TUMAINI FARAJA YA L E O | AHAD I NA U T H I B I T I SH O K AT I K A K I LA H A LI
Njia ya kuwa
SHUPAVU mambo yanapo kuwa mazito [p25]
NYIMBO HALISI toka kwa watu halisi
na jinsi walivyo pata tumaini [p7]
NJIA
maarufu ambayo
ITABADILI MAISHA YAKO [p49]
HEBU TAZAMA
HAUPO PEKEE YAKO KATIKA HII HALI [p38]
MAHALA SALAMA
MAMBO YANAPO KUWA YA KUTISHA [p33]
ZABURI 23 1
Bwana ndiye mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu. 2 Hunilaza katika malisho ya majani mabichi, kando ya maji matulivu huniongoza, 3
huifanya upya nafsi yangu.
Huniongoza katika njia za haki kwa ajili ya jina lake.
Hata kama nikipita katikati ya bonde la uvuli wa mauti, sitaogopa mabaya, 4
kwa maana wewe upo pamoja nami; fimbo yako na mkongojo wako vyanifariji.
Waandaa meza mbele yangu machoni pa adui zangu. Umenipaka mafuta kichwani pangu, kikombe changu kinafurika. 5
Hakika wema na upendo vitanifuata siku zote za maisha yangu, nami nitakaa nyumbani mwa Bwana milele. 6
KISWAHILI CONTEMPORARY VERSION Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission of Biblica, Inc.® All rights reserved worldwide. The Kiswahili Contemporary Version text may be quoted in any form (written, visual, electronic or audio), up to and inclusive of five hundred (500) verses without the express written permission of the publisher, providing the verses quoted do not amount to a complete book of the Bible nor do the verses quoted account for twenty-five percent (25%) or more of the total text of the work in which they are quoted. Permission requests that exceed the above guidelines must be directed to and approved in writing by Biblica, Inc.®, 1820 Jet Stream Drive, Colorado Springs, CO 80921, USA. Biblica.com Notice of copyright must appear on the title or copyright page as follows: Scripture quotations taken from The Holy Bible, Kiswahili Contemporary Version Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission of Biblica, Inc.® All rights reserved worldwide. When quotations from the Kiswahili Contemporary Version text are used by a local church in non-saleable media such as church bulletins, orders of service, posters, overhead transparencies, or similar materials, a complete copyright notice is not required, but the title (Kiswahili Contemporary Version) must appear at the end of each quotation.
Biblica, the International Bible Society, provides God’s Word to people through Bible translation & Bible publishing, and Bible engagement in Africa, Asia Pacific, Europe, Latin America, Middle East, North America, and South Asia. Through its worldwide reach, Biblica engages people with God’s Word so that their lives are transformed through a relationship with Jesus Christ.
P.O. Box 3619, Guelph Ontario, Canada N1H 7A2 Teléfono: 1 (888) 482-4253 | Fax: (519) 767-1913
hopemagazine@sharewordglobal.com www.sharewordglobal.com
Mkurugezi wa ubunifu Mchangiaji Mchoraji Picha
Kelvin Warkentin Paul Dunk Janette Drost Janette Drost Dennis Drost Scott deVries Julia Maier iStockPhoto
Kuhusu ShareWord Global Shauku yetu sisi hapa ShareWord Global, ni kushiriki injili ya Yesu Kristo na watu katika ulimwengu nzima na kuwapa fursa ya kusoma na kuskiza neno lake Mungu takatifu wao wenyewe. Tumekuwa tukifanya hivi kwa zaidi ya karne moja, kuanzia Canada na kuenea hadi dunia nzima. Tunafanya kazi kwa karibu na makanisa na huduma zingine husika ili kuhakikisha mikakati yetu imefikiwa. Kwa kuwapa wakristo mafunzo na nakala za neno la Mungu, tunaamini ya kuwa watajihisi kuwa mikono na miguu yake yesu katika jamii zao. Maandiko tunayopeana, yameundwa kwa njia ambayo humshirikisha msomaji kimaisha. Ikiwa ni Injili ya Yohana, Jarida la maandiko, Agano Jipya, Biblia nzima, nakala ya digitali ya kuskizwa—zote ni za kusambaza habari hiyo kwa msomaji kwa njia na lugha ya moyo wake. Jiunge nasi katika kuwakaribisha watu ulimwengu mzima kwake Yesu Kristo kwa kuwapa nakala ya neno la mungu mikononi mwao. Tutembelee kwenye tovuti yetu ambayo ni www.sharewordglobal.com ili kujifunza jinsi kushiriki injili katika jamii yako.
