Wajibu wa kutafuta elimu

Page 1

WAJIBU WA KUTAFUTA ELIMU (Duty of Acquiring Knowledge)

Mwandishi: Ustadh Shahid Murtadha Mutahhari

Kimetarjumiwa na: Salman Shou

13_16_Wajibu kutafuta Elimu (4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016.indd 1

6/18/2016 1:38:45 PM


©haki ya kunakili imehifadhiwa na: Al-Itrah Foundation ISBN: 978 - 9987 – 17 – 038 – 8 Kimeandikwa na: Ustadh Shahid Murtadha Mutahhari Kimetarjumiwa na: Salman Shou Kimehaririwa na: Al Haji Ramadhani S. K. Shemahimbo Kimesomwa-Prufu na: Ustadh Hemedi Lubumba Selemani Kimepitiwa na: Al Haji Mujahid Rashid Kimepangwa katika Kompyuta na: Al-Itrah Foundation Toleo la kwanza: Novemba, 2016 Nakala: 1000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. - 19701, Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 / 2127555 Barua pepe: alitrah@yahoo.com Tovuti: www.ibn-tv-com Katika mtandao: www.alitrah.info

13_16_Wajibu kutafuta Elimu (4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016.indd 2

6/18/2016 1:38:45 PM


Yaliyomo Dibaji.............................................................................................. 1 Neno la Mchapishaji...................................................................... 2 Hali ya Mataifa ya Kiislamu.......................................................... 6 Hadithi Nne:................................................................................... 8 Hadithi nyingine ni:....................................................................... 9 Hadithi ya tatu:............................................................................. 10 Kwa nini wajibu huu wa Kiislamu haukutimizwa?..................... 15 Elimu gani?.................................................................................. 17 Wajibu wa matayarisho:............................................................... 18 Kanuni ya kwanza: Uhuru na hadhi ya jamii ya Kiislamu.......... 20 Kanuni ya pili: Elimu kama msingi wa hadhi zote na uhuru....... 21 Elimu za kidini na za kisekula:.................................................... 22 Elimu ya wanawake..................................................................... 25 Kosa hili ni la nani?..................................................................... 29

13_16_Wajibu kutafuta Elimu (4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016.indd 3

6/18/2016 1:38:45 PM


Jihadi Tukufu:.............................................................................. 30 Wakati unapokuwa umepata elimu.............................................. 31 Kushindana katika kutoa huduma na katika wema:..................... 38

13_16_Wajibu kutafuta Elimu (4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016.indd 4

6/18/2016 1:38:45 PM


WAJIBU WA KUTAFUTA ELIMU

‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬

DIBAJI

K

itabu hiki ni toleo la Kiswahili la taasisi ya Al Itrah Foundation. Chapisho lake limelenga kukidhi mahitaji ya kiroho ya zama hizi pamoja na Ubongo na fikra zinazokuwa za Muislam. Jitihada kubwa zimefanywa na Taasisi kuweka chapisho hili la Kiswahili katika msingi wa haki na wenye kukubalika katika Uislam. Unaombwa kwa Taadhima ukisome kitabu hiki katika malengo yaliyokusudiwa. Pia Unaombwa kuwasilisha kwetu maoni yako huru juu ya chapisho letu hili, jambo ambalo tutashukuru sana. Kutangaza ujumbe wa Uislam ni kazi ambayo inahitaji ushirikiano wetu sote. Taasisi inakuomba kuungana na kushirikiana kama ilivyoagizwa katika aya ya Qur’an: (Surat Saba’ 34:46). Na rehma za Allah ziwe juu yako. Wako katika Uislam

Al Itrah Foundation Barua Pepe: alitrah@yahoo.com SMS: +255 778 300 140 1

13_16_Wajibu kutafuta Elimu (4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016.indd 1

6/18/2016 1:38:45 PM


WAJIBU WA KUTAFUTA ELIMU

‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬

NENO LA MCHAPISHAJI

K

itabu ulichonacho mikononi mwako chanzo chake ni makala kutoka jarida liitwalo, Message of Thaqalayn, toleo la 43, Na. 3, Majira ya Baridi 1431/2010, kwa lugha ya Kiingereza iliyoandikwa na: Shahid Murtadha Mutahhari. Mada kubwa ya makala hii ni kuhusu elimu, na msingi wake mkubwa ni hadithi ya Mtukufu Mtume pale aliposema: “Kutafuta elimu ni faradhi kwa kila Mwislamu.” Ziko hadithi nyingi za Mtukufu Mtume zinazotoa msisitizo juu ya elimu. Na katika Qur’ani Tukufu, aya tano za mwanzo kushuka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kutoka kwa Mola Wake zimebeba amri ya kusoma: “Soma kwa jina la Mola wako aliyeumba. Amemuumba mtu kwa pande la damu. Soma! Na Mola wako ni Karimu zaidi! Ambaye amefundisha kwa kalamu. Amemfundisha mtu aliyokuwa hayajui.” (96: 1-5)

2

13_16_Wajibu kutafuta Elimu (4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016.indd 2

6/18/2016 1:38:45 PM


WAJIBU WA KUTAFUTA ELIMU

Tumeiona makala hii ni yenye manufaa makubwa, hivyo, tukaamua kuifanya kuwa kijitabu kwa ajili ya wasomaji wetu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili, kwani huu ni wakati wa sayansi na tekinolojia ambapo ngano, hadithi za kale na upotoshaji wa historia ni vitu ambavyo kwa sasa havina nafasi katika akili za watu. Tunamshukuru ndugu yetu Salman Shou kwa kutarjumi makala hii kutoka lugha ya Kiingereza; pia tunawashukuru wale wote waliosaidia kwa njia moja au nyingine mpaka kuwezesha kitabu hiki kuchapishwa. Allah Mwenye kujazi awalipe wote malipo mema duniani na Akhera pia. MCHAPISHAJI AL-ITRAH FOUNDATION DAR ES SALAAM

3

13_16_Wajibu kutafuta Elimu (4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016.indd 3

6/18/2016 1:38:45 PM


WAJIBU WA KUTAFUTA ELIMU

‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬

‫قُلْ هَلْ يَ ْست َِوي الَّ ِذينَ يَ ْعلَ ُمونَ َوالَّ ِذينَ اَل يَ ْعلَ ُمونَ ۗ إِنَّ َما يَتَ َذ َّك ُر‬ ‫ب‬ ِ ‫أُولُو أْالَ ْلبَا‬ “…..Sema: Je wanalingana sawa wale ambao wanajua na wale ambao hawajui? Hakika ­wanaokumbuka ni wenye akili.” (39:9).

Mada yetu na maana yake iliyokusudiwa zimewekwa kwenye msingi wa hadithi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambayo inakubaliwa na madhehebu yote mawili: Shia na Sunni: “Kutafuta elimu ni faradhi kwa kila Mwislamu mwanamume na mwanamke.”

Kwa mujibu wa hadithi hii, mojawapo ya wajibu na faradhi ya Kiislamu ni kutafuta elimu. Katika lugha ya Kiarabu: “Faridhah” maana yake ni faradhi au wajibu na chimbuko lake ni neno la Kiarabu “Faradha” (kitenzi katika lugha ya Kiarabu) na maana yake ni “kuwa na uhakika” au “kulazimisha jambo.” Vile ambavyo tunaviita leo vitendo vya “wajib” au “mustahab” viliitwa katika kipindi cha mwanzo wa Uislamu “mafrudh” (ya lazima) na “masnuun” (yaliyopendekezwa). Lazima ielezwe kwamba maneno “wajib” na “wujuub” yalitumiwa katika zama hizo lakini sio mara 4

13_16_Wajibu kutafuta Elimu (4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016.indd 4

6/18/2016 1:38:45 PM


WAJIBU WA KUTAFUTA ELIMU

kwa mara kama “faridhat”, “mafrudh”, na “faradha”; ambapo neno “mustahab” na maana yake inayotumika leo linaonekana kubuniwa na mafakihi wa Kiislamu. Neno “mustahab” halikutumiwa katika Qur`ani Tukufu wala katika hadithi yoyote na hata wanasheria wa Kiislamu wa siku za mwanzo hawakulijumuisha katika fasiri zao. Huko nyuma siku zilizopita, walitumia maneno “masnuun” na “manduub” badala ya “mustahab.”Kutafuta elimu ni jambo la faradhi kwa kila Mwislamu na haiwi kwa tabaka au tabaka dogo la watu. Katika ustaarabu kabla ya ujio wa Uislamu, elimu ilikuwa ni ya upendeleo kwa wateule wachache. Katika Uislamu elimu ni faradhi na wajibu kwa kila mtu, kama ilivyo kwa utekelezaji wa swala za kila siku, kufunga saumu, kutoa zaka, kwenda Hijja, jihadi, na kuamrisha mema na kukataza mabaya. Tangu mwanzo wa Uislamu hadi sasa, madhehebu yote ya Kiislamu na wanazuoni wamekubaliana na hili. Kwa kawaida kuna mlango katika rejea za hadithi uitwao “Bab-u Wujuub-i Talab-i al-`Ilm” (Mlango juu ya wajibu wa Kutafuta Elimu). Hivyo, hadithi hiyo hapo juu inakubaliwa na wote na kama panahitajika mazungumzo yoyote mazungumzo hayo yatakuwa katika tafsiri na upeo wake.

