Ukweli uliofichika katika neno la allah

Page 1

Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

UKWELI ULIOFICHIKA KATIKA NENO LA ALLAH Machimbuko Mapya kutoka kwenye Baadhi ya Aya za Qur’ani

Kimeandikwa na: Sayyid Mujtaba Musavi Lari

Page A


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

B

7/16/2011

11:52 AM

Page B


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

ŠHaki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: 978 - 9987 - 17 - 012 - 8

Kimeandikwa na: Sayyed Mujtaba Musavi Lari

Kimetajumiwa na: Al-Hajj Ramadhani Salehe Kanju Shemahimb Kimehaririwa na: Al-Hajj Hemedi Lubumba (Abu Batul) Kimepangwa katika Kompyuta na: Hajat Pili Rajab Toleo la kwanza: Oktoba,2011 Nakala: 1000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Nukushi: +255 22 2127555 Barua Pepe: alitrah@raha.com Tovuti: www.ibn-tv-com Katika mtandao: w.w.w.alitrah.info

11:52 AM

Page C


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

NENO LA MCHAPISHAJI Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya Kiswahili ya kitabu cha Kiingereza kiitwacho, Hidden Truths in God’s Word, kilichoandikwa na Sayyid Mujtaba Musavi Lari. Sisi tumekiita, Ukweli Uliofichika katika Neno la Allah. Ukweli uliofichika katika neno la Allah - mwandishi alitumia maneno haya kwa kumaanisha Qur’ani Tukufu ambayo ni Ufunuio wa mwisho kwa mwanadamu kutoka kwa Muumba Wake kupitia kwa Mtukufu Mtume wa Uislamu. Mwandishi wa kitabu hiki amejaribu kufichua siri nyingi zilizomo katika baadhi ya aya za Qur’ani Tukufu na kuweka umuhimu mkubwa katika kuitafakari hii Qur’ani, kwani ni Mwongozo kwa wanadamu wote katika maisha yao ya hapa ulimwenguni na kesho Akhera. Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote, ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni mambo ambayo hayana nafasi tena katika akili za watu. Kutokana na ukweli huo, Taasisi ya Alitrah Foundation imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili. Tunamshukuru ndugu yetu, Al-Hajj Ramadhani Salehe Kanju Shemahimbo kwa kukubali jukumu hili la kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile

Page D


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake. Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa ni changamoto kubwa kwa wasomaji wetu. Mchapishaji: Al-Itrah Foundation

Page E


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

1

7/16/2011

11:52 AM

Page 1


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah

Utangulizi Hotuba, na uwezo wa kuwasiliana kupitia mazungumzo ni moja ya maajabu ya maumbile. Ni kupitia neema hii na uwelekevu huu ambapo wanadamu wanakuwa na uwezo wa kuanzisha mahusiano mmoja na mwingine, chochote kile mtu anachotaka kuwasilisha kinatolewa kwa urahisi kutoka ndani kabisa ya akili yake na kuchangiwa na wengine kupitia maongezi. Hali kadhalika, yule msikilizaji anakuwa na uwezo wa kutumia njia hiyo hiyo kuleta majibu yake mwenyewe na kuelezea fikra na mawazo yake kwenye hadhara yake. Kwa hiyo maneno na sentensi hudhihirisha nia na makusudio ya mzungumzaji na ndio njia ambayo kwayo anawasiliana na wenzake. Kwa namna nyingine, maneno ya Mwenyezi Mungu ni yale yale, hata hivyo, kuelewa ile maana iliyokusudiwa ya maneno ya Mwenyezi Mungu ndani ya Qur’ani – ambako kumekuwa ni chanzo cha mabadiliko makubwa katika historia ya mwanadamu – kunahitajia mawazo mazito na tafakari. Tafakari hii isije ikachafuliwa na mapendekezo, uharibifu na mawazo na dhana za kabla kwa sababu aya hizi zimekuja kutoka kwenye chanzo cha milele cha hekima, na ujumbe wake wote unalengwa kwenye ukweli usioweza kuharibiwa na madhubuti, ambao ni Mwenyezi Mungu. Hakika miyonzi ya elimu ya Mwenyezi Mungu inamulika ukamilifu wa maumbile yote. Kwa vile aya za Mwenyezi Mungu kimsingi zimezungumziwa kwa wanadamu, maana zake kuu na zisizoharibiwa kwa namna fulani ni lazima zishushwe katika mchangamano wake kwa namna ambayo inatilia maanani ukomo wa akili ya mwanadamu, uwezo na ujuzi ili kwamba ule ukweli mgumu ambao zinaubeba uweze kueleweka kwa kawaida. Huenda pengine ni kwa sababu hii ambapo kwamba Mwenyezi Mungu anatumia 2

Page 2


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah neno “Nuzul” (shuka) pale anaporejea kwenye maneno Yake. Kasha la kwanza kwa ajili ya kushuka kwa wahyi lilikuwa ni moyo mtukufu wa Mtume wa Mwisho (s.a.w.w.) na alikuwa ni mwanadamu tu aliyekuwa na uwezo wa kuuhimili wahyi moja kwa moja kutoka kwenye chanzo chake, na akafaulu kuelewa yaliyomo ndani yake.

“Hakika yeye ameiteremsha Qur’ani moyoni mwako kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, inayosadikisha yale yaliyokuwa kabla yake, na ni uongozi na bishara kwa waumini.” (al-Baqarah; 2:97) Na kwa wanadamu wote waliobakia ambao maneno ya Mwenyezi Mungu yanaelekezwa kwao, wanajifunza aya za Qur’ani kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Hii ni hatua ya mbele zaidi ya urahisishaji na ushukaji ili zile aya zipate kueleweka vizuri zaidi. Ndani ya Qur’ani, Mwenyezi Mungu ameweka fikra na uhalisia ambao unavutia kwenye tofauti ya viwango vyinavyotofautiana vya akili ya wanadamu na mawazo, na ujumbe wake unakuwa mng’aavu zaidi sanjari na ukuaji wa elimu ya mwanadamu. Mwanafikra mashuhuri mkubwa kama Mulla Sadra anapata kutoka kwenye aya ya Qur’ani dhana ya ‘burhan al-siddiqin’ katika tasnifu yake juu ya ‘hikmat al-muta’aliya’ – falsafa iliyozidi.

“Tutawaonyesha ishara zetu katika upeo wa mbali na katika nafsi zao mpaka iwabainikie kwamba haya ni kweli …..” (41:53) 3

Page 3


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah Kadhalika, wasomaji wengine wanaweza wakapata maamuzi kutoka kwenye aya hii kuhusu uhalisia wa Tawhiid kulingana na viwango vyao vya uelewa na akili zao. Mwenyezi Mungu anaendelea kuwataka waja wake kufikiri na kutaamali juu ya aya ya Qur’ani – ambayo ndio chanzo kitajiri sana na kilichokamilika, cha elimu kilichopo mikononi mwa wanadamu – na kwa namna fulani inaagiza kwamba ukweli unatafutwa kwa kupitia kutafakari kwa kina kizito. Kwa hiyo ili kuyaelewa maneno ya Mwenyezi Mungu, wanachuoni, zaidi kuliko mtu mwingine yeyote, wao wamewekwa wazi kwenye elimu isiyo na mipaka iliyoko ndani ya hotuba Yake. Mvuto wake wa kushangaza katika nyanja na mawanda mbali mbali inawavuta kwenda kunufaika nayo kwa kiwango cha uwezo wa akili zao. Kutokana na upana wa hazina yake ya kiroho, wanachuoni wa Kiislam katika zama tofauti wametoa tofauti ya maoni kuhusu yaliyomo ndani ya Qur’ani. Kwa kweli, chanzo kikubwa kama hicho na kisicho na ukomo hakiwezi kudhaniwa kwamba ni matokeo ya habari zilizokuwepo wakati wa Wahyi, kwa sababu kina habari kuhusu siri za maumbile na matukio ya nje ambayo yalikuwa hayawezekani kwa mwanadamu kujua kwa wakati ule. Qur’ani inasema:

“Je, hawaizingatii Qur’ani? Au kwenye nyoyo kuna makufuli?” (Surat Muhammad; 47:24).

4

Page 4


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah Maneno haya matatu, “Tadabbur” tafakari, “Qulub” nyoyo, na “Aqfal” makufuli, yanaonyesha nafasi maalum ya Qur’ani, huu muujiza wa milele, katika maisha ya mwanadamu. Aya hizo za Qur’ani zinamtaka mwanadamu kutafakari kwa kina ili aweze kufikia kwenye sera bora zaidi, na kufungua pingu za ujinga na kutojitambua na badala yake kuunururisha moyo. Zinamhimiza kuchunguza maumbile kwa vikomo vyake ili aweze kugundua mipaka ya kile kilichoko nje ya mipaka hiyo. Lengo la Qur’ani sio kutatua yale mambo yaliyo tofauti ya udadisi wa mwanadamu, kwa sababu maudhui hizi ziko nje ya uwanja wa kitabu cha muongozo. Hata hivyo, kwa kuhamasishwa na Qur’ani, ambayo kwa uchangamfu kabisa inalitukuza neno lililoandikwa na ukusanyaji wa elimu, ummah wenye ubunifu na hali ya shauku, ambao umekuja kuwa na elimu ya kushangaza na heshima yalitiwa moyo. Na mabadiliko makubwa ambayo yaliongoza kugeukia kwenye tofauti nyinginezo yanadaiwa shukurani kwenye ujumbe huu hasa unaoungwa mkono na Qur’ani. Qur’ani inaunyanyua mtazamo wa mwanadamu kwa kiasi kwamba anakuwa na uwezo wa kusafiri kutoka mahali panapojulikana na pa dhahiri na kwenda kwenye fukwe za kule ambako hakujulikani na kulikofichika na kwa namna hii akaanza kufumbua miujiza ya maumbile ambayo ina umuhimu wa maana kabisa kwa mwanadamu. Lengo ambalo Qur’ani inalitafuta ni lile la muongozo na malezi ya mwanadamu katika vipengele vyote vya maisha yake ili kwamba aweze kusonga mbele katika kupata utukufu. Njia pekee ambayo mwanadamu anaweza kupata ukamilifu ni kwa kuilea nafsi yake, kuubadilisha utu wake wa ndani kabisa, na kupata heshima katika nyanja zote za uhai wake kwa kufuata maagizo ya Mwenyezi Mungu yaliyomo ndani ya Qur’ani. Kwa namna hii ule wajibu wa msingi wa Qur’ani na mfumo wa maadili inaouunga mkono unakuwa wazi. Ni lazima tufahamu kwamba mwito wa kutafakari juu ya aya zake unakuja kutoka kwenye Qur’ani yenyewe. Kitabu hiki kitukufu, tofauti na vitabu 5

Page 5


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah vingine vya kawaida ambavyo vinahusika tu na taarifa na uchunguzi juu ya maudhui moja, hiki kinashughulikia namna mbalimbali za mada tofauti, kuanzia Usufii, maagizo ya kisheria, mipango ya kijamii na kibinafsi, haki na siasa, maadili, tabia na historia, kanuni za ibada na mambo mengine chungu nzima. Kwa upande mwingine, Qur’ani ni kitu kimoja ambacho kila sehemu yake inakubaliana na kanuni na sheria zake zote zilizobakia. Kuchunguza kanuni moja kunaweza kuleta ufunguo wa kufungulia kanuni nyingine, na sifa hii ya namna yake na ya kipekee inasisitiza ile hali ya kimsingi ya kimuujiza ya chemchem hii tajiri ya mwongozo. Kwa sababu hii mtu lazima asichukue njia finyu kwenye tafsir ya ufunuo huu wa kimungu kwa kuidhania kwamba imetulia na isiyonyambulika na kujiridhisha mtu na maoni ya wanachuoni wa nyakati za mwanzo, bali lazima kuwe na utafiti endelevu na maelezo na tafsir mpya kulingana na nyakati zinavyobadilika. Kwa kweli imesimuliwa kwamba mfasiri Qur’ani mashuhuri Allamah Tabatabai ameeleza, “Tafsiri mpya na maelezo ya Qur’ani ambayo inalingana na mahitaji ya wakati kuhusiana na Qur’ani lazima ichapishwe angalau mara mbili katika kila miaka kumi.” Kinachokubalika katika tafsir ya Qur’ani ni maelezo ya maoni yaliyopatikana kutokana na mazingatio na tafakari juu ya aya zake na tafsiri ya kiakili iliyoegemea kwenye hoja za maana; na kisichokubalika ni kuingia kwenye njia potovu ya tafsiri binafsi (tafsir bi’l ra’i) ya rai inayoegemea kwenye maelezo ya dhana na ubunifu badala ya maelezo ya kweli na thabiti, ambayo yatawasukuma wanadamu kuelekea kwenye laana ya milele. Kwa miaka mingi, watafiti na wanachuoni wengi na watu wachamungu wamefanya kazi bila kuchoka katika kuzielewa vizuri aya za Qur’ani, na hapo kufungua milango ya kufikia vilele vya juu kabisa vya elimu na hekima za Kiislam. Katika nyakati hizi za sasa pia, wanachuoni na wanasayansi lazima waelekeze juhudi zao kwenye utafiti kwa viwango mbalimbali ili kufichua ukweli ulioko kwenye aya za Qur’ani, na kunufaika na chanzo 6

Page 6


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah hiki halisi na cha kimuhutasari (concise) cha kanuni za elimu na hekima, ambacho sifa zake haziwezi kutiwa chumvi. Upeo mpana wa juhudi za mwanadamu unaweza kwa kweli kufichua hazina zilizofichika za Qur’ani na kutoa humo maana za kina na za hali ya juu za maneno ya Mwenyezi Mungu. Kwa hakika bahari ya maneno ya Mwenyezi Mungu haina mipaka, jinsi tunavyozama katika kutafuta ndani ya bahari hii pana, ndivyo tunavyopata vito ving’aavu sana na vyenye thamani zaidi mikononi mwetu. Qur’ani inaelezea:

“Sema: Lau bahari ingelikuwa ndio wino kwa maneno ya Mola wangu, basi bahari ingemalizika kabla ya kumalizika maneno ya Mola wangu, hata tungeleta mfano wake kuongezea.” (al-Kahf; 18:109) Kitabu hiki ni hatua ndogo katika kuyafikia malengo ambayo yalijadiliwa. Hata hivyo, kabla hatujaingia kwenye mjadala wa msingi, mambo mawili muhumu lazima yazingatiwe: 1. Ni dhahiri kwamba mbawa za mawazo ya mwanadamu haziwezi kamwe kupima urefu ama kina cha miujiza ya mikubwa na ya siri ya Qur’ani, na kile ambacho kimetajwa kama “umaizi wa neno la Mwenyezi Mungu uliofichika” ni mahitimisho ambayo yamekuja kwenye akili ya mwandishi. Maoni haya na maelezo haya kuhusu aya za Qur’ani hayawezi kuelezwa kwa uhakika kabisa kuwa ndio maana iliyokusudiwa na Mwenyezi Mungu; bali kila fasili inayofanya kutoka ndani ya aya tukufu, baada ya ufafanuzi wenye kufaa, lazima ihitimishwe na kwa maneno maarufu haya, “Wallahu ya ‘alam” (na Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye zaidi). 7

Page 7


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah 2. Kwa kuwasilisha mtazamo tofauti na ule wa tafsiri kuhusu mada ambazo zitajadiliwa, haikusudiwi kushauri kwamba maoni ya wale wanachuoni wakubwa hayana thamani. Hii ni kwa sababu, kama tulivyodokeza, haja ni kuchunguza baadhi ya ayah kutoka pembe tofauti na mwandishi anaangalia yaliyomo katika aya zinazopitiwa kwa namna maalum ambayo inatilia maanani yale mawazo ya wanachuoni hawa. Wakati wa kuthibitisha uhalali wa maoni haya, itakuwa ni muhimu kuzingatia kwa taadhima mawazo na maoni yenye thamani ya wafasiri wakubwa hawa na kuikubali hadhi yao ya uanachuo na maalum kabisa. Sayyid Mujtaba Musavi Lari Qum, Shahrivar 1387/Augosti 2008

1. MTAZAMO WA QUR’ANI JUU YA DU’A Na Mola wenu amesema: Niombeni nitawaitikia. Kwa hakika wale ambao wanajivuna kufanya ibada yangu wataingia Jahannamu wadhalilike. Aya hii ya Qur’ani ni moja kati ya zile zenye kuibua baadhi ya maswali. Ndani ya aya hii Mwenyezi Mungu anahakikisha kutorudisha du’a ya muombaji mikono mitupu na kukubali maombi yoyote ambayo waja wake wanaiwekaka mbele Yake. Hata hivyo, kivitendo, tunaona kwamba ingawa watu wanaendelea kumuomba Mwenyezi Mungu awajibu maombi yao, nyingi ya dua zao zinabakia bila kutimizwa. Kwa kweli, kama tukilinganisha ujazo wa maombi ambayo yanawekwa mbele ya Mwenyezi Mungu na idadi yenye ukomo ya watu ambao maombi yao yamejibiwa, inaonekana kwamba sehemu kubwa ya maombi hayana mafanikio. Katika hatua hii, hayo majibu ya du’a hizo inachukua maumbo tofauti, na tafsiri ya kila mmoja juu ya matokeo itategemea juu ya kiwango chake cha ujuzi na uelewa na falsafa yake ya kidunia. Yule anayeijua vizuri ile dhana halisi ya du’a na matokeo yake anapata mtazamo uliopanuka kuhusu kile 8

Page 8


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah kilichotokea ni nini, ambapo wale ambao hawana matarajio na wenye tabia za kuhuzunika wanalitazama jambo hilo katika mwanga tofauti. Matokeo yake ni kwamba, mara nyingi watu ambao du’a zao ni dhahiri hazijajibiwa, na ambao matumaini yao ni ya wimawima wanavunjika mioyo na wanapita katika mabadiliko ya maisha wakibadilika baina ya huzuni na kukata tamaa. Wanaigeuzia dini mgongo na kuangukia kwenye kosa la kukataa kudura za Mwenyezi Mungu. Swali linalojitokeza hapa ni kwamba kwa nini du’a za waombaji zinapita bila kujibiwa mbali na Mwenyezi Mungu kuahidi kujibu kinyume chake? Wafasiri wamejaribu kulijibu swali hili, na kubwa ni kwamba wamependekeza uwezekano namna mbili: 1. Ukubalikaji wa du’a unategemea juu ya hali mbalimbali, iliyo ya muhimu sana ikiwa ni utakaso wa ndani kabisa na kutokuwepo kwa uchafu wa kuzidi katika dhambi kwa kuasi amri za Mwenyezi Mungu. Hii ni kwa sababu kumuasi Mungu ndio jambo la msingi katika kukataliwa du’a, na kunamzuia mtu katika kupata wingi wa neema na baraka za Mwenyezi Mungu zisizo na ukomo. 2. Ujuzi wa Mwenyezi Mungu wa ni nini kilicho katika maslahi mazuri ya mtu, ambao umeegemea juu ya hekima, na vilevile elimu yake iliyokienea kila kitu na vipengele vyote vya jambo, unaishia katika kukubaliwa kwa baadhi ya du’a kukataliwa kwa baadhi nyingine. Hii ni kwa sababu Mwenyezi Mungu anatambua kile chenye manufaa kwa mwanadamu na kwa viumbe wote kwa jumla, ambao maisha yao yameunganishwa bila uwezekano wa kutengana. Mtu binafsi huyaangalia mambo kwa kujua ama kwa kutokujua, kulingana na yanavyomuathiri mwenyewe, na zile maana pana na mgandamizo wa du’a yake haviingii kwenye akili yake. Hata hivyo, elimu ya Mwenyezi Mungu inayokizunguka kila kitu haichukulii kila du’a yenye kufaa kwa ukubalikaji. Hata 9

Page 9


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah katika kiwango cha mtu binafsi, kila kitu ambacho muomba du’a anachoomba kinaweza kisiwe na manufaa kwake yeye, na kama ikiwa sio katika maslaha bora ya haraka kwake kutaka du’a zake kujibiwa, Mwenyezi Mungu hatofanya hivyo. Ingawa maelezo makuu haya mawili yanakubalika na ni sahihi kwa kiasi fulani, bado hayajawa ni majibu ya kutosheleza kikamilifu, na hayatulizi kabisa ule udadisi wa muulizaji, hasa kwa sababu Mwenyezi Mungu ameeleza kwa msisitizo katika aya iliyoko kwenye uchunguzi kwamba anahakikisha kujibu kila du’a. Kwa kweli maneno ya aya hiyo hayataji sharti lolote la kuhitaji kutekelezwa kabla ya du’a za muombaji kujibiwa. Zaidi ya hayo, kuziainisha zile du’a zinazoombwa sana kwa kawaida kuwa nje ya eneo la aya hii ya kawaida kunaweza kusiwe kunakubaliana na ufasaha wa maneno ya Mwenyezi Mungu, na kwa hiyo ni lazima tutafute namna ya ufafanuzi ambao uliojengeka vya kutosha na wakati huo huo ukubaliane na aya hiyo na pia umpatie muulizaji na mtafiti majibu ya msingi na yenye kufaa. Tunapoanza kuzichunguza aya za Qur’ani kwa umakini kiasi, tunakuta kwamba aina za du’a ambazo Mwenyezi Mungu ameahidi kuzijibu zina namna maalum ya uundaji, na kwa kuuzingatia na kuufuata, mtu anaweza akawa na matarajio ya kujibiwa kwa du’a yake. Kwa kweli Qur’ani inaonyesha vielelezo vya du’a ili kwamba waja wa Mwenyezi Mungu wawe wanaweza kuziiga na kuweka matakwa yao yanayofaa mbele ya Muumba, kwa uaminifu na kila aina matumaini ya kukubaliwa kwake. Du’a hiyo lazima iwe katika msawaziko na maendeleo ya mwanadamu kuelekea kwenye ukamilifu na iafikiane mwendo endelevu wa maumbile kuelekea kwenye uhai kamilifu; hapa ndipo du’a hizo zitapata majibu yatakiwayo na zitajibiwa na Mwenyezi Mungu.

10

Page 10


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah Kwa maneno mengine, du’a za mja mbele ya Mwenyezi Mungu lazima zikubaliane na kuendana na madhumuni ya kuumbwa kwa mwanadamu, ambazo bila kipingamizi zimeungana na kwenye uhai wake. Du’a ambayo itazidisha umaizi wa mwanadamu hadi kwenye mipaka ya peo za kiroho ni ile inayotengeneza mustakabali na kumuwezesha maendeleo yake katika kila kipengele ambacho ni muhimu kupata kilele cha ubora na mwinuko wa kiroho, ili kwamba aweze kusaidiwa na huruma ya ki-ungu kuweza kuongeza hadhi yake hata na zaidi. Hivyo du’a ya kweli hasa lazima iangaliwe kutokana na mtazamo huu, ambapo nyingi ya du’a za wanadamu hazina kabisa vionjo ama hamasa ya kiroho au kiwango na zinahusu matamanio ya binafsi ya kidunia, ama kuhusu msaada kutokana na matatizo ya kila siku ambayo kwa kawaida watu wanakabiliana nayo katika msongo wa maisha yao. Kama tulivyotaja hapo mwanzoni, kwa mujibu wa wafasiri wa Qur’ani, kuna vikwazo vikuu viwili ambavyo vinakwamisha kujibiwa kwa du‘a: dhambi na kutokuwepo kwa maslahi bora yake mtu; hata hivyo, kuhusiana na du’a halisi, hivi vipengele viwili hukoma kutumika kwa sababu wanaanza kwa kumuomba Mwenyezi Mungu maghfira kwa makosa, na msamaha Wake na huruma. Maombi juu ya maghfira yanapatikana katika moyo wa du’a mbili hizi ambazo waombaji wake walio na ubora wa kiroho na kiakili wakati wote wananong’ona kwenye kizingiti cha Mpaji wao asiye na kifani. Allah Mwenyewe amewaagiza wanadamu kwamba njia pekee ya kufuta madoa ya madhambi yao ni kujitakasa kupitia toba na nia thabiti ya kutokurudia na kujiweka mbali na zile tabia zilizopita. Ni hapo tu ambapo Mwenyezi Mungu kwa huruma na mapenzi Yake makubwa atakapoyakubali majuto ya mja Wake, ambayo sio jingine zaidi ya kurejea kwenye njia yake ya asili katika kutafuta kuelewa kuhusu Mola Wake, akitangaza imani yake juu Yake na kufanya marekebisho kwa ajili ya tabia mbaya zake zilizopita.

11

Page 11


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah Na kuhusu du’a hiyo kutokuwa katika maslahi bora binafsi ya muombaji, jambo hilo linakuwa halitumiki wakati du’a zinapokuwa na asili ya kiroho, kwa sababu muombaji ameomba kwa ajili ya neema ambazo zitaongeza mafhumu yake juu ya Mwenyezi Mungu, na kuishia kwenye ukuaji wa sifa na hadhi yake ya kiroho, kwa hakika kukubalika kwa du’a kama hii kutakuwa ni kwa maslahi ya muombaji, kwa sababu yale mambo ambayo yangefanya kukubaliwa kwa du’a kuwa kusikifaa yanakuwa hayapo tena katika aina hizi za du’a. Kwa hiyo inapokuja kwenye du’a ambazo zina kiambata cha kiroho, vizuizi viwili hivyo vikivyotajwa huwa havitumiki tena, na viwanja kwa ajili ya kukubaliwa maombi na du’a vimeandaliwa kikamilifu. Mifano bora kabisa ya du’a halisi inaweza kupatikana wazi kabisa ndani ya Qur’ani, na baada ya uchunguzi muhimu wa lazima, tunaweza kuwa na ujuzi nazo wa sawasawa. Mwenyezi Mungu amenukuu sampuli ya maombi ya Mitume Wake na waja Wake wa karibu ambayo yanaainisha kanuni na malengo ya Mwenyezi Mungu kumuumba mwanadamu, yaani kupata ujirani Wake. Na kama du’a na maombi ambayo yanatajwa ndani ya Qur’ani yakielekea kuwa na udhahiri wa kuhusu mambo ya kidunia, waliyatamka kama utangulizi wa kupatia sifa za hali ya juu kabisa, na yaliyofichika ndani mwao mmelala malengo matukufu na makubwa ya hali ya juu. Nabii Zakariyyah (a.s.) alitaka mtoto wa kiume wa kurithi kazi yake ya unabii na kuendelea kuwaongoza watu wa ummah wake baada ya kufa kwake, na sio kwa ajili ya furaha ya baba kupata mtoto. Maneno ya Nabii Zakaryyah (a.s.) na minong’ono yake na maombi yanayogusa moyo ni mazito sana kuweza kuyapita kwa usomaji wa wimawima. Neno alilotumia kwa ajili ya mtoto lilikuwa, mrithi (wali), na wala sio “mwana” (walad) akimaanisha kwamba tunda la uhai wake kuwa mtumishi wa karibu kwa Mwenyezi Mungu, na urithi wake matokeo yake ni muendelezo wa Utume na mwongozo kwa wanadamu. 12

Page 12


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah Atakayenirithi mimi na arithi ukoo wa Ya’qub. Ewe Mola wangu mjaaliye mwenye kuridhisha. Du’a ya Zakariyyah (a.s.) ilitakabaliwa na akajaaliwa na mtoto wa kiume yule ambaye alimtamani, ambaye aliendelea kuutangaza ujumbe wa Allah na kuwaongoza watu hadi siku za mwisho wa siku za uhai wake. Nabii Suleiman (a.s.) hakuomba utawala wenye nguvu sana na mamlaka kwa sababu bali ilikuwa ni shauku yake kuponyesha maradhi ya kiroho ya watu wake na kuwajulisha kwenye ukweli mtukufu, na hii ilikuwa ndio shabaha yake kuu. Hakuna wakati wowote ambapo historia inaonyesha kwamba Nabii Suleiman (a.s.) alitumia mamlaka zake kamwe kwa ajili ya tamaa zake au kwa manufaa yake binafsi; kwa kweli aliweka mamlaka yake makubwa na uwezo wake kwenye huduma kwa watu wake ili kuwaongoza na ili bendera ya Tawhiid iwekwe ikipepea juu na haki ienee katika dunia. Hii ndio ilikuwa du’a ya Nabii Musa (a,s.) kwa Mola Wake:

“Ewe Mola wangu! Nizindue niishukuru neema yako uliyonineemesha na wazazi wangu na nipate kutenda mema unayoyaridhia na uniingize kwa rehema yako katika waja wako wema.” (an-Naml; 27:19). Kinachofuata, hebu natuizingatie pia du’a ya Nabii Ibrahim (a.s.):

“Ewe Mola wangu! Nijaalie niwe mwenye kuisimamisha Swala na katika dhuria zangu pia. Ewe Mola wetu! Na utakabalie dua yangu. Ewe Mola wetu! Nighufirie mimi na wazazi wangu wawili na waumini siku ya kusimama hisabu.” (Ibrahim; 14:40-41) 13

Page 13


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah Suala pekee lililotajwa ndani ya Qur’ani ambapo du’a ya Nabii imekataliwa na wala haikukubaliwa ni ile ya Nabii Nuhu (a.s.) kuhusiana na wokovu wa mwanawe wa kiume kutokana na yale mafuriko. Du’a hii ilichukua shina kwenye mapenzi halisi ya baba kwa mwana tu, na du’a kama hizo huwa hazina uhakikisho wa kukubaliwa na Mwenyezi Mungu (hata kama zikitoka kwa Mtume mashuhuri vipi). Zile du’a ambazo Malaika na wabebaji wa Arshy ya Mwenyezi Mungu wanazoziomba kwa ajili ya watu wema na waumini kama ilivyoelezwa ndani ya Qur’ani, zote zinaelekezwa kwenye kumsaidia mwanadamu heri ya milele. Hivyo, wanaomba mlangoni kwa Mwenyezi Mungu wakimuomba Yeye azikubali toba za waumini na kuzifunga katika huruma na msamaha Wake

“Wale wanaobeba Arshi, na wanaoizunguka, wanamsabihi kwa kumuhimidi Mola wao, na wanamuamini na wanawaombea msamaha walioamini. Mola wetu! Umekienea kila kitu kwa rehema na ujuzi. Basi wasamehe ambao wametubu na wakaifuata Njia yako, na waepushe na adhabu ya Jahannamu. Mola wetu! Na waingize katika Bustani za Milele ulizowaahidi. Na pia waliofanya mema miongoni mwa wazee wao na wake zao na dhuriya zao. Hakika Wewe ni Mwenye nguvu, Mwenye hikima.” (Ghafir; 40:7-8) 14

Page 14


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah Qur’ani vilevile inazielezea du’a za wale marafiki wa karibu (awliya) na Mwenyezi Mungu. Kama tuonavyo, du’a hizi zina sifa kama zilezile za Mitume na malaika. Ifuatayo ni mifano ya dhahiri:

“Ambao humtaja Mwenyezi Mungu katika hali ya kusimama, na kukaa na kulala, na wanafikiria umbo la mbingu na ardhi. Mola wetu hukuviumba hivi bure. Utukufu ni wako, basi utuepushe na adhabu ya moto.” Mola wetu! Hakika wewe ambaye utamwingiza motoni utakuwa umemfedhehesha na hawatakuwepo wasaidizi kwa ajili ya madhalimu. Mola wetu! Hakika sisi tumemsikia mwenye kulingania anayelingania kwenye imani kwamba: mwaminini Mola wenu nasi tukaamini. Mola wetu! Tusamehe madhambi yetu na na utufutie makosa yetu na utufishe pamoja na watu wema.” Mola wetu! Na utupe uliyotuahidi kwa Mitume yako, wala usitufedheheshe siku ya kiyama. Hakika wewe huvunji ahadi.” (al-Imraan; 3:191- 194). Kama tukiziangalia zile aya za mwishoni mwa Surat al-Baqarah, tunaona kwa mara nyingine tena kwamba du’a za waumini zina vipengele kama vilevile vya maombi ya Mitume, malaika na waja wa karibu na Allah (awliya). 15

Page 15


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah “….. Mola wetu! Usituadhibu tukisahau au tukikosa. Na usitutwike mzigo kama uliyowatwika wale waliokuwa kabla yetu. Mola wetu! Usitutwike tusiyoyaweza na utusamehe na utughufurie na uturehemu wewe ndio Mola wetu na utunusuru na watu makafiri.” (2:286).

Du’a zote hizi ambazo Qur’ani inazinukuu kutoka kwa Mitume (a.s.), malaika wanaowaombea waumini, waja wa karibi sana na Mwenyezi Mungu na du’a za waumini juu yao wenyewe zote ni kwa ajili ya kunyanyua ngazi ya mtu, kupanua uelewa na ufahamu wa mtu na kupata ukaribu na Mwenyezi Mungu. Kwa sababu hii, baada ya kutaja aina hizi za du’a ndani ya Qur’ani, Mwenyezi Mungu anasema:

“Hivyo Mwenyezi Mungu alizikubali du’a zao …..”(3:195). Ni wazi kabisa kwamba hakuna sehemu yoyote katika mkusanyiko huu wa du’a ambapo kuna maombi juu ya faida binafsi ama ya kivitu au kwa ajili ya furaha za mpito za maisha. Katika aya nyingine, Qur’ani inasema:

“Na anawaitikia walioamini na wakatenda mema, na anawazidishia fadhila zake.” (42:26) Kwa mijibu wa baadhi ya wafasiri, aya hii inabana ukamilishaji wa maombi ya waumini kwenye ibada zao na utii, kwa sababu hilo huwongozea kwenye kupanda daraja kwao, na du’a kama hizi mara nyingi hukubaliwa na Mwenyezi Mungu.

16

Page 16


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah Baada ya kutaja taratibu za hijja, na kuwasihi sana waumini kuhusu utajo wa kumkumbuka Mwenyezi Mungu (dhikr), Qur’ani inaeleza kwamba watu wako wa namna mbili; baadhi yao wanasema:

“Mola wetu! Tupe (mema) hapa duniani; nao katika Akhera, hawana fungu lolote.” (2:200). Wakati wengine wanasema:

“….. Mola wetu! Tupe mema duniani na (tupe) mema Akhera, na utukinge na adhabu ya Moto. Hao ndio wenye fungu katika waliyoyachuma, na Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhisabu.” (2:201–202). Kama tunavyoona, du’a hii sio kwa ajili ya msukumo wa nafsi au kuinua kiwango cha hali ya kiroho ama kupata ukaribu na Mwenyezi Mungu; ni kuhusu upatikanaji wa vitu vya dunia hii, ama vya dunia hii na ya akhera. Kwa hiyo, katika majibu yaliyomo katika aya hizi kwa ajili ya makundi yote – wale wanaotamani vitu vya dunia hii tu na wakawa wameomba kwa ajili hiyo, na vilevile kwa wale wanaotamani vitu vya dunia hii na akhera, na wamekimbilia kwenye du’a ili kupata matamanio haya, ambayo hayana hata chembe ya kiroho ndani yake – Mwenyezi Mungu hataji kukubaliwa kwa du’a zao. Badala yake, ili kufikia malengo yao, Yeye swt. Amewaelekeza kufuata mfumo wa kawaida wa Kimbinguni ulioagizwa katika dunia hii; yaani, kutumia juhudi na vitendo ili kutimiza tamaa zao katika msingi wa hiari na uhuru wa kuchagua ambao amejaaliwa nao mwanadamu. 17

Page 17


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah Kwa njia hii, yeye anayajulisha makundi yote kwamba yatafanikiwa katika matamanio yao kwa kutekeleza juhudu na vitendo vinavyofaa; Qur’ani inaeleza kwamba: “Watapata sehemu ya kile walichokichuma.” Maimam ma’sumin (a.s.) vilevile wameonyesha mifano mizuri ya thamani juu ya namnana utaratibu huu wa du‘a, mfano wa wazi zaidi ukiwa ni ile Du’a ya Kumayl, kama alivyoifunzwa na Imam Ali (a.s.). Kifungu kimoja cha maneno katika du’a hii kinaeleza:

“Ewe Mola! Imarisha viungo vyangu kwa ajili ya kukutumikia na endeleza nguvu za mikono yangu kuweza kuhimili katika huduma yako na nijaalie uaminifu wa kukuhofia Wewe na kukutumikia ….. Nihurumie kupitia majibu yako bora na unipunguzie dhambi zangu na unisamehe mapungufu yangu.” Du’a hiyo inaenedelea mpaka kunatokea kauli ya kuvutia ambayo ina mwanga kama huu wa hii iliyoko kwenye mjadala sasa hivi: ? ?????? ?????? ? ???? ??? ???????