Tumaini Katika Dhoruba Kusubiri sijambo la furaha. Kama unasubiri jina lako kuitwa, kama unasubiri hundi yako muhimu ikufikie au kama uko kwa mlolongo kwenye duka – ni jambo ambalo wachache wetu hufurahia kufanya. Inahitaji kiwango kikubwa cha uvumilivu, mara kwa mara mioyo yetu hufanya kelele ili kupata jawabu la haraka. Pengine umepitia machungu na kupoteza masaa mengi hospitalini kwenye chumba cha kusubiri. Ulifanya uwezavyo hata kujisumbua ili kuhakikisha kusubiri hakutasababisha uchungu mwingi, lakini hakuna lililoonekana la msaada. Runinga iliyowekwa pembeni kuonyesha habari ilionekana kukosa umuhimu kwa kipindi hicho. Magazeti yaliyowekwa juu ya meza yaliyojaa maadishi muhimu na matangazo hayakuwa na maana kwako. Hata katika kupitapita, na kuzunguka zunguka hapa na pale hosipitalini hakukuweza kutuliza usimbufu uliokuwa moyoni mwako. Kusubiri ni kugumu sana. Uthabiti wa aina yeyote unaofikiri kuwa nao maishani mwako umetoweka mbali na sasa unalazimika kutupa mikono yako. Unaulizwa kuweka Imani yako kwa mtu fulani atatue migogoro katika maisha yako. Unaulizwa kutulia hapo na uwe na subrakwa kweli ni hali ambayo haina majibu. Katika hali hizo unapitia maishani mwako yaani dhiki, unaweza kutegemea sana katika
aina hizi za aya zipatikanazo katika gazeti hili. Haijalishi safari yako ya kiroho imekuaje ama unachokiamini kuhusu Mungu, ama kuhusu Bibilia, kuna kitu katika aya hizi kutoka kwa vitabu vya kale vya Zaburi hivyo ambavyio vitasababisha moyo wako kuwa na utulivu nyakati hizo za migogoro- na utazame zaidi ya uwezo wako wa kupata majibu. Mengi ya Mashairi haya yaliandikwa na watu ambao maisha yao yalijawa na dhiki mbalimbali ambazo hata zaweza kuwa zilikuwa mbaya kiasi kuwa haujawahi kupitia. Maisha yao yalikuwa na migogoro mingi na walihitaji msaada kweli kweli. Hata hivyio wakati mwingine katikati ya dhoruba kali, ushahiri ulioko katika shairi hivzi umejazwa na tumaini. Unaweza kupata tumaini hilo, katika kipindi hiki cha kusubiri. Weka tumaini lako kwa Mungu. Uwe na tumaini ukijua kwamba anaweza kukutoa gizani ulimo. Uwe na tumaini na uamini kwamba Mungu anampango kwa ajili yako - hata katikati ya mambo mengi yaliyovamia maisha yako. Tumaini hili la kiroho laweza kukutoa katika uchungu ulio nao. Shikamana na aya za gazeti hili, na uamini kwamba muumba wako Mungu anathibiti kila hali unayopitia. Huko peke yako. Kumbuka hivyo unaposubiri. Unapo omba. Unapo endelea kutumaini.
BWANA NI MCHUNGAJI W NI KIMBILIO L NGAO YANGU WA KUNIOKOA KUNILINDA NGUVU YANGU
ZABURI
WANGU: LANGU YA A
U
Mambo kuyahusu Kitabu Hiki Ikiwa umewahi kutaka kuwa mwaminifu na Mungu na umwambie kile ambacho unahisi maishani mwako,utapenda hizi Zaburi. Ni maelezo ya kimoyo ya tumaini katikakati ya machungu. Zinawahusu watu halisi walio na shida halisi ambao wanamtegemea Mungu wakati ambapo dunia nzima yaonekana kuwatoroka. Ni maelezo ya kishairi ya watu ambao wamemwamini Mungu kikamilifu wakati ambapo mioyo yao imejazwa na machungu. Kitabu cha Zaburi ni kitabu cha kale cha nyimbo kilichoandikwa kwa muda wa miaka elfu moja na watu kadhaa, akiwemo mfalme Daudi wa Israeli. Mashairi yalioandikwa kwa njia ya muziki yalikaririwa na kukusanywa kwa miaka hiyo hadi yalipoandikwa na kuwekwa kwa vikundi ambavyo twaviona leo. Zaburi ni hisia za kibinafsi, hisia za undani wa kiubinadamu. Utaweza kuona kwamba zinakuhusu wewe, na unaposoma baadhi yake,utahisi kana kwamba mwandishi anelezea kikamilifu unachohisi. Twatumaini kwamba unapozisoma utapata tumaini upya na mawazo mapya
kuhusu jukumu la Mungu maishani mwako. Anataka kukuongoza, kukupa makao, kukupa nguvu, na zaidi ya yote kukupenda. Zaidi ya yote, Zaburi nyingi ni ukumbusho wa ahadi ambazo Mungu amezitoa. Kuna tulizo katika kujua kwamba, tunapofuata uongozi wake maishani mwetu, atatuonyesha njia. Jinsi inavyosema katika Zaburi 119 msitari wa 114 (p37), “neno lako ni chanzo cha tumaini.’’
