Uwahabi haukubaliki

Page 1

Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo ‫الوهابية مرفوضة عقال و نقال‬

Mwandishi: Baba Mtumishi Kabwe Hussein

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 1

8/14/2017 1:18:22 PM


© Haki ya kunakili imehifadhiwa na: Al-Itrah Foundation ISBN No: 978 - 9987 – 17 – 008 – 1 Kimeandikwa na: Baba Mtumishi Kabwe Hussein Kimehaririwa na: Ustadh Haji Hemedi Lubumba Selemani Kimesomwa Prufu na: Al-Haj. Ramadhani S. K. Shemahimbo Kimepangwa katika Kompyuta na: Al-Itrah Foundation Toleo la kwanza: Decemba, 2017 Nakala: 2000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. - 19701, Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 / 2127555 Barua Pepe: alitrah@yahoo.com Tovuti: www.ibn-tv-com Katika mtandao: www.alitrah.info Vitabu vya Kiswahili mtandaoni: www.alitrah.info/ebooks/ ILI KUSOMA QUR’ANI MUBASHARA KWA NJIA YA MTANDAO, TEMBELEA www.somaquran.com

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 2

8/14/2017 1:18:22 PM


YALIYOMO Tabaruku.......................................................................................... 1 Dibaji................................................................................................ 2 Neno la Mchapishaji........................................................................ 3 Utangulizi......................................................................................... 5 Shukurani......................................................................................... 9 SEHEMUYA KWANZA............................................................ 11 Historia ya Uwahabi...................................................................... 11 Watoto wa Sheikh Muhammad Bin Abdul-wahab ....................... 13 Ni nani wa kwanza kuunga mkono Uwahabi baada ya kuibuka kwake?......................................................................... 14 Sheikh Abdul-Wahab na imani ya kukufurisha watu . .................. 15 Ni nani aliyepandikiza mbegu za madhehebu hii kwa mara ya kwanza?.................................................................... 19 Sababu za kuenea kwa madhehebu potovu ya uwahabi................ 20 Mazigazi......................................................................................... 23 Mapigano baina ya Sharif Ghalib, Amiri wa Makka na genge la Maharamia wa Kiwahabi............................................ 25 Mawahabi waivamia Iraq............................................................... 29 Kamwe hatutasahau mauaji ya Karbala......................................... 32 Kuvunjika kwa mkataba wa amani baina ya Sharif Ghalib na Mawahabi........................................................... 38 Barua ya wazi kwa Sharif Abdul-Muin......................................... 42

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 3

8/14/2017 1:18:22 PM


Maharamia wa Kiwahabi wauvamia mji wa Taif mwaka 1217 A.H.................................................................... 45 Maharamia wa Kiwahabi waingia Taif kwa mabavu..................... 47 Mawahabi waukamata mji wa Makka mwaka 1218A.H............... 47 Maharamia wa Kiwahabi watimuliwa Makka............................... 49 SEHEMU YA PILI..................................................................... 51 TAUHIDI....................................................................................... 51 Ukafiri wa Mawahabi nyuma ya mgongo wa tauhidi................... .51 Aina za tauhidi............................................................................... 53 TAUHIDI katika dhati ya Mwenyezi Mungu................................ 59 Vyanzo vya maarifa........................................................................ 54 Njia tano za fahamu....................................................................... 54 Akili............................................................................................... 56 Moyo.............................................................................................. 56 Hitimisho....................................................................................... 57 Je, Mwenyezi Mungu ni chanzo au matokeo?............................... 57 Je, aliyemuumba Adam yeye kaumbwa na nani............................ 58 TAUHIDI katika uumbaji.............................................................. 59 TAUHIDI katika malezi na uendeshaji wa ulimwengu................. 60 Je, neno Rabi maana yake ni muumba?......................................... 66 Tofauti kati ya maana na tamko..................................................... 66

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 4

8/14/2017 1:18:22 PM


Rabi katika Qur’ani........................................................................ 68 Mawahabi na tafsiri yao potovu..................................................... 73 TAUHIDI katika ibada................................................................... 80 Je, ni nini maana ya ibada?............................................................ 82 Njia ya kwanza............................................................................... 84 Njia ya pili...................................................................................... 87 Njia ya tatu..................................................................................... 89 Lengo la ibada kwa Wanatauhidi................................................... 91 Tabaka la pili.................................................................................. 93 Malengo ya Washirikina katika ibada............................................ 96 Lengo la kwanza: Kutafuta heshima na ushindi............................ 96 Lengo la pili: Masanamu yana nafasi ya uombezi......................... 97 Lengo la tatu: matendo ya kiungu.................................................. 98 Lengo la nne: Masanamu ni mithili ya Mwenyezi Mungu............ 99 SEHEMU YA TATU................................................................. 104 Bidaa............................................................................................ 104 Je, unafahamu nini linapotamkwa neno Bidaa?........................... 104 Bidaa katika dini.......................................................................... 104 Sifa na vigezo vya mpanga sheria kwa wanadamu...................... 106 Je, ni nani mwenye mamlaka ya kupanga sharia katika Uislam?............................................................................. 111

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 5

8/14/2017 1:18:22 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Je, kama haki ya kupanga sharia ni ya Mwenyezi Mungu peke yake, ni yapi majukumu ya baraza la sharia katika nchi za Kiislamu?................................................... 113 Kuchezea sharia ni Bidaa............................................................. 114 Maana ya Bidaa............................................................................ 115 Bidaa katika kamusi za Lugha ya Kiarabu.................................. 115 Maoni ya Wanachuoni katika uwanja huu................................... 116 Bidaa kwa mtazamo wa kielimu.................................................. 117 Nguzo za neno Bidaa................................................................... 120 Bidaa nzuri na Bidaa mbaya........................................................ 121 Vyanzo vya uharibifu wa sharia katika dini................................. 125 Utawa........................................................................................... 126 Kufuata matamanio...................................................................... 127 SEHEMU YA NNE................................................................... 129 Kutembelea makaburi.................................................................. 129 Azimio la Kiwahabi la kumdhalilisha Bwana Mtume ...... 129 Ususuavu wa moyo wa Kiwahabi wapevuka............................... 130 Msimamo wa Sheikh wa Mawahabi, Muhammad Bin Abdul-Wahab juu ya makaburi.................................................... 132 Kutumbelea makaburi ni maumbile ya kibinadamu.................... 134 vi

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 6

8/14/2017 1:18:23 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Kutembelea makaburi ya Wanachuoni........................................ 136 Kutembelea makaburi ya mashujaa wa Kiislaam........................ 138 Kutembelea kaburi la Bwana Mtume ............................... 145 Mtazamo wa Wanachuoni katika kutembelea kaburi la Bwana Mtume ............................................................... 148 Mtazamo wa Qur’ani juu ya kutembelea kaburi la Bwana Mtume  . ............................................................. 149 Kuna tofauti gani kati ya ukamilifu na utimilifu?........................ 151 Je, mwanamke anaruhusiwa kwenda kutembelea makaburi?..................................................................................... 152 Hoja chakavu za Kiwahabi.......................................................... 155 SEHEMU YA TANO................................................................ 159 Kumsomea maiti talakini............................................................. 159 Hoja chakavu za Kiwahabi katika kupinga talakini..................... 159 Majibu yetu.................................................................................. 159 Nabii Swaleh baada ya kuangamizwa watu wake....................... 163 Kisa cha Nabii Shuaib.................................................................. 166 Bwana Mtume na Manabii waliomtangulia................................. 167 Bwana Mtume katika vita vya Badri mwaka wa 2A.H. Sawa na 624 A.D............................................................... 167

vii

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 7

8/14/2017 1:18:23 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

SEHEMU YA SITA.................................................................. 170 Khitma.......................................................................................... 170 Je! Thawabu za kisomo cha khitma zinawanufaisha wafu?.................................................................. 170 Waumini waombewa na malaika................................................. 174 Je, maiti atanufaika na funga au Hijja ya niaba?......................... 176 Je, thawabu za sadaka zitamfikia maiti?...................................... 177 Hoja chakavu za Kiwahabi katika kupinga khitma...................... 178 Ya kwanza.................................................................................... 178 Majibu yetu.................................................................................. 178 Ya pili........................................................................................... 182 Majibu yetu.................................................................................. 182 SEHEMU YA SABA................................................................. 185 Maulidi......................................................................................... 185 Je! Ni kweli maulidi haina mashiko katika Qur’ani wala Sunnah?.................................................................. 185 Je! Ni zipi siku za Mwenyezi Mungu?........................................ 185 Je! Waislamu hatuna siku za kukumbuka?................................. 186 Alama za kufaulu......................................................................... 188 Hoja chakavu za Kiwahabi katika kupinga maulidi.................... 190 viii

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 8

8/14/2017 1:18:23 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Ya kwanza.................................................................................... 190 Majibu yetu ................................................................................. 190 Ya pili .......................................................................................... 191 Majibu yetu ................................................................................. 191 Kukubalika kwa Bwana Mtume Muhammad ................... 192 Mkataba wa amani wa Hudaybiyah............................................. 193 Sura ya mkataba wa amani wa Hudaybiyah................................ 196 Athari chanya za kisiasa na za kijamii za mkataba wa Hudaybiyah............................................................................ 197 Vyanzo vya umoja na amani duniani........................................... 199 Historia inajirudia........................................................................ 202 Umoja wa Kiislamu..................................................................... 204 Je, kwa nini maulidi ni tishio kwa wakoloni?.............................. 206 Kauli ya Mufti wa Serikali ya Kiwahabi ya Saudia..................... 208 Kusimama kiyamu katika maulidi ya Bwana Mtume  .............................................................................. 210 Je! Inafaa kuikumbuka siku ya kifo cha Bwana Mtume Muhammad  ?........................................................ 211 Huzuni na furaha kwa watu wa kale............................................ 211 Je! Umma wa Muhammad  una siku za huzuni?............... 213 Masharti ya kufaulu........................................................................... ix

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 9

8/14/2017 1:18:23 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Hoja chakavu za Kiwahabi katika kupinga kumtukuza Bwana Mtume  ............................................... 213 Ya kwanza ................................................................................... 214 Majibu yetu ................................................................................. 214 Mtume Muhammad  aifikisha dini kwenye kilele cha ukamilifu............................................................................... 215 Namna hii ndivyo Qur’ani ilivyoadhimisha siku ya kuzaliwa kwa Bwana Masihi (Yesu)............................................ 217 Mwanzo wa historia ya kuzaliwa kwa Bwana Masihi (Yesu)..... 218 Maryam Mtakatifu....................................................................... 219 Maana ya umaasumu.................................................................... 220 Je, umaasumu unaambatana na utume tu na hauingii sehemu nyingine?.......................................................... 221 Kuzaliwa kwa Bwana Masihi (Yesu)........................................... 221 Mjadala kuhusu muda wa ujauzito.............................................. 222 Wakati mgumu............................................................................. 223 Mjadala baina ya Bibi Maryam na watu wake............................. 224 Maafikiano kati ya Waislamu na Wakristo................................... 228 SEHEMU YA NANE................................................................ 229 x

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 10

8/14/2017 1:18:23 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Tawassul....................................................................................... 229 Je, kumwomba Mwenyezi Mungu kupitia kwa mmoja wa waja Wake wa karibu ni haramu?.............................. 229 Je, hadithi za Bwana Mtume  zatwambia nini kuhusiana na tawassul ?............................................................... 231 Ibnu Taimiyah akiri juu ya usahihi wa hadithi ya tawasul........... 232 Mwandishi wa Kiwahabi/Kianswar-suna naye pia akiri kuwa hadithi hiyo ni sahihi.................................................. 233 Tawassul kwa haki ya waombaji.................................................. 233 Mtume  atawassal kwa Baraka zake na Mitume waliomtangulia............................................................... 234 Dua-Kumail, ya Kumail Bin Ziyad ni aina nyingine ya tawassul................................................................................... 235 SEHEMU YA TISA.................................................................. 240 Utakatifu wa Ahlul-bayt  ...................................................... 240 Je, ni nani hao Ahlul-bayt waliotakaswa katika Qur’ani ?.......... 240 Ushahidi wa pili........................................................................... 242 Kuwatanguliza watu wa nyumba ya Mtume  ................... 243 Majibu ya Ibnu Taimiya............................................................... 246 Ahlul-bayt katika hadithi za Bwana Mtume ..................... 248 Utakaso wa watu wa nyumb ya Bwana Mtume ................ 248 xi

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 11

8/14/2017 1:18:23 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Je, aya hiyo inawatakasa viongozi kutoka katika nyumba ya Bwana Mtume ?.............................................. 251 Maana ya uchafu uliyotajwa katika aya hiyo............................... 251 Je, utashi wa Mwenyezi Mungu katika aya hiyo ni wa kikanuni au ni wa kimaumbile?......................................... 252 Je, ni akina nani hao watu wa nyumba ya Bwana Mtume  ?................................................................ 253 SEHEMU YA KUMI................................................................ 256 Ibnu Taimiyah na mitazamo kinzani na dini................................ 256 Je, itikadi za madhehebu mpya ya Uwahabi ni tofauti na zile za Maimamu wanne?............................................ 256 Majibu yetu.................................................................................. 256 Kundi la kwanza.......................................................................... 259 Kundi la pili................................................................................. 259 Sheikh Ibnu Taimiyah.................................................................. 260 Qur’ani imeshushwa kwa Lugha ya Kiarabu ili mpate kutafakari...................................................................... 261 Mwenyezi Mungu ana umbo....................................................... 262 Chuki na husuda za Sheikh Ibnu Taimiyah kwa watu wa nyumba ya Mtume  . ........................................... 263

xii

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 12

8/14/2017 1:18:23 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Kauli ya Sheikh Ibnu Taimiyah kuhusiana na watu wa nyumba ya Mtume  . ........................................... 264 SEHEMU YA KUMI NA MOJA............................................. 268 Ibnu Taimiyah na usalafi.............................................................. 268 Je, Sheikh Ibnu Taimiyah alikuwa ni mfuasi wa Salafi Swalih?......................................................................... 268 Maana ya neno salafi.................................................................... 268 Kaab Bin Maatii al-Himyary maarufu kwa jina la Kaab al-Ahbaar............................................................................ 274 Abdul-karim bin Abil-Aujaa........................................................ 275 Wahb bin Munabihu Al-swan’ani (34 – 114 AH)........................ 276 Tathmini....................................................................................... 277 Muhtasari..................................................................................... 280 SEHEMU YA KUMI NA MBILI............................................ 282 Athari za kale............................................................................... 282 Mawahabi na uondoshaji wao wa ushahidi wa kihistoria............ 282 Kusadikika kwa historia ya Kiislamu.......................................... 284 Ulimwengu wa majaribio............................................................. 288 Utunzaji wa athari za kale kwa kadiri ya Qur’ani....................... 291 Mtazamo chanya wa Qur’ani juu ya kujengea makaburi............ 294 xiii

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 13

8/14/2017 1:18:23 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Nukta ya maafikiano.................................................................... 295 Nukta ya hitilafu.......................................................................... 295 Kibali cha kuinuliwa baadhi ya nyumba...................................... 296 Maana ya neno buyut (nyumba).................................................. 297. Madhumuni ya neno kuinuliwa (turfaa)...................................... 298 Kuinuliwa kunakokusudiwa katika aya....................................... 299 Kwa nini Mawahabi wamethubutu kuvunja makaburi?.............. 300 Kujengea makaburi kwa kadiri ya ulimwengu wa Kiislamu....... 301 Maswali yaliyoelekezwa kwa Wanachuoni wa Madina.............. 303 Majibu ya Wanachuoni wa Madina............................................. 304 Hoja chakavu za Kiwahabi zasimamia juu ya nguzo mbili mbovu................................................................................. 304 Mtungo wa wapokezi wa hadithi hiyo......................................... 311

xiv

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 14

8/14/2017 1:18:23 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

َّ‫بِس ِْم ه‬ ‫َّح ِيم‬ ِ ‫للاِ الرَّحْ ٰ َم ِن الر‬

TABARUKU

K

wa kuwa sote tunaamini kuwa thawabu za matendo yetu mema zinaweza kuwafikia ndugu zetu waliotangulia mbele ya haki, nakitabarukia kitabu hiki mwanafunzi wangu mpendwa, nasi ­tunahuzuni juu yako Marehemu Khamis, aliyefariki dunia nami nikiwa katika uandishi, yaani Jumatano tarehe 30 Disemba 2015, na kuzikwa katika kijiji cha Marera, kata ya Mwanga, wilaya ya Mkalama, mkoani Singida tarehe mosi Januari 2016. Tunakuomba mpenzi msomaji usome Sura al-Fatihah (al-Hamdu) kwa ajili ya marehemu, na umkumbuke pia katika dua zako njema. Moyo wahuzunika, machozi yabubujika lakini sisemi yasiyompendeza Mwenyezi Mungu ilhali nimejawa na majonzi juu yako Khamis. Nafuta machozi japo machungu moyoni hayajaisha, na namwomba Mwenyezi Mungu akukutanishe na watu wa nyumba ya Bwana Mtume (s.a.w.w.) ambao ulikuwa katika mstari wao nyoofu mpaka mwisho wa maisha yako ya duniani. Amin. Baba Mtumishi Kabwe Hussein

1

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 1

8/14/2017 1:18:23 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

َّ‫بِس ِْم ه‬ ‫َّح ِيم‬ ِ ‫للاِ الرَّحْ ٰ َم ِن الر‬

DIBAJI

K

itabu hiki ni toleo la Kiswahili la taasisi ya Al Itrah Foundation. Chapisho lake limelenga kukidhi mahitaji ya kiroho ya zama hizi pamoja na Ubongo na fikra zinazokuwa za Muislam. Jitihada kubwa zimefanywa na Taasisi kuweka chapisho hili la Kiswahili katika msingi wa haki na wenye kukubalika katika Uislam. Unaombwa kwa Taadhima ukisome kitabu hiki katika malengo yaliyokusudiwa. Pia Unaombwa kuwasilisha kwetu maoni yako huru juu ya chapisho letu hili, jambo ambalo tutashukuru sana. Kutangaza ujumbe wa Uislam ni kazi ambayo inahitaji ushirikiano wetu sote. Taasisi inakuomba kuungana na kushirikiana kama ilivyoagizwa katika aya ya Qur’an: (Surat Saba’ 34:46). Na rehma za Allah ziwe juu yako. Wako katika Uislam Al Itrah Foundation Barua Pepe: alitrah@yahoo.com SMS: +255 778 300 140

2

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 2

8/14/2017 1:18:23 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

َّ ْ َّ ‫الر ْح َٰمن‬ َّ ‫الل ِه‬ ‫الر ِح ِيم‬ ‫ِبس ِم‬ ِ Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehma, Mwenye kurehemu.

NENO LA MCHAPISHAJI

K

itabu ulichonacho mikononi mwako, Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo, kimeandikwa kwa Kiswahili na Sheikh Kabwe Hussein. Hiki ni kati ya vitabu kadhaa vilivyoandikwa na masheikh wetu, hususan wa Shia, Ibadhi na Sunni wa hapa nchini (Tanzania) ili ­kuwarudi Mawahabi na itikadi zao za kuwakufurisha wale ambao hawafuati itikadi zao hizo. Katika kitabu hiki utaona jinsi mwandishi alivyozichambua i­tikadi hizo na imani zao nyinginezo na kuonesha walivyopotoka ­kielimu na kimaadili. Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni vitu ambavyo havina nafasi tena katika akili za watu. Kutokana na ukweli huu, Taasisi yetu ya Al-Itrah imeamua ­kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumini yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu na wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili. Tunamshukuru mwandishi wetu, Sheikh Kabwe kwa kazi ­kubwa hii ya kielimu ya kuwaelimisha kwa huduma hii adhimu. Allah Mwingi wa baraka ampe afya njema, ufahamu na elimu zaidi na 3

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 3

8/14/2017 1:18:23 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

maisha marefu ili azidi kuuhudumia Umma huu wa Kiislamu hususan, na wanadamu wote kwa jumla. Amin! Pia tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwa kitabu hiki. Allah awalipe wote malipo mema hapa duniani na kesho Akhera – Amin. Mchapishaji Al-Itrah Foundation

4

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 4

8/14/2017 1:18:23 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehma, Mwenye kurehemu.

UTANGULIZI

B

aada ya Mwenyezi Mungu kuumba ulimwengu na walimwengu, aliweka katiba zitakazotumika kama mwongozo wa maisha ya walimwengu, lakini katiba hizo zilikuja kimaeneo, japokuwa zilikuwa na lengo moja. Na mwisho wa yote Mwenyezi Mungu alileta katiba kamilifu ya kimataifa, inayopigania haki ya kila mtu bila kujali itikadi yake, na kuwataka wanadamu kujenga maisha yao juu ya msingi wa umoja na mshikamano. Kwa kuzingatia msingi huo wazee wetu waliishi kwa amani na upendo kama ndugu wa tumbo moja. Walishirikiana katika shida na raha, bila kukufurishana wala kudharauliana. Hakuna aliyemnyooshea kidole mwenzake na kumwita kuwa ni mtu wa Bidaa wala shirki, bali wote kwa pamoja walishirikiana katika kuadhimisha Maulidi ya Bwana Mtume 8 Sunni alihudhuria hafla ya Maulidi kwa Shia, na vilevile Shia na Ibaadhi walihudhuria hafla kwa Suni. Na hii inamaanisha kuwa Shia, Ibaadhi na Sunni ndio madhehebu ya kale hapa nchini. Na mfano halisi ni kule Pangani, kuna msikiti wa Shia uliojengwa tangu mwaka 1864, na kule Bagamoyo kuna msikiti wa Shia uliojengwa tangu mwaka 1889, na madhehebu zote hizo zilikuwa na heshima kubwa kwa Bwana Mtume 8, na zilikuwa na mila na desturi ya kumuenzi Mtukufu Mtume 8 na kizazi chake, kwa kutembelea makaburi yao na kutunza athari zao kama ushahidi kwa vizazi vijavyo, na mfano hai ni kule Kaole Bagamoyo ambako hadi leo hii makaburi ya Masharifu bado yapo na watu wanakwenda kumwomba Mwenyezi Mungu kila kukicha kupitia baraka zao. 5

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 5

8/14/2017 1:18:23 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Na hayo ndiyo maisha waliyoishi babu zetu, maisha ya amani, umoja, upendo. Kuheshimiana, kuvumiliana pamoja na mapenzi ya dhati kwa Bwana Mtume 8, na watu wa nyumbani kwake. Na amani hiyo haikuwa ni mali ya Waislamu tu, bali wao waliamini kuwa amani ni haki ya kila mwanadamu bila kujali itikadi yake ya kidini au ya kisiasa. Na kwa kuwa wanadamu wote wanaunganishwa na kitu kiitwacho ubinadamu, basi ni lazima washirikiane vilevile katika haki zote za kibinadamu, ikiwemo amani, heshima na upendo. Na yote hayo yanahitajia kutambuana na kuvumiliana. Kwa lugha nyepesi kila mmoja atambue mila na desturi za mwenzake kisha aziheshimu. Sasa yule atakayeona kuwa mwenzake ametoka kwenye njia nyoofu basi atafanya naye mazungumzo kwa lugha nzuri ya heshima na adabu iwezayo kuifungua akili ya mtu kwa wepesi na moyo kwa mahaba. Huo ndio mfumo wa kibinadamu tuliourithi toka kwa watu waliotutangulia tangu zama za Maswahaba hadi kufikia karne za babu zetu, lakini mfumo huo ukageuka kuwa ni tishio kwa maslahi ya Wakoloni, kwani lengo lao kuu lilikuwa ni kutugawa na kufisidi rasilimali zetu. Na kwa mantiki hiyo waliunda madhehebu zenye mitazamo kinzani na sheria tukufu ya Mwenyezi Mungu na haki za binadamu. Na moja ya madhehebu hizo ni Uwahabi ambao hapo awali ulitambulika kama Usalafi, lakini kutokana na umakini wa Wanachuoni madhehebu hii ilipotea kwa muda na kuibuka tena mnamo karne ya kumi na mbili kwa jina la Uwahabi. Madhehebu hii ya uzushi na uzandiki ni madhehebu katili isiyojua lugha ya kufahamiana na watu, madhehebu hii katika vidahizo vya kamusi yake huwezi kupata maneno yafuatayo: Hekima, heshima, huruma, amani, uadilifu na upendo. Yaani ni madhehebu katili isiyojua lugha ya kufahamiana na watu, madhehebu hii ni madhehebu ya watu wasio na hekima, heshima, huruma, upendo na uadilifu, na ni watu wasiotaka amani na maelewano na watu. Ndugu zangu katika utu, wakoloni waliuteka mji wa Hijjaz1 na kuufanya kuwa ndio makao makuu ya Serikali haramu ya Kiwahabi, 1

  Hijaz kwa sasa ndio Saudi Arabia 6

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 6

8/14/2017 1:18:23 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

ili kuhalalisha madai yao ya kwamba, wao ndio wanaoujua Uislamu sahihi kwa kuwa wanatoka palepale kwenye chimbuko la Uislamu. Na katika hilo wamefanikiwa kuwadanganya na kuwapotosha wengi wasiokuwa na hatia na kuwaingiza kwenye kundi la wakata suruali na kucheza karate misikitini, bila ya kujali heshima na matukufu ya misikiti, hususan vijana chipukizi. Mnamo mwaka wa 1968 madhehebu potovu ya Uwahabi iliweka mguu wake wa shari katika ardhi zetu lakini watu wake walijificha nyuma ya mgongo wa kunusuru suna za Bwana Mtume 8. Lakini suna zenyewe hawakuwa wakizinusuru bali walikwenda kinyume na suna zenyewe. Kwa mfano pale ambapo Bwana Mtume 8 aliposema: “Tembeleeni makaburi�, wao walishika bakora na kuwazuia Waislamu kwenda kutekeleza suna waliyodumu nayo kwa miaka mingi, na hapo ndipo waliposhtukiwa kwa haraka na wakalazimika kubadilisha jina na kujiita Salafi, lakini bado matendo yao yakawa ni yenye kukinzana na mwenendo wa Salafi, ambao ni Maswahaba wema wa Bwana Mtume 8 kama tutakavyoelezea huko mbele, Mungu akipenda. Kwa hiyo wakalazimika tena kubadilisha jina na kujibatiza jina la Ahlusuna wal-Jamaa (ambalo jina la madhehebu manne ya Sunni), lakini nyinyi msidanganyike kwa hayo majina wanayojibatiza kila siku bali angalieni matendo yao na sikilizeni maneno yao, bila shaka mtawagundua kwa haraka, maana wao lugha zao ni za kuchochea mauaji, vurugu na uvunjifu wa amani. Kwa mtazamo wao siku za sherehe za Idi huruhusiwi kumpelekea chakula jirani yako kwa kuwa yeye ni Mkristo, na yeye pia akikuletea chakula siku ya Krismas, ni haramu kula chakula hicho.2 Je huo ndio Uislamu wa Bwana Mtume Muhammad 8? Au maisha hayo ndiyo tuliyoyarithi toka kwa mababu? Ndugu yan2

  Hapa mwandishi anakusudia pale ambapo masharti mengine ya uhalali wa chakula yanapotimia. Kwa lugha nyingine mwandishi anakusudia kwamba, ukristo pekee si kigezo cha uharamu wa chakula cha mkiristo - Mhariri. 7

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 7

8/14/2017 1:18:23 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

gu mchele anaoupika Mkristo siku ya Krismas ni uleule unaoupika wewe siku ya Idi sasa iweje siku ya Idi uwe halali na siku nyingine ugeuke kuwa haramu? Au siku ya Krismas mchele huo unakuwa na madhara? Kama utakuwa na madhara basi uharamu utakuwa watokana na madhara na si kwa sababu ya Krismas, kwa kuwa kilichokuwa halali kwa Bwana Mtume Muhammad 8 kitabakia kuwa halali. Halafu pia uharamu huo unaodaiwa na Mawahabi hautawagusa watu wote bali wale waliopatwa na hayo madhara tu, na kwa wengine itakuwa ni halali. Ndugu zangu katika utu tuondoeni tofauti zetu za kiitikadi na kisiasa na za kijamii, ili tuweze kudumisha amani ya nchi yetu. Ndugu zangu, kitabu hiki kitawapatia mwanga ili muweze kuwafahamu waharibifu wa dini japo kwa muhtasari. Na pia Mimi sidai kuwa kitabu hiki kimefikia daraja ya ukamilifu, bali nasema kama alivyosema Mwalimu Wa Kwanza Sayyid Aristotle: “..Atakayekuta mapungufu azibe mapungufu hayo, na atakayekuta yanayofaa kurekebishwa basi arekebishe‌â€? Tunamwomba Mwenyezi Mungu atujalie kuwa katika wale wanaosikiliza neno na kufuata lile lililokuwa bora zaidi. Amin. Baba Mtumishi Kabwe Hussein Simu: +255 789 78 57 56 Barua pepe: husseinkabwe@yahoo.com 1 Mei, 2015

8

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 8

8/14/2017 1:18:23 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehma, Mwenye kurehemu.

SHUKURANI

A

wali ya yote, napenda kutoa shukurani zangu za dhati kwa ule uwepo wa asili ulioutokeza kila uwepo na kuutangulia, bila ya wenyewe kuhitajia uwepo mwingine ili kuufanya uwepo. Huyo ni Mungu Wenu, Mola mlezi wa walimwengu. Kisha mvua ya sala na amani imfikie Mtume wa kimataifa Bwana Muhammad 8 na watu wote wa nyumba ya utume. Natoa shukuruni pia kwa Familia ya Kabwe, kwa kuwa nami katika kipindi na wakati mgumu usiodumu, ikiniliwaza na kunipa faraja. Hali kadhalika nawashukuru wanangu wapendwa Hassanat, Hussein na Zakia Kabwe kwa uvumilivu wao kwangu, wakati nikitumia muda wao katika uandishi. Kutimia kwa kitabu hiki kumetokana na jitihada zangu katika kukesha usiku nikifanya utafiti kwenye vyanzo mbalimbali. Pia kuna watu muhimu waliochangia kwa njia moja au nyingine katika ufanikishaji wa kazi hii, napenda kutoa shukurani zangu za dhati kwao huku nikiwataja mmoja mmoja kwa jina: 1.

Maulana Sheikh Muhammad Abd: Bwana huyu alikuwa nami kila ambapo msaada wa hali na mali ulipohitajika. Mwenyezi Mungu ampe umri mrefu na amtilie wepesi katika mambo yake, na amfanye kuwa ni faraja kwa umma.

9

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 9

8/14/2017 1:18:23 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

2.

Sharif Sagaf Ahmed: Bwana huyu ni katika watu walionitangulia katika kazi hii na nimejifunza mengi kupitia uzoefu wake wa muda mrefu, Mwenyezi Mungu amzidishie kheri na amkutanishe na babu yake Bwana Mtume Muhammad 8.

3.

Al-Haj Muhammad Mputa: Bwana huyu alikuwa na mchango wa kipekee katika utimilifishaji wa kitabu hiki. Mwenyezi Mungu ampe subira kutokana na magumu anayokutana nayo katika jitihada za kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya Uislamu sahihi wa Bwana Mtume 8

4.

Sheikh Khalifa Khamis Mohammed: Bwana huyu kama itakuwa ni lugha sahihi basi ni bora niseme kuwa, kama si uwepo wake basi kazi hii isingewafikia wasomaji wengi ndani na nje ya nchi. Mwenyezi Mungu ampe nguvu katika kazi hii adhimu ya kusukuma mbele zaidi gurudumu la maendeleo ya kulitokomeza gonjwa hatari la Uwahabi.

5.

Alhaji Hemed Lubumba: Ndugu yangu huyu ana mchango mkubwa katika kufanikisha zoezi hili, kwa njia ya kunipa moyo na ushauri wa mara kwa mara utokanao na uzoefu wake wa muda mrefu katika kazi za uandishi. Mwenyezi Mungu amfungulie milango ya baraka, na kila zito liwe jepesi kwake.

Mwisho kabisa natoa shukurani zangu za dhati kwa wanafunzi wangu wote wa chuo cha theolojia cha Imam Swadiq D, hususan Bwana Jauz Hashimu, Ismail Nyopo, Mustafa H. Mkita Mustafa Hatibu na Haj Rajabu Mtereka kwa ushirikiano wao wa karibu. Namwomba Mola awafungulie milango ya maarifa na awakinge na shari ya yule mwovu Ibilis. Amin.

10

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 10

8/14/2017 1:18:23 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehma, Mwenye kurehemu.

SEHEMU YA KWANZA HISTORIA YA UWAHABI 1.

Je, inanasibishwa na nani madhehebu ya Uwahabi?

2.

Je, ni lini uliibuka Uwahabi?

3.

Je, ni nani wa kwanza kuunga mkono Uwahabi baada ya kuibuka kwake?

4.

Je, ni nani aliyeotesha mbegu za mtii huu (Uwahabi) kwa mara ya kwanza?

Madhehebu ya Uwahabi au Answar Sunnah inanasibishwa na Sheikh Muhammad bin Abdul Wahab, bin Suleiman, bin Ali, bin Muhammad, bin Ahmad, bin Rashid, bin Buraid, bin Mushrif, bin Umar, bin Ba’adhad, bin Ris, bin Zakhir, bin Muhammad, bin Ali, bin Wahib kutoka ukoo wa Tamim.3 Sasa cha kushangaza, ni pale tunaposikia madhehebu hii ikitambulishwa kwa jina la Al-wahabiyah, kwa kuinasibisha na Sheikh Abdul Wahab, ambaye ni baba wa mfufuaji wa madhehebu hii, badala ya kutambulishwa kwa jina la Al Muhammadiyah, kwa kuwa Sheikh Muhammad bin Abdul Wahab, ndiye aliyeifufua madhehebu kwa mara ya pili! 3

  Kashful irtiyab, uk. 14. 11

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 11

8/14/2017 1:18:23 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Sababu ya jina hilo ilikuwa ni tahadhari ya kutowachanganya watu, maana sisi Waislamu tunafahamika kama Al-Muhammadiyyin, yaani wafuasi wa Mtume Muhammad 8. Sasa endapo wafuasi wa madhehebu hii ya uzushi na ya uzandiki nao wangeitwa kwa jina hilohilo la Al Muhammadiyyin, basi watu wasingeweza kutofautisha kati ya wafuasi wa Muhammad wa ukweli na yule Muhammad bandia. Na haya machafu yote yanayojiri kupitia mikono ya Mawahabi yangeonekana kuwa ni wafuasi wa Muhammad 8 ndio wanaoyafanya. Sasa ili kutenganisha kati ya makundi haya mawili, ikabidi wale wafuasi wa madhehebu hii mpya ya uzushi waitwe Mawahabi. Sheikh Ahmad bin Zaini al-Dahlan anasema: Alizaliwa Muhammad bin Abdul-wahab mnamo mwaka wa 1111 hijiria na kufariki dunia mnamo mwaka wa 1207 hijiria, akiwa na umri wa miaka 96.4 Sheikh Muhammad bin Abdul-wahab, alipata masomo yake ya awali ya dini ya Kiislam kutoka kwa Sheikh Abdul-wahab ambaye ni baba yake mzazi. Mzee Abdul-wahab alikuwa ni katika watu wema na alikuwa ni katika wanachuoni wa madhehebu ya Imam Ahmad bin Hanbal. Baada ya hapo Sheikh Muhammad bin Abdul-wahab alikwenda Makka na Madina ili kujiendeleza kielimu, na huko alisoma kwa masheikh wa miji hiyo, lakini baada ya muda si mrefu masheikh walibaini athari za upotovu kwa mwanafunzi wao huyo, kwani alikuwa ni mtu mwenye mitazamo ya kishenzi, kama vile alivyokuwa akiamini kuwa fimbo yake ni bora kuliko Bwana Mtume Muhammad 8. Mitazamo kama hiyo iliwatia wasiwasi wanachuoni wa miji hiyo, na kibaya zaidi Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahab alikuwa 4

  Khulasatul kalaam fi umaraai el baladil haram. 12

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 12

8/14/2017 1:18:23 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

na tabia ya kujisomea vitabu vya watu waliokuwa wakidai utume hapo zamani, kama vile Musailamat al-Kadhab, Sujah, na Tulaihah al-Asadi, na wengineo. Sheikh Abdul-wahab ambaye ni baba mzazi wa Muhammad bin Abdul-Wahab, alikuwa akiwatahadharisha watu juu ya upotovu wa mtoto wake huyo. Naye Sheikh Suleiman ambaye ni kaka wa Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahab, aliwahi pia kuandika kitabu cha kubainisha madhara ya uwahabi na kupinga fikra za kiyahudi zinazoletwa na mdogo wake.5 Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahab aliacha watoto wanne. Watoto wa Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahab: 1. 2. 3. 4.

Abdullah Hassan Hussein Ali

Abdullah ndiye aliyeshika nafasi baada ya baba yake, naye alipofariki aliacha watoto wake wawili Suleiman kisha ndugu yake Abdurahman. Suleiman huyu yeye alikuwa ni zaidi ya ukiritimba, alikuwa na ususuavu wa moyo uliyokubuhu, matendo yake yalikuwa ni zaidi ya unyama. Lakini mnamo mwaka wa 1233 hijiria aliyekuwa gavana wa Misri Bwana Ibrahim Pasha alimuua Suleiman bin Muhammad bin Abdul-Wahab, kisha akamkamata aliyetarajia kushika nafasi ya usheikh baada yake, ambaye ni Abduraham tuliyemtaja hapo juu. Bwana huyu baada ya kukamatwa alipelekwa Misri na huko ndiko alikofia.(Ibrahim Pasha ndiye aliyeuangusha utawala wa kifalme wa Kisaud mwaka 1818 A.D lakini walijipanga upya na wakafanikiwa kuusimika tena utawala wao). 5

  Kitabu hicho kilitambulika kwa jina la: Al swawaaiqul-Ilaahiyyah fii radi alalWahhabiyyah (Vimondo vya kiungu katika kuupinga Uwahabi 13

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 13

8/14/2017 1:18:23 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Ama mtoto wa pili, Hassan, yeye alimwacha mwanawe Abdurahman. Bwana huyu aliwahi kuwa kadhi wa Makka katika zama zile Uwahabi uliposhika hatamu mjini humo, na aliishi miaka mia moja takriban. Ama Hussein na mdogo wake Ali, wao waliacha watoto wengi na mpaka sasa vizazi vyao bado vipo katika mji wa Dir’iyah, na wanaitwa Watoto wa Sheikh. Mpenzi msomaji, katika somo lililopita swali namba tatu lilihoji: Je, ni nani wa kwanza kuunga mkono uwahabi baada ya kuibuka kwake? Jibu: Wa kwanza kumuunga mkono Muhammad bin AbdulWahab, na kumsaidia kueneza itikadi zake, alikuwa ni Muhammad bin Saudi kisha baada yake akawa ni mwanawe Abdul-Aziz, kisha mjukuu wake Saud bin Abdul-Aziz, na Saud huyu katika utawala wake ndiye aliyeipiga Iraq na kuvunja kaburi la Imam Hussein mjukuu wa Bwana Mtume 8 mwaka 1216 – 1225, na akawazuia watu kuingia Makka kufanya ibada ya hijja, na hijja ilisimama katika utawala wake kwa miaka mingi, yote hayo tutayazungumza kwa mapana tukifika mahala pake. Chimbuko la uwahabi kama inavyosimuliwa, ni kwamba Waarabu hasa watu wa Yemen walihaditihia ya kwamba: Alikuwako mchungaji fakiri sana kwa jina la Suleiman. Aliota kuwa kaa la moto limetoka mwilini mwake, na kuenea ardhini na likawa likimuunguza kila anayekutana nalo, basi mchungaji yule akaenda kwa mfasiri wa ndoto ili kupata maana ya ndoto hiyo, basi mfasiri akamfasiria kuwa: Mtoto wako atazusha dola kubwa yenye nguvu. Na ndoto hiyo ikatimia kupitia mjukuu wake, Muhammad bin Abul-Wahab. Basi Muhammad bin Abdul-Wahab alipokuwa mkubwa alikuwa anaheshimika kwa watu wake kwa sababu ya ndoto hiyo ya babu 14

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 14

8/14/2017 1:18:23 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

yake, lakini kwa kipindi hicho hakupata wafuasi, basi akafanya safari kwenda ughaibuni na kurejea baada ya miaka mitatu, na hapo ndipo alipofika na kuzusha madhehebu yake hiyo ya kizushi na kuungwa mkono na mfalme wa hapo mjini Dir’iyyah, Muhammad bin Saud. Na kila mmoja alinufaika kutokana na mwingine, ufalme wa Muhammad bin Saud ulipata nguvu kwa njia ya dini kupitia mgongo wa Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahab. Na Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahab naye alinufaika kupitia msaada wa kipesa na wa kijeshi toka kwa mfalme. Kwa hiyo Sheikh akawa na uwezo wa kijeshi wa kuhujumu na kushambulia miji jirani na kuwataka watu wake waingie kwenye madhehebu yake kwa lazima, na alikuwa akiua kila anayekataa madhehebu yake. Na mkataba uliyosainiwa kati ya Sheikh Muhammad na Mfalme, ulikuwa ni, Sheikh kuendesha dini atakavyo bila kuingiliwa na mtu, na Mfalme naye atahusika na siasa ya utawala, na kwamba ataendesha nchi atakavyo bila kuingiliwa na yeyote katika maamuzi yake ya kisiasa. Basi wakaanza kuhujumu na kushambulia miji mbali mbali na kupora mali za wakazi wake, wakiamini kuwa ni ngawira, na mauaji yao waliamini kuwa ni jihadi. Na baada ya miaka 15 mfalme alifanikiwa kutanua mipaka ya utawala wake, na Sheikh akafanikiwa kuvuna watu kwa upanga, huku akiwaambia: “Hakika mimi nakuitieni TAUHIDI.” Lakini tauhidi hiyo sio ile tunayoifaham sisi. Je tauhidi aliyoikusudia ni ipi? Sheikh Abdul-Wahab na imani yake ya kukufurisha Waislamu: Anasema Mwanachuoni mashuhuri Mahmud Alusi katika kitabu chake Taarikh Najdi, kama alivyonukuliwa na Sayyid Muhsin Al-Amin: “Alizaliwa Muhammad bin Abdul-Wahab katika mji wa 15

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 15

8/14/2017 1:18:24 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Uyainah huko Najdi, na alisoma kwa baba yake elimu ya fikihi, kwa mujibu wa madhehebu ya Imam Ahamd bin Hanbal. Na alikuwa tokea utotoni mwake akiongea maneno ambayo watu hawayafahamu. Akiwapinga watu katika mengi ambayo ni sahihi kuyafanya kwa mujibu wa madhehebu yao, na akawa shadidi katika suala la watu kuomba Mungu kupitia kaburi la Bwana Mtume Muhammad 8. Kisha akaondoka kuelekea Najdi na baada ya hapo alikwenda Basra akikusudia kufika hadi Sham (Syria), na alipoingia Basra alibaki hapo muda wa miaka minne na hapo alisoma kwa Sheikh Muhammad Al-Majmuui. Baada ya hapo alikwenda Baghdad, nako alikaa miaka mitano, kisha akaenda Kurdistan akakaa mwaka mmoja, na miaka miwili alikaa katika mji wa Hamadan. Kisha akaenda Isfahan, kisha akaenda Qum. Baada ya hapo alikwenda Huraimalah, lakini miji yote aliyokuwa akipita hakuwa anaondoka kwa wema bali alikuwa anatimuliwa kama kwamba ni ndege kwenye shamba la mpunga. Lakini baada ya kuwasili Huraimalah alimkuta baba yake mjini hapo, basi akaambatana na baba yake, na akasoma tena kwa baba yake, kisha akadhihirisha itikadi zinazokinzana na zile za Waislam wa mji huo. Baba yake alimkataza lakini hakukoma mpaka ukaibuka ugomvi na mabishano baina yake na baba yake kwa upande mmoja, na baina yake na Waislamu mjini hapo kwa upande mwingine. Basi akaishi hapo miaka miwili na mzee wake akawa amefariki dunia mnamo mwaka 1153A.H., na hapo Sheikh akapata ujasiri wa kudhihirisha itikadi yake na kuwapinga Waislamu katika yale ambayo kwao yamethibiti kuwa ni sahihi. Muhammad bin Abdul-Wahab alipata wajinga wachache waliomuunga mkono, mpaka watu walipochoshwa na makala zake na kutaka kumuua ndipo alipokimbilia Uyainah ambako ndiko alikozaliwa. Uyainah wakati huo ilikuwa ikongozwa na Uthman bin Ahmad bin Muamar. Baada ya kuwasili Sheikh mjini hapo, alimtamani16

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 16

8/14/2017 1:18:24 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

sha kiongozi Uthman Muamar kuwa atamiliki Najdi nzima endapo atakubali kumsaidia na kumnusuru. Uthman Muamar akamsaidia na wakafanya makubaliano kuwa mfalme atampa Sheikh uhuru kamili wa kutangaza na kueneza itikadi zake, na Sheikh atamsaidia mfalme kutanua mipaka ya utawala wake hadi kuitawala nchi nzima ya Najdi kwa njia yoyote ile. Na ili kukomaza mahusiano yao, Amir Uthman alimuozesha dada yake aliyeitwa Jawharah kwa Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahab. Sheikh akamwambia mfalme kuwa ni matumaini yake kuwa Mungu atakuzawadia Najdi na vilivyomo. Muungano baina ya wawili hao, Sheikh na mfalme haukudumu kwa kipindi kirefu, kwani sheikh aliwapinga Waislam (kama kawaida yake). Baadhi ya watu walimfuata, na akafanikiwa kuvunja kuba kwenye kaburi la Zaid bin al-Khatwaab. Jambo hilo lilikuwa kubwa na habari ikamfikia Suleiman alHamiidi mfalme wa Ihsaa na Qatwiif. Suleiman alikuwa na nguvu zaidi ya Uthman mfalme wa Uyainah, basi akamwandikia barua Uthman na kumuamuru amuue Muhammad bin Abdul-Wahab, na akampa onyo ikiwa hatamuua. Uthman akamwambia mgeni wake achague mji wa kukimbilia na Sheikh akachagua kwenda Dir’iyah. Uthman akamteua bwana mmoja kwa jina Farid ili amsindikize Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahab na kumuulia njiani, lakini bwana yule hakuweza kuumua bali alimuachilia aende zake. Sheikh aliingia Dir’iyah mnamo mwaka 1160 A.H. Mji huo ulikuwa ukitawaliwa (kwa wakati huo) na Muhammad bin Saud, na hapo pia akamshawishi Muhammad bin Saud kuwa atamuwezesha kuitawala Najdi nzima. Mfalme alimuunga mkono na wakakubaliana kuanzisha vita dhidi ya Waislam wote wanaokataa mtazamo wa Sheikh na utawala wa Muhammad bin Saud. Na hiyo ndiyo tauhidi iliyokusudiwa na Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahab, na yeyote anayekwenda kinyume na mawazo yake huyo ni mushriki na damu yake ni 17

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 17

8/14/2017 1:18:24 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

halali. Basi mfalme akaamuru watu wa Dar’iyah kuingia katika jihadi ya kuuwa Waislam nao wakamkubalia. Mashambulizi yakaanza na wakawapiga watu wa Najdi na Ihsaa mara nyingi tu, mpaka baadhi yao wakatii kwa lazima na uongozi wa Najdi nzima ukawa chini ya ukoo wa Saud kwa kutumia nguvu na umwagaji damu za watu wasio na hatia. Mnamo mwaka 1207 A.H. alifariki Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahab kisha baada yake akafa mfalme Muhammad bin Saud na kumuacha mtoto wake Abdul-Aziz. Naye alifanya kazi ya kuinusuru madhehebu na kupigana na kuua Waislam kwa ajili ya kuieneza na kuinusuru madhehebu yao. Kisha akafa Abdul-Aziz na kumuacha mwanawe Saud, lakini Saud alikuwa shadidi mkali mno katika uwahabi zaidi ya baba yake. Saud huyu aliwazuia Waislam kwenda Hijja na akavuka mipaka katika kuwakufurisha wanaokwenda kinyume na wao. Saud naye alifariki na kumuacha mtoto wake Abdullah. 6 Wapenzi wasomaji huu ndio uwahabi uliojengeka juu ya misingi ya matusi chuki, mauaji, dhulma, kukufurisha Waislam, utovu wa nidhamu kwa wazazi, kama alivyokuwa Sheikh Muhammad bin AbdulWahab akigombana na baba yake hali kadhalika na mashekih wake. Na hayo ndiyo yanayojiri katika jamii yetu ya leo. Waislam wasio na hatia wanauawa kwa anuani ya jihadi, majumba ya ibada yanayomilikiwa na watu wenye imani ghairi ya Uislamu yanavunjwa na Mawahabi, kumbukumbu na athari za dini hazitakiwi kwa Mawahabi, ila kumbukumbu za wafalme wa Kisaud ndizo zitakiwazo katika jamii za Kiwahabi. Yote hayo tutayazungumza kwa mapana tukifikia mahala pake. Uwahabi ni genge la hujuma lililoasisiwa na wakoloni wa Uingereza kwa lengo la kuidondosha dola ya Bani Hashim na kuusimika 6

  Taarikh Najdi: uk. 98-99 18

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 18

8/14/2017 1:18:24 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

utawala haramu wa Kisaud. Sheikh Ahmad bin Zaini Dahlaan, katika kitabu chake Khulaasatul kalaam fi umarail balad alharam ameandika: “Hakika Mawahabi walipeleka wanazuoni wao 30 katika dola ya Sharif Masud bin Said bin Zaid aliyefariki mwaka 1165 A.H, basi Sharifu akawaamuru wanazuoni wa Makka na Madina wafanye nao mjadala. Basi wakajadiliana nao na kukuta itikadi zao ni mbovu, ndipo kadhi akatoa hukumu ya kuwakufurisha na akaamuru wafungwe, basi wakafungwa baadhi yao na wengine wakakimbia, dola ya Masharif Masud, Ahmad, Ghalib na wengineo tutazizungumzia mahala pake. Wapenzi wasomaji najua mtakuwa na shauku ya kupata jibu la swali namba 4 lililohoji: Je, ni nani aliyepandikiza mbegu za madhehebu hii kwa mara ya kwanza? Majibu: Mbegu hizo zilipandikizwa mwishoni mwa karne ya saba na mmoja wa wanazuoni wa madhehebu ya Hanbali, aliyefahamika kwa jina la Ahamad bin Abdul Halim, maarufu kwa jina la Ibnu Taimiyyah al-Harrani al-Damashqi aliyezaliwa mnamo mwaka 661 A.H. na kufariki mnamo mwaka 728 A.H. (Sheikh huyu tutamchambua vizuri mahala pake). Alikuwa mkiritimba katika madhehebu ya Hanbal, alifufua baadhi ya itikadi za madhehebu ya watu wa hadithi. Madhehebu hii inatumia hadithi zilizopokelewa na maswahaba katika kuthibitisha maswala ya kitheolojia (kiitikadi) na hawataki mijadala ya kiitikadi wala kutumia akili katika maswala hayo. Ibnu Taimiyyah alifufua baadhi ya mitazamo yao kama vile kumfananisha Mwenyezi Mungu na viumbe, kwa mfano Mungu ana macho, mikono, miguu, anakaa juu ya kiti nk. Ibnu Taimiyyah hakuishia hapo bali aliingiza katika itikadi za masheikh waliotangulia mambo ambayo hawakuyaacha katika vitabu vyao. 19

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 19

8/14/2017 1:18:24 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Kwenda kutembelea kaburi la Bwana Mtume 8 kwake ikawa ni Bida’a na shirki. Kutabaruku na athari za Mtume na watu wa nyumba ya utume pia kwake ilikuwa ni kinyume na mafundisho ya TAUHIDI. Alirithi fikra za waheshimiwa waliomtangulia za kumvunjia heshima na kumchukia Imam Ali, na kwa misingi hiyo akaunda harakati ya usalafi, (tutauzungumzia usalafi mahala pake) lakini kimbunga kikali kilimshambulia toka kila sehemu. Wanazuoni wakafanya kazi ya kubainisha upotovu wa madhehebu yake hiyo ya uzushi na ya uzandiki, na hawakuathirika na madhehebu hiyo ila wachache miongoni mwa wanafunzi wake kama vile Ibnu al-Kayim al-Jauziya (691-751 A.H), na baadhi ya wafuasi walikuwa Sham (Syria) na wengine wachache walikuwa Misri. Kwa hiyo mti wa Usalafi ukawa umekauka mapema mno lakini kwa muda maalum. Na mnamo karne ya kumi na mbili 12A.H aliibuka Muhammad bin Abdul Wahab na kuumwagilia tena maji mti huo na kuufufua kwa mara nyingine, na kufuata nyayo za Ibnu Taimiyyah.7 Na kwa sababu hiyo tu, Mawahabi wanamwita, Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahab: Sheikh al-Mujadid, yaani Sheikh mfufuaji wa suna zilizokuwa zimetoweka. Na mpaka hapa tunaweza kusema kuwa : Uwahabi ni Usalafi mambo leo. Sababu za kuenea madhehebu potovu ya Uwahabi: Kuna sababu mbili kuu za kuenea fikra za Uwahabi katika Bara Arabu, nazo ni: Ya kwanza: Ujinga uliokuwa umetawala katika jamii ya watu wa Najdi, na kuwa kwao mbali na mafundisho sahihi ya dini ya Mwenyezi Mungu. Na siku zote wajinga ni sawa na ardhi yenye rutuba inayompa mkulima fursa ya kuotesha mmea autakao. Kwa mantiki hiyo Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahab alitumia fursa hiyo kati7

  Bidaayatul maarifa uk. 52-54. 20

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 20

8/14/2017 1:18:24 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

ka kufanikisha zoezi lake na azma yake ya kuupotosha umma, na tunayo mifano hai ya namna Mawahabi wanavyotumia ujinga wa watu kama fursa adhimu ya kuwapotosha watu na kuwatoa katika mstari nyoofu, kwani wahubiri wa Kiwahabi hukusanya vijana wasiokuwa na maarifa na kuwakaririsha upotovu wao, halafu kila kijana mmoja anaambiwa awe na kundi la vijana watano, na hao watano nao kila mmoja anakuwa na wanafunzi wake watano. Kisha wanatawanyika katika maeneo mbalimbali, mijini na vijijini. Vijana hao wa Kiwahabi hutumia hoja chakavu katika upotoshaji wao, ikiwa ni pamoja na kufasiri aya za Qur’ani na hadithi kwa matamanio yao. Kwa mfano, Aya ya 70 katika Surat Yasin: “Ili imwonye aliye hai na ihakikike kauli juu ya makafiri.” Wao Aya hii huitumia kama ushahidi wa kuharamisha talakini, wakati Aya hiyo haina uhusiano wowote na maswala ya talakini. Lakini wao kwa tafsiri zao za kulazimisha wanataka Aya hiyo iharamishe talakini kwa lazima, na ukiwapa hoja yakinifu tu basi wao hupandwa na jazba mara moja na kuanza kuongea kwa ukali ili wakuogopeshe. Hao ndio Mawahabi ambao hata siku moja hawataweza kusimama mbele ya hadhira na kujitambulisha kwa jina la Uwahabi, bali utawasikia (waingiapo katika misikiti ya Ahlusunna) wakijinadi kuwa wao pia ni Ahlusunna wal-jamaa, na hapo ndipo ile kampeni yao huanza mara moja. Kampeni ya kuhakikisha kila Muwahabi anavuna waumini watano, na kuwafundisha Swala ya kupanua miguu, na kuwaonesha kuwa wao ndio wanaoijua Swala na kwamba wale wasiokuwa wao ni watu wa bidaa. Na hii ndiyo fikra ya Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahab, aliyedai kuwa watu wote walikuwa washirikina, kuanzia baba yake, masheikh wake wote mpaka miaka mia sita kurudi nyuma, wote hao hawakuwa na dini, mpaka hapo alipodhihiri yeye katika karne ya kumi na mbili, na kuwaletea wafuasi 21

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 21

8/14/2017 1:18:24 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

wake tauhidii ya kuua Waislam wasio na hatia, kwa maslahi yake binafsi. Hiyo ni sababu ya kwanza. Ya pili: Ni msaada wa kijeshi na wa kisiasa toka kwa familia ya kifalme ya Kisaudi, na kwa misingi hiyo Mawahabi waliweza kuendesha vita na mashambulizi ndani na nje ya Najdi, kama vile Yemen, Hijjaz, na sehemu za Syria na Iraq. Na miji waliyoiteka ilikuwa ni halali kwao, kuitumia watakavyo, wakiweza kuiweka chini ya himaya yao na mamlaka yao, wanafanya hivyo, ili kupanua mipaka ya utawala wa Saudi, na wasipoweza kufanya hivyo basi hutosheka na kupora mali za wakazi wa miji hiyo. Wapenzi wasomaji! Kwa yakini nadharia (mpya) yoyote ile inapodhihiri, hususan inapokuwa imebeba kaulimbiu ya dini na mabadiliko, basi ni lazima nadharia hiyo ivune wafuasi wa kuifuata, na ipenye katika nyoyo za watu, hasa pale nadharia hiyo inapoelezwa katika jamii iliyokosa maarifa sahihi. Ukichunguza kwa kina harakati za Sheikh Muhammad bin Abdul Wahab utazikuta zimejikusanyia sifa kuu mbili: 1.

Utakuta kuwa ni harakati zinazonadiwa kwa kwa jina la tauhidi na mabadiliko.

2.

Utakuta kuwa ni harakati zinazohubiriwa mbele ya hadhira isiyokuwa na maarifa, na kwa sababu hiyo tu harakati hiyo iliweza kuwadanganya wengi, na kuwaingiza katika genge la hujuma la Kiwahabi, lisilojua mipaka ya dini wala ya kibinadamu.

Mwalimu Sheikh Ja’far Subhani ananukuu kauli ya Jamiil Swidiq Al-Zahawi isemayo: “Pindi Muhammad bin Abdul Wahab alipoona jamii ya watu wa Najdi imegubikwa na ujinga, na kujitenga mbali na ulimwengu wa maarifa, kiasi ambacho hata elimu za kiakili kwao hazikuwa na nafasi, hapo ikawa ni rahisi kwake 22

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 22

8/14/2017 1:18:24 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

kupandikiza katika jamii mbegu zake za uharibifu, ambazo alitamani kuzipandikiza tokea zamani, ili kujipatia uongozi wa juu kwa jina la dini. Isipokuwa tu hakupata njia iwezayo kumfikisha katika matamanio yake, tofauti na kujiita: Almujaddid fid din, yaani, mfufuaji katika dini.8 Mazigazi: Kwa kuwa harakati za kijangili za Kiwahabi zilikuwa zikiendeshwa kwa jina la tauhidii, watu wengi walidanganyika na kuzipokea kwa anuani hiyo ya tauhidii, pasina kufahamu kuwa ni mazigazi tu ambayo mwenye kiu hudhania kuwa ni maji hali ya kuwa si maji. Sayyid Muhammad Ismail Amiri wa Yemen (1099 – 1886) aliposikia habari za tauhidi zilizoibuka huko Najdi, kwa kweli alivutiwa nazo, akiamini kuwa ni tauhidi ile aitakayo Mwenyezi Mungu, kumbe ni mazigazi pia. Kiongozi huyo wa Yemen baada ya kupata habari hizo kutoka Najdi, aliamua kutunga kaswida ya kumsifu Sheikh Muhammad bin Abdul Wahab isemayo:

‫سالم على نجد ومن حل في نجد‬ ‫وإنكان تسليمي على البعد ال يجدي‬ Amani iwe juu ya (mji) wa Najdi na aliyeingia katika mji wa Najdi, japo salamu yangu (ya kusalimia) nikiwa mbali hainufaishi. Kiongozi huyu baada ya kufanya uchunguzi kwa baadhi ya watu waliofika Yemen toka huko Najdi, alikuta ni tofauti na alivyokuwa amesimuliwa, na ndipo alipotunga kaswida nyingine ya kutubia ku8

Alwahhabiyyat baina mabanil fikri wanataijul amal, kutoka katika kitabu Alfajri Alswadiq uk. 14 23

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 23

8/14/2017 1:18:24 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

tokana na kaswida yake ya awali ya kumsifu Sheikh Muhamd bin Abdul Wahab. Kaswida ya pili ilisema:

‫رجعت عن القول الذي قلت في نجد‬ ‫فقد صح لي عنه خالف الذي عندي‬ Nimerudi nyuma toka kwenye kauli niliyoisema kuhusu Najdi. Kwa hakika nimepata usahihi (kuhusu hiyo Najdi) ambao ni tofauti na ule niliokuwa nao. Sayyid Muhammad Ismail alieleza bayana (baada ya toba yake aliyotubia kutokana na kupetuka kwake mipaka katika kuupenda Uwahhabi): “Kwa hakika alitufikia Sheikh Fadhil Abdurahman kutoka Najdi, na akatutajia katika sifa za Sheikh Muhammad Bin Abdul-Wahab, mambo ambayo hatukuyakubali, kama vile umwagaji damu, kunyang’anya mali za watu, kuwaua wanaompinga japo kwa siri bila ya watu wengine kufahamu, na kukufurisha umma wa Mtume Muhammad 8, basi tukabaki na tahayari, mpaka alipotufikia Sheikh Murbid akiwa na baadhi ya nyaraka za Ibnu Abdul-Wahab, ambazo aliziandika katika kukufurisha waumini na kuwaua na kuwapora mali zao. Na akatuhakikishia hali za Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahab, na ndipo tulipotambua kuwa bwana huyo hakufahamu chochote katika sheria isipokuwa mstari mmoja, na wala hakusoma kwa lengo la kutaka uongofu, na wala hakusoma kwa watu wenye taaluma, bali alijisomea baadhi ya vitabu vya Ibnu Taimiyyah na Ibnu Alqayyim, kisha akafuata mwenendo wao. Japo kuwa wawili hao Ibnu Taimiya na Ibnu Alqayim, wanaharamisha, suala la mtu kufuata mwenendo wa mtu mwingine.”9 9

Kashful Irtiyab uk. 22 24

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 24

8/14/2017 1:18:24 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Anasema Sayyid Muhsin Al-Amin: “Inaonesha kuwa Sayyid Muhammad Ismail Amiri wa Yemen, alirudi nyuma katika kuupenda Uwahabi, na kurejea kwake kulikuwa ni baada ya kuandika kwake kitabu alichokiita Tat’hirul Itikad, kwa kuwa kitabu hicho hazikupungua ndani yake nyaraka za Ibnu Abdul-Wahab. Amiri wa Yemen alifuata madhehebu hiyo kwa anuani ya kuacha bidaa na hali ya kuwa bidaa ndizo zilikuwa zimejaa katika madhehebu hiyo, lakini kwa kuwa alipetuka mipaka katika kuipenda madhehebu hiyo basi hata yaliyokuwa bidaa aliyaona kama sunnah.” Wapenzi wasomaji, hiyo ndiyo hali iliyopo leo hii, Mawahabi wanasema kila kitu ni Bidaa, lakini hapo hapo wanasema kuvaa saa mkono wa kulia ni sunnah. Sawa nitakubali ikiwa watathibitisha kwa maandiko sahihi, au labda niseme kama alivyosema Sheikh Abuu Idi: “Maneno hayo ni mazuri sana, lakini yanapatikana kitabu gani ?” Nadhani ndugu wasomaji wanakumbuka kuwa tuliwaahidi kuwaelezea habari ya Sharifu Masud na Sharifu Ahmad na dola zao. Masharifu hao ni kutoka katika ukoo wa Bani Hashim, unaotokana na Mtume kupitia Hassan Muthanna bin Hassan Sibti, mtoto wa Fatimah J binti Muhammad 8. Ukoo huo ulikuwa ukitawala Hijjaz, Makka na Madina, lakini baadaye uliondolewa kijeshi na utawala wa kifalme wa Kiwahabi wa ukoo wa Saudi. Mapigano baina ya Sharifu Ghalib Amir wa Makka na genge la majangili la kiwahabi, na kuiteka kwao Hijjaz katika zama za Sharifu, na mauaji waliyoyafanya ndani ya Hijjaz na Irak na kuwazuilia Waislamu ibada ya Hijja katika zama zao: Mauaji na vita kati ya Sharifu na Mawahabi ilikuwa ni matokeo ya amri ya kiongozi wa Kiwahabi, aliyehalalisha damu ya Waislamu 25

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 25

8/14/2017 1:18:24 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

wenye itikadi za Kisunni: “Ni halali kuwaua Waislamu wenye itikadi za kisunni na kutwaa mali zao.”10 Kwa itikadi chafu kama hiyo mimi naona kuwa: Jina lolote kutoa binadamu, lafaa kuwaita Mawahabi. Je, ni nani Sharifu Ghalib? Nasabu ya Sharifu Ghalib inakutana na Bwana Mtume Muhammad 8 kupitia kwa Hassan Muthana bin Hassan Sibti mtoto wa Bibi Fatimah J binti Muhammad 8. Ukoo wa Sharifu ulikuwa ukitawala Hijjaz, Makka na Madina, lakini baadaye uliondolewa kijeshi na utawala haramu wa kifalme wa Kiwahabi wa ukoo wa Saud. Tulikwisha kuzungumzia namna Mawahabi walivyokuwa wakiendesha mauaji ndani na nje ya Najdi, hadi wakafikia kuikamata Hijjaz, na mauaji hayo hayakuishia Hijjaz bali yaliendelea na yanaendea hadi leo katika maeneo mbalimbali ya ulimwengu, kwani nadharia ya uvamizi na mauaji na kujilipua mabomu, hii ni moja ya nguzo za dini ya Kiwahabi. Kwa hiyo mapigano ya muda mrefu ya vita zisizopungua hamsini yalishtadi baina ya Sharifu Ghalib kiongozi wa Makka na genge la Kiwahabi. Lakini vita ya kuwapiga Mawahabi haikuanzia kwa Sharifu Ghalib na Abdul-Aziz, bali ni vita ya muda mrefu. Mwalimu, Sheikh Ja’far Subhani anasimulia kuwa: Diham bin Dawaas aliyekuwa mtawala wa Riadh, alikuwa na vita na Mawahab takriban kila mwaka, na mwaka 1178 AH, watu wa Najran wa kabila la Bani Yaam, waliokuwa wakiongozwa na Sayyid Hassan Hibatullah, walifanya mapatano na makabila mawili ya Ihsaa, kabila la Bani Khalidi na kabila la Ajman kwenda Dir’iya na kuisambaratisha mamlaka ya Kiwahabi. 10

Kashfu-shub-hat 26

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 26

8/14/2017 1:18:24 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Makabila yaliondoka na silaha za kutosha, lakini kundi la Najran liliwasili mpakani kabla ya kundi la Ihsaa, na hapo waliwakuta askari wa Kiwahabi wakilinda amani. Watu wa Najran walikuwa peke yao lakini waliwapiga askari wa Kiwahhab na wakapigika. Wakaingia mpaka mjini, na Muhammad bin Saud akajificha kwa hofu. Hali ilikuwa tete mpaka kiongozi huyo wa serikali ya Kiwahabi Muhammad bin Saudi akajiharishia, na hapo bado lile kundi la Ihsaa lilikuwa halijafika. Kiongozi wa serikali ya Kiwahabi akataka kusalimu amri, lakini Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahab akainua juu bendera ya suluhu. Mkataba wa amani ukasainiwa kwa sharti jeshi la Najran lirudi nyuma, na wawaachie huru mateka wa Kiwahabi, na utawala wa Kiwahabi usivuke mipaka ya Dir’iya. Halafu serikali ya Kiwahabi itowe junaiyyah (jina la sarafu ya wakati huo) elfu moja kuwapa wanajeshi wa Najran. Na hilo ni kosa kubwa lililofanywa na Sheikh Hassan Hibatullah kwa maslahi yake binafsi. Sasa kundi la Ihsaa chini ya uongozi wa Khalidi lilipoingia, walikuta suluhu imeshafanywa, kwa hiyo wakawa hawana njia zaidi ya kukubaliana na suluhu iliyofanywa na ndugu zao. Na tangu kiongozi wa Kiwahabi ajiharishie, afya yake haikuwa nzuri tena, na huo ulikuwa ndiyo mwanzo wa maradhi yake, na mwaka 1179 alifariki Dunia, na nafasi yake ikashikwa na mtoto wake Abdul-Aziz bin Muhammad. Lakin kabla hajafa, Muhammad bin Saud alikuwa amekwisha mtawalisha mtoto wake huyo, kama ilivyopendekezwa na Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahhab, sawa na vile Muawiyyah alivyoacha. Anamtawalisha mtoto wake Yazidi, Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahhab anapiga vita bidaa halafu naye anapita njia hiyo hiyo.”11 Na kiongozi huyo mpya ndiye aliyepigana vita nyingi na Sharif Ghalib kama tulivyosema hapo awali. Mnamo mwaka 1213 A.H.,   Al-Milal wan-Nihal Jz. 4, uk. 584

11

27

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 27

8/14/2017 1:18:24 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

ilifanyika suluhu baina ya Sharifu na kiongozi wa Kiwahabi Abdul Aziz bin Muhammad, na wakaweka mipaka ya ardhi, na wakaelezana makabila yaliyokuwa chini ya himaya ya Sharifu Ghalib na yale yaliyokuwa chini ya serikali ya Kiwahabi. Basi mkataba wa amani ukasainiwa na wakakubaliana kusitisha mapigano, na Mawahabi waruhusiwe kwenda Hijja, maana katika zama za Sharifu ilikuwa ni marufuku kwa wakata suruali kuingia Makka. Kwa mujibu wa Sharifu ilikuwa ni uhuni kuonesha mandhari ya wavaa vimini mbele ya Al-Kaaba, lakini baada ya suluhu ilitangazwa amani na Mawahabi wakaruhusiwa kwenda Hijja. Na aliyehiji katika wanazuoni wao ni Hamd bin Nasir akiwa na kundi dogo la wakata suruali, lakini Amir wao hakuhiji, kwa sababu Suleiman Pasha, Gavana wa Baghdad aliandaa jeshi ili kwenda kumuua lakini bahati mbaya alifanikiwa kukimbia. Na mnamo mwaka 1214 A.H., alihiji Saud bin Abdul Aziz akiongozana na watu wengi, na wakakutana na Sharifu Ghalib katika hema mahala paitwapo Abtah. Mnamo mwaka 1214 A.H alihiji Saudi bin Abdul Azizi, akiwa na jeshi la watu wanaozidi 20,000, lakini kabla ya kuingia Makka alitanguliza zawadi nono kwa Sharifu Ghalib. Zawadi ziliwasilishwa na Hamd bin Nasir, Sheikh wa Kiwahabi. Zawadi yenyewe ilikuwa ni farasi 35, ngamia wazuri wa thamani walikuwa 10. Sharifu Ghalib alipokea zawadi, naye pia mkabala na zawadi hiyo aliwapa vitu vingine. Lakini Sharifu alikuwa kachukua tahadhari kabla ya ujio wa Mawahabi, maana watu hao hawajui mipaka ya sheria za ubinadamu achilia mbali za Mwenyezi Mungu. Sharifu alijenga ngome imara na madhubuti na aliweka ulinzi mkali katika njia zote kuu za kuingilia Makka na kuyataka makabila kuwa makini na kudhibiti njia zote ambazo adui angeweza kuzitumia. Lakini kiongozi wa serikali ya Kiwahabi hakuingia tena Makka, baada ya kuona kuwa ulinzi ni mkali mno, bali alishukia ka28

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 28

8/14/2017 1:18:24 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

tika viwanja vya Arafah. Mpenzi msomaji hebu jiulize kama kweli kiongozi wa serikali ya Kiwahabi alikuwa na nia ya kuhiji, kwa nini asitishe safari kwa sababu tu, Sharifu kaimarisha ulinzi? Bila shaka hapo lengo la safari ni hujuma na mauaji dhidi ya watu wasio na hatia kama ilivyo desturi ya Mawahabi. Na tarehe 12 ya mwezi wa mfunguo tatu yalitokea mapigino makali ya kubadilishana risasi baina ya Waarabu ambao ni wafuasi wa Sharifu, na watu wa kiongozi wa serikali ya Kiwahabi. Mapigano hayo yalipelekea umwagikaji wa damu ndani ya msimu wa ibada. Sharifu aliwazuia watu wake na akasitisha mapigano, na watu wakaondoka Mina kabla ya saa sita mchana kwa sababu za kiusalama, kwani hali haikuwa shwari. Na kiongozi wa genge la hujuma la kiwahabi alirejea mjini kwake Dir’iyah.12 Naam hao ndiyo Mawahabi na nadharia zao, nadharia chinja chinja. Watu wasio na huruma katika nyoyo zao, wala hekima vichwani mwao, sijui ni watu wa aina gani hawa. Hebu fikiria tangu karne ya 12 hadi leo watu wanarithishana itikadi potovu kizazi hadi kizazi. Kwa kweli sijui tuwaiteje watu hawa. Na hata tukiwaita Wapagani, naamini tutakuwa hatujawatendea haki Wapagani, kwani wapagani tunatofautiana nao katika imani tu, lakini tunasaidiana katika mambo mbalimbali ya kibinadamu na ya kijamii. Mawahabi waivamia Irak na kuwakumbusha Waislam masaibu ya Karbala kwa mara nyingine: Mnamo mwaka wa 1216 – 1225 A.H. Saud bin Abdul-Azizi kiongozi wa dola ya kifalme ya Kiwahabi aliandaa jeshi kubwa la Waarabu wa Najdi kwenda kuipiga Irak bila kosa na kuuzingira mji mtukufu wa Karbala. Waliingia Karbala kwa mabavu na uvamizi bila ya watu wa Karbala kuwa na maandalizi yoyote yale. Watu waliuawa wake kwa waume bali hadi watoto wachanga mikononi mwa mama zao. Katika 12

Khulaasatul kalaam fii umaraail baladil haraam uk. 267-269 29

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 29

8/14/2017 1:18:24 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

mashambulizi hayo hakusalimika mtu isipokuwa yule aliyekimbia au kujificha chini ya mizigo ya kuni nao wakashindwa kumuona. Hayo waliyafanya Mawahabi katika eneo lililokuwa jirani na kaburi la Sayyiduna Hussein Shahid ambaye ni mtoto wa Fatimah J bint ya Mtume Muhammad 8. Hawakutosheka na mauaji hayo bali waliingia ndani ya Haram, jengo alilozikwa ndani yake Sayyiduna Hussein na kulivunja kaburi lake na kungo’a madirisha yaliyokuwa kwenye jengo ambalo ndani yake kuna kaburi tukufu la Sayyiduna Hussein, na kupora vitu vya thamani vilivyokuwa jengoni humo, bila ya kulinda heshima ya Mtume wala kuzingatia nafasi aliyokuwa nayo Sayyiduna Hussein kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu 8, na tukio hilo lilirejesha upya tukio la mauaji yaliyofanywa na Bani Umaiyyah dhidi ya kizazi cha Bwana Mtume 8. Hiyo ndiyo dini ya Kiwahabi au ya Kianswar sunnah inayodai kufuata sunnah za Bwana Mtume, lakini yote hayo Mtume hakuyafanya kwa kuwa yeye alikuwa mkamilifu katika ubinadamu wake, achilia mbali dini yake. Sasa hawa Mawahabi mimi naona bila shaka kuwa wana mtume wao kutoka Najdi, mahala alikozaliwa kiongozi wao! Anasema Mwalimu Sheikh Ja’far Subhani: “Hakika mauaji ya kinyama ya kiwahabi ndani ya maeneo matakatifu, yameufifiza mno ukurasa wa historia ya Kiwahabi. Na mwandishi wa Kiwahabi, Swalaahud-din Al-Mukhtar amekiri kwa tukio hilo lenye kuumiza roho na kusema: Katika mwaka 1216 aliandaa Saud bin Abdul Aziz jeshi chinjachinja lililojumuisha watu wa Najdi, Hijjaz, Tihama na miji mingine, wakashika njia kuelekea Irak na kuwasili Karbala ndani ya mwezi wa mfunguo pili. Wakauzingira mji wa Karbala, na kuvunja ngome ya mji na minara yake na wakauingia mji kiubabe. Wakafanya mauaji na akauawa kila aliyekutwa sokoni, barabarani, nyumbani na maeneo mengineyo. Mpaka kufikia muda wa adhuhuri walikuwa 30

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 30

8/14/2017 1:18:24 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

wameishakusanya ngawira za kutosha. Walisitisha mashambulizi na kujipumzisha mahala paitwapo Abyadh. Mfalme akatwaa khumsi ya ngawira hiyo, na nyingine ikagawiwa mafungu, fungu la askari wa kikosi cha farasi, na fungu la askari wa chini.”13 Mwanahistoria mwingine Ibnu Bushri Najdi, yeye anaripoti kama ifuatavyo: “Ni desturi ya Mashia wa Irak kwenda Najaf kila mwaka ili kusherehekea sikukuu ya Ghadir, (ambayo kwa mujibu wa imani yao, Ghadir ni sikukuu ya kutangazwa rasmi Imam Ali D kuwa khalifa wa Mtume) basi wakazi wa Karbala walitoka na kwenda Najaf, na hakubaki mtu nyumbani isipokuwa yule asiyejiweza (na wengineo wenye nyudhuru mbalimbali). Basi majangili wa Kiwahabi au Answar sunna kama wanavyojiita wakakitumia kipindi hicho cha watu kwenda Najaf, kama fursa adhimu ya kufanya hujuma ndani ya mji wa Karbala. Wakaua kila aliyekutwa mjini humo, na hawakuacha hata mtu mmoja akiwa hai. Na wakapora mali za wakazi wa mji huo. Inakadiriwa idadi ya watu waliouawa kwa siku hiyo kuwa ilifikia watu elfu tatu (3,000). Ama kuhusu mali walizozipora Mawahabi kwa siku hiyo ni zaidi ya maelezo, na inasemekana kuwa ngamia mia mbili walisheheneshwa zaidi ya uwezo wao mali zilizoibwa, na wakatwaa hazina na kila chenye thamani bali hadi mapambo yaliyokuwa kwenye kuba ya kaburi la Sayyiduna Hussein pia waliyatwaa. Kutokana na mashambulizi hayo na mauaji hayo ya kinyama ya Kiwahabi, bali zaidi ya unyama, kwani kuna wakati mwingine hata simba huwa na huruma kwa binadamu, huenda baadhi ya watu wakadhania kuwa hayo walifanyiwa Mashia tu katika miji yao, na kwamba Waislamu wengine walikuwa kwenye amani. Vita na uvukaji mipaka kama huo haukuwagusa. Hii ni fikra chakavu na haina usahihi, bali ukweli ni kwamba dhulma za Kiwahabi ziliwakumba Waislamu wote, 13

Al-wahhabiyyat baina mabanil fikri, uk. 58 31

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 31

8/14/2017 1:18:24 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

(bali hata wasiokuwa Waislam pia) na wakazi wa miji ya Kiislam mingineyo kama vile huko Sham (Siria) Yemen kadhalika hawakusalimika na uvamizi wa Kiwahabi. Na hatuna shaka kuwa usajili wa matukio yote yasiyo ya kibinadamu yaliyofanywa na Mawahabi katika miji ya kiislam na isiyo ya Kiislam, unahitajia vitabu maalum. Haya yote tuliyoyataja hapa, hayakuishia huko tu, bali yanaendelea hadi leo hii, Kila siku mnasikia katika vyombo vya habari, na mnaona picha za mauaji na matukio ya kujitoa muhanga kwa kujilipua na mabomu yanayofanywa na Mawahabi, wanaojiita Boko Haram, al-Shabab, ISIS na pia mnashuhudia kila siku majumba ya ibada ya watu wenye imani ghairi ya Uislam yakivamiwa na Mawahabi kwa ujinga na elimu duni walizokuwa nazo, huku wakiamini kuwa watapata pepo, kwa misingi ya vurugu na uhuni kama huo. Mpenzi msomaji! Yote hii ni mifano hai tunayoishi nayo katika jamii yetu ya leo. Muwahabi mmoja yuko tayari kuvaa mabomu na kujilipua ndani ya gari lililobeba watu 200, aangamize watu wote hao, kwa sababu tu ndani ya gari lile kuna mtu mmoja tu, ambaye anatofautiana naye kiitikadi. Kila siku mnasikia mahubiri ya Kiwahabi yakichochea chuki na vita na mauaji dhidi ya Wakristo wasio na hatia, kwa anuani ya Jihadi. Na wanaambiwa kuwa wakiua japo Mkristo mmoja wataingia peponi. Huo sio tu unyama bali ni zaidi ya unyama. Kamwe hatutasahau mauaji ya Karbala: Uwahhabi ni dini iliyoasisiwa na wakoloni wa Kiingereza ili kuondoa si tu kinadharia bali kivitendo, matukufu ya dini yetu na kuvunja heshima ya Mtume wetu, huku wakijificha nyuma ya mgongo wa ndugu zetu Ahlu-Sunnah wal-jamaa. Nawaambieni ndugu zangu Ahlu-sunnah kuwa chukueni tahadhari kwani Mawahabi ni mithili 32

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 32

8/14/2017 1:18:24 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

ya panyabuku, wanaokula na kupuliza. Msipokuwa makini mtakwisha ndugu zangu. Katika somo lililopita tulisema kuwa: Mnamo mwaka wa 1216 – 1225 A.H Saud bin Abdul-Azizi kiongozi wa dola ya kifalme ya Kiwahabi, aliandaa jeshi kubwa la Waarabu wa Najdi kwenda kuipiga Irak bila kosa, na kuuzingira mji mtukufu wa Karbala. Waliingia Karbala kwa mabavu na uvamizi bila ya watu wa Karbala kuwa na maandalizi yoyote yale. Watu waliuawa wake kwa waume bali hadi watoto wachanga wakiwa mikononi mwa mama zao. Mpenzi msomaji! Mauji ya kinyama (bali zaidi ya unyama, kwani tukisema ya kinyama tutakuwa hatujawatendea haki wanyama) yaliyofanywa na Mawahabi yanatupeleka nyuma hadi mwaka 61 A.H, ambako historia yatwambia kuwa: Sayyiduna Hussein D, alipoona kuwa dini inachezewa na kuharibiwa, na hali imekuwa ni mbaya kufikia hatua ya kuifanya haramu kuwa halali na halali kuwa haramu, mipaka ya Mwenyezi Mungu haizingatiwi tena, achilia mbali ile ya ubinadamu, ndipo Imamu Hussein alipofunga safari kuelekea Irak, na kaulimbiu yake ilikuwa ni kuleta mabadiliko katika umma wa babu yake, pia kuamrisha mema na kukataza maovu. Kuamrisha mema ndiyo kuamrisha uadilifu, kukataza mabaya ndiyo kukataza dhulma. Sote tunatambua kuwa: Kuupenda uadilifu na kuichukia dhulma, hayo si maswala ya kidini tu bali ni maswala ya kimaumbile. Ni silika ya kila mwanadamu kupenda uadilifu, ni silika ya kila mwanadamu kuichukia dhulma. Kwa ibara nyingine tunaweza kusema kuwa Imamu Hussein alikwenda Irak kwa nia na madhumuni ya kupigania haki ya kila mwanadamu bila kujali dini rangi au kabila. Lakini Bani Ummaiyah waliona kuwa Hussein ni kikwazo kwa maslahi yao ya kidunia, yenye malengo ya kujaza matumbo yao kwa 33

