Uwanja wa mkusanyiko

Page 1

UWANJA WA MKUSANYIKO ‫صحراء املحشر‬

Mfululizo wa Mihadhara ya: Sayyid Hasan Nasrullah

Kimetarjumiwa na: Alhaj Hemedi Lubumba

Kimeandaliwa na: Taasisi ya Dar al-Mawaddah

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 1

1/17/2017 1:14:20 PM


‫ترجمة‬

‫صحراء املحشر‬ ‫سلسلة محاضرات لسماحة السيد حسن نصرهللا‬

‫إعداد‬ ‫داراملودة للترجمة والتحقيق والنشر‬

‫من اللغة العربية الى اللغة السواحلية‬

‫‪1/17/2017 1:14:20 PM‬‬

‫‪19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 2‬‬


©Haki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: 978 - 9987 –17 – 013 – 5 Mfululizo wa Mihadhara ya: Sayyid Hasan Nasrullah Kimetarjumiwa na: Alhaj Hemedi Lubumba Kimeandaliwa na: Taasisi ya Dar al-Mawaddah Kimehaririwa na: Alhaj Ramadhani S.K. Shemahimbo Kimepitiwa na: Mujahid Rashid Kimepangwa katika Kompyuta na: Al-Itrah Foundation Toleo la kwanza: Mei, 2017 Nakala: 1000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. - 19701, Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 / 2127555 Barua Pepe: alitrah@yahoo.com Tovuti: w.w.w.alitrah.info

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 3

1/17/2017 1:14:20 PM


YALIYOMO Dibaji.............................................................................................. 1 Neno la Mchapishaji...................................................................... 2 Dibaji.............................................................................................. 5 Utangulizi....................................................................................... 7 Ukweli wa Mauti na Maswali ya Lazima...................................... 8 Vipi Kuhusu Roho?...................................................................... 11 Matokeo ya Lazima Yatokanayo na Kuutambua Ulimwengu wa Akhera................................................................ 12 Dalili zinazothibitisha uwepo wa maisha ya baada ya mauti...... 16 Faslu ya Kwanza:......................................................................... 23 Kaburi na barzakh ndio kituo cha kwanza cha akhera................. 23 Dalili inayothibitisha uwepo wa ulimwengu wa Barzakh........... 26 Ufafanuzi kuhusu hatua za ulimwengu wa Barzakh.................... 29 Mgawanyo wa viumbe katika ulimwengu wa Barzakh............... 32 Hali za mashahidi katika ulimwengu wa Barzakh....................... 38 Kauli kuhusu kundi la tatu........................................................... 40 Mawaidha kwa ajili ya nafsi na Waumini.................................... 43 Faslu ya Pili: ............................................................................... 50 Hali za Kiyama kikubwa na misukosuko yake............................ 50 Utangulizi..................................................................................... 51 Matumizi ya Kilugha baina ya maana halisi na maana isiyo halisi......................................................................... 51 Maana halisi na maana isiyo halisi katika Qur’ani...................... 53 Viashiria vya Kiyama Kikubwa na Matukio yake....................... 55

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 4

1/17/2017 1:14:20 PM


Hali ya Viumbe Hai Katika Siku ya Kiyama............................... 58 Allah atawafishaje?...................................................................... 59 Ulimwengu Utakavyokuwa Siku ya Kiyama............................... 62 Tafakari fupi juu ya ushahidi wa maandiko ya Qur’ani............... 65 Kuwahuisha maiti na kurudi kuwakusanya................................. 70 Kusimama mbele ya Allah kwa ajili ya hesabu........................... 74 Basi ni kitu gani kitakachomfaa mtu siku hiyo?.......................... 82 Muhtasari kuhusu Sirati na Matokeo.......................................... 86 Neno Kuhusu Lengo la Utafiti Huu............................................. 88 Tukio la Karbala Katika Kipimo cha Kujituma kwa Ajili ya Akhera.......................................................................................... 93

v

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 5

1/17/2017 1:14:20 PM


19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 6

1/17/2017 1:14:20 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬

DIBAJI

K

itabu hiki ni toleo la Kiswahili la taasisi ya Al Itrah Foundation. Chapisho lake limelenga kukidhi mahitaji ya kiroho ya zama hizi pamoja na Ubongo na fikra zinazokuwa za Muislam. Jitihada kubwa zimefanywa na Taasisi kuweka chapisho hili la Kiswahili katika msingi wa haki na wenye kukubalika katika Uislam. Unaombwa kwa Taadhima ukisome kitabu hiki katika malengo yaliyokusudiwa. Pia Unaombwa kuwasilisha kwetu maoni yako huru juu ya chapisho letu hili, jambo ambalo tutashukuru sana. Kutangaza ujumbe wa Uislam ni kazi ambayo inahitaji ushirikiano wetu sote. Taasisi inakuomba kuungana na kushirikiana kama ilivyoagizwa katika aya ya Qur’an: (Surat Saba’ 34:46). Na rehma za Allah ziwe juu yako.

Wako katika Uislam Al Itrah Foundation Barua Pepe: alitrah@yahoo.com SMS: +255 778 300 140

1

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 1

1/17/2017 1:14:20 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬

NENO LA MCHAPISHAJI

K

itabu ulichonacho mikononi mwako kimetarjumiwa kutoka kitabu cha Kiarabu kwa jina la, Sahraa’ al-Mahshar, nasi tumekiita kwa Kiswahili, Uwanja wa Mkusanyiko. Kitabu hiki ni mkusanyiko wa khutba za Sayyid Hasan Nasrullah, kiongozi cha chama cha Hizbullah, alizotoa katika majlisi za maombolezo za masaibu ya Karbala katika mwaka 1437 Hijria mwafaka na mwaka 2015 Miladia. Katika majlisi hizi Sayyid amejikita katika kuelelezea maisha ya ulimwengu huu na maisha ya Akhera. Katika khutba zake ametukumbusha wajibu wetu kama waumini na wanadamu wote kwa ujumla makusudio ya kuumbwa kwetu, kama Allah anavyosema katika Qur’ani Tukufu: “Ambaye ameumba mauti na uhai ili awajaribu ni nani miongoni mwenu mwenye vitendo vizuri zaidi. Na Yeye ni Mwenye nguvu, Mwingi wa maghufira.” (2:67) 2

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 2

1/17/2017 1:14:20 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

“Na sikuwaumba majini waniabudu.” (51:56)

na

watu

ila

Hii ni moja kati ya kazi kubwa zinazofanywa na Taasisi ya al-Itrah katika kuwahudumia kielimu wasomaji wake wazungumzao Kiswahili. Na kwa maana hiyohiyo, imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa lengo lake lilelile la kuwahudumia Waislamu, hususan wanaozungumza Kiswahili. Hivyo, ni matumaini yetu kwamba wasomaji wetu watanufaika vya kutosha kutokana na kitabu hiki, kwani tumekiona ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya kielimu, sayansi na tekinolojia ambapo upotoshaji wa historia, ngano na hekaya ni vitu ambavyo havina nafasi katika vichwa vya watu. Tunamshukuru Sayyid Nasrullah kwa kazi kubwa anayofanya kwa ajili ya Umma huu wa Waislamu, Allah Azza wa Jalla amlipe kila kheri hapa duniani na huko Akhera Halikadhalika tunamshukuru ndugu yetu Alhaj Hemedi Lubumba kwa kukitarjumi kwa lugha Kiswahili kitabu hiki, insha’Allah na yeye Allah Azza wa Jalla amlipe kila la kheri hapa duniani na huko Akhera pia. Aidha hatuwasahau wale wote 3

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 3

1/17/2017 1:14:20 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

waliochangia kwa namna mmoja au nyingine mpaka kufanikisha kuchapishwa kwa kitabu hiki, Allah Mwenye kujazi awalipe wote malipo mema hapa duniani na huko Akhera pia. Mchapishaji Al-Itrah Foundation

4

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 4

1/17/2017 1:14:20 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬

DIBAJI

S

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

ote tunatambua kwamba sisi ni wenye kupita katika dunia hii, sawa uwe ni mrefu muda tutakaoishi katika dunia hii au ni mfupi. Na jambo hilo linaafikiana na itikadi ya dini yetu ya Uislamu, kama linavyoafikiana pia na itikadi za dini nyingine. Na kwamba uwepo wetu na maisha yetu katika dunia hii yenye kutoweka, si chochote isipokuwa ni mtihani unaolazimu mtu kupata neema za milele au kustahili adhabu ya milele. Na kwamba dunia ni sehemu ya mapito na chumo la Akhera. Na kwamba mauti ni tangazo la kuisha kwa kazi na kuanza kwa malipo, na ni daraja la kuvukia kutoka katika ulimwengu huu wa muda kwenda kwenye ulimwengu wa kudumu. Na kwamba yenyewe (mauti) ndio ukweli mkubwa usio na shaka, mzito na mchungu, na ndio haki kubwa ambayo haiwezekani kuikimbia. Hakika kukumbusha daima mauti na hesabu na Siku ya Kiyama, kunalirudisha upya kwenye udhibiti 5

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 5

1/17/2017 1:14:20 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

wa uwelewa, lile lengo la msingi la maisha ya mwanadamu. Na kunamwepusha na mtelezo, usahaulifu na mghafiliko kuhusu haki hii ya lazima. Na Mheshimiwa Sayyid Hasan Nasrullah, Mwenyezi Mungu amhifadhi, amewasilisha mazungumzo kuhusu mauti, uwanja wa mkusanyiko, na yale yatakayompata mwanadamu katika maeneo hayo mawili. Aliwasilisha hayo ndani ya mikesha ya Siku za Ashura, mnamo mwaka 1437 A.H. sawa na mwaka 2015 A.D.1 Na ni kutokana na umuhimu wa mihadhara hii miwili, tumeona ni muhimu kuiandika na kuitoa katika kitabu hiki, na hatimaye kuiwasilisha kwa msomaji mpendwa. Tunamuomba Mwenyezi Mungu atupe sisi na ninyi hatima njema na kufuzu kukubwa.

1

  Ni katika mikesha miwili ya mwezi saba na mwezi tisa Muharam, ­mnamo mwaka 1437 A.H. sawa na tarehe 20 na 22 Oktoba 2015. 6

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 6

1/17/2017 1:14:20 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬

UTANGULIZI Kukumbuka Mauti na Ulimwengu wa Akhera:

M

wenyezi Mungu amesema ndani ya Kitabu chake kitukufu:

َ َ َ َّ َ َ ْ‫َ آ‬ ‫أ َّم ْن ُه َو قا ِن ٌت آن َاء الل ْي ِل َس ِاج ًدا َوقا ِئ ًما َي ْحذ ُر ال ِخ َرة َو َي ْر ُجو‬ َ َ‫َ ْ َ َ َ ّ ُ ْ َ ْ َ ْ َ َّ َ َ ْ َ ُ َ َ َّ َ ا‬ ۗ ‫ين ل َي ْعل ُمو َن‬ ‫رحمة رِب ِه ۗ قل هل يست ِوي ال ِذين يعلمون وال ِذ‬ َ ْ‫َّ َ َ َ َ َّ ُ ُ ُ أ‬ َ ‫ال ْل‬ ‫اب‬ ‫ب‬ ‫ِإنما يتذكر أولو‬ ِ “Je, Afanyaye ibada nyakati za usiku kwa kusujudu na kusimama akitahadhari na Akhera, na akitaraji rehema za Mola Wake. Sema: Je, wanalingana sawa wale ambao wanajua na wale ambao hawajui? Hakika wanaokumbuka ni wenye akili tu.”2

Katika mazungumzo yafuatayo tutazungumzia mas’ala ya mauti na Akhera na mambo yanayohusu hayo mawili, kama vile Siku ya Kiyama, ulimwengu wa Akhera na mengineyo. Na kupitia uchunguzi wetu   Sura Zumar; 39: 9.

2

7

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 7

1/17/2017 1:14:20 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

tutaibua lile lililo wajibu wetu na jukumu letu mbele ya ulimwengu wa Akhera, kama watu tunaoishi katika dunia hii. Na kwa kweli mas’ala hii ina umuhimu mkubwa, kwani mambo mengi ya maisha ya mwanadamu na matendo yake katika dunia hii yanategemea ufahamu wake kuhusu mas’ala ya mauti na Akhera. Na kama mfano tu, hebu tutazame suala la Karbala, hakika yale matukio yaliyotokea Karbala na matokeo yaliyopatikana kutokana na matukio hayo, yote kwa daraja la kwanza sababu zake na chanzo chake kinarejea kwenye mas’ala hii, mas’ala ya dunia na Akhera, na mtazamo kuhusu Akhera, na namna ya kuamiliana nayo. Sawa iwe kwa upande wa kambi ya Imam Husein au kambi ya maadui.

Ukweli wa Mauti na Maswali ya Lazima: Na kabla ya kuzama katika uchunguzi, ni vizuri tukaashiria kwamba, kuna ukweli usiopingika ambao watu wote wanaukubali, na umewakusanya watu wote tangu zama za Adam  mpaka leo hii, na bado utaendelea kuwakusanya pamoja, nao ni ukweli wa mauti, kwamba watu wote ni lazima watakufa. Hakuna ubishi katika suala hili, na hata kama tutazunguka pande zote za ulimwengu hatutampata mtu mwenye akili timamu anayedai kwamba yeye ataishi milele hapa duniani, bali 8

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 8

1/17/2017 1:14:20 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

wote kila mmoja kwa nafsi yake anakiri kwamba atakufa. Katika hilo hakuna tofauti baina ya mwenye kuamini uwepo wa Allah na mwenye kukanusha uwepo Wake. Wala baina ya mwenye kumpwekesha na mwenye kumshirikisha, wale wenye kuabudu masanamu na mawe, wale wasiokiri uungu wa Mungu au wa chochote, wote wana yakini na mauti. Watu wa kipindi chote cha historia mpaka Siku ya Kiyama, wote wanakusanywa na ukweli huu, ukweli wa mauti ambayo Allah amewakahari kwayo waja Wake, kama anavyosema Kiongozi wa Waumini Ali bin Abutalib katika Dua ya Asubuhi: “Na akawakahari waja Wake kwa mauti na kutoweka.� Hivyo sisi tuko mbele ya ukweli usiokimbiwa, usio na mjadala, kwamba mtu vyovyote atakavyokuwa, bila kujali imani yake, au kiwango cha fikra zake, au itikadi yake, awe ana dini au hana dini, ni lazima atakufa. Isipokuwa ni kwamba, ni lazima ukweli huu uzalishe swali kubwa na la msingi, kwamba ni kitu gani kitafuata baada ya mauti? Nalo ni swali la kimantiki, la kawaida na la halali. Ni kitu gani kitafuata baada ya mauti? Kitu gani kitafuata baada ya kufa kwetu kama watu? Ndugu zetu waliokufa, na jamaa zetu waliokufa, hawa wamekwenda wapi ilihali dunia ingali ipo? Kitu gani kinawangojea? Kadhalika kipi kitafuata baada ya dunia hii kutoweka? Na kipi kitafuata baada ya ku9

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 9

1/17/2017 1:14:20 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

toweka ulimwengu huu? Kwani wanadamu kwa ujumla wao, na wasomi kwa upekee wao, wote wanakubaliana kwamba ulimwengu huu kitabia unaelekea upande wa kutoweka, upande wa kifo chake kitabia, sasa basi, ni kipi kitafuata baada ya hapo? Tunachokifahamu sote kwa uchunguzi na maumbile ni kwamba mtu anapokufa, na kila siku kuna watu wanaokufa ambao tunawaona wakiwa miili iliyotulia mbele yetu, ni nafsi au roho huwa imetoka kutoka katika mwili wa mtu huyu, mwili ambao wakati mwingine huwa ungali na viungo salama na wenye afya. Hauna maradhi yoyote wala tatizo au mgogoro wowote wa kiafya, lakini umejiwa na mauti na hatimaye roho imetoka na kutufanya tuwe mbele ya mwili uliotulia. Kisha mwili huu uliotulia, ambao kwa kawaida watu wengi huusindikiza na kuutekelezea wajibu za kidini, kila mmoja kwa mujibu wa dini yake, ambao huuzika katika kaburi katika kipande kidogo cha ardhi, na kuufukia kwa udongo, ambapo baada ya hapo athari zake hukatika na habari zake hutoweka, mwili huu utapatwa na nini ndani ya kaburi hili? Maiti huyu atapatwa na nini? Na pia sisi tunatambua kwamba, mwili huu mwisho wa siku baada ya muda fulani utatoweka, 10

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 10

1/17/2017 1:14:20 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

utaliwa na wadudu, na hakutabakia katika mwili huo isipokuwa muundo wa mifupa, kisha baada ya muda mrefu hakitabakia kitu katika mwili huo isipokuwa baadhi ya mifupa iliyooza,3 na baada ya muda mrefu huenda kisibakie kitu katika mwili huo isipokuwa udongo tu. Na wafiwa wa maiti huyu hawatakuwa na la kufanya isipokuwa kurudi (kutoka mazikoni) ili kwenda kupokea pole. Kisha watamkumbuka maiti wao kwa siku kadhaa au wiki kadhaa, lakini baada ya muda wataendelea na maisha yao ya kawaida, na kama isingelikuwa hivyo basi maisha yasingeendelea. Hakika hili linajulikana kwa wote.

Vipi Kuhusu Roho? Roho hii iliyokiacha kiwiliwili kilichogeuka kuwa mwili uliyotulia, je nayo pia inakufa? Au hubaki hai katika hali yake, kwa kuendelea kuwa na akili, hisia na kutambua yanayoendelea pembeni yake? Je huendelea kuhisi maumivu, huzuni na furaha? Ni ipi hali ya roho hii ambayo kwa lugha nyingine ukitaka iite nafsi? Inakwenda wapi? Inaishi wapi? Inakuwa wapi? Ni ipi hatima yake? Na maswali haya yanazalisha yenyewe maswali mengine, mfano: Je kuna ulimwengu mwing  Wanasema: Hivi kweli tutarudishwa hali ya kwanza? Pindi tutakapokuwa mifupa iliyooza? (Sura Naziat: 10 – 11).

3

11

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 11

1/17/2017 1:14:20 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

ine baada ya mauti? Ni ulimwengu upi huu? Ni zipi hali zake? Ni yapi mazingira yake? Ni zipi kanuni zake, vigezo vyake na tabia zake? Je ulimwengu huo ni sawa na ulimwengu wetu, au unatofautiana nao? Je kuna mafungamano yoyote baina ya ulimwengu wetu na ulimwengu huo? Je kutakuwa na hesabu katika ulimwengu huo au la? Na kama tutahesabiwa, je ni juu ya jambo tulilolitenda katika dunia hii au ni juu ya kitu gani? Kwa kweli maswali ni mengi nayo ni maswali ya halali na maarufu. Maswali haya na mengineyo, yanahitaji kutaamali na kutafakari kwa kina, kufanya uchunguzi wa kina wa kweli na wa dhati. Kwa sababu maswali hayo yana uhusiano na hatima ya kila mmoja wetu na hatima ya kila tunayempenda. Mtu anapompenda mwingine yeyote – mama yake, baba yake, mkewe, mwanawe, dada yake, kaka yake, ndugu zake na marafiki zake – bila shaka ni lazima atatilia umuhimu suala la kujua hatima yao na mwisho wao, atatafuta hatima yake yeye mwenyewe na hatima yao pia.

