Visa vya kweli 2

Page 1

VISA VYA KWELI SEHEMU YA PILI Kimeandikwa na: Sayyid Ali Akbar Sadaaqat

Kimetarjumiwa na: Dr. M. S. Kanju na Mwl. Aziz Njozi


B


ŠHaki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: 978 - 9987 - 512 - 28 - 7 Kimekusanywa na: Islamic Education Board - World Federation

Kimetarjumiwa na: Dr. M. S. Kanju na Mwl. Aziz Njozi Kimepangwa katika Kompyuta na: Ukhti Pili Rajab

Toleo la kwanza: Januari, 2014 Nakala: 1000

Kimetolewa na kuchapishwa na: Al-Itrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 / 2127555 Barua Pepe: alitrah@yahoo.com Tovuti: www.ibn-tv.com Katika mtandao: www.alitrah.info


YALIYOMO Utangulizi 21 – UCHAMUNGU (TAQWA)...............................................................8 1. Uchamungu usio sahihi...........................................................................9 2. Abudharr................................................................................................10 3. Mlevi Asiaminiwe.................................................................................11 4. Sheikh Murtaza Ansari..........................................................................12 5. Pingamizi la Aqil...................................................................................13 22 – KUMTEGEMEA MWENYEZI MUNGU....................................13 1. Mfanyabiashara aliyemtegemea Mwenyezi Mungu............................14 2. Mtukufu Mtume na kumtegemea Mwenyezi Mungu............................15 3. Maradhi ya Nabii Musa.........................................................................16 4. Hamad Ibn Habib...................................................................................17 5. Kumtegemea Mhudumu Mkuu wa kiume.............................................18 23 – UNYENYEKEVU.......................................................................... 19 1. Jibu la Imam......................................................................................... 20 2. Mu’adh Ibn Jabal................................................................................. .21 3. Jifunze Unyenyekevu kutoka kwa Njiwa.......................................... ...22 4. Sa’sah............................................................................................... .....23 5. Unyeyekevu mbele ya Hukumu............................................................24 24 - KUTAFAKARI.................................................................................25 1. Rabi’ah................................................................................................ 26 2. Kutafakari kabla ya kutenda.................................................................27 3. Aina za tafakari.....................................................................................27 4. Fikra za uongozi....................................................................................29 5. Ufalme wa Rey au kumuua Imam.........................................................30 25 – UDHALILISHAJI...........................................................................32 1. Mufadhal Ibn Umar................................................................................32 2. Mwenendo wa Mtukufu Mtume............................................................34


3. Matokeo ya kumdharau mtu..................................................................34 4. Mtoto mfupi na mwenye sura mbaya.....................................................35 5. Mlete aliye mbaya kuliko wewe!..........................................................36 26 – MAJIVUNO (KIBRI)......................................................................37 1. Abu Jahl.................................................................................................38 2. Walid Ibn Mughirah...............................................................................39 3. Tajiri mbele ya maskini..........................................................................40 4. Sulaiman ibn Abdul Malik.....................................................................41 5. Khusrow Parvez.....................................................................................42 27- UNYENYEKEVU............................................................................ 43 1. Unyenyekevu wa Salman Farsi..............................................................44 2. Bilal Muethiopia....................................................................................45 3. Unyenyekevu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)........................................45 4. Muhammad Ibn Muslim.......................................................................46 5. Isa na kuwaosha miguu wanafunzi wake.............................................47 28 – TOBA................................................................................................47 1. Aliyebuni Dini na Toba..........................................................................48 2. Mwajiriwa wa Bani Umayyah...............................................................50 3. Rejea kabla ya kifo................................................................................51 4. Abu Lubabah........................................................................................ 52 5. Buhlul, mchimba kaburi........................................................................55 29 – UJINGA............................................................................................58 1. Kamanda mjinga....................................................................................59 2. Mtoto mjinga wa Khalifa.......................................................................60 3. Mtu mwenye sura nzuri lakini mjinga...................................................61 4. Qais Ibn Asim........................................................................................62 5. Ndevu ndefu..........................................................................................63 30 – TAMAA............................................................................................65 1. Matope kutoka kaburini ni dawa ya mtu mwenye tamaa.....................66 2. Tamaa ya anasa.....................................................................................67 3. Isa na mtu mwenye tamaa.....................................................................69


4. Dhul Qarnain.........................................................................................71 5. Ash’ab ibn Jubair Madani (alikufa 154 Hijria)......................................72 31 – HUSDA.............................................................................................74 1. Rafiki wa Isa..........................................................................................75 2. Abdullah Ibn Ubayy...............................................................................76 3. Kitendo cha ajabu cha mtu mwenye husda...........................................78 4. Husda ya wanawake..............................................................................79 5. Madhara ya wivu...................................................................................81 32 – UKWELI NA UONGO...................................................................83 1. Haki ya Mwislamu aliyefariki...............................................................83 2. Mu’awiyah Ibn Yazid.............................................................................85 3. Kuukubali ukweli..................................................................................86 4. Aliyelewa abadilika na kuwa mwenye shukrani...................................87 5. Shukrani ya Abu Dharr..........................................................................88 33 – HALALI NA HARAMU.................................................................90 1. Wayahudi na chakula haramu................................................................91 2. Kwa njia za haramu...............................................................................91 3. Mtego wa Shetani..................................................................................92 4. Chakula cha Khalifa..............................................................................93 5. Aqil........................................................................................................94 34 – UVUMILIVU...................................................................................95 1. Usumbufu wa wafuga njiwa..................................................................96 2. Uvumilivu kwa matendo ya kamanda...................................................96 3. Qais Minqari..........................................................................................97 4. Imam Hasan na Msyria..........................................................................98 5. Sheikh Ja’far Kashif Al-Ghita...............................................................99 35 – STAHA..............................................................................................99 1. Musa na mabinti wa Shu’aib................................................................100 2. Staha ya macho....................................................................................190 3. Zulaikha...............................................................................................102


4. Staha ya Amirul Muuminin.................................................................103 36 – KHOFU........................................................................................ 103 1. Kijana mwenye khofu..........................................................................104 2. Lugha ya mawe isiyo na sauti..............................................................105 3. Adhabu ya mto.....................................................................................106 4. Wenye khofu........................................................................................107 5. Yahya...................................................................................................109 37 – HILA...............................................................................................110 1. Waziri mwenye Hila............................................................................111 2. Hila wakati wa ziara............................................................................113 3. Uasi wa Binti kwa baba yake...............................................................114 4. Mhindi na Imam wa Sita.....................................................................115 38 – ULIMWENGU...............................................................................119 1. Heshima na udhalili.............................................................................119 2. Ali na Hazina ya Umma.......................................................................121 3. Hadhrat Sulaiman................................................................................122 4. Mapenzi ya Talha na Zubair kwa ulimwengu.....................................124 5. Alichokitaka na kile ambacho hatimaye kilitokea...............................126 39- UONGO...........................................................................................128 1. Walid Ibn Uqbah..................................................................................129 2. Njaa na uongo......................................................................................130 3. Uongo wa mshairi................................................................................130 4. Zainab Muongo mkubwa...................................................................131 5. Uongo wa wazi wa Amir Husain.......................................................133 40 – WIZI...............................................................................................135 1. Imam na kukiri kwa mwizi..................................................................136 2. Ngamia wa Bedui................................................................................136 3. Buhlul na mwizi...................................................................................137 4. Msoma Qur’ani na kipofu ambaye ni mwizi......................................139

G


Neno la Mchapishaji Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiingereza kiitwacho, Anecdotes. Sisi tumekiita, Visa vya Kweli. Kitabu hiki kimekusanywa na Islamic Education Board - World Federation. Hiki ulichonacho mkononi mwako ni juzuu ya Pili. Kitabu cha Visa vya Kweli kimekusanya simulizi za visa vya kweli vilivyosimuliwa katika Qur’aniTukufu, hadithi na riwaya na vyanzo vingine sahihi. Kwa kweli, visa hivi hufundisha maadili mema kwa wanadamu, hivyo, kitabu hiki tunaweza kukiita kuwa ni cha maadili kwa kuwa visa vilivyoelezewa humu ni vya kimaadili. Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu ambapo kuna mmomonyoko mkubwa wa maadili. Kitabu hiki kitawafaa sana vijana walioko mashuleni na vyuoni, halikadhalika watu wa wazima. Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamua kukichapisha kwa lugha ya Kiswahili kwa malengo yaleyale ya kuwahudumia wasomaji wetu wazungumzao Kiswahili ili wapate kuongeza elimu yao ya dini na ya kijamii kwa ujumla. Tunawashukuru ndugu zetu, Dr. M. S. Kanju na Mwl. Aziz Njozi kwa kukubali jukumu hili la kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake. Mchapishaji: Al-Itrah Foundation

H


I



Visa vya Kweli sehemu ya Pili

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.

NENO LA AWALI Dhana ya maadili imekuwepo toka alipoumbwa mwanadamu. Siku za zamani kulikuwepo na tofauti za wazi kati ya maadili “mema” na maadili “mabaya.” Ingawa si mara zote watu walikuwa wakifuata maadili mema. Katika zama za sasa, tofauti kati ya maadili mema na mabaya imefifia na kwa kiasi kikubwa maadili yametibuliwa. Na matokeo yake, kuna hatari kwamba ufisadi utakuwa na nguvu zaidi kuliko maadili mema duniani kote. Hakuna kisingizio kwa Mwislamu kunasa katika hali hii mbaya na ya hatari. Kuna mwongozo ulio wazi kutoka kwa Allah kupitia Qur’ani Tukufu na Mitume (as) na Maasumina (as). Mtume Muhammad (s.a.w.w.) mwenyewe alisema: “Nimetumwa kama Mtume kwa lengo la kuyakamilisha maadili mema.” Moja ya njia bora kabisa za kuyaelewa maadili mema ni kwa kuisoma mifano halisi kutoka katika maisha ya Mitume na Maasumina (as). Vitabu vichache vimeshaandikwa juu ya hadithi za maadili mema kutoka katika ulimwengu wa Kiislamu, kimoja wapo kikiwa “Pearls of Wisdom” (Lulu za Hikma), kilichochapishwa na Islamic Education Board of World Federation, Machi mwaka 1993. Kwa kuzingatia umuhimu wa mada ya Maadili mema (Akhlaq), Bodi ya elimu ya Kiislamu ya World Federation inachapisha visa vya kweli kwa ajili ya kutafakari katika sehemu tano (5). Chanzo cha chapisho hili ni kitabu “Yaksad Mawzu wa 500 Dastani” cha Sayyid Ali Akber Sadaqaat. Tarjuma ya kutoka Kiajemi kwenda Kingereza ilifanywa na Sheikh Shahnawazi Mahdavi. Bodi ya Elimu ya Kiislamu ya World Federation ingependa kuwashukuru Sayyid Ali Akbar Sadaaqat na 2


Visa vya Kweli sehemu ya Pili Sheikh Shanawaz Mahdavi kwa jitihada zao na inawaombea kwa Allah awalipe vya kutosha. (Tunaomba) Allah aikubali kazi hii kama jitihada nyingine ya Bodi ya Elimu ya Kiislamu ya World Federation ya kueneza Uislamu. Bodi ya Elimu ya Kiislamu The World Federation of KSI Muslim Communities Shabani 1424 Oktoba 2003

3


Visa vya Kweli sehemu ya Pili

Bismillahir Rahmanir Raheem

UTANGULIZI Kuna njia nyingi kwa ajili ya mwanadamu kupata mwongozo na kuibuka kutoka kwenye giza na kuelekea kwenye nuru. Kwa ajili ya ustawi wa mwanadamu na ukamilifu wa maadili yake, Mwenyezi Mungu ameumba uthibitisho, ushahidi na dalili,1 katika idadi kubwa kiasi kwamba ziko nje ya uwezo wa kuhesabiwa wala kukokotolewa. Kwa ajili ya mwongozo wa mwanadamu alituma Mitume na dalili zilizo wazi,2 Vitabu, miujiza na ishara ili pengine watu wanaweza kuitambua njia iliyonyooka na kupata ustawi na mafanikio. Katika kipindi chote cha utume wake, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), katika suala la utakatifu wa kiroho na ukamilifu wa maadili, alikuwa ni kiigizo katika kauli na matendo, na hata alisema: “Nimetumwa (kama Mtume) kuja kuyakamilisha maadili”3 Tatizo la mwanadamu lipo katika kutozingatia kwake amali njema, kutenda kwake maovu, kupupia matamanio na utii kwa shetani. Baadhi ya watu wamejiachia (katika kufanya maovu) kiasi kwamba wanaendesha maisha yao kama wanyama. Kwa lengo la utakatifu na kuyaponya maadili ya wanadamu, kupunguza kasi na kudhibiti hulka ya asili, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alifanya kila aliloliweza na alielezea yote yaliyopaswa juu ya jambo hili. Kupata fanaka katika ulimwengu huu na ulimwengu ujao (Akhera) kunawezekana tu chini ya uangalizi wa mwalimu na wakati huo huo si kila mtu anaweza kuainisha hizo ncha mbili tofauti za mwenendo wa kimaadili 1 Qur’ani Tukufu, Sura Ibrahim – 14: 5 2 Suratul Hadiid 57:25 3 Safinah al- Bihar, Juz 1,uk 411 4


Visa vya Kweli sehemu ya Pili ili kuonyesha kwa vitendo njia ya kati na iliyo sawa. Yule mwenye Hikma isiyo na kikomo aliwaleta mitume wote na hususani Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kama “mwalimu na mkufunzi” wa maadili, ili kwa kufuata nyayo zake, watu wajitenge na maovu na wapate heshima ya Duniani na Akhera. Katika Qur’ani, kuna sura iitwayo Al-Qasas (masimulizi), ambayo yenyewe tu ni ushahidi kuwa mwanadamu anahitaji hadithi na masimulizi. Katika sehemu nyingi ndani ya Qur’ani, hadithi za mitume wafalme wa mataifa zimetajwa. Kwa kuongezea Mwenyezi Mungu amezungumzia masuala yanayohusiana na vita, amani, familia, dini, jamii na mada nyinginezo, katika muundo wa hadithi na masimulizi. Kwa kuvisoma visa hivi, watu wanaweza kuelewa na kutofautisha kati ya njia ya maendeleo na ile ya kuporomoka kwa maendeleo, na kupanda na kushuka katika kila kipengele, hususani maadili. Sura Yusuf yote imetumika kusimulia kisa cha Yusuf, Yaqub, Zulekha na nduguze. Mwanzoni mwa sura Mwenyezi Mungu anasema,

“Tuna kusimulia (Ewe Mtume) masimulizi bora kabisa kwa (kupitia) yale tuliyokufunulia katika Qur’ani hii.” Suratul Yusuf 12:3 Ambapo katika aya ya mwisho ya sura hii, anasema katika historia yao

“Kwa hakika kuna mazingatio kwa watu wenye akili” Suratul Yusuf 12: 111 Kwa hakika moja ya ustadi mkubwa kabisa wa Qur’ani ni hadithi hii ya Yusuf (as) iliyotajwa kuwa ni “simulizi bora kabisa” na mwisho (Qur’ani) 5


Visa vya Kweli sehemu ya Pili inasema: “katika hadithi hizi kuna mazingatio kwa wale wanaotaka kuadilika na kufuata njia ya watu watimilifu. Juu ya hili Amirul Muuminina (as) katika Nahjul Balaghah, anamwambia mwanawe Imam Hasan (as): “Ingawa sijafikia umri ule uliofikiwa na wa kabla yangu, nimezitazama tabia zao na nimetafakari matukio ya maisha yao. Nilitembea katika maanguko yao mpaka nikawa miongoni mwao. kwa kweli, kwa wema wa mambo yao niliyobahatika kujua, ni kama nimeishi nao mwanzo hadi mwisho. Hivyo nimeweza kubaini kilicho kichafu na kisafi na chenye manufa na chenye madhara. Nimekuchagulia bora kabisa ya mambo hayo na nimekukusanyia nukta nzuri huku nikiyaacha yale yasiyo kuwa na manufaa” Miaka kadhaa huko nyuma, nilikuwa nimeandika kitabu juu ya maadili (kwa ajili ya kutibu maovu), kwa jina la Ihyaul Qubul. Tokea wakati huo, nilikuwa nikitafakari juu ya kuandika kitabu, juu ya hadithi za maadili. Hivyo ilitokea kwamba, kwa bahati ya Mungu, fursa ilinijia pamoja na hamasa ya kufanya kazi hii. Licha ya ukosefu wa vitabu muhimu, nilitosheka na vile vilivyokuwepo na nikaanza kuandika kitabu hiki, nikiandika hadithi nne mpaka tano kwa kila mada. Kwa kweli sijakutana na kitabu chochote kilichoandikwa kwa mtindo huu. Vitabu kama Namunah-e- Ma’arif Islam na Pand-e-Taarikh vimekuwepo kwa takribani miaka 30 na nimevitumia pia (katika kuandaa mkusanyiko huu) lakini katika vitabu hivyo Aya za Qur’ani, Hadithi, Mashairi na analojia ya mkondo wa mambo vyote vimekusanywa pamoja, ambapo mimi nimetosheka kwa kutaja hadithi tu huku nikiepuka kutoa maelezo yanayohusiana na aya za Qur’ani, hadithi, mashairi na ulinganishaji, (vitu ambavyo) visingeongeza tu ukubwa wa kitabu bali pia vingeleta ugumu wa kueleweka kwa wasomaji wengi. Mkusanyiko huu ni kwa ajili ya umma kwa ujumla, watato na wakubwa pia, ambao wana elimu ya msingi 6


Visa vya Kweli sehemu ya Pili ya kusoma na kuandika. Kwa kadri nilivyoweza nimejitahidi kukwepa masuala ya kisayansi na vipengele vile vinavyohusiana na hadith ambavyo kueleweka kwake kungehitaji uangalifu mkubwa na kulazimisha kwa jumla juu ya umma. Ingawa baadhi ya visa vinawezekana visiwe na vipengele vyovyote vya uhalisi na uhakika, nilichokizingatia ni kunasihi na “kuchukua somo� la kipengele kilichomo humo, ambacho ninataraji wasomaji watukufu watafahamu na kuelewa. Kadiri suala la kuhusisha kisa na mada mahususi linavyohusika, sisemi kwamba visa hivyo vinadokezea kwenye mada moja tu au ile mahususi ambayo imetajwa hapa; bali ni visa ambavyo vinaweza kuhusishwa na mada nyingine pia, kwa nyongeza kwenye mada ambayo chini yake imetajwa hapa. Wakati nikisimulia maandishi au nikifanya tarjuma, sikujibana katika maana halisi, bali kwa utambuzi mzuri zaidi, nimeingia kwenye ufafanuzi wa maneno, kudokeza na maelezo yenye maana kidhana pia. Ili kuepuka kuingiliana kwa mada na kurefusha mjadala, nimeepuka kuleta mada zinazohusiana na zile ambazo tayari zimeshawasilishwa. Kwa mfano, Ithaar (tabia ya kufikiria wengine kuliko nafsi yako mwenyewe) imewasilishwa kama moja ya mada, lakini Infaaq (kutoa katika njia ya Allah) imeachwa. Ili kuzuia msomaji asipatwe na uchovu na uchoshi, na kwa ajili ya sababu mbali mbali, nimeacha kuwasilisha visa vya kukinaisha, kama vile vya wanafalsafa na washairi, lakini nimejitahidi kufanya mkusanyiko uwe tofauti tofauti. Kwa njia hii nataraji wasomaji watafurahia zaidi masimulizi haya. Kwa kuzingatia ukweli kwamba uaminifu lazima uzingatiwe, nimetaja kila 7


Visa vya Kweli sehemu ya Pili simulizi iliyowasilishwa hapa, imechukuliwa kutoka kwenye kitabu, juzuu gani, na ukurasa gani. Ni kwa ajili ya kupata mtiririko mzuri zaidi wa kazi kwamba nimejitahidi kusahihisha, kunakshi au kubadilisha baadhi ya maneno au sentensi za maandishi ya asili. Inatarajiwa kwamba baada ya wasomaji kuvipitia visa na simulizi hizi, watatafakari na kuchukua mazingatio ili waweze kujijengea nguvu za kwenda katika ukamilifu wa maadili, na Allah akipenda wale waliojaaliwa maadili yenye kusifika wawasimulie wengine, kwa ajili ya kuzirekebisha roho dhaifu zaidi. Sayyid Ali Akbar Sadaaqat Na dua yetu ya mwisho (ni): Sifa zote njema zinamstahiki Allah, Mola wa walimwengu Mordad, 1378 (July 1999)

21. UCHAMUNGU (TAQWA). Allah mwenye hikma amesema:

“lakini mafao bora kabisa ni mwenendo sahihi. Hivyo niogopeni, enyi wenye hikma” Suratul Baqara 2:197 Imam Ali (a.s) alisema: “Hakuna amali ndogo, ikiwa imeambatana na uchamugu.”7 Maelezo mafupi Uchamungu maalumu hupatikana kwa kujiepusha na yaliyokatazwa na mambo yenye mashaka, ambapo uchamungu wa jumla hupatikana kutokana na khofu ya adhabu na moto wa Jahanamu. 7 Al-Kafi, Juz. 2, uk. 61 8


Visa vya Kweli sehemu ya Pili Uchamungu ni sawa na maji ya mto ambayo hutiririka baina ya miti iliyomea katika kingo zake, kila mti ukinufaika nao (huo mto) kutokana na kipimo cha ulaini wake, na asili yake. Ingawa watu hunufaika na uchamungu kutokana na maarifa yao, ufahamu na kiwango cha imani, viwango vyao vya uchamungu hutofautiana katika amali na udhati. Kiuhalisia, uchamungu ni utii kamili bila ukengeukaji wowote, na ni maarifa bila ujinga wowote. Huwa ni sababu ya kukubaliwa kwa amali (njema) za mtu na humfanya yule mwenye nao (huo uchamungu), kuwa mtu maarufu na aliyeshinda wote.8 1. Uchamungu Usio Sahihi Wakati fulani, katika zama za Mtukufu Mtume (s.a.w.w), wanawake watatu walimwendea ili kulalamika juu ya waume zao. Mwanamke wa kwanza alilalamika: “Mume wangu ameacha kula nyama.” “Mume wangu ameacha kutumia mafuta mazuri.” Mwanamke wa pili alilalamika. Mwanamke wa tatu alilalamika kuwa mume wake hafanyi naye tendo la ndoa. (kwa kufanya hivi, waume hawa walikuwa na nia ya kufanya uchamungu na kujizuia). Hili lilimuudhi Mtukufu Mtume (s.a.w.w), kiasi kwamba alipokuwa akitoka nje ya nyumba yake, hakuvaa hata joho lake vizuri na hivyo lilikuwa likiburuza chini kwa nyuma yake. Akipanda juu ya mimbari mbele ya mkusanyiko wa watu, alimsifu Allah, na akasema: “Kwa nini baadhi ya masahaba zangu hawali nyama, hawatumii mafuta mazuri na hawajamiiani na wake zao? Enyi Waislamu! Jueni kwamba mimi pia ninakula nyama, natumia mafuta mazuri na ninajamiiana na wake zangu. Hii ndio mila yangu na anayejitenga na mila yangu hatokani na mimi.” Kwa kufanya hivi Mtukufu Mtume (s.a.w.w) aliuharibu msingi wa uchamungu usio sahihi na aliwashutumu watetezi wake.9 8 Tadhkiratul Haqaiq, uk. 79 9 Hikayat-ha-e-shanidad, Juz. 2, uk. 74, Al-Kafi, Juz. 5, uk. 496 9


Visa vya Kweli sehemu ya Pili 2. Abu Dharr Abu Dharr alisema: “Riziki yangu na akiba enzi za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mara zote ilikuwa ni kilo tatu za tende. Kwa muda wote nitakaoendelea kuishi, sitataka kumiliki zaidi ya kiasi hiki.” ‘At? anasema: Nilimuona Abu Dharr akisalia nguo kuu kuu. “Ewe Abu Dharr! Je huna nguo bora zaidi?” Nilimwuliza. Alinijibu, “Kama ningekuwa nayo, ungeniona nayo.” Nikasema, “Lakini punde nilikuona na nguo mbili.” Akanijibu: “Moja nilimpatia mpwa wangu aliyekuwa ni mwenye haja zaidi kuliko mimi.” “Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu! Wewe mwenyewe ni mhitaji.” Niliguta. Alinyanyua kichwa chake juu angani na kuomba, “Kwa hakika! Ewe Mola! Ninauhitaji msamaha wako.” Kisha alinigeukia na kuendelea, “Inaelekea kwamba umetokea kuuchukulia ulimwengu huu kuwa ni kitu muhimu sana na cha maana. Mbali na nguo hii unayoniona nayo sasa, ninayo nguo nyingine maalumu kwa ajili ya msikiti tu, mbuzi wanaonipatia maziwa, sanduku la mbao ninalobebea vitu vyangu na mke ambaye huniepusha na taabu za kupika ni neema gani zinaweza kuwa kubwa kuliko nilizonazo!” Baadhi ya watu walitoa pendekezo kwa Abu Dharr, “Je hutaki kujinunulia mali kama wengine walivyojifanyia?” “Ninauhitaji umwinyi na utukufu wa kazi gani?” Alijibu. “Kinywaji cha maziwa na maji kila siku na kiasi (kidogo) cha ngano kila wiki vinanitosha kabisa!”10 3. Mlevi Asiaminiwe Ismail, mtoto mkubwa kabisa wa kiume wa Imam Sadiq (a.s) alikuwa na fedha katika miliki yake. Alipojua kuwa mtu (mmoja) wa kabila la Quraishi aliyekuwa akiishi Madina alikuwa anakaribia kwenda Yemen, 10 Paighambar Wa Yaran, Juz. 1, uk. 47. Ayan Al - Shia, uk. 329-347 10


Visa vya Kweli sehemu ya Pili aliamua kumkabidhi fedha ili akamnunulie bidhaa kwa ajili ya biashara. Ismail alipoomba ushauri kwa baba yake, Imam Sadiq, (a.s), juu ya jambo hili, Imam (a.s) aliuliza: “Je mtu huyu anatumia vilevi?” “Watu wanasema hivyo, lakini tunajuaje kama wanasema ukweli?” alijibu Ismail. Imam (a.s) alimshauri, “sio jambo lenye maslahi kwako kumpatia mtu huyo fedha zako?” Lakini bado Ismail alimpatia mtu huyo fedha zake ambaye aliendelea na safari yake, na huko alizifuja fedha. Wakati wa msimu wa Hija, wote wawili, Imam Sadiq (a.s) na Ismail walikwenda kuhiji, Ismail alikuwa katika hatua ya kutufu Ka’ba Imam (a.s) alipobaini kuwa (mwanaye) alikuwa akimuomba Allah mfululizo ili abadilishe hasara zake. Akijisogeza katikati ya umati wa watu, Imam (a.s) alimfikia mwanawe na akaweka mkono wake juu ya bega lake, na kuliminya kidogo na akasema: “Mwanangu! Usiombe kitu kwa Allah kisicho na ulazima, kwani huna haki juu yake. Kwanza hukupaswa kumuamini mtu huyo. Sio, jukumu la wengine kuthibitisha makosa ya mtu.” “Watu walikuwa wakisema kuwa alikuwa akitumia vilevi lakini sikuwahi kumuona akitumia!” alisema Ismail.” Imam (a.s) alimshauri zaidi: “Yachukulie maneno ya waumini kuwa ni sahihi na usimwamini mlevi. Kuwa makini kuwapatia fedha wale ambao ni wapumbavu na wenye uelewa dhaifu kama ilivyoelezwa katika Qur’ani Tukufu.”11 Ni nani anaweza kuwa mpumbavu kuliko mlevi? Ushauri na usuluhisho wa mlevi katika masuala ya ndoa hayapaswi kukubaliwa wala mtu asimuamini juu ya mali yake kwani ataifuja. Mtu anayemwamini mlevi hana haki yoyote ya kumuomba Mwenyezi Mungu afidie hasara alizopata.12 11 Suratul Nisa 5:5 12 B? Bardun In Guneh Barkhord Konim, uk. 35. Biharul Anwar, Juz. 4, uk. 267 11


Visa vya Kweli sehemu ya Pili 4. Sheikh Murtadha Ansari Marehemu Sheikh Murtadha Ansari, akiwa pamoja na kaka yake, alisafiri kutoka Kashan kwenda Mash’had na baadaye kuwasili Tehran ambako hatimaye alifanya makazi katika madrasa ya Madershah akichangia chumba na mmoja wa wanafunzi. Siku moja Sheikh alimpa mwanafunzi fedha ili akanunue mkate kwa ajili yao wote. Mwanafunzi aliporudi, Sheikh alibaini kuwa alikuwa ameleta jemu. Pia ambayo aliiweka juu ya mkate. Akimgeukia mwanafunzi, alisema “Ulipata wapi fedha ya kununulia jemu?” “Nimekopa” alijibu mwanafunzi. Sheikh alichukua tu ile sehemu ya mkate ambayo haikuwa na jemu, akisema “Siwezi kula jemu kwani sina hakika kama nitaishi muda mrefu wa kutosha kulipa deni!” Miaka kadhaa baadaye, mwanafunzi alipokuja Najaf, alikwenda kwa Sheikh na kuuliza. “Sasa ukiwa mkuu wa Hawza Ilmiyyah na Marja’a wa ulimwengu mzima wa Kishia, niambie, ulifanya nini mpaka Mwenyezi Mungu akakupa mafanikio haya makubwa?” “Ni kwa sababu sikuwa na ujasiri wa kula hata ile sehemu ya mkate iliyokuwa chini ya halua, lakini wewe ulikuwa na ujasiri wa kula mkate pamoja na halua.” alijibu Sheikh.13 5. Pingamizi la Aqqil Wakati fulani, baada ya kuwa Khalifa, Imam Ali (a.s), alipanda kwenye mimbari na kumsifu Mwenyezi Mungu na akaiambia hadhara ile: “Naapa kwa Jina la Allah, ikiwa nitakuwa ninamiliki japo tawi la mtende, sitanyoosha mkono wangu kuelekea kwenye utajiri wenu. Ninajinyima mimi utajiri huu na ninawapeni nyinyi.” 13 Dastan-ha wa Pand-ha, Jz. 4, uk. 151, Zingadi wa Shakhsiyyat-e-Sheikh Ansari, uk. 70 12


Visa vya Kweli sehemu ya Pili Katika nukta hii, Aqqil, ndugu wa Imam (a.s) alisimama. “Naapa kwa Jina la Allah! Umeniweka mimi sawa na yule mtu mweusi kutoka Madina,” alisema. “Kaa chini! Hakuna yeyote isipokuwa wewe, ambaye hukupaswa kuzungumza katika mkusanyiko huu. Huna aina yoyote ya ubora juu ya yule mtu mweusi, kama kutangulia katika Uislamu, uchamungu na thawabu. Na haya ndiyo mambo yanayoleta ubora huko Akhera.” Imam Ali (a.s) alimtahadharisha.14

22- KUMTEGEMEA MWENYEZI MUNGU Allah, Mwenye Hikma, amesema: “Hivyo unapokuwa umeamua, basi mtegemee Allah, kwa hakika Allah huwapenda wale wanaomtegemea.”15 Imam Ali (a.s) amesema: “Kumtegemea Mwenyezi Mungu ni njia ya kuondokana na kila uovu.”16

MAELEZO MAFUPI Tawakkul (Kumtegemea Allah ni mtungi uliofungwa kwa lakiri ya Allah, na ni mtu yule tu anayemtegemea Allah, ndiye atakayeifungua lakiri ya mtungi na kula vilivyomo humo. Kiwango cha chini kabisa cha tawakkul ni ambapo mtu huwa hafanyi jitihada ya kutekeleza alichopanga kabla ya muda muafaka, na hajaribu kupata kuliko kile alichokadiriwa (na Allah). Kiini cha Tawwakul ni mtu kuyak14 Namunah-e-Ma’arif, Juz. 3, uk. 171, Al-Wafi, Juz. 3 uk. 60 15 Suratul Aali Imran 3:159 16 Biharul Anwar, Juz. 78, uk. 79 13


Visa vya Kweli sehemu ya Pili abidhisha mambo yake kwa Allah, na ikiwa mtu hajali sababisho halisi, yaani Allah, hatapata uhalisia wa Tawakkul.17 1. Mfanya biashara Aliyemtegemea Mwenyezi Mungu Katika enzi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipata kuishi mfanyabiashara, ambaye katika masuala yote, mara zote alikuwa akimtegemea Allah. Alikuwa akisafiri kutoka Syria kwenda Madina kwa ajili ya biashara na katika moja ya misafara yake, alikabiliana na jambazi ambaye alichomoa upanga wake na alikusudia kumuua. Yule mfanyabiashara alimsihi: “Ikiwa ni mali yangu ndiyo unayoitaka, njoo uichukue na mimi uniache (bila kunidhuru).” Kukuua wewe ni lazima, kwani nikikuacha huru utaondoka, utanibainisha kwa wenye mamalaka, alisema (yule) jambazi. “Ikiwa ni hivyo basi nipatie fursa hadi nitakaposali rakaa mbili.” Aliomba yule mfanyabiashara. Yule jambazi alikubali na mfanyabiashara alianza kusali. Alipomaliza kusali, alinyanyua mikono yake na kuomba: “Ewe Mola! Nimesikia kwa Mtume wako kuwa yeyote atakayekutegemea, atabakia kuwa amelindwa. Sina msaidizi katika jangwa hili na rehema yako ndio tumaini langu pekee.” Akiwa ameweka tumaini yake kwa Allah, alikuwa hata hajamaliza dua yake mpanda farasi akiwa juu ya farasi mweupe alitokea kwa mbali. Alipokaribia, alimkabili jambazi na kumuua kwa pigo moja la upanga wake. Kisha, akimgeukia mfanyabiashara, alisema: “Ewe, Mwenye kumtegemea Allah! Nimemuua adui wa Allah na amekuokoa kutokana naye (huyo jambazi).” “Wewe ni nani uliyekuja kunisaidia mimi katika hili jangwa?” aliuliza mfanyabiashara. “Mimi ni tawakkul yako, Allah alinitoa katika umbile la malaika na nilikuwa Peponi Jibril aliponiita na kusema “Fanya haraka 17 Tadhkirah al-Haqaiq, uk. 72.

