Uswalihina dhahiri na batini yake

Page 1

USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE ‫التدين بين المظهر والجوهر‬

Kimeandikwa na: Sheikh Hasan Musa as-Saffar

Kimetarjumiwa na: Abdul-Karim Juma Nkusui


‫ترجمة‬

‫التدين بين المظهر والجوهر‬

‫تأليف‬ ‫حسن بن موسى الصفار‬

‫من اللغة العربية إلى اللغة السواحلية‬


©Haki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION

ISBN: 978 - 9987 –17 – 075 – 3

Kimeandikwa na: Sheikh Hasan Musa as-Saffar

Kimetarjumiwa na: Abdul-Karim Juma Nkusui

Kimehaririwa na: Alhaji Hemedi Lubumba Na AlHaji Ramadhani S. K. Shemahimbo

Kimepangwa katika Kompyuta na: Al-Itrah Foundation

Toleo la kwanza: Septemba, 2014 Nakala: 2000

Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. - 19701, Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 / 2127555 Barua Pepe: alitrah@yahoo.com Tovuti: www.ibn-tv-com Katika mtandao: www.alitrah.info



Yaliyomo Neno la Mchapishaji........................................................................1

Utangulizi.........................................................................................3

Faragha ya Kiroho............................................................................6

Matokeo ya Kushikamana na Dini...................................................8

Kuwalea Watu Katika Maadili ya Kuwapenda Watu Wengine......34

Kuheshimu Utaratibu na Kanuni...................................................44

Mtazamo wa Kisharia Kuhusu Uzembe wa Wafanyakazi.............57

Taasisi za Afya na Umuhimu wa Wajibu Wao...............................65

Upotovu: Sababu na Utatuzi Wake................................................76

v


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

‫بسم اهلل الرحمن الرحيم‬ Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu. Sifa zote njema anastahiki Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa viumbe. Eee Mwenyezi Mungu mteremshie rehema Muhammad Mwisho wa Manabii na Hitimisho la Mitume, na kizazi chake chema kitwaharifu na Maswahaba wake wema.

vi


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

‫بسم اهلل الرحمن الرحيم‬ NENO LA MCHAPISHAJI

K

itabu ulichonacho mikononi mwako asili yake ni cha lugha ya Kiarabu kwa jina la, at-Tadayyun Bayna ‘l-Mudhhiri wa ‘lJawhar, kilichoandikwa na Sheikh Hasan Musa as-Saffar. Sisi tumekiita, Uswahilihina Dhahiri na Batini Yake. Mwandishi wa kitabu hiki anazungumzia kuhusu ibada za dhahiri ambazo utekelezaji wake una makusudio ya kumjenga muumini kusafisha moyo wake hadi kufikia kipeo cha takwa (takua). Miongoni mwa ibada hizo ni kufuata sheria katika vipengele mbalimbali cha maisha zikiwemo sheria za nchi, jamii, n.k. Lengo kubwa la muumini ni kufikia kiwango kizuri cha takwa, na ili kufikia lengo hili inahitajika juhudi kubwa katika matendo yote ya ibada. Uswalihina (ushikaji wa dini) hauko katika utekelezaji wa dhahiri tu wa ibada hizo za swala, saumu, zaka na Hija, n.k., bali shuruti yake ni kupatikana batini ya ibada hizo. Na batini ya ibada hizo ni udhati, usafi na unyenyekevu ambao humpandisha muumini katika daraja ya takwa (uchamungu) kwa kadiri ya utakasaji wake wa ndani. Kwa ufupi, uswahilina si udhahiri wa kuswali na kufunga tu, bali ni kuyajenga pia yale yaliyomo moyoni mwako ambayo hayaonekani ili kuwa na takwa. Katika kitabu hiki utajifunza namna ya utekelezaji wa masuala haya ambayo yatakufanya ufikie hali nzuri ya uchamungu. Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni vitu ambavyo havina nafasi tena katika akili za watu. 1


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

Kutoka na ukweli huu, taasisi yetu ya Al-Itrah imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumini yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili. Tunamshukuru ndugu yetu Abdul-Karim Juma Nkusui kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kukitarjumi kitabu hiki kwa Kiswahili kutoka lugha ya asili ya Kiarabu. Aidha tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake. Allah awalipe wote malipo mema hapa duniani na kesho Akhera – Amin. MCHAPISHAJI AL-ITRAH FOUNDATION

2


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

‫بسم اهلل الرحمن الرحيم‬ UTANGULIZI

D

ini ni utajiri mkubwa wa kiroho na ni hazina kubwa ya thamani, lakini wengi kati ya wanaojinasibisha na dini wanaghafilika juu ya ukubwa wa nafasi yake katika maisha yao, na juu ya nguvu kubwa ambayo inaizunguka dini ndani ya nafsi zao, na wanatosheka na dini kwa kutekeleza kwao muonekano wa ibada na kufanya minasaba bila ya kuzinduka ili kugundua nguvu yake kubwa, na uwezo wake wenye kuathiri ambao unaweza kutajirisha maisha yao kwa matumaini na wema, na kuelekeza nyendo zao ili kuzalisha, kujenga na kufanya kheri katika nyanja mbalimbali. Hakika dini ni maadili na misingi anayoiamini mwanadamu ili iongoze maisha yake, kutengeneza utu wake na kurekebisha nyendo zake, na sio itikadi ya kinadharia tu inayozunguka moyo wake, na wala sio vitendo vya ibada tu alivyozoea kuvitekeleza na kuvifanya. Na moja ya athari muhimu ya dini ni utulivu wa nafsi, ambapo mchamungu anaamini kwamba Mungu Muweza Mweye hekima, ndiye mwenye kuendesha mambo yake, ulimwengu na maisha yake, na hivyo nafsi yake hujaa hali ya kumtegemea na kumtawakali Mola Wake, na hapo anakuwa imara na mvumilivu mbele ya matatizo na changamoto, anaamiliana na ugumu wa maisha na matatizo yake kwa imani kwamba ni mitihani na majaribu, na hivyo anataka msaada kutoka kwa Mwenyezi Mungu ili kuivuka mitihani hiyo kwa uaminifu na ufaulu. Hakimbii matatizo wala hafikirii kujinyonga, hapatwi na masikitiko na wala hatawaliwi na hali ya kukata tamaa, yeye ni muumini na: 3


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

َ ‫س ِم ْن َر ْو ِح اللهَِّ إِ اَّل ْال َق ْو ُم ْال َكا ِف ُر‬ ‫ون‬ ُ َ‫إِنَّ ُه اَل َييْأ‬ “Hakika hawakati tamaa na faraja ya Mwenyezi Mungu isipokuwa watu makafiri.” (Surat Yusuf: 87).

Hakika anachukua utulivu na anapata azma kwa kuwasiliana kwake na Mola Wake na kuhudhurisha utajo wake (swt) katika moyo wake:

َ ‫الَّ ِذ‬ َِّ‫ين آ َمنُوا َو َت ْط َم ِئ ُّن ُقلُوبُ ُه ْم ِب ِذ ْك ِر اللهَِّ أَ اَل ِب ِذ ْك ِر الله‬ ُ ُ‫َت ْط َم ِئ ُّن ْال ُقل‬ ‫وب‬ “Wale ambao wameamini na zikatua nyoyo zao kwa kumdhukuru Mwenyezi Mungu. Ehee! Kwa kumdhukuru Mwenyezi Mungu nyoyo zinatua..” (Surat Ra’ad: 28).

Ama athari nyingine ya kushikamana na dini, ni tabia njema na mwenendo mzuri, ambapo mchamungu anapata msukumo katika kauli zake, vitendo vyake, harakati zake, misimamo yake kutokana na misingi ya haki, uadilifu na wema, na anatarajia radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu, hivyo anajiepusha na yanayomkasirisha Mwenyezi Mungu. Na mbele ya msomaji mpendwa kuna kurasa chache ambazo zinalenga kuelekeza uzingativu kwenye uhalisia wa uchamungu, mwonekano wake ndani ya nafsi na mwonekano wa mwenendo. Nataraji Mwenyezi Mungu atanijaalia mimi pamoja na msomaji mpendwa kuwa miongoni mwa wanaonufaika na ukumbusho na mawaidha kwa kusadikisha kauli yake (swt): 4


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

ِّ ‫َو َذ ِّك ْر َفإ َّن‬ ْ ‫الذ ْك َرىٰ َت ْن َف ُع ْالم‬ َ ‫ُؤ ِم ِن‬ ‫ين‬ ِ “Na kumbusha kwani ukombusho huwafaa Waumini.” (Surat Dhaariyyat: 55).

Hasan Musa as Safar, Qatif. 25 Ramadhan 1432 Hijiria, 25 Agosti 2011

5


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

‫بسم اهلل الرحمن الرحيم‬ FARAGHA YA KIROHO: HUZUNI NA MKANGANYIKO

H

akika mwanadamu katika maisha haya ana haja na mahitaji, na maisha yake hayaongoki isipokuwa anapopata mbele yake fursa ya kutimiza hayo mahitaji yake, na tunaweza kugawanya mahitaji yake katika aina tatu, kila aina miongoni mwazo inafungamana na nyanja fulani kati ya nyanja za utu wake.

Aina ya Kwanza: Mahitaji ya Kimada: Haya yanafungamana na mwili katika maisha ya mwanadamu kama vile mahitaji ya chakula, mavazi, malazi, matibabu na jinsia. Nayo ni mahitaji ya dharura, kama hayatapatikana basi maisha ya mtu na jamii yataparaganyika. Na inajulikana kwamba adha ya ufakiri na ukosefu hata kama ni katika sehemu ndogo tu katika jamii, inaweza kuondoa amani na utulivu katika jamii yote; kwa sababu inakuwa inatengeneza mazingira ya uasi na uovu, kwa ajili hiyo imepokewa kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) kwamba amesema: “Ufakiri unakaribia kuwa ni ukafiri.”1 Na inanukuliwa kutoka kwa Sahaba mtukufu Abu Dharr al-Ghafaariy (r.a) kauli yake: “Nimestaajabishwa na asiyepata chakula katika nyumba yake namna gani hatoki dhidi ya watu hali amechomoa upanga wake.”2 Aina ya Pili: Mahitaji ya Kiakili: Akili ambayo Mwenyezi Mungu amempa mwanadamu inahitaji elimu na maarifa, na inahitaji anzul-Ummal, Juz. 6, Chapa ya tano, 1985 (Beirut Muasasatu Risaala) Uk. 492, Hadith K namba: 16682 . 2 Rijalu Haula Rasuli, Chapa ya 1968 (Cairo: Darul-Kutubi al-Hadiythah) Uk. 100. 1

6


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

mazingira ambayo yanaipa uhuru wa kufikiri, njia na vifaa vinavyoisaidia katika harakari za kielimu na kifikira. Tangu wakati wa mwanzo ambao Mwenyezi Mungu alimuumba mwanadamu alimwandalia fursa ya elimu na kujifunza, anasema (swt):

َ ْ‫َو َعلَّ َم آ َد َم أ‬ ‫ال ْس َما َء ُكلَّ َها‬ “Na akamfundisha Adamu majina yote.” (Surat al-Baqarah: 31).

Na anasema (swt):

ْ‫َ َ إ‬ َ ‫ال ْن َس‬ ‫ان‬ ِ ‫َخلق‬ َ ‫َعلَّ َم ُه ْال َب َي‬ ‫ان‬ “Amemuumba mwanadamu na akamfundisha ubainifu.” (Surat Rahmaan: 3 - 4).

Na mwanadamu anapozuiwa harakati zake za kifikira na kunyimwa uhuru wake wa kielimu na kupokonywa haki ya maarifa, hakika anakosa sehemu muhimu katika uanadamu wake na kisha hatohisi heshima na raha. Na kwa sababu hiyo Uislamu umefaradhisha kutoa elimu na kutoa fursa ya kujua na kujifunza, imepokewa kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww): “Mwenye kuficha elimu yenye manufaa Mwenyezi Mungu atampiga kwa kijinga cha moto siku ya Kiyama.”3 Na katika tafsiri ya kauli yake (swt): “Na katika tuliyowaruzuku wanatoa..” (Surat al-Baqarah: 3), Imam Ja’far asSadiq (as) anasema: “Na katika tuliyowafundisha wanayasambaza.”4 iharul-An’war, Juz. 2, Chapa ya tatu 1403 Hijiria Beirut Darul-Ihiyaai Turathil-Islamiya, B Uk. 78. 4 Biharul-An’war, Juz. 70, Uk. 267. 3

7


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

Aina ya Tatu: Uelewa wa Kiroho wa Kimaanawi: Mwanadamu ni roho na mwili, na kama ambavyo mwili una haja zake na mahitaji yake, vile vile roho ina mahitaji yake, nayo yana athari kamili katika kuendesha upande wa kimada katika maisha ya mwanadamu, kama yatatimia mahitaji yake yote ya kimada, lakini akawa anaishi katika ukosefu na njaa ya kiroho, hakika maisha yake hayawezi kutulizana wala hawezi kufurahia. Mahitaji ya Roho: Roho inahitaji utulivu, uaminifu, ridhaa, raha, na hisia, na mahitaji ya kimada kwa kiwango chake, kwa mabadiliko yake, kwa upungufu wake na matatizo yake, hayampatii mwanadamu furaha, matumaini na utulivu wa kiroho. Hivyo ni lazima roho ya mwanadamu iwe na mawasiliano na nguvu ambayo ni zaidi ya mada, nguvu kuu ambayo haina mpaka, na ambayo ndio marejeo ya mambo yote. Ni sahihi kwamba mwanadamu anamiliki kiasi cha uwezo na nguvu, hususan katika zama hizi, ambapo uwezo wa mwanadamu umeongezeka na uwezo wake wa kielimu na kiteknolojia umeendelea, lakini mwanadamu anajua kwamba maisha yake, uwezo wake na nguvu zake sio za dhati, kwani amekuja katika uhai bila ya maamuzi yake mwenyewe na atatoka humo bila hiyari yake na wakati wowote, ambapo hawezi kupanga muda wa kutoka kwake. Mwanadamu anajua kwa fadhila ya maendeleo yake ya kielimu ya hivi sasa, upeo wa ufinyu wake na uchache wake ukilinganishwa na ulimwengu huu mpana ambao anaishi ndani wake, dunia ambayo anaishi juu yake umri wake unarejea kabla ya miaka bilioni 4 hadi 5, nayo pamoja na ukubwa wake ni sayari tu inayozunguka jua pamoja na sayari zingine tisa zinazounda mfumo wa jua, na jua hili ni kubwa 8


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

mara 1,300,000 kuliko ukubwa wa dunia, nalo ni nyota moja tu kati ya mabilioni ya nyota ambazo kwa pamoja zinaunda mjumuiko unaoitwa Path Trail au Track Route, na umri wake unakadiriwa kuwa ni kati ya miaka bilioni 10 na 15, na huu ni mjumuiko mmoja kati ya mabilioni ya mijumuiko ambayo inaelea katika uwanda wa ulimwengu.5 Na kama anavyosema mmoja wa wataalamu: “Lau tukitaka kuulinganisha ulimwengu tungesema: Hakika unafanana na bahari kubwa, na kila mjumuiko unafanana na kipande cha kisiwa katika bahari hiyo kubwa, na kila mkusanyiko wa jua katika mjumuiko unafanana na kipande cha ardhi katika kisiwa hicho, na ardhi yetu ambayo tunaishi juu yake ni sawa na sisimizi katika kipande cha ardhi ndani ya kisiwa miongoni mwa mamilioni ya visiwa katika bahari kubwa, hivyo ni upi ukubwa wa mwanadamu ukilinganisha na ulimwengu huu mkubwa?” Hakika mwanadamu anahisi udhaifu wake na kushindwa kwake, pamoja na yote aliyoyafanikisha na kuyafanya miongoni mwa maendeleo ya kielimu, na mafanikio ya kiteknolojia, na yanadhihirika hayo wazi pale anapopatwa na matukio ya kawaida kama vile matetemeko, volkano, mafuriko na dhoruba, naye anakosa udhibiti hata wa mwili wake na hisia zake. Wakati akiwa katika hali ya afya njema kabisa na uchangamfu, mara anashambuliwa na matatizo na magonjwa na anapatwa na uzee na ukongwe, na anapokuwa katika kilele cha furaha na sururi anaweza kupatwa na karaha na huzuni, vivyo hivyo anaingia katika hali na kwenda katika hali zingine mbalimbali, hawezi kujilinda mwenyewe na hali fulani na wala hawezi kuizuia nyingine. Hisia hii ya kina juu ya uduni na udhaifu wa uwezo, hisia kubwa ya uchache na kushindwa, inamsukuma mwanadamu kutafuta 5

Al- Mausu’atu al-Arabiya al- Alamiya, Juz. 14, Chapa ya pili ya 1999, Riyaadh Uk. 246. 9


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

chanzo chenye nguvu na uwezo, na upande unaotawala ulimwengu na uhai, ili nafsi yake ipate matumaini kwa kufungamana na nguvu hiyo, na ili moyo wake utulizane, na hisia zake zitulie kwa kujikuribisha katika nguvu hiyo. Na hii ndio dini, ambayo inampa mwanadamu jibu juu ya maswali yake yenye kutatiza kuhusu uwepo wake na hatima yake, na kufungua kwake njia ya mawasiliano na kuamiliana pamoja na Muumba wa ulimwengu na uhai. Uchamungu ni raghaba na utashi wa kimaumbile kwa mwanadamu katika muundo wake maalumu kuanzia na roho, akili na mwili. Anasema Wool Deyournet katika Qiswatul-Hadharah: “Hakika mchungaji hakuumba dini, lakini ameitumia kwa ajili ya malengo yake tu, kama anavyomtumia mwanasiasa mwanadamu yeyote kwa ajili ya msukumo wa kimaumbile na mazoea. Itikadi ya kidini haikuanza kutokana na uzushi au michezo ya makuhani bali imeanza kutokana na maumbile, kutokana na maswali yasiyoisha yaliyomo humo, na hali na hofu, huzuni, matarajio na kujihisi upweke zilizomo humo.�6 Lakini mwanadamu anaweza kupotea njia ya kwenda kwenye dini sahihi kama hajapata tawfiki ya uongofu wa Mwenyezi Mungu na ujumbe wa mbinguni. Maendeleo ya Kimada: Je Yanatosha? Baadhi wanaweza kufikiri kwamba jamii zetu zina haja ya kuinuka kielimu na kuendelea kiteknolojia, kubadilika kisiasa na kiuchumi ili kuungana na msafara wa ustaarabu na maendeleo, ama pande za kiroho na kidini zenyewe ni jambo la pembeni la ukamilisho, halina nafasi katika kutengeneza uhalisia wa mabadiliko na maendeleo. La6

ool Deyournet katika Qiswatul- Hadharah, Juz. 1, Uk. 117, Chapa ya 1988 (Beirut W Darul- Fikir). 10


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

kini pamoja na kukubali kwamba jamii zetu zina haja ya kuinuka kielimu na kiteknolojia, kisiasa na kiuchumi isipokuwa ni kwamba kushibisha upande wa kiroho ni jambo lenye umuhimu na kipaumbele kiasi kwamba haiwezekani kupuuza upande huu. Hakika jamii za Kimagharibi zilizoendelea ambazo tunatamani kuwa karibu na kiwango cha maendeleo yake, zinaishi katika matatizo makubwa ya kijamii ambayo yanazinyima utamu wa maendeleo, kwa sababu ya faragha na upweke wa kiroho unaowakabili. Utajiri wa kimada na kuinuka kielimu peke yake hakumpi mwanadamu furaha na utulivu, ikiwa hakujaza pengo la kiroho, hakika maisha ya mwanadamu katika hali hiyo yanakuwa na adhabu na mkanganyiko. Einstein ni Mfano: Mtu ambaye aliweka nadharia ya makadirio alikuwa ni mwenye kufeli katika maisha yake binafsi, bali Alberto Einstein alikuwa ni pipa (jalala) la wanawake, mbabe, mkali na mwenye muamala mgumu na watoto wake, na ni baba mlezi wa mtoto asiyekuwa wake kisharia, ambaye hakumuona wala hakumtambua anayeitwa Azoral, na nyaraka na barua binafsi zimefichua kwamba ndoa ya kwanza ya Einstein kwa Melega Marek ilipelekea talaka kwa sababu ya uhusiano wa siri na jamaa yake wa kike wa karibu aliyeitwa Elsa. Na barua zinaashiria juu ya ukali wa Einstein kwa mke wake Melega wakati wa kuachana kwao, jambo lililopelekea kuathirika kiakili ambapo hakupona hadi kufariki kwake. Na ukali huo ulihamia katika muamala wake na watoto wake, Hans Albert mtoto wake mkubwa na alikuwa na miaka kumi na tano alipoondoka mzazi wake katika nyumba ya familia, na Edward mtoto wake mdogo ambaye alichanganyikiwa baada ya kuachana wazazi wake na hatimaye ali11