Matokeo ya Lazima Yatokanayo na ­Kuutambua Ulimwengu wa Akhera: Tumetaja huko nyuma kwamba, uchunguzi kuhusu hali 12

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 12

1/17/2017 1:14:21 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

na uhalisia wa ulimwengu wa Akhera – ulimwengu wa baada ya mauti - ni jambo la lazima na la dharura, kwa sababu jambo hilo lina uhusiano na hatima ya mtu na mwisho wake. Na hapa tunasema: Hakika uchunguzu huu si uchunguzi wa kutaka tu kujua, bali ni kwamba sisi tunachunguza jambo lenye kutuhusu sisi kwa upande wa hatima yetu na maisha yetu katika ulimwengu huo. Upande wa neema zetu za kudumu au adhabu yetu ya milele, upande wa usalama wetu na amani yetu. Na kwa ajili hiyo uchunguzi huu ni miongoni mwa tafiti zinazohusu hatima yetu ambayo ni lazima iwe na matendo, mipango, mbinu, ratiba na maandalizi, kwa sababu sisi tutakuwa mbele ya safari ndefu na mbele ya maisha marefu. Na la ajabu, na tatizo hili linawagusa wote Waumini na wasiokuwa Waumini, ni kwamba ijapokuwa sisi tunatambua fika kuwa kila mmoja miongoni mwetu hataishi katika dunia hii isipokuwa miaka michache – lakini sisi, na kwa kujaalia kuwa tutaishi kipindi hiki cha muda maalumu, tunasoma, tunabobea katika taaluma, tunafanya tafiti mbalimbali, tunafanya biashara na kazi nyinginezo. Tunajenga majumba, tunakusanya samani na tunaoa. Tunaruzukiwa watoto, tunajiimarisha kimaisha, tunatafuta vyeo, na tunatafuta nguvu ili kuzihami nafsi zetu na kujiweka katika amani sisi na 13

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 13

1/17/2017 1:14:21 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

familia zetu. Tunajali afya zetu na siha za watu, na tunajituma ili kujihakikishia raha na starehe. Na tunafanya mengineyo mengi, yaani sisi tunatoa juhudi zetu nyingi katika kutengeneza na kuboresha mazingira ya maisha yetu haya ya muda mfupi. Ama maisha yetu ya Akhera, ambayo yataendelea na kudumu mamilioni ya miaka, bali ndio maisha ya milele, kwa nini hatujitumi katika kuyafanyia kazi?! Kwa nini hatuyatafakari?! Kwa nini hayatushughulishi?! Kwa nini hatuyafanyii maandalizi?! Kwa nini hatujijengei makazi katika ulimwengu huo?! Kwa nini hatujitengenezei mabustani humo?! Kwa nini hatujiandalii humo amani, usalama, sifa, raha, heshima, utukufu, vyeo na majirani?! Ilihali katika ulimwengu huo kuna adhabu ya moto ambayo haiwezekani hata kufikirika na akili ya mwanadamu. Hivi hatupasi kutenda ili kujiepusha nayo? Adhabu hii ijayo ambayo hakuna yeyote atakayeweza kuikimbia. Utendaji huu kutoka kwetu, kutoka kwa mtu mmoja mmoja na hata kutoka kwa jamii, ni wa ajabu sana. Unapingana na mantiki na akili, bali ni kwamba hauheshimu hata upande wa maslahi na manufaa ya mtu binafsi. Kwani kama mtu atakujia na kukwambia kwamba, tetemeko kubwa litapiga sehemu unayoishi kwa muda wa mwaka

14

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 14

1/17/2017 1:14:21 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

mzima au miaka miwili, na kwamba litaondoka na kila kitu chako, utafanya nini? Bila shaka lazima mhusika ataanza kutafakari namna ya kuuza nyumba yake na kumaliza mambo yake katika eneo hilo na kununua nyumba nyingine katika sehemu nyingine. Bali inawezekana akahama eneo hilo hata bila kujali kitu kingine isipokuwa kusalimika kwake na hatari ijayo. Tambua kwamba anafanya yote hayo kwa habari tu ya kielimu ambayo inaweza kweli ikatimia au isitimie. Na mfano mwingine ni kwamba kama mtu ataambiwa, katika njia uipitayo kuna adui anayevizia au mawe, naye ni lazima apite katika njia hii na si nyingineyo, je taarifa hiyo haimlazimishi kufanya maandalizi ya lazima, atafakari namna ya kuondoa au namna ya kupambana na adui anayevizia, ili aweze kuvuka na kufikia lengo akiwa salama salimini? Mtu ambaye hii ndio hali yake katika kuamiliana na dunia, kwa nini haamiliani kwa njia hiyo hiyo na maisha yake ya milele, na hatima yake na chanzo cha usalama wake, raha yake, neema yake na mustakbali wake wa maisha ya Akhera? Sisi katika miaka michache ya umri wetu tunapanga mipango, tunasoma, tunaandaa ratiba, tunafanya biashara na tunajituma usiku na mchana ili kujihakikishia chakula, vinywaji na mavazi. Ili kujihakikishia usalama na amani, kujilinda dhidi ya adui na kujihakikishia maisha ya kijamii yenye kukubalika 15

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 15

1/17/2017 1:14:21 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

na yenye kuingia akilini. Lakini ni kitu gani tumeandaa kwa ajili ya ulimwengu ujao? Tumeuandalia nini na tumefanya nini mbele yake? Hili ndio swali kubwa. Na kwa kweli ile dhana tu ya uwepo wa ulimwengu na maisha baada ya mauti inatosha kumfanya mtu ajitume na kuelekea upande wa matendo na maandalizi yake. Na hata kama mtu hatafika katika kiwango cha kuwa na yakini na uwepo wa ulimwengu wa Akhera na uwepo wa maisha baada ya mauti, bado ile dhana tu – kimantiki na kiakili – inatosha kumfanya mtu huyo achukue tahadhari, na hivyo ni juu yake kujiandaa na kujiweka tayari kutokana na dhana hii, kwa sababu baada ya mauti hakuna kabisa fursa tena ya kutenda. Ama wale wenye kumwamini Allah, majina Yake na sifa Zake, wenye kuamini uwezo wa Allah usio na mipaka, na ukamilifu Wake na ukarimu Wake, nguvu Zake na uwezo Wake, adhabu Yake na uadilifu Wake, nalo ndio kundi lenye kulengwa na maneno yetu kwa namna ya kipekee, hakika wao ndio wanaostahiki zaidi kujiandaa kwa ajili ya ulimwengu ujao, na wala haifai kwao kamwe kuzembea.

Dalili Zinazothibitisha Uwepo wa Maisha ya Baada ya Mauti:

Sisi tunaamini uwepo wa maisha ya baada ya mauti, na uwepo wa ulimwengu wa Akhera, na kwamba huko kuna 16

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 16

1/17/2017 1:14:21 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

hesabu, thawabu na adhabu juu ya kila tendo analolitenda mwanadamu, na kwamba kuna Pepo na Moto.4 Nami hapa sintoingia katika uwanda mrefu wa dalili, hivyo si vibaya kutaja baadhi ya dalili muhimu katika maudhui niliyoitaja.   Kuna Aya nyingi zitazazo Akhera, kama zilivypokelewa pia riwaya nyingi kutoka kwa Ahlulbayti , ikiwa ni pamoja na kutaja thawabu na adhabu, pepo na moto, mkusanyiko na hesabu. Bali ni kwamba utajo wa mambo haya ni mkubwa zaidi kiasi kwamba haijabaki nafasi yoyote ya shaka juu ya kutokea mambo haya, kwa mwenye kuamini sharia ya Muhammad . Miongoni mwa Aya zenye kutaja hayo ni kauli ya Allah: “Na iogopeni Siku ambayo nafsi haitaifaa nafsi (nyingine) kwa lolote. Wala hayatakubaliwa kwake maombezi (shufaa), wala hakitapokelewa kikomboleo; wala hawatanusuriwa.” (Sura al-Baqarah; 2:48). Na kauli ya Allah: “Mwenyezi Mungu hapana Mola ila Yeye. Kwa yakini atawakusanya Siku ya Kiyama. Halina shaka hilo. Na ni nani mkweli zaidi katika maneno kuliko Mwenyezi Mungu?” (Sura Nisaa: 87). Na kauli ya Allah: “Hakika saa (Kiyama) itakuja, nimekaribia kuificha, ili kila nafsi ilipwe kwa iliyoyafanya.” (Sura Twaha: 15). Na kauli ya Allah: “Hayo ndiyo makazi ya Akhera, tumewafanyia wale wasiotaka kujitukuza duniani wala ufisadi. Na mwisho ni wa wenye takua.” (Sura al-Qaswasw: 83). Ama upande wa riwaya kutoka kwa Ahlulbayti  imepokewa kutoka kwa Mtume  kuwa alisema: “Mauti ni lazima. Mauti yamekuja na yalichonacho. Yamekuja na raha na starehe ya peponi kwa watu wa nyumba ya kudumu. Ambao juhudi zao zilikuwa kwa ajili ya nyumba hiyo na hiyo ndio ilikuwa hamu yao. Na mauti yamekuja na majuto na masikitiko na hasara ya kuingia katika moto uwachomao watu wenye ghururi, ambao juhudi zao zilikuwa ni kwa ajili ya moto huo na hio ndio ilikuwa hamu yao.” (al-Kafiy, kitabu cha jeneza, mlango wa hekima, hadithi ya 27). Na siku moja alimwambia Abu Dhari: “Ewe Abu Dhari! Jitathmini kabla hujahesabiwa, hakika kufanya hivyo kutarahisisha hesabu yako kesho. Jipime kabla hujapimwa. Na jiandae na maonyesho makubwa siku utakayofichuliwa na hakuna chochote kitakachojificha kwa Allah.”

4

17

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 17

1/17/2017 1:14:21 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

Kwanza: Miongoni mwa mambo yanayosisitiza uwepo wa uhai baada ya mauti, ni kwamba Manabii wote wa Allah waliotumwa katika historia yote ya mwanadamu – ambao kwa mujibu wa baadhi ya riwaya idadi yao ni 124,0005 – wote wametueleza kuhusu maisha ya baada ya mauti. Hawa Manabii 124,000 wote walikuwa maarufu miongoni mwa watu wao kwa ukweli, uaminifu, wema na usalama, na wote hawa wametupa habari hiyo (ya maisha baada ya mauti) kutoka kwa Allah Mtukufu.6 Kama   Riwaya nyingi zimetaja idadi hii, miongoni mwazo ni ile iliyopokewa ndani ya kitabu al-Khiswal kutoka kwa Mtukufu Mtume  alipoulizwa na Abu Dhari kuhusu idadi ya Manabii, akasema: “Manabii laki moja na ishirini na nne elfu.” (Mizanul-Hikmah, Juz. 10, Hadithi ya 19495). Na miongoni mwa hizo ni ile iliyopokewa ndani ya Aamaliy kutoka kwake: “Allah ameumba Manabii laki moja ishirini na nne elfu, na mimi ndiye mbora wao kwa Allah, na wala si majivuno.” 6   Imethibiti katika sharia ya Uislamu kwamba Manabii wote kuanzia kwa Adam  mpaka kwa Nabii wa Uislamu , wote wameshirikiana katika kuwalingania watu kwenye imani ya kumwamini Allah Mmoja peke yake na kuamini siku ya mwisho. Na Qur’ani imetusimulia hilo katika eneo zaidi ya moja. Imepokewa kuhusu Nuhu  kauli ya Allah: “Hakika tulimtuma Nuh kwa watu wake. Akasema: Enyi watu wangu! Mwabuduni Mwenyezi Mungu, hamna Mungu mwingine zaidi Yake. Hakika mimi ninawahofia na adhabu ya siku iliyokuu.” (Surat Aaraf: 59). Na kuhusu Nabii Ibrahim : “Na aliposema Ibrahim: Ewe Mola Wangu! Ufanye huu uwe mji wa amani na uwaruzuku wakazi wake matunda, wale wanaomwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho katika wao. Akasema Mwenyezi Mungu: Na mwenye kukufuru pia nitamstarehesha kidogo; kisha nitamsukumiza katika adhabu ya Moto; napo ni mahali pabaya 5

18

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 18

1/17/2017 1:14:21 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

ambavyo pia vitabu vya mbinguni alivyoviteremsha Allah juu ya Manabii, navyo vyote vimetueleza kuhusu ulimwengu huo na kuhusu maisha hayo. Qur’ani Tukufu, kitabu cha milele na cha mwisho, na ambacho muujiza wake umethibiti kwa dalili za kiakili na kwa nukuu, kina takriba Aya Tukufu elfu moja zinazozungumzia ulimwengu wa Akhera na matukio yatakayotokea humo baada ya mauti. Kabla ya Kiyama na baada yake, kuanzia Pepo na Moto, kudumu kwake na mfano wa hayo. Kiasi kwamba hadi kuna Sura katika Qur’ani ambazo majina yake yana uhusiano na ulimwengu wa Akhera, kama vile Sura al-Jathiyah, al-Waqiah, al-Hashri, al-Mumtahinah, at-Taghabun, al-Haqah, al-Qiyamah, at-Takwiri, alInfitar, al-Ghashiyah, Zilzalah, na al-Qariah. Kama ambavyo pia kuna baadhi ya Sura ambazo madhumuni yake yote yanahusu maudhui hii hata kama jina kabisa pa kurejea.” (Sura al-Baqarah: 126). Na kuhusu Yusuf: “Ewe Mola Wangu! Hakika umenipa utawala na umenifunza tafsiri ya matukio. Ewe Mvumbuzi wa mbingu na ardhi! Wewe ndiye Mlinzi wangu katika dunia na Akhera. Nifishe hali ya kuwa ni Mwislamu na unikutanishe na watu wema.” (Sura Yusuf: 101). Na kuhusu Musa: “Na utuandikie mema katika dunia hii na katika akhera. Sisi tunarejea Kwako. Akasema: Adhabu Yangu nitamsibu nayo nimtakaye; na rehema Yangu imekienea kila kitu; nitaiandika kwa ajili ya wale wanaoogopa, na wanaotoa Zaka na wanaoziamini Ishara Zetu.” (Sura Aaraf: 156). Na nyingine nyingi zenye kuzungumzia Manabii waliotangulia kabla ya ujumbe wa Uislamu. 19

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 19

1/17/2017 1:14:21 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

la Sura husika halina uhusiano nayo, kama vile Sura al-Insan. Aidha ni kwamba, miongoni mwa mambo yanayothibitisha na kusisitiza uwepo wa ulimwengu huo na mas’ala hii ni ule ulazima utokanao na uadilifu wa Mungu. Imani yetu juu ya uadilifu wa Allah Mtukufu inalazimu kuwepo na maisha baada ya mauti, kwa sababu Waumini na watu wema katika dunia hii, kuanzia kwa Adam  mpaka siku ya kusimama Kiyama, wengi wao hawajapata malipo ya matendo yao mema. Wao wanauliwa, wanakufa kishahidi, wanaumia na wanakutana na matatizo mazito katika maisha haya, wakati ambapo wengine wanaishi kwa raha. Hivyo basi ni lazima kuwepo na ulimwengu mwingine ambao uadilifu wa Mungu utawapa hawa – Manabii 124,000 na maelfu ya waumini, watu wema na mashahidi waliopita katika historia yote ya mwanadamu - malipo ya matendo yao mema. Ni lazima kuwepo ulimwengu mwingine ambao humo watalipwa kwa kujitolea kwao, kwa majeraha yao, kwa machungu yao, kwa maumivu yao, kwa subira yao, kwa uvumilivu wao, kwa ufukara wao, kwa misukosuko na mitihani waliyoivumilia katika dunia hii kwa ukweli na ikhlasi. Aidha pia kwa upande mwingine, madhalimu, waovu, madikteta, makatili, wauaji, ambao wameijaza 20

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 20

1/17/2017 1:14:21 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

ardhi dhulma, uonevu, ufisadi na kiburi, watu mfano wa Firaun na Namrud7 na wale waliokuwa kabla yao na waliokuja baada yao, na kwa kweli madhalimu ni wengi katika ardhi hii, hawa bado hawajapata malipo yao duniani, hivyo uadilifu wa Mungu unalazimu kuwepo na ulimwengu mwingine ili na hawa nao wapate 7  Ama Firaun yeye ni muovu wa zama za Nabii Musa, alijitakabarisha ardhini na kuwakandamiza wana wa Israil, na akajitangizia umola. Ametajwa mara kadhaa ndani ya Qur’ani ikiwemo kauli ya Allah: “Hakika Firauni alitakabari katika nchi akawagawa watu wake makundi. Akidhoofisha taifa moja miongoni mwao, akiwachinja watoto wao wa kiume na akiwaacha watoto wao wa kike. Hakika yeye alikuwa katika wafisadi.” (Sura al-Qaswasw: 4). Na kauli ya Allah: “Je, imekujia hadithi ya Musa? Alipomwita Mola Wake katika bonde takatifu la Tuwaa: Nenda kwa Firauni. Kwani hakika yeye amepituka mpaka. Mwambie je, unataka kujitakasa? Na nikuongoze kwa Mola Wako upate kumcha? Basi akamwonyesha Ishara kubwa. Lakini akakadhibisha na akaasi. Kisha akarudi nyuma na akafanya juhudi. Akakusanya akanadi. Akasema: Mimi ndiye mola wenu mkuu. Basi Mwenyezi Mungu akamshika kumwadhibu kwa la mwisho na la kwanza.” (Sura Naziat: 15 – 25). Na kauli ya Allah: “Na hakika tuliwaokoa wana wa Israili katika adhabu ya kuwadhalilisha. Ya Firauni. Hakika yeye alikuwa jeuri katika wenye kupituka mipaka.” (Sura Dukhan: 30 – 31). Ama Namrud yeye ni muovu wa zama za Nabii Ibrahim . Ni miongoni mwa wafalme wa Babilon, Mungu alimpa ufalme wa kuwatawala jamaa zake na mara akaingiwa na kiburi hadi akajitangazia umola. Ametajwa katika Qur’ani katika kauli ya Allah: “Je, hukumjua aliyehojiana na Ibrahim juu ya Mola Wake kwa sababu Mwenyezi Mungu alimpa ufalme? Ibrahim aliposema: Mola Wangu ni yule ambaye huhuisha na kufisha. Yeye akasema: Mimi pia na huhuisha na kufisha. Ibrahim akasema: Hakika Mwenyezi Mungu hulichomoza jua mashariki, basi wewe lichomoze magharibi. Akafedheheka yule aliyekufuru, na Mwenyezi Mungu hawaongozi watu madhalimu.” (Sura al-Baqarah: 258). 21

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 21

1/17/2017 1:14:21 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

hesabu yao, walipwe na kuadhibiwa kwa makosa yao, ufisadi wao, jeuri yao na ukatili wao dhidi ya waja wa Mwenyezi Mungu na viumbe Wake. Hivyo basi, ni lazima kuwepo na ulimwengu huo na ni lazima siku hiyo itafika.

22

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 22

1/17/2017 1:14:21 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

FASLU YA KWANZA Kaburi na Barzakh ndio Kituo cha Kwanza cha Akhera

K

wa kurejea maswali tuliyouliza kwenye utangulizi, tunasema: Hakika kupata majibu ya maswali tuliyouliza huko, kutatufikisha kwenye kupata muhtasari ambao angalau utakuwa umejengeka juu ya misingi ya Uislamu na Qur’ani. Nasi hapa tutazungumzia misingi bila kuingia na kuzama ndani. Kwanza: Sisi tuna yakini na uwepo wa maisha baada ya mauti. Hiyo ni kwa mujibu wa dalili za kiakili na uthibitisho wa Qur’ani Tukufu, na kwamba kuna ulimwengu mwingine tutakaohamia, na kwamba maisha ya wanadamu, maisha ya mtu yeyote yule hayaishi kwa kufa kwake, bali kinachokwisha anapokufa ni hatua moja tu kati ya hatua za maisha yake. Na hata pindi dunia itakapokwisha, bado wanadamu hawatakwisha, bali wanadamu kwa asili yao kuanzia kwa Adam mpaka yule wa mwisho kuumbwa, watahamia katika ulimwengu mwingine kabla ya kusimama Kiyama. Huu ndio msingi na ndio itikadi yetu. Pili: Kwa mujibu wa mafundisho ya itikadi yetu ya Uislamu, maisha ya baada ya mauti yamegawa23

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 23

1/17/2017 1:14:21 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

nyika katika hatua mbili: Hatua ya katikati na hatua kubwa kama taabiri hii itakuwa ni sahihi. Au unaweza kusema kwamba: Hatua ya maandalizi na hatua ya maisha ya kweli ya milele, kama alivyoyaita Allamah Tabatabai mwandishi wa Tafsirul-Mizan. Hivyo dunia ilivyo ni sehemu ya matendo, mtihani na majaribu. Na kuna ulimwengu wa kati ambao unazingatiwa kuwa ni ulimwengu wa kujiandaa kwa ajili ya hesabu na malipo. Na kuna ulimwengu wa tatu, nao ni ulimwengu wa Akhera, ulimwengu wa hesabu na malipo. Huu ulimwengu wa kati unaitwa ulimwengu wa Barzakh, nao ni maarufu pia kwa jina la ulimwengu wa kaburi. Hivyo baina ya maisha ya duniani na Akhera kuna hatua ya kati ambayo kwa mujibu wa istilahi za Kiislamu huitwa ulimwengu wa Barzakh. Ulimwengu huu unaanza punde tu mauti yanapomfika mtu, anapohama kutoka katika dunia hii, na unaendelea mpaka pale Allah atakapotoa idhini ya kusimama Kiyama, kisimamo kikuu. Hatua hii ndio ulimwengu wa Barzakh, na kwa hali ilivyo ni kwamba ulimwengu wa Barzakh unatofutiana baina ya ulimwengu wa mtu mmoja na mwingine. Hiyo ni kwa kulingana na muda na kipindi alichoishi mtu ndani ya ulimwengu huu. Kwa mfano Baba yetu Adam na Mama yetu Hawa ď Š, wao wamo ndani ya 24

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 24

1/17/2017 1:14:21 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

ulimwengu wa Barzakh kuanzia muda waliokufa, na bado wangalimo humo mpaka sekunde hii, na wataendelea kuwemo mpaka Kiyama kitakaposimama. Hivyo basi, muda wa kuishi kwao humo ni mrefu zaidi kushinda muda atakaoishi mmoja wetu. Lakini sote mwisho wetu ni huko. Kila aliyekufa, na kila atakayekufa wote wanakwenda ulimwengu wa Barzakh. Na kama tulivyosema, ulimwengu huu hatuwezi kujua utadumu kwa muda gani, kwa sababu hakuna anayejua wakati kitakaposimama Kiyama isipokuwa Allah peke Yake. Neno Barzakh katika lugha ya Kiarabu humaanisha kizuizi kilichopo baina ya vitu viwili. Hivyo basi ulimwengu wa Barzakh ni kizuizi kilichopo baina ya hawa waliohama kutoka duniani na Akhera, unazuia baina yao na Akhera kwa ajili ya kungojea idhini ya Allah ya kusimama Kiyama na mkusanyiko mkubwa, ambao utawakusanya watu wote kuanzia wale wa zama za Adam mpaka wale wa wakati wa kusimama Kiyama. Na utawajumuisha wote kutoka pande zote. Hivyo inamaanisha kwamba hawawezi kuhamia katika ulimwengu wa Akhera kabla ya kupatikana idhini ya Allah, na wala hawawezi kurudi duniani isipokuwa kwa idhini Yake. Hivyo Barzakh inawazuia katikati baina ya dunia na Akhera. 25

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 25

1/17/2017 1:14:21 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

Kisha baada ya Barzakh inafuata hatua ya pili, hatua ya Kiyama na kuhamia katika ulimwengu wa milele, ambao unaanzia pale Mwenyezi Mungu atakaporudia kuutengeneza tena ulimwengu huu. Na hapo watu watashuhudia yale waliyoyasoma katika Aya Tukufu kuhusu hali ya Kiyama:

َ ْ‫َ ْ َ ُ َ َّ ُ أْ َ ْ ُ َ ْ َ أ‬ ْ َّ ُ ‫الس َم َاو‬ َّ ‫ال ْرض َو‬ ‫ات ۖ َو َب َر ُزوا ِلل ِه ال َو ِاح ِد‬ ‫يوم تبدل الرض غير‬ ِ َْ ‫الق َّه ِار‬ “Siku itakapobadilishwa ardhi kuwa ardhi nyingine na mbingu (pia). Nao watahudhuria mbele ya Mwenyezi Mungu Mmoja, Mwenye nguvu.” (Sura Ibrahim: 48).

