NENO
INTERNATIONAL CHRISTIAN EMBASSY JERUSALEMU//JANUARI/FEBRUARI 2019//TOLEO LA KISWAHILI
KUTOKA YERUSALEMU
MWANZO
.3
MUNGU WA WAKATI
K NA J – U A Y E MP A IC A Y AK PYA W M MA I AZ K A
1
NENO KUTOKA YERUSALEMU
M
KUTOKA
MEZA YA RAIS Ndugu marafiki,
Mwaka huu mpya, kwa njia nyingi, ni mwaka wa mwanzo mpya. Kwa ICEJ hapa Yerusalemu, 2019 ulianza kwa shukurani kwa zaidi ya miaka 20 tuliyojaliwa kuwa wapangaji wa jengo letu zuri linalomilikiwa na Jamhuri ya Ivory Coast. Kwa huzuni, msimu huu mkataba umefika mwisho.
Taasisi ya International Christian Embassy Jerusalem (ICEJ) ilianzishwa mwaka 1980 kwa kutambua umuhimu wa kibiblia kwa Yesalemu yote na muunganiko wake maalumu na Wayahudi. Leo hii ICEJ inawakilisha mamilioni ya Wakristo, makanisa na madhehebu kwa Israeli na watu wake. Tunatambua kutokana na urejesho wa Israeli uaminifu wa Mungu kutunza agano lake la kale kwa Wayahudi. Malengo yetu makuu ni: * Kusimama pamoja na Israeli kwa kuiunga mkono na kiurafiki; * Kuimarisha na kufundisha makanisa ya ulimwengu mzima kuhusiana na mpango wa Mungu kwa Israeli na mataifa ya Mashariki ya Kati; * Kuwa sauti hai ya upatanisho kati ya Wayahudi, Wakristo na Waarabu na kusaidia makanisa na makusanyiko yaliyoko katika Nchi Takatifu ya Israeli. Kutoka kwenye ofisi zake za makao makuu Yerusalemu, ICEJ inatoa huduma katika nchi zaidi ya 170 ikiwa na ofisi za matawi katika mataifa zaidi ya 90. Maono yetu ni: * Kufikia kila kipande cha jamii ya Israeli kwa ushuhuda wa Kikristo wa faraja na upendo, na * Kukusanya na kuwakilisha Israeli sadaka ya kuwabariki Wayahudi kutoka kwenye madhehebu, makanisa na kwa waumini wa kila taifa duniani. Christian Embassy ni huduma ambayo haifungamani na madhahebu inayoendeshwa kwa michango ya hiari ya wanachama wetu na marafiki zetu kutoka duniani kote. Tunakualika uungane nasi tunapoihudumia Israeli na Wayahudi ulimwenguni kwa kuchangia kazi inayoendelea na ushahidi wa ICEJ.
NENO KUTOKA JERUSALEMU
SHUKURANI Rais wa ICEJ: Dr Jürgen Bühler Makamu wa Rais Kimataifa: Mojmir Kallus Makamu wa Rais Fedha: David Van der Walt Makamu wa Rais Operesheni: Barry R. Denison Makamu wa Rais Msemaji Kimataifa: David Parsons Mhariri/Mkurugenzi Uchapishaji: Julaine Stark Mwandishi/Mhariri: Kayla Muchnik Msaidizi wa Uhariri: Lynzi Lapka Waandishi Waandamizi: Aaron Hecht, Lily Sironi Msanifu: Peter Ecenroad Utawala: Tobias H Picha: Watumishi wa ICEJ na kwenye Matawi WATAFSIRI: ICEJ Tanzania Mkurugenzi: Stanton Newton, Uandishi/Uhariri: Ebely Rugema, Olivia Ludovick, Tarimo Seraphim Msanifu: Daudi Mwaibula Biblia ya New King James (NKJ) imetumika kunukuu maandiko yote isipokuwa ilipoelezwa vinginevyo. Jarida la Neno Kutoka Yerusalemu linachapishwa na taasisi ya International Christian Embassy Jerusalem. Hairuhusiwi kulichapisha au kulinakili lote au kwa sehemu bila kibali cha maandishi kutoka kwa wachapishaji. Jarida hili haliuzwi na linachapishwa kwa michango ya hiari kutoka duniani kote. Michango yote inayotolewa kwenye huduma hii inakatwa kodi (katika nchi ambako inatendeka hivyo). Kwa habari zaidi, tutembelee kupitia www.icej.org INTERNATIONAL CHRISTIAN EMBASSY JERUSALEM P.O. Box 1192, Jerusalem • 9101002, ISRAEL Changia huduma yetu kwa njia ya mtandao kupitia www.icej.org
Tunawaomba muombe pamoja nasi tunapotafuta nyumba mpya inayofaa: ambayo itatuwezesha kukamilisha wito wetu wa kulifariji taifa la Israeli kulingana na Isaya 40:1, pamoja na kupanua na kuendeleza huduma kulingana na kile Bwana alichotuitia kufanya. Tafadhali pia omba kwa ajili ya upatikanaji wa fedha zinazohitajika kufanikisha mpango huu. Kumbukumbu Makini
Mauaji ya hivi karibuni ya kijana mmishenari wa Kikristo, John Chau huko visiwa vya Sentinal yanatukumbusha kwamba bado kungali na mataifa na makabila ambao hawajawahi kusikia habari njema za Yesu Kristo. Tukio hilo lilimleta Jim Elliot akilini, yule mmishenari aliyeuawa mwaka 1956 na watu wa kabila la Huaorani huko Ecuador akiwa na marafiki zake watano, walipojaribu kuwafikishia habari njema za Yesu Kristo. Ni mke wa Jim Elliot ambaye baadaye alipata mlango uliofunguliwa akawashirikisha neema iokoayo ya Yesu Kristo Wahuaorani, wakiwamo baadhi ya watu wale wale wa kabila hilo waliomuua mumewe. Yesu aliwatangazia wanafunzi wake: “Na Injili hii ya ufalme itahubiriwa ulimwenguni kote kwa ajili ya ushuhuda kwa mataifa yote, na kisha ule mwisho utakuja (Mathayo 24:14). Kama nyongeza ya urejesho wa Israeli, kuenea kwa Injili ya ufalme “kwa mataifa yote” ni moja ya ishara kuu za kurudi kwa Yesu. Urejesho wa Israeli na kutangazwa kwa Injili ni farasi wawili wanaovuta gari (mkokoteni) moja, kama alivyopenda kusema Juha Ketola aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Kimataifa wa ICEJ. Tunaishi katika nyakati za ajabu: Mungu ana kusudi la ajabu kwa kila mmoja wetu. Iwe umeitwa kuitumikia Israeli, mataifa, au vyote viwili, ninakupa changamoto ya kujitoa kikamilifu kwa Mwenye enzi kuu. Jim Elliot aliwahi kusema, “Si mpumbavu yeye atoaye asichoweza kukitunza, kupata kile asichoweza kukipoteza.” Nahimiza tena, tafadhali ombea ICEJ kuhusiana na mpango wetu wa makazi mapya na zingatia kuunga mkono kwa kuchangia miradi mbalimbali iliyotangazwa kwenye toleo hili la Neno Kutoka Yerusalemu. Asanteni sana kwa kusimama pamoja nasi,
Dr Jürgen Bühler Rais wa ICEJ
NENO
INTERNATIONAL CHRISTIAN EMBASSY JERUSALEMU//JANUARI/FEBRUARI 2019//TOLEO LA KISWAHILI
KUTOKA JERUSALEMU
PICHA YA MBELE:
Jua likichomoza juu ya Ulaya na Mashariki ya Kati
KUPATA MAJARIDA YALIYOPITA
Tembelea www.icej.org/media/word-jerusalem MWANZO
.3
MUNGU WA WAKATI
A UK AN J– PY ICE A M YA AK YA MW MAP ZI
KA
MA
Mwaka Mpya na Makazi Mapya WITO WA MAOMBI
Kadri mwaka 2018 ulivyokuwa ukielekea ukingoni, ICEJ ilianza kuwaza juu ya matarajio ya mwaka 2019, tulipata changamoto ya dharula ya kutafuta nyumba mpya kwa ajili ya ofisi za makao makuu jijini Yerusalemu! Uongozi wa ICEJ hivi sasa uko kwenye mchakato wa kutafuta nyumba mpya na tunahitaji maombi yenu!
