Upotoshaji dhahiri katika turathi ya kiislamu

Page 1

‫يم‬ ْ ِ‫ب‬ ِ ‫س ِم اللﱠـ ِه ال ﱠر ْح َم ٰـ ِن ال ﱠر ِح‬

Upotoshaji Dhahiri katika Upotoshaji Dhahiri Turathi (Hazina)ya katika Kiislamu

Turathi (Hazina)ya Kiislamu Mtungaji: Fakihi MhakikiMtungaji: Sheikh Ja’far Subhani Fakihi Mhakiki Sheikh Ja’far Subhani

Mtarjumi: Mtarjumi: Abdul Karim Juma Nkusui

Abdul Karim Juma Nkusui

Mhariri: Al Haj Hemedi Lubumba (Abu Batul)

Mhariri: Al Haj Hemedi Lubumba (Abu Batul)

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 1

7/5/2013 7:11:06 PM


‫ﺗﺮﺟﻤﺔ‬ ‫ﺗﺮﺟﻤﺔ‬ ‫ﺗﺮﺟﻤﺔ‬

‫ﻇﺎهﺮة اﻟﺘﺤﺮﻳﻒ‬ ‫اﻟﺘﺤﺮﻳﻒ‬ ‫ﻇﺎهﺮة‬ ‫ﻓﻲ‬ ‫ﻓﻲ‬ ‫اﻟﺘﺮاث اﻹﺳﻼﻡﻲ‬ ‫اﻟﺘﺮاث اﻹﺳﻼﻡﻲ‬ ‫ﻟﻴﻒ‬ ‫ﺗﺄﺗﺄ ﻟﻴﻒ‬ ‫ّﻖ‬ ‫اﻟﻔﻘﻴﻪ‬ ‫اﻟﻤﺤﻘﻘّﻖ‬ ‫اﻟﻔﻘﻴﻪ اﻟﻤﺤ‬ ‫ﺟﺟ ﺗﺄ‬ ‫ﺒﺤﺎﻧﻲ‬ ‫اﻟﺴ‬ ‫ﻟﻴﻒﺒﺤﺎﻧﻲ‬ ‫ﻌﻔﺮ اﻟﺴ‬ ‫ﻌﻔﺮ‬

‫اﻟﻔﻘﻴﻪ اﻟﻤﺤﻘّﻖ‬ ‫ﺟﻌﻔﺮ اﻟﺴﺒﺤﺎﻧﻲ‬ ‫اﻟﻠﻐﺔ‬ ‫اﻟﻰ اﻟﻠﻐﺔ‬ ‫اﻟﻌﺮﺏﻴﺔ اﻟﻰ‬ ‫اﻟﻠﻐﺔ اﻟﻌﺮﺏﻴﺔ‬ ‫ﺡﻠﻴﺔﻡﻦ اﻟﻠﻐﺔ‬ ‫اﻟﺴﻮا ﺡﻠﻴﺔﻡﻦ‬ ‫اﻟﺴﻮا‬

‫ﻣﻦ اﻟﻠﻐﺔ اﻟﻌﺮﺑﻴﺔ إﻟﻰ اﻟﻠﻐﺔ اﻟﺴﻮاﺣﻠﻴﺔ‬ ‫ﺡﻠﻴﺔﻡﻦ اﻟﻠﻐﺔ اﻟﻌﺮﺏﻴﺔ اﻟﻰ اﻟﻠﻐﺔ‬ ‫اﻟﺴﻮا ‪ ‬‬ ‫‪22‬‬

‫‪7/5/2013 7:11:07 PM‬‬

‫‪08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 2‬‬


©Haki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION

ISBN: 978 - 9987 - 17 - 036 - 4

Mtungaji: Fakihi Mhakiki Sheikh Ja’far Subhani

Mtarjumi: Abdul Karim Juma Nkusui Barua pepe: abdulkarimjuma@yahoo.com

Mhariri: Al Haj Hemedi Lubumba (Abu Batul)

Kimepangwa katika Kompyuta na: Al-Itrah Foundation

Toleo la kwanza: Oktoba 2013 Nakala: 2000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. - 19701, Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 / 2127555 Barua Pepe: alitrah@yahoo.com Tovuti: www.ibn-tv-com Katika mtandao: w.w.w.alitrah.info

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 3

7/5/2013 7:11:07 PM


08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 4

7/5/2013 7:11:07 PM


FAHARASI Neno la Mchapishaji.............................................................................. 01 Utangulizi.............................................................................................. 03 Turathi (Hazina) ya Kiislam ni amana ya Mwenyezi Mungu............... 07 1. Hadithi ya Siku ya Karamu ya Jamaa wa Karibu....................... 13 2. Al-Futuhatul-Makiyyah na kuondolewa kwa majina ya Maimamu Wa Ahlul-Bait (a.s.)................................... 18 3. Taarikh Ya’aqubiy na kupotoshwa kwa Hadithi ya Ghadir......... 24 4. Al-Adhkar an-Nawawiyyah na kupatwa na upotoshaji............... 26 5. Bukhari na Hadithi: “Na yeye ni kiongozi wenu baada yangu.”.................................................................... 31 6. Bukhari na Hadithi ya: “Litakuuwa kundi ovu.”......................... 36 7. Sahih Muslim na Hadith ya: “Wanawake bora ulimwenguni ni wanne.”............................................................. 39 8. Sahih Muslim na Hadith: “Mahdi, na yeye ni katika kizazi cha Fatimah”..................................................................... 39 9. Maarif Ibn Qutaybah na habari ya Fatimah kumporomosha Muhsin.............................................................. 40 10. Sawaiqul-Muhriqah na Hadith ya: “Kumtaja Ali ni Ibada.”........ 41 v

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 5

7/5/2013 7:11:07 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

11. Sawaiqul-Muhriqah na Hadith ya: “Ali alikuwa na Fadhila kumi na Nane.�............................................................... 42 12. Upotoshaji katika diwani za washairi.......................................... 44 i. Upotoshaji katika diwani ya al-Kumait:................................... 44 ii. Upotoshaji katika diwani ya Hasan:......................................... 44 iii. Upotoshaji katika Diwani ya Abi Tamam:................................ 45 iv. Upotoshaji katika Ruhul-Maaniy cha al-Alusiy:........................ 46 13. Kupotosha Sunnah ili kuwa mbali na mashia................................. 48 i. Kusawazisha kaburi ni Sunna inayoachwa kwa sababu ni alama ya Mashia: ............................................. 48 ii. Kusoma Bismillahi kwa jahara:................................................ 50 iii. Kumswalia muumini peke yake ni Sunna inayo kataliwa:.............................................................. 50 iv. Kuacha Sunna inapokuwa alama ya Mashia:........................... 52 v. Kuacha kufanya mema na kufanya maatam siku ya Ashura:........................................................................ 52 14. Udanganyifu na ongezeko lake kubwa katika hazina..................... 54

vi

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 6

7/5/2013 7:11:07 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

Neno la Mchapishaji

U

potoshaji Dhahiri katika Turathi (Hazina) ya Kiislamu ni kitabu kinachoelezea upotoshaji unaofanywa na baadhi ya watu kwa kutoa tuhuma mbalimbali juu ya Ushia bila ya kufanya utafiti wala kuangalia Mashia wanasema nini juu ya hayo wanayotuhumiwa nayo. Watu hawa wamekuwa wakiogolea katika dhana kwa karne nyingi, licha ya kutolewa majibu na maelezo mengi ya kina yaliyojaa hoja za msingi na za kielimu juu ya yale wanayotuhumiwa Mashia. Lakini bahati mbaya sana watu hawa hawajishughulishi kuangalia majibu hayo na badala yake wanarudiarudia kutoa tuhuma hizo kila mara wanapojisikia kufanya hivyo. Huu kwa kweli ni msiba mkubwa, kwani huonekana tofauti hizi kutumiwa na maadui wa Uislamu kuwachonganisha Waislamu. Na ndugu zetu hawa hawatanabahi kwani kwao hii ndio natija. Kitabu hiki kinatoa kwa mara nyingine maelezo na ufafanuzi wa baadhi ya masuala mbalimbali ambayo ni upotoshaji mkubwa unaofanywa katika hazina na mirathi ya Kiislamu. Sisi kama wachapishaji tunakiwasilisha kitabu hiki kama kilivyo kwa wasomaji wetu na kuwashauri wasome yaliyomo humo, wayafanyie kazi na kuyazingatia ili waepukane na upotoshaji huu unaofanywa kwa makusudi ili kukidhi malengo ya wapotoshaji. Hii ni moja kati ya kazi kubwa zilizofanywa na Taasisi ya Al-Itrah katika kuwahudumia kielimu wasomaji wake wazungumzaji wa Kiswahili. Na kwa maana hiyohiyo imeamua ku1

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 1

7/5/2013 7:11:07 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

kichapisha kitabu hiki chenye manufaa makubwa kwa lugha ya Kiswahili kwa lengo lake lilelile la kuwahudumia Waislamu, hususan wanaozungumza Kiswahili. Hivyo, ni matumaini yetu kwamba wasomaji wetu watanufaika vya kutosha kutokana na kitabu hiki, kwani tumekiona ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni vitu ambavyo havina nafasi tena katika akili za watu. Tunamshukuru mwandishi wa kitabu hiki fakihi ­mhakiki Sheikh Ja’far Subhani kwa kazi kubwa aliyoifanya kwa ­ajili ya Umma huu wa Waislamu, Allah ‘Azza wa Jallah ­amlipe kila kheri na amuingize Peponi kwa salama na amani insha’Allah. Halikadhalika tunamshukuru Ndugu yetu Abdul Karim Juma Nkusui kwa kukitarjumi kwa Kiswahili kitabu hiki, insha’Allah na yeye Allah ‘Azza wa Jallah amlipe kila kheri hapa duniani na Akhera pia, bila kuwasahau na wale wote waliochangia kwa namna moja au nyingine mpaka kufanikisha kuchapishwa kwake; Allah awalipe wote malipo mema hapa duniani na huko Akhera pia. Mchapishaji Al-Itrah Foundation.

2

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 2

7/5/2013 7:11:08 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

Utangulizi Utangulizi

‫يم‬ ْ ِ‫ب‬ ِ ‫س ِم اللﱠـ ِه ال ﱠر ْح َم ٰـ ِن ال ﱠر ِح‬ Kwa jina la Mwenyezi Mungu,Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu.

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa

Sifa zote njema ni za Mola mlezi wa Walimwengu, rehema na amani zimwendee mbora wa rehema Mwenye kurehemu. viumbe Vyake na hitimisho la Mitume Wake Muhammad (s.a.w.w.) na Ahali zake,ambao ni hazina ya elimu wenye ni kubebamikoba yake. wa Walimwengu, rehema ifayake zotenanjema za Mola mlezi

S

na amani zimwendee mbora wa viumbe Vyake na hitim-

Ama baad. Hakika hazina ya Kiislam ni utajiri wa kifikira usiolinganishwa na thamani la Mitume Wakebaada Muhammad na Ahali zake, Mungu yoyote, naisho umerithiwa na kizazi ya kizazi, (s.a.w.w.) nayo ni amana ya Mwenyezi ambayo niambao wajibu kuihifadhi na matukio yanayojitokeza na hilamikoba zakila zama.Vipi ni hazinakutokana ya elimu yake na wenye kubeba isiwe hivyo nayo ni rejea pekee ya itikadi na sharia katika kila zama na kizazi,laiti si hazina yake. hiyo isingesimama nguzo ya Uislamu na wala usingemea.

Ama baad. Hakika hazina ya Kiislam ni utajiri wa kifikira

Ni masikitiko makubwa sana kwamba kuna makundi yanayonyemelea hazina hii na kujaribu usiolinganishwa na thamani yoyote, na umerithiwa na kizazi kuichafua na hapa tutaashiria sababu mbili:

baada ya kizazi, nayo ni amana ya Mwenyezi Mungu ambayo 1: Kuna madalali wasiojali isipokuwa kununuana turathi za thamani za Kiislam kwa ni wajibu kuihifadhi kutokana matukio yanayojitokeza na thamani kubwa na hila kuzipeleka nchi za isiwe Magharibi za Kikristo kutaka kumiliki za kilakatika zama.Vipi hivyo nayo nikwa rejea pekee ya iti-utamaduni wetu na maendeleo yetu, na sababu hii ingali inafanya kazi katika wakati uliopita na uliopo. kadi na sharia katika aliyoyanukuu kila zama na kizazi, laitikatika si hazina hiyo Inatosha katika hayo yale maelezo Ibn Khalikaan maelezo yake juu ya nguzo ya Uislamu nabin wala usingemea. wasifu waisingesimama Tajud-Diyn Abul-Yaman Zaid bin Hasan Hasan bin Yazid bin Hasan bin Said al-Kindiy al-Baghdadiy ad-Dimishiqiy al-Masriy aliyefariki mwaka 613Hijiria.

Ni masikitiko makubwa sana kwamba kuna makundi hii naye: na kujaribu kuichafua na hapa Amesema yanayonyemelea katika maelezo yakehazina kuhusiana “Alizing’arisha zama zake katika fani za fasihi na kusifika, na umashuhuri wake unatosheleza kutorefusha wasifu wake. Aliondoka tutaashiria sababu mbili:

Baghdad katika ujana wake na akaishi Halab kwa muda, alikuwa ananunua manukato na kusafiri nayo hadi nchi ya Italia nawasiojali kurejea tena Halab, kisha alihamia turathi Damascus 1. Kuna madalali isipokuwa kununua zana akawa rafiki wa Amir Izzu Diyn Farukh Shah, naye ni mtoto wa ndugu yangu Swalahu thamani za Kiislam kwa thamani kubwa na kuzipeleka Diyn, akamfanya ni mahususi kwake na akaenda kwake na akasafiri kwa kusuhubiana naye hadi nchi za Magharibi za Kikristo kwa kumimiji ya Misri na katika akanunua miongoni mwa vitabu vya hazina zaokutaka kila chenye thamani na likinautamaduni na maendeleo na sababu hii kwake.”1 akarejea Damascus akaishi hapo,wetu watu wakamwendea na yetu, kuchukua elimukutoka 1

Wafayaatil- A’ayaani Juz.2, Uk.339 namba 249.

3

6 08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 3

7/5/2013 7:11:08 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

ingali inafanya kazi katika wakati uliopita na uliopo. Inatosha katika hayo yale maelezo aliyoyanukuu Ibn Khalikaan katika maelezo yake juu ya wasifu wa TajudDiyn Abul-Yaman Zaid bin Hasan bin Hasan bin Yazid bin Hasan bin Said al-Kindiy al-Baghdadiy ad-Dimishiqiy al-Masriy aliyefariki mwaka 613 Hijiria. Amesema katika maelezo yake kuhusiana naye: “Alizing’arisha zama zake katika fani za fasihi na kusifika, na umashuhuri wake unatosheleza kutorefusha wasifu wake. Aliondoka Baghdad katika ujana wake na akaishi Halab kwa muda, alikuwa ananunua manukato na kusafiri nayo hadi nchi ya Italia na kurejea tena Halab, kisha alihamia Damascus na akawa rafiki wa Amir Izzu Diyn Farukh Shah, naye ni mtoto wa ndugu yangu Swalahu Diyn, akamfanya ni mahususi kwake na akaenda kwake na akasafiri kwa kusuhubiana naye hadi miji ya Misri na akanunua miongoni mwa vitabu vya hazina zao kila chenye thamani na akarejea Damascus na akaishi hapo, watu wakamwendea na kuchukua elimu kutoka kwake.”1 Tajud-Diyn anawenzie wangapi waliomfano wake katika kupora utajiri wa fikra za Waislam hapo zamani na sasa? Na katika zama za leo mustashiriqiina wamekuwa wanashindana katika kupora hazina ya Kiislam hadi tumekuwa tunangojea ukarimu wa mikono yao baina ya muda na mwingine. Na hiki ni Chuo Kikuu cha “Barnastan” cha Marekani kimekusanya jumla ya miswada iliyoandikwa kwa hati za mikono za Kiarabu ambayo bado haijachapishwa, idadi 1

Wafayaatil- A’ayaani Juz.2, Uk.339 namba 249. 4

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 4

7/5/2013 7:11:08 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

yake inakadiriwa kuwa ni nakala 6000, ambapo Chuo hiki kimenunua kutoka kwa ustadh wa Kiyahudi wa Baghdad bidhaa moja kwa dola 72,000/= na Myahudi aliyetajwa amezunguka hadi nchi za Mashariki ya Kati hususan Misri na akakusanya toka katika nchi hizo maelfu haya ya vitabu ambavyo vilikuwa havijachapishwa na akavipeleka Marekani ambapo vipo katika maktaba ya Chuo Kikuu cha Barnastan.2 2. Kinachofanywa na taasisi za uchapishaji katika nchi mbalimbali za Kiarabu ni wakati wa kuhakiki vitabu na kuvichapisha, ambapo wanapotosha maneno kutoka katika mahala pake kwa kuondoa na kuongeza, wanaondoa wasiyoyapenda na wanaongeza yale wanayoelekezwa na matamaio yao. Wanayoyafanya ni uharibifu mkubwa mno unaoipata hazina. Na katika kitabu hiki kidogo tumetoa mfano wa aina za upotoshaji uliojitokeza katika vitabu vya Hadith, Historia na vinginevyo tangu zamani hadi leo hii, na ambayo tumeyatoa katika kitabu hiki si kingine isipokuwa ni sehemu ndogo tu ya yale aliyoyaona mtunzi katika kupitia kwake vitabu au ambayo ameyaona mwingine na akamweleza. Mwisho tunawaomba wachapishaji na wasambazaji wote, wahakiki, watunzi na wale wanaohusika na kuhifadhi turathi, kuhifadhi utajiri wa kifikra na amana ya Mwenyezi Mungu ambayo imo mikononi mwao ili ikifikie kizazi kinachokuja bila ya kupotoshwa wala kuharibiwa, anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

‫ت إِ َل ٰى أَھْ لِ َھا‬ ِ ‫ﷲ َيأْ ُم ُر ُك ْم أَنْ ُت َؤ ُّدوا ْاألَ َما َنا‬ َ َّ َّ‫إِن‬ 2

Jawlatu Fiy Durul-Kutubi al-Amrikiyatiuk. 46. 5

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 5

7/5/2013 7:11:08 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

“Hakika Mwenyezi Mungu anawaamuru kurudisha amana kwa wenyewe..” (Sura Nisaa 4:58).

