Viashiria vya uchamungu

Page 1

VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU (Indicators of Peity)

Mwandishi: Muhammad Ali Shomali

Kimetarjumiwa na: Salman Shou

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 1

1/17/2017 1:10:12 PM


©Haki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: 978 - 9987 – 17 – 014 – 2 Mwandishi: Muhammad Ali Shomali Kimetarjumiwa na: Salman Shou Kimehaririwa na: Al-Haj Ramadhani S.K. Shemahimbo Kimesomwa-Prufu na: Alhaj Hemedi Lubumba Selemani Kimepitiwa na: Alhaj Mujahid Rashid Kimepangwa katika Kompyuta na: Al-Itrah Foundation Toleo la kwanza: Mei, 2017 Nakala: 2000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. - 19701, Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 / 2127555 Barua Pepe: alitrah@yahoo.com Tovuti: w.w.w.alitrah.info

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 2

1/17/2017 1:10:12 PM


YALIYOMO Dibaji.............................................................................................. 1 Neno la Mchapishaji...................................................................... 2 Sehemu ya Kwanza........................................................................ 4 Sehemu ya Pili............................................................................. 19 Uchamungu katika hadithi:.......................................................... 20 Uchamungu katika Qur`ani Tukufu:............................................ 24 Sehemu ya Tatu............................................................................ 34 Wacha Mungu:............................................................................. 35 Imani Katika ghaibu:.................................................................... 35 Sehemu ya Nne............................................................................ 49 Mafanikio ya kweli:..................................................................... 50 Mambo ya furaha ya kidunia:...................................................... 52 Mambo ya mafanikio katika Akhera:........................................... 52 Maelezo ya waaminio:................................................................. 52 Waumini watakuwa warithi wa Pepo........................................... 57 Maelezo ya Waumini katika hadithi:........................................... 60 Sehemu ya Tano........................................................................... 72 Kumpenda Mwenyezi Mungu na kuwapenda wengine kwa ajili ya Mungu........................................................ 73

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 3

1/17/2017 1:10:12 PM


Dhahiri ya Siku ya Hukumu:....................................................... 78 Maana Pana zaidi ya kuwapenda wengine................................... 80 Msingi wa Uislamu...................................................................... 83 Uwalii (Wilayat) dhana na utekelezaji......................................... 84 Sifa za muumini........................................................................... 85 Kitendo kilicho bora zaidi:........................................................... 87 Wajibu wa akili............................................................................ 88 Ibada potofu................................................................................. 89

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 4

1/17/2017 1:10:12 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬

DIBAJI

K

itabu hiki ni toleo la Kiswahili la taasisi ya Al Itrah Foundation. Chapisho lake limelenga kukidhi mahitaji ya kiroho ya zama hizi pamoja na Ubongo na fikra zinazokuwa za Muislam. Jitihada kubwa zimefanywa na Taasisi kuweka chapisho hili la Kiswahili katika msingi wa haki na wenye kukubalika katika Uislam. Unaombwa kwa Taadhima ukisome kitabu hiki katika malengo yaliyokusudiwa. Pia Unaombwa kuwasilisha kwetu maoni yako huru juu ya chapisho letu hili, jambo ambalo tutashukuru sana. Kutangaza ujumbe wa Uislam ni kazi ambayo inahitaji ushirikiano wetu sote. Taasisi inakuomba kuungana na kushirikiana kama ilivyoagizwa katika aya ya Qur’an: (Surat Saba’ 34:46). Na rehma za Allah ziwe juu yako. Wako katika Uislam Al Itrah Foundation Barua Pepe: alitrah@yahoo.com SMS: +255 778 300 140 1

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 1

1/17/2017 1:10:12 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬

NENO LA MCHAPISHAJI

V

iashiria vya Uchamungu ni mkusanyiko wa mfululizo wa makala zilizochapishwa katika jarida liitwalo Message of Thaqalayn - Islamic Studies, nam. 57 hadi 61. Haya ni masomo yanayoelezea takwa (taqwa - uchamungu). Hii ni hali ya kiwango cha juu cha mwenye kumuabudu Mungu, na ndio lengo la kila muumini. Waumini hufanya ibada kwa nguvu zao zote na kwa unyofu na unyenyekevu ili kufikia daraja hii ya juu ya uchamungu (taqwa). Hata hivyo, ili kufikia daraja hii, mtu anatakiwa kurejea kwenye Qur’ani Tukufu, Sunna na Ahlul Bayt (a.s.). Hivyo, mwandishi wa makala hizi (ambazo zimekusanywa kama kitabu) humuelekeza msomaji kwenye viashiria hivyo ili iwe ni dira yake ya kufikia malengo yake ya uchamungu. Sisi kama wachapishaji tunakiwasilisha kitabu hiki kama kilivyo kwa wasomaji wetu na kuwashauri wasome yaliyomo humo, wayafanyie kazi na kuyazingatia ili wapate kufuzu katika safari hii ya kiroho ya kuelekea Akhera. 2

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 2

1/17/2017 1:10:12 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

Hii ni moja kati ya kazi kubwa zilizofanywa na Taasisi ya al-Itrah katika kuwahudumia kielimu wasomaji wake wazungumzao Kiswahili. Na kwa maana hiyohiyo, imeamua kukichapisha kitabu hiki chenye manufaa makubwa kwa lugha ya Kiswahili kwa lengo lake lilelile la kuwahudumia Waislamu wanaozungumza Kiswahili, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni vitu ambavyo havina nafasi tena katika akili za watu. Tunamshukuru mwandishi wa kitabu hiki kwa kazi kubwa aliyofanya kwa ajili ya Umma huu wa Waislamu, Allah Azza wa Jalla amlipe kila kheri na amuingize Peponi kwa salama na amani insha’Allah. Halikadhalika tunamshukuru ndugu yetu Salman Shou kwa kukitarjumi kwa lugha ya Kiswahili kitabu hiki, insha’Allah na Yeye Allah Azza wa Jalla amlipe kila kheri hapa duniani na huko Akhera pia. Aidha hatuwasahau wale wote waliochangia kwa namna mmoja au nyingine mpaka kufanikisha kuchapishwa kwa kitabu hiki. Allah Mwenye kujazi awalipe wote malipo mema hapa duniani na huko Akhera pia. Mchapishaji Al-Itrah Foundation.

3

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 3

1/17/2017 1:10:12 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬

SEHEMU YA KWANZA1

M

uhtasari: Viashiria vya uchamungu ni nini? Na tunawezaje kuhakikisha kwamba tunaelekea upande sahihi katika safari yetu ya kiroho? Mfululizo huu wa makala unafafanua sifa njema na matokeo ya ucha-Mungu kama inavyoonekana katika Qur’ani Tukufu na hadithi, na maisha ya Ahlul-Bayt, na unatambulisha viashiria ambavyo kwavyo mtu anaweza kupima uchamungu wake mwenyewe au, kama ikihitajika, na uchamungu wa wengine. Uchamungu, au Takwa, ni mojawapo ya sifa ya juu sana ambayo mtu anaweza kuipata; wachamungu huamini katika wahyi uliofichika na pia ule uliyoteremshwa kwa Mtume Muhammad 3 na Mitume wa kabla yake, kusimamisha Swala, na kutoa Zaka. Wale walionao uchamungu wanapaswa kushukuru, na wale wasiokuwa nao lazima wajitahidi kuupata kwani unamridhisha Mungu, unale1

Makala haya ni sehemu ya kwanza ya mfululizo wa masomo saba yaliyotolewa na mwandishi huko London, kwenye Kituo cha Kislamu cha Uingereza mnamo Julai mwaka 2011. Kozi hii ilikuwa ni jaribio la kutafiti kiini cha imani, uchamungu na maadili mema ambamo yameegemezwa. 4

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 4

1/17/2017 1:10:12 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

ta msaada Wake, na matokeo yake ni kukubalika kwa amali za mhusika. Sifa moja tunayotakiwa kuwa nayo ni kuweza kujitathimini sisi wenyewe na kuwatathmini wengine kwa kuzingatia tusiwe wenye kuhukumu. Katika maisha yetu ya kijamii, mara nyingi tunahitaji kuwatathmini au kuwachuja watu, mathalani: tunapotaka kuchagua rafiki, mchumba, mwalimu, au tunataka kumwajiri mtu fulani au kufanyakazi kwa mtu fulani. Watu ni watata na wagumu sana wenye mambo changamani. Unaweza kuwa unamfahamu mtu kwa miaka mingi lakini bado unakuwa huna uhakika kuhusu mtu huyo, au unaweza kuwa na maoni potofu kuhusu mtu fulani, kama vile kuamua kwa kutumia akili yako kwamba mtu huyo si mzuri, na halafu ghafla baada ya miaka mingi unashuhudia tabia zake nzuri. Hili linaweza pia kujitokeza kwa mtu mwenyewe binafsi. Sisi tuna uelekeo wa kuendeleza mawazo mazuri au mabaya kuhusu sisi wenyewe ingawaje katika mifano yote miwili inawezekana kuwa tunakosea. Ni vigumu sana kuweza kuwa na uelewa ulio kamili na sahihi wa watu wengine, ikiwa ni pamoja na watu wa familia yako na marafiki. Inahitaji jitihada kubwa na kwa hakika panahitajika aina

5

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 5

1/17/2017 1:10:12 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

fulani ya utambuzi. Kule tu kumsikiliza mtu au kuwa na uhusiano wa kindugu naye hakutoshi kupata kumwelewa kwa ukamilifu kwa sababu ya viwango vingi mbali mbali vya haiba. Zaidi ya hayo, wakati mwingine watu huweza kuficha baadhi ya mielekeo ya haiba zao, na hapo ndipo umaizi na uvumilivu unapohitajika kuweza kufahamu tabia zao za kweli. Wakati mwingine unahitaji kungojea hali fulani ijitokeze ili yale yaliyojificha yaweze kutokeza. Pale mtu anapotahiniwa tunaweza kuona tabia zake za kweli kwani binadamu wapo kama dimbwi la maji. Baadhi ya madimbwi huonekana safi kuanzia juu hadi chini na mengine ni masafi hapo juu tu: kama maji ya dimbwi hilo yakikorogwa, uchafu utajitokeza, na ni hapo tu ndipo utakapogundua kilichokuwa kimefichikana huko chini. Tabia za kweli za mtu hutokeza pale anapopatwa na changamoto nzito kama vile tukio la msiba, kazi ngumu, mapigano, au kutokukubaliana. Kama Imam Ali alivyosema:

ْ ‫ال ِّرجال َج َوا ِه ِر ِع ْل ُم ا‬ ‫ب‬ ِ ُّ‫ال فِي تَقَل‬ ِ ‫ال ُح َو‬ “Nafsi ya kweli ya mtu, hujulikana wakati wa ­mabadiliko ya mazingira.”2 2  Nahj al-Balaghah, Semi ya hekima ya 217

6

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 6

1/17/2017 1:10:12 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

Njia moja ya kuwajua watu ni kusafiri nao, kwani matukio yasiyotarajiwa hutokea katika safari, ambayo si kila mtu amejiandaa kwayo, na kwa hiyo hutenda kiasili zaidi badala ya hali bandia. Mathalani, wakati wa Hija, mara nyingi hutokeza hali ambapo mambo yanatoka nje ya udhibiti, hata kama mkiwa na viongozi wazuri sana wa Hija. Tukio lote zima ni fursa nzuri kuona vizuri zaidi tabia halisi za watu, kama vile: uvumilivu wao, uadilifu wao, ubinafsi wao, au ulafi na uchoyo wao. Katika hadithi moja fupi, palikuwepo na mtu ambaye siku zote alikuwa akiswali kwenye safu ya kwanza ya Swala ya jamaa ndani ya msikiti. Siku moja, alichelewa kuingia msikitini, na tayari Swala ilikwishaanza. Aliona soni, akifikiria jinsi gani watu wangemfikiria. Halafu ghafla alizinduka, na akajisemea mwenyewe, “Mungu Wangu! Huenda miaka yote hii nilikuwa nawahi ili kuwa katika safu ya kwanza kwa kujionesha tu.� Kwa hiyo wakati mwingine baada ya miaka mingi tunaweza kutambua kwamba palikuwepo nia mbaya ambayo ilikuwa ngumu kuitambua ambayo tulifikiri ilikuwa ni safi. Kuhusu nia, vyanzo vya madhehebu yote mawili: Sunni na Shia vinamnukuu Mtume Muhammad 3 akisema:

7

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 7

1/17/2017 1:10:12 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

“Unyemeleaji wa shirki (ni kumhusisha mtu au kitu na Mungu ambacho hapa kinarejelea kutokuwa na nia safi; al-shirk al-khafiyy) kwenye ummah wangu haujitokezi zaidi kuliko unyemeleaji wa mchwa mweusi juu ya jabali jeusi katika giza nene la usiku wa manane.”3 Kwa upande mwingine, inawezekana wakati mwingine ukatilia shaka nia yako ingawaje baada ya miaka mingi unakuja kutambua kwamba nia yako ilikuwa nzuri. Mathalani, katika hadithi moja fupi, palikuwepo na mtu mmoja ambaye alikuwa akiipatia familia fulani msaada wa kifedha. Siku moja, alikwenda kuitembelea familia hiyo na kwa sababu mahsusi familia hiyo ilimkasirikia mtu huyo, walimpigia makelele wakimwambia kwamba hakuwa amefanya jambo lolote jema kwao. Aliondoka nyumbani hapo akiwa mnyonge na aliyevunjiwa heshima mbele ya watu wengine. Hata hivyo, rafiki yake alimuona akiwa na furaha alipokuwa anarudi kutoka nyumbani kwa familia hiyo, na akamuuliza kwa nini amefurahi? Alimuelezea rafiki yake kile kilichotokea, na baada ya fedheha hiyo, alisema, “Mimi sikuhisi majuto yoyote na hii ina maana kwamba sikuwa ninawasaidia ili nipate kusifiwa. Yote hayo nilifanya kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.” 3

Muntakhab al-Anwar al-Mudi`ah, uk. wa 16 8

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 8

1/17/2017 1:10:12 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

Kwa vyovyote iwavyo, ni juu ya Mwenyezi Mungu kuwahukumu watu, lakini katika maisha yetu ya kijamii tunahitaji kuweza kuwatathimini watu na wakati huo huo tuwe tunajipima sisi wenyewe. Tunawezaje kuamua kama mtu fulani ni mwadilifu? Ni vipi viashiria vya uchamungu? Tunawezaje kuhakikisha kwamba tupo kwenye njia iliyo sahihi katika safari yetu ya kiroho? Siku zote waumini wanahangaika kuhusu wao wenyewe; wale wanaohisi wametosheka na msimamo wao wanahitaji kuwa na wasiwasi hata na zaidi. Kwa mujibu wa Imam Baqir B, siku moja wakati wa usiku, Mtukufu Mtume 3 aliulizwa na Mama wa Waumini Aisha mke wake, kwamba kwa nini alikuwa anajishinikiza sana kuhusu yeye mwenyewe ambapo Mwenyezi Mungu amemsamehe dhambi zake zote.4 Mtukufu Mtume 3 akajibu, “Ewe Aisha! Hivi nisiwe mimi ni mwenye kushukuru?” Mtukufu Mtume 3 aliamini kwamba kwa vyovyote vile atakavyomuabudu na kumtumikia Mwenyezi Mungu na alivyojaribu kuwaongoza watu, lakini bado alifanya zaidi kuonesha shukurani zake kwa neema na rehma za Mungu juu yake. Imam Baqir B alisema kwamba Mtukufu Mtume   Hii inarejelea kwenye Surah ya 48:2. Kwa hakika, hapa ‘dhambi’ haimaanishi ya kisheria au dhambi ya ki-fiqhi. Kwa mjadala zaidi, tafadhali rejea kwenye Tafsir ya Qur`ani Tukufu, kama vile Al-Mizan fi Tafsir al-Qur`ani, Juz. 18, uk. 255 & 256

4

9

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 9

1/17/2017 1:10:12 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

3 alikuwa akisimama kwa vidole vyake vya miguu (akiswali na kusoma Qur`ani) na ndipo Mwenyezi Mungu akateremsha: “Twaha. Hatukukuteremshia Qur`ani ili upate mashaka.” (20:1-2)5 Ni pale tu unapojihisi kwamba una haja kubwa ya fadhila na maghufira ya Mwenyezi Mungu ndipo unaweza kuboreka. Katika Du’a Abu Hamza, Imam Sajjad B anamwambia Allah:

‫إذا رأيت موالي ذنوبي فزعت وإذا رأيت عفوك‬ ‫طمعت‬ “Mola Wangu! Ninapoziangalia dhambi zangu ninapatwa na hofu lakini ninapouangalia usamehevu Wako ninakuwa mwenye matumaini.”6

Hivyo mtu kuchunguza tabia yake mbaya na mapungufu aliyonayo kunaweza kusababisha kukata tamaa; hata hivyo, kufikiria juu ya rehema na ukarimu wa Mungu huzalisha matumaini. Mahali pengine kwenye dua hiyohiyo, Imam Sajjad B anasema:

َ ‫إن لنا بك رجاء عظيما‬ ّ ‫يا رب‬ 5 6

Al-kafi, Juz. 2, uk. 95.   Bihar al-Anwar, Juz. 95, uk. 83. 10

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 10

1/17/2017 1:10:12 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

“Ewe Allah! Sisi tunayo matumaini makubwa Kwako.”7

Kama kuna jambo hapa duniani ambalo ni la uhakika, ni kwamba tunaye Mola Mpole sana, Mrehemevu, na Mwenye huruma, na jambo hili linapaswa kutupatia sisi matumaini makubwa. Hatupaswi kujidanganya sisi wenyewe kwa kuendeleza fikira iliyokuzwa kuhusu sisi wenyewe. Imam Sadiq B anasema: “Pale ujuba wa majisifu unapomwingia mtu, huwa ameangamia.”8 Sisi, inatubidi kujipima wenyewe kwa uangalifu. Kama kweli tunaona viashiria vya uchamungu au angalau baadhi ya hivyo ndani mwetu tunapaswa kumshukuru Mungu na tujitahidi kuvilinda viashiria hivyo; kama hatuvioni viashiria hivyo, sisi wenyewe tunatakiwa kujaribu kujirekebisha, na tuvipate viashiria hivyo kabla hatujachelewa sana. Takwa: Wakati mwingine Takwa hutafsiriwa kama vile kuwa mwangalifu juu ya Mwenyezi Mungu au kumuogopa-Mungu ambalo ni jambo zuri, lakini hapa tutaitafsiri Takwa kama uchamungu. Inaweza kuhojiwa kwamba kufuatana na Qur`ani Tukufu uchamungu ni sifa ya juu sana au angalau ni mojawapo ya sifa za juu sana ambazo mtu anaweza kuzifikia. Wakati huo huo, inawezekana kuhojiwa kwamba hakuna sifa chini   Bihar al-Anwar, Juz. 95, uk. 85.   Al-Kafi, Juz. 2, uk. 313