5

13_16_Wajibu kutafuta Elimu (4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016.indd 5

6/18/2016 1:38:45 PM


WAJIBU WA KUTAFUTA ELIMU

Hali ya Mataifa ya Kiislamu: Hapa hakuna haja ya kuzungumzia masuala yanayozunguka kama namna Uislamu ulivyowahimiza watu kwenye elimu na kutaja aya kutoka kwenye Qur`ani Tukufu na kunukuu baadhi ya hadithi kutoka kwa viongozi wa kidini na kuashiria kwenye sehemu za historia ya Kiislamu inayohusiana na mada yetu. Sitaki kuusifu Uislamu na kuvuta uzingativu wenu mara kwa mara kuhusu jinsi ambavyo Uislamu umeunga mkono elimu na kuwasukuma wanadamu kwa mintarafu ya elimu, kwa sababu mambo kama hayo yamekuwa yakisemwa na yanaendelea kusemwa sana na ninaamini hayaleti manufaa makubwa. Mambo haya yanakuwa hayana tija kama mtu akitazama mataifa ya Kiislamu na kuona kwamba ni mataifa yasiyo na elimu zaidi na yasiyoelimika kabisa hapa duniani. Mtu kama huyo, angalau, atakuwa na swali moja kwamba “kwa nini mataifa ya dunia yaliyo mbali kabisa na elimu ni mataifa ya Waislamu kama maneno hayo ni ya kweli na Uislamu umeunga mkono elimu kwa kiasi kikubwa hivyo?� Mimi ninaamini kwamba ni lazima tuwe wazingativu zaidi kwa mintarafu ya matatizo yaliyopo katika jamii zetu na tutafakari kuhusu chimbuko la sisi kuwa nyuma kisayansi, na tutafute ufumbuzi badala ya pro6

13_16_Wajibu kutafuta Elimu (4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016.indd 6

6/18/2016 1:38:45 PM


WAJIBU WA KUTAFUTA ELIMU

paganda zisizofaa zilizotajwa hapo juu ambazo athari zake za mwisho ni za kutufanya sisi tuwe na furaha isiyodumu. Katika mhadhara huu hapa, Sayyid Musa Sadr (Mungu amrehemu) alitaja baadhi ya shughuli ya Allamah Sharaf al-Din na akasema kwamba pamoja na kwamba Allamah Sharaf al-Din alikuwa na vitabu vingi vilivyo mashuhuri vya kuwatambulisha Shia na Watu wa Nyumba ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.); alipoona hali ya wafuasi wa Shia nchini Lebanon na kwamba walikuwa ndio masikini wa kutupwa na walikuwa hawana elimu inayofaa, na miongoni mwao walikuwepo walimu, madaktari na mainjinia wachache na badala yake, wapagazi, watunza mabafu ya kuogea na wazoa taka wote walikuwa ni Shia, alijifikiria yeye mwenyewe kuhusu athari ambayo vitabu vyake vingeweza kuwa nayo. Alipatwa na wasiwasi kwamba watu wangesema Uislamu wa madhehebu ya Shia ulikuwa ni imani bora, hali ya Mashia lazima ingekuwa bora zaidi. Hilo lilimfanya afikirie kuhusu shughuli za kisayansi na kuanzisha shule, taasisi, na vikundi vya kutoa misaada kwa lengo la kuunda vuguvugu tukufu na kuendeleza jumuiya ya Kishia nchini Lebanon. Kwa ujumla, Waislamu wakilinganishwa na watu wengine wa dunia wapo kama wafuasi wa madhehebu ya Shia wa Lebanon wakilinganishwa na Walebanon wengine mwanzoni mwa vuguvugu la Allamah Sharaf al-Din. 7

13_16_Wajibu kutafuta Elimu (4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016.indd 7

6/18/2016 1:38:45 PM


WAJIBU WA KUTAFUTA ELIMU

Chochote tunachosema kuhusu Uislamu, jinsi unavyounga mkono elimu na kuhamasisha kwa mintarafu ya kupata elimu hakiwezi kuwa na athari yoyote katika hali iliyopo sasa katika mataifa ya Kiislamu. Hasa zaidi ambalo hili linaweza kukifanya ni kuzua swali tu kwa ajili ya msikilizaji kwamba kwa nini Waislamu wanateseka katika hali hii kama maneno haya ni ya kweli. Ngoja niwaambieni kisa fulani, na kabla ya kufanya hivyo nitasoma hadithi nne kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuhusu elimu na kuzitolea maelezo kwa sababu zinahusiana na kisa hiki na halafu nitakwambieni kisa chenyewe baadaye.

Hadithi Nne: Moja ni hiyo Hadithi iliyotajwa hapo juu ambayo inaashiria kwamba ni wajibu kwa kila Mwislamu mwanamume na mwanamke, kutafuta elimu. Ni kwa ajili ya wote, wanamume na wanawake kwa sababu neno “muslim” maana yake ni Mwislamu; awe mwanamume au mwanamke. Bila shaka, neno “wa muslimah” (na Waislamu wanawake) limeongezwa kwenye baadhi ya rejea za hadithi za madhehebu ya Shia kama Bihar al-Anwar. Kufuatana na hadithi hii, kutafuta elimu ni wajibu wa jumla kwa wote na sio kwa ajili ya jinsia au tabaka maalum. Inawezekana kuwepo na jambo la 8

13_16_Wajibu kutafuta Elimu (4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016.indd 8

6/18/2016 1:38:45 PM


WAJIBU WA KUTAFUTA ELIMU

wajibu kwa ajili ya vijana badala ya watu wa makamo na wazee, au kazi ambayo ni ya wajibu kwa gavana na sio kwa watawaliwa, au kinyume chake au kitu ambacho ni wajibu kwa wanamume na sio kwa wanawake kama vile jihadi (vita) na swala ya jamaa ya Ijumaa ambazo ni faradhi kwa wanamume na sio kwa wanawake, lakini wajibu kutafuta elimu ni wa lazima kwa Waislamu wote na sio mahsusi kwa wateule wachache. Hadithi nyingine ni: “Tafuteni elimu tangu mwanzo mwa utotoni hadi kaburini.�

Maana yake ni kwamba kutafuta elimu sio jambo la kufanya katika kipindi fulani cha wakati na lazima elimu itafutwe siku zote. Kwa kuwa hadithi ya kwanza iliondosha mipaka ya kijinsia na tabaka na ikafanya ni nadharia ya jumla, hadithi hii inaifanya ni dhana ya jumla kutoka kwenye kipengele cha wakati. Inawezekana kwamba wajibu fulani umewekewa mpaka kwenye muda mahsusi na hilo linaufanya usiwezekane kufanyika katika wakati wowote. Mathalani, wajibu wa kufunga saumu kila siku umewekewa mpaka muda mahsusi katika mwezi wa Ramadhani. Swala za kila siku pia zimewekewa wakati mahsusi wa siku na lazima zitekelezwe katika 9

13_16_Wajibu kutafuta Elimu (4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016.indd 9

6/18/2016 1:38:45 PM


WAJIBU WA KUTAFUTA ELIMU

masaa maalum. Hijja pia ni wajibu ambao pamoja na kwamba inaweza kutekelezwa tu wakati wa mwezi wa Dhi`I-Hijjah. Lakini kutafuta elimu ni jambo ambalo halikuwekewa muda au umri.

Hadithi ya tatu: “Tafuteni elimu hata kama iko China.”1

Kwa dhahiri, China imetajwa katika hadithi kwa sababu ama ilikuwa ni sehemu iliyokuwa mbali zaidi hapa duniani ambapo watu wangeweza kwenda wakati huo au ilikuwa inajulikana kama chimbuko la sayansi na viwanda. Hadithi ambayo imetajwa inatoa ushauri kwamba kutafuta elimu sio jambo la kuwekewa mpaka wa mahali na muda. Inawezekana kwamba wajibu unakuwa na mpaka wa mahali na haiwezekani kufanyika mahali popote pale; mathalani; ibada za Hijja zote zimewekewa mpaka wa wakati na mahali. Waislamu wanatakiwa kutekeleza ibada za Hijja katika jiji la Makkah, katika nchi ambamo Uislamu ulianzia na kuenea duniani kote, na lazima zitekelezwe kwa kuzunguka nyumba ambayo ilijengwa na Ibrahim na mwanawe mtukufu Ismail. Waislamu hawawezi kukubaliana wao kwa wao na wachague sehemu nyingine ya kutekelezea ibada ya Hijja. Hivyo wajibu huu umewekewa mpaka; hata hivyo, kutafuta elimu, hakuna sehemu yoyote mah1

Bihar al-Anwar, `Allamah Majlisi, Juz. 1, uk. 180 10

13_16_Wajibu kutafuta Elimu (4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016.indd 10

6/18/2016 1:38:45 PM


WAJIBU WA KUTAFUTA ELIMU

susi ambayo imewekwa kwa ajili hiyo na mahali popote penye elimu lazima ichukuliwe, ama ni Makkah, Madinah, Misri, Syria, Iraq au sehemu za mbali sana hapa duniani. Tuna mlolongo wa hadithi kuhusu manufaa ya kuhama na kusafiri kwenda sehemu za mbali sana kwa ajili ya kutafuta elimu na hata aya ifuatayo imefasiriwa kulingana na usemi huo hapo juu: “….Na mwenye kutoka nyumbani kwake katika kuelekea kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, kisha yakamfika mauti, basi yamethibiti malipo yake kwa Mwenyezi Mungu…..” (4:100) na “kuhama na kusafiri kwa mintarafu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mtume Wake” inatafsiriwa kama kuhama na kusafiri kwa ajili ya kutafuta elimu. Imetajwa katika hadithi nyingi kwamba “Kama ungejua ni manufaa gani ambayo ungeweza kuyapata kama matokeo ya kutafuta na kupata elimu, ungekwenda kutafuta elimu hata kama damu yako ingemwagika wakati upo safarini au (kama) utahitajika kusafiri kupita kwenye bahari nyingi.2 Hadithi ya nne kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Hikma ni rasilimali inayokosekana kwa muumini, na mtu ambaye amepoteza kitu angekikamata popote pale ambapo angekiona.”   Bihar al-Anwar. Juz. 2 uk. 177. (Yapo mabadiliko madogo katika

2

tafsiri)

11

13_16_Wajibu kutafuta Elimu (4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016.indd 11

6/18/2016 1:38:45 PM


WAJIBU WA KUTAFUTA ELIMU

Neno hekima ni neno thabiti, kamilifu na lenye nguvu ambalo maana yake ni kugundua ukweli. Sheria yotote inayoendana na ukweli na haikutengenezwa kwa kufuata akili inaitwa hekima. Imam Ali (a.s.) anasema: “Usemi wenye hekima ni kitu cha muumini kilichopotea. Kwa hiyo, nufaika kwa usemi wa hekima hata kama unatoka kwa wanafiki. Nyinyi, waumini, mnastahiki zaidi kupata usemi huo.”3 Sharti moja linaloambatana na kutafuta elimu ni kwamba elimu inayopatikana lazima iendane na ukweli na uhalisia; na kama ni hivyo, basi usijali unajifunza elimu na hekima hiyo kutoka kwa nani. Kwa kweli, yapo masharti fulani pale ambapo mtu anakuwa na shaka kuhusu ukweli wa suala husika. Katika mazingira kama hayo, wale ambao hawawezi kutofautisha ukweli na udanganyifu ni lazima wasiwasikilize walio kwenye njia potovu. Lazima wawe waangalifu kuhusu wale ambao wana ushawishi juu yao. Kama hawatakuwa waangalifu, wapo katika hatari ya kukengeuka. Lakini zipo nyakati ambapo ni hakika kwamba maneno ni ya kweli, kama vile ugunduzi katika tiba au sayansi asilia. Imeagizwa kwamba katika mazingira kama hayo, mtu anatakiwa kujifunza. Imenukuliwa katika hadithi zetu kutoka kwa Isa bin Mariam (a.s.), kwamba: “Pata ukweli na uukubali ukweli huo, hata kama unatoka kwa 3

Nahjul Balaghah, ilitarjumiwa na`Askari Ja`far, semi na. 80 12

13_16_Wajibu kutafuta Elimu (4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016.indd 12