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 33

8/14/2017 1:18:24 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

njia yoyote ile iwayo, hata ile ya kuharibu dini ya Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo wakamuua Hussein, na kichwa chake kikapelekwa Sham (Syria) kwa Yazid bin Muawiyah na kikafanyiwa dhihaka ya hali ya juu zaidi. Lakini watu wa Madina waliposikia kuwa kiongozi wa Waislamu, Yazid bin Muawiyah amemuua Hussein, walitoka kwenda Sham ili kumuona huyo kiongozi wa waislam. Lakini cha kusikitisha walimkuta ni mtu mlevi na mcheza kamari, kila anapokaa lazima awe na ngedere pembeni yake. Basi watu wale waliporejea Madina, walisimulia hali waliyoikuta huko Syria. Watu wa Madina walisikitishwa mno na taarifa hiyo, na wasichana wa Madina walitoa tamko ya kuwa: “Laiti Madina pasingelikuwa na wanaume, basi wangetoka wenyewe kwenda kupigana na Yazid na jeshi lake.” Baada ya Yazid kupata taarifa hiyo, alituma jeshi kwenda kushambulia mji wa Mtume (Madina). Maswahaba wema wa Mtume waliuawa, na wasichana bikra elfu moja walinajisiwa hadharani, katika mashambulizi ya siku tatu ndani ya mji wa Mtume. Mwanachuoni maarufu, Dhahabi anasema: “Yazid alikuwa ni mtu mwenye ususuavu wa moyo, mlevi na mfanya maasi. Alianza utawala wake kwa kumuua Hussein mjukuu wa Mtume, na akamalizia kwa kuwaua Maswahaba na kubaka wasichana katika mji wa Mtume. Tukio hilo lilifahamika kwa jina la Tukio la Harrah. Basi watu wakamchukia, na hakubarikiwa katika maisha yake, na wengi baada ya Hussein walisimama dhidi yake..”14 Mpenzi msomaji tafakari tukio hilo kwa kina, kisha linganisha na matukio ya kigaidi yafanywayo na Mawahabi leo hii, utafahamu kuwa sera za Kiwahabi za Boko Haram za kubaka wasichana, ni mwendelezo wa sera za Bani Umaiyyah. Mauji yaliyofanywa na Bani Umaiyya dhidi ya watu wa nyumba ya Bwana Mtume yanam14

Siyar a’laamu nubalaa, J z. 4, uk 38 34

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 34

8/14/2017 1:18:24 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

liza kila mwenye roho ya ubinadamu, au kwa ibara sahihi, ni mauaji dhidi ya ubinadamu, maana watu wa nyumba ya Mtume walikuwa wakipigania ubinadamu wa kila mwanadamu. Sasa mtu anayewaua watu kama hao basi huyo ni adui wa ubinadamu. Inasikitisha mno leo hii kuona vijana wakitembea barabarani wamevaa vizibao na vipande vya suruali, wakitamani kuwa kama wanamgambo wa Al-shabab na Al-kaida, au Boko Haram. Vijana wengi hudhania kuwa makundi haya ya kigaidi ni makundi ya Kiislamu, na hiyo ni dhana yao njema. Lakini ukichunguza kazi za makundi haya utakuta kuwa ni: Uvamizi, ubakaji, kuua Waislamu wasio na hatia, kwa sababu tu, wanakwenda tofauti na itikadi zao. Kuua Wakristo na kutaka watu wote wawe wakata suruali kama wao na kwa muda wautakao wao. Na kwa matukio kama haya yanatosha kumfungua mtu akili na kumuonesha kuwa makundi ya kigaidi ya Kiwahabi si makundi ya Kiislamu, kwani yako nje ya mstari wa mafundisho sahihi ya dini yetu ya Kiislamu. Uislamu hauwezi kuruhusu ubakaji au uvamizi huo unaofanywa na makundi ya Kiwahabi au Salafi au Answar Suna kama wanavyojiita. Anasema mwanachuoni Sayyid Jawad Al-Amuli: “Mwaka 1216 A.H. Saudi, Muwahabi kutoka ardhi ya Najdi, alizusha aliyoyazusha katika dini, na akahalalisha damu za Waislamu, na kuharibu makaburi ya Maimamu watakatifu, na mwaka huo huo alishambulia kaburi la Imamu Hussein D (mjukuu wa Bwana Mtume) na akaua watu, wake kwa waume, bali hadi watoto wachanga pia aliwaua. Akapora mali za watu, na kufanya uharibifu kwenye kaburi la Imamu Hussein D ikiwa ni pamoja na kuvunja jengo lake, na nguzo zake.” Mwanachuoni Sayyid Jawad anaendelea kusema kuwa: “Usiku wa kuamkia tarehe 9 mwezi wa mfunguo tano mwaka 1221, kabla ya Swala ya asubuhi, Saudi Muwahabi alitufanyia mashambulizi ya 35

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 35

8/14/2017 1:18:24 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

ghafla katika mji wa Najaf, na walikaribia kuuteka mji, lakini ilikuwa kama muujiza, hali ambayo wao wenyewe walishindwa kuamini, maana walipigwa na wakapigika. Wengi wao walikufa, na wengine wakarejea wakiwa ni wenye kushindwa.” Sayyid Jawad anasema: “Mwaka wa 1222 Saud aliingia Irak na jeshi la zaidi ya watu 20,000. Tukahadharishwa kuwa anataka kubomoa Najaf, basi tukachukua tahadhari, kwa kutoka sisi sote na kwenda kwenye ngome ya mji (kwa ulinzi zaidi), na alipotujia usiku, alitukuta tuko makini tumeuzunguka mji kwa bunduki na silaha nyinginezo. Na hapo hakuweza kufanya chochote bali alikwenda katika mji wa Hillah, nako pia alikuta ulinzi ni mkali, na ndipo waliamua ghafla kuuelekea mji wa Karbala nyakati za mchana watu wakiwa hawajui hili wala lile. Wakauzingira mji vikali na wakazi wake wakasimama imara. Jeshi la Kiwahabi likaua watu, nao Mawahabi pia wakauliwa, kisha jeshi la Kiwahabi likarejea bila mafanikio baada ya kuibomoa Irak na kuuawa aliyeuawa. Kisha wakaja kuukamata miji ya Makka na Madina, na kuzuia ibada ya Hijja kwa muda wa miaka mitatu.”15 Mpenzi msomaji hebu jaribu kuvuta taswira ya mauaji ya Bani Umaiyyah dhidi ya Imamu Hussein katika mji wa Karbala, mwaka wa 61A.H, kisha linganisha na mauaji yaliyofanywa na Mawahabi katika mji wa Karbala mwaka 1216 – 1225, bila shaka utafahamu Wahabi ni nani. Halafu jaribu tena kuvuta hisia kama vile uko Madina unashuhudia tukio la Harrah, tukio ambalo Maswahaba wema waliuawa na jeshi la Yazidi bin Muawiyah na mabinti wao wakabakwa hadharani. Halafu linganisha tena ubakaji huo, na ubakaji unaofanywa leo hii na hao Maanswar-suna wa Boko Haram. Kwa kupitia matukio hayo bila shaka utafahamu kuwa mambo yote yanayofanywa na vikundi vya kigaidi vya Kiwahabi, ni mwendelezo wa fikra na njama za kuufanya Uislamu upoteze sifa zake chanya 15

Kashful Irtiab, uk 42. 36

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 36

8/14/2017 1:18:24 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

na haiba yake mbele ya watu wenye imani ghairi ya imani yetu ya Kiislamu kama tulivyosema hapo mwanzo. Ndugu yangu katika utu, hawa Mawahabi wanadai kuwa wanafuata mwenendo wa Mtume, hivi ni kweli bwana Mtume 8 alikuwa muuaji, mporaji na mbakaji kama wao? Tafakari kwa kina ili ugundue malengo ya vikundi hivi vya kigaidi kama vile Al-kaida, Boko Haram, na wengine wanaojiita: Lions of Monotheism (Simba wa Tauhidii). Cha kusikitisha ni pale unapokuta vijana wakishabikia makundi hayo, bila ya kufahamu malengo ya watu hao ni yapi! Uislamu ni dini ya amani na ulikwisha jieleza kwa vitendo siku ile uliposainiwa mkataba wa amani wa Hudaybiyah. Amani iliyoelezwa kwa vitendo katika mkataba, huo ndiyo ilikuwa chachu ya kuleta ushindi mkubwa, na kusukuma mbele zaidi gurudumu la maendeleo ya Uislamu. Watu wenye imani ghairi ya Uislamu walikiri kuwa Uislamu si dini ya kulazimishana. Lakini leo hii Mawahabi wanataka kuwalazimisha watu wote waingie katika dini yao. – Mawazo hayo ni mazuri sana lakini yanapatikana kitabu gani? Mwenyezi Mungu anasema katika Qur’ani:

“Hakuna kulazimisha katika Dini; uwongofu umekwisha pambanuka na upotofu. Basi anayemkataa taghuti na akamuamini Mwenyezi Mungu, hakika yeye ameshika kishikio madhubuti kisichovunjika. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mjuzi.”16

Aya hii inatufundisha kuwa tusiwalazimishe watu kuikubali itikadi yetu kabla ya kuwapa nguvu za hoja, bali tuzungumze nao 16

Surat Baqara; 2:256. 37

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 37

8/14/2017 1:18:25 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

kwa hekima na si kwa matusi, halafu wakikinaika na hoja zetu, basi watakuwa na hiari ya kufuata au kutofuata. Sasa kama watatufuata basi ni wajibu wetu kuwalazimisha kufuata yote ya wajibu yaliyopo katika dini yetu, na wasipotufuata basi hatuna mamlaka ya kuwalazimisha. Ewe Muwahabi! Usimlazimishe mkristo kukata suruali bali mthibitishie kwa hoja kuwa dini ya kukata suruali ya Kiwahabi ifanyayo mauaji na ubakaji kule Nigeria ni dini sahihi. Sasa akikubali kukufuata katika imani hiyo, basi mlazimishe kukata suruali maana kaikubali mwenyewe dini na masharti yake. Kuvunjika kwa mkataba wa amani baina ya Sharifu Ghalib na Mawahabi: Tuliwahi kuzungumzia suluhu iliyofanyika baina ya Mawahabi na Sharifu Ghalib, mnamo mwaka 1213, lakini mkataba huo wa amani na kusitisha mapigano uliosainiwa na watu wa pande zote mbili, haukudumu kwa kipindi kirefu sana, kwani watu wa upande wa pili, waliosaini mkataba huo, kwa ibara nyingine Mawahabi, hawakuwa waaminifu na wenye kutekeleza ahadi walizoahidi. Anasema Sheikh Dahlan katika kitabu chake cha KhulaasatulKalaam: “Baada ya suluhu, Saud hakuacha kuweka majasusi/ mashushushu, na kuwaandikia Masheikh wa Kiarabu kwa siri (kuwashawishi) kama vile Sheikh Muhail na Sheikh Bariq. Basi Masheikh hawa wawili wakawa wanashawishi na kuwaharibu kifikra na mawazo watu wa makabila mpaka ule mkataba wa amani ukavunjika, na makabila yote ya mji wa Hijjaz yakaingia kwenye Uwahabi. Basi Sharif aliposikia habari hizo, alimtumia ujumbe Gavana wake aliyekuwa katika mji wa Qunfudhah (Pwani ya bahari ya Sham) kumtaka aende kumpiga Sheikh Muhail, naye gavana alikwenda. Yakatokea baina yao (Sheikh na gavana wa Sharifu) mapi38

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 38

8/14/2017 1:18:25 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

gano makali mno na gavana yule alishinda vita, na akamiliki kila kilichokuwa katika uwanda wao, na akaunguza majumba kisha akarejea Qunfudhah. Kisha ikamfikia tena (Gavana) habari ya kuwa Mawahabi wamerudi na wamejikusanya tena na wamekuwa wakiwatishia amani wale wote wasiowatii. Gavana yule alimpa habari hiyo Sharifu, naye Sharifu akaandaa jeshi chini ya uongozi wa Sharifu Mandil. Basi akafanya vita na watu wa kabila la Bani Kinanah, na akaua wengi kati yao. Na habari nyingine ikamfikia Sharifu ya kuwa watu wa Hala wameingia kwenye uwahhabi. Sharifu bila kupoteza muda aliwaandalia jeshi, chini ya uongozi wa Sayyid Nasir bin Suleiman, naye aliua wengi kati yao na kutwaa ngawira, kisha akarejea Makka akiwa na baadhi ya watu wa mji wa Hala waliotubu. Na watu hao walimuomba Sharifu Ghalib awape jeshi la kuwarudisha mjini kwao, na Sharifu akakubali ombi hilo, akawapa jeshi lililoongozwa na Sayyid Mandil. Sayyid huyu alijenga ngome katika mji wa Hala na akaweka humo hazina nyingi, kwa kuhofia hujuma za maadui. Baada ya miezi minane habari ya ujio wa Mawahabi wakiongozwa na mtu aliyefahamika kwa jina la Hashri, ikamfikia Sayyid Mandil. Kikosi cha Mawahabi kilituma ujumbe kwa sheikh wa mji na kumshawishi akubali kuwazuia wapiganaji wa Sayyid Mandil kuingia katika ngome ya wapiganaji wa jeshi la Kiwahabi. Basi Sayyid alitoa baadhi ya watu katika kikosi chake, na watu wa mji wakabakia na wapiganaji hamsini tu. Mapigano yakashtadi baina ya askari wa Sayyid Mandil na wanamgambo katili wa Kiwahabi, na kutoka katika kila kundi, kati ya hayo mawili, idadi kubwa ilipoteza maisha. Mawahabi walishindwa, lakini walitumia njia mbadala ya kuwashawishi watu wa mjini hapo, nao kweli wakafanya usaliti na kumgeuka Sayyid Mandil. Mazingira yahakumruhusu tena Sayyid kuendelea 39

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 39

8/14/2017 1:18:25 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

kubakia hapo, kwa hiyo akarejea Makka. Kisha habari ikamfikia Sharifu Ghalib kwamba watu wa Pwani ya Yemen wameingia katika Uwahabi. Basi Sharifu akawatumia jeshi chini ya uongozi wa Sayyid Katadah, akawapiga na kuwapokonya mali, na akateka nyara watu kumi na tisa. Na wakati huo walikuwa tayari wamekwisha onja kisago kutoka kwa Gavana wa Kunfudhah, basi wakamfanyia hila ya makabila matatu kujifanya yametii, na wakamuandikia barua arudi tena ili wasaidiane kuwapiga Mawahabi, lakini walikuwa wameweka njama kuwa Gavana akifika tu wamkamate na kumuua. Basi Gavana akatoka na jeshi lake, nao wakaanza kumshambulia. Lakini Mwenyezi Mungu alimpa ushindi wa kishindo, akaua wengi kati yao, na kutwaa ngawira. Kisha akajumuika na askari wa Sayyid Sa’d, na ikamfikia habari kuwa Mawahabi wamekuja na wanajeshi wengi, na wamegawanyika makundi mawili. Gavana akawafuata nyuma, na huku nyuma yake kundi la pili likaingia ili kumshambulia Sayyid Sa’d. Lakini walipobaini kuwa hawana uwezo huo, walimuacha. Ama lile kundi la kwanza lilikuwa linaelekea Kunfudhah, lakini Gavana aliwakuta katika eneo liitwalo Dakan, na hapo mapambano yakashtadi na hawakusalimika ila watu wachache. Mwanzoni mwa mwaka wa 1217 Ma’di bin Shaar Sheikh Muhail, akakusanya jeshi la watu 12,000 kuelekea Kunfudhah. Basi Gavana alitoka na jeshi la watu mia saba watupa mishale, na farasi 13. Aliua watu mia nne, na kujeruhi mia mbili, na 200 walikamatwa mateka, na waliosalia wote wakakimbia. Gavana akachukua mifugo na silaha zao. Mapigano yalikuwa makali kiasi cha kuharibu majimbo mengi ya Yemen. Na pindi Saudi alipotambua kuwa mji wa Yemen utakuwa chini ya utawala wa Gavana wa Qunfudhah aliyesimikwa na Sharifu Ghalib, ndipo kiongozi wa Kiwahabi Saudi alipomuweka Salim bin Shakban ili kuyavuruga makabila ya Zahraan. Akaweka watu wake 40

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 40

8/14/2017 1:18:25 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

humo ili kutimiza azma yake, lakini Sharifu Ghalib alipogundua hilo, aliandika barua kwa Mfalme Abdul-Aziz na mwanawe Saudi akiwataka kutekeleza ahadi waliowekeana katika mkataba wa amani uliosainiwa mwaka 1213. Kila mmoja kati ya Abdul-aziz na mwanawe Saud, aliandika barua iliyojaa maelezo ya uongo, ya kwamba ni uvumi tu unaovumishwa na watu wao, ili kuvunja maafikiano hayo ya mwaka 1213. Lakini Sharifu hakutosheka na maelezo hayo yaliyotolewa na viongozi hao wa Kiwahabi, bali aliagiza mjumbe wake kwenda kwa makabila ya Zahran ili kupata ukweli. Ndipo watu wa makabila hayo (waliokwishaharibiwa na Mawahabi) wakamwambia yule mjumbe kuwa mlichoambiwa ni kweli. Sharifu baada ya kupata maelezo hayo (akajua kuwa ni yakweli) akamwagiza mume wa dada yake, Uthman bin Abdurahman Al-Mudhayifi, na Sharif Abdul-Hussein na Ibnu Hamid kwenda Dir’iyyah kufanya upya mkataba wao wa amani. Wajumbe hao walifika Dir’iyyah na Mfalme akawakaribisha, nao wakakabidhi ujumbe wa Sharifu kwa Mfalme Abdul-Aziz. Lakini mmoja wa wajumbe wa Sharifu, ambaye ni Sheikh Al-Mudhayif, alifanya usaliti, kwa kuomba kikao cha faragha baina yake na Mfalme Abdul-Aziz. Naye Mfalme alikubaliana na hilo. Sasa sikiliza muhtasari wa kikao hicho cha faragha: Sheikh Al-Mudhayif, alimuomba Abdul-Aziz ammilikishe Makka, na akamtajia majina ya wakuu wa makabila ambayo anataka kuyatawala. Basi AbdulAziz akaandika waraka kwa wakuu wa makabila hayo, akiwaambia kuwa amemteua Sheikh Al-Mudhayif kuwa kiongozi wao, na kuwa uongozi wake utajumuisha mji wa Taif na miji inayoizunguka Taif. Waraka huu ulibebwa na Sheikh Al-Mudhayif mwenyewe. Kisha Abdul-Aziz akaandika waraka mwingine ili kujibu ule waraka wa Sharifu Ghalib. Waraka huu ulikuwa umejaa ulaghai na uongo, na waraka huu ulikabidhiwa kwa wale wajumbe wengine, nao ha41

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 41

8/14/2017 1:18:25 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

wakujua kilichojiri baina ya Sheikh Al-Mudhayif na Abdul-Aziz. Wajumbe wakaanza safari ya kurudi kwa Sharifu, lakini walipofika Ubailah, eneo lenye umbali wa mwendo wa siku moja kuufikia mji wa Taif, na hapo palikuwapo na ngome na eneo hilo lilikuwa la mlimani, basi Sheikh Al-Mudhayif akabakia hapo, na kuwaambia wenzake watangulie na kuwa yeye yuko nyuma yao. Sheikh akaingia katika ngome ile na kuweka kambi yake hapo. Alitoa pia nyaraka toka kwa Abdul-Aziz zikionesha kuwa amepewa mamlaka juu watu wa mji huo. Nyaraka zikasambazwa kwa wakuu wa makabila yaliyo karibu naye nao wakamtii. Mpenzi msomaji, nadhani unakumbuka kuwa nilikwambia ya kwamba toka mahala alipobakia Sheikh Al-Mudhayif hadi Taif kuna umbali wa mwendo wa siku moja tu. Sasa wakati Sheikh Al-Mudhayif akitawala hapo Ubailah, kule Taif kulikuwako na Sharifu Abdul-Muin ambaye alikuwa ni mwakilishi wa ndugu yake Sharifu Ghalib. Barua ya wazi kwa Sharifu Abdul-Muin: Sheikh Al-Mudhayif alimtumia Sharifu Abdul-Muin waraka wa kumtaka ajiunge na genge la Mawahabi. Na wa kwanza kumtii katika makabila ni Taf-ha kisha Naf’a, wakafanya vita dhidi ya wale waliokataa Uwahabi kama kawaida yao. Na baadhi ya watu walitii baada ya mapigano kushtadi mno. Kisha akatoka (Al-Mudhayif) kwenda Al-Araj huko pia aliunguza majumba na kupora mifugo, lakini hawakumuweza Sharifu Abdul- Muin. Basi Sharifu Ghalib baada ya kupata habari hiyo, alikusanya jeshi linalokaribia watu elfu tatu 3,000 na akawaagiza kwenda Taif. Kuvunjika kwa mkataba wa amani baina ya Sharifu Ghalib na Abdul-Aziz kunatufundisha kuwa Mawahabi hawana mwamana hata kidogo, na dini yao ni dini ya vurugu. Kila mahala palipo na amani, muhubiri wa Kiwahabi atiapo mguu, basi huwa ndiyo mwisho wa 42

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 42

8/14/2017 1:18:25 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

amani katika eneo hilo. Tazama hali ya Afrika ya Kati kabla ya ujio wa Mawahabi, Afghanistan kabla ya Taleban na maeneo mengine mengi ya Dunia. Ndugu zangu hali si shwari nchini Nigeria. Watu wasio na hatia wanauawa, wasichana wanatekwa nyara, na kuozeshwa bila ridhaa yao, na wengine kati yao wakiwa na umri wa miaka tisa hadi kumi na mbili. Huo ni ubakaji mambo leo, na ni unyanyasaji wa hali ya juu zaidi na si unyama bali ni zaidi ya unyama. Jambo hilo ni kinyume na sharia na Mwenyezi Mungu alichukia. Mawahabi mnapata wapi maandiko? Yote hayo yanayofanywa na genge chinjachinja la Mawahabi wanaojiita Answar Sunah, hayapo kabisa katika mafundisho ya Dini yetu ya Kiislamu! Ndugu zangu hali si shwari chini Syria, Mawahabi wanaua watu kwa sababu tu, wana majina ambayo hayaendani na mitazamo yao ya Kiwahabi. Inafikia wakati mtu anaulizwa: Swala ya Asubuhi ina rakaa ngapi? Akishindwa kujibu basi huyo ni kafiri na damu yake ni halali. Huo ndio Uwahabi! Akili sifuri, jazba asilimia mia moja. Kwa ibara sahihi watu hawa hawana akili hata za kuazima. Kuua mtu asiye na hatia kwa kigezo cha kutofahamu idadi ya rakaa za Swala, si sahihi kwani wengine si Waislamu. Na hakuna mafundisho sahihi yanayoruhusu kuua watu kwa misingi hiyo isiyojali ubinadamu. Ndugu zangu hali si shwari ndani na nje ya Jiji la Dar es Salaam, vikundi vya Wahalifu wa Kiwahabi vinafanya uvamizi wa kuvamia misikiti katika maeneo mbalimbali hapa jijini. Watu wanajeruhiwa vibaya katika mashambulizi hayo ya kinyama na ya kikatili hadi kufikia hatua ya kulazwa mahospitalini. Na ukatili na ushenzi kama huo, Mawahabi wanauzingatia kuwa ni katika mafundisho ya dini. Na cha kumsikitisha na kumliza kila mwenye roho ya kibinadamu, ni pale uhalifu wa Kiwahabi unapofikishwa mbele ya vyombo vya usalama, halafu wahusika wanatoa tamko la kuunga mkono uhalifu, kwa kusema hayo ni mambo ya kidini! Ndugu zangu katika utu, hivi kweli mtu anauawa 43

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 43

8/14/2017 1:18:25 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

kikatili, au anajeruhiwa vibaya hadi anakaribia kupoteza maisha, halafu vyombo vya usalama vinasema hayo ni mambo ya kidini, hebu jiulize hawa watu wanaojibu majibu kama hayo, nadharia yao ni nadharia ya aina gani? Au tuseme kuwa watu hao wanaowapa nguvu wahalifu, hawajui maana ya dini? Nawaambia watu hao ya kuwa: Kama wanajua maana ya dini basi waache kuinasibisha dini na matendo ya kishenzi na yasiyojua thamani na heshima ya utu. Na kama hawajui maana ya dini basi nawapa muhtasari wa maana ya dini: Dini ni kanuni ya kiungu, ambayo ndani yake kunapatikana mfumo kamili wa maisha ya viumbe. Kwa hiyo Mwenyezi Mungu hajawahi kuufanya uhalifu kuwa ni mfumo kamili wa maisha ya viumbe. Bali Yeye Mwenyezi Mungu anaona kuwa uadilifu ndiyo mfumo sahihi na kamilifu wa maisha ya viumbe. Ili maisha ya viumbe yawe na amani, ni lazima uadilifu uwe ndiyo msingi wa maisha hayo, na uadilifu ukipatikana na amani pia hupatikana, kwani amani ni zao la uadilifu. Na uadilifu si suala linalonasibishwa na imani fulani, bali ni suala la kimaumbile, silika ya kila mwanadamu inapenda uadilifu na inachukia dhulma, na ndiyo maana tunaona mahakama hadi kwenye jamii zisizokuwa na dini, na lengo la kuanzishwa mahakama ni kuhakikisha kila mwenye haki anapewa haki yake. Sasa kama uadilifu ungekuwa na dini basi jamii zisizokuwa na dini zisingekuwa na haja ya mahakama. Sasa leo hii Mawahabi wanapovamia misikiti, wenye misikiti hiyo hawawezi kulikalia kimya suala hilo, bali ni lazima yaibuke mapambano kwa kuwa silika ya mwanadamu haikubali dhulma ya aina yoyote ile, iwe ya Kiwahabi au nyingineyo. Ndugu zangu katika utu, Mawahabi ni kikwazo sugu cha amani, na wao ndio uti wa mgongo wa kila uharibifu na kuvunjika kwa amani Duniani. Vita dhidi ya Uwahabi ni vita dhidi ya dhulma na kila mwanadamu mwenye kuichukia dhulma, ni wajibu wake pia kuwachukia 44

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 44

8/14/2017 1:18:25 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Mawahabi kwani watu hao si madhalimu tu, bali wao ndiyo dhulma yenyewe. Sasa kama wewe silika yako inaikubali dhulma, basi endelea kumkumbatia Muwahabi kama rafiki, lakini baadaye utalia na kusaga meno, kwani hata nyoka ngozi yake ni laini sana na nyororo, lakini ndani ana sumu kali iangamizayo‌na hapa sisemi kuwa Mawahabi wanasumu kama nyoka, bali nasema kuwa ni afadhali ya sumu ya nyoka kuliko ile ya Uwahabi, kwani sumu ya nyoka madhara yake ni ya kimwili tu, lakini sumu ya Uwahabi madhara yake ni ya kimwili na ya kiroho. Mpenzi msomaji, hayo yote tutayazungumzia tutakapoanza kuelezea itikadi potovu za Mawahabi, lakini kwa sasa bado tunazungumzia vita za Sharifu Ghalib na Mawahabi, na kuukamata kwao mji wa Makka, na pia matukio mbalimbali ya kikatili na yaliyo zaidi ya unyama waliyoyafanya katika sehemu mbalimbali na yale yanayoendelea kujiri hadi leo hii. Tukimaliza hili, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, tutazungumzia itikadi za Kiwahabi kwa mapana na marefu, na tutajibu hoja zao zote chakavu wanazozitegemea. Maharamia wa kiwahabi wauvamia mji wa Taif mwaka 1217 A.H. Katika somo lililopita tulizungumzia usaliti wa wazi uliyofanywa na Sheikh Al- Mudhayif, kutokana na uchu wake wa madaraka, na sasa tutaonesha jinsi alivyotaka kupanua mipaka ya utawala wake hadi kufikia mji wa Taif‌ Mnamo mwaka 1217 A.H, alitoka Sheikh Al-Mudhayif katika ngome yake akikusudia kwenda Taif kufanya mashambulizi, kama ilivyo desturi ya genge la uvamizi la Kiwahabi, lakini Sharifu Abdul-Muin alitoka kabla ya wanamgambo wa Kiwahabi hawajaingia Taif, na ndipo walipokutana katika bonde la Al-Araj, wakapigana hapo mchana kutwa, na Sharifu Abdul-Muin akashinda. Na watu 45

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 45

8/14/2017 1:18:25 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

wapatao sitini (60) katika jeshi la Sheikh Al-Mudhayif (Wahhabi) waliuawa. Na lau si kujingika na mlima, basi wote wangeteketea na asingelibakia hai yeyote kati yao. Baada ya kibarua hicho cha kutwa nzima, Sharifu Abdul-Muin akajikusanyia ngawira na kurejea mjini kwake Taif, na katika jeshi lake waliuawa askari kumi na tatu (13). Kisha akatoka Sharifu Ghalib mwenyewe kuelekea Ubailah. Bahati nzuri alikutana na ndugu yake Sharifu Abdul-Muin, basi wakaizunguka ngome (ngome hii ilikuwa mlimani) na kuishambulia lakini hawakufanikisha. Walirejea Taif, kisha wakarejea tena kwa mara ya pili, lakini hawakuruhusiwa kuingia, kwa hiyo wakarejea tena Taif. Kisha akatoka Sheikh Al-Mudhayif na waliokuwa pamoja naye kuelekea Taif. Wakauzingira mji wa Taif na Kiongozi au mtawala wa mji wa Bishah, Salim bin Shakban, akamtumia msaada wa kijeshi. Kundi kubwa la wanamgambo wa Kiwahabi likawasili kutoka mji wa Bishah, na mapigano yakashtadi hapo mchana kutwa, na jioni wote waliiacha ngome ya mji wa Taif na kurudi nyuma. Ilipofikia asubuhi ya siku iliyofuata, walirudi tena na wakapigana mchana kutwa, na jioni walirudi kwenye mahema yao baada ya kuwa wengi wao wameuawa. Na usiku ule Waarabu waliokuwa na Sharif Abdul-Muin walitawanyika na kumwacha Sharifu. Naye Sharif alitafuta mbinu za kuwafanya wabakie lakini walikataa na kutawanyiaka, pakatokea pengo katika ngome, na Masharifu wengine wakaondoka na kurejea Makka. Na hata ilipokuwa asubuhi ya siku ya pili, Sharifu alipata habari ya kuwa Sheikh Al-Mudhayif na Ibn Shakban pamoja na jeshi lao wanataka kuelekea Makka. Pale pale Sharifu alifanya utafiti ili kuhakiki usahihi wa habari hiyo, na alipopata usahihi wake, aliandaa wanajeshi wake na kuwataka wawe imara katika mapigano. Kisha yeye akaelekea Makka ili kupambana na jeshi la wanamgambo katili wa Kiwahabi, lakini huku nyuma nguvu ya jeshi haikuwa ya kutosha 46

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 46

8/14/2017 1:18:25 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

kwa hiyo watu waliobaki Taif wakawa wameshindwa kuwazuia maharamia wa Kiwahabi. Maharamia wa kiwahabi waingia Taif kwa mabavu: Mwezi wa mfunguo pili mwaka 1217 Maharamia wa Kiwahabi waliingia Taif kwa mabavu, wakafanya humo mauaji ya kimbari.Watu hao wasio na huruma katika nyoyo zao, waliwachinja watoto wachanga vifuani mwa mama zao. Na baadhi ya watu wa mji huo walikuwa tayari wamekwisha kimbia, lakini msafara wa Maharamia wa Kiwahabi uliwakuta njiani, basi wakawaua mauaji ya kinyama bali zaidi ya unyama, kisha wakamsaka kila aliyejificha ndani naye pia akauawa. Mauji hayakukomea hapo, bali waliingia mpaka misikitini wakaua watu wakiwa katika Swala, Sub-hanallah! Ushenzi ulioje! Damu ikatapakaa katika mji wa Taif, na wakawa Waarabu wanaingia Taif kila siku ili kujikusanyia mali za marehemu waliokufa kwa upanga wa Kiwahabi. Mali hizo zilikuwa zikipelekwa nje ya mji wa Taif, zilirundikwa hadi zikawa kama mlima. Baada ya kumaliza kukusanya, walitoa moja ya tano ya mali hizo kuwa ni fungu la Mfalme, na zilizosalia waligawana wenyewe (askari), kisha wakachukua misahafu na vitabu vinginevyo vya dini, wakavisambaza hovyo hovyo mitaani. Na walipopata habari kuwa kuna mali zingine zimezikwa ardhini, walifukua sehemu hiyo, na baada ya kukuta mali katika eneo hilo, basi walianza kufukua kila sehemu, na katika kila nyumba. Wakafukuwa hadi vyoo pamoja na makaro. Mawahabi waukamata mji wa Makka mwaka – 1218 A.H. Mwishoni mwa mwaka 1217 maharamia wa Kiwahabi waliazimia kuuteka mji wa Makka na kuuweka chini ya himaya yao, basi wakaandaa jeshi kubwa katika kufanikisha uvamizi huo haramu. Habari zikaenea katika anga la Makka na ikawafikia watu nao wakiwa katika msimu wa ibada ya Hijja. 47

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 47

8/14/2017 1:18:25 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Na katika mahujaji waliohudhuria katika Hijja ya mwaka huo ni Imamu wa Mascut: Sultan bin Said na mawaziri wake, na viongozi wa mahujaji wa Sham (Syria) na Misri, na wengineo, basi Sharifu Ghalib kiongozi wa Makka akawaomba msaada, nao wakamkatalia. Sharifu akatoa kwao wito wa kupigana jihadi na Mawahabi mara tu, baada ya kumaliza ibada ya Hijja, lakini Waarabu hao hawakuujali wito wa Sharifu, bali waliupuuza na kutoa visingizio visivyoeleweka. Sharifu alijaribu kuwakinaisha lakini hakupata sikio lililomsikiliza, na ndipo ilipomlazimu Sharif Ghalib kuondoka Makka akiongozana na wafuasi wake. Na wengi kati ya wakazi wa mji wa Makka waliondoka naye kuelekea katika mji wa Jidah kwa sababu za kiusalama. Hiyo ndiyo dini ya Kiwahabi! Sharifu anatolewa katika mji wa babu yake bwana Mtume 8 kwa dhulma ya wazi wazi. Na tarehe kumi ya mwezi wa mfunguo nne, Saudi bin AbdulAziz yeye na jeshi lake, waliwafikia Masharifu wa Makka bila vita, na akawafanyia watu wa Makka, kama yale ambayo wanajeshi wake waliwafanyia watu wa mji wa Taif. Na pia Saudi akawalazimisha watu wa Makka kufuata fikra za Sheikh wake Muhammad bin AbdulWahhab, na akalazimisha vitabu vya Muhmmad bin Abdul-Wahhab vifundishwe mashuleni. Aidha akawasitishia Waislam ibada ya Hijja na akavunja mahusiano ya kibiashara na ya kijamii yaliyokuwepo baina ya watu wa Makka na Madina. Na baada ya Mawahabi kuuteka mji wa Makka, walifika Mawahabi wengi kutoka Najdi, wakaingia Makka ili kutekeleza mipango yao iliyokuwa imekwisha kupangwa tokea awali, yakuwa tukiukamata mji wa Makka, basi kazi ya kwanza ni kuvunja na kufutilia mbali historia na kumbukumbu za Uislamu. Kwa hiyo wakalitekeleza hilo kwa vitendo pale walipovunja nyumba aliyozaliwa ndani yake Bwana Mtume Muhammad 8 na Quba ya Bibi Khadija, na ile ya Zamzam. Ndugu zangu katika utu hazikupita siku tatu, kumbu48

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 48

8/14/2017 1:18:25 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

kumbu zote za awali za Uislamu, zilikuwa zimekwisha kutokomezwa zikiwemo na zile za waja wema wa Mwenyezi Mungu. Maharamia wa kiwahabi watimuliwa Makka: Baada ya Sharifu kuona ya kuwa hali si shwari, hapo mjini Makka, aliamua kwenda Jidah kama tulivyosema hapo awali, ili kujipanga sawa sawa. Na katika kipindi cha kutokuwepo Sharifu, Mawahabi walikithirisha ufisadi katika mji mtakatifu wa Makka, hali ambayo ilimtia sana uchungu Sharifu na kumfanya aazimie kurudi haraka sana iwezekanavyo, ili kuusafisha tena mji wa Makka na kuurejeshea tena hadhi na heshima yake. Sharifu aliondoka Jidah akiwa na Amir (kiongozi) wa Jidah, pamoja na askari wengi, basi wakafanikiwa kuusafisha mji na kutokomeza imani taka za Kiwahabi zilizokuwa zimekithiri mjini humo. Kisha Sharifu akaanza kuyapiga makabila yaliyo jirani na Makka makabila ambayo yalikuwa yamejiunga na dini ya Uwahhabi Lengo la Sharifu lilikuwa ni kuutokomeza ufisadi na uharibifu wa Kiwahabi. Na machafuko yote hayo pamoja na vita alizopigana Sharifu zilikuwa zimelenga fitina na uharibifu, na uporaji na kuchafua matukufu ya dini ya Mwenyezi Mungu. Hiyo tu ndiyo ilikuwa azma ya Abdul-Aziz bin Saud. Na baada ya kifo chake, azma hiyo iliendelezwa na mtoto wake Saud bin Abdul-Aziz. Utawala wa Abdul-Aziz bin Muhammad ulianza baaada ya kifo cha baba yake Muhammad bin Saud mwaka 1179 na kuishia mwaka 1218. Historia yatwambia kuwa (1218) miaka miwili baada ya mauaji ya kinyama ya Kiwahabi yaliyofanyika mjini Karbala, bwana mmoja alikuja Dir’iyyah katika vazi la kidaruweshi, ili kulipiza kisasi kutokana na kuuliwa kikatili familia yake yote kwa jumla katika vita vya uvamizi vilivyoanzishwa na Abdul-Aziz. Bwana huyo baada ya kuwasili Dir’iyyah, alibaki hapo siku za kutosha huku akiswali ny49

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 49

8/14/2017 1:18:25 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

uma ya Abdul-Aziz kama muumini wa kweli wa Kiwahabi, na siku mazingira yalipomruhusu, ndipo alipomrukia Abdul-Aziz naye akiwa kwenye Swala. Akamshindilia kisu mgongoni na kutokezea tumboni. Abdul-Aziz alikufa papo hapo na huo ndio ulikuwa mwisho mbaya wa maisha yake ya kikatili na ya kinyama bali zaidi ya unyama. Naam, kifo hicho kwake kilikuwa ni sawa tu kwani hata yeye aliua watu katika mji wa Taif wakiwa msikitini wanaswali. Baada ya kuuawa Wahhabi huyo (Abdul-Aziz) watu walimkusanyikia yule muuaji na wakamuua. Mpenzi msomaji huu ulikuwa ni muhtasari wa vita za uchokozi na uvamizi za Kiwahabi. Vita na matukio ya fedheha ya Kiwahabi havielezeki ndani ya miaka mitano au kumi, kwani matukio ya fedheha ya Kiwahabi ni matukio endelevu, na Sheikh Dahlan katika kitabu chake anasema kuwa: “Sharif Ghalib alipambana na Mawahabi vita hamsini takriban, na sehemu kubwa ya vita hizo zilifanyika wakati wa utawala wa Abdul-Azizi bin Muhammad bin Saud.� Mwenye kuzitaka habari hizo kwa kina arejee vitabu: Khulasatul-kalaam fi umarail-baladil-haram na Kashful-irtiyab cha Sayyid Muhsin alAmin. Sayyid huyu ametaja sehemu kubwa ya vita hizo kwa mapana zaidi. Naamini kuwa msomaji aliyefuatilia vizuri mtiririko wa historia hii, atakuwa amefahamu vizuri kuwa Mawahabi ndio chanzo kikuu bali ndiyo uti wa mgongo wa machafuko ulimwenguni kote.

50

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 50

8/14/2017 1:18:25 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

SEHEMU YA PILI UKAFIRI WA MAWAHABI NYUMA YA MGONGO WA TAUHIDI

K

atika masomo yaliyopita tulisema kuwa: Ujinga uliyokuwa umetawala katika jamii ya watu wa Najdi, na kuwa kwao mbali na mafundisho sahihi ya dini ya Mwenyezi Mungu, ulikuwa ni moja ya sababu zilizochangia kupotosha watu. Kama mnavyoelewa kuwa siku zote wajinga ni sawa na ardhi yenye rutuba inayompa mkulima fursa ya kuotesha mmea autakao, kwa mantiki hiyo Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahab alitumia fursa hiyo katika kufanikisha zoezi lake na azma yake ya kuupotosha umma. Mwalimu Sheikh Ja’far Subhani ameandika katika kitabu chake kuwa: “Hakika nadharia yoyote mpya inapoibuka kwa jina la tauhidi na mabadiliko, ni rahisi mno kupenya na kuingia katika nyoyo za watu. Hasa pale nadharia hiyo inapoelezwa mbele ya watu wasio na maarifa, (na hiyo ndiyo njia aliyoitumia Muhammad Bin AbdulWahab).” Nadhani utakuwa na kumbukumbu kuwa toka Uwahabi uingie Afrika Mashariki hadi leo hii, Mawahabi hawana wanachokihubiri zaidi ya maneno matatu, tauhidi, shirki, Bidaa. Na kwa maneno hayo matatu na kwa ufahamu wao mdogo wamewatoa watu katika mstari mnyoofu. Nasi kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, tutazielezea mada zote hizo kwa usahihi zaidi ikiwa ni pamoja na kuvunja hoja zao chakavu wanazozitegemea, inshaa Allah. Mwenyezi Mungu anasema katika Qur’ani: 51

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 51

8/14/2017 1:18:25 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

“Na kwa hakika tulimtuma Mtume kwa kila uma kwamba mwabuduni Mwenyezi Mungu na mumwepuke taghuti..� (16:36).

Ni ukweli usiopingika kuwa Aya hii na nyinginezo mfano wake, ni ushahidi wa wazi kuwa: Tauhidi katika ibada ndiyo nukta kuu inayowaunganisha Manabii wote wa Mwenyezi Mungu, na kwamba hakuna Nabii aliyekuja bila ya ujumbe huo. Ibada ya kumwabudu Mwenyezi Mungu peke Yake pasina kumfanyia mshirika, na kukataa miungu yote ya batili, ndiyo fikra ya Manabii na Mitume, na ndiyo uti wa mgongo wa mafundisho yote waliyokuja nayo,pia ni uti wa mgongo wa fikra zao na mitazamo yao, na ndio maana twapata kuona kuwa dini zote zilizotangulia ziliiwekea tauhidi katika ibada msisitizo mkali, na kuiweka mbele katika orodha ya mafundisho yake. Kwa hakika nguzo hii muhimu tauhidi katika ibada, licha ya kuwa kadri siku zinavyopita katika historia ya maisha ya mwanadamu, na watu kutoka katika mstari mnyoofu na wengi kuabudu wanadamu wenzeo, badala ya Mwenyezi Mungu mmoja na wa pekee, lakini bado tunaikuta nguzo hii bado imethibiti katika nyoyo na akili za watu wenye dhamira safi na akili zenye nuru. Wao wanazingatia kuwa sheria zote zilizokuja na Manabii waliotangulia, ni sheria ambazo misingi yake ni tauhidi ya kumwabudu Mwezi Mungu, na kwamba tauhidi katika ibada ni nguzo pekee inayowaunganisha watu wa dini zote za tauhidi. Na kwa mantiki hiyo tunakuta Qur’ani katika mjadala na Mayahudi na Manaswara, inatilia sana msisitizo katika nguzo hii inayochangiwa na dini hizo na kuwahimiza warejee katika asili ya imani zao ambazo wamezitelekeza:

52

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 52

8/14/2017 1:18:25 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

“Sema: Enyi watu wa Kitabu! Njooni kwenye neno la usawa baina yetu na baina yenu. Kwamba tusimwabudu yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu, wala tusimshirikishe na chochote; wala baadhi yetu wasiwafanye baadhi kuwa waungu zaidi ya Mwenyezi Mungu. Wakikataa. Semeni: Shuhudieni kuwa sisi ni Waislamu.” (Al-Imraan; 3:64).

AINA ZA TAUHIDI: Hakika tauhidi ina ngazi na daraja, ambazo wamezifafanua wasomi wa Kiislam katika vitabu vyao vya tafsiri na vile vya kitheolojia, na kwamba tauhidi katika ibada inadhihiri kama moja ya matawi hayo mengi ya tauhidi. Hapa kwa bahati mbaya hatutaweza kuorodhesha vipengele vyote vya Tauhidi bali tutataja baadhi kama ifuatavyo: Tauhidi katika Dhati ya Mwenyezi Mungu: Maudhui inayozungumziwa katika aina hii ya tauhidi ni kuthibitisha kuwa Mwenyezi Mungu hana mfano na wala hafanani na chochote, kama vile tusemavyo: Juma ni kama Ali, yaani katika ubinadamu. Sasa Yeye Mwenyezi Mungu hafananishwi namna hiyo, bali Yeye ni wa pekee asiye na mfano. Qur’ani inasema:

53

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 53

8/14/2017 1:18:25 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

“Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa pekee. Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kukusudiwa kwa haja. Hakuzaa wala hakuzaliwa. Wala hana anayefanana naye hata mmoja.”17

Vyanzo vya maarifa: Swali liumizalo kichwa ni kutaka kujua kama Mwenyezi Mungu yupo ni kwa nini haonekani? Awali ya yote tungependa kuwajulisheni kuwa njia za maarifa/kujua kitu ni tatu. 1.

Njia tano za fahamu:

Kuona – kusikia – kunusa – kugusa – kuonja: Mwanadamu alizaliwa hali ya kuwa hajui kitu lakini alikuwa na mtaji wa kutafutia maarifa, nao ni hizo njia tano za ufahamu. Kwa njia ya macho aliweza kuona maumbile mbalimbali na kutofautisha kati ya rangi hii na ile. Na kwa njia ya kugusa mwanadamu aliweza kutofautisha kati ya joto na baridi ugumu na ulaini, na kwa njia ya kuonja aliweza kujua ladha tamu na chungu, chachu na nyinginezo, na kwa njia ya kusikia aliweza kutofautisha kati ya sauti za wanyama na zile za wanadamu, za kike na za kiume na kadhalika. Mpenzi msomaji, mwenye kumiliki njia zote hizo atakuwa na uwezo wa kujua vitu vyote vinavyopatikana kwa kupitia njia hizo. Na mwenye kupungukiwa na moja ya njia hizo basi atayakosa yale yote yanayopatikana kwa kupitia njia hiyo. Kwa mfano, mtu aliyezaliwa hali ya kuwa ni kipofu bila shaka mtu huyo hata umfafan17

Surat Ikhlas; 112:1-4 54

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 54

8/14/2017 1:18:25 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

ulie namna gani hawezi kufahamu muonekano wa rangi yoyote ile, hata ukimtajia mifano elfu kumi itakuwa ni kazi bure. Njia hizo tano ni moja kati ya vyanzo vya maarifa, lakini hazina uwezo wa kumuwezesha mwanadamu kujua kila kitu, bali njia hizo humsaidia mwanadamu kujua vitu vya kimaada tu. Lakini kuna mambo mengine yako nje ya njia hizo tano za fahamu, kwa hiyo tusiutilie shaka uwepo wa Mwenyezi Mungu kwa hoja ya kuwa Mwenyezi Mungu haonekani, mbona tunakubali kuwa akili zipo na hali ya kuwa hatuzioni? Je, waamini kuwa akili zipo? Sisi hatuna shaka kuwa unaamini juu ya uwepo wa akili. Lakini kabla ya kuendelea na somo letu, tunaomba kwanza tukusimulie kisa kizuri kilichojiri baina ya mwanafunzi na mwalimu wake, na tunaamini kuwa utapenda kukisikiliza. Siku moja mwalimu aliingia darasani na kuwafundisha wanafunzi wake kuwa: Kila kilichopo ni lazima kionekane, basi mwalimu yule akaanza kufafanua kauli yake kwa mifano, akasema: Je, huu ubao mnauona? Wanafunzi wakasema: Ndiyo, mwalimu akasema ni kwa sababu upo ndio maana mnauona. Akauliza tena: Je, Mimi mnaniona? Wakasema: Ndiyo. Mwalimu akasema ni kwa sababu nipo ndio maana mnaniona. Lakini Mungu hayupo na ndio maana hatumuoni. Basi mmoja wa wanafunzi wale, akanyoosha mkono akamuomba mwalimu ruhusa ya kusimama mbele ili wanafunzi wote waweze kumuona. Mwalimu bila kipingamizi akamruhusu, na mwanafunzi yule akasimama mbele ubaoni na kuanza kuwauliza wanafunzi wenzake: Watoto wenzangu je, Mimi mnaniona? Wote wakaitikia ndiyo, naye akasema ni kwa sababu nipo ndio maana mnaniona. Je mwalimu wetu mnamuona? Wote wakaitikia ndiyo, akasema ni kwa sababu mwalimu wetu yupo ndio maana mnamuona. Je akili za mwalimu wetu mnaziona wote wakasema: Hapana. Basi mtoto yule 55

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 55

8/14/2017 1:18:25 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

akasema: Ni kwa sababu mwalimu wetu hana akili kichwani ndio maana hatuzioni. Mwalimu alipatwa na hasira na kuona kuwa mtoto kamvunjia heshima, lakini mtoto hakuwa na kosa kwa kuwa hivyo ndivyo mwalimu alivyowafundisha, ya kwamba kila kilichopo ni lazima tukione, na tusichokiona basi hakipo. Nadharia ambayo si sahihi kabisa. Na hapo ndipo mwalimu alipobadilisha mtazamo wake na kusema kuwa: chenye kuonekana kipo, lakini siyo kila kilichopo kinaonekana. Baada ya kisa hicho cha kusisimua, sasa turudi tena kwenye somo letu. Ndugu wapendwa tunapomkosa Mwenyezi Mungu kwa kutumia njia tano za ufahamu, basi tusiseme kuwa hayupo bali tujaribu kumtafuta kwa kutumia njia nyingine, ambayo ni njia ya pili: 2.

Akili:

Kazi kuu ya akili ni kujenga hoja na kuthibitisha uwepo wa kile unachokitaka. Kwa mfano, mnapoangalia jengo la shule, swali la kwanza ni kutaka kumjua mjenzi. Na hiyo ni baada ya akili kujenga hoja ya kwamba shule haiwezi kujijenga yenyewe katika uwenyewe wake. Na kwa msingi huo akili inahukumu kuwa ulimwengu hauwezi kujiumba wenyewe bali ni lazima awepo fundi mweye ujuzi wa hali ya juu kuliko mafundi wote. Sasa njia hii hutumika kwa ajili ya kutufahamisha yale tusiyoweza kuyafahamu kwa kutumia njia ya kwanza, na mfano hai ni akili, ipo lakini tumeshindwa kuifahamu kwa kutumia njia ya kuona, kusikia, kunusa, kugusa na kuonja. 3.

Moyo:

Wasomaji wapendwa tunaposema moyo hatukusudii moyo ule unaofanya kazi ya kusukuma damu katika mwili wa mwanadamu, bali tunakusudia moyo kwa maana ya kituo cha hisia ambazo hazitam56

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 56

8/14/2017 1:18:25 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

buliki kwa kutumia njia ya kwanza wala ya pili. Njia hii ya tatu ni ngumu kwa kuwa inakuthibitishia uwepo wa Mwenyezi Mungu bila kutaka ushahidi, kama vile ambavyo mtu anajithibitishia uwepo wake mwenyewe bila ya dalili na ushahidi wa kumfanya ahisi kuwa yupo. Kwa hiyo kwa kadiri ambavyo mwanadamu anahisi uwepo wake, hivyo hivyo anahisi uwepo wa Mwenyezi Mungu. Kwa kadiri ambavyo mwanadamu anahisi upendo wa wazazi juu yake, hivyo hivyo anahisi upendo wa Mwenyezi Mungu juu yake. Watu waliokomaa kiimani humfahamu Mwenyezi Mungu kwa kupitia njia hii ya tatu, lakini walio wengi hutumia njia ya pili ambayo ni njia ya ujengaji hoja za akili kama tulivyofafanua. Hitimisho: Tunazo njia mbalimbali za kuthibitisha uwepo wa Mwenyezi Mungu, na njia hii ya tatu Mwenyezi Mungu ameizungumzia katika Qur’ani pale aliposema kuwa macho hayana upofu bali upofu ni wa nyoyo zilizoko vifuani. Na kwa mantiki hiyo sisi hatuna uwezo wa kumfanya Muwahabi amuone Mungu, kwa sababu sisi nyoyo zetu zinaona na za kiwahabi zina upofu, na mwenye macho hawezi kumuonesha kitu asiyekuwa na macho hata kama atamtajia mifano elfu kumi. Je, Mwenyezi Mungu ni chanzo au matokeo? Swali lingine liumizalo kichwa cha mwanafalsafa ni kutaka kujua je, nikionacho mbele ya macho yangu ninakiona katika uhalisia wake, au ni kitu cha kufikirika tu? Na kama kipo katika uhalisia wake je, kitakuwa ni chanzo au matokeo? Na kama ni matokeo chanzo chake ni nini? Na je, chanzo hicho ndicho chanzo kikuu au kuna chanzo kingine nyuma yake? Kwa Kiswahili chepesi, mwanafalsafa anataka kujua kwamba je, huyu mtu aliyesimama mbele yangu ni mtu kweli au ninaota tu? 57

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 57

8/14/2017 1:18:25 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Na kama ni mtu kweli je, kajileta mwenyewe katika uwepo huu au ameumbwa? Na kama ameumbwa je, huyo aliyemuumba, Yeye ndiye muumba mkuu au kuna muumba mwingine nyuma yake? Sasa tukianza kufuatilia mlolongo wa mwanadamu huyu tunayemwona mbele yetu, ni lazima tutaishia kwa Adam D. Na Adam tutakuta kuwa naye pia si chanzo kikuu cha uwepo wa mwanadamu huyo kwani na yeye pia ameumbwa. Je, aliyemuumba Adamu yeye kaumbwa na nani? Hapa kuna njia mbili za kujibu swali hilo. 1. Ni kufuatilia mlolongo wa mwanadamu, mpaka mwisho wake ambapo tunakuta chanzo ni Adam, kisha tunahoji Adam uwepo huu kautoa wapi? Tunapata jibu kuwa kapewa na Mungu. Kisha tunahoji Mungu kautoa wapi uwepo huo aliompa Adam? Hapo tutapata jibu kuwa uwepo ni asili yake, na asili huwa haitafutiwi sababu. Kwa mfano unapouliza kwa nini chai ni tamu? Jibu ni kwa sababu ina sukari, na kwa kuwa sukari asili yake ni utamu, basi hapo tunabakia bila swali, yaani hatuulizi tena kwa nini sukari ni tamu? 2. Njia nyingine ya kujibu swali hilo tunasema kuwa Mungu Naye ameumbwa na Mungu mwingine, kisha tunaanza mlolongo usio na mwisho, na hapo unatakiwa uiache akili yako huru itembee, kwa hiyo utasema: Mungu kaumbwa na Mungu mwingine na huyo mwingine kaumbwa na mwingine na huyo mwingine kaumbwa na mwingine. Utaendelea hivyo mpaka hapo itakapochokea akili yako na kuona ulazima wa kusitisha zoezi hilo. Kwa hiyo ukifikia hatua ya kuona hapa nilipofikia panatosha na huyu ndiye wa mwisho na hakutanguliwa na yeyote, basi huyo asiyetanguliwa na uwepo ndiyo Mungu, na wale wengine wote 58

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 58

8/14/2017 1:18:26 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

si miungu kwa sababu wameumbwa na kumiminiwa uwepo na huyo Mungu mwenye uwepo wa asili.

2 - TAUHIDI KATIKA UUMBAJI: Maudhuu inayozungumziwa katika aina hii ya Tauhidi ni kuthibitisha kwamba hakuna juu ya ardhi hii muumba mwingine na chanzo cha asili tofauti na Mwenyezi Mungu, lakini kuna vyanzo na sababu zingine za kimaumbile ambazo matokeo ya kazi zake huwa ni kwa idhini na baraka za Mwenyezi Mungu ambaye ndiye chanzo cha asili cha matokeo yote. Kwa mfano Bwana Masihi (Yesu) aliposema: Nitawafanyia kama namna ya ndege katika udongo; kisha nimpulizie awe ndege kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.18 Uumbaji huu wa Bwana Masihi (Yesu) ulikuwa ni kwa idhini na Baraka ya kutoka kwa Mwenyezi Mungu na wala si kwa uwezo wake Bwana Masihi (Yesu). Halikadhalika wewe na mimi tunapootesha mti, sisi tunakuwa ndiyo chanzo cha kupatikana kwa mti ule lakini si kwa uwezo wetu bali ni kwa baraka kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa kuwa Yeye pekee ndiye chanzo cha asili cha matokeo yote duniani.

Sema: Mwenyezi Mungu ndiye Muumba wa kila kitu na Yeye ni Mmoja, Mwenye kushinda. 19

Sasa hapa kwa ufahamu wa Mawahabi, mtu akiiba halafu akacharangwa mapanga hadi akafa wao husema: Ni mipango ya 18 19

  Surat al-Imran; 3:49   Surat Raad; 13:16 59

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 59

8/14/2017 1:18:26 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Mungu, kwa kuwa Mungu ndiye chanzo cha kila kitu duniani. Hebu tujadili madai hayo ya Kiwahabi kiakili. Mtu akimchoma mtu kisu basi yule mchomaji hupelekwa mbele ya sheria akiwa peke yake, wakati yeye hajatengeneza kisu. Kwa hiyo ilitakiwa akamatwe yeye pamoja na muuza visu, pamoja na kiwanda kilichotengeneza, pamoja na mchimbaji wa madini yaliyozaa kisu hicho. Wote hao wawajibishwe. Lakini mbona huwa hawawajibishwi? Wakati wao ndiyo wamesababisha kosa hilo la jinai? Jibu: Mwenye madini hajamuuzia mwenye kiwanda madini kwa sharti atengeneze kisu cha kuulia watu. Na mwenye kiwanda naye hakutengeza kisu kwa ajili ya mauaji, sasa wote hao kesi ya mauaji haiwahusu kwa kuwa muuaji ameua mwenyewe kwa akili yake na utashi wake. Na hivyo hivyo, Mwenyezi Mungu ni chanzo cha kila kitu kwa ajili ya matumizi mema, sasa wewe ukifanya shari, basi huo ni mzigo wako, kwani umetenda mwenyewe kwa akili yako na kwa hiari yako. Kwa hiyo hoja za Mawahabi, hazina mashiko sahihi na zinamchekesha kila mwenye akili timamu. Uwahabi ni dini inayowalenga watu wasio na maarifa ya dini, na hakuna hata siku moja ambayo Uwahabi umewahi kutangazwa mbele za wasomi, bali ni dini inayotangazwa mahala ambapo hakuna wasomi. Kwa ibara nyingine, Uwahabi hunadiwa kwa siri tena vichochoroni.

3 – TAUHIDI KATIKA MALEZI NA ­UENDESHAJI WA ULIMWENGU Maudhuu kuu ya aina hii ya tauhidi ni kuthibitisha kuwa hakuna mlezi na muendeshaji wa asili wa dunia na vilivyomo ndani yake isipokuwa Mwenyezi Mungu (swt) peke Yake, na hana mshirika katika hilo. Ama uendeshaji wa mambo unaofanywa na malaika, 60

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 60

8/14/2017 1:18:26 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

kadhalika na vyanzo vingine vya kimaumbile, ni kama tulivyosema hapo awali kuwa ni kwa amri ya Mwenyezi Mwenyezi Mungu:

“Hakika Mola Wenu ni Mwenyezi Mungu ambaye ameumba mbingu na ardhi katika siku sita, kisha akatawala kwenye Arshi. Yeye hutengeneza mambo. Hakuna mwombezi ila baada ya idhini Yake. Huyo ndiye Mwenyezi Mungu Mola Wenu, basi mwabuduni. Je hamkumbuki?”20

Sema: Atawafisha malaika wa mauti aliyewakilishwa kwenu; kisha mtarejeshwa kwa Mola Wenu.21

Aya hizi na nyinginezo nyingi za mfano wake, utendaji wa malaika unaodhihirika hapo, si wa malaika, wao wenyewe katika uwenyewe wao, bali ni kwa amri ya Mwenyezi Mungu. Na pia tukizichunguza kwa makini aya za Qur’ani, na tukavitupia macho vitabu vya theolojia, bila shaka tutafahamu wazi ya kwamba: Watu waliotangulia walikuwa wakiamini ile aina ya pili ya tauhidi (tauhidi katika uumbaji) bila ya kuhitilafiana. Tauhidi katika uendeshaji wa mambo na tauhidi katika ibada, aina hizi za tauhidi ndizo zilizowatofautisha, na hatimaye kila mmo20 21

Surat Yunus; 10:3   Surat Sajda; 32:11 61

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 61

8/14/2017 1:18:26 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

ja kushika muelekeo wake. Kwa maelezo ya wazi tunasema kuwa: Watu wengi waliamini juu ya uwepo wa Muumba mmoja wa hii Dunia, na Qur’ani imelizungumzia swala hilo zaidi ya mara moja, nasi tunakutajia baadhi tu ya Aya hizo:

“Na ukiwauliza ni nani aliyeumba mbingu na ardhi na akalitiisha jua na mwezi, bila shaka watasema ni Mwenyezi Mungu ..…”22

“Na ukiwauliza ni nani aliyeumba mbingu na ardhi na akalitiisha jua na mwezi? Bila ya shaka watasema ni Mwenyezi Mungu. Sema: Alhamdulillah. Bali wengi wao hawafahamu.”23

“Na ukiwauliza: Ni nani aliyeumba mbingu na ardhi? Bila shaka watasema: Mwenyezi Mungu. Sema: Je Mnawaonaje wale mnaowaomba badala ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu akitaka kunidhuru, wao wanaweza kuniondelea dhara Yake .….?”24   Surat Ankabut: 61   Surat Lukman: 25 24   Surat Zumar: 38 22 23

62

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 62

8/14/2017 1:18:26 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Kwa mujibu wa muongozo wa Aya hizo na nyinginezo ambazo hatukuzitaja, tumeona waziwazi namna ambavyo watu walivyokuwa wakiishi na imani juu ya muumba mmoja, lakini tofauti ni katika ibada (tauhidi katika ibada) kuainisha ni nani anayestahiki kuabudiwa, na pia katika kuainisha muendeshaji mkuu wa mambo yote ya dunia. Aya zimeweka wazi kwamba washirikina wa Kiarabu walioishi kabla na baada ya Qur’ani, wote waliamini uwepo wa muumba mmoja, tena bila ya kuwa na shaka katika hilo, licha ya kwamba imani yao hiyo haikuwa imefikia katika viwango vya tauhidi vilivyofafanuliwa katika Qur’ani. Lakini japo kwa uchache walikiri kuwa mbingu na ardhi na jua na mwezi vyote vimeumbwa na Mwenyezi Mungu, isipokuwa baadhi yao na si wote, waliamini kwamba Mwenyezi Mungu baada ya kuumba, alijivua jukumu la uendeshaji na ulezi na kulitelekeza mikononi mwa walezi wengine na watendaji wengi au mmoja, na viumbe hao waliotelekezewa majuku kwa mtazamo wao ni malaika, majini, sayari, na roho zilizotakasika. Kwa hiyo kila kimoja kati ya hivyo kilikuwa na mamlaka katika upande fulani wa dunia. Hayo ndiyo yalikuwa madai ya watu wa nadharia hiyo. Lakini watu hao hao pamoja na imani zao hizo, hawakuwa na imani juu ya uungu wa malaika na majini au jua, mwezi na vinginevyo. Bali waliamini kuwa vitu vyote hivyo ni nyenzo za kuwaweka karibu zaidi na Mwenyezi Mungu, kwa kuwa walikuwa wakiabudu jua kwa hoja ya kwamba jua ni mola mlezi na si kwa hoja ya kwamba jua ni Mola muumba. Kwa hiyo waliamini kwamba Mwenyezi Mungu hana mamlaka yoyote katika ulimwengu huu wa kimaunzi. Na kwa sababu hiyo Nabii Ibrahimu D alikuja kubatilisha itikadi hiyo ya kuamini kuwa jua ni mungu mlezi, kwa hoja nyepesi ambazo hazihitajii akili nyingi bali zahitajia akili kidogo tu japo 63

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 63

8/14/2017 1:18:26 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

ile ya kuvukia barabara, na tena kwa njia nzuri ya adabu na si ya jazba:

“Na Ibrahim alipomwambia baba yake Azar: Unawafanya masanamu kuwa waungu? Hakika ninakuona wewe na watu wako mko katika upotofu uliyo wazi.”25

“Na namna hii tukamuonesha Ibrahim ufalme wa mbingu na ardhi ili awe katika wenye yakini.

Na usiku ulipomwingilia, akaona nyota, alisema: Hii ni Mola wangu. Ilipotua akasema: Sipendi wanaotua.

Na alipouona mwezi unachomoza alisema: Huu ni Mola wangu. Ulipotua alisema: Asiponiongoza Mola Wangu, hakika nitakuwa katika watu waliopotea.

25

Surat An’am; 6:74 - 79 64

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 64

8/14/2017 1:18:26 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Na alipoliona jua linachomoza alisema: Hili ndilo Mola wangu. Hili ni kubwa kabisa. Lilipotua alisema: Enyi watu! Mimi simo katika hayo mnayoyashirikisha.

Hakika Mimi nimeuelekeza uso wangu kwa yule aliyeziumba mbingu na ardhi. Hali ya kuwa nimeacha dini za upotevu, tena mimi si katika washirikina.�

Sasa hebu tutazame kwa kina, ili tupate kuona ni kitu gani Nabii Ibrahim alikuwa anataka kukithibitisha kupitia kuchomoza kwa jua na kuzama kwake. Kwa mujibu wa itikadi za watu wa Nabii Ibrahim, ni kwamba sayari hizo ndizo zilizokuwa na mamlaka ya kupangilia na kuendesha mambo yote ya vilivyomo katika ardhi, akiwemo mwanadam. Kwa hiyo alitaka kuwaambia kwamba uwepo na uhai wa viumbe hautegemei uwepo wa hao wanaodhaniwa kuwa ni waungu. Sasa ikiwa Mungu atakuwa wa msimu, kwa maana asubuhi yupo jioni hayupo, basi Mungu huyo atakuwa na mapungufu. Na kuwepo kitu katika saa fulani na kutoweka katika saa nyingine, ni ushahidi tosha ya kwamba kitu hicho hakina mamlaka juu ya kiumbe chochote katika ulimwengu huu wa kimaamuzi. Lakini kwa Mawahabi tauhidi iliyozoeleka kwao ni: Tauhidi Rububiya: Kwa maana ya imani juu ya uwepo wa muumba mmoja wa ulimwengu. Na washirikina wote wa zama za Bwana Mtume walikuwa wakiamini hivyo. Lakini mimi nashangaa toka lini maana ya neno Rabi ikawa ni khalik? Ndugu zangu neno 65

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 65

8/14/2017 1:18:26 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Rabi lina maana ya mlezi, na wala halina maana ya muumba kama wanavyodai wakata suruali. Hapo ima lugha imewapiga chenga au ni katika ule upotoshaji wao wa maana ya maandiko ili kutimiza azma yao ya kupotosha watu wasio na maarifa ya kutosha katika dini. Ni kweli washirikina walikuwa wanaamini uwepo wa muumba mmoja (Khalik) lakini hawakuwa wakiamini juu ya uwepo wa mlezi na muendeshaji mmoja wa mambo yote ya viumbe. Mawahabi kwa nini hamna aibu, mnadanganya watu mchana kweupe ! Sasa kabla hatujasonga mbele zaidi kwanza tujue, nini maana ya neno Rabi litumikalo katika Tauhidi Rububiya? Je, neno Rabi maana yake ni muumba? Bado tungali katika aina ya tatu ya tauhidi ambayo katika somo lililopita tuliitambulisha kwenu kwa jina la Tauhidi katika malezi na uendeshaji wa ulimwengu. Ibara hii katika lugha ya Kiarabu inafahamika kama: Tauhidi fil Rububiya. Tauhidi hii kwa Mawahabi ina maana ya kuamini juu ya uwepo wa muumba mmoja. Hiyo ndiyo tauhidi iliyozoeleka kwa Mawahabi kama tulivyoeleza hapo awali, pia wana Tauhidi Fil Uluhiya nayo tutaizungumzia mahala pake. Sasa swali tunalowauliza Mawahabi ni: Je, neno Rabi maana yake ni muumba? Kama maana hiyo itathibiti basi madai yenu ya kufasiri Tauhidi fil Rububiya, kwa maana ya imani juu ya uwepo wa pekee wa muumba, yatakuwa (madai) sahihi. Tofauti kati ya maana na tamko: Kabla hatujaeleza maana ya neno Rabi, napenda kueleza tofauti iliyopo kati ya tamko na maana. Tamko ni lile neno unalolitamka ili kuwasilisha mbele ya hadhira kile unachotaka kuwajulisha, na maana ni kile kinachowakilishwa na tamko. Mfano tunaposema hii 66

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 66

8/14/2017 1:18:26 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

ni pikipiki, hapo maana ni kile chombo chenyewe cha usafiri, halafu tamko ni lile ulilotamka kwa muunganiko wa herufi, ili kuwasilisha maana ile mbele ya hadhira. Kwa hiyo matamshi yana kazi kubwa ya kumrahisishia mwanadamu zoezi la kufikisha mbele ya hadhira kila wazo analoliwaza na kila maana anayoikusudia. Hapana shaka kuwa wadhifa wa kamusi ni kuainisha mahala pa matumizi ya kila neno ni wapi. Kwa mfano neno simba, mahala pake litumike katika kuwasilisha aina fulani ya mnyama pori anayekula nyama, na hapo haitajalisha neno hilo litatumika katika maana hiyo au laa. Sasa neno linapohamishwa kutoka katika maana yake na kuwekwa katika kazi ya kuwasilisha maana nyingine, kwa kweli hilo liko nje ya jukumu la kamusi. Tukirudi katika mfano wetu wa neno simba, ambalo kwa mujibu wa kamusi ni mnyama, lakini utakuta neno hilo linatamkwa halafu haliwasilishi tena maana ile ya awali, bali linawasilisha maana nyingine nayo ni mwanadamu. Kama vile tusemapo: Simba anatamba jukwaani, sasa maana hii ya pili kwenye kamusi haitambuliki bali inatambulika kwa watumiaji wenyewe na hayo ndiyo mapungufu yanayojitokeza katika kamusi za lugha. Kwani mara nyingi utapata maneno matatu tofauti, au zaidi na yote yanawasilisha kitu kimoja, lakini msikilizaji anapoyasikia maneno hayo kwa mara ya kwanza anaweza kuamini kuwa kila moja kati ya hayo matatu au zaidi, linawasilisha maana yake maalumu. Lakini baada ya utafiti unakuta kuwa maneno hayo yote yanawasilisha maana moja, na hizi nyinginezo zinakuwa ni matawi ya ile maana ya asili. Na wakati mwingine pia utapata neno moja lakini katika umoja wake huo, linawasilisha maana mbalimbali, sasa neno Rabi kadhalika ni katika maneno ya sampuli hiyo. Baadhi ya waandishi kama vile Al-Maududi, yeye katika mtazamo wake, aliona kuwa neno Rabi lina maana tano za asili, na 67

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 67

8/14/2017 1:18:26 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

kila moja kati ya hizo tano aliitolea ushahidi kutoka katika Qur’ani tukufu. Huo ni mtazamo wake, lakini hapana shaka kuwa neno Rabi katika Qur’ani na vitabu vya lugha, halina maana ya asili zaidi ya moja. 1. Rabil-Waladi,mlezi wa mtoto. 2. Rabil-Bustaan, mwangalizi wa bustani. 3. Rabil-Qaum, kiongozi wa watu. 4. Rabil-Bait, mwenye nyumba. 26 Na katika riwaya ya bwana Mtume limetamkwa Rabi kwa maana ya umiliki: A Rabi ghanami am Rabi Ibil, je ni mmiliki wa kondoo au wa ngamia? Hakuna shaka kwamba tamko hilo katika sehemu tulizozitaja na nyinginezo ambazo hatukuzitaja, limetumika kwa maana moja tu ya asili, na hizo nyingine ni matawi tu ya ile maana ya asili, maana ambayo itamlenga yule aliyekabidhiwa jukumu la uendeshaji. Kwa hiyo mwenye shamba akiitwa Rabi, ni kwa sababu ya uangalizi na uendeshaji wake wa shamba hilo. Pia tukimwita kiongozi wa nchi Rabi, ni kwa sababu ya kuwa mambo ya nchi ile na uendeshaji na upangiliaji wa mikakati ya nchi uko chini ya mamlaka yake. Na mwenye nyumba akiitwa Rabi, kwa sababu ya kuwa yeye ndiye mmiliki na mwendeshaji wa mambo ya ndani ya nyumba hiyo. Kupitia mifano yote tuliyoitoa, neno Rabi mtaona kama limeleta maana mbali mbali zenye kutofautiana, lakini ukweli unabaki pale pale kuwa maana ya asili ya neno hilo itabaki kuwa ni malezi na uendeshaji, kama tulivyokwisha tanguliza hapo awali. Sasa Mawahabi, semeni kweli, je katika maana tulizozitoa, maana ya Muumba itapata nafasi japo ya kuweka unyayo? 26

  Surat Quraish; 106:3 68

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 68

8/14/2017 1:18:26 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Rabi katika Qur’ani: Nabii Yusuf, amani iwe juu yake, anatumia neno Rabi kwa Aziz wa Misri:

“Na bibi mwenye nyumba aliyokuwemo (Yusuf) alimshawishi kinyume cha nafsi yake. Na akafunga milango akasema: Njoo! Akasema: Najikinga Kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye (mume wako) ni bwana wangu, ameyatengeneza vizuri makazi yangu. Hakika waliodhulumu hawatengenekewi.”27

Hapo Yusuf katumia neno bwana (Rabi) kumwita Azizi kwa kuwa Azizi ndiye aliyekuwa akimiliki madaraka yote juu ya Yusuf kama mlezi wake. Na katika Aya nyingine Yusuf anamwita Aziz (Mfalme wa Misri) kuwa ni bwana (Rabi) wa mfungwa mwenzie kule gerezani:

“Enyi wafungwa wenzangu wawili! Ama mmoja wenu atamnywesha bwana wake mvinyo. Na ama mwingine atasulubiwa na ndege watamla kichwa chake..…”28

Hapo Azizi kama kiongozi wa nchi ameitwa Rabi kwa kuwa yeye ndiye aliyekuwa kashika hatamu na mambo yote yalikuwa chini yake, kama muangalizi wa maslahi ya nchi, na wananchi kwa jumla, na wala neno hilo halikutumika kwa maana ya Muumba kama wanavyodai Mawahabi. 27 28

Surat Yusuf; 12:23   Surat Yusuf; 12:41 69

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 69

8/14/2017 1:18:27 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Qur’ani inawaita watawa na makuhani wa Mayahudi: Rabi katika Aya hii:

“Wamefanya makuhani wao na watawa wao kuwa ni miungu badala ya Mwenyezi Mungu na Masihi mwana wa Maryam. Wala hawakuamrishwa isipokuwa wamwabudu Mungu mmoja hakuna Mungu ila Yeye Ametakata na wanayomshirikisha nayo.”29

Uungu unaozungumzwa hapo si kwa maana ya uumbaji, bali ni kwa sababu Mayahudi waliwapa makuhani wao hatamu ya kisheria na wakawazingatia kuwa ni wenye mamlaka juu yao sawasawa na Mwenyezi Mungu, bali waliamini kuwa Mwenyezi Mungu kajivua majukumu ya uendeshaji na kuwakabidhi kwa makuhani hao. Kwa hiyo Rabi inabaki katika maana yake ileile ya uendeshaji au malezi, Uungu katika aya hiyo umekuja kwa maana tuliyoeleza na si kwa maana ya uumbaji, kwani hata waabudu masanamu hawakuwa wakiamini ya kuwa masanamu yameumba, bali waliamini kuwa masanamu ndiyo yana mamlaka ya kuendesha mambo yao yote, kama tulivyoeleza hapo awali. Mwenyezi Mungu anajisifu katika Qur’ani ya kuwa Yeye ni Rabi:

“Mola wa mbingu na ardhi na vilivyomo kati yake, na ni Mola wa mashariki zote.” (Surat Swaffat; 37:5). 29

Surat Tauba; 9:31 70

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 70

8/14/2017 1:18:27 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Neno Rabi hapo limetumika kwa kuwa Mwenyezi Mungu peke Yake ndiye Mwenye mamlaka ya kuratibu (kupangilia) maswala yote ya mbingu na ardhi pamoja na vilivyomo kati yake. Na Mwenyezi Mungu anapojisifia kuwa Yeye ni Rabil-Bait (Mola wa Al-Kaaba), neno Rabi hapa lina maana ya msimamizi na si muumba, kwani Al-kaaba imejengwa na wala haijaumbwa. Sasa tafsiri ya neno Rabi kwa maana ya Muumba inataka kutulazimisha kukubaliana na fikra za Kiwahabi ya kuwa Mwenyezi Mungu ameumba Al-Kaaba, kwa tafsiri yao hiyo ya kufasiri neno Rabi kwa maana ya Muumba. Ni kamusi gani inafasiri hivyo? Mpenzi msomaji naamini hadi hapo utakuwa umefahamu japo kwa muhtasari maana ya Rabi. Sasa ugomvi mkubwa uliopo baina yangu na Mawahabi, ni pale wanaposema Tauhidi fil Rubuubiyyah maana yake ni kuamini juu ya uwepo wa Muumba mmoja wa ulimwengu, kitu ambacho si kweli, maelezo yao hayo ni tafsiri ya Tauhidii fil Khaaliqiyyah. Na madai yao ya kutafsiri neno Rabi kwa maana ya Muumba, hayana mashiko katika lugha, wala katika suna za Bwana Mtume, wala katika Qur’ani, na hapa kuna mlolongo wa aya zinazokanusha na kukataa neno Rabi kuwa na maana ya Muumba:

“Akasema: Bali Mola wenu ni Mola wa mbingu na ardhi ambaye ndiye aliyeziumba, na mimi ni katika wenye kuyashuhudia hayo.”30 30

Surat Anbiyaa, aya ya 56 71

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 71

8/14/2017 1:18:27 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Sasa kama kweli Rabi maana yake ni Muumba basi maana ya Aya hiyo itakuwa kama ifuatavyo: Bali Muumba wenu ni Muumba wa mbingu na ardhi ambaye ndiye aliyeziumba, na mimi ni katika wenye kuyashuhudia hayo. Sasa kuna haja gani ya neno Muumba kujirudia rudia, mpaka sentensi inapoteza vile vionjo vyake vya kilugha? Ingetosha kusema: Muumba wenu ni Muumba wa mbingu na ardhi, bila kurudia tena neno “ambaye ameziumba” kwa mara ya tatu.

“Enyi watu! Mwabuduni Mola Wenu ambaye amewaumba nyinyi na wale wa kabla yenu…”31 Huu ni ushuhuda mwingine wa kuonesha kuwa neno Rabi maana yake si muumba, na kama ingekuwa ni kweli basi pasingelikuwa na haja ya kutaja tena amewaumbeni. Lakini tukitafsiri kwa maana ya mlezi basi litakuwa neno amewaumbeni ni chanzo cha tauhidii katika malezi, yaani imani juu ya uwepo wa Mola mmoja mlezi wa ulimwengu, na mpaka hapo maana kamili ya Aya itakuwa ni: Yeye aliyewaumba ndiye anayeendesha mambo yenu.