Tangu mwaka 1996, ICEJ ilipata heshima ya kuwa wapangaji katika moja ya majengo mazuri sana jijini Yerusalemu. Kwa miaka 20 iliyopita mpangishaji wetu alikuwa Jamhuri ya Ivory Coast na tulifurahia mahusiano mazuri sana nao kwa miaka yote hiyo. Kwa bahati mbaya, mkataba wetu wa muda mrefu katika nyumba hiyo umefika mwisho na serikali ya Abidjani, kulingana na masuala ya kisheria nchini Israeli, haitaweza kutuongezea mkataba kwa kipindi kingine.
Kwa hiyo, sasa tunatafuta makao mapya ya ICEJ, nyumba ambayo itaturuhusu kuendelea—na huku tukipanua—huduma yetu hapa kwenye Mji Mtakatifu. Tunajua kwamba Mungu tayari ameshaandaa nyumba sahihi kwa ajili yetu na ameweka ndani ya mioyo ya viongozi wa ICEJ jijini Yerusalemu na Bodi ya Wakurugenzi wazo la kumiliki nyumba yetu wenyewe hapa Yerusalemu. Katika wiki na miezi ya hivi karibuni, watu mbalimbali walitukumbusha juu ya Isaya 54:3-4:
“Panua mahali pa hema yako, na wayatandaze mapazia ya maskani yako; usiwakataze; ongeza urefu wa kamba zako; vikaze vigingi vya hema yako. Kwa maana utaenea upande wa kuume na upande wa kushoto; na wazao wako watawamiliki mataifa; wataifanya miji iliyokuwa ukiwa kukaliwa na watu.” Tunawaomba msimame pamoja nasi katika maombi, tunaamini kwamba 2019 itaanza majira mpya kwa ICEJ.
TAFADHALI OMBA
l Mungu apanue ‘mahali pa hema yetu.’ l Mungu atupatie msaada wa kutatua mahitaji yetu yote na ambao utaimarisha huduma yetu hapa Yerusalemu. Inuka wakati tunapofanya mkakati huu muhimu.
l Tupate sehemu sahihi. l Kwa ajili ya upatikanaji wa fedha zitakazorahisisha mkakati huu.
Kumbukumbu la Torati 28:6 – “Utabarikiwa uingiapo, utabarikiwa na utokapo.”
Tafadhali pia omba Mungu alibariki taifa la Ivory Coast, kwa kuturuhusu kutumia jengo lao zuri kwa miaka yote hii.
Baraka nyingi kutoka Yerusalemu na tunawashukuru sana kwa kusimama pamoja nasi.
MAFUNDISHO/HABARI
YALIYOMO
6 7
CHUKI YA DAMU DHIDI YA ISRAELI
8
KITUONI HAIFA
16
SHALOM KUTOKA BURUNDI 4
AFRIKA YAIFUNGULIA MILANGO ISRAELI
12
JANUARI/FEBRUARI 2019
BODI MPYA YA ICEJ TANZANIA YAANZA KAZI
MAFUNDISHO/HABARI
MUNGU WA
WAKATI NA JĂœRGEN BĂœHLER RAIS WA ICEJ
K
ama tunavyoanza kila mwaka mpya, ni vema kujikumbusha mara zote kwamba Mungu ni Mungu wa mwanzo. Moja ya sifa kuu za Mungu ni asili yake ya umilele. Umilele ni wazo gumu sana kwetu kulielewa. Umilele ni hali isiyokuwa na mwisho lakini pia isiyokuwa na mwanzo: Daima ulikuwepo na daima utakuwepo. Moja ya mifano mikuu sana ya shauri hili la Mungu la nyakati zote na lisilotikisika ni historia ya watu wa Israeli. Msingi wa kusudi la Israeli unapatikana katika kusudi la milele la Mungu. 5
Hata kama mwaka mpya wako umeanza na magumu au changamoto zisizotazamiwa, kuwa na hakika kwamba Mungu atakamilisha kila alichokikusudia kwako. Yeye atakuonyesha matendo mema ambayo tokea awali Mungu alitangulia kuyaandaa kwa ajili yako (Waefeso 2:10). Kadri unavyokaa karibu na Yesu, ukichukua muda kuwa Naye na katika Neno Lake, Yeye atakuwa mwazilishi na mhitimishaji wa Imani yako (Waebrania 12:2). Mungu akubariki unapotembea katika kusudi Lake la milele mwaka 2019!
NENO KUTOKA YERUSALEMU
MAFUNDISHO/HABARI
Kumbukumbu ya wahanga wa shambulizi kwenye Sinagogi huko Pittsburgh Oktoba 2018 (Picha na AP).
