Uislamu na uwingi wa dini

Page 1

Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

UISLAMU NA UWINGI WA DINI Kimeandikwa na: Ayatullah Shahid Mutahhari

Kimetarjumiwa na:

7/15/2011

12:40 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

B

7/15/2011

12:40 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

ŠHaki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: 978 - 9987 - 512 - 86 - 7

Kimeandikwa na: Ayatullah Shahid Mutahhari

Kimetarjumiwa na: Dr. M. S. Kanju Kimepangwa katika Kompyuta na: Hajat Pili Rajab

Toleo la kwanza:Oktoba 2011 Nakala: 1000

Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Nukushi: +255 22 2127555 Barua Pepe: alitrah@raha.com Tovuti: www.ibn-tv.com Katika mtandao: www.alitrah.info

7/15/2011

12:40 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

YALIYOMO Dibaji........................................................................................................... Utangulizi...................................................................................................6 Mfumo unaotambua mawazo, misimamo mbali mbali kijamii..................8 Mfumo unaotambua dini mbalimbali........................................................11 Wasifu wa Hayati Ayatullah Murtadha Mutahhari....................................25 Matendo mema Mema ya wasio Waislamu.............................................39 Mwelekeo wa jumla wa mjadala .............................................................43 Dini yoyote haitakubaliwa zaidi ya Uislamu............................................46 Matendo mema bila Imani........................................................................50 Namna mbili za kufikiri............................................................................51 Mantiki ya tatu..........................................................................................52 Namna mbili za kufikiri.............................................................................51 Mantiki ya tatu...........................................................................................52 Wanaoitwa Wasomi...................................................................................53 Kundi lenye msimamo mkali....................................................................60 Maana ya Imani ......................................................................................64 Kuwajibika kwa sababu ya kutoamini.....................................................65 Viwango vya Unyenyekevu .....................................................................66 Uislamu wa kweli na Uislamu wa kamaeneo..........................................69 Dhati, sharti ya kukubaliwa amali.............................................................72

7/15/2011

12:40 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Ubora au wingi..........................................................................................79 Msikiti wa Bahlul ....................................................................................82 Imani juu Mwenyezi Mungu na Akhera...................................................83 Imani juu ya Utume na Uimamu...............................................................91 Kuharibika.................................................................................................96 Chini ya sifuri..........................................................................................104 Dhati za Waislamu...................................................................................118 Hali ya kimaumbile na hali ya kidesturi..................................................125

7/15/2011

12:40 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

NENO LA MCHAPISHAJI Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiingereza kiitwacho, Islam and Religious Pluralism, kilichoandikwa na Ayatullah Murtadha Mutahhari. Sisi tumekiita, Uislamu na Uwingi wa Dini. Kitabu hiki kinazungumzia suala muhimu sana la kuvumiliana hususan katika dini. Mara nyingi tumesikia katika nchi mbalimbali watu wakipigana na kuuana kwa sababu ya tofauti za itikadi zao za kidini. Baadhi ya wafuasi wa dini ni wachokozi na wengine wanashindwa tu kuwavumilia wenzao au itikadi za dini nyingine. Hii ni tabia ambayo imejengeka tu kwa watu, na wakati mwingine maadui wa dini hutumia mianya hii kuwagombanisha waumini wa dini moja au wa dini mbalimbali ili kukidhi malengo yao ya kisiasa. Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa utandawazi ambapo mambo mengi ya kupotosha yamepata mwanya wa kuingia katika jamii yetu kutokana na ulimwengu kuwa kama kijiji. Shahid Allama Murtadha Mutahhari alikuwa ni mwanachuoni mkubwa wa zama hizi, mtalaamu katika masuala ya dini. Ameyachambua masuala haya ya kuvumiliana katika dini kwa kina na kutuonesha njia. Kutokana na ukweli huo, Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili.

7/15/2011

12:40 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Tunamshukuru ndugu yetu, Dr. M. Kanju kwa kukubali jukumu hili la kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake. Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa ni changamoto kubwa kwa wasomaji wetu, hususan vijana wetu ambao ni waathirika wakubwa wa tamaduni hizi za Magharibi. Mchapishaji: Al-Itrah Foundation

7/15/2011

12:40 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu.

Abi Abdillah (Imamu Jafar ibn Muhammad as-Saqid a.s) anaripoti kutoka kwa baba zake (maimamu a.s) ambao wamesema: “Siku moja alikuja mtu mmoja kwa Mjumbe wa Allah (s.a.w.w) na akasema ‘Ewe Mjumbe wa Allah, elimu ni nini?’ Mtume alijibu ‘Ni ukimya,’ yule mtu akauliza, ‘kisha nini?’ Mtume akasema ‘kusikiliza,’ yule mtu akauliza, ‘kisha nini?’ Mtume akasema, ‘kisha kukumbuka’ yule mtu akauliza kisha nini? Mtume akasema, ‘Ni kuitumia elimu hiyo katika vitendo.’ Kisha yule mtu akauliza, ‘kisha nini ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu?’ Mtume akajibu, ‘ni kuwafundisha wengine (kile mtu alichojifunza).’”

Katika kuzingatia mafundisho ya Uislamu ya kuonyesha heshima na kuomba dua wakati wowote jina la Allah, Mtume wake na watu wengine wema na waongofu linapotajwa tumetumia herufi zifuatazo za Kiarabu baada ya majina hayo. Subhanahu wa Ta’ala (s.w.t) - Hutumika baada ya jina la Allah pekee yake. Lina maana Utukufu na Ukubwa wote ni wa Mwenyezi Mungu. Sallalah Alayhi wa Alihi wa Salam (s.a.w.w.)- Hutumika baada ya jina la Mtume Muhammad peke yake na ina maana baraka za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na familia yake. Alayhis Salam (a.s) - Hutumika baada ya jina la mmoja wa watu wa Ahlul Bait wa kiume au kwa Mitume wa Mwenyezi Mungu waliotangulia maana yake ni amani iwe juu yake. i

7/15/2011

12:40 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Alayhas Salam (a.s)- Hutumika baada ya jina la mtu wa kike wa Ahlu Bait wa Mtume au wanawake wengine watukufu na ina maana amani iwe juu yake. Alayhumus Salam- Hutumika kwa watu wawili au zaidi ambao ni Ahlul Bait au Mitume waliopita. Radhiallahu Anhu (r.a)- Hutumika kwa kila sahaba muongofu wa Mtume au sahaba wa maimamu wa Ahlul Bait. Ina maana Mwenyezi Mungu awe radhi naye. Quddisa Sirruh- Hutumika kwa ajili ya wanachuoni na watu wengine watukufu katika Uislamu. Ina maana Mwenyezi Mungu aibariki roho yake.

ii

7/15/2011

12:40 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

7/15/2011

12:40 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini

DIBAJI na Hasnain Walji Miaka kadhaa huko nyuma, katika mji wa Brampto Canada, majlisi yangu ya Muharram iliamsha swali; “ Je, Mama Terresa atakwenda wapi - Peponi au motoni?” Hii ilikuwa ni kutokana na hisia juu ya uwasilishaji wangu wenye changamoto juu ya mfumo wa jamii ya dini mbalimbali, mfumo ambao ulielekea kuwavutia wengi wa washiriki wa kongamano, ambao kutokana na majadiliano ya kielimu katika duru za kisomi walikuwa wakionekana kukubaliana kuwa ‘barabara zote zinaekea Roma.’ Majadiliano yangu ya tahadhari pamoja na baadhi ya wasomi hawa wa jamii yetu ilidhihirisha kutokutambua kwao kuwa dhana ya asili ya mfumo wa jamii ya dini mbalimbali, ulikuwa ni ulinzi tatanishi wa kuilinda itikadi ya wokovu kupitia kwa Kristo, na hivyo kuweka katika Ukristo dhana ya kuvumiliana kwenye dini nyingine. Kimsingi, mzizi ya mfumo wa jamii ya dini mbalimbali imeegemea kwenye maendeleo ya mfumo wa uhuru wa kisiasa huko Ulaya katika karne ya kumi na nane, ambapo Ulaya ilikuwa inayumba kutokana na simulizi za kutisha juu ya mateso ya kidini. Wanafikra walioelimika wa huko Ulaya wa wakati ule walikuwa wanaonyesha hisia juu ya hali ya kutovumiliana baina ya dini ambako kuliishia kuwa hali ya historia ya kivita vya kimadhehebu iepukwe kwa hali yoyote ile. Baada ya kuwa wameshuhudia madhara ya kutokuwa na uvumilivu wa kidini, Wazungu Wakristo walioishi katika karne ya kumi na nane walikuwa na shauku kubwa ya kuondokana na madhara haya kwa kupitia itikadi ambayo imefungwa katika kanuni za kidini na hivyo kupata athari yake ya kudumu ya kuhakikisha amani na maendeleo huko Ulaya kisiasa na kifalsafa - wakati huo huo wakilinda heshima na hadhi ya Ukristo. 2

7/15/2011

12:40 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini

Mtetezi mkuu (wa nadharia hii), Profesa John Hick, alibuni nadharia hii tete kueleweka ya mfumo wa jamii ya dini mbalimbali kwa kuishirikisha itikadi ya kikristo ya uwokovu, kuruhusu takriban mtu yeyote kuingia mbinguni (Peponi). Katika kujenga hoja yake, Hick ametumia miongoni mwa mambo mengine hekaya ya Rumi ya watu vipofu waliokuwa wakijaribu kumuelezea tembo. Hivyo anadokeza kwamba katika uonaji wetu wa ukweli halisi, tupo kama wale vipofu wanaojaribu kumuelezea tembo namna alivyo. Ukweli wetu halisi umewekewa mipaka na mifumo ya dini mbali mbali. Kwa maneno mengine, iwe ni kwa kushika mkonga, mguu au sikio, ilikuwa inatosheleza kumuwazia tembo alivyo. Wakati ambapo Rumi alitumia hekaya hii kuonesha mipaka yetu katika kuelewa ukweli halisi, Hick alielezea mfumo wa jamii ya dini mbalimbali kwa kudokeza kwamba imani mbali mbali zilizopo ulimwenguni zinazotofauti zinazoafikiana katika jitihada ya (kuujua) ukweli halisi. Kwa kweli ni hali ya mambo inayosikitisha kwamba, wakati sisi Waislamu tumebarikiwa kwa kuwa na majibu mazuri zaidi juu ya masuala magumu ya kipekee, lakini wasomi wa Kiislamu waweze kuridhishwa na maelezo dhaifu ya Hick yasiyoungwa mkono na yeyote isipokuwa wanafikra wa Kikristo waliotwezwa!! Tafsiri hii ya wakati muafaka ya Insha ya Kifursi juu ya Uislamu na mfumo wa jamii ya dini mbalimbali, iliyoandikwa na Ayatullah Shahid Mutahhar imekuja wakati muafaka na ni mchango unaohitajika sana katika kuendeleza mdahalo huu, ili kutuwezesha kuuelewa vizuri zaidi mtazamo wa Uislamu juu ya mfumo wa jamii ya dini mbalimbali. Kazi hii ni mfano mwingine wa uwezo wa uoni wa mbali kiwerevu wa marehemu Mutahhari, kwani miongo mingi iliyopita, alijitolea kulizungumzia masuala ya kisasa yaliyo tete na magumu yanayowakera 3

7/15/2011

12:40 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini vijana wa Kiislamu wanaokabiliwa na taaluma za ki-Magharibi. Kitabu hiki kinatoa majibu ya kimanki katika maswali kama vile je wavumbuzi na wanasayansi mashuhuri watakwenda motoni licha ya mchango wao mkubwa katika maendeleo na maisha ya mwanaadamu? Je watu kama Pasteur na Edison watakwenda motoni huku watu wavivu na tepevu waliomaliza umri wao katika kona ya msikiti wakienda peponi? Je Mwenyezi Mungu ameumba pepo kwa ajili ya Mashia peke yao? Tofauti na maoni dhaifu ya kuridhiana ya Hick, wanachuoni wa Kishia wanakubaliana kwa ujumla kuwa laana ya Mwenyezi Mungu haiwahusu vivi hivi tu wale wote ambao hawakuamini ufunuo Wake. Kwa mfano watasamehewa wale wasiokuwa na uwezo kama vile watoto wadogo na watu wazima wenye ulemavu wa akili. Wanachuoni wa Ahlul Bait wanatofautiasha baina ya wasiokuwa na uwezo (qasir) na wanaopuuzia (muqassir) ambao licha ya kuwa na uwezo wa kujifunza juu ya Uislamu au kuziona hoja zake wameziba nyoyo zao na kuweka imani zao mahali pasipostahili. Uchunguzi wa Shahidi Mutahhari juu ya tatizo la mfumo wa jamii ya dini mbalimbali anachambua kwa kinaganaga tofauti ya makundi haya mawili. Kinachofurahisha zaidi ni kuwa ameliezea lile kundi la qasir (wasiokuwa na uwezo) kwa kuwaingiza humo wale pia ambao Uislamu haukuwafikia. Kwa mfano makazi ya mbali ambako Uislamu haujaenezwa au wale wanaoishi katika mazingira ya hofu juu ya Uislamu “Islamaphobic” (ambapo kuna propaganda nyingi chafu dhidi ya Uislamu) ambayo imesababisha watu kuwa na dhana ya uelewal mbaya dhidi ya Uislamu. Ufafanuzi mahiri wa Shahid Mutahhir juu ya wasio na uwezo unajenga hoja kuwa Pepo haikuumbwa kwa ajili ya wachache tu ndani ya kundi dogo. Hivyo, kujibu kwa ujasiri fasaha itikadi za kulazimisha mambo (dogmatism) zinazoendelezwa kwa bidii na wale aliowaita ‘wenye akili finyu, wasioonyesha hisia, watakatifu (tagh nazari khushk muqaddasan). Matokeo ya ung’ang’anizi huu wa kulazimisha imani yamedhihirishwa katika dhana potavu mbali mbali za Kishia. Katika kulielezea hili siwezi 4

7/15/2011

12:40 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini kulielezea vizuri bila kunukuu mfano mmoja uliotolewa na Ayatullah Mutahhari: “Je tutaacha wasia kwamba sehemu kubwa kati ya fedha nyingi tulizozichuma katika njia zisizo nzuri au ambazo tungezitumia wakati wa uhai wetu katika mambo mema – lakini hatukufanya hivyo - wapewe waangalizi wa moja ya makaburi ya watu wema –watakatifu ili tuzikwe jirani na watakatifu hao ili malaika wasithubutu kutuadhibu. Watu kama hawa wajue kuwa wamepofushwa, na mapazia ya kutojali yamefunikwa machoni mwao.” Ninahitimisha kuwa kutafuta njia nyingine ya kuridhisha udadisi wa akili katika majadiliano haya, kwa hali yoyote ile kunaishia kwenye kuanguka kutoka katika kikaango cha “tang nazari khoshk muqaddasan” na kutumbukia katika moto wa mfumo wa jamii ya dini mbalimbali. Hasnain Walji Plano Texas, May 7th 2004-17th Rabiul Awwal 1425.

5

7/15/2011

12:40 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini

UTANGULIZI Je Uislamu ni njia pekee ya kweli iliyonyooka? Je as-Siratul Mustaqim ni njia moja tu au kuna njia nyingine nyingi ambazo zote zinafikia sehemu moja? Nini kitachotokea kwa watu wasiokuwa waislamu wanaoishi maisha ya uadilifu na heshima bila kuvunja haki za wengine? Je wanapata uokovu na kwenda peponi au hapana? Haya ni baadhi ya maswali makali yanayotawala zama hizi. Dhana ya mfumo wa jamii ya dini mbalimbali sio mpya, imewahi kujadiliwa katika namna moja au nyingine na wanafalsafa wa huko nyuma pamoja na wanateolojia (wajuzi wa dini) wa dini na madhehebu mbali mbali. Hata hivyo, kutokana na kuongezeka kwa maingiliano baina ya wafuasi wa dini mbali mbali na majadiliano baina ya imani mbali mbali, mfumo wa jamii ya dini mbalimbali umepata uhai mpya katika mkondo wa fikra za sasa. Wakati mwanafalsafa mkubwa, Ayatullah Murtaza Mutahhari alipoandika kitabu chake chenye maamuzi, ‘Adl-e Ilahi (uadilifu wa Mwenyezi Mungu) takriban miaka thelathini na tano iliyopita, midahalo juu ya mfumo wa jamii ya dini mbalimbali ilikuwa haijawa maarufu kiasi hiki nchini Iran. Ulichoshika mikononi ni tafsiri ya sura ya mwisho ya ‘Adl-e Ilahi’ juu ya ‘Amali njema za Wasio Waislamu.’ Sehemu muafaka zaidi pa kujadili juu ya mfumo wa jamii ya dini mbalimbali na mambo yanayohusiana nao ni chini ya dhamira ya ‘nubuwwah - Utume’ wakati wa kujadili dhana ya kuwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) ni Mtume wa mwisho, hata hivyo na swali ‘vipi kuhusu amali njema za wasio Waislamu’ linahusika kwenye dhana ya uadilifu wa Mwenyezi Mungu, na hivyo Ayatullah Mutahhari amelijibu mwishoni mwa ‘Adl-e illahi yake. 6

7/15/2011

12:40 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini Hata hivyo kabla ya kulijadili swali hilo kwa undani, Ayatullah Mutahhari pia ametoa maoni yake mafupi juu ya mfumo wenyewe wa jamii ya dini mbalimbali. Kama utakavyosoma wewe mwenyewe, anaelezea mtazamo uliopo sasa wa wanateolojia na wanafalsafa wa Kiislamu kuwa Uislamu ni njia pekee iliyo sahihi. Hata hivyo, muhimu zaidi ni kuwa anawatahadharisha wasomaji kuwa wasirukie hitimisho kuwa maadam Uislamu ndio njia pekee iliyo sahihi basi wasio Waislamu wote watakwenda motoni. Katika muongo mmoja na nusu uliopita suala la mfumo wa jamii ya dini mbalimbali limekuwa likijadiliwa kwa hamasa na hisia kali miongini mwa Waislamu wa Magharibi na wa Mashariki pia. Baadhi ya wasomi wa Kiislamu wamejaribu hata kudai kuwa chanzo cha dhana ya mfumo wa jamii ya dini mbalimbali ni Qur’an yenyewe. Ningependa kuchukua nafasi hii kuwasolisha mazungumzo haya kwa kifupi kama dibaji katika kazi ya huyu mwanachuoni mkubwa Ayatullah Murtaza Mutahhari. Wakati tukijadili dhana ya mfumo wa jamii ya dini mbalimbali kwa muktadha wa Uislamu, ni muhimu kwanza kuelezea maana ya istlahi hii ya ‘mfumo wa jamii ya dini mbalimbali’ vizuri. ‘Uwingi (pluralism) unaweza kutumika katika maana mbili: Mfumo wa mitazamo mbali – kijamii (social pluralism), kisosholojia ina maana jamii yenye imani au tamaduni mbali mbali. Mfumo unaotambua dini mbali mbali (religious Pluralism) kiteolojia ina maana ni dhana ambayo inazitambua dini zote kuwa za kweli na sahihi.

7

7/15/2011

12:40 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini

MFUMO UNAOTAMBUA MAWAZO, MISIMAMO MBALI MBALI KIJAMII. Kuhusiama na dhana hii, Uislamu ni dini inayotaka watu wa dini na tamaduni mbali mbali kuishi pamoja kwa amani na kuvumiliana. Miongoni mwa dini zote tatu zinazojinasibisha na Nabii Ibrahim, ni Uislamu tu unaozitambua dini za Ukristo na Uyahudi. Uyahudi haumtambui Yesu kama masihi aliyekuwa akisubiriwa wala kuwa ni Mtume wa Mungu, na Ukristo haumtambui Muhammad (s.a.w.w) kama Mtume wa kweli na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu. Kwa imani ya Kiislamu, Mwenyezi Mungu alituma Mitume wengi na manabii ili kumuongoza mwanaadamu, idadi iliyotolewa katika hadithi ni Mitume 124,000 (laki moja na ishirini na nne elfu) Mtume wa kwanza alikuwa ni Adam na Mtume wa Mwisho alikuwa ni Muhammad (s.a.w.w) - Mtume wa Uislamu. Hata hivyo sio kwamba Mitume wote walikuwa na hadhi na daraja sawa.1 Mitume watano katika hawa wamepewa daraja ya juu zaidi na hao ni Nuh, Ibrahim, Musa, Issa (Yesu) na Muhammad (s.a.w.w). Mwenyezi Mungu anasema katika Qur’an.

“Na Tulipoweka ahadi (agano) na Mitume, na wewe na Nuh, Ibrahim, Musa na Issa mwana wa Mariam…”Al-Qur’an 33:7/ 42:13. 1 Suratul Baqarah (2), aya 253; Al-Qur’an Surat Bani Israil; 17:55 Amekuamrisheni Dini ileile aliyomuusia Nuh na tuliyokufunulia wewe, na tuliyowausia Ibrahim na Musa na Isa…

8

7/15/2011

12:40 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini Mwislamu anapaswa kuwaamini Mitume wote, bila hivyo hawezi kuhesabika kuwa ni Mwislamu.2 Mtu kwa mfano akisema ninamuamini Muhammad, Isa, Ibrahim na Nuh lakini simuamini Musa kuwa ni miongoni mwa Mitume wa Mwenyezi Mungu basi huyu hawezi kukubalika kuwa ni Mwislamu. Halikadhalika mtu akiwakubali Mitume wote ila akamkataa Isa kuwa sio miongoni mwa Mitume wa Mwenyezi Mungu, basi huyo si Mwislamu. Hii ndio sababu Uislamu huziita jamii za Wakristo na Wayahudi kuwa ni ‘watu wa kitabu’ (Ahlul Kitab). Uislamu umefikia hata hatua ya kuwaruhusu wanaume Waislamu kuwaoa wanawake wa Kikristo au Kiyahudi lakini sio wanawake wa imani nyingine. Jambo muhimu la kuzingatia hapa ni kuwa Uislamu uliwatambua Ahlul Kitab karne kumi na nne zilizopita katika kipindi ambacho kulikuwa hakuna kabisa mazungumzo juu ya kuvumiliana baina ya dini mbali mbali, au japo kampeni za umoja wa madhehebu mbali mbali za Kikristo.3 Kisiasa na kijamii, serikali ya Kiislamu itakuwa tayari kuingia mkataba na makundi madogo ya wakristo na Wayahudi. Imam Ali Zainul Abidiin, ambaye ni kitukuu cha Mtume (s.a.w.w) ameandika: “Ni haki ya wasiokuwa Waislamu wanaoishi katika nchi ya Kiislamu kuwa muwakubalie yale ambayo Mwenyezi Mungu ame2 Al-Qur'an 3:84. 3 Ilichukua Kanisa Katoliki takriban miaka 2000 kuwatambua wasiokuwa Wakiristo kujumuisha na Waislamu. Halimashauri ya Pili ya Vatican, ilitangaza, katika mwaka wa 1964 kwamba: “Wale ambao kwa makosa ambayo si ya kwao, hawajui Injili ya Yesu Kristo au Kanisa lake, lakini wanamtafuta Mungu kwa moyo mkunjufu, na kwa rehema wanajaribu katika matendo yao kufanya utashi wake kama wanavyoujua kwa mwongozo wa dhamira zao – hao pia watapata wokovu.” Vatican: Council II: Conciliar and Post Conciliar: Documents (Wilmington, Delaware: Scholary Resouces, 1975) uk. 367. 9

7/15/2011

12:40 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini wakubalia … Na mjizuie kuwafanyia dhulma, kuwanyima ulinzi wa Mwenyezi Mungu na kuonyesha kibri na jeuri dhidi yao kinyume na maagizo ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Kwa sababu tumeambiwa kuwa Mtukufu Mtume alisema: “Yeyote atakayemfanyia dhulma asiyekuwa Mwislamu aliye chini ya himaya ya Uislamu, mimi nitakuwa adui yake Siku ya Kiyama.”4 Ingawa Uislamu haujawapa wafuasi wa dini nyingine hadhi kama iliyowapa Wakristo na Wayahudi, bado Uislamu unaamini kuwa wafuasi wa dini zote wanapaswa kuishi pamoja kwa amani. Moja ya ujumbe wa kuishi pamoja kwa amani uliotolewa na Mtume Muhammad (s.a.w.w) kwa waabudu masanamu wa Makka upo katika sura ya 109 ya Qur’ani: Sema: “Enyi makafiri! Mimi siabudu mnachokiabudu, wala nyinyi si wenye kuabudu ninayemuabudu, wala si mimi mwenye kuabudu mnachokiabudu wala nyinyi hamtamuabudu ninayemuabudu nyinyi mna dini yenu na mimi nina dini yangu.” Kwa mtazamo wa kihistoria, jamii za Kiislamu zilivyokuwa zikiwatendea jamii za walio wachache chini ya utawala wao hususan Wayahudi na Wakristo ni vizuri sana ikilinganishwa na jamii za walio wachache (minorities) zilivyokuwa zikitendewa katika Ulaya ya Kikristo.5 4 Imam Ali, Zainul Abidiin Risalatul Huquq, tarjuma ya SSA Rizvi (Vancouver: VIEF, 1989) Uk. 36. 5 Ira Lapidus anaandika hivi: ‘Watawala wa Ottoman kama ilivyokuwa kwa watawala wengine wa Kiislamu, walikuwa wakiwachukulia wasio Waislamu kama watu huru kuwa na utawala wao wa ndani ambao mambo yao ya kijamii, kidini na kijumuiya yaliendeshwa na taasisi zao za dini, lakini viongozi wao waliteuliwa, na kuwajibika kwenye dola ya Kiislamu. Tazama ‘A History of Islamic Societies, NY, Cambridge Unicersity Press, 1990, uk. 323. Pia tazama Marshall Hodgson, The Venture of Islam, vol.1- Chicago, University of Chicago Press, 1974, uk. 306. 10

7/15/2011

12:40 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini

MFUMO UNAOTAMBUA DINI MBALI MBALI. Mtetezi mkuu wa nadharia hii ya kisasa ya mfumo wa jamii ya dini nyingi ni John Hick, ambaye aliachana na uhafidhina wake wa kikatoliki na akaunda nadharia yake mahsusi katika miaka ya sabini. Nadharia ya Hick ya kuzitambua dini zote inadai kuwa kila dini kwa namna yake huwakilisha ufunuo halisi ya ulimwengu wa ki-mbingu na pia huwakilisha njia sahihi ya uokovu (uongofu). Anaamini kuwa dini zote ni majibu yaliyoundwa kitamaduni kwa ajili ya ukweli halisi na kwa hiyo dini zote zina thamani sawa, sahihi na mtu anaweza kuingia mbinguni (peponi) kwa kutumia yoyote katika dini hizi. Hick anatumia hadith maarufu ya fumbo la masufi wa kihindu katika kufafanua hoja yake: “Tembo aliletwa katika kundi la vipofu ambao walikuwa hawajawahi kukutana na tembo katika maisha yao. Mmojawao aligusa mguu na akasema kuwa tembo ni nguzo kubwa yenye uhai. Mwingine aligusa mkonga na akasema kuwa tembo ni nyoka mkubwa. Mwingine aligusa meno ya ndovu na akasema kuwa ni kama jembe la kulimia kwa ng’ombe na kadhalika. Kisha wote wakaanza kuzozana kila mmoja akidai yeye alivyoelezea ndio sawa na hivyo wengine wote ni waongo. Kwa kusema kweli wote walisema kweli lakini kila mmoja aliezea sehemu tu ya ukweli usio timilifu.”6 Kuna udhaifu mwingi katika nadharia ya Hick. Tatizo kubwa zaidi ni kujaribu kupatanisha madai-ya-kweli yanayokinzana baina ya dini mbali mbali (madai ambayo kila dini hudai yake ndio ya kweli); kwa mfano imani ya tawhidi (kuamini juu ya kuwepo kwa Mungu mmoja tu) ya Uislamu dhidi ya miungu wengi (shirki) katika dini ya Kihindu, imani ya 11

7/15/2011

12:40 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini kifo na ufufuo katika Uislamu na Ukristo dhidi ya imani kuwa roho ya marehemu huingia katika mwili wa mtu mwingine na kufikia hatua ya nirvana (yaani hali ya kujisahau binafsi kwa kuungana na Mungu) katika dini ya Budha; uokovu kupitia Utatu mtakatifu dhidi ya imani ya tawhidi n.k. Ili kutanzua tatizo la yale madai-ya-kweli yanayopingana (ambayo kila dini hudai imani yake ndio ukweli), Hick anapendekeza kwamba simulizi za kidini zinatofautiana katika mambo matatu: Mambo ya kihistoria Mambo ambayo hayawezi kuthibitishwa kihistoria. Dhana juu ya Mungu. Kisha anapendekeza suluhisho la tofauti hizi. Ama kwa kutokubaliana na habari za kihistoria, Hick anapendekeza kuwa haya ni mambo madogo madogo sana na yanaweza kutatuliwa kwa kutumia njia za kihistoria. Na kuhusiana na tofauti za ukweli ambao hauwezi kuthibitishwa kwa ushahidi wa kihistoria au kiutawala (kama vile, je ulimwengu utakuwepo milele au ni wa muda mfupi? Watu watakufa na kufufuliwa au roho zao zitaingia katika miili mingine? n.k. Juu ya hili anasema kuwa suluhisho juu ya tofauti hizi sio muhimu au lazima kwa ajili ya kupata uokovu na kwamba dini mbali mbali zinapaswa kukaa na kuzungumza zaidi ili kubadilisha kidogo imani zao. Na kuhusiana na tofauti juu ya dhana ya Mungu, Hick anaamini kuwa hadith za dini zote juu ya Mungu ni udhihirisho sahihi na kwamba mtazamo au imani yoyote juu ya Mungu alivyo ni dhihirisho sahihi la uso wa Mungu.7 Mwisho Hick anaamini kuwa imani yoyote ya dini ambayo itapingana na imani nyingine ya dini, na kama kwa kwa uhalisi ikawa ni kweli, ikafanya imani ya dini nyingine ni ya uongo, basi lazima imani hiyo ichukuliwe kuwa ni ya kubuniwa (ni ya uongo). Matokeo ya mwisho ya nadharia hii ni kuwa ili kuifanya iweze kufanya 7 Hick, An Interpretation of religion; New Haven: Yale University Press, 1989 Uk. 364-365. 12

7/15/2011

12:40 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini kazi, Hick angepaswa kutafsiri upya imani nyingi za kidini katika namna ambayo waanzilishi na wafuasi wa dini hizo wangeipinga vikali sana! Hebu chukua mfano wa hali ya kihistoria ya Yesu kwa mitazamo ya Uislamu, Ukristo na Uyahudi:

Dhana

Ukristo

Uislamu

Uyahudi

Kuzaliwa kimuujiza

Ndiyo

Ndiyo

Hapana

Miujiza.

Ndiyo

Ndiyo

Hapana

Cheo

Masihi na mwana wa Mungu

Mtume na Mjumbe wa Mungu

Hapana

Ufunuo

Injili iliandikwa na Injili ilifunuliwa Hapana waandishi mbalimbali na Mungu kwa Issa.

Kifo na baada ya kifo.

Alisubuliwa ili kuosha Hakusulubiwa, dhambi na alifufuka Alichukuliwa siku ya tatu. mbinguni.

Alisulubiwa na kufa.

Mbali na vipengele viwili vya mwanzo (na hivyo vilevile ni kati ya Uislamu na Ukirsto), dini zote hizi tatu zinazojinasibisha na Nabii Ibrahim (a.s) zinapingana na kutofautiana juu ya dhana mbali mbali juu ya Yesu. Kwa mujibu wa nadharia ya John Hick, imani mbili za mwanzo zinazofanana zitachukuliwa kuwa ni za “ukweli” (angalau kwenye Ukristo na Uislamu) wakati ambapo nukta nyingine za kutopatana lazima zishughulikiwe katika njia mbili zinazowezekana: Ama mitazamo hii inayogongana lazima itatuliwe kwa njia ya kihistoria au iwekwe katika kundi la “mithi13

7/15/2011

12:40 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini olojia (visasili)!” Suluhisho la kwanza litawalazimisha Wayahudi, Wakristo na Waislamu kuzikataa aya nyingi za vitabu vyao vitakatifu, ambapo suluhisho la pili litayaweka maelezo mengi ya Qur’ani na Biblia katika kundi la “mithiolojia (visasili).” Hakuna suluhu yoyote itakayokubalika kwenywe imani hizi tatu. Nafikiri kuwa mfano huu mmoja (vilevile wa Uislamu mkabala na Ukiristo na Uyahudi ambazo zipo karibu zaidi zenyewe kwa zenyewe kuliko Uislamu mkabala na Uhindu na Ubudha) unatosheleza kuonyesha kuwa nadharia ya Hick ya mfumo wa jamii ya dini nyingi hautekelezeki. Kwa kutegemea juu ya suluhisho la Hick juu ya masula yanahusiana na kifo na baada ya kifo, Waislamu watalazimika kuzichukulia zaidi ya Aya mia tano za Qur’ani juu ya kifo, ufufuo na maisha ya akhera kuwa sehemu ya mithiolojia (visasili)! Tukija katika tofauti ya tatu juu ya dhana juu ya Mwenyezi Mungu, Dr. John Hick anatutaka tuamini kuwa Utatu Mtakatifu wa Ukristo, uwingi wa masanamu wa dini ya Kihindu na Tawhidi ya Uislamu - imani zote hizi ni sawa, sahihi na za kweli. Nadharia hii hudhoofisha imani ya mtu katika dini yake na humsukumia mtu katika kuamini kuwa hakuna habari za Mungu wala hatuwezi kuzijua, kama sio kwenye ukafiri kabisa wa kuamini kuwa hakuna Mungu. Akitumia mtazamo wa Immanuel Kant wa makundi mawili mawili, Hick anasema kuwa kuna tofauti kati ya ‘kitu kilivyo hasa’ na ‘kinavyoonekana.’8 Kitu kinaweza kuwa kweli ‘chenyewe kama kilivyo’ lakini 8 John Hick, An Interpretation of Religion, uk. 241. Kwa maneno mengine hatuwezi kumjua Mwenyezi Mungu vilivyo, tunachokijua ni dhana zetu juu Yake. Wanafalsafa wa Kiislamu hawakubaliani na nadharia ya Kant. Kwa habari zaidi juu ya nadharia ya elimu kwa mtazamo wa Uislamu, Tazama kitabu cha Sayyid Muhammad Husayn Tabatabai kiitwacho, The Elements of Islamic Metaphysics, kilichotafsiriwa na S.A.Q Qarai (London; ICAS Press, 2003) uk. 115-132, na pia sehemu ya kwanza ya S.M Baqir as-Sadr, Our Philosophy, kilichotafsiriwa na Shams c. Inati (London: Muhammadi Trust, 1987). 14

7/15/2011

12:40 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini kinapotazamwa na wengine huwa ‘kwa kiasi ni kweli.’ Kwa msingi wa wazo hili, Hick anataka dini zote zikubali dhana zote zinazotofautiana juu ya Mungu kuwa zote hizi ni za kweli unaolingana kwa sababu hakuna hata moja (dhana) ambayo ni kweli kabisa, zote ni za ‘kwa kiasi ni kweli.’ Kwa jinsi Hick alivyoitumia nadharia ya watu vipofu na tembo anawachukulia watu wote wanaofuata dini kuwa vipofu na hawana uwezo wa kujua ukweli kamili. Kwa bahati mbaya, amekosa fundisho la kisa hikihiki (cha vipofu na tembo) kama lilivyotolewa na Maulana Rumi: “Baadhi ya wahindu wana tembo wa kumuonyesha. Hakuna yeyote hapa aliyewahi kumuona tembo. Wanamleta usiku na kumuweka katika chumba cha giza. Mmoja mmoja tunaingia gizani na kutoka tukieleza jinsi huyu mnyama alivyo. Mmoja wetu anabahatika kushika mkonga “Ni kiumbe aliye kama bomba la kupitisha maji.” Mwingine sikio. “Ni feni kubwa yenye nguvu, wakati wote inakwenda mbele na nyuma. Mwingine, mguu. “Nauona umetulia, kama nguzo kwenye hekalu.” Mwingine anagusa mgongo uliokunjika. “Ni kiti cha enzi cha ngozi.” Mwingine, jasiri zaidi, anagusa jino la tembo. “Ni upanga wa duara uliotengenezwa kwa udongo wa mfinyazi.” Anaona fahari kwa maelezo yake.

15

7/15/2011

12:40 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini Kila mmoja wetu anagusa sehemu moja na anaelewa kwamba tembo mzima yupo hivyo. Kiganja na vidole vinavyopapasa gizani ndivyo jinsi fahamu zinavyogundua uhalisi tembo. Kama kila mmoja wetu angeshika mshumaa pale, na kama tungeingia wote pamoja, tungemuona.9 Watu hawa walikuwa wanapapasa gizani kwa hivyo walimwelezea tembo visivyo. Kama wangetumia “mshumaa,” wangeona nuru! Katika Uislamu, Mwenyezi Mungu huwa hamuwachi anayetafuta ukweli akipapasa gizani.