“Sema: Je, nimtafute Mola mwingine asiyekuwa Mwenyezi Mungu; na hali Yeye ni Mola wa kila kitu?.....”32

Kwa mujibu wa aya hizi zinaonesha waziwazi kwamba tofauti iliyokuwepo kati ya Bwana Mtume 8 na washirikina wa zama zake, ilikuwa ni kuhusiana na tauhidi katika malezi na uendeshaji, je ni jukumu la Mwenyezi Mungu au laa? Kwa upande wa washirikina wao swala hilo waliliweka chini ya mamlaka ya viumbe, lakini Bwana Mtume 8 alikuwa na 31 32

Surat Bakara; 2:21   Surat An’am; 6:164 72

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 72

8/14/2017 1:18:27 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

jukumu kubwa la kubatilisha itikadi zao hizo. Lakini katika uumbaji, wote walikiri kwa moyo mkunjufu, ya kwamba Muumba wao ni Mwenyezi Mungu tu, kama tulivyoelezea hapo awali. Mawahabi na tafsiri yao potovu: Wapenzi wasomaji, bado tungali katika mada yetu ya kubatilisha tafsiri potovu ya Mawahabi, inayotafsiri neno Rabi kwa maana ya Mola Muumba. Katika somo lililopita tulitaja mtiririko wa aya za Qur’ani, na katika somo hili tunakuongezea Aya nyingine zinazounga mkono madai yetu ya kwamba neno Rabi haliwezi hata siku moja kutafsirika kwa maana ya Muumba:

“Na Mola wako alipowaleta katika wanadamu kutoka migongoni mwao kizazi chao, na akawashuhudilisha juu ya nafsi zao. Je, Mimi si Mola Wenu? Wakasema: Kwa nini! Tumeshuhudia. Msije mkasema siku ya Kiyama kuwa sisi tulikuwa tumeghafilika na haya.”33

Kwa mujibu wa Aya hii tunafahamu kuwa Mwenyezi Mungu alifanya agano na wanadamu wote, na wakakiri kuwa Yeye tu ndiye Mola Mlezi. Kwa sababu ya kukiri huko, Mwenyezi Mungu (Siku ya Kiyama) atamuuliza yule aliyekwenda kinyume na agano hilo:

33

Surat A’raf; 7:172 73

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 73

8/14/2017 1:18:27 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

“Au mkasema, baba zetu ndio walioshirikisha zamani, nasi tulikuwa kizazi nyuma yao, basi utatuangamiza kwa waliyofanya wabatilifu?” (7:173)

Hakika ujio wa Aya hii katika jamii na mazingira ya watu wanaomshirikisha Mungu, ni ushahidi tosha usio na shaka juu ya uwepo wa watu waliovunja agano lililokuwepo baina yao na Mwenyezi Mungu. Sasa kama Mawahabi wanatafsiri Rabi kwa maana ya Mola Muumba badala ya Mola mlezi, basi watupe ushahidi unaothibitisha kuwa washirikina walikuwa wanatofautiana na Bwana Mtume 8 katika imani ya kuamini juu ya uwepo wa Muumba mmoja. Ushahidi huo hawataupata, kwani Qur’ani ilikwishaweka wazi kuwa: Washirikina wanaamini uwepo wa Muumba mmoja, isipokuwa shirki yao ipo katika kuamini kwamba: Mamlaka ya ulezi na kusimamia mambo yote ya ulimwengu, yako chini ya baadhi ya viumbe kama vile jua, majini, na malaika, kama tulivyokwishaelezea katika masomo yaliyopita. Kwa hiyo walioabudu jua hapo zamani, hawakuliabudu kwa imani ya kuwa jua ndiye Muumba wa ulimwengu, bali waliamini uwepo wa Muumba wa kweli, na mkabala na imani hiyo waliamini kuwa: Maisha yao yote na uendeshaji wa kila kitu katika ulimwengu huu uko chini ya mamlaka ya jua. Sasa Mwenyezi Mungu anapowakumbusha lile agano, hamaanishi kuwa washirikina walikanusha kuwa Yeye (Mwenyezi Mungu) si muumba, bali lengo lilikuwa ni kuwauliza kuwa inakuwaje mnaweka jukumu la malezi na uendeshaji wa kila kitu chini ya mamlaka ya jua hali ya kuwa mlikiri wenyewe kwa utashi wenu ya kuwa Mimi ndiye Mola Wenu Mlezi? Kwa maelezo hayo, maana ya Rabi inabaki kuwa ni Mola Mlezi na muendeshaji wa ulimwengu. Katika kisa cha muumini aliyekuwa akimtetea Nabii Musa huku akificha imani yake na kujitokeza kuwa kama mmoja wa watu wali74

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 74

8/14/2017 1:18:27 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

omuamini Firauni, bwana huyu katika maelezo yake alionesha kuwa Mola Mlezi ni Allah, na si Firauni:

“Na Firauni akasema: Niacheni nimuue Musa, naye amwite Mola wake! Hakika Mimi nachelea asije kubadilisha dini yenu, au akadhihirisha uharibifu katika nchi.”(al-Mu’min; 40:26)

“Na Musa akasema: Hakika Mimi najikinga kwa Mola Wangu na Mola Wenu anilinde na kila mwenye kiburi asiyeamini Siku ya Hesabu.” . (al-Mu’min; 40:27)

“Na akasema mtu mmoja muumini, katika watu wa Firauni, anayeficha imani yake: Mtamuua mtu kwa sababu anasema Mola Wangu ni Mwezi Mungu? Na hali amewajia na hoja zilizo wazi? Na akiwa ni mwongo basi uongo wake ni juu yake mwenyewe, na akiwa ni mkweli yatawafika baadhi ya hayo anayowaahidi. Hakika Mwenyezi Mungu hamwongoi apindukiaye mipaka, mwongo mkubwa.” (alMu’min; 40:28) 75

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 75

8/14/2017 1:18:27 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Katika aya hizo imani ya Nabii Musa ilikuwa ni kuthibitisha kuwa Mola mlezi ni Mwenyezi Mungu na si Firauni, kwani yeye hakuwahi kudai kuwa ni Mola Muumba bali alikuwa anadai kuwa Yeye ni Mola Mlezi (rabi) kama ilivyo katika Aya hii:

“Akasema (Firauni): Je, hatukukulea utotoni, na ukakaa kwetu katika umri wako miaka mingi?”34

Firauni anatumia neno Rabi kwa maana ya mlezi na sio Muumba kama wanavyodai wapotoshaji wa Kiwahabi wanaopotosha maana za maneno bila aibu. Sasa ulezi huu aliyoudai Firauni (wa kumlea Musa alipokuwa mtoto) ndiyo uleule aliyoudai pale alipopituka mipaka na kusema:

“Akasema: Mimi ndiye Mola wenu mkuu.”35

Neno lililotumika hapo ni Rabi kwa maana ya Mola Mlezi na sio Mola Muumba. Firauni hata siku moja hakuwahi kutangaza kuwa yeye ndiye aliyeumba mbingu na nchi, na hii imethibiti katika historia ya Ma-Firauni wa Misri kuwa hakuna yeyote kati yao aliyedai kuwa yeye ndiye aliyeumba mbingu na nchi. Kwa hiyo Firauni alipojiita Rabi alikuwa anamaanisha Mola Mlezi, na ndiyo maana Nabii Musa alijibu kuwa Mola Wangu (mlezi) ni Mwenyezi Mungu “Rabiyallah”. Tamko hilo la kiarabu lenye maana: Mola Wangu Mlezi ni Mwenyezi Mungu, linarejesha haki zote za uendeshaji wa ulimwengu kwa Mwenyezi Mungu Muumba wa mbingu na nchi. 34 35

Surat Shuaraa; 26:18   Surat Naziat; 79:24 76

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 76

8/14/2017 1:18:27 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Haki ambazo washirikina walikuwa wamezikabidhi kwa asiyekuwa Mola Mlezi. Pia tunasoma kisa maarufu cha vijana wa pango katika Aya isemayo:

“Na tukazitia nguvu nyoyo zao, waliposimama wakasema: Mola wetu ni Mola wa mbingu na ardhi. Hatutamuomba Mungu mwingine badala Yake. Hakika tutakuwa tumesema jambo la kuvuka mpaka.”36

Hao ni vijana walioishi katika mazingira ya watu waliokuwa wakimshirikisha Mwenyezi Mungu, lakini jamii hiyo haikuwa na imani ya juu ya uwepo wa Muumba zaidi ya mmoja, hasa ukizingatia watu hao ni watu walioishi baada ya kuondoka kwa Sayyid Masihi ( Bwana Yesu). Katika kipindi hicho watu kwa uchache walikuwa na ule ufahamu wa kutambua japo uwepo wa Muumba mmoja. Halafu tofauti ikabaki katika imani juu ya malezi na uendeshaji, je ni jukumu la Mwenyezi Mungu, au kuna uwepo mwingine ambao una jukumu hilo, kama tulivyo sema hapo awali. Narudia tena kusema kuwa: Neno Rabi nafasi yake ni malezi na uendeshaji pamoja na upangiliaji wa mambo yote katika mbingu na nchi. Na ndiyo maana neno Rabi limejirudia katika Surat Rahman mara 31, tena limetajwa baada ya neno neema. Mwenyezi Mungu anasema:

36

Surat Kahfi; 18:14 77

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 77

8/14/2017 1:18:27 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

“Basi ni ipi katika neema za Mola wenu mnayoikanusha nyinyi wawili (binadamu na majini).”37

Nukta muhimu au hekima ya kutajwa neno Mola baada ya neno neema, ni kutaka kuonesha kuwa uneemeshaji au utoaji wa riziki ni jukumu la Mola Mlezi. Yeye tu ndiye anayewaruzuku viumbe wote, na kwamba Yeye ndiye chanzo kikuu cha neema zote unazoziona na usizoziona. Na kuna Aya tano katika Qur’ani, ambazo Mwenyezi Mungu anaambatanisha neno Rabi na shukurani:

Na alipotangaza Mola Wenu: Mkishukuru nitawazidishia na mkikufuru basi adhabu yangu ni kali.38

“…..Akasema (Nabii Suleiman): Ewe Mola wangu! Nizindue niishukuru neeme Yako uliyonineemesha na wazazi wangu na nipate kutenda mema unayoyaridhia na uniingize kwa rehema zako katika waja wako wema.39

“…..Haya ni katika fadhila za Mola wangu, ili anijaribu, nitashukuru au nitakufuru….”40

Surat Rahman; 55:13   Surat Ibrahimu; 14:7 39   Surat Namli; 27:19 40   Surat Namli; 27:40 37 38

78

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 78

8/14/2017 1:18:27 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Na tumemuusia mtu awafanyie uzuri wazazi wake wawili. Mama yake amebeba mimba yake kwa taabu, na akamzaa kwa taabu. Na kubeba mimba kwake na kumwachisha ziwa ni miezi thalathini. Hata anapofika kukomaa kwake, na akatimiza miaka arubaini. Husema: Mola Wangu! Nizindue nishukuru neema Yako uliyonineemesha na wazazi wangu…..”41

Hakika ilikuwa ishara kwa Wasabai katika maskani yao – bustani mbili, kulia na kushoto. Kuleni katika riziki ya Mola Wenu na mumshukuru. Mji mzuri na Mola mwenye maghfira.42

Aya zote hizo zinatilia mkazo tafsiri yetu ya neno Rabi kwa maana ya Mola mlezi na sio Mola Muumba kama wanavyodai Mawahabi na hoja zao chakavu tena za nguvu. Jukumu la Mlezi ni kuhakikisha anawapatia riziki wale anaowalea na kuendesha mambo yao ikiwa ni pamoja na kukidhi mahitaji yao. Kwa mantiki hiyo ni lazima ashukuriwe Mola Mlezi kwa malezi Yake hayo. Qur’ani inatusimulia kisa kizuri cha Nabii Nuhu:

41 42

Surat Ahkaf; 46:15   Surat Sabai; 34:15 79

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 79

8/14/2017 1:18:28 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

“Nikasema: Ombeni maghfira kwa Mola Wenu; hakika Yeye ni mwingi wa kusamehe.”43

“Atawaletea mvua nyingi.” “Na atawapa mali na watoto, na atawapa mabustani na atawafanyia mito. Yote hayo ni majukumu na sifa ya Mola Mlezi.” Mpenzi msomaji mpaka hapa utakuwa umeelewa japo kwa muhtasari maana ya neno Rabi.Ila tu neno hilo huambatana na neno Khaalik (Muumba) kwani Mwenyezi Mungu huumba kwanza halafu baada ya kuumba ndiyo analea viumbe wake,kwa hiyo ukisema Mungu ni Muumba basi lazima ukubali kuwa ni mlezi pia. Na unaweza ukakufuru upande wa malezi kwa kukufuru neema, lakini upande wa uumbaji ukabaki unaamini juu ya uwepo wa Muumba mmoja wa kweli na wa pekee, kama walivyokuwa wakifanya washirikina, ambao tumezungumzia habari zao katika Aya nyingi tulizozitaja katika masomo yaliyopita. 4- TAUHIDI KATIKA IBADA Katika masomo yaliyopita tulisema kuwa: Ibada ya kumwabudu Mwenyezi Mungu peke Yake pasina kumfanyia ushirika, na kukataa miungu yote ya batili, ndiyo fikra za Manabii na Mitume, na ndiyo uti wa mgongo wa mafundisho yote waliyokuja nayo. Pia ni uti wa mgongo wa fikra zao na mitazamo yao, na ndiyo maana twapata kuona kuwa dini zote zilizotangulia ziliiwekea tauhidi katika ibada msisitizo mkali, na kuiweka (tauhidi katika ibada) mstari wa mbele katika orodha ya mafundisho yake. Kwa hakika nguzo hii muhimu ya tauhidi katika ibada, licha ya kuwa kadri siku zinavyopita katika 43  Surat Nuh; 71:10 80

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 80

8/14/2017 1:18:28 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

historia ya maisha ya mwanadamu, na watu kutoka katika mstari mnyoofu na wengi kuabudu wanadamu wenzeo, badala ya Mwenyezi Mungu mmoja na wa pekee, lakini bado tunaikuta nguzo hii bado imethibiti katika nyoyo na akili za watu wenye dhamira safi na akili zenye nuru. Wao wanazingatia kuwa sheria zote zilizokuja na Manabii waliotangulia, ni sheria ambazo misingi yake ni tauhidi ya kumwabudu Mwenyezi Mungu, na kwamba tauhidi katika ibada ni nguzo pekee inayowaunganisha watu wa dini zote za tauhidi. Na kwa mantiki hiyo tunakuta Qur’ani katika mjadala na Mayahudi na Manaswara, inatilia sana msisitizo katika nguzo hii inayochangiwa na dini hizo na kuwahimiza warejee katika asili ya imani zao, ambayo ni tauhidi katika ibada, yaani imani juu ya uwepo wa Muumba mmoja anayestahiki kuabudiwa.

“Sema: Enyi watu wa Kitabu! Njooni kwenye neno la usawa baina yetu na baina yenu. Kwamba tusimwabudu yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu, wala tusimshirikishe na chochote; wala baadhi yetu wasiwafanye baadhi kuwa waungu zaidi ya Mwenyezi Mungu. Wakikataa. Semeni: Shuhudieni kuwa sisi ni waislamu.”44

Sasa mkabala na neno hili tauhidi katika ibada kuna neno shirki katika ibada, ambalo leo hii Mawahabi wanalitumia vibaya ilimradi tu waweze kukidhi mahitaji yao ya kupotosha watu wasio na hatia. 44

Surat al Imran; 3:64 81

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 81

8/14/2017 1:18:28 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Swali, je kuomba kwa kupitia mawalii (vipenzi) wa Mwenyezi Mungu, au kutafuta uombezi kwa Mitume, na kuadhimisha kuzaliwa kwao Mitume) na kufa kwao, je yote hayo yanaingia katika orodha ya ibada, ili atakayeyafanya tumhukumu kuwa ni mshirikina, anayebudu asiyekuwa Mwenyzi Mungu? Ndiyo, kuna watu wanaoamini kuwa yote hayo ni ibada ya kumwabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu, na ni katika mambo yanayomtoa mtu katika Uislamu!!! Kwa mantiki hiyo tumeona kuna ulazima mkubwa wa kuyatazama maswala haya kwa kina, ili tufahamu ukweli wa mambo katika maswala haya ambayo yamekuwa yakifanywa na Waislamu kila kukicha. Kama vile maulidi, hitima, kuomba dua kwa Baraka za watukufu kama vile Manabii na waja wema. Ni upi ukweli wa mambo hayo? Je, hayo ni katika mambo yanayokinzana na tauhidi na kuhukumiwa kuwa ni shirki? Je, kumwabudu Mtume ndiyo shirki na kutoka katika wigo wa tauhidi? Au kumtukuza na kuazimisha siku ya kuzaliwa kwake, na siku ya kufa kwake ni shirki nyingine imtoayo mtu katika dini? Wapenzi wasomaji, ili kupata utatuzi wa mgogoro huu na kufikia hitimisho sahihi kwa njia ya kielimu, ni lazima kwanza tueleze nini maana ya ibada, na tuitolee ufafanuzi ili tuweze kuweka mpaka unaotenganisha kati yake na vitu vingine ambavyo si ibada. Pia tufahamu tofauti kati ya kuabudu na kutukuza. Lakini tusipofanya hivyo basi kamwe hatutaweza kuwaokoa watu kutoka katika mtego mbovu wa Kiwahabi, unaonasa wasiokuwa na maarifa, na kuwatoa katika Sunna (walizokuwa wakizifuata toka zama za mababu) kwa hoja ya kuwa ni shirki na ni ibada ya kumwabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Je, ni nini maana ya ibada? Kwa hakika tafsiri ya neno lolote lile ili iwe nyoofu na isiyo na utata ndani yake, ni lazima iwe na sifa mbili: 82

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 82

8/14/2017 1:18:28 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

1.

Iwe ni tafsiri itakayokusanya sifa na vipengele vyote vinavyohusiana na neno husika, bila ya kuacha hata kipengele kimoja kando.

2.

Iwe ni tafsiri inayozuia sifa na vipengele vyote visivyohusiana na neno husika. Nukta hizi mbili ndiyo mtambo imara wa kudhibiti tafsiri za kulazimisha zinazotolewa na Mawahabi, pia kupitia nukta hizo tunaweza kufahamu wigo wa neno ibada na kutofautisha kati ya ibada na ile isiyokuwa ibada. Na kwa kudhibiti tafsiri ya neno kwa njia hii ndio tutakuwa tumewakwamisha wapotoshaji wa Kiwahabi, maana hawatakuwa na njia nyingine ya kutokea. Sasa kabla hatujaanza kulichambua neno ibada, hapa kuna njia tatu zinazotufikisha kwenye tafsiri sahihi ya neno ibada:

3.

Kamusi za Lugha ya Kiarabu, kwa kuwa neno lenyewe ni lenye asili ya kiarabu.

4.

Uchambuzi wa maandiko ya Qur’ani na hadithi ambayo ndani yake neno hilo limetajwa.

5.

Uchambuzi wa vipengele ambavyo ndio mihimili ya neno ibada, sawasawa ibada hiyo iwe kwa Waumini wa kweli au Washirikina.

Lakini tukitumia njia ya kwanza peke yake, haiwezi kutufikisha katika lengo letu tunalokusudia kulifikia, ambalo ni kupambanua kati ya maana mbili. Ni kitu gani kinasadikika kuwa ni ibada na ni kipi hakisadikiki kuwa ni ibada. Ila njia ambayo inaweza kutufikisha katika malengo yetu, pamoja na kuweka mipaka kati ya ibada na kisichokuwa ibada, ni njia ya tatu. Nasi kwa rukhsa ya Mwenyezi Mungu na uwezo Wake, tutaziweka wazi mbele ya wasomaji njia zote tatu, moja baada ya nyingine. 83

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 83

8/14/2017 1:18:28 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

NJIA YA KWANZA: 1.

Kamusi za Lugha ya Kiarabu:

Kama tulivyotangulia kusema kuwa njia ya kwanza ni kurejea kamusi za lugha husika, sasa hebu tuangalie kamusi yatwambia nini. Anasema Ibnu Mandhur katika kamusi yake maarufu kwa jina la Lisanul Arab: “Asili ya Ubudiyya (utumwa au kuwa mja) ni unyenyekevu au kujishusha.” Na anasema Raghib Isfahani katika kitabu chake kiitwacho AlMufradaat: “Al-Ubudiyyah (kuwa mja au mtumwa) ni kudhihirisha udhalilifu, na ibada ni daraja ya juu ya kujidhalilisha na haifai isipokuwa kwa yule mwenye fadhila za juu, juu zaidi kuliko wote, naye ni Mwenyezi Mungu, aliyetakasika.” Na anasema Feiruz Abadi katika kitabu chake, Kamusil Muhit: “Ibada ni utiifu.” Ama Ibnu Faris yeye anasema katika kitabu chake, Al-Maqayis: “Al abdu, neno abdu (mja) ni mnyambuliko wa neno Ibada (katika lugha ya Kiarabu), (neno hili) lina maana mbili za asili zinazokinzana, ya kwanza: Inaashiria ulaini na udhalilifu. Na ya pili inaashiria ukali na ususuavu.” Hiyo ni maana ya ibada kwa mujibu wa kamusi za lugha, lakini tukizichunguza tafsiri zote hizo, hazitoi maana halisi ya neno ibada bali zinatupatia maana inayojumuisha ibada halisi na isiyokuwa halisi. Lakini ukweli unabaki pale pale kuwa udhalilifu na utiifu na unyenyekevu, vyote hivi havitupatii maana halisi ya neno ibada. Na kama ni kweli tafsiri hiyo ndiyo tafsiri sahihi ya neno ibada basi Waislamu wote watakuwa wameshikamana na mambo ambayo hayafai kwao kushikamana nayo. Na kwa mantiki hiyo mtoto akionesha unyenyekevu mbele ya mzazi wake, atakuwa kamwabudu mzazi wake, na mwanafunzi akimtii mwalimu wake, 84

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 84

8/14/2017 1:18:28 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

atakuwa kamwabudu mwalimu, askari akitii amri ya mkuu wake, naye pia atakuwa kamwabudu mkuu huyo. Kitu ambacho si sahihi kabisa kwani Qur’ani inatuhimiza waziwazi kuwanyenyekea wazazi, inasema:

“Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa kuwaonea huruma na useme: Mola Wangu! Warehemu kama walivyonilea utotoni.”45

Na katika Aya nyingine tunakuta Mwenyezi Mungu anawaamuru Malaika wamsujudie Adamu:

“Na tulipowaambia Malaika: Msujudieni Adamu, wakamsujudia isipokuwa Ibilisi; alikataa na akatakabari; na akawa miongoni mwa makafiri.”46

Vilevile tusomapo kisa mashuhuri cha Nabii Yusuf na wazazi wake pamoja na ndugu zake 11. Tunaona kuwa walimsujudia Yusuf:

“Na akawapandisha wazazi wake kwenye kiti cha enzi na wakapomoka kumsujudia. Na akasema: Ewe baba yangu! Hii ndiyo tafsiri ya ile ndoto yangu ya zamani. Mwenyezi Mungu ameifanya iwe ya kweli…..”47   Surat Israa; 17:24   Surat Baqarah; 2:34 47   Surat Yusuf: 12:100 45 46

85

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 85

8/14/2017 1:18:28 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Sasa tukilifasiri neno ibada kwa tafsiri hii ya kilugha, basi Nabii Yakub atakuwa amemwabudu mwanawe Yusuf, na Malaika watakuwa wamemwabudu Adamu. Lakini tafsiri hii si sahihi kwani wigo wake ni mpana kwa, hiyo imejumuisha maana ya ibada na isiyokuwa ya ibada, kwani neno unyenyekevu wigo wake ni mpana mno. Kwa hiyo tunaweza kusema kuwa: Ibada ni unyenyekevu lakini si kila unyenyekevu ni ibada. Na hakuna Mwislamu hata mmoja juu ya ardhi hii anayesema kuwa Nabi Yakub alimwabudu Yusuf, au Malaika walimwabudu Adamu, labda mtu huyo awe ni mjukuu wa Sheikh Muhammad bin Abdul-wahab, aliyekosa adabu kwa wazazi wake hadi kwa Mitume wa Mwenyezi Mungu. Mpenzi msomaji kama tulivyosema kuwa tafsiri ya kilugha haitufikishi katika lengo letu, na tukiing’ang’ania basi tutakuwa tumekubali kuwaingiza Manabii na waja wema katika kundi la wasiomwabudu Mungu, kwa kuwa hakuna Mtume hata mmoja aliyekosa kumnyenyekea mzazi wake, Na kwa kuwa maana ya kilugha wigo wake ni mpana, basi ni lazima tafsiri iwe ni yenye kuzuia sifa na vipengele vyote visivyo husiana na neno husika, kama tulivyosema hapo awali. Ama kuhusu kitendo cha Malaika kumsujudia Adamu, baadhi ya wanazuoni wanasema kuwa: Aliyekuwa anasujudiwa ni Mwenyezi Mungu na wala si Adamu, bali Adamu alikuwa tu ni kibla cha Malaika, sawa sawa na Sisi Waislamu tunamsujudia Mungu hali yakuwa tumeelekea Al-Kaabah, lakini anayeabudiwa ni Mungu na wala si Al-Kaabah. Na nadharia hii itamwacha msomaji njia panda, kwani kama kweli aliyesujudiwa pale hakuwa ni Mwenyezi Mungu Mwenyewe kwa nini Ibilisi aseme: Je, nimsujudie uliyemuumba kwa udongo?48 48

Surat Israa : 61 86

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 86

8/14/2017 1:18:28 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Jibu sahihi ni kwamba aliyekuwa anasujudiwa hapo ni Adamu na wala si Mwenyezi Mungu, na kusujudu huko kulikuwa na maana ya kunyenyekea na si kuabudu, kwa hiyo maneno ya Ibilisi yanatafsirika hivi: Je nimnyenyekee uliyemuumba kwa udongo?

NJIA YA PILI: Katika somo lililopita tulijaribu kuelezea njia ya kwanza ya kufahamu maana ya neno ibada, ambayo ilikuwa ni kamusi ya lugha husika, na tukaifafanua njia hiyo ya kwanza kwa ufasaha wa hali ya juu. Na katika somo hili tutazungumzia njia ya pili ya kufahamu neno ibada, ambayo ni: 2. Uchambuzi wa matini ya Qur’ani na hadithi na matini zote za lugha, ambazo ndani yake neno ibada limetajwa. Mpenzi msomaji nadhani utakuwa unakumbuka kauli yetu ya kwamba njia ya kwanza ambayo ni kurejea kamusi ya lugha husika, haitufikishi katika lengo tunalokusudia kulifikia, nalo ni kupata tafsiri sahihi ya neno ibada, tafsiri itakayo tenganisha kati ya ibada halisi na ile isiyo halisi. Sasa tukiangalia njia ya pili tunakuta kuwa nayo vilevile haiainishi maana ya neno ibada, kwani kila tunapojaribu kurejea matini zote ambazo zimetaja neno ibada, tunakuta neno hilo limetumika kwa maana mbali mbali. Kwa hiyo, kwa kifupi ni kwamba njia hii nayo haitufikishi katika lengo letu. Kiarabu ni kama lugha nyinginezo tu, kwa hiyo kina sarufi yake na fasihi yake. Kwa hiyo mwanafasihi anaweza kutumia neno huku akilenga maana tofauti na ile iliyozoeleka, ilimradi tu pawepo nukta inayohusisha baina ya maana halisi ya neno na maana hii ya pili anayoikusudia mwanafasihi. Sasa matini nyingi zilizotaja neno ibada kwa kweli neno hilo limetumika kisitiari. Kwa mfano, utakuta neno ibada lime87

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 87

8/14/2017 1:18:28 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

tumika kwa mtu anayetii matamanio ya nafsi yake. Utasikia watu wakisema: Fulani ni mtumwa wa matamanio yake. Wakimaanisha kuwa anatii matamanio yake, kama vile ambavyo muumini anavyotii amri ya muumba Wake. Na mtu huyo anayetii matamanio yake haitwi mshirikina. Mfano mwingine ni pale tunapoona mtu anapenda madaraka na kuyatafuta kwa gharama yoyote ile, au anapenda pesa kupita kiasi, hapo utasikia watu wakisema: Fulani anaabudu pesa, au madaraka au anaabudu tumbo lake. Kwa hiyo mtu huyo hatuwezi kumuingiza katika orodha ya wasiomwabudu Mwenyezi Mungu, kwani neno kuabudu limetumika kisitiari kama tulivyokwisha kusema, na hapo linamaanisha kuwa: Fulani ameyakabidhi matamanio yake au tumbo lake hatamu ya mambo yake yote, kwa hiyo amekuwa ni mtu wa kupewa amri na tumbo lake au na tamaa zake za kimwili, halafu naye anatii. Hiyo ni maana ya kisitiari tu, na maana hiyo pia imetumika hata katika Qur’ani tukufu, Mwenyezi Mungu anasema:

“Je, sikuagana nanyi, enyi wanadamu, kuwa msimwabudu Shetani? Hakika yeye ni adui dhahiri kwenu.”49

Mtu aliyezitawalisha hasira au aliyebobea katika matamanio hadi matamanio yake yakamtoa katika mstari mnyoofu, akawa hajali kufanya ibada, anaacha kila ambalo Mwenyezi Mungu ameliwajibisha kwake, au akawa amebobea katika ulevi, au uzinzi mtu huyo ni mwenye kumtii Shetani, na kwa amri ya shetani anafanya maasi hayo. Lakini pamoja na hayo haimaanishi kuwa mtu huyu, anamwabudu Shetani kama vile aabudiwavyo Mwenyezi Mungu, au 49

Surat Yasin; 36:60 88

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 88

8/14/2017 1:18:28 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

kama vile washirikina wanavyoabudu masanamu. Kwa hiyo mtu huyu hawi mshirikina na wala hukumu ya shirki haimpati, na wala hatoki katika orodha ya Waislamu, pamoja na kuwa kwake katika watu wanaomwabudu shetani, lakini ibada hiyo si ibada kwa maana ile halisi inayokusudiwa katika vitabu vya theolojia, bali ibada hapo imetumika kwa maana ya sitiari. Na mpaka hapa hatuwezi kutegemea njia zote mbili zilizotumika kutafsiri neno ibada, japo zina faida kwa upande wake, lakini bado hazijatosha kutufikisha katika lengo letu tunalolikusudia kulifikia baada ya kutafsiri neno ibada kwa tafsiri ya kimantiki. Kwa hiyo hatuna budi kuingia katika njia ya tatu baada ya kuwa njia ya kwanza na ya pili zimeshindwa kutuainishia maana halisi ya neno ibada.

NJIA YA TATU: 3. Uchambuzi wa chembe msingi ambazo zinatengeneza kitu kiitwacho ibada, sawasawa ibada hiyo iwe kwa waumini wa kweli au washirikina. Hakika mtafiti wa mada hii atakapotaka kutanzua ufahamu wa maana ya neno ibada, na kuainisha chembe msingi zinazounda maana ya neno ibada, bila shaka atakutana na vipengele viwili vya kimsingi. Kimojawapo ni cha dhahiri (wazi) na kingine si cha wazi. Vipengele hivyo ni sanjari na chembe msingi mbili, Oksijeni na Haidrojeni zinazoungana kikemikali na kutengeza maji. Kwa hiyo ili kupata uhalisia wa maji ni lazima zipatikane chembe msingi hizo mbili. Kwa hiyo kuzifahamu chembe msingi zinazounda maana ya neno ibada kuna nafasi kubwa katika kumuwezesha mtu kupambanua kati ya ibada na isiyokuwa ibada. Na sifa zinazotofautisha kati ya ibada na isiyokuwa ibada tunaweza kuzifahamu kwa kupitia matendo ya 89

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 89

8/14/2017 1:18:28 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

waja na itikadi zao bila ya kutofautisha kati ya ibada ya waumini na ya wale wasiokuwa waumini. Kisha baada ya uchunguzi wa kina katika matendo ya watu hao tunafikia katika hitimisho la kusema kuwa, ibada kwa watu hao ni: Ibara ya unyenyekevu unaokwenda sanjari na itikadi maalum juu ya yule anayenyenyekewa. Na mpaka hapa tunafahamu kuwa chembe msingi zinazoungana na kutengeneza kitu ibada ni mbili tu. 1.

Tendo litokanalo na unyenyekevu na udhalilifu.

2.

Uwepo wa itikadi maalum inayokupa msukumo wa kumwabudu huyo mnyenyekewa.

Sasa kipengele hicho cha kwanza ndicho kinachowatatiza Mawahabi, kwa kuwa neno unyenyekevu lina maana pana zaidi inayojumuisha ndani yake ibada halisi na isiyokuwa halisi. Kama vile kurukuu na kusujudu ni unyenyekevu, ambao inasadikika ndani yake maana ya ibada. Na kuinamisha kichwa mbele ya mheshimiwa yeyote kama ishara ya heshima, huo pia ni unyenyekevu lakini ambao haisadikiki ndani yake maana ya ibada. Vile vile kuonesha utiifu au kuwatukuza Mitume na kuadhimisha siku za kuzaliwa kwao, yote hayo inasadiki ndani yake sifa ya unyenyekevu, lakini si ibada. Kwa hiyo hatuwezi kuifanya sifa hiyo ya unyenyekevu kuwa ndiyo sifa ya msingi inayoainisha ufahamu halisi na makusudio ya mwisho ya neno ibada, au kusema kuwa unyenyekevu unasadiki ndani yake kiukamilifu maana ya ibada. Bado kabisa neno hilo unyenyekevu lenyewe katika uwenyewe wake halijajitosheleza katika kutoa tafsiri kamili ya neno ibada. Hivyo basi hatuna budi kutafuta tena ukweli wa neno ibada, au tufanye utafiti wa kina ambao kupitia utafiti huo tutamakinika kuifahamu ibada inayokusudiwa, ikiwa 90

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 90

8/14/2017 1:18:28 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

ni pamoja na kupambanua baina yake na yale yanayodhihiri mbele yetu kama ibada hali ya kuwa si ibada katika uhalisia wake. Hapa tunasema kuwa: Hakika ufahamu wa malengo yaliyofichika, unapatikana ndani ya uchambuzi wa lengo la watu katika ibada na unyenyekevu. Ni katika mambo yasiyo na shaka kwamba lengo la muumini (katika ibada) ni tofauti na lengo la asiyekuwa muumini. Kwa ibara nyingine: Hakika waumini wote na waabudu masanamu wote, na waabudu jua na sayari nyinginezo, wanaamini juu ya uungu wa hivyo wanavyoviabudia. Kwa hiyo imani juu ya uungu wa mwabudiwa ndiyo chembe msingi inayotengeneza maana ya ibada, ila lengo la ibada kwa waumini ni tofauti na lile la wasiokuwa waumini kama tulivyosema, na mpaka hapa inatulazimu kuweka wazi hayo malengo. Lengo la waamini na wafuasi wa ujumbe wa tauhidi, linafungamana na usafi wa matendo yao, na kiwango cha maarifa yao na daraja ya ufahamu wao juu ya wanayemwabudu, naye ni Mwenyezi Mungu aliyetakasika. Kwa hiyo lengo kwa upande huu, ni kufikia kilele cha ibada, lakini kadri utakavyomfahamu Mwabudiwa kwa kina zaidi ndivyo utakavyomwabudu kwa kina zaidi. Na kwa ajili hiyo tunaweza kupangilia lengo mahususi la hao wanatauhidi, katika matabaka mawili, ambayo tutayafafanua mahala pake kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu. Lengo la ibada kwa wanatauhidi: 1.

Lengo linalokusudiwa (katika ibada) na watu maalum (kundi lenye maarifa ya juu) kati ya wanatauhidi.

2.

Lengo linalokusudiwa na waumini wote.

Watu wa tabaka hilo la kwanza, wao ni watu wenye maarifa ya juu zaidi, na wana mafungamano ya dhati na chanzo kikuu cha uka91

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 91

8/14/2017 1:18:28 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

milifu. Na katika mambo yasiyopingika ni kwamba watu hawa wana lengo maalumu na la kipekee nyuma ya ibada zao, ambalo linajieleza kama upendo na shauku na kuyeyuka kwao katika Mwabudiwa wao. Na kwamba ufahamu wao wa kumfahamu Mwenyezi Mungu ambaye ni chanzo cha wema wote, ufahamu huo umeufanya uwepo wao kubaki katika mstari mnyoofu, kwa msimamo wa hali ya juu na kuinamisha vichwa vyao kumnyenyekea mpendwa wao na mwabudiwa wao, pasina kufikiria hata chembe ya malipo, ya kimaada kama vile pepo au moto, au thawabu au adhabu. Kwa tafsiri nyepesi nyepesi tunasema kuwa: Hakika ya watu wa tabaka hilo la kwanza, injini ya msingi inayowaendesha na kuwafikisha kunako unyenyekevu na utiifu na udhalilifu mbele ya Mwenyezi Mungu ni ile hali ya kupenda wema na ukamilifu unaodhihirika kwa Mwenyezi Mungu aliyetakasika, na kuyeyuka kwao katika dhati ya Mwenyezi Mungu ambayo ni ukamilifu usio na kikomo wala mipaka ya kijografia. Kiasi ambacho hawakuona cha kuambatana nacho zaidi ya Mwenyezi Mungu. Bali Yeye akawa ndiyo kila kitu kwao, wakamtegemea Mwenyezi Mungu kama chanzo cha uwepo wao, na chanzo cha kubakia kwao katika Dunia hii mpaka siku maalum. Hadithi nyingi za Kiislamu zilizotufikia kupitia watu wa nyumba ya Mtume 8 zimeifafanua ibada ya watu hawa na kuiita kuwa ni ibada ya watu huru, ibada ambayo ndani yake haina matamanio ya ladha za kimaunzi (kimaada). Mapenzi yao kwa Mwenyezi Mungu, hayategemei uwepo wa maslahi fulani, bali ni upendo safi kama ule wa mama kwa mtoto wake, mama humpenda mtoto bila kuzingatia maslahi fulani. Moja ya hadithi hizo ni ile isemayo: “Watu wamemwabudu Mwenyezi Mungu kwa hali ya mapenzi tu, na hiyo ndiyo ibada ya waungwana.� Hapana shaka kuwa lengo hilo safi la ibada ulilolipata 92

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 92

8/14/2017 1:18:28 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

kwa tabaka hilo la kwanza, hutalipata katika kundi lingine la watu wa tauhidi tofauti na wao. Kwani wao ni watu waliojitolea katika ibada kwa moyo mkunjufu hadi wakafikia kilele cha ukamilifu wa kibinadamu, ambao chanzo chake ni ibada ambayo shina lake ni mapenzi ya dhati kwa Mwenyezi Mungu na kutambua kuwa Yeye tu ndiyo chanzo cha kila ukamilifu. Tabaka la pili: Watu wa tabaka hili la pili ni wale waumini wa kawaida ambao wanamwabudu Mwenyezi Mungu na kumnyenyekea lakini injini ya msingi katika ibada hiyo tunaweza kuigawa katika vipengele viwili vya msingi: 1.

Kutambua kwao ya kwamba Mwenyezi Mungu ndiyo chanzo na ulimwengu ni matokeo .

2.

Kutambua kwao ya kwamba licha ya Mwenyezi Mungu kuwa ni chanzo, Yeye huyo huyo ndiye Mola mlezi wa dunia na Mwenye mamlaka juu ya maswala ya viumbe, na kwamba ulimwengu katika uwepo kwa mara ya kwanza ulimtegemea Mungu, bali na hata katika kubakia kwake hadi siku ya mwisho bado unamtegea Mwenyezi Mungu. Na kwamba mustakabali wa maisha ya mwanadamu uko katika mamlaka Yake, na kuwa Yeye tu ndiye kimbilio la viumbe na kwamba ufumbuzi wa mambo yote, yale yanayowezekana na yasiyowezekana kwa mwanadamu, Kwake yanawezekana. Na mamlaka Yake ndiyo yenye uwezo wa kumuondolea mwanadamu mapungufu yake, na kukidhi haja zake zote.

Hakika ukitazama kwa kina Aya za Qur’ani utapata kuona namna Qur’ani ilivyolipangilia swala hili na kuliweka wazi katika sura zifuatazo: Baada ya watu hao kukiri kwamba Mwenyezi Mungu ndi93

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 93

8/14/2017 1:18:28 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

ye Muumba wa ulimwengu na mwanadamu, sasa sanjari na kukiri huko ni ushuhuda wao ya kwamba Mwenyezi Mungu tu ndiye Mola Mlezi na kila kitu kiko chini ya mamlaka Yake, na kwamba mamlaka Yake ndiyo yanayopangilia maswala yote ya ulimwengu na walimwengu kwa jumla. Baada ya nukta hii ya pili, tabaka hili linahamia katika nukta nyingine ambayo ni ibada, yaani baada ya nukta ya kwanza ambayo ni kukiri kwamba Mwenyezi Mungu ni Muumba, na nukta ya pili, kukiri kwamba mwenye mamlaka juu ya kila kitu ni Yeye tu. Sasa kupatikana ibada katika nukta ya tatu ya mlolongo huu, kunatupeleka katika hitimisho lifuatalo: Kwamba ibada ni zao la hisia mbili ndani ya mwanadamu, ya kwanza ni kuwa kwake Mwenyezi Mungu Muumba wa ulimwengu, ya pili ni kuwepo mamlaka ya malezi na ufumbuzi wa kila jambo katika mikono Yake, na kwamba Yeye ndiye mwendeshaji wa ulimwengu:

“Hakika Mola Wenu ni Mwenyezi Mungu ambaye ameumba mbingu na ardhi katika siku sita, kisha akatawala kwenye Arshi. Yeye hutengeneza mambo. Hakuna mwombezi ila baada ya idhini Yake. Huyo ndiye Mwenyezi Mungu, Mola Wenu, basi mwabuduni. Je, hamkumbuki ?�50

Aya hiyo ya 3 ya Surat Yunus imetaja mlolongo wa mambo manne nayo ni: 50

  Surat Yunus; 10:3 94

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 94

8/14/2017 1:18:28 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

1.

Hakika Mola Wenu ni Mwenyezi Mungu ambaye ameumba mbingu na ardhi.

2.

Yeye hutengeneza mambo.

3.

Hakuna mwombezi ila baada ya idhini Yake.

4.

Huyo ndiye Mola Wenu, basi mwabuduni.

Baada ya Aya hiyo kufafanua kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Muumba, na kwamba Yeye ndiye mtengenezaji wa mambo, na kwamba hakuna mwombezi ila baada ya ruhusa yake, nukta ya mwisho ndiyo inamalizia kwa kusema: Huyo ndiye Mola Wenu, basi mwabuduni, na hiyo ni kwa kuzingatia kuwa Yeye ndiye Mwenye kujitosheleza katika pande zote, Naye ndiye Mwenye kustahiki ibada, tofauti na mwingine yeyote yule, na kwa kuwa tofauti na Yeye hakuna aliyekamilika na kujitosheleza, na kwa misingi hiyo ni Yeye tu anayestahiki ibada milele yote, kwa hiyo tabaka hili linamwabudu kwa maslahi hayo. Ama wanatauhidi walioleleka katika mazingira ya utume na kunywa katika chemchem safi ya maji ya ufunuo wa kiungu, wao katika nyanja za maarifa walikwenda sanjari na mafundisho ya Mwenyezi Mungu, na walijipatia maarifa na elimu kwa haraka, wakafahamu kuwa Mwenyezi Mungu ndiye Muumba wao na Ndiye muendeshaji wa mambo yote ya ulimwengu na vilivyomo ndani yake, na kwamba hakuna kinachotendeka bila idhini yake. Kwa misingi hiyo wakamnyenyekea Mwenyezi Mungu pamoja na kuwa wadhalilifu mbele ya utukufu Wake na wakasimama mbele Yake hali ya kuwa ni wenye kumnyooshea Yeye viganja vyao kwa maombi. Wakimuomba msamaha kwa yale waliyomkosea, kama ambavyo walikuwa wakimuomba wakati wa matatizo ili awatatulie matatizo yao. Pia walifanyajitihada katika kuvuna radhi za Mwe95

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 95

8/14/2017 1:18:29 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

nyezi Mungu, na kujiepusha na kila limghadhibishalo, kwa kufuata yale anayowaamrisha, na kuacha yale anayowakataza. Sanjari na kukataa kila aina ya ibada kwa yeyote asiyekuwa Yeye, bila ya kujali ana hadhi gani katika jamii. Na kwa mantiki hiyo wakawa ni mfano hai wa Aya isemayo:

“Sema similikii nafsi yangu dhara wala nafuu isipokuwa apendavyo Mwenyezi Mungu.”51

Malengo ya washirikina katika ibada: Mkabala na malengo ya Waumini katika ibada, tunakuta malengo ya washirikina katika ibada, hakuna shaka kwamba kitendo cha Washirikina cha kutukuza na kuwanyanyuwa waabudiwa wao, kinazingatiwa kuwa ni ibada, japo kuwa ibada hiyo ni batili haimletei manufaa mwenye kuifanya, na wala haimuondolei madhara endapo yatamfika. Lakini pamoja na hayo hatuna budi kulitilia msisitizo somo la kujua malengo ya ibada kwa washirikina na siri iliyofichika nyuma ya ibada zao kwa hao waungu batili. Malengo hayo yanagawanyika sehemu kuu nne kama ifuatavyo: 1.

Lengo la kwanza: Kutafuta heshima na ushindi:

Ni ukweli usiopingika kwamba washirikina wa zama hizo za ujinga, walikuwa wakiamini kwamba nguvu, heshima na haiba ya jamii ya kibinadamu, na ushindi dhidi ya mahasimu, na maadui, yote hayo yamo katika mamlaka ya masanamu, wao ndiyo wanao uwezo wa kuhakiki upatikanaji wa mambo hayo muda wowote wautakao. 51

Surat Yunus; 10:49 96

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 96

8/14/2017 1:18:29 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Kwa misingi hiyo washirikina walikuwa wakiyanyenyekea masanamu na kudhalilika mbele yao huku wakiomba msaada, na ushindi dhidi ya wapinzani wao. Qur’ani katika aya zake imeelezea nadharia ya wanatauhidi na ile ya washirikina katika ibada, kisha ikaweka wazi tofauti ya msingi katika nadharia hizo mbili. Wanatauhidi wao wanaamini imani isiyo na chembe ya shaka ndani yake kwamba: Nguvu, ushindi, haiba na utukufu wa kijamii na mengineyo, yote hayo yamo katika mamlaka ya Mwenyezi Mungu. Kama inavyosimuliwa katika Qur’ani:

“Mwenye kutaka enzi basi enzi yote ni ya Mwenyezi Mungu.”52

Ama Washirikina wao huamini bila shaka ya kwamba yote tuliyoyataja yapo chini ya mamlaka ya masanamu ambayo wameyatengeneza wao kwa mikono yao:

“Na wamechukua miungu ghairi ya Mwenyezi Mungu ili iwape nguvu.”53

2.

Lengo la pili : Masanamu yana nafasi ya uombezi:

Lengo lingine linalopelekea washirikina kuabudu masanamu ni kwamba wanaamini kuwa masanamu yatawaombea Siku ya Kiyama, bali walikwenda mbali zaidi katika imani yao na kufikia imani ya kuwa uombezi wa masanamu hayo hauna masharti wala vipingamizi, bali unatakiwa tu kuabudu na kunyenyekea ili uweze ku52 53

Surat Fatir; 35:10   Surat Maryam; 19:81 97

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 97

8/14/2017 1:18:29 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

pata uombezi huo. Lakini Qur’ani iliipinga nadharia hiyo potofu na kubatilisha madai hayo yasiyokuwa na mashiko:

“Na ni nani huyo awezaye kuombea mbele yake bila ya idhini yake.”54 Na swala hilo limetajwa katika Aya mbali mbali za Qur’ani.

3.

Lengo la tatu: Matendo ya kiungu:

Lengo la tatu la kuabudu masanamu ni ile imani waliyokuwa nayo washirikina ya kuwa matendo yote yanayotendeka ambayo sisi tunaamini kuwa yanatendwa na Mwenyezi Mungu, kama vile utoaji wa riziki, uhai kwa viumbe, kufa kwa viumbe, uponyaji, na mengineyo, wao waliamini kuwa yote hayo yamo katika mamlaka ya masanamu. Kama tunavyosoma katika mjadala uliyojiri baina ya Nabii Ibrahimu D na washirikina, ambapo kwa Ibrahimu majukumu ya uponyaji, uongofu, kifo na uzima, kusamehe madhambi yote, na neema zote wanazoneemeka nazo wanadamu, yote hayo yapo chini ya mamlaka ya Mwenyezi Mungu:

“Ambaye ameniumba Naye ananiongoza. Na ambaye ananilisha na kuninywesha. Na ninapougua basi Yeye ananiponya. Na ambaye atanifisha kisha atanihuisha. Na ambaye ndiye ninayemtumai kunighufiria makosa yangu siku ya malipo.”55 54 55

Surat Baqarah; 2:255   Surat Shuaraa; 26:78 – 82 98

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 98

8/14/2017 1:18:29 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Lakini imani ya washirikina ya kwamba mambo hayo yanamilikiwa na masanamu, hiyo ndiyo iliyowafanya wayaabudu masanamu hayo kwa ndoto na tamaa za kupata neema hizo. 4.

Lengo la nne: Masanamu ni mithili ya Mwenyezi Mungu:

Aya hizi zifuatazo zinaonesha wazi kwamba washirikina waliyafanya masanamu yao kuwa sawa na Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo matendo yote ambayo Wanatauhidi (waumini) wanaamini kuwa ni matendo ya Mwenyezi Mungu peke Yake, washirikina waliamini kuwa hata masanamu yao, yenyewe katika uwenyewe wao yanaweza kufanya yote yanayofanywa na Mwenyezi mungu:

“Na katika watu kuna wanaofanya waungu wasiokuwa Mwenyezi Mungu, wanawapenda kama kumpenda Mwenyezi Mungu…..”56

Hayo ndiyo malengo yaliyopelekea washirikina kuabudu masanamu. Lakini tunaweza kuhitimisha somo letu kwa kutoa muhtasari wake: 1.

Hakika Washirikina wa zama za utume waliamini juu ya uwepo wa waungu wadogo ambao Mwenyezi Mungu - baada ya kuumba - aliwakabidhi mambo yote muhimu, moja wapo ni jukumu la kuendesha ulimwengu, kwa tafsiri nyepesi: Waliyatunukia masanamu nafasi ya malezi na uendeshaji wa kila kitu ulimwenguni. Na kwa misingi hiyo wakayaabudu masanamu hayo.

Uungu wa masanamu na utawala wao juu ya ulimwengu haukuwa na mipaka maalumu bali uligusa kila nyanja kama ilivyokuwa katika zama za Nabii Ibrahimu ambapo washirikina walinasibisha 56

Surat Baqarah; 2:165 99

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 99

8/14/2017 1:18:29 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

kwa masanamu, uponyaji, mvua, kusamehe madhambi, uombezi, na mengineyo. 2.

Baadhi ya watu wanaweza kufikiria kuwa nadharia ya washirikina juu ya uungu wa masanamu yao iliishia kuamini kuwa masanamu yanamiliki nafasi ya uombezi tu. Lakini si hivyo, kwani tukizichunguza kwa makini Aya zilizotangulia tunaona kuwa imani yao ilikwenda mbali zaidi hadi kufikia kuamini kuwa: Ushindi, kushindwa, msamaha, nguvu, yote hayo ni majuku ya masanamu yao. Yaani masanamu ndiyo yaliyokuwa yamebaba majukumu yote ya Mola Mlezi.

Kisha imani ya kuwa uombezi unaokubalika mbele ya Mwenyezi Mungu ni uombezi wa masanamu, bado haitoshi kuwa ni kigezo cha kuyafanya masanamu hayo kuwa sawa na Mwenyezi Mungu, na ndiyo maana watajuta Siku ya Kiyama kutokana na imani yao hiyo:

“Wallah! Hakika tulikuwa katika upotevu ulio wazi. Tulipowafanya sawa na Mola wa walimwengu wote.”57

Na huo ndiyo ukweli ya kwamba wao hawakuishia kuamini kuwa masanamu yatawaombea siku ya mwisho, bali walivuka mipaka na kuyafanya kuwa sawa na Mwenyezi Mungu. 3.

57

Malengo ya washirikina katika kuabudia masanamu yaliambatana na imani ya kwamba masanamu hayo yanamiliki nafasi nyeti katika kuendesha ulimwengu, na kwa misingi ya imani hiyo waliyaabudu na kuyanyenyekea wakiyazingatia kuwa ni miungu, inayowaongoza na itakayowaombea Siku Mwisho.

Surat Shuaraa; 26:97 - 98 100

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 100

8/14/2017 1:18:29 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

4.

Kwa kuzingatia mambo tuliyoyasema hapo awali, tunaweza kutoa tafsiri kamili na sahihi ya neno ibada kuwa: Ibada ni ibara ya unyenyekevu ufanywao na mnyenyekeaji kumfanyia yule anayemuamini kuwa ni mungu. Sasa wewe ukimnyenyekea mtu hali ya kuwa huamini juu ya uungu wake, unyenyekevu huo si ibada.

5.

Tulikwishaweka wazi kuwa ili ibada halisi ipatikane, ni lazima zipatikane chembe msingi zinazounda kitu ibada, nazo ni unyenyekevu na itikadi juu ya uungu wa yule unayemnyenyekea. Kwa tafsiri nyepesi ni kwamba unyenyekevu pasina kuambatana na imani ya kuamini kuwa unayemnyenyekea ni Mungu hiyo haitakuwa ibada, hata kama utanyenyekea kupita kiasi bado hautahesabika kuwa ni ibada maadamu tu unyenyekevu huo hauna imani ya uungu ndani yake. Kwa mantiki hiyo tunaweza kuyahukumu matendo yote yafanywayo na wafuasi wa Manabii kuwa si ibada, bali yanasadikiwa kuwa ni sehemu tu ya kuwaheshimu na kuwatukuza Manabii na wala si kuwaabudu. Kwa kuwa wapenzi wa Manabii wanapowatukuza Manabii wao, utukuzaji wao huwa haufungamani na imani juu ya uungu wa Manabii hao. Bali wao huamini kuwa Manabii ni waja wema wa Mwenyezi Mungu ambao hawamuasi Mwenyezi Mungu katika yale anayowaamrisha. Matendo yanayofanywa na wapenzi hao wa Manabii ni kama vile:

6.

Kubusu kuta za kaburi, na milango ya jengo ambalo ndani yake wamezikwa Manabii au Mawalii, au waja wema wa Mwenyezi Mungu. Kwa mfano tunapotembelea msikiti wa ngamia na kubusu kaburi la Sheikh wetu Mohamed Nassor tendo hilo si ibada kwani haliambatani na imani juu ya uungu wa Sheikh, bali tendo hilo linaashiria mapenzi yetu na heshima yetu kwa 101

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 101

8/14/2017 1:18:29 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Sheikh Mohamed Nassor. Pia linaashiria shauku yetu ya kutaka kuiga mapito yake, asaa huenda nasi tukajaliwa kuwa kama yeye, au kumkaribia japo kidogo. 7.

Kuswali kwenye maeneo walipozikiwa Manabii na Mawalii, ili kupata baraka ya ardhi hiyo ambayo imehifadhi miili hiyo mitukufu, kama vile tunavyosali katika makamu Ibrahimu, kwa kuitikia wito wa Mwenyezi Mungu:

“Na pafanyeni alipokuwa akisimama Ibrahimu ni mahali pa kuswalia.”58

8.

Kumwomba Mungu kwa kupitia Nabii Wake au walii Wake, kuomba huko ima uombe kupitia Nabii mwenyewe, kwa mfano ukasema kwa jina la Muhammad, au ukaomba kupitia baraka, ukasema kwa baraka za Mtume Muhammad, au kwa baraka za Sheikh Abdul Qaadir Jailani, au ukamwambia mtu mtakatifu akuombee kwa Mwenyezi Mungu, kama vile watoto wa Nabii Yakub walivyomwomba baba yao Nabii Yakub awaombee msamaha kwa Mwenyezi Mungu. Matendo yote hayo si ibada kwa kuwa hayana hata chembe ya imani juu ya uungu wa watakatifu hao.

9.

Kutafuta uombezi kwa Manabii si shirki kwa kuwa tunapotaka uombezi huo huwa tunautaka hali ya kuwa tunaamini ya kuwa Manabii ni watu waliopewa idhini ya kuwaombea watu msamaha. Na Qur’ani imelithibitisha hilo katika Aya nyingi tu. Mpenzi msomaji huo ndiyo muhtasari wa ibada na mipaka yake. Zingatia somo hilo kwani ni jibu la maswali mengi ya

58

Surat Baqarah; 2:125 102

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 102

8/14/2017 1:18:29 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

fitina yanayopandikizwa na Mawahabi katika jamii za Kiislamu ili kuwatatiza watu wasiokuwa na maarifa ya kutosha, na tayari wameshafanikiwa kuwapotosha wengi. Na wale ambao imeshindikana kuwapotosha, wote walinasibishwa na shirki wakaambiwa kuwa ni waabudu makaburi. Msomaji wetu utakuwa unakumbuka kuwa tuliwahi kusema kuwa: Mawahabi wamekuwa wakizunguka kila sehemu na maneno matatu, Tauhidi, Shirki na Bidaa, na kwa maneno hayo ambayo hawana ufahamu nayo, wamepotosha wengi wasiokuwa na maarifa. Na mpaka hapa tumefikia mwisho wa somo hili isipokuwa naona kuna ulazima katika somo lijalo kuzungumzia ufahamu wa Bidaa katika dini.

103

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 103

8/14/2017 1:18:29 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

SEHEMU YA TATU

BIDAA Je, unafahamu nini linapotamkwa neno Bidaa?

W

apenzi wasomaji, genge la Mawahabi hupotosha watu kwa maneno matatu ambayo hawana ufahamu nayo, maneno yenyewe ni: Tauhidi, Bidaa, na Shirki, na tumekwisha kuizungumzia tauhidi kwa kiasi tulichowezeshwa na Mwenyezi Mungu, kwani tauhidi ni mithili ya bahari isiyofahamika urefu wa kina chake. Katika somo hili tutazungumzia Bidaa, neno ambalo Mawahabi hulitumia kama uchochoro wa kufichia imani zao za kizandiki na chakavu za kukufurisha kila asiyekuwa Muwahabi. Na kwa misingi hiyo pia wamefanikiwa kupotosha wengi wasiokuwa na maarifa ya kutosha. Nasi tumeona ulazima wa kutoa utangulizi utakaobeba vipengele muhimu, kabla ya kuingia kwenye ufafanuzi wa maana ya neno Bidaa. Bidaa katika dini: Mwalimu wetu Sheikh Ja’far Subhani anasema: “Tauhidii ya Ibrahimu (ambayo ndiyo jiwe la msingi la dini zote zitokanazo na mafundisho ya mbinguni) ina ngazi na daraja nyingi. Wanatheolojia wa Kiislamu wamezifanyia utafiti mpana na wakazizungumzia katika pande zake zote na wakaandika vitabu na makala nyingi katika uwanja huo.” Sasa moja ya ngazi hizo nyingi za tauhidi ni: Tauhid Ii Fitashrii, yaani imani juu ya uwepo wa mamlaka moja inayopanga sheria na kanuni, na si mwingine bali ni Mwenyezi Mungu. Na hakuna yeyo104

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 104

8/14/2017 1:18:29 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

te mwenye haki ya kupanga sheria kwa mtazamo wake na kufanya kuwa ni wajibu kwa kila mwanadamu kuishi chini ya misingi ya sheria hiyo. Bali ni wajibu kwa kila muumini aamini kinadharia (sanjari na vitendo), kwamba haki ya upangaji wa kanuni na sheria na maelekezo, na mipangilio na kuainisha uhuru wa mwanadamu, na kipi kinamfaa na kipi hakimfai, yote hayo yako chini ya mamlaka ya Mwenyezi Mungu, bila kushirikiana na yeyote katika viumbe Wake. Yeye tu ndiye mwenye haki na maamuzi ya mwisho juu ya viumbe na vyote wanavyovimiliki. Yeye ndiye mtoaji wa amri na Yeye ndiye mwenye mamlaka ya kukataza jambo lolote analoliona kuwa halina maslahi au faida kwa wanadamu. Mpaka hapa tunaweza kuzithibitisha ngazi hizo za tauhidi kwa kupitia mifumo miwili mikuu ifuatayo: 1 - Mfumo wa kiakili 2 - Mfumo wa kunukuu maandiko. Tukianza na mfumo wa kwanza, tunasema kuwa: Hakika suala la kuhusisha upangaji wa sheria na Mwenyezi Mungu, si zao la upeo duni wa kifikara tulionao wanadamu, na si mtazamo mfinyu wala jazba zetu za kidini na kimadhehebu, bali ni zao la mtazamo chanya wa mambo katika uhalisia wake. Mtazamo huo ndiyo unaotushika mkono na kutupeleka katika imani ya kuamini juu ya uwepo mmoja, upangao sheria na kanuni katika nyanja zote za maisha ya mwanadamu, yawe ya kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiitikadi. Sasa tunaposoma mazingira katika uhalisia wake, tunajikuta kuwa hatuna budi kwanza kuangalia sifa na vigezo stahiki kwa mpanga sheria na kanuni kwa wanadamu, ili sheria na kanuni zake ziwe ni zenye kukidhi mahitaji ya wanadamu, na ziendazo sawia na nyakati, vivyo hivyo na mazingira tunayoishi ndani yake. 105

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 105

8/14/2017 1:18:29 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Sifa na vigezo vya mpanga sheria kwa wanadamu: 1.

Awe ni mwenye maarifa na ujuzi timilifu, juu ya mwanadamu na mazingira yanayomzunguka, katika pande zote mbili hasi na chanya.

2.

Apange kanuni na sheria zitakazomnufaisha mwanandamu, na zisiwe ni sheria za kulinda maslahi yake, binafsi. Kwa ibara nyingine asiwe muumini wa sera ya Mimi kwanza.

3.

Awe safi kwa maana ya kutosifika na kila sifa iashiriayo upungufu katika uwepo wake mtakatifu, kama vile tamaa za kimwili, uchoyo, umimi kwanza, na sifa nyinginezo zisizostahiki. Awe ni mwenye uhuru wa maamuzi (katika kila analoliona kuwa lina maslahi kwa waja wake) bila ya kuingiliwa katika maamuzi yake na madola yenye nguvu.

Msomi wetu mtukufu hebu tuachilie mbali ushabiki na tuseme kwa uadilifu: Hivi katika viongozi tulionao leo hii, ni wangapi tunaweza kuwakuta na sifa hizo zote tulizozitaja? Kama tutajibu kwa uadilifu bila ushabiki basi jawabu litakuwa ni hasi, yaani hakuna mwanadamu mwenye sifa hizo bali ni Mwenyezi Mungu pekee ndiye mwenye sifa hizo pasina kushirikiana na yeyote katika viumbe Wake. Na hii ni kutokana na sababu zifuatazo: a.

Ni lazima kwa mpanga sheria awe ni mwenye kumjua vizuri mwanadamu tena kwa kina ili kupitia ujuzi huo aweze kudhibiti hamasa na matamanio yake (mwanadamu) ikiwa ni pamoja na kumuwekea mstari mnyoofu atakaoufuata, na kanuni ziendazo sawia na matakwa yake. Kwa mfano mwanadamu ana tamaa za mwili lakini Mwenyezi Mungu ameweka sheria inayokwenda sawa na matamanio hayo ambayo ni sheria ya ndoa. Yote hayo yamewekwa na Muumba 106

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 106

8/14/2017 1:18:29 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

ili tu mwanadamu aweze kuitakasisha nafsi yake na kuilea malezi bora yatakayomfikisha kwenye kilele cha uongofu na ukamilifu, ambao ndiyo lengo la kuumbwa mwanadamu. Sanjari na kumjua mwanadamu, mpanga sheria ni lazima pia awe na ujuzi na elimu timilifu ya kuifahamu jamii kikamilifu katika pande zote, na hapo ndipo atakapoweza kujua nyadhifa na majukumu ya kila mmoja katika jamii, kwa namna moja, na kujua haki zilizo wajibu kutekelezwa na jamii (na si kutelekezwa) kwa namna nyingine. Vivyo hivyo mtunga sheria ni lazima ajue mwenendo wa harakati za wanajamii, na vikwazo viletavyo athari hasi katika harakati zao, na ajue pia radiamali waioneshayo mbele ya shinikizo na vikwazo. Hakuna shaka na ni ukweli usiopingika kuwa: Vigezo hivyo tulivyovitaja, ni vigezo ambavyo tunavipata kwa Mwenyezi Mungu, bila ya kuwepo yeyote katika waja Wake anayeshirikiana naye katika sifa Zake chanya, na yakinifu. Hata awe na elimu ya namna gani, bado elimu yake hiyo itakuwa na mapungufu mengi. Na ndiyo maana tunakuta kuwa Qur’ani ni Katiba inayoishi na zama zote, kutokana na ukweli usiopingika kuwa Katiba hiyo, imeundwa na mjuzi, anayemjua vizuri mwanadamu pamoja na mazingira yake, kwani yeye ndiye muumba wa kweli na wapekee. Kama tunavyosoma katika Qur’ani tukufu zile Aya zinazotilia msisitizo swala hili:

Hivi asijue aliyeumba, Naye ni Mpole, Mwenye habari.59

Kisha Mwenyezi Mungu ambaye aliyemuumba mwanadamu, katika umbo la kipekee na kustaajabisha, Yeye peke Yake ndiye 59

  Surat Mulk; 67:14 107

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 107

8/14/2017 1:18:29 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Mjumzi wa mahitaji yote ya mwanadamu, yale ya wazi na yale yaliyofichika, na Yeye tu Ndiye Mjuzi wa yale yenye manufaa na yenye madhara kwa mwanadamu. Na yenye faida na yenye hasara yote anayajua kwa kina zaidi, na wala hakuna anayemfikia katika maarifa na hakuna pia atakayemfikia milele yote. Na Yeye tu Ndiye Mjuzi wa mwenendo wa harakati za wanajamii, na mfumo wa maisha wanayotakiwa kuishi, na radiamali zao mbele ya sheria na kanuni. Na pia ni Mjuzi wa kuainisha nyadhifa na majukumu ambayo yaweza kuwa chachu ya mafungamano ya kijamii na kuipeleka jamii kwenye uhuru wa maamuzi sanjari na kuifikisha jamii hiyo kwenye kilele cha ukamilifu, na kumuweka mwanadamu mahala ambapo anastahiki kuwa. b. Uhalisia na ulindaji wa maslahi ya mwanadamu na manufaa yake, unamlazimu mpanga sheria kuwa mbali na kila aina ya matamanio, na asiwe na hata chembe ya umimi kwanza, na asiwe na pupa ya kutaka kujiletea maslahi yake kwanza, kupitia sheria anazozipanga. Na hiyo ni kutokana na kuwa matamanio yanayomshinikiza mwanadamu, kama vile umimi kwanza, yanazingatiwa kuwa ni ngome nzito na kizuizi kikuu kati ya mpanga sheria na uhalisia wa mambo, kwa kuwa mpanga kanuni na sheria kwa vyovyote vile atakavyojitahidi kadri ya uwezo wake, kujitakatifisha na kujikomboa kutoka katika gereza la matamanio na umimi kwanza, lakini bado kwani katika hali ya kutojitambua na bila ya hiari, yale matamanio hupenyeza athari zake hasi, zinazopelekea mpanga kanuni kuchezea kanuni alizozipanga, na hatimaye kutoka katika njia nyoofu na njia ya ukweli. Katika somo hili tunaendelea na kipengele kilichobakia. Kwanza kabisa ningependa kutoa muhtasari wa nukta tuliyoishia. Katika nukta yetu tuliyoishia tulisema kuwa: 108

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 108

8/14/2017 1:18:29 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Ili mpanga sheria aweze kupanga sheria itakayolinda maslahi ya jamii, ni lazima atakasike na kila sifa hasi. Asiwe na hata chembe ya umimi kwanza, ndipo atakapoweza kupanga sheria zenye manufaa kwa wanadamu, sheria ambazo misingi yake ni kumuinua mwanadamu na si kumnyonya, kama ilivyokuwa ni desturi kwa serikali nyingi, kupanga sheria kwa lengo na shabaha ya kulinda maslahi ya viongozi na kuwasahaulia mbali wananchi. c.

Hakika mapenzi na ushabiki wa kiitikadi au kisiasa, na uoga mbele ya madola yenye nguvu, yanayoingilia kimabavu maamuzi ya serikali nyingine, hiyo pia ni sababu nyingine iwezayo kumtoa mpanga sheria katika mstari uliyonyooka, kwani ni mara ngapi tumeshuhudia baadhi ya nchi zinazodai kuwa huru, zikipanga sheria kwa maslahi ya wananchi wake, lakini madola yenye nguvu yanaziingilia sheria hizo, na waliozipanga wanabaki kimya na hakuna wa kufungua mdomo.

Hakuna shaka kuwa mpanga sheria anayepanga sheria zake katika mazingira ya kuwaogopa watu fulani katika wale wenye mamlaka ya kuingilia maamuzi ya wenzao, bila shaka sheria hizo zitakuwa ni zenye kuzingatia maslahi ya watu fulani, na hazitakuwa kwa ajili ya kumnufaisha mwananchi, Kwa hiyo hata kama mwananchi atakuwa anakandamizwa namna gani, kiongozi huyo aliyepanga sheria hatojali kwa sababu tu, anachokifanya kinamridhisha bwana mkubwa. Kisha uwepo wa vitisho toka kwa watu wenye nguvu za kuwapangia wenzao sheiria, uwepo huo bado ni kikwazo kwa kiongozi, katika upangaji wake wa sheria na kanuni. Uwepo wa nguvu hiyo ni sawa na uwepo wa upanga mkali shingoni mwa yule kiongozi mpanga sheria, upanga ambao humuwezesha yule aliyeushika kumburuza yule mpanga she109

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 109

8/14/2017 1:18:29 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

ria na kumpeleka akutakako yeye, na kutekeleza kila alitakalo yule mheshimiwa mwenye upanga mkononi, kiasi ambacho yule mpanga sheria atabaki na hiari ya moja ya mambo mawili, ima akubali kutii udhalili wa kutii matakwa ya yule mheshimiwa, kwa kuhalalisha sheria zinazokubaliana na matakwa ya yule mheshimiwa, Kama vile ambavyo baadhi ya waheshimiwa walileta sheria ya ndoa ya jinsia moja, na kutaka wapanga sheria wa nchi mbali mbali wazihalalishe na wazifuate sheria hizo, udhalili ulioje huo!! Jambo la pili, ni ima akatae matakwa ya waheshimiwa, na hapo ndipo atakapokabiliwa na aina zote za upinzani. Atakabiliwa na vikwazo vya kisiasa, kiuchumi, vita za wenyewe kwa wenyewe, na atafikishwa katika mahakama za kimataifa, au atafukuzwa nchini na kwenda kuishi uhamishoni kama mkimbizi, na mengineyo mengi. Mpaka hapa tunaona umuhimu wa kupatikana vile vigezo tulivyovitaja hapo awali, na tunaona namna ambavyo uhuru wa maamuzi ulivyo na nafasi nyeti katika kupanga sheria. Na pia tunaona kuwa kujitosheleza na kutomuhitajia mtu kunaleta heshima kwa yule anayepanga sheria, kwani hakuna awezaye kumletea vitisho na masharti, kama vile ambavyo kiongozi asiyejitosheleza awekewavyo mashrti. Hupata kuambaiwa usipofanya kitu kadha hupati msaada, kwa hiyo hatimaye inamlazimu kuhalalisha hadi mambo machafu ili tu aweze kupata msaada huo. Kwa hiyo tukitaka kuwa na mpanga sheria mwenye uhuru wa maamuzi, asiyetaka mchango wa mawazo toka mashariki wala magharibi, na anayejitosheleza kwa kila kitu, hatuwezi kupata mwingine zaidi ya Mwenyezi Mungu. Yeye tu Ndiye Mwenye sifa zote hizo chanya. Na kwa misingi hiyo akastahiki kwa hukumu ya akili kuwa Ndiye Mwenye mamlaka hiyo ya kupanga katiba na kanuni inayotoa mfumo kamili wa maisha ya mwanadamu. 110

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 110

8/14/2017 1:18:29 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Na kwa bahati nzuri baadhi ya wanafikara wa Kimagharibi, wamezinduka na kuoana umuhimu wa kuwepo vigezo hivyo kwa mpanga sheria, ili kuweza kupata sheria itakayoweza kumlinda mwanadamu, sanjari na maslahi yake, badala ya kuwa na sheria inayomkandamiza na kutetea maslahi ya washimiwa fulani. Mmoja wa wanafikara hao wa Kimagharibi anasema katika kitabu chake kilichofasiriwa kwa Lugha ya Kiarabu kwa jina Al-Aqddul ijtimai: “Ili kupata kanuni bora zenye manufaa kwa mataifa yote, basi ni lazima ipatikane akili yenye kujua matamanio yote ya kibinadamu, lakini matamanio na mahitaji hayo yasiwe na nafasi kwake. Akili hiyo iwe ni akili ambayo haifungamani na maumbile ya kibinadamu, na wala hainyenyekei mbele ya shinikizo na vikwazo vya mataifa yenye nguvu, bali yenyewe katika uwenyewe wake inakuwa ni akili yenye kuyafahamu yote hayo ukweli wa kuyafahamu. Akili ambayo utukufu wake na ukamilifu wake hautegemei utukufu na ukamilifu wetu, isipokuwa akili hiyo ni akili yenye utayari wa kutusaidia sisi kwa kututoa katika usisi wetu na kutupeleka katika kilele cha ukamilifu unaotakiwa na kila mwanadamu.” Mpenzi msomaji, mpaka hapa utakuwa umefahamu japo kwa muhtasari hoja zetu za kiakili tunazozitumia katika kuthibitisha madai yetu ya kuwa: Mwenyezi Mungu peke Yake Ndiye Mwenye haki na mamlaka ya kupanga sheria na kanuni kwa wanadamu, na kutokuwepo yeyote anayeshirikiana naye katika hilo, hata awe ni mtu mwenye elimu na maarifa ya namna gani. Je, ni nani mwenye mamlaka ya kupanga sheria katika Uislam? Kwa hakika na ukweli usiopingika na kila mwenye akili huru ambayo haijajaladiwa ni kwamba: Qur’ani inaunga mkono hoja ya akili ya kukabidhi mamlaka ya kupanga sheria kwa Mwenyezi Mungu tu, kiasi ambacho Aya nyingi za Qur’ani zinazingatia kuwa, haki ya 111

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 111

8/14/2017 1:18:29 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

kuwapangia sheria viumbe ni ya Mwenyezi Mungu. Yaani ni haki inayomhusu Mwenyezi Mungu peke Yake bila ya kushirikiana na yeyote. Na wala haifai kwa wanadamu kuvuka mipaka katika haki hiyo. Na tukichunguza Aya zilizoshuka katika kuunga mkono suala hilo ni nyingi ila hapa tutataja baadhi tu kwa ajili ya kupigia mfano, na kuepuka kurefusha mada:

1. “Hapana hukumu isipokuwa ya Mwenyezi Mungu tu. Ameamrisha msimwabudu yeyote isipokuwa Yeye tu.

Hiyo ndiyo dini iliyonyooka, lakini watu wengi hawajui.”60

Aya hii inazungumza kwa lugha nyepesi kabisa kwamba: Aina zote za hukumu na kanuni ni katika mambo stahiki ya Mwenyezi Mungu. Na kwa kuwa ni katika mambo yanayomhusu Yeye tu, ndiyo maana katika Aya hiyo, baada ya kuzungumzia hukumu, pale pale ikafuata amri ya ibada, na unyenyekevu, Kwake Yeye tu.

2. “Wamewafanya makuhani wao na watawa wao kuwa ni miungu badala ya Mwenyezi Mungu na Masia mwana wa Maryamu…..”61

Aya hii pia inazungumza kwa lugha ya wazi na nyepesi kwa kila mwanadamu ambaye hajajaladia akili yake, kwamba: Watu 60 61

Surat Yusuf; 12:40   Surat Tauba; 9:31 112

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 112

8/14/2017 1:18:29 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

waliopewa Kitabu (Mayahudi na Manaswara) walivuka mipaka waliyowekewa, na kuikabidhi mamlaka ya sheria na kanuni kwa makasisi wao na watawa wao, badala ya kukifanya kitabu cha Mwenyezi Mungu kuwa ndiyo marejeo ya kutambua hukumu na sheria za Mwenyezi Mungu. Wao walirejea kwa makasisi wao hali ya kuwa inafahamika wazi kwamba makasisi wanaweza kuharamisha kitu ambacho Mwenyezi Mungu amekihalalisha, endapo tu kitu hicho kitakuwa dhidi ya maslahi yao. Na wanaweza pia kuhalalisha kitu ambacho Mwenyezi Mungu amekiharamisha, kwa ajili ya kuchunga na kulinda maslahi yao binafsi. Kwa sababu hiyo Qur’ani haiwatambui Mayahudi na Manaswara kama waumini wa uwepo Mmoja wenye mamlaka ya kupanga sheria kwa wanadamu, bali (yenyewe) Qur’ani inawachukulia kuwa ni watu waliotoka katika mstari wa imani hii ya kuamini juu ya uwepo Mmoja upangao sheria na kanuni zinazostahiki kufuatwa na wanadamu wote. Je, kama haki ya kupanga sheria ni ya Mwenyezi Mungu peke Yake, ni yapi majukumu ya baraza la sheria katika nchi za Kiislamu? Swali hili linaweza kupatiwa jibu kwa namna mbili zifuatazo: 1.

Hakuna shaka kuwa kila nchi hufanya jitihada ya kuleta ustawi na fanaka kwa watu wake, sanjari na kuweka sawa mipango ya kuendesha maisha katika mfumo sahihi. Kwa mantiki hiyo ni lazima ziandaliwe asasi zitakazoweza kubeba jukumu hilo, na kupanga mikakati na ratiba za kurahisisha harakati za nchi na mueleko wake. Sasa upatikanaji wa baraza au asasi itakayosimamia jukumu hilo, utakuwa ni jambo la maana na lenye manufaa.

113

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 113

8/14/2017 1:18:29 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

2.

Baada ya kufahamu umuhimu wa baraza la sheria katika nchi ya Kiislamu, na mpangilio wa harakati zake, hatuna budi kulitilia msisitizo suala la kubainisha wigo wa harakati za wajumbe wa baraza hilo. Je, wajumbe hao watakuwa ndani ya wigo wa matakwa yao, usiokuwa na mipaka, na ulio nje ya kanuni za Mwenyezi Mungu, na katika njia inayokinzana na sheria ya Mwenyezi Mungu? Ama watakuwa ndani ya wigo wa sheria na kanuni za mbinguni wakielea katika anga lake, wakitegemea misingi yote ya Uislamu?

Hakika usuli wa baraza la sheria katika nchi za Kiislam, ni sheria zilezile za Kiislam. Kwa hiyo baraza halitakuwa na jukumu la kuunda sheria zitakazokuwa nje ya wigo huo wa sheria za Mwenyezi Mungu, isipokuwa jukumu lake ni kuweka mpangilio na ratiba kwa kutegemea kanuni hizo, na misingi inayokubalika, yaani isiyokinzana na sheria. Uwepo wa baraza la sheria haumaanishi upatikanaji wa sheria dhidi ya zile za Mwenyezi Mungu, bali sheria za Baraza la Sheria zimo ndani ya wigo wa kanuni za Mwenyezi Mungu. Kuchezea sheria ni bidaa: Kama tulivyokwishasema kuwa haki ya sheria ni ya Mwenyezi Mungu, kwa hiyo haifai kwa mwanadamu kujitwalia majukumu hayo, kama ambavyo haifai kwa yeyote kufanya mchezo katika sheria kwa njia yoyote ile, iwe ya kuzidisha au kupunguza, yote hayo ni Bidaa na ni katika madhambi makubwa yenye kuangamiza. Na atakayeifanya Bidaa hiyo, atakuwa ametoka nje ya wigo wa Tauhidi Fitashrii, yaani atakuwa nje ya wigo wa imani ya kuamini juu ya uwepo mmoja upangao sheria. Na kwa kumaliza utangulizi huo hatuna budi kuitafsiri Bidaa tafsiri ya kimantiki na kuichambua kwa mapana katika pande zake 114

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 114

8/14/2017 1:18:29 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

zote, uchambuzi ambao waweza kuwa ni jibu la maswali na hoja zote chakavu zitokanazo na ufahamu duni wa Mawahabi. Maana ya Bidaa: Baada ya kumaliza mazunguzo juu ya utangulizi wa maana ya neno Bidaa, ambao ndani yake tulibainisha yale yote yanayohusu sheria, na tukatoa wasifu kamili wa mpanga sheria, na tukafafanua kuwa mabaraza ya sheria katika nchi za Kiislam, hayo si mabaraza ya kutunga sheria mpya, nje ya wigo wa sheria za Mwenyezi Mungu, bali sheria za mabaraza hayo huchukuliwa kutoka katika mfereji wa chemchem ya ufunuo wa Mwenyezi Mungu. Na mpaka hapa tumeona kuwa utangulizi huo watosha kumpa mwanga msomaji na kumwezesha kuingia katika somo rasmi la tafsiri ya maana ya Bidaa. Na tunapotaka kutafsiri neno Bidaa basi ni lazima tafsiri yetu iguse pande zote mbili: Upande wa kilugha na upande wa kielimu, yaani tafsiri ya neno kwa mjibu wa Lugha ya Kiarabu na kwa mujibu wa wanatheolojia. 1.

Bidaa katika kamusi za lugha ya Kiarabu:

Ni kuzusha kitu ambacho hakijawahi kuwa na uwepo, wala utajo, wala ujulikano.62 Ama Ibnu Faris yeye anasema kuwa, Bidaa ina maana mbili, lakini sisi tutataja moja ambayo inahusiana na somo letu. BIDAA: Ni kuanzisha kitu na kukitengeneza bila kuwa na mfano.63 Anasema Raghib al-Isfahani: Bidaa ni kubuni muundo bila kuiga.64   Kitabul ain, uk. 72.   Maqaayisu al Lughah, Jz. 1, uk. 209 64   Mufradaat Raghib, uk. 38-39. 62 63

115

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 115

8/14/2017 1:18:30 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Maoni ya wanachuoni katika uwanja huu: “Na ni katika mambo yasiyokuwa na shaka kuwa upenyesho na ubunifu, ni fikra inayomtawala mwanadamu, na ndiyo maana tunapata kumuona ni mwenye shauku ya vitu vya kisasa, ambavyo havijatanguliwa na uwepo hapo kabla. Na mwanadamu huyo huyo huwa hachelewi kuyapa mgongo maisha ya kimila yasiyokubali mabadiliko, na kuelea katika maisha ya kisasa na yanayobadilika kutokana na nyakati. Kwa hoja hiyo tumekuwa tukiona Wahandisi kila kukicha wao wako katika mchakato wa kila mmoja kuleta kitu ambacho mwingine hajawahi kuleta, na kila siku wanabuni kitu kipya tofauti na kile cha jana, kazi hiyo katika Lugha ya Kiarabu inaitwa bidaa kwa maana yaubunifu. Na kwa kuzingatia maana hiyo hiyo, Mwenyezi Mungu pia anaitwa, Mbunifu (Albadiu).

“Mbunifu wa mbingu na ardhi”65 kwa nini aitwe mbunifu, ni kwa sababu amezusha au amebuni umbo ambalo halijawahi kuwa na uwepo, tena kalitengeneza bila kuiga muundo kwa yeyote. Na vivyo hivyo amemuumba mwanadamu katika umbo zuri la kupendeza kwa ubunifu Wake Mwenyewe, na bila ya kuiga umbo hilo zuri kutoka kwa yeyote yule ajiitaye mbunifu.

Hiyo ndiyo maana ya BIDAA, yaani kuzusha kitu kipya ambacho hakijawahi kuwepo, na Bidaa kwa maana hiyo si lengo la somo letu hili, na vile vile Bidaa kwa maana hiyo si Bidaa ile inayoharamishwa na kukatazwa katika matini za dini (maandiko ya dini), kwa kuwa dini haiko dhidi ya maendeleo na wala haipingi upya katika maisha ya mtu binafsi au maisha ya jamii kwa jumla. Jamii ya wanadamu leo hii inaishi katika hali ya kutaka mabadiliko na mitindo mbali mbali katika nyanja zote. Kuanzia makazi, kila 65

Surat Baqarah; 2:117 116

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 116

8/14/2017 1:18:30 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

siku tunashuhudia mitindo mbalimbali ya majengo, kadhalika katika mavazi, na katika vipando. Kwa hiyo majumba yaliyokuwepo hapo zamani ni tofauti kabisa na yale tuyaonayo leo hii. Na mavazi yaliyotumika hapo zamani za kale ni tofauti kabisa na yale ya sasa. Vile vile usafiri uliotumika hapo zamani, ni tofauti na ule utumikao leo hii. Mbinu za ufundishaji za kileo ni tofauti na zile za kizamani, yote hayo ni zao la akili ya ubunifu aliyopewa mwanadamu. Mambo yote tuliyoyataja hapo juu yanaingia katika tafsiri ya neno Bidaa kwa mujibu wa Lugha ya Kiarabu, lakini Bidaa kwa maana hiyo si Bidaa ile inayokusudiwa kwa mtazamo wa wanazuoni kuwa ni katika madhambi makubwa. Hiyo ilikuwa sehemu ya kwanza ya tafsiri ya neno Bidaa kwa mujibu wa kamusi za Lugha ya Kiarabu. Lakini hilo si lengo letu la kuandaa somo hili, bali lengo letu ni kutafsiri Bidaa kwa mujibu wa vitabu vya theolojia na vitabu vya sheria, na hiyo ndiyo tafsiri ya kielimu. 2.

Bidaa kwa mtazamo wa kielimu:

Kwa mujibu wa wanatheolojia, na watu wa sheria ya Kiislamu, wao wanaona kuwa Bidaa ni katika mambo yasiyonashaka juu ya uharamu wake, na ni katika mambo ambayo sheria imesisitiza watu kuyaacha na kujiepusha nayo. Na pia sheria tukufu licha ya kuwakataza watu, inaizingatia Bidaa kuwa ni katika madhambi makubwa yawezayo kumfikisha mwenye kuifanya katika moto, sawa sawa Bidaa hiyo iwe kwa njia ya kuzidisha vitu vipya na sheria mpya katika dini, au iwe kwa njia ya kupunguza na kufuta baadhi ya vifungu vya sheria. Na kwa misingi hiyo wanatheolojia na wasomi wa sheria wote kwa pamoja wamelipa suala hili umuhimu mahsusi, na kulijali. Na wakalifanyia tahakiki na uchunguzi uliosheheneshwa hoja za ku117

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 117

8/14/2017 1:18:30 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

tosha. Jambo hilo kama litaashiria kitu basi litakuwa linaashiria umuhimu wa kutoipuuza Bidaa, na umuhimu wa kuzijua hatari zake kupitia mtazamo wa fikra ya Kiislam. Na wasomi na watafiti, wameitafsiri Bidaa kwa tafsiri aina mbalimbali zifuatazo: 1.

