Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Na Ushia Ndio Njia Iliyonyooka
Kimeandikwa na: Sayyid Abdul Muhsin Al-Musawi na Abdul Karim al-Husaini al-Qazwini
Kimetarjumiwa na: Hemedi Lubumba Selemani
Page A
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
Ubora wa Imam Ali Juu ya Sahaba
Kimeandikwa na: Sayyid Abdul Muhsin Al-Musawi
Kimetarjumiwa na: Hemedi Lubumba Selemani
B
12:36 PM
Page B
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
Š Haki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: 978 - 9987 - 512 -11 - 9 Kimeandikwa na: Seyyid Abdul Muhsin Al-Musawi Kimetajumiwa na: Hemedi Lubumba Selemani
Kimehaririwa na: Ustadh Abdallah Mohamed P.O. Box 19701, Dar es Salaam/Tanzania. Kupangwa katika Kompyuta na: Ukhti Pili Rajab. Toleo la kwanza: Julai, 2008 Nakala: 1000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Nukushi: +255 22 2127555 Barua Pepe: alitrah@raha.com Tovuti: www.alitrah.org Katika mtandao: www.alitrah.info
12:36 PM
Page C
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
YALIYOMO Ubora wa Imam Ali Juu ya Sahaba Utangulizi....................................................................................................2 Mwonekano wa Utu wa Imam Ali (a.s) upande wa elimu..........................2 Mwonekano wa Utu wa Imam Ali (a.s) upande wa Imani..........................5 Kisa cha kuzibwa mlango isipokuwa mlango wa Ali tu............................36 Mtukufu Mtume (s.a.w.w) kuunga udugu na Ali (a.s)..............................37 Khalifa wa Kwanza...................................................................................38
Ushia Ndio Njia Iliyonyooka Neno la jumuiya..............................................................................63 Utangulizi........................................................................................65 Mfumo wa uchunguzi ndani ya Uislamu........................................69 Mtume alitoa jina la Ushia...............................................................83 Ndugu yangu msomaji.....................................................................87
Page D
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Neno la Mchapishaji Kitabu kilichoko mikononi mwako ni mkusanyo wa tarjuma ya vitabu viwili vya Kiarabu. Cha kwanza kinaitwa, Afdhaliyyatu 'l-Imami 'Aliyyin 'Ala 's-Sahaabah kilichoandikwa na Sayyid Abdul Muhsin al-Musawi ambacho sisi tumekiita, Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba. Na cha pili kinaitwa, at-Tashayyyu' Huwa 's-Siraatu 'l-Mustaqiim kilichoandikwa na Abdul Karim al-Husaini al-Qazwini ambacho sisi tumekiita, Shia Ndio Njia Iliyonyooka. Tumevikusanya pamoja kwa vile tumeona maudhui yao yanakurubiana; kwani unapomzungumzia Imam Ali (a.s.) unazungumzia Ushia, na unapozungumzia Ushia unamzungumzia Imam Ali (a.s.). Vitabu hivi ni matokea ya utafiti wa kielimu pamoja na hoja zenye nguvu na utumiaji sahihi wa akili uliofanywa na wanavyuoni waandishi wa vitabu hivi: (1) UBORA WA IMAM ALI JUU YA MASAHABA Dalili ya kisheria yenye kuonyesha ubora wa Imam Ali bin Abi Talib (a.s.) haijakomea kwenye juhudi pekee za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na maneno yake ambayo yalikuwa yakitoka kwake kuelezea nafasi ya Ali (a.s.), bali juhudi hizo zimeambatana na uteremkaji wa aya nyingi za Qur'anI ambazo zimebeba jukumu la kudhihirisha fadhila za Ali (a.s.). Mwenye kufuatilia maelezo yote atayakuta kuwa upande mmoja yameangazia ubora wa Ali (a.s.) juu ya masahaba wote si kwa kulinganisha tu, bali maelezo hayo yanajumuisha zaidi ya maana hii, hivyo, kwa makusudio yake yanakusanya maana nyingine, nayo ni kuwa Ali (a.s.) kwa sifa zake takatifu ndiye mwanadamu aliyeandaliwa kuchukua Uimamu na Ukhalifa baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na wala si mwingine. (2) USHIA NDIO NJIA ILIYONYOOKA
Page E
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Hakika mirathi ya Ahlul Bait (watu wa nyumba ya Bwana Mtume) ambayo imehifadhiwa na kambi yao na wafuasi wao dhidi ya upotovu inaonyesha kambi iliyokusanya aina mbalimbali za taaluma za Kiislamu. Kambi hii imeweza kulea nafsi mbalimbali zilizo tayari kunywa kutoka kwenye chemchemu hiyo, na kuupa Umma wa Kiislamu wanavyuoni wakubwa wenye kufuata nyayo za ujumbe wa Ahlul Bait. Wanavyuoni waliokusanya vidodosa na maswali mbalimbali ya madhehebu na mitazamo tofauti ya kifikra kuanzia ndani ya desturi ya Kiislamu hadi nje ya desturi hiyo, huku wao wakitoa majibu na utatuzi makini juu ya maswali hayo ndani ya karne zote. Hakika uzoefu ambao umehifadhiwa ndani ya vitabu vya wanavyuoni wa kambi ya Ahlul Bait katika dhamira hii ni wa aina ya pekee, kwa sababu una akiba ya kielimu inayotegemea akili na hoja, huku ukijiepusha na matamanio na upendeleo uliokatazwa. Unazungumza na wasomi na wanafikra wenye fani maalumu, mazungumzo ambayo yanakubalika kiakili na yanapokewa na maumbile yaliyo salama. Mkusanyo wa vitabu hivi ni wenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote. Kutokana na ukweli huu, Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeona ichapishe vitabu hivi kwa lugha ya Kiswahili, kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili, ili kuongeza ujuzi wao katika masuala ya dini na ya kijamii. Tunamshukuru ndugu yetu, Hemedi Lubumba Selemani kwa kukubali jukumu hili la kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwa kitabu hiki. Mchapishaji: Al-Itrah Foundation S. L. P. 19701 Dar-es-Salaam, Tanzania
Page F
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
NENO LA JUMUIYA Hakika mirathi ya Ahlul-Bait ambayo imehifadhiwa na kambi yao na wafuasi wao dhidi ya upotovu inaonyesha kambi iliyokusanya aina mbalimbali za taaluma za kiislamu. Kambi hii imeweza kulea nafsi mbalimbali zilizo tayari kunywa kutoka kwenye chemchemu hiyo, na kuupa umma wa kiislamu wanachuoni wakubwa wenye kufuata nyayo za ujumbe wa AhlulBait. Wanachuoni waliokusanya vidodosa na maswali mbalimbali ya madhehebu na mitazamo tofauti ya kifikira kuanzia ndani ya desturi ya kiislamu hadi nje ya desturi hiyo, huku wao wakitoa majibu na utatuzi makini juu ya maswali hayo ndani ya karne zote. Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bait imefanya hima kutetea utukufu wa ujumbe wa Uislamu na ukweli wake ambao umechafuliwa na makundi, madhehebu na wanaharakati mbalimbali wenye chuki na Uislamu. Jumuiya imefuata nyayo za Ahlul-Bait na za wafuasi wa kambi yao njema ambayo imefanya hima kujibu madai yenye kuendelea na daima ikajaribu kubaki ndani ya msitari wa mapambano kwa kiwango kinachohitajika ndani ya kila zama. Hakika uzoefu ambao umehifadhiwa ndani ya vitabu vya wanachuoni wa kambi ya Ahlul-Bait katika dhamira hii ni wa aina ya pekee, kwa sababu una hakiba ya kielimu inayotegemea akili na hoja, huku ukijiepusha na matamanio na upendeleo uliokatazwa. Unazungumza na wasomi na wanafikra wenye fani maalumu,
Page G
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
mazungumzo ambayo yanakubalika kiakili na yanapokewa na maumbile yaliyo salama. Jaribio hili la Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bait limekuja kuwapa watafuta ukweli hatua mpya ya uzoefu wa thamani katika ulingo wa mazungumzo na maswali na kujibu hoja za utata zilizotolewa zama zilizopita au zinazotolewa leo kwa njia ya Tovuti, na hasa kwa kupewa nguvu na baadhi ya duru zenye chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu. Ikijiepusha na uchochezi uliyokatazwa, na ni yenye kuhangaikia kuzishauri akili zenye kufikiria na nafsi zenye kutafuta haki, ili ziweze kufikia kwenye haki ambayo inatolewa na Kambi ya AhlulBayt ulimwengu mzima, ndani ya zama ambazo akili inaerevuka na nafsi na roho zinaboreka kwa kasi ya pekee. Ni lazima tugusie kuwa mfululizo huu wa tafiti hizi umeandaliwa na Kamati maalumu toka jopo la wanachuoni watukufu, hivyo tunatoa shukurani njema kwa hawa wote na kwa wasomi na wahakiki kwa kila mmoja miongoni mwao kwa kupitia sehemu ya tafiti hizi na kutoa mchango wao wa thamani kuhusu tafiti hizi. Na sote tunategemea na kutaraji kuwa tutakuwa tumetoa kile tulichokiweza katika juhudi za kutekeleza baadhi ya wajibu tulionao mbele ya ujumbe wa Mtukufu Mola Wetu Mlezi ambaye alimtuma Mtume Wake na uongofu na dini ya haki ili aipe ushindi dhidi ya dini zote. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa shahidi. Jumuiya ya kimataifa ya Ahlu-Bait Kitengo cha utamaduni
i
Page i
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
ii
7/15/2011
12:36 PM
Page ii
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
1
7/15/2011
12:36 PM
Page 1
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba
UTANGULIZI Dalili ya kisheria yenye kuonyesha ubora wa Imam Ali bin Abi Talib (a.s.) haijakomea kwenye juhudi pekee za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na maneno yake ambayo yalikuwa yakitoka kwake kuelezea nafasi ya Ali (a.s.), bali juhudi hizo zimeambatana na uteremkaji wa Aya nyingi za Qur’an ambazo zimebeba jukumu la kudhihirisha fadhila za Ali (s.a.). Mwenye kufuatilia maelezo yote atayakuta kuwa upande mmoja yameangazia ubora wa Ali (a.s.) juu ya sahaba wote si kwa kulinganisha tu, bali maelezo hayo yanajumuisha zaidi ya maana hii, na hivyo kwa makusudio yake yanakusanya maana nyingine, nayo ni kuwa Ali (a.s.) kwa sifa zake takatifu ndiye mwanadamu aliyeandaliwa kuchukua uimamu baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) na wala si mwingine. Na hata tukifumbia macho utakaso na elimu ya asili ambayo inamilikiwa na Imam au karama ambazo zilikuwa zikidhihiri kwake na si kwa mwingine, bado Ali (a.s.) kwa uwezo wake, elimu yake na sifa zake anaendelea kuwa mbora kuliko sahaba wote, hali hiyo ni hata kama tukikubali kipimo cha kambi ya kisunni ambayo inamtazama Imam Ali (a.s.) kama sahaba tu bila cheo kingine. Na kuanzia hapa tutazungumzia mada ya ubora wa Imam Ali (a.s.) juu ya sahaba wote kwa kuangalia mambo yafuatayo:
Jambo la kwanza: Mionekano ya utu wa Imam Ali (a.s.). Hakika mwenendo wa Imam Ali bin Abi Talib (a.s.) na maumbile yake ya kiroho vinatengeneza mfano bora na kigezo chema kutoka kwa Mola. Kwa kudokoa tu baadhi ya mionekano yake ya kielimu na kitabia hatuwezi kufikia kina na siri ambazo zimebebwa na mfano huu bora, lakini mtazamaji hata kama ataishia kwenye baadhi ya mionekano yake basi itamtosha kuwa dalili juu ya ubora wa Imam Ali (a.s.) juu ya sahaba wote, si kwenye 2
Page 2
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba sekta maalumu tu bali kwenye kila sekta, kiasi kwamba kutokana na mionekano hiyo haitobaki shaka hata kidogo kuwa hakuna sahaba yeyote anayemfikia Ali (a.s.). Na ifuatayo ni baadhi ya mionekano ya utu wake (a.s.):
i. Mwonekano wa utu wa Imam Ali (a.s.) upande wa elimu: Kilichothibiti ni kuwa Imam Ali (a.s.) alikuwa ndiye mwenye elimu kuliko sahaba wote, ukamilifu wa elimu kwa Imam Ali (a.s.) ulifikia kiwango cha juu mpaka Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akauzungumzia kwa kusema: “Mimi ni Jiji la elimu na Ali ni mlango wake.”1Na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hajasema kauli kama hii kumwambia yeyote miongoni mwa sahaba (ila Ali tu.). Na hilo linaungwa mkono na kauli yake (a.s.): “Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alinifundisha milango elfu moja ya elimu, katika kila mlango inanifungukia milango elfu moja mingine mipya.”2 Ukinara wa Ali (a.s.) kwa elimu yake aliyotunukiwa pekee na Mola ulimpelekea kusema: “Laiti ningefunuliwa kifuniko basi nisingezidisha yakini yoyote.”3 Na akatamka waziwazi kuwa elimu aliyonayo ni kubwa mno hakuna sahaba yeyote awezaye kuibeba: “Fahamuni hakika hapa pana elimu yote laiti ningepata mbebaji.” Huku akiashiria kwenye kifua chake.4 1 - Al-Mustadrak Alas-Sahihayn 3: 126, 127. Ta’rikh Baghdad 11: 49 na 50. Jamiul-Usul 9: 473, Hadithi ya 6489. Usudul-Ghaba 4: 22. Al-Bidayah WanNihayah 7: 372. Na At-Tirmidhi ameipokea ndani ya Sunan yake 5: 63 kwa tamko: “Mimi ni Jiji la elimu na Ali ni mlango wake.” 2 - Tafsir Ar-Razi 8: 21 kwenye tafsiri ya kauli ya Mwenyezi Mungu: “Hakika Mwenyezi Mungu alimchagua Adam na Nuh na jamaa wa Ibrahim…” Sura AaliImran: 33. Kanzul-Ummal 13: 114, Hadithi ya 36372. 3 Al-Manaqib cha Ibnu Shahri Ashub 2: 38. Irshadul-Qulub 2: 14. BiharulAn’war 40: 153. 4 Nahjul-Balagha, hekima fupifupi: 147.
3
Page 3
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba Kauli hizi zinaonyesha kwa uwazi wote kuwa hakika Ali (a.s.) kielimu alifikia kiwango ambacho yeyote miongoni mwa viumbe hawezi kukifikia isipokuwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Na hili (a.s.) aliliashiria kwa kauli yake: “Bali nilijichanganya kwa kuyayuka kwenye hazina ya elimu, laiti nikijiengua nayo mtatetereka mtetereko wa kamba kwenye kisima chenye kina cha mbali.” Na imepokewa kutoka kwa Abi Tufaylu kuwa alisema: Nilimshuhudia Ali akisema: “Niulizeni, naapa kwa Mwenyezi Mungu hakuna kitu chochote mtakachoniuliza ila ni lazima nitawapa habari zake, na niulizeni kuhusu Kitabu cha Mwenyezi Mungu, naapa kwa Mwenyezi Mungu hakuna Aya yoyote ila mimi najua imeteremka usiku au mchana, bondeni au jabalini.”5 Na imepokewa kutoka kwa Said bin Al-Musayyib kuwa alisema: “Hakuna sahaba yeyote wa Mtume wa Mwenyezi Mungu aliyekuwa akisema: ‘Niulizeni’ isipokuwa Ali tu.’”6 Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alithibitisha zaidi ya mara moja ubora wa Ali na kuwa kwake juu kielimu kuliko sahaba wote. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimwambia Fatimah Az-Zahra (a.s.): “Hivi huridhii nikuoze kwa mtu wa kwanza kuukubali Uisilamu katika umma wangu, mwenye elimu kuliko wote na mwenye uvumilimu kuwashinda wote.”7 Na (s.a.w.w.) akasema: “Mwenye elimu mno baada yangu kuliko watu wote wa umma wangu ni Ali bin Abi Talib.”8 Na (s.a.w.w.) akasema: “Ali ni chombo cha elimu yangu na ni wasii wangu na mlango wangu ambao unafuatwa.”9 Na (s.a.w.w.) akasema: “Ali ni mlango wa elimu yangu na ndiye atakayeufafanulia umma wangu baada yangu yale niliyotumwa 5 Nahjul-Balagha: Hotuba ya 5. 6 Fathul-Bari 8 : 559 Suratul-Adhariyyat. Kanzul-Ummal 13: 165, hadithi ya 36502. Al-Jarhu Wat-Taadil 6: 192. Tahdhibul-Kamal 20: 487. Usudul-Ghaba 4: 22. Ar-Riyadh An-Nadhrah 3: 167. 7 Musnad Ahmad 5: 26. 8 Al-Manaqib cha Al-Khawarazami: 49, uhakiki wa Al-Mahmud. KanzulUmmal cha Al-Muttaqiy 11: 614, hadithi ya 32977. 9 Kifayat-Talib: 70 na 92. Shamsul-Akhbar: 29.
4
Page 4
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba kwayo.”10 Na (s.a.w.w.) akasema: “Ajuaye zaidi Sunna yangu na hukumu yangu baada yangu kuliko watu wote wa umma wangu ni Ali bin Abi Talib.”11 Na (s.a.w.w.) akasema: “Wewe utaufafanulia umma wangu watakayotofautiana kwayo baada yangu.”12 Na (s.a.w.w.) akasema: “Ewe Abil-Hasan nakuombea elimu ikustareheshe, kwani bila shaka umekunywa elimu sana na umeichota sana.”13
ii. Mwonekano wa utu wa Imam Ali (a.s.) upande wa imani Huu ni ukurasa wa maisha ya Imam Ali (a.s.) ambao ameujaza nguvu za kiroho na ameuchora sura bora kabisa kwa ajili ya vizazi vijavyo, na humo amesajili ukinara wake juu ya sahaba wote. Hivyo nguvu ya imani ni sifa ya pekee anayojitofautisha kwayo Ali (a.s.) na yenyewe imejengeka katika sura mbalimbali, hivyo katika ibada yeye ndiye mfano bora, kwani imekuja katika tafsiri ya kauli ya Mwenyezi Mungu: “ Utawaona ni wenye kuinama wenye kusujudu..” kuwa yenyewe iliteremka kwa ajili ya Ali (a.s.)14. Na akasema kuhusu suala hili: “Niliswali pamoja na Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu miaka saba kabla ya watu wote, na mimi ndiye wa kwanza aliyeswali naye.”15 Na akasema: “Simjui yeyote ndani ya umma 10 Kanzul-Ummal 11: 614, hadithi ya 32981. Kashful-Khifai 1: 204. 11 Ar-Riyadh An-Nadhrah 2: 194. Tafsir An-Nisabur ndani ya Sura Al-Ahqaf. Al-Manaqib cha Al-Khawarazami: 48. Tadhkiratul-Khawwas: 87. Faydhul-Qadir 4: 257 12 - Ameipokea Al-Hakim ndani ya Al-Mustadrak 2: 122. 13 -Al-Manaqib cha Ibnu Al-Mughazali: 420. Ta’rikh Ibnu Asakir 2: 498. 14 -Shawahidut-Tanzil 2: 183. Tafsirul-Khazin na pambizoni mwa An-Nasafi 4:
113. Tafsir Al-Kashif 3: 469. Ruhul-Ma’an 16: 117. 15 -Tadhkiratul-Khawwas: 63.
5
Page 5
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba huu aliyemwabudu Mwenyezi Mungu baada ya Mtume wetu zaidi yangu mimi…”16 Na akasema: “Niliukubali Uisilamu kabla ya watu wote kuukubali, na nikasali kabla ya kuswali kwao.”17 Hivyo Ali (a.s.) alikuwa mwanaibada mno kuliko watu wote na mwenye kusali na kufunga kuliko wao, na kutoka kwake watu wamejifunza Swala ya usiku, kutoachana na nyiradi na Swala za Sunna. Unasemaje kuhusu mtu ambaye kutokana na kudumisha uradi wake anatandikiwa mrago wa ngozi kati ya majeshi mawili usiku wa vita vya Suffin kisha anavuta uradi wake huku mishale ikimdondokea na kupita masikioni mwake kulia na kushoto lakini hatetereki, na wala hainuki mpaka anamaliza jukumu lake? Unasemaje kuhusu mtu ambaye paji lake la uso lilikuwa na sugu kama sugu ya ngamia kutokana na urefu wa sijida yake?18 Ali bin Husein Zainul-Abidina (a.s.) – Yeye alikuwa amefikia kiwango cha juu sana katika ibada - aliulizwa: Ipi nafasi ya ibada yako mbele ya ibada ya babu yako? Akajibu: “Ibada yangu mbele ya ibada ya babu yangu ni sawa na ibada ya babu yangu mbele ya ibada ya Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.).”19 Ama katika mwonekano mwingine wa imani tunamkuta yeye (a.s.) ni kilele katika usafi na tabia aziridhiazo Mola, na yeye ni mfano bora wa Qur’an ambao aliuleta kwa ajili ya maana ya ukweli. Mwenyezi Mungu amesema:
“Na wale walioamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, hao ndio wasema kweli..”-Suratul-Hadid: 19. 16 - Khasaisu Amiril-Mu’minin cha An-Nasai: 46. 17 - Sharhu Nahjul-Balagha 1: 10. 18 - Sharhu Nahjul-Balagha cha Ibnu Abil-Hadid 1: 27. 19 - Sharhu Nahjul-Balagha 1: 9.
6
Page 6
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba Aya hii kwa mujibu wa riwaya ya Ahmad yenyewe iliteremka kwa ajili ya Ali bin Abi Talib (a.s.).20 Na kuna Aya nyingi zinazothibitisha kuwa Ali (a.s.) ndiye mfano bora uliyo hai wa maana ya imani, Mwenyezi Mungu amesema: “Je, mnafanya kuwanywesha mahujaji na kuuamirisha Msikiti Mtukufu ni sawa na yule aliyemwamini Mwenyezi Mungu na siku ya Mwisho na akapigania dini ya Mwenyezi Mungu? Hawawi sawa mbele ya Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu hawaongozi watu madhalimu.”21 Aya hii na inayofuatia ziliteremka kwa ajili ya Ali (a.s.) pale Talha Ibnu Shayba na Abbas walipojifakharisha. Talha akasema: “Mimi ndiye mbora kwa ajili ya Nyumba kwani funguo zimo mikononi mwangu.” Abbas akasema: “Mimi ndiye mbora kwani mimi ndiye mnyweshaji na msimamizi wake.” Ali (a.s.) akasema: “Mimi ndiye mtu wa kwanza kuamini na mwenye jihadi zaidi kuliko wao.” Basi ndipo Mwenyezi Mungu akateremsha Aya hii ili kubainisha ubora wa Imam Ali bin Abi Talib juu yao.22 Na Mwenyezi Mungu amesema: “Je, muumini anaweza kuwa sawa na yule aliye muovu? Hawawi sawa.”23 Muumini ni Ali, na muovu ni Al20 - Ameipokea kwenye sura ya fadhila miongoni mwa fadhila za Ali (a.s.) kwenye hadithi ya 154 na 339. Minihaju As-Sunna iliyopo kwenye maelezo ya Shawahidu At-Tanzil 2: 224, humo mna: Ameipokea Al-Haskaniy kwa njia mbalimbali, Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Wasema kweli ni watatu: Habibu Seremala, muumini wa jamaa wa Yasin, Ezekiel muumini wa jamaa wa Firaun na Ali bin Abi Talib na huyu wa tatu ndiye mbora wao.”. Na ameipokea ndani ya As-Sawa’iqul-Muhriqah: 123. At-Tafsir Al-Kabir 27: 57. Dhakhairul-Uqba: 56. Ar-Riyadh An-Nadhra 2: 153. Faydhul-Qadir 4: 137. Ad-DurulMathur 5: 262. 21 - Surat Tawba: 19. 22 - Tafsir Ibnu Kathir 2: 241. Tafsir At-Tabari 10: 68. Jamiul-Usul 9: 477. At-Tafsir AlKabir 16: 10. Asbabun-Nuzul cha Al-Wahid: 139. Ad-Durul-Manthur 3: 318, 319. 23 -Surat As-Sajdah: 18.
7
Page 7
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba Walid.24Kwa Aya hii Qur’ani Tukufu inawapa watu mfano wake bora wa kiimani unaopatikana kwa Ali (a.s.). Mwenyezi Mungu amesema:
“Na wenye nasaba wana haki zaidi wao kwa wao katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu kuliko waumini na waliohama.”- Suratul-Ahzab: 6. Baadhi ya wafasiri wamesema kuwa Aya hii inamuhusu Ali (a.s.) kwa sababu yeye ndiye mwenye nasaba aliyehama.25 Kama ambavyo Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu alivyowafafanulia watu zaidi ya sehemu moja jinsi Ali (a.s.) alivyoupokea ujumbe na mafunzo yake na utanguliaji wake ndani ya Uislamu, na kuwa yeye ndiye mwanadamu mwenye uwezo wa kutatua matatizo kwa nguvu ya imani yake pindi yanapotatiza. Imepokewa kutoka kwa Ibnu Abi Dhari kuwa alisema:26 “Tuliingia kwa Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) tukamuuliza: Ni sahaba yupi umpendaye sana? Ili jambo likitokea tuwe pamoja naye na kama ni 24 - Tafsir At-Tabar 21: 68. Tafsir Ibnu Kathir 3: 462. Fa’hul-Qadir 4: 247. AsbabunNuzul: 273. Dhakhairul-Uqba: 88. Shawahidut-Tanzil 1: 444. Ansabul-Ashraf cha AlBaladhar 1: 162. Ta’rikh Damashqi 61: 199.