14


Visa vya Kweli sehemu ya Pili kampatie msaada bwana wako na umuue adui yake, na hapa nimekuja kumuondoa adui yako.” Aliposema haya alitoweka katika upeo wa macho. Mfanyabiashara alikwenda sajida ya kumshurkuru Allah, na imani yake ikawa na nguvu zaidi juu ya mafundisho ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) juu ya tawakkul. Alipofika Madina alikwenda kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kumsimulia kilichotokea. “Kwa hakika! Tawakkul humnyanyua mtu katika kilele cha mafanikio na mtu mwenye daraja hiyo, ni sawa na daraja ya mitume, marafiki wa Allah, waongofu na mashahidi,” alisema Mtume (s.a.w.w.).18 2. Mtukufu Mtume na Tegemeo katika Allah. Wakati Abu Sufyan, mkuu wa washirikina wa Makka, alipoona jeshi shupavu la Uislamu lenye askari elfu kumi (wakati wa kutekwa kwa mji wa Makka), alijawa na hofu na mshituko. Alipokuwa akitembea pembezoni mwa vikosi vya Mtukufu Mtume (s.a.w.w) alisema kwa kunong’ona: “Natamani ningejua kwa nini Muhammad amekuwa mshindi juu yangu. Aliweza vipi kujikusanyia jeshi lenye nguvu kiasi hiki licha ya kuwa peke yake na bila msaada kutoka Makka?” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimsikia. “Tumekushinda kwa sababu ya msaada wa Allah!” Alisema huku akiweka mkono wake juu ya bega la Abu Sufyan. Katika vita vya Hunain, wakati adui kwa ghafla na bila kutarajia alipolivamia jeshi la Uislamu, mkanganyiko ulitawala miongoni mwa Waislamu. Mtukufu Mtume (s.a.w.w) alipoona hali hii ya jeshi la Waislamu aliomba msaada wa Allah kwa kuweka tumaini lake Kwake, na aliomba: “Ewe Mola! Sifa zote njema na shukrani vinakustahiki Wewe tu. Ninaweka malalamiko yangu (juu ya hali ya mambo) mbele Yako, na ni Wewe tu Ambaye Kwake msaada huombwa.” Wakati huo, Jibril aliteremka kutoka peponi na kumuambia: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Umeomba 18 Khazinatul Jawashir, uk. 679, Majalis al-Muttaqin. (cha Shahid-e-Thalith)

15


Visa vya Kweli sehemu ya Pili dua ambayo Musa (a.s) aliomba ambapo bahari aligawanyika kwa ajili yake na aliokolewa dhidi ya uovu wa Firaun.19 3. Maradhi ya Nabii Musa Wakati fulani, Nabii Musa (a.s) aliugua. Wana wa Israil walimjia na kubaini alichokuwa anaumwa, (kisha) wakamshauri: “Ukitumia dawa hii na hii utapona maradhi yako.” “Sitatafuta tiba yeyote bali nitasubiri mpaka Allah atakaponiponya,” Musa (a.s) alisema kuwaambia. Ugonjwa wake uliendelea ndipo Allah akamfunulia: “Naapa kwa utukufu na Enzi Yangu! Sitakuponya mpaka utakapotumia dawa walizokushauri.” Musa (a.s) aliwaomba Bani Israil wamtibu kwa dawa walizokuwa wamependekeza awali. Walimtibu na muda mfupi baada ya hapo, Musa (a.s) alirudia katika afya yake. Lakini tukio hili lilimuacha Musa (a.s) na hisia za malalamiko na kutokuwa na furaha, lakini Allah alimfunulia: “Ulitaka kubatilisha Hikma Yangu kwa kupitia kunitegemea kwako. Mimi! Yupo mwengine mbali ya Mimi, aliyeweka uwezo na uponyaji na manufaa mengine katika mimea na vitu mbali mbali?”20 4. Hammad ibn Habib Hammad ibn Habib Kufi anasimulia: “Mwaka mmoja niliondoka kwenda Hijja nikiwa nimeambatana na baadhi ya watu. Tulipopita tu sehemu iitwayo Zubalah, upepo mbaya sana wenye vumbi jeusi ulianza kuvuma. Nguvu yake, ilikuwa kubwa kiasi kwamba kila mmoja katika kundi alitawanyika. Nilijikuta nikiwa pekee yangu na nimepotea katika sehemu isiyo na maji wala miti. Haikuchukua muda usiku ukaingia. Nilipotizama 19 Dars-hai Az Zindagi-e-Payambar-e-Islam, Uk. 216, Biharul Anwar, Juz. 21, uk. 150 20 Jame’al-Saadat, Juz. 3, uk. 228) (Ilm-e-akhlaq-e-eisalmi, Juz. 2 uk. 290 16


Visa vya Kweli sehemu ya Pili kwa mbali macho yangu yaliona kivuli cha mti mmoja na nikaanza kujikokota kukielekea. Nilipoukaribia mti, nilishuhudia kwamba kijana, aliyevaa nguo nyeupe na akiwa amejipulizia miski, naye alikuja kwenye ule mti. “Mtu huyu lazima atakuwa ni mmoja wa mawalii wa Mwenyezi Mungu,” niliwaza. Nilijificha nikiogopa kwamba kama ningejitokeza angeondoka kwenda sehehmu nyingine. Kijana alijiandaa kwa ajili ya Sala na akasoma: Yaa man haadha kulla shay’in malakuuta na kisha akaanza Sala yake. Nilibaini kwamba kulikuwa na chemchem ya maji pale jirani. Nilichukuwa udhu na kusimama nyuma ya kijana kwa ajili ya Sala. Nilibaini kuwa katikati ya Sala, kijana alipofikia aya inayozumgumzia adhabu, alikuwa akilia, akimwaga machozi na kulalama. Baada ya Sala, kijana alianza kuondoka kutoka katika sehemu yake, huku akisoma: Yaa man qaswadahu dhwaaluuna Kwa kuhofia kuwa ningeweza kumpoteza, nilimkimbilia na kumsihi: “Ninakuweka chini ya kiapo cha Yule ambaye ameondoa uchovu kutoka kwako na kukupatia furaha ya upweke huu! Nihurumie kwani nimepotea njia yangu na pia ninataka nijipambe na sifa na tabia zako.” “Kama kweli ungekuwa umemtegemea Allah kamwe usingekuwa umepotea njia, sasa nifuate,” alijibu kijana. Aliposema haya, alikwenda katika upande mmoja wa mti na aliushika mkono wangu na kunipeleka katika sehemu moja kwa njia ya tayy al-ardhi.21 Ilinidhihirikia kuwa alfajiri ilikuwa imepambazuka. “Habari njema kwako, kwani sehemu hii ni Makka,” alisema kijana. Nilibaini kuwa sasa nilikuwa ninaweza kusikia sauti za mahukadhi ambao walikuwa wamekuja hapo kwa ajili ya kuhiji. Nilimgeukia yule kijana na 21 Kuikunja ardhi, kwenda umbali mrefu kwa muda mfupi, kimiujiza.

17


Visa vya Kweli sehemu ya Pili kuuliza: Ninakuweka chini ya kiapo cha Yule, ambaye kwamba Kwake Yeye umeweka matumaini yako Kwake kwa ajili ya siku ya Hukumu! Niambie wewe ni nani?” “Kwa vile umeniweka chini ya kiapo, nitakujulisha mimi ni nani. Mimi ni Ali ibn Husain (Zainul-Abidin)”, yule kijana alijibu.22 5. Kumtegemea Mhudumu Mkuu wa Kiume wa Nyumba. Jibril alikuja kwa Nabii Yusuf (a.s) alipokuwa gerezani na akamuuliza: “Ewe Yusuf! Ni nani alikufanya uwe na sura nzuri kuliko wanaume wote?” Yusuf akajibu, “ni Allah.” Jibril akamuuliza tena, “Ni nani aliyekufanya upendwe kuliko watoto wote machoni pa baba yako?” “Mola Wangu” Yusuf alijibu. “Ni nani aliyeuelekeza msafara kwenye kisima (ulipokuwa umetupiwa)?” “Mola Wangu,” alijibu Yusuf. “Ni nani aliyekulinda dhidi ya jiwe lililotupwa na watu wa msafara kisimani?” Akajibu “Ni Allah” “Ni nani aliyekuokoa kutoka kisimani?” “Ni Mola Wangu.” “Ni nani aliyekukinga dhidi ya udanganyifu wa wanawake?” “Mola wangu”. Jibril hatimaye akamalizia, “Allah anasema: Ni nini kilichokufanya utafute mahitaji yako kwa mwingine asiyekuwa mimi? Kwa kitendo hiki, utakaa gerezani kwa miaka saba (kwa kosa la kuweka mategemeo yako kwa mhudumu wa baa ya Mfalme na kumuomba akakuombee uhuru wao kutoka kwa Mfalme).” Kwa mujibu wa hadithi nyingine, Allah alimfunulia: “Ewe Yusuf! Ni nani aliyekuonyesha ndoto ile?” 22 Pand-e-Tarikh, j. 5, uk. 182; Biharul Anwar, Jz. 11, uk. 24.

18


Visa vya Kweli sehemu ya Pili Yusuf akajibu, “Ni Wewe, Ewe Mola wangu!” “Ni nani aliyekukinga dhidi ya vitimbi vya mke wa Mfalme wa Misri?” Allah aliuliza. “Ni Wewe ewe Mola wangu!” Allah akasema, “Sasa kwa nini uliomba msaada kutoka kwa mwingine asiyekuwa Mimi? Lau ungeweka matumaini yako Kwangu, ningekutoa kutoka katika kifungo chako, lakini sasa kwa kuwa umeweka mategemeo yako kwa mwingine lazima ukae gerezani kwa miaka saba.” Baada ya tukio hili, Yusuf aliilia sana ndani ya gereza hadi wenzake wakaudhika na ikaamuliwa kuwa atakuwa analia siku moja halafu moja nyingine anaacha.23

23. UNYENYEKEVU Allah, Mwenye Hikma, amesema: “Na tumeamrishwa kwamba tujinyenyekeze kwa Mola wa ulimwengu.”24 Imam Baqir amesema: “Mja wa Allah aliye mbora zaidi ni yule ambaye hujinyenyekesha katika kadari ya Allah Aza wa Jala.25

23 Namunah-e-Ma’arif, Juz. 3 uk. 280, Layaliul Akhbar, uk. 92

24 Suratul An-am (6) :71 25 Jame”a-Sa’adat, Juz.3. uk. 204

19


Visa vya Kweli sehemu ya Pili MAELEZO MAFUPI Sifa ya taslim26 ina daraja kubwa kuliko zile za ridhaa’ 27 na tawakkul.28 Hii ni kwa sababu mtu mwenye sifa hii huwa hana shauku ya kutafuta ufumbuzi wa matatizo yanayomtatiza na badala yake hujitenga na mafungamano yake ya ndani kwa kiasi kwamba hujikabidhi mzima mzima kwa Allah. Katika sifa ya ridha, matendo kwa ujumla huendana na hulka za kibinadamu, ambapo katika tawakkul, watu humfanya Allah kuwa ndio wakala wao, lakini hivyo sivyo ilivyo katika sifa ya taslim, wateule wa Allah hukumbwa na aina mbalimbali za matatizo kama vile mke/mume muovu, umaskini, maradhi, kunyanyaswa na watu, na kadhalika, lakini kwa vile wameshajinyenyekesha kabisa kabisa, huwa hawalalamiki wala hawahisi aina yeyote ya kutokuwa na furaha kutokana na masaibu haya. 1. Jibu la Imam Imesimuliwa kwamba wakati fulani, Imam Sadiq (a.s) aliwakirimu wageni wake kwa halua na uji ambapo nyakati nyingine aliwapatia zaituni na mikate mitupu. Kuna wakati fulani mtu mmoja alimwambia: “Kama unaendesha mambo yako kwa hikma na kutizama mbali, mara zote utaishi maisha ya aina moja na hivyo utaweza kuwakirimu wageni wako kwa namna sawa mara zote.” “Uendeshaji wa mambo yetu upo katika mikono ya Allah (nasi tumenyenyekea kikamilifu kwenye Utashi Wake). Kila anapotupatia (riziki kubwa), tunawakirimu wageni wetu na sisi wenyewe kwa wasaa, lakini kila anapopunguza riziki yetu, sisi pia hurekebisha maisha yetu kwa mlingano wa hali halisi,” alijibu Imam (a.s). 29 26 Kujisalimisha kwenye utashi wa Allah 27 Kuridhika na kufurahi juu ya kadari za Mwenyezi Mungu 28 Kumtegemea moja kwa moja kwa Allah katika kila jambo.

29 Shanidani-ha-e-Tarikh, uk. 32; Mahajjatul Baida, Jz. 3, uk.43 20


Visa vya Kweli sehemu ya Pili 2. Muadh Ibn Jabal Muadh alisilimu akiwa katika umri wa miaka kumi na nane na alishiriki katika vita vya Badr, Uhud, Khandaq na vinginevyo. Mtukufu Mtume (s.a.ww) alijenga mafungamano ya undugu baina yake na Abdullah Ibn Masu’d. Kwa asili Muadh alikuwa rahimu na alikuwa na haiba njema. Mtukufu Mtume (s.a.w.w) alimpeleka Yemen kwenda kuwa gavana na alimpatia ushauri mwingi, moja ya ushauri ukiwa huu: “Usiwe mgumu sana kwa watu, tangamana nao katika namna ambayo watavutiwa na kauli na dini yako.” Wakati wa ukhalifa wa Khalifa wa pili, vita viliibuka baina ya Waislamu na Warumi na Muadh pia alishiriki katika vita hiyo. Mnamo mwaka 18 Hijria, katika mji wa Amwas, Syria, ugonjwa wa tauni ulianza kusambaa. Abu Ubaidah, kamanda wa jeshi la Wiaslamu, alipatwa na maradhi (haya ya tauni) na alipobaini kuwa kifo chake kilikuwa hakiepukiki, alimteua Muadh kuwa mrithi wake. Askari walimuomba Muadh aombe dua ili balaa hili liishe lakini alikataa kufanya hivyo. “Hili sio balaa. Bali ni dua ya Mtume wenu (s.a.w.w); ya kifo cha wachamungu waongofu, na shahada, ambayo Allah huwapatia wachache tu kutoka miongoni mwenu,” alisema. Kisha aliomba: “Ewe Mola! Ijaalie familia ya Muadh gawio kamili katika hii rehema yako (tauni).” Muda mfupi baadaye, watu wa familia yake walipatwa na ugonjwa huo na wakafa kutokana na ugonjwa huo. Yeye pia alipohisi athari yake katika kidole chake, aliweka kidole chake mdomoni na kuking”ata, (kisha) akaseme, “Ewe Mola! Hiki ni kidogo na chenye thamani ndogo, kibariki (ili kiwe kikubwa)” 21


Visa vya Kweli sehemu ya Pili Hatimaye alikufa kwa tauni hiyo (mwaka 18 Hijria) akiwa na umri wa miaka 38 na alizikwa karibu na Jordan.30 3. Jifunze Unyenyekevu kutoka kwa Njiwa. Katika enzi za mmoja wa Mitume, alipata kuishi mwanamke aliyekuwa na mwanawe wa kiume ambaye alikuwa katika (kipindi cha) ujana na ambaye alimpenda sana. Kwa kadari ya Mwenyezi Mungu, yule mtoto alikufa akimuacha mama akiwa na huzuni kubwa na akiwa amechanganyikiwa. Alikuwa katika hali ambayo ndugu zake ilibidi waende kwa Mtume wa wakati huo na kuomba msaada wake. Alipokuja kwa (yule) mama, Mtume yule alimkuta akiwa katika hali ya huzuni na mkanganyiko na alikuwa analia. Macho yake (Mtume yule) yakaangukia katika kiota cha njiwa kilichoko jirani. Alimgeukia yule mama na kuuliza. “Ewe mwanamke! Hiki ni kiota cha njiwa?” Yule mwanamke akajibu kuwa ndio (kilikuwa ni kiota cha njiwa). “Je njiwa huzaa watoto?” aliuliza Mtume. “Ndio” “Je watoto wote huwa wanakua mpaka wanaweza kuruka?” “Hapana, huwa tunawaua wengine kwa ajili ya nyama zao”, alisema yule mwanamke. Mtume yule aliendelea, “Na licha ya hivi, njiwa hawa huwa hawavikimbii viota vyao?” “Hapana, hawahami kwenda sehemu nyingine”, alijibu (yule) mwanamke. Kisha yule Mtume akashauri, “Ewe mwanamke! Ogopa usije ukawa duni kuliko njiwa hawa mbele ya macho ya Mola wako. Njiwa hawa, licha ya .30 Paighambar wa Yaran, Uk. 264-259, Tabaqat ibn Sa’d, Juz. 3, uk. 122-124

22


Visa vya Kweli sehemu ya Pili ukweli kwamba mnawaua na kuwala watoto wao mbele ya macho yao, hawakimbii. Ambapo wewe, kama matokeo ya kupoteza mwanao mmoja tu, umeelekeza hasira yako kwa Allah, umempatia kisogo, umeonyesha hofu yote hii na kutamka mambo yasiyofaa. Aliposikia maneno haya, machozi yake yaliacha kutoka na kamwe hakuonyesha ukosefu wa subira na kutoridhika.31

4. SA’SAH Ahnaf ibn Qais anasimulia: “Kuna wakati fulani nililalamika kwa ami yangu, Sa’sah, juu ya maumivu ya tumbo. Badala ya kunihurumia, alinifokea vikali kwa kusema: “Ewe Mwanangu! Kila unapojisikia vibaya unalalamika kwa kiumbe mwingine kama wewe, kuna uwezekano wa mambo mawili tu katika jambo hili, ama mtu unayemsimulia tatizo lako ni rafiki yako na hivyo ni wazi kwamba atakuhuzunikia, au ni adui yako, ambaye atafurahia hali yako. “Usidhihirishe tatizo lako kwa mtu ambaye ni sawa na wewe na hana uwezo wa kukuondoa katika (tatizo) hilo, badala yake tafuta hifadhi na wasilisha tatizo Kwake, aliyekupatia tatizo hilo, kwani ni Yeye anayeweza kukuondolea tatizo hilo. “Ewe Mwanangu! Ni miaka arobaini tangu moja ya jicho langu lilipopoteza uwezo wake wa kuona lakini sijamweleza yeyote juu ya hili – hata mke wangu hajui kuwa mimi ni kipofu katika jicho moja.32 5. KUNYENYEKEA MBELE YA HUKUMU. Shamba la mitende la Zubayr ibn Awwam (binamu yake Mtukufu Mtume (s.a.w.w)) lilikuwa linapakana na mmoja wa Answar (mwenyeji wa 31 Namunah-e-Ma’arif, Juz. 2 uk. 761 32 Pand-e-Tarikh, Juz. 5, uk. 188, Al-Kuna wa al-Alqab, Juz. 2, uk. 13 23


Visa vya Kweli sehemu ya Pili Madina). Kuna wakati ukatokea mzozo baina yao juu ya suala la umwagiliaji wa ardhi zao. Ili kutatua mzozo wao walimwendea Mtukufu Mtume (s.a.w.w) na kuwasilisha tatizo lao kwake. Kwa kuzigatia ukweli kwamba shamba la Zubair lilikuwa karibu na sehemu ya juu ya ardhi ambapo ndipo maji yalikuwa yakitoka (ilikuwa ni desturi kwamba sehemu ya juu ilikuwa inamwagiliwa kabla ya sehemu ya chini). Mtukufu Mtume (s.a.w.w) alihukumu kwamba Zubair atakuwa akimwagilia shamba lake kwanza akifuatiwa na yule Answar. Licha ya uadilifu wa kiasili katika hukumu hii, Answar yule hakuridhika na alimlalamikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w) akisema: “Umehukumu kwa kumpendelea Zubair kwa sababu ni binamu yako.” Mtukufu Mtume (s.a.w.w) alichukizwa sana na kauli hii ya upinzani (uadui) kiasi kwamba rangi ya uso wake ilibadilika. Hapa, aya ifuatayo ikateremshwa:

“Lakini hapana! Naapa kwa Mola wako! Hawatoamini kikweli kweli mpaka watakapokufanya wewe kuwa ni hakimu katika yale waliyohitilafiana baina yao, na wasione uzito wowote katika nyoyo zao katika yale uliyoamua na wanyenyekee kwa anyenyekevu kamili. SuratunNisaa (4):65 Aya hii inaonyesha kwamba hakuna mwislamu wa kweli anayeweza kuonyesha kutoridhishwa na hukumu ya kiongozi wa serikali ya Kiislamu ya Mtukufu Mtume na kufuata maoni yake. Mtu anapaswa kunyenyekea kikamilifu mbele ya hukumu iliyotolewa.34 34 Dastan-haa wa Pand-haa, Juz. 9 uk. 102, Majma’ul Bayan, Juz. 3 uk. 69 24


Visa vya Kweli sehemu ya Pili

24. KUTAFAKARI Allah, Mwenye Hikma, amesema:

“Je hawatafakari ndani ya nafsi zao: Allah hakuumba mbingu na ardhi na yale yaliyomo baina yake isipokuwa kwa haki na katika muda maalumu?” Suratul Ruum (30):8 Imam Ali (a.s) amesema: “Kutafakari humuita mtu katika amali njema na utekelezaji wake.”35 Maelezo Mafupi Mtu kutafakari hali yake na ile ya wengine hupelekea katika wema, kufutwa kwa madhambi na kuangaziwa kwa moyo. Huvuta akili za mtu kuelekea Akhera na huongeza amali zake njema. Kutafakari ni sifa na kitendo cha ibada, na mfano wake hakuna – kama alivyosema Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) “Saa moja ya kutafakari ni bora kuliko mwaka mzima wa ibada.” Ni yule tu ambaye katika moyo wake Allah ameutizama na kuuangazia kwa nuru ya kumuelewa yeye, anayeweza kufikia daraja ya kutafakari, ambapo huanza kuuelewa ulimwengu kwa maono ya uelewa na kujua, na kamwe hawi mzembe kwa Allah.36

1. Rabi’ah Rabi’ah Ibn Rabi’ah anasimulia: Wakati fulani Mtukufu Mtume (s.a.w.w) 35 Jame’al-Sa’adat, juz. 1 uk. 166 36 Tadhkrirah al-Haqaiq, uk. 29.

25


Visa vya Kweli sehemu ya Pili aliniambia “Ewe Rabi’ah umekuwa ukinitumikia kwa miaka saba na kwa hiyo je, huwezi kuomba kitu fulani kutoka kwangu ili nikupatie?” “Ewe Mtume wa Allah! Nipatie muda ili nitafakari juu ya jambo hili,” niliomba. Siku ya pili, nilipofika mbele yake, Mtume (s.a.w.w) alisema: “Ewe Rabi’ah! Sema ulitakalo.” “Omba kwa Allah ili anifanye niingie peponi pamoja nawe,” nilisema. Aliposikia ombi hili, aliuliza, “Nani aliyekufundisha uombe hili kutoka kwangu?” “Hakuna aliyenifundisha. Niliona kwamba nikiomba mali nyingi, hatimaye zitakwisha, kama ningeomba umri mrefu na watoto wengi, hatima yake ingekuwa ni kifo, hivyo ikawa matokeo ya tafakuri hii, hatimaye nilichagua ombi hili,” nilijibu. Mtukufu Mtume (s.a.w.w) aliinimisha kichwa chake kwa muda akiwaza, baada ya hapo alinyanyua kichwa, na akasema: “Nitaomba ulitakalo kwa Allah, lakini lazima unisaidie pia (katika jambo hili) kwa kuzidisha sijda.37

2. Kutafakari kabla ya kitendo Mmoja wa masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimwambia: “Mara zote ninapata hasara katika biashara zangu. Udanganyifu na ulaghai wa wauzaji na wanunuaji huwa kama uchawi na huniacha nimedanganyika.” Mtukufu Mtume (s.a.w.w) alishauri: “Katika kila makubaliano ya biashara unayohofu kuwa unaweza kulaghaiwa, dai kutoka kwa mtu huyo unayekubaliana naye, haki ya kuweza kubatilisha makubaliano ya kibiashara ndani ya siku tatu. Hii ni ili ikiwa utapata hawara, utaweza kurejeshewa fedha zako. Kwa kuongezea, kuwa na subira na mvumilivu katika mchakato wa mabadilishano ya kibiashara. 37 Khazinatul Jawahir, uk. 345, Al-Da’wat (cha Rawandi)

26


Visa vya Kweli sehemu ya Pili “Jua kwamba tafakuri na subira ni kutokana na Allah, wakati haraka na papara hutokana na shetani. Unaweza kujifunza somo hili kutoka kwa mbwa, kwani unapomtupia mbwa kipande cha mkate huwa haanzi kukila mara moja bali hukinusa kwanza na akiona kinafaa huanza kukila, hali kadhalika unapaswa unuse kila jambo linalokuja mbele yako (yaani tafakari juu ya faida na hasara zake na usilivamie bila uchunguzi wa awali). Wewe, kwa akili na busara yako sio duni kuliko mbwa, hivyo tafakari na waza kabla ya kila tendo” 38

3. Aina za Tafakari Miqdad mmoja wa masahaba watiifu wa Imam Ali (a.s) anasema: “Nilikwenda kwa Abu Hurairah ambaye alisema kuwa alikuwa amemsikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w) akisema: “Kutafakari kwa saa moja ni bora kuliko ibada ya mwaka mmoja.” Nilikwenda kwa Ibn Abbas na nilimsikia akisema kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w) alisema kwamba “Kutafakari kwa saa moja ni bora kuliko ibada ya miaka saba.” Nilikwenda kwa sahaba mwingine na nilimsikia akisimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w) alisema: “Saa moja la kutafakari ni bora kuliko miaka sabini ya ibada.” Nilishtushwa kusikia kila mmoja akisimulia tofauti na mwingine na hivyo, nilimwendea Mtukufu Mtume (s.a.w.w) na nilimjulisha juu ya maelezo hayo ya aina tatu. Akasema: “Wote (hao) watatu wanazungumza ukweli.” Kisha, ili kuthibitisha nukta yake, aliwaita watu wote watatu. Sisi wote tulikusanyika mbele ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w). Mtukufu Mtume (s.a.w.w) alimuuliza Abu Hurairah: “Wewe unatafakari vipi?” “Kama ilivyoelezwa na Allah katika Qur’ani: ‘(watu wenye akili) 38 Riwayat-ha wa Hikayat-ha, uk. 195, Dastan-ha-e-Mathnawi, Juz. 2 uk. 125 27


Visa vya Kweli sehemu ya Pili hutafakari juu ya kuumbwa kwa mbingu na ardhi.’39 Mimi pia hutafakri juu ya maajabu ya mbingu na ardhi,” alijibu. Mtukufu Mtume (s.a.w.w) alisema, “Saa moja ya kutafakari kwako ni bora kuliko mwaka mmoja wa ibada,” kisha akamgeukia Ibn Abbas, aliuliza, “Huwa unatafakari vipi?” “Huwa natafakari juu ya kifo na misukosuko ya Siku ya Hukumu,” alijibu Ibn Abbas. Mtukufu Mtume (s.a.w.w) akasema: “Saa moja ya kutafakari kwako ni bora kuliko miaka saba ya ibada”, kisha akamuuliza sahaba mwingine “Huwa unatafakari vipi?” Sahaba alijibu, “Huwa ninatafakari juu ya moto wa Jahannam na ukali na ubaya wake.” “Saa moja ya kutafakari kwako ni bora kuliko miaka sabini ya ibada.” Mtukufufu Mtume (s.a.w.w) alisema. Kwa njia hii suala likawa limetatuliwa na kuwa wazi kwamba malipo ya kutafakari yanagetemeana na nia iliyoambatana nayo.40

4. Fikra za Uongozi Saidi anasimulia: “Mmoja wa rafiki zangu aliyekuwa anasononeshwa kutokana na kipato chake kidogo, alilalamika kwangu juu ya kipato chake kidogo na familia kubwa. “Ili kulinda hadhi yangu, ninakusudia kuhama kwenda kwenye mji mwingine ili asiwepo wa kujua juu ya ubaya wa hali yangu,” alisema. “Unajua kwamba ninajua mahesabu na ninaweza kutunza mahesabu, nimekufuata ili utumie cheo na nafasi yako kunipatia kazi serikalini ili 39 Suratul Aali Imran (3) : 191

40 Dastan-ha Wa Pand- ha, Jz. 5, uk. 87; Tafsir Ruhul Bayan, Juz. 8, uk 440 28


Visa vya Kweli sehemu ya Pili niendeshe maisha yangu yaliyobaki kwa utulivu wa akili na nitakushukuru kwa jitihada zako!” Nikamwambia, “Kuendesha mahesabu ya mfalme kuna mambo mawili, kwa upande mmoja kunabeba matumaini ambapo kwa upande mwingine ni kazi inayopaswa kuogopwa. Usijiweke katika hali ya hatari. Kwa ajili ya matumaini ambayo kazi inayo.” “Kwa kuzingatia hali yangu, ushauri wako sio sawa, kwa kuongezea hujalijibu ombi langu kwa usahihi,” alisema rafiki. “Kwa hakika una uchamungu, maarifa na uaminifu lakini (pia tambua kwamba) watu wenye husda na wanaotafuta makosa huwa wamekaa wakikusubiri. Ni kwa maslahi yako kwamba uendeshe maisha yako kwa kuridhika na uachane na wazo la cheo cha juu”, nilimfafanulia. Rafiki yangu aliudhika aliposikia haya na alisema “Hii ni aina gani ya hoja na fikra? Ni wakati wa matatizo ambapo marafiki wanapaswa kujitokeza kusaidia, kwani wakati wa neema hata maadui hujifanya kuwa marafiki.” Nilipoona fadhaa yake juu ya ushauri wangu, nilimpeleka kwa waziri wa hazina niliyekuwa ninafahamiana naye. Nilimwelezea juu ya masaibu ya rafiki yangu na waziri alimpatia jukumu la kazi ndogo ndogo. Kwa kadri muda ulivyokwenda, maafisa waliona kwamba ni mchapakazi na ana tabia njema na hivyo walimpandisha cheo. Baada ya muda mrefu, nilisafiri kwenda Makka nikiwa na baadhi ya marafiki zangu. Nilipokuwa nikirejea, sio mbali sana kutoka katika mji wangu, nilikutana na rafiki yangu aliyeonekana kuwa katika hali ya masononeko. Alikuja kwangu akioneka mwenye huzuni.” “Kwa nini upo katika hali hiyo,?” nilimuuliza! “Kama ulivyokuwa umetabiri, kundi la watu lilinifanyia husda na likanishutumu kwa uhaini” alijibu. “Mfalme bila kufanya uchunguzi wowote, alinitupa gerezani na mpaka habari za kundi kwa mahukadhi zilipofika mjini, ambapo niliachi29


Visa vya Kweli sehemu ya Pili wa huru. Mfalme alikwenda mpaka kwenye hatua ya kupokonya urithi niliokuwa nimeupokea kutoka kwa baba yangu” Saidi anaendelea: Nikamwambia; “Nilikushauri hapo awali kwamba kufanya kazi na wafalme ni sawa na safari ya baharini ina manufaa lakini wakati huo huo ni hatari – ama unaweza kupata hazina au ukaishia kwenye maangamizi, lakini ulikataa kunisikiliza.”41 5. Ufalme wa Rey au kumuua Imam Yazid alimuagiza gavana wake, Ubaidullah Ibn Ziyad, kwamba ikiwa Husain (a.s) atakataa kutoa kiapo cha utii, atapaswa kupigana na Imam huyo (a.s). Kabla ya tukio la Karbala, Ubaidullah Ibn Ziyad alikuwa amemteua Umar Ibn Sa’d kama gavana wa jimbo la Rey, lakini kabla ya kwenda huko, Ubaidullah Ibn Ziyad alimtumia barua iliyokuwa na maelekezo yafuatayo: “Husain (a.s) ameshawasili Iraq. Kwanza nenda Iraq, pigana naye, muue na kisha nenda Rey.” Umar Ibn Sa’d alimwendea Ubaidullah na akaomba: “Ewe Amir! Niondolee jukumu hili?” “Nitakuondolea jukumu hili lakini pia nitakuondolea ugavana wa Rey.” Ubaidullah alijibu. Umar Ibn Sa’d alijikuta akisita kati ya kupigana na Imam (a.s) na kutawala himaya kubwa ya Rey. Alimuomba Ubaidullah ampe usiku mmoja ili akatafakari juu ya jambo (hilo). Ubaidullah alikubali na Umar Ibn Sa’d alikesha usiku kucha akitafakari juu ya jambo (hilo) hadi hatimaye alipochagua himaya ya Rey, ambayo ilikuwa mbele yake wakati huo, lakini alipuuzia Jahannam na Pepo, ambavyo vilikuwa katika ulimwengu ujao. Aliamua kupigana dhidi ya Imam (a.s). 41 Hikayat-ha-e Gulistan, uk. 65 30


Visa vya Kweli sehemu ya Pili Asubuhi yake alikwenda kwa Ubaidullah na kuelezea utayari wake wa kukubali jukumu la kupigana na Imam Husein (a.s). Ubaidullah aliweka jeshi kubwa chini yake ili aende Karbala kwa ajili ya lengo hilo. Imam Husein (a.s) aliingia Karbala tarehe mbili ya mwezi wa Muharram ambapo Umar Ibn Sa’d, akiwa kama kamanda mkuu wa jeshi lake, akiwa pamoja na askari shupavu elfu nne, aliwasili hapo tarehe tatu. Alimteua Shimr kuwa mkuu wa jeshi lake na tarehe 10 ya Muharram alifikia hatua ya kuamuru kuuliwa kwa Imam Husein (a.s) na watu 72 miongoni mwa watoto na sahaba zake kwa lengo tu la kuupata ugavana wa Rey.42

25. UDHALILISHAJI Allah, Mwenye Hikma amesema: “Enyi mlioamini! Kundi moja la watu lisilicheke kundi jingine…..”43 Mtukufu Mtume (s.a.w.w) amesema: “Mtu akimdhalilisha muumini, masikini au vinginevyo, Allah mara zote atamchukia na kumdhalilisha.44 Maelezo Mafupi Mambo kama majivuno, roho mbaya, wivu na yanayofanana na haya huwafanya baadhi ya watu kuwafikiria wengine ambao ama hawana elimu au hawana nguvu na ambao wamelazimika kufanya kazi dhalili na duni kwa dharau na fedheha. 42 Muntahal A’mal, Juz. 1 uk. 333. 43 Suratul Hujurat; 49: 11 44 Jame”al Sa’adat, Juz, 2, uk. 215. 31


Visa vya Kweli sehemu ya Pili Kuadhiri katika muundo wowote kumekatazwa, zaidi ya haya, ikiwa mtu aliyedhalilishwa atahisi fedheha au kuumia, hii litaelekea kumfikisha mtu katika matendo hewa ambayo yatakuja kudhihiri vibaya katika heshima na haiba ya mtenda kosa. Hivyo ni vizuri kuwaheshimu walio wanyonge kabisa kati ya viumbe wa Allah ili sisi pia tuzungukwe na rehema na huruma yake. 1. Mufadhal Ibn Umar Wakati fulani barua iliyosainiwa na wazee wa Kishia, ililetwa kwa Imam Sadiq (a.s) na wachache kati ya wale waliyoisaini. Barua ililalamika juu ya urafiki kati ya Mufaddhal Ibn Umar, mwakilishi wa Imam katika (mji) wa Kufa, na baadhi ya wafuga njiwa ambao kwa muonekano hawakuwa na tabia njema. Baada ya kuisoma barua, Imam (a.s) aliandika na kutuma barua kwa Mufaddhal kwa kupitia watu wale waliokuwa wamepeleka malalamiko kwake. Kwa bahati, barua ya Imam ilimfikia Muffadhal wakati baadhi ya wale waliosaini (ile) barua ya malalamiko wakiwemo katika nyumba yake. Aliifungua barua mbele yao, akaisoma na kisha akawakabidhi. Wale waliosaini barua ya malalamiko walipoisoma, walikuta kwamba ilikuwa na maelekezo kutoka kwa Imam (a.s) kwenda kwa Muffadhal, yakitaka akusanye kiasi kikubwa cha fedha. Barua haikutaja hata kidogo suala la urafiki kati ya Mufaddhal na wafuga njiwa. Kwa vile jambo lilihusu uchangaji wa fedha, wageni wa Mufaddhal waliinamisha vichwa chini na wakasema kwamba walihitaji muda ili wawaze juu ya hilo. Waliomba wasamehewe kutoa mchango wowote wa fedha. Muffadhal, mtu mwenye akili kiasi kile, aliwaomba wakae wasubiri chakula na aliwazuia kuondoka katika nyumba yake. Wakati huo, aliwatumia ujumbe wafuga njiwa akiwaomba waje nyumbani kwake. Walipowasili, aliwasomea barua ya Imam mbele ya lile kundi (la watu). Bila kupoteza 32


Visa vya Kweli sehemu ya Pili muda wowote, wafuga njiwa waliondoka, wakati kundi la awali likiendelea kula chakula, walirudi, wakakabidhi kiasi kikubwa cha fedha kwa Mufadhal na wakaondoka. Katika nukta hii Mufadhal aliwageukia walalamikaji na kusema: “Licha ya ukweli kwamba vijana hawa wanasaidia dini inapohitajika na kwamba kuna uwezekano mkubwa kwamba wanaweza kuifuata njia iliyonyooka, mnataka kwamba nisiwakirimu na nisitangamane nao? Mnafikiri Allah ana shida na sala zenu na funga zenu ambazo mnajivunia, lakini pindi likija suala la pesa, mnatafuta visingizio na mnakataa kuitikia wito wa Imam (a.s)? Wazee waliokuwa wanauona urafiki wa Mufaddhal na wale vijana kwa dharau, waliachwa wakiwa wameaibika na bila neno la kusema walipokuwa wakiondoka kwenye nyumba yake.45 2. Mwenendo wa Mtukufu Mtume. Mtukufu Mtume (s.a.w.w) na watu wengine wachache walikuwa wakila chakula alipoingia mtu aliyekuwa anaumwa tetekuanga kwenye mkusanyiko huo. Ugonjwa wake ulikuwa mkali kiasi kwamba majipu yalikuwa yameoza kwa wingi wa bakteria. Kila sehemu mgonjwa huyu alipotaka kukaa yule wa jirani yake alionyesha kuchukizwa kwa kusimama na kuondoka pale. Mtume (s.a.w.w) alipoona hivi, alimuita yule mtu akakaa pembeni yake na alioyesha upole mkubwa kwake.