7 8

11

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 11

1/17/2017 1:10:13 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

ya Takwa inayotosha. Kama imani ya mtu haifikii kiwango cha Takwa basi inahitajika jitihada. Takwa ni ukweli wa mwisho; ndio tu sifa inayomlinda mtu dhidi ya maumivu na mateso yaliyomo Akhera. Umuhimu wa takwa na sifa njema za wacha Mungu (muttaqin) zimezungumziwa kwenye aya nyingi, mathalani:

“Alif Lam Mim. Hiki ni Kitabu kisicho na shaka ndani yake; ni mwongozo kwa wenye takua. Ambao wanaamini ghaibu na wanasimamisha Swala, na wanatoa katika yale tuliyowapa. Na ambao wanaamini yaliyoteremshwa kwako, na yaliyoteremshwa kabla yako na akhera wana yakini nayo. Hao wako juu ya uongozi utokao kwa Mola Wao, na hao ndio wenye kufaulu.� (2:1-5)

Wale ambao hunufaika na yale yaliyomo kwenye Qur`ani Tukufu ni wacha Mungu. Ingawa Qur`ani Tukufu inatoa mwongozo wake kwa binadamu wote, wapo watu ambao huipuuza au kuipinga, na wapo watu ambao huikubali kinadharia bila ya kutekeleza

12

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 12

1/17/2017 1:10:13 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

mwongozo wake kwa vitendo. Kuiamini Qur`ani Tukufu na kuitendea kazi si jambo la kuisoma tu, kuihifadhi au kuigawa kama Mtume Muhammad 3 alivyosema, “Wapo wasomaji wengi wa Qur`ani Tukufu ambao wanalaaniwa na Qur`ani Tukufu.”9 Ni wacha Mungu gani ambao wanaweza kunufaika kwa kweli na Qur`ani Tukufu? Aya hizo hapo juu zimeorodhesha baadhi ya sifa zao. Wacha Mungu ni wale wanaoamini katika (a) yale yaliyoteremshwa kwa Mtume Muhammad 3 na Mitume wa Mungu wa kabla yake, (b) yale yaliyofichika, ambayo ni, Mungu, malaika, na Akhera, na (c) wanaosimamisha Swala na kutoa Zaka. Hivyo, Takwa ni ubora unaopatikana pale unapokuwa na sifa na matendo fulani. Pia inakuwa dhahiri kwamba Takwa ipo juu zaidi ya imani, Swala na Sadaka (zakat). Haya mambo matatu huishia kwenye kuwa na Takwa. Kwa mujibu wa Qur`ani Tukufu, Takwa ndicho tu kitu ambacho kinaweza kutuokoa sisi huko Akhera:

Bihar al-Anwar, Juz. 89, uk. 184.

9

13

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 13

1/17/2017 1:10:13 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

“Na wasomee habari za watoto wawili wa Adam kwa ukweli, walipotoa Sadaka, ikakubaliwa ya mmojawao, na ya mwingine haikukubaliwa. Akasema: Nitakuua! Akasema: Mwenyezi Mungu huwapokelea wenye takua tu.” (5:27)

Hivyo, Mungu hukubali matendo yatokanayo na wacha Mungu tu, na kama matendo hayakubaliki, huwa yanaishia kwenye kutokuwa na masurufu ya safari yake ya milele:

“……..Na kheri yoyote mnayoifanya Mwenyezi Mungu anaijua. Na chukueni masurufu, na hakika masurufu bora ni takua; na nicheni Mimi, enyi wenye akili.” (2:197)

Qur`ani Tukufu pia inaonesha kwamba Mungu huwapenda wacha Mungu, na kwa hakika mapenzi ya Mungu kwao ni mtaji mkubwa sana wanaoweza kuwa nao:

14

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 14

1/17/2017 1:10:13 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

“….basi Mwenyezi Mungu huwapenda wenye takua.” (3:76, 9:4, 9;7)

Nani asiyependa kupendwa na Mwenyezi Mungu? Baadhi ya watu hujisumbua wenyewe ili kupata mapenzi ya watu. Vipi kuhusu shauku ya mapenzi ya Mungu? Jambo la kuvutia ni kwamba mapenzi ya Mungu kwa wacha Mungu husababisha wao kupendwa na watu:

“Hakika wale ambao wameamini na wakatenda mema, Mwingi wa rehema atawajaalia mapenzi (ya viumbe Vyake).” (19:96)

Mungu hukubali matendo ya wacha Mungu tu: matendo hayakubaliwi bila ya Takwa. Inategemea juu ya nia, kwani Mungu anajua kile kilichomo moyoni mwa mtu na mtu huyo amefanya juhudi ya kiasi gani. Mtu anaweza kutoa pauni moja katika sadaka na ikakubaliwa, ambapo sadaka ya mtu mwingine ya pauni milioni moja inaweza kukataliwa kwa sababu ya nia mbaya. Katika kipindi cha uhai wa Imam Sadiq, B alikuwepo mtu ambaye alikuwa anaheshimika kwa 15

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 15

1/17/2017 1:10:13 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

mambo yake ya kiroho na uchamungu wake. Siku moja, Imam B alimshuhudia mtu huyu anaiba matunda mawili kutoka dukani na mikate miwili kutoka kwenye tanuri la kuoka mikate, na halafu akampa vitu hivyo mtu mgonjwa ambaye alimtembelea. Baada ya muda kidogo, Imam B alipomuuliza kwa nini alifanya hivyo, mtu huyu wa kuheshimika, akifikiria kuwa alikuwa mwerevu, akajibu “Kwani hujasoma ndani ya Qur`ani Tukufu kwamba kama ukifanya tendo moja jema Mungu anakulipa thawabu mara kumi, na kama ukitenda tendo moja baya Mungu atakuadhibu kwa kosa moja? Kwa hiyo ninayo matendo mema 36 bila ya kutumia hata peni moja ya fedha.” Imam B akajibu: “Kwani hujasoma ndani ya Qur`ani Tukufu kwamba Mungu hukubali yale tu yatokayo kwa wacha Mungu? Unawezaje kuiba fedha na kutumia fedha hiyo kutoa sadaka? Lazima uwe na fedha iliyo safi na nia safi, na ndipo unaweza kutoa fedha hiyo kwa ajili ya Mungu.”10 Qur`an Tukufu pia inatuambia kwamba Mungu yu pamoja na wacha Mungu: “……Mwenyezi Mungu yuko pamoja na wanaomcha.” (2:194; 9:36; 9:123)   Bihar al-Anwar, Juz. 47, uk. 238

10

16

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 16

1/17/2017 1:10:13 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

Kuwa na wacha Mungu maana yake ni kwamba Mungu huwapa msaada: “…..Na Mwenyezi Mungu ni Walii wa wenye Takwa.” (45;19) Ikielezea nafasi ya wacha Mungu katika Akhera, Qur`ani Tukufu inasema:

“Na wataambiwa wale waliofanya takua: Mola Wenu ameteremsha nini? Watasema: Kheri. Waliofanya wema katika dunia hii watapata wema. Na nyumba ya akhera ni bora zaidi. Na ni bora mno nyumba ya wenye takua. Bustani za milele wataziingia, hupita chini yake mito. Humo watapata watakacho. Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu awalipavyo wenye takua. Wale ambao malaika huwafisha katika hali njema. Wanawaambia, Salamun alaykum (amani iwe juu yenu) kwa yale mliyokuwa mkiyatenda.” (16:30-32).11

Pia Qur`ani Tukufu inatuambia kuhusu kufuzu kwa wacha Mungu;

Pia tazama aya hizi: 19;85; 44:51; 51:15 52:17; 54:54; 77:41

11

17

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 17

1/17/2017 1:10:13 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

“Musa akawaambia watu wake: Ombeni msaada kwa Mwenyezi Mungu na subirini. Ardhi ni ya Mwenyezi Mungu atamrithisha amtakaye katika waja Wake na mwisho ni wa wenye takua.” (7:128)12

Kumridhisha Mungu, ili matendo ya mtu yakubaliwe, ili mtu apate msaada Wake, na ulezi Wake, na kuweza kupata mwisho mwema, tunahitaji Takwa. Bila ya Takwa, neema yoyote kama vile elimu, hadhi, fedha, cheo au nafasi, familia na watoto ni mambo ambayo yataongezea kwenye uwajibikaji wetu, na moja au zaidi ya mambo haya yanaweza kutupiga vita sisi. Mathalani, Imam Sadiq B amenukuliwa akisema: “Dhambi sabini za mtu ambaye hana elimu zitasamehewa kabla ya dhambi moja ya mwanazuoni (Aalim) haijasamehewa.”13

Pia tazama aya 11:49; 28:83.

12 13

Al-Kafi, Juz. 1, uk. 47.

18

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 18

1/17/2017 1:10:13 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

SEHEMU YA PILI14

M

UHTASARI: Ni vipi viashiria vya uchamungu? Na tunawezaje kuwa na uhakika kwamba tunaelekea upande sahihi katika safari yetu ya kiroho? Mfululizo wa makala hizi unafafanua sifa njema na matokeo ya uchamungu kama ionekanavyo katika Qur`ani Tukufu, hadithi na maisha ya Ahlul-Bayt, na kutambulisha viashiria ambavyo mtu anaweza kuvitumia katika kujipima uchamungu wake au kama inahitajika, na uchamungu wa wengine. Kwa kweli uchamungu ni mojawapo ya dhana muhimu sana katika Qur`ani Tukufu ambayo ndiyo huwaweka watu katika madaraja mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwani sifa hii huenda mbali zaidi ya vitendo vya kimwili, na huhusishwa kwenye nia zilizo nyuma ya vitendo vyote. Katika sehemu iliyopita, sifa za uchamungu (Takua) zilichunguzwa kufuatana na isemavyo Qur`ani Tukufu. Katika sehemu hii, ufafanuzi wa uchamungu utachunguzwa sambamba na mambo ambayo huchangia katika ujenzi wake.   Makala hii ni ya sehemu ya kwanza ya mfululizo wa masomo saba yaliyotolewa na mwandishi huko London, Uingereza kwenye Kituo cha Kiislamu mnamo mwezi wa Julai, 2011. Mfululzo wa masomo haya ulikuwa ni jaribio la kuchunguza dhati ya imani na uchamungu na mienendo ya kimaadili ambamo humo ndimo ulimo msingi wa imani na uchamungu.

14

19

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 19

1/17/2017 1:10:13 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

Uchamungu katika hadithi: Kwa mujibu wa mafundisho ya Mtukufu Mtume 3 na Ahlul Bayt Fambayo huakisi mafundisho ya Qur`ani Tukufu, uchamungu unahitajika kwa furaha ya hapa duniani na Akhera. Hapa tunarejelea baadhi ya hadithi kuhusu umuhimu wa uchamungu. Imam Ali B alisema: “Uchamungu ni nahodha wa sifa bainishi wa tabia zote.” 15 “Takwa ndio hazina bora sana, ni hifadhi bora sana yenye kinga, ni hadhi ya utu iliyo bora sana yenye kutukuka.” 16 Tunatakiwa kutafuta Takwa ambayo huleta utajiri, ulinzi na heshima lakini baadhi ya watu hutafuta hazina za kidunia tu. Imam Ali B vilevile alisema: “Kwa hakika uchamungu ni jambo la msingi kabisa na linaloridhisha sana ambalo Mwenyezi Mungu analitaka kutoka kwa waja Wake.” 17   Nahjul Balaghah, Hikma ya 410, uk. 520   Sheikh Tusi, Al-Amali, sehemu ya 38, uk. 685. Hadithi namba 1456 (9) 17   Ghurar ul-Hikam wa Durar ul-Kalim, Mlango wa Fadhilatuhuma wattaghribi fihima, uk. 269. 15 16

20

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 20

1/17/2017 1:10:13 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

Mwenyezi Mungu hatutarajii sisi kuwa kama Malaika au kuwa miongoni mwa wale ambao wapo karibu Naye (Muqarrabun). Yeye anachotarajia kutoka kwetu ni kile chenye uwezekano kulingana na uwezo na hali zetu na anaweza kutuweka katika nafasi iliyo sahili karibu Naye. Mwenyezi Mungu anatutarajia sisi kuwa wacha Mungu, sifa kuu kabisa ambayo kwayo tunaweza kupanda kwenye viwango vya juu zaidi vya ukamilifu na kuwa miongoni mwa wale walio karibu Naye (Muqarrabun). Pia Imam Ali B amesema: “Enyi waja wa Mwenyezi Mungu ninakuusieni kuwa na Takwa.” 18 Uachie moyo wako uwe na uchamungu. Hiki ni kitu ambacho haiwezekani kutamkwa kwa maneno tu au hata kuonesha kwa vitendo vyako. Uchamungu sio tu kuswali, kutoa zaka au kitendo kingine chochote cha kiibada pamoja na kwamba vyote hivyo ni muhimu. Hata hivyo, kwa kumuona tu mtu anaswali hatuwezi kuzungumzia kuhusu ucha Mungu wa mtu huyo. Uchamungu unakwenda mbali zaidi ya vitendo vya   Nahjul-Balaghah, Hotuba ya 233. Maneno haya yanaweza kuonekana kwenye hotuba nyingi na hata siku hizi wahadhiri mara nyingi huanza hotuba zao kwa maneno hayo.

18

21

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 21

1/17/2017 1:10:13 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

kimwili. Uchamungu unapaswa kuhusika zaidi na moyo, na pamoja na nia iliyo nyuma ya vitendo. Hili linafanya iwe vigumu kutathmini uchamungu. Sisi wenyewe hata hatujui kwa usahihi yale yaliyomo ndani ya mioyo yetu seuze yale yaliyomo ndani ya mioyo ya wengine. Hii ndiyo sababu sisi hatuwezi na wala hatupaswi kutathimini kiwango cha uchamungu cha watu wengine. Baada ya maneno hayo hapo juu, Imam Ali B amezungumzia uchamungu na halafu amesema: “Uachilie uchamungu uingie moyoni mwako.” 19 Kitenzi cha Kiarabu ambacho kimetumika hapa ni ‘ash`iruha’ kutokana na chimbuko lilelile kama ‘sha`r’ (nywele). Katika hali halisi maana yake ni kukiacha kitu kugusa ngozi yako kama vile unywele unavyogusa ngozi yako hivyo kwamba pasiwepo umbali wowote. Sasa basi fungu hili la maneno linakuwa na maana zaidi kwamba mtu anapaswa kuruhusu uchamungu ufike moyoni mwake. Uchamungu sio kivazi; bali zaidi hiki ni kitu ambacho lazima kiguse moyo wako. Ni kwa sababu ya huu uhusiano wa karibu baina ya uchamungu na moyo kwamba unaweza kuwa na athari za kuponya juu ya moyo. Imam Ali B alisema:   Nahjul-Balaghah, Hotuba ya 233.

19

22

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 22

1/17/2017 1:10:13 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

“Kwa hakika uchamungu ni dawa ya maradhi ya moyo wako, uwezo wa kuona wa moyo wako ambao umepofuka, ponyo la mwili wako wenye maradhi, uimara wa vifua vyenu vilivyodhurika na utakaso wa uchafu wa nafsi zenu.” 20 Uchamungu unaweza kuponya hata maradhi ya kimwili. Yapo maradhi mengi siku hizi ambayo chanzo chake hakijulikani, kama vile wasiwasi wa aina mbalimbali au vurugu za mihangaiko na hofu. Mtu ambaye amejizatiti kwa uchamungu na ameweka imani yake kwa Mwenyezi Mungu hataathiriwa sana na mabadiliko ya majaaliwa ya dunia hii, na mabadiliko ya thamani ya fedha. Kwa hiyo watu hao wanapatwa na madhara kidogo zaidi ya mivurugiko ya wasiwasi. Sifa mojawapo ya watoto iliyobora ambayo imetajwa hata kwenye hadithi ni kwamba wao wanaweza kujitenga kwa urahisi. Mathalani, wanaweza kutumia muda wa saa nyingi kujenga kasri kwa kutumia mchanga halafu wanaivunja kasri hiyo kwa dakika chache tu. Muumini mcha Mungu ni budi aione dunia kwa mtulizano wa akili huo huo, kwamba ni mchezo tu, mchezo ambao sio kitu cha kutiliwa wasiwasi.   Nahjul-Balaghah, Hotuba ya 189

20

23

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 23

1/17/2017 1:10:13 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

Uchamungu katika Qur`ani Tukufu: Inaweza kusemwa kwamba uchamungu ni mojawapo ya dhana muhimu sana katika Qur`ani Tukufu na kigezo ambacho watu wanapangwa katika madaraja mbele ya Mwenyezi Mungu. Katika Qur`ani Tukufu Surah ya Hujurat, aya ya 13 tunasoma:

“Enyi watu! Hakika sisi tumewaumba kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumewafanya mataifa na makabila ili mjuane. Hakika mtukufu zaidi miongoni mwenu mbele ya Mwenyezi Mungu ni aliye na Takua zaidi yenu.� (Surah ya Hujurat, 49:13)

Katika aya hii, Mwenyezi Mungu anaelezea jinsi zilivyo tofauti zetu ili tuweze kujuana sisi kwa sisi na kuvutiwa na maisha ya wengine. Katika nukta hii, Mwenyezi Mungu anatambulisha uchamungu kama ndicho tu kitu chenye thamani ambacho kinaweza kumpandisha mtu daraja, ndicho tu kitu kinachoathiri nafasi yetu mbele ya Mwenyezi Mungu. Katika Surah ya Baqarah, aya ya 2 tunasoma:

24

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 24

1/17/2017 1:10:13 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

“Hiki ni kitabu kisicho na shaka ndani yake; ni mwongozo kwa wenye Takua.� (Surah Baqarah, 2:2)

