TOLEO LA TATU | NOVEMBA 2020
NEN O LA MSAL ABA
"JINSI YA KUPATA WOKOVU" NA MCHUNGAJI RAPHAEL MARKO SALLU
Mafunzo kwa kanisa la Mungu
0202 ABMEVON
UTAT AL OELOT
M S A L A B A
Neno
L A
NENO LA MSALABA
Yaliyomo 03 04
JUHUDI KATIKA MUNGU BILA MAARIFA.
HAKI IPATIKANAYO KWA IMANI INASEMA.
MAFUNZO KWA KANISA LA MUNGU
JINSI YA KUPATA WOKOVU
Nataka ni jadili juu ya somo hili,NAMNA YA KUUPATA WOKOVU. Kuna mawazo mbali mbali ya watu juu ya namna ya kuupata wokovu.Kuna ambao wanasema ili mtu apate wakovu inabidi aache dhambi,
pia kuna ambao wanasema ili mtu apate wakovu inabidi atende matendo fulani ili kuokoka,na mawazo mbali mbali mengine. Sasa tuangalie maandiko tuone Biblia inasema nini juu ya hilo.
JINSI YA KUPATA WOKOVU KUTOKUAMINI KWA WAISRAELI WARUMI 10: 1-10 Ndugu zangu, nitakayo sana moyoni mwangu, na dua yangu ni mwombayo Mungu, ni kwa ajili yao, ili waokolewe. Kwa maana nawashuhudia kwamba wana juhudi kwa ajili ya Mungu, lakini si katika maarifa. Kwa maana, wakiwa hawaijui haki ya Mungu, na wakitaka kuithibitisha haki yao wenyewe, hawakujitia chini ya haki ya Mungu. Kwa maana Kristo ni mwisho wa sheria, ili kila aaminiye ahesabiwe haki.
Kwa maana Musa aliandika juu ya haki itokayo kwa sheria, ya kuwa, Mtu afanyaye hiyo ataishi kwa hiyo. Bali ile haki ipatikanayo kwa imani yanena hivi,Usiseme moyoni mwako, Ni nani atakayepanda kwenda mbinguni? (Yaani, ni kumleta Kristo chini), Lakini yanenaje? Lile neno li karibu nawe, katika kinywa chako, na katika moyo wako; yaani, ni lile neno la imani tulihubirilo. Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.�(Warumi 10:1-10)
NENO LA MSALABA
Ukiiangalia hii mistari katika sura hii ya kumi ya kitabu cha warumi,tunapata mambo mbali
NA MCHUNGAJI RAPHAEL SALLU
mbali juu ya wokovu. Huu ndiyo uliyokuwa ujinga wao,ndiko kuliko JUHUDI KATIKA MUNGU BILA MAARIFA.
muonyesha Paulo kwamba ndugu zake hawana
Tusome tena haya maandiko tujifunze kwa
maarifa anasema,wakiwa hawaijui haki ya
undani.“Ndugu zangu, nitakayo sana moyoni
Mungu, walikuwa hawaijui haki ya Mungu,na
mwangu, na dua yangu nimwombayo Mungu, ni
kwa sababu hiyo walitaka kuithibitisha haki
kwa ajili yao, ili waokolewe. Kwa maana
yao wenyewe,hawakujitia chini ya haki ya
nawashuhudia kwamba wana juhudi kwa ajili
Mungu.
ya Mungu, lakini si katika maarifa.”(Warumi
wengi,hawataki
10:1-2).
Mungu,wanakazana
Unaona
hii kujitia
ni
shida
chini
ya
kwa
wenyewe.Sikia
ndugu,kama
kuhesabiwa
jitie
alikua
Mungu,nitakuonyesha huko mbele.
anaonyesha
hali
aliyonayo
moyoni
watu
haki
haki
Maneno haya yalisemwa na Mtume Paulo,
haki
ya
chini
ya zao
unataka ya
haki
ya
mwake,kwamba alikuwa na mzigo juu ya ndugu zake Waisraeli. Na akawa anawaombea kwa
Unajua
Mungu
kuhesabiwa
ili
waokolewe.Anasema,
tatizo
la
haki
kwa
waisraeli
,walitaka
sheria,kama
Musa
"anawashuhudia kwamba walikuwa na juhudi
alivyoandika. Unajua katika agano la kale watu
nyingi kwa ajili ya Mungu lakini si katika
walihesabiwa
maarifa."
sheria,sasa
haki waisraeli
kwa
matendo
hawakujua
ya
kwamba
katika agano jipya watu hawahesabiwi haki Yaani walikuwa hawana maarifa jinsi ya
kwa matendo ya sheria,hawakujua kuwa Yesu
kuupata wokovu.Inasikitisha sana mtu awe na
ni mwisho wa sheria.Mstari wa tano katika hii
juhudi juu ya Mungu halafu asijue namna
Warumi unasema hivi:
ambavyo Mungu anataka iwe.Jambo hili siyo tu kwa Wayahudi ambao Paulo aliwaombea, hata
“Kwa maana Musa aliandika juu ya haki
sasa kuna watu wengi sana hawana maarifa juu
itokayo kwa sheria, ya kuwa, Mtu afanyaye
ya Mungu.
hiyo ataishi kwa hiyo.”(Warumi 10:5).