Na Allah atahuisha viumbe vyote na kuvileta katika uwanja wa mkusanyiko kwa ajili ya hesabu, na hapa ndipo yataanza matukio makubwa ya Akhera au Kiyama kikubwa.

Dalili Inayothibitisha Uwepo waUlimwengu wa Barzakh: Kimsingi maulamaa na wafasiri wa Qur’ani wametumia Aya za Qur’ani katika kuthibitisha uwepo wa Barzakh. Mwenyezi Mungu anasema:

26

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 26

1/17/2017 1:14:21 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

َ ّ َ َ ‫َح َّت ٰى إ َذا َج َاء َأ َح َد ُه ُم المْ َ ْو ُت َق‬ ‫ال َر ِ ّب ا ْر ِج ُعو ِن ل َع ِلي أ ْع َم ُل‬ ِ ٌ‫صال ًحا ف َيما َت َر ْك ُت ۚ َك اَّل ۚ إ َّن َها َكل َم ٌة ُه َو َقائ ُل َها ۖ َوم ْن َو َرائه ْم َب ْر َزخ‬ َ ِ ِ ِ ِ ِ ِ ِ​ِ َ‫ا‬ َ ‫الصور َف اَل َأ ْن َس‬ ُّ ‫إ َل ٰى َي ْوم ُي ْب َع ُثو َن َفإ َذا ُن ِف َخ في‬ ‫اب َب ْي َن ُه ْم َي ْو َم ِئ ٍذ َول‬ ِ ِ ِ ِ ِ ُ َ ‫َيت َس َاءلو َن‬ “Mpaka yanapomfikia mmoja wao mauti, husema: Mola Wangu nirudishe. Ili nitende mema badala ya yale niliyoyaacha. Wapi! Hii ni kauli aisemayo yeye tu. Na nyuma yao kuna kizuizi mpaka siku watakapofufuliwa. Basi itakapopulizwa parapanda, hapo hakutakuwa na nasaba baina yao siku hiyo, wala hawataulizana.” (Sura Muuminuna: 99 – 101). Hapa Aya inazungumzia hali ya wakati wa kutoka roho, hali ambayo humpata mtu pindi anapotambua kwamba roho yake imeanza kutolewa, na kwamba amefika katika hatua ya kuhama na kuiacha dunia, hapo humwambia Allah kwamba ewe Mola Wangu nirudishe.

Katika hatua hii mtu huwa tayari amegusa hatari inayomkabili. Hufahamu fika kwamba uhai umekwisha na fursa ya kutenda imetoweka, na kwamba atahamia katika nyumba nyingine. Hivyo ameshuhudia hali ya kufa kwake na hatua za kutoka roho yake, na tayari ukweli wa ulimwengu wa Akhera umeanza kuonekana bayana katika macho yake, kama riwaya zinavyotaja, ame-

27

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 27

1/17/2017 1:14:21 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

kwishaanza kuwaona Malaika na mengineyo. Hivi sasa yeye anaona jinsi yanavyotokea makadara ya lazima, hivyo anaomba kwa kusihi apewe fursa ya kurudi. Haya yote hutangulia kabla ya hatua ya Akhera, kabla ya hatua ya kuingia peponi au motoni. Bali ni kwamba jambo hili huanza katika hatua ya kutoka roho, hivyo husema: “Mola Wangu nirudishe. Ili nitende mema badala ya yale niliyoyaacha.” Wakati huo hujiwa na jibu: “Wapi! Hii ni kauli aisemayo yeye tu. Na nyuma yao kuna kizuizi mpaka siku watakapofufuliwa.” Yaani, hakika mwanadamu kuanzia pale anapokufa mpaka muda atakaofufuliwa atakuwa katika ulimwengu maalumu na eneo la Barzakh. “Basi itakapopulizwa parapanda”, pindi viumbe vitakapopewa uhai upya “hapo hakutakuwa na nasaba baina yao siku hiyo, wala hawataulizana.” Watakwenda kwenye hesabu na kwenye uwanja wa mkusanyiko. Hivyo basi, mtu atapita katika hatua ya uhamisho, baina ya hatua ya kifo chake na kufufuliwa kwake kwa ajili ya hesabu, nayo ni hatua ya Barzakh. Na Aya zilizotangulia zinajulisha kwa uwazi kabisa maana hii. Na kwa nyongeza ni kwamba, kuna riwaya nyingi zinazozungumzia kwa undani kuhusu ulimwengu huu. Kama ambavyo pia kuna Aya nyingine zinazojulisha maana hii, tunaacha kuzitaja kwa lengo tu la kutaka kujikita katika kuwasilisha misingi ya maudhui hii. 28

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 28

1/17/2017 1:14:21 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

Ufafanuzi Kuhusu Hatua za Ulimwengu wa Barzakh: Kwanza kabisa tunataja mas’ala ya kiitikadi yaliyothibiti katika dini yetu, bali huenda tukasema kwamba Waislamu wote wameafikiana juu ya mas’ala hiyo isipokuwa wachache miongoni mwa watu wa rai binafsi. Madhumuni ya mas’ala hiyo ni kwamba Allah Mtukuka humtumia maiti malaika wawili watukufu pindi anapozikwa kaburini, ambao humuhoji kuhusu mambo ya msingi: Kuhusu Mola Wake, dini yake, Nabii wake na mengineyo. Akijibu ipasavyo, na ikawa kwa mujibu wa matendo yake na hali yake duniani ni miongoni mwa watu wema, basi Malaika hao humkabidhi kwa Malaika wa neema. Lakini kama atababaika au hakujibu ipasavyo au atazungumza kile kinachoonesha ubaya aliokuwa nao duniani, basi Malaika hao humkabidhi kwa Malaika wa adhabu, na humpata yale yanayoendelea katika kaburi hilo. Hakika wakati huo ni mzito sana, ni nyeti mno wenye kuonesha hatima ya mtu, kimsingi ni wakati huo ambapo huainika hatima ya mtu na hujulikana yeye ni mtu wa safu ipi. Safu ya neema, bila kujali aina na sifa za neema za Barzakh. Au safu ya adhabu na mateso, bila kujali pia aina na sifa za adhabu za ulimwengu wa Barzakh, yote hayo yametajwa na riwaya mbalimbali. 29

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 29

1/17/2017 1:14:21 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

Baada ya hapo ndipo mtu anaposimama katika hatua ngumu zaidi na ya kutisha zaidi, nayo ni hatua ya saa na siku za mwanzo za kuwa ndani ya kaburi. Mtu kutoka miongoni mwetu anapohama kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine, au kutoka mji mmoja kwenda mji mwingine wa nchi hiyo hiyo, kwa sababu ya kubadilisha mazingira, makazi, majirani na mambo, huwa katika hali ya upweke na unyonge mpaka pale anapooana na sehemu husika kisaikolojia. Sasa unaona itakuaje hali ya mtu pindi atakapohama kutoka duniani kwenda katika nyumba hiyo? Hakika misukosuko anayokabiliana nayo wakati wa kutoka roho na hatimaye kuhamia katika nyumba hiyo, yenyewe tu inatosha. Na ni kwa ajili hiyo utaona Manabii , Maimamu , wachamungu na watu wema walikuwa wakilia pindi wanapokumbuka au linapowajia wazo juu ya nyakati hizo. Kuhamia kaburini ni kuhama kutoka kwenye ulimwengu mpana kwenda kwenye shimo finyu ambalo Kiongozi wa Waumini, Ali bin Abutalib  analielezea kwa kusema: “Ni shimo ambalo lau lingezidishwa nafasi yake, na mikono ya mchimbaji wake kufanya wasaa, basi jiwe na udongo vitalikandamiza, na miyanya yake kuzibwa na mchanga uliorundikana!”8 Ni kuhamia kwe8

Nahjul-Balaghah, mlango wa barua zake na mikataba yake na usia wake. Barua ya 45, barua yake kwenda kwa Uthman bin Hunayfu al-Answariy. 30

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 30

1/17/2017 1:14:21 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

nye nyumba ya ugeni na upweke na khofu. Nyumba ya wadudu, ambapo atabaki mtu peke yake bila kuwa na mtu wa kumtetea wala kumsaidia. Maneno yake hayasikiki iwapo ataongea, na wala hana nguvu wala uwezo wa kufanya amali yoyote itakayoweza kubadili mazingira yake au kubadili hali yake mbaya kuwa nzuri. Ni nyumba ya udhaifu kamili na ufakiri kamili. Na yote haya sehemu yake ni kaburini. Na hapa ndipo inapodhihirika kwamba, ulimwengu huo una sifa ya kufichua ukweli, kwa sababu mtu awapo duniani huenda akakosea katika dhana yake, akajiona kwamba ni mtu mwenye uwezo, wasaa na mwenye kujitosheleza, wakati kiukweli ni fakiri, mjinga na asiyeweza lolote kama si kupewa na Allah neema ya elimu, utajiri, mali na cheo. Ama huko, ukweli utafichuka na kutadhihiri kushindwa kwa mtu, ufakiri wake, ujinga wake, udhaifu wake na uduni wake, yote hayo yatakuwa bayana. Kisha katika yaliyopita ongezea suala la mgandamizo wa kaburi, au kama wanavyosema, mbinyo wa kaburi, katika siku au saa za mwanzo za kuteremka kwake kaburini, nalo ni jambo lililotajwa na riwaya pia. Jambo ambalo kwa mujibu wa riwaya zilizopokelewa kwa Sunni na Shia na kwa Waislamu wote ni kwamba hatoepukana nalo isipokuwa watu wachache. Nalo ni jambo linalowajibisha mtu kuchukua tahadhari, kutafakari na 31

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 31

1/17/2017 1:14:21 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

kutaamali, kama ilivyo katika Aya tuliyoanza nayo: “Je, Afanyaye ibada nyakati za usiku kwa kusujudu na kusimama akitahadhari na Akhera, na akitaraji rehema za Mola Wake. Sema: Je, wanalingana sawa wale ambao wanajua na wale ambao hawajui? Hakika wanaokumbuka ni wenye akili tu.” (Sura Zumar: 9). Hivyo kaburi ni miongoni mwa vituo vya Akhera, bali ndio kituo chake cha kwanza. Kisha baada ya kuja Malaika na kumhoji mtu na hatimaye kumuweka katika fungu la watu waovu au watu wema, mwisho wake unakuwa nini? Baada ya hapo watu watakwenda wapi? Jambo hili lina mjadala wa kielimu ambao umewasilisha ndani yake mitazamo na rai za wanafalsafa, wanatheiolojia, na rai ya Qur’ani, nasi hatutaziwasilisha rai hizo hapa kutokana na ufinyu wa wakati. Lakini tutang’amua kutoka katika rai hizo kile kiwango kisicho na shaka ambacho wameshirikiana wote, kile kiwango walichoafikiana ambacho uthibitisho wake ni Qur’ani Tukufu na baadhi ya riwaya sahihi.

Mgawanyo waViumbe Katika Ulimwengu wa Barzakh: Tunapata kutoka katika mjumuiko wa dalili kwamba katika ulimwengu wa Barzakh watu watagawanyika 32

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 32

1/17/2017 1:14:21 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

makundi kadhaa. Kwanza ni kundi la watakaoadhibiwa ambao hawatapata neema. Pili ni kundi la watu watakaopata neema ambao hawataadhibiwa. Tatu ni kundi la watu wa kati kwa kati baina ya makundi hayo mawili ambalo tutalizungumzia baadaye. Hawa watu wa kundi la kwanza, wanapohama tu kutoka katika dunia hii hupokewa na Malaika kwa nguvu, adhabu na mateso ya aina mbalimbali. Ni kina nani hawa? Kabla ya kujibu swali hili hebu tusimame kwenye Qur’ani ambapo inataja kwa ufafanuzi adhabu itakayowapata hawa watu wa kundi la kwanza. Yamekuja ndani ya Qur’ani Tukufu, katika kisa cha Nabii wa Allah Musa  na Firaun, maneno yenye kufafanua hali ya kundi hili, Allah amesema akizungumzia kuhusu Musa :

َ​َْ ُ ُ َ َْْ َّ ُ َ َ َ َ َ َ ُ َ َ َ ‫الل ُه َس ّي َئ‬ ‫اب‬ ‫فوقاه‬ ِ ِ ِ ‫ات ما مكروا ۖ وحاق ِب ِآل ِفرعون سوء العذ‬

“Basi Mwenyezi Mungu akamlinda na ubaya wa hila walizozifanya. Na adhabu mbaya itawazunguka watu wa Firauni.” (Sura Ghafir: 45). Kisha Allah anaiunganisha kauli yake hii na maana ya adhabu mbaya, ambayo anaigawa katika sehemu mbili: Ya kwanza ni ile aliyoitaja katika kauli yake:

33

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 33

1/17/2017 1:14:21 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

ُ َ ُ َ َّ ُ ُ َ َ ْ َ َ ًّ َ َ ًّ ُ ُ َ ْ َ َ َ ُ َ ْ ُ ُ َّ ‫اعة أ ْد ِخلوا‬ ‫النار يعرضون عليها غدوا وع ِشيا ۖ ويوم تقوم الس‬ َ َ ْ َّ َ َ َ ْ َ ْ َ ‫اب‬ ‫ذ‬ ِ ‫آل ِفرعون أشد الع‬ “Wanaonyeshwa Moto asubuhi na jioni.” (Sura Ghafir: 46). Ya pili ni ile iliyopo katika kauli yake: “Na itapofika Saa (patasemwa): Waingizeni watu wa Firauni katika adhabu kali kabisa!” (Sura Ghafir: 46).

Hivyo sehemu ya kwanza ya adhabu ni kule kuonyeshwa kwao moto katika ulimwengu wa Barzakh. Na sehemu ya pili ya adhabu ni ile adhabu watakayoipata siku kitakaposimama Kiyama. Hivyo wao wataendelea kuwa katika adhabu bila kutoka. Lakini unaweza ukauliza ni ipi dalili inayojulisha kwamba kifungu cha kwanza cha Aya hiyo (Sura Ghafir: 46) kinajulisha Barzakh? Swali hilo wamelijibu wafasiri na maulamaa kwamba, kihusishi cha kwanza ni kule kutajwa asubuhi na jioni katika Aya. Tambua kwamba jahanamu ya Kiyama, yaani jahanamu ya milele, haina asubuhi wala usiku, na Aya hapa imetamka bayana kuwa wataoneshwa moto asubuhi na jioni, hivyo inafidisha kwamba jambo hili litatokea kabla ya kuhamia katika jahanamu ya Akhera. Na kihusishi kingine ni kauli ya Allah: “Na itapofika Saa (patasemwa): Waingizeni watu wa Firauni katika adhabu kali kabisa!” (Sura Ghafir: 46). Yenyewe inafidisha kwa uwazi na bayana kwamba Kiyama bado 34

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 34

1/17/2017 1:14:21 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

hakijasimama, na kwamba huku kuoneshwa moto kutatokea kabla ya kusimama Kiyama, hivyo watu wanaonyeshwa moto asubuhi na jioni kabla ya Kiyama kusimama, na pindi Kiyama kitakaposimama basi wakati huo Allah atasema: “Waingizeni watu wa Firauni katika adhabu kali kabisa!” (Sura Ghafir: 46). Na sasa hebu turejee kujibu swali letu. Ni kina nani hawa? Si Firaun peke yake ndiye anayehusika na eneo hili, bali maneno yanawajumuisha mafarao, manamrudi, viburi na mathwaghuti wa kila zama. Yanamjumuisha Abujahli,9 Abulahbi,10na viongozi wa Makurayshi ambao walimpiga vita Mtume wa Allah . Na kwa mujibu wa maelezo ya riwaya ni kwamba yanawajumuisha wale wote waliokunywa ukafiri halisi, yaani wale ambao ukafiri wao ni ukafiri halisi, na dhulma yao ni dhulma halisi, na ujeuri wao ni ujeuri halisi na ukandamizaji wao ni ukandamizaji halisi. Mtu ambaye hali   Yeye ni Amru bin Hisham bin Mughira kutoka kabila la Kinanah.   Yeye ni Abdul-Uzza bin Abdul-Mutalib, baba mdogo wa Mtume , jina lake la ubaba ni Abu Ut’bah, linatokana na jina la mwanawe mkubwa Ut’bah. Isipokuwa ni kwamba baba yake Abdul-Mutalib alimpa lakabu ya Abu Lahbi kutokana na mng’ao wa uso wake. Yeye alikuwa ni wa mwanzo kabisa kati ya watu waliodhihirisha uadui kwa Mtukufu Mtume na ujumbe wake, ametajwa katika Qur’ani katika Sura al-Masadd: “Imeangamia mikono ya Abu Lahab na yeye ameangamia. Haitamfaa mali yake na alichokichuma. Atauingia moto wenye miali. Na mkewe mchukuzi wa kuni. Shingoni mwake mna kamba iliyosokotwa.”

9

10

35

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 35

1/17/2017 1:14:21 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

yake ni hii kamwe hatapata raha baada ya hapo, kwa sababu yeye amechagua dunia kuwa pepo yake, kama alivyosema Imam Husein . Yaani yeye amemiliki kasri, neema ufalme, askari na watu duniani. Amekula, amekunywa, amestarehe, na ametumia mali zake katika kukidhi matamanio yake. Yote haya yatakwisha baada ya mauti, hivyo moja kwa moja itakapotolewa tu roho yake ataingia katika adhabu, uduni, udhalili na mateso. Aya hii inatumika pia kuthibitisha mas’ala mengine. Inajulisha uwepo wa hatua ya kati, nayo ni hatua ya Barzakh, na inajulisha uwepo wa uhai katika ulimwengu huo, kwa sababu haisihi kusema kuwa adhabu itavipata vitu visivyokuwa hai, bali ni kwamba adhabu itakipata kitu hai. Na pia inatumika kuthibitisha uwepo wa moto wa Barzakh ambao si ile Jahanam maarufu. Na inajulisha kwamba adhabu ya ulimwengu wa Barzakh hailingani na adhabu inayongojewa, ile ya siku ya Kiyama, bali hii ya Barzakh yenyewe ni ndogo zaidi ukiilinganisha na hiyo ya siku ya Kiyama. Kwani isingekuwa hivyo basi kusingekuwa na haja ya kuongeza kwamba “Na itapofika Saa (patasemwa): Waingizeni watu wa Firauni katika adhabu kali kabisa!” kama adhabu ya siku ya Kiyama isingekuwa ni kali zaidi kuliko adhabu ya Barzakh.

36

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 36

1/17/2017 1:14:21 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

Na hebu tuashirie hapa kwamba maneno haya haya yanasihi katika upande wa Pepo ya siku ya Kiyama, kwamba nayo ni ya juu zaidi kuliko neema za Barzakh. Imepokewa katika riwaya kadhaa kwamba watakaoadhibiwa katika Barzakh watasema: ‘Ewe Mola Wetu usikisimamishe Kiyama.’ Kwa sababu wao wanaona mateso yao na wanajua kwamba adhabu inayowangojea ni mbaya zaidi.11 Kinyume na wale watakaokuwa katika neema katika Barzakh, wenyewe watasema: ‘Ewe Mola Wetu! Kisimamishe Kiyama.’ Kwa sababu watakuwa wamejibashiria neema ya juu na tukufu zaidi kuliko ile waliyonayo katika ulimwengu wa Barzakh.12 Ama kundi la pili, kwa mujibu wa riwaya ni kwamba kundi hili linawajumuisha wale waliokunywa imani halisi. Yaani wale ambao imani yao duniani ilikuwa ni imani safi nyeupe isiyo na doa. Miongoni mwa watu hao ni Manabii, Mitume, Mawasii maasumina  na pia mashahidi, ambao tutasimama kidogo ili tutaje   Nayo ni hadithi iliyopokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq kwamba: “Roho za makafiri ziko motoni zinaoneshwa moto, wanasema ewe Mola Wetu usitubakishe hapa saa na wala usitutekelezee uliyotuahidi, na wala usimkutanishe wa mwisho wetu na wa mwanzo wetu.” (Mizanul-Hikma, Juz. 1, Hadith 1694). 12   Nayo ni hadithi iliyopokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq kwamba: “Roho za waumini ziko kwenye vyumba vya peponi, wanakula chakula chake na wanakunywa vinywaji vyake. Wanatembeleana humo na wanasema: Ewe Mola Wetu tubakishe humu ili ututimizie yale uliyotuahidi.” (Mizanul-Hikma, Juz. 1, Hadith 1689). 11

37

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 37

1/17/2017 1:14:22 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

hali zao kwa mujibu wa Aya za Qur’ani. Kuhusu kundi hili la pili hakuna mjadala kwamba wao wataanza kuneemeka punde tu watakapohama kutoka katika dunia hii. Wao watahamia katika neema na radhi za Allah, kwenye amani na usalama wa Allah, kwenye afya na heshima, kwenye yale aliyowaandalia Allah.