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

malizia maisha yake katika kiliniki ya wagonjwa wa akili ya Uswizi, na mzazi wake hakumtembelea hata mara moja.7 Na mfano wa Einstein ulitokea pia kwa Armstrong Neil Aulodan, naye ni mtu wa kwanza kukanyaga mwezini tarehe 20 July 1969, isipokuwa alikuwa hana raha na utulivu, alimtaliki mke wake na akakinzana na watoto wake na maisha yake yakapatwa na mkanganyiko na huzuni. Kuhusu Uhalisia wa Jamii ya Kimarekani: Jamii ya Kimarekani ipo kileleni katika ustaarabu wa kimada wa kisasa, lakini faragha ya kiroho katika jamii imezalisha ongezeko na matatizo makubwa katika maisha na tabia za Wamarekani, ambapo huzuni inazidi kusambaa, matukio ya kujinyonga yanazidi kuongezeka, makosa ya utumiaji nguvu hata katika kiwango cha wanafunzi wa shule za msingi yanaongezeka kwa kasi, kama ilivyozungumzwa na vyombo vya habari, ukiachilia mbali ufisadi wa kitabia ulionea. Katika mwaka uliopita ilitolewa orodha ya vitabu vyenye mauzo makubwa zaidi Marekani, kulingana na gazeti la New York Times, ni kitabu chenye anwani al-Khuruju Nihaiy ambacho ni utunzi wa mwingereza Derek Humphrey Sitendr ambaye anazungumzia kuhusu aina za kujinyonga na njia zake mbalimbali, kwa lugha ya uelekezi na mwongozo.8 Hali hii mbaya imegeuza mtazamo wa wanafikra wa Kimagharibi hadi kwenye dosari ya maendeleo ya kimada, nayo ni faragha na upweke wa kiroho, kama ambavyo imeyasukuma makundi ya jamii ya Kimarekani na ya Kimagharibi kutafiti kuhusu chanzo cha 7 8

Jarida la al-Hayaati la London, lililotolewa tarehe 14 Safar 1414Hijiria. Jarida la Safir – Beirut linalotolewa tarehe 30 Muharam 1412Hijiria. 12


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

fikra ya kiroho itakayoziba pengo hilo na kujaza upweke huo, ambao umetoa fursa ya kukuza mielekeo ya uongo na ukhorafi. Na anazungumzia hali hii mtafiti wa Kimarekani Rostow katika kitabu chake kizuri Marahil Numuwul-Iqtiswadiy ambapo anaona: Hakika nchi zinapita katika hatua mbalimbali: - Hatua ya jamii ya mwanzo, - Hatua ya kujiandaa na kuanza, - Hatua ya kupevuka, - Hatua ya watu kutumia, na inayofuatia baada ya hapo. Na anasisitiza kwamba Marekani ndio jamii pekee ambayo imefikia hatua ya kutumia, na kwamba inahamia katika hatua ambayo ni baada ya hapo, na miongoni mwa mwonekano wa hatua hii ni kwamba jamii inazalisha zaidi kuliko inavyotumia, na tatizo lake la kiuchumi linakomea katika kutengeneza maombi na sio kuandaa mahitaji, na vinatawala humo vyombo vya habari na mbinu za propaganda, hali ambayo inabadilika kutoka katika kujishibisha kimada na kuwa kile kinachoweza kuitwa ‘mwelekeo wa kiroho’, na kisha kunaenea humo ukhorafi (upotofu), dhana za uongo, madhehebu, uzushi na propaganda, sawa ziwe zinahusiana na dini au ziko nje ya dini au dhidi yake. Kama anavyoashiria kwamba jamii ya Kimarekani ina sifa maalumu, nayo ni utajiri, bali Marekani ni dola tajiri ulimwenguni, ambapo pato la jumla la taifa lake linazidi wastani wa dola trilioni 5.5, ambapo wastani wa pato la mtu binafsi ni dola elfu 22, lakini pamoja na kuongezeka kiwango cha uzalishaji na maendeleo ya teknolojia, na kuwa na umri wa kuzaa wenye kuheshimiwa katika maisha ya 13


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

Mmarekani, bado unaweza kushtushwa na matukio mbalimbali ya udororaji wa kijamii, hadi kufikia kiwango cha fujo za ndani ambazo hazina udhibiti. Na miongoni pia mwa mambo yanayozungumzwa na katika runinga za Marekani ni mas’ala ya kujua jambo la siri, kujua hadhi au kujua nyota, kutafuta kilichopotea hata kama atakuwa ni mpenzi au rafiki au pengine ni mali na cheo. Katika hali hii unachotakiwa ni uwasiliane tu na namba iliyoandikwa katika runinga na kueleza yanayokutatiza au unachotafuta au pengine unayoyataka au usiyoyataka na utapewa jawabu unalotaka: Je umepoteza mali? Je, umepoteza nyaraka muhimu? Ataonekana kwako katuni au tabibu anayekuongoza kwa ishara ili kupata ulichopoteza, na hatimaye anapata kutoka kwako haja yake nayo ni mali bila shaka.9 Somo na Zingatio: Makusudio sio kuonyesha uwezekano wa udhaifu na kasoro katika maendeleo ya kimada, na kutoa picha mbaya yenye giza ya maendeleo haya, wala sio tu kudhihirisha hali ya jamii hizo, kwani ni maendeleo ambayo yanakita himaya yake katika uhalisia wa maisha kwa mafanikio yake ya kielimu na kiteknolojia, bali ni wajibu jamii zetu zitamani kujiunga na msafara wake ulioendelea, isipokuwa kinachotakiwa ni kupambanua nukta zenye nguvu na zenye udhaifu katika maendeleo haya ya kimada ili tufahamu umuhimu wa upande wa kiroho, ili tusiupuuze na kuusahau wakati wa kupanga hali ya jamii zetu, bali tushikamane na ratiba na mikakati ambayo inakuza upeo wa kiroho na kuushibisha. Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu anahadharisha binadamu, kwamba kusahau upande wa kiroho kunasababisha huzuni kwa mtu 9

Jarida la al-Hayaati la London la tarehe 29 Shawwal 1415 Hijiria. 14


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

binafsi na mkanganyiko kwa jamii, na kisha dhiki ya maisha na hali mbaya, anasema (swt):

َ‫َو َم ْن أ‬ َ ‫ض َع ْن ِذ ْكري َفإ َّن لَ ُه َم ِع‬ َ ‫يش ًة‬ َ ْ ‫ض ْن ًكا‬ ‫ر‬ ‫ع‬ َ ِ ِ ٰ‫َو َن ْح ُش ُر ُه َي ْو َم ْال ِق َيا َم ِة أَ ْع َمى‬ “Na atakayejiepusha na mawaidha Yangu, basi hakika atapata maisha yenye dhiki. Na tutamfufua Siku ya Kiyama hali ya kuwa kipofu.» (Surat Twaha: 124).

Wakati ambapo wastani na ukamilifu katika kutimiza mahitaji ya mwanadamu katika mielekeo yake ya kimada, kiakili na kiroho inamhakikishia mwanadamu maisha mazuri yenye furaha:

‫صالِ ًحا ِم ْن َذ َك ٍر أَ ْو أُ ْن َثىٰ َو ُه َو ُم ْؤ ِم ٌن‬ َ ‫َم ْن َع ِم َل‬ ‫َفلَنُ ْح ِي َينَّ ُه َح َيا ًة َطيِّ َب ًة َولَ​َن ْج ِز َينَّ ُه ْم أَ ْج َر ُه ْم ِبأَ ْح َس ِن َما‬ َ ُ‫َكانُوا َي ْع َمل‬ ‫ون‬ “Mwenye kutenda mema, mwanamume au mwanamke, naye akawa ni muumini, tutamhuisha maisha mema; na tutawapa ujira wao kwa mazuri zaidi waliyokuwa wakiyafanya.” (Surat Nahl: 97).

Baina ya Mvuto wa Kimada na Utakasifu wa Kiroho: Mwenyezi Mungu amemuumba mwanadamu akiwa ni mchanganyiko wa vitu viwili, kimoja ni cha kimada na kingine ni cha kiroho, tapo la udongo na tapo la nuru, anasema (swt): 15


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

ْ َ َ ْ ‫ين‬ ٍ ‫إِذ َقال َربُّك لِل َم اَل ِئ َك ِة إِنِّي َخالِ ٌق َب َش ًرا ِم ْن ِط‬ ‫وحي َف َقعُوا لَ ُه‬ ِ ‫َفإِ َذا َس َّويْتُ ُه َو َن َف ْخ ُت ِفي ِه ِم ْن ُر‬ َ ‫اج ِد‬ ‫ين‬ ِ ‫َس‬ “Mola Wako alipowaambia Malaika: Hakika Mimi nitaumba mtu kutokana na udongo. Na nitakapomkamilisha na nikampulizia roho Yangu, basi mwangukieni kwa kusujudu.” (Surat Swad: 71 – 72).

Huu mchanganyiko uliotumika katika kuumbwa mwanadamu, mchanganyiko baina ya vitu viwili, mada na roho, umesababisha hali ya mapambano ya ndani kwa mwanadamu baina ya pande mbili za uwiano huu, udongo na roho, upande wa kimada au udongo unavutia kwenye ardhi na kuteremka naye kwenye mazingatio ya mada. Wakati ambapo upande wa kiroho unamsukuma kwenda juu na kumnyanyua katika upeo wa maadili na utukufu. Na katika mapambano haya ndio umefichikana mtihani wa mwanadamu na ni changamoto kubwa kwake, na kwa matokeo haya inaamuliwa hatima ya mwanadamu na unapangwa mustawa wake, ima awe katika mwelekeo mzuri, pindi anapoishi katika hali ya uwiano, na kufanya mazingatio yake ya kimada katika kivuli cha maadili na chini ya dari la maadili. Na ima awe duni kuliko wote walio duni, kama atayafanya matamanio yake kuwa ndio mungu wake na akatawaliwa na matamanio yake na matakwa yake. Na tunaweza kuainisha njia muhimu za mgongano na mwachano baina ya mielekeo miwili, katika maisha ya mwanadamu, katika pande tatu zifuatazo:-

16


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

Kwanza: Baina ya Matamanio na Kutumia akili: Kutokana na tapo la udongo kumepatikana kwa mawanadamu utashi na matamanio, nayo yanambana ili ayashibishe na kuyatimizia mahitaji ya kimwili na raghaba zake miongoni mwa chakula, vinywaji, jinsia ya pili, raha na yanayofungamana nayo miongoni mwa mali, cheo na jaha. Lakini kuelekea moja kwa moja kwenye mwelekeo huu, kunambadilisha mwanadamu hadi kwenye kiwango cha wanyama ambao hawana lengo isipokuwa utashi huu na hawana mazingatio isipokuwa haya, kwani wenyewe wanakula sehemu yoyote jalalani au mbungani, na wanakunywa maji yoyote safi au machafu, na wanatimiza matamanio yao ya kijinsia katika hali yoyote, kwa sababu wanaendeshwa na matamanio yao tu. Lakini hali ya kutumia akili kwa mwanadamu na ambayo inatokana na upande wa kiroho ndio ambayo inamuwekea mpaka na udhibiti katika kutimiza matamanio yake na raghaba zake, hivyo anakula, anakunywa, anaoa, anamiliki na anaongoza lakini yote hayo ndani ya maelekezo ya akili na mwongozo wake. Kuyanyenyekea sana matamanio inamaanisha kuteremka zaidi katika kina cha hali ya udongo wa kimada, wakati ambapo kutumia akili na kuyadhibiti vizuri zaidi matamanio na utashi inamaanisha kuinuka sana katika upeo wa kiroho wa kimaanawi. Pili: Baina ya Ubinafsi na Utukufu: Upande wa udongo unatilia mkazo hali ya ubinafsi na inamaanisha kuijali nafsi tu na maslahi binafsi kushinda kitu chochote kile, kwa sababu mada yenyewe kama mada haina uwezo wa kuelekea nje ya dhati yake, hivyo inaishi kwa dhati yake na kwa ajili ya dhati yake. Wakati ambapo upande wa kiroho unamwelekeza mwanadamu kwenye upeo mpana zaidi nje ya nafsi yake na kumwonyesha ridhaa ya 17


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

Mola Wake na Muumba Wake na kujali hali za wengine wanaomzunguka, na kufikiri katika maslahi ya watu wengine. Hakika ubinafsi unatokana na udongo, nao ndio unaomsukuma mwanadamu kufanya uadui katika haki za wengine ili apate yeye, nao ndio unaomzuia kutoa na kujitolea, ili yeye akusanye kiasi kikubwa cha uwezo kwa ajili ya nafsi yake mwenyewe. Lakini dhamira ya mwanadamu na utu wake unaotokana na kupuliziwa roho na Mwenyezi Mungu, ndio ambao unamkanya kutofanya dhulma na uadui na unamhamasisha kuwanufaisha wengine na kuwasaidia, bali na kuwapendelea wao zaidi ya nafsi yake. Hivyo mwanadamu kuijali zaidi nafsi yake ni kuporomoka katika kina cha hali ya udongo wa kimada, wakati ambapo kuwajali wengine na maslahi ya jamii ni kutukuka kiroho. Tatu: Baina ya Ufinyu na Maadili: Udongo ni mada inayohitaji kiasi makhususi cha wakati na sehemu, nayo inamzingira mwanadamu kwa mpaka wake finyu, na inamshughulisha kwa mahitaji yake na matumizi yake ya muda na ya haraka, wakati ambapo roho inafungamana na nguvu kuu isiyokuwa na mpaka wala kikomo, hakika ni pulizo kutoka kwa Mwenyezi Mungu: “Na nikampulizia roho yangu.” Na tamko “Yangu” hapa ni kwa ajili ya kumtukuza, vingenevyo Mwenyezi Mungu hana kiwiliwili au roho kwa maana inayofahamika kwetu. Na roho inamfungulia mwanadamu ulimwengu wa maadili na wema, nao ni ulimwengu mpana na mkubwa mno, ambapo mwanadamu anapoufahamu anatukuka kushinda mada zenye mipaka, na anaiandaa nafsi yake kwa ajili ya kutumikia misingi ya Mwenyezi Mungu yenye kudumu na anakuwa ni mlinganiaji wa kheri na kiongozi wa uadilifu na mtendaji kwa ajili ya haki. Na hivyo mwenye 18


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

kuimarisha maisha yake kwa ajili ya mada huwa amejitwalia upande wa udongo katika tabia yake, wakati ambapo mwenye kuionya nafsi yake kwa ajili ya misingi na maadili huwa amepanda katika ulimwengu wa roho, na ni mwenye kudumu katika neema na radhi za Mwenyezi Mungu.

19


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

MATOKEO YA KUSHIKAMANA NA DINI

D

ini ina nyanja mbalimbali zinazomzunguka mwanadamu na maisha, na baadhi ya wanadini wanaujali upande fulani katika dini na kuuzingatia kuwa ni upande muhimu zaidi, na kwamba unawakilisha undani wake na asili yake. Kwa mfano tu, baadhi wanatilia mkazo upande wa itikadi na wanayapa mambo yake na mas’ala yake umuhimu mkubwa kwa kuzingatia kwamba itikadi ndio asili ya dini. Wakati ambapo wengine wanaelekeza umuhimu wao upande wa sharia ya dini na ibada zake kama vile Swala, Swaumu, Hija na Zaka, kutokana na Aya na hadithi zilizopokewa kuhusu ibada hizo. Na baadhi wanatilia mkazo katika kutekeleza nidhamu za Kiislamu na kanuni zake katika kuendesha jamii, kwa sababu usalama wa maisha ya watu wa kawaida unaimarisha utawala wa dini na nguvu yake. Na pande zote hizo ni muhimu na za msingi isipokuwa ni kwamba kuna upande mwingine ambao ni haki kwetu kuuzingatia kuwa ni kina cha dini na asili ya dini, nao ni hali ambayo dini inalenga kuitengeneza na kuikuza katika nafsi ya mwanadamu, nayo ni kinga ya kidini au uchamungu kulingana na maneno ya Qur’ani na nususi za kidini. Na itikadi si kingine isipokuwa ni maandalizi ya kuzalisha hali hii, na isipopatikana hali hii basi itikadi inakuwa ni taarifa tu zilizohifadhiwa katika akili ya mwanadamu zisizo na kazi wala zisizoathiri katika maisha yake, na hilo ndilo tatizo la baadhi ya makafiri, ambao hawapungukiwi na itikadi kama taarifa tu na uhakika, lakini wao hawanyenyekei katika itikadi hizo katika maisha yao kwa kutokuwepo kinga hii katika nafsi zao. Kwa hiyo hakika Qur’ani Tukufu inasema kuhusu hilo: 20


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

َ ْ‫الس َماء َو أ‬ ‫ض أَ َّم ْن‬ ‫ر‬ ‫ال‬ ْ ِ َّ ‫ُق ْل َم ْن َي ْر ُز ُق ُك ْم ِم َن‬ ِ َ ْ‫الس ْم َع َو أ‬ ْ ‫ار َو َم ْن ي‬ ‫ُخ ِر ُج ْال َح َّي ِم َن‬ َّ ‫َي ْملِ ُك‬ َ ‫ْص‬ َ ‫الب‬ ْ ‫ِّت َوي‬ َ ‫ُخ ِر ُج ْال َمي‬ ‫ِّر‬ ُ ‫ِّت ِم َن ْال َح ِّي َو َم ْن يُ َدب‬ ِ ‫ْال َمي‬ َ ْ‫أ‬ َ ‫ون اللهَُّ َف ُق ْل أَ َف اَل َتتَّ ُق‬ َ ُ‫ال ْم َر َف َس َي ُقول‬ ‫ون‬ “Sema: Ninani anayewaruzuku kutoka mbinguni na ardhini? Au ni nani anayemiliki usikizi na uoni na ni nani amtoaye hai kutoka maiti na akamtoa maiti kutoka aliye hai na ni nani anayedabiri mambo yote? Watasema ni Mwenyezi Mungu. Waambie: Basi je hamuwi na takua?” (Surat Yunus: 31).

Na inasema:

ْ ْ ‫ُق ْل َم‬ ُّ ‫ش‬ ‫ب‬ ‫الس‬ ‫ات‬ ‫و‬ ‫ا‬ ‫م‬ ‫الس‬ ‫ب‬ ‫ر‬ ‫ن‬ َّ َّ َ َ َ ِ ِ ‫ْع َو َر ُّب ال َع ْر‬ ِ َ ْ ُ َّ‫ُ للِه‬ ْ ُ َّ َ َ ‫ون ِ قل أ َف اَل تتق‬ َ ‫يم َس َي ُقول‬ ‫ون‬ ‫ظ‬ ‫ع‬ ‫ال‬ َ ِ ِ “Sema, ni nani Mola wa mbingu saba na Mola wa arshi tukufu? Watasema, ni vya Mwenyezi Mungu. Sema, basi je, hamuogopi?” (Surat al- Muuminina: 86 – 87).

Hakika kumjua na kumfahamu Mwenyezi Mungu Mtukufu haitoshi bali kinachotakiwa ni hali hiyo kuleta matunda ya uchamungu katika nafsi yako. Na ibada za Kiislamu hazikusudiwi zenyewe kama zilivyo, bali kama inavyodhihirika katika nususi za kidini ni ratiba na njia ya kuleta hali ya uchamungu katika nafsi ya mwanadamu, kuhusu swala anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: 21


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

ُ‫ْات ُل َما أ‬ ْ ‫ْك ِم َن‬ َ ‫وح َي إلَي‬ َ ‫الص اَل َة إِ َّن‬ ‫ت‬ ‫ك‬ ‫ال‬ َّ ‫اب َوأَ ِق ِم‬ ِ ِ ِ ِ َّ َِّ‫الص اَل َة َت ْن َهىٰ َع ِن ْال َف ْح َشا ِء َو ْال ُم ْن َك ِر َولَ ِذ ْك ُر الله‬ َ ‫ص َنع‬ ‫ُون‬ ْ ‫أَ ْك َب ُر َواللهَُّ َيعْلَ ُم َما َت‬ “Soma uliyopewa wahyi katika Kitabu; na usimamishe Swala, hakika Swala inakataza machafu na maovu. Na hakika dhikri (utajo) ya Mwenyezi Mungu ni kubwa kabisa. Na Mwenyezi Mungu anayajua mnayoyafanya.” (Surat Ankabut: 45).

Nayo inalenga kutengeneza hali hii ambayo inazuia kufanya upotovu, na kama halijatimia lengo hili basi hakuna thamani ya Swala hiyo, kama ilivyopokewa kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww): “Ambaye Swala yake haijamkataza machafu na maovu hatozidi kwa Mwenyezi Mungu isipokuwa kuwa mbali.”10 Na saumu hekima ya kuanzishwa kwake ni kufikia daraja la uchamungu, anasema (swt):

ُ ‫ين آ َمنُوا ُك ِت َب َعلَي‬ َ ‫َيا أَُّي َها الَّ ِذ‬ ‫الص َيا ُم َك َما ُك ِت َب‬ ِّ ‫ْك ُم‬ َ ‫ين ِم ْن َق ْبلِ ُك ْم لَ َعلَّ ُك ْم َتتَّ ُق‬ َ ‫َعلَى الَّ ِذ‬ ‫ون‬ “Enyi mlioamini! Mmeandikiwa kufunga kama walivyoandikiwa waliokuwa kabla yenu, ili mpate kuwa na takua.” (Surat al-Baqarah: 183).

Na ni nini makusudio ya ibada ya Hija na nembo yake? Je Mwenyezi Mungu ana lengo lolote humo? Hakika Mwenyezi Mungu 10

Kanzul- Ummal, Juz. 7, Uk. 525 Hadith namba 20083. 22


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

kuhusu sadaka ya Hijja anaashiria kwamba, anayoyataka kupitia hilo ni kutengeneza hali ya uchamungu kwa mwanadamu, anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

َ ‫لَ ْن َي َن‬ ‫ل ِك ْن َي َنالُ ُه‬ ٰ َ ‫ال اللهََّ لُ ُحو ُم َها َو اَل ِد َما ُؤ َها َو‬ ٰ‫ِّروا اللهََّ َعلَى‬ ُ ‫التَّ ْق َوىٰ ِم ْن ُك ْم َك َذٰلِ َك َس َّخ َر َها لَ ُك ْم لِتُ َكب‬ ُ ‫َما َه َد‬ َ ‫اك ْم َو َب ِّش ِر ْال ُم ْح ِس ِن‬ ‫ين‬

“Nyama zao hazimfikii wala damu zao, lakini inamfikia takua kutoka kwenu. Kama hivyo tumewafanya hawa wawe dhalili kwenu ili mumtukuze Mwenyezi Mungu kwa alivyowaongoa. Na wabashirie wenye kufanya mema.” (Surat al-Haji: 37).

