Utokezo

Page 1

AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009. Final D.Kanju.qxd

UTOKEZO (AL-BADAA)

Kimeandikwa na:

Sayyid Abdul-Karim al-Bahbahani

Kimetarjumiwa na:

Abdul-Karim J. Nkusui

7/1/2011

11:19 AM

Page A


AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009. Final D.Kanju.qxd

©Haki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: 978 - 9987 - 512 - 26 - 3

Kimeandikwa na:

Sayyid Abdul-Karim al-Bahbahani

Kimetarjumiwa na: Abdul-Karim J. Nkusui

Kimepangwa katika Kompyuta na: Hajat Pili Rajab

Toleo la kwanza: Julai, 2009 Nakala: 1000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Nukushi: +255 22 2127555 Barua Pepe: alitrah@raha.com Tovuti: www.alitrah.org Katika mtandao: www.alitrah.info

7/1/2011

11:19 AM

Page B


AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009. Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

11:19 AM

Page C


AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009. Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

YALIYOMO

1. Al – badau katika Qur’an tukufu............................................................2 2. Kauli za Maulama wa Shia ithna ashariyah juu ya Al-badau.................7 3. Nafasi ya itikadi na malezi yenye kujenga ya Al-badau......................10 4. Maswali juu ya itikadi ya Al-badau.......................................................13 5. Hitimisho...............................................................................................15

11:19 AM

Page D


AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009. Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

NENO LA MCHAPISHAJI Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjumi ya kitabu cha Kiarabu kiitwacho, al-Badaa’. Sisi tumekiita, Utokezo. Kitabu hiki ni matokeo ya kazi ya kielimu iliyofanywa na mwanachuoni wa Kiislamu, Sayyid Abdul-Karim al-Bahbahani. Kumekuwepo na kutokuafikiana katika miji yetu ya Kiislamu, hususan miongoni mwa wanavyuoni kuhusu usahihi wa itikadi ya Badaa’ - yaani utokezo wa jambo fulani kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Baadhi wanasema kwamba itikadi hii ni sahihi na wengine wanasema si sahihi. Baadhi ya wanavyuoni wamekwenda mbali zaidi hadi kufikia kuwaita Waislamu wenzao wanaoitakidi juu ya Utokezo (Badaa’) kuwa ni washirikina au makafiri. Lakini je, Badaa’ haina asili katika dini? Ukweli ni kwamba ina asili katika dini kama utakavyoona katika kitabu hiki. Kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote, ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni mambo ambayo hayana nafasi tena katika akili za watu. Kutokana na ukweli huu, Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili, ili kuongeza ujuzi wao katika masuala ya dini na ya kijamii. Tunamshukuru ndugu yetu, Abdul-Karim J. Nkusui kwa kukubali jukumu hili la kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake. Mchapishaji: Al-Itrah Foundation S. L. P. 19701 Dar-es-Salaam, Tanzania.

11:19 AM

Page E


AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009. Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

NENO LA JUMUIYA Hakika mirathi ya AHLUL-BAYT ambayo imehifadhiwa na kambi yao na wafuasi wao dhidi ya upotovu inaonyesha kambi iliyokusanya aina mbalimbali za taaluma za kiislamu. Kambi hii imeweza kulea nafsi mbalimbali zilizo tayari kunywa kutoka kwenye chemchemu hiyo, na kuupa umma wa kiislamu wanachuoni wakubwa wenye kufuata nyayo za ujumbe wa Ahlul-Bayt. Wanachuoni waliyokusanya vidodosa na maswali mbalimbali ya madhehebu na mitazamo tofauti ya kifikra kuanzia ndani ya desturi ya kiislamu hadi nje ya desturi hiyo, huku wao wakitoa majibu na utatuzi makini juu ya maswali hayo ndani ya karne zote. Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bayt imefanya hima kutetea tukufu za ujumbe wa Uislamu na ukweli wake ambao umechafuliwa na makundi, madhehebu na wanaharakati mbalimbali wenye chuki na uislamu. Jumuiya imefuata nyayo za Ahlul-Bayt na za wafuasi wa kambi yao njema ambayo imefanya hima kujibu madai yenye kuendelea na daima ikajaribu kubaki ndani ya msitari wa mapambano kwa kiwango kinachohitajika ndani ya kila zama. Hakika uzoefu ambao umehifadhiwa ndani ya vitabu vya wanachuoni wa kambi ya Ahlul-Bayt katika dhamira hii ni vya aina ya pekee, kwa sababu una nguzo ya kielimu inayotegemea akili na hoja, huku ukijiepusha na matamanio na uzalendo uliokatazwa. Unazungumza na wasomi na wanaharakati wenye fani maalumu mazungumzo ambayo yanaituliza akili na yanapokewa na maumbile salaF

11:19 AM

Page F


AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009. Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

ma. Jaribio hili la Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bayt limekuja kuwapa watafuta ukweli hatua mpya ya uzoefu wa thamani katika ulingo wa mazungumzo na maswali na kujibu hoja za utata zilizotolewa zama zilizopita au zinazotolewa leo kwa njia ya Tovuti, na hasa kwa kupewa nguvu na baadhi ya nchi zenye chuki dhidi ya uislamu na waislamu. Jumuiya imejiepusha na udadisi uliokatazwa na ni yenye kuhangaikia kuzidadisi akili zenye kufikiria na nafsi zenye kutafuta haki ili ziweze kufikia kwenye haki ambayo inatolewa na kambi ya Ahlul-Bayt ulimwengu mzima, ndani ya zama ambazo akili inaerevuka na nafsi na roho zinaboreka kwa kasi ya pekee. Ni lazima tugusie kuwa mfululizo huu wa tafiti hizi umeandaliwa na Kamati maalum toka jopo la wanachuoni watukufu, hivyo tunatoa shukurani njema kwa hawa wote na kwa wasomi na wahakiki kwa kila mmoja miongoni mwao kupitia sehemu ya tafiti hizi na kutoa mchango wao wa thamani kuhusu tafiti hizi. Tunategemea na kutaraji kuwa tutakuwa tumetoa kile tunachokiweza katika juhudi za kutekeleza baadhi ya wajibu tulio nao mbele ya ujumbe wa Mtukufu Mola wetu Mlezi ambaye alimtuma Mtume Wake na uongofu na dini ya haki ili aidhihirishe juu kuliko dini zote. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa shahidi.