6/18/2016 1:38:45 PM


WAJIBU WA KUTAFUTA ELIMU

watu wadanganyifu, lakini usiuchukue au kuukubali udanganyifu, hata kama unatoka kwa watu wa ukweli.”4 Lazima uchambue kile ambacho kimesemwa. Hadithi kama hizi zimeondosha mipaka ya upatikanaji wa elimu kuhusu aina ya watu ambako Mwislamu anaweza kupata elimu. Hiyo ni kwa sababu wajibu inaweza kuwa na mipaka zaidi kutokana na msimamo huu, yaani swala ya jamaa lazima iwe na Imam, lakini kuwa Imam wa aina hiyo, yapo masharti ambayo ni: kuwa Mwislamu, muumini na mwadilifu; lakini kinyume chake, hakuna sharti la aina hiyo ambalo limewekwa katika kupata na kuigawa elimu. Sasa ngoja tuwasimulie kisa, ambacho kinahusiana na hadithi hizi. Rafiki yetu aliyeelimika, Bwana Sayyid Muhammad Farzan alisimulia kwamba hapo kale, mwanzoni mwa mapinduzi ya Kikatiba,5 Bwana Sayyid Hibat al-Ddin Shahrestani (Mungu amrehemu) alichapisha jarida la Kiarabu liitwalo “Al-`Ilm” (au “elimu”) na lilichapishwa kwa kipindi cha miaka miwili au mitatu. Kwenye jalada la nyuma la jarida hili, neno “AL-Ilm” liliandikwa katika mtindo wa kikaligrafia ya Nasta`liq na hadithi nne hizo hapo juu ziliandikwa kwenye pembe nne za jarida hilo. Wakati fulani, iliandikwa kwenye jarida hilo kwamba wakati fulani Mjerumani mmoja   Bihar al-Anwar, Allamah Majlisi, Jz. 2, uk. 96  Mashrutiyyat

4 5

13

13_16_Wajibu kutafuta Elimu (4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016.indd 13

6/18/2016 1:38:45 PM


WAJIBU WA KUTAFUTA ELIMU

ambaye alikuwa mustashiriki alikwenda kumtembelea Bwana Shahrestani na akaziona hadithi hizo zikiwa katika jalada la nyuma. Mjerumani huyo aliuliza ni kitu gani hicho kilichoandikwa na akaambiwa hizo zilikuwa amri nne kuhusu utafutaji wa elimu zilizosimuliwa na Mtume wetu (s.a.w.w.). Baada ya kuwaomba wazitafsiri hadithi hizo, Mjerumani huyo alifikiri kwa muda mfupi na akaonesha mshangao wake kuhusu hadithi ambazo zilitia moyo wa kupata elimu bila ya ubaguzi wa kijinsia, muda, mahali, na aina ya mwalimu na akauliza kwamba inakuwaje basi pamoja na hadithi hizi Waislamu wapo nyuma sana katika elimu na idadi ya wajinga wasio na elimu miongoni mwao ni kubwa sana. Kwa nini kanuni hii ya jumla imepuuzwa na haifikiriwi kama ni wajibu, na ni kwa nini amri hizo hapo juu hazijafanyiwa kazi na kunaendelea kuwa mwujiza. Kwa hakika, katika mkondo wa historia Uislamu ulifanya vuguvugu kubwa la kisayansi na kitamaduni hapa duniani na kwa kipindi cha karne nyingi uliongoza katika elimu, utamaduni na ustaarabu. Uislamu ni dini ambamo aya za kwanza zilizoshuka kwa Mtume wake zilianza na:

‫ك‬ َ ُّ‫ق ا ْق َر ْأ َو َرب‬ َ َ‫ق َخل‬ َ َ‫ك الَّ ِذي َخل‬ َ ِّ‫ا ْق َر ْأ بِاس ِْم َرب‬ ٍ َ‫ال ْن َسانَ ِم ْن َعل‬ ِ ْ‫ق إ‬ ‫ال ْن َسانَ َما لَ ْم يَ ْعلَ ْم‬ ِ ْ‫أْالَ ْك َر ُم الَّ ِذي عَلَّ َم بِ ْالقَلَ ِم عَلَّ َم إ‬ 14

13_16_Wajibu kutafuta Elimu (4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016.indd 14

6/18/2016 1:38:46 PM


WAJIBU WA KUTAFUTA ELIMU

“Soma kwa jina la Mola Wako aliyeumba. Amemuumba mtu kwa pande la damu. Soma! Na Mola Wako ni Karimu zaidi! Ambaye amefundisha kwa kalamu. Amemfundisha mtu aliyokuwa hayajui.� (96:1-5).

Hivyo, hili ni suala la kuhojiwa kwamba ni kwa jinsi gani dini ambayo kanuni yake ya kwanza ni Umoja na ambayo hairuhusu vizuizi vyovyote katika kufikiri na kujifunza iweze kushindwa kuunda ustaarabu mkubwa. Kwa nini wajibu huu wa Kiislamu haukutimizwa? Kwa hakika, mojawapo ya sababu zake ni kitendo kile kilichofanywa na serikali za ukhalifa ambazo zilisababisha matatizo katika maisha ya Waislamu. Serikali za ukhalifa zilitengeneza jamii yenye matabaka kitu amcho hakikuendana na sheria za Kiislamu. Halafu, jamii ikagawanywa katika tabaka la watu wa hali ya chini na tabaka la wafujaji, wabadhirifu, na wenye kiburi ambao hawakujua wafanye nini na rasilimali zao. Wakati hali ya watu inapodhoofishwa, itakuwa vigumu watu kuzingatia wajibu kama huo na hata baadhi ya masuala yatazuia kufanya ukamilishaji wao. Sababu nyingine ya tatizo ilikuwa kwamba elimu haikutiliwa maanani kwa sababu uzingativu ulielekezwa kwenye kitu kingine; ni kama vile muamana 15

13_16_Wajibu kutafuta Elimu (4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016.indd 15

6/18/2016 1:38:46 PM


WAJIBU WA KUTAFUTA ELIMU

fulani unahamishwa kutoka akaunti moja kwenda akaunti nyingine, mathalani, kama vile mtu anafungua akaunti benki akiwa na miamana kadhaa na halafu wenye mamlaka ya benki wanahamisha miamana hiyo kutoka kwenye akaunti hiyo na kupeleka kwenye akaunti nyingine. Wanadai kwamba sababu ya kutokutilia maanani kanuni za Kiislamu kuhusu elimu ilikuwa kwamba yote yale ambayo Uislamu ulifikiria kuwa hamasa kwa watu kujifunza, kuondoa ujinga, na ubora wa elimu yote yalichukuliwa kama muamala kwa wanazuoni (Ulamaa) wa Kiislamu kama vile kuwaheshimu wao, na watu badala ya kuzingatia suala la wao kusoma na kupata elimu wakawa wanatafuta ukaribu kwa wanazuoni wa Kiislamu na kuwaheshimu na yote haya ndiyo yalisababisha hali iliyopo sasa. Madai hayo hapo juu kwa kiwango fulani yapo sahihi, pamoja na kwamba wanazuoni wa Kiislamu hawajafanya vitendo vya upotoshaji kama hivyo. Haya yalikuwa ni matokeo ya kusikia kutoka kwa masheikhe wa kawaida wa mimbari kuhusu umuhimu wa kuwaheshimu watu wenye kuelimika kuliko kuheshimu elimu yenyewe. Tatizo lingine limekuwa kwamba wakati mwingine wanazuoni wa taaluma fulani ya elimu ya Kiislamu walisisitiza kudai kwamba faradhi (Faridhah) iliyotajwa katika hadithi hiyo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) 16

13_16_Wajibu kutafuta Elimu (4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016.indd 16

6/18/2016 1:38:46 PM


WAJIBU WA KUTAFUTA ELIMU

ilikuwa inatumika kwa ajili ya nidhamu yao tu na sio kwa watu wengine. Elimu gani? Katika “Al-Mahajjat al-Bayda,� ya marehemu Mulla Muhsin Fayd niliona nukta moja nzuri sana ambayo ni dhahiri aliichukua kutoka kwa Ghazali. Anasema kwamba wanazuoni wa Kiislamu wamegawanyika katika takribani makundi ishirini yakiegemea kwenye tafsiri ya hadithi iliyotajwa na kila kundi - bila kujali taaluma zao - limesisitiza kwamba hadithi iliyotajwa ilirejelea kwa nyanja ya uchunguzi wao tu. Mathalani, kuhusu hadithi iliyotajwa hapo juu wanatheolojia wanasema kwamba, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa na maana ya theolojia ya Kiislamu kwa sababu ni elimu ya kanuni za kidini. Watu wa elimu ya maadili wamesema kwamba lengo lilikuwa ni maadili yaani kujifunza vitendo vinavyomwongozea mtu kwenye furaha na vile ambavyo humzuia asiwe na furaha. Mafakihi walisema kwamba fikihi (elimu ya sheria za Kiislamu) ndio iliyokusudiwa. Kwamba kila mtu anatakiwa kujua wajibu wake wa kidini ama yeye mwenyewe kuwa mujitahidi (faqih) au kwa kuwafuata wanasheria waliobobea. Wafasiri walisema kwamba tafsiri ya Qur`ani Tukufu ndio iliyomaanishwa kwa sababu elimu ilimaanishwa kuwa 17

13_16_Wajibu kutafuta Elimu (4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016.indd 17

6/18/2016 1:38:46 PM


WAJIBU WA KUTAFUTA ELIMU

Kitabu cha Mungu. Wanazuoni wa hadithi wakasema kwamba ilikusudiwa kuwa ni elimu ya hadithi kwa sababu kitu chochote hata Qur`ani Tukufu yenyewe, lazima itafisiriwe kwa mujibu wa hadithi hiyo. Wafuasi wa Masufi (Gnostics) walisema kwamba usufi na elimu ya hatua za kiroho ndizo zilizokusudiwa. Baada ya kueleza sababu ya kila kundi, Ghazali anatoa maelezo ambayo kwa kiasi fulani yana maarifa mapana. Na kwa ufupi, ni kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakuwa na maana ya elimu yoyote pekee kati ya zile zilizotajwa hapo juu; na kama alikuwa na maana ya kuihusisha mojawapo ya elimu hizo, angeielezea. Tunachohitaji kufanya ni kugundua kwanza ni nini cha muhimu katika Uislamu kama wajibu wa kila mtu au wajibu wa watu wote, na halafu elimu yoyote ile inayohitajika kwa ajili ya kutekeleza huo wajibu wa lazima inakuwa faradhi. Wajibu wa matayarisho: Wanafikihi wa Kiislamu wanafikiria wajibu wa kupata elimu ni wa “matayarisho” na “kwa wenyewe.” Maana yake ni kwamba wajibu wa kupata elimu sio tu ni wa matayarisho kama yale masharti ya wajibu ambayo yenyewe sio ya wajibu; kutafuta elimu kwenyewe ni wajibu. Mafakihi wanasema kwamba wajibu huu wa matayarisho ni kwa ajili ya kujifunza hukumu, kama 18