Ja’far Subhani, Qum. Muasasatul- Imam as-Sadiq (as) 28Dhul- Qa’ad 1422 A.H.

6

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 6

7/5/2013 7:11:08 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

HAZINA YA KIISLAM NI AMANA YA MWENYEZI MUNGU

T

ahriyf (Upotoshaji): Katika lugha ya Kiarabu ni kugeuzana kubadilisha. Ibnu Mandhur amesema: “Tahriyf katika neno kwa kulitoa mahala pake, ni kulibadilisha.”3 Na katika istilahi: Kila nyongeza na badiliko unaloliweka katika maneno ya mwingine na katika athari yake, kwa namna ya kukhalifu makusudio yake, basi huo ni upotoshaji. Hakika hazina ya Kiislam ambayo tumeirithi kupitia vizazi baada ya vizazi, ni amana ya Mwenyezi Mungu juu yetu, inahaki kama zilivyo na haki hukumu zingine, na wala haipaswi kuzembea katika kuhifadhi hazina hii na kuijali, na nyongeza yoyote na mabadiliko yoyote yatakayofanywa humo kwa namna inayopelekea kupotosha makusudio inahesabiwa kuwa ni khiyana katika amana. Na Mwenyezi Mungu amesema:

‫ت إِ َل ٰى أَھْ لِ َھا‬ ِ ‫ﷲ َيأْ ُم ُر ُك ْم أَنْ ُت َؤ ُّدوا ْاألَ َما َنا‬ َ َّ َّ‫إِن‬ “Hakika Mwenyezi Mungu anawaamuru kurudisha amana kwa wenyewe..” (Sura Nisaa: 58).

ْ‫ع أَ َھ‬ ‫ُونلِ َھا‬ ‫ت َإِر َلا ٰى‬ ‫ﷲلَّذَيأْ َُم‬ ِ ‫األَع َمْھا ِ َدنا ِھ ْم‬ ‫ِين ُرھُك ْم ِأَألَنْ َما ُت َن َاؤت ُّد ِ​ِھ ْم‬ َ ْ ‫وا َو‬ َ ‫إِنَّ َو َّا‬

Na akasema:

‫ُون‬ َ ‫ِين ُھ ْم ِألَ َما َنات ِ​ِھ ْم َو َع ْھ ِد ِھ ْم َراع‬ َ ‫َوالَّذ‬ “Na wale ambao wanachunga amana zao na ahadi zao.” (Sura Muuminina: 8) 3

Lisanul- Arabi: 3 Madatu “Harif” 7

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 7

7/5/2013 7:11:08 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

Na akasema:

‫ﷲ َوالرَّ سُو َل َو َت ُخو ُنوا أَ َما َنا ِت ُك ْم‬ َ ‫َيا أَ ُّي َھا الَّذ‬ َ َّ ‫ِين آ َم ُنوا َال َت ُخو ُنوا‬ ‫ُون‬ َ ‫َوأَ ْن ُت ْم َتعْ َلم‬ “Enyi mlioamini! Msimfanyie khiyana Mwenyezi Mungu na Mtume na mkakhini amana zenu na hali mnajua..” (Sura Anfal: 27). َ ُ ْ ٰ

‫ون َھ َذا ِمنْ عِ ْن ِد‬ َ ُ‫ِيھ ْم ث َّم َيقُول‬ َ ‫ُون ال ِك َت‬ َ ‫ِين َي ْك ُتب‬ َ ‫َف َو ْي ٌل لِلَّذ‬ ِ ‫اب ِبأ ْيد‬

Na kati ya aina upotoshaji huo niule َ‫ت أ‬ َّ ulioً ‫ُوا ِب ِه َث َم ًنا َقل‬ َ ‫ َو ْي ٌل‬za ْ kubwa َ ‫ ِممَّا َك‬kabisa َ ۖ ‫ِيال‬ َ ‫ﷲ لِ َي ْش‬ ٌ ْ ْ ُ ‫ل‬ ‫ي‬ ‫و‬ ‫و‬ ‫م‬ ‫ِيھ‬ ‫د‬ ‫ي‬ ‫ب‬ ‫ت‬ ‫م‬ ‫ھ‬ ‫ل‬ ‫ف‬ ‫ر‬ ‫ت‬ َ َ َ ِ ْ ْ ِ fanyika katika vitabu vya Tafsiri, Hadith na Tarikh, ambavyo ‫ ْكسِ ب‬matawi ‫ َل ُھ ْم ِممَّا َي‬yake ndio tegemeo katika kufahamu misingi ya‫ُون‬ َ dini, na sira ya Mtukufu Nabii (s.a.w.w.). Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ameshatoa habari katika aya zaidi ya moja kwamba kazi ya kupotosha ni bidaa ya Kiyahudi, kundi hilo limerithishana kazi hiyo kizazi baadaya kizazi, wakapotosha maneno kutoka katika mahala pake kulingana na matamanio yao na kufuatana na masilahi yao.

َّ ‫ِين آ َم ُنوا َال َت ُخو ُنوا‬ ‫ﷲ َوالرَّ سُو َل َو َت ُخو ُنوا أَ َما َنا ِت ُك ْم‬ َ ‫َيا أَ ُّي َھا الَّذ‬

َ Katika zaidi ya Aya moja Mwenyezi Mungu amekosoa kazi ‫ُون‬ ‫َوأَ ْن‬ َ ‫ُت ْم َتعْ َلم‬muda hii ya jinai ambayo Mayahudi walikuwa wakiifanya baada ya muda. Mwenyezi Mungu amesema:

‫ون ٰ َھ َذا ِمنْ عِ ْن ِد‬ َ ُ‫ِيھ ْم ُث َّم َيقُول‬ َ ‫ُون ْال ِك َت‬ َ ‫ِين َي ْك ُتب‬ َ ‫َف َو ْي ٌل لِلَّذ‬ ِ ‫اب ِبأ َ ْيد‬ ً ‫ﷲ لِ َي ْش َترُوا ِب ِه َث َم ًنا َقل‬ ْ ‫ِيال ۖ َف َو ْي ٌل َل ُھ ْم ِممَّا َك َت َب‬ ‫ِيھ ْم َو َو ْي ٌل‬ ِ َّ ِ ‫ت أَ ْيد‬ ‫ُون‬ َ ‫َل ُھ ْم ِممَّا َي ْكسِ ب‬ “Basi ole wao wanaoandika Kitabu kwa mikono yao, kisha wakasema: Hiki kimetoka kwa Mwenyezi Mungu, ili wachukue kwacho thamani ndogo. Basi ole wao kwa 8

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 8

7/5/2013 7:11:08 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

yale iliyoyaandika mikono yao. Na ole wao kwa yale wanayoyachuma..”(Sura al-Baqarah 2:79).

Mayahudi walikuwa wanaandika vitabu vya mbinguni lakini kwa kubadilisha na kugeuza, wanaongeza ya kwao katika maneno ya Mwenyezi Mungu ili watu wakawaida wavinunue kwa thamani ndogo, licha ya kwamba wao huwa wameacha humo haki huwa wamedhihirisha batili ili wachukue mukabala wa hayo kitu kidogo. Mwenyezi Mungu amesema:

‫ون‬ َ ُ‫َف ِب َما َن ْقضِ ِھ ْم مِي َثا َق ُھ ْم َل َع َّنا ُھ ْم َو َج َع ْل َنا قُلُو َب ُھ ْم َقاسِ َي ًة ۖ ُي َحرِّ ف‬ ًّ ‫ْال َكلِ َم َعنْ َم َواضِ ِع ِه ۙ َو َنسُوا َح‬ ۚ ‫ظا ِممَّا ُذ ِّكرُوا ِب ِه‬ “Basi kwa sababu ya kuvunja kwao agano lao, tuliwalaani na tukazifanya nyoyo zao kuwa ngumu. Wanageuza maneno kutoka mahali mwake na wakaacha sehemu ya yale waliyokumbushwa.” (Sura Maidah: 13).

Aya zipo katika hali ya kumliwaza Nabii (s.a.w.w.), zinasema: Usishangae ewe Muhammad hawa Mayahudi ambao wamejaribu kunyoosha mikono yao kwako na kwa Masahaba wako na kutengua ahadi ambayo iko baina yako na baina yao na wanakufanyia khiyana, hakika hiyo ni tabia yao na kawaida ya watangulizi wao na wahenga wao, nilichukua ahadi kwao ya kunitii mimi wakati wa zama za Nabii Musa na nikawatumia viongozi kumi na wawili, lakini wakatengua ahadi yangu na agano langu, hivyo nikawalaani kwa kutengua kwao ahadi na agano hilo. Na kati ya vitendo vyao ni kwamba wao walipuuza Kitabu na wakapoteza mipaka yake 9

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 9

7/5/2013 7:11:08 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

na faradhi zake na wakaficha sifa za Nabii (s.a.w.w.) katika vitabu vyao, na walikuwa wanazijua kama wanavyowajua watoto wao. Mwenyezi Mungu anasema:

َّ‫ون أَ ْب َنا َء ُھ ْم ۖ َوإِن‬ َ ُ‫اب َيعْ ِرفُو َن ُه َك َما َيعْ ِرف‬ َ ‫ِين آ َت ْي َنا ُھ ُم ْال ِك َت‬ َ ‫الَّذ‬ ‫ُون‬ َ ‫ُون ْال َح َّق َو ُھ ْم َيعْ َلم‬ َ ‫َف ِري ًقا ِم ْن ُھ ْم َل َي ْك ُتم‬ “Wale tuliowapa Kitabu wanamjua yeye kama wanavyowajua watoto wao. Na hakika kundi katika wao wanaificha haki na hali wanaijua.”(Surat al-Baqarah 2:146).

ُ ‫َوإِ ْذ قُ ْل َنا ْاد ُخلُوا ٰ َھ ِذ ِه ْال َقرْ َي َة َف ُكلُوا ِم ْن َھا َحي‬ ‫ْث شِ ْئ ُت ْم َر َغ ًدا‬ Na uovu wao ulipita mipaka pale walipoamriwa kuomba َّ ‫اب سُجَّ ًدا َوقُولُوا ح‬ َ ‫رْ َل ُك ْم َخ‬dhambi ۚ ‫ ُك ْم‬na ‫طا َيا‬ ‫ِط ٌة َن ْغ ِف‬ ‫ َو ْاد ُخلُوا‬wakَ ‫ ْال َب‬mlango, msamaha kufutiwa kwa kuingia katika ageuza na wakabadili maneno ya Mwenyezi ‫ِين‬ ‫َس َن ِزي ُد َ َْالم‬mahala ‫َو‬ َ ‫ھُحْمسِ نْال ِك‬Mungu, َ ُ ُ َ َ َ َ ْ ْ‫ع‬ ْ‫ع‬ ُ ُ ُ ‫إ‬ ‫و‬ ۖ ‫م‬ ‫ھ‬ ‫ء‬ ‫ا‬ ‫ن‬ ‫ب‬ ‫أ‬ ‫ون‬ ‫ف‬ ‫ر‬ ‫ي‬ ‫ا‬ ‫م‬ ‫ك‬ ‫ه‬ ‫ن‬ ‫و‬ ‫ف‬ ‫ر‬ ‫ي‬ ‫اب‬ ‫ت‬ ‫( آت ْينا‬ngano). ‫ِين‬ َّ‫ن‬ َ َ َ َ َ َ َ َ ‫الَّذ‬ ْ ُ palipotajwa Hittwah (msamaha) wakasema Hintwah ِ ِ ِ ‫ُون‬ َ ‫ُون ْال َح َّق َو ُھ ْم َيعْ َلم‬ َ ‫َف ِري ًقا ِم ْن ُھ ْم َل َي ْك ُتم‬ Mwenyezi Mungu anasema:

ُ ‫َوإِ ْذ قُ ْل َنا ْاد ُخلُوا ٰ َھ ِذ ِه ْال َقرْ َي َة َف ُكلُوا ِم ْن َھا َحي‬ ‫ْث شِ ْئ ُت ْم َر َغ ًدا‬ َّ ‫اب سُجَّ ًدا َوقُولُوا ح‬ ۚ ‫ِط ٌة َن ْغ ِفرْ َل ُك ْم َخ َطا َيا ُك ْم‬ َ ‫َو ْاد ُخلُوا ْال َب‬ ‫ِين‬ َ ‫َو َس َن ِزي ُد ْالمُحْ سِ ن‬ “Na tuliposema: Ingieni mji huu na kuleni humo maridhawa popote mpendapo, na ingieni katika mlango (wake) kwa kunyenyekea, na semeni: Tusamehe. Tutawasamehe makosa yenu, na tutawazidishia wale wafanyao mazuri..” (Sura al-Baqarah: 58). 10

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 10

7/5/2013 7:11:09 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

Wafasiri wamekongamana kwamba waliamuriwa kuingia katika ardhi tukufu nayo ni Jerusalem au Arihaheneo ambalo ni karibu na Jerusalem na waliamuriwa kusujudu wakati wa kuingia na kusema: ”Hittwah” wakasema kwa kebehi ” Hintwah.” Mwenyezi Mungu anasema:

‫ِين َظ َلمُوا َق ْو ًال َغي َْر الَّذِي قِي َل َل ُھ ْم‬ َ ‫َف َب َّد َل الَّذ‬ “Wakabadilisha wale waliodhulumu kauli isiyokuwa ile waliyoambiwa...”(Sura al-Baqarah 2:59).

Hatupo katika fursa ya kubainisha aya zilizoshuka katika Qur’ani zikielezea upotoshaji wao na njia ambazo Mayahudi walizifuata katika kupotosha vitabu vya mbinguni, ambapo wakati mwingine ilikuwa ni kwa kupinga licha ya kuwepo maneno hayo, na wakati mwingine kwa kuondoa, na kwa aina nyingine za upotoshaji. Ikiwa hii ndio hali ya upotoshaji na msimamo wake katika Kitabu Kitukufu basi ni juu ya Mwislamu kuwa mbali na sifa hii, na kujitahidi sana kuhifadhi hazina yake, sawa iwe inaafikiana na matakwa yake au inakinzana na matakwa yake, kwani ni amana ya Mwenyezi Mungu ambayo ni wajibu kuipeleka kwa kizazi kinachokuja kama ilivyo. Lakini kadri unavyoishi utaona maajabu, tunaona kwamba kundi la baadhi ya waandishi na wahakiki au wachapishaji na wasambazaji huko Misri, Syria, Beirut (na kwingineko) wamejitahidi kupotosha hazina hii inapokhalifu matakwa yao, na kwa kuwa tumeona hilo ka11

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 11

7/5/2013 7:11:09 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

tika rejea nyingi, hali hiyoinatuzuia kusema kuwa upotoshaji huo ni makosa tu ya uandishi, au yametokea kwao kwa bahati mbaya na si kwa kudhamiria. Na sisi hapa katika makala haya tutaonesha baadhi ya sehemu ambazo upotoshaji umefanyika (kwa kudhamiria) ili msomaji aone kwamba madai yetu si madai yasiyokuwa na hoja.