“Mwenyezi Mungu ni Mlinzi wa walioamini, huwatoa gizani na kuwaleta kwenye nuru.” Qur’ani 2:257

Qur’ani na mfumo wa jamii ya dini nyingi. Baadhi ya wasomi wa Kiislamu wamejaribu kuisoma nadharia ya mfumo wa jamii ya dini nyingi katika Qur’ani yenyewe. Hoja mashuhuri wanayoitumia ni kuwa neno ‘Uislamu’ katika Qur’ani lisitumike kama nomino (jina) bali kama kitenzi. Wakati fulani wanatofautisha kati ya “Uislamu: (kitendo cha kujinyenyekesha kwa Mwenyezi Mungu) na Uislamu (dini); na wanasema kwamba ujumbe muhimu wa Mwenyezi Mungu na msingi wa wokovu ni kujinyenyekesha kwa Mwenyezi Mungu na haijalishi kama kujinyenyekesha huko kunafanyika kwa kupitia mafundisho ya Ibrahim, Musa, Isa au Muhammad (s.a.w.w). 9 The essential Rumi kilichotafsiriwa na C.Barks New Jewrsey Castle Books, 1997 uk. 525. 16

7/15/2011

12:40 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini Hapa hakuna jipya katika hili; hata Ayatullah Mutahhari; ndani ya kitabu hiki, ameandika: “Kama mtu atasema kuwa maana ya Uislamu katika aya hii sio hii dini yetu makhsusia, bali makusudi ni maana halisi ya neno hasa, au kujinyenyekesha kwa Mwenyezi Mungu, jawabu litakuwa bila shaka kuwa Uislamu ni kujinyenyekesha, na dini ya Uislamu ni dini ya kujinyenyekesha, lakini uhalisia wa kujinyenyekesha una muundo wake maalum katika kila zama. Na katika zama hizi muundo wake ni dini ile ile inayothaminiwa, iliyoletwa na Mwisho wa Manabii (Muhammad). Hivyo ina maana kuwa neno ‘Uislamu’ (unyenyekevu) linabaki lazima kutumika kwa kumaanisha dini ya Uislamu tu. “Kwa maneno mengine sharti kubwa la unyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu ni kukubali amri zake, na ni wazi kuwa ni lazima mtu atii amri za mwisho zilizoletwa na Mwenyezi Mungu. Na amri za mwisho za Mwenyezi Mungu ni zile zilizoletwa kwa Mtume wake wa mwisho, Muhammad (s.a.w.w).”10

Uislamu katika Qur’ani (3:19-20). Kwa mfano wakati Qur’ani inaposema: “Kwa hakika dini mbele ya Mwenyezi Mungu ni Uislamu,11 baadhi ya wasomi wa Kiislamu wanasema kwamba hapa neno Uislamu halimaanishi dini iliyoanzishwa karne ya saba na Mtume Muhamamd (s.a.w.w) wanasema hapa Uislamu una maana kujinyenyekesha mbele ya Mwenyezi Mungu kupitia dini yoyote katika zile zinazojinasibisha na Nabii Ibrahimu.

10 Tazama mjadala katika kitabu hiki. Ayatullah Mutahhari anafafanua kwamba “Ukweli wa kusalimu amri una muundo mahususi katika kila zama.” Vilevile ni ufunguo wa kuilewa Suratul Baqara (2) aya 62. 11 Qur’ani 3:19 17

7/15/2011

12:40 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini Katika jitihada zao za kusoma rai sahihi kisiasa katika Qur’ani wamepuuza hata muktadha wa aya – yaani jinsi ilivyotumika hapa. Hebu tusome kifungu hiki chote pamoja. “Kwa hakika DINI mbele ya Mwenyezi Mungu ni UISLAMU. Na wale waliopewa kitabu (Wakristo na Wayahudi) hawakupinga isipokuwa baada ya kuwajia elimu, kutokana na husda miongoni mwao. Na yeyote anayepinga aya za Mwenyezi Mungu, basi kwa hakika Mwenyezi Mungu ni mwepesi wa kuhesabu.” “Lakini wakibishana nawe, sema “Nimejinyenyekesha kwa Mwenyezi Mungu na amefanya hivyo pia kila anayenifuata.”

“Na kwa waliopewa kitabu (yaani Wakristo na Wayahudi) na kwa waabudu masanamu (wa Makka) sema; Je mnanyenyekea? Wakinyenyekea, basi hao wameongoka, lakini wakikataa, basi juu yako ni kufikisha ujumbe tu. Na Mwenyezi Mungu anawaona waja (wake).”3:20. Kifungu hiki kinaeleza yafuatayo: -“Al-Islam” Uislamu uliotajwa humu ni Ujumbe wa kunyenyekea kama ulivyoletwa na Mtume Muhammad (s.a.w.w). - Watu wa kitabu wanapinga na tafsiri hii ya kunyenyekea kwa Allah. - Mtume Muhammad (s.a.w.w) na wafuasi wake ni wafuasi wa ule Uislamu ulioletwa naye (Mtume s.a.w.w).

18

7/15/2011

12:40 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini - Watu wa Kitabu wanatakiwa kujinyenyekesha kwa Mwenyezi Mungu kupitia Mtume Muhammad (s.a.w.w) japo tayari ni wafuasi wa Nabii Musa (a.s) na Issa (a.s). - Halikadhalika ujumbe huo huo unatolewa kwa waabudu massanamu wa Makka. - Ikiwa watu wa kitabu hawatanyenyekea (kama Mtume Muhammad (s.a.w.w) na wafuasi wake walivyonyenyekea) basi watakuwa hawajaongoka.” Hivyo neno Uislamu, katika Aya hii linamaanisha “kujinyenyekesha kwa Mwenyezi Mungu” kupitia kwa ujumbe Wake wa mwisho ulioletwa na Mtume Muhammad (s.a.w.w) na sio kupitia Mitume waliopita.

Uislamu katika Qur’ani (3:83-85). Kifungu kingine katika sura hiyo hiyo kinafaa katika kuelewa maana ya neno “Uislamu”: “Je wanataka dini isiyokuwa ya Mwenyezi Mungu wakati kila kilichoko mbinguni na ardhini kinanyenyekea Kwake, kipende kisipende, na Kwake watarejeshwa?” “Sema: Tunamwamini Mwenyezi Mungu, na yale yaliyofunuliwa kwa Ibrahim, Ismail, Is’haq, Ya’qub na Makabila na yale aliyopewa Musa na Isa na Manabii kutoka kwa Mola wao. Hatutofautishi baina yao na Kwake tunajinyenyekesha.” “Na yeyote anayetaka dini isiyokuwa ya Kiislam haitakubaliwa kwake, na akhera atakuwa miongoni mwa wenye hasara.”

19

7/15/2011

12:40 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini Kifungu hiki kinaeleza yafuatayo: - Miongoni mwa imani za msingi ni kuamini “yale yaliyoteremshwa kwetu” (yaani Qur’ani waliyoteremshiwa Waislamu). - Islamu – unyenyekevu hufuatia tu baada ya mtu kuwaamini Mitume wote na akawa hatofautishi katika ukweli wa yeyote kati yao, akiwemo Mtume Muhammad (s.a.w.w).

“Uislamu” na “Imaan” katika Qur’ani (2:135-137). Aya zifuatazo katika sura ya pili ya Qur’ani zinafafanua zaidi maana “Uislamu–unyenyekevu” na halikdhalika “Imaan” - kuamini. “Na wanasema - kuweni Wayahudi au Wakristo na mtaongoka.” “Sema: Hapana! (Tunafuata) dini ya Ibrahim aliyekuwa na dhati, na hakuwa miongoni mwa washirikina.” “Sema: Tunamwamini Mwenyezi Mungu na yale yaliyofunuliwa kwetu na yale yaliyofunuliwa kwa Ibrahim, Ismail, Is’haq, Yaqub na makabila, na kwa yale yaliyoteremshwa kwa Musa na Isa na kwa Mitume (wengine) kutoka kwa Mola wao –hatutofautishi baina yao, na kwake (Allah) tunanyenyekea.” “Ikiwa Wayahudi na Wakristo wataamini kama mnavyoamini, basi watakuwa wameongoka; na wakikataa, basi wapo katika upinzani mkubwa, na Mwenyezi Mungu atakutosha (kuwa mlinzi) dhidi yao. Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua.” Aya hizi mbili zinaifafanua wazi wazi imani ya Waislamu tofauti na ile ya Wayahudi na Wakristo. Imani ya msingi ya Waislamu ni kuamini juu ya ufunuo wa Mitume wote, ukiwemo ufunuo wa Mtume Muhammad (s.a.w.w). Aya hizi zinaelezea wazi wazi kuwa ikiwa Wayahudi na Wakristo wataamini “kama mnavyoamini,” basi hapo ndio watakuwa 20

7/15/2011

12:40 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini wameongoka. Aya ya 285 ya Suratul Baqarah inathibitisha maana hii ya imani. “Mtume (Muhammad) ameamini yale yaliyoteremshwa kwake kutoka kwa Mola wake, na walioamini wote wanamuamini Mwenyezi Mungu, Malaika wake, Vitabu vyake na Mitume wake. Na wamesema; “Hatutofautishi baina ya Mitume wote.” Zingatia juu ya “hatutofautishi baina ya Mitume” au “hatufanyi tofauti yoyote kati ya yeyote miongoni mwao,” haina maana kuwa Mitume wote wa Mwenyezi Mungu wana daraja sawa. Tumeshasema hapo awali kuwa kuna Mitume watano ambao wana daraja ya juu zaidi kiroho. Ila tunaposema hatutofautishi baina yao tuna maana tunakubali madai yao ya utume, wote ni Mitume wa kweli. Hii ni tofauti na Wayahudi ambao wanawakubali Mitume wote lakini wanawakataa Issa (a.s) na Muhammad (s.a.w.w). Mtume Muhammad (s.a.w.w) na Dhana ya mfumo wa jamii ya dini nyingi. Wale wasomi wa Kiislamu wanaohubiri dhana ya mfumo wa jamii ya dini nyingi kutoka katika mafundisho ya Uislamu wanaelekea kusahau baadhi ya ukweli wa kihistoria wa Historia ya Uislamu na maisha ya Mtume. Ikiwa Uyahudi na Ukristo zingekuwa njia sahihi za kujinyenyekesha kwa Mwenyezi Mungu, kwa nini basi Mtume (s.a.w.w) alifanya bidii kubwa kiasi kile ya kufikisha ujumbe wake hata kwa Wayahudi na Wakristo? Kama tayari walikuwa katika njia iliyonyooka (sirat Mustaqim), kwa nini basi Mtume (s.a.w.w) aliona ni muhimu kuwaita katika Uislamu? Baadhi ya mkataba wa Hudaibiyya katika mwaka wa 6 A.H, Mtume wa Uislamu (s.a.w.w) alituma wajumbe kwenda kwa watawala na makabila mbali mbali ya Bara Arabu na nje yake kwa nia ya kuwaita katika Uislamu. 21

7/15/2011

12:40 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini Kwa mujibu wa wanahistoria Mtume (s.a.w.w) alituma takriban barua 25 kwa watawala na makabila mbalimbali.12 Miongoni mwa wale waliotumwa kwa watawala na makabila ya Kikristo ni Dihyah al-Kalbi aliyetumwa kwa Heraclius, Mfalme wa Byzantine, Amr bin Umayya Zamri kwa Negus Mfalme wa Abyssinia; Hatib bin Abi Balta’a aliyetumwa kwa Muqawqis, Mfalme wa Misri na makabila ya Ghassan na Hanifa (kaskazini mwa Arabuni). Barua tatu ni muhimu na muafaka kwa majadiliano yetu. Katika barua yake kwa Heraclius, Mfalme wa Byzentine, Mtume Muhammad (s.a.w.w.) aliandika: “… Amani iwe kwa yule anayefuata mwongozo. Ninakuita katika dini ya Uislamu. Ukubali na uufuate Uislamu na utafanikiwa na Mwenyezi Mungu atakulipa mara mbili. Lakini ukikataa, basi madhambi ya watu wako pia yatakuwa juu ya mabega yako. “Enyi watu wa kitabu njooni katika neno lililosawa baina yetu na baina yenu kuwa tusimuabudu yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu, na tusimshirikishe na chochote, na wala baadhi yetu wasiwafanye wengine kuwa waungu badala ya Mwenyezi Mungu. Lakini mkikengeuka, basi sema: Shuhudieni kuwa sisi ni Waislamu.” Katika barua yake kwa Negus, mfalme wa Abyssinia, Mtume (s.a.w.w) aliandika: “… Amani iwe juu ya yule anayefuata mwongozo. Sifa ni za Mwenyezi Mungu ambaye hakuna mungu mwingine isipokuwa Yeye, Mwenye Mamlaka, Mtakatifu, Mlinzi wa amani Mlinzi wa walioamini, Walii. 12 Muhammad Ibrahim Ayati, Tarikh-ePayghambar-e Islam (Tehran: Tehran University Press n.d.) uk. 480-482. 22

7/15/2011

12:40 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini “Ninashuhudia kuwa Yesu mwana wa Mariam ni roho iliyopuliziwa na Mwenyezi Mungu na ni neno lake, alilolipeleka kwa Bikira Mariam. Alimuumba Yesu kwa neno lake kama vile alivyomuumba Adam kwa mikono yake. “Sasa ninakuita kwa Mwenyezi Mungu ambaye ni Mmoja, hana mshirika na jitiishe kwake. Nifuate mimi na yaamini yale yaliyoteremshwa kwangu, kwani mimi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu. Ninakuita wewe na watu wako kwa Mwenyezi Mungu, Mwenye Nguvu, Mtukufu, Aliyetukuka. Nimefikisha ujumbe na ni juu yako kuukubali. Kwa mara nyingine tena, amani iwe juu ya yule anayefuata njia ya mwongozo.” Katika barua aliyoituma kwa Muqawqis, Mfalme wa Misri na mkristo wa ki-khibti (Copt), Mtume Muhammad (s.a.w.w) aliandika: “…Amani iwe juu ya yule anayefuata Mwongozo. Ninakuita uukubali ujumbe wa Uislamu. Ukubali Uislamu na utafanikiwa. Lakini ukikengeuka, basi juu yako zitakuwa dhambi za Wakhibti wote. “Enyi watu wa kitabu njooni katika neno lililo sawa baina yetu na baina yenu kwamba tusimuabudu yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu na kwamba hatutamshirikisha yeyote na Mwenyezi Mungu na kuwa hakuna yeyote miongini mwetu atakayechukua yoyote kuwa Mola badala ya Mwenyezi Mungu. “Na wakikengeuka, basi sema: Shuhudieni kuwa sisi ni Waislamu.”13 Hata kuja kwa Wakristo wa Najrani na jinsi Mtume (s.a.w.w) alivyowaita katika Uislamu na, hatimaye Mubahala ni kwa nia hiyo hiyo ya kuwaita Ahlul Kitab katika Uislamu.

23

7/15/2011

12:40 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini Barua zote hizi na mkutano na Wakristo wa Najrani zinathibitisha bila chembe yoyote ya shaka kwamba kama Ahlul-Kitab (watu wa Kitabu) wangekuwa katika njia iliyonyooka basi Mtume (s.a.w.w) hangekuwa na haja yoyote ya kuwaita katika Uislamu.

Tahadhari Muhimu. Katika kuhitimisha utangulizi huu, ningependa kurudia tahadhari kwamba kuamini kuwa Uislamu ndio njia pekee iliyonyooka na inayofaa kwa kujinyenyekeshea kwa Mwenyezi Mungu haipelekei kuamaini moja kwa moja kuwa wasio Waislamu wote watakwenda motoni. Wala hitimisho hili la kuwa Uislamu ndio njia pekee iliyonyooka haituzuii kukuza moyo wa kuvumiliana na kuishi pamoja kwa amani na wafuasi wa dini mbali mbali hasa Wayahudi na Wakristo. Wakati akizungumzia kuhusu wazazi washirikina, Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:

“Na kama wakisisitiza kuwa mnishirikishe (Mimi Mwenyezi Mungu) na yale msiyokuwa na elimu nayo, basi msiwatii, lakini ishini nao kwa wema katika dunia hii.” Qur’ani Tukufu 31:15 Kwa hiyo Mwislamu anapaswa kupinga kuathiriwa na mambo yasiyokubalika katika Uislamu, yanayofanywa na wasio Waislamu, lakini bado tuishi nao kwa wema. Kwa maneno mengine, japo njia zenu zitakuwa tofauti huko akhera, hii haikuzuii kuwa mpole, mkarimu, mwenye huruma na muadilifu kwa wasiokuwa Waislamu katika dunia hii. Sayyid Muhammad Rizvi, Toronto, Ontario. May 13th 2004/23rd of Rabiul Awwal 1425 A.H. 13 Ibid, uk. 483-494. 24

7/15/2011

12:40 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini

WASIFU WA HAYATI AYATULLAH MURTADHA MUTAHHARI Ayatullah Murtadha Mutahhari mmoja wa wajenzi wakubwa kifikra wa Iran mpya ya Kiislamu alizaliwa tarehe 2/2/1920, katika kilichokuwa kijiji cha Fariman, ambacho sasa ni mji uliopo kama kilomita sitini kutoka Mashhad; Mji mkubwa wa kielimu na Ziara kwa ajili ya Shi’a, mashariki mwa Iran.14 Baba yake alikuwa Muhammad Husain Mutahhari, mwanazuoni mkubwa aliyesoma Najaf na aliishi kwa miaka mingi Misri na Hijaz kabla ya kurejea Fariman, Iran. Mutahhari mkubwa alikuwa na hadhi isiyokubwa sana kama mwanawe, kwani mwanawe alikuwa aking’aa zaidi kuliko baba yake karibu katika kila fani. Baba yake alikuwa mpenzi wa kazi za mwanahadith mashuhuri Mullah Muhammad Baqir Majlis, ambapo mwanae alikuwa anamfuata shujaa mkubwa miongoni mwa wanachuoni wa Kishia wa zamani mwanateosofia (yaani imani kuwa wanadamu wanaweza kumfahamu Mungu na kuwasiliana naye kwa kutulia kabisa na kutafakari elimu) aliyeitwa Mulla Sadra. 14 Maelezo haya ya maisha na kazi za Ayyatullah Mutahhari kwa kiasi kikubwa ni kwa mujibu wa kitabu cha Muhammad Wa’izzada Khurasani kiitwacho Sayri dar Zindagi-yi ‘Ilmi wa Inqilabiiyi Ustadh Murtaza Mutahhari,” katika Yadnamayi Ustaadh Shahid Murtadha Mutahhari kilichohaririwa na Abdul Karim Surush, Tehran 1360 sh. /1981 uk. 319-380, makala yenye habari nyingi juu ya mambo mbali mbali ya historia ya hivi karibuni ya Iran ya Kiislamu. Baadhi ya maelezo pia yamepatikana katika makala ya Mujtaba Mutahhari ‘Zingagi-yi Pidaram’ iliyomo katika jarida la Harakat (jarida wa wanafunzi wa chuo kikuu cha Tehran kitivo cha teolojia) na. 1, uk. 5-16. Pia katika M. Huda, katika kumbukumbu ya Shahid Mutahhari, kitine kinachochapishwa na wizara ya muongozo wa utamaduni wa Kiislamu, Tehran April 1982; na pia katika wasifu ulioandikwa na yeye mwenyewe) ya Ayatullah Mutahhari alipokuwa anaandika utangulizi wa Ilal-i Girayish ba Maddigari, Qum, 1357 sh. /1978, uk. 7. 25

7/15/2011

12:40 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini Hata hivyo, Ayyatullah Mutahhari mara zote alikuwa anampenda na kumheshimu sana baba yake, ambaye pia alikuwa mwalimu wake wa kwanza, na alikitoa kitabu chake kimoja maarufu kama wakfu kwa ajili ya baba yake. Kitabu hicho kiliitwa, Dastan-e Rastan (Shairi la kuwasifu mashujaa waongofu) kilichochapishwa kwa mara ya kwanza mwaka 1960, na ambacho baadaye kilichaguliwa kuwa kitabu bora cha mwaka wa Iranian National Commission kwa niaba ya UNESCO mwaka wa 1965. Akiwa katika umri mdogo kabisa wa miaka 12, Mutahhari alianza masomo yake rasmi katika taasisi ya mafunzo ya Mashhad, ambapo kwa wakati huu hadhi ya taasisi hii ilikuwa inaporomoka kutokana na sababu za ndani na pia maelekezo ya Ridha Khan, dikteta wa kwanza kutoka ukoo wa Pahlavi. Lakini hapo Mashhad Mutahhari aligundua kuwa alikuwa na mapenzi makubwa na falsafa, teolojia na irfan (mysticism), mapenzi ambayo alibaki nayo katika maisha yake yote na yaliunda mtazamo wake mzima juu ya dini: “Ninaweza kukumbuka kuwa nilipoanza masomo yangu Mashhad na nilikuwa bado ninajifundisha Kiarabu cha msingi, wanafasafa, na wataalamu waliobobea katika mafundisho ya kumfikia Mungu kwa tafkira (mystics) na wanateolojia walinivutia mno kuliko wanachuoni na wanasayansi wengine, kama vile wagunduzi na wapelelezi. Ilivyo nilikuwa bado sijaelewa mawazo yao, lakini niliwachukulia kama mashujaa katika kiwango cha fikra.�15 Mtu aliyeamsha hamasa za Mutahhari pale Mashhad alikuwa Mirza Mahdi Shahid Razavi, mwalimu wa falsafa. Lakini alikufa mwaka wa 1936, kabla Mutahhari hajawa mkubwa wa kutosha kuanza kuhudhuria madarasa yake, na hii ikiwa ni moja ya sababu, Mutahhari aliondoka Mashhad mwaka mmoja baadaye na kwenda zake Qum ambako idadi ya wanafunzi ilikuwa inaongezeka. 15 Ilal-e-Girayish ba Maddigari, uk. 9 26

7/15/2011

12:40 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini Shukrani zimwendee Sheikh Abdul Karim Ha’iri kwa usimamizi wake. Qum ilikuwa inaelekea kuwa mji mkuu wa kielimu na kiroho wa Iran ya Kiislamu, na Mutahhari aliweza kufaidika huko kutokana na ufundishaji wa wanachuoni mbali mbali. Alijifunza Fiqh na Usul - masomo ya msingi ya mtaala wa kimapokeo kwa Ayattulah Hujjat Kuhkamari, Ayatullah Sayyid Muhammad Damand; Ayatullah Sayyid Muhammad Ridha Gulpayagani na Hajj Sayyid Sadr al-Din As-Sadr. Lakini muhimu zaidi kuliko wote hawa alikuwa ni Ayyatulah Burujerdi, mrithi wa Ha’ir kama mkurugenzi wa Uimarishaji wa kituo cha mafunzo ya Kiislamu cha Qum. Mutahhari alihudhuria madarasa yake tangu alipofika Qum mwaka 1944 hadi alipoondoka kwenda Tehran mwaka 1952, na alijenga heshima kubwa sana juu yake. Mutahhari alikuwa na mapenzi makubwa kwa mwalimu wake Mkuu wa Qum, Ayyatullah Ruhullah Khomeini. Mutahhari alipowasili Qum Ayyatullah Khomeini alikuwa mwalimu kijana, lakini tayari alikuwa anafahamika vyema kwa wenzake kwa uelewa wake mkubwa na mtazamo wake mpana wa Kiislamu na uwezo wake wa kuyafikisha hayo anayoyajua kwa wengine. Sifa hizi zilidhihirishwa katika khutba zake mashuhuri juu ya maadili alizoanza kuzitoa katika miaka ya 1930 katika mji wa Qum. Hotuba zake zilivuta wasikilizaji wengi kutoka nje na ndani ya kituo cha mafunzo na taathira kubwa sana kwa wole waliohudhuria. Mutahhari alianza kumjua Ayatullah Khomeini katika hotuba hizi: “Nilipohamia Qum, nilimkuta mtu mwenye haiba iliyokuwa katika Mahdi (Shahid Razavi) na sifa nyinginezo zilizokuwa za kwake peke yake. Nilitambua kuwa kiu ya roho yangu ingeweza kukatwa katika chemchem ya mtu huyu. Ingawa nilikuwa sijamaliza hatua za awali za masomo yangu na nilikuwa bado sijawa na sifa za kuanza masomo ya maarifa ya razini (mantiki) yaani maqulat, hotuba juu ya maadili zilizokuwa zikitolewa na mpendwa yule kila Alhamisi na Ijumaa hazikuwa zikiishia katika maadili tu katika maana kavu ya kitaalamu bali alizungumzia na safari za kiroho, na hivyo zilinielewesha. Naweza kusema bila kutia chumvi kuwa hotuba hizo zil27

7/15/2011

12:40 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini iamsha msisimko mkubwa wa kiroho niliobaki nao hadi Jumatatu au Jumanne au Jumatano iliyofuata. Sehemu muhimu ya haiba yangu ya kiakili na kiroho iliumbika chini ya taathiri ya hotuba hizo na madarasa yake mengine niliyohudhuria katika kipindi cha miaka kumi na mbili ya kiongozi huyu wa kiroho [Ayatulah Khomeini].�16 Katika mwaka 1946, Ayatulah Khomeini alianza kuhadhiri katika kundi dogo la wanafunzi lililowajumuisha wote Mutahhari na mwenzake aliyekuwa akiishi naye katika chuma kimoja Ayatullah Muntazari katika madrasa ya Fayziya, juu ya vitabu viwili muhimu sana vya falsafa; Asfar al-Arba’a cha Mulla Sadra na Sharh-e-Manzuma cha Mulla Hadi Sabzwari. Kushiriki kwa Mutahhari katika mihadhara ya kundi hili, iliyoendelea hadi mwaka 1951, kulimuwezesha kuwa na mahusiano ya karibu zaidi na mwalimu wake. Pia katika mwaka 1946, kwa mhimizo wa Mutahhari na Muntazari, Ayatullah Khomeini alifundisha kwa mara ya kwanza darasa rasmi la fiqh na Usul akitumia ushahidi wa kirazini (kimantiki) akitumia juzuu ya pili ya Kifayatal Usul cha Akhund Khurasani kama kitabu chake cha kiada. Mutahhari alizingatia masomo yake kwa umakini mkubwa, huku akiendelea na masomo yake ya Fiqh kwa Ayyatullah Burujerdi. Katika miongo miwili iliyofuatia baada ya vita, Ayatullah Khomeini aliwafundisha wanafunzi wengi katika mji wa Qum waliokuja kuwa viongozi wa mapinduzi ya Kiislamu na Jamhuri ya Kiislamu, ambapo kwa kupitia wanafunzi hao, haiba yake (Ayatulah Khomeini) iliweza kuonekana katika maendeleo na matukio muhimu ya muongo uliopita. Lakini hakuna mwanafunzi yeyote katika wanafunzi wake aliyekuwa na ukaribu naye kama Mutahhari, ukaribu ambao Ayyatullah Khomeini amekiri. Mwanafunzi na mwalimu walikuwa na mshikamano mkubwa mno katika kila nyanja za masomo ya kimapokeo na wote walikuwa na mtazamo mmoja juu ya kuwa Uislam ni mfumo kamili wa maisha ya imani, huku 16 Ilal-i Giraysh ba Maddigari, uk. 9. 28

7/15/2011

12:40 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini umuhimu zaidi ukiwekwa katika nyanja zake za kifalsafa na kutafakari Mwenyezi Mungu, utii kamili kwa taasisi ya kidini ukisukumwa na kujua haja ya mageuzi, kutaka mabadiliko ya kijamii na kisiasa, kukifuatiwa na mikakati sahihi na kwa muda muafaka, na uwezo wa kwenda nje ya wale watu wa kidini wa kimapokeo na kuwafikia pamoja na kupata usikivu na utii wa wasomi wa kisekula. Miongoni mwa walimu wengine waliokuwa na taathira/ushawishi kwa Mutahhari alipokuwa Qum ni mfasiri wa Qur’ani na mwanafalsafa, Ayatullah Sayyid Muhammad Husain Tabatabai. Mutahhari alishiriki katika madarasa ya Tabatabai juu ya shifa ya Abu Ali Sina kuanzia 1950-1953, na majlis za Alhamisi jioni zilizokuwa zikiendeshwa kwa maelekezo yake. Somo lililokuwa likifundishwa lilikuwa falsafa yakinifu, uteuzi wa kusifika kwa ajili ya kundi la wanachuo wa kimapokea. Mutahhari mwenyewe alipatwa na hamu kubwa katika falsafa yakinifu, hasa falsafa ya Marx mara tu baada ya kuanza kujifunza maarifa ya sayansi ya kirazini (mantiki). Kwa mujibu wa kazi alizoandika yeye mwenyewe, katika mwaka 1946 alianza kusoma tarjuma za vitabu vya Kifarsi vya fasihi ya Marx vilivyokuwa vikichapishwa na chama cha Tudeh, taasisi kubwa kabisa iliyokuwa ya ki-marx nchini Iran, na wakati huo chama hiki kilikuwa na nguvu kubwa kisiasa. Mbali na hivyo, pia alisoma vitabu vya Taqi Arani, mwananadharia mkuu wa chama cha Tudeh na alisoma pia vitabu vya kimarx vilivyokuwa katika lugha ya Kiarabu vikitokea nchini Misri. Awali alipata ugumu wa kuelewa vitabu hivi kwa sababu alikuwa hafahamu misamiati (istilahi) ya kisasa ya kifalsafa, lakini kutokana na jitihada kubwa (ambayo ilijumuisha kusoma ufupisho wa kitabu cha Georges Pulitzer kiitwacho ‘Elementary Principles of Philosophy’), alikuja kulimudu vizuri somo lote la falsafa yakinifu. Kulimudu huku kulimfanya awe mchangiaji mzuri na muhimu katika madarasa ya Tabatabai na baadaye, baada ya kuhamia Tehran alikuwa ni mpiganaji mahiri katika vita vya kiitikadi dhidi ya falsafa ya Marx na tafsiri za Uislamu zilizoegemea au zilizoathiriwa na falsafa ya Marx. 29

7/15/2011

12:40 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini Makanusho mengi juu ya Umarx yaliandikwa katika ulimwengu wa Kiislamu, Iran na kwingineko, lakini takriban zote zilishindwa kwenda nje ya mipaka ya wazi ya kutokukubaliana kwa ukomunisti na imani ya dini na kushindwa kisiasa na kutowiana kwa vyama vya siasa vya kikomunisti. Lakini, yeye Mutahhari kwa kinyume chake, yeye alikwenda katika mizizi ya falsafa hii na akaonyesha kwa hoja zenye nguvu kimantiki, hali ya kukinzana kinadharia kwa misingi mikuu ya ukomunisti. Maandishi yake ya kimjadala ya kupinga falsafa ya Marx (ukomunisti) yanaainishwa zaidi na hoja za kiakili zaidi kuliko ujanja wa maneno au msukumu wa kijazba. Hata hivyo, kwa Mutahhari, falsafa ilikuwa zaidi ya chombo cha ufasaha wa maneno au nidhamu ya kiusomi; ilikuwa ni staili fulani ya kuwa mshika dini, njia ya kuuelewa na kuujenga Uislamu, Mutahhari, kwa kusema kweli yupo katika utaratibu wa shughuli za kifalsafa za Shia ambazo zina historia ndefu toka enzi za Nasir ad-Din Tusi, mmoja wa watu mashujaa wa Mutahhari. Kusema kwamba mtazamo wa Mutahhari juu ya Uislamu ni wa kifalsafa haimaanishi kuwa hakuwa na imani ya kiroho au kuwa alikusudia kuyashusha mafundisho yote yaliyoteremshwa na Mwenyezi Mungu kwenye tafsiri za kifalsafa na kuingiza katika maeneo yote ya elimu ya shughuli za dini istilahi za kifalsafa, bali ina maana kuwa aliona kuwa kupata elimu na kuelewa kuwa ni lengo kuu na manufaa ya dini, na kwa sababu hiyo aliipa falsafa ubora (umuhimu wa pekee) fulani miongoni mwa nidhamu zilizoendelezwa katika taasisi hiyo ya dini. Katika hili alitofautiana na wanazuoni wengine wengi walioona kuwa Fiqh ilikuwa ndiyo mambo yote na mwisho wa yote wa mitaala, na wale wanaojiita wa kisasa ambao waliiona falsafa kama iliwakilisha uvamizi wa Uyunani (Kigiriki) katika ulimwengu wa Kiislamu, na wale wote ambao nguvu ya shauku ya mapinduzi iliwafanya wakose subira dhidi ya fikra makini za kifalsafa.17 17 Kauli yenye nguvu ya mtazamo huu ilitolewa na Sayyid Qutb katika kitabu chake “Khasa’is al-Tasawwur al-Islam wa Muqawwimatuhu”, Cairo, matoleo mengi ambayo kwayo yalitarjumiwa kwa Kifarsi na ambayo yana ushawishi fulani juu ya mitazamo kwenye filosofia. 30

7/15/2011

12:40 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Mfumo wa Jamii ya dini nyingi Shule mahususi ya filosofia ambayo Mutahhari alikuwa anafuata ilikuwa ni ile ya Mulla Sadra, “falsafa ya hali ya juu” (hikmat-i Muta’aliya) ambayo inatafuta kuchanganya taratibu za utambuzi (umaizi) wa kiroho pamoja na tafsiri za kifalsafa. Mutahhari alikuwa mtu wa amani na mtulivu wakati wote, katika staha ya kawaida na hata katika maandishi yake (vitabu vyake). Hata alipokuwa akishiriki katika majadiliano (ya kihoja), mara zote alikuwa mwenye heshima na alijiepusha na maneno ya jazba na kejeli. Lakini haya ndio yalikuwa mapenzi yake na namna yake ya kumuenzi Mulla Sadra kwamba mara zote na kwa mapenzi makubwa angeweza kumtetea na kumkingia kifua dhidi ya shutuma zozote nyepesi hata ndogo dhidi yake (Mulla Sadra), Na alichagua jina la Sadra kwa mjukuu wake wa kwanza na pia kwa ajili ya jumba la uchapishaji la Qum ambapo alikuwa akichapisha vitabu vyake. Kwa kiasi ambavyo shule ya falsafa ya mlengo wa Sadra ilikuwa inajaribu kuunganisha njia za utambuzi wa kiroho (ndani) na tafakuri za kiakili, haishangazi kuona kuwa mlengo huu wa falsafa umekumbwa na tafsiri zinazotofautiana kwa upande wa wale ambao wameelemea njia moja kuliko ile nyingine. Tukihukumu kutokana na kazi zake, Mutahhari alikuwa katika kundi la wale ambao vipimo vya kiakili vilikuwa vimeenea; kulikuwa na kidogo sana cha ki-irfani au nguvu za kiroho zilizokuwa zikionekana katika wafuasi wengine wa mlengo wa Sadri, labda kwa sababu Mutahhari aliuona uzoefu na hisia zake za ndani kutohusiana na kazi yake ya kuelekeza aliyokuwa anaifanya au kama siri ya moyoni iliyokuwa lazima aifiche. Hata hivyo, zaidi inaelekea upendeleo huu kwa ajili ya vipimo hasahasa vya kifilosofia vya “falsafa ya hali ya juu” ulikuwa ni kielelezo cha mwenendo na kipaji cha Mutahhari mwenyewe. Katika hili alitofautiana sana na mwalimu wake mkuu, Ayatullah Khomeini, ambaye hotuba zake nyingi za kisiasa zinaendelea kuwa zimejazwa lugha na mambo yanayohusiana na imani ya irfani (mafundisho ya kumfikia Mungu kwa tafakuri) na kiroho.

31

7/15/2011

12:40 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini Mwaka 1952, Mutahhari aliondoka Qum kwenda Tehran ambako alimuoa binti wa Ayatullah Ruhani na alianza kufundisha falsafa katika madrasa ya Marwi, moja ya taasisi kubwa kabisa ya mafundisho ya kidini katika mji huu mkuu. Huu haukuwa mwanzo wa kazi yake ya ufundishaji, kwani akiwa Qum tayari alikuwa ameshaanza kufundisha baadhi ya masomo kama mantiki, falsafa, teolojia na fiqh – akiwa yeye mwenyewe bado ni mwanafunzi. Lakini Mutahhari anaonekana kuanza kupoteza subira kutokana na mazingira ya kubanwa ya Qum, na huko kukiwa mgawanyiko miongoni mwa baadhi ya wanafunzi na waalimu wao na pia kutokana na kuwa mbali kwao na masuala ya kijamii. Majaaliwa yake pia pale Qum hayakuwa na uhakika. Akiwa Tehran, Mutahhari alikuta mazingira mapana na ya kuridhisha zaidi kwa ajili ya dini, elimu na hatimaye shughuli za kisiasa. Mwaka 1954, aliombwa kwenda kufundisha falsafa katika Kitivo cha Theolojia na Elimu za Kiislam cha Chuo Kikuu cha Tehran, ambapo alifundisha kwa miaka ishirini na mbili. Kwanza utaratibu wa kuhalalisha ajira yake na baadaye kupandishwa kwake cheo kufikia uprofesa kulicheleweshwa kutokana na wivu wa wenzake wa vyeo vya chini na kwa sababu za kisiasa (kwa sababu ukaribu wa Mutahhari na Ayatullah Khomeini ulikuwa unajulikana vyema). Lakini kuwepo kwa mtu kama Mutahhari katika chuo kikuu cha kisekula lilikuwa ni jambo la maana na lenye manufaa. Watu wengi waliotokea kwenye madrasa wamepata kuja kufundisha katika vyuo vikuu na mara nyingi walikuwa na ujuzi mkubwa. Hata hivyo, karibu wote waliachana na falsafa ya maisha ya kiislamu pamoja na vilemba na majoho yao. Mutahhari kinyume chake, alikuja chuo kikuu kama mtetezi mwenye uwezo wa maelezo fasaha na asiyeshaka, wa sayansi na hekima za Uislamu, takriban kama balozi wa taasisi ya Kiislamu katika jamii ya watu waliosoma elimu ya kisekula. Watu wengi walimwitikia, kwani ule uwezo wa ufundishaji aliounyesha mwanzoni huko Qum sasa ilifungulika kwa ukamilifu.