Bila shaka, baadhi ya watu wangetaka kupata uchamungu kwa kufuata Qur`ani Tukufu, lakini Qur`ani Tukufu bado inasema itawapa mwongozo watu ambao tayari wana ucha Mungu. Jambo hili linaweza kufanyika kwa namna gani? Kama mtu tayari ni mcha Mungu basi hakuna haja mtu huyo kuongozwa na Qur`ani Tukufu na kama mtu sio mcha Mungu basi Qur`ani Tukufu inasema haitampa mwongozo. Jibu ni kwamba uchamungu una viwango vinavyotofautiana na ni kiwango kidogo tu cha uchamungu kinachotosha kwa mtu kuweza kunufaika kutokana na mwongozo wa Qur`ani Tukufu na kuongezea kwenye uchamungu wake. Tunaweza kuelewa jambo hili vizuri zaidi kwa kutazama Waislamu wa mwanzoni wa Makkah ambao waliukubali ujumbe wa Mtukufu Mtume 3. Pale Mtukufu Mtume 3 alipoanza kazi yake baadhi ya watu walimuamini yeye na Qur`ani Tukufu ambapo wengine hawakumwamini. Ni sifa gani iliyokuwemo ndani ya

25

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 25

1/17/2017 1:10:13 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

baadhi ya watu ambayo iliwafanya waamini ujumbe wa Mtukufu Mtume 3? Watu kama Abu Dharr, Salman, na Ammar lazima walikuwa na chembe za sifa nzuri hata kabla ya kuukubali Uislamu, yaani kiwango fulani cha uchamungu. Hawa hawakuwa na kiburi na walikuwa tayari wazi kuipokea kweli. Uchamungu sio kuswali tu, kufunga, au kwenda Hijja pamoja na kwamba vitendo hivi ni muhimu sana. Hata hivyo, kuvutiwa katika ukweli pia ni kiwango cha uchamungu. Tutalielezea suala hili zaidi wakati ujao. Tirmidhi anasimulizi kutoka kwa Mtukufu Mtume 3 kwamba mawingu hayajaweka kivuli kwa yeyote ambaye ni mwaminifu kumzidi Abu Dharr. Mtukufu Mtume 3 alipotaka kuhama kutoka Makkah kwenda Madina, Abu Dharr alichukua jukumu la kumsindikiza. Kwa kuwa Mtukufu Mtume 3 hakutakiwa aonekane, basi Abu Dharr alimfunika asionekane. Hata hivyo mpagani mmoja alimuona Abu Dharr na akamuuliza kile alichokifunika ni kitu gani. Abu Dharr alisema alikuwa anambeba Mtukufu Mtume 3. Mpagani huyo ambaye hata hakuweza kufikiria kwamba mtu angeweza kuwa mwaminifu kiasi hicho alidhani kwamba huo ulikuwa ni mzaha tu na wala hakuchunguza zaidi. Ilikuwa ni kiwango hiki cha imani na kujisalimisha kwenye ukweli ambacho 26

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 26

1/17/2017 1:10:13 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

ndicho kilimsaidia kukubali Uislam mwanzoni kabisa. Mfano mwingine ni ule wa Hurr ambaye aliweza kutubu na kujiunga na jeshi la ukweli la Imam Husein B. Huyu hakuwa kama wengine katika jeshi la Umari bin Sa`d na ilikuwa kwa bahati tu kwamba alikubali Uislamu. Hurr alikuwa mtu mpole na mwaminifu ambaye alikubali sifa stahilifu za Imam Husein B. Alikuwepo hapo kumzuia Imam asiendelee na safari yake lakini wakati wa Swala alisimama na jeshi lake nyuma ya Imam na akaswali naye. Ndivyo ilivyo ukweli kuhusu watu wanaokubali Uislamu leo hii. Hawabadili imani kwa kubahatisha. Watu hao ni wanyenyekevu na waaminifu wanaoutafuta ukweli. Hawa ni watu ambao wana chembe ya nuru katika nyoyo zao na huamini papo hapo au baadaye, kwani hiyo nuru ya uchamungu huwa inawaongoza. Aya zifuatazo za Surah al-Baqarah, aya ya 3 hadi ya 5, zinaelezea wacha Mungu:

27

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 27

1/17/2017 1:10:13 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

“Ambao wanaamini ghaibu na wanaosimamisha Swala, na wanaotoa katika yale tuliyowapa. Na ambao wanaamini yaliyoteremshwa kwako, na yaliyoteremshwa kabla yako na Akhera wana yakini nayo. Hao wako juu ya uongozi utokao kwa Mola Wao, na hao ndiyo wenye kufaulu.” (al-Baqarah; 2:3-5).

Wacha Mungu huamini juu ya ghaibu. Lakini haya yanayoitwa ghaibu (ghayb) ni nini? Ni Mungu na malaika. Na sababu ya kwamba hawaonekani sio kwamba wamejificha; bali ni kwamba ni sisi ndiyo ambao hatuwezi kuwaona kwa sababu ya mapazia yaliyo mbele ya uwezo wetu wa kuona. Kama taa zikizimwa hatuwezi kukiona kila kitu ambacho tulikuwa tunakiona sekunde chache zilizopita. Pamoja na kwamba vitu hivyo bado vipo hapo lakini hatutaweza kuviona tena. Kwa msaada wa mwanga mdogo tu, tunaweza kuviona vitu hivyo tena. Ni ukweli kama huo kuhusu Mungu; kwetu sisi Yeye haonekani, lakini ni kipi ambacho kipo dhahiri kuliko Mwenyezi Mungu? Katika maombi yake kwenye Dua ya Arafa, Imam Husein B anasema: “Ni lini ulikuwa umejificha hivyo kwamba ningehitaji mtu wa kuniongoza ili niweze kukuona Wewe?”

28

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 28

1/17/2017 1:10:13 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

Kwa mtazamo wa Imam Husein B ni kwamba Mungu hakuwahi kutoonekana kamwe na wala hajatoweka kamwe. Kwetu sisi, hali haifafanani na hiyo - kwetu sisi Mungu hayuko dhahiri hivyo pamoja na kwamba tunamwamini, na hii ndiyo sifa mojawapo ya watu wacha Mungu. Wao wamekomaa vya kutosha kutambua kwamba katika dunia hii ambamo macho yamewekewa mpaka wa kuona umbali maalum tu wa mwanga, sio lazima kwamba uhalisia wote uonekane. Kisha aya zingine zinataja sifa nyingine ya wacha Mungu. Kama tunakiamini kitu lazima tukifanyie kazi. Mathalani, kama tunaamini kwamba dawa fulani inahitajika kutuponya maradhi yanayotusibu, haitakuwa ni uamuzi wa busara kukataa kutumia dawa hiyo. Ndivyo ilivyo hata katika masuala ya imani zetu za kidini. Kuamini dini kama ni mfumo wa maisha na sio nadharia tu kunahitajia utendaji, vinginevyo hatutaweza kunufaika. Kitendo kimojawapo muhimu kama kilivyotajwa katika aya ni kusimamisha Swala. Hakuna muumini ambaye haswali. Hii ndio sifa ya pili ya wacha Mungu ambayo imetajwa katika aya hii, yaani kusimamisha Swala. Jambo la kuvutia ni kwamba, aya ya 2:3 haisemi kwamba wale wanaoswali; bali hasa zaidi imesema wale wanaosimamisha Swala (yuqimuun as-salaat).

29

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 29

1/17/2017 1:10:13 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

Swala inapaswa kuchukua nafasi yake inayostahili katika jamii kwani yenyewe ni nguzo ya Uislamu.21 Kila kitu katika maisha kinatakiwa kujengwa katika mazingira ya Swala. Sifa ya tatu ni kwamba wacha Mungu hutumia kile alichowapa Mungu kwa malengo ya kutoa sadaka na misaada. Hili halikuwekewa mpaka kwenye mambo mengi na linajumuisha neema zote tunazopata kutoka kwa Mwenyezi Mungu: inaweza kuwa ni fedha, elimu, au hata wakati:

“Hamtapata wema mpaka mtoe katika vile mnavyovipenda; na chochote mnachokitoa, basi hakika Mwenyezi Mungu anakijua.” (al-Imraan; 3:92)

Ni suala la kutoa kile unachokipenda. Kwa maneno mengine, kama ukitoa kitu ambacho wewe hukihitaji au hukipendi sana, pamoja na kwamba kitu hicho kinaweza kutatua matatizo ya mtu, sadaka hiyo haitoshi kukufanya wewe uwe mtu bora zaidi. Halafu aya ifuatayo inataja nukta zingine kuhusu wacha Mungu: kwamba wanaamini kile ambacho   Sheikh Tusi, Amali, kikao cha 19, uk. 529:

21

30

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 30

1/17/2017 1:10:13 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

kimeteremshwa kwa Mtukufu Mtume 3 na yale ambayo yaliteremshwa kwa Mitume wa kabla yake.22 Mwisho, wacha Mungu wana yakini na Akhera. Kanuni tatu za dini zinajumuisha kumwamini Mwenyezi Mungu, utume na Akhera. Hata hivyo, aya iliyotangulia inawataja kama wamwaminio Mwenyezi Mungu na yale ambayo yameteremshwa kwa Mtukufu Mtume 3; hivyo yenyewe inarejelea kwenye imani na itikadi. Ambapo, pale inapotaja Akhera, aya inasema wacha Mungu wana yakini na ufufuo. Yakini ni kiwango madhubuti sana cha imani. Wapo Waislamu wengi ambao hawajapata yakini kuhusu Akhera kwani yakini hii lazima ifikie mahali ambapo mtu atatenda kana kwamba anaweza kujiona kama vile anaiona Pepo na Jahannam. Mtu ambaye anaweza kuiona Jahannam kamwe hatotenda kitendo ambacho kinaweza kusababisha yeye aingie huko. Kama wakati mwingine sisi tunatenda dhambi ni kwa sababu hatujafika katika kiwango hiki cha yakini.   Katika maelezo ya pembeni, aya hii ni mojawapo ya aya ambazo huonesha kwamba Uislamu una uwezo wa mazungumzo kwani ni ndiyo tu dini miongoni mwa dini zote duniani ambayo inakubali wahyi kwa Mitume waliotangulia. Waislamu wapo katika uwanja ulio rahisi sana kwa sababu kuwa Mwislamu maana yake ni lazima tumuamini Nabii Issa, Nabii Musa na mitume wote kabla ya Ibrahim.

22

31

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 31

1/17/2017 1:10:13 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

“Hakika hapana! Kama mngekuwa mnajua kwa yakini kwa kweli mngeiona jahannam, kwa kweli mngeiona kwa jicho la yakini.” (at-Takathur; 102:5-7)

Zipo aina tatu za yakini: ‘Ilm ul-yaqin,’ (elimu ya uhakika), ‘Haqq ul-yaqin’ (yakini ya kweli au uhalisia wake wote), na ‘Ayn ul-yaqin (jicho la yakini). Kuelezea hili, tutatumia mfano: Kuna njia tatu za kutambua kwamba kuna moto mahali fulani. Hatua ya kwanza: Unaweza kuona moshi na ukaamua kwamba lazima kuna moto ambao ndio umesababisha moshi. Bado hujaona moto lakini unakuwa na uhakika kwamba moto upo mahali fulani. Hatua ya pili: Unaweza pia kuona moto kwa macho yako. Sasa, umeuona moto wenyewe hasa. Hatua ya tatu: Sehemu ya mwili wako inaugusa moto: hiki ndio kiwango cha uhakika zaidi cha elimu chenye uzito. Hivyo, kuhusu Akhera, hatua kama hizo zinaweza kupatikana; kuwa wacha Mungu, tunatakiwa kuwa na angalau kiwango cha chini kabisa cha yakini. Imam Ali 32

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 32

1/17/2017 1:10:14 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

B anaelezea wacha Mungu katika kiwango cha juu zaidi: “Kuhusu Pepo, wacha Mungu wapo kama wale ambao wamefika huko na kuiona Pepo kwa hakika na wanafurahia neema zake; na kuhusu Jahannam ni kama wale ambao wamekwishafika huko na wakaiona Jahannam kwa uhakika na wanateseka humo.� Katika hotuba hiyohiyo, Imam Ali B anasema kwamba wacha Mungu wanaposoma aya za Qur`ani Tukufu zinazozungumzia Pepo huakisi sana, hivyo kwamba huhisi kama vile aya hizi huwa zinahusiana na hali zao wenyewe. Au wanaposoma aya ambazo zinaonya kuhusu Jahannam, husoma kwa moyo wote na huhisi kama vile wanaona mwako wake. Baada ya kutaja sifa za wacha Mungu, aya ifuatayo ya Surah al-Baqarah inataja hadhi ya wacha Mungu, wao huongozwa na Mola wao na ni wenye furaha. Na haya ni mafanikio makubwa yaliyoje!

33

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 33

1/17/2017 1:10:14 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

M

SEHEMU YA TATU23

UHTASARI: Mfululizo wa makala hizi unaelezea ubora na matokeo ya uchamungu (Takwa) kama inavyoonekana ndani ya Qur`ani Tukufu, hadithi na maisha ya Ahlul Bayt F. Uchamungu ni mojawapo ya dhana muhimu sana katika Qur`ani Tukufu ambayo ndio kipimo cha kuwapa watu madaraja mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kuwa huenda mbali zaidi ya vitendo vya mwili, na inahusishwa na nia ya vitendo vyote na inahitajika katika kumfikisha mtu kwenye uongofu. Katika Sehemu ya kwanza, sifa za uchamungu zilichunguzwa kwa mujibu wa Qur`ani Tukufu. Sehemu iliyopita ilichunguza ufafanuzi wa uchamungu (Takwa) pamoja na mambo yanayochangia katika uundaji wake. Sehemu hii inaendelea kuonesha sifa za uchamungu kufuatana na isemavyo Qur`ani Tukufu, kwamba wacha Mungu ni wale wenye kuamini ghaibu, wanaosimamisha Swala, wanaotoa Zaka, wanaoamini Akhera, wanaoamini yale ambayo yameteremshwa   Makala hii ni sehemu ya tatu ya mfululizo wa masomo saba ya mwandishi huko London, katika Kituo cha Kiislamu cha Uingereza mnamo mwezi wa Julai, 2011. Masomo haya yalikuwa ni jaribio la kuchunguza kiini cha imani, ushika dini, na maadili ambamo yametegemezwa

23

34

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 34

1/17/2017 1:10:14 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

kwa Mtukufu Mtume 3 pamoja na Mitume waliotangulia. Tayari tumekwishaelezea umuhimu wa uchamungu (Takwa) kufuatana na mafundisho ya Qur`ani Tukufu na hadithi, na tumeonesha kwamba uchamungu ndio sifa ya msingi inayohitajika kufikia kwenye wokovu. Ili kuweza kuelewa hali halisi ya uchamungu, uchunguzi zaidi wa maelezo ya Qur`ani Tukufu kuhusu sifa hii unahitajika. Kwa kurejelea kwenye aya za Qur`ani Tukufu ambazo zilinukuliwa kabla (2:2-5), Mwenyezi Mungu Mtukufu anawaelezea wacha Mungu kuwa ni wale wenye tabia fulani na kwa matokeo ya tabia hizo, hupata uchamungu na mwongozo, na hatimaye hupata mafanikio na furaha.

Wacha Mungu: a) Wanaamini katika ghaibu; b) wanasimamisha Swala; c) hutoa Zaka; d) huamini yale ambayo yameteremshwa kwa Mtukufu Mtume Muhammad 3 na Mitume wa kabla yake; na; e) wanaamini Akhera.

Imani Katika ghaibu: Ubora wa imani (iman) ndio jambo la msingi katika kupata uchamungu, bila hilo uchamungu unakuwa hau35

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 35

1/17/2017 1:10:14 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

wezekani. Kama inavyoonekana katika aya, imani ni sehemu ya sifa tatu miongoni mwa sifa tano za mcha Mungu. Katika hatua za mwanzoni mwa Uislamu dhana ya imani ilikuwa chini ya uchunguzi mkubwa na ilikuwa somo lililokuwa linajadiliwa sana. Wanatheolojia wa mwanzoni walikuwa na maoni yaliyotofautiana juu ya mtu aliyeamini ambaye anatenda dhambi kuu (murtakib al-kabirah), kwamba mtu kama huyo anaweza kuendelea kuwa muumini, au anaingia katika hali tofauti. Miongoni mwa hao, kundi la Muutazila24 waliamini kwamba mtu kama huyo huingia katika hali ambayo humfanya asiwe muumini au asiyeamini kabisa, ambapo kundi la Khawariji25 walikuwa na   K undi la Muutazilah lilitokeza wakati wa kipindi cha Hasan al-Basri (alifariki 110 AH), baada ya kuulizwa kama muumini akitenda dhambi kuu hubakia kuwa muumini. Mojawapo wa wanafunzi wake, Wasil bin Ata, alitoa maoni yake kwa kusema, ‘Hali iliyopo baina ya hali mbili (ya imani na kutoamini)’. Wasil akasimama na akaenda kukaa sehemu tofauti ya msikiti. Al-Basri akatangaza, ‘Mtu huyu ametuacha sisi au ‘Tuondokee’’ akitumia neno la Kiarabu kutoka kwenye chimbuko la neno Iitizaal, ambamo humo ndimo limechukuliwa jina Muutazilah. 25   Kharijites (kwa lugha ya Kiarabu ‫ خوارج‬Khawarij, maana yake halisi “wale waliondoka na kutoka nje”, kwa mmoja ni Khaarijii) ni jina la madhehebu ya Kiislamu. Watu wa madhehebu ya Khawarijites, ambao mwanzoni walikuwa wanaunga mkono mamlaka ya Ukhaifa wa Rashidun wa mwisho, Ali bin Abi Talib, mkwe na binamu wa Mtukufu Mtume Muhammad , baadaye waliukataa uongozi wake. Baada ya kipindi fulani, makundi ya Khawariji yalizidi kupungua idadi 24

36

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 36

1/17/2017 1:10:14 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

maoni kwamba mtu kama huyo angekuwa si muumini kabisa na matokeo yake angeuawa. Hivyo, haja ya kutoa ufafanuzi kwa usahihi ikachukua umuhimu mkubwa. Baadhi ya wanatheolojia walichukulia kwamba imani ni kutamka tu shahada mbili (shahadatayn) za imani. Wengine walisema kwamba kitu kingine zaidi kilihitajika, kama vile elimu, vitendo na unyenyekevu. Kutoka kwenye Qur`ani Tukufu na hadithi ni dhahiri kwamba ili mtu awe na imani, haitoshi kutamka tu imani juu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mtukufu Mtume Muhammad 3; bali, imani ni kitu kilichopo katika moyo.