Hali za Mashahidi Katika Ulimwengu wa Barzakh: Katika kutaja hali zao katika ulimwengu wa Barzakh, yamepokewa maelezo na ubainifu mzuri katika Qur’ani, nasi tutayategemea maelezo hayo katika sehemu hii. Allah anasema katika Kitabu chake Kitukufu:

َ َ‫َٰ ا‬ َّ َ ْ ُ ْ َ ُ ُ َ َ‫َ ا‬ ٌ ‫الله َأ ْم َو‬ َ ‫ات ۚ َب ْل أ ْح َي ٌاء َول ِك ْن ل‬ ِ ‫ول تقولوا لمِ ن يقت ُل ِفي س ِب ِيل‬ َ ‫َت ْش ُع ُر‬ ‫ون‬ “Wala msiseme kwamba wale wanaouawa katika njia ya Mwenyezi Mungu ni wafu…..” (Sura al-Baqarah: 154). Ni maelezo wanayoambiwa watu, kuanzia zama za Mtume wetu, mwisho wa Manabii  mpaka siku kitakaposimama Kiyama. Madhumuni yake ni kuwakataza watu kuwazingatia hawa kuwa ni wafu kama wengine wasiokuwa wao. Na kuwaelekeza 38

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 38

1/17/2017 1:14:22 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

watu kwamba hawa wamo miongoni mwa watu hai hivi sasa, hata kabla ya kusimama Kiyama wao wako hai. Wao ni hai lakini nyinyi hamtambui. Na kuna Aya iliyo bayana zaidi katika mtiririko na madhumuni hayo hayo, nayo ni kauli yake:

َ َ َّ ُ ُ َ َّ َّ َ َ ْ َ َ‫َ ا‬ ‫ين ق ِتلوا ِفي َس ِب ِيل الل ِه أ ْم َو ًاتا ۚ َب ْل أ ْح َي ٌاء ِع ْن َد‬ ‫ول تحسبن ال ِذ‬ ‫َ ِّرب ِه ْم ُي ْر َز ُقو َن‬

“Na usiwadhanie kabisa wale waliouawa katika njia ya Mwenyezi Mungu kuwa wamekufa, bali wako hai mbele ya Mola wao wanaruzukiwa.” (Sura Imran: 169). Yaani wao wako hai hivi sasa, na maana ya riziki yao iliyotajwa hapa si kula, kunywa na mali, bali maana yake ni ya ndani zaidi kuliko hiyo. Wao wanaruzukiwa heshima na daraja za juu, amani na usalama, heshima na utukufu, radhi na maridhiwa, neema na pepo, na mengineyo mengi. “Bali wako hai mbele ya Mola wao wanaruzukiwa. Wanafurahia aliyowapa Mwenyezi Mungu katika fadhila Zake,”13 hivi sasa na katika nyakati hizi. “Na wanawashangilia.”14 Wanawashangilia akina nani? Wao wanawashangilia ndugu zao, marafiki zao,   Sura Imran: 169 – 170).   Sura Imran: 170.

13 14

39

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 39

1/17/2017 1:14:22 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

vipenzi vyao na maswahiba zao ambao bado wangali katika dunia hii, wanawahutubia kwa kuwaambia: Enyi ndugu zetu mliyopo katika dunia! Enyi watu wa duniani! kama mngejua ni neema na uzuri gani tulionao huku, kama mngejua ni nuru, amani na heshima ipi tuliyonayo huku, kama mngejua tuko pamoja na nani na pembezoni mwa nani, basi nafsi zenu zisingeweza wala kuvumilia kubaki duniani hata sekunde moja. Lakini ninyi mmezibwa, mmengafilika na mmesahau. “Na wanawashangilia wale ambao hawajajiunga nao.”15 Na wanawapeni matumaini kwamba, hakika ninyi mtaendeleza njia yetu na Inshaallah mtaruzukiwa shahada kama tulivyoruzukiwa sisi. “Haitakuwa hofu juu yao wala hawatahuzunika. Wanashangilia neema na fadhila za Mwenyezi Mungu, na kwamba Mwenyezi Mungu hapotezi ujira wa waumini.” (Sura Imran: 170 – 171).

Kauli Kuhusu Kundi la Tatu: Baada ya kufunga maneno kuhusu makundi mawili, la kwanza na la pili, sasa tumefika katika kuzungumzia watu wengine waliobakia. Riwaya na rai za maulamaa zimetofautiana kuhusu watu hawa, bali tofauti hii imo hadi ndani ya madhehebu moja. Kwa kuwa uchunguzi   Sura Imran: 170.

15

40

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 40

1/17/2017 1:14:22 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

huu ni wa Kielimu, kifikra na kiitikadi, wenye kuhitaji mjadala mrefu, sintotoa hitimisho la moja kwa moja bali nitatosheka na kuwasilisha baadhi ya rai. Wapo maulamaa wanaoona kwamba kundi hili la tatu la watu, baada ya kuhojiwa na kupewa dozi yao ya kwanza kama itasihi kusema hivyo, dozi ya mbinyo wa kaburi na furaha au ghadhabu, wao wataachwa kama walivyo, wala Malaika hawatakuwa na kazi nao. Lakini hawafafanui kwa undani mtazamo huu. Na kuna kauli nyingine wanayoifuata wengine, wao wanaona kwamba kama maiti ni miongoni mwa watu wema chini ya kiwango cha watu wa kundi la pili (waliokunywa imani halisi), basi yeye hulala na Malaika humfungulia madirisha au milango katika kaburi lake kutoka peponi, hivyo hupatwa na harufu na saada ya pepo yake – na ni Allah pekee ndiye ajuaye ni kitu gani kitakachomjia wakati huo. Atalala na wala hataamka mpaka pale litakapopulizwa parapanda. Pale Allah atakapotoa idhini ya Kiyama kusimama. Na kadhalika kauli ni hiyo ikiwa ni miongoni mwa watu waovu chini ya kiwango cha watu wa kundi la kwanza (waliokunywa ukafiri halisi), atafunguliwa dirisha au tundu kaburini kwake kutoka motoni, na hivyo atakuwa anapatwa na sehemu ya moto wake, joto lake na giza lake. 41

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 41

1/17/2017 1:14:22 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

Na kuna rai nyingine ambayo madhumuni yake ni kwamba, hakuna tofauti baina ya hawa na kundi la pili au la kwanza, kwa sababu kanuni inajulisha kwamba kaburi la kila mtu ima liwe kiunga miongoni mwa viunga vya Pepo, au shimo miongoni mwa mashimo ya Moto. Lakini kuna tofauti katika kiwango cha adhabu ya watu hawa au neema yao. Adhabu yao ni chini kuliko adhabu ya watu wa kundi la kwanza, na neema yao ni chini kuliko neema ya watu wa kundi la pili. Na kutokana na kauli hii linajitokeza swali kuhusu wale watu wa kundi la pili watakaoneemeshwa (kama vile mashahidi na Manabii), je huko kuneemeshwa katika makaburi yao kutakuwa kwa kugeuzwa makaburi hayo kuwa kiunga miongoni mwa viunga vya peponi? Kama hali ilivyo kwa wale watakaoneemeshwa kutoka kundi la tatu, kama ilivyo kwa mujibu wa rai ya tatu? Au kuna pepo za Barzakh watakazokusanywa humo na kuneemeshwa ndani yake? Na kadhalika watu wa kundi la kwanza watakaoadhibiwa, je huko kuadhibiwa kwao kaburini kutakuwa kwa makaburi hayo kugeuzwa kuwa mashimo miongoni mwa mashimo ya Moto? Au kuna moto wa Barzakh watakaokusanywa humo watu kama hao? Katika jibu na ufafanuzi wa hili kuna riwaya, rai na kauli mbalimbali zenye kutofautiana. 42

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 42

1/17/2017 1:14:22 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

Mawaidha kwa Ajili ya Nafsi na Waumini: Ninalotaka kuashiriwa katika nukta hii ni kwamba, bila kujali usahihi wa rai yoyote kati ya rai hizo tatu, ule uwezekano tu wa kwamba rai ya tatu inaweza kuwa sahihi unatutosha. Kwa mfano, mimi hapa ninajizingatia inshaallah kuwa si miongoni mwa mafirauni, na ninataraji nimo miongoni mwa Waumini, lakini naizingatia nafsi yangu kwamba ni miongoni mwa watu wa kawaida, ni miongoni mwa hawa watakaohojiwa kuhusu hali yao. Hivyo basi, kwa upande wangu kuna dhana ya kwamba huenda nikapuuzwa na kuachwa, na kuna dhana ya kwamba huenda nikaachwa nilale na jambo langu liachwe mpaka siku ya hesabu, lakini pia kuna dhana nyingine isiyosema hivyo. Ninalotaka kusema hapa ni kwamba uwepo tu wa dhana na uwezekano wa kauli ya mwisho inayosema kwamba, kila kaburi ni kiunga miongoni mwa viunga vya peponi au ni shimo miongoni mwa mashimo ya moto, na kwamba neema na mateso huanza kwa mauti lakini kwa kulingana na mazingira ya Barzakh ambayo yanatofautiana na mazingira ya Kiyama, uwepo tu peke yake wa dhana hiyo unatosha kutufanya sisi tuishi katika hali ya mashaka, wasiwasi na khofu, bali tuishi katika hali ya tahadhari kubwa. Kwani mwisho ni kwamba

43

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 43

1/17/2017 1:14:22 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

sisi sote tutafikwa na mauti, wakati wowote na sehemu yoyote, na mtu anaweza kufia sehemu na wakati ambao hautarajii yeye wala mwingine. Sote tutakufa, na Allah anamwambia Nabii Wake mtukufu kwa kauli: “Kwa hakika wewe utakufa, na wao watakufa.” (Sura Zumar: 30), naye ndiye kiumbe akipendacho zaidi. Na sote mwisho tutafika Barzakh, tutafika katika kaburi ambalo tutaishi humo mamia au maelfu ya miaka, kwa sababu hakuna ajuaye Kiyama ni lini. Hivyo dhana ya tatu inawezekana kimantiki na kiakili, na inathibitishwa pia na baadhi ya riwaya, kadhalika na baadhi ya Aya, hivyo basi ni kitu gani tulichokiandaa na tulichojiandalia? Hii Barzakh – na maneno yetu yamefungika katika maudhui ya Barzakh na baadaye ndipo tutazungumzia Kiyama na maisha ya milele – na hili kaburi ni nyumba ya giza, ni nyumba ya ugeni, ni nyumba ya upweke, ni nyumba ya vitisho, ni nyumba ya wadudu, ni nyumba ya udhaifu na kutojiweza, ni nyumba ya njaa na ufakiri. Tumeandaa nini na tumeiandalia nini? Swali hili kubwa linatutaka sisi kila mmoja binafsi na kama jamii, tuketi, tutafakari, tutaamali, tudurusu, tupange, tutende na tufuatilie usiku na mchana. Na tuitumie kila dakika na kila sekunde na kila muda na kila siku ya umri wetu, katika kutenda, kujiandaa na kujiandalia masurufu, kama tunavyofanya katika kujiandaa na vita. Na kama 44

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 44

1/17/2017 1:14:22 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

unavyotukuta tukiketi na kupangilia namna ya kushungulikia mazingira yetu ya kiuchumi, kimaisha, kijamii, kisiasa na ulinzi na usalama. Na ni kama tunavyopanga mipango ya kuoa, kutafuta elimu na namna ya kupata kazi na ajira. Kama mambo hayo yanachukua wakati wetu, nayo ni mambo ya miaka michache katika dunia hii yenye kutoweka, basi lile linalostahiki zaidi kufanyiwa kazi na kujiandaa nalo, ambalo ni ulimwengu wa Barzakh, tumeliandalia nini? Tumeandaa nini kwa ajili ya nyumba hii mpya? Tumeandaa nini na tumeitumia nini miongoni mwa samani, mali, silaha na vifaa vingine? Tumetuma nini kwa amali zetu njema? Kwa sababu amali zetu njema ndizo zitakazobaki pamoja nasi kuanzia sekunde ya kwanza ya kifo chetu. Imepokewa katika habari iliyopokewa kutoka kwa Ahlulbayti wa Mtume , kwamba mtu baada ya kufa kwake huitazama mali yake – hii ni baada ya mauti au wakati wa kutoka roho yake -, kisha huiambia: ‘Wewe ndiye niliyetumia umri wangu kukukusanya na kukurundika, kwa njia ya halali na haramu, mimi hivi sasa niko katika mtihani, na mbele yangu kuna safari ndefu, basi nitapata msaada upi kutoka kwako juu ya safari hii?’ Mali yake humjibu: ‘Kwangu utapata sanda tu.’ Sanda tu, na mali nyingine watachukua warithi. Mtu ataulizwa kuhusu mali hii, aliitoa wapi, aliipata kwa njia 45

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 45

1/17/2017 1:14:22 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

ya halali au haramu? Lakini warithi ndio watakaostarehe nayo katika dunia hii kwa starehe zake mbalimbali. Kisha huwatizama watoto wake na familia yake na wapenzi wake, huwaambia: ‘Nilikuwa nakupeni ninyi vinywaji na chakula. Nilikuwa nakufundisheni na kukuleeni. Nilikuwa nakuteteeni na nilikuwa nakubebeni mabegani mwangu. Basi nitapata msaada gani kutoka kwenu juu yake?’ Nao husema: ‘Tutakubeba juu ya mabega yetu. Tutakusindikiza kwa kukupeleka katika shimo lako.’ Hivyo hatapata kutoka kwao ila kitendo cha wao kumbeba, na wala hawatamuacha barabarani ili riha ya mwili wake isambae. Kisha baada ya hapo hujiwa na mtu, na hatimaye yeye humuuliza mtu huyo: ‘Wewe ni nani?’ Hii huwa baada ya kuachwa na mali yake, watoto wake, vipenzi vyake na ndugu zake, ndipo hujiwa na kitu hiki ambacho humng’ang’ania bila kumwacha. Humuuliza wewe ni nani na una uhusiano gani na mimi? Nilikuona wapi? Nakujua au la? Hapo mtu huyo humjibu: ‘Ndiyo, mimi ni amali yako, na kuanzia sasa na kuendelea nitakuwa pamoja nawe na wala sikuachi hata sekunde moja.’ Amali hii kama ni njema itakuwa ni hazina, msaada, kinga, nguvu na auni kwa mtu huyu. Na kama ni amali mbaya miongoni mwa dhulma, ujeuri, ufisadi, maasi, matendo mabaya na madhambi, basi Allah peke yake Ndiye wa kuombwa 46

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 46

1/17/2017 1:14:22 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

msaada dhidi ya rafiki huyu ambaye, hatamwacha rafiki yake mpaka pale atakapotaka Allah Mtukuka. Mwisho tunasema: Sisi tunaamini uwepo wa ulimwengu wa Barzakh na maisha ya Barzakh. Na humo mna neema na adhabu. Na ilivyo ni kwamba neema zake hazilingani na neema yoyote ile ya duniani, na adhabu zake hazilingani na adhabu yoyote ile ya duniani. Lakini pamoja na hali hiyo bado neema ya Akhera na adhabu yake ni kubwa mno mara nyingi kushinda neema na adhabu ya Barzakh, isipokuwa ni kwamba tu, ulimwengu huu utakaokwisha kwa kusimama Kiyama una sifa zake na kanuni zake na mazingira yake makhususi, na kitu cha kutegemea katika ulimwengu huo ni amali tu. Na hata tukisema na kuamini msingi wa uombezi, uombezi wa Manabii ď ‡ kwa wenye dhambi na wenye maasi, na uombezi wa Ahlulbayti ď ‡ na mashahidi (radhi za Allah ziwe juu yao), na sisi ni miongoni mwa wanaoamini kwamba watu hawa wana heshima, nafasi na cheo kwa Allah Mtukuka ambacho kitawapa nafasi ya kuwaombea wengine, nasema hata tukiamini msingi huu wa uombezi, bado ni kwamba riwaya na Hadithi na kauli za maulamaa zimeashiria kwamba, ulimwengu wa Barzakh hauna uombezi.

47

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 47

1/17/2017 1:14:22 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

Haitakufaa chochote kusema: Mimi ni mzazi wa shahidi au mtoto wa shahidi. Haya yote hayasaidii chochote, bali kitakachofaa na kunufaisha ni amali njema tu. Kinyume na Akhera, ambako huko msingi wa uombezi unasaidia, na milango ya rehema ya Mungu itafunguka, uongofu wa Mungu utasambaa na upole Wake utaenea. Na ni Allah peke yake Ndiye ajuaye upana wa rehema Yake katika siku hiyo. Hivyo basi, ulimwengu wa Barzakh ni ulimwengu mzito, si wa kudharau. Na ni kwa ajili hiyo riwaya zimeelekeza kwamba, katika siku ya Kiyama mtu anaweza kumsaidia mtu mwingine, ama katika ulimwengu wa Barzakh hakuna nafasi hiyo. Hivyo basi, kila mtu ajitume yeye mwenyewe na atende kwa ajili ya ulimwengu huo, kwa sababu tegemeo lake katika ulimwengu huo halitakuwa isipokuwa juu ya nafsi yake mwenyewe na juu ya amali njema aliyojitangulizia kwa ajili ya nafsi yake, kuanzia ibada, wema, uchamungu, kheri, jihadi, ikhlasi, usafi na utakaso. Hakika ni safari ndefu inayohitaji maandalizi mengi na msaada utakaomsaidia, kama ambavyo safari ya duniani inavyohitaji maandalizi yanayonasibiana na safari husika. Wakati wa kupanda mlima, au wakati wa kusafiri maeneo yenye milima ni wajibu kwako kuandaa vitu vinavyonasibiana na safari hii ya milimani, miongoni mwa mavazi, nyenzo ya usafiri, vinywaji na vyakula. 48

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 48

1/17/2017 1:14:22 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

Ama hapa, sisi tuko katika safari ndefu ya mamia na maelfu ya miaka, safari hii ina mazingira haya, na ina kanuni na tabia hizi, hivyo ni wajibu kuiandalia masurufu. Jiandalieni masurufu Allah atakurehemuni, na tayari mmeshapata wito wa kusafiri, na takwa ndio masurufu bora.

49

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 49

1/17/2017 1:14:22 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

FASLU YA PILI Hali za Kiyama Kikubwa na Misukosuko Yake

K

atika mazungumzo yajayo tutakamilisha mazungumzo kuhusu mas’ala ya maisha ya baada ya mauti, na kuhusu Siku ya Kiyama na matukio ya Siku ya Kiyama. Tutajitahidi kufupisha maudhui kadiri itakavyowezekana. Katika baadhi ya maeneo tutafafanua zaidi, na katika maeneo mengine tutafupisha. Kimsingi katika uchunguzi huu tutategemea Aya za Qur’ani Tukufu, ile Qur’ani Tukufu ambayo ndio chanzo chenye kuaminika zaidi, ambacho kinaweza kutegemewa wakati wa kuzungumzia siku hiyo, kwa sababu habari za siku hiyo ni miongoni mwa habari za ghaibu, ambazo haiwezekani kuzijua isipokuwa kupitia habari zenye kuaminika. Na kabla ya kuzama katika ufafanuzi wa utafiti huu na kuwasilisha vipengele vyake, nawasilisha kwa ufupi na kwa muhtasari utangulizi wa utafiti huu, na hiyo ni kutokana na faida ninayoiona humo, sawa iwe kwa upande wa maudhui tunayotaka kuizungumzia hapa, au kwa upande wa kuyafahamu mas’ala ya Qur’ani kwa ujumla. 50

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 50

1/17/2017 1:14:22 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

Utangulizi: Matumizi ya Kilugha Baina ya Maana Halisi na Maana Isiyo Halisi: Ni jambo linalojulikana kwetu sote kwamba Allah Mtukuka aliiteremsha Qur’ani kwa lugha ya Kiarabu, na hivyo mwenye kutaka kuifahamu Qur’ani Tukufu na maana za Aya zake Takatifu ni lazima awe mjuzi wa lugha ya Kiarabu na kanuni zake. Na jambo hilo ni la lazima na dharura katika kufahamu maana za maneno na jumla zake, na muundo wa ibara zake ambao unaweza kutofautiana kutokana na kutofautiana maneno. Hivyo kuanzia hapa tunawajibika kuwasilisha katika maelezo yafuatayo vigawanyo vya matumizi ya kilugha ya maneno. Maulamaa wa lugha ya Kiarabu wamegawa matumizi ya maneno katika sehemu mbili: Kuna wakati watu wanatumia ibara fulani ili kufikisha maana fulani, na madhumuni yao huwa ni kufikisha ile maana yenyewe ambayo neno husika limewekwa kwa ajili yake. Kwa mfano, tunatumia neno Mlima ili kumaanisha maana yake halisi ambayo ni mwamba uliyoinuka.