Hata nidhamu na kanuni za kawaida lengo lake ni kuimarisha aina hii ya kizuizi cha kidini katika nafsi, kama anavyosema (swt) kuhusu sharia ya utaratibu wa kisasi na adhabu:

َ ْ‫صاص َح َيا ٌة َيا أُولِي أ‬ ْ ‫ال‬ ْ َُ ‫اب لَ َعلَّ ُك ْم‬ ‫ب‬ ‫ل‬ َ ِ ِ َ ‫َولك ْم ِفي ال ِق‬ َ ‫َتتَّ ُق‬ ‫ون‬

“Mna uhai katika kisasi, enyi wenye akili, ili msalimike.” (Surat alBaqarah: 179).

Ambapo uchamungu ni falsafa, lengo na natija kutoka katika kila pande za dini: Kutoka katika itikadi, ibada na utaratibu. Na ni uzuri ulioje wa aliyoyasema Amirul-Muuminina Ali (as): “Uchamungu ni kilele cha radhi za Mwenyezi Mungu kutoka kwa waja Wake na haja Yake kwa viumbe Vyake.” 11 11

yuunul- Mawaaidh Wal- Hikam, Chapa ya Kwanza (Qum tukufu U Uk. 154). 23

Darul-Hadith,


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

Kumweka Sawa Mwanadamu kwa Kanuni: Katika nafsi ya mwanadamu kuna mkusanyiko mkubwa wa sababu mbalimbali na zinazokinzana, kama anavyosema mwanafalsafa wa Kijerumani Bertrand Russell: “Mwanadamu ni mwenye utata zaidi katika mizozo yake na raghaba zake kuliko mnyama mwingine yeyote yule, na magumu yanayomkabili yanaanzia katika utata huu. Yeye sio mtu wa kijamii moja kwa moja kama vile sisimizi na nyuki, wala sio mtu wa kipekee moja kwa moja kama vile simba na chui, hakika yeye ni mnyama wa kijamii kiasi, na baadhi ya raghaba zake na mizozo yake ni ya kijamii, na baadhi yake ni ya kipeke.12 Hivyo yeye ni kiumbe wa kimada na kiroho, Mwenyezi Mungu amemuumba kutokana na tapo la udongo na pulizo la roho, na udongo una tabia zake na utashi wake, kama ambavyo roho ina matarajio yake na raghaba zake, jambo ambalo linamfanya awe ni medani ya mvutano baina ya pande mbili, na kulingana na kauli za baadhi ya wanafalsafa ni kwamba: “Hakika ni mkaazi wa dunia mbili, na zinampata mwanadamu hali tofauti tofauti za ridhaa na ghadhabu, furaha na huzuni, kukubali na kukengeuka, elimu na ujahili.” Kutokana na mvutano huu na msuguano wa ukinzani, mwanadamu anahitaji nguvu inayompatia udhibiti sahihi katika raghaba zake, utashi wake na mwelekeo wake kwa ajili ya wema wa nafsi yake na jamii yake, na wala haipatikani nguvu inayoweza kusimamia jukumu hili vizuri zaidi kuliko nguvu ya kidini na ambayo tunaiita kizuizi cha kidini (uchamungu), nayo ni nguvu inayomsukuma mwanadamu kwenye kheri na inamzuia na upotovu na shari. Na nguvu ya kanuni haiwezi hayo, kwa sababu kanuni ni askari wa mtengenezaji wake na inaweza kufanya hila na kujongea pemb12

r. Yusuf al- Qaradhwawiy katika al-Imaani Wal- Hayaati, Chapa ya sita 1993 (Beirut D Muasasatu risala) Uk.170. 24


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

ezoni kwake, kwa sababu inaamiliana na dhahiri ya mwanadamu na nje yake na wala haipenyi hadi kwenye dhati yake na ndani mwake, kama ambavyo pia mwanadamu anaweza kuponyoka katika adhabu kwa kukhalifu kwake kanuni, ukiachilia mbali kwamba kanuni inaweza kumwadhibu mkosaji lakini haimlipi mwema. Hakika kanuni za usalama barabarani – kwa mfano – zinamwadhibu anayekatisha taa nyekundu kama atadhibitiwa na askari, lakini nani atamwadhibu ikiwa hakuonwa na yeyote? Ama dini hakika yenyewe kama inavyomwadhibu huyu, hakika inamlipa yule, nayo inapanda katika moyo wa kila mtu mlinzi juu ya nafsi yake: “Mwabudu Mwenyezi Mungu kana kwamba unamuona na ikiwa humuoni basi Yeye anakuona.”13 Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

ُ ‫ون ِم ْن َع َم ٍل إ اَّل ُكنَّا َعلَي‬ َ ُ‫َو اَل َت ْع َمل‬ ‫ْك ْم ُشهُو ًدا إِ ْذ‬ ِ ُ ‫تُ ِف‬ َ ‫يض‬ ‫ون ِفي ِه‬ “Wala hamtendi kitendo chochote ila Sisi huwa ni mashahidi juu yenu mnaposhughulika nacho.” (Surat-Yunus: 61).

Na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) alikuwa anaposoma aya hii analia kilio kikali sana.14 Je, Elimu Inamdhibiti Mwanadamu? Baadhi wanaweza kuona kwamba maendeleo ya uelewa wa mwanadamu na maendeleo yake ya kielimu vinatosha kudhibiti nyendo zake na harakati zake, lakini linalosemwa ni kitu kingine na 13 14

Biharul- An’war, Juz. 25, Uk. 204. afsir Nuru Thaqalain, Juz. 3, Chapa ya kwanza 1422 Hijiria (Beirut Muasasatu Tarikh T al- arabiy), Uk.321. 25


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

uhalisia ni kitu kingine. Katika kiwango cha kawaida zimebadilika mbinu za utumiaji nguvu na njia za uhalifu na ufisadi, na zimeenea silaha za mauaji na silaha za maangamizi ya jamii, na elimu imetumika katika dola kubwa ili kuzidi kuyatawala na kuyadhibiti mataifa mbalimbali. Hakika Mionzi ya Leza (Laser) ambayo ilikuwa ni neema kwa binadamu kwa sifa yake katika ulimwengu wa tiba na huduma ya upasuaji, pia kukata almasi na madini magumu, na kompyuta za hali ya juu, na kufanya vipimo makini na mawasiliano, mionzi hiyo imeanza hivi sasa kugeuka na kuwa ni laana, kwani sifa hizo hizo ambazo zinasifika nayo na ambazo kwa ajili yake ni kigezo cha kutibu maradhi ya macho na aibu zake, sasa zinatumika kuharibu jicho hili na kulinyima neema ya kuona, kwa njia ya kuelekeza mionzi juu yake, na kisha kuunguza utando wake bila ya mlengwa kuhisi hayo, isipokuwa baadaye sana. Wanafanya hayo kwa njia ya utengenezaji wa bunduki za Leza ndogo au zile zilizoungwa katika bunduki za kawaida, ambazo zinatoa mionzi isiyoonekana inayolenga shabaha ya mbali, na kuunguza kabisa utando wa jicho kwa muda mchache mno kuliko nusu sekunde. Pamoja na jaribio la taasisi za kielimu kuja na utafiti wa kutatua hatari hii yenye kuangamiza kwa njia ya kutengeneza miwani maalum wanayoivaa askari kwenye macho yao, lakini imebainika kwamba kwa njia ya kubadilisha urefu wa mawimbi ya mwanga inaweza kushinda uzio wa kinga hii ya mwisho.15 Na katika kiwango cha mtu binafsi tunaweza kuzungumzia juu ya tatizo la uvutaji wa sigara, ambapo hakika madhara yake na ubaya wake uko wazi na umethibiti kielimu, na ambapo makampuni ya sigara yamelazimika kuandika katika kila pakiti ya sigara onyo linalosema: “Kuvuta sigara kuna madhara katika afya yako hivyo 15

Jarida la Sharqi al-Awsat la London Toleo la 20 April 1995. 26


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

jiepushe.� Lakini elimu hii na uelewa huu haukuzuia kuenea kwa wavutaji na biashara yake. Na taarifa ya Wizara ya Ugavi na Biashara ndani ya Misri inaashiria kwamba matumizi ya uvutaji kwa mtu binafsi huko Cairo yanazidi matumizi ya elimu, burudani, utamaduni na michezo. 16 Na kampuni moja inayofanya kazi ya kutengeneza sigara nayo ni Philip Morris, inapata pato linalofikia dola bilioni 30 kwa mwaka, kama ambavyo ulimwengu unatumia sigara bilioni elfu sita kwa mwaka. Na katika Saudia, taarifa ya Shirika la Habari la Saudia linaelezea juu ya ongezeko la ziada la matumizi ya tumbaku na vinavyotengenezwa kutokana na tumbaku kwa wakazi wa Saudia, ambapo katika mwaka 1995 ilikuwa ni mara dufu zaidi kuliko mwaka wa kabla yake, ambapo kiwango cha uagizaji kilifikia tani 22,000 kwa thamani ya riyali milioni 844, ambapo katika mwaka wa kabla yake kilifikia kiwango cha tani 9,000. Na Saudia inashika nafasi ya nne baina ya dola kumi na tano zinazoagiza sigara, na makadirio ya jumla ya kiasi kinachoingizwa ni sigara milioni 47 kila siku.17 Na ripoti ya mwisho imegundua kwamba idadi ya wavutaji sigara Saudia ni watu milioni sita, wakati ambapo idadi ya wavutaji katika vijana imefikia 772,000, na Saudia inazingatiwa kuwa ni ya nne kiulimwengu katika utumiaji wa tumbaku, kama ambavyo kiwango cha uvutaji baina ya wanafunzi kimefikia asilimia 10 ya wavutaji wa Saudia. Wafanyabiashara wa tumbaku wameagiza sigara bilioni 13 kwa wastani wa sigara 200 kwa kila mwanachi, na idadi ya wavutaji kwa vijana imefikia asilimia 30 katika jumla ya idadi yao. 18 Wakati ambapo taarifa ya Shirika la Afya Duniani inasema hakika tumbaku ni muuaji mjanja, kila mwaka inaua watu milioni tatu, Jarida la al-Hayaati, Toleo la 22 Juni 1995. Jarida la al-Muslimina la London, Toleo la 2 Mei 1997 18 Jarida la al-Jazira, Riyaadh, Toleo la 1409, lililotolewa 28 April 2011. 16 17

27


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

wavutaji hawawi wahanga baada ya sigara tu ya kwanza, wala vifo vinavyotokana na tumbaku havitokei ghafla baada ya kuanza tu kuvuta sigara, bali athari ya kurundikana na matokeo yenye kuchelewa hudhihirika baada ya kipindi cha baina ya miaka 30 na 40 tangu kuanza kuvuta sigara, na vifo vya wavutaji ni mara tatu zaidi ya vifo vya wasiovuta katika kila rika, kuanzia katika umri wa kubaleghe na ujana. Hii inamaanisha kwamba mtu ambaye anavuta sigara katika umri wake wote anakabiliwa na hatari ya kifo kutokana na kuvuta sigara, kwa wastani unaofanana na hatari ya mjumuiko wa sababu zote nyingine za vifo. Na mashirika ya kimataifa yanakadiria kwamba idadi ya wavutaji katika ulimwengu kwa sasa inakaribia watu bilioni moja na milioni mia moja, na kama ukiendelea mwelekeo wa matumizi ya sasa kwa namna hii hakika zaidi ya watu milioni mia tano miongoni mwa walio hai leo watakufa kwa tumbaku. Nusu ya hawa watakufa wakiwa katika umri wa uzee, yaani hakika kila mmoja atapata hasara baina ya miaka 20 na 25 katika umri unaotarajiwa. Ama idadi ya jumla ya watu ambao wanatarajiwa kufa kwa sababu ya tumbaku miongoni mwa ambao hivi sasa wako hai itazidi mara kumi zaidi ya jumla ya waliokufa kwa sababu ya vita kuu vya pili vya Dunia.19 Onyo la Shirika la Afya Duniani linaendelea, na nasaha za matabibu na matukio ya maradhi ambayo yanawapata watu kwa sababu ya kuvuta sigara, yote hayo ni elimu na ufahamu, lakini elimu hiyo imeshindwa kupambana na raghaba ya uvutaji au mazoea ya wavutaji. Nafasi ya Kinga ya Kidini: Ama uchamungu wa kweli hakika unaleta katika nafsi ya mwanadamu kinga ya kidini, inayomfanya awe ni mwenye kuhamasika 19

Jarida la al-Hayaat la London, Toleo la 28 Agosti 1996. 28


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

kwa ajili ya kheri na mwenye kujizuia na shari mwenye kuvuka mbinyo wa raghaba, matamanio na shahawati. Kunywa pombe ilikuwa ni ada iliyoenea katika zama za ujahilia, ambapo walikuwa wanakunywa pombe kupindukia na wanaizingatia kuwa ni kati ya fahari ambayo wanashindana katika vikao vyao, na wanajifaharisha na kujisifu kwayo katika mashairi, lakini iliposhuka Aya ya kuharamisha pombe, mwaka wa tatu hijiria jambo hili halikuhitajia zaidi ya mlinganiaji mmoja katika sehemu za Madina: “Eeee enyi watu hakika pombe imeshaharamishwa.” Yule ambaye mkononi mwake kulikuwa na glasi ya pombe aliivunja na ambaye katika kinywa chake kulikuwa na funda akalitema, na vikabomolewa vichochoro vya pombe na zikavunjwa chupa zake na jambo likamalizika kana kwamba hapakuwepo na ulevi wala pombe.20 Na amepokea al-Bukhariy kutoka kwa Anasi bin Malik, amesema: “Hakika mimi nilikuwa nimesimama namnywesha Abu Twalha na fulan na fulan, ambapo alikuja mtu akasema: ‘Je, imewafikia habari?’ Wakasema: ‘Na ni ipi hiyo?’ Akasema: ‘Pombe imeharamishwa.’ Wakasema: ‘Mwaga haya majagi ewe Anasi.’” Anasema: “Hawakuulizia wala hawakuirudia baada ya habari ya yule mtu.”21 Hivi ndivyo kinavyokuwa kizuizi cha kidini, hutawala katika vitendo vya mwanadamu na nyendo zake pamoja na mamlaka ya mazoea na nguvu ya raghaba. Na kama mfano tu wa mazungumzo, tunaashiria kwenye kisa cha kuharamisha tumbaku na sigara huko Iran mwaka 1312 Hijiria, pindi Shaha wa Iran Nasrudin al-Qajaariy alipotoa mamlaka ya kununua na kutengeneza tumbaku kwa kampuni ya Uingereza, kwa gharama ya uhuru wa nchi na maslahi ya uchumi wake, Marjaa wa dini wakati huo Mirzaa Muhammad Hasan Shiraziy alitoa fatwa ya kuharamisha tumbaku, kuuza, kununua na ayyid Qutub katika Fiy Dhilal- Qur’an, Juz.5, Chapa ya 15, 1988, Cairo Daarus Shariq, S Uk.97. 21 Sahih Bukhariy Juz. 6 kitabu Tafsir (Beirut: Maktabatu thaqafiya) Uk. 104 Hadith ya 139. 20

29


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

kuitumia. Watu na wananchi wote wa Iran walishikamana na kufuata fatwa yake, na idadi yao ilikuwa inazidi milioni ishirini, wakavunja mitemba yote na vyombo vyote vinavyotumiwa kwa ajili ya kutengenezea sigara, na hata wanawake wa kasri la Shaha pia nao wakavunja mitemba yote katika kasri, Shaha alipotaka aletewe mtemba kama kawaida yake, wakampa habari kwamba hakujabaki hata mtemba mmoja katika kasri kwa sababu Marjaa wa Kidini ameshaharamisha hayo! Jambo ambalo lilimpelekea kutengua mkataba wa kuipa haki kampuni ya Uingereza.22 Na tunaona namna gani wanadini wanajizuia mchana wa Ramadhani kutokana na raghba zao na mazoea yao katika chakula na vinywaji na vifunguzi vingine kwa kujilazimisha na amri ya dini. Katika Matamanio: Na miongoni mwa sehemu ambazo ni wajibu humo idhihirike wazi kinga ya kidini, ni pale yanapojitokeza matamanio ya uasi kwa mwanadamu kuelekea katika haramu kama vile matamanio ya ngono au mali au cheo, huo ndio mtihani wa kidini na kipimo cha uchamungu, je mtu atajisalimisha katika mbinyo wa matamanio na kufanya haramu? Au ataukandamiza na kuudhibiti uasi wake kwa kumuogopa Mwenyezi Mungu? Qur’ani Tukufu inatukumbusha kwa kirefu yaliyotokea kwa Nabii wa Mwenyezi Mungu Yusuf (a.s.) siku alipokuwa mtumwa na mtumishi katika nyumba ya mwanamke wa kiongozi wa Misri, na alikuwa ni kijana mbichi aliye katika umri wa ujana huku akiwa rijali kamili na kijana mzuri wa kuvutia. Mwanamke mwenye cheo na uzuri alimwita kwake, na akamwandalia mazingira yote yatakayomsaidia, lakini kinga ya kidini iliyo hai katika nafsi yake 22

A’yaan Shia, Juz. 5, Chapa ya 1986 (Beirut, Darul- Maarif) Uk. 306. 30


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

ilimkataza kumkubalia hata kama kukataa kwake kutampelekea kufungwa jela:

َ ‫َق‬ ‫الس ْج ُن أَ َح ُّب إِلَ َّي ِم َّما َي ْد ُعو َن ِني إِلَ ْي ِه‬ ِّ ‫ال َر ِّب‬ َ‫صر ْف َعنِّي َك ْي َد ُه َّن أ‬ َّ‫ا‬ َ‫ص ُب إل‬ ‫ْه َّن َوأَ ُك ْن ِم َن‬ ‫ي‬ ْ ِ ِ ِ ْ ‫َوإِل َت‬ َ ِ‫اهل‬ ‫ين‬ ِ ‫ْال َج‬ “Akasema: Ewe Mola Wangu! Gereza linapendeza zaidi kwangu kuliko haya wanayoniitia. Na kama hutaniondolea vitimbi vyao nitawaelekea na nitakuwa miongoni mwa wajinga.” (Surat Yusuf: 33).

Anapokuwa na Nguvu: Na sehemu nyingine, ikiwa mwanadamu yuko katika nafasi ya nguvu kuliko wengine, hakika hali hiyo inamuwezesha na kumfanya kutumia nguvu zake pasipo na haki dhidi yao, na hapa inahitaji uchamungu na kinga ya kidini ili aamiliane na walio chini ya mamlaka yake kwa heshima na uadilifu. Mtu mbele ya familia yake, Raisi mbele ya raia wake, kiongozi na wafuasi wake, wote wanakabiliwa na changamoto ya kuteleza, ikiwa hawatamuweka Mwenyezi Mungu mbele yao, na ikiwa kinga ya kidini haipo katika nafsi zao. Na kwa sababu hiyo Imam Ali (as) anamuusia Malik Ashtari wakati alipompa ugavana wa Misri kwa kusema: “Na ihisishe nafsi yako huruma kwa raia na mapenzi kwao, na upole kwao, na wala usiwe kama mnyama mkali kwao.”23 Na katika zama za Umar bin Abdul-Aziz gavana wake wa Basra alimwandikia: “Hakika watu miongoni mwa watumishi wamekata mali ya Mwenyezi Mungu na sitarajii kuirejesha kutoka kwao 23

Nahjul-Balaghah, Chapa ya kwanza 1967 (Beirut Darul- kitabi Lebnaaniy) barua ya 53. 31


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

isipokuwa kwa njia ya adhabu, kama Amirul-Muuminina ataniruhusu lolote katika hayo nitafanya hivyo.” Umar akamwandikia: “Ajabu sana kutaka kwako ruhusa kutoka kwangu ya kumwadhibu mtu kana kwamba mimi ni kizuizi katika adhabu ya Mwenyezi Mungu, na kana kwamba ridhaa yangu kwako inakuokoa na ghadhabu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Tazama ambaye ushahidi utathibiti basi mwadhibu kulingana na alivyokiri na Wallahi wao kukutana na Mwenyezi Mungu Mtukufu na hiyana yao inapendeza kwangu zaidi kuliko mimi kukutana na Mwenyezi Mungu na damu zao.”24 Na gavana mwingine alimwandikia: “Hakika mimi nimefika Muusil nimeikuta ni kati ya nchi zenye wizi mwingi na uporaji, kama utaniruhusu niwaadhibu watu kwa dhana na kuwapiga kwa tuhuma, basi nitafanya na hakitowarekebisha ila hicho.” Umar akamwandikia: “Wachukulie kwa ushahidi na katika mwenendo wa sunna, kama haki haitowarekebisha basi hawatorekebishika.”25 Na kabla ya hapo Imam Ali (as) aliwahutubia watu wa Kufah kwa kauli yake: “Hakika mimi ni mjuzi wa yanayowarekebisha na kuwanyoosha waliopinda miongoni mwenu, lakini mimi sioni haja ya kuwatengeneza nyinyi kwa kuiharibu nafsi yangu.”26 Huu ndio undani wa uchamungu, asili ya dini na uhalisia wake, ama mtu akikosa kinga ya kidini au ikidhoofika kwake, hakika kuamini tu kwa itikadi au kutekeleza ibada kama mwonekano, hiyo haimaanishi uchamungu wa kweli wala hakumpi manufaa mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:

Abdul-Aziz Sayyid al-Ahli al-Khalfatu Zahid Umar bin Abdul- Aziz (Beirut Darul-Ilimi lil malaayiini) Uk. 148. 25 Rejea iliyotangulia Uk. 170. 26 Nahjul-Balaghah, khutuba ya 69. 24

32


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

ُ ‫إنَّ َما َي َت َقب‬ َ ‫َّل اللهَُّ ِم َن ْالمُتَّ ِق‬ ‫ين‬ ِ “Mwenyezi Mungu huwapokelea wenye takua tu.” (Surat Maidah: 27).

