Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
12:28 PM
Page A
Umaasumu wa Mitume ('Ismatu 'l-Anbiyaa') Majibu ya Aya Zenye Utata
SEHEMU YA PILI
Kimeandikwa na: Sheikh Ja’far Subhani
Kimetarjumiwa na: Sheikh Harun Pingili
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
12:28 PM
Page B
©Haki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: 978 - 9987 - 512 - 04 - 1 Kimeandikwa na: Sheikh Ja’far Subhani Kimetarjumiwa na: Sheikh Harun Pingili Kimehaririwa na:
Hemedi Lubumba Selemani Kimepangwa katika Kompyuta na: Ukhti Pili Rajab Toleo la kwanza: Juni, 2008 Nakala: 1000 Kimetolewa na kuchapishwa na:
Al-Itrah Foundation P. O. Box 19701, Dar-es-Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Fax:
+255 22 2127555
Email: alitrah@raha.com Website: www.alitrah.org Online: www.alitrah.info
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
12:28 PM
Page C
YA LI Y OMO Ismah ya Adam na mti uliokatazwa..................................................2 Ismah ya Kongwe wa Manabii Nuhu (a.s)......................................33
Ismah ya Ibrahim Al-Khalil na maswala matatu.............................49
Ismah ya Yusuf................................................................................65
Ismah ya Musa, Kumua Mkibtiy na kumzoza nduguye................85
Ismah ya Daud (a.s) na hukumu ya kondoo...................................102
Ismah ya Nabii Sulayman (a.s) .....................................................109
Ismah ya Ayyubu (a.s) ................................................................. 129
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
12:28 PM
Page D
NENO LA MCHAPISHAJI Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabu kwa jina la 'Ismatu 'l-Anbiyaa' ambacho tumekiita Umaasumu wa Mitume kilichoandikwa na Sheikh Ja'far Subhani. Tumekigawa katika sehemu tatu, na hii sehemu uliyonayo sasa ni ya pili ambayo tumeiita: Majibu ya Aya Zenye Utata. Sehemu ya kwanza tumeiita: Faida na Lengo Lake, na Sehemu ya tatu tumeiita: Umaasumu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.). Suala la umaasumu ('ismah) wa Manabii na Mitume ni nukta ambayo imezua mjadala mkubwa miongoni mwa wanavyuoni na miongoni mwa madhehebu. Upande mmoja unasema kwamba Manabii ni wanadamu ambao wamehifadhiwa kutokana na dhambi na makosa ya aina yoyote. Upande mwingine unakataa na unasema kwamba Manabii wanaweza kukosea na kufanya dhambi. Upi ni ukweli? Mwandishi wa kitabu hiki ambaye ni mwanachuoni mkubwa wa Kiislamu, analifafanua suala hili kwa urefu kwa kutumia dalili za kielimu, Qur'ani na Sunna na kuhitimisha pasina shaka yoyote juu ya umaasumu wa Mitume. Sisi tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu. Hivyo, tunakitoa katika lugha ya Kiswahili ili wasomaji wetu wa Kiswahili wapate kufaidika na kulielewa suala hili vilivyo na kuongeza ujuzi wao katika masuala ya dini na ya kijamii.
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
12:28 PM
Page i
Tunamshukuru ndugu yetu Sheikh Harun Pingili, kwa kukubali jukumu hili la kukifanyia tarjuma kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwa kitabu hiki. Mchapishaji: Al-Itrah Foundation S. L. P. 19701
Dar-es- Salaam , Tanzania .
i
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
ii
12:28 PM
Page ii
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
12:28 PM
Page 1
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:28 PM
Page 2
Sehemu ya pili
Ismah ya Adam na mti uliokatazwa Lenye nguvu ambalo wameshikamana nalo wapinzani wa ismah, na wale wanaoruhusu kutokea maasi kwa mitume na manabii ni habari ya mti uliokatazwa usiliwe, na hayo yaonekana katika maneno yao na matamshi yao (vitabu vya Qasidah) katika uwanja huu, kwa minajili hiyo yatakiwa kufanya mjadala kwa wasaa na kufuatilia yanayoweza kuwa kisingizio cha mwenye mtizamo huu ulio kinyume na ukweli. Hivyo basi twasema: Kwa kweli habari ya mti imefafanuliwa katika sura tatu na hapa tunataja linalo husiana na utafiti tuufanyao: Amesema (s.w.t.) .
2
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:28 PM
Page 3
Sehemu ya pili
“Tulisema: Ewe Adam! Kaa wewe na mkeo katika Pepo na kuleni humo kwa raha mpendavyo, wala musiusogelee mti huu - kwa kufanya hivyo – mutakuwa miongoni mwa wadhalimu.* Basi Shetani aliwatia wasi wasi ili kuwafichulia tupu zao walizositiriwa , na akasema: Mola wenu hakukukatazeni mti huu ila msije kuwa Malaika au kuwa miongoni mwa watakao baki milele.* Naye- Shetani- akawaapia kuwaambia kwa hakika mimi ni miongoni mwa watoao nasaha kwenu. * Hivyo akawafikisha -kwenye kula mti - (wote wawili) kwa udanganyifu, na walipouonja mti ule, tupu zao zikawadhihirikia na wakaanza kujibandika majani ya ( miti ya huko) Peponi. Na Mola wao akawaita: Je, sijakukatazeni mti huo na kukwambieni kwamba shetani ni adui yenu aliye bayana!* Wakasema: Mola wetu! tumejidhulumu sisi wenyewe, na kama hutotughofiria na kutuhurumia, bila shaka tutakuwa miongoni mwa wenye khasara.* Akasema(swt): Shukeni, nyinyi kwa nyinyi ni maadui. Na makao yenu yatakuwa kait ka ardhi, na-mtapata - posho kwa muda.”. (Al-aarafu,19-24) Na anasema:
3
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
12:29 PM
Umaasumu wa Mitume
Page 4
Sehemu ya pili
“Na tulimuusia Adam hapo kabla na aliacha usia na wala hatukumuona kuwa na azma ya kuuhifadhi usia-au kuwa na subira nao. Tulipowaambia Malaika sujuduni kwa ajili ya Adam na walisujudu isipokuwa Ibilisi alikataa* Tukasema: Oh! We Adam huyu ni adui yako na wa mkeo-jihadharini naye musikubali chochote kutoka kwake kwani ni adui. Hivyo basi asikutoweni (nje ya) Pepo-(bustanini) - kwa kughafilika na vitimbi vyake na kwa kutotilia uzito vitimbi vyake, kwani utapata mashaka, mashaka ya ardhini na magumu yake *Kwa hakika hauto hisi njaa humo (yaani Peponi), wala hautojiona kuwa hauna vazi, na hakika hautohisi kiu humo wala hautopatwa na joto la Jua.* Shetani alimtia wasiwasi akasema: Oh! Adam, je nikujulishe mti wa milele na ufalme usiokwisha (mti hapo ni ule ulio katazwa). Wakala ule mti hapo hapo ikawadhihrikia kuwa wapo utupu bila ya nguo. Basi waliyaunganisha majani ya miti ya Bustani ili kwayo wajisitiri. Kwa kufanya hivyo Adam alimuasi Mola wake.” (Taaha 115-123 ) Hizi Sura tatu zimekusanya pande tatu zenye umuhimu kuhusu kisa hiki, kwa hiyo yatupasa tufafanuwe yaliyokuja humo miongoni mwa jumla na maneno ambayo yazingatiwa kuwa ndiyo kichocheo cha maswali ya fuatayo: Maswali kuhusu Aya hizi Hakika maswali yanayotolewa kuhusu Aya hizi ni: 1. Ni aina gani ya katazo katika kauli yake: “Musisogelee”? 2. Nini makusudio ya wasiwasi wa Shetani kwa Adam na mkewe? 3. Ni yapi makusudio ya kauli yake: “Shetani akawatelezesha” ? 4. Nini kinakusudiwa kwa kauli yake: “Adamu alimuasi Mola wake na akapotea.” Je kuasi na kupotea kunalazimiana na maasi kwa istilahi iliyopo? 5. Nini maana ya kukiri kwa Adam yeye mwenyewe dhulma yake katika kauli yake: “Oh! Mola wetu tumejidhulumu nafsi zetu”? 4
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
12:29 PM
Umaasumu wa Mitume
Page 5
Sehemu ya pili
6. Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anakusudia nini kwa kauli yake: “Basi Adam akapokea maneno kutoka kwa Mola wake, na akamkubalia toba yake…” Je toba ni dalili ya maasi? 7. Nini maana ya kauli yake “Na kama hutotughofiria na kutuhurumia”? Na tuanze kujibu maswali haya moja baada ya lingine na hatimaye mwisho wa mjadala itabainika kuwa Adamu baba wa wanadamu alikuwa ameepukana na waliyomuambatanisha nayo miongoni mwa tuhuma za kuwa amehalifu taklifu ya lazima ya kiungu ya Mola ambayo yalazimu adhabu, kama atakavyoelewa msomaji mpendwa. Aina gani ya katazo katika (La taqrabaa ) ? Kwa kweli katazo hugawanyika katika aina mbili: La lazima (ambalo ni lazima kujizuia). La mwongozo au nasaha njema (ambalo yapendeza kujizuia, na si lazima). Migawanyiko hiyo imeshirikiana kwenye nukta moja nayo ni kuwa, yote miwili imetoka kwa mtu wa ngazi ya juu kumwendea wa chini, hivyo tofauti kati ya migawanyiko hii miwili ni kwamba muamurishaji anaweza kuleta amri yake au katazo lake kutokana na hali ya ubwana na mamlaka yanayomfanya awe na nafasi ya mwamrishaji ambaye ni wajibu kumtii. Kwa hiyo anaamuru ambayo ni wajibu kumtii na anakataza ambayo ni wajibu kuliepuka. Kutokana na hali hiyo hupatikana thawabu kwa kumtii, na adhabu kwa kumuhalifu, na hii ndiyo hali ya amri zilizo nyingi na makatazo mengi yaliyokuja ndani ya Kitabu na Sunnah. Na inawezekana kuelekeza amri zake na makatazo yake kukatokana na nafasi ya Bwana mtoa nasaha na maelekezo, mwonyaji na mtoa mwongozo, bila ya kujiweka kwenye nafasi ya mwamrishaji ambaye ni wajibu kumtii. Bali anajiweka katika nafasi ya mtoa nasaha mwenye huruma, mwenye kukusudia kumfariji amsemeshaye na kumwepusha na mashaka, 5
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:29 PM
Page 6
Sehemu ya pili
kwa hiyo huwa anamwachia msemezwa nafasi ya kuchagua moja kati ya pande mbili, kati ya kufanya na kutofanya, na humzinduwa kuhusu athari mahsusi zitokanazo na kitendo chenyewe, bila ya uhalifu wake kufuatiliwa na malipizi yoyote. Na ukipenda waweza kusema kuwa: Kazi au kitendo chenyewe huwa kina athari za kimaumbile na matokeo mashuhuri yanayopatikana kila wakati na kila zama, bila ya tofauti kati ya mtendaji huyu na yule. Na Mola kwa kuzingatia kuwa ni mjuzi wa matokeo ya matendo na athari zake, humzinduwa mwanadamu dhidi ya matokeo ya kitendo chenyewe, kuanzia ufanisi hadi mashaka. Na huelekeza mtazamo wake kwenye matokeo ya kazi hizi na kumfanya awe katika nafasi ya mtu anayejua athari ya kitu, lakini humwachia hiari ya kuchaguwa moja ya pande mbili, kwa hiyo mtu huwa ni mwenye hiari ya kuchaguwa katika matendo yake na kuingia katika utendaji wa kazi yoyote. Na endapo atafuata nasaha za Mola na mwongozo wake ataepukana na athari mbaya ambazo zingepatikana, mfano kuangamia na kuhasirika. Na endapo atamhalifu Mola na asifuate nasaha zake atakuwa amenasa kwenye mtego wa msongamano uliojificha ndani ya kitendo chenyewe. Ili kuliweka hilo wazi tunaleta mfano: Kwa kweli tabibu au daktari, aelezapo dawa kwa mgonjwa na kumpa amri ya kutumia ile dawa, na kujiepusha na mambo mengine ( yawezayo kuiziwia dawa isiwe na athari yake), endapo mgonjwa atamtii tabibu na kutekeleza amri yake, siha na afya itakuwa ndiyo athari ya utii na utekekelezaji wa amri ya tabibu, na endapo atahalifu amri ya tabibu na maelekezo yake haitokuwa ila ni kubakia na ugonjwa na kuzidi kwa mnyong’onyeo utokanao na hali hiyo kwa kuwa yule tabibu hakumuandikia kile cheti ila ni kwa kuwa yeye ni mtoa nasaha na muuguzi mwenye huruma. Mfano huo ni sawa na kauli yake (s.w.t.): “Mumtii Mwenyezi Mungu na mumtii Mtume� baada ya kuwaamuru watu kutekeleza wajibu na 6
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
12:29 PM
Page 7
Umaasumu wa Mitume
Sehemu ya pili
kuwakataza ya haramu, basi endapo mukallafu atahalifu akaacha kutekeleza wajibu kama swala na swaumu, na akatenda yaliyokatazwa kama kusema uongo na kusengenya, hapo atakuwa amehalifu amri mbili: 1-Amri ya Swala na Swaumu. 2 - Amri ya kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hivyo kutokana na kuhalifu huko atapata adhabu moja na si mbili, hiyo ni kwa sababu amri ya pili haikuwa amri ya lazima bali ilikuwa amri ya mwongozo tu ambayo kule kuihalifu hakulazimu ila lile linalolazimu uhalifu wa amri ya kwanza. Kwa kuwa mwamrishaji katika ile amri ya pili hakujiweka kwenye nafasi ya wajibu kutiiwa, bali ni amri katika vazi la nasaha na kutoa mwongozo tu. Ukijua hilo twasema: Kwa kweli kuhalifu katazo la kula mti uliokatazwa kutahesabika kuwa ni maasi kwa maana iliyo katika istilahi pale tu itakapo kuwa katazo hilo ni katazo la lazima limetoka kwake (s.w.t.) akiwa katika hali ile ya Bwana mtowa amri ambaye ni wajibu kutiiwa katika anayoyaamrisha, wala si itakapokuwa amri hiyo ni amari ya mwongozo iliokuja kwa sura ya nasaha. Na vielelezo vilivyopo katika Aya vinathibitisha kuwa ni amri ya mwongozo amabayo uhalifu wake hauambatani ila na athari za kibinadamu na za kimaumbile zinazoambatana na tendo lenyewe, wala si za kiungu hata nyuma ya matendo hayo kuwe na adhabu ya kuhalifu na kwa sababu ya kufanya maasi. Vifuatavyo ni vielelezo hivyo: i. Lau lingekuwa katazo la kula mti ni katazo la lazima (maulawiy) ambalo ni wajibu kutiiwa ingelazimu athari zake zitoweke baada ya toba na kurejea, ilihali sisi twaona athari zinazoambatana na uhalifu ule zilibakia katika hali yake japokuwa Adam alitubia na alirejea kwa Mwenyezi 7
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:29 PM
Page 8
Sehemu ya pili
Mungu(swt) . Na hii ni dalili ya kuwa kutoka nje ya Pepo na kukabiliwa na maisha ya mashaka na tabu, ilikuwa ni athari ya kimaumbile ya kitendo chenyewe, na katazo lilikuwa kwa ajili ya kumuhifadhi Adam dhidi ya athari hizi na matokeo yake, kama vile tabibu amkatazapo aliyepatwa na maradhi ya sukari asile vyakula vyenye sukari. ii. Kwa kweli Aya zilizokuja ndani ya sura Twaha zinaweka wazi aina ya katazo hili, na zasema waziwazi kuwa katazo lilikuwa la mwongozo tu ili kumuhifadhi Adam asikabiliwe na matokeo mabaya na athari zinazochukiza, na hatima isiyohimidiwa. Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amesema:
“Hivo tulisema: Ewe Adamu! hakika huyu ni adui yako na wa mke wako, hivyo asikutoeni bustanini mtaingia mashakani.* Hakika hautokuwa na njaa humo wala hautokuwa uchi. Na kwa hakika hautopata kiu humo wala hautopata joto.” (Twaha:117-119). Hakika kauli yake (s.w.t.): “Hivyo asikutoeni bustanini mtaingia mashakani.” inatamka wazi kuwa athari ya utekelezwaji wa katazo ni kubakia ndani ya Pepo na kupata maisha ya furaha na ufanisi ambayo kielelezo chake kinapatikana katika kauli yake: “Hakika hautokuwa na njaa humo wala hautokuwa uchi. Na kwa hakika hautopata kiu humo wala hautopata joto.”. Na athari ya kuhalifu (katazo) ni kutoka nje ya Pepo na kuikabili tabu ambayo kielelezo chake kimo ndani ya maisha ambayo yana njaa, utupu, kiu na joto la Jua. Hayo yote yanabainisha kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) alipokuwa anakataza hakujiweka nafasi ya mkatazaji ambaye kumtii ni wajibu, bali alikuwa anakataza akiwa mtoa mwongozo, mnasihi na mtoa mwanga, na endapo nasaha na mwongozo wake hutotekelezwa basi kutapatikana tabu, mchoko na ugumu ndani ya maisha. 8
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:29 PM
Page 9
Sehemu ya pili
iii. Baada ya Adamu na mkewe kuonja mti ule tupu zao zilidhihiri na wakawa wanajikusanyia majani ya miti iliyokuwa ndani ya Bustani, hapo Mwenyezi Mungu alinadi: “Je, sikuwakatazeni mti ule na sikuwaambieni kuwa kwa hakika ya Shetani kwenu ni adui aliye bayana?!” (Alaarafu:22 ) Kwa hakika hii ni lugha ya mtoa nasaha mwenye huruma ambaye amemwongoza anayemsemesha kwa ajili ya maslahi yake na maharibifu yake maishani, lakini yeye alipofanya kinyume na bila kumsikiliza kauli yake alimrudia na kumsemesha kwa kauli yake: “Je! Sikukwambia… Sikukukataza jambo hili…?” iv. Kwa hakika yeye (s.w.t.) anabainisha kuwa wasiwasi wa Shetani kwao haukuwa ila ni kwa ajili ya kudhihirisha tupu zao zilizositirika, kwani anasema: “Basi shetani aliwatia wasiwasi ili kuwafichulia tupu zao walizofichiwa” (al-Aarafu:20). Hii yafichua kuwa matokeo ya wasiwasi, na baada yake Adam kuhalifu, hayakuwa ila ni kudhihiri na kuonekana kilichositirika kwao ambacho ni tupu, na hilo ni athari ya kimaumbile ya kitendo bila ya kuwa na athari yake nyingine, ile ya kuwa mbali na rehema yake (s.w.t.), na kunyimwa ukaribu na yeye, vitu ambavyo ndio athari ya kuhalifu maagizo ya lazima (yasiyokuwa ya nasaha). v. Kwa hakika yeye (s.w.t.) anaelezea kuwa wasiwasi wa Shetani kwao ulikuwa kwa sura ya nasaha na mwongozo pindi aliposema: “Na aliwaapia: Hakika mimi kwenu ni miongoni mwa watoao nasaha” (al-Aarafu; 7:21). Hii yafichua kuwa usemi wake (s.w.t) kwa wawili hawa Adamu na Hawa, nao ulikuwa kwa sura ya nasaha. Hili lipo wazi hata kwa mwenye kiwango cha chini mno cha kanuni za maneno. Vielelezo hivi na vinginevyo vilivyopo ndani ya Aya zilizokuja kuhusu kisa cha Adam waziwazi zajulisha kuwa katazo mahali hapa lilikuwa katazo la mwongozo tu si la lazima ambalo ni wajibu litiiwe, na lengo lilikuwa kumwepusha Adam ili awe mbali na sababu zisababishazo taabu na unyonge, lakini yeye hakusikiliza kauli ya mnasihi wake hivyo basi akaiingiza nafsi yake kwenye tabu, na akastahiki kuambiwa na Mwenyezi Mungu: 9
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:29 PM
Page 10
Sehemu ya pili
“Alisema: Teremkeni baadhi yenu ni maadui kwa wegine na mtakuwa na makazi ardhini na mtakuwa na njia ya maisha kwa muda.” ( alAarafu:24 ). Na alisema (s.w.t.):
“Ali sema:Teremkeni kutoka humo nyote baadhi yenu ni maadui kwa baadhi” (Twaha:123 ). Zaidi ya hayo ni kuwa hali ambayo alikabiliwa Adam na katazo hili (katazo la kula mti) haikuwa hali ya taklifu kiasi kwamba kuhalifu kwake kuhesabiwe kuwa ni maasi ya muktadha wake, kwani hali ya taklifu ni ndani ya mazingira yale aliyoteremka humo Adam na mkewe baada ya kukataa nasaha, ama mazingira yale – katika Pepo - yalikuwa yameandaliwa ili kumuelewesha mtu maadui zake na marafiki zake, na ni hatua yake ya kujielimisha kwa kushuhudia matokeo ya utii na athari za uhalifu. Yaani atambue matunda ya kukubali kauli yake (s.w.t.) ambayo ni ufanisi, na atambue matunda ya kuikubali kauli ya Ibilisi ambayo ni tabu. Katika mazingira kama yale katazo wala amri havihesabiki kuwa ni taklifu bali uhesabika kuwa ni njia ya kujielimisha na kupata utayarifu wa kubeba taklifu hapo baadaye. Kipindi kile cha maisha kilikuwa ni hatua ya maandalizi kwa baba wa wanadamu na mama yao ili auguse ukweli kwa mguso wa mkono. Raziy amesema ndani ya kitabu ‘Ismatul-Anbiyai’ alipoelezea utata kuhusu ismah ya Adam: “Tatu: Yeye alitenda lililokatazwa kulingana na kauli yake (s.w.t.): “Je! Sikuwakatazeni mti ule !” na kauli yake (s.w.t.): “wala musiukaribiye 10
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
12:29 PM
Page 11
Umaasumu wa Mitume
Sehemu ya pili
mti huu”, na kutenda lililokatazwa na dini ni dhambi”1. Akasema sehemu ya jibu: “Ama tatu: Jibu twasema: Hatukubali kuwa katazo ni kwa ajili ya uharamu tu, bali huwa lina maana mbili za ushirika kati ya uharamu na ubora. Na tafsiri yake ni kwamba katazo huwa lamaanisha upande wa kuacha wenye uzito kuliko upande wa kutenda. Ama upande wa kutenda, je! walazimu kustahiki adhabu au haulazimu? Hilo liko nje ya ufahamu utokanao na tamko, hali ikiwa hivyo basi haifai kutolea dalili. (kuwa katenda kinyume na katazo kwastahiki adhabu).” 2 Mpaka hapa limetimia jibu la swali la kwanza isipokuwa tu kuna jibu lingine wafasiri wengi wamelisema, na sisi twalisema kwa ufupi. Jibu lingine la ishkali hii: Kwa kweli wafasiri walio wengi miongoni mwa al-Adliyah wamechaguwa kuwa kuhalifu kwa Adam kulikuwa ni kuhalifu katazo la Mola lisilo la lazima nalo ni lile linaloitwa: “Kuacha lililo bora na kuacha lililo afadhali”. Ama kule kuliita kuwa ni maasi na vinginevyo miongoni mwa maneno yanayotia shaka katika suala hili, kwa muhtasari wanasema: Dhambi inagawanyika sehemu mbili. i. Dhambi ya moja kwa moja, ii. Dhambi inayotegemea hali fulani. Dhambi ya moja kwa moja ni tendo la kuhalifu irada ya katashauri ya lazima ya Mola mwenye hekima, bila ya tofauti kati ya mtu na mtu. Hivyo basi atakayemhalifu huwa ni mwasi bila kuwepo tofauti kati ya mtu na mtu. Dhambi inayotegemea hali fulani ni ile inayohesabika kuwa ni dhambi na jambo lisilo sawa kulingana na hali ya mtu na mtu. Yaani kitendo chenyewe kama kilivyo huwa ni halali na ni jambo linaloruhusiwa na ni 1. Ismatul-Anbiyai,Uk 25. chapa ya Jedah. 2. Ismatul-Anbiyai, Uk 27.chapa ya Jedah.
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:29 PM
Page 12
Sehemu ya pili
kitendo kinachofaa kisichokuwa kibaya, isipokuwa tu jamii inaona ni vibaya kitendo hicho kutendwa na mtu wa aina fulani, na inazingatia kuwa ni jambo lisilofaa kutendwa na mtu kama huyu, na si sahihi kutendwa na yeye na watu mfano wake. Na mifano yake ni kama ifuatavyo: Kwa kweli msaada wa mali ulio mdogo mno autowao mtu anayemiliki mamilioni ya shilingi, japokuwa waruhusiwa lakini wachochea hisia za tuhuma dhidi ya aliyetoa japokuwa yeye hajatenda tendo ovu. Kama ambavyo kusali sala bila ya kuelekeza moyo na bila ya unyeyekevu kunaepusha dhima na kunamuondolea mtu taklifu,-yaani anahesabika ameswali -isipokwa tu akiswali katika sura hiyo mtu kama Nabii (s.a) bila shaka hali hiyo itahesabika kuwa ni jambo lisilolingana na nafasi yake na lisilotazamiwa kwa mtu kama yeye. Kwa hiyo uzito wa kula mti uliokatazwa ni uzito wa watu wakubwa wenye heshma kutenda baadhi ya matendo yaliyo halali yanayoruhusiwa kiasili. Na kwa ibara iliyo wazi zaidi kuliko hiyo ni kuwa: Tukitambuwa kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) alimuenzi Adam kwa kumfundisha majina na kumfanya mwalimu wa Malaika na aliwaamuru wasujudu kwa heshima yake, na kutokana na hali kama hiyo Mwenyezi Mungu (s.w.t.) alimtaka (Adam) aache kula mti maalumu, (sio kwa lazima) baada ya kuwa alikwisha mruhusu kula kwa marefu na mapana vilivyomo ndani ya Pepo isipokuwa huu mti mahsusi, hivyo basi jambo lililokuwa linatazamiwa kwa mtu wa mfano wake ni aache aina yoyote ya kufanya kinyume, japo kwa kiwango kidogo ingawaje agizo na katazo si la lazima, kwa minajili hiyo tendo hili kwa kuzingatia sharti zilizomzunguka, lahesabika ni la maasi lahitajia toba. Jibu la tatu kuhusu ishkali hii: Jibu la tatu ni hilo hapa: Nalo ni kiini cha mjadala kwa wanatheiolojia katika suala la ismah ya manabii, maana yake ni mtu mukallafu kufanya kinyume na taklifu ya kiungu baada ya kuwekwa sheria na kuteremshwa vitabu. Na endapo hiki ndio kipimo basi haikuthibiti dhambi katika kisa 12
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
12:29 PM
Page 13
Umaasumu wa Mitume
Sehemu ya pili
cha Adam kwa sababu mazingira aliyoishi baba wa wanadamu kabla haja teremka ardhini, hayakuwa mahali pa sheria na taklifu wala hapakuwa na sheria yeyote. Hivyo kuhalifu katika mazingira haya hakuhesabiki kuwa kwatanguwa ismah. Baadhi ya maneno hayo yametangulia mwishoni mwa jibu la kwanza. Al-Fakhru Raziy amesema ndani ya tafsiri yake akiwa katika hali ya kutoa jibu la kupinga utata uliojitokeza kuhusu kisa cha Adam: “Jibu linalotegemewa kutokana na mitizamo saba ni useme: Maneno yenu yatakuwa timamu pale tu lau mungeleta dalili ya kuwa hilo lilikuwa katika hali ya unabii. Na hilo lazuwilika, basi ni kwa nini usiseme kuwa: Adam hakuwa Nabii pindi telezo lilipomtokea, na baada ya hipo ndipo akawa Nabii” 3 Hii ni ikiwa anakusudia unabii ni taklifu, ama ikiwa kusudio ni kufaa kutokea maasi kwa manabii kabla ya unabii, hili tumekwishathibitisha kubatilika kwake kama ulivyokwishatambua. Mpaka hapa imebainika kuwa uhalifu wa Adam dhidi ya katazo lake (s.w.t.) hakupingani na ismah yake, na umekwishayatambua majibu matatu, hivyo basi wakati umetimia wa kutafiti baadhi ya ufahamu uliyotokana na Aya ambazo zimetangulia kwako, na huenda baadhi ya hizo Aya zikahesabika kuwa ni dalili ya kuwa kuhalifu kwa Adam kulikuwa dhambi ya kisheria, kwa ajili hiyo ni wajibu juu yetu kuweka wazi ufahamu huu uliokuja katika kisa hiki. 1 -Nini maana ya wasiwasi wa Shetani kwa Adam? Ukweli wa swali hili warejea kwenye maana dhahiri ya Aya zilizopita nayo ni kuathiri Shetani katika nafsi ya Adam kwa kuingiza wasiwasi, Mwenyezi Mungu amesema:
“Hivyo shetani aliwatia wasi wasi .”(al-Aarafu; 7:20). 3. Tafsiru ya Fakhru Raaziy Jalada 1.Uk 221. 13
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:29 PM
Page 14
Sehemu ya pili
Na amesema Mwenyezi Mungu:
“Basi shetani akamtia wasi wasi, (Twaha :120) Hapo sasa hujiuliza: Kwa kweli kumwingiya wasiwasi Adam kutoka kwa Shetani yawezekana vipi kukutane na aliyoyaeleza Mwenyezi Mungu kuwa Shetani hawezi kuwa na mamlaka juu ya waja wa Mwenyezi Mungu wenye ikhlasi pale aliposema:
“Hakika waja wangu, wewe hutakuwa na mamlaka juu yao, isipokuwa yule mwenye kukufuata katika wapotovu.” “(Al-hajar:42 ). Na amesema akielezea kauli ya Ibilisi:
“Basi naapa kwa enzi yako nitawapoteza wote isipokuwa waja wako miongoni mwao ambao ni wenye ikhlasi walio takaswa.” (Swad:8283). Jibu: Kwa kweli makusudio ya wenye ikhlasi ni wale ambao Mwenyezi Mungu (s.w.t.) aliwachaguwa kati ya viumbe wake, Mwenyezi Mungu amesema akiashiria kundi la manabii:
“Hao ndio
aliowaneemesha Mwenyeezi Mungu, miongoni mwa 14
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
12:29 PM
Umaasumu wa Mitume
Page 15
Sehemu ya pili
Manabii, katika kizazi cha Adamu, na katika ambao tuliowachukua pamoja na Nuhu, na katika kizazi cha Ibrahim na Israeli, na katika ambao tuliowaongoza na kuwachagua.” (Mariyam; 19:58). Na amesema (s.w.t.) akiashiria kundi la manabii:
“Na miongoni mwa baba zao na vizazi vyao na ndugu zao na tuliwachaguwa na tuliwaongoza kwenye njia iliyonyooka.”(al-An’aam :87). Ikiwa wenye ikhlasi ni wale aliowachaguwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kwa aina fulani ya uchaguzi, basi Adam siku aliyofanya kinyume na katazo hakuwa miongoni mwa waliochaguliwa isipokuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) alimchaguwa baada ya tukio, amesema (s.w.t.):
“Adam alimuasi Mola wake akapotea kisha Mola wake alimchaguwa na alirejea kwake na akamwongoza.”(Twaha:121-122) Kutokana na hali hiyo wasiwasi wa Shetani kwa Adam hauwi kinyume na alilosema Mwenyezi Mungu kuwahusu waliochaguliwa, na kwa hakika Shetani hana hisa kwa wale wateule wala hana njia ya kuwaendea wao. Zaidi ya hayo ni kuwa wasiwasi wa Shetani katika vifuwa vya watu huwa kwa sura ya kuingia nyoyoni mwao na kuwa na mamlaka juu yao kiasi cha kuwaathiri, na ya kwamba yeye alikuwa hawezi kuwapokonya hiari na uhuru, na hilo la kuwa wasiwasi huwa kwa sura ya kuingia laungwa mkono na tamko la (fii-katika) katika kauli yake (s.w.t.)
“Anatiya wasi wasi katika nyoyo za watu.” (Annasu :5). 15
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
12:29 PM
Page 16
Umaasumu wa Mitume
Sehemu ya pili
Ama wasiwasi wa Shetani kwa baba wa wanadamu Adam (a.s.) haukuwa kwa sura ya kuingia na kumtamalaki, hilo ni kutokana na ushahidi wa kuja kwa tamko (lahuma) au (ilayhima ) katika sura Al-Aarafu: 20 na Taha:120. Tofauti hii katika kutoa ibara inamaanisha tofauti iliyopo kati ya wasiwasi hizi mbili na kuwa, moja kati ya hizo mbili ipo katika hali ya kuingia ndani ya vifuwa, na nyingine iko katika hali ya ukaribu tu. Ama kauli yake (s.w.t.):
“Lakini shetani akawatelezesha wote wawili.” (al-Baqarah :36). Na kauli yake:
“Hivyo aliwafikisha (wote wawili) kwa udanganyifu, na walipouonja mti ule, tupu zao zikawadhihirikia” (Al-Aaraf: 22). Hazijulishi kuwa kitendo walichotenda ni maasi kwa maana iliyo katika istilahi. Ama ibara iliyokuja ndani ya Aya hiyo ni kwa sababu kitendo cha Adam hakikuambatana na maslahi bali kilikuwa kimeambatana na tabu na kuwa mbali na maisha ya ufanisi, hivyo basi kila atakayezikosa baraka hizi na masilahi yake yathibiti kwake kuwa ameteleza au “Hakika Shetani amewatelezesha kutoka mahali pao kwa kuwadanganya”. Na kwa ufupi ni kuwa: Taabiri hizi zakutana hali ya kuwa katazo ni la mwongozo sio la lazima au katazo ni la Mola la ubora la kujitakasa kama ilivyokubalika katika majibu mawili ya mwanzo. 2- Nini maana ya usemi wake: Alimuasi na akapotea? Huenda mpinzani akashikamana na matamko haya mawili, pale (s.w.t.) aliposema: “Adam alimuasi Mola wake na akapotea” lakini ndani ya 16
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:29 PM
Page 17
Sehemu ya pili
maneno haya mawili hakuna dalili ithibitishayo mtazamo wa mtowa dalili. Ama tamko Aliasi ingawaje katika istilahi ya latumika kwa maana ya dhambi na kuhalifu utashi katashauri wa lazima, lakini hiyo ni istilahi mahsusi kwa mweka sharia, Qur’an haijajiri na istilahi hiyo bali hata lugha ya kiarabu. Ambalo ni dhahiri katika Qur’an na kamusi za lugha ya kiarabu ni kwamba kuasi ni kinyume cha utii. Ibnu Mandhur amesema: “Kuasi ni kinyume na kutii. Mja amemuasi Mola wake: Hutumika endapo atamkhalifu Mola wake. Na fulani amemuasi amiri wake: Hutumika endapo hamtii. Kwa hiyo yatupasa tulichunguze jambo ambalo lililoachwa kutekelezwa katika hali hii, kwani kila amri ya Mola ambayo ni ya lazima, kuihalifu ni dhambi. Na endapo itakuwa amri ni ya mwongozo au katazo la ubora na utakaso, kuihalifu si dhambi katika istilahi. Kwa ajili hiyo si sahihi kushikamana na tamko hili na kuthibitisha kuwa Adam ametenda dhambi. Ama tamko la pili yaani Akapotea kwa kweli kitenzi Ghawa ndani ya kiarabu hutumika kwa maana ya kutofanikiwa, mshairi amesema: Fa man yalqa khayran yahmaduhu nnasu amrahu Waman yaghwi la yaadam alalghayi laiman Yaani: Mwenye kupata kheri watu hulihimidi jambo lake. Na mwenye kufeli hakosi katika kufeli kwake mtu wa kulaumu. Na katika Hadithi ya Musa na Adam: Aghwaita nnasa, yaani: Umewafelisha watu. Pia hutumika kwa maana ya kuharibikiwa, na maana hiyo ndio iliyotafsiriwa kwenye neno lake (s.w.t.): “Faaswa Adamu Rabbahu faghawaa” yaani: Adam amemuasi Mola wake na ameharibikiwa na maisha yake.4 Ukitambuwa hilo basi twasema: Kwa kweli makusudio ya ghayu katika Aya ni kufeli na kutofanikiwa kwa Adam na kupata kwake hasara na kukosa kwake maisha ya raha ambayo yalikuwa hayana kiu wala utupu, bali yaliyo kuwa mbali na kila aina ya usumbufu na tabu. Wala si kila aina ya kufeli na kutofanikiwa inayomkabili mtu hutokana na dhambi inayotu4. Lisanul-Arabi. Jalada 15. Uk. 140.
17
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:29 PM
Page 18
Sehemu ya pili
mika katika istilahi, kama ambavyo yawezekana makusudio yake ikawa ni kuharibikiwa, na kwa ajili hiyo ndio maana Ibnu Mandhuri Mmisri ameifasiri kauli yake (s.w.t.) ndani ya kamusi yake Lisanul-Arabi kuwa: “Adamu alimuasi Mola wake akaharibikiwa maisha yake”.5 Wala hapana shaka kuwa maisha ya ndani ya Pepo hayawezi kulinganishwa na maisha katika ulimwengu wa kimada ambao ni nyumba ya uharibifu na kutoweka. Ndiyo, hata ikikubalika kuwa neno Al-ghayu maana yake ni upotovu ambao ni kinyume na uongofu, lakini sio kila aina ya upotovu ni maasi, kwani mwenye kupotea njia ya kuchuma au njia ya kujielimisha yathibiti kuwa amepotea, lakini si lazima awe amefanya maasi. Bwana wetu Ustadh Alamah Tabatabaiy (radhi za Mwenyezi Mungu zimfikiye) alikuwa akisema kwenye kikao cha mafunzo yake kuwa: “Kwa hakika tamko ghawaa linamaanisha hali ambayo humpata mnyama mfano wa mbuzi na kondoo anapojitenga na kundi, hapo hubaki ameduwaa, ana angalia kulia kushoto huku akiwa hawezi kujichukulia njia yake binafsi, na Adam baba wa wanadamu aliduwaa baada ya kuhalifu katazo la Mola wake na alipatwa na mtihani bila kujua vipi atatatuwa tatizo lake na vipi atajinasua na zahama hii.” Kwa ujumla ni kuwa neno Al-ghayyu likusudiwapo kuwa mbali na njia iliyo sawa ya Tawhid, na kwenda kombo mbali na alichochorewa mwanadamu miongoni mwa mambo ya wajibu na ya haramu, hilo kuna wakati lalazimiana na kufuru, na wakati mwinge lalazimiana na dhambi, lakini sio kila aina ya upotovu- endapo itakuwa ghayyu maana yake ni upotovu - yalazimu kosa na dhambi, kwani mwenye kupotea njia na akatangatanga mbali na malengo yake ya kidunia au masilahi ambayo ni lazima ayapate, inathibiti kuwa yeye amepotea dhidi ya uongofu, lakini hiyo hailazimu maasi kwa mujibu wa istilahi. Hapana shaka kuwa Adam baada ya kula mti uliokatazwa kula, tupu yake 5. Lisanul-Arabi. Jalada 15. Uk. 140.
18
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:29 PM
Page 19
Sehemu ya pili
ilidhihirika na alitoka nje ya Pepo na aliteremkia kwenye nyumba ya ufisadi hapo basi alipotea njia yake na kupoteza masilahi yake. Kwa ujumla ni kuwa sura hizi tatu zilizotajwa kuhusu ghawaa zimedhoofisha juhudi za kuthibitisha maasi kupitia zenyewe. 3. Nini maana ya kauli ya Adam: Mola wetu! tumejidhulumu sisi wenyewe! Dhulma maana yake ni kuweka kitu mahali pasipokuwa pake, na katika methali za kiarabu: “Mwenye kumlanda baba yake hakudhulumu”. Asmaiy amesema: “Dhulma ni kukiweka kitu mahali pasipo pake. Na katika methali: “Mwenye kumwamini mhaini amedhulumu”. Na kwa ajili hiyo kwenda kombo na njia kwahesabika ni dhulma, husemwa: “Hawakuachana na njia hawakuidhulumu” yaani hawakupita kwenye kitu kingine mbali na njia.”6 Hivyo basi madamu maana ya dhulma ni kuweka kitu mahali pasipokuwa pake na kuvuka mpaka, hailazimu kila dhulma iwe dhambi, bali ndani ya maana zake yajumuisha kitu kingine, hivyo asiyesikiliza kauli ya mtoa nasaha mwenye huruma na akatenda kinyume na kauli yake atakuwa ameliweka tendo lake mahali pasipo pake. Kama ambavyo mwenye kuhalifu katazo la ubora na utakaso atakuwa amekwenda kombo mbali na njia iliyo sahihi. Na kwa ujumla ni kuwa: Kila aina ya uhalifu na upotofu mbali na njia iliyo sawa ni dhulma, sawa amri iliyoendewa kinyume iwe ni ya lazima au ya mwongozo tu, au vinginevyo. Zaidi ya hayo ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anaihesabu dhulma ya mtu kujidhulumu nafsi yake ni kitu mbali na tendo ovu, Mwenyezi Mungu asema:
“Na mwenye kutenda ovu na akaidhulumu nafsi yake, kisha akaomba msamaha kwa Mwenyeezi Mungu, atamkuta Mwenyeezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.” (Anisaa:4 - 110). 6. Lisanul-Arabi. Neno “Dhulma”.