51

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 51

1/17/2017 1:14:22 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

Na tunatumia neno Mwezi ili kujulisha sayari ndogo iliyo karibu na dunia, ambayo inaizunguka dunia na inaonekana usiku ikiwa na mwanga. Na tunatumia neno Bahari ili kujulisha bahari ya maji ambayo sisi sote tunaijua. Na tukimuona simba porini tunasema porini kuna simba. Kutumia maneno mlima, mwezi, bahari na simba katika mifano iliyotangulia ilikuwa ni kumaanisha maana za msingi na za kawaida ambazo maneno haya yamewekwa kwa ajili yake. Na sehemu hii ya matumizi ya maneno ya kilugha huitwa ‘utumiaji maneno kwa maana halisi’, na maneno hapa huitwa hakika. Na wakati mwingine, kutokana na uwepo wa mahusiano ya kimaana baina ya maana moja na maana nyingine, pale panapokuwepo na ushirikiano katika pande fulani za maana zote mbili, husihi kulitumia katika kumaanisha maana ya pili, lile neno lililowekwa kwa ajili ya maana ya kwanza. Hivyo utatukuta tunamaanisha maana fulani kwa kutumia neno lililowekwa kwa ajili ya maana nyingine, lakini ni kwa sababu tu kuna ushirikiano kati ya maana hizo mbili katika upande fulani. Kwa mfano, tukimuona mtu mwenye nguvu na azma imara tunasema: ‘Nimeuona mlima’. Na hapa makusudio yetu hayawi mlima wa udongo na mchanga, bali makusudio yetu huwa ni yule mtu mwenye nguvu, thabiti na imara kama mlima. Kama unavyoona, matu52

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 52

1/17/2017 1:14:22 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

mizi haya yanasihi katika lugha kwa sababu kuna ushirikiano baina ya maana zote mbili, mlima na huyu mtu, maana zote zinakutana katika ugumu na uimara. Na mfano mwingine, ni tunapomuona mtu jasiri, shujaa asiyerudi nyuma katika vita tunasema ‘hakika fulani ni simba’ na hapo huwa hatumaanishi kwamba yeye ni Yule mnyama mwitu, bali huwa tumetumia neno hili kutokana na kuwepo ushirikiano, nao ni ushujaa. Na mifano mingine mingi, katika hali hii utumiaji wetu wa maneno huwa haulengi kumaanisha maana halisi za maneno, bali humaanisha maana nyingine zenye ushirikiano na maana halisi katika upande maalumu. Sehemu hii ya matumizi huitwa ‘utumiaji wa kinaya’ na maneno hapa huitwa kinaya. Na utumiaji huu kama unavyojua umeenea kwa wanalugha wote na wala haukomei kwa kundi maalumu.

Maana Halisi na Maana Isiyo Halisi Katika Qur’ani: Lazima tuutazame utangulizi uliopita wakati wa kuamiliana kwetu na maandiko ya Qur’ani, kwa sababu Qur’ani ilipoteremka iliteremka kwa lugha ya Kiarabu, na hakika yenyewe ilikuwa ni mfano wa juu kabisa wa fasihi na bayani, na ndani yake kuna utumiaji wa 53

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 53

1/17/2017 1:14:22 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

hakika na kinaya. Hivyo si maneno yote yaliyotumika katika Qur’ani yanachukuliwa kwa maana yake halisi na hakika, bali ni lazima kuchunguza na kutazama, na kwa mfano tunasoma kauli ya Allah: “Na aliyekuwa kipofu katika hii, basi Akhera atakuwa kipofu na aliyepotea zaidi njia.” (Sura Israi: 72), na ni maalumu kwamba neno ‘kipofu’ maana yake ni Yule mtu asiyeona, aliyepoteza uwezo wa kuona ima kwa kuzaliwa hivyo au kwa sababu ya tukio fulani. Katika mfano huu kama matumizi ya neno kipofu hapa ni kwa kumaanisha maana halisi na ya hakika basi itakuwa ni kupingana na hekima ya Allah Mtukuka na uadilifu Wake, kwani ana dhambi gani na ana kosa gani mtu aliyepatwa na majaribu katika dunia hii na hatimaye akapatwa na upofu, mpaka Allah amkusanye siku ya Kiyama akiwa kipofu na awe ni aliyepotea zaidi njia? Hakika mwelekeo sahihi wa mas’ala hii hauwi isipokuwa kwa kuzingatia kwamba utumiaji wa neno kipofu hapa ni kwa maana ya kinaya, anakusudiwa Yule aliye kipofu wa moyo, yaani aliyepotea na kupotoka. Na ni kama tunavyosoma katika Aya nyingine ibara: “Mkono wa Mwenyezi Mungu uko juu ya mikono yao.” (Sura al-Fat’hu: 10), isipokuwa ni kwamba sisi tunaamini kuwa Allah Mtukuka hana mwili, na hafanani na chochote. Na tunajua kwamba neno mkono ka54

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 54

1/17/2017 1:14:22 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

tika matumizi ya maneno kwa kumaanisha maana halisi humaanisha sehemu ya mwili. Hivyo haiwezekani kutoa mwelekeo sahihi wa ufahamu wetu juu ya maana ya Aya hii isipokuwa kwa kuzingatia kwamba, matumizi ya neno mkono hapa ni matumizi ya kinaya, kwa kumaanisha uwezo, kwa sababu matendo ya uwezo huwa kwa kuutumikisha mkono. Hivyo lugha ya Kiarabu ni lugha fasaha sana na inaruhusu utumiaji wa maneno katika mitindo mbalimbali. Na Qur’ani iliteremka kwa lugha hii, hivyo basi, ni wajibu wetu kuyachukulia baadhi ya maneno yake kwa maana halisi ya hakika, na kuyachukulia mengine kwa maana isiyo halisi, ya kinaya, iwapo tu patapatikana dalili au kihusishi au ishara au alama inayojulisha hivyo.

Viashiria vya Kiyama Kikubwa na Matukio yake: Baada ya utangulizi huu, sasa turudi kwenye maudhui tunayoizungumzia, nayo ni mas’ala ya kusimama Kiyama, nayo ndio hatua ya mwisho na kubwa. Hii ni baada ya kuwa tayari tumeshazungumzia mas’ala ya ulimwengu wa Barzakh katika faslu ya kwanza. Mwanzo kabisa tunasema kuwa, ni lini Kiyama kitasi55

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 55

1/17/2017 1:14:22 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

mama hilo ni jambo asilolijua yeyote isipokuwa Allah peke Yake. Jambo hilo ni miongoni mwa ghaibu binafsi za Allah, kwani zipo ghaibu ambazo Allah aliwajulisha Manabii na Mitume Wake , na wao kwa nafasi yao wakawajulisha watu ghaibu hizo. Na kuna ghaibu nyingine ambazo Allah amezifanya kuwa ni siri Yake Binafsi, hajamjulisha siri hiyo yeyote miongoni mwa Manabii Wake au mawalii Wake au malaika Wake. Na miongoni mwa ghaibu hizo ni suala la wakati wa kusimama Kiyama. Na ni kwa ajili hiyo hakuna yeyote anayejua Kiyama kitasimama lini - ni baada ya mwaka, au miaka mia moja, au miaka elfu moja, au miaka elfu kumi….- Na kusimama kwa Kiyama kutakuwa kwa ghafla, bali ni kwamba miongoni mwa alama zake makhususi na sifa zake za kipekee ni kwamba kitakuja ghafla. Na kwa mujibu wa riwaya mbalimbali ni kwamba wakati wa kusimama Kiyama watu watakuwa hawana hata mawazo nacho, watakuwa wameshughulishwa na mambo yao ya maisha ya kila siku, na ghafla kitawajia bila yeyote kutarajia16.   Limethibiti hili katika Qur’ani na katika hadithi za Ahlulbayri , Allah anasema: “Hakika wameshahasirika wale waliokadhibisha kukutana na Mwenyezi Mungu, na wamefuzu wale waliomwamini, mpaka itakapowajia ghafla saa (Kiyama) watasema: Oo! Majuto yetu juu ya yale tuliyoyapuuza! Nao watabeba mizigo yao migongoni mwao. Ehee! Ni mabaya mno wanayoyabeba.” (Sura An’am: 31). Na kauli ya Allah: “Wanauliza hiyo saa (Kiyama) kutokea kwake kutakuwa lini?

16

56

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 56

1/17/2017 1:14:22 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

Lakini ni matukio yapi yatakayotokea wakati Allah atakapoidhinisha Kiyama kisimame? Tunajibiwa swali hilo na maandiko, kwamba matukio hayo yana sehemu mbili. Yapo yenye uhusiano na viumbe hai tukiwemo sisi wanadamu, na yapo yenye uhusiano na viumbe visivyokuwa hai, kama vile jua, mwezi, milima, mabahari na vinginevyo. Ni vizuri tukaashiria hapa kwamba, hali ya jumla ya matukio haya na inayojitokeza, kuanzia mwanzo wake mpaka mwisho wake, ni kuenea kwa hisia ya mfadhaiko, khofu, woga, vitisho, mashaka, kutetemeka na wasiwasi kuhusu hatima yake. Na hali hiyo itamwandama mtu kuanzia mwanzo wa matukio mpaka pale itakapobainika hatima yake, pale watu wa peponi watakapoingia peponi na watu wa motoni watakapoingia motoni. Allah anasema mwanzoni mwa Sura al-Hajj:

َّ ‫َيا َأ ُّي َها‬ َ َّ ‫اس َّات ُقوا َرَّب ُك ْم ۚ إ َّن َ ْزل َ َزل َة‬ َ ‫اعة‬ ٌ ‫�ش ْي ٌء َع ِظ‬ ُ ‫الن‬ ‫يم َي ْو َم‬ ِ ‫الس‬ ِ َ ُّ ُ ُ َ َ َ ْ َ َ ْ َ َّ َ َ ْ ُ ُّ ُ ُ َ ْ َ َ َ ْ َ َ َ ْ ‫ات حم ٍل‬ ِ ‫ترونها تذهل كل مر ِضع ٍة عما أرضعت وتضع كل ذ‬ Sema: Ujuzi wake uko kwa Mola Wangu; hakuna wa kuidhihirisha kwa wakati wake ila Yeye tu; ni nzito katika mbingu na ardhi. Haitawafikia ila kwa ghafla tu. Wanakuuliza kama kwamba unaidadisi. Sema: Ujuzi wake uko kwa Mwenyezi Mungu tu, lakini watu wengi hawajui.” (Sura Aaraf: 187). Na kauli ya Allah: “Hawangoji ila Saa iwajie ghafla na hali wao hawatambui?” (Sura Zukhruf: 66). 57

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 57

1/17/2017 1:14:22 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

َّ َ َ َ َّ َٰ َ ٰ َ َ ُ ْ ُ َ َ ٰ َ َ ُ َ َّ َ َ َ َ َ ْ َ ‫اب الل ِه‬ ‫حملها وترى الناس سكارى وما هم ِبسكارى ول ِكن عذ‬ َ ‫ش ِد ٌيد‬ “Enyi watu! Mcheni Mola Wenu. Hakika tetemeko la saa ni jambo kuu. Siku mtakapoiona, kila mwenye kunyonyesha atamsahau amnyonyeshaye na kila mwenye mimba ataharibu mimba yake. Na utawaona watu wamelewa, na kumbe hawakulewa. Lakini adhabu ya Mwenyezi Mungu ni kali.” (Sura al-Hajj: 1 – 2).

Hali ya Viumbe Hai Katika Siku ya ­Kiyama: Sasa tuje kwenye aina ya kwanza ya matukio ambayo yana uhusiano na viumbe hai wakiwemo wanadamu. Qur’ani Tukufu inatueleza kwamba Allah Mtukuka ataamuru kufa kila kilicho hai wakati wa kusimama Kiyama, kuanzia wanadamu, majini, malaika na wanyama, na wala hakitabaki kilicho hai isipokuwa Yeye Mtukuka: “Kila kilicho juu yake kitatoweka. Na itabakia dhati ya Mola Wako Mwenye utukufu na ukarimu.” (Sura Rahman: 26 – 27). Na hapa hatuzungumzii viumbe vilivyopo tu duniani, kwa sababu tunajua katika viumbe hai vipo vile ambavyo uwepo wake haukomei duniani tu, kama vile Malaika. Wao wapo ardhini na mbinguni na sehemu nyingine miongoni mwa mazingi58

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 58

1/17/2017 1:14:22 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

ra ya uwepo. Na majini nao wao wapo katika mazingira yao maalumu, na vinginevyo miongoni mwa viumbe hai, na vyote vitafikwa na mauti, na hata wale waliokufa duniani ambao wako hai katika ulimwengu wa Barzakh, na wao pia wanaingia katika mauti hayo. Hivyo wakati huo Allah atakifisha kila kilicho hai, sawa kiwe kipo duniani au katika ulimwengu wa Barzakh au katika ulimwengu mwingine.

Allah Atawafishaje? Katika suala hili Qur’ani Tukufu inazungumzia mambo mawili: Kwanza, Ukelele, wenye kusifika kwa nguvu zake na ukubwa wake, na ambao katika sekunde moja utakifikia kila kilicho hai katika viumbe na kukifisha. Pili, mpulizo wa parapanda, na ndio uliozungumziwa katika Qur’ani kwa ibara: “Na itapulizwa parapanda, wazimie waliomo mbinguni na waliomo ardhini, ila ambaye Mwenyezi Mungu amemtaka. Kisha itapulizwa mara nyengine. Hapo watainuka wawe wanangojea.” (Sura Zumar: 68). Na neno Sur lililotumika katika Aya humaanisha parapanda katika lugha ya Kiarabu, na Mtume wa Allah  alipoulizwa kuhusu Sur alijibu kuwa ni parapanda litakalopulizwa. Na parapanda ni zana ya zamani iliyotegemewa huko nyuma kabla ya uvumbuzi wa vipaza sauti vya kisasa. Ilikuwa 59

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 59

1/17/2017 1:14:22 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

ikitumika jeshini wakati wa kuwakusanya askari waliotawanyika, hivyo ili kuwakusanya lilikuwa likipulizwa parapanda ili kila aliye kambini asikie na aharakishe kwenye uwanja wa mkusanyiko. Na wakati mwingine likitumika kuwakusanya watu wa mji kwa lengo la kuwafikishia jambo, na wao walikuwa wakikusanyika linapopulizwa. Hivyo parapanda ni zana maarufu tangu Allah alipomuumba Adam ď ‚ hadi kabla ya miaka kumi hivi, na bado baadhi ya mataifa wanaitumia zana hiyo mpaka leo hii. Lakini je makusudio hapa ni kama ilivyo katika baadhi ya riwaya na kauli, kwamba Israfil, ambaye ni mmoja kati ya Malaika watukufu na wakubwa, atabeba parapanda na kulipuliza – licha ya kwamba hakuna ajuaye sifa za parapanda hili na ukubwa wake – na hatimaye sauti inayotoka kwenye parapanda itakifikia kila kilicho hai na kukifisha? Maana hii inawezekana ikawa ndio inayokusudiwa, na inawezekana neno parapanda hapa limetumika kwa matumizi tuliyoyataja huko mwanzo, ya kumaanisha kinaya. Kwani matumizi ya parapanda kama ilivyopokewa yalikuwa ni kwa ajili ya kuwakusanya watu, na hivyo makusudio ya parapanda hapa yanakuwa ni ule ukulele atakaouumba Allah Mtukuka kwa uwezo Wake mkubwa usio na mwisho. Na rai zote mbili zina maulamaa wanaosema hivyo, lakini 60

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 60

1/17/2017 1:14:22 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

kilichothibiti bila shaka ni hitimisho lao, hitimishi ambalo ni kwamba kutakuwa na sauti kali yenye kutisha na kutetemesha ambayo itakifikia kila chenye akili, moyo na roho, na hapo watazimia waliomo mbinguni na waliomo ardhini. Na kwa kawaida kuzimia kunaweza kumfisha mtu au kusimfishe, lakini kuzimia huku kutawafisha wote hawa, na ndio kauli ya Allah: “Na itapulizwa parapanda, wazimie waliomo mbinguni na waliomo ardhini, ila ambaye Mwenyezi Mungu amemtaka.” (Sura Zumar: 68). Baadhi ya wafasiri wameizuia ibara “ila ambaye Mwenyezi Mungu amemtaka.” Wakazingatia kwamba, baadhi ya viumbe hawatafishwa kwa kuzimia, lakini wametofautiana katika kuwaainisha viumbe hao. Wapo wanaosema kuwa ni Jibril, Mikail, Israfil na Izrail, na wapo wanaosema kuwa ni Malaika wakubwa, na kama ilivyo katika baadhi ya riwaya kwamba ni baadhi ya mashahidi. Lakini hata hivyo tunawakuta wafasiri wengine wanazingatia kwamba ibara hii imekuja kama sehemu ya kuhifadhi haki tu, na kuelezea uwezo usio na mipaka, na si vinginevyo. Hali halisi ni kwamba watazimia wote waliomo mbinguni na ardhini bila kubagua. Hivyo kila kilicho hai – isipokuwa wale watakaoondolewa kama itasihi rai ya kwaza – kitazimia na kufa na hatabaki hai isipokuwa Allah Mtukuka. 61

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 61

1/17/2017 1:14:22 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

Na kwa wakati mmoja, wakati wa kutokea tukio hili la kwanza lenye uhusiano na viumbe hai, au kabla yake au baada yake, yatatokea matukio mengine yenye uhusiano na ulimwengu. Na inshaallah huko mbele tutataja Aya za Qur’ani zenye kuashiria matukio hayo. Lakini hata hivyo ni bora tukatanguliza ufupi wa hali itakavyokuwa ili tusihitajie tena kufasiri hizo Aya, ili iwe bayana kwa msomaji ile maana ya Aya hizo tutakapoziwasilisha.

Ulimwengu Utakavyokuwa Siku ya ­Kiyama: Ni kitu gani kitautokea ulimwengu? Jua ambalo ni chanzo cha mwanga na joto na maisha katika mfumo wetu wa sayari, ukiongezea faida nyingine linazotoa kwa viumbe wote wa ardhini, tunasema: Jua hili siku hiyo litakunjwa kunjwa, yaani litavingirishwa, kuzuiwa na mwanga wake kuzimwa. Na litakapozimwa mwezi hautakuwa tena na mwanga, kwa sababu wenyewe unachukua mwanga wake kutoka kwenye jua, na hapo dunia yote itafunikwa na giza, bali ni kwamba mfumo wote wa sayari na kila kinachoangaza kwa mwanga wa jua hili kitafunikwa na giza. Ama sayari nyingine za mbinguni na nyota, zenyewe zitazimwa na hatimaye zitatawanyika na kugongana na kuanguka na kusagika na 62

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 62

1/17/2017 1:14:22 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

kuyeyuka. Na hii ndio maana ya kauli ya Allah kwamba nyota zitaanguka. Na jambo hili kisayansi linawezekana, kwani kuna kitu kinachoitwa kifo cha nyota, na huenda mlishawahi kukishuhudia katika baadhi ya vituo vya kisayansi, na huenda hiyo ikawa ni moja ya maana za yale maelezo yaliyotangulia. Ama mbingu, mbingu hii iliyonyanyuka juu ya vichwa vyetu, yenyewe itafunguka, itapasuka na kutoboka. Ama milima, yenyewe itasagika na kuwa mchanga, vumbi jepesi, yaani kama vumbi la mchanga kiasi kwamba mlima utapeperushwa na upepo na kulingana sawa sawa na ardhi. Na kama tunataka kuvuta karibu sura ya hali itakavyokuwa basi inatutosha kufikiria jinsi mlima mmoja unavyosawazishwa, na lete picha ya khofu itakayotokea kwa kitendo hicho, na wasiwasi na woga utakaojikita katika nyoyo. Hali itakuwaje pindi milima yote itakaposawazishwa sawa na ardhi katika muda mmoja, ni nyoyo na akili zipi zinazoweza kufikiria hilo? Ama ardhi, yenyewe itatikiswa na kugongwa na kutolewa yaliyomo tumboni mwake. Itasawazika na kuwa sawa bila milima, wala mabonde wala kona, wala miinuko, wala maporomoko. Itakuwa ni ardhi iliyotandaa na kunyooka, ambayo inaandaliwa kuwa uwanja

63

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 63

1/17/2017 1:14:23 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

wa mkusanyiko ambao utakusanya mamilioni ya wanadamu na viumbe. Kisha mabahari, yenyewe yatatibuliwa, yatachemshwa na kulipuliwa kwa moto, maji yake yatawaka na kutoa moshi. Haitabaki bahari wala mlima wala bonde wala mti, uhai hautabaki katika chochote. Tunafahamu nini kutoka katika picha hii tuliyopewa na Qur’ani? Linalojulishwa na Aya hizi ni kwamba Allah Mtukuka hataumaliza kabisa ulimwengu bali atarudia kuutengeneza na kuujenga kulingana na mpangilio mpya na katika mfumo mpya. Na muulizaji anaweza kuuliza kuhusu upande wa ardhi baada ya kuibadili, ardhi ambayo watakusanywa juu yake watu, je watu watakusanywa na kuhesabiwa nayo ikiwa katika giza totoro? Kwani hakutakuwa na jua siku hiyo wala mwezi wala nyota. Kuhusu swali hilo jibu ni kwamba, Allah Mtukuka katika muundo huo mpya ataumba nuru ya moja kwa moja, nuru itakayowaangazia watu wa uwanjani, Allah anasema: “Na ardhi itang’ara kwa Nuru ya Mola Wake,” (Sura Zumar: 69). Hivyo sisi Siku ya Kiyama tutakuwa mbele ya ulimwengu mpya na uwepo mpya na tabianchi mpya, lakini ni tabianchi yenye ardhi, nuru, mwanga na mam-

64

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 64

1/17/2017 1:14:23 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

bo mengine. Na inshaallah baadaye tutazungumzia Pepo na Moto. Na hakika ulimwengu huo mpya kama tulivyotaja huko nyuma, una kanuni zake zilizo tofauti na kanuni za ulimwengu wetu huu, kuanzia kanuni za fizikia, kemia, maliasili, tiba, uhandisi, hesabu, maumbo na kila chenye uhusiano na sayari. Ni ulimwengu unaojitofautisha kwa mipangilio yake, tabia yake na mwenendo wake ukilinganisha na ulivyokuwa kabla ya kusimama Kiyama, na kwa ajili hiyo Allah anasema: “Siku itakapobadilishwa ardhi kuwa ardhi nyingine na mbingu (pia). Nao watahudhuria mbele ya Mwenyezi Mungu Mmoja, Mwenye nguvu.” (Sura Ibrahim: 48). Hivyo tutakuwa mbele ya ardhi mpya na mbingu mpya, atakayoitengeneza au atakayorudia kuitengeneza Allah, atakayoipangilia na kuiratibu baada ya kutoweka na kusagika maumbo ya ulimwengu huu.

