NENO LA MSALABA TOLEO LA KWANZA | SEPTEMBA 2020
KUNENA KWA LUGHA Mafunzo kwa Kanisa la Mungu NA MCHUNGAJI RAPHAEL MARKO SALLU
Mafunzo kwa kanisa la Mungu.
NENO LA MSALABA
NENO LA MSALABA
Yaliyomo 02
KUNA KUNENA KAMA KARAMA NA KUNA KUNENA KAMA ISHARA.
04
TUNAPOSEMA KWA LUGHA TUNASEMA KWA LUGHA MBALI MBALI.
04
SABABU TATU ZA MUHIMU AMBAZO INAPASA KILA MWAMINI ANENE KWA LUGHA.
MAFUNZO KWA KANISA LA MUNGU
Kunena kwa Lugha NA MCHUNGAJI RAPHAEL MARKO SALLU Nataka kuzungumzia somo zuri sana la kunena kwa lugha. Somo ambalo linasumbua watu wengi. Kuna mawazo tofauti juu ya somo hili.Kuna ambao wanasema siyo lazima kanisani watu wote wanene kwa lugha,na kuna ambao wanasema ni muhimu watu wote kanisani wanene kwa lugha mpya.
MAANDIKO YANASEMA NINI JUU YA SOMO HILI? HEBU TULIFUATILIE TUWEZE KUJIFUNZA. KUNA KUNENA KAMA KARAMA NA KUNA KUNENA KAMA ISHARA. KUNENA KAMA KARAMA Kunena kama karama si watu wote wanatakiwa kunena.kwa sababu karama Mungu anatoa tofauti tofauti,kama apendavyo,hivyo si wote wanaojaliwa karama hii. 02
MAFUNZO KWA KANISA LA MUNGU
Na wanaojaliwa karama hii ya kunena wanatakiwa ama wao wenyewe ama mtu mwingine atafisiri,imeandikwa hivi: “Kwa sababu hiyo yeye anenaye kwa lugha na aombe apewe kufasiri. (1wakorintho 14:13) Maneno kama haya, ndiyo wanayotumia watu ambao hawakubaliani na kunena kwa lugha kwa watu wote,wanasema haiwezekani watu wanene na isieleweke kinachoongelewa.Maandiko mengine wanayo yatumia nia haya: “ Je! Wote ni mitume? Wote ni manabii? Wote ni waalimu? Wote wanatenda miujiza? Wote wana karama za kuponya wagonjwa? Wote wanena kwa lugha? Wote wafasiri”?(1Wakorintho 12:29-30).
NENO LA MSALABA
NENO LA MSALABA
Wanatumia mistari hii kuthibitisha kwamba
NA MCHUNGAJI RAPHAEL SALLU
kunena kwa lugha si watu wote wanene,na ndiyo maana maandiko hapo yameuliza wote wanene kwa lugha? Ni kweli kama karama siyo wote.Kumbuka nimesema kuna kunena kama karama na kuna kunena kama ishara. Andiko jingine wanalotumia ni hili: “Kama mtu akinena kwa lugha, wanene wawili au watatu, si zaidi, tena zamu kwa zamu, na mmoja na afasiri.”(1Wakorintho 14:27)
Kama
wanene
mtu
wawili
au
akinena
kwa
watatu,na
lugha mmoja
afasiri.Kwa hoja hii mpaka upewe neema ya kufahamu
maandiko
kwanini
makanisani
Kwa sababu hii basi kunena kwa lugha si kwa baadhi ya watu tu. (2)Wote: Ni ishara inayoonyesha kwamba umejazwa na Roho Mtakatifu. Imeandikwa hivi: “Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka.”(Matendo 2:4) Hii ilikuwa siku ya pentekoste, ambapo waamini mia na ishirini walikua mahali pamoja wakisubiri ahadi ya kujazwa na Roho Mtakatifu.Maandiko yanasema wote kabisa
watu wananena wengi na hakuna mtafsiri,
wakajazwa na wakaanza kusema kwa lugha
lazima
nyingine.”wote”
utaona
wanaonena
namna
hiyo
wanakosea.Kwa hiyo niseme hivi,kunena kama karama si wote,na hii inaponenwa
Maandiko mengine yanayoonesha kwamba
lazima awepo mtafsiri.
kunena kwa lugha ni kwa wote ni haya:
KUNENA KAMA ISHARA
“ Petro alipokuwa akisema maneno hayo Roho
Kunena kama ishara,ni ishara inayoonesha
Mtakatifu akawashukia wote waliolisikia lile
kwamba
neno. Na wale waliotahiriwa, walioamini,
umepokea
ujazo
wa
Roho
Mtakatifu,na kwamba wewe ni mwamini.
wakashangaa, watu wote waliokuja pamoja na Petro, kwa sababu Mataifa nao wamemwagiwa
Ishara hizi: Imeandikwa hivi: “Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya;”(Marko 16:17.) Unaona maandiko haya? Ni maneno ya Bwana Yesu,alisema kuna ishara zitakazo fuatana na wanaoamini.Kama unamwamini Yesu lazima ishara hizo unazo,ni kitambulisho kinachoonesha kwamba wewe ni mwamini,umeokoka,na moja ya alama
kipawa cha Roho Mtakatifu. Kwa maana waliwasikia wakisema kwa lugha, na kumwadhimisha Mungu…”(Matendo 10:44-46). Hii
ilikuwa
nyumbani
kwa
Kornelio,wakati
Petro analisema Neno la Mungu mara ghafla mataifa
wale
wakajazwa
na
Roho
Mtakatifu.Biblia inasema Wayahudi walioamini ambao
walifuatana
na
Petro,walishangaa
kuona hata mataifa nao wamejazwa na Roho Mtakatifu.Nini
kiliwatambulisha,ni
ishara.