“Mabedui walisema: Tumeamini. Sema: Hamjaamini, lakini semeni: Tumesilimu. Kwani imani haijaingia katika nyoyo zetu. Na mkimtii Mwenyezi Mungu na yao na imani yao haikupata mvuto wowote katika vizazi vilivyofuata. Kutoka kwenye msimamo wao wa kisiasa wa asili, Khawaariji walianzisha mafundisho yenye msimamo mkali sana ambayo yalizidi kuwaweka mbali zaidi kutoka kwenye mkondo mkuu wa Waislamu wa madhehebu ya Sunni na Shia. Khawariji walifahamika hasa katika kuchukua msimamo mkali wa Takfiri, ambamo walitangaza kwamba Waislamu wengine kuwa ni makafiri kwa hiyo waliwaona kwamba wanafaa kuuawa (yamedondolewa kwa ufupisho kutoka Wikipedia). 37

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 37

1/17/2017 1:10:14 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

Mtume Wake, hatawapunguzia chochote katika vitendo vyenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira, Mwenye kurehemu.� (Surah Al-Hujurat, 49:14)

Katika aya hii, Mwenyezi Mungu Mtukufu anamwambia Mtukufu Mtume 3 kuwanasihi Mabedui kwamba imani ni hatua baada ya hatua ya kuukumbatia Uislamu, na kwa hiyo tamko la kuamini tu halitoshi kumuona mtu kwamba ni muumini. Kwa hiyo, imani ni hatua ya juu zaidi ya kuingia kwenye Uislamu. Baada ya kutangaza imani, hatua za ziada zinahitajika ili imani iweze kuingia katika moyo wa mtu. Kuongeza elimu tu kwenye tamko la mtu haitoshi kubadilika kuwa imani. Katika historia yote, mifano inaweza kuonekana ambapo watu walikuwa na elimu ya ukweli lakini hawakuwa waumini. Mathalani Muawiyah alijua kwamba uongozi wa kweli wa Waislamu uliwekwa kwa Ali bin Abi Talib lakini alikataa kukubali jambo hili. Vivyo hivyo, wapagani wa Kiarabu kwa marudio ya mara kwa mara walikataa kutambua sifa za utambulisho wa Mtukufu Mtume 3, pamoja na kwamba walijua kwamba yeye alikuwa Mtume wa kweli wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, kutokana woga wa ubinafsi wa kupoteza mamlaka na udhibiti wa Makka. Qur`ani Tukufu inasema:

38

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 38

1/17/2017 1:10:14 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

“Na wakazikataa kwa dhulma na kujivuna, na hali ya kuwa nafsi zao zina yakini nazo…..” (An-Naml; 27:14)

Hivyo, zaidi ya elimu, mtu lazima awe na sifa ya kukubali. Ukubalifu utajidhihirisha wenyewe katika namna ya kujisalimisha na unyenyekevu kwa mintarafu ya ukweli, bila kujali gharama yoyote binafsi, masuala magumu, na muhanga unaouhitajia. Kwa hiyo, imani na viendo lazima viambatane pamoja. Haioneshi kama ni jambo la kustahiki kwa mtu kukubali ukweli na halafu asifanye vitendo vinavyoendana na ukweli huo, au kutekeleza vitendo kufuatana na ukweli lakini bila kujiamini katika kuutangaza ukweli huo kwa wengine.26 Akielezea imani na vijenzi vyake, Mtukufu Mtume Muhammad 3 alisema:

26  Kwa hakika hapa haturejelei wakati ambapo watu lazima watumie mbinu ya kuficha imani yao ili kupata kinga, mfano ya maisha yao, kitendo ambacho Qur`ani Tukufu inakiafiki. Mathalani, rejea kwenye aya 16:6 na 40:28. 39

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 39

1/17/2017 1:10:14 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

“Imani si pambo (ambalo huvaliwa), wala haipatikani kwa kutaka tu, badala yake, imani ni kitu ambacho hutuama ndani ya moyo na huthibitishwa kwa vitendo.” 27 “Imani ni uthibitisho kwa njia ya kauli, kutambuliwa kwa moyo na vitendo kwa viungo vya mwili.”28 “Imani na vitendo ni kama ndugu wawili, ambao wameungana pamoja; Mwenyezi Mungu Mtukufu hakikubali kimojawapo bila ya mwenza wake.” 29 Riwaya hizi zinaonesha kwamba imani na vitendo ni vitu vya lazima kwa kitendo chochote kuweza kukubalika; na inapotokea hivyo, basi kwa mujibu wa Qur`ani Tukufu kinaelezewa kama ni uchamungu.

“…..Mwenyezi Mungu huwapokelea wenye takua tu.” (Al-Maidah, 5:27)   Bihar al-Anwar, Juz. 66, uk. 72   Bihar al-Anwar, Juz. 10, uk. 367 29   Mizan al-Hikmah, Juz. 1, uk. 193 27 28

40

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 40

1/17/2017 1:10:14 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

Kwa hiyo imani ya mtu inahitaji elimu na matokeo yake ni katika vitendo; imani huzalisha kauli za mdomo, lakini kwa kifupi ni utii na kukubali. Kuzidi kuelezea nukta hii, tunarejelea kwenye aya kadhaa ambamo sifa za muumini zinaelezewa:

“Hakika waumini ni wale ambao anapotajwa Mwenyezi Mungu nyoyo zao hujaa hofu, na wanaposomewa Aya Zake huwazidisha imani, na wanamtegemea Mola Wao. Ambao wanasimamisha Swala na wanatoa katika yale tuliyowaruzuku. Hao kweli ndio waumini; wao wanavyeo kwa Mola Wao, na maghufira na riziki bora.� (Surah Anfal, 8:2-4)

Ujenzi wa kisarufi wa aya hizi unaonesha namna ya upekee, yaani haiwezekani mtu kuonekana kuwa ni muumini bila kuwa na sifa zifuatazo: 1.

Anapotajwa Mwenyezi Mungu nyoyo zao hujaa hofu: Wakati mpenzi wa mtu anapotajwa, kwa kawaida husababisha moyo wa msikilizaji kutama-

41

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 41

1/17/2017 1:10:14 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

ni kwa mintarafu ya mpenzi wake wa kiume au wa kike, na hupitiwa na kitambo cha mapenzi ya hisia za moyoni. Pale mpendwa anapokuwa ni Mwenyezi Mungu Mtukufu, maelezo yaliyo sahihi ya hali hiyo ni kupata hisia za hofu. Kwa hiyo, dalili ya msingi ya mtu aliye muumini ni mapenzi yake kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Mapenzi haya yatatimia na kukamilika, kwa kuwa yatamwongozea utiifu wa hiari na furaha, si kwa sababu ya tishio au thawabu yoyote. Mathalani, mtoto anapomuomba mzazi wake ampe kitu fulani kama vile glasi ya maji ya kunywa, mzazi hutii. Hapa hukana hisia za kulazimisha au kushurutishwa kwa mzazi, wala hakuna tishio au thawabu inayohusishwa na kitendo hicho. Badala yake, mzazi humtii mtoto kwa furaha. Vivyo hivyo, kila mara mpendwa anaweza kutafuta njia za kufanya vitendo vya wema kwa ajili ya mpenzi wake hata pale ambapo hajaombwa kufanya hivyo. Utiifu huu wa hiari na huduma ndiyo ambao waumini wa kweli huonesha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na hatimaye hulainisha moyo.30   Katika msamiati wa Kiarabu moyo unaitwa qalb, ambayo maana yake halisi ni mabadiliko, kwa sababu moyo hubadilika kutokana na mapenzi, chuki, matumaini, na kukata tamaa na kadhalika. Inaonekana kwamba katika lugha zote neno moyo hutumika kumaanisha moyo wa kimaumbile na pia nafsi.

30

42

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 42

1/17/2017 1:10:14 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

2.

Na wanaposomewa Aya Zake huwazidisha imani: Kiwango cha imani ya mtu inaweza kuongezeka au kupungua; imeunganishwa na utii - kujisalimisha, na utii una viwango mbalimbali. Wakati hali ya maisha inapokuwa ngumu sana, huwa ni vigumu sana kujisalimisha na kuwa mtiifu. Mfano wa kitendo cha kujisalimisha kisichotetereka wakati hali inapokuwa ngumu sana ni kile cha Nabii Ibrahim B na Nabii Ismail B. Nabii Ibrahim B anamwambia Nabii Ismail B kwamba ameamriwa kumtoa kafara yeye, na Nabii Ismail B akakubali kwa utulivu kabisa.

“Akasema: Ewe baba yangu! Tenda unavyoamrishwa. Utanikuta mimi, Inshallah, katika wanaosubiri.� (Surah As-Saffat, 37:102)

3.

Na wanamtegemea Mola Wao: Mara nyingi watu huwategemea watu wengine au taasisi, kama vile watu wa familia moja, waalimu, maafisa wa polisi, wafanyakazi wa benki, au madaktari, lakini muumini wa kweli atakuwa ameweka tegemeo lake kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. 43

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 43

1/17/2017 1:10:14 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

4.

Husimamisha Swala na hutoa Zaka: Ndani ya Qur`ani Tukufu, mara nyingi imani hutajwa pamoja na Swala, na Swala nayo karibu kila mara inaunganishwa pamoja na sadaka. Swala na sadaka huweza kufikiriwa kama mbawa mbili za ndege, mbawa hizo zote zinahitajika katika kuruka kwenda juu zaidi na kupata mafanikio.

Watu waumini ambao hutekeleza vitendo hivi ndio wanaelezewa kama waumini halisi na wakweli ambao wapo karibu sana na Mola Wao. Na kama matokeo yake wanasamehewa na kupewa riziki nzuri. Mahali pengine Qur`ani Tukufu inasema:

“Na wale walioamini wakahajiri na wakafanya jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu na wale waliokaribisha na kusaidia, hao ndio waumini kweli; wana maghufira na riziki njema.� (Surah Al-Anfal, 8:74)

Kwa nyongeza ya vile vitendo vinne vilivyotajwa katika aya iliyotangulia, aya hii inaelezea wale ambao ni waumini wa kweli kuwa ni wale wanaowekeza juhudi kubwa zaidi na kufanya jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na wako tayari kwa hiari 44

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 44

1/17/2017 1:10:14 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

zao kufanya makafara binafsi. Qur`ani Tukufu pia inasema:

“Na waumini wanamume na waumini wanawake ni marafiki wao kwa wao; huamrishana mema na hukatazana maovu, na husimamisha Swala, na hutoa zaka, na humtii Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. Hao Mwenyezi Mungu atawarehemu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Mwenye hekima.� (Surah At-Tawba, 9:71).

Aya hii inaelezea majukumu muhimu ya kijamii ambayo waumini wanayo kama walezi wa kila mmojawao. Malezi (Wilaayah) si tu baina ya binadamu na Muumba, au baina ya Maasum na wafuasi wao, lakini hasa ni jambo linalowafungamanisha watu pamoja, na Maasumu na Mwenyezi Mungu Mtukufu vilevile. Waumini wana haki kwa kila mmojawao na hatima yao inategemeana. Kwa hiyo hutumia malezi yao kuhimiza matendo mema na kukataza matendo maovu kwani hujihisi kuwa wana wajibu juu ya kila mmojawao, kama familia moja, au kama abiria wanaosafiri kwenye

45

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 45

1/17/2017 1:10:14 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

mashua moja, ambamo vitendo vya mmojawao huathiri wengine. Hivyo, kwa mtu muumini, hakuna nafasi ya ubinafsi au tabia ya kutojali kuhusu hali njema ya mtu mwingine. Matokeo yake ni kwamba watu waaminifu kama hao punde wataoneshwa rehema maalumu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Mara wanapokuwa wamepata imani, wale waumini wa kweli hawaitilii shaka hali ya baadaye:

“Hakika Waumini ni wale tu waliomwamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake tena wasiwe na shaka, na wakapigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali yao na nafsi zao. Hao ndio wakweli.” (Surah Al-Hujurat, 49:15).

Hapa tunatakiwa kutofautisha baina ya shaka isiyo ya haki (rayb) na shaka halisi.31 Kwa moyo mkunjufu   Kwa mujibu wa hadithi kutoka kwa Imamu Sadiq  mtu mmoja alikwenda kwa Mtukufu Mtume Muhammad  akiwa na hofu, wasiwasi sana kwamba alikuwa amepoteza imani yake na kwa hiyo alikuwa ameangamia. Kabla ya mtu huyo hajasema tatizo hasa lilikuwa ni nini, Mtukufu Mtume  alisema: ”Shetani alikuja kwako na akakuuliza wewe: ‘Kama Mwenyezi Mungu Mtukufu ameumba kila kitu, basi ni nani aliyemuumba Mwenyezi Mungu Mtukufu?’ Yule mtu akasema: “Kwa Yule aliyekunyanyua kama Mtume kwa haki,

31

46

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 46

1/17/2017 1:10:14 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

Uislamu unahimiza uchunguzi, lakini mara tu ukweli unapodhihiri na kuonekana, majivuno na jeuri yasimzuie mtu kukubali ukweli, vinginevyo mtu kama huyo atajikuta anaishi katika kanusho la kudumu. Mmojawapo wa wanafunzi wa Ibn Sina (Avicenna) wakati mmoja alimwambia mwalimu wake: “Bwana, wewe una kipaji sana! Kama ungedai kuwa mtume watu wangekuamini!” Ibn Sina hakutoa jibu wakati huo. Katika siku nyingine, Ibn Sina na mwanafunzi wake huyo wakawa wanasafiri pamoja na usiku ulipoingia wakalala na hali ya hewa ilikuwa baridi sana. Ulipokaribia muda wa Swala ya Alfajiri, Ibn Sina alimwamsha mwanafunzi wake na akamtaka amletee maji ya kunywa. Mwanafunzi alikuwa ameliwazika kwa kujifunika vizuri na hakutaka kwenda nje kwenye baridi kuchota maji na kwa hiyo akaanza kutoa udhuru wa kwanini sio vizuri Ibn Sina kunywa maji ya baridi. Halafu wote wakasikia adhana kutoka kwenye msikiti wa karibu na pale walipolala. Ibn Sina alipohisi uzuri wa wakati akasema: “Wewe umekuwa mwanafunzi hilo ndilo lililokuwa tatizo.” Kisha Mtukufu Mtume akasema: “Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mtukufu hii ni imani safi kabisa.” (Al-Kafi, Juz. 2, uk. 425). Hii ina maana kwamba lile jambo la kwamba wakati unapopata swali kama hilo, ukawa na wasiwasi na ukataka kutafuta jibu sahihi kwa swali hilo inaonesha kwamba wewe ni muumini wa kweli. Hadithi hiyo inasomeka kama ifuatavyo: 47

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 47

1/17/2017 1:10:14 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

wangu kwa miaka mingi na mimi nilikuomba mara moja tu uniletee maji ya kunywa na ukaanza kutoa nyudhuru nyingi. Lakini yule mtu (muadhini) ambaye hata hakukutana na Mtume huenda kuadhini kwenye kilele cha mnara wenye baridi kila siku usiku na anatamka kumshuhudia Mtukufu Mtume Muhammad 3. Hii ndiyo tofauti baina yangu mimi na mtume.� Imani madhubuti na kusadiki huwarahisishia watu wenye imani kama hao kufanya jihadi kwa utajiri wao na maisha yao na kukubali matatizo; watu kama hao wamejaribiwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu na wakafuzu majaribu, na kwa hiyo aya inawaita watu hao kuwa wamefuzu.

48

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 48

1/17/2017 1:10:14 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

SEHEMU YA NNE32

M

UHTASARI: Viashiria vya Uchamungu vinalenga kwenye manufaa ya uchamungu (Takwa) katika Qur`ani Tukufu, hadithi, na maisha ya Ahlul Bayt F. Uchamungu - mojawapo ya sifa muhimu sana ambazo mtu anaweza kuwa nayo - ni namna ambavyo watu wanawekwa katika madaraja mbele ya Mungu kwani unahusiana na nia ya kwenye vitendo vyote na unahitajika kufikia kwenye wokovu. Sehemu ya kwanza na ya pili zilijikita kwenye sifa za uchamungu katika Qur`ani Tukufu na zikachunguza ufafanuzi wa uchamungu pamoja na mambo ambayo huchangia katika kuujenga uchamungu. Sehemu ya tatu ilionesha sifa za wacha Mungu kama ni wale wanaoamini ghaibu, kusimamisha Swala, kutoa Zaka, kuamini Akhera, na wanaamini katika yale yaliyoteremshwa kwa Mtukufu Mtume 3 na yale yaliyoteremshwa kwa Mitume wa kabla yake. Sehemu hii inafafanua zaidi kuhusu waaminio kwamba ndiyo hao watakaopata mafanikio ya   Makala hii imeegemezwa kwenye sehemu ya 4 na 5 ya mfululizo wa masomo saba yaliyotolewa na mwandishi huko London kwenye Kituo cha Kiislamu cha Uingereza mnamo mwezi wa Julai, 2011. Mfululizo huu wa masomo ulikuwa ni jaribio la kuchunguza kiini cha imani, uchamungu na maadili ambamo ndimo yameegemezwa.

32

49

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 49

1/17/2017 1:10:14 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

kweli na kuonesha mfano wa waaminio ni akina nani, na watapata nini hapa duniani na Akhera. Katika mfululizo uliotangulia tumethibitisha kwamba kwa mujibu wa Qur`ani Tukufu, uchamungu ni sifa muhimu ambayo kwayo tunaweza kupata mafanikio, na chochote ambacho ni pungufu ya hilo hakitaleta mafanikio yanayoridhisha hapa duniani na Akhera. Ili kuweza kuelewa zaidi, aya 2:2-5 zilinukuliwa, ambamo humo Mwenyezi Mungu amewaelezea wacha Mungu kuwa ni wale wenye kuamini ghaibu, yale yaliyoteremshwa kwa Mtukufu Mtume Muhammad 3, na yaliyoteremshwa kwa Mitume waliotangulia. Kinachofuata ni maelezo kwa mifano ya imani kama ambavyo imeelezewa katika Surah ya al-Muminuun:33

Mafanikio ya kweli: Surah ya al-Muuminuun inaanza na aya kumi na moja ambazo zinaelezea waaminio. Ndani aya ya kwanza kabisa, Mwenyezi Mungu anasema:

“Hakika wamefaulu waumini.” (23:1)   Surah ya 23 ya Qur`ani Tukufu.