25 - Ameipokea Ibnu Mardawihi ndani ya kitabu Al-Manaqib, na ameinukuu
ndani ya Ihqaqul-Haqi 3: 419 kutoka kwa At-Tirmidhi ndani ya ManaqibulMurtadhawi: 62. 26 - Ilalul-Hadith cha Ibnu Abi Hatim Ar-Razi: Hadithi ya 2664. ManaqibulMurtadhawi cha At-Tirmidhi: 95. Na ndani ya Kanzul-Ummal 13: 122, hadithi ya 36392 imepokewa kutoka kwa Ibnu Abbas kuwa Umar bin Al-Khatab alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu alisema: “Ewe Ali! Wewe ndiye muumini wa kwanza kuamini na wa kwanza wao kuukubali Uislamu.”
8
Page 8
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba msiba basi tuwe dhidi ya asiyekuwa yeye? Akajibu: “Ali, ndiye aliyewatangulia katika usalama na Uislamu.” Tunakomea na kiwango hiki cha dalili zinazoonyesha nguvu ya imani ya Ali (a.s.) na ubora wake ili tupate fursa ya kutazama upande wake wa jihadi. iii. Mwonekano wa utu wa Imam Ali (a.s.) upande wa jihadi Kuzama ndani ili kuthibitisha jihadi kwa Imam Ali (a.s.) ni sawa na kufafanua jambo lililo wazi mno na kuelezea jambo lisilohitaji maelezo, kwa sababu hakuna tofauti kati ya waislamu wote na hata wasio waislamu kuwa Ali katika jihadi alikuwa ni shujaa mno baada ya Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) kuliko sahaba wote na mwenye kutangulia mbele kuliko wote. Japokuwa ushujaa na kupenda jihadi ni sifa barizi kwa sahaba ndani ya maisha yao isipokuwa thamani yake kwa Ali (a.s.) inadhirika kwa uwazi mno kwenye mazingira magumu na pale watu wengine wanapokimbia na kutokuweza kuvuka. Hapo Ali (a.s.) hutangulia mbele kwa ushujaa wake wa juu kutoka kwa Mola ili kuvua kitanzi kwa waislamu. Na hili ndilo linalothibitishwa na vita ambavyo aliingia dhidi ya washirikina na watu wa kitabu katika vita vya Badr, Ahzab, Khaybar, Hunayn na vinginevyo.
Imepokewa kutoka kwa Abi Hurayra amesema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema siku ya Khaybar: “Nitampa bendera mtu ambaye anampenda Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na Mwenyezi Mungu atashinda mikononi mwake.” Umar alisema: “Katu kabla ya siku hiyo sikupenda uongozi, ndipo akaikabidhi kwa Ali (a.s.).” Akasema: “Akasema (s.a.w.w.): “Na wala usigeuke.” Akaenda kidogo, akasema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, tunapigana juu ya nini?” Akasema (s.a.w.w.): “Ili wakiri kuwa hapana Mola wa haki ila Allah, na hakika Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, basi iwapo watafanya hivyo damu yao na mali yao vitalindwa ila kwa haki yake, na hesabu yao ni juu 9
Page 9
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba ya Mwenyezi Mungu.”27 Katika vita vya Handaki Imam Ali (a.s.) aliweka mfano bora wa kupendeza kwa ajili ya kuinusuru haki na kwa mfano huo akatofautiana na sahaba wengine. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitukuza thamani ya tukio hili tukufu pale alipotamka waziwazi kuwa Ali anawakilisha haki yote. Sunni wamepokea kuwa: “Alipochomoza Amr bin Abdu Wuddi Al-Amiriy kwenye vita vya Handaki, baada ya kuwa tayari waislamu wameshashindwa kumkabili, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Imechomoza imani yote kupambana na shirki yote.”28 Na Ahmad bin Hambal amenukuu ndani ya Musnad yake amesema: “Hasan (a.s.) alihutubia akasema: “Jana amewatokeni mtu ambaye hakuna yeyote wa mwanzo aliyemtangulia katika elimu, wala hakuna yeyote atakayemfikia, Mtume wa Mwenyezi Mungu alikuwa akimtuma kwa kumpa bendera, Jibril anakaa kuliani mwake na Mikail kushotoni mwake basi harudi mpaka amletee ushindi.”29 Al-Khawarizmi amepokea amesema: Ametusimulia Ubaydullah bin Aisha kutoka kwa baba yake amesema: “Washirikina walikuwa wakiachiana usia pindi tu wanapomuona Ali vitani.”30 Na imepokewa kutoka kwa Jabir bin Abdullah amesema: Siku ya Hudaybiyyah nilimsikia Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akisema huku ameshika bega la Ali bin Abi Talib: “Huyu ni kiongozi wa watu wema na mteketezaji wa waovu, atapata msaada atakayemsaidia, 27 - Musnad Ahmad 3: 86, hadithi ya 8764. Maj’mauz-Zawa’id 9: 123. At-Ta’rikh Al-Kabir cha Bukhari 7: 263. At-Tabaqat Al-Kubra cha Ibnu Saad 2: 110, mlango wa Mtume wa Mwenyezi Mungu kuipiga Khaybar. Khasaisu Amiril-Mu’minin Ali bin Abi Talib cha AnNasai: 59. 28 - Sharhu Nahjul-Balagha cha Ibnu Abi Hadid 13: 261 na 285, na 19: 61. 29 -Musnad Ahmad bin Hambal 1: 199. 30 - Ibnu Al-Mughazaliy ndani ya Manaqib yake: 72: 106.
10
Page 10
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba atatelekezwa atakayemtelekeza.” Kisha akakokoteza sauti yake na kusema: “Mimi ni jiji la elimu na Ali ni mlango wake basi mwenye shida na jiji afuate mlango huu.”31 Imepokewa kutoka kwa Ibnu Abbas amesema: “Muhajirina siku ya Badri walikuwa sabini na saba, na watu wa Madina walikuwa mia mbili na thelathini na sita, aliyekuwa na bendera ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) ni Ali bin Abi Talib, na aliyekuwa na bendera ya watu wa Madina ni Saad bin Ubadah.”32 Imepokewa kutoka kwa Ibnu Abbas amesema: “Hakika bendera ya Muhajirina alikuwa nayo Ali (a.s.) kwenye mapambano yote, kuanzia siku ya Badri, siku ya Uhud, siku ya Khaybari, siku ya Ahzabu na siku ya ukombozi wa Makka, na iliendelea kuwa kwa Ali kwenye mapambano yote.”33 Na yeye mwenyewe Imam Ali bin Abi Talib anatusimulia usuhuba wake na Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) pale alipoazimia kuvunjavunja masanamu ambayo yalikuwa juu ya Al-Kaaba Tukufu, na (a.s.) alikuwa amepanda juu ya mabega ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), Ali (a.s.) anasema: “Nilikwenda pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) mpaka Al-Kaaba, ndipo Mtume wa Mwenyezi Mungu akapanda juu ya mabega yangu kisha (s.a.w.w.) akasema: “Inuka” nikainuka, basi Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alipoona udhaifu wangu akaniambia: “Kaa chini” nikakaa chini, basi Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akateremka na akakaa chini ili nipande, akaniambia: “Panda juu ya mabega yangu” nikapanda juu ya mabega yake akaniinua.” Ali (a.s.) anasema: “Basi nikawa naona kuwa kama nikitaka nitaugusa usawa wa mbingu, ndipo nikapanda juu ya Al-Kaaba na kulikuwa na sana31 -Ta’rikh Madinatu Damashqi 42: 383.
32 - Ta’rikh at-Tabar 2: 138. 33 - Ta’rikh Damashqi cha Ibnu Asakir, wasifu wa Imam Ali (a.s.) 1: 142. AlFusulul-Mi’ah 1: 307.
11
Page 11
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba mu la dhahabu au shaba, basi nikawa nakazana kulia na kushoto, mbele na nyuma na katikati ili niliondowe, mpaka nilipoweza, ndipo Mtume wa Mwenyezi Mungu akaniambia: “Litupe” nikalitupa likavunjikavunjika kama vivunjikavyo vigae vya fedha. Kisha nikateremka nikaondoka mimi na Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) tukiharakisha mpaka tukajisitiri kwa majumba tukihofia mtu yeyote asikutane nasi.”34 Na sura zote za mwenendo wa Imam Ali (a.s.) katika sekta zote zinajikusanya kwa ufupi pale Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) anapomfananisha na Manabi (a.s.) kwa Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) kusema: “Atakayetaka kutazama elimu ya Adam, azma ya Nuh, upole wa Ibrahim, haiba ya Musa na utawa wa Isa basi amtazame Ali bin Abi Talib.”35 iv. Mwonekano wa utu wa Imam Ali (a.s.) upande wa mwenendo na tabia Ukinara wa Ali bin Abi Talib (a.s.) na utofauti wake juu ya sahaba wote haukomei kwenye sekta tulizozitaja tu, bali kutokana na kutekeleza mafunzo ya Ujumbe, maana yake na maadili yake Ali amekuwa mfano bora ambao unaleta azma na ari ndani ya nafsi za sahaba, jambo lililomfanya awe eneo la sifa za kweli kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Na katika maelezo yafuatayo tutasimama kwenye maelezo yanayoonyesha mwenendo wake na tabia yake ambayo inamtofautisha na mwingine. 1. Mwenyezi Mungu anasema: “Na miongoni mwa watu kuna ambaye huiuza nafsi yake kwa ajili ya kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu.”36 Hakika yenyewe iliteremka kwa ajili ya Ali bin Abi Talib (a.s.) pale alipoachwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa ajili ya kulipa deni lake na 34 -Khasaisu Amiril-Muuminin cha An-Nasai: 113. Mustadrak Al-Hakim 2: 366. Musnad Ahmad 1: 84. Kanzul-Ummal 6: 407. Ar-Riyadh An-Nadhra 2: 200. Ta’rikh Baghdad 13: 302. Dhakhairul-Uqba: 85. 35 - Yanabiul-Mawaddah cha Al-Kunduzi, mlango wa 40. 36- Sura Al-Baqara: 207.
12
Page 12
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba kukabidhi amana yake wakati yeye (s.a.w.w.) alipohama, hivyo akalala juu ya kitanda chake na washirikina wakaizingira nyumba, basi Mwenyezi Mungu akamfunulia Jibrail na Mikail: “Hakika mimi nimeweka udugu kati yenu na nimefanya umri wa mmoja wenu kuwa mrefu kuliko wa mwingine, basi ni yupi kati yenu wawili atakayemwachia mwenzake uhai?” Kila mmoja akachagua uhai, ndipo Mwenyezi Mungu akawafunulia: “Mmeshindwa kuwa kama Ali bin Abi Talib, nimeweka udugu kati yake na Muhammad na amelala juu ya kitanda chake, kaitoa nafsi yake fidia kwa ajili yake (mtume) na kamwachia uhai. Teremkeni aridhini mkamuhifadhi dhidi ya adui zake.” Ndipo wakateremka, na Jibrail akawa miguuni, Jibrail akasema: “Hongera, hongera, ni nani mfano wako ewe mwana wa Abi Talib, Mwenyezi Mungu anajifaharisha kwa Malaika kupitia kwako.”37 2. Mwenyezi Mungu anasema: “Na huwalisha chakula masikini na yatima na mfungwa hali ya kuwa wanakipenda. Tunakulisheni kwa ajili 37 - Usudul-Ghaba 4: 25. Shawahudu At-Tanzil 1: 98. Mustadrak Al-Hakim 3: 132. Nurul-Absar: 86. Yanabiul-Mawaddah: 92. At-Tafsir Al-Kabir 5: 204. Musnad Ahmad 1: 331. Tafsir At-Tabar 9: 140. As-Sirat An-Nabawiyyah cha Dahlan pambizoni mwa As-Sirat Al-Halbiyah 1: 307. Ibnu Hajari amesema ndani ya kitabu Tahdhibut-Tahdhib: Imesemekana kuwa: Hakika Aya hii iliteremka kwa ajili ya Suhaybu Ar-Rumiyyu, lakini nasema: Hakika walioweka riwaya hii na mfano wa hii bila shaka ni wale maadui wa AhlulBayt (a.s.), na kama si hivyo basi ni kuwa, hata bila kufikiria sana inadhihirika kuwa: Hakika Aya hii Tukufu yenyewe ni fadhila ya mtu aliyeitoa nafsi yake katika njia ya Mwenyezi Mungu, na huyu si mwingine ila ni Ali bin Abi Talib (a.s.) siku ambayo alilala kwenye kitanda cha Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.). Na kinachoonyeshwa na riwaya inayomzungumzia Suhaybu Ar-Rumiy si kingine ila ni kutoa mali, na kuna uhusiano gani kati ya Aya na kitendo hicho, hakuna uhusiano wowote kati yake na Aya Tukufu.
13
Page 13
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba ya radhi ya Mwenyezi Mungu tu, hatutaki kwenu malipo wala shukurani.”38 Masunni wamepokea kuwa: Hasan na Husein waliugua, basi Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na waarabu wote wakawatembelea, ndipo Ali akaweka nadhiri ya kufunga siku tatu, pia mama yao Fatima na mtumishi wao Fidhah nao wakaweka nadhiri hiyo. Wakapona ilihali kwa ndugu wa Muhammad (s.a.w.w.) hawana kichache wala kingi, basi Ali (a.s.) akakopa pishi tatu za shairi, Fatimah akatwanga pishi moja na kutengeneza mikate kila mmoja mkate mmoja, Ali (a.s.) akaswali Magharibi kisha akaenda nyumbani akaweka chakula mbele yake ili afuturu, ghafla akawaijia masikini na kuwaomba, basi kila mmoja akampa chakula chake na hivyo wakashinda na kulala wakiwa hawajaonja chochote. Kisha wakafunga siku ya pili, Fatima akapika mikate pishi nyingine, alipoiweka mbele yao ili wafuturu akawaijia yatima na kuwaomba chakula, basi kila mmoja akatoa sadaka chakula chake. Walipokuwa katika saumu ya siku ya tatu na kikaja chakula ili wafuturu, ghafla aliwaijia mfungwa na kuwaomba chakula, basi kila mmoja akampa chakula chake, na ndani ya siku zote tatu hawakuonja chochote isipokuwa maji tu. Basi siku ya nne Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akawaona wakiwa wanatetemeka kwa njaa huku tumbo la Fatima likiwa limegusana na mgongo kutokana na ukali wa njaa na macho yake yamelegea, ndipo (s.a.w.w.) akasema: “Ewe Mwenyezi Mungu wasaidie, hivi ndugu wa Muhammad wanakufa kwa njaa?!!” Hapo akateremka Jibril na kusema: “Pokea pongezi alizokupa Mwenyezi Mungu kwa ajili ya watu wa nyumba yako.”39 Akasema: Ewe 38 - Surat Ad-Dahri: 8 – 9.
39 -Usudul-Ghaba 5: 530. Asbabun-Nuzul cha Al-Wahidi: 331. Ad-DurulManthur 6: 299. Dhakhairul-Uqba: 89 na 102. Nurul-Absar: 102. Ruhul-Maan 29: 157. Fat’hul-Qadir 5: 338. Sharhu Nahjul-Balagha cha Ibnu Abi Hadid 1: 7. Tafsir Al-Baydhawi 4: 235. Yanabiul-Mawaddah: 93. Shawahidu At-Tanzil 2: 298. AtTafsir Al-Kabir 30: 244 Amenukuu kutoka kwenye Al-Kashaf.
14
Page 14
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba Jibril ni kipo hicho ninachopokea?” Akamsomea: “Hakika ulimfikia..”. 3. Imam Ali (a.s.) aliulizwa huko Kufa akiwa juu ya mimbari kuhusu kauli ya Mwenyezi Mungu: “Wapo watu miongoni mwa waumini waliotimiza ahadi waliyoahidiana na Mwenyezi Mungu, baadhi yao wamekwishamaliza nadhiri zao, na wako miongoni mwao wanangojea, wala hawakubadilisha hata kidogo.”40 Akasema: “Ewe Mwenyezi Mungu tusamehe, hakika Aya hii iliteremka kwa ajili yangu na ami yangu Hamza na mwana wa ami yangu Ubaydah bin Al-Harith bin AbdulMuttalib. Ama Ubaydah yeye alitimiza ahadi yake akiwa shahidi siku ya Badri, na Hamza alitimiza ahadi yake akiwa shahidi siku ya Uhudi, ama mimi namngojea muovu mno atakayepaka damu hizi na hiki, (Akaashiria ndevu zake na kichwa chake) ni ahadi alioniachia kipenzi changu Abil Qasim (s.a.w.w.).”41 4. Kauli ya Mwenyezi Mungu: “….Hivi karibuni Mwenyezi Mungu ataleta watu atawapenda nao watampenda.”42 Aya hii iliteremka kwa ajili ya Ali bin Abi Talib (a.s.).43 5. Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Yeye ndiye aliyekusaidia kwa ushindi wake na kwa waumini.”44 Kutoka kwa Abi Hurayra amesema: Juu ya Arshi kumeandikwa: Hapana Mola wa haki ila Allah pekee asiye na mshirika. Muhammad ni mja Wangu na Mtume Wangu, nimempa nguvu kwa Ali bin Abi Talib, na hiyo ndio kauli ya Mwenyezi Mungu “Yeye ndiye aliyekusaidia kwa ushindi wake 40 - Sura Al-Ahzab: 23. 41 - Nurul-Absar cha Shablanji: 97. As-Sawaiqu Al-Muhriqah: 80. 42 -Sura Maidah: 54. 43 At-Tafsir Al-Kabir 12: 20. Mustadrak Al-Hakim 3: 132. Kanzul-Ummal 5: 428 na 6: 391 na 393 na 396. 44 -Surat Al-Anfal: 62.
15
Page 15
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba na kwa waumini.” yaani Ali bin Abi Talib (a.s.).45 6. Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Je, yeye anaweza kuwa sawa na yule anayeamuru kwa uadilifu naye yuko juu ya njia iliyonyooka?”46 Imepokewa kutoka kwa Ibnu Abbas kuwa ni Ali (a.s.).47 Aya hii inafafanua wazi sifa ya uadilifu kwa Ali, nayo ni miongoni mwa sifa ambazo kwazo amekuwa kinara, uadilifu kwake ulikuwa ndio kipimo kinachotawala mahusiano yake, mwenendo wake na msimamo wake tena kwa maana yenyewe halisi ya: “Na katika wale tuliowaumba, wako watu wanaoongoza kwa haki, na wanafanya uadilifu kwa haki hiyo.” Ali (a.s.) amesema: “Hao ni mimi na wafuasi wangu.”48 7. Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Wale watoao mali zao usiku na mchana, kwa siri na dhahiri”. Ali (a.s.) alichora sura ya utoaji na mazingira yake yenye kuhifadhi tena yaliyo masafi ambayo yanaitikia lengo la Mola katika njia ya utendaji, hivyo utendaji wake na utowaji wake wa sadaka ulikuwa upande mmoja unazingatia heshima ya mstahiki na upande mwingine unapelekea kuwavuta watu kwenye kitendo cha kutoa, na kwa ajili hiyo Qur’ani ikawa imemsifia kwa upande huu, nayo ni kauli ya Mwenyezi Mungu: “Wale watoao mali zao usiku na mchana, kwa siri na dhahiri.”49 Masunni wamepokea kuwa yenyewe iliteremka kwa ajili ya Ali (a.s.) kwani alikuwa na dirham nne, usiku akatoa dirham moja na mchana dirham moja, akatoa 45 - An-Nuru Al-Mushtaal ma Nazala Minal-Qur’an fi Ali cha Al-Hafidhu Ahmad bin Abdullah Al-Asbahaniy: 89. 46 - Surat An-Nahl: 76. 47 - Shawahidut-Tanzil 1: 59. Ameipokea Ibnu Mardawih ndani ya kitabu AlManaqib kama ilivyo ndani ya kitabu Kashful-Ghummah: 96. 48 - Yanabiul-Mawaddah: 109. Shawahidut-Tanzil 1: 204. 49 - Sura Baqarah: 274.
16
Page 16
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba dirham moja katika hali ya siri na dirham nyingine katika hali ya dhahiri.50 8. Kama ambavyo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alivyoamrishwa na Mwenyezi Mungu awe na unyenyekevu kwa waumini: “Na uinamishe bawa lako kwa yule anayekufuata katika wale walioamini.”51 pia kiongozi wa waumini Ali alikuwa kama kaka yake Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akifuata mwenendo wake, kwani alikuwa mnyenyekevu kwa waumini katika hali zake zote, katika nguvu zake na udhaifu wake, katika hali ya kutokuwa madarakani na akiwa madarakani, katika hali ya vita na usalama. Ibnu Abil Hadid Al-Mu’tazal amesema kutoka kwa Salih muuza mifuko kuwa: “Hakika bibi yake alikutana na Ali (a.s.) huko Kufa akiwa amebeba tende, basi akamsalimia na kumwambia: “Ewe kiongozi wa waumini! Tende hizi nikubebee hadi nyumbani kwako?” Akajibu (a.s.): “Baba wa familia ndiye mwenye haki zaidi ya kuzibeba.” Akasema: Kisha akaniambia: “Hauli katika hizi?” Nikasema: Sitaki. Akasema: Akaenda nazo nyumbani kwake, kisha akarejea akiwa amejifunika shuka hilo likiwa na maganda ya tende, akawaswalisha watu swala ya Ijumaa akiwa ndani ya shuka hilo.”52 9. Imepokewa kutoka kwa Abdullah bin Hasan bin Hasan amesema: “Zama za uhai wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) Ali (a.s.) aliwaacha huru watumwa elfu moja kwa mali yake aliyoichuma kwa nguvu zake na jasho lake. Alichukua ukhalifa na mali zikamfikia lakini hakuwa 50 - Asbabun-Nuzul cha Al-Wahidi: 64. At-Tafsir Al-Kabir 7: 98. Ad-DurulMathur 1: 363. Tafsir Al-Kashaf 1: 164. Tafsir Al-Khazin 1: 214. DhakhairulUqba: 88. Usudul-Ghaba 4: 25. As-Sawaiqul-Muhriqah: 87. Maj’mauz-Zawa’id 6: 334. Nurul-Absar: 70. 51 - Sura Shuaraa: 215. 52 - Sharhu Nahjul-Balagha cha Abi Hadid 2: 202.
17
Page 17
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba na vyakula vitamu ila tende, wala nguo isipokuwa kuukuu.” 53 10. Imepokewa kutoka kwa Zadhan amesema: “Hakika (a.s.) alikuwa akitembea kwa miguu masokoni peke yake na wakati huo huo akimwongoza mpotevu, akimsaidia dhaifu na akipita kwa wauzaji na watu wa mbogamboga kisha anawafunulia Qur’ani na kusoma: “Hivyo nyumba ya Akhera tutawafanyia wale wasiotaka kujitukuza katika ardhi.”54”55 11. Ama katika subira tunamkuta (a.s.) alitoa hoja siku ya shura kwa subira juu ya upotevu wa haki yake. Imepokewa kutoka kwa Abi Tufaylu Amir bin Wathilah amesema: “Nilikuwa mlangoni siku ya shura basi sauti zikanyanyuka kati yao, nikamsikia Ali (a.s.) akisema: “Watu walimchagua Abu Bakr ilihali wallahi mimi ni bora kwa jambo hilo kuliko yeye, na ni mwenye haki nalo kuliko yeye. Lakini nikasikia na nikanyamaza nikihofia watu wasije wakarudia kuwa makafiri, wakauwana wao kwa wao kwa mapanga. Kisha watu wakamchagua Umar ilihali wallahi mimi ni bora kwa jambo hilo kuliko yeye, na ni mwenye haki nalo kuliko yeye. Lakini nikasikia na nikanyamaza nikihofia watu wasije wakarudi na kuwa makafiri, wakauwana wao kwa wao kwa mapanga. Kisha nyinyi mnataka kumchagua Uthman?! Hivyo sisikii wala sinyamazi, na hakika Umar katika watu watano amenifanya mimi wa sita wao, hatambui ubora wangu wowote juu yao katika wema na wala hawautambui kwangu, sisi sote katika hilo tuko sawa, naapa kwa Mwenyezi Mungu nikitaka kuongea kisha asiweze kujibu sifa yeyote mwarabu yeyote, wala yeyote asiye mwarabu, wala mpwekeshaji wala mshirikina, naweza kufanya hivyo.” Kisha akasema: “Nawaapisheni Mwenyezi Mungu, hivi kati yenu yupo 53 - Sharhu Nahjul-Balagha cha Abi Hadid 2: 202. 54 -Sura Al-Qasas: 83. 55 - Al-Manaqib cha Ibnu Shahru Ashub 2: 104.