33


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

KUWALEA WATU KATIKA MAADILI YA KUWAPENDA WENGINE

M

iongoni mwa dalili ya utukufu wa Uislamu na ukweli wa daawa yake ni kuwalea watu wake katika maadili ya kuwapenda wengine, vyovyote watakavyokhitalifiana katika dini zao, kabila zao na mielekeo yao, na huu ndio mfumo wa Uislamu ambao unadhihirika katika muonekano mwingi, tunataja sehemu tatu miongoni mwazo: Kwanza: Mtazamo wa Kibinadamu: Uislamu unawapa watu wake mtazamo na utamaduni unaowafanya wawatazame watu wote kwa mtazamo wa heshima, na waamiliane nao kwa msingi wa upendo na kuwapendelea kheri watu wote, bila kujali dini zao na mitazamo yao, na hili liko wazi katika Aya za Qur’ani Tukufu, ambayo imezungumzia juu ya utukufu wa mwanadamu, anasema (swt):

ُ ‫َولَ َق ْد َك َّر ْم َنا َب ِني آ َد َم َو َح َم ْل َن‬ ‫اه ْم ِفي ْال َب ِّر َو ْال َب ْح ِر‬ َّ ‫اه ْم ِم َن‬ ْ‫ض‬ َ‫اه ْم َعل‬ َ َ َّ َ ُ ُ ‫َو َر َز ْق َن‬ ِّ ‫ير ِم َّم ْن‬ ‫ث‬ ‫ك‬ ‫ى‬ ٰ ‫ن‬ ‫ل‬ ‫ف‬ ‫و‬ ‫ات‬ ‫ب‬ ‫ي‬ ‫الط‬ َ َ ِ ِ ٍ ‫ضيل‬ ِ ‫َخلَ ْق َنا َت ْف‬ “Hakika tumewatukuza wanaadamu na tumewabeba nchi kavu na baharini na tumewaruzuku vitu vizuri na tumewafadhilisha kwa fadhila kubwa kuliko wengi miongoni mwa tuliowaumba.” (Surat Israi: 70). 34


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

Na aya hii ni ya jumla katika hoja yake katika kumtukuza mwanadamu kama mwanadamu bila ya kuangalia mwelekeo wake, rangi yake, lugha yake na dini yake. Na imepokewa kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) kwamba hakika yeye alisema: “Viumbe wote ni waja wa Mwenyezi Mungu, anayependeza zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni mwenye manufaa zaidi na waja wake.”27 Hakika mtazamo huu bora katika kumtazama binadamu, umepakwa matope na umepotoshwa na baadhi ya nadharia potovu na majaribio ya upotoshaji ambayo yanafanywa ili dini ionekane kuwa inawachukia wengine na kuwadharau na kuwaona wao ni duni, kama pale baadhi ya rai ambazo zinamtazama mwanamke kwa dharau zinaponasibishwa na dini, au pale mtu anapomdharau mwenye kunasibiana na dini nyingine au madhehebu nyingine na kunasibisha hilo na dini. Hakika mielekeo hii inakhalifu moyo na mafunzo ya Uislamu ambayo yanamtazama mwanadamu kwa heshima na kumtukuza. Pili: Kuzuia Ubaya na Uadui: Ambapo haijuzu katika sharia ya Uislamu kumfanyia uadui yeyote na vyovyote itakavyokuwa rangi yake, dini yake na madhehebu yake, isipokuwa kama mtu huyo atakuwa ni mwenye kufanya uadui, katika hali hii Uislamu unaruhusu kujitetea kwa ajili ya kuzuia uadui, anasema (swt):

َّ ‫ان إ اَّل َعلَى‬ َ‫َ ا‬ ْ َ َ ‫الظالِ ِم‬ ‫ين‬ ِ َ ‫فإِ ِن ان َت َه ْوا فل ُع ْد َو‬ “Na wakikoma, basi usiweko uadui ila kwa madhalimu.” (Surat al-Baqarah: 193). 27

anzul- Ummal, Juz. 6 Uk. 360, Hadith 16056, na inayofanana na hiyo katika Wasailu K Shia Juz. 16 Uk. 344, Hadith ya 21720. 35


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

Na anasema swt:

ُ ‫اع َت َدىٰ َعلَي‬ ْ ‫اع َت ُدوا َعلَ ْي ِه ِب ِم ْث ِل َما‬ ْ ‫ْك ْم َف‬ ْ ‫َف َم ِن‬ ٰ‫اع َت َدى‬ ُ ‫َعلَي‬ َ ‫اعلَ ُموا أَ َّن اللهََّ َم َع ْال ُمتَّ ِق‬ ْ ‫ْك ْم َواتَّ ُقوا اللهََّ َو‬ ‫ين‬ “Basi anayewachokoza, nanyi mlipizeni kwa kadiri ya alivyowachokoza. Na mcheni Mwenyezi Mungu na jueni kwamba Mwenyezi Mungu yuko pamoja na wanaomcha.” (Surat al-Baqarah: 194).

Na anasema:

ُ َ ‫يل اللهَِّ الَّ ِذ‬ ‫ين ي َُقا ِتلُو َن ُك ْم َو اَل َت ْع َت ُدوا‬ ِ ‫َو َقا ِتلوا ِفي َس ِب‬ َ ‫ُح ُّب ْال ُم ْع َت ِد‬ ‫ين‬ ِ ‫إِ َّن اللهََّ اَل ي‬ “Na piganeni katika njia ya Mwenyezi Mungu na wale wanaowapiga, wala msichokoze. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wachokozi.” (Surat al-Baqarah: 190).

Na imekuja katika hadith kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) kwamba amesema katika kumtambulisha kwake mwislamu: “Mwislamu ni ambaye watu wamesalimika kutokana na mkono wake na ulimi wake.”28 Hadithi iko wazi kwamba mwislamu wa kweli ni yule ambaye hawachokozi wengine kwa uchokozi wowote wa kimaanawi kwa kutuhumu au kwa kudharau 28

usnad Imam Ahmad, Juz. 2, Chapa ya 1419 Hijiria (Beirut A’alamul- kutub) Uk. 722, M hadith 7086. 36


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

au uadui wa kimada kama vile kupiga na kuiba. - Na imepokewa kutoka kwa Nabii (saww) kwamba amesema: “Mwenye kumuudhi mwenye dhima basi mimi ni mgomvi wake, na ambaye mimi ni mgomvi wake basi nitakuwa mgomvi wake Siku ya Kiyama.29 Tatu: Kuwafanyia Watu Wema: Kuna uhamasishaji na msukumo kutoka katika Uislam kwa kumtaka mwislamu kuwa mwema na mpole kwa watu na jamii ya kibinadamu, vyovyote zitakavyokuwa dini zao, madhehebu yao na jinsia yao, anasema (swt):

ُ ُ‫ين لَ ْم ي َُقا ِتل‬ ُ ‫اَل َي ْن َه‬ ِّ ‫وك ْم ِفي‬ َ ‫اك ُم اللهَُّ َع ِن الَّ ِذ‬ ‫ين َولَ ْم‬ ِ ‫الد‬ َ‫وك ْم ِم ْن ِد َيار ُك ْم أ‬ ُ ‫ُخر ُج‬ َ‫وه ْم َوتُ ْق ِس ُطوا إل‬ ْ َ ْ ُ ‫ْه ْم‬ ‫ي‬ ‫ر‬ ‫ب‬ ‫ت‬ ‫ن‬ ُّ َ ِ ِ ِ ِ ‫ي‬ َ ‫ُح ُّب ْال ُم ْق ِس ِط‬ ‫ين‬ ِ ‫إِ َّن اللهََّ ي‬ “Mwenyezi Mungu hawakatazi kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakuwapiga vita, wala hawakuwatoa makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu.” (Surat al-Mumtahinah: 8).

Na hadithi tukufu iliyopokelewa kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) iko wazi katika hoja yake juu ya maana hii, ambapo anasema (saww): “Viumbe ni waja Wangu, na anayependeza zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni yule mwenye manufaa zaidi 29

J ami’u Swaghir, Juz. 2, Chapa ya kwanza 1419 (Beirut Darul- fikri), Uk. 546, hadith ya 8270. 37


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

kwa waja Wake.” Ambapo hadithi imeashiria kwamba viumbe wote ni waja wa Mwenyezi Mungu na haikuzingira hayo kwa waumini na Waislamu tu. Na imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (as) kwamba amesema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) aliulizwa juu ya mtu anayependwa zaidi na Mwenyezi Mungu? Akasema: ‘Ni yule mwenye manufaa zaidi na watu.’”30 Na kutoka kwake (as) tena amesema (saww): “Msingi wa akili baada ya dini ni kuwapenda watu na kufanya kheri kwa mwema na muovu.”31 Kama ambavyo imepokewa kutoka kwa Amirul- Muuminina Ali bin Abi Twalib (as): “Wafanyie wema watu wote, hakika fadhila ya wema hailinganishwi na chochote kwa Mwenyezi Mungu.”32 Na mtu alisema mbele ya Imam Husain bin Ali (as): “Hakika wema anapofanyiwa asiyestahiki unapotea.” Imam Husain (as) akasema: ‘Sivyo hivyo, lakini itakuwa ni sawa na mfano wa maji ya mvua yanamfikia mwema na muovu.”33 Na miongoni mwa yaliyopokewa kuhusu hayo kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) ni kauli yake: “Fanya kheri kwa anayestahiki na kwa asiyestahiki, kama utamfikia asiyestahiki basi wewe unastahiki zaidi kwa wema huo.”34 Na kuna tukio analipokea mmoja wa wafuasi wa Imam as-Sadiq (as) naye ni Ma’aliy bin Khunais, amesema: “Nilitoka pamoja na Imam usiku huku akiwa na mfuko wa mikate, tukaenda eneo la Bani Sa’idah, tukakuta watu wamelala, Imam as-Sadiq akawa anaweka ustadrakul Wasail, Juz. 12, Chapa ya tatu 1991 (Beirut Muasasati Aalil bait lili ihiyaai M turathi) Uk. 390, hadith 14375. 31 Kanzul-Ummal, Juz. 8, Uk. 9, Hadith 5174. 32 Uyunul-Hikam Wal-Mawaa’idh, Uk. 75. 33 Tuhfatul-Uquul, Chapa ya tano 1394 Hijiria (Beirut Muasasatu al- A’alamiy) Uk. 176. 34 Uyun Akhibaar Ridhaa, Juz. 2, Chapa ya kwanza 1404 Hijiria (Beirut Muasasatu alA’alamiy), Uk. 38 Hadith 76. 30

38


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

mkate mmoja, miwili kando ya kichwa cha kila mtu miongoni mwao, hadi akamwendea wa mwisho wao kisha tukaondoka, nikasema: ‘Nijaaliwe niwe fidia kwa ajili yako, hawa wanajua haki? (wanaamini uimamu wako?)’ Akasema (as): ‘Kama wangeijua tungewasaidia na chumvi.”’35 Na katika riwaya kutoka kwa Masadifu (mmoja kati ya wanafunzi wa Imam as-Sadiq as) amesema: “Nilikuwa pamoja na Abi Abdillahi (as) baina ya Makka na Madina, tukapitia kwa mtu aliyekuwa katika shina la mti akiwa amejitupa hapo, akasema (as): ‘Tupitie kwa huyu mtu hakika mimi naogopa anaweza kuwa amepatwa na kiu.’ Tukapitia kwake, tukakuta ni katika watu wa Farashin mwenye nywele ndefu, akamuuliza: ‘Je, una kiu?’ Akasema: ‘Ndio.’ Akaniambia: ‘Shuka ewe Musadifu mnyweshe maji.’ Nikashuka na nikamnywesha maji kisha nikapanda na tukaondoka, nikasema: ‘Huyu ni mkiristo je unatoa sadaka kwa mkiristo?’ Akasema: ‘Ndiyo, ikiwa yuko katika hali hii.’”36 Na kutokana na nususi hizi na nyinginezo tunafahamu kwamba mfumo wa Uislamu ni kulea (watu) katika maadili ya kupenda watu, tena watu wote. Na kwa ajili hiyo hakika kati ya waliyoafikiana wanachuoni wa fiqhi wa Waislamu wote ni kwamba inasihi kutoa wakfu kwa ajili ya kuhudumia wasiokuwa Waislamu, kama vile mmoja kati ya Waislamu kutoa wakfu ili utumike kwa ajili ya mafakiri wa Kiyahudi au Kikristo au kwa ajili ya kufundishia watoto wao au kwa ajili ya kutibu wagonjwa wao na mengine yasiyokuwa hayo miongoni mwa manufaa ya jamii kwao. Na wala ruhusa ya wakfu haikomei kwa wasiokuwa Waislamu wenye amani tu bali inafika hata kwa wanaotupiga vita, kama ilivyo rai ya baadhi ya wanachuoni wa fiqhi kama vile Sayyid al-Yazdiy 35 36

al-Kafiy Juz. 4, Chapa ya 1405 Hijiria (Beirut Darul-Adhuwaai), Uk. 8. Wasaailu Shia Juz. 9, Chapa ya kwanza 1993, Uk. 49 Hadith 12350. 39


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

katika kiambatanisho cha Uruwatul-Wuthqa. Mfumo wa Kasumba: Huu ni mtazamo wa Uislamu katika kuamiliana na watu wengine, tunaoupata katika nususi zake tukufu, lakini kinachosikitisha ni kwamba hatupati wenye kuutangaza mtazamo huu na malezi yake matukufu ndani ya baadhi ya jamii za Kiislamu, bali kinyume cha hivyo tumekuwa tunasikia baina ya muda na mwingine zile kelele ambazo zinalingania kuchochea chuki, mifundo na bughudha baina ya binadamu. Badala ya kusambaa ndani ya Waislamu utamaduni wa mahaba na uelewano kumeenea ndani ya baadhi yao utamaduni wa kuchochea na kuwachukia wengine. Tunasikia baadhi ya nyakati katika hotuba za Ijumaa dua za kuwaombea kuhiliki na kuangamia Mayahudi na Wakristo, pamoja na kwamba Uislamu hauwafanyii uadui watu wa dini kwa ujumla wao bali una uadui na harakati na nyendo za uadui zinazofanywa dhidi ya Uislamu na Waislamu. Sio uadilifu kuulea umma wa Waislamu katika maadili ya kuwachukia wasiokuwa Waislamu kwa sababu ya baadhi ya misimamo inayochukuliwa na makundi ya wenye kujinasibisha na dini hizi. Na katika upande mwingine, namna gani Waislamu wataweza kutoa sura nzuri juu ya dini hii kwa wengine ikiwa wanatangaza chuki kwa wengine, mifundo na kuwaombea shari. Waislamu Wanasambaza Chuki Baina Yao: Na uchochezi huu haukuishia tu dhidi ya wasiokuwa Waislamu, bali mambo yameenda hadi kwa anayewakhalifu katika madhehebu, kuna uchochezi na uhamasishaji wa kujenga chuki baina ya Waislamu, wao kwa wao, kupitia njia mbalimbali kama vile fatwa, hotuba za Ijumaa, makala na katika baadhi ya mitaala ya kufundishia. 40


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

Na kwa hivyo Waislamu wamekuwa wanaishi baina yao katika hali inayotawaliwa na bughudha na chuki, hiyo ni kwa sababu ya uchochezi wa kibaguzi na wa kimadhehebu ambao unafanywa na kila upande dhidi ya wenginine. Bali tunakuta mas’ala yamevuka hadi kufikia katika uchochezi wa ukinzani baina ya watu wa madhehebu moja, wakati wanapogawanywa na mielekeo, na makundi mbalimbali, na ushahidi juu ya hayo ni mwingi na wa mwisho ni uliotokea Pakistani katika mji wa Karachi ambapo walikusanyika watu 50,000 wa kundi linaloitwa Tahariyku Sunnah – nalo liko katika Twariqah ya Bariylawiya – katika bustani ya umma kwa ajili ya kusherehekea maulidi ya Nabii (saww), kijana aliyevaa bomu la kujilipua akavamia kundi, na inaonyesha kijana huyu ni kutoka katika upande unaoona kwamba mfano wa hafla kama hii ni bidaa, na hivyo wakauliwa katika tukio hili watu 57 na wakajeruhiwa watu 100, na miongoni mwa waliojeruhiwa ni kiongozi wa kundi Maulana Abbas Qaadiriy (tarehe 12/4 2006).37 Na pia ndani ya jamii za Kishia tunaona zinatokea baadhi ya hali za uchochezi dhidi ya wengine wanaopinga rai na kufuata Marjaa mwingine, ambapo zinatoka fatwa za uchochezi, makala yenye kuchochea, na hotuba za mimbari zenye kuchukiza, jambo ambalo linaharibu uhusiano baina ya wanajamii, na hali inaweza kufikia kuharibu uhusiano baina ya watu wa familia moja kwa sababu ya hotuba hii ya uchochezi. Uchochezi wa Makundi Katika Silabasi za Masomo: Uchochezi huu wa chuki unaleta hali mbaya katika jamii ya Waislamu, hususan wakati unapoelekezwa kwa watoto wadogo na kufanywa kuwa ni silabasi ya kufundishia katika hatua za mafunzo ya 37

Magazeti na Mashirika ya habari. 41


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

mwanzo, hivyo watoto wanakulia katika makuzi yenye kasumba za kimakundi. Hakika silabasi hizi za uchochezi zinalaumiwa, hususan wakati zinapokuwa na ibara za kukufurisha, bidaa na tuhuma za ushirikina na upotovu, haya yanatutengenezea kizazi kilichojaa mifundo na ubaguzi uliojaa chuki na karaha dhidi ya upande mwingine. Na chakushangaza kuliko hayo ni baadhi ya waalimu wa baadhi ya mada za kidini kufanya kazi ya kuhubiri madhehebu katika jamii ambazo zinatofautiana nao kimadhehebu au kuchochea chuki baina ya wanafunzi katika jamii zilizoingiliana kimadhehebu. Hakika malezi haya yanaakisi uhusiano wa wananchi baadhi yao wao kwa wao, kwa sababu ya mahusiano yao mbalimbali, hivyo tunakuta wanafunzi wa kiume na wa kike katika jamii na vyuo vikuu wanahadharishwa kufanya uhusiano wa kawaida pamoja na wenzao kwa sababu tu ya malezi haya. Watu Ndio Muhanga: Hakika vyombo vya elimu, taasisi za kidini na familia katika malezi yao kwa kizazi hiki wanabeba majukumu makubwa, hivyo ni juu ya wale wanaomiliki sehemu za hotuba na matangazo, wazinduke na wala wasitumbukie katika mas’ala ya uchochezi wa kibaguzi na wa kimadhehebu. Wakati khatibu anapotekeleza jukumu lake la kutetea itikadi yake na kuwahamasisha watu dhidi ya upande mwingine na kundi lingine, hakika watu hawa ndio wanaokuwa muhanga wa uchochezi huu. Kijana wa kiume na kijana wa kike wanajikuta katika sehehmu za msuguano pamoja na pande hizi, ni sawa sawa iwe katika vyuo vikuu au katika sehemu za kazi, mmoja wao anapomfanyia vibaya mwingine uhusiano unaharibika na wanaishi katika hali ya ugomvi 42


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

na mvutano wa kimakundi, wakati ambapo khatibu ambaye amechochea na kuhamasisha habebi jukumu lolote. Ni wajibu kwa jamii yote kupinga uchochezi wowote na uhamasishaji wa ubaguzi, sawa iwe ndani ya Sunni au Shia, kwani uchochezi huo hautumikii isipokuwa uadui ambao unatunyemelea.