Biblia inasema maana waliwasikia wakisema
hiyo inayotambulisha kuamini kwako ni
kwa lugha.”Wote” .Fuatilia hayo maandiko
kunena kwa ugha.
utaona kwamba ni wote waliolisikia neno
03 02
walinena.Kunena kama ishara ni wote.
TUNAPOSEMA KWA LUGHA TUNASEMA KWA LUGHA MBALI MBALI. Hii kunena kwa lugha, tunaponena tunanena kwa lugha mbali mbali,ama za wanadamu ama za malaika,imeandikwa hivi: “Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika,…”(1Wakorintho 13:1) Paulo anaonesha kwamba mtu, anaponena anaweza kuwa ananena kwa lugha za wanadamu mbali mbali duniani au kwa lugha za malaika.Kwa sababu hii siyo lazima ieleweke kama ilivyokuwa siku ya Pentekoste.Ingelikuwa ni hivyo, kusingekuwa na haja ya kuwepo mtafsiri wakati tunanena kwa sababu kila mmoja angesikia kwa lugha yake kama ilivyokua siku ya Pentekoste.Lile lilikuwa jambo maalumu na hata sasa kwa makusudi ya Mungu ikibidi huwa inatokea. Wakati fulani miaka ya nyumba sana,nilikuwa namshuhudia kijana mmoja ambaye alikuawa hajamwamini Yesu. Yule kijana alikua anabisha sana habari ya wokovu.Tulikua na kaka mmoja wakati naongea naye,ghafla nikanena kwa lugha kama maneno matatu hivi.Yule kijana akamaka,akasema.”Wewe ni muemba?”Nikamwambia hapana mimi ni mzigua wa Korogwe,akasema hapana.”Wewe ni muwemba wa Zambia,mimi ni Muwemba na umesema kiwemba cha ndani sana!” Nikamwambia nimesema neno gani? Akasema,”Hilo neno kiwemba ni kama unamwita mtu mkubwa sana aje akusaidie.
SABABU TATU ZA MUHIMU AMBAZO INAPASA KILA MWAMINI ANENE KWA LUGHA. 1. kusema na Mungu mambo yako. “ Maana yeye anenaye kwa lugha, hasemi na watu, bali husema na Mungu; maana hakuna asikiaye; lakini anena mambo ya siri katika roho yake.”(Wakorintho 14:2) Maandiko yanasema,yeye anenaye kwa lugha hasemi na watu bali na Mungu.Kwa hiyo kunena kwa lugha ni njia ambayo Mungu ameiweka ili kuwasiliana na watu wake.Na kama ni namna moja wapo nzuri ya kuwasiliana na Mungu,bila shaka yeyote haiwezi kuwa ni kwa baadhi ya watu.Ila ni kwa watoto wa Mungu wote. Tafsiri nyingine ya Biblia mstari huo unasomeka hivi: “Kwa maana mtu yeyote anayesema kwa lugha,hasemi na wanadamu bali anasema na Mungu.Kwa kuwa hakuna mtu yeyote anayemuelewa,kwani anasema mambo ya siri kwa Roho.”(1kor14:2- NENO). Tafsiri ile nyingine inasema anena mambo ya siri katika roho yake, tafsiri hii ya Neno ,inasema. Anasema mambo ya siri kwa Roho. Ninachokipata mimi ni kwamba uko ushirikiano wa kimaongezi kati ya mtu na Mungu Kwa kuwezeshwa na Roho Mtakatifu.Hii inanipa kuona ni muhimu kila mtu anene.Maana inapofanyika hivi mtu binafsi hujijenga, kama tutakavyoona hapo mbele. NENO LA MSALABA | PAGE 04
2.Hujijenga nafsi. “Yeye anenaye kwa lugha hujijenga nafsi yake; …”(1wakorintho 14:4). Huu mstari sehemu hii ambayo tumeisoma,unaonesha kwamba mtu yeyote anayenena ,anajijenga nafsi yake,kiyunani kujijenga ni “oikodomei” Kwa hiyo utaona kwamba ni muhimu kwa kila mtoto wa Mungu ,kwanza awe na njia ya kiroho ya kuwasiliana na Baba yake,ambayo Biblia inasema ni pale mtu anaponena kwa lugha anasema na Mungu mambo ya siri yasiyoelewaka na binadamu,na pili ni pale anaponena kwamba anajijenga yeye mwenyewe jambo ambalo ni muhimu kujijenga.Maana unapojengeka ndipo unapoweza kuujenga mwili mzima yaani kanisa. Hii inanipa kutambua Mungu anataka kila mtu aliyeokoka anene kwa lugha ili ajijenge.