Tafakari Fupi Juu ya Ushahidi wa Maandiko ya Qur’ani: Baada ya kuwasilisha sura ya jumla ya hali ya ulimwengu katika Siku ya Kiyama, tutawasilisha hapa moja kwa moja baadhi ya ushahidi kutoka kwenye Aya za Qur’ani, ili tusimame nazo kisimamo cha tafakari, huenda kwa kufanya hivyo ikapatikana faida. Hapa 65

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 65

1/17/2017 1:14:23 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

hatutapanua maneno kwa ufafanuzi na undani, bali uwasilishaji wa hapa utakuwa kukamilisha sura tuliyoitoa huko nyuma. Allah Mtukuka anasema katika Sura al-Waqiah: “Itakapotikiswa ardhi kwa mtikiso.” (Sura al-Waqiah: 4). Na msomaji hebu sasa atafakari kutokea kwa tetemeko dogo na atafakari kiwango cha mfadhaiko na khofu ambayo itawapata watu. Hakika tetemeko dogo linalotokea katika eneo fulani halidumu hata nusu dakika, lakini linaweza kuwaacha watu wake katika tafrani wakiwa wamelala vifudifudi barabarani, majumba yamewabomokea na ardhi imewapasukia. Sasa itakuwaje ikiwa ardhi yote kwa wakati mmoja Allah ataitikisa? Hali itakuwaje? “Itakapotikiswa ardhi kwa mtikiso.Na milima itaposagwasagwa.Iwe mavumbi yanayopeperushwa.” (Sura al-Waqiah: 4 – 6). Hii ni kwa mujibu wa Sura al-Waqiah. Na katika Sura Mursalat, Allah anasema: “Hakika mnayoahidiwa bila ya shaka yatakuwa! Basi nyota zitakapofutwa. Na mbingu zitakapopasuliwa. Na milima itakapopeperushwa.”(Aya ya 7 – 10). Na katika Sura al-Haqqah Allah anasema: “Na itapulizwa parapanda mpulizo mmoja.” Ni mpulizo mmoja ambao hautahitajia wa pili. “Na ardhi na milima ikaondolewa, na ikavunjwa kwa mvunjo mmoja.” Na tetemeko hilo si la hatua moja baada ya nyingine, 66

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 66

1/17/2017 1:14:23 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

bali ni mvunjo mmoja tu. “Siku hiyo Tukio litatukia. Na mbingu zitapasuka, kwani siku hiyo zitakuwa dhaifu kabisa.”(Aya ya 13 – 16). Kwa nini mbingu zitapasuka na kuachana? Makusudio ni kwamba ganda la anga ambalo ndilo huzuia vimondo, nyota na mawe yaangukayo kutoka mbinguni litaondoka. Mbingu yote hii itapasuka na kuachana, na mara moja kila kitisho tunachokishuhudia katika filamu za kielimu kitaanguka juu ya ardhi. Na anasema katika Sura Muzzamil: “Siku ambayo ardhi itatikisika na milima, na milima itakuwa kama tifutifu la mchanga.” (Aya ya 14), yaani itakuwa imesambaa kama tifutifu la mchanga. Na anasema katika Sura Inshiqaq: “Mbingu itakapochanika. Na ikamsikiliza Mola Wake na ikafanya ndivyo. Na ardhi itakaponyooshwa. Na ikatupa vilivyo ndani na kuwa tupu.” (Aya ya 1 – 4). Na katika Sura Infitar: “Mbingu itakapopasuka. Na nyota zitakapopukutika. Na bahari zitakapopasuliwa. Na makaburi yatakapofukuliwa.” (Aya 1- 4). Kisha katika Sura al-Qariah anasema: “Inayogonga (siku ya Kiyama!)” yaani Kiyama kitakachogonga nyoyo, akili na roho. “Nini inayogonga? Na nini cha Kukujulisha nini inayogonga? Siku ambayo watu watakuwa kama panzi waliotawanyika.” Yaani kama panzi waliotawanyika 67

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 67

1/17/2017 1:14:23 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

wasiojua cha kufanya. “Na milima itakuwa kama sufi zilizochambuliwa!” yaani milima hii migumu na imara itageuka sufi nyepesi iliyochambuliwa yenye kupeperuka. “Basi yule ambaye mizani yake itakuwa nzito. Huyo atakuwa katika maisha ya kuridhiwa. Na yule ambaye mizani yake itakuwa hafifu. Basi mama yake atakuwa Hawiya! Na nini kitachokujulisha nini hiyo? Ni Moto mkali!” (Aya 1 – 11). Na katika Sura Zilzalah anasema: “Itakapotetemeshwa ardhi huo mtetemeko wake!” nalo ndio tetemeko la ukweli, ambalo ukililinganisha na matetemeko yote yaliyotokea ardhini, matetemeko hayo si chochote. “Na ikatoa ardhi mizigo yake! Na mtu akasema: Ina nini?” atakuwa katika mshangao na tahayari. “Siku hiyo itahadithia habari zake. Kwa sababu Mola Wako ameipa wahyi! Siku hiyo watu watatoka kwa mtawanyiko ili wakaonyeshwe vitendo vyao!”(Aya ya 1 – 6). Na katika Sura Tak’wir Allah anasema: “Jua litakapokunjwa kunjwa.” Na hili ni miongoni mwa matukio makubwa yatakayotokea siku hiyo, ambapo jua litazimwa na kufunikwa. “Na nyota zitakapoanguka. Na milima itakapoondolewa. Na ngamia wenye mimba watakapotupiliwa mbali. Na wanyama pori watakapokusanywa. Na bahari zitakapofurika.” Yaani italipuliwa kwa moto. “Na nafsi 68

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 68

1/17/2017 1:14:23 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

zitakapounganishwa (na miili). Na msichana aliyezikwa hai atakapoulizwa. Ni kwa dhambi gani aliuawa? Na madaftari yatakapoenezwa. Na mbingu itakapotanduliwa.” Na makusudio yake huenda yakawa ni yale tuliyoyataja, kwamba ni kuondolewa kwa ganda la anga. “Na moto utakapokokwa.” Na hii ni kukamilisha hali, ambapo Jahannam itaanza kuchemka ikijiandaa kuwapokea wageni wake. “Na Pepo itakaposogezwa.” Tazama, moto umekokwa na Pepo inaandaliwa na kuwekwa tayari kama makasiri yanavyoandaliwa kwa ajili ya wageni waheshimiwa. “Itajua kila nafsi ilichokihudhurisha.” (Aya 1 – 14). Baada ya matukio haya ya mfumo mzima wa ulimwengu, matukio ambayo yanaweza yakatokea yote kwa pamoja au yakatokea baadhi, uwepo wa viumbe hai utakwisha na tutakuwa mbele ya ulimwengu mpya. Na Allah Ndiye ajuaye tutakaa kwa muda gani mpaka Allah aje kuamrisha jambo jingine, nalo ni kule kutuhuisha tena na kuvipeleka viumbe na wanadamu katika hesabu. Ni saa, ni siku au ni maelfu ya miaka, Yeye Ndiye ajuaye. Jambo hilo ni miongoni mwa mambo ya ghaibu ambayo Qur’ani Tukufu haijatuelezea, wala hakuna yeyote mwenye uhakika na yakini kuhusu jibu la swali hili. Bali ni mpaka pale Allah Mtukuka atakapotaka kusimamisha Kiyama kikubwa. 69

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 69

1/17/2017 1:14:23 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

Kuwahuisha Maiti na Kurudi ­Kuwakusanya: Hapa tunarudi kuzungumzia hali za wanadamu zitakavyokuwa katika siku hiyo. Baada ya kuzungumzia suala la kuwafisha, hebu sasa suala la kuwarudishia uhai wao. Mazungumzo kuhusu suala la kuwahuisha yamegawanyika sehemu mbili, kama mgawanyo ule ule uliotajwa katika suala la kuwafisha: Kwanza ni tamko linalozungumzia ukelele, ambao utakuwa mkali, mzito na wa kutisha, ambao utawahuisha maiti wote na kuwatoa makaburini. Pili ni kuhusu mpulizo wa parapanda, nao ni mpulizo wa pili, ambao utawahuisha maiti na kuwatoa makaburini, nao ni mpulizo wa ufufuo na kurudisha uhai. Allah anasema: “Na itapulizwa Parapanda, mara watatoka makaburini wakikimbilia kwa Mola Wao.” Hebu fikiria hivi sasa hali ya ardhi ambayo imemeza makaburi, kuanzia ya wale waliozikwa makaburini hadi wale waliozikwa kwa kuangukiwa na sayari, nyota, milima na kwa tetemeko, na wote hao wamelala ndani ya ardhi. Kisha tafakari na ulete picha ya watu hawa sasa wanarudi katika uhai, miili yao inajijenga upya na inapewa uhai na kurudishiwa roho. Sasa makaburi yanafunguliwa ili watu hao watoke humo, mamil-

70

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 70

1/17/2017 1:14:23 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

ioni ya watu ndani ya muda mmoja wanatokea wakiwa wamefadhaika wenye kutetemeka. Na hili lililotajwa kwa kweli linaingia akilini, bali ni kwamba lilishawahi kutokea katika zama zilizotangulia, kwani imepokewa kwamba Nabii Isa  siku moja alipita karibu na kaburi, akamuomba Allah Mtukuka ampe uwezo wa kumuhuisha maiti aliyekuwemo ndani ya kaburi lile. Allah akampa idhini naye akamwita, basi kaburi likapasuka na maiti akatoka kutoka ndani ya kaburi lake. Alitoka akiwa amefazaika mwenye kutetemeka. Akamuuliza kuhusu uzee wake, akamjibu kuwa amezeeka muda huo huo kwa kudhania kwamba siku ya ufufuo imefika. Alidhani kuwa ni siku ya ufufuo, basi itakuwaje siku ya ufufuo wa kweli? Hebu sasa tukamilishe Aya, Allah anasema: “Na itapulizwa Parapanda, mara watatoka makaburini wakikimbilia kwa Mola Wao.” Yaani wanakwenda kwa Mola Wao na kwenye eneo ambalo ndipo watakapokusanywa. Watakwenda kwa haraka wakati wa kujitenga na makaburi yao. “Watasema: Ole wetu! Nani aliyetufufua malaloni petu? Haya ndiyo aliyoyaahidi Mwingi wa Rehema na wakasema kweli Mitume.” Sasa wamejua ukweli wa maudhui na kwamba si utani. Manabii na Mitume walikuwa tayari

71

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 71

1/17/2017 1:14:23 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

wameshawaonya lakini wao hawakuwasadikisha. Walikuwa katika mghafala na hilo. “Haitakuwa ila ukelele mmoja tu, mara wote watahudhurishwa mbele Yetu.” (Sura Yasin: 51 – 53). Na hii ni miongoni mwa adhama ya Allah Mtukuka. Sisi tukitaka kuwakusanya sehemu tu ya maelfu unadhani ni mkanganyiko kiasi gani utatokea. Au nchi ikitaka kuandaa maandamano ya mamilioni ya watu, ili kuzuia kusiwepo na fujo ni lazima vyombo vyake vyote vishiriki na kufanya kazi ya kuratibu maandamano hayo. Lakini Allah kwa ukelele mmoja atawakusanya mamilioni ya watu na zaidi katika uwanja wa mkusanyiko, na ni Yeye peke yake Ndiye ajuaye idadi yao. Na Allah anasema katika sehemu nyingine: “Siku itapowapasukia ardhi mbio mbio! Mkusanyo huo Kwetu ni mwepesi.” (Sura Qaf: 44), watatoka ndani ya makaburi yao, ardhi itapasuka na wao watatoka kwa haraka kwenda sehemu hiyo, na yote hayo ni mepesi kwa Allah. Anasema: “Siku watakaposikia ukelele wa haki. Hiyo ndiyo siku ya kutoka.” (Sura Qaf: 42), ambapo makundi ya watu yatatoka makaburini kwa haraka kwenda eneo la maswali na hesabu lililowekwa kwa ajili ya kusimama mbele ya Allah Mtukuka. Watatoka ndani ya makaburi yao bila sanda, ila wale baadhi waliotajwa katika riwaya. Watatoka miguu 72

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 72

1/17/2017 1:14:23 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

peku, uchi bila mavazi. Imam Zainul-Abidina  anaelezea hali ya mwanadamu katika siku hiyo, katika dua Abu Hamza Thumaliy: “Mara naangalia kuliani kwangu, na mara kushotoni kwangu, nawakuta viumbe kila mmoja akijishughulisha na jambo lake lisilokuwa langu.” Hakuna anayemtazama mwenzake, wala hakuna anayejali jambo la mwenzake, kila mmoja anajishughulisha na nafsi yake, akili yake na moyo wake vinatetemeka, amechanganyikiwa na ana wasiwasi kuhusu hatima yake na mustakabali wake. Ana wasiwasi juu ya maswali na hesabu na kusimama mbele ya Allah, na kwamba watasimama mbele ya Allah kwa muda mrefu. Aya za Qur’ani zinaelezea hali za watu zitakavyokuwa siku hiyo, zinasema: “Wakati nyoyo zitakapofika kooni, nao wamejaa huzuni.” (Sura Ghafir: 18). Nayo ni ibara inayoelezea ukubwa wa khofu yao. Na zinasema tena: “Na nyoyo zikapanda kooni.” (Sura Ahzab: 10), nayo ni ibara fasaha zaidi katika kuelezea khofu katika lugha ya Kiarabu. Hivyo nyoyo zimepanda kooni huku wakiwa na huzuni, hawawezi kutamka neno na wala hawawezi kupumua, isipokuwa kwa idhini kutoka kwa Allah. Kimya kitaenea na khofu itatawala. Watasimama muda mrefu, na sisi hatujui urefu wa siku hiyo, kwa sababu mfumo wa dunia utabadilika na urefu wa siku hautaendelea kuwa kama huu 73

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 73

1/17/2017 1:14:23 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

tuliouzoea, na hilo tumeshalitaja huko nyuma. Bali siku ya huko inatofautiana na ya huku, na miaka ya huko inatofautiana na ya huku, kama ilivyopokewa ndani ya Qur’ani, mpaka pale Allah Mtukuka atakapotoa idhini na kuamuru maswali na hesabu.

Kusimama Mbele ya Allah kwa Ajili ya Hesabu: Hivyo basi, hakuna anayejua kutakuwa na urefu wa muda gani kati ya kitendo cha kuwakusanya watu katika uwanja wa mkusanyiko na hatimaye kusimama wakiwa peku, uchi bila mavazi, wanatiririka jasho, wamejawa na woga, wenye njaa na kiu, na kati ya kukutana na hesabu na maswali. Na ni kwa ajili hiyo Siku ya Kiyama imepewa sifa ya kwamba ni Siku ya Njaa kubwa, ni Siku ya Kiu kali na ni Siku ya Mfazaiko mkubwa. Mtukufu Mtume  ameusia kuikumbuka muda wote siku hiyo, kama ilivyo katika hotuba yake maarufu ya kuupokea mwezi wa Ramadhan, aliposema: “Njaa yenu na kiu yenu katika mwezi huu iwakumbusheni njaa na kiu ya Siku ya Kiyama.” Na baada ya kuisha muda huu na kipindi hiki atakachotaka Allah Mtukuka, utafika wakati wa hesabu, na kwa mujibu wa maelezo ya Qur’ani ni kwamba vi74

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 74

1/17/2017 1:14:23 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

tawekwa vipimo. Na kwa kuzingatia tuliyoyataja katika utangulizi, ni kwamba kipimo hapa si mizani yenye mikono miwili, bali mizani ni kila kinachotumika kuoanisha, na ni kwa maana hiyo hata vina vya mashairi tumekuwa tukiviita mizani ‘Mizani za Kishairi’. Kadhalika humaanisha hivyo pindi wengine wanapotumia neno mizani kumaanisha akili, kwani yenyewe ndio hulinganisha na kupima ni kipi sahihi na kipi kibovu kati ya vile vinavyowasilishwa akilini. Hivyo tunapozungumzia mas’ala ya kupima matendo, tufahamu kwamba matendo hayana uzito wa vipimo kwa maana ya kimada, kwa maana ya kwamba yatawekwa matendo mkono huu na jiwe mkono huu ili kupima. Bali wafasiri wanasema kwamba makusudio yake ni maana ya kinaya, yaani watu watahojiwa kuhusu matendo yao na yatapimwa kwa kuzingatia wema na kheri au shari na uovu. Hivyo Yule ambaye mizani yake itakuwa nzito hapa ni Yule ambaye amali zake ni nzito, na uzito wa amali unatokana na umuhimu wake na zilivyo safi kwa ajili ya Allah. Na ni kinyume chake kwa mtu ambaye mizani yake itakuwa hafifu. Hivyo yataanza maswali na hesabu, hesabu ambayo inagawanyika katika maeneo kadhaa, hesabu ya mtu mmoja mmoja, hesabu ya taifa moja moja, na hesabu ya kundi moja moja. Ili kujua kwa undani maudhui hii ya hesabu ya kundi moja moja na taifa moja moja, unawe75

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 75

1/17/2017 1:14:23 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

za kurejea kwenye kitabu al-Mdrasat al-Qur’aniiyyah cha Shahid, Sayyid Muhammad Baqir as-Sadri, Mungu awe radhi naye. Hivyo mazungumzo yetu hapa yatakomea kwenye hesabu ya mtu mmoja mmoja. Kuhusu hali za watu katika Siku ya Kiyama, tunasoma kauli ya Allah: “Na kila mmoja kati yao atamfikia siku ya Kiyama akiwa peke yake.” (Sura Maryam: 95), yaani akiwa mbali na ndugu, baba, mtoto na rafiki. Wote hao kila mmoja atakuwa akijishughulisha na nafsi yake, na atasimama mtu mmoja mmoja kwa ajili ya hesabu mbele ya Allah mbele ya mashuhuda. Manabii, Malaika na wanadamu wote kuanzia zama za Adam  mpaka kusimama Kiyama, wote hawa watahudhuria hesabu yake. Na ni kwa ajili hiyo imepokelewa katika dua nyingi maombi ya kuomba Allah atusitiri Siku ya Kiyama. Yaani asitufedheheshe siku hiyo mbele ya mashuhuda, kwa sababu hapa duniani sisi tumetenda yanayofedhehesha bila kujali fedheha ya Siku ya Kiyama. Mtu anaweza kutenda maasi duniani kwa siri, kwa kuogopa watu wa nyumbani kwake, jirani zake, wenzake, na raia wenzake wasimuone. Lakini Siku ya Kiyama yatafichuliwa mbele ya watu wote yale aliyoyatenda, mbele ya mashuhuda wote wa kuanzia tangu alipoumbwa Adam  mpaka Siku ya Kiyama. Hivyo kama miogoni mwetu kuna mtu mwenye kujali hes76

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 76

1/17/2017 1:14:23 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

hima yake, ni wajibu kwake kutilia umuhimu suala la kutokutenda aibu au dhambi ambayo Allah ataifichua na kumfedhehesha kwayo Siku ya Kiyama. Mtu atatangulia mbele kwa ajili ya hesabu, hapo ataletewa kitabu chake. Tazama kitabu chako. Atakuta ndani yake kila kitendo alichokitenda katika maisha yake. Hakijaacha kidogo wala kikubwa isipokuwa imekihesabu. Na mtu anaweza kuuliza: Wale watu wa zamani ambao walikuwa umri wao unapindukia miaka elfu moja, vitabu vyao vitakuwa na ukubwa kiasi gani na vitakuwaje? Wakati ambao watu wa zamani walikuwa hawafafanui jibu juu ya swali hili na wanaegemeza mas’ala hii kwa Allah Mtukuka, wanadamu wa leo wao wamefika katika kiwango cha kugundua teknolojia inayotusaidia kufahamu na kuelewa mas’ala kama hii na kujibu swali hilo. Leo hii imekuwa ni kawaida mmoja wetu kubeba chombo kidogo kisicho na ukubwa wa zaidi ya kitanga cha mkono, lakini ndani yake kabeba maelefu bali malaki ya vitabu. Kama ambavyo pia inawezekana kitabu cha matendo yetu kikawa ni skrini inayoonesha matukio ya maisha yetu, dhana hiyo ipo na Allah Ndiye ajuaye. Mtu atakaposoma kitabu chake kilichopo mbele yake, atakosa kabisa fursa ya kukanusha. Katika ma-

77

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 77

1/17/2017 1:14:23 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

hakama za kidunia, kwa mfano tu, mtu anaweza kusema uwongo, kuzusha na kuapa kiapo cha uwongo. Na anaweza kuleta ushahidi wa kisanii ambao utabadili uhalisia mbele ya macho ya hakimu. Lakini Siku ya Kiyama hataweza hilo, kwa sababu kila kitu kimesajiliwa mbele yake katika kitabu, na Manabii, Malaika na watu wote wa ulimwenguni ni mashuhuda juu yake. Bali ni kwamba hata kuta na nyumba ambazo humo alitendea maasi zitatoa ushahidi dhidi yake. Ulimi wake, mkono wake, na miguu yake vyote vitakuwa mashahidi dhidi yake. Atakimbilia wapi? Na katika siku hiyo ni nani atakayekuwa hakimu? Ni Yule Mwadilifu ambaye Yeye ndiye uadilifu mtupu, ambaye hadhulumu hata kidogo, na ambaye kwake yeye hakuna watu wa kati wala mahesabu. Hamuogopi yeyote wala hatamani chochote, ametakasika mbali na hayo. Yeye ni mwadilifu, Mwenye kujitosheleza Mwenye uwezo, ambaye hakifichikani kitu Kwake na elimu Yake imedhibiti hali zote za waja na mazingira yao, na Yeye ndiye aliyewaumba. Hivyo basi, mtu atakimbilia wapi kumkimbia? Katika mahakama za duniani unaweza kupata mtu wa kukutetea. Unaweza kumweka wakili wa kukutetea. Ama huko, hakuna wa kukutetea, Allah Mtukuka anasema: “Siku ambayo kila nafsi itakujajitetea. Na kila nafsi 78

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 78

1/17/2017 1:14:23 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

italipwa sawa na yale iliyoyafanya, nao hawatadhulumiwa.” (Sura Nahli: 111). Hivyo hapatakuwa na wakili mjuzi wa sharia wa kuweza kukutetea, bali ni wajibu kujitetea mwenyewe, na mambo yote yatakuwa wazi bayana dhahiri shahiri mbele yako. Na matokeo yatakuwa kulingana na kitabu, maswali na majibu, na hapo maamuzi yatatolewa. Yule ambaye mizani yake itakuwa nzito, yaani ambaye amali yake ni nzito, na ameendesha maisha yake katika amali njema. Yule aliyekithirisha mambo mema, huyu ni wa Peponi. Na yule ambaye mizani yake itakuwa hafifu, yule ambaye amali yake njema ni chache, au hana kabisa amali njema, huyu ni wa Motoni. Mas’ala hayana sintofahamu wala haja ya kuhitaji kitabu cha haki za ulimwengu mwingine. Allah anasema: “Basi yule ambaye mizani yake itakuwa nzito. Huyo atakuwa katika maisha ya kuridhiwa. Na yule ambaye mizani yake itakuwa hafifu. Basi mama yake atakuwa Hawiya! Na nini kitachokujulisha nini hiyo? Ni Moto mkali!” (Sura al-Qariah: 6 – 11). Kisha hati na vitabu vitagaiwa, yule atakayepokea kitabu chake kwa mkono wa kulia hatima yake ni Peponi, na yule atakayekibeba kwa mkono wake wa kushoto au nyuma ya mgongo wake huyo hatima yake ni Motoni.