CHUKI YA DAMU DHIDI YA ISRAELI NA: DAVID PARSONS
M
auaji ya kutisha kwenye sinagogi huko Pittsburgh mwishoni mwa Oktoba mwaka jana yaliwaacha Wayahudi wa Marekani wakihaha kusaka mwarobaini wa kuongeza mifumo ya ulinzi na usalama katika jamii zinazowazunguka. Kwa huzuni kubwa, hawako mbali sana na Wayahudi wa Ulaya, ambao wamekuwa wakihisi na kujiona kama wamezingirwa kwa miaka kadhaa. Kwa hakika sasa hivi kuna walinzi wenye silaha na vifaa vya uchunguzi nje ya kila sinagogi la Kiyahudi, shule za kutwa na vituo vya huduma za kijamaii vinavyomilikiwa na Wayahudi kwenye kila kona ya dunia. Orodha ya mashambulio ya kigaida ya hivi karibuni yaliyolenga vituo vya Wayahudi yakivurumishwa kwenye hoteli moja ya kiyahudi huko Paris, shule ya kutwa ya Toulouse, nyumba ya makumbusho huko Brusels, na sinagogi la Copenhagen yameonyesha chuki ya damu na udhalilishaji dhidi ya Israeli. Hata huko Mumbai nchini India, na sehemu 6
ya ufukwe tulivu ya Bondi huko Austaralia, mashambulizi yaliyojificha dhidi ya Wayahudi yanaendelea. Kama ni Waisilamu wenye itikadi kali, watu wenye siasa kali ya mrengo wa kushoto, au Manazi—mamboleo wa mrengo wa kulia kama Pittsburgh muuaji—Watu wanaochukia Wayahudi wanaendelea kueneza chuki zao kila mahali. Katika kiini chake, Chuki dhidi ya Wayahudi ni maradhi ya kiroho; roho ya wivu na kuwakataa Wayahudi na wote lazima tuchague kukubaliana na hilo au la!
Katika nyakati hizi za giza, ni muhimu kwa Wakristo kukabiliana na watu wanaoeneza chuki dhidi ya Wayahudi leo hii. Watangulizi wa Imani yetu walifanya makosa makubwa walipoeneza uongo dhidi ya Wayahudi, ambao ulisababisha madhara makubwa. Hivyo, tunawajibika kimaadili kuwaeleza wale wanaochukia Wayahudi leo hii kwamba haikuwa sahihi na bado siyo sahihi. Lazima tuhakikishe kwamba hawarudii makosa yetu!
JANUARI/FEBRUARI 2019
MAFUNDISHO/HABARI
KITUO CHA HAIFA OFISI MPYA YA ICEJ NA: YUDIT SETZ Kipindi cha majira ya joto mwaka 2018, ICEJ ilipanua uwepo wake Haifa. Yudit Setz wa ICEJ pamoja na mume wake, Will, walihamia Haifa ili kufanya kazi kwa karibu zaidi katika Kituo cha Haifa kinachohudumia wahanga wa Mauaji dhidi ya Wayahudi yaliyotokea barani Ulaya karne ya 20, na wamekuwa wakifanya kazi kwa bidii sana katika mradi huo tangu hapo. Licha ya kuwa kwenye mabadiliko kwa miezi kadhaa, ofisi hii mpya ya ICEJ tayari imetoa faida nyingi za thamani. Jarida la NENO Kutoka Yerusalemu lilimuomba Yudit kutoa taarifa mpya za kile Mungu anachofanya kupitia ICEJ huko Haifa.
H
aifa pamekuwa nyumbani kwa miezi mitatu sasa, na tunaishi karibu sana na Kituo cha Haifa (cha wahanga wa mauaji ya halaiki ya Wayahudi barani Ulaya). Hii inatupatia fursa zaidi za kushiriki katika maisha ya kila siku ya wakazi, kufahamu mahitaji yao na mahitaji ya kituo kwa ujumla. Mume wangu Will Setz, kwa uzoefu wake mkubwa katika fani ya ujenzi, ukarabati na uwezo wa kuzungumza lugha za Kiebrania, Kiingereza na Kijerumani kwa ufasaha anaongoza timu ya watu wanaojitolea kufanya kazi za mikono. Maono yetu ni kuwaleta Wakristo wenye fani mbalimbali kufanya kazi kwa mikono yao kwenye kituo cha Haifa kwa ajili
ya wahanga wa mauaji ya halaiki ya Wayahudi na kuwatambulisha kazi za ICEJ.
Ukarabati wa ukuta wa nje karibu umekamilika kabisa ukiwa umewekewa madirisha mapya kabisa, na tunategemea kuanza ukarabati wa ndani ya nyumba katika miezi kadhaa ijayo baada ya kukamilisha mahitaji ya vibali vinavyotakiwa kwa ajili ya lifti na ghorofa za ziada. Kwa sasa, watu wengi wameonyesha kuvutiwa na wanataka kusaidia ukarabati wa nyumba mpya, kwa hiyo tunategemea kuwakaribisha watu wengi wa kufanya kazi za kujitolea kwa muda mfupi katika wiki na miezi michache ijayo.
Sasa ni fursa yako ya kuwabariki Wahanga hawa walionusurika kwenye Mauaji ya Wayahudi, ama kwa kuchangia fedha au muda wako wa kujitolea kufanya kazi. Kuchanga michango ya kifedha kwa ajili ya Kituo cha Haifa, tafadhali tembelea tovuti ya: int.icej.org/aid/haifa-home-holocaust-survivors Kwa ajili ya kujitolea kufanya kazi za mikono, tafadhali wasiliana na: Yudit.setz@icej.org 7
NENO KUTOKA YERUSALEMU
MAFUNDISHO/HABARI
David Parsons akiwa na Mosy Madugba kwenye mkutano wa ICEJ Tanzania.
David Parsons akiwa na viongozi wa ICEJ Tanzania.
AFRIKA YAIFUNGULIA MILANGO ISRAELI ICEJ TANZANIA YAONYESHA MOYO WA AFRIKA KUIBARIKI ISRAELI NA DAVID PARSONS, MSEMAJI MKUU KIMATAIFA
M
wishoni mwa Septemba, 2016 kiongozi wa Israeli Benjamin Netanyahu alisimama kwenye jukwaa la Umoja wa Mataifa na kutoa ujumbe mzito akisema: “Israeli imebeba neema kubwa ya wakati ujao katika Umoja wa Mataifa.� Kwa hakika, taasisi hiyo kubwa ulimwenguni imekuwa na mfululizo usiokwisha wa tuhuma dhidi ya Israeli kwa miongo kadhaa, lakini sasa inazo sababu za kuamini kwamba mambo yamebadilika. Netanyahu aligusia safari zake za hivi karibuni barani Afrika kama mfano wa mabadiliko hayo, ambapo alikaribishwa kwa mioyo ya furaha na shangwe ya idadi kubwa ya viongozi wa mataifa ya Afrika na umati wa watu waliojawa na furaha na shangwe. Mwezi Agosti, 2016 nilisafiri na kufika nchini Tanzania na kushuhudia kwa macho yangu mwenyewe jinsi Afrika sasa inavyoifungulia milango Israeli kuliko ilivyowahi kutokea. Niliambatana na Mkurugenzi wa ICEJ nchini Nigeria na Mratibu wa Afrika yote Mch. Mosy Madugba, na kwa pamoja tulifungua tawi jipya la ICEJ nchini Tanzania. Uzinduzi huo ulifanyika wakati wa kongamano la kitaifa la Israeli ambalo lilihudhuriwa na Wakristo zaidi ya 2000 kukota mikoa yote ya Tanzania na nchi sita za kiafrika. 8
Waamini hao walikuwa na njaa ya mafundisho ya kina kuhusu Israeli na Kanisa, walikuwa na shauku ya kuibariki Israeli kwa sadaka zao nyingi, na walifurahishwa sana na kujifunza zaidi kuhusiana na Israeli ya sasa na tekinolojia zake nyingi. Wahudhuriaji wengi wa kongamano hilo walikuwa wakijivunia mpango wa serikali ya Tanzania wa kufungua Ubalozi mpya nchini Israeli kwa ajili ya kuboresha mahusiano kati ya nchi hizo mbili. Hiyo inadhihirisha tu jinsi Afrika ilivyo tayari kurudisha na kupanua mahusiano na Taifa Takatifu la Wayahudi. Ufunguzi huo wa tawi jipya la ICEJ nchini Tanzania uliongozwa na Mwinjilist Stanton Newton ambaye amekuwa mwakilishi wa ICEJ kwa miaka miwili iliyopita. Amekuwa akijielimisha mwenyewe kwa muda wa miaka kumi kuhusiana na Israeli na ICEJ, hasa kuhusiana na ujumbe tunaosimamia kwenye Biblia na miradi yetu ya misaada.