43


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

KUHESHIMU UTARATIBU NA ­KANUNI

K

ila mtu miongoni mwa wanadamu ana haja yake, maslahi yake na raghaba zake kama zinavyokhitalifiana rai zao na mielekeo yao, na ni jambo la kawaida kutofautiana raghaba na mielekeo, kwani zilishaonekana tofauti hata kwa mapacha wa Siam, ambapo wasichana wawili wa Kiirani waliishi wakiwa wameungana pamoja kwa muda wa miaka kumi na nane kabla ya kufanyiwa upasuaji wa kuwatenganisha na wakafariki baada ya hapo, walikuwa wanatofautiana katika baadhi ya raghaba na rai. Na linapoishi kundi la watu katika mazingira mamoja hakika kutofautiana raghaba, maslahi na mielekeo kunaweza kupelekea kupingana na kugongana, kama mambo yataachwa kwa ushindi na nguvu, hakika maisha ya jamii yatatawaliwa na sharia za porini. Kwa hiyo mwanadamu ametambua tangu mwanzo wa ufahamu wake kwamba katika maisha ya kijamii ni dharura kuwepo utaratibu na kanuni inayoratibu maisha ya jamii na kudhibiti uhusiano baina ya nguvu zake na watu wake. Na historia ya binadamu imejua aina za taratibu na kanuni mbalimbali zinazotofautiana katika ukaribu wake na umbali wake katika uadilifu na haki. Lakini zilikuwa zinatimiza haja ya msingi katika asili ya uwepo wake, hata kama zilikuwa zina makosa na upotovu katika utaratibu, isipokuwa ni kwamba hilo ni bora kuliko kutokuwepo utaratibu, jambo ambalo linamaanisha kuwepo kwa fujo na mkanganyiko, na lililobaki ni jukumu la warekebishaji katika kila jamii ili kwenda mbio kubadilisha kanuni na kuzipeleka katika 44


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

mwelekeo sahihi na bora, na kuziba kasoro yake na kusahihisha makosa yake na kusawazisha upotovu wake. Na haja ya kuwa na utaratibu inaweza kuvuka kutoka kwenye upande wa kijamii katika maisha ya mwanadamu, hadi katika upande wa maisha yake binafsi na katika uhusiano wake na Mola Wake na mazingira anayoishi ndani yake, pande zote hizo zinahitaji aina ya utaratibu na kanuni. Sayyid Shiraziy anasema katika kitabu chake al-Qanun katika rejea yake ya kifiqhi: “Hakika mwanadamu amehitajia kanuni kwa sababu yeye ni binadamu, ana mahitaji binafsi na ya kijamii katika nyanja mbalimbali. Na sio kama alivyosema Mgiriki: ‘Kwamba ni kwa sababu ni mtu wa jamii, hivyo anahitajia kupata mahitaji ya kijamii, na mahitaji hayawezekani kuyaweka katika mwelekeo sahihi isipokuwa kwa kanuni.’ Ni kwa sababu hata kama mwanadamu angeishi peke yake katika pori au katika pango angehitajia kanuni vilevile ambayo inapangilia nyendo zake pamoja na nafsi yake, ukiongezea kanuni ambayo inaratibu nyendo zake pamoja na muumba Wake pamoja na ulimwengu kwa sura ya jumla. Na kwa hiyo imedhihirika kwamba kauli ya baadhi ya wanafalsafa: ‘Kwamba kama jamii bora ya mfano ingeundwa kutokana na wanafalsafa isingehitajia kanuni,’ si kauli kamilifu. Vipi? Hebu tujaalie kwamba wanafalsafa wote hao walikuwa wako katika daraja la juu sana la uadilifu na usafi, je kutofautiana rai si kunapelekea mzozo na msuguano baina yao? Je, hiyo haihitajii kanuni inayowekwa na aliye juu yao – kama watamwamini – au wanaiweka wengi wao, kama wataona hivyo, au kulingana na kura au kipimo chochote kingine watakachoafikiana juu yake? Hivyo kanuni ni lazima ili kupanga mambo ya jamii, vyovyote itakavyokuwa jamii, sawa iwe ya chini au ya katikati au iliyo bora 45


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

kabisa ambayo ipo katika kilele cha utukufu na daraja la juu, ambapo ni lazima kuwepo na kipimo cha safari ya mtu binafsi na jamii katika nyanja mbalimbali za maisha.38 Kufuata Kanuni: Utulivu wa jamii na mpangilio wa mambo unategemea uhusiano mzuri baina ya pande zake, kwa kadiri wanajamii watakavyojilazimisha kufuata kanuni inayotawala baina yao. Hiyo ni kwa sababu kukhalifu kanuni kunasababisha mgongano baina ya raghaba na ni kukiuka haki, kuzuia maslahi na ni kudumbukia katika madhara maradufu. Mfano, kukhalifu kanuni za usalama barabarani kunapelekea kutokea ajali za kutisha, miongoni mwa mambo yenye kuhilikisha nafsi na kusababisha vilema na hasara ya mali. Vivyo hivyo kukhalifu kanuni za afya kunasababisha kuenea kwa magonjwa na kuhatarisha maisha ya watu, na hali ni hiyo hiyo katika nyanja na pande zingine. Kama ambavyo kukhalifu kanuni inamaanisha kupoteza haiba ya utaratibu, na hatimaye kuenea fujo. Kwa sababu hiyo ni lazima kuwepo hisia na msukumo kwa wanajamii wa kufuata kanuni na kuchunga utaratibu kwa ajili ya kuhifadhi maslahi ya jamii. Hakika baadhi ya watu wanaheshimu kanuni inapokuwa katika maslahi yake na wanaikhalifu inapokuwa kwa maslahi ya mtu mwingine, au anapokosa maslahi yake katika kuifuata, na hili ni kosa kubwa; Kwa sababu utawala wa kanuni ni maslahi ya wote, faida yake inaakisi kwa wote na ni juu yake aione nafsi yake katika nafasi ya mwingine, je inamridhisha yeye wengine kukiuka maslahi yake? Na kuna anayeheshimu utaratibu anapoogopa adhabu kali, ama wakati wa kusalimika kutokana na adhabu au anapoweza kukim38

ayyid Muhammad al- Husainiy Shiraziy katika Fiqihi- al- Qanuni, Chapa ya pili 1998, S (Beirut: Muasasatul- balagha), Uk. 103 – 104. 46


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

bia, hakika anajasiri kukhalifu na kuasi, na hii inafichua kasoro katika nafsi na uelewa. Na baadhi wanaweza kuwa na upinzani juu ya baadhi ya taratibu na kanuni au kutoziamini na kutoridhishwa na chombo kilichozitunga, lakini hilo halisihi kuwa ni kisingizio cha kukhalifu, bali ni wajibu liwe ni msukumo kwa ajili ya kazi ya kwenda mbio kusahihisha na kunyoosha kasoro za utaratibu huo na kubadilisha upande wa sharia na kanuni kwa njia na mbinu zinazowezekana za kisharia, hivyo ili kupatikane hilo ni lazima kuchunga na kuheshimu taratibu na kanuni zilizopo. Kama hali ilivyo katika jamii za kidemokrasia, ambapo upinzani unapigia kelele baadhi ya kanuni na kuzipinga na kutoa mapendekezo mbadala, na wanafanya harakati za matangazo na za kisiasa ili kutimiza hilo, lakini wapinzani wanajikuta wanalazimika kuchunga na kuheshimu utaratibu uliopo na haikubaliwi kwao kuukhalifu. Ndiyo, idara ya jumuiya inayotaka mabadiliko na usahihishaji inaweza kuwa ni yenye kukhalifu kanuni katika mbinu za kazi za kufikia mabadiliko na masahihisho, kama hali ilivyo katika mipango ya migomo na uasi wa wananchi unaotokea katika baadhi ya miji, lakini hilo pia linakuwa kupitia kanuni au uongozi wenye kukubalika, na sio harakati binafsi au vitendo vya vurugu. Na kisha haisihi kwa mtu binafsi au kundi kukhalifu kanuni na taratibu kwa msimamo wao dhidi ya utawala au angalizo lao juu ya baadhi ya kanuni. Ndiyo, hakika mwislamu hatumii kanuni inayogongana na hukumu ya kisharia yenye kulazimu anapopata njia ya kufanya hivyo. Ulimwengu na Utawala wa Sheria: Aya nyingi za Qur’ani Tukufu zinatuzindua na kutupeleka kwenye utaratibu madhubuti ambao unazunguka ulimwengu, ulimwengu unafuata utaratibu makini, kila chembe humo ipo mahala pake kwa 47


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

hisabu makini, na uhusiano wake pamoja na vitu vingine unakwenda kwa mpangilio makini, anasema (swt):

‫إِنَّا ُك َّل َش ْي ٍء َخلَ ْق َنا ُه ِب َق َد ٍر‬ “Kwa hakika tumekiumba kila kitu kwa kipimo.” (Surat al-Qamar: 49).

Na anasema (swt):

ُّ ُ ْ ‫ار‬ ٍ ‫َوكل َش ْي ٍء ِع ْن َد ُه ِب ِمق َد‬ “Na kila kitu kwake ni kwa kipimo.” (Surat Ra’ad: 8).

Na anasema (swt):

‫َق ْد َج َع َل اللهَُّ لِ ُك ِّل َش ْي ٍء َق ْد ًرا‬ “Mwenyezi Mungu amejaalia kila kitu kwa makadirio” (Surat Twalaq: 3).

Na anasema (swt):

ْ ‫َو ْال َق َم َر َق َّد ْر َنا ُه َم َناز َل َحتَّىٰ َعا َد َك‬ َ ‫ُر ُجون ْال‬ ‫يم‬ ‫د‬ ‫ق‬ ‫ع‬ ‫ال‬ ْ ِ ِ ِ ِ ُ َّ َ َّ ‫اَل‬ ‫س َي ْن َب ِغي لَ َها أ ْن تُ ْد ِر َك ْال َق َم َر َو اَل الليْل‬ ُ ‫الش ْم‬ َّ ُ َ ‫ار َو ُك ٌّل ِفي َفلَ ٍك َي ْس َب ُح‬ ‫ون‬ ِ ‫َس ِابق الن َه‬ 48


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

“Na mwezi tumeupimia vituo, mpaka ukarudi kuwa kama karara la zamani. Haliwi jua kuufikia mwezi, wala usiku kuupita mchana. Na vyote vinaogelea katika njia.” (Surat Yaasin: 39 – 40).

Aya hizi tukufu na mfano wake na yote ambayo zinayasisitiza ikiwa ni pamoja na kueleza kuwa ulimwengu unanyenyekea chini ya mpangilio thabiti, na kanuni madhubuti ambazo mwanadamu anaziona na kuzishuhudia, na ambazo elimu inaendelea kuvumbua kila siku ziada na mapya miongoni mwa maajabu yake, hakika kwa yote hayo zinataka kumwelekeza mwanadamu kwenye fikra na utukufu wa Muumba Mtukufu. Na zaidi ya hayo ni kwamba hakika zinalenga kutengeneza utayari na mazingira katika nafsi ya mwanadamu na akili yake kwa lengo la kumlazimisha kufuata utaratibu na kanuni katika maisha yake binafsi na ya kijamii. Haya na yanayotamkwa na Aya nyingine yanamkataza mwanadamu kukhalifu mipaka na sharia, na yanamhimiza kushikamana nazo, anasema (swt):

َ ‫ِت ْل َك ُح ُدو ُد اللهَِّ َف اَل َت ْع َت ُد‬ َِّ‫وها َو َم ْن َي َت َع َّد ُح ُدو َد الله‬ َّ ‫ولٰ ِئ َك ُه ُم‬ َ ُ‫َفأ‬ َ ‫الظالِ ُم‬ ‫ون‬ “Hii ndiyo mipaka ya Mwenyezi Mungu; basi msiipetuke. Na watakaoipetuka mipaka ya Mwenyezi Mungu, basi hao ndio madhalimu.” (Surat al-Baqarah: 229).

Na anasema (swt):

‫َو ِت ْل َك ُح ُدو ُد اللهَِّ َو َم ْن َي َت َع َّد ُح ُدو َد اللهَِّ َف َق ْد َظلَ َم َن ْف َس ُه‬ 49


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

“Hiyo ndiyo mipaka ya Mwenyezi Mungu msiikiuke; na mwenye kuikiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu, amejidhulumu nafsi yake.� (Surat Twalaqa: 1).

Ibada na Malezi ya Kufuata Utaratibu: Tukitafakari hukumu za ibada kwa upana katika sharia za Kiislamu, hakika sisi tutagundua kwamba zinamlea mwanadamu mwislamu katika kufuata utaratibu na kanuni. Kwa mfano Swala, inatakiwa itekelezwe na mwanadamu katika wakati maalum, haisihi kabla yake hata kwa sekunde moja, kama ambavyo haijuzu kuichelewesha hadi nje ya wakati wake kwa hiyari hata kwa sekunde moja. Na Swala ina nguzo zake na wajibu zake ambazo haisihi kuzipuuza au kuacha kitu miongoni mwazo. Na vilevile Swaumu, hakika yenyewe ni wajibu katika mwezi maalumu, kuanzia mapambazuko ya alfajiri hadi kuzama kwa jua, haikubaliki kuichelewesha Swaumu hata kwa dakika moja tangu kuingia kwa mapambazuko ya alfajir, na mukabala wa hilo haisihi kuirefusha zaidi kwa saa moja baada ya kuzama kwa jua. Na faradhi ya Hija imewekewa wakati maalumu na sehemu maalumu, ndani ya vitendo vilivyopangwa ambavyo havivunjwi na raghaba za mwanadamu wala matamanio yake, na haijuzu kupuuza na kuacha chochote miongoni mwa mipaka yake. Na hali ni hiyo hiyo katika faradhi ya Zaka ambayo ni wajibu katika kiwango maalumu, na hukumu maalumu ambayo ni lazima kuichunga. Yote hayo kikawaida yanasaidia katika kumlea mtu na kumfanya mwenye utaratibu, mwenye kujali, na mwenye kujilazimisha kufuata utaratibu na kanuni, na aliye mbali na tabia ya kuacha na kukhalifu utaratibu.

50


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

Rai ya Kifiqhi: Wanachuoni wa fiqhi wametoa fatwa juu ya wajibu wa kuheshimu utaratibu na kanuni kwa ajili ya kuhifadhi utaratibu wa maisha ya jamii na kulinda maslahi ya jumla na kuheshimu haki zilizopo baina ya watu. Na wajibu wa kujilazimisha kufuata kanuni na uharamu wa kuzikhalifu, si makhususi tu katika nchi za Kiislamu, bali hakika mwislamu anakalifishwa hayo hata awapo katika nchi isiyokuwa ya Kiislamu kwa kuzingatia kuwa ameshailazimisha nafsi yake kuheshimu taratibu zilizipo humo, kupitia katika viza ya kuingia aliyopewa ambayo inaelekeza hilo, zaidi ya hapo ni kuwepo kwa kanuni (katika Uislamu) ya kuheshimu maslahi ya wengine na haki zao. Na kama mfano tu wa rai ya kifiqhi, tunaonyesha baadhi ya fatwa za Marjaa wa kidini Sayyid Ali Sistaniy akijibu maswali aliyoulizwa yanayofungamana na kuheshimu utaratibu na kanuni, muulizaji anasema: “Je, inamlazimu mukalafu aliyepata viza kujilazimisha na kanuni katika nchi isiyokuwa ya Kiislamu, ikiwa ni pamoja na kufuata kwa mfano alama za barabarani na kanuni za kazi na mfano wake?” – Akajibu: “Ikiwa atawaahidi – hata kama ni kwa ujumla – kuchunga kanuni za nchi yao, itamlazimu kutekeleza ahadi yake ikiwa haipingani na sharia tukufu. Na mfano wa alama za barabarani moja kwa moja inalazimu kuziheshimu, ikiwa kutoziheshimu kunapelekea – kwa kawaida – kudhurika kile ambacho ni haramu kukidhuru miongoni mwa nafsi na mali.39 Na katika lifuatalo: Kuna ibara ndani ya baadhi ya vyombo vya usafiri ya kutoruhusu kuvuta sigara, je, inaruhusiwa kuikhalifu? Sayyid Sistaniy alijibu: “Ikiwa hilo lipo ndani ya masharti ya anayetaka kupanda humo au ikiwa ni kanuni ya serikali na wameshalazi39

ayyid Ali Sistaaniy katika Fiqihi Lil-Mughtaribiina, Chapa ya tatu 2002 (Qum tukufu, S ofisi ya Sistaaniy) mas’ala 235. 51


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

mika kuheshimu kanuni za serikali, itamlazimu kufanya kulingana na masharti yake na ulazima wake.”40 Na katika kujibu swali lifuatalo: Je, inajuzu kwa mwislamu kutoa taarifa zisizo sahihi katika idara za serikali huko Ulaya ili kupata faida na wepesi wa kimali au wa kimaanawi, na kwa njia ya kanuni zao? Sayyid Sistaniy alisema: “Hiyo haijuzu, hakika ni uongo na yaliyotajwa sio miongoni mwa yanayohalalisha uongo.”41 Na pia aliulizwa: Je, inajuzu kudanganya katika shule za Ulaya? Je, inajuzu kudanganya katika shule za Kiislamu na zisizokuwa za Kiislamu? Akajibu: “Haijuzu kudanganya chochote miongoni mwa mambo yake.”42 Na kuhusu sehemu kama hizi waliulizwa wanachuoni wengine wa fiqhi na majibu yao na fatwa zao vyote vinatilia mkazo umuhimu wa kuheshimu na kufuata kanuni na utaratibu katika nchi na jamii yoyote ile. Aliulizwa Marjaa wa kidini marehemu Muhammad Ridhaa Gulbaiganiy swali lifuatalo: “Katika nchi za makafiri au ambazo hazihukumu kwa sharia ya Kiislamu je, inajuzu kukhalifu utaratibu wa jumla, ilihali hapana madhara? Akajibu: Hiyo haijuzu.43 Na ulazima wa kuheshimu utaratibu na kanuni katika nchi mbalimbali bila kujali dini au muundo wa utawala wake, ni rai vilevile ya Sayyid al-Khuiy, alishajibu (rm) kuhusu swali lifuatalo: Je, hukumu yenu ya kutojuzu kukhalifu utaratibu katika nchi za kikafiri imFiqihi Lil-Mughtaribiina, mas’ala 234 “ “ 238 . 42 “ “ 233. 43 Sayyid Husain al- Husainiy katika Ahkaamil-Mughtaribiina, Chapa ya kwanza 1420 Hijiria (Tehran Markazi Twiba’ah Wanashir Lil-Majmai al-A’alamiy li Ahlul-Bait), mas’ala 1244. 40 41

52


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

ejengeka katika tahadhari (ihtiyaati) au ni fatwa kamili? Akasema: “Hii ni hukumu ya fatwa, na sio tahadhari.”44 Na katika msimamo huu anatilia mkazo Marjaa wa kidini Sheikh Muhammad al-Fadhil al-Nakaraniy, ambapo alijibu swali lifuatalo: “Je, ni wajibu kwa waumini kujilazimisha na kanuni zote katika mfano wa nchi hizi, sawa iwe katika kanuni za barabarani, harakati za magari na vyombo au nyinginezo, kama vile kuzuia baadhi ya biashara katika baadhi ya vitu au kujifunga na kanuni za kupanga bei za bidhaa na kutokhalifu kulipa kodi na mfano wa hayo? Akajibu kwa kusema: “Dhahiri ni wajibu.”45 Na wanachuoni wa fiqhi wanapotoa fatwa juu ya wajibu wa kuheshimu utaratibu na kanuni, hakika wao kwa sera yao ya kielimu wanatoa mfano wa kivitendo katika kufuata fatwa hizi. Mmoja wa watafiti katika maisha ya Imam Khomeini (rm) ameandika fasili kamili katika kitabu chake juu Imam, chini ya anwani ya “Kuheshimu kanuni”, ameandika humo idadi ya ushahidi na matukio na misimamo ambayo inadhihirisha jinsi alivyokuwa akiheshimu na kufuata utaratibu na kanuni kivitendo katika kivuli cha serikali mbalimbali, tunadondoa kati yake mifano mitatu: Anasema mmoja kati ya waandamizi wake miongoni mwa maulamaa: Usiku mmoja nilikuwa kwa Imam Khomein huko Najaf, alipomjia mmoja wa wanafunzi na akamuuliza katika majilisi yake: ‘Je, inawezekana kununua kwa riyali mbili stempu ambayo thamani yake ni riyali nane, na kujizuia kulipa kiasi kilichobaki? Imam akajibu: “Amali hii haijuzu.” Kisha akasema: Hata kama mtawala ni Stalin, hakika kuheshimu utaratibu ni kati ya wajibu muhimu sana.”46 Rejea iliyotangulia, mas’ala 1246. Rejea iliyotangulia, mas’ala 1257. 46 Qabasaati Min Siratil-Imamil- Khumainiy – al-Qiyaadah, 2005 (Beirut Darul-Islaamiya), Uk. 326. 44 45

53


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

Miongoni mwa sifa mahususi zinazoonekana wazi kwa Imam Khomeini ni kwamba hata katika dola za kikafiri alikuwa anaheshimu haki na kanuni za kijamii katika jamii hiyo, na miongoni mwa hayo ni alipokuwa Ufaransa, ndugu walikusanya mali na wakanunua kondoo na wamkachinja nyuma ya uwanja ambao Imam Khomein alikuja humo kwa ajili ya Swala, wakaandaa chakula katika usiku wa Ashura na wakatuma kiasi cha nyama kwenye nyumba ya Imam. Na Ufaransa kulikuwa na kanuni inayozuia kuchinja mnyama yoyote nje ya machinjio kwa kuchunga mas’ala ya kiafya, Imam alipojua kanuni hii akasema: “Kwa kuwa hili linakhalifu kanuni ya serikali ya nchi hii mimi sintokula nyama hii.”47 Na mara nyingine Imam Khomeini alihitaji kurejea kitabu kilichokuwepo katika maktaba ya Husainiya ya Jamraan iliyo karibu na sehemu ya makazi yake huko Tehran, maktaba ambayo hupokea watu mbalimbali, akamtaka mwanae amletee kitabu, mtoto wake Sayyid Ahmad akamweleza kwamba kanuni ya maktaba inamkataza kutoa kitabu humo na inaruhusiwa kusomea ndani ya maktaba tu. Imam akajibu haraka: “Ni lazima kufuata na kuheshimu kanuni za maktaba na kutotoa kitabu.” Na hivyo akataka aletewe kitabu kutoka sehemu nyingine.48 Kwa nini Kuna Upuuzwaji wa Taratibu? Katika nchi zilizoendelea na jamii zilizoendelea unaona kuna hali ya wananchi kwa ujumla wao kujilazimisha na kuheshimu taratibu na kanuni. Ukiukwaji wa taratibu unaopatikana humo haufikii kiwango cha kuwa ndio tabia ya jamii yao. Wakati ambapo katika jamii za nchi zinazoendelea na nchi za ulimwengu wa tatu, utakuta ukiukwaji wa kanuni unawakilisha mwonekano wa tabia yao, ambapo inakuwa 47 48

Rejea iliyotangulia Uk. 327. Qabasaati Min Siratil- Imamil- Khumainiy – al- Qiyaadah, Uk. 328. 54


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

vigumu kwa watu kuheshimu na kufuata kanuni isipokuwa wanapolazimika katika hilo. Hakika kuna sababu na mazingira yanayosaidia watu kufuata na kuheshimu taratibu na kanuni, na miongoni mwayo ni haya yafuatayo: 1.