79

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 79

1/17/2017 1:14:23 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

Na wakati au kabla kidogo ya hukumu na maamuzi kutolewa, na kama ilivyo katika mahakama zetu za duniani, mtu atajitahidi kutaka kupata suluhisho na chaguo. Atatafuta kitu cha kufanya ili kujiokoa na msiba huo. Na maana zote hizi zimo ndani ya Qur’ani, isipokuwa ni kwamba nyudhuru, majuto na masikitiko vyote havitamsaidia chochote huko. Wala kukiri kosa na kujutia hakutamsaidia, kama ambavyo hakuna nafasi ya fidia wala dhamana itakayoweza kumtoa kwenye adhabu hiyo, kama ilivyo katika mahakama za duniani, ambapo mhukumiwa hukubaliwa kutoa fidia, huko hata akitoa dhahabu sawa na ujazo wa ardhi kamwe haitakubaliwa. Allah anasema: “Siku ambayo haitafaa mali wala wana. Isipokuwa mwenye kuja kwa Mwenyezi Mungu na moyo uliosalimika.” (Sura Shuaraa: 88 – 89). Hivyo hakuna mali itakayofaa wala mtoto atakayemfaa mzazi wake, isipokuwa mas’ala ya Mashahidi (wafiadini), na hiyo ni katika sehemu ya uombezi. Allah anasema: “Siku ambayo rafiki hatamfaa rafiki yake kwa chochote, wala hawatanusuriwa.” (Sura Dukhan: 41), hivyo hatakufaa chochote Sheikh wako, au mkuu wako au kiongozi wako. Na anasema tena: “Siku ambayo mtu atamkimbia nduguye. Na mama yake na baba yake, na mkewe na wanawe.” Licha ya 80

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 80

1/17/2017 1:14:23 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

kwamba ndiyo watu awapendao zaidi. “Kila mtu katika wao siku hiyo atakuwa na jambo la kumtosha.” (Sura Abbasa: 34 – 37). Hivyo hatafaliwa na yeyote, si ndugu, si mama wala baba, si mke wala mtoto. Bali kutokana na uzito wa hali huko, “Atatamani mkosefu lau ajikomboe na adhabu ya siku hiyo kwa kuwatoa fidia wanawe, na mkewe, na nduguye.” Wakati ambapo hapa duniani alikuwa yuko tayari kujitolea muhanga nafsi yake ili kuwalinda wanawe dhidi ya hatari na vitisho vyote. “Na ukoo wake uliokuwa ukimzunguka.” Yaani ukoo wake, kabila lake, kundi lake, nchi yake na jeshi lake. “Na wote waliomo ardhini, kisha aokoke.” Lakini hapo atafikiwa na jibu kwamba: “Sivyo! Kwa hakika huo ni Moto mkali kabisa. Unaobabua ngozi ya kichwa!” (Sura Maarij: 11 – 16), nao ni Jahannamu inawangojea madhalimu, hivyo hakuna chochote kitakachomfaa. Hivyo mali, watoto, fidia, ukaribu na nasaba, vyote havitafaa huko, kwani siku hiyo hakutakuwa na nasaba baina yao. Wala majuto na udhuru havitsaidia. Hakutamsaidia kusema kwake: “Mola Wangu nirudishe duniani,”17 kwani wakati huo dunia itakuwa imeshakwisha na ardhi imeshabadilika na kuwa ardhi nyingine, na pia mbingu imeshakuwa mbingu nyingine.   Sura Muuminuna: 99.

17

81

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 81

1/17/2017 1:14:23 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

Basi ni Kitu Gani Kitakachomfaa Siku Hiyo? Dhamana pekee yenye kufaa siku hiyo ni imani na amali njema. Na ni kwa ajili hiyo tunamkuta AmirulMuuminina  akisema: “Jiandalieni masurufu, Allah atakurehemuni, na tayari mmeshapata wito wa kusafiri, na takwa ndio masurufu bora.”18 Na takwa ni matokeo ya imani na amali njema. Na amali njema inabeba maana pana, kuanzia ibada, jihadi na tabia njema. Kutenda kheri na kuamrisha mema. Kutoa sadaka kwa wahitaji na kuwasaidia wenye kuhitaji na kutafuta msaada, na kutetea heshima za watu na mali zao. Yote hayo ni mifano halisi ya amali njema, nayo peke yake ndiyo itakayomfaa mtu Siku ya Kiyama. Mtu anaweza kusema, Allah ameacha mlango wazi wa uokovu, nao ni mlango wa uombezi. Uombezi wa   Haya ndio aliyoyataja Kiongozi wa Waumini Ali  aliposema: “Jiandaeni, Mwenyezi Mungu akurehemuni! Imenadiwa katika nyinyi kuondoka, jueni kwamba ubakiaji hapa duniani ni mfupi mno, na rejeeni na masurufu mema mliyonayo. Kwa kweli mbele yenu kuna vikwazo vigumu. Dogesheni kuitegemea dunia, na nendeni na mema mliyonayo miongoni mwa masurufu, kwa kuwa mbele yenu kuna mafikio yanayotisha, na ni ya hatari, hapana budi muyafike, na mbakie humo. Na jueni kuwa macho ya mauti yanakuelekeeni na yapo karibu, kama kwamba makucha yake yamekwisha washika, na mambo ya kufadhaisha na shida za yaliyotahadharishwa zimekuzongeni. Hivyo basi jikateni mbali na mafungamano ya dunia, na jisaidieni kwa masurufu ya uchamungu.»

18

82

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 82

1/17/2017 1:14:23 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

Manabii, Maimamu, Mawalii na Mashahidi. Licha ya kwamba hakuna yeyote anayeweza kujipa dhamana na hakikisho kwamba uombezi utamfikia, lakini mlango huo umebaki kuwa ni moja kati ya milango ya matumaini. Maneno kuhusu itikadi ya uombezi yamepokewa katika riwaya mbalimbali na katika Aya za Qur’ani, nao umethibiti kwa Mashahidi, kwamba wao watawaombea ndugu zao na jamaa zao nao watakubaliwa uombezi wao. Na pia umethibiti kwa Manabii, Maimamu maasumu na kwa baadhi ya Mawalii na kwa makundi mengine atakayoyaridhia Allah, makundi hayo yametajwa na riwaya mbalimbali.19 Hawa watakuwa na   Makundi yafuatayo ndiyo yatakuwa na Uombezi wa siku ya Kiyama kwa mujibu wa riwaya: 1. Mtukufu Mtume , imepokewa kuwa alisema: “Nimepewa mambo matano ambayo hajapewa yeyote kabla yangu. Nimefanyiwa ardhi kuwa sehemu ya kusujudia na kuchukulia tohara. Nimehalalishiwa ghanima. Nimenusuriwa na woga. Nimepewa ufasaha. Na nimepewa uombezi.” Na alisema pia: “Mimi nina ubora juu ya Manabii wengine, hakuna Nabii isipokuwa aliwaombea watu wake dua fulani, na mimi nimeliweka hilo kwa ajili ya umma wangu ili niwaombee siku ya Kiyama.” Na alisema pia: “Kitakaposimama Kiyama nitawaombea wenye madhambi makubwa kutoka katika umma wangu, na Allah atakubali uombezi wangu.” 2. Maimamu Maasumu na Manabii wengine : Imepokewa kutoka kwa Abu Abdillah Imam Ja’far as-Sadiq kwamba alisema: “Hakuna yeyote miongoni mwa Manabii wa Allah na Mitume Wake atakayemuombea mtu mpaka pale Allah atakapotoa idhini, isipokuwa Mtume wa Allah. Yeye Allah ameshampa idhini ya kuombea hata kabla ya kusimama Kiyama. Uombezi ni wake na

19

83

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 83

1/17/2017 1:14:23 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

uombezi kutokana na nafasi yao, daraja yao na cheo chao kwa Allah na kwa kuwa kwao karibu Naye. Na Yeye ni Mkarimu Mwingi wa utoaji na Mpole, hivyo atawakubalia uombezi wao. Hivyo baadhi ya watu waliostahili adhabu watatolewa motoni na kutoka kwenye adhabu. Jambo hilo litatimia kwa kufuata kanuni na nidhamu ya ulimwengu wa Akhera, na lina vigezo vyake na mipaka yake, na hata Manabii na Mashahidi, uombezi wao utakuwa kwa ajili ya makundi maalumu ya watu ambao, wao waombaji wanajua Allah ataridhia kuwaombea, na si kwa watu wote. Na kuna mlango mwingine wa uokovu, nao ni mlango wa rehema za Allah Mtukuka. Allah ni Mwingi

3.

4.

Maimamu kutoka katika kizazi chake . Kisha baada ya hapo ni wa Manabii wa Allah . Makundi maalumu ya Waumini: Mtume amesema: “Yeyote atakayemsaidia mtafutaji wa elimu atakuwa amewapenda Manabii na atakuwa pamoja nao. Na yeyote atakayembughudhi mtafutaji wa elimu atakuwa amewabughudhi Manabii, na malipo yake ni moto. Na hakika mtafutaji wa elimu atakuwa na uombezi kama uombezi wa Manabii.” Na Imam as-Sadiq  amesema: “Ewe Fadhlu, usiwanyanyapae mafakiri kutoka katika wafuasi wetu. Hakika fakiri miongoni mwao atakuwa na uombezi Siku ya Kiyama sawa na kabila la Mudhari na Rabiah.” Qur’ani Tukufu: Imam Ja’far as-Sadiq  amesema: “Atakayesoma Qur’ani wakati angali kijana ilihali ni muumini, Qur’ani itachanganyikana na nyama yake na damu yake, na Allah atamweka pamoja na waandishi wema, na Qur’ani itakuwa kinga yake siku ya Kiyama.” 84

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 84

1/17/2017 1:14:23 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

wa huruma, Mpole na rehema Zake huzifunika hata ghadhabu Zake. Hivyo anaweza kuwasamehe baadhi ya watu kati ya wale walioingizwa motoni, miongoni mwa wale waliomuasi na kumfanyia jeuri, miongoni mwa wale waliomshirikisha na wakakanusha uwepo Wake. Hiyo ni kutokana na jinsi rehema Yake itakavyoenea siku hiyo, na kusambaa kwa kiasi ambacho akili haziwezi kudhania. Na jambo hili limo mkononi Mwake na katika utashi Wake. Imepokewa katika baadhi ya riwaya kwamba, Allah atasambaza rehema Siku ya Kiyama, rehema ambayo hata Ibilisi ataitamani. Yaani Ibilisi ambaye hana mafikio isipokuwa Jahannam shingo yake itarefuka siku hiyo kwa kutamani rehema ya Allah Mtukuka, kwa kuwa anatambua kwamba Yeye Mtukuka ni Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu. Lakini mlango wa uombezi na rehema itakayoenea hauna dhamana na hakikisho la kuwa wazi kwa kila mmoja wetu. Hivyo imani na amali njema vinabaki kuwa ndio dhamana pekee. Kheri yoyote ile tuitendayo tutaikuta huko na wala hatutakuta kingine zaidi yake. Amali zetu njema zinatutangulia huko. Kheri tuitendayo katika dunia hii inatutangulia huko. Hii ndio dhamana yetu ya kweli.

85

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 85

1/17/2017 1:14:23 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

Muhtasari Kuhusu Sirati20 na Matokeo: Baada ya hatua hizo jambo litakuwa limeshaamriwa, watu wa Peponi wataelekezwa peponi, watakusanywa na kusindikizwa huko kama bibi harusi apelekwavyo kwa mumewe. Na watu wa motoni wataelekezwa motoni, watakusanywa na kusindikizwa huko kwa kukokotwa nywele za utosini na nyayo. Maelezo yote haya yamo ndani ya Qur’ani Tukufu na katika hadithi tukufu, nayo ni maeneo ambayo ni wajibu kuyatilia umuhimu na kuyasoma. Kwa mfano tu moja ya maeneo hayo ni Sura Zumar. Na hapa ndipo yanajitokeza mazungumzo kuhusu maudhui ya Sirati (Njia) ambayo imetajwa kuwa watu wataivuka kuelekea peponi. Kwa kuzingatia suala la kutumia maneno kwa kumaanisha maana halina maana ya kinaya, je Sirati ni daraja la kimada ambalo watembea kwa miguu watalipita likiwa juu ya moto ili waelekee peponi, au maana yake ni dini ambayo ndio njia ya Mungu, yaani njia iliyonyooka ambayo kama tutaifuata na kuipita tutafika peponi? Na kwa ibara nyingine ni kwamba, je neno Sirat limetumika kwa kumaanisha   Kwa mujibu wa Kamusi ya Kiswahili Sanifu, Toleo la Tatu iliyochapishwa na TUKI, Sirati ni “Njia inayoaminiwa na Waislamu kuwa itapitwa na binadamu siku ya malipo, ili wengine kwendea peponi na wengine motoni.” – Mtarjumi.

20

86

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 86

1/17/2017 1:14:23 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

maana yake halisi au kinaya? Katika hilo pia Maulamaa wametofautiana. Wapo wanaojengea kwa kufuata rai ya kwanza, na wapo wengine wanaofuata rai ya pili. Na mjadala huu ijapokuwa tumeupa mgongo lakini bado unazingatiwa kuwa ni mjadala muhimu na unaopaswa kutizamwa, kutokana na jinsi maudhui ya Sirati ilivyo na ufafanuzi na maelezo na mambo yanayohusu hatima ya binadamu. Na sasa watu walioingia peponi bila shaka wamefuzu na humo ndio sehemu yao ya kudumu. Ama watu wa motoni, wao wamegawanyika sehemu mbili, watakao ishi milele motoni, na wengine watakaokuja kutolewa baadaye, ima kwa kuwa wamechanganya kati ya amali njema na ovu, au kwa sababu ya kujumuishwa na rehema za Mungu, na au kwa sababu ya kuombewa na mmoja kati ya wale wenye uombezi, na hatimaye unatoka uamuzi wa kuwasamehe na kuhamishwa kutoka motoni hadi peponi. Ama ufafanuzi zaidi kuhusu watu wa namna hii hatutauzungumzia hapa, lakini ni vizuri kuujua na kuutafiti kwa kina. Ama lililo muhimu hapa ni kukanyana na kukatazana kutegemea ufafanuzi huo, mtu kusema kwamba mimi nachanganya matendo mema na maovu, hivyo nitaingia motoni kwa muda kisha nitatolewa. Kwani hakuna yeyote anayeweza kutaamali na kustahimili mngurumo na kufoka kwa moto 87

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 87

1/17/2017 1:14:23 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

ambao utapanda hadi vifuani. Mwisho wa hali ya Kiyama.

Neno Kuhusu Lengo la Utafiti Huu: Hakika lengo tulilotaka kulifikia katika maelezo na ufafanuzi tuliouwasilisha, ni kuwaamsha na kuwazindua walioghafilika, na ni kuwakumbusha uwepo wa majukumu makubwa na nyeti juu ya bega la kila mmoja wetu. Hivyo ni wajibu juu ya kila mmoja wetu kuiwekea nafsi yake njia na lengo mbele ya ufafanuzi uliotangulia, kwani hali tuliyotangulia kuitaja ni hali halisi ya kweli na itakayokuja, haina kizuizi. Na maandiko ya Qur’ani na hadithi yamesisitiza kutokea kwake, na wakati itakapotokea, toba na majuto havitamfaa mtu chochote. Mtu atajuta sana lakini majuto na masikitiko yake hayatamsaidia. Mtenda maasi atajuta kwa vitendo alivyotenda pindi atakapoona kitisho cha adhabu. Na mtiifu kwa Mungu atajuta na kusikitika kwa nini alizembea, pindi atakapoona ukubwa wa neema. Hivyo ni wajibu kwetu tuweke malengo mbele yetu, nayo ni kufikia kiwango cha kumtumikia Allah Mtukuka, bila kujali daraja za utumishi, kwamba kuna ibada ya wafanyabiashara, na ibada ya watumwa, na ibada ya waungwana huru. Na tuache kusema kwamba Mungu hatakubali ibada na utumishi wetu kwake mpaka pale 88

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 88

1/17/2017 1:14:23 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

tutakapofikia daraja ya juu zaidi kati ya daraja hizo za utumishi na ibada. Kwani daraja hiyo ni makhususi kwa Manabii na mawalii. Na wala haipasi kuwazuia watu kwa kuwatilia uzito katika suala la kuabudu na kumtumikia Mungu. Bali kauli sahihi ya kusema ni kuwa, ni wajibu kwetu kujituma ili kufikia maana ya utumishi mbele ya Allah, kwa kushikamana na maamrisho Yake na kuacha makatazo Yake. Na Allah anakubali hilo, sawa tuwe ni miongoni mwa wafanyabiashara au miongoni mwa watumwa. Allah anasema:

ْ َ ُ َ ُ ُ َ ْ َّ َ ُ َ َّ َ ْ َ ْ‫ُ ُّ َ ْ َ َ ُ لم‬ ‫ورك ْم َي ْو َم ال ِق َي َام ِة ۖ ف َم ْن‬ ‫س ذا ِئقة ا و ِت ۗ وِإنما توفون أج‬ ٍ ‫كل نف‬ ُ ‫الد ْن َيا إ اَّل َم َت‬ َّ َ َ ْ ُ ُّ ‫النار َو ُأ ْدخ َل ْال َج َّن َة َف َق ْد َو َما ْال َح َي ُاة‬ ‫اع‬ ِ ِ ‫زح ِزح ع ِن‬ ِ ُ ‫ْال ُغ‬ ‫ور‬ ‫ر‬ ِ

“Kila nafsi itaonja mauti. Na bila shaka mtatekelezewa malipo yenu Siku ya Kiyama. Mwenye kuepushwa na moto akatiwa peponi, basi huyo amefuzu.” (Sura Imran: 185), nalo ni lengo ambalo anapaswa mwanadamu kulitumikia katika kipindi chote cha uhai wake ili kulifikia. Hivyo inapasa lengo langu liwe ni kuepushwa na moto, na Siku ya Kiyama niwe katika amani, na siku ya mfazaiko mkubwa 89

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 89

1/17/2017 1:14:24 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

niwe katika utulivu, na rehema za Allah zinifunike na kunifikia. Na nisifedheheshwe mbele ya Allah, Malaika Wake, Manabii Wake na watu wote. Nataka heshima, utukufu, amani, neema, salama, na afya huko Akhera. Nataka kujisalimisha na adhabu ambayo roho haiwezi kuistahamili. Hili ndio lengo letu na ni wajibu juu yetu kuliwekea mbele yake yale aliyoyataka Allah kutoka kwetu.