13_16_Wajibu kutafuta Elimu (4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016.indd 18

6/18/2016 1:38:46 PM


WAJIBU WA KUTAFUTA ELIMU

vile inavyofikiriwa kwa ujumla kwamba utekelezaji wa wajibu wa Kiislamu unategemea juu ya ukweli kwamba Waislamu wanajua wajibu wao wenyewe na kwa kufanya hivyo, wataweza kutekeleza wajibu huo kwa kujiendesha wao wenyewe tu. Hivyo, wajibu wa elimu iliyopatikana ni kwamba Mwislamu lazima awe mwanazuoni wa elimu ya fikihi au awe mfuasi wa mmojawapo. Ambapo ni wazi kwamba pamoja na kujua wajibu na amri za kidini ambazo zinatakiwa kujifunza, vitendo vingi ambavyo ni wajibu katika Uislamu vinahitaji elimu, somo na ustadi. Mathalani, kufanya kazi ya utabibu ni wajibu wenye kuchangia ambao hauwezi kufanyika bila mtu kupata elimu ya utabibu, na kupata elimu kama hiyo ni wajibu na ni hivyo hivyo hata katika wajibu mwingine. Mtu ni lazima aone ni mahitaji na wajibu gani uliopo katika jamii ya Kiislamu na ambao hauwezi kutekelezeka vizuri bila kujifunza, kwa hiyo kupata elimu yake ni wajibu. Wajibu wa kupata elimu unategemea sana juu ya kiwango cha mahitaji ya jamii. Wakati fulani; kilimo kilihitaji viwanda, uchuuzi, na siasa haikuhitaji elimu. Wakati fulani watu wanaweza kuwa wanasiasa, mafundi stadi, au wafanya biashara kwa kupata mafunzo mafupi au muda wa kujifunza uanagenzi kama msaidizi wa mabingwa katika nyanja 19

13_16_Wajibu kutafuta Elimu (4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016.indd 19

6/18/2016 1:38:46 PM


WAJIBU WA KUTAFUTA ELIMU

hizi za kitaaluma. Lakini leo hii hakuna shughuli hizo zilizotajwa hapo juu ambayo inaweza kuendeshwa bila elimu katika namna ambayo inaweza kuendana na mtazamo wa dunia na maisha ya leo. Leo hii hata kilimo lazima kiendeshwe kisayansi na kuzingatia kanuni za kiufundi. Kama mfanyabiashara hajifunzi elimu ya uchumi, sio rahisi kuwa mfanyabiashara wa sawasawa hasa. Kanuni hiyo hiyo inatumika kwa wanasiasa. Leo hii pametokeza shughuli ambazo haziwezi kuendeshwa bila elimu na taaluma. Aina ya kazi ambazo zilikuwa zinasomewa kwa muda mfupi na kuwa kama msaidizi sasa hivi zimekuwa tofauti kwani kazi hizo hazifanyiki bila mtu kusomea kwenye shule au vyuo vya ufundi. Kazi zilizo nyingi zinahitaji mafundi stadi na mafundi sanifu. Kanuni ya kwanza: Uhuru na hadhi ya jamii ya Kiislamu. Hapa tunahitaji kuzingatia nukta kuu kadhaa za kikanuni. Kwanza tunapaswa kuona ni aina gani ya jamii inayotafutwa na Uislamu? Uislamu unatafuta jamii ambayo inaheshimika, iliyo huru na yenye kujitegemea na kwa kweli, Uislamu haukubali kwamba ummah wa Kiislamu kuwa chini ya taifa lisilo la Kiislamu: â€œâ€Ś.Mwenyezi Mungu hatawafanyia makafiri njia ya kuwashin20

13_16_Wajibu kutafuta Elimu (4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016.indd 20

6/18/2016 1:38:46 PM


WAJIBU WA KUTAFUTA ELIMU

da waumini.�(4:141). Pia Uislamu haukubali kwamba taifa la Waislamu siku zote liwe linaomba msaada ya bure kutoka taifa lingine. Zaidi ya hayo, Uislamu haukubali kwamba jamii ya Kiislamu iwe haina uhuru wa kiuchumi au kijamii. Uislamu kamwe hukubali kwamba Waislamu wawe hawana daktari au huduma za tiba wanapougua sana na wanavumilia maradhi na kwenda kwa watu ambao sio Waislamu. Na yote haya yanonesha kuwa na kanuni. Kanuni ya pili: Elimu kama msingi wa hadhi zote na uhuru. Kanuni nyingine ni kwamba pamefanyika mapinduzi hapa duniani kwamba mambo yote yanafanyika kwa kutegemea elimu na maisha yanapatikana kwa kutegemea elimu.Vipengele vyote vya maisha ya binadamu vinategemea elimu na hakuna hata kimojawapo ambacho kinaweza kushughulikiwa bila ufunguo wa elimu. Kanuni ya tatu: Elimu kama ufunguo wa utekelezaji wa wajibu nyingine mbalimbali. Utekelezaji wa wajibu mbalimbali ada za mtu binafsi na kijamii ya Kiislamu unategemea katika kupata elimu. Kwa ujumla elimu inajulikana kama ufunguo wa uka21

13_16_Wajibu kutafuta Elimu (4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016.indd 21

6/18/2016 1:38:46 PM


WAJIBU WA KUTAFUTA ELIMU

milishaji wa wajibu mbalimbali malengo ya Kiisalmu ambayo katika elimu ya sheria (fiqhi) huitwa ya wajibu wa matayarisho. Hivyo, kama mambo ya Waislamu yanaendelea na kunufaisha wengi kutokana na sayansi ya kutafuta elimu inakuwa muhimu zaidi na hupanuka zaidi katika uwanja wake. Suala la kupata elimu limezungumziwa katika sehemu mbalimbali za fiqhi na kanuni zake. Mathalani, katika kanuni za fiqhi (usul al-fiqh) wakati wa kuzungumzia “kanuni ya msamaha” (al-bara`ah) wanajifunza “umuhimu wa kupima (mahitaji ya) sababu.” Hapa wanajadili elimu. Katika sayansi ya sheria (al-fiqh) wanapozungumzia suala la “mustahabu au wajibu wa kujua hukumu za kivitendo za Shari`ah kuhusu biashara” wanasheria huchunguza umuhimu wa elimu. Pia wanasheria huzungumzia elimu wakati wanapochunguza ukubalikaji wa kulipwa kwa ajili ya kutekeleza vitendo vya wajibu. Elimu za kidini na za kisekula: Imekuwa ni tabia kwetu sisi kuziita baadhi ya elimu kuwa ni za kidini na baadhi ya zingine kuwa za kisekula. Elimu za kidini ni zile ambazo zinahusiana moja kwa moja na vitendo vya kitheolojia, kimaadili au matendo ya kidesturi au zile ambazo ni sharti kujifunza elimu 22

13_16_Wajibu kutafuta Elimu (4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016.indd 22

6/18/2016 1:38:46 PM


WAJIBU WA KUTAFUTA ELIMU

za Kiislamu, wajibu mbalimbali, na hukumu kama vile fasihi ya Kiarabu na mantiki. Baadhi ya watu wangedhani kwamba elimu zingine wala hazihusiani na dini, na chochote kile ambacho Uislamu umeelekeza kuhusu ubora wa elimu na thawabu za kuitafuta kwake, kimetengwa mbali na kile ambacho kinahau kinaitwa elimu ya kidini na kwa “wajibu wa kutafuta elimu”, kwa upekee Mtukufu Mtume  alikuwa na maana ya elimu ambazo zinaitwa elimu ya kidini. Ukweli ni kwamba hilo sio lolote bali ni nembo ya sifa tu. Katika msimamo mmoja, elimu ya kidini imetenganishwa na vitabu vya msingi, yaani Qur`ani Tukufu na hadithi halisi za Mtukufu Mtume  au warithi watukufu baada yake. Katika kipindi cha mwanzo wa Uislamu, wakati watu walipokuwa bado hawajaufahamu, ilikuwa ni wajibu kila mmoja kujifunza vile vitabu vikuu vilivyotajwa kabla ya kitu chochote. Wakati huo hapakuwepo na elimu za theolojia, mantiki, au historia ya Kiislamu. Mtukufu Mtume  alisema: “Kwa kweli, elimu ni ya aina tatu: aya madhubuti, wajibu wa haki, na hadithi sahihi.”6 Hii maana yake ni kwamba elimu imetengwa kwenye kujifunza aya za Qur`ani Tukufu, Hadithi za Kitume, na hukumu za kiutendaji. Badaye, Waislamu waliyazoea haya maandiko ya msingi ya Qur`ani Tukufu na hadithi ambazo zipo kama katiba ya   Usul al-Kafi, Sheikh Muhammad Kulayni, Jz. 1, uk. 32

6

23

13_16_Wajibu kutafuta Elimu (4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016.indd 23

6/18/2016 1:38:46 PM


WAJIBU WA KUTAFUTA ELIMU

Uislamu na kwa amri zao, walichukulia kutafuta elimu kama wajibu kamili na baadhi ya elimu zilianzishwa polepole. Kila elimu ambayo ina manufaa kwa Waislamu na inatatua matatizo ya Waislamu ni elimu ambayo lazima itafutwe kwa mujibu wa dini na inakuwa elimu ya kidini. Kwa nini tunatambua sarufi na msamiati wa Kiarabu kama elimu ya kidini? Hivi hilo linahifadhi dhahiri ukweli kwamba linanufaisha malengo ya Uislamu? Kwa nini huwa tunajifunza mashairi ya kimahaba ya Imra` al-Qays na mashairi ya mlevi Abu Nuwaas? Kwa kweli, ni kwa sababu yanatusaidia kuelewa Kiarabu, ambayo ni lugha ya Qur`ani Tukufu. Hivyo, elimu yoyote ambayo ina manufaa na muhimu kwa Uislamu lazima ichukuliwe kama sayansi ya kidini, na kama mtu anayo nia safi na anatafuta sayansi hiyo kutumikia Uislamu, atazawadiwa kama wale ambao wametajwa katika hadithi kwa ajili ya kutafuta elimu: “kwa kweli, malaika wanatandaza mabawa yao chini ya (miguu) ya watafutaji wa elimu.”7 Lakini kama mtu hana nia safi, hatapata thawabu hata kama akisoma aya za Qur`ani Tukufu. Kwa ujumla, hatuko sahihi tunapogawanya elimu zote katika makundi mawili: ya elimu ya kidini na ya 7

Usul al-Kafi, Sheikh Muhammad Kulayni, Jz. 1, uk. 34 24

13_16_Wajibu kutafuta Elimu (4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016.indd 24