“Kwani kwa hakika umeagiza ibada yako kwa ajili ya waja wako na umewaamrisha kuomba du’a kwako na ukawahakikishia kuwajibu.” Katika sehemu hii ya du’a ya Kumayl, Imam Ali (a.s.) anatoa dokezo kwenye ule uhakikisho uliotajwa kwenye hii aya ya Qur’ani tunayoichunguza akitaja ahadi ya Mwenyezi Mungu ya kumjibu kila muombaji kama matokeo ya zile du’a ambazo zimeegemea kwenye maombi ya kiroho na kiungwana. 18

Page 18


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah Kwa kweli Imam Ali (a.s.) ananuia kuonyesha kwamba du’a zilizofanywa katika namna walivyofanya mitume, malaika, waja wema wa karibu Naye na waumini ndio aina za du’a ambazo Mwenyezi Mungu amehakikisha kuzijibu na anatufundisha jinsi ya kumuomba Mwenyezi Mungu kwa namna hii ili kwamba tuweze kupokea majibu yake vilevile. Tunapogeukia kwenye du’a zilizomo ndani ya Sahifa Sajjadia ya Imam Ali Zainul-Abidiin (a.s.) tunaona mifano ya kipekee ya du’a ambazo zimefaulu kwa ajili ya kujibiwa; tunakuta kwamba zote zinaonyesha shauku ya uugwana na ya kiroho. Kadhalika tunapaswa kuchunguza du’a hii iliyofundiswa na Imam Mahdi (AF):

???? ? ?????? .....

Ewe Mwenyezi Mungu tuwafikishe kutii, na tuwembali na maasi, na tuwe na nia ya kweli, kuwatambua jamaa, tukirim sisi muongozo na msimamo, na uweke sawa ndimi zetu kwa ukweli na hekima zijaze nyoyo zetu elimu na maarifa, yatwaarishe matumbo yetu na haramu na kisichokuwa na uhakika. Katika ujumla wa du’a hii, hakuna utajo wa maombi yoyote ambayo yamekatazwa kwenye matamanio na starehe za kidunia. Maimam watukufu (a.s.) wengine vilevile wameacha hazina du’a zenye manufaa zenye ujumbe mzito na wa maana, zote zikiomba huruma ya Mwenyezi Mungu ili kufikia viwango vya hali ya juu vya kiroho. Masufii na wanachuoni wengine wamesisitiza kwamba umuhimu wa du’a na kuomba mlangoni kwa Mwenyezi Mungu ni haja ya kisilika, kwa 19

Page 19


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah sababu falsafa ya msingi ya du’a na siri ya maongezi ya mtu na Mola wake ni ili mwishowe kuleta mwongozo, maendeleo na kuinuliwa hata kama du’a hiyo ni kuhusu mahitaji ya kimada na ya muhimu. Kwa hiyo, du’a ya kweli – ambayo majibu yake yamehakikishwa na Mwenyezi Mungu kwa ajili ya wale watu waliotakasa fikra zao, wakajaza mioyo yao na mapenzi kwa Mwenyezi Mungu, na wamesafisha nafsi zao kutokana na kila alama ya ukafiri – ni ile du’a ambayo inamsaidia na kumnufaisha muombaji kwenye safari yake kuelekea kwa Mola Wake. Hata hivyo, hii sio kusema kwamba Mwenyezi Mungu, ambaye hazina zake za neema na upaji hazina mipaka haitikii maombi ya waja Wake wenye dhiki na wasiojiweza kutokana na huruma na fadhila Zake. Ni kwa sababu hii kwamba Maimam watukufu (a.s.) wakati wote wamesisitiza kwamba mtu aombe kwa ajili ya kila mahitaji yake kutoka kwa Mwenyezi Mungu na kuendelea kumuomba Yeye kwa njia ya du’a. Kwa hiyo, unapoomba kwa Mwenyezi Mungu kwa namna iliyo sahihi, njia ambayo inaishia kwenye kukubaliwa, muumini anaweza pia akaomba huruma na neema ya Allah, ili kwamba Mwenyezi Mungu aweze kukubali du’a zao kwa ajili ya mahitaji ya msingi na ya kidunia vilevile. Hata hivyo, hata kama ni kwa ajili ya kupunguza matatizo ya dunia hii, du’a kama hizo zisiwe zinakosa utajo wa yale mahitaji halisi, ambayo yako kwenye ulimwengu wa kesho akhera. Kama uwanja wa ile aya ya “Niombeni Mimi, Nami nitakujibuni” na uhakikisho wa kukubaliwa ni mpana sana kiasi kwamba unajumuisha du’a kwa ajili ya matamanio yote ya kidunia na ubora wa kimada na utafutaji usiokoma wa wepesi na wingi na yote yale ambayo mwanadamu anayatafuta katika uhai wa maisha yake, basi tunakabiliwa na namna fulani ya hitilafu. Dunia ni mahali pa mtihani kwa mwanadamu na katika mwendo wa maisha yao, uwezo wa kila mtu kukabiliana na matatizo umedhihirishwa. Mwenyezi Mungu kwa uhakika kabisa ameeleza kwamba dunia hii ni makazi ya mashaka, ambayo yanaitengeneza tabia ya wanadamu na 20

Page 20


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah kuwasababisha kuendelea na kusonga mbele. Mitume (a.s.) na waja wa karibu na Mwenyezi Mungu wamepitia kwenye baadhi ya matatizo magumu sana katika maisha yao, bado walionyesha upendo na kuabudu kwingi kwenye kizingiti cha Mwenyezi Mungu, na kwa njia hii wakapata ukaribu kwa Mola wao na wakapata rehema zinazofaa kwenye nafasi zao wenyewe zilizo kuu. Kama du’a ndio chote kinachohitajika katika kupunguza matatizo ya kawaida na ya siku hadi siku ambayo kwamba mwanadamu anakabiliana nayo katika ulimwengu huu, na Mwenyezi Mungu amehakikisha kukubaliwa kwa aina hizi za du’a, basi Yeye asingeruhusu amri na utaratibu ufuatao kuwepo juu ya ardhi, ambapo anasema: “Hakika tumemuumba mwanadamu katika taabu.” (90:4) Hakika matarajio haya na dhana ya kiakili ni kinyume kabisa na hekima ya Mwenyezi Mungu ambapo kwa upande mmoja, Mwenyezi Mungu atengeneze mfumo wa mitihani na matatizo ili kumjaribu mwanadamu, na kwa upande mwingine aweze kuondoa magumu yote haya wakati wa du’a zao. Kwani Yeye amesema ndani ya Qur’ani:

“Je, wanadhani watu wataachwa waseme tumeamini nao wasijaribiwe?” (29:2). Ni lazima isije kupuuzika kwamba sehemu nyingine ya masikitiko na matatizo ambayo mwanadamu anapambana nayo katika ulimwengu huu yanatokana na vitendo vyake vya kigoigoi na visivyo na busara, na kwa kumjaalia mwanadamu zawadi za akili na busara, Mwenyezi Mungu anamtaka ajaribu kwa kadiri ya uwezo wake kutatua matatizo yake mwenyewe na kuvishinda vikwazo vinavyozuia njia yake. 21

Page 21


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah Hoja ambayo inaweza kudokezwa kutokana na ile sehemu ya mwisho ya aya tuliyoijadili ni kwamba, kama tukichukulia neno “ibada” kama lilivyotajwa kwenye sehemu ya mwisho ya aya hii:

“Na Mola wenu amesema: Kwa hakika wale ambao wanajivuna kufanya ibada yangu wataingia Jahannamu wadhalilike.” (alMu’min; 40:60). ….. kumaanisha du’a, inalingana kabisa na ule mwanzo wa aya, ambapo Mwenyezi Mungu anamuamuru mwanadamu kuomba du’a, kwa sababu aya hii inazungumzia kuhusu du’a na kukubaliwa kwake, na du’a pia ni sehemu ya ibada. Kama mwanadamu anataka kufikia sehemu iliyoinukia hawezi kufanya hivyo isipokuwa kupitia njia ya kumkumbuka (dhikr) Allah kwa mfululizo na du’a. Kwa upande mwingine, ibada inaelezwa vizuri na maneno ya kumtukuza Mwenyezi Mungu na kwa asante na shukurani kwa ajili ya neema Zake na kwa kukubali hadhi Yake ya hali ya juu iliyotukuka. Hata hivyo, du’a ni kielelezo aminifu cha matamanio na matarajio ya mtu kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na kwa uhalisia zaidi, ni kukubali kwa mtu juu ya udhaifu na kutojiweza kwake mbele ya ukuu wa Mwenyezi Mungu; hapa ndipo fahari zenye mwembwe za watu wenye majivuno zinapowazuia kuomba du’a na kuonyesha unyenyekevu wao na udhalili wao mbele ya Mola Wao, na hivyo kukata mawasiliano yao pamoja na Yeye. Kama tukiwaza kuhusu tabia na fikra za wenye majivuno, tutaona kwamba kwa jumla, wanaelekea kumtukuza Mwenyezi Mungu kwa maneno matupu, na mtu haoni ukweli wala uaminifu wowote katika du’a zao. Watu 22

Page 22


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah hawa wenye kiburi hawako tayari kuonyesha unyenyekevu wao mbele ya Muumba wao na kukubali kutokuwa na thamani kwao halisi. Hii ndio sababu ya kwa nini Mwenyezi Mungu, Mola wa walimwengu Mwenye kudura anawaonya wale walionasa kwenye mtego wa fahari na makuu kwamba majivuno yao hayohayo yanayowazuia kuomba du’a kwa unyenyekevu mbele Yake mwishowe yatawaongozea kwenye hasara yao ya milele na adhabu katika Moto wa Jahannam. Hebu tuangalie kwa mara nyingine tena ile aya tuliyokuwa tunaijadili:

“Na Mola wenu amesema: Niombeni nitawaitikia. Kwa hakika wale ambao wanajivuna kufanya ibada yangu wataingia Jahannamu wadhalilike.” (40:60). 2. KUITAZAMA ILE MAANA YA “DHARABA” NDANI YA QUR’ANI

“….. Na ambao mnaogopa unashiza wao, basi wanasihini na muwahame katika vitanda na wapigeni…..” (4:34) Uchunguzi wa kuaminika wa Qur’ani unaweza kufanyika tu pale wakati akili inapokuwa huru kutokana na imani na dhana zilizoshikiliwa tangu huko nyuma, kwa sababu kuhukumu kabla na kuziangalia dhana zake bila busara kutaongozea tu kwenye kufungika akili na kutobadilika. Hii ni hatari moja ambayo kila mtafiti mpambuzi lazima aepukane nayo kwa gharama yoyote ile. Moja ya aya ambazo wapinzani wa Uislam na watetezi wa haki za wanawake waliyoiteua ili kuikosoa sheria ya Qur’ani ni hiyo iliyotajwa 23

Page 23


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah hapo juu. Aya hiyo inahusiana na suala la utelekezaji (nushuz – unashiza) wa wanawake. Badala ya kujaribu kuielewa bila upendeleo maana halisi ya aya hiyo, wao wamekimbilia ukosoaji wa makelele, bila ya kutambua kwamba mijadala iliyoegemea kwenye dhana isiyo sahihi kunamuondoa mtu kwenye ukweli na kuzuia kufikiri. Kwa kweli, kupitia uchunguzi wa kina na wa muhimu wa neno “Wadhribuhunna” (wapigeni) ndani ya aya hii, mtu anaweza kumaanisha maana mbili tofauti, ambazo tutazieleza kwa kiasi fulani hapa chini: Maana ya kwanza inapatikana kwa kuchukulia ile maana ya dhahiri ya neno dharaba, ambayo ni kupiga, na walio wengi wanaegemea kwenye tafsiri au maana hii. Maana ya pili, ambayo inakubaliana na uchunguzi wa muktadha wa jambo lenyewe linalojadiliwa ndani ya aya hiyo ni tafsiri mbadala ya neno hilo Dharaba, ambalo ni neno lenye maana mbalimbali. Mtu anaweza kuchukulia uwezekano wa hii maana ya pili, ambayo ni hasira na dharau, kama ni jibu la mtu kwa unashiza ulioonyeshwa na mke wake. Hii inakubaliana na ile maana pana ya dharaba, ambayo inajumuisha pamoja na kutengana na kufarakana.1 Maana nyingine ya neno Dharaba ni “kutoa kisogo” au “kukaa mbali,” kwa hiyo unaporejelea kwenye mazungumzo ya mtu ambaye anaongea upuuzi, au kwenye kipande cha maandishi yasiyo na msingi, mtu anaweza kusema: “fadhribuhu ‘ala ‘l- jidar” (itupilie ukutani), ambayo ni istiari ya “usiitilie maanani hiyo.” Maana ya kutengana na kufarakana kwa ajili ya dharaba inaweza pia kutumika kwenye aya iliyoko kwenye uchambuzi, na uchunguzi wa aya hiyo unaweza kufanyika juu ya msingi huu huu kwa sababu imeelezwa kwamba neno Dharaba limetumika hapa kwa vile linaashiria kutengana kwa 1 Huwa inasemwa, “Dharaba al-dahru baynana” kwa maana kwamba “kupita kwa wakati kumetufanya tutengane.” (al-Munjid, chini ya neno ‘Dharaba’) 24

Page 24


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah ghafla, tofauti na ule utengano wa taratibu.2 Kwa hiyo inaelekea kwamba Qur’ani hapa inamshauri mume ambaye amemkaripia bila mafanikio mke wake mkorofi kwa njia mbili kali sana, mwishowe kabisa kutengana (dharaba) naye. Hata hivyo, mume huyo anapaswa kuepuka ukali juu ya mkewe na angojee kwa subira juu ya kitendo chake kuleta athari, yeye anapaswa kumruhusu mkewe kufikiria juu ya mambo na kuchukua hatua kuelekea yale ambayo ni bora kwa mkewe. Kwa hiyo, wakati inapotafsiriwa kwa namna hii, tunaweza tukasema kwamba aya hii ina maana ya kusema: Kama mwanamke akikwepa wajibu wake na akatenda visivyofaa, basi mume lazima ajaribu kurekebisha mambo kwa hatua zilizoamrishwa. Kimsingi, mwanamume lazima amshauri mke wake, na amkumbushe juu ya wajibu wake, na amhimize kuangalia upya vitendo vyake ambavyo vimeishilizia kwenye hali ya kutokuwa na furaha katika maisha wanayoshirikiana pamoja. Hata hivyo, endapo juhudi za mume zitakuwa hazina mafanikio, na mke akaendelea na tabia yake isiyofaa, yeye lazima ajibu kwa tahadhari sana kwa kuondoka tu kwenye kitanda chao lakini abakie ndani ya nyumba na asifanye mabadiliko ya wazi kwenye utaratibu wa kawaida wa mambo ya nyumbani humo. Hii ni kwa sababu hiyo aya ya Qur’ani inatamka tu kitendo cha kususia kitanda katika hatua hii na wala sio zaidi. Kama kitendo hiki nacho pia kitakuwa hakileti mabadiliko katika tabia ya mke, na akawa anazidi kuwa na tabia dhidi ya maslahi yake mwenyewe, na juhudi za mumewe zote zikawa bure, hapo hatua kali zaidi inahitajika katika juhudi za kuvunja kutoafikiana huko. Hatua hii inamhitajia mume huyo kukata mawasiliano yote ndani ya nyumba na kuishi maisha ya utengano kabisa. Ni kana kwamba amemuondoa mke huyo kutoka kwenye sehemu ya kiini katika nyumba, kwa makusudi kwamba mke huyo abadili mawa2 Kwa maelezo zaidi rejea kwenye: Lisan al-‘Arab, Jz. 1, uk. 451-477; Mu’jam Muqa’is al-Lugha, Jz. 3, uk. 398-399. 25

Page 25


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah zo yake na kubadili hiyo tabia yake isiyokubalika ili kuzuia kuharibika zaidi kwa hali ya mambo. Ni kweli kwamba katika hali hii mke huyo bado anaishi ndani ya nyumba na ananufaika na vitu na faraja nyinginezo, lakini hatakuwa katika hali ya kiroho na kihisia ya kumuwezesha kuhisi amani, na hili huenda likampa hamasa ya kukubali wajibu wake kwa familia na kuchukua hatua za awali za kurejesha uelewano na kuiwezesha familia kusonga mbele kuelekea kwenye maisha ya furaha zaidi. Hata hivyo, kama tutachukulia neno dharaba hapa kumaanisha “kupiga,� na tukidhania kwamba Qur’ani inataka kwamba katika mazingira kama haya, mwanaume anapaswa kumlazimisha mke wake kurudia majukumu na wajibu wake kwa kumnyanyulia mkono, ili kwamba arejee kwenye fahamu zake, basi kufanyia kazi tafsiri hii huenda kukawa na athari zisizofaa kwa sababu zinazojadiliwa hapa chini: 1. Vitabu vya fiqhi vinaeleza kwamba ukatili wa kimwili mdogo kabisa wa mtu kwa mkwewe, kama ukimchubua ngozi yake, unabeba adhabu (diya) na kitendo cha adhabu kama hicho hakiruhusiwi kwa mwanamume kwa sababu yoyote ile. Kwa upande mwingine kuna mashaka kwamba pigo jepesi au laini linaweza kuwa na athari katika kumuadhibu mke mkorofi na kumsababisha kubadili tabia yake; kwa kweli haielekei kabisa kwamba kitendo kama hicho kinaweza kikaamua jambo lolote. Katika masuala ya unashiza, mafaqihi wanashughulika sana (kutunga sheria kwa) na kitendo cha mwanaume kuhusu kusimamisha uhudumiaji wa mke wake na sio upigaji au adhabu ya kimwili. Kama kanuni, mafaqihi hawakufanya uchunguzi wa sawasawa wa suala la kupiga, bali wamelenga juu ya maelezo yake ya matokeo yake; kama vile idadi na marudio ya mapigo, mazingira ambamo mkosaji anasamehewa kulipa faini au malipo ya fidia ya damu (diya), au kama mwanamke anaonyesha tabia yake ya ukaidi kwa muendelezo na kila siku, ni mara ngapi mwanaume ataamua kumpiga, na kwa muda kiasi gani ukatili 26

Page 26


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah huo unaruhusiwa na kadhalika. Maswali haya yanahitaji kujadiliwa kwa kirefu lakini hata uchunguzi mrefu unaweza kushindwa kuyashughulikia masuala yote yatakayojitokeza kuhusiana na hili. 2. Kwa kawaida uwajibishaji wa kimwili utamsukuma tu mwanamke kwenye hali ya uchungu na chuki, hususan wakati anapotambua kwamba mume wake ametumia kimbilio lake la mwisho na hawezi kufanya lolote tena kumzuia yeye, wakati huu anaweza kuhisi kwamba jambo jingine tena mume analoweza kumwelekezea. 3. Kitendo chochote cha kimwili kwa kawaida kinasababisha matokeo yasiyofaa, na kinaweza kumsukuma mwanamke kuwa madhubuti zaidi na mwenye kudhamiria katika tabia yake. Hii ndio hali hasa ilivyo hasa kwa wanawake ambao wana tabia ya kigomvi na ambao wamezoea sana uhasama kuliko kwa wanawake ambao wenye tabia ya ushwari na utulivu zaidi. Kwa hiyo matumizi ya adhabu na nguvu kwa namna kama hii ya wanawake kutazidisha tu ubishi wao, wakati mwingine kusababisha kupotea kwa udhibiti juu ya pande zote pamoja na matokeo yasiyotabirika. Wakati wowote mtu anapotwaa mbinu ya adhabu ili kuleta makubaliano na hatimae kurudisha uhusiano wa upendo baina ya wanandoa, wakati wote kuna uwezekano kwamba matokeo yanaweza yasiwe mazuri, au kwamba ule mpasuko baina yao unakuwa mkubwa zaidi au nafasi ya makubaliano ya pamoja ya baabaye yanadhoofika. 4. Kumlazimsha mwanamke kwenye makubaliano kupitia ukatili wa kimwili sio mwendo unaokubalika kisaikolojia kwa wanandoa wote wawili na hakutatoa uridhikaji wa ndani kabisa kwa yeyote kati yao. Baada ya muda itaondoa mapenzi ya kila mmoja juu ya mwenzie na hatimae inaweza kupelekea kuvunjika kwa ndoa hiyo. Kwa upande mwingine, inaelekea kwamba ile hatua iliyoelezwa kabla ya kutengana kabisa na mke wakati akiwa bado anaishi ndani ya nyumba hiyo hiyo inaweza kuwa ndio chachu inayoweza kumsababisha 27

Page 27


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah kuangali upya mambo na kufikiri juu ya mustakabali wa baadae na kumshawishi kubadili tabia yake. Zaidi ya hayo, kukataliwa huko na mume wake kunamchukiza mke na hataweza kukustahimili ama kuvumilia kwa muda mrefu. 5. Hakuna anayeweza kukanusha kwamba ile hatua ya mwisho katika mfululizo huu wa vitendo, ambao ni dhahiri kwamba haibadilishiki, ambamo mke anakuwa amekataa kwa makusudi kabisa juhudu zote za mumewe za kurudisha uhusiano wa maelewano, ni talaka. Talaka ndio kimbilio la mwisho kabisa wakati kila hatua ya kitendo inaposhindwa. Kwa hiyo, pale hatua zote zinaposhindwa kupata makubaliano ya mke, na hakuna kiasi chochote cha busara kinachoweza kumbadilisha tabia yake isiyofaa, mume anaanzisha mkondo wa kutengana kwa kudumu na uvunjaji wa ndoa yenyewe kwa kuomba talaka. Wakati mune anaporidhika kwamba hakuna kitakachovunja kutoafikiana huko na kwamba ule muungo wa kindoa umevunjika kabisa moja kwa moja, analeta ahueni kutokana na uhusiano wenye vurugu kwa njia ya talaka bila kuwa na haja ya adhabu yoyote ya kimwili ama kitendo. 6. Tunajua kwamba Uislam umetoa mazingatio maalum kwenye moyo na maana halisi ya maisha ya kidunia, na njia zinazoelekeza hatima yake bora. Kwa sababu hii, unaendeleza uhusiano mzuri baina ya watu wa familia moja na unatambua kwamba mshikamano wa mzito kati ya mume na mke utaishia kwenye familia yenye ustawi mzuri. Kama matokeo ya heshima kubwa iliyotolewa kwa wanawake katika kila kipengele cha maisha, mume hakuruhusiwa kuweka shinikizo japo kidogo juu ya mkewe katika kufanya kazi za nyumbani ama kumlazimisha kufanya jambo ambalo liko kinyume na silika yake. Kwa kweli, mke amepewa pia fursa ya kutaka malipo kutoka kwa mume wake kwa ajili ya kunyonyesha watoto wao. Kwa kuelewa kwamba Uislamu umechukua mkabala wa jumla kwenye masuala yanayohusiana na wanawake, ambao ni pamoja na 28

Page 28


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah haki na heshima zao ndani ya nyumba na katika jamii, sio jambo lisilowezekana kwamba kwa mtazamo wa Uislamu, wanaume hawawezi kuonyesha hisia kwa njia ya ukatili wa kimwili juu ya tabia ya uasi ya wake zao kwa sababu haiendani na maadili ya kijamii ya upendo na uelewano miongoni mwa wanandoa katika familia. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: Ninashangazwa na yule ambaye anampiga mke wake, ambapo yeye mwenyewe ndiye anayestahili zaidi kupigwa; msiwapige wake zenu kwa viboko kwa sababu kuna ulipizaji kisasi wa kisheria (qisas) kwa ajili ya hilo. Bali waadhibuni kwa upunguzaji katika matumizi yao; hivyo mtapata furaha katika ulimwengu huu na ule ujao wa Akhera.3 3 Mustadrak al-Wasa’il, Jz. 14, uk. 250, chapa ya Mu’asasa Ahlul-Bayt; na Bihar al-Anwar, Jz.103, uk.249 hadith ya 38. Inafaa kuangaliwa hapa kwamba kwa mujibu wa wanachuoni wa hadith na wanachuoni wa Rijal, hadith hii imewekwa katika daraja la hadith za kuaminika (Muaththaq) au kwa mujibu wa riwaya nyingine vile vile kama ni sahih (kama ile riwaya iliyosimuliwa kutoka kwa Abu Maryam). Kwa hiyo, riwaya nyingine zilizosimuliwa dhidi yake, kwa mfano, ile hadith ya al-adharb bi’l siwak (kupiga kwa mswaki wa mti) zina matatizo kwa namna mbili: kwanza kabisa kutokana na kipengele cha uaminikaji; kwa sababu ni riwaya yenye sanadi isiyokamilika (mursal); zaidi ya kutokeza katika Majma’ alBayan, haionekani kwenye chanzo chochote cha asili. Pili mafaqihi wakubwa wengi hawakujaribu kuieleza na kuihalalisha riwaya hii, na hilo lenyewe linaonyesha kwamba wao wanaona yale matumizi ya neno ‘dharaba’ kuwa katika maana mbali na ile ya dhahiri yake. Katika mjadala wake kuhusu nikah (ndoa) ndani ya kitabu chake ‘al-Masalik,’ Shahid al-Thani anaelezea kifungu hiki, “al-dharb bi’l siwak” hivi: “Imekusudiwa kuwa ya kimzaha, vinginevyo kitendo kama hicho hakielekei kuadhibu ama kurekebisha.” Marhum Bahrani katika kitabu chake “alHada’iq” anakubaliana na Shahid al-Thani kwamba ‘dharaba’ hapa haiko katika maana ya kupiga kimwili, kwa kuongezea “Sio kwa kuchapa kwa mjeledi ama kwa kiboko ….. na lazima kusiwe na majeraha ya kimwili kama matokeo yake.” (Al-Hada;iq, Jz. V, 22, uk.618). Mwishowe, kama mkazo wa ziada, tunaweza kunukuu riwaya kutoka al-Fiqh al-Mansub ila ‘l Imam al-Ridhaa (a.s.), ambamo Imam ar-Ridha (a.s.) katika kuifananua aya hiyo anasema: “Ni pigo la kirafiki (kimchezo) …..” Yote haya yanaonyesha kwamba neno “fadhribuhunna” katika aya hii halikutumika katika ile maana iliyozoeleka ya kugonga ama kupiga. 29

Page 29


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah Hapa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anawakumbusha watu kwamba ni faida kubwa kwao kupata usikivu wa wanawake kwa kuwaadhibu kwa kuwabania masurufu yao badala ya kuwapiga kimwili. Hii ni kwa sababu, kwa upande mmoja itawavunja moyo juu ya tabia za kikorofi na zisizofaa, na kwa upande mwingine wewe hutawajibika mbele ya Mwenyezi Mungu na katika akhera, utakuwa na utetezi juu ya vitendo vyako. 7. Mwishowe, inasisitizwa kwamba maana ya ‘dharaba’ katika aya hii kwa kweli ni kuadhibu kupitia njia za kimwili kama usomaji wa dhahiri unavyoshauri, ni lazima ielezwe kwamba hii sio amri ya wajib, kiasi kwamba hatua hii inakuwa ni ya faradhi juu ya mume ambaye mke wake anaonyesha unashiza (nushuz) au kumlazimisha mke wake ama ukaidi, na kwamba mume hana jinsi ila kugeukia kwenye adhabu ya kimwili. Kwa kweli kuna viashirio vinavyopendekeza matumizi ya njia mbadala, kama vile kuwapunguzia matumizi yao ya kimaisha, ambayo kwayo mume anaweza kushughulikia unashiza na kumlazimisha mkewe kubadilika. Hivyo hatua inayopendekezwa na aya hii ni ya maelekezo kwa kuwa inataja njia moja ya kurekebisha tabia ya mke na kumkumbusha juu ya wajibu wake. Kwa hiyo, kama katika nyakati ambazo fikra na busara za mwanadamu zilikuwa bado hazijakomaa, iliwezekana kukabili unashiza wa mke kupitia uadabishaji wa kimwili, ingawa kwa masharti maalum, katika nyakati hizi tunapokuwa katika zama zilizotaalimika zaidi, jibu tofauti kwa ajili ya unashiza linahitajika. Kwa sababu hii, ni muhimu kubadilisha na kurekebisha utaratibu uliopo na sio kupuuza mahitaji ya zama. Kwa hiyo siku hizi ambapo wanawake wamefikia kiwango cha juu zaidi cha elimu na ukomaavu wa fikra, mchakato wa hatua ya utengano uliopangwa na mume ili kuidhibiti tabia ya kikorofi ya mke wake ina mwelekeo wa kufanikiwa katika kumshawishi yeye kubadili msimamo wake. Unaweza ukasababisha mazingira ambayo hayana magomvi na uhasama, ambayo ni rahisi kupatikana, na kurudisha maelewano katika 30

Page 30


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah uhusiano na maisha ya kifamilia. Na hili linawezekana kwa kuziangalia maana zote zinazowezekana za neno dharaba katika neno la Mwenyezi Mungu, kama tulivyokwisha kueleza. Qur’ani inafaa kwa uwanja mpana wa tafsiri – na kwa kweli, hii ni sehemu ya muujiza wa maandiko haya yaliyojaaliwa na Mungu. Kwa sababu hii, chombo hiki huru na hai kitadumu milele. 3. NI NINI KINACHOMAANISHWA NA: “MKONO MWEUPE” WA MUSA (A.S.)?

“Na ingiza mkono wako katika mfuko wako utatoka mweupe pasipo ubaya. Ni katika ishara tisa kwa Firauni na watu wake. Hakika wao ni watu mafasiki.” (an-Naml, 27:12) Miongoni mwa Mitume wote wa Mwenyezi Mungu, Nabii Musa (a.s.) alikuwa ndiye aliyeonyesha miujiza mingi zaidi, pengine ni kwa sababu Bani Israil – Mayahudi – walikuwa ndio wakaidi zaidi miongoni mwa mataifa katika mtazamo na tabia zao. Mtu anaweza kusema kwamba kutokana na mwelekeo wa tabia yao ya ubishi na ukaidi wa kung’ang’ania kwenye mawazo yao, wao wamekuwa ni taifa la kipekee katika historia. Kutokana na mantiki yao iliyopotoka, wao kamwe hawakuwa wapokezi wa kweli, na kwa marudio walidai kwamba mitume wao wanaonyesha muujiza kulingana na desturi zao binafsi, udadisi wao uliobweteka na mawazo yao ya ajabuajabu yasiyo na msingi, baadhi yao hata wamethubutu kudai miujiza ambayo kimantiki ilikuwa haiwezekani. Walikuwa hawaelewi kwamba njia ya kutafuta usadikishaji, kuusaka ukweli na kupata mwongozo – ambayo ndio njia pekee ya wokovu – kunataka moyo na 31

Page 31


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah akili kuwa huru kutokana na mwelekeo wa kwenye ukaidi. Kwa nyongeza, miujiza inakuja tu kupitia mapenzi ya Mwenyezi Mungu, na kwa mujibu wa umuhimu na mazingira wakati huo, na sio kwa ajili ya burudani na mabadiliko ya ghafla ya watu wajinga. Ili kukamilisha neema Yake, Mwenyezi Mungu aliwatuma wengi wa Mitume Wake kwenye ummah huu, na wao waliwasilisha miujiza ya kustaajabisha na ya wazi kwa watu wao ili kwamba uso wa Haki usije ukafunikwa kwa mapazia ya udanganyifu na dhulma. Hata hivyo, Wayahudi hawakuwa na shukurani juu ya neema hizi na wakawauwa idadi kadhaa ya Mitume wa Mwenyezi Mungu. Licha ya tabia yao ya kikatili, Mwenyezi Mungu kwa subira na uvumilivu kabisa aliwasilisha hoja zake kwa kuendelea kuwatumia Mitume. Mtume maarufu na mkubwa kabisa aliyeteuliwa kama mjumbe kwa taifa hili alikuwa Nabii Musa (a.s.); yeye alitumwa kwa taifa ambalo, chini ya nira ya utumwa lilikuwa limepoteza maadili na ubora wote kabisa. Katika desturi yao uongo ulijifanya kama ndio kweli, na tabia zilisimama kwenye vigezo vya bandia. Musa (a.s.) alianza kazi yake kwa kulingania kwenye mzunguko mfinyu katika mazingira ambamo yameondolewa maadili ya matukufuna elimu, hadi alipoifanya jamii hii changa kuwa yenye nguvu na akaongeza ule utambuzi wao wa ndani. Kama wale Mitume wa kabla yake, alijaribu kukomesha fikra zao finyu na ngumu kwa kudukiza ndani yao upendeleaji wa maisha katika ulimwengu ujao wa akhera. Aya hiyo hapo juu inataja tu mmoja wa miujiza hiyo ya ajabu ya mtu huyu wa kimungu na una riwaya kadhaa na nukta za kupendeza, ambazo ufafanuzi wake ni huu ufuatao hapa chini: Kwa mujibu wa wanachuoni ambao wametoa maoni juu ya aya hii, yale maneno “mkono mweupe pasipo ubaya” yanamaanisha kwenye ule weupe wa mkono wa nabii Musa (a.s.) ambao aliuwasilisha kwa watu wake kama ushahidi wa madai yake utume. Matumizi ya kifungu “pasipo na ubaya” 32

Page 32


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah yanabatilisha ile dhana kwamba mkono wake ulishambuliwa au kudhuriwa na maradhi yoyote. Kwa kweli Qur’ani inathibitisha kwamba weupe huu ulikuwa tofauti kutokana na namna fulani ya ugonjwa unaofahamika. Maelezo haya ni dhaifu katika hali kadhaa: 1. Ule weupe wa mkono wa Nabii huyu wa Mwenyezi Mungu lazima uwe umefanana na weupe wa namna ya ugonjwa (mchafuko wa ngozi – vitiligo au mabaka – leucoderma) kwa ajili ya aya hiyo kutuliza wasiwasi wa wachunguzi na kuwahakikishia kwamba hapakuwa na shambulio lolote lililokuwepo. 2. Katika wakati wa Nabii Musa (a.s.) wachawi walifanya matendo ya kiajabu, na ingawaje vitendo hivyo vya wachawi na matapeli yalikuwa ni matokeo ya uwezo wao wa kibinadamu wenye ukomo na vilikuwa vimeegemea juu ya kiini macho, mafunzo na mazoezi tu, hata hivyo vilikuwa na athari kubwa sana katika akili za watu wa kawaida. Hata hivyo, muujiza wa namna hii (ya mkono mweupe) haukuwa wa kiwango sawa na ile miujiza mingine iliyoonyeshwa na Nabii Musa (a.s.) ambayo kila mmoja wao unashangaza na ni wa kipekee katika haki yake wenyewe. Zaidi ya hayo, ule muujiza wa mkono mweupe (kama unavyoelezwa sasa hivi) isingeweza kuwashawishi watu kwamba kitendo kisicho cha kawaida, kioja kilikuwa kinatokea, au kudhoofisha ile nafasi ya wachawi na kuwashawishi wao kuja kwenye uwanja wa makabiliano. 3. Muujiza huu ulikuwa ni wenye kuonekana kwa lile kundi ambalo lilikuwa limekusanyika karibu na Nabii Musa (a.s.) na ilikuwa ni vigumu kwa wale walikuwa japo mita chache tu mbali na alipokuwa kuweza kuona vizuri. Kutilia nguvu madai yetu kwamba hoja hizo hapo juu ni dhaifu, tunaweza kurejea kwenye aya nyingine:

33

Page 33


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah

“Akaitupa fimbo, mara ikawa nyoka dhahiri. Na akautoa mkono wake. Mara ukawa mweupe kwa watazamao.” (26:32-33) Aya hiyo hapo juu inaelezea jinsi Nabii Musa (a.s.) kwanza alivyoitupa fimbo yake mbele ya kundi kubwa la watu wa Farao na wengine waliokuwa wamekusanyika kumuangalia yeye. Fimbo hiyo iligeuka kuwa joka kubwa na likasababisha fadhaa ndani ya mkusanyiko huo; ilikuwa ni hapo tena ambapo alionyesha muujiza wake wa pili ambao ulikuwa ni ule mkono wake unaong’ara. Kama tukichukulia kwamba mkono wa Nabii Musa (a.s.) uligeuka mweupe tu kwa kiasi kwamba ulifanana na mtu mwenye ugonjwa unaohusiana na ngozi, usingeweza kuonekana isipokuwa kwa kikundi kidogo cha watu ambao walikuwa wamekusanyika, na usingeweza kuwa na sifa ya kuwa muujiza ambao ungetangaza hiyo kazi yake ya kuteuliwa mbinguni na ambao ulitumika kama ushahidi wake mkuu wa madai yake. Usingeweza kutosheleza katika kuleta ukubalikaji wa jumla katika Utume wake au kusababisha maajabu ambayo yangeleta mabadiliko mazito na ya wazi katika mioyo na akili za watu na kupanua upeo wa namna yao ya kufikiri. Kuhusu ule muda maalum ambamo muujiza huo ulitokea, Qur’ani inaeleza:“Akasema: Miadi yenu ni siku ya sikukuu na watu wakusanywe kabla ya adhuhuri.” (20:59) Inawezekana kwamba Nabii Musa (a.s.) alichagua muda huu maalum kwa ajili ya kuonyesha muujiza wake kwa sababu wakati huo jua lilikuwa katika kilele chake na siku ilikuwa katika mwanga wake mkali kabisa ili kwamba mtu yeyote asije akaweza kukanusha utokeaji na hali halisi ya muujiza huo na kila mtu angeweza kuuona waziwazi. 34

Page 34


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah Tutadhaniaje kwamba katika wakati wa siku kama huu kwenye mwanga mkali wa jua, muujiza wake ulifanana tu na mkono wa mtu mgonjwa, kiasi kwamba watu walikanganyikiwa na weupe wa mkono wa Nabii Musa (a.s.) wakidhani ni ukoma, ambapo Mwenyezi Mungu aliwajulisha kwamba walichokuwa wakishuhudia kilikuwa ni muujiza wa Mutume wao na sio aina ya madhara ya ngozi! Kwa tafsiri hii hatuwezi kutegemea kwamba maonyesho haya ya weupe wa mkono wake, ambao hauna mng’aro wala unururifu, kuweza kuibadilisha hadhira hiyo au kuwa na nguvu ya kuwashawishi kuacha imani zao potofu na kukubali madai ya Mtume wa Mwenyezi Mungu. Hii ni kwa sababu muujiza unaonyesha uhusiano wake na Muumba na Mjuzi wa wahyi, na uhalisi wake ni wa kiasi kwamba hauwezi kukosolewa na watu ambao hawana utambuzi wa dunia ya miujiza na wale ambao wanaushuhudia wanaona kwamba wamepewa fursa mpya ya kugundua ukweli. Kwa upande mwingine, Qur’ani inaeleza:

Na hatukuwaonyesha Ishara yoyote ila hiyo ilikuwa kubwa zaidi kuliko nyengineyo. Na tukawakamata kwa adhabu ili warejee. (azZukhruf; 43:49) Katika aya hii imeainishwa kwamba kila muujiza ambao Nabii Musa (a.s.) aliuonyesha ulifuatiwa na muujiza mkubwa na muhimu zaidi. Hii inaonyesha hoja yenye ustadi na umuhimu ambayo ni utaratibu wa kuhimiza nafasi iliyofahamishwa na kwa ajili ya maendeleo ya mwanadamu yaliyopiga hatua kufikia kiwango ambacho kwamba kufikiri kwake kunabadilika. Hii ni kwa sababu kama baadhi ya wale ambao fikra zao zilikuwa zimepotoka hawakuridhishwa na muujiza wa kwanza, basi muujiza wa pili unaweza ukavutia sana na kuwazindua na kuleta uhai kwenye nyoyo zao zilizokufa na kuwachochea kwenye kutafuta ukweli. 35

Page 35


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah Hivyo katika siku yao ya sikukuu, na katikati ya kundi kubwa la watu watiifu kwa Firauni, wakati Nabii wa Mwenyezi Mungu alipotupa fimbo yake ardhini na akauonyesha muujiza huo unaoogofya ambao ulisababisha mshangao na fadhaa kwa wote, kama tukidhania kwamba ule muujiza wa pili – wa mkono mweupe – ulifanana tu na weupe wa mkono wa mtu mwenye ugonjwa fulani, ni vipi tunaweza kusema kwamba ulikuwa mkubwa na muhimu zaidi kuliko ule muujiza wa kwanza? Wakati ambapo weupe kama huo (wa mgonjwa) sio tu kwamba hauonekani zaidi kuliko muujiza wa kwanza bali pia hauko sawa wala haulinganishiki nao. Kwa kutilia maanani hoja hizo hapo juu, inaelekea kwamba ile tafsiri ya mkono mweupe kufanana na ule wa mgonjwa haikubaliki na tunahitaji kuchunguza upya suala hili ili kuondoa matatizo yaliyotajwa hapo juu. Muujiza huu mtukufu unaweza ukaelezewa kwa namna ifuatayo: Kwa vile neno lililotumika kwa ajili ya weupe (baydha) pia ni kisawe – (neno lenye maana sawa) – cha neno jua, asili ya muujiza huu ni mwa mujibu wa uwezekano namna tatu: ama kiwango cha nuru na mng’aro wa mkono wa Nabii Musa (a.s.) kilikuwa cha ukali wa chini kuliko ule wa jua, ambao haukuweza kuonwa na watu; au vilikuwa sawa na ukali na ule wa jua, ambao kadhalika usingeweza kusababisha mshangao kiasi hicho; kwa hiyo uwezekano pekee uliobakia ni kwamba mng’aro wa mkono wa Nabii Musa (a.s.) lazima iwe ulikuwa mkali zaidi kuliko ule wa jua hivyo kwamba nuru yake inayopenya ingeweza kusababisha mshangao kwa kila mtazamaji. Kwa njia hii ungeweza kutuma ujumbe kwa wale waliotafuta njia ya haki na mwongoza wa kweli kuuchukulia muujiza huu kama ushahidi usio na shaka wa utume ambao unaanzia kwenye chanzo cha ki-Mungu, na hatimae kuwalazimisha watu wa Firauni kwa kinyongo waukubali ukweli.. Kwa mujibu wa elimu ya tiba, mng’aro na mmeremeto mkali zaidi ya ule wa jua hauwezi kustahimiliwa na macho ya mwanadamu, na kama ukali huo ni mkubwa kuliko uwezo wa kustahimili kwa macho, utakuwa ni wenye kuharibu kila jicho lililoelekezwa kwake. Hatari ya ziada pia inakuwepo ambayo kwamba itaharibu retina za macho kama vile tu mtu 36

Page 36


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah anapoliangalia jua kwa muda mrefu; kwa hiyo inaelekea kwamba Qur’ani inaashiria kwamba huu muujiza hapa ni kwamba ule mwanga unaong’ara kutoka kwenye mkono Musa (a.s.), ingawa ni mkali kuliko ule mwanga wa jua, hauna madhara kabisa kwenye utazamaji huo na hauharibu uoni wa watazamaji kwa namna yoyote ile. Sasa inakuwa dhahiri kwamba hii tafsiri mpya ya maneno “mweupe bila ubaya” inaweza ikaimarisha wazo la kwamba ule mwanga unaomeremeta ambao ulitoka kwenye mkono wa Nabii wa Mwenyezi Mungu, na ambao uliangaza mahali hapo, haukusababisha uharibifu wowote kwa hao watazamaji. Kwa kuzingatia akilini mjadala uliopita, maana ya neno “baydha” pia inakuwa wazi; hapa haiashirii au kumaanisha weupe wa kawaida, bali maana ya mng’aro na mmuliko inachukuana zaidi na aya hiyo.4 Maana hii 4 Marhum Mulla Muhsin Fayd katika tafsiri yake ya aya hii anaeleza: “Angetoa mkono wake kwenye nguo yake na kumulika mazingira yake.” (Tafsiir as-Safi, 4/89). Kwa hiyo, katika nyakati zile za siku hiyo, mng’aro wa mkono wa Nabii Musa (a.s.) ulikuwa na mwanga mkali zaidi kuliko jua, vinginevyo kauli ya kwamba mkono wake ulimulika mazingira yake wakati wa mchana isingeleta maana yoyote. Allama Majlisi anaeleza katika tafsiri yake ya aya hii: “ule mng’aro uliotoka kwenye mkono wa Nabii Musa (a.s.) ulikuwa na mwznga zaidi kuliko ule wa jua.” (Bihar al-Anwar, 13/78). Abul-Futuh Razi vile vile anaeleza katika maelezo yake juu ya aya hii kwamba: “Angeutoa mkono wake kutoka kwenye mfuko wake na ungeonekana mweupe na ungekuwa na mwanga zaidi kuliko jua.” (Tafsir Razi 27/12) Mwandishi wa Nasikh al-Tawarikh pia anaeleza: “Angeutoa mkono wake kutoka kwenye mfuko wake na ungekuwa na mwanga zaidi kuliko jua na ungemulika mazingira hayo wa namna ambayo hakuna mtu ambaye angeuangalia moja kwa moja” (Nasikh al-Tawarikh, 1/373). Kauli zote hizi zinaonyesha kwamba maelezo kuwa ule weupe wa mkono wa Nabii wa Mwenyezi Mungu ulikuwa sawa na weupe wa maradhi ya ngozi – ambayo wafasiri wakubwa wameyaamua kutokana na maneno “weupe bila ubaya” – hazikubaliani na riwaya yoyote kati ya hizo zilizotajwa hapo juu. 37

Page 37


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah ya baydha vilevile kwa kawaida inapatikana katika istilahi za kifiqh, kwa mfano katika usemi, “siku za mbaramwezi” (layaal al-baydh) ambazo ni zile siku mwezi unapowaka kwa nuru angavu zaidi. Mifano hii inaweza kufaa katika kudhihirisha mambo na kutoa uthibitisho mwingine kwa ajili ya suala lililojadiliwa hapo juu. Kutokana na yaliyotangulia, aya hii inaweza kutafsiriwa kama ifuatavyo:

“Na ingiza mkono wako katika mfuko wako utatoka mweupe pasipo ubaya. Ni katika ishara tisa kwa Firauni na watu wake. Hakika wao ni watu mafasiki.” (an-Naml; 27:12).

4. UDHIHIRISHAJI WA BUSARA ZA KIQUR’ANI KATIKA TARATIBU ZA MIRATHI

“Mwenyezi Mungu anawausia kwa watoto wenu; fungu la mwanamume ni kama fungu la wanawake wawili.” (an-Nisaa; 4:11)

“Na wakiwa ni ndugu wa kiume na wa kike, basi fungu la mwanamume ni kama fungu la wanawake wawili.”

38

Page 38


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah Kama ilivyoelezwa katika aya hizo mbili zilizotangulia, Uislama umeagiza kwamba fungu la mwanaume katika mirathi linapaswa kuwa mara mbili ya lile la mwanamke na umewataka wafuasi wake kutekeleza amri hii ya Mwenyezi Mungu. Suala hili linahitaji hadhari na uchambuzi; hata hivyo, kabla hatujaanza mjadala kuhusu hukmu hii, tunahitaji tujikumbushe wenyewe kwamba: Mjadala kuhusu urithi unaohusika wa wanaume na wanawake ni lazima usifungike katika kutetea haki za wanaume wakatu kukipuuzwa ile nafasi ya juu na haki halisi za wanawake; bali makusudio yawe ni kuulinda utukufu wa wahyi, ambao umeagiza njia iliyoegemea kwenye maumbile asili ya wanadamu na kile kilichoko kwenye maslahi yao ya kweli na bora. Kwa hiyo, inakuwa dhahiri kwamba mjadala uliopo mikononi hautaathiriwa na kanuni za kijamii zilizotengenezwa na wanadamu, ambazo ni zenye kupatwa mabadiliko katika kila zama, hata kama mazingira ya kijamii kwa namna yake yenyewe yakitoa athari kubwa kiasi gani katika fikira za watu kwamba unayumbisha pia maoni ya baadhi ya wasomi wake. Baada ya utangulizi huu, sasa tunaingia kwenye uchunguzi wa karibu sana juu ya jambo lenyewe: Uislam unawachukulia wanaume na wanawake katika namna ambayo ni pana, ukizingatia vipengele vyote vya maisha yao, katika kutambua nafasi yao ya thamani katika maumbile. Kwa upande mmoja, katika mwongozo wake wenye kuagiza (wahyi), Uislam unauona ubora wa asili na uwezo wa kiroho wa wanaume na wanawake kuwa ni sawa; kwa wote na kwa kila mmoja wao, kwa kupitia matendo yanayofaa, wanaweza kufikia uwezo wao wa hali ya juu unaostahili. Kwa upande mwingine, kama tukichukulia maoni na ugunduzi wa wanasaikolojia na wanafiziolojia kuhusu tofauti za kimwili, kiakili, kihisia na kiroho kati ya wanaume na wanawake yaliyoegama juu ya utafiti na uchunguzi, tunaona kwamba haki na wajibu wa mwanaume na mwanamke zimeagizwa kwa kuzingatia tofauti zao za ndani na halisi, ambazo haziathiri usawa wao wa msingi au hadhi yao kama wanadamu. Kwa maneno mengine, katika mtazamo wa kidini, tofauti hasa na za kimaum39

Page 39


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah bile za jinsia mbili hizi hazimaanishi kwamba kuna tofauti yoyote katika thamani zao husika. Hakuna shaka kwamba katika mkondo wa maendeleo ya kijamii ya wanadamu, jinsia ya kike wakati wote imekuwa ndio chombo cha maonevu na ukataliwaji wa haki. Mwanamke amepatwa na unyimwaji mkubwa mikononi mwa mwanaume. Kwa upande mwingine, hakuna shaka vilevile kwamba maendeleo mengi ya kurekebisha na makali sana kupitia zama zote yameelekea kwenye tofauti kumbwa mno; na majaribio ya kumaliza migongano hiyo hayajapata matokeo linganifu kuhusiana na hili, licha ya juhudu zenye nia njema. Miongoni mwa hayo, wale watafutaji wa haki za wanawake wenyewe hawana tofauti na mara nyingi sana tumeshuhudia tabia zao zisizowiana katika utetezi wao wa haki za wanawake. Na kwa lile jambo la kwamba usawa katika kila kipengele kati ya haki za wanaume na wanawake zimetangazwa kama haki ya msingi na iliyothubutu na wale wanaotetea haki za wanawake; ni lazima tuchambue ule msingi ambao umeunda maoni haya, na ni kwa kiasi gani ni wenye mantiki na iwapo unaendana na ukweli halisi. Ni kweli kwamba wote, wanaume na wanawake ni washirika katika ubinadamu, na wote wana haki sawa na ubora wa kibinadamu; hata hivyo kuna tofauti zisizopingika katika hali zao za kimwili na kihisia. Kwa kweli tofauti hizi sio mapungufu, ambayo kwamba jinsia moja inaweza kudai 5 Hadi leo hii, wale wanaotetea haki za wanawake wakati wote wamewasilisha ile kanuni ya haki sawa kama ni ya msingi na isiyokatalika na kwa hiyo wamehoji ni kwa nini kuna tofauti kati ya urithi wa mwanamume na mwanamke katika sheria ya Kiislam. Hata hivyo, wamepuuza ile nukta ya kwamba swali hasa ambalo wangelijibu kwanza ni kwamba, ni kwa msingi gani uliondiwa ile kanuni ya haki sawa kwa jinsia zote, wakati ambapo kuna tofauti za wazi kati ya wanaume na wanawake. 40

Page 40


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah ubora juu ya nyingine; bali ni tofauti ambazo zinafanya jinsia hizo ziwe na tofauti ya wazi kati ya moja na nyingine. Kwa sababu hiyo, pale inapodaiwa kwamba jinsia mbili hizo “lazima” ziwe na haki sawa na kila mojawapo, tunahitaji kuuliza, hii “lazima” inatokea wapi?5 Usawa wa haki za watu wa jinsia moja ni jambo ambalo ni la kimantiki na halali; hata hivyo, usawa wa haki katika vipengele vyote, wa jinsia mbili tofauti (kwa mtazamo wa tofauti zao za kihisia na kimwili) unahitaji ushahidi wa kuunga mkono madai hayo; na kama ushahidi juu ya usawa huu katika vipengele na vipimo vyote hautokezi au kutolewa, basi madai kwa ajili ya haja ya usawa wa haki hayana msingi wala mantiki; kwa ukweli, uhalali wenye nguvu wa madai haya bado haujapatikana. Kutupia macho kwa juujuu kwenye mawazo na maoni mbalimbali ya wenye kuitakidi usawa kati ya wanaume na wanawake yataonyesha ukweli wa masuala hayo yaliyoelezwa hapo juu. Itikadi ya utetezi wa haki sawa kwa wanaume na wanawake ilianzishwa huko Magharibi kama harakati ambayo ilitafuta haki za wanawake; ingawaje inawezekana kwamba watetezi wake, hasa wanawake, walianza harakati hizi kwa uaminifu kabisa ili kupata haki za kweli za wanawake, uwepo wa ubepari na sababu za kiuchumi nyuma ya utangazaji wa itikadi ya utetezi wa haki sawa kwa wanaume na wanawake kwenye hatua yake ya kwanza hauwezi kukatalika.6 Hata hivyo, mbali na mambo yaliyochochea kuchomoza kwa itikadi hii, hata leo hii, utetezi wa usawa wa kijinsia umebadilishwa kwenye idara nyingi za nadharia, na kila kundi linalotangaza itikadi hii limejiingiza kwenye njia yake ya pekee, mara nyingi likishutumu msimamo wa 6. Mazingira ya kihistoria ya itikadi hii na mlingano wake na kuanzishwa kwake ni mapinduzi ya kiviwanda huko Uingereza, ambayo yalipelekea kwenye harakati zinazodai haki ya wanawake kupiga kura. Juu ya mabadiliko ya kiviwanda ambayo yalikuwa yanapita Ulaya nzima, serikali zao ziliweza sasa kuwalipisha kodi wanawake, kwa sababu wale tu ambao walilipa kodi ndio waliokuwa na haki ya kupiga kura wakati wa chaguzi. 41

Page 41


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah wengine na kusisitiza kwamba mawazo yao wao ndio ya kimaendeleo zaidi. Watetezi wa haki za wanawake mwanzoni kabisa walipigania usawa wa haki kwa wanaume na wanawake. Maoni ya Simone de Beauvoir, kama yalivyoelezwa ndani ya kitabu chake, "The Second Sex" - ambacho kimekuwa maarufu kama "Biblia ya Utetezi wa Haki Sawa za Kijinsia" yameegemea katika kanuni ileile kwamba kwa kuwa wanaume na wanawake wote ni binadamu, basi wanapaswa kuwa na haki sawa. Hata hivyo, mkondo wa maendeleo ya kijamii uliwalazimisha wapigania haki za kijinsia (feminists) kuangalia upya fikra zao, kwa kiwango kiasi kwamba hawakuridhika tena na kuunga mkono haki sawa kwa wanaume na wanawake, bali walifika mbali zaidi kwamba wanawake ndio jinsia bora zaidi. Kimsingi, hii ilikuwa ni tofati hasa ya maoni ya mwisho ambayo yalikuwa yamewakosesha wanawake haki zao hapo mwanzoni kabisa. Wakereketwa walitokeza katika idara ya upigania haki za kijinsia, kwa kiasi kwamba mkereketwa mmoja mkali sana, Andrea Dworkin, alianzisha shutuma chungu za kuumiza juu ya hali ya kidume na akauchukulia ujanadume kama kimsingi una maana nyingine sawa na ukatili, kifo na maangamizi. Leo hii, katika vigezo vya kimatendo, kanuni ya usawa haitekelezwi wakati wote katika jamii za kimagharibi; kwa mfano, wanaposema kwamba wanaume na wanawake lazima wapate haki sawa kwa sababu ya ukweli kwamba wote ni wanadamu, katika suala la uangalizi wa mtoto mahakama zinahukumu kwa manufaa ya wanawake kwa msingi wa jinsia yao, na sio kwa msingi wa uwanachama wao katika ubinadamu. Kinyume na madai ya usawa katika kila hali, hii ni kanuni ya kisheria ambayo ni ya upendeleo wa wazi na isiyotenda haki kwa wanaume na ambayo vyombo vya sheria vinaiunga mkono wakati wote.

42

Page 42


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah Mwisho, kuibuka kwa hali ya usasa katika nyakati hizi, ambako kumeathiri itikadi nyingi za kisasa na vitivo vya fikra, vilevile kumebadilisha mwelekeo wa watetezi wa haki za kijinsia kuhusiana na ufuatiliaji wa haki za wanawake. Kwa hakika, kundi jipya la wapigania haki za kijinsia (feminists) wamesimama dhidi ya ziada za zama za usasa, umamboleo kwa kusisitiza umuhimu wa jukumu la umama la wanawake. Kwa kweli kundi hili linaamini kwamba wote wanaume na wanawake wanazo sifa maalum na za kipekee. Hivyo wanayatukuza masuala kama ya ujauzito na malezi ya watoto kama sifa bainifu ambazo ni za kipekee kwa wanawake, na wanawashutumu wakereketwa wa kupindukia kwa kuuliza ni vipi wanaweza wakaipuuza sifa hii ya kike yenye thamani wakati wanapofikiria haki za wanawake?7 Kwa hali yoyote, kwa kuzingatia mabadiliko katika dhana ya upigania haki sawa kwa wanawake na wanaume, kwa nyongeza kwenye swali lililokwisha kutajwa kuhusu ukosekanaji wa thibitisho za kimantiki na zenye uamuzi za kuhalalisha madai yao ya msingi, tunaweza pia kuhitaji kuuliza ni kwa muda kiasi gani na kwa kiwango gani maoni mbalimbali haya yanayopingana kuhusu haki za wanawake yataendelea kubadilika? Na ni wapi ambako maendeleo haya hatimaye yatakoma na kutulia? Zaidi ya hayo, ni nani mwenye kustahili zaidi kuchagua maoni sahihi kutoka miongoni mwa wingi wa maoni uliokithiri juu ya jambo hilo, na je, mawazo ya wataalamu hawa hayatapata kushutumiwa na kuhakikiwa baadae? Ni lazima isisahaulike kwamba ingawa watetezi wa haki sawa kwa wanaume na wanawake hawakuzungumzia kwa uwazi uwezo tofauti wa 7. Kwa uhakiki mpana zaidi rejea kitabu "Modern Political Ideologies" cha Andrew Vincent. (Mwandishi ametegemea juu ya tafsiri ya kitabu cha Murtadha Thabitfar); pia "Huquq-e-Zan dar Keshakesh-e Sunnat wa Tajaddud" cha Muhammad Hakimipur, "Faminesm 'Alayhi Zanan" cha Sayyid Ibrahim Husaini, kama ilivyonukuliwa katika Jarida juu ya Kitabu cha Tahkiki, Faslname-ye Kitab naqd, namba 17, Kipupwe cha Mwaka1379 H.A. 43

Page 43


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah kutafakari, akili, kazi na uongozi wa jinsia hizo mbili, hata hivyo, wao wakati wote wanazingatia sababu ya tofauti hizi zisizokanika na za msingi kwamba zinaunganika kwenye jinsia zote mbili na kuzitumia katika mengi ya mambo ya kijamii. Ukweli huu unatokana na takwimu ambazo zinachanganua jinsi, kwa vitendo na katika mandhari tofauti za kijamii, wanaume wanachaguliwa zaidi mara nyingi kuliko wanawake kwenye nafasi za uongozi. Wanaonyesha pia kwa uhakika kabisa jinsi ambavyo katika jamii ambazo zinadai kwa makelele kuhusu usawa wa haki kati ya wanaume na wanawake, uzalishaji wa kielimu na kikazi wa wanaume na wanawake unavyolipwa katika njia isiyolingana na ya upendeleo. Ni ukweli wa wazi kwamba maumbo ya kimwili ya wanaume na wanawake yanafaa kwenye majukumu maalum; wanaume wamechukuliwa kufaa kufanya kazi nzito na ngumu na kinyume chake, wanawake wanafaa zaidi kwenye kazi nyepesi na laini. Hii ni tofauti ambayo Muumba ameiweka katika asili ya hizi jinsia mbili. Ikiwa haki ya jinsia zote mbili ni lazima ziwe ni zenye kufanana, basi na kazi ambazo wawili hawa wanaweza kuzifanya lazima halikadhalika ziwe ni kugawanywa katika namna ya kufanana pia, kwa sababu haileti mantiki kwamba majukumu yawe tofauti na haki ziwe sawa! Jambo jingine linalotokana katika tofauti kwenye haki ni tofauti katika wajibati. Hebu tufikirie kiwanda, ofisi au mtambo wa kutengenezea bidhaa ambamo mna wafanyakazi wengi wakijishughulisha kufanya majukumu mbalimbali. Mmoja wao ndiye Raisi, na wengine kutegemeana na viwango vya ujuzi wao ni washauri, wafanyakazi na vibarua. Ni dhahiri kwamba haki za huyo Raisi ni tofauti na zile za kila mmoja mwinginewe na tofauti hii haiwezi ikachukuliwa kuwa sio halali, kwa sababu haki zake zinalingana na majukumu anayoyabeba. Huu ni mfumo wenye maana ambao umekubaliwa na jamii zote. Ikiwa wafanyikazi wote wa mshahara katika idara moja ni wanaume, au wote ni 44

Page 44


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah wanawake, au ni wote wanaume na wanawake wanaoendesha idara hiyo, hapo ndipo hali itakuwa ni ya usawa. Raisi hata kama ni mwanamke, yeye atakuwa na mshahara mkubwa kuliko waajiriwa wanaume, kwa sababu majukumu yake ni tofauti. Kwa hiyo, katika hali kama hizi, hakuna mtu atakayedai haki sawa kwa wanaume na wanawake. Tofauti hii katika majukumu na wajibu, ambayo baada ya hapo husababisha hizo tofauti katika haki, ni jambo la kawaida linalokubalika. Hapa swali linajitokeza kwamba wakati tofauti katika wajibu inapoishia kwenye tofauti katika haki – na jambo hili likawa halizui malalamiko au upinzani – basi kwa nini isiwe zile tofauti katika wajibati za wanaume na wanawake kutokana na maumbile yao na tabia, ambazo hazibadilishiki na zinarudi hadi kwenye asili ya uhai wao husika, zisiishie kwenye tofauti katika haki za wawili hao? Je, kuna hoja yoyote inayothibitisha kwamba zile tofauti katika wajibati ambazo zinainua na kushusha haki binafsi za mtu zimefungika kwenye wajibu wa kawaida tu na kwamba haizizunguki tofauti za kiasili na kiuhai? Maana ya swali hilo lililotangulia ni kwamba, kama watetezi wa haki sawa kati ya wanaume na wanawake wanataka kupuuza yale majukumu ya asili na ya dhahiri ya jinsia mbili hizi kwa kutunga sheria ama kanuni zilizoegemea kwenye haki sawa, basi wanakwenda kinyume na maumbili asilia. Sheria zinaweza wakati wote zikafanywa kwa mujibu wa mawazo yao ya ajabu na matamanio, lakini maumbile yenyewe hayawezi kubadilishwa! Na mwisho kabisa, hapa kuna swali jingine ambalo linaibuka nalo ni: Wakati makampuni ya kitaifa na ya binafsi yanaruhusiwa kufanya tofauti katika uainishaji wa kazi za waajiriwa wa kiume na wa kike, na hapo kupanga haki tofauti kwao, na jamii mbalimbali zikaupokea utaratibu huu kama ni wa kawaida, basi kwa nini madhehebu ya kidini isiruhusiwe kutamka haki za wanaume na wanawake ambao ni wafuasi kwa msingi wa wajibati ambazo imewapangia kila mmoja wao? 45

Page 45


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah Kama tofauti katika haki za kidesturi zinazotekelezwa na taasisi za kibinafsi na kijamii au na watu maalum hazikuleta upinzani wowote na ni kanuni zinazokubalika katika jamii zote, kwa nini zile tofauti katika haki kama zinavyoungwa mkono na dini zinapingwa? Wakati mwajiri wa kawaida anayo haki ya kuamua na kupanga kazi za wafanyakazi wanaotumika kwenye kampuni yake pamoja na haki zao vilevile, kwa nini mwasisi wa harakati kubwa ya kielimu na kiroho asiweze kufanya kama hivyo kwa wafuasi wake? Kwamba pia, dini ambayo imeweka wajibu mkubwa wa kifedha juu ya mabega ya wafuasi wake wa kiume; dini ambayo inamfanya mwanaume kuwajibika katika upatikanaji wa mahitaji muhimu kwa ajili ya mke wake kulingana na hadhi na nafasi yake; katika mazingira haya haki inataka kwamba fungu la wanaume na wanawake katika mirathi lazima liwe tofauti. Hebu tuchukulie kwamba baba anayetaka kutoa pesa kwa ajili ya vijana wake wawili wa kiume anampa yule aliyeoa mara mbili zaidi ya yule ambaye hajaoa. Kuna mtu yeyote atakayesema kwamba haki ya yule kijana ambaye hajaoa imekiukwa na kuvunjwa, au kwamba yeye amedhaifishwa kwa sababu amepokea kitu pungufu? Hapa pia kuna tofauti, lakini imeegemea kwenye haki na usawa, kwa sababu kama baba angewapa wanawe wote kiasi kilekile sawa sawa, dhamira itamsuta juu ya ubaguzi usio wa haki; kadhalika kuna tofauti katika mirathi ya wanaume na wanawake kulingana na kanuni ya Shari’ah; hata hivyo ni ugawaji wa haki ulioegemea kwenye majukumu mepesi yaliyowekwa juu ya mwanamke, na ambao unaakisiwa kwa usawa kabisa kwenye kiasi pungufu ambacho yeye anarithi. Huu ndio wakati ambapo kwa kawaida, kwa upande wa familia nyingi, mtu anaweza kusema kwa busara kabisa kwamba matumizi anayoyafanya mwanaume katika kumsaidia mke wake katika maisha yao ya ndoa ni makubwa kwa mara nyingi sana kuliko kiasi kile ambacho mwanamke angeweza kurithi kama angekuwa apokee mafungu yanayolingana sawasawa na kaka zake wawili. 46

Page 46


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah Kama desturi au kanuni, ule wajibu wa kifedha ambao mwanaume anaubeba una athari fulani; wakati mwanaume anapohakikisha kutimiza matumizi ya mke wake, yeye huwa anajisikia hisia kubwa ya uwajibikaji kwa mke wake. Hii itapelekea kuwepo hisia chanya kutoka kwa mke wake ambaye anajiona kwamba anawiwa na mume wake na akajitahidi kulipa deni hilo kwa kulea uhusiano na uamilianaji naye uliosimama juu ya upendo, heshima na ushirikiano. Kwa matokeo ya hisia za ziada za uwajibikaji kwa nafasi ya mwanaume kwa mke wake, kwa upande mmoja, na ile hisia ya kudaiwa kwa mwanamke kwa mumewe kwa upande mwingine, kuna ongezeko la mapenzi na upendo kati yao, na hili litasaidia kuimarisha msingi wa maisha ya familia. Athari hii hii ya ongezeko isingeweza kuibuka kama mwanamke angepata fungu kubwa katika urithi. Tangu kuchipukia kwa Uislamu hadi leo hii, Mamillioni ya Waislam wa kiume na kike, wake na waume zao wameishi bega kwa bega kwa ukunjufu wa nyoyo, bila hii tofauti katika mafungu ya mirathi kusababisha mvurugiko katika utaratibu wa maisha ya kifamilia ya Kiislamu; kwa kweli, wala hapakuwa na ushahidi wa kutosha wa kutoridhika kwenye upangaji huu ambao ungetupia kivuli juu ya uhusiano wao mkunjufu au kusababisha mpasuko miongoni mwa familia. Na yale matukio ya nadra ambapo kulitokea migogoro ya kifamilia kutokana na mafungu katika mirathi hayabatilishi ile hali ya jumla iliyoelezwa hapo juu. Moja ya hatua za maendeleo ya kuvutia katika nyakati za sasa ni ongezeko la welekeo wa wanawake huko Magharibi (ukilinganisha na wanaume) kugeukia kwenye Uislamu. Licha ya juhudi zote za baadhi ya mawakala wa kimagharibi za kuwashawishi wanawake kwamba Uislam unawanyima wanawake haki zao – na katika propaganda zao zilizoenea sana, wao hawajizuii kutokana na kutoa kila shutuma ya ukiukwaji wa haki – hata hivyo, wanawake wengi wanageukia kwenye Uislam kuliko wanaume. Ukweli huu unaweza kuonekana kwa urahisi kutoka kwenye taarifa za kitakwimu 47

Page 47


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah na ni lazima zisipuuzwe kirahisi; bali tunahitaji kulichunguza jambo hili kwa uangalifu na makini zaidi na kufikiria juu ya mambo ambayo yatamfanya mwanamke kutoka kwenye jamii ya kimagharibi awe tayari kupuuza zile haki sawa katika mirathi ambazo amepatiwa kupitia sheria za nchi yake (sheria ambayo imepitishwa kwa kuzingatia manufaa ya kimali ya mwanamke), kwa upendeleo wa dini ambayo imeelekeza kwamba fungu la mwanaume katika mirathi ni mara mbili ya lile la mwanamke. Inawezekana kutoliona lile jambo lenye kuathiri la asili ya maumbile ya mwanadamu (fitra), ambalo linahusiana na msingi halisi hasa wa wanadamu na kupuuza maumbile ya msingi ya dhahiri ya jinsia ya kike kuhusiana na hili? Hususan wakati tunapojua kwamba Uislamu umezingatia tofauti za kiroho na kimwili kati ya wanaume na wanawake kama msingi wa sheria za mirathi. Wakati sheria inapotungwa juu ya msingi wa haki na ikawa na mizizi ndani ya kina cha maumbile ya mwanadamu, kwa nini iwe yenye kupatwa na mabadiliko na mageuzi? Na ni nini itakachokiweka kama kiini chake badala ya haki na maumbile ya asili ya mwanadamu? Kama sheria zilizotengenezwa na wanadamu zingeshughulikia kwa uhakika mahitaji ambao yanaanzia kutoka kwenye vina vya wanadamu na kuridhisha hisia zake za ndani, basi mambo kama hayo yasingehitaji kufikiriwa. Kwa nyongeza juu ya yale ambayo tumekwisha kuyaelezea, kipengele kingine cha hekima ya Ki-ungu katika sheria ya mirathi ni kile kipengele cha uchumi; kwa hakika: Huko magharibi, utajiri unaowafikia wanawake kupitia mirathi ni sawa sawa na ule ambao wanaume wanaupokea kwa njia hiyo hiyo. Hata hivyo, katika hali nyingi utajiri wa wanawake unatumika kidogo sana katika njia za viwanda na biashara za maana, na sehemu yake kubwa kwa kawaida inatumika katika mapambo, sherehe zisizo na lazima, anasa na mapambo ya vito, bidhaa zisizo za lazima na maliwazo mbalimbali; huu sio kwamba ni uharibifu tu, bali vilevile ni kinyume na maadili ya heshima, yanayosababisha hisia za uchungu katika familia masikini na hatimaye kuishia kwenye unyonge wa kijamii na utamaduni wa uharibifu 48

Page 48


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah na israafu; inawezekana kwamba kama utajiri huu huu ungekuwa mikononi mwa wanaume, wao wangeutumia kuendeleza biashara na shughuli za kifedha na uwekezaji ambao ungeongezeka thamani, na kuishia katika uboreshaji wa hali zao za kiuchumi. Haiwi ni bila sababu kwamba maendeleo na kushamiri kwa uchumi mbalimbali katika jamii za kimagharibi kumekuja kutoka kwenye mali za wanaume, na nyingi ya shughuli na taasisi za kifedha katika jamii hizi hizi ambazo zinapiga makelele juu ya haki sawa kwa wanaume na wanawake, kwa kweli zinahusiana na wanaume. Jambo jingine ni kuhusiana na usimamizi wa familia. Kwa hali halisi, wajibu wa wanaume na wanawake ni kumkamilisha na kumstawisha mwenzie kwa kila mmoja wao, kwa hiyo matumizi sahihi ya uwezo wa kila mmoja wao katika kumsaidia mwenzie kunawezesha maisha yao ya pamoja kuendelea kwa ushwari kabisa, na huu mgawanyo wa majukumu na upangaji katika maisha yao ya kushirikiana kunahudumia kwa ajili ya mahitaji ya familia. Wakati Qur’ani inapoweka wajibu wa ulinzi na usimamizi kwenye mabega ya mwanaume kwa kusema:

“Wanaume ni walinzi juu ya wanawake …..” haina maana ya kusema kwamba wanaume ndio viongozi au kwamba jinsia moja ni bora kuliko nyingine katika kiwango cha ubinadamu. Wakati mwanaume na mwanamke wanapoishi pamoja kama wenza na wakaingia kwenye maisha ya kifamilia, hususan familia iliyosimama katika kanuni ya ushirikiano na maelewano, ni yupi mmoja kati yao ambaye ana uwezo wa kuisimamia familia hiyo na kutoa kwa ajili ya matumizi yao; ni mwanaume, mwanamke au watoto?1 1. Inawezekana kwamba katika baadhi ya hali wanawake wanakuwa wanafaa zaidi kusimamia kuliko waume zao, hata hivyo, wakati wote, sheria haitamki hali zote maalum, na imeshughulika tu na hali ya kawaida miongoni mwa wanadamu. 49

Page 49


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah Tunapoangalia hali iliyopo katika jamii sasa, tunaona kwamba mmiliki wa shughuli za kibiashara, ambaye ameajiri watu kadhaa, na ambaye anawalipa kwa ajili ya utumishi wao kwa kawaida huchukua jukumu la usimamizi wa watumishi wake bila ya kuteuliwa na mtu yoyote kwenye kazi hiyo. Hii ni desturi ya kawaida na waajiriwa hao huikubali hali hiyo bila ya maswali. Qur’ani vile vile inataja wajibu wa mwanaume kama msimamizi wa kitengo cha familia kama suala la desturi iliyokubalika na sio uzushi mpya. Inaunga mkono kile ambacho ni utaratibu wa kawaida katika jamii, na kwa matumizi ya maneno: “na kwa sababu wanatumia mali zao� (bimaa anfaquu), katika aya hiyo hapo juu, inaashiria kwenye suala hilo hilo kwamba sehemu kubwa ya mwanaume katika wajibu wa msimamizi na mlinzi imeunganishwa kwenye wajibu wa kutoa kwa ajili ya matumizi ya familia ambao unabaki juu ya mabega yake huyo mwanaume. Kanuni hii ya kimantiki imefumana na dhati ya uhai, ikiwa na maana kwamba, kwa nyongeza ya wanadamu ambao wamekubali, kwa silika zao za asili, ule wajibu wa mwanaume kama msimamizi na mlinzi, hali hiyo hiyo inakuwepo kwa kawaida katika jamii ya wanyama vile vile, na mifano ya tabia hii inaonekana waziwazi katika vipengele vyao vya maisha. Hapa inafaa kutaja jambo jingine pia; lile ambalo linasikika kwa kawaida kabisa huko magharibi kutoka kwenye vikundi vile vile vya wanafikra wasomi na watetezi wa uhuru ni haki ya mashoga, na kuna mwelekeo wa hata miongoni mwa wanafikra maarufu kabisa kwa kuvutwa kuelekea kwenye jambo hili kwa jina la utetezi wa uhuru. Huenda haitakuwa miaka mingi kabla ya haki za mashoga kuhudumiwa kwenye jamii yote ya magharibi na haki zao kukubaliwa kama hali ya kawaida inayotarajiwa kwa kiasi ambapo upinzani wowote utakaoibuliwa utaonekana kama kugeuka nyuma kusikokubalika na hakuna hata mtu mmoja atakayeweza kusema chochote au kuleta upinzani wowote kuhusu jambo hilo.