19
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:29 PM
Page 20
Sehemu ya pili
Aya inaonyesha kuwa dhulma ya mtu binafsi huenda ikawa si tendo baya, kutokana na hali hiyo ni wazi kuwa kauli ya Adam: “Mola wetu! tumejidhulumu sisi wenyewe!” hailazimu kukiri dhambi, kwa sababu dhulma ya mtu kuidhulumu nafsi yake si tendo ovu. Hivyo suala la kwanza lalazimu kuishusha nafsi daraja yake wala halilazimu kukiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu. Hali hiyo ni kinyume na suala la pili ambalo ni tendo ovu, kwani tendo ovu ni kukiuka mipaka wa Mwenyezi Mungu; kwa hiyo yajulikana kuwa makusudio ya kauli yake (s.w.t.): “Wala msiukaribie mti huu msijekuwa miongoni mwa waliodhulumu.” (Al-Baqara: 35) ni dhulma ya mtu binafsi inayolazimu kuiteremsha nafsi daraja yake, kinyume na tendo ovu linalolazimu kukiuka mipaka yake (s.w.t.). 4. Nini makusudio ya kauli yake : Akamkubalia toba yake Toba maana yake ni kurejea ikinasibishwa na Mwenyezi Mungu humwendea mtendewa kwa kutumia neno Alaa, Mwenyezi Mungu amesema:
“Kwa hakika Mwenyezi Mungu alirejea na rehema kwa Nabii na muhajirina na answar ambao walimfuata wakati wa dhiki” (AtTawbah:117). Yaani, alireja kwa rehema juu yao. Na endapo itanasibishwa na mja basi humfikia mtendewa kwa kutumia neno Ilaa. Mwenyezi Mungu amesema:
“Basi rejeeni kwa Muumba wenu jiuweni wenyewe” (Baqrah:54) Na amesema (s.w.t.):
“Je hawatubu kwa Mwenyeezi Mungu na kumuomba msamaha? Na Mwenyeezi Mungu ni mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.” (AlMaida:74). 20
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:29 PM
Page 21
Sehemu ya pili
Ikiwa toba maana yake ni kurejea, basi inapomwedea mtendewa kwa tamko Alaa maana ya kauli yake (s.w.t.): “Na akamkubalia toba yake, hakika yeye ndiye apokeaye toba, Mwenye kurehemu.” (Al-Baqarah: 37) inakuwa ni: Mwenyezi Mungu amerejea kwao kwa rehema, kwani toba katika jumla hii ni toba kutoka kwa Mwenyezi Mungu juu ya mja, si toba kutoka kwa mja kumwendea Mwenyezi Mungu. Na maana ya kwanza ni kurejea kwake (s.w.t.) juu ya mja kwa huruma na rehema. Na mfano kama huo ni kauli yake (s.w.t.):
“Kisha Mola wake akamchagua na akamkubalia toba na akamwongoza.” (Taha:122). Kwa hiyo toba hapa ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu kumwendea mja wake, na maana ya Aya ni kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) alimchagua Adam ili ampe maneno na ombi lake, hapo Mwenyezi Mungu (s.w.t.) akawa amerejea kwake kwa rehema na akamwongoza na kumtoa kwenye hali ya kufeli kulikomfunika, na giza lililomzunguka kwa sababu ya kutosikiliza nasaha zake (s.w.t.), na kuitanguliza nasaha ya mwingine mbali na yake (s.w.t.). Naam kwa kweli tamko “Na akamkubalia toba” katika Sura mbili za (alBaqarah na Taha) lajulisha kuwa Adam alitubu kwa Mola wake na kwa sababu ya toba yake kwa Mwenyezi Mungu na kurejea kwake kwa majuto, Mwenyezi Mungu alimkubalia toba, yaani alirejea kwake kwa rehema na mwongozo. Lakini hakuna dalili kuwa kila toba na kurejea kwa Mwenyezi Mungu kwajulisha kuwa alitenda dhambi, hususan tukiangalia tuliyotanguliza katika tafsiri ya pili kuhusu kuhalifu kwa Adam, tulisema kuwa tendo hilohilo laweza kuwa linafaa na laruhusiwa lakini likitendwa na baadhi ya watu wenye sifa fulani huwa ni baya na huangaliwa kuwa ni kitendo kisicho sawa.
21
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:29 PM
Page 22
Sehemu ya pili
Hivyo kurejea kwa watu wa aina hiyo kwa Mwenyezi Mungu katika hali kama hiyo si dalili ya kutokea dhambi upande wao, bali kwahesabika kuwa ni dalili ya wasaa wa elimu yao kuihusu utukufu wa Mola, na kwa ajili hiyo husemwa: “Mazuri ya watu wema ni maovu ya watu walio karibu.” Na amesema Nabii (s.a.w.w.) “Kwa hakika amesitiri moyo wangu na mimi namwomba maghfira Mwenyezi Mungu kila siku mara sabini.”7 Na wala istighfaru hizi si dalili ya kutokea dhambi, bali ni dalili ya wasaa wa elimu yake na undani wa utambuzi wake wa utukufu wa Mwenyezi Mungu (s.w.t.). 5. Nini maana ya ghufurani katika kauli yake: Kama hutotughofiria Hapa kumebaki neno moja nalo ni kuifafanuwa kauli yake (s.w.t.) nayo ni: “Na kama hutotughofiria na kutuhurumia kwa kweli tutakuwa miongoni mwa wenye hasara”. Huenda kwa mtizamo wa haraka haraka ikaingia akilini kuwa kipande hiki cha Aya chamaanisha kutokea dhambi upande wa baba yetu Adam, amani ya Mwenyezi Mungu imfikiye. Basi twasema: Hakuna dalili humo wala katika moja ya maneno yake inayothibitisha yale ayakusudiayo hasimu. Ufuatao ni ufafanuzi kuhusu lengo la Aya na maana ya maneno yake: Ama kuhusu neno Ghufrani asili yake ni Alghafru likiwa na maana ya kufunika na kusitiri, husemwa ndani ya kiarabu: ghafarahu, yaghfiruhu: Yaani amesitiri. Na kila ambacho umekisitiri basi umekighofiri, hivyo basi maadamu ghufranu maana yake ni kusitiri kwa hiyo hakuna ulazimiano kati ya kusitiri na dhambi, kwani kinachositiriwa chaweza kuwa dhambi au chaweza kuwa jambo linalofaa lisilotarajiwa kutendwa na mtu fulani, na kwa sababu hiyo Adam alimuomba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kulingana na mwenendo wa mawalii na watu wema katika kudogesha mambo mema wayatendayo na kukuza kwao kitu kidogo miongoni mwa aibu. 7. Sahih Muslim Jalada.8. Uk. 72. chapa ya 1993 A.D Beirut-Lebanon.
22
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:29 PM
Page 23
Sehemu ya pili
kitu hali wao wameumbwa? * Na wala hawawezi kuwanusuru, wala hawawezi kujinusuru wenyewe.”(Al-Aaraf:189 - 192) kuwa ni dalili ya Adam kutokuwa na ismah. Wanaokosoa ismah ya manabii wametoa dalili kutumia kauli yake (s.w.t.): “Basi anapowapa mwema, wanamuwekea washirika” kuwa wakilishi cha watu wawili sehemu zote mbili charejea kwa Adam na Hawaa ambao wameashiriwa mwanzoni mwa Aya kwa kauli yake (s.w.t.): “Katika nafsi moja na katika hiyo ameumba mwenzake”. Lakini kutumia Aya hii kama dalili msingi wake ni kauli isemayo kuwa makusudio ya “Katika nafsi moja” ni umoja wa mtu mmoja mmoja, na si umoja wa aina, yaani jenasi. Ili kuliweka wazi hilo ni kuwa hakika tamko hilo limetumika ndani ya Qur’an Tukufu kwa sura mbili: Ya kwanza: Ile inayokusudiwa umoja wa mtu mmoja mmoja, mfano wa kauli yake (s.w.t.):
“Oh! Ninyi watu! Mcheni Mola wenu ambaye amekuumbeni katika nafsi moja na ameumba kutokana nayo mke wake na ametawanya kutokana na wawili hao wanaume wengi na wanawake…” (An’nisaa:1). Kwa hiyo makusudio ya “katika nafsi moja” ni Adam na maana ya kumuumba mke kutokana naye ni kule kuwa katika jinsi yake. Na dalili ya kuwa makusudio ni umoja wa mtu mmoja mmoja ni ile kauli yake: “Na ametawanya kutokana na wawili hao wanaume wengi na wanawake”. Maana yake ni kuwa (s.w.t.) amewaumba viumbe kutokana na baba mmoja na mama mmoja, kwa hiyo hili kundi pamoja na wingi wake lakini lote 23
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:29 PM
Page 24
Sehemu ya pili
Hivyo akasema: “Kama hutotughofiria” yaani endapo hautotusitiri aibu yetu na “Kutuhurumia” yaani endapo hautorejea kwetu na rehema, tutakuwa miongoni mwa wenye hasara. Bila shaka Adam alipata hasara ya neema ambayo ilikuwa humo kwa kule kutofuata kwake nasaha za Mwenyezi Mungu (s.w.t.), kwa ajili hiyo alianza kumuomba arejee kwake kwa maghfira, yaani amsitiri aibu yake kwa rehema, yaani kwa kumtowa kwenye hasara iliyomkabili. Ukijua tulilolisema kuhusu Aya hizi na jumla na ukizizingatia kwa umakini na kwa kina itakudhihirikia kuwa kuitumia Aya hiyo kama dalili juu ya kutokea dhambi ya kiistilahi kwa Adam ni miongoni mwa matumizi ya dalili za kustaajabisha na za kushangaza. Wala haitomuia sahihi kwa mtafiti yeyote kuifasiri Aya bila msaada wa Aya nyingine katika ufahamu wake. Kwa hiyo inakuwa wazi kuwa njia tuliyoitumia katika kuitafsiri Qur’an ni njia sahihi ambayo inaondoa pazia kutoka kwenye nyuso za uhalisia ambao yawezekana ukawa umefichikana kwa watafiti walio wengi. Njia hii ndio njia ifaayo kukitafsiri kitabu cha Mwenyezi Mwenyezi Mungu kwa kukusanya Aya kadhaa zilizokuja kuihusu maudhui moja na kuzilinganisha zenyewe kwa zenyewe. Ismah ya Adamu dhidi ya kumfanyia Mwenyezi Mungu mshirika! Umeufahamu utata mkubwa kabisa wa mkosoaji manabii, kama ulivyofahamu jibu lake, hivyo basi njoo pamoja na mimi ili tudurusu utata wao mwigine ambao wameufanya kisingizio cha fikra zao mbovu pale walipo tumia kauli yake (s.w.t.): “Yeye ndiye aliyekuumbeni katika nafsi moja na katika hiyo ameumba mwenzake ili apate utulivu kwake. Na anapomwingilia hushika mimba nyepesi na kutembea nayo, anapokuwa mja mzito wakamuomba Mwenyezi Mungu, Mola wao: Kama ukitupa mwema, bila shaka tutakuwa miongoni mwa wanaoshukuru. * Basi anapowapa mwema, wanamuwekea washirika katika kile alichowapa, ametukuka Mwenyezi Mungu dhidi ya yale wanayomshirikisha. * Je! wanamshirikisha na wale ambao hawaumbi 24
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:29 PM
Page 25
Sehemu ya pili
lakomea kwao hawa wawili. Na mfano wa kauli hiyo ni kauli yake (s.w.t.):
“Oh! Ninyi watu! Hakika sisi tumewaumbeni kutoka mtu mwanaume na mwanamke na tumekufanyeni mataifa na makabila ili mtambuane…” (Al-Hujurati:13). Pili: Iliyokusudiwa umoja wa aina yaani jenasi, yaani baba wa kila mtu, na mama hivyo hivyo, mfano wake ni kauli yake:
“Amekuumbeni katika nafsi moja, kisha akamfanya mweziwe katika jinsi yake, na akakuumbieni wanyama, wanane madume na majike. Anakuumbeni tumboni mwa mama zenu umbo baada ya umbo katika giza tatu. Huyo ndiye Mwenyeezi Mungu Mola wenu, Ufalme ni wake hakuna aabudiwaye ila Yeye tu, basi nyinyi mnageuzwa wapi?” (AzZumar:6). Hivyo basi makusudio ya “Katika nafsi moja” ni umoja wa aina, na makusudio ni kila mmoja kati yetu amezaliwa kutoka baba mmoja na mama mmoja. Dalili ili kuthibitisha hilo ni kauli yake (s.w.t.): “Anakuumbeni tumboni mwa mama zenu umbo baada ya umbo katika giza tatu”. Na mfano wake mwingine ni Aya hii inayojadiliwa hapa, kwani makusudio si Adam mwenyewe baba wa wanadamu bali makusudio ni baba wa 25
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:29 PM
Page 26
Sehemu ya pili
kila mtu na mama yake, kwa hiyo jinsia mbili hizi zikisogeleana mtoto huzaliwa kutokana nazo, na maana tuliyoichaguwa inajulishwa na vielekezi vilivyomo ndani ya Aya zenyewe. Kielekezi cha kwanza: Kwa kweli Aya imekuja katika jumla ya Aya zinazoelezea ahadi ambayo mwanadamu alimpa Mola wake chini ya masharti makhsusi, lakini yeye alipopata neema na raha akaanza kuitanguwa ahadi hii, na hii ni tabia ya mwanadamu aliyeandaliwa kwa silika ya matamanio, hilo linaelekezwa na kauli Yake (s.w.t.).
“Na tunapomneemesha mwanadamu, hugeuka na kujitenga upande, na inapomgusa shari huomba sana.� (Fuswilat; 41:51). Ikiwa hii ndiyo tabia ya mwanadamu basi si vigumu kumuomba Mwenyezi Mungu amruzuku mtoto mwema, na ampe ahadi ya kumshukuru kwa ajili ya neema hiyo, lakini yeye aipatapo neema amfanyie Mwenyezi Mungu washirika kwa alichompa. Kwa mujibu huo Aya hii imekuja ujio wa mfano uliotolewa kwa wanadamu kuhusu uvunjaji wao wa ahadi yao waliyoithibitisha. Na dalili ya kuwa Aya imekuja katika nyanja hizo, ni yale yaliyokuja kabla ya Aya hii kuhusu kisa cha ahadi ambayo mwanadamu amempa Mola wake, lakini yeye baada ya hapo aliitenguwa, Mwenyezi Mungu (s.w.t.) alisema kabla ya Aya hii kuhusu Aya ya ahadi:
26
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:29 PM
Page 27
Sehemu ya pili
“Pale Mola wako alipochukuwa kutoka kwa watoto wa Adam-kutoka viunoni mwao-dhuria zao, na aliwashahidisha wenyewe. Je, siko Mola wenu! Wakasema: Ndiyo tume shuhudia. Musije mukasema siku ya Kiyama: Kuwa sisi tulikuwa tumeghafilika na haya, au musije mukasema: Baba zetu kabla yetu walifanya ushirikina sisi ni kizazi baada yao Je! Watuhilikisha kwa sababu ya waliyotenda wabatilifu!� (Al-aarafu:172-173). Ahadi iliyoelezwa ndani ya Aya tunayoizungumzia imeegemezwa kwenye ahadi ile ambayo imekuja katika Aya mbili katika suratil Aarafu, na hii ni dalili iliyo wazi kuwa makusudio ni kuiarifisha tabia ya mwanadamu na kuisifu kuwa yaweka ahadi kwanza, na kutanguwa pili, wala makusudio si kubainisha hali ya mwanadamu mmoja peke yake, yaani baba yetu Adam. Kielekezi cha pili: Muktadha wa Aya na lugha yake vyatufahamisha kuwa mtu ambaye alimuomba Mwenyezi Mungu amruzuku mtoto mwema alikuwa anaishi katika mazingira yaliyokuwa na mababa na watoto walio wema na walio waovu, aliwaangalia akatamani Mwenyezi Mungu amruzuku mtoto mwema kulingana na alivyoona, lakini Mwenyezi Mungu alipomruzuku mtoto yule mwema, aliitanguwa ahadi yake; yaani ya kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumruzuku watoto wema. Na hili halithibiti katika hali ya baba yetu Adam na mama yetu Hawa, kwani katika mazingira yao 27
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:29 PM
Page 28
Sehemu ya pili
hapakuwa na mababa na watoto wema na wabaya kiasi cha kuwafanya wao watamani mtoto mfano wa wale ambao Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ali waruzuku watu wengine. Raziy amesema katika kitabu chake IsmatulAnbiyai: “Na jibu sahihi: Kwa kweli sisi hatukubali kuwa “Katika nafsi moja” katika Aya hii amekusudiwa Adam (a.s.), wala katika Aya hakuna linalojulisha hivyo.8 Kielekezi cha tatu: Ni kwamba mwisho wa Aya waziwazi wathibitisha kuwa yenyewe haina mafungamano na mteule wa Mwenyezi Mungu Adam, hiyo ni kwa sababu Yeye (s.w.t.) asema mwishoni mwake: “Ametukuka Mwenyezi Mungu dhidi ya yale wanayomshirikisha”. Lau ingekuwa makusudio ya nafsina mkewe katika Aya ni watu wawili maalumu, kama vile Adam na Hawa basi ingefaa aseme: “Ametukuka Mwenyezi Mungu dhidi ya yale wanayomshirikisha wawili hawa” Na hii ni kinyume na ilivyokusudiwa nafsi na mkewe, bali kilichokusudiwa ni tabia ya uwanadamu wa pande mbili mwanaume na mwanamke, katika hali hiyo yafaa kutumia uwingi kwa sababu ya kukithiri kwa mifano yake. Kielekezi cha nne: Kwa kweli yeye (s.w.t.) anasema: “Je! wanamshirikisha na wale ambao hawaumbi kitu hali wao wameumbwa? * Na wala hawawezi kuwanusuru, wala hawawezi kujinusuru wenyewe.” Ni maarufu kuwa makusudio ya kushirikisha ni kushirikisha katika ibada, na Adam mteule wa Mwenyezi Mungu yumbali na uwezekano wa kuwa mshirikina katika ibada, vipi awe mshirikina hali Mwenyezi Mungu ameeleza kumhusu Adam kuwa ni mwenye kuchaguliwa, aliposema:
“Kisha Mola wake alimchagua na alimkubalia toba na alimuongoza.” (Taha: 122). 8. Ismatul-Anbiyai Uk. 29. Chapa ya Jidah.
28
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:29 PM
Page 29
Sehemu ya pili
Na amesema (s.w.t.):
“Ambaye Mwenyeezi Mungu anamuongoza, ndiye muongofu. (AlIsrau: 97). Na amesema (s.w.t.):
“Ambaye Mwenyeezi Mungu anamuongoza hakuna awezaye kumpoteza.” (Az-Zumar:37). Na amesema pia:
“Nani mpotovu zaidi kuliko anayemuomba asiyekuwa Mwenyezi Mungu ambaye hatoweza kumjibu mpaka siku ya Kiyama.” (AlAhqafu:5 ). Hizi Aya zote kwa wazi kabisa ni ushahidi kwamba Aya inalenga kukitaja kisa katika njia ya kutoa mfano na kubainisha kuwa hali ni sura inayowajumuisha watu wote katika wanadamu isipokuwa mwenye kujiokoa kwa imani, kama kwamba Mwenyezi Mungu anasema: Yeye ndiye ambaye amemuumba kila mmoja miongoni mwenu katika nafsi moja na amemuumba mkewe katika jinsi ya nafsi yake, mtu anayelingana naye katika ubinadamu, na mume alipomuinglia mke na kujitokeza mimba walimuomba Mola wao Mwenyezi Mungu endapo atawapa mtoto mwema aliyeumbika sawa watakuwa miongoni mwa wenye kushukuru neema zake, lakini Mwenyezi Mungu alipowapa mtoto mwema aliye sawa mke na mume walimfanyia Mwenyezi Mungu mshirika kwa mtoto aliyewapa. 29
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:29 PM
Page 30
Sehemu ya pili
Mara walimuhusisha na mada kama wasemavyo Dahria, na mara nyingine walimuhusisha na nyota kama ilivyo kauli ya wanajimu, na tatu walimuhusisha na sanamu kama ilivyo kauli ya waabudia sanamu. Hapo ndipo Mwenyezi Mungu akatoa jibu la kukanusha dhana hizo kwa kauli yake: “Ametukuka Mwenyezi Mungu dhidi ya yale wanayomshirikisha”.9 Kutokana na tuliyoyasema yawezekana ikawa makusudio ya ushirikina ni ushirikina katika kuendesha mambo na mfano wa hili haliwezi kuhusishwa na ambaye yuko chini ya manabii na mawalii kidaraja, basi itakuwaje ahusishwe nalo ambaye ni mteule wa Mwenyezi Mungu Adam (a.s.)! Na la mbali zaidi ambalo laweza kusemwa ni kwamba makusudio ya Nafsi moja na mkewe mwanzoni mwa Aya ni Adam na Hawa watu wawili, lakini Yeye (s.w.t.) alipofikia kauli yake: “Ili apate utulivu kwake” aligeuka na kuacha kuelezea watu wawili hawa na kuelekeza usemi wake kwa kila aliye mwanaume na mwanamke kuwahusu watoto wao au kuwahusu washirikina kutoka kizazi chao wawili hawa, hivyo basi maneno yatakadiriwa hivi “Alipomuingilia” yaani mume alipomuingilia mke katika kizazi chao hawa wawili “Mke alishika mimba nyepesi ...” mpaka mwisho wa Aya. Na hii huitwa katika elimu ya maani iltifatu nayo ina mifano mingi ndani ya Quran Tukufu. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema:
9. Mafaatihul-Ghaib. Jalada.4. Uk 343.
30
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:29 PM
Page 31
Sehemu ya pili
“Yeye ndiye anayekuendesheni katika bara na bahari, hata mnapokuwa katika majahazi na yanakwenda nao kwa upepo mzuri na wakafurahi nao, mara upepo mkali unayafikia na mawimbi yanawajia kutoka kila upande, na wanaanza kufikira kwamba wametingwa, ndipo wanamuomba Mwenyezi Mungu kwa kumtakasia utii: Ukituokoa katika haya bila shaka tutakuwa miongoni mwa wenye kushukuru.” (Yunus: 22 ). Waona kuwa Yeye (s.w.t.) amewasemesha jamaa kuhusu kuwafanyia wepsi misafara ya bara na baharini, kisha amewafanya wasafiri wa baharini hususan kuwa wao wameumbwa katika nafsi moja na mkewe nao ni Adam na Hawa, halafu akaendelea na maneno mpaka akazungumzia vizazi vyote vya Adam. Aina hii ameinukuu Al-Murtaza ndani ya kitabu TanzihulAnbiyai kutoka kwa Abu Muslim Muhammad bin Bahri Al-Isfahaniy.10 Na laajabu sana ni lile la Raziy ndani ya kitabu chake Ismatul-Anbiyai kwani aina hizi amezinasibisha na udhaifu, na mara nyingine akazinasibisha na utenganishi wa muundo, kana kwamba hajaziona Iltifati zilizotajwa ndani ya elimu ya Maani. Amesema alipokuwa akiondoa utata wa shirki dhidi ya Adam na Hawa: “Bali tunasema: Wanaambiwa makurayshi nao ni kizazi cha Qusway. Maana yake ni kuwa amekuumbeni katika nafsi ya Qusway na akaweka mke wake mwarabu mkurayshi katika jinsi yake ili apate utulivu. Basi alipowapa mwana mwema waliomuomba waliwapa watoto wao wanne majina ya Abdu Manafi “Mja wa Manafi”, Abdul-Uzza “Mja wa Uzza”, Abdu Qusway “Mja wa Qusway” na Abdu Dari “Mja wa Dari. Na kuwa nomino iliyopo kwenye kitenzi “Wanamshirikisha” inawaashiria wao wawili na vizazi vyao. Pia wametaja aina nyingine isiyokuwa hiyo na zote ni batili kwa sababu zifuatazo: Ya kwanza: Kuwa nomino zote zamuhusu Adam na Hawa, isipokuwa katika “Wanamuwekea” na “Wanamshirikisha” kwani hizi mbili zarejea kwa kizazi chao hawa wawili, na kadirio la maneno linakuwa: Mwenyezi 10. Tanzihul-Anbiyai, Uk 16.
31
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
12:29 PM
Page 32
Umaasumu wa Mitume
Sehemu ya pili
Mungu alipompa mtoto mwema Adam na Hawa waliyemuomba, makafiri katika watoto wao waliegemeza kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu, na sababu ya kutajwa wawili ni kwa kuwa wao ni jinsia mbili ya kiume na kike. Taawili hii yatiliwa nguvu na kauli yake: “Ametukuka Mwenyezi Mungu dhidi ya yale wanayomshirikisha”. na hilo lajulisha kuwa makusudio ya uwili ni lile tulilolitaja ambalo ni jinsia mbili. Ya pili yake: Ni kuwa kauli yake “Katika nafsi moja” ni Adam na amemuumba katika nafsi ile mke wake, naye ni Hawa, mpaka hapa yanakoma mazungumzo ya Adam na Hawa. Kisha aliwataja washirikina hususan miongoni mwa watoto wa Adam ambao waliomba waliloliomba na wakamwekea washiriki. Na yafaa kutaja kwa sura ya jumla kisha kutaja baadhi ya waliotajwa kwa sura mahsusi. Na mifano kama hiyo ni mingi katika maneno. Mwenyezi Mungu Mtukfu anasema: “Yeye ndiye anayekuendesheni katika bara na bahari, hata mnapokuwa katika majahazi na yanakwenda nao kwa upepo mzuri” (Yunus:22). Mwanzoni mwa Aya amejumuisha viumbe wote, kisha mwishoni akahusisha baadhi yao, na ndivyo ilivyo hapa. Jua kuwa mpingano huu kinaya zinazofuatana baada ya moja iliyotajwa peke yake baadhi yake huelekeza kwenye ile moja iliyotajwa na nyingine huelekeza kwenye kitu kingine, na hali hiyo huvuruga muundo”11. Twasema: Hii ni Iltifatu na wala sio kuvuruga muundo. Na amesma ndani ya sherhe ya kitabu Al-mawaqif katika kuwajibu walioshikilia Aya hiyo ili kuitolea dalili kuthibitisha dhambi ya Adam: “Na wala nomino katika kitenzi wanamuwekea sio ya Adam na Hawa, na hata kama itasihihi kuwa ni ya Adam (na mkewe) basi iko wapi dalili ya ushirikina katika uungu na kitendo chake (yaani huenda ushirikina uliyo tajwa katika Aya,) ikawa ni kuelemea kumtii shetani na kukubali wasiwasi wake pamoja na kujirudi kutokana naye na kuelekea kwa Mwenyezi 11. Ismatul-Anbiyai, Uk 29 - 30. Chapa ya Jidah.
32
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:29 PM
Page 33
Sehemu ya pili
Mungu Mtukufu (bila ya kumfuata shetani katika kitendo) na huo (mwelemeo unaotokana na wasiwasi) hauingii katika hiari, hivyo basi, hauwi maasi wala dhambi”12. Tayari tulikwishakanusha kuwa makusudio ya “Wanamuwekea” sio Adam na Hawa watu wawili, na tulitoa dalili kuwa makusudio yake ni asili ya kimaumbile yaani kila baba na mama. Ama kuhusu wasiwasi aliyoitaja pia tayari imeshatangulia kutoka kwetu kuwa kuna tofauti kati ya wasiwasi unaoingia vifuani ambao huwapata watu wasio manabii, nao ndio uliokusudiwa katika kauli Yake Taala katika Sura An-Nasi: “Ambaye hutia wasiwasi katika nyoyo za watu” na kati ya wasiwasi kwao bila ya kuingia vifuani, nao ndiyo wasiwasi wa Adam na Hawa. Na kuna aina nyingine za tafsiri ya Aya hazikutimia.13 Na katika tuliyotaja yatosha.
2 Ismah ya mkongwe wa manabii Nuhu (a.s.) Wasemao kuwa manabii hawana ismah wametumia Aya zifuatazo kama dalili ya kuwa Nuhu hana ismah:
12. Sharhul-Mawaqif, Juz 8, Uk 269. 13. Mafatihul-Ghayyi, Juz 4, Uk 343. Majmaul-Bayan, Juz 4, Uk 508 - 510. AmalilMurtaza, Uk 137 - 143.
33
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
12:29 PM
Umaasumu wa Mitume
Page 34
Sehemu ya pili
“Na Nuhu alinadi kumuomba Mola wake, akasema: Ewe Mola wangu! hakika mwanangu ni katika ahali wangu na kwa kweli ahadi yako ni kweli, na Wewe ni Mwenye hukumu iliyosawa mno kuliko ya Mahakimu.* Alisema: Ewe Nuhu kwa hakika yeye si miongoni mwa ahali wako kwa kuwa yeye ni tendo lisilo jema, hivyo usiniombe usilokuwa na elimu nalo. Kwa kweli mimi nakuonya usijekuwa miongoni mwa majahili.* Akasema: Oh! Mola wangu hakika mimi najikinga kwako nisiwe mwenye kukuomba nisilolijua na endapo hautonisamehe na hautonirehemu nitakuwa miongoni mwa wenye hasara.” (Sura Hud: 45 - 47). Wameitumia Aya hii kama dalili kwa hoja zifuatazo:i. Kwa kuwa dhahiri ya kauli yake (s.w.t.): “Kwa hakika yeye si miongoni mwa ahali wako” ni kuikadhibisha kauli ya Nuhu” “Hakika mwanangu ni katika ahali wangu” Na ikiwa Nabii haifai kwake uongo basi nini tafsiri ya usemi huo? ii. Kauli yake: “Hivyo usiniombe usilokuwa na elimu nalo. Kwa kweli mimi nakuonya usijekuwa miongoni mwa majahili.” kwa kuwa dhahiri ya kauli hii ni kuwa kujitokeza swali kwake ni jambo lisilolingana na heshima ya manabii, na kwa ajili hiyo amesemeshwa kwa lugha ya kulaumiwa na ameonywa asirudie. iii. Kauli yake: “Endapo hautonisamehe na hautonirehemu nitakuwa miongoni mwa wenye hasara.” Kwa kweli kuomba msamaha ni alama ya dhambi na haikai pamoja na ismah. Majibu ya hoja hizo tatu ni kama ifuatavyo: Hoja ya kwanza: Ufafanuzi wa jibu lake ni: Hakika Yeye (s.w.t.) alimuahidi Nuh kuwa atawaokoa ahali zake isipokuwa ambaye kauli ya hukumu imekwishapita kwake, akasema: 34
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:29 PM
Page 35
Sehemu ya pili
“Hata ilipofika amri yetu na chemchem ya maji ikabubujika, tukamwambia: Pakia humo jozi jozi dume na jike kutoka kila aina, na watu wako wa nyumbani isipokuwa yule ambaye imempitia hukumu, na walioamini, na hawakuamini pamoja naye ila wachache tu. (Hud:40) Kauli hii yaweka wazi kuwa Mwenyezi Mungu alimuahidi kwa maneno yake mkongwe wa manabii kuwa atawaokoa ahali wake, hii ni kwa upande mmoja na kwa upande mwingine yatubidi tufahamu hali ya mtoto wa Nuhu, kwani ima yeye alikuwa mwenye kuudhihirisha ukafiri na baba yake alikuwa anajua hilo, na ima alikuwa ni mwenye kudhihirisha imani na kuuficha ukafiri huku baba yake akiwa anamdhania kuwa ni miongoni mwa wanaomwamini. Kulingana na dhana ya kwanza inabidi isemwe kuwa: Nuhu aliifahamu kauli yake Mwenyezi Mungu (s.w.t.) “Na watu wako wa nyumbani isipokuwa yule ambaye imempitia hukumu” iliyomo katika sura mbili Hud: 40 na Muuminuna:28. Amesema katika Sura Hud: “Tukamwambia: Pakia humo jozi jozi dume na jike kutoka kila aina, na watu wako wa nyumbani isipokuwa yule ambaye imempitia hukumu”. Na amesema katika sura Muuminuna: “Uwaingize humo wa kila namna, dume na jike na ahli wako, isipokuwa ambaye kauli imepita wala usinitajie hao waliodhulumu, bila shaka wao watagharikishwa.” Nabii Nuhu alifahamu kutokana na Aya hizi kuwa utashi wa Mwenyezi Mungu wa kuokowa umeambatana na ahali wake wote wanaoungana naye kwa kamba ya nasaba na ya sababu, sawa wawe waumini au makafiri bighairi mkewe ambaye alikuwa mfano wa mke wa Lut ambaye alikuwa 35
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:29 PM
Page 36
Sehemu ya pili
anamfanyia uhaini usiku na mchana. Kwa mujibu huo makusudio ya kauli yake: “Isipokuwa ambaye kauli imepita” yanakuwa ni mkewe tu. Na Nuh alipoona mtoto amekabiliwa na gharika swali likamjia kifuani mwake: Vipi ahadi yake (s.w.t.) ya kuwaokoa ahali wote itakaa pamoja na kuangamia kwa mwanawe, hapo ndipo huzuni ilimshika akanyanyuwa sauti yake kwa dua akinadi: “Hakika mwanangu ni katika ahali wangu” bila ya kuomba chochote kingine isipokuwa alidhihirisha kilichokuwa kinazunguka moyoni mwake ambacho ni mgongano na tofauti iliyopo kati ya mambo mawili: Imani ya ukweli wa ahadi yake (s.w.t.) kama kauli yake inavyodhihrisha: “Kwa kweli ahadi yako ni kweli, na Wewe ni Mwenye hukumu iliyosawa mno kuliko ya Mahakimu.” na kati ya kuzama kwa mwanawe na kuangamia! Kulingana na mfano huo Nuhu (a.s.) hakusema uongo hata neno moja isipokuwa yeye alifahamu kutokana na kauli yake (s.w.t.): “Na ahli wako” kuokoka kwa wanaoambatana na yeye kwa uzawa au sababu, na hapo ndipo akadhihirisha ufahamu huu kwa kauli yake: “Hakika mwanangu ni katika ahali wangu”. Mtu hawezi kuzingatiwa kuwa ni muongo akidhihirisha alilokuwa akiamini na akilileta kwa kauli, japokuwa madhumuni yake ni kinyume na ukweli wenyewe, kwa ajili hiyo Mwenyezi Mungu (s.w.t.) akamjibu kuwa ahadi ya kuwaokowa ni ya watu wema miongoni mwa ahli wako na si wote wanaoambatana na wewe kwa kiungo cha uzawa au sababu. Kwa ibara nyingine ni kuwa: Kwa kweli mwanao japokuwa ni miongoni mwa ahli wako kwa nasaba lakini yeye si mwenye kuingia katika ahali nilioahidi kuwaokowa na kuwaepusha. Na kwa ibara ya tatu: Hakika mwanao ni mwenye kueunguliwa katika hilo, hivyo ni mwenye kuingia katika enguo la kauli Yake (s.w.t.): “Isipokuwa yule ambaye imempitia hukumu” kama ambavyo mkeo ni miongoni mwao pia. Jibu hili litakuwa sahihi na timamu bila ya vumbi juu yake endapo tu dhana 36
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:29 PM
Page 37
Sehemu ya pili
hii itakuwa sahihi, lakini asili ya dhana iliyoletwa nayo ni kuwa mtoto wa Nuhu alikuwa anadhihrisha ukafiri na baba alikuwa analijua hilo, dhana hii si timamu kutokana na mishkeli iliyomo ndani ya dhana hiyo. Raziy amesema ndani ya kitabu Ismatul-Anbiya katika kuwajibu wenye kushikamana na Aya hii kama dalili ya hoja yao ya Nuhu kutokuwa na Ismah na kumtuhumu kuwa amesema uongo: “Na jibu kuhusu la kwanza:Ni kuwa wafasiri wametofautiana kuhusu mtoto huyu, tofauti zafikia kauli tatu: Ya kwanza: Walio wengi wanasema kuwa alikuwa mtoto wake halisi, na hii ndiyo kauli yenye nguvu, kwa sababu ya usemi wake Mwenyezi Mungu mtukufu: “Nuh alimwita mwanawe.” kisha wametofautiana, miongoni mwao kuna aliyesema: Sio katika ahli wako ambao nilikuahidi kuwaokoa pamoja na wewe. Na imesemwa: Si katika ahli wa dini yako, Na hii ni kauli ya Ibnu Abbasi, Said bin Jubayri, Dhwahaki, Ikrimah na Maymun bin Mahran” 14 Kama tulivyokwishasema kuwa asili ya dhana hii haiko timamu, kutokana na dosari zinazojitokeza dhidi yake: Mishkeli inayojitokeza dhidi ya kauli hii: Nuhu alikuwa anajua fika kuwa mwanawe ni kafiri. Kwanza: Ni dhana iliyo mbali sana na ukweli kulingana na hadhi ya Nuhu kumwomba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kuwa asimbakishe yeyote yule juu ya ardhi miongoni mwa makafiri, kama inavyofafanuliwa na kauli yake (s.w.t.):
14. Ismatul-Anbiyai, Uk 32, chapa ya Jidah.
37
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:29 PM
Page 38
Sehemu ya pili
“Na Nuhu akasema: Ewe Mola wangu! Usimbakishe juu ya hii ardhi yeyote miongoni mwa makafiri.* Kwa kuwa wewe endapo utawabakisha watawapoteza waja wako, wala hatozaliwa isipokuwa kafiri muovu.” (Nuh: 26- 27). Kisha pamoja na hali hiyo haraka iingiye akilini mwake kuwa kauli yake (s.w.t.): “Na ahli wako” ni wote wanaoambatana na yeye sawa wawe waumini au makafiri. Bali dua yake hii ni ishara ya itikadi yake kuwa waliookoka katika ahli zake ni waumini tu sio makafiri, na kuwa makusudio ya “Isipokuwa yule ambaye imempitia hukumu” ni makafiri wote sawa wawe wanaambatana na yeye au hapana. Pili: Ni kwamba hapana dalili kuwa yeye alifahamu kutokana na kauli yake: “Isipokuwa yule ambaye imempitia hukumu” kuwa ni mkewe tu khususan, bali dhahiri ni kuwa yeye alifahamu kuwa makusudio ya walioenguliwa ni: Kila aliyempinga Mwenyezi Mungu na kumkanusha mjumbe wake bila ya tofauti katika hilo kati ya mke na mtu mwingine. Tatu: Kwa kweli yeye (s.w.t.) baada ya kumpa amri Nuhu ya kutengeza jahazi alimpelekea wahyi kwa kauli yake: “Wala usinisemeze katika wale waliodhulumu, kwa hakika wao wataghirikishwa.” (Hud:37 ). Dhahiri ni kuwa kutokana na kauli yake: “Wale waliodhulumu” ni washirikina wote wawe wapenzi au baki. Hiyvo kauli yake baada ya hiyo: “Na ahli wako isipokuwa yule ambaye imempitia hukumu”, pamoja na ile hali ya kuiacha jumla ya mwanzo “Wale waliodhulumu” bila ya mipaka ni ishara kuwa linalokusudiwa na neno “Ahli” ni waumini tu, sio madhalimu kati yao, kwani dhalimu miongoni mwa hawa anaingia chini ya kauli yake:“Wala usinisemeze katika wale waliodhulumu”. Ukitaka unaweza kusema: Kwa hakika uwazi wa jumla ya kwanza kwa kumwingiza mpenzi na asiyekuwa mpenzi ni ishara ya kuwa makusudio ya kauli yake: “Isipokuwa yule ambaye imempitia hukumu” ni madhalimu wote na makafiri sawa awe mke au mtu mwingine, awe ndugu wa kuzali38
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:29 PM
Page 39
Sehemu ya pili
wa au mwingine, na uwazi huu ni ishara kuwa aliyekusudiwa katika neno “Ahli” ni muumini tu, sio wote. Kwa ufupi ni kuwa lau dhana ingekuwa sahihi basi jibu lingekuwa sahihi, lakini dhana hiyo ni batili kutokana na vigezo vitatu tulivyovifafanua kwa kina. Dhana ya pili: Inavyoonekana dhana hii ndiyo ya kweli, na ilivyo ni kwamba mtoto wa Nabii Nuhu alikuwa anajidhihirisha kuwa ni muumini na huku akiuficha ukafiri. Hilo linajulishwa na kauli ya Nuhu kwa mwanawe alipokataa kwenda na baba yake jahazini: “Oh! Mwanangu panda pamoja na sisi wala usiwe pamoja na makafiri.” (Hud: 49 ) Yaani usiwe pamoja nao ukaja kushirikiana nao katika balaa, hivyo lau kama angekuwa anajua ukafiri wake ingempasa aseme “Usiwe katika makafiri” lakini kwa kuwa alikuwa hajui ukafiri wa mwanawe, bali alikuwa anaitakidi kuwa ni muumini akiwa na yakini kuwa anaingia katika kauli yake Taala: “Na ahli wako” aliingiwa na mshangao alipozama huyu mtoto, imekuwaje amezama hali ya kuwa Mwenyezi Mungu alimuahidi kuwa atawaokoa ahli zake wote na ahadi yake Mwenyezi Mungu ni ya kweli haiingiwi na shaka, basi hapo akadhihirisha la moyoni mwake na kusema: “Hakika mwanangu ni katika ahli zangu”. Mwenyezi Mungu (s.w.t.) akamjibu kuwa yeye hakukabiliwa na gharika isipokuwa ni kwa ajili ya ukafiri wake; kwa hiyo alikuwa amejumuishwa na kauli yake Taala ya kwanza: “Wala usinisemeze katika wale waliodhulumu bila shaka wao watagharikishwa.” na ni mwenye kuingia katika enguo la pili, yaani katika kauli yake: “Isipokuwa ambaye kauli imepita” na wala si mwenye kuingia katika kauli ya “Ahli wako”. Kulingana na ukaribu huu swali na jibu vinakuwa mahali pake, na Nuh ahukumiwi kuwa mwongo kwa kuwa yeye alikuwa anamdhania mwanawe kuwa ni muumini ndipo Mwenyezi Mungu (s.w.t.) alimtanabahisha kuwa yeye ni kafiri. Je uongo uko wapi katika hizi hukumu mbili? Na kauli yake (s.w.t.): “Yeye ni tendo lisilo jema” inajulisha kuwa udugu wa kidini unararuwa udugu wa nasaba, na kuwa nasaba yako ni ile dini 39
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:29 PM
Page 40
Sehemu ya pili
yako na itikadi yako, hivyo lau awe miongoni mwa watu wa mbali, kwa mfano awe Muhabeshi na wewe ni mkureshi basi huyo ni mwambata wako na ni muhusika wako, na asiye kuwa katika dini yako japo awe ndugu yako wa karibu mno wa kuzaliwa yeye ni mtu wa mbali mno na wewe. Kisha ibara kumuhusu mtoto wa Nuh kuwa yeye ni “Tendo lisilo jema” badala ya kauli “mwenye kutenda tendo lisilo jema” imekuja kwa ajili ya msisitizo katika kumlaumu, hiyo ninmfano wa kauli yake: “Si chochote ni mbele na nyuma”.15 kinyume na alivyodai Raziy ndani ya kitabu IsmatulAnbiyai baada ya kuteua kuwa kisono ni kwa irabu ya Raf’u na Tan’win, akasema: “Nomino hiyo hapana budi inarudi kwenye neno lililotajwa kabla, na neno lililotajwa kabla hapa huenda likawa ni swali na huenda likawa ni neno ibnu. Si jaizi nomino kurejea kwenye ibnu kwa sababu ibnu haiwezi kuwa tendo lisilo jema, bali huwa mwenye tendo lisilo jema, kwahiyo yatakikana ifichwe, na hali hiyo ni kinyume na asili, kwa hiyo yathibiti kuwa nomino yarejea kwenye ombi na hatimaye inathibiti kuwa hilo lilikuwa tendo lisilo jema.”16 Wala wenye utata huu hawakubainisha ni kwa nini ibnu hawi tendo lisilo jema baada ya kuwa tumebainisha sura ya msisitizo. Hususan baada ya Qur’an kuwa imejaa mifano ya balagha, majazi na istiara, hivyo ni wajibu kutanabahi na nukta hizi wakati wa kuzizingatia Aya za Qur’an. Hivyo basi nomino hairejei kwenye ombi bali hurejea kwenye ibnu. Kisha kulingana na usomaji wa Al-Kasaiy nayo ni amalan kwa fat’ha yaani amila amalan ghaira Swalihin kama ambavyo Raziy alivyonakili katika kitabu chake, na akaifanya kuwa ni kisomo chenye uzito, pia nominohairejei kwenye ombi bali yarejea kwenye ibnu kulingana na alivyonakili kutoka kwa Sharifu Aradhwiyu: Pamoja na kisomo hiki hakuna shaka ya kurejea maana ya maneno kwa ibnu na si kwenye ombi la Nuhu. Na 15. Al-Kashaf, Juz 2, Uk 101. 16. Ismatul-Anbiyai, Uk 32.