Kitu gani kilipelekea hata Paulo akasema
Musa aliandika juu ya haki itokayo kwa sheria,
maneno haya? Ukiuangalia mstari wa tatu
ambayo ilimtaka mtu afanye hiyo na aishi kwa
unaona sababu ambayo imepelekea aseme
hiyo,sasa ona alichosema Bwana wetu Yesu
kwamba wana juhudi katika Mungu lakini si
juu ya haki hiyo,imeandikwa hivi:
katika maarifa,hebu tuusome: “Kwa maana, wakiwa hawaijui haki ya Mungu,
“Maana nawaambia ya kwamba, Haki yenu
na wakitaka kuithibitisha haki yao wenyewe,
isipozidi
hawakujitia chini ya haki ya Mungu.”(Warumi
Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme
10:3)
wa mbinguni.”(Mathayo 5:20).
03
hiyo
haki
ya
waandishi
na
Ni maneno yenye uzito sana, haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na mafarisayo. Haki ya waandishi na mafarisayo ni haki gani? Ni haki iliyokuwa ikipatikana kwa matendo,na sasa haki hiyo Bwana alisema haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.Tunahitaji kuwa na maarifa,tusije tukawa kama wayahudi ambao walitaka kuithibitisha haki yao wenyewe,tukifanya hivyo hatuwezi kuuingia ufalme wa mbinguni. Labda mtu mmoja anajiuliza sasa haki yangu itazidi vipi? Ngoja nikujibu hivi: Ni kwa imani. Haki yetu inazidi haki ya waandishi na mafarisayo kwa kumwamini Yesu tu. Tusome hili andiko: “Kwa maana Kristo ni mwisho wa sheria, ili kila aaminiye ahesabiwe haki.”(Warumi 10:4). Kristo ni mwisho wa sheria,Yesu ni mwisho wa kuifuata torati,unajua kwanini? Kwa sababu torati ilikuwa ni kivuli cha mambo yajayo Yesu alipokuja ikawa ni mwisho wa kivuli kwa maana Yeye ni uhalisia wenyewe.Kwa hiyo kila anaye mwamini Yesu anahesabiwa haki, imeandikwa hivi: “na kwa yeye kila amwaminiye huhesabiwa haki katika mambo yale yote asiyoweza kuhesabiwa haki kwa torati ya Musa.”(Matendo 13:39).
tena nionekane katika yeye, nisiwe na haki yangu mwenyewe ipatikanayo kwa sheria, bali ile ipatikanayo kwa imani iliyo katika Kristo, haki ile itokayo kwa Mungu, kwa imani;”(Wafilipi 3:9). Hakutaka aonekane ana haki yake mwenyewe inayopatikana kwa sheria,bali ile inayopatikana kwa imani. Haki ile itokayo kwa Mungu. Hii ndiyo haki inayozidi haki ya waandishi na mafarisayo.Haki itokayo kwa Mungu.Ambayo inapatikana kwa imani tu.Na juu ya hili Paulo alifundisha kuhusu Ibarahimu, alisema hivi: “Basi, tusemeje juu ya Ibrahimu, baba yetu kwa jinsi ya mwili? Kwa maana ikiwa Ibrahimu alihesabiwa haki kwa ajili ya matendo yake, analo la kujisifia; lakini si mbele za Mungu. Maana maandiko yasemaje? Ibrahimu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa haki.”(Warumi 4:1-3) Unaona Paulo anavyo sisitiza ? Anasema kama Ibrahimu alihesabiwa haki kwa njia ya matendo yake,analo la kujisifia lakina si mbele za Mungu Ila Ibrahimu alimwamini Mungu ikahesabiwa kwake kuwa ni haki. Ndugu tunahesabiwa haki kwa njia ya imani tu. Si kwa matendo. HAKI IPATIKANAYO KWA IMANI INASEMA.