32

7/15/2011

12:40 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini Mbali na kujijengea sifa kama mhadhiri maarufu na mahiri mwenye mvuto wa chuo kikuu, Mutahhari alishiriki katika shughuli za taasisi mbali mbali za kitaalamu za Kiislamu (anjumanha) ambazo zilikuja kuwepo chini ya uongozi wa Mahdi Bazargan na Ayatullah Taleqani, akiwahadhiri madaktari, wahandisi, waalimu na kusaidia kuratibu kazi yao. Kwa hakika idadi ya vitabu vya Mutahhari vinajumuisha miswada iliyopitiwa upya ya mfululizo wa hotuba lilizotolewa katika jumuiya za Kiislamu. Matakwa ya Mutahhari ya kutaka kupenyeza zaidi kwa elimu ya dini ndani ya jamii, na ushiriki bora zaidi wa wanachuoni (wanazuoni) katika masuala ya kijamii ilimfanya mnamo mwaka wa 1960 achukue uongozi wa kikundi cha Maulamaa wa Tehran kilichojulikana kama Anjuman-emahana-yi Dini (mkusanyiko wa kidini wa kila mwezi). Wajumbe wa kikundi hiki, ambao ni pamoja na hayati Ayatullahi Behesht, aliyekuwa mwanafunzi mwenza wa Mutahhari, huko Qum, waliandaa hotuba za hadhara za kila mwezi zilizotengenezwa wakati huohuo kuonyesha kufaa kwa Uislamu katika mambo ya zama hizi, na vile vile kuhamasisha wanachuoni fikira za kimapinduzi miongoni wa Ulamaa. Hotuba hizi zilichapishwa chini ya kichwa cha habari Guftaar-e-Maah ‘Mazungumzo ya mwezi’ na zilipata umaarufu mkubwa, lakini serikali ilizipiga marufuku Machi 1963 wakati Ayatullah Khomeini alipoanza kushutumu hadharani utawala wa Pahlavi. Mradi mwingine muhimu zaidi alioanya mwaka 1965 ilikuwa ni kuunda taasisi ya Husayniya-e-Irshad, taasisi iliyokuwa kaskazini mwa Tehran, iliyoundwa ili kupata utii wa vijana wasomi wa kisekiula kwenye Uislamu. Mutahhari alikuwa miongoni mwa wajumbe wa bodi ya uelekezaji, alihutubia pia katika Husaynia-e Irshad na alihariri na kuchangia katika machapisho yake mbalimbali. Taasisi hii iliweza kuvuta umati mkubwa kila ilipofanya mikutano, lakini mafanikio haya ambayo kwa kweli yaliyazidi matarajio ya waanzilishi, yaligubikwa na matatizo mengi ya ndani. Moja ya matatizo haya ilikuwa muktadha wa kisiasa wa shughuli za taasisii hii, ambao uliibua maoni yanayotofautiana juu ya hali 33

7/15/2011

12:40 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini ya muafaka wa kwenda zaidi ya hotuba za kimageuzi mpaka kwenye makabiliano ya kisiasa. Maneno yanayotoka mdomoni huwa na taathiri kubwa zaidi na ya haraka katika kuhimiza mabadiliko ya kimapinduzi kuliko maneno yaliyoandikwa, na ingewezekana kutunga diwani ya hotuba muhimu, na mihadhara ambayo ingekuwa imeyasukuma mbele zaidi mapinduzi ya Kiislamu ya Iran. Lakini ufafanuzi wa yaliyomo katika itikadi ya mapinduzi na mipaka yake kutoka kwenye madhehebu zinazopinga au kushindana ulitegemea juu ya maneno ya maandishi, juu ya utungaji wa vitabu ambavyo vinafafanua misingi ya Kiislamu hatua kwa hatua, kwa kuzingatia matatizo ya zama hizi. Katika hili mchango wa Mutahhari ulikuwa wa pekee kwa ukubwa na upeo wake. Mutahhari aliandika vitabu vingi kwa uangalifu na mfululizo bila kuacha, tangu alipokuwa mwanafunzi Qum hadi mwaka 1979, mwaka aliokufa shahidi. Kazi zake nyingi (vitabu) zilikuwa na mwelekeo uleule wa kifalsafa na msisitizo wake ambao tayari umekwisha kuelezwa, na pengine kazi yake aliyoiona kuwa muhimu zaidi (kitabu) ni ‘Usul-e-Falsafa wa Ravish-e-Ri’alism (kanuni za falsafa na mbinu za Uhalisia) kumbukumbu ya mazungumzo ya Tabatabai katika madarasa ya Alhamisi jioni, Qum, iliyoongezwa na maoni ya Mutahhari mwenyewe. Lakini alikuwa hachagui mada za vitabu vyake kwa kutegemea anavyojisikia tu, au upendeleo wake, bali kwa kuzingatia mahitaji, kila ilipotokea kuwa kitabu juu ya mada fulani muhimu kwa Waislamu wa zama hizi hakipo (hakijawahi kuandikwa) basi yeye ndio alikuwa anakiandika. Akiwa peke yake alianza kujenga misingi mikubwa za makataba za Kiislamu zinazolingana na wakati. Vitabu kama Adl-e-Ilahi (uadilifu wa Mwenyezi Mungu), Nizam-e-Huquq-e-Zan dar Islam (Haki za wanawake katika Uislamu), Mas’ala-yi Hijab (mas’ala ya hijabu), Ashna’i ba Ulume-Islami (Utangulizi juu ya mtazamo wa ulimwengu juu ya Uislamu), na Muqaddima bar Jahanbinni-yi Islami (Utangulizi kwenye mtizamo wa ulimwengu wa Uislamu) vyote hivi vilikusudiwa kuziba pengo, kukidhi haja, kuchangia katika uelewa sahihi wa Uislamu na matatizo katika jamii 34

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini ya Kiislamu. Vitabu hivi vinaweza kuonekana kuwa ni mchango muhimu zaidi na wa kudumu katika kuzaliwa upya kwa Iran ya Kiislamu, lakini harakati zake pia zilikuwa na ukubwa wa kisiasa ambazo kwa kukiri kidogo, hazipaswi kupuuzwa. Akiwa mwanafunzi na mwalimu asiye na uzoefu huko Qum, alikuwa akiingiza utambuzi wa kisiasa miongoni mwa wasomi wenzake na hususan alikuwa karibu na wale waliokuwa wajumbe wa Fida’iyan-i Islam, kikundi cha kijeshi kilichoanzishwa mwaka 1945 na Nawwab Safawi. Makao makuu ya kikundi hiki katika mji wa Qum yalikuwa ni Madrasa-yi Fayzia, sehemu ambapo ndipo Mutahhari mwenyewe alipokuwa anaishi na alijaribu bila mafanikio kuwatetea wasiondolewe hapo madrasani na Ayatullah Burujerdi, ambaye alikuwa hataki kabisa mapambano yoyote ya kisiasa dhidi ya utawala wa Shah. Wakati wa harakati za utaifishaji wa shughuli za mafuta za Iran, Mutahhari alikuwa akiunga mkono jitihada za Ayatullahi Kashani na Dr. Muhammad Mussadiq, ingawa alimkosoa huyu wa pili kwa kwa ufuasi wake wa utaifa wa kisekula. Alipohamia Tehrani Mutahhari alishiriki harakati za uhuru za Bazargan na Taleqani, lakini hakuwahi kuwa mtu mashuhuri katika kundi hili. Mapambano yake ya kwanza makubwa dhidi ya utawala wa Shah yalikuja wakati wa uasi (machafuko) wa Khurdad 15, tarehe 06 Juni, 1963, alipojionyesha kuwa ni mfuasi wa Ayatullah Khomeini kisiasa na kiitikadi kwa kutawanya maazimio yake (ya Imam Khomeini) na kwa kuwahimiza kwake watu kumuunga mkono Imam Khomeyni katika hotuba alizotoa.18

18 Jina la Mutahhari lilikuwa la tisa katika orodha ya wafuasi waliotiwa kizuizini iliyotarishwa na ofisi ya mwendesha mashitaka wa jeshi ya mwezi wa Juni, 1963. Tazama nakala halisi ya orodha katika Dihnavi, Qiyam-e-Khunnin-i 15 Khurdad 42 ba Rivayat-e-Asnad, Tehran, 1360 sh./1981, uk. 77. 35

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini Alikamatwa kwa hiyo na kushikiliwa kwa siku arobaini na tatu. Baada ya kuachiliwa, alishiriki vilivyo katika taasisi mbali mbali zilizojitokeza ili kudumisha msukumo uliokuwa umeanzishwa na yale maasi, muhimu zaidi ni Jumuiya ya Wanachuoni wa kidini wanajeshi (Jamia yi Ruhaniyat-e Mubariz). Mnamo Novemba 1964, Ayatullah Khomeini aliingia mwaka wa kumi na nne akiwa uhamishoni nje ya nchi, ambayo baadhi yake aliishi Uturuki na kisha Najaf, na katika kipindi chote hiki Mutahhari alikuwa na mawasiliano ya moja kwa moja kwa kumtembelea Najaf na mawasiliano yasiyo ya moja kwa moja. Mapinduzi ya Kiislamu yalipokaribia kilele chake cha ushindi katika majira ya baridi ya mwaka 1978 na Ayatullah Khomeini alipoondoka Najaf kwenda Paris, Mutahhari alikuwa miongoni mwa waliosafiri kwenda Paris kumuona na kutaka ushauri wake. Ukaribu wake na Ayatullah Khomaini ulithibitishwa kwa kuteuliwa kwake kuwa katika Baraza la Mapinduzi ya Kiislamu, baraza ambalo Ayatullah Khomeini alilitangaza tarehe 12 Januari, 1979. Huduma alizokuwa akitoa Mutahhari kwa Mapinduzi ya Kiislam zilikatizwa kikatili kwa mauaji yaliyofanywa dhidi yake tarehe 01 Mei 1979. Mauaji yalifanywa na kundi linalojulikana kama Furqan, ambalo lilidai kuwa waongozaji (wahusika wakuu) wa “Uislamu wa kimaendeleo,� walidai kumuua ili kuepukana na ushawishi wake wa upotoshaji kwa wanachuoni wa kidini. Ingawa Mutahhari anaonekana kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ya Kiislamu katika kipindi alichouawa, lakini hii haikuwa sababu ya kuuawa kwake, aliuawa kama mwandishi na mwanafalsafa. Mwaka 1972, Mutahhari alichapisha kitabu Illal-i Girayish ba Maddigari (sababu za kugeukia kwenye Uyakinifu) kazi muhimu inayochambua usuli wa kihistoria wa Uyakinifu (metarialism) huko Ulaya na Iran. Wakati wa Mapinduzi, aliandika utangulizi wa toleo la nane la kitabu hiki, akiushambulia upotoshaji wa fikra ya Hafiz na Hallaj ambayo imekuwa ya mtindo 36

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini katika baadhi ya visehemu vya jamii ya Wairan na kukanusha baadhi ya tafsri za kiyakinifu za Qur’ani. Asili ya tafsiri hii ya Qur’ani ilikuwa ni kikundi cha Furqan, ambacho kilikuwa kinazikana baadhi ya dhana za msingi kabisa zilizomo katika Qur’ani kama vile nguvu kuu ya ki-Ungu na uhalisia wa maisha ya akheri. Kama ilivyo kawaida yake, katika kitabu hiki kauli yake ilikuwa ya kushawishi na kujali, haikuwa ya hasira wala kushutumu, na hata aliomba majibu kutoka kundi la Furqan na watu wengine wenye nia ya kutoa maoni yao juu ya alichoandika. Jibu lao pekee lilikuwa ni bunduki. Tishio la kuwaua wale wote waliowapinga tayari lilikuwa limetolewa katika machapisho yao (Furqan), na baada ya kuchapishwa kwa toleo jipya la Illal-e-Girayish ba Maddigari Mutahhari alionekana kuwa na wasiwasi wa kutokea kwa kifo chake cha kishahidi. Kwa mujibu wa mtoto wake, Mujtaba, alionyesha aina ya kijitenga na masuala ya kidunia, alizidisha sala zake za usiku na kusoma Qur’ani na wakati fulani aliota kuwa yuko pamoja na Mtume (s.a.w.w) yeye akiwa pamoja na Ayatullah Khomeini. Siku ya Jumanne terehe 01 Mei 1979, Mutahhari alikwenda katika nyumba ya Dr. Yaddullah Sahabi, walipokuwepo wajumbe wengine wa Baraza la mapinduzi ya Kiislamu. Katika majira ya saa nne na nusu usiku, yeye pamoja na mshiriki mwingine wa mkutano, Injinia Katira’i waliondoka katika nyumba ya Sahabi. Akiwa anatembea mwenyewe kwenye kichochoro (njia nyembamba) kilichokuwa kinaelekea kwenye gari lake mara alisikia sauti isiyojulikana ikimwita. Aligeuka kuangalia sauti ilikuwa inatokea wapi na mara akapigwa risasi kichwani, risasi iliingia chini ya sikio la kulia na kutokea juu ya jicho la kushoto, alikufa hapo hapo, na ingawa alikimbizwa hospitali ya jirani, hapakuwa na la kufanya zaidi ya kumlilia. Mwili uliachwa hospitali na Alhamisi katikati ya waombolezaji wengi, mwili wake ulipelekwa katika Chuo Kikuu cha Tehran kwa ajili ya sala ya maiti, na baadaye Qum, kwa ajili ya mazishi. Alizikwa jirani na kaburi la Shaikh Abdul Karim Ha’iri.

37

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini Ayatullah Khomeini alilia hadharani Mutahhari alipokuwa anazikwa Qum na alimwelezea kama ‘mwanawe kipenzi’ na kuwa alikuwa ni ‘matunda ya uhai wake’ na kuwa alikuwa ‘sehemu ya mwili wake.’ Lakini katika taabini yake (maneno ya kumsifia marehemu Mutahhari) alielezea kwamba pamoja na kuuawa kwa Mutahhari haiba yake haikupungua wala wimbi la mageuzi halijavurugwa. “Acha wataka uovu wajue kuwa kwa kuondoka Mutahhari haiba yake ya Kiislamu, falsafa yake na kisomo chake, havijatuacha. Mauaji hayawezi kuiharibu haiba ya Kiislamu, ya mashujaa wa Uislamu … Uislamu hukua kupitia kujitoa mhanga na vifo vya kishahidi vya wapendwa wake. Toka enzi za ufunuo wake hadi sasa, Uislamu umekuwa ukiambatana na vifo cha kishahidi na ushujaa.19 Umashuhuri na urithi aliotuachia Ayatullah Mutahhari bila shaka hautasahaulika katika Jamhuri ya Kiislamu na umebaki kukumbukwa kiasi cha kuwa uwepo wa haiba yake baada ya kifo chake umebaki kuwa mkubwa miongoni mwa watu kama ilivyokuwa enzi za uhai wake. Kumbukumbu ya kifo chake cha kishahidi hufanyika kila mwaka na picha na taswira yake ipo kila mahali nchini Iran. Kazi zake nyingi ambazo zilikuwa hazijachapishwa, zinachapishwa sasa kwa mara ya kwanza na mkusanyiko wa kazi zake zote unasambazwa na unasomwa na idadi kubwa ya watu. Katika maneno ya Ayatullah Khamenei, Rais wa Jamhuri, kazi za Mutahhari zinaunda miundo-mbinu wa kiakili wa Jamhuri ya Kiislamu. Jitihada zinafanyika kukuza utambuzi wa kazi za Mutahhari nje ya jamii ya wazungumzaji wa kifursi, na wizara ya muongozo wa Kiislamu imefadhili kazi za kutafsiri kazi zake katika lugha mbali mbali kama vile kispaniola, 19 Maandishi ya Ayatullah Khomeini katika taabini ya Mutahhari katika Yadnamayi Ustadh-i Shahid Murtadha Mutahhari, uk. 3-5 38

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini kimalay na nyinginezo nyingi. Inaaminika kuwa utakuwa ndio ukumbusho wa Mutahhari kama Iran ya kimapinduzi itathibitisha kuweza kujenga jamii ya watu wema, uchumi bora, utamaduni safi vyote hivi vikiwa vimejengwa kwa misingi sahihi na halisi ya Uislamu. Kwa vile maisha ya Mutahhari yalikuwa na malengo yaliyozidi hamasa binafsi, na kifo chake cha kishahidi kilikuwa ni kielelezo cha ufutaji huo wa nafsi.

MATENDO MEMA YA WASIO WAISLAMU. Dondoo ya majadiliano. Moja ya mambo yanayojadiliwa kuhusiana na ‘Uadilifu wa Mwenyezi Mungu’ ni suala la matendo mema yaliyofanywa na wasio Waislamu. Leo hii, suala la iwapo matendo mema ya wasio Waislamu yanakubaliwa na Mwenyezi Mungu au hapana, suala hili linajadiliwa miongoni mwa matabaka mbali mbali - ya wasomi na wasio wasomi, wanaojua kusoma na wasiojua kusoma. Ikiwa matendo yao mema yanakubaliwa, kuna tofauti gani sasa kati ya Mwislamu na asiyekuwa Mwislamu; kitu muhimu hapa itakuwa ni kutenda tu matendo mema katika dunia hii. Ikiwa mtu sio Mwislamu na hafuati dini yoyote, hajapoteza chochote. Na ikiwa matendo yao mema hayatakubaliwa na yakiwa batili bila malipo yoyote kutoka kwa Mwenyezi Mungu, sasa hapo uadilifu wa Mwenyezi Mungu uko wapi? Swali hili pia linaweza kuulizwa na mfuasi wa madhehebu ya Shia, ndani ya mipaka ya Uislamu, Je matendo (mema) ya Waislamu wasio kuwa Mashia yanakubaliwa na Mwenyezi Mungu, au ni batili? Kama matendo yao mema yanakubalika, sasa kuna tofauti gani ya mtu kuwa Muislamu wa Shia au kutokuwa Mwislamu wa Shia? Kitu muhimu ni kuwa Mwislamu; mtu ambaye sio Shia na haamini juu ya Wilayah (kuteuliwa kwa Ahlul Bait na Mwenyezi Mungu ili wawe viongozi wa Waislamu baada ya Mtume s.a.w.w) hajapoteza chochote. Na ikiwa matendo ya mtu huyo hay39

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini atakubaliwa na Mwenyezi Mungu, sasa hapa uko wapi uadilifu wa Mwenyezi Mungu? Huko nyuma, suala hili lilikuwa linajadiliwa na wanafalsafa tu na ndani ya vitabu vya falsafa. Lakini leo limeingia akilini mwa watu wa matabaka yote; ni watu wachache tu ambao bado hawajawahi kujadiliana juu ya hili au japo kuwajia akilini mwao. Wanafalsafa wanaotumia misingi ya dini wangelijadili suala hili kutokana na mwelekeo kwamba kama watu wote wasio na dini wataangamia na kuadhibiwa na Mwenyezi Mungu, kwa hiyo ina maana kwamba katika ulimwenguni, uovu na ulazimishaji ni mwingi sana. Hata hivyo, ukweli kuwa furaha na wema vinachukuliwa kama vitu bora duniani (sio uovu na udhalili) ni kanuni mkataa. Mwanadamu ni kiumbe bora kabisa wa viumbe wote, vitu vingine vyote vimeumbwa kwa ajili yake (bila shaka, kwa dhana njema inayoeleweka kwa watu wenye busara, sio kwa uelewa wa watu wenye mtazamo finyu). Ikiwa mwanadamu mwenyewe ameumbwa kwa ajili ya moto wa Jahanam, hii ni kuwa, ikiwa makazi ya mwisho ya wanadamu walio wengi ni Jahanamu basi mtu lazima akubali kuwa hasira ya Mwenyezi Mungu ni kubwa kuliko rehema Yake. Hii ni kwa sababu watu walio wengi hawaijui dini ya kweli; na hata wale waliomo ndani ya dini ya kweli wamezongwa na upotofu na kuishi kinyume na mafundisho, pindi inapokuja katika utekelezaji. Haya ndio yamekuwa majadiliano ya wanafalsafa huko nyuma. Kwa takriban nusu karne sasa, kutokana na kuongezeka na kuboreka kwa njia za mawasiliano, na maingiliano makubwa zaidi baina ya mataifa, suala la iwapo kuwa Mwislamu na muumini ni sharti muhimu la kukubaliwa kwa matendo ya mtu limekuwa likijadiliwa katika matabaka mbali mbali ya jamii hasa wale wanaojiita wasomi.

40

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini Watu hawa wanaposoma maisha ya wagunduzi na wanasayansi wa hivi karibuni ambao hawakuwa Waislamu lakini ambao walitoa mchango mkubwa katika kuboresha maisha ya wanaadamu, wanaona watu hawa wanastahili malipo. Kwa upande mwingine kwa vile walikuwa wakisoma kuwa matendo ya wasiokuwa Waislamu ni batili, wanapatwa na shakashaka. Kwa namna hii, suala ambalo kwa miaka lilikuwa la wanafalsafa tu sasa limeingia katika mazungumzo ya kawaida ya watu na limechukua sura ya pingamizi kuhusiana na uadilifu wa Mwenyezi Mungu. Kwa hakika, pingamizi hili halihusiani moja kwa moja na uadilifu wa Mwenyezi Mungu, linahusiana na mtazamo wa Uislamu juu ya watu na mtendo yao, na huhusiana na uadilifu wa Mwenyezi Mungu kwa vile huonekana kuwa mtazamo huo juu ya watu, matendo yao na jinsi Mwenyezi Mungu atakavyowatendea unapingana na uadilifu wa Mwenyezi Mungu. Katika mikutano ambayo nimepata kuwa nayo na wanafunzi na vijana, ni mara nyingi tu nimekumbana na swali hili. Wakati fulani wanauliza iwapo wagunduzi wakubwa na wanasayansi, pamoja na mchango wao wote wa thamani walioutoa kwa wanaadamu watakwenda motoni. Je watu kama Pasteur na Edison wataenda motoni wakati ambapo watu ambao hawakuwa na mchango wowote wa maana kwa wanadamu na ambao wameumaliza umri wao kwenye kona ya msikiti wataenda Peponi? Je Mwenyezi Mungu ameumba Pepo kwa ajili yetu Shia tu? Ninakumbuka wakati fulani jamaa mmoja ninayemfahamu kutoka katika mji wangu, ambaye alikuwa Mwislamu, anayeutekeleza Uislamu wake kwa vitendo, alikuja Tehran kunitembelea, na akauliza juu ya suala hili. Mtu huyu aliwahi kutembelea hospitali ya wagonjwa wa ukoma katika mji wa Mashhad na alitikiswa na kuathiriwa sana na jinsi alivyowaona manesi wa kikristo ambao kwa dhati (kwa mujibu alivyowaona yeye) walikuwa wakiwahudumia wagonjwa wa ukoma. Wakati huo, suali hili likamjia 41

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini kichwani mwake na akajikuta katika shaka. Unajua kuwa kumhudumia mgonjwa wa ukoma ni kazi ngumu sana na isiyovutia na hospitali hii ilipojengwa Mashhad, ni madaktari wachache sana walikuwa tayari kufanya kazi pale, na halikadhalika hakuna aliyekuwa tayari kuwahudumia wagonjwa. Matangazo ya ajira za wahudumu wa wagonjwa (manesi) yalitolewa katika magazeti Iran nzima, lakini hakuna aliyetaka kufanya kazi hiyo. Kundi dogo la wanaojiita wanawake watawa wa kikristo kutoka Ufaransa walikuja na kuchukua jukumu la kuwahudumia wakoma. Mtu huyu aliyeona ubindamu na matunzo yenye upendo wa wale manesi kwa wakoma, waliokuwa wametelekezwa hata na ndugu zao, aliathiriwa sana na manesi hawa. Alisimulia kuwa manesi hawa wa kikristo walivaa nguo ndefu, pana na mbali na nyuso na mikono yao, hakuna sehemu nyingine ya miili yao iliyokuwa inaonekana. Kila mmoja wao alikuwa na rosali ndefu yenye shanga labda elfu moja na kila walipokuwa na muda wa ziada, walijishughulisha na visomo vyao kwenye rozali. Kisha mtu huyu aliuliza kwa akili iliyotatizika na sauti ya kigugumizi endapo ni kweli wasio Waislamu hawataingia peponi. Kwa hakika, hivi sasa hatushughulishwi na malengo ya akina mama wale wa Kikristo. Hivi ilikuwa kweli ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, katika njia ya Mwenyezi Mungu, na walifanya hivyo kwa ajili ya misingi ya ubinadamu tu; au walikuwa na malengo mengine? Kwa hakika, hatutaki kuwafikiria bila matarajio, kama ambavyo hatuna matumaini mema sana, hoja yetu ni kuwa matukio haya yameweka watu wetu katika swali tete. Miaka mingi huko nyuma nilialikwa kutoa mada katika jumuiya fulani. Katika jumuiya hiyo, kwa mujibu wa taratibu zao, washiriki waliombwa kuandika maswali yoyote yale waliyokuwa nayo ili yajibiwe katika muda 42

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini muafaka. Maswali hayo yaliandikwa katika daftari, na nilikabidhiwa hilo daftari la maswali ili nichague mada ya hotuba yangu kutokana na mojawapo ya maswali hayo (yaliyo kwenye daftari). Niligundua kuwa swali lililokuwa limerudiwa mara nyingi kuliko maswali mengine yote lilikuwa ni iwapo ni kweli Mwenyezi Mungu atawapeleka wasiokuwa Waislamu wote Jahanamu. Je Pasteur, Edison, na Kokh watakuwa miongoni mwa hao watakaoadhibiwa huko Akhera? Ni kuanzia muda huo ndipo nikatambua umuhimu wa suala hili na kwa kiasi gani limewashughulisha watu. Sasa katika sehemu hii ya kitabu, tutajadili suala hili. Lakini kabla ya kuanza, tunahitaji kufafanua nukta mbili ili mada hii ieleweke wazi na vizuri.

MWELEKEO WA JUMLA WA MJADALA. Lengo la mjadala huu sio kufafanua hadhi na madaraja ya watu binafsi, kwa mfano kueleza ikiwa Pasteur atakwenda Peponi au motoni. Tunajua nini kuhusu fikra zake za kweli na imani yake? Nini yalikuwa malengo yake halisi? Zilikiwaje tabia zake kimaadili na utu wake? Na kwa kweli nini ilikuwa jumla ya matendo yake? Tunachokijua kwake ni huduma zake za kitaaluma tu basi. Hili sio kwa Pasteur tu. Kama suala la kanuni, hadhi ya mtu anaijua Mwenyezi Mungu tu; hakuna mtu mwenye haki ya kutoa maoni yake kwa uhakika kuhusu iwapo mtu imma atakwenda peponi au motoni. Kama ingekuwa tuulizwe, “Je, Shaykh Murtadha al-Ansari kwa kuzingatia utawa wake, uchamungu, imani na matendo yake, je, kwa hakika yeye ni miongoni mwa wakazi wa peponi? Jibu letu litakuwa, “Kutokana na jinsi tunavyomjua mtu huyu, kifikra na katika matendo yake hatujasikia jambo lolote baya. Tunachokijua kwake ni wema na matendo mema. Lakini kusema bila chembe yoyote ya shaka ikiwa ataenda peponi au motoni, hilo sio haki yetu. Ni Mwenyezi Mungu tu anayejua nia za watu wote, na anajua ya dhahiri na ya siri ya nafsi zote, na hesabu matendo ya watu wote pia iko 43

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini Kwake. Tunaweza kusema kwa uhakika juu ya wale tu ambao matokeo yao ya mwisho tyameelezwa na wenye mamlaka katika dini (Mitume na Maimamu a.s). Wakati mwingine watu wanajadiliana na kubishana miongoni mwao juu ya ni nani alikuwa mwanazuoni bora kabisa kwa ukaribu wao na Mwenyezi Mungu. Kwa mfano je alikuwa Sayyid Bahrul Uluum? Au Shaykh alAnsari? au wakati fulani wanauliza juu ya nani alikuwa bora kabisa miongoni mwa vizazi vya Maimamu (a.s). Kwa mfano je, Sayyid Abdul Adhim al-Hasan (a.s.) ni bora zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu au Sayidah Fatmah al-Ma’sumah(a.s.)? Wakati fulani, mmoja wa mujitahidi aliulizwa ikiwa Abbas ibn Ali (a.s.) alikuwa na ubora zaidi kuliko Ali al-Akbar (a.s). Ili kulipa swala mwelekeo wa kimatendo ili mujtahidi alazimike kulijibu, waliuliza, ikiwa mtu ataweka nadhiri ya kutoa kafara kondoo kwa ajili ya mbora wa watoto wa maimamu je nini wajibu wake? Je Abbas ibn Ali ni bora zaidi au Ali alAkbar?” Ni dhahiri kuwa majadiliano kama haya sio sahihi, na kujibu maswali haya sio wajibu wa faqihi wala mtu yeyote. Kupanga madaraja ya viumbe wa Mwenyezi Mungu sio jukumu letu. Linatakiwa aachiwe Mwenyezi Mungu, na hakuna yeyote mwenye maarifa hayo isipokuwa kupitia kwa Mwenyezi Mungu. Katika kipindi cha awali cha Uislamu, kulijitokeza matukio ambapo baadhi ya watu walitoa maoni kama haya yasiyokubalika, na Mtume (s.a.w.w) aliwakataza kufanya hivyo. Uthman ibn Ma’zun alipofariki mwanamke wa kiansari aliyeitwa Ummi Ali, ambaye alikuwa anaonekana kuwa mke wa baba mwenye nyumba ambamo Uthman bin Ma’zum alikuwa akiishi, na ambaye alikuwa mgeni wake, alisema mbele ya jeneza la Uthman, na Mtume Muhammad 44

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini (s.a.w.w) akiwepo: “Pepo iwe nzuri kwako!” Japokuwa Uthman ibn Ma’zum alikuwa mtukufu na maarufu na Mtume Muhammad (s.a.w.w) alimlilia sana wakati wa mazishi yake, na alijitupa kwenye jeneza lake na kumbusu, lakini maoni yasiyofaa ya yule mwanamke hayakumfurahisha. Alimgeukia kwa uso usio na furaha na kusema, “Wewe ulijuaje,?” Kwa nini umetamka maneno kwa ujinga? Je, umepokea ufunuo wa Mwenyezi Mungu? Yule mwanamke alijibu “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, alikuwa sahaba wako na mpiganaji shujaa (katika jihadi)!” Mtukufu Mtume (s.a.w.w) alimjibu kwa maneno haya ya kuvutia ambayo yanafaa kutajwa hapa, alisema: “Mimi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, lakini sijui nitafanywa nini.”20 Sentensi hii inakubalian na aya hii ya Qur’ani.

“Sema, mimi sio wa kwanza katika Mitume, wala sijui nitakachofanywa, au mtakachofanywa nyinyi (46:9). 21 22 20 Usd al-Ghaba, chini ya Uthman ibn Ma’zun. 21 Al-Qur’an 46:9 22 Unaweza kupata pingamizi akilini kuwa maana ya jumla ya aya hii ni kinyume na kile kinachojulikana na kukubalika kwa Waislamu wote kama ukweli; kwamba Mtume (s.a.w.w) alijulishwa juu ya cheo chake chenye utukufu Siku ya Kiyama na kuwa atawaombea shufaa wenye dhambi mbali mbali, na ni kinyume na maana ya jumla ya aya mbali mbali kama vile “Na kwa hakika Mola wako atakuruzuku mpaka utaridhika. (93:5) na “ili Mwenyezi Mungu akusamehe makosa yako yaliyopita na yajayo…” (48:2). Jibu ni kuwa maana ya jumla ya aya hii kama inavyojionyesha kwenye hadith inayofuata ni kuwa, matokeo ya mwisho ya matendo ya mtu hayajulikani kwa yakini na yeyote, ni Mwenyezi Mungu tu Mwenye elimu ya yakini juu ya matokeo ya mtu, na wengine wakijua basi ni kupitia ufunuo kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Hivyo aya inayokanusha ujuzi wa hatma ya mtu inamweleza Mtume Muhammad (s.a.w.w), au mtu mwingine kuwa asimtabirie mtu hatma yake kwa kutegemea matendo yake tu, na aya zilizoonyesha kuwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) ana elimu juu ya hatma yake na hatma za watu wengine elimu hiyo ameipata kupitia ufunuo kutoka kwa Mwenyezi Mungu. 45

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini Tukio kama hili pia limeripotiwa kutokea katika msiba wa Sa’d ibn Mu’adh. Katika tukio hili, pale mama yake Sa’d aliposema maneno kama hayo ya awali katika jeneza lake, Mtume (s.a.w.w) akamwambia, “Nyamaza, usifanye uamuzi kwa uhakika katika masuala ya Mwenyezi Mungu.”23

2. DINI YOYOTE HAITAKUBALIWA ZAIDI YA UISLAMU. Nukta nyingine ambayo lazima iwekwe wazi kabla ya kuanza majadiliano ni kuwa suala la matendo mema ya wasio Waislamu yanaweza kujadiliwa katika namna mbili, na kwa uhakika haya ni mijadala miwili, kwanza; je dini nyingine mbali na Uislamu inakubalika kwa Mwenyezi Mungu au Uislamu ndio dini pekee inayokubalika? Hii ni kusema, je ni lazima kwa mtu kuwa na dini, au kwa ubora kabisa afuate moja ya dini zinazohusishwa na Mitume wa Mwenyezi Mungu kama vile Uislamu, Ukristo, Uyahudi au dini za Zoroastria? Au ni kuwa kuna dini moja tu ya kweli katika kila zama? Baada ya kukubali kuwa dini ya kweli ni moja tu katika kila zama, mjadala mwingine ni ikiwa mtu ambaye hafuati dini ya kweli lakini anatenda tendo jema, tendo ambalo kwa hakina ni zuri na pia linakubaliwa na dini ya kweli, je, anastahiki malipo au la? Kwa maneno mengine, imani katika dini ya kweli ni sharti la mtu kulipwa matendo yake mema? Litakalojadiliwa hapa ni suala la pili. Kuhusiana na suala la kwanza, tunaweza kusema kwa kifupi kuwa kuna dini moja tu ya kweli katika kila zama, na watu wote wanalazimika kuifuata na kuiamini. Wazo ambalo hivi karibu limekuwa la kawaida miongoni mwa baadhi ya hao wanaoitwa wasomi kwamba dini zote za tukufu zina uhalili ulio sawa katika zama zote ni dhana yenye kupotosha. 23 Biharul-Anwar, Juz. 3, uk. 165.

46

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini Bila shaka, ni kweli kuwa hakuna migongano baina ya Mitume wa Mwenyezi Mungu. Mitume wote wa Mwenyezi Mungu huwalingania watu katika lengo moja na Mungu mmoja. Hawakuja kuunda makundi yanayogongana na madhehebu miongoni mwa wanaadamu. Lakini hii haimaanishi kuwa katika kila zama kuna dini nyingi za kweli na kwa hivyo watu katika kila zama wanaweza kuchagua dini yoyote wanayoitaka. Lakini kinyume chake, inamaanisha kuwa mtu anapaswa kuwaamini Mitume wote na akiri kuwa kila Mtume alitoa bishara za Mtume ajaye baada yake, hususan Mtume wa mwisho ambaye ni mkubwa kuliko wote; na halikadhalika kila Mtume aliwathibitisha wale waliomtangulia. Hivyo matokeo ya lazima ya kuamini juu ya Mitume wote ni kujinyenyekesha katika dini ya Mtume wa muda huo au zama hizo. Na kwa kweli ni lazima katika zama za mwisho tufuate na kutii amri za mwisho zilizoteremshwa na Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake wa mwisho. Na hivi ndivyo Uislamu unavyofanya, yaani kujinyenyekesha kwa Mwenyezi Mungu na kukubali ujumbe wa Mitume Wake. Watu wengi siku hizi wamekubaliana na maoni ya kuwa inatosha kwa mtu kumuabudu Mwenyezi Mungu kupitia dini yoyote inayohusishwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu, muundo wa maamrisho sio muhimu hivyo. Issa (a.s) alikuwa Mtume, Muhammad (s.a.w.w) alikuwa Mtume pia. Tukifuata dini ya Issa (a.s) na tukaenda kanisani mara moja kwa wiki, ni sawa tu, na tukifuata dini ya Mtume wa mwisho (s.a.w.w) na tukasali mara tano kwa siku, hii pia ni sahihi. Watu hawa wanasema kuwa la muhimu ni kumuamini Mwenyezi Mungu na kufuata moja ya dini zinazohusishwa na Mitume wa Mwenyezi Mungu. George Jordac, mwandishi wa kitabu, Imam Ali; Gibran Khalil Gibran, mwandishi maarufu wa Kilebanon ambaye ni mkristo, na wengine wa

47

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini mfano wao wana mtazamo kama huu.24 Hawa watu wawili wanazungumza juu ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) na Amirul Mu’minin Ali ibn Abi Talib (as) – na hususana Amirul Mu’minin Ali (as) – kama tu ambavyo Mwislamu angefanya. Baadhi ya watu wanauliza ilikuaje watu hawa, licha ya imani yao kwa Amirul Mu’minin Ali ibn Abi Talib (as) na Mtume Muhammad (s.a.w.w) bado ni Wakirsto. Kama wangekuwa wakweli, wangelikuwa Waislamu, na kwa vile hawakufanya hivyo, ni wazi kuna kitu nyuma ya pazia. Wanakuwa walaghai, na sio wakweli katika kauli zao za mapenzi na imani kwa Mtume Muhammad (saw) na Ali ibn Abi Talib (as). Jibu ni, sio kwamba hakuna ukweli katika maelezo yao ya imani na mapenzi kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) na Imam Ali (a.s). Hata hivyo, wana namna yao ya kufikiri juu ya utekelezaji wa dini. Watu hawa wanaamini kwamba wanaadamu hawalazimiki kufuata dini fulani; dini yoyote inatosha. Hivyo, wakati huo huo wao wakiwa ni wakris24 Maneno ya George Jordac kuhusu Mtume Muhammad (s.a.w.w) yanaonyesha kuwa alikuwa anaamimi juu ya Utume wake na kuteremshiwa kwake wahyi, na pia aliamini kwa dhati kuwa Imam Ali ibn Abi Talib (a.s) alikuwa ni mtu wa Mungu, na alikuwa akimfananisha na Issa (a.s) lakini wakati huo huo hakuuacha ukristo. Gibran Khalil Gibran anamzungumzia Imam Ali (a.s) kuwa: “Kwa mtuzamo wangu, Ali alikuwa ni Mwarabu wa kwanza kukutana na kuzungumza na nafsi ya watu wote [wa ulimwengu].” Anaonyesha mapenzi makubwa kwa Ali ibn Abi Talib kuliko hata kwa Mtume Muhammad (s.a.w). Anatoa maelezo yasiyo ya kawaida juu ya Ali ibn Abi Talib, kwa mfano anasema: “Alikufa huku sala ikiwa katika midono yake.” Pia anamzungumzia Ali ibn Abi Talib (a.s) kuwa ‘Ali alikuwepo kabla ya muda wake, na sijui kwa nini wakati fulani majaaliwa huwaleta watu duniani kabla ya muda wao.” Kwa bahati nukta hii ni maana ya moja ya kauli za Imam Ali ibn Abi Talib mwenyewe, aliposema: “Kesho mtaziona siku zangu na siri zangu zitaanikwa mbele yenu, na mtanijua baada ya kuondoka kwangu na nafasi yangu kuchukuliwa na wengine.” 48

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini to, wanajiona wenyewe kuwa ni watu wanaompenda sana na marafiki wa Ali ibn Abi Talib (a.s), na wanaamini pia kuwa yeye mwenyewe (Imam Ali (a.s) alikuwa na mtazamo kama wao. George Jordac mwenyewe anasema Ali ibn Abi Talib (a.s), alikataa kuwalazimisha watu kufuata dini fulani.” Hata hivyo sisi tunaiona rai hili kuwa batili. Ni kweli kuwa hakuna kulazimisha katika dini:

“Hakuna kulazimishana katika dini.” Qur’ani, 2:256 Lakini hii haina maana kuwa kuna dini zaidi ya moja katika kila zama ambazo zinazokubalika kwa Mwenyezi Mungu, na kwamba tuna haki ya kuchagua yoyote tunayoipenda. Hivi sivyo, katika kila zama kuna dini moja tu ya kweli na sio zaidi. Wakati wowote Mtume alipotumwa na Mwenyezi Mungu na dini mpya, watu waliwajibika ili kunufaika na mafundisho yake na kujifunza sheria na maamrisho yake, iwe ni matendo ya ibada au vinginevyo, mpaka zamu ya Mwisho wa Manabii ilipofika. Katika zama hizi mtu akitaka kuja karibu na Mwenyezi Mungu, ni lazima atafute mwongozo kutokana na maagizo ya dini aliyoileta. Qur’ani Tukufu inasema:

“Na yeyote anayefuata dini isiyokuwa ya Uislamu haitakubaliwa kwake, na akhera atakuwa miongoni mwa wenye hasara.” Qur’ani Tukufu, 3:85 Kama mtu angesema kwamba maana ya ‘Uislamu’ katika aya hii sio dini yetu hii makhususi, bali kusudio ni maana halisi ya maneno, au kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu, jibu litakuwa kwamba bila shaka Uislamu maana yake kujisalimisha na dini ya Uislamu ni dini ya kujisalimisha, lakini ukweli wa kujisalimisha una muundo maalumu katika kila zama. Na katika zama hizi, muundo wake ni ule wa dini iliyoletwa na Mwisho wa Manabii. Hivyo hufuatia kwamba neno Uislamu (kujisalimisha) hulaz49

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini imisha kutumika kwenye dini hii tu peke yake. Kwa maneno mengine, matokeo ya mwisho ya kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu ni kukubali maamrisho Yake, na ni dhahiri kwamba mtu anapaswa mara zote kuishi kwa kutekeleza maamrisho ya mwisho kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Na maamrisho ya mwisho ya Mwenyezi ni yale yaliyoletwa na Mtume wake wa mwisho.