6/18/2016 1:38:46 PM


WAJIBU WA KUTAFUTA ELIMU

kisekula jambo ambalo huwafanya baadhi ya watu kudhani kwamba hizo elimu ziitwazo za kisekula ni jambo geni kwa Uislamu. Ukweli kwamba Uislamu ni ujumbe wa mwisho wa Mungu wenye maarifa mengi unahitajia kwamba kila sayansi yenye manufaa na muhimu kwa jamii ya Kiislamu lazima ifikiriwe kuwa ni elimu ya kidini. Elimu ya wanawake. Kama ambavyo imetamkwa hapo juu, kutafuta elimu sio jambo la wanamume pekee. Hivyo Mtukufu Mtume 3 alisema: “Kutafuta elimu ni wajibu wa Waislamu wote,” na neno halisi ambalo limetumika ni (muslim) Waislamu, likiwa na muundo wake wa sarufi ya jinsia ya kiume, baadhi ya watu wamedhani kwamba kutafuta elimu ni wajibu wa wanamume tu. Kwanza, katika baadhi ya matini ya hadithi hii ambayo yapo katika rejea za madhehebu ya Shia, fungu la maneno, “wa muslimah” (“na wanawake Waislamu” katika Kiarabu) pia limejumuishwa. Pili, maelezo kama hayo huwa hayaoneshi upendeleo kwa jinsia mahsusi. Katika lugha ya Kiarabu, wakati neno “muslim” linapotumiwa likiwa peke yake na sio kinyume cha “muslimah” linaweza kurejelea kwa Mwislamu mwanamume au mwanamke. Mathalani, katika hadithi hii: 25

13_16_Wajibu kutafuta Elimu (4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016.indd 25

6/18/2016 1:38:46 PM


WAJIBU WA KUTAFUTA ELIMU

“Mwislamu ni yule ambaye kupitia ulimi wake na mkono wake Waislamu wengine wanakuwa salama,”8 kwa hakika, haijamaanishwa kwamba ni Waislamu wanamume tu ndio ambao lazima wawe hivyo. Mahali pengine, Mtukufu Mtume 3 amesema: “Waislamu ni ndugu wao kwa wao.”9 Hapa, mtu hawezi kusema kwamba hadithi hii inawahusu wanamume tu kwa sababu yeye Mtukufu Mtume 3 hakusema “Wanawake Waislamu ni dada wa wao kwa wao.” Neno “muslim” (katika lugha ya Kiarabu) linalo dhana mbili: kuwa Mwislamu na kuwa mwanadamu. Kila mtu anajua kwamba katika mifano kama hiyo jinsia haina umuhimu na kuwa Mwislamu tu ndio muhimu. Hata kama badala ya neno “muslim”, neno “rajul” (katika lugha ya Kiarabu maana yake ni “mwanamume” ndio lilitumiwa, lakini upande wake wa kijinsia unaweza kutotiliwa maanani. Hivi ndivyo wanavyoita wanafikihi, “ilgha’ al-khususiyyah” (kutokutilia maanani umaalum). Katika hadithi zingine katika masuala ya maarifa ya kifikihi, hadithi husika inawahutubia wanamume; yaani imeuliziwa kutoka kwa mmojawapo wa Maimamu E kwamba mwanamume ameshughulika namna ile na hilo likatokea, sasa atafanyaje? Na Imamu B amejibu swali hilo. Wanasheria wanasema kwamba 8 9

Usul al-Kafi, Sheikh Muhammad Kulayni, Jz. 2, uk. 234   Usul al-Kafi, Sheikh Muhammad Kulayni, Jz. 2, uk. 166 26

13_16_Wajibu kutafuta Elimu (4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016.indd 26

6/18/2016 1:38:46 PM


WAJIBU WA KUTAFUTA ELIMU

pamoja na kwamba neno “mwanamume” limetajwa katika hadithi hiyo, lakini katika masuala kama hayo, upendeleo hautiliwi maanani, kwa sababu ni dhahiri kwamba jinsia haiathiri hitimisho. Zaidi ya hayo, katika elimu ya fikihi ipo kanuni moja kwamba baadhi ya maneno ya ujumla hayaruhusu kuingiza vizuizi au marekebisho. Mathalani, suala kama hilo kama kile ambacho kimetajwa kuhusu elimu linaletwa katika Qur`ani Tukufu kuhusu “Takua” (ucha-Mungu). Kuhusu elimu, imetamkwa: “…Je, wanalingana sawa wale ambao wanajua na wale ambao hawajui? Hakika wanaokumbuka ni wenye akili tu.”(39:9). Kuhusu Takua, imeandikwa: “Je! Tuwafanye walioamini na wakatenda mema kama mafisadi katika ardhi? Je tuwafanye wenye takua kama waovu?” (38:28) na pia imetamkwa: “….Hakika mtukufu zaidi yenu mbele ya Mwenyezi Mungu ni aliye na takua zaidi yenu….” (49:13), na katika mifano yote hii, vihusishi ni vya kiume na haikusemwa: “Hivi Tutawatendea wanamume wenye takua na wanawake wenye takua” na haikusemwa: “mtukufu zaidi yenu mbele ya Mwenyezi Mungu ni aliye na takua zaidi yenu wanawake.” Hivi mtu anaweza kudai kwamba kwa sababu ya vihusishi ni vya kiume, kinachotamkwa kuhusu Takua ni mahsusi kwa wanamume na kuwatenga wanawake? Uislamu unaiona elimu kama nuru na ujinga kama giza kama 27

13_16_Wajibu kutafuta Elimu (4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016.indd 27

6/18/2016 1:38:46 PM


WAJIBU WA KUTAFUTA ELIMU

ambavyo imetamkwa katika Qur`ani Tukufu kwamba: “Sema, Je, anaweza kuwa sawa kipofu na aonaye? Au Je, Huwa sawa giza na nuru….?” (13:16). Kwa hiyo, Mtukufu Mtume 3 anaposema: “Kupata elimu ni wajibu wa Waislamu wote”10 lazima iwe faradhi kwa kila Mwislamu. Hivi mtu yeyote anaweza kuchukulia kwamba katika Uislamu wanamume wanapaswa kutoka kwenye giza na kuingia kwenye nuru, lakini wanawake bado wawepo kwenye giza? Na kwamba ni wajibu wa wanamume tu kutoka kwenye upofu huo lakini wanawake wabakie kwenye upofu huo? Mwishoni mwa aya, imetamkwa kwamba: “….Wanaokumbuka ni wenye akili tu.” (39:9) ikiwa na maana kwamba wale wenye akili wanajua vema masuala kama hayo. Kwa kweli, Qur`ani Tukufu inataka kusema kwamba suala kama hilo ni kitu kilicho dhahiri na kila mtu anaweza kulielewa. Imeelezwa kuhusu Mtukufu Mtume 3 katika aya nyingine: “….awasomee Aya Zake, na awatakase, na awafunze Kitabu na hikima….” (62:2). Katika aya hii, utakaso na mafundisho yametajwa kwa pamoja na yote hayo ni katika muundo wa jinsia ya kiume. Kama “kuwatakasa” inaweza kuwa mahsusi kwa wanamume, “kuwafundisha wao” pia inaweza kuwa mahsusi kwa wanamume.   Usul al-Kafi, Sheikh Muhammad Kulayni

10

28

13_16_Wajibu kutafuta Elimu (4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016.indd 28

6/18/2016 1:38:46 PM


WAJIBU WA KUTAFUTA ELIMU

Kosa hili ni la nani? Baada ya kusikia maelezo haya, baadhi ya watu watafanya haraka kusema: “Vipi wewe! Hivi unasema kwamba tuwapeleke mabinti zetu kwenye hizi shule zilizopo na wajifunze mambo ambayo ni kinyume na utamaduni wa kidini?� Jibu ni kwamba: kama yapo matatizo yoyote kwenye shule hizi na utamaduni; ni kosa la watu kwa sababu wao hawajazirekebisha. Na pamoja na kuwalazimisha watu kutafuta elimu, Uislamu umechukulia matayarisho ya kurekebisha jamii kama ni jambo la wajibu na hauwaruhusu watu kukaa majumbani na kungoja hadi hapo shule zitakapokuwa zinafaa asilimia mia moja kwa ajili ya watoto wao wanamume na wanawake ndipo wawapeleke watoto wao shule. Uislamu hauwaruhusu watu kulaumu bila kufanya lolote katika kuboresha hali iliyopo. Ni wajibu wetu kujenga shule nzuri zenye utamaduni mzuri. Kimsingi, mtu ambaye hajachukua hatua japo ndogo kwa ajili ya utamaduni, mtu ambaye hakushiriki katika kuanzisha jumuiya yoyote ya kitamaduni na hajachukua hata hatua moja katika kutekeleza wajibu wa kutafuta elimu haruhusiwi kukaa na kushutumu tu. Matatizo ya kitamaduni yalianzishwa pale ambapo wakosoaji hawakufanya wajibu wao wa kidini kuhusu utamaduni. 29

13_16_Wajibu kutafuta Elimu (4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016.indd 29

6/18/2016 1:38:46 PM


WAJIBU WA KUTAFUTA ELIMU

Inafaa ifahamike kwamba kwa jinsi ambavyo kuweka umaalum kunahusika, wanawake wanatakiwa kujaribu kubobea kwenye taaluma ambazo zinaendana na uwezo na vipaji vyao na wanaweza kutumikia jamii vema zaidi. Hivi mtu anaweza kusema kwamba jamii haihitaji madaktari wanawake au wapasuaji au wakunga? Jambo la kustaajabisha ni kwamba wakati suala linapohusu elimu ya wanawake, baadhi ya watu hukosoa na wakati haja inapojitokeza wanawake wanatakiwa kuwarejea madakitari wanamume au hata makafiri kwa ajili ya kupata dawa au hata kufanyiwa upasuaji. Jitihada Tukufu: Matokeo ya yote yaliyotajwa hapo juu ni kwamba leo hii wajibu mkubwa kabisa kuliko wajibu mwingine wowote ni kushiriki katika elimu ya ummah. Sharti hili sio wajibu wa wale ambao wanajishughulisha na mambo ya kitamaduni tu, lakini ni wajibu wa kila mtu ambaye ni Mwislamu na hao ambao wanadai kuwa Waislamu, ama awe ni mtu wa serikali au wa taifa. Wajibu kama huu lazima uendeshwe kama jitihada tukufu na katika namna ya kidini. Kwa hiyo wanazuoni wa kidini lazima wachukue heshima hii na kuwa watangulizi. Waumini na watu wa dini lazima wasiogope shule na 30

13_16_Wajibu kutafuta Elimu (4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016.indd 30

6/18/2016 1:38:46 PM


WAJIBU WA KUTAFUTA ELIMU

elimu na kudhani kwamba wakati sayansi ikiingia basi dini itakuwa imeondoka. Fikira hii inaonesha kukosa imani katika Uislamu. Uislamu ni dini ambayo hukua katika mazingira ya kisayansi vizuri zaidi kuliko katika mazingira ya ujinga. Tunatakiwa kuuogopa ujinga na kutokuwa na elimu kuliko kuiogopa sayansi na shule kama tungekuwa tunajua kile ambacho ujinga umetufanyia sisi na Uislamu. Wakati unapokuwa umepata elimu….. Wakati mwingine, tunawaona baadhi ya watu wanaweza kutumia shairi la Sana`i kuficha hofu yao ya elimu; shairi ambalo linasema: “Wakati unapopata elimu basi ogopa, kwani wakati wa usiku kama mwizi akija na mwanga, atachagua bidhaa vizuri zaidi.”