Kwa mujibu wa Sharif Murtaza: Bidaa ni kuzidisha au kupunguza katika dini pamoja na kuinasibisha nyongeza hiyo au punguzo hilo kuwa ni katika dini.

2.

Kwa mujibu wa Ibnu Hajar al-Asqalaani: Makusudio ya Bidaa ni kitu kilichozushwa pasina kuwa na mashiko katika sheria, ama chenye kuwa na mashiko yanayokiunga mkono katika sheria, si Bidaa.66

3.

Kwa mujibu wa Ibnu Hajar al-Haythami: Bidaa ni chenye kuzushwa katika dini, pasina kuwepo mashiko ya kisheria ya kuunga mkono uzushi huo. Hiyo ndiyo Bidaa kwa mtamzo wa kisheria.

Tutakomea katika tafsiri hizi tatu, na kuachilia mbali zilizobakia, kwa kuwa hazitofautiani sana na hizi tulizozitaja. Na tukizichunguza kwa kina tafsiri zilizotajwa, tutazikuta zinabeba nadharia ya kwamba chembe msingi zinazounda Bidaa haramu, na zenye kutofautiana na Sunna, ni tatu:

66

1.

Kuongeza au kupunguza katika dini imani au hukum.

2.

Ukosekanaji wa mashiko sahihi ya kuunga mkono nyongeza au punguzo hilo.

3.

Nyongeza na punguzo viwe na uvumi katika jamii.

  Fat-hul Bari, 5/156; 17/9. 118

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 118

8/14/2017 1:18:30 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Tunaanza na kifungu namba moja: Hakuna shaka kuwa kuongeza au kupunguza katika dini, au kwa ibara nyingine: Kuleta mabadiliko yoyote katika dini iwe ni katika misingi ya imani au katika hukumu za kisheria, na kuunasibisha uzushi huo kwa Bwana Mtume 8 hiyo ni Bidaa au kwa lugha nyepesi ni ubunifu ambao haukubaliki na unakataliwa katika sheria. Ama mtu akilenga kuleta maboresho, katika baadhi ya mambo ambayo hayagusi misingi ya dini na hukumu zake, kama vile kuweka vipaza sauti misikitini, kuwepo mazulia, saa za ukutani na mengineyo ambayo hayakuwepo wakati wa Bwana Mtume 8, bado mambo hayo hayatasadikika kuwa ni Bidaa kwa maana ile inayokatazwa na sheria, japo kwa upande wa kamusi za Lugha ya Kiarabu yatasadikika kuwa ni Bidaa. Kupitia maelezo hayo tunafahamu wazi kuwa baadhi ya matendo yetu (yawe ya halali au yale ya haramu), hayaingii katika wigo wa Bidaa. Kwa mfano kucheza mpira wa miguu au wa kikapu, na michezo mingineyo ya kisasa, yote hayo pamoja na kuwa ni mambo yaliyoshamiri katika jamii tunazoishi lakini bado kabisa hayajakidhi masharti ya kuingia kwenye wigo wa Bidaa haramu. Mfano mwingine, leo hii katika jamii zetu zilizoathiriwa na mila za kimagharibi, kuchanganyika wanawake na wanaume bila kujali mipaka ya kisheria ni jambo ambalo jamii imelipokea kwa mtazamo chanya, yaani ni jambo la kawaida tu, kama vile kupeana mikono, kukumbatiana, na mmoja kumbusu mwingine yote hayo ni ya kawaida, mambo yote hayo jamii inayaona kama mambo ambayo hayana madhara na jamii haijathubutu kuyakataza, na wala haijatoa tamko la kunasibisha mambo hayo na mwenendo wa Bwana Mtume 8. Kwahiyo mambo hayo yatabakia kuwa haramu na katika madhambi makubwa, ila hayaitwi kuwa ni Bidaa kwa sababu hayajatimiza vile vigezo na masharti ya Bidaa kwa mujibu wa mtazamo wa kisheria. 119

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 119

8/14/2017 1:18:30 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Nguzo za neno Bidaa: 1.

Kuongeza au kupunguza katika dini imani au hukum.

2.

Ukosekanaji wa mashiko sahihi ya kuunga mkono nyongeza au punguzo hilo.

3.

Kisha nyongeza na punguzo viwe na uvumi katika jamii.

Tunamwomba Mola atujalie sote kuwa ni katika wale wanaosikiliza neno na kkufuata lililokuwa bora zaidi. Sharti la pili la kufanya jambo kuwa Bidaa ni ukosekanaji wa mashiko sahihi yanayounga mkono kwa njia yoyote ile, ama ikiwa litaibuka jambo ambalo watu kwa mtazamo wao wanaliona kuwa geni lakini jambo hilo likawa na mashiko sahihi ya kuliunga mkono, basi jambo hilo hatuwezi kwa njia yoyote ile kuliingiza kwenye orodha ya vitu ambavyo ni Bidaa kwa mtazamo wa sheria, bali jambo hilo kama litaitwa kuwa ni Bidaa basi ni kwa kuzingatia ile maana ya Bidaa kwa mujibu wa kamusi ya Lugha ya Kiarabu. Lakini kisheria si Bidaa kwa kuwa lina mashiko. Bali tutasema tu kwamba aliyeleta jambo hilo hajaleta kitu kipya bali kaleta kitu ambacho kilikwishatajwa, halafu watu wakajisahau juu ya uwepo wa kitu hicho. Na hayo ndiyo makusudio ya neno tuliyoyasema katika tafsiri ya Bidaa kuwa ni kuzusha jambo ambalo halina mashiko katika dini. Kwa mantiki hiyo tunakuta kuwa mambo mengi ya kisasa hayaingii katika wigo wa tafsiri ya neno Bidaa kwa mtazamo wa kisheria, hata kama yatasadikika kuwa ni Bidaa kilugha. Bali tutakuwa na kila sababu ya kuyanasibisha matendo hayo na dini. Kwa mfano majeshi ya nchi za Kiislamu leo hii yanamiliki silaha za kisasa ambazo majeshi ya Kiislamu ya hapo kale zama za Bwana Mtume 8 hayakumiliki silaha za aina hiyo. Majeshi ya sasa yana nyenzo mbali mbali za kileo ambazo zinawawezesha wapiganaji kufikia 120

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 120

8/14/2017 1:18:30 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

malengo yao kwa kiwango kikubwa. Leo hii kuna chombo kama Rada ambacho jeshi linakitumia kujua adui yuko wapi, lakini hapo zamani watu walitumia farasi, badala ya Rada, kwa kuwa maadui walikuwa wakija juu ya farasi. Sasa Waislamu walikuwa wakipata habari kupitia farasi wao, kwa kuwa farasi ni mnyama ambaye Mwenyezi Mungu amempa uwezo wa kusikia milio ya kwato za farasi mwingine tangu akiwa mbali. Sasa farasi anaposikia hivyo huwa anatoa mlio fulani ambao unaashria hatari, na hapo watu walikuwa wanafahamu kuwa mbele yetu kuna maadui. Sasa leo hii majeshi yetu yanatumia Rada je wana mashiko sahihi ya kuhalalisha matumizi hayo? Je wanapotumia vifaru kuna mashiko yoyote kutoka kwenye Qur’ani au kupitia maneno ya Bwana Mtume 8? Jibu: Ndiyo mashiko yapo, kwani Mwenyezi Mungu alikwishatoa ruhusa kwa kusema:

“Na waandalieni nguvu kama vile muwezavyo na kwa farasi walioufungwa, ili mumtishe adui wa Mwenyezi Mungu na adui yenu…..” 67

Katika Aya hiyo kuna mambo mawili: 1.

67

Jambo la kwanza ni kuandaa nguvu bila kuainaisha aina ya nguvu hiyo. Na amri inapokuja bila kuainisha namna ya kile ulichoamrishwa kukifanya, huwa ni hoja tosha ya kuwa umepewa ruhusa kufanya utakavyoweza katika jambo hilo. Kwa mfano Mwenyezi Mungu ameamrisha tusome lakini hajatuainishia tusome nini, kwa hiyo sisi tutasoma kila kinachoitwa elimu. Mfano mwingine Mwenyezi Mungu aliposema kuleni,

Anfal; 8:60 121

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 121

8/14/2017 1:18:30 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

pale pale aliainisha chakula kinachofaa na kisichofaa, tufauti na hapo tungekula kila kitu. Sasa maboresho ya kisasa unayoyaona na mafunzo ya kileo wanayopewa askari katika majeshi ya Kiislamu, na matumizi ya rada na vifaru na zana mbali mbali za kivita, yote hayo yanaingia katika wigo mpana wa amri ya Mwenyezi Mungu ya kututaka tuandae nguvu, bila kuainisha ni za aina gani. Hakutaja tutumie zana aina gani. Kwa hiyo Aya hiyo tunaifasiri kama ruhusa ya sisi kutumia tuwezacho. 2.

Ama sehemu ya pili ya aya imetaja baadhi ya zana ambazo zilitumika wakati ule, kwa hiyo watu waliokuwepo kipindi hicho walitumia zana hizo na sisi hatuzitumii kwa kuwa zama zetu hizi tuna zana mbadala. Na si haramu kutumia kwa kuwa ile sehemu ya kwanza ya aya ilitwambia tuwaandalie nguvu kadiri tuwezavyo, kwa hiyo hata watu wale wa zamani kama wangeweza kuandaa zana hizi tulizonazo leo hii pasingekuwa na kizuizi. Kwa ufahamu wetu mzima katika Aya ni kwamba tuwaandalie maadui zana hizo zilizotajwa na nyinginezo ambazo tutaweza kuziandaa, kupitia akili ya ubunifu tuliyopewa na Mwenyezi Mungu.

3.

Jambo la tatu, ni kupatikana uvumi, yaani jambo hilo lililobuniwa lienee katika jamii, haya ndiyo mambo matatu ambayo ndiyo muhili wa neno Bidaa, yakikamilika hayo matatu basi Bidaa kwa maana ya kisheria inakuwa imekamilika. Lakini kipengele hiki cha tatu hakikutajwa katika tafsiri ya neno Bidaa isipokuwa tu kuna shuhuda nyingi zinazoonesha kuwa kuenea kwa jambo katika jamii kunaungana na masharti mawili ya mwanzo. Kwa mfano kuna riwaya na hadithi nyingi za Mtume zinazoamrisha kuupinga uzushi na wazushaji. Sasa ukisema kuwa kuenea jambo katika jamii si sharti katika kupatikana Bidaa, basi mimi 122

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 122

8/14/2017 1:18:30 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

nitajenga hoja kuwa: Ni vipi utaupinga uzushi ambao hauna uwepo mbele ya macho? Kwa mujibu wa riwaya ya Imamu Bukhari ni kuwa: “Atakayelingania kwenye uongofu atakuwa na malipo sawa na yule atakayemfuata.� Ufunuo tunaoupata kupitia hadithi hii ni kwamba kuzidisha au kupunguza chochote katika dini endapo utakuwa peke yako chumbani na hakuna wa kukufuata katika uzushi huo, basi maana ya Bidaa haitasadikika. Kwa mfano ukiwa chumbani kwako kisha ukaswali Swala ya Maghribi rakaa 4, maadamu hakuna aliyekufuata na kuufanyia kazi uzushi huo, bado maana ya Bidaa haijakamilika. Pamoja na kuwa jambo hilo ni haram na uasi mkubwa. Bidaa ni nadharia mbovu na ya uzushi inayoenezwa katika jamii kwa anuani ya sheria. Na katika jamii zetu kuna mifano mingi juu ya haya tunayoyasema. Bidaa njema na Bidaa mbaya: Baada ya kuelezea Bidaa kwa mapana na marefu na kufafanua nguzo kuu zinazotofautisha kati ya Bidaa kwa mujibu wa Lugha ya Kiarabu, na Bidaa inayokatazwa na shreria ya Dini Tukufu ya Kiislamu, tumeona kuna ulazima wa kutupia jicho katika tanzu za Bidaa ambazo zimeenea katika jamii ya Waislamu. Kama tulivyosema hapo awali kuwa Bidaa katika Lugha ya Kiarabu maana yake ni ubunifu, na ubunifu ni suala la kimaumbile, kila mwanadamu anapenda mabadiliko, anapenda mitindo mbali mbali tofauti na ile ya jana. Mwanadamu anapenda mitindo mipya katika chakula, mavazi, malazi, usafiri, na mengineyo, kwa hiyo ubunifu si haramu. Bidaa inayokatazwa ni ile tuliyoifafanua katika somo lililopita kuwa ni kuzidisha au kupunguza katika dini na kuhusisha tendo hilo na dini. Pili kwa sharti la kutokuwepo mashiko sahihi yanayounga mkono tendo hilo. Tatu kwa sharti la kuvumisha tendo hilo katika jamii na watu wakalipokea kama sehemu ya mafundisho ya dini, hiyo ndiyo 123

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 123

8/14/2017 1:18:30 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Bidaa haramu inayokusudiwa katika sheria, na ina sura moja tu ya uharamu na wala haina sura ya wema hata kidogo. Lakini Waislamu wanatatizika pale wanapofanya mambo ya kileo kisha wanasema hii ni Bidaa kwa kuwa Bwana Mtume 8 hakuifanya, halafu wanaita kuwa ni Bidaa njema (hasanat), ndugu zangu hiyo si Bidaa inayokusudiwa inayokatazwa katika sheria kama tulivyosema, kuwa Bidaa haramu kisheria sura yake ni moja tu. Anasema Mwalimu Mwanazuoni Sheikh Ja’far Subhani: Katika utanzuaji ulioenea kwa baadhi ya waandishi, ni ule wa kutanzua Bidaa katika tanzu mbili: Bidaa njema na Bidaa mbaya. Na ukweli ni kwamba kihistoria utanzuaji huu unakita mizizi yake katika mwaka wa 14 hijiria na katika kauli ya khalifa wa pili wa Waislamu Sayyiduna Umar K pindi alipowakusanya watu ndani ya Mwezi Mtukukufu wa Ramadhani, ili waswali swala ya sunnah, kwa jamaa nyuma ya Ubayyah bin Ka’ab, akaisifu swala hiyo kuwa ni Bidaa njema (niimal Bidaa hadhihi) Bidaa njema ni hii. Na imepokelewa na Imamu Bukhari katika Sahihi yake yakuwa: Anasema Abdu Rahman bin Abdul Qaari: Nilitoka usiku mmoja wa Ramadhani na Umar bin al-Khattab K kwenda msikitini. Mara tukakuta watu wametawanyika… Umar K akasema: Mimi naona laiti ningewakusanya nyuma ya Imamu mmoja ingekuwa vizuri zaidi. Kisha akawakusanya nyuma ya Ubayyah bin Ka’ab K. Kisha nikatoka naye usiku mwingine na watu wakiswali nyuma ya Imamu wao. Umar K akasema: Bidaa njema ni hii.” Lengo letu hapa si kuthibitisha kuwa Swala ya Sunah inafaa kuswaliwa jamaa au laa? Bali sisi tupo katika utanzuaji wa Bidaa ambao chanzo chake ni kauli ya Khalifa wa pili. Tumekwishaweka wazi kuwa Bidaa inayolengwa na Qur’ani na Sunnah ni kuingiza kitu au kupunguza katika misingi ya sheria pasina kuwepo mashiko ya kuunga mkono kwa njia yoyote ile. Sasa kwa 124

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 124

8/14/2017 1:18:30 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

misingi hiyo Bidaa haiwi jambo zuri hata siku moja bali itaendelea kuwa haramu, na wala haifai kuigawanya katika vigawanyo hivyo: Bidaa njema na Bidaa mbaya, kama tulivyotangulia kusema hapo awali. Ndiyo, kwani Bidaa kwa mujibu wa kamusi inaweza kutanzuka katika tanzu hizo mbili, na kila kitu kipya ambacho kimezuka, watu wanakitegemea katika maisha yao ya kila siku lakini hawajakihusisha na dini na chenyewe kikawa si haramu basi kitu hicho ni Bidaa njema, kwa kuwa ni ubunifu mpya wenye faida kwa jamii. Kama vile watu wanavyosherehekea sikukuu ya uhuru wa nchi zao, jambo hilo si haramu na wananchi hawajalihusisha na dini kwa njia moja au nyingine. Ama kilichokuwa haramu katika uwenyewe wake, kitabaki kuwa haramu, na hakitaingia katika Bidaa kwa kuwa uharamu unatokana na sababu za pembeni za kutokuwepo faida na maslahi katika jambo lenyewe, kwa mfano mwanamke kuingia kati ya wanaume bila sitara. Kwa hiyo Bidaa sura yake ni moja tu, na haiwezi kuwa njema kwa njia yoyote ile. Ama ikiwa ni kwa maana ya kilugha, hapo ni sawa, na yaweza kutanzuka na hapo inakuwa si Bidaa iliyokusudiwa katika sheria. Na ukweli wa mambo ni kwamba ugawaji huu wa Bidaa katika mafungu hayo mawili, Bidaa njema na Bidaa mbaya, uhalisia wake ni kutokana na kuchanganya kati ya Bidaa kwa mujibu wa kamusi na Bidaa kwa mujibu wa sheria. Vyanzo vya uharibifu wa sheria katika dini: Pamoja na uhalisia wa kwamba kiini cha dini ni kunyenyekea na kusalimu amri mbele ya matakwa ya Mwenyezi Mungu, na sehemu kubwa ya maswala ya imani na matendo inatokana na chanzo hicho, na hapo ndipo yanapoibuka maswali yafuatayo:

125

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 125

8/14/2017 1:18:30 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

1.

Anawezaje mtu kufanya mchakato wa kuharibu sheria za dini?

2.

Kitu gani kinachoweza kupelekea mtu huyo kufanya mambo hayo?

3.

Ni hatima gani anayoitegemea baada ya matendo hayo?

Hapa tutaelezea baadhi ya sababu na malengo ambayo yote yanaingia chini ya mwamvuli wa kufuata rai binafsi na kuacha maandiko: 1.

Utawa: Kuna mtu anafuata matamanio yake binafsi na kuleta utawa kwenye sheria ya dini, na kutaka dini iutambue kama sheria rasmi. Na historia imetutajia sehemu kubwa ya mifano hiyo. Nasi tutaelezea mfano mmjoa kati ya hiyo mingi, kama ifuatavyo: Inafahamika kwa wasomi kuwa kufunga safarini, ni haramu, na kwa sababu hiyo Mtukufu Mtume 8 alitoka siku moja ya Mwezi wa Ramadhan kwa ajili ya Fat’hul-Makka, na alipofika mahala ambapo kisheria haruhusiwi kufunga, aliagiza kikombe cha maji ili asitishe funga yake, na idadi kubwa ya Waislam waliokuwepo pamoja naye walifungulia pia. Lakini baadhi ya watu walijipa utawa ambao Mwenyezi Mungu hajawafaradhishia, na wakaendelea na funga kwa hoja ya kwamba kwenda kwenye jihadi ukiwa umefunga ni bora kuliko kwenda bila kufunga, na thawabu za aliyekwenda hali ya kuwa amefunga ni nyingi zaidi.

Lakini habari hiyo ilipomfikia Bwana Mtume 8 aliwazingatia watu hao kuwa ni waasi na wenye dhambi. Na katika hadithi nyingine, imepokewa kuwa Bwana Mtume 8 alitoka Madina ndani ya mwezi wa Ramadhani, kuelekea Makka akiwa pamoja na baadhi ya Waislamu, na kati yao walikuwepo waliokuwa wakitembea – bila vipando - lakini Bwana Mtume 8 alipofikia masafa 126

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 126

8/14/2017 1:18:30 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

ambayo kisheria hairuhusiwi kufunga, aliagiza kikombe cha maji na akanywa. Ilikuwa ni kati ya dhuhuri na alasiri. Baadhi ya watu waliokuwa naye wakanywa maji pia, na wengine wakaendelea na funga, na Bwana Mtume akawaita kuwa ni waasi, kwani ilitakiwa wafuate amri ya Bwana Mtume 8 ambayo ndiyo amri ya Mwenyezi Mungu. Sasa utawa huo ni sawa na ule unaofanywa na baadhi ya madhehebu katika Ukristo, ukiangalia maumbile ya kiume katika hali ya kawaida yanalazima kuwa na mwanamke, na ya kike yanalazimu kuwa na mwanaume, lakini walitokea watu na kuanzisha utawa ambao haupo katika sheria ya Mwenyezi Mungu. Wao waliona kuwa kuishi bila kuoa ndio bora zaidi kwani utapata muda mwingi wa kumtumikia Mwenyezi Mungu. Sasa kauli hii ni sawa na ile ya kusema kuwa kufunga ukiwa safarini au kwenye jihadi thawabu zake ni nyingi. Na hiyo ndiyo Bidaa maana huko ni kuingiza sheria mpya katika dini, sheria ambayo Mwenyezi Mungu na Mtume Wake hawaijui. 2.

Kufuata matamanio:

Inafahamika wazi kuwa kila jambo lina hukumu moja katika sheria, na si zaidi. Na haiwezekani jambo moja kuwa na hukumu zaidi ya moja na kwa wakati mmoja. Na kwa sababu hiyo tunakuta kwamba tofauti kubwa iliyopo baina ya Waislamu katika ufahamu wa hukumu, chanzo chake ni kufuata matamanio na matakwa binafsi ya mtu. Na kwa dhana njema tunasema kuwa tofauti hizo ni zao la kutofahamu makusudio rasmi ya hukumu, kama alivyoashiria Sayyiduna Ali bin Abu Twalib katika moja ya hotuba zake: “Enyi watu hakika chanzo cha kutokea fitina ni kufuata matamanio, na hukmu zinazoanzishwa zikiwa ni zenye kupingana na Kitabu na Sunnah za Bwana Mtume 8� 127

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 127

8/14/2017 1:18:30 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Historia imehadithia mifano mingi ya Bidaa hizo nasi tutataja baadhi tu: Moja ya tanzu za Hijja ni HijjaTamattui, nayo ni wadhifa wa Mwislamu ambaye kati yake na mji wa Makka kuna maili 48 au zaidi. Wadhifa wa mwenye kuhiji Hijja hiyo ni avue ihram baada ya kumaliza Ibada ya Umra, kisha yote yaliyokuwa haramu katika kipindi cha Hijja yanakuwa halali isipokuwa kuwinda. Kisha avae tena ihram siku ya tisa ya mwezi huo huo wa mfunguo tatu kwa nia ya HijjaTamattui, kisha anakamilisha matendo ya Hijja ya faradhi kwake. Sitaki kurefusha sana mada ila kwa kifupi ni kwamba mmoja wa Maswahaba aliikataza Hijja hiyo ya Tamatui.68 Sasa hii kisheria ni Bidaa na kilichothibiti kuwa ni Bidaa kisheria, basi sura yake huwa ni moja tu, kama tulivyokwishasema hapo awali. Jambo hilo la Swahaba huyo ni maamuzi yake binafsi ambayo hayana mashiko sahihi ya kuliunga mkono, lakini kwa bahati nzuri halikuenea na kudumu katika jamii ya Waislamu kwa muda mrefu, kwani watu walirejea tena kwenye Hijja Tamattui. Mfano mwingine ni ule unaohadithiwa na Imamu Malik kwamba mwadhini alikuja kwa Khalifa kipindi cha alfajiri na Khalifa alikuwa amelala, basi akamwambia: “Swala ni bora kuliko usingizi”, Khalifa pale pale aliamuru neno hilo liwekwe kwenye adhana ya alfajiri.

68

Sunan Abii Daud Jz. 2 hadith namba 1789. 128

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 128

8/14/2017 1:18:30 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

SEHEMU YA NNE

KUTEMBELEA MAKABURI Azimio la kiwahabi la kumdhalilisha Bwana Mtume 8: Katika somo hili tutazungumzia ziara ya makaburi, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa kuba juu ya kaburi. Ila tu kwa kuanzia tumeona bora tuanze na kaburi la Bwana Mtume 8 kama tabaruku, kisha tutaendelea na makaburi ya Manabii wengine pamoja na Mawalii. Wapenzi wasomaji, moja ya mambo ambayo ni haramu na Bidaa kwa ufahamu mdogo wa Kiwahabi ni suala la kutembelea makaburi. Suala hili kwa Mawahabi ni chanzo kingine cha kukufurishia Waislamu kwa hoja ya kwamba ni kuabudu kaburi. Kwa ibara nyingine ni kuabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Lakini Qur’ani yatwambia kuwa:

“Huo ndiyo mwisho wa upeo wao wa ujuzi….. ” 69

Wao pamoja na baba zao hawana ujuzi juu ya jambo hilo, na kibaya zaidi hawataki kukiri kuwa hawajui. Yaani watu hawajui halafu wao wenyewe hawajui kuwa wao hawajui, na huo ni ujinga maradufu, kwa kuwa hawajui lakini wanajiweka kwenye kundi la ujuaji na kudai kuwa wao ndiyo wako katika njia nyoofu. 69

Surat Najmi; 53:30 129

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 129

8/14/2017 1:18:30 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Khalifa wa nne wa Waislamu kama inavyosemekana Sayyiduna Ali bin Abu Twalib D, anasema: “Na mwingine amejiita mwanachuo hali ya kuwa si mwanachuo, isipokuwa amechukua ujinga kutoka kwa wajinga, na upotovu kutoka kwa wapotoshaji, na amewategea watu mtego uliyotengenezwa kwa kamba ya udanganyifu na maneno ya uongo. Anakitafsiri Kitabu (Qur’ani) kwa rai zake, na anayafanya matakwa yake kuwa ndiyo haki. Anawafanya watu wajione kuwa hawana hatia pindi wafanyapo madhambi makubwa, na makosa makubwa anayafanya kuwa mepesi. Anasema: Najizuia na mambo yenye utata hali ya kuwa ndani ya hayo ametumbukia, anasema : Najiepusha na Bidaa hali ya kuwa ameilalia, hivyo ni binadamu kisura, na mnyama kiroho. Hajui mlango wa uongofu ili aufuate, wala wa upotovu ili auepuke. Basi huyo ndiyo mfu kati ya waliohai (mfu anayetembea).” Hiyo ndiyo hali halisi ya Mawahabi, kujifanya kuwa wako mbali na Bidaa hali ya kuwa wameilalia. Sura zao ni za kibinadamu lakini roho zao ni mithili ya zile za wanyama. Kutofautisha kati ya Bidaa na sunnah si suala jepesi kama kutwaa kisu na kukata suruali, bali ni suala la kielimu, na Mawahabi wako mbali na elimu, umbali wa mbingu na ardhi. Wao ni watu wa kukurupuka, na kuendeshwa na matamanio yao. Lugha yao ni matusi, utovu wa nidhamu kwa Mitume na Mawalii, kukufurisha kila asiyekuwa Wahhabi, kuvunja amani katika jamii, kuhakikisha Uislamu unakosa haiba mbele ya kila asiyekuwa Mwislamu. Hoja zao ni Karate na Judo. Ni watu wasio na uelekevu hata kidogo. Ni watu wenye ususuavu wa moyo, na nyoyo zao ni kama chuma bali ni zaidi ya chuma. Ususuavu wa moyo wa Kianswar Sunna (kiwahabi) wapevuka: Jambo linalowathibitishia Waislamu kupevuka kwa ule ususuavu wa nyoyo walionao Mawahabi / Maanswar sunah, ni lile azimio lao lisi130

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 130

8/14/2017 1:18:30 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

lokuwa la kibinadamu la kutaka kufukua kaburi la Bwana Mtume 8. Ni utovu wa ni dhamu ulioje mpenzi msomaji!! Mwenyezi Mungu anasema katika Qur’ani:

“Ndivyo hivyo! Na anayezitukuza nembo za Mwenyezi Mungu, basi huo ni katika taqwa ya nyoyo.”70

Pendekezo la Mawahabi juu ya kuvunja msikiti wa Bwana Mtume 8 na kuvunja kuba ambalo ndiyo nembo na utambulisho wa msikiti huo, kwa lengo na shabaha ya kufutilia mbali ushahidi wa kihistoria, na kumbukumbu muhimu za dini yetu, kitendo hicho kinafaa kulaaniwa na kila Mwislamu. Ama kuufukua mwili wa Bwana Mtume 8 na kwenda kuuzika mahala ambapo mamilioni ya Waislamu hawapajui, kwa kweli suala hilo katika uhalisia wake linaleta sura mbili: 1.

70

Kuudhalilisha mwili mtukufu wa Bwana Mtume Muhammad 8, na jambo hilo ni kinyume na utu, na Mwenyezi Mungu analichukia, bali kila mtu mwenye chembe ya ubinadamu ndani ya moyo wake ni lazima alaani vikali kitendo hicho. Ndugu msomaji naandika ukurasa huu huku machozi yanatiririka, kutokana na pendekezo hilo la watu hao wasio na hata chembe ya ubinadamu katika nyoyo zao, watu ambao itikadi yao ni kumvunjia heshima Bwana Mtume kwa kisingizio cha tauhidii, neno ambalo hawalifahamu maana yake kwa kina.

Surat Al-Hajj; 22:32 131

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 131

8/14/2017 1:18:30 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

2.

Kuwanyima Waislamu fursa adhimu ya kufanya maombi yao kupitia kaburi hilo takatifu. Kitendo cha Waislamu kusimama mbele ya kaburi la Bwana Mtume 8 kwao ni pigo kubwa, kwani jambo hilo linaonesha heshima kwa Mtume na kwa Uislamu kwa jumla, kitu ambacho Mawahabi hawataki kabisa kukisikia.

Mimi kwa msimamo wangu binafsi nasema: Pendekezo hilo ni zaidi ya unyama, ni zaidi ya ususuavu wa moyo, na halifai kabisa kuwa ni wazo la mtu mwenye chembe ya ubinadamu ndani ya moyo wake, achilia mbali ya dini. Mfalme wa Mamlaka ya Kiwahabi ya Saudia afahamu kuwa: Matukio ya kifedhuli yaliyotokea nchini Iraq mwaka wa 1216 – 1225 kupitia utawala wa babu zake, watu wasio na hatia wakauawa na kuporwa mali zao, sanjari na kubomoa kaburi la mjukuu wa Mtume 8 Sayyiduna Hussein D, na mauaji katika mji wa Taif mwaka 1218, mauaji hayo ya kimbari bado yanamuuma kila Mwislamu. Sasa ikiwa Yeye na serikali yake ya Kiwahabi anataka kupetuka mipaka na kuparamia kaburi la Bwana Mtume 8 basi ajue ya kwamba hiyo ni bishara ya kuanguka kwa dola ya Kiwahabi ya Kisaudi, kwani suala hilo litaamsha hisia za wengi ndani na nje ya Saudia, na radiamali yake inaweza kusababisha athari hasi. Msimao wa Sheikh wa Answarsuna Muhammad bin Abdul-Wahab juu ya makaburi: Dr. Ahmad Rasem katika kitabu chake anasimulia yafuatayo: “Baada ya Sheikh Muhammad Bin Abdul-Wahab kuzizungushia akili za umma uliolala nyuzi zake za buibui, alikuja na uongo kupitia kisa cha masanamu ya watu wa Nabii Nuhu a.s,…” namna walivyokuwa wakiabudu masanamu yao. Sasa kwa ufahamu wake, anataka kutwambia kuwa kutembelea makaburi, ni sawa na kuabudu masanamu, kaburi na sanamu mbona hata maana hazikar132

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 132

8/14/2017 1:18:30 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

ibiani!! - Tafsiri hiyo ni nzuri sana ila tu, watwaambie inapatikana kamusi gani? Mwanadamu anazikwa chini ya ardhi ili maandiko yaliyonenwa na Mwenyezi Mungu yatimie: “Tumekuumbeni kutokana na udongo na ndani yake tutawarejesheni, na kutoka humo tutakutoweni kwa mara nyingine.” Sasa ni Mungu gani aliyezikwa ardhini (ambaye sisi tunaabudu kaburi lake)? Jibu la swali hilo liko wazi kwa kila mwanadamu ambaye hajajaladia akili yake, kwamba Qur’ani ilikwishajibu ya kuwa Muhammad si Mungu, Sema: “Hakika Mimi ni mwanadamu kama Ninyi.” Kwa mantiki hiyo hakuna Mwislamu anayeamini juu ya uungu wa Bwana Muhammad 8 wala yeyote katika waja wema waliotangulia. Bali sisi tunaposimama mbele ya kaburi tukufu la Bwana Mtume 8 lengo letu si ibada ya kumwabudu aliyekuwa ndani ya kaburi, ila lengo letu ni kufanya maombi kwa kupitia nafasi aliyonayo mwenye kaburi hilo mbele ya Mwenyezi Mungu, kama ilivyowekwa wazi katika Qur’ani, ya kwamba, na laiti kama wangekujia pindi walipojidhulumu wenyewe, kisha wakamwomba Mwenyezi Mungu msamaha na Mtume pia akawaombea, basi wangekuta Mwenyezi Mungu ni Msamehevu na Mwenye huruma. Tutaelezea kwa mapana tukifikia mahala pake. Hoja nyingine chakavu aliyoitegemea Sheikh Muhammad Bin Abdul-Wahab ni hadithi isemayo kuwa: “Mwenyezi Mungu aliwalaani Mayahudi na Manaswara kwa kuyafanya makaburi ya Manabii wao kuwa msikiti.” Kama alivyosema Dr. Rasem kuwa: “Akili za Mawahabi zimezungushiwa nyuzi za buibui” hadithi imetaja Mayahudi. Sawa tumekubali kwa sababu Makaburi yao yapo, halafu hadithi hiyo ikawataja Manaswara. Hapa nataka msomaji awe makini. Hadithi iliposema Manaswara, Naswara ni Mkristo, na Nabii aliyepelekwa kwa Wakristo ni Bwana Masihi (Yesu) tu, huo ni uongo 133

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 133

8/14/2017 1:18:30 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

wa kwanza wa Kiwahabi, wa kudai kuwa Manaswara wana makaburi ya Manabii wao hali ya kuwa wao wana Nabii mmoja aliyepewa Kitabu naye ni Bwana Masihi (Yesu). Uongo wa pili ni pale riwaya yao inaposema kuwa Manaswara wamefanya Makaburi ya Manabii wao kuwa msikiti, hali ya kuwa Bwana Masihi (Yesu) hajafa na wala hana kaburi.71 Labda wao Mawahabi watwambie kaburi la Bwana Masihi (Yesu) linapatikana wapi? Kutumbelea makaburi ni maumbile ya kibinadamu: Katika maisha tunayoishi hapa duniani, tunaishi na watu wa aina mbalimbali wakiwemo ndugu na marafiki. Tunaishi nao kwa amani na upendo na ushirikiano, katika nyanja mbalimbali za maisha, yawe ya kijamii, kisiasa, kiitikadi na mengineyo. Ndugu hawa huwa na nafasi kubwa ya kuishi ndani ya nyoyo zetu, kiasi ambacho wakifa, hatuwatoi ndani ya nyoyo zetu bali nyoyo zetu ambazo zilikuwa ni majumba yao wakati wa uhai wao, zinageuka kuwa makaburi yao baada ya kufa kwao. Kwa ibara nyingine tunasema kuwa, ndugu hawa waliishi ndani ya roho zetu na wakazikwa humo humo, na kifo si sababu ya wao kufutika katika kumbukumbu zetu, bali mahusiano yaliyokuwa baina yetu na wao hubakia vile vile mpaka mwisho wa uhai wetu. Mwalimu wetu Sheikh Ja’far Subhani anasema: “Kwa hakika wale wanaompoteza kipenzi wao (pamoja na kutokuwepo kwake) athari zake hubakia katika nyoyo zao na kumbukumbu zao, na kamwe hawatamsahau kutokana na mafungamano ya kiroho yanayowaunganisha. Na kwa hoja hiyo utawakuta wakimtaja mara kwa mara na kukumbuka siku ya kifo chake. Pamoja na kuwa kifo kimewatenganisha kimwili, wao hutafuta njia mbadala ya kukutana na kipenzi wao kiroho, iwe kwa njia ya mtu binafsi au ya makundi. Utawaona wanakusanyika kwenye kaburi la mtu wao na kufanya 71

Nakdhul-wahabiya 134

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 134

8/14/2017 1:18:31 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

dua ya kumwombea na kumzawadia thawabu za kisomo cha Suratul Faatiha na thawabu za metendo mema wanayoyafanya kwa niaba ya marehemu. Kwa hiyo huzuni ya kuondokewa na mmoja wa wale tuwapendao, na kufanya vikao vya kuwaenzi na kuwakumbuka, ni jambo lililoenea katika jamii mbali mbali za wanadamu. Na kwa hoja hiyo tunaweza kusema kuwa: Jambo hilo lina mizizi katika maumbile ya mwanadamu, na wala halihitajii ushahidi wa kimaandishi, na kwa ibara nyingine tunaweza kusema kuwa: Nguvu ile ile inayotufanya tuwapende ndugu na marafiki katika siku zote za maisha yao, ndiyo hiyohiyo inayotufanya tuwakumbuke baada ya kufa kwao na pia ndio hiyohiyo inayotufanya tuhudhurie kwenye makaburi yao, na kukutana nao kiroho. Na hili litaeleweka zaidi kama tutalitazama kwa mtazamo wa Kiislamu unaoamini kuwa roho ya mwanadamu haiozi baada ya kuoza mwili. Kwa hoja hiyo yanafunguka mbele yetu mahusiano mapya ya kiroho yanayotufanya twende kutembelea makaburi na kuwazawadia ndugu zetu thawabu za kisomo cha Qur’ani, pamoja na mema mengineyo tunayowafanyia marehemu wetu, kwa kuzingatia kuwa roho huwa haziozi, na hiyo ndiyo hoja idumishayo mahusiano ya kiroho kati yetu na wafu wetu.� Na kwa misingi hiyo si sahihi kuwakataza watu, na kuwakemea vikali (pale tunapowaona wakifanya kisomo cha kuwarehemu wafu), ili waachane na jambo hilo la kimaumbile, na kuwahimiza watu waende kinyume na mtazamo huo, na wauone kuwa ni ukafiri. Bali kinachotakiwa kufanya ni kuwahamasisha watu ili walipende jambo hilo la kimaumbile na kulipa umuhimu wa aina yake, kwa kufanya vikao vya kuwarehemu ndugu zetu, ikiwa ni sehemu mojawapo ya kuonesha mapenzi yetu kwao. Wakati tunafanya maadhimisho hayo tunapaswa kuzingatia miko na mipaka ya kisheria, tunatakiwa ku135

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 135

8/14/2017 1:18:31 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

hakikisha kuwa hatuchanganyi shughuli yetu na jambo lolote ambalo halitamridhisha Mwenyezi Mungu. Kutembelea makaburi ya wanachuoni: Tulikuwa tukizungumzia matembezi ya kutembelea makaburi ya wapendwa wetu, ambao baadhi yao ni urafiki ndiyo unaotuunganisha nao, na wengine tunaunganishwa nao kwa undugu wa damu, kwa hiyo mahusiano maalumu ya hisia za kiroho yaliyopo baina yetu, ndiyo yanayotupa msukumo wa kukusanyika kwenye makaburi ya wapendwa wetu na kusoma Qur’ani ili kuwazawadia thawabu za kisomo ambazo tungezipata sisi, na thawabu za matendo mengine mema ambayo tunayafanya kwa niaba yao. Kwa mfano tunaweza kuchimba kisima au tukafanya huduma yoyote yenye manufaa kwa jamii, kisha tukaweka nia ya kuwa thawabu ambazo tungezipata sisi tunaomba zimuendee mtu fulani katika wafu wetu. Hali hii hudumisha uhusiano wa kiroho kati yetu na wao, na kutufanya tuzidi kuwakumbuka na kutosahau makaburi yao. Tukiachilia mbali hao ndugu na marafiki, kuna tabaka lingine la watu muhimu ambao baina yao na sisi kuna mahusiano ya kiroho, ambayo yanaweza kuwa sawa na yale yaliyo kati yetu na ndugu zetu, au yanaweza kuwa zaidi ya hayo. Watu hawa katika tabaka hili ni Wanachuoni, waliojitolea maisha yao kafara kwa ajili ya kuwaangazia watu njia ili wapate kuongoka. Wao ni sawa na mshumaa unaoteketea kwa ajili ya kuwapatia watu mwanga. Wanachuoni na wanafikara, wameyatoa muhanga maisha yao, kwa ajili ya Umma bila ya kujali magumu wanayoyapata na bila kutanguliza mbele umimi. Walistahamili kila aina ya taabu na mashaka katika utafutataji wa elimu itakayoleta maendeleo mbali mbali katika jamii, ili waache hazina kubwa ya elimu na maarifa katika kizazi kilichopo na kizazi kijacho baadaye. Hazina ambayo itampandisha mwanadamu kwenye kilele cha ukamilifu wa kiroho, na ukamilifu katika maen136

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 136

8/14/2017 1:18:31 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

deleo ya kimaada. Kwa hiyo sidhani kama kuna mtu mwenye akili kamilifu anayeweza kusahau fadhila na hisani kama hizo. Ni nani asiyefahamu mchango wa Sheikh Ibn Sina katika jamii ya wasomi? Sidhani kama kuna mtu hata mmoja katika jamii hiyo asiyeshukuru juhudi za Sheikh huyo. Au ni madhehebu gani ya Kiislamu isiyofahamu mchango wa Mwalimu wa Maimamu Sayyid Jafar Swadiq D. Bali hata Mawahabi wenyewe wanamuenzi Shekih Muhammad bin Abdul Wahab kila kukicha, na kaburi la Ibnu Taimiyah limejengewa kifahari. Na hiyo inaonesha heshima yao kwa mtu huyo, na kamwe hawawezi kuwafuta katika kumbukumbu zao. Na hii ni hoja inayojitosheleza katika kuthibitisha kuwa suala hili ni suala la kimaumbile, na kwa mantiki hiyo kwenda kutembelea makaburi ya watu wetu muhimu kama hao wanachuoni, na kuwafanyia aina zote za takrima, na kuwasomea Qur’ani kisha kuwazawadia thawabu za kisomo hicho, yote hayo yanazingatiwa kuwa ni sehemu mojawapo ya kurejesha wema, na kuthamini kazi yao, na kuwatekelezea haki zao kutokana na kile walichoufanyia umma mkubwa kama huu. Pia inazingatiwa kuwa ni aina mojawapo ya kuienzi elimu na maarifa yao, na kwa upande mwingine ni njia ya kuwahamasisha watu waendeleze mwenendo wao, na wapite mapito yao katika kutafuta elimu na maarifa yenye manufaa kwa jamii. Hakuna shaka kuwa jamii inayowaheshimu wanachuoni wake kwa elimu na maarifa na fikara zao, basi jamii hiyo itakuwa ni jamii hai, na kamwe haitafilisika kielimu na maarifa hata siku moja, na itakuwa ni jamii yenye watu wanaoheshimiana pamoja na kulinda heshima ya yule ambaye si mmoja wao katika imani. Mpenzi msomaji hebu tazama jamii za Kiwahabi zilivyokuwa na utovu wa ni dhamu kwa Mitume, sembuse wanachuni. Na asiyeheshimu wanachuoni utovu wake wa nidhamu huanzia mbali, kwa 137

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 137

8/14/2017 1:18:31 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

hiyo msishangae kuona masheikh wa Kiwahabi hawana adabu. Utovu huo wa nidhamu wameutoa kwa Sheikh wao Muhammad bin Abdul-Wahab. Yeye alikuwa mtovu wa nidhamu kwa baba yake mzazi, hata ile Aya inayosema tuwanyenyekee wazazi, kwake haikuwa na maana yoyote. Hakuishia hapo tu bali alikuwa mtovu wa nidhamu kwa kaka yake na mwalimu wake Sheikh Suleiman bin Abdul-Wahab. Na si hapo tu, alikuwa ni mtovu wa nidhamu kwa masheikh waliomfundisha katika miji ya Makka na Madina. Sasa masheikh wa Kiwahabi wameiga tabia zote hizo za kishenzi. Hawana adabu, hawajui hata lugha ya kufahamiana na watu. Kukuita wewe kafiri kwao ni kitu cha kawaida, wakiingia nyumbani kwa mtu kama kuna picha ukutani, kitu cha kwanza wanaitoa bila ya kupata idhini ya mwenyeji wao, kwa madai ya kuwa ni Bidaa. Lakini huo ni utovu wa nidhamu wa hali ya juu. Haya yote yamefafanuliwa mahala pake, kwa hiyo hatuna haja ya kuyarefusha zaidi hapa. Cha msingi tufahamu kuwa jamii za Kiwahabi ni jamii zisizokuwa na adabu kwa mzazi wala kwa mwalimu, wala kwa Mtume, hali iliyopelekea jamii hizo kuwa ni jamii zilizofilisika kielimu na zenye ukame wa maarifa, kwa kutothamini kazi kubwa iliyofanywa na wanachuoni katika umma huu. Wao wanaona kama vile kifo ndio mwisho wa uhai. Mwenyezi Mungu anasema:

“Huo ndiyo mwisho wao wa ujuzi…..”72

Kutembelea makaburi ya mashujaa wa Kiislaam: Baadaya kuzungumzia ziara ya makaburi ya wapendwa wetu na wanachuoni wetu, tunatupia macho upande mwingine na kukuta kuwa 72

Surat Najmi; 53:30 138

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 138

8/14/2017 1:18:31 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

kuna kundi lingine la watu ambao wana nafasi muhimu katika jamii. Na hiyo ni kutokana na majukumu yao waliyoyatekeleza katika kuhuisha umma na kuurejeshea heshima yake iliyokuwa imepotezwa. Kundi hili ni kundi la wanamapinduzi na wapiganaji ambao nafsi zao hazikuwa radhi kuona maisha inayoishi jamii ni maisha yaliyojaa dhuluma na ufisadi. Jamii ilikuwa imepoteza heshima yake. Ubaguzi wa rangi, dini na ukabaila ulikuwa umetawala katika jamii. Sasa kundi hilo la wanamapinduzi lilitumia gharama zote, na kubwa zaidi ilikuwa ni wao kujitoa muhanga, damu yao ikamwagika ili kuhakikisha kuwa heshima ya jamii inarejea mahala pake na kuurejeshea umma hadhi yake na heshima yake iliyokuwa imevuliwa. Kwa hiyo kundi hilo lina nafasi maalumu na ya aina yake katika jamii, nafasi ambayo inawalazimu wanajamii kuikadiria utukufu wake. Kwa hiyo jamii ikaona (japo kwa uchache), baada ya kutoweka mashujaa hao basi wao wanajamii wawaenzi kwa kusimama mbele ya makaburi yao na kutoa heshima zao, na kudumisha utajo wao. Katika suala hili kuna mambo yanayomjengea mtu katika malezi mazuri yatakayoweza kumfikisha kwenye kilele cha roho ya utu na ubinadamu. Sasa maadui wa Uislamu waliliona hilo mapema, na hawakutaka hali hiyo au roho hiyo ya utu iendelelee katika jamii za Kiislamu, kwani uwepo wa roho ya utu na ubinadamu katika jamii za Kiislamu, ni kikwazo cha wao kufanikisha dhamira yao ya kuuchafua Uislamu. Kwa hiyo maadui hao wakaandaa wawakilishi wao ambao alama zao za dhahiri ni kukata suruali, kuvaa vizibao wakati wa joto, kufuga ndevu chafu, kunyoa vipara na kushika fimbo mkononi, pia utovu wa nidhamu kwa manabii hadi kwa wazazi wao, na kutokuwa na lugha ya maelewano kwa yeyote yule ambaye hakati suruali kwa kisu kama wao. 139

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 139

8/14/2017 1:18:31 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Vibaraka hao hutekeleza agizo la mabwana wao la kupinga suala la kutembelea makaburi, ili kuondoa ile roho ya utu tuliyoisema, ili watu wawe na nyoyo za chuma, kwani roho ya chuma ni zana kuu ya kubomolea jengo la Uislamu, kuupaka matope, na kuufanya ukose haiba yake mbele ya jamii hususan jamii za kimataifa. Hebu tazama matukio ya kinyama yanayofanywa na genge la Maharamia wa Kiwahabi la Daesh. Genge hili ni genge la mauaji, ubakaji na uporaji, lenyewe linadai kuwa ni kundi la Kiislamu. Sasa cha kushangaza ni pale tunapoona genge hilo ninaendesha mauaji dhidi ya Waislamu. Watu wanakatwa vichwa kisha vichwa hivyo vinachezewa. Wanaua hadi wanawake kisha wanachezea miili yao, wakati sheria hairuhusu kuchezea hata mzoga wa mbwa, achilia mbali maiti ya binadamu. Sasa hilo ni moja ya magenge ya Kiwahabi yanayofanya kazi ya kuuchafua Uislamu, na yako mengi si Daesh tu. Sasa watu kama hao ni watu ambao waliandaliwa mapema na wakalelewa katika malezi ya kutotembelea makaburi, ili waweze kuwa na roho za kinyama. Sasa leo Mawahabi wanapodai kuwa kutembelea makaburi ni mambo ya uzushi, lengo lao ni kutaka watu hususan Waislamu wawe na ususuavu wa nyoyo kama wao. Itikadi yetu iwe ni umwagaji damu, uporaji, ubakaji, chuki na mauaji kwa kila asiyekuwa Mwislamu, ilimradi tu jamii ya Kiislamu igeuke kuwa ni jamii chinja chinja, wakati Uislamu ni amani. Yote hayo ni matokeo hasi ya kuondoa mfumo wa kibinadamu wa kutembelea makaburi, uliosimikwa na Mtukufu Mtume 8, mfumo ambao umethibiti usahihi wake katika vitabu vya Kiislam kama vile Ibn Maaja, Kanzul Umaal, na vinginevyo. Kwa hiyo Mwislamu anaposimama mbele ya kaburi, lengo lake si kuabudia kaburi kama wanavyodai waumini wa genge la hujuma la Kiwahabi kutokana elimu zao za chekechea, bali lengo letu katika kusimama mbele ya makaburi ya Mashujaa Wetu, ni kudumisha na 140

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 140

8/14/2017 1:18:31 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

kutoa upya ahadi ya kwamba: Mimi nitapinga dhuluma kwa gharama yoyote ile na kulinda mwenendo wenu, kwani ni jambo lisilokuwa na shaka kwamba: Mapinduzi au mabadiliko ya kijamii hayaji hivi hivi bila gharama, bali ni lazima yagharamiwe, na gharama ya mapinduzi dhidi ya ukandamizaji, na kung’oa mizizi yake, gharama yake si mchezo kuimudu, kwani kazi hiyo inagharimu damu za watu. Sasa wanapotokea watu katika jamii wenye moyo wakujitolea damu zao kafara ili kuweza kuwatoa wanajamii katika dhuluma inayowakabili, basi hapo sidhani kama yupo mtu mwenye akili kamilifu atakayekataa kumuenzi shujaa huyo aliyejitoa muhanga ili kuinusuru jamii. Nakumbuka kisa kilichotokea nchini Iran. Mkulima mmoja aliyefahamika kwa jina Riz Ali, mkulima huyo siku moja alikuwa shambani kwake, shamba lililokuwa pembeni ya reli. Na Iran ni moja ya nchi zenye barafu, siku hiyo barafu ilidondoka kwa wingi mno hadi ukaibuka mlima wa barafu juu ya reli. Mara Riz Ali akasikia kipenga, treni iko njiani inakuja na imekaribia kufika kwenye eneo hilo la barafu. Haraka haraka Riz Ali akafikiria njia ya kuokoa watu. Akaona njia nzuri ni kuwasha moto, basi akatafuta majani kwa haraka haraka lakini hakuyapata. Bila kupoteza muda alivua nguo zake zote, na kubaki kama alivyozaliwa. Akakata tawi la mti, na nguo zile akazifunga kwenye tawi hilo kisha akawasha moto. Baada ya hapo akabeba mwenge wake huo na kukimbilia kule treni ilipokuwa inatokea na alipoikaribia treni alisimama kando ya reli na kuinua mwenge wake juu. Kwa bahati nzuri dereva aliiona ishara ile na akaanza kupunguza mwendo, maana breki ya treni si ya hapo kwa hapo. Basi treni ikaenda kidogo kidogo na hatimaye ikasimama karibu na mlima ule wa barafu. Dereva akashuka ili aangalia yanayojiri hapo mpaka ku141

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 141

8/14/2017 1:18:31 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

wekwa ishara ile ya moto. Abiria nao wote kwa pamoja walishuka chini na kwenda kumkuta Bwana Riz Ali yuko kama alivyozaliwa huku anatetemeka kutokana na baridi kali iliyokuwepo siku ile. Kitu cha kwanza kwa wasafiri wale kila mmoja alivua koti lake akitamani liwe la kwanza kupokelewa na Riz Ali, kisha wakamuuliza anapendelea zawadi gani mkabala na kazi kubwa aliyoifanya. Wakamwambia chochote utakacho leo hii utakipata, kwa kuwa umetuokoa. Sikiliza majibu ya shujaa Riz Ali: “Malipo yangu yako kwa Mwenyezi Mungu, kwani Yeye ndiye Mwenye malipo bora zaidi kwa waja. Na kuwaokoeni nyie kaka zangu na dada zangu naamini nimeokoa taifa langu.” Watu wakasaidiana kukwangua barafu ile hadi wakaimaliza na treni ikaendelea na safari yake. Riz Ali alipewa zawadi kubwa na wasafiri japo kuwa ile kubwa zaidi aliikataa na kusema kuwa atalipwa na Mwenyezi Mungu Siku ya Mwisho. Je, mtu kama huyu watu wanaweza kumsahau? Je watu wa Iran walifanya nini ili kumwenzi Riz Ali? Ndugu Wairan hadi leo hii tukio hili wameliandika vitabuni na vitabu vinafundishwa mashuleni na kila mtoto wa Kiiran hadithi hii anaifahamu. Sasa ikiwa watu mpaka leo hii wanamuenzi Riz Ali kwa kazi hiyo, vipi tusimuenzi Shujaa Imam Hussein aliyejitolea maisha yake kwa ajili ya ubinadamu wa kila mwanadamu, bila kujali dini yake, rangi yake, madhehebu yake, wala kabila? Kwa nini watu wasiwaenzi wale waliofanya jitahada za kuondoa ukoloni katika nchi zao? Imamu Hussein alipinga dhuluma na ukandamizaji kwa wanadamu, sasa ukienda kutembelea kaburi la Imamu Hussein utatoka huko na hamasa za kupinga dhuluma na ukandamizaji tunaofanyiwa na nchi za Kimagharibi, maadui wakubwa wa Mwenyezi Mungu. Mahatima Ghandi anasema: “Nimejifunza kwa Imamu Hussein namna ya ku142

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 142

8/14/2017 1:18:31 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

jikomboa na kutoka kwenye ukandamizaji.” Mawahabi hamna aibu hata kidogo wala hamna akili hata za kuazima? Mnakataza watu kutembelea kaburi la Imamu Hussein kwa kuogopa kuwa watarudi na hamasa za kupinga dhuluma iliyotawala kila sehemu, dhuluma inayofanywa na serikali ya Kiwahabi huko Saudia, na dhuluma mnayoifanya Mawahabi huko Palestina kwa kushirikiana na Mayahudi? Halafu mnajinadi kwa jina la kunusuru sunnah za Bwana Mtume 8 kumbe ninyi ndio mafisadi mnaozifisidi. Kwa hiyo sisi Waislamu kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na Mashujaa katika umma, tunaona ulazima wa kudumisha mwenendo wao na kufundisha historia yao kwa vizazi vyetu, na njia muhimu za kuendeleza fikra zao ni kutembelea makaburi yao na hapo ndipo tutaweza kuamsha hamasa zetu za kimapinduzi dhidi ya dhuluma na ukandamizaji. Pia tunaweza kujizidishia roho ya ushujaa kupitia ufunuo tunaoupata toka kwenye ushujaa wao na matendo yao yanayokumbukwa kila kukicha. Au kwa ibara nyingine tunaweza kusema kuwa: Kutembelea makaburi ya wakubwa kama hao ni ishara ya shukurani na kukadiria heshima yao kutokana na huduma kubwa waliyoifanyia umma. Na kwa upande mwingine ni somo kwa watu wa kizazi cha leo kuwa hii ndiyo heshima atakayoipata kila atakayepita mapito yao, na atapata malipo makubwa pia kwa Mwenyezi Mungu, si heshima ya hapa ulimwenguni tu. Tukiachilia mbali hayo, kuna mifano hai mingi tu ambayo tunaishi nayo katika maisha yetu ya kila siku, hapa nitakutajia baadhi kama nilivyoinukuu kutoka kwa Mwalimu Sheikh Ja’far Subhani: “Wale wanaokwenda Hijja huko Makka hulibusu Jiwe Jeusi na kuligusa kwa mikono yao kabla ya kuanza kuizunguka Al-Kaabah. 143

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 143

8/14/2017 1:18:31 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Mawahabi kutokana na ufahamu wao mdogo huona kama ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu katika ibada yake, lakini jambo hilo katika uhalisia wake linaashiria kutoa upya kiapo chetu cha utii kwa Ibrahimu, kwamba: “Sisi tunaunga mkono harakati zako, katika tauhidi na tunaahidi kukutii na kubaki katika mstari tukiendeleza tauhidi na kuisambaza kila mahala na kutokwenda kinyume na mwenendo wako.” Hiyo ndiyo maana ya kiapo cha utii. Sasa maneno hayo ilitakiwa kwa wale wanaokwenda Hijja wayatamke wakati wa kumpa mkono Nabii Ibrahimu, lakini kwa kuwa mikono yao haimfikii Nabii Ibrahimu, wao wakaona njia mbadala ya kumpa mkono Ibrahimu Nabii ni kwenda kwenye moja ya athari alizoziacha Ibrahimu, na Jiwe Jeusi ni moja ya athari hizo. Na kwa kuwa Jiwe hilo hata Ibrahimu Nabii alilishika pia. Hiyo ndiyo hekima ya Waislamu katika kugusa Jiwe Jeusi na kulibusu. Na ni mustahabu kusema :“Hii ni amana yangu nimeileta, na ahadi yangu niliyoiahidi ili uwe shahidi yangu kuwa nimetimiza ahadi.” Sasa Mawahabi wao wanaona kama vile Waislamu wanamkosea sana Mwenyezi Mungu kwa kitendo hicho. Huo ni ufahamu wao duni, na kibaya zaidi hawataki hata kuuliza ili waelimishwe. Ndugu zangu kizazi cha laana cha Banii Umaiyyah kilitaka kuung’oa Uislamu na mizizi yake, lakini kwa baraka za damu za Mashujaa ambao tunawaenzi kila kukicha, Uislamu umesimama hadi kufikia hapa tulipo, lakini Mawahabi wanafanya tena jitihada za kuuangusha Uislamu, na kuufanya uchukiwe na kila asiyekuwa Mwislamu. Uislamu wa Mtume Muhammad 8 misingi yake ni uadilifu wa kijamii, upendo, na maelewano kati ya wanadamu wote bila kujali tofauti zao za kiitikadi. Uislamu unaomtaka Mkristo na Mwislamu kukaa pamoja na kutatua tofauti zao kwa njia ya mazungumzo ya kielimu, huo ndiyo Uislamu sahihi. Lakini 144

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 144

8/14/2017 1:18:31 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Mawahabi hawataki kabisa kusikia Uislamu wa namna hiyo, bali Uislamu wao ni wa kujilipua na mabomu, kuua Wakristo bila hatia, kupandikiza chuki katika jamii ili wanajamii wachukiane wao kwa wao. Mawahabi ni zao la ukoloni wa Uingereza (na warithi wa Banii Umaiyyah) na ni mabolozi wa kuuchafua Uislamu duniani. Ndugu zangu, ikiwa kila ugonjwa una dawa yake basi, saratani hii ya Uwahabi pia ina dawa yake. Waislamu tufanye kazi kwa ushirikiano, ili kunusuru matukufu ya dini yetu, na kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu tutashinda. Namwomba Mola atujalie kuwa katika wale wanaosikiliza neno na kufuata lililo kuwa bora zaidi. Kutembelea kaburi la Bwana Mtume 8: Hakuna shaka kuwa kusimama mbele ya kaburi la Bwana Mtume 8 na Maimamu watakatifu kutoka nyumba yake, suala hili katika uwenyewe wake ni ishara tosha inayoashiria sifa na shukurani kwa Bwana Mtume na Maimamu, kutokana na kazi kubwa waliyoifanyia umma huu, ikiwemo ile ya kuwatoa watu gizani na kuwashika mkono hadi kuwafikisha pwani ya amani katika bahari yenye giza lililokomaa. Kwa hiyo matembezi ya kutembelea kaburi la Bwana ni agano baina yako wewe na Mtume 8, Mtume 8 ya kuwa utabakia kuwa mtiifu kwake na kuwa utafuata mwenendo wake na kubakia kwenye mstari na mafundisho aliyokuja nayo yeye au mmoja wa Makhalifa wake. Anasema Imamu Ali Bin Musa D, kuhusiana na matembezi ya kutembelea makaburi ya watukufu: “Hakika kila kiongozi ana agano na watu wake na wafuasi wake, na kwa hakika utimilifu wa utekelezaji wa agano ni kutembelea makaburi yao.� Ziara ya kaburi la Mtume katika uhalisia wake inazingatiwa kuwa ni agano analolianzisha yule mtembeleaji wa kaburi hilo baina yake na Mtume 145

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 145

8/14/2017 1:18:31 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

8, ya kwamba atabakia katika agano hilo na kufuata nyayo

zake pamoja na kulinda misingi ya dini na ubinadamu, aliyokuja nayo Bwana Mtume 8 au mmoja wa Makhalifa wake waongofu. Mtu anaposimama mbele ya kaburi la Mtume, kisimamo chake kinawasilisha kwa Bwana Mtume maneno yafuatayo: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu. Ewe Nabii wa utu. Ewe mwanadamu mkamilifu ambaye miguu yake imekanyaga sayari hii ya dunia. Ikiwa Muhajirina na Answar walikula kiapo cha kukutii huko Hudaibiyyah, na wakakupa mikono yao. Na ikiwa wanawake waumini wa Makka walikula kiapo cha kukutii na kwamba hawatamshirikisha Mwenyezi Mungu na wala hawatazini. Na ikiwa waumini ambao miguu yao iliteleza, wakaacha njia potofu na kufanya madhambi, watakujia na kukulilia uwaombee msamaha, kisha na wewe ukawaombea, watasamehewa kama isemavyo Qur’ani:

“.....Na lau kwamba walipojidhulumu wengekujia wakaomba maghufira kwa Mwenyezi Mungu na wakawaombewa maghufira na Mtume, wangelimkuta Mwenyezi Mungu ni Mwenye kutakabali toba, Mwenye kurehemu.”73

Basi na mimi nimesimama mbele yako na pembeni ya kaburi lako tukufu ili kufufua kile kiapo cha utii walichokitoa Waumini mbele yako, na ninaweka agano ya kwamba: Nitabakia kuwa mtiifu kwako na mwenye kutimiza agano langu, pamoja na kuyahami matukufu uliyokuja nayo, na kujiepusha na maasi, huku nikikuomba uniombee Mwenyezi Mungu aniwezeshe na anishike mkono na ku73

Surat Nisaa; 4:64 146

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 146

8/14/2017 1:18:31 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

nipeleka kwenye yale yaliyokuwa na kheri na maslahi, na anisamehe madhambi niliyotanguliza. Huu ndiyo ufunuo tunaoupata kupitia kitendo hicho cha kutembelea kaburi la Bwana Mtume 8. Lakini kuna tofauti kati ya matembezi ya kaburi yanayofanywa na waumini, na yale yanayofanywa na watalii. Lengo la waumini katika kutembelea kaburi la Bwana Mtume au Makhalifa wake ni kufufua lile agano lililopo baina ya wao na Mtukufu Mtume 8, ya kuwa wataendeleza yale aliyowaletea. Pili ni mkutano wa kiroho kati ya Wao na Mtume 8. Ama malengo ya watalii ni kuangalia mabaki ya kale na kukusanya taarifa mbali mbali za kihistoria, na mengineyo yanayopatikana katika maeneo husika. Wanahistoria wananukuu visa vilivyojiri katika matembezi ya kutembelea kaburi la Bwana Mtume 8 kama ifuatavyo: “Amepokea Sufiani bin Anbar Al-Atabi anasema: Nilikuwa nimekaa kaburini kwa Mtume 8 pindi alipokuja bedui kutoka nje ya mji na akasimama mbele ya kaburi tukufu la Mtume na akasema: ‘Amani iwe juu yako ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, nimemsikia Mwenyezi Mungu akisema: ‘Na lau kwamba wao walipojidhulumu wangekujia, wakaomba msamaha kwa Mwenyezi Mungu na wakaombewa msamaha na Mtume, wangelimkuta Mwenyezi Mungu ni Mwenye kukubali toba, Mwenye huruma.’74 Nami nimekujia hali ya kuwa ni mwenye kuomba msamaha kutokana na dhambi zangu, huku nikikutanguliza wewe mbele ya Mola Wangu.’” Kisha akalia. Bedui huyo alifahamu siri iliyofichika ndani ya ziara ya Bwana Mtume, kwa akili yake safi na maumbile salama. Hakuna shaka kuwa kutembelea makaburi ya ndugu na Mashujaa wetu na wanavyuoni na kaburi tukufu la mbora wa viumbe wa Mwenyezi Mungu na watu wa nyumbani kwake, ziara hizo zime  Surat Nisaa; 4:64.

74

147

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 147

8/14/2017 1:18:31 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

kusanya faida nyingi za kimaadili, kimalezi, kijamii, na nyinginezo. Mtazamo wa wanachuoni katika kutembelea kaburi la Bwana Mtume 8: Wanachuoni wa umma huu wamelipa suala hilo umuhimu wa kipekee, hasa ukizingatia kuwa Mtume alitumwa kuwa ni rehema kwa walimwengu, na akafanya jitihada zake zote ili kuutoa umma gizani na kuupeleka kwenye nuru. Na akavumilia kila aina ya taabu, dhiki na mateso aliyokutana nayo katika njia ya kufikisha ujumbe, maana wapinzani walimkabili kwa kila aina ya maudhi, lakini yeye aliweza kuyashinda majaribu. Kwa hiyo wanachuoni wametoa rai zao kuwa ni mustahabu, yaani inapendekezwa zaidi kutembelea kaburi la Bwana Mtume 8 na kuhamasisha watu kwenda kulitembelea ili kujizidishia baraka na neema kupitia matembezi hayo. Kati ya wanachuoni waliotoa kauli zao ni Imamu Taqii din al-Subki.75 Sheikh alSubki amethibitsha usahihi wa suala hilo kwa hoja zenye mashiko, na kwamba ni katika mambo yasiyo na shaka katika sheria ya Kiislamu. Mwanachuoni wa pili ni Allamah Amini, Yeye amekusanya kauli za Maimamu wanne na akataja zaidi ya kauli arobaini za Wanachuoni hao, hapa tutataja baadhi ya kauli hizo. 1. Anasema Abul-Hasan Ahmad Bin Muhammad al-Muhaili alShafi: Ni mustahabu kwa anayekwenda Hijja, baada ya kumaliza ibada ya hapo Makka, aende kutembelea kaburi la Bwana Mtume, 876 2. 75 76

Abul Hasan al-Marudhi anasema: Mahujaji walikuwa wanaelekea Madina kutembelea kaburi la Bwana Mtume 8, mara

  Shifaaus-Siqaam fi ziarat khairil anaam.   Shifaau siqaam: 65, al-Ghadir, Jz. 5, uk. 109 -125 148

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 148

8/14/2017 1:18:31 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

tu baada ya kumaliza ibada ya Hijja, ili wakusanye kati ya ziara ya nyumba ya Mwenyezi Mungu na ziara ya Bwana Mtume 8 ili kutunza heshima ya Mtume 8 na kutekeleza haki za utiifu kwake, na hilo si wajibu katika wajibu wa Hijja, bali ni katika mambo yanayopendekezwa kisheria.77 3.

Mwanachuoni wa tatu ni Sheikh Ghazal aliyefariki mwaka wa 505 A.H. Yeye amenukuu yafuatayo: “Atakayenizuru baada ya kufa kwangu ni kama vile amenizuru wakati wa uhai wangu.”78 Na mwenye kuwa na uwezo wa kunizuru kisha akaacha kunizuru basi huyo amenitenga.” Mpaka akasema mwenye kwenda ziara Madina basi awapo njiani amsalimie Mtume mara nyingi, na atakapoona ngome ya mji na miti yake, aseme: ‘Ewe Mola Wangu hili ni kaburi la Mtume Wako, lifanye kuwa ngao yangu dhidi ya moto, na amani dhidi ya adhabu na hukumu mbaya.

Kisha (Sheikh Ghazali) akataja taratibu za ziara na namna yake, ambayo ni sawa na ile ya ziara ya Baqii pamoja na waliozikwa hapo, kama vile Uthman Bin Affan K, na ziara ya kaburi la Sayyiduna Hasan bin Ali H. Mtazamo wa Qur’ani juu ya kutembelea kaburi la Mtume: Mwenyezi Mungu amewaamuru watu kufika kwa Mtume 8 ili wamwombe Mwenyezi Mungu msamaha kutokana na madhambi yao, na wamwombe Mtume 8 naye pia awaombee, kwa kuwa maombi ya Mtume hujibibiwa bila kizuizi:

77 78

Ahkaamu sultaaniyyah uk. 109.   Ihyaa uluumid-din Jz. 1, uk. 305 - 306. 149

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 149

8/14/2017 1:18:32 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

“.....Na lau kwamba walipojidhulumu wengekujia wakaomba maghufira kwa Mwenyezi Mungu na wakawaombewa maghufira na Mtume, wangelimkuta Mwenyezi Mungu ni Mwenye kutakabali toba, Mwenye kurehemu.”79

Na katika Aya nyingine Mwenyezi Mungu anawasema wanafiki kwa kutoitikia wito huo wa kuja kwa Mtume, ili awaombee, bali wao walikaidi wito huo na kufanya kiburi:

“Na wanapoambiwa: Njooni ili Mtume wa Mwenyezi Mungu awaombee maghufira, huvigeuza vichwa vyao, na unawaona wanageuka nao wamejaa kiburi.80

Mwanachuoni tuliyemtaja, Sheikh Taqii din Subki, yeye amerefusha mazungumzo katika Aya hiyo akasema: “Hukumu ya watu kwenda kwa Mtume ili awaombee haiwahusu Waislamu wa zama hizo tu, bali Aya hiyo inajumuisha na Waislamu wa zama hizi pia. Waislamu wa leo nao vile vile wanaweza kwenda kwa Mtume ili awaombee.” Katika aya hiyo tunasoma mambo matatu: 1. Aya inawahimiza watu kwenda kwa Mtume. 2. Kumwomba Mtume awombee. 3. Mtume kuwaombea. Sasa kama hayo yalifanyika kipindi cha uhai wa Mtume 8, basi yalikuwa ni ishara ya daraja na hadhi ya juu aliyopewa Bwana 79 80

Surat Nisaa; 4:64   Surat Munafikun; 63:5. 150

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 150

8/14/2017 1:18:32 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Mtume, na daraja au hadhi aliyopewa Mtume wakati wa uhai wake, haiwezi kushuka baada ya kifo chake. Mpenzi msomaji aya tuliyokutajia ni ya kuthibitisha kuwa Mtume 8 ana mamlaka ya kuwaombea watu wakati wowote, na kama hao askari chinja chinja (Mawahabi) wanasema kuwa Aya hiyo inahusu wakati wa uhai wa Mtume tu, basi mimi nawaambia kuwa Mtume bado yuko hai, kwani kifo si mwisho wa uhai bali ni safari toka sehemu moja kwenda sehemu nyingine. Kwa lugha nyepesi, ni safari ya kutoka kwenye uhai timilifu wa kidunia kwenda kwenye uhai kamilifu. Kwa hiyo uhai wa duniani ni timilifu, na uhai wa akhera ni kamilifu. Ili kufahamu maana ya maneno hayo inabidi kwanza tufahamu tofauti kati ya maneno hayo mawili, ukamilifu na utimilifu. Kuna tofauti gani kati ya ukamilifu na utilmilifu? Anasema Shahid Murtaza Mutahhari: Katika Lugha ya Kiarabu kuna maneno mawili yanayokaribiana kimaana, lakini hayana maana moja, nayo ni: Ukamilifu na utimilifu. Na maneno hayo mawili yote kwa pamoja kinyume chake ni neon: Upungufu. Neno hilo kuna wakati linatumika dhidi ya ukamilifu, na wakati mwingine linatumika dhidi ya utimilifu. Utapata watu wakisema: Hii imekamilika na ile imepungua, na wakati mwingine wanasema: Hii imetimia na ile imepungua, na maneno yote hayo mawili yametajwa kwenye Aya moja ya Qur’ani, pale Mwenyezi Mungu aliposema: “Leo hii nimekukamilishieni dini yenu na nimekutimizieni neema yangu,� na wala hakusema: Leo hii nimekutimizieni dini yenu, au nimekukamilishieni neema yangu. Na laiti angesema kama hivyo basi isingekuwa sahihi, basi kuna siri gani kati ya maneno hayo? UTILIMILFU: Ni kupatikana mahitaji yote ya lazima yawezayo kukifanya kitu kisiwe pungufu, na yasipopatikana mahitaji hayo basi 151

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 151

8/14/2017 1:18:32 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

kitu hicho kinapewa sifa ya upungufu, yaani hakijapatikana chote, kwa mfano tunaposema: Nyumba tunakusudia kuta milango, madirisha, dari na kadhalika. Vitu vyote hivyo vikipatikana, tunasema: Jengo limetimia, na visipopatikana vyote, tunasema: Jengo ni pungufu. Ama UKAMILIFU: Ni ngazi ambayo kitu kinaweza kuifikia baada ya kuwa kimetimia, kwa hiyo kama kitu si kamili haimaanishi kuwa hakijatimimia, bali kitu kinaweza kuwa kimetimia lakini kisiwe kikamilifu. Na tunaposema kuwa: Mtu fulani akili yake imekamilika hatumaanishi kuwa ilikuwa pungufu na sasa imetimia, bali tunamaanisha kuwa akili yake ni timilifu, isipokuwa tu kwa sasa imepanda kwenye ngazi ya ukamilifu, yaani imetoka kwenye daraja ya chini na kwenda kwenye daraja ya juu ambayo hakuna tena daraja nyingine juu yake. Kwa hiyo maisha yaliyokamilika ni yale maisha yaliyofikia daraja ya juu kiasi ambacho hakuna maisha bora juu yake. Je, mwanamke anaruhusiwa kwenda kutembelea makaburi? Mwanamke na mwanaume wote kwa pamoja wana ruhusa ya kutembelea makaburi ya ndugu na marafiki, ya Manabii, Maimamu, Wanachuoni na wengineo katika Mawalii wa Mwenyezi Mungu, na wala hakuna tofauti kati ya mwanamke na mwanaume katika swala hilo, kwa kuwa sheria tukufu ya Mwenyezi Mungu haimbagui mwanamke kwa uwanauke wake, bali Mwenyezi Mungu na Mtume Wake wanapohukumu jambo basi walengwa katika hukumu hiyo huwa ni wote wawili, wanawake na wanaume. Na hiyo ndiyo maana ya utashi wa kisheria, nao ni utashi unaotaka kutekelezwa na wote, bila kuchagua. Kwa mfano Mwenyezi Mungu aliposema: “Simamisheni Swala,� amri hiyo ilikuwa ni kwa wote na wala haikuwa kwa wanaume peke yao. Kwa hiyo tukichunguza kwa kina kauli ya Bwana Mtume 8 kwa jamii ya 152

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 152

8/14/2017 1:18:32 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Kiislamu, tutakuta kuwa alikuwa anawalenga wote wawili, mwanamke na mwanaume aliposema: “Tembeleeni makaburi, kwa hakika makaburi yanawakumbusheni Akhera.”81 Japo riwaya imetumia viwakilishi vya kiume, lakini hiyo si sababu ya kuwatoa wanawake katika hukumu hiyo, kama wanavyodai Maharamia wa Kiwahabi, kwani hata Aya inayoamrisha swala pia imetumia aina hiyo hiyo ya viwakailishi. Katika sarufi ya Lugha ya Kiarabu, unapozungumza na watu wa jinsia tofauti, yaani ya kike na ya kiume, hapo kwa mujibu wa sarufi ya lugha, utatumia viwakilishi vya jinsia ya kiume kuwakilisha jinsia zote mbili. Kwa hiyo mwenye kuwazuia wanawake wasiende makaburini, kwa hoja ya kuwa hadithi imetumia viwakilishi vya jinsia ya kiume tu, basi mimi namwabia kuwa: Hoja yako ni sahihi, na kwa misingi ya hoja hiyo basi hata swala pia haiwahusu wanawake, kwa kuwa Aya ya swala imekuja kwa muundo huo huo wa kisarufi, lakini swala inaswaliwa na wote wake kwa waume. Kwa mantiki hiyo ruhusa ya kutembelea makaburi inawahusu wote, mpaka hapo tutakapopata sheria inayomtoa mwanamke katika ruhusa hiyo, lakini kwa hadithi hiyo peke yake haitoshi kumzuia mwanamke kutembelea makaburi, kwa kuwa hukumu (kwa mujibu wa sarufi ya Lugha ya Kiarabu) ni ya watu wote. Pia kuna hadithi nyingi zinazounga mkono madai yetu: 1.

Hadithi ya Muslim katika Sahih yake: Kutoka kwa Bibi Aisha

O, anasema:

“Pindi ilipofikia zamu ya Bwana Mtume 8 kuwa kwangu, basi nilimuona usiku akichukua shuka na kuvaa viatu pole pole, kisha akafungua mlango pole pole, akatoka nje na kufunga mlango pole pole (akaondoka).” Bibi Aisha O anasema: “Nilivaa mavazi 81

Sunan ibn Majah, Jz. 1, Hadithi namba 1569. 153

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 153

8/14/2017 1:18:32 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

yangu na kumfuata nyuma, mpaka alipofika kwenye makaburi ya Baqii. Alisimama kwa muda mrefu kisha akainua mikono mara tatu.... mwisho akasema (kumwambia Bibi Aisha O): Jibril amenijia na kuniambia kuwa: “Hakika Mola Wako Mlezi anakuamuru kwenda kwenye makaburi ya Baqii na kuwaombea watu wa hapo.” Bibi Aisha O anasema: “Nikasema nisemeje Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? Bwana Mtume akasema: “Sema! Amani iwe juu yenu enyi watu wa miji hii Waislamu na Waumini, Mwenyezi Mungu awarehemu waliotangulia kati yetu na waliowafuatia, nasi Mwenyezi Mungu akipenda tutaungana nanyi.”82 Katika hadithi hiyo Bibi Aisha O anamwomba Bwana Mtume 8 amfundishe namna ya kutembelea makaburi, pamoja na yale

yasemwayo huko makaburini. Swali: Kama ni haramu kwa mwanamke kutembelea makaburi, kwa nini Bwana Mtume 8 amfundishe mke wake mambo ya haramu? Sasa ufahamu sahihi katika hadithi hiyo ni kwamba Bibi Aisha

O alipokuwa akiwasimulia Wanawake wa Kiislamu suala hilo

wao walilipokea kama jambo halali kwa wanawake kutembelea makaburi, na kwamba hakuna tofauti kati ya wanawake na wanaume katika suala hilo. 2.

82

Bibi Fatimah J, mtoto wa Bwana Mtume 8 na ni mmoja wa wale watakatifu ambao Mwenyezi Mungu kawazungumzia katika sura ya 33 aya 33, binti huyo wa Bwana Mtume alikuwa akitoka kila siku ya Ijumaa kwenda kutembelea kaburi la Sayyiduna Hamza, Baba yake mdogo na Bwana Mtume 8 na huko alikuwa akilia kumlilia Sayyiduna Hamza na kuswali rakaa mbili.

Sahihi Muslim, Kitabul janaizah . 154

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 154

8/14/2017 1:18:32 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Anasema Al-Hakim Nisaburi kuwa: Wapokezi wa hadithi hiyo wote kuanzia wa mwanzo hadi wa mwisho, ni watu wenye kukubalika, na wamekusanyikia kwenye hadithi hii, ili kuwahamasisha watu wapende kutembelea makaburi. 3.

Amepokea Tirmidhi kutoka kwa Abdullah Bin Malikah anasema: Alipofariki Abdurahman bin Abu Bakri - kaka yake na Bibi Aisha O – waliubeba mwili wake na kuupeleka Makkah kwa ajili ya mazishi, na Bibi Aisha O alipokuja Makkah akitokea Madina, alitembelea kaburi la kaka yake, na akasoma beti mbili za shairi.83

4.

Amepokea Imamu Bukhari toka kwa Anas kwamba: Siku moja Bwana Mtume 8 alimkuta mama mmoja akilia kwenye kaburi. Basi akasema kumwambia mama huyo: “Mche Mungu na ufanye subira.” Kwa mujibu wa maelezo ya hadithi hiyo tunafamu kuwa suala la kutembelea makaburi kama lingekuwa ni haramu kwa mwanamke, bisi Bwana Mtume 8 asingemuusia mama huyo kufanya subira, bali angemkemea na kumwambia aondoke katika eneo hilo.

Hoja chakavu za kiwahabi: Kuna hadithi mbili za Bwana Mtume 8 ambazo Mawahabi kwa ufahamu wao duni, wamezifanya hadithi hizo kuwa ni hoja ya kumzuia mwanamke kutembelea makaburi: 1.

83 84

Anasema Bwana Mtume 8: “Mwenyezi Mungu amewalaani wanawake wanaotembelea makaburi.”84 Kwa ufahamu wa kukurupuka wa Kiwahabi, ufahamu usiotaka kuuliza kwa nini, hadithi hiyo kwa mujibu wa ufahamu huo chakavu, ni

Sunan Tirmidhi, Jz. 3/371 hadithi namba 1055.   Sunan ibn Majah, Jz. 1, hadithi 1576. 155

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 155

8/14/2017 1:18:32 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

haramu kwa mwanamke kutembelea makaburi. Lakini mimi naona kama Mawahabi hawajatazama mbali, au hawajaitazama hadithi hiyo kwa kina, kwa nini? Kwa sababu wao sio watu wa kutumia akili bali ni watu wanaoendeshwa na matamanio, jazba na hamasa, na misimamo kinzani na Uislamu. Kwa hiyo hawawezi kuwa na muda wa kutafakari maandiko. Maneno ya Mtume hayafuti maneno ya Mwenyezi Mungu, bali maneno ya Mtume hufuta yaliyotangulia kusemwa, endapo maslahi yatalazimu maneno yale kubatilishwa. Basi hapo Mtume hutoa kauli ya kubatilisha kauli ya mwanzo. Kwa hiyo hadithi waliyoitegemea Mawahabi imefutwa na hadithi tuliyoisema hapo mwanzo, “Tembeleeni makaburi, hakika makaburi yanawakumbusheni Akhera.” Na wanachuoni, akiwemo Tirmidhi wanasema kuwa: Hadithi hiyo wanayoitegemea wakata suruali imefutwa. Na wanachuoni wengine wanasema: Hadithi ilikuwa ikitumika kabla ya ruhusa ya kutembelea makaburi kupatikana, sasa iliporuhusiwa kutembelea makaburi, ruhusa ile ikawajumuisha wote, mwanamke na mwanaume. Sasa anayekataa kwamba mwanamke haingii katika ruhusa hiyo inabidi alete hoja, maana hata Bibi Aisha O kafundishwa na Mtume namna ya kutembelea makaburi. Na sidhani kama Bwana Mtume 8 anaweza kumfundisha mke wake yale yaliyoharamishwa na Mwenyezi Mungu. Lakini Qurtubi anasema: Laana hiyo ni kwa wale wanawake wanaotembelea makaburi kupita kiasi, mpaka matembezi hayo yanakuwa ni chanzo cha kupoteza haki za waume wao.85 2.