**

**

**

Katika tukio jingine, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), pamoja na masahaba wengine wachache, walikuwa wakijishughulisha na kula chakula wakati mkoma alipowasili katika mkusanyiko huo. Watu waliokuwepo walionyesha kuchukia kwao kutokana na kuwasili kwake lakini Mtukufu Mtume 45 Ba Mardum katika Guneh Barkhord Konim, uk. 78; Manhajul Maqal cha Astarabadi uk. 343. 33


Visa vya Kweli sehemu ya Pili (s.a.w.w) alimuomba akae karibu yake na amkaribishe ale chakula. Mtu kutoka katika (kabila la) Quraish, aliyekuwa ameonyesha chuki yake alikumbwa na ugonjwa huu kabla ya kukutana na kifo chake.46 3. Matokeo ya kumdharau mtu. Alikuwepo mtu katika Bani Israil aliyekuwa muovu na asiye na maadili kiasi kwamba hatimaye ilibidi wamfukuze kutoka miongoni mwao. Wakati fulani alipokuwa anatangatanga, alikutana na mchamungu ambaye juu ya kichwa chake kulikuwa na njiwa akimpatia kivuli (hivyo kumkinga dhidi ya jua). Alijisemea: “Mimi ni mtu niliyefukuzwa lakini mtu huyu ni mchamungu, nikikaa karibu yake inawezekana kwamba kutokana na uchamungu wake, Allah anaweza akanirehemu mimi pia.” Akiwa na hili akilini, alimfuata (yule) mchamungu na alikaa chini pembeni yake. Alipomuona mtu aliyefukuzwa akikaa pembeni yake, (yule) mchamungu alijiwazia: “Mimi ni mchamungu wa kabila hili wakati yeye ni muovu duni, aliyefukuzwa na aliyedharauliwa, vipi anaweza kukaa chini karibu yangu?” Akigeuka kichwa chake pembeni, yule mchamugu alimuamuru yule mtu aondoke. Alipotamka tu maneno haya, Allah alimfunulia Mtume wa wakati ule: “Nenda kwa wale watu wawili kawaambie waanze amali zao upya kwani nimesamehe madhambi yote ya yule mtu asiye na maadili na nimefuta amali zote njema za mchamungu”, (kwa kuonyesha kibri na kumdharau mtu mwingine).47 46 Ilmi-e-Akhlaq-e-Islam, Juz. 1 uk. 435, Jame al-Sa’adat, Juz. 1 uk. 357. 47 Shanidani-ha-e-Tarikh, uk. 373, Mahajjatul baida, Juz. 6, kuk. 239. 34


Visa vya Kweli sehemu ya Pili 4. Mtoto mfupi na mwenye sura mbaya Saidi anasimulia: “Mfalme alikuwa na watoto wengi wa kiume, mmoja wao akiwa mfupi, mwembamba na mwenye sura mbaya. Mfalme alikuwa akimtazama yule mtoto mfupi kwa dharau na hivyo kumdhalilisha. Mtoto akiwa ni mwenye akili aligundua kwa nini baba yake alikuwa akimdharau na alimwambia: “Ewe baba! Mtu mfupi lakini mwenye busara ni bora kuliko mrefu mjinga. Yule ambaye ni mrefu zaidi sio lazima awe mzuri zaidi na bora, kondoo ni msafi, lakini tembo, kama mzoga mara zote ana harufu mbaya.” Maneno ya mtoto yalimfanya Mfalme acheke na wazee wa jumba la kifalme, waliyakubali aliyosema, lakini ndugu zake waliudhika. Ilitokea, katika siku hizo kwamba majeshi ya adui yaliuvamia ufalme na mtu wa kwanza kutoka katika jeshi la Mfalme, kupambana kishujaa alikuwa ni yule mtoto wa Mfalme mfupi na mwenye sura mbaya kwa kuonyesha ujasiri mkubwa, aliwadondosha wakuu wachache kati ya wanajeshi wa adui na kisha akarudi kwa baba yake na kutoa heshima, akisema: “Siku ya vita farasi dhaifu huwa na manufaa.” Licha ya ukweli kwamba kundi la askari wake lilikuwa limekimbia, mtoto alirudi kwenye uwanja wa vita. “Enyi wanaume! Jitahidini au sivyo vaeni nguo za wanawake” alipiga kelele kwa dhihaka chungu. Dhihaka hii ilitia uhai mpya katika jeshi ambao walipigana kwa nguvu mpya hadi hatimaye walipolishinda jeshi la adui na wakawa washindi. Mfalme alimbusu mwanae uso mzima na alimtaja kuwa ndiye mrithi wake, kuanzia wakati huo alikuwa akimtizama mwanae kwa heshima na staha. Matukio haya yaliwafanya ndugu zake wamuonee husda kiasi kwamba walimuwekea sumu kwenye chakula ili waondokane naye. Kwa bahati dada yake aliona kilichokuwa kinatokea kupitia kwenye mlango mdogo na alimtumia ishara ya onyo kaka yake kwa kufunga mlango kwa kelele. Yule kaka mwenye akili alikitilia mashaka chakula na alijiepusha kukila. 35


Visa vya Kweli sehemu ya Pili “Haiwezekani watu wenye ujuzi wafe wakati wasio na ujuzi wanaendelea kuishi na kuchukua nafasi yao” alisema. Mfalme alipojulishwa juu ya tukio (hili) aliwaonya vikali (wale) ndugu wengine na aliwapeleka katika sehemu ya mbali kabisa ya ufalme.48 5. Mtangulize Aliye duni Kuliko Wewe Allah alimfunulia Nabii Musa (a.s): “Siku nyingine utakayokuja kuzungumza na mimi, umlete aliye duni kuliko wewe.” Musa (a.s) aliondoka, kwenda kumtafuta mtu huyo lakini alishindwa kumpata kwa sababu kila mtu aliyekutana naye, hakuwa na ujasiri wa kufikiri kuwa yeye ni bora kuliko huyo mtu. Kisha aliamua kuelekeza jitihada zake katika kumtafuta huyu miongoni mwa wanyama, macho yake yaliangukia kwa mbwa mgonjwa. Aliamua kumchukua (huyo Mbwa). Alifunga kamba kuzunguka shingo ya mbwa na akaanza kumvuta lakini baada ya muda mfupi alijutia kitendo chake na kumuachia huru (yule) mbwa. Alirudi kuongea na Allah akiwa na mikono mitupu. “Kwa nini hukumleta mtu yeyote, kama nilivyokuamuru?” ilikuja sauti ya Allah. Musa (a.s) akaomba: “Ewe Mola! Nilishindwa kumpata yeyote aliye duni kuliko mimi.” Jibu lilitoka kwa Allah: “(Naapa) kwa nguvu Zangu na utukufu Wangu! Lau ungemleta yeyote, kwa kumuona kuwa ni duni kuliko wewe, kwa hakika ningelilifuta jina lako kutoka kwenye orodha ya Mitume (na ningekuondolea cheo cha utume)”49

26. MAJIVUNO (KIBURI) Allah, Mwenye Hikma, amesema: 48 Hikayat-ha-e-gulistan, uk. 43 49 Namunah-e-Ma’arif, Juz. 2, uk. 676, Layaliul Akhbar, uk. 197. 36


Visa vya Kweli sehemu ya Pili

“Wale wasioamini katika akhera, mioyo yao inakataa kujua, na wana jivuna” Suratul Nahl; 16 : 22. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Yule ambaye moyo wake una kiburi hata kama ni kama kipimo cha mbegu ya haradali, hataingia peponi.”50

Maelezo mafupi: Mtu mwenye majivuno na anayejisikia hujiona yeye kuwa ni bora kuliko wengine na kwa kutumia fikra tupu na za kujibambikia katika akili yake, hufuata mwenendo wa shetani ambaye alisema: “Nimeumbwa kwa moto wakati Adam ameumbwa kwa udongo, na moto una ubora kuliko udongo.” Dhambi ya kwanza kufanywa katika ulimwengu wa maumbile ilikuwa ni kiburi kwa upande wa shetani. Hivyo, kwa vile huu ni uovu, hapawezi pakawa na shaka au nadharia ya kushuku. Watu wenye kiburi na wanaojivuna huwadharau wengine na hutaka wengine wawasalimie na waonyeshe heshima na unyenyekevu kwao, mara zote wakiendekeza hali ya ubora na utukufu wao katika akili zao. Tofauti kati ya Ujb na Takabbur ni kwamba yule mwenye maradhi ya Ujb huwa anajiwazia yeye tu, ambapo yule mwenye maradhi ya takabbur huwa anajiona kuwa yeye ni bora kuliko wengine na ni kwa sababu hii kwamba maradhi yake (ya kiroho) ni makubwa kuliko ya yule mwenye Ujb.

1. Abu Jahl Abdullah Ibn Mas’ud, sahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w) alikuwa ni mtu wa kwanza kusoma Qur’ani hadharani mbele ya mkusanyiko. 50 Jami’al-Sa’adat, Juz. 1, uk. 346. 37


Visa vya Kweli sehemu ya Pili Alishiriki katika vita vyote vya Mtukufu Mtume (s.a.w.w), lakini alikuwa mfupi kiasi kwamba alikuwa hata akisimama miongoni mwa watu waliokaa, alikuwa hawezi kuwazidi! Ilikuwa ni kwa sababu hii kwamba katika vita vya Badr, alimuomba Mtukufu Mtume (s.a.w.w): “Sina nguvu za kupigana katika vita, unaweza kunipangia kazi (nyingine) ambayo inaweza kunipatia thawabu sawa na za wale wanaopigana?” “Tazama miongoni mwa makafiri wanaokufa na ukiona yeyote ambaye bado yuko hai, muue,” Mtume (s.a.w.w) alijibu. Abdullah anasimulia: “Nilivyokuwa nikitembea miongoni mwa watu waliokuwa wanaonekana kuwa wamekufa, nilimkuta Abu Jahl, adui mkubwa wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w). Bado alikuwa hai. “Ninamshukuru Allah kwamba amekudhalilisha,” nilisema huku nikikaa kwenye kifua chake. Abu Jahl alifungua macho yake na akakoroma: “Ole wako! Ni nani aliyeshinda?” “Ushindi ni wa Allah na Mtume wake, na ni kwa sababu hii kwamba nitakuua,” nilijibu huku nikiweka mguu wangu kwenye shingo yake. Kwa kiburi kikubwa, alilia: “Ewe kichungaji kiduchu! Umeweka mguu wako katika sehemu tukufu kabisa. Elewa kwamba hakuna kitu kinachouma zaidi kama kuuliwa na mbilikimo kama wewe. Oh! Kwa nini sikuuliwa na mmoja wa watoto wa Abdul Muttalib?” Nilikikata kichwa chake na nikaenda kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) “Biashara njema kwako, ewe Mtume wa Allah! Hiki ni kichwa cha Abu Jahl.”51 “Abu Jahl alikuwa muovu zaidi na mbaya mno kuliko Firauni wa wakati wa Musa (a.s). Firauni alipoyakinisha kuwa anaangamia, alimwamini Allah, wakati Abu Jahl alipoyakinisha juu ya kuangamia kwake, aliwaitia Lat na Uzza waje kumsaidia,” Mtume alisema baadaye.52 51 Paighambar wa Yaran, Juz. 4, uk. 206, Tabaqat Ibn Sa’d, Juz. 3, uk. 106 52 Safinatul Bihar, Juz. 1, uk.200 38


Visa vya Kweli sehemu ya Pili 2. Walid Ibn Mughairah Miaka mitatu tangu kuteuliwa kuwa Mtume na akiwa na watu wachache tu walioukabli Uislamu, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alifunuliwa: “Tangaza wazi wazi utume wako na usijali dhihaka na shari za washirikina, kwani tutakulinda na maovu yao.” Mmoja wa maadui alikuwa Waalid Ibn Mughairah. Wakati fulani Jibril, malaika mkuu alikuwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w) wakati Walid alipopita. Alipomuona, Jibril alimuuliza Mtukufu Mtume (s.w.w.w), “Huyu ni Walid Ibn Mughairah, je ni miongoni mwa wale wanokukejeli?” Mtukufu Mtume alipojibu kwa kukubali, Jibril alionyeshea kwenye unyayo wa Walid. Walid aliendelea kutembea mpaka alipofika sehemu ambapo mtu kutoka katika kabila la Khuza’ah alikuwa ananoa mishale. Walid alikanyaga juu ya vipande vikali na vilivyokuwa chini, na baadhi yake vilipenya ndani ya kisigino cha mguu wake. Kisigino chake kilichubuliwa vibaya huku damu ikianza kutoka. Kiburi cha Walid kilimzuia kuinama chini na kuchomoa vipande vile vya chuma kutoka kwenye kisigino chake. Alipofika nyumbani kwake alijitupa kwenye kiti na akalala, wakati binti yake akiwa amelala kwenye sakafu kando ya kiti. Wakati huo, damu iliendelea kutoka kwa nguvu kutoka kwenye kidonda cha Walid mpaka ikalifikia godoro la binti yake ambaye aliamka kutoka usingizini. Alimuuliza mtumwa wa kike kwa nini alikuwa hajafunga mfuniko wa ngozi ya maji. Walid akaeleza, “Haya sio maji kutoka katika mfuko wa ngozi wa maji. Ni damu kutoka kwa baba yako”. Kisha alitamka wosia wake wa mwisho na akauaga ulimwengu huu – kwenda Jahannam.53 3. Tajiri karibu ya Maskini. Tajiri akiwa amevaa nguo safi na za kifahari aliwasili mbele ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w) na akakaa chini mbele yake. Muda mfupi baadaye mtu maskini akiwa amevaa nguo kuu kuu na zilizochanika chanika alikuja na 53 Muntahal A’amal, Juz. 1. uk. 36 39


Visa vya Kweli sehemu ya Pili kukaa karibu na mtu tajiri, ambaye alizikusanya nguo zake nzuri kutoka karibu na mtu maskini na akazisogeza kwake. Baada ya kuona hivi, Mtukufu Mtume (s.a.w.w) alimwambia mtu tajiri. “Je uliogopa kwamba mtu maskini karibu yako anaweza kuzichafua nguo zako?” “Hapana,” alijibu yule mtu. “Sasa Kwa nini ulionyesha tabia hiyo?” aliuliza Mtukufu Mtume (s.a.w.w) “Ninaye mwenzi (nafsi) ambaye huvifanya vitendo vizuri vionekane viovu kwangu na kinyume chake. Ewe Mjumbe wa Allah! Kuwa kama adhabu kwa hiki kitendo changu hiki kibaya, ninamzawadia nusu ya mali yangu (huyu) mtu maskini.” Akimgeukia yule mtu maskini, Mtukufu Mtume (s.a.w.w) aliuliza, “Je unaikubali zawadi hiyo?” “Hapana, ewe Mtume wa Allah,” alisema yule maskini. Yule tajiri alipotaka kujua sababu, maskini alieleza: “Ninaogopa mimi pia ninaweza kupata kibri na majivuno (kama) haya yanayokusibu.”54 4. Sulaiman Ibn Abdul-Malik Ijumaa moja, Sulaiman Ibn Abdul Malik, (mmoja wa makhalifa wa Bani Marwan) alivaa nguo mpya, akajipulizia mafuta mazuri na kuamuru kifaa chenye vilemba vya kifalme kiletwe mbele yake. Akiwa na kioo katika mkono mmoja alikuwa anajaribu kilemba kimoja baada ya kingine mpaka hatimaye aliporidhishwa na kimoja. Kwa kujisikia na kunata, alikwenda msikitini. Alipoingia msikitini, alipanda katika mimbari, akionekana kuridhishwa kabisa na muonekano wake, na aliendelea kubadilisha mavazi yake. Hotuba aliyotoa ilimfanya 54 Rahnama-e-Sa’adat, Juz. 1, uk. 161, Al-Kafi, Juz. 2, Sura ya ubora wa waislamu maskini. 40


Visa vya Kweli sehemu ya Pili ajione mwenye furaha na mara nyingi wakati wa hotuba, alionekana kuziwaza nguo zake na aliwaza, “Mimi ni Sultan, kijana, ninayestahili kuheshimiwa na ni mkarimu sana.” Mwisho wa hotuba yake, aliteremka kwenye mimbari na kuelekea kwenye nyumba yake ya kifalme. Alipofika ndani, alimuuliza msichana aliyeonekana kuwa mmoja wa watumwa wake wa kike: “Ni nini maoni yako kuhusu mimi?” “Ninakuona kuwa ni mheshimiwa na mwenye furaha, ila tu lingekuwa sio shairi la mshairi!” Alijibu yule msichana – mtumwa. Sulaimani alishtushwa na maoni haya. Alisisitiza kutaka kulisikia shairi hilo, hivyo (msichana), alisema: “Wewe ni bidhaa na kitega uchumi kizuri, ikiwa tu utabakia milele. Lakini, tazama! Kwa mwanadamu, hakuna kubakia milele.” Mara tu alipolisikia, alianza kulia na aliendelea kulia kwa siku nzima. Jioni alimwita yule msichana mtumwa ili kujua ni nini kilimchochea kusoma shairi lile, lakini yule msichana aliapa kwamba mpaka siku hiyo hakuwahi kukutana na mshairi wala kusoma shairi. Wasichana watumwa wengine wote walishuhudia kuwa ni kweli. Ilimshitua Sulaiman kwamba tukio lile lilikuwa na mafungamano na kadiri isiyo ya kilimwengu na fikra hiyo ilimjaza hofu kubwa na wasiwasi. Muda si mrefu, aliondoka katika ulimwengu huu akiwa na majivuno ambayo yalikuja kumteka.55 5. Khusrow Parvez. Miongoni mwa wafalme ambao Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa amewapelekea barua za kuwaita katika Uislamu, mmoja wao alikuwa ni Khusrow Parvez, Mfalme wa Iran. Barua ilipelekwa kwake kupitia kwa Abdullah Ibn Hadhakah. 55 Pand-e-Tarikh, Jz. 3, uk. 37. 41


Visa vya Kweli sehemu ya Pili Alipoipokea barua, Khusrow aliamuru itafsiriwe. Ilipotafsiriwa, alibaini kuwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa ameandika jina lake kabla ya jina la Mfalme naye alishindwa kulistahamili hili. Aliichana barua kwa hasira, akampuuza kabisa Abdullah na akajiepusha kuijibu barua. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipojulishwa juu ya kitendo hiki, aliomba: “Ewe Mola! Wewe pia upasue ufalme wake” Khusrow alimuandikia barua Badhan, Mfalme wa Yemen: “Taarifa zimeyafikia masikio yangu kwamba kuna mtu amedai utume huko Hijaz. Andaa taratibu upeleke watu wawili wajasiri na wa kakamavu kwake ili wakamlete hapa kama mateka.” Badhan alipeleka watu wawili, Bahwaih na Khark Asrah kwenda Hijaz na waliiwasilisha barua ya Badhan kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Asubuhi yake walipokuja mbele yake, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwaambia; “Mjulishe Badhan kwamba usiku wa jana (Tarehe 10, Jamadiul Ula, mwaka 7 Hijiria), baada ya masaa saba ya usiku kupita, Mola wangu alimuua Khusrow Parvez katika mikono ya mwanaye Sheerwaih, na muda si mrefu tutaushinda ufalme wake, Ukiukubali Uislamu, unaweza kuendelea kutawala eneo lako.”56

27. UNYENYEKEVU Allah, Mwenye Hikima anasema:

“Na waja wa Allah Mwingi wa Rehema ni wale wanaotembea katika ardhi kwa unyenyekevu.” Suratul Furqan (25):63 56 Dastan-ha Wa Pand-ha, Juz. 2, uk. 126; Raudhatul Safa. 42


Visa vya Kweli sehemu ya Pili Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Hakuna mtu yeyote ambaye ataonyesha unyenyekevu kwa (ajili ya) Allah, isipokuwa Allah humpatia utukufu na heshima.”57 Maelezo mafupi: Unyenyekevu ni mzizi wa mema yote. Mtu mnyenyekevu mara zote ni mtiifu mbele ya utukufu wa Allah, na huweka msingi wa matendo yake ya ibada katika jukwaa la sifa hii njema. Hakuna anayeweza kuelewa uhalisia wa unyenyekevu isipokuwa wale Waliokaribu, miongoni mwa waja wa Allah ambao wameutambua upweke wa Allah. Utii na hofu (juu ya Allah) vinaweza tu vikatokana na unyenyekevu na ni kwa sababu hii kwamba wanyenyekevu wana muonekano ambao huwafanya waweze kutambuliwa na malaika na watu wenye ilmu ya kumjua Mungu (ma-Irifan). Muonekano wao na mwenendo wao wa kijamii na kifamilia huonyesha waziwazi kwamba wako mbali na kila aina ya kibri na majivuno.58 1. Unyenyekevu wa Salman Farsi. Salman alikuwa gavana wa moja ya miji ya Syria kwa muda fulani. Mwenendo wake katika kipindi cha utawala wake haukubadilika kutokana na ile ya kabla ya ugavana wake; wakati wote alikuwa anavaa nguo za kawaida, akitembea kwa miguu na alikuwa akiweka vitu vyake rehani (kwa ajili ya kukopa pesa). Siku moja, alipokuwa akitembea katika soko, alimuona mtu aliyekuwa amenunua majani ya wanyama na alikuwa akitafuta mtu wa kuyabeba na kumpelekea nyumbani kwake. Salman alimwendea huyo mtu ambaye 57 Jame al-Sa’adat, Juz. 1, uk. 359. 58 Tadhkiratul Haqaiq, uk. 55 43


Visa vya Kweli sehemu ya Pili alishindwa kumtambua Salman, ambaye alikubali kubeba mzigo wake bure. Mtu huyo aliweka mzigo wa majani ya wanyama katika mgongo wa Salman. Walipokuwa wakitembea, walikutana na mtu ambaye mara moja alimtambua Salman. “Ewe kiongozi! Unapeleka wapi mzigo huo,” alisema kwa mshangao. Alipo sikia maneno haya, mmiliki wa mzigo alibaini kuwa mtu aliyekuwa amebeba mzigo ule alikuwa ni Salman. Alipiga magoti chini na kuomba: “Nisamehe, kwani nilishindwa kukutambua.” “Hata hivyo, ni lazima niupeleke mzigo huu nyumbani kwako,” alisema Salman. Alipoufikisha alimuambia yule mtu, “Nimetekeleza ahadi yangu; sasa ni juu yako kuahidi kwamba kuanzia sasa hautataka huduma ya mtu yeyote kwa jambo lolote. (Na tambua!) Kwa wewe kubeba vitu unavyoviweza, hakutaakisi picha mbaya juu ya muruwa wako.”59 2. Bilal Muethiopia (Mhabeshi) Bilal alikuwa ni mmoja kati ya wale Waislam waliopiga hatua kubwa kiroho kiasi cha kuwa muadhini wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Yeye Mtukufu Mtume (saww) alikuwa akimwambia: Ewe Bilal! Hebu ichangamshe roho yangu (kwa adhana yako)” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) sio tu kwamba alimfanya msimamizi wa hazina, bali pia alimchukulia yeye kama ndugu yake wa damu. “Nitakapoingia peponi, nitasikia (sauti za) nyayo zako utakapokuwa ukitembea katika ardhi yake ya kijani” alimuambia Bilal. Hivyo Waislamu wengine walikuwa wakienda kumpongeza Bilal kwa 59 Jawame al- Hikayat, uk. 178 44


Visa vya Kweli sehemu ya Pili daraja tukufu alilojipatia, lakini kamwe hakuruhusu sifa zao zimfanye kiburi wala hakuruhusu sifa za watu zimbadilishe, kwa unyenyekevuu mkubwa, alikuwa akijibu sifa zao (walizo kuwa wakimpatia) kwa kusema” Mimi ni Muethiopia na hadi jana ni mtumwa.60 3 - Unyenyekevu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Abu Dharr anasimulia: Siku moja niliwaona Salman na Bilal wakiwasili mbele ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kwa heshima, Salman alianguka chini ya miguu ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na akaibusu. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alijitahidi kuumzuia asifanye kitendo hiki. “Usifanye vitendo ambavyo wasiokuwa waarabu huwafanyia wafalme wao” alishauri Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). “Mimi ni mja tu katika waja wa Allah ninakula wanachokula na ninakaa wanapokaa”61 4 - Muhammad ibn Muslim. Muhammad Ibn Muslim alikuwa ni mtu tajiri kutoka katika watukufu wa Kufa na sahaba wa Imam Baqir (as) na Imam Sadiq (a.s). Siku moja Imam Baqir (as) alimshauri: “Ewe Muhammad! Nilazima uwe mnyenyekevu na mwenye staha.” Aliporejea huko Kufa kutoka Madina, Muhammad Ibn Muslim alichukua mizani na mfuko wa tende. Kisha alikaa chini katika mlango wa msikiti mkuu wa huko Kufa na akaanza kutangaza: “Yeyote anayetaka tende naaje anunue kutoka kwangu.” (alifanya hivyo ili asibakiwe na hata chembe ya kiburi ndani ya nafsi yake). Ndugu zake walimlalamikia wakisema kwamba kitendo chake kinawadhalilisha. “Imam wangu ameniagiza nifanye kazi hii na siwezi kumuasi; siwezi 60 Hikayat-ha-e-Shanidani,Juz.4,uk 173;Tabaqat Ibn Sa’d ,Juz.3,uk.238 61 Dars-hai Az Zindagi-e-Payambar,uk.162;Biharul Anwar,Juz.76,uk.63 45


Visa vya Kweli sehemu ya Pili kuondoka hapa mpaka nitakapokuwa nimeuza tende zote zilizomo katika mfuko huu,” alisema Muhammad. “Ikiwa ndivyo unavyosema, basi pia unaweza kufanya kazi ya msaga unga” ndugu zake walimwambia kwa dhihaka. Kwa mshangao wao, Muhammad alikubali. Alinunua kinu cha kusaga kwa mkono na akawa anasaga ngano kuwa unga, nia ikiwa ni kujikwamua kutoka katika kibri na kujisikia.62 5. Isa na kuwaosha miguu wanafunzi wake. Isa Ibn Maryam (as) siku moja aliwaambia wanafunzi wake alikuwa anatafuta upendeleo kutoka kwao. “Unataka tufanye nini ?” waliuliza. Isa (as) aliondoka katika sehemu yake na kuwaosha nyayo wanafunzi wake wote! “Ewe roho wa Allah! Inatustahili zaidi sisi kuziosha nyayo zako!” walisema kwa mshangao. “Mtu anayestahili zaidi kutumikia ni yule ambaye ni mwanachuoni. Nimefanya hivi ili niwe nimeonyesha unyenyekevu kwa vitendo. Ninyi pia mnapaswa kujijengea sifa ya unyenyekevu na baada ya kuwa nimekwenda mnapaswa kutangamana na watu kwa unyenyekevu na staha. Kama nilivyo wafanyieni nyinyi sasa. Isa (as) alisema: “Ni kwa njia ya unyenyekevu na sio kibri ambapo kwamba busara hustawi, kama ambavyo ni katika udongo laini ambapo mimea hustawi, sio katika mwamba mgumu wa jabali.”63 62 Riwayat-ha Wa Hikayat-ha, uk. 103; Dastan-ha-e-Parakandeh, Jz. 3, uk. 18. 63 Namunah-e-Ma’arif, Juz.3, uk.223; Al-waf, Juz 1, uk. 4. 46


Visa vya Kweli sehemu ya Pili

28 –TOBA Allah Mwenye Busara anasema:

“Na kwamba muombe msamaha kwa Mola wenu kisha mtubie kwake…” Qur’ani Tukufu 11:3 Imam Sadiq (as) alisema: Kama mja anatubia kwa ukweli kabisa, Allah humpenda (na) huzificha dhambi zake.”64 Maelezo mafupi: Toba ni kamba ya Mungu ambayo wale wanaotubia lazima waikamate kwa nguvu; wanahitaji kusafisha dhambi zilizoko ndani mwao na kutoa ushahidi dhidi yao wenyewe mbele ya Mola wao. Lazima wawe ni wenye kutubia kutoka ndani ya nyoyo zao kuhusiana na matendo ya maovu yaliyopita, na kuwa wenye hofu na muda uliobaki wa maisha yao. Auliya (marafiki) wa Allah hutubia kwa ajili ya mawazo (yasiyofaa) ambayo yanaweza kupita katika akili zao, ambapo wale ambao ni maalumu hutubia kwa ajili ya kujishughulisha na chochote kisichokuwa Allah, hata kama umma kwa ujumla unatubia kwa ajili ya dhambi zilizotendwa na wao. Ni muhimu kwamba, ili kufanya marekebisho kwa ajili ya matendo (maovu) yaliyopita na kujizuia na kutenda dhambi siku zijazo, mtu anayetubia hapaswi kuichukulia dhambi yoyote kuwa ni ndogo na isiyo na 64 Jame’al-Sa’adat, Jz. 3, uk. 65. 47


Visa vya Kweli sehemu ya Pili muhimu, bali lazima siku zote awe anasikitika juu ya wakati wake uliopita, aweke nafsi yake mbali na aina mbalimbali za tamaa na aiongoze kwenye harakati (dhidi ya matamanio) na ibada.65 1. Mbunifu wa dini na Utubiaji. Imam Sadiq (as) alisimulia: “Katika zama za kale aliishi mtu ambaye alitaka kupata mahitaji yake ya maisha na kujipatia utajiri mkubwa kwa njia za halali lakini hakufanikiwa. Basi alifanya juhudi tena kufanikisha malengo yake kwa njia za haramu, lakini mara hii tena akashindwa. Shetani alimtokea na kumuambia: “Ulijaribu kupata utajiri mkubwa kwa njia za halali na halikadhalika kwa njia za haramu lakini hukufanikiwa. Je, unataka nikuoneshe njia anbayo kwamba sio tu utakuwa tajiri bali vilevile utavutia wafuasi wengi?” Yule mtu akaonesha kukubali kwake kwa kutaka kujua vipi atakuwa tajiri. “Buni dini na walinganie watu kwayo” alishauri shetani. Yule mtu akabuni dini na punde akawa na wafuasi wengi tu ambao kwawo alijipatia utajiri mkubwa. Siku moja akatambua kwamba amefanya kosa kwa kuwapotosha watu wengi, hivyo aliamua kuwajulisha watu wale uwongo wa dini yake na makosa ya mwenendo wake. Lakini kwa vyovyote alivyokazia kwa nguvu na kusisitiza, watu walikataa tu kuyakubali maneno yake. “Mitazamo yako ya mwanzo ilikuwa sahihi; je, sasa umekuwa mwenye kushuku dini yako mwenyewe?” Walimuuliza. Wakati aliposikia maneno haya alichukua pingu na kujifunga mwenyewe. Aliahidi kwamba hatajifungua mpaka Allah akubali toba yake. Allah akamjulisha (kwa njia ya wahyi) Mtume wa zama zile kumpelekea 65 Tadhkiratul Haqaiq, uk. 75. 48


Visa vya Kweli sehemu ya Pili ujumbe mtu yule: “Kwa Utukufu Wangu! Hata kama ungelia na kuomba kiasi kwamba kila mshipa katika mwili wako unaachia, kamwe sitakubali maombi yako, mpaka uwajulishe wale watu ambao wamekufa baada ya kupotoshwa na wewe na kutoka kwenye ukweli na waondoke kwenye dini yako.”66 2. Mfanyakazi wa Bani Umayyah Ali Ibn Hamza anasimulia: “Nilikuwa na rafiki ambaye alikuwa akifanya kazi kama mwandishi ndani ya utawala wa Bani Umayyah. Siku moja aliniomba nipange siku kwa ajili yake ya kuonana na Imam Sadiq (as). Nilitaka ruhusa kutoka kwa Imam (as) na alikubali kukutana naye. Siku na saa ya kiaga rafiki yangu na mimi tuliwasili katika hadhara ya Imam (as). Rafiki yangu alimsalimia Imam (as), akakaa chini na kusema: “Na nifanywe kuwa fidia yako! Nimekuwa nikishikilia cheo katika wizara ya hazina ya Bani Umayyah na nimeweza kupata utajiri mkubwa, ingawa pia nimetenda hatia fulani!” “Kama Bani Umayyah wasingekuwa na watu kama ninyi wa kukusanya kodi kwa ajili yao na kufuatana nao katika vita vyao, wasingeweza kutunyang’anya haki yetu,” alisema Imam Sadiq (as). “Kuna njia yoyote iliyopo kwa ajili ya wokovu wangu?” alisihi kijana yule. Imam (as) alimuuliza: “Kama nikikuambia utafanya kama nitakavyo kuelekeza?” Yule kijana akaitikia kwa kukubali. “Kutokana na mali ambayo imebaki kwako, rudisha ile ambayo wenyewe unawajua, na kwa ile ambayo wenyewe huwajui, itoe sadaka kwa niaba ya wenyewe. Kwa kubadilishana na kitendo hiki, nitakuhakikishia Pepo!” alisema Imam (as). 66 Pand-e-Tarikh, Jz. 4, uk. 251; Biharul Anwar, Jz. 2, uk. 277. 49


Visa vya Kweli sehemu ya Pili Huku akiwa ameinamisha kichwa, kijana yule alikubali baada ya kufikiria kwa muda mrefu: “Na nifanywe fidia yako! Nitafanya kama nilivyoelekezwa na wewe.” Ali Ibn Hamza anasema: Tulisimama na kuelekea huko Kufa. Kule, rafiki yangu yule alijiondolea mali zake zote – hata nguo zake – ama kurudisha kwa wenyewe au kuzitoa sadaka. Nilikusanya kiasi cha pesa kutoka kwa rafiki zangu ili kununua baadhi ya nguo kwa ajili yake na nilikuwa nikumtumia pesa kwa ajili ya matumizi yake. Miezi michache baada ya tukio hili, alishikwa na maradhi na tulikuwa tukimtembelea mara kwa mara wakati wa kuumwa kwake. Siku moja, wakati nilipomtembelea, nilimkuta ukingoni mwa kifo. Huku akifunua macho yake alisema: “Ewe Ali! Imam ametekeleza ahadi yake.” Kisha akafariki dunia. Tulimkosha, tukamvisha sanda na hatimaye tukamzika. Wakati mwingine baadae, nilimtembelea Imam (as). Mara tu macho yake yaliponiangukia, alisema: “Ewe Ali! Nimetekeleza ahadi yangu kwa rafiki yako.” “Na nifanywe kuwa fidia yako! Ni kama hivyo usemavyo. Yeye pia aliitaja (Hakikisho la Pepo) kwangu kabla ya kifo chake.” Nilisema.67 3. Kurejea Kabla Ya Kifo Mu’awiyah Ibn Wahab anasimulia: “Wakati tulipoondoka kuelekea Makka, kulikuwepo na mzee mmoja pamoja nasi ambaye alikuwa akijishughulisha na vitendo vya ibada, lakini alikuwa hashuhudii imani ya Shia. Mzee huyu alikuwa amefuatana na mpwa wake, ambaye yeye alikuwa ni Shia. 67 Shanidani-ha-e-Tarikh, uk. 55; Majjatul Baida, Jz. 3, uk. 254. 50


Visa vya Kweli sehemu ya Pili Wakati tukiwa safarini, yule mzee alishikwa na maradhi. Nilimuambia mpwa wake: “Kwa nini hamjulishi imani iliyo sahihi; Inawezekana kwamba Allah akamchukua kutoka katika ulimwengu huu katika hali ya imani ya kweli na Wilayah.” Hata hivyo, watu wengine wakamshauri kumuacha mzee huyo kama alivyo na kumuacha afe katika imani yake mwenyewe. Hata hivyo, yule mpwa wake hakuujali ushauri wao. Alikwenda kwa ami yake na kusema: “Ewe ami! Baada ya kifo cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) watu mbali na wachache ambao walishikamana na Amiru’l-Mu’minin (as) waliritadi licha ya kweli kwamba Ukhalifa (wa Amiru’l-Mu’minin as.) ulikuwa umekwisha kuelezewa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).” Aliposikia maneno haya, mzee yule alivuta pumzi na akasema: “Naikubali imani hii.” Kisha akafariki. Mu’awiyah Ibn Wahab anasimulia: “Tuliingia Madina na kuwasili kabla ya Imam Sadiq (as). Ali Ibn Sari, mmoja wa wenzetu katika safari alimsimulia Imam (sa) kisa cha kutubia kwa mzee yule na kukubali kwake uimam punde tu kabla ya kifo chake, Imam akasema: “Yeye ni mtu wa Peponi.” Ali Ibn Sarai akasema kwa mshangao: “Mzee yule alikuwa hajui chochote kuhusu imani yetu na alikuwa haelewi kabisa sheria na hukumu zake; ilikuwa ni wakati tu roho yake ilipokaribia kutengana na mwili wake ndipo akakubali imani hii.” Imam (as) akaelezea: “Unataka nini (zaidi) kwake? Kwa Jina la Allah! Amekwishaingia Peponi.”68 4. Abu Lubabah Abu Lubabah alikuwa mmoja wa masahaba maarufu wa Mtukufu Mtume 68 Khazinatul Awahir, uk. 312; Raudatil Anwar cha Sabzwari. 51


Visa vya Kweli sehemu ya Pili (s.a.w.w.) na alishiriki katika vita vya Uhud na katika ushindi wa Makka. Moja ya kipengele muhimu katika maisha yake ilikuwa ni tukio lake la kutubia. Wakati kabila la Bani Quraidhah walipovunja mkataba wao na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Mtukufu Mtume alituma jeshi dhidi yao na kuizingira ngome yao. Baadhi ya watu kutoka kabila la Aus walimuendea (Mtume) na wakamuomba: “Kama ulivyoshughulikia suala la kabila la Bani Qainaqa’a kuamuliwa na kabila la Khazraj, liache juu yetu suala hili la Bani Quraidhah liamuliwe na sisi.” Je, mtaridhika kama nikiwachagulieni mtu mmoja kutoka kabila lenu kuamua katika suala hili?” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwauliza. Walikubali. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimpendekeza Sa’d Ibn Mu’adh, lakini Bani Quraidhah walikataa kumkubali. Walimuambia amtume Abu Lubabah kwao ili waweze kushauriana naye. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akampa Abu Lubabah, ambaye ana nyumba, mali na familia katika ngome ya Bani Quraidha, jukumu la kufanya mashauriano pamoja nao. Mara tu Abu Lubadah alipoingia ndani ya ngome, wanaume na wanawake, wazee na vijana, walimzunguka na wakaanza kumlilia na kumlalamikia (juu ya hali ya mambo) kwa nia ya kuvuta huruma na upole wake. Kisha wakamuuliza: “Je, tujisalimishe mbele ya utawala wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)?” “Mnaweza kufanya hivyo,” alijibu, akionesha kwa ishara (kwa kuonesha kwenye shingo yake) kuonesha kwamba kujisalimisha kulikuwa sawa na kifo. Upesi sana alitambua kwamba kwa kutenda kitendo hiki, amekuwa si mwaminifu na ni mtovu wa utii kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Ilikuwa ni katika tukio hili aya ifuatayo iliteremshwa kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): 52


Visa vya Kweli sehemu ya Pili

“Enyi mlioamini msimfanyie khiana Allah na Mtume na msikhini amana zenu na hali mnajua. Na jueni kwamba mali zenu na watoto wenu ni mtihani, na kwamba kwa Allah yako malipo makubwa.” Qur’ani Tukufu 8:27-28. Akiwa amejawa na aibu, alitoka nje ya ngome na kuelekea moja kwa moja msikiti wa Madina na kujifunga mwenyewe kwenye nguzo mojawapo msikitini humo, kisha akasema kwa sauti kubwa: “Hakuna ruhusa mtu yeyote kunifungua mpaka Allah akubali toba yangu.” Alibakia katika hali hiyo kwa muda siku kumi hadi kumi na tano, akiruhusu yeye mwenyewe kufunguliwa kwa ajili ya Sala na kwenda chooni. “Kama Abu Lubabah angekuja kwangu, ningeomba msamaha kwa ajili yake lakini kwa vile yeye mwenyewe anasubiri msamaha wa Allah, mwacheni mpaka Allah amsamehe,” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema wakati alipojua kile alichofanya Abu Lubabah. Ummu Salama anasimulia: “Siku moja wakati wa mapambazuko ya asubuhi, nilimuona Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akiwa na tabasamu na furaha. ‘Allah akufanye uwe mwenye kutabasamu siku zote!’ ‘Ni nini sababu yake?’” Niliuliza. “Jibril amenijulisha kwamba toba ya Abu Lubabah imekubaliwa,” alisema. “Je, utanipa ruhusa yako nimjulishe kuhusu habari hizi njema?” niliuliza. “Unaweza kumjulisha kama unataka,” alijibu. Kutoka chumbani niliita kwa sauti: “Habari njema, Ewe Abu Lubabah! Allah amekubali toba yako.”