Na halafu wanasema: “Tazama! Madhara ya watu hawa waliosoma, kwa nchi ni mabaya mara 100 zaidi kuliko madhara ya wale wasio na elimu! Watu wasio na elimu hasa zaidi wanaweza kuiba vitu visivyo na thamani, lakini watu hawa waliokwenda shule wanaiba mamilioni ya Tumani!” Hapana shaka kwamba sayansi, kwa yenyewe tu, sio dhamana ya kuwa na jamii yenye ustawi. Jamii 31

13_16_Wajibu kutafuta Elimu (4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016.indd 31

6/18/2016 1:38:46 PM


WAJIBU WA KUTAFUTA ELIMU

inahitaji dini na imani pia. Hata hivyo, kama imani haikuungwa mkono na elimu haitakuwa na manufaa; itakuwa ni mzigo tu. Mtukufu Mtume  amesema: “Watu wa aina mbili wamevunja mgongo wangu: watu wenye elimu lakini hawana ucha-Mungu na watu wa dini ambao hawana elimu.”11 Uislamu wala hauhitaji mwanazuoni asiye mchamungu au mchamungu asiye na elimu. Pia ni hoja ya uongo kusema: “Kama mwizi akija na mwanga usiku anachagua vitu vizuri zaidi” kama mfano wa wale watu ambao wana elimu lakini hawana imani na kuhitimisha kwamba elimu ni kitu cha hatari zaidi kuliko ujinga. Kwa sababu mwizi anayekuja na mwanga na kuiba vitu vilivyochagua vizuri huwa anakuja usiku sio mchana. Na angeweza kuja usiku wakati mwenye nyumba amelala. Lakini, hangeweza kuiba wakati wa mchana au wakati wenye nyumba wapo macho. Mtu mwenye elimu lakini wasio na imani, hutumia ujinga na usingizi wa watu wengine katika kuiba. Kwa hiyo, ujinga wa watu wengi ni wenye ushawishi katika mkasa kama huu. Liangazie taifa lako kwa nuru ya elimu, iangazie kila nyumba iwe kama mchana, mwamshe kila mtu, mulika kila mahali na imarisha nguzo za imani na halafu yule mwizi hataweza kuiba. Sababu ambazo zimewezesha kufanyika   Bihar al-Anwar, `Allamah Majlisi, Juz. 2, uk. 111

11

32

13_16_Wajibu kutafuta Elimu (4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016.indd 32

6/18/2016 1:38:46 PM


WAJIBU WA KUTAFUTA ELIMU

wizi zimekuwa ni elimu ya mwizi huyo, kutokuwa na imani, na ujinga wa watu wa kawaida. Kwa hiyo, hapa ujinga pia unahusika. Hata hivyo, kama tunataka kuwa na dini halisi, tuepuke umasikini, kuyashinda maradhi, kusimamisha haki miongoni mwetu, kuleta demokrasia na uhuru na jamii yetu kuhamasika kuelekea kwenye kujishughulisha na mambo ya kijamii, kutakuwepo na njia moja nayo ni kutafuta na kupata elimu ambayo lazima iwe jumuishi na kuwa jitihada tukufu kupitia dini. Kama sisi hatutaanza jitihada hii tukufu, dunia itakuwa, na itanufaika kutokana na matokeo yake. Watu wengine watakuja kuelimisha taifa letu na Mungu anajua ni uharibifu wa kiasi gani kwa Uislamu utakaosababishwa na uzembe wetu Waislamu. Wanadamu dhidi ya ujinga: Kitabu kiitwacho “Men Against Ignorance - Wanadamu dhidi ya Ujinga�12 kimeripoti shughuli za UNESCO za kuwaelimisha watu katika nchi zinazoendelea. Pamoja na kwamba ni vizuri kuona kwamba kuna njia ambazo zinatolewa kwa ajili ya kuendeleza elimu miongoni mwa Waislamu kwa lengo la kufuta ujinga polepole 12

itabu kilichoandikwa na Ritchie Calder, Paris; UNESCO (Soleure, K kilichapishwa na Gassmann) 1953. 33

13_16_Wajibu kutafuta Elimu (4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016.indd 33

6/18/2016 1:38:46 PM


WAJIBU WA KUTAFUTA ELIMU

katika jumuiya zao, ni jambo la kujutia kwamba sisi Waislamu tunazembea katika kutekeleza wajibu wetu na kwamba watu wengine wanakuja kutoka nchi za nje, mbali, na kufanya juhudi kubwa katika kutimiza wajibu wetu na sio tu katika kuendeleza mafundisho ya kawaida, bali na kuanzisha mambo ya ziada ya taasisi za ushirika na afya na kuwasaidia watu katika kutibu maradhi yao, hujaza udongo kwenye vinamasi kwa lengo la kufutilia mbali mazalia ya mbu na kufutilia mbali malaria, na kurekebisha majiji yao na vijiji. Watakwenda sehemu za mbali ambazo hakuna mmoja wetu ambaye amewahi kufika huko kamwe katika nchi kama Pakistan na Afghanistan na kutoa huduma za ziada huko. Takwimu zilizopo katika kitabu hicho zinaonesha kwamba 96% ya baadhi ya nchi za Kiislamu zimekuwa na watu wasiojua kusoma hadi miaka michache iliyopita. Hali imeboreshwa na asilimia ya ujinga imepungua. Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, wawakilishi wa UNESCO walioko katika nchi za Asia walifanya kongamano huko Karachi na kupanga mpango wa elimu wa miaka 20 katika nchi za Asia. Mpango huu ambao uliundwa kuhakikisha usahihi ulioegemezwa kwenye takwimu zilizo thabiti na kufikiria fursa zote na nyenzo zinazowezekana. Wameamsha furaha na shauku miongoni mwa watu.

34

13_16_Wajibu kutafuta Elimu (4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016.indd 34

6/18/2016 1:38:46 PM


WAJIBU WA KUTAFUTA ELIMU

Makusudio yao katika kufanya hivi hayana maana. Huenda labda namna ya lengo la ukoloni lipo nyuma ya pazia. Ole wetu! Kama nguvu ya kikoloni imeingia kupitia shughuli hizi, basi tumekwisha! Ingawa hatujui madhumuni yao ya kweli, inatulazimu tusifunike makosa yetu kwa kifuniko cheusi kwa kuonesha hali ya kutokuwa na matarajio mema. Sisi Waislamu tuna tabia mbaya ya kutafsiri shughuli na makusudio ya watu wengine kuwa ni uovu ili tufiche makosa yetu. Iliandikwa katika kitabu hichohicho kilichochapishwa na UNESCO kwamba katika nchi mojawapo ya Kiafrika, mzalendo mmoja mwenye msimamo mkali aliwashutumu wakoloni na kusema kwamba ninyi Wazungu mmetambua kwamba nguvu yenu ya kikoloni imedhoofika na nguvu yenu ya kisiasa imepungua kwa hiyo sasa mnaficha nyuso zenu chini ya kivuli cha hisani na kuhudumia jamii. Malengo yao vyovyote yatakavyokuwa, hayana manufaa kwetu. Kinachotuathiri sisi ni kwamba tunaelewa kwamba kama Wazungu wakifaulu kuelimisha nchi za Kiislamu katika kipindi cha miaka 20 na kuwafanya watu wa nchi hizo kuelimika na kuwaondoa katika hali ya ujinga, umasikini, na maradhi, hivi kizazi kijacho kitahisi nini kwa mintarafu ya Uislamu na kuwa Mwislamu? Hivi hawatatuambia kwamba sisi tumekuwa Waislamu na tulifuata dini ya Muhammad 35

13_16_Wajibu kutafuta Elimu (4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016.indd 35

6/18/2016 1:38:47 PM


WAJIBU WA KUTAFUTA ELIMU

kwa karne 14 na tulikuwa tunaishi katika ujinga na uduni hadi hapo watu wengine waliponyoosha mikono yao kutoka upande mwingine wa dunia na kutunusuru? Patakuwepo na heshima gani itakayokuwa imebaki kwa ajili ya Uislamu? Hivi tutatoa jibu gani kwa Mtukufu Mtume  kama akiuliza: “Hivi nyinyi mlitii amri yangu ambayo ilisema ‘Kutafuta elimu ni wajibu wa Waislamu wote?’”13 Hii ni kanuni ya kimaumbile na kiroho kwamba: “binadamu ana deni na anapaswa kushukuru kwa fadhila.” Mtukufu Mtume  pia alisema kwamba: “Kama mtu akihuisha na kurutubisha ardhi isiyotumika basi itakuwa ya kwake.” Pamoja na kwamba huu ni uamuzi wa kisheria kuhusu ardhi, ni kweli kuhusu mambo ya maumbile. Yeyote aliyekuja na kuhuisha ummah na akaunusuru kutoka kwenye matatizo, umasikini, na ujinga, alizikonga nyoyo zao, roho zao na imani yao. Hivyo, kuhusu hali ilivyo sasa, tunaweza kutabiri bila shaka kwamba sisi sio wamiliki wa vizazi vijavyo. Mtu anaweza kusema kwamba Muislamu hawezi kubadili dini na kuingia kwenye dini nyingine, hususani kama watu wameelimika kamwe hawawezi kuondoka kwenye dini ya Mungu Mmoja (ya tawhiid) na kuingia dini nyingine. Ninasema kwamba inawezekana ikawa hivyo, lakini nukta ya uhakika ni kwamba hata kama hawatabadili imani, watu   Usul al-Kafi, Sheikh Muhammad Kulayni

13

36

13_16_Wajibu kutafuta Elimu (4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016.indd 36

6/18/2016 1:38:47 PM


WAJIBU WA KUTAFUTA ELIMU

hao watapoteza raghba yao katika Uisalmu na huenda wakommunisti wakanufaika kutokana na hali hiyo. Hivyo, lazima tuepukane na hatari hii. Lakini kwa jinsi gani? Je, inawezekana kupitia njia ya majibu hasi, kama ilivyo siku zote na kuanzisha ghasia na kupiga kelele kwamba UNESCO hawana haki ya kuwafundisha Waislamu, kujitahidi, na kutumia fedha kwa ajili ya lengo hili? Hili litakuwa na uhusiano gani na wao? Hivi unadhani kwamba msimamo wa namna hii unafaa? Tungeweza kukubali hili leo hii? Hivi mataifa ya Waislamu yanakubaliana na hili kutoka kwetu? Au ufumbuzi ni kwamba tufanye jitihada na tuanze juhudi (jihadi katika njia ya Allah) na kutimiza wajibu huu sisi wenyewe? Ilitolewa taarifa katika kitabu hichohicho kwamba nchini Indonesia, ambayo ni nchi ya Kiislamu yenye watu wengi zaidi, elimu ya jumla imekuwa ni jihadi tukufu na watu wanafuatilia elimu hiyo kama wanavyofuatilia wajibu mwingine wa kidini. Nchini Indonesia, yeyote anayejua kitu kuhusu kazi na anayo kazi hufikiria kuwa huo ni wajibu wake kwenda mashuleni na kufundisha, kwa sababu idadi ya walimu walioajiriwa na serikali haitoshi kwa shule zote. Hii ni amri ya Uislamu ambayo inafanya ni wajibu wa kila mtu kutafuta elimu. Muundo wa sasa wa amri hiyo ndio ulivyo nchini Indonesia, unatiiwa nchini humo.

