fmi اfi اﷲ اfmi
Ushia: Hoja na Majibu Uchunguzi kuhusu maswala kumi muhimu yaliyopo baina ya Mashia na Masunni
Kimeandikwa na: Ayatullah Nasir Makarim Shirazi
Kimetarjumiwa na: Alhaj Hemedi Lubumba Selemani
Kimehaririwa na: Alhaj Ramadhani Saleh Kanju Shemahimbo
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 1
11/25/2014 3:03:37 PM
ﺗﺮﺟﻤﺔ ﺗﺮﺟﻤﺔ
ﺗﺮﺟﻤﺔ
ﺗﺮﺟﻤﺔ
ﻴﻌﺔ ﺸّﻴﻌﺔ اﻟاﻟﺸّ ﻴﻌﺔردود اﻟ ردود ﺵﺒﻬﺎتﺸّ وو ﺵﺒﻬﺎت اﻟﺸّ ﻴﻌﺔ ردود ﺵﺒﻬﺎت و
وأهﻞ اﻟاﻟﺴﺴّﻨﺔ ّﻴﻌﺔ وأهﻞ َﻴﻦ اﻟاﻟﺸﺸّﻴﻌﺔ ﻡﻬﻤﻤّﺔّﺔ ﺑﺑَﻴﻦ ﻡﺴﺎﺋﻞ ﻡﻬ ﻋﺸﺮ ﻡﺴﺎﺋﻞ ﺣﻮل ﻋﺸﺮ ﺗﺤﻘﻴﻖ ﺣﻮل ﺗﺤﻘﻴﻖ ّﻨﺔ
ﺵﺒﻬﺎت و ردود
ﺗﺤﻘﻴﻖ ﺣﻮل ﻋﺸﺮ ﻡﺴﺎﺋﻞ ﻡﻬﻤّﺔ ﺑَﻴﻦ اﻟﺸّﻴﻌﺔ وأهﻞ اﻟﺴّﻨﺔ ﺗﺤﻘﻴﻖ ﺣﻮل ﻋﺸﺮ ﻡﺴﺎﺋﻞ ﻡﻬﻤّﺔ ﺑَﻴﻦ اﻟﺸّﻴﻌﺔ وأهﻞ اﻟﺴّﻨﺔ
ﺗﺄﺗﺄ ﻟﻴﻒ ﻟﻴﻒ اﻟﺸﻴﺮازي ﻡﻜﺎرم اﻟﺸﻴﺮازي ﻡﻜﺎرمﻡﻬﻤّﺔ ﺑَﻴﻦ اﻟﺸّﻴﻌﺔ وأهﻞ اﻟﺴّﻨﺔ ﺗﺤﻘﻴﻖ ﺣﻮل ﻋﺸﺮ ﻡﺴﺎﺋﻞ
ﺗﺄﺗﺄ ﻟﻴﻒ ﻟﻴﻒ ﻡﻜﺎرم اﻟﺸﻴﺮازي اﻟﺸﻴﺮازي ﻡﻜﺎرم ﻟﻴﻒ ﺗﺄ
اﻟﺸﻴﺮازياﻟﻠﻐﺔ اﻟﺴﻮا ﺣﻠﻴﺔ ﻡﻜﺎرم اﻟﻰ ﻡﻦ اﻟﻠﻐﺔ اﻟﻌﺮﺑﻴﺔ
ﻡﻦ اﻟﻠﻐﺔ اﻟﻌﺮﺑﻴﺔ اﻟﻰ اﻟﻠﻐﺔ اﻟﺴﻮا ﺣﻠﻴﺔ
ﻡﻦ اﻟﻠﻐﺔ اﻟﻌﺮﺑﻴﺔ اﻟﻰ اﻟﻠﻐﺔ اﻟﺴﻮا ﺣﻠﻴﺔ
ﻡﻦ اﻟﻠﻐﺔ اﻟﻌﺮﺑﻴﺔ اﻟﻰ اﻟﻠﻐﺔ اﻟﺴﻮا ﺣﻠﻴﺔ 22
11/25/2014 3:03:37 PM
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 2
ŠHaki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION
ISBN: 978 - 9987 - 17 - 035 - 7
Kimeandikwa na: Ayatullah Nasir Makarim Shirazi
Kimetarjumiwa na: Alhaj Hemedi Lubumba Selemani
Kimepangwa katika Kompyuta na: Al-Itrah Foundation
Toleo la kwanza: Septemba, 2013 Nakala: 2000
Toleo la pili: Aprili, 2015 Nakala: 2000
Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. - 19701, Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 / 2127555 Barua Pepe: alitrah@yahoo.com Tovuti: www.ibn-tv-com Katika mtandao: www.alitrah.info
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 3
11/25/2014 3:03:38 PM
Yaliyomo Neno la Mchapishaji...............................................................................01 Utangulizi...............................................................................................03 Maudhui Kumi.......................................................................................08 Maudhui kumi: Mada Ya Kwanza: Qur’ani Haina Mabadiliko.... 09 Vitabu viwili kutoka pande zote mbili...................................................10 Madhara ya tuhuma hizi........................................................................14 Dalili za kiakili na kimaandiko..............................................................16 Neno la mwisho.....................................................................................20 MADA YA PILI: TAQIYYAH KATIKA KITABU NA SUNNAH..... 22 Taqiyyah ni nini?...................................................................................22 Tofauti baina ya Taqiyyah na Unafiki....................................................23 Taqiyyah kwa mtazamo wa akili............................................................23 Taqiyyah ndani ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu..................................24 Taqiyyah ndani ya riwaya za Kiislamu..................................................27 Je Taqiyyah inaruhusiwa mbele ya makafiri tu?...................................27 Taqiyyah iliyo haramu...........................................................................32 Taqiyyah ya Umoja................................................................................33 MADA YA TATU: UADILIFU WA MASAHABA......................... 35 Rai mbili zenye kupingana....................................................................35 Usafishaji wa kupindukia.......................................................................36 Maswahaba ni akina nani?.....................................................................40 Sababu za msingi za itikadi ya kuwasafisha...........................................42 Je Maswahaba wote ni waadilifu bila kubagua......................................48 Aina za Maswahaba wa Mtukufu Mtume (saww)..................................55 Ushahidi wa Kihistoria...........................................................................58 Baadhi ya Maswahaba waliadhibiwa kisharia katika zama za Mtume (saww) na baada yake............................................................................62 Utetezi usiokubalika...............................................................................64 Dhulma aliyotendewa Imam Ali (a.s.)...................................................66 Kisa hiki kinastahiki kusimuliwa...........................................................67 iv
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 4
11/25/2014 3:03:38 PM
MADA YA NNE: KUHESHIMU MAKABURI YA WATUKUFU...... 70 Kuhusu mada hii....................................................................................70 Mifano ya kihistoria...............................................................................72 Dhana ya shirki katika kuzuru makaburi..............................................74 Je kuomba na kuombewa kwa Mwenyezi Mungu kunaoana na misingi ya tauhidi?............................................................................75 Maombi ya Mawalii si tu katika kipindi cha uhai wao..........................78 Wanawake na kuzuru makaburi.............................................................80 Safari haifungwi isipokuwa kwa ajili ya misikiti mitatu........................82 Je hairuhusiwi kujengea makaburi?......................................................83 Mawahabi wanabomoa kumbukumbu za kitamaduni...........................85 Visingizio wanavyotoa Mawahabi..........................................................86 Athari chanya za kuzuru makaburi ya watu watukufu.........................90 Jukumu kubwa la Ulamaa wa Kiislamu:...............................................92 MADA YA TANO: NDOA YA MUDA......................................... 94 Dharura na mahitaji...............................................................................94 Ndoa ya Misyar......................................................................................96 Ni ipi hiyo ndoa ya muda?.....................................................................98 Utumiaji hasi..........................................................................................101 Ndoa ya muda katika Kitabu, Sunnah na Ijmai ya umma.....................103 Ni nani aliyeharamisha Mut’a?..............................................................107 Njia bora ya kupata ufumbuzi................................................................116 MADA YA SITA: KUSUJUDU JUU YA UDONGO....................... 119 Umuhimu wa kusujudu baina ya ibada zote.........................................119 Hairuhusiwi kumsujudia asiyekuwa Mwenyezi Mungu.......................120 Ni wajibu kusujudu juu ya kitu gani?....................................................122 Dalili za mas’ala hii................................................................................125 Hadithi maarufu ya Mtume (saww) inayohusu kusujudu juu ya ardhi............................................................................................125 Sira ya Mtukufu Mtume (saww)............................................................126 Sira ya Maswahaba na Tabiina...............................................................128 MADA YA SABA: KUKUSANYA SALA MBILI............................... 131 Asili ya mada..........................................................................................131 v
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 5
11/25/2014 3:03:38 PM
Athari za kulazimisha watu wasali katika nyakati tano katika jamii za Kiislamu.........................................................................132 Riwaya zinazozungumzia kukusanya Sala mbili...................................134 Muhtasari wa riwaya zilizotangulia.......................................................137 Qur’ani na nyakati tatu za Sala..............................................................139 MADA YA NANE: KUPAKA MIGUU KATIKA UDHU........................144 Qur’ani na kupaka juu ya miguu...........................................................144 Utetezi wa ajabu.....................................................................................146 Ijitihadi na tafsiri ya rai binafsi mkabala na maandiko.........................147 Kupaka juu ya viatu...............................................................................150 Riwaya za Kiislamu na kupaka juu ya nyayo mbili...............................151 Riwaya za wenye kupinga......................................................................155 Sharia ni rahisi yenye unafuu................................................................156 Kupaka juu ya viatu kwa mtazamo wa akili na Sharia!!........................160 Hitimisho la mwisho la mada hii...........................................................170 MADA YA TISA: NAFASI YA BISMILLAHI KATIKA SURA AL-HAMDU.................................................................... 172 Kuisoma Bismillahi kwa jahara, kwa mujibu wa hadithi za Mtume (saww)......................................................................176 Qur’ani ni iliyopo baina ya jalada mbili................................................183 Muhtasari wa uchunguzi........................................................................185 MADA YA KUMI: KUTAWASALI KWA MAWALII WA MWENYEZI MUNGU................................................................ 188 Tawassuli kwa mujibu wa Aya za Qur’ani na dalili ya kiakili................188 Tawassul katika Aya tukufu...................................................................193 Tawassuli katika riwaya za Kiislamu......................................................198 Vidokezo muhimu vya kukumbushana.................................................202 Wazembe na wapindukiaji.....................................................................206 Tawassuli peke yake haitoshi.................................................................207 Tawassuli katika mambo ya kiasili.........................................................208 Bibliografia.............................................................................................211
vi
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 6
11/25/2014 3:03:38 PM
Ushia: Hoja na Majibu
NENO LA MCHAPISHAJI
U
shia: Hoja na Majibu ni kitabu kinachotoa majibu ya baadhi ya mambo ambayo kwayo Mashia wanatuhumiwa nayo na ndugu zao Masunni kwa kuyafanya; na wao wakiyaona kwamba hayafai kufanywa kwa sababu hayana asili katika dini.
Mwandishi wa kitabu hiki ambaye ni Ayatullah Nasir Makarimu Shirazi ameorodhesha matendo kumi ya kiibada ambayo Mashia hutuhumiwa kuyafanya kinyume cha Uislamu unavyofundisha, tuhuma ambazo hutolewa na ndugu zao Masunni. Mwandishi anatoa maelezo ya kina ya utafiti alioufanya kujibu tuhuma hizo na kuonesha pasina shaka yoyote kwamba matendo hayo ni sahihi kabisa kwa mujibu wa Qur’ani Tukufu, Sunna na katika matukio ya kihistoria Sisi kama wachapishaji tunakiwasilisha kitabu hiki kama kilivyo kwa wasomaji wetu na kuwashauri wasome yaliyomo humo, wayafanyie kazi na kuyazingatia ili kuondokana na dhana hii ya kutuhumu bila kufanya utafiti. Baadhi ya dhana nyingi ni dhambi kama ilivyosema Qur’ani Tukufu. Na wenye hekima na busara wanasema: “Hakuna utafiti, huna haki ya kusema (No research no right to speak).” Hii ni moja kati ya kazi kubwa zilizofanywa na Taasisi ya Al-Itrah katika kuwahudumia kielimu wasomaji wake wazungumzaji wa Kiswahili. Na kwa maana hiyohiyo imeamua kukichapisha kitabu hiki chenye manufaa makubwa kwa lugha ya Kiswahili kwa lengo lake lilelile la kuwahudumia Waislamu, hususan wanaozungumza Kiswahili. 1
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 1
11/25/2014 3:03:38 PM
Ushia: Hoja na Majibu
Hivyo, ni matumaini yetu kwamba wasomaji wetu watanufaika vya kutosha kutokana na kitabu hiki, kwani tumekiona ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni vitu ambavyo havina nafasi tena katika akili za watu. Tunamshukuru mwandishi wa kitabu hiki, Ayatullah Nasir Makarimu Shirazi kwa kazi kubwa aliyofanya kwa ajili ya Umma huu wa Waislamu, Allah ‘Azza wa Jallah amlipe kila kheri na amuingize Peponi kwa salama na amani, insha’Allah. Halikadhalika tunamshukuru Ndugu yetu Alhaj Hemedi Lubumba Selemani (Abul Batul) kwa kukitarjumi kwa Kiswahili kitabu hiki, insha’Allah na yeye Allah ‘Azza wa Jallah amlipe kila kheri hapa duniani na Akhera pia, bila kuwasahau na wale wote waliochangia kwa namna moja au nyingine mpaka kufanikisha kuchapishwa kwake. Allah awalipe wote malipo mema hapa duniani na huko Akhera pia. Mchapishaji Al-Itrah Foundation.
2
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 2
11/25/2014 3:03:38 PM
Ushia: Hoja na Majibu
UTANGULIZI Njia hii haifikishi kwenye umoja
T
ukitazama kwa mtazamo wa jumla hali ya ulimwengu wa leo tunaona unapigwa na tufani kubwa la kutisha, ambalo limeondoa pazia kwenye sura yake halisi, na ambalo limezungukwa na kaulimbiu za kupendeza kama vile tangazo la haki za binadamu na demokrasia. Huku serikali za dola mbalimbali zikiwa hazijiwezi chochote, wababe wa ulimwengu wao wameandaa mipango yao ya hatari ili kuweza kuzitawala nchi nyingine za ulimwengu, na katika hilo wameweka bayana kabisa nia zao. Uzuri ni kuwa wao wamesema kila kitu, na kwa mujibu wa usemi wa Kiajemi ni kuwa: “Hakika kubainisha kwao mipango yao kumetimiza hoja juu ya watu wote.� Hivyo katika ugomvi kama huu hakuna kimbilio baada ya huruma na msaada wa Mwenyezi Mungu isipokuwa kwenye uwezo na nguvu ya umma. Hivyo umma unapasa kuwa na nguvu katika utashi wake, katika mfumo huu wa dunia ulio dhaifu na duni. Kama Waislamu wa ulimwengu mzima wangeungana katika mazingira haya magumu na wakafaidika na uwezo mkubwa (wa kielimu na kirasilimali) wanaoumiliki, basi wangekuwa katika amani dhidi ya shari za watu wenye madaraka. Imepita miaka mingi huku mazungumzo kuhusu umoja wa Waislamu yakipaa katika kila sehemu, na zimetawala habari za kuanzisha Wiki ya Umoja, na yamefanyika 3
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 3
11/25/2014 3:03:38 PM
Ushia: Hoja na Majibu
makongamano na semina kadhaa kuhusu Umoja, huku kaulimbiu zikinyanyuliwa huku na kule. Mambo haya hata kama yana athari chanya katika medani za kisiasa na kijamii lakini mpaka leo bado hatujaweza kutimiza Umoja unaotakiwa utakaowezesha kusimama mbele ya tufani hii kubwa. Inawezekana kufupisha hilo katika mambo yafuatayo: 1. Hatua zilizochukuliwa hazikuwa za msingi, na maudhui ya Umoja haikuweza kupenya mpaka ndani ya jamii za Kiislamu, wala ndani ya mfumo wa elimu, na wala Waislamu wa ulimwengu hawakuandaliwa kuwa katika mwelekeo mmoja. 2. Maadui wamefanya kazi kwa uwanda mpana na kwa mipango madhubuti katika kueneza ukataji tamaa, dhana mbaya, tofauti na unafiki katika jamii za Kiislamu, kama linavyodhihirika hilo kupitia habari zinazonukuliwa. Wametumia mali nyingi katika kutimiza hilo, na wamewaandaa waasi na wenye chuki binafsi kutoka pande mbili ili kuweza kutekeleza mipango yao mibaya. Miongoni mwa mipango hiyo ni: a. Katika siku za hivi karibuni zimenukuliwa habari za uhakika kuwa Masalafi wenye chuki binafsi huko Saudia wamechapisha nakala milioni kumi za kitabu ili kueneza fitna na mfarakano, na wamezigawa kwa mahujaji. Hija ambayo inapasa kuwa njia ya kuleta Umoja baina ya Waislamu ulimwenguni wao wameifanya kuwa njia ya kuwatenganisha Waislamu na kuwagawa. Na kwa bahati mbaya sana ni kuwa kitendo hiki hujirudia kila mwaka. 4
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 4
11/25/2014 3:03:38 PM
Ushia: Hoja na Majibu
b. Makhatibu wa Kiwahabi wenye chuki binafsi wanatoa juhudi kubwa katika siku za Hija na Umra katika kueneza aina zote za sumu ili kuleta hali ya unafiki, hivyo licha ya kuwepo ukaribu wa kisiasa baina ya Iran na Saudia lakini bado sisi tunashuhudia mashambulizi yao dhidi ya Mashia yakienea zaidi na kuongezeka. c. Viko wazi kwa kila mtu vitendo vya Jeshi la Masahaba vyenye kujirudia mara kwa mara, na ambavyo hulenga kuwauwa watu wasio na hatia wanyonge waliodhulumiwa. Na lililo baya zaidi ya hilo ni kule kujifakharisha kwao na kufurahikia kwao matendo ya uuwaji na utekaji nyara. d. Na miongoni mwa matendo ya hatari wanayoyafanya ni kuyaendesha baadhi ya makundi yenye msimamo mkali kama vile kundi la Teleban, kupitia idara za ujasusi za Marekani - kulingana na ushahidi uliopo - ili kwa upande mmoja kuchafua sura ya Uislamu na kuudhihirisha kwa sura ya unyama na ukatili usio na huruma, na ulio mbali kabisa na elimu na maarifa. Na kwa upande mwingine ni ili kuleta mtengano na machafuko baina ya safu za Waislamu, licha ya kwamba hawa waliolelewa katika mapaja ya idara za ujasusi na siasa za Magharibi hivi sasa wameanza kujitoa kwenye mamlaka yao ili msiba na laana ziwashukie kutoka kwa wale waliowalea na kuwapa nguvu, ili walipe fidia ya yale waliyotenda. 5
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 5
11/25/2014 3:03:38 PM
Ushia: Hoja na Majibu
3.
Kutokuwajibika kwa baadhi ya viongozi wa Kiislamu, pale walipotanguliza maslahi yao binafsi na finyu kabla ya maslahi ya jamii ya ulimwengu wa Kiislamu. Hii ni moja ya sababu iliyozuia malengo ya msingi ya umoja yasiweze kutimia. Kwa mfano tu ni kuwa, baadhi ya dola za Kiislamu – maarufu – zimekuwa na mahusiano ya ushirikiano wa kirafiki na kundi la Kizayuni katika nyanja ya siasa na uchumi, ili kutimiza baadhi ya maslahi finyu na madogo, na dola hizo zinajulikana na watu wote, bali ni kwamba zimefikia hata kufanya mazoezi ya kijeshi ya pamoja!
Vyovyote iwavyo ni kuwa nafasi waliyonayo Ulamaa wa Kiislamu ni kukumbusha matokeo mabaya ya matendo haya, na kwamba siasa hizo za maangamizi na mabavu hazitaiacha salama katika amani na raha nchi yoyote ya Kiislamu wala kundi lolote la Kiislamu. Hakika kuwasilisha maswala haya ya kimadhehebu kwa mtindo bayana na wa uwazi kadiri iwezekanavyo, kutawanyima maadui fursa ya kusambaza sumu zao, na utazuia uenezwaji wa hali ya kutokuaminiana na kudhaniana vibaya kunakofanywa na baadhi ya makundi yenye msimamo mkali, yenye chuki binafsi toka pande zote mbili. Kwa ajili hii tunaweka kitabu hiki mbele ya mikono ya wasomaji wapendwa kwa njia mpya ya kuvutia, ili kuimarisha mshikamano, na kwa njia hii mas’ala hii itakuwa wazi kikamilifu, hasa ukizingatia kuwa mizizi ya maeneo muhimu yenye utata baina ya wafuasi wa madhehebu ya Ahlul-Baiti (as) na Masunni, imo ndani ya vitabu vyao maarufu, na kwamba kile wasemacho Mashia katika medani hii dalili zake zimo ndani ya vitabu vya Masunni, na kama anavyosema mmoja kati ya Ulamaa huru wa Kisunni kuwa: 6
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 6
11/25/2014 3:03:38 PM
Ushia: Hoja na Majibu
“Shia wanaweza kuthibitisha misingi yote na matawi yote ya madhehebu yao kutoka ndani ya vitabu vyao na utunzi wao.� Jambo hili likithibiti, na inshaallah litathibiti ndani ya kitabu hiki, haitabakia tena nafasi ya kuwa na chuki au kueneza utata dhidi ya itikadi za wafuasi wa madhehebu ya Ahlul-Baiti (as), na itakuwa ni sababu ya kuaminiana na kuunganisha safu zetu na kuondoa dhana mbaya kwa wale wenye uungwana na mantiki. Na itaendelea Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa nchi yenye nguvu yenye kuutetea Uislamu, kadhalika yenye kuyatetea madhehebu ya Shia katika ulimwengu wa Kiislamu. Sasa kazi ni kwenu dalili hizi hapa mikononi mwenu!
7
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 7
11/25/2014 3:03:38 PM
Ushia: Hoja na Majibu
MAUDHUI KUMI Maudhui muhimu ambazo zitahusu mazungumzo yetu na kujadiliwa baina yetu na wao ni kumi 1. Qur’ani Tukufu haina mabadiliko 2. Taqiyyah ndani ya Kitabu na Sunnah 3. Uadilifu wa Masahaba 4. Kuyaheshimu makaburi ya watu watukufu 5. Ndoa ya muda 6. Kusujudu juu ya ardhi 7. Kukusanya Sala mbili 8. Kupaka miguu wakati wa kutawadha 9. Bismillahi ni sehemu ya Sura Alhamdu 10. Kutawasali kupitia Mawalii wa Mwenyezi Mungu.
8
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 8
11/25/2014 3:03:38 PM
Ushia: Hoja na Majibu
MADA YA KWANZA QUR’ANI HAINA MABADILIKO
S
isi tunaamini – licha ya propaganda zote mbaya za kuwapaka matope Mashia – kuwa Qur’ani Tukufu iliyopo sasa kwetu na kwa Waislamu wote wa leo ndio ile ile Qur’ani iliyoteremka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) haina nyongeza au upungufu hata katika neno moja. Jambo hili tumelibainisha kwa uwazi zaidi katika vitabu vya tafsiri, misingi ya sharia na vitabu vinginevyo, na tumethibitisha hilo kwa dalili za kiakili na kimaandiko. Na sisi tunaamini kuwa Waislamu – wote Mashia na Masunni – wanakubaliana kuwa Qur’ani Tukufu iliyopo baina ya magamba mawili haijaongezwa chochote. Ama upande wa upungufu ni kuwa wahakiki wengi kutoka pande zote mbili wanasema hakuna upungufu katika Qur’ani Tukufu. Kuna watu kadhaa kutoka pande zote mbili wanaamini kuwa kuna upungufu ndani ya Qur’ani Tukufu, na wala hakuna mhakiki yeyote maarufu miongoni mwa Waislamu anayeunga mkono maneno yao.
9
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 9
11/25/2014 3:03:38 PM
Ushia: Hoja na Majibu
Vitabu viwili kutoka pande zote mbili
M
iongoni mwa watu hao ni Ibn Khatib al-Misriy, naye ni miongoni mwa Masunni, ameandika kitabu kwa anuwani isemayo “al-Fur’aqan Fii Tahrifil-Qur’ani”, yaani “Ubainifu kuhusu uwepo wa mabadiliko katika Qur’ani”, kitabu hiki kilisambazwa mwaka 1948 A.D. sawa na mwaka 1367 A.H. na pindi Chuo Kikuu cha Azhar kilipojua hilo kilifanya kazi ya kukusanya nakala zote na kuziharibu, isipokuwa ni kwamba kuna baadhi ya nakala ziliweza kudondokea mikononi mwa baadhi ya watu kinyume na utaratibu. Kadhalika kuna kitabu chenye anuwani isemayo “FaslulKhitab Fii Tahrif Kitabu Rabul-Arbabi” yaani “Ubainifu wa maneno kuhusu uwepo wa mabadiliko katika Kitabu cha Bwana wa mabwana,” kitabu hiki kiliandikwa na mmoja kati ya wanahadithi wa Kishia ambaye ni Alhaji Nuriy, na kilichapishwa mwaka 1291 A.H. na baada tu ya kuchapishwa Ulamaa wa Hawza ya Kielimu ya Najaf walikipinga kitendo hiki na wakaamrisha nakala zote za kitabu zikusanywe, na wakaandika vitabu kadhaa kumjibu, na miongoni mwa Ulamaa walioandika katika kujibu kitabu hiki “Faslul-Khitab Fii Tahrif Kitabu Rabul-Arbabi” ni: 1.
Mwanafiqhi mkubwa, marehemu Sheikh Mahmud bin Abil-Qasim, maarufu kwa jina la Muurab Twahraniy (alifariki mwaka 1313 A.H.) aliandika kitabu kwa anwani isemayo “Kashful-Irtiyab Fii Adami Tahrifil-Kitab”.
10
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 10
11/25/2014 3:03:38 PM
Ushia: Hoja na Majibu
2.
Marehemu Allamah Sayyid Muhammad Shahrastaniy (alifariki mwaka 1315 A.H.) katika kujibu kitabu “FaslulKhitab Fii Tahrif Kitabu Rabul-Arbabi” aliandika kitabu kwa anwani isemayo “Hifdhul-Kitab Sharif Ani Shubhatul-Qawli Bitahrif”.
3.
Marehemu Allamah al-Balaghiy (alifariki mwaka 1352 A.H.) naye ni mmoja kati ya wahakiki wa Hawza ya Kielimu ya Najaf, alitenga faslu makhususi katika tafsiri yake maarufu kwa jina la Alaur-Rahman ili kujibu kitabu “Faslul-Khitab Fii Tahrif Kitabu Rabul-Arbabi”1.
4.
Nasi kwa upande wetu katika kitabu chetu An’warulUsul tumechambua kwa upana zaidi suala la Qur’ani Tukufu kubadilishwa, na tumejibu kwa uyakinifu kabisa hoja zilizopo katika kitabu “Faslul-Khitab Fii Tahrif Kitabu Rabul-Arbabi”.
Hakika marehemu Alhaji Nuriy japokuwa yeye ni aalimu isipokuwa ni kwamba alitegemea riwaya dhaifu, kama alivyosema Allamah al-Balaghiy, na alijutia yale yaliyoandikwa na mkono wake baada ya kitabu husika kusambazwa, na Ulamaa wa Hawza ya Kielimu ya Najaf walihesabu kazi yake hii kuwa ni miongoni mwa makosa yaliyo bayana.2 Na la kuvutia ni kwamba Alhaji Nuriy baada ya kitabu chake kusambazwa na baada ya ukosoaji mkubwa aliokutana nao kutoka pande zote mbili, alilazimika kuandika ujumbe ambao aliweza kujitetea kupitia ujumbe huo na akabainisha kuwa kusudio lake katika hilo ni kutokuwepo na mabadiliko katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu, na kwamba wakosoaji walizielewa kimakosa ibara zake. 1
Tafsir Aalaur-Rahman, Juz. 1 Uk. 25.
2
Tafsir Aalaur-Rahman, Juz. 2 Uk. 311. 11
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 11
11/25/2014 3:03:38 PM
Ushia: Hoja na Majibu
Marehemu Allamah Sayyid Hibatud-Din Shahrastaniy anasema: “Nilipokuwa Samrau, mji ambao marehemu Mirza Shirazi mkubwa aliubadili na kuwa kituo cha elimu, kulikuwa na kelele kubwa dhidi ya Alhaji Nuriy na dhidi ya kitabu chake, na baadhi ya watu wakatoa kauli chafu na mbaya inayoshusha shakhsia yake.”3 Pamoja na yote haya, je inawezekana kusema kuwa Sheikh Nuriy anawakilisha itikadi ya Shia? Lakini kuna Mawahabi kadhaa wenye chuki binafsi – kwa kutumia hoja ya uwepo wa kitabu Faslul-Khitab Fii Tahrif Kitabu RabulArbabi – wanang’ang’ania kuwanasibisha Mashia na madai ya kuwa Qur’ani ina mabadiliko. Ikiwa rai ya mwandishi fulani ni dalili tosha kuwa Mashia wanaamini jambo hili, basi ni lazima suala hili la madai ya kuwa Qur’ani Tukufu ina mabadiliko linasibishwe pia na Ulamaa wa Kisunni, kwa sababu Ibn Khatib amelitaja jambo hili katika kitabu chake “al-Fur’aqan Fii Tahrifil-Qur’ani.” Na ikiwa kitendo cha Ulamaa wa Azhar kukerwa na kitabu hiki ni dalili ya kupinga kwao madhumuni yake, kadhalika ndivyo ilivyo kwa upande wa Ulamaa wa Najaf tukufu, kukipinga kwao kitabu Faslul-Khitab Fii Tahrif Kitabu Rabul-Arbabi ni dalili ya kukataa kwao madai ya kuwa Qur’ani ina mabadiliko. Tafsiri zote mbili, ya Qurtubiy na Durul-Manthur – nazo ni tafsiri maarufu kwa Masunni – zimenukuu kutoka kwa Aisha (mke wa Mtume (saww)) kauli yake: “Hakika yenyewe – yaani Sura Ahzab – ilikuwa na Aya mia mbili, na hazijabakia katika Sura hiyo isipokuwa Aya sabini na tatu.”4 Bali ni kuwa katika Sahih Bukhari na Sahih Muslim 3
Burhan Rawshan cha Kiajemi, Uk. 143.
4
Tafsirul-Qurtubiy Juz. 12, Uk. 113. Tafsiru Durul-Manthur Juz. 5, Uk. 180. 12
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 12
11/25/2014 3:03:38 PM
Ushia: Hoja na Majibu
kuna riwaya nyingi zinazotoa harufu ya kwamba Qur’ani ina mabadiliko.5 Lakini sisi hatuziruhusu nafsi zetu kuwanasibisha ndugu zetu Masunni na madai ya kwamba Qur’ani ina mabadiliko, kwa kutumia rai ya mwandishi, au kwa kuwepo riwaya dhaifu ndani ya vitabu vyao. Na wao hawapasi kunasibisha hilo na Mashia kwa kuwepo tu rai ya mwandishi fulani au kwa kuwepo riwaya dhaifu ndani ya vitabu vyao, riwaya ambazo Ulamaa wa Kishia hawazikubali. Na tukitazama kundi la riwaya alizozitegemea Sheikh Nuriy tutazikuta ni riwaya zilizopokewa kutoka kwa wapokezi watatu, nao ni ima mwenye madhehebu mbovu au mwongo au asiyejulikana, nao ni: 1.
Ahmad bin Muhammad Sayariy, mwenye madhehebu mbovu.
2.
Ali bin Ahmad al-Kufiy, ambaye ni mwongo.
3.
Abul Jarudi, ambaye hali yake haijulikani au asiyekubalika.6
5
S ahih Bukhar Juz. 8, Uk. 208 – 211. Sahih Muslim Juz. 4, Uk. 167, na Juz. 5 Uk. 116.
6
wa kutaka kujua zaidi hali za watu hawa watatu, rejea kitabu Rijalun-Najashiy K na Fahrasti Sheikh Tusiy, na vitabu vingine vya wasifu wa wapokezi. 13
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 13
11/25/2014 3:03:38 PM
Ushia: Hoja na Majibu
Madhara ya tuhuma hizi
K
una watu wanang’ang’ania kuelekeza kwa Mashia tuhuma ya madai ya kuwa Kitabu cha Mwenyezi Mungu kina mabadiliko, kana kwamba wao hawajui kuwa kuelekeza tuhuma hizi kwa sababu tu ya ugomvi wa kimadhehebu kunadhoofisha msingi wa Uislamu, hiyo ni kwa kuwa maadui wanasema: “Hakika suala la kuwa Qur’ani Tukufu haina mabadiliko halikubaliki na Waislamu wote, kuna kundi kubwa miongoni mwao linaloamini kuwa Qur’ani ina mabadiliko.” Hivyo sisi tunawasihi ndugu zetu hawa wasiufanye moyo wa Uislamu, ambao ni Qur’ani Tukufu kuwa shabaha kwa sababu ya tofauti na chuki za kimadhehebu. Uhurumieni Uislamu na Qur’ani ili maadui wasitumie wingi wa mazungumzo kuhusu madai ya kuwa Qur’ani ina mabadiliko kuwa njia ya kuuvunjia heshima Uislamu na Qur’ani Tukufu. Kwa bahati mbaya sana tuhuma hizi na uzushi huu umeenea kwa kiasi kikubwa, kiasi kwamba mimi mwenyewe katika moja ya safari zangu za kuiendea Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu kwa ajili ya Umrah, nilikutana na Waziri wa Mambo ya Dini wa Serikali ya Suudia, akaniambia: “Nimesikia kuwa nyinyi mna msahafu tofauti na msahafu wetu.” Nikamwambia: Kugundua jambo kama hili ni rahisi sana, inakupasa tu kwenda wewe mwenyewe huko Tehran, au kumtuma msaidizi wako huko, na kufanya uchunguzi katika nakala zote za Qur’ani zilizopo misikitini na majumbani, chagua msikiti wowote uupendao au nyumba yoyote uitakayo, na omba Qur’ani toka kwa mtu yeyote umtakaye, utakuta hakuna tofauti yoyote baina yake na nakala zote za Qur’ani 14
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 14
11/25/2014 3:03:38 PM
Ushia: Hoja na Majibu
zilizopo katika ulimwengu wa Kiislamu, hata katika neno moja. Na msomi mkubwa kama wewe hapasi kudhibitiwa na propaganda na uwongo kama huu. Na alhamdulilahi kwamba wasomi wetu wa Qur’ani wameshiriki katika mashindano mengi ya kimataifa ya usomaji wa Qur’ani na wameshika nafasi za mwanzo. Na mahafidhi wetu, hasa wenye vipaji miongoni mwao wamekuwa ni sehemu ya maajabu na kusifiwa na watu wengi kutoka nchi mbalimbali za ulimwengu wa Kiislamu. Na kila mwaka idadi ya wasomaji na mahafidhi wa Qur’ani inaongezeka kwetu, huku madrasa za kuhifadhisha Qur’ani, kufundisha usomaji wake na tafsiri yake, na vyuo vya taaluma ya Qur’ani, zimeenea kona zote za nchi yetu kubwa, na ni rahisi sana watu wote kuthibitisha hilo kwa kuangalia ratiba hizo kwa karibu. Na katika sehemu zote hizi hakuna Qur’ani nyingine isiyokuwa Qur’ani hii iliyo maarufu baina ya Waislamu wote, na hakuna yeyote anayeijua Qur’ani isiyokuwa hii, na wala hatuzungumzi kuwa Qur’ani ina mabadiliko, si katika mnasaba wowote ule wala katika hafla yoyote ile.
15
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 15
11/25/2014 3:03:39 PM
Ushia: Hoja na Majibu
Dalili za kiakili na kimaandiko
S
isi tunaamini kuwa kuna dalili nyingi za kiakili na kimaandiko zinazothibitisha kuwa Qur’ani haina mabadiliko, Mwenyezi Mungu amesema ndani ya Qur’ani Tukufu:
ِّ إِ َّنا َنحْ نُ َن َّز ْل َنا ُ الذ ْك َر َوإِ َّنا لَ ُه َل َحاف ون َ ِظ
“Hakika sisi tumeiteremsha Qur’ani, na hakika sisi ndio wenye kuilinda.” (Sura Hijri: 9). Na katika Aya nyingine anasema:
ِّ ِين َك َفرُوا ِب ٌالذ ْك ِر َلمَّا َجا َء ُھ ْم ۖ َوإِ َّن ُه َل ِك َتاب َ إِنَّ الَّذ ْ ۖ ْن َيدَ ْي ِه َو َال ِمنْ َخ ْل ِف ِه ِ َع ِزي ٌز َال َيأتِي ِه ْالبَاطِ ُل ِمنْ َبي ِيم َحمِي ٍد ٍ َت ْن ِزي ٌل ِمنْ َحك
“Kwa hakika wale wanaoyakataa mawaidha yanapowafikia (tutawaadhibu) bila shaka hicho ni Kitabu chenye kuheshimika. Hautakifikia upotovu mbele yake wala nyuma yake, kimeteremshwa na Mwenye hekima, Mwenye kuhimidiwa.” (Sura Fusilat: 41 – 42).
Ikiwa Mwenyezi Mungu amechukua ahadi ya kukilinda Kitabu hiki, je inawezekana Kitabu hiki kuguswa na mikono ya mabadiliko? Zaidi ya hapo ni kuwa Qur’ani Tukufu haikutelekezwa wala kusahauliwa mpaka mtu aje na kuongeza au kupunguza kitu humo, idadi ya waandishi wa wahyi iliongezeka kutoka watu 16
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 16
11/25/2014 3:03:39 PM
Ushia: Hoja na Majibu
kumi na nne mpaka watu mia nne, na walikuwa wanafanya kazi ya kuandika na kudhibiti kila Aya inaposhuka, na idadi ya mahafidhi wa Qur’ani Tukufu katika zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) ilifikia mamia ya watu, ambapo walikuwa wakihifadhi kila Aya inapoteremka. Usomaji wa Qur’ani katika zama hizo ulikuwa ni miongoni mwa ibada bora, ambapo ilikuwa ikisomwa usiku na mchana. Kama ambavyo pia Qur’ani ndio katiba ya Uislamu na kanuni ya matendo ya Waislamu, na ipo katika sehemu zote za maisha yao. Hivyo akili inatambua kuwa kitabu kama hiki hakiwezi kufikwa na mabadiliko sawa iwe ni upande wa nyongeza au upungufu. Na riwaya zilizotufikia kutoka kwa Maimamu maasumu (as) zinasisitiza ukamilifu wa Qur’ani Tukufu na kutofikwa na mabadiliko ya aina yoyote. Huyu hapa Amirul-Muuminina Ali bin Abu Talib (as) anatamka bayana ndani ya Nahjul-Balaghah kuwa: “Na amekuteremshieni Kitabu kinachobainisha kila kitu, na amemrefushia umri Nabii Wake kwa zama ndefu, kiasi cha kumkamilishia yeye na nyinyi Ujumbe (aliouteremsha Kitabuni mwake) ambao ni Dini Yake ambayo ameiridhia nafsini Mwake..”7 Na katika sehemu nyingi za Nahjul-Balaghah AmirulMuuminina Ali bin Abu Talib (as) anapogusia Qur’ani Tukufu hatuoni akizungumzia sehemu yoyote kuwa Qur’ani ina mabadiliko, bali anasisitiza bayana na waziwazi ukamilifu wa Qur’ani. Na Imam wa tisa Muhammad bin Ali al-Jawad katika moja ya hotuba zake kwa masahaba zake kuhusu watu walivyopotoka na kuacha njia ya haki anasema: “Na 7
Nahjul-Balaghah: Hotuba ya 85. 17
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 17
11/25/2014 3:03:39 PM
Ushia: Hoja na Majibu
miongoni mwa namna za kukiacha kwao Kitabu ni kuwa wamezisimamisha herufi zake kama zilivyo lakini wamebadili sheria zake.”8 Hadithi hii na nyinginezo mfano wa hii zinaashiria kuwa maandiko ya Qur’ani Tukufu yameendelea kuhifadhiwa lakini mabadiliko yalitokea kwenye maana, ambapo baadhi ya watu walitafsiri na kuzielekeza baadhi ya Aya kulingana na matakwa yao binafsi na manufaa yao binafsi kinyume na makusudio halisi. Na hapa ndipo linapotubainikia suala muhimu, nalo ni kuwa riwaya ambazo zinazungumzia uwepo wa mabadiliko katika Qur’ani zinazungumzia mabadiliko katika maana na tafsiri yenye kufuata rai binafsi, na si uwepo wa mabadiliko katika ibara na maandiko ya Qur’ani yenyewe. Na kwa upande mwingine tunaona kuwa kuna riwaya nyingi na zenye kukubalika ambazo zimetufikia kutoka kwa Maimamu maasumu (as) ambazo zinaamrisha kuzipima riwaya kwa Qur’ani Tukufu na hasa riwaya hizo zinapokinzana, ili kujua ni zipi riwaya sahihi na ni zipi zisizokuwa sahihi, zile zinazoafikiana na Qur’ani ndio sahihi na inaruhusiwa kuzifanyia kazi, na zile zinazopingana nayo ziacheni: “Zipimeni kwenye Kitabu cha Mwenyezi Mungu, zile zitakazoafikiana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu zichukueni, na zile zinazopingana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu ziacheni.”9 Hii ni dalili ya wazi kuwa hakuna mabadiliko yaliyofanywa ndani ya Qur’ani Tukufu, kwa sababu katika sura isiyokuwa hii haiwezi kuwa kipimo cha kupambanua ni ipi haki na ni ipi batili. 8
Usulul-Kafiy Juz. 8, Uk. 53.
9
Wasailus-Shiah Juz. 18, Uk. 80. 18
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 18
11/25/2014 3:03:39 PM
Ushia: Hoja na Majibu
Zaidi ya haya ni kuwa imepokewa pia hadithi ya Vizito Viwili ambayo ni maarufu na imenukuliwa kwa wingi katika vitabu vya Masunni na Mashia kuwa Mtukufu Mtume (saww) alisema: “Hakika mimi nimekuachieni vizito viwili: Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Kizazi changu, mkishikamana navyo kamwe hamtopotea.”10 Hakika hadithi hii tukufu inaonesha bayana kuwa Qur’ani na Kizazi cha Mtume ndio kimbilio salama na mwongozo wa watu mpaka Siku ya Kiyama. Hivyo ikiwa Qur’ani imebadilishwa itakuwaje iwe tena ni kimbilio salama na mwongozo wa watu dhidi ya upotovu.11
10
Biharul-An’war, Juz. 36, Uk. 331.
11
wenye kutaka ufafanuzi zaidi arejee kitabu chetu An’warul-Usul Juz. 2, Uk. M 340 na kuendelea. 19
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 19
11/25/2014 3:03:39 PM
Ushia: Hoja na Majibu
Neno la mwisho
N
eno la mwisho ni kuwa, moja ya madhambi makubwa mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ni kumtuhumu mwingine kwa mambo ambayo hajasema wala kutenda. Na sisi mara nyingi tumekuwa tukisema tena katika minasaba mbalimbali kuwa hakuna hata mtu mmoja miongoni mwa wahakiki na Ulamaa wa Kishia anayesema kuwa Qur’ani imebadilishwa, na vitabu vyao vinathibitisha hilo, lakini kuna kundi lenye chuki binafsi ambalo bado linaendelea kutoa tuhuma hizi, na sijui watajibu nini Siku ya Kiyama kuhusu tuhuma zote hizi na kuhusu kuivunjia heshima Qur’ani Tukufu na hadhi yake. Ikiwa kisingizio chenu ni uwepo wa baadhi ya riwaya dhaifu katika vitabu vyetu basi jueni riwaya hizo pia zimo ndani ya vitabu vyenu, na tumeshaashiria hilo huko nyuma. Na hakuna madhehebu yoyote inayojenga msingi wake juu ya riwaya dhaifu, wala sisi hatuwezi kuwatuhumu nyinyi kuwa mnaamini Qur’ani imebadilishwa, eti kwa kuwepo kitabu “al-Fur’aqan Fii Tahrifil-Qur’ani,” cha Ibn Khatib al-Misriy na kwa kuwepo riwaya dhaifu zilizopo kwenu zinazoonesha kuwa Qur’ani imebadilishwa, na wala hatuwezi kuitoa muhanga Qur’ani kwa ajili ya chuki binafsi zenye kuangamiza. Msizungumzie uwepo wa mabadiliko katika Qur’ani kwa njia hii na wala msiuvunjie heshima Uislamu, Waislamu na Qur’ani, msiishushe hadhi Qur’ani kwa sababu ya chuki zenu za kimadhehebu, Qur’ani ndio rasilimali kuu ya 20
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 20
11/25/2014 3:03:39 PM
Ushia: Hoja na Majibu
Waislamu wa ulimwengu wote, hivyo hazipasi ndimi zenu kuzungumzia uwepo wa mabadiliko katika Qur’ani, na wala msiwape maadui sababu, mkitaka kuwafanyia uadui Mashia na wafuasi wa Ahlul-Baiti (as) kwa njia hii, basi jueni kuwa nyinyi mnadhoofisha misingi ya Uislamu bila kujua, kwa sababu maadui wa Uislamu watasema: “Hakika kundi kubwa la Waislamu linaamini kuwa Qur’ani ina mabadiliko.” Na hii ni dhulma kubwa dhidi ya Qur’ani Tukufu. Mwishoni tunarudia tena kusema: Hakuna mtu miongoni mwa wahakiki wa Kishia na Kisunni anayesema kuwa Qur’ani ina mabadiliko, na hakika wao wanakiri kuwa Qur’ani iliyoteremka kwa Mtukufu Mtume (saww) ndio ile ile Qur’ani iliyopo sasa kwa Waislamu. Na wanaamini kama Qur’ani ilivyotamka bayana kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu alichukua ahadi ya kuihifadhi Qur’ani dhidi ya mabadiliko au upotoshaji au utowekaji. Lakini la kusikitisha ni kwamba wapo baadhi ya watu wenye chuki binafsi toka pande zote mbili ambao bila elimu na ujuzi wamewanasibisha wenzao na itikadi ya kwamba Qur’ani ina mabadiliko. Tunamuomba Mwenyezi Mungu awaongoe wote.
21
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 21
11/25/2014 3:03:39 PM
Ushia: Hoja na Majibu
MADA YA PILI TAQIYYAH KATIKA KITABU NA SUNNAH
T
aqiyyah ndio suala la pili ambalo wanalichukua hawa wachonganishi wenye chuki binafsi dhidi ya madhehebu ya Ahlul-Baiti (as); wanasema: Kwa nini mnatumia Taqiyyah, je Taqiyyah si moja kati ya aina za unafiki? Watu hawa wamekuza suala hili kiasi cha kuonekana kama Taqiyyah ni tendo la haramu au ni miongoni mwa madhambi makubwa au ni kubwa zaidi ya hapo. Wamesahau kuwa Qur’ani imeruhusu Taqiyyah katika Aya kadhaa, pale panapokuwa na mazingira makhususi, na riwaya zilizopo ndani ya vitabu vyao zinasisitiza maana hii, bali zaidi ya hapo ni kwamba akili inaamrisha Taqiyyah waziwazi pindi sharti zake zinapotimia, na zaidi ya hapo ni kuwa wengi miongoni mwa hawa hawa wanaoipinga wameitumia Taqiyyah mara kadhaa katika maisha yao binafsi. Hivyo ili kuweka wazi jambo hili ni lazima tutazame nukta zifuatazo: 1. Taqiyyah ni nini? Ni mtu kuficha itikadi yake ya kidini pindi anapohisi kuwa itamwingiza katika hatari mbele ya wanaoipinga au wenye chuki binafsi, mfano wa hilo ni kama pale Mwislamu 22
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 22
11/25/2014 3:03:39 PM
Ushia: Hoja na Majibu
mwanatauhidi atakapoangukia mikononi mwa kundi la waabudu masanamu na wapinzani, kiasi kwamba kama atadhihirisha itikadi yake ya tauhidi, hilo litasababisha damu yake kumwagika au kupata mateso au kupoteza mali yake na familia yake, hapo atawaficha itikadi yake ili abaki katika amani mbali na shari yao. Au pindi Mwislamu Shia anapokutana na Mawahabi wenye chuki binafsi ambao wanahalalisha kumwaga damu ya Mashia, hakika yeye atawaficha itikadi yake ili kuhifadhi nafsi yake, mali yake na familia yake. Na kila mwenye akili timamu anakiri kuwa kitendo hiki ni cha kimantiki, na akili timamu inahukumu hivyo, kwa sababu mtu hapaswi kuiangamiza nafsi yake kwa ajili tu ya kudhihirisha itikadi yake mbele ya watu wenye chuki binafsi. 2. Tofauti baina ya Taqiyyah na Unafiki: Unafiki ni kinyume na Taqiyyah, mnafiki ni yule asiyeamini misingi ya Uislamu kimoyo au mwenye shaka nayo, lakini anadhihirisha Uislamu baina ya Waislamu. Ama Taqiyyah tunayoamini sisi ni kuamini Uislamu sahihi kimoyo, na hili halioani na mtazamo wa baadhi ya Mawahabi wenye misimamo mikali ambao wanawakufurisha Waislamu wote – kasoro wao tu – na wanawazingatia kuwa ni makafiri na hivyo wanawashambulia na kuwatishia. Hivyo iwapo muumini atalificha kundi hili lenye chuki binafsi itikadi yake kwa lengo la kuilinda nafsi yake, mali yake na familia yake, hii ndio Taqiyyah ambayo mkabala wake ni unafiki. 3. Taqiyyah kwa mtazamo wa akili: Katika hali halisi Taqiyyah ni njiia ya kuilinda nafsi, na ndio maana katika riwaya zetu imetambulishwa kama “Ngao 23
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 23
11/25/2014 3:03:39 PM
Ushia: Hoja na Majibu
ya muumini.” Na hakuna akili timamu inayoruhusu mtu kudhihirisha itikadi yake ya kweli (ya moyoni) mbele ya watu wenye kupinga itikadi yake na wasiokuwa na mantiki ikiwa kufanya hivyo ni hatari kwa mhusika na kunaiweka nafsi yake katika mateso, hiyo ni kwa sababu kupoteza nguvukazi na uwezo bila faida si jambo linalokubalika kiakili. Taqiyyah ni sawa na kitendo cha kujificha kinachofanywa na wanajeshi vitani, kwa kuchagua mavazi yaliyo sawa na rangi ya miti, vichaka na maficho, ili kuzilinda nafsi zao na hatari. Hakika watu wote wenye akili timamu ulimwenguni huitumia Taqiyyah mbele za maadui wakali ili kuzilinda nafsi zao, na wala haiwezekani kumlaumu mtu mwenye kutumia njia hii, na wala hatuwezi kumpata mtu duniani mwenye kuikataa Taqiyyah pindi masharti yake yanapotimia. 4. Taqiyyah ndani ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu: Qur’ani Tukufu katika Aya kadhaa imeruhusu kutumia Taqiyyah dhidi ya makafiri na wapinzani, kwa mfano: a. Tunasoma kisa cha muumini aliyekuwa mmoja kati ya watu wa Firaun:
آل ِفرْ َع ْو َن َي ْك ُت ُم إِي َما َن ُه ِ َْو َقا َل َر ُج ٌل م ُْؤ ِمنٌ ِمن َّ ون َرج ًُال أَنْ َيقُو َل َرب َِّي ﷲُ َو َق ْد َجا َء ُك ْم َ ُأَ َت ْق ُتل ۖ ت ِمنْ َر ِّب ُك ْم ِ ِب ْال َب ِّي َنا
“Na akasema mtu Muumini aliyekuwa mmoja wa watu
wa Firaun anayeficha imani yake; je, mtamuua mtu kwa sababu anasema Mola wangu ni Mwenyeezi Mungu? Na kwa hakika amekuleteeni dalili za wazi wazi zitokazo kwa Mola wenu..” (Sura Muumin: 28), na baada tu ya hapo Aya ikaendelea kwa kusema: 24
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 24
11/25/2014 3:03:39 PM
Ushia: Hoja na Majibu
ُ ك َكا ِذبًا َف َع َل ْي ِه َك ِذ ُب ُه ۖ َوإِنْ َي ُ َوإِنْ َي صا ِد ًقا يُصِ ْب ُك ْم َ ك ٌﷲ َال َي ْھدِي َمنْ ھ َُو مُسْ ِرف َ َّ ََّبعْ ضُ الَّذِي َي ِع ُد ُك ْم ۖ إِن ٌَك َّذاب “Naye akiwa muongo, basi uwongo wake ni juu yake, na kama akiwa mkweli, yatakufikieni baadhi ya hayo anayo kuahidini. Bila shaka Mwenyeezi Mungu hamuongozi yule apitaye kiasi, muongo mkubwa.” (Sura Muumin: 28), Kwa msingi huu muumini aliyekuwa mmoja kati ya watu wa Firaun, wakati alipotumia Taqiyyah alitoa nasaha zake kwa kundi hilo lenye chuki ambalo lilikuwa linataka kumwaga damu ya Nabii wa Mwenyezi Mungu Musa (as).
b. Na katika sehemu nyingine tunasoma amri bayana isemayo: “Wenye kuamini wasiwafanye makafiri kuwa viongozi badala ya wenye kuamini, na atakayefanya hivyo, basi hana chochote kwa Mwenyeezi Mungu, ila mtakapojilinda nao kwa kujihifadhi..” (Sura Imran: 28). Aya hii inakataza kuwa na mahusiano ya upendo na maadui wa haki, isipokuwa kama kutokuwa na mahusiano na wao kutasababisha Waislamu kutumbukia katika matatizo na adha, hapo kuwa na mahusiano ya upendo pamoja nao kwa kutumia Taqiyyah kunakuwa ni moja ya aina za kuilinda nafsi. c. Wafasiri wote wa Qur’ani wananukuu kisa cha Ammar bin Yasir, mama yake na baba yake, kuwa wao wote watatu walidondokea mikononi mwa Mushrikina wa Kiarabu, nao wakawatesa na kuwalazimisha kumkana Nabii wa Uislamu. Mzazi wa kiume wa Ammari pamoja 25
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 25
11/25/2014 3:03:39 PM
Ushia: Hoja na Majibu
na mama yake wao waliwakatalia, na wakafariki wakiwa katika hali hii, ama Ammari yeye alitamka kwa Taqiyyah yale waliyoyataka, na baada ya hapo alikwenda mbele ya Mtukufu Mtume (saww) huku akilia, na ni wakati huo iliteremka Aya tukufu:
ا� ِمنْ َبعْ ِد إِي َما ِن ِه إِ َّال َمنْ أ ُ ْك ِر َه َو َق ْل ُب ُه ِ َّ َمنْ َك َف َر ِب ْ ص ْدرً ا َ ان َو ٰ َل ِكنْ َمنْ َش َر َح ِب ْال ُك ْف ِر ِ اإلي َم ِ ْ مُط َمئِنٌّ ِب ﷲ َو َل ُھ ْم َع َذابٌ عَظِ ي ٌم ِ َّ ضبٌ م َِن َ َف َع َلي ِْھ ْم َغ “Anayemkataa Mwenyezi Mungu baada ya imani yake (ataadhibiwa) isipokuwa yule aliyelazimishwa hali moyo wake unatulia kwa imani, lakini anayefungua kifua kwa kufru, basi ghadhabu ya Mwenyezi Mungu iko juu yao, na watapata adhabu kubwa.” (Sura Nahli: 106), Mtukufu Mtume akawahesabu wazazi wa Ammar kuwa miongoni mwa wafiadini, na akamfuta Ammar machozi na kumwambia: “Huna dhambi, wakirudia tena kukulazimisha rudia tena hayo maneno.”