50

Page 50


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah Wakati inapokuwa imekubalika kwenye sheria ovu juu ya matamanio ya aibu na duni ya ubinadamu, kila wema unaoheshimika utatupiliwa mbali na jamii itaangukia kwenye kushuka kwa utamaduni na maadili mema na kisha kuozeana. Ukweli ni kwamba mchakato wa sheria hii kimsingi haichukuani na maumbile asilia ya mwanadamu, na yale ambayo yanawasilishwa kwa jina la uhifadhi wa uhuru, lazima lifungike kwenye ile aina ya uhuru ambayo inarahisisha mahitaji ya mwanadamu yenye kuleta afya (yanayofaa) na yaliyo sawia, na wala sio madai yanayoibuka kutoka kwenye moyo usio wa kawaida na muovu. Kama chini ya bango la uhuru na ulinzi kwa sheria, tabia hii ya kingono isiyo ya kawaida na ya kipotofu inakuwa yenye kuenea na ya kawaida, basi, kama matokeo ya vitendo vya wanafikira hawa walioelimika na wenye mawazo mapana na watetezi wa haki za wanawake, nusu ya wanadamu katika jamii ya magharibi yenyewe – wanawake wake – watakuwa wamenyimwa haki ya kuolewa na kuwa na mahusiano ya kimwili ya kawaida pamoja na jinsia tofauti na katika ukamilifu wa wakati, jumuiya hii itabidi ikabiliane na tishio la kukoma kuwepo. Je utungaji wa sheria kama hizi unakuwa ni kwa maslahi bora ya mwanadamu na zina majawabu na matokeo yanayostahili kutetewa? Kama tukifanya mapitio kwenye historia ya utungaji sheria katika mataifa mbalimbali ya ulimwengu, tunakutana na sheria ambazo kwamba wanafikra na wataalamu wameweka mawazo na juhudi nyingi tu; bado kwa kupita kwa wakati na kwa tafakari na uchambuzi wa kina kabisa, kukosea kiutendaji kwa watunga sheria, na udhaifu, upungufu na kukosa uwezo kwa zile sheria hatimaye kumedhihirishwa. Lile ambalo mwaka wa jana liliokana kwa wenye kuona mbali kuwa ni namna ya mfano bora na wenye kufaa sana wa kuendesha jamii zao, limekuja kutambulika kama ni matokeo ya uelewa usio sahihi na kamilifu. 51

Page 51


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah Kwa hiyo wanageukia kwenye mfumo mpya wa utungaji sheria, na licha ya maendeleo yote katika maoni na mawazo ya wasomi na wataalamu, utafutaji (wa sheria kamilifu) bado unazishughulisha akili za watafiti. Ni mara ngapi kundi la wanachuoni kwa kauli moja wameunga mkono mfano fulani bado kwa kupita wakati na maendeleo ya elimu, udhaifu na makosa ya maoni yakathibitika kwa uhakika kabisa. Inakubalika mahali pote na wanasayansi wanaofanya kazi katika nyanja tofauti kwamba bila kuelewa na kuzingatia maumbile ya msingi ya mwanadamu, upangaji na utengenezaji wa mipango na programu utakuwa wa thamani ndogo sana. Haiwezi kukanushwa leo hii, licha ya elimu nyingi na kubwa iliyoko kwenye uwezo wa mwanadamu katika kila nyanja, kwamba kuna vilele vingi ambavyo bado havijapimwa, hususan katika masuala yanayohusiana na upeo wa ndani na wa kiroho ambao umo ndani ya mwanadamu; kwa kweli katika uwezo wake wa kiroho mwanadamu ni bahari ya kina kirefu na elimu yetu kuhusu hilo ni ndogo sana. Na kama matokeo, upangaji na uundaji wa sheria za kutawala maisha ya mwanadamu, ambaye utambulisho na asili yake vimefunikwa ndani ya kitendawili, ni sawa na kupanga utaratibu wa matibabu kwa ajili ya mtu asiye na thamani na ambaye maradhi yake hayafahamiki. Uundaji wa sheria sio tu unahitaji elimu kamilifu yenye kujumuisha mambo mengi kuhusu kila kipengele cha utu wa mwanadamu, bali inahitaji pia elimu ya sawasawa ya jamii na mahusiano ya kijamii yaliyofungamana na vilevile elimu ya viumbe wengine ambao maisha yao pia yanafungamana na mwanadamu. Ni juu ya mamlaka na elimu gani ambayo hawa wanaodai kwamba wanatamani ustawi na furaha ya jamii wanayoegemeza mipango na taratibu zao? Ukweli ni kwamba ile elimu na utambuzi wa mwanadamu bado haujawa 52

Page 52


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah na uwezo wa kuelewa kikamilifu ile sifa za ndani kabisa za kimwili na kiroho za wanadamu na miujiza ya tabia za kijamii inayoibuka kutoka kwenye muingiliano wa watu, mmoja na mwingine. Matokeo yake, mwanadamu hana uwezo wa kushughulikia mahitaji tofauti ya ubinadamu na kubaini ile njia sahihi kati ya njia nyingi ambazo zinajitokeza mbele yake. Hata kama zile kanuni zinazoongozea kwenye ukamilifu wa mwanadamu zikiwa zinaeleweka, elimu ya mwanadamu na akili yake inakuwa haina uwezo wa kujibu peke yake yale maswali lukuki yanayojitokeza, na kuchukua wajibu kamili wa kuongoza maendeleo ya wanadamu katika kila nyanja kwa mujibu wa mpango wa kimungu. Ni wakati ule tu ambapo mwanadamu anatafuta ndani yake mwenyewe na kuyatumia yale maadili ambayo yamezikwa ndani ya moyo na maumbile yake ambayo yatapata mafanikio na kuunda mfumo ambao unazingatia vipengele mbalimbali vya uhai wake. Ukweli ni kwamba wakati wa kutunga sheria, mwanadamu hawezi kubakia na kinga dhidi ya asili na tabia yake mwenyewe, tofauti miongoni mwa watu mmoja mmoja katika makuzi yao, desturi za kitamaduni na kijamii, mila za kifamilia na mambo mengine huathiri sana uelewa wao, maamuzi na maoni. Tafsiri ya maneno na mawazo haziwi ni zile zile kwa watu wote katika jamii, kila mmoja anaelewa kulingana na umaizi na maoni yake binafsi. Fikra na maoni ya watunga sheria na warekebishaji ambao wanajiingiza katika uchunguzaji wa maumbile ya mwanadamu huzama, ama kwa kujua au kwa kutokujua, kuelekea kwenye mawazo ya kabla yaliyopatikana kutoka kwenye mazingira yao husika na kwa hiyo wanakuwa hawana uwezo kufanya mchanganuo adilifu wa hali zenyewe. Haya yote yanaashiria kule kutokuwa na maana kwa kutegemea akili ya mwanadamu na elimu yake peke yake kuweza kuhudumia haja hii na ni uthibitisho wa dhahiri wa ukweli kwamba sheria za mwanadamu zinaweza kuwa zenye uharibifu kwa uwezekano mkubwa kabisa. Ni hapa ambapo ni 53

Page 53


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah lazima tukubali kwamba mtu hawezi kujitiisha kwa uhakika na kujiamini kabisa kwenye mfumo wenye mashaka kama huo na kuukabidhi ustawi wake kwenye mfumo huo. Hata kama tukichukulia kwamba siku itakuja ambapo ilmu ya mwanadamu itakuwa na uwezo wa kuvizunguka vipengele vyote vya uhai wa mwanadamu, hata hivyo hilo halitahakikisha raha na ustawi wa mwanadamu kwa sababu mwanadamu kwa asili amezoea kufanya maamuzi yanayotegemea juu ya maslahi yake binafsi na ya kichoyo. Kwa kuyatia akilini matatizo yote haya, yule mwanafikra mashuhuri ajulikanaye sana wa kimagharibi, Rousseau anaandika: “Ili kuzigundua sheria nzuri na bora ambazo zitakuwa zenye manufaa kwa mataifa, mtu anapaswa kwa lazima kabisa kutafuta mtu mwenye akili yenye uwezo kamilifu, ambaye ni mjuzi wa matamanio yote ya mwanadamu na udhaifu wake lakini yeye mwenyewe awe hakuathiriwa nayo hayo. Yeye awe hana mahusiano na maumbile lakini awe ana elimu timilifu juu yake. Ustawi wake binafsi usiwe unategemea juu yetu sisi, bali awe yuko tayari kutusaidia sisi katika kupata ustawi wetu …..” (Kitabu Social Conventions, uk. 81) Dr. Carrel anaandika juu ya suala hilo hilo: “Mifumo ya serikali, ambayo imeundwa yote kabisa katika akili za wana nadharia hazina maana yoyote wala thamani. Zile kanuni za Mapinduzi ya Ufaransa, mawazo ya Max na Lenin yanatumika tu katika kuwaweka mbali wanadamu. Ni lazima itambulike wazi kwamba sheria za mahusiano ya mwanadamu bado hazijajulikana. Elimujamii (sosiolojia) na uchumi ni elimu za kukisiwa tu – yaani, ni elimu za bandia.” Hivyo inaonekana kwamba mazingira ambamo sayansi na teknolojia vimefanikiwa katika kumuendeleza mwanadamu hayamfai, kwa sababu yameundwa bila utaratibu maalum, kwa kubahatisha, bila ya kujali nafsi yake 54

Page 54


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah halisi. (Kitabu; Man, the Unknown, uk. 30). Kwa hiyo haki ya kutunga sheria inastahiki zaidi Ambaye uhai wake mtakatifu hayashurutishwi na hali na ushawishi wa mazingira, wala kushindwa katika kazi yoyote kuweze kufikiriwa juu yake kamwe. Elimu yake isiyo na mipaka iwe inauzingira kabisa uhai na Awe anajua mahitaji ya msingi na halisi ya mwanadamu na anatambua mipaka ya uwezo wake na mabadiliko na maendeleo ambayo mwanadamu na ulimwengu mzima bado vitayapitia. Na Yeye ni Mwenyezi Mungu, na haki ya kuuwekea mfumo utungaji wa sheria ni wenye kufaa Kwake Yeye tu. Qur’ani tukufu inaeleza:

“Je wanataka hukumu za Kijahiliya. Na ni nani aliye mzuri zaidi kwa hukumu kuliko Mwenyezi Mungu; kwa watu wenye yakini.” (alMaidah; 5:50)

55

Page 55


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah 5. NJIA SAHIHI YA USULUHISHI NA MATOKEO YAKE YA HAKIKA

“Na ikiwa makundi mawili katika waumini yanapigana, basi yapatanisheni. Na likiwa moja la hayo linadhulumu jingine, basi lipigeni linalodhulumu mpaka lirejee kwenye amri ya Mwenyezi Mungu. Na likirejea basi yapatanisheni kwa uadilifu. Na hukumuni kwa haki. Hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wanaohukumu kwa haki.” (alHujurat; 49:9). Mwenyezi Mungu Mtukufu ameelezea kwamba miongoni mwa sifa za umati wa Mtume wa Uislam (s.a.w.w.) ni ukadiri na uwastani wao. Maelekezo ya Mwenyezi Mungu Mwenye hekima pia msingi wake uko juu ya sifa hizi, na kwa hakika ni sura muhimu ya hekima ya Mbinguni kwamba Mwenyezi Mungu anatetea njia ya kati na kati, iliyo tofauti na aina yoyote ya kuvuka mipaka, ijulikanayo kama ‘njia iliyonyooka’ (sirat al-mustaqiim). Katika aya hiyo hapo juu vile vile, ambayo inazungumzia kuhusu usuluhishi baina ya makundi mawili yanayogombana, vipengele vyote vimeangaliwa ili kwamba marekebisho yanayoagizwa hayaegemei tu juu ya hisia na mabadiliko, bali maafikiano yanaimarishwa kwa mantiki, na mazingatio ya maadili elekevu na ya kijamii yanafikiriwa vile vile. Ufafanuzi wa ujumbe halisi uliomo ndani ya aya hiyo ni kama ufuatavyo: Mgogoro au ugomvi kati ya makundi mawili hauwi wakati wote ni wa namna au aina moja; bali unatokana na namna mbalimbali za kutoelewana 56

Page 56


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah ambazo zinaweza kulipuka baina ya watu mmoja mmoja, kunakosababisha mvurugiko wa utulivu na amani katika jamii. Miundo na namna mbalimbali za kutoelewana na malengo yaliyoko nyuma yake na hali ya makabiliano kila moja litaathiri zile mbinu zinazochukuliwa katika kuyatuliza. Kwa sababu hii, ni lazima kuangalia kwa makini mambo yote ili mkakati wa marekebisho na juhudi za kisuluhishi hazielekei kwenye matokeo yasiyotakikana. Katika aya iliyoko kwenye mazingatio vilevile, namna za kutatua migogoro zinatofautiana kulingana na aina yenyewe ya mgogoro, na kila mgogoro mmoja ni lazima ikabiliwe kwa utendaji unaofaa. Kwa nadra, inawezekana kwamba shaka au kosa au uelewa mbaya unawakasirisha watu mmoja mmoja – na mara nyingi watakuwepo wale ambao watazichochea zile hali na kuongeza kutoaminiana zaidi sana – na kusababisha mabishano yanayoyaweka makundi hayo mawili kila moja kwenye makoo ya wenzao, hata wakati ambapo kimsingi hakuna upande uliokuwa umekusudia kuudhuru ule upande mwingine. Katika suala hili, Qur’ani inawashauri wenye nia njema na wasuluhishi wa amani wa jamii kuingilia kati na kupatanisha baina ya makundi mawili hayo na kujaribu kusuluhisha kabla hali haijaongezeka kutoka kwenye udhibiti na damu ikamwagika. Hata hivyo, tofauti na kipande cha mwisho cha aya hii, Qur’ani haielezei kimsingi kwamba kuleta amani kuwe ni kutegemea juu ya uadilifu, inaelezea tu kwamba wale watakia kheri lazima walete amani na usuluhishi kati ya makundi mawili (faslihu baynahuma). Hii ni katika suala maalum ambamo hakuna kundi lililokiuka au kuvunja haki za wenzao, ni mabishano tu yaliyotokea. Katika hatua hii haikuwa lazima kwa Mwenyezi Mungu kuamuru usuluhishi, ambao pia uliambatana na msisitizo juu ya uadilifu. Hata hivyo, kama moja ya makundi mawili hayo yanayogombana kwa shari tu likikimbilia kwenye tabia ya mabavu na akazikanyaga kanuni za uungwana na upole, basi ni lazima lisimamishwe kwa njia yoyote ile. Kama hatua kali zikisababisha wenye shari kuacha shari zao na kukubali 57

Page 57


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah sheria ya Mwenyezi Mungu, basi Qur’ani inaelekeza kwamba usuluhishi ufanyike kwa kuzingatia haki na uadilifu. Kuna jambo moja jepesi lakini la muhimu sana ambalo linaweza kudokezwa hapa kutoka kwenye aya hii, ambalo ni kwamba, katika kila hali mtu ni lazima azingatie malengo ya msingi ya Uislam ya kulea na kuendeleza jamii, na msisitizo wake katika kusimamisha na kuongoza ummah wa Kiislam katika misingi ya haki na uadilifu katika maana yake halisi na pana kabisa, na tamaa yake ya kuondoa kila mwelekeo wa dhulma na shari kutoka kwenye akili za mtu mmoja mmoja katika jamii; ni kupitia kwenye fikra hizi tu ambako kwamba tunaweza kupata uelewa wa kina wa ule msisitizo wa Qur’ani juu ya suluhu iliyoambatana na uadilifu. Wakati Qur’ani inapowashauri wapatanishi na wasuluhishi kusuluhisha kati ya makundi mawili yanayogombana kwa uadilifu kamini na usawa, haina maana ya kuwaonya wapatanishi hao kwamba wao wenyewe wasifanya dhulma juu ya kundi moja wakati wanapotafuta amani na muafaka, kwa sababu wapatanishi kwa kawaida hawana upendeleo na wenye nia njema. Kwa kweli nia ni kuwashauri kwamba ile namna ambamo wanajaribu kusuluhishia iwe kwamba kila kundi mara moja linapokea haki yake ya halali, wala isiwe ni kusamehe kitu au kupokea kitu chochote kisichostahili, hata kama ni kwa maelewano ya pande mbili. Kwa hiyo, hao wapatanishi wasilifanye ni lengo lao la mwisho kupata usuluhishi kwa gharama yoyote ile. Kwa uhalisia hii ina maana kwamba kutoa tahfifu kusiwe ni juu ya msingi wa usuluhishi na upatanishi, hata kama ikiwa ni kwa ridhaa ya lile kundi lililodhulumiwa, kwa sababu wale wenye shari wameleta makabiliano kwa makusudi ili kwamba waweze kupata tahafifu kwa nguvu. Katika masuala kama hayo, itakuwa ni makosa iwapo wapatanishi wanaotaka kufanya uchunguzi na kulithibitisha tukio kwa karibu mno, kabla ya kuchukua hatua za kuamua mgogoro kwa usuluhishi, wataelekeza juhudi zao katika kusisitiza juu ya upole na kusamehe yaliyopita katika jaribio la 58

Page 58


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah kumaliza mgogoro. Endapo watalishauri kundi moja kusamehe haki zake kwa faida ya lile jingine ili kupata amani na kwa namna hii wakafikia kulifunga suala hilo, hilo litasaidia tu katika kuongeza ukaidi wa wale washari ambao wamejaribu kupata udhibiti kupitia mabavu na uonevu. Na mara kwa mara, kila zinapojitokeza fursa siku za usoni, wao wataitumia mifano hii kama nguvu ya ushawishi kwa ajili ya faida binafsi; kwa kawaida wapatanishi vilevile, katika wakati wa kupatanisha, wanawaridhisha wakosaji kwa kuwapa tahafifu ili waache uvuka mipaka wao na kuacha tabia yao ya dhulma na uonevu, na kuwaacha waathirika wao katika amani. Hapa, madhalim wanakuwa washindi na wenye kuonewa na kudhulumiwa wanakuwa ndio wapotezaji wenye kushindwa. Kwa namna hii, amani inaweza kupatikana lakini haki haijafanyika. Ingawa lile kundi lililoonewa linaweza likaachia haki fulani ili kujiengua lenyewe kutokana na matatizo zaidi kutoka kwa wenye shari, tahafifu hizi, hata kama zikitolewa kwa hiari, wakati wote zitakuwa na matokeo hasi, matokeo mabaya. Kwa sababu hii Qur’ani inasisitiza kwamba suluhu lazima itekelezwe bila kukimbilia kuafikiana au kukana au kuacha haki za mtu. Katika mazingira haya, ikiwa wahalifu watasisitiza kuendelea katika mwenendo na njia yao hiyo, kwa mujibu wa Qur’ani, wao itabidi wakabiliane na ummah wote wa Kiislam, ambao unawajibika kutoka kuja kuwasaidia wale wa kundi linalodhulumiwa. Hivyo, sababu ya msisitizo wa Qur’ani juu ya usuluhishi unaoandamana na usawa katika aya tunayoingalia, ambao unaweza kuonekana kutokana na urudiwaji wa maneno ‘adl na qist yaani, uadilifu na usawa kwa mara tatu:

“…..basi yapatanisheni kwa uadilifu. Na hukumuni kwa haki. Hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wanaohukumu kwa haki.” (49:9) …..

59

Page 59


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah huwa inatambulika (sababu hiyo) pale wapatanishi, katika juhudi zao za usuluhishi, wanaiangalia sawasawa ile asili ya msingi ya mzozo huo na kutafakari kwa makini juu ya sababu zilizoko nyuma ya mgogoro huo. Kama wakigundua kwamba sababu ilikuwa ni mabavu na ukatili, basi hapo wao lazima watumie nguvu katika kuwazuia wakosaji kutokana na kutimiza malengo yao. Kama suluhu na uamuzi wa migogoro unafanyika katika namna isiyo sahihi, yaani kwa kutoa na kupokea tahafifu, itakuwa kama upanga wenye ncha mbili ambao utayaharibu makundi yote mawili; kwa upande mmoja, yule aliyedhulimiwa atahisi kwamba wapatanishi hawataweza kuzuia haki zake kutokana na kuingiliwa na kufanya uamuzi adilifu kwa sababu katika shuruti za kivitendo, mkosaji wake amenufaika kwa gharama yake mdhulumiwa. Kwa upande mwingine, yule mkosaji atahisi kwamba mbinu zake zisizo na maana hatimaye zimekuwa na mafanikio na zimempatia kile alichokitaka. Hata hivyo, kinachopasa kwa ajili ya jamii halisi ya Kiislam ni makubaliano ambayo ni ya usawa na haki kwa jumla, sio yale ambayo ndani yake mtu mmoja anajitenga na haki zake akimuachia mwingine kufanikisha malengo yake ya kidhalimu. Kama wakati wa mzozo huo, uwezekano wa suluhisho kwa maafikiano ukitokea, hapo basi mtu aliyekerwa anaweza yeye mwenyewe binafsi kujiengua kwenye mgogoro huo kwa kutoa msamaha na hapo kujitoa mwenyewe kutoka kwenye uovu wa yule mwenye shari. Katika suala hili, hakutakuwa na haja ya wengine kujiingiza katika jambo hilo na kutafuta suluhu. Hata hivyo katika aya hii, Qur’ani imeweka wajibu wa kusuluhisha kwenye mabega ya jamii ya Kiislam na kuulazimisha ummah wa kwa makusudi kabisa kusimama kwenye ulinzi wa huyu anayedhulumiwa wakati wowote wanapo dhulma yoyote ile. Lazima wakomeshe vitendo vya dhalimu na kumzuia, na sio kujaribu kulifanya kundi lililodhulumiwa likubali vile vitendo visivyo vya haki vinavyotendwa kimakosa dhidi yao, 60

Page 60


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah au kujiingiza kwenye njia ya vitendo ambavyo vinaishia kwenye manufaa ya mkosaji. Qur’ani inaeleza:

"Na mtakapohukumu baina ya watu muhukumu kwa uadilifu….." (4:58) Ni kweli kwamba katika suluhu ambayo tunaijadili hatuna maana ya kimbilio kwenye mahakama ya sheria. Bali tumekuwa tukihusika na juhudi za wapatanishi za kusuluhisha baina ya makundi mawili yanayozozana. Uislam unaweka umuhimu mkubwa kabisa kwenye mfumo wa haki unaoeleweka na wenye maarifa mengi; kwa kweli moja ya malengo makubwa ya Mitume watukufu (a.s.) lilikuwa ni wakati wote kujitahidi kusimamisha haki na usawa katika jamii za wanadamu. Kuhusiana na hili, Qur’ani tukufu inaelezea:

“Kwa hakika tuliwatuma Mitume wetu kwa dalili waziwazi, na tukateremsha Kitabu pamoja nao na mizani, ili watu wasimamie uadilifu, …..” (57:25). Kwa hiyo kama tukitafakari juu ya jambo hili kwa uangalifu zaidi, tutatambua kwamba kuvuka mipaka na kuvunja haki za wengine – katika kila wakati na kila hatua, hata katika suala la usuluhishi na upatanishi, na hata kwa makubaliano ya pande mbili – hakuendani na mtazamo wa Kiislam juu ya uadilifu.

61

Page 61


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah Kuacha na kusamehe haki zake mtu, wakati mwingine kunaweza kuwa ni kitendo muhimu na cha kupendeza pia, na chenye manufaa katika haki yake chenyewe; kinaweza kuleta matokeo mema na kwa kweli kikaweza kuleta mabadiliko ya moyo. Hata hivyo, inapokuwa ni kwa gharama ya uadilifu, sio tu kwamba si chenye kusaidia; ni chenye kuleta matokeo tofauti na matarajio na kama tulivyoeleza, hatimaye kitakuwa wakati wote kina athari hasi katika akili ya mkosaji ambaye alijiandaa kupata manufaa kupitia vitisho, na kitamhimiza na kumtia moyo kufanya mambo katika mtindo huo huo siku za usoni. Matokeo yatakuwa kwamba yeye atapata na kunufaika kutoka kwenye kila mzozo, ambapo lengo na madhumuni ya Uislamu ni kuondoa uonevu na dhulma kutoka katikati ya jamii za Kiislam, ili kwamba watu waweze kuhakikishiwa kwamba hakuna yeyote atakayekuwa na uwezo wa kupata chochote kwa kutumia nguvu au bila kutumia haki. Amirul-Mu’minin Ali (a.s.) - jemedari wa wachamungu amesema:

“Dhulma juu ya Ihsani (wema) ni kuifanya mahali pasipostahili.” (Ghuraral-Hikma, uk. 498) 6. UCHAMBUZI WA SEMI MBILI ZA QUR’ANI

“Na tukamwokoa Musa na waliokuwa pamoja naye wote. Kisha tukawazamisha hao wengine. Hakika bila shaka katika hayo ipo ishara lakini wengi wao si wenye kuamini. Na hakika Mola wako ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu.” (26:65-68) 62

Page 62


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah

“Kaumu ya Nuh waliwakadhibisha mitume.” (26:105)

“Basi tukamuokoa na walio pamoja naye katika jahazi iliyosheheni. Kisha tukawagharikisha baadaye waliobaki. Hakika bila shaka katika hayo ipo ishara, lakini wengi wao si wenye kuamini. Na hakika Mola wako ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu.” (26:119-122).

“A’d waliwakadhibisha mitume.” (26:123)

“Basi wakamkadhibisha na tukawahilikisha. Hakika bila shaka katika hayo ipo ishara, lakini wengi wao si wenye kuamini. Na hakika Mola wako ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu.” (26:139-140) “Thamuudi waliwakadhibisha mitume.”

“Basi ikawashika adhabu. Hakika bila shaka katika hayo ipo ishara, lakini wengi wao si wenye kuamini. Na hakika Mola wako ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu. (26:158-159). 63

Page 63


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah “Kaumu ya Lut waliwakadhibisha mitume.”

“Na tukawanyesheza mvua, basi ni uovu mno wa mvua ya waliyoonywa. Hakika bila shaka katika hayo ipo ishara, lakini wengi wao si wenye kuamini. Na hakika Mola wako ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu.” (26:173- 175)

“Watu wa mwituni waliwakadhibisha mitume.” (26:176)

“Basi wakamkadhibisha, ikawashika adhabu ya siku ya kivuli. Hakika hiyo ilikuwa adhabu ya siku kubwa. Hakika bila shaka katika hayo ipo ishara, lakini wengi wao si wenye kuamini. Na hakika Mola wako ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu.” (26:189-191). Historia ya mwanadamu, na uchanganuzi wa maendeleo yake vinadhirisha hazina ya kipekee ya taarifa; ukweli mwingi unadhihirishwa kupitia tafakuri ya kina juu ya matukio haya – kwa kweli ni moja ya njia timilifu kabisa ya kugundulia ukweli. Qur’ani inamhimiza mwanadamu kugundua kweli hizi kwa kuchunguza yale mambo ambayo yamepelekea kwenye kufanikiwa au kutofaulu, na kupanda na kushuka kwa umati zilizopita, na hatima ya wale waliokiuka ukweli. Kwa kudhamiria juu ya sheria na mielekeo ya kawaida ya historian a kuchunguza uchambuzi sahihi wa matukio ya kihistoria, anaweza 64

Page 64


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah kutafsiri vizuri zaidi kadhia mbalimbali na kupata mafunzo na kunufaika na matukio ya wakati. Neno “’aziz” (mwenye nguvu) ni moja ya sifa nzuri sana za Mwenyezi Mungu ambayo Qur’ani inatumia kwa msisitizo mkubwa na kwa mara nyingi. Sifa hii mashuhuri takriban wakati wote imetumika kwa kuunganishwa na neno “hakim” (hekima) ndani ya Qur’ani, na kuunganishwa huku ni kiashirio cha hekima ya maneno ya Mwenyezi Mungu; Mungu ambaye ni Mwenye nguvu na Mwenye uwezo, wakati huo huo ni Mwenye hekima. Hata hivyo, katika Surat Shu’araa, sifa hii imetajwa kwa kuunganishwa na sifa nyingine; “ar-rahiim” (Mwenye rehema). Kwa kweli, sifa hizi mbili zinajirudia tena katika aya zinazofuatana katika Sura hii, aya ambazo zinaelezea ile tabia ya kuchukiza ya ummati zilizosimama katika ukaidi dhidi ya Mitume waliotumwa kwao, na wakazikwaza jitihada zao za kuwaongoza watu. Kwa nyongeza katika matumizi ya semi hizi mbili bega kwa bega, kule kurudiwa kwao pia ni kwenye kuelekeza na kunakostahili kuzingatiwa, kama sasa hivi tutakavyoeleza: Surat ash-Shu’araa inataja matukio ambayo wakati wote yamekuwa yakiwatokea Mitume wa Mwenyezi Mungu (s.a.). Katika Sura hii, kisa cha Nabii Musa (a.s.) na Firauni kinaelezewa kwanza, na kisha baada ya kuelezea visa vya Manabii wengine, ambao ni Nabii Ibrahim (a.s.), Nuh (a.s.), Hud (a.s.), Saleh (a.s.) Lutwi (a.s.) na Shu’aib (a.s.), Qur’ani inazungumzia juu ya juhudi zao za bila kuchoka na zenye dhamira za kila mmoja wao kulingania ujumbe wake, ambao ulijaa ukweli wa msingi na wa kina, kote ulimwenguni. Na kwa kuelezea mapambano yao dhidi ya ushirikina, upotofu na dhulma ya zama zao, aya hiyo inamliwaza Mtume wa Uislam (s.a.w.w.) kuhusiana na maudhi na matatizo ambayo yeye alikuwa akikabiliana nayo, na kuimarisha moyo wake kwa maneno mazuri yafuatayo: “wa tawakkal ‘al’l ‘aziz l-rahiim,” – yaani, “hivyo umtegemee Mwenye nguvu Mwenye rehema.” 65

Page 65


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah Katika aya zote ambamo maneno ‘aziz na rahim yanatajwa kwa pamoja, maudhui inakuwa ni karipio la Mungu dhidi ya makafiri washupavu juu ya tabia yao ya ukaidi na upotovu maishani mwao mwote na kwa kukataa ukweli licha ya kushuhudia hoja na ushahidi wa wazi. Kuendelea kwao chini ya njia hii ya giza na uhalifu wao endelevu hatimaye ukasababisha nyoyo zao kupigwa muhuri, na kuwaacha daima kutangatanga ndani ya giza. Swali linalojitokeza hapa ni: Kwa nini Qur’ani inatumia mneno ‘aziz na rahiim kumuelezea Mwenyezi Mungu Mtukufu, baada ya kuelezea kushuka kwa ghadhabu Yake na adhabu iliyostahili juu ya ummah ambazo ziliangamizwa kwa ajili ya ukanamungu na ukaidi wao? Ili kulijibu swali hili, ni lazima tuelewe ile maana halisi iliyomo ndani ya sifa hizi mbili tukufu, na hususan ule umuhimu wa kurudiwa kwao katika Surat Shu’araa. Kwa nyongeza, tunahitaji kufichua ni ujumbe gani uliomo kwa ajili wa wanadamu katika matumizi ya semi hizi mbili katika kuziweka sambamba na ni somo gani tunaloweza kujifunza kutoka humo. Tunajua kwamba miongoni mwa kupenda kwa mwanadamu ni tabia yake ya ubinafsi na kupenda kwake madaraka. Katika jamii ya wanadamu huwa tunawaona watu ambao wana hali ya kujiona ya umaarufu binafsi na wana tabia ya kukweza tu mafanikio yao. Matakwa haya potovu yanafanya kazi ya kumpoteza tu na inaendelea kuongeza umiliki wa matamanio maovu kwenye akili ya mtu na kumsababishia mabalaa chungu nzima juu yake. Kwa kweli sifa hii ni dhaifu zaidi ndani ya baadhi ya watu kuliko ilivyo kwa wengine. Ingawaje kuna watu ambao vitendo vyao maishani kimsingi vinasababishwa na nia za kiungwana, ambao wana uwezo wa kutofautisha elementi za kianasa za tabia zao kutoka kwenye matakwa yao halisi na ya kweli, na wanajaribu sana kujizuia wao wenyewe kutokana na matamanio ya hisia kali na zisizopendeza, watu kama hao ni wachache sana kwa idadi na 66