JUMUIYA YA KIMATAIFA YA AHLUL-BAYT KITENGO CHA UTAMADUNI

G

11:19 AM

Page G


AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009. Final D.Kanju.qxd

H

7/1/2011

11:19 AM

Page H


AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009. Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

11:19 AM

Page 1


AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009. Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

Utokezo (al-Badaa)

AL-BADAU KATIKA QUR’AN TUKUFU Maudhui ya Badau yanazingatiwa kuwa ni kati ya masuala ya falsafa ya kitauhidi ambayo yamechochea utafiti wenye wigo mpana baina ya maulamaa wa elimu ya falsafa, hiyo ni kutokana na yanayopatikana humo miongoni mwa mas’ala ya kina na ya muhimu. Al-Badau katika lugha: Ina maana ya kudhihiri baada ya kufichikana, na inatumika katika mijadala ya kawaida katika nyanja za kubadilishana rai, fikra, maoni, malengo na makusudio. Hivyo husemwa: “Rai yake ilikuwa hivi kisha akabadili.” Ni dhahiri kwamba Al-Badau kwa maana hii ni kutotambua jambo mwanzo kisha ukalitambua baadaye na yote mawili hayapatikani kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kwa sababu elimu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ni ya dhati ambapo haijatanguliwa na ujahili. Lakini tukichunguza Al-Badau katika maana yake ya kilugha tunaikuta inaundwa na vitu viwili: Ujahili wa mwanzo na elimu mpya. Kubadilika kwa rai, nia na malengo kufuatana na elimu mpya aliyoipata. Kisha tunaulizana ni kipi kati ya hivi viwili kinapingana na tawhidi? Cha kwanza au cha pili au vyote viwili? Je, kuna uwezekano wa kutenganisha baina yake kiasi kwamba tunasalimika na aina ya kubadili na kugeuza ambapo hakutokani na ujahili uliotangulia wala elimu inayokuja baadaye? Ama kuhusiana na suala la kwanza: Kwa wepesi tunaona kwamba jambo la kwanza linapingana na tawhidi na hakuna Mwislamu anaekubali kuna2

11:20 AM

Page 2


AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009. Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

Utokezo (al-Badaa) sibisha ujahili kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na wala hatuhitaji kuleta aya wala riwaya juu ya hilo. Ama suala la pili: Ikiwa mabadiliko yanalazimiana na dhati ya kuwepo ujahili wa awali na kupatikana kwa elimu baadaye basi hali hii inapingana na tawhidi pia. Kama ambavyo ujahili unapingana na tawhidi vivyo hivyo unapingana na kila mabadiliko na mageuzi yanayosababishwa na hilo. Na ikiwa mabadiliko yana sababu nyingine katika hali hii hayapingani na tawhidi. Kubadili rai na mtazamo – mfano - ni kati ya mambo ya lazima ya dhati kwa ajili ya kudhihiri elimu na kuondoka kwa ujahili, hivyo basi haiwezekani kunasibisha ujahili kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Vivyo hivyo haiwezekani kunasibisha mabadiliko ya rai na mtazamo kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Bali dhana ya rai na mtazamo peke yake haiwezekani kunasibishwa kwa Mwenyezi Mungu tukiachilia mbali mabadiliko na mageuzi kwa sababu dhana hii inategemea maana ya kupata na kujifunza elimu, na elimu ya Mwenyezi Mungu haipatikani kwa njia ya kujifunza hadi isemwe kuwa huu ni mtazamo wa Mwenyezi Mungu na rai yake bali ni elimu ya dhati na inasimama juu ya dhati yake. Baada ya jawabu la maswali mawili kuwa wazi tunajaribu kutazama Qur’anTukufu ili tuangalie je, kunapatikana aya inayonasibisha mabadiliko au mageuzi katika jambo miongoni mwa mambo au nyanja kati ya nyanja? Kuna ambao wanafanya haraka kusema Qur’an inakataa kuwepo mabadiliko au mageuzi kwa Mwenyezi Mungu na hiyo ni kutokana na kauli yake (s.w.t.): “Lakini hutopata mabadiliko katika kawaida ya Mwenyezi Mungu”1 na kauli yake (s.w.t.): “Na wala hutopata mabadiliko katika kawaida ya Mwenyezi Mungu.”2 1 Suratu Fatir: 43 2 Suratul Ahzab: 62 3

11:20 AM

Page 3


AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009. Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