Kuafikiana kwa wafasiri wote kuwa Aya hii iliteremka kwa ajili ya Ammari na wazazi wake, na kuwa baada ya Aya ilifuata hadithi ya Mtukufu Mtume (saww), kunaashiria kuwa wote wamekubali suala la Taqiyyah. Lakini jambo linaloshangaza ni kuwa licha ya uwepo wa dalili zote hizi za Qur’ani madhubuti na maneno ya wafasiri wa Qur’ani wa Kisunni, bado wanawalaumu Mashia kwa kukubali kwao Taqiyyah. Ammari hakuwa mnafiki, wala muumini aliyekuwa katika watu wa Firaun hakuwa mnafiki, hiyo ni kwakuwa walifaidika na Taqiyyah kulingana na maamrisho ya Mwenyezi Mungu. 26
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 26
11/25/2014 3:03:39 PM
Ushia: Hoja na Majibu
5. Taqiyyah ndani ya riwaya za Kiislamu: Pia riwaya za Kiislamu zimezungumzia Taqiyyah kwa mapana, na kwa mfano tu ni katika Musnad Abi Shaybah, kitabu ambacho ni moja kati ya Musnadi maarufu kwa Masunni, yeye ananukuu kisa cha Musaylamah al-Kadhab, ambapo Musaylamah aliwateka watu wawili miongoni mwa masahaba wa Mtume (saww) katika mji aliokuwa anaudhibiti, na akamuuliza kila mmoja wao: “Je mnashahidia kuwa mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu?” Mmoja wao akakiri hilo na akawa ameiokoa nafsi yake, lakini yule wa pili hakukiri hivyo akakatwa kichwa chake. Zilipofika habari hizi kwa Mtukufu Mtume (saww) alisema: “Ama yule aliyeuawa alikuwa katika njia ya ukweli na haki. Na ama wa pili yeye ameruhusiwa na Mwenyezi Mungu na hana dhambi.”12 Na katika hadithi za Maimamu wa Ahlul-Baiti (as) - na hasa kutoka kwa Maimamu ambao waliishi katika zama za utawala wa Bani Umaiyyah na Bani Abbas ambao walikuwa wakimuuwa kila wanayemkuta kuwa ni mwenye kumpenda Ali bin Abu Talib (as) – tunakuta amri nyingi zinazoamrisha kutumia Taqiyyah, nao wameamrishwa kuzilinda nafsi zao kwa kutumia Taqiyyah, kuzilinda nafsi zao dhidi ya hawa wauwaji makatili. 6. Je Taqiyyah inaruhusiwa mbele ya makafiri tu? Baadhi ya wapingaji pindi wanapokutana na riwaya zinazotamka bayana Taqiyyah ambazo tumezitaja huko nyuma wanakuwa hawana nafasi isipokuwa kukubali suala la uwepo wa Taqiyyah kisharia, lakini wao hulihusisha hilo dhidi ya makafiri tu, na wala hawaoni kuwa Taqiyyah 12
Musnad Abi Shaybah Juz. 12, Uk. 358. 27
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 27
11/25/2014 3:03:39 PM
Ushia: Hoja na Majibu
inaruhusiwa kisharia dhidi ya Waislamu. Kwa ufafanuzi zaidi ni kuwa kutokana na dalili zilizotangulia hakuna tofauti katika hilo baina ya Mwislamu na asiyekuwa Mwislamu, hivyo tunasema: 1. Ikiwa maana ya Taqiyyah ni kuilinda nafsi, mali na familia dhidi ya watu waovu wenye chuki binafsi, basi ni ipi tofauti baina ya majahili miongoni mwa Waislamu wenye chuki binafsi na makafiri? Na ikiwa akili ndio inahukumu wajibu wa kuvilinda vitu hivi na kutokuimwaga damu bila uhalali, basi kuna tofauti gani baina ya Mwislamu na kafiri? a sisi tunajua kuwa kuna watu wasio na ufahamu sahihi N wameathiriwa na habari zenye sumu na propaganda mbaya, hawa wanaona kumwaga damu ya Shia kunawaweka karibu na Mwenyezi Mungu, hivyo Shia mwenye imani ya dhati ambaye ni mfuasi wa Imam Ali (a.s.) na watu wa Nyumba ya Mtume (saww) akikutana na watu hawa na wakamuuliza ni ipi madhehebu yake? Je mwenye akili timamu atathubutu kumtaka awajibu bayana kuwa yeye ni Shia ili aiweke nafsi yake katika hali ya kutendewa ubaya na kukatwa shingo yake?!
Kwa ibara nyingine ni kuwa laiti tukitoa hukumu kama wao wasemavyo, ya kuharamisha Taqiyyah mkabala na matendo waliyoyatenda Mushrikina dhidi ya Ammar bin Yasir, au mkabala na aliyoyatenda Musaylamah alKadhabu dhidi ya Masahaba wa Mtukufu Mtume (saww), au mkabala na matendo ya watawala wa Kibani Umaiyyah na Kibani Abbas, na kadhalika mkabala na matendo ya baadhi ya Waislamu majahili wanayoyatenda dhidi ya wafuasi wa Ali (a.s.), kuharamisha huko kutakuwa ni 28
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 28
11/25/2014 3:03:40 PM
Ushia: Hoja na Majibu
sababu ya kuteketea kwa maelfu ya wafuasi wa dhati wa Ahlul-Baiti (as), kwa sababu kidhahiri watawala hawa madhalimu ni Waislamu. ama Ahlul-Baiti (as) wasingesisitiza suala la Taqiyyah K kwa wingi kiasi cha kusema: “Tisa ya kumi ya dini ni Taqiyyah.”13 Basi idadi ya Mashia ambao wangeuwawa katika zama za Bani Umaiyyah na Bani Abbas ingekuwa ni maelfu ya watu mara dufu ya idadi ya wale waliouwawa kinyama bila huruma. Katika mazingira haya je inawezekana kuwa na shaka na uhalali wa Taqiyyah kisharia?! a sisi hatusahau zile damu zilizomwagwa baina ya N Masunni muda wa miaka kadhaa kwa sababu tu ya tofauti za kimadhehebu, likiwemo suala la je Qur’ani ni ya tangu milele au si ya tangu milele? Ugomvi ambao wahakiki wa sasa wanaona kuwa ni ugomvi usiokuwa na maana wala faida. Hivyo kundi linalodai kuwa liko katika haki likiangukia mikononi mwa wanaolipinga, je linapasa kujibu bayana maswali yao ya kiitikadi? Kuwa itikadi yetu ni kadha wakadha, hata kama kujibu huku bayana kutapelekea kumwaga damu zao bila umwagaji huu wa damu kuwa na athari na faida yoyote inayotarajiwa? 2. Fakhru Raziy katika tafsiri yake ya Aya tukufu: “Ila mtakapojilinda nao kwa kujihifadhi..” (Sura Imran: 28) anasema: “Dhahiri ya Aya inajulisha kuwa Taqiyyah ni halali inapokuwa ni dhidi ya makafiri wenye nguvu, isipokuwa madhehebu ya Shafi huhalalisha Taqiyyah kwa ajili ya kulinda nafsi pindi panapotokea hali tete 13
Biharul-An’war Juz. 19, Uk. 254. 29
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 29
11/25/2014 3:03:40 PM
Ushia: Hoja na Majibu
baina ya Waislamu na Mushrikina.” Baada ya Aya hiyo aliitumia kama dalili ya kuthibitisha kuwa Taqiyya inaruhusiwa kwa ajili ya kulinda nafsi, na je inaruhusiwa pia kwa ajili ya kulinda mali, inatarajiwa kuwa itakuwa inaruhusiwa kutokana na kauli ya (saww): “Heshima ya mali ya Mwislamu ni sawa na heshima ya damu yake.” Na kutokana na kauli yake (saww): “Ni mfiadini yule atakayeuwawa kwa ajili ya kutetea mali yake.”14 a pia tunasoma katika tafsiri ya Nisaburiy ambapo N katika tanbihi ya tafsiri Tabari imekuja: “Shafi amesema: Inaruhusiwa kufanya Taqiyyah baina ya Waislamu kama inavyoruhusiwa baina ya makafiri kwa ajili ya kuihami nafsi.”15 3. Na la kuvutia ni kwamba kuna kundi la wanahadithi wa Kisunni na kwa sababu ya kuamini kwao kuwa Qur’ani Tukufu ni ya tangu milele, walitumia Taqiyyah pindi walipojikuta chini ya ugandamizaji wa serikali ya Bani Abbas na wakakiri kuwa si ya tangu milele, ili kuziokoa nafsi zao. a mwanahistoria maarufu Ibn Saad katika kitabu N Tabaqat, pia Tabari katika kitabu chake mashuhuri Taarikh Tabari, wote wameashiria barua mbili kutoka kwa Maamun alizozituma kwenda kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi wa Baghdad Is’haqa bin Ibrahim, ambapo katika barua ya kwanza Ibn Saad amesema: “Maamun alimwandikia barua Is’haqa bin Ibrahim akiteua watu saba, miongoni mwao ni Muhammad bin Saad al-Waqidiy, 14
Tafsirul-Kabir cha Fakhru Raziy Juz. 8, Uk. 14.
15
Tafsiri Nisaburiy katika Tanbihi ya Tafsiri ya Tabari Juz. 3, Uk. 118. 30
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 30
11/25/2014 3:03:40 PM
Ushia: Hoja na Majibu
Abu Muslim Yazid bin Harun, Yahya bin Muin, Zuhair bin Harbu Abu Khaythamah, Ismail bin Daud, Ismail bin Abi Masuud, na Ahmad bin Dawraqiy, wakafika mbele yake na akawatahini na kuwauliza kuhusu kuumbwa kwa Qur’ani, wote wakajibu kuwa Qur’ani ni kiumbe.”16 Licha ya kwamba rai mashuhuri baina ya wanahadithi ni kuwa Qur’ani ni ya tangu milele (si kiumbe), na hii ndio itikadi waliyokuwa wanaamini watu hawa saba. Ndiyo hawa waliafikiana na Maamun kwa kukhofia adhabu yake kali na wakakiri kuwa Qur’ani ni kiumbe, naye akawaacha huru. a inafuata barua ya pili ambapo Tabari ananukuu barua N nyingine kutoka kwa Maamun ambayo nayo anamtumia Mkuu wa Jeshi la Polisi wa Baghdad, Tabari anasema: “Barua ya Maamun ilipofika, Is’haqa bin Ibrahim aliwaita mbele yake jamaa miongoni mwa wanafiqhi na wanahadithi, idadi yao ilifikia takribani watu ishirini na sita, akawasomea barua ya Maamun mara mbili mpaka wakaielewa, kisha akaanza kumwita mmoja baada ya mwingine ili wadhihirishe itikadi yao kuhusu Qur’ani, wote wakakiri kuwa Qur’ani ni kiumbe, hivyo akawaacha huru isipokuwa watu wanne ambao ni Ahmad bin Hanbal, Sajadah, al-Qawaririy na Muhammad bin Nuh. Mkuu wa Jeshi la Polisi akaamuru wafungwe minyororo na kuwekwa gerezani. Ilipofika siku ya pili aliwaita tena na kurudia mbele yao maneno kuhusu Qur’ani, hapo Sajadah akakiri kuwa Qur’ani ni kiumbe, hivyo akaachwa huru, lakini waliobaki wakaendelea kukhalifu, naye 16
aarikh Tabariy Juz. 7 Uk. 197. Tabaqat Ibn Saad Juz. 7 Uk. 167 chapa ya T Beirut. 31
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 31
11/25/2014 3:03:40 PM
Ushia: Hoja na Majibu
akawarudisha tena gerezani. Ilipofika siku ya tatu aliwaita na hapo al-Qawaririy akatengua msimamo wake naye akaachwa huru, lakini Ahmad bin Hanbal na Muhammad bin Nuh wakaendelea na msimamo wao, ndipo Mkuu wa Jeshi la Polisi akawapeleka uhamishoni katika mji wa Tartusi.” Na wale waliotumia Taqiyyah waliposhutumiwa na baadhi ya watu, walijitetea kwa kutumia msimamo wa Ammar bin Yasir dhidi ya makafiri.17 akika yote haya yanajulisha bayana kuwa pindi njia ya H uokovu wa mtu inapofungika katika Taqiyyah tu pindi anapokuwa katika mgandamizo mkubwa kutoka kwa madhalimu, anaweza kuchagua Taqiyyah kuwa njia ya kuilinda na kuihifadhi nafsi dhidi ya dhulma za makafiri au za Waislamu. 7. Taqiyyah ambayo ni haramu: Katika baadhi ya hali ni haramu kufanya Taqiyyah, na hiyo ni iwapo kutumia Taqiyyah kwa mtu kuficha itikadi yake au madhehebu yake, kutapelekea kuiweka misingi ya Uislamu katika hatari au kuiweka jamii ya Kiislamu katika madhara makubwa, katika hali kama hii ni wajibu mtu adhihirishe itikadi yake ya kweli hata kama kufanya hivyo kutampelekea yeye kutumbukia katika madhara. Na hawa wanadhani Taqiyyah ni kuiingiza nafsi katika maangamio, kwa sababu Qur’ani imekataza bayana kujiangamiza iliposema: “Msijiingize wenyewe katika maangamio.” (Sura al-Baqarah: 195). Na hii ni ishtibahi kubwa, kwa sababu kwa maana hii itakuwa ni haramu kuhudhuria katika medani ya Jihadi, wakati ambapo hakuna 17 Tarikh Tabari Juz. 7, Uk. 197. 32
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 32
11/25/2014 3:03:40 PM
Ushia: Hoja na Majibu
yeyote mwenye akili anayeweza kuthubutu kutamka hili. Na hapa ndipo inapobainika bayana kuwa mapinduzi ya Imam Husain bin Ali (a.s.) dhidi ya Yazid yalikuwa ni wajibu wa kidini, na Imam hakuwa tayari kumuimarisha Yazid na wafuasi wake na Bani Umaiyyah waliopora ukhalifa wa Waislamu, kwa sababu yeye alikuwa anajua kuwa hilo litauletea Uislamu madhara makubwa, na kwamba mapinduzi yake na kufa kwake kishahidi kutakuwa ni sababu ya Waislamu kuamka na kuokoka kwao dhidi ya ujahiliya. 8. Taqiyyah ya Umoja: Aina hii ya Taqiyyah hutumiwa na wanamadhehebu bila ya kusababisha madhara juu ya misingi ya dini au ya madhehebu, nayo ni kwa kusaidiana na makundi mengine ya Waislamu kwa lengo la kulinda umoja wao. Kwa mfano tu ni kwamba wafuasi wa madhehebu ya Ahlul-Baiti (as) wanaamini kuwa hairuhusiwi kusujudu juu ya busati, na ni lazima kusujudu juu ya jiwe au kitu kingine ambacho ni sehemu ya ardhi, na dalili yao katika hilo ni hadithi maarufu kutoka kwa Mtukufu Mtume (saww) ambapo anasema: “Nimefanyiwa ardhi hii kuwa ni sehemu ya kusujudia na kujitoharishia.�18 Hivyo wafuasi wa Ahlul-Baiti (as) wakitaka kulinda umoja baina ya Waislamu wanaweza kusali katika misikiti ya Waislamu wa madhehebu mengine au katika Msikiti Mtakatifu au katika Msikiti wa Mtume (saww) na kusujudu juu ya busati kama Waislamu wengine wenye kusali. Kitendo hiki kinaruhusiwa na Sala hii kwa mujibu wa itikadi yetu ni sahihi, na hii inaitwa Taqiyyah ya umoja, hiyo ni kwa sababu suala la kukhofia kupoteza nafsi na mali halihusiki, bali suala 18
S ahih Bukhar Juz. 1, Uk. 91. Sunanul-Bayhaqiy Juz. 2, Uk. 433. Na kuna vitabu vingine vingi ambavyo navyo vimepokea hadithi hii. 33
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 33
11/25/2014 3:03:40 PM
Ushia: Hoja na Majibu
linalohusika ni kuwa na umoja pamoja na makundi mengine ya Kiislamu. Na tunakamilisha mada ya Taqiyyah kwa mazungumzo ya mmoja kati ya Ulamaa wakubwa, ambapo mmoja kati ya ma-Ulamaa wakubwa wa Kishia alikutana na mmoja kati ya Masheikh wa Chuo Kikuu cha Azhari huko Misri, na Shekhe huyo akataka kumdhihaki aalimu huyu wa Kishia, akamwambia: “Tumesikia kuwa nyinyi mnatumia Taqiyyah!!” Aalimu wa Kishia akamjibu kwa kusema: “Mwenyezi Mungu amlaani anayetusababisha tutumie Taqiyyah.”
34
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 34
11/25/2014 3:03:40 PM
Ushia: Hoja na Majibu
MADA YA TATU UADILIFU WA MASAHABA
N
i jambo lisilo na shaka kuwa Masahaba wa Mtukufu Mtume (saww) wana sifa za kipekee, kwani wao walikuwa wanasikia Aya na wahyi wa Mwenyezi Mungu kupitia ulimi wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) na wanaona miujiza yake, na wanajifunza kupitia maneno yake na wanamfanya kiigizo cha kimatendo na kigezo chema. Na kwa shakhsia hizi za pekee ulimwengu wa Kiislamu ukachomoza, ukajifakharisha na kujisifu. Lakini suala muhimu hapa ni je Masahaba wote bila kumtoa yeyote miongoni mwao ni watu waumini, wema, wakweli, waaminifu, waadilifu? Au miongoni mwao wapo watu wasiokuwa wema? 1. Rai mbili zenye kupingana: Kuna rai mbili zenye kupingana kuhusu Masahaba: Rai ya Kwanza: Ni kuwa Maswahaba bila kumtoa hata mmoja, wote wana utakatifu maalumu, hivyo wao ni watu wema, wakweli, wachamungu na waadilifu. Na kwa msingi huu kila riwaya wanayoinukuu kutoka kwa Mtukufu Mtume (saww) ni riwaya sahihi na yenye kukubalika, na wala haiwezekani kabisa kuipinga, na ni lazima kuelekeza kwingine ukiukaji wowote unaojitokeza toka kwa Sahaba, na hii ndio rai na itikadi ya makundi mengi ya Kisunni. Rai ya Pili: Ni kuwa hata kama kuna watu watakashifu, wenye kujitolea na wachamungu baina ya Masahaba, ila 35
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 35
11/25/2014 3:03:40 PM
Ushia: Hoja na Majibu
pia wapo watu wengine miongoni mwao ambao ni wanafiki wasiokuwa wema, na Qur’ani Tukufu pamoja na Nabii wa Uislamu alionesha upinzani wake dhidi ya watu hawa. Kwa ibara nyingine ni kuwa hakika vigezo tunavyovitumia katika kupambanua watu wema na wasiokuwa wema ndio hivyo hivyo vinavyopasa kuwa vigezo vya kuainishia wema wa watu hawa (Maswahaba). Ndiyo, kwa kuwa wao ni Masahaba wa Mtukufu Mtume (saww), asili yao ni wema, lakini kuna ukweli ambao haiwezekani kuupuuza, haiwezekani kufumbia macho matendo waliyoyatenda ambayo yanapingana na uadilifu, ukweli na msimanmo wa sawa, kwa sababu matendo haya yana athari kubwa juu ya uhalisia wa Uislamu na Waislamu, na yanasaidia wanafiki kutekeleza matakwa yao katika jamii ya Kiislamu. Hivyo Shia na baadhi ya Masunni, wao wanafuata rai hii. 2. Usafishaji wa kupindukia Kuna kundi lenye kufuata fikra ya kuwasafisha Masahaba ambapo limepindukia katika kuwatetea, hivyo anapotokea mtu yeyote kuwakosoa (Masahaba) mara wao humtuhumu kwa uovu, na mara nyingine kwa upagani, uzandiki au huhalalisha damu yake. Miongoni mwa tunayoyakuta katika kitabu al-Iswabah kutoka kwa Abu Zar’ah, amesema: “Ukimuona mtu anamkosoa yeyote miongoni mwa Masahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu jua mtu huyo ni mzandiki, hiyo ni kwa sababu Mtume ni haki, Qur’ani ni haki, na aliyokuja nayo ni haki, na yote hayo tumefikishiwa na Masahaba. Na hawa mazandiki wanataka kuwatia doa mashuhuda wetu ili wabatilishe Kitabu na Sunnah, hivyo kuwatia doa wao ni bora zaidi.”19 19
Al-Iswabah Juz. 1, Uk. 22, Chapa ya Kwanza, Darul-Kutubu al-Ilmiyah, Beirut. 36
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 36
11/25/2014 3:03:40 PM
Ushia: Hoja na Majibu
Miongoni mwao ni Abdullah al-Muswiliy katika kitabu chake Hata La Nan’khadiu ambapo anasema: “Hakika wao (Masahaba) ni watu ambao Mwenyezi Mungu aliwateua kusuhubiana na Mtume wake (saww), kusimamisha dini yake na sheria yake. Na akawafanya Mawaziri wa Nabii wake (saww) na warithi wake baada yake, kuwapenda ni dini na imani na kuwachukia ni ukafiri na unafiki. Na ameuwajibisha umma wote kuwapenda wote na kutaja mema yao na fadhila zao na kunyamazia ugomvi uliotokea baina yao.”20 Wakati ambapo tunaona maneno haya ni kinyume na Kitabu na Sunnah. 3. Maswali yasiyo na majibu Mtu yeyote mwenye akili timamu na mwadilifu hawezi kukubali kufumba macho mbele ya maneno yasiyokuwa na dalili, na hapa ndipo yanapojitokeza maswali kadhaa: Mwenyezi Mungu Mtukufu anatwambia katika Qur’ani yake Tukufu kuhusu wake wa Mtume (saww):
ْاعف ِ َْيا ن َِسا َء ال َّن ِبيِّ َمنْ َيأ َ ُض َ ت ِم ْن ُكنَّ ِب َفا ِح َش ٍة ُم َب ِّي َن ٍة ي ﷲ يَسِ يرً ا َ ْن ۚ َو َك ِ َّ ان ٰ َذل َِك َع َلى ِ َل َھا ْال َع َذابُ ضِ عْ َفي “Enyi wake wa Nabii! Atakayefanya maovu dhahiri miongoni mwenu, atazidishiwa adhabu mara mbili, na hayo ni rahisi kwa Mwenyeezi Mungu.” (Sura Ahzab: 30).
Hata tukitafsiri Sahaba kwa maana yoyote ile bila shaka wake wa Mtume (saww) watakuwa ni miongoni mwa mifano yake halisi, lakini bado Qur’ani inatamka bayana kuwa Mwenyezi 20
Hata La Nan’khadiu Uk. 6, Darul-Iman. 37
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 37
11/25/2014 3:03:40 PM
Ushia: Hoja na Majibu
Mungu hatafumbia macho madhambi yao, bali atawaongezea maradufu adhabu. Sasa je tuchukue Aya au tuchukue maneno ya wenye kuwasafisha bila sharti na mipaka? Na pia Qur’ani Tukufu inatusimulia makosa ya mtoto wa Nuh (as) shekhe wa Manabii, inasema:
ۖ صال ٍِح َ ك ۖ إِ َّن ُه َع َم ٌل َغ ْي ُر َ ِْس ِمنْ أَھْ ل َ َقا َل َيا ُنو ُح إِ َّن ُه َلي “Akasema: Ewe Nuhu! Hakika huyo si miongoni mwa watu wako, hakika yeye ni (mwenye) mwendo usio mzuri…..” (Sura Hud: 46), na Mwenyezi Mungu akamhadharisha Nuh asiweze َُوا ا ْم َرأ َّ Nabii kumuombea. muhimu, َ َ َرأJe َ aliye ب ۖ ٍت لُوط َوا ْمniوح ت ُن ِين َك َفر ِ َم َث ًال لwa َ ض َر َ au Maswaَ لَّذmtoto ُﷲ ٍ yupi haba wa Mtume? َ ُ َ َّ َّ َ
َ َقا َلكا َني َتاا ن َتوحْ ُح ل كَن ۖا إِن َُه ص َاملا ٍِح َف ۖل ْم ي ُْغ ِن َيا ْن َْن َف َغ ْ َيخا ُر َن َتا ُھ َ ْس ِمنْ أعِھْ َبلِا ِد ٌِ صال َع َِح َمي ِ َ تإِن ُه َع ْبل َيدي ِين ار َم َع ال ا َوقِي َل ْاد ُخ َال الkuhusu ﷲ َش ْي ًئ َع ْن ُھ َما مwawili wa َ َّدا ِخلTukufu َ َّنinatusimulia ِ َّ َِنwake Na Qur’ani
Manabii, wa Nabii Nuh na Nabii Lut (as), inasema:
َّ ب َ َوح َوا ْم َرأ َ َِين َك َفرُوا ا ْم َرأ ۖ ٍت لُوط َ ض َر َ َ ﷲُ َم َث ًال لِلَّذ ٍ ت ُن َ َْكا َن َتا َتح ْن َف َخا َن َتا ُھ َما َف َل ْم ي ُْغ ِن َيا َ ْن ِمنْ عِ َبا ِد َنا ِ صال َِحي ِ ت َع ْب َدي ِين َ ار َم َع ال َّدا ِخل َ ﷲ َش ْي ًئا َوقِي َل ْاد ُخ َال ال َّن ِ َّ َع ْن ُھ َما م َِن “Mwenyezi Mungu amepiga mfano wa waliokufuru, kwa mke wa Nuh na mke wa Lut; hawa wawili walikuwa chini ya waja wema wawili miongoni mwa waja wetu, basi (wanawake hao) wakawafanyia khiyana, (lakini waume zao) hawakuwasaidia chochote mbele ya Mwenyezi Mungu, na ikasemwa ingieni Motoni pamoja na waingiao.” (Sura Tahrim: 10). Hawa ni wanawake wawili ambao waliwafanyia khiyana waume zao (Nuh na Lut) na wakashirikiana na maadui, na Manabii hawa wawili hawakuweza kuwaombea. 38
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 38
11/25/2014 3:03:40 PM
Ushia: Hoja na Majibu
Je Aya hii haijatamka bayana kuwa kipimo cha wema wa mtu na uovu wake ni kuwa na imani na matendo mema?! Na kipimo hiki kinahusika kwa mtoto wa Nabii au mke wake pindi matendo yake yanapokuwa mabaya. Je katika hali hii inasihi tufumbe macho yetu na tuseme: “Hakika kumpenda ni dini na imani, na kumkhalifu ni ukafiri na unafiki, kwa sababu tu yeye ni miongoni mwa Masahaba?” hata kama baadaye alijiunga na safu za wanafiki na akauudhi moyo wa Mtume na kuwasaliti Waislamu? Je mtu mwenye akili timamu au mwanafikra timamu anakubali maneno haya? Mmoja wao akisema: “Hakika Talha na Zubayri mwanzo walikuwa watu wema, lakini ilipokuja serikali yenye kukhalifu matamanio yao waliungana na mke wa Mtume (saww) (Aisha) baada ya kuwa wamempa Imam Ali (a.s.) kiapo cha utii pale Waislamu wote walipompa kiapo cha utii, wakawasha moto wa Vita vya Ngamia ambavyo wahanga wake walifikia Waislamu elfu kumi na saba, ambapo hao wawili waliacha njia nyoofu. Na damu zote hizi ambazo zilimwagika ni wao ndio watakaobeba mzigo wake na kuulizwa Siku ya Kiyama.” Je maneno haya si sahihi? Au je mtu kusema kuwa: “Hakika Muawiya ni mtu dhalimu kwa sababu ya kukataa kwake kumpa kiapo cha utii Ali (a.s.) na kwa kutokukubali kwake haki ambayo waliikubali Waislamu wote, wa kawaida na walio makhususi, na kwa kuwasha kwake moto wa Vita vya Suffin ambavyo wahanga wake walifikia zaidi ya watu laki mbili ambao damu zao zilimwagika.” Je kauli hii si sahihi? Je inawezekana kufumbia macho ukweli huu uliotokea katika historia? Kwa kweli hakuna yeyote mwenye akili timamu anayekubali visingizio hivyo pindi anapopita kwenye 39
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 39
11/25/2014 3:03:40 PM
Ushia: Hoja na Majibu
matukio haya yenye kusikitisha sana. Je kuwapenda watu hawa – kama asemavyo Abdullah al-Muswiliy – ni dini na imani na kuwachukia ni ukafiri na unafiki? Je wadhifa wetu ni kukaa kimya mbele ya ukiukaji huu ambao ulisababisha vifo vya maelfu ya watu? Ni akili gani inayohukumu hilo? Qur’ani inazungumzia uwepo wa kundi la wanafiki lililomzunguka Mtume (saww), je tunapasa kuzipuuza Aya hizi? Mwenyezi Mungu anasema:
ۖ ون ۖ َو ِمنْ أَھْ ِل ْال َمدِي َن ِة ِ َو ِممَّنْ َح ْو َل ُك ْم م َِن ْاألَعْ َرا َ ُب ُم َنا ِفق اق َال َتعْ َل ُم ُھ ْم ۖ َنحْ نُ َنعْ َل ُم ُھ ْم ۚ َس ُن َع ِّذ ُب ُھ ْم ِ َم َر ُدوا َع َلى ال ِّن َف ٍ ون إِ َل ٰى َع َذا ب َعظِ ٍيم َ ْن ُث َّم ي َُر ُّد ِ َمرَّ َتي “Na katika mabedui wanaokaa pembezoni mwenu kuna wanafiki, na katika wenyeji wa Madina (pia) wamebobea katika unafiki, huwajui, sisi tunawajua tutawaadhibu mara mbili, kisha watarudishwa kwenye adhabu kubwa.” (Sura Tawba: 101). Je hivi kweli mtu msomi mwenye akili timamu anaweza kukubali mantiki hii (ya kuwa Masahaba wote ni watu safi)?
4. Maswahaba ni akina nani? Jambo jingine muhimu hapa ni kujua maana ya Swahaba. Ni akina nani hao Maswahaba ambao wamezungushiwa usafi? Ulamaa wa Kisunni wana maelezo na utambulisho wenye kutofautiana kikamilifu kuhusu maana ya Swahaba: i. Baadhi yao wamepanua wigo wa maana ya Swahaba kiasi cha kumjumuisha kila aliyemuona Mtume (saww), maana hii ameitaja Bukhari ambapo anasema: 40
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 40
11/25/2014 3:03:41 PM
Ushia: Hoja na Majibu
“Mwislamu yeyote aliyemwandama Mtume (saww) au kumuona, huyo ni miongoni mwa Maswahaba zake.”21
Na Ahmad bin Hanbal naye pia anaona kuwa maana ya Swahaba ni pana, anasema: “Maswahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu ni kila aliyemwandama kwa muda wa mwezi au siku au saa, au aliyemuona.”22 ii. Baadhi yao wamechagua maana finyu kuliko iliyotangulia, miongoni mwao ni Kadhi Abu Bakri Muhammad bin Tayyib, ambapo anasema: “Japokuwa maana ya kilugha ya Swahaba ni pana, isipokuwa umma umejua kuwa istilahi hii haitumiki isipokuwa juu ya yule aliyemwandama Mtume kwa kipindi cha muda uliozoeleka, na si awe amemhudumia Mtume (saww) kwa muda wa saa au amefuatana naye hatua kadhaa, au amesikia kutoka kwake hadithi moja.” iii. Baadhi yao wamekwenda kwenye wigo mfinyu zaidi kuliko uliotangulia, miongoni mwao ni Said bin Musayyab ambapo anasema: “Maswahaba wa Mtume (saww) ni wale tu watu ambao walifuatana naye kwa muda usiopungua mwaka au miaka miwili, na wakashiriki na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) katika vita moja au vita viwili.”23
Huu ndio utambulisho, na kuna utambulisho mwingine ambao tumeuacha kwa kukhofia kurefusha maneno wakati wa kuunukuu, ambao haubainishi vizuri na bayana watu ambao 21
Sahih Bukhari Juz. 4, Uk. 188, Darul-Fikri – Beirut.
22
Usulus-Sunnah, Ahmad bin Hanbal Juz. 1, Uk. 40. Usudul-Ghabah Juz. 1, Uk. 7.
23
Tafsirul-Qurtubiy Juz. 8, Uk. 237. 41
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 41
11/25/2014 3:03:41 PM
Ushia: Hoja na Majibu
usafi huu unawahusu. Lakini wengi kati ya hao waliotoa maana hizo wamechagua maana iliyo pana, na kutofautiana huku katika maana hakuathiri mada yetu, kwani zaidi ya hapo kuna ukinzani mwingi ambao tutautaja baadaye ambao unawahusu wale ambao walifuatana na Mtume (saww) kwa muda mrefu. 5. Sababu za msingi za itikadi ya kuwasafisha: Kuna mfanano baina ya itikadi ya usafi wa kipekee wa Maswahaba na umaasumu ambao haujatajwa si katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu wala katika Sunnah ya Mtume Wake (saww), bali kilichomo ndani ya Kitabu, Sunnah na historia ni kinyume chake, mpaka pakasemwa: “Hakika itikadi hii haikuwepo katika karne ya kwanza, bali ilidhihiri katika karne zilizofuata.” Hivyo ni lazima tuchunguze sababu zilizopelekea kuanzishwa na ni ipi dalili yake. Kuna dalili kadhaa zinazobainisha sababu ya itikadi hii: iv. Hakika dalili bora juu ya kuanzishwa itikadi ya kuwasafisha Maswahaba – kama ilivyotangulia katika mada zilizopita – ni baadhi yao kudhani kuwa kama Maswahaba hawa wote watakosa usafi wao basi utavunjika uhusiano uliyopo baina yao (hao Waislamu) na Mtume (saww), kwa sababu Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah ya Mtume (saww) imetufikia kwa njia yao wao (Maswahaba). Lakini jibu la maneno haya liko bayana, kwa sababu hakuna mtu anayeamini kuwa Maswahaba wote ni waovu na waongo, kwani baina ya Maswahaba wapo wengine wengi ambao ni wa kutegemewa 42
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 42
11/25/2014 3:03:41 PM
Ushia: Hoja na Majibu
na waaminifu, na hawa wanaweza kuwa kiungo baina yetu na Mtukufu Mtume (saww), kama tunavyosema hilo kuhusu Maswahaba wa AhlulBaiti (a.s.). Na la kuangalia ni kwamba licha ya kupita karne nyingi lakini tatizo bado lipo, kwani sisi leo hii tunaungana na zama za Mtukufu Mtume (sawww) kwa njia ya viungo mbalimbali, lakini hakuna mtu anayesema kuwa: “Hakika viungo hawa wote ni waaminifu na wakweli wa kauli, na kwamba wao ni wasafi, na kuwa tusiposema hivyo basi dini yetu itakoma.” Bali wote wanasema: “Ni lazima riwaya zichukuliwe kutoka kwa watu waadilifu na waaminifu.” Na kwa ajili hii ndio maana vimeandikwa vitabu vya tasnia ya hali za wapokezi ili kujua walio waaminifu na wasiokuwa waaminifu. Sasa ni lipi lazuia vigezo hivi visitumike kwa Maswahaba kama vinavyotumika kwa watu wengine? v. B aadhi yao wanaona kuwatia hatiani baadhi ya Maswahaba kunadhoofisha cheo cha Nabii wa Uislamu, hivyo hairuhusiwi kuwagusa. Ni wajibu kumuuliza mtu mwenye kushikamana na dalili hii: Je Qur’ani Tukufu haijawakosoa vikali na kuwafichua wanafiki hawa waliokuwa wamemzunguka Mtume (saww)? Je kuwepo wanafiki pembezoni mwa Maswahaba wenye ikhlasi na walio wakweli kwa Mtume (saww), kunapunguza cheo chake adhimu na kitukufu?! 43
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 43
11/25/2014 3:03:41 PM
Ushia: Hoja na Majibu
Kwa muhtasari ni kuwa daima katika kila zama hakukosekani mtu mwema na mtu muovu, hata katika zama za Manabii watukufu (as), pamoja na hali hiyo bado mtu muovu hachafui cheo chao kitukufu. vi. Hakika kuwagusa Maswahaba kwa kuwatia hatiani na kukosoa matendo yao kutapelekea kuporomosha heshima ya Makhalifa wa mwanzo, hivyo ili kulinda heshima yao ni lazima kusisitiza usafi wa Maswahaba na kuwalinda, ili mtu yeyote asiweze kuviweka katika meza ya uchunguzi vitendo vilivyotokea zama za Uthman katika Hazina Kuu ya Waislamu na katika mambo mengine, na hatimaye Khalifa akawajibika kukosolewa na kuhojiwa juu ya vitendo vyake. Na kwa njia hii wataweza kuhalalisha matendo yote ya Muawiya, kumpinga kwake Kiongozi wa Waislamu Imam Ali (a.s.), kuwasha kwake moto wa vita angamizi na kuuwa kwake Waislamu, ili wamuache nje ya ukosoaji wa wakosoaji. Na lililo bayana katika maneno haya ni kuwa wanasiasa wa karne za mwanzo ndio waliopandikiza usafi huu, kama ilivyotokea katika tafsiri yao ya Aya: “Na wenye mamlaka miongoni mwenu.� (Sura Nisaa: 59) kwa kutafsiri kwa maana ya watawala wa kila zama, ili maana ya neno hili iwajumuishe watawala wote madhalimu wa Bani Umaiyyah na Bani Abbas, na haya yalikuwa ni matokeo ya mipango ya kisiasa ya watawala hawa. Na mimi sidhani kuwa matokeo ya maneno haya yanaoana na akili za wenye kuamini kuwa Masahaba wote ni wasafi. 44
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 44
11/25/2014 3:03:41 PM
Ushia: Hoja na Majibu
vii. Baadhi wanaamini usafi wa Maswahaba kwa sababu ya uwepo wa amri katika baadhi ya Aya za Qur’ani na hadithi za Mtume (saww). hahiri ni kuwa kati ya sababu zote hii ndio bora D zaidi, lakini tunapoijadili dalili hii inabainika kuwa katika Aya hizo au riwaya hizo hakuna mjumuisho katika lile wanalodai, na Aya muhimu wanayoshikamana nayo ni:
ِين ا َّت َبعُو ُھ ْم َ ار َوالَّذ َ ين َو ْاألَ ْن َ ج ِر َ ُون ْاألَوَّ ل َ َُّابق ِ ون م َِن ْال ُم َھا ِ َوالس ِ ص َّ ان َرضِ َي ٍ ﷲُ َع ْن ُھ ْم َو َرضُوا َع ْن ُه َوأَ َع َّد َل ُھ ْم َج َّنا ت َتجْ ِري َتحْ َت َھا ٍ ِبإِحْ َس ٰ ِين فِي َھا أَ َب ًدا ۚ َذل َِك ْال َف ْو ُز ْالعَظِ ي ُم َ ْاألَ ْن َھا ُر َخالِد “Na waliotangulia wa kwanza katika wahajiri na Ansari. Na wale waliowafuata kwa wema, Mwenyezi Mungu yuko radhi nao na wao wako radhi Naye; na amewaandalia Bustani ambazo hupita mito chini yake, watadumu humo milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa.” (Sura Tawba: 100).
Baadhi ya wafasiri wa Kisunni wametaja mwishoni mwa Aya hii, riwaya kutoka kwa Hamid bin Ziyad, kuwa alisema: “Siku moja nilimwambia Muhammad bin Kaab al-Qardhiy, nieleze kuhusu Maswahaba wa Mtume (saww) kwa yale yaliyotokea baina yao, nilikusudia machafuko. Akaniambia: ‘Hakika Mwenyezi Mungu ameshawasamehe wote na akawapa pepo ndani ya Kitabu chake, kuanzia mwema wao mpaka muovu wao.’ Nikamwambia: ‘Ni sehemu ipi ambapo amewapa pepo?’ Akasema: ‘Subhanallah! Hivi hausomi kauli yake Mtukufu: Na waliotangulia wa kwanza katika wahajiri na Ansari.’”24 24
At-Tafsirul-Kabir cha Fakhru Raziy Juz. 16, Uk. 171. 45
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 45
11/25/2014 3:03:41 PM
Ushia: Hoja na Majibu
Na la kuvutia ni kuwa Aya inasema: Hakika uokovu wa Tabiina una sharti la wao kuwafuata Maswahaba katika matendo mema na si katika matendo maovu, na maana yake ni kuwa Maswahaba wamedhaminiwa pepo, je inafahamika kutoka ndani ya maneno haya kuwa wao wako huru katika kutenda maasi? Je inawezekana Mtume (saww) ambaye amekuja kuwaongoa watu na kuwaweka sawa, awabague Maswahaba zake katika maasi wanayoyatenda!! Wakati ambapo Qur’ani Tukufu inawaambia wake wa Mtume (saww) – ambao ni miongoni mwa Masahaba wenye ukaribu sana kwake -:
ْاعف ِ َْيا ِن َسا َء ال َّن ِبيِّ َمنْ َيأ َ ض َ ت ِم ْن ُكنَّ ِب َفا ِح َش ٍة ُم َب ِّي َن ٍة ُي ﷲ يَسِ يرً ا َ ْن ۚ َو َك ِ َّ ك َع َلى َ ِان ٰ َذل ِ َل َھا ْال َع َذابُ ضِ عْ َفي “Enyi wake wa Mtume! Yeyote kati yenu atakayefanya uchafu dhahiri, atazidishiwa adhabu mara mbili. Na hilo kwa Mwenyezi Mungu ni jepesi.” (Sura Ahzab: 30).
َ ار َ ﷲ ۚ َوالَّذ ِ َّ م َُح َّم ٌد َرسُو ُل ِ ِين َم َع ُه أشِ َّدا ُء َع َلى ْال ُك َّف ون َفضْ ًال م َِن َ ُح َما ُء َب ْي َن ُھ ْم ۖ َت َرا ُھ ْم ُر َّكعًا سُجَّ ًدا َي ْب َت ُغ َ ر Na jambo muhimu katika maudhui hii ni kuwa hali ْضْب َويِّا ًنا َم ۖنْ سِ َييأ ْ َ ُ َّ َّ َ َ َ َ ْف ٍ ِّ ُ ٍ ع ا ُض ي ة ن ي ب م ة ش ح ا ف ب ك ن م ت ن ال ء ا ِس ن ا ي َّن ِ ِ ِ َ َ َ َ َ َ ْن ُو ُ ۚ د ُو ج س ال ر ث أ م م ِھ ھ ُو ج ِي ف ھ ا م ر و ﷲ ُّ ِ ِ َ َ ِ ْ ِ katika yoyote ya kutoeleweka ِ Ayaْ hii inaondolewa ِ ِ na Aya ya ِ ٰ ishirini na اtisa ya Sura al-Fathu ambayo inazungumzia َّ ان َذل َِك َع َلى ًﷲ يَسِ ير ْن ۚ َو َك َھا ْال َع َذابُ ضِ عْ َفيsifa َلza َ ِ ِ Maswahaba wa kweli wa Mtume (saww), ambapo inasema: َ ار َ ﷲ ۚ َوالَّذ ِ َّ م َُح َّم ٌد َرسُو ُل ِ ِين َم َع ُه أشِ َّدا ُء َع َلى ْال ُك َّف ون َفضْ ًال م َِن َ ُح َما ُء َب ْي َن ُھ ْم ۖ َت َرا ُھ ْم ُر َّكعًا سُجَّ ًدا َي ْب َت ُغ َ ر ۚ ﷲ َو ِرضْ َوا ًنا ۖ سِ ي َما ُھ ْم فِي وُ جُوھ ِِھ ْم ِمنْ أَ َث ِر ال ُّسجُو ِد ِ َّ 46
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 46
11/25/2014 3:03:41 PM
Ushia: Hoja na Majibu
“Muhammad, Mtume wa Mwenyezi Mungu, na walio pamoja naye, wana nguvu mbele ya makafiri, na wanahurumiana wao kwa wao. Utawaona wakirukuu na kusujudu wakitafuta fadhila na radhi za Mwenyezi Mungu. Alama zao zi katika nyuso zao, kwa athari ya kusujudu….” (48:29)
Je watu ambao waliwasha moto wa machafuko na vita huko Siffin na katika Jamal dhidi ya Imam Ali (a.s.) wakati huo, na wakawaua maelfu ya Waislamu, je wao ni mfano halisi wa sifa saba zilizotajwa ndani ya Aya hii? Na je walikuwa wanahurumiana wao kwa wao? Na je walikuwa na nguvu dhidi ya makafiri au dhidi ya Waislamu? Mwishoni mwa Aya Mwenyezi Mungu anataja bayana kwa ujumla shabaha na makusudio, kwa kusema:
َّ َو َع َد ت ِم ْن ُھ ْم ِ ين آ َم ُنوا َو َع ِملُوا الصَّالِ َحا َ ﷲُ الَّ ِذ َم ْغ ِف َر ًة َوأَجْ رً ا َع ِظيمًا “Mwenyezi Mungu amewaahidi walioamini na wakatenda mema katika wao maghufira na ujira mkubwa.” (Sura Fathu: 29), hivyo ahadi ya maghufira na msamaha mkubwa ni kwa watu hawa ambao wana sifa ya imani na matendo mema, na si wengine.
Je wale waliowauwa Waislamu na kuwasha moto katika Vita vya Jamal na vinginevyo, na wakafanya ubadhirifu wa mali kama ilivyotokea katika zama za Uthman, je hao ni miongoni mwa watu wema? Na cha kuvutia ni kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwalaumu baadhi ya Manabii wake watukufu (as) kwa 47
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 47
11/25/2014 3:03:41 PM
Ushia: Hoja na Majibu
sababu ya wao kuacha lililo bora, na alimtoa Nabii Adam (as) toka peponi kwa sababu ya yeye kuacha lililo bora. Na Nabii Yunus (as) alibakia kwa muda ndani ya tumbo la chewa kwa sababu ya yeye kuacha lililo bora, na hivyo akawekwa ndani ya giza tatu. Pia Nabii Nuh (as) alilaumiwa kwa sababu ya kumuombea mwanawe: “Hakika ni mwendo usio mwema.” Je inaingia akilini Maswahaba wa Nabii wa Uislamu (saww) kuwa ni waliobaguliwa toka ndani ya kanuni hii!! 6. Je Maswahaba wote ni waadilifu bila kubagua: Kama tulivyotaja kuwa wengi miongoni mwa Masunni wanasema: Hakika Maswahaba wote ambao waliishi katika zama za Mtukufu Mtume (saww) au ambao walimdiriki na wakawa pamoja naye katika kipindi cha muda fulani, wote ni waadilifu bila kubagua, na kwamba Qur’ani inathibitisha hilo. Bahati mbaya sana ndugu zetu hawa wameshikilia baadhi ya Aya za Qur’ani ambazo zinaelekeza masilahi kwao, na wamesahau Aya nyingine, Aya ambazo zinabagua jambo hili, na sisi tunajua kuwa mambo yote ya jumla yana mipaka makhususi. Hivyo tunasema ni uadilifu upi huu ambao Qur’ani Tukufu inabainisha kinyume chake katika sehemu kadhaa, miongoni mwa sehemu hizo ni ile iliyokuja katika Sura Imran:
ان إِ َّن َما َ إِنَّ الَّ ِذ ِ ين َت َولَّ ْوا ِم ْن ُك ْم َي ْو َم ْال َت َقى ْال َجمْ َع َّ ض َما َك َسبُوا ۖ َو َل َق ْد َع َفا َ اسْ َت َزلَّ ُھ ُم ال َّشي ِ ْْطانُ ِب َبع ُﷲ ﷲ َغفُو ٌر َحلِي ٌم َ َّ ََّع ْن ُھ ْم ۗ إِن 48
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 48
11/25/2014 3:03:41 PM
Ushia: Hoja na Majibu
“Hakika wale waliogeuka siku yalipokutana makundi mawili, shetani ndiye aliyewatelezesha kwa baadhi ya waliyoyafanya, na Mwenyezi Mungu amekwishawasamehe. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa Maghufira, Mpole.” (Sura Imran: 155). Ambapo inaashiria watu ambao walikimbia katika Vita vya Uhud na wakamuacha Mtukufu Mtume (saww) peke yake mbele ya maadui.
Na tunapata kwa uwazi kabisa kutokana na Aya hii kuwa kulikuwa na kundi lililokimbia, na vitabu vya historia vimetaja kuwa idadi yao ilikuwa kubwa, na kwamba shetani aliwadanganya na kuwashinda kwa sababu ya madhambi waliyotenda, hivyo dhambi zilizotangulia zikawapelekea kukimbia vitani, na kufanya hivyo ni dhambi kubwa. Licha ya kwamba mwishoni mwa Aya inasema kuwa Mwenyezi Mungu ameshawasamehe lakini kitendo cha Mwenyezi Mungu kuwasamehe kwa sababu ya Nabii (saww) haimaanishi wao ni waadilifu na kwamba wao hawajatenda dhambi, bali Qur’ani imetamka bayana kuwa wao walitenda madhambi mbalimbali. Na ni uadilifu upi huu ambapo baadhi yao Mwenyezi Mungu anawatambulisha kwa sifa ya ufasiki, aliposema:
ْاس ٌق ِب َن َبإٍ َف َت َب َّي ُنوا أَن ِ ين آ َم ُنوا إِنْ َجا َء ُك ْم َف َ َيا أَ ُّي َھا الَّ ِذ صيبُوا َق ْومًا ِب َج َھا َل ٍة َف ُتصْ ِبحُوا َع َل ٰى َما َف َع ْل ُت ْم ِ ُت ين َ َنا ِد ِم “Enyi ambao mmeamini! Akiwajia fasiki na habari yoyote, ichunguzeni, msije mkawasibu watu kwa kutojua, na mkawa wenye kujuta kwa mliyoyatenda.” (Sura Hujurat: 6). 49
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 49
11/25/2014 3:03:42 PM
Ushia: Hoja na Majibu
Ni maarufu baina ya wafasiri wa Qur’ani kuwa Aya inamzungumzia Walid bin Uqbah, pale alipotumwa na Mtukufu Mtume (saww), yeye na kundi fulani kwenda kuchukua Zaka kwa Bani Mustalaq, lakini akarudi na kusema: “Wamekataa kutoa Zaka na wameritadi.” Ambapo baadhi ya Waislamu walitosheka na maneno ya Walid na wakajiandaa kuwashambulia Bani Mustalaq na kuwakata vichwa vyao, lakini iliteremka Aya hii tukufu kuja kuwahadharisha Waislamu na kuwaeleza umuhimu wa kuhakikisha habari zinazoletwa na mtu muovu, ili wasije kuwadhuru watu na baadaye wakajutia walilotenda. Na matokeo yake yalikuwa ni kwamba baada ya kufanya uchunguzi waligundua kuwa kabila la Bani Mustalaq bado limo katika imani yake na kwamba lilikuwa linajiandaa kumlaki Walidi, na si kumshambulia Walid na kuritadi. Lakini Walidi – kwa sababu ya ugomvi wake binafsi na wao – alifanya hili kuwa ni sababu ya kuwachongea mbele ya Mtume wa Mwenyezi Mungu na kumpelekea habari zisizo sahihi. Hivyo japokuwa Walidi alikuwa miongoni mwa Maswahaba wa Mtume (saww), kwa maana ya watu ambao walimdiriki Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) na wakamtumikia, isipokuwa Qur’ani imemwita fasiki, sasa je hali hii inaoana na itikadi ya kwamba Masahaba wote ni waadilifu? Ni uadilifu upi huu wa mtu kusimama na kumpinga Mtukufu Mtume (saww) pindi alipotaka kugawa Zaka? Qur’ani Tukufu imenukuu upingaji huu katika Sura Tawba:
50
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 50
11/25/2014 3:03:42 PM
Ushia: Hoja na Majibu
ُ ْت َفإِنْ أُع طوا ِم ْن َھا َّ ك فِي ال ِ ص َد َقا َ َو ِم ْن ُھ ْم َمنْ َي ْل ِم ُز ُ َرضُوا َوإِنْ َل ْم يُعْ َط ْوا ِم ْن َھا إِ َذا ُھ ْم َيسْ َخ ون َ ط ُ ْت َفإِنْ أُع طوا ِم ْن َھا َّ ك فِي ال ِ ص َد َقا َ َو ِم ْن ُھ ْم َمنْ َي ْل ِم ُز ِيا قُل ُھ ْم ِينھافإِ َذ َ ط َ َ ون َط َْوالَّذ ِم ْن ٌض ون َما وب َيِھ ْسْم َ َخم َ ُر ضقُو َوإ َر ْذ َي َ ُْوا ُل َوإِ ْالنْ ُم َن َلا ِْفمقُ يُع ِ Ni uadilifu upi huu pale Mwenyezi Mungu katikaِ Qur’ani َّ Sura Tukufu anapozungumziaُورً ا Vita و َعدَ َناAhzab: ُغرvyaإِ َّالAhzab َرسُولُ ُهkatika ﷲُ َو َ “Na miongoni mwao wako wanaokulaumu katika sadaka. Wanapopewa katika hizo huridhika, na wasipopewa katika hizo huchukia.” (Sura Tawba: 58).
وب ِھ ْم َم َرضٌ َما َ ون َوالَّذ َ َُوإِ ْذ َيقُو ُل ْال ُم َنا ِفق ِ ُِين فِي قُل َّ َو َع َد َنا ﷲُ َو َرسُولُ ُه إِ َّال ُغرُورً ا “Na waliposema wanafiki na wale ambao wana maradhi katika nyoyo zao: Mwenyezi Mungu na Mtume Wake hakutuahidi ila udanganyifu.” (Sura Ahzab: 12). Wengine walikuwa wanafikiri kuwa Mtukufu Mtume (saww) atashindwa katika vita hivi na kwamba wao watauawa na Uislamu utamalizwa. Au ule wa kuhusu ile riwaya iliyonukuliwa na Mashia na Masunni katika kisa maarufu kuwa pindi Mtukufu Mtume (saww) alipokuwa akichimba Handaki alikuta jiwe kubwa akalivunjavunja, na hapo akawaahidi kuwa watashinda kwa kuifungua Sham, Iran na Yemen, baadhi yao wakaipokea habari hii kwa dhihaka, je hawa hawakuwa ni Maswahaba?!