Kwa mwaka mzima Stanton alisafiri nchi nzima akiyaeleza makanisa kuhusiana na kongamano hilo la kitaifa la Israeli akiwasihi wakusanye sadaka kwa ajili ya Israeli na kuzipeleka kwenye kongamano. Matokeo yake zilikusanywa Dola 9000 kwa ajili ya kuibariki Israeli. Sehemu ya
JANUARI/FEBRUARI 2019
MAFUNDISHO/HABARI
Wakristo wa Tanzania wakiombea mahusiano ya karibu kati ya taifa lao na Israeli.
michango hiyo aliahidiwa ielekezwe kwenye kazi yetu ya kusaidia wahanga wa Maangamizi ya Wayahudi, wakati sehemu kubwa ya michango hiyo iliahidiwa ielekezwa kwenye kazi ya kusaidia kurejesha familia za Wayahudi walioko Ethiopia kuwarudisha kwenye nchi yao ya Israeli. Kila mara watu wa mikoa mbalimbali walipojipanga kutoa sadaka zao, nilikuwa nikijiona moyoni mwanga kwamba ninashikilia “ile sadaka ndogo ya mjane� mikononi mwangu, kwa sababu kipato cha wastani nchini Tanzania ni Dola 600. Hata hivyo ukiri wa Imani ilikuwa kubwa sana: Kama tukiibariki Israeli tutabarikiwa! Tanzania ni nchi ya kipekee kwani kwa miongo kadhaa ilikuwa chini ya ushawishi ya China ya Kikomonisti. Hali hiyo licha ya kukumbwa na changamoto zake kimaendeleo kwa namna fulani, lakini pia iliwapa watu umoja na mshikamano kama taifa moja, kwa hiyo Tanzania haijakumbwa na migogoro ya kikabila wala vita vya wenyewe kwa wenyewe ambayo imezigubika nchi nyingi barani Afrika. Pia kuna umoja wa kipekee miongoni mwa Wakristo nchini Tanzania, kwani Maaskofu na 9
wachungaji kutoka makanisa mbalimbali kama vile Anglikana, Lutherani, Baptisti, Katoliki na Pentekoste wote walisimama pamoja kwa umoja kuiunga mkono Israeli kwenye jukwaa la ICEJ.
Umoja huo ulipeleka ujumbe mzito kwa viongozi wa serikali ya nchi yao, ambao tayari wameonyesha juhudi kubwa za kudumisha mahusiano na Israeli. Wakati huo huo kikundi cha viongozi wafanya biashara Wakristo, wakiongozwa na Waziri wa zamani wa mambo ya nje, tayari wamejipatia eneo la shamba la ekari 100 kwa ajili ya kujenga kituo cha shamba la mfano la Israeli litakaloonyesha tekinolojia mbalimbali za kilimo, matumizi yake na utaalamu kutoka Taifa Takatifu ya Israeli. Wanategemea viongozi wa serikali na wakulima kutoka kwenye nchi zote barani Afrika kutembelea shamba darasa hilo katika miaka ijayo.
Katika hotuba yake Umoja wa Mataifa, Netanyahu alidokeza tekinolojia ya kilimo ya Israeli kama sababu ya viongozi wa Afrika kutafuta uhusiano na Nchi Takatifu ya Israeli ili iwape majibu ya
NENO KUTOKA YERUSALEMU
MAFUNDISHO/HABARI
kweli ya namna ya kuwalisha na kuwalinda watu wao. Alidokeza pia jinsi Afrika inavyovutiwa sana na tekinolojia kubwa ya Israeli ya kudhibiti ugaidi na usalama wa mitandao. Wakati akiwa New York, alifanya pia mkutano na viongozi 15 wa mataifa ya Afrika ambapo walijadili fursa zinazotokana na kuongezeka kwa mahusiano biana yao na Taifa Takatifu la Israeli. Maelezo hayo ya Netanyahu kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa aliyatoa muda mfupi baada ya kufanya ziara ya kihistoria katika mataifa manne ya Afrika Mashariki kwa ajili ya kumbukumbu ya miaka 40 ya Operesheni Entebe nchini Uganda iliyosababisha kifo cha Yoni kaka yake Netanyahu mwaka 1976. Viongozi wengine wengi wa nchi mbalimbali barani Afrika walivutika kuja kujumuika na kushirikiana na ujumbe mkubwa kutoka Taifa Takatifu la Israeli katika sherehe hiyo. Pia maofisa wa Israeli waliingia kwenye makubaliano maalumu ya kibiashra na muungano wa kiuchumi wa nchi za Afrika Magharibi. Kwa hiyo serikali ya Israeli inalichukulia kwa uzito na umakini mkubwa suala la kurejeshe mahusiano ya kihistoria kati ya Afrika na Israeli, ambayo kwa asili yake yalianzishwa na Golda
Meir miaka ya 1950 na 1960.
Ingawa mahusiano hayo yaliathiriwa na shinikizo la nchi za kiarabu kufuatia Vita ya Siku Sita ya mwaka 1967, viongozi wa kiafrika sasa wanaona waziwazi umihimu wa Israeli kutokana na uvumbuzi wake wa tekinolojia inayohitajika sana katika mataifa yao kwa ajili ya kuongeza kasi ya maendeleo katika sekta mbalimbali na kujihakikishia usalama wa wakati ujao.
Bila shaka, ICEJ imekuwa mstari wa mbele kufanikisha yote haya. Viongozi wa Israeli waliona uwezekano na umuhimu wa kurejesha mahusiano na Afrika mwaka 2011 wakati tawi la ICEJ nchini Nigeria walipofanikiwa kumshawishi Rais wao kukataa kutambua uwepo wa kiti cha taifa la Palestina katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, na hivyo kukwamisha mkakati huo wa kidiplomasia.
Tangu wakati huo, tumekutana na viongozi wa nchi mbalimbali barani Afrika, ikiwa ni pamoja na zile zenye Waisilamu wengi, ambao wamekuwa wakituomba turudishe ujumbe wao Yerusalemu kwamba wanapenda na wanahitaji kurudisha mahusiano na Taifa Takatifu la Israeli. Kwa hakika, ni siku ya Sayuni kukubalika sana, na ni wakati wa Afrika kubarikiwa!