37

13_16_Wajibu kutafuta Elimu (4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016.indd 37

6/18/2016 1:38:47 PM


WAJIBU WA KUTAFUTA ELIMU

Kushindana katika kutoa huduma na katika kuwa mwema: Katika surah ya 5 aya ya 48, baada ya kurejelea Qur`ani Tukufu na maandiko matakatifu ya zamani na dini za kimungu, imeandikwa kwamba:

ً‫لِ ُكلٍّ َج َع ْلنَا ِم ْن ُك ْم ِشرْ َعةً َو ِم ْنهَاجًا ۚ َولَوْ َشا َء للاهَّ ُ لَ َج َعلَ ُك ْم أُ َّمة‬ ۚ‫ت‬ ِ ‫اح َدةً َو ٰلَ ِك ْن لِيَ ْبلُ َو ُك ْم فِي َما آتَا ُك ْم ۖ فَا ْستَبِقُوا ْال َخ ْي َرا‬ ِ ‫َو‬ “…..Na kila (umma) katika nyinyi, tumeujalia sharia yake na njia yake. Na kama Mwenyezi Mungu angelitaka, angewafanya umma mmoja, lakini ni kuwajaribu katika hayo aliyowapa. Basi shindaneni katika mambo ya kheri…..” (5:48).

Inaonekana kama vile aya hii inachukulia kuwa ni hekima kwamba mataifa yatofautiane yenyewe kwa yenyewe na huenda ina maana kwamba mataifa mbalimbali yashindane yenyewe kwa yenyewe kufanya vizuri zaidi katika vitendo vya kisayansi, na yanajaribiwa kwa njia hii ili kwamba taifa linalofanya vizuri zaidi linapata ushindi. Na aya hii inaagiza Waislamu kufanya jitihada kuchukua hatua kubwa zaidi na kushinda shindano hilo kwa faida yake. Kwa hiyo, njia ya kuepuka hatari iliyotajwa hapo juu sio kuiepuka UNESCO. Njia ya kuepuka hatari 38

13_16_Wajibu kutafuta Elimu (4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016.indd 38

6/18/2016 1:38:47 PM


WAJIBU WA KUTAFUTA ELIMU

hiyo ni kwamba sisi wenyewe tunaanza kazi hiyo na kuwa washindi. Na ninarudia kwamba hakuna kitakachofanyika hadi hapo ambapo kazi hiyo itakapochukuliwa kama jihadi katika njia ya Allah na wanazuoni wa kidini waiasisi kazi hiyo na kuiona ni ya kipaumbele kuliko masuala mengine yote. Ningeweza kuyaweka mazungumzo haya yote kwa yale yasemwayo na Uislamu kuhusu ubora wa elimu na kufanya kiasi cha propaganda kuhusu Uislamu, lakini kama nilivyosema mwanzoni, siamini katika propaganda kama hizo na ninaamini hazifanyi kazi. Ningependa zaidi badala yake kuzungumza kuhusu hali yetu ilivyo sasa na kazi yetu maalum. Mtu anaweza kusema kwa fahari kabisa kwamba Uislamu unasema: “Kutafuta elimu ni wajibu wa Waislamu wote”14 pale tu tutakapofanya jitihada kubwa na kushiriki katika jihadi hii tukufu na kupata kuendelea. Dakika chache baada ya kumaliza hotuba hii msikilizaji mwenye kuheshimika ambaye sikuwa namjua, alinipa kipande cha karatasi ambamo aliandika ukosoaji juu ya hotuba hii: “Ni kawaida mno kuzungumzia kuhusu elimu kufuatana na msimamo wa Uislamu. Wajibu wa jihadi tuku  Usul al-Kafi, Sheikh Muhammad Kulayni

14

39

13_16_Wajibu kutafuta Elimu (4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016.indd 39

6/18/2016 1:38:47 PM


WAJIBU WA KUTAFUTA ELIMU

fu ambayo lazima ianzie kwenye shule za msingi ilianzishwa, lakini njia yake nyepesi sana ya kuitekelezea haikutajwa. Mazungumzo kama haya yanaweza kuishia kwenye matokeo ya kukata tamaa kwetu kwamba kwa nini hakuna kinachoweza kufanyika. Tunaamini kwamba lazima tufikiri kuhusu hilo lakini hiyo ni taarifa tu na tabia yetu ya kujuta na kuacha mambo yaende hivyohivyo. Kwamba ilitajwa katika hotuba kwamba jihadi iliyoanzishwa na watu wengi (UNESCO) ni kitu cha kawaida. Kingeweza kutokea, tutake au tusitake, kwa ulinganiaji au bila ya ulinganiaji. Jambo la uhakika ni kwamba hata kama mitume wasingekuja, labda binadamu wangeelewa kile walichosema na huenda wangekuwa waumini, lakini dini ilikuja kuongeza kasi ya maendeleo ya mageuko yake. Wajibu wetu ni kueneza kuanzia kwenye hali yake ya kulegalega. Hivyo, taasisi na namna inayofaa ya kivitendo juu ya njia mahususi inahitajika inayofanana na shughuli za Sayyid Jamal al-Ddin Asad Abadi.�

Kwa kushukuru ukosoaji huu na kukiri umuhimu wa kile alichokisema, lazima niongezee na kutaja kwamba nukta muhimu sana katika masuala ya kidini ni kuwaelimisha watu wa kawaida kuhusu wajibu wao wa kidini; kama wakitambua na kushawishika kuhusu wajibu huo watautekeleza kama wajibu mwingine wowote ule.

40

13_16_Wajibu kutafuta Elimu (4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016.indd 40

6/18/2016 1:38:47 PM


WAJIBU WA KUTAFUTA ELIMU

Kuhusu wajibu mwingine wa kidini ambao watu wamekuja kwenye uelewa na imani kama hiyo, tunaona jinsi wanavyopambana kutekeleza kwa uaminifu wajibu huo. Takriban miaka 50 iliyopita, kwa sababu ya kukosa nyenzo na usalama, kutekeleza Hijja ilikuwa ni jihadi halisi. Mahujjaji walikuwa hawana uhakika kama wangeweza kurudi salama au hapana. Tuliona watu wengi hata miongoni mwa wakulima ambao walikuwa wanafunga saumu katika hali ya joto kali la msimu wa kiangazi na walikuwa wakienda kuvuna katika kipindi hicho hicho. Licha ya ufuatiliaji wa historia ya Uislamu wa siku za mwanzoni, hatukukuta kwamba watu wa kawaida wanapambana kwa bidii kwa ajili ya kupata elimu. Kama palikuwepo na jitihada yoyote baadaye iliendeshwa na wale ambao tayari walikwishapata kiasi fulani cha elimu na wakaanza kukifurahikia. Sasa fikiria ni vuguvugu kubwa kiasi gani lingetokea kama watu wangechukulia shughuli hii kuwa ni kama wajibu wa kidini, na hii sentensi: “Kupata elimu ni wajibu wa kila Mwislamu”15 badala ya kuipamba tu katika mbao za matangazo za mashuleni, ikafuatwa kama wajibu wa kidini wa maana kubwa na kuuchukulia kuwa ni sawa kama wajibu mwingine.   Usul al-Kafi, Sheikh Muhammad Kulayni

15

41

13_16_Wajibu kutafuta Elimu (4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016.indd 41

6/18/2016 1:38:47 PM


WAJIBU WA KUTAFUTA ELIMU

Orodha Ya Vitabu Vilivyo ­Chapishwa Na Al-Itrah Foundation 1.

i) Qur’ani Tukufu – Pamoja na Tarjuma ya Kiswahili ii) Qur’an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Thelathini 2. Uharamisho wa Riba 3. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza 4. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili 5. Hekaya za Bahlul 6. Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) 7. Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (a.s.) 8. Hijab vazi Bora 9. Ukweli wa Shia Ithnaashari 10. Madhambi Makuu 11. Mbingu imenikirimu 12. Abdallah Ibn Saba 13. Khadijatul Kubra 14. Utumwa 15. Umakini katika Swala 16. Misingi ya Maarifa 17. Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia 18. Bilal wa Afrika 19. Abudhar 20. Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu 42

13_16_Wajibu kutafuta Elimu (4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016.indd 42

6/18/2016 1:38:47 PM


WAJIBU WA KUTAFUTA ELIMU

21. Salman Farsi 22. Ammar Yasir 23. Qur’an na Hadithi 24. Elimu ya Nafsi 25. Yajue Madhehebu ya Shia 26. Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur’an Tukufu 27. Al-Wahda 28. Ponyo kutoka katika Qur’an 29. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii 30. Mashukio ya Akhera 31. Al Amali 32. Dua kwa Mujibu wa Ahlulbayt (a.s) 33. Udhuu kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna 34. Haki za wanawake katika Uislamu 35. Mwenyezi Mungu na sifa zake 36. Kumswalia Mtume (s) 37. Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) 38. Adhana 39. Upendo katika Ukristo na Uislamu 40. Qur’ani na Kuhifadhiwa Kwake 41. Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu 42. Kupaka juu ya khofu 43. Kukusanya Sala Mbili 44. Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara 43

13_16_Wajibu kutafuta Elimu (4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016.indd 43

6/18/2016 1:38:47 PM


WAJIBU WA KUTAFUTA ELIMU

45. Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya 46. Kusujudu juu ya udongo 47. Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s) 48. Tarawehe 49. Malumbano baina ya Sunni na Shia 50. Kupunguza Swala safarini 51. Kufungua safarini 52. Umaasumu wa Manabii 53. Qur’an Yatoa Changamoto 54. as-Salaatu Khayrun Mina -’n Nawm 55. Uadilifu wa Masahaba 56. Dua e Kumayl 57. Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu 58. Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake 59. Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata 60. Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mtume Muhammad (s) 61. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza 62. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili 63. Kuzuru Makaburi 64. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza 65. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili 66. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu 67. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne 68. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano 69. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita 44

13_16_Wajibu kutafuta Elimu (4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016.indd 44

6/18/2016 1:38:47 PM


WAJIBU WA KUTAFUTA ELIMU

70. Tujifunze Misingi Ya Dini 71. Sala ni Nguzo ya Dini 72. Mikesha Ya Peshawar 73. Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu 74. Ubora wa Imam ‘Ali na Ushia ndio njia iliyonyooka 75. Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake 76. Liqaa-u-llaah 77. Muhammad (s) Mtume wa Allah 78. Amani na Jihadi Katika Uislamu 79. Uislamu Ulienea Vipi? 80. Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) 81. Dhana ya Ndoa ya Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) 82. Urejeo (al-Raj’ah) 83. Mazingira 84. Utokezo (al - Badau) 85. Hukumu ya kujenga juu ya makaburi 86. Swala ya maiti na kumlilia maiti 87. Uislamu na Uwingi wa Dini 88. Mtoto mwema 89. Adabu za Sokoni Na Njiani 90. Johari za hekima kwa vijana 91. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza 92. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili 93. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu 94. Tawasali (AT- TAWASSUL) 45

13_16_Wajibu kutafuta Elimu (4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016.indd 45

6/18/2016 1:38:47 PM


WAJIBU WA KUTAFUTA ELIMU

95. 96. 97. 98. 99. 100. 101. 102. 103. 104. 105. 106. 107. 108. 109. 110. 111. 112. 113. 114. 115. 116. 117. 118. 119.