Utokezo (al-Badaa) Ila jawabu hili halitoshelezi kwa sababu uhalisia wa Qur’ani ni jambo linalotokana na Qur’ani yote na kinachopatikana katika upande mmoja tu hakiwakilishi isipokuwa nusu ya Qur’ani kwa sababu kinatokana na upande mmoja tu wa Qur’ani Tukufu. Kuna upande mwingine umenasibisha mabadiliko na mageuzi kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu mfano kauli yake (s.w.t.): “Mwenyezi Mungu hufuta ayatakayo na huimarisha (anayoyataka) na asili ya hukumu iko kwake.”3 Na kauli yake (s.w.t.): “Hakika Mwenyezi Mungu habadilishi yaliyoko kwa watu hadi wabadilishe yaliyoko katika nafsi zao.” 4 Aya ya kwanza inaonyesha kwamba Mwenyezi Mungu anafuta na kuthibitisha na katika hilo kunaashiria mabadiliko na mageuzi. Ama Aya ya pili imeweka wazi kwamba Mwenyezi Mungu anabadilisha hali za watu pindi wanapobadilisha yaliyopo katika nafsi zao. Hivyo hali ya kidini na kisiasa ya watu ni makadirio ya kiungu yanakubali mabadiliko pindi watu wanapoamua kubadilisha hali zao za kinafsi na kiutamaduni kutoka katika shirki kwenda kwenye imani, na kutoka kwenye upotovu kwenda kwenye uongofu. Hivyo kuna makadirio ya aina mbili, makadirio ya kiungu katika hali ya watu katika utii na makadirio ya kiungu katika hali zao katika maasi. Wanapochagua utiifu anawapitishia makadirio ya mwanzo, na wanapochagua uasi anawapitishia makadirio ya pili. Na aina hii Aya na riwaya zimeonyesha kuathiri baadhi ya vitendo katika riziki, vifo na balaa. Na haya hayakatai yeyote kati ya Waislamu bali ikhitilafu inatokea katika uelewa wa badau ilipochukuliwa kwa maana yake ya kilugha inayopingana na tawhidi, na ikhitilafu inaisha inapogundulika kuwa makusudio 3 Suratu Raad: 39 4 Suratu Raad: 11 4

11:20 AM

Page 4


AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009. Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

Utokezo (al-Badaa) yake ni maana ya kiistilahi isiyolazimu kunasibisha ujahili kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.). Hakika makusudio ya badau kwa Ahlul–Bait (a.s.) ni kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anamkadiria mja wake kulingana na hali fulani kisha Mwenyezi Mungu anabadilisha makadirio yake kutokana na hali mpya inayodhihiri kwa mja kutokana na amali fulani anayoifanya, pamoja na kutambua Kwake tangu awali mambo yote mawili na hali zote mbili. Na lau wangefahamu maana hii wangetambua kuwa ni kati ya mambo ambayo Waislamu wanaafikiana juu yake na ikhitilafu ipo katika matamshi tu. Amesema kweli Allammah as-Sayid Abdul-Husein Sharaf Diyn aliposema: “Ikhitilafu katika mas’ala haya baina yetu na Ahlus-Sunna ni ya matamshi tu.” Kisha amesema: “Aking’ang’ania asiyekuwa sisi tutamtaka arejee katika hukumu yake, hivyo abadilishe tamko la badau kama anavyotaka lakini amuogope Mwenyezi Mungu kwa ndugu yake muumini.”5 Na kabla yake alishaandika Sheikh Al-Mufiyd: “Ama kutamka tamko la badau, hakika nimelifahamu kupitia yaliyopokewa baina ya mja na Mwenyezi Mungu Mtukufu na lau kusingepokewa ambayo najua usahihi wake basi nisingekubali kutamka. Kama ambavyo lau nisingepokea kwamba Mwenyezi Mungu anakasirika na anaridhika, anapenda na kuchukia basi nisingesema hayo. Ninasema kwa maana ambayo haipingwi na akili na hakuna ikhitilafu baina yangu na Waislamu wote katika mlango huu, bali amekhalifu aliyewapinga katika tamko bila ya kupinga maana yake, na nimeshaeleza sababu yangu ya kusema hayo kwa kifupi, na huu ndio msimamo wa Mashia wote na kila aliyewakhalifu katika madhehebu anapinga niliyoyaeleza kwa jina tu bila ya kupinga maana yake na wala hayaridhii.”6 5 Ajiwibatul-Masa’ail Jarullah Uk: 79 6 Awaailul Maqalaat Uk: 92 - 93 5

11:20 AM

Page 5


AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009. Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

Utokezo (al-Badaa) Na kabla yake amesema Imamu Swadiq (a.s.) katika tafsiri ya kauli yake (s.w.t.): “Mwenyezi Mungu anafuta ayatakayo na huimarisha anayotaka na asili ya hukmu iko kwake.” Kila jambo analolitaka basi liko katika elimu yake kabla ya kulifanya, hakuna kitu kinachodhihiri ila kilishakuwa katika elimu yake. “Hakika Mwenyezi Mungu hakidhihiri kitu kwake ambako kunatokana na kutotambua.”7 Na amesema (a.s.): “Mwenye kudai kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu linadhihiri kwake jambo asilolijua basi jitengeni naye.”8 Kisha nguvu ya hoja za Shia katika mas’ala ya badau ni mambo matatu: Kauli yake (s.w.t.): “Mwenyezi Mungu anafuta ayatakayo na kuimarisha ayatakayo na asili ya hukumu iko kwake.”9 Na kauli yake (s.w.t.): “Humuomba Yeye kila kilichomo mbinguni na ardhini kila siku Yeye yumo katika mambo.”10 Kufanana mas’ala ya kufuta (nasikh) katika sharia, na badau ni nasikh katika maumbile, na nasikh ni badau ya kisharia, kama ambavyo waislamu wamethibitisha nasikh katika sharia kama vile kubadili kibla toka Masjidul-Aqsaa kuelekea Al-Ka’aba tukufu na hakukhalifu yeyote kati yao hilo, na hajazingatia yeyote kuwa hilo linakhalifu elimu ya milele ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) wala hailazimu kuthibiti ujahili wa mwanzo, vivyo hivyo katika badau na kubadilika katika hukumu za maumbile bila ya kulazimu ujahili wa mwanzo wala haikhalifu elimu ya Mwenyezi Mungu ya milele, kama yeyote atapinga badau basi upinzani wake pia utapinga nasikh na atakayoyataja katika mas’ala ya nasikh basi tunaweza kuyajibu pia katika mlango wa badau bila ya tofauti yeyote baina ya mambo hayo mawili.