Na la ajabu zaidi ni maelezo yaliyokuja katika Aya iliyofuata, inaposema:
51
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 51
11/25/2014 3:03:42 PM
Ushia: Hoja na Majibu
ْ َوإِ ْذ َقا َل ب َال ُم َقا َم َل ُك ْم َ ت َطا ِئ َف ٌة ِم ْن ُھ ْم َيا أَھْ َل َي ْث ِر ۚ َفارْ ِجعُوا “Na kundi moja miongoni mwao liliposema: Enyi watu wa Yathriba! Hapana pa kukaa nyinyi leo, basi rudini…” (Sura Ahzab: 13). Yaani wanawataka watu wa Madina warejee na kutopigana pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu. Au walilofanya baadhi yao kwa kumuomba idhini Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) ya kukimbia kutoka katika medani ya vita:
ْ َوإِ ْذ َقا َل ب َال ُم َقا َم َل ُك ْم َ ت َطا ِئ َف ٌة ِم ْن ُھ ْم َيا أَھْ َل َي ْث ِر ٌون إِنَّ ُبيُو َت َنا َع ْو َرة ٌ ُوا ۚنُ َف ِر َف َارْو َي ِجسْعَتأْ ِذ َ ُيق ِم ْن ُھ ُم ال َّن ِبيَّ َيقُول ون إِ َّال ف َِرارً ا َ ِي ِب َع ْو َر ٍة ۖ إِنْ ي ُِري ُد َ َو َما ھ
ٌون إِنَّ ُبيُو َت َنا َع ْو َرة ٌ َو َيسْ َتأْ ِذنُ َف ِر َ ُيق ِم ْن ُھ ُم ال َّن ِبيَّ َيقُول ون إِ َّال ف َِرارً ا َ ِي ِب َع ْو َر ٍة ۖ إِنْ ي ُِري ُد َ َو َما ھ “…Na kundi jingine miongoni mwao likaomba ruhusa kwa Mtume wakisema: Hakika nyumba zetu ni tupu. Wala hazikuwa ni tupu; hawakutaka ila kukimbia tu.” (Sura Ahzab: 13). Ambapo wafasiri wametaja sababu mbili zilizopelekea kushuka Aya hii:
Ya kwanza: Baadhi yao wamesema: Hakika inaashiria watu wa Abdullah bin Jubair ambao walikuwa wamekaa juu ya mlima katika Vita vya Uhud, Waislamu walipokaribia kuwashinda maadui, Abdullah pamoja na warusha mishale waliacha sehemu zao na kukimbilia kukusanya ngawira, licha ya kwamba Mtukufu Mtume (saww) alikuwa amewaamuru kutokuacha sehemu zao vyovyote iwavyo. Na baya zaidi ni lile walilosema, kuwa wanakhofia Mtume (saww) asije kupuuza hali zao katika ugawaji wake wa ngawira. Na kwa 52
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 52
11/25/2014 3:03:42 PM
Ushia: Hoja na Majibu
kweli kuna ibara kadhaa ambazo wamezitaja ambazo kalamu inaona aibu kuzitaja. Ya pili: Wameitaja Ibnu Kathir na Tabar mwishoni mwa tafsiri zao za Aya husika, kuwa kuna kipande cha kitambaa chekundu cha thamani ambacho kilitoweka katika Vita vya Badri, hivyo baadhi ya majahili wakamtuhumu Mtukufu Mtume (saww) kuwa amefanya khiyana, na haukupita muda mrefu kikawa kimepatikana, na ikabainika kuwa mmoja kati ya wanajeshi ndiye aliyekuwa amekichukua. Je kunasibisha mambo yote haya na Mtukufu Mtume (saww) kunaafikiana na uadilifu? Hivi tukiifanya akili iwe ndio mwamuzi je itakubali watu hawa kuwa ni waadilifu na wasafi, kiasi kwamba haipasi mtu yeyote kukosoa matendo yao? Sisi hatukatai kuwa wengi miongoni mwa Maswahaba walikuwa huru na wasafi, lakini hatutoi hukumu ya mjumuisho kwamba wote walikuwa safi kwa maji ya uchamungu na uadilifu, na kwamba mtu hana haki ya kukosoa matendo yao vyovyote vile, kwani kwa kweli hili linashangaza waziwazi. Ni uadilifu upi huu? Ambao unawaruhusu baadhi ya watu ambao kidhahiri wanahesabika miongoni mwa Maswahaba wa Mtukufu Mtume (saww), kama vile Muawiya, kujihalalishia kuwatukana na kuwalaani Maswahaba watukufu kama Ali (a.s.), na kuamrisha watu katika nchi zote kufanya kitendo hiki? Ni lazima kuwa makini na hadithi hizi mbili: i. Tunasoma katika Sahih Muslim nacho ndio kitabu chenye kuzingatiwa zaidi kwa Masunni: Kutoka kwa 53
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 53
11/25/2014 3:03:42 PM
Ushia: Hoja na Majibu
Aamir bin Saad bin Abi Waqas, kutoka kwa baba yake, alisema: “Muawiya bin Abu Sufiyan alimwamuru Saad akasema: ‘Ni kitu gani chakuzuia kumtukana Abu Turab?’ Akasema: ‘Kamwe sintomtukana pindi ninapokumbuka mambo matatu aliyoyasema Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) kuhusu yeye, mimi kuwa na moja kati ya hayo ni jambo nilipendalo sana kushinda hata ngamia mwekundu.”25 ii. Tunasoma katika kitabu al-Aqdu al-Farid, kitabu ambacho kimeandikwa na mmoja kati ya Ulamaa wa Kisunni, Ibn Abdurabih al-Undulusiy: “Alipofariki Hasan bin Ali (a.s.), Muawiya alikwenda Hija, alipoingia Madina alitaka kumlaani Ali bin Abu Talib juu ya mimbari ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww), ndipo akaambiwa: ‘Hapa yupo Saad bin Abi Waqas na hatudhani kama ataridhia jambo hili, hivyo mtumie mjumbe na uchukue rai yake.’ Muawiya akamtumia mjumbe na kumweleza jambo hilo, akasema: ‘Kama ukifanya hivyo basi hakika nitatoka msikitini na sintarudi tena msikitini.’ Ndipo Muawiya akajizuia kufanya hivyo mpaka alipofariki Saad, baada ya Saad kufariki alimlaani juu ya mimbari na akawaandikia barua maliwali wake kuwa wamlaani juu ya mimbari, nao wakafanya hivyo. Ummu Salamah mke wa Mtume (saww) akamwandikia barua Muawiya: ‘Hakika nyinyi mnamlaani Mwenyezi Mungu na Mtume wake juu ya mimbari zenu, hiyo 25
S ahih Muslim Juz. 14, Uk. 1871. Fadhailus-Sahabah. Fat’hul-Bariy Fii Sharhi Sahih Bukhari Juz. 7, Uk. 60. Na fadhila tatu zinazomuhusu Ali (a.s.) ambazo zimetajwa katika hadithi husika ni Hadithi ya cheo, Hadithi ya bendera ya Khaibar na Aya ya maapizano. 54
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 54
11/25/2014 3:03:42 PM
Ushia: Hoja na Majibu
ni kwa kuwa nyinyi mnamlaani Ali bin Abu Talib na mwenye kumpenda. Na mimi nashahidia kwamba Mwenyezi Mungu na Mtume Wake wanampenda.’ Lakini Muawiya hakujali maneno yake.”26 Je matendo haya mabaya yanaoana na uadilifu? Je kuna mtu yeyote mwenye akili timamu au mwadilifu anaruhusu kusimama na kumtukana au kumlaani - hasa katika sura hii bayana na pana – mtu mtukufu kama huyu (Ali), ambapo mshairi wa Kiarabu anasema: “Mnamlaani juu ya mimbari kwa kumtusi, wakati ni kwa upanga wake zimesimamishwa nguzo zake (za mimbari)?!. 7. Aina za Maswahaba wa Mtukufu Mtume (saww): Kwa ushahidi wa Qur’ani Tukufu tunaweza kuwagawa Maswahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) katika makundi makuu matano: La kwanza: Wasafi walio wema: Hawa ni kundi la waumini wenye imani ya dhati, ambao imani imeingia ndani ya vina vya nyoyo zao, na hawakusita hata kidogo kujitoa muhanga na fidia katika njia ya Mwenyezi Mungu na katika kulinyanyua Neno Lake, kama Aya ya Qur’ani ilivyowaashiria katika Sura Tawba:
َّ َرضِ َي ٍ ﷲُ َع ْن ُھ ْم َو َرضُوا َع ْن ُه َوأَ َع َّد َل ُھ ْم َج َّنا ت َتجْ ِري ِين فِي َھا أَ َب ًدا ۚ ٰ َذل َِك ْال َف ْو ُز ْالعَظِ ي ُم َ َتحْ َت َھا ْاألَ ْن َھا ُر َخالِد 26
l-Aqdu al-Farid Juz. 5, Uk. 114 na 115, Darul-Kutub al-Ilmiyyah. Jawahirula Matwalib Fii Manaqib Imam Ali bin Abi Talib Juz. 2, Uk. 228. Taalif Muhammad bin Ahmad Damashqiy Shafiiy (alifariki karne ya tisa ya Hijriyyah). 55
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 55
11/25/2014 3:03:42 PM
Ushia: Hoja na Majibu
“….. Mwenyezi Mungu yuko radhi nao na wao wako radhi Naye; na amewaandalia Bustani ambazo hupita mito chini yake, watadumu humo milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa.” (Sura Tawba: 100).
La pili: Waumini wenye dhambi: Hawa ni wale ambao licha ya wao kuwa wanasifika kwa imani na matendo mema lakini nyoyo zao huteleza na huchanganya matendo mema na mabaya, wanakiri madhambi yao na wanataraji kupatwa na msamaha na maghufira. Aya ya mia moja na mbili ya Sura Tawba imeashiria hilo baada ya kuwa imelitaja kundi la kwanza:
ُ وب ِھ ْم َخ َل َ َو صالِحً ا َ طوا َع َم ًال َ آخر ِ ُون اعْ َت َرفُوا ِب ُذ ُن َّ آخ َر َس ِّي ًئا َع َسى َ َو ۚ وب َع َلي ِْھ ْم َ ﷲُ أَنْ َي ُت “Na wengine wamekiri dhambi zao; wakachanganya vitendo vyema na vingine ُ خ َلHuenda َ وب ِھ ْم َ وakaصالِحً ا َع َم ًالviovu. طوا ُذ ُنMwenyezi ِبTawba: َرفُوا102) اعْ َت. Mungu ُون َ pokea َ آخر َ ِ (Sura toba zao…”
َْن
ُ ََ
َ ٌ
َ ُ
ُْ َّ َ ن
َّ
َ
ت َب َّينواWatenda عف َلياسِ ِْھ ْمق ۚ ِبن َبإٍ ف َي َُتجا َء َكHawa ِينس آى َم َو َيkwa ْوا أإِن آخا َرأ ُّي َھساِّي َ َ ًئالذ َعimewaita َ وب ْم La أtatu: maasi: ُنﷲQur’ani jina Mwenyezi ِين َما َف َع ْل ُت ْم َنna َع َل ٰىikaashiria َف ُتصْ ِبحُواhilo َھا َل ٍةkwa مًا ِب َجkauli ُوا َق ْوya صِ يب ُت َ مlaا ِدMafasiki, Mungu: ِْين آ َم ُنوا إِنْ َجا َء ُك ْم َفاسِ ٌق ِب َن َبإٍ َف َت َب َّي ُنوا أَن َ َيا أَ ُّي َھا الَّذ ِين َ ُتصِ يبُوا َق ْومًا ِب َج َھا َل ٍة َف ُتصْ ِبحُوا َع َل ٰى َما َف َع ْل ُت ْم َنا ِدم “Enyi ambao mmeamini! Akiwajia fasiki na habari yoyote, ichunguzeni, msije mkawasibu watu kwa kutojua, na mkawa wenye kujuta kwa mliyoyatenda.” (Sura Hujurat: 6). Na tafsiri zote za Shia na Sunni zimetaja mifano halisi ya Aya hii. 56
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 56
11/25/2014 3:03:42 PM
Ushia: Hoja na Majibu
La nne: Wenye kujionyesha kwa Uislamu: Hawa walikuwa wanadai kuwa ni Waislamu lakini imani haijaingia ndani ya nyoyo zao, Qur’ani imeashiria hilo kwa kusema:
ت ْاألَعْ َرابُ آ َم َّنا ۖ قُ ْل َل ْم ُت ْؤ ِم ُنوا َو ٰ َل ِكنْ قُولُوا ِ َقا َل وب ُك ْم ِ ُأَسْ َل ْم َنا َو َلمَّا َي ْد ُخ ِل ْاإلِي َمانُ فِي قُل “Mabedui walisema: Tumeamini. Sema: Hamjaamini, lakini semeni: Tumesilimu. Kwani imani haijaingia katika nyoyo zenu…” (Sura Hujurat: 14).
ون ۖ َو ِمنْ أَھْ ِل ِ َو ِممَّنْ َح ْو َل ُك ْم م َِن ْاألَعْ َرا َ ُب ُم َنا ِفق La tano: Wanafiki: Nao ni watu ambao waliishi baina ya اق ال ِّن َفbaadhi َع َلىyao َر ُدواwalikuwa ْال َمدِي َن ِة َ ۖ َمmaarufu Waislamu kwa roho ya unafiki, ِ ٰ ْ ِم ُنوا َو َل ِكنmaarufu قُولُواhawakuwa قُ ْل َل ْم ُت ْؤna ۖ َم َّناhawakuwa ْاألعْ َرابُ آnaت َقا َل ِ mchango na wengine wowote katika mapambano ya Uislamu na maendeleo ya َ وب ُك ْم ِ ُاإلي َمانُ فِي قُل ِ ْ أسْ َل ْم َنا َو َلمَّا َي ْد ُخ ِل Waislamu, na hili ndilo lililoashiriwa na Qur’ani Tukufu katika kauli yake:
ون ۖ َو ِمنْ أَھْ ِل ِ َو ِممَّنْ َح ْو َل ُك ْم م َِن ْاألَعْ َرا َ ُب ُم َنا ِفق اق ِ ْال َمدِي َن ِة ۖ َم َر ُدوا َع َلى ال ِّن َف “Na miongoni mwa mabedui walio pembezoni mwenu wamo wanafiki na katika wenyeji wa Madina wako waliobobea katika unafiki...” (Sura Tawba: 101).
Na hakuna shaka kuwa hawa wote walimuona Mtume (saww), wakamwandama na kuishi naye, na wengi wao walishiriki katika vita mbalimbali, na maana yoyote 57
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 57
11/25/2014 3:03:43 PM
Ushia: Hoja na Majibu
ya Swahaba inayajumuisha makundi yote matano, je inawezekana kusema hawa wote ni wasafi na watu wa peponi? Hivi si inafaa hapa kuchagua msitari wa kati baada ya maelezo haya bayana ya Aya za Qur’ani, na tuwagawe Maswahaba katika makundi matano kulingana na ugawaji wa Qur’ani, hivyo tuwape heshima kamili wale walio wasafi na wenye matendo mema, na tuliweke kila kundi katika sehemu yake inayofaa, na tujiepushe na upindukiaji, chuki na kuchupa mipaka, na tuwe waadilifu katika maamuzi yetu? 8. Ushahidi wa Kihistoria: Wenye kuamini na kutetea fikra ya kwamba Masahaba wote ni wasafi, hukutana na matatizo mengi kutokana na itikadi hii, miongoni mwayo ni matatizo ya kihistoria, kwa sababu sisi hatuwezi kuzingatia kuwa Maswahaba wote ambao kati yao kulitokea vita vikali – kama tuonavyo katika vitabu vya historia vilivyo maarufu na vya kutegemewa kwao, na hata katika hadithi zilizomo ndani ya vitabu Sahih – ni waadilifu, wema na wasafi, kwani kufanya hivyo ni sawa na kuziweka dhidi mbili pamoja, na jambo hilo ni muhali kiakili. Na hata tukiachilia mbali vita vya Jamal na Siffin ambavyo viliratibiwa na Talha, Zubayr na Muawiya dhidi ya Imam wa Waislamu Ali (a.s.), hatuwezi kufumbia macho matukio ambayo haina budi kukiri kuwa ni makosa na jinai za watu waliowasha moto wa vita hivi. Tuna ushahidi mwingi katika historia juu ya jambo hilo lakini sisi tutataja aina tatu tu kati ya ushahidi huo: a. Mwanahadithi mashuhuri Bukhari anataja katika Sahih yake katika kitabu cha tafsiri kuwa: “Siku moja Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) alisimama na kutaka 58
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 58
11/25/2014 3:03:43 PM
Ushia: Hoja na Majibu
kupumzishwa dhidi ya Abdullah bin Aubay huku akiwa juu ya mimbari, akasema: ‘Enyi kundi la Waislamu! Ni nani atakayenipumzisha na mtu huyu (akimkusudia Abdullah bin Salul, mmoja kati ya viongozi wa wanafiki), nimepata habari za maudhi yake kuhusu mke wangu, na Wallahi sijui kuhusu mke wangu isipokuwa kheri…’ ndipo akasimama Saad bin Muadh (Swahaba maarufu) ambaye ni ndugu wa Bani AbdulAsh’hal, akasema: ‘Mimi ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu nitakupumzisha, akiwa ni kutoka kabila la Awsi nitapiga shingo yake, na kama ni kutoka kwa ndugu zetu Makhazraji ulishatuamuru nasi tukatekeleza amri yako…’ “Aisha anasema: Saad bin Ubadah ambaye ni chifu wa kabila la Khazraj, wakati huo alikuwa bado ni mtu mwema lakini alikuwa na hasira, akamwambia Saad: ‘Naapa kwa Mwenyezi Mungu, umeongopa humuuwi wala huna uwezo wa kumuuwa, na kama angekuwa ni katika watu wa kundi lako usingependa auwawe.’ Akasimama Asid bin Hadhir ambaye ni binamu wa Saad, akamwambia Saad bin Ubadah: ‘Naapa kwa Mwenyezi Mungu, umeongopa hakika tutamuuwa, hakika wewe ni mnafiki unajadili kuhusu wanafiki.’ “Aisha anasema: Yakaamsha zogo makabila mawili ya Awsi na Khazraji mpaka wakataka kuuwana huku Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) akiwa juu ya mimbari. Aisha anasema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) aliendelea kuwatuliza mpaka wakanyamaza.”27 Je hawa wote walikuwa ni Maswahaba wema. 27
Sahih Buikhari Juz. 5, Uk. 57 na 58. 59
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 59
11/25/2014 3:03:43 PM
Ushia: Hoja na Majibu
b. Aalimu maarufu Baladhariy anasema katika kitabu Ansabul-Ashraf: “Uthman alimuuzulu Saad bin Abi Waqas aliyekuwa Liwali wa Kufa, na sehemu yake akamuweka Walid bin Uqbah, na Walid akamuomba Abdullah bin Mas’ud ufunguo wa Hazina, Ibnu Mas’ud akamtupia ufunguo na kumwambia: ‘Yeyote atakayegeuza basi Mwenyezi Mungu atageuza hali yake, na yeyote atakayebadili Mwenyezi Mungu atamkasirikia. Na simuoni jamaa yenu isipokuwa amegeuza na kubadili. Hivi kweli anauzuliwa Saad bin Abi Waqas na badala yake Walid anapewa uliwali…?’ Walid akamwandikia barua Uthman kumjulisha hilo na akasema: ‘Hakika yeye anakuaibisha na kukushutumu.’ Uthman akamwandikia barua akimwamuru kumrejesha (Madina)….. “Ibn Mas’ud alifika Madina wakati Uthman akiwa juu ya mimbari ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) akihutubia, alipomuona alisema: ‘Hakika amefika kwenu mdudu muovu, ambaye anatembea huku anakula chakula chake na akitapika na kujisaidia haja kubwa.’ Ibn Mas’ud akasema: ‘Mimi siko hivyo, lakini mimi ni Swahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu aliyekuwepo siku ya Badri na siku ya Kiapo cha Ridhaa.’ Aisha akanadi: ‘Ewe Uthman! Hivi kweli unamwambia haya Swahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu!’ Kisha Uthman akatoa amri atolewe, akatolewa msikitini kwa nguvu…. Na inasemekana kuwa Yahmumu mtumwa wa Uthman alimkaba kwa kumkunja miguu yake hadi shingo yake (Ibn Ms’ud) ikapita katikati ya miguu yake, akambamiza ardhini mpaka mbavu zake zikavunjika.”28 28
nsabul-Ashraf Juz. 6, Uk. 147. Taarikh Ibn Kathir Juz. 7, Uk. 136 na Uk. 183, A matukio ya mwaka 32. kwa muhtasari. 60
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 60
11/25/2014 3:03:43 PM
Ushia: Hoja na Majibu
c. Aalimu maarufu Baladhariy ananukuu katika kitabu Ansabul-Ashraf: “Katika Hazina ya Waislamu huko Madina kulikuwa na sanduku lenye mapambo na vito vya thamani, Uthman akachukua sehemu ya vito hivyo vile alivyovipenda mke wake, watu wakadhihirisha shutuma dhidi yake kwa hilo, na wakamtamkia maneno makali mpaka wakamkasirisha, ndipo akahutubia kwa kusema: ‘Hakika tutaendelea kuchukua mahitaji yetu kutoka kwenye fungu hili hata kama maelfu ya watu watachukia.’ Ali (a.s.) akamwambia: ‘Basi unazuiliwa kufanya hivyo na kunawekwa kizuizi baina yako na wewe.’ Ammar bin Yasir akasema: ‘Namfanya Mwenyezi Mungu shahidi, hakika mimi ndio mtu wa kwanza kuchukizwa na hilo.’ Uthman akasema: ‘Hivi unathubutu kuniambia hilo mimi ewe mtoto wa ….? Mchukueni.’ Akachukuliwa, Uthman akaingia akaomba aletwe, akampiga mpaka akazimia, kisha akatolewa akabebwa mpaka nyumbani kwa Ummu Salamah mke wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww), hakusali Dhuhri, Asri, na Maghrib, hivyo alipozinduka akachukua udhu na kusali, akasema: ‘Kila himidi njema ni ya Mwenyezi Mungu, hii si siku ya kwanza sisi kuteswa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.’”29 Akiashiria mateso aliyoyapata kutoka kwa Mushrikina mwanzo wa daawa. Na sisi hatupendi kunukuu matukio haya yenye kuumiza yaliyotokea katika historia ya Waislamu, na huenda haifai kutaja kadiri hii ya matukio kama si ndugu zetu kuendelea kung’ang’ania kuwa Maswahaba wote ni wasafi na pia vitendo vyao ni safi. 29
Ansabul-Ashraf Juz. 6, Uk. 161 na 162. 61
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 61
11/25/2014 3:03:43 PM
Ushia: Hoja na Majibu
Na sasa je inawezekana kuhalalisha shutuma, adha na maumivu ya mwili yaliyowapata watu hawa, watu ambao ni miongoni mwa Maswahaba bora na wasafi, ambao ni Saad bin Mua’dh, Abdullah bin Masu’d na Ammar bin Yasir? Ambao mmoja wao alipigwa mpaka akavunjika mbavu zake, na mwingine akapigwa mpaka akatokwa na fahamu na kupitwa na Sala. Je ushahidi huu wa kihistoria – ambao ni mwingi – unaturuhusu sisi kufumba macho yetu mbele ya matukio haya? Na tuseme: Hakika Maswahaba wote ni wema na matendo yao yote ni sahihi, na hatimaye tuanzishe jeshi kwa jina la Jeshi la Maswahaba na kuanza kutetea matendo yao yote bila sharti na mipaka? Je kuna yeyote mwenye akili timamu anayekubali fikra hizi? Na hapa tunarudia kauli hii mara nyingine kuwa baina ya Maswahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) wapo watu kadhaa ambao wamepambika kwa sifa ya imani, wema na kujinyima, lakini pia kuna watu ambao ni lazima tuyaweke matendo yao kwenye ukosoaji na uchunguzi na yapimwe kwa mizani ya akili, na hukumu itokane na kipimo hicho. 9. Baadhi ya Maswahaba waliadhibiwa kisharia katika zama za Mtume (saww) na baada yake: Tunaona katika vitabu Sahih na katika vitabu vingine vilivyo maarufu kwa ndugu zetu Masunni, sehemu ambazo baadhi ya Maswahaba walitenda madhambi katika zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww), dhambi ambazo zinawajibisha kuadhibiwa, na waliadhibiwa. Je pamoja na haya yote bado watasema kuwa hawa wote ni waadilifu?! Na kwamba 62
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 62
11/25/2014 3:03:43 PM
Ushia: Hoja na Majibu
hawakosei, ni uadilifu gani huu ambao licha ya mwenye nao kutenda dhambi kubwa na kuadhibiwa lakini bado upo? Kwa mfano tu tunataja baadhi ya sehemu hizo: a.
Kutoka kwa Aqabah bin Harith, amesema: “Aliletwa Naiman au mtoto wa Naiman akiwa amekunywa pombe, Mtukufu Mtume (saww) akawaamuru waliokuwa ndani ya nyumba wampige.” Anasema: “Mimi nilikuwa mmoja wao kati ya wale ambao walimpiga kwa kiatu.”30
b.
Kutoka kwa Jabir kwamba mtu mmoja kati ya watu waliosilimu, alikuja kwa Mtukufu Mtume na kukiri kuwa amezini, Mtukufu Mtume (saww) akamwacha mpaka akakiri mwenyewe mara nne, Mtume (saww) akamwambia: ‘Je una wendawazimu?’ Akasema: ‘Hapana.’ Akamwambia: ‘Je una mke?’ Akasema: ‘Ndiyo.’ Mtume akaamuru akapigwa mawe jirani na msikiti.”31
c.
Katika kisa cha watu kuzua uwongo wa tuhuma ya zinaa, Mtukufu Mtume (saww) aliamuru watu kadhaa waadhibiwe adhabu ya kumzushia mtu tuhuma ya zinaa.32
d.
Baada ya zama za Mtukufu Mtume (saww) aliletwa Abdur-Rahman bin Umar, na Uqbah bin Harith al-Badriy, kwa kosa la kunywa pombe, Umar bin al-Aswi aliyekuwa Liwali wa Misri akawaadhibu adhabu ya kisharia, kisha baadaye (Umar bin Khatab) alimleta mwanawe na kumwadhibu kwa mara nyingine.33
30
Sahih Bukhari Juz. 8, Uk. 13, Hadithi ya 6775, kitabu cha adhabu.
31
Sahih Bukhari Juz. 8, Uk. 22, Hadithi ya 6820, kitabu cha adhabu.
32
Al-Muujam al-Kabir Juz. 23, Uk. 128, na vitabu vingine.
33
As-Sunan al-Kubra Juz. 8, Uk. 312, na vitabu vingine vingi. 63
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 63
11/25/2014 3:03:43 PM
Ushia: Hoja na Majibu
e.
Kisa maarufu cha Walid bin Uqbah, ambaye alisali Sala ya Subhi rakaa nne huku akiwa amelewa, ambapo alifikishwa Madina na akaadhibiwa adhabu ya mtu aliyekunywa pombe.34
Na kuna sehemu nyingine nyingi ambazo tumejiepusha kuzitaja kwa sababu ya maslahi. Je pamoja na uwepo wa matukio haya bado inafaa sisi kuziba masikio yetu na macho yetu na tuseme: Hakika wao wote ni waadilifu? 10. Utetezi usiokubalika: a.
Wale ambao wanaunga mkono nadharia ya usafi wa Maswahaba bila sharti wala mipaka, wamelazimika baada ya mgongano huu, kujikinaisha kuwa hakika Maswahaba wote ni wanaijtihadi, na kila mmoja wao alitenda kulingana na ijtihadi yake. Na hii ni moja ya aina za kuizuia akili isifanye kazi, na ndugu zetu hawa wametumia hilo kuwa njia ya kujinasua na mgongano huu bayana. Je kweli hii ni ijtihadi!! Kumpiga Swahaba muumini mpaka anakosa fahamu na kupitwa na Sala yake, kwa sababu tu ya ukosoaji huu mdogo, au kwa sababu tu ya yeye kuamrisha mema na kukataza maovu katika jambo linalohusu uharibifu wa Hazina ya mali za Waislamu?
Na je hii ni aina ya ijtihadi!! Kuvunja mbavu za Swahaba maarufu kwa sababu tu ya yeye kupinga uteuzi wa kumfanya Walid mlevi wa pombe kuwa Liwali wa Kufa? Zaidi ya hapo ni kuwa je hii ni ijtihadi!! Kuwasha moto wa vita na kuwauwa maelfu ya Waislamu kwa ajili ya kupata 34
Sahih Muslim Juz. 5, Uk. 126, Hadithi ya 1707. 64
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 64
11/25/2014 3:03:43 PM
Ushia: Hoja na Majibu
madaraka na utawala wa serikali ya Kiislamu, na kusimama dhidi ya Imamu wa Waislamu aliyeteuliwa na watu wote ikiwa ni pamoja na kupata cheo chake kutoka kwa Mwenyezi Mungu? Ikiwa mambo haya na mengineyo ni ijtihadi na matawi yake, basi inawezekana kuyatetea makosa yote yaliyotokea katika historia kwa kisingizio hicho. Zaidi ya hapo ni je ijtihadi hii ni kwa hawa tu Maswahaba au wapo wanaijtihadi wengi katika umma wa Kiislamu? Na leo hii na kwa kukiri kwa wanafikra wa Kisunni na Ulamaa wa Kishia, wanasema kuwa mlango wa ijtihadi ungali wazi mbele ya Ulamaa wote wenye uwelewa, je mtu akitenda matendo kama haya, mko tayari kutetea matendo hayo kwa kisingizio hicho? Bila shaka hamko tayari. b. Na mara nyingine wanasema wadhifa wetu ni kunyamaza na kutozungumzia Maswahaba na matendo yao:
ْ ت ۖ َل َھا َما َك َس َب ْ ك أُم ٌَّة َق ْد َخ َل ۖ ت َو َل ُك ْم َما َك َس ْب ُت ْم َ ت ِْل ون َ ُون َعمَّا َكا ُنوا َيعْ َمل َ َُو َال ُتسْ أَل “Huo ni umma uliokwisha pita. Utapata uliyoyachuma nanyi mtapata mliyoyachuma, wala hamtaulizwa waliyokuwa wakiyafanya.” (Sura al-Baqarah: 134).
Ndiyo jambo hili ni zuri likiwa halina athari na hatima yetu, lakini ni kwamba sisi tunataka kuwafanya kiigizo na tuchukue riwaya za Mtukufu Mtume (saww) kupitia njia yao, hivi si wajibu juu yetu kujua ni nani mwaminifu na ni yupi asiye mwaminifu, ni nani mwadilifu na ni yupi fasiki, ili tutekeleze madhumuni ya Aya tukufu: 65
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 65
11/25/2014 3:03:43 PM
Ushia: Hoja na Majibu
ِين آ َم ُنوا إِنْ َجا َء ُك ْم َفاسِ ٌق ِب َن َبإٍ َف َت َب َّي ُنوا أَنْ ُتصِ يبُوا َ َيا أَ ُّي َھا الَّذ ِين َ َق ْومًا ِب َج َھا َل ٍة َف ُتصْ ِبحُوا َع َل ٰى َما َف َع ْل ُت ْم َنا ِدم “Enyi ambao mmeamini! Akiwajia fasiki na habari yoyote, ichunguzeni, msije mkawasibu watu kwa kutojua, na mkawa wenye kujuta kwa mliyoyatenda.” (Sura Hujurat: 6).
11. Dhulma aliyotendewa Ali (a.s.): Kila mtu anayesoma historia ya Kiislamu anakuta ushahidi wa jambo hili, na anaona ni jinsi gani Imam Ali (a.s.) – alama ya elimu na uchamungu, mtu aliye karibu zaidi na Mtukufu Mtume na mtetezi mkubwa wa Uislamu – alivyokutana na mambo yasiyofaa, ikiwemo kutukanwa, kukashifiwa na kudhalilishwa. Zaidi ya hapo ni wafuasi wake kutishiwa, kunyanyaswa na kuteswa kusiko na mfano katika historia, yote hayo yakifanywa na hawa ambao wanajiita Maswahaba wa Mtume (saww). Mifano tu juu ya hilo ni: a.
Siku moja watu walimuona Ali bin Jahmi al-Khurasaniy akimlaani baba yake mzazi, wakamuuliza kwa nini unafanya hivyo? Akasema: “Kwa sababu alinipa jina Ali.”35
b.
Muawiya aliandika nakala ya aina moja kwa Maliwali wake baada ya mwaka wa jamaa, ‘kuwa mimi nimejivua dhima ya mtu yeyote anayesimulia hadithi inayohusu fadhila za Abu Turab na watu wa nyumba yake (as).’ Basi mahatibu katika kila kona na kila mimbari
35
Lisanul-Mizan Juz. 4, Uk. 210. 66
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 66
11/25/2014 3:03:43 PM
Ushia: Hoja na Majibu
wakasimama na kuanza kumlaani Ali (a.s.), kujitenga naye na kumtusi yeye na watu wa nyumba yake.36 c.
Watu wa ukoo wa Umaiyyah (Bani Umaiyyah) walikuwa wanaposikia kuna mtoto jina lake ni Ali humuuwa. Maneno haya kayanukuu Salamah bin Shabib kutoka kwa Abu Abdur-Rahman al-Muqriu.37
d.
Zamakhshariy na Suyutiy wamenukuu kwamba: “Wakati wa Bani Umaiyyah, Imam Ali ( a.s.) alikuwa akitukanwa juu ya mimbari zaidi ya elfu sabini, na Muawiya ndiye aliyeasisi mwenendo huu.”38
e.
Alipokuja Khalifa Umar bin Abdul-Aziz na kuacha kulaani huku akiamrisha watu waache kulaani, watu walipiga kelele msikitini wakistaajabishwa na amri hiyo, wakasema: “Sunna imeachwa.”39 Wakati ambapo kwa mujibu wa riwaya sahihi zilizomo ndani ya vitabu vyao tegemewa, tunamkuta Mtukufu Mtume (saww) akisema: “Yeyote atakayemtukana Ali atakuwa amenitukana mimi, na atakayenitukana mimi atakuwa amemtukana Mwenyezi Mungu.”40
12. Kisa hiki kinastahiki kusimuliwa: Si vibaya na kwa kumalizia tu vizuri niwakumbushe wapendwa wasomaji kisa hiki ambacho kilitokea baina 36
An-Naswaihu al-Kafiyah Uk. 72.
37
Tahdhibul-Kamal Juz. 20, Uk. 429. Siratun-Nubalau Juz. 5, Uk. 102.
38
Rabiul-An’war Juz. 2, Uk. 186. Naswaihul-Kafiyyah Uk. 79, kutoka kwa Suyutiy.
39
aswaihul-Kafiyyah Uk. 116. Tahniatus-Swidiq al-Mahbub Uk. 59, cha Hasan N Saqaf.
40
meiandika al-Hakim na kusema ni sahihi. Na amekiri hilo Dahahbiy A (Mustadrakus-Sahihayn Juz. 3, Uk. 121. 67
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 67
11/25/2014 3:03:43 PM
Ushia: Hoja na Majibu
yangu na mtu mmoja katika Msikiti Mtakatifu. Katika moja ya safari zangu za Umra nilikutana na kundi la Ulamaa wa Hijazi katika Msikiti Mtakatifu, ilikuwa ni wakati wa baina ya Maghrib na Isha, na kulikuwa na fursa nzuri ya kuweza kujadiliana kuhusu madai ya kwamba Maswahaba wote ni wasafi, kwani kwa mujibu wa itikadi yao ni wajibu kutokuwakosoa kwa lolote. Nilimwambia mmoja wao: “Embu tufanye kuwa vita vya Siffin vimeanza sasa, wewe utakuwa katika kundi lipi, katika kundi la Ali (a.s.) au kundi la Muawiya?” Akajibu: “Lazima niwe katika kundi la Ali (a.s.).” Nikamuuliza: “Utafanya nini kama Ali akikuamuru kuchukua upanga na kumuuwa Muawiya?” Alitafakari kidogo kisha akasema: “Nitamuuwa Muawiya, lakini sintamkosoa kwa lolote.” Naam, haya ndio matokeo ya kushabikia itikadi bila mantiki, hivyo hata utetezi wake hautakuwa na mantiki. Ukweli ni kwamba Maswahaba na wafuasi wa Mtukufu Mtume (saww) kwa upande mmoja wamegawanyika katika aina tofauti, hiyo ni kwa ushahidi wa Qur’ani Tukufu na historia ya Uislamu. Kuna kundi la Maswahaba na wafuasi wa Mtukufu Mtume (saww) ambao tangu mwanzo walikuwa wasafi, wakweli na wema, na wakabakia hivyo mpaka mwisho, waliishi kwa wema na wakafa kwa wema. Na kwa upande mwingine kuna kundi lingine la watu ambao walikuwa katika safu za watu wema na wasafi katika zama za Mtukufu Mtume (saww), lakini wao baada ya hapo walibadili mwenendo wao kwa kutafuta vyeo na kupenda dunia, na hatima yao haikuwa nzuri.
68
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 68
11/25/2014 3:03:43 PM
Ushia: Hoja na Majibu
Na kuna kundi la tatu la watu ambao tangu mwanzo walikuwa katika safu za wanafiki na waabudu masanamu, na kwa ajili ya maslahi fulani walijiunga na Waislamu, na hao ni watu mfano wa Abu Sufiyan. (Na hao wote kwa mujibu wa maana ya Swahaba ni Maswahaba). Na hapa tunaliashiria kundi la kwanza kwa kusema:
ْ ون َر َّب َنا اغ ِفرْ َل َنا َ ُِين َجاءُوا ِمنْ َبعْ ِد ِھ ْم َيقُول َ َوالَّذ ان َو َال َتجْ َع ْل فِي َ إل ْخ َوا ِن َنا الَّذ ِ اإلي َم ِ ْ ِين َس َبقُو َنا ِب ِ ِ َو ِين آ َم ُنوا َر َّب َنا إِ َّن َك َرءُوفٌ َرحِي ٌم َ وب َنا غِ ًّال لِلَّذ ِ ُقُل “Na waliokuja baada yao wanasema: Mola Wetu! Tughufirie sisi na ndugu zetu waliotutangulia kwa Imani, wala usijaalie ndani ya nyoyo zetu undani kwa walioamini. Mola Wetu! Hakika Wewe ni Mpole, Mwingi wa rehema.” (Sura Hashri: 10).
69
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 69
11/25/2014 3:03:43 PM
Ushia: Hoja na Majibu
MADA YA NNE KUHESHIMU MAKABURI YA WATUKUFU Kuhusu mada hii
M
azungumzo yetu hapa ni baina yetu na Mawahabi tu wenye msimamo mkali, kwani tambua kuwa makundi yote ya Kiislamu yanaruhusu kuzuru makaburi ya watukufu kasoro kundi hili tu. Vyovyote iwavyo ni kuwa Mawahabi hutuuliza swali hili, nalo ni: Kwa nini mnakwenda kuwazuru viongozi wa dini? Na hutuita sisi watu wa makaburi. Wakati ambao tunaona mataifa katika pande zote za ulimwengu yakitilia umuhimu makaburi ya wahenga wao kwa kuyazuru na kuchukua mafunzo, Waislamu katika ulimwengu huu daima wanayapa umuhimu na heshima makhususi makaburi ya watukufu wao, na bado wanaendelea kufanya hivyo, na hakuna aliyekhalifu hilo isipokuwa kundi hili dogo la Mawahabi ambalo linadai kuwa linawakilisha Waislamu wote ulimwenguni. Naam, kuna baadhi ya Ulamaa maarufu miongoni mwa Mawahabi wametamka bayana kuwa ni mustahabu kulizuru kaburi la Mtukufu Mtume (saww), lakini kwa sharti isiwe kwa nia ya kulifungia safari, kwa maana ya kwamba aje kwa lengo la kuuzuru msikiti wa Mtume (saww) na kufanya ibada humo, au kwa lengo la kutekeleza Umra na kuizuru 70
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 70
11/25/2014 3:03:43 PM
Ushia: Hoja na Majibu
Madina, na ndani ya mambo hayo aweze kulizuru pia kaburi la Mtukufu Mtume (saww), lakini si kwa kulifungia safari. Mwanafiqhi maarufu wa Kiwahabi Ibn Baaz anasema katika mazungumzo yake na jarida la al-Jazirah: “Ni mustahabu kusali rakaa mbili katika raudha ya Mtukufu Mtume (saww) kwa mtu mwenye kuuzuru msikiti wake mtukufu, kisha amsalimu Mtukufu Mtume (saww). Na ni mustahabu pia kuzuru makaburi ya Baqii na kuwasalimu wafiadini waliozikwa huko.”41 Kwa mujibu wa nukuu za kitabu al-Fiqhi Alal-Madhahib alAr’baa, wanazuoni wanne wa fiqhi wa madhehebu ya Sunni wanaona ni mustahabu kulizuru kaburi la Mtukufu Mtume (saww) bila sharti lolote wala mipaka. Pale tunaposoma katika kitabu hiki kuwa: “Hakuna shaka kuwa kulizuru kaburi la Mustafa (a.s.) ni miongoni mwa mambo adhimu na matukufu zaidi yanayomkurubisha mtu kwa Mwenyezi Mungu.”42 Na kuna hadithi nyingi zenye madhumuni haya. Kundi hili la Mawahabi linatofautiana katika sura ya jumla na Waislamu wengine wa ulimwenguni katika nukta tatu: 1.
Katika kujengea makaburi.
2.
Kufunga safari kwa lengo la kwenda kuzuru makaburi.
3.
Na wanawake kuzuru makaburi.
Katika maudhui hizi tatu jamaa hawa wameshikilia baadhi ya riwaya ambazo zote hazikubaliki, ima kwa kuwa 41
Jaridatul-Jazirah, toleo la 6862, la tarehe 22/ 11/ 1411 A.H.
42
l-Fiqhi Alal-Madhahib al-ar’baah Juz. 1, Uk. 365, Darul-Kutubi al-Ilmiyyah, A Beirut, chapa ya 2, 1424 A.H. 71
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 71
11/25/2014 3:03:43 PM
Ushia: Hoja na Majibu
sanad yake ni dhaifu, na ima kwa kuwa hazina hoja husika. Inshaallah muda si mrefu tutafafanua hilo. Lakini inaonekana wana sababu nyingine zinazowapelekea kuzuia mambo hayo, wao wamepatwa na ugonjwa wa wasiwasi katika maudhui ya tauhidi na shirki, na huenda wamedhania kuwa kuzuru makaburi ni kuyaabudu, na kwa ajili hiyo Waislamu wote wanakuwa ni Washirikina na walahidi kasoro wao tu – kama wanavyodai. Mifano ya kihistoria Kuheshimu makaburi ya wahenga waliotangulia na khususan ya watu watukufu ni jambo lenye historia ndefu kabla ya maelfu ya miaka, jamii ya kibinadamu ilikuwa ikiwatukuza marehemu wao na kuheshimu makaburi yao khususan ya walio watukufu miongoni mwao, kwa sababu falsafa ya tendo hili ina athari na faida nyingi, kati ya hizo ni: Kwanza: Hakika faida ya kuwaheshimu wahenga ni kuhifadhi heshima ya wapendwa hawa na kuwatukuza, kwa sababu wao ni anwani ya utukufu na heshima ya utu, na ni sababu ya kuwaraghibisha vijana kupita njia yao. Pili: Ni kuchukua mafunzo na mazingatio kutoka kwenye makaburi hayo yasiyoongea, lakini wito wake ni dawa ya kuondolea kutu ya sahau katika moyo wa mwanadamu, na kumwamsha kutoka kwenye mghafala wa dunia na usingizi wake, na kumpunguzia utawala wa matamanio, na ni kama alivyosema Amirul-Muuminina (as): “Mauti mliyoyaona ni mawaidha tosha.”43 43
Nahjul-Balaghah, Hotuba 188. 72
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 72
11/25/2014 3:03:44 PM
Ushia: Hoja na Majibu
Tatu: Ni kuwaliwaza wafiwa, kwa sababu watu huhisi zaidi raha pindi wanapokuwa karibu na makaburi ya wapendwa wao, na ni kana kwamba wao wanaishi baina yao, hivyo ziara hii huwapunguzia machungu, na kwa ajili hii tunawakuta wakianzisha kaburi la alama ya marehemu wao, na wanakaa jirani yake kwa kuendeleza kumbukumbu yake. Nne: Kutukuza makaburi ya watukufu waliotangulia ni moja ya njia ya kuhifadhi kumbukumbu ya utamaduni wa kila kaumu na umma, na leo hii mataifa yako hai kupitia utamaduni wake wa zamani, na Waislamu wa ulimwengu wanamiliki utamaduni wa kutosha na hazina kubwa, na ulio muhimu zaidi ni makaburi ya wafiadini, Ulamaa wakubwa na mabingwa wa elimu na maarifa, khususan makaburi matukufu ya viongozi wakubwa wa dini. Kuhifadhi athari zao na kuhuisha utajo wao ilikuwa ni njia ya kuulinda Uislamu na Sunnah ya Mtukufu Mtume (saww), licha ya yote waliyotenda wale wasiokuwa na aibu kwa kuondoa athari adhimu za viongozi wa Uislamu huko Makka, Madina na katika miji mingine, ambapo jamii ya Kiislamu imepatwa na hasara kubwa. Na kwa kweli Masalafi wasiojua kitu kwa kutumia visingizio visivyo na maana wameuletea Uislamu hasara kubwa isiyoweza kuzibika katika kumbukumbu ya utamaduni. Je kumbukumbu hii kubwa ya kihistoria ni makhususi kwa ajili ya kundi hili tu mpaka iharibiwe kwa namna hii ya aibu? Hivi si ni wajibu jambo hili la kulinda athari hizi liachiwe kundi la Ulamaa wenye uwelewa toka miji yote? Tano: Hakika kuyazuru makaburi ya viongozi wakubwa wa dini na kuwaomba wakuombee kwa Mwenyezi Mungu, 73
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 73
11/25/2014 3:03:44 PM
Ushia: Hoja na Majibu
ikiwa ni pamoja na kutubu na kurejea kwenye medani ya utumwa wa kweli, kitendo hicho kina athari katika kuzilea nafsi na kuzistawisha kimaadili na kiimani. Na kuna watu wengi waliotenda dhambi na waliotenda maasi, ambao wamefanikiwa kutubu pembezoni mwa makaburi ya watukufu hawa, na bado wengine wanaendelea kutubu ili daima wawe watu wema, na wapande hadi daraja ya juu kabisa ya wema. Dhana ya shirki katika kuzuru makaburi Baadhi ya wajinga huwatuhumu kwa shirki wale wenye kuzuru makaburi ya viongozi wa dini, na kwa kweli laiti wangejua madhumuni ya ziara hizi na faida zake wangeona aibu kwa maneno yao haya. Hakuna mtu yeyote mwenye akili timamu anayemwabudu Mtukufu Mtume (saww) au Maimamu (as), bali hakuna mwenye fikra hii kabisa, na waumini wote wenye uwelewa sahihi wanakwenda kuwazuru kwa ajili ya kuwaheshimu na kuwaomba wawaombee kwa Mwenyezi Mungu. Watu wengi wenye kufanya ziara hutaja “Allahu Akbar” mara mia moja kabla ya kuanza kusoma matini ya Ziyara, kwa hili wao husisitiza msingi wa tauhidi mara mia moja ili kuondoa doa lolote la shirki toka ndani ya nafsi zao. Tunasema katika Ziyara maarufu kwa jina la Ziyarat Aminullah, na mbele ya makaburi ya Maimamu (as): “Nashahidia kuwa hakika wewe umepigana jihadi ya kweli katika njia ya Mwenyezi Mungu, umekifanyia kazi kitabu chake, na umefuata suna za Nabii wake mpaka Mwenyezi Mungu alipokuita kwenye ujirani wake.”44 Je kuna tauhidi kushinda hii? 44
Biharul-An’war Juz. 99, Uk. 129 na 130. 74
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 74
11/25/2014 3:03:44 PM
Ushia: Hoja na Majibu
Na tunasema kuwaambia watukufu hawa katika Ziyara maarufu kwa jina la al-Jamiah: “Mnalingania kwa Mwenyezi Mungu, mnajulisha ni nani Yeye, mnamwamini, mnajisalimisha kwake, mnatekeleza amri yake na mnaongoza kwenye njia yake.”45 Na dhamiri zote katika sentensi sita zilizotajwa zinarudi kwa Muumba Mtukufu. Hakika katika kila sehemu ya Ziyara hizi kuna tauhidi na kulingania kwa Mwenyezi Mungu, je hii ni shirki au imani? Na tunasema sehemu nyingine ya Ziyara hii: “Ni mwenye kuwaomba mniombee kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.” Hivyo ikiwa katika madhumuni ya baadhi ya Ziyara kuna utata, bila shaka ibara hizi zilizo bayana zinaondoa utata huo. Je kuomba kuombewa kwa Mwenyezi Mungu kunaoana na misingi ya tauhidi? Mkanganyiko mwingine muhimu walionao Mawahabi katika maudhui hii ni kulinganisha kitendo cha kuomba uombewe kwa Mwenyezi Mungu kupitia mawalii wake na kuomba msaada kutoka kwa masanamu – kutoka kwenye vitu ambavyo havina roho, akili wala hisia – wakati ambapo tunaiona Qur’ani Tukufu ikiashiria katika sehemu nyingi jinsi Manabii wa Mwenyezi Mungu walivyowaombea kwa Mwenyezi Mungu wale waliotenda dhambi, kwa mfano tu tunataja mifano ifuatayo: 1. Baada ya ndugu zake na Yusuf kujua utukufu wa ndugu yao waligundua makosa yao na walikwenda kwa baba yao na kumuomba awaombee, na baba yao alikubali ombi lao: 45
Biharul-An’war Juz. 99, Uk. 131. 75
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 75
11/25/2014 3:03:44 PM
Ushia: Hoja na Majibu
ِين َقا َل َ َقالُوا َيا أَ َبا َنا اسْ َت ْغ ِفرْ َل َنا ُذ ُنو َب َنا إِ َّنا ُك َّنا َخاطِ ئ ف أَسْ َت ْغ ِف ُر َل ُك ْم َربِّي ۖ إِ َّن ُه ھ َُو ْال َغفُو ُر الرَّ حِي ُم َ َس ْو “Wakasema: Ewe baba yetu! Tuombee maghufira kwa dhambi zetu, hakika sisi tulikuwa ni wenye hatia. Akasema: Nitawaombea maghufira kwa Mola Wangu. Hakika Yeye ni Mwingi wa maghufira, Mwenye kurehemu.” (Sura Yusuf: 97 – 98). Je Nabii Yaqub (as) alikuwa mushrik?
ﷲ َ َو َل ْو أَ َّن ُھ ْم إِ ْذ َظ َلمُوا أَ ْنفُ َس ُھ ْم َجاءُو َ َّ ك َفاسْ َت ْغ َفرُوا ﷲ َت َّوابًا َرحِيمًا َ َّ َواسْ َت ْغ َف َر َل ُھ ُم الرَّ سُو ُل َل َو َج ُدوا َّ ُ َّ
ُُ
َ
َ
ُ
ِين َقا إِنا كنا َخinawaraghibisha اسْ َت ْغ ِفرْ ل َنا ذنو َب َناna أ َبا َناkuwashajiisha َقالوا َيا َ Qur’ani َ اطِ ئTukufu 2. ل waliotenda dhambi na Mtukufu ُھ َُو ْال َغفwaombe ُ َلwamuombe َّ ِِّي ۖ إtoba ْ ف أَسْ َت ْ َس ُ ُ ُ م ِي ح ر و ه ن ب ر م ك ر ف غ و َّالر ِ َ َ ْ ُ Mtume (saww) awaombee, ambapo Mwenyezi Mungu anasema: ﷲ َ َو َل ْو أَ َّن ُھ ْم إِ ْذ َظ َلمُوا أَ ْنفُ َس ُھ ْم َجاء َ َّ ُوك َفاسْ َت ْغ َفرُوا ﷲ َت َّوابًا َرحِيمًا َ َّ َواسْ َت ْغ َف َر َل ُھ ُم الرَّ سُو ُل َل َو َج ُدوا “Na lau kwamba wao walipojidhulumu wangekujia wakaomba maghufira kwa Mwenyezi Mungu na wakaombewa maghufira na Mtume, wangelimkuta Mwenyezi Mungu ni mwenye kutakabali toba, mwenye kurehemu.” (Sura Nisaa: 64). Je uraghibishaji na ushajiishaji huu ni shirki.
76
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 76
11/25/2014 3:03:44 PM
Ushia: Hoja na Majibu
3. Qur’ani inasema katika kuwalaumu wanafiki:
ﷲ َلوَّ ْوا ُرءُو َس ُھ ْم ِ َّ َوإِ َذا قِي َل َل ُھ ْم َت َعا َل ْوا َيسْ َت ْغ ِفرْ َل ُك ْم َرسُو ُل ُ َو َرأَ ْي َت ُھ ْم َي ُون َ ون َو ُھ ْم مُسْ َت ْك ِبر َ ص ُّد “Na wanapoambiwa: Njooni ili Mtume wa Mwenyezi Mungu awaombee maghufira, huvigeuza vichwa vyao, na unawaona ْ َّ َم الرwamejaa ْش َر ٰى ي َُجا ِدلُ َناwanageuka و ُع َو َجا َء ْت ُه ْال ُبnao َعنْ إِب َْراھِيkiburi.” ب َ ( َف َلمَّا َذ َھSura Munafiqun: 5). Je Qur’ani Tukufu inawalingania makafiri na ْرا ِھي ُم فِي َق ْو ِم لُوطٍ إِنَّ إِب َْراھِي َم َل َحلِي ٌم أَوَّ اهٌ ُم ِن َ يبٌ َيا إِبshirki? wanafiki kufanya
ِّك ۖ َوإ َّن ُھ ْم آتِيھ ْم َ أَعْ رضْ َعنْ ٰ َھ َذا ۖ إ َّن ُه َق ْد َجا َء أَمْ ُر َرب
ِ ِ ِ ِ mwa 4. Bila shaka tunajua kaumu ya Lut ilikuwa miongoni َ ٌ( َع َذابas) kaumu ovu zaidi, na Sheikh wa Manabii, Ibrahim غ ْي ُر َمرْ ُدو ٍد aliwaombea kwa Mwenyezi Mungu, ambapo alimuomba ْ َيسْ َت ْغ ِفرhuenda َس ُھ ْمMwenyezi َلوَّ ْوا ُرءُوMungu ﷲ َل ُك ْم َرmuda ْم َت َعا َل ْواwakatubu, َوإِ َذا قِي َل َل ُھlakini ِ َّ سُو ُلawape kwa sababu wao walivuka katika ُ َيuovu ُون ون َو ُھ ْم م رأَ ْي َت ُھ ْمwalikosa َ ُسْ َت ْك ِبرmipaka َ ص ُّد َ َو hali ya wao kukubaliwa ombi lao, na ndipo yamekuja maelezo ya Nabii Ibrahim (as) akiacha kuwaombea: ب َعنْ إِب َْراھِي َم الرَّ ْو ُع َو َجا َء ْت ُه ْال ُب ْش َر ٰى ي َُجا ِدلُ َنا َ َف َلمَّا َذ َھ فِي َق ْو ِم لُوطٍ إِنَّ إِب َْراھِي َم َل َحلِي ٌم أَوَّ اهٌ ُم ِنيبٌ َيا إِب َْرا ِھي ُم ِيھ ْم َ أَعْ ِرضْ َعنْ ٰ َھ َذا ۖ إِ َّن ُه َق ْد َجا َء أَمْ ُر َرب ِ ِّك ۖ َوإِ َّن ُھ ْم آت َع َذابٌ َغ ْي ُر َمرْ ُدو ٍد “Basi hofu ilipomwondokea Ibrahim na ikawa ile bishara imemfikia, alianza kujadiliana nasi juu ya watu wa Lut. 77
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 77
11/25/2014 3:03:44 PM
Ushia: Hoja na Majibu
Hakika Ibrahim alikuwa mpole, mnyenyekevu mwepesi wa kurejea (kwa Mungu). Ewe Ibrahim! Achana nayo haya. Hakika amri ya Mola Wako imekwishakuja, na hakika wao itawafikia adhabu isiyorudishwa.” (Sura Hud: 74 – 76).
La muhimu kutaja hapa ni kuwa mkabala na ombi hili, Mwenyezi Mungu amemsifu Ibrahim kwa namna ya pekee, aliposema: “Hakika Ibrahim alikuwa mpole, mnyenyekevu mwepesi wa kurejea (kwa Mungu).” Lakini akamwambia kuwa muda umepita na hakuna tena muda wa maombi. Maombi ya Mawalii si tu katika kipindi cha uhai wao Wenye kutafuta upenyo wa kukwepa, walipoona Aya zilizotangulia zikitamka bayana uhalali wa uombezi wa Manabii na kwamba hakuna njia isipokuwa kuikubali, walikimbilia kwenye visingizio vingine, wakasema: “Hakika Aya hizi zinazungumzia uombezi katika hali ya uhai wa waombaji, wala hakuna dalili inayoonesha kuwa zinajumuisha pia uombezi wa baada ya kifo chao.” Na kwa maelezo haya wakaachana na kisingizio cha shirki na kushikilia kisingizio kingine. Lakini hapa kuna swali, nalo ni: Je Mtume (saww) amebadilika na kuwa udongo baada ya kufa kwake na ametoweka kabisa – kama alivyokiri mbele yetu mmoja kati ya Ulamaa wa kiwahabi – au kuna uhai wa Barzakh? Ukisema kuwa Mtume (saww) hana uhai tena, kauli hiyo ni batili, kwani inazusha baadhi ya mambo: Kwanza: Je nafasi ya Mtukufu Mtume (saww) ni ya chini kuliko nafasi ya mashahidi ambao Mwenyezi Mungu amesema: 78
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 78
11/25/2014 3:03:44 PM
Ushia: Hoja na Majibu
ﷲ أَمْ َوا ًتا ۚ َب ْل ِ َّ يل َ َو َال َتحْ َس َبنَّ الَّذ ِ ِين قُ ِتلُوا فِي َس ِب ون َ ُأَحْ َيا ٌء عِ ْندَ َرب ِِّھ ْم يُرْ َزق “Na usiwadhanie kabisa wale waliouawa katika njia ya Mwenyezi Mungu kuwa wamekufa, bali wako hai mbele ya Mola wao wanaruzukiwa.” (Sura Imran: 169).
