya nyumba ya Suwaylimu na wakiwazuwia watu dhidi ya 53. Al-Istiab kilichopo pembezoni mwa Al-Iswabati 1:201. 54. Al-Iswabatu fi Tamyizil-Swahabatu cha Al-asqalaniy 1: 429. 21
Uadilifu wa maswahaba final edit.qxd
7/15/2011
12:35 PM
Page 22
Uadilifu wa Masahaba kwa mtazamo wa Ahlul-Bait kumfuata Mtume wa Mwenyezi Mungu basi akaamrishwa yule aliyeichoma moto nyumba ya Suwaylimu.55 Huyu hapa Quzimani bin Al-Harth alishuhudia vita vya Badri na akapigana pamoja na Mtume mapambano makali, basi maswahaba wa Mtume wakasema: “Fulani hakutugawia fungu.” Mtume akasema: “Hakika yeye ni mtu wa motoni.” Na pindi alipopatwa na jeraha na akaanguka chini, aliambiwa: ‘Hongera kwa kupata Pepo ewe Abu Al-Ghaydaqu.’ Akajibu: “Pepo toka kwa Harmala, naapa kwa Mwenyezi Mungu hatukupigana vita isipokuwa ni kwa ajili ya nasaba tu.”56 Huyu hapa Al-Hakam bin Abul-Aas bin Umayya bin Abdu-Shamsi aliyefukuzwa na kulaaniwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu, na yeye ndiye mzazi wa Marwan na ni ami yake Uthman. Al-Faqihiyu amesimulia kwa njia toka kwa Az-Zahriyyu na Atau AlKhurasaniy kuwa maswahaba wa Mtume waliingia kwake wakamkuta akimlaani Al-Hakam ndipo wakamuuliza: “Amefanya nini ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?” Akajibu: “Ameingia kwangu kwa kupasua ukuta ilihali nikiwa na mke wangu fulani.” Siku moja Mtume akapita mbele ya Al-Hakam, basi Al-Hakam akaanza kumnyooshea Mtume kidole, ndipo Mtume akageuka na kumuona kisha akasema: “Ewe Mwenyezi Mungu mgeuze mjusi.” Basi hapo hapo akaanza kutambaa.57 Na ndani ya Hadithi ya Aisha ni kuwa yeye alimwambia Marwan bin Al-Hakam: “Nashuhudia kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu alimlaani baba yako ilihali bado ukiwa kwenye mifupa ya mgongo 55. Siratu ibnu Hisham 1: 332. 56. Al-Iswaba fi Tamyizis-Swahabatu cha Al-Asqalaniy 3:235. 57. Al-Iswaba fi Tamyizis-Swahabatu cha Al-Asqalaniy 1:346. 22
Uadilifu wa maswahaba final edit.qxd
7/15/2011
12:35 PM
Page 23
Uadilifu wa Masahaba kwa mtazamo wa Ahlul-Bait wake.”58 Hayo yote na mengine mengi yanahimiza kuwa miongoni mwa maswahaba wa Mtume wapo waliozama ndani ya vitendo asivyoviridhia Mwenyezi Mungu wala Mtume Wake na miongoni mwao wapo waliokwenda kinyume na Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna tukufu. Na bila shaka kauli ya uadilifu wa maswahaba wote waliomuona Mtume angalau siku moja ni jambo lisilokubaliana na hali halisi ya ujumbe wa Uislamu ambao unahimiza kuwa baadhi ya maswahaba, watoto na wake wa manabii walikuwa hawawaamini wao. Hivyo nadharia ya uadilifu wa maswahaba wote haikubaliani na maelezo ya Qur’ani na Sunna tukufu na historia.59 SABABU ZA KUANZA NADHARIA HII Bani Umayya wamecheza nafasi kubwa katika kuchafua historia na Sunna tukufu, na wao ndio waliotilia mkazo nadharia ya uadilifu wa kila sahaba na kutoa wito wa kutokuwatia dosari ili ukosoaji na utiaji dosari usiwafikie wao kutokana na vitendo vyao vibaya ambavyo walivitenda dhidi ya 58. Al-Imamus- Sadiq wal-Madhahibil-Arbaa cha Asadi Haydari 1:597. 59. Kwa urefu rejea: 1- Tarikh wal-Islami cha Al-Amiliy, 2- Adhuwau ala Sunnatil-Muhammadiyah cha Mahmud Aburiyah, 3- An-Nassu wal-Ijtihadu cha Sharafud-Din, 4- Ihqaqul-Haqi (Al-mul-haqatu) cha Al-Mar’ashiy An-Najafiy, 5Al-Fitnatul-Kubra cha Twaha Husein, 6- Iijazul-Qur’ani cha Rafiiy, 7-Abu Huraira cha Aburiyah, 8- Al-Ahadithul-Maudhuatu: Hadithi as’habi kan’nujumi, 9- Ansabul-Ashiraf Asimaul-munafiqina cha Al-Baladhariy, 10- Taawili Mukhtalafil-hadithi cha Ibnu Qutaybah, 11-Sharhul-Maqaswidi cha Taftazaniy na 12- An-Naswayihi Al-Kafiyah cha Ibnu Aqili. 23