12

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 12

7/5/2013 7:11:09 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

HADITHI YA SIKU YA KARAMU YA JAMAA WA KARIBU Tafsir Tabariy na Hadith ya “Siku ya Karamu ya Jamaa wa Karibu” Tafsir Ibn Kathir na Hadith ya “Siku ya Karamu ya Jamaa wa Karibu” Hayatu Muhammad na Hadith ya “Siku ya Karamu ya Jamaa wa Karibu” Wafasiri wametaja kwamba baada ya kuteremka kauli ya Mwenyezi Mungu:

‫ين‬ َ ‫ك ْاألَ ْق َر ِب‬ َ ‫ير َت‬ َ ِ‫َوأَ ْن ِذرْ عَش‬ “Na uwonye jamaa zako walio karibu..”

(Sura Shuarau: 214)

Nabii (s.a.w.w.) alimwita Ali (as) na watu arubaini katika viongozi wa Bani Hashim na wakuu wao na akaazimia kutangaza ujumbe wake katika karamu hiyo, na akamwamuru Ali (as) kuandaa chakula na mtindi, na baada ya kumaliza kula chakula Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alizungumza na akasema: “Hakika kiongozi hawadanganyi watu wake, naapa kwa Mwenyezi Mungu ambaye hakuna Mungu isipokuwa Yeye, hakika mimi ni Mtume kwenu na kwa watu wengine, Wallahi mtakufa kama mnavyolala na mtafufuliwa kama mnavyoamka (usingizini) na mtahesabiwa kwa mnayoyafanya, na kisha hakika ni pepo ya milele na moto wa milele.“ Kisha akasema: “Enyi watoto wa Abdul-Muttalib; hakika mimi simjui kijana katika waarabu aliyewajia watu wake na 13

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 13

7/5/2013 7:11:09 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

jambo bora kushinda lile nililokuleteeni mimi, hakika mimi nimekuleteeni kheri ya dunia na Akhera, na Mwenyezi Mungu Mtukufu ameniamuru nikuiteni kwenye jambo hilo, basi ni nani kati yenu ataniamini na kunisaidia katika jambo hili ili awe ndugu yangu, wasii wangu na khalifa wangu kwenu?” Ali (as) anasema: “Watu wote wakanyamaza, nikasema na hali mimi wakati huo nikiwa ni mdogo wao kwa umri na bado ni mwenye tongotongo, mwenye tumbo kubwa kati yao na mwenye miundi miembamba kati yao: ‘Mimi ewe Nabii wa Mwenyezi Mungu, nitakuwa msaidizi wako katika hilo.’ Akashika shingo yangu kisha akasema: ‘Hakika huyu ni ndugu yangu, wasii wangu na khalifa wangu kwenu basi msikilizeni na mtiini.’ Watu wakasimama huku wakicheka na kumwambia Abu Talib: ‘Amekuamuru kumsikiliza mtoto wako na kumtii.’”4 1. Muhammad bin Jarir Tabary katika kitabu chake Tarikh Tabariy ameitaja kwa kirefu hadithi ya “Siku ya Karamu ya Jamaa wa Karibu” lakini akapotosha Hadith kwa kuitoa mahala pake alipoitaja katika tafsiri yake, pale alipojaribu kufasiri kauli yake (swt): “Na uwonye jamaa zako walio karibu..” (Sura Shuarau: 214), hapo akataja yaliyopita katika kitabu chake Tarikh Tabariy lakini alipofika katika maelezo ya Mtume kuhusu‘udugu, wosiana ukhalifa wa Ali’akabadili kauli ya Mtume (s.a.w.w.) kwa kuweka kinaya. Maelezo yake ni haya hapa: “Akasema: ‘Enyi watoto wa Abdul-Muttalib hakika mimi simjui kijana katika waarabu aliyewajia watu wake na jambo 4

arikh Tabariy Juz. 2, Uk. 62 – 63, Tarikhul Kaamil Juz. 2, Uk. 40 – 41, Musnad T Ahmad Juz. 1, Uk. 111 na nyinginezo kati ya rejea zilizopo kuhusu nafasi hiyo. 14

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 14

7/5/2013 7:11:09 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

bora kushinda lile nililokuleteeni mimi, hakika mimi nimekuleteeni kheri ya dunia na Akhera, na Mwenyezi Mungu Mtukufu ameniamuru nikuiteni kwenye jambo hilo, basi ni nani kati yenu ataniamini na kunisaidia katika jambo hili ili awe ndugu yangu na kadha wa kadha.?’” Watu wote wakanyamaza. Nikasema – yaani Ali: Na hali mimi wakati huo nikiwa ni mdogo wao kwa umri ….: ‘Mimi ewe Nabii wa Mwenyezi Mungu, nitakuwa msaidizi wako katika hilo.’ Akashika shingo yangu kisha akasema: ‘Hakika huyu ni ndugu yangu na kadha wa kadha basi msikilizeni na mtiini.’”5 Hapana shaka kwamba ambacho kimemsukuma Tabary au mchapishaji wa kitabu chake – kwa dhana dhaifu - kufanya kosa hilo la upotoshaji ni kasumba yake ya kimadhehebu, kwa kuwa hakubali kwamba Imam Ali ni Khalifa wa Mtume bila ya utenganisho, na kwa upande mwingine hakika hayo maneno mawili: “Khalifa wangu na Wasii wangu” yanaeleza wazi wazi ukhalifa wa Ali kwa Nabii bila ya utenganisho, hivyo akageuza Hadith ili kuitetea madhehebu yake. 2. Ibnu Kathir (aliyefariki mwaka 774AH) na yeye amefanya mfano wa haya katika kitabu chake cha historia na katika tafsiri yake,6 akafuata njia ileile ambayo ameifuata aliyekuwa kabla yake, ambaye ni Tabary, kwa kutupilia mbali msingi wa uaminifu katika kunukuu. Na sisi hatumsamehe Ibn Kathir katika kitendo chake hiki abadani, kwa sababu amefanya kwa kudhamiria makusudi katika sehemu zote mbili kwa pamoja, katika riwaya zake za kihistoria na katika tafsiri yake. Ama Tabary yeye amefanya kosa 5 6

Tafsir Tabary Juz. 19, uk. 75. Tazama Tafsir Ibn Kathir Juz. 5, uk. 231 katika tafsri ya aya, na katika Tarikh yake ni Juz. 2, uk. 38 chapa ya Daarul- Kutubi Lebanon. 15

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 15

7/5/2013 7:11:09 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

hilo katika historia tu na sio katika tafsiri yake, na hapana shaka kwamba hakika yeye Ibn Kathir alipitia kisa hiki katika Tarikh Tabary lakini yeye pamoja na hivyo aliamua kutoka katika njia ya sawa, hivyo akaacha kunukuu riwaya ya kihistoria katika tukio hili na akadhamiria makusudi kunukuu riwaya ya tafsiri. 3. Na cha kushangaza zaidi kuliko hiyana hiyo ni yale aliyoyafanya katika zama zetu hizi, Dr. Haykal, waziri wa zamani wa elimu wa Misri, katika kitabu chake Hayat Muhammad, na kwa kitendo chake hiki akafungua mlango wa upotoshaji mbele ya kizazi cha leo. Hakika mtunzi katika utangulizi wake amewashambulia mustashiriqina kwa nguvu na akawakosoa kwa nguvu kwa kupotosha kwao ukweli wa kihistoria na kuzua kwao baadhi ya matukio, wakati ambapo yeye mwenyewe pia hakurudi nyuma kwa kutenda kosa hilo katika njia hii au ile: Kwanza: Katika chapa ya kwanza ya kitabu chake kilichotajwa amenukuu kwa namna ya mkato na kifupi sana tukio lililotajwa (Kuwalingania jamaa wa karibu wanaojulikana) katika tukio la “Siku ya Karamu ya Jamaa wa Karibu” au kwa Hadithi ya “Mwanzo wa daawa” na akatosheka kwa sentensi mbili za msingi kwa kutaja moja tu kati ya hizo mbili, nayo ni kauli ya Nabii kwa jamaa wa karibu waliohudhuria siku hiyo: “Nani atanisaidia ili awe ndugu yangu, wasii wangu na khalifa wangu” ambapo ameondoa sentensi ambayo aliisema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) kwa Ali baada ya kusimama kwa mara ya tatu na kutangaza usaidizi wake kwa Nabii, nayo ni kauli yake (s.a.w.w.): “Hakika huyu ni ndugu yangu, msaidizi wangu na khalifa wangu.” 16

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 16

7/5/2013 7:11:09 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

Pili: Hakika yeye alipiga hatua ya mbali zaidi katika chapa ya pili, ya tatu na ya nne, ambapo aliondoa sentensi zote mbili pamoja, na kwa hili ameelekeza pigo kubwa lenye kumaliza thamani ya kitabu chake.7 Ni juu ya msomaji kuto mbebesha Abu Ja’far Tabary moja kwa moja na kwa yakini mzigo wa upotoshaji, kwani upo uwezekano kuwa upotoshaji huo ulifanywa na wachapishaji wa tafsiri yake, lakini kasumba ya Ibn Kathir mfuasi wa Bani Umaiyya inaleta tumaini kwamba upotoshaji wake huo ni kitendo chake mwenyewe na wala si kutoka kwa wachapishaji wa kitabu chake. Kama ambavyo tunasema kwa uhakika kwamba kosa la upotoshaji katika kitabu Hayat Muhammad ni la mwandishi wake Muhammad Husein Haykal, kwani mabadiliko hayo katika kitabu chake yalitokea katika zama za uhai wake, na inasemekana kwamba alipata shinikizo kali kutoka kwa Maulamaa wa Azhari na hivyo akalazimika kupotosha na kugeuza katika chapa zilizofuatia.

‫ون ٰ َھ َذا ِمنْ عِ ْن ِد‬ َ ُ‫ِيھ ْم ُث َّم َيقُول‬ َ ‫ُون ْال ِك َت‬ َ ‫ِين َي ْك ُتب‬ َ ‫َف َو ْي ٌل لِلَّذ‬ ِ ‫اب ِبأ َ ْيد‬ ً ‫ﷲ لِ َي ْش َترُوا ِب ِه َث َم ًنا َقل‬ ْ ‫ِيال ۖ َف َو ْي ٌل َل ُھ ْم ِممَّا َك َت َب‬ ‫ِيھ ْم َو َو ْي ٌل‬ ِ َّ ِ ‫ت أَ ْيد‬ ‫ُون‬ َ ‫َل ُھ ْم ِممَّا َي ْكسِ ب‬ “Basi ole wao wanaoandika Kitabu kwa mikono yao, kisha wakasema: Hiki kimetoka kwa Mwenyezi Mungu, ili wachukue kwacho thamani ndogo. Basi ole wao kwa yale iliyoyaandika mikono yao. Na ole wao kwa yale wanayoyachuma.” (Surat al-Baqarah 2:79) 7

Rejea Hayat Muhammaduk. 142 chapa ya 13 ya Maktaba ya Nahadhati al- Misriyah ya Cairo ya mwaka 1968 17

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 17

7/5/2013 7:11:09 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

AL-FUTUHATUL-MAKIYYAH NA KUONDOLEWA

KWA MAJINA YA MAIMAMU WA AHLUL-BAIT (AS)

H

akika Nabii (s.a.w.w.) hakutosheka tu na kumsimika Ali (a.s.) katika cheo cha Uimamu na Ukhalifa, kama ambavyohakutosheka tu na kuurejesha ummah wa Kiislam kwa Ahlul-Bait wake na kizazi chake kitukufu, na hakuishia tu katika kuwafananisha wao na safina ya Nuhu katika Hadith maarufu: “Mfano wa Ahlul-Bait wangu ni kama safina ya Nuhu, mwenye kuipanda atanusurika na mwenye kuacha kuipanda ataghariki.”8 Bali pia alibainisha idadi ya Maimamu ambao watasimamia ukhalifa baada yake mmoja baada ya mwingine, ili kusibaki kwa mwenye wasiwasi shaka yoyote, wala kwa mwenye shaka, shaka yoyote. Na maelezo hayo yamekuja katika vitabu Sahihi Sitah na katika Musnad mbalimbali na kwa namna mbalimbali, na sisi hapatutaashiria Hadith moja tu. Amepokea Muslim kutoka kwa Jabir bin Samrah amesema: “Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu anasema: ‘Dini hii haitaacha kuwa yenye nguvu hadi watimie makhalifa kumi na mbili.’ kisha akasema neno ambalo sikulifahamu, ni-

8

S awaiqul-Muhriqah: 184 na 234 chapa ya Muhammadiyah Misri; Is’af ur-Raghibina: 109 na vinginevyo. 18

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 18

7/5/2013 7:11:09 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

kamwambia baba yangu; Amesemaje? Akasema: Amesema: ‘Wote ni katika Makuraishi.’”9 Na Maimau wa Kishia kumi na wawili ambao amewaashiria Nabii katika maneno yake ni: 1. Amirul-Muuminina Ali bin Abu Talib (aliyezaliwa kabla ya utume kwa miaka kumi na aliyekufa shahidi mwaka wa 40 Hijiria) na ambaye amezikwa huko Najaf tukufu, Iraq. 2. Imam Hasan bin Ali al-Mujtaba (aliyezaliwa mwaka 3 Hijiria na kufa shahidi mwaka 50 Hijiria) ambaye amezikwa katika makaburi ya Baqi’i katika Mji wa Madina. 3. Imam Husein bin Ali- Bwana wa wafia dini (aliyezaliwa mwaka wa 4 Hijiria na amekufa Shahidi mwaka wa 61 Hijiria) ambaye amezikwa huko Karbala, Iraq. 4. Imam Ali bin Husein bin Ali Zainul-Abidiin (aliyezaliwa mwaka 38 na kufa shahidi mwaka wa 94 Hijiria) ambaye amezikwa katika makaburi ya Baqi’i katika mji wa Madina. 5. Imam Muhammad bin Ali - Baqirul-Uluum (aliyezaliwa mwaka 57 na amekufa shahidi mwaka 114 Hijiria) ambaye amezikwa katika makaburi ya Baqi’i katika Mji wa Madina. 6. Imam Ja’far bin Muhammad as-Sadiq (aliyezaliwa mwaka 83 Hijiriah na amekufa shahidi mwaka 148 Hijiria) ambaye amezikwa katika makaburi ya Baqi’i katika mji wa Madina. 9

S ahihi Muslim Juz. 6, uk. 3, Kitabu cha uongozi, mlango wa watu kuwafuata Makuraishi. 19

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 19

7/5/2013 7:11:09 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

7. Imam Musa bin Ja’far al-Kadhim (aliyezaliwa mwaka 128 Hijiria na kufa shahidi mwaka 183 Hijiria) ambaye amezikwa katika mji wa Kadhimiya karibu na Baghdad, Iraq. 8. Imam Ali bin Musa ar-Ridhaa (aliyezaliwa mwaka 148 na kufa shahidi mwaka 203 Hijiria) ambaye amezikwa Khurasan, Iran. 9. Imam Muhammad bin Ali al-Jawad (aliyezaliwa mwaka 195 na kufa shahidi mwaka 220 Hijiria) ambaye amezikwa katika mji wa Kadhimiya, karibu na Baghdad Iraq. 10. Imam Ali bin Muhammad al-Had (aliyezaliwa mwaka 212 na kufa shahidi mwaka 254 Hijiria) ambaye amezikwa katika mji wa Samara Kaskazini mwa mji wa Baghdad, Iraq. 11. Imam Hasan bin Ali al-Askariy (aliyezaliwa mwaka 233 na kufa shahidi mwaka 260 Hijiria) na ambaye amezikwa katika mji wa Samara Kaskazini mwa mji wa Baghdad, Iraq. 12. Imam Muhammad bin Hasan maarufu kwa jina la Mahdi al-Hujjah (as), naye ndio Imam wa kumi na mbili, naye yuko hai hadi atakapodhihiri kwa amri ya Mwenyezi Mungu, (kulingana na ahadi iliyoahidiwa katika Qur’ani katika Surat Nuur: 45, Surat-Tawba: 33, Surat al-Fat’ha: 28 na Sura Swaf: 9) na kusimamisha serikali ya Mwenyezi Mungu katika Ulimwengu wote.10 10