MATENDO MEMA BILA IMANI Ni dhahiri sasa kuwa, kwanza kabisa, mjadala wetu una sura ya jumla, na hatutaki kupitisha maamuzi (hukumu) juu ya mtu au watu binafsi. Pili, mjadala wetu sio juu ya iwapo dini ya kweli ni moja au nyingi, bali tumekubali kwamba dini ya kweli ni moja na kwamba watu wote wanalazimika kuikubali. Tatu, mjadala wetu ni huu: Ikiwa mtu, bila kuikubali dini ya kweli, atafanya tendo ambalo dini ya kweli inaliona kuwa ni (tendo) njema, je mtu huyo atalipwa (na Mwenyezi Mungu) kwa kitendo hicho au hapana? Kwa mfanao, dini ya kweli imesisitiza kuwatendea mema watu wengine. Hii ni pamoja na huduma za kiutamaduni kama kuanzisha shule, sehemu za kusomea elimu, kuandika, na kufundishia; huduna za afya kama tiba, uuguzi, kuanzisha sehemu za kuteketezea taka na kadhalika; huduma za kijamii kama kusuluhisha migogoro, kuwasaidia masikini na walemavu, kusaidia haki za wenye kunyonywa, kuwapiga vita wanyonyaji na wakandamizaji, kuwasaidia walionyang’anywa, kusimamisha haki ambayo ndio madhumuni na lengo la ujumbe wa Mitume, kuweka njia za kuridhisha kwa ajili ya waliokata tamaa na wenye bahati mbaya na watu kama hao. Kila dini na kila Mtume amehubiri mambo haya. Kwa nyongeza, kufikiri na dhamiri ya kila mtu huhukumu kwamba mambo haya ni mazuri na yanayofaa.

50

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini Sasa, tunauliza iwapo asiye Mwislamu analipwa kama akitekeleza huduma hizi. Dini ya kweli inasema uwe mkweli na usiwe muwongo; kama asiye Mwislamu akitenda kwa mujibu wa kanuni hii, atalipwa au la? Kwa maneno mengine, je ni sawa sawa kwa asiyekuwa Mwislamu kuwa mwaminifu au msaliti? Je, uasherati na sala hulingana kwa upande wake? Hili ndilo suala tunalotaka kulijadili.

NAMNA MBILI ZA KUFIKIRI. Kwa kawaida, wale wenye mwelekeo wa kisomi husema kwa yakini kwamba hakuna tofauti kati ya Mwislamu na asiyekuwa Mwislamu, na pia hakuna tofauti kati ya anayeamini juu ya tauhidi (kuwa kuna Mungu mmoja tu) na mshirikina (anayeamini kuwa kuna miungu zaidi ya mmoja) yeyote atakayetenda matendo mema, huduma kama vile kuanzisha taasisi ya misaada, ya ugunduzi, au kitu kingine hustahili malipo kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Wanasema kuwa Mwenyezi Mungu ni muadilifu, na Mungu aliye muadilifu huwa habagui waja wake. Kuna tofauti gani kwa Mwenyezi Mungu ikiwa waja wake wanamtambua au la au wanamwamini au la. Kwa hakika, Mwenyezi Mungu hawezi kupuuza matendo mema au kupoteza malipo ya mtu, kwa sababu tu ya mtu huyu kutokuwa na uhusiano wa kumtambua na kumpenda (Mwenyezi Mungu). Na hata pia kwa uhakika zaidi, kama mtu anamwamini Mwenyezi Mungu na anafanya matendo mema, lakini hawatambui Mitume wa Mungu na hivyo hana uhusiano wa kumtambua wala mapatano ya urafiki nao, Mwenyezi Mungu hatafuta wala kubatilisha matendo yao. Kinyume kabisa na watu hawa kuna watu ambao huona kuwa watu wote wanastahili adhabu na huamini kuwa ni watu wachache sana ambao watakuwa na mwisho mwema na ambao matendo yao yatakubaliwa kwa heshima. Hawa wana kipeo rahisi kabisa; wanasema watu (kwa ujumla) imma ni Waislamu au wasio Waislamu. Wasio Waislamu, ambao ni takribani robo tatu ya watu wote duniani watakwenda motoni kwa sababu sio 51

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini Waislamu. Na waislamu kwa upande wao, wamo katika makundi, imma Shia au wasio Shia. Wasiokuwa Shia ni takriban robo tatu ya Waislamu wote duniani watakwenda motoni kwa sababu sio Shia. Na katika Shia wenyewe walio wengi, kama robo tatu ni Mashia wa jina tu, na ni kundi dogo tu miongoni mwao ambao wanajua japo wajibu wa msingi, ambalo ni kufuata taqlid ya mujtahidi, achilia mbali wajibati zao nyingine, na usahihi na ukamilifu wa wajibati hizo hutegemea wajibu huu. Na hata wale wanaofuata taqlid, wengi wao sio watekelezaji. Kwa hiyo ni watu wachache sana watakaoingia peponi. Hii ni mantiki ya pande mbili, mantiki ya wale ambao wanaweza wakaitwa wanaoondoa vikwazo vyote (kwa mtu kukubaliwa matendo yake), na mantiki ya wale ambao tunaweza kusema ni udhihirisho wa hasira ya Mwenyezi Mungu, wakitanguliza mbele hasira kuliko rehema.

MANTIKI YA TATU. Hapa kuna mantiki ya tatu, ambayo ni mantiki ya Qur’ani. Juu ya suala hili Qur’ani inatupatia dhana ambayo ni tofauti na hizo na ambayo ni ya pekee. Qur’ani haikubailani na wazo lisilo na maana la wanaoitwa wasomi wetu wala la wenye mtazamo finyu. Mtazamo wa Qur’ani umejichimbia katika mantiki ambayo yeyote, baada ya kuisoma, atakubali kuwa ni msimamo sahihi kuhusu suala hili. Na ukweli huu unatuongezea imani juu ya Kitabu hiki cha kustaajabisha (Qur’ani) na unaonyesha kuwa mafundisho yake bora yanajitegemea, hayaathiriwi na fikra za wanadamu na kuwa Kitabu hiki kimetoka mbinguni. Hapa tunaeleza ushahidi wa pande zote mbili zinazopingana (hao wanaojiita wasomi na hao wanaojiita wachamungu) na tunauchunguza (ushahidi) huo ili kwa kuuhakiki pole pole tuifikie mantiki ya tatu kuhusiana na suala hili ambayo itakuwa ni mantiki na falsafa ya Qur’ani.

52

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini

WANAOITWA WASOMI. Kundi hili linaleta thibitisho za aina mbili kwa mtazamo wao: kimantiki na kiusimuliaji. Uthibitisho wa kimantiki (kirazini). Uthibitisho wa kimantiki ambao unasema kwamba matendo mema huhitaji malipo bila kujali ni nani anayeyatenda, umetegemezwa katika matarajio mawili. Matarajio ya kwanza: Mwenyezi Mungu ana uhusiano ulio sawa na viumbe vyote. Uhusiano wake katika wakati na sehemu zote ni uleule; kama tu ilivyo kwamba Mwenyezi Mungu yupo Mashariki, pia Yupo Magharibi na kama ilivyo tu kuwa Mwenyezi Mungu yupo juu, pia Yupo chini. Yupo katika wakati huu, uliopita na ujao na uliopita havina tofauti yoyote kwa Mwenyezi Mungu, kama ilivyo tu kuwa Magharibi na Mashariki; juu na chini visivyokuwa na tofauti yoyote Kwake. Halikadhalika watumishi na viumbe Wake vilevile wako sawa Kwake; hana uhusiano ya kifamilia wala uhusiano maalumu na yeyote.

53

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini Hivyo, Mwenyezi Mungu kuonyesha rehema au hasira kwa watu vilevile ni hali moja, isipokuwa kama kuna tofauti baina ya watu wenyewe.25 Kwa sababu hii, hakuna ambaye ni kipenzi cha Mwenyezi Mungu bila sababu, na hakuna ambaye ni dhalili (mbele ya Mwenyezi Mungu) bila sababu. Mwenyezi Mungu hana mahusiano ya kindugu wala utaifa na yeyote; na hakuna mtu yeyote ambaye ni kipenzi au mteule wa Mwenyezi Mungu. 25 Ndio, kwa hakika hii haina maana kuwa vitu vyote vina uhusiano sawa kwa Mwenyezi Mungu na kwamba vinastahili kutendewa sawa sawa. Uhusiano wa vitu kwa Mwenyezi Mungu sio sawa lakini uhusiano wa Mwenyzi Mungu kwa kitu ni sawa. Ukaribu wa Mwenyezi Mungu kwa vitu vyote ni sawa lakini ukaribu wa vitu mbali mbali kutoka kwa Mwenyezi Mungu ni tofauti. Juu ya hili kuna sentensi ya kuvutia katika Dua al-Iftitah. Katika sentensi hii Mwenyezi Mungu ameelezewa kuwa “Ambaye yupo mbali na kwa hivyo hawezi kuonekana na ambaye yupo karibu na hivyo hushuhudia mazungumzo yote.” Kwa kusema kweli, sisi ndio tuko mbali Naye lakini Yeye yupo karibu yetu. Hili ni fumbo linalotatanisha, iweje vitu viwili visiwe na umbali sawa kutoka kimoja kwenda kingine. Lakini hapa ndivyo ilivyo; Mwenyezi Mungu yupo karibu na vitu, lakini vitu havipo karibu na Mwenyezi Mungu yaani vina ukaribu unaotofautiana kwa Mwenyezi Mungu. Nukta ya kufurahisha hapa ni kuwa inapomtaja Mwenyezi Mungu kuwa ‘mbali’ hutaja sifa ya viumbe Wake kuwa ni ushahidi, ambayo ni sifa ya kuona. “Hakuna yeyote ambaye anaweza kumuona.” Na inapotaja kuwa Mwenyezi Mungu Yupo ‘karibu’ hutaja sifa ya Mwenyezi Mungu kuwa ni ushahidi, ambayo ni sifa ya uwepo wa Mwenyezi Mungu (kila sehemu). Tunapojizungumzia sisi tunatumia sifa ya ‘umbali’ katika kumfikia Mwenyezi Mungu na tunapomzungumzia Yeye, tunatumia sifa ya; ukaribu’ katika kutufikia sisi.’ Sa’di anasema: “Ni rafiki aliye karibu na mimi kuliko mimi mwenyewe (nilivyo karibu yangu), na cha ajabu ni kuwa mimi nipo mbali Naye. Nifanye nini; nani ninayeweza kumwambia kuwa rafiki yangu yupo ubavuni mwangu, na nimetelekezwa.” 54

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini Maadamu uhusiano wa Mwenyezi Mungu kwa watu wote ni sawa, basi hapa hakuna sababu tena ya Yeye kukubali tendo jema la mtu mmoja na kukataa tendo jema la mtu mwingine. Ikiwa matendo ni yale yale, basi hata malipo yao yatakuwa sawa, maadamu uhusiano wa Mwenyezi Mungu kwa watu wote ni sawa. Hivyo hapa haki inataka Mwenyezi Mungu awalipe wema wale wote wanaotenda matendo mema bila kujali kuwa ni Waislamu au sio Waislamu. Matarajio ya pili: Uzuri au ubaya wa kitendo hautegemei juu ya maagano, bali uhalisia wake. Kwa kauli za wanateolojia na mafaqihi, ubaya au uzuri wa kitu ni wa asili. Yaani, matendo mema na mabaya yanatofautiana kwa asili yake. Matendo mema ni mema kwa asili yake na matendo maovu ni maovu kwa asili yake. Uaminifu, wema, kufanya mema, kusaidia wengine, n.k ni mambo mazuri kwa asili yake; na kusema uongo, kuiba na ukandamizaji ni vibaya kwa asili yake. Uzuri wa uaminifu au ubaya wa kusema uongo si kwa sababu Mungu amehalalisha uaminifu na kuharamisha uongo. Kinyume chake, ni kwa sababu uaminifu ni mzuri ndio maana Mwenyezi Mungu amefanya uwe wajibu na kwa sababu uongo ni mbaya ndio maana Mwenyezi Mungu ameuharamisha, na sio vinginevyo. Kutokana na vigezo hivi viwili, tunahitimisha kwamba kwa vile Mwenyezi Mungu hapendelei na kwa vile matendo mema ni mazuri kutoka kwa watu wote, yeyote yule atakayefanya tendo jema kwa hakika na kwa sharti atalipwa na Mwenyezi Mungu. Halikadhalika ni hivyo hivyo kwa matendo maovu, hakuna tofauti kati ya wale ambao wanayatenda. Uthibitisho kutoka kwenye masimulizi ya Qur’ani. Qur’ani huthibitisha katika Aya nyingi kanuni ya kutokubagua baina ya watu katika ulipaji wa matendo mema na adhabu kwa matendo maovu – jambo ambalo limetajwa katika uthibitisho wa kimantiki hapo juu.

55

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini Qur’ani imewapinga vikali Mayahudi, ambao wanaamini katika ubaguzi huo. Mayahudi waliamini – na bado wanaamini – kwamba Mayahudi ni taifa teule la Mungu; wanasema: Sisi ni watoto na marafiki wa Mungu. Endapo Mungu atatutia Motoni, haitakuwa zaidi ya muda mfupi.” Qur’ani inayaita mawazo haya kuwa ni matamanio tu na fikra za uongo na imeyapiga vita kwa nguvu sana. Qur’ani pia inaonyesha makosa ya baadhi ya Waislamu ambao nao wamedanganyika na wazo hili. Zifuatazo hapa ni baadhi ya aya kuhusiana na suala hili.

“Na wanasema, moto hautatuunguza isipokuwa kwa siku chache. Sema, je mmepata agano (ahadi) kutoka kwa Mwenyezi Mungu, ambalo Mwenyezi Mungu hawezi kulivunja, au mnasema juu ya Mwenyezi Mungu yale msiyoyajua? Bila shaka, wale wanaochuma uovu na ambao makosa yao yamewaviringisha ni wakazi wa motoni; na humo watakaa milele. Na wale wanaoamini na kutenda mema ni wakazi wa peponi, watakaa humo milele.” Qur’ani Tukufu, 2:80-82 Katika sehemu nyingine Qur’ani inasema kujibu mabunio (dhana) ya wayahudi:

56

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini

“Na waliyoyazua yaliwadanganya katika dini yao. Sasa, itakuwaje hali yao tutakapowakusanya katika siku ambayo haina shaka na kila nafsi italipwa kamili kile ilichochuma, na hawatadhulumiwa.” Qur’ani Tukufu, 3:24-25. Katika sehemu nyingine, Wakristo wamejumuishwa na Wayahudi, na wote wamepingwa na Qur’ani.

“Na wanasema, hakuna atakayeingia peponi isipokuwa Wayahudi au Wakristo; hizi ni fikra (kwa mujibu wa matamanio) zao, sema; leteni ushahidi wenu, kama nyinyi ni wakweli. Bali wale waliojisalimisha (waliosilimu) kwa Mwenyezi Mungu na wakafanya wema, watapata malipo kwa Mola wao, na hawatapata hofu wala hawatahuzunika.” Qur’ani Tukufu, 2:111-112 Katika Suratul Nisaa Waislamu pia wamejumlishwa katika kundi la Wayahudi; na Wakristo. Qur’ani inabomoa fikra za kibaguzi, bila kujali ni nani anayeziamini. Ni kama vile Waislamu wameathiriwa na fikra za Watu wa Kitabu, na katika sura ya wale ambao bila sababu yoyote nao walianza kujiona kuwa ni bora, nao (Waislam) wakajitwalia mawazo hayo juu yao wenyewe. Qur’ani inapinga vikali fikra hizi potofu. 57

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini

“(Hii) haitakuwa kwa matamanio yenu wala kwa matamanio ya watu wa kitabu. Yeyote atakayefanya uovu atalipwa kwalo. Hatapata mlinzi wala msaidizi (mwingine) badala ya Mwenyezi Mungu. Na yeyote atakayefanya wema akiwa mwanaume au mwanamke na ni muumini, hawa ndio watakaoingia Peponi na hawatadhulumiwa hata japo kokwa ya tende.” Qur’ani Tukufu, 4:123-124 Tukiachilia mbali aya zinazoshutumu madai yasiyo na msingi ya heshima na ukaribu kwa Mwenyezi Mungu, kuna aya nyingine ambazo zinasema kuwa Mwenyezi Mungu hapotezi ujira wa tendo lolote jema. Aya hizi pia zimechukuliwa kama uthibitisho wa kukubaliwa kwa vitendo vya watu wote, awe Mwislamu au asiye Mwislamu katika Suratul Zilzala, tunasoma:

“Yeyote atayefanya wema japo mdogo sana atauona na kila atakayefanya uovu japo mdono sana atauona.” Qur’ani Tukufu, 99:78. Sehemu nyingine Mwenyezi Mungu anasema:

“Kwa hakika Mwenyezi Mungu huwa hapotezi ujira wa watendao wema.” Qur’ani Tukufu, 9:120

58

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini Katika sehemu nyingine, Anasema:

“Kwa hakika hatupotezi ujira wa wale wanaofanya wema.” Qur’ani Tukufu, 18:30. Maneno ya aya hizi yanaonyesha kuwa maelezo ni kwa ajili ya watu wote bila kuwatenga baadhi ya watu. Wanachuoni wa misingi ya fiqhi (Usul Fiqh) wanasema kuwa maelezo fulani ya jumla hayakubali isipokuwa yaani kuwatenga baadhi ya watu. Inaposemwa “Hatupotezi ujira wa wanaotenda wema” inaonyesha kuwa Mwenyezi Mungu huhifadhi amali njema kwa hiyo haiwezekani Mwenyezi Mungu apuuze moja ya sifa (tabia) zake na apoteze amali njema. Kuna aya nyingine ambayo hutumiwa sana katika mjadala huu, na hudaiwa kuwa inaonyesha dhahiri utetezi wa madai ya kundi hili.

“Kwa hakika walioamini, Wayahudi, Wasabato na Wakristo wanaoamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho na wakatenda wema, hawatapata hofu wala hawatahuzunika.” Qur’ani Tukufu, 5:69. Katika aya hii kuna masharti matatu yaliyotajwa kwa ajili ya wokovu na usalama kutokana na adhabu ya Mwenyezi Mungu: kuamini Mwenyezi Mungu, kuamini juu ya Sikuu ya Hukumu, na matendo mema, hakuna sharti jingine linalotajwa. 59

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini Baadhi ya wale ambao kwa dhahiri ni wasomi wamekwenda hatua moja zaidi na kusema kuwa lengo la Mitume lilikuwa kuwaita watu katika haki na wema, na kwa kuafikiana na kanuni kuafikiana na roho na sio sheria’ tunaweza kusema kuwa haki na wema hukubaliwa hata kwa wale wasiomwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Hukumu. Hivyo wale ambao hawamwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho lakini wametoa michango mikubwa kiutamaduni katika tiba, uchumi na siasa kwa wanaadamu wanastahili ujira mkubwa. Ni kweli watu hawa wanaweza kutoa hoja kwa kutumia aya kama: “Hatupotezi ujira wa watendao wema” na “Hivyo yeyote atakayefanya wema japo mdogo sana atauona,” lakini aya kama hiyo hapo juu inapingana na dai lao. Hapa chini hebu tuangalie ushahidi wa kundi jingine.

KUNDI LENYE MISMAMO MKALI. Tofauti na hawa wanaodaiwa kuwa ni wasomi, wanaodai kuwa matendo mema ya kila mtu hukubaliwa na Mwenyezi Mungu katika hali zote, kuna ‘wachamungu wenye msimamo mkali,’ msimao wao unapishana kabisa na kundi la awali. Wanasema kuwa haiwezekanai matendo ya wasio Waislamu yakubaliwe. Matendo ya wasio Waislamu na hakikadhalika wasio Shia hayana thamani kabisa. Asiyekuwa Mwislamu na Mwislamu asiye Shia yeye mwenyewe amekataliwa; na matendo yao yanastahili kukataliwa zaidi. Kundi hili pia linaleta ushahidi wa namna mbili wa kimantiki na masimulizi (ya Qur’ani na hadith). Ushahidi wa kimantiki: Ushahidi wa kimantiki wa kundi hili ni kuwa ikiwa matendo ya wasio Waislamu na wasiokuwa Shia yatakubaliwa na Mwenyezi Mungu, sasa tofauti iko wapi kati ya Waislamu na wasio Waislamu? Tofauti hapa inatakiwa iwe ama matendo mema ya Waislamu 60

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini na Shia yakubaliwe na yale ya wasiokuwa Waislamu na wasio kuwa Shia yakataliwe, au Waislamu na Shia wasiadhibiwe kwa matendo yao maovu, bila kuadhibiwa wasiokuwa Waislamu na wasiokuwa Shia. Lakini tukisema matendo ya makundi yote yatakubaliwa na matendo maovu ya makundi yote yatasababisha waadhibiwe, sasa tofauti itakuwa nini baina yao? Na kuna athari gani ya kuwa Mwislam au kuwa Shia katika hali hii? Usawa wa Waislamu na wasio waislam, na kadhalika Shia na wasiokuwa Shia kuhusiana kuhesabiwa kwa matendo yao inamanisha kwamba kimsingi kuutekeleza Uislamu au Ushia hakuna maana wala faida yeyote. Ushahidi wa simulizi: Mbali na hoja hiyo hapo juu, kundi hili linatoa hoja kutoka katika Aya mbili za Qur’ani na hadith kadhaa. Katika aya chache za Qur’ani imeelezwa wazi wazi kuwa matendo ya wasioamini hayakubaliki, na halikadhalika katika hadith nyingi imeelezwa kuwa matendo ya wasiokuwa Shia yaani wale ambao hawana wilaya (uongozi ulioamrishwa na Mwenyezi Mungu) ya Ahlul Bait (a.s) hayakubaliwi. Katika Surat Ibrahim, Mwenyezi Mungu analinganisha matendo ya wasioamini na majivu ambayo hutawanywa na upepo mkali na kupotea.

“Mfano wa wale waliomuasi Mwenyezi Mungu. Matendo yao ni kama majivu ambayo upepo huyapuliza kwa nguvu katika siku yenye tufani: hawana nguvu juu ya chochote walichokichuma. Huo ni upotofu mkubwa.” Qur’ani Tukufu, 14:18. Katika aya ya Surat Nur, matendo ya wasioamini yamefananishwa na mazigazi ambayo huonekana kama maji lakini yakikaribiwa, hayaonekani tena. Aya hii inasema kwamba matendo makubwa huwapa watu ahueni, na katika mtazamo wa baadhi ya watu wenye akili za kawaida ni makubwa kuliko 61

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini huduma hata za Mitume, yote ni batili kama hayakubaliani na imani katika Mungu. Ukubwa wa matendo hayo si chochote bali ni mchezo, kama mazigazi. Maneno ya aya hiyo ni kama ifuatavyo:

“Ama kwa walio kufuru vitendo vyao ni kama mazigazi jangwani, mwenye kiu huyadhani ni maji hata ayafikiapo hapati chochote. Lakini hapo anamkuta Mwenyezi Mungu, naye humpa hesabu yake sawa sawa, na Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhesabu.” Qur’ani Tukufu, 24:39. Hili ni fumbo la matendo mema ya wasioamini, ambayo kwa nje huonekena kuwa ni mema. Hivyo ole wao kwa matendo yao maovu! Tunasoma fumbo lao katika aya ifuatayo kwa maneno haya:

“Au ni kama giza katika bahari yenye kilindi, inayofunikwa na mawimbi, juu ya mawimbi na juu yake kuna mawingu, giza juu ya giza anapotoa mkono wake anakarabia asiuone, na ambaye Mwenyezi Mungu hakumjaalia nuru, basi huyo hana nuru.” Qur’ani Tukufu, 24:40. Kwa kuongeza aya hii kwenye aya iliyopita, tunahitimisha kwamba matendo mazuri ya wasioamini, pamoja na udanganyifu wao wa dhahiri, ni mazigazi ambayo hayana ukweli. Ama kwa matendo yao maovu, ehee! Ni uovu juu ya uovu, giza juu ya giza 62

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini Aya hizo hapo juu zinafafanua hadhi ya amali za wasioamini. Na kuhusiana na Waislamu wasiokuwa Shia, kutokana na mtazamo wetu sisi Shia, hadith zilizotufikia kutoka kwa Ahlul Bait (a.s) zinafafanua msimamo wao. Hadith nyingi zimetufikia juu ya mada hii. Wale wanaopenda wanaweza kusoma al-Kafi, Jz. 1, ‘Kitab al-Hujjah’ na Jz. 2, ‘Kitab al-Iman wal kufr; Wasailul Shia Jz. 1, ‘Abwab Muqaddamat al-Ibadat;’ ‘Mustadrak wasail,’ Jz. 1, ‘Abwab Muqaddamat al-Ibadat,’ ‘Biharul Anwar.’ Majadiliano juu ya ufufuo, Sura ya 17 (sura juu ya ahadi, tishio, Ubatilisho wa matendo, na kafara) na Jz. 7 ya chapa ya zamani sura ya 227, na Jz. 15 ya chapa ya zamani, sehemu ya maadili, uk. 187. Kama mfano, tunasimulia hadathi moja kutoka Wasailush Shia: Muhammad ibn Muslim alisema, “Nilimsikia Imam Muhammad al-Baqir (a.s) akisema, ‘yeyote anayemuabudu Mwenyezi Mungu na hushikamana na ibada lakini hamtambui Imam (kiongozi) aliyeteuliwa na Mungu kwa ajili yake, matendo yake hayakubaliwi, na yeye mwenyewe amepotoka na amepotea, na Mwenyezi Mungu anayachukia matendo yake … na akifa katika hali hii, hufa kifo cha ukafiri. Ewe Muhammad ibn Muslim, jua kwamba viongozi wa udhalimu na wafuasi wao wako nje ya dini ya Mwenyezi Mungu. Wao wenyewe walipotoka na waliwapotosha wengine. Matendo yao ni kama majivu ambayo hupulizwa na upepo katika siku yenye tufani, na hawapati chochote katika waliyoyachuma. Huo ni upotevu wa dhahiri.” 26 Huu ni ushahidi wa wale wanaosema kuwa msingi wa wokovu ni imani. Wakati fulani baadhi ya watu kutoka katika kundi hili huenda mbali zaidi na kuchukuliwa tu dai la kuwa na imani, au kiuhalisia ushirikishaji rahisi, kuwa kigezo cha Hukumu. Kwa mfano, madhehebu ya Murji wakati wa 26 Wasailush Shia, Jz. 1, sehemu ya kwanza, uk. 90. 63

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini enzi za Bani Umayya walieneza wazo hili, na kwa bahati nzuri, baada ya kuanguka kwa utawala wa Bani Umayya nao walipotea. Katika enzi hizo, msimamo wa Shia wakiongozwa na Maimamu wa Ahlul Bait (a.s) ulikuwa kinyume kabisa na msimamo wa wafuasi wa Murji, lakini kwa bahati mbaya msimamo huu wa murji umechukua vazi jipya na kujikita miongoni mwa Shia wa kawaida. Baadhi ya Shia wenye mtazamo finyu huona kwamba kujishirikisha tu kiurahisi na Amirul Muuminina Ali bin Abi Talib (a.s) hutosha kwa ajili ya wokovu, na wazo hili ndio msingi wa hali duni ya Mashia katika zama hizi. Madarweshi na masufi wa zama hizi wanategemea (wanakwepa) kufanya matendo mema kwa njia mbali mbali na kwa visingizio mbali mbali wamefanya usafi wa moyo kuwa ni kisingizio licha ya kuwa moyo safi humhimiza mtu kufanya matendo mema. Tofauti na makundi haya, kuna wengine ambao wamepandisha thamani ya vitendo kiasi cha kusema kuwa mtu anayetenda dhambi kubwa ni kafiri. Hii ilikuwa imani ya Makhawariji. Baadhi ya wanateolojia walimchukulia mtenda dhambi kubwa kuwa si muumini wala kafiri na walishikilia kuwa kuna ‘hali baina ya hizi hali mbili.’ (Imani na kufuru). Jukumu letu ni kuona ipi kati ya misimamo hii ni sahihi. Je tuamini kuwa imani ndio bora zaidi au vitendo ndio bora zaidi? Au kuna njia ya tatu? Kwa kuanza hebu tujadili juu ya maana ya imani.

MAANA YA IMANI Ama kuhusiana na maana ya imani, mjadala utaendelea katika hatua tatu: Je, ukosefu wa imani katika ya misingi ya dini, kama vile upweke wa Mwenyezi Mungu, Utume, na Ufufuo – na kwa mujibu wa mtazamo wa Shia, ni hizi tatu pamoja na uadilifu wa Mwenyezi Mungu na Uimamu – 64

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini wakati wote haya ni lazima yawe ni sababu kwa ajili ya adhabu ya Mwenyezi Mungu kwa watu? Au je, inawezekana kwa baadhi ya wasioamini kusamehewa na wasiadhibiwe kwa kutokuwa na imani kwao? Je, imani ni sharti la lazima kwa kukubaliwa matendo mema? Kama vile hakuna matendo mema ya asiyekuwa Mwislamu au asiyekuwa Shia yanayokubaliwa na Mwenyezi Mungu? Je, kufru (kutokuamini) na kuukataa ukweli ni sababu ya kubatilisha matendo mema au hapana? Katika majadiliano yanayofuatia tutajadiliana kwa kugusia kila hatua katika hizi tatu.

KUWAJIBIKA KWA SABABU YA KUTOAMINI. Hakuna shaka kuwa kufuru ni ya aina mbili; moja ni kufuru inayotokana na ujeuri na ukaidi, ambayo inaitwa kufuru ya kukana na nyingine ni kufuru ya ujinga na kutojua ukweli. Kuhusiana na aina ya kwanza ushahidi wa kiakili unaonyesha kuwa mtu ambaye kwa makusudi na kwa kujua ataonyesha ukaidi dhidi ya ukweli na akajibidiisha kuukana, hustahili adhabu. Lakini kuhusiana na aina ya pili, ikiwa ujinga na kutojua hakutokani na kupuuzia, hao watasamehewa na Mwenyezi Mungu. Ili kuelezea nukta hili ni muhimu kuzungumzia kidogo juu ya unyenyekevu na ukaidi. Qur’ani inasema:

“Siku ambayo haitafaa mali wala watoto, isipokuwa mwenye kuja kwa Mola wake na moyo safi.” Qur’ani Tukufu, 26:88-89

65

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini

VIWANGO VYA UNYENYEKEVU Sharti muhimu kabisa la usafi wa moyo ni kujinyenyekeza katika ukweli. Unyenyekevu una hatua tatu, unyenyekevu wa mwili, unyenyekevu wa akili na unyenyekevu wa moyo. Wapinzani wawili wanapokutana katika mapigano na mmoja wao akahisi kuwa atashindwa, anaweza kujisalimisha au kujinyenyekesha kwa mwenzake. Katika kujisalimisha huko, kwa kawaida yule aliyeshindwa hunyanyua mikono yake juu kama dalili ya kushindwa na kutopenda kupigana, na hivyo kuwa chini ya himaya (utawala) wa mpinzani (adui). Yaani, hutenda kulingana na atakavyomridhisha na mpinzani wake. Katika aina hii ya unyenyekevu, mwili umenyenyekea, lakini akili na moyo havijanyenyekea, badala yake muda wote vinawaza juu ya kuasi, na kutafakari jinsi ya kupata nafasi ya kumshinda adui tena. Hii ndio hali ya akili na fikra zake, na hisia na mihemko yake vyote pia vinamkana adui. Aina hii ya unyenyekevu wa mwili ndio pekee inayoweza kupatikana kwa nguvu. Hatua inayofuatia ya unyenyekevu ni unyenyekevu wa akili na fikra. Nguvu inayoweza kuifanya akili inyenyekee ni mantiki na hoja. Hapa nguvu za kiumbo (kimwili) haziwezi kufanikisha lolote. Haiwezekani kabisa kwa kutumia nguvu za kimwili kumshawishi mwanafunzi aelewe kuwa jumla ya nyuzi za pembe tatu ni sawa na pembe mraba mbili. Hoja za kihesabu lazima zithibitishwe kwa hoja za kiakili na si kwa njia nyingine yoyote. Akili hulazimishwa kunyenyekea kwa kufikiri na kuchanganua hoja za kiakili. Ikiwa ushahidi wa kutosha upo na ukawasilishwa katika akili, na akili ikauelewa, basi hunyenyekea, hata kama dola zote za dunia zitasema usinyenyekee. 66

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini Inaeleweka vizuri kuwa Galileo aliteswa kwa imani yake juu ya mzunguko wa dunia na jua ya ukweli kuwa jua lipo katikati ya mfumo wa sayari, kwa hofu ya kuchomwa akiwa hai, Galileo alielezea kutubu kwake dhidi ya mtazamo wake wa kisayansi; katika hali hiyo, aliandika kitu fulani kisirisiri. Inasemekana kuwa aliandika kuwa, “Toba ya Galileo haitaifanya dunia isimame (isizunguke kama ninavyoamini kuwa inazunguka). Mabavu yanaweza kumlazimisha mtu akanushe maneno yake lakini akili ya binadamu huwa hainyenyekei isipokuwa inapokutana na mantiki na hoja za kiakili.

“Sema, Leteni ushahidi wenu, kama nyinyi ni wakweli.” Qur’ani ukufu, Qur’ani Tukufu, 27:64 Hatua ya tatu ya unyenyekevu ni unyenyekevu wa moyo. Uhalisi wa imani ni unyenyekevu wa moyo; Unyenyekevu wa ulimi au unyenyekevu wa fikra na akili visipoambatana na unyenyekevu wa moyo, bado sio imani. Unyenyekevu wa moyo ni sawa sawa na unyenyekevu wa mtu mzima na ni ukanushaji wa kila aina ya ukaidi na kibri. Inawezekana kuwa mtu anaweza akalikubali wazo kwa mujibu wa akili yake, lakini sio roho yake. Mtu anapoonyesha ukaidi kwa sababu ya chuki bila sababu au anakataa kuukubali ukweli kwa sababu ya maslahi yake binafsi, au akili na fikra zake zimenyenyekea, lakini roho imeasi na haina unyenyekevu, na kwa sababu hii hana imani, kwa sababu uhalisia wa imani ni unyenyekevu wa moyo na roho. Mwenyezi Mungu anasema katika Qur’ani

67

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini “Enyi mlioamini, nyenyekeeni hasa hasa, na msifuate nyayo za shetani. 2:208.