Watu kushiriki katika kutengeneza kanuni na taratibu, unapokuwepo ushirikiano wa wananchi kupitia utaratibu wa uchaguzi na kuchagua wawakilishi katika taasisi ya kutengeneza kanuni na taratibu, hakika ridhaa ya watu juu ya kanuni na hisia zao kwamba inawakilisha rai yao na inatumikia maslahi yao, inazingatiwa kuwa ni sababu ya msingi itakayowasukuma kuitekeleza kanuni hiyo.

2.

Viongozi wa mfano: Watu wanapoona viongozi na wakuu wa jamii yao wako msitari wa mbele katika kuheshimu na kufuata kanuni na utaratibu, hakika wao wanapata msukumo wa kuitekeleza. Ama wanapoona kilichotawala ni dhana tu na watekelezaji wa kuigwa (viongozi) wako juu ya kanuni na sheria, hakika haiba ya kanuni na thamani yake inaanguka katika nafsi za wanajamii.

3.

Uangalizi na kemeo: Hakika uwepo wa utaratibu wa kukemea unaolinda kanuni na unaozuia ujasiri wa kuikiuka na kuikhalifu, na pia uwepo wa ulinzi mkali na fursa na uwazi wa kufuatilia mwenendo wa utekelezwaji wa utaratibu na kanuni, vina nafasi kubwa katika kuhakikisha ufuatwaji na utekelezwaji wa kanuni unazingatiwa. Na haya ndio tunayoyaona katika nchi zilizoendelea, ambapo kuna taasisi zinazolinda na kudhibiti, vyombo huru vya mahakama, matangazo huru yanayoangalia kosa lolote na hususan katika upande wa utekelezaji, huku upinzani wa kisiasa ukiusukuma kila upande kutafuta makosa ya upande mwingine, 55


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

jambo ambalo linatengeneza kemeo na udhibiti dhidi ya ukiukwaji wa kanuni. Wakati ambapo katika ulimwengu wa tatu kuna ukiukwaji na uzembe unaotoa fursa ya kutapakaa hali ya ufisadi na ukiukwaji wa utaratibu na kanuni. 4.

Utamaduni wa kufuata na kuheshimu kanuni: Hakika malezi yanayomlea mtu katika kuchunga utaratibu na kanuni, ni wajibu yaanzie katika mzunguko wa familia na katika silabasi ya masomo na katika mazingira ya shule, sehemu zote hizo zina nafasi kubwa katika kuwaelekeza wananchi kuheshimu utaratibu, kama ambavyo vyombo vya kuelimisha na habari vinabeba sehemu muhimu katika jukumu la kuelekeza, kuhamasisha kuheshimu utaratibu na kanuni.

Na maulamaa wa kidini kutokana na nafasi waliyonayo katika kuathiri na kufikisha, ni wajibu wao kubainisha kwa watu upeo wa kisharia katika mas’ala ya kufuata na kuheshimu kanuni. Kama ambavyo mwislamu anawajibika kuheshimu na kufuata hukumu za Swala yake ni wajibu wake pia kuheshimu na kufuata taratibu za usalama barabarani. Na kama ambavyo inaharamishwa kwake kukiuka hukumu za Swaumu pia inaharamishwa kwake kukiuka kanuni ambazo zinaratibu mambo ya wananchi na jamii kwa ujumla. Hakika kuelimisha na kufundisha kuna nafasi kubwa na ya msingi katika upande huu, na hakika jamii zetu zina haja ya moyo wa utaratibu na tabia njema ya kuheshimu na kufuata kanuni kwa ajili ya kuhifadhi maslahi yetu ya jumla, na ili kunyanyua kiwango cha mafunzo ya dini yetu tukufu na ili tusirudi nyuma zaidi katika msafara wa jamii zilizoendelea.

56


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

MTAZAMO WA KISHARIA KUHUSU UZEMBE WA WAFANYAKAZI

M

wanadamu anaishi ndani ya jamii, na mahitaji yake yanaingiliana pamoja na wengine, hivyo hawezi kufanya mambo yake yote peke yake, bali kuna wengine wanaingia katika duara la mpangilio wa mambo yake na katika kuendesha mambo yake, kama ambayo yeye anaingia katika duara la wengine. Kwa sababu hiyo kunapatikana maafikiano (mikataba) baina ya watu, ambapo kila mmoja anajilazimisha na jambo la mwingine, hivyo kuuza na kukodisha ni katika mikataba. Na maafikiano yanaweza kuwa baina ya watu wawili, na yanaweza kuwa baina ya pande mbili zinazotambulika kishera kama vile serikali, kama ambavyo upande mmoja unaweza kuwa ni taasisi au shirika. Na ili serikali iendeshe mambo ya nchi inaanzisha wizara na taasisi na vyombo vya ulinzi na usalama, idara za elimu na mafunzo, idara za afya na idara nyingine katika sekta mbalimbali, na wanafanya kazi humo wafanyakazi ndani ya utaratibu wa kikazi wa kiidara unaotokana na maafikiano na mkataba unaotakiwa kufuatwa na kuheshimiwa. Mikataba yote hii ni wajibu kuitekeleza kwa mujibu wa kauli yake (swt):

ُ ‫ين آ َمنُوا أَ ْو ُفوا ب ْالع‬ َ ‫َيا أَُّي َها الَّ ِذ‬ ‫ُقو ِد‬ ِ “Enyi mlioamini! Tekelezeni mapatano.” (Surat al-Maidah: 1).

Na mkataba katika istilahi ni ulazima wa kubadilishana unaofungwa baina ya pande mbili. Aya tukufu inasema: “Enyi mlioami57


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

ni” wanaoambiwa ni waumini, “tekelezeni mapatano” kila maafikiano yanayopatikana baina ya pande mbili ni wajibu kuyatekeleza. Na neno Aufuu lililotumika katika Aya linatokana na neno Wafaa, na neno Wafaa linamaanisha kumaliza jambo katika ukamilifu wake. Hivyo Aya inawaamuru waumini kujilazimisha katika kukamilisha mikataba bila ya kupunguza kitu chochote katika mkataba baina ya pande mbili. Hakika maendeleo ya umma yanapatikana kwa njia ya tabia njema na kuamiliana kuzuri kwa pande zote, pale kila upande unapotekeleza kiukamilifu yale ambayo ni wajibu wake kuutekeleza upande mwingine. Ama ikiwa kuna kasoro katika kufuata na kuheshimu mapatano, ikiwa kuna kutengua maafikiano kwa pande zote, hakika umma ambao unatawaliwa na hali hii hautapata uhuru wa kuendelea. Na vivyo hivyo pindi utekelezaji wa mapatano unapokuwa hafifu hakika hali hiyo inaonyesha tabia mbaya. Na sasa kuna kipimo na mizani ya kimataifa ya kujua kiwango cha uzembe katika kazi na katika idara katika nchi mbalimbali za ulimwengu, na kuizingatia hali ya kutekeleza mapatano kuwa ni katika viashiria vya takwimu za ukuaji wa uchumi na maendeleo katika nchi. Qur’an Tukufu inazingatia utekelezaji wa mapatano (mkataba) kuwa ni sifa miongoni mwa sifa za imani:

ُ ‫ين آ َمنُوا أَ ْو ُفوا ب ْالع‬ َ ‫َيا أَُّي َها الَّ ِذ‬ ‫ُقو ِد‬ ِ “Enyi mlioamini! Tekelezeni mapatano.” (Surat al-Maidah: 1).

Kwa kuwa nyinyi ni waumini ni wajibu kuwepo na utekelezaji wa ahadi kutoka kwenu.

58


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

Na hivi karibuni vituo vya runinga vimetangaza mazungumzo ya Waziri Mkuu wa Israil akiwa Marekani, akizungumzia juu ya maafikiano ambayo hupatikana kutoka kwa Waarabu, na miongoni mwa aliyoyasema ilikuwa ni: “Hakika maafikiano ambayo hupatikana kutoka kwa Waarabu hayalingani na thamani ya karatasi ambayo inatumika kuandikia mapatano hayo.” Kwa hakika haya maneno ni ya kuamsha uadui, lakini kwa upande mwingine maneno haya yanaelezea uhalisia wa hali, hususan kuhusu yanayotokea ndani ya duara la Waarabu. Kwa sababu Waarabu wanalazimika kuheshimu mapatano yanayotokea baina yao na baina ya wengine, bila kuwepo ujasiri wa kutengua. Maneno haya yanaelezea sehemu ya ukweli unaopatikana ndani ya duara la Waarabu, na kwa hiyo utakuta mikataba mingi ambayo inafanyika baina ya nchi za Kiarabu inamalizika kana kwamba hakujatokea kitu chochote. Na hali ni hiyo hiyo katika mikataba inayofanyika baina makundi mbalimbali na pande mbalimbali. Kwanza: Ni wajibu kutekeleza mkataba hata kama upande mwingine sio wa Kiislamu, imepokewa kutoka kwa Nabii (saww) kwamba amesema: “Hakuna dini kwa asiyekuwa na ahadi.”49 Na amesema Imam Ja’far as-Sadiq (as): “Mambo matatu Mwenyezi Mungu hakutoa ruhusa (ya kukhalifu) kwa yeyote: Kutekeleza amana kwa mwema na muovu, kutekeleza ahadi kwa mwema na muovu na kuwafanyia wema wazazi wawili wawe ni wema au waovu.”50 Pili: Ni wajibu kutelekeza ahadi, sawa iwe ina manufaa au ina madhara (kwako). Tatu: Ni wajibu kutekeleza ahadi katika hali ya nguvu au ya udhaifu. 49 50

Mustadrakul-Wasaail, Juz. 16, Uk. 97, Hadith 19264. Wasaailu Shia, Juz. 21, Uk. 490, Hadith 27669. 59


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

Kazi ni Mkataba wa Lazima: Nini maana ya mwanadamu kuwa mfanyakazi? Inamaanisha kuwepo mkataba baina yake na upande ambao anaufanyia kazi, na mkataba huu una misingi, inaweza ikawa imeandikwa kwa ubayana ndani ya mkataba na inaweza kuwa ni ya jumla. Kazi hii inataka kwa mfanyakazi kuheshimu muda maalum wa kazi, na kazi maalumu. Si ruhusa kwa mfanyakazi kupunguza kitu katika misingi ya maafikiano yaliyopo baina yake na baina ya upande anaoufanyia kazi. Anasema mmoja wa Maulamaa: “Katika jamii zingine mkataba unakuwa baina ya pande mbili, ama katika jamii za kiimani kuna upande wa tatu, nao ni Mwenyezi Mungu Mtukufu.� Na kati ya matatizo makubwa ambayo wanakabiliwa nayo jamii katika ulimwengu wa tatu ni kile kinachoitwa: Uzembe wa kazi, au Ufisadi wa kiofisi. Nchi ina vyombo na taasisi, na kupitia taasisi hizi inapatikana huduma ya wananchi na uendeshaji wa mambo yao, na taasisi hizi zinalea kundi miongoni mwa wafanyakazi, na kuna mkataba baina ya hawa wafanyakazi na nchi, na kisha ni wajibu kuheshimu na kufuata misingi yote na haisihi kupunguza kitu chochote katika kutekeleza mkataba. Katika idara za nchi aghlabu kuna kuwa na upuuzaji wa kazi za kiidara, hakuna kuheshimu wakati wa kazi, kuanzia mwanzo wake, mwisho wake na ndani ya kazi. Mazungumzo yameshakuwa mengi kuhusu maudhui haya katika magazeti na kwingineko katika vyombo vya habari, na sababu yake ni hali ya kutokujali kazi kwa walio wengi kati ya wafanyakazi katika idara za serikali, ambapo baadhi wanajikuta wanalazimika kufuata na kuheshimu taratibu na kanuni pindi unapokuwepo ufuatiliaji, ama mazingira yanaporuhusu na kutoa fursa ya kupuuza na kutoheshimu, huwa hawajizuwii kutokukiuka kanuni na sheria. Na hii inaashiria hatari 60


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

inayotishia maendeleo ya nchi. – Na hapa inapasa kutilia mkazo nukta zifuatazo: Kwanza: Katika upande wa kisharia (Sharia ya Uislamu), ni wajibu mwanadamu mfanyakazi kutekeleza vipengele vyote vya maafikiano yaliyopo baina yake na upande anaoufanyia kazi, na ni mwenye kuwajibika kisharia kwa kasoro yoyote itakayojitokeza. Pili: Kuna tatizo la kisharia linalomkabili katika mshahara (anakula haramu), kutokana na muda wa kazi anaoupoteza, isipokuwa kama kuna ridhaa na maafikiano kutoka upande unaohusika. Tatu: Inapasa wote wahisi kuwa wanawajibika katika upande wa maslahi ya wananchi na maendeleo ya nchi, kwa kuzingatia kwamba sote ni wadau katika nchi. Na hakika hali tunayoiona ya nchi kutokuendelea, moja ya sababu zake ni kupuuza na kutojali kazi. Na kinachosikitisha ni kwamba nchi hizi ambazo Mwenyezi Mungu amezipa kheri na uwezo wa utajiri, pamoja na kwamba zina taasisi nyingi zilizopo chini ya serikali na mashirika ya kiraia, ikiwa ni pamoja na bajeti kubwa ambayo serikali inaiweka katika vyombo mbalimbali, lakini bado mwananchi wake anakabiliwa na matatizo mengi na upungufu katika huduma kutoka katika taasisi mbalimbali, na miongoni mwa sababu za msingi ni uzembe na upuuzi unaofanywa maofisini na kazini. Na wajibu unawahusu wote na hususan wafanyakazi au vyombo vya dola, ambapo ni wajibu wao kuheshimu kikamilifu maafikiano yaliyopo baina yao na pande wanazozifanyia kazi, na wala haijuzu kuacha kipengele chochote cha maafikiano isipokuwa ikiwa upande mwingine utaacha kuheshimu. Na mara nyingi unakuta mwananchi anakasirika kwa kuchelewa muamala wake wakati anapokwenda kupata huduma katika idara au shirika, na anaonyesha kuudhika kwake anapoona uzembe kutoka kwa wafanyakazi wa hospitali na vituo 61


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

vya afya, lakini na yeye pia anapokuwa sehemu yake ya kazi unaweza kumkuta anafanya hayo hayo ambayo anawakosoa wengine. Uzembe Kazini: Muhtasari wa maana ya uzembe kazini ni: Mfanyakazi kupuuza wajibu aliopewa, na ambao umeelezwa katika kanuni, taratibu, na pia kuchukua maamuzi ambayo yanaratibu kazi kwa namna ambayo inapelekea matokeo mabaya juu ya uzalishaji na mwenendo wa kazi. Na kutohudhuria kabisa kazini au baadhi ya muda, ni moja ya sifa kubwa za uzembe kazini, na huko kutohudhuria kunaweza kuwa na sura zaidi ya moja: Yawezekana mfanyakazi asifike kabisa katika kazi yake kwa kuzua baadhi ya visingizio na nyudhuru kama vile kudai anaumwa, au dharura za kifamilia na kijamii. Wakati ambapo kwa hakika anajishughulisha na kazi nyingine. Na wakati mwingine mfanyakazi anafanya hila katika utaratibu wa kufika katika eneo la kazi yake, kwa lengo la kutia saini katika daftari la mahudhurio na kuondoka zake. Na mfanyakazi anaweza kutoka kwa ajili ya jukumu la kikazi lakini harejei baada ya kukamilisha, na anatumia muda wa kazi uliobakia nje ya kazi kwa kivuli cha jukumu muhimu. Na baadhi ya wafanyakazi hawajilazimishi kuhudhuria mwanzo wa wakati wa kazi bali wanachelewa saa moja au pungufu au zaidi, na baadhi yao wanatoka kabla ya muda wa kazi kumalizika. Na baadhi wanatumia wakati wa kazi kwa maslahi yake mengine au katika mazungumzo na marafiki zake wafanyakazi wenzake. Hakika sura zote hizi ni kwenda kinyume na wajibu wa mfanyakazi na ni kinyume na sharia, na ni kupoteza maslahi ya wananchi, na mrundikano wake unazalisha hali ya kutokuendelea katika nyanja mbalimbali. 62


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

Fatwa za Kisharia: Hakika kuheshimu mkataba wa kazi na kuhudhuria katika kazi kwa wakati uliopangwa ni mas’ala ya kisharia ambayo ni wajibu mwanadamu mwislamu kuyachunga, kama ambavyo anaona kutopunguza rakaa au sijda katika Swala ni wajibu wake, pia ni wajibu azingatie kwamba kutopoteza sehemu yoyote ya muda wa kazi yake ni wajibu kisharia, bila kujali anafanya kazi kwa nani, sawa awe ni mfanyakazi katika taasisi za serikali ya Kiislamu au isiyokuwa ya Kiislamu, sawa iwe ni serikali adilifu au isiyokuwa adilifu, na hali ni hiyo hiyo katika mashirika maalumu, haitizami wamiliki wake ni Waislamu au si Waislamu, ni wema au ni waovu, maadamu kazi aliyoajiriwa kuifanya haingii katika aina za chumo lililoharamishwa. Aliulizwa Sayyid Sistaniy: Je, inajuzu kwa mfanyakazi mwislamu anayefanya kazi katika ofisi maalumu au idara ya serikali au mwenye mkataba katika kazi fulani kwa ajira ya masaa katika nchi isiyokuwa ya Kiislamu, kutoroka kazini katika baadhi ya nyakati au kupuuza au kuzembea kwa makusudi? Na je, anastahiki ujira wote? Akajibu: Hilo halijuzu kwake, na akifanya hatostahiki ujira wote.”51 Na Sayyid al-Khuiy aliulizwa: Ikiwa mfanyakazi anafanya kazi katika shirika la kikafiri je, inajuzu kwake kutoroka kazini? Je, anastahiki ujira kamili? Akajibu: “Hiyo haijuzu, bali ni lazima katika kustahiki ujira kutekeleza kazi ambayo ameajiriwa kwa ajili yake.”52 Na aliulizwa tena: Je, inajuzu mfanyakazi kutoroka katika kazi yake au kutohudhuria baadhi ya nyakati ikiwa hapewi ruhusa? Na je anastahiki malipo kamili? Akajibu: “Haruhusiwi kutoroka kwa kiasi chochote katika kazi ambayo ameajiriwa kwa ayyid Ali Sistaaniy katika Al- Fiqihi al- Muyassar, fatwa zinazohusiana na dola na mali S zake (Beirut Darul-Auliyaai), Uk. 318, mas’ala 15. 52 Sayyid Abul – Qasim al-Khuiy katika Swiratwa Najaati, Juz. 1, Chapa ya pili 1995 (Kuwait Maktabatu al-Fiqihiya), Uk. 258, mas’ala 707. 51

63


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

ajili yake, na wala hastahiki malipo kamili (akitoroka), isipokuwa kwa ridhaa ya mwajiri.”53 Hivi ndivyo sharia inavyowalea watu wake katika kutimiza ­wajibu wao na kutekeleza mikataba yao na kuheshimu haki za ­wengine na maslahi yao.