Page 66


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah wanapatikana kwa nadra miongoni mwa watu wa kawaida katika jamii. Hii ni kwa sababu kupata ulingano uliotulia namna hiyo kunahitaji mapambano makali na ya kudhamiriwa hasa dhidi ya nafsi. Kwa upande mwingine, wapo watu wengi, ambao kutokana na maadili yao dhaifu na tamaa ya kupata madaraka ya kiwango chochote wanachoweza kukikamata mikononi mwao, wao watakuwa tayari kuidhinisha makosa au uharibifu wowote ule ambao utawafanya wapate kile wanachokitafuta. Watashughulika vikali na mwenye mamlaka yeyote ambaye anajaribu kuwazuia wasifanikiwe wakati wanapojaribu kukata kiu yao isiyotoshelezeka juu ya madaraka. Hii ndio kawaida ya wale wanaotafuta kuwatawala wengine, ambao wakati wote wanatengeneza akilini mwao taswira ya kigezo chema ambacho kinaridhisha hisia zao za ubora juu ya wengine na kisha wanajaribu kujenga na kubadili haiba zao ipasavyo. Tunaona vilevile kwa uwazi kabisa kwamba tamaa ya makuu ya hali ya juu na utafutaji wa madaraka wakati wote umeambatana na utovu wa ustahimilivu unaojulikana. Hii haina mipaka kwenye suala la watu wa madaraka tu walioko juu ya nchi moja ama nchi mbalimbali, bali inadhihirika kwa viongozi wa mji au kijiji au hata kwenye idara ndogo kabisa. Hata yule kiongozi wa kikundi kidogo kabisa ni mwenye hisia kali kabisa na mtovu wa ustahimilivu juu ya uvunjaji kanuni mdogo kabisa kutoka kwa wale walio chini yake. Kwa upande mwingine, kuna uhusiano wa karibu sana kati ya madaraka na udhalimu, kwa kawaida, jinsi mtu anavyokuwa na madaraka zaidi ndivyo jinsi anavyokuwa mkosa huruma zaidi. Atashindwa kuvumilia na ataghadhibishwa na upinzani japo kidogo sana kwenye madaraka yake, atakuwa na kinyongo na kuwa na hisia za hasira na kulipiza kisasi na kujibu ukaidi wowote juu ya mamlaka yake kwa namna isiyojua kiasi, na tabia hii ya udhalimu vivyo itapanuka katika suala la kukosa utii kwa wale walioko karibu sana naye. 67

Page 67


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah Mitume wa Mwenyezi Mungu waliwafundisha watu kutafakari kuhusu ukweli na wakawakomboa kutokana na pingu za mila na ibada za kizamani zisizo na msingi. Ujumbe wao wa ufunguzi, ambao uliangaza peo za fikra za mwanadamu katika kila kizazi, ulikuwa ni wito wa Tawhiid (Upweke wa Allah) na ukanushaji wa kila namna ya ushirikina na uabudu masanamu; wao walisisitiza wokovu ulikuwa umo tu kwenye imani juu ya Mungu Mmoja. Kwa hakika, katika historia yote kila Mlinganiaji mtukufu alianza ujumbe wake kwa ufundishaji wa upweke, utukufu na umola wa Mwenyezi Mungu. Uelewaji wa ukweli huu wa msingi unamlazimisha mwanadamu, kwa kutembea katika njia hii tukufu, kurudisha nafasi yake na kupata ukamilifu katika uwiano na uhai uliobakia. Manabii wa Mwenyezi Mungu walivumilia taabu kubwa ambazo zilielekezwa kwao kwa subira kubwa na ustahimilivu ili kwamba, kwa kupita kwenye ujumbe wa Mwenyezi Mungu, wangeweza kutekeleza wajibu wao kwa uaminifu wa kuhakikisha furaha ya mwanadamu ambayo imewekwa mabegani mwao na Muumba. Baada ya hapo, kwa ajili ya wokovu wa jumuiya zao kutokana na kukamatwa na unyongevu wa kiroho katika mazingira ambamo misingi ya kiroho na kimaadili ilikuwa inamomonyoka na ambayo imewashusha wanadamu kutoka kwenye hali ya uungwana wao halisi, waliamrishwa kuwafundisha watu wao na kuwafanya wawe ni wenye kutambua uwezo wao. Waliwajulisha kwamba katika maisha yote ya ulimwengu huu, mwanadamu yumo katika hatari ya kupotea kwenye makosa, hivyo ni lazima ajitahidi kuelekea kwenye chanzo cha wema na furaha, na ajiweke mbali mwenyewe na tabia zake zilizopita na kujirekebisha. Manabii hawakutarajia malipo yoyote kwa ajili ya juhudi zao katika kupambana na uovu katika jamii zao, hata japo neno tu la shukurani. Wote walisema: “Malipo yetu yapo kwa Mwenyezi Mungu, Mola wa ulimwengu.� Ni hapa ambapo ubora wa haiba zao na tabia zisizo na ubinafsi zinapoweza kuonekana kwa uwazi kabisa. 68

Page 68


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah Miongoni mwa malengo mengine ya Mitume ni kubatilisha kule kuabudu madaraka na ubinafsi uliuokithiri na kubadilisha akili za watu ili kwamba waweze kufanya kazi endelevu ili kujiweka huru na pingu zao. Kwa njia hii, watu wanaweza kukusanya nguvu zao na kufanya kazi kwa pamoja ya kujitengenezea wenyewe mustakabali wenye maana, kwa sababu katika historia, uharibifu na hasara isiyorekebishika vimesababishiwa wanadamu kutokana na watu wabinafsi ya wenye uchu wa madaraka. Ujumbe wa zile aya za Surat Shu’araa ni kwamba zile jumuiya zenye kiburi, ubinafsi na uasi ambazo kwa kujua kabisa ziliikengeuka njia ya wokovu, na kwa ukaidi kabisa wakang’ang’ania kwenye njia zao tupu walikamatwa na adhabu ya Mwenyezi Mungu na wakafutwa kwenye kurasa za uhai; hizi zilikuwa ni jamii ambazo ziliwapinga Manabii wa Mwenyezi Mungu kwa ufidhuli na wakapuuza ushauri wao na wakaukataa ule ujumbe wa Mungu kwa uhuru wa kidanganyifu wa kishetani wa kutopaswa kuadhibiwa. Kwa sababu hiyo, siku hadi siku maisha yao yakakosa matumaini zaidi na kumbukumbu za uvukaji mipaka wao zikawa ndefu mpaka zikafunga milango yote ya kurejea nyuma yao, hivyo kwamba hapakuwa na matumaini ya ukarabati wao yaliyobakia na hakuna muda zaidi wa kupumua kuweza kutakasa nafsi zao na kupata msamaha kutokana na adhabu ya Mwenyezi Mungu. Wameziachia kirahisi zile fursa ambazo zilikuwa zimekwisha kutolewa kwao na sasa zimetatizwa katika mtego walioutengeza wao wenyewe; mtego ambao ulikuwa umejawa tu na adhabu na hukumu za Mwenyezi Mungu. Baada ya kila mwisho wa utajo wa kufedhehesha na wa maangamizi ya ummah ulioasi katika Sura hii, Qur’ani inafunga maelezo kwa kuelezea sifa ya Mwenyezi Mungu ya nguvu na uwezo (‘aziz), lakini vilevile mara tu inaongezea ile sifa ya rehema (rahim). Kwa mtazamo wa haraka haraka wa aya hii itaonekana kana kwamba rehema ya Mwenyezi Mungu haina chochote cha kuhusika na adhabu Yake na itakuwa inafaa zaidi kutaja sifa za kisasi au hasira au kudura za Mwenyezi Mungu. 69

Page 69


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah Ili kutambua ile hekima iliyojificha ndani ya aya hii ni lazima kwanza tuyaangalie maisha ya Manabii wa Mwenyezi Mungu; wale ambao walikuwa na njia ya kukifikia chanzo kitajiri na kikubwa cha habari na elimu, ili tuweze kuelewa ni vipi nafasi yao ya juu ya kiroho ilivyoweza kufikiwa. Moja ya njia ambazo kwazo Mitume (a.s.) walinyanyuliwa katika nafasi zao ilikuwa ni kwa upinzani wao dhidi ya upotofu, kutoamini (ukafiri) na ukaidi wa jamii (ummah) zao, ambazo ziliwasababishia kiasi kikubwa cha maumivu ya kiroho. Wale mitume ambao walikuwa imara zaidi mbele ya mitihani na taabu walinyanyuka juu zaidi katika cheo kwa mtazamo wa Mwenyezi Mungu. Mchukulie Nabii Nuh (s.a.) ambaye aliishi katika mwendeleo wa mbali sana katika historia; alitumia miaka 950 kati ya maisha yake ya miaka elfu moja katika kulingania dini ya Mwenyezi Mungu. Yake yalikuwa ni mapambano ya kudumu, magumu na marefu. Alipigana vita bila ya kuchoka dhidi ya uabudu masanamu na tabia ya kijinga ya umati wake wa kipumbavu. Bila ya hamaki aliendelea kujarivu kuwaongoza kwenye ukweli kwa kutoa mafundisho ya kiroho. Katika miaka yote hii mirefu, Nabii huyu mkubwa (a.s.) alikuwa hana msaidizi wala msaada isipokuwa mategemeo yake juu ya Mwenyezi Mungu, na bado hakuna kitu kingeweza kuzuia juhudi zake na dhamira yake ya kuwaongoza watu wake katika vipengele tofauti vya maisha yao. Hakuonyesha shaka yoyote katika kutekeleza wajibu wake na kulingania ujumbe wake; na kamwe hakusitasita katika kuelezea ujumbe wake kwa waziwazi kwenye hadhara yenye chuki na ya kijinga. Licha ya jitihada zote hizi za muda mrefu, hakupata majibu chanya kutoka kwenye umati wake, badala yake watu wa jamii hii ya kijinga na iliyoshuka kimaadili walishikilia katika ukanushaji wao na wakafuata desturi yao ya ushirikina.

70

Page 70


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah Nabii huyu wa Mwenyezi Mungu aliendelea na juhudi zote hizi za kweli kwa muda uliosonga mbele sana, licha ya mkazo usio na huruma ndani ya nafsi yake, katika matarajio yake kwamba angeweza kupita hadi kwa watu wake waasi na kurekebisha njia zao potofu, lakini matumaini haya kamwe hayakufanikiwa. Badala yake, kwa jinsi muda ulivyopita, ufidhuli na dharau zao vilizidi tu kuongezeka, na walizama kwa kina zaidi katika dimbwi la ujinga na ufisadi. Hatimae, kuelekea mwisho wa uhai wake, wakati alipokuwa amepoteza matumaini yote kabisa kwamba watu wake hawataweza kamwe kubadilika, yeye akawalaani. Manabii wengine walikuwa na uzoefu kama huo huo kwa watu wao, (uvumilivu na uimara mbele ya ufidhuli wa ummah zao na kukataa kwao kuukubali ujumbe wa Mbinguni, hadi walingeweza kupoteza matumaini). Katika ile hatua kuu, baada ya kupitia zile hatua tatu zilizotajwa hapo chini, Mitume (a.s.) hatimaye walizilaani jamii zao, ambazo ziliamua kuendelea katika kutoamini kwao na wakayatoa maisha yao moja kwa moja kwa Shetani. Manabii wangemuomba Mwenyezi Mungu kushusha adhabu Yake juu yao: 1. Subira na uvumilivu mkubwa mbele ya uso wa ukafiri, usugu na matusi ya watu wao. Wao wangeonyesha namna ya ustahimilivu ambao mtu wa kawaida asingeweza kuuonyesha. 2. Kukata tamaa na kupoteza matumaini kabisa katika urekebishaji wa watu wao, baada ya juhudi za mfululizo za kuwaongoza. Wakati ambapo juhudi na mawazo yao yote yalipokuwa bure na watu wakang’ang’ania katika kutokuutii ujumbe wa Mwenyezi Mungu. 3. Wakati washirikina waliposhikilia kuwadai wao kuleta adhabu ya Mwenyezi Mungu.

71

Page 71


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah Baada tu ya kuwa hatua zote hizi zimepitiwa, ndipo Manabii (a.s.) [kwa uhalali kabisa] wangeomba kisasa na adhabu ya Mwenyezi Mungu. Katika kadhia ya Nabii Yunus (a.s.) tunasoma kwamba alikuwa hakuonyesha subira ya kutosha na uvumilivu. Wakati juhudi zake katika kuwaongoza watu wake zilipokutana na dhihaka ya kijinga na ukaidi na wao waliposhikilia ibada zao potofu, yeye alipoteza subira juu yao na kabla hajaridhika kwamba hakukuwa na cha zaidi ambacho angeweza kufanya juu yao, alikimbilia kuomba adhabu ya Mwenyezi Mungu juu yao. Kutokana na kukata tamaa kwake kwa haraka na kukosa ustahimilivu wa muhimu katika kutekeleza majukumu yake, Mwenyezi Mungu akamtupa kwenye tumbo la nyangumi na akamkaripia kwa ukali sana ili kumfanya yeye atambue kwamba, katika mwenendo mzima wa kubeba ujumbe wake, kama angekuwa akabiliane na vikatisha tamaa, kushindwa na hata mateso, angepaswa kwa uimara kabisa kuona kwamba ujumbe wake unafika na kukaa mahali pake. Qur’ani inaelezea kwamba Manabii wengine walikuwa na uthabiti huu:

“Na Isma’il na Idris na Dhulkifl, wote walikuwa miongoni mwa wanaosubiri.” (Anbiya; 21:85). Mwishoni kabisa, wakati ummah wa Nabii Yunus (a.s.) waliposhuhudia dalili za adhabu ya Mwenyezi Mungu, walizidiwa na hofu dhalili kabisa na kutojiweza hasa, na wakatambua kosa lao kwa wakati muafaka tu. Walishikwa na majuto makubwa juu ya tabia zao za kimakosa zilizopita wa wakaangukia kwenye magoti yao wakiomba msamaha wa Mwenyezi Mungu na wakamuomba kwa dhati kabisa kuiondoa adhabu Yake iliyokuwa ikikaribia. Mwenyezi Mungu akawakubalia maombi yao na akawasamehe akaitangua adhabu Yake hiyo. Kutokana na kisa hiki tunaona wazi jinsi ambavyo, katika sura ya ufidhuli na ukaidi wa mwanadamu, Mwenyezi Mungu kwa subira kabisa inaiacha 72

Page 72


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah wazi milango ya Neema Zake wakati wote kwa ajili ya wanadamu kupita humo. Ni kweli neema na upole wa Mwenyezi ni kwa watu wote na imeenea kote, lakini hii haitangui uwezekano wa adhabu na hukumu. Neema na rehema za Mwenyezi Mungu zisizo na ukomo lazima zisieleweke vibaya kumaanisha kwamba katika utukufu Wake, wachamungu na waovu, wenye kudhulumiwa na madhalimu wote wako sawa. Kama Mwenyezi Mungu, Aliye Juu, ambaye utawala Wake upo juu ya kila mtawala na ambaye mamlaka Yake kamili juu ya kila dhalimu fidhuli, akawa haadhibu na kumuabisha kila mvuka mipaka, na akapuuza tabia ya kila muovu, basi haki na uwajibikaji vitapoteza maana zao. Je, Mwenyezi Mungu apaswe kutoa hifadhi kwa waonevu na kushughulika nao kwa upole na huruma? Je moto wa Jahannam sio adhabu inayofaa sana kwa fedhuli mwenye dhambi? Na mwishoni, ni kiini cha uadilifu kwamba uzito wa atom kama ni wa wema, au uzito wa atom kama ni wa uovu haupaswi kupuuzwa na kutoangaliwa. Moja ya udhihirisho wa wazi wa kudura na neema za Mwenyezi Mungu juu ya waja Wake wasio na shukurani na wabishi ni kwamba, baada ya kuja kwa Mtume wa Uislamu (s.a.w.w.), Yeye amesimamisha hukumu zote duniani na kuziakhirisha hadi Siku ya Kiyama. Kwa kweli, hata katika suala la Masihi (a.s.), yule Nabii mashuhuri ambaye alikuwa ni “roho wa Mungu,” ambaye alipatwa na mashaka mengi na hatimaye akaamuliwa kuuawa, Mwenyezi Mungu hakuwaadhibu hao wakosefu katika ulimwengu huu na akaihifadhi adhabu ya ufidhuli wao na ukaidi wao kwa ajili ya Siku ya Kiyama. Wanahistoria wamethibitisha kwamba, katika siku za mwanzoni kabisa za utume wake, watu wake walimsumbua yule Mtume mashuhuri wa Uislamu (s.a.w.w.) – Mtume ambaye alikuwa ni rehema kwa ulimwengu (rahmatun lil-‘alamin) – bila huruma na kuhujumu shughuli zake kwa visingizio mbalimbali na wakajaribu kupindua kazi yake kwa kutuma wahuni na wachochezi ili kuhanikiza na kumkemea kwa fujo; kwa kifupi, wao 73

Page 73


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah hawakuacha juhudi yoyote ile ya kumghasi yeye, kumkejeli na kumshusha tabia yake tukufu. Kupitia yote haya, yeye alidumisha umakini wake na kuonyesha subira kubwa sana. Mwenyezi Mungu pia aliwapa madhalimu hawa muhula na hakushusha adhabu Yake juu yao katika dunia hii. Kwa kuyachunguza mambo yote haya yaliyojadiliwa hapo juu, na kuzingatia akilini yale matukio yaliyotokea mwote katika mlolongo wa historia ndevu, tunagundua kwamba ummati hizi ambazo zilikamatwa ndani ya adhabu ya Mwenyezi Mungu katika dunia hii kwa kawaida ziliishi kwenye miji ambayo ilikuwa na watu wachache kabisa. Baada ya wafuasi wa Manabii kuondoka kwenye mandhari ambamo adhabu ilikuwa ishukie, ili waweze kuwa na kinga kutokana na ghadhabu ya Mwenyezi Mungu, tunaweza kusema kwamba wale waliobakia, ambao walikuwa ni katika madhalimu, mafidhuli na wasioamini miongoni mwa ummah husika, walikuwa ni wachache kwa ulinganisho. Kwa maneno mengine, wale ambao waliangamizwa na adhabu ya Mwenyezi Mungu ndani ya historia yote ya Mitume wa kale, historia ambayo inajumuisha maelfu ya miaka, walikuwa ni idadi ndogo ya watu kulinganisha kwa mfano na majeruhi na umwagaji damu ambao ulitokea katika vita mbalimbali ulimwenguni, au vile ambavyo vinasababishwa na nchi zinazotafuta madaraka, au hata bila sababu yoyote ya dhahiri kabisa,! ambamo watu chungu nzima waliuliwa. Katika nyakati zetu hizi, tunashuhudia kuenea kukubwa kwa umwagaji wa damu katika pembe kadhaa za dunia kutokana na uonevu wenye ubinafsi wa mataifa manyonge; kila moja ya vita hivi ni ushahidi wa maovu ya watu binafsi ambao wana njaa ya madaraka. Hii ni wakati ambapo hukumu na adhabu ya Mwenyezi Mungu ya mafidhuli katika siku za nyuma imekwisha kushuka – ingawaje ndani ya maeneo madogo, na kuhifadhi maadili ya mwanadamu na kuwaondoa madhalimu ambao hawakuwa tayari kutii amri za Mwenyezi Mungu kwa hali yoyote ile. Kwa nyongeza ya kuwaadhibu wenye hatia, hii ilikuwa ni onyo na somo kwa wengine, ambalo limewasimamisha na kuwazuia wengi katika 74

Page 74


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah kuendelea kwenye njia ya kiburi na upotofu. Ukweli ni kwamba, kutokana na vita vyote, ambavyo sababu halisi ilikuwa ni kuridhisha ubinafsi wa wachochezi wa vita, na ambavyo havina malengo ila kupata madaraka, mtu hawezi kutarajia matokeo chanya, mazuri; kwa hakika sio matokeo ambayo yanaweza kusababisha mazingira ambamo uchamungu na wema vinaweza kushamiri na ambayo yanaweza kuleta uongofu na maadili. Kwa kweli aina hizi za vita zinapotokea huleta mateso na dhulma, na dhiki na matatizo yanayokuja kujitokeza juu ya raia wa kawaida yasije yakapuuzwa kuzingatiwa. Kwa upande mwingine, kama wale waliogeuzia mgongo ukweli na wakajinyima wenyewe ulinzi wa hifadhi halisi, mara tu wakapata adhabu kwa ajili ya makosa yao na fimbo ya kifo na maangamizi ikawashukia mara moja na utaratibu huu ukaanzishwa kwa ajili ya wasioamini na wenye dhambi katika dunia hii, na Mwenyezi Mungu akawa hakuchelewesha adhabu yao tu mpaka Siku ya Hukumu, je, wanadamu wangekuwaje? Sasa hebu tufikirie mambo mbalimbali ya zama hizi za kisasa, kama vile ongezeko katika idadi ya miji na idadi ya watu ulimwenguni, kasi ya mawasiliano, wepesi ambamo kwamba mafundisho ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) yanaweza kusambazwa na kazi ya kuufanya ujumbe wa Uislam kufikia pembe zote za dunia, hata wakati ambapo mataifa mengi yamejawa na ukanaji Mungu na dhulma, au kwa maneno mengine, yamezama katika mtazamo mpya wa kisasa wa uabudu masanamu ambamo wenye kiburi na wafuasi wao wanachukua hatua ya uhasama dhidi ya Mwenyezi Mungu, ambalo ni ufidhuli usiosameheka. Sasa katika mazingira kama hayo, ambayo yamejaa ueneaji wa fitina, vurugu na ukosekanaji wa kizuizi, kama Mwenyezi Mungu angekuwa aamue kuonyesha ghadhabu Zake na kuwaadhibu wale ambao walikuwa wanastahili kuadhibiwa katika dunia hii, umati mkubwa wa watu wa dunia hii ungeangamizwa na kufutwa kwenye kurasa za uhai. 75

Page 75


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah Halafu tuzingatie akili ule uwezo usio na kikomo wa Mwenyezi Mungu, ambao mbele yake madaraka yenye mipaka na ya mpito ya kila mtawala mwenye amri katika ulimwengu huu inafifia na kutokuwa na maana, madaraka ambayo hayawezi kuhesabiwa au kutathminiwa, na ulimwengu mkubwa wote unakuwepo kutokana na sehemu ndogo sana ya mamlaka, uwezo na ukuu wa Muumba na kutokana na utashi Wake. Mamlaka haya yanaakisiwa katika kioo cha uhai ambacho kinanururisha kila atom katika ulimwengu mzima. Kiongozi wa waumini, Imam Ali (a.s.) amesema: “Oh, Allah! Hatuwezi kutamani kujua ukomo halisi hasa wa ukubwa Wako ….. tunayaona maumbile Yako na kushangaa juu yake kwa sababu ya uwezo Wako, na kuuelezea kama (ni matokeo ya) mamlaka Yako makuu, ambapo kile ambacho kimefichikana kwetu ….. ni kikubwa mno. – Nahjul-Balaghah, hotuba ya 160. Hakuna wakati wowote au mahali popote huko nyuma ama wakati huu wa sasa ambapo imeonekana kamwe kwamba mtawala mwenye nguvu sana, mwenye kutawala mambo yote katika miliki yake – sio kwa mazingatio ya kijamii ama kisiasa au kwa ajili ya kutafuta umaarufu, bali kwa sababu tu ya upendo wa kweli na mapenzi kwa wanadamu ambayo yametopea katika tabia zake – wakati wote akifanya mambo katika namna ya kibinadamu na kimaadili na akapuuza ukaidi na dharau za wapinzani wake ambao wako chini ya mamlaka yake, kwa kweli akafika mbali kiasi cha kushughulika na wale wanaompinga na kumdharau kwa huruma na kuwagubika kwa upendo wake bila ya kutarajia malipo na wema wowote kutoka kwao. Historia haiwezi kumtoa mtawala yoyote aliyekuwa na nguvu, katika zama zote, ambaye anazo sifa kama hizi, ingawa suala la vipindi vya utawala wa Mitume wa Mwenyezi Mungu (s.a.) ni masuala maalum ambayo hatuyazingatii kwa wakati huu. Kwa hiyo hizi sifa mbili za “madaraka” na “huruma” kamwe haziwezi kukutana ndani ya mtawala dhalimu. 76

Page 76


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah Ni mahali hapa ambapo tunapaswa kutafakari kwa kina ili tuweze kuuelewa ule ukubwa wa kupita kiasi wa udhihirisho wa ‘aziz na rahim, hizi sifa mbili za Mwenyezi Mungu kwa wanadamu. Tunahitaji kuwa wazoefu zaidi na zaidi katika ufahamu wa mamlaka na huruma Zake, hususan juu ya wale ambao wanathubutu kuwa waasi na wakosefu na wakaidi mbele ya Utukufu Wake; na njia moja ya kulielewa hili ni kutafakari juu ya msisitizo Wake uliokaririwa katika aya zote zilizotangulia, juu ya sifa Zake hizi mbili tukufu na mashuhuri. Kwa hiyo tunatambua kwamba Madaraka na Huruma halisi na za kweli zinamstahiki Mwenyezi Mungu peke Yake. Kwa hakika:

“Na hakika Mola wako ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu. (26:68)

7. ZAWADI KATIKATI YA MILIMA

“Je, huoni kuwa tumeteremsha kutoka mawinguni maji kutoka mbinguni na kwayo tumetoa matunda yenye kuhitalifiana rangi. Na katika milima imo mistari myeupe na myekundu yenye rangi mbalimbali na myeusi.” (35:27) Ndani ya Qur’ani, maelezo ya ulimwengu wa maajabu uliosanifiwa na Muumba yamegawanywa kimsingi mara mbili. Ya kwanza ni yale maelezo ya mfumo tatanishi wa maumbile na kuwepo kwa matukio ya kuvutia sana, yale maajabu ambayo mwanadamu anayashuhudia kote kwenye uwanda mpana wa maumbile. Kwa wale ambao imani zao binafsi zime77

Page 77


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah jitegemeza kwenye falsafa ya maisha ya kimungu na ambao wanauchukulia ulimwengu kama ulioasisiwa na usanifu wa kiakili na hekima kamilifu ya Muumba, kila wakati wanatoa muda wa kutafakari juu ya mwelekeo wa maisha, na wanakusanya masomo muhimu kutoka kwenye muundo na utaratibu wake. Kwa njia hii, wanapata kuuelewa ule utukufu na mwanga na ule mkono wa hekima ambao kwa madaha sana umetunga zile kurasa za uwepo wa dunia. Ya pili ni yale maelezo ya hali halisi zinazoshangaza ambazo ziko nje ya ulimwengu wa kawaida, ambazo ziko mbali na utaratibu wa uwanja wa kimaada, na zina peo pana ambazo hazitawaliwi na kanuni na sheria za kawaida ambazo sisi tumezizoea. Matokeo yake ni kwamba, utambuzi na uelewa wetu wa miujiza ya vipengele vilivyofichika vya uwepo wa dunia kwa kawaida una mipaka na kwa kweli elimu ya wanadamu wote ni kama tone dogo sana mbele ya bahari kubwa pale inapokuja elementi zisizojulikana na za siri, za ulimwengu usio wa kimaada. Wafasiri wa Qur’ani wametoa maoni juu ya haya maajabu ya aina ya pili kwa kirefu kiasi, ingawa kwa kweli, hakuna maelezo ya kifikra kuhusu miujiza hii – hata kama mtu ataweza kupasua mapazia yanayoyafunika maajabu hayo – ambayo yataweza kufafanua sehemu ndogo tu ya yanayotokea katika dunia ya nje na hii. Hii ni kwa sababu, kama ilivyoonyeshwa mapema, nyanja yote ya uwepo wa ulimwengu ni kubwa na pan asana kuliko hii dunia ya kawaida, na ndani yake, ulimwengu usio wa kimaada ni tajiri na pan asana kuliko ulimwengu wa kimaada na kutokana na mipaka ya asili, vyombo vya kisayansi vilivyoko mikononi mwa wanadamu havina nguvu ya kutosha ya kuchunguza na kuchanganua mengi ya mambo haya. Hata hivyo, hata katika suala maalum la matukio yanayotambulika katika dunia ya kawaida, tunaweza kuendesha utafiti wetu na kujaribu kuchunguza ukweli kwa njia mbili; moja ni kutafsiri aya za Qur’ani katika mwanga wa elimu ya kisasa na kuchanganua taratibu mbalimbali za asili (wanya78

Page 78


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah ma, uoto, viumbe wasio na uhai n.k.) na kulinganisha ugunduzi wa kisayansi na maelezo ya Qur’ani ili kuonyesha kwa uhakika kabisa kwamba hakuna mparaganyiko au ukinzani katika mawili hayo, na kwamba hekima na akili pia vinathibitisha neno la Mwenyezi Mungu. Lazima tuzingatie akili kwamba ingawa elimu ya kisayansi inatoa mwanga ambao umetatua baadhi ya miujiza, bado haina uwezo wa kuziondosha siri zote za maumbile (kwa kweli, mtu asije akalinganisha elimu iliyopatina kutoka kwenye Qur’ani na nadharia za kisayansi, kwa sababu sayansi imeegemea kwenye majaribio na utafiti, na tahakiki zinazotegemea juu ya kufanya majaribio ni dhaifu na zisizotegemeka, na katika historia yake yote, kanuni za kisayansi zimekumbwa na marekebisho na kisha yale mawazo ya zamani yanawekwa kwenye majalada. Kwa kweli, Qur’ani, ambayo ina rangi ya kudumu, na iko mbali na kila wasiwasi, inapaswa kuwa ndio kitu cha kwanza cha marejeo, ambayo juu yake usahihi wa ugunduzi wa kisayansi unapasa kupimwa na kuamuliwa kwayo.) Pili, kuhusiana na maajabu haya ya dunia ya kawaida na wakati wa kuchunguza viumbe mbalimbali ambavyo vinafanya hali ya kuwepo ni lazima vilevile tuzingatie mazingira yaliyopo wakati wa kushuka kwa Qur’ani, na uwezo wa hadhira ya watu ya wakati ule. Tunahitaji kuangalia kiwango cha uwezo, teknolojia na uelewa wa watu walioishi katika zama zile, na ambao kwa kijumla hawakuwa na njia na nyenzo za kuchunguzia baadhi au mengi ya mambo yaliyovichika ambayo hayajagunduliwa na yasiyojulikana ya kimaumbile. Na kwa kupitia hili tunaweza tukatambua ule ukubwa wa muujiza wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Na kwa kweli, kuhusu hii aya iliyoko kwenye uchunguzi, kiini cha msingi cha utafiti wetu ni cha namna hii ya pili, kama tutakavyoelezea hivi punde: Migodi yenye vito vya thamani vya rangi mbalimbali ni vyanzo vya mapato makubwa kwa ajili ya nchi zenye kumiliki hazina hizi za thamani. Mawe haya ya rangi mbalimbali yamehifadhiwa katika vina vya milima 79

Page 79


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah katika maeneo maalum kote ulimwenguni na yanachimbuliwa kwa vifaa mbalimbali na taratibu za kistadi kabisa. Baada ya hapo yanasafirishwa nchi za nje kote duniani na kuleta utajiri na umaarufu kwenye nchi yanakotoka mawe hayo. Ingawa migodi yenye mawe ya thamani inapatikana na kuchimbwa katika nchi nyingi, hata hivyo idadi ya migodi yenye utajiri katika nchi kama Iran Italia, China, Korea ya Kusini, India na Ureno ni mingi zaidi kuliko kwenye sehemu nyinginezo. Rangi za msingi za mawe haya ni nyeupe, nyeusi na nyekundu wakati ambapo rangi nyingine zinaweza kuchukuliwa kama za matokeo. Katika aya tunayoiangalia, Qur’ani inazielezea zile rangi za msingi za mawe yanayopatikana katika migodi kote duniani, na vilevile kuzitaja zile rangi za matokeo:

“Je, huoni kuwa tumeteremsha kutoka mawinguni maji kutoka mbinguni na kwayo tumetoa matunda yenye kuhitalifiana rangi. Na katika milima imo mistari myeupe na myekundu yenye rangi mbalimbali na myeusi.” (35:27) Kama ukweli wa mambo uliomo kwenye aya hiyo hapo juu ungekuwa hautoki kwa Muumba wa migodi hiyo – Muumba Mwenye enzi ambaye ameumba kila chembe (atom) katika ulimwengu na ambaye ana elimu pana na ya moja kwa moja juu ya kila sehemu ya uwepo – basi ni wapi kwingine tena ambako ungeweza kuwa umetoka? Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliishi maisha yake yaliyobarikiwa katika miji ya Makka na Madina, na alifanya safari fupi fupi mbili tu nje ya rasi 80

Page 80


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah (peninsula) ya Arabuni; mara moja katika utoto wake wakati alipoongozana na ammi yake ambaye alikuwa anapeleka msafara kwenda Syria, na wakati mwingine katika kipindi cha miaka ya ishirini ya umri wake, wakati alipoendesha shughuli za kibiashara akiwa wakala wa Bibi Khadija; mara nyingine tena kwenda Syria. Na kuhusu hiyo migodi mbalimbali yenye mawe ya thamani ya rangi mbalimbali, ambayo siku hizi inachukuliwa kama sehemu ya hazina ya taifa ya nchi mbalimbali na ambayo inatoa manufaa kwa mataifa, inapatikana tu katika nchi nyingine chache, na sio nchini Syria. Zaidi ya hayo, mawe hayo yanapatikana ndani sana katika matumbo ya milima, hivyo ni vipi ambavyo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alivyoweza kujua uwepo wao na hali zao kutoka kwenye chanzo kinginecho cha habari? Je, ingewezekana kwa mtu yoyote wa kawaida, ambaye hakuwa na umaizi wa ndani ama uhusiano wowote wa kiroho na chanzo cha uwepo wote (all existence), na ambaye hakuwa na njia ya kupata wahyi, kuweza kumiliki elimu kama hiyo katika siku zile? Na ule ukweli kwamba alikuwa anamiliki elimu kama hii sio ushahidi tosha kwamba alikuwa amehusiana na Muasisi wa maumbile na amepokea wahyi kutoka Kwake? Kwa hakika katika siku zile watu kwa kawaida hawatumia muda mwingi katika kutafakari kuhusu miujiza ya maumbile au kujaribu kufunua siri nyingi za maada na viumbe mbalimbali katika ulimwengu huu. Katika zama zile, ni binadamu gani aliyekuwa na elimu ngumu na inayotambulika vyema, ambapo hakuwa na utambuzi tu wa uwepo wa migodi hii, bali pia alizungumzia juu ya vizazi vitakavyokuja baadae ambavyo vitakuja kuchimbua mawe ya thamani (ambayo yaliotodheshwa sambamba na maji ya mvua kama moja ya neema za Mwenyezi Mungu) kutoka kwenye migodi hii ambayo ilikuwa imefichikana ndani sana katika vina vya milima? Mbali na hali ya ufasaha wa aya hiyo hapo juu, ambao unaweza kuwa na ufanano wa nje na kazi nyinginezo za kiuandishi, bado ina ubainifu wa 81

Page 81


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah kipekee na utukufu usiokanika ambao unaifanya kuvuka mipaka ya jitihada za mwanadamu. Aya inataja zawadi mbili na uhusiano wake wa ndani na maisha ya mwanadamu; moja ni zawadi ya mimea (vegetation) na nyingine ni zawadi ya vitu visivyo na uhai. Mimea katika muundo wa matunda ya rangi mbalimbali na baadhi ya nafaka ambavyo vimetajwa mwanzoni mwa aya hiyo vinahakikisha mahitaji ya kilishe ya mwanadamu na vinatia nguvu mwili wake, wakati ambapo ile zawadi ya pili, ile ya safu za milima, hutoa malighafi ambayo kwayo mwanadamu anaweza kujijengea mwenyewe makazi yake. Kwa ukweli, Qur’ani inazitaja zawadi hizi mbili na kuvuta mazingatio ya mwanadamu kwenye vyanzo viwili hivi vya mahitaji yake makuu na ya msingi kabisa, chakula na makazi. Muumba Mwenye hekima ameumba mawe yaliyoibuka juu kwa ajili ya mwanadamu kutumia wakati alipokuwa hajaendelea kupita kile kipindi cha historia kilichotuama kisayansi, ambapo Yeye swt. alikuwa ameweka mawe yenye rangi nyingi zaidi kwa ajili ya wanadamu kutumia wakati ustaarabu wao utakapostawi na elimu yao kukua ili waweze kuzalisha vifaa hivi bora kwa kujengea aina za kisasa za majengo. Tunajua kwamba katika nyakati za zamani, watu walikuwa hawana uwezo wa kuyafikia mawe yenye rangi nyingi mbalimbali na kuyatumia katika ujenzi wao. Katika siku zile, mengi ya mawe yaliyokuwa yakitumiwa na watu yalikuwa ni aina duni yaliyokuwa yakipatikana kwa kawaida katika safu za milima yote duniani, ambayo yalikuwa yanapatikana kwa urahisi kwa watu wote. Walikuwa wakiyatumia mawe hayo kwa kuweka misingi ya nyumba zao, au wakati mwingine kuweka mistari kwenye mapaa ya majengo yao. Ni katika zama za hivi karibuni ambapo kwamba mwanadamu amepata ustadi na kuendeleza zana na mashine za kisasa kuweza kuchimba kwa mafanikio mawe ya thamani kutoka kwenye sehemu za ndani kabisa za milima na kuyatumia katika majengo mbalimbali.