I metokea baadhi ya ikhitilafu katika historia katika mazazi na vifo vya baadhi ya Maimam na tumeshataja moja ya kauli, hivyo anayetaka ziada basi arejee katika ufafanuzi wa ziada. 20

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 20

7/5/2013 7:11:09 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

Imekuja katika maelezo ya maisha ya Maimam kumi na wawili katika vitabu vya historia na sira kwamba Imam wa kumi na mbili bado yungali hai na atashika cheo cha ukhalifa kwa matakwa ya Mwenyezi Mungu. Kisha Sheikh AbdulWahab Shaaraniy akatenga mlango mzima katika kitabu alYawaqitu Wal-Jawahir Fiy Bayan Aqaidil-Akabir akibainisha masharti ya Kiyama ambayo sharia imeyatolea maelezo na yote yatatokea kabla ya Kiyama, na kati ya hayo akasema ni kudhihiri Mahdi na akasema na Yeye ni katika watoto wa alHasan al-Askariy na kuzaliwa kwake ilikuwa ni katika nusu ya Shabani mwaka 255 Hijiria, naye atabakia hai hadi atakapokutana na Isa bin Mariyam (as), na umri wake hadi wakati wetu huu wa mwaka 958 Hijiria ni miaka 706. Kisha akasema: Ibara ya Sheikh Muhyi Diyn katika mlango wa 366 katika al-Futuhat iko hivi: “Najueni kwamba nilazima Mahdi atadhihiri, lakini hatatokea mpaka ardhi ijae ufisadi na dhulma, na ataijaza uadilifu na usawa, na lau kama umri wa dunia hautabaki ila siku moja tu, basi Mwenyezi Mungu atairefusha siku hiyo hadi Khalifa huyo atawale, naye ni katika kizazi cha Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) katika kizazi cha Fatmah (r.a), babu yake ni Husein bin Ali bin Abu Talib, na mzazi wake ni Hasan al-Askariy mtoto wa Imam Ali an-Naqiy, mtoto wa Imam Muhammad at-Taqiy, mtoto wa Imam Ali ar-Ridha, mtoto wa Imam Musa al-Kadhim, mtoto wa Imam Ja’far as-Sadiq, mtoto wa Imam Muhammad alBaqir, mtoto wa Imam Zainul-AbidinaAli bin Husein, mtoto wa Imam Husein, mtoto wa Imam Ali bin Abu Talib (r.a), jina lake linafanana na jina la Mtume wa Mwenyezi Mungu, Waislamu watampa yamini la utii baina ya Rukun na Maqam, anafanana na Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) katika tabia yake, na Mwenyezi Mungu amesema: 21

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 21

7/5/2013 7:11:09 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

‫ك َل َع َل ٰى ُخلُ ٍق َعظِ ٍيم‬ َ ‫َوإِ َّن‬ “Na hakika wewe una tabia tukufu.”

(Sura al-Qalam: 4)

Kisha akataja sifa za Mahdi (as) kwa kauli yake:“Ni mwenye paji gumu la ‫يم‬ ‫ك َل َع َل ٰى ُخل‬ ‫ َوإِ َّن‬ya kuchongoka, watu ِ‫ َعظ‬ni‫ُ ٍق‬mwenye َ pua ٍ uso, bora kwake ni watu wa mji wa Kufah, atagawa mali kwa usawa na atafanya uadilifu kwa raia...”11 Na tunaporejea katika al-Futuhatul-Makiyyah kitabu kilichochapishwa huko Misri, ambacho taasisi ya Darus-Sadir ya Beirut imerudia kukichapisha, tunakuta kimegeuzwa nakimebadilishwa, na haya ni maelezo yaliyokuja humo: “Tambua na Mwenyezi Mungu atuunge mkono, kwamba Mwenyezi Mungu ana Khalifa ambaye atatokea wakati ardhi itakuwa imejaa ufisadi na dhulma, hivyo yeye ataijaza uadilifu, na kama haitabakia katika umri wa dunia ila siku moja tu, basi Mwenyezi Mungu atairefusha siku hiyo hadi atawale Khalifa huyu ambaye anatokana na kizazi cha Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) katika kizazi cha Fatmah, jina lake linafanana na jina la Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na babu yake ni Hasan bin Ali bin Abu Talib, atapewa yamini la utii baina ya Rukun na Maqam, anafanana na Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) kwa umbo lake, na tabia yake ni chini ya tabia yake (s.a.w.w.), kwa sababu hakuna yeyote anayefanana na Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) katika tabia yake, na Mwenyezi Mungu anasema:

11

l- Jawahir Wal-Yawaqit Juz. 2, uk. 143 chapa ya ya mwaka 1378 AH sawa na A 1959 AD. 22

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 22

7/5/2013 7:11:10 PM


‫ك َل َع َل ٰى ُخلُ ٍق َعظِ ٍيم‬ َ ‫َوإِ َّن‬ Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

‫ك َل َع َل ٰى ُخلُ ٍق َعظِ ٍيم‬ َ ‫َوإِ َّن‬ “Na hakika wewe una tabia tukufu.”

(Sura al-Qalam: 4)”

Kwa kweli wewe unapolinganisha na aliyoyanukuu Sha’araniy katika kitabu chake na yaliyopo hivi sasa katika al-Futuhatul- Makiyyah ambayo tumenukuu maelezo yake, utaona kwamba mwandishi ameondoa majina ya Maimam kama ambavyo amebadili kwa kuondoa neno Husein na kuweka neno Hasan, ambapo amesema: “Babu yake ni Hasanbin Ali bin Abu Talib” na ilikuwa ni wajibu wake aseme babu yake ni Husein, na huu ni upotoshaji.

‫ير‬ ٍ ‫َو َال ُي َن ِّب ُئ َك م ِْث ُل َخ ِب‬ “Na hapana atakayekuambia kama Yeye Mwenye habari.” (Sura Fatir: 14)

23

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 23

7/5/2013 7:11:10 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

TAARIKH YA’AQUBIY NA KUPOTOSHWA KWA HADITHI YA GHADIR

H

akika Ahmad bin AbiYa’aqubiy ambaye ni mashuhuri kwa jina la Ibn Waadhul-Abbasiy (aliyefariki mwaka 290 AH) na mwandishi wa Taarikh al-Ya’aqubiy ametaja katika faslu isemayo“Sehemu ya Qur’ani iliyoteremka Madina” kauli yake: “Na imesemwa kwamba aya ya mwisho iliyoteremka kwake (s.a.w.w.) ni

ُ ِ‫ت َع َل ْي ُك ْم ِنعْ َمتِي َو َرض‬ ُ ْ‫ت َل ُك ْم دِي َن ُك ْم َوأَ ْت َمم‬ ُ ‫ْال َي ْو َم أَ ْك َم ْل‬ ‫يت َل ُك ُم‬ ‫ْاإلِسْ َال َم دِي ًنا‬ “Leo nimewakamilishia dini yenu na kuwatimizia neema Yangu na nimewapendelea Uislamu kuwa dini.” (Sura Maidah: 3).

Nayo ndio riwaya sahihi iliyothibiti waziwazi, na kuteremka kwake ilikuwa ni siku aliyomsimika Amirul-Muuminina Ali bin Abu Talib (as) huko katika bwawa la Khum.”12 Lakini katika chapa ya Darus-Sadir imekuja:Akasema baada ya kunukuu Aya: “Ni riwaya sahihi iliyothibiti waziwazi, na kuteremka kwake ilikuwa ni siku aliyojitenga mbali na Amirul-Muuminina Ali bin Abu Talib (as) baada ya kumhurumia.” amepotosha katika sentensi mbili: 1. Amepotosha katika “Siku aliyomsimika” kwa kuibadili na kusema “Siku aliyojitenga mbali” 12

arikh al-Ya’qubiy, Juz. 2, uk. 35, al-Maktabatu al-Hadariya Najaf 1383H sawa T na 1974 24

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 24

7/5/2013 7:11:10 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

2. Amepotosha katika “Bwawa la Khum” kwa kuibadili na kusema “Baada ya kumhurumia”13

‫ون أَ َّن ُھ ْم‬ َ ‫ض َّل َسعْ ُي ُھ ْم فِي ْال َح َيا ِة ال ُّد ْن َيا َو ُھ ْم َيحْ َس ُب‬ َ ‫ِين‬ َ ‫الَّذ‬ ُ ‫ون‬ ‫ص ْنعًا‬ َ ‫يُحْ سِ ُن‬ “Ambao juhudi yao katika maisha ya dunia imepotea bure, nao wanadhani kuwa wanafanya kazi nzuri.” (Sura Kahfi: 104).

13

Tarikh Ya’qubiy Juz. 2, uk. 43 chapa ya Daarus-Sadir, Beirut. 25

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 25

7/5/2013 7:11:10 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

AL-ADHKAR AN-NAWAWIYYAH NA KUPATWA NA UPOTOSHAJI

H

akika baadhi ya mifano halisi iliyotangulia kuhusu upotoshaji ilikuwa ni upotoshaji katika Hadith na historia, ima ni kutoka katika upande wa watunzi wenyewe au ni kutoka upande wa wachapishaji. Lakini kuna aina nyingine ya upotoshaji nje ya uzio huu, nayo ni kwamba ndani ya sehemu za uchapishaji huko Misri, Damascus na Beirut14 kuna vikundi vyenye kwenda mbio katika kubadili na kuondoa yaliyokuja katika vitabu vya wahenga kwa kufuata utashi wao au raghba ya taasisi zao ambazo zinawapa misaada, na hii ni hatari kubwa inayotishia hazina yetu kongwe ya Kiislamu ambayo imekuwa ni shabaha ya mzunguko wa kundi la mamluki wakulipwa ambao wameuza dini yao kwa dunia yao, na ifuatayo ni mifano ya aina hii katika upotoshaji. Hakika Hadith tukufu ambazo wamezipokea watu wa Hadith kuhusu kumzuru Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) ni nyingi kiasi kwamba zinatuondolea haja ya kuhakiki sanad zake na wapokezi wake, kwa sababu ya wingi wake na kuwa kwake mutawatir, na mahafidhi wa Hadith wameziandika kwa madhehebu zao zote za Kiislam katika vitabu vyao na Sahih zao, nazo kwa mkusanyiko wake zinaonyesha kwamba kuzuru kaburi la Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) ilikuwa ni kati ya Sunnah zilizothibiti, na lau tukitaka kutaja Hadithi zote hizo tutarefusha sana, hivyo basi hapa tutatosheka kwa kutaja moja kati ya hizo.

14

a kwa sababu itokanayo na yale yaliyotangulia ya kutokea upotoshaji katika N Tarikhul-Ya’qubiy. 26

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 26

7/5/2013 7:11:10 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

Kutoka kwa Abdullah bin Umar, amesema: “Hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: ‘Mwenye kuzuru kaburi langu anawajibika kupata uombezi wangu.’” Hadith hii imekuja katika kitabu al-Fiqhu Alaa MadhahibilArba’at, Juz. 1, uk. 590. Maulamaa wa Madhehebu manne wametoa fatwa kulingana na Hadith hii, na ili kujua rejea zake, rejea kitabu Wafaul-Wafai Bi akhbari Darul-Mustafa, Juz. 4 uk. 1336. Na katika mambo ambayo hakuna shaka humo ni kwamba Hadith ambayo imepokewa na Mahafidh wa Hadith na Maulamaa tangu katikati ya karne ya pili Hijiria hadi leo hii haiwezekani ikawa ni ya kuzua na isiyo na msingi. Hakika Imam Nawawi ad-Damashqiy (aliyezaliwa mwaka 631 na kufariki mwaka 676 AH) ametunga kitabu kiitwacho al-Adhkaru an-Nawawiyyah na ametaja humo kuzuru kaburi la Nabii na nyuradi zake, na ameandika faslu kama ifuatavyo:Faslu ya kuzuru kaburi la Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na nyuradi zake:

“Tambua ya kwamba inapasa kwa kila mmoja mwenye kuhiji kwenda kumzuru Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), ni sawa sawa (Madina) iwe ndio njia yake au si njia yake, kwani kumzuru kwake (s.a.w.w.) ni muhimu sana katika kujikurubisha na ni juhudi zenye manufaa na ni maombi bora mno, basi anapoondoka kwenda katika ziara azidishe kumswalia (s.a.w.w.) na amuombe Mwenyezi Mungu amnufaishe kwa kumzuru (s.a.w.w.) na imnufaishe ziara hiyo duniani na Akhera. Na aseme: ‘Eee Mwenyezi Mungu nifungulie milango ya rehema Zako na uniruzuku katika kuzuru kaburi la Nabii Wako (s.a.w.w.) yale ambayo umewaruzuku mawalii wako 27

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 27

7/5/2013 7:11:10 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

na watu wenye kukutii, na unisamehe na unihurumie, Ewe Mbora wa kuombwa.”’15 Haya ndio maelezo ya kitabu katika chapa ya kwanzaambayo Muhyi Diyn al-Mutaqiy amehakiki maelezo yake na hadithi zake na akatia ufafanuzi wake juu ya maelezo hayo, na kitabu kikachapishwa na Daaru Ibn Kathir ad-Damashqiy – Beirut. Katika chapa hiyo utaona humo anuani za faslu ni kama ifuatavyo: 1. Faslu katika kuzuru kaburi la Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.). 2. Na akasema kwamba kusudio la kukata masafa ni kumzuru Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) ambapo amesema: Kwenda kumzuru Mtume wa Mwenyezi Mungu. 3. Pia amesema vilevile katika maombi ya mwenye kuzuru: Na amuombe Mwenyezi Mungu amnufaishe kwa kumzuru kwake (s.a.w.w.). 4. Na yamepokewa maelezo kutoka kwake katika dua ya mwenye kuzuru ambapo amesema: Na uniruzuku kuzuru kaburi la Nabii (s.a.w.w.). Lakini kwa masikitiko makubwa tunaona upotoshaji mkubwa katika chapa nyingine ambayo ameisahihisha Abdul-Qadir al-Aurnaat na ikasambazwa na Daarul-Huda ya Riyadh mwaka 1408 Hijiria, na yafuatayo ni maelezo ya chapa hiyo: 15

Al-Adhkarun-Nuriyah , uk. 333. 28

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 28

7/5/2013 7:11:10 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

“Faslu katika kuzuru Msikti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.): Tambua kwamba ni mustahabu kwa mwenye kutaka kuzuru msikiti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) azidishe kumswalia (s.a.w.w.) katika njia yake, na jicho lake linapoona miti ya Madina na uzio wake na yale yanayoutambulisha (msikiti), azidishe kumswalia na kumsalimia (s.a.w.w.) na amuombe Mwenyezi Mungu amnufaishe kwa kuzuru kwake msikiti wake (s.a.w.w.), na amnufaishe kwa ziara hiyo duniani na Akhera, na aseme: ‘Eee Mwenyezi Mungu nifungulie milango ya rehema zako na uniruzuku katika kuzuru msikiti wa Nabii wako (s.a.w.w.) yale ambayo umewaruzuku mawalii wako na watu wenye kukutii na unisamehe na unihurumie, Ewe Mbora wa kuombwa.’”16 Amebadilisha maudhui manne: 1. Amebadili faslu na kuwa: Kuzuru msikiti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu. 2. Na amebadili makusudio ya safari ambapo amesema: Mwenye kutaka kuzuru msikiti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu. 3. Kama ambavyo amepotosha swali la muulizaji na akasema: Amnufaishe kwa kuzuru msikiti wake. 4. Amepotosha dua ya mwenye kuzuru na akasema: Katika kuzuru msikiti wa Nabii wako (s.a.w.w.). Yote hayo ni kwa kuwa Mawahabi hawathamini hata kido16

Al-Adhkaar an-Nuriyah, uk. 295 kimesambazwa na Daarul-Huda Riyadh chapa ya pili 1408 kimehakikiwa na Abdul- Qadir al-Arnaut. 29

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 29

7/5/2013 7:11:10 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

go kumzuru Nabii (s.a.w.w.), Aali zake wala Maswahaba wake licha ya kwamba hawaharamishi. Na kuna sababu nyingine ambayo imewafanya kupotosha, nayo ni madai yao kwamba kufunga safari kwenda kumzuru Nabii (s.a.w.w.) ni haramu, na anuani ya faslu iliyopo na madhumuni yaliyokuja humo, vyotevinaashiria kwamba ni mustahabu kufunga safari kwenda kumzuru Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), hivyo wao Mawahabi wameifanyia hiyana amana ya Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kuinusuru madhehebu yao (kwa njia ya kupotosha maandiko ya ulamaa). Tunamuomba Mwenyezi Mungu ahuishe amana ya Kiislam.