7.Bihrul Anuwari Juz: 4 uk: 121 Hadith Na.: 63 8 " " " " : 30 9.Suratu Rad: 39 10. Suratu Rahman: 29 6

11:20 AM

Page 6


AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009. Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

Utokezo (al-Badaa) Mushkeli katika badau ni kukariri mushkeli waliotoa mayahudi juu nasikh katika sharia, ambapo wao wanaona ubatili wa hilo na kutowezekana kunasibisha nasikh kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, kama ambavyo wamejibu maulamaa wa Kiislamu kwa mushkeli huu na kuthibitisha kwao uwezekano wa nasikh katika sharia bila kulazimu upungufu wowote katika uungu wake mtukufu inawezekana kutumiwa katika nasikh katika ulimwengu wa kimaumbile na mamlaka. Kitendo huathtiri katika maisha ya mwanadamu, na huu ni ukweli wa Qur’ani uliothibiti kwa kuongezea yaliyopo katika Sunna za Nabii (s.a.w.w.) kwa kutilia mkazo, nayo ni kwamba amali za mwanadamu imani, shiriki, utii, maasi wema kwa wazazi wawili na kuwaasi kwao, kuwasaidia mafakiri, kutoa, kuunga udugu na kuukata n.k kunaathiri katika riziki, baraka, kurefusha umri na furaha. Na mambo haya Qur’ani imeyataja mara nyingi na Sunna zinaunga mkono mara nyingi na Qur’ani imeyafupisha kwa kusema: “Hakika Mwenyezi Mungu habadilishi yaliyopo kwa watu hadi wabadilishe yaliyopo katika nafsi zao.” Na ambaye anapinga badau lazima atambue kwamba upinzani wake unapelekea kupinga mfano wa ukweli huu ulio wazi, na ikiwa anauamini basi atambue ya kuwa haya anayoyaamini ndio ambayo Shia wanayoyaita al-Badau.

KAULI ZA MAULAMAA WA SHIA KATIKA BADAU Hii ndio maana ya badau ambayo maulamaa wa Shia waliotangulia na waliokuja baadae wametilia mkazo. Sheikh Mufiyd anasema: “Kauli ya Shia katika al-badau njia yake ni ya kusikiwa na wala sio ya kutafakari, na makusudio yake sio kubadili rai na kutambua jambo lililokuwa limefichikana kwake, vitendo vya Mwenyezi Mungu vyote viko dhahiri kwa viumbe vyake kabla hata ya kuvimba, navyo vinatambulikana Kwake 7

11:20 AM

Page 7


AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009. Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

Utokezo (al-Badaa) na bado vingali vinatambulika.”11 Sheikh Tusi amesema: “Al-Badau katika lugha ni kudhihiri, hivyo husemwa umedhihri kwetu uzio wa mji na imetudhihirikia rai …” Ama likinasibishwa tamko hili kwa Mwenyezi Mungu humo kuna ambayo hayafai kunasibishwa Kwake; Ama ambayo yanafaa ni ambayo yanakusudia nasikh (kufuta) na kunasibisha hayo Kwake kuna wigo mpana, katika upande huu yanachukuliwa yote yaliyopokelewa kutoka kwa wakweli miongoni mwa habari zenye maana ya kunasibisha badau kwa Mwenyezi Mungu bila ya kunasibisha yasiyofaa kwake miongoni mwa kutambua baada ya kutotambua, na wajihi wa kuyasema hayo ni kwamba ikiwa yanayoonyesha nasikh inayodhihiri kwa mkalafu ambayo hayakuwa dhahiri kwao na kupata kwao elimu baada ya kutokuwa nayo, hayo huitwa “Al–badau.”12 Na amesema As-Sayyid Abdallah Shubar: “Al-Badau ina maana nyingi, baadhi yake zinajuzu na zingine hazijuzu nayo ni - kwa fatiha na madda -aghlab hutumika katika lugha kwa maana ya kudhihiri kitu baada ya kufichikana na kupata elimu kwayo baada ya kutojua. Na umma umeafikiana kukanusha hayo kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ila yale ambayo hayachupi mpaka Kwake, na mwenye kunasibisha hayo kwa Shia basi ameshawazulia uongo na Shia wako mbali nao.”13 As-Sayyid Abdul-Husein Sharaf Diyn amesema: “Na matokeo wanayosema Shia hapa ni kwamba Mwenyezi Mungu anapunguza riziki na kuongeza humo, vivyo hivyo katika vifo, afya maradhi furaha, matatizo, mitihani, balaa, imani ukafiri n.k. kama ilivyosema kauli Yake tukufu: “Mwenyezi Mungu hufuta atakayo na kuimarisha ayatakayo na asili 11 Taswihihul-Itiqaadatil Imamiyah Uk; 66 chapa ya Darul Mufiyd 12 Maswabihu Durar Juz: 1 Uk: 33 13 Udstul–Usul Juz: 2 Uk: 29 8

11:20 AM

Page 8


AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009. Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