40
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
12:29 PM
Page 41
Umaasumu wa Mitume
Sehemu ya pili
Sharifu amekitilia nguvu kisomo hiki na akaorodhesha ushahidi juu ya hilo kutoka kwenye maneno ya waarabu.17 Na hapa kuna nukta muhimu yapasa izingatiwe, nayo ni: Kuwa kiini kinachofanya anuwani ya Ahli iwe sahihi kwa mtizamo wa wana lugha na hali iliyo maarufu ni kunasibika mtu na mtu mwingine kwa njia ya kamba miongoni mwa kamba za nasaba au sababu, japo hao wawili wasiwe na mlandano na umoja kwa upande wa mwenendo na mfumo. Isipokuwa sheria ya kiungu imeingiza humo kipengele kingine nyuma ya nasaba ya kimaumbile, nacho ni kuungana mtu na mwingine kwa njia ya imani na umoja wa itikadi na maadili kwa kiwango fulani, lau kipengele hiki kikikosekana basi anuwani ile haitathibiti juu yake, bali kipengele cha imani chatosha kuthibitisha Ahli kwa watu wenye sifa hiyo, sawa wawe na kamba ya nasaba au hapana, kwa ajili hiyo twaona Mwenyezi (s.w.t) anatosheka na tamko la Ahli katika kuwaelezea waumini wote, asema katika kisa cha Nabii Lut:
“Basi tukamuokoa yeye (Luti) na ahli wake isipokuwa mke wake, alikuwa miongoni mwa waliokuwa nyuma.” (al-Aarafu: 83) Na pia amesema:
“Na kwa kweli Lut ni miongoni mwa waliotumwa. * Tulipomuokowa na ahli zake wote. * Isipokuwa bibi kizee katika waliobaki nyuma.” (Aswafaat: 133-135). 17. Pembezoni mwa Ismatul-Anbiyai, Uk 32. chapa ya Jidah. 41
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:29 PM
Page 42
Sehemu ya pili
Tunaona yeye Mwenyezi Mungu ametosheka na tamko la Ahli bila ya kuliambatanisha na tamko Waumini au Waliomwamini hali ya kuwa uokovu si mahususi kwa Ahli zake bali unawajumuisha waumini, hilo linaweka wazi kuwa imani yamfanya aliye baki kuwa Ahli, na ukafiri wamfanya wa karibu awe baki. Kwa ajili hiyo katika kisa cha Nabii Nuhu alitosheka na tamko la Ahli akasema:
“Na Nuhu alinadi hapo kabla tulimwitikia na tulimuokowa yeye na Ahli zake kwa kuwaepusha na dhiki kubwa”. (al-Anbiyau:76) Na amesema pia:
“Na kwa kweli Nuhu alituita kwa ombi nasi ni wema wa kulijibu ombi. Na tulimuokoa yeye na Ahli zake kwa kuwaepusha na dhiki kubwa.” (as-Saafaatu:75) Yajulikana kuwa uokovu sio mahsusi kwa Ahli tu, hilo ni kwa ushahidi wa kauli yake:
“Na Ahli zako isipokuwa ambaye imempitia hukumu, na walioamini” (Hud:40)
42
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:29 PM
Page 43
Sehemu ya pili
Kwa mujibu huo siri ya kauli yake (s.a.w.): “Sulaymani ni katika sisi Ahlulbayti” yabainika. Alimzingatia asiye mwarabu kuwa ni katika Ahlibayti wake na hii si kwa sababu nyingine ila ni ya mlandano wa kiroho ambao ni kiungo thabiti na kifungo imara, kama kulivyo kutengana kiroho ni chombo bora cha kukata kifungo na kubomoa uhusiano wa kimaumbile. Kwa ajili hiyo Imamu aliyetoharishwa Ali bin Musa Ar-ridhwa (a.s.) amesema kumuhusu mtoto wa Nuhu: “Kwa kweli alikuwa ni mwanawe, lakini alipomwasi Mwenyezi Mungu mwenye enzi na utukufu alimuengua mbali na baba yake, na hivyo hivyo kila aliyekuwa miongoni mwetu asiyemtii Mwenyezi Mungu mwenye enzi na utukufu si miongoni mwetu, na wewe ukimtii Mwenyezi Mungu basi wewe ni katika sisi Ahlul-bayti”. Ndiyo hatudai kuwa kila tulilolisema ndio istilahi pekee ya Qur’an bali Qur’an ina istilahi nyingine inayoafikiana na istilahi ya wanalugha na iliyo maarufu, nayo ni kutosheka na kiungo cha kimaumbile na twaona kila moja kati ya hizo istilahi mbili zimekuja ndani ya sura Hud, amesema (s.w.t.): “Na Ahli zako isipokuwa ambaye imempitia hukumu, na walioamini”. Amelitumia tamko la Ahli bila ya sharti lolote kwa kila aliyeungana na mkongwe wa manabii, sawa awe kafiri au muumini kisha alimtowa kafiri nje ya hukumu ile “wabebe” “jahaziini” si katika maudhui nayo ni Ahli, na akasema: “Na Ahli zako isipokuwa ambaye imempitia hukumu, na walioamini”. Na wakati huo huo anajibu wito wa dua ya Nuhu baada ya kauli yake: “Hakika mwanangu ni katika ahli wangu” kwa kauli yake “Kwa hakika yeye si katika ahli wako”. Kuhusu hoja ya pili: Umetambuwa yanayohusu swali la kwanza yale ya kumnasibishia uongo mkongwe wa manabii Nuh{a.s} katika kauli yake “Kwa hakika mwanangu ni miongoni mwa Ahli zangu”. Na sasa njoo pamoja nami tulidurusu swali la pili nalo ni kauli yake (s.w.t.): “Hivyo usiniombe usilokuwa na elimu nalo. Kwa kweli mimi nakuonya usijekuwa mion43
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:29 PM
Page 44
Sehemu ya pili
goni mwa majahili.” Yaonyesha kuwa kuna ombi lisilofaa kwenye uwanja wa manabii na kwa ajili hiyo amesemeshwa na kukatazwa asirudiye ombi hilo. Twasema: Kwa kweli Mwenyezi Mungu mwenye enzi na utukufu alimuahidi kuwaokoa Ahli zake pamoja na kuwaenguwa wale ambao wametanguliwa na hukumu, na kuenguliwa huku kulikuwa ni dalili ya kuwepo kwa yule ambaye adhabu imemuwajibikia katika jumla ya Ahli zake, na kwamba si wote watakaookoka na hapo ilikuwa yampasa Nuhu asiingiwe na utata pindi mwanawe alipokaribia kuzama, moja kwa moja ajue kuwa ni miongoni mwa walioenguliwa na si mwenye kuingia katika wasioenguliwa. Hivyo akalaumiwa kuwa ameingiwa na utata ambao ilimpasa yeye asiingiwe na utata huo. 18 Kwa mujibu huu makusudio ya kauli yake “Hivyo usiniombe usilokuwa na elimu nalo.” yanakuwa ni katazo la ombi ambalo halifai litolewe na liombwe ikiwa jawabu lajulikana kwa ishara na kwa kufikiri kwenye vipengele vya suala husika, na kama si hivyo basi ombi litakuwa linahusu kisichojulikana na si kinachojulikana. Hivi ndivyo alivyojibu mwandishi wa tafsiri ya Al-Kashafu, na kuna jibu la wazi zaidi na huenda likawa lalingana na uwanja wa manabii, nalo ni: “Alipomuahidi Nuhu kuwa atawaokowa Ahli kwa kauli yake: “Isipokuwa ambaye imempitia hukumu” Nuhu hakuwa anajua undani wa mwanawe isipokuwa alikuwa anaamini hali ya dhahiri kuwa yeye ni muumini, hivyo basi alibaki ameshikilia ibara ya mjumuisho ya Ahli na hakupingwa na yakini wala shaka kuhusu imani ya mwanawe, kwa hiyo alipiga ukelele wa ombi kwa Mola wake…” Ama kauli yake “Kwa kweli mimi nakuonya usijekuwa miongoni mwa majahili.” hairejei kwenye maneno yake na kunadi kwake, bali kumwom18. Al-Kashaaf, Juz 2.Uk 101. 44
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:29 PM
Page 45
Sehemu ya pili
ba kwake Mola wake katika hali hii kunakubalika na ombi lilikuwa sahihi na zuri, bali hiyo kauli yarejea kwenye ombi la hapo baadaye baada ya Mwenyezi Mungu kumjulisha undani wa mambo yake, na kwamba yeye Nuh endapo ataomba hapo baadaye atakuwa miongoni mwa majahili, na lengo lake ni kumpa kitakachombakisha yeye (a.s.) kwenye kusudi la ismah. Na onyo halilazimu dhambi iwe imetendeka, isipokuwa yawezekana lengo likawa kuhifadhi isije ikatokea dhambi hapo baadaye. Na kwa ajili hiyo alitekeleza (a.s.) katazo la Mola wake akasema: “Najilinda kwako nisije nikakuomba nisilolijua”.19
Jibu la tatu kuhusu hoja ya pili: Allama Tabatabai ana jibu la tatu amabalo lina uthabiti zaidi kuliko majibu mawili yaliyotangulia, amesema: “Kwa kweli kauli ya Nuh: “Hakika mwanangu ni miongoni mwa ahli wangu, na hakika ahadi yako ni haki, na wewe ni Mwenye haki kuliko Mahakimu” maumbile yalipasa kumsukuma kwenye ombi la kuokoka kwa mtoto wake hali akiwa hajui kuwa yeye si katika Ahli zake, ndipo akaingizwa kwenye msaada wa kiungu, na rekibisho la ghaibu likazuwia kati yake na ombi, hapo katazo likamuwahi kwa kauli yake: “Hivyo usiniombe usilokuwa na elimu nalo.” kwa kulizalisha katazo toka kwenye maelezo yaliyotangulia. Akampasha habari Nuh kuwa hakika mwanao si miongoni mwa Ahli zako kwa kuwa kwake tendo lisilo jema, hivyo wewe huna njia ya kujua hilo, basi jiepushe kufanya haraka kuomba kuokaka kwake kwani hilo ni ombi la jambo ambalo huna elimu nalo. Na kukataza kuomba usilokuwa na elimu hakulazimu kuthibiti kwa ombi, si kwa hapo baadaye wala si kwa undani. 19. Al-Intisafu cha Nasrud-Din Al-Iskandariy Al-Malikiy, JuZ 2, Uk 101, pambi-
zoni mwa Al-Kashaf. 45
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:29 PM
Page 46
Sehemu ya pili
Kukataza kitu hakulazimu kitu hicho kuwa kimetendwa hapo kabla, isipokuwa inatokana na kitendo kuwa cha hiari na mahali pa mukalafu kutahiniwa, hivyo miongoni mwa ismah ni Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kuwaweka sawa na kuwachunga katika matendo yao, na kila wakurubiapo kwenye jambo ambalo kwalo mtu anaweza kuteleza, Mwenyezi Mungu huwatanabahisha sura iliyo sahihi na kuwaita kwenye usawa wa mambo, na kuwaambatanisha na njia ya uja. Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amesema:
“Lau tusingekuweka katika hali thabiti ungekaribia kuwaelemea kidogo, kama ungefanya hivyo, tungekuonjesha sehemu mbili za adhabu katika maisha haya na sehemu mbili za adhabu baada ya kufa kisha hautopata yeyote atakayekusaidia dhidi yetu.”(Al-Israu :74-75). Na lijulishalo kuwa katazo katika kauli yake “Wala usiniombe” ni katazo la jambo ambalo bado halijatokea ni kauli ya Nuhu baada ya kusikiliza maelezo yake (s.w.t.): “Mola wangu hakika mimi najikinga kwako nisije kukuomba ambalo silijui”. Lau angekuwa alimuomba kitu kabla yake ingekuwa yampasa aseme: “Najikinga kwako na nililokuomba”, au mfano wa hilo. Na ambalo laweka wazi kuwa Nuhu hakuomba kitu kutoka kwa Mola wake ni kauli yake (s.w.t.): “Kwa kweli mimi nakuonya usijekuwa miongoni mwa majahili.” ni sababu ya katazo lake “Wala usiniombe” kwani lau Nuhu angekuwa amemwomba kitu kabla basi angekuwa miongoni mwa majahili kwa kuwa amemuomba asichokijua. Pia lau lingekuwa kusudio la katazo la kuomba ni asirudiye ombi kama hilo baada ya kutokea kwake mara moja basi ingekuwa yafaa akataze wazi46
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:29 PM
Page 47
Sehemu ya pili
wazi kuwa asirudiye mfano wa ombi kama hilo, na si kukataza asili ya ombi tu kama ulivyokuja mfano wake ndani ya Qur’an tukufu:
“Mlipoupokea kwa ndimi zenu na mkasema kwa vinywa vyenu msiyoyajua..” (An-nur:17) Na “Mwenyezi Mungu anakuonyeni msirudie kabisa mfano wa haya....” (An-nur:17).20 Mpaka hapa jibu la hoja ya pili limebainika, na imekuwa wazi kuwa hakupata kuomba ombi lisilolingana na hadhi yake. Maneno yamebaki katika hoja ya tatu nayo ndio tutakayoijadili kwenye mjadala ufuatao, na kabla ya huo tutataja maneno ya Raziy yaliyo ndani ya kitabu Ismatul-Anbiyai, amesema katika kuikanusha hoja ya pili: “Ama kuhusu kauli ya Nuh amani imfikiye: “Hakika mimi najikinga kwako nisikuombe nisilolijua” katika usemi huo hakuna dalili kuwa yeye alifanya hivyo, yaani kumuomba asilolijua.”21 Kuhusu hoja ya tatu: Yaliyomo ni kwamba; msamaha katika kauli yake: “Na endapo hautonighufiria na hautonirehemu nitakuwa miongoni mwa waliohasirika” haiwi pamoja na ismah. Nasema: Kwa hakika maneno haya, sura yake ni ya toba na ukweli wake ni shukrani kwa aliyoneemeshwa na Mwenyezi Mungu miongoni mwa taaluma na maadili. Ama dai la kwamba sura yake ni ya toba, ni kwa kuwa katika hilo kuna kurejea kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kuomba ulinzi na linalolazimu hilo ni kuomba msamaha wa Mwenyezi Mungu na rehema zake, yaani kumsitiri kwake mtu katika ambalo laweza kumtelezesha, na kuenea kwa msaada wake kwa hali yake.Na maghfira kwa maana ya kuomba sitara ina maana pana zaidi kuliko kuiomba kwa ajili ya maasi 20. Al-Miizan. Jalada 10 Uk .254. 21. Ismatul- Anbiyai.Uk.33. 47
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:29 PM
Page 48
Sehemu ya pili
yaliyo maarufu kwa wafanya sheria, na kila sitara ya kiungu humfanikishia mtu maisha bora ya furaha na huyaweka pamoja mambo yake. Ama kuhusu kuwa uhakika wake ni shukrani, hiyo ni kwa kuwa msaada wa kiungu uliozuia kati yake na ombi ambalo lingemfanya awajibike kuingia katika jumla ya majahili, ni sitara ya kiungu ya kutoteleza na kwenda na njia yake na ni rehema na neema ambayo Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amemneemesha, kwa hiyo kauli yake: “Na endapo hautonighufiria na hautonirehemu nitakuwa miongoni mwa waliohasirika� kwa maana ya kama haungeninasihi dhidi ya mitelezo ningepata hasara, hiyo ni sifa na shukrani kwa sababu ya mema yake.22 Ukweli wa maneno hayo unajitokeza kutokana na tuliyoyatanguliza katika kisa cha Adam, kwamba mambo mengi yanayoruhusiwa huhesabika dhambi kwa kiwango fulani kulingana na tabaka mahsusi ya mawali na manabii na pindi yatokeapo mfano wa hayo inakuwa wajibu kwao kukamilisha ismah yao, kuomba msamaha na rehema ili wasiwe miongoni mwa waliopata hasara. Na wala hasara haiishii katika kutenda maasi bali huenda kitendo halali kikahesabika hasara na kutofaulu endapo kitatokea upande wa tabaka la juu kama tulivyofafanuwa katika kisa cha Adam. Ndiyo hakikutokea kitendo upande wa mkongwe wa manabii katika hali ile, ila yeye alikuwa katika utambuzi wa kutokea kitendo kile, nako ni kuomba asilolijua. Kwa ajili hiyo ilikuwa sahihi kwake aombe sitara kuhusu hali ile ili apate uangalizi wa kiungu wenye kuzuwia kati yake na hali ya kutokea kitendo. Mpaka hapa yamebainika yaliyomaanishwa na Aya za Qur’an, na kwamba hakuna kinachoashiria kutokea kwa dhambi, bali hata ambalo lawajibisha lawama na kemeo. 22. Al-mizan, Juz 10, Uk 246 - 247. 48
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:29 PM
Page 49
Sehemu ya pili
Ismah ya Ibrahim Al-Khalil na maswala matatu23 Hakika Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amemsifu Ibrahim bingwa wa tawhiid kwa sifa nzuri mno, na alihimidi taabu yake katika njia yake (s.w.t.) himidi ya hali ya juu, na amekariri kulitaja jina lake katika kitabu chake zaidi ya sehemu sitini, na amedhihirisha vipaji vyake na neema zake kwake kwa wingi, na amesema (s.w.t.): “Kwa kweli tulimchaguwa duniani na kwa hakika yeye Akhera atakuwa miongoni mwa waliotenda wema” (alBaqrah:130). Mwenyezi Mungu (s.w.t.) aliyahifadhi maisha yake ya heshima na shakhsiya yake ya kidini alipoiita dini hii iliyo nyoofu kuwa ni: Uislamu, na kuitwa huku kumenasibishwa na yeye, Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema:
“Ni mila ya baba yenu Ibrahim, yeye aliyekuiteni Waisilam” (AlHajj:78 ) Na akasema:
“Sema: Hakika mimi Mola wangu ameniongoza kwenye njia iliyonyooka dini iliyo thabiti dini ya Ibrahim iliyo sawa na hakuwa miongoni mwa washirikina.” (al-Anamu:161. Ingawaje kuna sifa kama hizo nyingi kutoka kwake (s.w.t.) kumwelekea Ibrahim, twaona baadhi ya wanaowakosoa manabii wanataka kumnasi23. i= Kauli yake kuhusu nyita: Huyu ni Mola wangu. ii= Kauli yake: Bali amefanya mkubwa wao. iii= Kauli yake: Hakika mimi ni mgonjwa. 49
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:29 PM
Page 50
Sehemu ya pili
bisha au kumpakazia yasiyolingana na hadhi yake wakitolea dalili Aya ambazo tutazileta moja baada ya nyingine na hatimaye tutabainisha hali za Aya hizo. Kundi la kwanza: Ni kauli yake Taala: “Na kadhalika tunamuonesha Ibrahim ufalme wa mbinguni na ardhi ili awe miongoni mwa wenye yakini. * Na usiku ulipomfunika akaona nyota akasema: Hii ni Mola wangu. Lakini ilipotua, akasema: Siwapendi wanaotua. * Na alipouona mwezi unang’aa akasema: Huu ni Mola wangu. Lakini ulipotua, akasema: Asiponiongoza Mola wangu, bila shaka nitakuwa miongoni mwa watu wapotovu. * Na alipoliona jua linang’aa akasema: Hili ni Mola wangu, hili kubwa kabisa. Lakini lilipotua, akasema: Enyi watu wangu! mimi simo katika hayo mnayoyashirikisha” (Al-An’ami). Mkosowaji amesema kuwa kauli yake: “Hii ni Mola wangu” iliyopo sehemu hizo tatu zadhihirisha kuwa yeye (a.s.) alikuwa anaamini wakati fulani miongoni mwa nyakati uungu wa sayari hizi za mbinguni, na hili ni katika yasiyofaa kwa manabii kwa mtizamo wa Adliyah. Na endapo Adliyah watadhaniya kuwa yeye (a.s) aliongea hivyo kwa dhahiri tu na haamini ndani ya moyo wake, na hili pia sio sahihi kwa manabii kwakuwa atakuwa anasema kitu asichokiamini, nalo ni jambo baya mno sawa liitwe uongo au hapana. Na jibu: Dalili hii ni dhaifu kwa kuwa hali ya mambo haitoki nje ya moja kati ya sura mbili. Sura ya kwanza: Kwa kweli Ibrahim alikuwa katika ngazi ya kutafiti na kumtambuwa Mola mratibu wa ulimwengu, wakati ule hakuwa ameujua ukweli kwa kuwa yeye kulingana na ilivyosemwa alikuwa mdogo hajafikia 50
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
12:29 PM
Umaasumu wa Mitume
Page 51
Sehemu ya pili
balehe, na alikuwa kwenye lengo la kupata uhakika na uthibitisho, hivyo basi alileta nadharia tete nyingi moja baada ya nyingine, kisha alianza kubatilisha moja baada ya nyingine mpaka alifikia kwa Mola wa ukweli na mratibu wa ukweli. Raziy amesema akiwa katika nafasi ya kujibu utata huu kuhusu maneno haya: “Na jibu ni: Imesemwa kuwa ni maneno ya Ibrahim kabla hajabalehe, kwa kuwa yeye muda mfupi kabla ya taklifu ilipomjia akilini mwake hali ya kumthibitisha muumba alifikiri akaona nyota, akasema: “Hii ni Mola wangu”..... Na kuna ambao wamekubali kuwa yalikuwa maneno ya Ibrahim baada ya balehe kisha walitofautiana kuna ambaye anasema: Yawezekana yakawa hayo ni maneno yake alipokuwa katika hali ya kushughulika na utafiti na dalili. Kisha yeye alisema: “Hii ni Mola wangu” katika njia ya kuleta mfano, wala si katika njia ya kutoa habari. Kama ambavyo mmoja wetu akichunguza jinsi ya kutokea kwa miili husema: Kitu cha mwili ni cha milele? Makusudio yake hapo si kueleza kuwa vitu vya miili ni vya milele, bali yeye analeta mfano kuwa ni vya milele ili aje kudhihirisha ubaya utakaopatikana katika hali ya mfano huo. Na hiyo ndiyo hali ya “Hii ni Mola wangu”, hapa alipiga mfano kisha mwishowe akaleta linalojulisha ubaya wake, nalo ni kauli yake “Si wapendi wanao zama”.”24 Kisha ametaja nadharia nyingine akasema:… ..... “Na iliyo sahihi katika kauli hizi ni kuwa hiyo ilikuwa katika sura ya kutoa dalili si katika sura ya kutoa habari, kwa sababu hiyo hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu hakumlaumu Ibrahim (a.s) kwa tendo hilo, bali alimtaja kwa kumsifu na kumtukuza na yeye alimuonyesha hivyo ili awe miongoni mwa wenye yakini.”25 24. Ismatul-Anbiyai, Uk 34 - 35, chapa ya Jidah. 25. Ismatul-Anbiyai, Uk 35, chapa ya JIdah 51
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
12:29 PM
Page 52
Umaasumu wa Mitume
Sehemu ya pili
Na huu ni mfano wa wayafanyayo utafiti kuhusu sababu za dhahiri utawaona wanaweka juu ya meza ya uhakiki mlolongo wa nadharia tete na uwezekano kisha wanakusudia kuhakiki hali ya kila mojawapo katika hizo mpaka waifikiye sababu halisi, na kwa mujibu huu inakwa maana ya kauli yake “Hii ni Mola wangu” ni gezi tu sio kukiri moja kwa moja wala haihesabiki mfano kama huu kuwa haufai kwa hadhi ya manabii. Sayyid Murtadha anasema kwa lengo hili ikiwa ni jibu la hoja kuwa: “Yeye hakusema hivyo kwa kueleza, bali alisema kwa gezi akikadiria kifikra na kimazingatio, huoni kuwa yapendeza kwa mmoja wetu ikiwa anatafiti kitu na ana shaka juu ya moja ya sifa zake mbili akiletee mfano wa mojawapo ya sifa mbili ili aangaliye matokeo ya usahihi au ubatili wa mfano huo. Basi katika hali hiyo hawi muelezeaji wa hali ilivyo, kwa hiyo yafaa kwa mmoja wetu achunguzapo kuzuka kwa miili na umilele wake aweke mfano wa kuwa yenyewe ni ya milele ili apate kubainisha ubatili wa matokeo ya mfano huo.26 Na maana hii imeelezwa kutoka kwa Imam As-Sadiq (a.s) alipoulizwa kuhusu kauli ya Ibrahim: “Hii ni Mola wangu”, Je ameshirikisha katika usemi wake: “Hii ni Mola wangu”, Akasema (a.s.): “Hapana, isipokwa mwenye kusema hivyo hii leo basi yeye ni mshirikina wala haikuwa ni ushirikina kwa Ibrahim bali ilikuwa ni katika kumtafuta Mola wake, na hilo kwa mtu mwingine ni ushirikina.” Na katika riwaya nyingine kutoka kwa mmoja wao Al-Baqiru au As-Sadiq (a.s.): “Yeye alikuwa akitafuta kumtambuwa Mola wake, hakufikia ukafiri na yeyote mwenye kufikiri kwa mfano kama huo basi yeye atakuwa katika daraja yake.”27 Isipokuwa gezi hili huenda likawa haliridhishi kwa baadhi ya Adliyah28 kwa sababu manabii toka walipoachishwa kunyonya mpaka walipo lazwa katika sanda zao, walikuwa wanatambuwa tawhiidi yake (s.w.t.), kwa dhati 26.Tanzihul-Anbiyai, Uk 22. 27. Nuru Thaqalayn, Juz 1, Uk. 610 - 611, hadithi ya 149 hadi 151.
28. Adliyah ni: Miongoni mwa makundi ya theiolojia katika Waislamu. 52
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:29 PM
Page 53
Sehemu ya pili
na kwa kitendo, muumba na Mola, ingawaje kulikuwa na kuonyeshwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa kipenzi chake kama ilivyokuja katika kauli Yake “Na kadhalika tunamuonesha Ibrahim” ilikuwa ni kwa ajili ya kumzidishia maarifa na ili awe miongoni mwa wenye yakini.
Sura ya pili: Yeye alikuwa anatambua Umola wake, na mwenye kukanusha Umola wa mwingine yeyote yule, lakini kwakuwa alikuwa katika lengo la kuiongoza kaumu yake na kuiatua ili isiabudiye miili, alikwenda nao katika mantiki yao ili asiguse hisia zao na kutimua ukaidi na ung’ang’anizi wao, kwa hiyo alikwenda hatua kwa hatua katika kubatilisha Umola wa waabudiwa wao, mmoja baada ya mwingine, kwa hoja alizokuwa akizitumia mfano wa kuzama, kutoweka, kubadilIka, na kutikisika, miongoni mwa mambo ambayo hayafai ahusishwe nayo Mola mratibu. Na mfano kama huu unafaa kwa mwalimu ambaye anakusudia kuongoza jamii ya watu wakaidi wakiwa katika itikadi zao zilizo mbali na njia iliyo sawa, na hii ni moja ya njia ya kuongoza na kutoa malezi. Uko wapi basi usemi wa kishirikina ulio halisi kama wanavyodai? Razi amesema: “Miongoni mwao kuna waliosema: Alisema hayo baada ya kumaliza kwake utafiti na kuwa na yakini na Mwenyezi Mungu, kisha wakatofautiana katika hilo kwa mitizamo mitano, ikasemwa: Alisema hivyo kwa kuwa jambo liko hivyo kwao, yaani wao wana amini hivyo kama awezavyo mmoja wetu kumwambia Mushabihu kwa lengo la kukanusha, hakika mungu wake ni mwili wenye kubadilika. Mfano kama huo Mwenyezi Mungu Mtukufu ameutumia kwa kusema: “Basi mtazame mungu wako” yaani kulingana na dai lako”.29 Kwa mujibu wa jibu hilo Sayyid Murtadha katika maneno yake ameashiria kuwa Ibrahim (a.s) hakusema lililo ndani ya Aya kwa kutilia shaka wala si katika kipindi cha uchunguzi na utafiti bali alikuwa katika hali ile ya 29. Ismatul-Anbiyai, Uk. 35, chapa ya Jidah. 53
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:29 PM
Page 54
Sehemu ya pili
mwenye yakini mjuzi kuwa Mola wake Mwenyezi Mungu haifai awe katika sifa yoyote miongoni mwa sifa za sayari, isipokuwa alisema hivyo akiwa katika moja ya mitizamo miwili: Kwanza: Yeye ni Mola wangu kwenu nyinyi kwa mujibu wa madhehebu zenu, kama mmoja wetu awezavyo kusema akiwa katika njia ya kuwakanusha Mushabiha30 kwa kusema: Huyu mungu wake ni mwili unaotikisika na kutulia. Pili: Yeye alisema hivyo katika hali ya kuuliza, na ameacha kuitumia herufi ya kiulizo kwa kutoihitaji. 31. Na mtizamo wa kwanza katika sehemu mbili za jibu hili ni uko wazi, Raaziy amesema: “Na imesemwa: Makusudio yake ni swali, isipokuwa ameiacha herufi ya swali kwa kutoihitajia. Na imesemwa: Katika Aya ni ufupisho na usemi waweza kukadiriwa hivi: “Wanasema huyu ni Mola wangu” na mfano wake ni kauli
“Kumbuka alipokuwa Ibrahim anainuwa msingi wa nyumba na Ismaili, Mola wetu” (Al-Baqara:127) yaani na wakisema “Mola wetu”. Na imesemwa: Ibrahim alikuwa anataka kubatilisha kauli yao ya kuzienzi sayari. Kwa hiyo akajifanya binafsi kama kwamba anazienzi, kisha alimalizia kwa kutaja dalili juu ya kubatilika kwake.” 32
30. Mushabihu ni wenye imani ya kuwa Mungu anafanana na viumbe nna ana mada na maumbile kama ya viumbe. 31.Tanzihul-Anbiyai, Uk 23. 32. Ismatul-Anbiyai, Uk. 35, chapa ya Jidah 54
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:29 PM
Page 55
Sehemu ya pili
Kundi la pili: Usemi wake (s.w.t.): “Na hakika tulimpa Ibrahim mwongozo wake zamani na tulikuwa tukimjua.* Alipomwambia baba yake na watu wake: Ni nini masanamu haya mnayoyategemea? * Wakasema:Tuliwakuta baba zetu wakiyaabudu. * Akasema: Bila shaka nyinyi na baba zenu mlikuwa katika upotovu dhahiri. * Wakasema: Je, umetuletea haki au umo miongoni mwa wachezaji? * Akasema: Bali Mola wenu ndiye Mola wa mbingu na ardhi ambaye aliziumba na mimi kwa hilo ni miongoni mwa wenye kushuhudia. * Wallahi lazima nitayafanyia vitimbi masanamu yenu baada ya kunipa mgongo. * Basi akayavunja vipande vipande isipokuwa kubwa lao, ili wao walirudie.* Wakasema: Nani amewatendea hivi miungu yetu? Hakika huyo ni miongoni mwa madhalimu. * Wakasema: Tulimsikia kijana mmoja akiwataja vibaya anaitwa Ibrahim. * Wakasema basi mleteni mbele ya macho ya watu ili wamshuhudie. * Wakasema: Je, wewe umewafanya hivi waungu wetu ewe Ibrahim? * Akasema: Bali amefanya mkubwa wao huyu, kwa hiyo waulizeni kama wanaweza kutamka. * Wakajirudi kwenye nafsi zao na wakasema: Hakika nyinyi ni madhalimu. * Kisha wakainamisha vichwa vyao, hakika umeshajua kuwa hawa hawatamki. * Akasema: Je, mnaabudu badala ya Mwenyezi Mungu yasiyokufaeni chochote wala kukudhuruni? * Aibu yenu na hivyo mnavyoviabudu badala ya Mwenyezi Mungu, je, hamtumii akili ?.” (Sura Anbiyai: 51 - 67.) Kutokana na usemi huo wakosowaji wakadhania kuwa usemi wa Ibrahim: “Bali amefanya mkubwa wao huyu” kuwa ni uongo usio na shaka kwa kuwa yeye ndiye aliyevunja masanamu na kuyafanya vipande vipande na 55
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:29 PM
Page 56
Sehemu ya pili
aliliacha kubwa lao, basi vipi alihusisha uvunjaji wa sanamu kwa kubwa lao! Niwazi kuwa tuhuma hii haina msingi kabisa, ni mfano wa tuhuma iliyo tangulia, kwa sababu uongo unathibiti katika usemi endapo tu hakutokuwa na kielekezi kinachoonyesha kuwa msemaji hakulikusudia alilolitamka, kusudio la uhakika ila tu amesema kwa lengo lingine, lakini ikiwa kielekezi kipo hapo usemi hauzingatiwi kuwa ni uongo, na kielekezi katika maneno haya ni mambo mawili: La kwanza: Ni usemi wake (a.s.) wakati walipokuwa watu wa mji wanakwenda nje ya mji, aliwasemesha kwa kauli yake:
“Wallahi lazima nitayafanyia vitimbi masanamu yenu baada ya kunipa mgongo.” (al-Anbiyai:57). Haitokuwa sahihi kuuchukulia usemi huu kuwa alikuwa anausema moyoni na fikirani mwake na wala si kwa sura ya kutamka na kuwasemesha waziwazi, bali yachukuliwa kuwa yeye aliyatamka maneno haya na yalitoka mdomoni mwake, hilo ni kwa sababu Ibrahim alikuwa mashuhuri kwa uadui na uchukiji wa masanamu kiasi kwamba hata wao waliporudi mjini kwao na kuyakuta masanamu yao vipande vipande, hawakumdhania vibaya mwingine yeyote isipokuwa yeye, na wakamtuhumu kuyatendea uadui masanamu yao na kuyaharibu na
“Wakasema: Tulimsikia kijana mmoja akiwataja vibaya anaitwa Ibrahim.” (al-Anbiyau:60).