Yaliyomo katika jarida hili ni sehemu ndogo tu ya Zaburi 150 zilizo katika Bibilia. Tumekuchagulia mistari ambayo inalingana na mada ya kukupa tumaini katika hali ngumu. Maudhui mengine ambayo utagundua katika kitabu hiki ni nyakati za kuomboleza, sifa, hekima, shukrani na ibada. Kura zifuatazo zina jumbe zilizochaguliwa kutoka kwa Maandiko ya Agano la Kale na Agano Jipya. Bibilia kamili yaweza kupatikana bure ukipakua toka kwa mtandao kupitia kwa simu yako ya Android, iOS na kifaa cha Blackberry. Pakua nakala ya bure ya Newlife app kwa kifaa chako kwenye mtandao hapo www.newlife.bible.
8
ZABURI
TUMAINI
ZABURI 3 3
Lakini wewe, Ee Bwana, ni ngao pande zote;
umeniwekea utukufu na kuinua kichwa changu. 4
Ninamlilia Bwana kwa sauti kuu, naye ananijibu kutoka katika mlima wake mtakatifu.
ZABURI
1
TUMAINI
Ee Bwana, tegea sikio maneno yangu,
uangalie kupiga kite kwangu. LSikiliza kilio changu ili unisaidie, Mfalme wangu na Mungu wangu, kwa maana kwako ninaomba. 3 Asubuhi, unasikia sauti yangu, Ee Bwana; asubuhi naleta haja zangu mbele zako, na kusubiri kwa matumaini. 2
11
Lakini wote wakimbiliao kwako na wafurahi, waimbe kwa shangwe daima. Ueneze ulinzi wako juu yao, ili wale wapendao jina lako wapate kukushangilia. 12 Kwa hakika, Ee Bwana, unawabariki wenye haki, unawazunguka kwa wema wako kama ngao.
ZABURI 5
9
10
TUMAINI
ZABURI
ZABURI 6
BWANA AMESIKIA KILIO CHANGU KWA HURUMA, 9
Bwana amekubali sala yangu.
ZABURI 8 3
Nikiziangalia mbingu zako, kazi ya vidole vyako, mwezi na nyota, ulizoziratibisha, 4
9
mwanadamu ni kitu gani hata umkumbuke, binadamu hata umwangalie? Ee Bwana, Bwana wetu, tazama jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote!
7 2
9
NITAFURAHI NA KUSHANGILIA KATIKA WEWE, nitaliimbia sifa jina lako, Ewe Uliye Juu Sana.
Bwana ni kimbilio la watu wanaoonewa, ni ngome imara wakati wa shida. 10
Wote wanaolijua jina lako watakutumaini wewe, kwa maana wewe Bwana, hujawaacha kamwe wakutafutao.
ZABURI 9
8
14
TUMAINI
ZABURI
1
Ee Mungu, uniweke salama, kwa maana kwako nimekimbilia.
Nimemweka Bwana mbele yangu daima. Kwa kuwa yupo mkono wangu wa kuume, sitatikiswa. 8
9
Kwa hiyo moyo wangu una furaha na ulimi wangu unashangilia; pia mwili wangu utapumzika salama,
ZABURI 16
ZABURI
2
TUMAINI
Bwana ni mwamba wangu, ngome yangu na mwokozi wangu, Mungu wangu ni mwamba, ambaye kwake ninakimbilia.
Yeye ni ngao yangu na pembe ya wokovu wangu, ngome yangu. 30
Kuhusu Mungu, njia yake ni kamilifu, neno la Bwana ni kamili. Yeye ni ngao kwa wote wanaokimbilia kwake. 31 Kwa maana ni nani aliye Mungu zaidi ya Bwana? Ni nani aliye Mwamba isipokuwa Mungu wetu?