33

50

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 50

1/17/2017 1:10:14 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

Aya hii imetumia kitenzi cha wakati uliopita, sambamba na kishirikishi “qad” kwa ajili ya kuongeza msisitizo ambao unaashiria mafanikio ya wazi na uhakika kuhusu waaminio. Chimbuko la neno ambalo limetumiwa katika aya kuhusu kufuzu – falaah – kwa asili lina maana ya ‘kufungua’. Mkulima anajulikana kama fallah kwa sababu hufungua ardhi na kupanda mbegu katika udongo. Mwenyezi Mungu ametumia neno hili kwa ajili ya furaha ya binadamu, labda kwa sababu watu ni kama mbegu wenye uwezo wa kukua, almuradi wanapata ardhi iliyo na rutuba, ambayo ni imani. Hili baada ya hapo, husaidia makuzi ya mtu binafsi, na baadaye hutoa kivuli (yaani usalama na faraja) na matunda (yaani manufaa). Endapo inakuwa kinyume chake, basi fursa hufujwa na mtu ananyauka. Kidokezo kipana zaidi cha neno –falah - ni mafanikio na furaha katika dunia hii na Akhera. Kwa mujibu wa mwanaleksikografia mashuhuri al-Raghib al-Isfahani, neno hili linajumuisha mambo matatu ya furaha ya kidunia, na manufaa manne ya Akhera:

51

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 51

1/17/2017 1:10:14 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

Mambo ya furaha ya kidunia: 1.

Kuweza kuishi maisha yanayotosha kufanikisha malengo ya mtu.

2.

Kuishi kwa heshima na hadhi.

3.

Mtu kuwa na uwezo wa kumudu matumizi ya maisha yake.34

Mambo ya mafanikio katika Akhera: 1.

Maisha ya Milele.

2.

Heshima kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

3.

Utajiri wa kudumu bila kupungukiwa au ufukara.

4.

Kuwa na elimu ya ziada.

Maelezo ya waaminio: Aya 11 za kwanza za Sura al-Muuminuun zinajumuisha sura 6 za waaminio:   Wakati Uislamu ukihimiza mtindo wa maisha yaliyo rahisi, lakini pia unapinga vikali umasikini wa kifedha. Na serikali ya Kiislamu inayo kazi ya kuondoa ufukara miongoni mwa jamii. Jambo la kuvutia ni kwamba Qur`ani Tukufu inasema kwamba imani pia huwa na mchango wake katika utajiri wa rasilimali. (7:96)

34

52

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 52

1/17/2017 1:10:14 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

1.

ale ambao ni wanyenyekevu katika Swala W zao (23:2)

Qur`ani Tukufu inataja wale ambao huswali katika muktadha tofauti tofauti. Wakati mwingine kwa urahisi tu unapotaja wale wanaotekeleza Swala, inalalamika kuhusu nafasi yao:

“Basi ole wao wanaoswali. Ambao wanasahau Swala zao.� (107:4-5)

Kitendo cha kuswali tu hakilazimishi kuwa sababu ya mtu kuwa mwaminifu wa kweli; ni ubora wa Swala ndio humstahilisha mtekelezaji wa Swala kuwa miongoni mwa waumini. Waumini huwa wanyenyekevu mno katika Swala zao, na kwa sababu ya nyoyo zao nyenyekevu na laini, wanaweza kuwa makini wanaposwali. Yapo maneno mawili ambayo hutumiwa mara kwa mara katika muktadha wa adabu za mtu wakati wa Swala. Khudhuu: Muonekano wa kimwili wa kunyenyekea ambamo moyo unaweza kuwa au kutokuwa katika hali ya ulinganifu. 53

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 53

1/17/2017 1:10:14 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

Khushuu: Hali ya unyenyekevu iliyotegemezwa moyoni ambayo pia inaweza kuonekana kimwili. Aya hiyo hapo juu imetumia neno Khushui kumaanisha Swala ambayo imeswaliwa na muumini. Katika hadithi moja, Mtukufu Mtume Muhammad 3 alimuona mtu anaswali na wakati huohuo alikuwa anacheza na ndevu zake. Akasema, “Hakika, kama moyo wake ungekuwa unanyenyekea, pia viungo vyake vingekuwa vimenyenyekea.”35 Baadhi ya wafasiri mashuhuri kama Majma` alBayan na Tafsir al-Kabir wanataarifu kwamba kabla ya kuteremshwa kwa aya hizi, wakati mwingine Mtukufu Mtume 3 alikuwa akiangalia mbinguni akiwa katika hali ya unyenyekevu wakati wa Swala, lakini baada ya kuteremshwa aya hizi, wakati wote alikuwa akielekeza macho yake chini. 2.

mbao hujiepusha na mambo ya upuuzi A (23:3).

Waumini hujiepusha na kazi, mazungumzo au hata mawazo ya kipuuzi na yasio na maana. Kitu chochote kisicho na maana hakina faida, pamoja na kwamba hakikuharamishwa. Hata hivyo, waumini huwa hawaji35  Mathalani, tazama Bihar al-Anwar, Juz. 68, uk. 228. 54

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 54

1/17/2017 1:10:14 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

ingizi kwenye mambo kama hayo kwa sababu wao wanapata msukumo wa makusudio yaliyo dhahiri katika kila kitu wanachokifanya. Huthamini kila sekunde ya uhai wao kwa sababu wanakiona kifo kama kitu halisi na kinachokaribia kutokea. 3.

Na ambao kwa Zaka ni watendaji: (23:4)

Aya hii inarejelea kwenye mapana ya kitendo cha kutoa sadaka. Aya hizo hapo juu ziliteremshwa Makka, kabla ya kodi ya lazima ya Zaka haijarasimishwa kuwa sheria. Kwa hiyo neno ambalo limetajwa katika aya hii haliwezi kumaanisha kodi ya faradhi. Zaidi ya hayo, Qur`ani Tukufu kila wakati hutaja Swala na sadaka kwa pamoja. 4.

Na ambao wanazilinda tupu zao (23:5)

Waumini ni wale ambao hubakia katika mipaka ya ndoa na hudumisha uhusiano wa kimwili na wake zao wa halali tu. 5.

a wale ambao wanachunga amana zao na N ahadi zao. (23:8)

Waumini ni wale ambao huchunga ahadi zao katika hali ya kila namna, na kama anapewa dhamana ya kutunza rasilimali yoyote, basi hutekeleza ahadi hiyo kwa ua55

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 55

1/17/2017 1:10:15 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

minifu mkubwa. Imam Zaynul-Abidin B anatangaza kwamba kama angepewa dhamana na mwuaji wa Imam Hussain B ya upanga ambao ndiyo uliotumika kumuua baba yake huko Karbala, angeurudisha kwa mwenyewe. Vivyo hivyo, kabla Mtukufu Mtume Muhammad 3 hajahama kutoka Makka kwenda Madina alikuwa na amana kadhaa za watu wa Makka kwa sababu ya uaminifu wake maarufu. Alihakikisha amana hizo zinarudishwa kwa wenyewe kwa kumuagiza msaidizi wake Imam Ali B, aliyeshika nafasi yake hapo Makka kwa masharti yaliyo dhahiri ya kuondoka kwenda Madina baada tu ya kurudisha amana za watu. Mtukufu Mtume 3 hakutumia amana za watu vibaya pamoja na kwamba walikuwa na uadui naye. Kuhusu ahadi, waumini pia huhisi wajibu wao mkubwa katika kutimiza ahadi yao ambayo wamefunga na Mwenyezi Mungu:

“Na tekelezeni ahadi ya Mwenyezi Mungu mnapoahidi wala msivunje viapo baada ya kuvithibitisha, ilhali mmekwishamfanya Mwenyezi Mungu ndiye Mdhamini 56

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 56

1/17/2017 1:10:15 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

Wenu. Hakika Mwenyezi Mungu anayajua mnayoyafanya.” (16:91)

Hivyo, dhana ya kutekeleza ahadi ni pana sana na ni wajibu ambao waumini huwa wanautambua wakati wote. 6. Na ambao Swala zao wanazihifadhi (23:9) Kutajwa kwa Swala mara mbili katika dondoo hii inasisitizia umuhimu wake wa msingi. Kwa nyongeza kwenye hali yao ya unyenyekevu katika Swala, waumini huzingatia muda, adabu, na vitendo vya Swala zao vilivyopendekezwa. Huzilinda Swala zao zisiingiliwe na changamoto au tatizo lolote la ndani au nje. Waumini watakuwa warithi wa Pepo. Mwishoni mwa maelezo, Mwenyezi Mungu anasema:

“Hao ndio warithi. Watakaorithi Firdausi, wadumu humo.” (23:10-11)

Jambo la kustaajabisha ni kwamba Qur`ani Tukufu inatumia neno ‘rithi’, na kuhusiana na hili tunaweza

57

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 57

1/17/2017 1:10:15 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

kuona maoni matatu. Baadhi ya wanazuoni wa Kiislamu wanasema kwamba kwa namna ileile ambayo mtu hufaidika kutokana na urithi bila ya kuufanyia kazi urithi huo, pepo ni adhimu mno ambayo waumini wanapewa na Mwenyezi Mungu kutokana na huruma Yake, na ni zaidi sana ya fidia ya juhudi zao. Wale wenye kutenda matendo mema hawastahili pepo, ni sawa kabisa na zawadi isiyotarajiwa. Mtazamo huu unaweza kuonekana zaidi katika maelezo ya Qur`ani Tukufu kuhusu Pepo na Jahannam.

“Na Bustani (Pepo) itasogezwa kwa wenye Takua. Na Jahannam itadhihirishwa kwa wapotofu.� (26:90-91).

Wacha Mungu wametoa ishara kwa mintarafu ya pepo kupitia vitendo vyao katika maisha yao, lakini bado wanahitaji huruma ya Mwenyezi Mungu kuisogeza pepo kuwa karibu nao. Mwenyezi Mungu anaapa kuwapa pepo watu wema kwa kuisogeza karibu nao. Kuhusu jahannam, wapotofu tayari wanaishi humo; Kilichobakia ni kufunuliwa na kudhihirishwa tu kwao.

58

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 58

1/17/2017 1:10:15 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

Maoni ya pili yanaeleza kwamba kila mmoja anayo nafasi yake huko peponi, lakini watu wanaweza kupoteza nafasi hizo kwa sababu ya matendo yao. Mtukufu Mtume Muhammad 3 amesema: “Kila mmoja wenu anazo nyumba mbili: nyumba moja ipo peponi na nyingine ipo jahannam. Kama mtu akifariki dunia na anaingia jahannam, basi watu wengine watarithi nyumba ile iliyoko peponi.” Pepo haitabaki tupu, na hakuna nafasi ambayo itafujwa. Baadhi ya nafasi huko peponi zitarithiwa kutoka kwa wale ambao walishindwa kudai nafasi zao. Jambo la kuvutia ni kwamba sifa ya jahannam na pepo ni kwamba sehemu zote hizi mbili zinaweza kuwapatia nafasi wanadamu wote. Jahannam ina uwezo wa kupanua nafasi yake na kuwapatia nafasi watu wengi zaidi:

ْ َ‫يَ ْو َم نَقُو ُل لِ َجهَنَّ َم هَ ِل ا ْمتَ أ‬ ‫ت َوتَقُو ُل هَلْ ِمن َّم ِزي ٍد‬ ِ ‫ل‬ “Siku ambayo Tutaiuliza jahannam, ‘Je! Umejaa?’ Yenyewe itajibu, ‘Je! Wapo wengine zaidi?”

Maoni ya tatu, neno ‘kurithi’ linatumika kusisitiza kwamba pepo ni kitu ambacho anakiumba 59

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 59

1/17/2017 1:10:15 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

Mwenyezi Mungu tu. Hata hivyo, udhibiti wa pepo hii unakabidhiwa kwa wakazi wake ambao huishi humo, sio kama wapangaji ambao ukaaji wao wa baadaye unaweza kuwa hatarini, bali hasa ni kama wamiliki wenye udhibiti kamili.

Maelezo ya Waumini katika hadithi: Sasa kwa vile tumetoa maelezo ya waumini kwa mtazamo wa Qur`ani Tukufu, sasa tunaelekeza mazingatio yetu kwenye hadithi husika zilizojaa rejea juu ya imani. Ili kuweka mazungumzo yetu kwenye kiini, tutatosheka na hadithi ambazo zinahusiana na viashiria vya watu waaminio. Baadhi ya hadithi hurejelea kwenye viashiria vya nje vya imani ambapo nyingine zinarejelea kwenye viashiria vya ndani. Mathalani, riwaya hii mashuhuri kutoka kwa Imam Hasan al-Askari B inataja viashiria vitano nya nje.

‫ صالة إحدى وخمسين وزيارة‬:‫عالمات المؤمن خمس‬ ‫األربعين والتختم باليمين‬ ‫وتعفين الجبين والجهر ببسم هللا الرحمن الرحيم‬ 60

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 60

1/17/2017 1:10:15 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

“Alama za mtu muumini ni vitano: Utekelezaji wa rakaa 51 za Swala kila siku, usomaji wa dua ya Ziyarat al-Arba`in, kuvaa pete mkono wa kuume, kusujudu juu ya udongo, na kusoma Bism Allah al-Rahman al-Rahim kwa sauti kubwa (wakati wa Swala.)”36 Neno ambalo limetumika katika riwaya hii (‘alamat) chimbuko lake ni `ilm (elimu). Alama inafafanuliwa kama ‘kile kinachosaidia katika kuelewa’. Mathalani, ishara ya moto ni moshi, na wakati moshi unapoonekana, humsaidia mchunguzi katika kuelewa kwamba kuna moto mahali hapo. Pamoja na kwamba hadithi inataja viashiria vitano vya muumini, haijawekewa mpaka kwa viashiria hivi vitano. Imam al-Askari B amevitaja viashiria hivyo vitano kwa sababu ya umuhimu wao. Zaidi ya hayo, neno ‘muumini’ katika hadithi hii linarejelea kwa mfuasi wa Ahlul Bayt F na inataja viashiria ambavyo ni mahususi kwenye namna wanavyotekeleza Uislamu. Kiashiria (dalili) cha kwanza: Utekelezaji wa rakaa 51 za Swala kwa msingi wa kila siku. Hizo rakaa 51 zinakamilishwa na rakaa 17 za Swala za faradhi za kila siku na rakaa 34 za Swala za ziada za   Tusi, Tahdhib al-Ahkam, Juz. 6. uk. 52; `Amilii, Wasa`il al-Shia, Juz. 4, uk. 58.

36

61

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 61

1/17/2017 1:10:15 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

suna (nawafil), ambazo ni rakaa 8 kabla ya Swala ya faradhi ya Adhuhuri, rakaa 8 za kabla ya Swala ya faradhi ya Alasiri, rakaa 4 baada ya Swala ya faradhi ya Magharibi, rakaa 1 baada ya Swala ya faradhi ya Ishaa, rakaa 11 kama Swala za usiku wa manane na rakaa 2 kabla ya Swala ya faradhi ya Alfajiri. Hizi Swala za ziada zinachukua umuhimu mkubwa sana, na kama mtu hawezi kutekeleza Swala zote hizi basi angalau atekeleze baadhi yake, hususani zile Swala za ziada za Adhuhuri na zile za usiku wa manane. Zaidi ya hayo, hizo ndizo Swala za suna ambazo zinaweza kuswaliwa hata baada ya muda wao kupita kama kadhaa. Imam Zaynul-Abidin wakati mmoja aliwafundisha sahaba zake kwamba pale mtu anaposwali Swala za faradhi za kila siku, ni sehemu tu za Swala zilizoswaliwa kwa uhudhurishaji na uzingativu wa moyo ndizo hukubaliwa. Wakati sahaba zake walipojibu hoja kwa kusema kwamba hilo lilikuwa pendekezo gumu sana, Imam B aliwahakikishia kwamba utekelezaji wa Swala za ziada husaidia kufidia Swala za faradhi zilizoswaliwa baada ya muda wake kupita. Kiashiria cha pili: Usomaji wa Ziyarat al-Arbain, dua madhubuti sana ya ziyara inayosomwa mnamo siku ya 40 baada ya kuuawa kishahidi kwa Imam Husein B. Kutoka kwenye rejea nyingine za Kiislamu, tunajua 62

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 62

1/17/2017 1:10:15 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

kwamba tarakimu hii 40 ina maana muhimu maalumu. Inatumainiwa kwamba utekelezaji wa kitendo chochote kwa kipindi cha siku 40 kunakifanya kuwa desturi imara na kunakibadilisha kuwa hulka yake ya pili. Mtu anayeanza kumzuru Imam Hussain B katika ile siku ya kifo chake cha kishahidi, na akaendeleza hii dua ya Ziyara kwa kipindi cha siku 40 baada ya hapo, na akafikia kilele cha kusoma kwake katika siku ya 40, hujenga uhusiano imara usioweza kuyumba baina yake na Imam Hussain B. Uhusiano huu unatumainiwa kubaki kama fungamano la moyo la dhati. Hata hivyo, mtu ambaye anasoma Ziyara hii mnamo siku ya kuuawa kwake (Imam Hussain B) au kwa siku moja tu, akiwa katika faragha, peke yake hataweza kujenga uhusiano kama huo. Kiashiria cha tatu: Kuvaa pete mkono wa kulia. Hii inaweza kuwa ni njia ya haraka sana ya kumtambua mtu kwamba yeye ni mfuasi wa Ahlul Bayt F. Kiashiria cha nne: Waumini hutekeleza Swala zao kwa kusujudu juu ya udongo au vitu vingine

63

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 63

1/17/2017 1:10:15 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

vya asili.37 Wafuasi wa madhehebu ya Sunni wanazo hadithi nyingi kuhusu desturi hii lakini wao huliwekea jambo hili mpaka wa muda fulani katika historia kwa hiyo wao huwa hawafuati maamrisho haya nje ya kipindi hicho. Wanazuoni wa Shia hawakubaliani na madai kwamba Mtukufu Mtume 3 aliwaruhusu sahaba zake kusujudu juu ya nguo au nguo zao wenyewe. Historia inaonesha kwamba sahaba walikuwa wakibeba mchanga na pale wakati waliposujudu, walikuwa wakiweka mchanga ulio baridi chini na kusujudu juu yake, badala ya ardhi ambayo ilikuwa imeshika joto kutokana na jua. Kama Mtukufu Mtume aliwaruhusu wafuasi wake kusujudu juu ya nguo au mavazi yao, basi utaratibu huo wa kubeba mchanga unakuwa hauna maana. Katika riwaya nyingine, Suhayb mpwa wa Umm Salamah, mmojawapo wa wakeze Mtukufu Mtume 3, alikuwa akipuliza mchanga wakati anapotaka kusujudu kwa lengo la kukwepa vumbi. Umm Salamah alimwambia “Ewe mtoto wa kaka yangu! Usipulize   Kulingana na wanasheria wa madhehebu ya Shia, sio halali wakati wa swala kusujudu juu ya kitu chochote isipokuwa juu ya udongo na vitu vile ambavyo huota na kukua juu ya udongo na havitumiki kwa chakula au mavazi. Madhehebu mengine ya sharia yanaweza kuruhusu kusujudu juu ya mazulia na mabusati au kitu kingine chochote pamoja hata na sehemu ya kilemba cha mtu, almuradi ni tohara.