56
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:29 PM
Page 57
Sehemu ya pili
L a pili ni: Jambo linalokubalika kati ya Ibrahim na waabudia masanamu ni kuwa miungu yao, mdogo na mkubwa miongoni mwao hawawezi kutikisika na kutenda, na pamoja na ishara hiyo na kukubalika huko kuliko wazi kati yake na wao, bali pia na kati ya wenye akili wote, ghafla Ibrahim akajibu kwa usemi huu. Hivyo kutokana na hali hiyo inajulikana kuwa hakusema kwa lengo la kukusudia ukweli hasa bali lengo ni lingine, nalo ni ili watu wa kaumu hiyi watanabahi makosa yao. Raziy amesema katika kitabu Al-Aqiidah: “Ya nne: Kuwa yeye alisema ili kuwawajibisha kwa mujibu wa kauli yao, kuwa maadamu yeye ni mungu mkubwa na wamevunjwa wahudumu wake wa karibu kwake, basi haliwezi kutokea hili ila kwake” 33. Na hilo lazidi kufafanuliwa na yale yaliyokuja ndani ya kisa hiki kuwa: Ibrahim baada ya kuvunja masanamu madogo aliweka shoka kwenye shingo la kubwa lao ili aweze kulihusisha sanamu kubwa na uvunjaji wa masanamu kwa kutumia ishara hii ambayo ni chombo kilichotumiwa kutendea uhalifu kinatoa ushahidi kuwa sanamu kubwa ndilo mhalifu na wala si Ibrahim. Inajulikana wazi kuwa tendo hili na ushahidi huu unao dhaniwa kutoka kwa Ibrahim ni jambo linafanana sana na tendo lake la kuwadhihaki watu hawa na kuwakebehi kwa ajili ya wanayoamini. Japokuwa ishara hizo zilikuwepo lakini Ibrahim aliongea neno hili na wala hakuwa anakusudia uhalisia, bali alikuwa na lengo lingine kama Qur’an ilivyobainisha, kwa hiyo ikiwa uhalisia wa usemi wake umekosekana kwa ushahidi wa vielekezi basi uongo haupo. Ama lengo la maneno haya, ilihali yeye aliyaleta kwa sura ya uhalisia japo hakuwa analenga uhalisia, na akawaomba wayaulize masanamu yenyewe kuwa nani ameyatendea hivi, ni kutaka kupata utambuzi wa lile walilokiri ndani ya Aya; naukusudia usemi wao: “Umeshajua fika kuwa hayo hay33. Ismatul-Anbiyai, Uk 41. chapa ya Jidah. 57
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:29 PM
Page 58
Sehemu ya pili
atamki” ili (a.s.) aweze vizuru kuwakemea na kuwakaripia kuwa, ikiwa haya kama msemavyo hayana uwezo wa kutamka basi ni kwanini mnayaabudu “badala ya Mwenyezi Mungu yasiyokufaeni chochote wala kukudhuruni? * Aibu yenu na hivyo mnavyoviabudu badala ya Mwenyezi Mungu, je, hamtumii akili ?.” (Sura Anbiyai: 66 - 67.) Na anasema mahali pengine: “Mwaabudia mnavyovichonga. * Hali Mungu ndiye aliyekuumbeni na munavyovifanya” (Swafatu: 95-96). Kutokana na hayo imebainika kuwa kauli yake: “Bali amefanya mkubwa wao huyu” hayakuwa maneno kwa kukusudia hasa kiasi aweze kusifiwa kuwa muongo bali hayo ni maneno yamefanywa kwa sura ya umakini ili yawe kigezo cha kubatilisha ibada zao na ushirikina wao na itikadi zao kuelekea haya masanamu. Vielekezi vilikuwa vinathibitisha kutokuwepo na makusudio na niya ya uhalisia katika maneno haya. Lau maneno haya yangetoka kwa mtu mwenye akili asiyekuwa Nabii (a.s.), tungeona kuwa inafaa tuseme: Kwa kweli lengo lilikuwa kuwadhihaki na kuwakebehi waabudia sanamu ili kwa hoja hiyo wapate kutanabahi kuwa itikadi zao ni batili. Na aina hii ya mazungumzo na utoaji hoja alioufanya Ibrahim kwa kuwa ulikuwa na nguvu na umadhubuti kwa upeo wa juu kabisa, hawa jamaa hawakuwa na jibu lake isipokuwa kumhukumu aadhibiwe kwa kuunguzwa, na hii ni hali ya kila mfanya mjadala usio wa haki na mbishi endapo atashindwa jibu na kufumbwa mdomo, kama ambavyo (s.w.t.) anasema : “Wakasema mjengeeni tanuli na mumtumbukize ndani ya moto. * Walimfanyia njama tukawafanya wenye kuaibika mno.” (Swafat:97-98). Na katika Aya nyingine: “Wakasema muunguzeni na muwanusuru miungu wenu mkiwa wafanyaji) (al-Anbiyau:68). Huu ndiyo ukweli wa wazi kwa mwenye kukifuatilia kisa hiki ndani ya Qur’an Tukufu, na mwenye kuchunguza kwa makini humo atakuta jibu ni hilo tulilolisema.
58
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:29 PM
Page 59
Sehemu ya pili
Jibu lingine kuhusu swali hili: Na huenda ikajibiwa hivi: Yeye hakusema uongo isipokuwa alikinasibisha kitendo kwa mkubwa wao kwa sharti si kwa kuhitimisha usemi kuwa alifanya, na uongo utathibiti iwapo tu angemnasibishia kitendo kwa kuhitimisha kuwa kilitendeka, kwani alisema: “Bali amefanya mkubwa wao huyu, kwa hiyo waulizeni kama wanaweza kutamka.�. Hivyo inakuwa kama amesema: Amefanya mkubwa wao tendo hili endapo kama masanamu yaliovunjwa yana uwezo wa kutamka. Na kwa sababu kitu ambacho hupatikana kwa kutimia sharti hukosekana endapo sharti lake litakosekana, na kwa sababu sharti halikutimia basi na hali ya mkubwa wao kuwa mvunjaji nayo imekosekana. Sharti hapa ni kule kutamka kwa masanamu. Jibu hili haliendi sawa na maana dhahiri ya Aya kwa sababu Aya ina vitenzi viwili: Kimoja kipo karibu na sharti na kingine kipo mbali na sharti, na kwa mujibu wa kanuni za lugha ya kiarabu ni kuwa sharti latakiwa lihusike na kitenzi cha karibu kati ya vitenzi viwili na si cha mbali, na kuhusika na vitenzi vyote viwili ni kinyume na kanuni na ni kinyume na dhahiri. Ufatao ni ufafanuzi: i. Bali amefanya mkubwa wao huyu: Kitenzi kiko mbali na sharti. ii. Yaulizeni: Kitenzi kiko karibu na sharti. iii. Ikiwa yanatamka: Hili ndilo sharti. Hivyo sharti kuhusika na kitenzi cha kwanza peke yake au vyote viwili ni kinyume na dhahiri, na linaloainika ni kuhusika na kitenzi cha pili, kwa hiyo uamuzi unakuwa aliyefanya ni mkubwa wao hasa kwa hitimisho na si kwa sharti. Bwana Raziy amesema akijibu tuhuma hii: “Tatu: Katika usemi kuna kutanguliza na kurudisha nyuma, inakuwa kana kwamba amesema: Ni 59
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:30 PM
Page 60
Sehemu ya pili
mkubwa wao huyu endapo wanatamka waulizeni, kwa hiyo kukiegemeza kitendo kwa mkubwa wao ni kwa sharti wawe wanatamka, na maadamu si wenye kutamka imezuilika wawe ndio waliofanya”34. Kundi la tatu: Wakosowaji wa ismah ya Ibrahim wametoa dalili kutumia kundi hili la Aya, nazikusudia kauli zake (s.w.t.):
“Na hakika Ibrahim alikuwa katika kundi lake. * Alipomfikia Mola wake kwa moyo safi.* Alipomwambia baba yake na watu wake: Mnaabudu nini? * Je kwa uongo tu, mnataka miungu mingine badala ya Mwenye enzi Mungu? * Basi ni nini fikra yenu juu ya Mola wa walimwengu? * Kisha akatazama mtazamo katika nyota. Na akasema: Hakika mimi mgonjwa. * Nao wakamwacha, wakampa kisogo. * Basi alikwenda kwa siri kwa miungu yao na akasema: Je, nyinyi hamli?” (Aswafati: 83 - 91). Neno “Hakika mimi mgonjwa” wamelitumia kama dalili wakasema: “Hakuwa mgonjwa isipokuwa alisema hilo ili liwe kisingizio cha kuacha 34. Ismatul-Anbiyai cha Al-Fakhru Raziy, Uk 40 - 41, chapa ya Jidah. 60
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:30 PM
Page 61
Sehemu ya pili
kwenda pamoja nao nje ya mji. Zaidi ya hilo ni kuwa usemi wake: “Kisha akatazama mtazamo katika nyota.” tendo lake hilo lafanana na wayafanyayo wanajimu, kwani wao wanafichuwa matukio ya hapa duniani kutokana na hali ya kinyota ilivyo. Jibu: Msingi wa tuhuma ni kuwa yeye (a.s.) alisema “Hakika mimi mgonjwa” hali akiwa si mgonjwa, na hakuna dalili iliyothibitisha madai hayo, kuwa hakuwa mgonjwa, kwa kuwa yawezekana alikuwa mgonjwa kweli wakati ule. Ama kuhusu usemi wake: “Kisha akatazama mtazamo katika nyota.” kwa kuwa inawezekana kabisa kuwa aliangalia mbinguni akiwa anafikiri ili aangalie hali yake je anaweza kwenda pamoja nao au hapana, na waarabu husema kwa mwenye kufikiri: “Aliangalia mbinguni”, yaani alifikiri ili ajibu swali la kaumu, kama ambavyo mmoja wetu anaweza kufanya hivyo anapokusudia kufikiri kitu. Hilo laungwa mkono na hali halisi kwani yeye (a.s.) aliwaambia walipomwita atoke pamoja nao kwa ajili ya sherehe ya sikukuu, ndipo akaziangalia nyota na akawapa habari kuwa yeye ni mgonjwa, na yajulikana kuwa kutoka nje ya mji kwa ajili ya safari fupi ya furaha haikuwa usiku isipokuwa ilikuwa asubuhi-majira ya saa mbili hivi, hivyo kwa kuwa wito wao ulikuwa wakati wa kuchomoza jua na mwanzo wa nyakati za asubuhi isingewezekana kuangalia nyota kwa maana ya kuchunguza hali ya kinyota kwani nyota zilikuwa zimekwisha zama wakati wa kuchomoza jua, kwa hiyo mtazamo huu haukuwa na lengo zaidi ya kufikiri na kuzingatia. Ndiyo lau wangemwita usiku ili waende mchana basi kuziangalia nyota kungekuwa na dhana hiyo waliyoisema lakini hilo halikuthibiti. Naam kuna maana nyingine ya usemi wake: “Kisha akatazama mtazamo katika nyota.” nayo ni (a.s.) alikuwa na homa ya vipindi inayompata wakati mahsusi, wakati huo hujulikana kwa kuchomoza nyota au kuzama kwake, kwa ajili hiyo aliangalia mbinguni na akajua kuwa kipindi cha homa kipo karibu, waarabu huita kukaribia kwa kitu kuwa kimeingia, na kwa ajili 61
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:30 PM
Page 62
Sehemu ya pili
hiyo mtu aliyedhoofishwa na maradhi na anahofiwa kufa wao husema ni maiti. Na Mwenyezi Mungu alimwambia Nabii wake: “Kwa hakika wewe ni maiti na wao ni maiti” (Az-zumar:30). Bwana Raziy amesema: “Ama sura ya pili, nayo ni usemi wake: “Hakika mimi mgonjwa” kuwa nao ni uongo, jibu lake ni: Hatukubali kuwa hakuwa mgonjwa katika wakati ambao ungefuata. Kama ambavyo wewe uwe umejua kuwa utakuwa mgonjwa wakati wa adhuhuri, kisha mtu akualike kwenye dhifa hali ikiwa wajua kuwa hapana budi utakaa na jamaa wakati wa adhuhuri, utasema mimi nina homa, ukiwa unamaanisha kuwa utakuwa mgonjwa wakati huo. Na pia huenda alipokuwa amekurubia kuwa mgonjwa alijiita binafsi mgonjwa, kama ilivyokuja katika kauli yake (s.w.t.): “Kwa hakika wewe ni maiti na wao ni maiti”, Na pia alikusudia mimi ni mgonjwa wa moyo, na makusudio yaliyo moyoni mwake ni miongoni mwa huzuni na majonzi kwa sababu ya ukafiri wao na ubishi wao.”35 Ama kutumia neno ‘katika’ sehemu ya ‘kwenye’ katika kauli yake: “Katika nyota” ni kwa sababu herufi moja huchukuwa nafasi ya nyigine, Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: “Kwa hakika nitakusulubuni katika vigogo vya mitende”, alilokusudia ni juu yake. Mshairi amesema: “Fungua mlango na uangalie katika nyota. Wingi ulioje wa vipande vya usiku vya giza”. Jibu lingine la tuhma: Na yawezekana tuhuma ikajibiwa kuwa: Ni mfano wa mikingamo katika usemi, na mikingamo hapa maana yake ni mtu aseme kitu akiwa anakusudia kitu kingine, na afahamike kinyume na anavyokusudia, kwa hiyo huenda aliangalia kwenye nyota uangaliaji wa mwanatawhidi katika uumbaji wake Mwenyezi Mungu Mtukufu ambao autolea dalili kwa muumba wake na sifa zake, lakini ile kaumu ikamdhania anazitazama mtizamo wa mna35. Ismatul-Anbiyai, Uk 42, chapa ya Jidah.
62
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
12:30 PM
Page 63
Umaasumu wa Mitume
Sehemu ya pili
jimu ili atolee dalili za matukio akasema: “Hakika mimi mgonjwa.”36 Ni wazi kuwa jibu hili msingi wake ni endapo alikuwa si mgonjwa wakati ule, na hilo halijathibiti, na ya kwamba mikingamo haifai kwa manabii kwa sababu ya kutoweka uaminifu kwenye maneno yao. Kwa ajili hiyo hujulikana thamani ya yale waliyoyasema wana sihahi na sunan kupitia njia nyingi kutoka kwa Abu Huraira: Kuwa mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) alisema: Ibrahim hakusema uongo ila mara tatu, mbili katika dhati ya Mwenyezi Mungu: Usemi wake: “Hakika mimi ni mgonjwa” na usemi wake: “Bali amefanya mkubwa wao huyu” na kauli yake kumuhusu Sara: “Yeye ni dada yangu”. 37 Na tayari umeshajua kuwa Ibrahim hakusema uwongo katika sehemu mbili za mwanzo, ama kuhusu ya tatu hiyo imeelezwa ndani ya Taurati iliyopotoshwa je baada ya hayo yawezekana kuitegemea riwaya hii?! La ajabu ni kwamba Ibnu Kathir amekuwa katika kusudio la kuisahihisha riwaya hii na amesema: “Hili halipo kwenye mlango wa uongo wa kweli ambao msemaji wake hulaumiwa, lahasha sivyo ila tu huu umeitwa kuwa ni uongo kimatamko tu, hivyo wenyewe ni miongoni mwa mikingamo katika usemi kwa kusudio la kisharia la kidini kama ilivyokuja katika Hadithi: “Hakika katika mikingamo kuna wasaa wa kutolazimika kusema uongo.”38 Na kadhalika Raziy amesema ndani ya kitabu Ismatul-Anbiyai kama jibu la Hadithi hii: “Nilisema hizi ni miongoni mwa habari zisizo pokewa kwa uwingi, hivyo haiwezi kuipinga dalili ya yakini kama ile ambayo tumeisema. Kisha iwapo ni sahihi basi dhahiri yake ni uongo. Ama usemi wake kumhusu Sara: “Hakika yeye ni dada yangu”, maana yake yeye ni dada yangu katika dini, au kwa kuangalia kunasibika kwake na Adam au kuna36 Tafsir Al-Qur’an Al-Adhim cha Ibnu Kathir, Juz 4, Uk 13. 37. Tafsir Al-Qur’an Al-Adhim cha Ibnu Kathir, Juz 4, Uk 13. 38. Tafsir Al-Qur’an Al-Adhim cha Ibnu Kathir, Juz 4, Uk 13 63
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:30 PM
Page 64
Sehemu ya pili
sibika kwake na mababu wengine�39. Na sisi hatutoi maoni yoyote kuihusu Hadithi hii wala muelekeo alioufanya Ibnu Kathiri na Raziy, isipokuwa tunaacha uwamuzi kwenye dhamira ya msomaji mpendwa, na yatosha udhaifu wa Hadithi hii kuwa ni miongoni mwa riwaya za Abu Huraira, kama itoshavyo kuwa ni Hadithi za Israiliyati ambazo zimekuja ndani ya Taurati iliyopotoshwa. Lakustaajabisha sana ni waelezaji wa Hadithi hii wanawatuhumu Shia kwa usemi wao wa Taqiyah, kuwa inalazimu uongo, ilihali taqiya ni miongoni mwa mikingamo ambayo Qur’an imeruhusu na Sunnah chini ya masharti mahsusi na kwa watu maalumu. Hizi ndizo Aya walizozitumia wakosoaji kuwa ni dalili za kutokuwa na ismah kwa shujaa wa Tawhidi, na tayari umekwishatambua maana yake, na kuna Aya nyingine zimeshuka kumuhusu yeye na huenda zimeangukia mikononi mwa wakosoaji hao na wakazifanya kuwa ni visingizio vyao, na kwa sababu madhumuni ya Aya hizo yako wazi hatuoni haja ya kuziongelea. Katika kusudio hili yatutosha aliyoyasema Sayyid Murtadha katika kitabu chake Tanzihul-Anbiyai kwa atakaye kuyafahamu arejee huko. Pia wao wamezitolea dalili Aya zilizoshuka kumuhusu Yakobo (a.s.) ili kumkosowa, na kwa sababu tuhuma hizi ni dhaifu tumeacha kuziongelea na tumeielekeza hatamu ya kalamu kwenye baadhi ya waliyoyatolea dalili wakosoaji katika kusudio hili kumuhusu mkweli wa zama zake na mtakatifu wa zama zake bwana wetu Yusufu iwe juu yake na juu ya Nabii wetu rehma na amani.
39. Ismatul-Anbiyai, Uk 42. 64
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
12:30 PM
Umaasumu wa Mitume
Page 65
Sehemu ya pili
4 Ismah ya Yusuf Kwa kweli miongoni mwa Aya zilizokuja katika Sura Yusuf ni dalili zilizo wazi mno kuwa yeye ni mtu bora, ambaye hana kifani, na asiyeweza kukurubiwa katika ubora wake. Vipi asiwe hivyo! ilihali Aya zimeonyesha kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amemchaguwa tokea mwanzoni mwa uhai wake na tokea zama za utoto wake na Mwenyezi Mungu alimuelimisha tafsiri ya semi na akamtimizia neema zake. Qur’an imefuatilia kisa hiki na ikakiita kuwa ni kisa kizuri mno miongoni mwa visa, ndani yake mna uthibitisho wa wazi juu ya usafi wake na utakatifu wake na ismah yake dhidi ya dhambi na kuhifadhika kwake dhidi ya kila maasi, na kumalizika kwake katika ridhaa za Mwenyezi Mungu, vipi asiwe hivyo ilihali Mwenyezi Mungu (s.w.t.) alimpa majaribu mema na akamkuta ni nmwenye subira, mwenye kuimiliki nafsi yake kwenye matamanio na yaliyoharamishwa na mwenye kuokoka kutoka kwenye machungu ambayo haokoki kutoka humo isipokuwa aliyefunikwa na ismah Yake (s.w.t.), kwa majaribu haya umedhihiri undani wake na hali yake ya siri, na kwayo ukweli wake umejidhihrisha, na ikabainika kuwa yeye ni mtu ambaye woga wa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) umemsuguwa akawa haghafiliki kumuelekea Mwenyezi Mungu hata kwa kadiri ya mpepeso wa jicho na wala haibadilishi ridhaa yake (s.w.t.) na kitu chochote. Na mwenye kukizingatia kisa hiki atajua kuwa, kuokoka kwa Yusuf kutoka kwenye makucha ya matamanio na hadaa ya mke wa mfalme, kulikuwa si jambo la kawaida, hivyo lau sio ismah yake uokovu haungewezekana bali jambo lingekuwa lashabihiyana na njozi kuliko la mtu aliye macho. Na katika lengo hili Allamah Tabatabai anasema: “Alikuwa mtu mwanaume, na katika silika ya wanaume ni kuvutika kuwapenda wanawake, naye alikuwa kijana, aliyefikia balehe yake, na huo ndio mwanzo wa kuchemka shahawa na kupenya kwa matamanio makali, 65
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:30 PM
Page 66
Sehemu ya pili
na alikuwa mzuri mno kiasi cha kuziduwaza akili na kuzitoa akili, uzuri na urembo huita kwenye matamanio! Hii ni kwa upande mmoja. Na kwa upande mwingine alikuwa amezama katika neema na maisha ya raha, amepambwa na makazi ya heshima, na hali hiyo ni miongoni mwa sababu za kupenda kwa bidii, na malikia alikuwa kijana mzuri mno kama vile hali ya mambo huwa katika nyumba za wafalme na wakubwa, na bila shaka alikuwa amejipamba na mapambo yanayouvuta kila moyo, naye ni mtukufu wa Misri, pamoja na hayo amemuashki huku akiwa ni mwenye huzuni, nafsi yake inampenda, na hapo nyuma amemtendea Yusuf ukarimu na hisani, na hayo yote ni miongoni mwa yanayomzuia mtu kusema na kumfumba mdomo. Na alijitambulisha kwake, na alimwita kwa ajili yake na subira baada ya kujitokeza hayo ni ngumu mno. Huyu mwanamke mzuri sana alimtaka Yusuf na alifanya kila ambalo liko kwenye uwezo wake miongoni mwa ishara na hila na aling’ang’ania kiasi kwamba alifikia kumvuta mpaka akaichana kanzu yake, na subira katika hali hii ni ngumu mno. Huyu mwanamke mwenye enzi hakurudi nyuma wala kusitisha rai yake, naye alimlea Yusuf ikiwa ni jukumu mahsusi alilokabidhiwa na mfalme. Na wawili wote walikuwa ndani ya kasri zuriIkulu zuri- miongoni mwa kasri za kifalme lenye mandhari nzuri ya hali ya juu inayofanya macho yasioni kwa kuzidiwa na mwanga na kuita kwenye maisha ya raha. Na walikuwa wawili hawa katika faragha na alikwishafunga milango na kuteremsha pazia, hali ambayo kukataa kusingemuacha salama dhidi ya shari, na alikuwa mahali paaminifu kiasi kwamba jambo hili lisingetoka nje kwa sababu yeye ni mwanamama mwenye enzi, mkononi mwake mna nyenzo za kulisitiri na kulifanya lisionekane, wala muungano huu haukuwa wa kupita mara moja bali ulikuwa ufunguo wa maisha marefu ya raha, na Yusuf alikuwa anaweza kuufanya muungano huu na upendo kuwa ni sababu ya kuyafikia matumaini na matarajio mema ya maisha kama ufalme, enzi na mali.
66
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:30 PM
Page 67
Sehemu ya pili
Kwa hiyo hizi ni sababu na mambo makubwa, lau yangeelekezwa kwenye jabali yangelipasuwa, au kama yangekutanishwa na jiwe kubwa yangeliyeyusha, hivyo hapakuwa na linalodhaniwa kuwa ni kizuwizi isipokuwa hofu ya kufichuka jambo hili au kizuwizi cha nasaba ya Yusuf au ubaya wa kumsaliti mfalme: Ama hofu ya jambo hili kufichuka imekwishaelezwa kuwa alikuwa katika hali ya usalama. Lau ingekuwa hapana budi hilo litokee, ingekuwa katika uwezo wa malkia kulipa tafsiri kama alivyofanya ilipofichuka habari ya kumtaka kwake Yusuf kinyume na ridhaa yake, alifikia kiasi cha kuiridhisha nafsi ya mfalme, kwa hiyo mfalme hakumchukuwa kuwa ana kosa lolote, na malkia alibadilisha adhabu badala ya kuadhibiwa yeye aka adhibiawa Yusuf kwa kutiwa jela. Ama kizuwizi cha nasaba kama kingekuwa chazuwia basi kingewazuwia nduguze Yusuf wasitende ambalo ni dhambi kubwa na mbaya kuliko zinaa kwani wao walikuwa watoto wa Ibrahim, Is’haka, na Yakub sawa na Yusuf, utukufu wa nasaba haukuzuia kusudio la kumuuwa Yusuf na kumtumbukiza kisimani, na wamuuze kwa wasafiri uuzwaji wa watumwa na walimuhuzunisha baba yao Yakobo Nabii (a.s.) akalia mpaka macho yake yakapofuka. Ama ubaya wa usaliti na uharamu wake ni miongoni mwa kanuni za kijamii, na kanuni za kijamii huathiri tu kwa malipizi yatakayofuatia endapo kutafanywa kinyume, na hilo hutokea endapo mtu atakuwa chini ya mamlaka tekelezi yenye nguvu na serkali adilifu, na endapo ikighafilika nguvu tekelezi au ikawa fasiki na ikazembea au uovu ukafichika mbele ya macho yake au ukatoka nje ya mamlaka yake, hapo kanuni hizi hazitokuwa na athari yeyote. Kwa hiyo Yusuf (a.s.) hakuwa na kitakachomuwezesha kujilinda nafsi yake na kuzishinda sababu hizi zenye nguvu alizokuwanazo malkia dhidi ya Yusuf isipokuwa ni asili ya tawhidi ambayo ni kumuamini Mwenyezi Mungu. Na ukipenda utasema: Mahaba ya kiungu ambayo yalijaza uwepo wake na yakaushughulisha moyo wake hayakuki67
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
12:30 PM
Umaasumu wa Mitume
Page 68
Sehemu ya pili
achia kitu kingine nafasi hata nafasi ya kidole.”40 Huu ndio ukweli wa kisa lakini baadhi ya wakosowaji hawakuridhia Yusuf awe na heshima na ubora na wameendelea kutolea dalili yaliyokuja ndani ya Qur’an ili wathibitishe kutokuwa kwake na ismah kuhusiana na mke wa mfalme wa Misri yule ambaye yeye Yusuf alikuwa nyumbani mwake. Amesema (s.w.t.):
“Na ambaye yeye nyumbani mwake alikuwamo akamtamani kinyume na nafsi yake, na akafunga milango na akasema: Njoo. Akasema: Najikinga kwa Mwenyezi Mungu, bila shaka (mumeo) yeye ni bwana wangu ametengeneza makazi yangu vizuri. Hakika madhalimu hawafanikiwi. * Na hakika alimkazia nia na akamkazia nia, laula asingeliona burhani ya Mola wake. Hivyo ndivyo ilivyotokea ili tumuepushie kila jambo la aibu na uovu. Hakika yeye alikuwa miongoni mwa waja wetu waliotakaswa.” (Yusuf: 23-24). Na mahali panapojengewa hoja ya dalili ni kauli yake: Na akamkazia nia” kwani kumkusudia kwake yule mwanamke kulikuwa sawa na kusudio la mwanamke kwake, na lau asingeona burhani ya Mola wake angefanya, kuiona burhani kumemzuia asifanye kosa baada ya kulikusudia. Na kwa ibara nyingine: Kwa hakika mkosoaji ameifanya kiungwa na kiungiwa , yaani kauli “Na hakika alimkazia nia” na kauli “Na akamkazia nia” kila 40. Al-Miizan. Jalada 11 Uk 137 - 139. 68
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:30 PM
Page 69
Sehemu ya pili
moja kuwa usemi unaojitegemea usiotegemea chochote, kwa hiyo inakuwa kama amesema: “Na hakika alimkazia nia”, yaani bila sharti na kizuizi chochote. “Na akamkazia nia”, kwa dhumuni na lengo lisilo na sharti. Kisha baada ya hayo, yaani baada ya kutoa habari ya kuthibiti uamuzi toka pande zote mbili akarejea kusema kuwa malikia alibaki na upendo mpaka aliposhindwa, lakini Yusuf aliacha kutenda kwa sababu ya kuiona burhani ya Mola wake, na kwa ajili hiyo alisema: “Laula asingeliona burhani ya Mola wake.” yaani lau kama si uonaji wa burhani angetenda madhambi, lakini yeye aliona, kwa hiyo hakufanya wala hakutenda. Hivyo jibu la tamko Laula halipo, hivyo linakisiwa kuwa ni Angefanya. Kisha wakosoaji wametafsiri Aya kwa msaada wa Hadithi zinazotajwa kuwa ni Israiliyati ambazo hazifai kunakiliwa kwani hadithi zisizokuwa na wapokezi wengi hunakiliwa ili tu msomaji awe anazijua. Wamesema: Yusuf alikaa ukaaji wa msaliti na ilimuwahi burhani ya Mola wake na ilimuokoa asiangamie. Kisha wao wamefuma fikra za kimawazo katika kuitafsiri burhani hii inayoonwa wakasema: Kwa kweli ndege alituwa juu ya bega lake na akamnong’oneza sikioni: Usifanye ukifanya utaporomoka kutoka kwenye daraja ya manabii. Tafsiri nyingine inasema kuwa: Alimwona Yakobo (baba yake) ameuma kidole na akasema: Oh! Yusuf! Je, haunioni mimi. Na kuna tafsiri nyingine mbali na hizo za upotovu ambazo kalamu inaona haya kuzinakili. Ila tu ili kuiondoa pazia kwenye dhumuni la Aya kunategemea uchunguzi kuhusu mambo kadhaa: i. Nini maana ya Al-Hammu, yaani kumkazia nia katika kauli yake “Na akamkazia nia”? ii. Nini jibu la “Laula asingeliona burhani ya Mola wake.”? Na hii ndio nguzo katika tafsiri ya Aya. iii. Nini maana ya burhani? iv. Dalili ya Aya juu ya ismah ya Yusuf. Ufuatao ni ufafanuzi wake na tafsiri yake moja baada ya jingine. 69
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
12:30 PM
Umaasumu wa Mitume
Page 70
Sehemu ya pili
I. Nini maana ya al-Hammu - Kumkazia nia: Ibnu Mandhur amefasiri katika kitabu chake Lisanul-Arabi kuwa: “Amekinuwia. Amekitaka na Amekiazimaia. Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amesema: “Na wakaazimia wasiyoweza kuyafikia” (Tawba:74). Wanahistoria wameeleza kuwa kundi katika wanafiki waliazimia kumuuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s .a .w.) alipokuwa akirudi kutoka Tabuk, kwa ajili hiyo walisimama kwenye njia yake, walipomkaribia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) aliamuru waondolewe na aliwataja majina mmoja mmoja 41. Hii ndio maana ya al-Hammu na yaungwa mkono maana hii na Aya zingine ambazo neno al-Hammu limo humo, na endapo litatumika kwa maana ya kuwaza kitu akilini japokuwa azma ya kitu hicho haijatokea basi matumizi hayo ni ya nadra sana na Kitabu kitukufu hakichukuliwi kwa maana hiyo. Zaidi ya hayo ni kuwa al-Hammu sehemu hizi mbili ina maana moja, na kwa kuwa al-Hammu ya malikia ilikuwa ni azma na utashi, itawajibika kuichukulia al-Hammu ya Yusuf nayo kwa maana hiyo hiyo na si kwa maana ya kuwaza kitu akilini, kinyume na hivyo itakuwa ni kutenganisha kati ya matamko mawili katika maana bila ya dokezo. Lakini kuthibiti kwa moja kati ya al-Hammu mbili bila ya nyingine nayo kuthibiti, ni kwa sababu al-Hammu ya Yusuf ilikuwa kwa sharti la kutoiona burhani ya Mola wake, na kwa kuwa kisichokuwepo kimegeuka na kuwa kipo na akaiona burhani basi kimsingi haikuthibiti al-Hammu hii, kama itakavyokubainikia. Ndio hatukatai kuwa al-Hammu huenda ikatumika mkabala na azma kwa msaada wa dokezo, Kaabu bin Zuheir amesema: “Kiwango gani wamefahamu kutoka kwa Sayyid mutawasii. Na kutoka kwa mtenda mema ametaka au ameazimia.”
41. Majmaul-Bayani. Jalada 3. Uk. 51. na nyingine. 70
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:30 PM
Page 71
Sehemu ya pili
Lakini kupambanisha kati ya al-Hammu na azma imewajibisha kuichukulia al-Hammu kwa maana ya kuwaza akilini, na laiti kama si hivyo basi ingechukuliwa kwa maana hiyo hiyo ya azma. Kama ambavyo huenda ikatumika kwa maana ya kukaribia, kwa hiyo waarabu husema: Alikuwa karibu kufanya kitu fulani na fulani, hivyo hutumia neno al-Hammu kwa maana ya kukaribia. Na kwa vyovyote vile ni kuwa maana inayodokezwa na neno al-Hamu katika Aya ni azma na utashi. II. Nini jibu la: Laula? Hapana shaka kuwa Laula katika usemi wake (s.w.t.): “Laula asingeliona burhani ya Mola wake.” huiingia mwanzo wa sentensi kwa mujibu wa kiarabu, hivyo haiingii isipokuwa mwanzoni mwa sentensi. Ibnu Maliki amesema: “Laula hulazimiana na mwanzo wa sentensi. Na miongoni mwa yasiyokuwa na shaka ni kuwa Laula ambayo huingia mwanzoni mwa sentensi huwa yahitajia jawabu, na aghlabu jawabu huwa limetajwa. Mfano wa usemi wa msemaji: “Walikuwa thamanini au walizidi wanane. Laula si kukutumainia wewe wangekwishauliwa watoto wangu”. Kwa hakika riwaya zimekithiri kutoka kwa Khalifa Umar bin AlKhatabi kuwa amesema kwenye maeneo ya hatari: Laula si Ali Umar angeangamia.”. Na huenda jawabu lake likaondolewa kwa sababu ya kuwepo dokezo lijulishalo na kufahamisha jibu kutokana na mtiririko wa maneno kama usemi Wake (s.w.t.):
“Na laula si fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema yake, na kwamba Mwenyezi Mungu ni Mpokeaji wa toba, Mwenye hekima” (An-Nuru:10).
71
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:30 PM
Page 72
Sehemu ya pili
Yaani laula si fadhila za Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema zake mngeangamia. Na huenda jawabu likaondolewa kwa sababu ya kujulishwa na sentensi ya nyuma yake, mfano wa usemi wake: “Ungelihiliki laula si kukuwahi kwangu”. Na usemi wake: “Ungeliuwawa laula si kukuokoa kwangu.” Maana yake ni kuwa laula si kukuokowa kwangu ungeangamia. Na laula si kukuokoa kwangu ungeuwawa. Na mfano wa laula ni huo huo kwa herufi zingine za sharti. Raziy amesema : Haiwezi semwa hivi: Inabidi jibu la tamko Laula liwe limeitangulia sentensi na ikisiwe hivi: “Laula asingeliona burhani ya Mola wake angemkazia nia kwa kumkaribia”. Na kutangulia jibu la Laula haifai. Kwa sababu sisi tunasema: Hatukubali kuwa kutangulia kwa jawabu la Laula haifai… Na dalili juu ya hilo ni kauli Yake (s.w.t.): “Alikaribia kudhihirisha laula tusingemuimarisha moyo wake”. Na pia lau asingeitanguliza sentensi ya kabla ya Laula kuwa ndio jibu lake, basi jawabu lake lingekuwa limeondolewa. Na endapo suala litajiri kati ya jibu kuondolewa na kutangulizwa, bila shaka kutangulizwa jibu ni bora. Na ukisema: Ni faida gani iliyopo katika kauli yake: “Na akamkazia nia laula asingeliona burhani ya Mola wake.” Nitasema: “Faida iliyopo ni kutoa habari kuwa kuiacha azma ya jambo na kuacha kumjibu malikia utashi wake hakukuwa kwa sababu ya kutopenda wanawake kwa ajili ya kutoweza lakini yeye aliacha hilo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu akitaka thawabu Yake (s.w.t.) na kuikimbia adhabu yake kali.”42 Na kwa ujumla: Hapana ishkali kuwa jibu la herufi ya sharti ni jumuishi na jibu la Laula ni mahsusi, huondolewa kwa sababu ya kufahamika kwake kutokana na mtiririko wa maneno au kwa dalili ya maneno yaliyotangulia, na hali ya hili tunalolijadili ni sawa na hili la pili, kwa hiyo kauli Yake 42. Ismatul-Anbiyai cha Fakhru Raziy. Uk. 55-56. Chapa ya Jidah. 72
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:30 PM
Page 73
Sehemu ya pili
(s.w.t.): “Na hakika alimkazia nia na akamkazia nia, laula asingeliona burhani ya Mola wake.” huchanguka na kuwa sentensi mbili: Moja haina sharti na nyingine ina sharti. Ama isiyokuwa na sharti ni kauli yake “Na hakika alimkazia nia” hiyo yajulisha kuthibiti kwa al--Hammu kutoka kwa malikia wa Misri bila ya kusitasita. ama iliyo na sharti ni kauli yake: “Na akamkazia nia laula asingeliona burhani ya Mola wake.” Na kisio lake ni “Laula asingoona burhani ya Mola wake angemkazia nia.”. Kwa usemi huu yajulisha kutothibiti al--Hammu upande wa Yusufu alipoiona burhani ya Mola wake. Ama kuhusu sentensi iliyoitangulia Laula, ambayo ni kauli yake “Na akamkazia nia” haijulishi kuthibiti kwa al-Hammu na kwa kuwa yenyewe sio sentensi iliyojitenga mbali na ile ya baada yake, hata ijulishe kuthibiti kwa al-Hammu bali imechukuwa nafasi ya jawabu, basi yenyewe inakuwa ni sharti iliyotungikwa. Ufafanuzi utakufikia kikamilifu hivi punde. III. Burhani ni nini? Burhani ni hoja na huwa yakusudiwa sababu inayoleta yakini, yaani sababu inayomfanya mtu aelewe kitu kwa yakini bila shaka yoyote, Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amesema: “Basi hizo zitakuwa burhani mbili zitokazo kwa Mola wako kwa ajili ya Firaun na wakuu wake.” (alQaswasu:32). Na amesema (s.w.t.): “Enyi watu! bila shaka imewafikieni burhan kutoka kwa Mola wenu” (an-Nisaa :174). Na amesema (s.w.t.): “Je, kuna mungu mwingine asiye Allah? Sema leteni burhani zenu ikiwa kweli ni wakweli” (an-Nahlu :64). Kwa mujibu huo burhanu ni hoja yenye yakini ambayo yaudhihirisha ukweli wala haiachi shaka kwa mwenye shaka, kwa hiyo ni wajibu ijulikane ni burhani ipi hii aliyoiona Yusuf? Na ambalo laweza kuwa sadikisho la burhani eneo hili ni elimu ya wazi na yakini ionwayo ambayo yaikokota nafsi ya mwanadamu kuelekea kwenye 73
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:30 PM
Page 74
Sehemu ya pili
utii ambao haumpotoshi na kumpeleka kweye maasi, na ni ufuataji usio na uhalifu. Na tulifafanuwa tulipokuwa tunajadili uhalisiya wa ismah kuwa mojawapo ya misingi ya ismah ni elimu ya yakini kuhusiana na matokeo ya madhambi na uhalifu, elimu isiyoghilibiwa, na kufichuka kusiko shindwa. Na hii ni elimu ambayo aliyokuwanayo Yusuf ndiyo iliyomzuia asifanye alilolipendekeza mke wa muheshimiwa mfalme. Na yawezekana ikawa kusudi lake ni mambo mengine ambayo yanabubujisha ismah kwa waja, mambo ambayo tuliifafanua hali yake katika utafiti wa uhalisiya wa ismah. Raziy amesema alipobainisha burhani hii ambayo Yusuf (a .s) aliiona: “Endapo utasema: Ni burhani gani ambayo Yusuf (a.s.) aliiona? Nitasema: Jibu kuhusiana na swali hilo, kuna mitizamo minane: Wa kwanza: Ni hoja ya Mwenyezi Mungu katika kuharamisha zinaa na elimu ya yatakayomkabili mzinifu miongoni mwa adhabu, hilo amelisema Muhammad bin Kaaby. Wa pili: Alichompa Mwenyezi Mungu miongoni mwa adabu za manabii wake miongoni mwa utawa na kuilinda nafsi kwa kuiweka mbali na matendo machafu… Wa nne: Kutoka kwa Imam Swadiqi (a.s.): “Unabii uzuiao kutenda machafu”.43 IV. Aya ni dalili juu ya ismah ya Yusuf. Kwa hakika Aya hii pamoja na upande waliokwenda wakosowaji lakini bado yajulisha juu ya ismah ya Yusuf kabla ya kujulisha kinyume chake. Ufafanuzi wake ni kuwa: Kwa kweli (s.w.t.) ametaja al-hammu ya malikia kwa sura ya isio na sharti lolote, akasema: “Na hakika alimkazia nia” na ameibainisha al-hammu ya Yusuf kwa aina ya sharti, amesema: “Na akamkazia nia laula asingeliona burhani ya Mola wake.”, na sentensi yenye maneno yenye sharti haijulishi kupatikana kwa pande mbili, husu43. Ismatul-Anbiyai cha Fakhru Raaziy. Uk. 56. Chapa ya Jidah. 74
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:30 PM
Page 75
Sehemu ya pili
sani ikiwa ina neno Laula lijulishalo kutotokea kwa pande mbili. Na endapo utasema: Kwa kweli al-hammu zote mbili hazina sharti lolote hata ile al-hammu iliyokuja kumuhusu Yusuf, ila tu yalazimu kulihusisha ikiwa tutasema kuwa inaruhusiwa jawabu la Laula ya kuzuia kutangulia kabla ya laula yenyewe, ilihali haifai kwa maafikiano ya wanalugha. Kwa hiyo kauli yake: “Na akamkazia nia” inakuwa haina sharti lolote, kwa sababu sio jawabu la neno Laula. Nitasema: Kwa hakika jawabu la Laula limeondolewa na kisio lake ni “Angelimkazia nia” na wala jumla iliyotangulia si jawabu lake hata isemwe kuwa kutangulia jawabu haifai kwa maafikiano, pamoja na hivyo bado sentensi hiyo si isiyo na sharti, bali nayo pia imewekewa sharti lilelile lililoko kwenye jibu, kwa sababu endapo jibu likiwa limewekewa sharti basi sentensi itakayochukuwa nafasi yake itakuwa mfano wake. Na hili lina mfano katika Kitabu Kitukufu mfano wa kauli yake: “Na laula tusingelikuimarisha ungelikuwa karibu kuwaelekea kidogo” (al-Israa:74). Maana yake ni kuwa yeye (s.w.t.) amemfanya Nabii wake abaki thabiti hivyo kuelemea wala kukaribia vyote viwili havikupatikana. Na amesema (s.w.t.):
“Na laula si fadhila za Mwenyezi Mungu juu yako na rehma zake, bila shaka kundi moja miongoni mwao lingekusudia kukupoteza, wala hawazipotezi ila nafsi zao wala hawatakudhuru chochote.” (Annisaa:113). Na maana ni kuwa fadhila zake (s.w.t.) juu ya Nabii wake zimegeuka na kuwa sababu ya kutokukusudiwa na kundi kutompoteza, na Aya hii ni mfano wa Aya mbili ila tu jawabu katika Aya hii limeondolewa kwa sababu sentensi iliyotangulia inajulisha kinyume na zile mbili. 75
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:30 PM
Page 76
Sehemu ya pili
Na matunda ya maneno haya ni kwamba katika Aya hii na nyinginezo zinazofanana jawabu huwa halipo kwa sababu ya kukosekana sharti lake, ila tu sentensi hizi hutumika endapo tu kutakuwa na mazingira mazuri ya kuthibiti jawabu lake japo halijathibiti kwa sababu ya kukosekana sharti, na kwenye Aya hii mazingira ya kupatikana al-hammu yalikuwepo upande wa Yusuf kwa sababu ya kuwa na nguvu ya matamanio na aina nyinginemiongoni mwa nguvu za matamanio ya nafsi. Hali hizi zilikuwa ni sababu za msingi za kutokea al-Hammu ya machafu, lakini haikufanikiwa na haikuathiri chochote kwa sababu ya kuiona burhani ya Mola wake, na ufunuo wa yakini ambao humzuia Nabii kutenda maasi au kuyakusudia. Na ukipenda utasema: Yamemzuia mapenzi ya kiungu yaliyotawala uwepo wake na yameushughulisha moyo wake, kwa hiyo hayakuacha nafasi kwa kitu kingine hata kwa kadiri ya unyayo, hivyo yakazuwia kila kinachokuwa kinyume na mapenzi haya. Hili ndilo funzo la Aya hii, na mwenye kuchunguza tangulizi nne tulizozitanguliza hatokuwa na shaka ndani yake. Kwa mujibu huo kwa kuwa Lam katika kauli yake (s.w.t.): “Wa laqad hammat bihi” ni ya kiapo, basi maana ya kauli yake “Na akamkazia nia” inakuwa katika hukumu moja sawa la ile sentensi ya kuungia, na hapo maana yake inakuwa: Wallahi mke wa mfalme alimkazia nia na wallahi laula Yusuf asingeliona burhani za Mola wake, naye pia angemkazia nia, lakini yeye kwa ajili ya kuiona burhani na kuhifadhika kwake, Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amemuondolea uovu na uchafu, kwa hiyo yeye hakukusudia chochote wala hakufanya kitu kwa ajili ya muono ule.