ت ِ ص ْو َ ِين آ َم ُنوا َال َترْ َفعُوا أَصْ َوا َت ُك ْم َف ْو َق َ َيا أَ ُّي َھا الَّذ Pili: Je salamu tunayomtolea Mtume (saww) katika ْو ِل َك َجھ ِْر َبعna ْ ِب ْال َقWaislamu ِّال َّن ِبيtofauti: ض جْ َھرُوا َل ُهwote َو َال َتbila ٍ ْم لِ َبعna ْ ضِ ُكinayotolewa tashahudi “Salamu iwe juu yako ewe Nabii…”, َ أَنْ َتحْ َبmtu ْ ال َت ُ ُأَعْ َمالtunamtolea َ ْم َوأَ ْن ُت ْمhuwa ُ ُون ر ع ش ك ط َ wa kufikirika tu asiye na uwepo? َّ يل َ َو ﷲ أَ ْموا ًتا ۚ ب ْل ِين قُ ِتلُوا ال َتحْ َس َبنَّ الَّذndani َmnapokuwa ِ فِي َس ِبkuwa Tatu: َ Hivi َ si ِ mnaamini ya msikiti wa Mtume ni wajibuون ُد َرب ِِّھ ْم يُرْ َزقkwa أَحْ َياpindi َ ٌء عِ ْنupole َ kuzungumza mnapokuwa jirani na kaburi lake tukufu? Kwa sababu Qur’ani Tukufu inasema:
ت ِ ص ْو َ ِين آ َم ُنوا َال َترْ َفعُوا أَصْ َوا َت ُك ْم َف ْو َق َ َيا أَ ُّي َھا الَّذ ض ٍ ْال َّن ِبيِّ َو َال َتجْ َھرُوا َل ُه ِب ْال َق ْو ِل َك َجھ ِْر َبعْ ضِ ُك ْم لِ َبع ُون َ أَنْ َتحْ َب َط أَعْ َمالُ ُك ْم َوأَ ْن ُت ْم َال َت ْش ُعر “Enyi mlioamini! Msinyanyue sauti zenu kuliko sauti ya Nabii, wala msiseme naye kwa kelele kama mnavyosemezana nyinyi kwa nyinyi, visije vitendo vyenu vikaanguka, na hali hamtambui.” (Sura Hujurat: 2). Na Aya hii imeandikwa katika ubao na kutundikwa juu ya kaburi la Mtukufu Mtume (saww). Mnayakubali vipi maneno haya yenye kupingana?
79
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 79
11/25/2014 3:03:45 PM
Ushia: Hoja na Majibu
Nne: Hakika mauti si mwisho wa uhai bali hasa ni mwanzo wa uhai mwingine mpya: “Watu wamelala, watakapofariki watazinduka.”46 Tano: Tunasoma katika hadithi maarufu ambayo imekuja katika chanzo chenye kutegemewa na Masunni, kwamba Abdullah bin Umar alinukuu kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) kuwa alisema: “Atakayezuru kaburi langu atawajibika kupata uombezi wangu.”47 Na imekuja katika hadithi nyingine ambayo ameinukuu mpokezi huyo huyo kutoka kwa Mtukufu Mtume (saww): “Atakayenizuru baada ya kifo changu ni kama amenizuru katika wakati wa uhai wangu.”48 Hivyo hali hii ya kutofautisha baina ya zama za uhai na zama za mauti ni mawazo ya kipuuzi. Hivyo kwa kupitia mjumuisho uliyopo katika hadithi hizi zilizotajwa tunaweza kusisitiza uhalali wa kufunga safari kwa lengo la kwenda kumzuru Mtukufu Mtume (saww). Wanawake na kuzuru makaburi Wanawake wanahitaji kuzuru makaburi ya wapendwa wao kwa ajili ya kujiliwaza, na kwa sababu wao ni wenye mapenzi na huruma zaidi. Kama ambavyo pia uzoefu umethibitisha kuwa wana mapenzi makubwa zaidi kuliko wanaume katika kuzuru makaburi ya mawalii wa Mwenyezi Mungu. Lakini kuna kundi la Mawahabi wenye msimamo mkali kwa bahati mbaya sana na kwa sababu ya hadithi dhaifu 46
Iwalil-Lialiy Juz. 2, Uk. 73.
47
S unan cha Darqutuniy Juz. 2, Uk. 278, Allamah Amin ametaja vyanzo 41 vya hadithi hii kutoka kwenye vitabu maarufu vya Masunni, al-Ghadir Juz. 5, Uk. 93.
48
Al-Ghadir Juz. 5, Uk. 101. 80
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 80
11/25/2014 3:03:45 PM
Ushia: Hoja na Majibu
wanawazuia wanawake kwa nguvu kuzuru makaburi, mpaka imekuwa mashuhuri katika ndimi za Mawahabi wa kawaida huko Kusini mwa Iran kuwa mwanamke mwenye kusimama kwenye kaburi, mwenye kaburi humuona utupu wake. Mmoja wa Ulamaa anasema: “Nikawaambia: ‘Hakika kaburi la Mtukufu Mtume (saww) na la Khalifa wa kwanza na la Khalifa wa pili, yote yamo ndani ya chumba cha Aisha, chumba alichokuwa akiishi au kuingia na kutoka, hivyo tukisema hakuna ubaya kusimama kwenye kaburi la Mtume (saww) katika sura mnayodai, basi ni vipi kuhusu kusimama kwake katika sura hii – ya kuonekana utupu wake – katika kaburi la Khalifa wa kwanza na la Khalifa wa pili? Jambo hili linahitaji tafakari. Vyovyote iwavyo ni kuwa dalili yao ni hadithi maarufu ambayo wanainasibisha na Mtume (saww) kuwa alisema: “Mwenyezi Mungu awalaani wanawake wenye kuzuru makaburi.” Na katika baadhi ya vitabu badala ya “Wanawake wenye kuzuru makaburi” imekuja: “Wanawake wenye kuzuru sana makaburi.” Kwa kanuni ya kukuza. Baadhi ya Ulamaa wa Kisunni akiwemo Tirmidhiy49 wamesema: “Hakika hadithi hii inahusu wakati ambao Mtume (saww) alipokuwa amekataza kuzuru makaburi, lakini hukumu hii ilifutwa baadaye.” Na aalimu mwingine miongoni mwa Ulamaa wao anasema: “Hakika yenyewe inawahusu tu wanawake ambao wanatumia muda mwingi katika kuzuru makaburi kiasi kwamba inawapelekea kupoteza haki za waume zao, na dalili yao juu ya hilo ni kanuni ya kukuza “Wanawake wenye kuzuru sana” ambayo imepatikana katika baadhi ya nakala. 49
S unan Tirmidhiy Juz. 3, Uk. 371, Mlango unaozungumzia ruhusa ya kuzuru makaburi. 81
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 81
11/25/2014 3:03:45 PM
Ushia: Hoja na Majibu
Lakini ndugu zetu hawa vyovyote watakavyojaribu kukanusha hawawezi kukanusha kitendo cha Aisha cha kulibakisha kaburi la Mtukufu Mtume (saww), kaburi la Khalifa wa kwanza na la Khalifa wa pili chumbani kwake. Safari haifungwi isipokuwa kwa ajili ya misikiti mitatu Historia inaeleza kuwa Waislamu kwa muda wa karne nyingi walikuwa wakifunga safari kwenda kumzuru Mtukufu Mtume (saww) na hakukuwa na tatizo lolote kwa yeyote. Mpaka ilipofika zamu ya Ibn Taymiyyah katika karne ya saba akawa amewakataza wafuasi wake kitendo hiki, na akasema: “Hakika safari haifungwi isipokuwa kwa ajili ya misikiti mitatu, na hairuhusiwi kwa ajili ya misikiti mingine, mara hii akatumia hadithi ya Abu Huraira kuwa dalili. Abu Huraira anasema: “Safari haifungwi isipokuwa kwa ajili ya kwenda kwenye misikiti mitatu: Msikiti wangu huu, Msikiti mtakatifu na Msikiti wa mbali.”50 Wakati ambapo kwanza: Maudhui ya hadithi inazungumzia misikiti na si kuzuru sehemu nyingine yoyote, na kwa ajili hii maana ya hadithi inakuwa ni safari haifungwi kwa ajili ya kwenda msikiti wowote ule isipokuwa tu kwa ajili ya kwenda katika misikiti hii mitatu. Pili: Hadithi hii imenukuliwa kwa tamko lingine ambapo katika tamko hilo hakuna dalili yoyote inayoonesha makusudio yao, tamko hilo ni: “Safari hufungwa kwa ajili ya kwenda misikiti mitatu.”51 Kwa kweli hii ni namna ya kuraghibisha 50
Sahih Muslim Juz. 4, Uk. 102.
51
Sahih Muslim Juz. 4, Uk. 126. 82
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 82
11/25/2014 3:03:45 PM
Ushia: Hoja na Majibu
kitendo hiki bila kukataza kufunga safari kwenda sehemu nyingine, na katika istilahi ni kwamba: “Hakika kuthibitisha kitu hakukanushi kingine.” Hivyo ikiwa haijulikani tamko asili la hadithi ni kwa tamko la kwanza au kwa tamko la pili, hadithi inakuwa ni maelezo ya jumla na haifai kuwa dalili. Inaweza kusemwa kuwa katika kitabu hicho hicho kuna tamko lingine: “Hakika safari ni kwa ajili ya kwenda misikiti mitatu….”52 Na kwa tamko hili inakuwa ni ruhusa kufunga safari kwa ajili ya kwenda misikiti mitatu tu. Jibu la ukosoaji huu liko wazi: Kwanza: Kuna ijmai ya umma juu ya kuruhusiwa kufunga safari kwa ajili ya makusudio mbalimbali sawa yawe ya kidini au yasiyo ya kidini, na safari si kwenda tu kwenye misikiti mitatu, hivyo hitimisho lake ni kuwa mabano haya ni mabano ya ziada, nayo yanamaanisha kuwa safari hufungwa kwa ajili ya kwenda misikiti mitatu tu kati ya misikiti yote. Pili: tamko la hadithi linatofautiana, hivyo haijulikani ni lipi hasa la kweli, je ni la kwanza au la pili au la tatu? Na haiwezekani Mtukufu Mtume (saww) kuelezea jambo hili kwa ibara tatu tofauti, na dhahiri ni kwamba wapokezi wa hadithi walinukuu hadithi kwa maana, na hivyo hadithi hii si bayana, na hadithi inapokuwa si bayana inakosa nguvu ya kuwa dalili. Je hairuhusiwi kujenga makaburi? Zilipita karne nyingi huku Waislamu wakiendelea kujenga majengo mengi ya kihistoria na ya kawaida juu ya makaburi 52
Sahih Muslim Juz. 4, Uk. 126. 83
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 83
11/25/2014 3:03:45 PM
Ushia: Hoja na Majibu
ya viongozi wa Uislamu, na walikuwa wanakwenda kuzuru makaburi na kutabaruku nayo, na hakuna mtu yeyote aliyepinga, na kwa kweli kulikuwa na ijmai na mwenendo wa kimatendo juu ya amali hii, na haukuonekana upingaji wowote. Wanahistoria kama vile al-Masuudiy, mwanahistoria ambaye aliishi katika karne ya nne ya Hijriyya, ametaja katika kitabu Murujud-Dhahbi, na pia mabingwa wa kusafiri kama Ibn Jubair na Ibn Batutah ambao waliishi katika karne ya saba na nane, wote wamesema kuwa waliyashuhudia majengo hayo makubwa ya kipekee. Mpaka alipodhihiri Ibn Taymiyyah katika karne ya saba na mwanafunzi wake Muhammad bin Abdul-Wahab katika karne ya kumi na mbili, wakadai kuwa kujengea makaburi ni bidaa, haramu na shirki. Kwa kweli Mawahabi wana maradhi ya wasiwasi ya ajabu, hasa katika suala la tauhidi na shirki, hiyo ni kwa sababu ya kiwango duni cha uwezo wao wa kielimu katika kuchambua mambo, na hukimbilia kupinga pindi wanapojikuta wamekwama katika maudhui yoyote ile, ikiwemo maudhui ya kufanya ziara, kuomba kuombewa, kujengea makaburi na nyinginezo, mambo haya yote kwa mtazamo wao ni mambo yaliyo kinyume na sharia, na wanayaunganisha na suala la shirki na bidaa na wanayapinga. Na suala muhimu kati ya haya ni suala la makaburi ya viongozi wa dini, wakati ambapo katika nchi mbalimbali za ulimwengu wa Kiislamu kasoro Suudia tunaona majengo makubwa kwenye makaburi ya Manabii waliopita na pia ya viongozi wa Uislamu. Tunakuta raia wa nchi hizo kuanzia Misri, India, Algeria mpaka Indonesia wanaheshimu mabaki ya athari za Kiislamu zilizopo katika nchi zao, na wanalipa 84
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 84
11/25/2014 3:03:45 PM
Ushia: Hoja na Majibu
umuhimu wa pekee suala la kuzuru makaburi ya viongozi wa dini. Lakini katika nchi ya Suudia hatuoni hali hii ya kujali athari hizi, na dalili juu ya hilo ni kutokuwepo uchambuzi salama wa dhana za Kiislamu. Mawahabi wanabomoa kumbukumbu za kitamaduni Katika karne iliyopita kulitokea tukio la kuumiza katika mji wa wahyi, tukio ambalo lilipelekea kuwanyima moja kwa moja Waislamu athari za historia ya Uislamu, na tukio hili lilitokea kwa sababu ya Mawahabi kutawala nchi hiyo. Kabla ya miaka themanini iliyopita, katika mwaka 1344 Mawahabi walipoitawala Hijaz, walianza harakati ya kubomoa athari zote za historia ya Uislamu kwa kisingizio cha shirki na bidaa, na wakazisawazisha zote sawa na ardhi. Lakini hawakuwa na ujasiri wa kutosha wa kuligusa kaburi tukufu la Mtukufu Mtume (saww) kwa kukhofia kuwa Waislamu wote watasimama dhidi yao, na kwa istilahi ni kwamba wapingaji wa Taqiyyah walitumia Taqiyyah dhidi ya Waislamu. Katika mwaka mmoja nilipokuwa nimekwenda kuhiji Nyumba takatifu ya Mwenyezi Mungu, wakati wa mazungumzo ya kindugu nilimuuliza mmoja kati ya wakubwa wao kuhusu sababu iliyowafanya walibakishe kaburi tukufu la Mtume wa Uislamu baada ya makaburi yote kubomolewa, kwa kweli hakuwa na jibu juu ya hilo. Vyovyote vile ni kuwa maisha ya mataifa mbalimbali yanafungamana na mambo mengi, miongoni mwa mambo hayo ni kuhifadhi athari za kitamaduni na kumbukumbu za kielimu na kidini. Lakini la kusikitisha sana ni kwamba ardhi ya wahyi hasa Makka na Madina imedondokea mikononi 85
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 85
11/25/2014 3:03:45 PM
Ushia: Hoja na Majibu
mwa kundi lisilo la kawaida na lenye chuki binafsi, hivyo likafanya kazi ya kufuta athari zote za thamani za utamaduni wa Kiislamu, kwa visingizio visivyo na maana, athari ambazo kila moja inaonesha msimamo miongoni mwa misimamo muhimu na mitukufu na ya historia ya Uislamu. Miongoni mwa makaburi yaliyobomolewa ni makaburi ya Maimamu wa Ahlul-Bait (as) katika makaburi ya Baqii, na dhahiri ni kwamba watu hawa wanafanya kazi ya kuondoa kila athari ya maana katika historia ya Uislamu, na kwa kupitia njia hii wanawatia Waislamu hasara isiyoweza kuzibika. Kwani athari hizi humchukua mtu mpaka kwenye kina cha historia kwa sababu ya mvuto wake na kuathiri kwake kwa ajabu, hivyo makaburi ya Baqii ambayo yalikuwa ni mandhari ya kuvutia huku kila kona yake ikielezea tukio muhimu la kihistoria, leo yamegeuka na kuwa jangwa tupu linaloogopesha kutazama, huku yakiwa katikati ya hoteli nzuri na majengo makubwa, na milango yake ya chuma isiyo na makufuli inafunguliwa kwa muda wa saa moja au saa mbili kwa siku, kwa ajili ya wanaume tu wanaofanya ziara. Visingizio wanavyotoa Mawahabi Kisingizio cha kwanza: Haipasi kuyafanya makaburi kuwa sehemu za ibada: Mara wanasema: Kujengea makaburi kunapelekea kuyaabudu, na hadithi ya Mtume inathibitisha kuwa jambo hilo haliruhusiwi: “Mwenyezi Mungu awalaani Mayahudi, kwani wamefanya makaburi ya Mitume wao kuwa ni sehemu za ibada.”53 53
S ahih Bukhari Juz. 1, Uk. 110. Na pia imekuja katika Sahih Muslim Juz. 2, Uk. 67 kwa kuongeza “na Wakristo”. 86
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 86
11/25/2014 3:03:45 PM
Ushia: Hoja na Majibu
Lakini jambo hili liko wazi kwa Waislamu wote, hakuna yeyote anayeyaabudu makaburi ya Mawalii wa Mwenyezi Mungu, kwani kuna tofauti bayana baina ya ziara na ibada (kwa maana makhususi), kama tunavyokwenda kuwazuru watu hai na kutoa heshima zetu kwa wakubwa na kuwaomba dua, ndivyo tunavyokwenda kuwazuru wafu kwa ajili ya kuwaheshimu viongozi wa dini na mashahidi wa Uislamu, na kuwaomba dua. Je kuna mtu yeyote mwenye akili timamu anayesema: “Kuwazuru watu watukufu kwa sura niliyoitaja katika zama za uhai wao ni kuwaabudu, ni shirki na ukafiri? Na hivyo hivyo kuwazuru baada ya kifo chao? Hakika Nabii wa Uislamu (saww) alikuwa anakwenda kuzuru makaburi ya Baqii, na kuna riwaya nyingi katika vitabu vya Masunni vinaashiria hilo. Ndiyo Mwenyezi Mungu awalaani Mayahudi, kwani wamefanya makaburi ya Mitume wao kuwa ni sehemu za ibada, lakini hakuna Mwislamu yeyote aliyelifanya kaburi lolote kuwa ni sehemu ya ibada. Mwenye kutazama kwa makini ataona kuwa kuba la kaburi la Mtukufu Mtume (saww) liko juu pembeni ya Msikiti wa Mtume (saww), na Waislamu wote hata hao Mawahabi wenyewe wanasali Sala tano katika nyakati tano katika raudha tukufu ambayo ipo pembeni mwa Msikiti wa Mtume ikiwa imeungana nao, na wanasali pia Sala za sunna katika nyakati nyingine. Je kufanya hivi ni kuyaabudu makaburi na ni haramu? Au kaburi tukufu la Mtume halihusiki na hukumu hiyo, je dalili za kufanya shirki na kumwabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu zinahusu baadhi na kuacha baadhi?! Kuzuru makaburi hakuna uhusiano wowote na kuliabudu, na wala hakuna tatizo lolote katika kusali jirani na kaburi la 87
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 87
11/25/2014 3:03:45 PM
Ushia: Hoja na Majibu
Mtukufu Mtume (saww) na makaburi mengine ya Mawalii, na hadithi iliyotajwa inazungumzia wale wenye kuyaabudu makaburi yenyewe. Hivyo wale wenye kujua jinsi Mashia ulimwenguni wanavyoyazuru makaburi ya Maimamu wao (as) wanajua kuwa wao huelekea kibla pindi mwadhini anaponyanyua sauti ya kusimamisha Sala ya wajibu ya jamaa, na huanza kwa takbira pindi wanapotaka kufanya ziara, na wanapomaliza husali rakaa mbili za sunna kwa kuelekea kibla, ili ibainike wazi kuwa anayestahiki kuabudiwa ni Mwenyezi Mungu tu mwanzo hadi mwisho. Lakini kwa bahati mbaya sana na kwa ajili ya sababu maalumu, mlango wa tuhuma, uwongo na uzushi umekuwa wazi, ambapo kundi dogo la Kiwahabi linafanya kazi ya kuwatuhumu kwa tuhuma mbalimbali Waislamu wote wenye kuwakhalifu wao. Na kauli nzuri tunayoweza kusema ni kwamba wao hawana uwezo wa kuchambua mambo kwa namna sahihi, kwa sababu ya kiwango duni cha elimu walichonacho, na hawakuweza kuujua ukweli wa shirki na tauhidi, na wala hawajui vilivyo tofauti iliyopo baina ya ziara na ibada. Kisingizio cha pili: Wamenukuu hadithi kutoka kwenye Sahih Muslim kwamba Abil Hayyaj alipokea riwaya hii kutoka kwa Mtukufu Mtume (saww): “Ali bin Abu Talib aliniambia: Je, nikutume kwa jambo ambalo Mtume wa Mwenyezi Mungu alinituma kwamba, usiache sanamu yoyote ila uiondoshe wala kaburi lolote lile lililonyanyuka isipokuwa ulisawazishe.”54 Na kwa sababu ya ufahamu wao wa makosa kuhusu hadithi wameinua nyundo zao na kubomoa makaburi yote ya watu 54
Sahih Muslim Juz. 3, Uk. 61. Musnad Abi Ya’la Juz. 1, Uk. 455, Darul-Maamun. 88
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 88
11/25/2014 3:03:45 PM
Ushia: Hoja na Majibu
watukufu katika Uislamu kasoro kaburi la Mtukufu Mtume (saww), kaburi la Khalifa wa kwanza na la Khalifa wa pili yaliyopo pembezoni mwa kaburi la Mtukufu Mtume (saww) ambapo wameyaacha kama yalivyokuwa, na wala hakuna dalili yoyote juu ya ubaguzi huu. Lakini kuna mambo kadhaa ya kukosoa katika hadithi hii: Kwanza: Hakika katika sanadi ya hadithi hii kuna watu wasiokuwa waaminifu kati ya wapokezi wa hadithi wa upande wa Masunni, na baadhi yao walikuwa ni waongo hususan Sufyan Thawriy na Ibn Abi Thabit. Pili: Na hata tukijaalia kuwa hadithi hii ni sahihi, bado maana yake itakuwa ni kaburi liwe sawa bila nundu, na katika hilo kuna wanafiqhi wengi ambao wametoa fatwa kuwa ni wajibu kaburi liwe sawa bila nundu, hivyo hakuna uhusiano kati ya hilo na suala tunalozungumzia. Tatu: Na hata tukijaalia kuwa maana ya hadithi ni kuwa kaburi liwe sawa na ardhi bila mwinuko, bado pia maudhui hii haina uhusiano wowote na suala la kujenga juu ya kaburi. Hebu tufanye kuwa juu ya kaburi la Mtukufu Mtume kuna jiwe lililo sawa na ardhi, na wakati huo huo juu ya kaburi kuna kuba – kama tunavyoliona leo), bila shaka hali hiyo haipingani na hukumu iliyotajwa. Kama ambavyo pia sisi tunasoma katika Qur’ani Tukufu pindi ilipofichuka siri ya Vijana wa Pangoni, watu wakasema ni lazima tujenge jengo juu ya makaburi yao, na baadaye wakasema: “Wakasema wale walioshinda katika shauri lao. Hakika tutajenga msikiti juu yao.” (Sura Kahfi: 21). Hivyo Qur’ani Tukufu imetaja kisa hiki bila kuwakosoa, na hii inamaanisha kuwa hakuna kizuizi katika kujenga msikiti pembezoni mwa makaburi ya watu watukufu. 89
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 89
11/25/2014 3:03:45 PM
Ushia: Hoja na Majibu
Athari chanya za kuzuru makaburi ya watu watukufu Tukiweza kuwaongoza watu kwa namna inayofaa ili wajiepushe na aina yoyote ya uzembe na upindukiaji mipaka, na wamtaje Mwenyezi Mungu Mtukufu pembeni mwa makaburi haya matukufu, watubu kwa Mwenyezi Mungu, na wachukue mafunzo na fikra kutoka kwa Mawalii wa Mwenyezi Mungu, bila shaka makaburi haya matukufu yaliyopo yatakuwa ni vituo vya malezi, mafunzo, toba, marejeo kwa Mwenyezi Mungu na kuziadabisha nafsi. Hakika uzoefu umetufunza kwamba mamilioni ya watu ambao huenda kuyazuru makaburi matukufu ya viongozi wa dini au makaburi ya mashahidi wa njia ya haki, hurejea majumbani kwao wakiwa na ari ya hali ya juu, nafsi safi na zenye nuru na nyoyo safi, na athari hizi hubaki kwao muda mrefu. Wakati hawa wanaomba kuombewa mbele ya Mwenyezi Mungu ili wafutiwe madhambi na kutatuliwa matatizo yao ya kidini na kidunia, ni lazima wajenge mahusiano ya kiroho na Mawalii wa Mwenyezi Mungu, mpaka wajitenge na maasi kadiri iwazekanavyo, na waelekee katika kutenda kheri. Zaidi ya hapo ni kuwa kujielekeza kwao kwa Mawalii wa Mwenyezi Mungu na kuomba kupitia kwao na kuwaomba wawaombee kwa Mwenyezi Mungu, kunaongeza ari yao na uwezo wao wa kuweza kupambana na changamoto zinazowakabili, na kunazuia upatikanaji wa hali ya kukata tamaa na kuvunjika moyo, na kunapunguza machungu yao ya kiroho na kimwili, na pia kuna athari na baraka nyingine nyingi. Kwa nini tunawanyima watu hawa baraka zote hizi za kimaanawiya, kiroho, na kimwili, kwa sababu tu ya 90
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 90
11/25/2014 3:03:45 PM
Ushia: Hoja na Majibu
ufahamu wa kimakosa juu ya suala la kufanya ziara, kuomba kuombewa, na kuomba kupitia watu wema? Ni nani mwenye akili timamu anayeruhusu jambo hili? Kwa sababu kuzuia meza hii ya kimaanawiya kunapelekea hasara kubwa, zaidi ya hapo ni kwamba wasiwasi usio wa kawaida katika masuala ya tauhidi na shirki yanapelekea kulinyima kundi kubwa faida hizi. Kisingizio cha nne Kisingizio kingine ni kuwa wale wanaokwenda kuzuru makaburi ya watu watukufu huenda kwa ajili kutafuta baraka na kubusu makaburi, na amali hii ina shirki ndani yake. Na kwa ajili hii ndio maana wenye kuzuru Nyumba takatifu ya Mwenyezi Mungu huwaona askari wakali wamesimama kwa kulizunguka kaburi la Mtukufu Mtume (saww) wakiwazuia watu wasilikaribie, na baadhi wanalinasibisha jambo hili na Ibn Taymiyyah na Muhammad bin Abdul-Wahab. Kwa kweli hawa watu wawili waasisi, wa madhehebu ya Kiwahabi laiti wangekuwepo zama za uhai wa Mtukufu Mtume wa Uislamu (saww) na wakaona kwa macho yao matukio ya Sulhu ya Hudaibiya au tukio la Kuikomboa Makka, pindi Mtukufu Mtume (saww) alipokuwa akichukua udhu huku Maswahaba wake na wafuasi wake wakishindana kupata matone ya maji ya udhu wake kiasi kwamba hakuna tone hata moja linalodondoka ardhini,55 wangesema kwa siri kuwa hakika hili haliafikiani na hadhi ya Mtume (saww) na hili lina shirki ndani yake, kama wasingekuwa na 55
a tukio hili limetokea mara nyingi katika muda wote wa uhai wa Mtukufu N Mtume (saww), rejea Sahih Muslim Juz. 4, Hadithi ya 1943. Kanzul-Ummal Juz. 16, Hadithi ya 249. 91
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 91
11/25/2014 3:03:45 PM
Ushia: Hoja na Majibu
ujasiri wa kutamka hilo wazi wazi. Na ni hivyo hivyo kama wangekuwepo huko Madina baada ya kufariki Mtukufu Mtume (saww) na wakaona kwa macho yao jinsi Abu Ayub al-Ansariy mwenyeji wa kwanza wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) alivyoweka uso wake kwenye kaburi la Mtume (saww) ili kutafuta Baraka.56 Au kama wangeona alilofanya Bilal, mwadhini wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) ambapo alikaa pembeni ya kaburi lake (saww) na kulia kwa sauti ya juu huku akiuchakaza uso wake kwa udongo wa kaburi, wangesimama na kumchukua Bilal na Abu Ayub na kuwatupilia mbali, kwa sababu kwao wao kitendo hiki ni shirki, kama wanavyofanya leo wafuasi wa madhehebu hii ya Kiwahabi kuwafanyia watu wanaolizuru kaburi la Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww). Wakati hakuna uhusiano wowote hata kidogo kati ya kutafuta Baraka na ibada, bali kutafuta Baraka ni aina moja ya heshima na adabu, kwa kutaraji kuwa kwa ajili ya heshima hii Mwenyezi Mungu Mtukufu atawashushia baraka zake wenye kumzuru Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww). Jukumu kubwa la Ulamaa wa Kiislamu Ni wajibu juu ya Ulamaa wote na wanafikra wa Kiislamu kuzuia matendo yasiyofaa yanayotendwa na baadhi ya watu wa kawaida pembeni mwa kaburi la Mtukufu Mtume (saww) au kwenye makaburi ya Maimamu waliozikwa huko Baqii na ya Maimamu wengine maasumu, na pia kwenye makaburi ya mashahidi na viongozi wa Uislamu. Na wawafunze maana halisi ya dhana ya kufanya ziara, kutawasali, kutabaruku 56
Mustadrakus-Sahihayn Juz. 4 Uk. 560. Taarikh Ibn Asakir Juz. 7 Uk. 137. 92
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 92
11/25/2014 3:03:45 PM
Ushia: Hoja na Majibu
na kuomba kuombewa, ili wapingaji wasigeuze hilo kuwa kisingizio. Waambieni watu: Hakika mambo yote yako mikononi mwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na Yeye ndiye chanzo kikuu cha sababu zote, Mwenye kukidhi haja zote, Mwenye kuondoa matatizo yote na Mwenye kutosheleza katika mambo yote, hivyo mnapoomba kupitia Mtukufu Mtume (saww) na Maimamu (as), Mwenyezi Mungu huwajibu kupitia wao na huwakubalia uombezi wao Kwake, hiyo ni kwa ajili ya nafasi yao tukufu na nafsi zao safi, na hivyo haja zenu hukubaliwa kwa heshima waliyonayo Kwake. Hakika kitendo cha baadhi ya watu wa kawaida kusujudu mbele ya kaburi tukufu na kutamka baadhi ya ibara ambazo zina chembechembe ya kutaja uungu wao, au kufunga mafundo kwenye makaburi yao na mfano wa matendo hayo yasiyo sahihi, yanaleta matatizo na kuchafua sura nzuri na imara ya kufanya ziara, na kupelekea kuwa kisingizio cha huyu na yule cha kuwanyima watu baraka za kufanya ziara.
93
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 93
11/25/2014 3:03:45 PM
Ushia: Hoja na Majibu
MADA YA TANO NDOA YA MUDA (MUT’A)
U
lamaa wote wa Uislamu wanaamini kuwa ndoa ya muda ilikuwepo katika zama za Mtume wa Uislamu (saww) kwa kipindi cha muda fulani. Na baadhi yao wanasema hakika iliharamishwa zama za ukhalifa wa Khalifa wa pili kwa amri ya Khalifa mwenyewe. Na wengine wanasema kuwa iliharamishwa tangu zama za Mtukufu Mtume (saww). Ama sisi wafuasi wa madhehebu ya Ahlul-Bait (as) tunaamini kuwa haikuharamishwa kabisa, na bado iko katika hali yake kwa sharti zake. Kuna kundi dogo la Masunni linaafikiana nasi katika itikadi hii, lakini aghlabu yao wanatofautiana na rai yetu, na daima walikuwa wakitulaumu kwa hilo, na ndoa hii si sehemu ya kukosoa bali ni nukta muhimu ya kutatua matatizo mengi ya kijamii. Hivyo mtasoma ufafanuzi wa mada hii katika vipengele vifuatavyo: Dharura na mahitaji Hakika watu wengi na hasa vijana hawana uwezo wa kufunga ndoa ya daima, zaidi ya hapo ni kuwa ndoa ya daima inahitaji vitangulizi na uwezo na uwajibikaji katika majukumu mbalimbali, na mambo hayo hayapatikani kwa baadhi, kwa mfano tu: a. Vijana wengi hawana uwezo wa kuoa katika kipindi cha masomo - hasa katika zama zetu hizi ambapo masomo 94
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 94
11/25/2014 3:03:45 PM
Ushia: Hoja na Majibu
huendelea kwa kipindi kirefu – kwa kutokuwa na kazi, makazi yanayofaa na mahitaji mengine. Na hata akijaribu kukomea kwenye mahitaji ya dharura katika hafla ya ndoa, pamoja na hilo bado kwa kiwango cha chini kabisa atahitaji baadhi ya mahitaji ya kimaisha ambayo hana. b.
Kuna watu wenye ndoa ambao hukumbwa na shinikizo la kuhitaji kufanya mapenzi wawapo katika safari zao za nje, na hasa inapokuwa ni safari ya muda mrefu, na wao hawana uwezo wa kufuatana na wake zao katika safari hizo, na hawana uwezo wa kuoa ndoa ya daima kwa mara nyingine wawapo ugenini.
c.
Kuna watu ambao wake zao wanasumbuliwa na maradhi mbalimbali na matatizo kadhaa, na wake hao hawana uwezo wa kukidhi mahitaji ya kimapenzi ya waume zao.
d.
Wapo askari wanaokwenda kwenye majukumu kwa muda mrefu kwa ajili ya kuhifadhi mipaka na wajibu mwingine, na hawa wanaweza kupatwa na shinikizo la kutaka kufanya mapenzi kwa sababu ya kuwa kwao mbali na wake zao. Kama tutakavyoona lilivyotokea jambo hilo katika zama za Mtukufu Mtume (saww), ambapo tatizo hili liliwapata askari wengi wa jeshi la Waislamu, jambo ambalo lilipelekea ndoa hii ya muda kuhalalishwa kisharia.
e.
Baadhi ya wanaume - hasa vijana - wanaweza kupatwa na matatizo ya kisaikolojia kwa sababu ya kutokuwa karibu na wake zao kwa muda mrefu, katika kipindi cha ujauzito, kwa sababu ya mazingira maalumu ambayo kikawaida husuhubiana naye. 95
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 95
11/25/2014 3:03:45 PM
Ushia: Hoja na Majibu
Hakika dharura hizi na matatizo haya ya kijamii daima yalikuwepo na yataendelea kuwepo, na hayahusu tu zama za Mtukufu Mtume (saww), bali inawezekana katika zama zetu yamekuwa makubwa zaidi, hiyo ni kwa sababu ya kuongezeka vyanzo vya matatizo hayo, vyanzo ambavyo vimeizingira jamii yetu kwa sasa. Hivyo katika hali hii watu wamesimama njia panda, ima waingie katika uchafu (Mwenyezi Mungu aepushe hilo) au watumie ndoa ya muda, ndoa nyepesi ambayo haiwajibishi matunzo ambayo yanawajibishwa na ndoa ya daima, na kwa ndoa hiyo mtu akidhi mahitaji yake ya kimapenzi. Pendekezo la kujinyima na kujizuia kwa kufumbia macho mambo yote mawili (kutokuzini na kutokuoa ndoa ya muda) ni pendekezo zuri, lakini liko nje ya uwezo wa watu wengi, na kwa uchache ni kwa hawa watu ambao wanaona jambo hilo la kujizuia ni jambo la kifikra tu. Ndoa ya Misyar La kushangaza ni kwamba watu wengi miongoni mwa Masunni wenye kuikanusha ndoa ya muda, kidogo kidogo kwa sababu ya vijana na watu wengine kupatwa na mashinikizo ya kufanya mapenzi, wamelazimika kuikubali ndoa inayoshabihiana kwa namna fulani na ndoa ya muda, ndoa ambayo huitwa “Ndoa ya Misyar,� japokuwa wao hawajaiita ndoa ya muda lakini haina tofauti na ndoa ya muda, nayo ni kwamba mtu aliyedharurika anaruhusiwa kumuoa mwanamke kwa namna ya ndoa ya daima hata kama amenuwia kumtaliki baada ya muda mfupi, na amempa sharti la kutowajibika kumpa matunzo, kutokuwa na haki ya kulala na 96
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 96
11/25/2014 3:03:45 PM
Ushia: Hoja na Majibu
kurithi. Kwa kweli yenyewe katika uhalisia inashabihiana na ndoa ya muda katika sehemu kubwa isipokuwa katika kutengana, ambapo katika ndoa hii kunatimia kwa talaka ya kawaida, ambapo katika ndoa ya muda kunatimia ima kwa mwanaume kumzawadia mwanamke muda uliobaki au kwa kuisha muda waliokubaliana. Lakini ndoa zote mbili (ya Muda na ya Misyar) zina muda maalumu ambao umeainishwa tangu mwanzo. La kuvutia katika jambo hili ni kuwa baadhi ya vijana wa Kisunni kwa sababu ya matatizo na mashinikizo yanayowakabili katika njia ya kupata ndoa ya daima, wamekuwa wakiwasiliana nasi siku za hivi karibuni kwa njia ya Mtandao wa Intaneti, na wametuuliza swali hili: “Je kuna kizuizi chochote katika suala la ndoa ya muda kufuata fatwa ya Shia?” Tukawajibu: “Kamwe hakuna kizuizi.” Hawa wanaokataa ndoa ya muda wanaikubali ndoa ya Misyar, hivyo hata kama wao hawaikubali ndoa ya muda kwa jina lake wanaikubali kwa uhalisia wake. Ndio; dharura zinazompata mtu zinaweza kumshurutisha mtu kukubali mambo kwa uhalisia wake, hata kama ni kwa jina tofauti. Hivyo kwa matokeo haya na kwa kuendelea kwao kung’ang’ania kuikataa ndoa ya muda ni kuwa wao wanaiandalia zinaa njia, isipokuwa kama watabuni aina nyingine yenye kushabihiana kama hali ilivyo katika ndoa ya Misyar, na kwa ajili hii zimekuja riwaya za Ahlul-Bait (as) zikisema: “Laiti kama si kukhalifu kwao ndoa ya muda ya Uislamu basi hakuna mtu yeyote ambaye angepatwa na zinaa.”57 57
I mam as-Sadiq (a.s.) anasema: “Laiti kama si Umar kukataza ndoa hiyo basi asingezini isipokuwa muovu wa kupindukia.” Wasailus-Shia Juz. 14, Uk. 440, Hadithi ya 24. na hadithi hii imekuja mara nyingi katika vitabu vya Masunni, nayo ni kauli ya Imam Ali (a.s.): “Laiti si Umar kukataza Mut’a basi asingezini 97
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 97
11/25/2014 3:03:45 PM
Ushia: Hoja na Majibu
Pamoja na haya yote bado wamefanya kazi ya kuipotosha maudhui ya ndoa ya muda ambayo imehalalishwa kisharia ili kukidhi dharura na mahitajio ya wasio na kitu, na kuidhihirisha kwa sura mbaya, na kwa njia hii wameandaa mazingira ya kuenea uharibifu kwa njia ya zinaa katika jamii ya Waislamu. Kwa kweli wao ni washiriki wa watenda dhambi katika kutenda maasi, kwa sababu wao wamewakataza watu kutumia njia sahihi ya kufunga ndoa ya muda. Vyovyote iwavyo ni kuwa Uislamu umeweka kanuni zinazooana na maumbile ya binadamu, ili kuweza kukidhi mahitaji yake halisi, na hivyo ndoa ya muda haiwezi kuondolewa katika orodha ya hukumu zake. Muda si mrefu itabainika kuwa ndoa ya muda ililetwa na Qur’ani Tukufu na hadithi za Mtume (saww) na ikatekelezwa kivitendo na kundi la Maswahaba, isipokuwa kundi jingine linadai kuwa hukumu hii ya Uislamu ilifutwa, na tutaona huko mbele kuwa hawamiliki dalili yoyote yenye kukinaisha juu ya kufutwa huko wanakodai. Ni ipi hiyo ndoa ya muda? Baadhi yao bila elimu wamesimama na kutoa maana isiyofaa kuhusu ndoa ya muda, na bado wanaendelea kufanya hivyo, ambapo wameielezea kuwa ni: “Kuukubali rasmi uchafu, ngono na uhuru wa kufanya mapenzi.” Kama watu hawa wangekuwa ni kutoka jamii ya watu wa kawaida ingekuwa rahisi, lakini la kusikitisha ni kwamba wapo baadhi ya Ulamaa kutoka upande wa Masunni wanaounga isipokuwa muovu wa kupindukia.” Tafsir Tabari Juz. 5, Uk. 119. Tafsir DurulManthur Juz. 2, Uk. 140. Tafsirul-Qurtubiy Juz. 5, Uk. 130. 98
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 98
11/25/2014 3:03:45 PM
Ushia: Hoja na Majibu
mkono tuhuma hii mbaya, na mimi nina yakini kuwa wao hawajajilazimisha kusoma vitabu vya wenye kuikubali ndoa ya muda, na huenda hawajawahi kusoma hata msitari mmoja, na jambo hili linasikitisha sana. Na sisi katika muhtasari huu tunalazimika kuelezea masharti ya ndoa ya muda, na kubainisha vizuri tofauti iliyopo baina yake na ndoa ya daima, ili hoja ya Mwenyezi Mungu itimie juu ya watu wote. Hakika hukumu na masharti mengi yaliyopo katika ndoa ya muda ndio hayo hayo yaliyopo katika ndoa ya daima: 1.
Ni wajibu kupata ridhaa kutoka kwa mwanamume na mwanamke juu ya ndoa yao, tena kwa hiyari kamili bila upande mmoja kuulazimisha upande mwingine.
2.
Ni wajibu tamko la ndoa liwe kwa “Ankahtuka” au “Zawajtuka” au kwa “Mataatuka”, wala haisihi kwa lafudhi nyingine.
3.
Ni sharti kupata idhini ya walii ikiwa anayeolewa ni bikra, wala si sharti kufanya hivyo iwapo si bikra.
4.
Ni lazima kuainisha vizuri muda na mahari, na kama muda hautatajwa kwa kusahau basi itageuka na kuwa ndoa ya daima, hiyo ni kwa mujibu wa fatwa za Ulamaa wengi wa fiqhi. Na hii ni dalili ya kwamba sifa za asili za ndoa zote mbili ni moja kasoro katika jambo moja, nalo ni katika kutaja muda na kutotaja muda.
5.
Kumalizika muda ndio sawa na talaka, na baada ya hapo ni wajibu moja kwa moja mwanamke akae eda ya talaka, ikiwa alimwingilia. 99
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 99
11/25/2014 3:03:45 PM
Ushia: Hoja na Majibu
6.
Eda ya ndoa ya daima ni tohara tatu, na atakapoiona tu tohara ya tatu eda inakuwa imekamilika. Lakini eda ya ndoa ya muda ni tohara mbili si zaidi.
7.
Watoto wanaozaliwa kutokana na ndoa ya muda ni watoto halali kisharia, na wana haki zote sawa na watoto waliozaliwa katika ndoa ya daima, na wanarithi kwa baba na mama na kwa ndugu wote. Na hakuna tofauti katika haki baina ya watoto wa aina hizi mbili za ndoa.
8.
Watoto wa ndoa ya muda ni wajibu wawe chini ya uangalizi wa baba na mama, na ni lazima kutoa matunzo na matumizi yao yote kama ilivyo kwa watoto wa ndoa ya daima.
Huenda baadhi ya watu wakastaajabu sana pindi watakaposikia maneno haya, wana haki ya kufanya hivyo, kwa sababu bongo zao sio salama na hazijui chochote kinachohusu ndoa ya muda, na huenda wanaamini kuwa ni ndoa isiyo halali na isiyo kamili na iko nje ya mipaka ya sharia, na kwa ibara nyingine ni ndoa yenye kushabihiana na zinaa. Wakati ambapo ukweli wake si hivyo kabisa. Ndio, kuna tofauti baina ya ndoa hizi mbili upande wa mume na mke, wajibu alionao kila mmoja wao juu ya mwenzake ni mdogo zaidi katika ndoa ya muda kuliko ule alionao katika ndoa ya daima, kwa sababu lengo la ndoa ya muda ni kurahisisha na si kutia uzito, hivyo miongoni mwa tofauti hizi ni: 1.
Hakika katika ndoa ya muda mwanamke hana matunzo wala urithi, hii ni ikiwa hakukuwa na sharti hilo tangu mwanzo, kama lilivyosema hilo kundi la Ulamaa, hivyo kama mwanamke ataweka sharti hilo (la kupewa 100
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 100
11/25/2014 3:03:45 PM
Ushia: Hoja na Majibu
matunzo au kurithi) ni wajibu kutenda kwa mujibu wa sharti hilo. 2.
Katika ndoa ya muda mwanamke yuko huru katika kuchagua kazi ya kufanya nje ya nyumba, wala si sharti kwake kuomba idhini na wala mume hana haki ya kumzuia. Lakini katika ndoa ya daima mwanamke haruhusiwi kufanya hivyo isipokuwa kwa kuafikiana.
3.
Katika ndoa ya muda si wajibu mwanamume kulala kwa mkewe.
Bila shaka kwa kuziangalia kwa makini hukumu tulizozitaja watu wengi watabainikiwa na majibu ya maswali, hukumu za uwongo na uzushi unaozushwa, na wataondokewa na dhana za uwongo na mbaya zinazoenezwa kuhusu hukmu hii tukufu ya Kiislamu. Kwa kweli hakuna mfanano wowote baina ya ndoa ya muda na zinaa au matendo yenye kuondoa staha. Bila shaka watu hawa wanaolinganisha baina ya aina mbili hizi za matendo hawana aina yoyote ya maarifa kuhusu ukweli wa ndoa ya muda na masharti yake. Utumiaji hasi Kuyatumia vibaya mambo ya haki huwa kunatoa fursa kwa wenye ndimi chafu, na pia hutoa visingizio na hoja kwa mwenye kutafuta njia ya kukosoa, hivyo hutumia hali hiyo kama kigezo cha kukosoa mambo hayo ya haki na ya halali kisharia. Ndoa ya muda ni miongoni mwa mifano halisi ya wazi ya mada hii, na kwa bahati mbaya sana baadhi ya watu wenye malengo yao binafsi na wafuasi wa matamanio wamefanya 101
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 101
11/25/2014 3:03:45 PM
Ushia: Hoja na Majibu
kazi ya kuichafua na kuipotosha ndoa hii, ambayo kiasili ilihalalishwa kisharia ili iwe suluhisho la baadhi ya matatizo makubwa ya kijamii na ya dharura, wamefanya hivyo ili wawape wapingaji wa ndoa hii sababu na visingizio vya kuikosoa sharia hii iliyojaa hekima. Lakini swali hapa ni: Ni hukumu ipi ambayo haijaguswa mpaka leo hii na mikono ya walaghai wenye kutumia vibaya mambo, na ni kanuni ipi ya thamani ambayo haijatumiwa vibaya na makundi yasiyohusika? Hivi siku moja ikiwekwa misahafu kwa uwongo na udanganyifu juu ya vichwa vya mikuki ili kuhalalisha serikali ya madhalimu na wenye chuki binafsi, je hii inamaanisha kuwa tuitenge mbali Qur’ani? Hivi ikiwa kundi la wanafiki walijenga msikiti wa kuudhuru Uislamu, na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) akaamuru ubomolewe na kuchomwa moto, je hii inamaanisha kuwa tuiache misikiti moja kwa moja. Vyovyote iwavyo ni kuwa sisi tunakiri kuwa kuna baadhi ya watu wameitumia hukumu hii muhimu ya Kiislamu vibaya, lakini sisi hatuwezi kufunga milango ya msikiti kwa sababu ya kundi fulani la waacha Sala, au kuwasha moto kwa sababu ya leso ya Kaisari. Ni wajibu tufunge milango mbele ya wafuasi wa matamanio na walaghai wenye kutumia mambo vibaya kwa maslahi yao, na tuweke masharti na vigezo sahihi vya ndoa ya muda, hasa katika zama zetu hizi, ambapo haiwezekani kutekeleza jambo hili bila mipango sahihi na mizuri, hivyo ni lazima kundi la wabobezi na wenye ujuzi waweze kuandika kanuni za kuweza kuinadhimu na kuitekeleza, ili kuzuia mikono ya kishetani isiifikie, na ili kuhifadhi utukufu wa sharia hii iliyojaa hekima, na ili kuziba mwanya dhidi ya makundi yote 102
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 102
11/25/2014 3:03:46 PM
Ushia: Hoja na Majibu
mawili: Kundi la wafuata matamanio na kundi la wakosoaji wenye chuki binafsi. Ndoa ya muda katika Kitabu, Sunnah na Ijmai ya umma Katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu ndoa ya muda imekuja kwa neno Mut’a, ambapo Mwenyezi Mungu anasema:
ۚ ض ًة َ ُورھُنَّ َف ِري َ َف َما اسْ َتمْ َتعْ ُت ْم ِب ِه ِم ْنھُنَّ َفآ ُتوھُنَّ أُج اض ْي ُت ْم ِب ِه ِمنْ َبعْ ِد َ َو َال ُج َنا َح َع َل ْي ُك ْم فِي َما َت َر ان َعلِيمًا َحكِيمًا َ ْال َف ِر َ ﷲ َك َ َّ َّيض ِة ۚ إِن “Ambao mmefunga nao ndoa ya muda katika wao, basi wapeni mahari yao yaliyolazimu. Wala si vibaya kwenu katika yale mliyoridhiana baada ya (kutoa) kile kilichowalazimu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye hekima.” (Sura Nisaa: 24).
Na nukta muhimu hapa ni kuwa kuna riwaya nyingi zimenukuliwa kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) ambazo ndani yake limekuja neno Mut’a kwa maana ya ndoa ya muda, na huko mbele tutawasilisha riwaya hizo kwa mheshimiwa msomaji. Zaidi ya hapo ni kuwa ndani ya vitabu vya Ulamaa wa sharia ya Uislamu – Shia na Sunni – ndoa ya muda imeelezwa kwa neno Mut’a, na kwa kweli kukataa maudhui hii ni sawa na kukataa vitu vilivyokubalika na wote. Na Inshaallah huko mbele tutawasilisha kwenu kundi la maneno ya Ulamaa wa sharia ya Uislamu. 103
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 103
11/25/2014 3:03:46 PM
Ushia: Hoja na Majibu
Pamoja na yote haya bado baadhi yao wanang’ang’ania kutafsiri neno Istimtai lililopo katika Aya husika kwa maana ya kustarehe, na wamesema: Maana ya Aya hii ni kumpa mahari mke ambaye anakusudia kustarehe naye kimapenzi. Hapa tunataja majibu mawili juu ya kauli yao hiyo: Kwanza: Hakika kinachowajibisha kutoa mahari ni ndoa, kwa maana ya kwamba kwa kitendo cha kutimia tu ndoa mwanamke anaweza kuomba mahari kamili hata kama bado hajamwingilia, au hata kabla ya kutokea aina yoyote ya kuchezeana. Ndiyo, iwapo talaka itatokea kabla ya kumwingilia hapo mahari inakuwa nusu. Pili: Hakika istilahi ya Mut’a kama tulivyoitaja katika tasnia ya sharia na katika maneno ya wanafiqhi wa Kishia na Kisunni, na kama ilivyokuja katika riwaya, humaanisha ndoa ya muda, na muda si mrefu tutaona dalili nyingi zenye kuunga mkono hilo. Huyu hapa Sheikh Tabrasiy mfasiri maarufu na mwandishi wa tafsiri Maj’maul-Bayan, katika tafsiri yake ya Aya hii anatamka wazi wazi kuwa kuna nadharia mbili katika tafsiri ya Aya hii: Ya kwanza: Nadharia ya mtu aliyetafsiri Istimtai hapa kwa maana ya kustarehe. Na akataja kundi la Maswahaba, Tabiina na wengineo. Ya pili: Nadharia ya mtu aliyefasiri Istimtai hapa kwa maana ya ndoa ya muda, na hii ndio rai ya Ibn Abbas, Ibn Mas’ud na kundi la Tabiina. Sheikh anaendelea katika mazungumzo yake na anasema: “Nadharia ya pili iko wazi, kwa sababu neno Mut’a na Istimtai 104
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 104
11/25/2014 3:03:46 PM
Ushia: Hoja na Majibu
katika tasnia ya Sharia humaanisha ndoa ya muda, zaidi ya hapo ni kuwa wajibu wa kumpa mahari mwanamke hauna sharti la kustarehe naye.”58 Huyu hapa Qurtubiy anasema katika tafsiri yake: “Makusudio ya Aya kwa mtazamo wa jamuhuri ni ndoa ya muda ambayo ilikuwepo mwanzoni mwa Uislamu.”59 Na Suyutiy katika Durul-Manthur, Abu Hayan, Ibn Kathir na Thaalabiy, wote katika tafsiri zao wameashiria maana hii. Hakika suala la kuwepo ndoa ya muda zama za Mtukufu Mtume (saww) ni jambo linalokubalika na Ulamaa wote wa Uislamu, sawa wawe Mashia au Masunni, isipokuwa kuna kundi la Ulamaa kutoka kwa Masunni ambao wanaamini kuwa hukumu hii ilifutwa baadaye, na kuna tofauti kubwa baina yao katika kuainisha ni wakati gani ilifutwa. Haya ndiyo aliyosema aalimu maarufu kwa jina la anNawawi katika ufafanuzi wake wa kitabu Sahih Muslim: 1.
Baadhi wanasema ilikuwa halali katika vita vya kwanza vya Khaibari, na ikaharamishwa baadaye.
2.
Ilikuwa halali kwenye Umrah tu ya kulipa.
3.
Ilikuwa halali siku ya kwanza ya Ukombozi wa Makka, kisha ikaharamishwa baadaye.
4.
Iliharamishwa katika vita vya Tabuk mnamo mwaka wa nane Hijiriyah.
5.
Ilikuwa halali katika vita vya Awtasi tu mnamo mwaka wa nane Hijiriyah.
58
Majmaul-Bayan Juz. 3. Uk. 60.
59
Tafsirul-Qurtubiy Juz. 5. Uk. 120. Fathul-Ghadir Juz. 1 Uk. 449. 105
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 105
11/25/2014 3:03:46 PM
Ushia: Hoja na Majibu
6.
Iilikuwa halali katika Hija ya kuaga mnamo mwaka wa kumi Hijiriyah.”60
Na la kuchunguza zaidi ni kuwa katika maudhui hii kumenukuliwa riwaya zenye kupingana na kugongana, hasa riwaya zinazodai imeharamishwa katika vita vya Khaibar, na riwaya zinazodai imeharamishwa katika Hija ya kuaga iliyo maarufu, ambapo kundi la wanafiqhi kutoka kwa Masunni wametoa juhudi kubwa katika kujaribu kuziweka pamoja riwaya hizi lakini wameshindwa kutoa suluhisho sahihi.61 Na la kuchunguza zaidi ni maneno yaliyonukuliwa kutoka kwa Shafi, aliposema: “Sikijui kitu zaidi ya Mut’a ambacho Mwenyezi Mungu alikihalalisha kisha akakiharamisha, kisha akakihalalisha kisha akakiharamisha.”62 Na wakati huo huo Ibn Hajar amenukuu kutoka kwa Suhayliy kuwa: “Hakuna mtu yeyote miongoni mwa mabingwa wa historia na wapokezi wa hadithi aliyenukuu kuwa kuharamishwa kwa Mut’a kulitokea siku ya Khaibar.”63 7.