Utokezo (al-Badaa) ya hukumu iko kwake.”14 Na huu ndio mtazamo wa Umar bin Khattab na Ibnu Mas’ud, Abi Wail na Qatadah. Na amepokea Jabir kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na wengi wa Salaf wanaomba na kunyenyekea kwa Mwenyezi Mungu awajaalie wawe wema na wala wasiwe waovu, na yamepokewa hayo kwa tawaatur kutoka kwa Maimamu wetu katika dua zao zilizopokelewa, na imepokewa katika Sunna kwamba sadaka kwa namna yake, wema kwa wazazi wawili, kufanya wema, haya yanabadili uovu kuwa wema na yanaongeza umri. Na imesihi kwa Ibnu Abbas kwamba yeye amesema: “Tahadhari hainufaishi kitu katika Qadar lakini Mwenyezi Mungu anafuta kwa dua anayotaka miongoni mwa Qadar.” Hii ndio badau ambayo wanaisema Shia, inajuzu kuinasibisha badau kwake kwa uhusiano wa kufanana. Ikhitilafu katika hili baina yetu na Ahlus-Sunna ni ya matamshi tu, na anayosema Shia katika badau kwa maana tuliyoitaja wanaisema Waislamu wote.15 Sheikh Agha Bazarak at-Twaharaniy anasema: “Al-Badau maana yake katika lugha ni kudhihiri rai ambayo haikuwepo na kusahihisha kitu kilichojulikana baada ya kutojulikana, lakini haifai kunasibishwa kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kulazimu kudhihiri rai juu ya kitu ambacho hakikuwepo kwa kutokijua Kwake awali au kushindwa Kwake na Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ametakasika na hayo. Al-Badau wanayoisema Shia ni kwa maana ambayo lazima kila mwislamu anaitakidi mkabala na wayahudi wanaosema kwamba Mwenyezi Mungu amemaliza kazi hivyo hakidhihiri kitu chochote kwake: “Mkono wa Mwenyezi Mungu umefumba” au mwenye kufuata kauli za wayahudi wenye kudai kwamba Mwenyezi Mungu ameumba vyote vilivyopo mara moja hivyo hakuna kitu ila alichokiumba awali au alikuwa anaitakidi mfumo wa ulimwengu kwa kusema kwamba Mwenyezi Mungu ameumba 14 Suratu Raad: 39 15 Ajuwibatu Masaail Jarullah Uk: 101 -103 9

11:20 AM

Page 9


AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009. Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

Utokezo (al-Badaa) mfumo wa ulimwengu nao uko nje umevuliwa katika mamlaka yake, mifumo mingine ndio inaoiendesha, ambapo lazima kila mwislamu akanushe kauli hizi na aitakidi kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu “ kila siku yuko katika mambo”16

NAFASI YA ITIKADI NA MALEZI YENYE KUJENGA KATIKA BADAU Imedhihiri katika yaliyotangulia kwamba al- badau ina maana ya Qur’ani imeenea baina ya waislamu wote na kwamba Shia hawatofautiani na waislamu wengine isipokuwa katika jina ambalo kwalo linafahamika kosa la kunasibisha ujahili kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na imebainika kutosihi kunasibisha huku, na kilicho muhimu kwetu sasa ni kueleza upande mwingine wa utafiti, nao ni umuhimu wa fikra ya badau kuhusu itikadi ya mwanadamu mwislamu, kwani fikra zinapimwa kwa misingi yake ya kielimu na hoja zake za kimantiki na kwa malengo yake na matunda yake kwa upande mwingine. Na katika maudhui ya badau inaweza kusemwa kwa njia ya kuuliza: Ikiwa makadirio ya awali hayatakuwa na kazi bali yatamalizikia kwa kufutwa, nini faida ya kutoa taarifa juu yake? Na nini matunda yanayopatikana kwa kuitakidi al-Badau wakati huo? Jawabu: Hakika kuitakidi al-Badau kunarejea kwenye umuhimu mkubwa sana katika pande mbili: Upande wa itikadi na upande wa malezi. Ama upande wa kiitikadi yanatutosha maneno ya Allammah al-Majlisiy ambapo ameandika anasema: “Hakika wamevuka mpaka katika al-Badau kwa kuwajibu Wayahudi ambao wanasema: “Hakika Mwenyezi Mungu amemaliza kazi na utawala.” Na baadhi ya Mu’tazila wanasema: “Hakika 16 Suratu Rahman: 29 10

11:20 AM

Page 10


AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009. Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

Utokezo (al-Badaa) Mwenyezi Mungu ameumba viumbe mara moja kama ilivyo hivi sasa miongoni mwa madini, mimea, wanyama, wanadamu, na wala kuumbwa Adamu hakujatangulia kuumbwa watoto wake, na kutangulia ni katika kudhihiri kwake sio katika kuumbwa kwake na kuwepo kwake, bali wamechukua makala haya kwa watu wa falsafa wenye kusema kuhusiana na mfumo wenye kuendesha ulimwengu, na wenye kusema kwamba mamlaka ya Mwenyezi Mungu hayakuathiri isipokuwa katika uumbaji wa awali tu, hivyo wao wanamuengua Mwenyezi Mungu (s.w.t.) katika mamlaka Yake na wananasibisha uendeshaji kwenye mfumo wa ulimwengu na wala sio kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.” 17 Kwa maana kwamba mkazo wa Maimamu (a.s.) juu ya al-Badau umekuja ili kubatilisha kila fikra zinazofanya uwezo wa Mwenyezi Mungu na matakwa Yake (s.w.t.) kuwa na kiwango maalum, na kuthibitisha kuwa ni uhakika wa jumla kwa pande zote hata katika upande wa Qadar ambayo anaikadiria Mwenyezi Mungu Mtukufu mwenyewe katika ulimwengu wa maumbile, uumbaji, uendeshaji na malezi. Na kwamba makadirio ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) katika makadirio hayo, hayamfanyi kuwa ni mwenye kupokonywa hiari Yake na matakwa Yake kutokana na hayo. Kama ambavyo al-Badau imekuja ili kutilia mkazo juu ya hiari ya mwanadamu na matakwa yake wakati wa kubainisha uwezo wa kiungu, humo kuna Lauhul-Mahfuudh haikubali mabadiliko, na Lauhu nyingine ni ya kufuta na kuthibitisha ambayo anayakadiria Mwenyezi Mungu (s.w.t.) tangu mwanzo wa kuumba, hii inakubali mabadiliko kulingana na anayoyafanya mwanadamu miongoni mwa amali katika dunia. Kana kwamba itikadi ya al-Badau imekuja ili kukamilisha itikadi ya Qadhwaa na Qadar ili kuondolewa “Ghuluu” kuchupa mpaka na kufifiliza katika itikadi ya Qadhwaa na Qadar, na isichukuliwe kwa maana ambayo itapokonya hiari kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na kwa mwanadamu. Hivyo hakuna budi kuikamilisha kwa itikadi ya badau ambayo imekuja kutilia mkazo kwam17 Biharul-Anwar Juz: 4, Uk: 129 – 130 chapa ya Tehran 11