Maswali na majibu Kwa ajili ya kuondoa pazia kwenye ukweli kikamilifu ni wajibu kuyajibu maswali kadhaa yanayochochewa kuhusiana na Aya hizi, ubainifu na majibu yake yanakujia kama ifuatavyo: Swali la kwanza: Kwa hakika tafsiri ya al-Hammu iliyokuja katika Aya kwa maana ya kuaz76
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:30 PM
Page 77
Sehemu ya pili
imia maasi pande zote mbili, upande wa Yusuf na wa malikia ni marudio yaliyokuja kutoka Aya iliyotangulia kwa sura ya wazi kabisa, nayo ni kauli Yake: “Na ambaye nyumbani mwake alikuwamo, akamtamani kinyume cha nafsi yake, na akafunga milango, na akasema: Njoo...” Kwa ubainifu huu uliyo wazi hakuna sababu ya kuirudia mara ya pili kwa usemi Wake: “Na hakika alimkazia nia na akamkazia nia” hususan katika: “Na hakika alimkazia nia” kwani madhumuni ya ibara hiyo yamo katika Aya iliyotangulia tena kwa sura ya wazi kabisa, yaani katika kauli Yake (s.w.t.): “Njoo...”?! Jibu: Sababu ya kukariri sio kuifahamisha maana ileile mara ya pili bali sababu ni kubainisha jinsi Yusuf alivyookoka dhidi ya shari hii. Na kwa ajili hiyo amerejea kwenye maudhui ileile ili akumbushe matokeo ya kisa na mwisho wake. Na huu ni mfano wa mtu ahadithiapo kuhusu watu wawili wanaozozana na mmoja kati yao kumdhuru mwingine na utayarifu wa ule upande mwingine kujilinda, akishaleta taswira hiyo hutaka kuashiria matokeo ya mzozo huo hivyo hurejea tena kubainisha asili ya kisa ili matokeo yake yawe wazi na matokeo yake ya mwisho yajulikane. Aya mbili hizi ziko katika mfano huo. Kwa mujibu huo inadhiri kuwa yale aliyoeleza mwandishi wa tafsiri ya almanar katika wazo hili sio sawa, pale aliposema kuwa: Kutokana na kisa hiki imejulikana fika kuwa huyu mwanamke alikuwa ameazimia alilomtakia azma thabiti, tena mwenye kusisitiza bila kutaradadi hata chembe, na wala hapana kizuwizi upande wa Yusuf kinachoweka pingamizi kwa litakiwalo, hivyo basi haifai isemwe kuwa: Malikia alimkusudia kwa kusudi lisilo na sharti, kwa sababu al-Hammu ni kukikurubia kitendo chenye kutaradadiwa.44 Maneno yamebakia katika tafsiri ya al-Hammu nayo kulingana na tafsiri yake maana yake ni kukikurubia kitendo anachotaradadi kukifanya. Maana 44.Tafsirul-Manar Jalada 12. Uk. 286. 77
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:30 PM
Page 78
Sehemu ya pili
hiyo haitokuwa sahihi katika kauli Yake (s.w.t.): “Na wakafunga nia ya kumfukuza Mtume” (al-Tawbah:13) yaani kumtoa Mtume Makka, wao walikuwa wamekata shauri kufanya hivyo na walimfanyia njama usiku maalumu wajulikana katika sira na historia. Kama ambavyo sio sawa katika kauli Yake (s.w.t.): “Na wakaazimia wasiyoweza kuyafikia” (Tawbah:74) walipojaribu wanafiki kumfurusha ngamia wa Nabii (s.a.w.) katika Aqabah alipokuwa akirejea kutoka kwenye shambuliola Tabuk. Swali la pili: Kwa kweli kuitafsiri Burhani kuwa ni ismah haiendi sawa na matumizi yake mengine ndani ya Qur’an, kwa mfano Burhani katika kauli Yake (s.w.t.): “Basi hizo zitakuwa burhani mbili zitokazo kwa Mola wako” (Al-qaswasu:32) maana yake ni miujiza ya Musa miongoni mwa fimbo, mkono mweupe, kwa mujibu huo ni wajibu kuifasiri burhani kwa maana ya kitu kinachowafikiana na muujiza na wala sio ismah ambayo miongoni mwa maana zake ni elimu?! Jibu: Kwa kweli Burhani kwa maana ya hoja, kuna mara yaafikiana na muujiza na mara nyingine yaafikiana na elimu kwa maana ya mtu kufichukiwa kikamilifu, na yakini ionwayo ambayo yamlinda mtu asitende maasi, na tulikwishaeleza katika utafiti kuhusu uhalisiya wa ismah kuwa, yenyewe haimuondolei uwezo na hiari. Hivyo yenyewe ni hoja ya Nabii katika wakati wake wa baadae na hivi punde, na ni dalili maishani mwake mpaka afikapo kwenye maisha yake ya furaha. Swali la tatu: Kwa kweli kauli Yake (s.w..): “Hivyo ndivyo ilivyotokea ili tumuepushie kila jambo la aibu na uovu.” ni dhahiri kuwa aibu si uovu, hivyo iwapo kauli yake: “Na hakika alimkazia nia na akamkazia nia” itatafsiriwa kwa maana ya kuazimia maasi basi italazimu maneno hayo yawe na maana moja, nayo ni kinyume na maana yake ya dhahiri?! 78
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:30 PM
Page 79
Sehemu ya pili
Jibu: Kwa hakika makusudio ya aibu, ni al-Hammu na azma, na linalokusudiwa na uovu ni kitendo chenyewe, kwa hiyo Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ameondoa al-Hammu yenyewe kwa baraka ya ismah na akakanusha kutenda vyote viwili. Allamah At-Tabatabaiy amesema: “Yafaa mno kusema kuwa: Maana ya aibu ni kulikusudia tendo na kulielemea, kama ambavyo maana ya uovu ni kutenda uovu, nayo ni zinaa”. Kisha amesema: “Na miongoni mwa ishara nzuri ni ile kauli Yake: “Ili tumuepushie kila jambo la aibu na uovu.” kwani amefanya aibu na uovu kuwa vitu vilivyoepushwa mbali na yeye, na si kuepushwa mbali na wao wawili. Kwa sababu kwenye hili la pili kuna dalili kuwa yeye alikuwa na jambo ambalo lapelekea kujiingiza kwenye mawili hayo na yahitaji aepushwe nalo, na hilo lapingana na ushahidi Wake (s.w.t.) kuwa yeye ni miongoni mwa waja waliotakaswa, nao ni wale ambao Mwenyezi Mungu amewatakasa na kuwachaguwa kwa ajili yake, hakuna yeyote anayeshirikiana nao katika kitu chochote na wala hawamtii mwingine yeyote miongoni mwa ushawishi wa shetani, au pambo la nafsi au sababu yoyote mbali na Mwenyezi Mungu (s.w.t.). Kisha Mwenyezi Mungu akasema: “Hakika yeye alikuwa katika waja wetu waliotakaswa” alipoelezea sababu ya kauli yake: “Hivyo ndivyo ilivyotokea ili tumuepushie kila jambo la aibu na uovu.”, maana yake ni kuwa tumemtendea Yusuf kama hivi kwa kuwa yeye ni miongoni mwa waja wetu tuliowatakasa na kuwachaguwa. Kutokana na Aya hii yadhihiri kuwa ni hadhi ya watakaswa kuona burhani ya Mola wao, na kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) huwaepushia mbali kila aina ya aibu na uovu na wala hawatendi maasi wala hawayakusudii kwa vile Mwenyezi Mungu anawaonyesha burhani yake, na hii ndiyo ismah ya kiungu.45
45. Al-Mizan, Juz 11, Uk 142. 79
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:30 PM
Page 80
Sehemu ya pili
Swali la nne: Lau makusudio ya “burhani ya Mola wake” ni ismah basi kwa nini (s.w.t.) amesema “Asingeliona burhani ya Mola wake” kwa kuwa neno hili linawiana na vitu vinavyohisiwa, kama miujiza na karama, na wala sio ismah ambayo yenyewe ni elimu inayoshinda haishindwi na yamlinda mwenye kuwa nayo asifanye maasi?! Nasema: Kwa sababu Arru’uya “kuona” hutumika katika kuona viyu vya kimada vya hisia na vinavyoonekana kwa macho, pia hutumika katika idraki ya kimoyo na kuona kwa jicho la moyo, Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amesema: “Moyo haukukosea ulichoona” (An-najmu:11). Na kauli yake (s.w.t.): “Mwenye kupambiwa matendo yake maovu na akayaona kuwa ni mema!” (Faatir:8). Na kauli Yake (s.w.t.): “Walipojuta na kuona kuwa wamekosa walisema; lau Mola wetu asingeturehemu na kutughofiria tungekuwa miongoni mwa waliohasirika”. (Aarafu:149) Aya hizi na zilizo mfano wake kwa wazi zaonyesha kuwa Ru’uya “kuona” hutumika katika utambuzi wa moyo, kuwaza na kuhisi kwa ndanindani. Kwa mujibu huo Yusuf mkweli aliposimama mkabala wa maono yale yanayochombeza, ambayo huondoa ubongo na akili kwa mwanadamu, na ilikuwa yatazamiwa kwa kuwa yeye ni binaadamu basi aelemee kwenye kuingiliana naye na kuazimia kutenda maasi, lakini yeye alipotambuwa kwa elimu ya mkato athari ya maasi yale, elimu ile ilimuhifadhi asifanye azma na kusudio la kuingiliana naye. Hii ndiyo maana teule katika Aya hii na kwayo wadhihiri utakasifu wa Yusuf dhidi ya aina yoyote ya kusudi na azma ya kuingiliana naye. Na kuna tafsiri nyingine ya Aya hii inaafikiana na maana teuliwa katika kumtakasa Yusuf dhidi ya kila lisilolingana na hadhi ya unabii, ingawa kuafikiana kwa maana hii na Aya ni kwa daraja la pili. Maana hii ndio aliyoichaguwa mwandishi wa tafsiri ya Al-Manar, na baadhi ya watu wa kileo wameipamba na kuiremba. Ufafanuzi wa mwandishi wa Al-manar na 80
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:30 PM
Page 81
Sehemu ya pili
yaliyoelezwa na wanaenzi hii utakuijia katika utafiti ujao. Maana ya pili ya Aya Kwa kweli makusudio ya al-Hammu sehemu zote mbili ni kuazimia kupiga na kuuwa, mfano wa kauli Yake (s.w.t.): “Na wakaazimia wasiyoweza kuyafikia” (Atawbah:74) kwa kuwa washirikina walikusudia kumuuwa Nabii (s.a.w.) alipokuwa akirudi kutoka Tabuk, kwa hiyo maana inakuwa: Mke wa mfalme wa Misri alikusudia kumpiga na kumjeruhi, na kwa kawaida Yusuf hakuwa na lakufanya ila kujilinda binafsi lakini aliona hilo lingesababisha kumjeruhi mke wa mfalme, nalo lingempa kisingizio mkononi mwake kumtuhumu Yusuf na kumzulia uongo, naye aliitambuwa hali hii kwa hiyo alikimbilia mlangoni ili kujiepusha naye. Kwa mujibu huo maana ya al-Hammu sehemu zote mbli ni kupiga, lakini hilo upande wa malikia lilikuwa kwa msukumo na kwa upande wa Yusuf kwa msukumo mwingine. Na elekezo hili linalingana na hali ya mwenye ashki mwenye huzuni anapopupia kulipata alipendalo na moyo wake una shauku ya kulipata, huyu akiwa katika msimamo kama huu hali yake ya ndani humsukuma kulipiza kisasi kwa ampendae ambaye hakuwa pamoja naye kwa alilolitaka, na wala hakumtimizia lengo lake. Na hili lilitokea kwa malikia, kwani yeye alipopupia kulipata alilolitaka kwa Yusuf mawazo yalimsukuma ahisi kuwa amevunjwa moyo nahapo akapupia kumkomowa Yusuf, na hii ndio maana ya kauli yake: “Na hakika alimkazia nia” kwa kuiachia bila ya sharti lolote. Yusuf hakuwa na la kufanya katika hali hii isipokuwa kujilinda nafsi yake, lakini yeye alipoona kumpiga malikia huenda kukafanywa kisingizio cha kuzushiwa uongo na kutuhumiwa, alijizuwia kumpiga na kumkusudia, na hii ndio maana ya kauli yake: “Na akamkazia nia laula asingeliona burhani ya Mola wake.”.
81
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:30 PM
Page 82
Sehemu ya pili
Na maana hii ndio iliyochaguliwa na baadhi ya wanatafsiri na pia ameichaguwa mwandishi wa Al-manar, na alifanya juhudi kuifanya iwe na nguvu kwa kauli Yake (s.w.t.): “Wallahi mwanamke alimkusudia kumpiga kwa sababu ya kutotii amri yake huku akijiona kuwa ni bibi mwenye mamlaka juu yake, naye Yusuf ni mtumwa kwake na tayari amejidhalilisha nafsi yake kwake, kwa kule kumtaka wazi wazi baada ya hila ya kumtaka kinyume na nafsi yake, na kulingana na hali ya mwanamke ndiye huwa mtakiwa na si mtakaji, lakini huyu mtumwa wa kiebrania amegeuza mambo kinyume na ameiparaganya nidhamu ya kimaumbile kwa kumtoa mwanamke nje ya tabia yake ya kike kwa kule kuhifadhika kwake, na amemteremsha bibi malikia kutoka kwenye enzi ya mamlaka yake. Hapo ndipo alipomkusudia kumuonyesha mabavu ghadhabu zilipompanda, nacho ni kisasi kilichozoeleka kwa watu mfano wake, na walio chini yake katika kila zama na mahali.”46 Kisha mmoja miongoni mwa wanakileo ameichaguwa maana iliyotajwa ila tu amelifasiri neno “Burhani ya Mola wake” kwa sura nyingine isiyokuwa hiyo iliyotajwa katika rai hii, bali ameifasiri kwa maana ya kufunguka mlango kwa utashi wa Mwenyezi Mungu (s.w.t.), kwa kuwa mke wa mfalme alikuwa amekwishafunga milango na kuziimarisha komeo zake. Na baada ya kutokea hali hii ya mvutano kati yake na Yusuf, aliukimbilia mlango kumkimbia yule mwanamke na hapo mlango ulifunguka kwa ajili ya Yusuf kwa utashi wake Mwenyezi Mungu (s.w.t.), na hii ndiyo burhani ya Mola aliyoiona. Na linalojulisha hili ni kuwa Qur’an inaeleza wazi wazi kufungwa kwa milango wala haijataja chochote kuhusu kufunguka, na hii yajulisha kuwa makusudio ya “Burhani ya Mola wake” ni kufunguka mlango kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) mbele ya Yusuf kwa heshima yake. Haujifichi udhaifu wa tafsiri hii, hiyo ni kwa sababu lau makusudio ya burhani ni kufunguka mlango ingelazimu itajwe kwenye kauli yake: “Na 46. Al-Manaar. Juz. 12. Uk. 278.
82
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:30 PM
Page 83
Sehemu ya pili
wote wawili wakakimbilia mlangoni” au kabla yake na sio katika Aya iliyoitangulia, nalo ladhihiri kwa kuzizingatia zote mbili pamoja aliposema:“Na hakika alimkazia nia na akamkazia nia, laula asingeliona burhani ya Mola wake.” na “Na wote wawili wakakimbilia mlangoni, na mwanamke huyo akairarua kanzu yake kwa nyuma, na wakamkuta mume wake mlangoni”. Hivyo twaona kuwa yataja kumkusudia kwake na kuiona burhani katika Aya moja, kisha yataja kukimbizana kwao kuelekea mlangoni katika Aya nyingine huku kati ya Aya hizo mbili kukiwa na kitenganishi, ikiwemo kauli yake: “Hakika yeye alikuwa miongoni mwa watakaswa”. Hivyo lau makusudio ya “Kuiona burhani” ingekuwa ni kufunguka kwa mlango ingefaa kutaja kushindana kabla yake. Na linaloonekana dhahiri katika kauli Yake: “Na akafunga milango” ni kufunga milango kwa kawaida na sio kuifunga kwa maana ya kuitia kufuli ili isifunguke kwa urahisi, ila tu hakufunga kwa makufuli kwa kuwa yeye hakuwa anatazamia kuwa Yusuf hatomkubali na kutotii amri yake. Maana ya tatu ya Aya hii Kwa hakika al-Hammu upande wa Yusuf ni kuwaza kitu akilini japo hajaazimia. Na huenda al-Hammu ikatumika katika maana hiyo, Kaabu bin Zuheir amesema: “Kwa kiwango gani wamefahamu kutoka kwa bwana mwenye wasaa. Na kutoka kwa mtenda mema awazapo au aazimiapo.” Mshairi huyu ametumia msamiati al-Hammu kwa maana ya kuwaza. Raziy amesema: Al-Hammu katika lugha imekuja na maana nne:…..ya pili: Kuwaza kitu akilini, Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: “Makundi mawili miongoni mwenu yalipotaka kufanya woga kuwa watashindwa na hali Mwenyezi Mungu ndio mlinzi wao” (Al-Imran:122), alilolikusudia Mwenyezi Mungu mtukufu ni kuwa kushindwa ni wazo lililoingia akilini mwao, na lau kusudio hapa lingekuwa ni kuazimia basi haingefaa Mwenyezi Mungu kuwa mlinzi wao… na pia maana hiyo yajulishwa na kauli ya Kaabu bin Zuhayr: “Kwa kiwango gani wamefahamu kutoka kwa bwana mwenye wasaa. Na kutoka kwa mtenda mema awazapo au aaz83
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:30 PM
Page 84
Sehemu ya pili
imiapo.” ametumia msamiati al-Hammu kwa maana ya kuwaza.47 Haifichikani kuwa tafsiri hii haiko sahihi, kwa sababu ni dhahiri kuwa maana ya al-hammu sehemu zote mbili ni moja, na wala haikuwa alHammu upande wa malikia isipokuwa ni kuazimia, na kutenganisha kati ya al-hammu mbili ni kinyume na maana dhahiri. Hivyo kwa makadirio yoyote yale ni kuwa, kisa cha Yusuf kilichokuja ndani ya Qur’an kinajulisha utakasifu wake tokea mwanzo wa suala hili mpaka mwisho, na kuwa hapakuthibiti upande wake kusudio wala hakukusudia kuingiliana naye, si kwamba eti yeye alikusudia na kuazimia na kisha ndipo akatokwa na azimio kwa sababu maalumu. Ametaja Ar-Razi ndani ya Ismatul-Anbiyai maana nyingine ya Al-hammu, amesema: “Ama al-hammu yake Yusuf tumetoa dalili kuwa haifai iwe inaambatana na ovu na wala dhahiri ya Aya haielekezi hilo, kwa hiyo si vibaya tukiiambatanisha na kule kumsukuma mbali dhidi yake, kama asemavyo msemaji: “Nilikuwa nimemkusudia fulani yaani nimwangushiye kipigo.”48 Na jibu lake ni lilelile, nalo ni kwamba kutenganisha maana ya al-hammu kati ya al-hammu ya Yusuf na ya malikia ni kinyume na maana dhahiri. Kisha Raziy baada ya hivyo kulingana na tafsiri hii ameiondoa maana ya Aya, maana ile iliyotangulia kimsingi na kwenda kwenye maana ya mbali isiyo na ushahidi katika Aya hizi, aliposema: “Haiwezi semwa: Basi ni faida gani ya taawili hii katika usemi wake Taala: “Laula asingeliona burhani ya Mola wake.”, na kumsukuma mbali naye ni utii usiyomuondolea burhani? Kwa sababu sisi tunasema: Yawezekana alipomkusudia kumsukuma na kumpiga aliona burhani kuwa endapo atatekeleza aliloliazimia watu wa yule mama watamwangamiza na kumuuwa, na kuwa yeyemalikia atadai dhidi yake kuwa amemtaka kwa mabaya na kumhusisha 47. Ismatul-Anbiyai cha Al-Fakhru Raziy, Uk 54, chapa ya Jidah. 48. Ismatul-Anbiyai cha Al-Fakhru Raziy, Uk 55, chapa ya Jidah. 84
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:30 PM
Page 85
Sehemu ya pili
kuwa alimwita kwa ajili yake na kuwa alimpiga kwa sababu ya kule kumkataa kwake, Mwenyezi Mungu alimpa habari kuwa amemwondolea ubaya na uchafu ambao ni kuuwa na kutongoza.................................”49
5 Isma ya Musa, kumuua Mkibtiy, na kumzoza nduguye Kwa kweli Kalimullah Musa bin Imrani (a.s.) ni mmoja miongoni mwa manabii watukufu, Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amemsifu kwa sifa timamu na zilizo kamili mno, amesema Msemaji Mwenye enzi:
“Na mtaje Musa katika Kitabu, hakika yeye alikuwa alikuwa mwenye kutakaswa na alikuwa Mtume Nabii.* Na tukamwita upande wa kuliya wa mlima na tukamkurubisha kwa faragha.* Nasi tukampa katika rehma zetu nduguye Harun Nabii.” (Mariam:51-53). Na amesema (s.w.t.):
“Na tulimpa Musa na Haruna Furuqan na mwanga na ukumbusho kwa wacha mungu.” (Al-Anbiyau: 48).
49. Ismatul-Anbiyai.Uk.55 chapa ya Jeddah. 85
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
12:30 PM
Umaasumu wa Mitume
Page 86
Sehemu ya pili
Na amekisifu kitabu chake kwa kauli yake:
“Na hapo kabla kulikuwa kitabu cha Musa mwongozo na rehema�.(Al-ahqafu:12) Pamoja na hayo yote mpinzani ametoa dalili ya yeye Musa (a.s.) kutokuwa na ismah, amedai hilo kupitia mambo mawili: La kwanza: Kumuuwa kwake mkibtiy na aliposifu kuwa ni miongoni mwa kazi ya shetani. La pili: Kuzozana kwake na nduguye Harun hali akiwa hakuzembea: Ufuatao ni mjadala wa kila moja kati ya hayo: I: Ismah ya Musa na kumuua Mkibtiy: Amesema msemaji Mwenye Enzi:
86
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:30 PM
Page 87
Sehemu ya pili
“Na alipo komaa kiumri na kutuwama tulimpa busara na elimu, ni kama hivyo tunawatunukia watendao mema. *Na aliingia mjini wakati watu wake wako katika mghafiliko, humo aliwakuta watu wawili wanapigana mmoja akiwa katika Shia wake na huyu mwingine akiwa kutoka kwa adui zake, yule ambaye alikuwa katika Shia wake alimuomba amnusuru dhidi ya ambaye ni adui wake, Musa alimpiga ngumi na alikufa, akasema hii ni miongoni mwa kazi ya Shetani kwani yeye ni adui mpotovu aliye bayana. * Alisema (Musa): Oh Mola wangu! kwa hakika mimi nimejidhulumu binafsi ni ghufiriye, na alimghufiria kwa kweli yeye ni mwenye kughofiri sana na mwingi wa rehema. * Alisema: Mola wangu kwa kuwa umeniniimesha sintokuwa msaidizi wa waovu” (al-Qasasu:14-17.). Na Qur’an inakitaja kisa hiki kwa ufupi ndani ya sura Ashuaraa, anasema (s.w.t.):
“Hatujakulea ukiwa mtoto mchanga, na ukakaa kwetu miaka ya umri wako? * Na ukatenda tendo lako (ovu) ulilotenda, ukawa miongoni mwa wasioshukuru.* Akasema: Nilifanya hayo, hapo nilipokuwa miongoni mwa wale wasioelewa.”(Ashuara :18-20 ) Aya hizi zinajulisha kuwa Musa aliingia mjini wakati ambao watu wa mjini hapo hawana habari ya uingiaji wake, yawezekana kuwa ni kwa sababu aliingia katikati ya mchana hali watu wakiwa katika usingizi mwepesi au yawezekana aliingia mwanzoni mwa usiku na yawezekana kwa sababu zingine mbali na hizo. Akawakuta humo mjini watu wawili, mmoja wao alikuwa Mwisraili na mwingine ni Mkibtiy nao walikuwa wanapigana, 87
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:30 PM
Page 88
Sehemu ya pili
yule ambaye ni Shia wa Musa alimuomba amnusuru dhidi ya yule mwingine, hapo Musa akamnusuru kwa kumpiga ngumi kifuani na hatimaye ikamuuwa, na alipomaliza suala hilo, alijuta na kuieleza kazi hii kama ifuatavyo: 1-Hii ni miongoni mwa kazi za Shetani 2-Ewe Mola wangu kwa kweli nimeidhulumu nafsi yangu 3-Nisamehe alimsamehe 4-Nilifanya tendo hilo nikiwa miongoni mwa wasioelewa. Sentensi hizi nne zabainisha kuwa uuwaji huu ni jambo ambalo si la kisheria. Kwa ajili hiyo mara amelielezea tukio hili kuwa ni miongoni mwa kazi za Shetani, na mara nyingine kuwa alikuwa amejidhulumu binafsi, na alikiri mbele ya Firauni kuwa alipokuwa akitenda alilotenda alikuwa miongoni mwa wasioelewa, na aliomba msamaha. Nasema kabla ya kuzifafanuwa nukta hizi nne tunaamsha maoni ya msomaji mpendwa ili ayaelekeze kwenye baadhi ya maovu waliyokuwa nayo mafirauni miongoni mwa matendo ya kihalifu. Ili kukuthibitishia hayo yatosha kauli Yake Mwenyezi Mungu (s.w.t.):
“Kwa hakika Firauni alijitukuza aridhini akawafanya watu wa huko makundi makundi, akalidhoofisha taifa moja miongoni mwao, akiwachinja watoto wao wanaume na kuwaacha hai wanawake wao, hakika yeye alikuwa miongoni mwa waharibifu.� (Al-qasas:4). Na Firauni alikuwa anayatenda matendo haya kupitia wafanyakazi wake makibti ambao walikuwa wasaidizi wake. Na chini ya kivuli cha usaidizi 88
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:30 PM
Page 89
Sehemu ya pili
huu mafirauni waliwatamalaki wana wa Israeli wanaume na wanawake wakawafanya watumwa kama inavyobainisha hilo kauli Yake (s.w.t.):
“Hivyo hiyo ni neema waweza kunisimbulia, nawe unawafanya bani Israeli watumwa.” (Shuaraa:22)
hali ukiwa
Firauni alipomwambia Musa: “Je hatujakulea ukiwa mtoto mchanga…” Musa alimjibu kuwa: “Hivi wanisimbulia kwa hilo na wewe umewafanya waisraeli watumwa?” Kwa mujibu huo, kumuuwa mmoja miongoni mwa wasaidizi wa wapuuzi wakosefu ambao wamewachinja mamia bali maelfu ya watoto katika waisraeli na kuwabakisha hai watoto wa kike wao, haihesabiki na mahakama ya akili na dhamira kuwa ni tendo ovu lisilo sahihi. Zaidi ya hilo ni kuwa Mkibti aliyeuwawa alikuwa katika lengo la kumuuwa Mwisraeli lau Musa asingelimnusuru, hilo ni kulingana na ielezavyo kauli yake (swt): “Wanapigana”. Lau kama Mkibti angemuuwa, tendo lake la kuuwa lisingekuwa na athari ya kitendo, kwakuwa yeye alikuwa na uhusiano na serekali tawala ambayo ilikuwa yaendelea kuwaangamiza Wasraeli na yamwaga damu zao miaka nenda miaka rudi, kwa hiyo kumuuwa kwake kwa mtizamo wa Firauni ni sawa na kuuwa kwa mtu sharifu mmoja wa watumwa wake endapo amehalifu amri yake. Ukielewa hayo hebu na turejee kwenye ufafanuzi wa sentensi ambazo amezielewa mkosoaji aliyezitolea dalili kuwa zajulisha Musa hana ismah. Kwa kweli kauli Yake “Hii ni miongni mwa kazi za Shetani” kauli hiyo ina uwezekano wa maana mbili: Ya kwanza: Liwe tamko hii au huu laashiria kwenye mjadala uliojiri kati ya Mkibtiy na Mwisraeli, na uliishia kuuwawa wa kwanza; na kwa mtizamo huu hakuna chochote humo kinachojulisha alichokusudia mtowa 89
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:30 PM
Page 90
Sehemu ya pili
dalili… Ibnu Al-jahamu ameeleza kutoka kwa Imamu Ridhwa (a.s) Maamun alipomuuliza kuhusu kauli Yake (s.w.t.): “Hii ni miongoni mwa kazi za Shetani”. Akajibu: “Kupigana kulikotokea kati ya watu wawili, sio kule kumuuwa kulikotendwa na Musa”50. Ya pili: Kwa kweli tamko hii au huu laashiria kule kumuuwa Mkibtiy, na ameelezea kuwa ni kazi ya Shetani kwa mitizamo miwili: i. Kwa kweli tendo hili lilikuwa kosa tupu, lime msukumia kwenye matokeo mabaya yaliyomfanya alazimike kuiacha nyumba na watani, baada ya siri yake kuvuja na Ikulu ya Firauni ikajua kuwa Musa amemuuwa mmoja wa wasaidizi wa Firauni, kwa ajili hiyo walifanya njama dhidi yake wamuuwe, lau kama si muumini wa watu wa Firauni kumjulisha ukweli wa hali ya mambo ulivyo, basi askari wangemchukuwa na kuyateketeza maisha yake kama Mwenyezi Mungu alivyosema:
“Na akaja mtu kutoka mji wa mbali huku akikimbia akasema: Ewe Musa, kwa kweli wakuu wanakufanyia kikao wakuuwe, toka hakika mimi ni mnasihi mnyoofu kwako.” (Al-qasas:20). Kazi ile haikuwa na faida yeyote kwa mtu mmoja mmoja au jamii isipokuwa ilimfanya alazimike kuyaacha makazi na kufanya msafara nchi ya ugeni (Madyan) na kujishughulisha na kuchunga kondoo akiwa mwajiriwa wa Shuaibu (a.s.). Kama ambavyo maasi hunasibishwa na shetani, amesema (s.w.t.):
50. Al-Burhani, Juz 3, Uk 224. Uyunu Akhbar Ridhwa, Juz 1, Uk 199. 90
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:30 PM
Page 91
Sehemu ya pili
“Pombe na kamari na sanamu na mishale ya kuagulia ni uchafu miongoni mwa kazi za Shetani jiepusheni navyo huenda mtafanikiwa.” (Al-Maidah; 90). Vilevile matendo ya makosa yatokanayo na mipango mibaya na upotovu wa juhudi ambavyo humsukumia mwanadamu kwenye matokeo mabaya pia hunasibishwa na yeye Shetani. Kwa hiyo maasi na matendo yaliyokosewa vyote viwili vyafaa kuhusishwa na shetani, kwa kigezo cha kuwa yeye ni adui mwenye kumpoteza mwanadamu, na adui haridhiki na ustawi na ufanisi wa adui yake, bali humsukumia kwenye ambalo lina madhara kwake, yachelewayo na ya haraka, kwa ajili hiyo ndiyo maana alisema baada ya kumtokomeza: “Hii ni miongoni mwa kazi ya Shetani kwani yeye ni adui mpotovu aliye bayana.”. ii. Kwa kweli kumuuwa Mkibtiy ilikuwa ni tendo lililotokana na haraka katika jaribio la kumtokomeza adui, hivyo lau yeye angelisubiria uchungu wa maisha kidogo basi Mkibti angetupwa yeye na wenzake wote baharini bila kuwa na matokeo mabaya. Kama alivyosema (s.w.t.):
“Tulimchukuwa na askari wake tukawatupa baharini basi angalia jinsi ulivyokuwa mwisho wa wadhalimu.” (Qasas:40) Kwa mujibu huo lafahamika faidisho la sentensi ya pili ambayo ni katika jumla ya vishiko vya mtoa dalili; naikusudia kauli Yake: “Oh Mola wangu! kwa hakika mimi nimejidhulumu” kwani maneno hayaendani na maasi na ya kumhalifu Mola, bali ni kukiweka kitu mahali pasipo pake, kama walivyosema wazi hilo viongozi wa lugha, na tayari tulitanguliza 91
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:30 PM
Page 92
Sehemu ya pili
kauli halisi tulipokuwa kwenye mjadala wa ismah ya Adam, na ulikwisha tambuwa kuwa tendo la Musa lilifanyika mahali pasipo pake, na lilikuwa ni kosa kwa pande mbili: kwanza: Lilimsukumia kwenye matokeo machungu, kwa sababu alilazimika kuwaacha ahali na mji wake. Pili: Na kwa upande mwingine lilikuwa tendo lililotokana na kuharakia kumwangamiza adui bila ulazima, kwa ajili ya pande mbili hizo lilikuwa tendo lililotendeka halipo mahali pake, kwa hiyo imekuwa sahihi tendo lielezwe kuwa ni la dhulma, na mtendaji aitwe dhalimu. Liwekalo wazi hilo ni kuwa yeye ameifanya kuwa ni dhulma ya nafsi yake sio ya Mola, lau ingekuwa ni maasi dhulma ingekuwa ni ya Mola wake na kuzikiuka haki zake, kama hali ilivyo kwenye ushirikina, hii huwa ni dhulma ya Mola na kumkiuka, amesema (s.w.t.):
“Usimshirikishe Mwenyezi Mungu kwa kweli ushirikina ni dhulma kubwa mno”. (Luqmanu:13). Ama sentensi ya tatu, namaanisha kauli Yake: “Nighufurie naye alimghufiria hakika yeye ni mghufiriaji sana mwenye huruma” kuomba kughufuriwa sio dalili ya kutokea maasi, kwani ghufrani ina maana ya kusitiri. Na makusudio yake ni kubatilisha matokeo mabaya ya kitendo chake, na kumuokowa mbali na majonzi, na kumuepushia shari ya Firauni na wakuu wake, na (s.w.t.) ameieleza ibara hii: “Na ulimuuwa mtu, lakini tulikuokowa kutoka tabu na tulikufanyia majaribu mbali mbali.” (Twaha:30) Mwenyezi Mungu alimuokowa kupitia mtu katika watu wa Firauni aliye mpa habari ya njama dhidi yake, hivyo akatoka Misri kwa woga na kwa 92
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:30 PM
Page 93
Sehemu ya pili
hadhari, mpaka akafika ardhi ya Madyan nyumbani kwa Shuaibu na alimhadithia kisa. Shuaibu alimwambia
“Umeokoka kutoka kaumu ya watu madhalimu”. (Qasas:25). Kwa ajili hiyo alimghufuria na alisitiri tendo lake na alimuokoa (s.w.t.) kutoka machoni mwa Firauni. Na alimuwezesha kufika kwenye maji ya Madiyan na kufikia kwenye nyumba ya mmoja wa manabii wake. (a.s.). Ongeza juu ya hayo: Kumuua Mkibtiy ingawaje halikuwa tendo la maasi lakini lililotarajiwa kutoka kwa Musa ni kuacha na hangelifanya. Kwa hiyo kutokea kwa tendo kama hilo kwa Musa yafaa aombe msamaha kwa kuwa mema ya watu wema ni maovu kwa watu wa karibu. Kwani kazi inayoruhusiwa ambayo mtu wa kawaida hachukuliwi kuwa katenda makosa huenda ikawa ni makosa kwa mtu mjuzi, sembuse mtu wa kiungu. Ilikuwa yafaa kwa heshima ya mtukufu kama huyu kusubiri na kuwa na msimamo katika matukio ya maisha: kama vile utamu wake, uchungu wake, na kuwaamua wanaopigana kwa maneno laini, Mwenyezi Mungu ali muamuru hivyo alipomtuma kwa Firauni alimwagiza amwambiye kwa kauli laini pale (s.w.t.) aliposema:
“Mwambiyeni kwa kauli laini huenda atakumbuka au ataogopa.” (Taha:44). Tulifafanua maana ya neno hili kwenye mjadala wa Adam na Hawa waliposema:
“Walisema: Ewe Mola wetu, tumezidhulumu nafsi zetu kama hauto93
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:30 PM
Page 94
Sehemu ya pili
tughufuria na kuturehemu tutakuwa miongoni mwa wenye hasara”.(al-Aarafu:23) Ama kauli yake (s.w.t.): “Nilifanya hayo, hapo nilipokuwa miongoni mwa wale wasioelewa.” makusudio ya kutoelewa hapa ni mghafiliko wa litakaloambatana na tendo miongoni mwa matokeo mabaya na kusahau, nalo si jambo geni. Neno dhalalu ‘kupotea” limetumika kwa maana hizi mbili ndani ya Kitabu chenye hekima (Quran), amesema (s.w.t.): “Katika wale muwaridhiao kuwa mashahidi, ili akisahau mmojawapo akumbushwe mmoja wapo na mwingine” (Baqara: 282). Kwa hiyo makusudio ya kupotea hapo ni kusahau mmoja kati ya mashahidi wawili na kughafilika kwake alichokishuhudia. Na amesema (s.w.t.):
“Na walisema:Hivi tukipotea ardhini eti ni kweli tutarudishwa katika umbo jipya!” (Assajdah:10) Yaani tukizama humo. Amesema ndani ya kamusi Lisanularabi: Adhalalu: ni kusahau, na katika Quran: Yaani inatoweka kwenye kumbukumbu yake, na miongoni mwake ni kauli Yake Taala: “Katika wale muwaridhiao kuwa mashahidi, ili akisahau mmojawapo akumbushwe mmoja wapo na mwingine” na “Nilifanya hayo, hapo nilipokuwa miongoni mwa wale wasioelewa.”...... na “Hivi tukipotea ardhini eti ni kweli tutarudishwa katika umbo jipya!”51 Kwa ujumla hakika Kalimullahi Musa (a.s.) anakiri kwa sentensi hiyo pindi Firauni alipompinga kwa kauli yake: “Na ukatenda tendo lako (ovu) ulilotenda, ukawa miongoni mwa wasioshukuru.” akamtolea udhuru kwa kusema: “Nilifanya hayo, hapo nilipokuwa miongoni mwa 51. Lisanul-Arabi. Juz.11 .Uk 392-393. 94