37

64

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 64

1/17/2017 1:10:15 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

mchanga huo, kwa sababu nilimsikia Mtukufu Mtume 3 akimwambia mtumishi wake Yasar ambaye alipuliza mchanga ‘Kwa ajili ya Mungu, uwache uso wako uwe na vumbi,’38 kwa sababu vumbi kwenye uso wa mtu huhimiza unyenyekevu na huonesha utumwa kabisa. Riwaya zingine zinaeleza kwamba masahaba walikuwa wakisujudu juu ya majani ya mitende na ni riwaya chache tu zinaeleza kwamba masahaba walitumia ncha za vilemba vyao. Hivyo, msimamo ambao umechukuliwa na Ahlul Bayt F angalau ni msimamo wenye kutahadharisha na ni utaratibu ambao hauna pingamizi na unakubaliwa na Waislamu wote, ambapo kusujudu juu ya nguo ni kitendo kinachopingwa na baadhi ya Waislamu na kwa hiyo ni kosa linalowezekana. Kiashiria cha tano: Utongoaji wa Bismillah (Kwa Jina la Mwenyezi Mungu) katika Swala. Kati ya Swala tano za faradhi za kila siku, Sura za Qur`ani Tukufu zinazosomwa katika rakaa mbili za mwanzo za Swala   Musnad Imam Ahmad bin Hanbal, Baqi Musnad, Hadithi ya Umm Salamah, hadithi ya 25360. Pia ipo hadithi inayofanana na hii kutoka kwenye chanzo hicho hicho (hadithi na. 25519) ambayo inaashiria kwamba Umm Salamah alimwambia mtoto wa kaka yake, “Usipulize, kwa sababu Mtukufu Mtume  alimwambia mtumishi wetu, aliyeitwa Ribaah, ‘Uache uso wako uwe na vumbi., ewe Ribaah.” Hadithi kama hiyo inaweza kuonekana katika vyanzo vingine vingi. Mathalani, rejea Sunan Tirmidhi, mlango wa Swala, hadithi ya 348.

38

65

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 65

1/17/2017 1:10:15 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

ya Alfajiri, Magharibi na Ishaa zinasomwa kwa sauti ya kusikika. Katika Swala ya Adhuhuri na Alasiri, sehemu hizi husomwa kwa mnong`ono, lakini inapendekezwa kwamba Bismillah itongolewe kwa sauti ya kusikika. Kuhusu Bismillah, Imam Ja`far al-Sadiq anasema, “Ni aya tukufu sana iliyoibiwa na Shetani.39 Leo hii, Waislamu wengi huswali Swala zao bila kutongoa Bismillah, pamoja na kwamba aya hii ni ya muhimu sana kiasi kwamba Mwenyezi Mungu aliiteremsha mara 114. Ahlul Bayt F wanaichukulia aya hii kuwa ni sehemu ya mwanzo wa kila Sura isipokuwa sura ya 9 tu, lakini hata hivyo imejumuishwa mara mbili katika Sura ya ishirini na saba.40 Kurudiwa kwa aya hii kunaonesha kwamba Mwenyezi Mungu anataka waja Wake kukumbuka majina Yake, hususani yale matatu ambayo yametajwa kwenye aya: Allah, Rahmaan (Mwenye huruma), na Rahim (Mwingi wa Rehema). Mtukufu Mtume 3 amesema: “Kila jambo muhimu lisiloanza na Bismillah halitakuwa na matokeo mazuri.” 40

.‫ أعظم آية سرقتها شيطان‬39   Sura ya 9 ya Qur`ani Tukufu ambayo imebeba maonyo makali kwa wapagani, na kwa hiyo haianzi na aya hii. Jambo la kuvutia ni kwamba, Mwenyezi Mungu hachagui mbadala wowote, mathalani ‘Kwa Jina la Mlipiza kisasi’ au ‘Kwa Jina la Mlazimishaji’. Labda hii ni kwa sababu Yeye anataka atambuliwe kama mwenye huruma na mwingi wa rehema, au bila chochote kabisa. 66

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 66

1/17/2017 1:10:15 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

Kutokana na mafundisho haya tunaweza kudondoa nukta mbili: 1.

Mwenyezi Mungu anatutaka sisi tumwelewe Yeye kama Mola ambaye ni mwingi wa rehema na mrehemevu. Pamoja na kwamba anayo majina yanayofika mamia, anatutaka sisi tumtambue Yeye hususani kwa sifa hizi. Jina Rahmaan linamaanisha urehemevu Wake kwa jumla kwa viumbe Vyake vyote na ni nomino inayomstahiki Yeye pekee.

Jina Rahim linamaanisha rehema Yake maalumu ambayo imehifadhiwa kwa ajili ya waumini. Rehema ya Mungu ni kitu cha karibu sana na dhati Yake isiyo na kina. Anapotaja rehema Yake anasema: “…..Akasema: Adhabu Yangu nitamsibu nayo nimtakaye; na rehema Yangu imekienea kila kitu…..”.(7:156). 2.

Aya inawatia moyo wale wenye imani kwa Mungu kama huyo kuziendeleza sifa hizi ndani mwao. Kwa kumkumbuka wakati wote kwa sifa hizi wanapaswa kuzidhihirisha sifa hizi katika sifa zao wenyewe, vinginevyo usomaji wa utaratibu huu unakuwa wa kinafiki. Kwa hiyo waaminio wanayo huruma na rehema kwa viumbe vingine vyote, pamoja na kwamba hususani ni kwa 67

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 67

1/17/2017 1:10:15 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

waumini wenzao, kwani hao ndiyo wanaostahili zaidi, ijapokuwa katika namna isiyo ya kibaguzi. Hii ni kama vile kuwapenda watoto wote, lakini mtu kuwa na upendo wa ziada na mahusiano kwa watoto wake mwenyewe. Ishara hizi tano ni ishara za nje na kila mojawapo inaweza kuonekana kwa urahisi katika tabia ya nje ya mtu. Hii inaweza kusaidia haraka kuwatambua wale ambao sio waaminifu. Hata hivyo, haijuzu kwamba wale wenye dalili hizi lazima wawe waumini. Kwa ajili ya hilo, tunahitaji dalili zingine zaidi. Imam al-Baqir B amesema:

,‫ حسن التقدير في المعيشة‬:‫من عالمات المؤمن ثالث‬ ‫والصبر على النائبة والتفقه في الدين‬ “Miongoni mwa dalili za watu wenye kuamini ni tatu: usimamizi mzuri wa uchumi wa familia yake, subira wakati wa msiba mkubwa, na elimu ya kina juu ya dini.” 41

Hadithi hii inarejelea dalili tatu za ziada miongoni mwa ishara nyingi za mtu aliye muumini: Dalili ya kwanza: Mtu aliye muumini ataweza kusimamia na kupanga uchumi wa familia yake.  Tusii, Tahdhib al-Ahkaam, Juz. 7, uk. 236.

41

68

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 68

1/17/2017 1:10:15 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

Hii maana yake ni kwamba yeye wala sio bakhili au mwenye kufanya matumizi mabaya na ufujaji (israaf). Kujiepusha na matumizi mabaya na kuthamini walichonacho katika mali pia ni sifa ya waumini wanayoifanya ndani ya familia zao. Mtu mmoja mwoka mikate alimwambia mwanaye wa kiume ambaye alikuwa anakaribia balehe kwamba angemfikiria kuwa amekuwa mtu mzima pale ambapo angeweza kupata kipato cha dirham moja.42 Kwa hiyo kijana huyo bila ya juhudi yoyote alichukua dirham moja kutoka kwa mama yake, na alipomwonesha baba yake, baba yake alisema kwamba dirham hiyo haikubaliki na akaitupa dirham hiyo ndani ya oveni. Tukio hili lilijirudia tena katika siku chache zilizofuata, na kijana huyo alizidi kufadhaika kwamba baba yake alijuaje kwamba dirham aliyokuwa anampa hakuitolea jasho. Mama wa mtoto huyo alimshauri kijana huyo kupata dirham kwa kufanya kazi na aioneshe kwa baba yake. Hatimaye kijana huyo alikubali na akafanya kazi kwa bidii na akapata dirham moja, na alipoionesha dirham hiyo kwa baba yake kwa mara nyingine dirham hiyo ilitupwa kwenye oveni. Ndipo mtoto huyo alipoingiza mkono kwenye oveni kwa hasira sana na akaitoa nje dirham hiyo, bila kujali hatari ya kuungua. Ndipo baba   Sarafu ya madini ya fedha.

42

69

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 69

1/17/2017 1:10:15 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

yake alipokubali kwamba dirham hiyo ilipatikana kwa kufanya kazi, na akasema kwamba alikuwa akijua kwamba dirham za nyuma hazikuwa zinapatikana kwa kufanya kazi kutokana na kitendo cha kutoonyesha hisia za raghba. Somo hili lilikuwa ni kumfundisha mwanae kujua thamani ya fedha na kwamba inapaswa kutumiwa kwa busara. Dalili ya pili: Kuwa na subira wakati wa matatizo. Hali ngumu ya maisha huwa kama chekecheke ambamo tabia na dhamira ya mtu hujaribiwa. Katika hadithi inasimuliwa kwamba subira ni sifa ya msingi katika mafanikio ya mtu, kama vile kilivyo kichwa kwa kiwiliwili. Dalili ya tatu: Waumini wanavutiwa sana, na kuambatana sana na dini, na hujitahidi kusoma na kuweza kujua zaidi. Maisha ya waumini yameelekezwa zaidi katika kumpendeza Mola Wao na kujifunza njia za dini yao. Inafaa kutamka hapa kwamba elimu inayozungumziwa katika hadithi hii ni (tafaqquh) ambayo inarejelea kwenye uelewa mkubwa badala ya elimu ya juujuu. Kutokana na semi hizi mbili imekuwa ni dhahiri kwamba imani ina muonekano wa nje na vilevile dalili za ndani ambazo zinahusisha utu, shauku na ustadi na 70

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 70

1/17/2017 1:10:15 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

hatimaye itatua moyoni. Kila hadithi inarejelea seti moja ya dalili.

71

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 71

1/17/2017 1:10:15 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

SEHEMU YA TANO 43

U

FUPISHO: Mfululizo huu wa makala za Viashiria vya Uchamungu unalenga juu ya manufaa ya uchamungu (takwa) katika Uislamu. Uchamungu ni mojawapo ya sifa muhimu sana ambayo mtu anaweza kuwa nayo kwani ina uhusiano na nia nyuma ya vitendo vyote na inatakiwa ili kufikia kwenye wokovu. Wakati sehemu ya kwanza na ya pili zilichunguza kwa undani sifa za uchamungu na zikagundua ufafanuzi wake na mambo ambayo huchangia katika uundaji wake, sehemu ya tatu na ya nne zilionesha tabia za mcha Mungu na kueleza kuwa waumini ni wale ambao watapata mafanikio ya kweli hapa duniani na Akhera. Sehemu hii inatafiti katika sifa za kumpenda Mwenyezi Mungu na kuwapenda watu wengine kwa ajili Yake, wajibu wetu kwa mintarafu ya jumuiya yote ya Ahlul Bayt F, na umuhimu wa ukweli, haki, na kutimiza ahadi. Katika mijadala iliyopita tuliichukulia imani kuwa mojawapo ya nguzo za uchamungu, na tukachunguza   Makala hii imeegemezwa juu ya makala ya tatu na ya nne ya mlolongo wa masomo saba ambayo yametayarishwa na mwandishi huko London, Kituo cha Kiislamu cha Uingereza mnamo Julai mwaka wa 2011. Kozi hii ilikuwa ni jaribio la kuchunguza asili ya imani, ushikadini, na maadili ambamo yameegemezwa.

43

72

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 72

1/17/2017 1:10:15 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

dalili za nje ambazo husaidia kumwelewa mtu aliye muumini. Halafu tukatathimini idadi kadhaa ya utendaji wa nje wa muumini: jinsi mtu anavyo shughulikia matumizi ya familia yake, jinsi mtu alivyo na uwezo wa kustahamili misiba, na ni kwa undani kiasi gani mtu anaelewa dini yake. Sasa tuelekeze uzingativu wetu kwa mintarafu ya dalili za ndani za imani, na sifa ambayo inaweza kujengewa hoja kuwa ni sehemu muhimu zaidi ya umuumini wa mtu lakini kwa masikitiko huwa mara nyingi inapuuzwa, yaani kiungo madhubuti kati ya mapenzi ya mtu kwa Mwenyezi Mungu na mapenzi ya mtu kwa watu wengine, yote kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na sababu za Kimungu. Kigezo chake cha msingi ni kwamba kama mtu anampenda Mungu kwa uaminifu, basi ataweza kuwapenda au kuwachukia watu wengine kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, badala ya sababu zingine zozote au sababu za ubinafsi.

Kumpenda Mwenyezi Mungu na kuwapenda wengine kwa ajili ya Mungu. Imamu Muhammad al-Jawad B amesimulia kwamba Mwenyezi Mungu aliwaambia baadhi ya Mitume:

73

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 73

1/17/2017 1:10:15 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

“Mlijizuia na dunia lakini hiyo haikuwa kwa ajili Yangu - mlifanya hivyo ili muweze kugeuzwa ili msiwe wenye kujishughulisha na maisha ya kidunia. Mlijitenga na dunia ili mpate heshima na umashuhuri. Lakini hivi umepata kumchukia au kumpenda mtu kwa ajili Yangu?”44 Muumini ni mtu ambaye anatengeneza uhusiano wake kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Mtukufu Mtume 3 amezidi kuweka wazi juu ya suala hili anaponukuu tukio kutoka kwenye maisha ya Nabii Musa B: “Mwenyezi Mungu alimuuliza Nabii Musa B: ‘Hivi umepata kutekeleza kitendo kwa ajili Yangu tu?’ Musa akajibu: ‘Nimeswali kwa ajili Yako, nimefunga saumu kwa ajili Yako, na nimetoa Zaka kwa ajili Yako!’ Mwenyezi Mungu akasema: ‘Kuhusu Swala zako huo ni uthibitisho wako mnamo Siku ya Hukumu (yaani zitakusaidi wewe), Saumu yako ni hifadhi kwa ajili yako, zaka yako ni kivuli chako na sadaka zako ni nuru…. Haya yote yalikuwa kwa ajili yako. Sasa ni kitu gani umefanya kwa ajili Yangu?’ Musa akasema:   Bihar al-Anwar, Juz. 66, uk. 238.

44

74

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 74

1/17/2017 1:10:15 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

‘Basi niambie, ni kitendo kipi ambacho ni kwa ajili Yako tu?’ Mwenyezi Mungu akajibu: ‘Hivi umepata kumpenda mtu kwa ajili Yangu?’ Baada ya kusikia hivi Musa akatambua kwamba amali iliyo bora sana miongoni mwa amali zote ni kumpenda mtu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kumchukia mtu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.”45 Katika riwaya nyingine Imamu al-Baqir B anasimulia kutoka kwa Mtukufu Mtume Muhammad 3: “Enyi watu! Kile ambacho nimekihalalisha kitabakia kuwa halali hadi Siku ya Hukumu….. Kweli mojawapo ya mambo makubwa sana ambayo humuongezea mtu kwenye imani ni kumpenda mtu mwingine aliye muumini. Wakati waumini wakipendana wao kwa wao kwa ajili ya Mungu, wanakuwa kama mwili mmoja; ambapo kama kiungo kimoja cha mwili kikipatwa na maumivu viungo vingine vyote havitatulia; vitafanya bidii kukisaidia kiungo kilichopatwa na maumivu.” Kuhusiana na suala hili Saad, mshairi mashuhuri   Mustradak al-Wasa`il, Juz. 12, uk. 220.

45

75

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 75

1/17/2017 1:10:15 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

wa Irani, anasema: “Watoto wa Adam ni viungo vya mwili mmoja, vilivyoumbwa kutoka kwenye asili moja; kiungo kimoja kikipata maumivu viungo vingine haviwezi kupata utulivu.”46 Waumini ni viungo vya mwili moja, kila kiungo huwa na wajibu wake muhimu kwa ajili ya afya na uhai wa mwili huo. Ni hapo tu viungo vyote vinaposhikamana na kufanya kazi pamoja ndipo mwili unaweza kuendelea kuishi na kuneemeka. Mtukufu Mtume Muhammad 3 wakati fulani aliwauliza masahaba wake: “Ni mpini upi wa imani wenye nguvu zaidi?” Mashaba walitoa majibu yaliyotofautiana - baadhi walisema Swala, wengine wakasema Zaka. Hatimaye walikubali kushindwa na wakamwomba Mtukufu Mtume 3 awape jibu sahihi. Yeye akatamka: “Kupenda kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kuchukia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.”47 Mara tu mtu anapojipamba na tabia hii, sifa zingine za kiungwana hufuata. Ni kawaida yetu kama binadamu kufuata kile tunachokipenda na kuepuka   Shairi hili pia linaonekana kwenye mojawapo ya kuta za Umoja wa Mataifa huko New York - Marekani. 47   Bihar al-Anwar, Juz. 66, uk. 243. 46

76

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 76

1/17/2017 1:10:15 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

kile tunachokichukia. Hivyo, kama suala la msingi la kupenda na kuchukia mambo kulingana anavyotaka Mungu likijengeka ndani ya mtu, basi mapenzi mengine yote na chuki zingine zote zitafuata mkondo. Katika Misbah al-Shari`ah 48 Imamu al-Sadiq B amenukuliwa kwamba alisema: “Mtu anayependa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ni kipenzi cha Mwenyezi Mungu. Na mtu anayependwa na wengine kwa ajili ya Mungu ni kipenzi cha Mwenyezi Mungu.”49 Mtu ambaye anaweza kuishi maisha yake katika njia ambayo watu wengine ambao ni waumini wanampenda hatimaye atapendwa na Mwenyezi Mungu. Hii ni kwa sababu watu wengine ambao ni waumini watampenda yeye kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na wanampenda yeye kwa sababu wanaona kwamba yu karibu na Mwenyezi Mungu. Halafu Imamu al-Sadiq B anamnukuu Mtukufu Mtume Muhammad 3 kwa mara nyingine kwamba alisema: “Mtu atafufuliwa pamoja na yule ambaye anampenda.” Kwa maneno mengine, kama kweli watu wanawapenda wale watu watukufu,   Hiki ni kitabu mashuhuri sana katika Kiarabu juu ya maadili na mambo ya kiroho ambacho pia kimetafsiriwa katika lugha ya Kiingereza kwa jina la The Lantern of the Path (Fanusi ya Njia). 49   Mustradak al-Wasa`il; Juz. 12, uk. 220. 48

77

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 77

1/17/2017 1:10:15 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

watafufuliwa pamoja nao. Na katika simulizi nyingine tena, Mtukufu Mtume Muhammad 3 anasema: “Watu walio bora sana hapa duniani na Akhera – mbali na Mitume - ni wale ambao wanampenda Mwenyezi Mungu na wanapendana wao kwa wao kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Upendo wa aina nyingine yoyote utakuwa na uadui mnamo Siku ya Hukumu.”50 Inapotokea mtu anampenda Mwenyezi Mungu kwa uaminifu wa kweli, pia atakipenda kile ambacho kina uhusiano na Mwenyezi Mungu. Kwa mfano wa kawaida, anapofariki mtu anayependwa, mara nyingi watu huchukua vitu fulani vya marehemu, kama vile nguo, na hutazama vitu hivi kumkumbuka marehemu. Kwa mujibu wa Mtukufu Mtume Muhammad 3 mapenzi yote ambayo hayana uhusiano na Mwenyezi Mungu yatakuwa ni uhasama Siku ya Hukumu.