ُ ْ َ َ ْ ُ َ ُ ْ َ ُ ُ َ َ َّ َ ُّ َ َ َّ ‫ود َها‬ ُ ‫يك ْم َنا ًرا َو ُق‬ ُ ‫الن‬ ‫اس‬ ‫يا أيها ال ِذين آمنوا قوا أنفسكم وأه ِل‬ ْ ُ ‫َوال ِح َجا َرة‬

“Enyi mlioamini! Jilindeni nafsi zenu na ahali zenu na Moto ambao kuni zake ni watu na mawe.” (Sura Tahrim: 6). Na tunapoweka lengo hili mbele ya macho yetu, ni wajibu kwetu kwa lengo la kuweza kulifikia lengo hilo, kushikamana na vitendo na njia ya kivitendo, nami naifupisha hapa kwa kutaja hatua kadhaa: Kwanza: Tuikumbuke Akhera. Tusiisahau wala kughafilika nayo. Wala kukumbuka kwetu Akhera, kaburi, barzakh, matukio ya Kiyama, matokeo yake, pepo na moto, kusiwe ni kukumbuka kwa msimu, katika baadhi ya minasaba tu, kama vile katika mikesha ya Lay-

90

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 90

1/17/2017 1:14:24 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

latul-Qadri, au pindi anapofariki kipenzi. Bali iwe ni kumbukumbu ya saa zote, kwani mauti yatakuja ghafla na wala hatujui Kiyama kitakuwa lini. Hivyo kukumbuka daima mauti na Akhera ndio hatua ya kwanza, na ndio jambo litakaloweka uhai kwetu na kutuhisisha thamani ya saa na siku ambazo zinaweza kwisha. Na wala hakuna kitenganishi kitakachoweza kututenganisha na Akhera yetu wala na mauti yetu. Pili: Tuchukue tahadhari kuhusu Akhera. Nayo ndiyo maana iliyoashiriwa katika Aya tuliyoigusia katika utangulizi. Na madhumuni yake ni kwamba tuiogope Akhera, tuikhofu na kuwa makini nayo. Isiwe ni kuikumbuka tu bila kitu, hivyo tuichukulie tahadhari yenyewe pamoja na mazito yake. Tatu: Tutende kwa ajili ya Akhera. Kama ambavyo kila moja wetu anavyoyawekea malengo maisha yake ya dunia na anajituma kuweza kuyafikia na kuyatimiza malengo yake, kiasi unamkuta mtu anaweka mipango, anatenda, anakesha usiku na anajituma mchana, basi je, maisha ya Akhera hayastahiki mtendaji huyo kuyafanyia kazi na kujitolea katika njia ya kuyatengeneza kwa juhudi zake zote? Kwa nini mtu asimuombe maghufira Mola Wake na kutubia Kwake kutokana na dhambi zake zilizopita, kwanza. Pili, kwa nini asilipe Swala na

91

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 91

1/17/2017 1:14:24 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

ibada zilizompita, na atekeleze katika mali yake haki ya muombaji na aliyenyimwa. Kwa nini asiizindue nafsi yake kutoka kwenye mghafala wa kutenda madhambi na maasi katika kila jambo. Maelekezo haya nayaelekeza zaidi kwa kizazi cha vijana, ambao bado wangali katika umri wa ujana, wanamiliki nguvu na uchangamfu, vitu ambavyo wazee hawanavyo tena. Lakini simaanishi kuwa hawa (wazee) wamepitwa na fursa, bali ninalokusudia ni kwamba fursa ya vijana ni kubwa zaidi. Hivyo ni wajibu kwetu sote kutenda amali njema na kuutumia uwepo wetu katika dunia hii, kutumia mengine tuliyonayo miongoni mwa siha, afya njema, na pia kutumia mengine tunayoyamiliki miongoni mwa mali, uwezo na wakati, na umri wetu uliobakia. Mambo yote hayo inapasa kuyatumia katika njia ya kutengeneza Akhera yetu ambayo, urefu wake si miaka hamsini au mia moja, bali ni mamilioni ya miaka na zaidi, kwani yenyewe ni nyumba ya milele, na Allah Ndiye ajuaye. Na hakika maelezo muhimu zaidi katika ratiba hii ya kimatendo ni kutoipenda dunia na kuing’ang’ania, kuanzia mali, vyeo na matamanio mengine. Kwa sababu kuipenda dunia huwa kunarahisisha mbele ya macho yetu hali ya kutenda haramu na kufuata mata-

92

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 92

1/17/2017 1:14:24 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

manio yake. Ni watenda maasi wangapi wameyataka matamanio na starehe ya dunia, na hatimaye nafsi iamrishayo maovu imewasukuma kuthubutu kutenda maasi kwa lengo la kuyafikia matamanio hayo. Wala hapa hatusemi kwamba mtu akate uhusiano wake na dunia, kwani dunia ni chumo la Akhera, na kila mmoja wetu ndani ya dunia hii ana mke, watoto na maslahi. Lakini kinachotakiwa ni kwamba uhusiano wake huu na dunia usiwe kwa namna ambayo kama mtu ataombwa kutoa mali, au mtoto au kuhudhuria kwenye medani ya jihadi, atakataa. Na mwenye kuihama dunia kwa maana hii niliyoikusudia, bila shaka yeye anaipenda Akhera kwa moyo wake, kwani anafaidika na dunia, na anaishi duniani kama wanavyoishi na walivyoishi watu wema. Maana hii ndio muhtasari wa safari ya Husein ď ‚ na waliokuwa pamoja naye miongoni mwa watu wa Karbala.

Tukio la Karbala Katika Kipimo cha ­Kujituma kwa Ajili ya Akhera: Na kwa kuendelea na mtiririko ule ule uliopita, tunasema kwamba, baadhi ya watu wanaweza kufaulu kupitia yale tuliyowasilisha, kwa kujituma kuelekea katika kujisalimisha na moto na kufuzu kwa kupata pepo. Na wengine wanaweza kupanda daraja na hivyo wakafaulu 93

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 93

1/17/2017 1:14:24 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

katika juhudi na kujituma kwao, bali wanaweza kuwa hata sababu ya wengine kuokoka. Lakini kiwango cha juu kabisa cha juhudi na kujituma huku ni mtu kujituma katika njia ya kuwatafutia uokovu watu wote wa aridhini. Na huu ndio uliokuwa wajibu wa Manabii na Maimamu. Na ndivyo ilivyokuwa hali ya Imam Husein . Imam Husein  pale Karbala, kwa shahada yake na mapinduzi yake alikusudia kuwaepusha watu na njia ya motoni, na aliwaachia njia ya kuelekea peponi ikiwa wazi mpaka siku ya kusimama Kiyama. Ni upi muhtasari wa tukio la Karbala? Ukweli ni kwamba sisi hatuko mbele ya jamii ambayo haijui haki na batili, bali haki ilikuwa bayana na kadhalika batili. Waislamu wote wa zama zile walikuwa wanajua ni nani Husein na ni nani Yazid. Husein ni mjukuu wa Mtukufu Mtume , naye katika umma huu ana nafasi na cheo kikubwa kiasi kwamba haisihi kwa yeyote kudai kuwa hakijui. Hivyo haki ilikuwa bayana na batili ilikuwa wazi. Vita vilikuwa wazi na malengo yalikuwa bayana. Lakini tatizo lilikuwa hapa, kwamba baadhi ya watu waliipupia dunia yao wakaing’ang’ania. Waliogopa kupoteza mali zao na watoto wao, nyumba zao na mambo mengine ya kidunia yenye kutoweka. Hivyo wakamtelekeza mjukuu wa Mtume wa Allah , si hivyo tu bali walimuuwa kikatili. Baadhi yao kwa ajili ya kutaka 94

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 94

1/17/2017 1:14:24 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

cheo huko Ray, au Kufa au Basra, walimtelekeza Husein  na wakamuuwa. Hivyo wakaikosaAkhera, bali Allah aliwafedhehesha mpaka wakakosa hata kuipata hiyo dunia. Mkabala na watu hao tunawakuta watu – nao walikuwa wachache - ambao walimtambua Allah na wakaingiwa na khofu kwa kuogopa wakati wa kusimama na kuhojiwa mbele Yake. Hao ni watu mfano wa Habib bin Madhahir, aliyekuwa mtu mzima sana. Na Zuhayri bin Qayni, Abbas bin Ali, Qasim na wengineo miongoni mwa wanaume na wanawake waliokuwa Karbala. Hawa wameshamaliza wajibu wao. Lakini kesho tutakapokusanywa katika uwanja wa mkusanyiko, mbele ya Allah Mtukuka na tukiulizwa kuhusu safari ya Husein mwana wa binti wa Mtume wa Allah , ambaye alikuwa katika njia ya kuitetea dini yetu na kuamrisha mema na kukataza maovu, na tukiulizwa kuhusu wajibu wa kumtetea na kumnusuru ulio juu yetu, je tulimnusuru au la? Hakika jibu letu litakuwa: Ndiyo ewe Mola Wetu. Tulisimama pamoja naye na tulibaki pamoja naye. Tuliumizwa na kiu pamoja naye na tulipigana pamoja naye. Tuliuwawa mbele yake na tulikatwakatwa viungo mbele yake ili tufufuliwe Siku ya Kiyama tukiwa ni wenye nyuso ze-

95

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 95

1/17/2017 1:14:24 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

nye kung’aa. Siku ambayo baadhi ya nyuso zitang’aa na nyingine zitasawijika. Hiki ndio kisa cha Karbala kwa kina na uhakika. Amani iwe juu yako ewe Bwana wangu na Kiongozi wangu! Ewe Abu Abdillah Husein. Ewe mwana wa Mtume wa Allah. Iwe juu yako na juu ya roho zenye makazi katika kaburi lako. Amani ya Allah iwe juu yenu nyote kutoka kwangu, muda wote nitakaoendelea kubaki na kadiri usiku na mchana utakavyoendelea kuwepo. Na wala Allah asiifanye hii kuwa ndio mara yangu ya mwisho kuwazuru ninyi. Amani iwe juu ya Husein, na juu ya Ali bin Husein, na juu ya watoto wa Husein, na juu ya maswahaba wa Husein.

Kila sifa njema anastahiki Allah, Mola Mlezi wa viumbe wote.

96

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 96

1/17/2017 1:14:24 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

Orodha Ya Vitabu Vilivyo ­Chapishwa Na Al-Itrah Foundation 1.

i) Qur’ani Tukufu – Pamoja na Tarjuma ya Kiswahili ii) Qur’an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Thelathini 2. Uharamisho wa Riba 3. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza 4. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili 5. Hekaya za Bahlul 6. Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) 7. Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (a.s.) 8. Hijab vazi Bora 9. Ukweli wa Shia Ithnaashari 10. Madhambi Makuu 11. Mbingu imenikirimu 12. Abdallah Ibn Saba 13. Khadijatul Kubra 14. Utumwa 15. Umakini katika Swala 16. Misingi ya Maarifa 17. Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia 18. Bilal wa Afrika

97

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 97

1/17/2017 1:14:24 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

19. Abudhar 20. Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu 21. Salman Farsi 22. Ammar Yasir 23. Qur’an na Hadithi 24. Elimu ya Nafsi 25. Yajue Madhehebu ya Shia 26. Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur’an Tukufu 27. Al-Wahda 28. Ponyo kutoka katika Qur’an 29. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii 30. Mashukio ya Akhera 31. Al Amali 32. Dua kwa Mujibu wa Ahlulbayt (a.s) 33. Udhuu kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna 34. Haki za wanawake katika Uislamu 35. Mwenyezi Mungu na sifa zake 36. Kumswalia Mtume (s) 37. Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) 38. Adhana 39. Upendo katika Ukristo na Uislamu 40. Qur’ani na Kuhifadhiwa Kwake 41. Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu 42. Kupaka juu ya khofu 43. Kukusanya Sala Mbili

98

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 98

1/17/2017 1:14:24 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

44. Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara 45. Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya 46. Kusujudu juu ya udongo 47. Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s) 48. Tarawehe 49. Malumbano baina ya Sunni na Shia 50. Kupunguza Swala safarini 51. Kufungua safarini 52. Umaasumu wa Manabii 53. Qur’an Yatoa Changamoto 54. as-Salaatu Khayrun Mina -’n Nawm 55. Uadilifu wa Masahaba 56. Dua e Kumayl 57. Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu 58. Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake 59. Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata 60. Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mtume ­Muhammad (s) 61. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza 62. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili 63. Kuzuru Makaburi 64. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza 65. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili 66. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu 67. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne 68. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano 99

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 99

1/17/2017 1:14:24 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

69. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita 70. Tujifunze Misingi Ya Dini 71. Sala ni Nguzo ya Dini 72. Mikesha Ya Peshawar 73. Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu 74. Ubora wa Imam ‘Ali na Ushia ndio njia iliyonyooka 75. Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake 76. Liqaa-u-llaah 77. Muhammad (s) Mtume wa Allah 78. Amani na Jihadi Katika Uislamu 79. Uislamu Ulienea Vipi? 80. Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) 81. Dhana ya Ndoa ya Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) 82. Urejeo (al-Raj’ah) 83. Mazingira 84. Utokezo (al - Badau) 85. Hukumu ya kujenga juu ya makaburi 86. Swala ya maiti na kumlilia maiti 87. Uislamu na Uwingi wa Dini 88. Mtoto mwema 89. Adabu za Sokoni Na Njiani 90. Johari za hekima kwa vijana 91. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza 92. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili 93. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu 100

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 100

1/17/2017 1:14:24 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

94. 95. 96. 97. 98. 99. 100. 101. 102. 103. 104. 105. 106. 107. 108. 109. 110. 111. 112. 113. 114. 115. 116. 117. 118.

Tawasali (AT- TAWASSUL) Imam Mahdi katika Usunni na Ushia Hukumu za Mgonjwa Sadaka yenye kuendelea Msahafu wa Imam Ali Maimamu wa Ahlul Bait – Ujumbe na Jihadi Idi Al-Ghadir Kusoma sura zenye Sijda ya wajibu Hukumu zinazomuhusu mkuu wa kazi na Mfanyakazi Huduma ya Afya katika Uislamu Sunna za Nabii Muhammad (saww) Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza) Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili) Shahiid Mfiadini Mwanamke Na Sharia Ujumbe -Sehemu ya Kwanza Ujumbe - Sehemu ya Pili Ujumbe - Sehemu ya Tatu Ujumbe - Sehemu ya Nne Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu Hadithi ya Thaqalain Ndoa ya Mutaa Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza Ukweli uliopotea sehemu ya Pili Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu

101

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 101

1/17/2017 1:14:24 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

119. Ukweli uliopotea sehemu ya Nne 120. Ukweli uliopotea sehemu ya Tano 121. Mkutano wa Maulamaa wa Baghdad 122. Safari ya kuifuata Nuru 123. Fatima al-Zahra 124. Myahudi wa Kimataifa 125. Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi 126. Visa vya kweli sehemu ya Kwanza 127. Visa vya kweli sehemu ya Pili 128. Elimu ya Ghaibu ya Maimamu 129. Mwanadamu na Mustakabali wake 130. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Kwanza) 131. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Pili) 132. Khairul l’Bariyyah 133. Uislamu na mafunzo ya kimalezi 134. Vijana ni Hazina ya Uislamu 135. Adhana ni Ndoto au ni Wahyi? 136. Tabaruku 137. Saada Kamili – Kitabu cha Kiada cha Maadili 138. Vikao vya furaha 139. Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje? 140. Visa vya wachamungu 141. Falsafa ya Dini 142. Kuhuzunika na Kuomboleza 102

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 102

1/17/2017 1:14:24 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

143. Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah 144. Mjadala wa Kiitikadi 145. Kuonekana kwa Allah 146. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza) 147. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili) 148. Ndugu na Jirani 149. Ushia ndani ya Usunni 150. Maswali na Majibu 151. Mafunzo ya hukmu za ibada 152. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 1 153. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 2 154. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 3 155. Abu Huraira 156. Vipengee kadhaa katika Swala ya Jamaa na Msikiti. 157. Mazingatio kutoka katika Qur’an - Sehemu ya Kwanza 158. Mazingatio kutoka kaitka Qur’an - Sehemu ya Pili 159. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya kwanza 160. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya Pili 161. Shia na Qur’ani – Majibu na Maelezo 162. Falsafa ya Mageuzi ya Imam Husein (a.s) 163. Amali za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani 164. Elimu ya Tiba za Kiislamu - Matibabu ya Maimamu 165. Uislamu Safi 166. Majlisi za Imam Husein Majumbani 167. Je, Kufunga Mikono 103

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 103

1/17/2017 1:14:24 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

168. Uislam wa Shia 169. Amali za Makka 170. Amali za Madina 171. Asili ya Madhehebu katika Uislamu 172. Sira ya Imam Ali kuhusu Waasi 173. Ukweli uliofichika katika neno la Allah 174. Uislamu na Mifumo ya Uchumi 175. Umoja wa Kiislamu na Furaha 176. Mas’ala ya Kifiqhi 177. Jifunze kusoma Qur’ani 178. as-Sahifatul Kamilah as-Sajjadiyyah 179. Hayya ‘Alaa Khayri’l-’Amal Katika Adhana 180. Ukweli kuhusu Funga ya Siku ya Ashura 181. Dua za Miezi Mitatu Mitukufu (Rajabu, Shaabani na Ramadhani) 182. Uadilifu katika Uislamu 183. Mahdi katika Sunna 184. Maswali Ya Uchunguzi Kuhusu Uislam 185. Kazi na Bidii ni njia ya maendeleo 186. Abu Talib – Jabali Imara la Imani 187. Ujenzi na Utakaso wa Nafsi 188. Vijana na Matarajio ya Baadaye 189. Historia maana na lengo la Usalafi 190. Ushia – Hoja na Majibu 191. Mateso ya Dhuria wa Mtume (saww) 192. Maombolezo – Msiba wa Bwana wa Mashahidi (a.s.) 104

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 104

1/17/2017 1:14:24 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

193. Shahidi kwa Ajili ya Ubinadamu 194. Takwa 195. Upotoshaji Dhahiri katika (Turathi) Hazina ya Kiislamu 196. Amirul Muuminina (as) na Makhalifa 197. Tawheed Na Shirki 198. Kuvunja hoja iliyotumika kutetea Uimamu wa AbuBakr 199. Adabu za vikao na mazungumzo 200. Hija ya Kuaga 201. Uwazi baina ya Maslahi na Vikwazo 202. Fadhila za watukufu watano katika Sahih Sita 203. Mdahalo baina ya Mwanachuoni waKisunni na Kishia (Al- Muraja’aat) 204. Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (as) 205. Imam Husain ni Mfumo wa Marekebisho na Mageuzi 206. Mtazamo kuhusu msuguano wa Kimadhehebu 207. Nchi na Uraia – Haki na wajibu kwa Taifa 208. Mtazamo wa Ibn Taymiyyah juu ya Imam Ali (as) 209. Uongozi wa Kidini – Maelekezo na Utekelezaji wa Kijamii 210. Maadili ya Ashura 211. Mshumaa – Shahidi na Kifo cha Kishahidi 212. Mizani ya Hekima – Hadithi za Ahlul Bait (as) – Sehemu ya Kwanza 213. Imam Ali na Mambo ya Umma 214. Imam Ali na Mfumo wa Usawa 215. Uimamu na Tamko la Kutawazwa 216. Mfumo wa Wilaya 105

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 105

1/17/2017 1:14:24 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

217. Vipi Tutaishinda Hofu? 218. Kumswalia Mtume ni Ufunguo wa Utatuzi wa Matatizo 219. Maeneo ya Umma na Mali Zake 220. Nahju ‘L-Balagha– Majmua ya Khutba, Amri, Barua, ­Risala, Mawaidha na Semi za Amirul-Muuminin Ali bin Abu Talib (a.s.) 221. Mukhtar – Shujaa aliyelipiza kisasi dhidi ya wauaji wa Imam Husein (as) hapo Karbala 222. Mazingatio Katika Swala 223. Imam Hasan na Mfumo wa Kujenga Jamii 224. Vyakula Na Vinywaji 225. Kuelewa Rehema ya Mwenyezi Mungu 226. Imam Mahdi na Bishara ya Matumaini 227. Mtazamo Mpya - Wanawake katika Uislamu 228. Shia Na Sahaba - Majibu na Maelezo 229. Majanga Na Jukumu la Jamii 230. Shia Na Hadith - Majibu na Maelezo 231. Upotofu Ndani ya Kitabu cha Mitaala kwa Shule za Sekondari 232. Ugaidi Wa Kifikra Katika Medani Ya Kidini 233. Yafaayo kijamii 234. Uswalihina Dhahiri Na Batini Yake 235. Mkakati wa Kupambana na Ufakiri 236. Mwanamke Katika Harakati Za Mageuzi 237. Jihadi 238. Hija Katika Maneno Na Ujumbe Wa Imam Khomeini (R.A) 106

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 106

1/17/2017 1:14:24 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

239. Tiba Ya Maradhi Ya Kimaadili 240. Yusuf Mkweli 241. Taqiyya Kwa Mujibu Wa Sheria Ya KIISLAMU 242. Imam Mahdi (A.S) Imam Wa Zama Hizi Na Kiongozi Wa Dunia 243. Talaka Tatu 244. Safari Ya Kuelekea Kwa Mwenyezi Mungu 245. Hotuba Za Kiislamu Juu Ya Haki Za Binadamu 246. Mashairi Ya Kijamii 247. Ngano Ya Kwamba Qur’ani Imebadilishwa 248. Wito Kwa Waumini: “Enyi Mlioamini” 249. Imam Husain (a.s) ni Utu na Kadhia 250. Imam Husain ni Kielelezo cha Kujitoa Muhanga na Fidia 251. Imam Mahdi ni Tumaini la Mataifa 252. Kuchagua Mchumba 253. Mazungumzo ya Umoja – Ukosoaji na Usahihishaji 254. Utamaduni wa Mwamko wa Kijamii 255. Hekima za kina za Swala 256. Kanuni za Sharia za Kiislamu 257. Utamaduni kufuatana na Qur’ani na Utekelezaji wa ­Kivitendo (Sehemu ya Kwanza) 258. Kauli sahihi zaidi katika kufafanua Hadithi

107

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 107

1/17/2017 1:14:24 PM


UWANJA WA MKUSANYIKO

KOPI ZIFUATAZO ZIMETAFSIRIWA KWA LUGHA KINYARWANDA 1.

Amateka Na Aba’ Khalifa

2.

Nyuma yaho naje kuyoboka

3.

Amavu n;amavuko by;ubushiya

4.

Shiya na Hadithi

5.

Kor’ani Nziranenge

6.

Kwigisha Mu Buryo Bw’incamake Uka Salat Ikotwa

7.

Iduwa ya Kumayili

ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION KWA LUGHA YA KIFARANSA 1.

Livre Islamique

108

19_16_Uwanja wa Mkusanyiko_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 108

1/17/2017 1:14:24 PM


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.