53


Visa vya Kweli sehemu ya Pili Watu wakakurupuka kwenda kumfungua lakini akasema: “Nakuwekeni juu ya kiapo cha Allah kwamba mtu yeyote asinifungue, isipokuwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe.” Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipowasili msikitini kwa ajili ya Sala ya asubuhi alimfungua Abu Lubabah kutoka kwenye nguzo ambayo mpaka sasa ipo katika msikiti wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mashuhuri kwa jina la ‘Nguzo ya Toba’ au Nguzo ya Abu Lubabah.’69 5. Buhlul70 Mchimbaji Kaburi Muadh Ibn Jabal alikuwa katika majonzi wakati alipowasili mbele ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kumsalimu. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alijibu salamu yake na akamuuliza: “Kinakuliza nini?” “Hapo kwenye mlango wa msikiti kuna kijana mzuri ambaye analia kwa uchungu kama mama ambaye amefiwa na kijana wake, na anataka kuonana na wewe.” Alijibu Muadh. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akakubali kukutana naye. Kijana yule akaingia na kumsalimia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambaye aliitikia salamu yake na akauliza: “Kwa nini unalia?” “Kwa nini nisilie? Nimetenda dhambi ambayo Allah kamwe hatasamehe na Yuko tayari kunitupa motoni.” Alisema kijana yule. “Umemshirikisha Allah na kitu chochote?” “Hapana.” “Umeuwa mtu yeyote?” 69 Paighambar Wa Yaaraan, Jz. 1, uk. 129; Majma’ al-Bayan, chini ya njadala unaohusu aya ya 102 sura ya Tawba. 70 Neno la mchapishaji: Asije akafikiriwa kuwa ni Buhlul aliyeishi zama za Imam Ridha (as) 54


Visa vya Kweli sehemu ya Pili “Hapana.” “Hata kama dhambi zako zina ukubwa wa milima, Allah atazisamehe.” Alisema Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). “Dhambi zangu ni kubwa kuliko milima.” Kijana alisema. Dhambi zako zina ukubwa wa ardhi saba, bahari, mchanga, miti, vyote ambavyo vinalala katika ardhi, katika mbingu, nyota, Arshi na Kiti cha Enzi?” aliuliza Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). “Dhambi zangu ni kubwa kuliko vitu vyote hivyo.” “Ole wako! Dhambi zako ni kubwa kuliko Mola wako?” Yule kijana akainamisha kichwa na akajibu: “Allah yu mbali na dosari zote; ni Mola wangu, ambaye ni mkubwa mno.” “Je, hunisimulii moja ya dhambi zako? Aliuliza Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) “Kwa nini nisikusimulie?” Alijibu yule kijana, ambaye jina lake lilikuwa ni Buhlul: “Kwa muda wa miaka saba nimekuwa nikichimba makaburi ya wafu, nikiwavua sanda zao na kuziuza. Usiku mmoja mwanamwali mmoja kutoka miongoni mwa Answar alikufa na alizikwa makaburini. Wakati nilipochimbua kaburi lake ili kumvua sanda yake, shetani akanishawishi na nikatenda dhambi kubwa (kuzini na maiti yule). Wakati nikiwa ninarudi, ile maiti ikaniita: “Ewe kijana! Humuogopi Mtawala wa Siku ya Hukumu? Ole wako na moto wa Siku ya Hukumu.” Baada ya kusimulia hivi, kijana yule alitaka kujua kitu cha kufanya. “Ewe muovu! Kaa mbali na mimi kwani naogopa kwamba na mimi vilevile naweza kuungua katika moto wako!” aliguta Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Yule kijana akaondoka, na moja kwa moja akaelekea milimani. Alifunga mikono yake kwenye shingo yake na kujishughulisha sana katika ibada, madua na kuomba msamaha. 55


Visa vya Kweli sehemu ya Pili Kwa muda wa siku arobaini, alilia usiku na mchana kwa kiasi kwamba hata wanyama waporini waliathiriwa na kulia kwake. Baada ya siku arobaini alimuomba Allah ama amuadhibu kwa njia ya moto au amsamehe, ili kwamba asije akakabiliana na fedheha ya Siku ya Hukumu. Allah akateremsha aya ifuatayo, ambayo hutaja msamaha wa Buhlul:

“Na wale ambao wanapofanya uchafu au wakidhulumu nafsi zao humkumbuka Allah wakaomba msamaha wa madhambi yao, na ni nani anayesamehe madhambi isipokuwa Allah, na hawaendelei na (maovu) waliyofanya hali wanajua.” Qur’ani Tukufu 3:135 Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisoma aya hii huku akiwa na uso wa tabasamu na kisha akasema: “Nani atanipeleka kwa yule kijana?” Mu’adh alikubali kumpeleka. Akifuatana na Mu’adh, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) walikwenda mpaka sehemu ambayo alikuwepo yule kijana. Alimuona akiwa amesimama katikati ya majabali mawili, mikono ikiwa imefungwa kwenye shingo yake huku akiwa anajishughulisha na maombi. Uso wake umekuwa mweusi kwa sababu ya jua kali na nyusi zake zote zimeondoka kwa sababu ya kulia sana. Wanyama wa porini wamemzunguka ambapo ndege wanazunguka juu ya kichwa chake wote wanalia juu ya huzuni na hali ya kutia huruma. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimsogelea, akafungua mikono yake na akaondoa udongo juu ya kichwa chake.

56


Visa vya Kweli sehemu ya Pili “Ewe Buhlul! Hizi ni habari njema kwa ajili yako; umeokolewa na Allah kutoka kwenye moto (wa Jehannamu),” alisema. Kisha akawageukia sahaba zake, akasema: “Hivi ndivyo ambavyo mnatakiwa kufanya katika kurekebisha madhambi yenu.”71

29 – UJINGA Allah, Mwenye Busara, amesema:

“Shikamana na kusamehe na amrisha mema na wapuuze wajinga.” Qur’ani Tukufu 7:199. Imam Ali (as) amesema: “Ujinga ni chanzo cha maovu yote.”72 Maelezo Mafupi: Ujinga ni hali ambayo ipo ndani ya wanadamu na mtu ambaye anao humpeleka kwenye giza, ambapo mtu ambaye huuweka mbali naye hufikia mwanga na kupata utambuzi na umaizi. Kama mtu anachagua njia isiyo sahihi kwa ajili yake mwenyewe na kuruhusu ujinga umuongoze katika vitendo vyake, atachukuliwa kama muovu na mtu wa motoni. Hata hivyo, kama atajiweka katika njia iliyo sahihi, na akatenda kwa mujibu wa misingi ya elimu na utambuzi, atakuwa miongoni mwa watu waliookolewa.

71 Risalah Liqaullah, uk.62; Majalis as-Saduq. 72 Ghurar al-Hikimah, Hadithi ya 819. 57


Visa vya Kweli sehemu ya Pili Mtu kuridhika juu ya vitendo vyake ni ufunguo ambao hufungua mlango wa ujinga, na tabia mbaya ya mtu mjinga ni kudai kwamba ana elimu licha ya yeye kuwa ni mjinga. Mtu mjinga, wakati akijua makosa yake mwenyewe, hajisikii vibaya wala aibu, na anaposhauriwa, hajali ushauri huo. Licha ya kuuelewa ujinga wake (unaitwa ujinga mwepesi wa kawaida) bado anafanya makosa. 1. Kamanda Mjinga Ya’qub Laith Saffar (amekufa 265 A.H.) alikuwa na kamanda aitwaye Ibrahim ambaye licha ya kuwa shujaa na mwenye ari, alikuwa mjinga mno. Wakati mmoja wa kipindi cha kipupwe Ya’qub aliagiza kwamba nguo zake binafsi za kipupwe apewe Ibrahim. Ibrahim alikuwa na mtumishi aitwaye Ahmad Ibn Abdullah ambaye alikuwa na chuki juu yake. Wakati Ibrahim aliporudi nyumbani, Ahmad akamuuliza: “Je, unajua kwamba yeyote yule ambaye Ya’qub Laith anampa nguo zake binafsi, humuuwa mtu huyo ndani ya wiki moja?” “Oh hapana! Nilikuwa sina habari ya hili. Ni njia ipi ya kuepukana na hili?” aliuliza Ibrahim. Ahmad akamshauri kwamba ni lazima akimbie sehemu hiyo. Pia alikubali kumfuata Ibrahim na akapanga kukutana naye siku ifuatayo. Baadae Ahmad kwa siri alikwenda kwa Ya’qub Laith na akamjulisha kwamba Ibrahim anakusudia kukimbilia Sistan ambako ataanzisha uasi dhidi ya Ya’qub Laith. Ya’qub akatafakari kwa muda na ilikuwa karibu aamuru jeshi lake kujiandaa kwa ajili ya kupambana na Ibrahim wakati Ahmad alipotoa ombi. “Niruhusu mimi peke yangu nikuletee kichwa cha Ibrahim mbele yako.” Ahmad alimuambia Ya’qub. 58


Visa vya Kweli sehemu ya Pili Ya’qub Laith alikubali. Wakati Ibrahim alipokuwa anakaribia kuondoka mjini pale na jeshi lake, Ahmad alimshambulia kwa nyuma, akakata kichwa chake kwa upanga wake na akakipeleka mbele ya Ya’qub Laith. Ya’qub akaitoa nafasi ile ya Ibrahim, kamanda wake mjinga na kumpa Ahmad ambaye kwa njia hiyo akaja kufaidi heshima kubwa machoni pake.73 2. Mtoto Mjinga Wa Khalifa Mahdi Abbasi, Khalifa wa tatu wa Bani Abbas, alikuwa na mtoto aitwaye Ibrahim, ambaye alikuwa ni mtu aliyepotoka. Alionesha uadui mkali na uovu mahsusi kwa Amiru’l-Muminin (as). Siku moja alimuendea Ma’mun, Khalifa wa saba wa Bani Abbas, na akamuambia: “Nilimuona Ali (as) katika ndoto. Tulikuwa tukisafiri naye mpaka tulipofikia darajani ambapo alinipa upendeleo wa kwanza kulivuka. Nikamuambia: ‘Unadai kuwa wewe ni Amir wa waumini, lakini sisi tunastahiki zaidi katika cheo hiki.’ Ali (as) hakunipa jibu sahihi.” “Alikujibu nini?” Ma’mun aliuliza. “Alinisalimia tu mara nyingi kwa kusema ‘Amani, Amani,” alijibu Ibrahim. “Kwa Jina la Allah! Amekujibu kwa sauti kubwa na kwa uwazi,” alieleza Ma’mun. Ibrahim alishangazwa. Ma’mun akaendelea: “Alikuona wewe kama mtu mjinga usiyefaa kujibiwa. Hii ni kwa sababu Allah Anaelezea waja wake maalumu katika Qur’ani, anasema:

73 Namunah-e-Ma’arif, Jz. 4, uk. 93. 59


Visa vya Kweli sehemu ya Pili

“Na waja wa Allah Mwenye Rehema ni wale ambao hutembea katika ardhi kwa unyenyekevu, na kama wajinga wakiwasemesha, husema: Amani,’” Qur’an Tukufu 25:63 (usemi) ambao huonesha kutojali kwao (kuhusiana na wajinga) na ukubwa wao (binafsi). “Ali (as) alikuchukulia wewe kama mtu mjinga na akajihusisha na wewe kama Qur’ani ilivyopendekeza wakati wa kushughulika na watu wajinga.”74 3. Mtu Mtanashati Lakini Mjinga Mtu anayeonekana wa kupendeza na mwenye heshima aliingia kwenye mahakama ya Abu Yusuf Kufi (aliyekufa 182 A.H.), Kadhi wa Harun Rashid ambaye alimchukulia kwa heshima kubwa sana. Mtu yule alikaa kwenye mkusanyiko kwa ukimya na heshima, kiasi kwamba ilimshawishi Kadhi yule kumuona kama mtu mwenye utukufu mkubwa. Alimuuliza kama anataka kusema neno lolote. “Nataka jibu kwa swali,” akasema mtu yule “Kile ninachojua nitakujibu,” alijibu yule Kadhi kwa unyenyekevu. Yule mtu akauliza: “Ni wakati gani mtu anaweza kufungua saumu yake?” “Wakati jua likizama,” Kadhi alijibu. 74 Hikayat-ha-e-Shanidani, Jz. 2, uk. 20; Safinatul Bihar, Jz. 1, uk. 79. 60


Visa vya Kweli sehemu ya Pili “Vipi kama jua halizami mpaka usiku wa manane?” Aliposikia hivi, yule Kadhi akacheka sana na akasema: “Usahihi ulioje wa mshairi Jarir Ibn Atiyyah (Mshairi wa zama za Bani Umayya, ambaye alikufa katika mwaka wa 110 A.H.) alisema: ‘Ukimya ni uzuri kwa mtu ambaye ni dhaifu na mjinga;’ kwa hakika akili ya mtu hujulikana kwa mazungumzo yake, kama vile ambavyo upungufu wake wa akili unavyodhihirika kwa matokeo ya mazungumzo yake.” Hivyo, Kadhi yule akaelewa ujinga wa mtu yule mwenye mwonekano mzuri wa kupendeza.75 4. Qais Ibn Asim Qais Ibn Asim alikuwa kiongozi wa kikabila wakati wa zama ya ujinga lakini baadae alikubali Uislamu. Wakati fulani, katika kipindi cha uzee wake, aliwasili kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ili apate njia ya kurekebisha matendo yake mabaya ya zamani, alisema: “Zamani, ujinga uliwashawishi kina baba wengi kuwazika mabinti zao wasio na hatia wakiwa hai. Mimi vilevile, nimewazika mabinti zangu kumi na wawili wakiwa hai katika vipindi vifupi. Mke wangu alijifungua kwa siri binti wa kumi na tatu na akafanya ionekane kwangu kama vile mtoto haikuwa riziki, alimpeleka kwa siri mtoto yule kwa ndugu zake ili wamlee. Miaka ilipita mpaka siku moja niliporudi nyumbani, ghafla na bila kutegemea, kutoka moja ya safari zangu, nikamkuta msichana mdogo nyumbani kwangu. Kwa vile alifanana na watoto wangu, nilijiona mwenyewe nimechanganyikiwa mpaka hatimaye nikaja kujua kuwa alikuwa ni binti yangu. 75 Lataif al-Tawaf, uk. 412 61


Visa vya Kweli sehemu ya Pili Mara moja nilikamata mkono wa msichana yule ambaye alikuwa analia sana na nikamchukua mpaka kwenye sehemu ya mbali, mwenyewe sikutaka niathiriwe na kilio chake. Aliendelea kunisihi, ‘nitarudi kwa wajomba zangu na sitakuja nyumbani kwako tena,’ lakini sikujali ombi lake na nikamzika akiwa hai.” Wakati alipokwishasimulia haya, Qais aliona kwamba machozi yalikuwa yanatiririka kwenye macho ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na alimsikia akinung’unika: “Mtu ambaye hana huruma kwa wengine, hatahurumiwa.”76 Kisha akamgeukia Qais, akasema: “Una wakati mgumu mbele yako!” “Nifanye nini kuufanya mzigo wa maovu yangu kuwa mwepesi?” aliuliza Qais. “Kwa kila binti uliyeuwa, muache huru msichana mtumwa,” alijibu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).77 5. Ndevu Ndefu Jahidh Basri (alikufa 249 A.H.) ambaye ana kitabu kwa jina lake katika kila tawi la elimu, anaeleza: “Ma’mun Abbasi na watu wengine wachache walikusanyika pamoja na walikuwa wanajishughulisha na maongezi. “Mtu ambaye anaweka ndevu ndefu ni mpuuzi na mpumbavu,” mmoja wao alisema. Baadhi ya wengine walipinga wakisema: “Bali kinyume chake, tumewaona watu wenye kufuga ndevu ndefu lakini ambao walikuwa ni werevu na wenye akili.” 76 77 Dastan-ha Wa Pand-ha, Jz. 1, uk. 15; Ahiliyyat Wa Islam, uk. 632. 62


Visa vya Kweli sehemu ya Pili “Haiwezekani!” Ma’mun aliguna. Wakati huo huo, mtu mwenye ndevu ndefu aliyekuwa amepanda ngamia alikuja kuelekea kule walikokuwa wamekaa. Ili Ma’mun apate kuthibitisha nukta yake, alimuita mtu yule na kumuuliza jina lake. “Abu Hamdwaih,” alijibu yule mtu. “Jina lako la utani ni nani?” aliuliza Ma’mun. “Alawiyyah,” alijibu yule mtu. Ma’mun akawaambia wale waliokuwa wamemzunguka: “Mtu ambaye ni mjinga hivyo kiasi kwamba hawezi kutofautisha kati ya jina na jina la utani, matendo yake yote mengine yatakuwa vilevile yatahusishwa na ujinga huo huo.” Akamgeukia yule mtu mara nyingine tena, akamuuliza: “Unafanya kazi gani?” “Mimi ni mwanasheria na mtaalamu katika sayansi mbalimbali. Kama mfalme anataka anaweza kuniuliza.” “Mtu mmoja aliuza kondoo kwa mtu mwingine, ambaye alimchukuwa kondoo yule katika miliki yake. Lakini akiwa bado hajamlipia mnyama yule, alitoa kinyesi ambacho kiliangukia kwenye macho ya mtu mwingine na kumpofusha. Katika mazingara haya, nani anawajibika kulipa fidia kwa maumivu yaliyosababishwa?” aliuliza Ma’amun. Yule mtu mwenye ndevu ndefu alitafakari kwa muda kisha akasema: “Fidia lazima ilipwe na muuzaji na sio mnunuzi.” Wale waliokuwa pale wakataka kujua sababu yake.

63


Visa vya Kweli sehemu ya Pili “Ni kwa sababu muuzaji hakumjulisha mnunuzi kwamba ameweka manati ndani ya sehemu ya nyuma ya kondoo, ambayo hutumika kwa kutupia mawe kwa ajili ya kujilinda mwenyewe.” Alielezea yule mtu. Waliposikia vile Ma’amun na wale waliomzunguka pale waliangua kicheko. Mtu yule alipewa pesa kidogo na akaondoka. “Ukweli wa maelezo yangu umekuwa dhahiri mbele yenu kwamba wahenga wamesema78: Mtu mwenye ndevu ndefu ni mpumbavu.” Alisema Ma’mun.79

30 – UROHO Allah, Mwenye Busara amesema: “Hakika mtu ameumbwa hali ya kuwa mwenye pupa.”80 Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Kadiri mtu anavyokuwa mzee, sifa mbili ndani yake hugeuka kuwa za ujana – uroho na tamaa za hali ya juu.”81 Maelezo Mafupi Kama mtu ni mroho wa kupata kitu, hatapata ujirani wa Allah, kwa vile ameacha sifa ya tawakkul (tegemeo kwa Allah), hatosheki na alichokadiriwa na Allah na amekuwa mwenye pupa, ambayo ni njia ya Shetani. 78 Kuna hadithi ambazo zinakataza kufuga ndevu ndefu. Moja ya vitu ambavyo Imam Ali (as) alivyovitaja katika kuwakosoa watu wa Basra ni ndevu zao ndefu. Mtukufu Mtume anaona kutofuga ndevu ndefu kama moja ya furaha za mtu. (Safinatul Bihar, Jz. 2, uk. 509) 79 Jawame al-Hikayat, uk. 300. 80 Qur’ani Tukufu 70: 19. 81 Jame al-Sa’dat, Jz. 2, uk. 100. 64


Visa vya Kweli sehemu ya Pili Allah ameumba ulimwengu unaofanana na kivuli; kufuata kivuli hakuleti natija yoyote isipokuwa kuchoka na uchovu. Kama mtu anautaka ulimwengu kwa ziada ambayo kwamba ni muhimu, sio tu kwamba haupati bali vilevile hupata matatizo na mateso. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Mtu mroho siku zote huwa ametengwa.” Na mtu aliyetengwa huchukiwa na kulaumiwa. Mawazo ya mtu mroho yamevurugika na matatizo yake ni mengi - wakati wote anajishughulisha na kufanya mahesabu ya utajiri, hana amani katika ulimwengu huu wala mwelekeo wa Akhera.82 Tope La Kaburini Ni Dawa Ya Mtu Mroho Sa’id anasimulia: “Nilikuwa nimesikia kwamba mchuuzi ambaye alimiliki watumwa arobaini na ngamia mia moja na hamsini waliobeba mizigo ya dhahabu alikuwa akisafiri kutoka mji huu kwenda mji mwingine kwa ajili ya biashara. Usiku mmoja, katika kisiwa cha Kish, alinikaribisha chumbani kwake. Nilikwenda chumbani kwake lakini usiku wote ule alikuwa anahangaika. Alikuwa akizungumza bila mpangilio na bila kukoma, na akisema: “Ghala yangu ile na ile iko Turkistan, mzigo wangu fulani uko India, hii ni hati ya kuuza ardhi fulani, mzigo mwingine unashikiliwa kwa sababu ya baadhi ya bidhaa, mtu fulani yule ni mdhamini wa mkopo… nafikiria kusafiri kwenda Alexandria, lakini bahari ya Mediteraniani ina mawimbi makali kwa sasa… “Ewe Sa’id! Ninayo safari nyingine mbele yangu, ambayo kama nitaikamilisha, nitatumia maisha yangu yaliyobaki katika faragha na kamwe sitafanya safiri nyingine tena.” “Ni safari ipi hiyo, ambayo baada yake hutasafiri tena.?” Nilimuuliza. 82 Tadhkiratul Haqaiq, uk 33. 65


Visa vya Kweli sehemu ya Pili Akajibu: “Nataka kuchukua salfa ya Iran niipeleke China, kwani nimesikia kwamba inauzika kwa bei kubwa kule; kutoka China, nitachukua mabakuli ya kauri na kuyapeleka Roma; kutoka Roma nitanunua hariri nzuri sana ya Kiroma kwa ajili ya kuuza India; kutoka India nitachukua chuma cha India kwa ajili ya kuuza Halab (Syria) kutoka huko nitanunua vioo vya Halabi, na kuelekea Yemeni; kule nitanunua nguo za Yemeni na kuzileta Iran ambapo baada ya hapo nitaacha kusafiri nitapumzika na kushughulika na duka.” Aliendelea kuongea mpaka mwisho akachoka na akashindwa kuongea zaidi, akaniambia: “Ewe Sa’id! Hebu niambie, unafikiria nini kutokana na haya uliyoyasikia hivi punde.” Nikasema: “Unajua kwa hakika kwamba katika sehemu ya mbali sana kutoka nchi ya Ghour (kati ya Hiraat na Ghaznah) wakati mchuuzi alipoanguka kutoka kwenye kipando chake na kufa, mtu mmoja akasema: “Vitu viwili tu vinaweza kumtosha mtu mroho mwenye mapenzi ya dunia – kutosheka au udogo wa kaburi.”83 2. Uroho Kwa Ajili Ya Starehe Yazid ibn Abdul Malik (Khalifa wa kumi wa Banu Umayyah) alikuwa Khalifa baada ya Umar Ibn Abdul Aziz, kinyume na mtangulizi wake, alikuwa akijishughulisha usiku na mchana katika starehe, mikusanyiko ya sherehe, ulevi na kuwa na kushereheka pamoja na wawili wa vijakazi wake, Salamah na Hababah, ambao walikuwa waimbaji wazuri mno. Hatimaye Hababah alimweka kando mpinzani wa Salamah na kuchukua hatamu za khalifa mikononi mwake. Maslamah Ibn Abdul Malik, alimwendea kaka yake Yazid na akamuambia: “Umar Ibn Abdul Aziz alikuwa mtu mwadilifu mno, wakati ambapo wewe, 83 Hikayat-ha-eGulistan, uk. 166. 66


Visa vya Kweli sehemu ya Pili kinyume chake unakunywa pombe na kujishughulisha na starehe mbali mbali na umeutoa ufalme kwa muimbaji, Hababah. Aidha, wakati watu wako wanapenda sana kukuona mara moja, umeangukia mikononi mwake msichana huyo. Achana naye na zingatia masuala ya ukhalifa.” Yazid akaamua kusikiliza ushauri wa ndugu yake na akaamua kusalisha sala za Ijumaa. Wakati huohuo, Hababah amewaelekeza vijakazi wake kumjumlisha punde tu Khalifa akitoka nje. Mara tu vijakazi wale walipomjulisha kwamba ametoka nje, alijitokeza mbele yake, akiwa na fidla mkononi mwake na huku akighani kwa sauti ya kupendeza, akisoma shairi lifuatalao: “Kama mtu anayependezwa mno amepoteza akili yake, usimlaumu; kitu kibaya ni kuonesha uvumilivu kutokana na maumivu yake makali.” Khalifa kumuona mpenzi wake kwenye hali ile na kusikia sauti yake ya kuteka, alifunika uso wake kwa mikono yake. “Hababah! Basi inatosha!” alipiga kelele kisha akasoma shairi lifuatalo: “Maisha si chochote isipokuwa kuishi kwa anasa na kujitukuza mwenyewe; hata kama watu watakulaumu.” Na kisha akapiga yowe: “Ewe mpendwa wa wapendwa! Umesema kweli. Allah amuangamize yeyote yule ambaye ananikosoa kwa kuwa na mapenzi na wewe! Ewe Mtumwa! Nenda kamuambie kaka yangu Maslamah aende msikitini na asalishe sala kwa niaba yangu.” Kisha kwanza alikwenda kwenye ukumbi wake wa starehe, na baadae, kwa ajili ya starehe na shagwe kuu, alielekea Bait al-Rass, ambayo iko karibu na Damascus. Alipokuwa kule alisema kuwaambia watumwa wake: “Watu wanafikiri kwamba hakuna starehe bila machungu yoyote na nataka kuonesha uongo wa dhana yao hii.” Alikaa kule ili kwamba kusiwe na habari au barua kamwe inayoweza kum67


Visa vya Kweli sehemu ya Pili fikia kule. Alikaa kule akiwa amezama kabisa kwenye starehe bila tatizo lolote lile. Hata hivyo, kama majaliwa yalivyokuwa, siku moja mbegu ya komamanga ilimsakama Hababah kooni, na kufuatiwa na kikohozi kikali, na hatimaye akafariki. Usiku na mchana, Khalifa aliipakata maiti ya Hababah mikononi mwake na kumwaga machozi juu yake, na ilikuwa tu kwa msisitizo wa ndugu wa marehemu kwamba mwili ule ulikuwa ukitoa harufu hatimaye ulizikwa. Khalifa naye pia, baada ya tukio hili hakuishi zaidi ya siku kumi na tano alizikwa karibu na kaburi la Hababah.84 3. Isa (as) Na Mtu Mroho Nabii Isa (as) alikuwa anasafiri akiwa amefutana na mtu mmoja, baada ya kusafiri kwa kipindi fulani walishikwa na njaa. Waliwasili kwenye kijiji ambako Isa (as) alimuomba msafiri mwenzake kwenda kijijini hapo kuleta mkate, wakati yeye akiwa anajishughulisha na sala. Yule mtu akarudi na mikate mitatu na akamngojea Isa ili wawe pamoja, lakini kwa vile sala zake ziliendelea kwa muda mrefu, mtu yule kimya kimya akala mkate mmoja. “Iko wapi ile mikate mitatu?” Isa (as) aliuliza baada ya kumaliza kusali sala zake. “Hapana kulikuwa na mikate miwili tu.” Alijibu yule mtu. Muda mfupi baada ya kula chakula chao, walianza tena safari yao na wakiwa njiani walikutana na kundi la paa. Isa (as) aliita mmoja wa paa wale, na kisha akamchinja, na wote wakakaa wakamla. Wakati walipomaliza kula, Isa (as) akaamrisha: Ewe paa! Tembea kwa amri ya Allah!” Paa yule ghafla akafufuka na kuanza kutembea. 84 Rahnama-e-Sa’adat, Jz. 3, uk. 657; Tarikh-e-Tamaddun-e-Islam Jz. 1, uk. 86. 68


Visa vya Kweli sehemu ya Pili Wakati akishuhudia hivi, yule mtu alisimama akiwa hana la kusema na akasema: “Subhanallahi (Mwenyezi Mungu ametakasika).” “Nakuweka chini ya kiapo cha Yule Ambaye amedhihirisha ishara ya uwezo Wake mbele yako! Niambie imekuaje kuhusu mkate wa tatu?” Isa (as) alimuuliza. “Kulikuwa na mikate miwili tu.” Alijibu yule mtu. Waliendelea na safari yao na punde wakawasili kwenye kiunga cha kijiji kikubwa ambako waliona matofali matatu ya dhahabu yamelala mbele yao. “Inaonekana kuwa kuna utajiri mkubwa hapa.” Mtu yule alisema. “Ndio. Tofali moja kwa ajili yako, la pili ni kwa ajili yangu na la tatu nitalitoa kwa mtu aliyekula ule mkate.” Alisema Isa (as). Yule mtu mroho akaropoka: “Nilikula mimi mkate ule wa tatu.” Nabii Isa (as) aliachana na mtu yule na akamkabidhi matofali yote ya dhahabu, akasema: “Matofali yote matatu sasa ni mali yako.” Yule mtu akakaa chini mbele ya matofali yale ya dhahabu na akazama kwenye mawazo ya jinsi gani atayabeba na kuweza kuitumia dhahabu hiyo, wakati akiwa katika kutafakari mara wakatokea watu watatu. Wakati macho yao yalipoangukia kwenye matofali yale ya dhahabu, walimuua mtu yule na kuchukuwa umiliki wa dhahabu ile. Kwa vile walikuwa na njaa, waliamua mmoja wao aende kwenye kijiji cha jirani akanunue mikate. Yule mtu aliyekwenda kununua mikate alijiwazia mwenyewe: “Nitaitia sumu mikate ili wale (wenzangu) wengine wawili wakila wafe na kisha nitachukua matofali yote matatu ya dhahabu kuwa mali yangu.” Wakati huohuo, wale rafiki zake wawili nao vilevile walikula njama 69


Visa vya Kweli sehemu ya Pili kumuua wakati akirudi ili wagawane wao wenyewe mgao wake. Wakati aliporudi walimuua kama walivyopanga, na kwa kuridhika kwao kukubwa kwa kitendo chao hicho, wakaanza kula ile mikate. Kabla ya muda mrefu kupita na wao pia walifariki kutokana na sumu ile iliyokuwa kwenye mikate. Wakati Nabii Isa (as) alipokuwa anarudi aliona maiti zile za watu wanne zikuwa zimelala karibu na matofali yale matatu ya dhahabu, akasema:85 “Hivi ndivyo ulimwengu unavyojiendesha wenyewe pamoja na wale wanaoutamani sana.”86 4. Dhul Qarnain 87 Wakati wa safari yake Dhul Qarnain, aliwasili Dhulumat, ambako alifika sehemu ambapo alimuona kijana amesimama pale ambaye amevaa mavazi meupe, uso wake ameunyanyua angani na mikono yake ameiweka kwenye midomo yake. Yule kijana alipomuona alimuuliza: “Wewe ni nani?” “Dhul Qarnain.” Alijibu. Kijana yule (ambaye ni malaika Israfil) akamuambia: “Wakati Siku ya 85 86 Pand-e-Tarikh, J. 2, uk. 124; Nwarul Nu’Maniyah, uk. 353. 87 Jina hili (maana yake pembe mbili) limetajwa katika Sura ya Al-Kahf ya Qur’ani Tukufu; Ni Alexander yule yule wa kizazi cha Nabii Nuh (as) ambaye alisafiri kwenda mashariki ya ulimwengu na kujenga mji wa Alexandria. Kwa vile alikuwa akikusanya nywele zake katika muundo wa pembe mbili karibu na paji lake la uso, akaja kujulikana mashuhuri kama Dhul Qarnain – ‘Mwenye pembe mbili.’ Aliishi takriban karne mbili na amezishinda na kuzitawala nchi 36 ulimwenguni. 70


Visa vya Kweli sehemu ya Pili Hukumu ikiwadia, nitapuliza Baragumu.” Kisha akaokota jiwe na akampa Dhul Qarnain, akasema: “Kama jiwe hili likishiba na wewe pia utashiba, na kama jiwe hili likitokea kuwa na njaa, na wewe pia utakuwa na njaa!” Dhul Qarnain akalichukuwa jiwe lile mpaka kwa rafiki zake na akaliweka kwenye mizani ili kulipima, lakini licha ya kuwa na uzito sawa dhidi ya mawe elfu moja, bado lilikuwa na uzito zaidi wa mawe yote yakikusanywa pamoja.88 Wakati huo huo, Mtume Khidhr (as) aliwasili; aliweka jiwe upande mwingine wa mizani, aliweka udongo juu ya jiwe ambapo ghafla, wote waliona kwamba mizani ililingana sawa sawa kwa ukamilifu. Dhul Qarnain alitaka kujua sababu hii kutoka kwa Mtume Khidhr (as) ambaye alielezea: “Allah anataka kukuonya kwamba licha ya kuzishinda na kutawala nchi nyingi, bado hujatosheka; mtu hawezi kutosheka mpaka ukafi wa udongo unatupwa kwenye uso wake, na hakuna kinachoweza kujaza tumbo lake isipokuwa udongo.” Dhul Qarnain alianza kulia na akarudi (alikotoka). Katika tukio jingine, alikutana na mtu aliyekuwa amekaa karibu na makaburi akicheza cheza na baadhi ya mifupa iliyooza na mafuvu ya vichwa ambayo yalikuwa yamelala mbele yake. Alimuuliza yule mtu kitu alichokuwa anafanya. Yule mtu akajibu: “Nataka kutenganisha mifupa ya wafalme na ile ya masikini lakini najiona siwezi kufanya hivyo.” Dhul Qarnain alipita na akajiwazia mwenyewe: “Kitendo chake kile kilikuwa kimekusudiwa kwa ajili yangu.” Kisha alifanya makazi yake katika Daumah al-Jandal, 89 aliachana na kiu yake ya kuutawala ulimwengu na akajishughulisha katika kumuabudu Allah. 90 88 Ilikuwa ni kitendo cha kimuujiza, kilichofanywa ili kumshitusha Dhul Qarnain awe makini na kumuongoza kwenye unyenyekevu na utiifu kwa Allah. 89 Fakhr Razi anaeleza: Dhul Qanain alirudi Iraq na akashikwa na maradhi katika mji wa Zur, ambako hatimaye alifariki. (Safinatul Bihar, Jz. 2, uk. 426) 90 Namunah-e-Ma’arif, Jz. 4, uk. 234; Layaliul Akhbar, uk. 46. 71


Visa vya Kweli sehemu ya Pili 5. Ash’ab Ibn Jubair Madanii (alikufa 154 AH) Alikuwa ni mtu mwenye makengeza, upara pande mbili za kichwa na alikuwa hawezi kutamka herufu r, (ree) na l, (lam). Alikuwa na uroho wa hali ya juu sana juu ya utajiri wa dunia na chakula kiasi kwamba hakuonekena kutosheka kuhusiana na vitu hivyo. Alipoulizwa kuhusu sifa yake, alijibu: “Kila mara nikiona moshi unatoka kwenye nyumba ya mtu fulani, huhisi kwamba wanatengeneza chakula kwa ajili yangu na hukaa kungojea chakula. Lakini licha ya kungojea kwa muda mrefu hakuna dalili ya chakula, basi huchovya mkate mkavu kwenye maji na kuula! “Na wakati nikisikia kisomo kikisomwa kwa ajili ya maiti, nahisi kwamba marehemu ametenga theluthi moja ya utajiri wake kwa ajili yangu, na nikiwa na mawazo haya kichwani mwangu, huenda kwenye nyumba ya marehemu na kusaidia kumkosha, kumvisha sanda na mwishowe kushiriki katika kumzika. Lakini baada ya mazishi yake hakuna dalili ya utajiri, narudi nyumbani nikiwa nimechukia. “Na kama nikitembea mitaani hutandaza jicho langu kwa matumaini kwamba pengine mtu wakati akitupa kitu kutoka gorofani kwake au dirishani kumtupia jirani yake, kitu hicho kingeangukia kwenye joho langu.” Inasemekana kwamba wakati fulani alipokuwa anapita mtaani, aliwakuta watoto wanajishughulisha katika michezo. Aliamua kuwaeleza uwongo. “Enyi watoto! Kwa nini mnasimama hapa wakati ng’ambo ya barabara kuna mtu anagawa mzigo wake wa matufaha mekundu na meupe na kuwapa watu bure?” aliwaambia wale watoto. Waliposikia hivi watoto wale walikimbia mara moja kuelekea ng’ambo ile ya barabara. Wakati wakikimbia Ash’ab yeye mwenyewe alipandwa na uroho naye pia akaanza kukimbilia kuelekea ng’ambo ile ya barabara.