18
Page 18
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba yeyote aliye ndugu wa Mtume wa Mwenyezi Mungu kuliko mimi?” Wakasema: “Hapana.” Akasema: “Hivi miongoni mwenu yupo yeyote kuliko mimi mwenye ami mfano wa ami yangu Hamza bin Abdul-Muttalib, simba wa Mwenyezi Mungu na simba wa Mtume Wake?” Wakasema: “Hapana.” Akasema: “Hivi miongoni mwenu yupo yeyote mwenye binamu mfano wa binamu yangu Mtume wa Mwenyezi Mungu?” Wakasema: “Hapana.” Akasema: “Hivi miongoni mwenu yupo yeyote mwenye ndugu wa kiume mfano ndugu yangu Jafar aliyepambwa kwa mbawa mbili anayeruka pamoja na Malaika Peponi?” Wakasema: “Hapana.” Akasema: “Hivi miongoni mwenu yupo yeyote mwenye mke mfano wa mke wangu Fatima binti ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) bibi mbora kuliko wanawake wote wa umma huu?” Wakasema: “Hapana.” Akasema: “Hivi miongoni mwenu yupo yeyote asiyekuwa mimi aliye na wajukuu wawili mfano wa Hasan na Husein wajukuu wa umma huu watoto wawili wa Mtume wa Mwenyezi Mungu?” Wakasema: “Hapana.” Akasema: “Hivi miongoni mwenu yupo yeyote aliyewauwa washirikina wa kikurayshi kabla yangu?” Wakasema: “Hapana.” Akasema: “Hivi miongoni mwenu yupo yeyote aliyempwekesha Mwenyezi Mungu kabla yangu?” 19
Page 19
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba Wakasema: “Hapana.” Akasema: “Hivi miongoni mwenu yupo yeyote asiyekuwa mimi ambaye Mwenyezi Mungu ameamuru kumpenda?” Wakasema: “Hapana.” Akasema: “Hivi miongoni mwenu yupo yeyote aliyemuosha Mtume wa Mwenyezi Mungu kabla yangu? Wakasema: “Hapana.” Akasema: “Hivi miongoni mwenu yupo yeyote asiyekuwa mimi aliishi ndani ya msikiti anaopita humo akiwa na janaba?” Wakasema: “Hapana.” Akasema: “Hivi miongoni mwenu yupo yeyote asiyekuwa mimi aliyerudishiwa jua mpaka akasali Alasiri baada ya kuwa limezama?” Wakasema: “Hapana.” Akasema: “Hivi baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) kuletewa nyama ya ndege na kupendezwa nayo yupo yeyote miongoni mwenu asiyekuwa mimi aliambiwa na Mtume: “Ewe Mwenyezi Mungu niletee kiumbe ukipendacho mno kile pamoja nami ndege huyu?” Ghafla nilikuja huku nikiwa sijui kauli yoyote aliyoitanguliza na nikaingia kwake, (s.aw.w.) akasema: Huyu hapa ewe Mola Mlezi, huyu hapa ewe Mola Mlezi.” Wakasema: “Hapana.” Akasema: “Hivi miongoni mwenu yupo yeyote kuliko mimi aliyekuwa shujaa mno katika kuwauwa washirikina wakati wa kila gumu linalompata Mtume wa Mwenyezi Mungu?” Wakasema: “Hapana.” Akasema: “Hivi miongoni mwenu yupo yeyote ambaye alikuwa fidia kubwa sana kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kuliko mimi pindi nilipo20
Page 20
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba lala kwenye kitanda chake na kumkinga kwa nafsi yangu na kutoa damu ya moyo wangu kwa ajili yake?” Wakasema: “Hapana.” Akasema: “Hivi miongoni mwenu yupo yeyote asiyekuwa mimi na Fatima ambaye alikuwa akichukua Khumsi?” Wakasema: “Hapana.” Akasema: “Hivi miongoni mwenu yupo yeyote Mwenyezi Mungu ametimiza nuru yake kutoka mbinguni mpaka akasema: “Basi mpe jamaa haki yake,”?56 Wakasema: “Ewe Mwenyezi Mungu hapana.” Akasema: “Hivi miongoni mwenu yupo yeyote asiyekuwa mimi alizungumza faragha na Mtume wa Mwenyezi Mungu mara kumi pindi ilipoteremka: “Enyi mlioamini! Mnaposema siri na Mtume, basi tangulizeni sadaka kabla ya kumsemeza,”57? Wakasema: “Ewe Mwenyezi Mungu hapana.” Akasema: “Hivi miongoni mwenu yupo yeyote asiyekuwa mimi alichukua jukumu la kumfumba macho Mtume wa Mwenyezi Mungu?” Wakasema: “Hapana.” Akasema: “Hivi miongoni mwenu yupo yeyote asiyekuwa mimi alikuwa mwishoni mwa uhai wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na akaendelea mpaka akamlaza ndani ya kaburi lake?” Wakasema: “Hapana.58” Pamoja na kuwepo fadhila hizi na ubora huu lakini (a.s.) alifanya subira kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na ndani ya mipaka ya Mwenyezi Mungu 56 - Sura Rum: 38. 57 - Sura Al-Mujadilah: 12. 58 - Faraidus-Samtwayn 1: 319, namba 251..
21
Page 21
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba ili asiwafarakishe Waislam, na wala watu wasirudi wakawa makafiri na kuuwana wao kwa wao. Subira hii ndio subira bora mno na ina malipo yasiyo na mfano. 12. Katika usamehevu (a.s.) alikuwa msamehevu mno dhidi ya mabaya kuliko watu wote na mwenye kutoa msamaha mno kwa mwenye kumkosea na alikuwa akisamehe wakati wa ujinga wa watu, na yeye ndiye mfano bora wa usamehevu. Amesema kweli Mtume wa Mwenyezi Mungu aliposema: “Laiti usamehevu ungekuwa ni mtu basi angekuwa Ali (a.s.).”59 Siku ya vita vya Jamal tunamkuta (a.s.) amemshinda Mar’wan bin AlHakam ambaye alikuwa adui mkubwa kwake na mwenye chuki mno juu yake (a.s.), lakini alimsamehe. Abdullah bin Zubayri alikuwa akimkashifu mbele ya watu, na siku moja wakati wa vita vya Basra alitoa hotuba na kusema: “Amekuijieni baradhuli muovu Ali bin Abi Talib.” Na Ali (a.s.) alikuwa akisema: “Zubayri aliendelea kuwa mtu miongoni mwetu AhlulBait mpaka alipopevuka Abdullah.” Lakini alipomshinda siku ya vita vya Jamal na kumchukua mateka alimsamehe na kumwambia: “Nenda zako nisikuone tena.” Hakumfanya kitu zaidi ya maneno hayo….60
Jambo la pili: Aya zilizoteremka kwa ajili ya Imam Ali (a.s.) na hazijateremka mfano wa hizo kwa ajili ya mwingine yeyote. Katika kipengele hiki tutachagua baadhi tu ya Aya zilizoteremka kwa ajili ya Ali (a.s.) na ambazo zinafafanua ubora wake juu ya sahaba wote, na wala si Aya zote ambazo zinafafanua ubora wake na ambazo ziliteremka kwa ajili yake moja kwa moja. Kwa sababu hili linahitaji mada yenye kujitegemea, kwani miongoni mwa Aya zipo ambazo zinamuhusu Ali (a.s.) pekee wala hazimuhusu mwingine yeyote, na kwa Aya hizo unathibiti ubora wake juu ya sahaba wote na kisha zinafafanua kiwango cha uhusiano 59 -Faraidus-Samtwayni 2: 68 namba 392. 60 - Sharhu Nahjul-Balagha cha Ibnu Abi Hadid 1: 22
22
Page 22
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba wa Ali (a.s.) na Qur’ani. 1. Imepokewa kutoka kwa Ibnu Abbas kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Hakuna Aya yoyote yenye “Enyi mlioamini” isipokuwa Ali ni kinara wake na kiongozi wake.”61 2. Pia imepokewa kutoka kwa Ibnu Abbas kuwa alisema: “Ilipoteremka “Sema: Kwa hayo siombi malipo yoyote kwenu isipokuwa mapenzi kwa ndugu wa karibu,”62 wakamwambia: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Ni nani akaraba zako ambao tumewajibishwa kuwapenda?” Akasema: “Ali, Fatima na watoto wao wawili wa kiume.”63 Kwa Aya hii inakuwa ni wajibu kwa sahaba mwingine kumpenda Ali (a.s.). 3. Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na uniwekee waziri katika jamaa zangu.”64 Imepokewa kutoka kwa Ibnu Abbas kuwa alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alimshika mkono Ali (a.s.) na mkono wangu tukiwa Makka akaswali rakaa nne kisha akainua mkono wake mbinguni na kusema: “Ewe Mwenyezi Mungu, hakika Musa bin Imran alikuomba na mimi Muhammad Mtume wako nakuomba unipanulie kifua changu, na ufungue fundo katika ulimi wangu wapate kufahamu kauli yangu, na uniwekee waziri katika jamaa zangu, ndugu yangu Ali bin Abi Talib, nitie nguvu kwa ndugu yangu, na umshirikishe katika kazi yangu.” Ibnu Abbas amesema: Nikasikia mnadi akinadi: “Ewe Ahmad umeshapewa ulichokiomba.”65 4. Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Hakika kiongozi wenu khasa ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na walioamini, ambao husi61 - An-Nuru Al-Mushtaal kutoka kwenye kitabu “Ma Nazala Minal-Qur’an fi Ali” cha Al-Hafidhu Ahmad bin Abdullah Al-Asbahaniy: 26. 62 - Sura Shura. 23. 63 - Khasaisul-Wahyi Al-Mubiin cha Ibnu Bitariq: 81. 64 - Sura Taha: 29. 65 - Khasaisul-Wahyi Al-Mubiin cha Ibnu Bitariq: 245.
23
Page 23
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba mamisha Swala na hutoa Zaka na hali ya kuwa wamerukuu.”66 Qur’ani Tukufu hasa katika Aya hii imebainisha ubora wa Imam Ali (a.s.) juu ya sahaba mwingine yeyote kwa kutegemea mfumo wa kuonyesha sehemu fulani ya mwenendo wenye kuandamana na tamko la wazi kuwa Ali ndiye mtawala wa waumini. Wote wamekubaliana juu ya kuteremka Aya hii kwa ajili ya Ali bin Abi Talib pindi alipotoa sadaka kwa kumpa masikini pete yake akiwa ndani ya Swala mbele ya sahaba. Zamakhshari amezungumzia kauli ya Mwenyezi Mungu: “Hali ya kuwa wamerukuu,” akasema: Imesemekena: Ni hali ya wenye kutoa Zaka, yaani wanaitoa ndani ya rukuu zao ndani ya Swala, na yenyewe iliteremka kwa ajili ya Ali, Mwenyezi Mungu (auhifadhi uso wake), pindi alipoombwa na ombaomba ilihali yeye akiwa mwenye kurukuu ndani ya Swala yake, ndipo akamtolea pete yake kana kwamba ilikuwa imelegea katika kidolepete chake, uvuaji wake haukumlazimu kitendo kinachobatilisha Swala yake. Ukisema: Vipi umuhusu Ali ilihali tamko ni la uwingi? Nitakwambia: Imekuja kwa tamko la uwingi japokuwa sababu ni mtu mmoja ili watu watamanishwe kitendo kama hiki na hivyo wapate mfano wa thawabu zake, na awazindue kuwa tabia za waumini ni wajibu ziwe kwa kiwango kama hiki katika kupupia kufanya wema na ihsani na kuwatunza mafakiri hata kama wakiwa ndani ya swala kisha likawalazimu jambo lisilokubali kucheleweshwa hawalicheleweshi mpaka mwisho wa Swala.67 66 - Sura Maida: 55. 67 - Al-Kashaf cha Zamakhshar 1: 648. Tafsir At-Tabari cha Ibnu Jarir At-Tabar 6: 186. As-Suyut ndani ya Ad-Durul-Manthur mwishoni mwa tafsiri ya Aya ya “Hakika kiongozi wenu khasa ni Mwenyezi Mungu na Mtume Wake…” katika Sura Maida, amesema: Al-Katib ametoa katika Hadithi muttafaqu kutoka kwa Ibnu Abbas amesema: Ali (a.s.) alitoa pete yake sadaka akiwa ndani ya rukuu, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akamuuliza ombaomba: “Nani aliyekupa pete?” Akajibu: “Yule mwenye kurukuu.” Basi Mwenyezi Mungu akateremsha: “Hakika kiongozi wenu khasa ni Mwenyezi Mungu na Mtume Wake…”.
24
Page 24
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba 5. Mwenyezi Mungu amesema: “Ewe Mtume! Fikisha uliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wako Mlezi….”68 Maimamu wa tafsiri na Hadithi wametamka wazi kuwa yenyewe iliteremka kwa ajili ya kubainisha ubora wa Ali (a.s.) siku ya Ghadir, siku ambayo Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) aliushika mkono wa Ali (a.s.) na kusema: “Yule ambaye mimi ni mtawala wake basi Ali ni mtawala wake, ewe Mola mpende ampendaye na mfanyie uadui atakayemfanyia uadui, msaidie atakayemsaidia na mtelekeze atakayemtelekeza na izungushe haki pamoja naye popote vyovyote atakavyozunguka.”69 Na kumpa Ali cheo hiki kutoka kwa Mola kwa mujibu wa Aya hii kunathibitisha kuwa yeye (a.s.) ndiye mbora baada ya Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu na wala si mwingine. 6. Mwenyezi Mungu amesema: “Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu watu wa nyumba na kukutakaseni kabisa.”70 Aya inaeleza kuhusu utashi wa Mwenyezi Mungu kukomea kwenye kuondoa uchafu dhidi ya Ahlul-Bayt na kuwatakasa kabisa kiukamilifu. Hakika kikomo hiki ni kwa yale tu yanayowahusu Ahlul-Bayt kwani Mwenyezi Mungu ana utashi mwingi wa kisheria na wa kiuumbaji wa lazima, hivyo maana yake ni kuwa utashi wa kuondoa uchafu na kutakasa ni muhtasi kwao bila kuhusisha wasiokuwa wao. 68 -Al-Maida: 67. 69 - Hiyo imetolewa kwa wingi mno na Maimam wa hadithi na historia, na pia uwingi wa kuteremka Aya hii Tukufu siku ya Ghadiri na hotuba ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) siku hii, tena mbele ya watu laki moja au zaidi, na wamenukuu uthibitishaji wa Ahlul-Bayt na sahaba wengine wengi, basi sisi kwa ajili ya muhtasari tutakomea kutaja vyanzo vichache mno kati ya vyanzo vingi mno vya tukio hilo, na kati ya hivyo ni Shawahidu At-Tanzil 1: 187. Ad-Durul-Manthur 2: 298. Fathul-Qadir 3: 57. Ruhul-Ma’an 6: 168. Al-Manar 6: 463. Tafsir At-Tabari 6: 198. As-Sawaiqul-Muhriqah: 75. 70- Al-Ahzab: 33.
25
Page 25
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba Hivyo inasihi kusema: Enyi Ahlul-Bayt, ninyi tu ndio ambao Mwenyezi Mungu ametaka kuwaondolea uchafu na kuwatakaseni na machafu, hivyo utashi huu bila kizuizi ni wa kiuumbaji, kwani hakika utashi wa kisheria wa kutakasa hauhusu kaumu fulani na kuiacha kaumu nyingine au nyumba hii na kuiacha nyumba nyingine. Utashi wa kiuumbaji toka kwa Mwenyezi Mungu hauachani na muradi, hivyo utakaso wa Ahlul-Bayt dhidi ya uchafu ni jambo lililotokea kwa utashi wa Mwenyezi Mungu, na hivyo wao ni Watakasifu dhidi ya madhambi na makosa. Hii ndio hali ionekanayo toka kwenye sentensi yenyewe bila kuangalia maelezo yaliyo kabla yake. Riwaya zinazothibitisha kuwa ilishuka kwa ajili ya Ahlul-Bayt - watu wa nyumba ya ufunuo waliotakasika Mtume Muhammad, Ali, Fatima, Hasan na Husein - na si kwa wengine ni nyingi sana, ni zaidi ya Hadithi sabini toka pande zote mbili. Hivyo ikiwa riwaya kama hizi hawazitegemei juu ya suala hili basi ni Hadithi ipi baada yake wataiamini?! Riwaya hizi ambazo Shia kwa njia yao wamezipokea toka kwa kiongozi wa waumini Ali na Ali bin Husein na Muhammad bin Ali na Jafar bin Muhammad na Ali bin Musa Ar-Ridha (a.s.) na toka kwa Ummu Salama na Abi Dharr na Abi Layla na Abi Aswadi Ad-Dawli na Ummari bin Maymuna Al-Awdiy na Sa’ad bin Abi Waqas. Na Sunni wamezipokea kwa njia zao toka kwa Ummu Salma na Aisha na Abi Said Al-Khidri na Saad na Wailatu bin Al-Askau na Abil-Hamra na Ibnu Abbas na Thaubani mtumishi wa Mtume na Abdallah bin Jafar na Ali bin Abi Talib na Hasan bin Ali (a.s.), zote zinaonyesha kuwa Aya hiyo ilishuka kwa ajili ya watu watano safi: Mtume wa Mwenyezi Mungu na Mwana wa ami yake Ali na Binti yake Fatima na wajukuu zake wawili Hasan na Husein (a.s.), na wao ndio muradi wa tamko Ahlul-Bayt na si wengine.71 71- Rejea Al-Imamatu Wal-wilayatu cha Jopo la wanazuoni: 150.
26
Page 26
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba Abdallah bin Ahmad bin Hanbali amepokea ndani ya Musnad yake kutoka kwa baba yake kutoka kwa Shadadu Abi Ammari amesema: “Niliingia kwa Wailu bin Al-Askau nikamkuta akiwa na watu na wakamtaja Ali, basi walipoondoka akasema: “Je nikupe habari niliyoyaona toka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu?” Nikasema: “Ndiyo.” Akasema: “Nilikwenda kwa Fatima kumuuliza kuhusu Ali, akasema: Ameelekea kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu. Basi nikamsubiri mpaka Mtume akaja akiwa pamoja na Ali, Hasan na Husein, akiwa amemshika mkono kila mmoja kati ya hao wawili. Akamsogeza Ali na Fatima na kuwakalisha mbele yake na akamkalisha Hasan na Husein kila mmoja juu ya paja lake, kisha akawafunika nguo - au shuka - kisha akasoma Aya hii: “Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu watu wa nyumba na kuwatakaseni kabisa,” na akasema: “Ewe Mwenyezi Mungu hawa ni Ahlul-Bayt wangu na watu wa nyumba yangu ndio wenye haki.”72 Na kwa maelezo haya Imam anamiliki nguvu ya utakaso ambayo yenyewe 72- Musnad Ahmad 4:107, Wafasiri wameafikiana juu ya kuteremka Aya ya utakaso nyumbani kwa Ummu Salama ikihusu ubora wa watu wa chini ya shuka, na imepokewa na watu wengi toka kwa Maimam wa Ahlul-Bayt na sahaba wengi, na ufuatao ni mfano tu wa vyanzo Hivyo: Al-Hafidhul-Kabiru Al-Hanafi maarufu kwa jina la Al-Hakim Al-Haskani ndani ya Shawahidut-Tanzili 2:10- 192 amepokea kwa njia mbalimbali. Na Al-Hafidhu Jalalud-Dini As-Suyuti ndani ya AdDurul-Man’thuri 5:198 Kaipokea kwa njia nyingi. Pia At-Tahawi ndani ya Mush’kilul-Athari 1:238-332. Na Al-Hafidhu Al-Haythami ndani ya Maj’mauz-
Zawaidu 9:121 na 146 na 169 na 172. Na Ahmad bin Hambali ndani ya AlMus’nadi 1:230 na 4: 107. Na Ibnu Hajar ndani ya As-Sawaiqu: 85. Na AtTabari ndani ya Tafsiri yake 22: 5 na 6 na 7. Na Ibnul-Athiri ndani ya Usudul-Ghaba 4: 29. An-Nasai ndani ya Khasais yake: 4.
27
Page 27
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba inatosha kabisa kuwa dalili kuwa yeye ni mbora kuliko wote waliyopo juu ya ardhi isipokuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.). 7. Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na atakayebishana nawe katika hili baada ya ujuzi uliokuijia, basi waambie: Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wanawake wetu na wanawake wenu, na nafsi zetu na nafsi zenu, kisha tuombe kwa unyenyekevu na tuiweke laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie wenye kusema uongo.”73 Amri ya kuita watoto, wanawake na nafsi imebeba tamko la uwingi sehemu zote na hivyo utekelezaji wa amri hii unahitaji kuhudhurisha kuanzia watu watatu kwenye kila anuani na si chini ya hapo ili itimie maana ya uwingi (jam’u’)-ndani ya kiarabu. Lakini kwa ushahidi wa Hadithi sahihi na historia, aliowaleta Mtume katika kutekeleza amri hii hawakuwa idadi hiyo, na kitendo chake hicho hakina sababu nyingine ila ni ile hali ya mfano halisi kukomea kwa wale tu aliowaleta. Hivyo tunapoangalia namna ya utekelezaji wa Aya hii kwa mujibu wa Mtume alivyofanya inaonyesha kuwa hawa ndio ambao walikuwa wanafaa kushiriki pamoja naye kwenye maapizano, na kuwa wao ndio vipenzi vyake kuliko viumbe wote na ndio watu maalumu na mahususi kwake, na hali hiyo inatosha kuwa fahari na fadhila kwao. Na kinachotia nguvu dalili juu ya hilo ni kuwa, yeye (s.a.w.w.) alikuwa na wanawake wengi lakini hakuja hata na mmoja miongoni mwao isipokuwa binti yake tu. Hilo halibebi ujumbe mwingine isipokuwa ni kuwa umahususi wake kwake na mapenzi yake kwake kwa ajili ya ukaribu wake – wa binti yake – kwa Mwenyezi Mungu na heshima yake kwake. Kama pia ilivyo hali ya kukomea anuani ya (nafsi) kwa Imam Ali tu na si kwa mtu mwingine inaonyesha ukubwa wa ubora wake na utukufu wa sifa 73 - Aali-Imran: 61.
28
Page 28
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba zake (a.s.), kiasi kwamba akachukua cheo cha nafsi ya Mtume (s.a.w.w.).74 Na hali hiyo inasisitizwa na kuungwa mkono na riwaya iliyopokewa na makundi yote mawili kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kuwa alimwambia Ali (a.s.): “Wewe kwangu mimi una cheo kama cha Haruna kwa Musa isipokuwa ni kuwa hakuna nabii baada yangu”75. Na kauli ya Mtume: “Wewe unatokana na mimi na mimi natokana na wewe.”76 Kiongozi wetu kiongozi wa waumini alitoa dalili kutumia ubora huu siku ya kamati ya watu sita, na watu wote wakakiri ubora huu na hakuna yeyote aliyempinga. Ubora huu umekuwa wazi mno kiasi kwamba nafsi haikubali kuukanusha hata nafsi ya mtu kama Ibnu Taymiyya. Hakika amekiri usahihi wa Hadithi hii akasema: “Hakika nafsi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) katika Aya ni Ali (a.s.) isipokuwa msingi wa kupewa nafasi hiyo ni undugu wa karibu.” Na alipogeukia kitendo cha kumpiku kwake ami yake Abbas, kwani ami ni ndugu wa karibu mno kuliko mtoto wa ami yake, akasema: “Hakika Abbas hakuwa miongoni mwa waumini wa mwanzo na wala hakuwa na umahususi kwa Mtume kama wa Ali.” Hivyo akalazimika kukiri kuwa msingi wa Ali kuchukua nafasi ya nafsi ya Mtume77 si tu undugu wa karibu bali pia alimtangulia kwenye Uislamu na akawa mtu muhtasi kwa 74 -At-Tafsir Al-Kabir cha Al-Fakh’rud-Din ar-Radhi: 8 / 81, tafsiri ya Aya ya 61 ya Surat Al-Imrani, Suala la tano. 75- Al-Bahrani amepata Hadithi mia moja zikiwa ni riwaya toka njia ya masunni na Hadithi sabini toka njia ya Mashi’a zote zikiwa na ibara hii. Rejea ndani ya Ghayatul-Marami Wahujatul-Khiswami: 1 / 109 -152. 76 - Khasais Amiril-Mu’minin cha An-Nasai: 88. 77 As-Sunan At-Tirmidhi: 5 / 596, hadithi ya 3724.
29
Page 29
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba Nabii, umahsusi wake kwa Mtume hautokani na chochote isipokuwa kwa ajili ya ubora wake kuliko mwingine yeyote na ukuruba wake kwa Mwenyezi Mungu.78 Kisha ndani ya kauli: “Tuwaite watoto wetu” kuna ishara kuwa mwenza ana hadhi maalum katika wito wa maapizano kiasi likajumuishwa tamko la watoto wa wanawake kwa mzungumzaji pamoja na mwenza wake ilihali mpingwaji alikuwa ni yeye tu, kama inavyoonyeshwa na kauli: “Na atakayebishana nawe.” Na hili ndilo tunalolipata toka kwenye kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na anaifuata na shahidi atokaye kwake”79 na kauli ya Mwenyezi Mungu: “Sema: hii ndiyo njia yangu, ninalingania kwa Mwenyezi Mungu kwa ujuzi, mimi na wanaonifuata.”80 Kama inavyoungwa mkono na riwaya zilizopokewa kuhusu hilo na ndio sababu ya msingi wa Mtume kumpa nafasi bila mipaka pale alipomwambia Ali: “Wewe kwangu mimi una nafasi kama ya Haruna kwa Musa”, na hilo linaungwa mkono na kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na tuiweke laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie wenye kusema uongo,”81 kwani muradi wa wenye kusema uongo hapa si kila aliye muongo katika kutoa habari na madai, bali muradi ni waongo wenye kulenga upande mmoja kati ya pande mbili za mabishano na maapizano. Hivyo hakuna kipingamizi kuwa kila upande kati ya pande mbili ni lazima mtoa madai awe ni zaidi ya mtu mmoja, na kama si hivyo basi ilifaa isemwe: “Na tuiweke laana ya Mwenyezi Mungu imshukie mwenye kusema uongo,” ili isihi kuitumia kwa mtu mmoja pia. Hivyo washiriki wenza na Mtume katika maapizano ni washiriki wenza katika madai. Kwa kuwa mabishano yalitokea kati ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na wakristo na si kwa ajili ya madai tu bali kwa ajili ya kuwaita kwenye 78 -Minhajul-Sunati cha Ibn Taymiyya: 4 / 33, Dalili ya Tisa 79 - Hud: 17. 80 - Yusuf: 108: 81 Aali-Imran: 61.