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:30 PM
Page 95
Sehemu ya pili
wale wasioelewa.” Na uwiano wa mahali pakutolea udhuru ni ile tafsiri ya dhalalu kwa maana ya ghafiliko la yatakayoambatana na tendo kama matunda na kule kuyasahau. Na matokeo yake ni kwamba, mghafala umenitelezesha wakati wa kuuwa na yalifichikana kwangu yatakayoambatana nalo miongoni mwa lipizi la kitendo na ubaya wa matokeo, hivyo basi nikafanya niliyofanya. Na ni miongoni mwa kosa la wazi kuitafsiri dhalalu kuwa ni dhidi ya hidaya. Itakuwaje hivyo hali ikiwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) alimsifu kabla hajatenda uuaji kwa kauli yake: “Tulimpa hukumu na elimu na hivyo ndivyo tunavyowalipa wenye kufanya mema.” (Qasas:14) Kama ambavyo Musa mwenyewe baada ya kuomba aghufiriwe na kuhisi kujibiwa dua yake alisema: “Akasema: Mola wangu! kwa sababu umenineemesha basi sitakuwa kabisa msaidizi wa waovu” (Qasas:17). Je ni sahihi baada ya haya kuitafsiri dhalalu kwa maana ya kupotea dhidi ya hidaya? La hasha haiwezi kuwa hivyo! Haya yote kuhusu kishiko cha kwanza, na maanisha kumuuwa Mkibtiy, haya sasa njoo pamoja nami tudurusu kishiko cha pili cha hasimu kuhusiana na kumtuhumu Kaliimullah mtukufu (a.s.) kuwa hana ismah: ii. Mahojiano na nduguye Harun (a.s.), kwa hakika Mwenyezi Mungu (s.w.t.) alimuahidi Musa baada ya kuangamia Firauni kuwa aende upande wa kulia wa mlima Sinai ili amkamilishiye Taurati ambayo ndani yake kuna ubainifu wa sheria na hukumu na anayoyahitajia. Na maafikiano yalikuwa atekeleze ahadi hiyo akiwa na kundi la watu miongoni mwa wakuu wa kaumu yake hivyo Musa alifanya haraka kati yao kwa shauku ya Mola wake aliwatangulia kwa sharti ya wao waungane naye na Mwenyezi Mungu (s.w.t.) alipomsemesha kwa kauli yake: “Kitu gani 95
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:30 PM
Page 96
Sehemu ya pili
kimekuharakisha hata umekuwa mbali na watu wako ewe Musa?” Akamjibu kuwa: “Wao wako nyuma yangu watanikuta hivi punde.” Hapo (s.w.t.) alimjulisha kuwa amewapa mtihani watu wake baada ya kujitenga nao na Saamiriyu amewapoteza. Hapo Musa alirejea kwa waisraeli kutoka kwenye ile ahadi akiwa na huzuni ameghadhibika akaona kuwa Assamiriy amewatolea ndama mwili wenye sauti na akasema: Kwa hakika huyu ndio mungu wa wana wa Israeli wote na walimfuata watu wa ngazi ya chini na watu wa kawaida. Musa alikutana na Harun alitupa mbao na kuanza kumlaumu Harun, na kujadiliana naye. Hili ndilo ambalo Mwenyezi Mungu (s.w.t.) analolieleza katika Sura mbili anasema:
“Na Musa aliporudi kwa kaumu yake hali akiwa ameghadhibika mwenye masikitiko akasema: Ni maovu mliyonifanyia nyuma yangu. Je, mmeiharakia amri ya Mola wenu? Na akazitupa zile mbao na akakamata kichwa cha nduguye na kukivutia kwake. Akasema: Ewe mwana wa mama yangu! Hakika kaumu wamenidharau na hata walikaribia kuniua, basi usiwafurahishe maadui juu yangu, wala usiniweke pamoja na watu madhalimu.” (A’araf 150) Na anasema (s.w.t.):
96
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:30 PM
Page 97
Sehemu ya pili
“Musa alirejea kwa kaumu yake hali ameghadhibika sana mwenye huzuni, Akasema: Ninyi watu Mola wenu hajakuahidini ahadi njema! Je(muda wa) ahadi umekuwa mrefu kwenu au mumetaka ikufikeni ghadhabu kutoka kwa Mola wenu ndio maana mumekhalifu ahadi yangu…” Twaha: 86 Na anasema:
“Akasema ewe Harun nini kilikuzuia ulipowaona wamepotea usinifuate je! Uliasi amri yangu? Akasema (Harun): Ewe mwana wa mama, usizishike ndevu zangu wala kichwa changu hakika mimi niliogopa usije ukasema umewafarikisha kati ya wana wa Israeli na hukuheshimu kauli yangu.”(Twaha: 92, 94). i. Kwanini alizitupa mbao? ii. Kwanini alimzoza nduguye hali akiwa ametekeleza wajibu wake? Na uchambuzi wa maswli haya mawili wakujia baada ya kubainisha utangulizi ufuatao: Kwa kweli Musa alimuacha nyuma Harun alipokuwa akienda kwenye ahadi, Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amemnukuu Musa kwa Kauli hii:
97
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:30 PM
Page 98
Sehemu ya pili
“Kwa kweli Musa alimwambiya nduguye Harun: Chukuwa nafasi yangu katika kaumu yangu fanya vyema wala usifuate njia ya mafasidi.” (Aarafu:142). Na Harun alitekeleza wadhifa wake katika kaumu yake, na pindinSamiriy alipowapoteza Harun alifanya nao mdahalo kwa kauli yake:
“Oh! watu wangu, mmepotoshwa naye, Mola wenu si mwingine ni ArRahman nifuateni na mutii amri yangu.”(Twaha:90). Alitosheka katika kutekeleza wadhifa wake kwa kuwabainishia na kuwalaumu wala hakuwa anawapiga na kuwaadhibu, na alibainisha hilo kwa nduguye kwa kauli yake:
“Kwa hakika mimi nilihofia usije ukasema umewatenganisha wana wa Israeli na wala haukuchunga kauli yangu.” Twaha: 94 Haya ndiyo yamuhusuyo Harun, ama yanayorejea kwa Musa (s.w.t.) ametoa habari ya Saamiriyu kuwapoteza watu wake kwa kauli yake: “Hakika sisi tumeijaribu kaumu yako baada yako na Saamiriyyu amewapoteza” (Twaha:85). Na akasema: “Na Musa aliporudi kwa kaumu yake hali akiwa ameghadhibika mwenye masikitiko akasema: Ni maovu mliyonifanyia nyuma yangu. Je, mmeiharakia amri ya Mola wenu?” Na akasema: “Ninyi watu Mola wenu hajakuahidini ahadi njema! Je(muda wa) ahadi umekuwa mrefu kwenu” Na katika hali hii ngumu Kaliimullahi alidhihirisha ghadhabu yake kwa kufanya matendo mawili: 1 - Kuzitupa mbao kando. 98
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:30 PM
Page 99
Sehemu ya pili
2 - Kumkemea nduguye kwa kauli yake: “Kitu gani kilikuziwia ulipowaona wamepotea usinifuate! Je uliasi amri yangu?� (Twaha:9293). Hapo ndipo yanazuka yale maswali mawili. Kwanini alitupa mbao kwanza? Na kwa nini alimkemea nduguye na kugombana naye hali alitekeleza wadhifa wake. Pili, kwa hiyo twasema: Hapana shaka waliyoyatenda wana wa Israeli ambayo ni kuabudu ndama yalikuwa miongoni mwa matendo mabaya mno na yakufedhehesha, vipi washindwe kukumbuka kuwa Mwenyezi Mungu amemuhilikisha adui yao na amewarithisha ardhi yao, hivyo ambalo lilikuwa langojewa kutoka kwao ni kubaki imara katika njia ya Tawhid na kupambana na ushirikina, lakini yasikitisha kuwa wao wameikufuru neema yake kubwa, na waliacha ibada Yake (s.w.t.), na walijiunga na mlolongo wa ushirikina wakiwa hawajuwi ubaya wa matendo yao na kufedhehesha kwa kazi yao. Kwa kweli umma wa Kalimullah ingawaje ulikuwa umeghafilika kutambuwa ni kwa umbali gani wafikia ubaya wa tendo lao, lakini mkuu wao na Mtume wao alikuwa mjuzi wa hatari ya hali hii na kukiuka kwa umma, hivyo akahisi kuwa ikiwa hatopambana nao kwa ukali na mkazo na wala asisimame mbele yao kukemea na kudhihrisha kuhuzunishwa na kughadhibika kwake, huenda ile kaumu ingeendelea katika upotovu wake, na ingedhania haikutenda ila ni dhambi isiyo na uzito au ni uhalifu mdogo, wala isingetanabahi na hivyo hata kama wao wangerudi kwenye njia iliyo sawa na wakafuata Tawhid ya kweli, huenda mabaki ya ushirikina yapo ndani ya kina cha fahamu zao, hivyo kwa ajili ya kuwafahamisha fadhaisho la tendo lao alisimama katika nafasi ya kurekebisha kama alivyo mkurugenzi mkuu anayepambana na ufisadi ghafla katika eneo lake la kazi hali akiwa hajui uchafu huu umejipenyeza kutokea wapi. Kwa hiyo la kwanza linalokuja haraka akilini ni jinsi ya kumkabili na kumuwajibisha aliyeshika mahali pake, na aliyewakilisha kwake funguo za mambo, ukithibiti utakatifu wake, usafi wake, na kuwa alitekeleza wajibu wake kwa uzuri kabisa kulingana na hali halisi na kwa kiasi cha uwezo 99
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:30 PM
Page 100
Sehemu ya pili
wake atamwacha mpaka ayafahamu mambo ipasavyo na sababu zake halisi zilizosababisha ufisadi uliotokea na kuporomoka. Ni kama hivi alifanya Kaliimullah katika kurekebisha suala hili, na tukio la kusitusha ambalo lau lingebaki katika hali yake, lingeishia kwenye hali ya kujipenyeza ushirikina kwa wana wa Israeli wote, na juhudi yake ya miaka mingi ingepotea bure. Hivyo basi alilolifanya kwanza, alimkabili nduguye aliyechukuwa nafasi yake alipokuwa hayupo kwa nguvu na ukali ili wengine waliobaki awatambulishe kuwa hali ya mambo ni hatari mno. Kwa hiyo alimshika ndevu zake na kichwa chake akiwa juu yake akijiuliza kwa nini ushirikina umejipenyeza mpaka kwa kaumu yake pamoja na kuwa yeye yupo kati yao? Lakini ilipombainikia kuwa yuko safi na alitekeleza wadhifa wake kama anavyoelezea (s.w.t.) kwa kauli yake: “Hakika kaumu wamenidharau na hata walikaribia kuniua, basi usiwafurahishe maadui juu yangu, wala usiniweke pamoja na watu madhalimu.” Hapo alichupa na kumwelemea kwa upendo na alimuombea akisema:
“Mola wangu nighufiriye mimi na ndugu yangu na tuingize katika rehema zako na wewe ni mwenye kurehemu mno miongoni mwa wenye kurehemu.” (al-Aarafu:151). Kwa kweli kuomba msamaha kwa ajili yake na kwa nduguye hakujulishi kutokea kwa uhalifu kwao wawili, kwani manabii na mawalii kwa huomba msamaha kwa ajili ya hatari ya hali ya mambo na ukubwa na utukufu wa majukumu, wao huomba msamaha wa Mwenyezi Mungu na rehema zake ili daraja yao ipande, kama ilivyo wazi kwa mwenye kufuatilia hali zao. Ubainifu wake utakufikia wakati wa kutafiti ismah ya Nabii mtukufu (s.a.w.w). 100
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:30 PM
Page 101
Sehemu ya pili
Na baada ya kubainika kuwa sababu hasa ya kuingia ushirikina katika kaumu yake ni As-Samiriyyu na wakamfuata walio na unyonge kifikra na wenye nafsi dhaifu, akaanza kuwalaumu na kuwahadharisha kwa hotuba kali na maneno mazito, yametajwa katika sura mbili al-Aaraf na Twaha. Na sisi twatosheka na baadhi yake aliyowasemesha waabudu ndama kwa kauli yake:
“Kwa kweli ambao wamemchukuwa ndama (kumwabudu) itawapata ghadhabu kutoka kwa Mola wao na udhalili katika maisha ya dunia, ni kama hivyo tunawalipa wazushi.” (Al-aarafu:152). Na alipomkabili Samiriy alimsemesha kwa kauli Yake (s.w.t.):
“Ni jambo gani hili kubwa umelileta ewe Samiriya? Akasema: Nimeona ambalo hawakuliona nikachota gao la unyayo wa Mtume. nikalitupa, kama hivyo nafsi yangu ilinishawishi. * Akasema: Nenda kwa hakika itakuwa adhabu yako katika maisha haya, utasema: Usiniguse, na unayo ahadi haitokukosa. * Na mwangaliye mungu wako ambae umebaki ukimwabudu kwa hakika tutamchoma kisha 101
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:30 PM
Page 102
Sehemu ya pili
tutampeperusha baharini. * Hakika Mungu wenu ni Allah ambaye hapana mungu mwingine ila ni yeye tu, elimu yake imekienea kila kitu.” (Taha: 95 - 98).
Ismah ya Daud (a.s.) na hukumu ya kondoo Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amemsifu Nabii Daud (a.s.) kwa sifa ya hali ya juu awezayo kusifiwa mtu mkamilifu, amesema: “Na mkumbuke mja wetu Daud mwenye nguvu daima alirejea (kwa Mwenyezi Mungu).” Na alipanuwa ufalme na mamlaka yake juu ya milima na ndege kwa namna inayowakilisha uwezo mkubwa alioweza kuupata binadamu muda wote wa kuwa kwake khalifa aridhini. Amesema (s.w.t.):
“Hakika sisi tuliitiisha milima inafanya tasbihi pamoja naye jioni na asubuhi. * Na ndege wamekusanywa wote warejea (kutii amri) kwake. * Na tuliimarisha ufalme wake na tulimpa hekima na uwezo wa kumaizi mambo.”(Swad:18-20) Katika Aya ya mwisho ameeleza kuwa alipewa hekima na uwezo wa kumaizi mambo, jambo ambalo lazingatiwa kuwa ni muhimili katika kukata mashauri kwa njia sahihi ya wanaogombana kutoka matawi yake na vipengele vyake. Kisha Yeye (s.w.t.) baada ya hivyo ananakili jinsi alivyokuwa akihukumu anasema: 102
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:30 PM
Page 103
Sehemu ya pili
“Na je, imekujia habari ya mahasimu walipopindukia mihrabuni. * Walipomwingilia Daud na akawaogopa, wakasema: Usiogope, sisi ni mahasimu wawili mmoja wetu amemdhulumu mwenzie, basi tuhukumu baina yetu kwa haki wala usipendelee, na utuongoze kwenye njia iliyo sawa.* Hakika huyu ni ndugu yangu, anao kondoo majike tisini na tisa, nami nina kondoo mmoja tu, lakini anasema: Nipe huyo, na amenishinda katika maneno. * Akasema: Kweli amekudhulumu kwa kukuomba kondoo wako kuongeza katika kondoo zake, na bila shaka washirika wengi hurukiana wao kwa wao, isipokuwa wale walioami103
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
12:30 PM
Umaasumu wa Mitume
Page 104
Sehemu ya pili
ni na kutenda mema, nao hao ni wachache. Na Daud akaona kuwa tumemjaribu, akaomba msamaha kwa Mola wake na akaporomoka kunyenyekea na akaelekea.* Na tukamsamehe hayo, na kwa hakika alikuwa mbele yetu mwenye cheo cha kukaribiana na mahala pazuri. *Ewe Daud! Hakika tumekufanya khalifa aridhini, basi uwahukumu watu kwa haki wala usifuate matamanio yakakupoteza katika njia ya Mwenyezi Mungu. Hakika wanaopotea njia ya Mwenyezi Mungu wao watapata adhabu kali kwa sababu waliisahau siku ya Hesabu.” (Saad:21-26) Mkosowaji wa ismah ya manabii amejiambatanisha na kauli Yake Taala: “Akaomba msamaha kwa Mola wake na akaporomoka kunyenyekea na akaelekea.” alipodhania kuwa: Kuomba msamaha na kumsamehe kwake (s.w.t.) ni ishara na alama ya kutokea kwa dhambi. Ili kuujibu utoleaji wa dalili kama huu, kwa kutumia Aya hii yahitajia kubainisha maana za misamiati ya Aya na kukiweka wazi kisa hiki, kwa hiyo tunasema: Kwa kweli tafsiri ya Aya hii itatimia baada ya kubainisha mambo kadhaa: i. Kuweka wazi misamiati yake, ii. Kufafanua kisa hiki, iii. Je mahasimu hawa wawili walikuwa katika jinsi ya binaadamu! iv. Kwa nini Daud aliomba msamaha, na je uombaji wake msamaha ulikuwa kwa ajili ya dhambi au kwa ajili ya kuacha lililo bora? Ufuatao ni ubainisho wa mambo haya: I. Kuweka wazi maana ya misamiati ya kisa: a. Hasimu: Limekusudiwa watu wawili ambao walikuja ili wapitishiwe hukumu na Daud (a.s.) b. Kupindukia: Kupanda juu ya ukuta, yaani ukuta mrefu, ni kama litumikapo na neno numdu, humaanisha kupanda juu ya nundu ya ngamia..... 104
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:30 PM
Page 105
Sehemu ya pili
c. Mihrabu: Makusudio ya mihrabu katika Aya ni chumba. d. Kuogopa: Ni hali ya mfadhaiko na kutopenda ambayo humpata mwanadamu aonapo kitu cha kutisha, ni katika jinsi ya kuvunjika moyo. e. Kondoo: Hapa ni kondoo jike. f. Nipe huyo: Makusudio ya kauli Yake: Nipe huyo, yaani mfanye awe chini ya mamlaka yangu na uangalizi wangu. g. Amenishinda katika maneno: Yaani amenishinda katika usemi. Hayo yote yanahusu ufafanuzi wa misamiati ya kisa hicho. II. Kukifafanuwa kisa hiki Daud (a.s.) alikuwa ameketi chumbani mwake ghafla waliingia chumbani mwake watu wawili bila ya idhini yake na bila ya kumtambulisha kabla, walikuwa ni ndugu wawili mmoja wao anamiliki kondoo tisini na tisa na mwingine anamiliki kondoo mmoja tu. Wa kwanza alimuomba nduguye ampe kondoo ambae yupo chini ya miliki yake, akidai kuwa ana haki katika alipendekezalo kwa nduguye, na huyu mwenye kondoo mmoja ali elekeza usemi wake kwa namna ambayo iliamsha hisia za huruma ya Daud. Daud alitoa uamuzi kulingana na madai ya mlalamikaji bila ya kusikiliza usemi wa mlalamikiwa, akasema: “Akasema: Kweli amekudhulumu kwa kukuomba kondoo wako kuongeza katika kondoo zake”. Alipong’amuwa kuwa aliyoyafanya hayakulingana na hadhi yake, na kwamba mashitaka haya yaliyoletwa kwake ilikuwa ni mtihani kutoka kwake (s.w.t.) kwa Nabii wake: “Akaomba msamaha kwa Mola wake na akaporomoka kunyenyekea na akaelekea”.
105
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:30 PM
Page 106
Sehemu ya pili
III. Je mahasimu wawili walikuwa jinsi ya binaadamu? Kwa kweli Aya imezungukwa na ishara zinazojulisha kuwa hawa mahasimu wawili hawakuwa katika jinsi ya wanadamu na ishara hizo ni: 1. Kuparamia kwao mihrabu na kuingia kwao kwake (a.s.) kwa namna isiyo ya kawaida pamoja na kuwa hali ya mambo inabidi mihirabu yake iwe imezungukwa na walinzi na kwa kadiri ilivyo haikosi kuwa na anayemjulisha mambo. Lau uingiaji ungekuwa kwa idhini basi Daud (a.s.) angekuwa anatambuwa hilo hivyo hapangekuwa na sababu ya kufadhaika. 2- Usemi wa mahasimu wawili kwa Daud (a.s.) kwa kauli yao: “Usiogope” hali ikiwa usemi kama huu haifai utoke kwa raia amsemeshae mtawala na mwangalizi, kulingana na hali ya mambo yabidi mtawala ndiyo amsemeshe raia kwa kauli hiyo. 3- Kwa hakika usemi wao kwa Daud (a.s.) ulivyokuja katika Aya washabihiyana mno na usemi wa mgeni wa Ibrahim kwake (a.s.), Anasema (s.w.t.):
“Wape habari kuhusu mgeni wa Ibrahim. * Ghafla walipoingia kwake wakasema salamu, akasema sisi tunawaogopa. * Wakasema usiogope kwa hakika sisi tunakubashiria mtoto aliye tunukiwa elimu.” (Alhajar: 51-53). Na anasema (s.w.t.):
“Waliwaogopa wakasema: Usiogope na walimbashiria mtoto aliyetunukiwa elimu.” (Adhariati:28)
106
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:30 PM
Page 107
Sehemu ya pili
4- Kule kutanabai kwake (a.s.) kuwa suala hili lilikuwa majaribu kwake kutoka kwa Mwenyezi Mungu na ni mtihani kutoka kwake (s.w.t.) kwajulisha kuwa tukio lilikuwa sio la kawaida, na hii inawiana na kitendo wito kuwa umekuja kutoka Kwake (s.w.t.) kupitia Malaika. 5- Kwa kweli lengo la kuleta tukio hilo ni kumuweka sawa katika ukhalifa wake na hukumu zake kati ya watu ili atekeleze ukadhi kwa namna inayooana na hadhi yake na asighafilike na uthabiti katika suala analolitolea hukumu, kwa ajili hiyo (s.w.t.) alimsemesha baada ya hukumu yake ile: “Ewe Daud! Hakika tumekufanya khalifa aridhini, basi uwahukumu watu kwa haki�. Hayo yote yatiliya nguvu kuwa mahasimu wawili ni katika Malaika wamekuja kwa sura ya wanaume wawili binadamu. Naam, kisa na kupeleka madai kwake vilikuwa ni jambo la kweli na limetokea kama mfano wa kisa cha wageni wa Ibrahim (a.s.) na si kwa njia ya njozi na mfano wake. IV. Kuomba msamaha hulitokana na kuacha lililo bora Mkosoaji ametolea dalili kule kuomba msamaha kwake na kurejea kwake kwa Allah, kuwa dhambi imetokea kwake. Lakini hiyo dalili haijulishi hivyo. Kwanza: Kwa kweli hukumu yake haikuwa kwa namna ya kukata shauri na uamuzi wa mwisho kuhusu mashitaka, lakini ulikuwa uwamuzi wa kujengea hoja, kwani kwa kweli mwenye kumiliki kondoo tisini na tisa na asitosheke nao na bado anataka kuongezea juu yao kondoo mmoja wa nduguye, mtu kama huyu kamdhulumu nduguye. Na nafasi baada ya hapo ilikuwa wazi kwa mwenye kupinga, ingawaje ilikuwa bora na ilipendeza mno kulingana na hadhi yake baada ya kuwa amesikiliza madai kutoka kwa mmoja wa mahasimu wawili, aulize upande wa pili: Ni kipi ulicho nacho kuhusiana na madai haya? Hivyo asingeharakia kuamuwa na kutoa hukumu, japo iwe hukumu ya kukadiria tu. 107
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:30 PM
Page 108
Sehemu ya pili
Ambalo lilimfanya aharakiye hukumu ya kukadiria ni kwa kuwa yeye (a.s.) alisitukizwa na suala hili kwa kuingia kwake mahasimu wawili kwa namna isiyo ya kawaida, kwa hali hiyo hakutafuta uthibitishaji wa madai unaolingana na hadhi yake. Na alipong’amuwa hivyo na kutambuwa kuwa lililotokea lilikuwa majaribu na mtihani kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kumuhusu yeye “Akaomba msamaha kwa Mola wake na akaporomoka kunyenyekea na akaelekea� ili kuliwahi lililomtokea ambapo ilikuwa bora kwake aliache, hilo ni la kwanza, la pili ni kuonyesha shukrani na kuienzi neema ya kutanabahishwa ambayo haraka ilipatikana baada ya kuteleza. Pili: Yawezekana hukumu yake ilikuwa kabla ya kusikiliza usemi wa mlalamikiwa, kwa sababu ya kubainikiwa na ukweli kwa njia mojawapo miongoni mwa njia, kuwa haki ni ya mlalamikaji, kwa hiyo alihukumu bila ya kutaka kusikiliza usemi wa mlalamikiwa. Ndiyo, ilikuwa ni bora kwake hata katika sura hii asingeharakia kulitolea hukumu, bali yabidi maamuzi yawe baada ya kusikiliza usemi wa mlalamikiwa, hivyo basi, alipoacha ambalo ni bora kulingana na hali yake aliomba msamaha kwa ajili hiyo, na neno hili limerudiwa sana kuwa kuacha lililo bora kwa manabii ni dhambi kwa mtizamo fulani ingawaje sio dhambi ya moja kwa moja. Tatu: Na yalivyokuwa mashitaka yameletwa kwake kupitia Malaika na katika mazingira ya mfano huku mazingira hayakuwa ya taklifu, kosa la Daud litakuwa katika mazingira yasiyokuwa ya taklifu kama vile kosa la Adam (a.s.) lilikuwa katika Pepo na Pepo sio mahali pa taklifu, lakini pamoja na yote hayo madamu kufanya haraka katika kutoa hukumu kwa sura kama hii ni jambo linalochukiza, Daud alilazimika kuomba msamaha na kurejea kwa Mwenyezi Mungu, kwani alitambuwa kuwa kuacha lililo bora yahesabika ni dhambi kwake inayohitaji kuomba msamaha. Ndiyo katika tafsiri nyingi zimekuja Hadithi zikiwa ni tafsiri ya Aya hizo, lakini mwenye akili lau kwa kiwango kidogo hatokuwa na shaka kuwa ni Hadith Israiliyati zimejipenyeza kwenye umma wa Kiislamu kupitia 108
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
12:30 PM
Page 109
Umaasumu wa Mitume
Sehemu ya pili
wanazuoni wa Kiyahudi na watawa wa Kikristo. Kwa hiyo ni bora kuzitupilia mbali. Muktadha wa Aya wafichuwa kuwa telezo lake lilikuwa katika nyanja ya hukumu tu, kinyume na wanavyodai maaskofu wajinga, kuwa alipatwa na mtihani ambao kalamu yaona haya kuuandika. Kwa ajili hiyo Imamu Ali (a.s.) anasema kuwahusu waweka maneno haya ya batili na kumnasibishia Nabii Daud (a.s): “Daud hatoletewa mtu anayedai kuwa Daudi alimuoa mwanamke ila ni lazima Daud atamwadhibu kwa hadi mbili: Hadi ya unabii na hadi ya Uisilamu.”52
Ismah ya Nabii Sulayman (a.s.) Kwa kweli Nabii Sulayman ni mmoja wa manabii, yeye anatambulika kuwa alimiliki uwezo mkubwa mno na utawala na ushindi mrefu mno na imara zaidi, Mwenyezi Mungu (s.w.t.) alimpa hukumu, akili, na elimu. Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amesema:
“Kwa hakika tumempa Daud na Sulemani elimu” (An-namlu:15). Na amesema mwenye enzi:
“Na kila mmoja tulimpa hukumu na elimu”. (al-Anbiyau:79) Na alimfundisha lugha ya ndege amesema (s.w.t.): “Ee ninyi watu tume elimishwa matamshi ya ndege” (an-Namlu:16). Na Mwenyezi Mungu aliuelezea uwezo wake Sulayman {a.s}.) kwa kauli yake: 52. Majmaul-Bayan.Ju 4.Uk. 472. 109
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:30 PM
Page 110
Sehemu ya pili
“Na alikusanyiwa Sulaimani askari wake miongoni mwa majini, watu na ndege…” (An-namlu:17) Na nyinginezo kama hizo miongoni mwa Aya zilizokuja kuelezea uwezo wake na wingi wa elimu yake na daraja ya juu ya elimu yake. Wanahistoria wameeleza kuwa: Sulaymani aliswali swala ya mwanzo ya Adhuhuri kisha akaketi kwenye kiti chake huku farasi wakinyeshwa mbele yake mpaka jua likazama. Akasema: “Nimeelemea mapenzi ya farasi na nimesahau kumdhukuru Mola wangu. Kwa kweli farasi hawa wamenishughulisha kiasi cha kuisahau swala ya Alaasiri” Hapo akatoa amri farasi warudishwe na akawa anapiga hatamu zao na shingo zao kwa sababu wao walikuwa sababu ya Swala yake kumpita.53 Na katika baadhi ya tafsiri ni kuwa makusudio ya kurudishwa ni ombi la kurudishwa jua, hivyo jua likarudishwa akaswali Swala ya laasiri.54 Na baadhi ya hao wanadai kuwa kisa walichokileta kinajulishwa na Aya zifuatazo, na maanisha kauli Yake (s.w.t.):
“Na tulimpa Daud Sulaimani aliyekuwa mtu mwema, bila shaka alikuwa mnyenyekevu mno. * Alipopelekewa jioni farasi walio kimya wasimamapo, wepesi wakimbiapo. * Basi akasema: Navipenda vitu 53. Tafsiri Tabarasiy, Juz 3, Uk 99 - 100. Durul-Manthur, Juz 5, Uk 39. 54. Majmaul-Bayan, imenasibishwa kwake, Juz 4, Uk 475. 110
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:30 PM
Page 111
Sehemu ya pili
vizuri kwa kumkumbuka Mola wangu, kisha wakafichikana nyuma ya pazia. * Warudisheni kwangu na akaanza kuwapangusa miundi yake na shingo.”(Saad:30-33.). Na ili kukikosoa kisa hiki kilichodaiwa yatakiwa kwanza kuweka wazi mafunzo Aya hizi ili msomaji apate kuelewa kuwa hiyo ni sawa na kuitafsiri Quran kwa rai, jambo ambalo limezuiliwa na ni miongoni mwa uzushi wa wanazuoni wa Ahlul-kitab uliobebeshwa Qur’an nayo ikiwa mbali na uzushi huo. Nasema: 1- Aswafinaatu: Ni farasi aliyesimama kwa miguu mitatu aliyeweka ncha ya kwato ya nne aridhini ili iwe juu ya ncha ya kwato ile ya chini. 2- Al-Jiyadu: Ni farasi mwenye mwendo wa kasi, kana kwamba anafanya juhudi kukimbia. 3- Al-Khayru: Ni kinyume cha shari. Na neno hilo pia hutumika kumaanisha mali, kama lilivyotumika katika kauli Yake (s.w.t.): “Akiacha khayran” yaani mali (al-Baqrah:180). Na makusudio yake hapa ni farasi, na waarabu huwaita farasi kuwa ni khairun, na Nabii alimwita Zaidu Al-khaylu kwa jina la Zaidu Al-khayru. Na amesema (s.a.w.): “Kheri imefungwa kwenye nywele za utosi wa farasi mpaka siku ya kiyama”. Vipi asiwe kheri hali bado angali ahesabika kuwa ni nyenzo ya maisha katika miji mingi kama si yote. 4-Kupenda ni kinyume na kuchukia. 5- Navipenda vitu vizuri: Yajulisha mtendewa aliyeondolewa katika usemi, na kadirio la usemi ni kama hivi: Kwa hakika mimi nimependa farasi upendo wa kuipenda kheri. Anakusudia: Kuwapenda kwangu farasi ni kule kule kupenda kwangu kheri. Kwa sababu farasi kama ulivyojua ni nyenzo ya mafanikio ya mtu katika maisha yake binafsi na ya kijamii, khususan wakati wa vita dhidi ya adui na anaposhambuliwa. Na yawezekana ikawa Navipenda vitu vizuri ni mtendewa na sio kiwakilishi cha mtendewa.
111
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:30 PM
Page 112
Sehemu ya pili
6- Kwa kumkumbuka Mola wangu ni bainisho la chanzo cha mapenzi yake ya kheri na sababu yake, na ya kuwa kupenda kwake kwatokana na kumdhukuru Mola wake (s.w.t.) na amri yake kwa kuwa amewapa amri waja wake wateule wajiandae binafsi kwa ajili ya jihadi na kupambana na ushirikina na kuung’owa ufisadi kwa upanga na farasi. Na kwa ajili hiyo nimejihusisha na maonyesho ya farasi, hayo yote katika kutekeleza amri yake (s.w.t.) sio kuitikia wito wa silika ambayo kwa kawaida mwanadamu haepukani nayo, kama ambavyo (s.w.t.) ameashiriya kwa kauli yake:
“Watu wamepambiwa kupenda matamanio ya wanawake, na vijana wa kiume0, na mali mengi ya dhahabu na fedha, na farasi wazuri wazuri, na wanyama na mimea. Hivyo ni vitu vya kustarehea katika uhai wa ulimwenguni, na kwa Mwenyezi Mungu ndiko kwenye marejeo mazuri.” (al-Imran:14). Na kuna mfano wa wito huo katika Kitabu chenye hekima, amesema (s.w.t):
“Na waandalieni nguvu muwezayo, na kwa farasi waliofungwa muogopeshe maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui zenu.” (alAnfalu:60).
112
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:30 PM
Page 113
Sehemu ya pili
Raziy amesema: “Navipenda vitu vizuri kwa kumkumbuka Mola wangu” ndani yake kuna mitizamo mitatu: Wa kwanza: Neno Navipenda liwe na maana ya kitendo kinachomwendea mtendewa kwa herufi “an”, kwa hiyo inakuwa kama imesemwa: Nimeleta upendo wa farasi kuliko kumdhukuru Mola wangu. Ya pili: Navipenda kwa maana ya nimejihusisha zaidi na kheri kuliko kumkumbuka Mola wangu, kuliko kukikumbuka Kitabu cha Mola wangu, nacho ni Taurati au kingine, kama ambavyo kuambatana na farasi katika Kitabu chetu kwasifiwa, hivyo hivyo katika kitabu chao. Na maelezo haya ni bora kuliko ya kwanza kwa kuwa katika haya kuna utambuzi wa dhahiri”. 55 7- Mtendaji wa kitendo katika kauli yake: “Kisha wakafichikana nyuma ya pazia.” yaani ni farasi wenye mwendo wa kasi, na linalokusudiwa ni kuwa: Yeye aliamrisha warejeshwe baada ya kuwa wameghibu mbali na macho yake. Raziy amesema: Nomino katika “Kisha wakafichikana” na katika “Warudisheni” yawezekana yarejea kwenye jua kwa sababu ya kutajwa kile chenye mafungamano nalo nacho ni “jioni”. Na inawezekana yarejea kwenye farasi. Na mtazamo huu ni bora kwa kuulinganisha na ile miwili.” 56 8- Hapo sasa liulizwe swali nalo ni: Kwa nini aliamrisha kurudishwa, na lengo lilikuwa nini? Alibainisha jibu kwa kauli Yake: “Na akaanza kuwapangusa miundi na shingo.” yaani alianza kupangusa manyoya ya farasi wake na miguu yao kwa mkono wake kuonyesha heshima kwa wapandaji wake na waangalizi wake ambao wametekeleza wajibu wao kuandaa zana za jihadi. Mpaka hapa zimekuwa wazi maana za Aya, misamiati yake na sentensi zake. Kwa mujibu huo Aya zinalenga kuleta taswira ya gwaride la kiaskari 55. Ismatul-Anbiyai cha Al-fakhri Raziy. Uk.74. chapa ya Jedah. 56. Ismatul-Anbiyai cha Al-fakhri Raziy. Uk.74. chapa ya Jedah. 113
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:30 PM
Page 114
Sehemu ya pili
aliloliongoza mmoja katika manabii wenye mamlaka na uwezo, alilifanya siku za utawala na uwezo wake. Na matokeo ni kuwa: Kwa hakika Nabii Suleman Ambaye Qur’an imeashiria ufalme wake, uwezo, ushindi na kule kulitawala jeshi lake miongoni mwa binadamu na majinni, na kuitambuwa kwake lugha ya ndege na yasiyo hayo katika aina ya uwezo wake na utukufu wake ambao ameufanya makhsusi kwa ajili yake kati ya manabii, jioni ya mojawapo ya siku alifanya gwaride la kiaskari akawapandisha farasi wenye mwendo wa kasi wakawa wanakimbia mbele yake mpaka jua likazama mbele ya macho yake akawaamrisha swahaba zake wawarudishe kwake mpaka walivyofika kwake alisimama kuthamini juhudi zao kwa kupangusa shingo za farasi na mshipa wa vungu za magoti yao. Kufanya kwake hivyo hakujakuwa kwa sababu ya kujionyesha uwezo na ushindi au kujigamba au dharau na utashi wa nafsi, bali kwa kutii amri Yake (s.w.t.) na utajo wake ili wanatawhiidi wafanye nyadhifa zao na wajiandae kupambana na kujilinda wawezavyo na watayarishe zana zihitajikazo katika uwanja huu. 57 Na hili ndilo linalolengwa na Aya hizi na zalingana nalo kwa uwazi kabisa, basi njoo pamoja nami ili tuidurusu maana ambayo Aya zimelazimishwa hali zikiwa mbali na maana hiyo na zikiwa zimeepukana nayo.