72


Visa vya Kweli sehemu ya Pili “Mwenyewe umebuni kisa cha uwongo, sasa kwa nini unakimbia?” watu walimuuliza. Alijibu: “Watoto wale wanakimbia kwa umakini ambapo mimi nakimbia kwa uroho. Huenda pengine kweli kuna mtu huko anagawa matufaha na mimi sitaki niyakose.” 91

31 – Husuda Allah, Mwenye Busara amesema: “Au wanawahusudu watu kwa yale aliyowapa Allah kwa fadhila Zake?...”92 Imam Sadiq (as) alisema: “Muumini wa kweli hufurahia, lakini kamwe hahusudu.”93 Maelezo Mafupi Husuda huchipua kutokana na upofu wa moyo na kukataa baraka za Allah – zile mbawa mbili za kufr na kukosa imani. Uhusuda wa mtu hasidi humuathiri yeye mwenyewe kabla ya kuathiri mwenye kuhusudiwa; kama vile Ibilisi, ambaye husuda yake imechochea nafsi yake na kumfanya kuwa aliyelaaniwa milele ambapo Adam alipata cheo cha Utume. Mizani ya matendo ya mtu mwenye husuda ni nyepesi, na hapo hufanya Jahannam kuwa makazi yake, ambapo mizani ya matendo ya mtu mwenye kuhusudiwa ni nzito, na hapo humpeleka Peponi. Kwa mtazamo huu, Qabil, ambaye alimuua ndugu yake Habil kwa sababu ya uovu wake alijitupa mwenyewe motoni wakati ambapo alimpeleka ndugu yake Peponi. 91 Lataif al-Tawaif, uk. 361. 92 Qur’ani Tukufu 4:54 93 Jame’al-Sa’adat, Jz. 2, uk. 54.. 73


Visa vya Kweli sehemu ya Pili Kama uovu huu ukipenyeza kwenye moyo wa mtu, hawezi kutubia (kwa ajili ya matendo yake) bali badala yake, wakati wote atakuwa anatafuta sababu za kuleta madhara na maumivu kwa wale ambao, ama wako juu yake au wana nafasi nzuri kuliko yake.94 1. Rafiki wa Isa (as) Imam Sadiq (as) amesema: “Jiepusheni na husuda na msiwe na kijicho kuhusiana na ninyi wenyewe kwa wenyewe.” Aliposema haya Imam (as) aliendelea: “Moja ya shughuli ambazo Nabii Isa (as) amezifanya ni kusafiri kutoka mji huu kwenda mji mwingine. Wakati wa moja ya safari zake, alifuatana na mwenza ambaye alikuwa mfupi na ambaye pia ametokea kuwa mmoja wa wahudumu wake. Baada ya muda walifika kwenye bahari. Isa (as) akataja jina la Allah, na akakanyaga juu ya maji na akaanza kutembea bila juhudi yoyote. Yule mwenza alirejea kila alichofanya Isa (as), akataja jina la Allah na akaanza kumfuata juu ya maji. Katikati ya bahari alijiwazia mwenyewe: ‘Isa ni Mtume na anatembea juu ya maji na mimi pia natembea juu ya maji, sasa ana ubora gani aliokuwa nao juu yangu?’ Kabla hata mawazo hayo hayajapita akilini mwake, ghafla alianguka majini na akaanza kumsihi Isa (as) amsaidie. Isa (as) alikamata mkono wake na akamvuta kutoka kwenye maji. ‘Ni nini ulichosema kikakusababisha kuanguka kwenye maji?’ Isa (as) alimuuliza. Yule mwenza akakiri kile kilichompitia katika mawazo yake. ‘Umejiweka katika nafasi mbali na ambayo Allah amekadiria kwa ajili yako, na hiyo ikawa ni sababu ya ghadhabu Yake,’ alisema Isa (as). ‘Omba msamaha ili uweze kukipata tena cheo chako cha zamani.’ Mara tu yule mwenza alipoomba msamaha, alianza kumfuata tena Isa (as) juu ya maji.’” 94 Tadhkiratul Haqaiq 74


Visa vya Kweli sehemu ya Pili Baada ya kusimulia hadithi hii Imam Sadiq (as) alinasihi: “Muogopeni Allah na jiepusheni na husuda.”95 2. Abdullah Ibn Ubayy Wakati watu wa Madina wakiwa katika shamra shamra za kumkubali Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika idadi kubwa, Abdullah Ibn Ubayy, mmoja wa viongozi wa Mayahudi akawa na husuda zaidi juu ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), na hivyo akapanga kumuua. Alimkaribisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Ali (as) na Masahaba wengine kwa ajili ya karamu ya harusi ya binti yake. Wakati huohuo, alichimba shimo kubwa katika ua wa nyumba yake, chini ya shimo lile alijaza panga, mishale na mikuki, na akalifunika kwa zulia juu yake. Kwa nyongeza ya hili, aliweka sumu kwenye chakula na vilevile akaficha baadhi ya mayahudi ndani ya nyumba wakiwa na silaha pamoja na panga zilizotiwa sumu. Madhumuni yake yalikuwa kwamba, wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na masahaba zake watakapokanyaga juu ya zulia watatumbukia ndani ya shimo ambapo wale Mayahudi wenye silaha watawavamia na kuwaua. Ametia sumu kwenye chakula ili kwamba kama mpango huu ukishindikana watauwa kwa sumu iliyoko kwenye chakula. Jibril (as) kwa amri ya Allah aliifichua mipango hii miwili kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambayo ilianzia kwenye husuda na kijicho kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na akamuambia: “Mola wako anasema: Nenda nyumbani kwa Abdullah Ibn Ubayy na kaa popote atakapokuambia kukaa na kula chochote atakacholeta mbele yako, kwani Mimi nitakuwa natosha kwa ajili yako na nitakulinda na mipango yake ya uovu.” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Amir’l-Muuminin (as) na masahaba wengine waliingia nyumbani kwa Abdullah Ibn Ubayy. Abdullah akawaelekeza waelekee kwenye ua wa nyumba. Kama alivyowaomba 95 Shanidani-ha-e-Tarikh, uk. 316; Mahajjatul Baida, Jz. 5, uk. 328. 75


Visa vya Kweli sehemu ya Pili wote walikaa juu ya shimo, lakini kwa mshangao mkubwa wa Abdullah, hakuna kilichotokea. Kisha aliamuru chakula kile chenye sumu kiletwe. Kilipoletwa mbele yao, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuambia Ali (as) asome kisomo kifuatacho juu ya chakula kile: “Kwa jina la Allah, Mponyaji; kwa jina la Allah, Mwenye kutosheleza; kwa jina la Allah, Mwenye kuacha huru; kwa jina la Allah, Ambaye kwa jina Lake hakuna kitu au ugonjwa, katika ardhi au katika mbingu kinachoweza kuleta madhara, na ni Mwenye kusikia Mwenye kujua.” Kisha wote wakala chakula kile na wakatoka nje ya mkusanyiko ule bila madhara yoyote. Mkanganyiko wa Abdullah haukujua mipaka; akachukulia kwamba kile chakula hakikuwekwa sumu na hivyo kuamuru wale mayahudi wenye silaha kula chakula kile, ambapo matokeo yake wote wakafariki. Wakati huohuo, binti yake ambaye alikuwa Bi-harusi aliamua kukaa juu ya zulia lililofunika lile shimo. Mara tu alipokaa alitumbukia ndani ya shimo. Kilio chake kilijaza anga lote, na hatimaye kufariki dunia. Abdullah alitoa amri kwa watumishi wake wasije wakasema sababu za vifo hivyo ndani ya nyumba yake. Wakati habari za tukio hilo zilipomfikia Mtume (s.a.w.w.), alimuuliza hasidi Abdullah ni nini kilichotokea. “Binti yangu alianguka kutoka kwenye paa la nyumba; ama kwa wale wengine walikufa kwa sababu ya kuharisha,” alijibu.96

96 Khazinah al-Jawahir, uk. 344; Biharul Anwar, Jz. 6. 76


Visa vya Kweli sehemu ya Pili 3. Kitendo Cha Ajabu Cha Hasidi Mmoja Wakati wa ukhalifa wa Hadi Abbasi,97 aliishi mjini Baghdadi mtu mmoja tajiri ambaye alikuwa mtu mwema na mwenye hisani. Katika ujirani wake aliishi mtu mmoja ambaye alikuwa juu ya husuda na utajiri wake huo, na haidhuru ni mara ngapi alijaribu kutia dosari hadhi ya tajiri yule na kumuadhiri, hakufanikiwa. Mwishowe, alinunua mtumwa, akamfundisha na kumtumia kutekeleza dhamira yake ya uovu. Siku moja, baada ya mwaka mmoja kupita, alimuuliza mtumwa wake: “Una utii kiasi gani kwa bwana wako?” Yule mtumwa akajibu: “Kama ukinitaka nijitupe kwenye moto, nitafanya hivyo.” Mtu yule alifurahi mno aliposikia hivyo. “Jirani yangu ni tajiri na nina uadui naye. Nataka utekeleze maelekezo yangu. Usiku wa leo, wote mimi na wewe tutapanda juu ya paa la nyumba yake ambako utaniuwa ili ashitakiwe kwa mauwaji yangu na kwa njia hiyo atauawa na serikali kama adhabu ya kuniuawa,” alimuambia yule mtumwa. Kadiri mtumwa yule alivyosisitiza ili asitekeleze maagizo hayo, haikuwezekana na mtu huyo aling’ang’ania shauri lake hilo. Wakati wa usiku, kwa amri ya bwana wake hasidi, mtumwa yule akakata kichwa cha bwana wake juu ya paa la nyumba ya jirani tajiri na akarudi upesi kitandani kwake. Siku iliyofuatia, kifo cha yule hasidi kilijulikana kwa watu na Hadi Abbasi aliamuru yule tajiri akamatwe, na kufanya ahojiwe. Kisha alimuita yule mtumwa na akamhoji naye pia. Yule mtumwa, akaona kwamba yule tajiri alikuwa hana hatia kabisa, ali97 Alikuwa ni ndugu (kaka) yake Harun al-Rashid na ambaye alikuwa khalifa kwa takriban mwaka mmoja ambapo baada ya hapo ukhalifa ulikwenda kwa Harun. 77


Visa vya Kweli sehemu ya Pili fichua lile tukio la yule hasidi na mwishowe kumuuwa. Kusikia tukio hilo, Khalifa akainamisha kichwa chake, akatafakari kwa muda na kisha akanyanyua kichwa chake tena. “Ingawa umeuwa mtu, umeonesha ujasiri na kumuokoa mtu asiye na hatia, kwa hiyo, nitakuacha huru.” Khalifa alimuambia yule mtumwa. Kwa namna hii, madhara ya hasidi yalimrudia hasidi mwenyewe.98 4. Wivu wa Akina Mama Ibn Abi Laila alikuwa ni Kadhi wakati wa ukhalifa wa Mansur Dawaniqi. “Kesi nyingi za ajabu na za kuvutia huletwa mbele ya makadhi na ninataka unisimulie moja ya hizo,” Mansur alimuambia Ibn Abi Laila. Ibn Abi Laila akasimulia: “Siku moja bibi moja dhaifu alinifuata na akanisihi nilinde haki yake na kumuadhibu mbaya wake. Nilimuuliza ni nani aliyetaka kumlalamikia juu yake.” Alijibu: “Mpwa wangu.” Niliamuru mpwa yule kuletwa mbele yangu. Wakati alipowasili, niliona kwamba anaonekana kuwa mchangamfu na umbo la kuvutia. Nilimuuliza sababu za shangazi yake kulalamika ambapo alisimulia suala lote kama ifuatavyo: “Mimi ni binti wa kaka yake huyu bibi kizee na yeye ni shangazi yangu. Baba yangu alifariki wakati nilipokuwa bado mtoto mdogo na shangazi yangu huyu alinichukua na kunilea na kamwe sijakuwa mzembe kuhusiana na kulelewa kwangu. Wakati nilipokuwa mkubwa, kwa idhini yangu, aliniozesha kwa sonara. “Maisha yangu ya furaha yalimfanya shangazi yangu huyu kunionea wivu. 98 Dastan-ha-e-Ma, Jz. 2, uk. 138; Mustadikul Wasa’il, Jz. 3 (katika wasifu wa Fadhlullah Rawandi) 78


Visa vya Kweli sehemu ya Pili Alimpamba binti yake na akamleta mbele ya mume wangu, ambaye alitekwa naye na akataka amuoe. “Huyu shangazi yangu akatoa masharti kwamba angemuozesha binti yake tu kama mamlaka ya kuniweka au kunitaliki inawekwa mikononi mwake binti huyo. Mume wangu akakubalina na sharti hili. “Baada ya muda, shangazi yangu alinifanya mimi niachike na nikatengana na mume wangu. Wakati huo huo mume wa shangazi yangu, ambaye alikuwa safarini, alirejea nyumbani. Baada ya kutambua kilichotokea, kila mara alikuwa akiniliwaza. Nilijitokeza kwake kwa hali ambayo alivutiwa na mimi. Hatimaye, alinipenda na akaonesha nia yake ya kunioa. “Nilimuambia: ‘Nitakubali tu kwa masharti kwamba mamlaka ya kumtaliki shangazi yangu inawekwa mikononi mwangu.’ “Alikubali na baada ya kuolewa naye, nilimfanya shangazi yangu kuachika na niliendelea kuishi na mume wake, ambaye alikufa baada ya muda. Siku moja, mume wangu wa kwanza alinifuata na kuonesha msimamo wake wa kunioa tena. “Nikamuambia: ‘Nakubali kuolewa na wewe tena lakini kwa masharti kwamba lazima unipe mamlaka ya amma kumweka au kumtaliki binti ya shangazi yangu.’ “Alikubali na kwa mara nyingine niliolewa na mume wangu wa kwanza, na kwa mamlaka ambayo imewekwa juu yangu, mimi vilevile nilifanya binti ya shangazi yangu aachike. “Sasa unaweza kuhukumu kwamba sijafanya kosa lolote; yote niliyofanya ni kufidia wivu usio na msingi wa shangazi yangu.”99 99 Pand-e-Tarikh, Jz. 2, uk.156; I’laam al-Naas (cha Atlidii), uk. 44. 79


Visa vya Kweli sehemu ya Pili 5. Matokeo Ya Husuda Wakati fulani, kipindi cha ukhalifa wa Mu’tasim Abbas, msomi mmoja aliwasili katika baraza yake. Mu’tasim alivutiwa sana na mazungumzo yake kiasi kwamba alimuamuru kuja kwenye baraza lake kila baada ya siku chache. Basi mtu yule akawa anakuja mara kwa mara na haikuchukua muda akawa msiri wa Khalifa. Msiri mwingine wa Khalifa akapatwa na husuda kwa mtu huyu na akaogopa kwamba atachukua wizara yake, akafikiria njia za kuondokana naye. Siku moja wakati wa Dhuhr, wakati alipokuwa anaondoka kwenye mkusanyiko wa Khalifa pamoja na yule msomi, alimuomba wafuatane naye nyumbani kwake ili wapate kuongea na kula chakula cha mchana pamoja. Yule mtu akakubali mwaliko huo. Wakati walipokaa na kuanza kula, kitunguu saumu pia kiliwekwa pamoja na chakula na yule mtu akala kwa wingi kile kitunguu saumu. Wakati wa al-Asr, yule hasidi alikwenda kwa Khalifa na kumuambia: “Kwa vile nimesheheneka kwa fadhila na ukarimu wako, siwezi kuficha siri hii kwako. Huyu mtu msomi ambaye ni msiri wako, amekuwa akilalamika kisiri siri kwa watu kwamba harufu mbaya kutoka kwenye mdomo wa Khalifa inamuudhi sana lakini Khalifa mara kwa mara anamuita kwenda kwake.” Khalifa alikasirika sana kusikia hivi na akaagiza msomi yule aletwe mbele yake. Kwa vile amekula kitunguu saumu kwa wingi, alifunika mdomo wake kwa kitambaa na akakaa mbali na Khalifa. Kuona hivyo, Khalifa akawa na uhakika wa ukweli wa maneno ya waziri. Aliandika barua kwa mmoja wa wasaidizi wake na kumuelekeza kumuuwa mtu mwenye barua hiyo na akamuambia yule msomi aipeleke kwa huyo msaidizi. Yule msiri hasidi alikuwa anangojea nje ya chumba. Mara tu yule mtu alipotoka nje baraza la Khalifa akiwa na barua mkononi mwake, msiri yule hasidi akadhani kwamba barua ile ina amri ya Khalifa kwa ajili ya kiasi kikubwa cha pesa ili apewe huyo mtu, na hili likaongeza moto katika husu80


Visa vya Kweli sehemu ya Pili da yake ambayo tayari inawaka moto. Alijitolea kumpa mtu yule dirham elfu mbili ili ampe barua hiyo yeye. Yule msomi akakubali kupokea pesa zile na kisha alikubali ombi la msiri yule hasidi la kutokwenda kwa Khalifa kwa muda wa siku chache. Msiri yule hasidi, aliipeleka barua ile kwa msaidizi wa Khalifa ambaye mara moja alidengua kichwa chake. Siku kidogo baadae, Khalifa akauliza: “Yuko wapi yule msomi? Amekwenda Safari?” Wale waliokuwa pamoja naye wakamuambia. “Hapana, tumemuona hivi karibuni.” Khalifa akaagiza aletwe mbele yake. Wakati alipowasili kwa mshangao mkubwa Khalifa alimuuliza: “Nilikupa barua kupeleka kwa msaidizi wangu, je, hukufanya kama nilivyokuelekeza?” Yule mtu akaelezea tukio la barua ile na waziri yule hasidi. Khalifa akasema: “Nitakuuliza swali; usiongope, Ulimueleza waziri msiri wangu kwamba harufu mbaya ya mdomo ya Khalifa inakuudhi wewe? Yule msomi akakataa kwamba hakusema kitu kama hicho. “Basi kwa nini ulikaa mbali na mimi mara ya mwisho ulipokuja kuniona na ukafunika mdomo wako kwa kitambaa?” akauliza Khalifa yule aliyeshangaa. “Msiri wako alinichukua nyumbani kwake na akanilisha kitunguu saumu hivyo wakati nilipowasili kwenye hadhara yako, niliogopa harufu ile isije ikakuudhi.” Alijibu yule mtu. Kusikia hivi, Khalifa akatamka: “Allahu Akbar!” na kisha akasimulia kadhia yote kwa wale waliokuwa pale pamoja naye. Wote walishitushwa na kushangazwa mno.100

100 Rangarang, Jz. 1, uk. 358. 81


Visa vya Kweli sehemu ya Pili

32 - HAKI NA BATILI Allah, Mwenye Busara Anasema:

“Na sema: haki imedhihiri na batili imetoweka; kwa hakika batili ni yenye kutoweka.” Qur’ani Tukufu 17:81 Imam Ali (as) alisema: “Mtu anayesaidia batili, ameikandamiza (na kuifanyia dhulma) haki.”101 Maelezo Mafupi Kuna hatua nyingi za kutambua haki na batili, na watu hutofautiana mno kuhusiana na kuzikubali na kuzikataa. Kanuni kubwa, kuhusiana na haki, ni kwamba moyo lazima uelekee kwa Allah, amri Zake na uhalisi wa mambo, ambapo kanuni inayohusiana na batili, ni kwamba moyo lazima uwe unachukia vitu ambavyo vimeharamishwa, na kuhusishwa kwa mwingine asiyekuwa Allah, na upande wa ndani lazima uwe mbali na uchafu na fungamano chafu za tamaa ya mwili. Mchamungu anatambua kwamba batili humuondoa mtu kutoka kwenye ukweli na utakoma kuwepo, na ni ukweli tu ambao umejikita ndani na kuendelea kuwepo. Hivyo, mtu lazima ajiambatanishe na watu wakweli na kukaa mbali na watu waongo. 1. Haki ya Maiti ya Mwislamu Zurarah anasimulia: “Nilikuwa nafuatana na Imam Baqir (as) kwenye msafara wa mazishi ya mtu mmoja wa kikureshi. Ata, mwanachuoni wa Makka, alikuwa mmoja wa wale waliokuwepo kwenye msafara ule wa mazishi. Ghafla anga ilijaa kelele za bibi mmoja aliyekuwa anaomboleza. 101 Ghurar al-Hikam, Hadithi Na. 6041. 82


Visa vya Kweli sehemu ya Pili Ata akamshauri anyamaze au vinginevyo hataendelea na msafara huo wa mazishi. Lakini bibi yule aliendelea kulia, hivyo Ata akajitoa kwenye msafara ule wa mazishi. Nilimjulisha Imam (as) kuhusu kuondoka kwa Ata.” “Kwanini?” aliuliza Imam (as) Nilijibu: “Kwa sababu ya maombolezo ya bibi mmoja. Alimuambia anyamaze na alipoendelea kuomboleza, aliondoka.” Imam Baqir (as) akasema: “Kaa na mimi na tutaifuata maiti. Kama tukiona batili pamoja na haki na kuacha haki kwa sababu ya batili hiyo, tutakuwa hatukutekeleza haki ya Mwislamu.” Yaani kusindikiza jeneza na mazishi ya Mwislamu, ambayo ni haki yake, haipaswi kuachwa kwa sababu ya kulia kwa mwanamke huyo (kitu ambacho, kwa mujibu wa madhehebu mengine yasiyokuwa ya Shia, imekatazwa na kuzuiwa). Wakati swala ya maiti ilipokwisha kuswaliwa, ndugu wa marehemu akamuambia Imam (as): “Allah akuhurumie! Unaweza kurudi kwani huna nguvu za kutembea.” Imam (as) aliendelea kufuata msafara wa mazishi. Zurarah akaendelea: “Nilimuambia Imam (as): Ndugu wa marehemu amekuruhusu kuondoka.” “Kama una kazi za kufanya, unaweza kwenda,” alisema Imam (as) kisha akaendelea: “Sikuja hapa kwa ruhusa yake wala sihitaji ruhusa yake kuondoka. Nimekuja hapa kutafuta thawabu, kwani mtu atalipwa kwa kipimo ambacho kwamba hufuata msafara wa mazishi.102 2. Mua’wiyah Ibn Yazid Baada ya miaka mitatu ya ukhalifa wa Yazid ambaye alisababisha mauwaji ya Imam Husein (as), uporaji na uhalifu katika mji wa Madina na 102 Ba Mardum katika Guneh Barkhord Konim, uk. 55; Al-Kafi, Jz. 3 uk. 171. 83


Visa vya Kweli sehemu ya Pili kuifanyia kufuru Ka’ba, ukhalifa ukamfikia mtoto wake Mua’wiyah. Wakati Mua’wiyah anapolala wakati wa usiku, vijakazi wawili walikaa macho, mmoja karibu na kichwa chake na mwingine karibu na miguu yake, ili kumzuiya asipatwe na usumbufu. Usiku mmoja, wakidhania kuwa Khalifa amelela, vijakazi wale wakaanza kuongea wenyewe. “Khalifa ananipenda sana mimi kuliko wewe na kama hakuniona mara tatu kwa siku, anapata taabu sana na hajisikii raha,” yule kijakazi aliyekaa karibu na kichwa cha Khalifa alisema. “Jahannamu ni makazi yenu nyinyi wote,” alisema yule kijakazi mwingine. Akiwa ameshindwa kulala, Mua’wiyah alisikia mazungumzo yale. Kwa kubashiri, alisikia hamu ya kuamka na kumuuwa kijakazi yule, lakini alijizuia na kungojea kusikia zaidi juu ya mazungumzo yao. Kijakazi wa kwanza alitaka kujua kwa nini yule wa pili amesema vile. Alipata jibu lifuatalo: “Mua’wiyah na Yazid, babu na baba yake huyu Mua’wiyah, walikuwa waporaji wa Ukhalifa, kwa vile cheo hiki ni haki na fursa ya watu wa nyumba ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).” Wakati Mua’wiyah aliposikia haya, alizama katika tafakari ya kina na hatimaye aliamua kujiuzulu kutoka kwenye ukhalifa wa bandia na akawajulisha watu kiongozi wa kweli. Siku iliyofuatia aliwataka watu wote kuwepo msikitini. Wakati msikiti ulipojaa, alipanda kwenye mimbari na baada ya kumshukuru Allah, alisema: “Enyi watu! Ukhalifa ulikuwa wa Imam Sajjad (as) ambapo kwamba babu yangu, baba yangu na mimi tuwaporaji wa cheo hiki.”

84


Visa vya Kweli sehemu ya Pili Alishuka kutoka kwenye mimbari, na kurudi nyumbani kwake, akajifungia na akakataa mtu yeyote kuja kumuona. Wakati mama yake alipojulishwa kuhusu kadhia hiyo, alimfuata, akampiga kichwani kwa mikono yake: “Ewe! Natamani kwamba ungekuwa damu yangu ya mwezi na kwamba nisingeshuhudia kitendo kama hiki kutoka kwako!” Mua’wiyah akasema: “Kwa jina la Allah! Natamani ningekuwa tu kama ulivyotamani na kwamba usingenizaa mimi!” Kwa muda wa siku arobaini hakutoka nyumbani kwake. Wakati huo huo, Marwan Ibn Hakam alichukuwa hatamu za ukhalifa. Kisha Marwan akamuoa mama yake Mua’wiyah (Mke wa Yazid) na baada ya siku chache kwa amri yake Mua’wiyah akapewa sumu, akafariki.103 3. Kuukubali Ukweli Usiku mmoja, Sa’id Ibn Musayyab aliingia msikiti wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambako alimuona mtu anaswali. Alikuwa akisoma kwa sauti nzuri. Sa’id alimuagiza mtumwa wake kwenda kumuambia mtu yule asome kwa sauti ya chini. “Msikiti sio mali yetu; huyu mtu ana haki juu yake pia,” alisema yule mtumwa. Sa’id akaamua kuifanya kazi ile yeye mwenyewe. Aliita kwa sauti kubwa: “Ewe Mfanya ibada! Kama unaswali kwa ajili ya Allah, basi shusha sauti yako, lakini kama unafanya ibada yako kwa ajili ya watu (basi tambua) hawatakufaa kwa kitu chochote.” Mtu yule akaona ukweli kwenye ushauri huu, alishusha sauti yake na akamalizia sala yake kwa kusoma kwa sauti ya chini. Mara tu alipomaliza kusali alichukua viatu vyake akatoka msikitini. Baadae akiwa amek103 Dastan-ha Wa Pand-ha, Jz. 9, uk. 154; Jame’al-Nurain, uk. 316. 85


Visa vya Kweli sehemu ya Pili wishaondoka, ilifahamika kwamba mtu yule alikuwa ni Umar Ibn Abdul Aziz, mtawala wa Madina. 104 4. Mlevi Ageuka Kuwa Mwenye Shukurani Dhunnun Misrii anasimulia: “Nilikuja Misri kwa ajili ya matembezi na nilikuwa natembea ukingoni mwa mto Naili huku nikiangalia maji yake, wakati ghafla tu nilimuona ng’e akitembea kwa haraka, nilishangaa ni wapi anakwenda. Mara alipovuka kwenye ukingo wa mto, chura alijitokeza nje ya maji; yule ng’e akapanda juu ya mgongo wake na yule chura akaanza kuogelea katika maji. “Kuna kitu cha ajabu kuhusiana na tukio hili,” nilijiwazia mwenyewe. Nijitupa majini nikaanza kuogelea kuwafuata huko waendako. Niliona kwamba wakati yule chura alipofika nchi kavu, yule ng’e akashuka juu ya mgongo wa yule chura. Niliendelea kumfuata yule ng’e mpaka nilipofika kwenye mti, nikamuona kijana amelele kivulini mwake. Kando yake kuna nyoka mweusi ambaye alikuwa karibu anataka kumng’ata. Ghafla, yule ng’e akakimbia mbele na kumng’ata yule nyoka mgongoni. Yule nyoka akafa pale pale. Baada ya tukio hili yule ng’e akaondoka na kuelekea mtoni, akapanda juu ya mgongo wa chura na kumvusha upande wa pili. Nilisimama huku nikiwa nimepigwa na butwaa. “Kwa hakika mtu huyu ni moja wa auliya (rafiki wa karibu) wa Allah!” nilinong’ona. Nilikuwa karibu nibusu miguu yake wakati nilipogundua kwamba mtu yule alikuwa amelewa, na hili likafanya uongeze mshangao wangu. Nilingojea kwa subira ili yule kijana azindukane kutoka kwenye ulevi wake na wakati alipopata fahamu, aliniona mimi nimesimama karibu yake. 104 Shanidani-ha-e-Tarikh, uk. 18; Mahajjatul Baida, Jz. 2, uk. 230. 86


Visa vya Kweli sehemu ya Pili “Ewe ambaye ni kiongozi wa wakati wako! Umesimama karibu na muovu na kumheshimu,” aliguta kwa mshangao. Nilimuambia aachane kwanza na kuropoka, bali amuangalie yule nyoka kando yake. Alipomuona yule nyoka karibu yake, alijipiga makofi usoni na akauliza ni kitu gani kilichotokea. Nilimuelezea tukio lote la ng’e, chura na nyoka. Aliposikia hivi, na kuona rehema ya Allah juu yake, alinyanyua kichwa chake kuelekea mbinguni na akalia: “Ee Mola! Kama rehema Yako kwa mlevi iko kiasi hiki, ni kiasi gani itakuwa juu ya rafiki Zako?” Kisha baada ya kuchukua wudhu katika mto Naili, alirudi nyumbani kwake. Kuanzia wakati ule na kuendelea alijishughulisha mwenyewe katika kujirekebisha mpaka akafika hatua na cheo ambacho kwamba kila mgonjwa anayemuombea hupona maradhi yake.”105 5. Shukurani za Abu Dharr Wakati Abu Dharr alipopata habari kwamba Mtume amejidhihirisha mjini Makka, alimuelekeza ndugu yake Anis aende akaulizie habari kiasi kuhusiana naye. Ndugu yake yule akaenda Makka, akarudi na kumuelezea Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alivyokuwa. “Hukuweza kutuliza moto ambao unawaka moyoni mwangu,” Abu Dharr akalalamika. Kwa hivyo aliandaa safari ya kwenda Makka yeye mwenyewe. Alipowasili, alitafuta sehemu katika pembe moja ya msikiti akakaa hapo kwa muda wa siku tatu, Ali (as) alimchukua na kumpeleka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na akamsalimia. 105 Jawame al-Hikayat, uk. 46; Siyar as-Salihin. 87


Visa vya Kweli sehemu ya Pili Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipomuuliza jina lake na kutaka kujua habari zake, Abu Dharr alimpa majibu, ambayo yalifuatia kukubali kwake Uislamu. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akamshauri: “Rudi mjini kwako na usikae hapa Makka kwani nahofia kwamba wanaweza kukutesa ukiwa hapa.” “Kwa yule ambaye nafsi yangu iko mikononi mwake, nitatangaza kwa sauti ya juu mbele za watu kuhusu kukubali kwangu Uislamu,” alijibu Abu Dharr. Alielekea moja kwa moja Masjidul-Haram ambako kwa sauti kubwa alishuhudia Upweke wa Allah na Utume wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Waliposikia hivi watu wa Makka walimkimbilia na kumpiga mpaka akadondoka chini, akiwa amezimia. Abbas ami yake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipoona tukio hilo, alijitupa mbele ya Abu Dharr na akawapigia kelele watu wale: “Enyi watu! Ole wenu! Hamuoni kwamba mtu huyu anatokana na kabila la Ghaffar na alikuwa katikati yenu wakati mlipokuwa safarini kwenda Syria?” Kwa maneno haya, aliweza kuokoa maisha ya Abu Dharr. Siku iliyofuatia, hali yake iliendelea kuwa nzuri lakini Abu Dharr kwa mara nyingine tena alitangaza imani yake mpya na alipigwa tena vibaya zaidi. Kwa mara ya pili na siku nyingine nyingi, Abbas aliingilia na kumuokoa kutokana na kipigo chao. Baada ya hili, Abu Dharr akarudi mjini kwake.”106

33 – HALALI NA HARAMU Allah Mwenye Busara Amesema:

106 Paighambar Wa Yaaraan, Jz. 1, uk. 45; Ayan al-Shi’a, uk. 316 88


Visa vya Kweli sehemu ya Pili Enyi watu! Kuleni vilivyomo ardhini halali (na) vizuri… Qur’ani Tukufu 2:168 Imam Kadhim (as) alisema: “Kwa hakika, vitu haramu havikui (na kuongezeka) na kama vikikua, katu haviwi na baraka.”107 Maelezo Mafupi Ulaji wa vitu halali huleta matokeo ya afya nzuri na Akhera nzuri, wakati ambapo kula vitu haramu husababisha ugumu wa moyo – maradhi mabaya mno ya moyo. Athari zake mbaya pia huonekena kudhihiri katika kizazi cha mtu na hata huwa ni sababu ya mtu kuwa mpinzani wa Allah! Mitume na Mawalii Wake kamwe hawali vitu haramu na wakati wote hushauri umma wao kujipatia kipato halali na kujizuia kutokana na vitu haramu. Kwa nini mtu ambaye hatimaye atahitaji kipande kidogo tu cha ardhi na mita chache za kitambaa kwa ajili ya sanda, afanye juhudi kubwa ya kujikusanyia utajiri kwa njia za haramu na kuishia kuuacha kwa wengine, bila ya kutaja taabu zake na majukumu yake? Kwa kuhusiana na kipato cha halali, imesimuliwa kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ibada ina sehemu sabini, iliyo bora zaidi miongoni mwao ni kupata kipato halali. Kitendo cha kupata kipato halali hufanya moyo wa mtu kuwa na nuru, matendo yake ya ibada kukubaliwa, na mtu hujiona mwenyewe katika ulinzi endelevu wa Allah. (Safinatul Bihar, Jz. 1, uk. 297) 1. Mayahudi na Chakula Haramu Wakati Mtukufu Mtume alipokuwa na umri wa miaka saba (wakiwa wametambua dalili za utume ndani yake na hivyo wakaamua kumjaribu) walijadiliana miongoni mwao: “Tumesoma ndani ya vitabu vyetu kwamba 107 Jame al-Sa’adat, Jz. 2, uk. 167. 89


Visa vya Kweli sehemu ya Pili Mtume atajiepusha na chakula cha haramu na chenye utata, hivyo ngoja tumjaribu.” Hivyo, waliiba Ndege (wa kufugwa) na wakamtoa zawadi kwa Abu Talib ili jamaa wa familia yake (akiwemo Mtume) wapate kumla. Wote walikula, isipokuwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambaye hakukigusa chakula hicho. Wakati alipoulizwa, alijibu: “Ndege huyu sio wa halali na Allah amenikinga na vitu vya haramu.” Baada ya tukio hili, Mayahudi wakamshika ndege wa jirani kwa nia ya kulipa baadae na wakampeleka kwa Abu Talib, lakini kwa mara nyingine tena Mtukufu Mtume alikataa kula chakula kile, akasema: “Chakula hiki kina utata (pamoja na kuwa kwake halali).” Wakati mayahudi walipojua matukio haya, wakasema: “Mtoto huyu atakujapata cheo na hadhi ya hali ya juu sana.”108 2. Kwa Njia za Haramu Wakati ambapo Imam Baqir (as) alikuwa mfungwa wa Mansur Dawaniqi (Khalifa wa pili wa Banu Abbas), alikuwa akila chakula kidogo sana. Wakati mmoja, bibi mwema ambaye alikuwa mfuasi wa Ahlul Bayt alitayarisha mikate miwili kwa njia ya halali na akaipeleka kwa Imam (as) ili aweze kuila. Askari wa Gereza akamuambia Imam (as): “Bibi mmoja mchamungu ambaye ni mfuasi wako ameleta mikate hii kama zawadi kwako na ameapa kwamba imetengenezwa kwa njia za halali na anakuomba uile.” Imam (as) akakataa kuipokea mikate ile na akaomba irudishwe kwa bibi yule. “Muambie: Tunajua kwamba chakula chako ni halali; hata hivyo, kwa vile imefanya kitufikie kwa njia zisizo halali, hatustahiki sisi kukila’” 108 Dars-hai Az Zindagi-e-Payambar, uk. 31; Biharul Anwar, Jz. 15, uk. 336 90


Visa vya Kweli sehemu ya Pili alisema.109 3. Mtego wa Shetani Mmoja wa wanafunzi wa Ayatullah Sheikh Murtadha Ansari anaeleza: “Usiku mmoja, wakati tulipokuwa Najaf tukijishughulisha na masomo chini ya malezi ya Sheikh (huyo), nilimuona shetani kwenye ndoto zangu. Alikuwa amesheheni kamba na vigwe vingi mikononi mwake. “Kamba zote za nini?” nilimuuliza. Alijibu: “Huziweka hizi kwenye shingo za watu, huwavuta kuja kwangu na kuwashawishi. Kama ambavyo nimefanya, niliweka moja ya kamba hizi imara katika shingo ya Sheikh na niliweza kumburuza na kumtoa chumbani mwake mpaka katikati ya mtaa ambako kuna nyumba yake, lakini kwa bahati mbaya aliponyoka kwenye makucha yangu na akarudi nyumbani kwake.” Asubuhi yake wakati nilipokwenda kumuona Sheikh, niliisimulia ndoto ile kwake. “Shetani amesema Kweli,” Sheikh akaelezea: “Huyo maluuni alitaka kunipoteza, lakini kwa baraka za Allah, niliweza kuponyoka kwenye mtego wake. Jana, nilikuwa sina pesa za kununua kitu kwa ajili ya nyumbani kwangu. Nilijisemea mwenyewe: ‘Ninayo reyali mmoja kutokana na pesa za Imam al-Zaman (as) Na bado kuna muda ambao naweza kuitumia. Nitaikopa sasa na kuilipa baadae.’ “Nilitoka nyumbani kwangu na pesa hiyo, lakini nilipokuwa nataka kununua kitu nilichotaka, nilijisemea mwenyewe: ‘Hivi ninajuaje kwamba nitakuwa na uwezo wa kulipa deni hili?’ Nilitetemeka na kisha ghafla tu nikaamua kutokuendelea na ununuzi huo. Mara niliporudi nyumbani nilirudisha na kuiweka pesa ile mahali pake.”110 109 Lataif al-Tawaif, uk. 44. 110 Sima-e-Farzanegan, uk. 430; Zindagani Wa Shaksiyyat-e-Sheikh Ansari, uk. 88. 91


Visa vya Kweli sehemu ya Pili 4. Chakula cha Khalifa Wakati mmoja, katika mkusanyiko wa Harun Rashid (Khalifa wa tano wa Banu Abbas), ambao ulijumuisha idadi kadhaa ya mamwinyi, mazungumzo yalihama na kuelekea kwa Bahalul (Bahalul) na uchizi wake. Wakati wa chakula cha mchana ulipowasili, meza ya Mfalme iliandaliwa, na chakula kitamu kilichoandaliwa maalumu kwa ajili ya Harun kiliwekwa mbele yake. Harun alimpa mtumwa wake chakula kile ampelekee Bahalul, kwa matumaini ya kumvutia kwake kwa kitendo hiki cha ukarimu. Wakati mtumwa yule alipoleta chakula kile mbele ya Bahalul, ambaye alikuwa amekaa katika hame la nyumba iliyobomoka, aliona kwamba baadhi ya watu karibu na nyumba ile walikuwa wanatafuna mzoga wa punda. Bahalul alikataa chakula kile. “Tafadhali Kiweke chakula hicho mbele za mbwa hao,” alimuambia yule mtumwa. “Hiki ni chakula maalum kwa ajili ya Khalifa na amekuletea wewe kwa sababu ya kukuheshimu. Usimtukane Khalifa!” alisema yule mtumwa. Bahalul akajibu: “Sema kwa sauti ya chini kwani kama mbwa hao watalijua hili, hata wao watakataa kula chakula hiki.” (Kwa vile kuhusiana na utajiri wa Khalifa, haijulikani ni sehemu gani ya utajiri huo ni halali na sehemu ipi ni haramu).111 5. Aaqil Wakati fulani, Aaqil, ndugu yake Imam Ali (as), alipoona baadhi ya misaada ya fedha, alimuomba Imam (as) ampe kitu kidogo kwani alikuwa masikini. Imam (as) akasema: “Kuwa na subira mpaka nigawanye pesa 111 Hikayat-ha-e-Shanidani, Jz. 1, uk. 120. 92


Visa vya Kweli sehemu ya Pili hizi miongoni mwa Waislamu, kisha nitakupa na wewe pia mgao wako.” Lakini wakati Aaqil aliposisitiza ombi lake hilo, Imam (as) akamuambia mtu mmoja pale: Mchukue Aqil mpaka sokoni na muambie avunje kufuli la moja ya maduka ya hapo na kisha achukue kila kitu kutoka humo.” Mara moja Aqil akasema: “Unataka mimi nishikwe kama mwizi?” “Na mimi kwa kukupa wewe pesa kutoka kwenye hazina ya umma wa Waislamu, unataka mimi nifungwe kama mwizi?” Imam alisema. “Nitakwenda kwa Mua’wiyah,” alijibu Aqil. Imam Ali (as) akamshauri afanye kama anavyotaka. Aqil alikwenda kwa Mua’wiyah kuomba msaada kutoka kwake ambapo Mua’wiyah alimpa dirham elfu mia moja na akasema: “Panda juu ya mimbari na uwajulishe watu jinsi Ali alivyokufanyia na jinsi nilivyoshirikiana na wewe.” Aqil alipanda juu ya mimbari na baada ya kumshukuru Allah, akasema: “Enyi watu! Wakati nilipoomba kutoka kwa Ali (as) dini yake, alinitupa mimi – ndugu yake, na akashikamana na dini yake. Hata hivyo, wakati nilipomfuata Mua’wiyah alinipa kipaumbele juu ya dini yake.”112

34- UVUMILIVU Allaha, Mwenye Busara, anasema:

“Kwa hakika Ibrahim alikuwa mpole, mwenye kumuomba sana Allah, mwepesi wa kurejea. Qur’ani Tukufu 11:75. Imam Sadiq (as) alisema: “Kama wewe sio mvumilivu, basi jioneshe wewe mwenyewe kama mtu 112 Pand-e-Tarikh, Jz. 1, uk. 180; Al-Sawaiqul-Muhiriqah. 93


Visa vya Kweli sehemu ya Pili mwenye uvumilivu.”113 Maelezo Mafupi. Uvumilivu ni taa ya Allah ambayo kutokana na mwanga wake mtu hupata ujirani wa Allah. Mtu mvumilivu, katika kukabiliana na kutendewa vibaya na familia, marafiki na watu wengine, huonesha uvumilivu kwa ajili ya ridhaa ya Allah. Ukweli wa uvumilivu ni wakati mtu licha ya kuwa na uwezo na nguvu za kulipiza kisasi, humsamehe mtu aliyemsababishia madhara na maumivu; tunasoma kwenye vitabu vya du’a: “Ewe Mola, neema Zako ni za thamani sana na uvumilivu Wako ni mkubwa sana, kiasi kwamba utaniadhibu kwa ajili ya matendo yangu na kunifedhehesha kwa ajili ya dhambi zangu.” Hivyo, kwa vile umuhimu wa muumini wa kweli ni zaidi kuliko wa mtu yeyote yule, ni sharti kwake kuonesha uvumilivu katika kukabiliana na matatizo na usumbufu wa watu wajinga, kwani kama angesimama na kukabiana nao, ingelikuwa ni sawa na kuongeza mafuta kwenye moto na kulikuza tu suala hilo.114 1. Usumbufu wa Mpenda Njiwa Sheikh Abu Ali Thaqafi alikuwa na jirani ambaye ni mpenda njiwa. Njiwa wake wakati mwingine hutua juu ya paa la nyumba ya Sheikh na ili kuwafanya waruke, huwatupia mawe kitendo ambacho husababisha matatizo na usumbufu kwa Sheikh. Siku moja, Sheikh alikuwa amekaa nyumbani kwake akisoma Qur’ani Tukufu, wakati jirani yule alipowatupia jiwe njiwa. Jiwe lile lilimpiga Sheikh kwenye paji lake la uso, likamuumiza na kusababisha damu kuchuruzika chini kutoka kwenye paji lake la uso. Wafuasi wa Sheikh walifurahi na wakajisemea wenyewe miongni mwao: 113 Jame’ al-Sa’adat, Jz. 1, uk. 297. 114 Tadhkiratul Haqaiq, uk. 54. 94


Visa vya Kweli sehemu ya Pili “Kesho, Sheikh atalalamika kwa gavana wa mji na mara moja tutaondokana na usumbufu wa mpenzi huyu wa njiwa.” Sheikh akamuita mtumishi wake na akamtuma alete tawi la mti. Wakati mtumishi yule alipoleta lile tawi, Sheikh Akamuambia: “Sasa chukua tawi hili na umpelekee jirani yangu mpenda njiwa na muambie kwamba asitupe mawe na badala yake atumie hili tawi kuwafanya njiwa waruke.”115 2. Uvumilivu Kwenye Matendo ya Amri Wakati ambapo Hisham Ibn Ismail (mjomba wake Abdul Malik Ibn Marwan) alipokuwa gavana wa Madina, akiwa ameteuliwa na Yazid, alizoea kumnyanyasa Imam Sajjad (as) kwa nguvu sana. Wakati alipoondolewa katika wadhifa huo, Walid alichukuwa nafasi yake, akaagiza (Hisham) akamatwe na awekwe ndani ili watu wote wale ambao wana malalamiko dhidi yake waweze kujitokeza na kuomba fidia. Hisham akasema: “Simuogopi yeyote isipokuwa Ali Ibn Husein (as).” Hofu hii ni kwa sababu alimpatisha Imam (as) matatizo mengi. Hata hivyo, Imam (as) aliwaelekeza baadhi ya watu anaowajua (na ambao wamesaidia katika kukamatwa kwa Hisham) wasimsababishie madhara yoyote, hata kutumia maneno mabaya. Pia alimpelekea ujumbe Hisham unaosema: “Sikiliza, kama huna uwezo wa kulipa pesa ambazo zimelazimu juu yako kama fidia na adhabu, tunaweza kupanga ili zilipwe kwa ajili yako. Nakuhakikishia usiwe na wasi wasi, amma kuhusiana na sisi au kuhusiana na wafuasi wetu.” Wakati Hisham alipotambua uungwana wa Imam (as) na heshima aliyoonesha kwake licha ya tabia yake mbaya, alisoma kwa sauti ya juu:116 115 Namunah-e-Ma’arif, Jz. 4, uk. 368

116 Qur’ani Tukufu 6:124

95


Visa vya Kweli sehemu ya Pili “…Allah ndiye Ajuaye zaidi wapi pakuweka ujumbe wake…” 117 3. Qais Minqarii Msimuliaji mmoja anasema: “Nilijifundisha uvumilivu kutoka kwa Qais Minqarii, siku moja nilimuangalia akiwa anahubiri na kunasihi watu akiwa ameegemea kwenye upanga wake mbele ya nyumba yake. Wakati akiwa anahubiri, niliona kwamba baadhi ya watu walikuja kwake na maiti na pamoja na mtu mmoja ambaye mikono yake ilikuwa imefungwa. “Huyu ni mpwa wako na amemuuwa mtoto wako,” walimuambia Qais. Msimuliaji akaendelea: “Wallahi Qais hakuacha kuendelea na khutba yake mpaka alipomaliza, ambapo baada ya hapo alimgeukia mpwa wake na akasema: “Ewe mpwa! Umetenda kitendo kiovu sana, kumuasi Mola wako, kukata undugu wako, kutumia silaha yako kwa (kumuuwa) mtu wa koo wako mwenyewe na umewavunjia heshima watu wa ukoo wako!” Kisha, akamgeukia mtoto wake mwingine, akasema: “Fungua mikono ya binamu yako, mzike ndugu yako na mpe mama yako kutoka kwenye mali yangu, ngamia mia mmoja kama fidia kwa ajili kifo cha ndugu yako, kwa vile yeye anatokana na familia tofauti,”118 4. Imam Hasan na Msiria Siku moja Imam Hasan (as) alikuwa amekaa katika sehemu yake wakati alipokabiliwa na mtu mmoja ambaye ametokea Syria. Mara tu mtu yule macho yake yalipoangukia kwa Imam (as) alianza kumlaani na kumtukana; lakini Imam (as) alikaa kimya mpaka alipomaliza hasira zake. Wakati aliponyamaza, Imam (as) alimgeukia, akamsalimia, akatabasamu 117 Ba Mardum katika Guneh Barkhord konim, uk. 22; Tarikh Tabari, Jz. 8, uk. 61 118 Payghambar Wa Payghambar Wa Yaran, Jz. 5, uk. 180; Asad al-Ghabah,

Jz. 4, uk. 229 96


Visa vya Kweli sehemu ya Pili na kisha akasema: “Ndugu yangu! Naona wewe ni mgeni hapa na kwa dhahiri umekosea. Kama unataka mimi nipuuze tabia yako na nikusamehe, nitafanya hivyo; kama unataka kitu chochote kutoka kwangu, nitakupatia; kama unataka mimi nikuongoze, nitafanya hivyo; kama una njaa, nitakulisha; kama una haja ya nguo, nitakupatia; kama ni muhitaji, nitakupa yale yote unayohitaji; kama umefukuzwa, nitakupatia hifadhi na kama una hamu ya kitu, nitatekeleza kwa ajili yako. Kama unaweza kuwa mgeni wangu kwa muda utakaokaa hapa, itakuwa kwa faida yako, kwa vile nyumba yangu ni kubwa na ina huduma zote.” Aliposikia maneno haya ya Imam Hasan (as), yule mtu aliangua kilio na akasema: “Nashuhudia kwamba wewe ni Khalifa wa Allah juu ya ardhi na Allah anajua zaidi wapi pakuweka ujumbe Wake na ukhalifa. Kabla ya mkutano huu na wewe, nilikuwa nakuchukulia wewe na baba yako kama maadui wangu wakubwa miongoni mwa watu, lakini sasa umpenzi kwangu zaidi ya wote.” Mtu yule alikaa na Imam Hasan (as) kama mgeni wake kwa muda wote aliokaa Madina, na hatimaye akawa mfuasi mwaminifu wa Ahlul Bayt. 119 5. Sheikh Ja’far Kashif al-Ghita Sheikh Kashif al-Ghita alikuwa mmoja wa wanachuoni maarufu ambaye alikuwa anajulikana kuwa mwenye uvumilivu wa hali ya juu. Siku mmoja, Sheikh aligawanya pesa miongoni mwa watu masikini wa Isfahan ambapo baada ya hapo alianza kuongoza Swala za jamaa. Katikati ya Swala mbili, wakati watu walipokuwa wanashughulika na maombi, Sharifu120 mmoja masikini aliingia msikitini, akasimama mbele ya Sheikh na kwa ukali alipiga kelele: “Ewe Sheikh! Kabidhi pesa za babu yangu (khums) kwangu.” 119 Mutahal Amal, Jz. 1, uk. 222. 120 Mwenye Nasaba na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kupitia Hasan na Husein kwa upande wa watoto wa kiume. 97


Visa vya Kweli sehemu ya Pili “Umechelewa kuja; kwa bahati mbaya hakuna kilichobakia kwangu,” Sheikh akajibu. Yule Sharifu kwa ufedhuli mkubwa, alimtemea mate kwenye ndevu zake! Badala ya kujibu kwa ukali, Sheikh akatandaza joho lake na akaanza kutembea kwenye safu za watu, akisema: “Yeyote yule anayezipenda na kuziheshimu ndevu za Sheikh, lazima amsaidie Sharifu huyu.” Watu wakiwa wameshuhudia kilichotokea kati ya wawili hao, mara moja walitii na punde tu joho la Sheikh lilijazwa pesa. Alimkabidhi yule Sharifu pesa yote kisha akaendelea kusalisha Swala ya Alasiri.121

35- STAHA (HAYA) Allah, Mwenye Hikma anasema:

“(Tabia) kama hiyo humuudhi Mtume: anaona haya kuwafukuza, lakini Allah haoni haya (kuwaeleza) ukweli.” Suratul Ahzab; 33:53 Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Kila aina ya staha ni wema”122 Maelezo mafupi Staha ni nuru, ambayo kiini chake ni imani, na hivyo staha hutokana na imani na inapaswa kuongezewa nguvu kwa imani. Mtu mwenye staha hujipatia kila aina ya wema - kujiepusha na kitendo kinachochukiza na kichafu – lakini yule asiye kuwa na staha na aibu, hupata kila aina ya uovu, ingawa anaweza kuonekana akijishughulisha na 121 Seema-e-Farzanegan, uk. 338; Fawaid al-Radawiyyah, uk. 74. 122Jame al-Sa’adat, Juz. 2, uk. 385 98


Visa vya Kweli sehemu ya Pili matendo ya ibada. Mtu asiyekuwa na sifa hii (ya staha) atanyimwa rehema na ataadhibiwa kwa adhabu ya Akhera. Staha katika hatua za awali, hubadilika na kuwa “hofu ya kumuogopa Allah,” ambapo katika hatua ya mwisho hubadilika na kuwa “utambuzi juu ya Allah.” Mtu mwenye sifa hii huwa anamjali Allah, huwa mbali na madhambi na uasi, na huwa amejivisha heshima na upendo”123 1. Musa na mabinti wa Shuaib Wakati Musa alipomuua mtu wa kutoka Qabt, wafuasi wa Firaun walipanga kumuua, na hivyo alikimbia kutoka Misri. Aliposafari kati ya siku tatu na nne na kwa kustahamili shida nyingi, alifika katika mji wa Madiyan, ambapo alikaa na kupumzika chini ya mti uliokuwa karibu na kisima. Alibaini kwamba kulikuwa na wanawake wawili waliokuwa wamesimama karibu na kisima, wakisubiri wachungaji wamalize kuchota maji ili nao pia wachote maji kutoka kwenye kisima. Aliwaelekea na akajitolea kuwachotea maji. Kama matokeo ya msaada wa Musa, wale wanawake walipeleka maji nyumbani mapema kuliko ilivyo kawaida na hili lilimfanya baba yao, Shuaib (as) kuuliza “Mmeweza vipi leo kuleta maji mapema kuliko ilivyo kawaida?” Walimsimulia kisa chote kisha Shuaib akasema, “Nendeni kwa huyu mwanaume na kisha mleteni kwangu ili nimlipe kwa kitendo chake.” Wale wanawake walimfuata Musa (as) walipomfikishia tu ujumbe wa baba yao, alikubali mara moja, kwani alikuwa na njaa, amechoka na mgeni katika sehemu hiyo. Wale wanawake waliongoza njia huku Musa (as) akiwafuata, lakini walivyokuwa wakitembea, miraba ya miili yao ilionekana na hili halikuonekana ni jema kwa staha ya Musa (kutazama). Hivyo aliwaambia: “Mimi nitaongoza njia wakati nyinyi mtakuwa mkifuata nyuma yangu; nirekebisheni nikiwa ninaelekea muelekeo usio (au tupeni mawe mbele yangu ili nijue sehemu ya kwenda. Kwani sisi watoto wa Yaqub, 123 Tadhikratul Haqaiq, uk.93 & 128. 99


Visa vya Kweli sehemu ya Pili huwa hatutizami migongo ya wanawake.” Wale wanawake walipokwenda kwa Shuaib (as) na kumsimulia tukio hilo, alimuozesha Musa binti yake, kutokana na msaada wake, staha, utasi (wa roho), uaminifu na nguvu za kimwili.124 2. Staha ya macho Imesimuliwa katika Tafsir Ruhul-Bayan kwamba katika mji mmoja waliishi ndugu watatu. Ndugu mkubwa alikuwa ni muadhini wa msikiti wa mji na alikuwa akiadhini kutoka juu ya mnara wake. Baada ya kutoa huduma zake kwa miaka kumi, alikufa na ndugu wa pili alichukua kazi ya kaka yake. Miaka michache huyu ndugu pia alikufa na watu walimfuata ndugu wa tatu wakimsihi akubali jukumu hili na asiache sauti ya adhana ikakoma. Lakini alikataa kabisa. “Tutakupa kiasi kikubwa cha fedha,” walimwambia. Lakini alijibu “Hata mkinipa mara mia ya kiasi hiki (bado) sitakubali kazi hii” “Je kusoma adhana ni kitendo kiovu? Walimuuliza. “Hapana, lakini sitaadhini nikiwa juu ya mnara.” Walipotaka kujua sababu ya kukataa kwake, alisema, “Mnara huu ni sehemu ambayo iliyosababisha ndugu zangu wawili mafukara wafe bila imani. Nilikuwa karibu na kaka yangu mkubwa alipokuwa anavuta pumzi yake ya mwisho na nilitaka kusoma Suratul-Yasini ili kupunguza maumivu ya kifo chake lakini alinikataza kusoma. “Ndugu wa pili pia aliondoka kwa namna hiyo hiyo. Ili kujua sababu ya tatizo hili Allah alinirehemu nilimuona kaka yangu mkubwa katika ndoto, akiwa katika adhabu. Nikamwambia: “Sitakuachia mpaka uniambie kilichosababisha nyinyi wote wawili mfe bila imani.” Nilisema: “Kila 124 Tarikh-e-Anbiya, Jz. 2, uk. 65-71. 100


Visa vya Kweli sehemu ya Pili tulipokuwa tukipanda kwenye mnara tulikuwa tukiwatizama wanawake katika majumba ya watu, bila aibu na staha. Hiki kitendo chetu kilikuwa kikituingia mioyoni na kuzitawala fikra zetu, zikituacha tukiwa hatumjali Allah, na hiki ndicho kilichotusababisha tuwe waovu na tukachuma akhera mbaya.”125 3. Zulaikha Wakati Zulaikha alipomfuata Yusuf ili kukidhi haja zake na akapendekeza kufanya dhambi, ghafla Yusuf alibaini kwamba alikuwa amefunika kitu kifuani kwa kipande cha nguo. “Ulifanya nini? alimuuliza “Nimefunika uso wa sanamu ili lisinione ninapofanya dhambi, alijibu. Aliposikia hivi Yusuf alisema, “Ikiwa unaonyesha haya na staha mbele ya jiwe ambalo halioni, (basi) inanifaa zaidi kuonyesha aibu na staha mbele ya Yule, ambaye huona na ambaye huyajua ya dhahiri kuhusu mimi na yaliyofichika ndani yangu.126 4. Staha ya Amirul Mu’uminin Utaratibu wa ndoa kati ya Imam Ali (as) na Hazrat Zahra (as) ulisomwa mwaka wa 2 Hijiria, lakini harusi ilifanyika baadaye (baada ya mwezi mmoja au mwaka mmoja kwa mujibu wa taarifa zinazotofautiana). Katika kipindi hiki Ali (as) kutokana na haya, alikuwa hawezi kutamka jina la Fatimah (as) na Fatimah naye alikuwa hivyo hivyo. Hii iliendelea mpaka siku moja wake za Mtukufu Mtume (s.a.w.w) walipomfuata Ali (as) na kuuliza: “Kwa nini unachelewesha sherehe ya harusi? Ikiwa unahisi aibu au uoga, turuhusu tukamueleze Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) juu ya hili” Imam Ali (as) aliwapa ruhusa. 125 Riwayat ha wa Hikayat-ha, uk.105, Dastan-ha-Parakanden, Juz.1, uk.123 126 Namunah-e-Ma'arif, Jz. 4, uk. 385; BahrulMahajjah (cha Ghazzali), uk. 94. 101


Visa vya Kweli sehemu ya Pili Walifika mbele ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). “Ewe Mtume wa Allah! Kama Khadija angekuwa hai, harusi ya Fatimah ingemfanya kuwa na furaha mno, na Fatimah (as) pia angefurahi kumuona mume wake. Ali pia anamsubiri mkewe, tunalisubiria tukio hili la furaha.” Aliposikia jina la Khadija machozi yalitirirka katika macho yake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Huku akishusha pumzi alisema: “Yuko wapi mfano wa Khadija?” Na kisha akaongeza, “lakini kwa nini Ali hakunifuata moja kwa moja kwa ajili ya hili?” Wake (zake) wakajibu, “Staha yake ilimzuia kufanya hivyo” Aliposikia hivi, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwaagiza wafanye maandalizi ya harusi.127

36. HOFU Allah, Mwenye hekma amesema:

“Na muombeni kwa hofu na kutumainia.” Suratul Araf; 7:56 Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Mkamilifu zaidi miongoni mwenu katika akili ni yule mwenye kumuogopa zaidi Allah zaidi.”128 Maelezo mafupi Hofu juu ya Allah ni mlinzi wa moyo; hii ni kwa sababu mtu mwenye hofu, hubaki ni mwenye kukumbuka radhi za Mwenyezi Mungu na hukwea katika vilele vilivyotukuka. Hushuhudia vitisho vya Mwenyezi Mungu na maonyo, na hivyo hujiepusha na matendo ambayo huchochewa na matamanio ya kinyama na dunia. 127 Fatimah al-Zahra, uk. 283 128 Jame’al-Sa’adat, Juz. 1, uk. 225 102


Visa vya Kweli sehemu ya Pili Mtu anayemuabudu Allah kwa sababu ya kumhofu kamwe huwa hapotoki na hatimaye hufikia lengo na kusudio lake. Anaweza vipi kumudu kutokuwa na hofu hususani kwa vile hana maarifa ya hatima yake ya mwisho itakuwaje na hajui kitabu chake cha amali kama kitakuwa chepesi au kizito. Mtu mwenye hofu hujikuta akiwa katika hofu mbili – hofu ya yaliyopita na hofu ya yajayo. Hofu husaidia kuikandamiza roho isiyo makini na roho ya mtu inapokandamizwa katika matamanio yake ya kinyama na yanayobadilika, moyo wake hupata uhai. Hii husababisha ustahamilivu ambao hatimaye huandaa mazingira kwa ajili ya moyo kuwa na matumaini na huwa na matumaini (ya rehema za Mwenyezi Mungu).129 1. Kijana Mwenye Hofu Salman Farsi alikuwa akipita katika soko la wahunzi la mji wa Kufa alipoona kundi la watu limemzunguka kijana aliyekuwa amelala chini, (akiwa) hana fahamu. Watu walipomuona Salman, walimuomba asome dua ili yule kijana azinduke. Salman alipokaribia yule kijana alisimama na kusema “Sina tatizo. Nilikuwa ninapita tu katika soko hili nilipowaona wahunzi wakigonga chuma kwa nyundo yao ya chuma na hili lilinikumbusha yale aliyoyasema Allah ndani ya Qur’ani: ‘Kwa nyongeza kutakuwa na fimbo ya chuma (kuwaadhibia)’”130 (Suratul Hajj; 22:4). Aya hii ilipopita akilini mwangu, nilikumbwa na hali hii. Salman alivutiwa na kijana huyo, alimpenda na kumfanya (kuwa) ndugu yake. Mara zote walikuwa marafiki mpaka siku moja alipougua na alikuwa anakaribia kufariki. Salman alikaa chini karibu na kichwa chake na akimueleza Izrail, alisema: “Ewe Izrail! kuwa mvumilivu na mpole kwa mdogo wangu na kuwa mtaratibu kwake.” 129 Tadhkiratul Haqaaiq, uk. 83. 130 Qur’ani Tukufu 22:21 103


Visa vya Kweli sehemu ya Pili “Ewe mja wa Allah! Mimi ni rafiki wa waumini wote na ni mpole kwao wote” Izrail alijibu.131 2. Lugha ya jiwe isiyosema (isiyotoa sauti) Imesimuliwa kuwa katika safari zake, mmoja wa Mitume alilikuta jiwe na akaona kwamba kiasi kikubwa cha maji kilikuwa kikitoka katika jiwe (hilo) ambalo lilisema: “Tangu niliposikia kuwa watu na mawe watakuwa ni kuni za moto wa Jahannam, nimekuwa katika hali ya kutoa machozi (kwa hofu kwamba ninaweza kuwa miongoni mwa mawe hayo).” Kisha jiwe likamuomba Mtume huyo aliombee ili libaki kusalimika na moto (wa Jahannam), na mtume huyo alikubali ombi lake na akaliombea. Ilitokea kwamba baada ya kipindi, mtume huyo alipita tena sehemu ile na alipoona kwamba bado maji yalikuwa yanaendelea kutoka katika jiwe kama zamani, akaliuliza: “Ni nini kinakufanya ulie sasa?” Jiwe lilijibu: “Kabla sijaridhishwa na kuokolewa kwangu kutokana na moto (wa Jahannam) machozi yalitokana na hofu, lakini sasa, ninalia kwa shukurani na kutokana na furaha.132 3. Kuadhibiwa kwa Moto Wakati fulani, Amirul-Mu’minin (as) alikuwa na sahaba zake, mtu (mmoja) alipomfuata na kusema: “Ewe Amirul-Mu’minin! Nitakase kwani nimefanya liwati na mvulana.” 131 Dastan-e-Jawanan, uk. 94. 132 Shanidani-ha-e Tarikh, uk.388; Mahajjatul Baida, Juz.7, uk.142 104


Visa vya Kweli sehemu ya Pili “Nenda nyumbani kwani unaonekana kuwa umeathiriwa na nyongo au umechanganikiwa.” Alishauri Imam (as). Siku ya pili yule mtu alikwenda tena na kukiri kitendo chake kichafu lakini Imam (as) alirudia alichokuwa amekisema mwanzo. Siku ya tatu pia alikiri tena na Imam (as) akarudia ushauri wake. Mtu yule alipowasili siku ya nne na kukiri uhalifu wake, Imam (as) alisema: “Sasa kwa vile umekiri mara nne, chagua moja kati ya adhabu tatu, ambapo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ameziweka kwa ajili ya kitendo hiki - kukatwa kichwa kwa upanga, kutupwa chini kutoka kwenye sehemu ya juu au kuchomwa huku mikono na miguu yako imefungwa.” “Ni adhabu gani kati ya hizi ni kali zaidi kwangu?” Aliuliza yule mtu. “Kuungua kwa moto” alisema Imam. “Ewe Ali (as), ninachagua adhabu hii” Imam (as) akamuambia ajiandae kwa adhabu (kwa adhabu hiyo). Yule mtu alisimama, akasali rakaa mbili na kuomba: “Ewe Mola! Nimefanya dhambi na wewe unanifahamu. Kwa kuogopa hasira yako, nimemuendea mrithi na binadamu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na nimemuomba anitakase kwalo. Aliniomba nichague moja kati ya adhabu tatu na nimechagua kali zaidi. Ewe Mola! Ninakuomba kwa rehema zako ukufanye kuungua kwangu katika ulimwengu huu (kuwe) ni fidia ya dhambi yangu na usinichome huko akhera!” Baada ya kusema haya, alisimama akaanza kulia na kisha akajitupa katika shimo la moto uliokuwa unafoka. Imam (as) akaanza kulia alipoona hivi na halikadhalika masahaba zake; kisha akasema kwa sauti kubwa: “Ewe mtu! Inuka kwenye moto kwani umewafanya malaika walie. Allah ameikubali toba yako. Toka na usirudie kitendo hicho!” Imesimuliwa katika hadithi nyingine kwamba mtu alimuuliza Ali (as), 105


Visa vya Kweli sehemu ya Pili “Ewe Amirul-Mu’minin (as)! Unabatilisha adhabu ya Allah?” Imam Ali (as) akajibu, “Ole wako! Kila panapokuwa na Imam aliyeteuliwa na Allah na muovu akaja kutubia dhambi yake, ni wajibu kwa Allah kumsamehe.”133 4. Wenye Hofu Wakati aya hii: “Na kwa hakika moto wa Jahannam ni mahala walipoahidiwa wao wote. Una milango saba, kutakuwa kundi tofauti miongoni mwao,”134 ilipoteremshwa kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), alilia sana mpaka akawafanya masahaba zake pia walie, lakini hakuna aliyejua kile Jibril alichokiteremsha kilichomfanya Mtume (s.a.w.w.) alie namna hiyo. Mmoja wa masahaba alikwenda kwa Fatmah (as) na kumjulisha juu ya tukio hilo. Akivaa baibui lake lililokuwa limeshonwa viraka kumi na mbili kwa majani ya mchikichi, akitoka nje ya nyumba. Macho ya Salman Farsi yaliangukia kwenye hijabu hiyo, aliitizama kwa mshangao kisha akaanza kulia na kusema. Wafalme wa Urumi na Iran wanavaa nguo za hariri na zilizopambwa kwa dhahabu lakini binti wa Mtukufu Mtume anajitanda kwa hijabu kama hiyo! Fatma (as) alipokuja kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Mtume alimwambia Salman: “Binti yangu yupo katika kundi ambalo limechukua umuhimu mkubwa katika utii na unyenyekevu kwa Allah”. Kisha Fatima (as) akauliza, “Baba! Ni nini kilichokuhuzunisha?” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisoma aya zilizoletwa na Jibril. Kutajwa kwa moto wa Jahannam na adhabu ya moto kulimuacha na hofu kiasi kwamba magoti yake yalishindwa kuubeba uzito wake na alianguka kwenye sakafu 133 Dastan-ha-e-Zindagi.e- Ali(as), uk. 51; Qadhawat-ha-eMuhayyir al-Uqul 134 Suratul Hijr 15 : 43-44 106