82

Page 82


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah Katika aya inayofuata, Mwenyezi Mungu anasema:

“Na katika watu na wanyama na wanyama howa pia rangi zao zinahitalifiana. Hakika si mengineyo wanaomcha Mwenyezi Mungu, katika waja wake ni wale wajuzi Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye maghufira.” (35:28). Mbali na rangi za vitu na mawe ndani ya milima, katika aya hii Mwenyezi Mungu anaelezea zile rangi tofauti zinazopatikana miongoni mwa watu, ambao ni weupe na wenye ngozi nyeusi; na kuhusu wanyama vilevile, kuna maelezo ya ubao mpana wa rangi mbalimbali ambao wanauonyesha. Kama tulivyoona, Qur’ani anaashiria wazi kwenye tofauti pana ya rangi zinazopatikana kote kwenye jamii ya madini, ya mimea wanyama na ya wanadamu na inafungua milango ya uchunguzi ili kwa kila mtu anaweza kuyaangalia maumbile na mpangilio wake na maajabu kwenye mfumo wake wa kutatanisha ambao uliopo hata katika chembechembe ndogo kabisa katika muumbo mpana kabisa wa hali ya uwepo (existence). Qur’ani inatangaza kwamba haya maajabu ya maumbile, ambayo kila moja ni ishara ya elimu na hadhi ya utukufu usio na mwisho na uwezo wa Mwenyezi Mungu, yanaweza kueleweka vizuri tu kwa wale wenye akili – wale ambao bongo zao zimeng’arishwa na nuru ya umaizi, hekima na muono uliokomaa – ambao wanatambua kwamba ujenzi mkubwa na mfumo wa ulimwengu pamoja na uzuri wake sio chochote bali ni udhihirishaji mdogo sana wa nguvu na uwezo Wake. Wanachukulia ukamilifu wa kurasa za kitabu cha maumbile kuwa ni ushahidi wa mvuto wa usanifu na akili ya hali ya juu ambayo iko nyuma ya uumbwaji wake. Hapana shaka! Wale walio na umaizi na akili, wanaposhuhudia ule usani83

Page 83


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah fu muundo wa ajabu na lengo na upangaji na hekima ya kuona mbali ambayo inadhihirika katika ulimwengu uanaowazunguka na katika maumbile ya mbinguni na katika moyo ya atom na mawe na katika kila kipengele cha ulimwengu, kuanzia kwenye kitu kidogo hadi kwenye kikubwa wanavutika moja kwa moja kwenye ukamilifu usio na mipaka wa Muumba na wakati wote wanakimbilia haraka Kwake kwa shauku, hamasa na imani kamilifu. Maelezo na fasili ya aya hii vinaonyesha mfano mwingine wa muujiza wa maneno ya Mwenyezi Mungu, ambayo hayakufikiriwa na wafasiri wakubwa katika vitabu vyao. 8. KUFUFULIWA KUTOKA KWENYE USINGIZI WA KIFO

“Macho yao yatainama; watatoka makaburini, kama kwamba wao ni nzige waliotawanyika.� (54:7) Sitiari na tashbihi (mfanano) ni ala za uzungumzaji fasaha zenye nguvu zinazotumika katika fasihi katika kufikisha kwa ufasaha maana inayokusudiwa. Mambo matatu yanaunda kila tashbihi: la kwanza ni kitu chenyewe hasa, la pili ni kitu kinacholinganishwa na cha kwanza na ufanano kati ya viwili hivyo. Hata hivyo, nukta muhimu ili kuelewa ufasaha wa msemaji au umahiri uliotumika katika kuunda ile tamathali iliyomo katika kifungu cha maneno ni kuelewa kufanana huko kwa usahihi wake, kwani sababu ya kutumia tashbihi hiyo kufikisha ile maana iliyokusudiwa imewekwa katika hiyo namna ya kufanana ambayo imetumika.

84

Page 84


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah Hususan katika suala la wahyi na aya za Qur’ani, ambazo ni sahihi na zilizojaa maana, ni muhimu kutafakari kwa uangalifu zaidi kuhusu vipengele mbalimbali vya ufanano kati ya vitu viwili ambavyo vinatumika katika tashbihi, ili kufunua hata zaidi ya siri zinazovutia sana zilizomo katika maneno ya Mwenyezi Mungu na kumuwezesha mwanadamu kuchota kutoka kwenye bahari zisizo na ukomo za elimu ya Mwenyezi Mungu kwa kiasi cha uwezo wake mwenyewe. Katika ufafanuzi wao juu ya aya hii, wafasiri maarufu wa Qur’ani wameelezea kwamba msingi wa kufanana huko ni kule kutoka kwa binadamu makaburini kwa makundi na kutawanyika kwenye mawanda ya sehemu ya kukusanyikia (mahshar), kwa sababu ya ujio muhimu sana wa Siku ya Kiyama. Tukio la ulipukaji litatangazwa kwa kuangamizwa kwa ulimwengu na kuporomoka kwa ghafla kwa utaratibu wa dunia nzima na kutoka kwa wanadamu kwenye makaburi yao. Litakuwa ni tukio la kuhofisha na kuogofya kiasi kwamba watu watatawanyika katika ghasia na kusambaa ovyo kama vile tu nzige wanavyotoka kwa makundi kutoka kwenye viluwiluwi vyao. Wataanza kuondoka lakini bila fahamu sawasawa kuelekea upande wowote. Wafasiri wameeleza kwa usahihi kabisa matumizi ya tashbihi hii iliyoegemea kwenye maelezo (muntashir) ambayo yanajitokeza mwishoni mwa aya hiyo, na wametengeneza picha ya hali isiyo ya kawaida ya rabsha na hofu itakayokuwepo juu ya wanadamu katika siku hiyo, wakati kila mpangilio wanaoufahamu wao utakuwa umebadilika; hata hivyo, itakuwa bora kutofungia mjadala wetu huu kwenye kipengele kimoja tu cha kufanana, bali na kuigundua maana ya vipengele vingine pia. Hii itaturuhusu sisi kupata uelewa mzuri wa lengo la aya hii, ambayo ni kuelezea mandhari za kushangaza za siku hiyo kubwa ya hukumu. Hapana shaka kwamba siku moja huu utaratibu wa ulimwengu uliopo sasa utakuja kukumbwa na msukosuko wa vurugu, na kufuatia tukio la tetemeko kubwa, utafikia kwenye mwisho wa ghafla. Sio kwamba ni dunia tu 85

Page 85


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah itakayopatwa na tetemeko na machafuko, bali na nyota nazo zitakufa na makundi ya nyota yatavunjika na kutaanguka kimya; kwa maneno mengine, kwamba mpasuko wa ulimwengu utaziteketeza mbingu na dunia kwa wakati mmoja, na mfumo na utaratibu katika maumbile uliopo kwa sasa utakuwa umebadilika kabisa, na kusababisha mwisho wa uhai wa ulimwengu na wakazi wake na kumbukumbu ya vyote vilivyoumbwa. Kwa kweli, huu uangamiaji wa jumla wa ulimwengu, ambamo hakutakuwa na kiumbe yeyote atakayeweza kutambulika, ndio mustakabali usioepukika wa dunia yetu. Kisha, makaburi yatapinduliwa, na ardhi pia, katika utiifu wa maagizo ya Mola Wake itadhihirisha vilivyomo vya tangu enzi na siri ambazo ilikuwa imezificha katika tumbo lake, na kupunguza mzigo wake. Kama mwanadamu ataangalia vinavyoujenga mwili wake mwenyewe, ambao umetengenezwa kwa elementi mbalimbali zinazopatikana kwenye ardhi na maji, atatambua kwamba siku moja mwili huu utakuja kuzama na kupotelea ardhini na kutoa mbolea kama chakula cha matunda na mimea na hivyo kutawanyika kote duniani; au molekyuli zake hatimaye zinaweza kuwa katika umbile la matone ya maji na kuingia kwenye bahari pana. Elementi zinazotengeneza miili yetu ni matokeo ya mabadiliko ambayo yametokea chini ya kundi maalum la visababishi na namna za hali, sio tu kwamba mwili wa kila mwanadamu unafikia umbo lake kupitia mwenendo huohuo, bali pale unapoharibika na kuoza na kuwa atom mwishoni mwa maisha yake, kwa mara nyingine tena unakuwa ni lishe inayopatikana tayari kwa ajili ya maumbo mengine ya uhai. Na kwa njia hii zile elementi za sehemu za mwili mmoja zinakuwa zimehifadhika, hata wakati zinapokuwa zinabadilishwa katika ulimwengu. Kwa nini isiwezekane kuunganisha tena vitu hivi vilivyotawanyika, ambavyo vimeenea kwenye kila pembe ya mbali, kwa kuvikusanya vyote kutoka kwenye kumbatio la ardhi na mishiko ya upepo, na kuvileta pamoja katika namna mpya ya umbo? Kwa kweli, hapo mwanzo wa kuumbwa 86

Page 86


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah kwake, jambo kama hilo hilo lilitokea, na kwa namna hiyohiyo. Huu ulikuwa ni utupia macho wa kwenye kipengele kimoja cha ukubwa wa kushangaza na wa kudumu wa Mwenyezi Mungu kuhusiana na kuwadia kwa Siku ya Kiyama. Hata hivyo, inaelekea kwamba kilicho muhimu na cha kuvutia katika tashbihi hii iliyotumika katika aya hiyo hapo juu ikielezea kuenea na kusongamana kwa watu katika siku ya mkusanyiko (mahshar), ni kule kutokeza kwao kutoka makaburini mwao ambako kunafanana na kutoka katika makundi kwa nzige nje ya ardhi. Ule mwanzo wa aya unadokezea kwenye hilo vile vile. Wanadamu wanalala ndaini ardhi baada ya kufa kwao kwa kipindi cha mpito, wakisubiri amri ya Mwenyezi Mungu ya kuwarudisha wafu kwenye uhai na kuchomoza kutoka makaburini mwao. Hili litatokeza baada ya mpulizo wa baragumu (tarumbeta) la pili na ule ukelele mkali ambao utagubika viumbe wote na mara moja kuwarudisha wanadamu kwenye uhai na kutoka nje ya makaburi yao. Halikadhalika, viluilui vya nzige vinalala kwa kutulia na kuzikwa ndani ya ardhi kama vile wafu wa binadamu. Wale nzige wenye mimba huingiza miili yao kwenye udongo na kutaga mayai yao ndani kabisa ya ardhi na kisha kumwaga umajimaji juu ya mayai hayo ili kuyavunika. Umajimaji huu unayalinda kutokana na elementi na kwa kweli hutengeneza kaburi la muda kwa ajili yao. Kapsuli (kidonge) ya kiluwiluwi cha nzige hubakia kutulia katika ardhi kama vile tu maiti ya mfu katika kaburi ambalo limetayarishwa kwa ajili yake na kuzikwa humo; ingawaje ina ukuta mwembamba na laini sana, ukuta huo unatosha kukilinda kiluwiluwi kwa muda unaohitajika. Kwa kweli, ni kama sanda tu ambayo imefungwa kwenye mwili wa binadamu aliyekufa.

87

Page 87


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah Wakati wa miezi ya kupukutika majani (autumn) na wa kipupwe, viluwiluwi hivyo hutulia bila kutingishika na kisha wakati wa msimu wa kuchipua unapowadia, vinafunguka na kutoa nzige waliomo ndani yao. Wadudu hao sasa wako tayari kufikisha mwisho wa kusubiri kwao (barzakh) na kutoka kwenye makaburi yao. Baada ya kutokeza nje kwenye ardhi, kwa mujibu wa baadhi ya vipengele na mazingira wanaanza kuruka. Kwa kweli hali ilivyo kwa binadamu waliokufa ni sawasawa na hiyo. Sehemu mbalimbali za mwili wa binadamu ambazo zimeozea kwenye udongo huwa zinabadilishwa kama kila kitu kinginecho, kulingana na kanuni ya maumbile. Kwa utashi wa Mwenyezi Mungu, vitakuwa vimechangamka katika ujio wa Siku ya Hukumu, na kama vile tu kwa nzige walioanguliwa, watatokeza kutoka kwenye makaburi yao na kukimbilia kwenye sehemu ya makutano iliyoteuliwa ya mahshar. Wataonyesha sura zao za asili ambazo zilikuwa zimevikwa sanda na kufichwa; kwa mara nyingine tena mwanadamu atakuwa na uhai wake wa halisi ukiwa umehifadhiwa katika umbo jipya. Tashbihi iliyotumiwa na Qur’ani inawezekana kuwa ndio ufananaji sahihi na mahiri zaidi kuhusiana na hili, na unaweza kueleweka kwa urahisi na kutambuliwa na kila mtu. Aya yenyewe inatoa taswira kwa uwazi kabisa ya hali ya mwanadamu wakati anaporejeshwa upya kwenye uhai. Mwenyezi Mungu anawajulisha waja Wake na kuwashauri waangalie wale nzige walioanguliwa vile wanavyotoka kwenye makaburi yao katika ardhi, na kisha wazingatie mwanzo wa maisha mapya yao wenyewe wakati ambapo na wao pia watakapotoka nje ya ardhi. Kwa namna hii wataridhika kwamba tukio hili kwa hakika litakuja kupita na kwamba majaliwa yao wenyewe yatakuja kukunjuka katika namna hii hii na kwamba siku hiyo inawangojea. Umbo la mwanadamu linaweza kukubali mabadiliko kadhaa lakini halitakubali kwamba kiini cha uhai wake kiweze kuwa hakipo tena. Kwa mfano huu, ataona kwamba, kama miili mingine, sifa za umbo lake zimepotea lakini hakuna kilichopungua katika asili yake. Kwa kweli, asili 88

Page 88


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah na nafsi yake vinabakia na fahamu na visivyoharibika mwote katika mabadiliko yake yote hadi siku yake ya malipo ya mwisho itakapowadia. Kulingana na maoni yaliyotolewa hapo juu na kupitia kutumia tashbihi maridadi kama hiyo, mtu anaweza kutafsiri aya iliyoko kwenye uchunguzi kama ifuatavyo: “Wanatoka makaburi mwao kama nzige na wametawanyika katika mawanda ya sehemu ya kukusanyikia (Mahshar),” kinyume na tafsiri ya kawaida ambayo inasema: “Watatoka makaburini, kama kwamba wao ni nzige waliotawanyika kwenye uwanja wa mahshar.”2 9. USHAURI WA BUSARA WA LUQMAN

“Na Luqman alipomwambia mwanawe akiwa anampa mawaidha: Ewe mwanangu! Usimshirikishe Mwenyezi Mungu na chochote. Hakika shirki ndio dhulma kubwa.” (Luqman; 31:13) Maisha ya mwanadamu yanatawaliwa na mfumo wa wajibu binafsi. Majukumu yanaanza tangu kwenye hatua za awali kabisa za maisha na kuendelea hadi mwisho wake; hakuna wakati wowote ambao mwanadamu anaweza kudai kuwa huru au na utengano kutokana na namna fulani wa wajibu. Madhali uwezo unakuwepo, unakuwa na wajibu shirikishi ulioambatanishwa nao, na ni pale tu kifo hatimae kinapomkuta mtu, kinakuja kufunga orodha ya majukumu yake. 2. Katika elimu ya balagha ('ilm al-ma'ani) kuna mjadala kuhusu kukanusha (salb) na kuthibitisha (ijab) katika sentensi; kama kufanana katika tashbihi ni chanya (tashbihi ya kuthibitisha), basi inatumika kwa vyote, kivumishi na nomino za tashbihi hiyo. Sasa katika aya inayojadiliwa, neno jirad (nzige) limeelezewa kama kivumishi Muntashir (tawanyika), kwa hiyo kufanana ambako ni "kutoka makaburini" kunatumika kwenye muntashir na jirad halikadhalika. 89

Page 89


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah Kwa kawaida, hisia za uwajibikaji zimeegemea kwenye kanuni za kiakili, na sababu ya kushikamana na sheria za dini vilevile zinarudi kwenye kanuni zizi hizi. Hii ni kwa sababu katika mambo ya kijamii na pia maisha binafsi, sheria za kidini na maagizo vinaendana na utambuzi wa kawaida wa akili. Vile uelewa na utambuzi wa mtu unapozidi, kupenda na kuwa tayari kwake kutekeleza wajibu wake kutaongezeka na kukua, kwa sababu utambuzi wa majukumu yake mtu na wajibu wake ni sharti la msingi kwa ajili ya furaha na wanadamu. Athari ya tabia na vitendo ni kubwa sana kuliko ile ya mazungumzo na hotuba; sifa binafsi za mwalimu na namna ya tabia yake vina athari nzito na ya msingi juu ya wanafunzi wake. Mafunzo ya vitendo kwa mfano, yana athari ya maana sana katika akili za wale wanaolelewa, na huvutia tabia zao kwa kiasi ambacho kwamba hakiwezi kulinganishwa na kushauri sana kutupu kwa maneno na mdomo. Wakati mtu anapotaka kuwa mshauri na akaangalia mafundisho ya kiroho na maadili ya wengine, hata kama atatumia mbinu za hali ya juu za ufundishaji, bado anahitaji kuwa na sifa binafsi bora ili aweze kutengeneza mazingira mazuri kwa ajili ya kukuza ubora. Ni lazima awe na uwezo wa kuhamisha hazina ya taq-wa kwenda kwenye akili zao na mawazo ili aweze kuleta mapinduzi ya ndani katika maagizo na amri zake, la muhimu kabisa likiwa ni kuendeleza uadilifu wa uaminifu (ikhlaas) na ulinzi wa akili zao kutokana na upotofu. Kwa hiyo mtu anayetafuta mafanikio katika ulezi ni lazima yeye mwenyewe aonyeshe uadilifu mema na tabia nyofu, ili kwamba maneno yake ushauri viwe na athari ile inayotakikana; vinginevyo, kama ni mzembe katika utekelezaji wa majukumu yake, ni dhahiri kwamba juhudi zake katika kuwalea wengine zitakuwa bure tu. Hii ndio hali hasa wakati vitendo na tabia zake vinapotazamwa kwa ukaribu sana na wanafunzi wake ambao baadae hugundua kwamba maneno yake hayalingani na vitendo vyake. 90

Page 90


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah Wakati nafsi ya ndani kabisa ya mshauri inapokosa taqwa ya Muumba wa vyote na yeye mwenyewe akawa haishi maisha ya kiadilifu, watu watamtathmini na kumhukumu na kugundua kwamba tabia yake haifai, na hatimae uaminifu wa kawaida juu yake utakuwa na wasiwasi na kudhoofika. Watu tena hawatakuwa tayari kumkubali yeye kama kiongozi na kigezo cha mfano ili kupata ubora wa kimaadili. Katika aya iliyoko kwenye mjadala, kupitia mlolongo wa mapendekezo na ushauri wake wa busara, tunatambulishwa kwenye hekima za Luqman, ambaye alikuwa na njia ya kufikia kile chanzo halisi cha elimu na taarifa. Uso wake mng’aavu ulikuwa umezoeleka na maarufu miongoni mwa watu wake; na mazungumzo bora kabisa na umaizi wa kila siku havikuweza kulingana hata na dondoo za kauli zake. Mwanachuoni huyu mwenye hekima anageuzia mazingatio yake kwenye ufundishaji wa maadili kwa mwanawe kwa uangalifu na ubunifu maalum. Anaongea na mwanawe kwa kumpa ushauri wenye manufaa, na kwa kumuelezea juu ya njia sahihi na hali halisi ya majukumu yake. Anamuonyesha jinsi ya kuendesha maisha ya kiungwana, ambapo kupitia hayo, maneno ya hekima za kiroho na maadili mema yaweze kueleweka dhahiri kwa ubora zaidi. Mwanzoni kabisa, ili kumhamasisha mwanawe, kutia nguvu ule ukweli wenye uwezo wa kujulisha uliofichika ndani yake yeye na kumuongoza kuelekea kwenye lengo lake la mwisho, anamuandalia kwa uwazi kabisa wajibu wake kwa Muumba na anamkumbusha kuhusu upweke wa Mwenyezi Mungu. Hii ni kuangaza akili na umaizi wake ili kwamba awe na uwezo wa kujizuia mwenyewe kutokana na kupotoka kutoka kwenye njia ya upweke wa Mungu (tawhiid) na kupotelea kwenye ushirikina (shirk). Hivyo anamshauri kwa maneno yafuatayo:

91

Page 91


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah

“Na Luqman alipomwambia mwanawe akiwa anampa mawaidha: Ewe mwanangu! Usimshirikishe Mwenyezi Mungu na chochote. Hakika shirki ndio dhulma kubwa. Na tumemuusia mtu kwa wazazi wake, mama yake amebeba mimba yake kwa udhaifu juu ya udhaifu na kumwachisha ziwa (kunyonya) kwa miaka miwili, kwamba unishukuru mimi na wazazi wako. Marudio ni kwangu.� (Luqman; 31:13-14). Katika hiyo aya ya kwanza imeelezwa jinsi Luqman anavyovuta nadhari ya mwanawe kwenye ukweli huu mtukufu ili kwamba asije akatoka nje yake na kuingia kwenye dimbwi la makosa, bali agundue kwamba nyuma ya ulimwengu wa dhahiri na mchangamano tata wa maumbile, kuna Mwenye Uwezo Mmoja pekee Ambaye ndiye aliyeasisi huu mfumo wa ulimwengu na ambaye anausimamia na kuudhibiti kwa mujibu wa mpango angalifu na kusudi na lengo la ujuzi kabisa. Dhati tukufu kama hiyo ndio inayostahili kuabudiwa. Kwa hali hii, yeye lazima atimize wajibu wake kwa hii Dhati ya Milele, Isiyohitajia na kuonyesha muendelezo wa shukurani zake Kwake. Katika aya ya pili, maneno ya Luqman yamekatwa, na kimya chake hapa kinazua swali: Kwa nini Luqman anaacha kuzungumza hapa alipofikia? Baada ya kumuelezea mwanawe majukumu yake mbele ya Mola Wake, ilikuwa ni muhimu baada ya hapo kumpa mukhtasari wa wajibu wake kwa wazazi wake ili kwamba aweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo kwa mama na baba yake. 92

Page 92


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah Inaelekea kwamba sababu ya Luqman kuwa kimya hapa na hakuelezea juu ya wajibu wa mtoto kwa baba na mama yake imo kwenye hoja ya werevu kwamba katika suala hili, ilikuwa Luqman mwenyewe ndiye baba. Kama angelileta hili suala la wajibu wa mtoto, ambao unajumuisha upole, heshima na shukurani kwa baba, ingekuwa kana kwamba anamuomba mwanawe kuonyesha tabia hii kwake yeye binafsi. Ingekuwa ni sawa na kumtaka mwanawe kumlipa yeye kwa ajili ya juhudi zake zote na malezi kwa kipindi chote cha utoto wake na miaka ya baadae, kuyatii maagizo yake na kamwe kwamba asisahau fadhila zake juu yake yeye. Maneno ya mtu mashuhuri na mwenye hekima kama Luqman, ambaye alikuwa amekusanya katika nafsi yake mema mbalimbali hayawezi kukatishwa kwa namna hii, na kwa kweli, itakuwa ni dhulma kwenye nafasi yake kufanya hivyo. Pili, kwa yeye mwenyewe kumkumbusha mwanawe wajibu wake kama mtoto, Luqman kwa hakika anamuelekeza mwanawe wajibu wake na ile hali ya kuwa na deni kwake juu yake yeye mwenyewe, kitendo ambacho hakimstahiki mtu ambaye amefikia daraja ya hali juu kama hiyo ya kiroho. Kwa kulingalia jambo hili la kiwerevu na maana sana la nasaha, tunaweza kuelewa sababu ya kwa nini Luqman anasimama kuongea anapofikia mahali hapa, na kupitia kimya chake hiki chenye maana kubwa, tukazitambua sifa zake za maadili ya kupigiwa mfano. Vile Luqman anavyopiga kimya na kujizuia kuzitaja wajibat za mtoto, wahyi mtukufu unachukua nafasi hiyo na kuwaagiza wanadamu kuhusu haki za wazazi. Kwa kawada, mtoto wa Luqman pia anawajibika kuchapa kazi kwa juhudi zake zote ili kutimiza wajibu wake kwa baba na mama yake katika kutii amri ya Mwenyezi Mungu. Kwa mara nyingine tena, Luqman anaanza kuongea na kuendelea kumshauri mwanae, safari hii akimshauri kuhusu majukumu yake mbele ya ummah:

93

Page 93


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah

“Ewe mwangu! Simamisha Swala na uamrishe mema na ukataze mabaya na subiri kwa yanayokusibu, hakika hayo ni katika mambo ya kuazimiwa. Wala usiwapindie watu uso wako kuwabeua. Wala usitembee katika nchi kwa maringo. Hakika Mwenyezi Mungu hampendi kila anayejivuna anayejifaharisha.� (31:17-18). Katika kipande hiki cha hotuba, Luqman anamshauri mwanae kuhusu tabia bainifu za nje za kimsingi ambao anapaswa kuzitwaa ili kwamba aweze kujihifadhi yeye mwenyewe kutokana na kuidhulumu nafsi yake; kwa njia hiyo hiyo, kutoka miongoni mwa maadili maovu mengi, yeye anateua moja. Anamuasa mwanawe, ambaye anakaribia kuingia na kushiriki katika jamii, kuwa muangalifu juu ya kuwa na tabia ya makuu, ambayo itakuwa ni udhihirisho wa nje wa mielekeo hasi ya haiba yake, na itakuwa na matokeo yanayofika mbali. Kama majivuno yakiwa ni sehemu ya tabia ya mtu, basi yataathiri kila mwelekeo wa mwingiliano wake binafsi na wa jamii, na kuishia bila kukwepa kwenye kuanguka kwake na kufedheheka katika jamii. Kwa nyongeza, majivuno wakati wote husababisha hisia mbaya kutoka kwa watu na kufungua mlango wa chuki za kawaida kwa yule mwenye kujishauwa. Kupishana huku kunafanya maisha ya kijamii kuwa magumu kwa kila mtu na hivyo, ilikuwa ni muhimu kwa mtoto wa Luqman kuchukua ushauri wa baba yake kwa makini sana na aliepuka kile ambacho, katika ushauri wa baba yake, kilikuwa ni kinyume na utaratibu wa kimaadili wa maisha ya kijamii, na ambacho hufanya kuwa vigumu kuunda uhusiano mzuri na raia wenzake. Ni lazima atambue kwamba ubinafsi 94

Page 94


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah na umimi unapelekea tu kwenye hasara na wala kamwe sio njia inayopendeza; aidha Mwenyezi Mungu anachukia tabia ya makuu. Mwisho, ubinafsi ni jambo ambalo linadumaza maendeleo ya kiroho ya mtu na kuwa ni kizuizi katika safari yake ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu. Baada ya pale, Luqman anamshauri mwanae kujipandikizia ndani yake sifa bainifu za uadilifu na kutakasa nafsi yake kutokana na kile ambacho kinaweza kuikoroga, kwani hii ilikuwa ndio njia ya kwenye furaha kamili na uokovu. Anamhimiza awe wakati wote ni mwenye kutwaa njia ya wastani katika tabia zake akisema:

“Na ushike mwendo wa katikati. na uinamishe sauti yako. Hakika sauti mbaya zaidi ni sauti ya punda.” (Luqman; 31:19). 10. DUNIA YENYE MTANUKO

“Na ardhi tumeitandaza, basi sisi ni watandazaji wazuri walioje.” (51:48).

“Na ardhi tumeitandaza na tumeweka humo milima na tumeotesha kila kitu kwa wizani. Na tumejaalia humo maisha. Na ya ambao nyinyi sio wenye kuwaruzuku.” (15:19-20) 95

Page 95


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah

“Je, hatukuifanya ardhi ni chombo? Kwa walio hai na wafu?” (77:2526) Moja ya matawi ya elimu ya mwanadamu inayoendelea kuongezeka katika nyakati za sasa hivi ni metholojia (kanuni za utaratibu) ya kuchimba rasilimali za ardhini na hazina alizojaalia Mwenyezi Mungu. Wanasayansi wakati wote wamekuwa na wasiwasi kwamba matumizi yasiyopangiliwa ya rasilimali zilizopo yanaweza kupelekea matatizo kwa vizazi vijavyo. Kwa sababu hii, mipango iliyochanganuliwa vizuri na ya muda mrefu na miradi kadhaa imeundwa na wataalamu ili kuweza kutumia vizuri zaidi hizo rasilimali, ambazo ni jambo lenye kuvutia katika uazimiaji wa ustawi bora wa jamii za wanadamu. Mikutano mingi imeendeshwa katika kujadili njia bora zaidi za kuchimba maliasili, kiasi kwamba mazingatio ya kutosha yanafanywa juu ya mahitaji ya msingi na muhimu ya wanadamu na vilevile kuhakikisha kwamba mahitaji haya yanafikiwa katika namna ya uwiano na haki na usawa. Hakuna mwanasayansi atakayeidhinisha kanuni ya kwamba kila mtu anayo haki ya kutumia vitu vya asili kwa namna ambayo ni kwa manufaa yake pekee yasiyo na ukomo. Hata hivyo, Mwenyezi Mungu Mwenye hikma – ambaye hekima Zake zinaakisiwa kwa nadra na elimu nzima ya wanadamu – pia amefanya mipango kwa ajili ya jambo hili muhimu wakati wa kuumbwa kwa dunia; hakika huu ni ushahidi wa ile akili, elimu na usanifu wenye uwezo ambao unaweka mhimili wa uhai. Alimfanya mwanadamu kutambua neema hizi na kumtaka azifanyie matumizi halali. Mwanadamu ametakiwa kupata manufaa ya zawadi hizi za Mwenyezi Mungu ndani ya ardhi kwa namna ya uangalifu na asiruhusu ziada na uharibifu katika kujaribu kupata kwa wingi iwezekanavyo, ambavyo hatimae vitasababisha hitalafu baina ya mahitaji na matumizi. Kama rasilimali hizi zitasimamiwa kwa usahihi kupitia mfumo mpangilio na udhibiti, basi upungufu hautawaathiri wala 96

Page 96


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah maliasili hizi nyingi hazitamalizika. Katika zile siku ambazo idadi ya watu ilikuwa haijafikia hata theluthi ya idadi ya watu waliopo sasa na nyingi ya rasilimali za ardhi zilikuwa bado hazijagunduliwa, umasikini na njaa kutokana na mazao yaliyoharibika vilikuwa ni kawaida sana kuliko ilivyo hivi sasa. Ufukara na njaa vilikuwa na huzuni ya endelevu na vingekuwa wakati mwingine vikisababisha vifo vilivyoenea miongoni mwa jamii za watu. Siku hizi, ingawa idadi ya watu duniani imeongezeka maradufu, yale mazingira yasiyopendeza hayapo tena kwa wingi kama ilivyokuwa, ingawa kuridhika na wastani katika matumizi sio tu kwamba kumepungua kuliko zamani, bali pia kumetoa mwanya kwenye israfu na kupindukia. Zaidi ya hayo, ili kusawazisha masoko yao, nchi nyingi kwa kweli huharibu kiasi kingi cha mazao yao ya kilimo kwa mwaka, jambo ambalo linamhuzunisha moyo kila mtu mwenye fikra huru. Hivyo, umasikini na uhaba unatokea kutokana na utaratibu wa utumiaji rasilimali na ugawaji usiowiana – na sio kwa sababu ya upungufu wa maliasili zenyewe za dunia – na kutokana na mgongano kati ya mahitaji na ulanguzi na uharibifu ambao unajitokeza kama matokeo, mfumo wa jamii na utulivu vinapasuka na kufumuka kabisa; kwa uhalisia haya matumizi mabaya ya rasilimali ni kutokana na utamaduni wa visingizio kwa upande mmoja, na kukosekana kwa kutosheka, na uchu wa kutokuridhika wa watu walafi na wabinafsi wa leo kwa upande mwingine. Hebu tutupie jicho huko nyuma kabisa: Haijulikani ni lini hasa dunia ilipata uwezo wa saidia uhai na lini viumbe hai wa kwanza walitokeza, kuendelea na kuongezeka juu yake. Tarehe hasa ya wakati ambapo mwanadamu alitembea juu ya ardhi kadhalika imefungika katika muujiza na kwa hiyo hakuna jibu la kuridhisha kwenye kitendawili hiki ambalo limetolewa na watafiti. Chochote kile ambacho kimekubalika kuhusu hili kimeegemea kwenye mlolongo wa nadharia na dhana na sio juu ya ukweli uliothubu na kukubalika hasa. 97

Page 97


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah Kama tukiifikiria hii dunia, tunagundua kwamba hatujui ina umri gani, wala hatuna hata mbinu ya kuweza kugundua umri wake kwa uhakika wowote ule, na kila maoni juu ya jambo hili si chochote zaidi ya makisio, ambayo hayatoi mwanga zaidi juu ya ukale wake na asili yake halisi. Wakati ambapo wanahistoria kwa kawaida hawakubaliani kuhusu matukio ambayo ni ya karne chache tu zilizopita, ni aina gani ya nadharia inayoweza kuelezea kwa kuaminika hasa kadhia iliyojitokeza katika mfumo wa uumbaji mamilioni kadhaa bali hata mabilioni ya miaka iliyopita? Wala hatujui ni lini uhai na hatimae binadamu vilianza kutokea duniani, kile tunachojua kwa yakini hata hivyo ni kwamba Mwenyezi Mungu ameruzuku vitu vingi vya aina mbalimbali kwa ajili ya manufaa na mahitaji ya kila kiumbe hai (wanadamu, wanyama na mimea) bila ya ubakhili japo kidogo. Kila kiumbe na mmea vinaweza kupata riziki na virutubisho kwa ajili ya uhai wake na maendeleo kutoka ardhini. Kwa vile ardhi ina mipaka katika ukubwa wake, kwa maana hiyo hata chakula inachozalisha kina mipaka pia. Mipaka hii inaelekea kuashiria kwamba ardhi inaweza kukosa uwezo kwa ajili ya mahitaji ya wakazi wake kwa muda wa kipindi kirefu cha wakati. Licha ya hayo, kupitia mfumo tata na uliodhibitiwa ambao unatawala sayari hii ndogo – ambayo ina vipengele vingi tofauti na vya aina mbalimbali na ambayo imeunganishwa kitatanishi kwenye hifadhi ama ghala la rasimali zake – kila kiumbe hai na mmea unapokea riziki yake. Na hii imekuwa ndio hali kuanzia mwanzo uliogubikika wa uumbaji, na itaendelea hadi mwisho wa wakati, ambapo hizo rasilimali zitakuwa hazijamalizika ama kupungua. Muujiza huu wa kushangaza wa maumbile ni jambo ambalo halikataliki na kwa kuhusiana na hili, Qur’ani inatamka kwamba hii ardhi ina uwezo wa kuwasaidia wakazi wake wote na kukidhi mahitaji yao mbalimbali na tofauti: 98