Na kuna kauli nyingine inasema: Hakika Mut’a ilikuwa halali zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) na ndipo baadaye Umar akaiharamisha, kama tunavyosoma hilo katika Sahih Muslim ambayo ni miongoni mwa vitabu vyenye kutegemewa zaidi kwa Masunni: Kutoka kwa Abu Nadhrah amesema: “Nilikuwa kwa Jabir bin Abdillah, mara alimjia mtu fulani akamwambia: ‘Ibn Abbas na Ibn Zubayr wanahitilafiana kuhusu
60
Sharhu Sahih Muslim, Juz. 9. Uk. 191.
61
Sharhu Sahih Muslim, Juz. 9. Uk. 191.
62
al-al-Mughniy cha Ibn Qudamah Juz. 7, Uk. 572.
63
athul-Bariy Juz. 9, Uk. 138. Sahih Muslim Juz. 4 Uk. 59, Hadithi ya 3307, F Darul-Fikri, Beirut. 106
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 106
11/25/2014 3:03:46 PM
Ushia: Hoja na Majibu
Mut’a mbili (Mut’a ya Wanawake na Mut’a ya Hija)’ basi Jabir akasema zote mbili tulizifanya zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) kisha akatukataza Umar basi hatukurejea tena (kuzifanya).”64 Je baada ya tamko hili bayana lililopo ndani ya Sahih Muslim, inawezekana tena kusema kuwa Mut’a iliharamishwa zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww)?
Ni nani aliyeharamisha Mut’a? Maneno yaliyotajwa hapo nyuma tuliyoyanukuu kutoka kwa Jabir bin Abdullah al-Ansariy yanaashiria hadithi maarufu ambayo imenukuliwa na kundi kubwa la wanahadithi, wafasiri na wanafiqhi wa Kisunni katika vitabu vyao, kutoka kwa Khalifa wa pili. Hadithi yenyewe iko hivi: “Mut’a mbili zilikuwa halali katika zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww), na mimi nakataza, Mut’a ya Hijja na Mut’a ya Wanawake.” Na katika baadhi ya hadithi imekuja: “Na nitatoa adhabu kwa atakayezifanya.” Kusudio la Mut’a ya Hijja ni Umra ya kwanza ambayo anaifanya Hujaji ili kujitoa kwenye ihram yake, na baada ya muda mrefu au mfupi anaanza upya ihramu yake ili kujiandaa na Hijja. Hii ni moja ya hadithi zilizonukuliwa kutoka kwa Umar ikiwa na tofauti kidogo, ambapo alisimama na kubainisha hilo mbele za watu akiwa juu ya mimbari. Na tutaashiria vyanzo saba vya hadithi, fiqhi na tafsiri ambavyo vimeitaja hadithi hii: 64
Sahih Muslim Juz. 4, Uk. 59, Hadithi ya 3307, Darul-Fikri, Beirut. 107
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 107
11/25/2014 3:03:46 PM
Ushia: Hoja na Majibu
1.
Musnad Ahmad Juz. 3, Uk. 325.
2.
Sunanul-Bayhaqiy Juz. 7, Uk. 206.
3.
al-Mabsut cha Sarkhasiy Juz. 4, Uk. 27.
4.
al-Mughniy cha Ibn Qadamah Juz. 7, Uk. 571.
5.
al-Muhali cha Ibn Hazmi Juz. 7, Uk. 107.
6.
Kanzul-Ummal Juz. 16, Uk. 521.
7.
Tafsirul-Kabir cha Fakhru Raz Juz. 10, Uk. 52. Hadithi hii inafichua mas’ala mbali mbali, nayo ni:
Kwanza: Uhalali wa Mut’a katika kipindi cha Khalifa wa kwanza Hakika Mut’a au ndoa ya muda ilikuwa halali muda wote wa kipindi cha uhai wa Mtukufu Mtume (saww) na hata kipindi cha Khalifa wa kwanza, na ndipo Khalifa wa pili alipokuja kukataza. Pili: Rai binafsi dhidi ya tamko la Mtume Khalifa wa pili alijipa ruhusa ya kuweka kanuni dhidi ya tamko bayana la Mtukufu Mtume (saww), wakati ambapo Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema ndani ya Qur’ani Tukufu:
ۚ َو َما آ َتا ُك ُم الرَّ سُو ُل َف ُخ ُذوهُ َو َما َن َھا ُك ْم َع ْن ُه َفا ْن َتھُوا ب ِ ﷲ َشدِي ُد ْال ِع َقا َ َّ َّﷲ ۖ إِن َ َّ َوا َّتقُوا 108
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 108
11/25/2014 3:03:46 PM
Ushia: Hoja na Majibu
“Na anachowapa Mtume kichukueni, na anachowakataza jiepusheni nacho. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.� (Sura Hashri: 7).
Je kuna mtu yeyote mwenye haki ya kufanya atakavyo katika hukumu za Mwenyezi Mungu zaidi ya Mtukufu Mtume (saww), je mtu anaweza kusema: Hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) alifanya hivi basi na mimi nafanya vile? Je inaruhusiwa kutumia rai binafsi mbele ya tamko la Mtukufu Mtume (saww) ambalo kiuhalisia ni maneno ya Mwenyezi Mungu? Kwa kweli ni jambo la kushangaza sana kuona kanuni ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) inawekwa pembeni licha ya kuwepo tamko hili bayana!!! Zaidi ya hapo ikiwa mlango wa ijtihadi dhidi ya tamko la Mtume uko wazi basi ni kwa dalili ipi wengine hawana haki ya kufanya hivyo? Je ijtihadi hiyo ni halali kwa mtu mmoja tu na wengine si halali kwao? Na suala hili ni miongoni mwa masuala muhimu, kwani kuuwacha wazi mlango wa ijtihadi dhidi ya tamko la Mtume kunapelekea hukumu za Mwenyezi Mungu kubaki bila ulinzi na kusababisha fujo na uholela katika hukumu za kudumu za Uislamu, na hivyo kuziweka hukumu za Mwenyezi Mungu katika hatari. Tatu: Kwa nini Umar alijitokeza kupinga hukumu hizi mbili? Alidhani kuwa katika Hijja ya Tamatui ni wajibu juu ya Mwislamu pindi anapokuja Hijja, kutimiza Hijja yake na Umrah yake ili ajitoe katika ihramu yake na akurubiane na mke wake. Ama akifanya Umrah Tamatui na baada ya siku kadhaa 109
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 109
11/25/2014 3:03:46 PM
Ushia: Hoja na Majibu
awe amejitoa kutoka katika ihramu yake na baada ya hapo awe huru katika mambo yake, kufanya hivi si sahihi wala hakuendani na uhalisia wa Hijja. Hii ndio ilikuwa dhana ya Umar, wakati ambapo hakika rai hii si sahihi, kwa sababu matendo ya Hijja si yenye kuungana na Umrah, hivyo mtu anaweza kutekeleza Umrah mwezi mmoja kabla ya matendo ya Hijja, hivyo Waislamu katika mwezi wa Shawal au Dhulqaadah hupata heshima ya kuizuru Makka na kutekeleza matendo ya Umrah, na huwa huru mpaka siku ya mwezi nane Dhulhaji, baada ya hapo huhirimia kwa ajili ya matendo ya Hijja na kwenda Arafa. Hivyo liko wapi tatizo katika jambo hili, tatizo ambalo lilisumbua akili yake? Ama kuhusu maudhui ya Mut’a na ndoa ya muda baadhi yao wanadhani kuwa ikiwa ndoa ya muda ni inayoruhusiwa basi ni vigumu kutofautisha baina ya ndoa na zinaa, kwa sababu mwanamume yeyote atakapokutwa na mwanamke (wakijamiina) anaweza kudai kuwa ni mke wake wa ndoa ya muda, na hili litapelekea zinaa kuenea. Hakika dhana hii ni dhaifu zaidi kuliko ya kwanza, kwa sababu ni kinyume chake kabisa, kwa sababu kuzuia kufunga ndoa ya Mut’a ndiko kunakosaidia zinaa kuenea na kutokuwepo na staha, hiyo ni kama tulivyoashiria hapo mwanzo kuwa vijana wengi hawamiliki uwezo wa kufunga ndoa ya daima, au wake zao wako mbali na wao, hivyo wao hubaki njiapanda, ima wafunge ndoa ya muda au wafanye zinaa, hivyo kuwazuia kufunga ndoa ya muda – iliyopangiliwa kwa sharti zake na kwa usahihi – kunapelekea wao kuangukia katika uwanja wa maasi na kuzama katika zinaa na kutokuwa na staha. Na kwa ajili hii imenukuliwa kutoka kwa Imam Ali 110
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 110
11/25/2014 3:03:46 PM
Ushia: Hoja na Majibu
(a.s.) hadithi mashuhuri: “Laiti si Umar kuwakataza watu Mut’a basi asingezini isipokuwa muovu wa kupindukia.”65 Nne: Tofauti kubwa kuhusu ni lini iliharamishwa Kundi kubwa la wanahadithi, wafasiri na wanafiqhi wa Kisunni limepokea hadithi iliyotajwa (ya Umar kukataza Mut’a), na tunaweza kufaidika nayo kwa namna iliyo bayana kuwa Mut’a iliharamishwa katika zama za Umar, na si katika zama za Mtukufu Mtume (saww), na kuna riwaya nyingine nyingi kutoka ndani ya vyanzo hivyo hivyo zimenukuliwa zikiunga mkono hilo (la kuwa Umar ndiye aliyeharamisha), hapa tunataja baadhi tu kama mfano: 1.
Msimulizi maarufu wa hadithi Tirmidhiy ananukuu kwamba: “Hakika mtu mmoja kati ya watu wa Sham (Syria) alimuuliza Abdullah bin Umar kuhusu Mut’a ya Wanawake, akajibu: Ni halali. Muulizaji akasema: ‘Hakika baba yako Umar aliikataza.’ Abdullah akasema: ‘Waonaje ikiwa baba yangu aliikataza na Mtume wa Mwenyezi Mungu aliifanya, basi je niache Sunnah na nifuate amri ya baba yangu?!”’66
65
Tafsirul-Kabir cha Fakhru Raz Juz. 10 Uk. 50.
66
adithi hii haimo ndani ya Sahih Tirmidhiy inayopatikana sasa mikononi mwetu, H badala ya neno Muta ya Wanawake imebadilishwa na kuandikwa Muta ya Hijja. Lakini Zainul-Abidin maarufu kwa jina la Shahid wa pili ambaye ni miongoni mwa Ulamaa wa karne ya kumi, ameitaja katika kitabu Lum’atud-Damashqiy, na pia Sayyid Ibn Tawus ambaye ni miongoni mwa Ulamaa wa karne ya saba, ameitaja katika kitabu Taraif, wote wameitaja kwa neno Muta ya Wanawake. Na hii inaonesha kuwa katika nakala za chapa ya zamani ya kitabu Sahih Tirmidhiy hadithi hii ilikuwa katika sura hii ya Muta ya Wanawake, lakini chapa zilizokuja baadaye zilibadilishwa na kugeuzwa kwa sababu zinazojulikana, na ni katika maudhui nyingi wamefanya hivyo. 111
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 111
11/25/2014 3:03:46 PM
Ushia: Hoja na Majibu
2.
Na tunasoma katika hadithi nyingine kutoka kwa Jabir bin Abdullah akisema: “Tulikuwa tunafunga ndoa ya Mut’a kwa gao la tende na unga kwa siku kadhaa, katika zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) na (zama za) Abu Bakr mpaka Umar alipokataza kutokana na suala la A’mri bin Hurayth.”67
3.
Na katika hadithi nyingine ndani ya kitabu hicho hicho imekuja: “Nilikuwa kwa Jabir bin Abdillah, mara alimjia mtu fulani akamwambia: ‘Ibn Abbas na Ibn Zubayr wanahitilafiana kuhusu Mut’a mbili (Mut’a ya Wanawake na Mut’a ya Hija)’ basi Jabir akasema zote mbili tulizifanya zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) kisha akatukataza Umar basi hatukurejea tena (kuzifanya).”68
4.
Ibn Abbas ambaye ni wino wa umma huu alikuwa ni miongoni mwa wenye kupinga madai ya kufutwa kwa hukumu ya Mut’a katika zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) na ni shahidi juu ya hilo katika ugomvi ambao ulitokea baina yake na Abdullah bin Zubayr, ambapo imekuja katika Sahih Muslim kuwa: “Hakika Abdallah bin Zubayr alisimama Makkah akasema: ‘Kuna watu Mwenyezi Mungu amezifanya pofu nyoyo zao kama alivyoyafanya mapofu macho yao, wanafutu kuruhusu Mut’a. (Akimkusudia Ibn Abbas).’ Ibn Abbas akamwita na akamwambia: ‘Hakika wewe ni mtu ovyo usiye na akili. Naapa kwa umri wangu, Mut’a ilikuwa ikifanywa zama za Kiongozi wa wacha-Mungu (Akimkusudia Mtume wa Mwenyezi Mungu saww).’ Ibn Zubayr
67
Sahih Muslim Juz. 2, Uk. 131.
68
Sahih Muslim Juz. 2, Uk. 131. 112
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 112
11/25/2014 3:03:46 PM
Ushia: Hoja na Majibu
akamjibu: ‘Jaribu wewe mwenyewe kufanya. Wallahi ukifanya, nitakupiga kwa mawe yako.’”69 Na hii ni akili ya dhulma na unyanyasaji. Inaonekana mazungumzo haya yalitokea katika siku ambazo Abdullah bin Zubayr alipata mamlaka ya kuitawala Makkah, na kwa ajili hii alipata nguvu na ujasiri wa kumfanyia jeuri aalimu mkubwa Ibn Abbas ambaye alikuwa sawa na baba yake kiumri, na kwa upande wa elimu hakuwa analingana naye, na hata tukijaalia kuwa alikuwa analingana naye kiumri bado hakuwa na haki ya kuongea naye kwa sura hii, kwa sababu iwapo mtu atatenda jambo hili (Mut’a) kwa mujibu wa fatwa yake basi kubwa linaloweza kusemwa ni kuwa “Amefanya Shubha.” Na hivyo kumwingilia kwake ni kuingilia kwa Shubha, na kuingilia kwa Shubha hakuna adhabu, hivyo kumtishia kumpopoa mawe hakuna maana yoyote na ni maneno ya mtu jahili. Na mara nyingi misimamo mibaya kama hii hutokea kwa kijana jahili asiye na tabia nzuri mfano wa Abdullah bin Zubayr. Na cha kuvutia ni kwamba Raghib Isfahaniy amenukuu tukio hili katika kitabu chake al-Muhadharat, kuwa: “Abdullah bin Zubayr alimtoa dosari Abdullah bin Abbas kwa kuhalalisha kwake Mut’a, Abdullah bin Abbas akamwambia: ‘Muulize mama yako ni vipi yalitokea mapenzi kati yake na baba yako (walipendana vipi)?’ Akamuuliza mama yake, akasema: ‘Sikukuzaa isipokuwa ni kwa kupitia ndoa ya Mut’a (Ndoa ya muda).’ Ibn Abbas alisema: ‘Hakika mapenzi ya kwanza kuchomoza katika Mut’a ni mapenzi ya mke wa Zubayr.”’70 69
Sahih Muslim Juz. 2, Uk. 133.
70
l-Muhadharat Juz. 2, Uk. 214. Sharhu Nahjul-Balaghah cha Ibn Abil-Hadid A Juz. 20, Uk. 130. 113
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 113
11/25/2014 3:03:46 PM
Ushia: Hoja na Majibu
1.
Tunasoma katika Musnad Ahmad bin Hanbal kuwa: “Ibn Huswayn alisema: Aya ya Mut’a iliteremshwa katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu na tukaifanya, na haikuteremshwa Aya yoyote kuifuta mpaka Mtume (saww) anafumba macho yake kwa kuiacha dunia.”71
Hii ni mifano tu ya riwaya ambazo zinakanusha bayana madai ya kufutwa kwa hukumu ya Mut’a. Mkabala na riwaya hizi kuna riwaya nyingine zinazoonesha kuwa hukumu ya Mut’a ilifutwa katika zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww), lakini riwaya hizo haziko katika msitari mmoja wala hazijakubaliana, na bahati mbaya sana zinatofautiana kuhusu ni wakati upi ilifutwa: 1.
Katika baadhi ya riwaya imekuja kuwa hukumu ya kufutwa Mut’a ilitolewa katika vita vya Khaibar mnamo mwaka wa saba Hijiriyah.72
2.
Na kuna riwaya nyingine zimetaja kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) aliruhusu Mut’a huko Makkah katika mwaka wa Ukombozi wa Makkah mwaka wa nane Hijiriya, na akaikataza mwaka huo huo baada ya muda mfupi.73
3.
Na imekuja katika riwaya nyingine kuwa yeye (saww) aliruhusu kwa muda wa siku tatu katika vita vya Awtas ambavyo vilitokea baada ya Ukombozi wa Makkah katika mji wa Hawazin ambao uko karibu na Makkah, na akaikataza baada ya hapo.
71
Musnad Ahmad Juz. 4, Uk. 436.
72
Tafsir Durul-Manthur Juz. 2, Uk. 486.
73
Sahih Muslim Juz. 4, Uk. 133. 114
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 114
11/25/2014 3:03:46 PM
Ushia: Hoja na Majibu
Kwa kweli tungekuwa na kifua kipana cha kuweza kuhoji kauli hizi zenye kutofautiana katika mada hii, basi suala lingekuwa kubwa zaidi ya hapa, kwa sababu mwanafiqhi maarufu wa Kisunni Nawawi, katika Sharhu Sahih Bukhari amenukuu kauli sita kuhusu mas’ala hii, na kila rai kaitajia riwaya zinazoihusu, kauli hizo ni: a.
Mut’a ilihalalishwa katika vita vya Khaibar na ikaharamishwa baada ya siku kadhaa.
b.
Iliruihusiwa katika Umra ya kulipa, na baada ya hapo ikaharamishwa.
c.
Iliruhusiwa siku ya Ukombozi wa Makkah na baada ya hapo ikaharamishwa.
d.
Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) aliiharamisha katika vita vya Tabuk.
e.
Iliruhusiwa katika vita vya Awtas katika ardhi ya Hawazin.
f.
Ilikuwa ni halali katika Hijja ya kuaga mnamo mwaka wa mwisho wa umri wa Mtukufu Mtume (saww).74 Na la kustaajabisha zaidi ni maneno ya Shafi anaposema: “Sikijui kitu zaidi ya Mut’a ambacho Mwenyezi Mungu alikihalalisha kisha akakiharamisha, kisha akakihalalisha kisha akakiharamisha.”75 Kila mtafiti anapoona mgongano na mkinzano huu katika riwaya hizi anazidi kupata uhakika kuwa riwaya hizi ziliwekwa ili kutimiza malengo ya kisiasa.
74
S harh Sahih Muslim cha Nawawi Juz. 9, Uk. 191. al-Mughniy cha Ibn Qadamah Juz. 7, Uk. 572.
75
al-al-Mughniy cha Ibn Qudamah Juz. 7, Uk. 572. 115
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 115
11/25/2014 3:03:46 PM
Ushia: Hoja na Majibu
Njia bora ya kupata ufumbuzi Hakika kauli hizi zenye kutofautiana na kupingana zinamlazimisha mtu kujisomea kwa uhakika, la sivyo basi ni ipi sababu ya kuwepo kadiri hii kubwa ya mkinzano katika riwaya, na ni kwa nini kila mwanahadithi au mwanafiqhi anachagua rai yake katika hilo? Na tutawezaje kuzikusanya pamoja riwaya hizi zenye kupingana? Je kadiri hii ya tofauti sio dalili tosha kuwa mas’ala hii husika ina hisia za kisiasa, jambo ambalo liliwafanya baadhi ya waweka hadithi za uwongo kuweka baadhi ya hadithi za uwongo kwa kutumia majina ya baadhi ya Maswahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) na wafuasi wake, na wakanasibisha kwao, na hatimaye wakaonekana wananukuu kutoka kwa Mtukufu Mtume (saww) kuwa alisema kadha wa kadha. Hakika mas’ala ya kisiasa si mengine ni yale aliyosema Khalifa wa pili: “Mut’a mbili zilikuwa halali katika zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww), na mimi nazikataza, Mut’a ya Hijja na Mut’a ya Wanawake.” Hakika hadithi hii ina matokeo mabaya ya ajabu, ikiwa mmoja kati ya wanaummah au Makhalifa anaweza kubadili waziwazi hukumu za Uislamu - hakuna dalili inayoonesha ubadilishaji huu ni makhususi kwa ajili ya Khalifa wa pili tu - basi na wengine pia wana haki ya kufanya ijtihadi dhidi ya tamko la Mtukufu Mtume (saww), na hili litapelekea kuwepo fujo na tofauti za ajabu katika hukumu za Uislamu, kuna mambo yaliyo wajibu na mengine haramu, lakini baada ya muda fulani Uislamu hautabaki na chochote katika hukumu. Hivyo ili kufidia athari hii ya ajabu ya jambo hili wakalazimika kulipa kazi kundi fulani ya kutunga hadithi za 116
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 116
11/25/2014 3:03:46 PM
Ushia: Hoja na Majibu
uwongo ili liseme kuwa: “Hakika Mut’a mbili ziliharamishwa katika zama za Mtume (saww).” Hivyo wakaweka hadithi na kuzinasibisha na Maswahaba wa Mtukufu Mtume (saww), na kwa sababu si za ukweli kukatokea mgongano na mkinzano wa ajabu na hatimaye jambo likafichuka. Kama si hivyo basi itawezekanaje kufasiri mkinzano na mgongano wote huu katika riwaya hizi, mpaka baadhi ya wanafiqhi na kwa ajili ya kutaka kuzikusanya pamoja wamesema: “Mut’a ilikuwa halali kwa muda, baada ya hapo iliharamishwa, kisha ikahalalishwa tena kisha ikaharamishwa.”!! Hivi hukumu za Mwenyezi Mungu zimegeuka mchezo na upuuzi?!! Na hata tukifumbia macho yote hayo bado tunasema: Hakika kuhalalishwa Mut’a katika zama za Mtukufu Mtume (saww) ni lazima ilikuwa ni kwa sababu ya dharura, na dharura hiyo inaweza kupatikana pia katika zama zilizofuata, na hasa katika zama zetu hizi, ni kwa nini basi iwe haramu? Na dharura hii inawajumuisha vijana au wasafiri wenye kwenda nchi za mbali kwa safari ya muda mrefu na hasa katika nchi za Magharibi. Katika zama zile ulimwengu wa Kiislamu haukuwa katika sura hii ya kutisha, hakukuwa na wanawake wenye kutembea uchi wasiokuwa na hijabu, wala hakukuwa na filamu chafu katika runinga, intaneti, tovuti na katika mitandao ya kijamii, wala hakukuwa na mabaraza ya uharibifu na vyombo vya habari vyenye kupotosha, vitu ambavyo vinawaweka vijana wengi katika mtihani. Je inawezekana kweli kukubali maneno haya kuwa Mut’a ilikuwa ni halali katika zama zile kwa sababu ya dharura, kisha ikafutwa moja kwa moja milele? Na hata tukifumbia macho hili pia na tujaalie kuwa kuna kundi kubwa la wanafiqhi linaona kuwa ndoa ya muda 117
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 117
11/25/2014 3:03:47 PM
Ushia: Hoja na Majibu
iliharamishwa, bado kuna kundi lingine pia linaona ndoa hiyo ni halali, na hivyo ni suala lenye tofauti, na hivyo haifai huyu mwenye kusema ni halali kuwatuhumu wenye kupinga na kuwaona kuwa ni watu wasiofuata hukumu za dini, na hivyo hivyo mwenye kuharamisha hapaswi kuwatuhumu wenye kuhalalisha kuwa wanaeneza zinaa. Watamjibu nini Mwenyezi Mungu wale wenye kuwatuhumu wenzao kwa zinaa? Jambo kubwa linaloweza kusemwa katika maudhui hii ni kwamba hii ni tofauti katika ijtihadi. Fakhru Razi anasema katika tafsiri yake na kwa ushabiki makhususi katika aina hii ya mas’ala: “Sehemu kubwa ya ummah inaona kuwa ndoa hiyo ilifutwa, na wengine miongoni mwao wanaona kuwa ilibaki kama ilivyokuwa.”76 Kwa ibara nyingine ni suala lenye tofauti. Na hadi hapa tumemaliza mada ya ndoa ya muda, na tunawaomba watu wote wasitoe hukumu kabla ya kufanya utafiti, na wala wasinasibishe kauli kwa namna isiyokuwa sahihi, hivyo ni lazima kurejea kufanya utafiti na uhakiki kisha ndipo hukumu ifuate, na bila shaka watapata uhakika kuwa Mut’a bado ni hukumu halali ya Mwenyezi Mungu, na kama masharti yake yatazingatiwa basi matatizo mengi yatatatuka.
76
Tafsirul-Kabir ya Fakhru Razi Juz. 10, Uk. 49. 118
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 118
11/25/2014 3:03:47 PM
Ushia: Hoja na Majibu
MADA YA SITA KUSUJUDU JUU YA UDONGO 1. Umuhimu wa kusujudu baina ya ibada zote:
K
wa mtazamo wa Uislamu kusujudu ni ibada muhumu zaidi kati ya ibada nyingine, au ni miongoni mwa ibada muhimu zaidi, na kama ilivyokuja katika riwaya: “Ni katika sijda ndipo mtu huwa karibu zaidi na Mola Wake.” Na hivyo viongozi wetu watukufu walikuwa na sijda ndefu, na hasa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) na Ahlul-Bait wake (as). Hakika kusujudu sijda ndefu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kunalea roho ya mtu, na kusujudu huko ni miongoni mwa mifano halisi ya utumwa na unyenyekevu wa dhati mbele ya Mwenyezi Mungu, na kwa sababu hii ndio maana sharia imekuja na sijda mbili katika kila rakaa moja ya Sala. Na miongoni mwa mifano halisi ya sijda ni sijda ya kushukuru, ukiongezea sijda za wajibu na za Sunna za kisomo cha Qur’ani. Hakika katika hali ya kuwa katika sijda mtu husahau kila kitu isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na huona kuwa nafsi yake iko karibu zaidi na Yeye, na kwamba amechukua nafasi yake katika busati la ukaribu. Hivyo walimu wa Sira, tabia na irfani, na pia walimu wa maadili, wanasisitiza sana mas’ala ya kusujudu. Na hakika tuliyoyataja ni dalili ya wazi juu ya hadithi mashuhuri: “Hakuna amali inayomuudhi shetani kama mtu kumsujudia Mola Wake.” Na unasoma katika hadithi nyingine kuwa Mtukufu Mtume (saww) alimwambia 119
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 119
11/25/2014 3:03:47 PM
Ushia: Hoja na Majibu
mmoja wa Maswahaba zake: “Ukitaka Mwenyezi Mungu akufufue pamoja na mimi Siku ya Kiyama, basi refusha sijda yako mbele ya Mwenyezi Mungu Mmoja wa pekee Mwenye nguvu.”77 2. Hairuhusiwi kumsujudia asiyekuwa Mwenyezi Mungu: Sisi tunaamini kuwa hairuhusiwi kumsujudia asiyekuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu Mmoja wa pekee mwenye kukusudiwa kwa haja, kwa sababu kusujudu ndio kilele cha unyenyekevu, na ndio mfano wa juu kabisa wa ibada, hivyo ibada ni makhususi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Hakika ibara:
ض ِ � َيسْ ُج ُد َمنْ فِي ال َّس َم َاوا ِ َّ ِ َو ِ ْت َو ْاألَر …… “Na vilivyomo mbinguni na ardhini vinamsujudia Mwenyezi Mungu ...” (Sura Ra’d: 15), na kwa kutanguliza neno “Lilahi” mwanzoni mwa jumla iliyotajwa kunaonesha umakhususi, na hii inamaanisha kuwa vyote vilivyomo mbinguni na ardhini havimsujudii isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kadhalika jumla “…Na wanamsujudia.” (Sura A’raf: 206), ni ishara nyingine inayoonesha kuwa kusujudu ni makhususi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Kiuhalisia kusujudu kunawakilisha daraja la juu kabisa la unyenyekevu, nalo ni makhususi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu tu, na hivyo iwapo tukimsujudia mtu au kitu, hii 77
Safinatul-Bihar: Neno Sujud. 120
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 120
11/25/2014 3:03:47 PM
Ushia: Hoja na Majibu
humaanisha kuwa tumekifanya kitu hicho au mtu huyo mshirika wa Mwenyezi Mungu, na amali hiyo si sahihi. Na sisi tunajua kuwa moja kati ya maana za tauhidi ni tauhidi katika ibada, kwa maana ya kwamba inapasa ibada iwe kwa ajili ya Mwenyezi Mungu tu, na bila maana hiyo tauhidi haikamiliki. Na kwa ibara nyingine ni kuwa kumwabudu asiyekuwa Allah ni moja kati ya matawi ya Shirki, na kusujudu ni moja kati ya aina za ibada. Ama kitendo cha Malaika kumsujudia Adam (as) kama ilivyokuja katika baadhi ya Aya, maana yake ni kama walivyosema baadhi ya wafasiri kuwa: “Maana yake ni kumtukuza na kumheshimu na kumkirimu Adam, na si kwa maana ya kumwabudu. Au ni kwa maana ya kuonesha unyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu, kwa sababu wao walitii amri ya Mwenyezi Mungu na wakatekeleza walichoamrishwa. Au ni kusujudu kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu.” Ama sijda ambayo Ya’qub (as), mke wake na watoto wake walimsujudia Yusuf (as) kama ilivyokuja katika Qur’ani Tukufu:
ش َو َخرُّ وا َل ُه سُجَّ ًدا ِ َْو َر َف َع أَ َب َو ْي ِه َع َلى ْال َعر “Na akawapandisha wazazi wake kwenye kiti cha enzi na wakaporomoka kumsujudia.” (Sura Yusuf: 100), ima ni sijda ya kumshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu, au ni aina fulani ya kumheshimu na kumtukuza.”
121
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 121
11/25/2014 3:03:47 PM
Ushia: Hoja na Majibu
Na la muhimu kutaja hapa ni kuwa katika kitabu WasailusShiah – nacho ni moja ya vyanzo maarufu kwetu – chini ya anwani “Hairuhusiwi kumsujudia asiyekuwa Mwenyezi Mungu,” katika mlango wa kusujudu katika Sala, zimepokewa hadithi saba kutoka kwa Mtukufu Mtume (saww) na Maimamu maasumina (as) zikionesha kuwa hairuhusiwi kumsujudia asiyekuwa Mwenyezi Mungu.78 Tumedokeza hili hapa ili tufaidike nalo katika vipengele vinavyofuata. Ni wajibu kusujudu juu ya kitu gani? Wafuasi wote wa madhehebu ya Ahlul-Bait (as) wamekubaliana juu ya kutokuruhusiwa kusujudu juu ya kitu chochote kisichokuwa ardhi, na wanaamini pia kuwa inaruhusiwa kusujudu juu ya mazao ya ardhi, kwa sharti kuwa mazao hayo yasiwe ni yale yanayoliwa wala kuvaliwa, (isiwe ni kisamvu, mchicha, miwa na mfano wake). Wakati ambapo Ulamaa wote wa fiqhi wa Kisunni wanaamini kuwa inaruhusiwa kusujudu juu ya kila kitu, ndiyo kuna kundi miongoni mwao linasema kuwa hairuhusiwi kusujudu juu ya sehemu ya nguo uliyoivaa, au ya kilemba na mfano wake. Wafuasi wa madhehebu ya Ahlul-Bait (as) wanasisitiza itikadi hii kwa kutegemea riwaya zilizonukuliwa kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) na Maimamu wa Ahlul-Bait (as), na hivyo wanaona ni bora kutosujudu juu ya mazulia yaliyomo ndani ya Msikiti mtakatifu na Msikiti wa Mtukufu Mtume (saww), na ni lazima kusujudu juu ya jiwe au juu ya mikeka (mabusati, majamvi) ambayo mara nyingi huenda nayo huko. 78
Wasailus-Shiah Juz. 4, Uk. 984. 122
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 122
11/25/2014 3:03:47 PM
Ushia: Hoja na Majibu
Hakika misikiti yote iliyopo Iran, Iraq na miji mingine ya Kishia imetandikwa mazulia, kwa ajili hiyo wao huandaa vipande vya udongo vinvyoitwa Turba na kuviweka juu ya mazulia wakati wa kusali ili wasujudu juu yake, na ili paji la uso liguse udongo mbele ya Mwenyezi Mungu, ili mwenye kusali adhihirishe unyenyekevu na udhalili wake wote mbele ya Mwenyezi Mungu, na mara nyingi Turba hizi hutengenezwa kutokana na udongo wa Mashahid, ili kuleta nyoyoni mwao taswira ya mihanga ya watu hawa waliyoitoa katika njia ya Mwenyezi Mungu, ili iwe ni sababu ya nyoyo zao kuwa hadhiri katika Sala. Na hakika wanapendekeza zaidi Turba itokanayo na udongo wa Mashahid wa Karbala, lakini si sharti daima iwe ni Turba hii au udongo huu, kama tulivyotaja hapo mwanzo kuwa inaruhusiwa pia kusujudu juu ya mawe yanayofunika ardhi ya msikiti kama ilivyo katika Msikiti Mtakatifu na Msikiti wa Mtume (saww). Na vyovyote iwavyo ni kuwa wafuasi wa Ahlul-Bait (as) wana dalili nyingi zinazothibitisha wajibu wa kusujudu juu ya ardhi, na miongoni mwa dalili hizo ni hadithi zilizopokewa kutoka kwa Mtukufu Mtume (saww) na pia sira ya Maswahaba ambayo tutaitaja katika vipengele vijavyo, na pia riwaya zilizopokewa kutoka kwa Maimam wa Ahlul-Bait (as) ambazo ni punde tu tutazitaja. La kustaajabisha hapa katika jambo hili ni kwa nini baadhi ya Masunni wamelichukulia jambo hili kwa ubaya na kuleta upinzani mbaya dhidi ya fatwa hii, ambapo mara wanaona ni bidaa na mara nyingine wanaona ni ukafiri na kuabudu masanamu? Hivi tukithibitisha kupitia vitabu vinavyokubalika na kutegemewa na ndugu zetu hawa, kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) yeye na Maswahaba zake walisujudu 123
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 123
11/25/2014 3:03:47 PM
Ushia: Hoja na Majibu
juu ya ardhi, je hii itakuwa ni bidaa?!! Na je tukithibitisha kuwa baadhi ya Maswahaba wa Mtukufu Mtume (saww) kama vile Jabir bin Abdullah al-Ansariy alikuwa anabadili fungu la changarawe toka mkono huu na kuziweka katika mkono mwingine ili zipoe – kutokana na joto kali linalofanya changarawe na mchanga viwe vya moto - ili aweze kuweka paji la uso wake juu ya changarawe hizo wakati wa kusali, je mtamzingatia Jabir kuwa ni mwabudu masanamu au muasisi wa bidaa?!! Je mtu mwenye kusujudu juu ya mkeka au anaona bora kusujudu juu ya mawe ambayo yamefunika ardhi ya Msikiti Mtakatifu au Msikiti wa Mtume (saww) anakuwa ni mwabudu mkeka au mwabudu mawe hayo?!! Hivi si ni wajibu kwa ndugu zetu kusoma vitabu vyetu vingi tu vya fiqhi ili waone kuwa si haki wala si sahihi yale wanayotunasibisha nayo?! Je Mwenyezi Mungu Mtukufu atawasamehe kirahisi Siku ya Kiyama wale wanaowatuhumu wengine kwa bidaa, ukafiri na kuabudu masanamu? Bila shaka baada ya kuitafakari hadithi hii iliyopokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (as) itabainika ni kwa nini Shia husujudu juu ya ardhi. Nayo ni kutoka kwa Hisham bin alHakam – ambaye ni miongoni mwa wanahikma na wafuasi wa Imam (as) – amesema: “Nilimwambia Abu Abdillah, niambie ni kitu gani inaruhusiwa kusujudu juu yake na ni kipi hakiruhusiwi? Akasema: ‘Hairuhusiwi kusujudu isipokuwa juu ya ardhi au juu ya mazao ya ardhi, isipokuwa linaloliwa au kuvaliwa.’ Nikamwambia: Mimi ni fidia kwako, kuna sababu ipi katika hilo? Akasema: ‘Kwa sababu kusujudu ni kunyenyekea kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, hivyo haipasi kuwe juu ya kitu kinacholiwa wala kuvaliwa, kwa 124
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 124
11/25/2014 3:03:47 PM
Ushia: Hoja na Majibu
sababu watu wa duniani ni watumwa wa vile wanavyokula na wanavyovaa. Na mwenye kusujudu anapokuwa katika sijida yake huwa katika kumwabudu Mwenyezi Mungu hivyo haipasi wakati wa kusujudu kwake kuweka paji la uso wake juu ya kile wanachokitumikia watu wa duniani, ambao wamehadaika kwa hadaa yake. Na Kusujudu juu ya ardhi ni bora kwani kunazidisha unyenyekevu na udhalili kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.”79 4. Dalili za mas’ala hii: Hebu sasa tutaje dalili, kwanza tuanze na maneno ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww): a. Hadithi maarufu ya Mtume (saww) inayohusu kusujudu juu ya ardhi: Hadithi hii imenukuliwa na Shia na Sunni kutoka kwa Mtukufu Mtume (saww) akisema: “Nimefanyiwa ardhi kuwa mahala pa kusujudia na tohara.”80 Na baadhi yao wamedhani kuwa maana ya hadithi ni kwamba ardhi na vyote vilivyopo juu yake ni sehemu ya kumwabudia Mwenyezi Mungu na wala hakuna sehemu makhususi kwa ajili ya ibada, si kama wanavyosema Mayahudi na Manasara kuwa ni lazima iwe kanisani au sehemu makhususi za kufanyia ibada. Lakini ukitafakari kidogo utaona kuwa tafsiri hii (ya kwamba ardhi na vyote vilivyopo juu yake ni sehemu ya kumwabudia Mwenyezi Mungu na wala hakuna sehemu 79
Ilalus-Sharaiu cha as-Saduq Juz. 2, Uk. 341.
80
S ahih Bukhari Juz. 1, Uk. 91. Sunanul-Bayhaqiy Juz. 2, Uk. Na imepokewa pia na wengine kati ya waandishi wa Sahihi Sita na vitabu vya Sunnah. 125
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 125
11/25/2014 3:03:47 PM
Ushia: Hoja na Majibu
makhususi kwa ajili ya ibada), haioani na maana halisi ya hadithi husika, kwa sababu Mtukufu Mtume (saww) amesema: “Nimefanyiwa ardhi kuwa mahala pa kusujudia na tohara.” Na tunajua kuwa kilicho tohara ambacho tunaweza kutayamamia kama vile udongo na changarawe kinatokana na ardhi, na kwa ajili hii ni lazima sehemu ya kusujudia iwe inatokana na udongo huo huo na changarawe. Na laiti Mtukufu Mtume (saww) angekuwa anataka kubainisha maana waliyoichukua wanafiqhi wa Kisunni kutoka katika hadithi hii, basi angesema: “Nimefanyiwa ardhi kuwa mahala pa kusujudia na udongo wake ni tohara.” Lakini yeye hakusema hivyo. Hitimisho ni kuwa hakuna shaka kwamba maana ya “mahala pa kusujudia” hapa ni sehemu ya kusujudia, na sehemu ya kusujudia ni lazima iwe inatokana na kitu kilekile ambacho inaruhusiwa kutayamamia. Hivyo Mashia hawajakosea pindi walipoona ni sharti kusujudu juu ya udongo bila kuruhusu kusujudu juu ya mazulia na vitu mfano wake, kwa sababu wao wanatenda kwa mujibu wa maamrisho ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww). b.
Sira ya Mtukufu Mtume (saww):
Mtukufu Mtume (saww) alikuwa akisujudu juu ya ardhi na si juu ya mazulia au nguo au vinginevyo, na hiyo ni kwa mujibu wa kundi la riwaya mbalimbali, ambapo tunasoma hadithi inayonukuliwa na Abu Huraira akisema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) alisujudu siku ya mvua kali kiasi kwamba nikawa naona alama za sijda kwenye paji lake na pua yake.”81 Ikiwa inaruhusiwa kusujudu juu ya mazulia na 81
l-Muujam al-Awsat cha Tabaraniy Juz. 1, Uk. 36. Majmauz-Zawaid Juz. 2 Uk. A 126. 126
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 126
11/25/2014 3:03:47 PM
Ushia: Hoja na Majibu
nguo basi hakuna haja ya Mtukufu Mtume kusujudu juu ya ardhi siku yenye mvua. Pia Aisha anasema: “Sikuwahi kumuona Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) akikinga uso wake na kitu.”82 Yaani wakati wa kusujudu. Ibn Hajar katika ufafanuzi wake juu ya hadithi hii anasema: “Hadithi hii inaashiria kuwa asili katika sijda ni paji la uso kugusa ardhi, lakini kama haiwezekani si wajibu kutimiza hilo.”83 Na imekuja katika riwaya nyingine kutoka kwa Maimunah ambaye ni mmoja kati ya wake za Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww): “Na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) akisali na kusujudu juu ya khumra.” Yaani kipande cha mkeka. Na lililo wazi kutoka kwenye maana ya hadithi hii ni kwamba Mtukufu Mtume (saww) alisujudu juu ya mkeka. Na zimekuja hadithi nyingi katika vyanzo maarufu vya Masunni kwamba Mtukufu Mtume (saww) alikuwa akisalia juu ya mkeka. Na la kustaajabisha katika jambo hili ni kwamba Shia anapoweka mkeka kwa ajili ya Sala kama alivyofanya Mtukufu Mtume (saww) basi kundi lenye chuki binafsi linamtuhumu kwa bidaa na wanamtazama kwa jicho la ghadhabu, wakati ambapo hadithi hizi zinasema kuwa hakika Mtukufu Mtume (saww) ndiye aliyeasisi amali hii, na inauma sana Sunnah hizi zinapozingatiwa kuwa ni bidaa!! Na kamwe sintasahau tukio lililotokea katika moja ya ziara zangu za kuizuru Nyumba takatifu ya Mwenyezi 82
Musanaf cha Ibn Abi Shaybah Juz. 1, Uk. 397.
83
Fat’hul-Bariy Juz. 1, Uk. 404. 127
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 127
11/25/2014 3:03:47 PM
Ushia: Hoja na Majibu
Mungu, nilipokuwa katika Msikiti wa Mtume (saww) na nikataka kusalia juu ya kipande cha mkeka, mara alikuja mmoja kati ya Ulamaa wa kiwahabi wenye chuki binafsi akachukua mkeka – huku uso wake umevimba – na kuutupa pembeni, na dhahiri ni kwamba alikuwa anaona Sunnah hii ni bidaa. c.
Sira ya Maswahaba na Tabiina:
Miongoni mwa maudhui yenye kuvutia katika uhakiki huu ni kuchunguza kwa makini hali za Maswahaba na kundi lililokuja baada yao ambalo ni maarufu kwa jina la Tabiina, uchunguzi unaonesha kuwa walikuwa wakisujudu juu ya ardhi, na kwa mfano tu tunataja mifano ifuatayo: 1.
Jabir bin Abdullah al-Ansariy anasema: “Nilikuwa nikiswali pamoja na Mtume (saww) Swala ya Dhuhri, na nikichukua fungu la changarawe mikononi mwangu na kuziweka mkono wa pili ili zipowe kutokana na joto kali, kisha naziweka kwa ajili ya paji langu ili nisujudu juu yake.”84 Hadithi hii inaonesha vizuri kabisa kuwa Maswahaba wa Mtukufu Mtume (saww) walikuwa wamefungika katika kusujudu juu ya ardhi hata katika mazingira magumu yenye joto kali, kama kusujudu juu ya ardhi si lazima basi kusingekuwa na haja ya kuvumilia taabu zote hizi.
2.
Anas bin Malik anasema: “Tulikuwa tukiswali pamoja na Mtukufu Mtume (saww) katika siku za joto kali, na kila mmoja wetu akichukua changarawe mkononi
84
Musnadi Ahmad Juz. 3, Uk. 327. Sunanul-Bayhaqiy Juz. 1 Uk. 439. 128
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 128
11/25/2014 3:03:47 PM
Ushia: Hoja na Majibu
mwake, zinapopoa huziweka na kusujudu juu yake.”85 Ibara hii inaonesha kuwa kitendo hiki kilikuwa kimeenea baina ya Maswahaba. 3.
Abu Ubayda ananukuu kwa kusema: “Hakika Ibn Masuud hasujudu – au alisema: Hasali – isipokuwa juu ya ardhi.”86 Ingekuwa makusudio ya ardhi hapa ni mazulia basi kusingekuwa na haja ya yeye kubainisha hili, hivyo makusudio ya ardhi hapa ni udongo, changarawe, mchanga na mfano wake.
4.
Katika kutaja hali za Masruq bin Jad’an ambaye ni mmoja kati ya wafuasi wa Ibn Masuud, imekuja kwamba: “Alikuwa haruhusu kusujudu juu ya kitu kisichokuwa ardhi hata awapo ndani ya jahazi, na alikuwa anabeba ndani ya jahazi kitu cha kusujudia juu yake.”87
5.
Ali bin Abdullah bin Abbas alimwandikia barua Razin kuwa: “Nitumie vipande vya mawe ya Mar’wa ili niwe nasujudu juu yake.”88
6.
Na imeandikwa katika kitabu Fat’hul-Bariy Fi Sharhi Sahih Bukhari kuwa: “Umar bin Abdul-Aziz alikuwa hatosheki na Khumra bali alikuwa anaweka udongo juu ya Khumra na kusujudu juu yake.”89
Basi ni kitu gani tunachokifahamu kutoka kwenye kundi hili la riwaya? Tunachofahamu ni kwamba sira ya 85
Sunanul-Kubra cha Bayhaqiy Juz. 2, Uk. 106.
86
Musanaf cha Ibn Abi Shaybah Juz. 1, Uk. 397.
87
Tabaqatul-Kubra cha Ibn Saad Juz. 6, Uk. 53.
88
Akh-baru Makkah cha Azraqiy Juz. 2, Uk. 151.
89
Fat’hul-Bari Juz. 1, Uk. 410. 129
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 129
11/25/2014 3:03:47 PM
Ushia: Hoja na Majibu
Maswahaba na ya wale waliokuja baada ya Maswahaba, katika karne za mwanzo, ilikuwa ni kusujudu juu ya ardhi, yaani juu ya udongo, changarawe na mchanga. Hivyo ikitokea mtu miongoni mwa Waislamu anataka kuhuisha Sunnah hii, je ni wajibu kuzingatia kuwa suala hilo ni bidaa?!! Hivi si wajibu juu ya wanazuoni wa fiqhi wa Kisunni kuwa mbele katika kuhuisha Sunnah hii ya Mtukufu Mtume (saww)?!! Amali hii ambayo inaonesha ukamilifu wa unyenyekevu mbele ya Mwenyezi Mungu, na inaoana kabisa na maana halisi ya kusujudu. Inshaallah tunataraji ipo siku hilo litatimia.
130
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 130
11/25/2014 3:03:47 PM
Ushia: Hoja na Majibu
MADA YA SABA KUKUSANYA SALA MBILI Asili ya mada
S
ala ndio kiunganishi muhimu zaidi cha kiibada baina ya viumbe na Muumba, na ndio njia bora zaidi ya kimalezi, na ndio njia ya kuilea nafsi na kuitakasa, yenyewe inakataza machafu na maovu, na ni ngazi ya kupandia kwa Mwenyezi Mungu, na Sala ya jamaa huwapa Waislamu nguvu na uwezo, na huleta umoja baina yao na kuinua hadhi ya jamii ya Kiislamu. Na kila siku mchana na usiku hutekelezwa Sala tano ili moyo wa mtu na roho yake isafike kwa kuendelea na chemchem hii safi ya Mwenyezi Mungu, ambapo Mtukufu Mtume (saww) alisema: “Furaha ya macho yangu ipo katika Sala.”90 Na “Sala ni ngazi ya muumini.”91 Na “Sala ni sadaka ya kila muumini.”92 Na mazungumzo katika maudhui hii yanahusu je kutenganisha baina ya Sala tano katika nyakati tano ni hukumu ya wajibu kiasi kwamba bila kufanya hivyo Sala inakuwa batili? Kama ilivyo kwa mtu mwenye kusali Sala kabla ya wakati. Au mtu anaweza kusali Sala zake tano katika nyakati tatu kwa kusali pamoja Sala ya Dhuhri na Asri, na pia Sala ya Maghrib na Isha. 90
Makarimul-Akhlaq Uk. 461.
91
Biharul-An’war Juz. 79, Uk. 249 na 303.
92
Usulul-Kafiy Juz. 3, Uk. 265, Hadithi 26. 131
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 131
11/25/2014 3:03:47 PM
Ushia: Hoja na Majibu
Wanazuoni wa Kishia wafuasi wa madhehebu ya Ahlul-Bait (as) wameafikina kuwa inaruhusiwa kutekeleza Sala tano katika nyakati tatu, licha ya kwamba ni bora kuzitekeleza katika nyakati tano. Lakini wanazuoni wengi wa Kisunni wanaona ni wajibu kusali Sala tano katika nyakati zake tano isipokuwa wachache miongoni mwao. Na wameruhusu kukusanya baina ya Sala ya Dhuhri na Asri siku ya Arafah, na kukusanya baina ya Maghrib na Isha katika usiku wa Idd Udh’ha huko Muzdalifa tu. Na wengi miongoni mwao wameruhusu kukusanya safarini au katika siku za mvua ambazo ni vigumu kwenda na kurudi msikitini kutekeleza Sala ya jamaa. Ama kwa mtazamo wa wanazuoni wa Kishia ni kama tulivyosema kuwa wao wakati wanasisitiza ubora wa kutekeleza Sala tano katika nyakati zake tano, pia wanaruhusu kutekeleza Sala hizo katika nyakati zake tatu, na hiyo inazingatiwa kuwa ni zawadi ya Mwenyezi Mungu kwa viumbe wake ili kuwarahisishia amri ya Sala na kuwapa unafuu watu, na wanaona kuwa hali hiyo inaoana na uhalisia wa Uislamu kwani Sharia ni nyepesi yenye kuleta unafuu. Na uzoefu unaonesha kuwa kulazimisha watu wasali Sala tano katika nyakati zake tano kunaweza kumpelekea mtu kusahau asili ya Sala na baadhi ya watu kuacha kabisa Sala. Athari za kulazimisha watu wasali katika nyakati tano katika jamii za Kiislamu Kwa nini Uislamu uliruhusu kukusanya baina ya Sala ya Dhuhri na Asri katika siku ya Arafah, na Sala ya Maghrib na Isha katika usiku wa Iddi Udh’ha huko Muzdalifa? Kwa nini 132
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 132
11/25/2014 3:03:47 PM
Ushia: Hoja na Majibu
wanaona kuwa inaruhusiwa kukusanya baina ya Sala mbili safarini au katika siku ya mvua kwa mujibu wa riwaya za Mtume? Bila shaka ni kwa sababu ya kuurahisishia umma. Urahisishaji huu unawajibisha iwepo ruhusa ya kukusanya baina ya Sala mbili wakati wa dharura pia, sawa iwe ni huko nyuma au sasa. Kwa kweli maisha ya watu yamebadilika katika zama hizi, na mazingira yaliyopo hayamsaidii mtu kutekeleza Sala tano katika nyakati tano kutokana na kuwepo wafanyakazi wengi viwandani, watumishi wengi maofisini na wanafunzi wengi shuleni na vyuoni, na hasa kwa sababu kazi ni nzito na ngumu sana. Hakika kutenda kwa mujibu wa riwaya zilizopokewa kutoka kwa Mtukufu Mtume (saww) na kusisitizwa na Maimamu wa Ahlul-Bait (as), riwaya ambazo zinawaruhusu watu kukusanya Sala mbili, kutapelekea kuwapa nafuu katika utekelezaji wa Sala, jambo ambalo litaongeza idadi ya wenye kusali na ari ya wao kuitekeleza, kinyume na hivyo kutokufanya hivyo kutapelekea watu wengi kuacha Sala na hivyo idadi ya wenye kuacha Sala itazidi, na huenda hii ndio sababu inayofanya vijana wengi wa madhehebu ya Sunni kuacha Sala kama wasemavyo, ambapo ni kinyume kabisa na hali ilivyo kwa upande wa vijana wa madhehebu ya Shia, kwao wao wenye kuacha Sala ni wachache mno. Ukweli ni kwamba hakika kwa mujibu wa “Na nimeletwa nikiwa na Sharia rahisi yenye unafuu� na kwa mujibu wa riwaya mbalimbali ambazo zimenukuliwa kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) ni kuwa wakati ambao yeye (saww) anasisitiza ubora wa kusali Sala tano katika nyakati tano, bali bora zaidi ikiwa ni kwa jamaa, ni wakati huo huo pia anawaruhusu watu kusali Sala zao tano katika nyakati 133
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 133
11/25/2014 3:03:47 PM
Ushia: Hoja na Majibu
tatu hata kama itakuwa ni kwa mtu binafsi, ili kuzuia watu kuacha Sala kwa sababu ya mihangaiko ya kimaisha. Hebu sasa turudi kwenye Qur’ani Tukufu na kwenye riwaya za Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) na za Maasumu (as) ili kutafiti suala hili bila upendeleo na bila chuki binafsi na ushabiki. Riwaya zinazozungumzia kukusanya Sala mbili Vyanzo maarufu kama vile Sahih Muslim, Sahih Bukhar, Sunan Tirmidhiy, Muwatau ya Malik, Musnad Ahmad, SunanunNasaiy, Musannaf ya Abdur-Razaq, na vyanzo vingine na vyote vikiwa ni mashuhuri na maarufu kwa Masunni, vimetaja karibuni riwaya thelathini zikiruhusu kukusanya Sala mbili Dhuhri na Asri, na Maghrib na Isha, bila udhuru wowote, kama vile safari au mvua au kukhofia kupatwa na madhara. Na katika asili riwaya hizi zinarejea kwa wapokezi wao watano, nao ni: 1.
Ibn Abbas.
2.
Jabir bin Abdullah al-Ansariy.
3.
Abu Ayub al-Ansariy.
4.
Abdullah bin Umar na
5.
Abu Huraira.
Na tutamuonesha mpenzi msomaji sehemu ya riwaya hizo kama ifuatavyo: 1.
Ametuhadithia Abu Zubair kutoka kwa Said bin Jubair kutoka kwa Ibn Abbas kuwa amesema: “Mtume wa 134
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 134
11/25/2014 3:03:47 PM
Ushia: Hoja na Majibu
Mwenyezi Mungu (saww) aliswali Dhuhri na Asri zote kwa pamoja akiwa Madina, pasipo na hofu wala safari.”
Amesema Abu Zubair: Nikamuuliza Said: Kwa nini Mtume alifanya hivyo? (Said) akasema: Nilimuuliza Ibn Abbas kama ulivyoniuliza, akanijibu: “Alitaka asimtie katika taabu mtu yeyote katika ummah wake.”93 Yaani hataki kuutia uzito ummah wake.
2.