Makamu wa Rais wa ICEJ Kimataifa, Mch. Mojmir Kallus akipokea sadaka ya kuibariki Israeli kutoka kwa Askofu Bruno Mwakiborwa. Kushoto ni Mwenyekiti wa ICEJ Kanda ya Pwani, Mchungaji Samson Mwaipaja 10
JANUARI/FEBRUARI 2019
MAFUNDISHO/HABARI
Mkurugenzi mpya wa Uchapishaji wa ICEJ, Julaine Stark, akiwa dukani Yerusalemu linakochapishwa Jarida la Neno Kutoka Yerusalemu.
Mkurugenzi mstaafu wa Uchapishaji wa ICEJ, Dan Herron, akikagua kituo kipya cha hifadhi na uokoaji wa wahanga wa mabomu huko Gaza.
MSIMU MPYA WA UCHAPISHAJI ICEJ
M
simu wa kiangazi mwaka 2017 uliashiria mwanzo mpya kwenye kitengo cha uchapishaji cha ICEJ wakati Dan Herron, aliyekuwa Mkurugenzi alipoachia ngazi mnamo July 2017 kwa ajili ya kwenda masomoni Yerusalemu.
Dan anakusudia kufanya masomo yake Yerusalemu, kwa sasa anasoma kozi ya kukabiliana na ugaidi na sera ya mambo ya nje ya Uturuki kwenye chuo kikuu cha Waebrania (Hebrew University). Pamoja na masomo yake huko chuo kikuu, Dan anaendelea na utumishi wake wa kuhamasisha mpango wa kusaidia Wayahudi kurejea Israeli (Aliyah) na pia atafanya kazi na vijana walio katika mazingira hatarishi, na wanajeshi wapweke katika jeshi la Israeli (IDF). Julaine Stark alitoka katika nafasi yake ya mpito ya Makamu wa Rais wa ICEJ wa Operesheni na kuongoza timu hiyo.
“Tunafurahi sana kuwa na Julaine akitekeleza majukumu katika nafasi yake mpya. Uaminifu wake na kujitoa kwake kwa ICEJ pamoja na wito wake na akili yake ya kipekee ndivyo hasa vitakavyosaidia kuongoza idara ya Uchapishaji katika msimu ujao wa kutimiza uwakili wetu katika nchi ya Israeli”, alisema Dkt. Jürgen Bühler, wakati akizungumzia uteuzi huo mpya.
11
NENO KUTOKA YERUSALEMU
MAFUNDISHO/HABARI
BODI MPYA YA ICEJ TANZANIA YAANZA KAZI EBELY RUGEMA, ICEJ TANZANIA
M
AKAMU wa Rais wa Taasisi ya International Christian Embassy Jerusalem (ICEJ) inayojishughulisha na kuunganisha Waisraeli na Wakristo wa mataifa yote duniani, Mch. Mojmir Kallus wiki iliyopita alisaini makubaliano maalumu na wanachama waanzilishi na Bodi ya Wadhamini wa taasisi hiyo kwa upande wa Tanzania ambayo yatawasilishwa serikalini kwa ajili ya kuanzisha rasmi tawi la ICEJ hapa nchini.
Akionekana mwenye furaha baada ya kusaini makubaliano hayo akiwa pamoja na jumla ya wanachama waanzilishi 12 wanaowakilisha madhehebu yote ya Kristo Tanzania Bara na Visiwani, Mch. Mojmir alisema tawi hilo la ICEJ Tanzania litakuwa chini ya uangalizi wa makao makuu yake yaliyoko Yerusalemu kwa muda wa miaka mitatu. Mch. Mojmir alisema baada ya miaka hiyo mitatu ICEJ Tanzania itakuwa huru kujiendesha na kuwa kitovu cha kusaidia kuanzisha matawi mengine katika nchi jirani za Afrika Mashariki na Kati huku akifafanua kwamba majukumu ya taasisi hiyo ni kuwaelimisha Wakristo juu ya wajibu wao kwa Israeli na wajibu wa Israeli kuwabariki na kuwashirikisha vipawa vya Mungu wa Israeli.
Alisema ICEJ inalo jukumu la kuwahamasisha Wakristo wa madhehebu mbalimbali kuombea nchi na serikali yao pamoja na Amani ya Yerusalemu kama ilivyoandikwa kwenye Isaya 62 na maandiko mengine ya Biblia.
Aidha, Mch. Mojmir alisema ni muhimu kwa kila Mkristo kutambua wajibu wake kwa Israeli kwamba anapaswa kushiriki kwa kuchanga fedha kiasi chochote anachoweza ili kuendeleza mpango unaoratibiwa na ICEJ wa kuwarejesha Wayahudi kwenye nchi takatifu 12
ya Israeli, jukumu ambalo ni la watu wa mataifa (wasiokuwa Wayahudi).
Alisema kitendo cha Wayahudi kurudi kwenye nchi Takatifu ni cha kiroho na kihistoria kinachotimiza maandiko na unabii wa Biblia na kuhimiza Wakristo wa Tanzania kujiunga na ICEJ ili kutimiza wajibu wao wa kiroho na kihistoria na kuwa tayari kuvuna baraka ya tekinolojia ya kisasa ya Israeli inayoweza kulisha dunia nzima kipitia kilimo, viwanda na ufugaji wa kisasa. Naye Mkurugenzi wa ICEJ nchini, Bw. Stanton Newton alimshukuru Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kufungua Ubalozi wa Tanzania nchini Israeli ambao umekuwa kiungo muhimu kati ya Tanzania na Israeli.
Bw. Stanton alimuomba Mch. Mojmir kumkumbuka Rais JPM, serikali anayoiongoza na nchi ya Tanzania katika maombi huko Yerusalemu. Mch. Mojmir alipokea ombi hilo kwa furaha na kuahidi kwamba atapeleka jina la Rais JPM moja kwa moja kwenye madhabahu ya Yerusalemu yanapofanyika maombi kila siku asubuhi.
Maombi hayo yanaratibiwa na ICEJ inayofanya kazi kwa ushirikiano wa karibu na ofisi ya Waziri Mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu.
JANUARI/FEBRUARI 2019
MAFUNDISHO/HABARI
Watumishi wa ICEJ Nicole Yoder and Dan Herron wakipokea maelezo kutoka kwa Meya katika chumba cha uokoaji wa wahanga wa mabomu kilichoko Manispaa ya Sdot Negev.