30
Page 30
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba Uislamu, na kuhudhuria kwenye maapizano kulitokana na madai na wito huo, basi mahudhurio ya aliyehudhuria ni dalili kuwa wahudhuriaji ni washiriki wenza katika madai na wito vyote viwili pamoja. Riwaya zilizotoka kwa sahaba kuhusu Aya ya maapizano ni nyingi mno, kama vile Riwaya ya Jabir bin Abdillah na Al-Barau bin Azibu na Anas bin Malik na Uthman bin Affan na Abdurahmani bin Auf na Talha na Zubeir na Saad bin Abi Waqas na Abdallah bin Abbas na Abi Rafiu mtumishi wa Mtume na wengineo. Na riwaya ya kundi la Tabiina akiwemo As-Saadiyu na As-Shaabiyu na AlKalbiyu na Abi Saleh. Na tabaka la wasimulizi wa hadithi na wanahistoria na wanatafsiri kwa kuiweka ndani ya vitabu vyao vya maarifa, kama vile Muslimu, At-Tirmidhi, At-Tabari, Abil-Fidau, As-Suyuti Az-Zamakhshari na Ar-Radhi wote wakipokea na kuafikiana kuhusu usahihi wake.82 Jabir amesema: “Kwao iliteremka: “Tuwaite watoto zetu na watoto zenu.” Jabir amesema: ‘Nafsi zetu” ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na Ali (a.s.). Na “watoto zetu” ni Hasan na Husein. Na “wanawake zetu” ni Fatima.83 8. Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Hakika wale walioamini na kutenda mema, hao ndio wema wa viumbe.”84 Imepokewa kutoka kwa Jabir bin Abdullah amesema: “Tulikuwa kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akaja Ali bin Abi Talib, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Hakika amewaijieni ndugu yangu.” Kisha akageukia Al-Kaaba na kuipiga kwa mkono wake, kisha akasema: “Naapa kwa yule ambaye nafsi yangu imo mikononi mwake, hakika huyu na wafuasi wake ndio wenye kufuzu Siku ya Kiyama.” Kisha akasema: “Hakika yeye ni wa kwanza wenu kuamini pamoja nami, mtekelezaji wa ahadi ya Mwenyezi Mungu kuliko nyinyi, mwenye msimamo zaidi katika dini ya Mwenyezi Mungu kuliko nyinyi, mwadilifu zaidi kwa raia kuliko 82 -Al-Imamatu Wal-wilayatu cha Jopo la wanazuoni: 138. 83 -Ghayatul-Marami: 301 Hadithi ya 7. 84 - Sura Al-Bayyinah: 8.
31
Page 31
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba nyinyi, mgawaji kwa usawa mno kuliko nyinyi na mwenye ubora mbele ya Mwenyezi Mungu kuliko nyinyi.” Akasema: Ikateremka: “Hakika wale walioamini na kutenda mema, hao ndio wema wa viumbe.” Akasema: Ikawa anapotokea Ali sahaba wa Muhammad husema: Amekuja mwema wa viumbe.”85
Jambo la tatu: Matamko jumuishi ya waziwazi kutoka kwenye Sunna ya Mtukufu Mtume yanasisitiza ubora wa Ali (a.s.) Lengo letu si kuonyesha riwaya zote kwa ukamilifu zilizotoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) kuhusu haki ya Ali (a.s.), au ambazo kupitia kwazo kinagundulika kina cha uhusiano wao wawili na sifa zake mahususi, au Ali huyo ndio mfano bora kutoka kwa Mola aliyeteuliwa kubeba amana baada ya Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), bali lengo letu ni kuchagua baadhi tu ya mifano ya riwaya ambazo kwazo Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amedhihirisha na kutoa ubora wa Ali (a.s.) juu ya sahaba, na tena si kwa lengo lingine bali ni kwa ajili ya yeye (s.a.w.w.) kutaka kuufikishia umma yale ayatakayo Mwenyezi Mungu. Miongoni mwa riwaya hizo ni: 1. Kutoka kwa Ali bin Abi Talib (a.s.) amesema: “Hakika Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwakusanya makurayshi kisha akasema: “Hakuna yeyote anayefaa kunilipia deni langu ila Ali.”86 85 - Ta’rikh Damashqi cha Ibnu Asakir 42: 371, wasifu wa Ali bin Abi Talib (a.s.). Wanachuoni wamepokea kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) kuwa mbora wa viumbe ni Ali na wafuasi wake. Miongoni mwao ni As-Suyuti ndani ya Ad-Durul-Manthur 6: 379. Ibnu Hajar ndani ya As-Sawaiq: 96, 159. As-Shawkaniy ndani ya Fat’hul-Qadir 5: 464. Al-Ulus ndani ya Tafsiir yake 30: 207. At-Tabar ndani ya Tafsiir yake 3: 171. As-Shablanji ndani ya Nurul-Absar: 105. Al-Hakim Al-Haskaniy ndani ya Shawahidu At-Tanzil 2: 356. 86 - Ta’rikh Damashq cha Ibnu Asakir 42: 47.
32
Page 32
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba 2. Kutoka kwa Abdullah amesema: “Imam Ali aligonga mlango wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) katika nyumba ya Ummu Salamah, Mtume akamwamuru mkewe aufungue, na tayari alikuwa keshamwambia kuwa, atakayegonga ni mtu anayempenda Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, basi alipoingia akasema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.): “Ewe Ummu Salamah! Unamjua?” Akajibu: ndiyo ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, huyu ni Ali bin Abi Talib. Mtume akasema: “Umesema kweli, ni bwana nimpendaye, nyama yake inatokana na nyama yangu na damu yake inatokana na damu yangu na yeye ndiye msiri wa nyumba yangu, sikia na shuhudia, na yeye ndiye atakayewauwa wavunja kiapo, wenye kujitenga na haki na wenye kutoka ndani ya dini basi sikia na shuhudia, na yeye ndiye atakayetekeleza usia wangu basi sikia na shuhudia, naapa kwa Mwenyezi Mungu yeye ndiye atakayehuisha Sunna yangu basi sikia na shuhudia. Laiti mja atamwabudu Mwenyezi Mungu miaka elfu moja baada ya miaka elfu moja, na miaka elfu moja akiwa kati ya Ruknu na Maqam, kisha akakutana na Mwenyezi Mungu akiwa ni mwenye kumchukia Ali bin Abi Talib na kizazi changu, Siku ya Kiyama Mwenyezi Mungu atamwingiza ndani ya Moto wa Jahannam huku pua yake ikiwa chini.”87 3. Iliyopokewa kutoka kwa Ali (a.s.) kuwa alisema: “Watu kutoka kwa makurayshi walimjia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kumwambia: “Ewe Muhammad! Sisi ni jirani zako na rafiki zako, na miongoni mwa watumwa wetu wapo waliyokuja kwako huku wakiwa hawana raghba na dini wala raghba na elimu, bali wamekimbia kutokana na ukabwela wetu na mali zetu basi warudishe kwetu.” Akamwambia Abi Bakr: “Unasemaje?” Akasema: “Wamesema kweli wao ni jirani zako na rafiki zako.” Basi uso wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ukabadilika, kisha akamwambia Umar: “Unasemaje?” Akasema: “Wamesema kweli wao ni jirani zako na rafiki zako.” Basi uso wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ukabadilika, kisha akasema: 87-Ta’rikh Damashq cha Ibnu Asakir 42: 47.
33
Page 33
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba “Enyi kundi la makurayshi! Naapa kwa Mwenyezi Mungu hakika Mwenyezi Mungu atawatumia mtu miongoni mwenu ambaye Mwenyezi Mungu ameutahini moyo wake kwa imani ili awapige nyinyi kwa ajili ya dini au awapige baadhi yenu.” Abu Bakr akasema: “Ni mimi ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?” Akajibu: “Hapana.” Umar akasema: “Ni mimi ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?” Akajibu: “Hapana, lakini ni yule anayeshona viatu.” Na alikuwa tayari ameshampa Ali (a.s.) viatu anavishona.”88 4. Az-Zamakhshari amepokea kwa njia yake akasema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Fatima ni damu ya moyo wangu na wanae ni matunda ya kifua changu na mumewe ni nuru ya macho yangu na maimam kutoka kwenye kizazi chake ni wasiri wa Mola Wangu Mlezi na kamba iliyonyooka kati Yake na viumbe Wake, basi atakayeshikamana nao ataokoka na atakayewaacha ataangamia.”89 Na kwa ajili hii (a.s.) wanakuwa wabora kuliko yule mwenye kushikamana nao, kwa sababu wao wanamwongoza upande wa uongofu, na kwa njia bora kabisa wanakuwa (a.s.) wabora kuliko sahaba yeyote anayewakhalifu, kwa sababu Mwenyezi Mungu na Mtume Wake wako pamoja na yule mwenye kushikamana nao na si yule mwenye kuwakhalifu. Na inajulikana waziwazi kuwa sahaba wengi si kwamba waliwakhalifu tu bali pia waliwapiga vita vikali. Na Ali (a.s.) ameshaweka wazi msimamo wake juu ya 88 - Tadhkiratul-Khuwwais: 40. Al-Mustadrak 2: 137. Kanzul-Ummal 13: 127, hadithi ya 36403. Sharhu Maanil-Athar 2: 408. Manaqib cha Ibnu Shahr Ashub 2: 44. 89 - Ameipokea Az-Zamakhshar ndani ya kitabu chake Al-Manaqib: 213. Sheikh Jammalud-Din Al-Hanafiy Al-Muuswiliy ndani ya kitabu Duraru BahrulManaqib: 116. Al-Hafidhu Muhammad bin Abil-Fuwwaris ndani ya kitabu AlArbaun: 14. Ihqaul-Haq 4: 228 na 9: 198. Na ameipokea Sheikh Sulayman ndani ya Yanabiul-Mawaddah: 82. Na Al-Muwathaqu Al-Khawarazamiy ndani ya Maqtalul-Husayni: 59.
34
Page 34
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba baadhi ya sahaba kama ilivyo ndani ya hotuba maarufu ijulikanayo kwa jina la Shaqshaqiyyah. Pia msimamo wa Az-Zahrau uko wazi mno kupitia hotuba yake aliyoitoa ndani ya msikiti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) baada ya kifo cha baba yake baada ya kuonekana picha halisi ya kiwango cha uasi wa baadhi ya sahaba dhidi ya njia ya Ali (a.s.). 5. Imepokewa kutoka kwa Abi Said Al-Khudri kuwa alisema: “Tulikuwa tumeketi tukimngojea Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na ndipo alipotutokea akitokea kwenye nyumba ya mmoja ya wakeze.” Akasema: “Basi tukasimama pamoja naye na ghafla kiatu chake kikakatika na akamuacha Ali akikishona. Basi Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akaondoka na tukaondoka pamoja naye, kisha akasimama akimngojea nasi tukasimama pamoja naye, ndipo akasema: “Hakika miongoni mwenu yupo atakayepigania maana ya Qur’ani hii kama nilivyopigania uteremkaji wake.” Basi kila mmoja akajitanguliza akiwemo Abu Bakr na Umar. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akasema: “Hapana, lakini ni mshona viatu.” Akasema: Tukaja kumbashiria, na alikuwa kama keshazisikia. Na katika riwaya nyingine amesema: Hakuinua kichwa kwa ajili ya habari hizo kana kwamba keshazisikia.”90 Kwa aina hili ya riwaya Ali (a.s.) anapata ubora juu ya sahaba wote kwa sababu ndiye mwenye kuchukua nafasi ya kuthibitisha haki kipindi cha baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), na ni wajibu kwa sahaba wote kumfuata. 6. Imepokewa kwa njia mbalimbali kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Hakika Ali anatokana na mimi na mimi natokana na Ali, na yeye ndiye mtawala wa kila muumini baada yangu, yeyote hafikishi 90 - Musnad Ahmad bin Hanbal 3: 83. Na ndani ya Hilyatul-Awliyai cha Abi Naim imo yenye maana hii. Na Usudul-Ghaba cha Ibnu Athir 3: 283.
35
Page 35
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba kuhusu mimi ila mimi au Ali.”91 7. Msimamo wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) dhidi ya makhalifa wawili katika suala la kumuoa Fatima unadhihirisha jinsi gani Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alivyomjali Ali (a.s.) kipekee kuliko wao wawili. Imepokewa kutoka kwa Abdullah bin Yazid kutoka kwa baba yake amesema: “Abu Bakr na Umar walimposa Fatima, Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akasema: “Hakika yeye bado mdogo.” Ali (a.s.) akamposa na akamuoa.”92 8. Kisa cha kuzibwa milango isipokuwa mlango wa Ali tu Imepokewa ndani ya kitabu Musnad cha Ahmad kwa njia mbalimbali kuwa: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliamuru milango yote izibwe ila mlango wa Ali (a.s.), basi watu wakanung’unika, ndipo Mtume wa Mwenyezi Mungu akatoa hotuba, akamuhimidi Mwenyezi Mungu na kumsifu kisha akasema: “Ama baada, hakika mimi nimeamrishwa kuziba milango hii isipokuwa mlango wa Ali, hivyo baadhi yenu wamenung’unika, lakini naapa kwa Mwenyezi Mungu sikuziba chochote wala kukifungua ila ni kitu nilichoamrishwa nami nikafuata.”93 91 - Musnadu Ahmad 4: 164 na 165, katoa kwa njia tano. Khasais AmirilMu’minin cha An-Nasai: 19 na 20, katoa kwa njia mbili. Sahih Bukhari 3: 229. Sawaiqu Al-Muhriqah: 74. Kanzul-Ummal cha Al-Mutaqiy Al-Hindi 11: 607, hadithi ya 32938. Sunan At-Tirmidhi 5: 591, hadithi ya 3712. 92 -As-Sunan Al-Kubra cha An-Nasai 3: 265, hadithi ya 5329. Sahih Ibnu Habban 15: 399. Mawaridu Ad-Daman cha Al-Haythami: 549. Al-Manaqib cha Ibnu Shahri Ashub 3: 345. Tadhkiratul-Khuwwas: 306. 93 - Al-Qawlu Al-Musaddad fi Musnad Ahmad: 17. Sharhu Nahjul-Balagha 9: 173. KanzulUmmal 11: 598, hadithi ya 32877, na 618 hadithi ya 33004. Faydhul-Qadir 1: 120. Musnad Ahmad 1: 175 na 4: 369. Mustadrak Al-Hakim 3: 4, 116 na 125. Khasais cha An-Nasai: 13. Sahih At-Tirmidhi 2: 301. Ad-Durul-Manthur 6: 122. As-Sawaiq Al-Muhriqah: 76.
36
Page 36
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba 9. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aunga udugu na Ali (a.s.) Tunamkuta Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ameweka undugu kati ya watu na akimuacha Ali awe wa mwisho wao akiwa haoni ni nani ndugu yake, akasema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Umeweka undugu kati ya sahaba zako na umeniacha?” Akasema (s.a.w.w.): “Hakika nimekuacha kwa ajili yangu mwenyewe, wewe ni ndugu yangu na mimi ni ndugu yako, yeyote akikusema basi sema: Mimi ni mja wa Mwenyezi Mungu na ndugu wa Mtume Wake, hakuna yeyote atakayedai hayo mawili baada yako ila ni mwongo. Naapa kwa yule aliyenipa utume kwa haki, sikukubakiza isipokuwa ni kwa ajili yangu mwenyewe.”94 10. Baadhi ya fadhila pekee za Ali (a.s.) zinapatikana kwa muhtasari ndani ya riwaya iliyopokewa kutoka kwa Saad bin Abi Waqas, amesema: “Naapa kwa Mwenyezi Mungu, kuwa na kimoja kati ya vitu vitatu ni jambo nilipendalo mno kuliko kuwa na yote yaliyochomozewa na jua. “Awe ameniambia yale aliyomwambia alipomzuia asiende Tabuk: “Hivi uridhii kuwa na nafasi kwangu kama ya Harun kwa Musa isipokuwa ni kuwa hakuna Nabii baada yangu.” Ni jambo nilipendalo mno kuliko kuwa na yote yaliyochomozewa na jua. “Awe ameniambia yale aliyomwambia siku ya Khaybar: “Hakika nitamkabidhi bendera mtu anayempenda Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, Mwenyezi Mungu atashinda mikononi mwake na si mkimbiaji.” Ni jambo nilipendalo mno kuliko kuwa na yote yaliyochomozewa na jua. “Na niwe na binti yake na niwe nimepata mtoto kutoka kwake kama aliye naye. Ni jambo nilipendalo mno kuliko kuwa na yote yaliyochomozewa na 94 - Usudul-Ghaba cha Ibnu Al-Athir 4: 29, wasifu wa Ali bin Abi Talib. Tahdhibul-Kamal 5: 126. Ar-Riyadhu An-Nadhirah 2: 168. Kanzul-Ummal 13: 140, hadithi ya 36440. At-Taju Al-Jamiu Lil-Usul 3: 335. Maswabihus-Sunnah 2: 199. Dhakhairul-Uqba: 92. Usudul-Ghaba 3: 317. Khasais cha An-Nasai: 18.
37
Page 37
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba jua.”95
Jambo la nne: Mtazamo wa sahaba kuhusu utu wa Imam Ali (a.s.) Hakika harakati za ujumbe na juhudi za kiroho ambazo Imam Ali bin Abi Talib (a.s.) alizidhihirisha ili kutimiza ujumbe na kuinua juu neno la haki tangu (s.a.w.w.) kupewa utume mpaka mwisho wa ujumbe wake zimeacha athari na taswira chanya zenye kuathiri ndani ya nafsi za sahaba, kiasi kwamba hatua zake zimetengeneza kituo cha nguvu na harakati, sawa iwe zama za utume au baada ya kifo cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kwani yeye ndiye marejeo ya Makhalifa pindi yanapowabana mambo magumu na akili zao kushindwa kujua malengo ya Sheria na ukweli wake halisi. Jambo hili halihitaji ufafanuzi na ubainishaji zaidi, kwani hilo limejaa ndani ya vitabu vya historia na sera. Vyovyote vile ni kuwa, hakika mitazamo na maono ya sahaba kuhusu Ali (a.s.) ni jambo lisilowezekana kuchambuliwa lote ndani ya kifungu hichi tu, lakini pamoja na hayo sisi tutakomea kwenye baadhi tu ya matamshi ya waziwazi ya sahaba kuhusu Ali (a.s.) na ubora wake juu ya sahaba wote kama ifuatavyo:
1. Khalifa wa kwanza: Tunamkuta khalifa wa kwanza Abu Bakr akirejea kwa Imam katika kutafuta utatuzi wa matatizo mbalimbali, kwa mfano Abu Bakr alipotaka kuishambulia Rumi kivita aliomba ushauri toka kwa baadhi ya sahaba wa Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), wakawa wameakhirisha vita. Ndipo akamtaka ushauri Ali bin Abi Talib (a.s.), yeye akamshauri apigane, akamwambia: “Ukipigana utashinda.” Abu Bakr akassema: 95 -Murujud-Dhahab 2: 61. Sunan At-Tirmidhi 2: 300. Musnad Ahmad 1: 185. Khasaisu Amiril-Mu’minin cha An-Nasai: 116.
38
Page 38
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba “Umetabiri kheri.” Abu Bakr akasimama katikati ya watu akawahutubia na kuwaamuru wajiandae kuelekea Rumi.96 Ama upande ya tafsiri tunamkuta anakiri kuwa hawezi kutafsiri baadhi ya Aya za Qur’ani. Imepokewa kutoka kwa Abi Malikah amesema: “Abu Bakr aliulizwa tafsiri ya herufi toka ndani ya Qur’ani akasema: Ni mbingu ipi itanifunika na ni ardhi ipi itanimeza na ni wapi nitakwenda na nitafanyaje iwapo nikitafsiri herufi toka ndani ya Kitabu cha Mwenywezi Mungu kwa tafsiri asiyoitaka?”97 Na alikuwa ameulizwa kuhusu kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na matunda na malisho.”98 Basi yalipomfikia kiongozi wa waumini yale aliyoyasema, akasema (a.s.): “Ewe Mwenyezi Mungu umetakasika! Hivi hakujua kuwa neno Abba ni malisho na machungio, na kuwa kauli ya Mwenyezi Mungu “Na matunda na malisho.” Ni orodha kutoka kwa Mwenyezi Mungu ya neema Zake juu ya viumbe Wake kwa yale aliyowalisha na kuyaumba kwa ajili yao na kwa ajili ya wanyama wao miongoni mwa mambo ambayo kwayo anawapa uhai na kwayo miili yao inakuwa bora.” 99 Kama alivyotamka waziwazi khalifa wa kwanza kuwa yeye hana uwezo wa kumwelezea kwa undani Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kama alivyo, na Imam Ali bin Abi Talib ndiye mwenye uwezo juu ya hilo, kwa sababu yeye ndiye aliyekuwa karibu mno na ndiye ajuaye sana siri za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na utume. Imepokewa kutoka kwa Ibnu Umar amesema: “Mayahudi walikwenda kwa Abu Bakr wakamwambia: “Tupe wasifu wa rafiki yako.” Akasema: 96 - Ta’rikh Al-Yaaqubiy 2: 111. 97- Muntakhabu Kanzul-Ummal kwenye maelezo ya Musnad Ahmad bin Hambal 5: 396. 98- Sura Abasa: 31. 99 - Al-Irshad cha Sheikh Al-Mufidu 1: 200, uhakiki wa taasisi ya Ali Al-Bayti (a.s.).
39
Page 39
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba Enyi mayahudi, bila shaka mimi nilikuwa naye kwenye pango kama vidole vyangu hivi viwili, na hakika nilipanda naye mlima wa Hira huku kidole changu kidogo kikiwa kwenye kidole chake kidogo, lakini kutoa wasifu wake ni jambo gumu mno, huyu hapa Ali bin Abi Talib.” Basi wakamwendea Ali (a.s.) na kumwambia: “Ewe baba Hasan, tupe wasifu wa binamu yako.” Akasema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu hakuwa mrefu mno wala mfupi wa kupindukia bali alikuwa amevuka kati kidogo, mwenye rangi nyeupe, mwekundu usoni, mwenye nywele zisizo fupi mno, nywele zake zinafika juu ya pua, mwenye paji la ubapa lililochomoza, mwenye macho mapana yaliyo meusi mno, huku akiwa na mapitio membamba ya machozi. Meno yake ya mbele ni yenye kung’aa mno, mwenye pua nyembamba yenye mwinuko, shingo yake ni kama birika la fedha. Ana nywele ndogondogo kuanzia mwanzo wa kifua hadi kwenye kitovu, zenyewe ni kama tawi la mti mweusi wa miski, mwilini mwake na kifuani kwake hana nywele nyingine zaidi ya hizo. Alikuwa mwenye kitanga na nyayo ngumu, anapotembea hutembea kama anainama, na anapogeuka hugeuka mwili mzima, na anaposimama watu humfika shingoni, na anapoketi huwa juu zaidi ya watu, anapoongea huwanyamazisha watu, na anapohutubia huwaliza watu. Alikuwa mwenye huruma kwa watu kuliko watu wote, kwa mayatima alikuwa kama baba mwenye huruma, kwa wajane alikuwa mkarimu. Alikuwa shujaa mno kuliko watu wote na mwenye mkono wa kutoa mno kuliko wao na mzuri wa uso kuliko wao. Vazi lake ni joho, chakula chake ni mkate wa shayiri na siagi yake ni maziwa, mto wake ni ngozi iliyojazwa maganda ya mtende, kitanda chake ni mghiliyani100 halisi kilichopambwa kwa johari. Alikuwa na vilemba viwili kimoja kikiitwa mawingu na kingine kikiitwa nyota, upanga wake ulikuwa ni wenye ncha mbili, na ben100 - Jina la mti – (Mtarjumi.)
40
Page 40
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba dera yake ilikuwa na mng’ao mweupe, ngamia wake alikuwa ni mwenye masikio ya kupasuka, nyumbu wake alikuwa mwenye kunesa, punda wake alikuwa ni mbuzimawe, farasi wake alikuwa ni mtoa sauti, mbuzi wake alikuwa ni mwenye kutoa maziwa sana, upinde wake ulikuwa mrefu mwembamba, bandera yake ilikuwa ni yenye kusifiwa. Alikuwa akimfunga kamba ngamia na akimlisha aliyopo manyweshoni, alikuwa akisafisha nguo na akishona viatu.”101
2. Khalifa wa pili: Imam Ali (a.s.) ndani ya nafsi yake aliacha athari nyingi mpaka maneno yake: “Laiti kama si Ali basi Umar angeangamia.”102 Yakawa mashuhuri katika maeneo mbalimbali. Na kauli yake: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Hajachuma mchumaji mfano wa fadhila ya Ali, humwongoza sahaba wake katika haki na humzuia na angamio.”103 Imepokewa kutoka kwa Muhammad bin Khalid Ad-Dhabi amesema: Siku moja Umar bin Al-Khattabi aliwahutubia akasema: “Hivi tukiwaondoa toka kwenye yale myajuayo na kuwapeleka kwenye yale msiyoyapenda, mtafanya nini?” Amesema: Wakanyamaza, akarudia maneno hayo mara tatu. Akasimama Ali (a.s.) na kusema: “Ewe Umar! Tutakuomba uombe toba, ukitubu tutakukubali.” Akasema: Iwapo nisipotubu? Akasema: “Tunatupilia mbali unayoyakodolea macho.” Akasema: “Kila sifa njema ni za Mwenyezi Mungu ambaye amemuweka ndani ya umma huu mtu ambaye tunapopinda hunyoosha mpindo wetu.”104
101 - Ar-Riyadhu An-Nadhirah fi Manaqibil-Ushrah cha Abi Jafar At-Tabari 3: 162.102 - Kanzul-Ummal 1: 154. Dhakhairul-Uqba: 82. Faydhul-Qadir 3: 356. Mustadrakul-Hakim 1: 457. Al-Isti’ab pambizoni mwa Al-Isabah 3: 39. 103 - Ar-Riyadhu An-Nadhirah cha Al-Muhibu At-Tabari 3: 189. 104 - Manaqibul-Khawarazam. Muwaffaqu Ibnu Ahmad Al-Hanafiy: 98, uhakiki wa Malik Al-Mahmudiy.