Page 98


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah

Na tumewajaalia humo maisha. Na ya ambao nyinyi sio wenye kuwaruzuku. (15:20) Na kwa hiyo tunaona maendeleo ya kudumu na endelevu katika dunia ambayo yanasonga mbele kwa kushirikiana mfumo maalum wa udhibiti kwenye njia iliyokwishapangwa na kulindwa kabla. Wakati mwanadamu alipotaka kujenga nyumba na vifaa alivyokuwa akihitaji ni matofali, mawe na chokaa, Mwenyezi Mungu aliweka vifaa hivi rahisi kwa ajili yake ili aweze kuchukua hatua za kurahisisha haja yake ya msingi na ajifanyie makazi yake. Hata hivyo, siku hizi kutokana na ongezeko kubwa la watu mijini, hususan vile watu wanavyohamia kwenye miji mikuu, na kutokana na matatizo yanayohusiana mlundikano na uongezekaji wa mawasiliano ya watu, mwanadamu anahitaji majengo yenye hata zaidi ya ghorofa mia moja. Katika hekima na elimu Yake isiyo na ukomo inayokizunguka kila kijichembe katika ulimwengu wa uhai, Mwenyezi Mungu alijaalia ndani ya dunia – mamilioni mengi ya miaka yaliyopita – malighafi ambayo siku moja zitakuja kutumika kwa ajili ya ujenzi (mawe, na ufinyanzi na chuma) katika umbile la kokoto na madini. Kisha akawapa wanadamu mzinduko wa kuunda na kugundua na kutengeneza vitu hivi anavyoweza kuvifikia ili aweze kuendelea katika ulimwengu kwa kuchimbua maghala haya yaliyoandaliwa kabla kutoka kwenye vina vya ardhi na kuzitumia kwa kumpatia mahitaji yake. Mazungumzo yaliyopita yameelezea utoshelezaji wa rasilimali za dunia katika kuhudumia mahitaji ya mwanadamu na viumbe wenzie mwote katika historia na kwa kipindi chote ambacho namna za uhai zinakuwepo juu yake na kutaka kufanya matumizi ya vile inavyovitoa. 99

Page 99


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah Qur’ani pia inasisitiza nukta hii hii, na inaongeza kwamba ardhi haimudu tu kila kiumbe hai, bali inaingiza ha wafu vilevile:

Je, hatukuifanya ardhi ni chombo? Kwa walio hai na wafu? (77:2526). Ingawa maendeleo na mabadiliko ya mwanadamu kamwe hayataondoka kwenye utu wake wa msingi na asili ya uhai na muundo, hata hivyo, katika vifaa vya mavazi, mwanadamu amefika mbali katika mpito wa wakati, na hili liko wazi duniani kote. Kifo ndio mwisho usiokwepeka wa kila kiumbe hai ambacho kinakaa duniani na dunia yenyewe iko tayari wakati wote kupokea mabaki ya vilivyokufa na kuvikumbatia. Mwishowe miili ya wanadamu hurudi ardhini, kama ilivyo kwa mizoga ya wanyama. Kila aina ya mimea – kuanzia majani hadi kwenye mashina ya miti – halikadhalika huanguka na kuchanganyika kwenye maghala ya ardhi. Kwa hiyo ardhi mara moja huwa mhimili mkuu wa maisha ya wanadamu na chanzo ambacho humo wanadamu wanaweza kukusanya neema, na vilevile ni sehemu ya maziko kwa viumbe hai vyote; hivyo Qur’ani inaeleza:

Je, hatukuifanya ardhi ni chombo? Kwa walio hai na wafu? (77:2526). Kinachovuma pamoja na kanuni za maumbili ni lengo na kutafuta ukamilifu; kwa kweli hizi ndio sifa za wazi na zenye kujulikana sana ambazo zinayaenea maumbile na ndio matunda ya haraka na ya mfululizo ya mpan100

Page 100


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah go wa Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo, dosari na upungufu – ambavyo ni matokeo ya mpango wa vurugu na usio na busara – havina nafasi au maana katika mfumo wa uhai. Hivyo, wakati tunapotafakari misingi ya uhai, tunakuja kutambua kwamba umejaa utukufu, hadhi na ukuu. Qur’ani inaelezea kuhusu hili:

“…..Huoni tafauti yoyote katika uumbaji wa Mwingi wa Rehema. Hebu rudisha jicho! Unaona kosa lolote?” (67:3) Nyuma ya mfumo wa maumbile wa Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehma mtu hataona upungufu au vurugu; angalia kwa uangalifu tena na tena, je unaona hitilafu yoyote? La hasha! Kwa hiyo, kutojali na ujinga juu ya mambo mbalimbali ambayo yamedhihirishwa katika dunia na kile kinachoendelea katika kumzunguka mwanadamu, kuna matokeo ambayo yatatengeneza vikwazo kwenye furaha kamili ya wanadamu. 11. MWONGOZO KATIKA MAUMBILE

“Na akaweka katika ardhi milima ili isiyumbe nanyi. Na mito na njia ili mpate kuongoka. Na alama nyingine. Na kwa nyota wao wanajiongoza.” (16:15-16) Neno “mwongozo” wakati wote linaleta kwenye akili ya mtu ile dhana ya 101

Page 101


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah maagizo na maelekezo ya kiroho. Hata hivyo, kwa upande wa Mwenyezi Mungu na neema Zake zisizokoma na zilizoenea, hatuwezi kulifunga neno hili katika maana finyu kama hiyo. Uchunguzi wa mpango mkuu wa ulimwengu na maelezo yenye utatanishi ya kuumbwa kwetu wenyewe kunatufanya tufikie hitimisho kwamba mfumo wa uhai umeundwa juu ya seti ya kanuni za msingi ambamo kila kiumbe na kila jambo lina mahali pake maalum na jukumu lake makhsusi. Muumba amekiongoza kila kimoja cha viumbe Wake kwa mujibu wa asili na uumbwaji wake na ameandaa mpango kwa ajili ya kila kipengele na muhula wa uhai wake. Haiwezekani kwa kiumbe kupata uhai au kufikia ukamilifu na bado kisitegemee malezi na uwezo wa Mwenyezi Mungu, kutoa uhai mpya, kujaalia neema na kutunukia fadhila ni miongoni mwa haki bainifu za Muumba, na ishara za utiaji nguvu huu na utoaji na fadhila za kudumu ziko dhahiri kabisa na zenye kuonekana katik kila kiumbe: 1. Mwongozo wa kiuhai au wa kiulimwengu (hidayatul-takwinii): Wanafikra wa Kiislam wanakubaliana kwa kauli moja kwamba ndani ya mpango wa uumbaji, Mwenyezi Mungu hukiongoza kila kiumbe kwenye ukamilifu wa hali yake halisi ya kimwili, kuanzia kwenye chembe ndogo kabisa ambayo michakato yake ya ndani inaendeshwa na mfumo maalum hadi kuwa kitu kizuri kabisa katika ulimwengu – licha ya maajabu yote, wakati wowote vinapopata daraja fulani vinahitaji na kupokea huo mwongozo uliohifadhiwa kwa ajili ya daraja hilo. Kwa hakika kila kitu kipo katika kumhitajia kabisa Yeye ili kwamba sio tu akiruhusu kupata uwezo wake wa ndani, bali pia ili kwamba akibembeleze polepole kwenye uelekeo sahihi wa maendeleo katika nuru Yake yenye kupenya. Kama isingekuwa kwa muongozo huu, ulimwengu wote usingeweza kamwe kudumu na kusimama imara – kwa kweli usingeweza kutambua hata alama ya uhai.

102

Page 102


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah 2. Mwongozo wa kisheria au kimaagizo (hidayatut-tashri’i): Kama vile utaratibu wa uhai ulivyochimbukia kutoka kwenye hikma na elimu ya Mwenyezi Mungu isiyo na mipaka, kadhalika muongozo kuhusu lengo la mwanadamu katika mfumo wa uhai ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu, kwa sababu matokeo muhimu ya maisha na akili ni kuwa na lengo na madhumuni. Mbali na elimu ya kipawa ambayo ni ya asili ndani ya kila mwanadamu na ambayo inamsaidia kutambua kweli fulani fulani ili aweze kuchagua njia yake, kwa uhuru kabisa, bila ya kuwa na mawazo ya kabla, kutegemea huu uwezo wa asili wa ndani kabisa (fitra), mwongozo wa nje ambao utaimarisha na kusaidia akili na fitra vilevile ni muhimu. Hili liko hivi ili kwamba yeye aweze kurekebisha dalili za uasi na nyingi katika tabia zake na vilevile kuilinda akili yake na fitra kutokana na upotovu. Kama vile tu Mwenyezi Mungu alivyomuongoza mwanadamu kutafuta ukamilifu wa kimwili kupitia silika ya maslahi binafsi, Yeye kadhalika alimuongoza katika kufikia ukamilifu wa kibinadamu kupitia ule uwakala wa sheria au amri zenye kuagiza, kwa nyongeza ya muongozo wa fitra. Hii ni kwa sababu wakati muongozo wa kimaumbile unapokabiliana na maslahi binafsi, huwa unahitaji kiasi fulani cha msaada. Mwenyezi Mungu aliwateua Manabii (a.s.) kuja kusaidia mwanadamu, kumshika mkono na kumtambulisha kwenye uwezo stadi wenye kufahamika uliofichika katika fitra yake mwenyewe na kuchangamsha mielekeo na hamasa zake chanya na tukufu na kumzindua kuutumia welekevu hizi katika namna ambamo zimekusudiwa kutumika, na kumuonyesha vikwazo vyote ambavyo vingeweza kukwaza safari yake kuelekea kwenye ukamilifu. Ni lazima ifahamike kwamba muongozo huu ni udhihirisho wa neema za Mwenyezi Mungu na maandalizi ya kuchunguza umuhimu wa mhusika na kuamua aina ya malipo atakayochuma kupitia vitendo 103

Page 103


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah vyake; haukumaanishwa kumuondolea mwanadamu chaguo au nguvu ya mawazo huru ya kibusara na kuzima nuru ya hiari yake, bali hii ndio namna ambamo kipimo cha ubora na kasoro za watu zinajidhihirisha. Kila mwanadamu anaweza kutumia muongozo wa ndani na wa nje wa kimungu ulioko kwenye mamlaka yake katika kutukuzisha vitendo vyake na kupanda ngazi kuelekea kwenye ukomavu wa kiakili na ukamilifu. Kwa kweli njia ya kwenye ukamilifu haikubali mkwamo na upandaji wa mwanadamu hautatokea mpaka atakapochukua hatua kwa ufahamu kabisa za kujirekebisha mwenyewe kimsingi kabisa. 3. Muongozo kuhusu mahitaji ya maisha (hidayatuz-zisti): Tunapoangalia miundo ya maisha iliyopo ulimwenguni kwa jumla na kuchambua vipengele vyao mbalimbali, tunakuta kwamba wanachama wote wa mfumo huu wanashika nafasi inayofaa kwa hali yao maalum. Na wakati sehemu makhsusi ya mgawanyiko wa maumbile inapokumbwa na kanuni za maumbile asili huanza kufanikiwa katika muelekeo wake iliopangiwa kabla. Kwa mtazamo huu tunaweza kuona wazi ule mlingano wa jumla uliopo ulimwenguni kati ya wanachama hawa wa maumbile (ndani ya jamii za wanadamu, wanyama na mimea), wote hao ambao kila mmoja ana muongozo wake wenyewe halisi wa asili. Tukizichambua sifa za wanyama tunahitimisha kwamba maumbo yao ya asili na makazi yao ni tofauti kabisa na maada ya mimea, kwa sababu maumbile hayawawekei riziki zao kwenye milki zao, bali wanyama wanalazimika kutafuta chakula chao bila kukoma na kuwinda ili kujipatia wenyewe chakula, na ni dhahiri kwamba hili linahitajia kukua kwa zana zinazofaa na viungo vilivyotokeza mwilini kwa ajili ya kazi hiyo. Hata hivyo, mwanadamu ambaye amefikia daraja za juu na ambaye ana dhamiri na hiyari, bado yuko katika kiwango cha chini inapokuja kwenye suala la silika zake. Umbo lake la kimwili kwa mfano ni dhaifu sana na lililoandaliwa vibaya na yeye ana uwezo mdogo sana wa 104

Page 104


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah kuhimili kihoro kuliko wanyama; kwa kweli, inamchukua yeye miaka mingi kuweza kuwa mwenye kujitosheleza mwenyewe na kuweza kujihudumia kwa mahitaji yake mwenyewe. Sifa hizi makhsusi ambazo zinawazunguka viumbe wote ndio njia kwa ajili ya kukua kwao taratibu kuelekea kwenye ukamilifu. Aya hiyo hapo juu inaelezea aina ya mwongozo ambao unamsaidia mwanadamu katika maisha yake ya kila siku, na inatoa mwanga juu ya baadhi ya uhalisia wa kimuujiza wa maumbile. Mwenyezi Mungu Mtukufu, ambaye ndiye chanzo cha rehema, na ambaye neema Zake zinaendelea kumiminika kote ulimwenguni hakupuuza kuumba wingi wa hali za asili na mchanganyiko wa maumbo katika mfumo tata wa ulimwengu ambao unafanya kazi ya kuongoza wakazi wake wakati wa mfululizo wa maisha yao ya kidunia. Muumba wa ulimwengu – Yule Msanifu Mkubwa na Mmiliki wa nguvu zisizo na mipaka – amewapa viumbe Wake uwezo wa utambuzi na hisia za ajabu ili viweze kuishi na kustawi na kufikia ukamilifu. Uwezo huu unawawezesha kushika njia sahihi katika safari ambayo kila kimoja lazima kiifanye katika dunia hii na kuviongoza katika mfululizo wa maisha yao ya kushangaza. Wakati nabii Musa (a.s.) alipotakiwa na Firauni kumtambulisha Mola wake, yeye alijibu:

“Akasema: Mola wetu ni yule aliyekipa kila kitu umbo lake kisha akakiongoza.” (20:50). Wanyama na ndege wana hisia kali upande wa mwelekeo ambazo kwazo wanaongoza masafa ya umbali. Katika mfululizo wa maisha yao, ndege 105

Page 105


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah wanatumia hisia hii ya ajabu katika kuruka kwa urahisi baina ya viota vyao na sehemu za malisho zilizoko mbali bila ya kupoteza kamwe njia zao za kurudia. Elimu ambayo kila kiumbe anayo ni neema ambayo imewekwa katika asili yake na utukufu na hadhi ya umbaji imedhihirishwa vya kutosha zaidi na huu uwezo wa ajabu ambao tunauona katika viumbe mbalimbali. Ndege wahamaji wakati mwingine wanasafiri kuvuka mamia ya kilometa ili kufikia mwisho wa safari zao ambako wanakaa kwa muda mrefu kabla ya kuruka kurejea kupitia njia ile ile mpaka wanarejea kwenye kituo chao cha mwanzo kwa uhakika kabisa bila kukosea. Ni aina gani ya bikari (compass) wanayotumia ndege hawa, ambayo haina makosa kiasi hicho na iliyo sahihi kuweza kuvuka masafa marefu, wakakaa katika nchi ngeni kwa muda wa miezi kadhaa na kisha wakarejea kwenye kituo chao cha asili? Hata mpaka leo hii sayansi ya mwanadamu haijaweza kufumbua muujiza huo! Wanasayansi wengi wamefanya majaribio mbalimbali kadhaa katika kujaribu kuelewa zaidi kuhusu hiyo hisia ya uelekeo ambayo ndege wote wanakuwa nayo na hawakuweza kuituliza katika mnyama (hata kwa kuanzisha mambo mbalimbali ya kumchanganya akili); ndege hao wanaweza pia kutumia mfumo huu uliokadiriwa kutoa mienendo mingi ya ajabu ya kisarakasi ndani yao wenyewe ambayo ni sehemu ya mfumo huo huo usiojulikana. Wakati wa kuhama kwao, ndege hawa hufanya makundi ya angani na kukutana kutokea sehemu tofauti na wakati mwingine hubadilishana sehemu na kuunda umbo zuri la kuvutia sana katika kuruka kwao. Ni chombo gani kimewekwa katika asili na maumbile yao kinachowawezesha kuruka katika mitindo madhubuti na kamilifu bila ya wao kugongana? 106

Page 106


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah Fikiria ndege (airplanes) ambazo zina vijenzi vya kutatanisha vingi tu na vyenye hisia na vyombo vya kisasa; zinapofanya mienendo ya angani haziwezi kamwe kuruka kwa pamoja kwa ukaribu sana kwa idadi hizi kubwa na zikafanya kwa usalama kabisa ile mienendo mbalimbali inayofanywa na ndege viumbe bila ya maguvu. Mara nyingi, hata ndege za kisasa ambazo zinapitia majaribio ya makali kisheria na zinapitishwa kwenye hali halisi zilizopangwa katika jaribio la kustahimili matukio yasiyotarajiwa, zimepata ajali na migongano mibaya sana wakati ziliposhiriki katika maonyesho ya angani. Mbali na ndege, wanyama wengine na wadudu pia hufuata mfumo ulioundwa na huonyesha namna nyingi za miujiza na tabia zisizofahamika; ili kukamilisha mahitaji yao wanatumia uwezo wa kushangaza wa kutambua mahali, ambao ni wa kipekee kwenye spishi zao. Wanyama wamefumbwa macho na kuhamishiwa tena mamia ya kilomita mbali na makazi yao ya kawaida, na bado kwa mshangao kabisa wanaweza kurejea kwenye makazi yao bila ya kukosea kabisa. Hata hivyo, kwa mujibu wa Qur’ani:

“………. Na binadamu ameumbwa dhaifu.” (4:28) Mwanadamu ameumbwa mdhaifu kiasi kimwili na hana mfumo wa uelekeo/mahali wa ndani wa kuzungumzia. Wakati huo huo anayo akili nzuri na yenye ubunifu na akili yenye nguvu ambayo ni bora kuliko kila kiumbe kingine chochote.

107

Page 107


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah Kwa hali yoyote ile, mikono ya Mwenyezi Mungu imeunda matukio ya kawaida ya kufidia haya mapungufu ndani ya miili ya wanadamu ili kwamba yaweze kuwahudumia wanadamu kama milingoti na nguzo za alama kwa ajili yake, na kumtahadharisha na kumlinda katika safari zake kutokana na hatari zinazowezekana kutokea kwenye safari yake. Katika nyakati za zamani namna ya usafiri ilikuwa katika mipaka ya wanyama wa mizigo. Mara nyingi, wakati wa safari ambazo zilifanyika kuvuka majangwa na mawanda ambayo yalikuwa hayana milima na vilima, wasafiri walikuwa wakipoteza njia zao na kukabiliwa na hatari kubwa. Katika matukio mengi walipotelea kwenye njia zisizojulikana na matokeo yake wakapoteza maisha yao. Hata hivyo, kwenye njia ambazo zilizungukwa na milima kwa upande mmoja, kulikuwa na uwezekano mdogo wa watu kupotea kwa sababu waliweza kuitumia milima hiyo kama alama za kuwaongozea kufika waendako. Aya zilizoko kwenye uchunguzi zinaweka wazi kwamba ili kufidia ukosefu wa mfumo wa rada ya ndani kwa mwanadamu – mfumo ambao upo kwa namna mbalimbali ndani wa viumbe hai wengineo – Mwenyezi Mungu alimuandalia mwanadamu mfumo asili wa kutambua uelekeo wa upande katika sura ya milima na vilima na vijito na mito na mianya ndani ya milima ili kwamba wakati mwanadamu anaposafiri katika ardhi kutoka sehemu moja kwenda nyingine, sura hizi zisizobadilika zingefanya kazi ya kuwa alama na ishara kwa ajili yake kuweza kupanga mwelekeo wake wa safari. Hata katika nyakati zetu hizi, pamoja na maendeleo katika elimu ya sayansi, marubani wa ndege, mbali na kutegemea mifumo yao ya elekroniki kutambua mahali walipo, vilevile na wao wanatumia safu za milima, mito na sura za kijogorafia katika kuweka alama ya mielekeo ya njia zao. Hii ni moja na neema zisizo idadi za Mwenyezi Mungu na ni ushahidi wa matumizi na manufaa mengi ambayo mambo haya ya asili yanatoa kwa 108

Page 108


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah wakazi wa dunia kulingana na mpango wa Mwenyezi Mungu, mojawapo ikiwa ni kuongoza na kuwaelekeza wanadamu. Faida ya sura hizi za asili zinaonekana wazi wazi wakati jua linapowaka kwa joto na mwanga wakati wa mchana; joto na mwanga vyote vya hili umbo tukufu la mbinguni vinasaidia wakazi wa dunia katika harakati zao na safari zao. Kwa ajili ya safari za usiku vilevile, Mwenyezi Mungu ameumba mfumo wa nyota mbinguni ambazo mwanga wake na mng’aro huwaongoza wakazi wa dunia katika nchi kavu na baharini. Mfumo wa mienendo ya sayari, nyota, jua na mwezi vile zinavyotembea kwenye mizunguko yao iliyopangwa, zinafanya kazi ya kuwaongoza wanadamu.

“….. Na kwa nyota wao wanajiongoza.” (16:16) Uchunguzi juu ya peo za macho na ukaguzi wa jinsi matukio mbalimbali ya asili yalivyo na manufaa kwa mwanadamu yenyewe ni chanzo cha mzinduko wa kiroho na elimu kuhusu Mwenyezi Mungu. Tunajua kwamba ulimwengu hauishi kamwe na kwa hiyo kujua na kuelewa siri zake zote vilevile ni kazi ngumu mno, elimu ya mwanadamu inayoendelea bado haina uwezo wa kuelezea mingi ya miujiza nyuma ya matukio ya kimaumbile ambayo yameumbwa kwa ajili yake. Licha ya kila moja ya alama na mifumo hii, ambayo inaweza kushuhudiwa na kueleweka katika maumbile, iliyopo katika viwango vya juu, haiwezi kulinganishwa na umbo tatanishi na lenye hisia la binadamu na pia na akili ya mwanadamu. Kwa mtu ambaye ana akili na umaizi – ambavyo pia vinatolewa utashi bunifu wa Mwenyezi Mungu – jambo hili ni lenye maelekezo sana. Kuwepo kwa alama hizi za nchi katika safari yote ya mtu kuanzia mahali pamoja hadi pengine ni jambo la faraja na amani ya akili, na kila mtu anaweza kuchagua njia nyepesi zaidi ya kufikia anakokwenda kuvuka mil109

Page 109


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah ima ya asili, mito na makorongo. Kwa nyongeza, katika kusafiri kupitia sura hizi za asili wao wanaweza kutafakati juu ya alama hizi za Mwenyezi Mungu na kuzichambua; wakati wanaposhangaa kwenye mandhari nyingi za kushangaza zilizoenea duniani kote, wanaweza wakashuhudia uwezo wa upangaji wa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Katika kila chembe (atom) katika upana wa maumbile wataona ushahidi wa kuwepo kwa Chanzo cha maumbile na kwa hiyo wakazinduliwa na kuongozwa. Qur’ani inasema:

“Ambaye amewafanyia ardhi kuwa tandiko, na akawafanyia ndani yake njia mpate kuongoka.” (43:10). Kutokana na neno “tahtadun” – kuongozwa sawa – katika aya mbili hizo zilizotangulia, maana zote zinaweza kupatikana na kutokana nazo zote tunaweza kupata mwongozo; tunanufaika kutokana na milima na mito na njia za asili katika mienendo ya safari zetu na kusafiri hadi mwisho wa safari zetu bila ya wasiwasi wala hofu ya kupoteza njia yetu na pia tunanufaika kwa kushuhudia haya matukio hai ya asili makubwa na ya kustaajabisha, na kwa kupitia hayo tunautambua ule uhalisia mkubwa na yule Chanzo asiyehitajia, wa kipekee na mwenye kudura, Ambaye sifa zake zinaakisiwa na mwanadamu mwenyewe kwa ufahamu mdogo kabisa. Ni kweli kwamba uelewa wa mwanafiziolojia au mwanasayansi mdadisi ambaye anachunguza zile kazi zenye utatanishi za ndani kabisa ya mnyama umeondolewa mbali kabisa na ule wa mtu wa kawaida ambaye anafanya uchunguzi mwepesi tu wa mnyama, hata hivyo, ingawaje wote wanayaangalia maumbile kutoka kwenye pembe tofauti, bado wanakuja kwenye hitimisho moja.

110

Page 110


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah 12. DHORUBA YENYE KUANGAMIZA

“Enyi ambao mmeamini! Zikumbukeni neema za Mwenyezi Mungu zilizo juu yenu; pale yalipowafikia majeshi, tukayapelekea upepo na majeshi msiyoyaona na Mwenyezi Mungu anayaona mnayoyatenda. Walipowajia kutoka juu yenu na kutoka chini yenu; na macho yakakodoka na nyoyo zikapanda kooni. na mkamdhania Mwenyezi Mungu dhana mbali mbali. Hapo waumini walijaribiwa na wakatikiswa mtikiso mkali.” (33:9-11). Kazi kubwa ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ilikuwa ni kufikisha ujumbe uliotukuka wenye nuru wa Mwenyezi Mungu swt. kwa wanadamu na kwa sababu hiyo, mbili ya sifa zake maarufu ni “mtoa habari njema” (mubashir) na “muonyaji” (Mundhir). Hata hivyo, wakati ujinga unapofikia kilele chake na wanadamu wakawa wananyimwa uhuru wao wa kuamua na kuchagua njia sahihi ya utendaji, na hakuna fursa nyingine inayobakia ya kukabiliana na hali hiyo, basi matumizi ya mapambano ya silaha yanakuwa ni halali. Juu ya adui mwepesi wa kukimbilia vita, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alilazimika kujibu kwa namna hiyo hiyo, kwa kweli kujibu huku ni kwa kawaida na kwenye mantiki. Kwa hiyo, kila wakati makafiri na washirikina walipowapa Waislamu changamoto ya vita, na uhai wa Uislam ukawa hatarini, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angechukua hatua za kulinda uhai wa maadili matukufu ndani ya jamii na kuutetea Uislamu. Nyingi ya vita vya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) 111

Page 111


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah vilikuwa katika asili ya kujihami, na vilipiganwa katika kujibu mashambulizi ya maadui hao. Hata hivyo, kwa kuwa kazi yake kimsingi ilikuwa ni kufikisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu na kuimarisha Upweke Wake, Mwenyezi Mungu alimpendelea na kumsaidia Mtume Wake (s.a.w.w.) ambaye alikuwa ndiye mbora kabisa wa viumbe vyake. Katika vita dhidi ya adui pia, Mtukufu Mtume alipokea msaada wa Mwenyezi Mungu ili aweze kubeba jukumu la kuwaongoza wanadamu, na kuwanasua binadamu kutoka kwenye makucha ya ushirikina na uchafu wa kiroho, na kufikisha ujumbe wake wa watu wote kwenye kila pembe ya ulimwengu ili aweze kuwasilisha dhana mpya katika muundo wa mpango mzima wa maisha. Hivyo kanuni ya migogoro na vita katika Uislamu ni tofauti kabisa na dini nyinginezo kwa sababu inatafuta malengo makubwa na ya kibinadamu. Katika Uislam, kukimbilia makabiliano ya silaha ni halali tu katika kumkomboa mwanadamu katika maana halisi na kuziweka akili huru kutokana na kutekwa na shaka na kila kifungo kinachofunga wanadamu. Katika vita vya Ahzab ambavyo sehemu yake imeelezwa katika aya zilizotangulia, hali ilikuwa kiasi kwamba vikundi kadhaa, ndani yake wakiwemo washirikina na makabila ya Wayahudi, ambao mamlaka yao yalitishiwa na ujumbe wa Uislam, vilikuwa vikijaribu kumgeuza Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kutoka kwenye kazi yake. Wakati juhudi zao zote ziliposhindwa, walikimbilia kuungana pamoja kupigana vita dhidi ya Waislam. Muungano wao ulifanyika katika mazingira ambapo viapo vya kikabila vilikuwa na nguvu sana wakati ambapo Uislam ulikuwa unafundisha ujumbe ambao ulizipita sana nadhari kama hizo. Ushirikiano huo ulilizidi sana jeshi la Waislam katika nguvu na vifaa, na mpangilio wao ulioratibiwa vyema uliweka ukuta mzito dhidi ya majeshi ya Uislamu. Imesimuliwa kwamba waliwazidi Waislam kwa watu watatu kwa mmoja, ambao bila shaka ni ulingano usio sawa. 112

Page 112


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah Katika vita hivi, ambavyo vilitokea karibu na Madina, askari wa Kiislamu walikuwa katika mazingira magumu sana kutokana na upungufu wao katika idadi na uwezo. Mambo yalikuwa yakiendelea kwa namna ambayo kwamba ilielekea kuwa lile jeshi kubwa na lililoandaliwa vizuri kwa vyovyote vile lilikuwa lishinde lile jeshi dhaifu. Washirikina walikuwa na uhakika kwamba watayasambaratisha kwa urahisi majeshi ya Waislam, na kuwapa kipigo cha kudhoofisha na kuharibu huo mfumo mchanga wa Uislamu. Wakati huo huo, wanafiki na wasaidizi wa kisiri siri wa maadui wa Uislam walianza kuelekeza juhudi zao katika kudhoofisha morali wa Waislamu. Walitumia kila njia kupanga njama na kuwasha moto kwenye hali hiyo katika jaribio la kuzuia kuenea kwa ushawishi wa Uislam uliokuwa unasambaa, na ambao ulikuwa unatishia mbinu zao na mila na desturi za tangu zama za kupenda makuu. Ilikuwa ni katika nyakati hizi ngumu ambapo kwamba msaada wa Mwenyezi Mungu ulikuja kuwanusuru Waislam. Katika namna ilivyoelezwa katika aya hizo, Mwenyezi Mungu alituma majeshi mawili kuja kuwasaidia waumini hao. Moja ya majeshi haya lilikuwa linaonekana na jingine lilikuwa halionekani; hili jeshi lisiloonekana lilikuwa haliwezi kuonwa na makundi yote katika vita hivyo, ambapo hili linaloonekana lilihisiwa wazi na pande zote. Hili jeshi lisiloonekana, ambalo Qur’ani inalitaja, lilikuwa la malaika, ambao waliwasaidia Waislam na kuimarisha morali wao, na kuwafanya kuwa madhubuti dhidi ya adui yao. Lile jeshi ambalo uwepo wake ulihisika lilikuwa ni la tufani kali ambalo athari zake za uharibifu zilikuwa dhahiri kwa Waislamu na kwa maadui kadhalika. Tufani ama dhoruba hiyo ambayo ilitokea kwenye medani ya vita na wakati wa mapambano ilikuwa haikutarajiwa kabisa na ya ghafla kiasi kwamba ilileta mparaganyiko kwenye safu za maadui kwa muda mdogo sana, na kusababisha kushindwa kwao. 113

Page 113


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah Waislam walielewa wazi na kutambua kwa uhakika kabisa kwamba jeshi lisiloonekena la malaika lilikuwa limekuja kuwasaidia katika wakati muhimu ambapo walikuwa wamezidiwa vibaya kwa idadi na wakikabiliana na jeshi la adui lililojiandaa , kwa sababu walijua kwamba ushindi wao haukuwa wa kawaida au matokeo yaliyotazamiwa; washirikina hawakuwa na imani kama hiyo juu ya malaika. Na kwa ule msaada wa wazi ambao ulikuwa ni dhoruba kali, athari zake zilikuwa zimeonekana kwa pande zote za mapambano hayo. Jeshi la Waislam na vilevile yale majeshi ya adui waliishuhudia dhoruba hiyo ya ghafla kwa wakati mmoja na kwa macho yao wenyewe. Hapa Qur’ani kwa mkazo kabisa inatangaza dhoruba hiyo kama chanzo cha kushindwa kwa maadui na tukio hili limetajwa kama mfano wa neema maalum za Mwenyezi Mungu na huruma kwa wapiganaji wa Kiislam. Na kama dhoruba kali ya namna yake kama hii, ambayo waabudu masanamu wenyewe iliwapitia na ambayo ilisababisha kushindwa kwao kuzima isingetokea, wangepokea kwa hasira, na kuipinga waziwazi tafsiri ya Qur’ani juu ya matukio. Wasingepoteza fursa yoyote kueneza propaganda dhidi ya Uislam na Qur’ani na wangetangaza kila mahali kwamba hakukuwa na dhoruba yoyote, na hili lingeweza kuwa na uwezo wa kuvunja imani ya Waislamu na kukanusha madai ya Qur’ani. Hata hivyo, ukweli ni kwamba baada ya kushuka kwa aya hizo, waabudu masanamu na wanafiki ambao walikuwa daima wakitafuta njia ya kuutia fedheha Uislam, na ambao wangeweza kuzihoji aya za Qur’ani kwenye kisingizio chochote kidogo kabisa, walibakia kimya na hawakutoa maelezo mbadala yoyote yale juu ya kushindwa kwao. Hili peke yake ni dalili kwamba waliukubali ukweli wa maelezo ya Qur’ani; kwamba dhoruba ililiangamiza jeshi la makafiri na kuwasababishia kushindwa kwao kwenye kufedhehesha; kwamba pia dhoruba ambayo ilisukasuka kwenye lile eneo dogo ambalo majeshi hayo yalijipanga hapo, likilenga tu kwenye upande wao na kuangamiza jeshi lao wakati lile jingine likisalimika. Mwishoni 114

Page 114


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:52 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah walilazimishwa kuuacha uwanja wa vita na kuwa adui dhaifu. Inafaa kuzingatiwa kwamba vita vya Ahzab, kama ilivyotajwa mapema, vilichochewa na ushirikiano wa makabila mbalimbali miongoni mwa waabudu masanamu na Wayahudi; licha ya hili, hakuna hata mtu mmoja kutoka kwenye safu za Wayahudi, waabudu masanamu au wanafiki aliyeweza kuwasilisha maelezo kinyume na maelezo ya wazi na yenye uamuzi yaliyotajwa katika Qur’ani. Katika miaka iliyofuatia tukio hili, wakati wapinzani walipokuwa wakitafuta, kwa muda wote, njia na mbinu za kuhujumu imani za Waislam, hata wanahistoria wenye chuki miongoni mwao hawakuweza kukanusha kwa uhalali kauli ya Qur’ani kuhusu kile hasa kilichotokea siku ile, na kuweza kuthibitisha kwamba ile dhoruba ya kuangamiza inayotajwa na Qur’ani kama chanzo cha vurugu katika jeshi lao na kushindwa kwao mswishoni kusikodhanika, kamwe haikutokea. Hili lenyewe peke yake ni udhihirisho wa mujiza wa Qur’ani, ambao ni lazima ufanyiwe tafakari juu yake, na sio kupitwa kama jambo la kawaida tu. Kama makundi haya hasimu yangetaka kusonga mbele kutoka kwenye zama zao za giza, na daima kuweka pembeni urithi wao wa mila zisizo na msingi, ambao ulikuwa ni chanzo muhimu cha kukwama kwao kiakili, na kunufaika kutokana na nuru ya mafundisho ya Mbinguni, basi tukio hili la ajabu ambalo walilishuhudia kwa macho yao wenyewe lilikuwa linatosha. Kama wangekuwa tayari kubadilika, hali kwa hakika ingewafanya wafikirie upya imani zao potovu na kutelekeza ukaidi wao na kuikubali dini ambayo ilimfungulia mwanadamu milango ya kwenye maendeleo binafsi, muongozo na ukamilifu, na ambayo ilileta pamoja nayo funguo za ustawi wa binadamu. Tunapaswa pia kuangalia zile aya za Suratut-Tawba ambazo zinasema:

115

Page 115


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:53 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah

“Watawatolea udhuru mtakaporudi kwao, Sema, msitoe udhuru; hatutawaamini. Mwenyezi Mungu amekwishatueleza habari zenu. Na Mwenyezi Mungu na Mtume wake, ataviangalia vitendo vyenu. Kisha mtarudishwa kwa Mjuzi, wa ghaibu na dhahiri awaambie mliyokuwa mkiyatenda. Watawaapia Mwenyezi Mungu mtakaporudi kwao ili muachane nao. Basi achaneni nao. Hakika wao ni uchafu, na makazi yao ni Jahanamu; ni malipo ya yale waliyokuwa wakiyachuma. Wanawaapia ili muwe radhi nao. Kama mkiwa radhi nao, basi hakika Mwenyezi Mungu hatakuwa radhi na watu mafasiki.” (9:94-96). Katika aya hizi, Qur’ani inaelezea hali ya wanafiki mwishoni mwa vita vya Tabuk, kabla ya kurejea kwa jeshi la Waislam kwenda Madina na inamfanya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) awatambue kwamba wanafiki, ambao walikuwa hawakushiriki katika msafara huo wa Tabuk, walikuwa wanapanga kuligeukia lile jeshi la ushindi katika kurejea kwao Madina, na kuwasilisha visiingizio vya kuwaelezea kule kutokuwepo kwao katika vita hivyo. Aya zinaweka wazi kwamba maneno yao yalikuwa ni uongo mtupu na kwamba watajaribu pia kuwashawishi wapiganaji hao na kuwaghilibu Waislam kwa kutoa viapo vya uongo ili wasije wakabanwa kutoa maelezo juu ya tabia yao mbaya ambayo walikuwa na hatia kwayo. 116

Page 116


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:53 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah Qur’ani vilevile inafichua sababu zao za kuapa viapo hivi hewa na kuwafanya Waislam watambue ukweli wa mambo ili kwamba wawe wamejiandaa kabla namna ya kuwajibu hao wanafiki na wasiingie kwenye mtego wa ghilba yao na kushughulika nao vizuri ipasavyo. Kwa hiyo, Waislam walitakiwa kuyajibu maneno ya wanafiki yasiyo na msingi kwa kuwaambia kwa kusisitiza kwamba hawatavikubali visingizio vyao au kuamini maneno yao, kwa sababu Mwenyezi Mungu, Ambaye ni mtambuzi wa ya dhahiri na ya siri ya kila mtu alikuwa amewafahamisha juu ya mpango wao wa kishetani na ule mtego waliokuwa wameutega ili kuwalaghai Waislam. Qur’ani inawaambia wapiganaji hao kimsingi kwamba: “Mara tu mtakaporejea kwao wataapia kwa jina la Allah ili kwamba mpuuze jinai yao, lakini ninyi msije mkadharau uzito mbaya wa vitendo vyao kwa sababu wao ni mafasiki wakubwa.” Rejea Surat-Tawba, aya ya 96. Hapa uwezekano namna mbili unaweza kuangaliwa. Wa kwanza ni kwamba hao wanafiki walikuwa wametambua ule wahyi wa zile aya kuwahusu wao kabla Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hajarejea Madina. Kama suala lilikuwa ni hili, bila shaka wangefanya kinyume na zile aya zilizoshuka wakati walipokutana na Waislam, yaani, wao wasingetoa visingizio vyovyote vile wala wasingeapa kiapo chochote, na kwa sababu hiyo wakashinda pigo mkataa la kipropaganda dhidi ya Qur’ani, kwa sababu walikuwa na tahadhari wakati wote juu ya fursa yoyote ile ya kuwadhoofisha Waislamu. Kwa nini basi hawakuzihujumu zile aya kwa kufanya kinyume nazo na badala yake wakafanya kile hasa kilichokwisha kuelezwa na Qur’ani? Uwezekano mwingine ni kwamba hao wanafiki walikuwa hawatambui huo ufunuo wa aya hizi na bila kujua wakatoa visingizio vyao na kuchukua viapo vya uongo. Katika suala hili hizo aya za Qur’ani ni utabiri ambao ulikuwa sahihi kabisa. 117

Page 117


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:53 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah Kwa hiyo , katika hali zote, swali linabakia kwamba mbali na Mwenyezi Mungu Mwenye nguvu zote – Aliye Mtambuzi wa siri na mawazo ya ndani kabisa ya wanadamu – ni nani mwingine tena ambaye angeweza kutabiri kwa uhakika kabisa vile vitendo vya upotovu vya wanafiki, na kwa usahihi kabisa akatangaza maneno yao ya baadae? Bila shaka tukio hili ni muujiza wa Qur’ani ambao haukuweza kukanushwa na wapinzani wowote wale wa Uislamu.