MTUMISHI WA ICEJ ANASA KWENYE KIZUIZI CHA MABOMU NA MAROKETI Yote ilianzia kwenye safari ya kawaida ya kutembelea baadhi ya vituo vyetu vya misaada kwenye mpaka wa Gaza. Kwenye asubuhi moja angavu ya Novemba, niliungana na Mkurugenzi wa Misaada wa ICEJ, Nicole Yoder kwa ajili ya kutembelea miradi tunayoifadhili huko Negev magharibi. Lakini mpaka mchana, hakuna kilichokuwa kawaida kuhusu siku hiyo, kwani tulinasa kwenye kizuizi kikubwa mno kuwahi kutokea cha mabomu na maroketi kutoka Gaza kilichodumu kwa muda wa siku nzima. Kwa zaidi ya masaa 24 yaliyofuata, karibu mabomu 500 na makombora yalipigwa kwenye makazi ya Waisraeli wanaoishi mpakani.
Nicole na mimi tulikumbana na uhitaji wa haraka wa mahali pa kujihifadhi, lakini tulitiwa moyo na 13
Mpaka wa Gaza
wasimamizi wa vyumba vya kuokolea wahanga wa mashambulizi ya mabomu na maneno yao ya shukurani kwa ajili ya misaada ya ICEJ. Tumejenga vituo 70 vya kujihifadhi na kuokolea maisha ya wahanga wa mabomu, na kutoa magari 17 ya zima moto kwa ajili ya kuzima miale ya moto inayotokana na mabaluni yanayochomwa kwa nia mbaya ya kuhatarisha usalama. Hata hivyo, cha kusikitisha, Hamas wanaendeleza mashambulizi kutokea Gaza. Bado kuna mengi ya kufanya ili kudumisha usalama katika mpaka huu uliozingirwa. Tunashukuru kwa kutusaidia wakati huu tunaposimama pamoja na watu wa Israeli.
Saidia Israeli kujiandaa na kustahimili katika mazingira ya migogoro kwa kutembelea tovuti ifuatayo: int.icej.org/aid/israel_in_crisis
NENO KUTOKA YERUSALEMU
MAFUNDISHO/HABARI
Waziri Mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu akisikiliza hotuba ya mmoja wa viongozi waandamizi wa Israeli katika mkutano wa kimataifa wa vyombo vya habari vya Kikristo uliofanyika Yerusalemu Oktoba mwaka jana.
I
CEJ iliwakilishwa vema kwenye Mkutano wa pili wa kila mwaka wa Kimataifa wa Vyombo vya Habari vya Kikristo uliofanyika Yerusalemu Oktoba mwaka jana chini ya uenyeji wa Idara ya Habari ya Serikali ya Israeli.
Mkutano huo wa Vyombo vya Habari vya Kikristo kwa mara nyingine ulithibitika kuwa na masuala nyeti na uliofanyika katika muda mwafaka kwani ulikwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 70 ya kumbukumbu ya kuzaliwa upya kwa taifa la Israeli mwaka 1948.
Makamu wa Rais wa ICEJ, David Parsons kwa mara nyingine alifanya kazi kama mshauri maalumu wa masuala ya Kikristo wa Idara ya Habari ya Serikali ya Israeli kuhusiana na mkutano huo ambao ulihudhuriwa pia na dozeni ya Wakurugenzi wa ICEJ katika mataifa mbalimbali na wafanyakazi wa makao makuu.
Alimkaribisha pia Balozi wa Marekani, David Friedman kutoa salamu, kabla ya Ujumbe wa Wakristo wenye asili ya Kiyahudi kutoka Marekani kuanza kunukuu maneno ya Yesu kuhusiana na vita ya vyombo vya habari akisema, “Kweli itawaweka huru.”
Zaidi ya waandishi wa habari za Kikristo 200, wachapishaji na watangazaji kutoka kwenye mataifa 35 walihutubiwa na Waziri Mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu, Rais Reuven Rivlin, Naibu Waziri Mkuu, Michael Oren, Meya wa Yerusalemu Nir Barkat, Balozi wa zamani wa Umoja wa Mataifa, Dore Gold na viongozi waandamizi wengine kadhaa wa Israeli, na wasomi na wachambuzi.
14
Waziri Mkuu Netanyahu alionekana mtulivu na mwenye furaha katika hotuba yake ya kufungua mkutano huo, ambapo alijibu maswali 20— ambayo ni mengi zaidi sana kwani kulingana na kawaida yake huwa hana muda wa kujibu maswali mengi kiasi hicho katika mikutano yake ya mara kwa mara na waandishi wa habari nchini mwake na wale wa kigeni.
JANUARI/FEBRUARI 2019
MAFUNDISHO/HABARI
ZIARA YA MAKAMU WA RAIS WA ICEJ KIMATAIFA MCH. MOJMIR KALLUS NCHINI TANZANIA DESEMBA 2018
Wanachama wa ICEJ na marafiki wa Israeli nchini Tanzania wakikabidhi sadaka zao za binafsi za kuibariki Israeli kwa Makamu wa Rais wa ICEJ Kimataifa, Mch. Mojmir Kallus Desemba mwaka jana.
15
Makamu wa Rais wa ICEJ Kimataifa, Mch. Mojmir Kallus akitoa maneno baraka baada ya kupokea sadaka wa Wakristo wa Tanzania. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa ICEJ Tanzania, Mch. Stanton Newton, Askofu Bruno Mwakiborwa wa Kanisa la EAGT Mito ya Baraka jijini Dar es Salaam, na Mwenyekiti wa ICEJ Tanzania, Kanda ya Pwani, Mch. Samson Mwaipaja.
Makamu wa Rais wa ICEJ Kimataifa, Mch. Mojmir Kallus akiomba baraka kwa ajili ya wanachama wa ICEJ na marafiki wa Israeli nchini Tanzania waliohudhuria ibada maalumu ya kusimika wajumbe wa Bodi mpya ya ICEJ tawi la Tanzania.
NENO KUTOKA YERUSALEMU
MAFUNDISHO/HABARI
SHALOM KUTOKA BURUNDI
NA AMANDA GROSS
“Tunaiheshimu Israeli kama ya kwanza, kwa sababu Israeli ni mzaliwa wa kwanza wa Mungu miongoni mwa mataifa,” ndivyo alivyotangaza mke wa Rais wa Burundi, Mheshimiwa Mch. Denise Buchumi Nkurunziza wakati akitambulisha ujumbe wetu wa ICEJ kutoka Israeli. Tulikaribishwa kwa furaha na salamu ya “SHALOM”, kwa sababu “shalom” ni salamu ya kawaida nchini Burundi.
Tukiwakilisha makao makuu ya ICEJ, Jo Olsen, Jannie Tolhoek na mimi tulipewa heshima ya kushiriki katika mkutano wa kwanza wa Kimataifa wa Wanawake Viongozi uliofanyika nchini Burundi chini ya kauli mbiu ya: “Wanawake wenye mamlaka inukeni, jipeni moyo na kushughulikia mambo yanayowahusu.”
Mkutano huo ulihudhuriwa na wanawake 500 wa Burundi na wawakilishi 116 kutoka mataifa 24, wakiwemo mke wa Rais wa Zambia, Mheshimiwa Esther Nyawa Lungu na mke wa Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Mheshimiwa Brigitte Touadera. Mke wa Rais wa Burundi ni Mchungaji mwenye maono ya kuunganisha wanawake wa Burundi kutambua wajibu wao kama viongozi, siyo tu 16
katika nyumba zao lakini pia katika taifa lao.