Uadilifu wa maswahaba final edit.qxd
7/15/2011
12:35 PM
Page 24
Uadilifu wa Masahaba kwa mtazamo wa Ahlul-Bait Uislamu, basi wakaenda wakiwapa majina ya kafiri na mzandiki wale waislamu wanaowatia dosari na wakiwatolea fat’wa za kuwaua. Na ilikuwa wanapotaka kumuua mpinzani wa utawala wao basi humtuhumu kuwa anawatusi maswahaba, na maana ya kuwatusi maswahaba ni kule kuwakosoa na kuwatia dosari wao.60 Mafunzo haya yaliboreka zama za utawala wa Bani Umayya kwa sababu nadharia hii inajenga ngome imara kwa utawala wao na kuhalalisha vitendo vyote visivyokuwa vya kisheria. Kutokana na hili ndipo Muawiya alipojichukulia yeye mwenyewe kuwa ni khalifa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu akaona analazimika katika hali kama hii kuweka kigezo cha kisheria kinachompa nguvu na hivyo hoja bora ni nadharia ya uadilifu wa maswahaba wote ambao yeye ni mmoja wao. Baada ya hapo ni kitu gani kitamzuia Muawiya kuwa khalifa wa Mtume na mtawala wa waisilamu maadamu kuna Aya na riwaya nyingi ziashiriazo uadilifu wake?! Nadharia ya uadilifu wa kila sahaba inahalalisha vitendo vyote vya Bani Umayya kuanzia kumuwekea sumu Hasan na kumuua Husein na tukio la uvamizi wa Madina na kuwaua wengi miongoni mwa Muhajirina na Ansari na kumtesa Basri bin Ar’taah, na waliyoyafanya kwa wana wawili wa Ubaydullah bin Abbas. Vitendo hivi vinahalalishwa na nadharia ya uadilifu wa kila swahaba ambayo inasihisha vitendo vya Bani Umayya, kwa sababu pindi sahaba anapoua kwa dhuluma maana yake hawi katenda kosa kwa kuwa yeye ni mwadilifu katika kila kitu, na wala haisihi kwa wengine kumkosoa hata kwa maswahaba wenzake.
60. Tarikh Baghdad cha Al-Khatib Al-Baghdadiy 14:7. 24
Uadilifu wa maswahaba final edit.qxd
7/15/2011
12:35 PM
Page 25
Uadilifu wa Masahaba kwa mtazamo wa Ahlul-Bait
MFUMO WA SHI’A KUHUSU MAANA YA USUHUBA NA SAHABA Miongoni mwa wanaopinga nadharia ya uadilifu wa kila aliye sahaba ni wafuasi wa Ahlul-bait, kwa ajili hiyo ndio maana wakaitwa kuwa ni mazandiki kwa sababu wao wanawatia dosari baadhi ya maswahaba au kuwatuhumu kuwa ni waovu. Imepokewa toka kwa Abu Zur’a kuwa alisema: “Ukimwona mtu anamtia dosari yeyote miongoni mwa maswahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu basi jua yeye ni mzandiki, ni kwa sababu Mtume wa Mwenyezi Mungu ni haki na Qur’ani ni haki na aliyoyaleta ni haki na bila shaka hayo yote tulifikishiwa na maswahaba na hawa (Mashi’a) wanataka kuwatia dosari mashuhuda wetu ili wabatilishe Kitabu na Sunna, hivyo ni bora kuwatia dosari wao na wao ndio mazandiki.61 Yuko wapi huyu mbele ya kauli ya Imam Ali (a.s.): “Hakika haki na batili havijulikani kwa kuwatazama watu lakini ijue haki utamjua mwenye nayo na ijue batili utamjua aliyeileta.”62 Kuanzia hapa ndipo utawakuta Shi’a wana haki ya kutafuta kwa sahaba yeyote yule neno la haki na kulichukua pia hatua ya haki na kusimama juu yake. Ama tuhuma ya kutusi na kuwakashifu maswahaba ambayo wanatupiwa Mashi’a toka kwa wenye chuki dhidi yao haina usahihi wowote. Hakika Shi’a huwaweka waislamu wote katika kipimo kimoja, hawatofautishi kati ya sahaba na aliyekuja baada ya sahaba na ni kwamba uswahaba kama uswahaba wenyewe si ngao itakayomzuia mwenye 61. Al-Iswaba fi Tamyizis-Swahabatu cha Al-Asqalaniy 1: 18. 62. Tarikh Yaaqubi 2: 210. Rejea Nahjul-balagha, hekima fupi fupi 262. BiharulAnwar cha Al-Majlisiy 22: 105 na Jz. 32: 228. 25