11:20 AM

Page 11


AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009. Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

Utokezo (al-Badaa) ba Qadar haifikii kiwango cha kupokonya hiari ya Mwenyezi Mungu wala haipokonyi hiari ya mwandamu. Na katika upande wa malezi tunaona kwamba itikadi ya al-Badau ina athari ya kimalezi yenye kujenga katika maisha ya wanadamu, na Allammah al-Majlisiy anabainisha athari hii katika kukamilisha maana yake yaliyopita juu ya sababu za kutilia mkazo Maimamu (a.s.) juu ya alBadau, ambapo kwanza anataja faida ya kuitakidi ambazo tumezitaja na akaongezea kwa kutaja faida ya kimalezi kwa kusema: “Hivyo Maimamu (a.s.) wakakataza hayo na wakathibitisha kwamba (s.w.t.) kila siku yuko katika kazi miongoni mwa kuondoa, kuleta kingine, kumfisha mtu na kumhuisha mwingine, n.k. ili waja wasiache kunyenyekea kwa Mwenyezi Mungu, kuomba, kutii, kujikurubisha kwake kwa yale yanayofaa katika mambo ya dunia yao na akhera yao, na ili wataraji wanapotoa sadaka kwa mafakiri, kuunga udugu, kuwafanyia wema wazazi wawili, kufanya mema na ihsani kwa yale waliyoahidiwa katika kuongezewa umri na kuongezewa riziki.� Na katika upande mwingine itikadi ya al-Badau ni kuhamasisha juu ya uzuri wake katika itikadi ya toba na masharti ya kukubaliwa mbele ya Mwenyezi Mungu, kama ambavyo toba ina athari nzuri katika kumjenga mwanadamu, na kwa upande mwingine ni kufunga mianya ya kukata tamaa na kufungua milango ya matumaini na matarajio na kujenga moyo wa mageuzi na maandalizi ya mafanikio, vivyo hivyo badau ina athari hii katika maisha ya mwandamu, bali badau ni dharura kati ya dharura za toba na vigezo vyake ni katika amali, kwani kati ya dharura za toba ni mwenye kutubia kuitakidi kwamba kalamu ya Mwenyezi Mungu bado wino wake haujakauka katika ubao wa kufuta na kuthibitisha, hivyo Mwenyezi Mungu anaweza kufuta na kuthibitisha anayotaka, anamneemesha amtakaye na kumfanya amtakaye kuwa muovu kulingana na anavyojipamba mja miongoni mwa tabia njema na amali njema, au kulingana na anavyofanya amali mbaya, na wala matakwa ya Mwenyezi Mungu hayaji bure bure tu, bila ya kudhibitiwa na hekima. Bali lau mja akitubu na kutekeleza 12

11:20 AM

Page 12


AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009. Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

Utokezo (al-Badaa) ya wajibu na kushikamana na wema anatoka katika kundi la watu waovu na kuingia katika kundi la waja wema, na kinyume chake pia ni sahihi. Na katika hayo yote tunaweza kufahamu maana ya maneno ya Maimamu (a.s.) kwamba: “Hajaabudiwa Mwenyezi Mungu kwa chochote mfano wa anavyoabudiwa kwa badau.”18 Na wala “Hajatukuzwa Mwenyezi Mungu mfano wa anavyotukuzwa kwa al-Badau.”19 Na “Mwenyezi Mungu hajatuma Nabii hadi achukue kwake ahadi ya mambo matatu: Kukubali ibada ya Mwenyezi Mungu, kuivua shirki, na kwamba Mwenyezi Mungu hutanguliza ayatakayo na huchelewesha ayatakayo.” 20

MASWALI KUHUSU ITIKADI YA BADAU Hapa tunatoa maswali yanayotaka majibu yenye kutosheleza nayo: 1. Hakika kauli ya al-Badau inasababisha Mwenyezi Mungu kufanya upuuzi kwani pamoja na kutambua yatakayotokea kwake miongoni mwa mabadiliko na kudhihiri, basi kutoa taarifa kwa makadirio ya mwanzo itakuwa ni upuuzi? Jawabu: Hakika itakuwa ni upuuzi kama tutajaalia kutokuwepo lengo na manufaa yanayotarajiwa kutokana na kutoa taarifa ya makadirio ya mwanzo, na haya ni ambayo hatuwezi kuyathibitisha, hivyo inawezekana kuwepo lengo na manufaa yanayorejea kwa mja kwa faida kubwa kutokana na taarifa hiyo. 2. Hakika Nabii au Imamu akitoa taarifa ya kitu kisha ikatokea al-Badau katika kutokea kwake, ni lazima ategemee katika taarifa yake ya awali kwenye kitu kinachokuwa ni chanzo (rejea) cha taarifa yake na asili ya chanzo cha elimu yake, sasa ni kwa jambo gani atategemea Nabii au Imamu katika taarifa yake ya awali? 18 Usulul-Kafiy Juz: 1, Uk: 146 19 Usulul-Kafiy : Jz. 1, Uk. 146 kitabu Tawhid Babul-Badai 20 Usulul-Kafiy : Jz. 1, Uk. 146 kitabu Tawhid Babul-Badai 13