Kama sehemu ya kongamano hilo, tulisafiri kwa masaa matatu kaskazini kwenda mkoa wa Ngozi ambako tulishiriki uzinduzi wa kampeni ya “Uhuru wa Kung’ara”, yenye lengo la kukomesha maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa kujifungua. Tulitembelea pia kituo cha watoto yatima cha “Msamaria Mwema” kinachohudumia watoto yatima 40. Tulipata fursa ya kuwaombea watoto yatima na walezi wao, pamoja na kuwabariki kwa zawadi mbalimbali.
Baada ya kutoka kwenye mkutano huo, nilivutiwa sana na maisha ya mke wa Rais wa Burundi na mikakati yake. Pia Ilikuwa inagusa moyo kuona upendo halisi uliochomoza kutoka kwa watu wa Burundi. Watu wengi waliohudhuria mkutano huo walikuja kwenye meza yetu wakisema wanaiombea Israeli na wana ndoto ya kutembelea nchi hii takatifu ya Israeli moja ya siku. Mungu alijidhihirisha sana katika mkutano huo, na tunatumaini kuona kile Mungu atakachoendelea kufanya kupitia wakati huu wa kihistoria katika historia ya Burundi!
JANUARI/FEBRUARI 2019
MAFUNDISHO/HABARI
SUPPORTING ETHIOPIAN ALIYAH Do you feel led to help God’s chosen people return to the land of Israel? You can be a part of bringing Ethiopian Jewish families back together in their biblical homeland by donating to the ICEJ today!
How to Pray for Ethiopian Aliyah
SUPPORTING ETHIOPIAN ALIYAH
1. Pray that the door would open for the Jews of Ethiopia to return to Israel and the government of the nation would cooperate with Israel in the Aliyah process. Do you feel led to help God’s chosen people return to the land of Israel? You can be a part 2. Pray for the reuniting of family members within Israel and for the healing of old wounds of of bringing Ethiopian Jewish families back together in their biblical homeland by donating to separation loss. the ICEJand today! 3. Pray with us for the assimilation of the Ethiopian community into the fibre of Israeli society, Je, unajisikia kuongozwa kuwasaidia wateule wa Mungu kurudi kwenye nchi yao ya Israeli? Unaweza kushiriki kwa kuchangia mpango wa kusaidia How to Pray for Ethiopian and for them to find purpose Aliyah in their homeland of Israel. familia za Wayahudi walioko Ethiopia kurudi kwenye nchi yao ya kibiblia ya Israeli kupitia ICEJ leo.
SAIDIA WAYAHUDI WA ETHIOPIA KURUDI ISRAELI
1. Pray that the door would open for the Jews of Ethiopia to return to Israel and the government of the nation would cooperate with Israel in the Aliyah process. Jinsi2. ya kuombea Wayahudi wa Ethiopiayour wanaorudi Israeli. Pray for the reuniting of family members within copy Israel and the healing of of old wounds ofat: Donate today and receive offorJourney Dreams 1. Ombea mlango and ufunguke separation loss. kwa ajili ya Wayahudi wa Ethiopia kurejea Israeli na serikali ya taifa hilo ishirikiane na Israeli int.icej.org/documentary katika mchakato wathe kurudi kwenye nchi yaoEthiopian ya ahadi.community into the fibre of Israeli society, 3. Pray with us for assimilation of the 2. Ombea tenapurpose wa wanafamilia nchini Israeliofna uponyaji wa majereha ya kutengana na kupotezana. andmuunganiko for them to find in their homeland Israel. 3. Omba pamoja nasi kwa ajili ya kuwaingiza jamii ya Wayahudi wa Ethiopia kwenye mkondo mkubwa wa jamii ya Waisraeli ili na wao waweze kupata na kutumikia kusudi katika nchi yao ya ahadi ya Israeli.
Donate today and receive your copy of Journey of Dreams at: int.icej.org/documentary Changia Dola 50 za Marekani au zaidi upate nakala yako ya filamu ya Safari ya Ndoto (Journey of Dreams) int.icej.org/documentary
ICEJ NORTHERN IRELAND & IRELAND 38 Lough Moss Park Carryduff • Belfast BT8 8PD icej.ire@btinternet.com
ICEJ HEAD OFFICE 20 Rachel Imeinu · PO Box 1192 Jerusalem, Israel · 9101002 Tel: +972 2 539 9700 · Fax: +972 2 566 9612 ICEJ HEAD OFFICE www.icej.org · icej@icej.org 20 Rachel Imeinu · PO Box 1192 Jerusalem, Israel · 9101002 Tel: +972 2 539 9700 · Fax: +972 2 566 9612 www.icej.org · icej@icej.org
ICEJ NORTHERN IRELAND & IRELAND 38 Lough Moss Park Carryduff • Belfast BT8 8PD icej.ire@btinternet.com
ICEJ NEW ZEALAND ICEJ AUSTRALIA PO Box 100474 Level 40, 140 William Street ICEJ NEW ZEALAND ICEJ AUSTRALIA North Shore · North Shore · 0745 Melbourne 3000, Australia PO BoxCity 100474 Level 40, 140 William Street Tel: North +649Shore 837 ·5384 Tel: +61 3 8001 6001 North Shore City · 0745 Melbourne 3000, Australia Tel: +649 837 5384 Tel: +61 3 8001 6001 icejnz@ihug.co.nz Connect@icej.org.au icejnz@ihug.co.nz
ICEJICEJ
INTERNATIONAL
INTERNATIONAL CHRISTIAN CHRISTIAN EMBASSY JERUSALEM EMBASSY JERUSALEM
Connect@icej.org.au
ICEJ UNITED KINGDOM ICEJ UK PO Box 717, WIGAN, WN1 9PP Tel. 07503624135 or 01744 894374 ICEJ UNITED KINGDOM ICEJ UKinfo@icejuk.org PO Box 717, WIGAN, WN1 9PP Tel. 07503624135 or 01744 894374 info@icejuk.org
ICEJ SOUTH AFRICA ICEJ CANADA 3 Transvalia Avenue 20 Bloor Street East · PO Box 75149 ICEJ SOUTH AFRICA ICEJ CANADA Union Park 20 Bloor Street East Toronto M4W 3T3 3 Transvalia Avenue · PO BoxON 75149 Stellenbosch Union Park Tel: 416 Toronto ON M4W 3T3 324 9133 Stellenbosch 7600 Tel: 416 9133 Toll324 Free Tel: 1 866 324 9133 866 324 9133 Tel.7600 +27 21 8833301 Toll Free Tel: 1info@icejcanada.org Tel. +27 21 8833301 info@icejcanada.org office@icej.org.za office@icej.org.za
ISRAELI INAKABILIANA NA MAHITAJI LUKUKI YA KIJAMII. Hata hivyo, kama Wakristo tunayo fursa ya kipekee17kubariki watuKUTOKA wake katika tendo la upatanisho na upendo. Uzoefu wetu mkubwa na mtandao NENO YERUSALEMU wa mahusiano ya kijamii katika ardhi ya Israeli utakuhakikishia kwamba zawadi yako ya baraka inatumika kikamilifu iwezekanavyo. Michango inawezesha kusimamia na kugharamia miradi ya dharula, na kuanzisha mipango mipya ya kuisaidia Israeli katika nyakati hizi za hatari. Tembelea www.icej.org/donate
BEGINNINGS
THE BEGINNING OF EVERYTHING THAT EXISTS WAS MADE BY AND THROUGH HIM
$ 470
OCTOBER 13 -18, 2019
18
Full registration includes admission to all public Feast-related events including Ein Gedi, Communion at the Garden Tomb and the Jerusalem March.