Tunasoma katika hadithi nyingine kutoka kwa Ibn Abbas kuwa: “Aliswali Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) Dhuhri na Asri kwa kukusanya pamoja, na Maghribi na Isha kwa kukusanya pamoja huko Madina, pasipo na hofu wala safari.” Mwishoni mwa riwaya imekuja: “Ibn Abbas akaulizwa: Alikusudia nini Mtume (saww) kwa tendo hili? Akajibu: Alitaka asimtie mtu taabu.”94 Yaani asiutie uzito ummah wake.
3.
Abdullah bin Shaqiq anasema: “Siku moja Ibn Abbas alitutolea hotuba baada ya Sala ya Asri mpaka jua likazama na nyota zikadhihiri. Watu wakawa wanasema: ‘Sala! Sala!’” Akasema (mpokezi): “Kisha akaja mtu mmoja miongoni mwa Bani Tamim akiwa hachoki wala kupumzika, akasema ‘Sala! Sala!’, Ibn Abbas akamjibu kwa kusema: ‘Je unanifundisha Sunnah (za Mtume) ewe usiye na mama wee!’ Kisha akasema: ‘Mimi nimemwona Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) akikusanya Dhuhri pamoja na Asri, na Maghribi pamoja na Isha.’” Abdullah bin Shaqiq akasema: “Jambo hilo likanikera moyoni mwangu na kunitia shaka. Nikam-
93
Sahih Muslim Juz. 2, Uk. 151.
94
Sahih Muslim Juz. 2, Uk. 152. 135
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 135
11/25/2014 3:03:47 PM
Ushia: Hoja na Majibu
wendea Abu Huraira nikamuuliza. Yeye akasadikisha maneno ya Ibn Abbas.”95 4.
Ametusimulia Jabir bin Zaid kutoka kwa Ibn Abbas amesema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) aliswali nane kwa pamoja na saba kwa pamoja.”96 Akiashiria kukusanya baina ya Sala ya Maghribi na Isha na baina ya Sala ya Dhuhri na Asri.
5.
Alitusimulia Said bin Jubair kutoka kwa Ibn Abbas kuwa alisema: “Aliswali Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) Dhuhri na Asri kwa kukusanya pamoja, na Maghribi na Isha kwa kukusanya pamoja huko Madina, pasipo na hofu wala safari.” Mpokezi anasema: “Ibn Abbas akaulizwa: Alikusudia nini kwa tendo hilo? Akajibu: ‘Alitaka asiutie taabu umma wake’.”97
6.
Ahmad bin Hanbal amenukuu katika Musnad yake riwaya inayoshabihiana kwa ukaribu na hiyo iliyotangulia.98
7.
Malik Imam maarufu kwa Masunni amenukuu ndani ya kitabu chake Muwatau hadithi kutoka kwa Ibn Abbas kuwa alisema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) aliswali Dhuhri na Asri kwa kukusanya pamoja, na Maghribi na Isha kwa kukusanya pamoja, pasipo na hofu wala safari.”99
95
Sahih Muslim Juz. 2, Uk. 151.
96
Sahih Bukhari Juz. 1, Uk. 140, mlango unaozungumzia wakati wa Maghrib.
97
Sunan Tirmidhiy Juz. 1, Uk. 121, Hadithi ya 187.
98
Musnad Ahmad Juz. 1, Uk. 223.
99
Muwatau ya Malik Juz. 1, Uk. 144. 136
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 136
11/25/2014 3:03:47 PM
Ushia: Hoja na Majibu
8.
Imekuja ndani ya kitabu Musannaf cha Abdur-Razaq, kutoka kwa Umar bin Shuaib, amesema: Abdullah alisema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) alitusalisha na akakusanya Sala baina ya Dhuhri na Asri, na baina ya Maghribi na Isha, hali tukiwa nyumbani na si safarini. Mtu mmoja akamuuliza Ibn Umar: ‘Unaona ni kwa nini Mtume (saww) amefanya hivyo?’ Akajibu: ‘Ili asiupe taabu umma wake iwapo mtu atakusanya.’”100
9.
Jabir bin Abdullah alitusimulia, akasema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) alikusanya baina ya Dhuhri na Asri, na baina ya Maghribi na Isha huko Madina, kwa hiyari pasipo na khofu wala udhuru wowote.”101
10.
Abu Huraira anasema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) alikusanya baina ya Sala mbili huko Madina pasipo na Khofu.”102
11.
Pia Abdullah bin Masuud ananukuu kuwa: “Alikusanya Mtume wa Mwenyezi Mungu Dhuhri na Asri, Maghribi na Isha. Akaulizwa kuhusu hilo, yeye akasema: ‘Nimefanya hivyo ili umma wangu usitaabike.”103 Na hadithi nyingine nyingi.
Na hapa kuna maswali mawili yanajitokeza: Kwanza: Muhtasari wa riwaya zilizotangulia Riwaya zote tulizozitaja na ambazo ni kutoka kwenye vyanzo maarufu na vitabu vya daraja la kwanza kwa Masunni, ri100
Musannaf cha Abdur-Razaq Juz. 1, Uk. 556.
101
Maanil-Athar Juz. 1, Uk. 161.
102
Musnadul-Bazzar Juz. 1, Uk. 283.
103
al-Muujam al-Kabir cha Tabaraniy Juz. 10, Uk. 219, Hadithi ya 10525. 137
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 137
11/25/2014 3:03:48 PM
Ushia: Hoja na Majibu
waya ambazo zinakomea kwa kundi la Masahaba wakubwa, zote zinasisitiza nukta mbili: Nukta ya kwanza: Hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) alikusanya baina ya Sala mbili pasipo kuwepo mazingira yoyote makhususi, kama vile safari, khofu au kuwepo adui. Nukta ya pili: Hakika lengo lilikuwa ni kuupa unafuu umma na kuuondolea taabu na uzito. Je hali hii inaoana na ukosoaji usio na maana, wa kusema kuwa ukusanyaji huu ulihusu hali na mazingira ya dharura? Kwa nini mnafumba macho yenu mbele ya ukweli huu na badala ya kuchukua maneno ya Mtume wa Mwenyezi Mungu yaliyo bayana mnatanguliza rai zenu zisizokuwa haki? Mwenyezi Mungu na Mtume wake wamesamehe na kurahisisha lakini katika umma kuna kundi lenye chuki binafsi halitaki kusamehe na kurahisisha, kwa nini? Kwa nini hatuwapi nafasi vijana wa Kiislamu ya kutekeleza wadhifa muhimu zaidi katika Uislamu, nao ni Sala tano za kila siku, katika hali yoyote aliyo nayo na katika sehemu yoyote aliyopo, sawa awe katika nchi ya Kiislamu au nje, awe chuoni au ofisini au kiwandani? Sisi tunaamini kuwa Uislamu unakubali kutekelezwa katika zama zote na sehemu zote mpaka mwisho wa ulimwengu. Na tuna yakini kuwa Mtukufu Mtume (saww) kwa mtazamo wake wa kina na wa mbali alitizama mazingira ya Waislamu wote wa zama zote, hivyo kama angewafunga Waislamu wote katika kutekeleza Sala tano katika nyakati tano basi kungekuwepo na kundi la waacha Sala, na hili ndilo tunaloliona leo, na kwa ajili 138
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 138
11/25/2014 3:03:48 PM
Ushia: Hoja na Majibu
hii akauhurumia umma wake na kuupa nafuu ili uweze kutekeleza daima Sala tano za kila siku, kwa raha na kila zama na kila sehemu. Qur’ani Tukufu inasema:
ۚ ين ِمنْ َح َر ٍج ِ َو َما َج َع َل َع َل ْي ُك ْم فِي ال ِّد “…..Wala hakuweka juu yenu uzito katika dini…..” (Sura Hajj: 78.)
Pili: Qur’ani na nyakati tatu za Sala Miongoni mwa mambo ya kushangaza katika mas’ala hii ni kwamba Qur’ani Tukufu inapozungumzia nyakati za Sala tano yenyewe imetaja nyakati tatu tu kwa ajili ya Sala tano za kila siku, lakini la kustaajabisha katika jambo hili ni kwa nini hawa ndugu zetu wanang’ang’ania wajibu wa kusali Sala tano katika nyakati tano? Sisi hatukanushi ubora wa nyakati tano, sisi tunafuata nyakati tano tunapoafikishwa kufanya hivyo, lakini tatizo hapa ni kuhusu wajibu wa kusali katika nyakati tano!! Zifuatazo ni Aya zinazozungumzia nyakati za Sala: Aya ya kwanza ni ya Sura Hud:
َ ۚ ار َو ُز َل ًفا م َِن اللَّي ِْل ِ َوأق ِِم الص ََّال َة َط َر َفيِ ال َّن َھ
“Na simamisha Swala katika sehemu mbili za mchana na nyakati za usiku zilizo karibu na mchana….” (Sura Hud: 114). 139
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 139
11/25/2014 3:03:48 PM
Ushia: Hoja na Majibu
Ibara “Sehemu mbili za mchana” inaashiria Sala ya Subhi ambayo husaliwa mwanzoni mwa mchana, na Sala ya Dhuhri na Asri ambazo wakati wake hudumu hadi magharibi. Na kwa ibara nyingine ni kwamba kutokana na Aya hii tunapata kwa bayana kabisa kuwa wakati wa Sala ya Dhuhri na Asri unaendelea mpaka jua linapozama.
Ama ibara: “Nyakati za usiku zilizo karibu na mchana,” ukitazama aliyosema Raghib katika kitabu chake al-Mufradat na Mukhtarus-Sahih utakuta hakika neno Zulafa lililopo katika Aya ni wingi wa Zulfatu, nalo humaanisha sehemu ya kwanza ya usiku, ambapo ni kuashiria wakati wa Sala ya Maghribi na Isha. Hivyo ikiwa Mtukufu Mtume (saww) ana ada ya kutekeleza Sala zake tano katika nyakati tano basi ni kwa sababu ya kuchunga wakati wenye ubora, na hili ndilo tunaloitakidi sote, hivyo ni kwa nini tukimbilie kwenye dhana bila kutazama dhahiri ya Aya?! Aya ya pili ni:
آن َ ْمْس إِ َل ٰى َغ َس ِق اللَّي ِْل َوقُر ِ أَق ِِم الص ََّال َة لِ ُدلُوكِ ال َّش ان َم ْشھُو ًدا َ آن ْال َفجْ ِر َك َ ْْال َفجْ ِر ۖ إِنَّ قُر “Simamisha Sala linapopinduka jua mpaka giza la usiku, na Qur’ani ya alfajiri; hakika Qur’ani ya alfajiri imekuwa ni yenye kushuhudiwa.” (Sura Israi: 78).
Duluk humaanisha kuelemea, na hapa neno hili linaashiria kuelemea kwa jua kutoka kwenye msitari unaogawa mchana, yaani ni kukengeuka kwa jua na kuingia adhuhuri.
140
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 140
11/25/2014 3:03:48 PM
Ushia: Hoja na Majibu
Ghasaqi Layli humaanisha giza la usiku, na baadhi yao wamelifasiri neno hili kwa maana ya mwanzo wa usiku, na wengine wakasema nusu ya usiku, kwa sababu alichosema Raghib katika al-Mufradat ni kuwa humaanisha giza kali, na hiyo ndio nusu ya usiku. Hivyo hitimisho ni kwamba hakika ibara “Linapopinduka jua” inaashiria mwanzo wa wakati wa Sala ya Dhuhri, na ibara “Giza la usiku” inaashiria mwisho wa wakati wa Sala ya Maghribi na Isha, na ibara “Qur’ani ya Alfajiri” inaashiria Sala ya Subhi. Vyovyote iwavyo ni kuwa Aya tukufu imebainisha nyakati tatu za Sala tano za kila siku, na si nyakati tano, na hii ni dalili ya kwamba inaruhusiwa kusali ndani ya nyakati tatu. Kwa Fakhri Razi kuna maelezo mazuri anapotafsiri Aya hii, ambapo anasema: “Laiti tukitafsiri giza la usiku kwa maana ya kuingia kwa giza la mwanzo, basi ibara giza la usiku itamaanisha mwanzo wa magharibi, na kwa maana hii nyakati zilizotajwa na Aya zitakuwa ni tatu: Wakati wa kupinduka kwa jua, wakati wa kuanza magharibi na wakati wa alfajiri. Na hali hii inapelekea kupinduka kwa jua kuwe ni wakati wa Dhuhri na Asri, hivyo wakati huu unakuwa ni wa kushirikiana kati ya hizi Sala mbili. Na mwanzo wa magharibi uwe ni wakati wa Maghribi na Isha, hivyo wakati huu nao ni wa kushirikiana kati ya hizi Sala mbili. Hivyo hii inapelekea kuruhusiwa kukusanya katika hali yoyote ile kati ya Dhuhri na Asri, Maghribi na Isha.”104 Tunaona hadi hapa Fakhru Razi ameichambua mada vizuri, na amefahamu maana ya Aya kwa usahihi, na 104
Tafsirul-Kabir cha Fakhru Razi Juz. 21, Uk. 27. 141
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 141
11/25/2014 3:03:48 PM
Ushia: Hoja na Majibu
ameibainisha kwa sura bayana, lakini baada ya hapo anasema: “Lakini tunayo dalili inayoonesha kutoruhusiwa kukusanya Sala mbili isipokuwa katika udhuru au safari.”105 Na ni wajibu tuseme kuwa si tu hatuna dalili inayoonesha kuwa kukusanya ni makhususi katika hali ya udhuru, bali ni kwamba pia tunazo riwaya nyingi – na tumeshataja baadhi yake – zinazoonesha kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) katika baadhi ya nyakati alikuwa akikusanya baina ya Sala mbili ya Dhuhri na Asri, na Sala ya Maghribi na Isha, pasipo udhuru wala safari, ili aufanyie unafuu umma wake, na umma utumie vizuri ruhusa hii. Vyovyote iwavyo hatuwezi kuachana na maana bayana ya Aya ambayo inabainisha nyakati tatu, hivyo kutokana na uchambuzi uliotangulia tunapata hitimisho lifuatalo: 1.
Hakika Qur’ani imebainisha bayana na kuruhusu kutekeleza Sala tano katika nyakati tatu.
2.
Riwaya za Kiislamu kutoka kwenye vitabu vya makundi yote mawili (Sunni na Shia) zimebainisha kuwa Mtukufu Mtume (saww) alikusanya Sala mbili mara nyingi tu, pasipo yeye kuwa safarini au kuwa na udhuru wowote ule. Na hii inachukuliwa kuwa ni ruhusa kwa Waislamu ili wasitumbukie katika taabu.
3.
Ijapokuwa kusali Sala tano katika nyakati tano ni bora, lakini kung’ang’ania ubora mkabala na ruhusa kutapelekea watu wengi – na hasa rika la vijana – kupuuza Sala, na mzigo huu wataubeba wale wenye kupinga ruhusa, hivyo kwa uchache Ulamaa wa Kisunni wanapasa kuwataka vijana wao kutenda kwa mujibu
105
Tafsirul-Kabir cha Fakhru Razi Juz. 21, Uk. 27. 142
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 142
11/25/2014 3:03:48 PM
Ushia: Hoja na Majibu
wa fatwa zetu sisi wafuasi wa Ahlul-Baiti (as), kama aalimu mkubwa Sheikh wa Azhar, Sheikh Mahmud Shaltut alivyoruhusu kutenda kwa mujibu wa fatwa za madhehebu ya Ja’fariyyah (Shia Ith’naasharia). Tunasisitiza tena kuwa ni lazima kukubali kuwa ni vigumu sana katika zama zetu hizi tulizonazo, kwa wafanyakazi wengi, watumishi wengi, wanafunzi wengi na wanavyuo wengi na pia watu wa makundi mengine, kutekeleza Sala tano ndani ya nyakati tano, hivyo je si inatupasa tutumie ruhusa ya Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) ambayo aliitoa kwa ajili ya siku kama hizi, ili vijana na makundi mengine yasipate nguvu ya kuacha Sala? Je inasihi kung’ang’ania Sunnah ikiwa inapelekea kuacha faradhi?
143
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 143
11/25/2014 3:03:48 PM
Ushia: Hoja na Majibu
MADA YA NANE KUPAKA MIGUU KATIKA UDHU Qur’ani na kupaka juu ya miguu
K
upaka juu ya miguu ni moja ya mambo ambayo baadhi ya Ulamaa wa Kisunni huwakosoa Mashia na wafuasi wa madhehebu ya Ahlul-Baiti (as) kwalo, ambapo Masunni wengi wanaona ni wajibu kuosha miguu na kutotosheka na kupaka miguu. Wakati ambapo Qur’ani Tukufu imeamuru wazi wazi kupaka juu ya miguu, na wafuasi wa Ahlul-Baiti (as) wanatenda kwa mujibu wa Qur’ani na kwa mujibu wa hadithi nyingi ambazo ni zaidi ya thelathini. Na kupaka ilikuwa ni tendo la Masahaba wengi na pia Tabiina, na si kuosha. Lakini cha kusikitisha baadhi ya wenye kupinga wamefumba macho mbele ya dalili hizi, na hawajazihimiza nafsi zao kufanya utafiti vya kutosha, bali wao wameelekeza mashambulizi yao kwa wafuasi wa madhehebu ya Shia kwa kuwakosoa na kuwaudhi kwa maneno mazito na yasiyofaa na yaliyo mbali na haki na uadilifu. Ibn Kathir ambaye ni mmoja kati ya Ulamaa maarufu kwa Masunni anasema katika kitabu chake Tafsirul-Qur’ani alAdhim: “Rawafidhu wamekhalifu hilo (kuosha miguu miwili) bila ya egemeo, bali kwa ujahili na upotovu…. Kadhalika Aya hii tukufu yajulisha wajibu wa kuosha miguu miwili ikiwa 144
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 144
11/25/2014 3:03:48 PM
Ushia: Hoja na Majibu
ni pamoja na ilivyothibiti kwa tawaturi kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) alitenda kulingana na ilivyojulisha Aya tukufu, na wao (Mashia) wanakwenda kinyume na hayo yote, na wala hawana dalili iliyo sahihi katika suala lenyewe.”106 Na likamfuata kundi jingine kwa macho yaliyopofuka na kwa masikio yaliyoziba bila kuhakiki mas’ala husika, na hivyo na wao wakawasha moto wa tuhuma dhidi ya Mashia kadiri na jinsi wapendavyo. Na wakadhani kuwa wote wanaowaambia ni watu wa kawaida, na wala hawajafikiri kuwa wapo wahakiki na Ulamaa ambao siku moja watasimama na kukosoa maneno yao, na hivyo wao wataendelea kujuta mbele ya historia ya Uislamu juu ya uzushi wao. Na sasa na kabla ya kila kitu hebu tuelekee kwenye Qur’ani Tukufu, yenyewe inatueleza katika Sura al-Maidah, Sura ambayo ndio ya mwisho kumshukia Mtume wa Uislamu (saww):
ْ ِين آ َم ُنوا إِ َذا قُ ْم ُت ْم إِ َلى الص ََّال ِة َف اغسِ لُوا َ َيا أَ ُّي َھا الَّذ وُ جُو َھ ُك ْم َوأَ ْي ِد َي ُك ْم إِ َلى ْال َم َراف ِِق َوا ْم َسحُوا ِب ُر ُءوسِ ُك ْم ۚ ْن ِ َوأَرْ ُج َل ُك ْم إِ َلى ْال َكعْ َبي “Enyi mlioamini! Mnaposimama kwa ajili ya Swala, basi osheni nyuso zenu na mikono yenu mpaka vifundoni, na mpake vichwa vyenu na miguu yenu mpaka vifundoni….” (Sura Maidah: 6).
Na ni dhahiri kwamba neno “Miguu yenu” limeunganishwa na “Vichwa vyenu” hivyo inakuwa ni lazima kuvipaka vyote 106
Tazama Tafsir Ibn Kathir Juz. 2 Uk. 518. 145
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 145
11/25/2014 3:03:48 PM
Ushia: Hoja na Majibu
viungo viwili, sawa tukisoma kwa Fat’ha au kwa Kasra, zingatia hilo. Vyovyote iwavyo ni kwamba Qur’ani Tukufu imeamuru kupaka nyayo mbili. Utetezi wa ajabu Lakini kuna kundi lilipoona kuwa hukumu za mwanzo walizozichukua haziafikiani na tamko la Qur’ani Tukufu limekimbilia kutoa na kufuata sababu zinazomfanya mtu awe katika mbabaiko, na miongoni mwa utetezi huo ni: 1.
Hakika Aya hii ilifutwa kwa Sunnah ya Mtukufu Mtume (saww) na kwa hadithi zilizonukuliwa kutoka kwake, Ibn Hazmi anasema katika kitabu chake al-Ihkam Fii UsululAhkam: “Kwa kuwa kuosha kumekuja katika Sunnah basi ni lazima kukubali kuwa kupaka kulifutwa.”
Tunamjibu kuwa: Kwanza: Hakika wafasiri wote wa Qur’ani wamesema kuwa Sura Maidah ndio Sura ya mwisho iliyoteremka kwa Mtukufu Mtume (saww) na hakuna ufutwaji wowote katika Aya zake. Pili: Kama itakavyofuata baadaye kuwa mkabala na riwaya zinazoonesha kuwa Mtukufu Mtume (saww) aliosha nyayo zake wakati wa kutawadha, pia zipo riwaya nyingi nyingine zinazosema kuwa Mtukufu Mtume (saww) alipaka nyayo zake wakati wa kutawadha. Hivyo itakuwaje asili ambayo ni Qur’ani ifutwe kwa riwaya za uwongo ambazo hii ndio hali yake? Na hata tukifumbia macho hili ni kwamba katika mlango wa mgongano wa riwaya imetajwa kuwa riwaya zinapopingana ni wajibu kuzipima kwa Qur’ani, zile 146
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 146
11/25/2014 3:03:48 PM
Ushia: Hoja na Majibu
zinazoafikiana na Qur’ani zichukuliwe na zinazopingana nayo zitupiliwe mbali na kuachwa. 2.
Wapo wengine kama vile Jasas anasema katika kitabu chake Ahkamul-Qur’ani kuwa: “Hakika Aya ya udhu haiko wazi, hivyo ni lazima tutende kwa mujibu wa tahadhari, tuoshe nyayo mbili, hapo itakuwa imepatikana kuosha na kupaka.”107 Na sisi sote tunajua kuwa kuna tofauti kubwa na bayana kati ya maana ya kuosha na kupaka, na kupaka hakujumuishi kuosha. Lakini tutafanya nini!! Hukumu za mwanzo ambazo hutolewa bila utafiti hazituruhusu kutenda kwa mujibu wa dhahiri ya Qur’ani Tukufu.
3.
Fakhru Razi anasema: “Hata tukisoma “Arjulakum” (miguu yenu) kwa Kasra, kwa kuiunganisha na “Ruusikum” (vichwa vyenu), bado itaonesha wazi wazi kupaka. Isipokuwa ni kwamba makusudio yake si kupaka juu ya nyayo mbili, bali makusudio ya kupaka hapa ni kutokumwagia maji mengi wakati wa kuosha nyayo mbili.”108
Kwa kweli tukikubali aina hii ya ijitihadi na kutafsiri Aya za Qur’ani kwa rai binafsi, basi hakutabakia dhahiri yoyote ya Qur’ani tutakayoifanyia kazi. Tukiweza kusema kwa utashi wetu kuwa hapa kupaka inamaanisha kuosha basi tunaweza kutafsiri dhahiri nyingine za Qur’ani kwa namna nyingine tutakavyo. Ijitihadi na tafsiri ya rai binafsi mkabala na maandiko Kuna vielelezo vingi vinavyoonesha ubaya na kutokukubalika kwa aina hii ya ijitihadi ambayo huwa mkabala na maandiko 107
Ahkamul-Qur’ani Juz. 2, Uk. 434.
108
Tafsirul-Kashaf: Juz. 1 Uk. 610. 147
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 147
11/25/2014 3:03:48 PM
Ushia: Hoja na Majibu
yaliyoenea katika zama zetu hizi, na hali hii ya kukataa na kupinga haikuwepo katika zama za mwanzo za Uislamu. Na kwa ibara nyingine ni kwamba hakika hali hii iliyopo kwetu leo hii ya kufuata na kutii moja kwa moja Aya za Qur’ani Tukufu na maneno ya Mtukufu Mtume (saww), katika zama hizo haikuwa hivi kwa nguvu hii na mkazo huu uliopo sasa. Kwa mfano tu ni kwamba pindi Umar bin Khattab alipotoa rai yake maarufu kuwa: “Mut’a mbili zilikuwa ni halali zama za Mtume (saww) na mimi naziharamisha na ninatoa adhabu kwa mtendaji wake: Mut’a ya wanawake na Mut’a ya Hijja,” hatukusikia yeyote miongoni mwa Masahaba aliyemkosoa au kumwelekezea lawama kwa kusema: “Huku ni kufanya ijtihadi mkabala na maandiko.” Ambapo leo hii katika zama zetu laiti atajitokeza aalimu mkubwa wa Kiislamu na kusema: “Hakika amali fulani ilikuwa halali zama za Mtume (saww) na mimi naiharamisha.” Basi watu wote watashangazwa na msimamo wake huu na wataonesha kumpinga na watasema rai yake hii haina uzito na haikubaliki, na kwamba hakuna mtu mwenye haki ya kuharamisha halali ya Mwenyezi Mungu wala kuhalalisha haramu yake, kwa sababu hapaswi mtu kufanya ijitihadi mbele ya maandiko wala kufuta hukumu zilizothibiti. Lakini hali haikuwa hivyo zama za mwanzo, na kwa dalili hii ndio maana tunawaona baadhi ya Ulamaa wa fiqhi wakiwa wamejipa ruhusa ya kukhalifu hukumu za Mwenyezi Mungu, na huenda kukataa kupaka nyayo mbili na hatimaye kubadili hukumu hiyo kwa kuosha ni miongoni mwa aina hizi za ijitihadi na tafsiri ya rai binafi mkabala na maandiko.
148
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 148
11/25/2014 3:03:48 PM
Ushia: Hoja na Majibu
Na huenda baadhi yao walidhani ni bora kuosha nyayo mbili kwa sababu daima zenyewe ndio huchafuka, hivyo kuna faida gani ya kupaka? Na hasa ukizingatia kuwa baadhi ya Waislamu walikuwa katika zama hizo wakitembea peku peku, na kwa ajili hii ilikuwa ni miongoni mwa adabu maarufu kwao wakati wa kuwapokea wageni, kuleta maji ili wageni waoshe miguu yao. Na ushahidi juu ya maneno haya ni yale aliyosema mwandishi wa tafsiri al-Manar mwishoni mwa Aya ya udhu, anapotetea maneno ya wale wenye kusema miguu huoshwa, anasema: “Hakika kupaka mikono miwili juu ya nyayo mbili zilizotapakaa vumbi au uchafu, si tu hakuna faida bali pia kunazidi kuzichafua kuliko zilivyokuwa mwanzo, na pia uchafu huo utahamia kwenye mkono.” Ibn Qadamah ambaye ni mwanafiqhi maarufu kwa Masunni (alifariki mwaka 62 A.H.) ananukuu kutoka kwa baadhi yao kuwa: “Hakika nyayo mbili ziko katika hatari ya kuchafuka kinyume na kichwa, hivyo inafaa nyayo zioshwe na kichwa kipakwe.”109 Hapa tunaona jinsi gani ameitanguliza ijitihadi hii na pendekezo hili mkabala na dhahiri ya Aya ya Qur’ani, na ameacha kupaka na kuielekeza Aya kwenye mwelekeo usiokuwa salama kwa utetezi wake. Na dhahiri ni kwamba kundi hili limesahau kuwa udhu ni mjumuiko wa usafi na ibada, hivyo kupaka kichwa hakuna uhusiano wowote na usafi wake, na hasa kwa kuzingatia baadhi ya fatwa ambazo zinasema inatosha kupaka kwa kidole, na kadhalika kupaka nyayo hakuna uhusiano wowote na usafi wake, na ukweli ni kwamba kupaka kichwa na nyayo mbili ni ishara ya mtu mwenye kutawadha kukubali na kutii amri za Mwenyezi Mungu kutoka kichwani hadi chini ya 109
Al-Mughniy cha Ibn Qadamah Juz. 1 Uk. 117. 149
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 149
11/25/2014 3:03:48 PM
Ushia: Hoja na Majibu
nyayo mbili, kwani kupaka kichwani hakuleti usafi wala kupaka nyayo mbili. Vyovyote iwavyo ni kuwa sisi ni wenye kufuata hukumu za Mwenyezi Mungu na hatuna haki kubadili maamrisho ya Mwenyezi Mungu kwa akili zetu finyu. Wakati inapomteremkia Mtume (saww) Sura ya mwisho ya Qur’ani na kuamuru kuosha uso na mikono miwili na kupaka kichwa na nyayo mbili, ni wajibu juu yetu kutoikhalifu na kutokukimbilia kutetea ukhalifu huo kwa kuyatafsiri maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa njia isiyo sahihi kwa akili zetu finyu za kibinadamu. Ndiyo, tafsiri ya rai binafsi mkabala na maandiko ni balaa kubwa na ni yenye kudhuru sana misingi ya Sharia ya Uislamu katika baadhi ya sehemu. Kupaka juu ya viatu Na miongoni mwa maajabu ya dahari ambayo yanamshangaza kila mhakiki mwadilifu ni kuwa wakati ambao wanasisitiza kuwa hairuhusiwi kupaka juu ya nyayo katika udhu na ni lazima kuosha nyayo mbili, ni wakati huo huo wengi wao wanatamka wazi kuwa inaruhusiwa kupaka juu ya viatu badala ya kuosha nyayo mbili, tena pasipo na udhuru wala safari, bali ni katika hali ya hiyari, ya kutokuwa safarini na katika hali yoyote ile. Kwa kweli hukumu hizi – za ima kuosha miguu au kupaka juu ya viatu - zinashangaza sana. Ndiyo, kwa mtazamo wa fiqhi ya Masunni ni kuwa kuna kundi dogo la watu kama vile Ali bin Abu Talib (a.s.), Ibn Abbas na Malik ambaye ni mmoja kati ya Maimamu wa Kisunni, yeye katika moja ya 150
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 150
11/25/2014 3:03:48 PM
Ushia: Hoja na Majibu
fatwa zake, pamoja na hao wawili hawaruhusu kupaka juu ya viatu. Na la kuvutia ni kwamba Aisha ambaye ndugu zetu Masunni wanazipa umuhimu mkubwa fatwa zake na riwaya zake anasema katika hadithi maarufu: “Kukatika nyayo zangu mbili hizi ni kitu nikipendacho zaidi kuliko kupaka juu ya Khoffu mbili.”110 Na yeye alikuwa anaishi na Mtukufu Mtume usiku na mchana na anaona udhu wake. Vyovyote iwavyo lau ndugu zetu hawa wangefuata hadithi za Ahlul-Bait (as) na ambazo zinaoana na dhahiri ya Qur’ani basi wasingekubali isipokuwa kupaka nyayo mbili. Mtukufu Mtume (saww) anasema katika hadithi sahihi: “Nimekuachieni vitu ambavyo mkishikamana navyo kamwe hamtopotea: Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu watu wa nyumba yangu. Na hakika hivyo viwili havitaachana mpaka vitakaponikuta katika Hodhi.”111 Na anasema Imam al-Baqir (as) katika riwaya sahihi: “Katika mambo matatu simuogopi (simfanyii taqiyyah) yeyote: Katika kilevi, kupaka Khoffu mbili, na Mut’a ya Hijja.”112 Riwaya za Kiislamu na kupaka juu ya nyayo mbili Wanafiqhi wa madhehebu ya Imamiyyah wamekubaliana kuwa katika udhu tendo lililo kinyume na kupaka nyayo mbili halikubaliki, na riwaya zilizopokewa kwa njia ya AhlulBaiti (as) zinatamka wazi wazi maana hii, na bila shaka mmeshaona hilo katika hadithi iliyotangulia punde tu ya Imam 110
Al-Mabsut cha Sarkhasiy Juz. 1, Uk. 98.
111
Kamalud-Din Watamamun-Ni’mah Uk. 237.
112
Usulul-Kafiy Juz. 3, Uk. 32. 151
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 151
11/25/2014 3:03:48 PM
Ushia: Hoja na Majibu
al-Baqir (as), na bado kuna hadithi nyingi sana kuhusu suala hili. Lakini hadithi zilizokuja ndani ya vyanzo vya Kisunni zimetofautiana kikamilifu, kuna makumi ya hadithi ambazo zimeashiria mas’ala hii ya kupaka juu ya nyayo mbili, au zinasema: Hakika baada ya Mtukufu Mtume (saww) kupaka kichwa chake alipaka nyayo zake mbili. Na kuna hadithi nyingine wamezinasibisha kwa Mtukufu Mtume (saww) ambazo zinasema aliosha, na nyingine zinasema alipaka juu ya Khoffu mbili. Kundi la hadithi ambazo zimetaja kupaka tu zimetajwa katika vitabu maarufu kama vile: Sahih Bukhar, Musnad Ahmad, Sunan Ibn Majah, Mustadrakul-Hakim, Tafsir Tabariy, ad-Durul-Manthur, Kanzul-Ummal na vinginevyo miongoni mwa vitabu vyenye kukubalika na kupewa kipaumbele kwa Masunni. Na wapokezi wa hadithi hizi ni watu mfano wa Amirul-Muuminin (a.s.), Ibn Abbas, Anas bin Malik, Uthman bin Affan, Basru bin Said, na Rifaah. Nasi hapa tutataja riwaya tano tu kama mfano, na kwa kweli maneno ya kuajabisha zaidi ni yale waliyosema baadhi yao akiwemo mfasiri maarufu Alusiy, aliposema: “Hakuna riwaya zaidi ya moja kwa Mashia iliyo dalili juu ya hilo.”113 Riwaya hizo ni: 1.
Kutoka kwa Ali bin Abu Talib (a.s.) amesema: “Nilikuwa naonelea kuwa chini ya nyayo mbili ndiko kunastahiki kupakwa kuliko juu yake, mpaka nilipomuona Mtume wa Mwenyezi Mungu anapaka juu ya nyayo mbili.”114
113
Tafsir Ruhul-Maaniy Juz. 6, Uk. 87.
114
Musnad Ahmad Juz. 1, Uk. 124. 152
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 152
11/25/2014 3:03:48 PM
Ushia: Hoja na Majibu
Hadithi hii imetajwa vizuri na bayana kwamba Mtukufu Mtume (saww) alipaka juu ya nyayo zake, na kwa njia ya mtu mfano wa Imam Ali (a.s.). 2.
Kutoka kwa Abu Matar alisema: “Wakati sisi tukiwa tumeketi pamoja na Ali (a.s.) msikitini, alikuja mtu kwa Ali (a.s.) na alisema: ‘Nionyeshe udhu wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww).’ Ali (a.s.) alimwita Qanbar na kumwambia: ‘Niletee kimtungi cha maji.’ Akaosha mikono yake na uso wake mara tatu, aliingiza baadhi ya vidole vyake kinywani na alipandisha maji puani mara tatu, na aliosha dhiraa zake mbili mara tatu na alipaka kichwa chake mara moja na miguu yake miwili mpaka katika fundo mbili.”115
3.
Kutoka kwa Bisru bin Said alisema: “Uthman alileta kigoda, kisha akaomba maji, akasukutua na kuvuta maji puani kisha akaosha uso wake mara tatu na mikono yake mara tatu tatu, na akapaka sehemu ya kichwa chake na miguu yake mara tatu tatu, kisha akasema kuliambia kundi la Maswahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) waliokuwepo kwake: ‘Nilimuona Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) akitawadha kama hivi, enyi mliopo, ndivyo hivi?’ Wakasema: ‘Ndiyo.’”116 Hadithi hii inaashiria wazi wazi kuwa namna ya udhu wa Mtume (saww) ilikuwa ni kupaka, na ushahidi huu haukomei tu kwenye kauli ya Uthman peke yake, bali Maswahaba wote wanathibitisha hilo. Na hata kama imetajwa kuwa alipaka kichwani na katika nyayo mbili mara tatu tatu
115
Kanzul-Ummal Juz. 9, Uk. 448.
116
Musnad Ahmad Juz. 1, Uk. 67. 153
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 153
11/25/2014 3:03:49 PM
Ushia: Hoja na Majibu
lakini inaweza kutafsiriwa kuwa kufanya hivyo mara tatu ni mustahabu, au mpokezi amekosea. 4.
Kutoka kwa Rufa’ah bin Rafi’u alisema kuwa alimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) akisema: “Hakika Sala ya mmoja wenu haitimii mpaka akamilishe udhu kama Mwenyezi Mungu alivyoamuru, aoshe uso wake na mikono yake miwili mpaka kwenye viwiko vyake viwili, na apake sehemu ya kichwa chake na miguu yake mpaka kwenye fundo zake mbili.”117
5.
Kutoka kwa Abu Malik al-Ash’ariy kuwa aliiambia kaumu yake: “Jikusanyeni niwasalisheni Sala ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww).” Walipojikusanya, alisema: “Je kati yenu kuna ambaye si katika ninyi?” Wakasema: “Hapana, isipokuwa mtoto wa dada yetu.” Akasema: “Mtoto wa dada wa kaumu ni miongoni mwao.” Akaagiza bakuli ndani yake mna maji, akatawadha na akasukutua na kupandisha maji puani, akaosha uso wake mara tatu na dhiraa zake mbili mara tatu, na akapaka sehemu ya kichwa chake na juu ya nyayo zake mbili, kisha akawasalisha.”118
Kwa kweli riwaya tulizozitaja ni sehemu ndogo sana ya riwaya zilizopo ndani ya vitabu vya kutegemewa vya Masunni zinazozungumzia kupaka, na ambazo zimenukuliwa na wapokezi maarufu. Ama watu ambao wamesema kuwa hakuna hadithi yoyote inayoonesha kupaka miguu miwili, au kwamba hakuna zaidi ya hadithi moja inayoonesha hilo, hakika hao ni watu wasiojua kitu na wenye chuki binafsi na ushabiki, ambapo walidhani kuwa kwa kufumba macho na 117
Sunan Ibn Majah Juz. 1, Uk. 156.
118
Musnad Ahmad Juz. 5, Uk. 342. 154
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 154
11/25/2014 3:03:49 PM
Ushia: Hoja na Majibu
kukataa ukweli watafanikiwa kuufuta ukweli. Wao ni kama yule aliyekanusha wajibu wa kupaka unaotokana na dalili ya Aya tukufu ya Surat Maidah, mpaka jambo hili likawapelekea kusema (uwongo) kuwa Aya inaamrisha kuosha, kama tulivyobainisha huko nyuma. Riwaya za wenye kupinga Hatukatai kuwa katika vyanzo maarufu vya Masunni kuna makundi mawili ya riwaya zenye kupingana na kundi la riwaya tulizozitaja punde tu. Kundi moja la riwaya linasema kuwa Mtukufu Mtume (saww) alikuwa akiosha miguu yake wakati wa udhu, na kundi lingine la riwaya linasema kuwa miguu haioshwi wala kupakwa bali ni kupaka juu ya Khoffu mbili!! Lakini hatupaswi kusahau kanuni ya tasnia ya Misingi ya Sharia inayokubalika, ambayo inasema: “Yanapopingana makundi mawili ya riwaya kuhusu mas’ala moja, ni wajibu kwanza kuondoa mgongano huo kwa kuziweka pamoja dalili za riwaya hizo kwa mujibu wa vipimo vya uelewa wa kijamii. Na kama tusipoweza kufanya hivyo ni wajibu kuzipima kwa Kitabu cha Mwenyezi Mungu ili tuweze kuona ni kundi lipi kati ya hayo mawili lenye kuafikiana na Qur’ani ili tuweze kulichukua, na ni lipi lenye kukhalifu Qur’ani ili tuweze kuliacha.” Na njia hii imethibiti kwa dalili zenye kukubalika. Hivyo tunaweza kuziweka pamoja riwaya za kupaka na kuosha kwa kusema kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) alitekeleza wajibu wa udhu kwa kupaka nyayo zake, kisha akasafisha miguu yake miwili kwa kuiosha bila kitendo cha kuosha kuwa sehemu ya udhu wake, na hivyo 155
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 155
11/25/2014 3:03:49 PM
Ushia: Hoja na Majibu
baadhi ya watu walioona tukio hili wakadhani kuwa kuosha miguu miwili ni sehemu ya matendo ya udhu. Na mtindo huu hutumika sana na Mashia, baada ya kutekeleza wajibu wao wa kupaka miguu yao katika udhu huosha pia miguu kikamilifu ili kuisafisha. Na kwa sababu ya hali ya hewa kuwa na joto kali katika baadhi ya maeneo, kitendo hiki huwa ni cha dharura wanapokuwa wamevaa malapa na si viatu, kwa sababu malapa hayazuii vumbi kikamilifu. Vyovyote iwavyo, kupaka juu ya nyayo mbili ndio wajibu wa kisharia unaopaswa kutekelezwa, nacho ni kitendo chenye kujitegemea kilicho tofauti na kuosha. Ama baadhi ya wanafiqhi kufanya ijtihadi mkabala na maandiko yaliyopatikana, kwa kutoa fatwa ya ulazima wa kuosha miguu miwili, ni kwa sababu wao wanaamini kuwa kuondoa vumbi na uchafu kwenye miguu miwili hakutimii isipokuwa kwa kuosha miguu, na hivyo wanajitenga mbali na wajibu wa kupaka nyayo mbili uliyopatikana kutoka kwenye dhahiri ya Aya iliyopo katika Surat Maidah, kama ilivyokuja katika maneno ya baadhi ya Ulamaa wa Kisunni katika vipengele vilivyotangulia, ambapo walisema: “Ni bora kuosha miguu kwa sababu ya uchafu, na kupaka hakutimizi lengo.� Sharia ni rahisi yenye unafuu Sisi tunaamini kuwa Uislamu ni dini ya kimataifa kwa ajili ya ulimwengu wote na kwa ajili ya zama zote na karne zote, na wakati huo huo wenyewe ni sharia rahisi yenye unafuu kikamilifu. Hebu fikiria kwamba kulazimisha kuosha miguu miwili katika udhu mara tano kwa siku kumesababisha baadhi ya matatizo makubwa ulimwenguni, jam156
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 156
11/25/2014 3:03:49 PM
Ushia: Hoja na Majibu
bo ambalo limepelekea baadhi ya watu kuichukia dini na kuacha udhu na Sala kwa sababu ya taabu, na jambo hilo ni kinyume na asili ya Sharia ambayo ni rahisi na yenye unafuu. Na haya ni matokeo ya ijitihadi zinazofanywa mkabala na maandiko na zilizopelekea kuacha riwaya zinazoelekeza kupaka. Na haiko mbali dhana ya kwamba baadhi ya riwaya zinazoelekeza kuosha ziliwekwa na kuzushwa zama za utawala wa Bani Umaiyyah, hiyo ni kwa sababu katika zama hizo suala la kuweka hadithi za uwongo lilichukua nafasi kubwa kwa sababu ya kiasi kikubwa cha fedha kilichokuwa kikitolewa na Muawiya kwa mtu mwenye kuweka hadithi moja tu ya uwongo, kwa sababu watu wote wanajua kuwa Imam Ali (a.s.) alikuwa miongoni mwa wenye kuunga mkono wajibu wa kupaka miguu miwili, na Muawiya alikuwa akimkhalifu Ali (a.s.) katika kila kitu. Tunakuomba uchunguze kwa makini hadithi hizi mbili: 1.
Imekuja katika Sahih Muslim kutoka kwa Aamir bin Saad bin Abi Waqas, kutoka kwa baba yake, alisema: “Muawiya bin Abu Sufiyan alimwamuru Saad akasema: ‘Ni kitu gani chakuzuia kumtukana Abu Turab?’ Akasema: ‘Kamwe sintomtukana pindi ninapokumbuka mambo matatu aliyoyasema Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) kuhusu yeye, mimi kuwa na moja kati ya hayo ni jambo nilipendalo sana kushinda hata ngamia mwekundu.” Baada ya hapo alitaja kisa cha Vita vya Tabuk na sentensi: “Hivi huridhii kuwa wewe kwangu mimi una cheo cha Harun kwa Musa.” Akabainisha pia kisa cha Vita vya Khaibar na sentensi muhimu aliyoise157
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 157
11/25/2014 3:03:49 PM
Ushia: Hoja na Majibu
ma Mtukufu Mtume (saww) kuhusu Ali (a.s.), na pia akataja kisa cha Maapizano.119 Hakika hadithi hii inaonesha ni kiasi gani Muawiya alivyong’ang’ania kumkhalifu Imam Ali (a.s.) na ni kwa kiwango gani alimkhalifu. 2.
Na kutokana na riwaya mbalimbali tunapata kuwa kuna makundi mawili yalijitolea kuweka hadithi za uwongo katika karne ya kwanza ya historia ya Uislamu:
Kundi la kwanza: Ni kundi la watu ambao kwa muonekano wao wa nje ni watu wema na wenye kujinyima dunia, lakini si watu werevu na makini, walifanya kazi ya kuweka hadithi za uwongo kwa nia ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu, na kati yao ni lile kundi la watu ambao kwa muonekano wa nje ni washika dini, ambao walitunga hadithi za ajabu za uwongo kuhusu fadhila za baadhi ya Sura za Qur’ani ili kuwavutia watu katika kusoma Qur’ani, na wakazinasibisha hadithi hizo na Mtukufu Mtume (saww), na bahati mbaya sana watu hawa hawakuwa wachache. Aalimu maarufu kwa Masunni al-Qurtubiy anasema ndani ya kitabu chake at-Tadhkar: “Hakuna kuwekea maanani riwaya za uwongo kuhusu fadhila za Sura za Qur’ani, ambazo ziliwekwa na waweka hadithi za uwongo. Kitendo hiki kilifanywa na watu wengi kuhusu fadhila za Sura za Qur’ani, bali hata kuhusu fadhila za baadhi ya matendo, waliweka hadithi za uwongo kwa nia ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu kwa kuwavutia watu na kuwashajiisha kutenda 119
Sahih Muslim Juz. 7, Uk. 120. 158
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 158
11/25/2014 3:03:49 PM
Ushia: Hoja na Majibu
amali njema, na inaonekana kuwa hakuna ukinzani baina ya uwongo, kujinyima dunia na Sharia.”120 Katika kitabu hicho hicho kwenye ukurasa uliofuata alQurtubiy ananukuu kutoka kwa al-Hakim na kutoka kwa baadhi ya mashekhe wanahadithi kuwa: “Mmoja kati ya watu wenye kujinyima dunia aliweka hadithi ya uwongo kuhusu fadhila za Qur’ani na Sura zake, kwa nia ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu, na alipoulizwa kwa nini umefanya kitendo hiki? Alijibu: ‘Nimeona watu hawaijali Qur’ani hivyo nikaona niwashajiishe watu zaidi juu ya Qur’ani.’ Walipomwambia: Hakika Mtukufu Mtume (saww) alisema: ‘Yeyote atakayenisemea uwongo basi na ajiandae kuyaweka makalio yake motoni.’ Alijibu: ‘Hakika Mtukufu Mtume (saww) alisema: ‘Yeyote atakayenisemea uwongo…’ na mimi sijasema uwongo dhidi ya Mtukufu Mtume (saww) bali uwongo wangu ulikuwa kwa maslahi ya Mtukufu Mtume (saww).’” Mambo hayakukomea tu katika kiwango hicho alichonukuu al-Qurtubiy, bali kundi lingine la Ulamaa wa Kisunni limenukuu hadithi hizi, na ili kujua zaidi rejea kitabu al-Ghadir, juzuu ya tano, mlango unaozungumzia waongo na waweka hadithi za uwongo. Kundi la pili: Ni kundi la watu ambao walikuwa wanachukua fedha nyingi ili kuweka hadithi za uwongo kwa maslahi ya Muawiya na Bani Umaiyyah, na ili kumkashifu Amirul-Muuminin Ali (a.s.). Miongoni mwa hao ni Samrah bin Jundub ambaye alichukua kutoka kwa Muawiya fedha kiasi cha dirhamu laki nne, ili aweke hadithi ya uwongo 120
At-Tadhkar cha Qurtubiy Uk. 155. 159
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 159
11/25/2014 3:03:49 PM
Ushia: Hoja na Majibu
ya kumkashifu Imam Ali (a.s.) na kumsifu aliyemuuwa Ali (a.s.), na akasema Aya:
ۗﷲ ِ ضا ِ َّ ت َ ْاس َمنْ َي ْش ِري َن ْف َس ُه ا ْبت َِغا َء َمر ِ َوم َِن ال َّن َّ َو ﷲُ َرءُوفٌ ِب ْال ِع َبا ِد َّ ت ْ َمرyuko ْ َمنkwa ا ْب ِت َغا َءauzaye ي َن ْف َس ُه َي ْش ِرyake اس َوم َِنradhi ِ ضا ِ katika َ watu “Naۗ ﷲ nafsi ِ ال َّنkutaka ya Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ni Mpole kwa َّ ْ ٌُوف ﷲ و د ا ب ع ال ب ء ر ِ ِ َ َ َ ُ ِ Abdur-Rahman waja.” (Sura al-Baqarah: 207) iliteremka kumpongeza bin Muljimu ambaye ndiye aliyemuuwa Imam Ali ْ ُ ْ َ ك ق ْول ُه فِي ال َح َيا ِة ال ُّدن َيا َوم َِنNa َ اس َمنْ يُعْ ِج ُب ِ ( ال َّنa.s.). kwamba Aya: ِص ِام َ ﷲ َع َل ٰى َما فِي َق ْل ِب ِه َوھ َُو أَ َل ُّد ْالخ َ َّ َو ُي ْش ِھ ُد ك َق ْولُ ُه فِي ْال َح َيا ِة ال ُّد ْن َيا َ اس َمنْ يُعْ ِج ُب ِ َوم َِن ال َّن ص ِام َ ﷲ َع َل ٰى َما فِي َق ْل ِب ِه َوھ َُو أَ َل ُّد ْال ِخ َ َّ َو ُي ْش ِھ ُد “Na katika watu kuna ambaye kauli yake inakupendeza katika maisha ya duniani, naye humshuhudiza Mwenyezi Mungu kwa yaliyo moyoni mwake, na hali ni hasimu mkubwa kabisa.” (Sura al-Baqarah: 204) iliteremka kumuumbua Ali (a.s.).121
Kwakweli tunajikinga kwa Mwenyezi Mungu na uwongo huu. Hivyo si ajabu kuwa riwaya za kuosha miguu katika udhu ziliwekwa ili kumkhalifu Imam Ali (a.s.). Kupaka juu ya viatu kwa mtazamo wa akili na Sharia!! 121
I bn Abil-Hadid al-Muutazaliy, amenukuu kutoka kwenye Mun’tahal-Maqal, katika ufafanuzi wa hali ya Samrah. 160
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 160
11/25/2014 3:03:49 PM
Ushia: Hoja na Majibu
Kama tulivyoashiria huko nyuma kuwa ndugu zetu hawa wameng’ang’ania kutoruhusu kupaka juu ya nyayo mbili wakati wa udhu na wamewajibisha kuosha, wakati ambapo wanaruhusu kupaka juu ya viatu wakati wa udhu, kwa kutegemea baadhi ya hadithi zilizonukuliwa kutoka kwa Nabii wa Uislamu (s.a.a.w.w.), wakati ambapo hadithi za AhlulBait (as) zinapinga hilo, na kadhalika kuna riwaya zenye kuzingatiwa kutoka kwa Masunni ambazo zimepinga hilo wazi wazi. Ufafanuzi wa hilo ni kwamba wanafiqhi wote wa madhehebu ya Imamiyah kwa kufuata riwaya za Ahlul-Bait (as) wamekubaliana kuwa hairuhusiwi kabisa kupaka juu ya viatu, lakini wengi miongoni mwa wanafiqhi wa madhehebu ya Sunni wanaruhusu hilo moja kwa moja nyumbani au safarini, isipokuwa baadhi yao wanaruhusu hilo kwa sharti kuwepo na dharura. Na hapa kuna maswali kadhaa ya kuuliza: Kwanza: Inakuwaje si ruhusa kupaka juu ya miguu wakati ambapo ni ruhusa kupaka juu ya viatu? Wakati ambapo waliposema inatakiwa kuosha miguu walisema: Hakika ili kuondoa uchafu kuosha ni bora kuliko kupaka. Je kupaka juu viatu vyenye uchafu kunaweza kuwa mbadala wa kuosha? Na pia wapo wengi miongoni mwao waliosema kuwa mtu ana hiyari baina ya kuosha miguu au kupaka juu ya viatu. Pili: Kwa nini mmeacha kushikamana na dhahiri ya Qur’ani Tukufu ambayo inaelekeza kupaka kichwa na miguu, na mmekwenda kwenye kupaka viatu? Tatu: Kwa nini hamchukui riwaya za Ahlul-Bait (as) ambazo zote zinakubaliana kuwa hairuhusiwi kupaka juu ya 161
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 161
11/25/2014 3:03:49 PM
Ushia: Hoja na Majibu
viatu, watu ambao Mtume (saww) aliwafanya njia ya uokovu sambamba na Kitabu cha Mwenyezi Mungu? Nne: Ni sahihi kwamba kuna riwaya zimepokewa kutoka kwa Mtukufu Mtume (saww) zinasema kuwa yeye (saww) alipaka juu ya viatu, lakini mkabala na hizo tunazo riwaya nyingine zenye kukubalika ambazo zinasema kuwa hakika Mtukufu Mtume (saww) alipaka miguu miwili, hivyo basi ni kwa nini haturejei na kukimbilia kwenye Aya ya Qur’ani pindi riwaya zinapogongana, na kuifanya Qur’ani kuwa rejea na hakimu pindi zinapopingana riwaya hizi? Kwa kweli kila tunapozama zaidi katika mas’ala hii tunazidi kupata mshangao, kwani tunasoma katika kitabu al-Fiqhi Alal-Madhahib al-Arba’ah kuwa: “Hakika kupaka juu ya Khoffu mbili ni wajibu katika hali ya dharura na udhuru, ama pasipo na dharura ni ruhusa, na kuosha ni bora kuliko kupaka.” Na baada ya hapo ananukuu kutoka kwa Mahanbali kauli yao isemayo: “Hakika kupaka juu ya Khoffu ni bora kuliko kuzivua na kuosha miguu, kwa sababu Mwenyezi Mungu anapenda watu wachukue ruhusa yake ili wahisi neema yake juu yao, hivyo wamshukuru kwa neema hiyo. Na baadhi ya Mahanafi wameafiki juu ya hili.”122 Baada ya hapo akadai kuwa kupaka juu ya Khoffu mbili kumethibiti kwa hadithi nyingi sahihi zinazokaribia kiwango cha kuwa mutawatiri.123 Na la kuvutia zaidi ni kwamba aligusia kwa undani zaidi katika kitabu hiki masharti ya aina hii ya Khoffu mbili, na pia kadiri inayopaswa kupakwa na muda wake, mambo 122
al-Fiqhi Alal-Madhahib al-Arba’ah Juz. 1, Uk. 135.