Kuikosoa tafsiri iliyolazimishwa dhidi ya Qur’an Kwa hakika katika Aya zenyewe kuna dalili na shuhuda zijulishazo kuwa kisa hiki kilichochukuliwa kuwa ndio tafsiri ya Aya hizi ni batili. Ufuatao ni ubainifu wa shuhuda hizo: 57.Tafsiri hii kaichagua Sayyid Al-Murtaza ndani ya kitabu Tanzihul-Anbiyai, Uk 95 - 97. Na pia Ar-Raziy ndani ya kitabu Mafatihul-Ghaybi, Juz 7, Uk 136. Na AlMajlisiy ndani ya kitabu Al-Bihar, Juz 14, Uk 103 - 104, chapa mpya. 114
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:30 PM
Page 115
Sehemu ya pili
Kwa kweli Qur’an Al-hakiimu inakieleza kisa hiki baada ya kumsifu Sulaimani (a.s.), yasema: “Na tukampa Daud Sulaimani aliyekuwa mtu mwema, bila shaka alikuwa mnyenyekevu mno.” Na kulingana na sheria na taratibu za fani ya balagha zalazimisha baada ya sifa hiyo isitajwe chochote kinachoitanguwa na kinachopingana na sifa hiyo. Basi uko wapi uwiano wa sifa yake ya kuwa mja mwema na mwenye kurejea sana kwa Mwenyezi Mungu katika mambo ya dini yake na dunia yake ukilinganisha na kuzama kwake katika kushughulikia maonyesho ya farasi akiwa ameghafilika kutekeleza wajibu wa Swala?! Lau tuweke mfano wa kuwa tukio hili ni sahihi basi kulingana na ulazima wa fani ya balagha kingetajwa kisa hiki mahali pengine, na kisingetajwa baada ya sifa na himidi zilizotajwa katika Aya husika. Raziy amesema katika hali hii: “Jua kuwa hikaya hii pamoja na kuwa hakuna dalili kuihusu ndani ya Aya hii kabisa, lakini ndani ya Aya yenyewe kuna ambalo lakinzana na hikaya hii kwa njia tano: Ya kwanza: Kwa kweli yeye Taala amemsifu Sulaymani (a.s.) mwanzoni mwa Aya kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu amemtunukia Daud Sulaimani (a.s.) katika toleo la kumkirimu. Hali hiyo yapingana na ile hali ya kumalizia kwa kumsema Sulaymani kuwa alikuwa ni mwenye kuacha Swala na ya kuwa yeye ni mnyenyekevu mno wakati walipoonyeshwa farasi kwake kwani tamko “alipo” lajulisha hivyo. Na yeye kuwa ni mnyenyekevu mno na mwacha Swala kwa wakati mmoja ni muhali.” 58 2- Itakuwa sahihi kuichukulia kauli yake: “Navipenda vitu vizuri kwa kumkumbuka Mola wangu” kulingana na ilivyokuja katika kisa hiki endapo kitendo tu “Navipenda” itakuwa na maana ya kutilia uzito, na kuchaguwa, na kukadiria, yaani nimetilia uzito kupenda kheri nikiitanguliza kuliko kumdhukuru Mola wangu na ni mwenye kuchaguwa hilo 58. Ismatul-Anbiyai cha Al-Fakhru Raziy. Uk.75-76. chapa ya Jidah. 115
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:30 PM
Page 116
Sehemu ya pili
kabla ya kumdhukuru Mola wangu”. Na hii yahitajia dalili. Ikiwa tutasema maana hiyo imo kwa ndani, itakuwa ni lazima mahali “Kwa kumkumbuka Mola wangu” iwe “Kuliko kumkumbuka Mola wangu” yaani nimetiliya uzito kupenda kheri na nimekuchaguwa kuliko kumdhukuru Allah. Kama ilivyokuja katika kauli yake (s.w.t.):
“Walitilia uzito sana kupenda upofu kuliko mwongozo” (Fuswilat:17). Na kauli yake Taala:
“Endapo watatilia uzito sana kuchaguwa ukafiri kuliko imani” (Attawbah:23). 4- Kwa hakika dhamiri au nomino ya kitendo katika kauli Yake (s.w.t.): “Wakafichikana” yarejea kwenye neno “farasi” lililotajwa katika Aya. Na kulingana na tafsiri iliyolazimishwa yarejea kwenye Jua, hali ikiwa halikutajwa katika Aya hii. Na dai la kuwa tamko “Jioni” kuwa lajulisha hivyo ni dhaifu mno. Raziy anasema: “Kwa hakika kurudi nomino iliyopo kwenye “Wakafichikana” kwenye Jua inalazimu kulipa uzito neno lisilotajwa na kulipa uzito la mbali kuliko la karibu, hali ikiwa kufanya hivyo sio sahihi, na endapo litakubaliwa hilo basi hukumu ya kurudi nomino ya kitenzi “Warudisheni” kwenye “farasi” ni kuzitenganisha nomino zilizo shekili moja kutumia vitu vilivyo mbali mbali”.59 5-Dhamiri au nomino katika kauli yake “Warudisheni” kulingana na utaratibu uliochaguliwa yarudi kwenye “farasi” na kulingana na tafsiri 59. Ismatul-Anbiyai.Uk 76. chapa ya Jidah. 116
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:30 PM
Page 117
Sehemu ya pili
iliyolazimishwa yarejea kwenye “Jua” hali ikiwa neno jua halikutajwa kabisa katika Aya hizo. 6-Kwa kweli usemi katika kauli yake “Warudisheni” kulingana na tulivyochaguwa waelekezwa kwa viongozi wa majeshi na hapo ndipo mahali pake, na kwa mujibu wa tafsiri iliyonakiliwa kutoka kwa baadhi yao60 inakuwa ni yenye kuelekezwa kwa Malaika, na hali hiyo hailingani isipokuwa iwe warudisheni imetoka Kwake (s.w.t.) kwa sababu ya kuwa daraja yake ni ya juu, na si kwa mtu mfano wa Sulaimani kwa kumlinganisha na wao Malaika. 7- Hapana shaka kuwa wateule katika waja Wake (s.w.t.) wana mamlaka kimaumbile na uwezo waliotunukiwa kuyatumiya maumbile kwa idhini yake subhanahu, kwa malengo matakatifu ili kuthibitisha unabii wao na kuwa wao wametumwa na Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ili wawaongoze waja wake. Na hilo lajulishwa na Aya nyingi baadhi yao tumezitaja katika vitabu vyetu vikubwa kama vile Mafaahiimul-Quran katika juzuu ya kwanza.61 Na hapa suala halikuwa mahali pa mabishano kiasi suala lifikiye kwenye kutumia muujiza na kuyatumia maumbile kwa kuliamuru Jua lirudi, kwakuwa swala iliyopita wakati wake ikiwa ni ya wajibu kuifidia kwake ni kuiswali kadha, na endapo itakuwa ya Sunnah hapana ishkali itakuwa imepitwa na wakati wake. Hivyo basi hapakuwa na ulazima wa kuyatumia maumbile kinyume na utaratibu wakena kuwaamuru Malaika wa Mwenyezi Mungu walirudishe Jua ili apate kuswali swala ya Sunnah. 8- Lau yangekuwa makusudio ya “Warudisheni” ni kuwaomba Malaika Wake (s.w.t.) walirudishe Jua ingelazimu ataje lengo la kurejeshwa kwake, kama vile aseme: Ili niweze kutawadha niswali, na hili halikutajwa ndani ya Aya hii bali lililtajwa ni kauli yake:“Na akaanza kuwapangusa miundi na shingo.” Na hili ladhihirisha kuwa lengo lililoambatana na rudisho 60. Tabarasiy ameinasibisha kwa Al-Qaylu. 61. Angalia juz 1. Uk.444 - 446. 117
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:30 PM
Page 118
Sehemu ya pili
ni kupangusa miundi na shingo sio kutawadha na kuaswali. 9- Kwa kweli kulitafsiri neno mas’hu ambalo lamaanisha kupaka kwa maana ya kukata, ni tafsiri bila ya dalili, kwa kuwa maana inayokuja haraka akilini kutokana na neno mas’hu ni kupitisha mkono juu yake na sio kuikata na kuiondoa. Na lau makusudio yangekuwa haya kulingana na ilivyo kuja katika kisa hiki ingekuwa yafaa mno aseme: Alianza kuipiga milundi sio kuipaka. 10- Kwa kweli tafsiri iliyokwishatajwa inaishia kwa maaskofu waongo kama vile Kaabu ambaye alikuwa anaingiza visa na habari kwa misukumo yake ya Kiyahudi, na atakaye kuufahamu zaidi mchango wake katika kuingiza uongo na mengine yasiyokuwa hayo itampasa arejee kwenye mjadala wetu ndani ya kitabu Al-milalu Wannahlu. 11- Na kuna baadhi ya wafasiri wameitafsiri kauli Yake: “Na akaanza kuwapangusa miundi yake na shingo.” kwa maana ya kupaka kwa maji ikiwa ni mahali pa wudhu. Na maana hiyo udhaifu wake ni kama uonavyohauna kificho. Kwa sababu lau kama makusudio yangekuwa kama waliyo yataja hao baadhi, basi ni kwanini wamebadilisha “kuosha kwa kupaka?” na “miundi miwili miundi mingi?” na “shingo moja kwa shingo nyingi?”hali ikiwa Sulayman hakuwa isipokuwa na miundi miwili na shingo mmoja.? 12- Kwa kweli kuwauwa farasi ambao Suleyman mwenyewe amewasema kuwa ni kheri kwa hoja kuwa shughuli ya maonyesho ya farasi kwake (a.s.) ilikuwa ndio sababu ya kumpita wakati wa Swala, hili ni sawa na tendo la mtu asiyekuwa na akili kabisa, na Sulaymani ameepukana na tendo kama hili, kwa kuzingatia kuwa Sulaymani ni yule ambaye Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amempa hukumu, elimu mamlaka juu ya ardhi pamoja na wale waliomo humo miongoni mwa majini na wanadamu, pia na mbinguni. Kitendo kama hiki ambacho hakiwezi kutendwa na mtu miongoni mwa watu duni isipokuwa wenda wazimu miongoni mwao, sio watu wakawaida wa sokoni, sembuse manabii wa Mwenyezi Mungu na 118
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:30 PM
Page 119
Sehemu ya pili
mawalii wake waliotakaswa. Na mwishowe tunageuza mtizamo wa msomaji uelekee kwenye usemi wa Sayyid Qutbiy ndani ya tafsiri yake kuhusiana na Aya hizi: Amesema: “Ama kuhusu kisa cha farasi: Kwa kweli Suleyman alifanya maonyesho ya farasi wake jioni, hivyo basi swala ambayo alikuwa akiiswali kabla ya kuzama Jua ilimpita, akasema: Warudisheni kwangu, wakawarudisha kwake, akaanza kuwapiga shingo zao na miundi yao ikiwa ni malipo yao kwa vile walimshughulisha asiweze kumdhukuru Mola wake. Na katika riwaya nyingine imeelezwa kuwa alianza kuwapangusa miundi yao na shingo zao kuonyesha heshima kwao kwa kuwa walikuwa farasi kwa ajili ya njia ya Mwenyezi Mungu.” Kisha akasema- yaani Sayed Qutub-: “Na riwaya hizi mbili zote hazina dalili ya kuthibitisha madai hayo, na inakuwa vigumu kukata shauri kuhusiana nazo.”62 Lakustaajabisha kumhusu Sayyid Qutbiy ni kuwa riwaya zote mbili amezipa daraja moja, hali ikiwa riwaya ya kwanza inapingana na maamuzi ya kiakili na sera za manabii na za wanavyuoni, kwa hiyo ni rahisi kukata shauri kuwa ni riwaya batili. Ama kuhusu ya pili inaafikiana kikamililifu na dhahiri za Aya zilizohusika, nayo imeelezwa kutoka kwa Hibrul-Umma Ibnu Abbasi. Raziy amesema ndani ya kitabub Ismatul-Anbiyai kuhusu hikaya hizi: “Kisha kwa kweli Suleyman (a.s.) aliketi ili farasi waonyeshwe kwake, kisha alibainisha kuwa hilo halikuwa kwa sababu ya kupenda dunia kwa kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu amelikiri alilolisema: “Navipenda vitu vizuri kwa kumkumbuka Mola wangu” kisha aliamrisha wakimbiye mpaka walifichika nyuma ya pazia, yaani mpaka walitoweka machoni mwake kisha aliamrisha warudishwe, akaanza kuwapangusa miundi yao na shingo zao ikiwa ni heshma kwao na kubainisha utukukufu wao kwa kuwa wao ni usaidizi mkubwa mno kumsukuma adui… Haya tuliyo yasema ni maneno yanayoafikiana na tamko na yanakubaliana na yaliyo kabla ya Aya na yaliyo baada yake…” 63 62. Fi dhwilalil-Quran al-kariim Juz 23. Uk 100. 63. Ismatul-Anbiyai cha Al-fakhri Raziy. Uk 76. chapa ya Jidah. 119
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:30 PM
Page 120
Sehemu ya pili
Na imenakiliwa riwaya ya kwanza64kutoka kwa watu waliokuwa hawajihadhari kuchukuwa riwaya kutoka kwa mapadri wanaojifanya waisilamu, kwa hiyo Tabariy ameinakili ndani ya tafsiri yake kutoka kwa Asidiy na Qutada mpaka kiasi kwamba Tabariy katika kuchagua riwaya bora kati ya riwaya mbili aliichaguwa kauli ya Ibnu Abbasi na akaitolea sababu, akasema: “Kwa kweli Nabii wa Mwenyezi Mungu hakuwa wakumuadhibu mnyama kwa kumchinja na aiangamize mali katika mali yake bila ya sababu ila tu ni kwa sababu alizuilika kuswali kwa kuwaangalia, wala wao hawana dhambi kwa kuzuwilika kwake kuswali kwa kuwaangalia kwake.65 Na si haba aliyoyanakili Suyuti katika kitabu Adurulmanthur kwa kuyalinganisha na haya miongoni mwa Hadithi za kubuni kuhusiana na farasi hawa hivyo imeelezwa kutoka kwa Ibrahim Atamimiy kuwa amesema: “Walikuwa farasi ishirini elfu wenye mbawa akawachinja” wakati huohuo alinukuu kauli ya Ibnu Abbas kuhusu tafsiri ya mas’hu: “Sulayman alikuwa akipangusa vishungi vya farasi na ukano wa mvungu wa goti la farasi.”66 Hii ndiyo hali ya tafsiri iliyobebeshwa juu ya Aya. Na kuna kishiko kingine kuhusiana na kisa hiki cha Nabii wa Mwenyezi Mungu Suleyman kutoka kwa wakosoaji tutakileta. Mtihani aliyotahiniwa Sulayman: Amesema (swt):
“Na hakika tulimjaribu Suleymani na tukauweka mwili juu ya kiti 64. Nayo ni riwaya ya Sulayman kusahau swala na kuzamia kwenye maonyesho ya farasi. 65.Tafsir Tabarasiy, Juz 3, Uk 100. 66. Ad-Durul-Manthur, Juz 5, Uk 309. 120
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:30 PM
Page 121
Sehemu ya pili
chake, kisha akarejea.* Akasema: Mola wangu! Nisamehe na unipe ufalme, asiupate yeyote baada yangu, bila shaka wewe ndiye Mpaji.” (Saad:34-35). Na ili kuwadhihisha faidisho la Aya hii yatakiwa kwenda hatuwa moja baada ya nyingine kwa kujadili mambo kadhaa: i. Ni mtihani upi ambao Sulaymani (a.s.) alitahiniwa? ii. Nini maana ya kuomba msamaha ilihali ameshikilia kamba ya ismah? iii. Kwa nini anajiombea ufalme binafsi? iv. Kwa nini anaomba ufalme ambao haifai uwe kwa mwingine yeyote baada yake? Ama kuhusu swali la kwanza: Katika Aya zilizokuja kuhusiana na habari hizi hakuna kinachoweka wazi ukweli wake. Ama riwaya wamenakili wanazuoni wa Hadithi riwaya kadhaa zikibainisha mtihani,baadhi ya riwaya zaonesha kuwa ni Israiliyati, zimesambazwa na wanazuoni wa kiyahudi kati ya Waislamu, na Waislamu wamekumbwa na mtihani huu katika nyanja nyingi za tafsiri, historia na za kiitikadi na … kwa hiyo tarajio ni kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) awajaaliye jamaa miongoni mwa wanataaluma na wahakiki na awape tawfiki ya kubadili mkondo na kurekibisha vitabu vya kiislamu na kuvisafisha viwe mbali na riwaya zao. Lakini kati ya riwaya hizi ambayo yaweza kutegemewa ni ile iliyosemwa: Kuwa Suleyman alikuwa na mtoto kijana mwerevu, alikuwa akimpenda sana. Mwenyezi Mungu alimfisha ghafla bila ya ugonjwa wowote akiwa kwenye kiti chake cha enzi, ikiwa ni majaribu kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kwa Nabii wake Sulaymani ili kuona subira yake katika kumfisha mwanawe na aliudondosha mwili wake juu ya kiti chake67. Na bwana Raziy amenakili hekaya hii kwa sura ya uwezekano wa tatu, lakini katika hali inayoashiria kuingia kwa Israiliyati humo, alisema: “Alizaliwa mtoto wa Suleyman, hapo Shetani walifanya hila ya kumuuwa, 67.Tanziihul-Anbiyai. Uk. 99. chapa ya zamani. 121
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:30 PM
Page 122
Sehemu ya pili
wakasema: Tunaogopa asije tuadhibu kama anavyotuadhibu baba yake. Basi Suleymanu {a.s} ) aliyaamrisha mawingu yalimbeba na aliuamrisha upepo ukamchukuwa kuwahofia Shetani, hivyo basi mtoto alifariki hapo na maiti ilitupwa juu ya kitanda chake kumtihani alipowahofia Shetani.68 Na shuhuda za kuwa riwaya hii ni ya kuwekwa ziko wazi, kwa sababu mienendo ya mashetani ilikuwa imefungika kwa Sulayman, na baadhi yao walikuwa wanafanya kazi mbele ya Sulayman, kwa hiyo itakuwaje awaogope kiasi cha kukimbilia kwenye kazi kama hii! Na tukifumbia macho aliyoyanakili Raziy tunasema: Wala hapana shaka kuwa kupata mtihani wa kufiwa na mtoto kijana ni miongoni mwa mitihani mikubwa mno, na subira katika hali hii na kulikabidhi swala hili kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ni dalili ya ukamilifu wa nafsi. Hivyo basi lengo la mtihani halikuwa isipokuwa kuimarisha ukamilifu uliohifadhika ndani ya dhati yake, ili uweze kujitokeza kutoka kwenye hali ya nguvu na kuja kwenye kitendo. Atakaye ziyada kuhusu falsafa ya majaribu na mitihani basi arejee tuliyo yaandika ndani ya juzuu ya tano ya kitabu Mafahiimul-Quran kwenye mjadala wa majaribu ya Ibrahim ya maneno.69 La ajabu ni kuwa Sayyid Qutbiy amezitegemea riwaya zinazoonekana kuwa ni miongoni mwa Israiliyaati katika kutafsiri neno mtihani, riwaya alizozichukuwa Abu Hurera kutoka kwa Kaabu Al-Ahbari amesema: “Sijaipata athari iliyo sahihi niwezayo kuitumainia katika tafsiri ya mwili uliodondoshwa juu ya kiti cha enzi cha Suleymani isipokuwa Hadithi sahihi. Lakini uhusiano wake na mojawapo ya matukio haya mawili hauna uhakika. Na Hadithi hii ni ile aliyoieleza Abu hurera kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.), na Bukhari ameileta ndani ya Sahih yake kwa sifa ya Hadithi ya kuvushwa (marfuu), na tamko lake ni kama ifuatavyo: “Nabii wa Mwenyezi Mungu Suleymanu alisema: Wallahi nitawazungukia 68. Ismatul-Anbiyai, Uk 78, chapa ya Jidah. 69. Mafahimul-Qur’an, Juz 5, Uk 206. 122
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
12:30 PM
Umaasumu wa Mitume
Page 123
Sehemu ya pili
usiku huu wa leo wanawake sabini kila mmoja wao atazaa askari mpanda farasi atakayepigana katika njia ya Mwenyezi Mungu na wala hakusema “In shaallahu”. Hivyo Suleymani aliwazungukia, na wala hakubeba mimba ila mwanamke mmoja ambaye alizaa upande mmoja wa mwanaume. Naapa kwa yule ambaye nafsi yangu iko mikononi mwake: Lau angesema Inshaallah wangepigana katika njia ya Mwenyezi Mungu wote wakiwa askari wapanda farasi.” Kisha Sayyid Qutbiy alisema: “Mtihani huu unaoashiriwa na Aya hizi ambao ni mwili huu inawezekana ukawa ni huyu mzaliwa kipande, lakini hii ni dhana tu ya uwezekano.”70 Na Raziy ameileta hikaya hii kwa sura ya tafsiri ya ule mwili katika namna nyingine kutoka kwa Nabii (s.a.w.), nayo ni kuwa: “Suleymani alisema: Nitawazungukia usiku huu wanawake mia moja… na wala hakusema Inshaallah, naye aliwazungukia wala hakubeba mimba isipokuwa mmoja akazaa nusu kijana wa kiume, basi mkunga akamleta na kumtupia mbele yake juu ya kiti chake, na lau angesema Inshaallah ingekuwa kama alivyosema.”71 Na mtoa maoni yake kuhusiana na Hadithi hii katika kitabu hiki amesema: “Hadithi hii ameieleza Bukhari na Muslim kutoka kwa Abu Hureira kwa tamko lisilokuwa hili”.72 Na sisi hatusemi kitu kuhusiana na Hadith hii, tunaacha uwamuzi kwa msomaji aamuwe, na yatosha Hadith hii kuwa dhaifu kwa kule kuwa ni miongoni mwa riwaya za Abu hureira, na Sayyid Qutbiy ameieleza kuwa ni uwezekano tu kama ulivyokwishatambuwa.
70. Fi dhwilalil-Quran al-kariim Juz 23. Uk 99. 71. Ismatul-Anbiyai.Uk.77. Chapa ya Jidah. 72. Pambizoni mwa Ismatul-Anbiyai.Uk.7. Chapa ya Jidah. 123
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:31 PM
Page 124
Sehemu ya pili
Kwa mujibu huo lajulikana jibu kuhusiana na swali la pili, kwa hiyo ni wazi kuwa yeye (a.s.) alikuwa na matumaini na matarajio naye, lakini Mwenyezi Mungu alimfisha na kumtupa kwenye kiti chake, ili amzinduwe kuwa ukweli wa uja ni kumkabidhi mambo Mwenyezi Mungu na kusalimu amri kwake, na yawezekana kadiri hii ya matumaini na matarajio kwa mtoto yahesabika kuwa ni aina ya kujitenga mbali na Mwenyezi Mungu na kumwelekea mtoto. Na kujiambatanisha kama huku na mtoto japokuwa sio maasi lakini linalo pendeza zaidi kulingana na hali ya mawalii isiwe hivyo, kwa ajili hiyo alipotambuwa wadhifa wake unaolingana na nafasi yake na la lazima kwa daraja yake, alirejea kwa Mwenyezi Mungu na aliomba msamaha kama ambavyo (s.w.t.) asemavyo: “Kisha akarejea” na “Akasema: Ewe Mola wangu nisamehe.” Na imerudiwa rudiwa kutoka kwetu kuwa, kuomba msamaha sio dalili ya maasi na kutokea kwa dhambi, bali huwa kutenda au kuacha, kulikotokea kwa baadhi ya watu wenye kutambuwa uhakika wa umola na uhakika wa uja, wenye kutambuwa kuwa ni bora na inafaa sana wao wawe kinyume na kitendo hiki au katazo lile hulazimu kuomba msamaha, japokuwa tendo lililoachwa au lililotendwa sio maasi na wala haikuwa ni kumhalifu Muumba kulingana na mantiki ya kisheria. Kwa ajili hiyo mawalii wa Mwenyezi Mungu bado waomba msamaha kila mchana na usiku kwa sababu ya hisia zao na utambuzi wao mkali kuhusu ukubwa wa wadhifa mbele ya utukufu wa Muumba. Ama kuhusu swali la tatu: Namaanisha kuomba ufalme kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.). Ufalme ulioombwa haukukusudiwa dhati yake, kwa sababu ufalme kama huo hauepukani na dhulma na kukiuka na kuziponda haki, na yasiyokuwa hayo katika jumla ya yaliyoashiriwa na kauli yake Taala:
124
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:31 PM
Page 125
Sehemu ya pili
“Akasema: Hakika wafalme wanapouingia mji wana uhauribu na wanawafanya watukufu wake kuwa dhalili, hivyo ndivyo wanavyofanya.” (an-Namlu: 34) Na katika kauli yake:
“Ama ile jahazi ilikuwa ya masikini wafanyao kazi baharini, na nilitaka kuiharibu, na nyuma yao alikuwako mfalme anakamata majahazi yote”. (al-Kahfu:79) Hivi ndivyo ulivyokuwa mwendo wa wafalme na hayo ndio yalazimianayo na ufalme katika zama zilizopita, bali hata za sasa na katika kila zama, kwa hiyo ufalme ni ukandamizaji, kutaka kuabudiwa, kunyang’anya mali, kuuwa nafsi ipasayo kuheshimiwa, na kujiambatanisha na kila aina ya ukiukaji unyanyasaji na dhulma. Hilo liko wazi kwa mwenye kuchunguza historia ya masultani na sera zao katika zama zilizopita na za hivi sasa. Nabii wa Mwenyezi Mungu Suleymani aliomba lililo kinyume na hilo, kwa hakika alimuomba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ufalme utakaomfanya awe mtu aliyepewa elimu hukumu na kutunukiwa unabii na wahyi, na ambao utamfanya awe mtu aliyetunukiwa elimu na hukumu na kupata sharafu ya unabii na wahyi. Basi kutokana na hali yake hii ufalme uliyoombwa si ufalme kama ufalme, bali huwa umeombwa ili uwe nyenzo katika njia ya kuithibitisha haki na kuibatilisha batili na kuwahudumiya viumbe wa Mwenyezi Mungu (s.w.t.). 125
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:31 PM
Page 126
Sehemu ya pili
Na huenda hilo likatiwa nguvu na alilolisema Raziy katika kitabu Ismatulanbiya aliposema kuhusu jibu la utata huu: “Jibu lake lipo ndani ya sababu saba: Ya kwanza: Ni kuwa muujiza wa kila Nabii yapasa ulingane na hali za watu wa wakati wake, na ilipokuwa kukabiliana na watu wa zama zake kulihitajia kuwa na mali na mamlaka aliomba mamlaka inayozizidi mamlaka zote ili iwe muujiza kwake”.73 Lakini kwa kuwa linaloingia haraka akilini mwa watu wa kawaida ni ufalme wa kidhalimu tunaona Qur,an Tukufu inapomsifu Mwenyezi Mungu kwa ufalme inaambatanisha na sifa ya Qudusu yaani Mtakatifu ili kuashiria kuwa ufalme wake na mamlaka yake watofautiana na mamlaka zingine kwa hiyo yeye alivyokuwa mfalme wa ulimwengu, yeye ni Qudusu mwenye kutakasika na kila aibu na dosari na kila ukiukaji na kwa hiyo yeye ni
“Mfalme, Mtakatifu, Mwenye salama, Mtoaji wa amani, Mwangaliaji, Mwenye nguvu, Jabari, Mkubwa, Mwenyezi Mungu yu mbali na hao wanaomshirikisha.” (al-Hashru:23). Wanahistoria wamenakili kuwa Nabii (s.a.w.) alikuwa akisema: “Mimi si mfalme” hali ya kuwa alikuwa hakimu wa kiungu na Rais wa dola ya kiislamu aliyeiasisi tokea alipoingia Madina. Makusudio yake kuwa yeye si mfalme ni kujiweka mbali na yale yanayoharakia kwenye uelewa wa watu wa kawaida wasikiapo tamko hilo. Kuwa yeye si katika kundi la hao, bali yeye ni hakimu wa kiungu anaefanya juhudi kuurekibisha umma huu kulingana na kanuni za kiungu. Kwa ujumla ni kuwa kuna tofauti kati ya mamlaka yanayohodhiwa na silika za kinafsi na kutumiwa na utashi wa kibinafsi na kutumikishwa na upendo wa mtu mwenyewe ukiamuliwa na umimi, na kati ya mamlaka 73. Ismatul-Anbiyai. Uk.78. chapa ya Jidah. 126
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:31 PM
Page 127
Sehemu ya pili
inayochungwa na unabii na maasi yake kuzuiliwa na hofu ya Mwenyezi Mungu, na ashki ya ridhaa zake, ambayo ni kwa ajili ya kuwahudumia waja wake. Na ambao Suleimani aliuomba ndani ya Aya hii ni huu wa pili, nao ni kazi ya kiungu na ni kwa ajili ya kutoa huduma ya dini, ni kazi inayomkurubisha kwa Mwenyezi Mungu, wala siyo ule wa kwanza. Na ili akili za swahaba zisiharakiye kwenye maana inayofahamika kutokana na tamko mfalme, Mtume wa Mungu (s.a.w.) alifafanuwa alilo liomba Suleiman kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) Alisema: “Je mmeona alichopewa Suleiman bin Daud katika ufalme wake, huo ufalme haukukumzidishia isipokuwa unyenyekevu, alikuwa hainui macho yake mbinguni kwa ajili ya kumnyenyekea Mola wake.”74 Tayari tumeshafafanua mamlaka iliyoletwa na Kitabu na Sunnah, tumeonyesha misingi yake, fifa zake na malengo yake ndani ya kitabu chetu Mafahimul-Qur’an basi rejea huko75. Kutokana na hayo jibu la swali la nne la fahamika, na ya kuwa kwa nini alisema: “Asiupate yeyote baada yangu”. Yeye hakusema hivyo kwa choyo na ubakhili dhidi ya mtu mwengine, bali alisema hivyo kwa kuwa aliomba ufalme ambao haufai kwa mantiki ya kiakili na kisheria autumikishe mtu mwingine, au aliye mfano wake katika elimu na imani, hivyo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amebainisha ishara za hukumu hii katika Aya nyingine na anasema:
“Basi tukamtiishia upepo ukaenda polepole kwa amri yake anakotaka kufika.* Na mashetani kila ajengaye na azamiaye. * Na wengine 74.Ruhul-Bayan Jalada la 8. Uk.39. 75. Tazama juzuu ya kwanza na ya pili sehemu ya kwanza, Uk 11 - 72. 127
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:31 PM
Page 128
Sehemu ya pili
wafungwao minyororoni.* Hiki ndicho kipawa chetu bila ya hesabu, basi fanya ihsani au zuia. * Na kwa hakika alikuwa mbele yetu mwenye cheo cha kukaribiana na mahala pazuri.” Sad:36-40. Kwa hiyo Aya katika usemi wake: “Basi tukamtiishia” yajulisha kuwa hakuomba ufalme kama ufalme ili uwe ni mamlaka ambayo anaweza kumwongoza mwanadamu ajulikanaye katika watu, khususan akiwa miongoni mwa watu wema, bali aliomba uwezo unaomfikisha kwenye kutiishiwa upepo, anga na mashetani. Na uwezo kama huu haiwezekani kwa mantiki ya kiakili uwe kwenye uwezekano wa kufikiwa na mikono ya watu wa kawaida, kwa sababu kuwepo kwa mamlaka kama hiyo mkononi mwa mtu ambaye sio maasumu itamfikisha kwenye ukiukaji na kubomoa mipaka na kudai uungumtu, na mengineyo yasiyokuwa hayo miongoni mwa ufisadi mkubwa. Lakini itaambatana na wema na kuwa ndiyo sababu ya ufanisi endapo tu itakuwa chini ya matumizi ya Nabii anayetambuwa utukufu wa jukumu, kwanza mbele ya Mwenyezi Mungu, na mbele ya akili na dhamira pili, na mbele ya viumbe tatu. Kwa ajili hiyo anasema: “Asiupate yeyote baada yangu”, huyu yeyote anamlenga mtu wa kawaida asiye na maandalizi ya kubeba jukumu kama hili na asiyeshikamana na kamba ya ismah, na asiyekuwa na sifa ya unabii, kwa kuwa ufalme huu kama vile ulivyotambuwa haumfai yaeyote bali wamfaa Suleymani na mwenye kuwa katika daraja yake ya uhifadhi na ismah. Hayo tuliyoyasema ameyaashiria Murtadha kwa kusema: “Aliomba ufalme wake uwe alama ya unabii wake, kwa ajili yake ajitofautishe dhidi ya yule asiyekuwa miongoni mwa manabii. Na kauli yake: “Asiupate yeyote baada yangu” alikuwa anakusudia kuwa huo asiupate yeyote asiyekuwa mimi miongoni mwa wale ambao mimi nimetumwa kwao, wala hakukusudia baada yake mpaka siku ya kiyama miongoni mwa manabii”.76
76. Tanziihul-Anbiyai. Uk.100. 128
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
12:31 PM
Page 129
Umaasumu wa Mitume
Sehemu ya pili
8 Ismah ya Ayyubu (A. S.) Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amemsifu Nabii wake mtukufu Ayyubu kwa sifa zilizo tukufu mno amesema: “Bila shaka tilimkuta ni mwenye subira, mja mwema, kwa hakika alikuwa mnyenyekevu mno.” (Sad:44). Pamoja na yote hayo bado mkosowaji ameleta dalili kuwa Ayubu hana ismah yeyote, amesema hivyo kwa kutumia maana ya dhahiri ya baadhi ya Aya ilihali zenyewe hazijulishi lile walikusudialo. Aya zenyewe ni hizo: Amesema (s.w.t.):
“Na Ayubu alipomwita Mola wake ya kwamba imenigusa dhara nawe ndiye unayerehemu zaidi kuliko wanaorehemu. * Basi tukamkubalia na tukamwondolea dhara aliyokuwa nayo na tukampa watu wake na mfano wa pamoja nao ni rehema kutoka kwetu, na ukumbusho kwa wafanya ibada.” (Anbiyau: 83-84) Na akasema:
129
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:31 PM
Page 130
Sehemu ya pili
“Na mkumbuke mja wetu Ayubu, alipomwita Mola wake: Kwa hakika shetani amenifikishia udhia na tabu.* Kaza mwendo, hapa mahala baridi pakuogea na kinywaji.* Na tukampa watu wake na wengine kama wao pamoja nao, kwa rehema itokayo kwetu na mawaidha kwa watu wenye akili.* Na shika kicha cha vijiti mkononi mwako, kisha mpige nacho wala usivunje kiapo bila shaka tulimkuta ni mwenye subira, mja mwema, kwa hakika alikuwa mnyenyekevu sana.” (Sad:41-44). Mkosowaji ametowa dalili kuthibitisha utokeaji wa dhambi kwa manabii kwa kutumia yale yaliyokuja ndani ya Aya hizi, naikusudia kauli yake : i. Shetani amenifikishia ii. Udhia na tabu Bila shaka wamedhania kuwa kufikishiwa na Shetani kwa lazimu kutokea dhambi upande wa Ayubu, wakiwa wameghafilika kuwa jumla hii ni ibara nyingine ya ile iliyokuja ndani ya sura Anbiyai ambayo ni kauli yake: “Imenigusa dhara” kama ambavyo wamedhania kuwa tabu maana yake ni adhabu ya kiungu wakiwa wameghafilika kuwa tabu maana yake ni kila ambalo litialo usumbufu na mashaka kwa mwanadamu, na hiyo ndiyo makusudio ya neno tabu, mchoko, maumivu na machungu. Hayo yote yana maana zinazolingana. Kwa ujumla Aya haina dalili ya kutokea dhambi aslani, bali usemi uko katika kubainisha sababu ya mtihani wa Ayubu kwa machungu haya! Na haya yatakuwa wazi baada ya kuzibainisha Aya na kutafsiri misamiati yake. Twasema: Raghibu amesema ndani ya kitabu chake Mufradatul-Quran: “Dhara ima ni hali mbaya ndani ya nafsi yake itokanayo na uchache wa elimu, ubora na kukosa utawa, na ima ni hali mbaya ya mwilini mwake kwa sababu ya dosari, au ya hali yake ya nje itokanayo na uchache wa mali na cheo.”