41
Page 41
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba Kisha tunamkuta khalifa wa pili akimtaka ushauri kuhusu pombe na kipimo cha adhabu yake, kwani imepokewa kutoka kwa Thawru bin Yazad AdDayliyu kuwa Umar bin Al-Khattab alimtaka ushauri kuhusu pombe anayokunywa mtu, Ali bin Abi Talib akasema: “Mpige viboko themanini, kwani atakapokunywa atalewa na atakapolewa ataweweseka na atakapoweweseka atazua uwongo.” Ndipo Umar akaanza kutoa adhabu ya viboko themanini kwenye pombe.”105 Na imepokewa kutoka kwa Udhaynah kuwa nilimjia Umar na kumuuliza: Nianzie wapi kufanya Umra? Akasema: “Nenda kamuulize Ali (a.s.).”
3. Khalifa wa tatu: Uthman bin Affan ana matukio mengi aliyorejea kwa Imam katika mambo tata ambayo hakuwa na utatuzi wake, kwani imepokewa kutoka kwa Ujah bin Abdullah Al-Juhayni amesema: “Mwanaume kutoka kwetu alioa mwanamke kutoka kabila la Juhaynah kisha akamzalia mtoto akiwa na miezi sita tangu waowane, basi mume akaenda kwa Uthman bin Affan na hivyo akatoa amri apigwe mawe, habari hizo zikamfikia Ali (a.s.) ndipo alipomjia na kusema: “Unafanya nini?” akasema: “Amezaa ndani ya miezi sita kamili, hivi hilo linawezekana?” Ali (a.s.) akajibu: “Hivi hujasikia Mwenyezi Mungu anasema: “Na kumbeba na kumwachisha ziwa ni miezi thelathini,” inabaki mingapi? Hakuna zaidi ila miezi sita.” Uthman akasema: “Wallahi sikulijua hili.”106” Na kutoka kwa Muhammad bin Yahya bin Habban amesema kuwa: Kwa babu yake Habban bin Munqidhu kulikuwa na wanawake wawili, mmoja wa kihashim na mwingine wa kiansari, basi yule wa kiansari akatalikiwa ilihali akiwa ananyonyesha, na ukapita mwaka mzima bila kuona damu yake ya mwezi, kisha mwanaume akafariki, ndipo yule wa kiansari akasema: Mimi nitamrithi kwani sijaona damu yangu ya mwezi.” Ndipo 105 -Kanzul-Ummal 3: 100. Sharhul-Muwatau cha Az-Zarqaniy 4: 25. 106 - Ad-Durul-Manthur 6: 40.
42
Page 42
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba wakapeleka mzozo wao kwa Uthman bin Affan naye akahukumu apewe mirathi, basi yule wa kihashim akamlaumu Uthman bin Affan na ndipo Uthman akamwambia: “Hii ni kazi ya binamu yako, kwani ndiye aliyetupa ushauri huu, yaani Ali bin Abi Talib.”107 Na imepokewa kutoka kwenye mtiririko wa Hadithi za Uthman kuwa: “Uthman bin Affan aliletewa mtu aliyemlawiti kijana wa kikurayshi, Uthman akasema: “Ameshaoa?” Wakasema: “Ndiyo, kamuoa mwanamke lakini bado hajamwingilia.” Ali akamwambia Uthman: “Angekuwa kishamwingilia ingekuwa ni halali kupigwa mawe, ama ikiwa hajamwingilia mchapeni viboko vya kisheria.” Abi Ayyub akasema: “Nashuhudia hakika mimi nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akisema hili alilolisema Abal Hasan.” Uthman akaamuru achapwe viboko, na akachapwa viboko.”108
4. Ibnu Abbas: Amesema (r.a.): “Wallahi hakika Ali alipewa tisa ya kumi ya elimu, naapa kwa Mwenyezi Mungu na moja iliyobaki kashiriki nanyi.”109 Amesema (r.a.): “Elimu ya Mtume inatokana na elimu ya Mwenyezi Mungu, na elimu ya Ali inatokana na elimu ya Mtume, na elimu yangu inatokana na elimu ya Ali, na elimu yangu na elimu ya sahaba si chochote isipokuwa ni sawa na tone la maji ndani ya bahari saba.”110 Na amesema (r.a.): “Elimu ni sudusi sita, Ali ana sudusi tano na waliobaki wana sudusi moja, na bila shaka ameshiriki nasi katika sudusi hiyo moja 107 - Kanzul-Ummal 5: 829, hadithi ya 14505, imenukuliwa kutoka kwenye kitabu Al-Muwatau cha Malik na Sunan cha Al-Bayhaqiy. 108 -Kanzul-Ummal 5: 469, hadithi ya 13642, imenukuliwa kutoka kwenye AlMuujam Al-Kabir cha At-Tabaran. 109 - Al-Isti’ab cha Ibnu Abdul-Bari 3: 41. Ar-Riyadhu An-Nadhirah 2: 149. 110 - Yanabiul-Mawaddah: 70.
43
Page 43
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba mpaka yeye amekuwa ndiye mjuzi mno wa sudusi hiyo moja kuliko sisi.”111
5- Ibnu Mas’ud: Amesema (r.a.): “Tulikuwa tukizungumza kuwa mjuzi mno wa hukumu kuliko watu wote wa Madina ni Ali.”112 Na amesema (r.a.): “Hekima iligawanywa sehemu kumi, Ali akapewa sehemu tisa na watu wakapewa sehemu moja, na Ali ndiye mjuzi mno wa sehemu hiyo moja.”113 Na amesema (r.a.): “Mjuzi mno wa faradhi ni Ali bin Abi Talib.”114 Na amesema (r.a.): “Mjuzi mno wa faradhi na hukumu katika watu wa Madina ni Ali.”115 Na amesema (r.a.): “Hakika Qur’ani iliteremshwa kwa herufi saba, na hakuna yoyote ile kati ya hizo ila ina maana ya nje na ndani, na hakika kwa Ali bin Abi Talib ndiko kuna maana ya nje na ndani.”116
6. Adiyy bin Hatim: Katika hotuba yake: “Wallahi ikiwa ni kwenda kwenye elimu ya Kitabu na Sunna basi ni kwa Ali, kwa mjuzi mno wa hivyo viwili kuliko watu wote, na ikiwa ni kwenda kwenye Uislamu basi ni kwa ndugu wa Mtume na wa kwanza ndani ya Uislamu, na ikiwa ni kwenda kwenye akili na ukamilifu basi ni kwa mwenye akili mno kuliko watu wote na mwenye uzalendo bora kuliko wao.”117 111 -Al-Manaqib cha Al-Khawarazami: 55. Faraidu As-Samtwayn 1: 366. 112 Al-Mustadrak 3: 41. Asnal-Matalib cha Al-Jazari: 14. As-Sawaiq AlMuhriqah cha Ibnu Hajar: 76.
113 -Kanzul-Ummal 5: 156 na 401.114 - Al-Isti’ab 1: 41. Ar-Riyadhu AnNadhrah 2: 194. 115 - Ar-Riyadhu An-Nadhrah 2: 198. Ta’rikhul-Khulafai cha As-Suyuti: 115. 116 -Miftahu As-Saadah 1: 400. 117 -Jamharatu Khutubul-Arab 1: 202.
44
Page 44
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba 7. Abi Sa’id Al-Khudri: Amesema: “Mjuzi mno wa hukumu ni Ali.”118
8. Aisha: Amesema: “Ali ndiye mjuzi mno wa Sunna kuliko watu wote.”119
9. Atau: Atau aliulizwa: “Je, katika sahaba wa Muhammad alikuwepo mjuzi kuliko Ali?” Akasema: “Hapana, Wallahi simjui.”120
10. Said Al-Musayyib: Amesema: “Umar alikuwa akijikinga kwa Mwenyezi Mungu dhidi ya tatizo lolote asipokuwepo Abil Hasan.”121
11. Muawiya bin Abi Suf’yan: Amesema: “Umar alikuwa anapotatizwa na kitu hukichukua kutoka kwa Ali.”122 Na mtu mmoja akaenda kwa Muawiya na kumuuliza kuhusu suala fulani, akajibu: “Hilo muulize Ali bin Abi Talib yeye ndiye mjuzi mno.” Akasema: “Ewe kiongozi wa waumini! Jibu lako nalipenda mno kuliko jibu la Ali. Akasema: “Ni baya sana ulilosema, unamchukia mtu ambaye 118 -Fat’hul-Bari cha Ibnu Hajar 8: 136. 119 - Al-Isti’ab 3: 40. Ar-Riyadh An-Nadhirah 2: 193. Manaqibul-Khawarazam: 45. As-Sawaiqu: 76. Ta’rikhul-Khulafai: 115. 120 -Al-Isti’ab 3: 40. Al-Futuhati Al-Islamiyyah 2: 337. 121 -Al-Isti’ab cha Ibnu Abdul-Bar pembezoni mwa Al-Isabah 3: 39. WasfatusSaf’wah cha Ibnu Al-Jawzi 1: 121. Al-Isabah 2: 509. Ar-Riyadhu An-Nadhrah 2: 194. As-Sawaiqu cha Ibnu Hajar: 76. Faydhul-Qadir cha Al-Munawi 4: 357. 122 - Ar-Riyadhu An-Nadhirah 2: 194. Matalibu As-Suul: 30.
45
Page 45
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alikuwa akimwagia mvua ya elimu, na bila shaka alimwambia: “Nafasi yako kwangu ni sawa na nafasi ya Harun kwa Musa isipokuwa hakuna Nabii baada yangu.”123”
12. Said bin Ghaflah: Niliingia kwa Ali bin Abi Talib (a.s.) nikamkuta ameketi huku mbele yake kukiwa na sahani yenye maziwa huku yakitoa harufu kali kutokana na uchachu wake, na mikononi alikuwa na kipande cha mkate, huku nikiona athari za pumba za shayiri usoni kwake, akawa anaukata kwa mkono wake, na unapomchosha huukata kwa goti lake na kuuweka ndani ya maziwa. Akaniambia: “Sogea, upate chakula chetu hiki.” Nikasema: “Mimi nimefunga.” Akasema: “Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akisema: “Mwenye kuzuiliwa na Saumu kula chakula akipendacho basi ni haki kwa Mwenyezi Mungu kumlisha chakula cha Peponi na kumnywesha kinywaji chake.”124
13. Ibnu Umar: Amesema: “Ali alikuwa na mambo matatu, kuwa na moja kati ya hayo ni jambo nilipendalo mno kuliko ngamia mwekundu: Kumuoa Fatima (s.a.), kupewa bendera siku ya Khaybari na Aya ya mazungumzo ya faragha.”125
Jambo la tano: Mambo ya pekee ambayo kwayo Ali (a.s.) aliyojitenga dhidi ya sahaba wengine Bila shaka Imam Ali (a.s.) alikuwa anamiliki sifa nyingine za pekee alizotunukiwa na Mwenyezi Mungu kwa lengo la kutekeleza jukumu la uimam baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) kama vile elimu ya mambo ya ghaybu aliyotunukiwa na Mwenyezi Mungu, na kwa ajili hii 123 -Ar-Riyadhu An-Nadhirah 3: 162. 124 -Rejea Kashful-Ghummah 1: 163. 125 -Tafsir At-Tha’alabi: 254.
46
Page 46
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba tunamkuta anatoa habari za matukio ya mustakbali yatakayotokea baadae. Kama pia alivyopata hadhi kupitia harakati za Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) zilizotilia mkazo ulinzi wa njia ya Ali (a.s.) baada ya kifo chake (s.a.w.w.), na kwa ajili ya jambo hili ndio maana tunaona baadhi ya riwaya katika uzinduaji wake zimejikita juu ya mustakbali wa utume na wakati huohuo zikisisitiza umuhimu wa kushikamana na nji ya Ali (a.s.). Pia tunakuta harakati nyingine alizozifanya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) nazo ni kutupia jicho dhidi ya maadui wa Ali (a.s.) na wenye chuki naye. Msaada huu kutoka kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake kwa ajili ya Ali (a.s.) hatujakuta katendewa yeyote mwingine asiyekuwa yeye. Kwanza: Jicho la Qur’ani dhidi ya maadui wa Ali (a.s.): Qur’ani katika kutoa sifa za Ali (a.s.) na mwenendo wake tulioutaja mwanzo pia imetumia mfumo wa kuwafunga watu pembezoni mwa Ali (a.s.) kwa sababu yeye ndiye mwenye kuwaokoa dhidi ya upotovu, na njia yake kutoka kwa Mola ndio kitenganishi kati ya haki na batili na misimamo yake inayooana na Qur’ani ni kipimo cha haki ambacho kwacho matendo hupimwa. Kuanzia hapa Qur’ani inapanua ombi lake linalohusu uhusiano na Ali (a.s.) ili zaidi liwe akilini na hivyo kwenda mpaka kwenye uhusiano wa huruma na mapenzi ya dhati, kama sharti la utawalishaji linalomsukuma mtu kutenda, kutekeleza na kuungana na msitari wa Ali (a.s.), kwa ajili hiyo Mwenyezi Mungu akasema: “Sema: Kwa haya siombi malipo yoyote kwenu isipokuwa mapenzi kwa ndugu zangu.”126 Imepokewa kutoka kwa Ibnu Abbas amesema: “Ilipoteremka “Sema: Kwa haya siombi malipo yoyote kwenu isipokuwa mapenzi katika ndugu zangu.”127 Walimuuliza: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu ni kina nani 126 -Sura Shuraa: 23. 127 -Sura Shuraa: 23.
47
Page 47
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba ndugu zako ambao tumewajibishwa kuwapenda?” Akasema: “Ali, Fatima, Hasan na Husein.”128 Imepokewa kutoka kwa Ibnu Abbas kuhusu kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na wasimamisheni, hakika wao wataulizwa.”129 Na kutoka pia kwa Abi Said Al-Khudri kuwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Kuhusu utawala wa Ali bin Abi Talib.”130 Ama kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na hasa utawafahamu kwa namna ya usemi wao,”131 imepokewa kutoka kwa Abi Said Al-Khudri kuwa alisema: “Kwa kumchukia kwao Ali (a.s.).”132 Aya Tukufu ifuatayo inabainisha kiwango cha uhusiano wa Imam Ali na Mtukufu Mtume kiasi kwamba imefanya msimamo wa kumpinga Ali ndio msimamo wa kumpinga Mtume wa Mwenyezi Mungu, hivyo Mwenyezi Mungu aliposema: “Na wakapingana na Mtume baada ya kuwabainikia mwongozo wao,”133 Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Katika suala la Ali (a.s.).”134 Hivyo ndivyo ilivyoendelea Qur’ani katika Aya zake nyingi kuwashambulia wanaompinga Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) katika suala la ukuruba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa Ali na kumtenga kwa 128 - Ad-Durul-Manthur 6: 7. Tafsir At-Tabari 25: 14 na 15. Mustadrakul-Hakim 2: 444. Musnad Ahmad 1; 199. Yanabiul-Mawaddah: 15. As-Sawaiq AlMuhriqah: 11 na 12. Dhakhairul-Uqba: 25. 129 - Sura As-Swafati: 24. 130 - As-Sawaiqul-Muhriqah: 79. Shawahidu At-Tanzil 2: 106. Kifayatu At-Talib: 247. 131 - Surat Muhammad: 30. 132 -Ad-Durul-Manthur 6: 66. Ruhul-Ma’an 26: 71. Fat’hul-Qadir 5: 39. Usudul-Ghaba 4: 29. 133 - Surat Muhammad: 32. 134 - Tafsirul-Burhani 4: 189.
48
Page 48
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba mambo binafsi na majukumu pekee ambayo Mtume alikuwa akimpa Ali (a.s.). Na Qur’ani imefichua hali ya ndani ya Mtume na uchungu wa nafsi uliyokuwa ukimpata kutoka kwa mwenye kumchukia Ali (a.s.), kwani katika kauli ya Mwenyezi Mungu: “Basi ni nani dhalimu mkubwa kuliko yule anayemzulia uongo juu ya Mwenyezi Mungu na kukadhibisha ukweli umfikiapo.”135 Ni yule anayepinga kauli ya Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) kuhusu Ali (a.s.).136 Ama kauli ya Mwenyezi Mungu: “Kwa hakika wale wanaomuudhi Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, Mwenyezi Mungu amewalaani katika dunia na Akhera, na amewaandalia adhabu yenye kufedhehesha.”137 Inafichua dhuluma anayofanyiwa Ali na wanafiki, na inabainisha utakaso wake, kwani imepokewa kuwa iliteremka kwa ajili ya Ali (a.s.), kwa sababu kundi fulani la wanafiki lilikuwa likimuudhi na kumpinga.138 Na Aya Tukufu ifuatayo inaweka wazi kuwa Mwenyezi Mungu atalipiza kisasi kwa maadui wa Ali, na kwa ajili hii inalazimu kila aliyempiga vita Ali kuwa adui wa Mwenyezi Mungu: “Na kama tukikuondoa, basi hakika sisi tutajilipiza kisasi kwao.”139 Ibnu Abbas amesema: “Kwa Ali (a.s.).”140 Imepokewa kutoka kwa Abi Abdullah Al-Jadli amesema: Ali (a.s.) aliniambia: “Je, nikwambie jema ambalo atakayelitenda basi Mwenyezi Mungu 135 -Surat Az-Zumar: 32. 136 -Ameipokea Ibnu Mardawihi ndani ya kitabu Al-Manaqib, kama inavyopatikana pia ndani ya Kashful-Ghummah: 93. Na Tafsirul-Burhan 4: 76. 137 -Surat Al-Ahzab: 58. 138 - Tafsirul-Qurtubi 4: 24. Asbabun-Nuzul: 207. Shawahidu At-Tanzil 2: 93. Tafsirul-Khazin 3: 511. 139 -Surat Az-Zukhruf: 41. 140 -Ad-Durul-Manthur 6: 18. Yanabiul-Mawaddah: 98. Shawahidu At-Tanzil 2: 151. Manaqib Ibn Al-Maghazali: 274.
49
Page 49
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba atamwingiza Peponi, na baya ambalo atakayelitenda basi Mwenyezi Mungu atauangusha uso wake Motoni na wala hatomkubalia amali yoyote?” Nikasema: Ndiyo. Kisha akasoma: “Atakayeleta mema, basi atapata mema kuliko hayo, nao katika mahangaiko ya siku hiyo watasalimika. Na watakaoleta ubaya, basi zitaangushwa nyuzo zao Motoni,”.141 Kisha akasema: “Ewe Abi Abdullah! Jema ni kutupenda na baya ni kutuchukia.”142 Harakati za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) zimeungana na Qur’ani Tukufu katika kuwatupia jicho maadui wa Ali bin Abi Talib (a.s.), kwani kuna baadhi ya riwaya zimepatikana huku, katika maana yake zinagawa watu sehemu mbili: Yule mwenye kumpenda Ali na yule mwenye kumchukia Ali, na wala hazitenganishi kati ya yule mwenye kumpenda Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na yule asiyempenda Ali, bali imani ya kweli ni kuwapenda wote wawili pamoja kwa sababu ujumbe wao ni mmoja. Imekuja ndani ya kitabu Musnad Ahmad kwa njia mbalimbali kuwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Atakayemuudhi Ali basi bila shaka ameniudhi mimi.”143 Na akasema: “Enyi watu! Atakayemuudhi Ali atafufuliwa Siku ya Kiyama akiwa myahudi au mkiristo.”144 Na pia ndani ya kitabu Musnad Ahmad: Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Hakupendi ila muumini na wala hakuchukii ila mnafiki.”145 Mtume wa Mwenyezi Mungu akasema huku akimwashiria kiongozi wa 141 - Sura Naml: 89 – 90. 142 - Khasaisul-Wahyi Al-Mubin cha Ibnu Bitariqi Al-Hilliy: 217. 143 -Musnad Ahmad 3: 483. Dhakhairul-Uqba: 65. As-Sawaiq Al-Muhriqah: 73. 144 - Mizanul-Iitidal 3: 151. Lisanul-Mizan 3: 90 na 4: 251. Warajihul-Matalib: 119. Yanabiul-Mawaddah: 251. 145 - Musnad Ahmad 1: 84 na 95 na 128. Sahih Muslim 1: 41. At-Taju Al-Jamiu Lil-Usul 3: 335. Sahih At-Tirmidhiy 2: 301. Sunan An-Nasai 2: 271. Khasaisu cha An-Nasai: 27. Dhakhairul-Uqba: 43. Ta’rikhul-Khulafai: 170. As-Sawaiqu AlMuhriqah: 74.
50
Page 50
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba waumini Ali (a.s.): “Enyi watu! Watahinini watoto zenu kwa kumpenda, kwani hakika Ali haiti kwenye upotovu na wala haepushi na uongofu, hivyo atakayempenda basi ni miongoni mwenu na atakayemchukia basi si miongoni mwenu.”146 Pili: Harakati za Mtukufu Mtume na kuhami kwake mustakbali wa uimam. Mtukufu Mtume alisisitiza ndani ya akili za umma umuhimu wa nafasi ya Imam Ali (a.s.) na dharura ya kuhami njia yake na ulazima wa kushikamana nayo, njia ambayo inauokoa umma na kuukinga dhidi ya utelezi na upotovu, na kwa ajili hii Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akamwambia Ammar: “Baada yangu kutakuwa na machafuko na mfarakano ndani ya umma wangu mpaka watabebeana panga na kuuwana wao kwa wao, huku wao kwa wao wakitengana….Ewe Ammar! Atakayebeba upanga kumsaidia Ali dhidi ya adui yake, Mwenyezi Mungu atamvisha cheni mbili za nuru Siku ya Kiyama. Na atakayebeba upanga kumsaidia adui yake, Mwenyezi Mungu atamvisha cheni mbili za Moto, ukiona hilo basi ni juu yako kushikamana na huyu aliyoko kuliani kwangu – akimaanisha Ali.”147 Qur’ani Tukufu imeashiria machafuko ambayo yataupata umma baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kiasi kwamba yataupelekea umma kugawanyika na kufarakana, jambo ambalo matokeo yake yatakuwa ni makundi mengi yenye kupingana kuingia Motoni, na wala halitookoka ila kundi moja tu ambalo linamtawalisha Imam Ali (a.s.) na linafuata nyayo zake. Na kwa ajili hii Imam anaweka rekodi ya ubora wa kiwango cha juu mno kuliko Waislam wote waliobakia. 146 - Wasifu wa Imam Ali (a.s.) ndani ya Ta’rikh Madinat Damash’qi 2: 147 - Yanabiul-Mawaddah: 128. Na inapatikana kwa tamko lingine ndani ya kitabu Usudul-Ghaba cha Ibnu Athir 5: 287. Ta’rikh Baghdad 13: 186. Maj’mauzZawaid 6: 236. Fadhailul-Khamsah Minassahah As-Sitah 2: 397.
51
Page 51
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba Imepokewa kuhusu kauli ya Mwenyezi Mungu: “Hakika wale waliofarakisha dini yao na wakawa makundimakundi,” kuwa Zadhani Abi Umar amesema: “Ali (a.s.) aliniambia: “Ewe Abi Umar! Unajua mayahudi waligawanyika makundi mangapi?” Nikasema: Mwenyezi Mungu na Mtume Wake ndio wajuao zaidi. Akasema: “Waligawanyika makundi sabini na moja yote ni ya Motoni ila moja tu ndilo lenye kuokoka. Unajua umma huu utagawanyika makundi mangapi?” Nikasema: Mwenyezi Mungu na Mtume Wake ndio wajuao zaidi. Akasema: “Utagawanyika makundi sabini na tatu yote ni ya Motoni ila moja tu ndilo lenye kuokoka. Unajua utagawanyika makundi mangapi kuhusu mimi?” Nikasema: Hivi wenyewe utagawanyika kuhusu wewe? Akasema: “Ndiyo utagawanyika makundi kumi na mbili kuhusu mimi, yote ni ya Motoni ila moja tu ndilo lenye kuokoka, na wewe Abi Ammar ni miongoni mwao.”148” Na Aya: “Basi waulizeni wenye ukumbusho ikiwa nyinyi hamjui,”149 inasisitiza kuwa Imam Ali (a.s.) ndiye marejeo pekee baada ya Mtukufu Mtume pale mambo yanapotatiza na machafuko kuzidi na kutokujulikana usahihi ni upi na ufahamu mpya uliozuka sasa ni upi. Katika tafsiri ya Aya hii imepokewa kutoka kwa Jabir Al-Jaafiy kuwa alisema: “Ilipoteremka “Basi waulizeni wenye ukumbusho ikiwa nyinyi hamjui,”150 Ali (a.s.) alisema: “Sisi ndio wenye ukumbusho.”151 Kwa maelezo haya Ali anakuwa ndio Imam wa kundi lenye kuokoka na yeye ndiye mwalimu wa sahaba wengine akihofia wasije wakazama ndani ya makundi yenye kupotea bila elimu yoyote. Imepokewa kutoka kwa Said Al-Khudri amesema: “Tulikuwa tumeketi tukimngojea Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na ndipo alipotu148 - Khasaisul-Wahyi Al-Mubin cha Ibnu Bitariqi: 214. Ta’rikhu Damashqi 18: 4. 149 - Surat An-Nahli: 43. 150 -Sura An-Nahli: 43. 151 - Tafsir Ibnu Jarir At-Tabari 17: 5.