123
al-Fiqhi Alal-Madhahib al-Arba’ah Juz. 1, Uk. 136. 162
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 162
11/25/2014 3:03:49 PM
Ushia: Hoja na Majibu
yaliyo sunna katika kupaka huko na yaliyo makuruhu, yanayobatilisha kupaka juu ya Khoffu mbili na hukumu za Khoffu mbili, kinachovaliwa juu ya Khoffu mbili na aina zake, na je ni wajibu ziwe zimetengenezwa kwa ngozi au hata zisizotengenezwa kwa ngozi zinatosha pia, na hukumu za Khoffu zilizo wazi na zisizo wazi… mambo ambayo yamechukua sehemu kubwa ya kitabu hiki.124 Tano: Kwa nini riwaya zinazoonesha kupaka juu ya viatu hatuzitafsiri kuwa zinahusu wakati wa dharura au safarini au vitani, au katika maeneo ambayo haiwezekani kuvua viatu, au iwapo kufanya hivyo kutapelekea taabu kubwa? Maswali haya hayana majibu isipokuwa hukumu zilizotangulia ambazo hazijafanyiwa utafiti na ambazo zinasababisha fujo katika mas’ala ndogo na nyepesi. Kwani siku moja nilikuwa katika uwanja wa ndege wa Jidah, na nikamuona mtu mmoja kati ya ndugu zetu hawa alipokwenda kuchukua udhu, aliosha miguu yake vizuri badala ya kupaka, mara akaja mwingine, yeye aliosha uso wake na mikono yake, kisha alipaka kwa mkono wake juu ya viatu vyake, na alikwenda kusali. Hilo likanishangaza, nikasema: Je inawezekana kweli kwa mtu mwenye hekima kama Mtukufu Mtume (saww) kutoa amri kama hizi ambazo haziwezi kufasirika? Baada ya maswali haya ni lazima tutaje sasa dalili za msingi, na katika kutoa dalili hizi ndipo tutagundua chanzo cha msingi cha fatwa hizi, na kadhalika njia ya kutatua tatizo hili inayokubalika kiakili. Kwa kweli dalili ni kundi la riwaya ambazo tunaweza kuzigawa katika makundi kadhaa: 124
al-Fiqhi Alal-Madhahib al-Arba’ah Juz. 1, Uk. 135 - 147. 163
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 163
11/25/2014 3:03:49 PM
Ushia: Hoja na Majibu
a.
Riwaya ambazo zimenukuliwa kutoka kwenye vyanzo vya Ahlul-Bait (as) na ambazo zinakataa kabisa kupaka juu ya viatu, na kwa mfano tu riwaya hizo ni:
1.
Sheikh Tusiy ananukuu kutoka kwa Abu Wardi, amesema: “Nilimwambia Abu Ja’far (as): Kwa hakika Abu Dhabyanu amenihadithia kuwa alimuona Ali (a.s.) alimwaga maji kisha alipaka juu ya Khoffu mbili, akasema: ‘Amesema uwongo Abu Dhabyani, hivi haijakufikia kauli ya Ali (a.s.) kwenu nyinyi, kwamba kitabu kimetangulia Khoffu mbili.’ Nikasema: Je kuna ruhusa katika Khoffu mbili? Akasema: ‘Hapana isipokuwa kwa adui wamchelea, au kwa theluji unayohofia juu ya miguu yako.’”125 Kutokana na hadithi hii tunapata mambo kadhaa:
Kwanza: Hakika lililo mashuhuri katika riwaya za Masunni ni kwamba Imam Ali (a.s.) haruhusu kupaka juu ya Khoffu mbili, ikiwa hivi ndivyo inakuwaje Abu Dhabyanu na watu mfano wake wanajipa ujasiri wa kumzushia uwongo Imam Ali (a.s.), je kuna njama yoyote? Jibu la swali hili litabainika hapo baadaye. Pili: Imam Ali (a.s.) anaelekeza njia na anasema: Qur’ani Tukufu hutangulizwa kabla ya kila kitu wala hakitangulizwi kitu kingine kabla ya Qur’ani, hivyo tukiona riwaya inakwenda kinyume na Qur’ani ni lazima kuiletea tafsiri nyingine, hii ni pamoja na kwamba Aya ya udhu katika Surat Maidah ni miongoni mwa Aya ambazo bila shaka hazikufutwa. Tatu: Imam al-Baqir (a.s.) anaashiria kuwa riwaya zinazoelekeza kupaka juu ya Khoffu mbili zinapaswa 125
Tahdhib Juz. 1, Uk. 347, Hadithi ya 1092. 164
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 164
11/25/2014 3:03:49 PM
Ushia: Hoja na Majibu
kutafsiriwa kuwa ni za wakati wa dharura, kama wakati wa baridi kali ambayo mtu anakhofia isije ikadhuru miguu yake. 2.
Marehemu as-Saduq, ndani ya kitabu chake Man’la Yahdhuruhul-Faqihu ananukuu hadithi kutoka kwa AmirulMuuminin (a.s.) kuwa amesema: “Hakika sisi AhlulBaiti (as) hatupaki juu ya Khoffu mbili, hivyo yeyote ambaye ni miongoni mwa wafuasi wetu atufuate sisi na achukue mwenendo wetu.”126
3.
Katika hadithi nyingine imenukuliwa ibara ya ajabu kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s.), anasema: “Yeyote atakayepaka juu ya Khoffu mbili atakuwa amemkhalifu Mwenyezi Mungu, Mtume wake na Kitabu chake, na udhu wake hautakuwa umetimia, na Sala yake haitatosheleza.”127
Ninapozitazama riwaya zilizopokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s.) kuhusu kutoruhusiwa kupaka juu ya Khoffu mbili, zinanikumbusha maneno ya Fakhru Razi anapoelezea mas’ala ya kuisoma Bismillahi kwa sauti na kwa kuficha, ambapo kuna kundi linasema ni lazima kuisoma kwa kuficha huku Imam Ali (a.s.) akiona ni lazima kuisoma kwa sauti, Fakhru Razi anasema: “Yeyote atakayemfanya Ali Imam wa dini yake basi ajue ameshikamana na kishikio madhubuti katika dini yake na nafsi yake.”128 Licha ya hali hii hebu sasa tuendelee kutaja riwaya nyingine. 126
Man’la Yahdhuruhul-Faqihu Juz. 4, Uk. 415.
127
Wasailus-Shia Juz. 1, Uk. 279.
128
Tafsirul-Kabir ya Fakhru Razi Juz. 1, Uk. 207. 165
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 165
11/25/2014 3:03:49 PM
Ushia: Hoja na Majibu
b.
Riwaya ambazo zinaruhusu kupaka juu ya Khoffu mbili zimegawanyika sehemu mbili:
Kundi la kwanza: Ni riwaya za moja kwa moja zisizo na sharti, kama vile riwaya ya kuvushwa (isiyo na mlolongo wote wa wapokezi) ya Said bin Abi Waqas kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) kuhusu kupaka juu ya Khoffu mbili, amesema: “Hakuna ubaya kuchukua udhu kwa kupaka juu ya Khofu mbili.”129 Na katika hadithi nyingine ambayo kainukuu al-Bayhaqiy kutoka kwa Abu Hudhayfah, amesema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) alikwenda kwenye jalala la watu akajisaidia haja ndogo wima, halafu aliomba maji. Nilimpelekea maji, alitawadha na kupaka Khoffu zake.” Na al-Bayhaqiy ameeleza kuwa hadithi hii ameipokea Bukhari ndani ya Sahih kutoka kwa Adam bin Abi Abbas, na ameipokea pia Muslimu kwa njia nyingine kutoka kwa A’mashi.130 Sisi tuna uhakika kuwa hadithi hii imewekwa na baadhi ya wanafiki ambao wanataka kumshusha hadhi na utukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww), na hivyo kwa sababu ya waandishi kukosa umakini waliandika hadithi hii katika vitabu mbalimbali vyenye kutegemewa kwa Masunni mfano wa kitabu Sahih Bukhari na Sahih Muslim. Hivi kweli mtu tu wa kawaida mwenye kujiheshimu anaweza kufanya kitendo kama hiki kwa njia isiyofaa na ambayo kalamu inaona haya kuifafanua? Na linalosikitisha zaidi ni kuwepo riwaya kama hizi ndani ya vitabu Sahih, na ambavyo bado daima vinatumika kama dalili!131 129
As-Sunan al-Kubra Juz. 1, Uk. 269.
130
As-Sunan al-Kubra Juz. 1, Uk. 270.
131
Na la kusikitisha kuliko yote ni baadhi ya Masheikh kwa kujua au kutokujua 166
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 166
11/25/2014 3:03:49 PM
Ushia: Hoja na Majibu
Vyovyote iwavyo ni kuwa riwaya hizi na mfano wake hazijaweka sharti lolote wala sifa yoyote au mpaka wowote katika kupaka juu ya Khoffu mbili. Kundi la pili: Riwaya hizi zinaruhusu kupaka juu ya Khoffu mbili wakati wa dharura tu, mfano wa riwaya hizo ni kama hii aliyoipokea Miqdam bin Sharihu kutoka kwa Aisha, anasema: “Nilimuuliza (Aisha) kuhusu kupaka juu ya Khoffu mbili. Akasema: ‘Nenda kwa Ali (a.s.) kwani yeye alifuatana na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) safarini.’ Nilikwenda kwa Ali (a.s.) nikamuuliza kuhusu kupaka, akasema: ‘Tulikuwa tunaposafiri pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) alikuwa anatuamrisha kupaka juu ya Khoffu zetu.”’132 Taabiri hii inaashiria wazi wazi kuwa kupaka juu ya Khofu mbili ilikuwa inahusu mazingira ya dharura, kwa sababu anasema: Tulikuwa tunaposafiri anatuamrisha kufanya hivyo. Na kuna riwaya nyingine mfano wa hii. Na baada ya kuchunguza makundi ya riwaya zilizopo katika vyanzo maarufu na vya kutegemewa vya Masunni, na kabla ya kutoa hukumu iliyotangulia, yanabainika mambo yafuatayo: Kwanza: Kulingana na kanuni maarufu katika Elimu ya Misingi ya Sharia (kanuni na kuondoa mgongano baina uchafu wa riwaya hizi na dosari zake bado mpaka leo wanazitumia kama dalili ya kuthibitishia matakwa yao, maudhui zao na mijadala yao. Na si ajabu kumsikia Shekhe bila aibu wala haya au kuona vibaya akitoa mawaidha na kutaja hadithi hizi kwa sauti nzuri na hamasa ya juu eti ataka kuthibitisha mafunzo au utukufu na fadhila za Swahaba fulani aliyepokea hadithi husika na daraja lake kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)! Ewe Mola Wangu kama ushekhe ndio huu basi nifishe kabla haujanifikia! – Mtarjumi. 132
As-Sunan al-Kubra Juz. 1, Uk. 272. 167
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 167
11/25/2014 3:03:49 PM
Ushia: Hoja na Majibu
ya maneno yasiyofungwa na sharti lolote na yale yenye kufungwa na sharti, ambapo ni kuyafunga kwa sharti na mpaka yale yasiyo na masharti na mipaka.) ni lazima kuzitafsiri riwaya zinazoruhusu kupaka juu ya Khoffu mbili kuwa zinahusu wakati wa dharura (sharti na mpaka), kama vile safarini au katika uwanja wa vita au sehemu nyingine kama hizo. Na la kuvutia ni kwamba al-Bayhaqiy ametenga mlango makhususi wenye kujitegemea kuhusu kipindi cha muda unaoruhusiwa kupaka juu ya Khoffu mbili, na akabainisha kupitia baadhi ya riwaya kuwa ni muda wa siku tatu safarini na siku moja nyumbani.133 Hivi riwaya zote hizi si ni dalili bayana juu ya ukweli huu? Nao ni kwamba riwaya zote ambazo zimetaja kupaka juu ya Khoffu mbili zinahusu wakati wa dharura, ama katika hali ya kawaida hakuna maana ya kutokuvua Khoffu mbili na kutokupaka miguu miwili. Ama wasemalo baadhi kuwa kufanya hivyo ni ili kuuondolea umma uzito na taabu, hayo ni maneno yasiyokubalika kwa mwenye akili timamu, kwa sababu kuvua Khoffu mbili za kawaida hakuhitaji juhudi. Pili: Ukiwa makini na riwaya mbalimbali zilizonukuliwa katika vyanzo maarufu vya madhehebu ya Ahlul-Bait (as) na ya Sunni, utaona Imam Ali (a.s.) anasema kuwa kupaka huku kulifanyika kabla ya kuteremka Aya ya sita ya Sura Maidah inayohusu udhu, ama baada ya Aya hiyo kuteremka haikuwa ni ruhusa pia kupaka juu ya Khiffu mbili, hata katika vita na safarini, kwa sababu katika hali ambayo ni vigumu kuvua Khoffu mbili mbadala wa udhu ni tayamamu, kwa sababu 133
As-Sunan al-Kubra Juz. 1, Uk. 275 na 276. 168
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 168
11/25/2014 3:03:49 PM
Ushia: Hoja na Majibu
amri ya tayamamu imekuja mwishoni mwa Aya kwa namna ya jumla. Tatu: Ikiwa baadhi ya waliokuwepo waliona Mtukufu Mtume (saww) alipaka juu ya Khoffu mbili, basi inawezekana kuwa viatu vya Mtukufu Mtume vilikuwa na uwazi na mpasuko unaomwezesha kupaka juu ya nyayo. Marehemu Sheikh as-Saduq ambaye ni mmoja kati ya wanahadithi maarufu kwa Mashia, anasema katika kitabu chake maarufu Man’la Yahdhuruhul-Faqihu kuwa: “Hakika Najashi alimpa Mtukufu Mtume (saww) zawadi ya Khoffu, na sehemu za juu za unyayo za Khofu hizo zilikuwa na uwazi, hivyo Mtukufu Mtume (saww) akapaka juu ya miguu yake huku akiwa kavaa Khoffu zake, hivyo watu wakasema kuwa yeye (saww) amepaka juu ya Khoffu zake.”134 Bila ya kung’amua kuwa yeye (saww) hakupaka juu ya Khoffu zenyewe bali juu ya miguu yake iliyo na Khoffu. Al-Bayhaqiy ambaye ni mwanahadithi maarufu, katika kitabu chake as-Sunan al-Kubra ametenga mlango chini ya anwani isemayo Mlango unaozungumzia Khoffu ambayo Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) alipaka juu yake: “Na kutokana na baadhi ya hadithi za mlango huu tunapata kuwa…” “Na hata Khoffu za Muhajirina na Ansari pia nazo zilikuwa zimepasuliwa na kuwekewa uwazi.”135 Na kutokana na maelezo yaliyotangulia punde inaonekana watu hawa walikuwa wakipaka pia juu ya nyayo zao. Na la kushangaza katika mada hii ni kwamba wapokezi wa hadithi za kupaka juu ya Khoffu mbili ni watu ambao 134
Man’la Yahdhuruhul-Faqihu Juz. 1, Uk. 48.
135
As-Sunan al-Kubra Juz. 1, Uk. 283. 169
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 169
11/25/2014 3:03:49 PM
Ushia: Hoja na Majibu
walipata heshima ya kumhudumia Mtukufu Mtume (saww), lakini Imam Ali (a.s.) daima alikuwa mbele ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww), na kamwe hakukubali maneno yenye kuoana na hadithi zilizo maarufu kwa Masunni. Na la kushangaza zaidi ni maneno aliyonukuu Aisha ambaye mara nyingi alikuwa karibu na Mtukufu Mtume (saww), aliposema: “Kukatika nyayo zangu mbili hizi ni kitu nikipendacho zaidi kuliko kupaka juu ya Khoffu mbili.”136 Hitimisho la mwisho la mada hii 1.
Imebainika kwamba Qur’ani Tukufu inaona kuwa kupaka juu ya miguu miwili ndio wajibu wa kisharia wa msingi katika udhu, kadhalika Aya tukufu ya udhu iliyopo katika Surat Maidah na riwaya zote za Ahlul-Bait (as), ikiwemo pia fatwa za tabiina, zote zimeafikiana juu ya hilo.
2.
Wanafiqhi wengi wa Kisunni wanaona kuwa wajibu wa msingi katika udhu ni kuosha miguu, lakini wengi miongoni mwao wanaona kuwa inaruhusiwa kupaka juu ya Khoffu mbili katika hali ya hiyari, lakini baadhi yao wanaona inaruhusiwa wakati wa dharura tu.
3.
Hakika mgongano na kupingana kwa riwaya zinazohusu kupaka juu ya Khoffu mbili, riwaya zilizomo katika vyanzo vya Masunni, kunamtia shaka yeyote miongoni mwa wahakiki, kwani baadhi zinaruhusu moja kwa moja bila sharti wala mipaka kupaka juu ya Khoffu mbili, na nyingine zinaweka sharti la wakati wa
136
Al-Mabsut cha Sarkhasiy Juz. 1, Uk. 98. 170
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 170
11/25/2014 3:03:49 PM
Ushia: Hoja na Majibu
dharura tu, kwa kuainisha kiwango maalumu, ambapo safarini ni siku tatu na nyumbani ni siku moja. 4.
Hakika njia bora ya kuondoa mgongano baina ya riwaya hizi ni kusema kuwa wajibu wa asili katika udhu ni kupaka juu ya miguu, na kwa mujibu wa itikadi yao ni kuosha miguu, lakini kama kuna dharura kama vile vita, safari ngumu au kuna ugumu katika kuvua Khoffu mbili, hapo wajibu unakuwa ni kupaka juu ya Khofu mbili, kama ilivyo katika udhu wa bandeji.
171
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 171
11/25/2014 3:03:50 PM
Ushia: Hoja na Majibu
MADA YA TISA NAFASI YA BISMILLAHI KATIKA SURA AL-HAMDU
P
indi wafuasi wa Ahlul-Baiti (as) wanapopata heshima ya kuhiji Nyumba Takatifu ya Mwenyezi Mungu, na kwa ajili ya kulinda umoja wa Waislamu kama walivyoelekezwa na Ahlul-Baiti (as), hushiriki pamoja na Masunni katika Sala za jamaa, ili wapate fadhila za kusalia ndani ya Msikiti Mtakatifu na Msikiti wa Mtume (saww), na jambo la kwanza kabisa ambalo huwashtua ni kitendo cha Maimamu wa Sala za jamaa kutokusoma Bismillahi Rahman Rahim mwanzoni mwa Surat al-Hamdu, au huisoma kwa moyo hata katika Sala za jahara mfano Sala ya Subhi, Maghrib na Isha. Wakati ambapo wanaona Sura al-Hamdu ina Aya saba katika misahafu yote iliyopo Makka na ambayo aghlabu kuchapishwa huko, huku Bismillahi ikiwa ni sehemu ya al-Hamdu. Kwa kweli hili huwashangaza sana, hujiuliza kwa nini Aya muhimu katika Qur’ani ambayo ni Bismillahi inawekwa katika hali hii?!! Na mshangao wao huongezeka pindi tunapowanukulia kisa cha kutofautiana kwa riwaya zinazohusu Bismillahi kwa Masunni, hivyo ni lazima kwanza tunukuu fatwa kuhusu mas’ala hii kisha baadaye ndipo tunukuu riwaya zilizopokewa kuhusu mada hii. Kwa ujumla wanafiqhi wa Kisunni wamegawanyika makundi matatu kuhusu mas’ala hii: 172
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 172
11/25/2014 3:03:50 PM
Ushia: Hoja na Majibu
Kundi la kwanza: La kwanza linasema ni wajibu kusoma Bismillahi wakati wa kuanza kusoma Surat al-Hamdu, hivyo inapasa kusomwa kwa jahara katika Sala za jahara, na itasomwa kwa moyo katika Sala za kusoma kwa moyo. Kauli hii ni ya Imam Shafi na wafuasi wake. Kundi la pili: Linasema ni wajibu kuisoma kwa moyo wakati wote. Kauli hii ni ya Mahanbali, wafuasi wa Ahmad bin Hanbal. Kundi la tatu: Linasema kuwa haisomwi kabisa. Kauli hii ni ya wafuasi wa Imam Malik, na iko karibu na kauli waliyosema wafuasi wa Abu Hanifa. Na ibara ya Ibn Qudamah mwanafiqhi mashuhuri kwa Masunni, iliyomo ndani ya kitabu chake al-Mughniy ni: “Hakika kusoma Bismillahi Rahman Rahim mwanzoni mwa al-Fatiha ni sharia, na pia mwanzoni mwa kila sura kwa kauli ya wanazuoni wengi. Malik na al-Awzaiy wamesema: ‘Hapasi kuisoma mwanzoni mwa Sura al-Fatiha…na wala hazitofautiani riwaya kutoka kwa Ahmad kwamba kuisoma kwa jahara si sunna…. Na imepokewa kutoka kwa Atau, Taus, Mujahid na Said bin Jubayri kuwa yapasa kuisoma kwa jahara, nayo ndio madhehebu ya Shafi.”137 Ambapo katika ibara hii amenukuu kauli tatu. Na katika tafsiri al-Manar imepokewa kutoka kwa Wahbah Zahiliy kwamba: “Mamaliki na Mahanafi wamesema kuwa Bismillahi si Aya katika Sura al-Fatiha wala katika Sura nyingine isipokuwa katika Surat Naml…. Isipokuwa ni kwamba Mahanafi wamesema kuwa mwenye kusali binafsi (si katika jamaa) atasoma Bismillahi kwa moyo katika 137
Al-Mughniy cha Ibn Qadamah Juz. 1, Uk. 521. 173
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 173
11/25/2014 3:03:50 PM
Ushia: Hoja na Majibu
kila rakaa asomapo al-Fatiha…. Na Mashafi na Mahanbali wamesema kuwa: Bismillahi ni Aya katika Sura al-Fatiha na ni wajibu kuisoma katika Sala, isipokuwa ni kwamba Mahanbali wamesema kama walivyosema Mahanafi kuwa ataisoma kwa moyo na si kwa jahara. Na Mashafi wamesema: Ataisoma kwa moyo katika Sala za kuficha na ataisoma kwa jahara katika Sala za jahara.”138 Kutokana na maelezo yaliyotangulia kauli ya Shafi ndio iliyo karibu zaidi na kauli ya wanafiqhi wa Kishia kuliko kauli nyingine, isipokuwa ni kuwa watu wetu wanaona kuwa ni mustahabu kusoma Bismillahi kwa jahara katika Sala zote, na wameafikiana kuwa ni wajibu kuisoma katika Sura al-Hamdu na kwamba yenyewe ni sehemu ya Sura zote. Na kwa kweli mtafiti anapatwa na mshangao pindi anapoona kwamba Mtukufu Mtume (saww) ambaye aliishi baina yao muda wa miaka ishirini na tatu, mara nyingi alikuwa akisali jamaa pamoja nao, na wao wanasikia asemacho katika Sala zake, lakini baada ya muda mfupi wao wanatofautiana sana kuhusu namna ya Sala yake, baadhi hawaruhusu kusoma Bismillahi huku wengine wakisema ni wajibu, wengine wanaona ni wajibu kuisoma kwa moyo huku wengine wakisema ni wajibu kuisoma kwa jahara katika Sala za jahara!!! Hivi huoni kuwa tofauti hii ya ajabu na isiyotegemewa inaashiria kuwa mas’ala hii haikuwa ya kawaida, na kwamba kuna kikundi cha kisiasa kinafanya kazi kwa siri ya kuweka hadithi za uwongo zenye kupingana na kugongana na kisha kuzinasibisha na Mtukufu Mtume (saww)? Hakika tutafafanua hilo hapo baadaye. 138
Tafsirul-Manar Juz. 1, Uk. 46. 174
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 174
11/25/2014 3:03:50 PM
Ushia: Hoja na Majibu
Bukhari katika Sahih yake anapokea hadithi ambayo kupitia hadithi hiyo tunaweza kufichua njama hizo zilizopangwa, anasema: “Mutarifu ananukuu kutoka kwa Imran bin Haswin kauli yake: Wakati Ali (a.s.) alipokuwa akisali huko Basra, nilisema: Mtu huyu ametukumbusha Sala ambayo tulikuwa tunaisali pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww).”139 Ndiyo, imebainika kuwa wao walibadili kila kitu hadi Sala. Shafi katika kitabu chake maarufu kwa jina la al-Ummu ananukuu kutoka kwa Wahbi bin Kisani kuwa: “Sunnah zote za Mtume wa Mwenyezi Mungu zilibadilishwa hadi Sala.”140 Kuisoma Bismillahi kwa jahara, kwa mujibu wa hadithi za Mtume (saww) Kuna makundi mawili ya riwaya zinazohusu mas’ala hii, katika vitabu maarufu na vya kutegemewa vya Masunni, nazo ni zenye kutofautiana kabisa, na jambo hili ndilo lililopelekea fatwa zao kutofautiana. Na cha kustaajabisha zaidi katika jambo hili ni kwamba mpokezi mmoja ananukuu riwaya kadhaa zenye kupingana na kugongana, hilo tutaliona kwenye hadithi zitakazofuata. Kundi la kwanza: Ni la riwaya ambazo zinasema Bismillahi ni sehemu ya Sura al-Hamdu, bali zinaona ni mustahabu kuisoma kwa jahara au ni wajibu kuisoma. Katika kundi hili tutatosheka kwa kutaja riwaya tano kutoka kwa wapokezi watano maarufu: 1.
Ad-Darqutniy ndani ya kitabu chake as-Sunan ananukuu hadithi kutoka kwa Amirul-Muuminin Ali (a.s.) mwenye
139
Sahih Bukhari Juz. 1, Uk. 190.
140
Al-Ummu Juz. 1, Uk. 269. 175
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 175
11/25/2014 3:03:50 PM
Ushia: Hoja na Majibu
cheo kikubwa na kinachojulikana kwa watu wote, ambaye aliandamana na Mtukufu Mtume (saww) safarini, nyumbani, katika siri na katika dhahiri, anasema: “Mtukufu Mtume (saww) alikuwa akisoma Bismillahi Rahmani Rahim kwa jahara ndani ya Sura zote mbili.”141 2.
al-Hakim ananukuu katika al-Mustadrak kutoka kwa Anas bin Malik mtumishi maalumu wa Mtukufu Mtume (saww) tangu ujana wake, anasema: “Nilisali nyuma ya Mtume (saww) na nyuma ya Abu Bakr na nyuma ya Umar na nyuma ya Uthman na nyuma ya Ali, na wote walikuwa wakisoma Bismillahi Rahmani Rahim kwa jahara.”142
3.
Ad-Darqutniy ananukuu kutoka kwa Aisha ambaye katika hali ya kawaida alikuwa na Mtume (saww) usiku na mchana, anasema: “Hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) alikuwa akisoma Bismillahi Rahmani Rahim kwa jahara.”143
4.
Vitabu Sahihi vinanukuu kutoka kwa Abu Huraira ambaye ni mpokezi maarufu wa ndugu zetu Masunni – ambapo vitabu Sahihi na vinginevyo vyenye kutegemewa hunukuu riwaya zake nyingi – kuwa anasema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) alikuwa akisoma Bismillahi Rahmani Rahim kwa jahara katika Sala.” Hadithi hii imepatikana ndani ya vitabu vitatu maarufu:
141
S unan ad-Darqutniy Juz. 1, Uk. 302. Na hadithi hii hii kainukuu Suyutiy ndani ya tafsiri yake ad-Durul-Manthur Juz. 1 Uk. 22.
142
Mustadrakus-Sahihayn Juz. 1, Uk. 232.
143
Tafsiru ad-Durrul-Manthur Juz. 1, Uk. 23. 176
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 176
11/25/2014 3:03:50 PM
Ushia: Hoja na Majibu
as-Sunan al-Kubra144, Mustadrakul-Hakim145 na Sunan adDarqutniy146. 5. Na katika hadithi nyingine: Hakika pia Jibril (as) alipotaka kumfunza Sala Mtume (saww) alisoma Bismillahi kwa sauti ya juu, ambapo Ad-Darqutniy ananukuu kutoka kwa Nuuman bin Bashir kuwa alisema: “Hakika Mtume (saww) alisema: ‘Jibril alinisalisha kwenye Kaaba, akasoma Bismillahi Rahmani Rahim kwa jahara.”147 Na riwaya nyingine nyingi. Na la kuvutia ni kwamba baadhi ya Ulamaa maarufu ambao wametaja hadithi zinazoelekeza kusoma Bismillahi kwa jahara wametamka wazi wazi mwishoni mwa baadhi ya riwaya kuwa wapokezi wa hadithi hizo wote ni watu waaminifu, kama alivyosema al-Hakim ndani ya al-Mustadrak. Na hapa ni lazima tuongezee kuwa Bismillahi katika vitabu vya Fiqhi na hadithi vya madhehebu ya Ahlul-Baiti (as) imetajwa kwa anwani yake kuwa ni sehemu ya Sura alHamdu, na riwaya zake ni mutawatiri, na riwaya nyingine zimetamka bayana kuwa inapasa kuisoma Bismillahi kwa jahara. Na ili kuzijua vizuri riwaya hizi rejea kitabu WasailusShiah,148 na pia kuhusu hili zimenukuliwa riwaya nyingi makumi kwa makumi kutoka kwa Ahlul-Baiti (as), katika vitabu mfano wa al-Kafiy, Uyunu Akhbarur-Ridhaa (as) na Mustadrakul-Wasail.149 144
As-Sunan al-Kubra Juz. 2, Uk. 47.
145
Mustadrakus-Sahihayn Juz. 1, Uk. 208.
146
Sunan ad-Darqutniy Juz. 1, Uk. 306.
147
Sunan ad-Darqutniy Juz. 1, Uk. 309.
148
asailus-Shiah, Milango inayohusu kusoma katika Sala, mlango wa 11, 12, 21, W na 22.
149
Mustadrakul-Wasail, Milango inayohusu kusoma Qur’ani ndani ya Sala. 177
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 177
11/25/2014 3:03:50 PM
Ushia: Hoja na Majibu
Hivi si inapasa sasa kuifuata hadithi ya vizito viwili ambayo imenukuliwa na makundi yote mawili Sunni na Shia kutoka kwa Mtukufu Mtume (saww), na ambayo inatamka bayana wajibu wa kushikamana na Qur’ani na Ahlul-Bait (as) ili watu wasipotee baada yake – na kukimbilia kwa Ahlul-Bait (as) pindi tunapokutana na mas’ala kama haya yenye tofauti ili tuweze kuwafuata katika lile watakalotuelekeza?!! Kundi la pili: Ni la riwaya ambazo hazioni kuwa Bismillahi ni sehemu ya Sura al-Hamdu, na kwazo wanazuia kuisoma jahara, miongoni mwa riwaya hizo ni: 1.
Tunasoma katika Sahih Muslim hadithi aliyoinukuu kutoka kwa Qatadah kuwa Anas alisema: “Nilisali pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu, pamoja na Abu Bakr, pamoja na Umar na pamoja na Uthman, na sikumsikia yeyote kati yao akisoma Bismillahi Rahmani Rahim.”150 Tazama, hadithi hii haijataja kusoma kwa Ali (a.s.)!
Kwa kweli ni jambo linalotia shaka, kwamba atajwe mtu makhususi –mfano wa Anas - waziwazi, kuwa yeye alisali nyuma ya Mtukufu Mtume (saww) na nyuma ya Makhalifa watatu wa mwanzo na nyuma ya Ali (a.s.), na kwamba wote walisoma Bismillahi kwa sauti ya juu kabisa, kisha sehemu nyingine aseme kuwa: Yeye alisali nyuma ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) na nyuma ya Makhalifa watatu wa mwanzo na kuwa hakuna hata mmoja kati yao aliyesoma Bismillahi. Vipi kuhusu kusoma kwao kwa sauti ya juu!! 150
S ahih Muslim Juz. 2, Uk. 12, Mlango unaozungumzia hoja ya mwenye kusema: Bismillahi haisomwi jahara. 178
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 178
11/25/2014 3:03:50 PM
Ushia: Hoja na Majibu
Hivi si inatosha kwa mtu mwenye kutafakari kugundua kuwa mikono ya wawekaji wa hadithi za uwongo ilifanya kazi ya kuweka hadithi ya pili ili kubatilisha hadithi ya kwanza – ni hivi karibu tu itabainika dalili yake – na wakainasibisha hadithi hiyo na Anas, na hawakutaja jina la Ali (a.s.) ili hila hii isifichuke, kwa sababu watu wote wanajua kuwa Imam Ali (a.s.) na wafuasi wake huisoma Bismillahi kwa jahara. 2.
Al-Bayhaqiy ananukuu kutoka kwa Abdullah bin Maghfalu amesema: “Baba alinisikia nikisoma: Bismillahi Rahmani Rahim; akasema: ‘Ewe mwanangu mpendwa, umezua bidaa? Nilisali nyuma ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) na Abu Bakr na Umar na Uthman, na sikumsikia hata mmoja kati yao akisoma Bismillahi Rahmani Rahim kwa jahara.”151 Na hapa pia tunaona jina la Imam Ali (a.s.) halijatajwa.
3.
Tunasoma katika al-Muujam al-Wasit cha Tabaraniy kutoka kwa Ibnu Abbas kuwa alisema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) alikuwa asomapo Bismillahi Rahmani Rahim, mushrikina hutetemeka na kusema: ‘Muhammad anataja Mungu wa Al-Yamama.’ Na Musaylamah alikuwa akijiita Rahmani, hivyo iliposhuka Aya hii Mtume akaamrisha isisomwe kwa jahara.”?!! Bila shaka katika riwaya hii athari za uzushi ziko bayana, hiyo ni kwa sababu:
Kwanza: Hakika neno Rahman katika Qur’ani halijatajwa katika Bismillahi tu, bali limetajwa mara hamsini na sita sehemu mbalimbali, na katika Sura Mariyam limerudiwa 151
As-Sunan al-Kubra Juz. 2 Uk. 52. 179
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 179
11/25/2014 3:03:50 PM
Ushia: Hoja na Majibu
katika Aya kumi na sita, hivyo kwa mujibu wa hadithi hiyo ni wajibu pia kutokusoma Sura nyingine za Qur’ani ili Sura hizo zisiwe sehemu ya dhihaka za mushrikina. Pili: Mushrikina wanadhihaki Aya zote za Qur’ani, na kwa ajili hii ndio maana tunasoma katika Aya mbalimbali ndani ya Qur’ani Tukufu ikiwemo kauli ya Mwenyezi Mungu:
ﷲ ِ ب أَنْ إِ َذا َس ِمعْ ُت ْم آ َيا ِ َو َق ْد َن َّز َل َع َل ْي ُك ْم فِي ْال ِك َتا ِ َّ ت ُي ْك َف ُر ِب َھا َويُسْ َتھ َْزأ ُ ِب َھا َف َال َت ْق ُع ُدوا َم َع ُھ ْم َح َّت ٰى ﷲ ُوا فَع َل ْي ض َل َيو َُقخ ْدو َن َّز ِ ب أَنْ إِ َذا َس ِمعْ ُت ْم آ َيا ِ ث ْال َ ِغك َيتا ِْر ِه ِ َّ ت ٍ ِي ُك ْ َمحدفِيِي ُھ ْم َح َّت ٰىwateremshia َف َال َت ْق ُع ُدوا َم َعkatika َْزأ ُ ِب َھاKitabu َويُسْ َتھhiki ُر ِب َھاkwamba ُي ْك َف “Na amekwisha mtakaposikia Aya za Mwenyezi Mungu zinakanushwa ٍ َحدِيnao ي ِْر ِهpamoja ث َغ فِيmpaka وضُواwaingie َي ُخna kuchezewa shere, basi msikae (Sura Nisai: 140). Na pia tunakatika َ ٰmazungumzo َ ص ََّال ِة ا َّت خ ُذو َھاsoma: َوإِ َذا َنادَ ْي ُت ْم إِ َلى ال ُھ ُز ًوا َو َل ِعبًا ۚ ذل َِكmengine...” ون َ ُِبأ َ َّن ُھ ْم َق ْو ٌم َال َيعْ ِقل َوإِ َذا َنا َد ْي ُت ْم إِ َلى الص ََّال ِة ا َّت َخ ُذو َھا ُھ ُز ًوا َو َل ِعبًا ۚ ٰ َذل َِك ون َ ُِبأ َ َّن ُھ ْم َق ْو ٌم َال َيعْ ِقل “Na mnaponadi Swala, wanaifanyia mzaha na mchezo. Hayo ni kwa sababu wao ni watu wasiokuwa na akili.” (Sura Maidah: 58). Je Mtukufu Mtume (saww) aliamuru kuacha adhana au kuisoma kwa sauti ya chini, ili isiwe ni sehemu ya dhihaka za mushrikina?
Kiasili ni kwamba mushrikina walikuwa wakidhihaki shakhsiya ya Mtukufu Mtume (saww): 180
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 180
11/25/2014 3:03:50 PM
Ushia: Hoja na Majibu
ك إِ َّال ُھ ُز ًوا أَ ٰ َھ َذا َ ِين َك َفرُوا إِنْ َي َّتخ ُِذو َن َ آك الَّذ َ َوإِ َذا َر ُون َ الَّذِي َي ْذ ُك ُر آلِ َھ َت ُك ْم َو ُھ ْم ِبذ ِْك ِر الرَّ حْ ٰ َم ِن ُھ ْم َكا ِفر “Na wanapokuona wale ambao wamekufuru hawakufanyii
ُ خhuyu wenu? Na َ َِوإ َّ ِك إ ُ ُھmzaha: َ وJe, ز ًوا أَ ٰ َھ َذاila ال ن ِذ إِنْ َي َّتndiye ُواdhikri َك َفرanayewataja ِين آك َ َ yaالَّذMwingi َ ذا َرmiungu hao ndio wanaokataa wa rehema.” َّ ِ{ إ95}juu(Sura َ ْ ْال ْم ُُسhiyo َ ْيni َك َفwajibu ِين ئ ْز ھ ت اك ن ا ن َ َ ٰ َّ ِ Anbiyaa: 36) . Hivyo kwa mujibu wa riwaya ya ْ ُ َ َ ُون َ الذِي َيذك ُر آلِ َھتك ْم َو ُھ ْم ِب ِذك ِر الرَّ حْ َم ِن ُھ ْم كا ِفر
Mtume (saww) ajifiche asionwe na watu. Na hata ukiachilia mbali yote hayo bado Mwenyezi Mungu anamwambia Mtume Wake (saww) wazi wazi:
ِين َ اك ْالمُسْ َتھ ِْزئ َ { إِ َّنا َك َف ْي َن95} “Hakika Sisi tunakutosha na wafanyao isthizai.” (Sura Hijri: 95).
Tatu: Hakika Musaylamah hakuwa mtu wa kutisha kiasi hiki, bali alikuwa duni kiasi ambacho Mtukufu Mtume (saww) hawezi kuficha Aya za Qur’ani au kuzisoma kwa moyo eti kwa sababu jina lake ni Rahman, na hasa ukizingatia kuwa madai haya ya Musaylamah yalienea katika karne ya kumi ya Hijiriyyah, wakati ambao Uislamu ulikuwa katika nguvu zake na uwezo wake. Kwa kweli ukweli huu unaonesha waziwazi kuwa wawekaji wa hadithi hii ya uwongo walikuwa bado wachanga sana na wasio na ujuzi katika kazi yao hii ya kuweka hadithi za uwongo. Nne: Tunasoma katika hadithi aliyoitaja Ibn Abi Shaybah katika al-Musannaf yake kutoka kwa Ibn Abbas, anasema: “Kuisoma Bismillahi Rahmani Rahim kwa jahara ni usomaji 181
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 181
11/25/2014 3:03:50 PM
Ushia: Hoja na Majibu
wa mabedui.”152 Na wakati huo huo tunayo hadithi nyingine kutoka kwa Ali bin Zayd bin Jad’an akisema: “Hakika akina Abdullah (Abdullah bin Abbas, Abdullah bin Umar na Abdullah bin Zubair) walikuwa wanaanza kusoma kwa kusoma Bismillahi Rahmani Rahim kwa jahara.”153 Na zaidi ya hapa ni kwamba sira ya Imam Ali bin Abu Talib (a.s.) ilikuwa ni kuisoma Bismillahi kwa jahara, na jambo hili ni mashuhuri katika vitabu vyote vya Mashia na vya Masunni, je Imam Ali (a.s.) alikuwa miongoni mwa mabedui? Hivi hadithi hizi zenye kupingana na kugongana si zinatosha kuwa dalili tosha kuwa mas’ala hii ilikuwa na mkondo wa kisiasa? Ndiyo, ukweli ni kwamba Imam Ali (a.s.) alikuwa akisoma Bismillahi kwa jahara, na Muawiya – baada ya kuuwawa Imam Ali (a.s.) na katika kipindi cha ukhalifa wa Imam Hasan (a.s.) na baada ya kupata utawala - alikuwa akiendelea kufuta kila athari na alama za Ali (a.s.) katika ulimwengu wa Kiislamu, zaidi ya hapo alikuwa akiitikadi kuwa athari za kifikra na kimaanawi za Imam Ali (a.s.) zikiendelea kuwepo katika fikra za Waislamu basi hali hiyo itajenga hatari kubwa dhidi ya utawala wake. Na ushahidi juu ya maneno haya tunausoma katika hadithi ambayo kaitaja al-Hakim katika al-Mustadrak kutoka kwa Anas bin Malik mtumishi makhususi wa Mtukufu Mtume (saww): “Muawiya alikuja Madina na akashiriki katika moja ya Sala za jahara (Maghrib au Isha), akasoma Bismillahi katika Sura al-Hamdu na hakuisoma katika Sura ya pili, na alipotoa tu salamu katika Sala yake, zilinyanyuka juu sauti za kundi la Muhajirina na Ansari toka pande zote zikisema: ‘Umeiibia Sala au umesahau?’ hivyo katika Sala iliyofuata Muawiya 152
Al-Musannaf Ibn Abi Shaybah Juz. 2, Uk. 89.
153
Tafsiru ad-Durul-Manthur Juz. 1, Uk. 21. 182
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 182
11/25/2014 3:03:50 PM
Ushia: Hoja na Majibu
akasoma Bismillahi mwanzoni mwa Sura al-Hamdu na pia mwanzoni mwa Sura ya pili.”154 Huenda Muawiya kwa amali hii alitaka kujua hisia za Muhajirina na Ansari juu ya kuisoma Bismillahi jahara, lakini aliendelea na amali yake hii katika miji mingine kama vile Sham na kwingineko. Qur’ani ni iliyopo baina ya jalada mbili Hakika bila shaka maneno yaliyopo baina ya jalada mbili ndio Qur’ani, na Bismillahi ni sehemu ya Qur’ani, ama maneno wasemayo baadhi yao kuwa Bismillahi si sehemu ya Qur’ani bali yenyewe ni kwa ajili ya kutenganisha tu baina ya Sura, hilo tunajibu kuwa: Kwanza: Hakika maneno haya hayajumuishi Sura alHamdu, kwa sababu Bismillahi ni sehemu ya Sura al-Hamdu na inahesabiwa miongoni mwa Aya saba, kama ilivyo katika nakala zote za Qur’ani. Pili: Kwa nini utenganishaji huu hausemwi katika Sura al-Baraa? Ikisemwa: Hakika muktadha wa Aya za mwisho wa Sura An’fal hauoani na muktadha wa Aya za mwanzo wa Sura al-Baraa, tutajibu kuwa: Katika Qur’ani kuna Sura nyingi ambazo mwisho wake hauoani na mwanzo wa Sura inayofuatia, lakini pamoja na hali hiyo Bismillahi imekuja baina ya Sura hizo. Ukweli ni kwamba Bismillahi ni sehemu ya kila Sura kama ilivyo katika Qur’ani, ama kutokutajwa Bismillahi mwanzoni mwa Sura al-Baraa, hiyo ni kwa sababu Sura al-Baraa inaanza 154
Mustadrakus-Sahihayn Juz. 1, Uk. 232. 183
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 183
11/25/2014 3:03:50 PM
Ushia: Hoja na Majibu
kwa kutangaza vita dhidi ya wale waliovunja ahadi, na hii hainasibiani na kitendo cha kutajwa Rahman Rahiim, kwa sababu sifa hizo mbili ni dhihiriko la rehema ya jumla na makhususi.
184
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 184
11/25/2014 3:03:51 PM
Ushia: Hoja na Majibu
Muhtasari wa uchunguzi Muhtasari wa mada ya nafasi ya Bismillahi katika Sura al-Hamdu ni
K
wanza: Hakika Mtukufu Mtume (saww) alisoma Bismillahi mwanzoni mwa Sura al-Hamdu, na mwanzoni mwa Sura nyingine, hiyo ni kwa mujibu wa riwaya nyingi ambazo zimenukuliwa na watu waliokuwa na ukaribu zaidi na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww), na kwa mujibu wa riwaya kadhaa aliisoma Bismillahi kwa jahara. Pili: Hakika riwaya ambazo zinapinga riwaya zilizotajwa hapo nyuma punde tu na ambazo zinasema kuwa Bismillahi si sehemu ya Sura yeyote, au Mtume (saww) alikuwa akiisoma kwa sauti ya chini, riwaya hizo si za kweli ni za uwongo zilizowekwa na wawekaji wa hadithi za uwongo, hiyo ni kutokana na vielelezo vilivyopo katika riwaya zenyewe, na Bani Umaiyyah ndio waliokuwa nyuma ya riwaya hizi ili kutimiza baadhi ya malengo yao ya kisiasa, kwa sababu kitendo cha Imam Ali (a.s.) kuwa anaisoma Bismillahi kwa jahara kilikuwa mashuhuri na maarufu, na siasa ya Bani Umaiyyah ilikuwa inahitaji kwenda kinyume na kila linalomhusu Imam Ali (a.s.) hata kama jambo hilo litakuwa linaafikiana na sira ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww). Na Maswahaba walimkosoa kwa nguvu zote Muawiya juu ya maudhui hii, na vielelezo na ushahidi tulioutaja hapo nyuma unasisitiza hilo. 185
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 185
11/25/2014 3:03:51 PM
Ushia: Hoja na Majibu
Tatu: Maimamu wa Ahlul-Bait (as) walikuwa wakisoma Bismillahi kwa jahara kwa kumfuata Amirul-Muuminin Ali (a.s.) ambaye alikunywa elimu ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) kwa muda wa miaka mingi, na wao wameafikiana juu ya rai hii mpaka Imam as-Sadiq (a.s.) akasema: “Aali Muhammadi wamekubaliana juu ya kuisoma Bismillahi Rahman Rahiim kwa jahara.”155 Na ikiwa inapasa wao kutenda kwa mujibu wa riwaya ya vizito viwili na kuchukua riwaya za Ahlul-Bait (as) basi ni wajibu kwa wanafiqhi wote wa Kisunni kama vile Shafi, kuisoma Bismillahi kwa jahara, au kwa uchache kuzingatia kuwa ni wajibu kuisoma kwa jahara katika Sala za jahara. Nne: Kwa kumalizia tunanukuu ibara mbili za Fakhru Razi kutoka kwenye kitabu chake cha tafsiri: a.
Anasema: “Hakika Ali alikuwa amezidisha kuisoma Bismillahi kwa jahara, hivyo dola ilipofika mikononi mwa Bani Umaiyya wao walizidisha katika kuzuia kuisoma kwa jahara, ikiwa ni kujitahidi kubatilisha athari za Ali (a.s.).”156 akika ushahidi wa aalimu huyu mkubwa wa Kisunni H unaweka wazi bila shaka kuwa hukumu ya kuficha Bismillahi au kuiondoa kabisa ilikuwa ni moja ya njia za kutimizia malengo ya kisiasa.
b.
Katika sehemu nyingine ya kitabu chake hicho baada ya kuonesha nukuu ya al-Bayhaqi inayosema: “Hakika Umar bin Khatab, Ibn Abbas, Abdullah bin Umar na Abdullah bin Zubair wote walikuwa wakisoma Bismillahi
155
Mustadrakul-Wasail Juz. 4 Uk. 189.
156
At-Tafsiru al-Kabir cha Fakhru Raz Juz. 1 Uk. 206. 186
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 186
11/25/2014 3:03:51 PM
Ushia: Hoja na Majibu
kwa jahara.” Anaongeza kuwa: “Ama kwamba Ali (a.s.) alikuwa akisoma Bismillahi kwa jahara, hilo limethibiti kwa uwingi (ni mutawatiri), na atakayemfuata Ali bin Abu Talib katika dini yake basi ameongoka. Na dalili juu ya hilo ni kauli ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww): ‘Ewe Mwenyezi Mungu izungushe haki pamoja na Ali popote atakapozunguka.’”157
157
At-Tafsiru al-Kabir cha Fakhru Raz Juz. 1 Uk. 204 - 205. 187
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 187
11/25/2014 3:03:51 PM
Ushia: Hoja na Majibu
MADA YA KUMI KUTAWASALI KWA MAWALII WA MWENYEZI MUNGU Tawassuli kwa mujibu wa Aya za Qur’ani na dalili ya kiakili
H
akika kutawasali kupitia Mawalii wa Mwenyezi Mungu ili kutatua matatizo ya kimada na kimaanawi ni miongoni mwa mambo yenye mjadala mkubwa baina ya Mawahabi na Waislamu wengine ulimwenguni. Mawahabi wanatamka wazi kuwa kutawasali kwa Mwenyezi Mungu kupitia matendo mema ni jambo lisilo na mushkeli wowote, lakini hairuhusiwi kutawasali kupitia Mawalii wa Mwenyezi Mungu, na wanaona hiyo ni namna mojawapo ya shirki, wakati ambapo Waislamu wengine ulimwenguni wanaona kuwa inaruhusiwa kutawasali kupitia Mawalii wa Mwenyezi Mungu, kwa maana ambayo tutaifafanua huko mbele. Mawahabi wamedhani kwamba baadhi ya Aya za Qur’ani zinazuia kutawasali, na zinazingatia kuwa jambo hilo ni shirki, na miongoni mwa Aya hizo ni kauli ya Mwenyezi Mungu:
ﷲ ُز ْل َف ٰى ِ َّ َما َنعْ ُب ُد ُھ ْم إِ َّال لِ ُي َقرِّ بُو َنا إِ َلى 188
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 188
11/25/2014 3:03:51 PM
Ushia: Hoja na Majibu
“Sisi hatuwaabudu ila wapate kutujongeza tu kumkaribia Mwenyezi Mungu…” (Sura Zumara; 39: 3), ambayo inaelezea hali waliyokuwa nayo Mushrikina wa zama za ujahiliya kuhusu vile walivyokuwa wakiviabudu, kama vile Malaika na vinginevyo, na Qur’ani inaona maneno haya ni shirki. Na katika Aya nyingine Mwenyezi Mungu anasema:
ﷲ أَ َح ًدا ِ َّ � َف َال َت ْدعُوا َم َع ِ َّ ِ َوأَنَّ ْال َم َسا ِج َد ﷲ أَ َح ًدا ِ َّ � َف َال َت ْدعُوا َم َع ِ َّ ِ َوأَنَّ ْال َم َسا ِج َد
“Na hakika misikiti yote ni ya Mwenyezi Mungu, basi msimuombe yoyote pamoja na Mwenyezi Mungu.” (Sura Jinn: (18). Na katika Aya nyingine anasema:
ُون ِمنْ ُدو ِن ِه َال َ ِين َي ْدع َ َل ُه دَ عْ َوةُ ْال َح ِّق ۖ َوالَّذ ُون ِمنْ ُدو ِن ِه َال َل َيُهسْ َد َتعْ ِج َيوبةُ َْال َ ِين َي ْدع َ ُون َح َل ِّ ُھق ْم ۖ ِبَوا َشلَّيْذ ٍء ُون َل ُھ ْم ِب َشيْ ٍء َ َيسْ َت ِجيب
“Kwake ndio maombi ya haki. Na hao wanaoomba badala Yake hawajibiwi chochote..” (Sura Ra’d; 13:14).
Mawahabi wamefikiri na kudhani kuwa Aya hizi zinakataza kutawasali kupitia Mawalii wa Mwenyezi Mungu, na zaidi ya hili wana mada nyingine nayo ni kuwa hata tukijaalia kuwa ni ruhusa kutawasali kupitia Mtukufu Mtume (saww) katika zama za uhai wake, kama baadhi ya riwaya zisemavyo, lakini hatuna dalili zinazoonesha kuwa ni ruhusa pia baada ya kifo chake. Huu ndio ufupi wa lile wasemalo. Lakini kwa bahati mbaya na kwa sababu ya maneno haya yasiyo na dalili, Mawahabi wanawatuhumu Waislamu wengi 189
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 189
11/25/2014 3:03:51 PM
Ushia: Hoja na Majibu
kwa shirki na ukafiri, na wamehalalisha damu zao na mali zao, na kwa kisingizio hiki wamemwaga damu nyingi na kupora mali nyingi. Hebu sasa baada ya kutambua itikadi yao vizuri turejee kwenye asili ya mada na tuzungumzie maudhui ya kutawasali kuanzia kwenye mizizi yake. Kwanza tutaonesha maana ya tawassuli katika lugha ya Kiarabu na katika Aya za Qur’ani na riwaya. Tawassuli katika lugha ya Kiarabu: Kilugha Tawassuli ina maana ya kuchagua al-Wasilah, na al-Wasilah ni jambo analolitumia mtu kujiweka karibu na mtu mwingine.158 Ibn Mandhur katika kitabu chake maarufu Lisanul-Arab anasema: “Fulani ametumia al-Wasilah kwa Mwenyezi Mungu: Pindi anapotenda amali itakayomkurubisha kwake… na al-Wasilah ni jambo analolitumia mtu kujiweka karibu na mtu mwingine.”159 Na katika kitabu Misbahul-Lughah imekuja: “al-Wasilah: Ni jambo analolitumia mtu kujiweka karibu na kitu, na wingi wake ni al-Wasailu.” Na tunasoma katika kitabu MaqayisulLughah: “al-Wasilah: Ni raghaba na ombi.” Na kwa maana hii al-Wasilah humaanisha kujikurubisha, na pia jambo ambalo hulitumia mtu kujiweka karibu na mtu, hivyo al-Wasilah ina maana pana sana. 158
159
Kwa mujibu wa Kamusi ya Kiswahili Sanifu, Toleo la Pili, iliyochapishwa na Oxford University Press, Kutawasali ni kuomba Mungu kwa kuunganisha maombi hayo na Baraka au jaha ya mtu au watu wenye cheo kwa Mungu – Mtarjuma. Lisanul-Arabi cha Ibnu Mandhuri, Juz. 11, Uk. 724, Kitomeo: Wasala. 190
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 190
11/25/2014 3:03:51 PM
Ushia: Hoja na Majibu
Ama kwa upande wa Qur’ani yenyewe imetumia istilahi ya al-Wasilah katika Aya mbili: Ya kwanza: Katika kauli ya Mwenyezi Mungu:
ﷲ َوا ْب َت ُغوا إِ َل ْي ِه ْال َوسِ ي َل َة َ َيا أَ ُّي َھا الَّذ َ َّ ِين آ َم ُنوا ا َّتقُوا ُون َ َو َجا ِھ ُدوا فِي َس ِبيلِ ِه َل َعلَّ ُك ْم ُت ْفلِح “Enyi mlioamini! Mcheni Mwenyezi Mungu na tafuteni njia (al-Wasilah) ya kumfikia mfanye juhudi katika njia Yake ili mpate kufaulu.” (Sura al-Maidah: 35). Aya hii inawaamrisha Waislamu wote, na ina amri tatu:
a.
ف َ ون َك ْش َ ِين َز َعمْ ُت ْم ِمنْ ُدو ِن ِه َف َال َي ْملِ ُك َ قُ ِل ْادعُوا الَّذ ً الضُّرِّ َع ْن ُك ْم َو َال َتحْ ِو يال Amri ya kumcha Mwenyezi Mungu.
b.
Amri ya kuchagua njia (al-Wasilah) ambayo itatuweka karibu na Mwenyezi Mungu Mtukufu.
c.
Amri ya jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu.
Na matokeo ya kukusanyika pamoja sifa hizi tatu َّ قُواyanapatikana (uchamungu, ْال َوسِ ي َل َةtawassuli َت ُغوا إِ َل ْي ِهna َوا ْبjihadi) ﷲ ِين آ َم ُنوا ا َّت َيا أَ ُّي َھاwa َ الَّذmwisho َ Aya hii, nayo ni: “Ili mpate kufaulu.”