Hii ni kuwa, roho yako iwe vitani dhidi ya akili yako, hisia zako na iwe vitani dhidi ya utambuzi wako. Kisa cha shetani kilichotajwa katika Qur’ani ni mfano wa kufuru ya moyo, japokuwa akili imenyenyekea. Shetani alimtambua Mwenyezi Mungu, aliamini juu ya Siku ya Hukumu, aliwatambua Mitume vizuri pamoja na warithi wao na alizitambua nafasi zao; na wakati huo huo Mwenyezi Mungu anamwita asiyeamini:

“Na akawa miongoni mwa wasioamini…” Qur’ani ukufu, 2:34 Ushahidi kuwa, kwa mtazamo wa Qur’ani, shetani alimtambua Mwenyezi Mungu ni kuwa Qur’ani inasema wazi wazi kuwa alikiri kuwa Yeye ni Muumba. Akimweleza Mwenyezi Mungu alisema:

“Uliniumba kwa moto, na yeye ulimuumba kwa udongo.” Tukufu, 7:12.

Qur’ani

Na ushahidi kuwa aliamini juu ya Siku ya Hukumu ni kuwa alisema:

“Nipe fursa mpaka Siku watakapofufuliwa.” Qur’ani ukufu, 7:14. Na ushahidi kuwa aliwatambua Mitume na maasumu ni kuwa alisema: “(Naapa) kwa utukufu wake, nitawapotosha wao wote isipokuwa waja wako waliotakasika miongoni mwao.” Qur’ani ukufu, 38:82-83

68

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini Maana ya waja waliotakasika, ambao ni twahiri, sio tu katika matendo yao bali kuwepo kwao kote kumetakasika na wameepukana na madhambi yote, ni marafiki wa Mwenyezi Mungu; na maasumu, shetani aliwatambua pia na aliamini juu ya kutakasika kwao. Qur’ani, huku ikimwelezea shetani kuwa anayajua yote haya, bado inamwita kuwa asiyeamini. Hivyo hapa tunaelewa kuwa kutambua na kuelewa peke yake, au kunyenyekea kwa akili, hakutoshelezi kwa mtu kuhesabika kuwa ni muumini. Kitu cha zaidi kinahitajika. Kwa mantiki ya Qur’ani, kwa nini shetani ameitwa asiyeamini licha ya elimu yake? Ni dhahiri kwamba, licha ya kuwa utambuzi wake ulikubaliana na uhalisia, hisia zake zilipinga, moyo wake uliipinga akili yake, alionyesha kiburi, alikosa unyenyekevu wa moyo.

UISLAMU WA KWELI NA UISLAMU WA KIMAENEO. Kwa kawaida tunaposema fulani ni Mwislamu au sio Mwislamu, mtazamo wetu sio juu ya uhalisia wa jambo. Wale ambao kijiografia wanaishi katika eneo fulani na ni Waislamu wa kuiga na kurithi kutoka kwa wazazi wao tunawaita Waislamu, na wale wanaoishi katika eneo tofauti na wamenasibika na dini nyingine au hawana dini kabisa, kwa mara nyingine tena kutokana na kurithi/kuiga kutoka kwa wazazi wao, tunawaita wasiokuwa waislamu. Inafaa ieleweke kwamba kipengele hiki hakina maana sana, si ile ya kuwa Mwislamu wala ile ya kutokuwa Mwislamu na asiyeamini. Wengi wetu ni Waislamu wa kuiga au wa kijiografia, ni Waislamu kwa sababu mama zetu 69

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini na baba zetu walikuwa Waislamu na tulizaliwa na kukulia katika eneo ambalo watu wake ni Waislamu. Chenye thamani kiuhalisi ni Uislamu wa kweli, na hii ni kwa yule ambaye hunyenyekea/hukubali ukweli kutoka moyoni mwake. Katika hali ya kuufungua moyo wake kwa ajili ya kuupokea na kuutekeleza ukweli, na Uislamu ambao ameukubali lazima uwe umeegemea katika misingi ya kutafiti na kusoma katika upande mmoja, na unyenyekevu pamoja na kutokuwa na chuki isiyo na sababu juu ya hilo analolitafiti kwa upande mwingine. Ikiwa mtu ana tabia ya kuukubali (kunyenyekea) ukweli anapouona na kwa sababu yoyote ile mtu akawa hakuufikia uhalisi wa Uislamu bila ya yeye mwenyewe kukaidi, bila shaka Mwenyezi Mungu atajiepusha kumuadhibu na atauepuka moto wa Jahanamu. Mwenyezi Mungu anasema:

“Na hatuadhibu isipokuwa baada ya kutuma mjumbe.” Qur’ani Tukufu, 17:15. Yaani, haiwezekani kwa Mwenyezi Mungu, Mwenye Hikma na Mkarimu, kumuadhibu mtu ambaye ushahidi wa ukweli haujamfikia au haujakamilika. Wanazuoni wa misingi ya fiqhi (Usulul fiqh) wameeleza maana ya jumla ya aya hii ambayo huthibitisha matumizi ya akili (hukubaliana na akili), na wameiita “kutokuwa sahihi kwa adhabu bila maelezo ya awali.” Wanasema kuwa mpaka Mwenyezi Mungu aweke uhalisia wazi wazi kwa mtu, vinginevyo itakuwa sio haki kwa Yeye kumuadhibu mtu huyo. Kuonyesha ukweli kwamba inawezekana kuwapata watu ambao wana roho za unyenyekevu bila kuwa Waislamu kwa jina, Descartes, Mwanafalsafa wa Kifaransa kwa mujibu wa maneno yake mwenyewe – ni mfano mzuri. Katika wasifu wake, wameandika kuwa alianza falsafa yake kuanzia kwenye shaka, alivitilia shaka vitu vyote alivyovijua na alianzia kutoka 70

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini sifuri. Aliifanya fikra yake yeye mwenyewe kuwa nukta ya kuanzia, na alisema: “Kwa hiyo, nafikiri ni mimi.” Baada ya kuthibitisha kuwepo kwake alithibitisha kuwepo kwa roho na halikadhalika kuwepo kwa mwili, na alidhihirikiwa kuwa Mwenyezi Mungu yupo, polepole wazo la kuchagua dini lilijitokeza, alichagua Ukristo, ambao ulikuwa dini ya rasmi ya nchi yake. Lakini pia anasema, “Sisemi kuwa Ukristo ndio dini bora kabisa duniani kote, ninachosema ni kuwa katika dini ambazo hadi sasa ninazijua na ambazo ninaweza kuzifikia, Ukristo ni dini bora. Sina ugomvi na ukweli; labda katika sehemu nyingine za dunia kuna dini bora kuliko Ukristo.” Ilitokea tu akaitaja Iran kama nchi ambayo hana taarifa zake na hajui dini yake; anasema: “Ninajuaje? Labda kuna dini Iran ambayo ni bora kuliko Ukristo.” Watu kama hawa hawawezi kuitwa wasioamini, kwani hawana ukaidi; sio kwamba wanaitafuta kufru kwa makusudi. Hawahusiki katika kuficha ukweli, jambo ambalo ndio msingi wa kufru. Watu hawa ni “Waislamu wa kimwelekeo.” Ingawa hawawezi kuitwa Waislamu, pia hawawezi kuitwa wasioamini, kwani upinzani wa Mwislamu na asiyeamini si sawa na upinzani wa kukubali na kukana au kati ya kuwepo kwa kitu na wajuzi wa mantiki na wanafalsafa. Badala yake, ni upinzani wa kinyume wa vitu viwili, yaani kinyume cha vitu viwili vilivyopo, sio ule wa kimoja kilichopo na mwingine wa kile ambacho hakipo. Hapa tumemtaja Descartes kama mfano na hatukuwa na nia ya kuondoka katika kanuni yetu tuliyoeleza mwanzo. Tulieleza tokea mwanzo kuwa hatutatoa maoni yetu kuhusu mtu mmoja mmoja. Nia yetu katika kumtaja Descartes kama mfano ni kuwa ikiwa tutajalia kuwa alichosema ni kweli na kuwa ni mnyenyekevu mbele ya ukweli kama maneno yake yanavyoonyesha, na kwa upande mwingine kweli hakuwa na uwezo zaidi wa kufanya utafiti, basi ni Mwislamu wa kimwelekeo. 71

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini

DHATI, SHARTI LA KUKUBALIWA AMALI. Jambo la pili katika tuliyoyataja katika maana ya imani ni kuwa imani ina ushawishi gani katika kukubaliwa kwa matendo. Awali, tulipokuwa tukieleza uthibitisho wa wale wanaosema kuwa matendo mema ya wasioamini yatakubaliwa na Mwenyezi Mungu, tulisema kuwa wanasema kuwa uzuri au ubaya wa matendo unahusiana na asili yake. Matendo mema, yawe ya muumini au asiyeamini ni mazuri kwa asili yake na ni lazima kwa namna yoyote ile yakubaliwe na Mwenyezi Mungu, kwa vile wema ni wema tu, bila kujali ni nani ameutenda, na uovu ni uovu tu bila kujali ni nani ameufanya, na ikizingatiwa kuwa uhusiano wa Mwenyezi Mungu kwa watu wote ni sawa. Sasa tungependa kuongeza kuwa japokuwa kilichotajwa hapo juu ni sawa, kuna nukta moja muhimu ambayo imepuuzwa. Kuelezea nukta hii, ni lazima tuelezee istilahi nyingine kutoka katika somo la misingi ya fiqh ambayo ni kwamba wema au uovu ni wa aina mbili: unaohusiana na tendo na unaohusiana na mtendaji. Kila tendo lina pande mbili na kila upande una kanuni yake kuhusiana na uzuri au ubaya wake. Inawezekana tendo likawa jema katika upande mmoja na likawa si zuri katika upande mwingine. Halikadhalika kinyume chake kinawezekana, na pia inawezekana jambo likawa zuri au baya katika pande zote. Pande mbili zinajumuisha manufaa au madhara ya kitendo katika ulimwengu wa nje pamoja na malengo madhumuni ya kiroho ya mtu huyo yaliyohamasisha mtendaji kutenda tendo hilo.

72

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini Kutokana na upande wa kwanza, mtu anapaswa kutathmini ukubwa wa faida au hasara za kitendo. Na kutokana na upande wa pili, mtu anapaswa kutathmini ni aina gani ya kitendo mtendaji amefanya katika hali ya kiakili na kiroho na anafanya kwa malengo gani. Matendo ya wanadamu, kwa mujibu wa ukubwa wa manufaa na madhara yake, huandikwa katika vitabu vya historia, na historia hupitisha hukumu juu yao. Huwasifu au huwalaumu. Lakini malipo ya kiroho hurekodiwa katika vitabu vya ulimwengu mwingine (vya amali). Vitabu vya historia hupenda matendo makuu na yenye ushawishi na huyasifu matendo haya lakini vitabu vya rekodi vya akhera, mbali na haya vitabu vya rekodi ya akhera vinatafuta matendo ambayo yana roho. Qur’ani inasema:

“Ambaye ameumba kifo na uhai ili kuwajaribuni, ni nani miongoni mwenu aliye na matendo bora...” Qur’ani ukufu, 67:2. Aya hii inazungumzia ‘mateno bora’ sio ‘matendo zaidi’ kwa vile kitu muhimu kwetu ni kujua kwamba tunapotenda kitendo kwa ushawishi wa kiroho, mbali na muonekano wa nje wa kitendo ambao ni mfululizo wa harakati, na kina athari na thamani yake kijamii – kiroho, kwa hakika tunaelekea mwelekeo fulani na tunapita katika njia fulani. Suala hili sio rahisi kiasi hicho kama kusema, “Vyote vile ambavyo vipo ni ‘kitendo,’ kazi, nishati ya misuli ambayo imetumika. Na kuhusiana na fikra na nia, thamani yake ipo katika kujiandaa kwa ajili ya kitendo; sio tena kama fikra na kitangulizi. Na hata maandalizi ya awali yaweje, kitu kikubwa ni kitendo chenyewe.” Kinyume chake, umuhimu wa fikra na nia sio mdogo kama ule wa kitendo. Namna hiyo ya kufikiria ambayo hudumisha ubora wa kitendo kuliko ubora wa nia na imani, ni fikra ya kiyakinifu. Chini ya majina: “busara” na “unafsi” huifanya imani na nia nyuma ya 73

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini kitendo kuwa thamani ya kitangulizi na sio zaidi. Tukiachilia mbali ukweli kwamba ubatili wa madhehebu hii uko wazi katika haki yake yenyewe, chenye uhakika ni kuwa mafundisho ya Qur’ani hayawezi kutafsiriwa juu ya misingi ya njia kama hizo za kufikira. Kwa mtazamo wa Qur’ani haiba yetu ya kweli na nafsi ni roho. Katika kila tendo la hiari, roho husogea kutoka kwenye uwezekano kwenda kwenye uhalisia na hupata athari na sifa inayolingana na nia na lengo lake. Athari hizi na tabia huwa sehemu ya haiba yetu na hutupeleka katika ulimwengu unaoafikiana nazo kutoka miongoni mwa nyanja za uhai. Hivyo, kutokana na kipimo cha kwanza, wema na uovu wa matendo hutegemea athari za nje za matendo hayo; na kutokana na kutoka kipimo cha pili, wema na uovu hutegemea ni kwa namna gani mtendaji alitenda kitendo hicho. Katika hali ya kwanza, msimamo wetu juu ya kitendo umejengwa juu ya athari zake za nje na matokeo ya kijamii; na katika hali ya pili msingi wake uko juu ya athari za ndani na za kifikra za kitendo juu ya mtendaji wake. Ikiwa mtu atajenga hospitali au atafanya kitendo kingine cha ukarimu katika kuhusiana na mambo ya kiutamaduni, afya au uchumi wa taifa, bila shaka, kwa mtazamo wa kijamii na wa kihistoria, kitendo hicho ni kizuri. Yaani, ni kitendo ambacho huwanufaisha viumbe wa Mwenyezi Mungu. Katika hili, haidhuru ni nini ilikuwa nia ya mtu yule aliyejenga hospitali au taasisi nyingine ya kihisani. Ikiwa nia ilikuwa kujionyesha na kuziridhisha silika zake binafsi, au ikiwa nia ilikuwa ni ubinadamu na uungwana, kwa mtazamo wa kijamii, taasisi ya kusaidia wenye shida tayari imeshajengwa. Uamuzi wa kihistoria kuhusiana na matendo ya watu siku zote unatoka kwenye kipengele hiki na katika mtazamo wa kipimo hiki mahususi. Historia haina haja na nia za watu. Wakati kazi bora za sanaa na ufundi ujenzi za Isfahan zinapotajwa, hakuna mwenye shida ya kujua nia au lengo la mjenzi wa Msikiti wa Sheikh Lutfullah, Msikiti wa Shah au daraja liitwalo Thelathini na Tatu; historia huangalia sura ya nje na hukiita kitendo 74

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini hicho “tendo jema.� Hata hivyo tunapohakiki wema unaohusiana na mtendaji uangalifu wetu hauendi kwenye manufaa ya nje au ya kijamii ya tendo. Badala yake tunaangalia ni jinsi gani kitendo kinahusiana na mtendaji. Kwa hesabu hizi, haitoshi kwa kitendo kuwa na manufaa ili kihesabike kuwa tendo jema. Kinachozingatiwa ni, je, nini ilikuwa nia ya mtendaji wakati wa kutenda tendo husika na alikuwa anataka kupata maslahi gani. Ikiwa mtendaji wa tendo jema alikuwa na nia njema, na alifanya kitendo hicho kwa matarajio mema na kitendo ni kizuri, yaani kina wema unaohusiana na mtendaji. Kitendo chenyewe ni sura mbili; yaani huendelea katika sura mbili: sura ya kihistoria na kijamii, na sura ya kiroho. Lakini kama mtendaji alitenda ili kujionyesha au kuvutia maslahi ya kiyakinifu, basi kitendo hicho kitakuwa na kipimo kimoja. Kinakwenda mbele tu katika wakati na historia, na sio katika kipimo cha kiroho; na katika istilahi ya Kiislamu, kitendo hicho hakipandi kwenye uwanja wa juu. Kwa maneno mengine, katika hali kama hiyo, mtendaji atakuwa ameitumikia jamii na kunyanyua viwango vyake lakini hakunufaika, na kwa hakika inaweza kuwa ametenda uovu. Badala ya kupanda kiroho kwa kufanya kitendo hicho, nafsi ya mtendaji yaweza kuwa imeshuka kwenye kiwango cha chini kiroho. Kwa hakika, dhamira yetu sio kwamba wema unaohusiana na kitendo, wa kitendo chenyewe umetenganishwa kabisa na wema unaohusiana na mtendaji, na kwamba kwa mtazamo wa kiroho mtu hana cha kufanya kwa matendo ambayo ni yenye faida kwa jamii. Dhamira ni kwamba kitendo kinachonufaisha jamii, ni chenye manufaa tu kiroho iwapo wakati wa kufanya kitendo hicho roho halikadhalika imesafiri katika njia ya kiroho, huku ikiwa imekiacha kituo cha ubinafsi na utafutaji wa starehe na kuweka mguu kwenye kituo cha unyofu na utakaso. Uhusiano wa wema unaotakana na kitendo na wema unaotokana na mtendaji ni uhusiano wa mwili na roho. Kiumbe hai ni muunganiko wa mwili na roho. Halikadhalika, aina ya pili ya wema lazima ipuliziwe katika mwili 75

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini wa kitendo chenye aina ya kwanza ya wema kwa ajili ya kitendo hicho kuwa hai. Hivyo, uthibitisho wa kimantiki wa wanaojiita wasomi ni wa kimakosa. Uthibitisho huu hueleza kwamba: “Uhusiano wa Mwenyezi Mungu na viumbe wake wote ni sawa, na wema au uovu wa vitendo umo ndani ya vitendo vyenyewe. Hivyo matendo mema yako sawa kwa watu wote. Na matokeo ya usawa huu ni kuwa huko akhera, malipo ya waumini na wasiokuwa waumini yatakuwa sawa.” Kwa hoja hii, matendo na usawa wa viumbe mbele ya Muumba vimezingatiwa, lakini mtendaji na haiba yake, lengo, nia na njia ya kiroho – vyote ambavyo kwa kujuzisha husababisha matendo yasifanane na kusababisha tofauti baina yao, kama tofauti ya aliyehai na mfu – yamesahauliwa kabisa. Wanasema kuna tofauti gani kwa Mwenyezi Mungu ikiwa mtendaji wa tendo njema anamtambua Mwenyezi Mungu au hamtambui? Ikiwa alifanya kitendo hicho kwa kumridhisha Mwenyezi Mungu au la kwa Mwenyezi Mungu kuna tofauti gani? Jibu ni kuwa, haina tofauti yoyote kwa Mwenyezi Mungu, lakini huweka tofauti kwa mtu (mtendaji) mwenyewe. Ikiwa mtu hamtambui Mwenyezi Mungu, kitendo chake kitakuwa na upande mmoja wa kiroho, na ikiwa anamtambua Mwenyezi Mungu, tendo lake litakuwa na pande mbili. Ikiwa mtu hamtambui Mwenyezi Mungu tendo litakuwa na upande mmoja, tendo litakuwa na wema wa kihistoria. Lakini kama mtu anamjua Mwenyezi Mungu, tendo lake litakuwa na pande mbili, na litakuwa pia na wema unaotokana na mtendaji na wema wa kiroho. Ikiwa mtu anamjua Mwenyezi Mungu tendo lake litapanda juu kwa Mungu na ikiwa mtu hamjui Mungu tendo hilo halitapanda, kwa maneno mengine, kwa Mwenyezi Mungu hayaleti tofauti yoyote, ila tofauti iko kwenye kitendo. Kwa mmoja tendo litakuwa hai, likipanda juu, na katika mtu mwingine, tendo litakuwa limekufa, likishuka chini. Wanasema kuwa Mwenyezi Mungu, ambaye ni Mwenye Hikma na Muadilifu, bila shaka hawezi kubatilisha matendo mema ya mtu kwa 76

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini sababu ya kutokuwa na uhusiano Naye. Sisi pia tunaamini kuwa Mwenyezi Mungu hawezi kubatilisha matendo yao. Lakini lazima tuangalie kama kweli mtu ambaye hamtambui Mwenyezi Mungu hufanya kitendo kizuri ambacho kina pande zote mbili, upande wa athari zake, na upande wa uhusiano wake na mtendaji wake, kizuri kwa mtazamo wa kijamii na vile vile kizuri kwa mtazamo wa kiroho kwa mtendaji. Ubovu wa hoja hii unatokana na sisi kuchukulia kuwa kwa kitendo kuwa na maslahi kwa jamii basi inatosha kukiita kitendo hicho ‘tendo jema.’ Tukijaalia lisilowezekana, kuwa ikiwa mtu hamjui Mungu na bado akapanda kwa Mwenyezi kupitia matendo yake, basi bila shaka Mwenyezi Mungu hawezi kumrudisha. Lakini uhalisia ni kuwa mtu asiyemjua Mwenyezi Mungu huwa hawezi kupenya pazia na kuingia ufalme wa kiroho, hasafiri kutoka kituo chochote cha kiroho kuelekea cha juu yake, na hapandi kuelekea kwenye ufalme wa kiroho wa Mungu ili matendo yake yaweze kupata umbo na sura ya kiroho ambayo itakuwa chanzo cha faraha, mafanikio na wokovu wake. Kukubaliwa kwa kitendo na Mungu hilo si lolote zaidi ya kitendo kuwa na sifa hizi. Moja ya tofauti za msingi kati ya Sheria za Mwenyezi Mungu na zile zilizotungwa na binadamu ni nukta hii; sheria za Mwenyezi Mungu zina pande mbili na zile zinazotungwa na binadamu zina pande moja. Sheria za kibinadamu hazina lolote juu maisha au maendeleo ya kiroho ya mtu. Serikali inapoweka sheria ya kodi kwa maslahi ya nchi, lengo lake huwa ni kupata fedha za kugharamia matumizi ya nchi. Serikali haishughulishwi na nia za walipa kodi, je wanalipa kwa mapenzi ya nchi na serikali yao au kwa sababu ya uwoga? Nia ya serikali ni kupata fedha tu hata kama mlipa kodi atakuwa akiilaumu serikali kimoyomoyo, haijalishi ili mradi lengo la serikali limeshatimia. Halikadhalika serikali inapoyaita majeshi yake kulinda nchi, haishughulishwi na nia za askari; inataka askari wapigane na adui yake vitani. Haijalishi kwa serikali ikiwa askari atapigana kwa hiari yake au kwa 77

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini sababu ya uwoga wa bunduki, au ikiwa kupigana kwake ni kwa kujionyesha, kutokana na upumbavu wake, au anapigania ukweli na haki. Lakini sheria za Mwenyezi Mungu haziko hivyo. Katika sheria hizi, kinachotakiwa sio fedha na wapiganaji tu, lakini pia nia safi na hitajio la kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu. Uislamu hutaka matendo yenye roho, sio matendo yasiyo na roho. Hivyo Mwislamu akilipa zaka, lakini kwa kujionyesha, haitakubalika. Sheria za Mwenyezi Mungu zinasema kuwa askari aliyelazimishwa hana manufaa yoyote; Ninataka askari mwenye roho ya uaskari, aliyeukubali wito:

“Kwa hakika Mwenyezi Mungu amenunua roho na mali za waumini ili awalipe pepo.” Qur’ani Tukufu 9:111 Imesimuliwa kutoka kwa mtukufu Mtume wa Uislamu (saw) katika hadithi iliyosimuliwa kwa mfululizo miongoni mwa wote, Masunni na Mashia ambayo inasema: “Thamani ya matendo inategemea nia.” “Kila mtu atalipwa kwa kile alichokikusudia.” “Hakuna tendo litakayokubaliwa bila nia.” 27 Hadith nyingine imesimuliwa kwa maneno yafuatayo: “Thamani ya matendo iko kwenye nia zake, na mtu atalipwa kile tu alichokusudia. Hivyo yeyote aliyehijiri (hama) kwa ajili Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, kuhama kwake kutakuwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, na yeyote aliyehama kwa ajili ya mali za kidunia au kwa ajili ya mwanamke anayetaka kumuoa, basi kuhajiri kwake (malipo yake) kutakiendea kitu hicho.” 28 27 Hii na mbili za mwanzo ziko katika Wasailush Shia Juz. 1, uk. 8 28 Sahih Muslim, Juz. 6, uk. 48 78

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini Imam Jafar as-Sadiq (a.s) alisema, “Tendeni matendo yenu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na sio kwa ajili ya watu, kwa sababu chochote kilichofanywa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, hupanda (huenda) Kwake, na chochote ambacho ni kwa ajili ya watu hakiendi kwa Mwenyezi Mungu. Nia ni roho ya kitendo, na kama ilivyo kwa mwili wa mwanadamu kwamba ni mtukufu kwa sababu ya roho ya binadamu, halikadhalika utukufu wa kitendo cha mwanaadamu hutegemea roho yake. Ni nini roho ya kitendo? Roho ya kitendo ni ikhlasi. Qur’ani Tukufu inasema:

“Na hawakuamrishwa isipokuwa kumuabudu Mwenyezi Mungu, wakiielekeza imani yao yote Kwake.” Qur’ani Tukufu, 98:5

UBORA AU WINGI? Kutokana na majadiliano hayo hapo juu, hitimisho la kuvutia laweza kupatikana ambalo ni kwamba kwa hesabu za Mwenyezi Mungu, thamani ya matendo ni ubora wake na sio wingi wake. Kutozingatia nukta hii kumewafanya baadhi ya watu kuleta visa vya ajabu kuhusiana na manufaa makubwa yasiyo ya kawaida ya matendo ya watu watukufu, wakati wanapoona mwelekeo wa kijamii wa matendo hayo kuwa hayakuwa na thamani yoyote. Kwa mfano, kuhusiana na pete ambayo Imam Ali ibn Abi Talib alimpa muombaji yeye Imam Ali alipokuwa katika rukuu, ambapo Aya ya Qur’ani iliteremka kusifia kitendo hiki, baadhi ya watu wanasema thamani ya pete ile ilikuwa sawa na kodi ya Syria yote. Ili watu waiamini, waliitungia hadith. Kwa mtazamo wa watu hawa, ilikuwa vigumu kuamini kuwa aya tukufu ya Qur’ani ingeteremshwa kwa sababu ya kutoa pete isiyokuwa na thamani. Na kwa sababu hawakuweza kuamini jambo hili, waliunda hadith 79

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini na wakapandisha thamani ya pete (bei yake). Hawakuweza kufikiri kuwa pete yenye thamani ya kodi ya nchi yote ya Syria isingeweza kukutwa kwenye kidole cha Imam Ali bin Abi Talib (a.s). Tujaalia kwamba Imam Ali (a.s) alikuwa na pete yenye thamani kama hiyo kwenye miliki yake, asingeitoa tu kwa ombaomba mmoja; badala yake, kwa pete hiyo angeifanya Madina kustawi na kukidhi mahitaji yote ya mjini hapo – Madina. Akili za watu hawa wanaobuni mambo ya ajabu hazijajua kuwa kwa Mwenyezi Mungu kitendo kikubwa kina hesabu tofauti na ile ya hesabu ya vitu vya kidunia. Inakuwa kana kwamba wanaona kuwa ukubwa wa thamani ya pete ya Ali ibn Abi Talib (a.s) ndio uliomvutia Mwenyezi Mungu na kulazimika kumsifu Ali ibn Abi Talib (a.s) kwa ukubwa wa kitendo alichokifanya, Mwenyezi Mungu ameepukana na hilo! Sifahamu ni kitu gani walichofikiria watu hawa wenye mtazamo mfupi juu ya vipande vya mkate ambavyo Ali ibn Abi Talib (a.s) na familia yake walitoa kuwapa maskini kama sadaka na hivyo kupelekea kushuka kwa Sura ‘Hal Ata.’29 Bila shaka watasema unga wa mikate ile haukuwa shayiri (jamii ya ngano) bali umetokana na vumbi la dhahabu. Lakini kwa kweli hivyo sivyo hali ilivyo. Umuhimu wa kitendo cha Ali ibn Abi Talib (a.s) na familia yake sio katika mwelekeo wa kiulimwengu ambao unavutia nadhdari yetu; umuhimu wa kitendo chao ni kwamba kilikuwa safi na kwa ajili ya Mwenyezi Mungu tu; kilikuwa katika kiwango cha unyofu ambao uko nje ya mipaka yetu hata kuweza kutambuliwa na sisi, unyofu ambao uliakisiwa katika upeo wa juu kabisa na sifa na utukuzaji wa ki-mbingu wenye mvuto. Kwa maneno ya Sheikh Fariud Din al-Attar:

29 Suratul Dahr - vilevile hujulikana kama Suratul Insan 80

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini “Ni nje [ya uwezo] wa dunia hii kuelezea mkuki wake, ni nje ya uwezo wa dunia ile kuelezea vipande vyake vitatu vya mkate.” Umuhimu wa kitendo chao upo katika kauli yao ambayo Qur’ani imeunukuu:

“Tunawalisha kutaka radhi za Mwenyezi Mungu tu; hatutaki kutoka kwenu malipo wala shukrani.” Qur’ani, 76:9 Haya ni maneno kutoka mioyoni mwao ambayo Mwenyezi Mungu, Mjuzi, Amefanya yajulikane; yaani, bila ubinafsi wowote na kujitoa muhanga, hawakutamani chochote kutoka kwa Mwenyezi Mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu Mwenyewe. Ukweli kwamba Qur’ani inaziona amali za wasioamini kama mazigazi yasiyo na kitu ndani, na yasiyo na uhalisia, ni kwa sababu matendo yao yana mapambo ya nje yanayopotosha, lakini kwa vile yamefanywa kwa maslahi binafsi na si kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, hivyo hayana mwelekeo wa kiroho. Zubayda, mke wa Khalifa wa ukoo wa Bani Abbas, Harun Rashid, kwa juhudi zake alisababisha mto kuchimbwa katika mji wa Makka ambao umekuwa ukitumiwa na wageni wa Mwenyezi Mungu toka enzi hizo mpaka leo. Tendo hili linaonekana ni la wema sana kwa nje. Uamuzi wa Zubaydah ulifanya mto huu utiririke katika mji wa Makka uliokuwa jangwa kutoka katika sehemu yenye majabari (miamba) mingi, sehemu iliyo katikati ya Ta’if na Makka, na umekuwa ukitumiwa na mahujaji wenye kiu kwa takriban karne kumi na mbili sasa.

81

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini Kwa mtazamo wa kidunia, hili ni tendo kubwa kabisa, lakini vipi kwa mtazamo wa kiroho? Je malaika wanalihesabu tendo hilo kama tunavyoliheshabu sisi? Je mazingatio yao ni kama yetu, yanavutika tu kwenye ukubwa dhahiri wa tendo hili? Hapana, hesabu yao ni tofauti. Kwa kutumia mizani wa Ki-Mungu wanapima pande nyingine za kitendo hicho. Hutilia maanani ni wapi Zubayda alipata fedha hizi za kufanyia kitendo hiki. Zubaydah alikuwa mke wa mtu dhulumati, mkandamizaji aliyekuwa anamiliki hazina ya Umma wa Waislamu na alikuwa na uwezo wa kufanya apendavyo. Zubaidah hakuwa na fedha zake mwenyewe, na hakutumia fedha zake mwenyewe katika kitendo hiki cha ukarimu; alitumia fedha za watu kwa ajili ya watu. Tofauti yake yeye na wanawake wengine waliokuwa na nafasi kama yake ni kuwa wengine walikuwa wakitumia mali ya umma kwa matamanio yao wenyewe tu, na yeye alitumia sehemu ya fedha hizi za Umma kwa manufaa ya Umma. Sasa ni nini yalikuwa malengo ya Zubaidah katika kitendo hiki? Je alitaka jina lake libaki katika historia? Au alikuwa anataka radhi za Mwenyezi Mungu? Ni Mwenyezi Mungu tu ndiye anayejua. Ni kutokana na kukosea mahesabu ya mwelekeo huku, kwamba inasemekana kuwa mtu mmoja alimuona Zubaidah ndotoni na akamuuliza kuwa Mwenyezi Mungu amemlipa nini kutokana na mto aliochimbisha. Alimjibu kuwa malipo yote ya kitendo kile yamekwenda kwa wamiliki halisi wa fedha zile (walipa kodi).

MSIKITI WA BAHLUL Inasemekana kuwa kuna wakati msikiti ulikuwa unajengwa, kisha Bahlul akafika na kuuliza, ‘Mnafanya nini?” wakajibu: “Tunajenga msikiti.” Bahlul akauliza: “wa nini?” Wakamjibu: “swali gani hilo? Tunajenga msik82

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini iti kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.” Bahlul alitaka kuwaonyesha watendaji wa kitendo hiki chema kiwango chao cha unyofu. Kwa siri, alikuwa na jiwe liliochongwa maneno ‘Msikiti wa Bahlul,’ na usiku alilifunga juu ya geti la msikiti. Wajenzi wa msikiti walipokuja walikasirika. Walimfuata Bahlul na kumpiga kwa kujimilikisha kitu walichokihangaikia wengine. Bahlul alijibu; “Lakini hamkusema kuwa mnajenga msikiti kwa ajili ya Mwenyezi Mungu? Tuchukulie kwamba watu kwa makosa wanafikiri mimi ndiye niliyejenga, Mwenyezi Mungu hawezi kufanya kosa hilo (la kunilipa mimi thawabu badala yenu)!” Kuna matendo mangapi makubwa yanayoonekana ni makubwa machoni mwetu lakini kwa Mwenyezi Mungu hayana thamani yoyote! Labda majumba mengi makubwa iwe misikiti, makaburi makubwa, mahospitali madaraja, majumba ya kupumzikia wageni, au mashule yanaonekana hivyo, hesabu za vitu hivyo iko kwa Mwenyezi Mungu.

IMANI JUU YA MWENYEZI MUNGU NA AKHERA. Uhusianao wa dunia hii na Akhera ni sawa na uhusiano wa mwili na roho, au uhusiano wa sura ya nje na sura ya ndani. Dunia hii na ijayo (akhera) sio dunia mbili tofauti kabisa, dunia hii na Akhera ni kitu kimoja, kama ilivyo kwa karatasi au shilingi kuwa na pande mbili. Dunia hii hii tuliyonayo hapa ulimwenguni inaonekana huko Akhera katika sura ya ulimwengu mwingine. Mimea na vitu vya dunia hii vitaonekana huko Akhera katika sura ya ulimwengu mwingine. Kimsingi Akhera ni Muundo wa ki-mbingu au malakut wa ulimwengu huu uliopo. Sharti la kitendo kupata mwelekeo mzuri wa huo ulimwengu mwingine ni kufanywa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na ili kiweze kupanda juu katika ufalme wa Mwenyezi Mungu. Ikiwa mtu haamini juu ya Mwenyezi 83

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini Mungu, na hana mazingatio juu ya Mungu, kitendo chake hakitakuwa na mwelekeo wa ulimwengu mwingine na hivyo hakitapanda katika ufalme wa juu. Mwelekeo wa ulimwengu wa Akhera ni wa juu zaidi, na mwelekeo wa ulimwengu huu ni wa chini. Maadamu kitendo hakipati mwanga na usafi kupitia nia, imani na kuamini, hakiwezi kufikia kwenye ufalme wa juu zaidi; ni kitendo tu chenye roho ndicho kinachoweza kufikia kituo hicho. Na roho ya kitendo ni mwelekeo wake wa ulimwengu mwingine. Kwa maneno mazuri, Qur,an inasema:

“Kwake hupanda maneno safi, na Yeye huzipandisha amali njema.” Qur’ani Tukufu 35:10 Aya hii inaweza kueleweka kwa namna mbili, na zote zimeelezwa katika vitabu vya ufafanuzi wa Qur’ani. Ya kwanza ni kuwa tendo njema huleta maneno safi na imani safi na nyingine ni kuwa maneno safi na imani safi huleta matendo mema na kuyafanya kuwa na sura ya kiakhera. Maelezo haya ya namna mbili ambayo yote ni sahihi, ambayo pia inawezekana yote yamekusudiwa – kwa pamoja yanatujulisha kanuni kwamba ina athari katika kukubaliwa au kukataliwa kwa kitendo na kupanda kwake kwa Mwenyezi Mungu, na matendo yana athari katika kuikamilisha imani na katika kuongeza kiwango cha imani. Kanuni hii inakubalika katika mafundisho ya Kiislamu. Rejea yetu katika aya hii inategemea maelezo ya pili, ingawa kama tulivyoonyesha, kwa mtazamo wetu inawezekana kuwa Aya hii imekusudia maana zote mbili kwa wakati mmoja. Kwa vyovyote vile ni makosa kwetu kufikiri kuwa matendo ya wale ambao hawamwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Hukumu yatapanda juu na kupata mwelekeo wa dunia nyingine. Kama tukiambiwa kuwa mtu fulani amechukua ile barabara kuu ya kuelekea kaskazini kutokea Tehran, na akaendelea kusafiri kuelekea 84

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini kaskazini kwa siku kadhaa, ni dhahiri kuwa hatutatarajia mtu huyu afike Qum, Isfahan au Shiraz (miji ambayo iko kusini mwa Tehran); ikiwa mtu atashikilia uwezekano huo tutamcheka na kumwambia kuwa ikiwa mtu huyo alitaka kwenda katika moja ya miji hii, angechukua barabara inayoelekea kusini kutokea Tehran na kutembea juu yake. Haiwezekani mtu asafiri kuelekea Uturuki na bado afike kwenye Ka’aba. Pepo na Moto ni vituo vya mwisho vya safari ya mtu kiroho. Huko Akhera kila mtu hujiona katika kituo chake cha mwisho, mwingine juu, mwingine chini, mwingine juu zaidi kuliko wote na wengine chini zaidi kuliko wote.