85

Hadithi ya pili itumiwayo na hao wakata suruali ni ile hadithi ya Ibnu Majah kutoka kwa Sayyiduna Ali D, ya kwamba siku moja Bwana Mtume 8 aliwakuta wanawake wamekaa, na

Fat-hul barri, Jz. 3/ hadithi 149 156

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 156

8/14/2017 1:18:32 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

alipowauliza kipi kiwakalishacho walijibu: Tunasubiri jeneza. Bwana Mtume akawauliza je, ninyi ni wabebaji? Wakasema: Hapana... na mwisho wa majadiliano yao aliwaambia rejeeni.86 Hadithi hii hatuwezi kuifanya kuwa ni hoja ya kuwazuia wanawake kutembelea makaburi, kwa kuwa ina utata katika mlolongo wa wapokezi wake, na pia hata katika maana. Kwa upande wa wapokezi hadithi hiyo ni dhaifu kwa kuwa mmoja wa wapokezi wake ni Amru bin Dinar. Bwana huyo wanachuoni wa elimu ya hadithi wanasema kuwa alikuwa na sifa ya uongo, kama alivyoeleza Mwalimu Sheikh Ja’far Subhani katika kitabu chake, Alwahhabiyyah baina Mabanil fikri. Pamoja na kuwepo sifa hiyo ya uongo vipi mtu huyo anaweza kuwa katika orodha ya wapokezi wa hadithi, halafu na watu waipokee hadithi hiyo kwa mikono miwili? Kama tutaachilia mbali udhaifu wa hadithi hii kwa upande huo wa wapokezi wake, bado tutakutana na utata mwingine upande wa maana ya hadithi, kwani hadithi hiyo inawahusu wale wanawake wanaokusanyika kwenye jeneza kwa ajili ya kushangaa tu bila kuwa na shughuli yoyote ya kufanya mbele ya jeneza hilo. Na suala hilo halina uhusiano wowote na kutembelea makaburi. Kushangaa jeneza na kutembelea makaburi ni vitu viwili tofauti. Kauli ya Bwana Mtume 8: ‘Rejeeni,’ ilikuwa inawalenga wale waliokuwa wanataka kushangaa jeneza, na wala haikuwa inawalenga wale wanaokwenda kutembelea makaburi, kwani anayefunga safari kutoka nyumbani kwake hadi makaburini, ni lazima awe na lengo maalum, na mtu hawezi kutoka nyumbani kwake kwenda makaburini kwa ajili ya kushangaa tu. Mpenzi msomaji! Dini ya Uwahabi haijui ubinadamu. Sasa Mawahabi wanawaharamishia wanawake kutembelea makaburi ili wanawake wetu wapoteza ile roho yao ya ubinadamu halafu wawe 86

Sunan Ibn Majah, Jz. 1, uk. 5023. 157

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 157

8/14/2017 1:18:32 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

na nyoyo za chuma kama za wanawake wao wa Kiwahabi. Lakini nawaambia kina dada kuwa: Uislamu ni dini ya huruma, upendo, na maelewano, na si dini ya ususuavu kama ule walionao Mawahabi. Kwa mfano, kama mwanamke wa Kiislamu amefiwa na mtoto wake, ni njia ipi iwezayo kumpunguzia machungu na simanzi mwanamke huyo? Bila shaka njia ya kuweza kumfariji kwa haraka haraka ni kwenda kwenye kaburi la marehemu huyo na kumlilia, pamoja na kumwombea dua Mwenyezi Mungu amlaze mahala pema peponi. Kisha mama huyo ataendelea kufanya matendo mengineyo katika yale yaliyokuwa mema, na kumwomba Mwenyezi Mungu amfikishie marehemu thawabu za matendo hayo, kama tulivyokwishafafanua mahala pake. Sasa endapo Uislamu utamzuia mama huyo kufanya hivyo, basi Uislamu utakuwa na dhamira ya kumzidishia simanzi, wakati Uislamu ni dini ya utu, dini inayokwenda sanjari na maumbile ya wanadamu. Na roho ya utu inapompa mtu msukumo wa kwenda kutembelea kaburi la mmoja wa wapendwa wake, basi Uislamu hauwezi kulitilia kipingamizi suala hilo, kwa kuwa Uislamu wenyewe ni dini ya huruma na unatuamuru kuhurumiana, na moja ya njia ya kuhurumiana ni kutembeleana na kuombeana dua njema. Na mmoja wetu anapofariki, mahusiano yetu hubakia kama yalivyokuwa, na yale matembezi ya kumtembelea rafiki huyo nyumbani kwake, yanabadilika na kuwa ni matembezi ya kumtembelea kaburini kwake.

158

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 158

8/14/2017 1:18:32 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

SEHEMU YA TANO

KUMSOMEA MAITI TALAKINI:

K

wa hakika talakini ni katika mambo ambayo Mawahabi wanafanya jitihada kila kukicha, kuhakikisha suala hilo linafutika kabisa na kukosa mahala pa kuweka mguu katika ardhi hii. Na ili kutimiza azma yao hiyo, wamekuwa wakipotosha maana za maandiko ya Mwenyezi Mungu, ili mradi tu, wawapotoshe watu wenye maarifa machache katika jamii, kwa hoja ya kuwa maiti hasikii. Maiti atanufaishwa na matendo yake tu. Na ili kuthibitisha upotovu wao huo, wanatumia baadhi ya Aya za Qur’ani kisha wanazitafsiri kwa mawazo yao, na matamanio yao. Lakini wazo lolote lile ni lazima lipate wafuasi hata kama ni la upotovu, hususan pale wazo hilo linapoelezwa mbele ya watu wenye ufahamu mdogo. Na kwa misingi hiyo Mawahabi walifanikiwa kupata wafuasi wengi kutoka kwenye jamii za watu wasiokuwa na maarifa ya dini, hususan vijana wa mitaani, wanafunzi wa vyuo, wazee na wengineo. Hoja chakavu za kiwahabi katika kupinga talakini: Mwenyezi Mungu anasema katika Qur’ani tukufu: “Wala hawalingani wazima na wafu. Hakika Mwenyezi Mungu humsikilizisha amtakaye, nawe huwezi kuwasikilizisha waliomo makaburini.” Kupitia aya hiyo Mawahabi wanatwambia kwa ufahamu wao wapupa kuwa haifai kusoma talakini kwa kuwa maiti hasikii, na yale tunayomfundisha saa ile hayatamsaidia kwa chochote kile. Majibu yetu: Ni ukweli usiopingika kuwa Qur’ani ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu kilichokuja kuwatoa watu gizani na kuwaonguza kwenye njia 159

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 159

8/14/2017 1:18:32 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

iliyonyooka. Kwa mantiki hiyo zoezi la kuwafikishia watu ujumbe kama huo wa uongofu, hufanywa na Mitume katika jamii hai na si jamii ya wafu. Sasa katika jamii kuna watu wenye akili huru na zenye kuonywa zikaonyeka, hiyo ndiyo jamii ya watu hai. Na wale wenye vichwa vigumu na nyoyo ngumu mithili ya chuma, watu hao hawawezi kusikia neno la uongofu na kulifuata, na ndiyo maana Mwenyezi Mungu akawafananisha na wafu waliomo makaburini, kwani wafu hawawezi kunufaika na ujumbe wa uongofu kwa kuwa ujumbe huo unahitajia kutekelezwa kwa vitendo, na kaburini si mahala pa matendo bali ni sehemu ya watu kusubiria siku ya ufufuo ili wakahukumiwe kutokana na matendo waliyoyatenda duniani. Waislamu wanaposoma talakini huwa hawakusudii kumlingania maiti aliye kaburini au kwa lugha nyepesi huwa hawakusudii kumfikishia maiti ujumbe wa haki ili aufanyie kazi huko kaburini, bali wao hukusudia kumkumbusha ile imani aliyotaka nayo duniani, nayo ni imani ya TAUHIDI. Imani ya kuamini juu ya uwepo wa Mungu Mmoja wa kweli na wa pekee, na pia kuamini kwamba Bwana Muhammad 8 ni Mtume Wake na kwamba Al-Kaabah ndiyo kibla pekee kwa Waislamu wote ulimwenguni, na Qur’ani ndio Kitabu cha Waislamu wote na muongozo kwao. Na mafundisho kama haya hufundishwa mtu wakati wa uhai wake ili ayafanyie kazi kwa vitendo, na anapofariki dunia ndipo ndugu zake Waislamu husimama kaburini kwake na kumsomea maneno hayo (ambayo ni agano baina yake na Mola Wake) si kwa lengo la kumfundisha, bali kumkumbusha kwa kuwa imani hiyo yule marehemu alikuwa akiiamini wakati wa uhai wake. Sasa mimi sidhani kama Mawahabi hawaelewi suala hili, laa. Ukweli ni kwamba wanafahamu ila tu wanachokitaka ni kutimiza malengo yao ya kuuharibu Uislamu na kuupaka matope, na ndiyo maana harakati zao zote huzielekeza kwa jamii isiyokuwa na maarifa ya kutosha. 160

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 160

8/14/2017 1:18:32 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Hoja nyingine itumiwayo na Mawahabi ni ile Aya ya Qur’ani isemayo:

“Ili imwonye aliye hai na ihakikike kauli juu ya makafiri”87

Mawahabi kwa kuwa roho zao ni roho zenye ususuavu na ugumu mithili ya chuma, basi kwao kuchukua Qur’ani na kuitafsiri kama gazeti kwao ni jambo dogo na jepesi kabisa. Yaani hawaheshimu maandiko matakatifu. Sasa katika ususuavu wao wamethubutu kuitafsiri Aya hiyo ya 70 kwa mujibu wa matamino kuwa “Ili imnufaishe aliye hai na ihakikike kauli juu ya makafiri.” Aya hiyo imetumia neno “indhaar” kwa maana ya kuonya lakini wao wanapotaka kuwachanganya watu wanawapa tafsiri ya “kunufaisha” badala ya kuonya. Sasa Mwislamu mwenye ufahamu mdogo akisikia kuwa Qur’ani haimnufaishi asiyekuwa hai, hapo ni lazima afuate mkumbo na aingie kwenye chama cha kukata suruali na kufuga ndevu chafu. Sasa huo ni upotoshaji dhahiri na wa makusudi unaofanywa na genge hilo la Mawahabi. Na hata wakitafsiri kwa maana ya kuonya bado tafsiri hiyo pia haitoshi kuwa ni hoja ya kuharamisha talakini, kwani hiyo Aya inasema Qur’ani inamwonya aliye hai, na talakini haionyi kwa kuwa kaburini si mahala pa matendo kama tulivyosema hapo awali. Kwa hiyo talakini inamkumbusha mtu mambo yale yale 87

Surat Yasin; 36:70 161

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 161

8/14/2017 1:18:33 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

aliyokuwa akiyaamini tangu zama za uhai wake. Naamini mpaka hapa mpenzi msomaji utakuwa umefahamu kuwa Uwahabi umesimama juu ya nguzo mbili tena mbovu kuliko nyumba ya buibui: 1.

Maiti hasikii.

2.

Qur’ani haimnufaishi asiyekuwa hai.

Na nguzo zote mbili tumekwishazitolea maelezo na kufafanua makusudio sahihi ya Aya hizo ambazo Mawahabi wanazitafsiri kwa rai zao na kuzilazimisha ziharamishe talakini, japo malengo yake si kuharamisha talakini. Huo ni upotoshaji wa Kiwahabi wa kupotoa Aya za Mwenyezi Mungu kwa makusudi ili waweze kuwapotosha watu wasiojua kitu, na kuwaingiza kwenye genge la wavaa kaptula misikitini na kucheza karate humo bila ya kujali heshima ya misikiti. Lakini Mwenyezi Mungu anaapa kuwa atailinda Qur’ani yake kutokana na shari za Maibilisi na uharibifu wa Mawahabi. Kwa hiyo tunasema kuwa: Madai ya kusema kuwa maiti hasikii, ni madai batili na hayana mashiko sahihi. Bali watu wote wanaoamini ufufuo wanaamini kuwa siku ya mwisho litapigwa parapanda na wafu wote wataamka ili kila mtu akahukumiwe kwa haki kutokana na matendo yake, na Mawahabi wanalikubali hilo. Halafu pamoja na imani hiyo ya wafu kuamka baada ya kusikia parapanda, bado wanadai kuwa maiti hasikii. Sasa kama maiti hasikii hiyo parapanda ataisikiaje? Na ukisema kuwa maiti hatasikia parapanda maana yake unasema kuwa wafu watabaki makaburini bila kufufuliwa, kitu ambacho si sahihi kabisa, bali ni ukafiri wa wazi kukanusha ufufuo ambao Qur’ani imeunadi katika Aya zake. Na ukisema kuwa maiti atasikia parapanda tu, na hana uwezo wa kusikia sauti nyingine, hapo sasa utakuwa mchekeshaji, kwani Qur’ani inatusimulia visa mbali mbali vilivyojiri baina ya Mitume wa Mwenyezi Mungu na watu wao. Na visa vyote katika mtiririko 162

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 162

8/14/2017 1:18:33 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

wake vinathibisha kuwa maiti anasikia. Lakini kabla ya kuvizungumzia visa hivyo kwanza kabisa hatuna budi kufahamu maana ya mauti, na tutakapofahamu maana yake ndipo tutaweza kujua kama kweli maiti anasikia au hasikii. Mauti ni safari toka ulimwengu wa kimaunzi kwenda ulimwengu wa kirazini, au kwa lugha nyepesi ni safari toka ulimwengu wa dunia kwenda ulimwengu wa Akhera. Na ulimwengu huo ni kamilifu kiasi ambacho roho itakuwa imetosheka na kutohitajia ile nguo ya kimaunzi, yaani mwili. Kwa hiyo kama mwili utafufuliwa ni kwa malengo mengine ya kiuadilifu ili Mungu aulipe mwili nao kwa kazi yake, lakini si kwamba mwili utafufuliwa kwa kuwa roho inashida nao, hapana. Na mwenye kupenda kujua mada hii kwa mapana arejee vitabu vya theolojia, hapa mada hii si mahala pake. Wanatheolojia wanasema kwamba: Mauti si mwisho wa maisha ya mwanadamu, bali maisha ya ukweli huanza kwa kifo chake. Kwa maelezo hayo tunaweza kuhukumu kuwa imani ya Kiwahabi ina misingi ya kuamini kuwa maisha ndiyo mwisho wa kila kitu. Yaani mtu akifa ndiyo basi kila kitu kimefika mwisho, na hiyo si itikadi yetu Waislamu bali ni itikadi iliyokuwa nje ya Uislmu na hapo ni lazima utakubaliana na mimi kuwa: Uwahabi si Uislamu bali ni dini inayojitegemea katika itikadi yake potovu. Baada ya kufahamu maana ya kifo, sasa turudi kwenye vile visa vilivyojiri kati ya Mitume wa Mwenyezi Mungu na watu wao: Nabii Swaleh baada ya kuangamizwa watu wake: Nabii huyo aliwalingania watu wake katika njia ya ibada ya kumwabudu Mungu Mmoja wa kweli na pekee asiye na kifani. Naye Swaleh alikuwa na ngamia ambaye hakuzaliwa, ngamia huyo alikuwa ni muujiza wa Nabii Swaleh wa kuthibitisha madai yake ya kuwa yeye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Lakini watu hao pamo163

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 163

8/14/2017 1:18:33 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

ja na kushuhudia kwao muujiza huo, bado waliendelea kumpinga, naye Swaleh akawanasihi vya kutosha na kuwataka waache kuubeza muujiza wake huo, lakini kwa ususuavu wa nyoyo zao wakamuua ngamia wa Mtume wao Swaleh. Qur’ani inatusimulia tukio hilo:

“Wakamchinja ngamia na wakaasi amri ya Mola Wao na wakasema: Ewe Swaleh! Tuletee unayotuahidi ikiwa wewe ni miongoni mwa Mitume.”88

“Ukawanyakua mtetemeko, wakawa wameanguka hawajimudu majumbani mwao.” (7:78).

“Basi Swaleh akawaacha na kusema: Enyi watu wangu! Kwa hakika nimewafikishia ujumbe wa Mola Wangu na nikawanasihi, lakini (nyinyi) hampendi wenye nasaha.” (7:79).

Mpenzi msomaji naomba uweke akili yako huru ili tuweze kuutafakari mtiririko wa Aya hizo. Aya ya kwanza inaonesha wazi watu 88

Surat A’raf; 7:77 - 79 164

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 164

8/14/2017 1:18:34 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

walivyokuwa wakijiombea adhabu kwa hiari yao. Aya ya pili inasisitiza kuwa ni kweli adhabu waliyoiomba waliipata, na wote walikufa majumbani mwao. Aya ya tatu inaeleza kwa lugha nyepesi kabisa kwamba: Nabii Swaleh aliwazungumzisha wafu hao ya kuwa: “Nimewafikishia ujumbe wa Mola Wangu na nikawanasihi lakini hampendi wenye nasaha. Mpenzi msomaji hebu rudia tena kauli hiyo “ ….lakini hampeni wenye nasaha.” Kauli hiyo aliisema Nabii Swaleh baada ya kuangamizwa watu wake. Ukiitazama Aya hiyo mwanzo wake ilianza kwa wakati uliopita: “Basi Swaleh akawaacha na kusema: Enyi watu wangu! Kwa hakika nimewafikishia ujumbe wa Mola Wangu…..” sasa cha kushangaza ni ile ibara isemayo “… lakini hampendi wenye nasaha.” Ibara hiyo ingekuwa hivi: Nimewafikishia ujumbe wa Mola Wangu na nikawanasihi lakini hamkupenda wenye nasaha, kwa kuwa wakati Swaleh anaongea maneno hayo wale watu hawakuwa hai, sasa kulikuwa na hekima gani katika kuwaambia, lakini hampendi wenye nasaha! Kauli hiyo inaonesha upinzani wa hali ya juu kabisa kiasi ambacho watu hao walimpinga na bado wanaendelea kumpinga. Pili kauli hiyo “lakini hampendi wenye nasaha” inaonesha kuwa watu hao walikuwa wanasikia maneno ya Nabii Swaleh, na kama wangekuwa hawasikii na hawapo mbele yake, basi Nabii Swaleh angesema: “Lakini hawakupenda nasaha,” kwa kutumia nafsi ya tatu, na si nafsi ya pili kama ilivyokuja katika Aya hiyo. Kwani unapotumia nafsi ya pili katika mazungumzo, unamaanisha kuwa yule unayemzungumzisha yuko mbele yako na anasikia maneno yako. Kwa hiyo tunaposoma talakini, huwa tunazungumza na watu ambao wanatusikia, japokuwa hawawezi kutujibu, na sisi pia hatuna haja na majibu yao. 165

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 165

8/14/2017 1:18:34 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Kisa cha Nabii Shuaib: Qur’ani inaendelea kutusimulia visa vilivyojiri baina ya Mitume wa Mwenyezi Mungu na watu wao. Hapa Qur’ani inatupeleka moja kwa moja mpaka Madian, kwa Nabii Shuaib:

“Ukawanyakua mtetemeko, wakaamkia majumbani mwao wamejifudikiza.” (7:91)

“Wale waliomkadhibisha Shuaib wakawa kama kwamba hawakuwepo. Wale waliomkadhibisha Shuaib ndiyo wenye hasara.” (7:92).

“Basi Shuaib akaachana nao na akasema: Enyi watu wangu! Kwa hakika nimewafikishia ujumbe wa Mola Wangu na nikawanasihi, basi vipi nihuzunike juu ya watu makafiri.”89

Mtiririko huu wa kisa cha Nabii Shuaib, ni sawa na ule uliyopita katika kisa cha Nabii Swaleh bila tofauti, kwani Manabii wawili hao, kila mmoja kwa muda wake aliwazungumzisha wafu waliompinga 89

Surat A’raf; 7:93 166

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 166

8/14/2017 1:18:34 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

katika umma wake. Visa hivi vinathibitisha wazi kuwa wafu wanasikia, na Aya kama hizo ni nyingi ndani ya Qur’ani na zote zinaonesha uwepo wa mawasiliano baina yetu na wafu. Bwana Mtume na Manabii waliomtangulia: Mtukufu Mtume Muhammad 8 ni Mtume wa mwisho, lakini kuna Mitume wengi waliopita kabla yake, na hakuna hitilafu juu ya suala hilo. Na Mwenyezi Mungu anamwambia Mtume Wake:

“Na waulize Mitume wetu tuliowatuma kabla yako: Je, tulifanya miungu mingine iabudiwe badala ya Mwnyezi Mungu) mwingi wa rehema?”90

Pamoja na kuwa Mtume Muhammad hakuishi zama moja na Mitume waliomtangulia, Mwenyezi Mungu anamwambia: “Waulize Mitume wetu….” Je, wakati Mwenyezi Mungu anasema: “Waulize Mitume wetu….” Mitume hao walikuwa hai? Jibu liko wazi kwamba walikuwa wameshakufa miaka mingi iliyopita. Sasa kama walikuwa wameshakufa je, walikuwa na uwezo wa kusikia swali la Mtume? Jibu ni ndiyo. Na kama wafu hawasikii basi Mwenyezi Mungu asingemwamuru Mtume kuwauliza watu wasiosikia. Kwa hiyo Aya hii pia inaonesha uwezekano wa Mtume kuwasiliana na Mitume waliomtangulia na kuwauliza maswali. Na ikiwa ni kweli maiti hasikii kama wanavyodai Mawahabi, basi elimu ya Mwenyezi Mungu itakuwa na mapungufu, yaani hajui kwamba wafu hawasikii na ndiyo maana akamwambia Mtukufu Mtume awaulize Mitume waliomtangulia. Mungu atuepushe na maradhi hayo ya Uwahabi. Mungu 90

Surat Zukhruf : 45 167

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 167

8/14/2017 1:18:34 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

hana sifa ya ujinga, kwani yeye ni Mjuzi wa kila kitu, na Mawahabi ni waongo, wanafiki na mazandiki. Bwana Mtume katika vita ya Badri mwaka wa 2 A.H. sawa na 624 A.D: Badri ni kijiji kilichopo Kusini Maghari mwa mji wa Madina, kijiji ambacho yalishtadi humo mapambano makali baina ya Waislamu na washirikina, na ikawa kilele cha mapambano ni Waislamu kuwashinda Washirikina. Baadhi yao walikimbia, na wengine 70 waliuawa. Bwana Mtume aliamuru waliouawa watiwe ndani ya shimo, kisha yeye 8 akasimama na kumwita mmoja mmoja kwa jina: “Ewe Utbah bin Rabiah, ewe Shaibah bin Rabiah, ewe Umaiyah bin Khalaf, ewe Abu Jahli (na hao ndiyo walikuwa magwiji na viongozi wa Washirikina) hivi mmekuta aliyoyaahidi Mola Wenu ni ya kweli……?” Baadhi ya maswahaba wakauliza: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu hivi unawaita wafu? Bwana Mtume 8 akawajibu:

‫ما أنتم بأسم َع لما أقول منهم ولكنهم ال يستطيعون أن يجيبوني‬ “Ninyi hamsikii ninayoyasema zaidi yao hao, isipokuwa wao hawawezi kunijibu.”

Kwa mujibu wa maelezo ya Bwana Mtume 8 ni kwamba wafu wanasikia zaidi yetu, tofauti ni kwamba wao hawawezi tu kutujibu. Taz: Sirat ibn Hisham, Jz. 1, uk. 639. Sayydul Mursalin, Jz. 2, uk. 83. Muhtasari: Maiti anasikia maneno yanayosomwa kwenye talakini, japokuwa hajibu. Aya isemayo kuwa Qur’ani inamuonya aliye hai, haihusiani kabisa na talakini, kwani talakini haionyi bali inamkumbusha maiti imani yake ile ile ya zamani kabla ya kufa kwake. Aya zote wana168

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 168

8/14/2017 1:18:34 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

zozitumia Mawahabi kama hoja ya kuharamishia talakini, aya hizo wanazitafsiri kwa matakwa yao tena kwa makusudi ili wapotoshe watu wasiokuwa na ufahamu wa kutosha katika mambo ya dini. Namwomba Mola atujalie kuwa katika wale wanaosikiliza neno na kufuata lililokuwa bora zaidi.

169

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 169

8/14/2017 1:18:34 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

SEHEMU YA SITA

KHITMA

J

e! thawabu za kisomo cha khitma zinawanufaisha wafu?

Tumewahi kusema kuwa: Kifo katika uhalisia wake hakimaanishi mwisho wa uhai, bali kifo ni kuhama toka sehemu hadi sehemu nyingine, au kwa lugha nzuri, ni safari ya kutoka ulimwengu huu, kwenda ulimwengu wa akhera. Na pia imethibiti katika tafiti za kielimu kuwa: Uhalisia wa mwanadamu si mwili huu wa kimaunzi, na ikiwa ni mwili basi baada ya kuoza kwake na kusambaratika mavumbini, hapo itakuwa ndiyo mwisho wa kila kitu, lakini mwanadamu kusadikika kwake ni roho iliyopo ndani ya vazi hili la kimaunzi (mwili). Kwa hiyo baada ya kutokomea mwili na kuoza, roho huendelea kuishi katika ulimwengu wa kiroho (Barzakh), na katika ulimwengu huo, roho huingia katika mwili mpya unaoendana na mazingira ya ulimwengu huo. Barzakh ni mapokezi ima ya moto au ya pepo, kwa hiyo kama mtu alikuwa ni mwema basi ataanza kupata neema za pepo akiwa hapo Barzakh, na akiwa mwovu basi mateso ya kule aendako ataanza kuyaonja hapo hapo Barzakh. Ni kama ambavyo muhalifu hupata mateso ya gereza tangu akiwa mahabusu, akisubiria siku ya hukumu. Na kwa kuwa Barzakh ni kituo cha mtu kusubiria hukumu yake, basi ni lazima uhai uendelee hapo. Na kama uhai unaendelea, swali ni kwamba: Je, kama mtu aliye hai atafanya matendo mema na kumzawadia marehemu thawabu za matendo hayo, marehemu yule atanufaika na thawabu hizo? Kwa mfano mtu kasoma Qur’ani kisha akasema: Ewe Mwenyezi Mungu nakuomba ufikishe thawabu za ki170

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 170

8/14/2017 1:18:34 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

somo nilichosoma kwa marehemu fulani, hivi kisomo hicho kitamfikia marehemu au ni kupoteza muda tu? Ili kujibu swali hilo hatuna budi kurejea Aya za Qur’ani na hadithi za Bwana Mtume 8. Lakini kabla ya kuingia kwenye uchambuzi huo, kuna umuhimu wa kutambua kuwa: Kwa mujibu wa mafundisho sahihi ya Uislamu, imani isiyofungamana na matendo, imani hiyo haina faida wala manufaa, na pia haiwezi kuwa ni sababu ya wokovu katika ulimwengu wa kiroho, na kwa mnasaba huo Qur’ani inatwambia: “Wale walioamini na kutenda mema….”91 Aya hiyo kwa lugha nyepesi imeambatanisha imani na matendo, kwa hiyo haiwezekani kwa mwanadamu, kutegemea pepo kwa imani tu, bila matendo. Imani hiyo kavu kavu haitampeleka mtu popote. Sasa moja kwa moja nakupeleka mwishoni mwa karne ya kwanza na mwanzoni mwa karne ya pili ambako tunakuta kundi la watu wanaojiita Murjiah. Watu hawa katika nadharia zao, waliamini kuwa imani bila matendo inaokoa, kwa hiyo mtu akishahidilia kuwa Mungu ni mmoja na Muhammad ni Mtume wake, basi akiamini hayo, huyo ni mtu wa peponi hata kama hakutenda matendo mema. Lakini nadharia hiyo haikuchelewa kuanguka kwani Maimamu na Makhalifa waongofu walisimama imara katika kuitetea imani sahihi ya Uislamu na wakawabainishia wafuasi wao athari mbaya za nadharia kama hizo. Vile vile wakawahimiza wazazi na walezi kuwafundisha watoto wao maadili mema mapema na haraka iwezekekanavyo kabla ya Murjiah hawajawatangulia na itikadi zao potovu.92 Na kwa upande mwingine Makhalifa waongofu walikutana na nadharia nyingine inayofanana na hiyo, iliyokuwa ikidai kuwa: Uwepo wa undugu baina ya mtu na watu wa nyumba ya utume, hiyo 91 92

Surat Maida; 5:18   Al-Kafi, Jz. 6, uk. 174 hadithi 5. 171

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 171

8/14/2017 1:18:34 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

ni sababu tosha ya mtu kuokoka, na kuingia katika uzima wa milele. Makhalifa waongofu vile vile waliishambulia nadharia hiyo na kuifananisha na nadharia ya Kiyahudi inayodai (bila mashiko sahihi) kuwa wao ni watoto wa Mwenyezi Mungu na wao ndiyo vipenzi wa Mwenyezi Mungu. Lakini baada ya madai yao hayo Qur’ani ilijenga hoja kwa kusema “Leteni hoja zenu ikiwa nyinyi ni wasema kweli.” 93 Mpaka hapo tumeelewa kuwa wokovu wa mwanadamu uko katika imani yake inayoambatana na matendo mema, lakini kutegemea imani peke yake, au kutegemea mahusiano ya undugu kati yako na watu wa nyumba ya Mtume, fikra hiyo ni potovu na batili na haifai kwa yeyote kuikumbatia nadharia kama hiyo. Qur’ani inasema:

“Basi itakapopulizwa parapanda, hapo hakutakuwa na nasaba baina yao siku hiyo, wala hawataulizana” 94

Na Imamu Ali D anasema: “Leo ni kazi na hakuna malipo, na kesho ni malipo na hakuna kazi.”95 Sasa kama umekubaliana na maelezo hayo kuwa imani bila matendo ni kazi bure, basi nakuruhusu uendelee kunihoji lile swali lako: Je, maiti anaweza kunufaika na thawabu anazozawadia na watu walio hai? Au kwa Kiswahili chepesi, je khitima tunazozisoma zinawanufaisha wafu huko kaburini? Jawabu ni kama ifuatavyo: Thawabu za matendo anazozawadiwa maiti, zina aina mbili: 1.

Maiti awe na mchango katika thawabu hizo:

Surat Baqarah; 2:111   Surat Muuminun; 23:101. 95   Nahju al Balaghah, khutba ya 42. 93 94

172

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 172

8/14/2017 1:18:34 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Je, atachangia namna gani? Maiti katika uhai wake anaweza kutoa huduma endelevu katika jamii yake, kama vile kujenga shule, hospitali, kuchimba kisima na mengineyo. Kwa kazi hiyo atapata thawabu na akifa thawabu zitaendelea kumfikia huko katika makazi yake mapya. Sasa thawabu kama hizi hatuwezi kusema kuwa maiti kazawadiwa bali tunasema kuwa ni kazi aliyoitenda mwenyewe wakati wa uhai wake hapa duniani. Na hiyo ndiyo maana ya swadaqatul jaariah (sadaka endelevu) katika hadithi ya Bwana Mtume 8: “Atakapokufa mwanadamu, hukatikiwa na amali (matendo) yake, isipokuwa mambo matatu: Sadaqatul jaaria (sadaka yenye kuendelea), elimu ambayo watu watanufaika nayo, na mtoto mwema wa kumwombea dua.” Thawabu za matendo hayo chanzo chake ni marehemu mwenyewe, bali hata mtoto anapomwombea dua mzazi wake basi mzazi huyo ni chanzo cha kupatikana dua hiyo, kwani kama si juhudi zake za kumwandaa mtoto katika maadili na malezi sahihi ya Kiislamu, bila shaka mtoto asingekuwa na malezi hayo ya kuwarehemu wazee wake. Na yote hayo yamepatikana kwa baraka za malezi bora ya yule mzazi aliyetangulia mbele ya haki. Na katika vitabu vya Waislamu kuna hadithi nyingi tu ambazo zinaashiria haya tunayoyasema, kama vile hadithi ya Jarir bin Abdullah Ansaar iliyopokelewa na Imamu Muslim katika Sahih yake: “Atakayeanzisha sunna njema katika Uislamu na ikafanyiwa kazi baada yake basi atalipwa mithili ya malipo ya yule aliyeifanyia kazi…..” Kwa hiyo athari yoyote ya matendo yawe mema au mabaya, athari hiyo inapomrejea maiti, ni kutokana na mchango wake katika matendo hayo. Sasa tuangalie aina ya pili ya matendo ambayo thawabu zake humfikia maiti: 2.

Maiti hana mchango wowote katika upatikanaji wa thawabu hizo: - Hii ni aina nyingine ya matendo ambayo humfikia mai173

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 173

8/14/2017 1:18:34 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

ti bila ya yeye mwenyewe kuwa na mchango wowote katika matendo hayo, bali ni ndugu zake waumuni wamependa tu kumzawadia thawabu za kisomo cha Qur’ani au thawabu za mengineyo katika matendo mema, na aina hii ya matendo ndiyo chanzo cha mjadala wetu, kwani katika aina hii ya matendo maiti hakuwa na mchango wowote katika upatikanaji wa thawabu hizo, je thawabu za namna hiyo zitamnufaisha maiti au hazitamnufaisha? Ndugu mpendwa! Hakika Qur’ani na hadithi za Bwana Mtume 8 kwa pamoja vimetilia msisitizo juu ya uwezekano wa maiti kunufaika na matendo ambayo hakuyafanya kwa mikono yake wala hakushiriki kwa njia moja au nyingine katika kusababisha upatikanaji wa matendo hayo. Kwa mfano kama mtu atafunga, au atatoa sadaka kwa niaba ya ndugu yake aliyefariki, kisha akamzawadia marehemu thawabu za funga hiyo na sadaka hiyo, bila shaka thawabu hizo zitamfikia marehemu. Au hata kama mtu atatoa sadaka au atafunga bila kunuia niaba, kisha akasema: Ewe Mwenyezi Mungu peleka thawabu za sadaka au funga au swala hii kwa marehemu fulani, thawabu hizo bila shaka zitamfikia marehemu na atanufaika nazo. Na tuna mifano mingi kutoka katika Qur’ani inayoonesha namna ambavyo malaika wanawaombea Waumini. Waumini waombewa na malaika: Hebu fuata mtiririko huu kisha tujadili kwa pamoja:

174

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 174

8/14/2017 1:18:34 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

“Wale wanaobeba Arshi, na wanaoizunguka, wanamsabihi kwa kumhimidi Mola wao, na wanamwamini na wanawaombea msamaha walioamini. Mola Wetu! Umekienea kila kitu kwa rehema na ujuzi. Basi wasamehe ambao wametubu na wakaifuata njia Yako, na waepushe na adhabu ya Jahannamu.”96

Ikiwa maiti hatanufaika kupitia kazi ambayo hakuifanya kwa mikono yake, basi hiyo dua ya malaika ni mchezo na upuuzi mtupu, kumwombea maiti hali ya kuwa maombi hayo hayamnufaishi maiti huyo kwa cho chote kile. Na katika Aya nyingine:

“Zinakaribia mbingu kutatuka juu yao. Na malaika wakimsabihi Mola Wao kwa kumhimidi na wakiwaombea maghufira waliomo kwenye ardhi. Ehee! Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwingi wa maghufiraa Mwenye kurehemu.”97

Katika Aya hizo tumeona khitima ya malaika kwa waumini, na sasa tuangalie khitima ya waumini kwa waumini wenzao:

“Na waliokuja baada yao wanasema: Mola Wetu! Tughufirie sisi na ndugu zetu waliotutangulia kwa imani, wala usijaalie ndani ya 96 97

Surat Ghafir; 40:7   Surat Ash-Shura; 42:5 175

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 175

8/14/2017 1:18:35 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

nyoyo zetu undani kwa walioamini. Mola Wetu! Hakika Wewe ni Mpole, Mwingi wa rehema.”98 Katika Aya ya kwanza na ya pili tumeona khitima ya malaika kwa waumini, na katika Aya ya tatu tumeona khitima ya waumini wakiwaombea waumini wenzao. Lakini jambo hili haliishi hapo tu bali faida ni pana zaidi kama inavyosisitizwa katika hadithi nyingi zilizoenea katika vitabu vya hadithi, kuwafanyia ihsani wafu, na njia pekee ni kwa matendo yetu hata kama wao hawakuchangia kwa njia moja ama nyingine kama tulivyosema. Je, maiti atanufaika na funga au Hijja ya niaba? Amesema Bwana Mtume 8: “Atakayekufa na deni la funga, basi afunge walii wake kwa niaba yake.”99 Amepokea Ibnu Abbas ya kuwa: “Mwanamke mmoja alikuja kwa Bwana Mtume 8 na akamwambia: Hakika mama yangu alifariki na deni la funga ya mwezi mmoja. Bwana Mtume 8 akamwambia: ‘Je unaonaje kama mama yako angekuwa na deni hivi ungelilipa?’ Yule mwanamke akasema: Ndiyo. Bwana Mtume akamwambia: ‘Basi deni la Mwenyezi Mungu lina haki ya kulipwa zaidi ya deni lingine.’100 Amepokea Abdallah bin Ataa, kutoka kwa Abdallah bin Buraidah kutoka kwa baba yake alisema: Nilipokuwa nimekaa kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu 8 alikuja mwanamke mmoja na kusema: Hakika mimi nimemtoa mjakazi wangu sadaka kwa ajili ya marehemu mama yangu. Basi Bwana Mtume akasema ‘Ni wajibu kupata malipo kwa hilo.’ Kisha mwanamke yule akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, mama yangu alikuwa na deni la funga ya mwezi mmoja, je nifunge kwa niaba yake? Akamwambia funga. Akasema:   Surat Hashri; 59:10   Sahihi Muslim Jz. 3, uk. 155 100   Chanzo hichohicho 98 99

176

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 176

8/14/2017 1:18:35 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Mama yangu hakuwahi kwenda Hijja je, nihiji kwa niaba yake? Bwana Mtume akamwambia hiji. Mpenzi msomaji acha kujaladia akili yako bali iweke huru na ujiulize swali hili: Ikiwa ni kweli maiti hanufaiki na amali ambayo hakuitenda kwa mikono yake, kwa nini Bwana Mtume alimruhusu yule mama kufunga na kwenda Hijja kwa niaba ya mzazi wake? Je, thawabu ya sadaka itamfikia maiti? Ikiwa Hijja ya niaba inamfikia maiti basi hakuna kizuizi cha kuzuia thawabu za sadaka kumfikia maiti. Labda tu kwa kuthibitisha madai yetu tutaje hadithi moja: Imepokelewa kutoka kwa Saad bin Ubadah ya kuwa alisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa hakika mama Saad amefariki je, ni ipi sadaka bora zaidi kuliko nyingine? Bwana Mtume 8 akasema: “Maji.� basi Saad akachimba kisima na akasema hii ni kwaajili ya mama Saad. Kwa hiyo Mwislamu anapotoa sadaka yake kwa nia ya kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu, kisha akaamua kuwa thawabu ya sadaka yake imwendee mmoja wa watu waliotangulia, bila shaka thawabu hizo zitamfikia marehemu, kama ilivyothibiti katika hadithi za Bwana Mtume 8. Lakini thawabu tunazopata wanadamu hatuzipati kwa kuwa tunastahiki kuzipata, hapana bali tunazipa kwa huruma na hisani ya Mwenyezi Mungu. Neema za Mwenyezi Mungu kwa mwanadamu hazina idadi, na mwanadamu hawezi kuzishukuru ipasavyo. Kwanza kila anaposhukuru kidogo Mwenyezi Mungu anamzidishia zaidi, kwa hiyo hawezi kushuru kikamilifu, na wala hawezi kumwabudu ipasavyo. Kumwabudu ibada itakayoweza kufidia wema wa Mwenyezi Mungu, hiyo haitawezekana. Ikiwa mtu hawezi kufidia kazi iliyofanywa na mama yake mzazi ni vipi aweze kufidia kazi ya Mwenyezi Mungu ili kesho aweze kusema kuwa ana haki ya kulipwa pepo? Jibu ni 177

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 177

8/14/2017 1:18:35 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

kwamba: Pepo itapatikana kwa huruma na hisani tu ya Mwenyezi Mungu na si kwa hoja ya kuwa sisi tumemwabudu Mwenyezi Mungu kama ipasavyo.

HOJA CHAKAVU ZA KIWAHABI: Ya kwanza: Moja ya hoja zinazotumiwa na Mawahabi ili kuwatoa watu katika mstaari mnyoofu, ni Aya hii:

“Na kwamba hatapata mtu ila aliyoyahangaikia.”101

Na kwa kupitia aya hiyo wamefanikiwa kuwapotosha watu wasiokuwa na maarifa, na kuwafanya wapoteze ile roho ya utu ya kuwakumbuka ndugu zao waliotangulia japo kwa kuwasomea khitima. Hoja ya Mawahabi katika Aya hiyo ni kwamba Qur’ani imeweka wazi kuwa mtu atanufaishwa na kile alichokitenda na kukifanyia juhudi yeye mwenyewe binafsi. Sasa kwa mujibu wa aya hiyo iweje sisi tudai kuwa kuna uwezekano wa mtu kunufaika na matendo ya mtu mwingine? Majibu yetu: Kama Mawahabi wangefuatilia mtiririko wa Aya zilizoitangulia Aya hiyo, bila shaka wasingetoa hoja za kukurupuka kama hizo. Aya hiyo tuliyotaja inazungumzia adhabu atakazopewa mwanadamu kutokana na uovu wake, na kwamba kila mwanadamu atalipwa kwa yale aliyoyatenda kwa mikono yake. Yaani mtu hataadhibiwa kwa dhambi ya mtu mwingine, kwa hiyo aya hiyo inazungumzia adhabu na wala haina mafungamano yoyote na masuala ya   Surat Najmi; 53:39

101

178

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 178

8/14/2017 1:18:35 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

thawabu za khitma au matendo mema anazozawadiwa maiti, anagalia mtiririko wa Aya zilizoitangulia Aya hiyo:102

“Je, umemwona yule aliyegeuka? Na akatoa kidogo, kisha akajizuia. Je, anayo elimu ya ghaibu, basi ndio anaona. Au hakuambiwa yaliyomo katika vitabu vya Musa? Na vya Ibrahimu aliyetimiza ahadi? Kwamba habebi mbebaji mzigo wa mwingine? Na kwamba hatapata mtu ila aliyoyahangaikia. Na kwamba mahangaiko yake yataonekana. Kisha ndio atalipwa malipo yake kwa ukamilifu. Na kwamba kwa Mola Wako ndio mwisho.” (53:33-42)

Ukizitafakari Aya hizo kwa akili huru utafahamu wazi kuwa Aya hizo katika mtiririko wake zinaongelea adhabu atakayoipata mwanadamu kutokana na matendo yake, kama tulivyosoma katika Aya ya 38 kuwa mtu habebi mzigo wa mtu mwingine. Na katika Aya ya 39 tumesoma kuwa, na kwamba hatapata mtu ila aliyoyahangaikia. Kwa lugha nyepesi tunasema kuwa mtu hatapata dhambi au hataadhibiwa kwa dhambi ambayo hakuitenda mwenyewe kwa mikono yake, au kushiriki kwa njia moja au nyingine katika upatikanaji wa dhambi hiyo. Kwa mantiki hiyo mtu akiiba mali ya mtu hawezi kusema: Ewe Mwenyezi Mungu nakuomba ufikishe dhambi za wizi huu kwa marehemu fulani. Au useme, Ewe Mwenyezi Mungu fikisha dhambi   Anzia aya ya 33-42 Surat Najmi, utaugundua ubabaishaji wa Mawahabi

102

179

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 179

8/14/2017 1:18:35 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

za ulevi wangu kwa marehemu fulani, kamwe suala hilo halitatimia kwa kuwa wewe unataka kumbebesha marehemu mzigo wa dhambi ambazo hakuzitenda. Na hayo ndiyo makusudio ya Aya hizo katika mtiririko wake huo. Lakini kwa ufahamu wa Kiwahabi wao wanaposoma Aya hizo hufahamu kuwa mtu hatanufaika kwa kitu ambacho hakukihangaikia. Kwa kweli hata ufahamu wa mtoto mdogo haukubaliani na mawazo kama hayo. Hapa nitatoa mfano mmoja kuhusiana na mtu kunufaika na kitu ambacho hakukifanyia kazi: Rafiki yangu Bwana Kisagase ni mkulima, siku ya mavuno akiamua kuniletea zawadi ya gunia moja la mahindi, bila shaka zawadi hiyo itaninufaisha, lakini madai ya Mawahabi yanachekesha kwamba mtu hawezi kunufaika na kile ambacho hajakihangaikia. Sasa mbona nimenufaika na zawadi ya Bwana Kisagase hali ya kuwa sijaifanyia kazi? Kauli hiyo inathibitisha wazi kuwa Mawahabi ni wababaishaji, na hawana mashiko sahihi. Mpaka hapo tumeona akili mgando za Kiwahabi na itikadi zao zilizojengewa juu ya misingi mibovu ya fikara, ya kwamba kimnufaishacho mtu ni lazima kitokane na jasho lake. Na kama mtu atadai kuwa Aya hiyo inajumuisha dhambi na thawabu, yaani mwanadamu hataadhibiwa kwa dhambi ambayo hakuitenda, na hapati thawabu ambayo hakuitafuta wakati wa uhai wake wa duniani, basi hapo patakuwa na mambo mawili ambayo tunapaswa kuwa makini nayo, na kutoyachanganya: 1.

Wema na ubaya wa mtu unategemea matendo yake na mwenendo wake: Hii inamaanisha kuwa kama mtu ni mtenda mema, basi hatima yake pia ni njema, na akiwa ni mwovu basi hatima yake pia ni hasara. Na hiyo ndiyo asili kama ilivyotiliwa msisitizo katika Qur’ani: 180

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 180

8/14/2017 1:18:35 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

“Anayetenda mema basi anajitendea mwenyewe, na anayetendaa uovu basi ni juu yake; Na Mola wako si Mwenye kuwadhulumu waja.”103

Kwa mantiki hiyo, asili ya mafanikio ya mwadamu ni zao la juhudi yake mwenyewe, kama ambavyo hasara ni zao la uzembe wake mwenyewe. 2. Kama mtu atafanya jema lolote lile, kisha thawabu za jema hilo akazizawadia kwa mmoja wa watu wema waliokwishakufa, bila shaka thawabu za jema hilo zitamnufaisha marehemu. Na hapo hakuna mjadala katika asili hizo mbili. Asili ya kwanza ni ile inayozungumzia kwa jumla kuhusuiana na mafanikio na hasara, kuwa ni zao la juhudu yake au uzembe wake mwenyewe, lakini asili ya pili inaonesha hali tofauti na ya kipekee, na tunaweza kuifafanua kwa kupitia mfano huu: Kama mtu atampa mtoto wake nasaha ya kuwa: Mafanikio na hasara maishani mwako ni kutokana na juhudi yako katika kazi, au uzembe wako, na kuwa na matumaini ya mafanikio bila kuonesha juhudi, hiyo ni ndoto batili. Je! Nasaha hii inamaanisha kuwa mtoto huyu hana haki ya kupokea zawadi kutoka kwa marafiki au kwa ndugu? Na kama akipokea zawadi hizo ni kweli hazitamnufaisha, kwa hoja ya kuwa hakuzihangaikia? Je, au kupokea zawadi hizo ni kupinga na kukaidi nasaha alizopewa na baba? Jibu kwa herufi kubwa ni hapana. Kwa sababu baba hakumkataza mtoto kupokea zawadi endapo itapatikana, bali (baba) alikuwa anamjengea mtoto misingi sahihi na imara ya maisha yake, nayo ni mtu kutegemea juhudi yake kwanza, kabla ya kutegemea msaada wa mtu, na hiyo haimaanishi   Surat Fuswilat; 41:46 .

103

181

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 181

8/14/2017 1:18:35 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

kuwa ukipewa msaada basi hautakuwa na manufaa kwako, hapana, manufaa yatakuwepo ila tu manufaa hayo yawe ni ya ziada kiasi ambacho hata kama yakikosekana huwezi kuathirika kwa chochote. Lakini sio sahihi mtu kujenga maisha yake juu ya misingi ya uzembe na kutegemea watu. Sasa nasaha kama hizo kutoka kwa mzazi, hazimzuii mtoto kupokea zawadi au msaada pale unapohitajika. Kwa hiyo ile Aya ambayo mawahabi wanaitafsiri kwa matakwa yao, iko katika mfumo huo wa nasaha, kwamba mtu ategemee sana juhudi zake mwenyewe. Lakini Aya hiyo haimaanishi kuwa mtu akizawadiwa thawabu za matendo mema basi atakuwa amepinga nasaha, hapana, bali huo ni ufahamu wa pupa wa kiwahabi, ufahamu ambao misingi yake ni kuendeshwa na matamanio badala ya akili. Ya pili: Katika hoja hii, mawahabi wametegemea hadithi ya Bwana Mtume 8 tuliyokwisha kuitanguliza kuwa anapokufa mwanadamu matendo yake hukatika isipokuwa mambo matatu, sadaka endelevu, mtoto mwema mwenye kumwombea, elimu yenye manufaa kwa watu. Kwa hiyo hoja ya kiwahabi ni kwamba maiti atanufaishwa na hayo mambo matatu au moja yake, sasa suala la mtu kusoma Qur’ani na kumzawadia mwenzako thawabu limetoka wapi, mbona halikutajwa kwenye hadithi hiyo? Majibu yetu: Kwa hakika hadithi iliyotumiwa na Mawahabi, imelenga yale matendo ambayo mwanadamu huyafanya anapokuwa hai, hayo ndiyo hukoma pale mtu anapofariki dunia hapo, isipokuwa hayo matatu ambayo athari zake hubakia baada ya yeye kufa. Na kwa misingi hiyo hakuna uhusiano baina ya hadithi na mtu kunufaika kupitia kazi ya mtu mwingine, bali muundo wa hadithi umevua yale matendo ambayo hufanywa na mtu wakati wa uhai wake. 182

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 182

8/14/2017 1:18:35 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Kwa hiyo malengo ya hadithi ni kubainisha kuwa matendo atendayo mwanadamu kipindi cha uhai wake yote husimama pale anapokufa, yaani hawezi tena kufanya tendo lolote kwa mikono yake, lakini mambo matatu athari zake huendelea, kama tulivyokwishafafanua hapo awali, na hadithi hii haikuwa na lengo la kubainisha kuwa mtu anaweza kunufaika na thawabu anazozawadiwa na Waislamu wenzake au laa! Ya tatu: Kuna aina mbili za ibada: Ya kwanza inakubali niaba, yaani mtu anaweza kufanya ibada hiyo kwa niaba ya mtu mwingine, kwa mfano Hijja na sadaka. Na aina ya pili haikubali niaba, yaani mtu hawezi kufanya ibada hiyo kwa niaba ya mtu mwingine kwa mfano, Swala, kusoma Qur’ani na kufunga, kwa hiyo mtu anaweza kufanya ibada kwa niaba ya mmoja wa watu wake waliotangulia mbele ya haki, kwa sharti tu, ibada hiyo iwe ni katika zile ibada zinazokubali niaba. Majibu yetu: Sheria pekee ndiyo yenye mamlaka ya kuainisha matendo yanayokubali niaba na yale yasiyoikubali. Kwa mfano mtu akitamka shahada mbili kwa niaba ya ndugu yake aliyekufa kafiri, shahada hiyo hata kama itatamkwa mara elfu kumi, haitamnufaisha yule kafiri kwa chochote, kwa kuwa Uislamu haukubali niaba katika suala la imani bali inatakiwa mtu atamke mwenyewe shahada mbili baada ya kuwa ametosheka kwa nguvu za hoja kuwa Uislamu ni dini sahihi. Lakini ibada ya funga, hadithi zilizotangulia zimeonesha msisitizo wa kufunga kwa niaba ya wenzetu na kwamba funga hizo tutakazozifunga zitapokelewa. Ama kauli ya kusema kuwa swala haikubali niaba, au haiwezekani mtu kuswali kwa niaba ya ndugu yake aliyetangulia mbele ya haki, kwa kweli kauli hiyo ya kiwahabi inachekesha kama si kuliza, kwani mawahabi wanakubali kuwa mtu anaweza kuhiji kwa niaba ya 183

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 183

8/14/2017 1:18:35 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

mtu mwingine, na moja katika matendo ya Hijja ni Swala ya Twawafu, na Swala hiyo ikikosekana na Hijja pia ni batili. Sasa ikiwa swala haikubali niaba itakuwaje Hijja ya niaba iwe sahihi wakati ndani yake kuna swala ya Twawafu na swala haiswaliwi kwa niaba ya mtu mwingine? Ni wazi kwamba amali ikishakubali niaba basi yale yote yanayofungamana na amali hiyo pia yataruhusiwa. Kwa mfano tukisema kuwa hairuhusiwi kusoma Qur’ani kwa niaba ya mtu mwingine, halafu wakati huo huo tunasema kuwa mtu anaruhusiwa kuswali kwa niaba ya ndugu yake aliyetangulia mbele ya haki, hapo tutachekesha watu kwani katika swala kuna Suratu al-Fatiha, nayo ni Qur’ani na swala haikubaliwi bila ya sura hiyo. Kwa hiyo madai ya kiwahabi ya kwamba swala haiswaliwi kwa niaba, au Qur’ani haisomwi kwa niaba ya mtu mwingine, madai yote hayo yanabatilishwa na kauli yao wenyewe ya kwamba mtu anaweza kuhiji kwa niaba ya mtu mwingine. Sasa kama swala haina niaba mbona kwenye Hijja kuna swala ya Twawafu? Na kama Qur’ani haina niaba mbona swala hiyo ya Twawafu ndani yake kuna Suratal-Fatiha? Imethibiti kutoka kwa Imamu Ahmad bin Hanbal kuwa: “Surat Yasin ni Moyo wa Qur’ani, atakayeisoma kwa kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu atamsamehe, basi wasomeeni wafu wenu.”104 Mawahabi mpaka lini mtafanya kazi ya kupotosha watu, kwa ajili ya kutafuta radhi za mabwana zenu wa Uingereza?

A l-Wahabiya baina mabani al fikri… Kutoka kitab Musnad Ahmad Bin Hanbal Jz. 4, uk. 26.

104

184

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 184

8/14/2017 1:18:35 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

SEHEMU YA SABA MAULIDI

J

e! ni kweli maulidi haina mashiko katika Qur’ani wala Sunnah?

Siku ya kuzaliwa kwa Bwana Mtume 8 ni katika siku ambazo Qur’ani inataka zikumbukwe, kama inavyoelezwa katika Surat Ibrahim:

“Hakika tulimtuma Musa pamoja na miujiza Yetu, kuwa itoe kaumu yako gizani kwenda kwenye nuru. Na uwakumbushe Siku za Mwenyezi Mungu…. Hakika kaatika hayo kuna ishara kwa kila mwenye kusubiri, mwenye kushukuru.”105

Je! ni zipi Siku za Mwenyezi Mungu? Siku zote ni za Mwenyezi Mungu, na hakuna hata siku moja ambayo si ya Mwenyezi Mungu! Lakini lugha hiyo inaweza kumwacha msomaji na maswali mengi, ila ukiitafakari utakuta kuwa hata sisi katika matumizi yetu ya kila siku huwa tunaitumia lugha kama hiyo. Pale tunaposema kuwa Hussein ni mwanaume, kwa hakika kauli hiyo haimaanishi kuwa Musa ni mwanamke, bali naye pia ni mwanaume lakini kila mwanaume katika uwanaume wake, ana mambo yake ya kipekee yanayomtofautisha na mwanaume mwingine. Sasa Mwenyezi Mungu aliposema: “Na uwakumbushe siku za Mwenyezi Mungu” makusudio yake ilikuwa ni zile siku ambazo   Surat Ibrahim; 14:5

105

185

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 185

8/14/2017 1:18:36 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

zina matukio ya kihistoria ambayo hayatakiwi kusahauliwa. Utume wa Musa ulikuwa na malengo ya kuwatoa wana wa Israel gizani na kuwapeleka kwenye nuru, na kuwakomboa kutoka kwenye nyumba ya utumwa, kwani wana hao wa Israel walikuwa wakiishi chini ya utawala wa kiongozi asiyejua halali wala haramu. Kiongozi aliyevuka mipaka na kudai uungu. Kiongozi huyo alikuwa akichinja kila mtoto wa kiume na kumwacha hai kila mtoto wa kike. Tukio la kwanza la kustaajabisha ni pale alipozaliwa Musa D, kiongozi huyo alishindwa kumchinja na badala yake alimlea kama mtoto wake, na Mwenyezi Mungu akaiita siku hiyo kuwa ni siku Yake kutokana na maajabu aliyoyafanya ndani ya siku hiyo. Na pia akawataka wana wa Israili wakumbushwe siku hiyo, ili wasiisahau. Tukio la kupasua njia katika bahari, siku hiyo pia Mwenyezi Mungu anataka wana wa Israil waikumbuke, kutokana na miujiza ya Kiungu iliyofanyika ndani ya siku hiyo, ambayo ni kuwakomboa wana wa Israili na kumwangamiza kiongozi yule aliyevuka mipaka, yeye na kundi lake. Na tunaposoma uvukaji mipaka wa kiongozi huyo wa Kimisri tunaukuta hautofautiani sana na uvukaji mipaka unaofanywa na kundi la kiwahabi la Daesh, tofauti ni kwamba kiongozi huyo wa Kimisri alikuwa anachinja watoto wa kiume tu, lakini Daeshi (Mawahabi) wanachinja watu wazima na wanachinja watoto wote bila kutofautisha kati ya mwanamke na mwanaume. Kwa mantiki hiyo tunasema kuwa Firauni alikuwa mbaya lakini Mawahabi ni wabaya zaidi. Je! Waislamu hatuna siku za kukumbuka? Tukiutafakari utume wa Muhammad 8 kupitia Aya iliyotangulia, tutaukuta na wenyewe pia una malengo sawa na yale ya utume wa Musa D, ila tofauti ni kwamba utume wa Musa ulikuwa ni kwa Waisraeli tu, wakati utume wa Muhammad ni utume wa kimataifa, 186

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 186

8/14/2017 1:18:36 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

na ni utume uliokuja kuukomboa ulimwengu mzima. Utume huo ndiyo una haki zaidi ya kuwa na matukio ya kukumbukwa. Wakati Mtukufu Mtume Muhammad 8 alipokabidhiwa utume, hali haikuwa salama katika jamii za Kiarabu, watu walikuwa wanaua watoto wa kike kwa madai ya kuwa watoto wa kike ni aibu na fedheha kwa familia. Lakini kwa baraka za utume huo wa kimataifa tabia hiyo ya Waraabu ikawa imekomea hapo. Hiyo ilikuwa ni neema kubwa ya Mwenyezi Mungu ndani ya siku hiyo ambayo inapaswa kukumbukwa. Watu walikuwa wakiishi nje kabisa ya wigo wa utu na maadili mema, lakini kwa baraka ya utume wa kimataifa wa Muhammad 8 maisha ya kijamii yalisimama juu ya misingi ya uadilifu, hali ambayo ilipelekea upendo, mshikamano, na usawa katika utu, na biashara ya utumwa ikakosa mahala pakuweka unyayo. Masiku yote hayo ni masiku ya Mwenyezi Mungu ambayo tunatakiwa kuyakumbuka, na hatuwezi kukumbuka ushindi mkubwa kama huo bila kumkumbuka aliyeuleta. Na siamini kama yuko mtu mwenye akili huru anayekubali kukumbuka matukio hayo bila kumkumbuka aliyechangia katika upatikanaji wake. Mpenzi msomaji leo hii kama utawaambia ndugu zetu Wahindi waadhimishe uhuru wa taifa lao lakini wasimtaje kabisa Mzee Mahatima Ghandi, bila shaka watakupeleka hospitali kwanza ili ukapimwe akili. Na sisi Waislamu ukitwambia tukumbumbuke ukombozi wa Mtume Muhammad lakini yeye mwenyewe tusimkumbuke, hapo ni lazima tuushakie Uislamu wako, kwani ukombozi wa Mtume Muhammad umempatia nafasi ya kupenya na kuingia ndani ya moyo wa kila muumini. Na ili mtu aingie kwenye orodha ya waumini ni lazima kwanza ampende Mtume wetu mapenzi ya kweli, na mapenzi ya kweli ndiyo yatakayomfanya mtu kuwa ni mwenye kufuata nyayo za Mtume wetu 8. Mwenyezi Mungu anasema: 187

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 187

8/14/2017 1:18:36 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

“Sema ikiwa baba zenu, na wana wenu, na ndugu zenu, na wake zenu, na jamaa zenu, na mali mlizozichuma, na biashara mnazohofia kuharibikiwa, na majumba mnayoyapenda, ni vipenzi zaidi kwenu kuliko Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na jihadi katika njia Yake basi ngojeni mpaka Mwenyezi Mungu alete amri yake…..”106

Kwa hiyo lengo letu katika maulidi ni kuthibitisha upendo wetu juu ya Mtume wetu na kwamba hakuna mwenye nafasi ndani ya nyoyo zetu zaidi ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na katika hadithi Bwana Mtume 8 anasema: “Naapa kwa anayemiliki pumzi yangu, hataamini mmoja wenu mpaka anipende zaidi katika watu kuliko baba yake na mtoto wake.” Kwa hiyo kwa ibara nyingine maulidi ni njia mojawapo ya kudhihirisha upendo wetu na heshima zetu juu ya Bwana Mtume 8. Alama za kufaulu: Mwenyezi Mungu anasema katika Qur’ani:

“….. Basi wale walioamini na wakamheshimu na wakamsaidia na wakafuata nuru iliyoteremshwa pamoja naye, hao ndiyo wenye kufaulu.” 107

Katika Aya hiyo kuna mambo manne ambayo endapo mtu atayashikilia basi atakuwa ni mwenye kufaulu:   Surat Tauba; 9:24   Surat A’raf; 7:157

106 107

188

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 188

8/14/2017 1:18:36 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

a.

Kumwamini

b. Kumheshimu c.

Kumnusuru

d. Kufuata nuru iliyotteremshwa pamoja naye. Kinachotakiwa kwa Mwislamu kwanza kabisa ni kumwamini Mtukufu Mtume 8, kisha kumheshimu yeye na kumtukuza, na mengineyo kama ilivyo katika orodha hiyo. Sasa kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa Bwana Mtume 8 si jambo lililokuwa nje na mpangilio wa Aya tuliyoitaja, bali ni jambo lililoko ndani ya Aya na katika kifungu (b). Nasi kwa kufuata kifungu hicho, sisi tutaendelea kumtukuza Mtume wetu, na Maulidi yake tutailinda kwa gharama yoyote ile, ili kuhakikisha utajo wa Bwana Mtume unabaki hadi milele. Na moja katika neema za Mwenyezi Mungu kwa Mtume Wake ni ile kauli isemayo:

“Na tukakunyanyulia utajo wako.”108

Kwa mujibu wa Aya hiyo ni kwamba Bwana Mtume 8 atatukuzwa daima. Labda tuwaulize hao wenye chuki na Mtume: Endapo maulidi itafanywa kwa kuzingatia mipaka ya kisheria, hiyo itakuwa ni kumtukuza Mtume au itakuwa ni katika mambo yanayomdhalilisha? Maulidi ndiyo iliyoufikisha Uislamu hapa ulipo leo hii. Maulidi ndiyo chombo kilichowaunganisha Waislamu bila kujali itikadi zao za kimadhehebu. Sasa umoja huo ulikuwa ni pigo kubwa kwa maadui, maana wao siku zote hufanya jitihada za kuwatenganisha. Miaka ya   Surat Inshirah; 94:4

108

189

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 189

8/14/2017 1:18:36 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

1970 kwenda mbele waliibuka vibaraka wa ukoloni wa Uingereza na madhehebu bali na dini mpya ya kucheza karate misikitini. Lengo kuu la madhehebu hiyo ni kuvunja ile sehemu ya Aya inayotaka Mtume atukuzwe, na kueneza fikra chafu dhidi ya Mtume 8 na Uislamu kwa jumla. Vibaraka hao walilenga sana kundi la vijana na watu wazima wasio na uwelekevu katika dini, kwani watu hao ni rahisi kudanganywa kwa hoja mbovu kuliko nyumba ya buibui.

HOJA CHAKAVU ZA KIWAHABI KATIKA KUPINGA MAULIDI Ya kwanza: Wenye chuki na Mtume 8 wanasema: Hakika maulidi haina mashiko katika Qur’ani wala katika hadithi za Mtume, na kisichokuwa na mashiko katika Qur’ani au katika hadithi za Bwana Mtume, ni Bidaa na ni haramu kwa mujibu wa sheria. Majibu yetu: Katika masomo yaliyopita tumewahi kusema kuwa Bidaa Ni kuzidisha au kupunguza katika dini, bila ya kuwepo mashiko yanayounga mkono uzidishaji au upunguzaji huo. Kwa hiyo ufahamu sahihi wa maneno ni kwamba kitakachokuwa na mashiko katika Qur’ani hakiwezi kuwa Bidaa! Kwa hiyo maulidi sio Bidaa kwa sababu ina mashiko katika Qur’ani. Maulid lengo lake ni kumtukuza Mtume na Mwenyezi Mungu anasema:

190

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 190

8/14/2017 1:18:36 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

“….. Basi wale walioamini na wakamheshimu na wakamsaidia na wakafuata nuru iliyoteremshwa pamoja naye, hao ndiyo wenye kufaulu.”109

Lengo lingine katika kusoma maulidi ni kudhihirisha mapenzi yetu kwa Bwana Mtume 8 kama isemavyo hadithi: “Naapa kwa anayemiliki pumzi yangu, hataamini mmoja wenu mpaka anipende zaidi katika watu kuliko baba yake na mtoto wake.” Hatuna sababu ya kurefusha mazungumzo kwani somo hili limekwishaelezwa kwa kina katika mahala pake katika kurasa za nyuma. Ya pili : Kumtukuza binadamu ni aina ya ibada, na anayestahiki kuabudiwa ni Mwenyezi Mungu peke Yake, na hakuna binadamu mwenye haki hiyo ya kunyenyekewa na kutukuzwa. Majibu yetu: Ibada ni unyenyekevu lakini si kila unyenyekevu ni ibada. Kwa hiyo ili maana sahihi ya ibada itimie ni lazima tupate nguzo zifuatazo: a.

Unyenyekevu

b. Imani juu ya uungu wa yule mnyenyekewa. Kwa hiyo nyenyekea uwezavyo lakini kama hutaamini kuwa unayemnyenyekea ni Mungu basi unyenyekevu wako bado haujatimiza vigezo na masharti ya kuitwa ibada. Kwa mantiki hiyo sisi tunamtukuza sana Mtukufu Mtume 8 na tunamsifu kadiri ya uwezo wetu, sifa zote tunampa ila hatuamini kuwa Bwana Mtume ni Mungu, na kwa mujibu wa nguzo hizo mbili za neno ibada, utukuzaji wetu bado haujafikia kiwango cha kuitwa ibada.   Surat A’raf; 7:157

109

191

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 191

8/14/2017 1:18:36 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Kama kweli madai ya Mawahabi ni sahihi kwamba unyenyekevu ni ibada basi dunia nzima imejaa Washirikina, maana hata Manabii waliwanyenyekea wazazi wao, na Qur’ani pia inatuamrisha kuwanyenyekea wazazi, sasa kama unyenyekevu ni ibada kwa nini Mwenyezi Mungu anatuamrisha kuwaabudu wazazi? Ndugu zangu katika utu tudumu katika mila na desturi za kudumisha matukufu ya dini yetu. Uwahabi ni uzumbukuku na ubabaishaji. Kwa hiyo msidanganyike kwa hoja mbovu zaidi kuliko nyumba ya buibui, zinazoletwa kwenu na madhehebu hii ya uzushi, hali ya kuwa mnatambua kuwa maulidi ndio iliyoufikisha Uislamu hapa ulipo leo hii. Kukubalika kwa Bwana Mtume Muhammad 8: Ni ukweli usiopingika kuwa Bwana Mtume Muhammad 8 alikuwa ni kiongozi wa kimataifa, lakini tabia yake pia ilikuwa ni chachu yeye kuweza kupenya na kuingia katika nyoyo za watu kwa haraka. Tabia zake ndizo zilizoanza kuwavutia watu kabla ya ujumbe aliokuja nao. Lakini Mwenyezi Mungu naye anamsifu Mtume wake kuwa:

“Na hakika wewe una tabia tukufu.110

Hii ina maanisha kuwa kama maadili mema yangelikuwa ni mlima mrefu basi tungemkuta Bwana Mtume Muhammad 8 juu ya kilele cha mlima huo, na kwa mantiki hiyo tunasema kuwa: Bwana Mtume 8 ni zaidi ya maadili mema kwa sababu yeye yuko juu ya maadili, na maadili yako chini yake. Kisha Mwenyezi Mungu anaendelea kumsifu Mtume wake kwa kusema:   Suratul Qalam; 68:4

110

192

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 192

8/14/2017 1:18:36 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

“Kwa sababu ya rehema itokayo kwa Mwenyezi Mungu umekuwa ni laini kwao. Lau ungelikuwa mkali mwenye moyo mgumu bila shaka wangelikukimbia.....”111

Huo ndio wasifu kamili wa Bwana Mtume 8. Yeye alikuwa ni mpole na mwenye maneno mazuri yamuingiayo mtu akilini kwa urahisi, na moyoni kwa mahaba, na yawezayo kumbadilisha adui kuwa rafiki. Kwa hiyo ile dhana ionayo kuwa Uislamu ulienea kwa upanga, ni dhana ya kikoloni inayoenezwa kivitendo na Mawahabi, na dhana hiyo haina mashiko katika Qur’ani wala katika Sunah za Bwana Mtume 8 isipokuwa tu dhana hiyo ilikuwa na malengo ya kuuchafua Uislamu na kuufanya uonekane kuwa ni dini ya wahuni, wakosa busara, watovu wa nidhamu kwa Mwenyezi Mungu na Mitume achilia mbali kwa wazazi. Mpenzi msomaji hebu tazama mambo yanayofanywa na vibaraka wa wakoloni wanaojiita Answar Suna halafu uyalinganishe na moyo wa huruma aliokuwanao Bwana Mtume 8 ndipo utakapofahamu kuwa Mawahabi ni maharamia waliokuja kuharibu matukufu ya dini kwa anuani ya kunusuru Sunnah. Je, ni Sunah ya Mtume gani inayoruhusu kuua watu wasio na hatia kwa tofauti za kiitikadi? Na machafu yote hayo yanayofanywa na Mawahabi, yanafanywa kwa jina la jihadi, na jihadi kwa kadiri ya Kamusi Sanifu ya Kiwahabi ni kuwalazimsha watu wote wafuate itikadi zao. Na hapo maana yake ni kuwatenza watu kwa nguvu kufuata imani za kiwahabi. Lakini hiyo siyo siasa ya Bwana Mtume 8 bali siasa yake aliyoitumia hadi akakubalika ilikuwa ni hekima na busara. Hebu tu  Surat al Imran; 3:159

111

193

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 193

8/14/2017 1:18:36 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

rudi nyuma hadi mwaka wa sita wa Hijiria ili tuone hekima iliyotumika wakati huo hadi kuikomboa Makka.

MKATABA WA AMANI WA HUDAIBIYAH Mnamo mwaka wa 6 Hijiria, Bwana Mtume 8 aliondoka na Maswahaba kuelekea Makka, na Waislamu wengi walivutiwa na hilo isipokuwa baadhi yao walijizuia na safari hiyo. Basi wale waliokuwa na Bwana Mtume 8 waliovaa vazi rasmi (ihraam) walikuwa watu 1,400 na hawakuwa na silaha zaidi ya panga ambazo kwa kadiri ya zama hizo upanga ulikuwa ni silaha ya msafiri. Na walipofika Asfan eneo lililopo karibu na mji wa Makka, ilisikika tetesi kuwa Makuraishi wamejipanga na wameazimia kumzuia Bwana Mtume 8 asiingie Makka. Na walipofika Hudaibiya, kijiji kilicho umbali wa kilo mita 20 au 26 kutoka Makka, Bwana Mtume aliwaamuru Maswahaba kupiga kambi katika eneo hilo. Maswahaba wakasema ‘Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, hakika sehemu hii haina maji wala usalama.’ Basi Mwenyezi Mungu akaandaa maji kwa njia ya muujiza kupitia kisima kikavu kilichokuwepo katika eneo hilo. Kisha wawakilishi wa Makuraishi na wale wa Bwana Mtume 8 wakaanza kutafuta mbinu za kutatua mgogoro kwa njia yoyote ile. Na hatimaye alikuja bwana mmoja kutoka kambi ya upinzani, Ur’wah al Thaqafi. Bwana Mtume 8 akamwambia: “Hakika sisi hatukuja kwa ajili ya kugombana na yeyote bali tumekuja kwa ajili ya ibada.” Lakini Ur’wah alishangaa kuona Bwana Mtume 8 akifanyiwa mambo ambayo hajawahi kumshuhudia kiongozi yeyote akifanyiwa na watu wake, kwani Bwana Mtume 8 wakati wa kutawadha alikuwa akizungukwa na Maswahaba, ambao walikuwa wakiyagombania yale maji yaliyokuwa yakidondoka wakati wa kutawadha kwake, na hawakuruhusu hata tone moja kufika chini. Na Ur’wah 194

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 194

8/14/2017 1:18:36 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

aliporejea kwa Makuraishi aliwaambia: “Kwa hakika nimetembelea majumba ya wafalme, Kisra (Iran) Kaisari (Roma) Najash (Ethiopia) na sikupata kuona kiongozi mwenye haiba mbele ya watu wake kama vile Muhammad mbele ya Maswahaba wake...” Kisha akaongezea kuwa: “Ikiwa mnadhania kuwa Maswahaba wa Muhammad wanaweza kumuacha basi mnakosea mno... nyinyi mko katika mapambano na watu ambao wanaamini kuwa si hasara kwao kupoteza roho zao kwa ajili ya Mtume wao, kwa hiyo mnapaswa kujua ni jinsi gani mtapambana nao.” Kisha Bwana Mtume alimwamrisha Umar K kwenda Makka ili kuwafahamisha viongozi na wakuu wa Makuraishi lengo la safari yake 8 kutoka Madina kwenda Makka, lakini kwa bahati mbaya Umar K aliomba radhi na akasema kuwa, kuna uadui baina yake na Makuraishi naye anahofia hilo kwa hiyo ni bora aende Uthman K. Naye Uthman aliondoka kuelekea Makka na haukupita muda mrefu, habari ikasikika kuwa Uthman K ameuawa. Bwana Mtume 8 akafanya maandalizi ya kupambana vikali na Makurishi! Basi akawataka Maswahaba wake watoe kiapo cha utii katika hilo, nao wakafanya kama walivyotakiwa kufanya, na wakaahidi kuendeleza mapambano hadi pumzi ya mwisho. Kitendo hicho cha Maswahaba kuunga mkono fikra ya mapambano dhidi ya Makuraishi kiliitwa Baiat Ridh’wan. Lakini kwa bahati nzuri haukupita muda mrefu Uthman K akawa amerejea akiwa salama. Na kwa upande wa Makuraishi wao pia walimtuma mtu wao, Suheil bin Amru kwenda kwa Bwana Mtume 8 kuomba suluhu ili kuleta amani kati ya pande mbili, isipokuwa wao Makuraishi walisisitiza kuwa Bwana Mtume 8 asiingie Makka ndani ya mwaka ule. Na baada ya mazungumzo marefu yaliyojiri baina ya Bwana Mtume 8 na mjumbe wa Makuraishi, uliandaliwa mkataba wa amani baina ya pande hizo mbili, na moja ya vipengele 195

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 195

8/14/2017 1:18:36 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

vya mkataba kilikuwa ni hicho tulichokitaja kuwa Bwana Mtume 8 asiingie Makka mpaka mwaka ujao. Na katika mkataba palikuwa na vipengele vilivyohusu usalama wa nafsi na mali kwa ajili ya Waislamu na pia kwa wasafiri watokao Madina kwenda Makka. Mkataba ulilenga kusitisha kwa muda mapigano ya muda mrefu baina ya Waislamu na Washirikina, na pia haikutakiwa kwa pande zote mbili kuvunja masharti ya mkataba kabla ya kumalizika muda huo ulioafikiwa na pande zote mbili. Sura ya mkataba wa amani wa Hudaibiya: 1.

Waislamu wamekubaliana na Makuraishi kusitisha mapigano kwa muda wa miaka kumi.

2.

Mkuraishi atakayekimbilia kwa Muhammad bila idhini ya kiongozi wake basi arudishwe, na Mwislamu atakayekimbilia kwa Makuraishi asirudishwe.

3.

Mwenye kupenda kuunga urafiki na Muhammad basi aruhusiwe, na mwenye kupenda kuunga urafiki na Makuraishi pia hakuna kizuizi.

4.

Muhammad asiingie Makka bali arejee Madina hadi mwaka ujao, na Makuraishi wataondoaka Makka ili kumpisha afanye ibada zake, naye atabakia humo kwa muda wa siku tatu tu kwa sharti asije na silaha zaidi ya upanga, ambao ni silaha ya kila msafiri.

5.

Uhuru wa kuabudu na mtu asilazimishwe kuacha dini yake. Na Waislamu wamwabudu Mungu huko Makka wazi wazi bila kujificha (na Uislamu usiwe dini ya siri kwa kuwaogopa Makuraishi) na asiudhiwe yeyote. 196

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 196

8/14/2017 1:18:36 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

6.

Pasiwepo wizi wala hiana bali kila mmoja aheshimu mali za mwingine.

7.

Makuraishi hawatamsaidia yeyote dhidi ya Muhammad. 112

8.

Na baada ya mkataba huo kusainiwa na pande zote mbili, nakala moja ilipelekwa kwa Makuraishi na nyingine ilibakia kwa Bwana Mtume 8 lakini sharti la kurejea bila kufanya ibada lilikuwa gumu kwa baadhi ya Waislamu isipokuwa Bwana Mtume 8. Alionesha mfano yeye mwenyewe kwanza, alichinja mnyama wake na akavua vazi la ihraam na ndipo Waislamu walipotambua kuwa hiyo ilikuwa ni hukumu mahsusi ambayo Mwenyezi Mungu amemuamuru Nabii Wake.

Kwa hiyo Waislamu wakawa hawana budi ila kutekeleza amri ya Bwana Mtume 8. Wote walirejea Madina kwa huzuni kubwa baada ya kuona kwamba malengo yao hayakutimia. Kwa kweli walisononeka mno na hiyo ni kwa sababu hawakujua kuwa nyuma ya mkataba huo kuna ukombozi mkubwa kwa Waislamu na mustakabali wa Uislamu. Na ndani ya kipindi hicho ilishuka Surat Fat-hu, na Bwana Mtume 8 akabashiriwa ushindi wa wazi113 Athari chanya za kisiasa na za kijamii za mkataba wa Hudaibiya: Tukilichunguza tukio la Mkataba wa Amani wa Hudaibiya tutalikuta kuwa ni tukio ambalo ndani yake kuna vipengele vingi vilivyowawezesha Waislamu kupata ushindi wa wazi, ikiwa ni pamoja na wao kupata nguvu kubwa ambayo haikuwa na upinzani kutoka upande wa pili. Hapa tutakutajia faida zilizopatikana baada ya mkataba huo:  Sayyed al Mursalina, Jz. 2, uk. 339   Al Amthal, Jz. 13, uk. 11 - 13.

112 113

197

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 197

8/14/2017 1:18:37 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

1.

Waislamu waliweza kuwabainishia washirikina wa Makka kwa vitendo kuwa wao hawakuwa na nia ya vita na yeyote wala kumwaga damu, na kwamba wao wanaiheshimu Kaaba tukufu. Na jambo hilo lilikuwa ni sababu ya wengi kuvutiwa na Uislamu.

2.

Kwa mara ya kwanza Makuraishi waliweza kukiri na kuutambua rasmi Uislamu na Waislam, na hiyo ilikuwa ni sababu ya Uislamu kupata nafasi katika Rasi la Uarabu.

3.

Baada ya mkataba huo, Waislamu waliweza kwenda kokote kwa amani na utulivu, na bila ya kuhofia usalama wao na wa mali zao, na wakaweza kufanya mawasiliano ya karibu na washirikina yaliyoacha athari chanya kwa washirikina hao. Na hiyo ilikuwa ni fursa nyingine kwa Uislamu kuzidi kujulikana.

4.

Njia ilifunguka na Uislamu ukaenea na athari chanya za msimamo wa Bwana Mtume 8 katika kupatanisha migogoro ya Makabila ya Kiarabu, na makabila yote hayo yalibadilisha mitazamo yake na badala yake yaliuelekea Uislamu na Mtume wake.

5.

Mkataba wa amani wa Hudaibiya uliandaa njia ya kuikomboa Khaybar na kung’oa saratani hii inayowakilishwa na Mayahudi, na ambayo ilikuwa inatengeneza hatari kubwa kwa matendo na nguvu dhidi ya Uislamu na Waislamu.

6.

Na kwa msingi huo, hakika kitendo cha Makurayshi kujizuia kupambana na jeshi ambalo lilikuwa linaundwa na Waislamu elfu moja na mia nne tu, na huku hajabeba yeyote kati yao silaha yoyote ila silaha ya safari, na kisha wakakubali Makurashi mkataba wa amani, hili lenyewe pia katika uwenyewe wake 198

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 198

8/14/2017 1:18:37 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

lilikuwa ni sababu muhimu ya kuimarisha ari ya kiroho ya Waislamu na kushindwa kwa maadui wa Uislamu mpaka kufikia kiwango kwamba walikuwa wanaogopa kupambana na Waislamu. 7.

Na baada ya mkataba huo wa amani Nabii 8 aliandika barua na ujumbe mbalimbali kwenda kwa wakuu wa dola kubwa (Iran, Urumi, Uhabeshi), na kwenda kwa wafalme wakubwa wa ulimwenguni, akiwaita katika Uislamu. Na hili lenyewe linajulisha kuwa mkataba uliwajengea Waislamu hali ya kujiamini na kufunguka, sio tu katika Rasi ya Uarabuni bali pia katika ulimwengu wote.

Vyanzo vya umoja na amani duniani: Katika hii dunia tunaishi watu wa itikadi mbali mbali katika nyanja mbali mbali, za kisiasa, kiuchumi, kijamii hadi za kidini, kwa hiyo kama tunataka amani inatubidi tuwe ni watu waelewa tunaoelewa hisia za wenzetu. Tuheshima mila na desturi zao na bila ya kukejeli matukufu ya dini zao, na vivyohivyo wao pia wawe ni watu waelewa wanaoelewa hisia zetu. Pia waheshimu mila na desturi zetu na wasiyafanyie dhihaka matukufu ya dini yetu. Na hii ndio maana ya kutambuana, kama ilivyonenwa katika Qur’ani:

“Enyi watu! Hakika Sisi tumewaumba kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumewafanya mataifa na makabila ili mjuane. Hakika mtukufu zaidi yenu mbele ya Mwenyezi Mungu ni aliye na takua ziadi yenu. Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye habari. ”114   Hujurat; 49:3.