‫ُون‬ َ ‫أَ َال إِ َّن ُھ ْم ُھ ُم ْال ُم ْفسِ ُد‬ َ ‫ون َو ٰ َل ِكنْ َال َي ْش ُعر‬ “Ehee! Hakika wao ndio mafisadi, lakini hawatambui.” (Sura al-Baqarah: 12).

30

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 30

7/5/2013 7:11:10 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

BUKHARI NA HADITHI: “NA YEYE NI KIONGOZI WENU BAADA YANGU.”

H

akika hata kama Bukhari ametaja kiasi fulani katika fadhila za Ali (a.s.) na watu wa nyumbani kwake na wafuasi wake, isipokuwa kalamu yake inatetemeka anapofika kwenye fadhila zao na hivyo inazichezea Hadith kadri inavyoweza, na hii hapa ni mifano: Hakika Hadith ya uongozi, yaani kauli ya Nabii (s.a.w.w.) kuhusu haki ya Ali: “Ali anatokana na mimi na mimi natokana na Ali, naye ni kiongozi wenu baada yangu.” Ni kati ya Hadith zilizo enea ambazo zimepokewa na zaidi ya mtu mmoja kati ya maimamu wa Sahihi Sita, Sunan na mahafidhi wa Hadith, na kundi kubwa kati ya maimamu wakubwa wa Hadith wameinukuu hadithi hiyo, na pengine idadi yao inafikia wanahadithi na mahafidhi wa hadithi 65, hiyo ni kulingana na alivyopokea mhakiki mfuatiliaji Sayid Hamid Husein al-Kufiy (aliyefariki mwaka 1306 Hijiria) katika kitabu chake Abaqatul-An’wari, na kati yao ni: 1. Suleiman bin Daud Tayalisiy (aliyefariki mwaka 204 ­Hijiria) 2. Abu Bakri, Abdullah bin Muhammad bin Abi Shaibah (aliyefariki mwaka 239 Hijiria) 3. Ahmad bin Hanbal (aliyefariki mwaka 241 Hijiria) 4. Muhammad bin Isa Tirmidhiy (aliyefariki mwaka 279 Hijiria) 31

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 31

7/5/2013 7:11:10 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

5. Ahmad bin Shuaib an-Nasaiy (aliyefariki mwaka 303 Hijiria) na wengineo kati ya maimamu, mahafidhi wa hadithi na wasimulizi wa hadithi.17 Lifuatalo ni tamko la Hadith: 1. An-Nasaiy amepokea katika Khasaisu yake kwa kusema: Ametusimulia Wail bin Abdil-A’laa kutoka kwa Ibn Fudhaylu, kutoka kwa Aaraj, kutoka kwa Abdullah bin Buraydah, kutoka kwa baba yake, amesema. “Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.)alitutuma Yemen pamoja na Khalid bin Walid, na akamtuma Ali katika kikosi kingine, na akasema: ‘Kama mtakutana basi Ali atakuwa kiongozi wa watu na mkitawanyika basi kila mmoja kati yenu ataongoza kundi lake.’ Basi tukawakuta Bani Zubayda miongoni mwa watu wa Yemen, na hapo Waislamu wakawashinda washirikina basi tukawauwa wapiganaji na tukawateka wanawake, Ali akachagua kijakazi kwa ajili yake binafsi kati ya mateka wale, ndipo Khalid akamwandikia Nabii barua juu ya hilo na akaniamuru nimtie doa. Nikamkabidhi (Mtume) barua na nikamtia doa Ali, mara uso wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) ukabadilika, nikasema: Hapa ni mahala pa kujilinda, umenituma pamoja na mtu na umeniamuru nimtii na nimefikisha niliyotumwa na yeye. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akaniambia: Ewe Buraidah! Acha kumtia dosari Ali, hakika Ali anatokana na mimi na mimi nimetokana na yeye, na yeye ni kiongozi wenu baada yangu.”18 17 18

Tazama Nafahatul-Azihar Fiy Khulaswati Aqabatil- An’war Juz. 15, uk. 51 – 54. Khasaisu Ali bin Abu Talib, uk. 167, kimehakikiwa na Muhammad Baqir alMahamudiy, chapa ya kwanza 1403 A.H. 32

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 32

7/5/2013 7:11:10 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

2. Na amepokea Ahmad katika Musnad yake kutoka kwa Ibn Abbas kutoka kwa Buraydah amesema: Nilipigana vita pamoja na Ali huko Yemen, nikaona kwake kosa, tulipofika kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) nikamtaja Alikwa kumkosoa, mara nikaona uso wa Mtume wa Mwenyezi Mungu unabadilika, akasema: “Ewe Buraydah, je mimi si mwenye mamlaka kwa waumini kuliko waliyonayo juu ya nafsi zao wenyewe?” Nikasema: Ndio ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu. Akasema: “Basi ambaye mimi ni kiongozi wake Ali ni kiongozi wake.”19 Na maelezo yaliyokuja katika Hadith ambayo ameipokea an-Nasaiy katika kauli yake (s.a.w.w.) “Ali anatokana na mimi na mimi natokana na yeye, na yeye ni kiongozi wenu baada yangu.” hayapingani na yaliyonukuliwa kutoka katika Musnad Ahmad, na huenda Mtume (s.a.w.w.) alikusanya baina ya maneno mawili au mpokezi amenukuu kwa maana, hivyo akasema: “Ambaye mimi nilikuwa kiongozi wake basi huyu Ali ni kiongozi wake.” Vyovyote iwavyo ni kwamba Hadith ilikuwa inamalizia kwa maelezo yanayoonesha uongozi wa Ali baada ya kuondoka Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Na linalounga mkono hayo ni kwamba Imam Ahmad amepokea Hadith kutoka kwa Imran bin Haswin kwa namna ifuatayo: 3. Amesema: “Mtume wa Mwenyezi Mumgu (s.a.w.w.) alituma kikosi na akampa uongozi Ali bin Abu Talib (r.a) basi watu wanne katika maswahaba wa Mtume Muhammad wakapanga kueleza jambo lake kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu.” Imran anasema: “Na tulikuwa tunapowasili kuto19

Musnad Ahmad bin Hanbal Juz. 5, uk. 347. 33

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 33

7/5/2013 7:11:10 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

ka katika safari yetu tunaanzia kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) tunamsalimia.” Anasema: “Wakaingia kwake (s.a.w.w.), mtu mmoja kati yao akasema: ‘Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Hakika Ali alifanya kadha wakadha.’ Lakini Mtume akampuuza.” Kisha akanukuu kitendo cha kusimama watu wengine watatu na kurudia kwao kauli ile ya mtu wa kwanza na Mtume alivyowapuuza wote, akaendelea kunukuu hadi alipofika kwenye kauli yake: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akamwelekea wa nne wao huku uso wake ukiwa umebadilika, akasema: ‘Mwacheni Ali, hakika Ali anatokana na mimi na mimi natokana na yeye, na yeye ni kiongozi wa kila muumini baada yangu.’”20 4. Tirmidhiy amepokea kutoka kwa Imrani bin Haswin na amenukuu Hadith kama alivyoinukuu Ahmad bin Hanbal, mpaka aliposema: Akasimama mtu wa nne, na yeye akasema kama walivyosema wenzake, ndipo Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akamwelekea – huku ghadhabu ikionekana katika uso wake – akasema: “Mnataka nini kwa Ali! Mnataka nini kwa Ali! Mnataka nini kwa Ali! Hakika Ali anatokana na mimi na mimi natokana na yeye, na yeye ni kiongozi wa kila muumini baada yangu.”21 Unaona riwaya inazungumzia uongozi huku ikionesha kwamba yeye (as) ni Imam baada ya kuondoka Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), lakini Bukhari kama kawaida yake ameipokea Hadith kutoka kwa Buraydah, akataja sehemu ya Hadith na akaondoa ubeti wa kaswida katika hadithi hiyo. 20 21

Musnad Ahmad Juz. 4, uk. 437. Sunan Tirmidhiy Juz. 5, uk. 632. 34

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 34

7/5/2013 7:11:10 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

Ameipokea Hadith kutoka kwa Abdullah bin Buraydah kutoka kwa baba yake kwa namna ifuatayo: Akasema: Nabii (s.a.w.w.) alimtuma Ali kwa Khalid ili kwenda kuchukua khumsi, na nilikuwa namchukia Ali, na alikuwa ameshaoga (janaba), nikamwambia Khalid: Je humuoni huyu? Tulipowasili kwa Nabii (s.a.w.w.) nikaeleza hayo kwake. Akasema: “Ewe Buraydah unamchukia Ali?” Nikasema: Ndio. Akasema: “Usimchukie hakika ana haki katika khumsi zaidi ya hiyo (ya kumchukua kijakazi).”22 Bila shaka umeona mwenyewe Bukhari ameondoa ibara ya mwisho katika Hadith ambayo ni sawa na ubeti wa kaswida, nayo ni: “Hakika Ali anatokana na mimi na mimi ninatokana na Ali, na yeye ni kiongozi wenu baada yangu.” Na yanayosikitisha zaidi ni kwamba Mashekhe wawili: Bukhari na Muslim hawakunukuu hadithi kutoka kwa Ali (as) katika Sahih zao isipokuwa Hadith 43 tu,23 na wakati huohuo wamenukuu kutoka kwa Abu Huraira karibuni Hadith 607.24 Wa kwanza (Ali) ni mlango wa elimu ya Nabii na mtu wa kwanza kumwamini na ameandamana naye tangu utotoni mwake hadi wakati wa kuondoka Nabii (s.a.w.w.). Na wa pili (Abu Huraira) amesilimu mwaka wa saba Hijiria na akawahi miaka minne ya utume, mwaka mmoja ameumaliza Bahrain na akasuhubiana na Nabii takriban miaka mitatu tu.

Sahihu Bukhari Juz. 5, uk. 163. Al-Jam’u Baina Sahihain ya al- Hamidiy Juz. 1, uk. 153 – 157. 24 “ “ “ 3/5, uk. 322. 22 23

35

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 35

7/5/2013 7:11:11 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

BUKHARI NA HADITHI YA: “LITAKUUWA KUNDI OVU”

Z

imepokea pande mbili kutoka kwa zaidi ya swahaba mmoja mmoja kauli ya Nabii (s.a.w.w.) juu ya Ammar: “Furahi, litakuuwa kundi ovu.” Isipokuwa ni kwamba Bukhari ameichezea Hadith hii na akainukuu kwa namna ya kigutu. Bukhari amepokea kutoka kwa Ikrimah – Huria wa Ibn Abbas (r.a) - amesema: “Ibn Abbas aliniambia mimi na mtoto wake Ali: Nendeni kwa Abi Saidi mkasikilize Hadith yake, tukaondoka tukamkuta yuko katika bustani anaitengeneza, akachukua shuka lake akajitanda kisha akaanza kutusimulia hadi akataja habari za kujenga msikiti, akasema: “Tulikuwa tunabeba tofali moja moja na Ammar anabeba tofali mbili mbili. Nabii (s.a.w.w.) akamuona akawa anampangusa vumbi na anasema: ‘Maangamio! Ammar anawaita kwenda peponi na wao wanamwita kwenda motoni.’ Akasema: Ammar akasema: ‘Najikinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na fitina.’”25 Na katika riwaya nyingine ni kwamba Ibn Abbas alimwambia yeye na Ali bin Abdullah: “Mwendeeni Abi Said na mkasikilize Hadith yake.” Anasema: Tukamwendea yeye na tukamkuta yeye na ndugu yake wakiwa katika bustaniyao, tukamsalimia, alipotuona akaja akajitanda na akakaa na akasema: “Tulikuwa tunabeba tofali za msikiti tofali moja moja na Ammar anabeba tofali mbilimbili. Nabii (s.a.w.w.) akapitia kwake na akapangusa vumbi kichwani mwake na akasema: ‘Maangamio! Ammar anawaita wao kwenda kwa 25

SahihBukhari, Swala Juz. 1, uk. 541 (447). 36

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 36

7/5/2013 7:11:11 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

Mwenyezi Mungu na wao wanamwita kwenda motoni.’ Ammar akasema. ‘Najilinda kwa Mwenyezi Mungu kutokana na fitina.’”26 Al-Humaidiy amesema katika al-Jam’u Baina Sahihain: Katika Hadith hii kuna ziada mashuhuri ambayo hakuitaja asilani Bukhari katika njia za Hadith hii, na huenda haikumfikia kwa njia hizo au ilimfikia lakini akaiondoa kwa lengo makhususi alilodhamiria! Na ziada hiyo wameipokea Abu Bakri alBurqaniy naAbu Bakri Ismailiy kabla yake (Bukhari). Hadith hii kwao wao wawili inasema: “Hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: ‘Maangamio! Ammar litamuuwa kundi ovu, anawaita wao kwenda peponi na wao wanamwita kwenda motoni.’” Abu Mas’ud ad-Dimashqiy amaesema katika kitabu chake:“Bukhari hakutaja ziada hii, nayo ipo katika Hadith ya Abdul-Aziz bin al-Mukhtar, Khalid bin Abdullah al-Wastiy, Yazid bin Zari’iy, Mahbub bin Hasan na Shuubah. Wote wamepokea kutoka kwa Khalid al-Hadhau kutoka kwa Ikrimah, na ameipokea Is’haq kutoka kwa Abdul-Wahab. Ama hadithi ya Abdul-Wahab ambayo ameiandika Bukhari bila ya ziada hii, yenyewe haijatufikia kupitia mwingine yeyote zaidi ya hadithi ya Bukhari mwenyewe.” Haya ndio maelezo ya mwisho aliyoyasema Abu Mas’ud.27 Na Ibnu Athir – baada ya kunukuu maneno ya al-Humaidiy kama tulivyonukuu, amesema: “Mimi nilisema: Na ambayo nimeyasoma katika kitabu cha Bukhari katika njia ya Abil-Waqti Abdul-Awwal as-Sajziy (r.m) katika nakala ambayo niliisoma na humo kuna hati 26 27

Sahih Bukhari, Jihad, Juz. 6, uk. 30 ( 2813). Al-Jam’u Baina Sahihain ya al- Hamidiy Juz. 3/5, uk. 322. 37

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 37

7/5/2013 7:11:11 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

yake, ni kwamba katika matini za kitabu imeondolewa ziada hiina ameiandika pambizoni na kusema ni sahihi. Na akaiweka katika jumla ya Hadith, na kwamba yenyewe ni katika riwaya ya Abil-Waqti, hiyo ni katika sehemu mbili katika kitabu husika. Ya kwanza ni katika: ‘Mlango unaozungumzia kusaidiana katika ujenzi wa msikiti, katika faslu ya Jihadi.’ Na ya pili ni katika ‘Mlango unaozungumzia kufuta vumbi kichwani, katika faslu ya Jihadi.’ Sijapata ziada hii katika nakala nyingine yoyote zaidi ya hii, kama alivyosema al-Humaidiy na aliyekuwa kabla yake, na Mwenyezi Mungu ndiye Mjuzi zaidi.”28 Na vyovyote iwavyo ni kwamba ziada hii imekuja katika sehemu mbili zifuatazo katika nakala zilizochapishwa, zikiashiria kwa “Laa” kwamba ziada hiyo haipo katika nakala ya asili: 1. Faslu ya Swala, Mlango unaozungumzia kusaidiana katika ujenzi wa msikiti, namba 447. 2. Faslu ya Jihadi, Mlango unaozungumzia kufuta vumbi kichwani, namba 2812, Chapa ya Daarul- Fikri. Kama ilivyokuja katika Fat’hul-Baariy, Juz. 1, uk. 430, Mlango unaozungumzia kusaidiana katika ujenzi wa msikiti.