53

Rejea iliyotangulia mas’ala 707. 64


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

TAASISI ZA AFYA NA UMUHIMU WA WAJIBU WAO

U

makini na ufanisi unatakiwa katika kazi yoyote anayoifanya mwanadamu, na katika harakati yoyote anayoifanya, lakini kila kazi inapokuwa ni muhimu zaidi na kubwa zaidi basi ufanisi humo unakuwa ni muhimu zaidi, na huwenda kati ya kazi muhimu zaidi ni ile ambayo inahusiana na maisha ya watu na roho zao, mfano utabibu na kazi katika huduma ya afya, ikiwa wale wanaofanya kazi katika kazi mbalimbali wanafanya kazi aghlabu kwa kuamiliana na vitu na vifaa, hakika tabibu na watu wa afya wanaamiliana na roho za watu na maisha yao, na kwa ajili hiyo hakika ufanisi katika sekta ya tiba ni wa dharura zaidi na muhimu zaidi, kwa sababu kosa lolote na uzembe wowote au upuuzi wowote unaweza kusababisha kuteketeza roho na unaweza kusababisha matatizo ya daima. Mas’ala ya makosa na uzembe katika sekta ya afya na tiba yamekuwa ni mas’ala yenye kutia huzuni katika kiwango cha kimataifa. Na nchi zinatofautiana katika upana na daraja ya uzembe huu na makosa haya. Ripoti imefichua kuwa mwaka 1999 walifariki watu elfu 98 kwa mwaka huko Marekani, kwa sababu ya kosa la kuainisha maradhi na kukosea katika kuandika maelezo ya kitabibu au katika njia ya kutumia dawa. Na imeeleza kwamba idadi ya Wamarekani ambao wanakufa kwa sababu ya makosa haya ya kitabibu inazidi idadi ya wale ambao wanakufa kwa sababu ya saratani ya matiti au ajali za barabarani au maradhi ya ukosefu wa kinga mwilini (Ukimwi).54 Na haya yanatokea Marekani licha ya kuwa na maendeleo katika kanuni na vyombo, mambo ambayo yanatarajiwa kupunguza ma54

Jarida la Zamaan linalotolewa London, Toleo la Ijumaa ya tarehe 3/12/1999. 65


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

kosa haya, sasa itakuwaje katika nchi nyingine, na pengine sifa ya kipekee Marekani ni kuwepo takwimu na ripoti zinazofichua mambo haya, wakati ambapo yanazuiliwa haya katika nchi nyingine, hivyo basi tatizo ni la kiulimwengu. Tiba ni Kazi ya Kibinadamu: Elimu ya nafsi ya kijamii inasema: Hakika wale ambao wanaamiliana pamoja na mwanadamu wao ni wenye kuelemea zaidi katika kushikamana na maadili ya kibinadamu, na kuwa huru kutokana na maadili ya sokoni na biashara, kuliko wasiokuwa wao katika watu wa kazi, ambazo zinaamiliana na bidhaa katika njia ya faida na mfano wake kabla ya mazingatio mengine. Na maumbile ya kibinadamu yaliyo sawa yanamsukuma mwanadamu kuokoa maisha ya mwanadamu mwenzake anapokabiliwa na hatari bila ya kuangalia mazingatio mengine. Mtu anapomuona mwingine anayehofiwa kughariki au anayekaribia kuungua au anayekabiliwa na tukio lolote la hatari au anayekabiliwa na kiu yenye kuhilikisha, hakika dhamira yake na utu wake huwa haumruhusu kupuuzia na kushangalia kuhiliki kwake. Kutokana na mantiki hii hakika mwenye ujuzi wa tiba anahisi wajibu wa kibinadamu kwa mgonjwa. Na wanachuoni wa fiqhi wa Kiislamu wamezungumzia juu ya wajibu wa kumtibu mgonjwa ili kuokoa maisha yake au kuokoa kiungo chochote kinachotishiwa na uharibifu. Na wamezingatia kuchukua malipo kwa matibabu ni jambo linalojuzu. Imam Shiraziy anasema: “Haijuzu kwa mwanadamu kuacha tiba hadi afe au hadi apofuke au hadi mkono wake upooze. Na kama ambavyo inaharamishwa kwa mwanadamu kuacha nafsi yake hadi ahiliki, au kiungo chake kiharibike au nguvu zake, kadhalika ni wajibu kwa tabibu kumpa dawa yule anayetaka kuangamia kama hakuna ta66


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

bibu mwingine anayemtibu, lakini inajuzu kwake kuchukua malipo kwani hakuna dalili ya ulazima wa kutibu bure, hivyo kukusanya baina ya haki mbili kunapelekea wajibu wa kutibu kwa malipo kama ilivyo katika fani nyingine za wajibu wa kila mmoja au wa kutosheleza. Na dhahiri ni kwamba ni wajibu kutibu nguvu na kiungo, hivyo ikiwa kutokutibu mkono kutapelekea kuukata, au ikiwa kutokutibu jicho kutapelekea kupofuka, hapo ni wajibu kufanya matibabu. Na hilo linathibitishwa na riwaya ya Ibana bin Taghlab kutoka kwa Imamu Ja’far as-Sadiq (as) amesema: Masihi (as) alikuwa anasema: ‘Hakika ni mshirika wa aliyejeruhi, yule mwenye kuacha kumtibu majeruhi kutokana na jeraha lake.’ Na nyinginezo miongoni mwa riwaya.”55 Lakini yanayomkabili mwanadamu sasa hivi katika kivuli cha maendeleo ya kimada, ni kuibadilisha kazi ya tiba kwa walio wengi kuwa ni kazi ya biashara kabisa na kuwa ni soko huria linalotawaliwa na maadili ya soko na faida kama shughuli zingine za kibiashara. Marekani ni Mfano: Na hapa tunaashiria baadhi ya yale ambayo yamezungumzwa na baadhi ya ripoti, kuhusu hali ya taasisi za afya huko Marekani, na huu ni kama mfano tu wa hali hii hatari. Hakika maamuzi yanayohusu mas’ala ya uhai na mauti yameanza kuhama kutoka katika mikono ya matatibu, viongozi na wenye jukumu, na kwenda kwenye mikono ya mashirika yanayoshughulika na faida tu, na warasimu walio mbali na matatizo ya wagonjwa. Imetawala akili hiyo ambayo Dkt. Paulo ameiita kuwa ni akili au tabia 55

ayyid Muhammad al-Husainiy as-Shiraziy katika Fiqihi, Juz. 90, Chapa ya tatu 1987 S (Beirut Darul- Ulum) Uk. 74 – 74. 67


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

ya shirika la biashara. Akili ambayo imesambaa sana katika hospitali na taasisi za tiba za Marekani, hadi watafiti wa mauzo ya hisa katika viwanda vya tiba wamekuwa wakiwaashiria wagonjwa kwamba wao ni vyanzo vya mapato. Hakika mapato ya viwanda vya tiba ni tirioni moja kwa mwaka, katika mapato hayo mashirika yenye kumiliki hospitali yanapata zaidi ya dola bilioni mia nne, na matabibu wanapata takriban bilioni mia mbili, na mashirika ya dawa yanapata bilioni mia moja. Utafiti uliofanyika mwaka 1991 katika hospitali 277 umebainisha kwamba asilimia 40 ya hospitali hizo zimekataa kupokea wagonjwa waliopelekwa na magari ya wagonjwa, kwa hoja ya msongamano. Kama ambavyo utafiti umedhihirisha kwamba hospitali nyingi hazifanyi uchunguzi unaokubalika wa huduma anayotakiwa kufanyiwa mgonjwa, kujua je ni wajibu huduma husika ifanyike au je imefanyika kwa njia sahihi. Na baadhi ya watafiti wamethibitisha hoja ya kwamba chama cha matatibu hakina tabia nzuri, kutokana na kuungana kwao pamoja na mashirika ya utengenezaji wa sigara, na muungano huu umetoa ushahidi katika baadhi ya hali, kwamba kuna ulazima wa kufanywa utafiti wa ziada kabla hayajaongezeka madhara ya uvutaji. Na imebainika katika hali nyingine, kwamba chama cha matabibu wa Marekani kilikuwa kinanunua hisa katika mashirika ya kutengeneza sigara. Kisha hakika wengi kati ya matabibu wanataka uchunguzi wa ziada kwa mgonjwa, sio tu kwa ajili ya kupata uhakika au kuepuka kukabiliwa na malalamiko ya kisheria, bali vilevile ni kwa sababu hao matabibu ndio wamiliki wa hizo maabara ambazo wanawapeleka wagonjwa wakafanyiwe uchunguzi huko. Imebainika katokana na utafiti wa Florida kwamba asilimia 40 kati ya matabibu wa jimbo hili wanamiliki maabara ambazo wa68


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

nawapeleka wagonjwa wakafanyiwe uchunguzi huko, bali wamekuta kwamba matabibu ambao wanamiliki maabara wanawataka wagonjwa kufanya utafiti wa ziada zaidi ya ule ambao wanautaka matabibu ambao hawamiliki maabara zao maalum. Na imebainika kutokana na utafiti uliofanyika Michigan kwamba matabibu elfu sita ambao wanamiliki vifaa vya x – ray waliwaamuru wagomjwa wao kufanyiwa uchunguzi wa M.R.I kwa kiasi ambacho ni zaidi ya mara nne ya uchunguzi ambao wameutaka wale matabibu ambao hawamiliki mfano wa vyombo hivi. Na katika namna ya kuainisha, Neil Postmenr katika kitabu chake Technoply amefikia kwamba kuna mambo yanayosababisha huzuni kwa wagonjwa katika ripoti ambayo inakadiriwa kwamba asilimia 40 ya upasuaji ambao umefanyika Marekani sio wa ­dharura. Na mwisho ni mashirika ya utengenezaji wa dawa, na pengine ndio mabaya zaidi katika merkebu ya watengenezaji wa bidhaa za kitabibu, ambayo yana mbinu mbalimbali za udanganyifu. Hakika faida ya mashirika ya kutengeneza madawa ndio inayoongoza katika orodha ya mashirika mia tano yenye faida nyingi Marekani. Na moja ya utafiti wa Public Citizen Health Research (Utafiti wa Afya ya Jamii kwa Raia) umepata kwamba idadi ya wakazi wenye umri mkubwa wanapata matibabu yasiyo ya dharura kabisa, na kwamba wengi wa matabibu wanahisi kwamba inatarajiwa kutoka kwao vyeti vya dawa ambavyo watawapa wagonjwa wao wanapomaliza kuwahudumia, na kwamba bei za jumla za madawa mapya ni mara sita hadi nane zaidi ya gharama za maandalizi yake. Na imebainika kwamba baadhi ya mashirika ya dawa yanawahonga baadhi ya matabibu kwa njia za ulaghai ili waandike dawa zao kinyume na 69


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

nyinginezo, licha ya kwamba dawa zao hizo si bora na wala si za gharama ndogo.56 Ikiwa hii ni baadhi ya hali inayotokea katika sekta ya afya huko Marekani, licha ya kuwa na maendeleo katika kanuni na vyombo, pamoja na taasisi za uangalizi na matangazo na hali ya ushindani ambao unausukuma kila upande kudhihirisha makosa ya upande mwingine, sasa hali itakuwaje katika nchi nyingine? – Ndiyo, inawezekana kusema kwamba jamii ambazo zina daraja ya chini ya tamaa ya kimada, na zinazotawaliwa na mazingira ya maadili mema ndio zina hali bora zaidi na zenye uovu mchache zaidi. Uzembe na Uvivu: Mengi ni matukio ambayo yanafichua uwepo wa makosa mabaya ya kitabibu, ni wangapi wamepoteza maisha yao kwa sababu ya uzembe. Baadhi ya majarida ya habari yamechapisha habari kuhusu mgonjwa wa kike ambaye alifanyiwa upasuaji wa kuondoa kidole tumbo, na maumivu yakabakia yakimsumbua, kisha ikabainika baada ya uchunguzi kwamba wao walisahau taulo ndani ya tumbo lake. Na kosa hili limesababisha tatizo la kiafya ambalo limewalazimisha kukata sehemu ya utumbo, jambo ambalo limemsababishia kilema cha kudumu.57 Na jarida la Ikaadh limetaja kwamba kijana mwenye umri wa miaka 23 aliingia hospitalini huko Jiddah akilalamika maumivu katika tezi, na baada ya saa kadhaa akafariki.58 Na sababu ya hilo ilikuwa ni kosa la kitabibu lililomaliza maisha yake. Na jarida la leo limezungumzia juu ya mwananchi aliyeingia hospitali kwa maumivu ya J arida la al-Hayaati, Uk. 15, Toleo la 1167, Alhamis 19 Januari 1995, 18 Sha’aban 1415Hijiria. 57 Jarida la al-Hayaati la London lililotolewa tarehe 28/ 12/ 1418 Hijiria. 58 Jarida la Akaadh, Jiddah, la tarehe 26 Dhul-Qaad 1418 Machi, 1998. 56

70


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

nyongo akafanyiwa upasuaji katika ubongo.59 Na yanatokea mfano wa haya baina ya wakati na mwingine, bila shaka kuna makosa ya kitabibu yanayofanyika miongoni mwayo ni: Kutokuwa na Uwezo wa Kutosha: Tabibu ambaye anakabiliana na baadhi ya hali anaweza asiwe na uwezo unaotakiwa, na hali hii inazidi pale hospitali inapoliachia majukumu shirika linalotoa na kudhamini matabibu, na linaweza kuchagua matabibu wenye mshahara na malipo madogo ili liweze kupata faida kwa kubana matumizi, na cha ajabu kuliko hayo ni kwamba baadhi ya matabibu wanaoletwa hujifunza kupitia wagonjwa katika nchi zetu. Tabibu mpya aliyehitimu hakatai kukubali kazi kwa mshahara mdogo unaomuwezesha kupata ujuzi, kisha baada ya hapo anahama na kwenda katika nchi yake au nchi nyingine kwa cheti cha ujuzi ambao utamsaidia katika kupata kazi bora zaidi. Hivyo uwezo duni wa kitabibu ni sababu ya msingi kati ya sababu zinazosababisha makosa ambayo yanatokea na kusababisha matatizo. Imepokewa kutoka kwa Amirul Muuminina Ali (as) kwamba alisema: “Ni wajibu kwa Imam kuwaweka mahabusu mafasiki kati ya wanachuoni na majahili miongoni mwa matabibu…”60 Udhaifu Katika Uwezo wa Kupokea Wagonjwa: Kila hospitali na kila tabibu ana mpaka na uwezo katika kupokea wagonjwa. Mfano ikiwa tabibu anaweza kupokea wagonjwa 20 kwa siku, na ikatokea kwamba wameingia kwake wagonjwa maradufu ya idadi hiyo, hakika hatoweza kufanikisha kazi yake kwa ufanisi. Kadiri unavyodhoofika uwezo wa kupokea wagonjwa ndivyo unavyoongezeka mbinyo katika kituo au kwa tabibu, na ndivyo unavyodhoofika uwezo unaotakiwa katika kutekeleza majukumu. Na hali hii inaweza Jarida la kila siku la Damam, Toleo la 9039 lililotolewa Jumapili tarehe 18 Dhul Qaad 1418Hijiria, 15 machi, 1998. 60 Man Laa Yahudhuruhul-Faqiihi, Juz. 3, Chapa ya pili (Qum: Jamiatul-Mudarissina) Uk. 32. Tahadhiybul-Ahkaami, Juz. 6, Uk. 319. 59

71


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

kupatikana kwa sababu ya ukata na ufinyu wa bajeti au kwa sababu ya uendeshaji mbaya au kwa sababu nyingine mbalimbali. Udhaifu Katika Maandalizi: Kadiri hospitali inavyokuwa imeandaliwa na ina mahitaji ya lazima ikiwa ni pamoja na maabara, ndivyo uwezo wa kutibu unavyokuwa bora zaidi. Na kinyume chake ikiwa maandalizi ni ya kizamani au mabovu au hayatoshi na hayalingani na idadi ya wagonjwa inayopokea hospitali, basi kwa sababu hiyo unadhoofika uwezo na makosa yanaongezeka, na wakati mwingine inaweza kutokea kwamba mgonjwa anahamishiwa hospitali nyingine kwa ajili ya kuchukua picha au kuchunguzwa kwa kutopatikana vifaa vya kutosha katika hospitali ya kwanza, pamoja na hatari yote inayoizunguka kazi ya kumhamisha. Na unaweza kuongezeka mbinyo kwa sababu ya kuwa na kifaa kimoja cha tiba katika eneo pana, na hali hiyo inaweza kusababisha msongamano wa kusubiri kwa muda mrefu, jambo ambalo linaweza kusababisha kifo kwa huyu mgonjwa. Uzembe wa Tabibu: Tabibu anaweza kuzembea katika kufanya wajibu wake kwa namna inayotakiwa, ima kwa udhaifu wake katika kuhisi majukumu, au kwa sababu anataka kulipiza kisasi kutokana na hali yake ambayo hairidhii, wakati anaopoathiriwa na hisia yake ya kwamba anadhulumiwa na kunyonywa basi hisia hii inajiakisi katika kazi yake. Na wakati mwingine baadhi ya matabibu huonekana wakiwa hawatoi juhudi yoyote katika kumchunguza mgonjwa, na hali hiyo inaweza kuwa mbaya zaidi kiasi cha kufikia kwamba cheti cha maelezo ya kitabibu na cha dawa kinakuwa kimeandaliwa kwa kila anayelalamika maradhi maalumu bila ya kutoa juhudi katika kumchunguza na kumuuliza mgonjwa kuhusu undani wa maradhi yake. Hakika tabibu anabeba majukumu makubwa mbele ya Mwenyezi Mungu. Na haya ni mas’ala ya kisharia, tabibu anaweza kuwa ni 72


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

muuwaji kama uzembe wake na uvivu wake utapelekea kufariki kwa mgonjwa. Anapozembea na kutokana na uzembe huu huyu mtu akafariki, basi yeye ndiye mwenye kuwajibika kwa damu yake mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na katika upande wa kisharia tabibu anawajibika kwa fidia na hususan anapozembea hivyo ni juu yake kutoa fidia,61 ukiachilia mbali kwamba yeye ni mwenye kuwajibika kwa uzembe mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Uwelewa wa Mwananchi: Inapasa mwanadamu awe na kiwango fulani cha maarifa kuhusu afya, mtu kuwa na kiwango fulani cha maarifa kuhusu afya kutamuwezesha kujua muamala sahihi wa kuamiliana na tabibu, hospitali na matumizi ya dawa. Na kunapatikana vitabu kwa ajili ya kuelimisha hilo, vipindi na rejea za kutosha za taarifa za kitabibu, na ni juu ya mwanadamu kupata daraja fulani la kiwango cha elimu ya afya ili kujiondolea adha katika nafsi yake na kwa jamaa zake na kwa alio pamoja nao. Na kuna anayeisalimisha nafsi yake na kutegemeza mambo yake au ya jamaa yake kwa tabibu au hospitali bila ya kuwa na ujuzi au elimu ya awali kuhusu mas’ala ya afya. Elimu ya afya ni muhimu sana na wala hakuna udhuru kwa mwanadamu sasa hivi kama atazembea kuwa na elimu hiyo, vitabu viko vingi na kuna majarida mahususi ya tiba na afya. Na hususan ikiwa mwanadamu ni mwenye maradhi fulani au ni mwenye wajibu kwa mtu mwenye maradhi kama vile kisukari au maradhi ya moyo au mfano wa hayo, hivyo ni wajibu wake atumie sehemu ya muda wake ili kupata elimu ya afya katika nyanja hii. Hivyo ni juu yake ajue ni maradhi gani na mambo gani ambayo yanasababisha kuongezeka kwake na njia zipi za kujik61

J awahirul-Kalaami, Juz. 43, Chapa ya kwanza 1992 (Beirut: Muasasatul-Murtadha alAlamiya), Uk. 44. 73


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

inga nayo? Na namna gani inapasa aamiliane nayo? Elimu ya afya inafaa katika kufikia matokeo bora. Inaelezwa kwamba matabibu wa Kijapani wanahisi vibaya sana kutokana na wagonjwa wao, kwa sababu baadhi ya wagonjwa wanazungumza na matabibu mambo ya kielimu yanayohusiana na maradhi yao, mambo ambayo inawezekana hata tabibu hayajui, na inawezakana ili kujua mambo hayo tabibu akahitajia kusoma au kufanya utafiti tena, kiasi kwamba matabibu wanauliza je, sisi tuko katika kuwahudumia wagonjwa au katika kitivo cha tiba? Na mkabala na hali hiyo tunaona jamii zetu zimejaa watu ambao wamezoea kusalimisha nafsi zao au wagonjwa wao kwa matabibu bila ya kuwa na elimu au maarifa ya awali katika misingi ya maradhi yanayowasumbua. Hakika elimu ya afya kwa mgonjwa inakuwa ni msaada kwa tabibu vilevile, na ni kinga ya kutokea baadhi ya makosa. Kama ambavyo pia inapasa kuwe na uangalizi na mazingatio kutoka kwa wananchi, maadamu tabibu anakabiliwa na makosa au uzembe basi inapasa kwa mgonjwa au msimamizi wake awe mwelewa na mwenye kuzinduka. Haisihi kuyachukulia mambo kuwa ni ya kawaida, sawa iwe ni katika kuamiliana na tabibu au na muuguzi. Katika baadhi ya nyakati yanatokea matatizo katika upande wa wauguzi wakati wahusika wanapokuwa hawana ujuzi wa kutosha au hawana ikhilasi katika kazi yao. Na hapa ndipo inapokuja dharura ya uangalizi na ufuatiliaji katika utekelezaji wa huduma za hospitali, hivyo ni wajibu kwa wananchi wanapoona udhaifu au kasoro au uzembe katika utekelezaji wa baadhi ya taasisi za afya wasinyamazie hilo, bali watoe maoni yao na watoe malalamiko yao kwa upande unaohusika hospitalini au wizarani. Kuna idara ya mambo ya afya, na kuna waziri mwenye dhamana na ni juu ya watu kuwaeleza viongozi. 74


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

Serikali inazungumzia kujali kwake maudhui haya, hivyo ni juu ya mwananchi kujali na kufikisha habari serikalini kupitia mamlaka zinazohusika, kwani kunyamazia makosa kama haya kunapelekea kuongezeka na kuendelea kwake, kwa sababu taasisi zinatokana na pato la nchi, nazo ni mahala pa mazingatio ya dola na serikali, na inaweza kuwa serikali haiwezi kudhibiti kila jambo kwa njia ya moja kwa moja, hivyo hapa inakuja nafasi ya mwananchi katika kurekebisha kasoro na jamii. Lakini urekebishaji wa wananchi katika jambo mfano wa hili unatofautiana, miongoni mwao kuna anayeshikamana na maamuzi ya haraka na kujaribu kurekebisha na kuondoa kasoro, na miongoni mwao kuna ambaye anazidiwa na uzembe au uvivu au kulala, na anatosheka na kutangaza ghadhabu yake katika vikao bila ya kuchukua hatua yoyote yenye faida, na hili ni kosa kubwa, tunalipa thamani yake kwa afya zetu na afya za watoto wetu na wapendwa wetu. Misingi na Maadili: Hakika kutawala misingi ya kidini na maadili katika jamii ndiko kunakomfanya kila mtu kati ya wanajamii kuwa mwenye kuzingatia maslahi ya jamii kwa kujali haki za wengine, wakati ambapo matamanio ya kimada yanapotawala huwa ndio sababu kubwa ya uadui na ufisadi. Na taasisi za afya na wanaofanya kazi humo wanapasa daima kukumbuka misingi ya dini na misingi ya tabia njema ili iwe mbele ya macho ya watendaji. Na maelekezo ya kidini katika jamii ni wajibu yamkumbushe kila mwenye kazi ni upi wajibu wake mbele ya Mwenyezi Mungu na mbele ya jamii yake na nchi, na kwamba kutekeleza wajibu huu ni katika msingi wa kushikamana na dini. Dini sio nembo tu na ibada (swala na funga au mfano wake) bali kabla ya hapo ni kushikamana kimwenendo na wajibu wa kijamii.