114

199

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 199

8/14/2017 1:18:37 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Mwenyezi Mungu aliposema kujuana hakumaanisha kujuana majina bali alimaanisha kama tulivyofanunua kuwa sisi tuwajue wenzetu na wao watujue sisi katika mfumo mzima wa maisha yetu. Kisha baada ya kujuana kila mmoja amvumilie mwenzake. Mambo hayo yakifanikiwa basi ile dhana ya dunia nzima kuwa ni kijiji kimoja chenye serikali moja na katiba moja na msemaji mmoja itakamilika, na watu wote bila kujali dini zao wataishi kwa amani na upendo kama ndugu wa tumbo moja bila kuchukiana wala kudharauliana. Na Yule atakayeona kuwa mwenzake kateleza kiimani, basi atafanya naye mazungumzo kwa hekima na busara na kwa lugha tamu iliyojaa heshima, lugha iwezayo kufungua akili kwa wepesi na moyo kwa upendo. Ndugu msomaji! Majadiliano ni njia ya kuufikia ukweli kwa sharti tu majadiliano hayo yafanywe kwa kuzingatia heshima baina ya pande zote mbili zinazotofautiana. Lakini endapo yakifanywa bila kuzingatia masharti hayo, tena kwa lugha kali za Kiwahabi, basi lengo la kutatua mgogoro na kuleta amani halitakamilika. Mtu mwenye busara anapotaka kumwongoza ndugu yake katika utu husema hivi:

“.....Na hakika sisi au nyinyi bila shaka tuko kwenye uongofu au upotevu ulio wazi.�115

Kwa ibara nyepesi, usimwambie ndugu yako kuwa wewe umepotea, kwa asilimia zote, na mimi nimeongoka, kwani ukisema hivyo utagusa hisia zake na yeye atataka kufanya radiamali, na hapo amani itatoweka. Kwa hiyo lugha ya adabu ni kumwambia ndugu yako   Sabai : 24

115

200

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 200

8/14/2017 1:18:37 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

kuwa huenda mimi nimepotea na wewe umeongoka, au yawezekana mimi nimeongoka na wewe umepotea. Sasa ili tuufikie ukweli uliofichika baina yetu, njoo tuzungumze. Kwa amani bila jazba wala kupandishiana sauti, na bila kutumia lugha kali zinazoweza kutuvua sifa zetu za ubinadamu. Bwana Mtume 8 alifanya mazungumzo na watu wenye itikadi tofauti na yake na lugha aliyoitumia ilikuwa ni lugha ya kupendeza:

“Sema: Enyi watu wa kitabu! Njooni kwenye neno la usawa baina yetu na baina yenu.....�116

Bwana Mtume 8 alitaka kuwahakikishia watu wa upande wa pili kuwa tofauti za kiitikadi baina yetu zisiwe ni sababu ya kuvunja amani na maelewano kati yetu bali njooni tufanye mazungumzo ili tuweze kutatua mgogoro na kudumisha amani kati yetu. Ndugu msomaji! Vipengele vya mkataba wa amani vinaeleza waziwazi namna ambavyo Bwana Mtume 8 alikuwa akilijali suala la amani katika jamii. Na kama Bwana Mtume angelikuwa ni mtu wa fujo basi kwa vyovyote vile asingekubali kusaini mkataba wa amani wa Hudaibiya kutokana na masharti magumu yaliyojitokeza ndani ya vipengele vya mkataba huo. Amani ni maslahi ya umma na siyo maslahi ya Waislamu peke yao wala Wakristo peke yao. Mkataba wa amani uliyosaniwa Hudaibiya haukulenga kuleta amani kwa wakazi wa Makka na Madina tu, bali ulimwengu mzima. Kwa lugha nzuri tunasema kuwa Bwana Mtume 8 alitaka kuwafundisha wanadamu kivitendo kwamba hakuna haki ya kumuua Mkristo kwa sababu ya tofauti za kiitikadi, na vilevile Mkristo hana haki ya ku  Surat al Imran : 64

116

201

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 201

8/14/2017 1:18:37 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

muua Mwislamu kwa sababu ya tofauti hizo. Hali kadhalika serikali haina haki ya kuuwa watu fulani au kuwafunga kwa sababu tu watu hao hawauamini mfumo wa serikali hiyo. Kwa hiyo ukiona serikali inaua watu basi ujue ni kwa makosa ya uhaini na usaliti wa kuisaliti nchi na watu wake. Na hivyohivyo dola ya Kiislamu inapovamiwa na maadui basi wajibu wa dola ni kujihami, na kujihami si kuvunja amani bali ni kudumisha amani ndani ya nchi inayokaliwa na watu wa dini mchanganyiko. Amani ambayo wakoloni wanafanya jitihada za kuiondoa kwa vitendo kupitia vibaraka wao Mawahabi wanaoendesha mauaji na kuvanja amani kwa jina la Uislamu, wakati Uislamu wenyewe ulikwishaonesha msimamo wake tangu siku ile Bwana Mtume 8 aliposaini mkataba wa amani baina yake na Makuraishi waliokuwa na imani tofauti na yake. Makuraishi ambao walikuwa wakiamini kuwa Bwana Mtume Muhammad 8 alikuwa ni mtu wa vurugu na mpenda madaraka na imani hiyo wakaieneza kila mahala, na watu wengi wakaamini kuwa ni kweli, lakini tukio la Hudaibiya lilimsafisha Mtume na kumvua kila sifa mbaya aliyovishwa na Makuraishi. Historia inajirudia: Bwana Mtume 8 alipata upinzani wa hali ya juu kutoka kwa viongozi na wakuu wa Makuraishi, wakuu ambao waliamini kuwa Bwana Mtume anatafuta madaraka ili kujipatia umaarufu. Kwa dhana hiyo walijitokeza wengi na kumuahidi mambo mengi ukiwemo ufalme ikiwa tu atakubali kuacha harakati za kupigania uadilifu, na kuitaka jamii ijitambue na iache kulala. Lakini Bwana Mtume 8 hakushawishika na yote aliyoahidiwa, kwa nini? Kwa sababu yeye si mbinafsi kwanza, bali yeye ni Mtume wa Kimataifa anayeweka mbele maslahi ya umma kabla ya tumbo lake. Yeye ni rehema ya Mwenyezi Mungu kwa walimwengu wote bila kujali tofauti zao za kiitikadi. 202

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 202

8/14/2017 1:18:37 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Sasa Wakuu wa Makuraishi waliposhindwa kupambana naye kwa hoja waliamua kumpakazia kila sifa chafu katika jamii, lakini yale waliyoyavumisha ndio yaliyompatia ushindi na kuweza kuikomboa Makka mnamo mwaka wa nane wa Hijiriya tena kwa amani. Na wakuu wa madola yenye nguvu kama wanavyojiita wenyewe (Super Power) waliposhindwa kuuzima Uislamu kwa hoja, waliamua kuazima mbinu za Kikuraishi na kuwapatia vibaraka wao wanaojiita Answar Suna ili wafanye mauaji, uporaji, ubakaji na kila kiwezacho kuondoa amani kwa walimwengu wote na kuondoa umoja wa Kiislamu kwa njia moja au nyingine kwa jina la jihadi, ilimradi tu Uislamu uonekane mbele ya jamii za kimataifa kuwa ni dini ya Wahuni wavaa kaptula na kucheza karate misikitini bila ya kujali kuwa misikiti ni nyumba za Mwenyezi Mungu na inabidi ziheshimiwe. Na tayari watu wengi wamekwishaamini kuwa Uislamu ni dini ya vurugu na mauaji kwa watu wasiokuwa na hatia, dini ya uchokozi, uvamizi, dini isiyoheshimu imani za watu wengine na mengineyo. Napenda kusimulia kisa kilichomkuta rafiki yangu Mkristo. Bwana huyu aliponitembelea nyumbani aliniambia: Hivi ni kwa nini Uislamu unakuwa ni dini ya kunyanyapaa wasiokuwa Waislamu? Nikamwambia Uislamu katika mafundisho yake hauruhusu hayo, kwani watu wamegawanyika sehemu mbili, sehemu ya kwanza ni ndugu katika dini na sehemu ya pili ni ndugu katika ubinadamu. Kwa hiyo yule ambaye mliyekutana katika imani unapaswa kuishi naye kwa kuzingatia misingi ya sheria ya imani yenu inayolinda haki ya kila mmoja wenu. Na yule mliyekutana katika ubinadamu basi unapaswa kuishi naye kwa kuzingatia misingi ya sheria za ubinadamu. Basi yule rafiki yangu akaanza kunisimulia yaliyojiri baina yake na Mwislamu mwenye imani ya kufuga ndevu chafu na kukata suruali, kisa kilikuwa hivi: 203

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 203

8/14/2017 1:18:37 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

“Nilipokuwa nasoma katika shule ya upili nilikuwa ninakaa bweni moja na Mwislamu ambaye tulizoeana kama marafiki. Siku moja mwenzangu alipatwa na shida na hapakuwa na mtu wa karibu kwa wakati ule zaidi yangu. Basi mimi nikaona ni wajibu wangu kumsaidia ndugu yangu huyo. Lakini baada ya kutatua tatizo hilo, siku iliyofuata nilimsikia ndugu yangu anawasimulia wanafunzi kuwa, msaada niliompatia haukuwa kwa hiari yangu bali ni Mungu ndiye alinisukuma kwenda kumsaidia yeye Mwislamu, na kwamba Mwislamu akiwa na shida basi ni lazima Kafiri atampelekea msaada pasina kujitambua. Maneno hayo yaliniuma mno.” Mpenzi msomaji hebu tujiulize swali hili: Kama kweli Mawahabi wanafuata Uislamu wa Bwana Mtume 8 ambao ndio Uislamu wa amani, mbona huyu Mwislamu alimkosesha amani ya roho mwanafunzi mwenziwe? Je tunawezaje kumthibitishia kijana huyo aliyesononeshwa kuwa Uislamu ni dini ya amani? Au tunawezaje kuwathibitishia wale wote wanaoumizwa na ususuavu wa Kiwahabi kuwa Uislamu ni dini ya amani? Jibu ni jepesi mno, kwani historia inajirudia na yote yanayofanywa na Mawahabi ni marudio tu. Kwa hiyo njia zilezile alizozitumia Bwana Mtume 8 kuwathibitishia Makuraishi kwa vitendo kuwa Uislamu ni dini ya amani, ndizo tutakazozitumia kuuthibitishia ulimwengu kwa vitendo kuwa Uislamu ni dini ya amani, ili watu wasidanganywe tena na wakoloni kupitia vibaraka wao Mawahabi. Umoja wa Kiislamu: Imethibiti katika elimu za kiakili kwamba matokeo ni lazima yawe na chanzo, na amani pia imethibiti kwa watu wenye akili kuwa ni matokeo. Kwa hiyo kama ni matokeo basi ni lazima yawe na chanzo chake, na chanzo chake si kingine bali ni uadilifu, kwani uadilifu ndio uletao upendo na amani, na watu wakishakuwa na amani basi ni lazima wawe pamoja, na Mwenyezi Mungu anasema katika Qur’ani kwamba: 204

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 204

8/14/2017 1:18:37 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

“Na mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake wala msizozane, msije mkavunjika moyo na zikapotea nguvu zenu, na subirini; Hakika Mwenyezi Mungu yuko pamoja na wanaosubiri.117

Kwa hiyo kuna mambo mengi yanayotukusanya kama binadamu, bila kujali itikadi zetu za kidini, au rangi za ngozi zetu. Halafu kwa upande wa pili wa shilingi kuna mambo mengi yanayotukutanisha sisi kama Waislamu, na moja ya mambo hayo ni vile vikao ambavyo watu hukaa na kuadhimisha siku ya ukombozi wa mwanadamu, nayo ni siku ya kuzaliwa Bwana Mtume 8. Lakini wakoloni walikwishasoma kwamba watu wakikaa pamoja ni lazima watafanya jambo la maana na watakuwa na msemaji mmoja atakayeweza kuwafikisha kwenye malengo yao makuu. Na pia wale wenye akili ziendazo kasi, watawaamsha wale waliolala ili waweze kujitambua na hatimaye ukoloni hautafikia malengo yake ya kuhodhi maeneo na kunyonya rasilimali zetu. Mpenzi msomaji! Tunaamini utakuwa unakumbuka kuwa wazungu walipokuja huku kwetu walikuja na Biblia mikononi mwao, na wezee wetu walikuwa wanamiliki maeneo makubwa ya ardhi, lakini haukupita muda mrefu wazungu walimiliki mashamba makubwa na wazee wetu wakabakia na Biblia mikononi, wakiamini kwamba tajiri hataingia peponi mpaka ngamia apenye kwenye tundu la sindano. Maneno hayo akiyasikia mtu mwenye ufahamu mdogo ni lazima akabidhi kwa wakoloni mali zake zote. Na yote hayo yaliyojiri ni   Surat Anfal; 8:46

117

205

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 205

8/14/2017 1:18:37 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

kwa sababu ya watu kutokuwa na kiongozi wa kuwafikisha katika malengo yao makuu, na kiongozi hatuwezi kumpata bila ya kukaa pamoja. Na ndio maana wakoloni wanafanya kazi kila kukicha kwa kuwaamrisha vibaraka wao Mwahabi, wafanye kazi ya kuvisambaratisha vikao vya kuadhimisha siku ya kuzaliwa Bwana Mtume 8 kwa kutumia kigezo cha Bidaa na shirki. Maneno ambayo hawana ufahamu nayo, isipokuwa ubabaishaji tu, au upotoshaji wa makusudi ilimradi wapate ujira wao kutoka kwa wakuu wao wa Uingereza. Kwa nini maulidi ni tishio kwa wakoloni? Malengo makuu ya maulidi ni kuwaamsha watu ili waweze kujitambua, wawe ni jamii iliyokuwa hai. Sasa endapo hilo litafanikiwa basi litakuwa ni kikwazo sugu kwa wakoloni kufikia malengo yao kama tulivyosema. Maulidi ni jukwaa la uamsho, jukwaa la malezi ya kuilea jamii katika maadili yanayomridhisha Mwenyezi Mungu. Katika vikao vya maulidi huwa tunalenga mambo yafuatayo:I.

Kudumisha umoja na mshikamano:

Umoja huu unaopigwa vita na vikanzu vifupi ndio uliyotufikisha hapa tulipo leo hii. Lakini kuna mbinu mbalimbali na za kisasa zinazotumika ili kutugawa makundi makundi, na kuhakikisha hakuna kauli moja inayotuongoza. II. Kuwapatia watu somo la ukombozi: Vikao vya maulidi ni fursa adhimu na ya dhahabu, ya kuwajulisha watu madhara ya ukoloni. Na somo hilo limo ndani ya historia ya Bwana Mtume 8, kwani katika historia yake tunakuta kuwa yeye aliuondoa ukoloni kivitendo kwa kusitisha biashara ya utumwa na badala yake alitetea haki ya kila mwanadamu. Wakoloni waliliona hilo mapema kuwa watu wakisimuliwa historia ya Mtume 8 206

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 206

8/14/2017 1:18:37 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

wataamka kutoka katika usingizi wao mzito. Na hilo pia litakuwa ni pigo kali dhidi ya mikakati yao ya kutaka kuendeleza ukoloni duniani kwa maslahi ya matumbo yao, hususan katika nchi changa na za wanyonge. Kwa mantiki hiyo wakaandaa vibaraka watakaoandaa mazingira ya kuhakikisha somo hilo adhimu haliwafikii walengwa, na vibaraka hao ndio wale waliovaa vazi la suna kwa lengo la kuzifisidi. III. Kuwaandaa watoto kuwa ni taifa la kesho badala ya kuwa mafisadi wa kesho: Katika vikao vya maulidi tunapata fursa ya kukutana na wazazi na kuwaambia kuwa: Watoto ni taifa la kesho, endapo mtawaandalia mustakabali wa maisha yao kwa kuwapatia elimu bora watakuwa taifa bora. Lakini elimu bila maadili mema ni sawa na imani bila matendo. Na kwa mantiki hiyo mtakuwa mmewaandaa watoto wenu kuwa mafisadi wa tafa la kesho badala ya taifa bora la kesho kama mlivyotarajia. Kwa hiyo ili kupata taifa bora la kesho ni lazima kuwafundisha watoto au kuwanywesha mapenzi ya kumpenda Mtume wao Bwana Muhammad 8. Au kwa ibara nyingine na fasaha zaidi, tuwanyweshe wake wetu mapenzi ya kumpenda Bwana Mtume 8 ili wao wayatie vifuani mwao yachanganyike na maziwa halafu wawanyonyeshe watoto wao. Na mtoto aliyefinyangwa kwa mapenzi ya kumpenda Bwana Mtume 8 hawezi hata siku moja kuwa mtumwa wa mtu bali atakuwa ni mtu huru na atakayeweza kuwakomboa wengine, na ndio maana wakoloni wanavishambulia vikao vya maulidi kwa sababu vinafua wanaharakati wa kweli. Chakusikitisha ni pale tunapoona watu wakiacha shughuli zao, na familia zao ili kuzunguka maeneo yote ya mjini kukataza watu wasimsifu Bwana Mtume 8, kwa hoja ya kuwa ni Bidaa. Historia yake ya ukombozi pia hawataki ita207

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 207

8/14/2017 1:18:37 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

jwe. Bwana Mtume asipewe heshima kama kiongozi wa kimataifa aliyeyakusanya mataifa yote na kuyafanya kuwa ni kijiji kimoja chenye msemaji mmoja. Utovu wa nidhamu ulioje huo!! Kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa mkombozi wetu ni shirki lakini maadhimisho ya kifahari yanayofanywa na serikali ya Kiwahabi ya Saudia kwa ajili ya wafalme na viongozi wao ni halali! Hebu tuangalie Jarida la Al-Faisal, toleo la 102 limekusanya kwa mapana maadhimisho makubwa ambayo yalifanywa na utawala wa mabavu wa serikali ya Kiwahabi ya Saudia. Waliadhimisha siku ya kurejea kwa Amir Sultan kutoka katika safari ya anga ndani Rocket iitwayo Discovery. Katika maadhimisho hayo kuliimbwa nyimbo mbalimbali za kumsifu Amir Sultan pamoja na kuusifu ufalme wa Saud kwa sifa nyingi zilizovuka mipaka ya dini. Pia jarida hilo lilionesha gharama kubwa iliyotumika katika kuadhimisha upuuzi huo. Safari hiyo ya anga iliandaliwa na Marekani, utawala wa Saud ukasifiwa tena kwa millioni nyingi kutoka katika mfuko wa pesa za umma tena bila faida yoyote. Sasa hili liwe halali au kwa ibara nyingine liwe ni katika siku za Mwenyezi Mungu ambazo alitaka zikumbukwe, ila kuadhimisha siku ya kuzaliwa mkombozi wetu iwe ni haramu na shirki! Nyie Mawahabi nani kakulogeni. Kauli ya Mufti wa serikali ya kiwahabi ya Saudia: Gazeti la Mizani toleo la 128 Januari 9, 2015 limenukuu kutoka Gazeti la Arab News la Januari 3, 2015 kauli ya Mufti wa Kiwahabi Sheikh Abdul-Aziz bin Abdallah Al-Sheikh: “Vinginevyo ni Bidaa na dhambi kubwa zilizopenyezwa katika Uislamu karne ya tatu baada ya kufa Mtume Muhammad 8. Ni lazima kwa Mwislamu yeyote kufuata mafundisho ya Mtume kama yanavyodhihirika katika Sunnah zake.” Alisema Sheikh Abdul-Azizi alipokuwa akihutubia katika Msikiti wa Imam Turki Abdallah mjini Riyadh. Sheikh Abdul-Aziz alisema: “Wote wanaowaagiza watu kusherekea 208

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 208

8/14/2017 1:18:37 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

siku ya kuzaliwa kwa Mtume ni wakosefu na walioharibikiwa. Kwa vile hilo halijaagizwa popote katika Qur’ani tukufu wala hadithi za Mtume mwenyewe,” alidai mjukuu huyo wa Muhammad Abdul Wahhab mwasisi wa kikundi hicho cha kitakfir cha Kiwahabi. “Mapenzi ya kweli kwa Mtume huonyeshwa kwa kufuata matendo yake na Sunnah zake, ndiyo namna pekee ya kuonyesha mapenzi kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu 8.” Akinukuu Aya za Qur’ani tukufu, Sheikh Abdul-Azizi alisoma Aya ifuatayo: “Sema ikiwa mnampenda Mwenyezi Mungu basi nifuateni mimi. Mwenyezi Mungu atakupendeni na kuwasameheni dhambi zenu.” “Ni wajibu wa kila Mwislamu, kumuamini na kumheshimu yeye kama mjumbe wa Mwenyezi Mungu. Ni jukumu lao pia kumlinda na kumhami dhidi ya wale wanaotafsiri vibaya na kupotosha mafundisho yake, makafiri wanaomkana pamoja na wale wanaomdhihaki na kumtumsi. Hii ndiyo njia sahihi ya kumuenzi Mtume Muhammad 8 wala siyo kuingiza ushirikina katika dini ya Mwenyezi Mungu kwa kufanya sherehe za kuadhimisha kuzaliwa kwake.” Wakati Mufti huyo wa serikali ya kiwahabi akitoa ufafanuzi huo, Gazeti la Mizani toleo la 128 Januari 9, 2015 linanukuu katika ukurasa wake wa 4 kwamba “Saud Al Faisal aliyekuwa waziri wa kigeni wa Saudia aliongoza Maulidi (Birthday) ya kutimiza miaka hamsini na moja ya kuzaliwa Condoleezza Rice aliyekuwa Waziri wa Nje wa Marekani. Hata hivyo Mufti wa Saudia anakufurisha Maulidi kwa ajili ya Mtume 8 huku serikali ya Saudia ikimfanyia Condoleezza Rice, ambaye anaonekana na thamani zaidi humo. Waziri wa mashauri ya kigeni wa Saudi Arabia mwana Mfalme Saud Al Faisal aliongoza Maulid hiyo (Birthday) ya kutimiza miaka hamsini na moja ya kuzaliwa Condoleezza Rice ambaye alikuwa waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani. Katika kuima209

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 209

8/14/2017 1:18:37 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

risha urafiki baina ya Marekani na Saudia, waziri huyo wa mambo ya nje wa Saudia alimkirimu waziri huyo wa kigeni wa Marekani kwa keki ya chokoleti katika kusherekea siku ya Maulid yake huku zikipepea bendera za mataifa hayo mawili.� Sasa iko wapi kauli ya Mufti wa serikali ya Kiwahabi? Mbona serikali yake haitii kauli zake ambazo alizitilia msisitizo kwa Aya za Qur’ani tukufu? Hapo utapata jibu kuwa utawala wa Saudia umejipa nafasi ya kuwa juu ya sheria za Mwenyezi Mungu nchini humo. Na pili hukumu zinazotolewa na Mufti wao ni kwa ajili ya kutokomeza matukufu ya dini yetu, na kuendeleza matukufu na tamaduni za wakoloni kupitia mawakala wao waliosimikwa madarakani katika nchi ya Bwana Mtume kwa mabavu, tangu mwaka 1930. Kusimama kiyamu katika maulidi ya Bwana Mtume 8: Katika shereha za kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa Bwana Mtume 8 kuna desturi ya kusimama kiamu pale inapofikia mahali pakutaja kuzaliwa kwake. Na hii sio Bidaa bali ni ishara ya heshima na taadhima kwa Kiongozi wa Kimataifa Bwana Mtume 8. Kama ambavyo leo hii tunashuhudia namna viongozi wa kisiasa wanavyopewa heshima kubwa. Watu wote wanatambua kuwa siku za kitaifa kama vile sherehe za siku ya uhuru, siku ya mashujaa na nyinginezo, wafanyakazi hupewa mapumziko ikiwa ni sehemu ya kuzitukuza siku hizo. Na hakuna ubaya kufanya hivyo kwa sababu watu wanawakumbuka viongozi wao na historia ya nchi yao. Sasa iweje kuadhimisha siku ya kuzaliwa Bwana Mtume 8 iwe kero na kejeli? Watu wanawanyanyukia viongozi wa kisiasa, lakini watambue kuwa kumnyanyukia Mtume wa Mwenyezi Mungu na mpigania amani na haki za wanadamu ni bora zaidi na ni jambo la heshima kubwa. 210

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 210

8/14/2017 1:18:37 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Waislamu ili kuurudisha Uislamu wa Bwana Mtume ulioharibiwa na Mawahabi, ni lazima kudumisha amani, na umoja na tuushike utandawazi wa Mwenyezi Mungu, kwa maana ya dunia kuwa kama kijiji. Kisha kijiji hicho tukitafutie msemaji mmoja mwadilifu atakayeweza kusimamia katiba ya haki na uadilifu, na kutufikisha kwenye malengo yetu. Tunamwomba Mwenyezi Mungu atujalie kuwa katika wale wanaosikiliza neno na kufuata lililokuwa bora zaidi. Je! inaafaa kuikumbuka siku ya kifo cha Bwana Mtume Muhammad 8? Siku ya kifo cha Bwana Mtume 8 ni katika siku ambazo Qur’ani inataka zikumbukwe, kama inavyoelezwa katika Surat Ibrahim: “Kwa hakika tulimtuma Musa pamoja na miujiza yetu, kuwa watoe watu wako gizani kuwapeleka kwenye nuru. Na uwakumbushe siku za Mwenyezi Mungu.” Wapenzi Waislamu, ulimwengu wa Kiislamu hugubikwa na wingu la majonzi huzuni na simanzi, kila ifikapo tarehe 28 mfungo tano, kwani Mkombozi na mpigania uhuru wa kila mwanadamu, Mtume Muhammad 8 alifariki dunia ndani ya tarehe hiyo. Kwa hiyo ni jukumu la kila mwenye chembe ya ubinadamu ndani ya roho yake, kuimbuka siku hiyo ya huzuni, kwani ni moja ya siku za Mwenyezi Mungu. Huzuni na furaha kwa watu wa kale: Siku zote ni za Mwenyezi Mungu, na hakuna hata siku moja ambayo sio ya Mwenyezi Mungu, lakini lugha hiyo inaweza kumwacha msomaji na maswali mengi. Ila ukiitafakari utakuta kuwa hata sisi katika matumizi yetu ya kila siku huwa tunaitumia lugha kama hiyo, pale tunaposema kuwa Hussein ni mwanaume, kwa hakika kauli hiyo haimaanishi kuwa Musa ni mwanamke. Sasa Mwenyezi Mungu aliposema: “Na uwakumbushe siku za Mwenyezi Mungu” makusudio yake ilikuwa ni zile siku ambazo zina matukio ya kihistoria ya 211

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 211

8/14/2017 1:18:37 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

kufarahisha na kuhuzunisha pia ambayo hayatakiwi kusahauliwa, kama walivyofurahi watu wa Musa siku ya ukombozi wao toka kwenye nyumba ya utumwa. Na kwa upande mwingine wa sarafu, ni kama walivyohuzunika katika nchi ya Misri kutokana na mateso waliyokuwa wakiyapata chini ya utawala dhalimu wa Firauni, mateso hayo pia yanafaa kukumbukwa. Utume wa Musa ulikuwa na malengo ya kuwatoa wana wa Israel gizani na kuwapeleka kwenye nuru, na kuwakomboa kutoka kwenye nyumba ya utumwa, kwani wana hao wa Israel walikuwa wakiishi chini ya utawala wa kiongozi asiyejua halali wala haramu. Kiongozi aliyevuka mipaka na kudai uungu. Kiongozi huyo alikuwa akichinja kila mtoto wa kiume na kumwacha hai kila mtoto wa kike. Lakini tukio la kwanza la kustaajabisha ni pale alipozaliwa Musa D. Kiongozi huyo alishindwa kumchinja na badala yake alimlea kama mtoto wake, na Mwenyezi Mungu akaiita siku hiyo kuwa ni siku yake kutokana na maajabu aliyoyafanya ndani ya siku hiyo. Na pia akawataka wana wa Israeli wakumbushwe siku hiyo ili wasiisahau. Tukio la kupasua njia katika bahari, siku hiyo pia Mwenyezi Mungu anawataka wana wa Israeli waikumbuke, kutokana na miujiza ya Kiungu iliyofanyika ndani ya siku hiyo, ambayo ni kuwakomboa wana wa Israeli na kumwangamiza kiongozi yule aliyevuka mipaka, yeye na kundi lake. Na tunapousoma uvukaji mipaka wa kiongozi huyo wa Kimisri (Firauni), tunaukuta kuna tofauti kubwa kabisa kati ya uvukaji mipaka unaofanywa na makundi ya Kiwahabi Daesh, Boko Haramu, Al-shababi na kadhalika, kwani kiongozi huyo wa Kimisri alikuwa anachinja watoto wakiume tu, lakini Makundi ya Kiwahabi (Mawahabi) yanachinja watu wazee, vijana, haijalishi ni wanawake au wanaume, na wanaua hadi watoto wachanga, wawe wa kike au wa kiume. Kwa mantiki hiyo tunasema kuwa Firauni alikuwa mbaya 212

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 212

8/14/2017 1:18:37 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

lakini Mawahabi ni wabaya zaidi. Kwa hiyo wana wa Israeli hawana budi kumkumbuka Nabii Musa kutokana na kazi hiyo ya kuwakomboa kutoka mikononi mwa Firauni. Je! Umma wa Muhammad 8 hauna siku za huzuni? Tukiutafakari utume wa Muhammad 8 kupitia Aya iliyotangulia, tutaukuta na wenyewe pia una malengo sawa na yale ya utume wa Musa D, ila tofauti ni kwamba utume wa Musa ulikuwa ni kwa Waisrael tu, wakati utume wa Muhammad ni kwa ulimwengu mzima, na ni utume uliokuja kuukomboa ulimwengu mzima. Utume huo ndiyo una haki zaidi ya kuwa na matukio ya kukumbukwa. Wakati Muhammad 8 alipokabidhiwa utume, hali haikuwa salama katika jamii za Kiarabu, watu walikuwa wanaua watoto wa kike kwa madai ya kuwa watoto wa kike ni aibu na ni fedheha kwa familia. Lakini kwa baraka ya utume huo wa kimataifa tabia hiyo ya waraabu ikawa imekomea hapo. Hiyo ilikuwa ni neema kubwa ya Mwenyezi Mungu ndani ya siku hiyo ambayo inapaswa kukumbukwa. Watu walikuwa wakiishi nje kabisa ya wigo wa utu na maadili mema, lakini kwa baraka ya utume wa kimataifa wa Mtume Muhammad 8 maisha ya kijamii yalisimama juu ya misingi ya uadilifu, hali ambayo ilipelekea upendo, na mshikamano, na usawa katika utu, na biashara ya utumwa ikakosa mahala pakuweka unyayo. Masiku yote hayo ni masiku ya Mwenyezi Mungu ambayo tunatakiwa kuyakumbuka, na hatuwezi kukumbuka ushindi mkubwa kama huo bila ya kumkumbuka aliyeuleta, na siamini kama yuko mtu mwenye akili huru anayekubali kukumbuka matukio hayo bila ya kumkumbuka aliyechangia katika upatikanaji wake. Mpenzi msomaji leo hii kama utawaambia ndugu zetu Wahindi waadhimishe uhuru wa taifa lao lakini wasimtaje kabisa Mzee Mahatima Ghandi, bila shaka watakupeleka hospitali kwanza ili ukapimwe akili. 213

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 213

8/14/2017 1:18:37 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Na sisi Waislamu ukitwambia tukumbumbuke ukombozi wa Mtume Muhammad lakini yeye mwenyewe tusimkumbuke, hapo ni lazima tuushakie Uislamu wako, kwani ukombozi wa Mtume Muhammad umempatia nafasi ya kupenya na kuingia ndani ya moyo wa kila muumini. Na ili mtu aingie kwenye orodha ya waumini ni lazima kwanza ampende Mtume wetu mapenzi ya kweli, na mapenzi ya kweli ndiyo yatakayomfanya mtu kuwa ni mwenye kufuata nyayo za Mtume wetu 8. Mwenyezi Mungu anasema:

“Sema ikiwa baba zenu na wana wenu na ndugu zenu na wake zenu na jamaa zenu, na mali mlizozichuma, na biashara mnazohofia kuharibika, na majumba mnayoyapenda, ni vipenzi zaidi kwenu kuliko Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na jihadi katika njia Yake, basi ngojeni mpaka Mwenyezi Mungu alete amri Yake…”118

Kwa hiyo lengo letu katika kuadhimisha siku ya kifo cha Bwana Mtume, ni kuthibitisha upendo wetu kwa Mtume wetu na kwamba hakuna mwenye nafasi ndani ya nyoyo zetu zaidi ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na katika hadithi Bwana Mtume 8 anasema: “Naapa kwa anayemiliki pumzi yangu, hataamini mmoja wenu mpaka anipende zaidi katika watu kuliko baba yake na mtoto wake.” Kwa hiyo kwa ibara nyingine maadhimisho haya ni njia mojawapo ya kudhirisha upendo wetu na heshima zetu kwa Bwana Mtume 8.   Tauba; 9:24

118

214

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 214

8/14/2017 1:18:38 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Mtume Muhammad 8 aifikisha dini kwenye kilele cha ­ukamilifu: Uislamu ndiyo dini ya mwisho na hakuna dini baada yake, na hakuna utume baada ya Mtume Muhammad 8. Na kwa kuwa Uislamu ndiyo dini ya mwisho, basi ni lazima iwe kamilifu kiasi ambacho hatutahitajia dini nyingine badala yake. Licha ya ukombozi mkubwa uliyofanywa na Bwana Mtume 8 bado kuna kazi nyingine kubwa zaidi aliyoifanya, nayo ni kuifikisha dini kwenye kilele cha ukamilifu, na si kilele cha utimilifu. Je, ni kazi ndogo hiyo aliyoifanya Mtume Muhammad? Je, kwa kazi kama hiyo hastahiki kusifiwa na kutukuzwa milele? Je, akili kamilifu inakubali kuushangilia ushindi na ukombozi wa Muhammad 8 bila ya kumtaja Yeye mwenyewe? Muhammad 8 ni hazina yenye thamani, tutakumbuka mazazi yake na kifo chake, kwa gharama yoyote ile, ambayo ni sahihi hata kama makafiri watakerwa na kuomboleza kifo chake ni suala la kimaumbile. Kwa ibara nzuri, mtu kumlilia mtu mwingine si jambo la hiari kwa mwanadamu. Sasa nashangaa kusikia Mawahabi/Maanswar sunnah wanakataza watu kumlilia Mtume, achilia mbali mtu wa kawaida. Hawataki kabisa kutuona tukilia kwa kuondekewa na kipenzi chetu, wakati Nabii Yakub D alimlilia mtoto wake Nabii Yusuf, hadi akawa hawezi kuona na kipindi hicho Yusuf alikuwa hai, lakini kitendo cha Yusuf kuwa mbali kilimfanya Nabii Yakub alie kiasi hicho. Inaonesha kuwa kama Nabii Yakub angeishi katika zama hizi, basi Mawahabi kwa ukosefu wao wa adabu wangethubutu kumwambia kauli hiyo kuwa kumlilia mtoto wake ni Bidaa na ni haraam! Ndugu zangu, amkeni mna macho lakini hamuoni. Bendera ya upotovu wa Kiwahabi inapepea mbele yenu kwa jina la kuinusuru Sunnah. Watu wanadanganyika kwa majina mazuri ambayo Mawahabi wanaji215

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 215

8/14/2017 1:18:38 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

batiza kila kukicha; utawasikia wakijiita Salafi, au Ahlusuna wal jamaa, lakini ukweli ni kwamba hakuna Sunnah inayonusuriwa na hao wakata suruali, na kufuga ndevu chafu, pamoja na kunyoa vipara. Kazi yao kubwa ni kumvunjia heshima Bwana Mtume 8. Utawasikia wahubiri wao wakisema: “Muhammad ni mtu kama wewe hata litakalofanyika baada ya dakika tano mbele halijui.” Subhaanallah! Kweli watu hawa hawana adabu hata za kuazima na wala hawasomi kabisa, kwani Bwana Mtume 8 amewahi kutabiri jambo litakalotokea baada ya miaka kadhaa mbele, achilia mbali la dakika tano. Mwenyezi Mungu anasema: “Warumi wameshindwa, katika nchi iliyo karibu. Nao baada ya kushindwa kwao watashinda...”119 Je, utabiri huo ulitimia baada ya muda gani, ikiwa ni kweli Mtume hafahamu hata la dakika tano mbele? Hiyo ni sehemu tu ya utovu wao wa nidhamu kwa Bwana Mtume 8. Na si kwa Mtume tu bali hata kwa Mwenyezi Mungu, kwani Mawahabi hao hao ndio wanaomfananisha Mwenyezi Mungu na mwanadamu, kwa kudai kuwa Mungu ana mikono, miguu, meno na macho, lakini macho yake ni makubwa sana si kama yetu. Kazi yao nyingine ni kututenganisha Waislamu kwa kupandikiza chuki kati yetu. Na sasa wameanza kutembelea misikiti mbali mbali wakijifanya kuwa wanahubiri umoja, halafu wakati huo huo wanawabeza wasiokuwa na itikadi za ususuavu kama za kwao, umoja gani huo tunaoletewa! Umoja wanaoukusudia ni watu wote kuwa kama wao. Ndugu zangu zindukeni Mawahabi ni zaidi ya Saratani, na wanakula na kupuliza mithili ya panya buku. Lakini jambo lingine muhimu zaidi linalowafanya Mawahabi kuyapiga vita maadhimisho ya siku ya kifo cha Bwana Mtume 8 ni kwa sababu ya kuwa Waislamu wakikumbuka uongozi kamilifu wa Mtume 8 unaotetea haki ya kila kiumbe ni lazima watajiuliza swali lifuatalo, je   Surat Rum; 30:1 - 3

119

216

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 216

8/14/2017 1:18:38 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

ikiwa Bwana Mtume 8 alikuja kama msimamizi wa sheria na kuhakikisha maisha yanasimama juu ya misingi ya uadilifu, je ni kitu gani alichotuachia kama dira na mwongozo wetu baada yake? Tunamwomba Mwenyezi Mungu atujaalie sote kuwa katika wale wanaosikiliza neno na kufuata lililokuwa bora zaidi. Namna hii ndivyo Qur’ani ilivyoadhimisha siku ya kuzaliwa kwa Bwana Masihi Yesu Kristo: Ikiwa Chrismass120 itatafsiriwa kwa maana ya kuzaliwa kwa Bwana Yesu, basi watu hawana budi kuikumbuka, kwani siku hiyo itakuwa ni moja ya siku za Mwenyezi Mungu, na Mitume wote walikuja kwa lengo moja tu nalo ni kuwaokoa wanadamu kwa kuwaonesha njia iendayo uzimani, Qur’ani Tukufu inasema:

“Hatutofautishi baina ya yeyote katika Mitume Wake.” 121

Siku ya kuzaliwa kwa Bwana Yesu ni katika siku ambazo Qur’ani inataka zikumbukwe, kama inavyoelezwa katika Surat Ibrahim:

“Hakika tulimtuma Musa pamoja na miujiza Yetu, kuwa itoe kaumu yako gizani kwenda kwenye nuru. Na uwakumbushe Siku za ­Mwenyezi Mungu…..”122   Hapa mwandishi hasemi kuwa siku ya tarehe 25 Desemba ndio tarehe hasa yenyewe aliyozaliwa Masihi , anachokusudia hapa ni ile sherehe yenyewe ya kuzaliwa bila kujali tofauti za tarehe yenyewe – Mhariri. 121   Surat Baqarah; 2:285. 122   Surat Ibrahim; 14:5 120

217

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 217

8/14/2017 1:18:38 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Mwanzo wa historia ya kuzaliwa kwa Bwana Yesu: Historia ya kuzaliwa kwa Bwana Yesu katika Qur’ani, inaanzia kwa Bibi Yake, pale alipopata shauku ya kuwa na mtoto wa kiume, na akaweka nadhiri ya kumtoa mtoto huyo wakfu, katika nyumba ya ibada. Qur’ani tukufu inasimulia kisa hicho kama ifuatavyo:

“Aliposema mke wa Imran: Mola Wangu! Nimeweka nadhiri kwako aliyemo tumboni mwangu kuwa wakfu, basi nikubalie kwa hakika wewe ndiwe usikiaye uliye mjuzi.”123

Katika aya hiyo, mke wa Imran ambaye ni bibi mzaa mama wa Bwana Yesu aliweka nadhiri ya kuwa: Nikizaa mtoto wa kiume nitamtoa katika njia ya Mwenyezi Mungu, ili awe mtumishi katika nyumba ya ibada, lakini mambo hayakuwa kama alivyotarajia kwani mtoto aliyezaliwa alikuwa ni wa jinsia tofauti na ile aliyokuwa akiitarajia, soma Aya ifuatayo:

“Alipomzaa alisema: Mola Wangu! Nimemzaa mwanamke - na Mwenyezi Mungu anajua sana aliyemzaa - Na mwanamume si kama mwanamke, na mimemwita Maryam. Na mimi namkinga Kwako, yeye na kizazi chake (uwalinde) na shetani aliyefukuzwa.” (3:36).   Surat al Imran; 3:35

123

218

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 218

8/14/2017 1:18:38 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Mama huyo pale aliposema: Na mwanamume si kama mwanamke, kauli hiyo haioneshi kutoridhika na jinsia ya kike, wala haimaanishi kuwa mtoto wa kiume ni bora kuliko wa kike, bali lengo lake lilikuwa ni kupata mtoto wa kiume atakayekuwa mtumishi katika nyumba ya ibada, kwani hali ya maumbile ya mtoto wa kiume inamruhusu kufanya kazi wakati wowote, lakini hali ya maumbile ya mtoto wa kike, haimruhusu kuingia katika nyumba ya ibada kila siku, kutokana na dharura za kimaumbile kwa mwanamke. Pia hata kazi anazozifanya mtoto wa kiume ni tofauti na zile zifanywazo na mtoto wa kike. Ni kwa hoja hiyo tu, mama huyo (mke wa Imran) alistahabu kupata mtoto wa kiume. Mke wa Imran hakupata mtoto wa kiume na badala yake alimzaa Bibi Maryam, ambaye ndiye Mama wa Bwana Yesu. Maryam mtakatifu: Bibi Maryam alikulia katika mazingira mema, chini ya himaya ya Nabii Zakaria na uangalizi wa Mwenyezi Mungu. Bibi Maryamu alikuwa na akili kamilifu iliyomuwezesha kujua kwamba hatima ya madhambi ni kuingia katika Jehanam, na kwa misingi hiyo aliweza kujitenga mbali, na kila aina ya dhambi, hadi akakaribia daraja ya unabii. Qur’ani Tukufu inasema:

“Na Malaika waliposema: Ewe Maryam! Hakika Mwenyezi Mungu amekuteua na akakutakasa na akakuteua juu ya wanawake wa ulimwenguni.”124   Surat al Imran; 3:42

124

219

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 219

8/14/2017 1:18:38 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Kuna baadhi ya Waislamu wanaoamini kwamba wasiofanya madhambi ni Mitume peke yao, kwani wao wamehifadhika kutokana na kila aina ya uchafu, na ni vigumu kwa mtu wa kawaida kufikia daraja hiyo. Mpenzi msomaji! Neno kuhifadhika linafahamika katika Lugha ya Kiarabu kama Umaasumu, na kila mwanadamu anaweza kujihifadhi na asifanye dhambi milele yote. Na ili kukuondolea utata mpenzi msomaji, kwanza tukuelezee maana ya Umaasumu. Maana ya umaasumu: Umaasumu ni ngazi katika ngazi za elimu, au ni tabaka katika matabaka ya elimu. Kama mwanadamu atakuwa na yakini katika mambo yote yawezayo kumletea madhara basi ni lazima atajiepusha nayo, kwa hiyo tunasema kuwa kila mwanadamu hujihifadhi baada ya kujua athari mbaya zitakazotokea baada ya kufanya tendo fulani baya. Au kwa tafsiri nyepesi ni kwamba Umaasumu ni elimu ya yakini inayokuzuia kuingia kwenye mazingira hatarishi. Kwa mfano tukiweka nyaya za umeme ambazo hazina gamba la juu, kisha nyaya zile ziwe na moto, hivi yuko mtu mwenye akili timamu anayeweza kuzishika kwa mkono wake? Jibu ni hapana, kwa nini? Kwa sababu anajua kwa yakini kuwa akizishika atahatarisha maisha yake, kwa hiyo mwanadamu huyu atakuwa ni mwenye kujilinda na hataweza kuisogelea hatari hiyo, na hawezi kufanya kosa hapo. Na huo ni mfano mdogo tu. Sasa mwanadamu atakaposimama mbele ya maasi kisha akajua kwa yakini kuwa hatima ya kufanya maasi ni moto mkali, bila shaka atajiepusha na maasi yale, na huyo atakuwa amehifadhika na maasi baada ya kuelewa hatima yake mbaya. Kwa mantiki hiyo, Bibi Maryam alijiepusha na maasi kwa kuwa aliona kwa jicho la yakini kuwa nyuma ya maasi kuna 220

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 220

8/14/2017 1:18:38 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

maangamio na ndiyo maana hakuweza kuyasogelea kabisa maasi, maisha yake yote. Mke wa (mfalme) Aziz wa Misri anasema nilimtamani (Yusuf) naye akajizuia (fasta’aswama), kwa nini? Kwa kuwa ana elimu ya kujua kwamba hatima ya maasi ni kuangamia, Qur’ani imesimulia kwa mapana yale yaliyojiri kati ya Yusuf na mama yake mlezi. Baadhi ya Waislam, hususan wale wanaovaa vipande vya suruali na kufuga ndevu chafu wanapotusikia tukisema kuwa Bibi Marim hakuwa na madhambi, wao hushangaa sana na kusema kuwa sisi tunamfanya Bibi Maryam sawa na Mitume, sasa labda tuwaulize hili: Je, umaasumu unaambatana na utume tu na hauingii sehemu nyingine? Tumekwishaeleza kuwa Umaasumu125 chanzo chake ni elimu ya yakini juu ya hatima mbaya ya mambo, na kila atakayefahamu kwa yakini hatima mbaya ya matendo machafu, ni lazima ajiepushe nayo, na wala hatujasema kuwa chanzo cha Umaasumu ni utume laa, bali chanzo chake ni elimu ya yakini. Kwa hiyo Bibi Maryam, bali Manabii wote wa Mwenyezi Mungu walijihifadhi na kutofanya madhambi kutokana na elimu hiyo ya yakini, na wewe na mimi tukiwa na elimu hiyo basi tutakuwa tumetakasika na kila aina ya uovu. Kuzaliwa kwa Bwana Yesu: Qur’ani Tukufu inasimulia kisa cha kuzaliwa kwa Bwana Yesu, kwa mtiririko wake wa kipekee tofauti na ule uliyopo katika kitabu cha Mathayo Mtakatifu. Qur’ani ina kitabu kamili kiitwacho kitabu cha Maryam, Waislamu wanakiita Surat Maryam. Kitabu hicho ni cha kumi na tisa katika vitabu vya Qur’ani. Mwenyezi Mungu anasema:   Isma tunayokusudia hapa ni ile hali inayomzuia mtu na kila aina ya uchafu wa kimetafizikia “mtunzi”

125

221

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 221

8/14/2017 1:18:38 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Na mtaje Maryam katika Kitabu, alipojitenga na watu wake mahali upande wa mashariki. Na akaweka pazia kujikinga nao. Tukampelekea roho Wetu, akajifananisha kwake sawa na mtu.126 Akasema: Hakika mimi najilinda kwa Mwingi wa rehema aniepushe nawe, ukiwa ni mwenye takua.127Akasema: Mimi ni mjumbe wa Mola Wako ili nikupe mwana mtakatifu. Akasema: Nitakuwaje na mwana hali hajanigusa mtu yeyote wala mimi si malaya. Akasema: Ndivyo hivyo, Mola Wako amesema, haya Kwangu ni mepesi! Na ili tumfanye kuwa ni ishara kwa watu na rehema itokayo Kwetu. Na hilo ni jambo lililokwishapitishwa. Basi akachukua mimba yake akaondoka nayo mahali mbali.”

Mjadala kuhusu muda wa ujauzito: Kuna mjadala mkubwa kati ya wanachuoni kuhusu muda wa ujauzito, baadhi wanasema ujauzito huo ulidumu kwa miezi tisa, na wengine wanasema ni miezi sita, na wengine wanasema ni siku nzima,   Surat Maryam; 19:16 - 17   Surat Maryam; 19:18 - 22

126 127

222

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 222

8/14/2017 1:18:38 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

na kuna wanaosema ni saa chache tu na wala si siku nzima. Na rai hii ya mwisho haiko mbali na usahihi, kwani katika Aya zilizotangulia tumesoma kuwa: “Na mtaje Maryam katika kitabu, alipojitenga na watu wake mahali upande wa mashariki.”128 Ibara hiyo na ile isemayo: “Basi akachukua mimba yake akaondoka nayo sehemu (iliyo) mbali.”129 Ni ushahidi tosha kuwa Bibi Maryam alitoka kwa muda mfupi tena bila kumtaarifu yeyote, na kurejea nyumbani haraka kabla ya watu kuanza kumtafuta. Sasa kama angekaa huko miezi tisa au miezi sita basi familia ingeanza kumtafuta kila sehemu, lakini historia haioneshi kuwa Bibi Maryam aliwahi kutafutwa na familia yake. Wakati mgumu: Katika Aya ya 22 tumesoma kuwa, Bibi Maryam alichukua ujauzito na kuondoka nao mbali. Lakini Aya ya 23 inaainisha kuwa safari iliishia kwenye shina la mtende pale alipopatwa na udhaifu wa kibinadamu, na wala si udhaifu wa kike kwa maana Mwenyezi Mungu anasema kuwa mwanadamu ameumbwa dhaifu, na wala hakusema kuwa mwanamke ameumbwa dhaifu. Mwenyezi Mungu anasema:

Surat Maryam; 19:16   Surat Maryam; 19:22

128 129

223

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 223

8/14/2017 1:18:38 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

“Uchungu ukampeleka kwenye shina la mtende; akasema: Laiti ningelikufa kabla ya haya nikawa mwenye kusahaulika kabisa. Pakanadiwa kutoka chini yake kwamba usihuzunike; hakika Mola Wako amejaalia chini yako kijito cha maji.130 Na litikise kwako shina la mtende utakuangushia tende freshi zilizo mbivu. Basi Kula na kunywa na uburudishe jicho. Na pindi ukimuona mtu yeyote basi sema hakika mimi nimeweka nadhiri kwa Mwingi wa rehema ya kufunga. Kwa hiyo leo sitasema na mtu.”

Basi baada ya kuzaliwa mtoto, Bibi Maryam alirejea nyumbani akiwa kabeba mtoto, hali ambayo ilimshangaza kila mtu, na kuzua mgogoro mkubwa kati yake na watu wake. Mjadala baina ya Bibi Maryam na watu wake: Kutokana na utakatifu aliyokuwa nao Bibi Maryam basi isingeweza kuingia akilini kwa yeyote kuwa Bibi Maryam anaweza kuwa na mtoto kwa njia isiyokuwa ya kisheria, kwa maana alikuwa hajaolewa. Mwenyezi Mungu anasema:

“Akaenda naye kwa jamaa zake amembeba. Wakasema: Ewe Maryam! Hakika umeleta kitu cha ajabu.”131

Kuzaliwa mtoto asiye na baba mwenye kutambulika kisheria hilo lilikuwa ni jambo ambalo halijawahi kutokea katika historia ya familia ya Mzee Imran. Basi kwa kuwa Bibi Maryam alikuwa kaishapata amri ya kutosema na yeyote, basi ilimbidi aashirie kwa mkono, kuwa wamuulize mtoto mwenyewe, nao wakaona kama vile Bibi Maryam anawadhihaki, wakasema:   Surat Maryam; 19:23 - 26   Surat Maryam; 19:27

130 131

224

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 224

8/14/2017 1:18:38 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

“Ewe dada wa Harun! Baba yako hakuwa mtu muovu wala mama yako hakuwa kahaba. Ndipo akaashiria kwake. Wakasema: Tutamsemezaje aliye bado mdogo susuni?”

Basi pale pale Bwana Yesu alianza kuongea na kutajitambulisha kwa jina la Mja wa Mwenyezi Mungu, Qur’ani Tukufu inasema:

“Akasema: Hakika mimi ni mja wa Mwenyezi Mungu amenipa kitabu na amenifanya ni Nabii. Na amenijaalia ni mwenye kubarikiwa popote pale niwapo. Na ameniusia Swala na Zaka muda wa kuwa niko hai. Na kumtendea mema mama yangu. Wala hakunifanya niwe jeuri muovu. Na amani iwe juu yangu, siku niliyozaliwa na siku nitakayokufa na siku nitakayofufuliwa.”132

Kisha Qur’ani ikamalizia hadithi kwa kusema:

Surat Maryam; 19:30-33

132

225

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 225

8/14/2017 1:18:39 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

“Huyo ndiye Isa mwana wa Maryam, kauli ya haki ambayo wanalifanyia shaka. Haiwi kwa Mwenyezi Mungu kuwa na mwana, Yeye ametakasika! Anapolipitisha jambo basi huliambia tu: Kuwa! Likawa. Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mola Wangu na Mola Wenu basi mwabuduni. Hii ndio njia iliyonyooka. Lakini makundi yakahitilafiana baina yao. Basi ole wao waliokufuru kuhudhuria siku iliyo kuu.”133

Ndugu wapendwa! Manabii wote walikuwa na lengo moja tu, nalo ni kufundisha maadili mema katika jamii, maadili yatakayo wabainishia watu njia itakayowafikisha kwenye kilele cha ukamilifu. Sasa kama wewe unamfuata Mtume Muhammad 8 basi tambua kuwa maadili ya Bwana Mtume 8 ndiyo yale yale ya Bwana Yesu. Sasa unapovunja makanisa ya Wakristo bila sababu hapo unakuwa unakwenda kinyume na mafundisho kwani mafundisho ya Uislamu wa Mtume Muhammad, ni Mwislamu na Mkristo kukaa meza moja, kwa amani, kama ndugu wa tumbo moja, huo ndiyo Uislamu wa Mtume Muhammad 8. Na hata kipindi Waislamu walipokuwa katika wakati mgumu, wakipata mateso mbali mbali toka kwa wakuu wa tawala zilizokuwa madarakani, Bwana Mtume 8 aliwaambia wafuasi wake wakimbilie Ethiopia. Huko Ethiopia walipokolewa na kupewa hifa  Surat Maryam; 19: 34-37

133

226

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 226

8/14/2017 1:18:39 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

dhi, lakini Mfalme wa Ethiopia aliyewapa hifadhi Waislamu, yeye mwenyewe hakuwa Mwislamu bali alikuwa ni Mkristo, lakini aliwapa Waislamu, chakula, mavazi na malazi. Sasa wewe Mwislamu mfuasi wa makundi ya ugaidi, unapokataa kula chakula cha jirani yako siku ya Chrismass kwa madai ya kuwa wewe ni Mwislamu safi, hivi wewe unaujua sana Uislamu zaidi ya Mtume Muhammad 8? Mbona Yeye aliishi na watu wa dini tofauti kwa kuheshimu misingi ya ubinadamu? Bali hata pale Mtume 8 alipokuwa na Dola ya Kiislamu hakuna aliyefanyiwa uhaini na ugaidi kama huu tunaoushuhudia leo hii. Ndugu zangu Wakristo, kiongozi aliyestahiki kushika madaraka ya dola ya Uislamu baada ya Mtume Muhammad 8 ni Imamu Ali G, Imamu huyu anasema: “Watu wako aina mbili, ima ni ndugu yako katika dini, au ni mwenzio katika ubinadamu (kwa maneno mengine ni: Ndugu yako katika Adamu).� Kauli hiyo inatufundisha namna ya kuishi na watu, yaani yule ambaye mmechangia imani basi ishi naye kwa wema kama ilivyoamrishwa katika imani yenu, na yule ambaye mmetofautiana kiimani, basi ishi naye kwa wema kwa kuzingatia misingi ya haki za kibinadamu na kama wana wa Adamu D. Kwa hiyo Waislamu na Wakristo wanaunganishwa na kitu kiitwacho ubinadamu. Na katika ubinadamu ni wewe kushirikiana na binadamu wenzio katika shida na raha. Wanapokuwa na furaha basi nenda ukawapongeze, tafuta japo zawadi ndogo uwapelekee na wao wakikuletea chakula ambacho kinaruhusiwa kwa mujibu wa itikadi yako basi pokea. Na wanapokuwa na simanzi nenda ukawafariji, huo ndiyo ubinadamu. Aliyekuwa Kiongozi wa wa kiroho wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Imamu Khomein Mungu amrehemu. Wakati alipokuwa Ufaransa, siku ya Chrismass aliuliza kuhusu mila na deturi za Wafaransa 227

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 227

8/14/2017 1:18:39 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

katika kusherekea Siku hiyo, akaambiwa kuwa Wafaransa wanapenda sana maua. Basi Imamu Khomein alinunua vishada vya maua na akawapelekea majirani, ili kuwapongeza kwa Sikukuu yao hiyo. Maafikiano kati ya Waislamu na Wakristo: Wakristo na Waislamu wote kwa pamoja wanaafikiana kuwa Bwana Yesu alizaliwa, na kwamba kuzaliwa kwake ni muujiza katika miujiza ya Kiungu. Lakini tofauti iliyopo kati yao ni kuhusiana na tarehe ya tukio hilo je, ni tarehe 25 mwezi wa kumi na mbili, au ni tarehe 10 mwezi wa nne? Sasa tofauti ya tarehe isiwe sababu ya kuwagombanisha watu wenye akili timamu, bali ni suala la kukaa mezani kwa heshima na taadhima, ili kufanya mazungumzo na kufikia mwafaka. Na hata kama tarehe ya kuzaliwa kwa Bwana Yesu haitafahamika, hiyo haiwezi kuwa ni sababu ya kutokukumbuka tukio hilo la kihistoria. Tukio litabaki pale pale na litakumbukwa hata kama siku itakuwa ni tofauti na siku ya tukio lenyewe, kwani mbona Qur’ani Tukufu imelikumbuka tukio hilo na haikutaja tarehe? Mbona Kitabu cha Mathayo Mtakatifu kimelikumbuka tukio hilo pia, lakini tarehe haikutajwa? Hii inaashiria kuwa cha msingi ni kukumbuka tukio lenyewe, hususan ule ukombozi ulioletwa na Nabii huyo hata kama hatujui ilikuwa ni siku gani. Bali ni suala la sisi kuchagua siku ya kufanya maadhimisho hayo. Na ndio maana utakuta katika jamii za Waislamu wakifanya maulidi mara kwa mara hata kama ni nje ya mwezi na tarehe ya tukio. Tunamwomba Mola atujaalie sote kuwa ni katika wale wanaosikiliza neno na kufuata lile lililokuwa bora zaidi.

228

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 228

8/14/2017 1:18:39 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

SEHEMU YA NANE TAWASSUL

I

likuwa ni desturi ya Waislam, kumwomba Mwenyezi Mungu kwa kupitia kwa mmoja wa watu watakatifu kama vile Manabii au Mawalii na waja wema. Lakini desturi hiyo iliyodumu kwa karne nyingi, na bila ya kupingwa na yeyote kati ya wasomi, iligeuka kuwa ni Bidaa na kuabudu asiyekuwa Mungu pale tu alipodhihiri Ibn Taimiyyah mnamo karne ya nane Hijiria, na madai yake ya ubabaishaji, kasha akaibuka Sheikh Abdul-Wahhab mnamo karne ya 12 na kuendeleza uzushi na upotovu huo hadi leo hii. Suala la kumwomba Mwenyezi Mungu kwa kupitia kwa Mitume na Mawalii ni suala linalofahamika katika jamii za Kiislamu ulimwenguni kote, na zimepokelewa hadithi nyingi kuhusiana na jambo hili na kulipendekeza. Kwa hiyo kutawassuli si jambo geni bali ni jambo la kidini linalofahamika kwa Waislamu toka mwanzoni mwa ujio wa Uislamu hadi leo hii, isipokuwa mwanzoni mwa karne ya nane na mwishoni mwa karne ya saba aliibuka Ibn Taimiyyah, na fikra ya kupinga kila jambo zuri linalofanywa na Waislamu katika dini hata likiwa na dalili na mashiko katika Qur’ani na hadithi, atajaribu kutaka kuzidhoofisha hadithi hizo kwa kutumia ubabaishaji na hoja chakavu kama vile: Je! Kumwomba Mungu kupitia kwa mmoja wa waja Wake wa karibu ni haramu?

1.

Wanachuoni wetu wamesema haijuzu.

2.

Hawakuinukuu hadithi hii Maimamu wetu wa hadithi. 229

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 229

8/14/2017 1:18:39 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

3.

Haijapokelewa na wenye elimu na maarifa ya kunukuu.

4.

Haijapokewa na Salafi Swalih.

Lakini kwa bahati mbaya utakaposoma huoni akiwataja hao Wanachuoni wao. Na ukichunguza vitabu vya hadithi unakuta imetoka kwenye moja ya vitabu sita sahihi. Sasa ni Maimamu gani wa hadithi wasiokuwa hawa wa vitabu hivyo? Ni kina nani hao wenye elimu anaowataka zaidi ya Bukhari, Muslim, Ibn Majah, Tabarani, al-Hakim, al-Nisai, na Abi Daud? Tunavyoelewa sisi Salafi Swalih ni Maswahaba wa Bwana Mtume 8, sasa yeye alikusudia kina nani pale aliposema Salafi Swaleh? Ukisoma vitabu vyake unaweza kulia kama si kucheka, kutokana na jinsi maneno yake yanavyokinzana. Utapata kitabu kimoja, kinaharamisha jambo fulani na kulifanya kuwa Bidaa na uzushi, kisha jambo hilo hilo kwenye kitabu kingine ukilifanya unapata thawabu, na hapo ndipo utakapochoka. Bwana huyu aliwahi kufungwa na kufia gerezani huko nchini Syria kutokana na maneno yake yanayokinzana na jumuia ya Waislamu wote. Na baada ya kifo chake, bendera ya upotovu ilishikwa na wafuasi wake kina Ibn Kayim al-Jauziya, na hatimaye kushikwa na Sheikh Muhammad Bin Abdul-Wahab chini ya madhehebu yake ya uzushi Modern Salafism (usalafi asilia wa kisasa) kwa jina maarufu Uwahabi. Bwana huyu aliendeleza fikra ile ile ya kusema kuwa tawassul kwa Mitume na Mawalii ni shirki na ni kumwabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Mpenzi Msomaji, fahamu kuwa kuna aina mbili za kumwomba Mwenyezi Mungu kupitia kwa Mitume na Mawalii Wake, nazo ni: 1.

Kumwomba Mwenyezi Mungu kupitia kwa Mitume na Mawalii Wake, wao wenyewe katika uwenyewe wao. Kwa mfano: 230

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 230

8/14/2017 1:18:39 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninaelekeza haja yangu Kwako, basi kupitia kwa Mtume Wako Muhammad 8 nikubalie haja yangu. 2.

Kumwomba Mungu kwa heshima, utukufu, na baraka za Mitume, na Mawalii. Kwa mfano: Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninaelekeza haja yangu kwako, basi kwa heshima na nafasi aliyonayo Muhammad Kwako naomba unikubalie haja yangu.

Aina zote hizo mbili za tawassul ni uzushi na ni haramu, kwa mujibu wa itikadi za Kiwahabi zinazotokana na ufahamu duni wa maandiko, au upotoshaji wa makusudi na nia zao mbaya za kutaka kuuvuruga Uislamu ili kukidhi matakwa ya wakuu wao wa Ulaya, ambao wanawalipa kwa ajili ya kuupaka Uislamu matope na kuufanya uwe na sifa mbaya katika jamii, hususan jamii za kimataifa na mbele ya kila asiyekuwa Mwislamu. Ili mradi tu Uislamu uonekane kuwa ni dini ya wahuni, wauaji, watu wasio na lugha ya maelewano na yeyote asiyekuwa na mitizamo chakavu kama yao. Watu wasiokuwa na nidhamu wala heshima kwa Mitume na Mawalii, achilia mbali wazazi. Hiyo ndiyo sura ambayo Mawahabi wanataka tujitokeze nayo mbele ya jamii. Lakini mafundisho sahihi ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake yako mbali kabisa na hayo yafanywayo na Mawahabi. Je, hadithi za Mtume 8 zatwambia nini kuhusiana na tawassul? Hakuna hadithi sahihi ya Bwana Mtume 8 inayopinga suala la kumwomba Mwenyezi kupitia kwa mmoja wa watu watakatifu, kama vile Mitume na Mawalii. Bali hadithi zinazothibitisha suala hili hazina idadi. Hapa tutakutajia baadhi yake:

231

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 231

8/14/2017 1:18:39 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Imepokelewa kutoka kwa Uthman bin Hunaif, anasema: Mtu mmoja aliyekuwa kipofu alikuja kwa Bwana Mtume 8 akamwambia: Niombee kwa Mwenyezi Mungu aniponye upofu. Bwana Mtume akamwambia: Ukipenda nitaomba, na ukipenda vumilia na ndiyo bora. Bwana yule akamwambia Mtume 8: Mwambie Mwenyezi Mungu aniponye. Basi Mtume akamwambia atawadhe, na aswali rakaa mbili, na aombe kwa kusema hivi: ‘Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi nakuomba na ninaelekea Kwako kupitia kwa Mtume Wako, Mtume wa rehema. Ewe Muhammad, hakika mimi naelekea kwa Mola Wangu ili ikubaliwe haja yangu. Ewe Mwenyezi Mungu mfanye Muhammad kuwa mwombezi wangu.’ Anasema Ibn Hunaif: Wallahi wakati tukiendelea na mazungumzo na kabla hatujatawanyika, aliingia bwana yule aliyekuwa kipofu, kama kwamba hakuwa kipofu. Ibn Taimiyyah akiri juu ya usahihi wa hadithi ya Tawasul: Pamoja na ususuavu aliyokuwanao Ibn Taimiyyah katika kudhoofisha hadithi za Bwana Mtume 8 bila kuwa na aibu hata kidogo, lakini hadithi tuliyoitaja ilimshinda kuidhoofisha. Anasema Ibn Taimiyyah: “Makusudio ya Abu Ja’far, jina lililotajwa katika mtungo wa wapokezi wa hadithi hiyo, huyo ni Abu Ja’far al-Khatmi, bwana huyu ni mpokezi wa hadithi anayetegemewa.” Ibn Taimiyyah anaendelea kusema: “Ama katika kitabu Musnad Ahmad cha Imamu Hanbal, ametajwa kwa jina la Abu Ja’far al-Khatmi. Na katika Sunan ibn Majah ametajwa kwa jina la Abu Ja’far tu.” Huyo ndiyo Imamu wa Mawahabi anavyokiri juu ya usahihi wa hadithi tuliyoitaja kuhusiana na tawassul. Sasa hebu tugeukie upande wa pili tuangalie wafuasi wake nao wana maoni gani juu ya suala hili? 232

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 232

8/14/2017 1:18:39 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Mwandishi wa kiwahabi / kianswarsunna naye pia akiri kuwa hadithi hiyo ni sahihi: Mwandishi asilia wa Kiwahabi anayefahamika kwa jina al-Rifai, ambaye kila hadithi inayopingana na itikadi yake ya uzushi, huidhoofisha hata kama ni hadithi sahihi, hususan zile hadithi zinazohusu tawassul, lakini hadithi hii ameshindwa kuidhoofisha (kama alivyoshindwa Sheikh wake Ibn Taimiyyah) na hatimaye akaishia kusema kuwa: “Hapana shaka kwamba hadithi hii ni sahihi, mashuhuri. Na imethibiti bila wasiwasi wala shaka, kwamba macho ya kipofu yalirejea (akawa anaona) kwa sababu ya dua ya Mtume 8”134 Tawasul kwa haki ya waombaji: Amepokea Atiya al Aufi kutoka kwa Abu Said al-Khudri, kwamba Mtume 8 amesema: “Yeyote atakayetoka nyumbani kwake na akaenda msikitini kwa ajili ya Swala na akasema: ‘Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi nakuomba kwa haki na baraka ya wanaokuomba, na ninakuomba kwa haki ya mwendo wangu huu, kwani mimi sikutoka kwangu kwa ajili ya maringo na majivuno, wala kujionesha, wala kutaka sifa, bali nimetoka kwa kuogopa ghadhabu Zako. Basi ninakuomba unilinde kutokana na moto, na unisamehe dhambi zangu, kwani hakuna anayesamehe dhambi ila Wewe.’135 Atakayesema hivyo, Mwenyezi Mungu atamwelekea mtu huyo kwa dhati Yake, na malaika sabini elfu watamtakia msamaha.” Tukiitafakari hadithi hiyo kwa akili huru ambazo hazijajaladiwa, basi tutafahamu kupitia maana yake iliyo wazi kwamba mtu anaruhusa ya kumwomba Mwenyezi Mungu kupitia kwa Mitume na Mawalii, au daraja na heshima walizonazo mbele ya Mwenyezi Mungu, ili kulitilia wepesi jambo lake, na kuweza kukubaliwa haraka na Mwenyezi Mungu kupitia kwa watukufu hao. Katika hadithi   Al -Wahabiyat fil Mizan   Sunan Ibn Majah, Jz. 1, uk. 256 hadithi namba 778.

134 135

233

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 233

8/14/2017 1:18:39 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

hii tumeona uwezekano wa watu kumwomba Mungu kwa baraka za watu wengine wanaomwomba, bali ni vizuri mno kumwomba Mungu kwa heshima za watukufu, kwa mfano kama tunavyosoma katika sura za Qur’ani:

“.....Na lau kwamba walipojidhulumu wengekujia wakaomba maghufira kwa Mwenyezi Mungu na wakawaombewa maghufira na Mtume, wangelimkuta Mwenyezi Mungu ni Mwenye kutakabali toba, Mwenye kurehemu.”136

Mtume 8 atawassali kwa baraka zake na Mitume waliomtangulia: Alipofariki Bibi Fatimah JBint Asad, mama yake Imamu Ali, D Bwana Mtume 8 aliingia mahala alipofia (chumbani) akakaa upande wa kichwani kwake, akasema: “ Mwenyezi Mungu akurehemu ewe mama yangu.” Kisha Bwana Mtume akamwita Usama Bin Zayd na Umar ibn al Khattab, na kijana mwingine ili wakachimbe kaburi. Basi walichimba kaburi hilo, na walipofikia kuchimba mwanandani, Bwana Mtume 8 alichimba mwanandani Yeye Mwenyewe huku akitoa mchanga kwa mikono yake mitukufu, na alipomaliza alilala ndani ya mwanandani, na kusema: “Mwenyezi Mungu ndiye anayehuisha na kufisha na Yeye ni hai wala hafi. Ewe Mwenyezi Mungu msamehe mama yangu Fatimah Bint Asad J na uyapanue makazi yake, kwa haki ya Mtume Wako na Manabii waliopita kabla yangu.” Hapa Mtume ameomba kupitia Mitume waliomtangulia. Tukiachilia mbali hayo, twende kwenye maisha yetu ya kila siku, tutaku  Surat Nisaa; 4:64

136

234

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 234

8/14/2017 1:18:39 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

ta mifano mingi tu. Nakutajia mfano mmoja tu: mtoto anapokuwa na shida ya kitu kwa mfano anataka kalamu, utaona mtoto huyu akienda kumwambia mama yake ili mama akamwombee kwa baba. Sasa hawa Mawahabi mbona wanaharamisha mambo ambayo hayahitajii elimu kubwa bali hata akili ya mtoto mdogo wa chekechea inatosha. Ndugu zangu tawassul ni suala la kimaumbile, lakini Mawahabi wanayapinga hadi maumbile yao ili kukidhi matakwa ya wakuu wao wa Ulaya, ambao wanawalipa kwa ajili ya kuharibu matukufu ya dini yetu. Mwenyezi Mungu tunakuomba kwa utukufu wa Mtume Muhammad 8, uvinusuru vizazi vyetu kutokana na upotovu wa Madhehebu hii ya uzushi na ya uzandiki ya Uwahabi. Dua ya Kumail bin Ziyad ni aina nyingine ya tawassul: Moja ya mambo yanayopelekea Mawahabi kuwakufurisha wafuasi wa Ali bin Abi Twalib D, ni husuda, kwa kuona kwamba Ali D, kawaachia Wafuasi Wake hazina nyingi na zenye thamani, ambapo wao Mawahabi hawana hazina waliyoirithi zaidi ya mikasi ya kukatia suruali za watu bila ridhaa zao. Na sisi moja ya hazina tulizoachiwa kama urithi wetu ni dua ambazo hazina idadi, na katika dua hizo nyingi sisi tumechagua Dua al Khizri inayofahamika kwa wengi kama Dua ya Kumail, ili tuweze kufaidika na mafunzo yake ya kiroho ambayo ndiyo njia pekee ya kutakatifisha nafsi zetu na kutufikisha kwenye kilele cha ukamilifu. Dua hii ni katika hazina za siri ambazo Imamu Ali D alimfundisha mwanafunzi wake mpendwa Kumail bin Ziyad ili urithi huo uwafikie wafuasi wote wa Mtume 8 na wa watu wa nyumbani kwake. Imependekezwa kwamba dua hii isomwe tarehe 15 ya Mwezi Shaaban, na kila usiku wa kuamkia Ijumaa, na mwenye kuweza asome kila siku, au isomwe kwa mwezi mara moja, na ikishindikana basi kwa mwaka isomwe mara moja, ikishindikana basi katika umri wa mtu aisome 235

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 235

8/14/2017 1:18:39 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

mara moja tu, hebu jiulize kuna siri gani iliyofichika kwenye dua hiyo ?

} ‫{ أللهم إنّي أسألك برحمتك التي وسعت ُكل شيء‬ {Ewe Mola wangu, kwa hakika mimi ninakuomba kwa rehema zako zilizokienea kila kitu}

Hakuna kitu kilichopo nje ya rehema za Mwenyezi Mungu, bali kila ukionacho kinategemea katika uwepo wake rehema za Mwenyezi Mungu, kwani rehema zake hazina kikomo wala mipaka. Kwa rehema hizo jua lake huangaza kwa watu wote bila kubagua, na pia mvua yake huwafaidisha viumbe wote. Hii inaashiria utajiri usio na kikomo, Naye Mwenyezi Mungu akalitilia msisitizo suala hilo kwa kusema:

“Enyi watu! Nyinyi ndio wenye haja kwa Mwenyezi Mungu; Na Mwenyezi Mungu ni Mkwasi, Msifiwa.”137

Kutokana na kwamba sisi ni wenye haja, na Mwenyezi Mungu ni mwenye kujitosheleza, alituamuru tumuombe Yeye ili atumiminie katika rehema Zake, na akaahidi kuwa atajibu maombi yetu, na pia akaahidi kuwatia katika Moto wa Jehanamu wala wote wanaojivuna, na kutomuomba. Kwa nini? Kwa sababu kumuomba Yeye ni ibada, na asiyefanya ibada huyo anazingatiwa kuwa ni mwenye kiburi. Na anayejiweka katika nafasi ya wenye kujitosheleza hali ya kuwa nafasi hiyo ni ya Mwenyezi Mungu peke yake. Qur’ani Tukufu inasema:   Surat Fatir; 35:15

137

236

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 236

8/14/2017 1:18:39 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

“Na Mola Wenu amesema: Niombeni nitawaitikia.Kwa hakika wale ambao wanajivuna kufanya ibada Yangu wataingia Jahanamu wadhalilike.”138

Na hiyo ndio hali tunayoishuhudia leo hii. Kiburi kimetawala kuanzia ngazi ya mtu binafsi, familia, mpaka jamii nzima. Leo hii imefika hatua ya mtu kujiona kuwa yeye ni bora kuliko mwingine. Na mwingine ana kiburi kwa sababu ya kale kagari kake, akitembea barabarani anawarushia maji machafu watu wanaotembea kwa miguu. Halafu mtu huyo huyo anajiita mfuasi wa Bwana Mtume Muhammad 8. Kwa yakini hayo ni madai yake anayoyadai kwa mdomo wake, kwani Mwenyezi Mungu amekwishatutajia sifa za wafuasi wa Mtume Muhammad 8 kwa kusema:

“….. “Muhammad, Mtume wa Mwenyezi Mungu, na walio pamoja naye, wana nguvu mbele ya makafiri, na wanahurumiana wao kwa wao. Utawaona wakirukuu na kusujudu wakitafuta fadhila na radhi za Mwenyezi Mungu. Alama zao zi katika nyuso zao, kwa athari ya kusujudu.....”139   Surat Ghafir; 40:60   Surat Fat-hu; 48:29

138 139

237

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 237

8/14/2017 1:18:39 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Hao ndio wafuasi wa Bwana Mtume, Muhammad 8 na ndio wafuasi wa Ali ibn Abi Twalib D. Wafuasi hao wanahurumiana wao kwa wao, kwa kupitia ile rehema ya Mwenyezi Mungu iliyokigubika kila kitu katika uwepo, na rehema hiyo ndio ile ile tunayoitumia kama njia ya kujibiwa maombi yetu pale tunaposema:

}‫{أللهم إنّي أسألك برحمتك التي وسعت ُكل شيء‬ {Ewe Mola wangu, kwa hakika mimi ninakuomba kwa rehema zako zilizokienea kila kitu}.

Sasa kwa nini tusiseme: Ewe Mola Wangu kwa hakika mimi ninakuomba kwa kupitia kwa Mtume Wako na watu wa nyumbani kwake? Jibu: Ni kwa sababu tunataka dua yetu ipitie kwa kitu ambacho kina ukaribu na Mwenyezi Mungu, lakini hakuna chenye ukaribu na dhati ya Mwenyezi Mungu zaidi ya rehema yake iliyokigubika kila kitu, bali hata Bwana Mtume 8 amegubikwa na rehema hiyo. Na hapo Wahhabi ni lazima aulize: Ikiwa rehema ndiyo iko karibu zaidi na dhati ya Mwenyezi Mungu, kwa nini mnawafundisha watu shirki, kwa kuwaambia wamuombe Mwenyezi Mungu kwa kupitia kwa watu wema na Manabii? Jibu: Ni kwa sababu hatuna usafi wa kiroho, midomo yetu ni michafu, kwa hiyo tunahisi aibu kusimama mbele ya Mwenyezi Mungu na hali kama hiyo. Kwa maana hiyo tunasimama nyuma ya watu wema na Manabii ili wao watuombee kwa Mwenyezi Mungu kwa kupitia kwenye rehema hiyo. Naye Mwenyezi Mungu atajibu maombi yetu kama alivyotuahidi. Ndugu zangu katika utu! Hivi mtu kama Wahhabi au Answar Sunnah au Salafi, anatarajia kuwa Mwenyezi Mungu atamsikiliza bila ya 238

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 238

8/14/2017 1:18:39 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

kupitia kwa watakatifu? Kwa yakini hilo haliwezekani, kutokana na uchafu wao wa kiroho na wa kimwili. Kwanza ndevu zao chafu, na mavazi yao ndio sitaki hata kusema. Midomo yao ni michafu kila siku wanawakufurisha Waislamu na kuwagombanisha. Na Mawahabi hao hao ndio watovu wakubwa wa nidhamu kwa Mwenyezi Mungu na Mitume Wake, na pia hawana nidhamu hata kwa wazazi wao. Je! Watu kama hao hawahitajii kumuomba Mwenyezi Mungu kwa kupitia baraka za watakatifu Wake? Bila shaka wao ndio wanahitajia hasa msaada wa watakatifu hao, ila tu hawajitambui

239

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 239

8/14/2017 1:18:39 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

SEHEMU YA TISA

UTAKATIFU WA AHLUL-BAYT Je! ni nani hao Ahlul-bayt waliotakaswa katika Qur’ani? Tujuavyo sisi ni kwamba wake wa Bwana Mtume 8 ndiyo watu wa nyumbani kwake, na kwamba watu hao ndiyo walengwa katika aya 33 ya Surat Ahzab, inayowatakatisha watu wa nyumba ya Mtume 8. Hivyo ndivyo tunavyofahamu, lakini je! ufahamu huo ni sahihi? Waislamu wote wanakubali kuwa Mtume 8 ni kiongozi wao, na hakuna mjadala kati yao kuwa wake wa Bwana Mtume 8 ni mama wa waumini wote. Hilo limethibi usahihi wake, na hakuna akanushaye. Lakini mjadala unabaki kwenye utakatifu uliotajwa katika Aya hiyo ya Surat Ahzab, kwamba utakatifu huo unawahusu wake wa Mtume pia au hauwasuhu? Imepokelewa kutoka kwa Ummu Salama O kwamba alisema: Bwana Mtume 8 alikuwa amekaa na Bibi Fatimah J, Imamu Ali G,, Imamu Hasan G, na Imamu Hussein G, na walikuwa wakila chakula na hawakuniita kula nao. Na desturi ya Bwana Mtume 8 alikuwa hali chakula mpaka aniite. Baada ya kumaliza chakula, Bwana Mtume 8 alijifunika shuka yake (kisaa) na akawaingiza ndani ya shuka hiyo, Sayyiduna Ali, Bibi Fatimah J, Sayyiduna Hasan G, Sayyiduna Hussein G, pamoja na yeye Mwenyewe wakawa watano. Kisha Bwana Mtume akasema: Ewe Mwenyezi Mungu hakika watu hawa ndiyo Ahlulbayti wangu (watu wa nyumba yangu). Basi akashuka Sayyiduna Jibril D, huku akisoma Aya hii: 240

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 240

8/14/2017 1:18:40 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

“Hakika si mengineyo, Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume, na kuwatakasa kabisa kabisa.”140

Kwa mujibu wa maelezo ya Mama wa waumini Ummu Salama ni kwamba Aya hiyo imewatakasa watu hao walioingia ndani ya shuka hiyo, kwa hiyo mwenye kudai kinyume na hivyo inabidi atukinaishe kwa hoja, kama isemavyo Qur’ani:

“Sema leteni hoja zenu ikiwa nyinyi ni wasema kweli.”141

Pia imepokewa kutoka kwa wake wa Bwana Mtume 8 Bibi Aisha O na Ummu Salama (radhi za Allah ziwaendee) kwamba Aya hii haiwahusu wao. Lakini watu wenye chuki hujaribu kukarabati hadithi na kuwachomeka mama wa waumini katika utakaso uliyotajwa kwenye Aya hiyo. Madai hayo ni ya uongo na hayana mashiko sahihi, na ushahidi wa Bibi Aisha O na Ummu Salama O unawapiga msumari wa mdomo wasemao maneno hayo yasiyo na mashiko. Ahlul-bayt kwa mujibu wa Aya ya Qur’ani ni hao waliotajwa, bali hata Ummu Salama O alitaka kuingia pamoja nao lakini Bwana Mtume 8 alimzuia na kumwambia kuwa “Wewe uko kwenye kheri.” Kwa hiyo sisi pamoja na heshima yetu kwa wake wa Mtume, tunasema kuwa Aya hiyo ni mahsusi kwa Ahlul kisaa (watu waliongia ndani ya shuka) peke yao, na wao ndiyo waliotakasika. Ila   Surat Ahzab; 33:33   Surat Baqarah; 2:111.