“Sivyo hakika kumbu kumbu (maandishi) ya watu wema ipo katika Illiyin (mahala patukufu). Qur’ani Tukufu, 83:18

“Sivyo hakika kumbu kumbu ya waovu ipo katika sijjin (gereza).” Qur’ani Tukufu, 83:7 Inawezekana vipi mtu asafiri kuelekea kituo fulani au asafiri kuelekea njia ya kinyume nacho, na bado afike kituo hicho? Kwenda kuelekea mbigu (Pepo) ya juu zaidi (Illiyyin) huhitaji nia na hamu ya kufika huko, na huhitaji utambuzi na imani katika upande mmoja, unyenyekevu na urahisishaji kwa upande mwingine. Kama mtu hana imani juu ya mashukio kwenye kituo hicho, au hana sifa za urahisishaji na unyenyekevu, na kwa ufupi hana haja wala hachukui hatua hata ile ndogo ya kufika kwenye kituo hicho, vipi mtu atamtarajia mtu huyo kufikia kituo hicho? Bila shaka, kila njia huelekea kwenye kituo chake, na ni mpaka Mungu awe ndio kituo

85

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini hicho, vinginevyo njia hiyo haiwezi kumuelekeza kwa Mungu. Qur’ani inasema:

“Anayetaka ya upesi upesi (dunia) tutamharakishia humo tunayoyataka kwa tunayemtaka; kisha tunamwekea Jahannam; ataiingia hali ya kuwa ni mwenye kulaumiwa mwenye kufurushwa. Na mwenye kutaka ya mwisho (Akhera) na akayahangaikia kwa mahangaikio yake huku akiwa ni mumin, basi hao mahangaikio yao yatakuwa ni yenye kushukuriwa.” Qur’ani Tukufu, 17:18-19 Hii ni kuwa, ikiwa mtu uwezo wake wa kufikiri sio zaidi ya dunia hii, au hana lengo jingine zaidi ya ulimwengu huu, haiwezekani kwa mtu huyu kulifikia lengo la juu la Akhera; lakini Rehema na Ukarimu Wetu wa KiMungu unataka kuwa tumpe kitu fulani cha malengo ya kidunia anachotaka kukipata. Kuna nukta ya kutatiza hapa, ulimwengu huu ni ulimwengu wa kimaada ni ulimwengu wa visababishi na sababu. Visababishi vya kidunia vinakinzana, na vikwazo pia vipo katika ulimwengu huu wa kimaada. Hivyo kwa mtu ambaye lengo lake ni dunia hii, hakuna uhakikisho kuwa lengo lake litatimia. Maneno ambayo Qur’ani imeyachagua kuelezea nukta hii ni kuwa: “Tutamharakishia humo tunayoyataka kwa tunayemtaka.” Lakini, yule mwenye malengo makubwa katika safari yake ya kiroho, hauelekezi moyo wake wote katika malengo yasiyo na thamani, na ambaye 86

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini hukuza imani yake, anapiga hatua kumwelekea Mwenyezi Mungu, bila shaka atalifikia lengo lake kwani Mwenyezi Mungu anatambua thamani ya tendo njema, huyakubali matendo nema yanayowasilishwa mbele Yake na hutoa malipo yake. Hapa jitihada na bidii ni muhimu, kwani haiwezekani kwa mtu kwenda mbele na kufikia lengo bila kuchukua hatua. Kisha katika aya inayofuata, Qur’ani inasema

“Wote hao tunawasaidia, hawa na hao, katika kipawa cha Mola wako; na kipawa cha Mola wako hakizuiliki kumfikia mja wake.” Qur’ani Tukufu, 17:20 Hii ni kuwa, rehema Zetu hazina mipaka, yeyote anayepanda mbegu, tunaifanya izae matunda; yeyote anayeliendea lengo, tunamsaidia kuliendea lengo hilo. Watu watukufu wenye hekima wanasema kwamba Mwenyezi Mungu ambaye kwa kila hali yupo, kimsingi ni Mwenye kuwepo kutoka mielekeo yote na pande zote. Hivyo, alikulihali ni Mwenye Neema (Fayyadh). Kwa ajili hiyo, yeyote anayetaka kitu fulani, Mwenyezi Mungu humsaidia. Sio suala la kwamba mtu akitaka ya dunia, Mwenyezi Mungu humwambia “Umepotoka na umekwenda kinyume na mwongozo wetu na maelekezo, hivyo Hatutakusaidia.” Hivi sivyo hali ilivyo. Anayeitaka dunia pia husaidiwa na Mwenyezi Mungu katika kutafuta dunia hii na faida zake, kutokana na rehema Zake zisizokwisha, ndani ya mipaka iliyoruhusiwa na ulimwengu huu wa visababishi, upekee wa pande mbili na matokeo yanayokinzana.

87

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini Kwa maneno mengine, ulimwengu huu ni sehemu muafaka kwa kupanda, kukuza, kuongeza, na kuvuna. Inategemeana na mbegu gani mtu anachagua kupanda, kuikuza na ni nini anataka kuvuna. Mbegu yoyote atakayoipanda ndiyo itakayoota na kukua katika ardhi ya ulimwengu huu yenye rutuba. Ni kweli kuwa kuna msaada wa kipekee, maalumu tu kwa watu wa haki, unaitwa neema ya rahimiyya (ya kipekee), wanaoitaka dunia hii wamenyimwa neema hii, kwa sababu hawaitafuti. Lakini rahmaniyyah – rehema ya jumla ya Mwenyezi Mungu huwaendea watu wote na katika njia zote. Katika maneno ya Sa’di anasema: “Uso wa dunia ni meza Yake, ilozunguka vyote. Meza ambayo kwayo hushiriki wote, iwe rafiki au adui.” Kutokana na yaliyosemwa katika mjadala huu, sehemu ya masuala yanayochunguzwa imeshajibiwa. Tumeweka wazi kwamba wema unachohusiana na kitendo hautoshi kwa malipo katika ulimwengu ujao – Akhera; wema unaohusika na mtendaji ni muhimu vile vile. Wema unaotokana na kitendo ni kama mwili, na wema unaotokana na mtendaji ni kama roho na uhai wa kitendo hicho. Na tumeelezea kuwa kumwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya mwisho ni sharti la msingi la wema unaotokana na mtendaji. Hali hii Shurtishi haisimamii kwenye makubaliano ya watu, bali ni hali muhimu ya asili na ya kweli, kama ilivyo kwa hali ya kimasharti ya njia makhususi kuhusiana na nia ya kufika kituo makhususi. Hapa ni muhimu kufafanua nukta moja, ambayo ni kwamba baadhi ya watu pengine watasema kwamba wema unahusika na mtendaji sio lazima uwe na nia ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu; ikiwa mtu atafanya wema kwa sababu ya dhamiri yake au huruma au upendo, hiyo inatosheleza kwa kitendo chake kuwa na wema unaohusika na mtendaji. Kwa maneno mengine sababu ya kibinadamu inatosheleza kutimiza sharti 88

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini la wema unaohusiana na mtendaji maadamu mtendaji hakuwa na maslahi binafsi, hapa wema unaotokana na mtendaji upo, haijalishi kuwa lengo ni “Mungu” au “ubinadamu.” Nukta hii ni inafaa kuangaliwa. Wakati hatuungi mkono ule mtazamo kuwa hakuna tofauti ikiwa nia ni Mungu au ubinadamu, na hatuwezi kuingia katika majadiliano ya kina kwa sasa, lakini kwa kweli tunaamini kuwa wakati wowote kitendo kinapofanywa kwa nia ya kutenda wema, kuwatumikia wengine, na kwa ajili ya ubinadamu, sio sawa na kitendo kinachofanywa kwa sababu ya ubinafsi hasa. Bila shaka, Mwenyezi Mungu hawezi kuwaacha watu hawa bila malipo. Hadith mbali mbali zinaonyesha kwamba kwa ajili ya matendo yao mema waliyoyafanya, washirikina kama Hatam al-Tai hawataadhibiwa au adhabu ya watu hao itapunguzwa, japokuwa walikuwa washirikina. Tunaweza kuelewa nukta hii kutokana na hadith nyingi ambazo tunazo mbele yetu: 1. Allamah Majlis ananukuu kutoka katika kitabu Thawabul A’mal cha Sheikh Saduq kuwa Ali ibn Yaqtin amesimulia kutoka kwa Imamu Musa ibn Ja’far al-Kadhin (a.s) kuwa amesema: “Miongoni mwa Banu Israeli kulikuwa na muumini ambaye jirani yake alikuwa sio muumini. Yule mtu ambaye hakuwa muumini alikuwa mara zote akionyesha upole na tabia njema kwa jirani yake muumini. Huyu asiyekuwa mumini alipokufa Mwenyezi Munu alimtengenezea nyumba kutokana na aina ya tope ambayo ilimkinga kutokana na joto la moto, na riziki yake ilikuwa akipeewa kutoka nje ya mazingira yake ambayo yalikuwa ni ya moto. Akiambiwa “Hii ni kwa sababu ya upole na wema wako kwa jirani yako aliyeamini.”30 Allamah Majlis baada ya kunukuu hadith hii, anasema: “Hadith hii na nyinginezo kama hii ni ushahidi kuwa adhabu ya baadhi ya makafiri itaon30 Biharul Anwar, Juz. 3, uk. 377 89

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini dolewa, na aya za Qur’ani zinazosema kuwa adhabu ya makafiri haitapunguzwa inawahusu wale ambao hawakutenda wema wowote. 2. Pia anasimulia kutoka kwa Imam Muhammad ibn Ali al-Baqir (a.s) kuwa amesema, “Kuna muumini aliyeishi katika nchi ambayo mfalme wake alikuwa mkandamizaji. Yule mfalme alimtishia huyu muumini, na hivyo yule muumini alikimbilia nchi isiyo ya Kiislamu, na alifikia kwa mshirikina. Mshirikina alimuweka pembeni yake na akamhudumia vizuri sana. Yule mshirikina alipokufa, Mwenyezi Mungu alimwambia, “Ninaapa kwa Heshima na Utukufu Wangu kuwa kama peponi kungekuwa na sehemu ya washirikina ningekuweka huko, lakini ewe moto, muogopeshe lakini usimdhuru.” 65 Kisha Imam alisema, “Kila asubuhi na jioni alikuwa akiletewa riziki yake kutoka nje ya mazingira yale.” Imam aliulizwa, ‘Je ni kutoka Peponi?’ Yeye akajibu, “Kutoka anakopenda Mwenyezi Mungu.” 3. Mtukufu Mtume (s.a.w.w) alisema juu ya Abdillah ibn Jud’an ambaye alikuwa miongoni mwa makafiri waliofahamika sana katika enzi za ujinga na mmoja wa machifu wa Kiquraishi kuwa, “Mwenye adhabu nyepesi kabisa katika Moto (Jahanamu) ni ibn Jud’an.” Aliulizwa kwa nini, akajibu: ‘Alikuwa akiwalisha watu.’” 4. Kwa nyongeza, Mtume Muhammad (s.a.w.w) alisema juu ya watu mbali mbali walioishi enzi za ujinga, “Niliwaona motoni mmiliki wa kanzu fupi na mtu mwenye fimbo aliyekuwa akiwafukuza mahujaji, na mwanamke aliyekuwa na paka aliyemfungia ndani na akawa hamlishi wala kumwachilia ili ajitafutie chakula chake. Nilipoingia Peponi nilimkuta mtu aliyemuokoa mbwa aliyekuwa na kiu kwa kumpa maji.”31 Watu hawa ambao wapo katika kila zama, watapunguziwa adhabu yao au adhabu yao itaondolewa kabisa. Kwa maoni yangu, kama kuna watu wanaowafanyia wema watu wengine au hata viumbe wengine wawe – binadamu au mnyama bila matarajio yoy31 Biharul Anwar, Juz. 3, uk. 382 90

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini ote, sio hata kwa sababu wao wenyewe wanajiona katika ulimwengu wa wanyonge (yaani, kuogopa kuwa siku moja, wanaweza kuwa katika shida hiyo, sio kipengele kinachovutia katika wanachokifanya), na baadala yake nia ya kufanya wema na kuhudumia wengine ni kubwa kiasi cha kuwa japo wanajua kuwa hawatafadika kwa lolote na hata kama hakuna mtu atakayejua walichofanya au kusema (kwa kuwaombea) hata angalau “Mungu awabariki,� na bado wanaendelea kufanya matendo mema, na hawajaathiriwa na tabia na vitu kama hivi. Mtu lazima aseme kwamba ndani kabisa ya dhamiri zao kuna nuru ya kumtambua Mungu. Na ikiwa wanaikana kwa ndimi zao, wanakiri ndani ya dhamiri zao; kukataa kwao ni katika ukweli wa kukataa kwa kiumbe wa kufikirika ambayo waliyatambua kama badala ya Mungu, au ni kukikana kitu kingine walichokiwazia badala ya kurejea kwaMwenyezi Mungu na Siku ya Hukumu, sio kuukana uhalisia wa Mwenyezi Mungu na Siku ya Ufufuo. Kupenda wema na haki na kufanya wema kwa sababu ni mzuri na haki na unafaa, bila kigezo kingine chochote, ni alama ya upendo wa ile Asili iliyotawaliwa ya Uzuri Halisi; kwa hiyo, hakuna mushkili kwamba watu kama hawa kwa hakika hawatafufuliwa miongoni mwa makafiri ingawa kwa ndimi zao wanachukuliwa kama waliokana. Na Mwenyezi Mungu anajua zaidi.

IMANI JUU YA UTUME NA UIMAMU. Sasa tutajadili upande mwingine wa suala hili, ambao ni nafasi ya wale wasiokuwa Waislamu lakini wanaamini kuwa Mungu ni Mmoja na wanaamini juu ya Siku ya Mwisho na wanafanya matendo yao kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Miongoni mwa watu wa Kitabu, wanaweza kupatikana watu ambao hawaamini kuwa Yesu (mwana wa Maryam), wala Ezra kuwa ni wana wa Mungu, sio waabudu moto wala hawaamini kuwa kuna miungu wawili. 91

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini Hawasemi ‘masihi ni mwana wa mungu, wala Uzayr ni mwana wa Mungu, wala Ahraman ni mungu wa uovu, pia wanaamini juu ya Siku ya Hukumu. Ni nini matokeo ya matendo ya watu kama hawa? Hivi sasa mjadala wetu sio juu ya wale wagunduzi, wavumbuzi na watumishi wa ubinadamu ambao ni wayakinifu na wanakana kuwepo kwa Mungu, ambao malengo yao kivitendo hayajavuka nyanja ya kimaada. Kutokana na mjadala unaoendelea, tumeweka mtazamo wetu wazi juu yao kwa mujibu wa Uislamu. Mjadala wetu katika sehemu hii unawahusu wale wanaotenda wema ambao wanaanini Mwenyezi Mungu na siku ya Ufufuo, na hivyo wana uwezo wa kuwa na malengo makubwa zaidi katika matendo yao na wanafanya kazi kuelekea katika lengo linalovuka upeo wa maada. Inasemekana kuwa Edison na Pasteur walikuwa watu wa aina hii, kuwa walikuwa watu wa dini na walikuwa na malengo ya kidini. Hii ni kuwa, katika matendo yao, kamavile tu Waislamu washika dini, Walifanya kazi kutaka radhi za Mwenyezi Mungu na kwa sababu za kidini. Kiuhalisia hawa Wakristo (Edison na Pasteur) sio wakristo (wanaweza kuitwa Waislamu wa kimwelekeo), kwa sababu kama wangekuwa wakristo na kuamini katika itikadi iliyopo ya Ukristo, wangeamini kuwa masihi ni Mungu, basi moja kwa moja isingewezekana kwao kuwa wanaoamini juu ya Mungu Mmoja tu, labda Wakristo wasomi wachache wa leo wanaamini juu ya uzushi wa Utatu Mtakatifu. Ili kujibu swali hili, ni muhimu kueleza ni kwa namna gani imani juu ya Utume na Uimamu (viongozi walioteuliwa na Mwenyezi Mungu) ni muhimu, na kwa nini imani hii ni sharti la kukubaliwa matendo ya mtu. Inaonekana kuwa imani juu Mitume na mawalii wa Mwenyezi Mungu inahusika katika kukubaliwa au kukataliwa kwa matendo ya mtu kwa sababu mbili.

92

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini Kwanza, kuwatambua wao kunarudi nyuma hadi kumtambua Mwenyezi Mungu. Kiuhalisia, kumtambua Mwenyezi Mungu na mambo Yake hakukamiliki bila kuwatambua mawalii Wake. Kwa maneno mengine, kumtambua Mwenyezi Mungu kiukamilifu ni kutambua udhihirisho wa muongozo wake. Pili, kukitambua kituo cha Utume na Uimamu ni lazima kwa sababu bila hivyo, haiwezekani kupata mpango sahihi na kamili wa matendo ili kupata muongozo. Tofauti kubwa kati ya Mwislamu mtenda mema na mtenda mema ambaye hajaamini ni kuwa yule ambaye hajaamini lakini anatenda mema hana mpango sahihi wa kupata uongofu na hivyo ana nafasi ndogo sana ya kufanikiwa. Tofauti na huyu asiyeamini, Mwislamu ambaye amenyenyekea katika dini ambayo ina mpango sahihi na inayoeleweka ya uongofu, amehakikishiwa mafanikio ikiwa ataitekeleza mipango hiyo kiusahihi. Matendo mema sio kuwatendea wengine wema tu, matendo yote, ya faradhi, yaliyokatazwa, yaliyopendekezwa na yasiyopendeza pia yanaunda mpango wa matendo mema. Mkristo wa vitendo aliye nje ya Uislamu na ambaye hana mpango sahihi amekosa zawadi kubwa kwani anafanya matendo yaliyokatazwa. Kwa mfano pombe imekatazwa, lakini anakunywa. Tunajua kuwa pombe imekatazwa kwa sababu ya madhara ya kiafya kwa mtumiaji, madhara ya kijamii na kiroho, na ilivyo yeyote atakayekunywa pombe atapata madhara yake, sawa na mtu ambaye hakupata mwongozo wa daktari anaweza kufanya kitu ambacho kinaweza kuudhuru moyo wake, ini au moja kwa moja kufupisha maisha yake. Katika mpango wa Uislamu kuna baadhi ya amri ambazo ni lazima zitiiwe ili kupata ukamilifu wa kiroho na maendeleo. Ni dhahiri kwamba 93

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini asiyekuwa Mwislamu, hata awe hana chuki kiasi gani au asiwe na ukaidi kiasi gani, kwa kukosa kwake mipangilio kamili ya ukamilifu wa mwanadamu, atakosa faida zake. Mtu huyo atalazimika kukosa matendo makubwa ya ibada, kama sala tano za kila siku, kufunga mwezi Ramadhani na Hijja. Ni kama mtu anayepanda mbegu bila utaratibu maalumu wa mbinu za kilimo, kwa namna yoyote mazao ya mtu huyu hayawezi kuwa sawa na yule anayepanda mbegu kwa utaratibu maalumu, anapanda katika msimu sahihi, na anapalilia katika wakati sahihi, na kwa kifupi anafanya na kufuata hatua zote za kiufundi. Tofauti kati ya Mwislamu mtenda mema na asiye Mwislamu mtenda mema inaweza kuelezwa hivi: Mwislamu mtenda mema ni kama mgonjwa aliye chini ya uangalizi na maelekezo ya daktari bingwa; chakula chake na dawa vyote anapewa kwa maelekezo ya daktari, nyakati zake na kiasi anafanya kama alivyoagizwa. Lakini mtenda mema asiye kuwa mwislam ni kama mgonjwa ambaye hana program hiyo na anafanya anavyotaka anakula chakula chochote anachotaka na anatumia dawa yoyote inayofika mikononi mwake. Mgonjwa huyu wakati fulani anaweza kunywa dawa yenye manufaa na ikaleta matokeo mazuri, lakini pia inaelekea kuwa anaweza kutumia dawa ambayo ina madhara au inayoweza hata kuua. Halikadhalika anaweza kula chakula chenye manufaa, lakini kwa kutokuwa mwangalifu au kwa kula chakula kisichofaa, anaweza kubatilisha manufaa ya chakula cha awali. Kwa maelezo haya inakuwa wazi kuwa tofauti kati ya Mwislamu na asiyekuwa Mwislamu lakini anayemwamini Mwenyezi Mungu ni kuwa Mwislamu ni mtu anayemwamini Mwenyezi Mungu mwenye mpango maalum, ambapo asiyekuwa Mwislamu anafanya matendo yake bila mpangilio sahihi. Kwa maneno mengine, Mwislamu ameongoka na asiyekuwa mwislam japo anamuamini Mwenyezi Mungu, amepotoka. Juu ya hili Qur’ani inasema:

94

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini “Hivyo kama wakinyenyekea, watakuwa wamepata uongofu.” Qur’ani Tukufu, 3:20. Kutokana na tuliyoyasema katika sehemu mbili za mwisho, imekuwa wazi kuwa si wote wasiokuwa Waislamu wako sawa kwa namna watakavyolipwa matendo yao mema; kuna tofauti kubwa kati ya asiyekuwa Mwislamu ambaye hamwamini Mwenyezi Mungu na siku ya ufufuo na yule ambaye anamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Hukumu lakini wamekosa zawadi ya imani ya Utume. Kwa kundi la kwanza, haiwezekani kufanya kitendo kinachokubalika kwa Mwenyezi Mungu ambapo kwa kundi la pili inawezekana. Inawezekana kwa kundi hili kwenda peponi kwa masharti fulani, lakini kwa kundi la kwanza haiwezekani. Kwa inavyoonekana, sababu ya Uislamu kutofautisha kati ya washirikina na watu wa Kitabu katika sheria zake za maingiliano ambapo kwamba hauwavumilii washirikina lakini unawavumilia watu wa Kitabu, unawalazimisha washirikina kuacha imani yao lakini hauwalazimishi watu wa Kitabu - ni kuwa mshirikina au kafiri, kwa sababu ya ushirikina wake au kumkana kwake Mwenyezi Mungu anajifungia lango la uwokovu kwa ajili yake mwenyewe milele, na yupo katika hali ya kujinyima kuuvuka ulimwengu wa kimaada na kuingia katika ulimwengu wa juu na Pepo ya milele. Hata hivyo watu wa Kitabu wapo katika hali ambayo wanaweza kufanya matendo mema, japo katika hali ya upungufu, na kwa masharti fulani wanaweza kupata matokeo ya matendo yao. Qur’ani inasema, inapoongea na watu wa Kitabu:

95

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini “Njooni katika neno lililosawa baina yetu na baina yenu, kwamba tusimuabudu yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu na tusimshirikishe na yeyote, na tusimfanye yeyote kuwa mungu badala ya Mwenyezi Mungu.” Qur’ani Tukufu, 3:64 Qur’ani Tukufu imewapa watu wa Kitabu wito huo, lakini haijawapa kabisa na haiwapi wito huo washirikina na wanaomkana kabisa Mwenyezi Mungu.

KUHARIBIKA Suala la tatu ambalo linastahili kuangaliwa kuhusiana na thamani ya imani ni thamani hasi ya ukafiri na ukaidi. Yaani, je ukafiri na ukaidi hufanya tendo njema libatilike na kupoteza athari yake, na kulifanya liwe baya kama kuharibika kunavyofanya? Kwa maneno mengine, ikiwa mtu atatenda tendo njema kwa masharti yote ya wema unaotokana na kitendo na wema unaotokana na mtendaji, na bado kwa upande mwingine mtu huyo anaonyesha ukaidi kuhusiana na haki, hususan haki ambayo ni moja ya misingi ya dini, katika hali hii, je kitendo hiki ambacho ni kizuri kwa chenyewe, kwa masharti ya ulimwengu mwingine, na kinang’ara na hakina kasoro kutokana na vipimo vitukufu na vya kimbinguni - kinabatilika na kutofaa kwa sababu ya huu ukaidi na ujeuri au hali nyingine za kiroho zisizo halali? Hapa suala la kuharibika linajitokeza. Inawezekana kwa kitendo kuwa na wema wa pande zote mbili, wa kitendo na wa mtendaji, kwa maneno mengine, kuwa na hivi vyote, mwili safi na roho na moyo safi, kuwa kizuri kwa mtazamo wa duniani na akhera na bado wakati huo huo kikaharibika na kuwa kubatilika kwa mtazamo wa akhera kwa kuharibika, kama vile tu mbegu nzuri iliyopandwa katika ardhi yenye rutuba na hata pengine ikatoa matunda, lakini ikaangukia kwenye matatizo kabla haijatumiwa, na inaharibiwa, kwa mfano na nzige au radi. Qur’ni inauita uharibifu huu habt au kuporomoka. 96

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini Uharibifu huu sio wa wasioamini tu, unaweza kutokea hata kwenye matendo mema ya Waislamu pia. Inawezekana Mwislamu akatoa zaka kumpa mhitaji anayestahili kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, lakini mtendaji akaiharibu baadaye na kuifanya ibatilike kwa kumuwekea masharti mtu aliyempa au namna nyingine ya mateso ya kiakili. Qur’ani inasema:

“Enyi mlioamini, msiziharibu sadaka zenu kwa masimango na kashfa.”Qur’ani Tukufu, 2:264. Kingine kinachobatilisha matendo mema ni wivu, kama ilivyosemwa: “Wivu hula thawabu sawa na moto unavyokula kuni.” 32 Kingine kinachobatilisha matendo mema ni juhuud au ukanusho, au hali ya kupingana na ukweli, Ukanusho una maana mtu anautambua ukweli, lakini wakati huo huo anaupinga. Kwa maneno mengine kanusho ni pindi akili inaponyenyekea kupitia hoja za kiakili na mantiki na ukweli umekuwa dhahiri katika akili yake, lakini roho na hisia zake za kibinafsi na ujeuri vinaasi na vinakataa kunyenyekea. Chimbuko la ukafiri ni upinzani na ukinzani dhidi ya ukweli na hali akili ikiutambua. Awali, tulipokuwa tukijadili viwango vya unyenyekevu, tulielezea juu ya hali hii. Hapa tutatoa maelezo zaidi yenye kuhusika na majadiliano ya ubatilishaji wa matendo. Imam Ali Ibn Abi Talib (a.s) alipokuwa anaelezea maana ya Uislamu alisema: “Uislamu ni unyenyekevu”33 32 Biharul Anwar, Juz. 15, sehemu ya 3, uk. 132-133.

33 Nahjul Balaghah, hutba na. 125. 97

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini Hii ni kuwa pindi maslahi binafsi, chuki binafsi au tabia inapopingana na ukweli au uhalisia, mtu kuhiari kuyaacha yote haya na mengine yasiyokuwa ukweli ndio Uislamu. Ukanusho maana yake hali ya kukataa ukweli kwa hiari, hali aliyokuwa nayo Abu Jahl. Alijua kuwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w) alikuwa Mtume wa kweli lakini kwa sababu ya chuki binafsi, hakumwamini. Wakati fulani watu wanaweza kusikika wakisema; “Tuko tayari kwenda Motoni, ila sio kufanya hiki na kile!” Yaani hata kama kitu hicho ni ukweli (haki), bado hatuko tayari kukikubali. Maneno mengine kama vile kuwa ‘nyumbu’, kuwa asiyetawalika’ na mengine kama hayo, yote yanaelezea sifa ya ukanusho. Qur’ani imeelezea vizuri sana kuwepo kwa watu wa aina hii pale iliposema:

“Na waliposema, ‘Ewe Mwenyezi Mungu kama huu ni ukweli kutoka kwako tuteremshia mvua ya mawe kutoka mbinguni au tuletee adhabu yenye kuumiza.” Qur’ani Tukufu, 8:32. Unaona picha ambayo Qur’ani inatuchorea, kwa kusimulia sentensi moja, imeonyesha maradhi ya kiakili ya baadhi ya watu. Mtu mkaidi ambaye maneno yake yamenukuliwa katika aya hii, badala ya kusema: “Ewe Mwenyezi Mungu, kama huu ni ukweli kutoka kwako, basi ufanye moyo wangu uwe tayari kuukubali,’ anasema; “Kama huu ni ukweli, niteremshie adhabu na niagamize kwa sababu sina nguvu za kubaki hai kukabiliana na ukweli.” Hali hii ni ya hatari sana, hata ikiwa katika mambo madogo madogo. Na inawezekana wengi wetu tunaumwa maradhi haya. Mwenyezi Mungu 98

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini atuepushie. Chukulia kwamba daktari mahiri, mujtahidi, au msomi mwingine bingwa anayekubalika duniani kote anatoa maoni yake kuhusiana na mambo ya fani yake; kisha, daktari asiyejulikana, au mwanfunzi kijana, naye akatoa maoni yanayopigana na yule bingwa juu ya jambo hilo hilo moja, na akatoa ushahidi wake wa kutosheleza mpaka yule msomi akaridhika moyoni mwake kuwa ukweli ni ule aliosema yule kijana, lakini watu wengine wakabaki hawajui kama walivyojua zamani, na kwa mtazamo wa kusifika kwa mtu huyu akilikubali wazo la yule kijana, na kukiri makosa yake basi huyu ni Mwislamu wa wa kweli, kwa sababu Uislamu ni unyenyekevu na huu unaweza kuwa mfano katika aya;

“Yule anayejinyenyekesha kwa Mwenyezi Mungu …” Qur’ani Tukufu, 2:112 Mtu huyo ameepukana na tabia hizo za kukana ukweli. Lakini akijiingiza katika kuukana na kuupinga ukweli kuokoa heshima na umaarufu wake, atakuwa anaukana ukweli kwa makusudi. Ikiwa daktari huyo kwa mfano, akiwa hakukosa uadilifu moja kwa moja anaweza asikanushe maneno yake, lakini anaweza kubadilika kiutendaji, na kama sio muadilifu kabisa hawezi hata kubadilika kiutendaji, na akatoa matibabu yaleyale na pengine kumuua mgonjwa, kisha akasema mgonjwa alikuwa hawezi kutibika – na hali hii inawahusu wanazuoni wengine maarufu. Na kinyume cha hali hii pia hutokea mara kwa mara. Kuna hadithi katika al-Kafi ambayo inatoa mwanga juu ya ukweli huu. Muhammad ibn Muslim alisimulia kuwa alimsikia Imam Muhamamd ibn Ali al-Baqir (as) akisema: “Kitu chochote kinachotokana na kukiri na kutii hiyo ni imani na kitu chochote kinachotokana na kukana ama kukataa (ukweli) hiyo ni kufru.” 34 34 Al-Kafi, Jz. 2, uk. 387. 99

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini Wanasema kuwa marehemu Ayatulllah Sayyid Husayn Kuhkamari (r.a.) ambaye alikuwa mmoja wa wanafunzi wa mtunzi wa Jawahirul Kalam na Mujtahidi mashuhuri na mwalimu aliyetambulika, alikuwa akienda kila siku katika muda maalum, kama ilivyokuwa kawaida yake, kufundisha katika moja ya misikiti ya Najaf. Kama tunavyojua nafasi ya kufundisha kiwango cha ‘kharij’ ya fiqh na kanuni zake ni misingi kwa ajili ya uongozi na mamlaka ya kidini. Uongozi na mamlaka ya kidini kwa mwanafunzi wa seminari ina maana kuanza mara moja kuanzia sifuri hadi kwenye namba isiyohesabika, kwani mwanafunzi si chochote kama yeye sio msomi wa kidini (marja), na maoni na imani yake havipewi umuhimu, na kwa kawaida anaishi maisha duni. Lakini mara tu anapokuwa ni msomi wa kidini (marja), ghafla maoni yake hutiiwa na hakuna yeyote wa kusema lolote juu ya maoni yake. Kifedha na kitaalamu ana busara kamili bila kuwajibika kwa mtu yeyote. Hivyo, mwanazuoni, anayepata bahati ya kuwa marja hupitia hatua nyeti; hayati Sayyid Husain Kuhkamari alikuwa katika hatua kama hiyo. Siku moja alikuwa anarudi kutokea sehemu fulani, labda kutembelea mtu fulani, na ilikuwa imebaki kama nusu saa kabla ya darasa lake kuanza. Aliwaza kuwa kwa muda ule mdogo uliobaki akienda nyumbani hataweza kufanya lolote, hivyo aliona ni bora aende darasani akawasubiri wanafunzi wake. Alikwenda na kukuta hakuna mwanafunzi yeyote aliyefika, lakini alimuona kwenye kona ya msikiti Sheikh aliyeonekana mnyenyekevu akiwa amekaa akifundisha kundi la wanafunzi. Hayati Sayyid alisikiliza maneno yake na kwa mshangao aligundua kuwa mafundisho ya sheikh yalikuwa ya kisomi cha hali ya juu sana. Siku iliyofuata aliamua awahi ili aje asikilize maneno ya yule Sheikh. Hivyo alikuja na kusikiliza na kushawishika kwake kuanzia ile siku iliyopita kukawa kukubwa zaidi. Hii iliendelea kuruduwa kwa siku kadhaa na marhum Sayyid Husayn akawa na uhakika kuwa Sheikh yule alikuwa na elimu kumzidi yeye na kuwa angenufaika na mihadhara yake, na kama wanafunzi wake wangehudhuria mihadhara ya Sheikh, wangefaidika zaidi. 100

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini Hapa ilikuwa kwamba, yeye alijiona kama amepewa fursa ya kuchagua kati ya utii na ukaidi, kati ya imani na kufru, kati ya Akhera na dunia hii. Siku inayofuata wanafunzi walipokuja na kukusanyika, akasema, ‘Rafiki zangu, leo ninataka kuwaelezeeni kitu kipya. Yule Sheikh aliyekaa kwenye pembe ile ya msikiti na wanafunzi wachache anastahili zaidi kufundisha kuliko mimi, na mimi mwenyewe ninafaidika na mafundisho yake, hivyo sisi wote twende kwenye hotuba zake.” Toka siku ile alijiunga kwenye kundi la wanafunzi wa Sheikh yule mnyenyekevu ambaye macho yake yalikuwa yamevimba kidogo na ambaye kwake dalili za umaskini zilikuwa zinaonekana. Huyu sheikh mwenye maadili ndio yule mwanazuoni ambaye badae alikuja kuwa maarufu kama Sheykh Murtadha al-Ansari na kupata cheo cha “mwalimu wa wanachuoni wa zama zijazo.” Sheikh Ansari wakati huo alikuwa amerudi kutoka katika safari ya miaka mingi huko Mashhad, Isfahaan na Kaashaan na alikuwa amepata elimu kubwa katika safari yake hiyo, hasa kutoka kwa marhum Hajj Mulla Ahmad Naraaqi katika mji wa Kaashaan. Yeyote ambaye hali hii inapatikana kwake ni mfano wa aya hii “Ambaye hunyenyekea kwa Mwenyezi Mungu.” Hivyo kufru, na kukana ina maana kusimama dhidi ya ukweli kwa makusudi na kuonyesha ukaidi. Baadaye tutataja kuwa kwa maoni ya Qur’ani, yule asiyeamini ameitwa kafiri kwa sababu yupo katika hali ya kukanusha na kukaidi ambapo wakati huohuo anautambua ukweli, na ni hali hii ambayo husababisha ubatilishaji na kuchukuliwa kama kuporomoka kwa matendo mema. Hii ndio maana kuhusiana na matendo ya wasioamini, ambayo yamelinganishwa na majivu ambayo upepo mkali huyapuliza na kuyaharibu, Mwenyezi Mungu anatwambia:

101

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini

“Mfano wa wale wanaomkana Mola wao: Matendo yao ni kama majivu ambayo juu yake upepo hupitia na kuyapuliza kwa nguvu katika siku yenye tufani.” Qur’ani Tukufu, 14:18. Tuchukulie kwamba Pasteur alifanya utafiti wake wa kisomi ambao ulisababisha kugunduliwa kwa bakteria kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kwamba nia yake ni kuwatumikia wanaadamu na kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu, hii haitoshi kwake kulipwa na Mwenyezi Mungu mwisho wa safari. Kama ana sifa za ukukanaji ukweli na nyingine kama hizo na alikuwa ni mwenye chuki kwa ajili ya kupendelea imani zake, basi bila shaka matendo yake yote ni batili, kwa vile katika hili yupo katika hali ya kukana ukweli, na hali hii ya kuukana ukweli huharibu jitihada zote za mtu. Suala lingekuwa hivi, kama kwa mfano, angeambiwa: “Ukristo ni imani ya eneo na ya mababu tu kwako; je, umefanya utafiti na ukaona iwapo kuna dini bora na kamili zaidi kuliko Ukiristo au hapana?” Na akayakataa maneno haya - bila kuwa tayari kujifunza na kutafiti akasema “Dini bora ni Ukristo.” Matendo ya mtu katika hali kama hii, huwa kama majivu, yanayopulizwa na upepo mkali. Tumemtaja Pasteur tu hapa lakini hatuna maana kuwa Pasteur alikuwa hivi. Ni Mwenyezi Mungu tu ndio anajua hilo. Sisi pia kama ni wakaidi dhidi ya ukweli, tutaangukia kwenye kanuni hii. Ewe Mola! Tukinge dhidi ya kufru, ukaidi na kuuupinga ukweli. Mbali na yaliyotajwa, vilevile kuna uporomokaji mwingine ambao hutokea kwenye matendo mema. Labda moja ya uharibifu huo ni hali ya kutojali kutetea ukweli na uadilifu. Mtu sio tu anapaswa kuepuka kukataa na kuupuza ukweli, bali kwa nyongeza, mtu hapaswi kubaki bila upande wowote, na badala yake anapaswa kutetea ukweli. Watu wa Kufa walijua 102