130
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:31 PM
Page 131
Sehemu ya pili
Na kauli yake: “Na tukamwondolea dhara aliyokuwa nayo” yawezekana ni kwa haya matatu yaliyotajwa, isipokuwa tu dhara hapa ina maana inayolingana na maradhi ambayo si maana ya pili aliyoitaja Raghibu, na kwa ajili hiyo Allamah Tabatabaiy amesema: “Dhara ni linalogusa nafsi miongoni mwa madhara kama maradhi, kuisha nguvu kwa kuchoka au kumalizika kifikra na mfano wa mawili hayo, na mwisho wa Aya hizo watilia nguvu maana hii. Ama Udhia ni usumbu. Na Kaza mwendo ni kukimbia kwa mguu. Hizi ndio lugha zilizomo katika Aya, na baada ya kujua maana zake sasa turejee kwenye tafsiri ya Aya. Utatambuwa kuwa haipatikani humo hata harufu ya kutokea maasi yeyote kwa Nabii Ayubu ambaye ni dhihirisho la subira, uvumilivu na mapambano. Tafsiri ya kauli yake: Imenigusa dhara. Ama iliyokuja ndani ya sura Anbiyai haijulishi zaidi ya kuwa alipatwa na dhara na kukumbwa na balaa hapo akamnyenyekea (s.w.t.) akamsihi akisema: “Imenigusa dhara nawe ndiye unayerehemu zaidi kuliko wanaorehemu.”. Basi hapo rehema ya kiungu ikamuenea na akaingizwa kwenye uangalizi wa Mwenyezi Mungu. Mungu (s.w.t.) alimuondolea dhara alizokuwanazo, na ni yumkini kabisa kuwa makusudio ni maradhi na Mwenyezi Mungu alimponya maradhi hayo aliyokuwa amekumbwa nayo kwa miaka mingi. Bali Mwenyezi Mungu aliwahuisha ahli zake na kumwongezea wengine mfano wao, hayo yote ni rehema kutoka kwake, na haikuwa kazi hiyo ila ni mtihani kutoka Kwake (s.w.t.) kwenda kwa Ayubu na wengine miongoni mwa wachamungu ili watiye akilini na wajuwe kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) huwashushia balaa mawalii wake kisha huwapa ujira wao na wala haupotezi ujira wa watu wema. Na balaa au mtihani sio jambo lingine ila ni kwa ajili ya kufunguka ukamilifu huo uliofichwa na kuhifadhiwa ndani ya dhati ya mtahiniwa, na wala hautodhihiri ukamilifu huo ila pale 131
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
12:31 PM
Umaasumu wa Mitume
Page 132
Sehemu ya pili
mwanadamu atakapokuwa katika kalibu la mtihani, hapo hujitokeza yaliyo ndani yake na yaliyo siri yake miongoni mwa ukamilifu na vipaji, na hilo tumeliweka wazi katika baadhi ya maandiko yetu. Amirul-Muuminina (a.s.) anasema katika uwanja huu: “Na maana yake ni kuwa yeye anawatahini kwa mali na watoto ili abainike mwenye kuikasirikia riziki yake na mwenye kuuridhia mgao wake japokuwa yeye (s.w.t.) anawajua vyema kuliko wanavyojijua wao wenyewe, lakini ili kujitokeze vitendo ambavyo kwavyo hustahiki thawabu na adhabu.”77 Tafsiri ya: Shetani amenifikishia Ama Aya zilizokuja ndani ya sura Swad ndizo zilizoangukia kwenye visingizio vya baadhi ya wakosowaji eti kuwa (s.w.t.) alimtia Ayubu kwenye balaa la baadhi ya maradhi ya kuchukiza. Hali ikiwa hakuna ndani ya Aya hizo ishara wala dokezo juu ya hilo isipokuwa katika baadhi ya Hadithi ambazo zashabihiyana na Israiliyati. Amesema (s.w.t.): “Na mkumbuke mja wetu Ayubu, alipomwita Mola wake: Kwa hakika shetani amenifikishia udhia na tabu.” Umekwishatambuwa maana ya Udhia, ama kuhusu neno Tabu maana yake haivuki mapana zaidi ya kinachoudhi roho miongoni mwa hali mbaya, kwa hiyo kauli yake: “Shetani amenifikishia” ni ibara ya maana ile aliyoisema katika sura Anbiyai kwa kauli yake: “Imenigusa dhara”, hivyo katika sura hii aliuhusisha uteremkaji wa udhia na tabu na Shetani, lakini yeye alinyamaza kumtaja mtendaji wake katika sura Anbiyai, hapo basi ni lazima kuzingatia maana ya jumla hii, kwa hiyo twasema: Yawezekana moja ya maana mbili: 1- Iwe madhara na maradhi yaliyomgusa yanaegemezwa kwa Shetani kwa aina fulani ya sababu na taathira, badala ya kuegemeza kwenye sababu za kawaida za kimaumbile kama ambavyo mwanadamu husibiwa na taabu 77. Nahjul-Balagha, sehemu ya hekima, namba 93. 132
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:31 PM
Page 133
Sehemu ya pili
kwa njia ya sababu za kimaumbile, pia husibiwa na taabu kwa aina fulani ya kuguswa na Shetani, na hayo yote ni kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.). Na hii ndiyo maana ambayo mtu anaweza kuielewa kutokana na riwaya, nayo japokuwa haiungwi mkono na maana ya dhahiri ya Aya, ila tu kwangu ni miongoni mwa mambo yaliyo muhali kwa kuwa ikiwa sababu za kimaumbile zina mamlaka juu ya manabii kuhusu maradhi yao basi hakuna kiziwizi Shetani kuwa na mamlaka hususan katika uwanja huu wa kuwapotosha na kuathiri ndani ya mioyo yao na itikadi zao, yote hayo kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.), hususani endapo hayo yatakuwa kwa ajili ya mtihani. Na Zamakhshari amekanusha mamlaka kama hii akisema kuwa “Sio jaizi Mwenyezi Mungu ampe Shetani mamlaka juu ya manabii wake yawafikishe kwenye kuwaadhibu na kuwatia taabuni ili akidhi haja yake, na akiliweza hilo hatouacha wema isipokuwa atauweka kwenye maafa na kuuangamiza, na Qur’an imekariri kuwa yeye Shetani hana mamlaka isipokuwa kutia wasiwasi tu.”78 Nasema: Litakuwa sahihi alilolisema iwapo tu Shetani atakuwa na uwezo usio na mipaka na wa kuwaenea swalihina na waumini wote, kwa ajili hiyo hatomuacha mwema ila atakuwa amembadilisha endapo ataiweza njia ya hilo. Na hii sio kauli ile isemayo kuwa ana uwezo wa kuwatawala baadhi tu, nao ni Ayubu kwa idhini kutoka Kwake (s.w.t.), na wala hakuna dalili ya kuzuilika kadhia ya baadhi. Itakuwaje hivyo ilihali (s.w.t.) ame eleza kwa kauli yake kumuhusu kijana wa Musa naye ni nabii Yoshua kwa kauli yake: “Hakika mimi nimesahau yule samaki na wala hakunisahaulisha ila ni Shetani nisimkumbuke.” (Al-kahfu:63). 2- Makusudio ya “Kwa hakika shetani amenifikishia udhia na tabu” ni wasiwasi wa Shetani kwa watu kwa kujiweka mbali na Ayubu na kuwahimiza wajiepushe naye, na kumuhama pale maradhi yalipomzidi, kwa hiyo maneno yalikuwa kutoka kwa watu lakini kwa wasiwasi wa kuto78. Al -Kashafu, Jalada la 3. Uk 16. 133
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:31 PM
Page 134
Sehemu ya pili
ka kwa Shetani, hivyo ibara hii yenyewe na maneno yao haya vilikuwa ni udhia na ni tabu kwa Ayubu, kwa hiyo makusudio ya udhia na tabu ni maneno yatokanayo na wasiwasi wa Shetani. Kwa makadirio yoyote yawayo hakuna dalili ya neno tabu lililopo baada ya udhia, kuwa ilikuwa ni adhabu kutoka Kwake (s.w.t.) kwa Nabii wake Ayubu. Imamu Jafar As-Sadiq (a.s.) anasema: “Kwa hakika Mwenyezi Mungu alimpa Ayubu mtihani bila ya dhambi akavuta subira mpaka alipoaibishwa, na kwa kweli manabii hawavumilii kuaibishwa.”79 Ama kuhusu Hadithi zilizokuja kuhusiana na kisa cha Ayubu, eti kuwa alipatwa na ukoma kufikia kiasi cha kukatika viungo vyake vya mwili. Imamu Al-Baqir (a.s.) asema kumhusu Ayubu: “Kwa kweli Ayubu alitahiniwa bila ya dhambi, na kwa kweli manabii hawatendi dhambi, kwa sababu wao ni maasumin wamehifadhiwa wametahirishwa, hawatendi dhambi wala hawapotoki, hawafanyi dhambi kubwa wala ndogo.” Na alisema: “Kwa kweli Ayubu ingawaje alipatwa na mitihani yote hiyo hakutowa harufu mbaya wala sura yake kuwa mbaya wala mwili wake haukuwa unatoa damu wala usaha wala hakuonwa kinyaa na yeyote aliyepata kumuona, wala mtu yeyote aliyepata kumuona hakumtelekeza na wala hakutoka wadudu. Ni kama hivi Mwenyezi Mungu Mtukufu huwaweka wote anaowapa mtihani miongoni mwa manabii wake na mawali wake wenye heshma mbele yake. Na watu walijitenga mbali naye bila kumuunga mkoono na kumfariji kwa sababu ya ufakiri wake na udhaifu wake katika hali ya dhahiri ya mambo yake kwa sababu ya kutokujua kwao hadhi aliyokuwa nayo mbele ya Mola wake. Na hakika Nabii (s.a.w.) alikwishasema: “Wenye kukabiliwa na balaa kubwa mno katika watu ni manabii kisha walio mfano wao.” Mwenyezi Mungu Mtukufu alimfanyia mtihani mkubwa mno ambao unamdhalilisha kwa watu wote ili wasimdaiye uungu waonapo yale ambayo Mwenyezi 79. Biharul-An’war, Juz 12, Uk 347, amenukuu kutoka kitabu An’warut-Tanzil. 134
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
12:31 PM
Umaasumu wa Mitume
Page 135
Sehemu ya pili
Mungu anataka kumpa miongoni mwa neema zake kubwa kubwa, ili wamuonapo iwe ni dalili kwao kwa hilo kuwa ni thawabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu amezitaja kwa namna mbili: Ya kustahiki na ya kufanywa mahususi kwa ajili yake na ili wasimdharau mtu mnyonge kwa unyonge wake, wala fakiri kwa ufakiri wake, na ili wajuwe kuwa Yeye (s.w.t.) humfanya mgonjwa amtakae na humponya amtakaye apendapo, Naye amekuwa na enzi na ametukuka katika yote hayo, ni mwadilifu katika maamuzi yake na ni Mwenye hekima katika matendo yake hawatendei waja wake ila jema mno kwao na wala hawana nguvu ila kwalo.”80 Riwaya hii itokayo nyumba ya wahyi na utume inabainisha itikadi ya maimamu kuwahusu manabii kwa ujumla na kumuhusu Nabii Ayubu khususan, na kwamba manabii hawapatwi na maradhi ya kuchukiza, kwani hayo hayaafikiani na lengo la kutumwa, na kwamba kutahiniwa kwa Ayubu kulikuwa kwa ajili ya malengo ya kimalezi ambayo yameashiriwa ndani ya riwaya. Sayyid Murtadhwa amesema: “Mnasahihisha yaliyoelezwa kuwa alipatwa na ukoma mpaka viungo vyake vya mwili vilipakatika? Tutajibu: Ama magonjwa yanayochakaza mfano wa ukoma ambayo huyachukia, humsononesha na humuhuzunisha yule ayaonayo, haifai hata kidogo kama hayo kwa manabii kulingana na yaliyotangulia.”81 Na Allamah Majlisiy amesema baada ya kunakili habari hizi kutoka kwa Imamu Baaqir (a.s.): “Habari hizi zaafikiana mno na wanatheiolojia wa Imamia, kwa kuwa wao wanawatakasa dhidi ya yale yanayosababisha hali ya tabia ya kuwachukia, kwa hiyo habari nyingine zinatafsirika kwa aina nyingine ya tafsiri.”82 80. Al-Khiswal, Juz 2, Uk 400, chapa ya Al-Ghafariy 81. Tanziihul-Anbiyai. Uk 64. 82. Al-Bihar. Juz 12. Uk. 349. 135
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:31 PM
Page 136
Sehemu ya pili
Wanaopinga kauli ya ismah na waonao kuwa yafaa manabii kufanya makosa wametoa dalili juu ya kutokuwa na ismah kwa Nabii Yunus kwa Aya zilizokuja kuhusiana na kisa chake, nasi tunataja muhtasari wa yaliyo kuja katika uwanja huo, kisha tutafafanua makusudio yake, kwa hiyo twasema: Kisa kimekuja kwa namna ya ufafanuzi na kwa sura ya ujumla ndani ya sura nne: 1. “Basi mbona haukuwako mji ulioamini na imani yake ikaufaa, isipokuwa watu wa Yunus. Walipoamini tuliwaondolea adhabu ya fedheha katika maisha ya dunia na tukawastarehesha kwa muda.” (Yunus:98). 2. “Na Dhun Nun alipoondoka hali amechukia, na akadhani kuwa hatutamdhiki basi aliita katika giza kwamba: Hakuna aabudiwaye isipokuwa wewe tu, umetakasika, hakika mimi nilikuwa miongoni mwa madhalimu.” (al—Anbiyau:87). 3. “Basi tukampokelea na tukamwokoa katika huzuni, na hivyo ndivyo tunavyowaokoa wenye kuamini.” (al-Anbiyau:88). 4. “Na hakika Yunus alikuwa miongoni mwa waliotumwa.* Alipokimbia katika jahazi iliyosheheni.* Na wakapiga kura, basi akawa miongoni mwa walioshindwa.* Mara samaki alimmeza hali yakuwa mwenye kulaumiwa.* Na angelikuwa hakuwa katika wanaomtakasa Mwenyezi Mungu.* Lazima angelikaa tumboni mwake mpaka siku watakayofufuliwa.* Lakini tukamtupa ufukoni hali yakuwa mgonjwa.* Na tukamuoteshea mmea wa mung’unya.* Na tulimpeleka kwa laki moja au zaidi.* Basi waliamini na tukawastarehesha kwa muda.” (Swafatu:139-148). 5. “Basi subiri hukumu ya Mola wako, wala usiwe kama mmezwa na samaki, alipomwita na hali yeye alikuwa mwenye huzuni nyingi.* Kama isingelimfikia neema kutoka kwa Mola wake, bila shaka angelitupwa ufukoni na hali yakuwa mwenye kulaumiwa.* Lakini Mola 136
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
12:31 PM
Umaasumu wa Mitume
Page 137
Sehemu ya pili
wake alimchagua na akamfanya miongoni mwa watu wema.” (alQalamu:48-50). Hizi ndizo Aya zilizokuja kuhusiana na kisa cha Yunus, na kwa kukielewa kisa kizima ndiyo mtu anaweza kujibu maswali yaliyoletwa kuhusiana nacho japo baadhi ya Aya hazina fungamano na ismah. Ama miongoni mwa riwaya zilizokuja kuhusiana na kisa hiki ni kuwa zote ni riwaya zisizo na wapokezi wengi, haiwezekani kutegemewa kwenye mambo mahususi yaliyokuja humo, bali baadhi ya yaliyomo humo hayalingani na hadhi ya mtu wa kawaida, sembuse Nabii, kwa ajili hiyo tumeacha kuyataja. Na ambalo riwaya zimesaidiana ni kuwa yeye alipowalinganiya watu wake waamini Uislamu hawakumwitikia, aliwaombea laana na alipojua kuwa dua yake ya laana imejibiwa aliwapa habari kuwa adhabu itawashukia, na ishara za adhabu zilipodhihirika huku baina yao kukiwa na mwanachuoni mchamungu, ndipo alipowashauri wamuelekee Mwenyezi Mungu na wamnyenyekee huenda atawarehemu na kuwaepushia mbali adhabu, wakamuuliza: Tutafanyeje! Akasema: Jikusanyeni na mtoke nje ya mji jangwani, na muwatenganishe watoto na mama zao na kati ya watoto wa ngamiya na mama zao… kisha liyeni na muombe. Walikwenda na kufanya hayo walipiga kelele na kulia, Mwenyezi Mungu aliwarehemu na kuwaepushia adhabu.83 Hivyo basi twasema: Ili kuweka wazi faidisho la Aya lazima kutafiti mambo kadhaa: I. Kwa nini aliwaepushia adhabu watu wa Yunus na si wengine! Kauli yake Mwenyezi Mungu:“Basi mbona haukuwako mji ulioamini na imani yake ikaufaa, isipokuwa watu wa Yunus. Walipoamini tuliwaondolea adhabu ya fedheha katika maisha ya dunia na tukawastarehesha kwa muda.” (Yunus:98). Aya hii yabainisha wazi kuwa umma wa Yunusi ni 83. Biharul-An’war, Juz 14, Uk 380, chapa mpya. 137
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:31 PM
Page 138
Sehemu ya pili
umma pekee uliofaidika na imani yake kabla ya kushuka kwa adhabu, aliwaondolea adhabu, na hivyo ni kwa sababu ya tamko isipokuwa ........ yaani: Hapakuwa na kijiji miongoni mwa vijiji hivi vilivyoijiwa na Mitume yetu na wakawakidhibisha na vikaamini kabla ya kushukiwa na adhabu na vikanufaika na imani hiyo! Hapajatokea kitu hicho isipokuwa kwa kaumu ya Yunusi, walipoamini tuliwaondolea adhabu twezi. Hapana shaka kuwa watu wa Yunus imani yao iliwanufaisha lakini Firaun hakunufaika na imani yake. Hapo ndipo linapozuka swali hili: Ni tofauti ipi iliyopo kati ya imani hizi mbili? Imani ya watu wa Yunus ambayo iliwanufaisha na imani ya Firauni na wafuasi wake na wengine ambayo haikuwanufaisha, kwani Mwenyezi Mungu anasema kwa kauli yake:
“Na tukawavusha bahari wana wa Israel, hapo Firauni na majeshi yake wakawafuata kwa dhulma na uadui hata ilipomfikia kuzama, akasema: Naamini ya kwamba hakuna aabudiwaye ila yule wanayemwamini wana wa Israil, nami ni miongoni mwa wanaotii.* Je, hivi sasa! Na hali uliasi hapo kabla na ukawa miongoni mwa waharibifu.* Basi leo tutakuokoa kwa mwili wako ili uwe dalili kwa ajili ya nyuma yako. Na kwa kweli watu wengi wameghafilika na Aya zetu.�(Yunus:90-92) Jibu: Tofauti kati ya imani mbili ni: Kwa sababu imani ya watu wa Yunus 138
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:31 PM
Page 139
Sehemu ya pili
ilitokana na utashi, azma na uthabiti, na kwa ajili hiyo walibakia katika imani yao baada ya kuondolewa adhabu. Na imani ya mafirauni ilikuwa imani ya kulazimika ya wakati, imekuja kwa sababu ya kuiona adhabu tu wala haikuwa yatokana na mhemko wa kiroho, dhidi ya kufuru na sanamu, bali ilizalishwa na kule kuiona adhabu na kucharuka kwa mawimbi. Wala sisemi kuwa imani ya watu wa Yunus ilikuwa ya uhakika ya umakini, na imani ya wengine ilikuwa ya sura ya nje tu sio ya uhakika bali zote zilikuwa za uhakika, isipokuwa tofauti tu ni kuwa moja imekuja kwa hiari na nyingine imetokana na hofu na kulazimika. Na kwa ibara nyingine: moja ya hizo imekuja na kichocheo cha ndani na ya pili imetokana na kichocheo cha nje. Na dalili juu ya hilo ni kuimarika na kuthibiti kwa watu wa Yunus katika imani baada ya kuondolewa adhabu kwa ushahidi wa kauli Yake (s.w.t.): “Na tukawastarehesha kwa muda.” (Yunus:98). Na anasema (s.w.t.): “Na tulimpeleka kwa laki moja au zaidi.* Basi waliamini na tukawastarehesha kwa muda.” (Swafatu:147-148). Na ilivyo dhahiri katika Aya hii ni kuwa Yunus baada ya kuokoka kwake kutokana na balaa lililomfika, alitumwa kwa watu wake wale wale wakampokea kwa shangwe na walistarehe chini ya kivuli cha imani mpaka muda uliowekwa katika elimu ya Mwenyezi Mungu. Ama mafirauni sera yao na dini yao ni kuamini wakati wa kushuka adhabu na kurejea kwenye ufisadi waliokuwa nao mwanzo baada ya kuondolewa adhabu, sawa uwe ufisadi wa kiitikadi au ufisadi wa matendo. Na Qur’an Tukufu yaeleza wazi hilo katika Aya zifuatazo:
139
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:31 PM
Page 140
Sehemu ya pili
“Wakasema: Dalili yoyote utakayotuletea ili uturoge kwayo hatutakuamini.* Ndipo tukalwapelekea tufani, nzige, chawa, vyura na damu kuwa dalili mbalimbali lakini wakatakabari na walikuwa watu wabaya.* Na ilipowaangukia adhabu, wakasema: Ewe Musa! tuombee kwa Mola wako yale aliyokuahidi, endapo utatuondolea adhabu bila shaka tutakuamini na kwa hakika tutawapeleka wana wa Israeli pamoja nawe.* Lakini tulipowaondolea adhabu mpaka muda fulani wao waufikie, mara wakavunja ahadi.” (Al-aarafu:132-134). Kuthibiti kwa watu wa Yunus kwenye imani na kutorejea kwenye ukafiri baada ya kuondolewa adhabu, na kule kukiuka kwa mafirauni baada ya kuodolewa adhabu, ni dalili tosha kuwa imani ya watu wa Yunus ilikuwa imani ya hiari iliyo imara na iliyotokana na yakini, na imani ya mafirauni ilikuwa ya kulazimika iliyotokana na hofu. Na kwa ibara nyingine imani ya watu wa Yunus ilitokana na toba na kujuta na kuona kuwa wametenda kosa na dhambi kwa hiyo tendo lao lilikuwa mfano wa tendo la mwenye kutubia ambaye amejing’oa kutoka hali yake ya mwanzo na akaitakasa niya yake kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kwa minajili hiyo walithibiti. Hali ikiwa imani ya mafirauni ilikuwa kwa ajili ya kujikinga na adhabu na kujiepusha na maafa waliyoyaingia, bila ya imani hii kuwa na athari nyoyoni mwao, kwa ajili hiyo walirejea kwenye ukafiri. Imani ya kwanza inatobowa paziya la ujinga na mwanadamu anashuhudia uja wake kwa jicho la kiroho na utukufu wa Mola na nuru ya imani, kwa hiyo anakuwa mnyenyekevu mbele ya Mwenyezi Mungu, anamuabudu Yeye wala haabudu miungu wengine mbali na Yeye. Na ya pili yazunguka mzunguko wa kuwepo kichocheo cha kulazimika na kubidika, kwa hiyo yeye huamini kinapokuwepo kichocheo hicho na hukufuru kinapotoweka, kwa hiyo imani yake ni kwa kadiri ya dharura yake ili kuondoa adhabu. Hivyo imani hii haihesabiki kuwa ni ukamilifu wa kiro140
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:31 PM
Page 141
Sehemu ya pili
ho na haina thamani katika soko la maarifa. anasema (s.wt):
“Na kama angelitaka Mola wako bila shaka wangeliamini wote waliomo katika ardhi. Basi je, wewe utawalazimisha watu hawa wawe Waumini?” (Yunus: 99). Hapana shaka Mwenyezi Mungu (s.w.t.) utashi wake wa kisheria umeambatana na imani ya watu wote kwa ushahidi wa kutumwa manabii na kuwapeleka Mitume. Lakini utashi wake wa kimaumbile haukuambatana na imani yao, kama si hivyo basi lau ungefungamana utashi wake na imani yao haungekosana na makusudio yake na watu wote wangekuwa waumini, imani ya kulazimishwa si kwa hiari, lakini kwa kuwa imani iko nje ya wigo wa hiari na imetokana na kulazimishwa na kudharurika ndio maana utashi wake (s.w.t.) haukuambatana na imani yao. Mwenyezi Mungu anagusia hilo katika kauli yake (s.w.t.): “Na kama angelitaka Mola wako bila shaka wangeliamini wote waliomo katika ardhi.” II. Je kuwaondolea adhabu ilikuwa ni kulikadhibisha kamio la Yunus (a.s.) ! Kwa kweli ameahidi (s.w.t.) ndani ya kitabu chake kitukufu kuwa atawaunga mkono Mitume wake na atawanusuru na wala hatowakadhibisha, na Yeye ndiye msemaji aliye na enzi katika wasemaji: “Hakika sisi tutawanusuru mitume wetu na wale walioamini katika uhai wa dunia na siku watakayosimama mashahidi” (Ghafir:51). Hivyo basi akimpa habari Nabii miongoni mwao kuwa tukio fulani litatokea au kuwa rehema itateremka au adhabu juu ya watu fulani, hapana budi yatokee madhumuni ya habari alizozitoa wakati fulani ujao, kwa sura ambayo hailazimu yeye (s.w.t.) kuwa amemkadhibisha Mtume wake, na hilo huwa 141
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:31 PM
Page 142
Sehemu ya pili
katika aina mbili: Ima kwa kutokea lilelile lililoandaliwa kama hali ilivyokuwa kuhusu habari ya Nabii Swaleh (a.s.) kwa watu wake aliposema: “Stareheni katika mji wenu kwa siku tatu, hiyo ni ahadi isiyokadhibishwa.” ulipofika muda uliopanga “Na wale waliodhulumu aliwaangamiza ukalele, na wakawa ndani ya majumba yao wameanguka kifudifudi.* Kama kwamba hawakuwamo. Sikilizeni! Hakika Thamud walimkufuru Mola wao, sikilizeni! Thamud wamepotelea mbali.” ( Huud:67-68). Na pili: Ima kwa kujitokeza alama na ishara zijulishazo ukweli wa kauli ya Nabii na habari alizozitoa, japo isithibiti adhabu yenyewe, kwa sababu ya kubadilika kwa majaaliwa kwa ajili ya dua na matendo mema, amesema (s.w.t.): “Na kama watu wa miji wangeamini na kumcha lazima tungeliwafungulia baraka za mbingu na ardhi” (Aarafu:96), Na amesema:
“Hayo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu habadilishi kabisa neema aliyowaneemesha watu mpaka wabadilishe waliyomi ndani ya nafsi zao, na kwamba Mwenyezi Mungu ni Msikivu, Mjuzi mno.” (Anfalu:53). Hii ni desturi ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) katika uteremshaji wa neema na adhabu na uondoaji wake. Na ile ambayo Yunus aliitolea habari ilikuwa katika aina hii, alitoa habari ya kuteremka kwa adhabu, na watu waliona alama zake na dalili zake…84 walianza kutubu na kurejea kwa Mwenyezi Mungu kama alivyowaelekeza yule mwanachuoni na Mwenyezi Mungu 84. Angalia tafsiri ya Tabariy, Juz 11, Uk 117-118. Na Durul-Manthur, Juz 3, Uk 317-318. Na Al-Bihaaru, Juz 14, Uk 396.Chapa mpya. 142
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:31 PM
Page 143
Sehemu ya pili
akawaondolea adhabu. Katika hilo hakuna kitendo cha Yunus (a.s.) kufanywa muongo. Lau kusingekuwa na usadikisho basi wasingeugusa ukweli wa usemi wake kwa kuziona alama za adhabu, ila tu Mwenyezi Mungu (s.w.t) ana desturi katika maisha, kwa hiyo kumlipiza mkiukaji kwa kukiuka kwake ni desturi, na kumsamehe mwenye kutubu kwa toba yake pia ni desturi na kila mojawapo lina maudhui yake mahsusi. Na hii ndiyo maana ya al-Badau isemwayo na Imamia, hii ni al-Badau ambayo lau ndugu zetu Ahlu Sunnah wangetambuwa ukweli wake basi wangeikubali ndani ya nyoyo zao halisi, lakini propaganda batili zimezuwia kati yao na kati ya kutambuwa waliojijengea Imamiya katika lengo hili, na tayari tulikwishafafanuwa hali ya mambo ndani ya risala ya al-Badau katika Kitabu na Sunnah, na apendae kufahamu hali halisi ya mambo arejea humo.85 III. Maswali matatu kuhusu Ismah ya Yunus (a.s.). a)-Nini maana ya kuwa kwake ameghadhibika, na nani aliyeghadhibikiwa? b)- Inakusudiwa nini kwa kauli yake: “Na akadhani kuwa hatutamdhiki” c)-Vipi Ismah itaafikiana na kutambuwa kwake kuwa yu miongoni mwa madhalimu ? Haya ndiyo maswali nyeti katika kisa cha Yunus (a.s.), mkosoaji ameshikamana nayo, na ufafanuzi wake wakujia mmoja baada ya mwingine. Ama la kwanza: Mkosowaji amedhania kuwa maana yake ametoka amemghadhibikia Mola wake kwa kutowateremshia adhabu watu wake, lakini hii ni kutafsiri Qur’an kwa rai, bali ni kuwazulia manabii na kuwadhania vibaya, na wala hamghadhibikii Mola wake ila aliye adui yake na ambaye ni mjinga wa hukumu zake katika matendo yake, na hali kama 85. Al-Bada’u 143
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:31 PM
Page 144
Sehemu ya pili
hiyo hailingani na mtu muumini sembuse Nabii. Ghadhabu yake ilikuwa kwa ajili ya watu wake kwa kuendelea kwao kumkadhibisha na kung’ang’ania ukafiri wao, na yakuwa yeye alikatishwa tamaa na toba yao ndipo akatoka kando nao.86 Ni kama hivi alifasiri Imamu Ridhwa (a.s.) Maamun alipomuuliza kuhusu maana ya Aya akajibu: “Huyo ni Yunus bin Matayo alikwenda akiwa amewangadhibikia watu wake”.87 Raziy amesema katika kuujibu utata huu: “Jibu la swali la kwanza: Ni kuwa Aya imejulisha kuwa yeye aliondoka hali ameghadhibika wala haikujulisha kuwa alimghadhibikia Mwenyezi Mungu, au vipi! Na kumghadhibikia Mwenyezi Mungu haiwi jaizi kwa mmoja yeyote katika Waislamu basi itakuwaje kwa Nabii (a.s.)! Huenda yeye alitoka akiwa amewaghadhibikia watu wake basi kwa nini mmesema kuwa hayo ni maasi?”88 Na amesema ndani ya sharehe ya al-Mamawaqif: “Huenda ghadhabu yake ilikuwa juu ya watu waliokufuru waliokithirisha ukaidi na mukabara mpaka akaishiwa uvumilivu na hakuweza kuwavumilia, basi hii ni ghadhabu ya Mwenyezi Mungu juu ya maadui zake nayo haiwi dhambi.”89 Raziy amesema ndani ya tafsiri yake akijibu utata huu na alirefusha maneno kuwa: “Ndani ya Aya hakujatajwa aliyeghadhibikiwa lakini sisi tunakata shauri kuwa haifai Nabii awe amemghadhibikia Mola wake kwa kuwa hiyo ni sifa ya asiyejua kuwa Mwenyezi Mungu ni mmiliki wa amri na katazo, na asiyemjua Mwenyezi Mungu si muumini sembuse kuwa Nabii!. Na inapothibiti kuwa sio jaizi kuielekeza ghadhabu hii kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) lazima makusudio ya kuwa yeye alitoka hali akiwa ameghadhibika itakuwa ni amemghadhibikia mwiginme na sio Mwenyezi Mungu. Na aghlabu itakuwa yeye alimghadhibikia anayemuasi yeye (Yunusu) asemalo au kuamrisha, kwa hiyo yumkini aliwaghadhibikia watu 86 Tanzihul-Anbiyai, Uk 102. 87. Biharul-An’war, Juz 14, Uk 387. 88. Ismatul-Anbiyai cha Al-Fakhru Raziy, Uk 80, chapa ya Jidah. 89. Sharhul-Mawaqif, Juz 8, Uk 276. 144
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:31 PM
Page 145
Sehemu ya pili
wake au mfalme au wote wawili. Na maana ya kuwaghadhibisha watu wake ni kuwa yeye aliwakasirisha kwa kujitenga nao kwa hofu yao ya kukabiliwa na adhabu wakati ule yeye hayupo. Ama usemi wa kuwa kuwaghadhibikia watu kulikuwa kumehadharishwa kwa usemi wake Mwenyezi Mungu (s.w.t.): “Wala usiwe kama mtu wa samaki” Twasema: Hatukubali kuwa ulikuwa umehadharishwa kwa kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) alimuamuru kuifikisha risala ile kwao na wala hakumuamrisha abaki nao na asitoke abadan…”90 Ama la pili: Namaanisha “Na akadhani kuwa hatutamdhiki” kwani kitenzi nacho ni: Naqdira chatokana na al-qadru kwa maana ya kumdhiki, sio kutokana na Al-qudrah yenye maana ya uwezo. Amesema “Na kwa ambaye riziki yake imekuwa dhiki na atowe ambacho Mwenyezi Mungu amempa” (Talaaqu:7). Na amesema (s.w.t.): “Kwa kweli Mwenyezi Mungu huikunjua riziki ya amtakaye na huidhiki” (Israu:30). Kwa hiyo maana ya Aya ni kuwa alidhania kuwa mambo hayatomuia dhiki kwa kutovuta subira na kuwavumilia watu wake, si kwa maana ya kuwa yeye aliwaza dhana hii akilini mwake, bali kwenda kwake na kuwaacha watu wake ni sawa na hali ya aliyedhani kuwa hatutamdhiki akiwa ametoka na kuwaacha watu wake bila ya kungoja amri ya Mwenyezi Mungu, ikawa kujitenga na watu wake kunawakilisha hali ya anayemdhania Mola wake hivyo. Ama tafsiri ya kuwa alidhania kuwa (s.w.t.) hawezi kumdhiki, hiyo ni tafsiri isiyo sahihi kuinasibisha na watu wasiojua katika watu wa kawaida sembuse mawalii na manabii. Amesema katika sherehe ya al-Mawaqif: “Alidhania hatutamdhiki kwa kuwa neno latokana na al-Qadru, ni mfano wa kauli Yake: “Anaikunjua riziki kwa amtakaye na huidhiki” na sio kutokana na al-Qudrah, yaani uwezo.”91
90. Tafsir Ar-Raziy, Juz 6, Uk 149. 91. Sharhul-Mawaqif, Juz 8, Uk 271. 145
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:31 PM
Page 146
Sehemu ya pili
Na kwa kuwa kujitenga na watu wake bila ya idhini kutoka kwa Mwenyezi Mungu kulikuwa kwawakilisha hali ya anaye dhania Mola wake hatomdhiki92, ndipo Mwenyezi Mungu alimpa mtihani wa chewa akammeza. Alipotambua kuwa ameacha lililo bora kutenda, akajutia tendo lake, na akanadi akiwa gizani kuwa hapana Mola wa haki apasaye kuabudiwa ila Wewe. Raziy amesema ndani ya tafsiri yake katika kuondoa utata wa “Na akadhani kuwa hatutamdhiki” kuwa: “Yalazimu taawili kwa nadharia kadhaa: Moja wapo: Yaani hatutomdhiki, nayo ni sawa na kauli Yake (s.w.t.): “Kwa kweli Mwenyezi Mungu huikunjua riziki ya amtakaye na huidhiki”. Ya pili: Hii iwe katika upande wa kupigia mfano kwa maana hali yake ilikuwa yafanana na hali ya anayedhania kuwa hatomdhiki kwa kutoka kwake na kujitenga kwake na watu wake bila ya kungojea amri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Ya tatu: Ni uwezo uleule wa pitisho la Mola, kwa hiyo maana inakuwa: Akadhania hatutomhukumia shida, nayo ndiyo kauli ya Mujahidu, Qutadah, Dwahaqu, Kalbiy na riwaya ya Aufiy ameieleza kutoka kwa Ibnu Abbas na amechaguwa Alfarrau na Az-zujaju…”93 Zamakhshariy amenakili ndani ya tafsiri yake Al-Kashaafu: “Kutoka kwa Ibnu Abbas kuwa yeye aliingia kwa Muawiyah akasema Muawiya: Nimepigwa na mawimbi ya Qur’an jana nikazama humo sikumpata wa kuniokoa isipokuwa wewe. Akasema ni mawimbi gani ewe Muawiyah? Akaisoma Aya hii na akasema: Je adhania Nabii wa Mwenyezi Mungu kuwa hatomuweza? Akasema: Hii ni katika kudhiki sio katika kuweza.” Kisha mwandishi wa Al-Kashafu akaongeza : “Inasihi tafsiri ya uwezo kwa 92. Raziy amesema kama haya ndani ya Ismatul-Anbiyai, Uk 80, chapa ya Jida. 93. Tafsir Fakhru Raziy, Juz 6, Uk 150. 146
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:31 PM
Page 147
Sehemu ya pili
maana ya hatutomfanyia uwezo wetu. Na iwe katika mlango wa kupigia mfano kwa maana ya hali yake ilikuwa inafanana na hali ya anayedhania kuwa hatutomdhiki katika kuwaacha watu wake bila ya kungoja amri ya Mwenyezi Mungu. Na yajuzu hilo limtanguliye katika mawazo yake kwa wasiwasi wa Shetani kisha aikinze na kumjibu kwa dalili kama afanyavyo muumini wa kweli kwa misukumo ya Shetani na wasiwasi autiao kila wakati.94 Haikujificha kuwa alilonakili Ibnu abbas ndilo la kutegemewa, kwa ushahidi wa kutumika kwake ndani ya Qur’an kwa maana ya dhiki. Nayo yalingana na limaanishwalo na Aya. Ama sura mbili zingine hazifai kutegemewa hususan sura ya mwisho, kwa sababu manabii daraja zao ni za juu zaidi kuliko mioyo yao kuzungukwa na minong’ono ya Shetani mpaka ufumbuzi wake uje kwa burhani, kwani yeye shetani hana mamlaka juu ya watakaswa miongoni mwa waja wa Mwenyezi Mungu, na shetani amekiri hilo yeye mwenyewe aliposema: “Isipokuwa waja wako waliotakaswa miogoni mwao” (Swad:83). III. Ama swali la tatu Ime tanguliya kuwa neno Dhulma katika lugha ya kiarabu maana yake ni: Kukiweka kitu mahali pasipo pake, hivyo bila shaka kujitenga mbali na watu wake na kuwatelekeza katika wakati mgumu na hali ya mfadhaiko lilikuwa jambo lisilotarajiwa kutokea kwake japokuwa haikuwa kuasi amri ya Mola wake, kwani huruma na upendo vitazamiwavyo kutoka kwa manabii ni tofauti ukilinganisha na vitazamiwavyo kutoka kwa watu wengine, kwa hiyo inachukuliwa kuwa kitendo chake kilitokea mahali pasipo pake. Na yawezekana kitendo kilichotokea kwake mahali pasipo pake ni kule kuwaombea adhabu watu wake na kuacha kuvuta subira, na hilo laungwa mkono na kauli yake (s.w.t.):
94. Al-Kashaf, Juz 2, Uk 335 - 336. 147
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
12:31 PM
Umaasumu wa Mitume
Page 148
Sehemu ya pili
“Basi subiri hukumu ya Mola wako, wala usiwe kama mmezwa na samaki, alipomwita na hali yeye alikuwa mwenye huzuni nyingi.” (Qalamu:48). Ni dhahiri kuwa liammbatanalo na wito katika Aya ni kutaka adhabu iteremke kwa watu wake kwa muktadha wa kauli yake: “Hali yeye alikuwa mwenye huzuni nyingi.” yaani alikuwa amejawa na ghadhabu au huzuni na maana inakuwa: Ewe Nabii usiwe mfano wa mwenzi wa samaki (yaani Yunus) lisitokee kwako mfano wa lililotokea kwake akapasukwa na ghadhabu kwa hiyo akapatwa na balaa lake. Vuta subira kwa ajili ya uamuzi wa Mola wako kwani yeye huwangojea, wala usiwafanyie haraka adhabu kwa kukufuru kwao. Amesema ndani ya Sharhul-Mawaqif: “Hakika mimi nilikuwa miongoni mwa madhalimu” nimeidhulumu nafsi yangu kwa kuacha lililo bora. Yaani kwa hiyo kukiri kwake kufanya dhulma ni kuiponda nafsi yake na kulikuza lililotokana nayo, na hali hiyo ni kwenda mbali sana katika unyenyekevu. “Wala usiwe kama mwenzi wa samaki yaani katika uchache wa subira” juu ya shida na maafa ili kupata daraja zilizo bora, wala maana yake sio usiwe mfano wake katika kutenda dhambi…95 Na yamaanishwa na baadhi ya riwaya kuwa sababu ya kulaumiwa kwake na kukatazwa kwake kulikuwa ni jambo lingine la tatu nalo ni alipobaini kuwa watu wake wameokoka alighadhibika na kulitoka eneo.96 Mitizamo miwili wa kwanza na wa pili ndiyo iliyo sahihi.
95. Sharhul-Mawaqif, Juz 8, Uk 286. 96. Biharul-An’war, Juz 14, Uk 381, chapa mpya. 148
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:31 PM
Page 149
Sehemu ya pili
Na kutokana na tulilotaja yajulikana maana ya kauli yake (s.w.t.): “Alipokimbia katika jahazi iliyosheheni.�. Kwa hiyo aliishabihisha hali yake na ya mja aliyekimbia, na hilo laja kutokana na yaliyo angulia kuwa kutoka kwake katika hali kama hii kulikuwa kwawakilisha hali ya mja aliyekimbia kumhudumia bwana wake, kwa ajili hiyo Mola wake hapo basi alimchukua kwa balaa kwa ajili ya hilo. Maneno yamebaki kuhusu ismah ya mtukufu Nabii Muhammad (s.a.w.) tutatoa usemi wa hilo katika utafiti ufuatao.
149
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume
12:31 PM
Page 150
Sehemu ya pili
ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION: 1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9. 10. 11. 12. 13. 14. 15. 16. 17. 18. 19. 20. 21. 22. 23. 24. 25. 26. 27. 28. 29.
Qur'an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka kumi na Tisa Uharamisho wa Riba Uharamisho wa uwongo Juzuu ya kwanza Uharamisho wa uwongo Juzuu ya pili Hekaya za Bahlul Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.) Hijab vazi Bora Ukweli wa Shia Ithnaashari Madhambi Makuu Mbingu imenikirimu Abdallah Ibn Saba Khadijatul Kubra Utumwa Umakini katika Swala Misingi ya Maarifa Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia Bilal wa Afrika Abudharr Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu Salman Farsi Ammar Yasir Qur'an na Hadithi Elimu ya Nafsi Yajue Madhehebu ya Shia Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur'an Tukufu Al-Wahda Ponyo kutoka katika Qur'an Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii 150
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
Umaasumu wa Mitume 30. 31. 32. 33. 34. 35. 36. 37. 38. 39 40. 41. 42. 43. 44. 45. 46. 47. 48. 49. 50. 51. 52. 53. 54. 55. 56. 57. 58. 59. 60. 61. 62. 63
12:31 PM
Page 151
Sehemu ya pili
Mashukio ya Akhera Al Amali Dua Indal Ahlul Bayt Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna Haki za wanawake katika Uislamu Mwenyeezi Mungu na sifa zake Amateka Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) Adhana. Upendo katika Ukristo na Uislamu Nyuma yaho naje kuyoboka Amavu n’amavuko by’ubushiya Kupaka juu ya khofu Kukusanya swala mbili Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Kusujudu juu ya udongo Maulidi Tarawehe Malumbano baina ya Sunni na Shia Kupunguza swala safarini Kufungua safarini Kuzuru makaburi Umaasumu wa Manabii Qur’an inatoa changamoto Tujifunze misingi ya dini Nahjul Balagha Sehemu ya Kwanza Nahjul Balagha Sehemu ya Pili Dua Kumayl Uadilifu wa masahaba Asalaatu Khayrunminaumi Sauti ya uadilifu wa binadamu Umaasumu wa Mitume Sehemu ya kwanza Maswali na Mishkili Elfu Sehemu ya kwanza 151
Umaasumu wa mitume Lubumba final.qxd
7/16/2011
12:31 PM
Umaasumu wa Mitume
Page 152
Sehemu ya pili
BACK COVER Suala la ismah ya Manabii ni nukta ambayo imezua mjadala mkubwa miongoni mwa wanachuoni na miongoni mwa madhehebu. Upande mmoja unasema Manabii ni binadamu ambao wamehifadhiwa kutokana na dhambi na makosa ya aina yoyote. Upande mwingine unasema hapana, Manabii wanaweza kukosea na kufanya dhambi. Upi ni ukweli; mwandishi ya kitabu hiki ambaye ni mwanachuoni mkubwa wa Kiislamu analifafanua suala hili kwa urefu kwa kutumia dalili za kielimu, Qur’an na Sunna na kuhitimisha pasina shaka yoyote juu ya Umaasum wa Mitme. Kimetolewa na kuchapishwa na:
Al-Itrah Foundation P. O. Box 19701, Dar-es-Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Fax: +255 22 2127555 Email: alitrah@raha.com Website: www.alitrah.org Online: www.alitrah.info
152