28

Jamiul-Usul Juz. 1, uk. 31. 38

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 38

7/5/2013 7:11:11 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

SAHIH MUSLIM NA HADITH YA: “WANAWAKE BORA ULIMWENGUNI NI WANNE.”

A

mepokea al-Hakim katika al-Mustadrak kutoka kwa Abu Said al-Khudriy (r.a) amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Fatmah ni bibi wa wanawake wapeponi isipokuwa yaliyokuwa yanatokana na Mariam binti Imran.” Akasema: Hadith hii ni sahihi katika sanad na hawakuiandika (mashekhe wawili). Na akasema: Bali Muslim peke yake ameiandika Hadith ya Abi Musa kutoka kwa Nabii (s.a.w.w.): “Walio bora katika wanawake wa ulimwenguni ni wanne.”29 Na hakuna athari yoyote ya Hadith hii katika nakala za Sahih Muslim tulizonazo.

SAHIH MUSLIM NA HADITH: “MAHDI, NA YEYE NI KATIKA KIZAZI CHA FATIMAH”

A

mepokea al-Mutaqiy al-Hindiy kutoka katika Sahih Muslim na Sunan Abi Daud kauli yake (s.a.w.w.): “Mahdi ni katika kizazi changu kutoka katika kizazi cha Fatimah.”30 29 30

Mustadrakul-Hakim, Juz. 3, uk. 154. Kanzul-Ummal, Juz. 14, uk. 264 namba 38662. 39

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 39

7/5/2013 7:11:11 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

Na amesema Ibnu Hajar al-Haythamiy katika SawaiqulMuhriqah: Na miongoni mwa hayo ni yale ambayo ameyapokea Muslim, Abu Daud, an-Nasaiy, Ibn Majah, al-Bayhaqiy na wengineo: “Mahdi anatokana na kizazi changu kutoka katika kizazi cha Fatimah.”31- Na hatujaiona hadithi hiyo katika Sahih Muslim licha ya kuitafuta sana na kwa umakini.

MAARIF IBN QUTAYBAH NA HABARI YA FATIMAH KUMPOROMOSHA MUHSIN

A

mepokea Ibn Shahar Aashub katika faslu inayosema: ‘Pambo la Fatimah na historia yake.’Amesema: “Watoto wake ni Hasan, Husein na Muhsin aliyeporomoka, na katika kitabu Maarif cha Qutaybah ni kwamba Muhsin aliharibika kutokana na mbinyo mkali wa uadui, na Zainabu na Ummu Kulthum.”32 Na amesema Abu Abdullah Muhammad bin Yusuf bin Muhammad al-Qarshiy al-Kanjiy Ashafiiy aliyeuawa mwaka 658 Hijiria, katika kitabu Kifayatut-Talib FiiManaqib Ali bin Abi Talib: “…. Na akaongezea juu yamaneno ya jamhuri, akasema: Hakika Fatimah (as) aliporomosha mimba ya mtoto wa kiume baada ya (kufariki) Nabii (s.a.w.w.), Mtume wa Mwenyezi Mungu alikuwa alishampa jina la Muhsin, na jambo 31 32

Swawiqul-Muhriqah , uk. 163, chapa ya maktabatul-Qahirah ya mwaka 1385. Al-Manaqib cha Ibn Shahar Ashub chapa ya Beirut ya Daarul- Adhuwaa Juz. 3, uk. 407. 40

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 40

7/5/2013 7:11:11 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

hili halijapatikana kwa yeyote kati ya watu wenye kunukuu isipokuwa kwa Abdullah bin Qutaibah.33 Lakini katika chapa ya Maarif imeandikwa: Wakati wakutaja watoto wa Ali bin Abu Talib: Na ama Muhsin bin Ali alifariki akiwa mdogo.”34

SAWAIQUL-MUHRIQAH NA HADITH YA: “KUMTAJA ALI NI IBADA.”

H

akika kitabu Sawaiqul-Muhriqah kilichotungwa na Ahmad bin Hajar al-Haythamiy al-Makiy aliyezaliwa mwaka 899 na kufariki mwaka 974 Hijiria, kilichochapishwa mwaka 1312 A.H. Misri, kilichopigwa chapa na al-Maymaniyah, katika kitabu hicho imo Hadith hiyo (Kumtaja Ali ni ibada) katika ukurasa wa 74 mstari wa 34. Amepokea Daylamiy kutoka kwa Aisha kwamba Nabii (s.a.w.w.) amesema: “Mbora wa ndugu zangu ni Ali na mbora wa ami zangu ni Hamza, kumtaja Ali ni ibada.” Lakini katika chapa ambayo ameihakiki Abdul-Wahab Abdu Latif mwaka 1385 Hijiria, hadithi hiyo imepotoshwa, na yafuatayo ndio maelezo yaliyokuja katika chapa hiyo:

“Amepokea Daylamiy kutoka kwa Aisha kwamba Nabii (s.a.w.w.) alisema: Mbora wa ndugu zangu ni Ali na mbora wa ami zangu ni Hamza.”35 (kipande cha “kumtaja Ali ni ibada,” ameacha kukinukuu). Kanzul-Ummal, Juz. 14, uk. 264 namba 38662. Al-Maarif , uk. 122 Daarul- Kutubi al-Ilimiyah, Beirut ya mwaka 1407. 35 Tazama ukurasa 124, Msitari wa mwisho. 33 34

41

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 41

7/5/2013 7:11:11 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

SAWAIQUL-MUHRIQAH NA HADITH YA: “ALI ALIKUWA NA FADHILA KUMI NA NANE”

K

atika chapa ya al-Maymaniyah, ukurasa wa 76 mstari 14 kuna Hadith ifuatayo: Na amepokea Ibn Asakir kutoka kwake, amesema: “Hazijateremka (Aya) kumhusu yeyote katika kitabu cha Mwenyezi Mungu kama zilivyoteremka kwa Ali.” Na amepokea kutoka kwake vile vile kuwa amesema: “Zimeshuka Aya 300 kumhusu Ali.” Na Tabaraniy amepokea kutoka kwake kuwa amesema: “Ali alikuwa na fadhila kumi na nane ambazo hakuna yeyote mwingine aliyekuwa nazo katika ummah huu.” Na amepokea Abu Ya’liy kutoka kwa Abu Huraira ..hadi mwisho. Lakini maelezo hayo tuliyoyanukuu yamepotoshwa katika chapa ya pili, ambamo imekuja Hadith katika ukurasa wa 127 mstari wa 12 kama ifuatavyo: Amepokea Ibn Asakir kutoka kwake, amesema: “Hazijateremka (Aya) kumhusu yeyote katika kitabu cha Mwenyezi Mungu kama zilivyoteremka kwa Ali.” Na amepokea kutoka kwake vile vile kuwa amesema: “Zimeshuka Aya 300 kumhusu Ali.” Na amepokea Abu Ya’liy kutoka kwa Abu Huraira … hadi mwisho. Unaona mwenyewe kauli yake: “Ali alikuwa na fadhila kumi na nane ambazo hakuna yeyote aliyekuwa nazo katika umma huu” imeondolewa kabisa.

42

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 42

7/5/2013 7:11:11 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

UPOTOSHAJI KATIKA DIWANI ZA WASHAIRI

H

akika upotoshaji una aina mbalimbali, na katika vigawanyo vyake ni kupotosha kaswida za washairi wa Kishia katika kuwasifu Maimam wa Ahlul-Bait (as), na sisi tunataja kwa haraka haraka kutokea kwa upotoshaji huo katika diwani ya Washairi wa Kishia ambao kaswida zao zilikuwa zina mvumo mpana katika zama zilizopita, napengine kaswida kadhaa kati ya hizo zilikuwa na athari katika diwani yote katika kuathiri hisia na kuangazia akili na kukusanya rai ya watu dhidi ya madhalimu. 1. Upotoshaji katika diwani ya al-Kumait: Na hii ndio kaswida ya mshairi bingwa al-Kumait (aliyezaliwa mwaka 60 Hijiria na kufariki mwaka 126 Hijiria) ambayo mwanzo wake ni: “Amezuia juu ya jicho lako usingizi wa fofofo, na huzuni inatiririsha machozi.” Mkono wa wachapishaji usio na uaminifu ulifanya uharibifu katika chapa yake kwa kuvunja uaminifu wa kielimu kwa kupunguza kiasi kikubwa ambacho hakiwezi kupuuzwa. Mhakiki Aminiy amesema: “Imefika wakati kwa mkono wa upembuzi kuondoa pazia katika jinai hii iliyofichikana, hakika kaswida hii iliyochapishwa huko Leiden mwaka 1904 ina beti 536. Na ile chapa iliyoshereheshwa na kalamu ya Ustadh Muhammad Shakir ina beti 560, na ile chapa iliyoshereheshwa na Ustadh Rafi’iy ina beti 458.” Kisha akataja sehemu zilizopotoshwa katika chapa hii.36

36

ifayatut-Talib Fii Manaqib Ali bin Abu Talib, katika faslu ya kutaja idadi ya K watoto wake Uk. 372 chapa ya Beirut, mwaka 1413 Hijiria. 43

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 43

7/5/2013 7:11:11 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

2. Upotoshaji katika diwani ya Hasan: Na anasema kuhusu diwani ya Hasan: “Hakika Hasan ana kaswida nyingi za kumhusu Kiongozi wetu Amirul-Muuminina (as) za kumsifu, isipokuwa mkono usio na uaminifu haukufanya uaminifu wakati ulipoigusa diwani yake, hivyo ukapotosha maneno kwa kuyatoa sehemu yake, na hivyo diwani ya Hasan ikachezewa kama zilivyochezewa nyinginezo miongoni mwa diwani, vitabu na kamusi ambazo zimeondolewa humo sifa za Ahlul-Bait (as) na fadhila zao na utajo mzuri wa wafuasi wao, kama vile walivyopotosha diwani ya Farazdaq ambaye wameondoa katika diwani yake shairi lake mashuhuri la mimiyah alilolisoma kumsifu Maulana Imam Zainul-Abidin (as), licha ya kwamba mchapishaji ameliashiria katika utangulizi wa ufafanuzi wa diwani yake, na limetajwa sana ndani ya vitabu na enklopedia. Na mfano mwingine ni diwani ya Kumait, hakika nayo beti zake zimepotoshwa kama ambavyo zimeongezwa humo beti nyingine. Na pia diwani ya kiongozi wa washairi, Abi Farasi, pia diwani ya Kashajim ambayo humo wameondoa sehemu muhimu inayohusu maombolezo ya Bwana wetu, Imam wetu na Shahidi mjukuu wa Mtume (s.a.w.w.). Na pia kitabu al-Maarif cha Ibnu Qutaybah ambacho humo mpotoshaji ameongeza yale yaliyotakiwa na matamanio yake, naamepunguza yale yanayoafikiana na njama zake, hiyo ni kwa ushahidi wa vitabu vilivyonukuu kutoka kwake baada yake. Na pia vitabu vinginevyo ambavyo vimefanyiwa uharibifu na wachapishaji au vimefanyiwa upotoshaji wakati wa kunukuu.37 37

Al-Maarif , uk. 122 Daarul- Kutubi al-Ilimiyah, Beirut ya mwaka 1407. 44

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 44

7/5/2013 7:11:11 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

ni kwa ushahidi wa vitabu vilivyonukuu kutoka kwake baada yake.Na pia vitabu vinginevyo ambavyo3.vimefanyiwa uharibifu wachapishaji au vimefanyiwa Upotoshaji katikanaDiwani ya Abi Tamam: upotoshaji wakati wa kunukuu.37

Abu Tamam ni Habib bin Aus, mmoja kati ya viongozi wa Imamiya kamaDiwani alivyosema al-Jahidh, 3. Upotoshaji katika ya Abi Tamam:38 na ni wa pekee kati ya masheikh waAus, Kishia katika fasihi katika zama zakama mwanzo, Abu Tamam ni Habib bin mmoja kati ya viongozi wa Imamiya alivyosema al38ni mwenye diwani maarufu, na humo ana shairi lake linalJahidh, na ni wa pekee kati ya masheikh wa Kishia katika fasihi katika zama za mwanzo, ni mwenyeoishia diwaninamaarufu, na humoana lake linaloishia herufi Rau, ambalo shairi utangulizi wake ni: na herufi Rau,ambalo

utangulizi wake ni:

‫أظبـــيـة حــيث استنت الكثب العـــــفر * رويدك ال يغــــتـــالك اللوم والـــزجـر‬ ‫أســـري حــــــذارا لـــــم يقــــيدك ردة * فــــيحـــسر مـــاء من محاسنك الھذر‬ Na imekuja humo kauli yake:

Na imekuja humo kauli yake:

‫ويــوم الغدير استوضح الحق أھله * بضــحيآء ال فيھا حجاب وال ستر‬

‫ويوم الغدير استوضح الحق أھله بضيآء ال فيھا حجاب و‬ ‫ال ستر‬

An-Najashiy amenukuu kutoka kwa rafiki yake Ahmad bin Husein al-Ghadhairiy kwamba, yeye aliiona nakala ya kale yadiwani ya ushairi wa Abi Tamamambayo iliandikwa katika zama zake au karibu na zama zake, na humo kulikuwa kuna kaswida ambayo inataja 39 Maimamu hadi kwa Abu Ja’far wa pili, kwa sababukwa yeyerafiki alifariki katika zama zake. An-Najashiy amenukuu kutoka yake Ahmad bin Lakini sasa katika diwani yake hakunakaswida yoyote inayoelezea juu ya ufuasi wake na itikadi Huseinileal-Ghadhairiy kwamba, yeye aliiona nakala ya kale yake, isipokuwa inayoishia na herufi Rau.

yadiwani ya ushairi wa Abi Tamam ambayo iliandikwa katika

Mhakiki al-Amini amesema: “Hakika mkono usio na uaminifu katika kuchapisha vitabu, zama zakehizo au wakati karibuwanakuipeleka zama zake, humo kulikuwa kuna umeondoa kaswida diwanina katika uchapishaji, kama ulivyofanya kaswida ambayo Maimamu hadi kwa Abuwakati Ja’farwa wakuchapisha,au pili, katikadiwani nyinginezo, au inataja ni kwamba haikumfikia (mchapishaji) kilichochapishwa ni muhtasari wa Abil-Alaai Vipi39isiwe hivyo wakati an-Najashiy kwa sababu yeye alifariki katikaal-Ma’ariy. zama zake. Lakini sasa katika anaeleza kuwa ana mashairi mengi juu ya Ahlul-Bait.Hii ni mifano tu katika upotoshaji diwani yake hakuna kaswida yoyote inayoelezea ambao umezikumba diwani za washairi wa Kishia na nyaraka zao. juu ya ufuasi

wake na itikadi yake, isipokuwa ile inayoishia na herufi Rau.

4. Upotoshaji katika Ruhul-Maaniy al-Alusiy: Mhakiki al-Amini amesema: cha “Hakika mkono usio na ua-

minifu katika kuchapisha vitabu, umeondoa kaswida hizo Na kati ya upotoshaji mbaya zaidi ni kuondoa sehemu maalumu kutoka kwenye kitabu, kwa sababu wakati tu haiafikiani na itikadi ya mchapishaji, na ikiwa unamashaka na haya, wa kuipeleka diwani katika uchapishaji, kama ulivyo- soma tunayokusomea katika kitendo cha Nu’man al-Alusiy mtoto wa Allamah al-Araaq Sheikh katika diwani nyinginezo, Mahmudfanya al-Alusiy mtunzi wa tafsiri Ruhul-Maaniy.au ni kwamba haikumfikia 38 39

Tazama ukurasa 124, Msitari wa mwisho. Al-Ghadir Juz. 2, uk. 181.