Dhahiri ya Siku ya Hukumu: Qur`ani Tukufu inasema:

Mustradak al-Wasa`il: Juz. 12, uk. 220 na 227.

50

78

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 78

1/17/2017 1:10:15 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

“Siku hiyo marafiki watakuwa maadui wao kwa wao, isipokuwa wenye takua.” (43:67)

Wenye takua watabakia kuwa marafiki hata huko Akhera na hawasahauliani wao kwa wao. Lakini mapenzi ambayo yamechanganyika na matamanio na ubinafsi yatakuwa ni uhasama; kwa kweli, hili linaweza pia kuonekana hapa duniani vilevile. Imam Ali B amesema: “Jambo ambalo linapendeza sana huko peponi ni kumpenda Mwenyezi Mungu na kupenda kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.”51 Wakati akifika mbinguni ataweza kufurahia neema ambazo ataweza kuzibeba na kwenda nazo hadi mbinguni zile ambazo alizichuma katika maisha ya hapa duniani. Kama mtu akifika katika eneo la Akhera akiwa hasama na ubinafsi basi watu hao hawawezi kuwemo katika furaha kamili ya Peponi. Mtukufu Mtume Muhammad 3 amesema: “Ninaapa kwa Yule ambaye uhai wangu upo mikononi Mwake, hamtaingia peponi hadi muamini; na hamtaamini hadi hapo mtakapopendana nyinyi kwa nyinyi.”52 Mustradak al-Wasa`il; Juz. 12, uk. 221.   Mustradak al-Wasa`il; Juz. 12, uk. 222.

51  52

79

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 79

1/17/2017 1:10:15 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

Wale wapendanao wao kwa wao kwa ajili ya Mwenyezi Mungu nyuso zao zitakuwa zinag`ara hiyo Siku ya Hukumu, na watakuwa kwenye mimbari za nuru; wao hawatakuwa na hofu ambapo watu waliowazunguka watakuwa wanaogopa, na hawatahuzunika ambapo wengine watakuwa wanahuzunika. “Ehee! Mawalii wa Mwenyezi Mungu hawana khofu wala wao hawahuzuniki.”1153 (10:62) Hawa ‘vipenzi’ wa Mwenyezi Mungu ni haohao ambao wanampenda Mwenyezi Mungu na wanawapenda wengine kwa ajili Yake.

Maana Pana zaidi ya kuwapenda wengine. Imamu Ali B amesema: “Yeyote anayetamani kwamba imani yake iwe kamilifu, mapenzi yake lazima yawe kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na chuki yake, furaha yake, na kero zake vyote lazima viwe kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.”54 Wakati mtu muumini anapompenda mtu mwingine, mapenzi hayo yanapaswa yawe sio kwa ajili ya sababu yoyote ya kibinafsi kama vile uhusiano wa kifamilia au kirafiki, lakini yanapaswa kuwa kwa ajili ya daraja la mtu huyo na ukaribu wake kwa Mwenyezi   Mustradak al-Wasa`il; Juz. 12, uk. wa 225.   Mustradak al-Wasa`il; Juz. 12, uk. 228.

53 54

80

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 80

1/17/2017 1:10:15 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

Mungu. Kinadharia maana yake ni kwamba tunaweza tukaishia kumpenda mtoto mwingine zaidi ya watoto wetu wenyewe. Mfano mzuri wa hili ni yale mapenzi tunayokuwa nayo kwa watoto wa Imamu al-Husayn B, ambao waumini wanaweza kwa hakika kudai kwamba wanawapenda zaidi sana watoto hao kuliko watoto wao wenyewe kutokana na watoto wa Imamu al-Husayn kuwa na ukaribu na Mwenyezi Mungu. Hivyo, endapo mtoto mbali na mtoto wako wa kumzaa akionesha uwezekano wa ubora wa kiroho kuliko mtoto wa kumzaa mwenyewe, lakini akakosa njia ya kuweza kumfikisha kwenye ubora huo, basi muumini anatakiwa kuwa na mwelekeo wa kumsaidia mtoto huyo akue na aendelee, kwa kutumia fedha au njia zingine. Mtukufu Mtume Muhammad 3 pia amesema: “Mapenzi ya Mungu ni muhimu kwa ajili ya watu wanaopendana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kwa ajili ya watu ambao huanzisha urafiki kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kwa ajili ya watu ambao hutembeleana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na kwa ajili ya watu ambao hupeana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.”55   Mustradak al-Wasa`il; Juz. 12, uk. 225.

55

81

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 81

1/17/2017 1:10:16 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

Imamu Ali B pia anaelezea umuhimu wa watu kupendana kwa namna ifuatayo: “Wafuasi wetu ni wale ambao husaidiana kwa ajili yetu sisi, ambao hupendana kwa ajili yetu, ambao hutembeleana na kuona ni jinsi gani wanaweza kuendeleza ujumbe wetu. Ni watu hao ambao wakati wanapokasirika hawafanyi jambo lisilo la haki, na wanapofurahi hawawi wabadhirifu. Wao ni chanzo cha neema kwa wale walio karibu nao, na chanzo cha amani kwa wale wenye maingiliano nao.” 56 Shia mzuri, kufuatana na asemavyo Imamu Ali B, anaweza kupimwa kwa kile ambacho yupo tayari kufanya kwa ajili ya waumini wenzake. Zaidi ya hayo, Shia aliye bora, ni yule ambaye anapompenda mtu mwingine hatapuuza kutilia maanani makosa na dhambi za wengine, na anapomchukia mtu atatilia maanani matendo yao mema na ya kiungwana. Bali hasa ni kwamba, watatathimini na kupima kila kitu kufuatana na mtazamo wa mapenzi ya Mungu na amri Zake.  Al-Kulayn, Usul al-Kafi, Juz. 2, uk. 236 – 237.

56

82

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 82

1/17/2017 1:10:16 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

Msingi wa Uislamu. Katika hadithi moja Imamu al-Baqir B amesema: “Uislamu umewekwa juu ya msingi wa mambo matano: Swala, Zaka, Saumu, Hijja, na Uwalii (Wilayat). Na hakuna ambacho kimesisitizwa zaidi kama ulivyosisitizwa uwalii. Watu wamekubali mambo manne ya mwanzo lakini wameacha hili la mwisho.”57 Wakati Imamu al-Baqir B anapotaja wale ambao wametelekeza Wilayah huwa anarejelea makundi mawili ya watu; 1.

Wale ambao hawafuati uongozi na mamlaka ya Ahlu Bayt; mathalani, baadhi ya madhehebu ya Waislamu.

2.

Wale Waislamu ambao, wakati ambapo wao ni wafuasi wa dhahiri wa Ahlul Bayt F, hawatambui kwamba wilayah ni wajibu kwa mintarafu ya jumuiya yote ya Ahlul Bayt F.

Fikira hiyohiyo imegusiwa katika dua ya Ziyarat Ashurah ambamo inaeleza:   Al-Kafi, Juz. 2, uk. 18.

57

83

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 83

1/17/2017 1:10:16 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

“Hakika nipo katika amani na yeyote ambaye yupo katika amani na wewe na nipo katika vita na yeyote ambaye yupo vitani na wewe; mimi ni adui wa yeyote ambaye anaonesha uadui kwako na mimi ni rafiki wa yeyote anayeonesha urafiki na wewe…. “Ewe Aba Abdillah! Hakika ninatafuta ukaribu na Mwenyezi Mungu, na kwa Mtukufu Mtume 3, na kwa Imamu Ali, na kwa Bibi Fatimah, na Imamu Hasan, na kwako wewe, kupitia mapenzi yako na kupitia mapenzi ya marafiki zako.” Kama sisi ni vipenzi wa kweli wa Imamu alHusayn, basi hatutakiwi kuwa katika migogoro na yeyote miongoni mwa wafuasi wake.

Uwalii (Wilayat) dhana na utekelezaji. Ni jambo la kuvutia kuona kuwa Imamu al-Baqir B ametaja dhana ya uwalii sambamba na vitendo vinne vya utendaji. Hii ni kwa sababu wilaya sio dhana tu, bali hasa zaidi ina mazoezi madhubuti ya kiutendaji. Vivyo hivyo, tawalli (yaani kuwapenda maasumu na yote hayo yanayohusiana nao) na tabarri (yaani kuwa-

84

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 84

1/17/2017 1:10:16 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

chukia maadui wa maasumin na yote yale yanayohusiana nao) ni mambo ambayo yote yametajwa sambamba na vitendo vingine vinane vya Uislamu kama ‘matawi ya dini.’ Kwa hiyo, haitoshi kuwapenda tu Ahlul Bayt F na wafuasi wao, lakini inahitajika hatua ya ziada kwa ajili hiyo ili iweze kuonekana katika vitendo. Kama mtu anataka kufanya huduma kwa ajili ya mmoja wa Ahlul Bayt F basi ingefaa kutenda huduma hiyo kwa mmojawapo wa wafuasi wa Ahlul Bayt na jumuiya ya Ahlul Bayt F.

Sifa za muumini Sasa tuelekeze uzingativu wetu kwenye baadhi ya sifa muhimu zaidi za muumini ambazo zingemwongoza kwenye ukaribu na Mwenyezi Mungu na mafanikio katika dunia hii. Imamu Zaynul-Abidin B aliulizwa na sahaba wake Abi Malik: “Niambie kuhusu sheria zote za dini.” Imamu akajibu: “Kusema kweli, kuhukumu kwa haki, na kuchunga ahadi.” Binadamu hufanya maamuzi na kutoa hukumu wakati wote, juu ya msingi wa kila siku. Kulingana na riwaya hii wa Imamu Zaynul-Abidin, uamuzi wowote kama huo ni lazima ufanywe katika msingi wa haki, na sio kufuatana na matamanio ya ubinafsi au upendeleo 85

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 85

1/17/2017 1:10:16 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

wa mtu. Kama Mwislamu na asiyekuwa Mwislamu wana mgogoro, basi muamuzi wakati wote anatakiwa kuwa upande ulio sahihi, bila kujali imani. Sifa za ukweli na haki ni muhimu zaidi kuliko kitu kingine chochote.

“Enyi mlioamini! Kuweni wasimamizi madhubuti kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, mtoao ushahidi kwa uadilifu. Wala kuchukiana na watu kusiwapelekee kutofanya uadilifu. Fanyeni uadilifu ndiko kunakokurubisha kwenye takua. Na Mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ana habari za mnayoyafanya.� (5:8)

Katika njia hiyo hiyo, kutimiza ahadi ni sifa nyingine muhimu ya muumini. Ahadi, ziwe ama kwa kauli au kwa maandishi, na ama ziwe kwa maslahi yetu au dhidi yetu, siku zote lazima zitimizwe. Uislamu unasema kwamba kama jamii haiambatani na kanuni hii, isiwe sababu kwamba mtu muumini pia aitelekeze kanuni hii. Yeyote anayeweza kuwa nazo sifa hizi hakika atakuwa ni sehemu ya rejea kwa watu wa imani zote.

86

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 86

1/17/2017 1:10:16 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

Kitendo kilicho bora zaidi: Imamu al-Sadiq B amesimulia: “Vitendo bora kuliko vyote ni vitatu: kuwatendea wengine inavyostahili, kushirikiana na ndugu yako (katika imani) kwenye mali yako, na kumkumbuka Mwenyezi Mungu katika mazingira yoyote yale.”58 Waumini wanapotenda mambo kwa uadilifu juu ya nafsi zao, hawachukulii kwamba siku zote wapo sahihi na hawatafuti hoja dhaifu kuweza kuthibitisha mambo yao. Waumini pia ni wale ambao hutafuta fursa ya kugawana utajiri wao na wengine. Humkumbuka Mwenyezi Mungu wakati wote na katika mazingira yote, iwe katika raha au matatizo. Kumkumbuka Mwenyezi Mungu sio lazima iwe kwa matamshi ya mdomo kama vile kudhukuru jina Lake au dua za kidini; kwa usahihi zaidi, maana yake ni kukubali na kutekeleza chochote kile ambacho amehalalisha na kuacha chochote kile ambacho ameharamisha, kwa sababu kumkumbuka Mwenyezi Mungu ni kutenda kufuatana na ridhaa Yake. Tabia kama hizo ni ngumu zaidi kuzitawala kuliko hata kusali Swala za usiku (salat al-layl) kwa sababu tabia hizi zinaweza kuhitajika katika mlolongo wa mazingira magumu.  Al-Kulayni, Usul al-Kafi, Juz. 2, uk. 144.

58

87

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 87

1/17/2017 1:10:16 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

Wajibu wa akili. Mtukufu Mtume Muhammad 3 amenukuliwa akisema: “Nahodha wa vitendo bora kuliko vyote hapa duniani na Akhera ni akili. Na kila kitu kina nguzo na nguzo ya muumini ni akili yake. Kuwianisha akili yake ni ibada yake kwa Mola Wake.”59 Muumini atahakikisha kwamba vitendo vyake vinaendana na akili yake, na sio hisia tu. Mwenyezi Mungu humpa kila binadamu hujja za aina mbili: moja ya nje, yaani Mitume na Maimamu, na nyingine ya ndani, yaani akili. Umashuhuri wa akili ni sura muhimu ya madhehebu ya Shia ndani ya Uislamu. Madhehebu ya Shia yana desturi ya kujivunia ya sayansi za kiakili, ikiwa ni pamoja na masomo kama falsafa, ambapo madhebu mengine ya Kiislamu hayaipatii akili umashuhuri unaostahili. Ahlul Bayt F wamewahimiza wafuasi wao kuwa na fikira za kihekima na kimantiki, na kufanya maamuzi yao kufuatana na mahitaji ya akili. Katika al-Kafi, kuna hadithi ya kimungu (al-hadith alqudsi), ambamo, akizungumzia kuhusu akili, Mwenyezi Mungu anasema: “Ninakuamrisheni na kuwakatazeni.   Bihar al-Anwar, Juz. 1, uk. 96.

59

88

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 88

1/17/2017 1:10:16 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

Ninawalipa thawabu na kuwaadhibuni.”60 Hivyo akili ni jambo la msingi katika kurekibisha maisha ya mtu aliye muumini.

Ibada potofu. Imamu al-Sadiq B anawaonya wafuasi wake juu jinsi ya kumtambua muumini wa kweli: “Msidanganywe na Swala zao na saumu zao, kwani kwa kweli mtu anaweza kuswali na kufunga saumu mara kwa mara lakini kama asipotekeleza vitendo hivyo atajisikia vibaya. Kwa usahihi zaidi, wapimeni kwa mambo mawili: ukweli katika maneno yao na utekelezaji wa amana na ahadi zao.”61 Watu wa dini wakati mwingine huambatana na vitendo vya ibada zao kwa sababu ya mazoea tu. Mathalani, mtu anayefunga saumu mara kwa mara anaambiwa kwamba kwa sababu ya afya yake mbaya hawezi kufunga saumu, na hivyo anaweza kuhuzunika pamoja na kwamba hiyo ni amri ya Mwenyezi Mungu kwamba afya ya mtu inapewa kipaumbele kuliko kufunga. Mtu kama huyo lazima afikirie kama alifunga   Al-Kafi Juz. 1, uk. 10.   Bihar al-Anwar, Juz. 2, uk. 104.

60 61

89

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 89

1/17/2017 1:10:16 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

kweli kwa ajili ya Mwenyezi Mungu au kwa sababu ya kujiridhisha yeye mwenyewe. Mtu muumini atatekeleza vitendo vya ibada, lakini kwa sababu zilizo sahihi, yaani katika kujinyenyekeza kwa Mwenyezi Mungu na amri Zake, vyovyote zitakavyokuwa. Zaidi ya hayo, muumini atakuwa na sifa ya uaminifu katika mazingira yote na kutimiza wajibu kwa uaminifu kabisa. Kadhalika, wakati mwingine tunawaona watu wa dini ambao hutegemea hisia za ndani ya nafsi na mihemko kuliko yale ambayo Uislamu umeamuru. Wakati wanapofanya dhambi wanaweza kusema wanahisi furaha mahususi ya kiroho. Au, matahalani, wanapendelea kuswali peke yao badala ya kuswali jamaa kwani wanadai kwamba hilo linawapa wao hisia za umakinifu zaidi. Hii inaweza kuwa ni zana za Shetani. Uislamu ungewashauri wao kufuata mafundisho ya dini badala ya hisia zozote za kinafsi ambazo zinaweza kutafsiriwa vibaya kwa urahisi sana. Kuhusu umuhimu wa kukamilisha tabia kabla ya kuingia kwenye elimu yoyote ya kidini kwa undani zaidi, Amr bin Abi al-Miqdam anasimulia kutoka kwa Imamu al-Baqir B: “Jifunzeni ukweli kabla ya kujifunza hadithi yoyote.”62   Bihar al-Anwar, Juz. 2, uk. 104.