11:20 AM

Page 13


AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009. Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

Utokezo (al-Badaa) Jawabu: Inahitaji kubainisha mfano kama lau mwanadamu akila sumu yenye kuangamiza inayosababisha kifo chake hakika utakapoona tukio hili unaweza kumpa taarifa ya kutokea kifo chake baada ya masaa, nayo ni habari ya kweli kulingana na hali halisi isiyo na shaka, na kama mauti hayakutokea kwa sababu ya kutokea kizuizi kisichotarajiwa kama vile kutokea tabibu wa kumtibu mwenye ujuzi wa hali ya juu, taarifa hiyo haiwi ya uongo wala haihesabiwi kuwa ni taarifa isiyo na chanzo, vivyo hivyo katika taarifa ya mbinguni ambayo inatoa taarifa za kutokea baadhi ya mambo katika siku zijazo, kwani ni za kweli kulingana na hali ya kutokuwepo na kizuizi wala hakuna ubaya katika jambo hili isipokuwa kutotambua Nabii au Imamu kupatikana kwa kizuizi hapo baadae. Hivyo tuseme kwamba Mwenyezi Mungu amempa Nabii taarifa ya jambo na hakutaka kumpa taarifa ya kutokea kwa kizuizi baadaye kwa maslahi yanayohusiana na waja. 3. Hakika kutokea badau inasababisha Nabii au Imam kutuhumiwa kwa uongo. Jawabu: Hakika kutuhumiwa Nabii au Imamu kwa uongo ni jambo ambalo dhambi yake inamwangukia mwenye kulifanya, na tuhuma kama itatoka kwa kafiri basi hii sio ajabu kwake baada ya kukataa kuamini asili ya tawhidi, utume na marejeo, na kama itatoka kwa muumini tunajaalia kuwa imani yake itamzuia juu ya hilo, na kama haitamzuia basi hiyo ni dalili ya udhaifu wa imani yake. Cha muhimu ni kwamba badau sio sababu ya kimantiki ya kumtuhumu kwa uongo bali hali nyingi za badau zilikuwa zikiambatana na yanayosadikisha ukweli, kama ilivyo katika kisa cha Ibrahim (a.s.) pale alipoamrishwa kumchinja mtoto wake, kwani amri mpya ya fidia inamaanisha kusadikisha amri ya awali ya kumchinja Ismail (a.s.) na kama hiyo taarifa ya awali haikuwa ya kweli basi amri ya kuchinja kondoo isingekuja ni fidia badala yake, hivyo fidia ni kwa maana ya badala.

14

11:20 AM

Page 14


AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009. Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

Utokezo (al-Badaa)

HITIMISHO Hakika al-Badau kwa maana ya kubadili rai haitokei kwa Mwenyezi Mungu na wala Shia hawasemi hivyo, bali wanasema kutowezekana hilo na ukafiri wa mwenye kusema hivyo, na kwamba inalazimu kujiepusha na anayesema hivyo.21 Ndio, al-Badau inayokubaliwa na ambayo ni wajibu kuitakidi kwayo imeelezwa na Aya za Qur’ani tukufu: “Mwenyezi Mungu anafuta ayatakayo na huimarisha anayoyataka na asili ya hukumu iko kwake.” Na kufuta huku na kuimarisha kunakuwa wazi na kuthibiti katika anayoyadhihirisha Mwenyezi Mungu miongoni mwa mambo kwa ulimi wa Nabii wake au Walii wake katika dhahiri kwa masilahi yanayohitajia kudhihirishwa, kisha anayafuta na yanakuwa yale yasiyodhihiri mwanzo pamoja na kutambua hilo tangu mwanzo kwa elimu yake. Badau inafanana na nasikh (kufuta) hukumu za kisharia zilizotangulia kabla ya Nabii Muhammad (s.a.w.w.) au nasikh ya baadhi ya hukumu ambazo zimekuja katika sharia ya Nabii wetu (s.a.w.w.) kwa hukumu zilizofuata baadaye.22 Hakika ambaye haamini itikadi hii ya badau basi atakuwa amemuwekea Mwenyezi Mungu kikomo katika uwezo Wake na matakwa Yake yasiyo na mpaka, kama ilivyoashiria Qur’ani tukufu juu ya hilo katika itikadi ya kiyahudi kwa kauli yake: “Wamesema Wayahudi mkono wa Mwenyezi Mungu umefumba, bali imefumba mikono yao.”23 Na haya ndio ambayo yameenea kwa baadhi ya makundi ya Kiislamu yasiyokuwa Shia Ithina Ashariyah. 21 Aqaidul-Imamiyah cha Mudhafar uk: 45 chapa ya pili ya Najaf 22 Aqaidul-Imamiyah cha Mudhafar uk: 45 chapa ya pili ya Najaf 23 Suratul Maida: 64 15

11:20 AM

Page 15


AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009. Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

Utokezo (al-Badaa)

ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION: 1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9. 10. 11. 12. 13. 14. 15. 16. 17. 18. 19. 20. 21. 22. 23. 24. 25. 26. 27.