13. UFAFANUZI JUU YA AYA YA NURU (AYATUN-NUR)

“Mwenyezi Mungu ni nuru ya mbingu na ardhi. Mfano wa nuru yake ni kama shubaka ndani yake mna taa. Taa hiyo imo katika tungi. Tungi hilo ni kama nyota inayomeremeta, inayowashwa kwa mafuta yanayotokana na mti uliobarikiwa, mzaituni. Si wa mashariki wala magharibi. Yanakurubia mafuta yake kung’aa ingawa hayajaguswa na moto – Nuru juu ya nuru. Mwenyezi Mungu humuongoza kwenye nuru yake amtakaye. Na Mwenyezi Mungu huwapigia watu mifano; na Mwenyezi Mungu ni mwenye kujua kila kitu.” (An-Nur; 24:35).

118

Page 118


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:53 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah Wakati wowote kunapokuwa na mjadala kuhusu kupata elimu kamili na pana ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, tunakubali kwamba binadamu atalazimika kukiri kutoweza na upungufu wake wa kuelewa ile Dhati Halisi Iliyotukuka, ambayo ndio Dhati halisi pekee katika nyanja ya uhai. Upeo mdogo wa akili ya mwanadamu hauna nguvu ya kutosha kufanya maamuzi katika nyanja ya Mbinguni, au kufumbua siri za Mwenyezi Mungu zisizoeleweka au kufikia uelewa kuhusu Dhati hii Tukufu, kwa uchunguzi na fikra. Hata kama binadamu alikuwa arefushe dhana yake na mawazo hadi kwenye upeo wao au kutumia uwezo wake wa kushangaza wa fikra – ambao unaweza kufichua miujiza ya dunia yote ya asili – kufikiri na kushauriana na wenzake, bado hatakuwa na zana za lazima za kufikia lengo lake. Ni kwa sababu hii kwamba hata maelezo ya kinaganaga yanashindwa kufikia kuielezea Dhati Yake, kwa sababu chochote kile mwanadamu atakachoweza kuelewa kutoka kwenye maumbile na sayansi kimeumbwa na Mwenyezi Mungu mwanzoni kabisa, na ni matokeo ya amri na utashi Wake. Akili zetu zenye ukomo kadhalika hazina uwezo kabisa wa uelewa mzuri wa asili ya sifa Zake kwa sababu kwamba wakati zinapotolewa kwa Chanzo cha uhai, sifa zinakuwa tofauti kabisa na wakati zinapohusishwa na viumbe wengine. Na juu ya yote, ni dhana zinazofikiriwa na kutungwa na akili za wanadamu, ambazo zenyewe ni mateka wa mipaka ya kimaada, kwa sababu chote kile ambacho kinaweza kufikiriwa katika nyanja za mawazo ya binadamu kinaainishwa na mipaka na kufikia na kuhukumu kwa akili kadhalika kunakuwa kumezuilika na elimu ya mwanadamu licha ya maendeleo mengi, inakuwa haitoshi kabisa, ambapo Mwenyezi Mungu ni wa Milele na Asiye na Mipaka. Hata hivyo, hata pale tunapokiri kukosa uwezo kwetu na nguvu ya kupata uelewa kamilifu na elimu ya uhalisia wa kiroho ya kina na pana juu ya hii Dhati isiyo na mipaka, vivyo hivyo tunapata kiwango fulani cha ukaribu na uelewa kiasi wa daraja Lake Tukufu na tawhiid. Hata wakati akili ya mtu 119

Page 119


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:53 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah na mawazo yake havijakomaa kikamilifu kufikia uwezo wake wa juu kabisa, bado anao uwezo wa kutumia uwezo wake wa kushangaza wa tafakari – ambao ni neema inayopatikana kutoka kwenye amri ya yule yule aliye Chanzo kisicho na mipaka, ambayo Yeye ameiweka katika nafsi zetu ili tuweze kutafuta njia ya kwendea Kwake na kujaribu kumuelewa Yeye – na kutumia ushahidi wa kimantiki na hekima na kupata uelewa kiasi fulani wa ile Dhati ya Milele, kwa ulingano na kiwango cha umaizi wetu binafsi na akili zetu. Kwa njia hii, tunaweza kutambua kikamilifu uwepo wa yule Dhati halisi wa wakati wote, Ambaye anaakisiwa katika upana wote wa uhai na maumbile, nyuma ya kila kitu tunachokitazama. Moja ya aya za Qur’ani zenye utatanishi sana ni aya ya nuru (ayatun-Nur), ambayo wafasiri, masufi’i, na wanafalsafa wote wameijadili, na ambayo kuhusu hiyo kila mmoja ametoa maoni yake kulingana na mielekeo yao mwenyewe wanayohusika nayo. Bila shaka, mbinu ya kuridhisha kabisa ya kuelezea mambo yasiyofahamika ni kwa kutumia istiari, mifano na tashbih; kwa ukweli mtindo huu wa utambulishaji na ufahamishaji wa mambo ya kweli, unaundwa na vipengele muhimu na vya msingi viwili; cha kwanza ni kwamba kile kilichojificha kizuri na cha kistadi ndani ya sitiari kinaufanya moyo wa msikilizaji kuelemea kwenye kile kinachoelezwa, na pili zile siri na miujiza tata ya kitu chenyewe vinaweza kuja kujulikana vema kwa msikilizaji kwa msaada wa sitiari na mifano inayotumika. Aya hiyo hapo juu pia inaangukia kwenye kundi la istiari, lakini hata hivyo, ni kwa kiwango tu cha kufikia uwezo wa kiakili wa mwanadamu, na elimu yake ndogo aliyonayo na kwa upande mwingine, kujaribu kuutambulisha ule uwepo usio na mipaka na mtakatatifu wa Mwenyezi Mungu. Lazima isibakie bila kusemwa kwamba ingawa katika tafsiri zao juu ya aya hii, wafasiri wakubwa wa Kiislam hawakutaja zile nukta muhimu ambazo tutazijadili baadae, hata hivyo kile walichowasilisha kuhusu zile dhana zilizomo kwenye aya hiyo, na maelezo yao na ufafanuzi wa vipengele 120

Page 120


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:53 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah mbalimbali umechanganyika na nukta nzito na zinazotatanisha ambazo zinaendana na mwelekeo wa ndani kabisa wa Qur’ani na zilizoegemea kwenye kuelewa kwa watafiti ziko wazi na zenye kukubalika. Hata hivyo, nukta ambazo tutazijadili sasa hivi zinaweza kupangwa kama maelezo mbadala yenye uwezekano ya aya hii ya nuru. Mwenyezi Mungu ni nuru ya mbingu na ardhi. Ile Dhati Tukufu Ambaye anazizunguka daraja zote za ukamilifu kwa mara moja; nuru Yake takatifu inauzingira uhai wote na inaangaza mbingu na ardhi. Yeye ndiye Muumba Mjuzi wa yote ambaye nuru Yake isiyokwisha huingiza uhai kwenye viumbe na hutoa usaidizi kwao. Yeye anavidhibiti, anavilea na kuvikamilisha kupitia Uwezo Wake, Nuru ya uhai Wake huangaza na kuonekana wazi kwenye uwepo wote wa maisha. Hakuna pembe ya ulimwengu inayoweza kujificha ambayo Nuru ya Dhati Yake tukufu haiawezi kuangazia, hata hivyo, kila kiumbe kinaneemeka kutokana na nuru hii kulingana na nafasi na uwezo wake, kuanzia kwenye uwezo wa msingi hadi kwenye manufaa makubwa ambayo mwanadamu hujikusanyia kwa ajili ya hali bora yake mwenyewe na kufikia vilele vya ukamilifu wa binadamu, ambavyo ndio lengo kuu la malezi ya kimungu. Kwa kuziandaa akili za wasikilizaji ili waweze kulielewa jambo hilo vyema, Mwenyezi Mungu anaielezea nuru Yake kwa tashbihi ifuatayo:

“Mfano wa nuru yake ni kama shubaka ndani yake mna taa. Taa hiyo imo katika tungi. Tungi hilo ni kama nyota inayomeremeta, …..” (24:35). 121

Page 121


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:53 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah Qur’ani ambayo ndio chanzo kikuu cha msingi kwa ajili ya kupata utambuzi wa Mwenyezi Mungu na kupata muongozo wa wazi kuhusu njia ambayo binadamu lazima waipitie ili kumfikia Mwanzilishi wa uhai, inalinganisha ile Nuru tukufu na kitu cha kawaida kabisa ambacho kinamuongoza mwanadamu na kumulika njia yake katika vina vya giza: yaani, taa. Swali la kwanza ambalo linajitokeza hapa ni kwamba, kwa nini Mwenyezi Mungu aliinganisha nuru Yake na kitu ambacho ndio chenye mng’aro zaidi na chenye kutoa mwanga katika ulimwengu huu, ambacho ni jua, ambalo mbali na ukubwa na ung’aavu wake, linatoa athari nyingi na manufaa kwa ajili ya wakazi wa dunia? Kwa nini Nuru ya Mwenyezi Mungu imelinganishwa na taa iliyotengenezwa na binadamu badala yake? Ni lazima ielezwe katika kujibu kwamba: Kwanza kabisa, jua pamoja na mwanga wake wote, manufaa na athari juu ya viumbe hai bado ni moja kati ya viumbe vya Mwenyezi Mungu katika mfumo wa ulimwengu; linatekeleza tu ile kazi liliyopangiwa. Kama Mwenyezi Mungu amelinganisha nuru Yake na ile ya jua, ingeashiria upungufu kutoka kwenye hali ya Muumba kwa kiwango cha kilichoumbwa, na hii ni kinyume na asili tukufu ya Mwenyezi Mungu, ambaye Uwezo Wake unazidi juu ya viumbe wake wote; muumini wa kawaida wakati anapotembea kupita kwenye maumbile asili na kutafakari juu ya vitu hivihivi vya kimbinguni na lengo lililoko nyuma ya kuumbwa kwao ataweza kutambua na kuelewa uwepo Wake. Pili, mu’mini na asiye muumini na kila binadamu, bila kujali itikadi zao na imani, wanatafuta na kupata manufaa yaleyale kutoka kwenye jua, ambapo Nuru ya Mwenyezi Mungu yenye kung’ara yenyewe inamulika kurasa za nyoyo za waumini, na mwanga Wake wa milele unang’arisha akili na nafsi za watu wenye utambuzi na kuweka juu yao matumaini na huruma, ambavyo ni chanzo cha kutosheka kwa moyo; Yeye hainyooshi neema sawa na hiyo kwenye nyoyo za wasioamini, ambao wamefungwa na mapazia yao giza. 122

Page 122


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:53 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah Sasa kwa nini Nuru ya Mwenyezi Mungu imefananishwa na taa, licha ya kwamba ni kitu kilichotengenezwa na binadamu na zaidi ya hayo mwanga wake unaweza kumulika sehemu ndogo sana – ambapo mwanga wa jua unamulika na kuwaka juu ya eneo pana la ardhi? Majibu ni kama ifuatavyo: Sifa zote za taa ambazo zimetajwa ndani ya aya hii hazikutengenezwa na Mwenyezi Mungu ili ziwe ni viumbe wa Muumba, wala hazifanani hasa na chombo kama hicho hasa kilichotengenezwa na binadamu, kwa sababu ung’avu wa taa hii yenye kung’ara na sifa zake za kipekee ambazo haziwezi kupatikana katika eneo lote pana la uhai, umechukuliwa kama msingi wa huko kufanana. Kufanana kwa nuru ya Mwenyezi Mungu na ile ya taa:

“Mfano wa nuru yake ni kama shubaka ndani yake mna taa….” Kama mtu anataka kusafiri kwa umbali fulani katika giza nene, ni lazima kwanza apate taa ili aweze kumulika njia yake iliyo mbele yake na kwa msaada wa mwanga huo atakuwa hawezi kupoteza njia yake na hivyo kufika mwisho wa safari yake salama salimini. Itakuwa haina maana na ni ushauri mbovu kuanza safari katika giza tupu na kusafiri kupita kwenye milima na mabonde na bado mtu ujione huna haja ya mwanga ambao kwamba unaweza kumulikia njia yako. Ili kusafiri katika njia ya haki na kuepuka giza la moyo na akili, na hatimae kuwa umelindwa kutokana na kupotea, mtu anahitaji mwanga mwingine, na mwanga huo ni mwongozo ambao unamulika ile njia ya mawazo ya maana na kugundua ukweli. Endapo mtu ameazimia kutafuta wokovu, yeye ni lazima ajifanye kupatana na usafiri endelevu wa viumbe na watu ambao wanasafiri kwa matumaini yasiyo shaka ya kukutana na Mola (liqa’ Allah), ili kwamba siku moja waweze kufikia ukaribu mtakatifu wa 123

Page 123


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:53 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah Mwenyezi Mungu na kuweka mguu kwenye kizingiti Kitukufu cha mlango; hii ina maana ya kupata kila kilele cha uwezo wake na haiwezi kupatikana isipokuwa kwa kusafiri kwa msaada wa mwanga wa Mbinguni kuelekea kwenye Nafsi yake ya isiyo na mwisho. Sasa, ni nini ambacho kile kioo kinachoifunika na kuilinda taa, kilichotajwa kwenye aya kinachoweza kuwa kinaashiria? Kazi ya kioo hicho ni kuukinga ule mwale kutokana na kuzimwa na nguvu za upepo na dhoruba; kule kuendelea, uhai na uangazaji wa mwale huo kunategemea juu ya kioo na kuwepo kwake endelevu kama chombo cha ulinzi dhidi ya vitu kama hivyo. Kama vile tu muendelezo wa huo mwanga unavyounganishwa na kuwepo kwa kioo hicho, ambacho kinafanya kazi kama kizuizi chenye kulinda, Nuru ya Mwenyezi Mungu kadhalika kwa uendelevu inategemea juu ya Uhai Wake wa milele. Kwa vile nuru hii inachimbukia kwenye Nafsi Yake Takatifu, ambayo inadumu daima, na haina kupatwa na mabadiliko yoyote, uangazaji wake vilevile umeunganishwa kwenye umilele na unajikimu daima. Hivyo Nafsi Yake inadukiza uhai kwenye ulimwengu, na ambapo Nuru Yake inauangaza (kwa mwongozo). Baada ya hapo, aya inazungumzia uangavu wa kile kioo chenye kulinda ambacho kinarusha mwanga mbele kama nyota yenye kumetameta, kwa sababu hicho kioo angavu hakizuii upitishaji wa mwanga japo kidogo; bali kwa wakati huo huo, kule kuwepo kwa kioo kunaunda kizuizi ambacho kitamzuia mwanadamu kukifikia kile chanzo cha mwanga huo. Inawezekana kwamba kizuizi king’aavu hiki chenye kukinga, ambacho kinarusha mwanga huo ni kiashirio kwa malaika wa cheo cha juu kabisa na wabebaji wa Arshi ya Mwenyezi Mungu. Qur’ani inaelezea hivi:

124

Page 124


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:53 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah

“Wale wanaobeba Arshi, na wanaoizunguka, wanamsabihi kwa kumuhimidi Mola wao,…..” (40:7) Na wakati huohuo uhai wa malaika wenyewe umejaa unururifu:

“…..Tungi hilo ni kama nyota inayomeremeta, …..” (24:35) Tunapowachukulia wabebaji wa Arshi kama tashbihi ya kile kioo kinachoufunika mwanga, tunafikia hitimisho kwamba katika mfano huu, kwa sababu kioo kinasimama kama kizuizi cha kumzuia mwanadamu kupata njia ya kukifikia chanzo cha mwanga, hao malaika pia wamewekwa katika kuta nne na kuunda kizuizi kisichopenyeka. Mwanadamu, ambaye ni kiumbe cha kimaada, hawezi akapenya kwenye nyanja ya viumbe wasio wa kimaada kama hao malaika, achilia mbali hicho Chanzo cha Nuru Takatifu chenyewe, ambacho undani wa Dhati yake uko nje ya kila ufahamu, fikra na hisia. Amirul-Mu’minin Ali bin Abi Talib (a.s.) anatamka kuhusu hili: “Utukufu uwe juu Yake Yule ambaye ……. Wala mawazo ya werevu hayawezi kufikia kumtambua.” (wa la yanaluhu ghaws al-fitan) – Nahjul-Balaghah, hotuba ya kwanza, Kwa mujibu wa hayo yaliyotangulia, wazo la kioo ambacho kinafunika huo mwanga ni kupitisha nuru hiyo kwa manufaa ya binadamu. Hao wabebaji wa Arshi tukufu na wale walio kwenye ukaribu (Mukarrabun) hali kadhalika ni mifereji ambamo ule udukizi wa ki-Mungu na neema humiminika kutoka kwenye Dhati Yake Takatifu kuelekea kwa wanadamu.

125

Page 125


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:53 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah Zaidi ya hayo, kama vile watu wanavyofaidika kutokana na mwanga wa taa ambayo imewekwa karibu yao, Mwenyezi Mungu pia yupo karibu na mwanadamu, sio tu pembeni yake bali karibu zaidi na yeye kuliko hata mshipa wake wa shingo (jugular):

“Na hakika tumemuumba mtu, na tunayajua yanayoitia wasiwasi nafsi yake. Na Sisi tuko karibu naye kuliko mshipa wa shingo. (50:16) Tunaona pia kwa uwazi kabisa kwamba jinsi taa inavyokuwa karibu na mtu, ndio anavyoweza kufaidika zaidi kutokana na mwanga wake; sasa kwa vile Mwenyezi Mungu Mtukufu yuko karibu na wanadamu kuliko chanzo kingine chochote cha mwanga – karibu sana naye kuliko hata mshipa wake wa shingo – Nuru Yake yenye kumetameta inasafirisha nyoyo na akili hadi kwenye nyanja za elimu na ufahamu, na kumuwezesha mwanadamu kuona ukweli mwingi. Ndani ya taa hii kuna mafuta ambayo yamepatikana kutoka kwenye mti wa neema wa mzaituni, ambao una ile sifa ya kipekee kwamba haupo katika upande wa ‘Mashariki au Magharibi’ wa kiunga cha mitunda. Huenda fungu hili la maneno limetumika kuashiria ule ukweli kwamba kwa vile mashariki ndio upande wa mawio ya jua na magharibi ni upande wa machweo ya jua, wakati aya inapoeleza kwamba “sio mashariki,” inamaanisha kudokeza kwamba mwanga wa kitu hicho cha mbali sio unaochomoza, au kwa maneno mengine, kina mahali pa chimbuko. Hali kadhalika “sio magharibi,” ikimaanisha kwamba sio mwanga ambao unafifia kamwe, au kwa maneno mengine, hauna mahali pa kukomea vilevile. Ni wa milele. Kama vile tu Muumba wa ulimwengu anavyoishi milele, ndivyo mwanga huo ambao daima unawaka kutoka kwenye Chanzo cha milele. 126

Page 126


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:53 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah Ingawaje uhusikaji wa dhahiri wa maelezo ya “sio Mashariki wala Magharibi” unaelekea kuelekezwa kwa mti wa mzaituni, kuhusika maalum na makhsusia kwa kifungu hicho cha maneno kulikotumika kunaweza kutumika zaidi katika kuelezea nuru hiyo ya Dhati ya Mwenyezi Mungu isiyo na waa. Baadhi ya wafasiri wamependekeza kwamba maneno hayo, “sio Mashariki wa Magharibi” yametumika kuashiria kwamba nuru ya Mwenyezi Mungu inaangaza Mashariki na Magharibi ya ulimwengu. Wazo hili haliendani dhahiri na ile maana iliyojificha ya aya hiyo, kwa sababu swali linajitokeza, “kama ina maana ya Mashariki na Magharibi ya ulimwengu, basi ni vipi kuhusu Kaskazini na Kusini na maeneo mengineyo?” Wakati ambapo tunajua kwamba ile nuru ya Uhalisia ambayo imekuwepo katika kila zama na katika kila nchi inazingira kila sehemu katika uwepo. Mwanga wa nuru Yake unamulika mfululizo kila chembe katika ulimwengu; kwa hiyo, maana iliyokusudiwa ya maneno ya Mwenyezi Mungu hapa sio inayorejelea kwenye mipaka ya kijogorafia, kwa sababu uwepo Wake mtukufu umeepukana na masharti kama hayo.

“….. Yanakurubia mafuta yake kung’aa ingawa hayajaguswa na moto …..” (24:35) Kila mwanga ulioko katika ulimwengu una hali ambayo kwamba ili kuwa mng’aavu unahitaji cheche mwanzoni inauwasha na kufanya athari zake. Kile kitu kinachouwasha kina wajibu wa msingi; hata hivyo, Nuru ya Mwenyezi Mungu ndio ya kipekee. Nuru Yake iko huru kutokana na kila kitu kwa mtazamo kwamba nuru inachimbukia kutoka Dhati Yake Takatifu, na huyu ni wa kipekee kwa sababu sifa Zake, maelezo na heshima viko ndani Yake Mwenyewe na hakuna ubora unaoweza kudhaniwa mbali na Asili Kamilifu, kwa maneno mengine, Nuru Yake si kingine zaidi ya Dhati Yake. 127

Page 127


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:53 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah

“….. Nuru juu ya nuru. …..” (24:35) Ni sahihi kwamba Nuru Yake ni Dhahiri na hakuna kikomo au mpaka uliopo kwa ajili yake; hata hivyo katika hatua za kujiweka wazi, udhihirikaji wake unahusiana na uwezo na sifa za mpokeaji. Vile mwanadamu anavyozidi kupanda kwenye viwango vya juu zaidi vya utambuzi katika tawhiid, vivyo hivyo yeye ananufaika kwa mwanga zaidi katika njia yake ya kiroho: Kipande hiki cha aya pia ni sampuli kwa ajili ya maana hii hasahasa kwa sababu baada ya kujaalia zawadi ya uhai, Mwenyezi Mungu anawaongoza viumbe Wake wastahilifu kuelekea kwenye ukamilifu wa uwezo wao kwa kuwapa neema nyinginezo na kuwafanya wapokezi wa muongozo Wake. Kile ambacho kinampelekea mwanadamu kwenye kuridhika halisi na furaha ni juhudi zake za dhati za kutumia vipaji vyake vilivyofichika na uwezo wake ili kunufaika kutokana na muongozo na Nuru ya Muumba Wake mwema na mkarimu, kwa sababu njia zote za kwenye ustawi na wokovu huishia hapo. Katika du’a ya daku tunasoma kama ifuatavyo:

“Ewe Mola! Tunakuomba kutoka kwenye Nuru Yako ile yenye kung’ara sana, na Nuru Zako zote zinaangaza; Ewe Mola nakuomba kwa Nuru Zako zote.” Baada ya kujadili mambo yaliyoibuka hapo juu, kadhalika inatupasa kufikiri kuhusu mwisho wa aya yenyewe:

128

Page 128


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:53 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah

“….. Na Mwenyezi Mungu huwapigia watu mifano; na Mwenyezi Mungu ni mwenye kujua kila kitu.” (24:35). Na Mwenyezi Mungu anajua vizuri zaidi.

129

Page 129


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:53 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah

ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION 1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9. 10. 11. 12. 13. 14. 15. 16. 17. 18. 19. 20. 21. 22. 23. 24. 25.

Qur'an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Thalathini Uharamisho wa Riba Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili Hekaya za Bahlul Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.) Hijab vazi Bora Ukweli wa Shia Ithnaashari Madhambi Makuu Mbingu imenikirimu Abdallah Ibn Saba Khadijatul Kubra Utumwa Umakini katika Swala Misingi ya Maarifa Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia Bilal wa Afrika Abudharr Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu Salman Farsi Ammar Yasir Qur'an na Hadithi Elimu ya Nafsi Yajue Madhehebu ya Shia 130

Page 130


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

Ukweli uliofichika katika neno la Allah 26. 27. 28. 29. 30. 31. 32. 33. 34. 35. 36. 37. 38. 39 40. 41. 42. 43. 44. 45. 46. 47. 48. 49. 50. 51. 52. 53. 54. 55. 56.

Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur'an Tukufu Al-Wahda Ponyo kutoka katika Qur'an. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii Mashukio ya Akhera Al Amali Dua Indal Ahlul Bayt Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna. Haki za wanawake katika Uislamu Mwenyeezi Mungu na sifa zake Amateka Na Aba'Khalifa Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) Adhana. Upendo katika Ukristo na Uislamu Nyuma yaho naje kuyoboka Amavu n’amavuko by’ubushiya Kupaka juu ya khofu Kukusanya swala mbili Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Kusujudu juu ya udongo Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s) Tarawehe Malumbano baina ya Sunni na Shia Kupunguza Swala safarini Kufungua safarini Umaasumu wa Manabii Qur’an inatoa changamoto as-Salaatu Khayrun Mina -'n Nawm Uadilifu wa Masahaba Dua e Kumayl 131

11:53 AM

Page 131


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:53 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah 57. 58. 59. 60. 61. 62. 63. 64. 65. 66. 67. 68. 69. 70. 71. 72. 73. 74. 75. 76. 77. 78. 79. 80. 81. 82. 83. 84. 85.

Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mitume Muhammad (s) Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili Kuzuru Makaburi Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita Tujifunze Misingi Ya Dini Sala ni Nguzo ya Dini Mikesha Ya Peshawar Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu Ubora wa Imam 'Ali Juu ya Maswahaba Na Ushia ndio njia iliyonyooka Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake Liqaa-u-llaah Muhammad (s) Mtume wa Allah Amani na Jihadi Katika Uislamu Uislamu Ulienea Vipi? Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) Urejeo (al-Raja’a ) Mazingira Utokezo (al - Badau) Sadaka yenye kuendelea 132

Page 132


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

Ukweli uliofichika katika neno la Allah 86. 87. 88. 89. 90. 91. 92. 93. 94. 95.

Msahafu wa Imam Ali Uislamu na dhana Mtoto mwema Adabu za Sokoni Johari za hekima kwa vijana Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu Tawasali Imam Mahdi katika Usunni na Ushia

96.

Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu

97.

Hukumu ya kujenga juu ya makaburi

98.

Swala ya maiti na kumlilia maiti

99.

Shiya na Hadithi (kinyarwanda)

100.

Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu

101.

Hadithi ya Thaqalain

102

Fatima al-Zahra

103.

Tabaruku

104.

Sunan an-Nabii

105.

Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza)

106.

Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili)

107.

Mahdi katika sunna

108.

Kusalia Nabii (s.a.w)

109.

Ujumbe -Sehemu ya Kwanza

110.

Ujumbe - Sehemu ya Pili

111.

Ujumbe - Sehemu ya Tatu

112.

Ujumbe - Sehemu ya Nne 133

11:53 AM

Page 133


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

Ukweli uliofichika katika neno la Allah 113.

Ngano ya kwamba Qur’ani imebadilishwa

114.

Iduwa ya Kumayili.

115.

Maarifa ya Kiislamu.

116.

Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza

117.

Ukweli uliopotea sehemu ya Pili

118.

Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu

119.

Ukweli uliopotea sehmu ya Nne

120.

Ukweli uliopotea sehmu ya Tano

121.

Johari zenye hekima kwa vijana

122.

Safari ya kuifuata Nuru

123.

Idil Ghadiri

124.

Myahudi wa Kimataifa

125.

Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi

126.

Visa vya kweli sehemu ya Kwanza

127.

Visa vya kweli sehemu ya Pili

128.

Muhadhara wa Maulamaa

129.

Mwanadamu na Mustakabali wake

130.

Imam Ali binamu ya Mtume Sehemu ya Kwanza

131.

Imam Ali binamu ya Mtume Sehemu ya Pili

132.

Khairul Bariyyah

133.

Uislamu na mafunzo ya kimalezi

134.

Vijana ni Hazina ya Uislamu.

135.

Yafaayo kijamii

136.

Kusoma sura zenye Sijda ya wajibu

137.

Taqiyya

138.

Vikao vya furaha 134

11:53 AM

Page 134


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

Ukweli uliofichika katika neno la Allah 139.

Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje?

140.

Uislamu na Mazingatio Sehemu ya Kwanza

141.

Uislamu na Mazingatio Sehemu ya Pili

142.

Azadari-Kuhuzunika na Kuomboleza

143.

Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah

144.

Mtazamo Mpya - Wanawake katika Uislamu

145.

Kuonekana kwa Allah

146.

Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza)

147.

Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili)

148.

Ndugu na Jirani

149.

Ushia ndani ya Usunni

150.

Maswali na Majibu

151.

Mafunzo ya hukmu za ibada

152.

Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisusunni No 1

153

Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisusunni No 2

154.

Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisusunni No 3

155.

Abu Huraira

156.

Kati ya Alama kuu za dini Swala ya Jamaa.

157.

Mazingatio kutoka katika Qur’an sehemu ya Kwanza

158.

Mazingatio kutoka kaitka Qur’an sehemu ya Pili

159.

Mazingatio kutoka katika Uislamu sehemu ya kwanza

160.

Mazingatio kutoka katika Uislamu sehemu ya Pili

161.

Hukumu zinazomuhusu mkuu wa kazi na Mfanyakazi

162.

Falsafa ya mageuzi ya Imam Husein (a.s)

163.

Huduma ya Afya katika Uislamu 135

11:53 AM

Page 135


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

Ukweli uliofichika katika neno la Allah 164.

Hukumu za Mgonjwa

165.

Falsafa ya Mageuzi ya Imam Husein

166.

Uislamu Safi

167.

Majlis ya Imam Husein

168.

Mshumaa

169.

Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

170.

Uislam wa Shia

171.

Amali za Makka

172.

Amali za Madina

173.

Uislamu na mfumo wa Jamii ya dini nyingi

174.

Sira ya Imam Ali kuhusu Waasi

175.

Ukweli uliofichika katika neno la Allah

176.

Elimu ya Tiba za Kiislam Matibabu ya Maimamu

177.

Falsafa ya Dini

178.

Visa vya wachamungu

136

11:53 AM

Page 136


Ukweli uliofichika katika neno la Allah Luabumba final.qxd

7/16/2011

11:53 AM

Ukweli uliofichika katika neno la Allah

BACK COVER Ukweli uliofichika katika neno la Allah - mwandishi alitumia maneno haya kwa kumaanisha Qur’ani Tukufu ambayo ni Ufunuio wa mwisho kwa mwanadamu kutoka kwa Muumba Wake kupitia kwa Mtukufu Mtume wa Uislamu. Mwandishi wa kitabu hiki amejaribu kufichua siri nyingi zilizomo katika baadhi ya aya za Qur’ani Tukufu na kuweka umuhimu mkubwa katika kuitafakari hii Qur’ani, kwani ni Mwongozo kwa wanadamu wote katika maisha yao ya hapa ulimwenguni na kesho Akhera. Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote, ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni mambo ambayo hayana nafasi tena katika akili za watu. Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Nukushi: +255 22 2127555 Barua Pepe: alitrah@raha.com Tovuti: www.ibn-tv-com Katika mtandao: w.w.w.alitrah.info

137

Page 137


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.