Visa vya Kweli sehemu ya Pili na kusema: “Ole wake atakayeuingia moto” “Oh, natamani ningekuwa kondoo niliyeliwa na ngozi yangu ikachanwa ili kamwe nisijekuwa niliyepaswa kusikia juu ya moto wa Jahannam,” alisema Salman. “Oh natamani mama yangu asingekuwa amenizaa ili kamwe nisisikie juu ya moto wa Jahannam” alisema Abu Dharr. “Natamani ningekuwa ndege katika jangwa ili nisiwe na kuhesabiwa wala adhabu, na nisiwe nimesikia juu ya moto wa Jahannam” kisha akiweka mikono yake kichwani, alianza kulia, “Oh! Ni safari ndefu iliyoje siku ya Hukumu! Ole wao wale ambao hawakujiandalia masurufu kwa ajili ya siku ya Hukumu, wataongozwa kuelekea motoni; Enyi wagonjwa ambao mtakuwa katika vifungo vya mateka na ambao majeraha yao kamwe hayatatibiwa. Hakuna atakayejitokeza kuwafungua; moto utakuwa ni chakula chao na maji yao, watageuzwa kichwa chini miguu juu katika vituo mbalimbali vya moto wa Jahannam.135

5. Yahya Wakati Nabii Yahya (as) alipokuwa akiwaona viongozi wa kidini wa Baytul Maqdas walikuwa wamevaa majoho yaliyotengenezwa kwa kitambaa chenye manyoya na vitambaa vya pamba, alimuomba mama yake amtengenezee nguo kama hiyo. Baadaye alianza kusali nao katika Baytul Maqdas. Siku moja Yahya (as) aliutazama mwili wake uliokuwa umekonda kwa kiasi kikubwa, na akaanza kulia. Allah alimfunulia: “Unalilia mwili wako uliokonda? (Naapa) kwa utukufu wangu! Lau ungekuwa na elimu japo kidogo ya moto (wa Jahannam) ungevaa makoti yaliyotengenezwa kwa 135 Pand-e-Tarikh, Juz. 4, uk. 221; Biharal Anwar, Juz.10, uk. 26 107


Visa vya Kweli sehemu ya Pili chuma, na sio nguo hizi zilizoshonwa.” Aliposikia hivi, Yahya alilia mno kiasi kwamba minofu ya mashavu yake iliisha. Zakaria (as) alimuambia mwanawe, “Nilikuomba kwa Allah ili uwe tuhafa la macho yangu. Kwa nini unafanya hivyo?” “Baba, lakini haikuwa wewe uliyesema: ‘kwa hakika baina ya pepo na moto wa Jahannam kuna njia na hakuna yeyote atakayeweza kupita isipokuwa wale wanaolia sana kwa sababu ya hofu ya Allah’” Yahya alijibu. “Ndio nilisema!” alikiri Zakariyya (as). Kila wakati Zakariyya (as) alipokuwa akikusudia kuhubiri na kuwatolea mawaidha Bani Israil, alikuwa kwanza akitizama huku na kule, na ikiwa alimuona Yahya (as) miongoni mwao, alikuwa akijiepusha kutaja chochote juu ya pepo na moto. Wakati fulani Zakariyya (as) alikuwa akiwahutubia watu ambapo Yahya (as), amekifunika kichwa chake na joho, aliwasili na kukaa miongoni mwa watu. Zakariyya (as) ambaye hakuwa amemuona Yahya (as) alihubiri: Allah amesema: “Jahannam kuna mlima uitwao Sakaran ambao kando kando yake kuna jangwa liitwalo Ghadhaban, ambamo kuna kisima ambacho kina chake ni sawa na miaka mia moja ya kusafiri. Ndani ya kisima hiki kuna makasha ya moto na ndani ya makasha kuna masanduku ya moto, ambayo nayo yana nguo na minyororo ya moto” Mara Yahya (as) aliposikia jina ‘Sakran,’ alinyanyua kichwa chake, akapiga mayowe na katika hali ya msongo mkubwa na sononeko, alitoka nje na akaelekea porini. Zakariyya na mama yake Yahya walitoka na kwenda kumtafuta; baadhi ya vijana wa Bani Israil pia, kutokana na heshima ya mama yake Yahya waliungana kumtafuta. Walikutana na mchungaji wakamuuliza ikiwa amemuona kijana mwenye maumbile ya Yahya. “Je mnamtafuta Yahya Ibn Zakaryya?” aliuliza mchungaji. 108


Visa vya Kweli sehemu ya Pili “Ndiyo” walijibu “Hivi sasa yupo katika sehemu moja, miguu yake ikiwa ndani ya maji na macho yake yakitizama mbinguni, akisali na kuwasiliana na Mola Wake,” alieleza. Kundi lililokuwa likimtafuta lilikwenda sehemu hiyo na kumkuta. Mama yake alimuita Yahya (as), alimuweka chini ya kiapo cha Allah na alimuomba arudi nyumbani. Punde, Yahya alirudi nyumbani na mama yake.136

37. HILA Allah Mwenye Hikma, amesema:

“Kwa hakika Allah hampendi yule ambaye ni mwenye hila, muovu.” Suratul Nisa (4): 107 Imam Sadiq (as) amesema: “Haifai mkamuamini mtu mwenye hila.”137 Maelezo mafupi Ikiwa kitu kama fedha, biashara, gari au mfano wa hivyo vitawekwa kwa mtu kama amana, mtu hapaswi kutokuwa muaminifu, kuharibu au kukana kuwa alikipokea kama amana. Mtu mwenye uovu huu hana uaminifu mbele ya macho ya Allah wala 136 Risalah Liqaullah, uk. 157-164; Amali ya al Saduq

137 Biharul Anwar, Juz. 78, uk. 248

109


Visa vya Kweli sehemu ya Pili mbele ya macho ya watu. Hudondoka kutoka katika daraja la imani na matokeo (ya uovu) ya kitendo chake hudunda (na kumrudia) - yakimuathiri yeye, mali yake na familia yake katika namna yenye madhara. Imeshauriwa sana kwamba mtu asidanganyike na sala (ndefu) za mtu na funga (nyingi) – kwani inawezekana kwamba mtu anaweza tu akapenda kufanya vitendo hivi, badala yake mtu ampime mtu kwa uaminifu, na uaminifu katika amana (zilizowekwa chini ya uangalizi wake). Kamwe mtu akiweka amana yake kwa mtu asiyekuwa muaminifu, kumkopesha fedha au kumuozesha binti yake mtu mwenye hila kumekatazwa na mtu akifanya hivyo na kisha ikatokea akapata hasara au madhara, ni yeye mwenyewe ndiye anapaswa kujikosoa na kujilaumu. 1. Waziri mwenye hila Wakati wa utawala wake, Gushtasp alikuwa na waziri aliyeitwa Rast Rawishan.138 Kutokana na jina lake zuri, Gushtasp alikuwa akimheshimu sana na alikuwa akimpenda kuliko mawaziri wengine. Huyu waziri alimshawishi Gushtasp kuwakandamiza watu na kuwapokonya mali zao kwa imani kwamba kunyooka kwa masuala ya ufalme kulikuwa kunategemea hazina na kwamba wananchi wanapaswa kuwa masikini ili waendelee kuwa watiifu. Yeye mwenyewe sio tu kwamba alikuwa amejikusanyia mali nyingi bali alikuwa amejenga uadui na Gushtasp. Siku moja, Gushtasp alipokuja hazina, alitambua kwamba hapakuwa na fedha za kuwalipa wafanya kazi wake. Isitoshe, miji yake ilikuwa inaporomoka na kuwa magofu na watu walikuwa katika sononeko. Hili lilimuacha Gushtasp katika hali ya mshangao. 138 Kilugha jina hili maana yake ‘mfanyakazi mkweli.’ 110


Visa vya Kweli sehemu ya Pili

Akiwa amekata tamaa kabisa, alipanda farasi wake na alielekea porini. Alipokuwa akienda, macho yake yaliangukia kwenye kundi la kondoo kwa mbali. Aliposogea karibu aliona kwamba kondoo walikuwa wamelala huku mbwa akiwa amening’inizwa kwenye mti wa kunyongea. Kwa mshtuko, alimuuliza mchungaji sababu ya kumuua mbwa, mchungaji akajibu “Mbwa huyu alikuwa ni mnyama mtiifu; nilimlea na kumuamini kuwalinda kondoo. Baada ya muda, alikutana na mbwa mwitu jike na wakawa marafiki. Usiku ulipoingia, mbwa mwitu alikuwa akikamata kondoo, akila nusu na kumbakishia mbwa huyu nusu. “Siku moja, niligundua upungufu wa idadi ya kondoo na baada ya uchunguzi, nikaja kugundua juu ya hila ya mbwa huyu. Hivyo nimemning’iniza juu ya mti wa kunyongea ili ieleweke kwamba matokeo ya hila na uovu ni mateso na adhabu!” Aliposikia hivi, Gushtasp alijifikiria: Raia wangu ni kama kondoo hawa na mimi ni kama mchungaji; lazima nichunguze na kusoma hali ya watu ili nijue sababu ya hali yao mbaya” Alirudi katika Kasri lake na kuomba orodha ya wafungwa waliofungwa gerezani. Alipoichunguza orodha alihitimisha kwamba waziri wake, Rast Rawishan, (ndiye) aliyekuwa amewafunga wao wote na kwamba yeye ndiye aliyekuwa sababu ya uovu na matatizo. Alimnyonga yule waziri na akakiri kwamba alikuwa amedanganywa na jina lake. Pole pole aliufanya ufalme kuwa ni wenye ustawi, alirekebisha uharibifu wa nyuma, akaiangalia hali ya wafungwa na akaepuka kumuamini yeyote tena.139

139 Jawame al-Hikayat, uk. 313; Siyasatnameh-e-Khwajah Nidham al-Mulk 111


Visa vya Kweli sehemu ya Pili 2. Hila Wakati wa Ziara Al-Hajj Hasan, mtoto wa Ayatullah al-Hajj Husain Tabaitabai Qummi, anasimulia: “Nilikuwa nimekuja Tehran kutokea Mash’had kwa ajili ya matibabu ya macho yangu. Katika kipindi hicho, mmoja wa wafanya biashara wa Tehran niliyekuwa nafahamiana naye, alikuwa amesafiri kwenda Khurasan kwa ajili ya ziara ya Imam Ridha (as). Usiku mmoja niliota nikiwa katika msikiti mtakatifu wa Imam Ridha (as) aliyekuwa amekaa kwenye kaburi. Ghafla niliona kwamba mfanyabiashara alimtupia mshale Imam (as) ambao ulimsumbua sana. Kwa mara ya pili, kutokea upande wa pili wa kaburi, alirusha mshale mwingine kuelekea kwa Imam (as) na tena Imam (as) aliudhika sana. Kwa mara ya tatu, mfanyabiashara alirusha mshale kutokea kwa nyuma lakini mara hii Imam (as) aliangukia mgongo wake. Nikiwa nimeshtushwa na kuogopeshwa niliamka kutoka kwenye usingizi wangu. Matibabu yangu ya macho yalipokamilika, nilitaka kurudi Khurasan lakini nikaamua kukaa mpaka mfanyabiashara atakaporudi kutoka Khurasan. Aliporudi niliongea naye na kumuuliza baadhi ya maswali lakini sikuweza kupata kiini cha habari. Hatimaye nilimsimulia ndoto yangu, ambapo huku machozi yakitiririka kutoka kwenye macho yake, alieleza: “Siku moja, nikiwa nimeingia kwenye eneo la msikiti mtukufu wa Imam Ridha (as) mbele yangu nilimuona mwanamke akiwa ameweka mkono wake kwenye kaburi. Niliweka mkono wangu juu ya mkono wake na hivyo yule mwanamke akaenda upande wa pili wa kaburi. Nilimfuata huko na kwa mara nyingine nikaweka mkono wangu juu ya mkono wake. Mwanamke yule alienda nyuma ya kaburi. Alipokuwa ameweka mkono wake, nilifanya kama awali na nikamuuliza ametokea wapi. Alijibu kwamba alikuwa ametokea Tehran; tukawa marafiki na tukarudi Tehran pamoja.”140

140 Rahnama-e-Sa’adat, Juz. 1, uk.257, Jame al-Durar, Juz. 1uk. 448 112


Visa vya Kweli sehemu ya Pili 3. Uasi wa Binti kwa Baba Yake Saatrun, ambaye jina lake lilikuwa Dhizan alikuwa ni Mfalme wa Hadhar, nchi iliyopo kati ya mito ya Tigris na Eupharates. Katika nchi ya Hadhar kulikuwa na jumba zuri la kifame kwa jina la Jausaq. Siku moja, Mfalme alivamia mji uliokuwa chini ya Shapur; alipora na kuuharibu, aliuwa idadi kubwa ya watu na hatimaye akaukalia mji huo. Katika mchakato huo aliweza kumchukua dada yake Shapur kama mateka. Shapur alipolifahamu hili, alikusanya jeshi lake na akaenda kwa Mfalme. Dhizan alikuwa amejifungia kwenye ngome imara ambayo Shapur aliizingira. Uzingiraji uliendelea kwa kipindi cha miaka mine lakini Shapur hakuweza kuipenya ngome. Siku moja, Binti wa Dhizan, Nadhrah mwali mrembo kabisa, alikuwa akitembea nje ya ngome macho ya Shapur yalipomuangukia. Alimtumia ujumbe kwamba ikiwa angesaidia kuteka ngome angemuoa. Katika moja ya usiku Nadhirah, ambaye naye alikuwa amempenda Shapur, aliwalewesha walinzi wa ngome na akawafungulia milango wanajeshi wa Shapur. Katika vita vilivyopiganwa, hatimaye baba yake, Dhizan iliuawa. Katika kutekeleza ahadi yake Shapur alimuoa Nadhrah. Usiku mmoja, alibaini kuwa kulikuwa na damu katika kitanda chake. Alipochunguza sababu yake, aligundua kwamba fundo la nywele nene zilikuwa kwenye kitanda chake na hizi zilikuwa zimesababisha mwili wake laini na mwororo kuchubuka na kuumia. “Baba yako alikuwa akikulisha nini? alimuuliza. “Kiini cha mayai, ubongo wa wanakondoo, siagi na asali; alijbu. Aliposikia hivi Shapur alitafakari kwa muda kisha akasema: “Licha ya raha hizi ulizopewa na baba yako bado hukuwa mwaminifu kwake; ni vipi 113


Visa vya Kweli sehemu ya Pili unaweza kuwa mtiifu na mwaminifu kwangu? Aliamuru kwamba afungwe kwenye mkia wa ngamia na mnyama akimbizwe jangwani hadi miiba ya jangwa ikatapakaa rangi ya damu ya huyu binti mwenye hila na asiye kuwa mwaminifu”.141 4. Mhindi na Imam wa sita Imam Kadhim (as) anasimulia: “Siku moja, nilikuwa na baba yangu ambapo rafiki aliingia na kumwambia baba yangu kuwa (kuna) watu walikuwa wamesimama nje, wakisubiri kumuona. Baba yangu aliniambia nikaangalie walikuwa ni akina nani. Nilipokwenda nje niliona ngamia wengi wakiwa wamesheheni maboksi makubwa, mwanaume alikuwa amekaa juu ya farasi. “Wewe ni nani?” nilimuuliza mtu huyo. “Nimetoka India na ninataka heshima ya kuonana na Imam (as),” alijibu. Nilirudi kwa baba yangu na nilimjulisha juu ya mtu aliyopo nje. “Usimruhusu mtu huyu najisi na mwenye hila aingie ndani ya nyumba,” aliagiza, na hivyo nilifanya kama nilivyoagizwa, watu hao walijenga mahema katika sehemu hiyo hiyo karibu na nyumba na walisubiri kwa muda mrefu mpaka Yazid Ibn Sulaiman na Muhammad Ibn Sulaiman walipoingilia na wakawaombea kuonana na baba yangu. Mhindi alipoingia, alikaa chini mbele ya Imam (as) akiwa amekunja miguu na akasema: “Nakuombea afya njema! Ninatokea India na Mfalme amenituma mimi pamoja na zawadi ambazo zinapaswa kuwasilishwa kwako. Kwa siku nyingi nimekuwa nikiomba ruhusa ya kuingia lakini umekuwa 141 Namunah-e- Ma’arif, Juz.5, uk.142, Al-Mustatraf, Juz.1 uk210 114


Visa vya Kweli sehemu ya Pili ukikataa kuonana na mimi. Je watoto wa Mitume huwa wana mwenendo huu?” Baba yangu aliinamisha kichwa chake chini na kujibu: “Utajua sababu yake baadaye,” kisha aliniomba nifungue barua ambayo Mhindi alikuwa ameileta. Ndani ya barua, Mfalme alikuwa ametuma salamu, kisha alikuwa ameandika: “Ni kwa sababu yako kwamba nimeongoka. Nilikuwa nimeletewa binti mtumwa mzuri (wa sura) na nikaona hakuna mwingine isipokuwa wewe anayestahili kummiliki na hivyo pamoja na nguo, mapambo na manukato, ninakuzawadia (binti huyo). Kati ya watu elfu moja, nilichagua mia moja, na katika mia moja nilichagua kumi, na katika kumi, nimemchagua mmoja, Mizan Ibn Khabbab, ambaye ni mwaminifu. Ninamtuma kwako pamoja na binti mtumwa na zawadi.” Baba yangu alimgeukia Mhindi na kusema, “Ewe mtu usiyekuwa mwaminifu! Rudi, kwani kamwe siwezi kuikubali amana ambayo imefanyiwa ufisadi.” Yule mhindi aliapa kuwa hakufanya hila, hata hivyo baba yangu alimuambia, “Kama nguo zako zikitoa ushahidi kwamba haukuwa mwaminifu kwa huyu binti mtumwa utakuwa mwislamu?” “Nisamehe!” aliomba Mizan. “Basi andika matendo yako (kwenda) kwa Mfalme wa India” “Ikiwa unajua lolote kuhusu jambo hili liandike” alisema Mizan Mtu huyu alikuwa na ngozi ya kondoo katika mabega yake; Imam alimwambia aiweke chini. Kisha baba yangu alisali rakaa mbili kisha akasujudu na kuomba:

115


Visa vya Kweli sehemu ya Pili Akinyanyua kichwa chake, aliigekia ngozi ya kondoo na kusema: “Sema yote unayoyajua kuhusu huyu Mhindi” Ngozi ya kondoo ilianza kuongea Kama kondoo, na kusema: “Ewe mtoto wa Mtume wa Allah! Mfalme alimuona mtu huyu kuwa ni mwaminifu na alimsisitizia sana juu ya kumlinda binti mtumwa na zawadi. Tulipokuwa tumesafiri umbali fulani, tulifikia jangwa ambapo mvua alitunyeshea. Vitu vyote vililoa kutokana na mvua. Wakati huo, huyu mtu asiyekuwa mwaminifu alimuita mtumishi aliyekuwa ameambatana na binti mtumwa (kijakazi) na alimtuma kwenda mjini kununua kitu fulani. Mtumishi alipokuwa amekwenda, alimwambia mjakazi: “Ingia ndani ya hema hili tulilolisimika kwenye jua ili nguo zako na mwili ukauke. Mjakazi aliingia ndani ya hema na akavuta nguo zake hadi kwenye magoti. Alipoona miguu yake aliingiwa na tamaa na akamrubuni kijakazi kutokuwa mwaminifu.” Mhindi, akiwa amechanganyikiwa na mwenye usongo kwa kushuhudia, ngozi ya kondoo (ikiongelea madhambi yake), alikiri kosa lake na akaomba msamaha. Ngozi ya kondoo ikarudia hali yake ya kawaida na Imam (as) akamuamuru aivae. Alipoiweka tu mabegani mwake, ilijizungusha shingoni kwake na kumbana na ilikuwa inakaribia kumnyonga wakati Imam (as) aliposema: “Ewe ngozi ya kondoo! Muache ili arudi kwa Mfalme ambaye atakuwa ni mtu muafaka wa kumwadhibu mtu huyo kwa kutokuwa mwaminifu kwake.” Ngozi ya kondoo ilirudia hali yake ya kawaida. Yule Mhindi akiwa amejaa hofu, alimuomba Imam (as) azikubali zawadi. “Ukiwa mwislam nitakuzawadia kijakazi huyu,” alisema Imam (as). Lakini alikataa zawadi hiyo. Imam (as) alizikubali zawadi zile, lakini alikataa kumchukua kijakazi, na yule mtu akarudi India. 116


Visa vya Kweli sehemu ya Pili Baada ya mwezi mmoja, barua iliwasili kutoka kwa Mfalme wa India, ambamo baada ya salamu aliandika: “Ulikubali kile kisicho kuwa na thamani kubwa na ukakataa kile kilicho na thamani. Hili lilinisumbua sana na nikajisemea: ‘Watoto wa Mitume wana maono na busara za kimungu na inawezekana kwamba mtu aliyemsindikiza mjakazi, alifanya kitendo kisichokuwa cha uaminifu.’ Na hivyo nilijiandikia barua yenye jina lako kuja kwangu, na nikamwambia yule mtu kwamba barua yako imenifikia ambamo ulitaja kutoaminika kwake. Nilimwambia: “Hakuna chochote kitakacho kuokoa isipokuwa ukweli,” ambapo alikiri na akanisimulia kisa chote cha udanganyifu wake kuhusiana na mjakazi na tukio la ngozi ya kondoo. Mjakazi pia alikiri hivyo nikaamuru wote wakatwe vichwa. “Ninashuhudia upweke wa Allah na utukufu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na ninaeleza kwamba nitakuja mimi mwenyewe kwako baadaye” Muda si mrefu aliwasili Madina baada yakuwa amejiuzulu ufalme wake na akajibadilisha na kuwa mwislamu wa kweli.142

38. ULIMWENGU Allah Mwenye Busara, anasema: “Na maisha ya dunia hii si chochote isipokuwa mchezo na yapitayo”143 Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Yule anayeamka asubuhi huku kitu muhimu kabisa kwake ni ulimwengu, hatapata chochote (katika ulinzi wa) kwa Allah”144 142 Pande-e-Tarikh, Juz.1, uk. 217; Biharul Anwar, Juz.11, uk.136 143 Suratul An-am (6):32 144 Jame’al-Sa’adat, Juz. 2, uk.24 117


Visa vya Kweli sehemu ya Pili Maelezo mafupi Ulimwengu ni kama umbo ambalo kichwa chake ni kibri, macho yake ni ulafi, masikio yake ni tamaa; ulimi wake ni msigano, mikono yake ni hawaa, miguu yake ni majisifu na moyo wake ni upuuzaji. Yeyote anayependa ulimwengu, utamvutia katika kibri na majivuno, yeyote anayependa ulimwengu, utamfanya awe na tamaa na ulimwengu, na yeyote anayeutaka ulimwengu atasukumizwa kuelekea kwenye kutamani vya watu. Mtu aliyeusifu ulimwengu, amejivisha vazi la udanganyifu, yule ambaye lengo na kusudio lake ni ulimwengu huu, moyo wake hujawa na majivuno, na yule anayeuamini ulimwengu huu, huelemewa na uzembe na kutojali (masuala ya Allah). Matokeo yake, Jahannam yatakuwa ni makazi ya wanaoupenda ulimwengu.145 1. Heshima na udhalili Harun Rashid, khalifa wa (ukoo wa) Banu Abbas, alikuwa anapenda sana familia ya Barmaki. Walikuwa ni masahibu zake maalumu na wa karibu, kwa ujumla wakishikilia nafasi za uwaziri, na katika hao alikuwa akimpenda sana Ja’far Barmaki. Heshima hii iliendelea kwa zaidi ya miaka 17. Mnamo mwaka 189 Hijiria, kutokana na matukio fulani, familia ya Barmaki ilikuwa ni mhanga wa Harun, na matokeo yake wote walipita katika vipindi vigumu kabisa. Muhammad Ibn Abdul Rahman Hashim anasimulia: “Katika siku ya Eidul Adh’ha, nilimfuata mama yangu aliyekuwa anaongea na mwanamke aliyevaa nguo kuukuu. “Je unamfahamu huyu mwanamke?” mama yangu aliniuliza. Nilisema simfahamu.

145 Tadhikiratul Hqaiq, uk.35 118


Visa vya Kweli sehemu ya Pili “Huyu ni Ubadah, mama wa Ja’afar Barmaki,” alisema. Nilikwenda kwa Ubadah na kuongea naye kwa muda fulani, muda wote nikishangazwa na hali aliyokuwa nayo. “Ewe mama! Umeona nini katika maajabu ya ulimwengu?” nilimuuliza Ubadah alijibu, “Ewe mwanangu! Nilishuhudia katika siku ya Idd kama siku hii ya leo (Eidul Adh’ha,) nilipokuwa na wajakazi mia nne wakiwa wamesimama mbele yangu kunihudumia na bado nilikuwa ninalalamika kwamba mwanangu Ja’far alikuwa hajanipa haki yangu (kikamilifu) kwani nilipaswa kuwa na wajakazi zaidi wakinitumikia. Leo ni siku nyingine ya Idd lakini ninakabiliwa na hali ambayo vitu ninavyovihitaji ni ngozi mbili za kondoo, moja ya kutumia kama tandiko na nyingine ya kutumia kama blanketi.” Muhammad Hashim aliendelea: “Nilimpa dirham mia tano, zilizomfanya afurahi sana kiasi cha kukaribia kufa kwa sababu ya furaha, Ubadah aliendelea kuja nyumbani kwetu kila baada ya muda fulani, hadi hatimaye alipofariki”146 2. Ali na hazina ya Umma Shu’bi anasimulia: “Nikiwa nimeambatana na vijana wengine, mimi pia niliingia kwenye uwanja mkubwa wa wazi wa Kufa ambapo nilimuona Amirul Mu’uminin (as) akiwa ameshika bakora ndogo mkononi mwake na akiwa amesimama jirani na makontena mawili yakiwa yamejaa sarafu za dhahabu na fedha. Alikuwa akitumia bakora kuurudisha nyuma umati wa watu uliokuwa umekusanyika alipokuwa anagawa fedha. Imam (as) aliendelea kugawa fedha hadi ikawa hakuna kilichobaki kwa ajili yake, na akarudi nyumbani akiwa hana kitu, mimi pia nikaenda nyumbani. 146 Tatimmah al-Muntaha, uk.181 119


Visa vya Kweli sehemu ya Pili “Nimeshuhudia kitu cha ajabu leo na ninashindwa kuelewa ikiwa kitendo hicho kilikuwa kizuri au kibaya, ambapo hakujibakizia chochote!” Nilimuambia baba yangu. Baba yangu aliniuliza ni kitu gani nilichokuwa naongelea. Nilimsimulia yote niliyoshuhudia ambapo baba yangu alianza kulia, akaniambia: “Mwanangu, umemuona mtu bora kabisa miongoni mwa watu.’”147

* * * Zadhaan anaripoti: “Qambar na mimi tulikwenda kumuona Amirul Muuminin (as). Tulipomfikia Qambar akasema: “Ewe Amirul Muuminin! Inuka, kwani nimekufichia hazina nzuri kwa ajili yako” “Ni hazina gani hiyo?” Aliuliza Imam (as) “Inuka na uambatane nami ili nikuonyeshe,” alisisitiza Qambar. Imam (as) aliinuka na kumfuata ndani ya nyumba. Qambar alileta mfuko wa kitani uliokuwa umejaa vifuko vidogo vidogo vikiwa na dhahabu na fedha. “Ewe Ali! Ninajua kwamba unagawa kila kitu miongoni mwa watu na wewe hujibakizii chochote na hivyo, nimehifadhi hii maalum kwa ajili yako!” Alisema Qambar. Imam (as) akasema, “Ningepedelea uichome nyumba hii na kuunguza kila kitu.” Aliposema hivi, aliupiga mfuko kwa upanga wake, akisababisha sarafu za fedha kumwagika. Kisha alituamuru tuzigawe kwa watu. Baada ya kuwa tumetekeleza maagizo yake, Imam (as) alisema: “Shuhudieni kuwa sijachukua chochote kwa ajili yangu na sikuwa mzembe katika ugawaji wa fedha miongoni mwa waislamu. Ewe dhahabu na fedha! 147 Al-Gharat, Juz.1, uk.55; Dastan-hal-Az Zindagi Ali (as), uk. 114 120


Visa vya Kweli sehemu ya Pili Kamdanganye mwingine sio Ali.”148 3. Hadhrat Sulaiman. Sulaiman Ibn Dawud (as) alikuwa ni mmoja wa wale Mitume wa Allah aliowapatia mamlaka juu ya Mashariki na Magharibi ya ulimwengu. Kwa miaka aliwatawala majini, watu, wanyama, ndege na alijua lugha za viumbe wote, mamlaka ambayo yalikuwa makubwa na mapana kiasi kwamba yalikuwa mazuri kiasi cha kutowezekana kuyaelezea. Alikuwa amemuomba Allah: “Nipatie ufalme ambao hautampatia mwingine kwa mfano wake baada yangu” Baada ya Allah kumrehemu na kumtukuza kwa ufalme huo, Hadhrat Sulaiman (as) aliwaambia watumishi wake siku moja: “Sijawa na siku hata moja ambayo nimekuwa na furaha asubuhi hadi usiku. Kesho nitaingia kwenye kasri yangu, nitapanda kwenye paa lake na kuwaona raia wangu. Msiruhusu mtu yeyote kuja kuniona isije furaha yangu ikabadilika na kuwa huzuni.” Asubuhi iliyofuata, alichukua fimbo yake, akapanda sehemu ya juu kabisa ya kasri yake na akasimama huko, huku akiegemea fimbo yake, akiutizama ufalme na raia wake, huku akifurahia yale Allah aliyompatia. Alipokuwa akitizama hivi, ghafla alimuona kijana mtanashati, akiwa amevaa nguo safi, akitokea kwenye upande wa kasri yake. “Ni nani aliyekupa ruhusa ya kuingia kwenye kasri?” alimuuliza kijana. “Mola” alijibu kijana yule. “Wewe ni nani?” aliuliza Sulaiman (as). “Izrail.” “Kwa nini umekuja?” “Kuchukua roho yako, Sulaiman” 148 Dastan-hai. Az Zindagi Ali (as), uk. 128; Nahjul Balagha (Ibn Hadid), Juz., uk. 181

121


Visa vya Kweli sehemu ya Pili “Nilikuwa ninataka siku ya leo iwe siku yangu ya furaha lakini Allah ametaka vinginevyo; tekeleza amri uliyopewa” alisema Sulaiman (as) Izrail alichukua roho yake huku akiwa amesimama, ameegemea kwenye fimbo yake wakati watu waliokuwa wakimtizama kutokea mbali, walifikiria yuko hai. Muda ulipopita, ulizuka mzozo baina ya watu. Baadhi walisema, “Ni siku nyingi zimepita akiwa hajala wala kunywa chochote hivyo ni mungu wetu.” Kundi jingine lilisema, “Ni mchawi; amefanya ionekane kwamba amesimama, ambapo kiuhalisia sio hivyo. Kundi la watu lilisema, “Yeye ni Mtume wa Allah.” Allah alituma jeshi la mchwa (kwenda) kula fimbo yake na matokeo yake fimbo ilivunjika na Sulaiman akaangua. Wakati huo ndio watu wakabaini kuwa alifariki siku nyingi kabla.149 4. Mapenzi ya Talha na Zubair kwa ulimwengu Talha na Zubair walikuwa miongoni mwa watu wazima katika kipindi cha awali cha Uislamu na walitoa mchango mkubwa katika vita. Baada ya kufariki kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), wote wawili, na hususani Zubair, walimuunga mkono kwa nguvu Amirul Muuminin (as) na hawakusita kutoa msaada wao kwake. Kumuunga mkono kwao kuliendelea hadi Uthman alipouawa na watu wakamchagua Imam Ali (as) kama kiongozi wao. Hili lilipotokea, wawili hawa walimfuata Imam (as) na kumuomba rasmi kwamba awateue kuwa magavana wa baadhi ya miji. Lakini, walipokataliwa na Imam Ali (as), walimtumia ujumbe mkali kupi149 Hayat al-Qulub, Jz. 1, uk. 370.