140 141

241

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 241

8/14/2017 1:18:40 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

sisemi kuwa wake wa Mtume si watakatifu, bali kauli yangu ni kama vile nisemavyo Jauz ni mwanaume, hapo nakuwa simaanishi kuwa Mustafa ni mwanamke, na kuthibitisha kitu si kukanusha kingine. Ushahidi wa pili: Ushahidi huu umethibiti kupitia Surat al-Imran, aya ya 61, Mwenyezi aliposema:

“Na watakaokuhoji (kuhusu Nabii Isa) baada ya kukufikia elimu hii, waambie: Njooni, tuwaite watoto wetu na watoto wenu na wanawake zetu na wanawake wenu, na nafsi zetu na nafsi zenu, kisha tuombe kwa unyenyekevu tutake laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie waongo.”142

Sababu ya kushuka kwa Aya hii, ni pale viongozi wa Kikristo wa Najran, walipokuja Madina mnamo mwaka wa 9 Hijiria, kwa lengo la kutaka kujadiliana na Bwana Mtume 8 kuhusiana na Nabii Isa D. Bwana Mtume 8 akawajibu viongozi wale kwa kuwaambia:

“Hakika mfano wa Isa kwa Mwenyezi Mungu, ni kama mfano wa Adamu; alimuumba kutokana na udongo, kisha akamwambia ‘Kuwa’ na akawa.”143   Surat al-Imran; 3:61.   Surat al-Imran; 3:59.

142 143

242

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 242

8/14/2017 1:18:40 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Viongozi wale pamoja na kupewa majibu hayo lakini bado waliendeleza mabishano, na ndipo iliposhuka Aya hiyo ya 61 kumwambia Mtume ikiwa wataendeleza mjadala na kutotosheka na majibu yako, na kukuona wewe kama mwongo, basi waite waje kwenye maapizano, kama ilivyoashiriwa katika Aya hiyo. Maana ya watoto wetu katika Aya hiyo ni Hasan na Hussein, na maana ya wanawake wetu ni Bibi Fatimah J, na maana ya Nafsi zetu ni Bwana Mtume 8 na Sayyiduna Ali D. Tazama kitabu Maalim Tanzil. Anasema Saad Bin Abi Wiqqas K, iliposhuka Aya hiyo ya 61 ya Surat al-Imran, Bwana Mtume 8 alimwita Sayyiduna Ali, Bibi Fatimah J, Sayyiduna Hasan, na Sayyiduna Hussein, kisha akasema: “Ewe Mola Wangu, hawa hapa ndio watu wangu.”144 Kuwatanguliza watu wa nyumba ya Mtume 8: Sasa tuangalie itikadi ya kuwatanguliza watu wa nyumba ya Mtume, kwa mujibu wa kauli ya Mwenyezi Mungu, kisha tuiangalie itikadi hiyo hiyo kwa mujibu wa mawazo ya Ibnu Taimiyya. Mwenyezi Mungu swt, anasema:

“Hakika Mwenyezi Mungu na Malaika Wake wanamswalia Nabii. Enyi ambao mmeamini! Mswalieni na mumsalimu kwa salamu.”145

Iliposhuka Aya hii Maswahaba walimuuliza Bwana Mtume 8 namna ya kumsalia, “Ewe Mtume! Ama kukusalimia tuna  Sahihi Muslim Jz. 4, uk. 1871 hadithi nambari 2404 . Sunan Tirmidhi Jz. 5 uk.

144

638 hadithi nambari 3724.

Surat Ahzab : 56.

145

243

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 243

8/14/2017 1:18:40 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

jua ni Assalaam alayka yaa Rasulullah! Huku kukuswalia kunakofaradhishwa na Qur’ani ni vipi? Bwana Mtume 8 akasema, semeni: ALLAHUMMA SWALLI ALAA MUHAMMAD WA ALAA AALI MUHAMMAD, KAMA SWALLAITA ALAA IBRAHIMA WA ALAA AALI IBRAHIMA.146 Tamko hilo wa alaa Aali Muhammad, ndilo ambalo limefanywa wajibu kwa kila Mwislamu atamke namna hiyo kwenye Swala yake. Na Swala haitatimia bila ya kutamka ibara hiyo. Imekuwaje kuwatanguliza watu wa nyumba ya Mtume kuwe ni sehemu muhimu na ya wajibu katika Swala? Imamu Shafii anasema: “Enyi watu wa nyumba ya Mtume, kuwapenda nyinyi ni faradhi kutoka kwa Mwenyezi Mungu, aliyoishusha katika Qur’ani, yatosha kwenu kuwa ni fahari kubwa ya kwamba asiyekuswalieni hana Swala.” Hiyo ndiyo namna ya kumswalia Mtume, iwe ni katika Swala au nje ya Swala, lakini Mawahabi wanajaribu kuiondosha kidogo kidogo swala hiyo, wakati mila na desturi ya wazee wetu, ilikuwa ni kukaa msikiti baada ya Swala hususan Swala ya asubuhi na kusoma swalat alaan-Nabii. Hii ni maarufu sana kwa Wanatwariqa, lakini walipokuja hao Waislamu wenye vipara na ndevu ndefu, waliukarabati mfumo walioukuta na badala yake wakaweka neno Takbiir, Allaahu Akbar, alimradi tu wapingane na Aya isemayo “Na tukakunyanyulia utajo wako”. Juhudi kubwa ya Mawahabi ni kuhakikisha wanautokomeza huo utajo wa Mtume na watu wa nyumbani kwake, na cha kushangaza ni pale inaposemwa, msalieni Mtume, wao husema: Allahumma swalli wasallim alee. Lakini wakati wa Swala hawasemi hivyo bali wanasema: Allahumma swalli alaa Muhammad wa alaa aali Muhammad, kwa nini? Kwa sababu wanajua kuwa wasiposema hivyo Swala itakuwa batili, lakini utafikia wakati hata   Sahihi Bukhari Jz. 6, uk. 217 hadith mutafak alaih

146

244

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 244

8/14/2017 1:18:40 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

hapo kwenye Swala za kila siku pia watageuza, maana watu hawa ni hatari zaidi ya saratani. Ndugu zangu sisi hatukanushi ukuu wa Mwenyezi Mungu, lakini kila kitu kina mahala pake, yaani kila sehemu ina mazungumzo yake, na kila mazungumzo yana sehemu yake. Sasa kuweka neno takbiir mahala pa mswalie Mtume, hiyo ni mbinu ya kujaribu kuutokomeza kabisa utajo wa Bwana Mtume 8. Waislamu zindukeni msiingie kwenye mtego wa Kiwahabi. Lakini tujiulize, ni kwa nini watu hao wamekuwa ni wajibu kwetu kuwataja mpaka kwenye Swala zetu za wajibu, na bila ya wao Swala zinakuwa batili? Anasema Mwenyezi Mungu (swt) kuwa:

“Na tukamtunukia (Ibrahim) Is-haqa na Yakub; kila mmoja tulimuongoza. Na Nuh tulimwongoza zamani. Na kizazi chake Daud na Suleiman na Ayub na Yusuf na Musa na Haruna. Na kama hivyo tunawalipa wafanyao mema.”147

Kisha akaendelea kusema katika Aya inayofuatia:

Surat An’am; 6:84

147

245

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 245

8/14/2017 1:18:40 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

“Na Zakaria na Yahya na Isa (Yesu) na Ilyas (Elisha) wote ni katika (watu) wema. Na Ismail na Ilyasaa na Yunus na Lut; na kila mmoja tulimfadhilisha juu ya walimwengu wote. Na katika baba zao na vizazi vyao na ndugu zao. Na tukawachagua na kuwaongoza katika njia iliyonyooka.” (6:85-87).

Kwa nini tuwatangulize Ahlul-Bayt? Na majibu ya Ibnu Taimiyyah Baada ya kumaliza uchambuzi wa Aya za Qur’ani, kuhusiana na suala la kuwatanguliza watu wa nyumba ya Bwana Mtume 8, sasa tuangalie mtazamo wa Ibnu Taimiyyah, ambaye ndiye mwanzilishi wa fikra hii ya kukufurisha Waislamu, kwa sababu tu wanawaweka mbele watu wa nyumba ya Mtume 8. Ibnu Taimiyyah bila ya woga wala aibu anajibu kwa kauli moja tu: “Kwa hakika kutanguliza kizazi cha Mtume (Ahlul-bayt) ni katika athari za kijahiliyyah, katika kuwatanguliza viongozi wao.” Huo ni mtazamo wa Ibnu Taimiyyah. Yeye anaona kuwa kuwatanguliza watu wa nyumba ya Mtume ni katika mambo yaliyopitwa na wakati. Nini maana ya ujahiliyyah? Aliposema ujahiliyyah alikuwa anakusudia zama za kabla ya Uislamu. Na maisha ya watu kabla ya Uislamu ni maisha ya kuabudu masanamu, watu kuwanyenyekea wafalme wao hata kama ni watu waovu. Sasa Ibnu Taimiyyah anawaambia wafuasi wake kuwa kuwatanguliza watu wa nyumba ya Mtume, hayo ni mabaki ya fikra za washirikina kabla ya Uislamu. Subhaanallah! Hapo ndipo utakapokubali maneno yangu kuwa Masalafi/Mawahabi, si Waislamu japokuwa wanajificha nyuma ya tamko la shahada mbili. Mpenzi msomaji, ni ususuavu wa moyo wa namna gani huo wa mtu kuukosoa uteuzi wa Mwenyezi Mungu, na kusema kuwa ni athari za fikra zile walizokuwanazo watu kabla ya Uislamu! Katika mtiririko wa Aya tulizozitaja, Mwenyezi Mungu amewachagua Mitume kizazi kwa 246

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 246

8/14/2017 1:18:40 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

kizazi kitokanacho na wao kwa wao, je! Mwenyezi Mungu hakufahamu kuwa kufanya hivyo ni kufuata athari za watu wa zamani waliokuwa wakifuata mila chafu kabla ya Uislamu? Kwa hiyo Qur’ani inatuletea mawazo ya ujahilyyah (ya zama za ujinga) kabla watu hawajaelimika! Mungu atulinde na aviepushe vizazi vyetu kutokana na ukafikri huo. Hilo ndilo kundi lenye husuda, chuki na uadui dhidi ya watu wa nyumba ya Mtume, halafu wanajinadi hadharani kuwa wao ndiyo watetezi wa Sunnah za Bwana Mtume. Je, huo ni utetezi wa Sunnah za Bwana Mtume au ni utetezi wa wakuu wao wa Uingereza? Mawahabi wanawachukia mno watu wa nyumba ya Bwana Mtume, pamoja na vizazi vitokanavyo na wao, ambao ni watu tuwaitao Sayyid au Sharif. Anasema Sheikh Muhammad Bin Abdul Wahab kuwa neno ( Ilaahu/Mungu) walilitumia washirikina kuyaita masanamu yao, lakini washirikina wa zama hizi wanatumia neno Sayyid. Neno Ilaahu maana yake ni mungu na washirikina walilitumia neno hilo (Ilaahu/mungu) kuyaita masanamu yao. Lakini Waislamu wa leo wanaposema Sayyid wanakuwa na maana ile ile ya washirikina, kwa hiyo kama Ilaahu kwa washirikina maana yake ni mungu basi na neno Sayyid au Sharif kwa Waislamu maana yake ni mungu!!! Ni matusi ya namna gani hayo Waislamu mnatukanwa kwa sababu tu mnawapenda watu wa nyumba ya Bwana Mtume 8 na vizazi vyao, yaani masharifu. Mawahabi kinachowasumbua ni chuki na husuda tu, lakini sisi hatutaacha kuwapenda watu wa nyumba ya Mtume 8. Mwenyezi Mungu anasema:

“Huo ni mwongozo wa Mwenyezi Mungu. Kwa huo humwongoza amtakaye katika waja Wake…..”148   Surat An’am; 6:88

148

247

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 247

8/14/2017 1:18:40 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Ahlulbayti katika hadithi za Bwana Mtume 8: Amesema Bwana Mtume 8: i.

“Hussein anatokana na mimi, na mimi ninatokana na Hussein, Mwenyezi Mungu humpenda mwenye kumpenda Hussein.”

ii. “Hasan na Hussein ni Mabwana wa vijana wa peponi.” iii. “Fatimah J ni pande la nyama ya mwili wangu mwenye kumpenda Fatimah J amenipenda mimi, na mwenye kumchukia Fatimah J amenichukia mimi.” Hebu nileteeni hadithi ya Mtume 8 isemayo mwenye kumpenda Abdul Wahab, amenipenda mimi. Enyi Mawahabi, Mayahudi mliyovaa joho la Uislamu ili kuufisidi, mkiona sisi hatuwatangulizi viongozi wenu kama vile Sheikh Muhammad Bin Abdul Wahab, au Ibnu Taimiyyah au viongozi wa Saudia, na Boko Haram, Daesh n.k, msije mkadhania kuwa ni chuki, bali ni kwa sababu hakuna ushahidi wa Aya wala hadithi unaotuamrisha kuwatanguliza watu hao. Tunamwomba Mola atujalie sote kuwa ni katika wale wanaosikiliza neno na kufuata lililokuwa bora zaidi. Utakaso wa watu wa nyumba ya Mtume 8: Katika somo hili tutazungumzia utakaso wa watu wa nyumba ya Mtume 8 kwa mujibu wa Qur’ani. Lakini kabla hatujazungumzia ushahidi wa Qur’ani, kwanza kabisa hatuna budi kufahamu maana ya utakaso, (kuhifadhika kutokana na madhambi) uliotajwa katika Qur’ani. Na je hali hiyo inawahusu wao tu, au hata sisi tunaweza kuwa watakatifu, yaani watu wasiokuwa na dhambi? Maana Mawahabi wanadanganya watu kila kukicha ya kwamba Mitume tu ndio hawatendi dhambi katika baadhi ya nyakati, halafu 248

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 248

8/14/2017 1:18:40 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

wanashindwa kuithibitisha kielimu nadharia hiyo iliyojaa utovu wa nidhamu kwa Manabii wa Mwenyezi Mungu. Utakatifu ni hatua katika hatua za elimu yakinifu, au ni tabaka katika matabaka ya elimu hiyo. Mwanadamu akiwa na yakini katika mambo yote yawezayo kumletea madhara basi ni lazima atajiepusha nayo. Kwa hiyo tunasema kuwa kila mwanadamu ni mwenye kujihifadhi katika baadhi ya vitu, au kwa tafsiri nyepesi tunasema kuwa kujilinda ni matokeo ya elimu ya yakini uliyonayo juu ya hatima mbaya ya matendo machafu. Kwa mfano kama tukiweka nyaya za umeme ambazo ziko wazi bila gamba kisha nyaya zile ziwe na moto, hivi yuko mtu mwenye akili timamu anayeweza kuzishika kwa mkono wake? Jibu hapana, kwa nini? Kwa sababu anajua kwa yakini kuwa akizishika atahatarisha maisha yake. Kwa hiyo mwanadamu huyu atakuwa ni mwenye kujilinda katika jambo hili, na hawezi kufanya kosa hapo hata kidogo. Na huo ni mfano mdogo tu, sasa mwanadamu atakaposimama mbele ya maasi kisha akawa na yakini ya kwamba hatima ya kufanya maasi ni moto mkali wa Jehannam, bila shaka atayaepuka maasi yale, na huyo atakuwa ni mwenye kuhifadhika na maasi baada ya kuelewa hatima yake mbaya. Kwa mantiki hiyo, Watu wa nyumba ya Mtume 8 bali Manabii wote wanaepukana na maasi kwa kuwa wanaona kwa jicho la yakini kuwa nyuma ya maasi kuna maangamio na ndiyo maana hawayasogelei maasi hata kidogo. Labda tuulize swali lifuatalo:- Je, ni nani yuko tayari kuchukua kitita cha pesa ili ashike nyaya za umeme zilizo wazi? Jibu hakuna mwenye akili timamu awezaye kuthubutu, sababu anajua ataangamia na pesa hiyo hataitumia. Na vivyo hivyo watu wa nyumba ya Bwana Mtume 8 na Manabii wote, kwa maarifa yao ya kufahamu kuwa, hatima ya maasi ni maangamio ya milele au ya muda mrefu, hivyo hata siku moja hawakuweza kuyasogelea maasi. 249

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 249

8/14/2017 1:18:40 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Mke wa Aziz (mfalme) wa Misri anasema nilimtamani Yusuf naye akajizuia (fasta’aswama). Kwa nini, kwa kuwa ana elimu yakinifu juu hatima mbaya ya maasi. Lakini kuna baadhi ya Waislam wanapotusikia tukisema kuwa watu wa nyumba ya Mtume 8 hawafanyi madhambi, wao hushangaa sana na kusema sisi tunawafanya watu hao kuwa sawa na mitume. Sasa labda tuwaulize hili: Je, utakatifu unaambatana na utume tu na hauingii sehemu nyingine? Tumekwishaeleza kuwa utakatifu chanzo chake ni elimu ya yakini juu ya hatima mbaya ya mambo, kila atakayefahamu kwa yakini hatima mbaya ya matendo mchafu, ni lazima ajiepushe nayo. Na wala hatusemi kuwa chanzo cha utakatifu ni utume, laa, bali chanzo chake ni elimu yakini. Kwa hiyo Manabii ni watakatifu kutokana na elimu hiyo, na wewe na mimi tukiwa na elimu hiyo, na tukaweza kuitumia kikamilifu, basi tutakuwa tumetakasika na kila aina ya uovu. Qur’ani inasema:

“Na Malaika waliposema: Ewe Maryamu! Hakika Mwenyezi Mungu amekuteua na akakutakasa na akakuteua juu ya wanawake wa ulimwenguni.”149

Na uchafu unaozungumziwa hapo si uchafu wa kimaunzi bali ni uchafu wa kirazini. Ni uchafu ambao huwezi kuuona kwa macho, wala kuusikia kwa masikio, wala kuushika kwa mikono, wala kuuonja kwa ulimi, wala kuunusa kwa pua. Uchafu unaokusudiwa hapo ni madhambi, kwa hiyo Maryamu alikuwa safi, kaepukana na uchafu huo na wala hakuwa Mtume. Kwa hiyo hakuna ulazima wowote wa kuambatanisha utakatifu na utume. Mtume ni lazima   Surat al-Imran aya: 42.

149

250

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 250

8/14/2017 1:18:40 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

awe mtakatifu lakini hakuna ulazima kwa kila mtakatifu awe ni Mtume. Na tunaweza kusema kuwa kila Nabii ni Mtakatifu lakini si kila mtakatifu ni Nabii, na mfano hai ni Bibi Maryamu. Alikuwa ni mtakatifu, na wala hakuwa Nabii. Watu wa nyumba ya Mtume (.a.w.w) kadhalika, wote walikuwa ni watakatifu na hawakuwa Manabii. Baada ya kufahamu hayo sasa tutupie macho kwenye Sura Ahzab aya 33. Je, Aya hiyo inawatakasa viongozi kutoka katika nyumba ya Mtume 8?

“Na kaeni majumbani mwenu wala msidhihirishe mapambo kwa madhihirisho ya kijahiliya ya zamani. Na simamisheni Swala, na toeni Zaka, na mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. Hakika si mengineyo Mwenyezi Mungu anataka kuwaondelea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume, na kuwatakasa kabisa kabisa.� (Ahzab; 33:33)

Kabla ya kuingia katika uchambuzi wa Aya hiyo, ni lazima tubainishe baadhi ya mambo: 1.

Maana ya uchafu uliyotajwa katika Aya hiyo:

Uchafu uliyokusudiwa kama wanavyotueleza wanachuoni, si uchafu ule unaoonekana kwa macho, na kusikiwa kwa masikio, na kunuswa harufu yake kwa pua, bali ni uchafu wa kiroho, ambao kwa tafsiri nyepesi tunasema kuwa ni mambo machafu na ya haramu na kila 251

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 251

8/14/2017 1:18:40 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

lililokuwa kinyume na misingi ya maadili bora. Hiyo ndiyo maana ya uchafu. Na kwa kuwa Aya imesema kuwa Mwenyezi Mungu anataka basi hatuna budi kuufahamu utashi huo. 2.

Je, utashi wa Mwenyezi Mungu katika Aya hiyo ni wa kikanuni au ni wa kimaumbile?

Tofauti kati ya utashi wa kikanuni na utashi wa kimaumbile ni kuwa utashi wa kikanuni ni sheria inayotakiwa itekelezwe na wote waliopewa amri hiyo. Kwa mfano, mwalimu anaposema andikeni. Hii ni amri ya kikanuni ambayo ni lazima itekelezwe na wanafunzi wote darasani. Sasa utashi huo wa mwalimu kwa kuwa ni wa kisheria, wanafunzi wanaweza kutii sheria au wasitii. Mfano wa pili wa utashi wa kisheria, ni pale Mwenyezi Mungu katika utashi Wake wa kisheria alipotaka malaika wote wamsujudie Adamu, lakini ibilisi alipinga utashi huo wa Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo mpaka hapa mpenzi msomaji, utakuwa umefahamu kuwa utashi wa kikanuni, ni sheria inayowataka watu wote waifuate. Ama utashi wa kimaumbile ni mfumo ambao Mwenyezi Mungu anataka uwe katika baadhi ya vitu. Kwa mfano, mfumo wa Jua kutoka Mashariki kwenda Magharibi ni amri ya Mwenyezi Mungu ya kimaumbile. Ameliamuru Jua kimaumbile kufuata utaratibu huo, na Jua halina uwezo wa kwenda kinynume na mfumo huo alioutaka Mwenyezi Mungu. Ngamia kutofanya mapenzi na dada yake au mama yake huo ni utashi wa Mwenyezi Mungu katika maumbile ya ngamia, na mnyama huyo hawezi kwenda kinyume na utashi huo. Sasa tofauti iliyopo kati ya utashi wa kisheria na ule wa kimaumbile ni kwamba katika utashi wa kisheria, sheria inaweza kutaka jambo kwa watu wote, lakini wao wasitekeleze jambo hilo au baadhi wakaasi na wengine wakatekeleza. Lakini 252

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 252

8/14/2017 1:18:41 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

utashi wa kimaumbile unakuwa ni kwa baadhi ya vitu, halafu vile vitu ambavyo Mungu ametaka viwe katika maumbile yale, ni lazima viwe hivyo alivyotaka Mwenyezi Mungu na huwezi kupata ukinzani wa aina yoyote ile katika utashi wa kimaumbile. Amri ya kimaumbile inapotaka mtoto atoke tumboni hali ya kuwa kafanana na baba yake, basi ni lazima iwe hivyo na mtoto yule ni lazima atii amri ile ya kimaumbile. Kwa hiyo kauli ya Mwenyezi Mungu ya kusema “ANATAKA� utashi huu si wa kisheria bali ni wa kimaumbile, kwa nini? Kwa sababu ungekuwa ni utashi wa kisheria basi sheria hiyo ingekuwa ni ya watu wote na siyo ya watu mahsusi na idadi mahsusi, maana sheria huwa inafuatwa na watu wote. Mpenzi msomaji katika aya hiyo ya 33 Ahzab tumejifunza mambo manne: 1.

Maana ya utakatifu na chimbuko lake.

2.

Uhusiano kati ya utume na utakatifu.

3.

Maana ya uchafu.

4.

Aina ya utashi aliyoutaka Mwenyezi Mungu juu ya watu wa nyumba ya Mtume 8.

Baada ya utangulizi huo sasa tunaweza kuingia rasmi katika somo la kuwajua Ahlul-Bayt, yaani watu wa nyumba ya Mtume 8. Je, ni akina nani hao watu wa nyumba ya Mtume? Mada hii sitaki kuirefusha sana ila nitataja baadhi ya nukta zinazokubaliana na madai yetu, kuwa watu wa nyumba ya Mtume katika Aya hiyo, si wake wa Mtume kama wanavyodhani baadhi ya Waislam. 253

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 253

8/14/2017 1:18:41 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

a.

Gender (jinsia) zilizotumika zote 6 ni za kike lakini walipotajwa Ahlulbayti, jinsia ilibadilika na ikatumika ya kiume, kuonesha kuwa hapo wake wa Mtume wameshawekwa pembeni, na kutolewa kwenye ule utashi wa kimaumbile.

b. Wake wa Mtume hawakuwa wakiishi katika nyumba moja bali kila mmoja alikuwa na nyumba yake, ndiyo maana Aya imeanza kwa kusema Na kaeni majumbani mwenu, yaani kila mmoja akae nyumbani kwake. Sasa ikiwa wake wa Mtume ndio walengwa katika Aya basi Aya ingesema: Enyi watu wa majumba ya Mtume, lakini aya inasema, enyi watu wa nyumba ya Mtume kuonesha kuwa ni watu wa nyumba moja tu ya Mtume na si watu wa majumba yote ya Mtume. Na ikithibiti kielimu kuwa wake wa Mtume wanahusika, basi atakuwa ni mke mmoja tu, kwa sababu Aya imetangaza kuwatakasa watu wa nyumba moja. Na kwa kuwa Aya hiyo ilishukia nyumbani kwa Ummu Salama O basi mama huyo ndio mhusika. Lakini hii ni nadharia isiyokuwa na mashiko, kwani iliposhuka Aya hiyo Bwana Mtume 8 aliwakusanya, Ali, Fatimah J, Hasan, Hussein, kisha akawafunika shuka na Yeye mwenyewe Mtume 8 akaingia humo, kisha Sayyiduna Jibril naye akaingia humo na kusoma Aya hiyo ya 33:33. Bwana Mtume 8 akasema: “Ewe Mola Wangu kwa hakika hawa ndio watu wangu.” Lakini Ummu Salama O alipoomba kuingia ndani ya hema lile Bwana Mtume 8 alimwambia: “Hakika wewe uko katika kheri, hakika wewe ni katika wake wa Mtume.” Na ziko riwaya nyingi zinazothibitisha kuwa Ahlulbayti katika aya hiyo ni watu watano tu, kama tulivyofafanua kwa mapana katika kurasa zilizopita. 254

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 254

8/14/2017 1:18:41 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Na baada ya kushuka aya hiyo Bwana Mtume 8 alikuwa akipita mlangoni kwa Bibi Fatimah J kila asubuhi akinadi Swala huku akisoma Aya hiyo kwa muda wa miezi sita, kisa hiki ni maarufu sana na hakuna haja ya kukirefusha hapa. Ama ushahidi juu ya utakatifu wa Makhalifa kutoka nyumba ya Bwana Mtume 8 ni kama tulivyosema kuwa utakatifu chanzo chake ni elimu ya yakini, kwa hiyo wao wamejitakatisha kupitia njia hiyo, kama tulivyoona kwa Bibi Maryamu. Halafu ziko riwaya nyingi sahihi zijulishazo utakatifu wao, na kuwataja kwa majina mmoja baada ya mwingine. Tunamwomba Mola atujalie sote kuwa ni katika wale wanaosikiliza neno na kufuata lililokuwa bora zaidi.

255

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 255

8/14/2017 1:18:41 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

SEHEMU YA KUMI

IBN TAIMIYA NA MITAZAMO ­KINZANI NA DINI Je! itikadi za madhehebu mpya ya uwahabi ni tofauti na zile za maimamu wanne? Swali la msomaji wetu: Msomaji wa mtiririko wa makala zetu katika Gazeti la Mizani, Bwana Khamis Miraji, Mkazi wa Mbagala jijini Dar-es-Salaam, ametuletea swali lifuatalo:“Asalamu aleykum Sheikh. Nimeona umeandika kwamba kuna madhehebu mapya kama Wahabi. Naomba moja katika itikadi yao wanayotofautiana na hawa Maimamu wanne, mfano wa wanachuoni mnaowaandika Ibn Taymiya, Muhammad Abdulwahabi. Na naomba unitajie kitabu alichosema yeye mwenyewe usinukuu mtu mwingine na ukurasa katika gazeti lako la Mizani ndio kuna habari hizo.” Majibu yetu: Waislamu wengi walihadaika na majina mazuri yanayotumiwa na wafuasi wa madhehebu hii ya uzushi. Utawasikia wazushi hao wakijibatiza majina mazuri kwa mfano, Answar Sunna, Salafi Swaleh, Ahlus-Sunnah wal-Jamaa, na kwa majina hayo watu walidanganyika na kuwakumbatia Mawahabi kama ndugu, kumbe wamemkumbatia adui aliyevaa vazi la Usunni, lakini ukweli ni kwamba Mawahabi katika itikadi zao, si kwamba wanawapinga Maimamu wanne tu, bali wanampinga kwanza Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, 256

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 256

8/14/2017 1:18:41 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

halafu ndiyo wanawapinga hao Maimamu. Kisha wanamkufurisha kila Mwislamu asiyekubaliana na mitazamo yao, katika somo hili tutaonesha tofauti zao, kwa mujibu wa vitabu vyao. Majibu yetu: Waislamu wengi walihadaika na majina mazuri yanayotumiwa na wafuasi wa madhehebu hii ya uzushi. Utawasikia wazushi hao wakijibatiza majina mazuri kwa mfano, Answar Sunna, Salafi Swaleh, Ahlus-Sunnah wal-Jamaa, na kwa majina hayo watu walidanganyika na kuwakumbatia Mawahabi kama ndugu, kumbe wamemkumbatia adui aliyevaa vazi la Usunni, lakini ukweli ni kwamba Mawahabi katika itikadi zao, si kwamba wanawapinga Maimamu wanne tu, bali wanampinga kwanza Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, halafu ndiyo wanawapinga hao Maimamu. Kisha wanamkufurisha kila Mwislamu asiyekubaliana na mitazamo yao, katika somo hili tutaonesha tofauti zao, kwa mujibu wa vitabu vyao. Qur’ani Tukufu imebainisha kuwa lengo la kuumbwa kwa mwandamu ni ibada:

“Na sikuwaumba majini na watu ila waniabudu.”150

Kwa mujibu wa Aya hiyo, ukamilifu wa utu wa kila mtu hauwezi kupatikana isipokuwa kwa njia ya ibada ya kumwabudu Mwenyezi Mungu, na pasina kumwabudu Mwenyezi Mungu mtu atabakia katika daraja ya wanyama au chini ya hapo, lakini ngazi ya uwanadamu uliyokamilika hawezi kuifikia ila kwa ibada kamilifu. Na wasifu wa kwanza wa Manabii, tunaoupata katika Qur’ani, ni wao kuwa waja wa Mwenyezi Mungu, kama inavyosimuliwa katika Qur’ani Tukufu:   Dhariat; 51:56

150

257

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 257

8/14/2017 1:18:41 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

“Kutakata na mawi ni kwa ambaye aliyempeleka mja wake…..”151

Na wala Aya hiyo haikusema, aliyempeleka mbora wa Manabii, au Imamu wa Manabii, lakini neno lililotumika ni mja, kwa sababu kuwa kwake mja mwenye kumwabudu Mwenyezi Mungu ndiyo kunampandisha daraja na kumfanya awe mbora wa viumbe. Kadhalika sisi katika Swala zetu za kila siku tunasema: ..wa ashhadu an-na Muhammadan abduhu wa rasuuluhu, kwanza tunaanza na neno abduhu, yaani mja Wake kisha Rasuuluhu yaani mjumbe Wake, hiyo inamaanisha kwamba, uja ndiyo uliomfikisha Mtume kwenye daraja ya utume ambao hakuna tena utume baada yake. Kwa hiyo uhalisia wa uwanadamu hataufikia mwanadamu na wala hawezi kuwa khalifa wa Mwenyezi Mungu katika ardhi yake ila baada ya kufika ngazi ya juu katika ibada ya kumwabudu Mwenyezi Mungu. Ndiyo, ukamilifu ni zao la ibada lakini ibada haiwezi kuzaa matunda yake duniani wa akhera, ila baada ya kumfahamu huyo Mwenye kustahiki kuabudiwa, naye ni Mwenyezi Mungu. Na laiti mwanadamu atamwabudu Mungu asiyemjua, basi atakuwa sawa na mwendaji asiyejua njia itakayomfikisha aendako. Na huko ndiko Sheikh Ibnu Taimiyyah anataka watu waelekee, maana yeye anamtambulisha Mwenyezi Mungu kwa sifa ambazo si zake, na wale wote wanaomwabudu Mwenyezi Mungu kwa kufuata rai hizo za Sheikh wao Ibnu Taimiyyah basi ibada zao si sahihi kwa kuwa hawajamfahamu Mwenyezi Mungu. Ndugu yangu, ili ibada iweze kutufikisha kwenye kilele cha ukamilifu na kuonekana waja bora wa Mwneyezi Mungu, ni la  Israa; 17:1

151

258

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 258

8/14/2017 1:18:41 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

zima tumfahamu kwanza Mwenyezi Mungu. Swahaba Mtukufu Sayyiduna Ali anasema: “Mwanzo wa dini ni kumjua Yeye (Mwenyezi Mungu)”, kwa hiyo kumjua Mwenyezi Mungu ndiyo uti wa mgongo wa ibada, na bila elimu ya kumjua kwanza Mwenyezi Mungu, ibada haina maana yoyote, na ni sawa na kwenda mwendo kasi hali ya kuwa hujui njia. Kwa hiyo kadiri unavyoongeza mbio ndivyo unavyozidi kupotea zaidi, lakini kadiri elimu ya mtu ya kumjua Mwenyezi Mungu inapozidi ndivyo ibada inavyopanda thamani. Na kwa utangulizi huo tumebaini nukta mbili muhimu: 1.

Lengo la kuumbwa mwanadamu.

2.

Ibada pasina kumjua mwabudiwa ni kazi bure.

Kwa misingi hiyo yaliibuka makundi mawili yenye nadharia tofauti kuhusiana na Mwenyezi Mungu: Kundi la kwanza: Hili ni lile kundi lenye itikadi inayofuatwa na Wanachuoni wengi wa Kiisalmu, Sunni, Shi’ah, Mu’utazilah, Ashaira, Sufi, Wanafalsafa, Wanateolojia, wote hao wanaamini kwamba Mwenyezi Mungu hafanani na chochote, hana umbo na wala hana uzito wa kuchukua nafasi, na wala hana sifa yoyote inayoashiria mapungufu kwake. Kundi la pili:Hili ni kundi la wanachuoni wachache ambao idadi yao haizidi ile ya vidole vya mkono mmoja. Na sidhani kama ni sahihi kuwaita wanachuoni, kwani tutakuwa tumewavunjia heshima wale wanachuoni wa ukweli. Kwa hiyo mazungumzo yetu yatajiri katika imani ya kundi hili la pili, ili tuone itikadi zinazonadiwa na masheikh wao kwa jina la TAUHIDI je, ni TAUHIDI ile ile ya Waislamu wote? 259

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 259

8/14/2017 1:18:41 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Sheikh Ibnu Taimiyyah: Bwana huyu alipokuwa akijadili na kuzikosoa nadharia za kundi la kwanza, na ambalo ndilo kundi la Maimamu wanne, alisema: “Ama katika kukanusha, (ana kusudia kukanusha kuwa Mungu ana miguu na mikono) basi mmemkanushia Mwenyezi Mungu mambo ambayo Qur’ani haikuyatamka, wala sunnah, na wala hayakutamkwa na mmoja wa Maimamu wa Waislamu, bali hata akili huru haihukumu hivyo. Na mkasema kuwa akili imekanusha hayo, na ndipo mlipoipinga sheria kwa Bidaa. Na mkakhalifu akili huru na kusema kuwa Mwenyezi Mungu hana umbo (wala kiwiliwili) wala uzito wa kuchukua nafasi.”152 Kwa mujibu wa Sheikh Ibnu Taimiyyah ni kwamba kusema kuwa Mwenyezi Mungu hana umbo wala hana mikono na miguu, huko ni kusema kitu ambacho Qur’ani haikijui, wala Sunnah, wala Maimamu wa Waislamu. Sasa ni Maimamu gani anaowataka Sheikh Ibnu Taimiyyah tofauti na hao tuliowataja katika kundi la kwanza? Basi mpenzi msomaji hayo ndiyo mapito ya Sheikh Ibnu Taimiyyah, yeye utamsikia akisema hadithi hii haikupokelewa na Maimamu wetu wa hadithi, lakini huwa ni mwiko kwake kuwataja hao maimamu kwa majina yao, bali majina huwa anayajua yeye mwenyewe, uzushi ulioje huo! Sheikh huyu ambaye fikra zake ndizo zilizozaa Uwahabi, yeye si kwamba amepingana na Maimamu wanne tu, bali anampinga Mwenyezi Mungu na Mtume Wake pia. Kwa mujibu wa maelezo ya kitabu tulichokitaja ni kwamba Mwenyezi Mungu ni kama mwanadamu wa kawaida, yaani ana macho, uso, mikono. Anakaa kwenye kiti, na mengineyo mengi tu. Sasa itikadi kama hiyo haipo kwa Maimamu wa Waislamu. Na kama Mawahabi wataleta hoja kwa kusema kuwa mbona Qur’ani imesema kuwa Mwenyezi Mungu ana macho na mikono, basi tunawaambia wakasome kwanza   Bayan Talbis el Jahmiya, Jz. 3, uk. 44 – 45

152

260

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 260

8/14/2017 1:18:41 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

lugha ya Kiarabu, kabla ya kukurupuka na kuwatolea watu fatwa za ajabu. Qur’ani imeshushwa kwa lugha ya Kiarabu ili mpate kutafakari: Sote tunafahamu kuwa Qur’ani imekuja kwa Lugha ya Kiarabu, na Kiarabu ni lugha kama lugha nyinginezo. Kwa hiyo ni lazima lugha hiyo iwe na sarufi yake, mfumo na fasihi. Sasa unapotaka kutafsiri neno lolote, kwanza waulize wenye lugha husika, je, neno hilo wanalitumia kwa maana gani? Kwa mfano Waswahili wanapotaka kuuzungumzia ubakhili wa Idi, husema: “Idi ana mkono wa birika.” Sasa kuna uhusiano gani kati ya mkono wa birika na ubakhili wa Idi? Au nini maana ya mkono wa birika? Makusudio ya mkono wa birika, ni kwamba mtu akitaka kumpa mtu kitu hunyoosha mkono wake, sasa kwa kuwa Idi ni mchoyo, hakunjui mkono, na ndiyo maana mkono wake ukafananishwa na wa birika katika hali ya kutokunjuka. Hiyo ndio tafsiri sahihi ya ibara hiyo. Lakini Sheikh Ibnu Taimiyyah, anatafsiri maneno ya Kiarabu kwa ufahamu wake binafsi. Lakini pamoja na hayo bado ananasibishwa na elimu na maarifa, na wanamwita “Sheikh ul Islamu” yaani Sheikh wa Uislamu. Masheikh wa Kiawahabi wanapinga matumizi ya sitiari katika Qur’ani kwa hoja ya kwamba Mwenyezi Mungu hawezi kutumia lugha hiyo. Pale aliposema kuwa mikono yake imekunjuka kama angekuwa anakusudia kuwa Yeye ni mkarimu angesema wazi wazi, kwani anamwogopa nani? Kwa hiyo Aya ikisema Mwenyezi Mungu ana mkono basi makusudio ni mkono kweli, lakini Mawahabi wanasahau kwamba kabla ya ujio wa Qur’ani kwa Bwana Mtume 8. Waarabu walikuwa wakiitumia lugha yao, kwa kuzingatia misingi ya sarufi na fasihi. Sasa ujio wa Qur’ani kwa lugha hiyo si sababu ya 261

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 261

8/14/2017 1:18:41 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

kubatilisha matumizi ya sarufi na fasihi katika lugha hiyo, ila kama kuna ushahidi kwamba sarufi na fasihi haina kazi katika Qur’ani basi watuletee! Mwenyezi Mungu ana umbo: Kwa mujibu wa kitabu tulichokitaja ni kwamba Mwenyezi Mungu ni maada, na Sheikh Ibnu Taimiyyah amethibitisha kuwa kukanusha, ni kusema mambo ambayo Qur’ani haikuyatamka wala Maimamu wa Waislamu. Hivi ndio kusema kuwa Sheikh Ibnu Taimiyyah hafahamu kuwa maada ni kitu chenye uzito wa kuchukua nafasi! Na kitu chenye uzito wa kuchukua nafasi, kikiwa sehemu moja basi hakiwezi kuwa sehemu nyingine kwa wakati huo huo. Sasa Sheikh Ibnu Taimiyyah anaifahamu namna gani Aya hii:

“Na waja Wangu watakapokuuliza habari Yangu, Mimi niko karibu. Naitikia maombi ya mwombaji anaponiomba…..”153

Sasa wakipatikana waombaji wawili, mmoja akawa katika mji wa Ujiji na mwingine akawa Kondoa, halafu Mwenyezi Mungu akawa karibu na yule wa Ujiji, hapo kwa mujibu wa Sheikh Ibnu Taimiyyah ni kwamba Mwenyezi Mungu hawezi kuwa karibu na yule aliye Kondoa. Hii ndiyo picha tunayoipata katika maneno yake, yaani kama tutajenga misingi ya fikara ya kimantiki basi hitimisho ni kama hivyo. Itikadi potovu za Sheikh Ibnu Taimiyyh, zinazokinzana na itikadi za Wanachuoni wote wa Kiislamu, hasa katika mlango wa TAUHIDI, ndizo zilizosababisha awekwe gerezani na hatimaye kufia humo. Mwingine aliyepita mapito ya Sheikh Ibnu Taimiyyah ni mwanafunzi wake, Ibnu al-Kayim al-Jauziya. Yeye kwa mtazamo wake   Surat al-Baqarah; 2:186

153

262

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 262

8/14/2017 1:18:41 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

ni kwamba kila mwenye kwenda kinyume na mtazamo wake ni kafiri. Kila mwenye kukanusha kwamba Mwenyezi Mungu hana umbo, basi amemvua sifa zake, kwani Yeye anasema kuwa anaona na anasikia, na macho na masikio hayawezi kupatikana kama hakuna kiwiliwili.154 Chuki na husuda za Sheikh Ibnu Taimiyyah kwa watu wa ­nyumba ya Mtukufu Mtume 8: Chuki dhidi ya Watakatifu wa nyumba ya Bwana Mtume 8 ni moja ya itiakdi za viongozi wa Kiwahabi, na fikra hii inakinzana na fikra za wanachuoni wa Kiislamu, kwani baada ya Mwenyezi Mungu kushusha Aya ya kuwatakasa watu hao, wanachuoni wa Kiislamu waliuheshimu utakaso huo, na kuwatukuza watu wa nyumba ya Mtume 8 kwa kuzingatia kuwa ni watu waliotakaswa na Mwenyezi Mungu. Na walikuwa wakiwatanguliza kwa kila jambo, mpaka maombi yalikuwa yakifanywa kwa kupitia kwa watu hao. Na katika wanachuoni waliokuwa na mapenzi ya kweli kwa watu wa nyumba ya Bwana Mtume 8 ni Imamu Shafii (r.a). Yeye anasema katika mashairi yake: “Kizazi cha Mtume ni njia yangu na wasila wangu kwa Mwenyezi Mungu. Kwao wao kesho natarajia kupewa kitabu changu kwa mkono wa kulia.” Imamu Shafii anaendelea kusema: “Enyi watu wa nyumba ya Mtume, kuwapenda nyinyi ni faradhi kutoka kwa Mwenyezi Mungu, aliyoishusha katika Qur’ani, yatosha kwenu kuwa ni fahari kubwa ya kwamba asiyekuswalieni hana Swala.” Ndugu msomaji, hayo ndiyo maneno ya Mchamungu na Mwanachuoni mkubwa mwenye fani mbali mbali za elimu ya dini. Maneno hayo aliyasema kule Iraq, ikawa ni sababu ya yeye kuchukiwa, na watu wakakatazwa kusikiliza masomo yake, na mihadhara yake.   Sawaiq al Mursalah alal-Jahmiyyah. Jz. 3, uk. 934

154

263

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 263

8/14/2017 1:18:41 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Na kwa sababu hiyo tu alitoka Iraq na kuhamia Misri, na aliwahi hata kuzushiwa kuwa yeye ni Shia. Kauli ya Sheikh Ibnu Taimiyyah kuhusiana na watu wa nyumba ya Mtume 8: Hapa naomba msomaji atulize kichwa ili aone tofauti kati ya Mawahabi na Waislamu. Baada ya kauli hiyo ya Imamu Shafii juu ya watu wa nyumba ya Mtume 8 sasa nakupa mtazamo wa Kiwahabi. Hii ni kauli ya Imamu wao Sheikhul Islamu Ibnu Taimiyyah: “Kwa hakika kutanguliza kizazi cha Mtume (Ahlul-bayt) ni katika athari za kijahiliyyah, katika kuwatanguliza viongozi wao.”155 Huo ni mtazamo wa Sheikh Ibnu Taimiyyah. Yeye anaona kuwa kuwatanguliza watu wa nyumba ya Mtume ni katika mambo yaliyopitwa na wakati. Nini maana ya ujahiliyyah? Aliposema ujahiliyyah alikuwa anakusudia zama za kale kabla ya Uislamu. Na maisha ya watu wa kale kabla ya Uislamu yalikuwa ni maisha ya kuabudu masanamu, watu kuwanyenyekea wafalme wao hata kama ni watu waovu. Sasa Sheikh Ibnu Taimiyyah anawaambia wafuasi wake kuwa kuwatanguliza watu wa nyumba ya Mtume hayo ni mabaki ya fikra za washirikina kabla ya Uislamu. Subhanallah! Hapo ndipo utakapokubali maneno yetu kuwa Masalafi/ Mawahabi, si Waislamu japokuwa wanajificha nyuma ya tamko la shahada mbili. Mpenzi msomaji, ni ususuavu wa moyo wa namna gani huo wa mtu kuukosoa uteuzi wa Mwenyezi Mungu, na kusema kuwa ni athari za fikra zile walizokuwanazo watu kabla ya Uislamu! Mwenyezi Mungu amewachagua Mitume kizazi kwa kizazi kitokanacho na wao kwa wao, je! Mwenyezi Mungu hakufahamu kuwa kufanya hivyo ni kufuata athari za watu wa zamani waliokuwa wakifuata mila chafu kabla ya Uislamu? Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anasema kuwa:   Minhaju Suna Jz. 3, uk. 269. Minhaju sunnah Jz. 1, uk. 6

155

264

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 264

8/14/2017 1:18:41 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

“Na tukamtunukia (Ibrahim) Is-haqa na Yakub; kila mmoja tulimuongoza. Na Nuh tulimwongoza zamani. Na kizazi chake Daud na Suleiman na Ayub na Yusuf na Musa na Haruna. Na kama hivyo tunawalipa wafanyao mema.”156

Kisha akaendelea kusema katika Aya inayofuatia:

“Na Zakaria na Yahya na Isa (Yesu) na Ilyas (Elisha) wote ni katika (watu) wema. Na Ismail na Ilyasaa na Yunus na Lut; na kila mmoja tulimfadhilisha juu ya walimwengu wote. Na katika baba zao na vizazi vyao na ndugu zao. Na tukawachagua na kuwaongoza katika njia iliyonyooka.” (6:85-87).

Kwa hiyo kwa mujibu wa Sheikh Ibnu Taimiyyah, Qur’ani imetuletea mawazo ya ujahilyyah (ya zama za ujinga) kabla watu hawajaelimika, Mungu atulinde na aviepushe vizazi vyetu kutokana na ukafikri huo. Hilo ndilo kundi lenye husuda, chuki na uadui juu watu wa nyumba ya Mtume, halafu wanajinadi hadharani kuwa wao ndiyo watetezi wa Sunnah za Bwana Mtume 8. Je, huo ni utetezi   Surat An’am; 6:84

156

265

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 265

8/14/2017 1:18:41 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

wa Sunnah za Bwana Mtume 8 au ni utetezi wa Sunnah za wakuu wao wa Uingereza? Mawahabi wanawachukia mno watu wa nyumba ya Bwana Mtume, pamoja na vizazi vitokanavyo na wao, ambao ni watu tuwaitao Masayyid au Masharifu. Anasema Sheikh Muhammad Bin Abdul Wahab kuwa: “Neno Ilaahu maana yake ni Mungu na washirikina walilitumia neno hilo (Ilaahu/Mungu) kwa kuyaita masanamu yao lakini washirikina (yaani Waislamu) wa leo wanaposema Sayyid wanakuwa na maana ile ile ya washirikina.”157 Kwa hiyo kama Ilaahu kwa washirikina maana yake ni Mungu basi na neno Sayyid au Sharifu kwa Waislamu maana yake ni Mungu pia. Je, ni nani kati ya Maimamu wanne aliyeongea maneno kama hayo? Matusi yalioje hayo! Waislamu mnatukanwa kwa sababu tu mnawapenda watu wa nyumba ya Bwana Mtume 8 na vizazi vyao yaani Masharifu. Mpenzi msomaji kama umesoma bila kujaladia akili yako, bila shaka utakuwa umefahamu msimamo wa Maimamu wa Waislamu kuhusu kumfahamu Mwenyezi Mungu na sifa zake, na pia utakuwa umefahamu msimamo wa Kiwahabi, wa kuwa Mwenyezi Mungu ana mikono, miguu, anakaa juu ya kiti, na mengineyo yaliyotajwa ndani ya vitabu vyao. Hiyo ni tofauti ya kwanza inayowatenganisha Waislamu na madhehebu mpya ya Kiwahabi. Suala la Mwenyezi Mungu kuwatakasa watu wa nyumba ya Mtume 8 na kuamrisha watu kuwatii, na Wanachuoni wetu wakasalimu amri, huo ni utiifu wa hali ya juu wa kuitii Qur’ani na mafundisho ya Bwana Mtume 8. Lakini kauli ya Kiwahabi ya kusema kuwa kuwatukuza watu wa nyumba ya Mtume 8 ni mabaki ya fikra za watu wa zama za ujinga, kauli hii ya Sheikh Ibnu Taimiyyah inaashiria utovu wa nidhamu kwa Mwenyezi Mungu na   Matnu Kashfi shub-hat, uk. 8-9; Shar-hu Kashfu Shub-hat uk. 19

157

266

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 266

8/14/2017 1:18:41 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Mtume Wake, na hiyo ni tofauti nyingine inayowatenganisha Waislamu na Mawahabi. Sasa anayepingana na Mwenyezi Mungu na Mtume Wake bila aibu atashindwa kupingana na Maimamu wanne? Ndugu zangu katika utu, Sheikh Ibnu Taimiyyah alijinadi kwa jina la Salafi lakini hakuwa mfuasi wa hao Salafi wema, kama tutakavyofafanua katika somo lijalo, Mwenyezi Mungu akituwezesha.

267

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 267

8/14/2017 1:18:41 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

SEHEMU YA KUMI NA MOJA

IBNU TAIMIYYAH NA USALAFI

M

Je, Sheikh Ibnu Taimiyyah alikuwa ni mfuasi wa Salaf Swaleh?

adhehebu mpya ya uzushi na uzandiki iliyoanzishwa na Sheikh Ibnu Taimiyyah, na kuendelezwa na Sheikh Muhammad Bin Abdul-Wahab, hapo awali ilifahamika kwa jina la Salaf Swaleh, lakini hatupaswi kutosheka na jina tu, kwani mtu anaweza kustahabu kuitwa jina lolote litakalomfurahisha hata kama haliendi sanjari na matendo yake. Kwa mfano utakuta mtu anaitwa Karimu lakini kivitendo hana hata chembe ya ukarimu, sasa ndugu zangu tusihadaike na jina Salafi bali tujiulize je, Sheikh Ibnu Taimiyyah alikuwa ni Salafi kwa vitendo au jina tu? Kabla ya kujibu swali hilo, awali ya yote hatuna budi kueleza maana ya neno Salafi, kwa mujibu wa Lugha ya Kiarabu, na kwa mujibu wa makubaliano ya wanachuoni katika neno hilo. Maana ya neno Salafi: Neno Salaf katika Lugha ya Kiarabu lina maana mbali mbali lakini sisi tumechagua maana iliyokaribu na mazungumzo yetu ambayo ni “Kila aliyekutangulia katika mababu au ndugu wa nasabu. Akiwa mmoja ni Salafi, wakiwa wengi ni: Aslaaf.”158 Kwa hiyo maana ya Salafi katika Lugha ya Kiarabu ni ndugu au mababu waliotangulia. Kwa mantiki hiyo mtu akisema kuwa Aslaaf wake walitokea Kongo, hapo anakusudia kuwa babu zake walitokea Kongo, kwa hiyo yeye pia ni Mkongo asilia.   Al-Munjid chapa ya 43 Beirut 2008 Dar al Mashriq, uk. 346.

158

268

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 268

8/14/2017 1:18:41 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Maana nyingine ni: Mtu aliyekutangulia katika jambo fulani, liwe la kidini au linginelo. Kama tunavyosoma katika Qur’ani Tukufu:

“Kisha tukawafanya kuwa watangulizi na mfano kwa (watakaokuja) baadaye.”159

Hiyo ilikuwa ni maana ya neno Salaf kwa mujibu wa Lugha ya Kiarabu. Ama katika vitabu vya wanatheolojia, wanaposema Salaf, wao hukusudia wale maswahaba wema waliotutangulia katika imani. Mwanachuoni Sheikh Ja’far Subhani anasema: “Kwa hakika wapenzi wa Ibnu Taimiyyah na wenye kufuata nyayo zake, wanamsifu kwa usalafi na wanavumisha kuwa alikuwa ni mfufuaji wa madhehebu ya Salafi, kama tutajalia Salaf ni madhehebu. Lakini Salaf si madhehebu katika madhehebu za fikihi wala za kitheolojia, bali ni ibara ya mtu anayefuata mwenendo wa Maswahaba wema waliotangulia na wale waliokuja baada yao, hadi kufikia karne ya saba. Lakini rai zake (Ibnu Taimiyyah) zinakinzana na rai za hao Maswahaba wema waliotangulia (Salaf Swaleh) kwani Maswahaba wema bali na Waislamu wote hadi kufikia karne ya saba, walikuwa wakiliheshimu kaburi la Bwana Mtume 8 na kulitembelea, na katika zama hizo matembezi ya kulitembelea kaburi la Bwana Mtume 8 hayakuwahi kuwa ni chanzo cha kumuingiza mtu kwenye shirki.”160 Kwa mujibu wa Sheikh Tabriz Subhan ni kwamba hapakuwa na madhehebu ya kifikihi wala ya kitheolojia yaliyokuwa yakitambulika kwa jina la Salaf Swaleh, bali kama tulivyotangulia kusema kuwa: Salafi ni Maswahaba wema waliotangulia. Lakini tukichun  Zukhruf; 43:56   Al-Milalu wa Nihal, Jz. 4, uk. 36

159 160

269

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 269

8/14/2017 1:18:42 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

guza Mwenendo wa Sheikh Ibnu Taimiyyah tunaukuta kuwa ni tofauti na mwenendo wa Maswahaba wema na wale waliokuja baada yao, hadi kufikia karne ya saba. Kwani kipindi chote hicho Waislamu walikuwa wakifuata mila na desturi walizorithi kutoka kwa Maswahaba wema wa Bwana Mtume, na walikuwa wakiheshimu matukufu ya dini ya Mwenyezi Mungu. Kwa mfano, tukitazama mjadala uliojiri baina ya Imamu Malik na Mansur Dawaniq ndani ya Msikiti wa Mtume 8 kama ilivyosimuliwa na Ibnu Hamid, ni kwamba: “Abu Ja’far (Mansur) alijadiliana na Malik ndani ya Msikiti wa Mtume 8. Malik akasema kumwambia Mansur: Ewe kiongozi wa Waumini, usinyanyue sauti yako ndani ya Msikiti huu, kwani Mwenyezi Mungu aliwakanya watu kwa kusema: ‘Msinyanyue sauti zenu kuliko sauti ya Nabii.’161 Kisha akawasifu watu wengine akasema: ‘Kwa hakika ambao wanateremsha sauti zao mbele ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, hao ndio ambao Mwenyezi Mungu amezitahini nafsi zao kwa uchamungu. Hao watakuwa na msamaha na malipo malipo makubwa.’ Na akawashutumu wengineo, akasema: ‘Hakika ambao wanakuita nyuma ya vyumba wengi wao hawana akili.’’ Kisha Imamu Malik akaongezea kusema: Hakika heshima yake (Mtume) katika hali ya umauti ni sawa na heshima yake katika hali ya uhai wake. Basi hapo Mansur akawa dhalili, hana hoja akasema kumwambia Imamu Malik: Ewe Abu Abdillah: Je, nielekee kibla niombe au nimwelekee Mtume wa Mwenyezi Mungu 8? Imamu Malik akasema: Usigeuzie uso wako pembeni. Yeye Mtume 8 ndiye kiunganishi baina yako na Mwenyezi Mungu na ni kiunganishi baina ya Mwenyezi Mungu na baba yako Adamu hadi siku ya mwisho. Mwelekee Mtume 8 na utafute uombezi kwake, na Mwenyezi Mungu   Hujrat; 49:2 - 4

161

270

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 270

8/14/2017 1:18:42 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

anasema: ‘Na lau kwamba walipojidhulumu wengekujia wakaomba msamaha kwa Mwenyezi Mungu na Mtume akawaombea, wangemkuta Mwenyezi Mungu ni mwenye kukubali toba, mwenye kurehemu.’162 Mpenzi msomaji huo ndio ulikuwa msimamo wa Waislamu kwa kipindi chote walichoishi mpaka kufikia karne ya saba Hijiria, alipoibuka Shekh Ibnu Taimiyyah na madhehebu ya uzandiki na ya uzushi akidai kuwa yeye ni mfuasi wa Salafi Swaleh, Maswahaba wema waliotangulia... na waliokuja kufuata mwenendo wao baada yao. Lakini cha kushangaza ni pale alipoanza kuwakataza watu zile mila na desteri walizozirithi kutoka kwa Maswahaba wema. Kwa kadiri ya Sheikh Ibnu Taimiyyah, kuheshimu kaburi la Bwana Mtume 8 ni Shirki. Kumuomba Mwenyezi Mungu kupitia kwa mmoja wa waja Wake wema pia ikawa ni sawa na kuwaabudu watu hao. Kuwatukuza watu watukufu wa nyumba ya Bwana Mtume 8 ikawa ni mila za kijinga, wakati Mwenyezi Mungu ametuamuru kuwapenda watu hao: “Sema: Kwa haya siwaombi malipo yoyote kwenu isipokuwa mapenzi katika ndugu (Ahlul-Bayt).”163 Iliposhuka Aya hiyo Bwana Mtume 8 aliulizwa ni kina nani hao ndugu zako ambao ni wajibu juu yetu kuwapenda? Akasema: “Ni Ali, Fatimah J, na watoto wao.” Hadithi hii inaungwa mkono na ile iliyopokelewa kutoka kwa Ali D: “Nilimshtakia Mtume wa Mwenyezi Mungu husda za watu juu yangu. Akaniambia: Je, huridhii kuwa ni wanne katika wanne: Wa kwanza kuingia peponi ni Mimi na wewe na Hassan na Hussein na wake zetu watakuwa kuliani kwetu na kushotoni kwetu...” Na pia imepokelewa kutoka kwa Bwana Mtume 8 ya kwamba: “Pepo ni haramu kwa atakayewadhulumu watu wa nyum  Al wahhabiyat baina mabanil fikri, kutoka kitabu al- Shifaa J2/41.   Shura; 42:23 .

162 163

271

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 271

8/14/2017 1:18:42 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

bani kwangu, na akaniudhi katika kizazi changu.” Na katika hadithi nyingine Bwana Mtume 8 anasema: “Mwenye kufa na mapenzi juu ya watu wa Muhammad, amekufa shahid (kafa kifo cha kishujaa). Mwenye kufa na mapenzi juu watu wa Muhammad, amekufa ni mwenye kusamehewa. Mwenye kufa na mapenzi juu ya watu wa Muhammad amekufa ni mwenye kutubia makosa yake. Mwenye kufa na mapenzi juu ya watu wa Muhammad, amekufa ni muumini mwenye imani kamilifu. Mwenye kufa na mapenzi juu ya watu wa Muhammad, atabashiriwa pepo na malaika wa mauti. Mwenye kufa na mapenzi juu ya watu wa Muhammad, atapelekwa peponi kama apelekwavyo bibi harusi kwa mume. Mwenye kufa na mapenzi juu ya watu wa Muhammad, atafunguliwa kaburini kwake milango miwili iendayo peponi. Mwenye kufa na mapenzi juu ya watu wa Muhammad, Mwenyezi Mungu atalifanya kaburi lake kuwa ni mahala watembeleapo malaika wa rehema. Mwenye kufa na mapenzi juu ya watu wa Muhammad, amefia katika Sunnah na mshikamano.” Kisha Bwana Mtume 8 akaongezea kusema kuwa: “Mwenye kufa na chuki juu ya watu wa Muhammad, amekufa kafiri. Na mwenye kufa na chuki juu ya watu wa Muhammad, hatainusa harufu ya pepo.”164 Mpenzi msomaji! Aya tulizozitaja na hadithi tulizozitanguliza, ni mila na desturi ya kijinga kwa kadiri ya Sheikh Ibnu Taimiyyah. Sheikh huyu hakutosheka na hayo bali alichupa mipaka katika utovu wa nidhamu, na akafikia hatua ya kumfananisha Mwenyezi Mungu na viumbe Wake. Basi Mwenyezi Mungu akawa na mikono miwili, mguu, meno, macho. Anavaa nguo fupi na kadhilika. Lakini yote hayo hayakuwepo katika zama za Maswahaba wema wala Waislamu   Tafsir al Kashaf, Jz. 4, uk. 220

164

272

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 272

8/14/2017 1:18:42 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

wa baada yao mpaka kufikia karne ya saba. Watu walioishi katika kipindi hicho hawakuwa na itikadi kama hizo za Sheikh Ibnu Taimiyyah. Kama kweli Sheikh Ibnu Taymiyyah anawafuata Maswahaba wema, mbona hatujawahi kusikia kuwa Sayyiduna Ali D alikuwa akimfananisha Mwenyezi Mungu na viumbe Wake? Mbona hatujawahi kusikia kuwa Sayyiduna Ali na Maswahaba wengineo, walikuwa wakizipinga hadithi za Bwana Mtume 8 ? Ni mwenendo wa Swahaba gani huo anaoufuata Sheikh Ibnu Taimiyyah na genge lake? Maswahaba wema na Waislamu baada yao waliiamini sana Qur’ani na Sunnah za Bwana Mtume 8. Huo ndio ulikuwa mwenendo wa Salafi Swaleh (maswahaba wema) na Wasilamu waliokuja baada yao, mpaka hapo ilipodhihiri fitina mwishoni mwa karne ya saba, kama tulivyokwisha elezea toka awali. Ujio wa Sheikh Ibn Taimiyyah ulikuwa ndio chanzo cha kubadilisha Sunnah na kuzifanya kuwa ni Bidaa isipokuwa kufuga ndevu chafu zinazoambatana na vipara na kukata suruali. Hata kumlilia mtu aliyekufa pia ikawa ni Badaa, hali ya kuwa kulia ni suala la kimaumbile na haliko katika matendo ya hiari ya mwanadamu. Bwana Mtume Mwenyewe alilia kumlilia Hamza. Nabii Yakub alimlilia Yusuf miaka 40. Ila kinachokataliwa wakati wa kulia ni kutamka maneno ambayo hayamridhishi Mwenyezi Mungu, na kwa msingi huo kulia si haramu bali haramu ni hicho kitendo cha kutamka hayo maneno machafu yasiyomridhisha Mwenyezi Mungu. Ndugu zangu! Je kuna Mtume wa Mwenyezi Mungu aliyekosa huruma moyoni mwake? Je, kuna swahaba yeyote katika Maswahaba wema aliyekosa huruma moyoni mwake? Ikiwa Maswahaba wema hawakuwa na utovu wa nidhamu kwa Mwenyezi Mungu na Mitume, je huyu Imamu wa Mawahabi Sheikh Ibn Taimiyyah mafundisho aliyokujanayo ni kutoka kwenye kitabu gani? 273

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 273

8/14/2017 1:18:42 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Ndugu msomaji! Ukizitazama kwa kina itikadi za Sheikh Ibnu Taimiyyah utafahamu kuwa kwa kadiri ya Shekih huyo Maswahaba wema tunaowajua sisi ni tofauti na wale anaowakusudia yeye, kwani matendo yake yanakinzana na mafundisho ya Mwenyezi Mungu na Mitume, na yanakinzana na mwenendo wa Maswahaba wema, na yanakinzana hata na maumbile. Halafu yanakubaliana kwa asilimia zote na mafundisho ya Kiyahudi yaliyosimuliwa na makasisi wa Kiyahudi waliosilimu kwa maslahi maalumu. Makasisi hao walihadithia hadithi nyingi kutoka kwenye vitabu vya kale vya Kiyahudi. Na hadithi hizo za uongo walizisimulia kwa jina la Bwana Mtume 8, na baadhi ya Maswahaba wakazipokea kama hadithi sahihi. Kwa muhtasari labda tukutajie majina ya Wayahudi hao: 1.

Kaab bin Maati al-Himyary, maarufu kwa jina la Kaab al-Akhbaar:

Bwana huyu alikuwa ni katika wanachuoni wakubwa wa kiyahudi aliyesilimu katika zama za utawala wa Khalifa Abu Bakri K kwa maslahi yake mwenyewe. Aliingia Madina wakati wa utawala wa Khalifa Umar K na Maswahaba walipokea habari nyingi za watu wa kale kutoka kwake, na hatimaye alifariki dunia mwaka wa 34 A.H. Imepokelewa kutoka kwa Atau Bin Abi Mar’wan kutoka kwa baba yake, anasema kuwa: “Kaab aliwahi kuapa mbele yake kwa jina la Mwenyezi Mungu aliyempasulia Musa bahari, na akasema: (Kaab) Hakika sisi tumekuta imeandikwa katika Taurati ya kwamba: Daud alikuwa akisema baada ya Swala: Ewe Mwenyezi Mungu nirekebishie dini yangu ambayo umeifanya kuwa ni ngao kwangu, na unirekebishie dunia yangu ambayo umeweka maisha ndani yake. Ewe Mwenyezi Mungu najikinga na ridhaa Yako kutokana na ghadhabu Yako.”165   Al-Uluwwu ya Saqqaf uk. 22, kutoka Sunnan al-Sughra, hadithi 1346.

165

274

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 274

8/14/2017 1:18:42 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Mpenzi msomaji! Hadithi hiyo inadhihirisha uongo kwa njia mbili, kwanza kabisa uongo unadhihiri pale iliposemwa kuwa imeandikwa katika Taurat kuwa Daud alikuwa akisema kadha wa kadha, wakati Taurat ni kitabu cha Mwenyezi Mungu alichokabidhiwa Nabii Musa, na wakati huo Nabii Daudi bado hajazaliwa. Sasa Taurat iliwezaje kusimulia matendo ya mtu ambaye hajazaliwa? Lakini kama Taurat ingesema kuwa atazaliwa mtoto ambaye ataitwa Daudi, halafu mtoto huyo akikua, baada ya Swala zake atakuwa anasema kadha wa kadha, hapo tungesema huo ni utabiri. Lakini kusema alikuwa anasema kadha wa kadha, wakati Daudi mwenyewe bado hajazaliwa, huo ni uzushi wa ajabu. Pili habari hiyo ni katika hadithi zinazoelezea desturi na mwenendo wa maisha ya Manabii. Kwa hiyo Mwenyezi Mungu asingeweka maombi ya Daudi baada ya Swala ndani ya Taurat, kwa sababu maisha ya Daudi yangefaa kuandikwa na Maswahaba wake baada yake na siyo ndani ya kitabu cha Mwenyezi Mungu. Na mfano hai ni dua alizokuwa akiomba Bwana Mtume 8 baada ya kila Swala, hazikuandikwa ndani ya Qur’ani bali dua na matendo yote ya Bwana Mtume 8 kama vile kupiga mswaki, kutembelea wagonjwa, majirani na kadhalika yote utayapata kwenye vitabu vya hadithi na vitabu vya historia ya maisha yake na siyo ndani ya Qur’ani.166 2.

Abdul-Karim bin Abil-Aujaa:

Bwana huyu alijitahidi naye kuingiza hadithi za kuchonga ndani ya vitabu vya Waislamu, na mpaka siku alipohukumiwa kifo, alisema: “Hata mkiniua ni kazi bure kwani nimeshaingiza kwenye vitabu vyenu hadithi elfu nne (4,000) za uongo.”167   Al-uluwwu ya Sayyed Saqqaf uk. 23   Bidaayat al Ma’arifah, uk. 43.

166 167

275

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 275

8/14/2017 1:18:42 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

3.

Wahb bin Munabbihu al-Swan’ani 34 – 114 A.H:

Bwana huyu alikuwa ni mtaalamu wa vitabu vya kale, na fundi wa kutunga visa vya kufikirika (visa dhahania), hususan visa vya Kiyahudi, alikuwa akisema kuwa: “Nimesikia vitabu 92 vyote vimetoka mbinguni, 72 katika hivyo viko makanisani, na 20 viko mikononi mwa watu, na wanaovijua ni wachahe.” Na katika hadithi alizoingiza Wahb ni ile isemayo kwamba: “Hakika mbingu na bahari viko kwenye hekalu, na hekalu liko kwenye kiti cha enzi, na miguu ya Mwenyezi Mungu iko juu ya kiti, na kiti kikabaki kama ndala miguuni mwake (Mwenyezi Mungu).” Hebu angalia jinsi Mwenyezi Mungu anavyofananishwa na mwanadamu, katika suala la kuwa na miguu na ndala miguuni au mfano wa ndala. Sasa hadithi kama hiyo inakinzana na mafundisho ya Kiislamu yaliyoletwa kwetu na makhalifa waongofu kutoka kwa Bwana Mtume 8 Kwa hiyo ni dhahiri kwamba Wahab alinakili mafundisho hayo kutoka kwenye vitabu vya imani tofauti na ya Kiislamu, kama ilivyo katika kitabu cha Mtakatifu Mathayo: “Usiape kwa mbingu kwani ni kiti cha enzi cha Bwana Mungu wako, wala kwa nchi maana ni mahala pakuwekea miguu ya Bwana Mungu wako.” Ndugu wapendwa! Huu ni mfano tu wa baadhi ya Wayahudi waliosilimu na kuanza kuingiza mafundisho ya Kiyahudi ndani ya Uislamu. Kama ni kweli walikinaika kwa hoja kuwa Uislamu ndio dini sahihi na Uyahudi ni batili, kulikuwa na haja gani tena ya kutwaa mafundisho ya dini batili na kuingia nayo kwenye Uislamu? Hapo bila shaka utakubaliana na maneno yetu kuwa makasisi hao hawakuwa na lengo zuri bali waliingia katika Uilsamu ili waweze kuufisidi kwa njia kama hiyo. Na fikra yoyote inapoelezwa mbele za watu ni lazima ipate wafuasi hususan pale inapoelezwa mbele ya watu wasiokuwa na uelekevu wa kutosha. Sasa baada ya maelezo 276

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 276

8/14/2017 1:18:42 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

yote tuliyoyatanguliza hebu tumuangalie Sheikh Ibnu Taimiyyah kama tutamkuta japo na harufu ya usalafi kama alivyodai, na madai yake yakaendelezwa na wanafunzi wake. Tathmini: Tumeelezea kwa mapana maana ya neno Salafi katika Lugha ya Kiarabu na kwa kadiri ya wanachuoni wa theolojia. Na tukaelezea itikadi, desturi na mwendo wa hao watu tunaowaita Salafi, na maisha ya kiitikadi ya Waislamu walioishi baada yao. Yote hayo tumeyafafanua na tukaona kuwa ni watu waliokuwa na heshima kubwa kwa Bwana Mtume 8. Lakini tulipoangalia mwenendo wa makasisi wa Kiyahudi walioingia Uislamu, tuliukuta unakinzana na mafundisho ya Uislamu wa Bwana Mtume 8 kwa kuwa wao waliingiza hadithi nyingi za kumfananisha Mwenyezi Mungu na viumbe Wake. Sasa cha kusikitisha na cha kuliza ni pale alipoibuka Sheikh Ibnu Taimiyyah na itikadi zilezile za Kiyahudi. Wayahudi katika imani zao hawamuheshimu Bwana Mtume 8 na wala hawautambui utume wake. Na kwa kadiri ya Sheikh Ibnu Taimiyyah Bwana Mtume ni mtu wa kawaida tu, na wala hastahiki heshima zote tunazompatia. Na kwa msingi huo aliwakataza wafuasi wake kwenda kulitembelea kaburi la Bwana Mtume 8 na kuwaheshimu watu wa nyumbani kwake, kwa madai ya kuwa hayo ni mabaki ya zile mila za kishenzi za watu wa kale walioishi kabla ya Uislamu, kama tulivyofafanua katika masomo yaliyopita.168 Sheikh Ibnu Taimiyyah hakutosheka na hayo bali alimkufurisha kila anayekwenda kinyume na mitazamo yake. Kilichonenwa kwa midomo mitukufu ya Bwana Mtume 8 kuwa ni Sunnah, basi kwake ilikuwa ni shirki na Bidaa. Na kubwa zaidi ni ile itikadi yake   Minhaju Sunna

168

277

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 277

8/14/2017 1:18:42 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

ya kumfananisha Mwenyezi Mungu na wanadamu, na hapo ndipo Waislamu walipogundua kuwa Sheikh Ibnu Taimiyyah ni balozi wa Kiyahudi ndani ya Uislamu. Kwa kuwa ile itikadi ya Kiyahudi ya kusema kuwa Mwenyezi Mungu ana miguu, anakaa kwenye kiti, anapatikana baadhi ya maeneo, na Sheikh Ibnu Taimiyyah naye pia alikuwa akiifuata itikadi hiyo na kuiamini. Kwa bahati nzuri wanachuoni wa zama hizo walikuwa makini, kwa hiyo walifanya kazi ya ziada ya kuandika na kuhubiri ili kuwabainishia Waislamu upotovu huo, na walifanikiwa kwa kiasi kikubwa. Kama tulivyosema kuwa kila nadharia ni lazima ipate wafuasi, Sheikh Ibnu Taimiyyah na yeye pia alipata baadhi ya wajinga wenzake wa kumuunga mkono, kama vile Ibnu Al-Qayyim al-Jawziyyah na wanafunzi wengine wachache. Na hapo hali ilitulia kidogo hadi kufikia karne ya kumi na mbili, ndipo ilipoibuka fitina huko katika nchi ya Najd kwa kuzaliwa Sheikh Muhammad Bin Abdul-Wahab. Bwana huyu hakuwa na jipya bali aliendeleza fikra za Kiyahudi zilizoachwa na Imamu wake Sheikh Ibnu Taimiyyah, na kuanzia karne hiyo wafuasi wa fikra hizo za Kiyahudi waliitwa Wahhabiyyah. Lakini kutokana na ususuavu wa moyo aliokuwa nao Sheikh Muhammad Bin Abdul-Wahab, na utovu wake wa nidhamu kwa Mwenyezi Mungu hadi kwa wazazi na waalimu wake, jina Wahhabiyya lilipoteza haiba yake katika jamii, na badala yake wakajiita Answar Sunnah ili kuficha maovu yao na utovu wao wa nidhamu. Ndugu msomaji, naamini kuwa mpaka hapa utakuwa umefahamu itikadi na mwenendo wa Maswahaba wema (Salaf Swaleh) na pia mwenendo wa Waislamu waliokuja baada yao hadi kufika karne ya saba. Hakuna yeyote aliyemvunjia heshima Bwana Mtume 8 na watu wa nyumbani kwake, na wala hakuna yeyote kati yao aliyemkosea adabu Mwenyezi Mungu na kumfananisha na viumbe Wake. Bali yote hayo kama tulivyokusimulia ni katika zile 278

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 278

8/14/2017 1:18:42 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

itikadi za Kiyahudi zilizoletwa na Mabwana tuliowataja. Sasa kwa mwenendo na itikadi za Sheikh Ibnu Taimiyyah je, ni halali kumwita kuwa ni mfuasi wa Maswahaba wema, yaani Salafi Swaleh? Je, hao Maswahaba wema amewafuata katika lipi? Je, Maswahaba wema walikuwa wanawagawa Waislamu? Je, Maswahaba wema walikuwa ni watovu wa nidhamu? Je, walikuwa wanamfananisha Mwenyezi Mungu na wanadamu? Ndugu zangu katika utu hivi hamuoni kuwa huo ni Uyahudi ndani ya Uislamu? Je, hamuoni kama Maswahaba wema kwa mujibu wa Sheikh Ibnu Taimiyyah ndio hao makasisi tuliowataja? Bila shaka ndugu zangu mtakubaliana na sisi kuwa Maswahaba wema waliokusudiwa na Sheikh Ibnu Taimiyyah ni hao makasisi wa Kiyahudi tuliowataja kwa majina, na wala si wale wanaojulikana kwa Waislamu wote. Ndugu mpendwa! Je, uko tayari kuwaita wafuasi wa makasisi wa Kiyahudi kuwa ni Salafi Swaleh (wafuasi wa Maswahaba wema)? Ndugu zangu kwa hakika wafuasi wa Sheikh Ibnu Taimiyyah wana tabia ya kuficha upotovu wao kwa majina mazuri, na ndio maana wamekuwa wakijibatiza majina kila kukicha. Kama tulivyokueleza kuwa madhehebu ya uzushi ya Sheikh Ibnu Taimiyyah iliyoficha upotovu wake nyuma ya mgongo wa Salafi Swaleh (maswahaba wema waliotangulia) haikudumu na badala yake aliibuka Sheikh Muhammad Bin Abdul-Wahab na kuifufua madhehebu hiyo mnamo karne ya kumi na mbili. Lakini ndani ya karne hiyo ilitambulika kwa jina Al-Wahhabiyyah lakini utoafauti ni wa jina tu, ila itikadi ni zilezile za Sheikh Ibnu Timiyyah. Na jina hilo pia baada ya kukosa haiba waliamua kujiita Answar Sunnah. Na jina hili pia nalo lilipoteza haiba yake kutokana na matendo yao machafu, kwa hiyo wakaanza kujificha nyuma ya mgongo wa Ahlus-Sunnah. Lakini jina hili liliwaumbua haraka kwa kuwa wenye jina hili ni wapenzi wa Bwana Mtume 8 na wanamuheshimu ipasavyo. 279

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 279

8/14/2017 1:18:42 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Wao wanafanya maulidi za kumsifu Bwana Mtume 8 kila mwaka kwa mapenzi makubwa na kwa gharama kubwa. Sasa wao baada ya kujitwisha jina hilo wakasema kuwa maulidi ni shirki na ni Bidaa. Hapo Waislamu wenye maarifa wakashtukia na ndipo walipoamua kurejea tena kwenye kichaka chao cha zamani, yaani kujiita kwa jina Salafi Swaleh. Lakini pamoja na hivyo bado wanaendelea kulitumia jina la Ahlus-Sunnah, hususan pale wanapokutana na Ahlus-Sunnah wasiojitambua, hapo utawasikia na wao pia wakijiita Ahlus-Sunnah. Lakini wakikutana na Ahlus-Sunnah wanaojitambua basi hapo utawasikia wakijiita Salafi Swaleh. Ndugu zangu msidanganyike na jina bandia la Salafi Swaleh, kwani wanaotambulika kwa jina hilo ni wale Maswahaba wema waliotangulia. Sasa wao wanafuata Maswahaba wema katika jambo gani? Kama ni ukatili basi Maswahaba walikuwa katika kilele cha utu na ukarimu ndio maana wakaitwa masahaba wema. Kama ni katika uvaaji wa vizibao wakati wa joto basi Maswahaba wema hawakuwahi kuvaa vizibao wakati wa joto wala wakati wa baridi. Na kama ni kucheza karate msikitini basi Maswahaba wema hawakuwahi kucheza karate msikitini hata siku moja, bali wao waliuheshimu msikiti kama nyumba ya ibada. Na wala Maswahaba wema hawakuwahi kuwa na ndevu chafu wala kuvaa vipande vya suruali, na wala hawakuwahi kuweka mikasi ndani ya misikiti kwa ajili ya kukata kanzu na suruali za watu bila ridhaa zao. Ndugu zangu hivyo ni vituko vilivyoibuka mnamo miaka ya 1970 kwenda mbele. Muhtasari: ď ś Salafi katika Lugha ya Kiarabu, ni mababu waliotangulia. Au ni watu waliotangulia, ambao waliokuja nyuma yao huwafanya kama dira yao. Lakini Wanachuoni wa Kiislamu wanaposema Salafi huwa wakimaanisha Maswahaba wema waliotangulia am280

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 280

8/14/2017 1:18:42 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

bao hawakwenda kinyume na mafundisho ya Mwenyenyi Mungu na Mtume wake 8.  Waislamu waliofuata nyayo za Maswahaba wema, walikuwa wakiheshimu na kulinda matukufu ya dini kwa hali na mali mpaka kufikia karne ya saba A.H.  Maswahaba wema na Waislamu baada yao hawakuwahi kuamini kuwa Mwenyezi anafanana na viumbe Wake, kwani imani ya kumfananisha Mwenyezi Mungu na viumbe ni imani ya Kiyahudi iliyoletwa na makasisi tuliowataja, na ambao walisilimu kwa malengo mahususi.  Sheikh Ibnu Taimiyyah na wafuasi wake wote wa zamani na wa sasa sio wafuasi wa Maswahaba wema, bali ni wafuasi wa nadharia za Kiyahudi zilizoletwa na makasisi, Kaab al-Akhbaar, Abdulkarimu Bin Abil-Aujaa, Wahb Bin Munbbihu al-Swan’ani na kadhalika. Waislamu msidanganyike na majina mazuri yanayotumiwa na wahalifu wa Kiwahabi, ili kutimiza azma yao ya kufisidi madhehebu na dini kwa jumla. Ndugu zangu haifai kwa Mwislamu kutumia jina Salafi katika kuwaita waharibifu wa dini.