7/15/2011

12:41 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini kuwa haki ilikuwa kwa Husain ibn Ali (a.s) na walikuwa wamekiri ukweli huu lakini walipuuzia kuitetea na kuilinda haki. Hawakuonyesha msimamo na ustahimilivu. Kutokuunga mkono haki ni kuikataa haki kivitendo. Bibi Zainab bint Ali (a.s) katika hotuba yake maarufu kwa watu wa Kufah, anawakaripia kwa kupuuza kwao kuja kutetea haki na kwa kuutendea dhulma juu yake. Alisema: “Enyi watu wa Kufah! Enyi watu wa ulaghai, usaliti na uasi, je mnalia? Basi na machozi yenu yasikauke, na vilio vyenu visiishe! Mfano wenu ni wa mwanamke aliyefumua kitambaa chake baada ya kuwa ameshakikamilisha.”35 Balaa zingine zinazoweza kuharibu matedno mema ni majivuno na kujisifu. Mtu kujisifu kwa ajili ya matendo yake, kama kwa husda, majivuno na ukanushaji, hilo vilevile huharibu matendo mema. Kuna hadith inayosema; “Wakati fulani mtu hufanya tendo nzuri na safi, na tendo lake hilo hupata nafasi katika ‘Illiyyin’ lakini baadaye hulitaja tendo hilo hadharani na kujisifia nalo. Hili husababisha tendo lile liporomoke chini. Akilitaja tena huporomoka zaidi na akilitaja tena mara ya tatu huharibika kabisa, na wakati fulani hubadilishwa na kuwa uovu.” Imam Muhammad ibn al-Baqir (as) alisema: “Kuihifadhi tendo jema ni kugumu kuliko kulitenda tendo lenyewe.” Msimuliaji aliuliza maana ya kuhifadhi tendo. Imam alijibu, “Mtu hufanya tendo jema na hutoa kitu fulani katika njia ya Mwenyezi Mungu, na huandikwa kama tendo lililofanywa kwa siri. Kisha hulitaja, hivyo hufutwa na kuandikwa kama tendo liliyofanywa hadharani. Kisha hulitaja tena, hivyo hufutwa na kuandikwa kama tendo liliofanywa ili kujionyesha.” 36 35 Nafas al-Mahmum, uk. 393 36 Wasailush Shia, Juz. 1, uk. 55 103

7/15/2011

12:42 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini

CHINI YA SIFURI. Hadi sasa mjadala wetu umekuwa juu ya kukubaliwa au kutokubaliwa kwa matendo ya ibada na matendo mazuri na bayana ya wasiokuwa Waislamu, na kwa maneno mengine mjadala huu umekuwa juu ya yale yaliyo juu ya nukta ya sifuri; mjadala ulikuwa ni iwapo matendo yao mema yanawafanya wapande juu au hapana. Sasa hebu tuangalie hali ya yale yaliyo chini ya mstari wa sifuri, yaani nini kinatokea kuhusiana na maovu na dhambi za wasiokuwa Waislamu. Je yote ni sawa kwa mwelekeo wa majadiliano yetu, au kuna tofauti? Na kwa nyongeza, katika matendo haya ambayo ni maovu na humshusha mtu chini, kuna tofauti kati ya Mwislamu na asiyekuwa Mwislamu? Na halikadhalika kwa Shia, na wasiokuwa Shia? Je, Mwislamu na hususan Mwislam Shia ana aina ya ulinzi fulani dhidi ya matendo haya au hapana? Katika mas’ala yaliyopita imekuwa wazi kuwa Mwenyezi Mungu huwaadhibu watu wanapofanya matendo mabaya kwa makusudi (taqsir), yaani, wanapofanya kwa makusudi na hali wanajua na sio kwa sababu hawawezi kuiepuka dhambi hiyo (qusur). Awali tulitafsiri na kuielezea aya ya Qur’ani ambayo wanazuoni wa kanuni za fiqh (usul-fiqh) hutoa kanuni inayosema: “Ni kosa kumuadhibu mtu kabla ya kumfafanulia jukumu lake.” Sasa tukiainisha hali ya wasiokuwa Waislamu kuhusiana na matendo ambayo yanaangukia chini ya alama ya sifuri na kuchunguza adhabu yao maovu wanayoyafanya, hatuna hiari bali tunaanzisha suala jingine ambalo limegusiwa katika maarifa ya kiislamu na lenye mizizi yake katika Qur’ani Tukufu, na hili ni suala la “kutokuwa na uwezo” na “kutokuwa na nguvu” (istidh’af). Hapa tunaaza mjadala wetu chini ya kichwa cha habari hiki:

104

7/15/2011

12:42 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini

WASIOKUWA NA NGUVU NA WASIO NA UWEZO Wanazuoni wa Kiislamu wanatumia istilahi mbili; wanasema baadhi ya watu hawana nguvu (mustadh’afin) au wanasubiri amri ya Mwenyezi Mungu (murjawn li-amrillah). Wasio na nguvu ni wale wenye bahati mbaya na wasio na uwezo; ‘wanaosubiri amri ya Mwenyezi Mungu’ inamaanisha wale ambao mambo yao na hadhi zao ni za kuchukuliwa kuwa ziko kwa Mwenyezi Mungu na mikononi Mwake, Mwenyezi Mungu Mwenyewe atawatendea kwa mujibu wa Hekima na rehema Yake. Istilahi zote hizi zimechukuliwa kutoka katika Qur’ani: Katika Suratul Nisaa, aya za 97-99, Mwenyezi Mungu anasema: “Na wale ambao malaika huchukua roho zao na hali wakiwa ni wenye kujidhulumu nafasi zao. (Wataulizwa); ‘Mlikuwa na hali gani?’ Watasema, ‘Tulikuwa wadhaifu katika ardhi. Malaika watasema, Je ardhi ya Mwenyezi Mungu haikuwa pana, mkahamia huko? Hivyo makazi ya watu hao ni moto, na ni makazi mabaya isipokuwa wale wasio na nguvu miongoni mwa wanaume, wanawake na watoto ambao hawana njia yoyote wala hawajaongoka katika njia yoyote; hivyo labda Mwenyezi Mungu anaweza kuwasamehe, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe sana.” Katika aya ya kwanza, yametajwa mahojianao ya baadhi ya watu na Malaika wa kaburini. Malaika wanawauliza, “Ilikuwaje hali yenu duniani?” Wanatanguliza udhuru; “Tulikuwa na bahati mbaya njia zetu zilikuwa hazitoshelezi (na hatukuwa na uwezo wa kubadilisha hali zetu).” Malaika watasema, “Sio kwamba hamkuwa na nguvu, maadamu ardhi ya Mwenyezi Mungu ilikuwa pana na mlikuwa na uwezo wa kuhama kutoka 105

7/15/2011

12:42 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini katika nchi zenu za asili na kwenda katika sehemu yenye nafasi bora zaidi; hivyo mlifanya makusudi na mnastahili adhabu.” Katika aya ya pili, hali ya watu wengine imetajwa ambao ni kweli hawana nguvu, wawe wanaume, wanawake au watoto. Hawa ni watu ambao hawakuwa na namna yoyote. Katika aya tatu, Qur’ani inatoa bishara na matumaini kuwa Mwenyezi Mungu anaweza kulisamehe kundi la pili. Katika tafsiri yake ya Qur’ani, Al-Mizan, mwalimu wetu anayeheshimika zaidi, Allamah Tabatabai, ana haya ya kusema kuhusian na aya hizi. “Mwenyezi Mungu huchukulia ujinga wa dini na kila namna ya kuzuia kusimamishwa kwa dalili za dini kuwa ni udhalimu, na msamaha wa Mwenyezi Mungu haulifikii kundi hili. Hata hivyo, msamaha umetolewa kwa wale ambao hawakuwa na nguvu, na hawakuwa na uwezo wa kuhama na kubadilisha mazingira. Msamaha huu umetajwa katika namna ambayo sio pekee kwa hali ya kutokuwa na nguvu inapochukua sura hii. Kama ilivyo tu kuwa inawezekana chanzo cha kutokuwa na nguvu kikawa ni kutokuwa na uwezo wa kubadilisha mazingira, inawezekana kwa hilo pia kwa sababu akili ya mtu haijui ukweli, na hivyo kubaki ameukosa ukweli.” 37 Hadith nyingi zimesimuliwa ambapo watu wale ambao, kwa sababu mbali mbali wamebakia kutokuwa na uwezo, wamehesabiwa miongoni mwa “wasiokuwa na nguvu.” 38 Katika aya ya 106 ya Surat-Tawbah, Mwenyezi Mungu anasema: “Na wengine ambao wanasubiri amri ya Mwenyezi Mungu, ama atawaadhibu au atawasamehe na Mwenyezi Mungu ni mwenye kujua, Mwenye Hikma.” 37. al-Mizan, Jz. 5, uk. 51. 38 Rejea kwenye al-Mizan, Jz. 5, uk. 56-61. “Majadiliano ya Hadithi.” 106

7/15/2011

12:42 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini Neno murjawn li-amrillah (wale wanaosubiri amri ya Mwenyezi Mungu) limechukuliwa kutoka katika Aya hii. Imesimuliwa kuwa Imam Muhammad ibn Ali al-Baqir (a.s) alisema yafuatayo kuhusiana na Aya hii: “Kwa hakika kulikuwa watu katika kipindi cha awali cha Uislamu ambao waliwahi kuwa washirikina na walifanya madhambi makubwa sana, walimuua Hamza na Ja’far na watu kama hao miongoni mwa Waislamu. Baadaye, wakawa Waislamu, wakaachana na ushirikina na kuambatana na tauhidi, lakini imani haikupata nafasi katika mioyo yao kwa wao kuhesabiwa miongoni mwa waumini na kustahili pepo, na wakati huo huo walikuwa wameachana na kumkana Mwenyezi Mungu na ukaidi, mambo ambayo yalikuwa sababu ya kustahili kwao kuadhibiwa. Hawakuwa waumini wala makafiri, hawa basi ndio murjawn li-amrillah ambao suala lao liko kwa Mwenyezi Mungu. 39 Katika hadith nyingine, imesimuliwa kuwa Humra ibn A’yan alisema: “Nilimuuliza Ja’far ibn Muhammad as-Sadiq (a.s) juu ya wasio na nguvu, akajibu, “Sio waumini wala makafiri, hawa ndio ambao suala lao liko kwa Mwenyezi Mungu. 40 Ingawa maana ya jumla ya aya hii kuhusiana na wale ambao suala lao linasubiri amri ya Mwenyezi Mungu ni kwamba mtu anatakiwa aseme tu; suala lao liko kwa Mungu, bado, kutokana na mwelekeo wa aya kuhusiana na wasio na nguvu, kidokezo cha msamaha wa Mungu kinaonekana hapa. Kinachoeleweka kwa jumla hapa ni kuwa watu ambao hawakuwa na uwezo, na hawana lawama, hawataadhibiwa na Mwenyezi Mungu.

39. Al-Mizan, Juz. 9, uk. 406, kutoka Al-Kafi. 40. Al-Mizan, Juz. 9, uk. 407, kutoka Tafsir Ayash. 107

7/15/2011

12:42 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini Katika al-Kafi kuna hadith kutoka kwa Hamzah ibn Tayyar aliyesimulia kwamba Imam Ja’far ibn Muhammad as-Sadiq (a.s) alisema: “Watu wapo katika makundi sita, na mwisho wanabaki makundi matatu; kundi la imani, kundi la kufru, na kundi la upotovu. Makundi haya yanatokea kutokana na ahadi ya Mwenyezi Mungu na maonyo Yake kuhusiana na Pepo na Moto. (Yaani, watu wamegawanyika kwenye makundi haya kutokana na mwelekeo wao kuhusiana na ahadi na maonyo haya). Yale makundi sita ni waumini, makafiri, wasio na nguvu, wale wanaosubiri amri ya Mwenyezi Mungu, wale ambao wamekiri madhambi yao na wamechanganya mema na mabaya na watu wa juu (a’raf).” 41 Pia katika al-Kafi, imesimuliwa kutoka kwa Zurarah kuwa alisema: “Nilimtembelea Imam Muhammad ibn Ali al-Baqri (a.s) na ndugu yangu Humrah au ndugu yangu Bukahir. Nilimwambia Imam: “Tunawapima watu kwa utepe wa kupimia; Yeyote ambaye ni Shia kama sisi, awe ametokana na kizazi cha Ali au vinginevyo tunafanya naye urafiki (kama Mwislamu na ambaye atapata uokovu). Na yeyote anayepinga madhehebu yetu, tunajitenga naye (kama mtu aliyepotoka na ambaye hatapata uokovu).’” Imam alisema: “Zurarah, neno la Mwenyezi Mungu ni kweli zaidi kuliko neno lako, unachosema ni sahihi, lakini vipi kuhusiana na maneno ya Mwenyezi Mungu pale aliposema: ‘Isipokuwa wasiokuwa na nguvu miongoni mwa wanaume, wanawake na watoto ambao hawana njia yoyote?’ Vipi kuhusiana na wale wanaosubiri amri ya Mwewnyezi Mungu? Vipi kuhusiana na wale ambao Mwenyezi Mungu amesema, ‘Walichanganya amali njema na mbaya?’ Nini kilichotokea kwa watu wa juu? Ni nani basi ambao mioyo iwaelekee?” Hammad, katika simulizi yake ya tukio hili kutoka kwa Zurarah anasimulia kwamba amesema: “Kufikia hapa Imamu na mimi tukaanza kubishana. 41. Al-Mizan, Juz. 9, uk. 406, kutoka Al-Kafi. 108

7/15/2011

12:42 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini Wote tukapaza sauti, kiasi kwamba wale waliokuwa nje ya nyumba walitusikia.” Jamal ibn Darraj anasimulia kutoka kwa Zurarah katika tukio hili kwamba Imamu alisema: “Zurarah! Mwenyezi Mungu amefanya ni wajibu kwake kwamba awachukue waliopotoshwa awaingize Peponi (sio makafiri na wakanushaji).” 42 Pia katika al-Kafi, imesimuliwa kuwa Imam Musa ibn Ja’far al-Kadhim (a.s) amesema ‘Ali ni mlango katika milango ya mwongozo, yeyote anayeingia katika mlango huu ni muumini na yeyote anayetoka katika mlango huu sio muumini; na yule ambaye haingii wala hatoki (katika mlango huu) ni miongoni mwa wale ambao wanasubiri amri ya Mwenyezi Mungu.” Katika hadithi hii Imamu anataja waziwazi kundi ambalo si miongo mwa wenye imani, unyenyekevu na uokovu wala si miongoni mwa wakanushaji na watakaoangamia. 43 Pia katika al-Kafi imesimuliwa kutoka kwa Imam Ja’far ibn Muhammad as-Sadiq (a.s) kwamba: “Ikiwa watu, wakiwa wajinga, wakanyamaza na wasikanushe, hawatakuwa makafiri.” 44 42 Al-Kafi, Juz. 2, uk. 382. Maneno ya mwisho ya hadithi ni: ‘Haqa alaa llahi an yudkhila al-dhwulala al-Janat.’ Kama ilivyo tarjuma yake hapo juu. Lakini katika baadhi ya maandishi, ni kama ifuatavyo: ‘Haqa alaa llahi an la yudkhila aldhwulala al-Janat.’ Ambayo ingemaanisha kwamba Imamu (as) amebadilisha maoni yake na kukubali yale ya Zurarah. Kwa dhahiri, hii sio sahihi. Bali kwa kutegemea juu ya maandishi haya, maana nyingine inawezekana, ambayo ni kwamba Imamu (as) huenda alikusudia kwamba watu hawa hawataadhibiwa, lakini pia hatakwenda Peponi. 43 al-Kafi, Juz. 2, uk. 388 44 al-Kafi, Juz. 2, uk. 388 109

7/15/2011

12:42 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini Tukizitafakari hadith zilizotujia kutoka kwa Maimamu watukufu (a.s), na ambazo nyingi katika hizo zimekusanywa katika ‘Kitab al-Hujjat’ na ‘Kitab al-Iman wa al-Kufr’ katika al-Kafi tutaona kuwa msimamo wa Maimamu ulikuwa ni kwamba mtu ataadhibiwa tu ikiwa alipelekewa ukweli na akaonyesha chuki binafsi dhidi ya ukweli au ukaidi au kwa uchache alikuwa na nafasi ya kutafiti na kutafuta ukweli lakini hakufanya hivyo. Na kuhusiana na watu ambao, kwa sababu ya kutoelewa, au sababu nyingine, hawakanushi ukweli wala hawapuuzi ukweli, hawahesabiwi kuwa miongoni mwa wakanushaji wala maadui. Wanahesabiwa kuwa miongoni mwa wasio na nguvu na wale ambao wanasubiri amri ya Mwenyezi Mungu. Na inaonekana kutokana na hadith za Maimamu waliotakasika wanaona kuwa watu wengi wapo katika kundi hili. Katika al-Kafi, sehemu ya ‘Kitab al Hujjah’ Sheikh Kulayn anasimulia hadith nyingi kuhusiana na mada hii kuwa: “Yeyote anayemtii Mwenyezi Mungu na akajibidiisha, lakini hana Imamu aliyeteuliwa na Mwenyezi Mungu, jitihada zake hazitakubaliwa. 45au pia; “Mwenyezi Mungu huwa hakubali kitendo cha mja Wake, alichokifanya bila kumtambua Imamu wake.” 46 Na wakati huo huo, katika sehemu ya‘Kitab al-Hujjah’ ya al-Kafi, imesimuliwa kutoka kwa Imam Ja’far Sadiq (a.s) kuwa: “Yeyote mwenye kututambua sisi ni muumini, na yeyote anayetukataa sio muumini, na yeyote ambaye hatutambui wala hatukanushi amepotoka mpaka atakaporejea katika mwongozo wa utii kwetu ambao Mwenyezi Mungu amemuamrisha. Hivyo akifa katika hali hiyo Mwenyezi Mungu atafanya atakavyo. 47 45 al-Kafi, Juz. 2, uk. 183 46 al-Kafi, Juz. 2, uk. 203 47 al-Kafi, Juz. 2, uk. 187 110

7/15/2011

12:42 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini Muhammad ibn Muslim anasema; “Nilikuwa na Imam Ja’far Sadiq (a.s), nilikuwa upande wake wa kushoto na Zurarah upande wa kulia. Abu Basir aliingia na kuuliza, ‘Unasemaje juu ya mtu mwenye mashaka juu ya Mwenyezi Mungu (kuwa yupo)?’ Imam alijibu ‘sio muumini.’ ‘Unasemaje juu ya mtu mwenye mashaka juu ya Mjumbe wa Mwenyezi Mungu?’ Sio muumini alipofika hapa Imam alimgeukia Zurarah na kusema ‘kwa hakika mtu huyo atakuwa sio muumini ikiwa atakanusha au kuonyesha ukaidi.’” 48

Pia katika al-Kafi, Kulayn anasimulia kuwa Hashim ibn al-Barid (sahib alBarid) alisema: “Muhammad ibn Muslim, Abdul Khattab, na mimi tulikuwa pamoja sehemu moja; Abul Khattab akauliza, ‘ni nini imani yako juu ya yule asiyejua suala la Uimamu?’ Nikasema, ‘Kwa maoni yangu sio muumini.’ Abul Khattab akaesma: ‘Maadam ushahidi haujamkamilikia, yeye sio kafiri sio muumini, kama ushahidi ukimkalimilikia na bado akawa hauamini basi ni kafiri.’ Muhammad ibn Muslim akasema, ‘Mwenyezi Mungu ametukuka! Kama hamtambui Imamu na haonyeshi ukaidi wala kuwakanusha, vipi anaweza kuhesabiwa kuwa si muumini?’ Hivyo sisi watatu tulikuwa na imani tatu zinazopoingana. “Kipindi cha Hijja kilipofika nilikwenda kwa Imam Sadiq (a.s), nilimweleza juu ya majadiliano yetu sisi watatu na nikamuuliza Imamu maoni yake. ‘Nitalijibu swali hili mtakapokuwepo ninyi wote watatu. Mimi na nyinyi tutakutana usiku kule Mina karibu na Jamarat ya katikati.’” “Usiku ule sisi watatu tulikwenda, Imam akiwa ameegemea juu ya mto alianza kutuuliza. ‘Je mnasemaje juu ya watumishi, wanawake na watu wa familia zenu? Je hawashuhudii kuwa Mungu ni Mmoja?’

48 al-Kafi, Juz. 2, uk. 399 111

7/15/2011

12:42 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini Nilijibu, ‘Ndio’ ‘Wanaamini juu ya Utume wa nabii Muhammad (s.a.w.w)?’ “Ndiyo.” “Je wanautambua Uimamu na Wilayah (mamlaka yaliyoteuliwa na Mwenyezi Mungu kama nyinyi?’ ‘Hapana.’ ‘Sasa ni nini maoni yenu?’ ‘Maoni yangu ni kuwa yeyote ambaye hamtambui Imamu sio muumini.’ “Mwenyezi Mungu ni Mtukufu! Je, wewe hukuwaona watu wa mitaani na sokoni? Hukuwaona wabebaji maji?’ ‘Ndio nimewaona na ninawaona.’ ‘Je, hawafungi? Hawahiji? Je hawashuhudii kuwa Mwenyezi Mungu ni Mmoja na Utume wa Muhammad?’ ‘Ndio’ ‘Vizuri, je wanamtambua Imamu kama unavyofanya?’ ‘Hapana.’ ‘Hivyo basi wao wako katika hali gani?’ ‘Maoni yangu ni kuwa yeyote asiyemtambua Imam sio muumini.’ ‘Mwenyezi Mungu ametukuka! Je huioni hali ya al-Kaaba kuzunguka kwa watu hawa? Je huwaoni watu wa Yemen wakishikilia mapazia ya alKaaba? 112

7/15/2011

12:42 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini ‘Ndio nimewona.’ ‘Je, hawashuhudii umoja wa Mungu na kumwamini Mtume? Je, hawaswali, hawafungi na kuhiji? ‘Ndio.’ ‘Je, wanamtambua Imamu kama wewe?’ ‘Hapana.’ ‘Nini imani yako kuhusu wao?’ ‘Kwa mtazamo wangu, yeyote yule ambaye hamtambui Imamu si muumini.’ ‘Mwenyezi Mungu atukuzwe! Imani hii ni imani ya Makhawariji.’ Kufikia hapa Imamu (as) akasema: ‘Sasa mnataka mimi niwajulishe ukweli?’ Hashim, ambaye kwa maneno ya marehemu Faydh al-Kashani, alijua kwamba mtazamo wa Imamu ulikuwa kinyume na imani yake mwenyewe, akasema: ‘Hapana.’ Imamu (as) akasema: ‘Ni vibaya sana kwenu ninyi kusema kitu kwa maoni yako mwenyewe kitu ambacho hukusikia kutoka kwetu.’ Hashim baadaye aliwaambia wenzake: “Nilihisi kuwa Imam alikubaliana na maoni ya Muhammad ibn Muslim na alitaka tukubali maoni yake.” 49 Katika al-Kafi, baada ya hadith hii, Shaykh Kulayni anasimulia hadith maarufu ya majadiliano kati ya Zurarah na Imam Muhammad ibn Ali alBaqir (a.s) juu ya hili, ambayo ni majadiliano marefu. 49 al-Kafi Juz. 2, uk. 401, sura juu ya upotofu (Dhalal), uk. 401 113

7/15/2011

12:42 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini Katika al-Kafi mwisho wa Kitab al-Iman wal al kufr, kuna sura iitwayo “Hakuna kitendo kinachosababisha madhara kwa sababu ya imani na hakuna kitendo kinacholeta faida kwa kuambatana na kufru.” 50 Lakini hadith tulizozipitia katika kichwa hiki cha habari hazikubaliani na baadhi ya hadith kama vile: “Yaqub ibn Shuayb alisema “Nilimuuliza Imam Ja’afar ibn Muhammad as-Sadiq (a.s): “Je kuna yeyote mbali na waumini atakayepata malipo kutoka kwa Mwenyezi Mungu? Akajibu; “Hapana.” 51 Maana ya jumla ya hadith hii ni kuwa Mwenyezi Mungu hajatoa ahadi ya malipo kwa yeyote isipokuwa waumini, na bila shaka atatekeleza ahadi yake. Hata hivyo, mbali na waumini, Mwenyezi Mungu hajatoa ahadi yoyote kwa ajili Yake kutekeleza hilo (kwa wasiokuwa waumini), na kwa vile hajatoa ahadi yoyote, ni juu Yake Mwenyewe kuwalipa au kutowalipa. Kwa maelezo haya Imamu anataka kueleza kuwa wasiokuwa waumini wanahesabika katika wasiokuwa na nguvu na wale ambao suala lao linasubiri amri kutoka kwa Mwenyezi Mungu ikiwa Mwenyezi Mungu atawalipa au la, lazima isemwe kwamba suala lao liko kwa Mwenyezi Mungu kwa ajili ya Yeye kuwalipa au la. Mwishoni mwa sura hii ya al-Kafi, kuna baadhi ya hadith ambazo tutazitaja baadaye katika kichwa cha habari, “Dhambi za Waislamu.” Kwa kweli hadith kuhusiana na hili sio hizi tu, zipo nyingine pia. Hitimisho kutokana na hadith zote hizi ni hilo tulilotaja hapo juu. Ikiwa mtu hakubaliani na mtazamo wetu, anaweza akaelezea, kwa ushahidi mtazamo wake na pengine sisi pia tunaweza kunufaika. 50 al-Kafi Juz. 2, uk. 463 51 al-Kafi Juz. 2, uk. 464 114

7/15/2011

12:42 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini Kwa Mtazamo wa Wenye Busara wa Kiislamu. Wanafalsafa wa Kiislamu wamelijadili suala hili kwa namna totauti lakini hitimisho walilofikia mwisho ni sawa na letu tulilolipata kutokana na aya na hadith. Ibn Sina (Avecenna) anasema: “Watu wamegawanyika katika makundi matatu kwa kutegemea na uzuri wao wa miili, kundi moja lililo katika hatua ya ukamilifu wa uzuri, jingine ni baya sana au gonjwa, makundi yote haya ni madogo. Kundi lenye watu wengi zaidi ni la kati kulingana na hali ya afya na uzuri; sio zuri moja kwa moja au lenye afya nzuri, wala hawawi, kama wale waliolemaa, wenye kusumbuliwa na ulemavu au maradhi ya kudumu; wala hawako wazuri sana au wabaya.” “Halikadhalika kwa mtazamo wa kiroho, watu huangukia katika makundi hayo hayo; kundi moja linapenda ukweli, kundi jingine ni la maadui wakaidi. Kundi la tatu linajumuisha wale wa kati na ndio wengi, ambao wala hawaupendi ukweli kama lile kundi la kwanza, wala sio maadui wa ukweli kama lile kundi la pili. Hawa ni watu ambao hawajaufikia ukweli, lakini kama wakionyeshwa ukweli hawatakataa kuukubali.” Kwa maneno mengine, kwa mtazamo wa Kiislamu na kwa mtazamo wa kifiqihi, wao sio Waislamu, lakini kwa hali halisi ni Waislamu. Hii ni kwamba wanaukubali ukweli na hawana ukaidi juu yake. Baada ya mgawanyo huu Ibn Sina anasema: “Amini kwamba rehema ya Mwenyezi Mungu hukizunguka kila kitu.” 52 Katika majadiliano juu ya wema na uovu wa al-Asfar, Mulla Sadra anataja nukta hii kama pingamizi: “Unasemaje kuwa wema huzidi uovu, na hali tukimuangalia hata mwanaadamu ambaye ndiye mbora wa viumbe vyote, 52 Al-Isharat, mwishoni mwa sehemu ya saba (nama) 115

7/15/2011

12:42 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini tunaona kwamba watu wengi wamenasa katika matendo maovu kwa kigezo cha mazoea yao, wamezama katika imani dhaifu, na ujinga mchanganyiko kwa kigezo cha imani zao hizo? Na matendo maovu na imani za potofu zitaiporomosha nafasi yao Siku ya Kiyama, na hivyo kuwafanya wastahili adhabu. Hivyo, hatma ya mwanaadamu, ambaye ni mbora wa viumbe ni uovu na mkosi.” Mulla Sadra katika kujibu pingamizi hili anaelekeza kwenye maneno ya Ibn Sina na kusema: “Katika maisha yajayo, watu watakuwa kama walivyo katika maisha haya kwa kigezo cha siha imara zao na furaha. Kama vile tu wale imara kabisa na wale wazuri kupita kiasi kwa upande mmoja, na halikadhalika wale wagonjwa sana na wabaya kupindukia, walivyo wachache katika dunia hii, wakati walio wengi ni wa kati na kati na kwa kiasi fulani wako imara, vivyo hivyo huko Akhera wale walio wakamilifu, ambao kwa maneno ya Qur’ani ni al-Sabiquun, au “walio mbele zaidi” na halikadhalika wanyonge ambao katika lugha ya Qur’ani ni as-hab alShimaal au ‘watu wa upande wa kushoto,’ ni wachache, na walio wengi ni watu wa wastani, ambao Qur’ani imewaita as-Habul Yamin au watu wa upande wa kulia.” Baada ya hapa Mulla Sadra anasema: “Hivyo watu wa rehema na wenye uimara ndio wengi, duniani na Akhera pia.” Mmoja wa wenye busara kabisa, huenda ni marehemu Aqa Muhammad Ridha Qumshi’i, alikuwa ana beti za kipekee za ushairi juu ya ukubwa wa rehema za Mwenyezi Mungu. Katika beti hizi anaakisi imani za wenye busara na upeo mkubwa wa msimamo wa watu wa Irifan (mystics) anasema: Fikiria vyote kuwa vya Mola, vilivyo kubaliwa na ambavyo havikukubaliwa. Kwa rehema kilianza, na kwa rehema kitarejea. Kutoka kwenye rehema, vilivyoumbwa ndiko 116

7/15/2011

12:42 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini vilikotokea, na vinakwenda kwenye rehema. Hii ni siri ya mahaba, ambayo inakanganya akili. Viumbe wote waliumbwa, pamoja na uasilia wa Upweke wa Mungu Mmoja. Ushirikina huu ni ziada, na ziada hupungua Siri ya ukweli endelea kuificha; Busara ndivyo huesma. Ni kipi akili inayodadisi itakifanya kwa upendo ambao huvutia pembeni mapazia? Fikiria kisa cha ambacho kilikuwa, na ambacho kitakuwa kwa kuwa kitone. Kitone hiki mara hupanda, na mara hushuka. Si chochote bali nilijitihadi kutunza amana, Imma muniite dhulumati, au muniite mjinga. Mjadala wa wenye busara unahusika kwenye maeneo madogo madogo ya hoja, sio makubwa. Hawajajadili vigezo vya kitendo kizuri ni nini au vigezo vya kukubaliwa kwa matendo, mjadala wao ni juu ya binadamu, kuhusu wazo ambalo kulizungumzia kiasi, kivitendo, watu walio wengi - kwa madaraja tofauti - ni wema, watabaki kuwa wema, watakufa wakiwa wema na watafufuliwa wakiwa wema. Wanachotaka kusema ni kuwa ingawa wale waliojaaliwa kuukubali Uislamu ni wachache, watu wana Uislamu wa maumbile (fitrah) na watafufuliwa na Uislamu wa maumbile ni wengi.

117

7/15/2011

12:42 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini Kwa imani ya wanaounga mkono mtazamo huu, kilichoelezwa kwenye Qur’ani juu ya Mitume kuwaombea watu ni juu ya wale watu ambao dini yao ni ya maumbile, na sio dini ya kutafutwa, ambayo, kwa sababu ya kutokuwa na uwezo hawakuifikia, lakini hawakuonyesha ukaidi.

DHAMBI ZA WAISLAMU Kuhusiana na dhambi za Waislamu, jambo hili lina sura kinyume kabisa na ile ya awali (juu ya amali njema za wasio Waislamu) na ni ukamilisho wa mjadala wa awali. Suala ni iwapo dhambi zilizofanywa na Waislamu ni sawa na dhambi za wasio Waislamu kuhusiana na adhabu, au la. Kuanzisha mjadala wa awali ilikuwa muhimu kutokana na mwelekeo wa kuwa kwake ni suala la imani ya kiakili, lakini kuanzisha mjadala huu ni umuhimu wa lazima, kwa sababu moja ya mambo katika kuanguka na kuangamia kwa jamii za Waislamu katika zama hizi, ni kibri na majivuno yasiyo na maana ambayo siku hizi yameenea na kukomaa miongoni mwa Waislamu wakiwemo pia Mashi’a wengi. Watu hawa wakiulizwa iwapo matendo ya wasio Mashia yanakubalika kwa Mwenyezi Mungu, wengi wao wanajibu ‘hapana.’ Na wakiulizwa ni hukumu gani kwa madhambi na maovu ya Mashia, wanajibu: “Yote husamehewa.” Kutokana na sentensi hizi mbili, inahitimishwa kwamba matendo hayana thamani; hayana thamani chanya wala hasi. Sharti muhimu na la lazima la kujihakikishia furaha na wokovu ni kwa mtu kujiita Shia, hilo tu basi. Kwa kawaida kundi hili hutoa hoja zifuatazo: Kwanza, kama dhambi zetu na za wale ambao sio Shia zitahesabiwa sawa sawa, basi kuna tofauti gani kati ya Shia na wasio kuwa Shia?

118

7/15/2011

12:42 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini Pili, kuna hadith inayoeleweka vizuri; “Kumpenda Ali ibn Abi Talib ni tendo jema ambalo hakuna tendo baya linaloweza kuliharibu.” Katika kuijibu hoja ya kwanza, lazima tuseme hapa kuwa tofauti kati ya Shia na wasiokuwa Shia huonekana dhahiri pindi Shi’a wanapofuata mpango ambao viongozi wake wamempa na wasiokuwa Shia nao wanafuata mafundisho ya dini yao. Kwa njia hii ubora wa Shia utakuwa dhahiri katika dunia hii na Akhera. Yaani, tofauti zitazamwe kwenye upande wa chanya na sio upande hasi. Tusiseme kwamba Shia na wasio Shia wakiyaweka pembeni (wakiyapuuza) mafundisho ya dini yao lazima kutakuwa na tofauti fulani kati yao – na kama hakuna tofauti katika hali hiyo, basi kuna tofauti gani kati ya Shia na wasiokuwa Shia? Mfano wake ni wagonjwa wawili ambao walipelekwa kwa madaktari, mmoja alipelekwa kwa daktari bingwa na mwingine kwa daktari mwenye ujuzi kidogo, lakini wanapoandikiwa dawa na maelekezo yake, hakuna anayezingatia maelekezo haya. Kisha mgonjwa wa kwanza analalamika kuna tofauti gani kati yangu na yule ambaye alipelekwa kwa daktari asiyekuwa bingwa? Kwa nini bado ninaumwa kama yeye, wakati mimi nilipelekwa kwa daktari bingwa na yeye alipelekwa kwa daktari asiye bingwa? Basi, kama ilivyo kwa mfano wa hawa wagonjwa wawili, sio sahihi kwetu kumtofautisha Ali ibn Abi Talib (a.s) na wengine kwa kusema kuwa kama tusipofuata amri zake, hatutadhurika, lakini wao, hata wakifuata au wasifuate maneno ya viongozi wao, watakuwa kwenye hasara. Mmoja wa masahaba wa Imam Ja’far ibn Muhammad as-Sadiq (a.s) alimwambia Imam: “Baadhi ya Shia wako wamepotoka na wanavifanya vilivyo haramu kuwa ni halali, wakisema dini ni kumtambua Imamu na si zaidi; hivyo ukishamtambua Imamu unaweza kufanya chochote unachotaka?” Imam As-Sadiq (a.s) akasema: “Kwa hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu na kwake ndio marejeo yetu. Hawa wasioamini wametafsiri yale 119

7/15/2011

12:42 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini wasioyoyajua kwa mawazo yao wenyewe.” Sentensi sahihi ni kuwa “Mtambue Imamu na kisha tenda matendo mema unayotaka, na itakubaliwa; kwani Mwenyezi Mungu hakubali amali bila mtendaji kumtambua Imamu.” 53 Muhamamd ibn Marid alimuuliza Imam Ja’far ibn Muhammad as-Sadiq (a.s) Je, ni kweli kuwa umesema kwamba ukishamtambua Imamu basi fanya vyovyote utakavyo?” Imam akasema. “Ndio ni sahihi.” Akasema, “Tendo lolote hata zinaa, wizi au kunywa pombe?” Imam (a.s) akasema, “Sisi ni wa Mwenyezi Mungu na kwake ndio marejeo yetu. Ninaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kuwa wametutendea vibaya. Sisi Maimamu wenyewe tunawajibika kwa matendo yetu; vipi jukumu linaweza kuondolewa kwa Shia wetu? Nilichosema ni kuwa ukishamtambua Imamu, fanya chochote unachopenda katika matendo mema, kitakubaliwa.” 54 Na kuhusiana na hadith isemayo: “Kumpenda Ali ibn Abi Talib (a.s) ni tendo jema ambalo hakuna tendo ovu litakaloliharibu,” lazima tuangalie ni nini tafsiri yake. Mmoja wa wanachuoni mashuhuri nafikiri alikuwa Wahid Bihbahani ameitafsiri hadith hii vizuri sana. Anasema kuwa maana ya hadith hii ni kuwa ikiwa mtu mapenzi yake kwa Ali ibn Abi talib (a.s) ni ya kweli, hakuna dhambi itakayomdhuru. Hii ni kuwa ikiwa upendo kwa Ali ibn Abi Talib (a.s) ambaye ni mfano wa ukamilifu wa ubinadamu uaminifu, utii kuwatumikia wengine na maadili ni wa dhati na usio na ubinafsi, utazuia kutenda madhambi, ni kama chanjo ambayo huongeza kinga ya mwili na huuzuia ugonjwa usimfikie aliyechanjwa. Kumpenda kiongozi kama Ali ibn Abi Talib (a.s), ambaye ni nembo ya matendo mema na uchamungu, humfanya mtu aipende tabia ya Ali ibn Abi Talib, huondoa fikra za kutenda dhambi kutoka katika akili yake, kwa shar53 Mustadrak al-Wasail, Juz. 1, uk. 24 54 al-Kafi, Juz. 2, uk. 464. 120

7/15/2011

12:42 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini ti kuwa upendo huo ni wa kweli. Haiwezekani kwa mtu anayemtambua Ali ibn Abi Talib (a.s) uchamungu wake, sala zake zilizojaa machozi, dua zake katikati ya usiku, na mtu anayempenda mtu huyu atende kinyume na amri zake, yeye ambaye mara zote aliwaamrisha wengine kuwa wachamungu na kufanya matendo mema. Mwenye kupenda yeyote huheshimu matakwa ya mpendwa wake na hutii amri za mpendwa wake. Utii kwa unayempenda ni matokeo muhimu ya upendo wa kweli, hivyo sio kwa Ali ibn Abi Talib (a.s) tu, upendo wa kweli kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) ni hivyo hivyo. Hivyo maana ya hadith kwamba upendo kwa Ali bin Abi Talib (a.s) ni tendo jema ambalo huzuia matendo mabaya kuleta madhara, hii ni kuwa huzuia kutokea kwake. Haionyeshi maana ambayo wajinga wameielewa, kwamba kumpenda Ali ibn Abi Talib (a.s) ni tiketi ambayo hata ukifanya madhambi, hayatakuwa na matatizo. Baadhi ya madarweshi kwa upande mmoja wanadai kumpenda Mwenyezi Mungu, lakini kwa upande wa pili wanatenda madhambi kuliko watenda madhambi wote, hawa pia wanatoa madai ya uongo. Imam Jafar (a.s) alisema: “Unamuasi Mwenyezi Mungu huku ukidai kumpenda. Hii (naapa) kwa maisha yangu ni amali isiyosadikika. Kama upendo wako ni wa kweli, ungemuitika; kwa hakika mwenye kupenda huonyesha utii kwa mpendwa wake.” Marafiki wa kweli wa Amirul Muuminina Ali ibn Abi Talib (a.s) walikuwa mara zote wakijiepusha na madhambi, uongozi wake (wilaya) uliwazuia kutenda madhambi, haukuyahimiza.”