Uadilifu wa maswahaba final edit.qxd
7/15/2011
12:35 PM
Page 26
Uadilifu wa Masahaba kwa mtazamo wa Ahlul-Bait makosa kukosolewa. Kwa mfumo huu ambao unapokewa na akili timilifu umewahalalishia Mashi’a kuwakosoa maswahaba na kutafiti kiwango cha uadilifu wao kwa kila kipimo ili kumpata aliyekuwa mwaminifu wa kweli katika uswahaba wake au aliyegeuka kwa nyayo zake mpaka Mwenyezi Mungu akataka kumbadili kwa kuleta mbora kuliko yeye. Hayo yote ni kwa ajili ya kutaka kumjua sahaba muumini wa kweli ili tuchukue riwaya yake na sahaba muongo ili tujitenge na hadithi yake.
26
Uadilifu wa maswahaba final edit.qxd
7/15/2011
12:35 PM
Page 27
Uadilifu wa Masahaba kwa mtazamo wa Ahlul-Bait MUHTASARI WA RAI YA SHI’A JUU YA MASAHABA Madhehebu ya Ahlul-bait yanaona kuwa hali ya maswahaba upande wa uadilifu ni kama hali ya wasio maswahaba, miongoni mwao yupo mwadilifu na asiye mwadilifu na wala si kila aliyemsuhubu Mtume alikuwa mwadilifu na wala uswahaba hauna nafasi yoyote katika uadilifu wa sahaba ikiwa hajafuata mwenendo wa Mtume wa Mwenyezi Mungu katika matendo yake na misimamo yake. Hivyo kipimo ni mwenendo wa kivitendo, na kila ambaye mwenendo wake utaoana na mwenendo wa Uislamu basi yeye ni mwadilifu. Rai hii inaoana na Qur’ani tukufu na Sunna tukufu kwani Qur’ani imeashiria kuwa miongoni mwa maswahaba wamo waumini wa kweli na hao imewasifia kwa mazuri na miongoni mwao wamo wanafiki ambao Mwenyezi Mungu amehabarisha kuhusu uongo wao, na miongoni mwao wamo waliokusudia kula njama za kumuuwa Mtume usiku wa AlAqabah.63 Hii ndio rai ya Shi’a Imamiya kuhusu maswahaba ambayo ndio rai ya wastani miongoni mwa rai zote kwani wao hawajavuka kipimo kama Ghulati na wala hawajakipunguza kama masunni.64 Imetarjumuwa na: Hemedi Lubumba Selemani. 0715-017178. 0773-017178. 0754-017178.
63. Ni usiku ambao Mtume alikwenda kukutana na ujumbe wa waisilamu wa Madina ili kuchukua kiapo chao cha utii juu yake na kuandaa mazingira ya kuhamia Madina. 64. Al-Fusulul-Muhimma cha Abdul-Husein Sharafud-Din:189 27
Uadilifu wa maswahaba final edit.qxd
7/15/2011
12:35 PM
Page 28
Uadilifu wa Masahaba kwa mtazamo wa Ahlul-Bait
ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION 1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9. 10. 11. 12. 13. 14. 15. 16. 17. 18. 19. 20. 21. 22. 23. 24. 25. 26. 27. 28. 29. 30.
Qur'an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka kumi na Nane Uharamisho wa Riba Uharamisho wa uwongo Juzuu ya kwanza Uharamisho wa uwongo Juzuu ya pili Hekaya za Bahlul Muhanga wa Imamu Husein (a.s.) Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (a.s.) Hijab vazi Bora Ukweli wa Shia Ithnaashari Madhambi Makuu Mbingu imenikirimu Abdallah Ibn Saba Khadijatul Kubra Utumwa Umakini katika Swala Misingi ya Maarifa Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia Bilal wa Afrika Abudhar Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu Salman Farsi Ammar Yasir Qur'an na Hadithi Elimu ya Nafsi Yajue Madhehebu ya Shia Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur'an Tukufu Al-Wahda Ponyo kutoka katika Qur’an. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii Mashukio ya Akhera 28
Uadilifu wa maswahaba final edit.qxd
7/15/2011
12:35 PM
Page 29
Uadilifu wa Masahaba kwa mtazamo wa Ahlul-Bait 31. 32. 33. 34. 35. 36. 37. 38. 39. 40. 41. 42. 43. 44. 45. 46. 47. 48. 49. 50. 51. 52.