Qur'an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Ishirini na Nne Uharamisho wa Riba Uharamisho wa uwongo Juzuu ya kwanza Uharamisho wa uwongo Juzuu ya pili Hekaya za Bahlul Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.) Hijab vazi Bora Ukweli wa Shia Ithnaashari Madhambi Makuu Mbingu imenikirimu Abdallah Ibn Saba Khadijatul Kubra Utumwa Umakini katika Swala Misingi ya Maarifa Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia Bilal wa Afrika Abudharr Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu Salman Farsi Ammar Yasir Qur'an na Hadithi Elimu ya Nafsi Yajue Madhehebu ya Shia Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur'an Tukufu Al-Wahda 16

11:20 AM

Page 16


AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009. Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

Utokezo (al-Badaa) 28. 29. 30. 31. 32. 33. 34. 35. 36. 37. 38. 39 40. 41. 42. 43. 44. 45. 46. 47. 48. 49. 50. 51. 52. 53. 54. 55. 56. 57. 58. 59. 60.

Ponyo kutoka katika Qur'an. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii Mashukio ya Akhera Al Amali Dua Indal Ahlul Bayt Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna. Haki za wanawake katika Uislamu Mwenyeezi Mungu na sifa zake Amateka Na Aba'Khalifa Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) Adhana. Upendo katika Ukristo na Uislamu Nyuma yaho naje kuyoboka Amavu n’amavuko by’ubushiya Kupaka juu ya khofu Kukusanya swala mbili Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Kusujudu juu ya udongo Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s) Tarawehe Malumbano baina ya Sunni na Shia Kupunguza Swala safarini Kufungua safarini Umaasumu wa Manabii Qur’an inatoa changamoto as-Salaatu Khayrun Mina -'n Nawm Uadilifu wa Masahaba Dua e Kumayl Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mitume Muhammad (s) 17

11:20 AM

Page 17


AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009. Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

Utokezo (al-Badaa) 61. 62. 63. 64. 65. 66. 67. 68. 69. 70. 71. 72. 73. 74. 75. 76. 77. 78. 79. 80. 81. 82. 83. 84. 85. 86. 87. 88. 89. 90. 91.

Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili Kuzuru Makaburi Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu Tujifunze Misingi Ya Dini Sala ni Nguzo ya Dini Mikesha Ya Peshawar Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu Ubora wa Imam 'Ali Juu ya Maswahaba Na Ushia ndio njia iliy onyooka Shia asema haya, Sunni asema haya, Wewe wasemaje? Liqaa-u-llaah Muhammad (s) Mtume wa Allah Amani na Jihadi Katika Uislamu Uislamu Ulienea Vipi? Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) Urejeo (al-Raja’a ) Shahidi kwa ajili ya Ubinadamu Kuanzia ndoa hadi kuwa wazazi Myahudi wa Kimataifa Uislamu na dhana Mtoto mwema Adabu za Sokoni Johari za hekima kwa vijana Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu Tawasali Imam Mahdi katika Usunni na Ushia

92.

Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu 18

11:20 AM

Page 18


AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009. Final D.Kanju.qxd

Utokezo (al-Badaa) 93.

Hukumu ya kujenga juu ya makaburi

94.

Swala ya maiti na kumlilia maiti

95.

Shiya na Hadithi (kinyarwanda)

96.

Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu

97.

Hadithi ya Thaqalain

98.

Fatima al-Zahra

99.

Tabaruku

100.

Sunan an-Nabii

101.

Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza)

100.

Idil Ghadiri

102.

Mahdi katika sunna

103.

Kusalia Nabii (s.a.w)

104.

Ujumbe -Sehemu ya Kwanza

105.

Ujumbe - Sehemu ya Pili

106.

Ujumbe - Sehemu ya Tatu

107.

Ujumbe - Sehemu ya Nne

108.

Shiya N’abasahaba

109.

Iduwa ya Kumayili

110.

Maarifa ya Kiislamu.

111.

Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza

112.

Ukweli uliopotea sehemu ya Pili

113.

Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu

114.

Ukweli uliopotea sehemu ya Nne

115.

Ukweli uliopotea sehmu ya Tano

19

7/1/2011

11:20 AM

Page 19


AL-BADAU - PROOFREAD BYA SHEMAHIMBO ON 04 - 02 - 2009. Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

Utokezo (al-Badaa)

BACK COVER Maudhui ya Utokezo (Badaa’) yanazingatiwa kuwa ni kati ya masuala ya falsafa ya Kitawhidi ambayo yamechochea utafiti wenye wigo mpana baina ya maulamaa wa elimu ya falsafa, hiyo ni kutokana na yanayopatikana humo miongoni mwa masuala ya kina na ya muhimu. Kumekuwepo na kutokuafikiana katika miji yetu ya Kiislamu, hususan miongoni mwa wanavyuoni kuhusu usahihi wa itikadi ya Badaa’ - yaani utokezo wa jambo fulani kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Baadhi wanasema kwamba itikadi hii ni sahihi na wengine wanasema si sahihi. Baadhi ya wanavyuoni wamekwenda mbali zaidi hadi kufikia kuwaita Waislamu wenzao wanaoitakidi juu ya Utokezo (Badaa’) kuwa ni washirikina au makafiri . Lakini je, Badaa’ haina asili katika dini? Ukweli ni kwamba ina asili katika dini kwani uhalisi wake umeelezwa katika Qur’ani Tukufu, kama utakavyoona katika kitabu hiki. Hivyo ungana na mwaandishi wa kitabu hiki, Sayyid Abdul-Karim al-Bahbahani katika utafiti wake huu wa kielimu. Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Nukushi: +255 22 2127555 Barua Pepe: alitrah@raha.com Tovuti: www.alitrah.org Katika mtandao: www.alitrah.info

20

11:20 AM

Page 20


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.