$1049and up The ICEJ also offers a land package programme to provide hotel accomodations for seven nights and transportation to Feast events including the Jerusalem March. Land package rates begin at $1049.00 and include the registration fee.
feast.icej.org
JANUARI/FEBRUARI 2019 Come to Jerusalem for the Feast and begin a New Chapter – in 2019!
SIKUKUU YA VIBANDA 2018
Shuhuda za Eben-ezeri KUTOKA SIKUKUU YA VIBANDA YA ICEJ Ndipo Samweli akachukua jiwe, na kulisimamisha kati ya Mispa na Sheni, akaliita jina lake, Eben-ezeri, akisema, Hata Sasa BWANA ametusaidia.” (1Samweli 7:12)
E
ben-ezeri inamaanisha, jiwe la msaada, na lilisimamishwa na Samweli kama alama na kumbukumbu ya msaada wa Mungu na fadhili zake. Kila mwaka, ICEJ inapokea taarifa mbalimbali za miujiza inayotendeka wakati wa Sikukuu ya Vibanda inayoandaliwa na ICEJ. Baada ya sikukuu ya mwaka 2018, wafanyakazi wa ICEJ na wengine binafsi waliorodhesha mifano mikuu ya jinsi Mungu alivyotusaidia “mpaka hapa” na anavyoendelea kuwa Eben-ezeri. Zifuatazo ni baadhi tu ya shuhuda: Siku kadhaa kabla ya ufunguzi huko Ein Gedi, polisi walisema jioni ya sikukuu hiyo lazima ifutwe. Siku moja kabla ya tukio, Mungu alifanya muujiza kwa kutupatia kibali tulichokuwa tunahitaji kwa ajili ya mkesha wa ufunguzi kuendelea kama tu vile hakuna kilichokuwa kimetokea! Wakati Daniel Kolenda alipoomba mguso wa Mungu wa uponyaji kwa mkutano wote wa Ein Gedi, mwanamke wa zaidi ya miaka 80 aliponywa maumivu ya miguu ya muda mrefu na mgongo uliokuwa umemtesa kwa miaka mingi sana. Baada ya kugundua Mungu amemponya, alianza kucheza na kumsifu Mungu!
Makamu wa Rais na Msemaji Mkuu wa ICEJ, David Parsons, akiwa anaumwa kichwa na mafua na homa wakati wa Sikukuu, alitiwa nguvu na Mungu kila siku, ambaye alimwezesha kusherehesha, kuhutubia, na kuunganisha watu wakati wote wa Sikukuu. Rais wa ICEJ, Jürgen Bühler, aliyekuwa ametoka kwenye upasuaji muda si mrefu, alijisikia Mungu akiendelea kumtia nguvu na uwezo wa kuhudumu kama mnenaji mkuu kwenye mkesha wa tukio la ufunguzi na kuhudhuria kweye Sikukuu kila siku. Mchungaji wa miaka 84 kutoka Ufilipino aliyekuja Israeli kwa mara ya kwanza, katika moja ya ibada za Sikukuu ya Vibabanda Mungu alimponya ugonjwa wa moyo ambao ulikuwa umemtesa kwa miaka kadhaa. Christine kutoka Marekani alitushirikisha kwamba, “Mume wangu alibadilisha mtazamo kuhusu Israeli baada ya kusoma jarida la ICEJ la Neno Kutoka Yerusalemu, na hatimaye akafunguliwa kuja Israeli. Niko na mume wangu hapa kwenye mkutano.” Tunataka kusikia kutoka kwako! Tushirikishe ushuhuda wako wa Eben-ezeri wa kile Mungu alichokutendea kwenye maisha yako kupitia barua pepe: media@icej.org
MWANZO
MWANZO WA KILA KITU KILICHOPO KILIUMBWA NA YEYE KUPITIA YEYE
SIKUKUUU ya VIBANDA IMETOLEWA NA INTERNATIONAL CHRISTIAN EMBASSY JERUSALEM
OKTOBA 13-18, 2019 JISAJILI LEO: FEAST.ICEJ.ORG/REGISTER 19
NENO KUTOKA YERUSALEMU
Njoo Yereusalemu usherehekee nguvu Zake za kugeuza mambo na ahadi zake za milele
TOLEO MAALUMU LA KUMBUKUMBU YA MIAKA 70
LEMU KA YERUSA NENO KUTO
Sherehekea Israeli ya wakati uliopita - Bariki wakati wake ujao Unaweza kuwa baraka kwa watu wa Israeli! Taifa la Israeli limekuwa na linaendelea kutubariki, je utaungana nasi kuonesha shukurani zetu kwa njia inayoonekana dhahiri? Mchango wako unafanya kitu kikubwa cha tofauti kwenye maisha ya Waisraeli! Kwa mchango wako wa Dola 7o za Marekani au zaidi, utapokea toleo hili maalumu la kipekee bure kama zawadi (lililochapishwa na la kielektroniki).
MUUJIZA WA KUDUMU WA MUNGU
NENO KUTOKA LEMU YERUSA
hili? Ni nani aliyesikia neno kama haya? Ni nani aliyeona mambo kama ? moja siku liwa kuza za Je! nchi yawe ? Taifa laweza kuzaliwa mara ona utungu, Maana Sayuni, mara alipo Alizaa watoto wake.
Toleo hili maalumu la kurasa 40 lina muhutasari wa miaka kumi kumi wa historia ya Israeli ya sasa na inatoa mafundisho ya thamani sana na maelezo muhimu ya kihistoria.
PATA TOLEO LAKO MAALUMU KUPITIA
SAFARI YA VIJANA WATU WAZIMA NCHINI ISRAELI INAYOBADILISHA MAISHA
SAFARI YA
GHARAMA ZA SAFARI
DOLA 1399
• Malazi na kifungua kinywa • Usafiri wa kutoka uwanja wa ndege wakati wa kuingia na kutoka • Safari zote na malipo ya viingilio kwenye hifadhi za taifa • Huduma ya malazi hotelini kwa siku 10 kwa masharti ya watu watatu kuchangia chumba. • Bei hii haihusiani na nauli ya ndege.
20
JANUARI/FEBRUARI 2019
JISAJILI LEO