37

Al-Ghadir Juz. 2, uk. 42. Rijalun-Najashiy, Namba 365. 39 Rijalun-Najashiy, Namba 365. 38

45

28 08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 45

7/5/2013 7:11:11 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

(mchapishaji) wakati wa kuchapisha, au kilichochapishwa ni muhtasari wa Abil-Alaai al-Ma’ariy. Vipi isiwe hivyo wakati an-Najashiy anaeleza kuwa ana mashairi mengi juu ya AhlulBait. Hii ni mifano tu katika upotoshaji ambao umezikumba diwani za washairi wa Kishia na nyaraka zao. 4. Upotoshaji katika Ruhul-Maaniy cha al-Alusiy: Na kati ya upotoshaji mbaya zaidi ni kuondoa sehemu maalumu kutoka kwenye kitabu, kwa sababu tu haiafikiani na itikadi ya mchapishaji, na ikiwa unamashaka na haya, soma tunayokusomea katika kitendo cha Nu’man al-Alusiy mtoto wa Allamah al-Araaq Sheikh Mahmud al-Alusiy mtunzi wa tafsiri Ruhul-Maaniy. Mtunzi wakitabu Rudud Alaa Shubhati as-Salafiyyah anasema: “Hakika upotoshaji na kuondoa Hadith ni jambo la Masalafi na ndio dini yao, hakika Nu’man al-Alusiy amepotosha tafsiri ya mzazi wake mtukufu Allamah al-AraaqSheikh Mahmud al-Alusiy (Ruhul-Ma’aniy), na kama si upotoshaji wake ingekuwa ni tafsiri ya kipekee na yenye kukusanya mambo. Ama kuhusu upotoshaji kwa kuondoa na kufuta ibara na Hadith, zilizozungumzia wala usiwe na shaka. Wamechapisha kitabu al-Mughniy cha Ibn Quddamah al-Hanbaliy wakaondoa humo maudhui ya Istighathah (kuomba msaada), na wakachapisha Sharhu ya Sahih Muslim na humo wakaondoa Hadith zinazozungumzia sifa za Mwenyezi Mungu. Haya ndio tuliyoyakuta miongoni mwa hiyana zao za kielimu na ubaya wa uovu wa vitendo vyao, na Mwenyezi Mungu atawahesabu kwa ubaya wa vitendo vyao, na Yeye anaviona hata kama vyafichikana kwetu.”40 40

Ar-Rududu Alaa Shubhaati as-Salafiyyah: 249. 46

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 46

7/5/2013 7:11:11 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

Na mwishoni mwa makala ya al-Kauthariy ya Ahmad Khairiy kuna kauli yake kuhusu41 Nu’man: “Naye si mwaminifu juu ya tafsiri ya mzazi wake, na lau angekabiliana na yeyote mwenye nakala iliyohifadhiwa leo katika maktaba ya Raghib Pasha huko Istanbul, nayo ninakala aliyoitoa zawadi kwa Sultan Abdul–Hamid Khaan, angepata lenye kumpa matumaini.”

ۖ‫ت‬ ِ ‫ضاعُوا الص َ​َّال َة َوا َّت َبعُوا ال َّش َھ َوا‬ َ َ‫ف ِمنْ َبعْ ِد ِھ ْم َخ ْلفٌ أ‬ َ ‫َف َخ َل‬ ‫ف َي ْل َق ْو َن َغ ًّيا‬ َ ‫َف َس ْو‬ “Wakafuata baadae wazawa wabaya walioiacha Swala na wakafuata matamanio. Basi watakujakuta malipo ya ubaya.” (Sura Maryam: 59).

41

Rijalun-Najashiy, Namba 365. 47

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 47

7/5/2013 7:11:11 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

KUPOTOSHA SUNNA ILI KUWA MBALI NA MASHIA

H

akika Sharia ya Kiislam ni mwisho wa sharia na Nabii wake ni hitimisho la Manabii, na Kitabu chake ni mwisho wa vitabu, na sharia yake ni yenye kudumu, halali ya Muhammad ni halali hadi Siku ya Kiyama na haramu yake ni haramu hadi Siku ya Kiyama bila ya tofauti baina ya wajibu na haramu, Sunnah na ibada, hivyo si haki ya Mwislamu kubadili hukumu zake katika nyanja yoyote ile. Lakini tunaona kwamba baadhi ya Masunni wamependelea kuacha Sunnah ya Nabii na wakaiita kuwa ni Bidaa kwa hoja ya kwamba, baadhi ya watu kati ya Waislamu wanajilazimisha kuifanyia kazi, hivyo ili kujiepusha kufanana nao wakaamua kuchukua Bidaa na kuacha Sunnah. Hebu sasa tutaje mifano ya aina hii ya Bidaa: 1. Kusawazisha kaburi ni Sunnah inayoachwa kwa sababu ni alama ya Mashia: Amesema Sheikh Muhammad bin Abdur-Rahman adDamashqiy:“Sunnah katika kaburi ni kulisawazisha, nayo ni bora kwa mujibu wa madhehebu ya Shafi.”42 Amesema Abu Hanifa, Malik na Ahmad: “Kulinyanyua ni bora kwa sababu kulisawazisha imekuwa ni alama ya Mashia.” Amesema al-Ghazaliy na al-Mawaridiy: “Hakika kusawazisha kaburi ndio sharia, lakini Mashia walipoifanya kuwa ni alama yao tukaachana nayo na tukahamia kwenye kulinyanyua.” 42

d-Damashqiy: Katika Rahmatul-Umma Fii Ikhtilafil-Aimmah Juz. 1, uk. 88, A katika Sharhu ya al-Mizani cha Shaaraniy. 48

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 48

7/5/2013 7:11:11 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

Amesema mtunzi waal-Hidayah wa Kihanafi: “Hakika sharia ni kuvaa pete mkono wa kulia lakini Mashia walipoifanya kuwa ni alama yao basi tukaifanya iwe katika mkono wa kushoto.”43 Na amesema Raafi’i: “Hakika Nabii (s.a.w.w.) alisawazisha kaburi la mtoto wake Ibrahim, na imepokewa kutoka kwa Qasim bin Muhammad kuwa alisema: Nimeona kaburi la Nabii, la Abu Bakr na la Umar yakiwa yamesawazishwa.” Na amesema Ibn Abi Huraira: “Hakika ilivyobora hivi sasa ni kuacha kusawazisha na kwenda kwenye kunyanyua, kwa sababu kusawazisha imekuwa ni alama ya Mashia, ni bora kuwakhalifu na kuihifadhi maiti na watu wake kuliko kutuhumiwa kwa Bidaa.” Na mfano wake ni yale yaliyoelezwa kwamba kusoma Bismillahi kwa jahara inapokuwa ni alama ya Mashia basi ni Sunnah kutosoma kwa jahara ili kuwakhalifu. Na wakatoa hojakwamba Nabii (s.a.w.w.) alikuwa anasimama linapoonekana jeneza, mara akapewa habari kwamba Mayahudi wanafanya hivyo, ndipo akaacha kusimama baada ya hapo. Na mwelekeo huu ndio aliouchukua na kuelemea hukoSheikh Abu Muhammad, na akafuatwa na al-Qadhi Rawiyaniy, lakini jamhuri wako na madhehebu ya awali. Wakasema: “Kama tutaacha yaliyothibiti katika Sunnah na kufuata baadhi ya Bidaa hilo litatupelekea kuacha Sunnah nyingi sana, na tunapokimbilia katika jambo, kukimbilia kwetu kunalifanya lisihesabiwe kuwa ni alama ya wanabidaa.”44 43 44

Al-Ghadir Juz. 10, uk. 209. al-Aziz Fii Sharhil-Wajiz, Juz. 2, uk. 453. 49

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 49

7/5/2013 7:11:11 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

2. Kusoma Bismillah kwa jahara: Imam Raziy amesema: “Amepokea al-Bayhaqiy kutoka kwa Abu Huraira, amesema: ‘Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alikuwa anasoma Bismillahi Rahman Rahim katika Sala kwa jahara.’ Na Ali bin Abu Talib (r.a) alikuwa anasema: ‘Eee ambaye utajo wake ni utukufu kwa wenye kumtaja.’ Itafaa vipi kwa mwenye akili kuisoma kwa siri katika hali kama hii? Na Mashia wamesema: Sunnah ni kusoma Bismillahi kwa jahara, sawa iwe katika Sala za jahara au za kusoma kwa siri, lakini jamhuri ya wanachuoni wanawakhalifu wao – aliendelea hadi akasema: Hakika Ali alikuwa anazidisha kiasi katika kusoma Bismillahi kwa jahara, hivyo dola ilipofika kwa Bani Umaiyyah na wao wakazidisha kiasi katika kukataza kuisoma kwa jahara ili kuzima nyendo za Ali (r.a).”45 3. Kumswalia muumini peke yake ni Sunnah inayokataliwa: Zamakhshariy amesema katika tafsiri ya kauli yake (swt):

ۚ ِّ‫ون َع َلى ال َّن ِبي‬ َ ُّ‫ُصل‬ َ ‫ﷲ َو َم َال ِئ َك َت ُه ي‬ َ َّ َّ‫إِن‬ “Hakika Mwenyezi Mungu na malaika Wake wanamswalia Nabii...” (Sura Ahzab: 56).

‫صلِّي َع َل ْي ُك ْم‬ َ ‫ھ َُو الَّذِي ُي‬

“Kama utasema: Utasemaje katika kumswalia asiyekuwa yeye? Nasema: Kipimoni kwamba inajuzu kumswalia kila muumini kwa kauli Yake (swt): 45

Mafatihul- Ghayb, Juz. 1, uk. 205 – 206. 50

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 50

7/5/2013 7:11:12 PM


ُّ‫ُصل‬ ۚ ِّ‫ي‬Upotoshaji ‫ون َع َلى ال َّن ِب‬ ‫و َم َال ِئ َك َت‬Turathi َ Dhahiri َ ‫ ُه ي‬katika َ ‫ﷲ‬ َ َّ َّ‫إِن‬ ‫ُصلِّي َع َل ْي ُك ْم‬ َ ‫ھ َُو الَّذِي ي‬ “Yeye Ndiye anayewaswalia...”

(Sura Ahzab33:43)

Na kauli yake (swt):

َّ ‫َع َسى‬ ‫ﷲ َغفُو ٌر َرحِي ٌم‬ َ ‫ﷲُ أَنْ َي ُت‬ َ َّ َّ‫وب َع َلي ِْھ ْم ۚ إِن‬ “Na uwaombee rehema. Hakika maombi yako ni utulivu kwao...” (Sura Tawba: 102).

Na kauli yake (s.a.w.w.): ‘Eee Mwenyezi Mungu waswalie Aali Abi Aufiy.’ Lakini Maulamaa wanamaelezo katika hayo, nayo ni kwamba hakika ikiwa ni katika njia ya kufuata, kama vile kauli yako: ‘Mwenyezi Mungu msalie Nabii na Aali zake’ basi hakuna maneno katika hilo, ama kumsalia peke yake yeyote miongoni mwa Ahlul-Bait wake kama ambavyo tunamsalia yeye (s.a.w.w.) peke yake, kufanya hivyo ni makuruhu, kwa sababu kitendo hicho kimekuwa ni nembo ya kumtaja Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), na kwa sababu kufanya hivyo inapelekea kutuhumiwa kwa ushia.”46 Na katika kitabu Fat’hul-Bariy imeandikwa: “Kuna tofauti kuhusukumtolea salamu asiyekuwa Nabii baada ya kuafikiana juu ya uhalali wake kisheria awapo hai, ikasemekana kuwa inaruhusiwa bila sharti lolote, na ikesemekana kuwa inaruhusiwa kwa kufuata na si kwa peke yake kwa sababau kufanya hivyo imekuwa ni alama ya Mashia. Na amenukuu hilian-Nawawiy kutoka kwa Sheikh Abi Muhammad al-Juwayniy.”47 46 47

al-Kashaaf, Juz. 2, uk. 549. Fat’hul-Bariy, Juz. 1, uk: 14. 51

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 51

7/5/2013 7:11:12 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

Na maana yake ni kwamba hakupata kigezo cha kisharia kinachohalalisha kuacha yale yaliyoruhusiwa na Uislamu isipokuwa kitendo cha Mashia kutekeleza Sunnah ya Uislamu, na lau likisihi hilo basi italazimu kwa msemaji kuacha faradhi na Sunnah ambazo wanazifanya Mashia. 4. Kuacha Sunna inapokuwa alama ya Mashia: Ibn Taymiya amesema – katika kufafanua hali ya kufanana na Mashia: “Na hapa ameona aliyeona miongoni mwa wanachuoni kwamba inapasa kuacha baadhi ya Sunnah inapokuwa ni alama yao, hata kama kwa sababu hiyo haitakuwa kuacha ni wajibu, lakini katika kudhihirisha kushabihiana nao kutapelekea kutojulikana Sunni ni yupi na Shia ni yupi, na masilahi yanayopatikana katika kujitofautisha na wao kwakuwahama na kuwakhalifu wao ni bora zaidi kuliko masilahi ya kutekeleza Sunnah hii.”48 5. Kuacha kufanya mema na kufanya maatam siku ya Ashura: Ameeleza al-Barsawiy kutoka katika kitabu Uqud-Durar WalLaaliy Wafadhilis-Shuhuri Wallayaaliy cha Sheikh ShihabudDin mashuhuri kwajina la Rassam: Sehemu ya tatu: Kilicho Sunnah siku hiyo- Siku ya Ashura –ni kufanya kheri, kutoa sadaka, kufunga, nyuradi na visivyokuwa hivyo, na haipasi kwa muumini kushabihiana na Yazid aliyelaaniwa katika baadhi ya vitendo, na pia na Mashia na Khawarji vile vile. Yaani asiifanye siku hiyo kuwa ni siku ya Sikukuu au maombolezo, hivyo mwenye kupaka wanja siku ya Ashura ameshajifananisha na Yazid aliyelaaniwa na kaumu yake, ingawa kupaka wanja katika siku hiyo katika asili ni sahihi, 48

Minhajus-Sunnah Juz. 2, uk. 143. 52

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 52

7/5/2013 7:11:12 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

kwani hakika kuacha Sunnah ni Sunnah ikiwa itakuwa ni alama ya wanabidaa, kama vile kuvaa pete mkono wa kulia, hakika ni Sunnah katika asili, lakini ilipokuwa ni alama ya wanabidaa na madhalimu ikawa ni Sunnah ivaliwe katika kidole cha mkono wa kushoto katika zama zetu hizi kama ilivyo katika ufafanuzi wa al-Qahastaaniy. Na mwenye kusoma katika siku za Ashura na mwanzo wa Muharram mauaji ya Husein (r.a) basi ameshajifananisha na Mashia hususan ikiwa ni kwa matamshi yenye kuwahuzunisha wasikilizaji, na katika Karahiyatul-Qahastaaniy imeandikwa: “Lau akitaka kutaja mauaji ya Husein inapasa kwanza ataje mauaji ya Masahaba wote ili asifanane na Mashia.” al-Ghazaliy amesema: “Ni haramu kwa mtoa mawaidha na mwingineo kusimulia mauaji ya Husein na kisa chake na yaliyotokea baina ya Masahaba miongoni mwa ugomvi na mizozo, kwani inachochea chuki kwa Masahaba na kuwatuhumu, na wao ni alama ya dini, na yaliyotokea baina yao katika ugomvi basi yanachukuliwa katika mapito sahihi na huenda hayo ni katika makosa ya ijitihadi na wala si kutaka madaraka na dunia kama ambavyo haifichikani.”49 Lakini nini thamani ya ijitihadi, katika kisingizio cha kumwaga damu ya maelfu ya Waislamu katika vita vya Jamal na Siffin!