62

90

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 90

1/17/2017 1:10:16 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

Abu Kahmas anasimulia kwamba alikutana na Imamu Al-Sadiq B na akawasilisha salaam za Abdullah ibn Abi Ya`fur.63 Imamu akasema: “Amani iwe kwako na kwake pia. Wakati mwingine utakapokutana na Abdullah basi fikisha salaam zangu kwake na umwambie: “Kwa kweli Ja`far bin Muhammad anakwambia: ‘Zingatia yale ambayo aliyafanya Ali ili awe karibu zaidi na Mtukufu Mtume 3, na wewe pia ufanye hivyo. Kwani hakika Ali B alifika hatua hiyo kwa Mtukufu Mtume 3 kwa kusema kweli na kutekeleza wajibu.”64 Imamu Ali B alikuwa karibu sana na Mtukufu Mtume Muhammad 3 kupitia sifa hizi mbili. Kwa hakika, ukweli na uaminifu huathiri ibada katika kuipandisha hatua moja juu zaidi. Zaidi ya hayo, Mungu anayeabudiwa anajulikana kama Haqq (ukweli); kwa hiyo, kwa mtu kufikiria kwamba ibada yake kama ni yenye athari wakati bado anakuwa sio mwaminifu, haitaleta maana yoyote. Kwa mara nyingine Imamu alSadiq B anasema: “Usizingatie sana rukuu ndefu na sijida ndefu za mtu kwani vitendo hivi vinaweza kuwa ni   Mmojawapo wa masahaba mashuhuri wa Imam al-Sadiq  na msimuliaji muhimu wa hadithi. 64   Al-Kafi, Juz. 2, uk. 104. 63

91

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 91

1/17/2017 1:10:16 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

kutokana na mazoea tu kwani kama angeviacha angejihisi vibaya. Badala yake zingatia ukweli katika mazungumzo yake na namna utekelezaji wake wa ahadi na amana.”65 Swala ndefu za mtu sio lazima ziwe dalili ya kweli ya mtu kuwa mwema. Mtukufu Mtume 3 anaelezea zaidi kuhusu suala hili: “Je, niwaambie kuhusu sifa bora zaidi za dunia hii na Akhera? Sifa hizo ni kumsamehe mtu ambaye amekukosea, kumtembelea mtu ambaye amekata uhusiano na wewe, na kumfanyia wema mtu ambaye amekufanyia ubaya.”66 Tabia za kushangaza kama hizi hujulikana kama Makarim al-akhlaq (ni sifa zilizo tukufu sana) na Mtukufu Mtume 3 amesema kwamba ujumbe wake ulikuwa ni kukamilisha sifa kama hizo. Mtu ambaye anaweza kutambua makosa yake mwenyewe na mapungufu yake kwa kweli yupo kwenye nafasi maalumu na anapaswa kusifiwa, kwa sababu hiyo ni hatua ya kwanza katika kujirekebisha. Tunaweza kuwa na uhakika kwamba mtu ambaye   Al-Kafi, Juz. 2, uk. 105.   Al-Kafi, Juz. 2, uk. 107.

65 66

92

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 92

1/17/2017 1:10:16 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

ni mwaminifu, mnyenyekevu, anayejizuia kukasirika, anayeepuka mihemko, na mpole kwa watu ambao wamemfanyia ubaya ni mtu ambaye yupo karibu sana na Mwenyezi Mungu Mtukufu. Katika kipindi cha uhai wa Mtukufu Mtume 3 walikuwepo masahaba ambao ni wazi kabisa walikuwa vipenzi wa Mwenyezi Mungu. Mmojawapo miongoni mwa Masahaba hao ni Salman al-Farsi, ambaye aliiacha familia yake, vitu vyake, na hadhi yake kwa sababu ya kutafuta ukweli. Kwanza Salman aliingia kwenye Ukristo na halafu akasikia kwamba atakuwepo Mtume katika mwisho wa wakati katika Rasi ya Arabia. Ndipo alipoamua mwenyewe kusafiri kwenda huko kwa lengo la kumtafuta Mtume huyo, Salman alikubali kuwa Mwislamu baada ya kukutana na Mtume, na tangu hapo inaonesha alikuwa na kiwango cha juu sana cha imani kwani yeye alikuwa anatafuta ukweli, hata hivyo yeye alikuwa anahitaji uwepo wa Mtume na Qur`ani Tukufu ili kumuunganisha sawasawa inavyofaa na Mwenyezi Mungu. Vivyo hivyo, yule sahaba mashuhuri Abu Dharr, ambaye kumhusu yeye Mtukufu Mtume 3 alisema kwamba mbingu hazijapata kutoa kivuli kwa yeyote ambaye ni mwaminifu kuliko Abu Dharr.67 68 Mojawapo   Bihar al-Anwar, Juz. 10, uk. 123.   Historia inatuambia kwamba ule usiku ambamo Abu Dharr alimsaidia Mtukufu Mtume  kutoroka kutoka Makkah, alimficha Mtukufu

67 68

93

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 93

1/17/2017 1:10:16 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

ya uzuri wa wale ambao huingia katika Uislamu ni kwamba wameonesha kujali kwao na kutafuta ukweli, bila kujali malezi na makuzi yao, familia, na mazingira. Ndugu zetu waume na akina dada waliosilimu na kuwa Waislamu wamefuzu mtihani ambao wale waliozaliwa katika Uislamu wanaweza kuwa hakuupitia. Tunamuomba Mwenyezi Mungu atujaalie mafanikio katika kuzipata sifa hizi na maadili ya kibinadamu, na kutupatia msukumo wa uaminifu, toba, na mwongozo. Tunamuomba Mwenyezi Mungu atusaidie siku zote tuwe tunatafuta ukweli na halafu tujifunge kwa dhati kwenye ukweli ambao umegunduliwa. Mwisho ya sehemu ya tano.

Mtume  chini ya blanketi wakati maadui zake walikuwa wanamtafuta. Maadui wa Mtukufu Mtume  walipomkaria Abu Dharr, walimuuliza ni nani aliyekuwa chini ya blanketi, huo ulikuwa ndio uaminifu wake kwani alijibu kwamba ni Mtukufu Mtume  ndiye aliyekuwa chini ya blanketi. Maadui hawakumuamini na hawakufanya uchunguzi zaidi. 94

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 94

1/17/2017 1:10:16 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

Orodha Ya Vitabu Vilivyo ­Chapishwa Na Al-Itrah Foundation 1.

i) Qur’ani Tukufu – Pamoja na Tarjuma ya Kiswahili ii) Qur’an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Thelathini 2. Uharamisho wa Riba 3. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza 4. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili 5. Hekaya za Bahlul 6. Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) 7. Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (a.s.) 8. Hijab vazi Bora 9. Ukweli wa Shia Ithnaashari 10. Madhambi Makuu 11. Mbingu imenikirimu 12. Abdallah Ibn Saba 13. Khadijatul Kubra 14. Utumwa 15. Umakini katika Swala 16. Misingi ya Maarifa 17. Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia 18. Bilal wa Afrika 95

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 95

1/17/2017 1:10:16 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

19. Abudhar 20. Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu 21. Salman Farsi 22. Ammar Yasir 23. Qur’an na Hadithi 24. Elimu ya Nafsi 25. Yajue Madhehebu ya Shia 26. Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur’an Tukufu 27. Al-Wahda 28. Ponyo kutoka katika Qur’an 29. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii 30. Mashukio ya Akhera 31. Al Amali 32. Dua kwa Mujibu wa Ahlulbayt (a.s) 33. Udhuu kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna 34. Haki za wanawake katika Uislamu 35. Mwenyezi Mungu na sifa zake 36. Kumswalia Mtume (s) 37. Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) 38. Adhana 39. Upendo katika Ukristo na Uislamu 40. Qur’ani na Kuhifadhiwa Kwake 41. Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu 42. Kupaka juu ya khofu 43. Kukusanya Sala Mbili

96

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 96

1/17/2017 1:10:16 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

44. Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara 45. Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya 46. Kusujudu juu ya udongo 47. Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s) 48. Tarawehe 49. Malumbano baina ya Sunni na Shia 50. Kupunguza Swala safarini 51. Kufungua safarini 52. Umaasumu wa Manabii 53. Qur’an Yatoa Changamoto 54. as-Salaatu Khayrun Mina -’n Nawm 55. Uadilifu wa Masahaba 56. Dua e Kumayl 57. Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu 58. Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake 59. Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata 60. Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mtume ­Muhammad (s) 61. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza 62. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili 63. Kuzuru Makaburi 64. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza 65. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili 66. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu 67. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne 68. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano 97

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 97

1/17/2017 1:10:16 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

69. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita 70. Tujifunze Misingi Ya Dini 71. Sala ni Nguzo ya Dini 72. Mikesha Ya Peshawar 73. Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu 74. Ubora wa Imam ‘Ali na Ushia ndio njia iliyonyooka 75. Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake 76. Liqaa-u-llaah 77. Muhammad (s) Mtume wa Allah 78. Amani na Jihadi Katika Uislamu 79. Uislamu Ulienea Vipi? 80. Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) 81. Dhana ya Ndoa ya Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) 82. Urejeo (al-Raj’ah) 83. Mazingira 84. Utokezo (al - Badau) 85. Hukumu ya kujenga juu ya makaburi 86. Swala ya maiti na kumlilia maiti 87. Uislamu na Uwingi wa Dini 88. Mtoto mwema 89. Adabu za Sokoni Na Njiani 90. Johari za hekima kwa vijana 91. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza 92. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili 93. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu 98

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 98

1/17/2017 1:10:16 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

94. Tawasali (AT- TAWASSUL) 95. Imam Mahdi katika Usunni na Ushia 96. Hukumu za Mgonjwa 97. Sadaka yenye kuendelea 98. Msahafu wa Imam Ali 99. Maimamu wa Ahlul Bait – Ujumbe na Jihadi 100. Idi Al-Ghadir 101. Kusoma sura zenye Sijda ya wajibu 102. Hukumu zinazomuhusu mkuu wa kazi na Mfanyakazi 103. Huduma ya Afya katika Uislamu 104. Sunna za Nabii Muhammad (saww) 105. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza) 106. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili) 107. Shahiid Mfiadini 108. Mwanamke Na Sharia 109. Ujumbe -Sehemu ya Kwanza 110. Ujumbe - Sehemu ya Pili 111. Ujumbe - Sehemu ya Tatu 112. Ujumbe - Sehemu ya Nne 113. Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu 114. Hadithi ya Thaqalain 115. Ndoa ya Mutaa 116. Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza 117. Ukweli uliopotea sehemu ya Pili 118. Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu

99

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 99

1/17/2017 1:10:16 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

119. Ukweli uliopotea sehemu ya Nne 120. Ukweli uliopotea sehemu ya Tano 121. Mkutano wa Maulamaa wa Baghdad 122. Safari ya kuifuata Nuru 123. Fatima al-Zahra 124. Myahudi wa Kimataifa 125. Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi 126. Visa vya kweli sehemu ya Kwanza 127. Visa vya kweli sehemu ya Pili 128. Elimu ya Ghaibu ya Maimamu 129. Mwanadamu na Mustakabali wake 130. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Kwanza) 131. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Pili) 132. Khairul l’Bariyyah 133. Uislamu na mafunzo ya kimalezi 134. Vijana ni Hazina ya Uislamu 135. Adhana ni Ndoto au ni Wahyi? 136. Tabaruku 137. Saada Kamili – Kitabu cha Kiada cha Maadili 138. Vikao vya furaha 139. Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje? 140. Visa vya wachamungu 141. Falsafa ya Dini 142. Kuhuzunika na Kuomboleza 100

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 100

1/17/2017 1:10:16 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

143. Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah 144. Mjadala wa Kiitikadi 145. Kuonekana kwa Allah 146. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza) 147. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili) 148. Ndugu na Jirani 149. Ushia ndani ya Usunni 150. Maswali na Majibu 151. Mafunzo ya hukmu za ibada 152. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 1 153. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 2 154. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 3 155. Abu Huraira 156. Vipengee kadhaa katika Swala ya Jamaa na Msikiti. 157. Mazingatio kutoka katika Qur’an - Sehemu ya Kwanza 158. Mazingatio kutoka kaitka Qur’an - Sehemu ya Pili 159. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya kwanza 160. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya Pili 161. Shia na Qur’ani – Majibu na Maelezo 162. Falsafa ya Mageuzi ya Imam Husein (a.s) 163. Amali za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani 164. Elimu ya Tiba za Kiislamu - Matibabu ya Maimamu 165. Uislamu Safi 166. Majlisi za Imam Husein Majumbani 167. Je, Kufunga Mikono 101

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 101

1/17/2017 1:10:16 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

168. Uislam wa Shia 169. Amali za Makka 170. Amali za Madina 171. Asili ya Madhehebu katika Uislamu 172. Sira ya Imam Ali kuhusu Waasi 173. Ukweli uliofichika katika neno la Allah 174. Uislamu na Mifumo ya Uchumi 175. Umoja wa Kiislamu na Furaha 176. Mas’ala ya Kifiqhi 177. Jifunze kusoma Qur’ani 178. as-Sahifatul Kamilah as-Sajjadiyyah 179. Hayya ‘Alaa Khayri’l-’Amal Katika Adhana 180. Ukweli kuhusu Funga ya Siku ya Ashura 181. Dua za Miezi Mitatu Mitukufu (Rajabu, Shaabani na Ramadhani) 182. Uadilifu katika Uislamu 183. Mahdi katika Sunna 184. Maswali Ya Uchunguzi Kuhusu Uislam 185. Kazi na Bidii ni njia ya maendeleo 186. Abu Talib – Jabali Imara la Imani 187. Ujenzi na Utakaso wa Nafsi 188. Vijana na Matarajio ya Baadaye 189. Historia maana na lengo la Usalafi 190. Ushia – Hoja na Majibu 191. Mateso ya Dhuria wa Mtume (saww) 192. Maombolezo – Msiba wa Bwana wa Mashahidi (a.s.) 102

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 102

1/17/2017 1:10:16 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

193. Shahidi kwa Ajili ya Ubinadamu 194. Takwa 195. Upotoshaji Dhahiri katika (Turathi) Hazina ya Kiislamu 196. Amirul Muuminina (as) na Makhalifa 197. Tawheed Na Shirki 198. Kuvunja hoja iliyotumika kutetea Uimamu wa AbuBakr 199. Adabu za vikao na mazungumzo 200. Hija ya Kuaga 201. Uwazi baina ya Maslahi na Vikwazo 202. Fadhila za watukufu watano katika Sahih Sita 203. Mdahalo baina ya Mwanachuoni waKisunni na Kishia (Al- Muraja’aat) 204. Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (as) 205. Imam Husain ni Mfumo wa Marekebisho na Mageuzi 206. Mtazamo kuhusu msuguano wa Kimadhehebu 207. Nchi na Uraia – Haki na wajibu kwa Taifa 208. Mtazamo wa Ibn Taymiyyah juu ya Imam Ali (as) 209. Uongozi wa Kidini – Maelekezo na Utekelezaji wa Kijamii 210. Maadili ya Ashura 211. Mshumaa – Shahidi na Kifo cha Kishahidi 212. Mizani ya Hekima – Hadithi za Ahlul Bait (as) – Sehemu ya Kwanza 213. Imam Ali na Mambo ya Umma 214. Imam Ali na Mfumo wa Usawa 215. Uimamu na Tamko la Kutawazwa 216. Mfumo wa Wilaya 103

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 103

1/17/2017 1:10:16 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

217. Vipi Tutaishinda Hofu? 218. Kumswalia Mtume ni Ufunguo wa Utatuzi wa Matatizo 219. Maeneo ya Umma na Mali Zake 220. Nahju ‘L-Balagha– Majmua ya Khutba, Amri, Barua, ­Risala, Mawaidha na Semi za Amirul-Muuminin Ali bin Abu Talib (a.s.) 221. Mukhtar – Shujaa aliyelipiza kisasi dhidi ya wauaji wa Imam Husein (as) hapo Karbala 222. Mazingatio Katika Swala 223. Imam Hasan na Mfumo wa Kujenga Jamii 224. Vyakula Na Vinywaji 225. Kuelewa Rehema ya Mwenyezi Mungu 226. Imam Mahdi na Bishara ya Matumaini 227. Mtazamo Mpya - Wanawake katika Uislamu 228. Shia Na Sahaba - Majibu na Maelezo 229. Majanga Na Jukumu la Jamii 230. Shia Na Hadith - Majibu na Maelezo 231. Upotofu Ndani ya Kitabu cha Mitaala kwa Shule za Sekondari 232. Ugaidi Wa Kifikra Katika Medani Ya Kidini 233. Yafaayo kijamii 234. Uswalihina Dhahiri Na Batini Yake 235. Mkakati wa Kupambana na Ufakiri 236. Mwanamke Katika Harakati Za Mageuzi 237. Jihadi 238. Hija Katika Maneno Na Ujumbe Wa Imam Khomeini (R.A) 104

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 104

1/17/2017 1:10:16 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

239. Tiba Ya Maradhi Ya Kimaadili 240. Yusuf Mkweli 241. Taqiyya Kwa Mujibu Wa Sheria Ya KIISLAMU 242. Imam Mahdi (A.S) Imam Wa Zama Hizi Na Kiongozi Wa Dunia 243. Talaka Tatu 244. Safari Ya Kuelekea Kwa Mwenyezi Mungu 245. Hotuba Za Kiislamu Juu Ya Haki Za Binadamu 246. Mashairi Ya Kijamii 247. Ngano Ya Kwamba Qur’ani Imebadilishwa 248. Wito Kwa Waumini: “Enyi Mlioamini” 249. Imam Husain (a.s) ni Utu na Kadhia 250. Imam Husain ni Kielelezo cha Kujitoa Muhanga na Fidia 251. Imam Mahdi ni Tumaini la Mataifa 252. Kuchagua Mchumba 253. Mazungumzo ya Umoja – Ukosoaji na Usahihishaji 254. Utamaduni wa Mwamko wa Kijamii 255. Hekima za kina za Swala 256. Kanuni za Sharia za Kiislamu 257. Utamaduni kufuatana na Qur’ani na Utekelezaji wa ­Kivitendo (Sehemu ya Kwanza) 258. Kauli sahihi zaidi katika kufafanua Hadithi

105

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 105

1/17/2017 1:10:16 PM


VIASHIRIA VYA UCHAMUNGU

KOPI ZIFUATAZO ZIMETAFSIRIWA KWA LUGHA KINYARWANDA 1.

Amateka Na Aba’ Khalifa

2.

Nyuma yaho naje kuyoboka

3.

Amavu n;amavuko by;ubushiya

4.

Shiya na Hadithi

5.

Kor’ani Nziranenge

6.

Kwigisha Mu Buryo Bw’incamake Uka Salat Ikotwa

7.

Iduwa ya Kumayili

ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION KWA LUGHA YA KIFARANSA 1.

Livre Islamique

106

20_16_Viashira Vya Uchamungu_(4-75 inch x 7 inch)_17_January_2017 .indd 106

1/17/2017 1:10:16 PM


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.