281

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 281

8/14/2017 1:18:42 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

SEHEMU YA KUMI NA MBILI

ATHARI ZA KALE Mawahabi na uondoshaji wao wa ushahidi wa kihistoria:

K

ila mwanadamu ana matukio aliyoyafanya katika maisha yake, na ambayo anafanya bidii ya kuyatunza kwa matumizi ya baadaye. Kama matukio yale yatakuwa ni mabaya basi atayatumia kama somo la kuwatahadharisha wengine na njia hiyo mbaya, na yakiwa ni matukio mazuri basi vilevile atayatumia kama kigezo cha kuhamasisha watu kupita njia hiyo aliyoipita yeye. Kwa kadiri ya imani yetu ni kwamba kila mfumo sahihi katika jamii ni lazima uanzie ndani ya mtu mwenyewe katika uwenyewe wake, kisha uhamie katika ngazi ya familia na hatimaye kwa jamii nzima. Halikadhalika suala la kutunza matukio ni suala la kimaumbile na linaanzia kwa mtu binafsi, kisha familia, na hatimaye kuenea katika jamii nzima. Na ndio maana tunakuta kila mtu ana historia yake binafsi, pia wana familia wana historia ya familia yao, na wana jamii wana historia ya jamii zao. Familia yenye kutunza historia yake ni familia hai, na jamii yenye kutunza historia yake ni jamii hai. Kwa mantiki hii suala la kujenga majumba ya makumbusho ni la enzi na enzi na hata mababu walilikuta. Labda ni kuulize wewe mpenzi msomaji, hivi ni nchi gani unayoifahamu iliyokosa jumba la makumbusho? Bila shaka jibu ni hakuna nchi isiyokuwa na makumbusho. Sasa iweje leo wazuke watu na vikanzu vyao vifupi na kutwambia kuwa suala hilo ni Bidaa? Na kama ni Bidaa au shirki hukumu hiyo ni hukumu kwetu tu? Mbona huko Saudia wanatunza historia ya utawala wa mabavu wa Kiwaha282

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 282

8/14/2017 1:18:42 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

bi, ikiwa ni pamoja na kuadhimisha matukufu yake? Mbona Mawahabi wamelifumbia macho suala hilo na hawasemi kuwa ni shirki, ambapo huko ndio chimbuko lao na kwa wakubwa zao? Historia ni moja ya njia za kueneza utamaduni wa jamii husika, na ni utambulisho wa jamii hizo mbele ya jamii zinginezo, hususan zile za kimataifa. Umma wowote uliopoteza historia yake ni sawa na mtoto aliyepoteza wazazi kisha akawa hajui chimbuko lake, bali ni sawa na mti uliokosa mizizi. Na kwa mantiki hiyo serikali nyingi duniani zimekuwa zikiandaa bajeti maalumu kwa ajili ya suala hili la utunzaji wa athari za kihistoria, na mpaka vimejengwa vyuo kwa lengo hilo na utunzaji wa athari za kale ukawa ni moja ya taaluma ambazo watu wanazisomea. Na hii inaonesha wazi kuwa suala hili ni zaidi ya muhimu. Hapana shaka kuwa utamaduni wa Kiislamu ni utamaduni mpana mno na wenye historia ndefu. Na inasimuliwa kuwa ulianza sanjari na Bwana Mtume 8 kukabidhiwa utume bali sanjari hata na kuzaliwa kwake. Kisha utamaduni huo ni endelevu kupitia mikononi mwa Maswahaba wema waliofuata nyao za Bwana Mtume 8 na wakafanya jitihada kubwa katika uwanja huu kwa kipindi kirefu. Kumbukumbu za kihistoria na majengo yanayofungamana na Bwana Mtume 8 na Maswahaba wake wema vyote hivyo ni sehemu ya urithi wa kiutamaduni kwa umma wa Kiislamu, na siyo miliki ya ukoo fulani au mtu fulani ili aweze kuwa na haki ya kutumia hazina hizo za umma kwa namna atakavyo au apendavyo. Bali ni miliki ya umma mzima wa Kiislamu na ni miliki ya ubinadamu kwa jumla. Kwa hiyo hakuna haki kwa yeyote yule awe mtu binafsi au serikali, kufanya maamuzi yoyote katika urithi huo bila ridha ya Waislamu, kama ambavyo tumekuwa tukishuhudia leo hii kumbukumbu muhimu zinabomolewa ikiwa ni pamoja na makaburi ya Manabii wa Mwenyezi Mungu. Kumbukumbu kama hizo zinapotezwa na 283

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 283

8/14/2017 1:18:42 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Mawahabi kwa kisingizio cha kulinda tauhidi!! Na kwa kaulimbiu hiyo wamedanganya wengi hususan wale wasiokuwa na maarifa ya kutosha katika dini. Na hili ni tatizo kubwa linalozikabili jamii zetu. Watu wanapewa maneno kama vile Bidaa, tauhidi, shirki, kisha na wao wanayapokea na kuyafanyia kazi bila ya kuhoji kwa kina maana sahihi ya maneno hayo. Historia yatwambia kuwa Bwana Mtume 8 alizaliwa mnamo mwaka 570 A.D, na kutangazwa rasmi kuwa Mtume baada ya kutimiza miaka 40. Baada ya kupewa utume alikaa Makkah miaka kumi na tatu 13 akifanya kazi ya kufikisha ujumbe na kuilingania dini ya Mwenyezi Mungu. Kisha akafunga safari na kuelekea Madina ambako alikaa miaka kumi. Alimtumikia Mwenyezi Mungu na kutoa huduma mbali mbali za kijamii na kupambana na washirikina kwa ajili ya kuihami dini. Hii ilikuwa ni harakati adhimu, ambayo kwamba watu walijitolea muhanga na damu zikamwagika kwa ajili ya dini tukufu ya Kiislamu. Mwaka wa kumi na moja Hijiria, Bwana Mtume 8 aliitika wito wa Mwenyezi Mungu, lakini bendera ya Uislamu ilibakia kuwa ni yenye kupepea na kuenea katika maeneo mbalimbali ya Rasi ya Uarabu na miji mingineyo ya ulimwengu. Athari na kumbukumbu zinazohusiana na maisha ya Bwana Mtume 8 na watu wa nyumbani kwake na Maswahaba wake wema, ndio jiwe la msingi la utamaduni wa Kiislamu, utamaduni ambao hauna budi kuzingatiwa kama ishara ya uwepo wa kusadikika kwa Uislamu, na ni wajibu kuulinda utamaduni huo kwa gharama yoyote ile na kuuepushia kila aina ya hatari inayoukabili. Kusadikika kwa historia ya kiislamu: Tukio lolote linapotokea katika jamii huwa ni lenye kusadikika kwa wale waliolishuhudia. Lakini kwa kadiri zama zinavyosonga mbele ndivyo linavyozidi kupoteza ile hali ya kusadikika kwake kidogo 284

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 284

8/14/2017 1:18:42 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

kidogo, mpaka kufikia hatua ya tukio hilo kuonekana kwa baadhi ya vizazi kuwa ni la kufikirika, yaani halijawahi kuwa na uwepo wa kweli. Sasa ili kuyalinda matukio hayo yasionekane kuwa ni ya kufikirika ni lazima athari zake zilindwe kwa ajili ya vizazi vijavyo, hususan tunapozingatia kuwa Uislamu ni dini ya mwisho na dini kamilifu, na Qur’ani ndio Katiba ya mwisho katika mtungo wa katiba za kiungu na yenye kudumu na kwenda sanjari na maisha ya mwanadamu, ili kumpatia mwongozo mpaka mwisho wa uhai wake. Na hakuna shaka kuwa itakuwa ni rahisi kwa vizazi vijavyo kufuata ujumbe wa Uislamu utokanao na mfereji wa chemchemu ya ufunuo wa kiungu, endapo watapata yakini juu ya kusadikika kwa ujumbe huo na uhalisia wake. Sisi hatuna shaka kuwa moja ya mambo yawezayo kuhifadhi ujumbe wa Mwenyezi Mungu, usuli wake na kusadikika kwake na kuishamirisha mizizi yake ni kutunza athari zinazohusiana na maisha ya Bwana Mtume 8 uongozi wake na harakati zake za kijamii na zile za kijeshi. Na kwa msingi huo, kutunza kumbukumbu za kihistoria kunaizidishia sheria ya dini yetu hali ya kusadikika, hususan mbele ya wale wasiokuwa na imani ya Kiislamu. Au mbele ya wale wenye shaka juu ya usahihi wa imani hiyo pamoja na shaka juu ya mapambano ya umma katika kuuhami Uislamu. Na kwa sababu hiyo wanachuoni wetu walijitolea kwa hali na mali katika kuhifadhi kumbukumbu za kihistoria ili kuzifikisha kwa uaminifu kwa vizazi vilivyopo salama salimini. Sasa leo ukiona mtu anaondosha kumbukumbu ambazo wanachuoni walizilinda kama amana yenye thamani kubwa ili zitufikie zikiwa salama, mtu kama huyo usimuweke katika kundi la Waislamu bali muone mithili ya chui aliyevaa ngozi ya kondoo. Juhudi na huduma zilizofanywa na wanachuoni katika kuhifadhi kumbukumbu za matukio ya kihistoria zilikuwa na athari kubwa 285

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 285

8/14/2017 1:18:42 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

katika kuufanya Uislamu uonekane kuwa ni dini yenye uwepo wa kusadikika na siyo uwepo dhahania. Na kwa kutumia athari hizo za kihistoria Waislamu wanaweza kuizungumzia dini yao ya Uislamu na kuwalingania wengine bila ya hofu na pia wanaweza kuongea na ulimwengu kwa ujasiri na kuuambia kuwa: Katika nchi ya Hijjaz kuna mtu alipewa utume, mnamo miaka 1400 iliyopita kwa lengo la kuongoza jamii ya wanadamu, na alipata ushindi katika kipindi cha miaka ishirini na tatu, ambayo tunaweza kuigawa katika mafungu mawili, fungu la kwanza ni ile miaka kumi na tatu aliyokaa Makkah na fungu la pili ni ile miaka kumi 10 aliyokaa Madina. Sasa endapo ulimwengu utataka ushahidi zaidi basi sisi tutawaonesha kuwa, nyumba hii ndio mahala alipozaliwa Mtume wetu, na huu ndio msikiti wake, na hii ndio nyumba aliyozikwa ndani yake, na hizi ndizo nyumba za wake zake. Na alikuwa akifanyia ibada zake katika pango hili kabla ya utume, na ufunuo wa kiungu (wahyi) ulimshukia pangoni hapo akiwa na umri wa miaka arubaini, na hapo ndipo zilipoanza harakati za Kislamu, watu wakamwamini na wengine wakampinga. Bwana Mtume 8 alipata upinzani mkali katika nyanja za kisiasa, kijamii, na kiuchumi. Mazingira yakawa magumu na kumlazimu kutobakia mjini humo na kuhamia katika mji wa Yathriba ambao baadaye ulifahamika kama Madinat Rasul (Mji wa Mtume 8). Bwana Mtume 8 aliendeleza harakati mjini humo, lakini alipokuwa njiani kuelekea huko, alijificha katika pango la Thaur (Ghar Thaur) lililoko kusini mwa mji wa Makkah. Na alipoingia Madina alipokelewa na watu wa Kabila la Ausi na Khazraj. Mjini Madina aliweza kuanzisha Dola ya Kiislamu, na huko pia alipambana na Mayahudi na Washirikina, na watu wengi walikufa kishujaa katika vita mbalimbali kama vile Badri, Uhud, Khaibar, Hunain, hiyo ni kwa upande mmoja. 286

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 286

8/14/2017 1:18:42 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Lakini tukitazama upande wa pili wa shilingi tunakuta kuwa Bwana Mtume 8 aliagiza watu kwenda maeneo mbali mbali ya Rasi ya Uarabu kupeleka ujumbe wa nadharia ya kuabudu Mungu mmoja na kuacha shirki, na baada ya kukamilisha jukumu lake hilo kwa usahihi zaidi. Na mnamo mwaka wa kumi na moja 11 H.A. Bwana Mtume 8 aliitika wito wa Mwenyezi Mungu na bendera aliyoisimika ilipokelewa na watu wa nyumbani kwake, pamoja na Maswahaba wema. Wote hao kwa pamoja walifuata nyayo zake na kupita mapito yake, katika kueneza mafundisho ya Qur’ani katika pande zote za dunia. Mpenzi msomaji! Historia kama hiyo inayoambatana na ushahidi uonekanao, bila shaka inaufanya Uislamu kuwa ni dini yenye uwepo wa kweli, na kwamba Bwana Mtume Muhammad 8 ni mtu mwenye uwepo wa kusadikika, kwa sababu tu, watu wanaona mabaki ya historia yake kama vile nyumba yake, kaburi lake na mengineyo. Sasa tukiondosha athari hizo tutakuwa tumeondoa vishiario na ushahidi wa uwepo wake wa kweli. Na kwa upande mwingine wa sarafu tutakuwa tumewaandalia maadui wa Uislamu mazingira mazuri ya kusema walitakalo na hata kama wakisema kuwa Muhammad alikuwa ni mtu dhahania au wa kufirika hatutakua na hoja ya kuvunja madai hayo kwa sababu ya kutokuwepo na kiashirio hata kimoja kinachoashiria juu ya uwepo wa Bwana Mtume Muhammad 8 na watu wa nyumbani kwake na Maswahaba wake. Ndugu zangu kubomoa athari za Kiislam ni vita dhidi ya Bwana Mtume 8 inayopinga mizizi ya utume wake na viashirio vya dini yake tukufu. Hakika Uislamu ni dini hai, na inayodumu milele na itabakia kuwa ni dini ya wanaadamu wote mpaka siku ya mwisho. Na vizazi vijavyo havina budi kutambua na kukiri juu ya uasilia wa dini hii na utukufu wake. Na ili kufanikisha hilo tunapaswa kutunza athari za matukio ya historia ya Bwana Mtume 8 ili tuwe 287

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 287

8/14/2017 1:18:42 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

tumepiga hatua katika kuendeleza na kuidumisha dini hii milele kwa ajili ya vizazi vijavyo, na ili tusifungue mlango kwa yeyote kuja kuutilia shaka Uislamu na ujumbe wake kwa kutokuwepo na ushahidi wa kihistroria na hatimaye Uislamu kuonekana kuwa ni dini ya kubuni na ya kufikirika. Waislamu wamelipa kipao mbele suala la kutunza historia ya Mtume wao mpaka wakafikia hatua ya kusajili kila alichokifanya Bwana Mtume 8 katika maisha yake binafsi, na kila kinachohusiana naye, kama vile pete yake, viatu vyake, mswaki wake, upanga wake, ngao na mkuki wake, farasi wake, ngamia wake, ‌ na mpaka visima ambavyo aliwahi kunywa maji yake na maeneo aliyoyatoa wakfu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, bali hata chakula alichokuwa akipendelea zaidi kutumia. Na hata ndevu zake alikuwa akizitunza namna gani na mengineyo mengi. Sehemu kubwa ya kumbukumbu hizo bado zipo hadi leo hii.169 Ulimwengu wa majaribio: Mwanadamu ni mwepesi mno wa kufahamu yale yanayopatikana kwa kutumia njia tano za fahamu, ambazo ni kuona, kusikia, kugusa, kunusa, kuonja. Ukiona mtoto anaogopa moto ni kwa sababu aliwahi kuushika na akaungua, au alishuhudia kwa macho yake mtu akiungua na baada ya hapo akapata yakini kuwa moto ni hatari. Na mtoto hawezi kufahamu madhara ya wembe mpaka pale utakapomkata, na namna hii ndivyo njia za ufahamu zinavyofanya kazi ya kumletea mwanadamu ufahamu juu ya mambo mbalimbali yanayohusiana na njia hizo. Na kwa msingi huohuo mwanadamu huamini sana kile anachokiona kuliko kile anachokisikia (Kusadiki kwa Toma ni kuona). Kwa hiyo njia bora zaidi ya kumfanya mwanadamu ayaamini kwa   Al-Wahabiyya baina Mabani Al-fikr kutoka Tabakat Al-Kubra Juz. 1, uk. 360-506.

169

288

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 288

8/14/2017 1:18:42 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

wepesi yale anayoambiwa ni kuwepo maeneo rasmi ya kuhifadhia athari za matukio ya kale, na maeneo ya matukio yawekewe alama ya kumbukumbu kwa ajili ya kuwaelimishia wale watakaokuja baadaye na hapo bila shaka maelezo watakayopewa yatawakinaisha kwa kuwa yameambatana na ushahidi wa athari za watu hao waliotangulia. Kwa mfano ukimwambia mtoto kuwa babu yake alikuwa na kichwa kikubwa halafu ukamuonesha na kofia aliyokuwa akiivaa babu huyo, hapo mtoto ataamini bila ubishi, kwa sababu tu maelezo yameambatana na ushahidi unaoonekana. Leo hii watu wa jamii zilizopatwa na balaa la mauaji ya kimbari (Genocide) waliathirika sana na mandhari hiyo ya kinyama na ya kutisha. Lakini ili kuibakisha athari ile, walihifadhi mifupa ya wafu wao na mafuvu yao kwa ajili ya vizazi vijavyo, ili nao wapate kujifunza kupitia tukio hilo lililotokea kabla yao. Mwenyezi Mungu anasema:

“Kwa hakika katika simulizi zao mna mazingatio kwa wenye akili…..”170

Tukiichunguza historia ya sheria za kiungu zilizopita tutakuta kuwa Bwana Masihi (Yesu) ni mfano hai wa haya tunayoyasema. Lakini ni katika mambo yasiyokuwa na shaka kwetu, kwamba sisi Waislamu kupitia Qur’ani na mafundisho ya Bwana Mtume 8 tunaamini juu ya uwepo wa kweli wa Bwana Masihi (Yesu), na tunaamini kwa kina kuwa Yeye ni mwendelezo wa mtungo mrefu wa Manabii waliotangulia, na hatimaye kuishia kwa Mtume Muhammad 8. Na kwamba Yeye Masihi (Yesu) alikuja na mwongozo kwa watu wake kupitia kitabu chake cha Injili.   Surat Yusuf; 12:111

170

289

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 289

8/14/2017 1:18:42 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Lakini cha kusikitisha ni pale tunapowakuta vijana wa Kimagharibi, kwa kutoifahamu kwao Qur’ani ufahamu sahihi, na kutoamini kwao Uislamu kama dini sahihi aliyokuja nayo Bwana Mtume Muhammad 8 na inayoweza kutoa picha sahihi na ya kweli ya Manabii waliotangulia, akiwemo Bwana Masihi - Yesu D, vijana hao kwa kutoamini hivyo leo hii tunawaona wakimwangalia Bwana Masihi (Yesu) kwa mtazamo wa shaka, na si kwa sababu nyingine bali ni kwa sababu ya kutokuwepo na kumbukumbu yoyote katika yale aliyokuja nayo. Hakuna kitabu hata kimoja ambacho wao wanakubaliana kuwa ndio kitabu kilichoachwa na Bwana Masihi (Yesu), bali kinyume chake wanaambiwa kuwa Biblia iliandikwa na watu arubaini (40). Na kila mmoja kati yao ananasibisha maandiko yake na Bwana Masihi (Yesu). Luka hakuwa katika orodha ya wanafunzi wa Bwana Yesu, na wala hakumuona lakini naye pia ana nasibisha maandiko yake na Bwana Yesu. Hakuna kaburi linalosadikika kuwa ni la Bwana Yesu wala la mama yake. Sasa kwa hali kama hii ni lazima kwa vijana wa Kikirsto hususan katika nchi za Magharibi wawe na shaka juu ya uwepo wa kweli wa Bwana Yesu pamoja na mama yake. Kwa msingi huo ni lazima tujifunze kupitia historia hiyo ya Bwana Yesu na tujitahidi kwa gharama yoyote iwezekanayo ili kulinda athari zote za matukio ya Kiislamu, na athari yoyote inayohusiana na Bwana Mtume 8 hata kama ni unywele wake mmoja basi tuuhifdhi katika makumbusho, kwani ni ushahidi hai juu ya kusadikika kwa dini yetu na uwepo wa kweli wa Mtume wetu 8 . Na tujiepushe na fikra za kubomoa kumbukumbu kama vile makaburi ya Baqii na nyumba ya Bwana Mtume 8 kwa kisingizio cha kulinda tauhidi kama wafanyavyo Mawahabi, kuvunja kumbukumbu zote muhimu za Kiislamu kwa hoja ya kupinga shirki, neno ambalo hawajui mipaka ya maana yake. Ndugu zangu tusipokuwa 290

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 290

8/14/2017 1:18:42 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

makini vizazi vijavyo vitaingia katika balaa lilelile la kuwa na shaka na Uislamu kama dini ya kweli, na Mtume Muhammad kama mtu mwenye uwepo wa kweli. Utunzaji wa athari za kale kwa kadiri ya Qur’ani: Qur’ani katika mtiririko wa Aya zake inasimulia kwa msisitizo wa hali ya juu zaidi kuwa watu wa kale walikuwa wakilipa kipaumbele suala la utunzaji wa mabaki ya kale, hususan athari za Manabii. Walikuwa wakizitumia hata wakati wa vita ili kupata ushindi kupitia athari hizo. Moja ya mifano iliyotajwa katika Qur’ani kama kulitilia msisitizo suala hili, ni sanduku la Wana wa Israel, ambalo ndani yake lilikuwa na mabaki ya vile vilivyoachwa na Watu wa Musa na wa Harun. Mwenyezi Mungu anasema:

“Na Nabii wao akawaambia: Hakika alama ya ufalme wake ni kuwajia lile sanduku ambalo ndani yake mna kitulizo na mabaki ya yale waliyoyaacha watu Musa na wa Harun, wakilibeba Malaika. Hakika katika hayo mna dalili kwenu ikiwa nyinyi ni wenye kuamini.”171

Sanduku hilo ni katika mabaki ya yale yaliyoachwa na watu wa Musa na wa Harun. Na kitendo cha sanduku hilo kubebwa na viumbe watukufu kama Malaika ni ishara tosha kuwa sanduku hilo si kama masanduku ya kawaida bali ni sanduku tukufu na lenye ubora wa kipekee na wa aina yake. Kwa mantiki hiyo ikiwa kuhifadhi mabaki   Surat al- Baqarah; 2:248

171

291

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 291

8/14/2017 1:18:43 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

ya kale hususan yale yenye utukufu ni jambo lisiliofaa kushikamana nalo, ni kwa nini Qur’ani inalizungumzia suala hili kwa mtazamo mzuri, mtazamo chanya ambao unadhihirisha kuwa Qur’ani pia inaunga mkono suala la kuhifadhi mabaki ya kale? Na kwa nini sanduku hilo libebwe na Malaika tu? Na kwa nini zoezi la kulirejesha sanduku hilo liwe ni dalili za kusadikika kwa kiongozi huyo wa kijeshi aliyekuwa anahitajiwa na Wana wa Israil kwa wakati ule? Mpenzi msomaji! Mabaki ya kale ni hazina muhimu ambazo hatuna budi kuzilinda kwa nguvu zote, lakini kuna wajinga wasiojitambua. Na ndio wale vibaraka wa wakoloni; wao wana kazi kubwa ya kubomoa hazina ambazo zingebakia kama urithi wa vizazi vyetu vitakavyokuja baadaye. Na kibaya zaidi watu hao wamekuwa wakiwashawishi watu wenye maarifa machache kufuata nyao zao, na wao kwa uchache wa maarifa wakakubaliana nao. Baadhi wakasambaza makaburi ya mababu zao, na wengine wakachana picha za wazazi wao ambazo walikuwa wamezitunza kwa muda mrefu kabisa, kabla ya kujiwa na vibaraka hao wa kikoloni. Lakini umma wenye akili timamu bado unaendelea kutunza mabaki ya kale kwa namna ambayo haitofautiani kwa njia moja au nyingine na ile waliyoitumia watu wa zamani katika kutunza athari za watu waliowatangulia. Ndugu wapendwa mtu yeyote anayechezea historia ya kabila lako, mtu huyo ni adui mkubwa na anataka kukupotezea utambulisho wako wa kitaifa. Na ukishapoteza utambulisho wako basi umekwisha, wewe ni sawa na mfu. Mtu mwenye akili timamu ni lazima atunze historia, halikadhalika mila na desturi za kabila lake. Hapa nitawatajia mfano mmoja tu: Nchini Zambia kuna mikoa 9 na idadi ya watu milioni kumi na nne 14,000,000 na nchi hiyo ina makabila 72. Zambia ina zaidi ya sherehe ishirini za kiutamaduni kila mwaka. Sherehe hizo ni za kuadhimisha historia za makabila mbalimbali nchini humo, kwa mfano, N’cwala Traditional Ceremony: 292

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 292

8/14/2017 1:18:43 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Hii ni sherehe ya kiutamaduni inayoadhimishwa na kabila la Wangoni ambalo ni moja ya makabila makubwa mashariki mwa Zambia. N’cwala (Nchwala) ni moja ya sherehe muhimu sana katika historia ya nchi ya Zambia, ni sherehe inayofanyika mwezi wa pili (February) kila mwaka. Sherehe hiyo pamoja na kuvutia na kuhudhuriwa na watu mbalimbali kutoka makabila mengine nchini kote, idadi kubwa ya watalii toka nchi mbalimbali duniani huhudhuria pia. Machifu wakishirikiana na serikali wamekuwa wakihimiza sherehe za kitamaduni kama njia mojawapo ya kuhifadhi, na kuenzi na kuimarisha utamaduni wa kabila husika. Pia sherehe hizo zimekuwa ni vyanzo vya mapato hususan kwa vijana, na nafasi mwafaka kwa serikali kutangaza utalii kupitia utamaduni. Lengo kuu la Wangoni nchini Zambia ni kuadhimisha ushindi wa vita nyingi walizoshinda katika ardhi yao, na kukumbuka siku waliyovuka Mto Zambezi mnamo mwaka 1835 na kuingia Zambia kutoka Afrika ya Kusini. Katika sherehe hiyo utawaona Wangoni katika mavazi ya asili na silaha za jadi mikononi. Na kwa namna hii wamefanikiwa kuilinda historia yao na kuibakisha hai ili iwe ni urithi wa vizazi vijavyo. Halikadhalika mtu yeyote anayechezea historia ya taifa lako na kufuta kumbukumbu zake, mtu huyo ni adui na ana lengo la kukupotezea utambulisho wako mbele ya jamii za kimataifa. Na yeyote anayechezea historia ya dini yako na kuondosha kivitendo kumbukumbu zake, tambua kuwa mtu huyo anaandaa mazingira ya kupotosha vizazi vijavyo kwa kuwaambia kuwa dini yao ni ya kufikirikia na Mtume wao hakuwa na uwepo wa kweli. Kwa sababu kama angekuwa na uwepo wa kweli basi tungeona japo kaburi lake, na tungekuta mabaki japo ya baadhi ya vitu alivyokuwa akivitumia, lakini mbona havina uwepo katika majumba ya makumbusho? Na hapo ni lazima wakose jibu la kuvunja hoja chakavu kama hizo. Sasa 293

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 293

8/14/2017 1:18:43 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

ili kuzuia balaa hilo, wanachuoni wa Kiislamu wanatumia nguvu zote kuhakikisha athari zote za Kiislamu na za Mtume wake na watu wa nyumbani kwake pamoja na Maswahaba wema, zinahifadhika ili ziwe urithi kwa vizazi vijavyo. Tunamwomba Mola atujaalie kuwa katika wale wanaosikiliza neno na kufuata lililokuwa bora zaidi. Mtazamo chanya wa Qur’ani juu ya kujengea makaburi: Wamepata hasara wale walioondosha ushahidi wa kihistoria, kwa kubomoa makaburi ya Manabii wa Mwenyenyezi Mungu, na ya mababu zao, kwa ujinga na bila ya kuwa na elimu juu ya jambo hilo. Na kibaya zaidi hawakupenda kuwauliza wenye maarifa, bali kwa ufahamu wao duni na wa pupa walidhania kuwa wanamfurahisha na kumridhisha Mwenyezi Mungu. Ubaya ulioje wa maamuzi mabaya yatokanayo na ufahamu wa kukurupuka walionao watu hao!! Lakini ni ipi sera ya watu wa kale, kuhusiana na hilo, na ni upi mtazamo wa Qur’ani Tukufu? Kutunza athari za kale na kujengea makaburi kwa lengo la kuhifadhi historia isipotee, ni katika masuala ya kimaumbile na yaliyoshuhudiwa katika umma zilizotangulia, mpaka kufikia zama za Mtume wa mwisho Bwana Muhammad 8 na Qur’ani Tukufu imelitazama suala hilo kwa mtazamo chanya. Na mfano hai ni pale ilipotusimulia kisa cha kijana Maxmilianos na wenzake, pindi walipolala pangoni kwa muda wa miaka mia tatu (300). Habari yao ilipowafikia watu, kwa haraka walikimbilia huko kwenye eneo la tukio ili kushuhudia tukio hilo la ajabu. Na kwa kuwa jamii ile ilikuwa na watu wenye imani tofauti, watu hao waligawanyika kwa mujibu wa itikadi zao juu ya utunzaji wa eneo hilo. Kwa hiyo ikapatikana nukta ya makubaliano baina yao kwa upande mmoja, na nukta ya hitilafu kwa upande mwingine. 294

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 294

8/14/2017 1:18:43 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Nukta ya maafikiano: Mwafaka uliofikiwa baina ya pande mbili, bila ya kujali tofauti zao za kiitikadi, ilikuwa ni kuweka kumbukumbu au alama ambayo itatumika kama kiashirio cha kuashiria uwepo wa kitu adhimu katika eneo hilo. Nukta ya hitilafu: Hitilafu iliyojitokeza baina ya pande hizo mbili, ilikuwa ni katika kuainisha alama itakayotumika. Mzozo uliendelea kati yao na wale wasiokuwa na imani ya Mungu mmoja, walisema kuwa: “Lijengwe jengo juu yao� kwa kuwa jengo kama jengo likisimama basi itakuwa ni alama tosha na ya kudumu. Mtazamo huu ulizingatia kutunza historia tu, kwa ajili ya vizazi vijavyo. Lakini mtazamo wa kundi la pili ambao ulikuwa ni mtazamo wa watu wenye imani ya kuamini juu ya uwepo wa Mungu mmoja, ulitazama mbali zaidi kuliko mtazamo wa kundi la kwanza. Mtazamo huu wa kiumini ulizingatia mambo mawili muhimu sana:1.

Kuhifadhi sehemu hiyo ya vijana hao watukufu waliojitolea maisha yao katika njia ya kutetea imani ya dini ya kweli, ili vijana wa vizazi vijavyo waikute sehemu hiyo na waweze kujifunza kupitia vijana wenzao waliolala hapo. Somo la kuwa na msimamo imara mbele ya batili na kutopoteza imani kwa sababu ya vikwazo au mazingira magumu yanayosababishwa na serikali zisizojali mipaka ya sheria za Kiungu, achilia mbali za kibinadamu.

2.

Kunufaika kiroho kupitia mlango mpana wa utukufu na ukaribu wa vijana hao kwa Mwenyezi Mungu swt. Kwa mantiki hiyo waliipenda sehemu hiyo iwe ni sehemu endelevu ya ibada na maombi kwao na kwa vizazi vijavyo pia. Kwa hiyo walipende295

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 295

8/14/2017 1:18:43 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

keza uwepo wa jengo ambalo litakidhi mahitaji yao, badala ya jengo tupu kama ilivyopendekezwa na watu wa kundi la kwanza. Na kwa msingi huo jengo liwezalo kukidhi haja ya watu hawa wa kundi hili la pili ni msikiti. Na mwisho wa mjadala wao wale watu wenye mtazamo wa kuamini juu ya uwepo wa Mungu mmoja hoja yao ilipata ushindi, na msikiti ukajengwa kama inavyosimuliwa katika Aya ifuatayo:-

“…..Walisema: Jengeni jengo juu yao. Mola Wao anawajua zaidi. Wakasema wale walioshinda katika shauri lao. Hakika tutajenga msikiti juu yao.”172

Kwa mujibu wa aya hiyo tunafahamu kuwa eneo hilo liligeuka kuwa ni kituo cha watu kutoa heshima zao, na uwepo wa msikiti katika eneo hilo ni kwa ajili ya ibada ya kumwabudu Mwenyezi Mungu Mmoja tu, na kufanya maombi kwa baraka na utukufu wa vijana hao. Kwa hiyo kama tendo hilo lingekuwa ni shirki kama wanavyodai Mawahabi basi Mwenyezi Mungu angelisimulia tukio hilo kwa sura hasi.

KIBALI CHA KUINULIWA BAADHI YA ­NYUMBA:

Surat Al-Kahf; 18:21

172

296

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 296

8/14/2017 1:18:43 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

“Katika nyumba ambazo Mwenyezi Mungu ameruhusu ziinuliwe na kutajwa humo jina Lake, wanamtakasa humo asubuhi na jioni. Watu ambao biashara wala kuuza hakuwashughulishi na kumdhukuru Mwenyezi Mungu na kusimamisha swala na kutoa zaka…..” (24:36-37)

Sheikh Muhammad Ridha al Mudhafar anasema: “Mara nyingi hutokea migogoro katika nyanja za elimu mbalimbali zikiwemo zile za kisiasa na za kijamii, kwa sababu ya kutoweka wazi maana halisi ya maneno yatumikayo.” Kwa msingi huo tunapaswa kuainisha mambo mawili yafuatayo:1.

Maana ya neno Buyut (nyumba):

Ama kuhusiana na jambo la kwanza, tunasema: Makusudio ya nyumba katika aya hiyo si misikiti peke yake, bali neno hilo lina maana pana ikiwemo misikiti na maeneo mengineyo ambayo ­linatajwa humo jina la Mwenyezi Mungu, kwa hiyo yawezekana ikawa ni misikiti au nyumba za Manabii, Maimamu na Mawalii wa Mwenyezi Mungu, ambao biashara haiwashughulishi na ­kuwapumbaza hadi kuwasahaulisha swala na kumtaja Mwenyezi Mungu. Nyumba hizo ni mifano ya kusadikika iliyowazi katika Aya hiyo. Bali tunaweza kusema kuwa neno nyumba hapo halimaanishi misikiti, kwani neno (bait) nyumba, ni mkusanyiko wa kuta nne zenye sakafu ya juu. Hali kadhalika Al-Kabah imeitwa nyumba kwa sababu ya kuwa na sakafu ya juu na Qur’ani Tukufu inazingatia kuwa nyumba ni sehemu / jengo lenye sakafu ya juu:

297

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 297

8/14/2017 1:18:43 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

“Na lau isingekuwa watu watakuwa kundi moja tungeliwajaalia wanaomkufuru Mwingi wa rehema nyumba zao zina dari ya fedha, na ngazi zao pia wanazopandia.”173

Kwa mujibu wa Aya hii ni dhahiri kwamba nyumba ni lazima iwe na dari lakini msikiti hauna sharti hilo, kama unakumbuka tuliwahi kusema kuwa maana ya neno nyumba ni pana zaidi kuliko ile ya msikiti. Kwa hiyo tunaposema nyumba, msikiti pia unasadikika kuwa ni nyumba, lakini tunaposema msikiti hapo tunamaanisha baadhi ya nyumba tu nazo ni zile ambazo zinazosadikika kuwa na maana ya msikiti. Au kwa lugha nyepesi tunasema: Msikiti ni nyumba lakini siyo kila nyumba ni msikiti. 1.

Madhumuni ya neno kuinuliwa (turfaa):

Katika neno kuinuliwa hapo kuna maana mbili zinazotegemewa. Ima kuinua huko kuwe ni kwa kifizikia ambako utimilifu wake unahitajia uwepo wa nguzo zitakazosimamisha jengo, kama tunavyosoma katika Aya ifuatayo:-

“Na Ibrahimu alipoinua misingi ya ile Nyumba (al-Kaabah) na Ismail (wakaomba): Ewe Mola Wetu! Tutakabalie; hakika wewe ndiye Msikivu, Mjuzi.”174

Huko ni kuinua ambako kusadikika kwake ni katika ulimwengu wa kimetafizikia tu. Ama aina ya pili ya kuinua ni ile inayofungamana na ulimwengu wa kimetafizikia, na ulimwengu huu uko nje ya milango mitano ya fahamu. Mwenyezi Mungu anasema:   Surat al Zukhruf; 43:33   Surat al-Baqarah; 2:127

173 174

298

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 298

8/14/2017 1:18:43 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

“Na mtaje katika Kitabu, Idris. Hakika yeye alikuwa mkweli na alikuwa Mtume, Nabii. Na tukamwinua mahali pa juu.�175

Kutokana na ushahidi wa Aya hizo, kama kuinuliwa kwa Idris kungekuwa ni kule kwa kifizikia basi tungelimkuta Idris juu ya kitu kilichomuwezesha kuwa juu, au tungeona ngazi aliyopandia hadi kufika huko juu. Lakini kutokuwepo na nyenzo iliyomuwezesha kuwa juu ni dalili tosha ya kwamba kuinuliwa kwake ni kule kwa kifizikia kama tulivyosema. Na baada ya kuelezea aina hizo mbili za kuinua sasa tuangalie kuinuliwa kunakonasibiana na somo letu ni kupi? Kuinuliwa kunakokusudiwa katika Aya: Kutokana na aina za kuinuliwa tulizozitaja hebu tuangalie ile iliyokaribu na mazungumzo yetu kama ni ile ya kimetafizikia au nyingineyo: 1.

Ikiwa kuinuliwa kunakokusudiwa ni kule kwa kifizikia, basi makusudio ya Aya ni kuziimarisha nyumba za Manabii na Mawalii. Katika kipindi cha uhai wao, na baada ya kufa kwao, nyumba zao zibakie kama zilivyokuwa, na tusisahau kuwa Bwana Mtume 8 alizikwa ndani ya nyumba yake. Halikadhalika baadhi ya Maimamu na Mawalii wa Mwenyezi Mungu pia wamezikwa ndani ya nyumba zao, kwa hiyo kuzibakisha nyumba hizo katika hali zake, na kuziepushia kila aina ya uharibifu (unaofanywa na mafisadi kwa anuani ya kunusuru Sunnah) ni ruhusa kwa mujibu wa matini ya aya tukufu iliyotangulia.

  Surat Maryam; 19:56- 57

175

299

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 299

8/14/2017 1:18:43 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

2.

Na ikiwa kuinuliwakunako kusudiwa ni kwa kimetafizikia kama vile alivyoinuliwa Nabii Idris, basi kibali alichokitoa Mwenyezi Mungu ni cha kuzitukuza nyumba hizo, kuziheshimu, kuzienzi na kuzitakasa kutokana na kila kisichoendana na hadhi ya nyumba hizo. Na kwa nini nyumba hizo zipate hadhi kubwa kama hiyo? Ni kwa sababu ya uwepo wa watu wema wanaomwabudu na kumtukuza Mwenyezi Mungu asubuhi na jioni.

Na baada ya Aya hiyo na nyinginezo mfano wake, lakini bado utovu wa nidhamu wa genge la Kiwahabi unadhihirika kupitia vitendo vyao vichafu (visivyokuwa na hata chembe ya ubinadamu) vya kubomoa nyumba hizo za Manabii na Mawalii kwa lengo la kuwavunjia heshima watakatifu hao na kuondoa ushahidi wa kihistoria. Na katika utovu wao wa nidhamu uliovuka mipaka ni ule wa kuchezea nyumba ambayo ilikuwa ni mafikio ya Malaika wa Mwenyezi Mungu, na makao makuu ya kueneza dini na sheria Zake. Kwa nini mawahabi wamethubutu kuvunja makaburi ya Manabii? Moja ya maswali yaumizayo kichwa cha kila Mwislamu mwenye chembe ya utu moyoni mwake, ni kutaka kujua ni kwa nini Mawahabi wamekuwa na jasara ya kuvunja makaburi ambayo maelfu bali mamilioni ya Waumini walikuwa wakiyatembelea kwa kuzingatia utukufu wa watu waliozikwa humo? Je, ina maana kuwa Sheikh Ibnu Taimiyyah aliyeibuka mnamo karne ya saba na Sheikh Muhammad Bin Abdul Wahab aliyeibuka huko Najd karne kumi na mbili, wao tu ndio wanaujua sana Uislamu kuliko wanachuoni wote waliotangulia? Kama jibu lako ni hasi, basi ni lazima utakubaliana nasi kwamba lengo la Mawahabi ni kuondosha kivitendo ushahidi wa kihistoria, ili vizazi vijavyo vikose hoja ya kuwakinaisha mahasimu wao juu 300

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 300

8/14/2017 1:18:43 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

ya uhalisia wa dini yao na uwepo wa kweli na wa kusadikika wa Mtume wao. Mwenyezi Mungu swt, anasema: “Katika nyumba ambazo Mwenyezi Mungu ameruhusu ziinuliwe na kutajwa humo jina lake, wanamtakasa humo asubuhi na jioni.” (24:36). Siku moja Bwana Mtume 8 alisoma Aya hiyo, basi bwana mmoja akamuuliza kwa kusema: Ni nyumba gani hizo ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? Bwana Mtume 8 akajibu: “Hizo ni nyumba za Manabii.” Sayyiduna Abu Bakri Swidiq K naye akauliza ewe Mtume wa Mwenyenzi Mungu! Je, na nyumba hii pia ni mojawapo? (akaashiria nyumba ya Ali D na Fatimah J). Bwana Mtume 8 akasema: “Na ni katika bora zaidi ya hizo.”176 Kujengea makaburi kwa mujibu wa ulimwengu wa Kiislamu: Kujengea makaburi ni ada endelevu katika Umma wa Kiislamu, na hakuna Nabii wala Swahaba au Mwanachuoni aliyethubutu kuharamisha suala hilo. Lakini mwaka 1344 A.H. sawa na 1923 A.D. baada ya utawala wa uvamizi wa ukoo wa Kiwahabi wa Kisaudi kuiteka miji miwili mitukufu ya Makkah na Madina na miji inayoizunguka, utawala huo wa mabavu katika hali ya kutaka kuhalalisha upotovu wao na itikadi zao kinzani na mafundisho ya Uislamu, kitu walichokifanya wakuu wa utawala huo ni kutafuta hoja za kulazimisha uhalali wa kubomoa makaburi ya Baqii (mahala walipozikwa wajukuu wanne wa Bwana Mtume 8) na kufuta athari za watu watakatifu wa nyumba ya Bwana Mtume 8 na Maswahaba wake wema. Hivyo walimtuma mwakilishi wao kwenda kwa Wanachuoni wa Madina ili kuwataka watoe tamko la kuharamisha kujengea makaburi, ili wapate kisingizio mbele ya watu wenye mtazamo wa Ki  Taz, Ad-Durrul Manthur Jz. 5, uk. 91

176

301

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 301

8/14/2017 1:18:43 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

islamu ambao hauoni kizuizi katika suala hilo - hususan Watu wa Hijjaz – kwa maana wao (Mawahabi) walifahamu wazi kuwa suala la kubomoa makaburi na kufuta athari za watu watakatifu lingeweza kuamsha hisia za wengi mjini humo, kwa kuwa itikadi ya Waislamu wa Hijjaz ilikuwa sanjari na ile ya Waislamu katika miji mingine. Wote kwa pamoja waliamini juu ya karama za Mawlii wa Mwenyezi Mungu na utukufu wao, na pia walikuwa na imani juu ya uhalali wa kujengea makaburi yao kwa lengo la kutunza athari za kihistoria. Lakini Serikali ya Kiwahabi ya ukoo wa Saudi ilifanya jitihada za kuuvalisha uharamia wao vazi la Uislamu, kwa lengo la kuuangamiza Uislamu na kuing’oa mizizi ya matukufu yake. Kwa hiyo serikali ya Kiwahabi ilimtuma Kadhi Mkuu wa Najd, Sheikh Suileman Bin Bulaihd akiwa na maswali maalumu kwenda Madina (kama tulivyosema) na kutaka tamko la wanachuoni mjini humo juu ya uharamu wa kujengea makaburi ya mawalii mjini humo, lakini maswali yenyewe ndani yake yalikuwa na madhumini ya majibu yanayoendana na mtazamo wa Kiwahabi. Na hapo ndipo Sheikh Ja’far Subhani anasema: “Nadhani maswali na majibu yalikuwa yamekwishaandaliwa toka zamani katika waraka maalumu kisha waraka ule ukapelekwa kwa Wanachuoni wa Madnina ili watie sahihi tu.” Sheikh anaendelea kusema: “Kwani isingekuwa rahisi kwa wanachuoni hao kubadilisha ghafla itikadi waliyodumu nayo kwa miaka mingi, isipokuwa kubadilika huko kulitokana na kutambua kwao kuwa kutoa tamko linalokinzana na Serikali ya Kiwahabi matokeo yake ni kukufurishwa na kufilisiwa mali na hatimaye kuuawa endapo kama hutakubali kutubia.” Gazeti la Ummul Qura la mjini Makka katika toleo lake la 69 la mwaka 1344 A.H sawa na 1923A.D lilichapisha maswali hayo pamoja na majibu yake, ili kuwakinaisha Waislamu kuwa Wanachuoni wa Madina ndio waliotoa tamko hilo la kuharamisha kujengea maka302

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 302

8/14/2017 1:18:43 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

buri. Na suala hilo liliibua hisia za Waislamu wengi Sunni na Shia kwa pamoja, kwa kuwa walielewa wazi kuwa majibu yaliyochapisha kwenye gazeti hilo hayakutokana na hisia za Wanachuoni wa Madina bali yalitokana na shinikizo la kutishiwa kuhatarisha maisha endapo watasema kinyume na matakwa ya Serikali ya Kiwahabi. Tukio hilo kwa mtazamo wa Waislamu liliashiria utangulizi wa kubomoa makaburi na mashahidi yaliyojengwa juu ya viongozi watukufu wa dini yetu. Na baada ya tamko hilo kuwasilishwa mjini Makkah toka kwa Wanachouni kumi na tano wa Madina, Serikali ya watu wasiokuwa na ubinadamu ndani ya nyoyo zao ilisambaza majibu hayo na kisha ikatekeleza na si kutelekeza kwa vitendo zoezi la kinyama la kuvunja makabari ya watu watakatifu wa nyumba ya Bwana Mtume 8 na sahaba zake, ususuavu wa moyo ulioje huo!! Hayo yalijiri mnamo tarehe nane mfungo mosi mwaka 1344A.H sawa na 1923A.D. Athari za Maswahaba na zile za familia ya Bwana Mtume 8 zikasambaratishwa. Tendo hilo ndugu msomaji liliwaliza wote wenye nyoyo za ubinadamu bila kujali dini zao. Maswali yaliyoelekezwa kwa wanachuoni wa Madina: Hapa tutaorodhesha baadhi ya maswali, ambayo mjumbe wa Kiwahabi aliyapeleka Madina: 1.

Je, ni lipi tamko la wanachuoni wa Madina - Mwenyezi Mungu awazidishie fahamu - juu ya kujengea makaburi na kuyafanya kuwa ni misikiti, inaruhusiwa au laa?

2.

Na kama jambo hilo halifai bali ni lenye kukatazwa makatazo makali je, ni wajibu kuyabomoa na kuzuia Swala sehemu hiyo?

3.

Na ikiwa kujenga kwenye ardhi iliyotolewa wakfu ni kuwazuilia manufaa, je huoni kama ni uporaji, upaswao uon303

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 303

8/14/2017 1:18:43 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

dolewe kwa kuzingatia kuwa ni dhulma ya kuwazuilia haki zisiwafikie wanaostahiki? Majibu ya wanachuoni wa Madina: Baada ya shinikizo na vitisho vikali, wanachuoni wa Madina walitoa majibu kama ilivyotakiwa na Serikali ya Kiwahabi: Ama kuhusu suala la kujengea makaburi, hilo ni lenye kuzuiliwa, kwa mujibu wa makubaliano ya wanachuoni kwa kuzingatia hadithi zilizopokelewa katika kukataza hilo. Na kwa msingi huo wanachuoni wengi wametoa tamko juu ya ulazima wa kubomoa makaburi kwa kutegemea hadithi ya Ali (r.a) ya kwamba yeye alimwambia Abul Hayaj kuwa “…..Nakutuma kwa yale aliyonituma kwayo Mtume wa Mwenyezi Mungu, usiache sanamu isipokuwa umelivunja na wala kaburi isipokuwa umelisawazisha “177 Na hadithi hii maharamia wa Kiwahabi wameifanya kuwa ni hoja ya kuhalalisha ushenzi wao wa kubomoa makaburi ya Manabii na Mawalii wa Mwenyezi Mungu (swt). Mpenzi msomaji, kama ulivyoona katika hadithi hiyo, Bwana Mtume 8 anasema: “Wala kaburi isipokuwa umelisawazisha.” Hivi neno kusawazisha katika Kamusi Sanifu ya Kiwahabi, ni kisawe cha kubomoa? Hayo ni madai ya Kiwahabi tu, lakini neno kusawazisha na kubomoa ni maneno mawili tofauti na yenye maana tofauti, lakini Mawahabi wanataka kuyafanya kuwa ni maneno mawili yenye maana moja. Huo ni mtazamo wao nasi tutakufafanulia kwa kina huko mbele maana ya maneno hayo. Hoja chakavu za Kiwahabi zasimamia juu ya nguzo mbili mbovu: 1.

Makubaliano ya wanachuoni juu ya uharamu wa kujengea makaburi.

Sunan Tirmidhi: Kitabu janaiz, babu maajaa fii tas-wiyatil kubur hadith namba 1049. Sahihi Muslim, Kitabu janaiz uk. 256

177

304

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 304

8/14/2017 1:18:43 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

2.

Hadithi ya Abul Hayaj kutoka kwa Sayyiduna Ali D.

Majibu yetu juu ya hoja hizo: a.

Ama kuhusu hoja yao ya kwanza iliyodai kuwa wanachuoni wamekubaliana juu ya uharamu wa kujengea makaburi, madai hayo hayana hata chembe ya ukweli ndani yake. Na kama yangekuwa na ukweli basi wangetutajia majina ya hao wanachuoni. Naye Sheikh Najdi anaeleza katika makala yake iliyochapishwa kwenye Gazeti la Ummul Qura mwezi wa mfunguo tisa mwaka 1340 A.H: “Kujengea kuba juu ya makaburi kulikuwa kumeenea tangu karne ya tano hijiria.”

Historia yatwambia kuwa Wanachuoni wa Madina walikuwa na desturi waliyoikuta tokea zama za mababu zao, ya kujengea na kuhifadhi athari za Manabii, bali walikuwa wakitoa wito kwa Waislamu wote kudumisha desturi hiyo, pia walikuwa wakitembelea makaburi ya watakatifu. Hata Aya za Qur’ani pia zimezungumzia suala la kutunza athari za Manabii na Mawailii, kama tulivyoashiria katika kisa cha vijana wa pangoni. Ili kuthibitisha uzushi wa Kiwahabi hebu tuangalie huko huko Hijjaz (Saudia) ambako inadaiwa kuwa wanachuoni wameafikiana juu ya kubomoa makaburi. Katika mji wa Makkah tena pembezoni mwa pembe ya Al-Kaabah kuna - Hijri Ismail – sehemu ya kaburi la Sayyiduna Ismail na la mama yake Bi Hajir. Na Bwana Mtume 8 aliyakuta makaburi hayo na akafanya ibada ya kuizunguka Kaabah na makaburi yakiwa pale pale. Baada ya Bwana Mtume 8 Maswahaba walifanya ibada hapo na Waislamu wote walikuwa wakifanya ibada hapo, na hakuna hata mmoja aliyetamka utovu huo wa nidhamu, bali hata wao wenyewe Mawahabi wanapofanya twawafu (ibada ya kuizunguka Kaabah) huwa wanayazunguka makaburi hayo. Na kwa lugha nyepesi kila anayekwenda Hijja huwa anayazunguka makaburi hayo mawili. 305

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 305

8/14/2017 1:18:43 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Kwa hiyo kauli ya kubomoa makaburi ni katika uzushi wa madhehebu potovu na ya kizandiki ya Kiwahabi, uzushi ambao genge la kiharamia la Kiwahabi liliwashinikiza Wanachuoni wa Madina mwaka 1344 A.H kutoa tamko la kuhalalisha uharamia huo wa kuchezea matukufu ya dini. Tukiachana na mji wa Makkah, moja kwa moja nakupeleka nchini Iraq na huko tunakuta makaburi ya Manabii:Hud, Swaleh, Yunus na Dhul-Kifli. Tukiwa mbele ya makaburi haya mpenzi msomaji unaweza kuuliza swali lifuatalo: Mbona Swahaba Mtukufu Ali D aliishi hapa kama makao ya serikali yake, na hakuwahi kutoa tamko la kuhalalisha kubomoa makaburi haya? Ndugu yangu msomaji kubomoa makaburi ni mtazamo hasi wa Kisalafi ambao kwa sasa unatambulika kama Uwahabi na AnswarSuna maana kila siku wanajibatiza majina mapya. Ni kweli kabisa ndugu msomaji kwamba Swahaba Mtukufu Ali D aliishi hapa, na makaburi haya yalikuwepo, na wala yeye hakuwa na mtazamo hasi juu ya makaburi haya. Lakini cha kumsikitisha na kumliza kila mwenye ubinadamu ndugu yangu msomaji, ni kile kitendo cha kuibuka watu mnamo mwaka 2014, wakiwa wamevaa vipande vya suruali na bendera nyeusi mikononi mwao, na kuanza kubomoa kaburi la Nabii wa Mwenyezi Mungu Yunus D, kwa lengo la kupoteza ushahidi wa kihistoria juu ya uwepo wa kweli wa Nabii huyu. Baada ya maelezo haya mpenzi msomaji nakupeleka nchini Iran, endelea kuwa nami. Hapa tumekuta kaburi la Nabii Daniel, katika mji wa Shush likiwa salama. Kutoka Shush sasa tuelekee (Quds) Palestina na huko kuna makaburi ya Manabii Ibrahimu, Is-haq, Yakub na Yusuf. Makaburi ya Manabii hawa mpenzi msomaji yalikuwa huko Misri, lakini Nabii Musa aliihamisha miili ya Watakatifu hawa na kuizika Quds kama alivyoamrishwa na Mwenyezi Mungu. Makaburi hayo yapo hadi leo hii na yamejengewa madhubuti, na kila moja lina alama yake. 306

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 306

8/14/2017 1:18:43 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Lakini tukirudi nyuma mpaka Hijjaz, kule tulikoanzia safari yetu, tukifika katika mji wa Jidah kuna kaburi la mama yetu Hawa. Kaburi hili lilikuwa na alama zinazoonekana, lakini baada ya genge la hujuma la Kiwahabi kuiteka Hijjaz, walifuta athari zote kwa makusudi!! Mwisho kabisa napenda nikupeleke nchini Jordan, nchi hii inatawaliwa na serikali ya kifalme. Huko kuna makaburi ya Manabii wengi na yamejengewa kwa majengo imara. Mpenzi msomaji naamini kuwa katika safari yetu ya kutembelea athari za kale umejifunza mengi na umeona mengi ya kusikitisha na kuliza na pia ya kufurahisha. Sasa naomba tukae chini tupumzike kutokana na uchovu wa safari. Na baada ya kunywa kikombe cha kahawa, tujiulize maswali haya: Kwa nini Bwana Mtume 8 hakutoa tamko dhidi ya makaburi aliyoyakuta katika mji wa Hijjaz? Kwa nini Mwenyezi Mungu amuamuru Nabii Musa D kuhamisha miili ya Manabii waliokuwa Misri kutoka nchini humo na kuipeleka (Quds) Palestina? Kwa nini Swahaba Mtukufu kama Ali D aliishi Iraq na hakubomoa makaburi ya Manabii waliozikwa huko? Kwa nini Maswahaba na Waislamu walioishi baada yao mpaka kufikia karne ya Usalafi, hawakuwa na mitazamo hasi dhidi ya makaburi ya Manabii na Mawalii? Je, ina maana watu wote hao hawakuwa na dini sahihi bali dini sahihi ni hii tuliyoletewa na Mawahabi? Ndugu yangu kuwa makini na Uwahabi. Na laiti kama madai yao yangekuwa sahihi basi wanachuoni wa Kiislamu wangekuwa wamekwishalitolea hukumu suala hili hata kabla ya ujio wa Sheikh Ibnu Taimiyyah na mwanafunzi wake Sheikh Muhammad Bin Abdul Wahab. Lakini ndio kwanza tunakuta kuwa wanachuoni kwa miaka mingi walikuwa na desturi ya kuyaenzi na kuyakarabati, na kuyaboresha kutokana na mitindo ya zama husika. Yote hayo waliyadumisha ikiwa ni ishara ya heshima kwa watukufu hao na kuwatukuza, na wala hawakuwa na lengo la kuwaabudu Manabii na Mawalii 307

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 307

8/14/2017 1:18:43 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

hao. Anasema Sheikh Ibnu Taimiyyah: “Pindi ilipokombolewa Quds, makaburi ya Manabii yalikuwa yamejengewa lakini milango yake ilikuwa imefungwa mpaka kufikia karne ya nne hijiria.”178 Mwalimu Sheikh Tabriz Subhani anasema: “Kama kujengea makaburi kungekuwa ni haramu, basi ingekuwa ni wajibu kuyabomoa na wala pasingekuwa na hoja katika kuyaacha kama yalivyo hali ya kuwa ni yenye kufungwa milango, bali ingekuwa ni wajibu kuyabomoa haraka sana, kama tukizingatia usahihi wa kauli ya Ibnu Taimiyyah kuwa milango ilifungwa mpaka karne ya nne.” Mpenzi msomaji! Kama kusimamisha jengo kwenye kaburi ni haramu kisheria kwa kuchelea watu kuingia humo na kuabudu kaburi kama wanavyodai Mawahabi, basi kwa nini jengo hilo lisibomolewe kwa kuzingatia kuwa kuboma ndiyo njia pekee ya kutokomeza ibada ya makaburi? Kufunga milango tu, hakusaidii kitu, kwani watu wanaweza kusimama nje ya jengo na kuanza kubusu kuta zake ili kuonesha ishara ya upendo na heshima kwa yule aliye ndani ya jengo. Kama ilivyokuwa maarufu katika kisa cha Mwehu aliyempenda Leilat - Leilat wa Majnun - na hilo la kubusu ukuta pia ni shirki katika mantiki ya Kiwahabi, kwa hiyo kauli ya Sheikh Ibnu Taimiyyah inathibitisha ubabaishaji wake wa wazi, na kwamba alikuwa na lengo la kuwatoa watu kwenye mstari mnyoofu. Na kwa mantiki hiyo sisi tunasema kuwa majibu yaliyodaiwa kuwa ni kauli za wanachuoni juu ya kubomoa makarburi, ni batili na hayana ukweli ndani yake, bali ilikuwa ni shinikizo la Kiwahabi la vitisho kwa wanachuoni hao kama tulivyoashiria hapo awali. Kama kweli suala la kubomoa makaburi lingekuwa katika makubaliano ya wanachuoni basi Mawahabi wasingepata la kusema kwani wasingekuta kaburi hata moja, kwani yote yangekuwa yamekwishavunjwa kabla ya ujio wao.   Kashful Irtiyab kutoka kitabu Swiratul Mustaqima.

178

308

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 308

8/14/2017 1:18:43 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Na kwa upande wa pili wa shilingi tunaweza kusema kuwa suala hilo ni la kimaumbile na ndio maana hata jamii za watu wenye imani tofauti na imani ya Kiislamu wao pia wanajengea na kuhifadhi makaburi yao, ili wawe na ushahidi wa kuonekena kwa vizazi vijavyo. Na hii ndiyo falsafa ya kutunza makaburi pamoja na athari zote za kale zinazohusiana na mtu binafsi, familia, kabila na taifa zima kwa jumla. Ili kukupa mfano hai mpenzi msomaji niruhusu nikupeleke mara moja Mkoani Morogoro, ili uweze kumwona mkulima mahiri, aliyeishi katika mazingira magumu ya kiuchumi. Riziki yake na ya familia ilitegemea kazi ya kilimo na kuchoma mkaa. Lakini kwa sababu Mwenyezi Mungu swt, hata siku moja huwa hapotezi juhudi ya mtu mwenye kujishughulisha, hali ya mkulima huyo ilibadilika kiuchumi na kuwa nzuri. Mkulima huyo katika hali ya kutaka kutunza historia yenye ushahidi, aliweka shoka kwenye ofisi yake ya shambani, ili iwe somo kwa vizazi vijavyo, na shoka hilo lipo hadi leo kama athari au ushahidi unaoonekana juu ya kazi yake ya kukata miti kwa ajili ya kuchoma mkaa. Kwa hiyo siku Muwahabi akifika hapo na kumwambia mkulima huyo kuwa ameweka sanamu ndani, ni lazima mkulima huyo autilie shaka utimilifu wa akili ya Wahabi huyo. Ndugu yangu, yeyote mwenye akili timamu ni lazima atakubaliana na sisi kuwa Mawahabi ni watu wanaoendeshwa kwa matamanio na wala hawatawaliwi na akili. Watu wa maeneo mbalimbali hapa nchini, hususan mjini Kigoma walikuwa na desturi ya kupalilia makaburi, na kuwarehemu ndugu zao na Waislamu wenzao waliotangulia, na Masheikh wote waliunga mkono desturi hii ya kimaumbile na hakuna yeyote kati yao aliyetamka kuwa tendo hilo ni ushirikina. Lakini cha kusikitisha na kumliza kila mwenye chembe ya utu moyoni, katika miaka ya 1968 kwenda mbele waliibuka vibaraka wasiojitambua kule nchini Burundi, na kuenea kidogokidogo 309

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 309

8/14/2017 1:18:43 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

mpaka wakafika Tanzania na Afrika Mashariki kwa jumla. Vibaraka hao waliwakaririsha watu maneno matatu – tauhidi, shirki na Bidaa. Na kwa maneno hayo yasiyokuwa na ufafanuzi sahihi, watu walianza kubomoa makaburi ya mababu zao, na baadhi ya watu hususan wale wasiokuwa na maarifa ya sheria ya dini waliupokea udanganyifu huo na kuukumbatia kama Sunna ya Bwana Mtume 8!! Mwenyezi Mungu aepushe vizazi vyetu na janga la Uwahabi. b. Hoja ya pili ni kuhusu hadithi ya Abul Hayaj kutoka kwa Imamu Ali D ya kwamba: “Nakutuma kwa yale aliyonituma kwayo Nabii 8 ya kwamba: Usiache kaburi refu isipokuwa umelisawazisha na wala usiache sanamu isipokuwa umelivunja.” Mpenzi msomaji napenda kukukumbusha kauli ya Sheikh alMudhafar: “Mara nyingi yatokea migogoro katika nyanja za kielimu na hata za kisiasa na kijamii, kwa sababu ya kutoweka ainisho la maana ya maneno yatumiwayo.” Na kwa msingi huo hatuna budi kuweka wazi maana ya neno kusawazisha lililotumika katika hadithi hiyo, kwani kuna tofauti kubwa kati ya neno kusawazisha na kulinganisha. Neno kulinganisha hutumika baina ya vitu viwili, na hutamkwa Linganisha na.... kwa mfano: Jauz namlinganisha na Mustafa, na wala huwezi kusema: Jauz namsawazisha na Mustafa. Ila unawezakusema: Nimemsawazisha Mustafa. Na hapo utakuwa na maana ya kumrekebisha Mustafa na kumuweka sawa. Kwa mantiki hiyo, maana ya kusawazisha ni kurekebisha kitu na kukiweka katika mpangilio mzuri. Katika Lugha ya Kiarabu neno tas-wiyat huwa na maana ya kulinganisha kitu kimoja na kingine, endapo litatamkwa: Sawaituhu bi…‫سويت كذا بكذا‬, lakini lisipofuatana na neno (bi) huwa halileti maana nyingine zaidi ya kurekebisha kitu katika uwenyewe wake na kukiweka katika hali nzuri kama ilivyotumika katika hadithi hiyo “( ‫) أن ال تدع قبرًا مشرفا إال سويته‬. 310

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 310

8/14/2017 1:18:43 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

Na wala (usiache) kaburi refu isipokuwa umelisawazisha.” Lakini neno kusawazisha kwa mujibu wa kamusi Sanifu ya Kiwahabi, lina maana ya kubomoa na kusambaza, na kwa mantiki hiyo kama kinyozi atakuwa ni Muwahabi/Msalafi halafu wewe ukaenda kumwambia asawazishe nywele zako basi naamini kuwa hapo ni lazima utoke na para, maana kwa ufahamu wake, utakuwa umemwambia kuwa amalize nywele zote kichwani. Na baada ya kuweka wazi maana ya neno kusawazisha, napenda kuweka wazi pia maana ya neno lingine lililotumika ndani ya hadithi hiyo, nalo ni Mushrifa )‫ (مشرفًا‬. Neno hili kwa mujibu wa kamusi ya Lugha ya Kiarabu, kama litatumika kwa kukusudia sehemu basi litakuwa na maana ya sehemu iliyoinuka juu.179 Na katika ngamia neno hilo linamaanisha nundu ya mgongoni (sanaamu). Kwa hiyo madhumuni ya hadithi ni kulisawazisha kaburi na kuliweka katika utaratibu liinuke kwa vipimo vyake maalumu vinavyo kadiriwa katika vitabu vya sheria kuwa ni wastani wa nchi 6, na lisiwe kama kichuguu au nundu ya ngamia japo Maimamu wa madhehebu manne wamestahabu kaburi kuwa katika muundu huo, isipokuwa Imamu Shafii peke yake.180 Na mpaka hapa tumeona kuwa hadithi inayotegemewa na Mawahabi haina uhusiano wowote na suala la kuvunja makaburi, na kama hadithi ingekuwa na maana ya kuvunja na kusambaza makaburi basi ingesema hivi: }‫“ {وال قبرًا مشرفًا إال سويته باألرض‬Wala (usiache) kaburi refu isipokuwa umelilinganisha na ardhi.” (Kwa maana ya kusambaza). Mtungo wa wapokezi wa hadithi hiyo: Tunapotumia hadithi kama hoja ya kuthibitisha moja ya hukumu za Mwenyezi Mungu, basi awali ya yote ni lazima hadithi hiyo ikamilishe masharti mawili yafuatayo:   Al-Munjid, uk. 383 chapa ya Beirut toleo la 43 la mwaka 2008   Fiq-hu alal madhahib al arbaa, Jz. 1, uk. 420.

179 180

311

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 311

8/14/2017 1:18:44 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

i.

Usahihi wa sanad: Wapokezi wote waliotajwa katika hadithi wawe ni watu waaminifu, na ambao hadithi zao watu wanaweza kuzitegemea kama hoja ya kuhalalisha au kuharamisha jambo.

ii. Madhumuni ya hadithi: Matamshi ya hadithi yaoneshe wazi kile tunachokikusudia katika matamshi hayo, kiasi ambacho kila mwenye kufahamu lugha ile na sarufi yake pia aweze kufahamu kwa wepesi kile tunachotaka kukithibitisha. Ama kuhusu wapokezi waliotajwa katika hadithi hiyo: i.

Wakii,

ii. Sufiyan Thawriy, iii. Habib bin Abu Thabit iv. Abu Wail Asadiy. 1.

Wapokezi wote hao wamekosolewa na kutiwa dosari na Hafidh Ibnu Hajar al-Askalan katika kitabu Tahdhib tahdhib kama alivyopokea kutoka kwa Imamu Ahmad bin Hanbal ya kwamba alikosea (Wakii) katika hadithi 500.

2.

Anasema Ibnu Hajar, kutoka kwa Ibnu Mubaraka: Sufian alisimulia hadithi, nami nikamjia na kumkuta akiwa katika hali ya kupotosha (maana ya hadithi, kwa Kiswahili cha vijana kuchakachua) pindi aliponiona alipatwa na aibu.

3.

Ibnu Hajar anasema kuwa: Bwana huyu (Habib) naye pia alikuwa ni mtaalamu wa kukarabati hadithi.

4.

Bwana huyu (Al-Asadi) alikuwa ni katika watu wanaompiga vita Imamu Ali D, na Bwana Mtume 8 anase312

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 312

8/14/2017 1:18:44 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

ma: “Ewe Ali, hakupendi wewe isipokuwa muumini na wala hakuchukii wewe isipokuwa mnafiki.”181 Halafu nukta nyingine muhimu ni kwamba Abul Hayaj hana hadithi katika Sahih sita isipokuwa hiyo inayodaiwa na Mawahabi kuwa ni ushahidi wa kusambaza makaburi. Kwa hiyo hoja waliyoitegemea Mawahabi katika kubomoa makaburi, imekosa vigezo hivyo viwili tulivyovitaja, ambavyo ni madhumuni ya maneno yaliyotumika, na mlolongo wa wapokezi ambao hawana dosari itakayopelekea kuwavua sifa ya uadilifu. Halafu kama kweli wanachuoni waliafikiana juu ya suala la kubomoa makaburi, basi kwanza kabisa wangebomoa kaburi la Bwana Mtume 8 ambaye alizikwa nyumbani kwa Bibi Aisha O, lakini badala ya kulibomoa kaburi hilo, waliongeza Kaburi la Abu Bakri K kisha kaburi la Umar K, ili Maswahaba hao wapate baraka za Bwana Mtume 8. Na nyumba hiyo iliwekewa ukuta katikati ikawa upande mmoja wa nyumba hiyo ni makaburi, na upande mwingine ikawa ni makazi ya Bibi Aisha O, na kipindi chote hicho wanachuoni hawakuona uharamu katika suala hilo mpaka pale Mawahabi walipoikalia nchi ya Hijjaz kimabavu tena kwa kuwezeshwa na wakuu wao Waingereza. Ewe Mwenyezi Mungu tunakuomba utujalie kuwa katika wale wanaosikiliza neno na kufuata lile lililokuwa bora zaidi. Amin. Baba Mtumishi Kabwe Hussein Dar-es-Salaam. Tanzania. Simu: +255-789-78 57 56 Email : husseinkabwe@yahoo.com   Sharhu Nahjul-Balaghah ya Ibnu Abil Hadid.

181

313

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 313

8/14/2017 1:18:44 PM


‫‪Uwahabi Haukubaliki‬‬ ‫‪kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo‬‬

‫‪VITABU REJEA‬‬ ‫‪ .1‬‬

‫القرآن الكريم‬

‫‪ .2‬‬

‫نهج البالغة‬

‫‪ .3‬‬

‫كشف اإلرتياب‬

‫‪ .4‬‬

‫بحوث في الملل و النحل ‪ -‬للشيخ جغفر السبحان‬

‫‪ .5‬‬

‫الملل و النحل للشهرستان‬

‫‪ .6‬‬

‫الكتاب المقدس‬

‫‪ .7‬‬

‫عقائد اإلمامية – للشيخ محمد رضا المظر‬

‫‪ .8‬‬

‫منطق المظفر‬

‫‪ .9‬‬

‫التوحيد عند الشيخ ابن تيمية – للعالمة السيد الحيدري‬

‫‪ .10‬‬

‫كتاب اإللهيات للشيخ جعفر السبحاني‬

‫‪ .11‬‬

‫صحيح مسلم‬ ‫‪314‬‬

‫‪8/14/2017 1:18:44 PM‬‬

‫‪09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 314‬‬


‫‪Uwahabi Haukubaliki‬‬ ‫‪kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo‬‬

‫‪ .12‬صحيح البخاري‬ ‫‪ .13‬‬

‫نقض الوهابية‬

‫‪ .14‬‬

‫الصواعق اإللهية في الرد على الوهابية‬

‫‪ .15‬‬

‫الوهابية في الميزان‬

‫‪ .16‬‬

‫القاالت السنية للشيخ عبد هللا الهرري‬

‫‪ .17‬‬

‫العلو للعلي الغفار للسيد السقاف‬

‫‪ .18‬صحيح شرح العقيدة الطحاوية‪ ,‬للسيد السقاف‬ ‫‪ .19‬أخي السلفي‬ ‫‪. 20‬‬

‫ألوهابية بين المباني الفكري والنتائج العملية ‪ -‬للشيخ السبحاني‬

‫‪ .21‬التفسير الكبير لالمام الفخر الرازي‬ ‫‪ .22‬‬

‫بداية الحكمة للسيد الطباطبائي‬

‫‪ .23‬‬

‫الدر المنثور للسيوطي‬

‫‪ .24‬‬

‫الكشاف للزمخشر‬ ‫‪315‬‬

‫‪8/14/2017 1:18:44 PM‬‬

‫‪09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 315‬‬


‫‪Uwahabi Haukubaliki‬‬ ‫‪kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo‬‬

‫‪ .25‬الميزان للسيد الطباطبائي‬ ‫‪ .26‬‬

‫إبن تيمية فكرا و منهجا للشيخ السبحاني‬

‫‪ .27‬شواهد التنزيل للحافظ الحسكاني‬ ‫‪ .28‬خالصة الكالم في أمراء البلد الحرام‬ ‫‪ .29‬بحار األنوار‬ ‫‪ .30‬تفسير األمثل للشيخ مكارم الشيرازي‬ ‫‪ .31‬‬

‫المعاد للسيد كمال الحيدري‬

‫‪316‬‬

‫‪8/14/2017 1:18:44 PM‬‬

‫‪09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 316‬‬


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

ORODHA YA VITABU VILIVYO ­ ­CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION: 1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9. 10. 11. 12. 13. 14. 15. 16. 17. 18. 19. 20. 21. 22. 23. 24. 25. 26.

i) Qur’ani Tukufu – Pamoja na Tarjuma ya Kiswahili ii) Qur’an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Thelathini Uharamisho wa Riba Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili Hekaya za Bahlul Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (a.s.) Hijab vazi Bora Ukweli wa Shia Ithnaashari Madhambi Makuu Mbingu imenikirimu Abdallah Ibn Saba Khadijatul Kubra Utumwa Umakini katika Swala Misingi ya Maarifa Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia Bilal wa Afrika Abudhar Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu Salman Farsi Ammar Yasir Qur’an na Hadithi Elimu ya Nafsi Yajue Madhehebu ya Shia Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur’an Tukufu 317

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 317

8/14/2017 1:18:44 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

27. 28. 29. 30. 31. 32. 33. 34. 35. 36. 37. 38. 39. 40. 41. 42. 43. 44. 45. 46. 47. 48. 49. 50. 51. 52. 53. 54. 55. 56. 57.

Al-Wahda Ponyo kutoka katika Qur’an Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii Mashukio ya Akhera Al Amali Dua kwa Mujibu wa Ahlulbayt (a.s) Udhuu kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna Haki za wanawake katika Uislamu Mwenyezi Mungu na sifa zake Kumswalia Mtume (s) Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) Adhana Upendo katika Ukristo na Uislamu Qur’ani na Kuhifadhiwa Kwake Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu Kupaka juu ya khofu Kukusanya Sala Mbili Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Kusujudu juu ya udongo Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s) Tarawehe Malumbano baina ya Sunni na Shia Kupunguza Swala safarini Kufungua safarini Umaasumu wa Manabii Qur’an Yatoa Changamoto as-Salaatu Khayrun Mina -’n Nawm Uadilifu wa Masahaba Dua e Kumayl Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu 318

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 318

8/14/2017 1:18:44 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

58. Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake 59. Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata 60. Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mtume Muhammad (s) 61. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza 62. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili 63. Kuzuru Makaburi 64. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza 65. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili 66. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu 67. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne 68. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano 69. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita 70. Tujifunze Misingi Ya Dini 71. Sala ni Nguzo ya Dini 72. Mikesha Ya Peshawar 73. Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu 74. Ubora wa Imam ‘Ali na Ushia ndio njia iliyonyooka 75. Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake 76. Liqaa-u-llaah 77. Muhammad (s) Mtume wa Allah 78. Amani na Jihadi Katika Uislamu 79. Uislamu Ulienea Vipi? 80. Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) 81. Dhana ya Ndoa ya Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) 82. Urejeo (al-Raj’ah) 83. Mazingira 84. Utokezo (al - Badau) 85. Hukumu ya kujenga juu ya makaburi 86. Swala ya maiti na kumlilia maiti 87. Uislamu na Uwingi wa Dini 319

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 319

8/14/2017 1:18:44 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

88. 89. 90. 91. 92. 93. 94. 95. 96. 97. 98. 99. 100. 101. 102. 103. 104. 105. 106. 107. 108. 109. 110. 111. 112. 113. 114. 115. 116. 117. 118.

Mtoto mwema Adabu za Sokoni Na Njiani Johari za hekima kwa vijana Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu Tawasali (AT- TAWASSUL) Imam Mahdi katika Usunni na Ushia Hukumu za Mgonjwa Sadaka yenye kuendelea Msahafu wa Imam Ali Maimamu wa Ahlul Bait – Ujumbe na Jihadi Idi Al-Ghadir Kusoma sura zenye Sijda ya wajibu Hukumu zinazomuhusu mkuu wa kazi na Mfanyakazi Huduma ya Afya katika Uislamu Sunna za Nabii Muhammad (saww) Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza) Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili) Shahiid Mfiadini Mwanamke Na Sharia Ujumbe -Sehemu ya Kwanza Ujumbe - Sehemu ya Pili Ujumbe - Sehemu ya Tatu Ujumbe - Sehemu ya Nne Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu Hadithi ya Thaqalain Ndoa ya Mutaa Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza Ukweli uliopotea sehemu ya Pili Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu 320

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 320

8/14/2017 1:18:44 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

119. Ukweli uliopotea sehemu ya Nne 120. Ukweli uliopotea sehemu ya Tano 121. Mkutano wa Maulamaa wa Baghdad 122. Safari ya kuifuata Nuru 123. Fatima al-Zahra 124. Myahudi wa Kimataifa 125. Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi 126. Visa vya kweli sehemu ya Kwanza 127. Visa vya kweli sehemu ya Pili 128. Elimu ya Ghaibu ya Maimamu 129. Mwanadamu na Mustakabali wake 130. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Kwanza) 131. mam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Pili) 132. Khairul l’Bariyyah 133. Uislamu na mafunzo ya kimalezi 134. Vijana ni Hazina ya Uislamu 135. Adhana ni Ndoto au ni Wahyi? 136. Tabaruku 137. Saada Kamili – Kitabu cha Kiada cha Maadili 138. Vikao vya furaha 139. Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje? 140. Visa vya wachamungu 141. Falsafa ya Dini 142. Kuhuzunika na Kuomboleza 143. Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah 144. Mjadala wa Kiitikadi 145. Kuonekana kwa Allah 146. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza) 147. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili) 321

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 321

8/14/2017 1:18:44 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

148. 149. 150. 151. 152. 153. 154. 155. 156. 157. 158. 159. 160. 161. 162. 163. 164. 165. 166. 167. 168. 169. 170. 171. 172. 173. 174. 175. 176. 177. 178.

Ndugu na Jirani Ushia ndani ya Usunni Maswali na Majibu Mafunzo ya hukmu za ibada Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 1 Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 2 Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 3 Abu Huraira Vipengee kadhaa katika Swala ya Jamaa na Msikiti. Mazingatio kutoka katika Qur’an - Sehemu ya Kwanza Mazingatio kutoka kaitka Qur’an - Sehemu ya Pili Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya kwanza Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya Pili Shia na Qur’ani – Majibu na Maelezo Falsafa ya Mageuzi ya Imam Husein (a.s) Amali za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani Elimu ya Tiba za Kiislamu - Matibabu ya Maimamu Uislamu Safi Majlisi za Imam Husein Majumbani Je, Kufunga Mikono Uislam wa Shia Amali za Makka Amali za Madina Asili ya Madhehebu katika Uislamu Sira ya Imam Ali kuhusu Waasi Ukweli uliofichika katika neno la Allah Uislamu na Mifumo ya Uchumi Umoja wa Kiislamu na Furaha Mas’ala ya Kifiqhi Jifunze kusoma Qur’ani as-Sahifatul Kamilah as-Sajjadiyyah 322

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 322

8/14/2017 1:18:44 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

179. Hayya ‘Alaa Khayri’l-’Amal Katika Adhana 180. Ukweli kuhusu Funga ya Siku ya Ashura 181. Dua za Miezi Mitatu Mitukufu (Rajabu, Shaabani na Ramadhani) 182. Uadilifu katika Uislamu 183. Mahdi katika Sunna 184. Maswali Ya Uchunguzi Kuhusu Uislam 185. Kazi na Bidii ni njia ya maendeleo 186. Abu Talib – Jabali Imara la Imani 187. Ujenzi na Utakaso wa Nafsi 188. Vijana na Matarajio ya Baadaye 189. Historia maana na lengo la Usalafi 190. Ushia – Hoja na Majibu 191. Mateso ya Dhuria wa Mtume (saww) 192. Maombolezo – Msiba wa Bwana wa Mashahidi (a.s.) 193. Shahidi kwa Ajili ya Ubinadamu 194. Takwa 195. Upotoshaji Dhahiri katika (Turathi) Hazina ya Kiislamu 196. Amirul Muuminina (as) na Makhalifa 197. Tawheed Na Shirki 198. Kuvunja hoja iliyotumika kutetea Uimamu wa AbuBakr 199. Adabu za vikao na mazungumzo 200. Hija ya Kuaga 201. Uwazi baina ya Maslahi na Vikwazo 202. Fadhila za watukufu watano katika Sahih Sita 203. Mdahalo baina ya Mwanachuoni waKisunni na Kishia (Al- Muraja’aat) 204. Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (as) 205. Imam Husain ni Mfumo wa Marekebisho na Mageuzi 206. Mtazamo kuhusu msuguano wa Kimadhehebu 207. Nchi na Uraia – Haki na wajibu kwa Taifa

323

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 323

8/14/2017 1:18:44 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

208. Mtazamo wa Ibn Taymiyyah juu ya Imam Ali (as) 209. Uongozi wa Kidini – Maelekezo na Utekelezaji wa Kijamii 210. Maadili ya Ashura 211. Mshumaa – Shahidi na Kifo cha Kishahidi 212. Mizani ya Hekima – Hadithi za Ahlul Bait (as) – Sehemu ya Kwanza 213. Imam Ali na Mambo ya Umma 214. Imam Ali na Mfumo wa Usawa 215. Uimamu na Tamko la Kutawazwa 216. Mfumo wa Wilaya 217. Vipi Tutaishinda Hofu? 218. Kumswalia Mtume ni Ufunguo wa Utatuzi wa Matatizo 219. Maeneo ya Umma na Mali Zake 220. Nahju ‘L-Balagha– Majmua ya Khutba, Amri, Barua, R­isala, Mawaidha na Semi za Amirul-Muuminin Ali bin Abu Talib (a.s.) 221. Mukhtar – Shujaa aliyelipiza kisasi dhidi ya wauaji wa Imam Husein (as) hapo Karbala 222. Mazingatio Katika Swala 223. Imam Hasan na Mfumo wa Kujenga Jamii 224. Vyakula Na Vinywaji 225. Kuelewa Rehema ya Mwenyezi Mungu 226. Imam Mahdi na Bishara ya Matumaini 227. Mtazamo Mpya - Wanawake katika Uislamu 228. Shia Na Sahaba - Majibu na Maelezo 229. Majanga Na Jukumu la Jamii 230. Shia Na Hadith - Majibu na Maelezo 231. Upotofu Ndani ya Kitabu cha Mitaala kwa Shule za Sekondari 232. Ugaidi Wa Kifikra Katika Medani Ya Kidini 233. Yafaayo kijamii 234. Uswalihina Dhahiri Na Batini Yake 235. Mkakati wa Kupambana na Ufakiri 324

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 324

8/14/2017 1:18:44 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

236. Mwanamke Katika Harakati Za Mageuzi 237. Jihadi 238. Hija Katika Maneno Na Ujumbe Wa Imam Khomeini (R.A) 239. Tiba Ya Maradhi Ya Kimaadili 240. Yusuf Mkweli 241. Taqiyya Kwa Mujibu Wa Sheria Ya KIISLAMU 242. Imam Mahdi (A.S) Imam Wa Zama Hizi Na Kiongozi Wa Dunia 243. Talaka Tatu 244. Safari Ya Kuelekea Kwa Mwenyezi Mungu 245. Hotuba Za Kiislamu Juu Ya Haki Za Binadamu 246. Mashairi Ya Kijamii 247. Ngano Ya Kwamba Qur’ani Imebadilishwa 248. Wito Kwa Waumini: “Enyi Mlioamini” 249. Imam Husain (a.s) ni Utu na Kadhia 250. Imam Husain ni Kielelezo cha Kujitoa Muhanga na Fidia 251. Imam Mahdi ni Tumaini la Mataifa 252. Kuchagua Mchumba 253. Mazungumzo ya Umoja – Ukosoaji na Usahihishaji 254. Utamaduni wa Mwamko wa Kijamii 255. Hekima za kina za Swala 256. Kanuni za Sharia za Kiislamu 257. Utamaduni kufuatana na Qur’ani na Utekelezaji wa Kivitendo (Sehemu ya Kwanza) 258. Kauli sahihi zaidi katika kufafanua Hadithi

325

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 325

8/14/2017 1:18:44 PM


Uwahabi Haukubaliki kwa Hoja za Kiakili wala za Kimapokeo

KOPI ZIFUATAZO ZIMETAFSIRIWA KWA LUGHA KINYARWANDA 1.

Amateka Na Aba’ Khalifa

2.

Nyuma yaho naje kuyoboka

3.

Amavu n;amavuko by;ubushiya

4.

Shiya na Hadithi

5.

Kor’ani Nziranenge

6.

Kwigisha Mu Buryo Bw’incamake Uka Salat Ikotwa

7.

Iduwa ya Kumayili

ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION KWA LUGHA YA KIFARANSA 1.

Livre Islamique

326

09_17_Uwahabi Haukubalik_14_August_2017.indd 326

8/14/2017 1:18:44 PM


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.