ُون َ َو َجا ِھ ُدوا فِي َسبيلِ ِه َل َعلَّ ُك ْم ُت ْفلِح
Ya pili: Ni Aya ya hamsini na saba ِ ya Sura Israi, na ili kuielewa vizuri Aya hii tunaanza kwanza na Aya iliyoitangulia, nayo ni:
ف َ ون َك ْش َ ِين َز َع ْم ُت ْم ِمنْ ُدو ِن ِه َف َال َيمْ لِ ُك َ قُ ِل ْادعُوا الَّذ ً الضُّرِّ َع ْن ُك ْم َو َال َتحْ ِو يال 191
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 191
11/25/2014 3:03:51 PM
Ushia: Hoja na Majibu
“Sema: Waombeni hao mnaodai badala Yake. hawawezi kuwaondolea madhara wala kuyabadilisha.” (Sura Israi; 17:56). Na kwa kuangalia jumla: “Sema: Waombeni hao mnaodai badala Yake.” Inabainika kuwa mkusudiwa katika Aya hii sio masanamu na mengineyo – kwa sababu “Hao” hutumika kwa wenye akili – bali mkusudiwa hapo ni Malaika ambao walikuwa wakiabudiwa badala ya Mwenyezi Mungu, au ni Nabii Isa (as) ambaye alikuwa akiabudiwa na baadhi ya watu badala ya Mwenyezi Mungu, hivyo Aya inatamka wazi wazi kwamba hao Malaika au Masihi mnayemwabudu badala ya Mwenyezi Mungu hawawezi kuwaondolea nyinyi madhara wala hawawezi kuwatatulieni matatizo yenu.
Aya inayofuatia ndio sehemu ya mada yetu, nayo ni kauli ya Mwenyezi Mungu:
ون إِ َل ٰى َرب ِِّھ ُم ْال َوسِ ي َل َة أَ ُّي ُھ ْم َ ُون َي ْب َت ُغ َ ِين َي ْدع َ ِك الَّذ َ أُو ٰ َلئ اب َ ون َع َذا َب ُه ۚ إِنَّ َع َذ َ ُُون َرحْ َم َت ُه َو َي َخاف َ أَ ْق َربُ َو َيرْ ج ان َمحْ ُذورً ا َ ِّك َك َ َرب “Hao wanawaomba, wao wenyewe wanatafuta njia ya kujikurubisha kwa Mola Wao, hata walio karibu miongoni mwao, na wanataraji rehema Zake na wanaihofu adhabu Yake. Hakika adhabu ya Mola Wako ni ya kuchukuliwa hadhari.” (Sura Israi: 57). Kosa kubwa walilotumbukia ndani yake Mawahabi ni kudhani kwao kwamba maana ya kutawasali kupitia Mawalii wa Mwenyezi Mungu ni kuwa wao Mawalii wanaondoa madhara na kutatua matatizo. Na wakadhani kuwa kukidhi kwao haja na kuondoa kwao matatizo kunatimia kwa namna ya kujitegemea, wakati ambapo tunachokusudia katika kutawasali si maana hii. 192
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 192
11/25/2014 3:03:51 PM
Ushia: Hoja na Majibu
Tawassul katika Aya tukufu Ama Aya ambazo zimeng’ang’aniwa na Mawahabi, zenyewe zinahusu ibada, na hakuna mtu mwenye kuwaabudu Mawalii wa Mwenyezi Mungu. Hivi je kutawasali kwetu kupitia Mtukufu Mtume (saww) kunamaanisha kumwabudu? Na hivi je tunaamini kuwa Mtukufu Mtume (saww) anaathiri na kuondoa matatizo kwa namna ya kujitegemea. Tawassuli ambayo Qur’ani Tukufu inailingania ni kutawasali kwa njia ambayo itatuweka karibu na Mwenyezi Mungu, kwa maana ya kwamba hawa wanatuombea kwa Mwenyezi Mungu, kama tulivyotaja hilo katika mada ya uombezi. Na uhalisia ni kwamba hakika ukweli kuhusu Tawassuli na uombezi ni kitu kimoja, kuna Aya nyingi zinazojulisha uombezi, na Aya mbili zinajulisha Tawassul, na cha kuvutia ni kwamba Aya ya hamsini na saba ya Sura Israi inasema: “hata walio karibu miongoni mwao”, ambapo inawapa hiyari ya kuchagua njia iliyo karibu zaidi baina ya Malaika na Masihi, na hakika dhamiri “Miongoni mwao” ni ya uwingi wa vitu vyenye akili (malaika na binadamu), hii inamaanisha kuwa wao wanatawasali kupitia waswalihina na Mawalii wa Mwenyezi Mungu. Vyovyote iwavyo kwanza ni wajibu tuweke wazi nini maana ya kutawasali kupitia Mawalii wa Mwenyezi Mungu; na je ni kuwaabudu wao? Lahasha si hivyo kabisa! Je wanaona kuwa wao wanajitegemea katika kuathiri kwao? Lahasha, hapana si hivyo kabisa! Au je wao binafsi wana uwezo wa kukidhi haja na kuondoa matatizo? Lahasha, hapana si hivyo kabisa! Hakika wao humuombea kwa Mwenyezi Mungu yule anayetawasali kupitia kwao, kama pale tunapotaka kwenda 193
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 193
11/25/2014 3:03:51 PM
Ushia: Hoja na Majibu
kwenye nyumba ya mtu mzito ambaye hatumjui, hivyo tunakimbilia kwa mtu mwenye uhusiano mzuri na wa karibu na mtu huyo, na tunapitia kwake ili twende pamoja naye kwa mtu huyo mzito, ili akatutambulishe kwake na kutuombea kwake, kitendo hiki si kumwabudu mtu huyu na wala faida tutakayopata si kutoka kwa mtu huyu yeye kama yeye binafsi. Na hapa inafaa tusome maneno mazuri ya Ibn Alawi katika kitabu chake maarufu Mafahim Yajibu An’tuswahahu, ambapo anasema: “Watu wengi wameshindwa kufahamu ukweli wa Tawassuli, na kwa ajili hii tutabainisha maana sahihi ya Tawassuli kwa mujibu wa mtazamo wetu, na kabla ya kufanya hivyo ni lazima tukumbushane kwa kubainisha baadhi ya nukta: 1.
Tawassuli ni moja ya aina za dua, na ukweli yenyewe ni mlango miongoni mwa milango ya kujielekeza kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, hivyo mlengwa na mkusudiwa wa asili na halisi ni Mwenyezi Mungu Mtukufu, na mtu anayemtumia katika kutawasali kwake ni kiungo tu na njia ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu, na anayeitakidi kinyume na hivi basi huyo ni miongoni mwa mushirikina.
2.
Na yeyote anayetawasali kwa Mwenyezi Mungu kupitia mtu fulani, ni kwa sababu mtu huyo ni mahabubu kwake na anamwamini, na anaamini kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu anampenda mtu huyo, hivyo lau ikitokea kwamba imedhihiri kinyume na hivyo basi muombaji atajitenga moja kwa moja na mtu huyo na kumkhalifu, kwa sababu kigezo ni mtu huyo kuwa anapendwa na Mwenyezi Mungu. 194
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 194
11/25/2014 3:03:51 PM
Ushia: Hoja na Majibu
3.
Iwapo mtu atatawasali na akaamini kuwa anayemtumia katika kutawasali anaathiri katika maombi yake kwa namna ya kujitegemea yeye mwenyewe binafsi, kama ilivyo kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, basi mtu huyo ni miongoni mwa mushrikina.”
4.
Tawassuli si jambo la wajibu wala la lazima, wala dua haijibiwi kwa Tawassuli tu, hivyo jambo la muhimu ni dua na kukimbilia kwa Mwenyezi Mungu kwa namna yoyote ile, kama Mwenyezi Mungu asemavyo:
ُ اع َ َوإِ َذا َسأ َ َل ِ ك عِ َبادِي َع ِّني َفإِ ِّني َق ِريبٌ ۖ أ ِجيبُ َدعْ َو َة ال َّد ُ ْان ۖ َف ْل َيسْ َت ِجيبُوا لِي َو ْلي ُْؤ ِم ُنوا ِبي َل َعلَّ ُھ ْم َير ون َ ش ُد ِ إِ َذا َد َع “Na waja Wangu watakapokuuliza habari Yangu, Mimi niko karibu. Naitikia maombi ya mwombaji anaponiomba. Basi nawaniitikie Mimi na waniamini Mimi ili wapate kuongoka.” (Sura al-Baqarah: 186).”
Baada ya kutoa utangulizi huu, Ibn Alawi ametaja rai za Ulamaa, wanafiqhi na wanatheiolojia wa Kisunni, akasema: “Hakuna tofauti baina ya Waislamu kuhusu uhalali wa kisharia wa kutawasali kwa Mwenyezi Mungu kupitia matendo mema, kama vile mtu kufunga au kusali au kusoma Qur’ani au kutoa sadaka katika njia ya Mwenyezi Mungu, kisha atawasali kwa Mwenyezi Mungu kupitia matendo haya na ajikurubishe kwayo kwake. Jambo hili ni miongoni mwa mambo yenye kukubalika na wote na hayana mjadala. Na aina hii ya Tawassuli inakubaliwa hata na Masalafi, na miongoni mwao ni Ibn Taymiyah, kama ilivyotajwa ndani ya vitabu vyake mbalimbali na hasa risala yake al195
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 195
11/25/2014 3:03:52 PM
Ushia: Hoja na Majibu
Qaidah al-Jaliyah Fit-Tawassuli Wal-Wasilah. Ibn Taymiyah anatamka wazi kuwa aina hii ya Tawassuli inaruhusiwa, yaani kutawasali kupitia matendo mema, ikiwa ndivyo hivyo ni wapi basi penye ikhtilafu? Penye ikhtilafu ni katika kutawasali kwa kitu kisichokuwa tendo jema, kama vile kutawasali kupitia Mawalii wa Mwenyezi Mungu, kwa mfano mtu aseme: ‘Ewe Mungu Wangu, hakika mimi natawasali kwako kupitia Nabii Wako Muhammadi.’” Na baada ya hapo anaongeza kwa kusema: “Kutofautiana katika maana hii, na Mawahabi kupinga kutawasali kupitia Mawalii wa Mwenyezi Mungu, kiukweli ni mojawapo ya aina tofauti za kimaneno tu na kimatamshi na si tofauti ya kiasili, na kwa ibara nyingine ni mzozo wa kimatamshi, kwa sababu Tawassuli ya kupitia Mawalii wa Mwenyezi Mungu kiuhalisia inarejea katika kutawasali kupitia matendo mema, na jambo hilo ni halali kisharia. Hivyo laiti wapingaji wangelitazama jambo hili kwa macho ya uadilifu na ujuzi basi jambo hili lingekuwa wazi mno kwao, na hapo tatizo litaondoka na moto wa fitina utazimika na wala haitafika zamu ya kuwatuhumu Waislamu kwa shirki na upotovu.” Na ili kufafanua maneno haya, Ibn Alawi anaongeza baada ya hapo kwa kusema: “Ikiwa mtu anatawasali kupitia mmoja kati ya Mawalii wa Mwenyezi Mungu, hiyo ni kwa sababu mtu huyo ni mahabubu kwake. Lakini ni kwa nini mtu huyo ni mahabubu kwake? Ni kwa sababu ni mtu mwema au ni kwa kuwa anapendwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, au ni kwa kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu anampenda, au mtu mwenyewe anaipenda njia hii (anayopitia), na tunapotazama 196
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 196
11/25/2014 3:03:52 PM
Ushia: Hoja na Majibu
kwa kina mambo yote haya tunakuta kuwa yanatokana na amali, yaani kiuhalisia Tawassuli inapatikana kutokana na matendo yaliyo mema mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na hii ndio maana walioafikiana Waislamu wote.”160 Ndiyo, sisi tutaashiria hapo baadaye kuwa kutawasali kupitia baadhi ya watu ni kwa utukufu wao na si kwa ajili ya matendo yao, ni kwa kuwa wao ni watu wenye jaha, watukufu na walio adhimu mbele ya Mwenyezi Mungu, au kwa dalili yoyote iwayo ni kwa kuwa wao si wenye kujitegemea wenyewe katika kuathiri maombi, bali ni kwa kuwa wao ni waombezi mbele ya Mwenyezi Mungu, na Tawassuli hii si ukafiri wala si haramu. Na Aya za Qur’ani mara kadhaa zimegusia aina hii ya Tawassuli, hivyo shirki ni mtu kuitakidi kuwa kuna kitu mkabala na Mwenyezi Mungu chenye kuathiri chenyewe binafsi, na hivyo kosa la Mawahabi ni wao kuchanganya baina ya ibada na uombezi uliopo katika Aya:
ﷲ ُز ْل َف ٰى ِ َّ َما َنعْ ُب ُد ُھ ْم إِ َّال لِ ُي َقرِّ بُو َنا إِ َلى ….. “Sisi hatuwaabudu ila wapate kutujongeza tu kumkaribia Mwenyezi Mungu…” (Sura Zumar: 3), na wakadhani pia kuwa uombezi ni shirki, wakati ambapo shirki ni kuwaabudu hawa watu wa kati na si kuomba wakuombee au kutawasali kupitia kwao.
160
Mafahim Yajibu An’tuswahahu, Uk. 116 na 117. 197
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 197
11/25/2014 3:03:52 PM
Ushia: Hoja na Majibu
Tawassuli katika riwaya za Kiislamu Ukiachilia mbali kwamba Aya za Tawassuli hazijafungwa na sharti lolote, ambapo humaanisha kuwa Tawassuli yoyote isiyokhalifu itikadi sahihi ya Uislamu inaruhusiwa, pia tuna riwaya nyingi kuhusu Tawassuli ambazo zinafika kiwango cha mutawatiri au karibu na mutawatiri. Na nyingi kati ya riwaya hizi zinahusu kutawasali kupitia Mtukufu Mtume (saww) yeye mwenyewe, baadhi yake zinahusu kabla ya kuzaliwa Mtume (saww), nyingine baada ya kuzaliwa kwake, nyingine zama za uhai wake na nyingine baada ya kufariki kwake. Na pia kuna kundi lingine la riwaya linahusu kutawasali kupitia asiyekuwa Mtukufu Mtume (saww) miongoni mwa Ulamaa wa dini. Tunaongeza kuwa baadhi ya riwaya hizo zimekuja kwa lugha ya maombi na dua, na nyingine kwa lugha ya kuomba kuombewa kwa Mwenyezi Mungu, na nyingine zinaonesha jinsi Mwenyezi Mungu anavyobainisha cheo cha Mtukufu Mtume (saww). Na kwa ufupi ni kuwa sisi tutatazama vizuri aina zote za Tawassuli zilizopo kwenye riwaya hizi kwa namna ambayo itaziba mlango wa visingizio wanavyoving’ang’ania Mawahabi. Na hebu sasa tuone baadhi ya mifano ya riwaya hizi: 1. Adam (as) alitawasali kupitia Mtukufu Mtume (saww) kabla ya kuzaliwa kwake: al-Hakim ndani ya alMustadrak na jamaa wengine miongoni mwa wanahadithi, wote wamenukuu hadithi hii kutoka kwa Mtukufu Mtume (saww) kuwa alisema: “Adam alipotenda kosa, alisema: ‘Ewe Mola nakuomba unisamehe kwa haki ya Muhammad.’ 198
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 198
11/25/2014 3:03:52 PM
Ushia: Hoja na Majibu
Mwenyezi Mungu akasema: ‘Ewe Adam, umemjuaje Muhammad na bado sijamuumba?’ Akasema: ‘Ewe Mola, kwa sababu uliponiumba kwa mkono wako na kunipulizia roho yako niliinua kichwa changu nikaona nguzo za Arshi zikiwa zimeandikwa: Hapana mungu isipokuwa Allah, Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Nikajua kuwa hakika wewe haujamuunganisha kwenye jina lako isipokuwa kiumbe umpendaye zaidi.’ Mwenyezi Mungu akasema: ‘Umesema kweli ewe Adam, hakika yeye ndiye kiumbe nimpendaye zaidi, endelea kuniomba kwa haki yake kwani nimeshakusamehe, na laiti kama si Muhammadi nisingekuumba.’”161 2. Hadithi nyingine inahusu kutawasali alikofanya Abu Talib kupitia Mtukufu Mtume (saww) alipokuwa mtoto: Muhtasari wa hadithi kama alivyoinukuu Ibn Hajar ndani ya kitabu chake Fat’hul-Bariy ni: “Ukame ulipoipata Makka, Makuraishi walikwenda kwa Abu Talib na kumwambia: ‘Bonde limepatwa na ukame na familia hazina kitu, njoo utuombee mvua.’ Abu Talib akatoka akiwa pamoja na mtoto ambaye anang’aa kama jua, Abu Talib akamchukua na kuegemeza mgongo wake kwenye Kaaba na kuomba kupitia kwake, yaani alitawasali kupitia mtoto huyu, wakati huo mbinguni hakukuwa na mawingu hata kipande kimoja, mara mawingu yakaanza kujikusanya toka huku na kule na hatimaye mvua ikanyesha na bonde likapasuka kutokana 161
l-Mustadrak ya Al-Hakim Juz. 2, Uk. 615, na kainukuu al-Hafidh Suyutiy A katika al-Khasaisu an-Nabawiyyah na ameizingatia kuwa ni hadithi sahihi. Na ameinukuu al-Bayhaqiy katika Dalailun-Nubuwah, naye hapokei hadithi dhaifu. Na ameinukuu al-Qastalaniy na Zarqaniy katika al-Mawahib ad-Daniyyah na ameizingatia kuwa ni hadithi sahihi. Na kwa ufafanuzi zaidi rejea kitabu Mafahim Yajibu An’tuswahahu, Uk. 121. 199
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 199
11/25/2014 3:03:52 PM
Ushia: Hoja na Majibu
na mvua nyingi na ardhi yote ikastawi. Na hapo Abu Talib akasoma shairi la kumsifu Mtukufu Mtume (saww) likiwa na beti zaidi ya themanini, kati ya beti hizo ni: ‘Mweupe ambaye kwa uso wake mawingu yanabubujisha mvua, ni msaada kwa mayatima na muhimili kwa wajane.’”162 3. Kipofu alitawasali kupitia Mtukufu Mtume (saww): Mtu mmoja kipofu alikwenda kwa Mtukufu Mtume (saww) zama za uhai wake akatawasali kupitia kwake na Mtume (saww) akamuombea, na hatimaye akapona na kuona.163 Muhtasari wa hadithi hii ni kwamba: “Mtu mmoja kipofu alikwenda kwa Mtume (saww) akasema: ‘Niombee kwa Mwenyezi Mungu aniponye.’ Mtume akamwambia: ‘Ukipenda nitaomba na ukipenda vumilia na ndiyo bora kwako.’ Yule mtu akamwambia Mtume: ‘Muombe Mwenyezi Mungu.’ Basi Mtume akamwamuru atawadhe vizuri na aombe dua hii: ‘Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi nakuomba na ninaelekea Kwako kupitia kwa Mtume Wako Muhammad (saww), Mtume wa Rehema. Ewe Muhammad, hakika mimi naelekea kwa Mola Wangu Mlezi kupitia kwako katika haja yangu ili unikidhie. Ewe Mwenyezi Mungu mfanye Muhammad kuwa mwombezi wangu.’ Mtu yule akasimama na akafanya aliloambiwa na Mtume (saww). Uthman bin Umair mpokezi wa hadithi hii anasema: “Tulikuwa tumeketi katika kikao hicho tukizungumza, mara baada ya muda mfupi kipofu yule alikuja kwenye kikao huku akiwa anaona kama zamani kiasi kwamba hana athari yoyote ya upofu.” 162
Fat’hul-Bariy Juz. 2, Uk. 494. Kadhalika As-Siyratul-Halabiyyah Juz. 1, Uk. 116.
163
S ahih Tirmidhiy Uk. 119, Hadithi ya 3578. Sunanu Ibnu Majah Juz. 1, Uk. 441, Hadithi ya 1385. Musnad Ahmad Juz. 4. Uk. 138, Hadithi ya 16789. 200
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 200
11/25/2014 3:03:52 PM
Ushia: Hoja na Majibu
Na la kuvutia ni kwamba wengi miongoni mwa Ulamaa wakubwa wa Kisunni wametamka wazi wazi kwamba hadithi hii ni sahihi, Tirmidhiy anaona ni hadithi sahihi, na Ibn Majah anasema: “Ni hadithi sahihi.”164 Na Rifa’iy amesema: “Hakuna shaka kwamba hadithi hii ni sahihi na mashuhuri.”165 4. Kutawasali kupitia Mtukufu Mtume (saww) baada ya kifo chake: ad-Daramiy ni mmoja kati ya Ulamaa maarufu wa Kisunni, anasema katika kitabu chake maarufu SunanudDaramiy chini ya anwani: “Mlango unaozungumzia yale aliyomkirimu Mwenyezi Mungu Nabii wake (saww) baada ya kifo chake.” Mlango huu umewekwa ili kubainisha makarama ambayo Mwenyezi Mungu Mtukufu alimpa Mtume (saww) baada ya kifo chake: “Wakazi wa Madina walipatwa na ukame mkali, wakamlalamikia hilo Aisha, yeye akasema: ‘Litazameni kaburi la Mtume (saww) na lifanyeni sehemu ya kutazamia mbinguni kiasi kwamba kusiwe na kizuizi baina yake na mbingu.’ Wakafanya hivyo tukapata mvua nyingi mpaka majani yakachipua na ngamia wakanenepa mpaka wakapasuka kwa mafuta, na mwaka huo ukaitwa mwaka wa ngamia kupasuka.”166 5. Kutawasali kupitia ami ya Mtukufu Mtume (saww) Abbas: Bukhari ananukuu katika Sahih yake kwamba: “Umar bin Khattab alikuwa kila wanapopatwa na ukame huomba mvua kupitia Abbas bin Abdul-Muttalib (ra) na alikuwa 164
Sunanu Ibnu Majah Juz. 1, Uk. 441.
165
wa ufafanuzi zaidi unaweza kurejea kitabu ar-Rasail Wal-Masail Juz. 18 Uk. K 1, Chapa ya Beirut, ambapo anasema: “Hakika ibara halisi ya Ibn Taymiyah ni: “Hakika an-Nasaiy na Tirmidhiy wamepokea hadithi sahihi kwamba Mtukufu Mtume (saww) alimfundisha mtu mmoja kuomba, amuombe Mwenyezi Mungu kisha amsemeshe Mtukufu Mtume (saww) kwa kutawasali kupitia kwake, kisha amuombe Mwenyezi Mungu akubali uombezi wake.”
166
Sunan ad-Daramiy Juz. 1, Uk. 43. 201
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 201
11/25/2014 3:03:52 PM
Ushia: Hoja na Majibu
akisoma dua hii: ‘Ewe Mungu Wangu tulikuwa tukitawasali kwako kupitia Mtume wetu (saww) na ukitupa mvua, basi sasa tunatawasali kwako kupitia ami ya Mtume wetu basi tupe mvua.’ Mpokezi anasema: ‘Basi hupewa mvua nyingi.’”167 6. Ibn Hajar al-Makiy ananukuu katika as-Sawaiqul-Muhriqah kutoka kwa Imam Shafi ambaye ni mmoja kati Ulamaa maarufu kwa Masunni, kuwa yeye alikuwa akitawasali kupitia Ahlul-Baiti (as), na ananukuu shairi maarufu kutoka kwake: “Kizazi cha Mtume, wao ni njia yangu na wao ni wasila wangu.. Kupitia wao kesho nataraji kupewa kitabu changu kwa mkono wa kulia.”168 Rifa’iy ameiandika hadithi hii katika kitabu chake at-Tawasul Ilaa Haqiqatut-Tawassul.169 Vidokezo muhimu vya kukumbushana Mawahabi wenye chuki binafsi na ushabiki, ili kuthibitisha makusudio yao na malengo yao wameng’ang’ania mambo mengi katika kuwakufurisha Waislamu na kuwatuhumu kwa ufasiki, eti kwa kuwa Waislamu hao wanatawasali kupitia watu wema, na hivyo kwa visingizio hivi ambavyo vinafanana na visingizio vya watoto wanapotofautiana wao kwa wao, Mawahabi wamekhalifu Aya na riwaya zilizotajwa hapo nyuma ambazo zinathibitisha kuwa Tawassuli kwa aina zake mbalimbali ni halali na ni ruhusa. Mara wao husema: Kilichozuiliwa ni kutawasali kupitia watu watukufu na walio wema, ama kutawasali kwa maana ya kuomba dua na kutaka kuombewa na hawa, hilo ni jambo linaloruhusiwa. 167
Sahih Bukhar Juz. 2, Uk. 16. at-Tawasul Ilaa Haqiqatut-Tawassul Uk. 329.
168
Tazama katika As-Sawaiqul-Muhriqah Uk. 274 – Mtarjumi.
169
at-Tawasul Ilaa Haqiqatut-Tawassul Uk. 329. 202
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 202
11/25/2014 3:03:52 PM
Ushia: Hoja na Majibu
Na mara husema: Hakika Tawassuli inayoruhusiwa ni ile inayofanyika zama za uhai wao, ama baada ya kifo chao hairuhusiwi, kwa sababu uhusiano wetu na wao unakatika pale tu wanapoihama nyumba hii ya dunia, kwa sababu Qur’ani Tukufu inasema:
ص َّم ال ُّد َعا َء إِ َذا ُّ ك َال ُتسْ ِم ُع ْال َم ْو َت ٰى َو َال ُتسْ ِم ُع ال َ إِ َّن ين َ َولَّ ْوا م ُْد ِب ِر “Kwa hakika wewe huwezi kuwasikilizisha wafu wala kuwasikilizisha viziwi wanapogeuka kurudi nyuma.” (Sura Namli: 80).
Lakini ukosoaji huu usiyo na mashiko kwa kweli unatia aibu, hiyo ni kwa sababu: Kwanza: Aya za Qur’ani zinazohusu aina zote za Tawassuli hazijafungwa na sharti lolote, na hivyo kwa mujibu wa hukumu ya kutokuwepo masharti na mipaka katika Aya hizo, Tawassuli ni halali na inaruhusiwa. Na wala hakuna ukinzani wowote baina yake na dhana ya Tauhidi katika ibada au dhana ya Tauhidi katika matendo, kwani Qur’ani Tukufu inasema: “Na tafuteni njia (al-Wasilah) ya kumfikia,” na tulisema kuwa al-Wasilah (njia) ni kitu anachokitumia mtu kujiweka karibu na Mwenyezi Mungu. Ndiyo, ni kitu gani kinaweza kuwaweka karibu na Mwenyezi Mungu kama dua ya Mtukufu Mtume (saww), au cheo cha Mtukufu Mtume (saww) au yeye mwenyewe Mtukufu Mtume (saww), na hiyo ni kwa sababu ya utiifu wake, unyenyekevu wake, kumwabudu kwake Mwenyezi Mungu Mtukufu na sifa zake zenye kumuweka karibu zaidi na Mwenyezi Mungu. Hivyo 203
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 203
11/25/2014 3:03:52 PM
Ushia: Hoja na Majibu
mtu huomba kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu kupitia mambo haya, na wala hakuna dalili inayofunga na kuzuia al-Wasilah (njia) kwenye amali njema tu, kama wasemavyo Mawahabi. Na tuliyoyataja hayakinzani na dhana ya Tauhidi katika ibada, kwa sababu anayeabudiwa ni Mwenyezi Mungui tu na si Mtukufu Mtume (saww), na wala pia hayakinzani na dhana ya Tauhidi katika matendo, kwa sababu chanzo cha kheri na shari hakiwezi kuwa kitu kingine isipokuwa ni Mwenyezi Mungu, na kila anachokimiliki mwanadamu ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu na ni kwa kupitia yeye Mwenyezi Mungu. Basi tunangojea nini baada ya Aya hizi kutofungwa na sharti lolote? La sivyo hali yetu itakuwa sawa na hali ya mtu anayetafuta kisingizio pindi Qur’ani inaposema: “Basi someni kilicho chepesi katika Qur’ani…” (Sura Muzamil: 20), yeye anasema: ‘Je inaruhusiwa kusoma Qur’ani tukiwa tumesimama au la? Au tukiwa tumelala au la?’ Hakika kutokuwa na mipaka katika Aya kunasema: Hakika aina zote za usomaji zinaruhusiwa, sawa iwe nyumbani au safarini, tukiwa na udhu au bila udhu, isipokuwa kama itapatikana dalili nyingine inayothibitisha kinyume na hivyo. Hakika matamko yasiyofungwa na sharti wala mpaka yaliyopo ndani ya Qur’ani yanafanya kazi maadamu tu hayajafungwa kwa sharti lolote, na Aya za Tawassuli nazo ndivyo zilivyo hazijafungwa na sharti lolote, hivyo matamko ya Aya za Qur’ani ambayo hayajafungwa na sharti lolote yanafanya kazi ikiwa tu hatujapata sharti lolote lenye kuyafunga, na hivyo tunaweza kutenda kwa mujibu wa matamko hayo, na wala si sahihi kutafuta visingizio ili kuleta mjadala usio na maana yoyote. 204
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 204
11/25/2014 3:03:52 PM
Ushia: Hoja na Majibu
Pili: Riwaya zilizopatikana katika mada ya Tawassuli – na ambazo tumeshataja sehemu katika hizo – zina aina tofauti za Tawassuli, na aina zote hizi zinaruhusiwa, nazo ni: 1.
Kuatawasali kupitia Mtukufu Mtume mwenyewe (saww) kama ilivyokuja katika kisa cha kipofu.
2.
Kutawasali kupitia kaburi la Mtukufu Mtume (saww) kama ilivyokuja katika baadhi ya riwaya.
3.
Kutawasali kupitia dua ya Mtukufu Mtume (saww).
4.
Kutawasali kwa uombezi wa Mtukufu Mtume (saww).
Na aina nyingine ambazo zimepatikana katika riwaya, na hivyo kuwepo huku kwa aina mbalimbali na tofauti za Tawassuli hakuachi tena nafasi ya watu wa mijadala na visingizio kujadili. Tatu: Inamaanisha nini kutawasali kupitia Mtukufu Mtume mwenyewe? Ni kwa nini Mtume (saww) anakuwa mheshimiwa kwetu? Na kwa nini tunamfanya muombezi wetu mbele ya Mwenyezi Mungu? Kwa sababu Mtukufu Mtume (saww) anajitofautisha kwa utiifu na unyenyekevu wa kina na wa dhati kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Hivyo kutawasali kwetu kupitia Mtume (saww) yeye mwenyewe ni kutawasali kupitia utiifu wake, ibada zake na matendo yake. Na hii ndio aina yenyewe ya Tawassuli wanayoiruhusu Mawahabi wenye chuki binafsi na ushabiki, nayo ni Tawassuli ya kupitia matendo ya utiifu, hivyo ugomvi uliopo ni wa kimatamshi tu. Na la kustaajabisha ni kwamba baadhi yao wanakanusha maisha ya barzakhi ya Mtukufu Mtume (saww), na wanaitakidi 205
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 205
11/25/2014 3:03:52 PM
Ushia: Hoja na Majibu
kuwa kifo chake ni sawa na kifo cha makafiri, wakati ambapo Qur’ani Tukufu imetaja kuwa mashahidi wako hai milele:
ﷲ أَمْ َوا ًتا ۚ َب ْل ِ َّ يل َ َو َال َتحْ َس َبنَّ الَّذ ِ ِين قُ ِتلُوا فِي َس ِب ون َ ُأَحْ َيا ٌء عِ ْن َد َرب ِِّھ ْم يُرْ َزق “Na usiwadhanie kabisa wale waliouawa katika njia ya Mwenyezi Mungu kuwa wamekufa, bali wako hai mbele ya Mola wao wanaruzukiwa.” (Sura Imran: 169). Je cheo cha Mtukufu Mtume ni kidogo kuliko cha mashahidi? Achilia mbali hilo, vipi kuhusu salamu tunayomtolea katika Sala? Ikiwa hatujui kuwa kutawasali baada ya kifo chake ni kutawasali kupitia mtu aliye hai milele basi salamu zote hizi hazina maana. Na ni Mwenyezi Mungu tu ndiye wa kumkimbilia dhidi ya chuki hii binafsi yenye kupofua macho na kuziba masikio, ambayo inampeleka mwanadamu katika ujinga. Na bahati nzuri ni kwamba baadhi yao wanaamini uwepo wa maisha ya barzakhi, na kwa ajili hiyo ni lazima ukosoaji wao utoweke.
Wazembe na wapindukiaji Kundi la kwanza ni la wazembe: Nao ni wale wenye kukanusha kutawasali kupitia Mawalii wa Mwenyezi Mungu, na sisi tunasimama baina ya makundi mawili, lenye kuzembea na kupindukia. Yeyote atakayezembea katika kufahamu mas’ala ya Tawassuli na akaikataa kabisa Tawassuli, na akadai hairuhusiwi Tawassuli ambayo imeruhusiwa na Aya za Qur’ani na riwaya, na akadhani kuwa itampelekea kukanusha Tauhidi, basi mtu huyo yumo katika makosa, kwani kutawasali kupitia Mawalii wa Mwenyezi Mungu kwa ajili 206
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 206
11/25/2014 3:03:52 PM
Ushia: Hoja na Majibu
ya utiifu wao, ibada zao, matendo yao na ukuruba wao kwa Mwenyezi Mungu, ni kusisitiza mas’ala ya Tauhidi, ambapo hao wenye kutawasali wanaomba yote wanayoyataka kutoka kwa Mwenyezi Mungu tu Muweza. Kundi la pili: Hili ni la wenye kupindukia: Nao ni wale ambao wanafanya Tawassuli kama njia ya kupindukia mipaka, na hatari ya hawa si ndogo kuliko hatari ya kundi la kwanza, ni watu ambao ibara zao hazioani na dhana ya Tauhidi katika matendo, au wana ibara ambazo haziafikiani na dhana ya Tauhidi katika ibada, wakati ambapo hakuna mwenye kuathiri katika ulimwengu isipokuwa Allah. Kutokana na hili kama ambavyo tunakabiliana na wenye kukanusha Tawassuli sahihi ndivyo tunavyowaongoza, kuwaelekeza, kufichua na kusahihisha makosa ya hao wenye kupindukia, hivyo ni lazima kuwaelekeza wapindukiaji na watu wenye mlengo wa kupindukia, na kuwarejesha katika njia sahihi. Na ukweli ni kwamba tunaweza kusema kuwa hakika moja ya sababu zilizopelekea kuwepo watu wenye kukanusha Tawassuli ni kule kupindukia na kuvuka mipaka kwa watu wenye kuunga mkono Tawassuli, kwani pindi watu hawa wanapowasilisha sura ya upindukiaji basi ni lazima mbele yao kujitokeze kundi lenye kuzembea, na kwa kweli kanuni hii hujitokeza katika mas’ala yote ya kiitikadi, kijamii na kisiasa, hivyo daima kuna ulazima baina ya makundi haya ya kimakosa, na yote mawili yanashirikiana katika kosa, yote mawili hayako sahihi. Tawassuli peke yake haitoshi Ni lazima tuwaelimishe watu kuwa wasitosheke tu kutawasali kupitia Mawalii wa Mwenyezi Mungu na watu wema, kwa sababu kiasili kutawasali ni somo kwetu, kwa nini tunata207
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 207
11/25/2014 3:03:52 PM
Ushia: Hoja na Majibu
wasali kupitia watu hawa? Ni kwa sababu matendo yao ni mema, hivyo basi ni wajibu juu yetu kutenda matendo mema, hivyo Tawassuli inatupa somo kwamba kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu hupatikana kwa njia ya matendo mema na kwa kutawasali kupitia Mawalii wa Mwenyezi Mungu kwa sababu ya matendo yao mema, wao ni watu walio karibu na Mwenyezi Mungu, na sisi tunawaomba watuombee kwa Mwenyezi Mungu, hivyo ni wajibu juu yetu kupita njia walioipita, hivyo ni lazima tuibadili Tawassuli na kuifanya chuo cha kumlea mwanadamu na kumstawisha, na wala tusikomee kwenye kutawasali tu na tukasahau malengo ya juu ya Tawassuli, na hili ni jambo muhimu yapasa kulizingatia. Tawassuli katika mambo ya kiasili Nukta nyingine ni kwamba Tawassuli ya kupitia ulimwengu wa sababu inapatikana katika mambo ya kisharia kama inavyopatikana katika mambo ya kiasili, na Tawassuli zote mbili hazikinzani na dhana ya Tauhidi, kwani sisi tunapotaka kupata matokeo mazuri katika maisha yetu ya kilimo tunakimbilia kwenye sababu, hivyo tunailima ardhi, tunapanda mbegu, tunamwagilia maji mimea, tunapambana na maafa, na tunavuna mavuno katika wakati wake, ili tufaidike nayo katika maisha yetu. Je kupitia sababu hizi ili kufikia lengo kunatufanya tumsahau Mwenyezi Mungu? Na hivi je kuitakidi kwamba ardhi huilisha mizizi ya mimea, au mwanga wa jua na matone ya mvua ambayo huleta uhai ndio huotesha maua na matunda, na kwa jumla ni kuwa hivi je kuamini ulimwengu wa sababu kunakinzana na dhana ya Tauhidi katika matendo?
208
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 208
11/25/2014 3:03:52 PM
Ushia: Hoja na Majibu
Ukweli ni kwamba hakukinzani na dhana ya Tauhidi, kwa sababu sisi tunakimbilia kwenye ulimwengu wa sababu huku tukiamini kuwa chanzo kikuu cha sababu na msababishaji mkuu ni Mwenyezi Mungu Mtukufu, na ni kama methali isemayo: “Sifa zote hizi anastahiki Mfalme adhimu.”170 Hivyo kama ambavyo kutawasali kupitia sababu za asili hakukinzani na dhana ya Tauhidi katika matendo, ndivyo hivyo hivyo katika ulimwengu wa sharia, kwa sababu kutawasali kupitia Manabii, Mawalii na Maasumu na kuwataka watuombee kwa Mwenyezi Mungu hakukinzani kamwe na dhana ya Tauhidi. Ndiyo, hapa kumezuka kundi la upindukiaji ambalo linakataa ulimwengu wa sababu, kwa sababu wao wanadhani kuwa kuamini ulimwengu wa sababu kunakinzana na dhana ya Tauhidi katika matendo, hivyo wanasema: Hakika moto hauchomi, bali Mwenyezi Mungu ndiye anayekichoma kitu hicho pindi kinapokuwa karibu na moto. Na hakika maji hayazimi moto bali Mwenyezi Mungu ndiye anayeuzima pindi maji yanapoufikia moto, hivyo hivyo wanakataa mahusiano yaliyopo kati ya sababu na kisababishwa, mahusiano ambayo yako wazi dhahiri shahiri katika ulimwengu wa maumbile. Wakati ambapo Qur’ani Tukufu inakiri kuwepo kwa ulimwengu wa sababu na unautangaza wazi wazi kwa kusema:
َو ِمنْ آ َيا ِت ِه ي ُِري ُك ُم ْال َبرْ َق َخ ْو ًفا َو َط َمعًا َو ُي َن ِّز ُل م َِن ض َبعْ دَ َم ْو ِت َھا ۚ إِنَّ فِي َ ْال َّس َما ِء َما ًء َفيُحْ ِيي ِب ِه ْاألَر ٍ ٰ َذل َِك َآل َيا ون َ ُت لِ َق ْو ٍم َيعْ ِقل 170
Ni methali ya Kiajemi. 209
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 209
11/25/2014 3:03:53 PM
Ushia: Hoja na Majibu
“Na katika Ishara Zake ni kuwaonyesha umeme kwa hofu na tamaa, na kuwateremshia maji kutoka mbinguni, na kwayo akaihuisha ardhi baada ya kufa kwake. Hakika katika hayo kuna ishara kwa watu wenye akili.” (Sura Rum: 24). Hivyo neno “na kwayo akaihuisha ardhi” inamaanisha mvua huihuisha ardhi, na Aya hii ina dalili bayana na ya wazi ikikiri na kukubali uwepo wa ulimwengu wa sababu, lakini sababu hizi haziathiri kwa kujitegemea zenyewe binafsi, kila zilichonacho ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
Hivyo athari hizi zinazoonekana ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu, hivyo kama ambavyo wenye kukanusha na kukataa asili wako katika makosa na mghafala, kadhalika wenye kukataa sababu katika ulimwengu wa sharia. Tunataraji watayatia akilini yale yaliyotajwa na watajitenga na chuki binafsi na ushabiki na watarejea katika njia sahihi na wataacha safari ya kukufurisha na kuwatuhumu Waislamu kwa ufasiki na wataungana pamoja na Waislamu wa ulimwengu, na watasimama dhidi ya maadui ambao wamemfanya Mwenyezi Mungu, Qur’ani na Uislamu kuwa shabaha ya mashambulizi yao, na watabainisha mafunzo ya Uislamu kwa jamii yote ulimwenguni huku yakiwa hayana shirki, upindukiaji wala upungufu. Shaban tukufu 1426 Nasir Makarim Shirazi.
210
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 210
11/25/2014 3:03:53 PM
Ushia: Hoja na Majibu
BIBLIOGRAFIA 1.
Qur’ani Tukufu
2.
Nahjul-Balaghah.
3.
Alaur-Rahman cha Muhammad Jawad al-Balaghiy.
4.
Ahkamul-Qur’ani cha Ahmad bin Ali Razi al-Jasas.
5.
Ahkbar Makkah cha al-Azruqiy.
6.
al-Ahkam cha Ali bin Hazmi al-Undulusiy.
7.
al-Iswabah Fii Tamyizis-Swahabah cha Ibn Hajar alAsqalaniy.
8.
at-Tawasul Ilaa Haqiqatut-Tawassul cha Muhammad Nasib Riqa’iy.
9.
al-Khasaisun-Nabawiyyah cha al-Hafidh as-Suyutiy.
10.
as-Sunan al-Kubra cha Ahmad bin Husain al-Bayhaqiy.
11.
al-Aqdu al-Farid cha Ahmad bin Muhammad bin Abdu Rabih al-Undulusiy.
12.
al-Ghadir cha allamah al-Amin.
13.
al-Fiqhi Alal-Madhahib al-Arba’ah cha Abdur-Rahman al-Jaziriy.
14.
al-Mabsut cha Shamsud-Din Abu Bakri Sarkhasiy.
15.
al-Muujam al-Kabir cha Sulayman bin Ahmad Tabaraniy. 211
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 211
11/25/2014 3:03:53 PM
Ushia: Hoja na Majibu
16.
an-Naswayihu al-Kafiyah.
17.
Ansabul-Ashraf cha Ahmad bin Yahya al-Baladhiriy.
18.
Biharul-An’war cha Allamah al-Majlisiy.
19.
Taarikh Ibn Asakir cha Ibn Asakir.
20.
Taarikh Ibn Kathir cha Ismail bin Kathir al-Qarashiy.
21.
Taarikh Tabariy cha Muhammad Jariri Tabari.
22.
Tafsir ad-Durul-Manthur cha Jalalud-Din as-Suyutiy.
23.
Tafsirul-Qur’ani al-Adhim cha Ibn Kathir ad-Damashqiy.
24.
Tafsirul-Manar cha Muhammad Rashid Ridha.
25.
at-Tafsiru al-Munir cha Wahbah Zuhayliy.
26.
Tafsirul-Qurtubiy cha Abu Abdullah Muhammad bin Ahmad al-Qurtubiy.
27.
at-Tafsiru al-Kabir cha Imam Fakhru Raziy.
28.
Tafsirul-Kashaf cha Jarullah Zamakhshari.
29.
Tahniatullah as-Sadiq al-Mahbub cha Saqaf.
30.
Jaridatul-Jazirah, Toleo la 6826.
31.
Jawahirul-Matalib Fii Manaqib Imam Ali bin Abi Talib cha Muhammad bin Ahmad ad-Damashqiy as-Shafi’iy.
32.
Hata La Nan’khadiu cha Abdullah al-Muwaswiliy.
33.
Dalailun-Nubuwah cha Ahmad bin Husain al-Bayhaqiy.
34.
Rijalun-Najashiy cha Ahmad bin Ali an-Najashiy.
35.
Ruhul-Maaniy cha Mahmud al-Alusiy. 212
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 212
11/25/2014 3:03:53 PM
Ushia: Hoja na Majibu
36.
Safinatul-Bihar cha Sheikh Abbas al-Qummiy.
37.
Sunan Tirmidhiy cha Muhammad bin Isa Tirmidhiy.
38.
Sunan Daramiy cha Abdullah bin Bahram ad-Daramiy.
39.
Sharhu Muniyatul-Muswaliy cha Ibrahim bin Muhammad al-Halbiy.
40.
Sahih Bukhari cha Muhammad bin Ismail Bukhari.
41.
Sahih Muslim cha Muslim bin Hujjaj Nisaburiy.
42.
at-Tabaqat al-Kubra cha Ibn Saad.
43.
Ilalus-Sharaii cha Sheikh as-Saduq.
44.
Awailul-Lialiy cha Ibn Abi Jamhur al-Ihsaiy.
45.
Fat’hul-Bariy Fii Sharhi Sahih Bukhari cha Ibn Hajar al-Asqalaniy.
46.
Fadhailus-Sahabah cha Ahmad bin Hanbal.
47.
Fahrasti cha Sheikh Tusiy.
48.
al-Kafiy cha Muhammad bin Ya’qub al-Kulayniy.
49.
Kanzul-Ummal cha Ali al-Mutaqiy al-Hindiy.
50.
Majmauz-Zawaid cha Ali bin Abu Bakri al-Haythamiy.
51.
Majmuatur-Rasail Wal-Masail cha Ibn Taymiyyah.
52.
Mustadrakus-Sahihayn cha al-Hakim an-Nisaburiy.
53.
Musnadul-Bazzaz cha Abu Bakri Ahmad bin Amru bin Abdul-Khaliq al-Atiqiy al-Bazzaz.
54.
Musnad Abi Shaybah cha Abdullah bin Muhammad bin Abi Shaybah. 213
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 213
11/25/2014 3:03:53 PM
Ushia: Hoja na Majibu
55.
Musannaf Abdur-Razaq cha Abdur-Razaq bin Hamam as-San’aniy.
56.
Muujamul-Buldan cha Yaqut bin Abdullah al-Hamawi.
57.
al-Mughniy cha Ibn Qadamah.
58.
Mafatihul-Ghaybi cha Imam Fakhru Razi.
59.
Mafahim Yajib An’tuswahahu cha Yusuf bin Alawi alMalikiy.
60.
Man Layahdhuruhu al-Faqihu cha Sheikh as-Saduq.
61.
al-Mawahib ad-Daniyyah cha Ahmad bin Muhammad al-Qastalaniy – Muhammad bin Abdul-Baqiy az-Zarqaniy.
62.
Wasailus-Shiah cha Sheikh al-Huru al-Amiliy.
214
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 214
11/25/2014 3:03:53 PM
Ushia: Hoja na Majibu
ORODHA YA VITABU VILIVYOCHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION 1. Qur’ani Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka ya Thelathini 2.
Uharamisho wa Riba
3.
Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza
4.
Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili
5.
Hekaya za Bahlul
6.
Muhanga wa Imamu Husein (A.S.)
7.
Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.)
8.
Hijab vazi Bora
9.
Ukweli wa Shia Ithnaashari
10.
Madhambi Makuu
11.
Mbingu imenikirimu
12.
Abdallah Ibn Saba
13.
Khadijatul Kubra
14. Utumwa 15.
Umakini katika Swala
16.
Misingi ya Maarifa
17.
Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia 215
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 215
11/25/2014 3:03:53 PM
Ushia: Hoja na Majibu
18.
Bilal wa Afrika
19. Abudharr 20.
Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu
21.
Salman Farsi
22.
Ammar Yasir
23.
Qur’ani na Hadithi
24.
Elimu ya Nafsi
25.
Yajue Madhehebu ya Shia
26.
Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur’ani Tukufu
27. Al-Wahda 28.
Ponyo kutoka katika Qur’ani.
29.
Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii
30.
Mashukio ya Akhera
31.
Al Amali
32.
Dua Indal Ahlul Bayt
33.
Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna.
34.
Haki za wanawake katika Uislamu
35.
Mwenyezi Mungu na Sifa Zake
36.
Kumswalia Mtume (s)
37.
Nafasi za Ahlul Bayt (a.s)
38. Adhana. 39
Upendo katika Ukristo na Uislamu 216
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 216
11/25/2014 3:03:53 PM
Ushia: Hoja na Majibu
40.
Tiba ya Maradhi ya Kimaadili
41.
Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu
42.
Kupaka juu ya khofu
43.
Kukusanya swala mbili
44.
Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara
45.
Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya
46.
Kusujudu juu ya udongo
47.
Kusherehekea Maulidi Ya Mtume (s)
48. Tarawehe 49.
Malumbano baina ya Sunni na Shia
50.
Kupunguza Swala safarini
51.
Kufungua safarini
52.
Umaasumu wa Manabii
53.
Qur’ani inatoa changamoto
54.
as-Salaatu Khayrun Mina -’n Nawm
55.
Uadilifu wa Masahaba
56.
Dua e Kumayl
57.
Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu
58.
Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake
59.
Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata
60. Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mtume Muhammad (s) 61.
Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza 217
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 217
11/25/2014 3:03:53 PM
Ushia: Hoja na Majibu
62.
Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili
63.
Kuzuru Makaburi
64.
Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza
65.
Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili
66.
Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu
67.
Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne
68.
Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano
69.
Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita
70.
Tujifunze Misingi Ya Dini
71.
Sala ni Nguzo ya Dini
72.
Mikesha Ya Peshawar
73.
Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu
74. Ubora wa Imam ‘Ali Juu ya Maswahaba Na Ushia ndio njia iliyonyooka 75.
Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake
76. Liqaa-u-llaah 77.
Muhammad (s) Mtume wa Allah
78.
Amani na Jihadi Katika Uislamu
79.
Uislamu Ulienea Vipi?
80.
Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s)
81.
Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s)
82.
Urejeo (al-Raja’a )
218
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 218
11/25/2014 3:03:53 PM
Ushia: Hoja na Majibu
83. Mazingira 84.
Utokezo (al - Badau)
85.
Hukumu ya kujenga juu ya makaburi
86.
Swala ya maiti na kumlilia maiti
87.
Uislamu na Uwingi wa Dini
88.
Mtoto mwema
89.
Adabu za Sokoni
90.
Johari za hekima kwa vijana
91.
Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza
92.
Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili
93.
Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu
94. Tawasali 95.
Imam Mahdi katika Usunni na Ushia
96.
Hukumu za Mgonjwa
97.
Sadaka yenye kuendelea
98.
Msahafu wa Imam Ali
99.
Ngano ya kwamba Qur’ani imebadilishwa
100. Idil Ghadiri 101. Kusoma sura zenye Sijda ya wajibu 102
Hukumu zinazomhusu mkuu wa kazi na Mfanyakazi
103. Huduma ya Afya katika Uislamu 104. Sunan an-Nabii 219
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 219
11/25/2014 3:03:53 PM
Ushia: Hoja na Majibu
105. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza) 106. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili) 107. Shahiid Mfiadini 108. Kusalia Nabii (s.a.w) 109. Ujumbe -Sehemu ya Kwanza 110. Ujumbe - Sehemu ya Pili 111.
Ujumbe - Sehemu ya Tatu
112. Ujumbe - Sehemu ya Nne 113. Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu 114. Hadithi ya Thaqalain 115. Maarifa ya Kiislamu 116. Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza 117. Ukweli uliopotea sehemu ya Pili 118. Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu 119. Ukweli uliopotea sehmu ya Nne 120. Ukweli uliopotea sehmu ya Tano 121. Johari zenye hekima kwa vijana 122. Safari ya kuifuata Nuru 123. Fatima al-Zahra 124. Myahudi wa Kimataifa 125. Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi 126. Visa vya kweli sehemu ya Kwanza 220
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 220
11/25/2014 3:03:53 PM
Ushia: Hoja na Majibu
127. Visa vya kweli sehemu ya Pili 128. Muhadhara wa MaUlamaa 129. Mwanadamu na Mustakabali wake 130. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Kwanza) 131. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Pili) 132. Khairul Bariyyah 133. Uislamu na mafunzo ya kimalezi 134. Vijana ni Hazina ya Uislamu. 135. Yafaayo kijamii 136. Tabaruku 137. Taqiyya 138. Vikao vya furaha 139. Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje? 140. Visa vya wachamungu 141. Falsafa ya Dini 142. Azadari-Kuhuzunika na Kuomboleza 143. Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah 144. Mtazamo Mpya - Wanawake katika Uislamu 145. Kuonekana kwa Allah 146. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza) 147. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili) 221
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 221
11/25/2014 3:03:53 PM
Ushia: Hoja na Majibu
148. Ndugu na Jirani 149. Ushia ndani ya Usunni 150. Maswali na Majibu 151. Mafunzo ya hukmu za ibada 152. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 1 153
Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 2
154. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 3 155. Abu Huraira 156. Vipengee kadhaa katika Swala ya Jamaa na Msikiti. 157. Mazingatio kutoka katika Qur’ani - Sehemu ya Kwanza 158. Mazingatio kutoka kaitka Qur’ani - Sehemu ya Pili 159. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya kwanza 160. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya Pili 161. Qur’ani Tukufu – Pamoja na Tarjuma ya Kiswahili 162. Falsafa ya Mageuzi ya Imam Husein (a.s) 163. Amali za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani 164. Elimu ya Tiba za Kiislamu - Matibabu ya Maimamu 165. Uislamu Safi 166. Majlisi za Imam Husein Majumbani 167. Mshumaa. 168. Uislam wa Shia 169. Amali za Makka 222
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 222
11/25/2014 3:03:53 PM
Ushia: Hoja na Majibu
170. Amali za Madina 171. Asili ya Madhehebu katika Uislamu 172. Sira ya Imam Ali kuhusu Waasi 173. Ukweli uliofichika katika neno la Allah 174. Uislamu na Mifumo ya Uchumi 175. Umoja wa Kiislamu na Furaha 176. Mas’ala ya Kifiqhi 177. Jifunze kusoma Qur’ani 178. As-Sahifatul Kamilah as-Sajjadiyyah 179. Hayya ‘Alaa Khayri’l-’Amal Katika Adhana 180. Ukweli kuhusu Funga ya Siku ya Ashura 181. Dua za Miezi Mitatu Mitukufu (Rajabu, Shaabani na Ramadhani) 182. Uadilifu katika Uislamu 183. Mahdi katika Sunna 184. Jihadi ya Imam Hussein (‘as) 185. Kazi na Bidii ni Njia ya Maendeleo 186. Abu Talib – Jabali Imara la Imani 187. Ujenzi na Utakaso wa Nafsi 188. Vijana na matarajio ya baadaye 189. Usalafi – Historia yake, maana yake na lengo lake 190. Ushia – Hoja na Majibu
223
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 223
11/25/2014 3:03:53 PM
Ushia: Hoja na Majibu
191. Mateso ya Dhuria wa Mtume (saww) 192. Maombolezo – Msiba wa Bwana wa Mashahidi (a.s.) 193. Shahidi kwa Ajili ya Ubinadamu 194. Takwa 195. Mwonekano wa Upotoshaji katika Hazina ya Kiislamu 196. Amirul Muuminina (‘as) na Makhalifa 197. Uongozi na Utawala katika Mwanendo wa Imam ‘Ali (‘a) 198. Kuelewa Rehema ya Mwenyezi Mungu 199. Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (as) 200. Upotoshaji Dhahiri katika Turathi ya Kiislamu 201. Mtazamo kuhusu msuguano wa Kimadhehebu 202. Nchi na Uraia - Haki na wajibu kwa Taifa 203. Mtazamo wa Ibn Taymiya kwa Imam Ali (as)
224
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 224
11/25/2014 3:03:53 PM
Ushia: Hoja na Majibu
VITABU VINNE VIFUATAVYO VIMETAFSIRIWA KWA LUGHA KINYARWANDA 1.
Amateka Na Aba’Khalifa
2.
Nyuma yaho naje kuyoboka
3.
Amavu n’amavuko by’ubushiya
4.
Shiya na Hadithi
225
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 225
11/25/2014 3:03:53 PM
MUHTASARI
226
03_Ushia - Hoja na Majibu_13_June_2013.indd 226
11/25/2014 3:03:53 PM