ِ‫ُون َمنْ أَصْ َحابُ الص َِّراط‬ َ ‫قُ ْل ُك ٌّل ُم َت َربِّصٌ َف َت َر َّبصُوا ۖ َف َس َتعْ َلم‬ ‫الس َِّويِّ َو َم ِن اھْ َتدَ ٰى‬ “Sema: Kila mmoja anangoja; basi ngojeni punde mtajua nani mwenye njia sawa na nani aliyeongoka.” (Sura Twaha: 135). 49

Ruhul-Bayaani, Juz. 4, uk. 142. 53

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 53

7/5/2013 7:11:12 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

UDANGANYIFU NA ONGEZEKO LAKE KUBWA KATIKA HAZINA

H

akika upotoshaji kwa maana ya kugeuza ukweli na kudhihirisha kisichokuwa cha ukweli ni alama ya watu wengi miongoni mwa wasimulizi wa hadithi na wapokezi ambao majina yao na upokezi wao umejaza vitabu vya wapokezi wa Hadith. Na huyu hapa nial-Hakim anataja majina ya wasimulizi wakubwa wa hadithi waliopokea kutoka kwa watu bila kusikia kutoka kwa watu hao lakini wao wanadai wamesikia maneno hayo kutoka kwao, anasema: “Na atambue mwenye Hadith kwamba Hasan hajasikia kutoka kwa Abu Huraira wala kutoka kwa Jabir wala kutoka kwa Ibn Umar wala kutoka kwa Ibn Abbas chochote kamwe, na kwamba al-A’amash hajasikia kutoka kwa Anasi, as-Shaabiy hajasikia kutoka kwa Swahaba yoyote isipokuwa Anas, na kwamba As-Shaabiy hajasikia kutoka kwa Aisha wala kutoka kwa Abdullah bin Mas’ud wala kutoka kwa Usamah bin Zaid wala kutoka kwa Ali bali amemuona katika ndoto, wala kutoka kwa Mua’adh bin Jabal wala kutoka kwa Zaid bin Thabiti, na kwamba Qatadah hajasikia kutoka kwa Swahaba yeyote isipokuwa Anas, na kwamba Hadith nyingi za Amru bin Dinaar ni kutoka kwa Masahaba wasiojulikana, na Hadith nyingi za Makuhul ni kutoka kwa Sahaba hewa, na kwamba hayo yote hayafahamiki isipokuwa kwa wenye kuhifadhi Hadith.”50

Hakika udanganyifu ni aina ya uongo na uzushi, al-Hakim anapokea kutoka kwa Hamad bin Zaid kwamba anase50

Maarifatul-Ulumil-Hadith, uk. 111 Na 103. 54

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 54

7/5/2013 7:11:12 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

ma: “Mdanganyifu anatosheka kwa ambayo hajapewa, inanukuliwa kutoka kwa Abdu Swamad bin Abdil-Warith kwamba anasimulia kutoka kwa baba yake kuwa amesema: ‘Udanganyifu ni udhalili.’ Suleiman amesema: ‘Udanganyifu, ghushi, kiburi, hadaa na uongo utafufuliwa Siku ya Kiyama katika sehemu moja.’”51 Na baada ya kutaja vigawanyo vya udanganyifu na majina ya makundi ya wadanganyifu, amesema na haya ni matamshi yake: “Na amesema Abu Abdullah: Nimeshataja namna sita za aina za udanganyifu ili atafakari mwenye kutafuta elimu hii, na apime wingi kwa uchache, nasikupendezwa kutaja majina ya wenye kudanganya kati ya Maimam wa Waislam ili kuzilinda Hadith na wapokezi wake, isipokuwa mimi naashiria kwa ujumla ili kwa ujumla huo mtafiti aweze kuwajua Maimam waliodanganya na wale ambao hawakudanganya kwa kumcha Mungu.”52 Pamoja na kwamba Dhahabiy ni kati ya wenye kuzipa Hadith na wasimulizi wa Hadith heshima makhusus, na anajaribu kuwasitiri wengi kwa aibu zao na tuhuma zao, lakini pamoja na hayo ametunga kitabu juu ya madhaifu, ambapo imekuja humo majina ya watu 7855 ambao ni wapokezi na wasimulizi wa hadithi walio dhaifu ambao si hoja Hadithi yao na wala haichukuliwi, na inatosha katika hayo kurejea kwenye kitabu chake al-Mughaniy Fii Dhu’afai kilichohakikiwa na Abi Zahra Hazim al-Qadhiy. Ama kuhusiana na waongo na wadanganyifu ambao wameelezwa wazi wazi na Maimam wa uchambuzi wa Hadith kwa sifa zao na uongo wao, ni wengi mno, Allammah al51 52

Maarifatul-Ulumil-Hadith, uk. 111. Maarifatul-Ulumil-Hadith, uk. 111. 55

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 55

7/5/2013 7:11:12 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

Aminiy amekusanya majina 700 ya waongo na wadanganyifu katika rejea ya kitabu al-Ghadir.53 Ibn Hiban ananukuu katika kitabu chake al-Majuruhina Minal-Muhadithina Wadhu’afai Wal-Maturukina kutoka kwa Yahya bin Mu’in amesema: “Tumeandika juu ya waongo na tukawasha tanuri tukaoka kwalo mkate ulioiva, na alipofariki Yahya bin Mu’in katika mji wa Mtume (s.a.w.w.) na akabebwa katika jeneza mara niliona wakinadi: ‘Enyi watu huyu ni aliyejitolea katika uongo katika kumsingizia Mtume wa Mwenyezi Mungu katika kadha wa kadhaa mwaka mzima.’”54 Na haya tuliyoyataja ndio ambayo yametoka katika kalamu ya hawa kwa bahati, na lau kama wangekuwa wanakusudia kuondoa pazia kikweli kweli ungetambua kwamba uongo na udanganyifu ni hali ya wengi kati ya wapokezi na wasimulizi wa Hadith isipokuwa ni kwamba kupenda kusitiri kumezuia kubaini ukweli. Dhahbiy amesema: “Kisha inajulikana kwamba ni lazima kumlinda mpokezi na kumsitiri…. na lau ningefungua katika nafsi yangu hali ya kufanya sahali katika mlango huu, wasingesalimika kwangu isipokuwa wachache, ambapo wengi hawajui wanayoyapokea wala hawajui jambo hili, bali walisikiwa udogoni mwao na wakafanywa hoja katika daraja la sanad yao ukubwani mwao, tegemeo ni kwa waliowasoma, na kwa aliyethibitisha kusikiwa kwao, kama ilivyozoeleka katika elimu ya Hadithi.”55 Na anasema vile vile katika kitabu Ma’arifat RuwatilMutakalim FiiHim: “Lau tukifungua mlango huu wa “JarhulMaarifatul-Ulumil-Hadith, uk. 111 Na 103. Al-Majuruhina cha Ibn Hiban uk. 56. 55 Mizanul- I’itidaal Juz. 1 Uk. 4. 53 54

56

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 56

7/5/2013 7:11:12 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

Aimmah” katika nafsi zetu, wataingia humo wengi kati ya Masahaba, Tabiina na Maimam, kwani baadhi ya Masahaba waliwakufurisha wenzao.56 Kama al-Hakim An-Nisaburiy anaficha majina ya waliodanganya miongoni mwa Maimam wa Waislam kwa ajili ya kulinda Hadith na kutaka kumlinda mpokezi na kumsitiri, basi mtafiti mkubwa mfano wa Dhahbiy hawezi kufichua ukweli au hawezi kufanya sahali katika mlango huu- kulingana na maneno yake – na je, kuna uaminifu wowote unaobakia katika Sihahi, Sanad na Sunan? Haya na yale ndio ambayo yanamlazimu mtafiti kusoma historia ya Hadith upya na kuweka vidhibiti maalum katika kupambanua Hadith za Mtume na Sunnah ya Abil-Qasim (s.a.w.w.) na yale yaliyozuliwa na kutiwa katika ulimi wake. Wakutegemewa ni Mwenyezi Mungu.

‫ِين آ َم ُنوا إِنْ َجا َء ُك ْم َفاسِ ٌق ِب َن َبإٍ َف َت َب َّي ُنوا أَنْ ُتصِ يبُوا‬ َ ‫َيا أَ ُّي َھا الَّذ‬ ‫ِين‬ َ ‫َق ْومًا ِب َج َھا َل ٍة َف ُتصْ ِبحُوا َع َل ٰى َما َف َع ْل ُت ْم َنا ِدم‬ “Enyi ambao mmeamini! Akiwajia fasiki na habari yoyote, ichunguzeni, msije mkawasibu watu kwa kutojua, na mkawa wenye kujuta kwa mliyoyatenda.” (Sura Hujurat: 6).

56

Al-Ghadir Juz. 5, uk. 207 – 275. 57

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 57

7/5/2013 7:11:12 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION 1. Qur’an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Thelathini 2. Uharamisho wa Riba 3. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza 4. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili 5. Hekaya za Bahlul 6. Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) 7. Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.) 8. Hijab vazi Bora 9. Ukweli wa Shia Ithnaashari 10. Madhambi Makuu 11. Mbingu imenikirimu 12. Abdallah Ibn Saba 13. Khadijatul Kubra 14. Utumwa 15. Umakini katika Swala 16. Misingi ya Maarifa 17. Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia 18. Bilal wa Afrika 58

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 58

7/5/2013 7:11:12 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

19. Abudharr 20. Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu 21. Salman Farsi 22. Ammar Yasir 23. Qur’an na Hadithi 24. Elimu ya Nafsi 25. Yajue Madhehebu ya Shia 26. Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur’an Tukufu 27. Al-Wahda 28. Ponyo kutoka katika Qur’an. 29. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii 30. Mashukio ya Akhera 31. Al Amali 32. Dua Indal Ahlul Bayt 33. Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna. 34. Haki za wanawake katika Uislamu 35. Mwenyeezi Mungu na sifa zake 36. Kumswalia Mtume (s) 37. Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) 38. Adhana. 39 Upendo katika Ukristo na Uislamu 40. Tiba ya Maradhi ya Kimaadili 59

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 59

7/5/2013 7:11:12 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

41. Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu 42. Kupaka juu ya khofu 43. Kukusanya swala mbili 44. Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara 45. Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya 46. Kusujudu juu ya udongo 47. Kusherehekea Maulidi Ya Mtume (s) 48. Tarawehe 49. Malumbano baina ya Sunni na Shia 50. Kupunguza Swala safarini 51. Kufungua safarini 52. Umaasumu wa Manabii 53. Qur’an inatoa changamoto 54. as-Salaatu Khayrun Mina -’n Nawm 55. Uadilifu wa Masahaba 56. Dua e Kumayl 57. Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu 58. Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake 59. Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata 60. Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mtume Muhammad (s) 61. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza 62. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili 60

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 60

7/5/2013 7:11:12 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

63. Kuzuru Makaburi 64. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza 65. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili 66. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu 67. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne 68. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano 69. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita 70. Tujifunze Misingi Ya Dini 71. Sala ni Nguzo ya Dini 72. Mikesha Ya Peshawar 73. Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu 74. Ubora wa Imam ‘Ali Juu ya Maswahaba Na Ushia ndio njia iliyonyooka 75. Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake 76. Liqaa-u-llaah 77. Muhammad (s) Mtume wa Allah 78. Amani na Jihadi Katika Uislamu 79. Uislamu Ulienea Vipi? 80. Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) 61

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 61

7/5/2013 7:11:12 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

81. Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) 82. Urejeo (al-Raja’a ) 83. Mazingira 84. Utokezo (al - Badau) 85. Hukumu ya kujenga juu ya makaburi 86. Swala ya maiti na kumlilia maiti 87. Uislamu na Uwingi wa Dini 88. Mtoto mwema 89. Adabu za Sokoni 90. Johari za hekima kwa vijana 91. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza 92. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili 93. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu 94. Tawasali 95. Imam Mahdi katika Usunni na Ushia 96. Hukumu za Mgonjwa 97. Sadaka yenye kuendelea 98. Msahafu wa Imam Ali 99. Ngano ya kwamba Qur’ani imebadilishwa 62

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 62

7/5/2013 7:11:12 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

100. Idil Ghadiri 101. Kusoma sura zenye Sijda ya wajibu 102 Hukumu zinazomhusu mkuu wa kazi na Mfanyakazi 103. Huduma ya Afya katika Uislamu 104. Sunan an-Nabii 105. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza) 106. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili) 107. Shahiid Mfiadini 108. Kusalia Nabii (s.a.w) 109. Ujumbe - Sehemu ya Kwanza 110. Ujumbe - Sehemu ya Pili 111. Ujumbe - Sehemu ya Tatu 112. Ujumbe - Sehemu ya Nne 113. Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu 114. Hadithi ya Thaqalain 115. Maarifa ya Kiislamu 116. Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza 117. Ukweli uliopotea sehemu ya Pili 118. Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu 119. Ukweli uliopotea sehemu ya Nne 120. Ukweli uliopotea sehemu ya Tano 121. Johari zenye hekima kwa vijana 63

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 63

7/5/2013 7:11:12 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

122. Safari ya kuifuata Nuru 123. Fatima al-Zahra 124. Myahudi wa Kimataifa 125. Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi 126. Visa vya kweli sehemu ya Kwanza 127. Visa vya kweli sehemu ya Pili 128. Muhadhara wa Maulamaa 129. Mwanadamu na Mustakabali wake 130. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Kwanza) 131. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Pili) 132. Khairul Bariyyah 133. Uislamu na mafunzo ya kimalezi 134. Vijana ni Hazina ya Uislamu. 135. Yafaayo kijamii 136. Tabaruku 137. Taqiyya 138. Vikao vya furaha 139. Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje? 140. Visa vya wachamungu 141. Falsafa ya Dini 142. Azadari-Kuhuzunika na Kuomboleza 64

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 64

7/5/2013 7:11:12 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

143. Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah 144. Mtazamo Mpya - Wanawake katika Uislamu 145. Kuonekana kwa Allah 146. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza) 147. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili) 148. Ndugu na Jirani 149. Ushia ndani ya Usunni 150. Maswali na Majibu 151. Mafunzo ya hukmu za ibada 152. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 1 153 Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 2 154. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 3 155. Abu Huraira 156. Vipengee kadhaa katika Swala ya Jamaa na Msikiti. 157. Mazingatio kutoka katika Qur’an - Sehemu ya Kwanza 158. Mazingatio kutoka kaitka Qur’an - Sehemu ya Pili 159. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya kwanza 160. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya Pili 161. Qur’ani Tukufu – Pamoja na Tarjuma ya Kiswahili 162. Falsafa ya Mageuzi ya Imam Husein (a.s) 163. Amali za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani 164. Elimu ya Tiba za Kiislamu - Matibabu ya Maimamu 65

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 65

7/5/2013 7:11:12 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

165. Uislamu Safi 166. Majlisi za Imam Husein Majumbani 167. Mshumaa. 168. Uislam wa Shia 169. Amali za Makka 170. Amali za Madina 171. Asili ya Madhehebu katika Uislamu 172. Sira ya Imam Ali kuhusu Waasi 173. Ukweli uliofichika katika neno la Allah 174. Uislamu na Mifumo ya Uchumi 175. Umoja wa Kiislamu na Furaha 176. Mas’ala ya Kifiqhi 177. Jifunze kusoma Qur’ani 178. As-Sahifatul Kamilah as-Sajjadiyyah 179. Hayya ‘Alaa Khayri’l-’Amal Katika Adhana 180. Ukweli kuhusu Funga ya Siku ya Ashura 181. Dua za Miezi Mitatu Mitukufu (Rajabu, Shaabani na Ramadhani) 182. Uadilifu katika Uislamu 183. Mahdi katika Sunna 184. Jihadi ya Imam Hussein (‘as) 185. Kazi naBidii ni njia ya maendeleo

66

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 66

7/5/2013 7:11:12 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

186. Abu Talib – Jabali Imara la Imani 187. Ujenzi na Utakaso wa Nafsi 188. Vijana na Matarajio ya Baadaye 189. Usalafi – Historia yake, maana yake na lengo lake 190. Ushia – Hoja na Majibu 191. Mateso ya Dhuria wa Mtume (saww) 192. Maombolezo – Msiba wa Bwana wa Mashahidi (a.s.) 193. Shahidi kwa Ajili ya Ubinadamu 194. Takwa 195. Mwonekano wa Upotoshaji katika Hazina ya Kiislamu 196. Amirul Muuminina (‘as) na Makhalifa 197. Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.) 198. Kuelewa Rehma ya Mwenyezi Mungu 199. Mtazamo kuhusu msuguano wa kimadhehebu

200. Upotoshaji Dhahiri katika Turathi ya Kiislamu 201. Nchi na Uraia – Haki na wajibu kwa Taifa 202. Mtazamo wa Ibn Taymiyyah kwa Imam Ali (a.s.) 203. Uongozi wa kidini – Maelekezo na utekelezaji wa Kijamii

67

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 67

7/5/2013 7:11:13 PM


Upotoshaji Dhahiri katika Turathi

NAKALA NNE ZIFUATAZO ZIMETAFSIRIWAKWA LUGHA KINYARWANDA 1. 2. 3. 4.

Amateka Na Aba’Khalifa Nyuma yaho naje kuyoboka Amavu n’amavuko by’ubushiya Shiya na Hadithi

68

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 68

7/5/2013 7:11:13 PM


MUHTASARI

69

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 69

7/5/2013 7:11:13 PM


MUHTASARI

70

08_Upotoshaji Dhahiri_05_July_2013.indd 70

7/5/2013 7:11:13 PM


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.