121

7/15/2011

12:42 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini Imamu Muhammad Baqir (a.s) alisema: “Uongozi (ulezi) wetu haupatikani isipokuwa kwa matendo na uchamungu.” 55 Sasa tuangalie hadith zinazounga mkono nukta hii. Tawus al-Yaman anasema, “Nilimuona Ali ibn Husein (a.s) akitufu katika Nyumba ya Mwenyezi Mungu na alijishughulisha na ibada tokea wakati wa Isha hadi sehemu ya mwisho ya usiku. Alipojikuta peke yake, alitazama angani na kusema ‘Ewe Mwenyezi Mungu! Nyota zimetoweka kwenye upeo na macho ya watu yamelala, na milango Yako imefunguliwa kwa wale wanaotafuta …” 1. Tawus alisimulia sentensi nyingi juu ya hili kutoka kwenye ibada za unyenyekevu na dua za Imam (a.s) na alisema (kuhusiana na Imamu): “Mara nyingi katika kuomba dua kwake alilia.” Kisha (Tawus) akasema: “Kisha akapomoka na kusujudu ardhini. Nilimsogelea, akiweka kichwa chake kwenye magoti yangu, alilia sana. Machozi yangu nami yalitiririka na kudondokea usoni mwake. Aliinuka, akakaa na kusema: “Ni nani amenishughulisha ninapomkumbuka Mola wangu? Nikasema “Ni mimi Tawus, ewe mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, wasi wasi na fadhaa yote hii ya nini? Sisi ambao ni wenye dhambi ndio tungefanya haya. Baba yako ni Husein ibn Ali, mama yako ni Fatuma Zahra na Babu yako ni Mtume Muhammad (s.a.w.w) - yaani, kwa nasaba tukufu kama hii, na kiungo shariif kama hiki, kwa nini unajitia shida na wasi wasi?” Alinitazama na kusema: “Sivyo kabisa, ewe Tawus, sivyo kabisa, acha kuongelea juu ya nasaba yangu. Mwenyezi Mungu aliumba pepo kwa ajili ya wale wanaomtii na kutenda mema hata kama atakuwa mtumwa wa Ethiopia (Abyssinia), na aliumba moto kwa ajili ya wale wanaomuasi, hata kama atakuwa ni kijana wa Kiquraishi. Je haujayasikia 55 Biharul Anwar, juz. 12 122

7/15/2011

12:42 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini maneno ya Mwenyezi Mungu: ‘Hivyo baragumu litakapopulizwa, hakutakuwa undugu miongoni mwao, wala hawataulizana?’ Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu, hakuna kitakachokunufaisha kesho isipokuwa matendo yako mema uliyoyatanguliza.”56 2. Mtume (s.a.w.w), baada ya kuiteka Makka alipanda juu ya kilima cha alSafa na akaita, “Enyi watoto wa Hashim! Enyi watoto wa Abdul Muttalib!” Ukoo wa Hashim na Abdul Muttalib walijikusanya, walipotimia pamoja Mtume (s.a.w.w) aliwaambia: “Kwa hakika mimi ni Mjumbe wa mwenyezi Mungu kwenu; kwa hakika ninawatakia kheri. Msiseme Mtume Muhammad anatokana na sisi, kwani ninaapa kwa Mwenyezi Mungu, marafiki zangu kutoka miongoni mwenu na kutoka miongoni mwa watu ni wachamungu tu. Hivyo msinifanye niwaone Siku ya Kiyama mkiwa mmeibeba dunia mabegani mwenu, wakati wote wengine watakuwa wamebeba Akhera. Sijaacha kusema lolote hivyo hakuna kisingizio baina yangu na baina yenu, na baina ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na nyinyi. Kwa hakika mimi nina matendo yangu na nyinyi mna matendo yenu.” 57 3. Vitabu vya historia vimeandika kwamba Mtume (s.a.w.w) katika siku za mwisho za uhai wake, alikwenda usiku katika makaburi ya Baqii na aliwaombea msamaha waliozikwa humo. Baada ya hapo aliwaambia masahaba zake, “Kila mwaka Jibril hunionyesha Qur’ani mara moja, na mwaka huu amenisomea Qur’ani mara mbili. Nafikiri hii ni ishara kuwa kifo changu kimekaribia.” Siku iliyofuata alikwenda kwenye mimbari na kutangaza, “Muda wa kifo changu umekaribia. Yeyote ambaye nimemuahidi kitu aje ili niitekeleze ahadi, na yeyote anayenidai aje ili nimlipe.” Kisha aliendelea kusema: 56 Biharul Anwar, Juz. 11, uk. 25, sura ya maadili ya Imam wa nne 57 Biharul Anwar (chapa ya Akhundi), Juz. 21, uk. 111, kutoka sifa za Shia cha Shaykh Saduq 123

7/15/2011

12:42 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini “Enyi watu! Kwa hakika hakuna undugu kati ya mtu yeyote na Mwenyezi Mungu wala hatamlipa yeyote wema isipokuwa kwa mujibu wa matendo yake. Basi yeyote asidai wala kutaka vinginevyo. Ninaapa kwa Yule aliyenileta na ukweli, hakuna kitakachowapa wokovu isipokuwa matendo mema pamoja na rehema, na hata mimi kama ningeasi, ningeangamia. Ewe Mwenyezi Mungu nimefikisha.” 58 4. Imam Ali ibn Musa al-Ridha (as) alikuwa na ndugu yake aliyeitwa Zayd al-Naar. Tabia ya ndugu huyu wa Imam ilikuwa haimridhishi Imam. Siku moja, wakati huo ambapo Imam alikuwa Marw, Zayd alikuwepo katika mkusanyiko ambao ndani yake kulikuwa watu wengi waliokuwa wanazungumza. Imam alipokuwa anazungumza, aligundua kuwa Zayd alikuwa akiongea na kundi la watu juu ya daraja la watu wa Nyumba ya Mtume, na kwa majivuno alikuwa kila mara akisema, “Sisi hivi…, sisi vile…” Imam alimkatisha maneno yake na kumwambia Zayd: “Ni vitu gani hivi unavyozungumza? Ikiwa unayosema ni kweli na kizazi cha Mtume (s.a.w.w) wana daraja la pekee, yaani, kama Mwenyezi Mungu hatawaadhibu waovu kutoka kizazi cha Mtume, basi wewe una daraja kubwa zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu kuliko baba yako Musa bin Jafar (a.s), kwa sababu alikuwa akimuabudu Mwenyezi Mungu mpaka akafikia daraja ya ukaribu na Mwenyezi Mungu, wakati wewe unafikiri kuwa bila ibada unaweza kufikia daraja la Musa ibn Jafar (a.s).” Kisha Imam (a.s) akamgeukia Hassan ibn Musa al-Washsha, mmoja wa wanazuoni wa Kufah aliyekuwepo katika mkusanyiko huo, akasema: “Wanazuoni wa Kufah wanaisomaje aya hii: “Ewe Nuh! Kwa hakika huyu si katika familia yako ni mtendaji wa maovu” Alijibu: Wanaisoma hivi: “yaani kuwa, sio mtoto wako, na hatokani na mbegu yake; ni mtoto wa mwanaume muovu” 58 Sharh Nahjul Balagha ya Abil Hadid, Juz. 2, uk.863 124

7/15/2011

12:42 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini Imam (a.s) akasema: “Sivyo ilivyo. Wanaisoma aya visivyo na wanaitafsiri visivyo. Maana ya aya ni kuwa: “Huyu mtoto wako mwenyewe hafai. Alikuwa mtoto wa Nuh; alifukuzwa kwa Mwenyezi Mungu na alizamishwa majini kwa sababu yeye mwenyewe hakuwa muongofu, japokuwa alikuwa mtoto wa Nabii Nuh (a.s).” Hivyo, kuwa unatokana na kizazi cha Mtume au Imam sio sababu ya kuweza kunufaika, amali njema zinatakiwa.”59

HALI YA KIMAUMBILE NA HALI YA KIDESTURI Kwa kawaida, watu wanalinganisha kanuni za Mwenyezi Mungu katika maumbile, thawabu na adhabu, na wokovu na adhabu, (hulinganisha) na kanuni za kijamii za binadamu, ingawa mambo haya yanaafikiana na mazingira ya kimaumbile na hali halisi, na ni katika sehemu yao, wakati ambapo mazingira ya kijamii na kanuni hufuata sheria za kidesturi zilizotengenezwa na watu. Kanuni za kijamii zinaweza kufuata mazingira ya kawaida, lakini kanuni za maumbile, na miongoni mwazo thawabu na adhabu ya Mwenyezi Mungu, haziwezi kufuata mazingira haya, na badala yake hufuata masharti ya kimaumbile. Ili kufafanua tofauti kati ya mfumo wa kimaumbile na mfumo wa kidesturi, hebu tuangalie mfano huu: Tunajua kuwa katika mifumo ya kijamii, kila nchi ina sheria na kanuni zake za kipekee. Kanuni za kijamii, katika baadhi ya masuala, hutofautisha kati ya watu wawili japo wako sawa kwa masharti ya kimwili na kimaumbile, lakini wako tofauti kuhusiana na hali ya kidesturi. Kwa mfano, wakati wanapotaka kuajiri mtu fulani nchini Iran, ikiwa Muiran na Muafghani wataomba kazi hiyo na wote wako sawa katika hali za kimaumbile, inawezekana Muiran akaajiriwa badala ya Muafghani, kwa 59 Biharul Anwar, Juz. 10, uk. 65 125

7/15/2011

12:42 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini sababu tu sio Muiran. Hapa Muafghani anaweza kusema niko sawa kabisa kimaumbile na Muiran, aliyeajiriwa kama ana afya, mimi pia nina afya, kama ni kijana mimi pia ni kijana, kama ni bingwa katika fani hii na ile, mimi pia ni bingwa atajibiwa kuwa kanuni za kiutawala hazituruhusu kukuajiri wewe. Kwa kutengemea juu ya uamuzi wa kidesturi na maamuzi yaliyotengenezwa na watu, hadhi ya Muafghani huyu huyu inaweza kubadilika na kuwa kama wengine, yaani anaweza kuomba na kupata uraia wa Iran. Ni wazi kuwa makaratasi ya uraia hayajambadilisha chochote katika haiba yake, lakini kwa mtazamo wa kanuni za kijamii, amekuwa mtu mwingine. Kwa kawaida, uzingatiwaji wa mazingira ya kidesturi hufuatana pamoja na kukosekana uzingatiaji wa usawa katika mazingira halisi na ya kimaumbile. Lakini katika masuala ambayo hayafuati kanuni za kijamii na za kidesturi badala yake yanafuata tu mazingira ya kimaumbile, hali ni tofauti. Kwa mfano – Mwenyezi Mungu aepushilie mbali – kama maradhi au ugonjwa wa mlipuko utakuja Iran, hauwezi kutofautisha kati ya raia wa Iran na yule wa nchi nyingine. Ikiwa Muirani na Muafghani wako sawa kitabia na kimazingira, na hali nyingine zote, haiwezekani bakteria anayesababisha maradhi akabagua na aseme kwamba kwa vile Muafghani sio raia wa nchi hii nimuache tu sina haja naye. Hapa suala ni la uumbaji na maumbile, sio jamii na desturi za kijamii, suala linahusiana na maumbile sio utungaji wa sheria na kanuni. Sheria za Mwenyezi Mungu kuhusiana na malipo na adhabu na wokovu na laana ya milele kwa watu binafsi zinategemea kwenye hali halisi na za kimaumbile. Sio suala la kwamba ikiwa mtu atadai “Mimi jina langu limeandikwa katika rejista ya Uislamu na ni Mwislamu kwa jina basi lazima nipewe huduma maalumu,” basi itakubaliwa juu yake.

126

7/15/2011

12:42 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini Kusiwe na mkanganyiko hapa; tunashughulishwa hapa na suala la malipo na adhabu, wokovu na kulaaniwa, na ada ya Mwenyezi Mungu katika kuwatendea waja Wake; hatuzungumzii juu ya sheria ambazo Uislamu umezihukumu katika maisha ya kijamii ya Waislamu. Hapana shaka kwamba sheria za Uislamu, kama sheria nyingine zote duniani, ni mfululizo wa sheria za kawaida, na pia mfululizo wa mazingira ya kawaida yamezingatiwa. Na katika sheria hizi ambazo zinahusiana na maisha ya kidunia, wanaadamu, imewalazimu, kufuata mwelekeo wa hali ya kidesturi. Lakini matendo ya Mwenyezi Mungu, na utendaji wa utashi wa Mwenyezi Mungu katika mfumo wa uumbaji – ikiwa ni pamoja na kutoa wokovu na kuelekeza kwenye laana ya watu binafsi, na kuwalipa na kuwaadhibu – hayafuati kanuni za kijamii, na badala yake ni za aina tofauti kabisa. Mwenyezi Mungu katika kutekeleza utashi Wake kamili, hatendi juu ya misingi ya kanuni za kawaida. Masuala ya kawaida ambayo yana athari kubwa katika mfumo wa kijamii hayana kazi yoyote katika utashi wa kiuumbaji wa Mwenyezi Mungu. Kutokana na mtazamo wa kanuni ambazo Uislamu umetunga kuhusiana na mienendo ya wanaadamu, pindi mtu anapotamka shahada mbili,60 atatambuliwa kuwa Mwislamu na atanufaika na fursa za Uislamu. Lakini kwa mujibu wa kanuni za Akhera na kwa mtazamo wa mwenendo wa Mwenyezi Mungu, sheria za:

60 Ikiwa na maana kwamba mtu anashuhudia kwamba hakuna kiumbe au mungu anayefaa kuabudiwa isipokuwa Allah na Muhammad ni Mtume na Mjumbe Wake. (mtarujuma wa Kiingereza) 127

7/15/2011

12:42 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini

“Yeyote anayenifuata, anatokana na mimi,” Qur’ani Tukufu, 14:36. Na:

“Kwa hakika aliye mbora zaidi mbele Mwenyezi Mungu ni yule mchamungu zaidi.” Qur’ani Tukufu, 49:13. Mtume (s.a.w.w) amesema: “Enyi watu! Kwa hakika baba yenu ni mmoja, na Mola wenu ni mmoja. Nyinyi wote mnatokana na Adam, na Adam alitokana na udongo (vumbi). Hakuna ubora wa Mwarabu juu ya asiyekuwa Mwarabu isipokuwa kwa uchamungu.” 61 Salman Farsi aliyejitahidi sana kuufikia ukweli alifikia daraja ambalo Mtume (s.a.w.w) alimwambia: “Salman ni miongoni mwetu, Ahlul Bayt.” Wapo walioingia katika ushawishi wa minong’ono ya shetani na ambao wameridhika na fikra kuwa: “Jina letu ni miongoni mwa majina ya marafiki wa Ali bin Abi Talib (a.s). Vyovyote tuwavyo, tunahesabika kuwa wafuasi wake. Au tutaweka wosia kuwa kiasi kikubwa cha fedha tulizozipata kwa ajili za haramu au ambazo tungekuwa tuzitumie wakati wa uhai wetu katika njia za heri - lakini hatukuzitumia - wapewe waangalizi wa makaburi matakatifu ili tuzikwe karibu na watakatifu wa Mwenyezi Mungu ili malaika wasithubutu kutuadhibu.” 61 Tarikh Ya’qubi, Juz. 2, uk. 110 128

7/15/2011

12:42 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini Watu kama hawa wajue kuwa wamepofuka na pazia la kutojali limefunika macho yao. Macho yao yatafunguka watakapojikuta wamezamishwa katika adhabu ya Mwenyezi Mungu na watajuta sana kiasi kwamba kama ingekuwa inawezekana kufa wangekufa mara elfu. Hivyo waamke kutoka usingizini, usingizi wa uzembe leo, watubie, na wayafidie yaliyowapita.

“Na waonye juu ya siku ya majuto, jambo litakapoamuliwa wakiwa hawana habari na hawaamini.” Qur’ani Tukufu, 19:39 Kwa mtazamo wa Qur’ani na hadith, ni wazi kuwa muovu, hata kama ni Mwislamu, ataadhibiwa na Mwenyezi Mungu. Ni kweli, kwa vile ana imani baadaye atapata kuondolewa motoni, lakini baada ya miaka ya machungu na adhabu. Madhambi ya baadhi ya watu yatasafishwa kwa uchungu wa kufariki, kundi jingine watalipia fidia ya madhambi yao kaburini na barzakh (ulimwengu wa mpito kati ya dunia hii na akhera), kundi jingine litapata adhabu zake katika hofu na misukosuko ya kufufuliwa na ugumu wa kuhesabiwa matendo yao na bado wengine watakwenda motoni na kudumu huko kwa miaka kadhaa wakiadhibiwa. Imesimuliwa kutoka kwa Imam wa sita, Jafar as-Sadiq (a.s) kuwa aya:

“…Watadumu humo kwa zama.” Qur’ani Tukufu, 78:23 Inawahusu wale watakaopata uokovu kutokea motoni. 62 Hapa tutataja baadhi ya mifano ya hadith zinazozungumzia adhabu wakati wa kufa na baada ya kufa ili zitusaidie kujua, kuamka na kujiandaa kwa safari hiyo ya kuogofya na ya hatari iliyopo mbele yetu. 62 Biharul Anwar (chapisho la Kumpani), Juz. 3, uk. 376-7 129

7/15/2011

12:42 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini 1. Shaykh Kulayni anasimulia kutoka kwa Imam Ja’far (a.s) kuwa Ali ibn Abi Talib (a.s) kuna wakati alikuwa anaumwa jicho. Mtume (s.a.w.w) alikwenda kumuona katika wakati ambao Ali (a.s) alikuwa analia kwa maumivu. Akasema (Mtume) “Je kulia huku ni kwa sababu ya kukosa subira au kwa sababu ya ukali wa maumivu? Amirul Muminina Ali ibn Abi Talib (a.s) akajibu; “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, sijawahi kupata maumivu makali kama haya ya leo.” Mtume (s.a.w.w) akaanza kusimulia ugumu wa mambo na hali ya kutisha itakayowapata makafiri wakati wa kufariki. Kusikia hivi, Ali (a.s) akakaa na kusema; “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu hebu rudia maelezo haya kwani yamenifanya nisahau maumivu yangu. Kisha akauliza, “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kuna yeyote katika Ummah, wako atakayekumbana na kifo cha namna hii?” Akasema, “Ndiyo, Mfalme mkandamizaji, anayekula mali za yatima na anayetoa ushahidi wa uongo.” 63 Sheikh Saduq anasimulia katika kitabu ‘Man La Yahduruhu al-Faqih’ kuwa wakati Dharr, Mtoto wa Abu Dharr al-Ghiffar alipokufa, Abu Dharr alisimama pembeni ya kaburi lake, aliweka mkono wake juu ya kaburi na kusema: “Mwenyezi Mungu akurehemu; ninaapa kwa Mwenyezi Mungu ulikuwa mwema kwangu na sasa ulivyoniacha niko radhi nawe. Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu sina wasi wasi kwa kuondoka kwako, hakuna kilichopungua kwangu na simuhitaji yeyote ila Mwenyezi Mungu. Na isingekuwa kule kuhofia muda wa taarifa, ningetamani kwenda badala yako. Lakini sasa ninataka kufidia yale yaliyopita na kujiandaa na ulimwengu ujao, na bila shaka huzuni yangu kwa ajili yako imenizuia nisikuhuzunikie (yaani nimezama katika kufikiri kitu ambacho kingekunufaisha na hivyo sina muda wa kuhuzunikia kutengana kwetu). Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu kuwa sijalia kwa sababu ya kuondoka kwako bali nimelia kwa sababu ya kuwaza ni jinsi gani na ni mambo gani unayokabiliana nayo. Natamani kujua ulichosema na ulichoambiwa. Ewe Mwenyezi Mungu nimesamehe haki zangu ambazo zilikuwa wajibu kwa 63 Shaykh Abbas Qummi, Manzilul Akhirah, (chapisho la Islamiyya) uk. 5-6 130

7/15/2011

12:42 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini mwanangu, hivyo na Wewe pia msamehe haki Zako juu yake, kwani ukarimu unakufaa zaidi Wewe.” 64 Imam Ja’far (a.s) anasimulia kutoka kwa baba zake kuwa Mtume Muhamamd (s.a.w.w) alisema: “Kubanwa mbavu kaburini kwa muumini ni kufidia dhambi alizozifanya.” 65 Ali ibn Ibrahim anasimulia kuwa Imam Jafar as-Sadiq (a.s), kuhusiana na aya: “…na mbele yao ni kizuizi mpaka siku watakapofufuliwa.” Qur’ani Tukufu, 23:100. Alisema: “Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu siwahofii chochote isipokuwa Barzakh; kwani jambo linapofanywa kwa ajili yetu, tunakuwa na umuhimu zaidi kwenu.” 66 Yaani, kuwaombea kwetu kunahusiana na baada ya barzakh, hakuna uombezi ndani ya barzakh. Kwa ujumla kuna Aya nyingi za Qur’ani na hadith za wazi juu ya adhabu ya madhambi kama vile kusema uwongo, kusengenya, tuhuma za uwongo, usaliti, ukandamizaji, kupora mali za watu, kunywa pombe, kucheza kamari, kusambaza habari za watu, kuchafua sifa za watu, kuacha sala, kuacha kufunga, kuacha hijja kuacha Jihad, na mengineyo ambayo hatuwezi kuyahesabu. Haya sio kwa ajili ya wasioamini au wasio kuwa Shia tu, ni pamoja na Shia. Katika Kisa cha Miiraji (safari ya Mtume Mbinguni), tunakuta sehemu nyingi ambapo Mtume (s.a.w.w) anasema: “Niliyaona makundi mbali mbali ya umma wangu, wanaume na wanawake, katika sura mbali mbali, wakiadhibiwa kwa adhabu mbali mbali kwa sababu ya dhambi mbali mbali.” 64 Shaykh Abbas Qummi, Manzilul Akhirah, (chapa ya Islamiyya), uk. 24-25 65Biharul Anwar (chapisho la Kumpani), Juz. 3, uk. 153, kutoka Thawabul A’mal na al-Amali cha sheikh Suduq. 66 Biharul Anwar, Juz. 3, uk. 151 131

7/15/2011

12:42 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini

Mukhtasari Na Hitimisho. Kutokana na yote yaliyosemwa katika sehemu hii juu ya Matendo mema na mabaya ya Waislamu na wasiokuwa Waislamu, hitimisho linaweza kuwa hivi: 1. Vyote wokovu na adhabu vina viwango, wala sio watu wote watakaookoka wana madaraja sawa wala wale wa kuangamia (pia hawana viwango sawa). Viwango hivi vya tofauti vinaitwa darajaat ‘viwango vya kupanda) kuhusiana na watu wa Peponi na darakaat ‘viwango vya kushuka’ kuhusiana na wakazi wa Motoni. 2. Sio suala la kwamba watu wote wa Peponi watakwenda huko toka mwanzo, kama ambavyo watu wote wa motoni hawatakaa humo milele. Wakazi wengi wa Peponi watakwenda huko baada ya vipindi vigumu sana vya adhabu za Barzakh au Akhera. Mwislamu Shia na asiye Shia anapaswa kujua kuwa, ikiwa atakufa na imani safi, na ikawa - Mwenyezi Mungu aepushie mbali – kwamba alifanya madhambi, dhulma na uhalifu, ana hatua ngumu sana mbele yake, na baadhi ya madhambi yana hatari kubwa na yanaweza kumfanya mtu abakie motoni milele. 3. Watu ambao hawamwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, kwa kawaida hawafanyi matendo kwa nia ya kupanda juu kwa Mwenyezi Mungu, na maadamu hawafanyi vitendo kwa nia hii, basi hawasafiri kumuelekea Mwenyezi Mungu na Akhera. Hivyo kwa kawaida hawapandi juu kwa Mwenyezi Mungu na katika nyanja za juu, na hawafiki peponi. Yaani, kwa vile walikuwa hawasafiri kuelekea huko, hivyo hawataufikia mwisho huo. 4. Kama watu wanaomwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, watafanya vitendo kwa nia ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu, na wana dhati katika matendo yao, matendo yao yatakubaliwa na Mwenyezi Mungu na wanastahiki malipo yao na Pepo, wawe Waislamu au wasiwe Waislamu. 132

7/15/2011

12:42 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini 5. Wasio Waislamu wanaomwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho na wanafanya vitendo vizuri kwa nia ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu, kwa maana ya kutokuwa na baraka ya Uislamu, kwa kawaida wananyimwa kunufaika na mpango huu wa Mwenyezi Mungu. Ila sehemu ya matendo yao inayokubaliwa ni ile inayokwenda sawa na mpango wa Mungu, kama vile desturi nzuri za fadhila na huduma kwa viumbe wa Mungu. Lakini matendo ya kubuni ya ibada ambayo hayana msingi, kwa kawaida hayakubaliki, na mfululizo wa unyimwaji unaotokana na kutokuwepo na mpango kamili hutumika hutumika juu yao na kuwajumuisha. 6. Matendo mema yanayokubalika, yawe ya Mwislamu au mwingine yana huzuni fulani ambazo zinaweza kuja baadae na kuyaharibu. Juu ya mateso yote haya ni ukanushaji (ukweli), ukaidi na kufuru ya makusudi. Hivyo, kama watu wasiokuwa Waislamu watafanya matendo makubwa kwa nia ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu, lakini pindi ukweli wa Uisalmu ukiletwa kwao wataonyesha chuki binafsi na ukaidi na wakaweka pembeni haki na kutafuta ukweli, matendo yote yale mazuri yanabatilika (na kuwa sifuri), “kama majivu yanavyopulizwa na upepo mkali katika siku ya tufani.� 7. Waislamu na wale wote wengine waumini wa kweli katika Mungu Mmoja, kama wakitenda maovu na kuruka mipaka na wakausaliti mwelekeo wa kimatendo wa mpango wa Mwenyezi Mungu, wanastahili adhabu ya muda mrefu huko Barzakh na Siku ya Hukumu, na kwa baadhi ya madhambi kama kumuua muumini asiye na hatia kwa makusudi wanaweza kubaki motoni milele. 8. Matendo mema ya watu ambao hawamwani Mwenyezi Mungu na Siku ya Hukumu na pengine wakamshirikisha Mwenyezi Mungu yatafanya adhabu yao ipunguzwe na pengine iondolewe. 9. Furaha (ya peponi) na kuangamia (motoni) ni kwa mujibu wa mazingira halisi na ya kimaumbale, sio mazingira ya kawaida na ya kibinadamu. 133

7/15/2011

12:42 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini 10. Aya na Hadith zinazoonyesha kuwa Mwenyezi Mungu hukubali matendo mema, haziangalii wema wa matendo tu, kwa mtazamo wa Uislamu, kitendo huwa na thamani kinapokuwa na wema wa pande mbili, unaotokana na kitendo na unaotokana na mtendaji. 11. Aya na Hadith zinazoonyesha kuwa vitendo vya wale wanaokana Utume na Uimamu, havikubaliwi, zinafanya hivyo kwa mtazamo kuwa wanafanya hivyo kwa ukaidi huku wakiujua ukweli, lakini kukanusha kunakotokana na kukosa kukiri kwa sababu ya kutokuwa na uwezo (qusur) ndiko kunakozungumziwa na Aya na Hadith hizi. Kwa mtazamo wa Qur’ani wakanushaji hao wanahesabika kuwa mustadhaf (wasio na nguvu) na murjawn li’amrillah (wanaosubiri amri ya Mwenyezi Mungu). 12. Kwa mtazamo wa baadhi ya wafasiri wa Kiislamu kama Ibn Sina na Mulla Sadra, wengi wa ambao hawajaukiri ukweli hawana uwezo na watasamehewa, kama watu hawa hawamjui Mungu, hawataadhibiwa ingawa pia hawatakwenda Peponi, na kama wakimwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho na kufanya matendo mema kwa nia ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu, watalipwa matendo yao. Watakaoadhibiwa ni wale tu waliofanya kwa makusudi. Ewe Mwenyezi Mungu! Ufunge mwisho wetu kwa wema na furaha, na utufishe tukiwa Waislamu na tuweke pamoja na watu wema, Muhammadi na kizazi chake kitukufu (s.a.w.w).

134

7/15/2011

12:42 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini

ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION 1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9. 10. 11. 12. 13. 14. 15. 16. 17. 18. 19. 20. 21. 22. 23. 24. 25. 26.

Qur'an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Thalathini Uharamisho wa Riba Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili Hekaya za Bahlul Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.) Hijab vazi Bora Ukweli wa Shia Ithnaashari Madhambi Makuu Mbingu imenikirimu Abdallah Ibn Saba Khadijatul Kubra Utumwa Umakini katika Swala Misingi ya Maarifa Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia Bilal wa Afrika Abudharr Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu Salman Farsi Ammar Yasir Qur'an na Hadithi Elimu ya Nafsi Yajue Madhehebu ya Shia Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur'an Tukufu 135

7/15/2011

12:42 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini 27. 28. 29. 30. 31. 32. 33. 34. 35. 36. 37. 38. 39 40. 41. 42. 43. 44. 45. 46. 47. 48. 49. 50. 51. 52. 53. 54. 55. 56. 57.

Al-Wahda Ponyo kutoka katika Qur'an. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii Mashukio ya Akhera Al Amali Dua Indal Ahlul Bayt Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna. Haki za wanawake katika Uislamu Mwenyeezi Mungu na sifa zake Amateka Na Aba'Khalifa Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) Adhana. Upendo katika Ukristo na Uislamu Nyuma yaho naje kuyoboka Amavu n’amavuko by’ubushiya Kupaka juu ya khofu Kukusanya swala mbili Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Kusujudu juu ya udongo Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s) Tarawehe Malumbano baina ya Sunni na Shia Kupunguza Swala safarini Kufungua safarini Umaasumu wa Manabii Qur’an inatoa changamoto as-Salaatu Khayrun Mina -'n Nawm Uadilifu wa Masahaba Dua e Kumayl Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu 136

7/15/2011

12:42 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini 58. 59. 60. 61. 62. 63. 64. 65. 66. 67. 68. 69. 70. 71. 72. 73. 74. 75. 76. 77. 78. 79. 80. 81. 82. 83. 84. 85. 86.

Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mitume Muhammad (s) Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili Kuzuru Makaburi Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita Tujifunze Misingi Ya Dini Sala ni Nguzo ya Dini Mikesha Ya Peshawar Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu Ubora wa Imam 'Ali Juu ya Maswahaba Na Ushia ndio njia iliyonyooka Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake Liqaa-u-llaah Muhammad (s) Mtume wa Allah Amani na Jihadi Katika Uislamu Uislamu Ulienea Vipi? Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) Urejeo (al-Raja’a ) Mazingira Utokezo (al - Badau) Sadaka yenye kuendelea Msahafu wa Imam Ali 137

7/15/2011

12:42 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini 87. 88. 89. 90. 91. 92. 93. 94. 95.

Uislamu na dhana Mtoto mwema Adabu za Sokoni Johari za hekima kwa vijana Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu Tawasali Imam Mahdi katika Usunni na Ushia

96.

Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu

97.

Hukumu ya kujenga juu ya makaburi

98.

Swala ya maiti na kumlilia maiti

99.

Shiya na Hadithi (kinyarwanda)

100.

Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu

101.

Hadithi ya Thaqalain

102

Fatima al-Zahra

103.

Tabaruku

104.

Sunan an-Nabii

105.

Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza)

106.

Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili)

107.

Mahdi katika sunna

108.

Kusalia Nabii (s.a.w)

109.

Ujumbe -Sehemu ya Kwanza

110.

Ujumbe - Sehemu ya Pili

111.

Ujumbe - Sehemu ya Tatu

112.

Ujumbe - Sehemu ya Nne

113.

Ngano ya kwamba Qur’ani imebadilishwa 138

7/15/2011

12:42 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini 114.

Iduwa ya Kumayili.

115.

Maarifa ya Kiislamu.

116.

Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza

117.

Ukweli uliopotea sehemu ya Pili

118.

Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu

119.

Ukweli uliopotea sehmu ya Nne

120.

Ukweli uliopotea sehmu ya Tano

121.

Johari zenye hekima kwa vijana

122.

Safari ya kuifuata Nuru

123.

Idil Ghadiri

124.

Myahudi wa Kimataifa

125.

Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi

126.

Visa vya kweli sehemu ya Kwanza

127.

Visa vya kweli sehemu ya Pili

128.

Muhadhara wa Maulamaa

129.

Mwanadamu na Mustakabali wake

130.

Imam Ali binamu ya Mtume Sehemu ya Kwanza

131.

Imam Ali binamu ya Mtume Sehemu ya Pili

132.

Khairul Bariyyah

133.

Uislamu na mafunzo ya kimalezi

134.

Vijana ni Hazina ya Uislamu.

135.

Yafaayo kijamii

136.

Kusoma sura zenye Sijda ya wajibu

137.

Taqiyya

138.

Vikao vya furaha

139.

Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje? 139

7/15/2011

12:42 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini 140.

Uislamu na Mazingatio Sehemu ya Kwanza

141.

Uislamu na Mazingatio Sehemu ya Pili

142.

Azadari-Kuhuzunika na Kuomboleza

143.

Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah

144.

Mtazamo Mpya - Wanawake katika Uislamu

145.

Kuonekana kwa Allah

146.

Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza)

147.

Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili)

148.

Ndugu na Jirani

149.

Ushia ndani ya Usunni

150.

Maswali na Majibu

151.

Mafunzo ya hukmu za ibada

152.

Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisusunni No 1

153

Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisusunni No 2

154.

Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisusunni No 3

155.

Abu Huraira

156.

Kati ya Alama kuu za dini Swala ya Jamaa.

157.

Mazingatio kutoka katika Qur’an sehemu ya Kwanza

158.

Mazingatio kutoka kaitka Qur’an sehemu ya Pili

159.

Mazingatio kutoka katika Uislamu sehemu ya kwanza

160.

Mazingatio kutoka katika Uislamu sehemu ya Pili

161.

Hukumu zinazomuhusu mkuu wa kazi na Mfanyakazi

162.

Falsafa ya mageuzi ya Imam Husein (a.s)

163.

Huduma ya Afya katika Uislamu

164.

Hukumu za Mgonjwa 140

7/15/2011

12:42 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini 165.

Falsafa ya Mageuzi ya Imam Husein

166.

Uislamu Safi

167.

Majlis ya Imam Husein

168.

Mshumaa

169.

Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

170.

Uislam wa Shia

171.

Amali za Makka

172.

Amali za Madina

173.

Uislamu na mfumo wa Jamii ya dini nyingi

174.

Sira ya Imam Ali kuhusu Waasi

175.

Ukweli uliofichika katika neno la Allah

176.

Elimu ya Tiba za Kiislam Matibabu ya Maimamu

177.

Falsafa ya Dini

178.

Visa vya wachamungu

141

7/15/2011

12:42 PM


Uislamu na dhana ya

mfumo wa Jamii ya dini nyingi = PROOFREAD BY =RSKShemahimbo.qxd

Uislamu na Uwingi wa Dini

BACK COVER Kitabu hiki kinazungumzia suala muhimu sana la kuvumiliana hususan katika dini. Mara nyingi tumesikia katika nchi mbalimbali watu wakipigana na kuuana kwa sababu ya tofauti za itikadi zao za kidini. Baadhi ya wafuasi wa dini ni wachokozi na wengine wanashindwa tu kuwavumilia wenzao au itikadi za dini nyingine. Hii ni tabia ambayo imejengeka tu kwa watu, na wakati mwingine maadui wa dini hutumia mianya hii kuwagombanisha waumini wa dini moja au wa dini mbalimbali ili kukidhi malengo yao ya kisiasa. Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Nukushi: +255 22 2127555 Barua Pepe: alitrah@raha.com Tovuti: www.ibn-tv.com Katika mtandao: www.alitrah.info

142

7/15/2011

12:42 PM


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.