122


Visa vya Kweli sehemu ya Pili tia kwa Muhammad Ibn Talha, uliosema: “Tulijitolea sana kawa ajili ya Ukhalifa wako na sasa kwa sababu una hatamu za madaraka mikononi mwako, unafanya kama dikteta, unawaweka mbele (watu) wa mfano wa Malik Ashtar na kutusukumia nyuma?!” Imam Ali (as) alituma ujumbe kupitia kwa Muhammad Ibn Talha akisema: “nifanye nini ili mridhike?” “Mteue mmoja wetu awe gavana wa Basra na mwingine kama gavana wa Kufa,” walijibu. “(Naapa) kwa Allah! Wakati wao mimi siwaoni kuwa waaminifu hapa katika sehemu hii (Madina), ni vipi ninaweza kuwaweka juu ya watu wa Kufa na Basra?” aliuliza Imam Ali (as). Kisha alimuagiza Muhammad Ibn Talha kwenda na kuwaeleza, “Enyi masheikh! Muogopeni Allah na Mtume wake kuhusiana na Umma wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na msiwakandamize waislamu, je hamjamsikia Allah akisema:

“(Na kwa) hayo makazi yajayo, Tunawapa wale ambao hawana haja ya kujitukuza katika dunia wala kufanya uharibifu na mwisho mwema ni kwa wachamungu.” Suratul Qasas (28):83 Baada ya kushindwa kufanikisha ndoto zao za madaraka na utajiri, Talha na Zubair waliamua kwenda Makka. Walimuendea Imam Ali (as) na kumuomba ruhusa ya kwenda Makka kufanya (hijja ya) Umra. Imam (as) aliwaambia kuwa hawakuwa wanakusudia kwenda kufanya Hijja ya Umra, lakini waliapa kwamba hawakuwa na malengo mengine na walikuwa thabiti na waaminifu katika kiapo chao cha utii. 123


Visa vya Kweli sehemu ya Pili Kwa amri ya Imam, walirudia kiapo chao na kisha wakaondoka kwenda Makka. Huko, walivunja kiapo, wakakusanya jeshi wakiwa na Aisha, waliondoka kwenda Basra kwa ajili ya vita vya ngamia (Jamal)! Njiani walikutana na Ya’li Ibn Munabbah, ambaye alikuwa amebeba dinar takriban laki nne kwa ajili ya Imam Ali (as) kutoka Yemen. Hao watu wawili, kwa nguvu walimnyang’anya fedha na wakazitumia kwa ajili ya kupigana na Imam Ali (as). Katika vita hivi (mwaka 36 Hijiria), askari kumi na tatu elfu kutoka katika jeshi la Talha na Zubair na askari elfu tano kutoka kwa Imam Ali (as) waliuawa. Hatimaye Talha aliuawa kwa mshale uliorushwa na Marwan, aliyekuwa kwenye jeshi lake mwenyewe. Baada ya kumuua, Marwan alitangaza, “Nimelipiza kisasi cha damu ya Uthman kutoka kwa Talha.” Zubair alijitoa katika vita na njiani aliuawa na Ibn Jurmuz. Matokeo ya kupenda kwao madaraka na hulka katika matamanio ya kidunia hayakuwa chochote isipokuwa kifo cha aibu.150 5. Alichokitaka na hatimaye kilitokea! Tarehe 23 Muharram mwaka 169 Hijiria, Mahdi Abbas, alifariki huko Masabdhaan na ukhalifa ukaenda kwa mwanawe Musa, mwenye cheo cha Hadi Abbasi, ambaye wakati huo, alikuwa amekwenda Jordan kupigana na watu wa Tabaristan.151 Harun Rashid, kaka yake alichukua kiapo cha utii kwa niaba yake kutoka kwa watu wa Masabdhaan na Baghdad na alituma ujumbe kumjulisha juu ya hali hiyo. Haraka Hadi alirudi katika mji mkuu. 150 Hikayat-ha-eShanidani, Juz. 2, uk. 169 151 Modern day Mazandaran 124


Visa vya Kweli sehemu ya Pili Harthamah Ibn A’ayum anasimulia: “Usiku mmoja Hadi Abbasi aliniita kufanya naye mkutano wa siri.” “Unajua usumbufu nilionao kwa sababu ya huyu mbwa kafiri Yahya Ibn Khalid? Amewageuza watu kuwa dhidi yangu na amewahamasisha kumuunga mkono Harun. Lazima uende gerezani mara moja na ukamkate kichwa,” alisema. “Kisha nenda kwenye nyumba ya Harun na umuuwe. Baada ya hili, chunguza gereza na muuwe kila mtu anayetokana na kizazi cha Abu Talib. Baada ya kutekeleza maagizo haya, andaa jeshi na elekea Kufa, ukifika huko waondoe watu wote wa kizazi cha Abbas kutoka katika majumba yao na zichome moto nyumba zao.” Niliposikia maelezo haya, baridi iliniingia mwilini mwangu. “Sina nguvu ya kutekeleza kazi hizi kubwa na ngumu,” niliomba. “Ukifanya uzembe katika kutii amri yangu nitakuuwa,” alisema, na aliniamuru nisimame pale nilipokuwa wakati akienda katika sehemu ya wanawake. Niliwaza kwamba kwa vile nilikuwa nimeonyesha chuki dhidi ya matendo haya, angemteuwa mtu mwingine na kisha angeniua. Nilijiahidi kwamba kama ningenusurika na balaa hili, ningeenda sehemu ambayo hakuna ambaye angenijua. Ghafla mtumwa alijitokeza na kunijulisha kuwa Hadi Abbasi alikuwa ameniita. Nikatarajia kifo, nilishuhudia upweke wa Allah utume Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na nikaenda mbele. Katikati ya njia nilisikia mwanamke akisema “Ewe Harthamah! Mimi ni Khaizran, mama yake Hadi. Njoo uone msiba uliotufika” Nilivyoingia chumbani, Khaizran aliyekuwa nyuma ya pazia, alisema: “Hadi alipoingia ndani ya nyumba, niliondoa mtandio wangu kutoka kichwani na nikamuombea msamaha Harun, lakini alikataa. Wakati huo huo 125


Visa vya Kweli sehemu ya Pili ghafla akapatwa na kikohozi kikali. Alikunywa maji na haikusaidia na alifia hapo (18 Rabiul Awal, 170 Hijiria). Sasa nenda kamjulishe Yahya Ibn Khalid juu ya kifo chake ili ale kiapo cha utii kwa mwanangu Harun.” Harthamah anaendelea: “Nilimjulisha Yahya juu ya kifo cha Hadi na kisha nikaenda kwenye nyumba ya Harun, ambako nilimkuta anasoma Qur’ani Tukufu. Nilimjulisha kuwa amekuwa Khalifa lakini alikataa kuamini na hivyo nikamsimulia kisa kizima. Usiku huo huo Harun alijulishwa juu ya kuzaliwa kwa mwanae wa kiume, Mamun.152

39 - UONGO Allah mwenye Hikma, anasema: “(Ni) wasikilizaji wa uwongo, walaji wa yaliyokatazwa.” SuratulMaidah; 5:42 Imam Askari (as) amesema: “Maovu yote yamewekwa katika nyumba na uwongo umefanywa kuwa ni ufunguo wake.”153 Maelezo mafupi Kusema uwongo mdogo au mkubwa, kwa maskhara au kwa dhati hairuhusiwi kwani imeshaelezwa: “Maovu yote yamewekwa katika nyumba na uwongo umefanya kuwa ni ufunguo wake,” huwa ni muhimu sana kujiepusha na kitendo hiki. Kwa vile uongo huzungumzia yasiyo kuwepo, na yule anayesema uwongo 152 Rangarang, Juz.1,uk 24 153 Taz. Jame al-Sa’adat, Juz. 2, uk. 323 126


Visa vya Kweli sehemu ya Pili hafanyi hivyo kwa lengo la kuikuza nukta yake wala kwa ajili ya kupatanisha pande mbili zinazopigana, huwafanya malaika wajitenge na mtu huyo. Huleta maangamizi ya imani yake, kupungua kwa riziki yake na udhalili na fedheha mbele ya watu - kiasi kwamba ikiwa uwongo atasingiziwa Allah na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika mwezi wa Ramadhani, (hili) hubatilisha saumu.”154 1 - Walid Ibn Uqbah Abi Mu’iit Walid Ibn Uqbah alikua Mwislam ambaye awali alionekana kuwa ni mtu mwongofu kiasi kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimpa jukumu la kukusanya Zaka na sadaka kutoka katika kabila la Mustalaq. Watu wa kabila hilo walipojua juu ya kuwasili kwa mwakilishi wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), walitoka kuja kumkaribisha. Katika zama za ujinga, kulikuwa na uadui kati ya Walid na kabila hili, na alipoona watu wanamjia katika kundi kubwa, alifikiri kwamba walikuwa wamejiandaa kumuua. Haraka aligeuka na kurudi madina. Alikwenda kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na akamwambia kwamba watu wa kabila hilo hawakuwa tayari kutoa Zaka zao, jambo ambalo ni wazi halikuwa kweli, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliudhika sana aliposikia hivi na alianza kuwaza kupeleka jeshi kwenye kabila (hilo), Allah alipomshushia aya ifuatayo:

“Enyi mlioamini! Ikiwa mtu muovu atakujieni na habari, ichunguzeni kwa makini,155 (ili kuthibitisha ukweli wake).”156 154 Ihya al-Qulub, uk.151. 155 Suratul Hujurat (49):6 156 Safinatul Bihar, J. 2, uk. 361. 127


Visa vya Kweli sehemu ya Pili Baada ya kuteremshwa aya hii Walid alikuja kujulikana kama mtu fasiki. “Ni katika watu wa Jahannam” alisema Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuhusu Walid. Baadaye Walid aliungana na Amr Ibn ‘Aas na hao wawili walikuwa wakinywa pombe na wakajenga hisia za uadui dhidi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Amirul muuminin (as). Khalifa wa tatu, wakati wa ukhalifa wake, alimteua kuwa gavana wa Kufa na asubuhi moja, akiwa katika hali ya ulevi, aliongoza katika sala ya jamaa ya Asubuhi kwa kusalisha rakaa nne badala ya mbili zilizoamriwa.157 2 - Njaa na Uongo Asma Bint Umais, amesimulia: “Katika usiku wa harusi ya Aisha na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wanawake wachache na mimi tulikuwa naye, tukimvalisha. Tulipo kwenda kwenye nyumba ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hatukukuta chakula chochote isipokuwa bakuli moja la maziwa. Mtume (s.a.w.w.) alikunywa kidogo kisha akampatia Aisha. Lakini huku akiwa amezidiwa na aibu hakulichukua bakuli lile. “Usimkatalie Mtume wa Allah, chukua na unywe hayo maziwa,” nilimuambia. Kwa aibu alichukua bakuli na kunywa kiasi cha maziwa hayo. “Pitisha bakuli kwa wenzako ili nao wanywe pia,” Mtukufu Mtume alimuagiza. Wanawake tuliokuwa nao wakasema, “Hatuna njaa.” Aliposikia hivi Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema, “Msikusanye njaa na uwongo pamoja (yaani kwa nini mnasema uongo na wakati huohuo mnabakia na njaa?).” “Ewe Mtume wa Allah! Ikiwa tuna hamu ya kitu fulani lakini tunakana kuwa nayo (hamu hiyo), tutakuwa tumesema uongo?” Niliuliza. 157 Ibid, uk. 688

128


Visa vya Kweli sehemu ya Pili “Uwongo hata ukiwa mdogo, hurekodiwa katika kitabu cha amali,” alisema Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).158 3 - Uongo wa Mshairi Khusro Hirawi aliishi zama za Abd al-Rahman Jaami, na ubeti ufuatao ni utunzi wake: “Ua la uso wako limemwagilia bustani ya uzuri, na yamekuwa ni mawimbi ya nywele zako ambayo yametoa kupinda pinda kwa maua ya urujuani.” Imesimuliwa kuwa alisema kwamba: “Baba yangu, ambaye ameandaa chakula wakati wa kutahiriwa kwangu, alitumia kilo mia tatu za binzari zilizosagwa” Walio kuwa naye walimuuliza ni chakula gani alichokuwa ametia kiasi kikubwa hivyo cha binzari. “Kilo mia moja na ishirini za bizari zilitiwa kwenye wali, kilo tisini kwenye supu ya choroko, kilo thelathini kwenye nyama ya kuku iliyokaangwa kisha ikatengenezwa mchuzi (fricassee) na kilo thelathini kwenye halua,” alijibu. “Hii ni sawa na jumla ya kilo 270, ni vipi kuhusu kilo nyingine 30?” wenzake waliuliza. Akiwa ameduwaa Khusro, alifikiria kwa muda kisha akanyanyua kichwa chake na akadanganya kwa furaha na bashasha kubwa “Nimekumbuka sasa alitumia kilo 30 za mwisho katika quttab!”159 na 160 4 – Zainab, Yule Muongo Mkubwa Wakati wa ukhalifa wa Mutawakkil Abbas, mwanamke mmoja alidai kuwa yeye ni Zainab binti wa Fatimah Al-Zahra (as). 158 Shanidad-ha-e-Tarikh, uk294; Mahajjatul Baida, Juz. 5, uk. 249

159 Haluwa 160 Latif al-Tawaif, uk 414.

129


Visa vya Kweli sehemu ya Pili “Miaka imepita tangu zama za Zainab, lakini wewe unaonekana kuwa mdogo.” Mutawakkil alimuambia. “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alinishika kichwa na kuomba kwamba kila baada ya miaka arobaini niwe kijana tena!” alisema huyu mwanamke. Mutawakkil aliwaita wazee kutoka katika kizazi cha Abu Talb, Abbasi na Waquraish na akaliweka suala mbele yao. Wote kwa pamoja walisema kwamba mwanamke huyu ni mwongo kwa sababu Zainab alifariki mwaka 62 Hijiria. Zainab, mwongo mkubwa alisema: “Wao ndio wanaodanganya, nilikuwa nimejificha kutokana na watu na hakuna aliyejua niliko mpaka leo.” “Lazima mthibitishe uwongo wa madai yake kwa ushahidi” alisisitiza Mutawakkil kwa wale wazee. “Muombe Imam Hadi (as) athibitishe uwongo wake” walishauri. Mutawakkil alimuita Imam (as) na kumjulisha suala (hilo). “Amesema uwongo kwani Zainab alifariki mwaka fulani,” alisema Imam (as). “Leta ushahidi wako kuthibitisha uwongo wa madai yake alisema Mutawakkil. Imam (as) alisema “Miili ya watoto wa Fatimah (as) imeharamishwa wanyama wa mwitu; mpelekeni mbele ya simba ikiwa anasema ukweli!” Mutawakkil alimgeukia yule mwanamke kutaka jibu. “Kwa njia hii anataka kuniua” alisema yule mwanamke. “Idadi (kubwa) ya watu kutoka katika kizazi cha Fatma (as) ipo hapa, unaweza kumpeleka yeyote umtakaye (mbele ya wanyama wa mwitu,” alijibu Imam (as). 130


Visa vya Kweli sehemu ya Pili Msimuliaji anaeleza: “Nyuso za masharifu wote wa kike waliokuwepo kwenye mkusanyiko huo zilipayuka. Baadhi walisema, “Kwa nini asiende yeye mwenyewe badala ya kuwaonyeshea wengine?” Mutawakkil alimuuliza Imam (as) kwa nini yeye mwenyewe asiende mbele ya simba? Imam (as) mara moja alikubali kwenda. Mutawakkili aliagiza iletwe ngazi, na Imam (as) akaingia katika wigo ambamo simba walikuwa wanatunzwa. Wale wanyama wa mwitu, kwa unyenyekevu na udhalili, waliweka vichwa vyao ardhini mbele ya Imam (as) naye akawapapasa vichwani. Baadaye kidogo aliwaamuru wasogee pembeni na wote wakatii! Waziri wa Mutawakkil alimshauri, “muambie Imam Hadi (as) atoke upesi kwani watu wakishuhudia muujiza huu watajazana kwake. Ngazi iliwekwa tena na Imam (as) akatoka. “Yeyote ambaye ni mtoto wa Fatima (as) ajitokeze na akae miongoni mwa wanyama wa mwitu; alisema Imam Hadi (as). (Yule) mwanamke (baada ya kuona tukio hilo) alikiri: “Ewe Imam! Madai yangu ni ya wongo. Mimi ni binti wa masikini mmoja, na umasikini (ndio) ulinisukuma katika udanganyifu huu.” Mutawakkil aliwaamuru walinzi wamtupie mwanamke huyu kwenye simba lakini mama yake aliingilia na kumuombea Zainab ambaye alisamehewa.161 5 - Uongo wa wazi wa Amir Husain Sultan Husain Baayaqra ambaye alitawala Khurasan na Zabolistan na Ya’qub Mirza ambaye alitawala Azerbaijan, walikuwa ni marafiki ambao mara kwa mara walikuwa wakitumiana barua na zawadi. 161 Muntahal A’mal Juz. 2, uk. 368

131


Visa vya Kweli sehemu ya Pili Wakati fulani, Sultan Husain alikabidhi vitu vizuri sana na vya thamani kwa mtu aitwaye Amir Husain Abyurdi na akamwagiza akachukue kitabu ‘Kulliyat Jami’ kutoka maktaba na kukiwasilisha kwa Sultani Ya’qub Mirza pamoja na vitu vingine. Amir Husain alimfuata mkutubu na akaomba kitabu, lakini mkutubu kwa makosa akamkabidhi kitabu Al-Futoohat Al-Makkiyyah cha Muhyuddeen Arabi, ambacho kilikuwa kinafanana sana na kitabu Kulliyat Jami kwa ukubwa na unene. Amir Husain aliondoka kuelekea Azerbaijan na alipowasili mbele ya Ya’qub Mirza, alimkabidhi barua ya Sultan na zawadi. Baada ya kupitia yaliyomo kwenye barua, Ya’qub aliuliza juu ya afya ya Sultan Husain na mawaziri wengine. Kisha aliuliza juu ya afya ya Amir Husain na kuhusu safari ndefu ya miezi miwili ambayo Amir Husain alikuwa amesafiri hadi kumfikia, alisema: “Lazima kwa hakika utakuwa ulikuwa na mwenzi wa kuifanya safari yako kuwa nzuri.” “Ndio, nilikuwa na kitabu Kulliyat Jami ambacho kimeandikwa hivi karibuni, katika safari nzima nilikuwa nikikisoma na nilikifurahia sana” alijibu Amir Husain. Mara tu Ya’qub Mirza aliposikia jina la Kulliyat Jami alisema, “Nilikuwa ninakitaka kitabu hiki na nimefurahi sana kwamba umekileta.” Amr Husain alimtuma mmoja wa watumishi wake kwenda kukileta, na kilipoletwa alikikabidhi kwa Ya’qub Mirza. Ya’qub Mirza alipokifungua kitabu, aliona kwamba kilikuwa Al-Futoohat Al-Makkiyyah. Alimgeukia Amir Husain na kuuliza: “Hiki sio Kulliyat Jami kwa nini umedanganya?” Amir Husain, akiwa amefadhaika na ameaibika, hakusubiri hata kuchukua majibu ya barua, bali aliondoka mara moja kurudi Khurasan.

132


Visa vya Kweli sehemu ya Pili “Uwongo wangu ulipogundulika nilitamani ningekufa.” alisema Amir Husain baadaye.162

40. WIZI Allah mwenye Busara amesema:

“Na (kwa) mwanaume anayeiba na mwanamke anayeiba, kateni mikono yao.” Qur’ani Tukufu Suratul Maida (5):38 Imam Sadiq (as) alisema: “Mwizi anapoiba, mikono yake hukatwa na hulazimishwa alipe (au arejeshe) kile alichoiba.”163 Maelezo mafupi Kumnyima mke mahari, mtu kutolipa madeni yake, kutolipa Zaka za wajibu na kadhalika, yote ni mifano ya wizi, lakini maana inayokuja mara moja akilini baada ya kusikia wizi ni “kuchukua/kumiliki mali na utajiri wa wengine, kwa siri na kwa udanganyifu.” Hii ndio maana halisi iliyokusudiwa hapa. Kama kungekuwa hakuna ulinzi (katika jamii) watu wasingeweza kulala kwa amani kwa kuhofia wezi. Ni kwa madhumuni ya ulinzi na kudumisha usalama kwamba Uislamu umeamuru vidole vya mwizi vikatwe; hata kama kitendo kimefanywa na mtoto, anapaswa akemewe vikali kwa namna fulani, ili ajizuie kutenda uovu huu katika siku za baadae. 162 Muntahal A’mal Juz. 2, uk. 368 163 Khazinatul Jawahir, uk. 640; Tarikh Jaib al-Sir

133


Visa vya Kweli sehemu ya Pili Ni kutokana na kutoielekeza hukumu hii ya Uislamu ndio maana idadi inayoongezeka ya wezi inapatikana hata katika jamii za kiislamu siku hizi. 1- Imam na Kukiri kwa Mwizi Mtu alimjia Imam Ali (as) na akakiri kuwa alikuwa ameiba. “Unaweza kusoma chochote kutoka katika Qur’ani tukufu?” Imam (as) alimuuliza. “Ndiyo, ninajua Suratul Baqarah,” alijibu yule mtu. Imam (as) akasema, “Ninakusamehe kwa sababu ya Suratul Baqarah.” Ash’ath Ibn Qais, aliyekuwepo hapo, alimuuliza Imam (as) akiwa anaweza kuondoa adhabu iliyowekwa na Allah. “Wewe ni kipi unachojua? Ikiwa mtu atakiri uhalifu wake, Imam ana mamlaka ya kumuadhibu au kumsamehe, lakini ikiwa watu wawili watashuhudia uhalifu wa mtu, haiwezekani kuondoa adhabu na kumsamehe”, Imam (as) alijibu.164 2 - Ngamia wa Bedui Sheikh Tawus al-Haramain anasimulia: “Nilikuwa nimesimama karibu na Masjid Haram (katika mji wa) Makka nilipomuona Bedui akija na ngamia wake. Alipofika msikitini, aliteremka, akamkalisha ngamia wake chini, akamfunga magoti yake na kisha, akakinyanyua kichwa chake angani akaomba: “Ewe Mola! Ninamuwekeza Kwako huyu ngamia na mzigo uliopo juu yake,” kisha aliingia Masjid alHaram. Alipokuwa amemaliza kutufu Ka’ba na kusali, alitoka nje ya msikiti na hakumkuta ngamia wake. Alitizama juu angani. 164 Tafsirul Mu’in, uk. 114 134


Visa vya Kweli sehemu ya Pili “Imesemwa katika Sheria takatifu kwamba mali inapaswa kutafutwa kutoka kwa yule, ambaye iliwekezwa kwake kama amana. Nilimuwekeza ngamia wangu Kwako, hivyo nirudishie Ngamia wangu” alisema. Alikuwa hata hajamaliza kutamka maneno haya nilipomuona mtu akitokea nyuma ya mlima wa Abu Qubbais, akiwa na hatamu za ngamia katika mkono wa kushoto na mkono wa kulia ukiwa umening’nizwa kwenye shingo yake. Alikuja karibu na Bedui. “Ewe kijana! Chukua ngamia wako” alisema. “Wewe ni nani na umefikaje katika hali hii?” Bedui aliuliza. “Nilikuwa masikini na mhitaji na hivyo nikaiba ngamia wako,” alisema yule mgeni. Nilikwenda nyuma ya mlima wa Abu Qubais ambapo ghafla nilimuona mpanda (farasi) akinijia. Aliponikaribia alipiga kelele: nyoosha mkono wako. Niliponyoosha mkono wangu aliukata kwa pigo la upanga wake, na akauning’iniza kwenye shingo yangu, akasema: Mrudishe ngamia huyu kwa mmiliki wake mara moja.”165 3 - Bahalul na Mwizi Kila wakati Bahlul alipokuwa akiwa na fedha nyingi kuliko mahitaji yake, alikuwa akijiwekea akiba kwa kuzificha katika kona moja ya nyumba gofu na iliyobomoka; hii iliendelea hadi hatimaye kiasi kikafikia dirhamu 300. Mara nyingine alipokuwa ameweka dirham kumi na alikuwa amekwenda sehemu hiyo ili kuongeza akiba yake aliyoificha, mfanyabiashara aliyekuwa anaishi jirani, aliyaona maficho yake. Bahalul alipoondoka tu kwenye maficho yule jirani alizichimba fedha zilizokuwa zimefichwa chini ya udongo. 165 Qadhawat-ha-e-Amirul Muuminin (as), uk. 119, kilichotungwa na Tustari 135


Visa vya Kweli sehemu ya Pili Mara nyingine Bahalul alipokuja sehemu ile, hakukuta fedha zake na mara moja akajua kuwa ilikuwa ni kazi ya mfanyabiashara. Aliamua kumuendea mfanyabiashara. “Nataka nikusumbue kwa kueleza siri yangu” Bahalul alimuambia mfanyabiashara. Nimeweka fedha zangu katika sehemu mbalimbali,” kisha alianza kuzitaja sehemu mpaka idadi ya fedha ikafikia dirham 3000. “Sehemu nilipoweka dirham 310 ndio salama zaidi kuliko zote. Sasa ninataka kuzihamishia fedha zangu zote katika sehemu hii kwenye nyumba iliyobomoka.” Aliposema hivi, alimuaga mfanyabiashara na akaondoka. Mfanyabiashara aliamua kurudisha zile dirham 310 pale alipokuwa ameziiba kwa nia kwamba Bahalul akiweka fedha zake hapo, ataiba kiasi kilichoongezeka. Siku kadhaa baadaye, Bahalul alirudi kwenye yale magofu na akazikuta dirham 310 katika sehemu yake ya awali. Alichukua fedha na akajisaidia haja kubwa hapo kisha akafunika kwa udongo. Mara tu Bahalul alipoondoka mfanyabiashara alikwenda haraka kwenye sehemu ile na akaondoa udongo akitaka kuchukua fedha zote (lakini) alijikuta akichafua mikono yake kwa kinyesi. Hivyo akautambua udanganyifu wa Bahalul. Siku chache baadaye Bahalul alimtembelea. “Nataka unipigie hesabu kuhusiana na fedha zangu,” alisema Bahalul. “Inakuwa ni dirham ngapi ukijumlisha dirham thelathi ukijumlisha na dirham hamsini ukijumlisha na dirham mia moja na idadi hii ikijumlishwa na harufu mbaya inayotoka kwenye mikono yako?” Alivyosema hivi akatimua mbio. Mfanyabiashara akamkimbiza kwa nguvu lakini akashindwa kumkamata.166

166 Rahnama-e-Sa’adat, Juz. 2, uk. 272; Khulasatul Akhbar, uk. 526 136


Visa vya Kweli sehemu ya Pili 3 Msoma Qur’an Kipofu ambaye ni Mwizi Allaam Ibn Al-Thamaan anasema: “Nilikuwa nimeajiriwa na mfanya biashara mmoja wa Basra ambapo siku moja, nililazimika kusafiri kwenda katika mji wa Ubullah. Niliweka dirham 500 katika mfuko na nikaanza safari. Nilifika katika kingo za mto Tigris ambapo nilikodi boti. Nilipokuwa nikipita eneo liitwalo Mismar, nilimuona mtu mmoja kipofu akiwa amekaa kwenye ukingo wa mto akisoma Qur’ani. Kwa sauti ya huzuni sana aliita: “Ewe nahodha nichukue kwenye boti kwani ninaogopa wanyama wanaweza kuniua usiku. Awali nahodha alikataa lakini nilipomfokea aliridhia. Kipofu alikaa ndani ya boti na alikuwa akisoma Qur’ani mfululizo kwa kichwa hadi tulipokaribia Ubullah, ambapo aliacha kisomo chake na akaanza kushuka kutoka kwenye boti. Ghafla nikabaini kwamba zile fedha za mfanyabiashara nilizokuwa nimepewa kama amana hazikuwepo. Wote nahodha na yule mtu kipofu walitoa nguo zao ili kuthibitisha kuwa walikuwa hawajachukuwa fedha. Nilijiwazia. “Yule mfanyabiashara lazima ataniua. Maelfu ya mawazo yalizunguka kichwani mwangu na nikaanza kulia na kusali. Nilivyokuwa nikitembea kueleleka Ubullah, mtu mmoja alinijia na akataka kujua sababu ya kulalama kwangu. Nilimjulisha juu ya wizi (uliofanyika) wa fedha za mfanyabiashara. “Nitakuonyesha njia (ya kuponyoka kwenye tatizo hili) alisema: “Nunua chakula kizuri, nenda gerezani na msihi mlinzi wa gereza akuruhusu uingie. Ndani ya gereza, nenda kwa Abu Bakr Naqqash na mpatie chakula. Atakuuliza juu ya tatizo lako na akifanya hivyo, msimulie kisa kizima.” Nilifuata maelekezo yake na nilipokuwa nimemsimulia tatizo langu Abu Bakr Naqqash, alisema: “Sasa nenda katika kabila la Bani Hilal na nenda katika nyumba fulani. Fungua mlango na ingia ndani ya nyumba. Hapo utaona leso zikining’inia nyuma ya mlango. Funga leso moja kiunoni mwako na kaa chini kwenye kona. Kundi la watu litaingia na kuanza kun137


Visa vya Kweli sehemu ya Pili ywa pombe, utapaswa uchukue bakuli pia na baada ya kusema, “Kwa afya ya mjomba wangu, Abu Bakr Naqqash, anza kunywa. Baada ya kusikia jina langu, watakuuliza juu ya afya yangu. Wapatie ujumbe huu. “Jana, fedha za mpwa wangu ziliibiwa. Tafadhali mrudishieni, nao watakukabidhi fedha.” Nilifanya kama nilivyoelekezwa na wao bila kupinga hata kidogo, walinikabidhi fedha. Niliwaomba wanijulishe jinsi mfuko wangu wa fedha ulivyoibiwa. Baada ya kusita sana, moja wao aliniuliza kama nilimtambua. Nilipomtazama kwa makini, nikabaini kuwa ni yule yule kipofu aliyekuwa anasoma Qur’ani, wakati yule mwingine alikuwa ni nahodha wa boti. “Mmoja wa washirika wetu huwa anaogelea majini nyuma ya boti,” alieleza. “Qur’ani inaposomwa, msafiri huwa anashughulishwa sana kiasi kwamba huwa habaini kuwa tumezitupia fedha zake ndani ya maji. Huchukuliwa na mwenzetu ndani ya maji na kupelekwa ufukweni kwenda kugawiwa miongoni mwetu pindi tunapokutana siku inayofuata. Leo ilikuwa ni siku ya kugawana fedha, lakini kwa kuwa tumepokea amri kutoka kwa mkuu wetu Abu Baqr Naqqash, tumekurudishia fedha.” Nilichukua fedha hizo na nikamshukuru Allah kwa kuniokoa kutoka katika utata huu.167

167 Dastan-ha wa Pand-ha, Juz. 2, uk. 71. Khazain Naraqi.

138


Visa vya Kweli sehemu ya Pili

ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION 1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9. 10. 11. 12. 13. 14. 15. 16. 17. 18. 19. 20. 21. 22. 23. 24.

Qur'an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Thelathini Uharamisho wa Riba Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili Hekaya za Bahlul Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.) Hijab vazi Bora Ukweli wa Shia Ithnaashari Madhambi Makuu Mbingu imenikirimu Abdallah Ibn Saba Khadijatul Kubra Utumwa Umakini katika Swala Misingi ya Maarifa Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia Bilal wa Afrika Abudharr Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu Salman Farsi Ammar Yasir Qur'an na Hadithi Elimu ya Nafsi 139


Visa vya Kweli sehemu ya Pili 25. 26. 27. 28. 29. 30. 31. 32. 33. 34. 35. 36. 37. 38. 39 40. 41. 42. 43. 44. 45. 46. 47. 48. 49. 50. 51. 52. 53.

Yajue Madhehebu ya Shia Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur'an Tukufu Al-Wahda Ponyo kutoka katika Qur'an. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii Mashukio ya Akhera Al Amali Dua Indal Ahlul Bayt Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna. Haki za wanawake katika Uislamu Mwenyeezi Mungu na sifa zake Kumswalia Mtume (s) Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) Adhana. Upendo katika Ukristo na Uislamu Tiba ya Maradhi ya Kimaadili Maana ya laana na kutukana katika Qur'ani Tukufu Kupaka juu ya khofu Kukusanya swala mbili Bismillah ni sehemu ya Qur'ani na husomwa kwa Jahara Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Kusujudu juu ya udongo Kusherehekea Maulidi Ya Mtume (s) Tarawehe Malumbano baina ya Sunni na Shia Kupunguza Swala safarini Kufungua safarini Umaasumu wa Manabii Qur'an inatoa changamoto 140


Visa vya Kweli sehemu ya Pili 54. 55. 56. 57. 58. 59. 60. 61. 62. 63. 64. 65. 66. 67. 68. 69. 70. 71. 72. 73. 74. 75. 76. 77. 78. 79. 80. 81.

as-Salaatu Khayrun Mina -'n Nawm Uadilifu wa Masahaba Dua e Kumayl Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mtume Muhammad (s) Nahju'l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza Nahju'l-Balaghah - Juzuu ya Pili Kuzuru Makaburi Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita Tujifunze Misingi Ya Dini Sala ni Nguzo ya Dini Mikesha Ya Peshawar Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu Ubora wa Imam 'Ali Juu ya Maswahaba Na Ushia ndio njia iliyonyooka Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake Liqaa-u-llaah Muhammad (s) Mtume wa Allah Amani na Jihadi Katika Uislamu Uislamu Ulienea Vipi? Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) 141


Visa vya Kweli sehemu ya Pili 82. 83. 84. 85. 86. 87. 88. 89. 90. 91. 92. 93. 94. 95. 96. 97. 98. 99. 100. 101. 102 103. 104. 105. 106. 107. 108. 109. 110.

Urejeo (al-Raja'a ) Mazingira Utokezo (al - Badau) Hukumu ya kujenga juu ya makaburi Swala ya maiti na kumlilia maiti Uislamu na Uwingi wa Dini Mtoto mwema Adabu za Sokoni Johari za hekima kwa vijana Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu Tawasali Imam Mahdi katika Usunni na Ushia Hukumu za Mgonjwa Sadaka yenye kuendelea Msahafu wa Imam Ali Ngano ya kwamba Qur'ani imebadilishwa Idil Ghadiri Kusoma sura zenye Sijda ya wajibu Hukumu zinazomuhusu mkuu wa kazi na Mfanyakazi Huduma ya Afya katika Uislamu Sunan an-Nabii Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza) Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili) Shahiid Mfiadini Kumswalia Nabii (s.a.w) Ujumbe - Sehemu ya Kwanza Ujumbe - Sehemu ya Pili 142


Visa vya Kweli sehemu ya Pili 111. 112. 113. 114. 115. 116. 117. 118. 119. 120. 121. 122. 123. 124. 125. 126. 127. 128. 129. 130. 131. 132. 133. 134. 135. 136. 137.

Ujumbe - Sehemu ya Tatu Ujumbe - Sehemu ya Nne Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu Hadithi ya Thaqalain Maarifa ya Kiislamu Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza Ukweli uliopotea sehemu ya Pili Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu Ukweli uliopotea sehemu ya Nne Ukweli uliopotea sehemu ya Tano Safari ya kuifuata Nuru Fatima al-Zahra Myahudi wa Kimataifa Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi Visa vya kweli sehemu ya Kwanza Visa vya kweli sehemu ya Pili Muhadhara wa Maulamaa Mwanadamu na Mustakabali wake Imam Ali ('a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Kwanza) Imam Ali ('a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Pili) Khairul Bariyyah Uislamu na mafunzo ya kimalezi Vijana ni Hazina ya Uislamu. Yafaayo kijamii Tabaruku Taqiyya Vikao vya furaha 143


Visa vya Kweli sehemu ya Pili 138. 139. 140. 141. 142. 143. 144. 145. 146. 147. 148. 149. 150. 151. 152 153. 154. 155. 156. 157. 158. 159. 160. 161. 162. 163. 164. 165. 166.

Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje? Visa vya wachamungu Falsafa ya Dini Kuhuzunika na Kuomboleza - Azadari Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah Mtazamo Mpya - Wanawake katika Uislamu Kuonekana kwa Allah Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza) Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili) Ndugu na Jirani Ushia ndani ya Usunni Maswali na Majibu Mafunzo ya hukmu za ibada Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 1 Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 2 Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 3 Abu Huraira Vipengee kadhaa katika Swala ya Jamaa na Msikiti. Mazingatio kutoka katika Qur'an - Sehemu ya Kwanza Mazingatio kutoka kaitka Qur'an - Sehemu ya Pili Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya kwanza Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya Pili Qur'ani Tukufu - Pamoja na Tarjuma ya Kiswahili Falsafa ya Mageuzi ya Imam Husein (a.s) Amali za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani Elimu ya Tiba za Kiislamu - Matibabu ya Maimamu Uislamu Safi Majlisi za Imam Husein Majumbani Mshumaa 144


Visa vya Kweli sehemu ya Pili 167. 168. 169. 170. 171. 172. 173. 174. 175. 176. 177. 178. 179. 180. 181. 182. 183. 184. 185. 186. 187. 188. 189. 190. 191. 192. 193. 194. 195.

Uislam wa Shia Amali za Makka Amali za Madina Asili ya Madhehebu katika Uislamu Sira ya Imam Ali kuhusu Waasi Ukweli uliofichika katika neno la Allah Uislamu na Mifumo ya Uchumi Umoja wa Kiislamu na Furaha Mas'ala ya Kifiqhi Jifunze kusoma Qur'ani As-Sahifatul Kamilah as-Sajjadiyyah Hayya 'Alaa Khayri'l-'Amal Katika Adhana Ukweli kuhusu Funga ya Siku ya Ashura Dua za Miezi Mitatu Mitukufu (Rajabu, Shaabani na Ramadhani) Uadilifu katika Uislamu Mahdi katika Sunna Jihadi ya Imam Hussein ('as) Kazi na Bidii ni njia ya maendeleo Abu Talib - Jabali Imara la Imani Ujenzi na Utakaso wa Nafsi Vijana na Matarajio ya Baadaye Usalafi - Historia yake, maana yake na lengo lake Ushia - Hoja na Majibu Mateso ya Dhuria wa Mtume (saww) Maombolezo - Msiba wa Bwana wa Mashahidi (a.s.) Shahidi kwa Ajili ya Ubinadamu Takwa Amirul Muuminina ('as) na Makhalifa Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.) 145


Visa vya Kweli sehemu ya Pili 196. 197. 198. 199. 200. 201.

Kuelewa Rehma ya Mwenyezi Mungu Mtazamo kuhusu msuguano wa kimadhehebu Upotoshaji Dhahiri katika Turathi (Hazina) ya Kiislamu Nchi na Uraia - Haki na wajibu kwa Taifa Mtazamo wa Ibn Taymiyyah kwa Imam Ali (a.s.) Uongozi wa kidini - Maelekezo na utekelezaji wa Kijamii

KOPI NNE ZIFUATAZO ZIMETAFSIRIWA KWA LUGHA KINYARWANDA 1. 2. 3. 4.

Amateka Na Aba'Khalifa Nyuma yaho naje kuyoboka Amavu n'amavuko by'ubushiya Shiya na Hadithi

146


Visa vya Kweli sehemu ya Pili

BACK COVER Katika Qur’ani, kuna sura iitwayo al-Qasas (Masimulizi), ambayo yenyewe tu ni ushahidi kuwa mwanadamu anahitaji hadithi na masimulizi. Katika sehemu nyingi ndani ya Qur’ani, hadithi za Mitume na wafalme wa mataifa zimetajwa. Kwa kuongezea Mwenyezi Mungu amezungumzia masuala yanayohusiana na vita, amani, familia, dini, jamii na mada nyinginezo, katika muundo wa hadithi na masimulizi. Kwa kuvisoma visa hivi, watu wanaweza kuelewa na kutofautisha kati ya njia ya maendeleo na ile ya kuporomoka kwa maendeleo, na kupanda na kushuka katika kila kipengee, hususan maadili. Kitabu hiki ambacho kiko katika sehemu tano, kimekusanya takriban visa vya kweli 500 juu ya maadili mema katika masuala ya uaminifu, imani, misiba, uchamungu, toba, ujinga, maombi, subira na mengine mengi. Inatarajiwa kutoka kwa wasomaji kwamba, baada ya kuvipitia visa na simulizi hizi, watatafakari na kuchukua mazingatio ili waweze kujijengea nguvu za kwenda katika ukamilifu wa maadili, na Allah akipenda wale waliojaaliwa maadili yenye kusifika wawasimulie wengine ili kuzirekebisha roho dhaifu. Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 / 2127555 Barua Pepe: alitrah@yahoo.com Tovuti: www.ibn-tv.com Katika mtandao: www.alitrah.info

147


Visa vya Kweli sehemu ya Pili

148


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.