52
Page 52
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba tokea akitokea kwenye nyumba ya mmoja ya wakeze.” Akasema: “Basi tukasimama pamoja naye na ghafla kiatu chake kikakatika na akamuacha Ali akikishona. Basi Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akaondoka na tukaondoka pamoja naye, kisha akasimama akimngojea nasi tukasimama pamoja naye, ndipo akasema: “Hakika miongoni mwenu yupo atakayepigania maana ya Qur’ani hii kama nilivyopigania uteremkaji wake.” Basi kila mmoja akajitanguliza akiwemo Abu Bakr na Umar. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akasema: “Hapana, lakini ni mshona viatu.” Akasema: Tukaja kumbashiria, na alikuwa kama keshazisikia. Na katika riwaya nyingine amesema: Hakuinua kichwa kwa ajili ya habari hizo kana kwamba keshazisikia.”152 Na ili kutenganisha mfano halisi wa njia ya Imam Ali dhidi ya nyingine ili iwe wazi kiasi kwamba isibakie hoja yoyote kwa wale wanaojitenga na Imam Ali, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimwambia Ammar aliyekuwa akimtawalisha Ali na akimsaidia: “Litakuuwa kundi ovu.” Imepokewa kutoka kwa Ikrima kuwa Ibnu Abbas alimwambia yeye na mwanae Ali: “Nendeni kwa Abi Said Al-Khudri mkasikie hadithi yake.” Amesema: “Basi tukaenda tukamkuta yuko bustanini kwake na alipotuona akachukua shuka yake akaja na akaketi, basi akaanza kutusimulia mpaka akafika kwenye suala la ujenzi wa msikiti, akasema: “Tulikuwa tukibeba tofali moja moja na Ammar bin Yasir akibeba mawili mawili.” Amesema: “Basi Mtume wa Mwenyezi Mungu akamwona ndipo akaanza kumfuta udongo na huku akisema: “Ewe Ammar! Kwa nini usibebe tofali kama wanavyobeba rafiki zako?” Akasema: “Hakika mimi nataka malipo kutoka kwa Mwenyezi Mungu.” Amesema: “Basi akawa anamfuta udongo huku akisema: “Ole wako Ammar, litamuuwa kundi ovu, analiita kwenda Peponi na wao wanamuita kwenda Motoni.” Ammar akaanza kusema: Ninajilinda 152 - Musnad Ahmad bin Hambal 3: 83. Na ndani ya Hilyatul-Awliyai cha Abi Naim 1: 67 imo yenye maana hii. Na Usudul-Ghaba cha Ibnu Athir 3: 283.
53
Page 53
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba kwa Mwenyezi Mungu dhidi ya fitina.”153 Na miongoni mwa ishara za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na tahadhari zake juu ya matukio ya mustakbali na ambazo zinafichua sifa ya mchanganyiko na muungano wa njia ya Ali na njia ya Utume, na kuwa yeye (a.s.) ndio mwendelezo sahihi wa ujumbe huo, na wakati huohuo zinatimiza ulinzi wa umma na kuukinga dhidi ya madhara ya mbiu za upotovu na madai ya uovu ni pale (s.a.w.w.) alipotahadharisha kuhusu hatari ya harakati za kundi la Makhawariji ambalo litadhihiri baadaye na kujitenga na Ali (a.s.). Kwa tahadhari hii Imam Ali anawakilisha njia ya uimam na anatekeleza amri za Mola. Ama madai yaliyobaki yanaelekea upande wa udanganyifu na upotovu. Imepokewa kutoka kwa Abi Said Al-Khudri amesema: “Tukiwa kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) huku akigawa kifungu, ghafla akajiwa na Dhul-Khuwaysarah – naye ni mtu kutoka kabila la Tamim – akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu fanya uadilifu. Mtume akamjibu: “Adhabu kali itakupata, ni nani atafanya uadilifu iwapo mimi sifanyi uadili? Umefeli na umepata hasara ikiwa mimi sifanyi uadilifu.” Umar akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Unaniruhusu nimkate shingo yake? Akasema: “Mwache, kwani anao wafuasi ambao mmoja wenu atadharau sala yake (yaani ya Dhul-Khuwaysarah) pamoja na sala yao, na funga yake pamoja na funga yao, wanasoma Qur’ani lakini haivuki mitulinga yao, watachupa kutoka kwenye dini kama mshale uchupavyo kutoka kwenye upinde.” Akaendelea mpaka akasema: “Alama yao ni mtu mweusi ambaye moja ya sehemu za kati ya muundi na bega iko mfano wa chuchu za mwanamke au kipande cha nyama chenye kujaa, na watatoka dhidi ya kundi la watu 153 - Sahih Bukhar, kitabu cha swala. Sahih Muslim kitabu cha fitina. Sunan AtTirmidhi 5: 628. Manaqib Ammar bin Yasir, hadithi ya 3800. Mustadrak AsSahihayn 2: 148. Musnad Ahmad 3: 516, hadithi ya 11451. Ta’rikh Baghdad cha Al-Khatib Al-Baghdadiy 13: 186.
54
Page 54
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba bora.” Abi Said amesema: “Nashuhudia hakika mimi niliisikia Hadithi hii kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na nashuhudia kuwa Ali bin Abi Talib (a.s.) aliwauwa nikiwa pamoja naye, basi akaamuru mtu huyo atafutwe, kisha akaletwa na nikamuona akiwa na sifa zilezile alizoeleza Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).154 Na kuna riwaya nyingine zimepatikana kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) zikielekea kumuhami Imam Ali (a.s.) na kwa namna isiyo na mipaka, yaani zinabainisha ubora wa Imam Ali (a.s.) juu ya mwingine, sawa awe yule aliyeishi zama zake pamoja na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) au atakayekuja mbele. Pia zinaweka wazi kuwa mwenendo wa Imam na misimamo yake si hali inayojitokeza na kumwepuka katika baadhi ya mazingira, bali kitendo cha Ali kushikamana na haki, au uhusiano wa Ali na haki na uhusiano wa haki na Ali ni uhusiano wa mawazo kuungana na mfano halisi. Imepokewa kutoka kwa Thabit mtumishi wa Abi Dhari amesema: “Niliingia kwa Ummu Salamah nikamwona analia na akimtaja Ali (a.s.) na akasema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu akisema: “Ali yuko pamoja na haki na haki iko pamoja na Ali, na hawatoachana mpaka wanikute kwenye hodhi Siku ya Kiyama.”155 Pia imepokewa kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa njia mbalimbali: “Hakika Ali anatokana na mimi, na mimi natokana na Ali, na yeye ndiye mtawala wa kila muumini baada yangu, hafikishi kuhusu mimi ila mimi mwenyewe au Ali.”156 154 - Sahih Bukhari katika kitabu cha mwanzo wa kuumba. Khasais cha AnNasai: 137. Mizanul-Iitidal cha Ad-Dhahabi 2: 263. 155 - Ta’rikh Baghdadi cha Al-Khatib Al-Baghdadiy 14: 321. Al-Hakim ndani ya Mustadrak As-Sahihayn 3: 124. Sahih At-Tirmidhiy 2: 298. 156 - Musnad Ahmad 4: 164 na 165 ameipokea kwa njia tano. Khasais AmirilMu’minin cha An-Nasai: 19 na 20 kapokea kwa njia mbili. Sahih Bukhari 3:
229. As-Sawaiq Al-Muhriqah: 74. Sunan Al-Bayhaqiy 8: 5. 55
Page 55
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba Tatu: Utabiri na karama kwa Imam Ali (a.s.). Imam Ali bin Abi Talib amejitofautisha na sahaba wengine kwa karama mbalimbali mpaka utabiri wake wa matukio ya mbele ukawa ni tukio lenye kushuhudiwa ndani ya maisha yake. Miongoni mwa mambo aliyotabiri na yakatimia ni haya yafuatayo: 1. Utabiri wake (a.s.) kuhusu utawala wa Baghdadi na ufalme wa kizazi cha Abbas, na akaelezea hali zao na kuja kuangamia kwao, akasema (a.s.): “Kitu gani kitakujulisha ni ipi hiyo Baghdadi! Ni ardhi yenye miti ya Athli, itajengwa majengo makubwa, itaongezeka wakazi na wana wa Abbas wataifanya makazi, na kwa mapambo yao wataifanya maskani na itakuwa nyumba yao ya upuuzi na michezo. Na kwa ardhi hiyo watakuwa na ujeuri, dhuluma na viongozi waovu, wasomi waovu na mawaziri wahuni na watatumikiwa na vizazi vya Uajemi na Rum, hawatoamrishana mema watakapoyajua, wala hawatokatazana maovu watakapoyachukia…”157 2. Kuna mtu mmoja alikwenda kwa kiongozi wa waumini Ali (a.s.) na kusema: “Ewe kiongozi wa waumini! Hakika mimi nimepita kwenye ardhi ya kijiji kimoja nikamwona Khalid bin Irfatah amekufa, muombee msamaha. Ali (a.s.) akasema: “Hakika yeye hajakufa na wala hafi mpaka aongoze jeshi la upotovu, na mshika bendera yake ni Habib bin Jammaz.” Basi akasimama mtu kutoka chini ya mimbari na kusema: Ewe kiongozi wa waumini! Hakika mimi ni mfuasi wako na mimi ni mwenye mapenzi nawe. Akamwambia: “Wewe ni nani?” Akasema: Mimi ni Habib bin Jammaz. Akasema (a.s.): “Ni wewe utaibeba, na bila shaka utaibeba na kuingia nayo kupitia mlango huu.” Akaashiria mlango wa Al-Faylu. Basi alipofariki kiongozi wa waumini (a.s.) na akafariki mwanae baada yake na kumfika Husein yaliyomfika, Ibnu Ziyad alimtuma Umar ibnu Sa’ad kwa Husain (a.s.) na akamweka Khalid bin Irfatah mbele na akamfanya Habib bin Jammaz kuwa mbeba bendera yake mpaka wakaingia 157 -Kashful-Yaqin
56
Page 56
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba msikitini kupitia mlango wa Al-Faylu.158 3. Imepokewa kutoka kwake kuwa pindi alipoelekea kwenye vita vya Siffin kumpiga Mu’awiya na akawa amefika Karbala alisimama upande mmoja wa kikosi cha jeshi kisha akatazama kulia na kushoto na kusema: “Wallahi hii ndio sehemu ya vipando vyao na eneo la maoteo yao.” Kisha akalia sana. Akaulizwa: Ewe kiongozi wa waumini! Ni eneo gani hili? Na ni kina nani hawa? Akajibu: “Hii ni Karbala, kundi toka kizazi cha Muhammad litauawa hapa kwa kudhulumiwa na kwa uadui, pamoja nao watauawa watu ambao wataingia Peponi bila hesabu.” Kisha (a.s.) akaendelea na safari. Watu walikuwa hawajui tafsiri ya maneno yake mpaka yalipomfika Husein yale yaliyomfika. 159 4. Ali (a.s.) alipotoka kwenda kuwakabili watu wa Nahrwan alikuja mtu miongoni mwa sahaba wake waliokuwa mbele huku akikimbia mpaka kwa Ali (a.s.) na kusema: “Bishara njema ewe kiongozi wa waumini!” Akamuuliza: “Ni bishara ipi?” akasema: “Hakika wamevuka mto walipopata habari kuwa umefika, jibashirie hakika Mwenyezi Mungu amekutunukia mabega yao.”Ali (a.s.) akamwambia: “Mwogope Mwenyezi Mungu, ni kweli umeona wamevuka!” Akasema: “Ndiyo.” Basi akamwapisha mara tatu na mara zote akisema ndiyo. Ali (a.s.) akasema: “Wallahi hawakuvuka na wala hawatovuka na hakika kifo chao kitakuwa eneo la Ladun-Nutfah, naapa kwa yule aliyetoa mbegu na kuumba nafsi hawatofika Athlathu wala kasri la Bawazin mpaka Mwenyezi Mungu awauwe, na bila shaka amepata hasara yule aliyezua uongo.”160 Amesema: Kisha akaja mpanda farasi mwingine huku akikimbia, naye 158 -Tazama Kashful-Yaqin: 79. Irshadul-Qulub 2: 34. Nahjul-Haqi: 243. AlManaqib cha Ibnu Shahri Ashub 2: 270 anapoelezea balaa na matatizo. Rejea Sharhu Nahjul-Balagha cha Ibnu Abi Hadid 2: 287. 159 -Rejea Kashful-Ghummah 1: 282. Kashful-Yaqin: 80. Irshadul-Mufid: 175. 160 - Biharul-An’war 33: 348, kutoka kwenye Sharhu Nahjul-Balagha cha AlMuutazili 2: 271, kutoka kwenye kitabu Al-Khawariji cha Al-Madainiy.
57
Page 57
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba akasema kama yale yaliyosemwa na wa kwanza, lakini Ali (a.s.) hakujali maneno yake. Wakaja wapanda farasi wawili huku wakikimbia na wakasema mfano wa yale yale, Ali (a.s.) akasema: “Miongoni mwao hawatobaki ila wachache chini ya kumi, wala hawatouawa miongoni mwa sahaba wangu ila wachache chini ya kumi.” Kisha Ali (a.s.) akasimama na kuzungusha mgongo wa farasi wake. Amesema: Basi kijana mmoja miongoni mwa watu akawa anasema: “Wallahi nitakuwa karibu naye, na ikiwa wamevuka mto basi nitaiweka ncha ya mshale huu ndani ya jicho lake, anadai anajua mambo ya ghaybu?” Basi alipofika (a.s) mtoni aliwakuta watu wameshavunjavunja ala za panga zao na wamekata mishipa ya visigino vya ngamia wao na wameketi juu ya vipando vyao na kwa pamoja wakamwachia uamuzi kwa sauti kubwa yenye ukulele. Basi kijana yule akateremka na kusema: “Ewe kiongozi wa waumini! Hakika mimi mwanzo nilikuwa nimekutilia shaka, na hakika mimi natubu kwa Mwenyezi Mungu na kwako basi nisamehe.” Ali (a.s.) akasema: “Hakika Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kusamehe madhambi, basi muombe msamaha.”161 5. Imepokewa kutoka kwa Isma’il bin Rajai amesema: “Aasha Bahilah162 – kipindi hicho akiwa ni kijana mdogo – alisimama mbele ya Ali (a.s.) huku Ali akiwa anatoa hotuba na akitaja fadhila mbalimbali. Basi akasema: “Ewe kiongozi wa waumini! Mazungumzo haya yanafanana sana na ngano za kuchekesha!” Ali (a.s.) akasema: “Ewe kijana ikiwa ni mwenye makosa katika uliyoyasema basi Mwenyezi Mungu akukutanishe na kijana mwerevu.” Kisha akanyamaza. Ndipo wakasimama watu na kumuuliza: “Ewe kiongozi wa waumini ni nani huyo kijana mwerevu?” Akasema: “Ni kijana 161 - Sharhu Nahjul-Balagha cha Ibnu Abi Hadid 2: 271. Kashful-Ghummah, mlango wa fadhila 1: 375. Maelezo ni ya Ibnu Abi Hadid na yale yaliyopo kati ya mabano ni kutoka ndani ya Kashful-Ghummah. 162 -Aasha Bahilah, jina lake ni Amir bin Al-Harith.
58
Page 58
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba atakayetawala mji wenu huu na hatoacha heshima yoyote ya Mwenyezi Mungu ila ataivunja, na atapiga shingo la kijana huyu kwa upanga wake.” Wakasema: “Ewe kiongozi wa waumini! Atatawala miaka mingapi?” Akasema: “Ishirini ikiwa atautawala.” Wakasema: “Atakufa kifo cha kuuwawa au kifo cha kawaida?” Akasema: “Bali atakufa kifo cha kawaida kwa ugonjwa wa tumbo, na hivyo kitanda chake kitatoboka kutokana na wingi wa yale yatakayotoka tumboni mwake.”
Isma’il bin Rajai amesema: “Basi Wallahi hakika nilimwona Aasha Bahilah kwa macho yangu haya mawili akiwa miongoni mwa kundi la mateka ambao walitekwa na jeshi la Abdur-Rahman bin Muhammad bin Al-Ash’ath na kuletwa mbele ya Al-Hujjaj basi akamlaumu na kumfokea. Na akamwomba amsomee shairi lake ambalo linahimiza vita kwa AbdurRahman. Kisha akakatwa kichwa chake katika hadhara hiyo.163 Na miongoni mwa karama zake (a.s.) ni ile iliyomo ndani ya tafsiri ya AlFakhru Ar-Razi mwishoni mwa tafsiri ya Aya: “Je, unafikiri kwamba watu wa pangoni na zilizoandikwa walikuwa ajabu katika hoja zetu?”164 Amesema: “Ama kuhusu Ali (a.s.) imepokewa kuwa mmoja miongoni mwa watu wampendao aliiba na alikuwa ni mtumwa mweusi, basi akaletwa kwa Ali (a.s.) naye akamuuliza: “Umeiba kweli?” Akasema: “Ndiyo.” Basi mkono wake ukakatwa. Basi akatoka kwa Ali (a.s.) na ndipo akakutana na Salman Al-Faris na Ibnu Al-Kawwau, Ibnu Kawwau akasema: “Nani aliyekata mkono wako?” Akajibu: “Kiongozi wa waumini, jemedari wa Waislam, mkwe wa Mtume na mume wa Al-Batul.” Akamwambia: “Amekukata mkono na bado unamsifu?” Akasema: “Na kwa nini nisimsifu ilihali kaukata mkono wangu kwa haki na ameniokoa na Moto.” Basi Salman akayasikia hayo na akaenda 163 - Sharhu Nahjul-Balagha cha Ibnu Abi Hadid 2: 289. 164 -Sura Al-Kahf: 9.
59
Page 59
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba kumweleza Ali (a.s.), ndipo akamwita mtumwa yule mweusi kisha akauweka mkono wake juu ya muundi wake kisha akaufunika kwa kitambaa na akaanza kuomba baadhi ya dua. Ndipo tukasikia sauti kutoka mbinguni ikisema: “Ondoa kitambaa kwenye mkono, tukakiondoa na kukuta mkono umepona kwa idhini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na kwa tendo lake zuri.165
Imepokewa kutoka kwa Abi Dharr, amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu alinituma nikamwite Ali (a.s.), nikaenda nyumbani kwake nikamwita lakini hakunijibu. Nikarudi na kumpa habari Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), ndipo akaniambia: “Rudi tena ukamwite hakika yeye yumo ndani.” Amesema: “Nikarudi kumwita, ndipo nikasikia jiwe la kusagia likisaga, ndipo nikachungulia nikaona jiwe la kusagia likisaga peke yake bila kuwa na mtu yeyote, basi nikaendelea kumwita na ndipo akatoka akiwa na furaha. Nikamwambia: Hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu anakuita, basi akaja. Kisha nikaendelea kumtazama Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na yeye akinitazama, kisha akaniambia: “Ewe Abi Dhari! Una jambo gani? Nikasema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Ni maajabu ya ajabu, nimeliona jiwe la kusagia likisaga nyumbani kwa Ali (a.s.) likiwa halina mtu yeyote anayelisagisha.” Akasema: “Ewe Abi Dharr! Hakika Mwenyezi Mungu ana malaika wenye kufanya ibada aridhini na wamepewa jukumu la kuwahudumia jamaa wa Muhammad (s.a.w.w.)”166
165 - At-Tafsir Al-Kabir cha Al-Fakhru Ar-Razi 21 – 22: 88. 166 -Ar-Riyadhu An-Nadhirah 3: 202.
60
Page 60
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba
Muhtasari Imam Ali (a.s.) aliacha picha za kheri ndani ya nafsi za sahaba, jambo lililofanya matamko yao ya wazi kuhusu ubora wake juu ya sahaba wote yajae vitabu vya tafsiri, Hadithi na historia. Kama ambavyo Ali (a.s.) kwa mwenendo wake wa imani na uwezo wake wa kielimu, kijihadi na kimaadili alitekeleza yale yaliyoandikwa na utume waziwazi yasiyofichikana kwa yeyote. Hivyo akawa mfano bora kabisa katika utekelezaji huo baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), wakati ambapo sahaba wengine wameshindwa kufikia. Qur’ani Tukufu imethibitisha na kauli za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) zimetamka waziwazi ubora wa Ali (a.s.) juu ya sahaba wote, kama tulivyotaja hilo sehemu zaidi ya moja. Na Ali (a.s.) alikuwa ndiye marejeo makuu ya sahaba katika utatuzi wa matatizo yao kwa sura ya ujumla na ya Makhalifa kwa sura ya pekee. Kutokana na hilo Imam Ali bin Abi Talib (a.s.) anakuwa ndiye mbora kuliko sahaba wote katika kila kitu baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) bila mpinzani. Na mwisho wa dua zetu ni kumshukuru Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu.
61
Page 61
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
Ushia njia iliyonyooka
USHIA NDIO NJIA ILIYONYOOKA
Kimeandikwa na: Abdul Karim Al-Huseini Al-Qazwini
Kimetajumiwa na: Hemedi Lubumba Selemani
62
12:36 PM
Page 62
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ushia njia iliyonyooka
NENO LA JUMUIYA Hakika mirathi ya Ahlul-Bait ambayo imehifadhiwa na kambi yao na wafuasi wao dhidi ya upotovu inaonyesha kambi iliyokusanya aina mbalimbali za taaluma za kiislamu. Kambi hii imeweza kulea nafsi mbalimbali zilizo tayari kunywa kutoka kwenye chemchemu hiyo, na kuupa umma wa kiislamu Wanachuoni wakubwa wenye kufuata nyayo za ujumbe wa AhlulBait. Wanachuoni waliokusanya vidodosa na maswali mbalimbali ya madhehebu na mitazamo tofauti ya kifikira kuanzia ndani ya desturi ya kiisilamu hadi nje ya desturi hiyo, huku wao wakitoa majibu na utatuzi makini juu ya maswali hayo ndani ya karne zote. Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bait imefanya hima kutetea tukufu za ujumbe wa Uislamu na ukweli wake ambao umechafuliwa na makundi, madhehebu na wanaharakati mbalimbali wenye chuki na Uislamu. Jumuiya imefuata nyayo za Ahlul-Bait na za wafuasi wa kambi yao njema ambayo imefanya hima kujibu madai yenye kuendelea na daima ikajaribu kubaki ndani ya msitari wa mapambano kwa kiwango kinachohitajika ndani ya kila zama. Hakika uzoefu ambao umehifadhiwa ndani ya vitabu vya Wanachuoni wa kambi ya Ahlul-Bait katika dhamira hii ni wa aina ya pekee, kwa sababu una akiba ya kielimu inayotegemea akili na hoja, huku ukijiepusha na matamanio na upendeleo uliokatazwa. Unazungumza na wasomi na wanafikra wenye fani maalumu, mazungumzo ambayo yanakubalika kiakili na yanapokewa na 63
Page 63
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ushia njia iliyonyooka maumbile yaliyo salama. Jaribio hili la Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bait limekuja kuwapa watafuta ukweli hatua mpya ya uzoefu wa thamani katika ulingo wa mazungumzo na maswali na kujibu hoja za utata zilizotolewa zama zilizopita au zinazotolewa leo kwa njia ya Tovuti, na hasa kwa kupewa nguvu na baadhi ya duru zenye chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu. Ikijiepusha na uchochezi uliokatazwa, na ni yenye kuhangaikia kuzishauri akili zenye kufikiria na nafsi zenye kutafuta haki, ili ziweze kufikia kwenye haki ambayo inatolewa na Kambi ya AhlulBaiti ulimwengu mzima, ndani ya zama ambazo akili inaerevuka na nafsi na roho zinaboreka kwa kasi ya pekee. Ni lazima tugusie kuwa mfululizo huu wa tafiti hizi umeandaliwa na Kamati maalumu toka jopo la Wanachuoni watukufu, hivyo tunatoa shukurani njema kwa hawa wote na kwa wasomi na wahakiki kwa kila mmoja miongoni mwao, kwa kupitia sehemu ya tafiti hizi na kutoa mchango wao wa thamani kuhusu tafiti hizi. Na sote tunategemea na kutaraji kuwa tutakuwa tumetoa kile tulichokiweza katika juhudi za kutekeleza baadhi ya wajibu tulionao mbele ya ujumbe wa Mtukufu Mola Wetu Mlezi ambaye alimtuma Mtume Wake na uongofu na dini ya haki ili aipe ushindi dhidi ya dini zote. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa shahidi. Jumuiya ya kimataifa ya Ahlu-Bait Kitengo cha utamaduni
64
Page 64
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ushia njia iliyonyooka
UTANGULIZI Mwislamu anaposafiri kwenda kutekeleza faradhi ya Hijja na kutekeleza Umra bila shaka ndani ya misimu hii anapata ladha ya kuabudu kwake na uislamu wake na kukomaza imani, na huishi kwenye uwenyeji wa Mwenyezi Mungu na hali ya kiroho. Lakini kwa bahati mbaya sana hukumbana na tukio la kuumiza na tabia kavu na maadili yenye ujahiliya mtupu, na kauli za kumzushia Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, na tuhuma batili na uzushi wanaozushiwa waislamu na waumini, na hapo matarajio yake ya safari yake ya kiroho hugeuka na kuwa tukio chungu na kavu linalouudhi uislamu na waislamu kwa jumla. Na kwa bahati mbaya sana hilo linatokea kwenye maeneo ya ibada na misikiti mitukufu ambayo ndio misikiti mitukufu mno kwa waislamu, ilihali inahamasishwa kuwa Mwislamu apate ndani ya umri wake angalau fursa moja tu ya kuwepo hapo, kustarehe hapo na apate shauku kubwa ya kukaa kwenye maeneo yake ili kuimarisha imani yake na uchaji wake. Lakini ghafla hukumbana na jicho baya, ulimi mchafu, vitendo vibaya na tabia chafu kutoka kwa watu wanaojulikana kwa kurefusha ndevu, kuvaa mavazi mafupi huku wakidhani kwa kufanya hivyo
“Kwamba wanafanya vitendo vizuri.” Sura Al-Kahf: 104. Lakini vitendo vyao hivi na kuwazushia kwao uwongo waumini si chochote bali ndio mfano halisi wa Aya:
“Hakika hilo ni uchafu na ni jambo lenye kuchukiza na ni njia mbaya.”Sura An-Nisai: 22.