75


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

UPOTOVU: SABABU NA UTATUZI WAKE:62

J

amii yoyote ya kibinadamu haiepukani na hali za upotovu zinazodhihiri baina ya wakati mmoja na mwingine katika mwonekano wake, baadhi yake ni za kibinafsi na nyingine ni za kijamii, na hali hizo zinafichua uwepo wa kasoro fulani katika jengo la jamii hiyo, nazo ni kama hali ya maradhi ambayo inaashiria kuwepo kwa maradhi. Na kila hali inaweza kuhitajia kuainishwa tabia yake ili kujua aina ya maradhi yanayoisukuma kudhihiri. Na jambo la kushangaza zaidi ni kudhihiri hali za upotovu hatari katika jamii yetu ya Kiislamu na yenye kufuata dini, na kuendelea kutokea hali hizo hadi kugeuka kuwa hali ya kawaida. Na linaloshangaza zaidi ni mauaji kuwa hali ya kawaida, na kutumia njia za mabavu na maudhi kuwa ni hali ya kawaida. Hakika inawezekana baadhi ya hali za kuuwa na kuwafanyia watu uadui kwa kuwajeruhi au kuwapiga zina chanzo na sababu zenye nguvu, lakini linalotahadharisha hatari ya hali hii ni pale sababu zinazopelekea kutokea matendo hayo zinapokuwa ni za kipuuzi na dhaifu, kama vile kukhitalifiana pande mbili katika kiwango kidogo cha mali na mmoja wao kumuuwa mwingine kwa sababu hiyo, au kwa sababu ya ugomvi mdogo uliyotokea baina ya watoto, au mzozo wa maneno kuhusu jambo dogo. Katika hali kama hizi inapasa kuamiliana na sura hii kwa mazingatio makubwa na uelewa kamili. Na ijapokuwa matukio ya hali hizi yaliyotokea katika Saudia ni machache na yenye kuhesabika ukilinganisha na kiwango cha matukio kama hayo yanayotokea katika jamii nyingine, lakini ni kwamba bado ingalipo hali inayotutaka sisi na wenye kuijali jamii, 62

Jarida la al-Bilaadi, tarehe 19 Dhul- Qaad 1321 Hijiria. 76


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

kufanya utafiti wa kimaudhui na uchambuzi wa kina. Hiyo ni kwa kuwa nchi zetu na jamii zetu – katika mtazamo wa jamii nyingine za Waislamu – ndio kigezo na mfano, humu kuna miji miwili mitakatifu na humu ndimo ulimoteremka ujumbe na mbegu ya tawhidi, na inawakilisha marejeo ya kidini ambayo Waislamu wanaelekea upande wake (Kaaba), na ina hali nzuri ya amani na utulivu wa kijamii. Na kuanzia hapa tunasema kwa kweli kujitolea kwa jarida la alBilaadi, kuwasilisha maudhui haya na kuibua mjadala kuhusu suala hili ni juhudi nzuri na zinazopasa kuthaminiwa na kushukuriwa, na inaonyesha uelewa walionao kuhusu maslahi ya umma kwa ajili ya nchi na jamii. Miongoni mwa Sababu za Hali Hii: Kwanza: Faragha ya Kiroho: Kujiingiza sana katika mada na kwenda mbio nyuma ya faida za kimada bila ya kuchunga maadili na misingi kunazuia moyo wa mwanadamu kusikia wito wa dhamira na kelele ya maadili kutoka kwa mtoa mawaidha huyu au yule. Katika mazingira yanayotawaliwa na ukame wa kiroho na ukame wa kimaanawi si vigumu kabisa kutokea hali hii, lakini hutopata hali kama hiyo kama kutakuwa na uwepo mkubwa wa maadili na njia za mawasiliano zenye nguvu na mshikamano pamoja na Mwenyezi Mungu Mtukufu, ambapo nafasi ya mada, mbinyo wa matamanio na ubinafsi vitapungua, ambapo sauti ya haki, maadili na tabia njema vitakuwa juu. Mpaka wa kimada ni mfinyu na unapotawala maisha unafanya nafasi ya kukutana baina ya mtu na wengine ni finyu, na kuwafanya wanaotofautiana kuwa karibu zaidi na kitendo cha kukimbiana kuliko kukutana. Na pengine kutokana na hilo ndio maana tunapata nususi nyingi za kiroho kwa Waislamu, ambazo anazisoma mwan77


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

adamu wakati wa dua na kumuomba Mwenyezi Mungu, zinahimiza kusahihisha upande huu katika nafsi ya mwanadamu. Tazama kauli yake (swt):

ْ ‫ون َربَّ َنا‬ َ ُ‫ين َجا ُءوا ِم ْن َب ْع ِد ِه ْم َي ُقول‬ َ ‫َوالَّ ِذ‬ ‫اغ ِف ْر لَ​َنا‬ ُ َ ‫َول ْخ َوا ِن َنا الَّ ِذ‬ ْ‫إ‬ ‫ان َو اَل َت ْج َع ْل ِفي‬ ِ ‫الي َم‬ ِ ‫ين َس َبقو َنا ِب‬ ِ​ِ‫إ‬ َّ ًّ‫ُقلُوب َنا ِغ ا‬ ٌ ‫ين آ َمنُوا َربَّ َنا إنَّ َك َر ُء‬ َ ‫وف َر ِحي ٌم‬ ‫ذ‬ ‫ل‬ ‫ل‬ ‫ل‬ ِ ِ ِ ِ “Na waliokuja baada yao wanasema: Mola Wetu! Tughufirie sisi na ndugu zetu waliotutangulia kwa Imani, wala usijaalie ndani ya nyoyo zetu undani kwa walioamini. Mola Wetu! Hakika Wewe ni Mpole, Mwingi wa rehema.” (Surat al-Hashir: 10).

Na kauli yake (swt):

َ ‫ْر ْال َفا ِت ِح‬ َ ‫َربَّ َنا ْاف َت ْح َب ْي َن َنا َو َبي‬ ‫ين‬ ُ ‫ْن َق ْو ِم َنا ِب ْال َح ِّق َوأَ ْن َت َخي‬ “Mola Wetu! Hukumu baina yetu na baina ya kaumu yetu kwa haki, Nawe ndiwe bora wa wenye kuhukumu.” (Surat al-A’raf: 89).

Pili: Udhaifu wa Uwelewa na Elimu: Kuna watoa mawaidha na waelekezaji wengi katika jamii ya Kiislamu na hususan katika Saudia, nayo ni hali wanayotuonea wivu watu wengi, na hali hii yenyewe ilivyo inapasa iwe ni sababu yenye nguvu ya kuimarisha maadili na misingi katika jamii yetu, na inawalazimu hawa watoa waadhi kufanya kazi kubwa katika kutatua matatizo halisi 78


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

ya jamii ambayo watu wanaishi nayo. Na kwa kweli harakati za watoa nasaha na mawaidha zinahitaji juhudi nyingi na maboresho, ili ziweze kutatua matatizo ya eneo husika na wanayoishi nayo jamii husika. Waadhi unaotolewa kwa njia ya juu juu au kwa njia ya haraka haraka haupenyi hadi ndani, au kuzungumza kwa lugha ya kulazimisha na kuwajibisha bila ya kuchunga ugumu na vikwazo, au kutumia lugha ya mabavu au kukufurisha na mfano wa hayo, yote hayo na mengineyo yanaukosesha upande huu na upande unaotarajiwa faida inayotakikana, na zaidi ya hayo ni kwamba kadiri muda unavyozidi kupita ndivyo pengo la mapenzi baina ya watu na tabaka hili linavyozidi kuongezeka. Na hapa inapasa kwa watu wenye elimu na maimamu na waongozaji kuboresha hotuba zao na mbinu zao na wafikie kiwango cha uwezo wa kuathiri na kubadilisha na kutatua matatizo mbalimbali ya watu. Na hilo halitotimia isipokuwa kwa kupendekeza suluhisho la kweli la matatizo yaliyopo na kutengeneza mazingira na hali inayofaa katika kuyatatua, na kuvumbua lugha ya mazungumzo yanayoweza kuvutia watu katika kubeba majukumu na kutoa ushirikiano wa kweli katika kumaliza matatizo ya kijamii. Na haya yanaweza kuwalazimisha watoa waadhi na waelekezaji kubadilika na kuwa waasisi na wadau katika kuimarisha taasisi za kijamii zinazotoa utatuzi wenye mantiki katika matatizo, na watekeleze jukumu la waadhi na nasaha kupitia juhudi za kivitendo na sio kusubiri na maneno matupu tu. Tatu: Kusambaa na Kuelewa: Katika baadhi ya jamii zilizoendelea kuna vyombo na taasisi zinazoweza kuamiliana na upotovu wenye mabavu na zinaweza kuamiliana na watu ambao wanatumia mabavu ili kufikia malengo yao, na baadhi ya taasisi zinafanya kazi ya kuvuta utambi wa mabavu kabla ya mlipuko wake. Wajuzi wa 79


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

jamii, washauri wa mambo ya kisaikolojia, akili na nafsi, na kundi la kukabiliana na wapotovu, pande zote hizo zinajaribu kupunguza hali za mvutano zinazoweza kutokea kutokana na vitendo vya kuporomoka au kukabiliana na matatizo ya kiuchumi au ya kijamii, au zinazoweza kutokea kwa sababu za kinafsi au mazingira mengine yasiyojulikana. Hivyo imeshakuwa ni dharura katika kila jamii kuwepo na taasisi za ushauri ambazo watu wanarejea huko wakati wanapohisi wanakabiliwa na tatizo fulani, na kazi yake katika mpaka wa kidunia ni kutoa fursa kwa watu ya kueleza matatizo yao, kueleza wanayohisi katika nafsi zao pamoja na kueleza changamoto yoyote inayowakabili. Na kazi hii inaweza kufanywa na wabobezi wa mambo ya kisaikolojia, viongozi wa kijamii, watu wa elimu wenye maarifa, na watu wa rai na wajuzi katika jamii. Na ikiwa mambo katika jamii nyingine yanakwenda kwa namna ambayo mwenye tatizo ndiye anayeeleza tatizo, basi sisi tunahitaji watu wenye rai na hekima ndio wawaanze kwa kutoa nafasi kwa wenye matatizo kueleza matatizo yao. Hakika kuhisi tu mtu kwamba upande fulani unamsikiliza na unafahamu mazingira yake na matatizo yake, kutapunguza sana hali ya tatizo kwake na kumfanya akinaike zaidi kuwa uwezekano wa kutatua tatizo hilo upo.

80


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION 1. Qur’an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Thelathini 2.

Uharamisho wa Riba

3.

Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza

4.

Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili

5.

Hekaya za Bahlul

6.

Muhanga wa Imamu Husein (A.S.)

7.

Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.)

8.

Hijab vazi Bora

9.

Ukweli wa Shia Ithnaashari

10. Madhambi Makuu 11. Mbingu imenikirimu 12. Abdallah Ibn Saba 13. Khadijatul Kubra 14. Utumwa 15. Umakini katika Swala 16. Misingi ya Maarifa 17. Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia 81


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

18. Bilal wa Afrika 19. Abudharr 20. Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu 21. Salman Farsi 22. Ammar Yasir 23. Qur’an na Hadithi 24. Elimu ya Nafsi 25. Yajue Madhehebu ya Shia 26. Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur’an Tukufu 27. Al-Wahda 28. Ponyo kutoka katika Qur’an 29. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii 30. Mashukio ya Akhera 31. Al Amali 32. Dua Indal Ahlul Bayt 33. Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna. 34. Haki za wanawake katika Uislamu 35. Mwenyezi Mungu na sifa zake 36. Kumswalia Mtume (s) 37. Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) 38. Adhana 39

Upendo katika Ukristo na Uislamu 82


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

40. Tiba ya Maradhi ya Kimaadili 41. Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu 42. Kupaka juu ya khofu 43. Kukusanya swala mbili 44. Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara 45. Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya 46. Kusujudu juu ya udongo 47. Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s) 48. Tarawehe 49. Malumbano baina ya Sunni na Shia 50. Kupunguza Swala safarini 51. Kufungua safarini 52. Umaasumu wa Manabii 53. Qur’an inatoa changamoto 54. as-Salaatu Khayrun Mina -’n Nawm 55. Uadilifu wa Masahaba 56. Dua e Kumayl 57. Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu 58. Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake 59. Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata 60. Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mtume Muhammad (s) 61. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza 83


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

62. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili 63. Kuzuru Makaburi 64. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza 65. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili 66. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu 67. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne 68. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano 69. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita 70. Tujifunze Misingi Ya Dini 71. Sala ni Nguzo ya Dini 72. Mikesha Ya Peshawar 73. Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu 74. Ubora wa Imam ‘Ali Juu ya Maswahaba Na Ushia ndio njia iliyonyooka 75. Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake 76. Liqaa-u-llaah 77. Muhammad (s) Mtume wa Allah 78. Amani na Jihadi Katika Uislamu 79. Uislamu Ulienea Vipi? 80. Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) 81. Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) 82. Urejeo (al-Raja’a )

84


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

83. Mazingira 84. Utokezo (al - Badau) 85. Hukumu ya kujenga juu ya makaburi 86. Swala ya maiti na kumlilia maiti 87. Uislamu na Uwingi wa Dini 88. Mtoto mwema 89. Adabu za Sokoni 90. Johari za hekima kwa vijana 91. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza 92. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili 93. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu 94. Tawasali 95. Imam Mahdi katika Usunni na Ushia 96. Hukumu za Mgonjwa 97. Sadaka yenye kuendelea 98. Msahafu wa Imam Ali 99. Ngano ya kwamba Qur’ani imebadilishwa 100. Idi Al-Ghadir 101. Kusoma sura zenye Sijda ya wajibu 102 Hukumu zinazomhusu mkuu wa kazi na Mfanyakazi 103. Huduma ya Afya katika Uislamu 104. Sunan an-Nabii 85


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

105. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza) 106. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili) 107. Shahiid Mfiadini 108. Kumsalia Nabii (s.a.w) 109. Ujumbe -Sehemu ya Kwanza 110. Ujumbe - Sehemu ya Pili 111. Ujumbe - Sehemu ya Tatu 112. Ujumbe - Sehemu ya Nne 113. Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu 114. Hadithi ya Thaqalain 115. Ndoa ya Mutaa 116. Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza 117. Ukweli uliopotea sehemu ya Pili 118. Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu 119. Ukweli uliopotea sehemu ya Nne 120. Ukweli uliopotea sehemu ya Tano 121. Mkutano wa Maulamaa wa Baghdad 122. Safari ya kuifuata Nuru 123. Fatima al-Zahra 124. Myahudi wa Kimataifa 125. Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi 126. Visa vya kweli sehemu ya Kwanza 86


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

127. Visa vya kweli sehemu ya Pili 128. Elimu ya Ghaibu ya Maimamu 129. Mwanadamu na Mustakabali wake 130. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Kwanza) 131. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Pili) 132. Khairul Bariyyah 133. Uislamu na mafunzo ya kimalezi 134. Vijana ni Hazina ya Uislamu 135. Yafaayo kijamii 136. Tabaruku 137. Taqiyya 138. Vikao vya furaha 139. Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje? 140. Visa vya wachamungu 141. Falsafa ya Dini 142. Azadari-Kuhuzunika na Kuomboleza 143. Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah 144. Mtazamo Mpya - Wanawake katika Uislamu 145. Kuonekana kwa Allah 146. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza) 147. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili) 87


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

148. Ndugu na Jirani 149. Ushia ndani ya Usunni 150. Maswali na Majibu 151. Mafunzo ya hukmu za ibada 152. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 1 153 Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 2 154. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 3 155. Abu Huraira 156. Vipengee kadhaa katika Swala ya Jamaa na Msikiti. 157. Mazingatio kutoka katika Qur’an - Sehemu ya Kwanza 158. Mazingatio kutoka kaitka Qur’an - Sehemu ya Pili 159. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya kwanza 160. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya Pili 161. Qur’ani Tukufu – Pamoja na Tarjuma ya Kiswahili 162. Falsafa ya Mageuzi ya Imam Husein (a.s) 163. Amali za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani 164. Elimu ya Tiba za Kiislamu - Matibabu ya Maimamu 165. Uislamu Safi 166. Majlisi za Imam Husein Majumbani 167. Je, Kufunga Mikono 168. Uislam wa Shia 169. Amali za Makka 88


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

170. Amali za Madina 171. Asili ya Madhehebu katika Uislamu 172. Sira ya Imam Ali kuhusu Waasi 173. Ukweli uliofichika katika neno la Allah 174. Uislamu na Mifumo ya Uchumi 175. Umoja wa Kiislamu na Furaha 176. Mas’ala ya Kifiqhi 177. Jifunze kusoma Qur’ani 178. As-Sahifatul Kamilah as-Sajjadiyyah 179. Hayya ‘Alaa Khayri’l-’Amal Katika Adhana 180. Ukweli kuhusu Funga ya Siku ya Ashura 181. Dua za Miezi Mitatu Mitukufu (Rajabu, Shaabani na Ramadhani) 182. Uadilifu katika Uislamu 183. Mahdi katika Sunna 184. Maswali Ya Uchunguzi Kuhusu Uislam 185. Kazi na Bidii ni njia ya maendeleo 186. Abu Talib – Jabali Imara la Imani 187. Ujenzi na Utakaso wa Nafsi 188. Vijana na Matarajio ya Baadaye 189. Usalafi – Historia yake, maana yake na lengo lake 190. Ushia – Hoja na Majibu

89


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

191. Mateso ya Dhuria wa Mtume (saww) 192. Maombolezo – Msiba wa Bwana wa Mashahidi (a.s.) 193. Shahidi kwa Ajili ya Ubinadamu 194. Takwa 195. Upotoshaji dhahiri katika Turathi (Hazina) ya Kiislamu 196. Amirul Muuminina (‘as) na Makhalifa 197. Uongozi na Utawala katika Mwenendo wa Imam ‘Ali (‘a) 198. Kuvunja hoja iliyotumika kutetea Uimamu wa AbuBakr 199. Adabu za vikao na mazungumzo 200. Hija ya Kuaga 201. Uwazi baina ya Maslahi na Vikwazo 202. Fadhila za watukufu watano katika Sahih Sita 203. Mdahalo baina ya Mwanachuoni wa Kisunni na Mwanachuoni wa Kishia (Al-Muraja’aat) 204. Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (as) 205. Mjadala wa Kiitikadi 206. Mtazamo kuhusu msuguano wa Kimadhehebu 207. Nchi na Uraia – Haki na wajibu kwa Taifa 208. Mtazamo wa Ibn Taymiyyah juu ya Imam Ali (as) 209. Uongozi wa Kidini – Maelekezo na Utekelezaji wa Kijamii 210. Maadili ya Ashura 211. Mshumaa – Shahidi na Kifo cha Kishahidi

90


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

212. Mizani ya Hekima – Hadithi za Ahlul Bait (as) – Sehemu ya Kwanza 213. Imam Ali na Mambo ya Umma 214. Imam Ali na Mfumo wa Usawa 215. Mwanamke na Sharia 216. Mfumo wa Wilaya 217. Vipi Tutaishinda Hofu? 218. Kumswalia Mtume ni Ufunguo wa Utatuzi wa Matatizo 219. Maeneo ya Umma na Mali Zake 220. Nahjul-Balagha – Majmua ya Khutba, Amri, Barua, Risala, Mawaidha na Semi za Amirul-Muuminin Ali bin Abu Talib (a.s.) 221. Mukhtar – Shujaa aliyelipiza kisasi dhidi ya wauaji wa Imam Husein (as) hapo Karbala 222. Uimamu na Tamko la Kutawazwa 223. Imam Husain ni Mfumo wa Marekebisho na Mageuzi 224. Saada Kamili – Kitabu cha Kiada cha Maadili 225. Imam Hasan na Mfumo wa Kujenga Jamii 226. Adhana ni Ndoto au ni Wahyi? 227. Maimamu wa Ahlul Bait – Ujumbe na Jihadi 228. Qur’ani na Kuhifadhiwa Kwake 229. Shia na Qur’ani – Majibu na Maelezo

91


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

KOPI NNE ZIFUATAZO ZIMETAFSIRIWA KWA LUGHA KINYARWANDA 1.

Amateka Na Aba’Khalifa

2.

Nyuma yaho naje kuyoboka

3.

Amavu n’amavuko by’ubushiya

4.

Shiya na Hadithi

92


USWALIHINA DHAHIRI NA BATINI YAKE

ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION KWA LUGHA YA KIFARANSA 1.

Livre Islamique

93


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.