Al-Amali Dua Indal Ahlul Bayt Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna. Haki za wanawake katika Uislamu Mwenyezi Mungu na sifa zake Amateka Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) Adhana. Upendo katika Ukristo na Uislamu Nyuma yaho naje kuyoboka Amavu n’amavuko by’ubushiya Kupaka juu ya khofu Kukusanya swala mbili Bismillahi ni sehemu ya Qur’ani Sauti ya uadilifu wa Binadamu Kufungua Safarini. Kusujudu juu ya udongo. Tarawehe Kufungua safarini Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Kupunguza swala safarini As-Swalaatu khayrun minan-Nawm
29
Uadilifu wa maswahaba final edit.qxd
7/15/2011
12:35 PM
Page 30
Uadilifu wa Masahaba kwa mtazamo wa Ahlul-Bait
BACK COVER Sheria ya Kiislamu ni ya kipekee kwa kuwa inahusika na kila jambo huku ikiweka utatuzi wa matatizo yote yanayompata mwanadamu katika sekta zote za maisha yake, hivyo Mwenyezi Mungu akasema: "Leo nimewakamilishieni dini yenu na kuwatimizieni neema Yangu na nimewapendeleeni Uislamu uwe dini yenu." (5:3). Isipokuwa kuna masuala madogo madogo ambayo wanazuoni wa sheria wamehitilafiana kwa sababu ya kutofautiana kwao kuhusu riwaya ambazo zimenasibishwa kwa Mtume. Jambo ambalo limesababisha kutofautiana kuhusu masuala madodo madogo ya sheria. Je, Masahaba wote ni waadilifu? Hili ni suala ambalo wanachuo wetu wamehitalifiana; ndani ya madhehebu moja na kati ya madhehebu. Kwa hiyo hii sio hitilafu ya madhehebu, bali ni hitilafi ya wanachuo wa madhehebu zote, wamehitilafiana juu ya suala hili. Lakini bahati mbaya Waislamu wengi hawaitambui hitilafu hii kwa usahihi na hivyo kuogelea katika dhana na kusababisha mizozo isiyokuwa na maana. Kutokana na hali hii Sheikh wetu, Sayyid Abdur-Rahim al-Musawi amelifanyia utafiti wa kina suala hili na kuweka wazi asaili ya hitilafu hii, kisha akamuachia msomaji mwenyewe kutoa uamuzi. Kwa kuwa ukweli hutokana na utafiti basi hakika katika mtiririko wa masomo haya mwandishi amejaribu kuliweka swala hili juu ya meza ya utafiti, kwani huenda ikawa ndio njia ya kuunganisha mtazamo na kusogeza hatua katika uwanja huu. Kwani tofauti iliyopo si katika asili na misingi ya dini hata isababishe kuwa na uadui na chuki, bali tofauti iliyopo ni kuhusu riwaya zilizonasibishwa na Mtume, nalo ni jambo dogo ukilin30
Uadilifu wa maswahaba final edit.qxd
7/15/2011
12:35 PM
Page 31
Uadilifu wa Masahaba kwa mtazamo wa Ahlul-Bait ganisha na mambo mengi ambayo tunaafikiana kati ya madhehebu za Kiislamu. Na mwongozo wetu katika njia hii ni kauli ya Mwenyezi Mungu: "Na shikamaneni katika kamba ya Mwenyezi Mungu nyote wala msifarakiane. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu, mlipokuwa maadui na akaziunganisha nyoyo zenu, hivyo kwa neema Zake mkawa ndugu." (3:103) Kimetolewa na kuchapishwa na:
Al-Itrah Foundation P. O. Box 19701, Dar-es-Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Fax: +255 22 2127555 Email: alitrah@raha.com Website: www.alitrah.org Online: www.alitrah.info
31
Uadilifu wa maswahaba final edit.qxd
7/15/2011
12:35 PM
Page 32
Uadilifu wa Masahaba kwa mtazamo wa Ahlul-Bait
32
Uadilifu wa maswahaba final edit.qxd
7/15/2011
12:35 PM
Page 33
Uadilifu wa Masahaba kwa mtazamo wa Ahlul-Bait
33