ZABURI 18
8
Maagizo ya Bwana ni kamili,
nayo hufurahisha moyo.
Amri za Bwana huangaza, zatia nuru machoni.
ZABURI 19
15
16
ZABURI
TUMAINI
Kwa maana hakupuuza wala kudharau mateso ya aliyeonewa; 24
hakumficha uso wake bali alisikiliza kilio chake ili amsaidie.
ZABURI 22 ZABURI 27
Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu, nimwogope nani? 1
Bwana ni ngome ya uzima wangu, nimhofu nani? 14 Umngojee Bwana, uwe hodari na mwenye moyo mkuu, nawe, umngojee Bwana.
ZABURI 28
Bwana ni nguvu zangu na ngao yangu, moyo wangu umemtumaini yeye, nami nimesaidiwa. 7
Moyo wangu unarukaruka kwa furaha nami nitamshukuru kwa wimbo.
ZABURI 29 Mpeni Bwana Enyi mashujaa, mpeni Bwana utukufu na nguvu. 2 Mpeni Bwana utukufu unaostahili jina lake; mwabuduni Bwana katika uzuri wa utakatifu wake. 1
Sauti ya Bwana iko juu ya maji; Mungu wa utukufu hupiga radi, Bwana hupiga radi juu ya maji makuu. 4 Sauti ya Bwana ina nguvu; sauti ya Bwana ni tukufu. 5 Sauti ya Bwana huvunja mierezi; Bwana huvunja vipande vipande mierezi ya Lebanoni. 6 Hufanya Lebanoni irukaruke kama ndama, Sirioni urukaruke kama mwana nyati. 7 Sauti ya Bwana hupiga kwa miali ya umeme wa radi. 8 Sauti ya Bwana hutikisa jangwa; Bwana hutikisa Jangwa la Kadeshi. 9 Sauti ya Bwana huzalisha ayala, na huuacha msitu wazi. Hekaluni mwake wote wasema, “Utukufu!” 3
Bwana huketi akiwa ametawazwa juu ya gharika; Bwana ametawazwa kuwa Mfalme milele. 11 Bwana huwapa watu wake nguvu; Bwana huwabariki watu wake kwa kuwapa amani. 10
ZABURI 30 Uligeuza maombolezo yangu kuwa kucheza, ulinivua nguo za gunia ukanivika shangwe,
11
12
tili moyo wangu uweze kukusifu na usikae kimya. Ee Bwana Mungu wangu, nitakushukuru milele.
ZABURI 31 24
Iweni hodari na mjipe moyo,
ninyi nyote mnaomtumaini Bwana.
ZABURI 33 Sisi tunamngojea Bwana kwa matumaini, yeye ni msaada wetu na ngao yetu. 21 Katika yeye mioyo yetu hushangilia, kwa maana tunalitumainia jina lake takatifu. 20
22
Upendo wako usio na mwisho ukae juu yetu, Ee Bwana, kama vile tunavyoweka tumaini letu kwako.
ZABURI 34 Nitamtukuza Bwana nyakati zote, sifa zake zitakuwa midomoni mwangu siku zote. 2 Nafsi yangu itajisifu katika Bwana walioonewa wasikie na wafurahi. 3 Mtukuzeni Bwana pamoja nami, naam, na tulitukuze jina lake pamoja. 4 Nilimtafuta Bwana naye akanijibu, akaniokoa kwenye hofu zangu zote. 5 Wale wamtazamao hutiwa nuru, nyuso zao hazifunikwi na aibu kamwe. 6 Maskini huyu alimwita Bwana akamsikia, akamwokoa katika taabu zake zote. 7 Malaika wa Bwana hufanya kituo akiwazunguka wale wamchao, naye huwaokoa. 1
Onjeni mwone kwamba Bwana ni mwema, heri mtu yule anayemkimbilia. 9 Mcheni Bwana enyi watakatifu wake, kwa maana wale wamchao hawapungukiwi na kitu cho chote. 10 Wana simba wenye nguvu hutindikiwa na kuona njaa, bali wale wamtafutao Bwana hawatakosa kitu cho chote kilicho chema. 11 Njoni, watoto wangu, mnisikilize, nitawafundisha kumcha Bwana. 12 Ye yote kati yenu anayependa maisha na kutamani kuziona siku nyingi njema, 13 auzuie ulimi wake na mabaya na midomo yake kutokana na kusema uongo. 14 Aache uovu na atende mema, aitafute amani na kuifuatia. 8
4
Macho ya Bwana yako kwa wenye haki na masikio yake yako makini kusikia kilio chao; 16 uso wa Bwana uko kinyume na watenda mabaya, kufuta kumbukumbu lao duniani. 17 Wenye haki hulia, naye Bwana huwasikia, huwaokoa katika taabu zao zote. 18 Bwana yu karibu nao waliovunjika moyo na huwaokoa waliopondeka roho. 19 Mwenye haki ana mateso mengi, lakini Bwana humwokoa nayo yote, 20 huhifadhi mifupa yake yote, hata mmoja hautavunjika. 21 Ubaya utamwua mtu mwovu, adui za mwenye haki watahukumiwa. 22 Bwana huwakomboa watumishi wake, wale wanaomkimbilia yeye hawatahukumiwa hata mmoja wao. 15
NILIMTAFUTA BWANA
naye akanijibu, akaniokoa kwenye hofu zangu zote. ZAMURI 34
20
TUMAINI
ZABURI
7 UPENDO WAKO, EE BWANA, UNAFIKA HADI KATIKA MBINGU, 5
6
uaminifu wako hadi kwenye anga. Haki yako ni kama milima mikubwa, hukumu zako ni kama kilindi kirefu sana.