Imam Mahdi katika Usunni na Ushia Hukumu za Mgonjwa Sadaka yenye kuendelea Msahafu wa Imam Ali Maimamu wa Ahlul Bait – Ujumbe na Jihadi Idi Al-Ghadir Kusoma sura zenye Sijda ya wajibu Hukumu zinazomuhusu mkuu wa kazi na Mfanyakazi Huduma ya Afya katika Uislamu Sunna za Nabii Muhammad (saww) Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza) Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili) Shahiid Mfiadini Mwanamke Na Sharia Ujumbe -Sehemu ya Kwanza Ujumbe - Sehemu ya Pili Ujumbe - Sehemu ya Tatu Ujumbe - Sehemu ya Nne Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu Hadithi ya Thaqalain Ndoa ya Mutaa Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza Ukweli uliopotea sehemu ya Pili Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu Ukweli uliopotea sehemu ya Nne

46

13_16_Wajibu kutafuta Elimu (4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016.indd 46

6/18/2016 1:38:47 PM


WAJIBU WA KUTAFUTA ELIMU

120. Ukweli uliopotea sehemu ya Tano 121. Mkutano wa Maulamaa wa Baghdad 122. Safari ya kuifuata Nuru 123. Fatima al-Zahra 124. Myahudi wa Kimataifa 125. Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi 126. Visa vya kweli sehemu ya Kwanza 127. Visa vya kweli sehemu ya Pili 128. Elimu ya Ghaibu ya Maimamu 129. Mwanadamu na Mustakabali wake 130. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Kwanza) 131. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Pili) 132. Khairul l’Bariyyah 133. Uislamu na mafunzo ya kimalezi 134. Vijana ni Hazina ya Uislamu 135. Adhana ni Ndoto au ni Wahyi? 136. Tabaruku 137. Saada Kamili – Kitabu cha Kiada cha Maadili 138. Vikao vya furaha 139. Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje? 140. Visa vya wachamungu 141. Falsafa ya Dini 142. Kuhuzunika na Kuomboleza 143. Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah 47

13_16_Wajibu kutafuta Elimu (4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016.indd 47

6/18/2016 1:38:47 PM


WAJIBU WA KUTAFUTA ELIMU

144. Mjadala wa Kiitikadi 145. Kuonekana kwa Allah 146. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza) 147. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili) 148. Ndugu na Jirani 149. Ushia ndani ya Usunni 150. Maswali na Majibu 151. Mafunzo ya hukmu za ibada 152. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 1 153. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 2 154. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 3 155. Abu Huraira 156. Vipengee kadhaa katika Swala ya Jamaa na Msikiti. 157. Mazingatio kutoka katika Qur’an - Sehemu ya Kwanza 158. Mazingatio kutoka kaitka Qur’an - Sehemu ya Pili 159. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya kwanza 160. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya Pili 161. Shia na Qur’ani – Majibu na Maelezo 162. Falsafa ya Mageuzi ya Imam Husein (a.s) 163. Amali za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani 164. Elimu ya Tiba za Kiislamu - Matibabu ya Maimamu 165. Uislamu Safi 166. Majlisi za Imam Husein Majumbani 167. Je, Kufunga Mikono 168. Uislam wa Shia 48

13_16_Wajibu kutafuta Elimu (4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016.indd 48

6/18/2016 1:38:47 PM


WAJIBU WA KUTAFUTA ELIMU

169. Amali za Makka 170. Amali za Madina 171. Asili ya Madhehebu katika Uislamu 172. Sira ya Imam Ali kuhusu Waasi 173. Ukweli uliofichika katika neno la Allah 174. Uislamu na Mifumo ya Uchumi 175. Umoja wa Kiislamu na Furaha 176. Mas’ala ya Kifiqhi 177. Jifunze kusoma Qur’ani 178. as-Sahifatul Kamilah as-Sajjadiyyah 179. Hayya ‘Alaa Khayri’l-’Amal Katika Adhana 180. Ukweli kuhusu Funga ya Siku ya Ashura 181. Dua za Miezi Mitatu Mitukufu (Rajabu, Shaabani na Ramadhani) 182. Uadilifu katika Uislamu 183. Mahdi katika Sunna 184. Maswali Ya Uchunguzi Kuhusu Uislam 185. Kazi na Bidii ni njia ya maendeleo 186. Abu Talib – Jabali Imara la Imani 187. Ujenzi na Utakaso wa Nafsi 188. Vijana na Matarajio ya Baadaye 189. Historia maana na lengo la Usalafi 190. Ushia – Hoja na Majibu 191. Mateso ya Dhuria wa Mtume (saww) 192. Maombolezo – Msiba wa Bwana wa Mashahidi (a.s.) 193. Shahidi kwa Ajili ya Ubinadamu 49

13_16_Wajibu kutafuta Elimu (4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016.indd 49

6/18/2016 1:38:47 PM


WAJIBU WA KUTAFUTA ELIMU

194. Takwa 195. Upotoshaji Dhahiri katika (Turathi) Hazina ya Kiislamu 196. Amirul Muuminina (as) na Makhalifa 197. Tawheed Na Shirki 198. Kuvunja hoja iliyotumika kutetea Uimamu wa AbuBakr 199. Adabu za vikao na mazungumzo 200. Hija ya Kuaga 201. Uwazi baina ya Maslahi na Vikwazo 202. Fadhila za watukufu watano katika Sahih Sita 203. Mdahalo baina ya Mwanachuoni waKisunni na Kishia (Al- Muraja’aat) 204. Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (as) 205. Imam Husain ni Mfumo wa Marekebisho na Mageuzi 206. Mtazamo kuhusu msuguano wa Kimadhehebu 207. Nchi na Uraia – Haki na wajibu kwa Taifa 208. Mtazamo wa Ibn Taymiyyah juu ya Imam Ali (as) 209. Uongozi wa Kidini – Maelekezo na Utekelezaji wa Kijamii 210. Maadili ya Ashura 211. Mshumaa – Shahidi na Kifo cha Kishahidi 212. Mizani ya Hekima – Hadithi za Ahlul Bait (as) – Sehemu ya Kwanza 213. Imam Ali na Mambo ya Umma 214. Imam Ali na Mfumo wa Usawa 215. Uimamu na Tamko la Kutawazwa 216. Mfumo wa Wilaya 217. Vipi Tutaishinda Hofu? 50

13_16_Wajibu kutafuta Elimu (4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016.indd 50

6/18/2016 1:38:47 PM


WAJIBU WA KUTAFUTA ELIMU

218. Kumswalia Mtume ni Ufunguo wa Utatuzi wa Matatizo 219. Maeneo ya Umma na Mali Zake 220. Nahju ‘L-Balagha– Majmua ya Khutba, Amri, Barua, ­Risala, Mawaidha na Semi za Amirul-Muuminin Ali bin Abu Talib (a.s.) 221. Mukhtar – Shujaa aliyelipiza kisasi dhidi ya wauaji wa Imam Husein (as) hapo Karbala 222. Mazingatio Katika Swala 223. Imam Hasan na Mfumo wa Kujenga Jamii 224. Vyakula Na Vinywaji 225. Kuelewa Rehema ya Mwenyezi Mungu 226. Imam Mahdi na Bishara ya Matumaini 227. Mtazamo Mpya - Wanawake katika Uislamu 228. Shia Na Sahaba - Majibu na Maelezo 229. Majanga Na Jukumu la Jamii 230. Shia Na Hadith - Majibu na Maelezo 231. Upotofu Ndani ya Kitabu cha Mitaala kwa Shule za Sekondari 232. Ugaidi Wa Kifikra Katika Medani Ya Kidini 233. Yafaayo kijamii 234. Uswalihina Dhahiri Na Batini Yake 235. Mkakati wa Kupambana na Ufakiri 236. Mwanamke Katika Harakati Za Mageuzi 237. Jihadi 238. Hija Katika Maneno Na Ujumbe Wa Imam Khomeini (R.A) 239. Tiba Ya Maradhi Ya Kimaadili 51

13_16_Wajibu kutafuta Elimu (4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016.indd 51

6/18/2016 1:38:47 PM


WAJIBU WA KUTAFUTA ELIMU

240. Yusuf Mkweli 241. Taqiyya Kwa Mujibu Wa Sheria Ya KIISLAMU 242. Imam Mahdi (A.S) Imam Wa Zama Hizi Na Kiongozi Wa Dunia 243. Talaka Tatu 244. Safari Ya Kuelekea Kwa Mwenyezi Mungu 245. Hotuba Za Kiislamu Juu Ya Haki Za Binadamu 246. Mashairi Ya Kijamii 247. Ngano Ya Kwamba Qur’ani Imebadilishwa 248. Wito Kwa Waumini: “Enyi Mlioamini” 249. Imam Husain (a.s) ni Utu na Kadhia 250. Imam Husain ni Kielelezo cha Kujitoa Muhanga na Fidia 251. Imam Mahdi ni Tumaini la Mataifa 252. Kuchagua Mchumba 253. Mazungumzo ya Umoja – Ukosoaji na Usahihishaji 254. Utamaduni wa Mwamko wa Kijamii 255. Hekima za kina za Swala 256. Kanuni za Sharia za Kiislamu 257. Utamaduni kufuatana na Qur’ani na Utekelezaji wa Kivitendo (Sehemu ya Kwanza) 258. Kauli sahihi zaidi katika kufafanua Hadithi

52

13_16_Wajibu kutafuta Elimu (4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016.indd 52

6/18/2016 1:38:47 PM


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.