65
Page 65
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ushia njia iliyonyooka Na Aya
“Nao watabeba mizigo yao miongoni mwao, angalieni ni mabaya wanayoyabeba.”Sura Al-An’am: 31. Na pia wao wamehifadhi kitu na hawana vitu vingi, kama alivyosema mshairi: “Mwambie yule anayedai kuwa ana maarifa katika elimu: Umehifadhi kitu na hauna vitu vingi!” Na sisi tunawaambia hawa yafuatayo: Kwanza: Kushikamana na Qur’ani na Sunna kuna sharti zake na kanuni zake, wala kushikamana navyo hakumaanishi tu kurefusha ndevu na kuvaa kanzu fupi, bali ni lazima Mwislamu ashikamane navyo kwa ukamilifu kwa kutekeleza wajibu mbalimbali na kuacha mambo ya haramu, kinyume na hivyo ataingia chini ya Aya:
“Je, mnaamini baadhi ya Kitabu na kuyakataa mengine? Basi hakuna malipo kwa mwenye kufanya hayo katika nyinyi ila fedheha katika maisha ya dunia na Siku ya Kiyama.” Sura Baqarah: 85. Pili: Miongoni mwa mambo yanayokubalika ndani ya uislamu bila kuhitaji dalili ni kuwa kuwazulia waumini uwongo na kuwanasibisha na tuhuma na batili ni miongoni mwa mambo yaliyoharamishwa kwa mkazo ndani ya 66
Page 66
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ushia njia iliyonyooka uislamu. Hilo amelikataza Mwenyezi Mungu kupitia Aya nyingi miongoni mwa Aya hizo ni:
“Basi wenye kumzulia Mwenyezi Mungu uongo baada ya hayo, basi hao ndio wenye kudhulumu.” Sura Aali Imraan: 94. Pia akasema akiwazungumzia hawa wazushi:
“Wanaozua uwongo ni wale tu wasioziamini Aya za Mwenyezi Mungu,”Sura An-Nahli: 105. Itaruhusiwaje kwa hawa kuwazushia uongo waumini ilihali wao wamejitenga na hayo wanayozushiwa, hivi hapa vitabu vyao na hizi hapa imani zao zinaonyesha ukweli wa imani yao na uislamu wao. Na wao wanakiri hilo na wanajifaharisha kwalo, na nyinyi mnawazushia uwongo ilihali Mwenyezi Mungu amewakataza kufanya hivyo na nyinyi bado mnaendelea kuyakataa maneno ya Mwenyezi Mungu anaposema:
“Wala msimwambie mwenye kuwapa salamu: Wewe si muumini.” Sura An-Nisai 94. Na huku ni kumpinga Mwenyezi Mungu na Mtume Wake bila hoja yoyote, na Mwenyezi Mungu anasema ndani ya Kitabu Chake: “Ambao wanajadiliana katika Aya za Mwenyezi Mungu pasipo dalili yoyote iliyowafikia, ni chukizo kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu na mbele ya wale walioamini, hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu anavyopiga muhuri juu ya kila moyo wa jeuri ajitukuzaye.” Sura Muumin: 35. 67
Page 67
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ushia njia iliyonyooka Tatu: Hakika mimi mara nyingi nimekutana na watu miongoni mwa hawa katika viwanja vya msikiti mtukufu na msikiti wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na wao wanatangaza kwa sauti kabisa kuwa nyinyi Shia ni makafiri na washirikina, mnaabudu makaburi ya Maimam wenu. Uzushi huu ni uwongo mtupu na ubatilifu wake uko wazi laiti kama wangekuwa na akili. Nao kwa mujibu wa sheria ni haramu uwapo maeneo ya kawaida, vipi maeneo ya nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu na msikiti wa Mtume (s.a.w.w.), ambayo yenyewe ndio msingi wa umoja, muungano na imani. Nne: Hakika mimi nawaomba hawa wasikie ukweli na uhalisi angalau kipindi cha muda mfupi mno kwa kusoma kurasa hizi kwa uzingativu na umakini, kisha baada ya hapo wana haki ya kutuhukumu kwa uzuri au ubaya, lakini iwe kwa hoja na dalili. Kwa sababu kurasa hizi ni jibu juu ya tuhuma moja kuhusu Ushia na ukweli wake. Mada hii imechambuliwa kwa ujumla huku ikitegemea dalili za Kitabu na Sunna. Sisi tumejiandaa kwa ukamilifu kujibu maswali yao, au utata wowote utakaojitokeza kwao mpaka waijue haki na wenye nayo, ikiwa kweli wanaupenda uislamu na wanatilia umuhimu kitendo cha kujua ukweli na uhalisia, na Mwislamu wa kweli ni yule ambaye anaupenda ukweli na anavutika kwenye ukweli huo. Qur’ani Tukufu inawaomba wasiokuwa waislamu wafanye uchunguzi na watambue ukweli, basi itakuwaje kwa waislamu wenyewe wao kwa wao, na Mwenyezi Mungu anasema:
“Sema: Enyi watu wa Kitabu! Njooni katika neno lililo sawa baina 68
Page 68
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ushia njia iliyonyooka yetu na baina yenu, tusimwabudu ila Mwenyezi Mungu tu, wala tusimshirikishe na chochote, wala baadhi yetu wasiwafanye baadhi kuwa ni waungu badala ya Mwenyezi Mungu. Basi wakikataa, waambieni: Shuhudieni kwamba sisi ni wenye kunyenyekea.� Sura Aali Imran: 64. Tano: Kurasa hizi ni matokeo ya mazungumzo kati yangu na mmoja kati ya mawahabi, naye ni mtu anayeongoza kundi moja la watu hawa, na ni mtumishi mwenye cheo kikubwa katika utumishi wake, jina lake ni Umar‌., wala sipendi kutaja jina lake kwa ukamilifu ili isiwe usumbufu kwake. Lakini mtu huyu pamoja na chuki yake na uzalendo wake nimeweza kuondoa ndani ya fikira zake tuhuma kuhusu Ushia kwa sababu ni fikira ya kupandikizwa isiyokuwa na mizizi yoyote ya uislamu. Namshukuru Mwenyezi Mungu, yeye ameiona haki na ameongozwa kwa kufuata madhehebu ya Ahlul-Bayt (a.s.) na katika ibada zake anafuata fiqhi ya Ahlul-Bayt (a.s.). Hayo ni matunda ya uchunguzi wa mada husika na kuthibitisha dharura ya kufuata madhehebu hii, kwa sababu yenyewe ndio njia iliyonyooka ya uislamu.
Mfumo wa uchunguzi ndani ya Uislamu Uislamu una njia maalumu na ya pekee hivyo unawalea wafuasi wake na waumini wa ujumbe wake katika njia hiyo, nayo ni kuutafuta ukweli na kuwa na shabaha na uhalisia. Njia hii ndiyo inayomfikisha mwanadamu kwenye ukweli, na ndio inayomwepusha na matabaka yake ya kimadhehebu, kikabila na kitaifa. Na pindi mtu atakapojiepusha na matabaka haya ndipo atakapofikia ubora na ukweli na atakuwa anaishi kwa akili zake na si kwa tabaka lake na matamanio yake. Na ili kufikia ukweli halisi inahitaji mambo yafuatayo: Kwanza: Ajiepushe kufuata matamanio yake, na tabaka lake la kinafsi na 69
Page 69
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ushia njia iliyonyooka kifikra na la namna yoyote ile. Pili: Mada anayotaka kuichunguza aitazame kama mada bila kuitangulizia uamuzi wowote ule mpaka afike kwenye ukweli na afike kwenye hali halisi. Tatu: Asitoe uamuzi wowote katika madhehebu yake au fikira yake ila baada ya kujua misingi yake na maana zake anazoamini, na baada ya hapo ndipo ahukumu ubaya au uzuri. Nukta hizi tatu ni miongoni mwa misingi ya asili ya mwanzo kabisa inayomfikisha mtafiti kwenye haki na hali halisi, na kwa mwanadamu mwislamu inapasa kujipamba nayo na akitolee kitu uamuzi kwa kufuata misingi hiyo, na kwa ajili hii tunamwona Mwenyezi Mungu anamwambia Mtukufu Mtume Wake (s.a.w.w.) kwa kusema:
“Wala usifuate usiyo na elimu nayo, hakika masikio na macho na moyo, hivyo vyote vitaulizwa.� Sura Bani Israil: 36. Ikiwa tamko hili linaelekezwa kwa Mtukufu Mtume Wake (s.a.w.w.) aliye mtakasifu dhidi ya makosa, itakuwaje kwa mwanadamu asiyekuwa mtakasifu, basi ni bora kwetu tusiseme kitu bila kuwa na elimu nacho, na wala tusikitolee kitu uamuzi kabla ya uchunguzi, kwani kwa mujibu wa maana ya imani ya kweli ni kujifunga ndani ya njia hii na kushikamana na mfumo huu.
Ushia na Uislamu Baada ya kutoka kwenye utangulizi huu sasa hebu tuchunguze kuhusu 70
Page 70
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ushia njia iliyonyooka Ushia ndani ya uislamu, na je, Ushia ni fikira iliyozuka juu ya uislamu? Na je, wenyewe ni jambo geni ndani ya uislamu? Au wenyewe umetokana na uislamu wenyewe? Kiasi kwamba hauachani nao kwa hali yoyote ile? Haya ndiyo tutakayojifunza kwa muhtasari na kwa uwazi mno, uwazi usio na pazia wala uficho, tutatazama hilo katika maeneo matano:
Eneo la kwanza: Ushia na maana yake: Tunalichunguza neno Shia katika pande mbili: Kilugha na kiistilahi. Ama kilugha: Lenyewe humaanisha ufuasi na mwandamano, kama alivyosema maana hii mwandishi wa kamusi, amesema: “Shia wa mtu ni wafuasi wake na wasaidizi wake.”1 Maana hii imepatika ndani ya Qur’ani katika kauli ya Mwenyezi Mungu:
“Na hakika Ibrahim alikuwa katika kundi lake. Alipomfikia Mola wake Mlezi kwa moyo safi”Sura As-Saafat: 83 – 84. Yaani miongoni mwa waliomfuata katika misingi ya dini au aliyemfuata katika uvumilivu ndani ya dini ya Mwenyezi Mungu na kuwa na subira dhidi ya wapingaji.2 Ama upande wa istilahi: Hakika neno Shia limeenea na kuwa alama kubwa pekee ya yule anayemfuata Ali (a.s.) na kumtawalisha, anamfuata na kumnusuru, na hii inabeba maana mbili: i. Hutumika kukusudia maana ya mapenzi na mawada, na maana hii ni faradhi ya kidini ndani ya Uislamu na ni amri ya Qur’ani juu ya waislamu wote. Hilo limekuja ndani ya maelezo ya Qur’ani kwa kauli ya Mwenyezi Mungu: 1 -Qamusil-Lugha 2: 246 2 - Tafsiri Al-Kashaf cha Az-Zamakhshari 2: 483.
71
Page 71
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ushia njia iliyonyooka
“Sema: Kwa haya siombi malipo yoyote kwenu isipokuwa mapenzi katika akraba (wangu).” Sura Shuraa: 23. Sisi tunajiuliza je, kuna mtu wa karibu aliye karibu mno na Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) kuliko Ali, Fatima, Hasan na Husein (a.s.)? Basi mapenzi na mawada kwa Ahlul-Bayt (a.s.) ambayo ni sehemu ya Ushia yanakuwa ni faradhi iliyofaradhishwa kwa maelezo ya Qur’ani kama tulivyotaja hilo. Na Al-Baydhawi amenukuu ndani ya tafsiri yake kuwa: “Imepokewa kuwa ilipoteremka Aya ya mapenzi. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) aliulizwa ni nani akraba zako hawa ambao tumewajibishwa kuwapenda?” Mtume (s.a.w.w.) akajibu kwa kusema: “Ali, Fatima na vijana wao wawili.”3 ii. Hutumika neno Shia kumaanisha ufuasi na kupita njia ya Ahlul-Bayt (a.s.) na kuchukua kauli zao na mafunzo yao. Na hilo nalo ni faradhi ya kidini ndani ya uislamu, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amefaradhisha hilo juu ya waislamu wote na akawaamuru kwa hilo. Kama lilivyopotikana hilo ndani ya Hadithi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ijulikanayo kwa jina la ‘Hadithi ya Safina,’ nayo ni kauli yake (s.a.w.w.): “Mfano wa Ahlul-Bayt wangu kwenu ni sawa na Safina ya Nuh, atakayeipanda ataokoka na atakayejiepusha nayo atapotea na kuangamia.”4 Hadithi hii inakubalika ndani ya madhehebu zote za kiisilamu, na ime3 -Tafsirul-Baydhawi 5: 53, chapa ya vitabu vya kiarabu, Misri mwaka 1330 A.H. 4 - Hadithi hii kaipokea Al-Hakim ndani ya kitabu chake Al-Mustadrak 3: 151. Na Al-Khatib ameitoa ndani ya Ta’rikh yake 12: 91. Nayo imepokewa kutoka kwa Abi Dharr na kutoka kwa Ibnu Abbas, Anas, Abi Said Al-Khudri, Ibnu Zubayr na wengineo, tazama kitabu Al-Ghadir 2: 301.
72
Page 72
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ushia njia iliyonyooka walazimisha waislamu wote kufuata kauli zao na kushikamana na mafunzo yao ili waokoke dhidi ya upotovu na uovu. Kuanzia hapa tuna haki ya kujiuliza je, katika watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w.) yupo aliye wa karibu mno na mjuzi mno kuliko Ali hata tuweze kufuata kauli yake na kufuata uongofu wake na mafunzo yake? Ili tuokoke dhidi ya upotovu. Kisha Hadithi hii si inakomea kwa Ali, Fatima na vijana wao wawili? Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anapoamuru kufuata kauli za Ahlul-Bayt inamaanisha yeye kafaradhisha wajibu juu ya waislamu wote, kwa sababu kauli ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kitendo chake na ridhaa yake ni hoja ya amri juu ya waislamu wote, kwa sababu yeye (s.a.w.w.) kama Qur’ani alivyomwelezea:
“Wala hasemi kwa tamaa. Hayakuwa haya ila ni Wahyi uliofunuliwa.”Suratun-Najmi: 3 - 4. Na pia ikasema:
“Na anachokupeni Mtume basi pokeeni, na anachokukatazeni basi jiepusheni,”Sura Hashir: 7. Kutokana na maelezo haya yanabainika yafuatayo: 1. Hakika kurejea na kufuata mawazo ya wanachuoni wa Ahlul-Bayt ni faradhi iliyofaradhishwa ndani ya maarifa ya Uislamu, hilo ni kwa mujibu wa maelezo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) yaliyotangulia. Ilihali kurejea na kufuata mawazo ya wanachuoni wengine si faradhi kwa sababu hilo halijaungwa mkono na maelezo yoyote ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wala Qur’ani tukufu, na hasa pindi unapopatikana mgongano wa mawazo. 73
Page 73
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ushia njia iliyonyooka 2. Tukikubali na tukasema turejee kwa wanachuoni, basi wanachuoni wa Ahlul-Bayt ndio wa mwanzo kwa sababu wao ni kundi bora kama ushuhuda wa historia ulivyothibitisha hilo kwa Ahlul-Bayt, zaidi ya hapo ni maelezo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambayo yanahimiza kuchukua kauli zao kama ilivyo wazi ndani ya ‘Hadithi ya Safina.’ 3. Katika hali ya mgongano kati ya kauli mbili, yaani kauli ya mwanachuoni wa Ahlul-Bayt na mwanachuoni asiye wa Ahlul-Bayt, lililo la wajibu kwa mujibu wa sheria na akili ni kufuata kauli ya mwanazuoni wa Ahlul-Bayt, kwa sababu ina yakini na upatiaji wa hukumu halisi na imeepukana na upotovu. Hilo linaungwa mkono na maelezo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika ‘Hadithi ya Safina.’ Ilihali kuifanyia kazi kauli ya mwanazuoni asiye wa Ahlul-Bayt kunamwacha mwanadamu ndani ya shaka; je, amepatia hukumu halisi au hakupatia? Hali hiyo ni kwa kuwa ndani ya hukumu hiyo hamna maelezo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Na mwislamu halisi na wa kweli haachi yakini na kwenda kwenye shaka bali anatakiwa awe kinyume, yaani afanyie kazi yakini na aache chenye shaka. 4. Hapa tunajiuliza: Kwa nini Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitamka Hadithi hii tukufu? Kutamka huko kuna faida gani? Na je, alitamka Hadithi hii kwa kupamba na kupendezesha mazungumzo? Ilihali yeye hatamki kwa matamanio bali ni Wahyi anaofunuliwa, au alikuwa anautakia umma wake uokovu ndio maana akaitamka? Basi ni kwa nini waislamu wengi hawaitekelezi Hadithi hii? Na hasa wakati wa kutofautiana mawazo ili wapate kuokoka dhidi ya upotovu? Kama alivyotamka wazi hilo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ndani ya Hadithi yake hii. 5. Hakika kutokufuata kauli ya wanachuoni wa Ahlul-Bayt na hasa katika sura ya mgongano na mpishano bila shaka kunaonyesha ukazaniaji na ubobeaji ndani ya uovu na upotovu, kama alivyoelezea hilo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ndani ya ‘Hadithi ya Safina’ tuliyoitaja mwanzo “Na 74
Page 74
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ushia njia iliyonyooka atakayejiepusha nayo atapotea na kuangamia.”5 6. Kufuata kauli za Maimam wa Ahlul-Bayt ndio mfano halisi miongoni mwa mifano halisi ya mapenzi na mawada yaliyofaradhishwa kwa maelezo ya Qur’ani Tukufu: “Sema: Kwa haya siombi malipo yoyote kwenu isipokuwa mapenzi kwa akraba zangu.”6 Na kutokufuata kauli yao maana yake ni kuzinyanyapaa na kutozijali na kutokuzitilia umuhimu, na hiyo ni aina moja ya kunyanyapaa haki zao. Na hili linapingana na Aya ya mapenzi iliyotajwa hapo mwanzo, zaidi ya hapo ni upotovu na upotevu kama alivyotamka wazi hilo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika Hadithi ya safina kama tulivyoitaja.
Eneo la pili: Ushia ulianza lini na wakati gani? Hebu sasa tusome tukio la kuanza Ushia na historia yake kwa kufuata historia ya kuanza kwake na kuasisiwa kwake ili tuweze kuutolea maamuzi mazuri au mabaya. Tutakapochunguza mitazamo inayozungumzia kuanza kwa Ushia tutaikuta kama ifuatavyo: 1. Hakika Ushia ulianza zama za Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) ndiye mwasisi wake, mjenzi wake na mpandaji wa mbegu yake. 2. Ulianza baada ya kifo cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) baada ya yale yaliyotokea ndani ya ukumbi wa Saqifa wa kizazi cha Saadah, pale kundi la baadhi ya Muhajirina na Ansari liliposimama bega kwa bega na Ali (a.s.) na wakakataa kumpa kiapo cha utii asiyekuwa Ali. 5 - Hadithi hii kaipokea Al-Hakim ndani ya kitabu chake Al-Mustadrak 3: 151. Na Al-Khatib ameitoa ndani ya Ta’rikh yake 12: 91. Nayo imepokewa kutoka kwa Abi Dharr na kutoka kwa Ibnu Abbas, Anas, Abi Sa’id Al-Khudri, Ibnu Zubayr na wengineo, tazama kitabu Al-Ghadir 2: 301. 6 - Sura Shuraa: 23.
75
Page 75
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ushia njia iliyonyooka 3. Ulianza baada ya vita vya Jamal pale sahaba wakubwa waliposimama bega kwa bega na Ali (a.s.) na wakapigana pamoja naye. 4. Ulianza baada ya kuuwawa Husein (a.s.) na kupatikana mapinduzi ya wenye kutubu na yale ya Al-Mukhtari. 5. Ulianza zama za kuzuka madhehebu mbalimbali ndani ya karne ya nne, ndani ya zama za utawala wa kizazi cha Abbas, pale yalipozuka madhehebu ya kifiqhi kama vile, madhehebu ya Hanafiy, Shafiy, Malikiy na Hambaliy na ndipo ikazuka madhehebu ya ki-Shia ya Ja’afariya. 6. Ulizuka zama za mwishoni kabisa ukianzishwa na Waajemi. Ilihali sisi tutakapochunguza tunakuta haukuwepo uhusiano wa uwingi wa Waajemi ndani ya Ushia, bali wengi wao walikuwa wakifuata madhehebu za kisunni mpaka karne ya sita7 ya hijira. Na hakika Abi Hanifa kiongozi wa madhehebu ya Hanafiy yeye ni miongoni mwa Waajemi. Huu ndio muhtasari wa kauli kuhusu kuanza kwa Ushia, lakini mtu msomi na mtafutaji wa ukweli anakuta kuwa kuna maelezo ya kihistoria ya tangu zamani mno yanaelezea waziwazi kuhusu wafuasi wa Ali, nayo ni Hadithi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kama ilivyopokewa kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) pindi ilipoteremka Aya hii:
“Hakika wale walioamini na kutenda mema, hao ndio wema wa viumbe.”Sura Al-Bayinnah: 7. Zimepatikana riwaya mbalimbali kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa njia za kisunni zikielezea hilo kama ifuatavyo: 1. Ibnu Asakir ametoa kutoka kwa Jabir bin Abdullah amesema: “Tulikuwa 7 - Bali hadi karne ya kumi. Rejea vitabu vya historia.
76
Page 76
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ushia njia iliyonyooka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na ghafla akaja Ali, basi Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Naapa kwa yule ambaye nafsi yangu imo mikononi Mwake hakika huyu na wafuasi wake ndio wenye kufuzu Siku ya Kiyama.”8 Ikateremka:
“Hakika wale walioamini na kutenda mema, hao ndio wabora wa viumbe.”- Sura Al-Bayinnah: 7. Basi ikawa anapokuja Ali sahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) husema: Amekuja mbora wa viumbe.” 2. Pia As-Suyuti ametaja ndani ya Tafsir yake9: Ametoa Ibnu Adiy kutoka kwa Ibnu Abbas amesema: Ilipoteremka:
“Hakika wale walioamini na kutenda mema, hao ndio wabora wa viumbe.” Sura Al-Bayinnah: 7. Mtume wa Mwenyezi Mungu akamwambia Ali (a.s.): “Wewe na wafuasi wako mtakuja siku ya Kiyama mkiwa mmeridhia, na wenye kuridhiwa.” 3. At-Tabari ndani ya Tafsiri yake amesema: Imepokewa kutoka kwa Abi Al-Jarud kutoka kwa Muhammad bin Ali kuhusu ‘hao ndio wabora wa viumbe,’ akasema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Ni wewe Ali na wafuasi wako.”10
8 - Tafsir Ad-Durul-Manthur cha As-Suyuti 6: 379. 9 - Tafsiru Ad-Durul-Manthur cha As-Suyuti 6: 379, chapa ya Al-Mayniyyah, Cairo mwaka 1314 A.H. Na Al-Khawarazami ameitaja nyingine yenye maana hii ndani ya kitabu chake Al-Manaqib: 66. 10 -Tafsiru At-Tabari 3: 146.
77
Page 77
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ushia njia iliyonyooka 4. Al-Khawarizmi amepokea ndani ya kitabu chake kauli: Kutoka kwenye njia ya Al-Hafidh Ibnu Mardawihi kutoka kwa Yazid bin Sharahabil AlAnsar mwandishi wa Ali (a.s.) amesema: Nilimsikia Ali akisema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu alinisimulia ilihali akiwa ameegamia kwenye kifua changu, akasema: “Ewe Ali! Hujasikia kauli ya Mwenyezi Mungu:
“Hakika wale walioamini na kutenda mema, hao ndio wabora wa viumbe.” Sura Al-Bayinnah: 7. Ni wewe na wafuasi wako, na ahadi yangu mimi na nyinyi ni Hodhi, pindi nyumati zitakapokuja kwa ajili ya hesabu basi mtaitwa kundi mashuhuri.”11 5. Na mwandishi wa kitabu Al-Ghadir amesema: Al-Hafidhu JammaludDin Az-Zindiy ametoa kutoka kwa Ibnu Abbas (r.a.) kuwa: “Ilipoteremka Aya hii, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimwambia Ali (a.s.): “Ni wewe na wafuasi wako, utakuja wewe na wafuasi wako Siku ya Kiyama mkiwa mmeridhia, na wenye kuridhiwa, na atakuja adui yako akiwa amekasirika mwenye kukasirikiwa.” Akasema: Ni nani adui yangu? Akasema (s.a.w.w.): “Atakayejitenga na wewe na akakulaani.” Kisha Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akasema: “Atakayesema: Mwenyezi Mungu amrehemu Ali, basi atarehemewa na Mwenyezi Mungu.”12 6. Al-Baghdadiy ametaja ndani ya historia yake: “Hakika Mtume (s.a.w.w.) alimwambia Ali (a.s.): “Wewe na wafuasi wako ni watu wa Peponi.”13 7. Na ndani ya kitabu Murujudh-Dhahab imekuja kauli ya Mtume 11 - Al-Manaqib cha Al-Khawarazim: 178. 12 -Tazama kitabu Al-Ghadir 2: 58. 13- Tarikh Baghdad 12: 289.