Sasa swali kwanini watu wananena na hakuna mtafisiri,na wakati maandiko yanasema mtu anaponena wanene wawili au watatu na mwingine atafisiri? Ni hivi: Kwanza tuelewe Paulo alipokua anaandika waraka huu alikua akitatua matatizo mbali mbali yaliyojitokeza kule Korintho, na moja wapo ya mambo aliyo yatatua,ni utaratibu katika ibada na matumizi ya karama,walikua hawana utaratibu,kwamba labda nabii alikua anahutubu yaani anatoa ujumbe wakati huo huo mtu mwingine anaenena kama karama , na wakati huo huo mwingine anatafsiri.Hii ndiyo iliyopelekea akasema hivyo. Sasa kama watu wamefudishwa na karama ya kunena ikawa inatumika na Mungu anataka kutoa ujumbe kwa watu wake, watu watanyamaza tu kusikiliza ujumbe ,hii imetokea mara nyingi na mimi nikiona hivyo.Ila kama hakuna ujumbe watu wataendelea kuomba kwa kunena. Si kila wakati wanapokutana watu Mungu ana ujumbe,wakati mwingine watu wanaomba kwa lugha tu na kumsimfu Mungu.
Na wanapofanya namna hiyo watu wanajijenga wenyewe. Zingatia kwamba Paulo katika sura hii ya kumi na nne alikua akitatua tatizo na kutaka karama hizi zinapotumika watu watilie maanani kujengwa kwa mwili mzima yaani kanisa, ndipo akawaambia yeye ahutubuye,yaani anayetoa unabii ni mkuu kuliko anenaye kwa lugha.Ni vigumu kuelezea habari hii kwa maandishi,soma sura yote hiyo utaelewa Paulo ameshauri nini kwa tatizo lililokuwepo. 3.Lugha hutasidia kuomba “Maana nikiomba kwa lugha, roho yangu huomba, lakini akili zangu hazina matunda. Imekuwaje, basi? Nitaomba kwa roho, tena nitaomba kwa akili pia; nitaimba kwa roho, tena nitaimba kwa akili pia. “(1Wakorinto 14:14-15) Maandiko haya yanaonesha kwamba lugha hutusaidia kuomba na hata kuimba kiroho.Ni rahisi kuomba kwa muda mrefu kwa njia ya kunena kuliko kuomba kwa akili.Na tukiomba kwa roho na kwa akili tutakua na muda mwingi wa kushirikiana na Mungu.Hii ndiyo maana ninasema,hii nayo ni sababu ya muhimu kwanini kila mtoto wa Mungu anene kwa lugha, kwamba yuko peke yake ,ama kwenye kusanyiko kwa utaratibu wa kusanyiko hilo,maana kila kusanyiko lina utaratibu waliojiwekea,ili mradi huo utaratibu ufuate upendo uwe kwa ajili ya kulijenga kanisa. Ninapo malizia ngoja nijibu swali hili. Lugha ni ishara kwa waaminio au kwa wasioamini? Jibu: Ni ishara kwa wote kwa mujibu wa maandiko.
NENO LA MSALABA | PAGE 05
1.Kwa wasioamini “Basi, hizi lugha ni ishara, si kwao waaminio, bali kwao wasioamini”.(1Wakorintho 14:22). 2.Kwa waamini “Na wale waliotahiriwa, walioamini, wakashangaa, watu wote waliokuja pamoja na Petro, kwa sababu Mataifa nao wamemwagiwa kipawa cha Roho Mtakatifu.
Na hiyo ndiyo iliyomjulisha Petro na wale waliotahiriwa walioamini kuwa mataifa nao wamemwagiwa kipawa cha Roho Mtakatifu,Biblia inasema maana waliwasikia wakinena kwa lugha mpya,kwa ishara hiyo Petro akasema ni nini kinachozuia hawa wasibatizwe watu waliompokea Roho kama sisi? Kwa hiyo lugha ni ishara kwa wote.
Kwa maana waliwasikia wakisema kwa lugha, na kumwadhimisha Mungu. Ndipo Petro akajibu, Ni nani awezaye kuzuia maji, hawa wasibatizwe, watu waliopokea Roho Mtakatifu vile vile kama sisi”?(Matendo 10:45-47) Mwanzoni mwa somo nilisema,kuna kunena kama karama na kuna kunena kama ishara.Na nikasema hii ishara inaonesha kwanza wewe ni mwamini,kama maandiko yanavyosema kwamba,na ishara hizi zitafuatana na waaminio.Lakini pili nilisema ni ishara inayoonesha kwamba wewe umejazwa na Roho Mtakatifu.
Mungu awabariki nyote kwa kusoma ujumbe huu. Neema na iwe kwenu. Amina. MCHUNGAJI RAPHAEL MARKO SALLU EMAIL: raphaelsallu2@gmail.com MOBILE: +255 713 830 788
NENO LA MSALABA Mafunzo ya Kanisa la Mungu