Ndugu zangu kuhesabiwa haki ni kwa imani tu! Ni ajabu kwamba kuna mtu anasema ameokoka lakini anataka ahesabiwe haki kwa njia ya matendo yake! Ni kukosa maarifa. Paulo alijihadhari sana ili asije akataka ahesabiwe haki kwa njia ya sheria,alisema hivi:
“Bali ile haki ipatikanayo kwa imani yanena hivi, Usiseme moyoni mwako, Ni nani atakayepanda kwenda mbinguni? (Yaani, ni kumleta Kristo chini),”(Warumi 10:6).
NENO LA MSALABA | 04
Paulo anasema,ile haki ipatikayo kwa imani inasema.Inasemaje? Inasema hivi: (1) Usiseme moyoni mwako,yaani usijiulize,usiwaze kwamba Ni nani atakayepanda kwenda mbinguni? Anasema kusema hivyo,ni kumleta Kristo chini,ni kutokujua uweza wake,yaani ni kama kusema hajafufuka na kupaa. Lakini (2) Usiseme,”au, Ni nani atakayeshuka kwenda kuzimuni? (Yaani, ni kumleta Kristo juu, kutoka kwa wafu.)”(Warumi 10:7).
Haki ipatikanayo kwa imani inakukataza usiseme ni nani aliyeshuka kwenda kuzimuni anasema kusema hivyo ni sawa na kusema Kristo hakufa na kufufuka kwa ajili ya dhambi zetu.Kama una maarifa usiseme hivyo. Lakini (3) Haki ipatikanayo kwa imani inasema hivi: “Lakini yanenaje? Lile neno li karibu nawe, katika kinywa chako, na katika moyo wako; yaani, ni lile neno la imani tulihubirilo.”(Warumi 10:8). Haki itokayo kwa Mungu yasema Lile neno li karibu nawe sana! Wapi? Katika kinywa chako na katika moyo wako anasema yaani lile neno la imani tunalolihubiri liko kwenye kinywa chako na moyo wako. Si mbali mpaka wende kwa mtu, hapana ni katika kinywa chako na moyo wako, hapo hakuhitaji usafiri ili kupata haki,hapana ni katika kinywa chako na moyo wako. Anamalizia kwa kusema hivi: “Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.”(Warumi 10:9) Andiko hili linatuonyesha jinsi mtu anavyookoka,linasema,ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu utaokoka. Unaona ni namna hiyo tu ,ni kukiri na kuamini. Kukiri nini? Kukiri kwamba Yesu ni Bwana,na kuamini kuwa Mungu alimfufua katika wafu. 05
Hivyo tu,hakuna kuongeza jambo lolote ,kwa sababu wokovu ni kutokana na kazi ya Yesu pale msalabani. Si sawa kumwambia mtu anayetaka kuokoka kwamba aache dhambi, mwanadamu hawezi kuacha dhambi,anamwitaji mwokozi na ndiyo maana Yesu alikuja ulimwenguni ili atuokoe,kumwambia mtu aache dhambi ili apate wakovu,maana yake ni kumwambia ajiokoe.Sikia ndugu kazi ya wokovu aliishaifanya Yesu na akasema pale msalabani,imekwisha.kwa upande wa mtu anayetaka kuokoka. Ni kumkiri Yesu kuwa ni Bwana,na kuamini kuwa Mungu alimfufua katika wafu,basi. Mtu mmoja aliuliza hivi kwenye Biblia: “kisha akawaleta nje akasema, Bwana zangu, yanipasa nifanye nini nipate kuokoka? Wakamwambia, Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako.”(Matendo 16:30-31) Huyu alikua askari aliyeshuhudia muujiza pale gerezani akaguswa,akauliza inampasa afanye nini apate kuokoka? Akina paulo hawakumwambia aache dhambi zake wala hawakumwambia akiri dhambi zake,bali walimwamba, Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako. Hivyo ndivyo tuvyopaswa kuwaelekeza watu. “Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.”(Warumi 10:10). Ni kwa moyo na kwa kinywa.Kwa kumwamini Bwana Yesu na kumkiri tunahesabiwa haki na kupata wokovu. Mungu akubariki.Neema na iwe pamoja nawe. Amina. Mch. Raphael Marko Sallu Divine Grace Church - Kange, Tanga- Tanzania Raphaelsallu2@gmail.com +255 713 830 788
NENO LA MSALABA
Mafunzo kwa Kanisa la Mungu
Toleo la Tatu - Novemba 2020
MBUNIFU JARIDA Mch. Avitus Leonard +255 677424916 aleonard@divinegracetz.org Dar es Salaam,Tanzania
MHARIRI Andrew Caus +255 684670440 andrewsextus@gmail.com Dar es Salaam, Tanzania