78
Page 78
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ushia njia iliyonyooka (s.a.w.w.): “Itakapofika Siku ya Kiyama watu wataitwa kwa majina yao na majina ya mama zao isipokuwa huyu – Yaani Ali na Wafuasi wake – kwani hakika wao wataitwa kwa majina yao na majina ya baba zao kwa sababu ya usahihi wa uzawa wao.”14 8. Na mwandishi wa As-Sawaiq ametaja: Hakika Mtume (s.a.w.w.) alimwambia Ali (a.s.): “Ewe Ali, hakika Mwenyezi Mungu amekusamahe wewe, wajukuu zako, kizazi chako, mke wako, wafuasi wako na mwenye kuwapenda wafuasi wako.”15 9. Imekuja ndani ya kitabu Maj’mauz-Zawaid kuwa: Hakika Mtume (s.a.w.w.) alimwambia Ali (a.s.): “Wewe utakuwa mtu wa kwanza kuingia Peponi katika umma wangu, na wafuasi wako watanizunguka wakiwa juu ya mimbari za nuru, wenye furaha huku nyuso zao ziking’ara, nitawaombea Shufaa na hivyo kesho watakuwa majirani zangu Peponi.”16 10. Al-Hakim ndani ya kitabu Al-Mustadrak amesema: Hakika imepokewa kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) kuwa alisema: “Mimi ni mti na Fatima ni tawi na Ali ni mrutubishaji wake, na Hasan na Husein ni matunda yake, na wafuasi wetu ni majani yake. Asili ya mti ni kutoka Pepo ya Aden na vyote vilivyobaki ni kutoka Pepo nyingine.”17 11. Imekuja ndani ya Ta’rikh Ibnu Asakir kuwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimwambia Ali: “Ewe Ali! Hakika wanne wa mwanzo kuingia Peponi ni mimi, wewe, Hasan na Husein na vizazi vyetu vitakuwa nyuma ya migongo yetu, na wake zetu nyuma ya vizazi vyetu, na wafuasi wetu wakiwa kuliani na kushotoni mwetu.”18 14- Muruju Ad-Dhahbi 2: 51. 15- As-Sawaiqu Al-Muhriqah: 96 na 139 na 140. 16- Maj’mauz-Zawaid 9: 131. Kifayatul-Athar: 135. 17- Al-Hakim ameitaja ndani ya Al-Mustadrak 3: 160. Ibnu Asakir ndani ya Tarikh yake 4: 318. Ibnu As-Sabaghu ndani ya Al-Fusuul: 11. 18- Tarikh Ibnu Asakir 4:318. Tadhkiratus-Samtwiyn: 31. As-Sawaiqu AlMuhriqah: 96
79
Page 79
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ushia njia iliyonyooka 12. Na imekuja ndani ya Ta’rikhul-Khatib kuwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Shufaa ya umma wangu ni kwa atakayewapenda Ahlul-Bayt wangu na hao ndio wafuasi wangu.”19 13. Al-Haythami ametaja ndani ya kitabu chake Maj’mauz-Zawaid kuwa: Katika hotuba ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Enyi watu! Atakayetuchukia sisi Ahlul-Bayt Mwenyezi Mungu atamfufua Siku ya Kiyama akiwa Yahudi.” Jabir bin Abdullah akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Hata kama akifunga na kuswali? Akasema: “Ndio hata kama akiswali na akifunga na kudai kuwa ni Mwislamu, atazuiliwa hayo mwenye kumwaga damu yake na kutoa kodi kwa mkono ilihali amedhalilika20Nilifananishiwa umma wangu udongoni basi wakapita wabeba bendera mbele yangu, ndipo nikamwombea msamaha Ali na wafuasi wake.”21 14. Kutokana na riwaya tulizozitaja inabainika kuwa mpandaji wa mbegu ya Ushia ni yeye mwenyewe Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa sababu mtu wa kwanza kabisa aliyetamka na kudhihirisha istilahi ya neno Shia kwa maana ya wafuasi wa Ali ni yeye mwenyewe Mtume wetu Muhammad (s.a.w.w.) hivyo ndiye mpandaji halisi na wa kwanza wa mbegu ya Ushia na mwenye kuihudumia na kuwalingania watu waelekee huko, na Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: “Na anachokupeni Mtume basi pokeeni, na anachokukatazeni basi jiepusheni,”22. Hivyo ni wajibu kwa Mwislamu muumini kufuata kauli ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) pindi anapotaka kuufikia ukweli halisi, kwa sababu 19 -Ta’rikh Al-Khatib 2: 146. 20 -Yaani Yahudi hata akisali na kufunga na kufanya ibada ilimradi hajawa Mwislamu basi hayo hayatomsaidia kitu siku ya Kiyama – Mtarjumi-. 21 -Maj’mauz-Zawaid 9: 172. 22 -Sura Hashir: 7.
80
Page 80
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ushia njia iliyonyooka Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hatamki kwa matamanio yake bali ni Wahyi anaofunuliwa, na kwa msingi huu inatubainikia kuwa Uislamu wa haki ndio ulioasisi Ushia na wenyewe ndio chemchemu safi ya Uislamu.23
Dalili za kupasa kushikamana na madhehebu ya AhlulBayt (Ushia) Lililo wajibu kwa kila Mwislamu ni kutenda kwa mujibu wa madhehebu ya Ahlul-Bayt (Shia) (a.s.) kwa sababu maana hii ndio ipatikanayo toka kwenye Hadithi nyingi zilizopatikana kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) zikitamka waziwazi neno Shia. Hivyo zenyewe zinaonyesha kuwa lengo la Uislamu haliwezi kutimia isipokuwa ni kwa Ushia, hivyo madhehebu hii ndio chemchemu safi ya uislamu. Na kutokea ndani ya Hadithi hizi tunagundua wajibu wa kishikamana na mafundisho ya Ahlul-Bayt na kufuata kauli zao, kwa sababu zenyewe ndio zenye kuokoa dhidi ya upotovu na upotevu, kama alivyotamka waziwazi Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambaye hatamki kwa matamanio yake bali ni kwa Wahyi anaofunuliwa. Na Hadithi hizo ni kama zifuatavyo: i. Kauli ya (s.a.w.w.): “Hakika mimi ninawaachia vizito viwili ambavyo mkishikamana navyo kamwe hamtopotea: Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu watu wa nyumba yangu (Ahlul-Bayt). Hakika hivyo viwili havitoachana mpaka vitakaponifikia kwenye Hodhi.” Al-Allamah Az-Zarqaniy Al-Malikiy amefidisha maana hii kama alivyosimulia ndani ya kitabu Sharhul-Mawahibi kutoka kwa Al-Allamah As-Samhudi kuwa alisema: “Habari hii inafahamisha kuwa ndani ya kila 23 - Kutokana na ushuhuda huo, basi kwa lugha nyepesi tunasema: Uislamu sahihi na halisi aliouleta Mwenyezi Mungu kupitia Mtukufu Mtume ni Ushia. Na Ushia ndio uislamu sahihi aliouleta Mwenyezi Mungu kupitia Mtukufu Mtume. Hakuna tofauti kati ya Uislamu wa Mtume na Ushia. Kama ambavyo Hadithi na riwaya nyingi sahihi zilizosheheni ndani ya vitabu vya kisunni zilivyoonyesha hilo – Mtarjumi.
81
Page 81
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ushia njia iliyonyooka zama mpaka kusimama Kiyama yupo yule inayefaa kushikamana naye kutoka kwenye kizazi chake ili muhimizo uliotajwa wa kushikama naye uelekee kwake. Na Kitabu nacho ni kama hivyo, ndio maana wakawa ni kinga kwa watu wa aridhini, basi wakitoweka na watu wa aridhini wanatoweka.”24 ii. Kauli ya (s.a.w.w.): “Anayependa kuishi maisha yangu na afe kifo changu na aishi ndani ya Pepo ya Aden aliyoipanda Mola wangu Mlezi basi amtawalishe Ali baada yangu na amtawalishe atakayemtawalisha. Na awafuate watu wa nyumba yangu baada yangu, kwani hakika wao ni kizazi changu wameumbwa kutokana na udongo wangu na wameruzukiwa fahamu yangu na elimu yangu. Adhabu kali ni kwa wenye kupinga ubora wao ndani ya umma wangu, wenye kuukata uhusiano wangu kwao, Mwenyezi Mungu hatowapa Shufaa yangu.”25 iii. Kauli ya (s.a.w.w.): “Ndani ya kila karne ya umma wangu kuna waadilifu kutoka ndani ya watu wa nyumba yangu wanaoondoa ndani ya dini hii upotoshi wa wenye mapenzi ya kupindukia na imani za makundi ya wapotovu na tafsiri ya wajinga. Fahamuni kuwa hakika Maimam wenu ni ujumbe wenu kwa Mwenyezi Mungu, basi tazameni ni nani mnayempa ujumbe wenu.”26 iv. Kauli ya (s.a.w.w.): “Hakika mfano wangu na watu wa nyumba yangu ni sawa na safina ya Nuhu atakayeipanga ataokoka na atakayejitenga nayo ataangamia.”27 24- Sharhul-Mawahib 7: 8. Kitabul-Ghadir 3: 80. 25-Ameitoa Abu Naim ndani ya Al-Hilyah 1: 68. Tabariy na Ar-Rafiqiy kama ilivyo ndani ya Jam’ul-Jawamiu 6: 217. 26-Ameitoa At-Tabariy ndani ya Dhakhairul-Uqba: 17. As-Sawaiq: 141. 27- Ameitoa Al-Baghdad ndani ya Tarikh 12: 91. Al-Hakim ndani ya AlMustadrak 3: 151, na amesema ni hadith sahihi.
82
Page 82
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ushia njia iliyonyooka v. Kauli ya (s.a.w.w.): “Nyota ni kinga kwa watu wa ardhini dhidi ya kuangamia, na watu wa nyumba yangu ni kinga kwa umma wangu dhidi ya mtengano, basi kabila lolote litakapowatenga litatengana na kuwa kundi la Ibilisi.”28
Eneo la tatu: Ushia ndio njia iliyonyooka: Hakika Ushia ni chemchemu safi na ya asili ya Uislamu, kwa sababu wenyewe ni madhehebu ambayo ilimepewa jina na kuanzishwa na Uislamu, na Maimam wake wakasimikwa na Uislamu. Dalili yetu juu ya hilo ni hii ifuatayo:
Mtume alitoa jina la Ushia: Madhehebu pekee ambayo jina lake linatokana na tamko la wazi la Mtume (s.a.w.w.) ni madhehebu ya Ahlul-Bayt (Shia), hili limesemwa na vitabu vya ndugu zetu Sunni kama inavyopatikana ndani ya Tafsir Ad-DurulManthur cha Al-Hafidh As-Suyuti, na tayari maelezo yake yameshapita huko nyuma. Al-Allamah Al-Majlisi ndani ya kitabu chake Biharul-An’war ametaja yafuatayo: “Abi Sa’id Al-Khudri amesema: Siku moja Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alikuwa ameketi akiwa na kundi la sahaba zake akiwemo Ali bin Abi Talib (a.s.), basi Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Atakayesema: Hapana Mola wa haki ila Allah, ataingia Peponi.” Sahaba zake wawili wakasema: “Sisi husema: Hapana Mola wa haki ila Allah.” Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akasema: “Hakika shahada ya: Hapana Mola wa haki ila Allah hukubaliwa kutoka kwa huyu na Shia wake ambao Mola wetu Mlezi amechukua ahadi yao.”29
28- Ameitoa Al-Hakim ndani ya Al-Mustadrak 3: 149 na amesema ni hadith sahih. 29- Tazama Biharul-An’war 93: 203.
83
Page 83
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ushia njia iliyonyooka Eneo la nne: Mtukufu Mtume ndiye aliyetuita Shia Ithna’ashari (wafuasi wa Maimamu kumi na wawili): Ushia ndio madhehenu pekee ambayo imeshikamana na Sunna ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) herufi kwa herufi hata katika jina lake na idadi ya Maimam wake. Imam Ahmad bin Hanbal amesema ndani ya Musnad yake kuwa: “Imepokewa kutoka kwa As-Shaabiy kutoka kwa Masruq amesema: “Tulikuwa tumeketi kwa Abdullah bin Mas’ud huku akitusomea Qur’ani, basi mtu mmoja akamwambia: Ewe Abi Abdur-Rahman! Je, mlimuuliza Mtume wa Mwenyezi Mungu umma huu utakuwa na makhalifa wangapi?” Abdullah bin Mas’ud akasema: “Hakuna yeyote kabla yako aliyeniuliza swali kama hili tangu nije Irak.” Kisha akasema: “Ndiyo, tulimuuliza Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akasema: “Kumi na wawili kama idadi ya makabila ya wana wa Israil.”30 Na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anatilia mkazo Hadithi hii iliyotajwa kwa kusema: “Dini hii itaendelea kusimama mpaka kisimame Kiyama na watawaliwe na Makhalifa kumi na mbili, wote kutoka kabila la Qurayshi.”31 Ni lazima tuwachunguze makhalifa waliyochukua cheo cha ukhalifa idadi yao ni wangapi. Ifuatayo ni idadi yao: i. Makhalifa waongozao ukimjumuisha na Imam Hasan (a.s.) ni watano. ii. Makhalifa kutoka kizazi cha Umayyah ni kumi na nne. iii. Makhalifa kutoka kizazi cha Abbas ni ishirini na tatu. Hivyo jumla ni makhalifa arubaini na wawili. Hakika riwaya hii iliyotoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) huwezi 30 - Musnad Ahmad 1: 657, hadithi ya namba 3772. 31- Sahih Muslim 3: 1452.
84
Page 84
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ushia njia iliyonyooka kuitafsiri ila ni kwa mujibu wa madhehebu ya Ahlul-Bayt (Ushia) kwani yenyewe ndio madhehebu pekee ambayo imeshikamana na Sunna ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) herufi kwa herufi mpaka kwenye jina alilolitoa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuwa wao ni Shia Ithna’ashar, yaani wafuasi wa makhalifa kumi na mbili. Ukitaka uchambuzi wa mada hii kwa urefu basi rejea kitabu “Nadharia ya unabii, uimam na ukhalifa.”32 Ikiwa Ushia ndio Wahyi ulioletwa na Kitabu na Sunna, na ndio madhehebu ambayo imeshikamana na hivyo viwili herufi kwa herufi hata kwenye jina lake na idadi ya Maimam wake, basi ni kwa nini linazushiwa uwongo?
Eneo la tano: Ni kipi kitambulisho cha Shia? Mwanadamu mwenye kufuata kambi ya Ahlul-Bayt (a.s.) na mwenye kuchukua mafunzo yao na kufuata mwenendo wao na nyayo zao na uongofu wao ni lazima abebe kitambulisho bayana kisichokuwa na uficho wowote. Alama za kitambulisho hiki zimetajwa na kuainishwa na Imam Muhammad Al-Baqir mwana wa Imam Zaynul-Abidin Ali bin Husain Ibnu Imam Ali bin Abi Talib (a.s.), aliainisha alama hizo pale alipoulizwa na mmoja wa wafuasi wake naye ni Jabir bin Yazid Al-Jaafiy kuhusu utu wa Shia, akasema: “Ewe mwana wa Mtume wa Mwenyezi Mungu! Hivi inatosha kwa yule anayejinasibisha na ufuasi wenu aseme tu, mimi nawapenda Ahlul-Bayt?” Imam akamjibu kwa kusema: “Hapana ewe Jabir, Shia wetu si mwingine bali ni yule atakayemcha Mwenyezi Mungu na kumtii, na walikuwa hawajulikani ila kwa unyenyekevu, uoga (kwa Mwenyezi Mungu), kutubu na kukithirisha kumtaja Mwenyezi Mungu, swaumu, swala, kusoma Qur’ani, kuwajulia hali majirani, kuanzia masikini hadi wenye shida. Na walikuwa ni waaminifu katika vitu vya jamaa zao.” Jabir akasema: “Ewe mwana wa Mtume wa Mwenyezi Mungu! Hivi leo 32- Tazama kitabu “Nadharia ya uimam na ukhalifa” cha As-Sayyid AbdulKarim Al-Qaz’winiy: 45.
85
Page 85
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ushia njia iliyonyooka kuna yeyote hajulikani kwa sifa hizo?” Imam akamwambia: “Ewe Jabir, angalia madhehebu yasikubebe; hivi inatosha mtu aseme tu mimi nampenda Ali na kumtawalisha bila kuwa mtendaji? Laiti mtu akisema mimi nampenda Mtume wa Mwenyezi Mungu, na Mtume wa Mwenyezi Mungu ni mbora kuliko Ali, kisha akawa hatendi Sunna zake na wala hafuati mwenendo wake basi mapenzi yake hayatomsaidia chochote. Mcheni Mwenyezi Mungu na mumtii, hakuna yeyote mwenye ukaraba kati yake na Mwenyezi Mungu ila yule tu atakayemcha Mwenyezi Mungu. Hivyo mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu huyo ndiye adui wetu, na mwenye kumtii Mwenyezi Mungu huyo ndiye mwenye kutupenda.”33 Hizi ndio sifa na baadhi ya alama za Mwislamu Shia mwenye kufuata madhehebu ya Ahlul-Bayt (a.s.), na linalotakiwa kwake ni kujipamba kwa sifa hizi ili aweze kuwa mwanafunzi wa kweli na mwenye kufaulu katika matendo yake na vitendo vyake. Ama kujinasibisha tu na kubeba jina bila kutenda na kushikamana nao kwenyewe hakunufaishi na wala hakuleti mapenzi ya kweli, na mwisho anakuwa kama alivyosema mshairi: “Kila mmoja anadai ana uhusiano na Layla Na Layla hakiri chochote katika madai yao hayo
33 - Utawezaje kumtii Mwenyezi Mungu bila kujua anataka nini na hataki nini? Utamtii vipi bila kujua namna ya utekelezaji wa utii huo? Utajuaje hayo bila kufunzwa na anayejua? Ni nani anayejua kama si yule aliyeambiwa na Mtume: “Mimi ni Jiji la elimu na Ali ni mlango wake.”? Utaingiaje Jiji bila kupita mlangoni? Utapitaje mlangoni bila kuwa usawa wa mlango? Utakuwaje usawa wa mlango bila kuikubali hali halisi na kuwa jasiri katika kuipokea haki? – Mtarjumi
86
Page 86
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ushia njia iliyonyooka
Ndugu yangu msomaji! Kurasa hizi zimebeba baadhi ya mazungumzo kuhusu Ushia na Shia wenyewe, mazungumzo ambayo yalifanyika huko Makka Tukufu na Madina yenye nuru. Tuliyachambua uchambuzi unaohusu mada hii tu jambo lililowapelekea baadhi kujiunga na madhehebu ya Ahlul-Bayt (s.a.w.w.) miongoni mwa watu wapenda ukweli ambao lengo lao ni uislamu na njia yake iliyonyooka huku wakitafuta haki na wenye nayo. Nataraji msomaji wa kurasa hizi atapata jaribio la kwanza la kutaka kugundua madhehebu asili ya uislamu kwa mujibu wa Kitabu Kitukufu na Sunna Tukufu ya Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.). Na mwisho wa maombi yetu ni kumshukuru Mola Mlezi wa walimwengu.
87
Page 87
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba
Rejea 1. Qur’ani Tukufu na tafsiri zake. 2. Tafsir At-Tabari. 3.Tafsir Al-Baydhawi. 4. Tafsir Al-Kashaf cha Az-Zamakhshar. 5. Tafsir Ad-Durul-Manthur cha As-Suyuti. 6. Nahjul-Balagha, kutoka kwenye hotuba za Imam Ali (a.s.). 7. Al-Mustadrak cha Al-Hakim. 8. Musnad Ahmad bin Hanbal. 9. Sahih Muslim. 10. Biharul-An’war cha Sheikh Al-Majlis. 11. Al-Ghadir Fil-Kitabi Was-Sunnah cha Sheikh Al-Amin. 12. Al-Manaqib cha Al-Khawarizmi. 13. As-Sawaiqul-Muhriqah. 14. Tadhkiratul-Samtwayn. 15. Al-Fusulul-Muhimmah cha Ibnu As-Swabagh. 16. Kifayatut-Talib. 17. Sharhul-Mawahib. 18. Dhakhairul-Uqba. 19. Nadhariyatu An-Nubuwah Wal-Imamah cha mwandishi wa kitabu hiki. 20. Vitabu vya lugha na historia. 21. Qamusul-Muhiti Fil-Lughah. 22. Tarikh Baghdad cha Al-Khatib Al-Baghdadiy. 23. Tarikh Murujud-Dhahab cha Al-Mas’udiy. 24. Tarikh Ibnu Asakir. 25. Maj’mauz-Zawaid. 26. Kifayatul-Athar. 27. Murujudh-Dhahab. 88
Page 88
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba
ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION: 1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9. 10. 11. 12. 13. 14. 15. 16. 17. 18. 19. 20. 21. 22. 23. 24. 25. 26. 27. 28.
Qur’ani Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka kumi na Tisa Uharamisho wa Riba Uharamisho wa uwongo Juzuu ya kwanza Uharamisho wa uwongo Juzuu ya pili Hekaya za Bahlul Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.) Hijab vazi Bora Ukweli wa Shia Ithnaashari Madhambi Makuu Mbingu imenikirimu Abdallah Ibn Saba Khadijatul Kubra Utumwa Umakini katika Swala Misingi ya Maarifa Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia Bilal wa Afrika Abudharr Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu Salman Farsi Ammar Yasir Qur’ani na Hadithi Elimu ya Nafsi Yajue Madhehebu ya Shia Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur’ani Tukufu Al-Wahda Ponyo kutoka katika Qur’ani 89
Page 89
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba 29. 30. 31. 32. 33. 34. 35. 36. 37. 38. 39 40. 41. 42. 43. 44. 45. 46. 47. 48. 49. 50. 51. 52. 53. 54. 55. 56. 57. 58. 59.
Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii Mashukio ya Akhera Al Amali Dua Indal Ahlul Bayt Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna Haki za wanawake katika Uislamu Mwenyeezi Mungu na sifa zake Amateka Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) Adhana. Upendo katika Ukristo na Uislamu Nyuma yaho naje kuyoboka Amavu n’amavuko by’ubushiya Kupaka juu ya khofu Kukusanya swala mbili Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Kusujudu juu ya udongo Maulidi Tarawehe Malumbano baina ya Sunni na Shia Kupunguza swala safarini Kufungua safarini Kuzuru makaburi Umaasumu wa Manabii Qur’ani inatoa changamoto Tujifunze misingi ya dini Nahjul Balagha Sehemu ya Kwanza Nahjul Balagha Sehemu ya Pili Dua Kumayl Uadilifu wa masahaba 90
12:36 PM
Page 90
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba 60. 61. 62. 63 64. 65. 66. 67. 68. 69. 70. 71.
Asalaatu Khayrunminaumi Sauti ya uadilifu wa binadamu Umaasumu wa Mitume Sehemu ya kwanza Maswali na Mishkili Elfu Sehemu ya kwanza Umaasumu wa Mitume Sehemu ya pili Umaasumu wa Mitume Sehemu ya tatu Maswali na Mishkili Elfu Sehemu ya pili Maswali na Mishkili Elfu Sehemu ya Tatu Sala ni nguzo ya dini Malezi ya mtoto katika Uislamu Shia asema haya, Sunni asema haya, wewe, wewe wasemaje? Mikesha ya Peshawar
91
Page 91
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
12:36 PM
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba
BACK COVER (1) UBORA WA IMAM ALI JUU YA MASAHABA Dalili ya kisheria yenye kuonyesha ubora wa Imam Ali bin Abi Talib (a.s.) haijakomea kwenye juhudi pekee za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na maneno yake ambayo yalikuwa yakitoka kwake kuelezea nafasi ya Ali (a.s.), bali juhudi hizo zimeambatana na uteremkaji wa aya nyingi za Qur'anI ambazo zimebeba jukumu la kudhihirisha fadhila za Ali (a.s.). Mwenye kufuatilia maelezo yote atayakuta kuwa upande mmoja yameangazia ubora wa Ali (a.s.) juu ya masahaba wote si kwa kulinganisha tu, bali maelezo hayo yanajumuisha zaidi ya maana hii, hivyo, kwa makusudio yake yanakusanya maana nyingine, nayo ni kuwa Ali (a.s.) kwa sifa zake takatifu ndiye mwanadamu aliyeandaliwa kuchukua Uimamu na Ukhalifa baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na wala si mwingine. (2) USHIA NDIO NJIA ILIYONYOOKA Hakika mirathi ya Ahlul Bait (watu wa nyumba ya Bwana Mtume) ambayo imehifadhiwa na kambi yao na wafuasi wao dhidi ya upotovu inaonyesha kambi iliyokusanya aina mbalimbali za taaluma za Kiislamu. Kambi hii imeweza kulea nafsi mbalimbali zilizo tayari kunywa kutoka kwenye chemchemu hiyo, na kuupa Umma wa Kiislamu wanavyuoni wakubwa wenye kufuata nyayo za ujumbe wa Ahlul Bait. Wanavyuoni waliokusanya vidodosa na maswali mbalimbali ya madhehebu na mitazamo tofauti ya kifikra kuanzia ndani ya desturi ya Kiislamu hadi nje ya desturi hiyo, huku wao wakitoa majibu na utatuzi makini juu ya maswali hayo ndani ya karne zote. Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Nukushi: +255 22 2127555 Barua Pepe: alitrah@raha.com Tovuti: www.alitrah.org Katika mtandao: www.alitrah.info 92
Page 92
Ubora wa Imam Ali Juu Ya Maswahaba final Edit Lubumba.qxd
7/15/2011
Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba
93
12:36 PM
Page 93