8
ZABURI
7
TUMAINI
21
Ee Bwana, wewe huwahifadhi mwanadamu na mnyama. Upendo wako usiokoma ni wa thamani mno!
Wale wa daraja ya juu na ya chini miongoni mwa wanadamu hupata kimbilio katika uvuli wa mbawa zako. ZABURI 36
22
YOHANA
TUMAINI
7 Mtumaini Bwana na utende yaliyo mema, ukae katika nchi ukafurahie malisho salama. 4 Jifurahishe katika Bwana naye atakupa haja za moyo wako. 3
Mkabidhi Bwana njia yako, mtumaini yeye naye atatenda hili: 6 yeye atafanya haki yako ing’ae kama apambazuko, hukumu kama jua la adhuhuri. 5
8
YOHANA
TUMAINI
TULIA MBELE ZA BWANA NA UMNGOJEE KWA UVUMILIVU; 7
usisumbuke watu wanapofanikiwa katika njia zao, wanapotekeleza mipango yao miovu.
Wokovu wa wenye haki hutoka kwa Bwana, yeye ni ngome yao wakati wa shida. 40 Bwana huwasaidia na kuwaokoa, huwaokoa kutoka kwa waovu na kuwahifadhi, kwa maana wanamkimbilia. 39
ZABURI 37
23
24
TUMAINI
ZABURI
Nilimngoja Bwana kwa saburi, naye akaniinamia akasikia kilio changu. 2 Akanipandisha kutoka shimo la uharibifu, kutoka katika matope na utelezi; akaiweka miguu yangu juu ya mwamba na kunipa mahali imara pa kusimama. 1
Akaweka wimbo mpya kinywani mwangu, 3
wimbo wa sifa kwa Mungu wetu. Wengi wataona na kuogopa na kuweka tumaini lao kwa Bwana.
ZABURI 40
ZABURI
ZABURI 42 Kama vile paa aoneavyo shauku vijito vya maji, ndivyo nafsi yangu ikuoneavyo shauku, Ee Mungu. 2 Nafsi yangu inamwonea Mungu kiu, Mungu aliye hai. Ni lini nitaweza kwenda kukutana na Mungu? 3 Machozi yangu yamekuwa chakula changu mchana na usiku, huku watu wakiniambia mchana kutwa, “Yuko wapi Mungu wako?” 4 Vitu hivi ninavikumbuka ninapoimimina nafsi yangu: Jinsi nilivyokuwa nikienda na umati wa watu, nikiongoza maandamano kuelekea kwenye nyumba ya Mungu, kwa kelele za shangwe na za shukrani katikati ya umati wa watu wanaoadhimisha sikukuu. 5 Ee nafsi yangu kwa nini unasononeka? Kwa nini unafadhaika hivyo ndani yangu? Weka tumaini lako kwa Mungu, kwa sababu bado nitamsifu, aliye afya ya uso wangu Mwokozi wangu na 1
TUMAINI
Mungu wangu. Nafsi yangu inasononeka ndani yangu; kwa hiyo nitakukumbuka kutoka nchi ya Yordani, katika vilele vya Hermoni, kutoka Mlima Mizari. 7 Kilindi huita kilindi, katika ngurumo za maporomoko ya maji yako; mawimbi yako yote pamoja na viwimbi vimepita juu yangu. 8 Mchana Bwana huelekeza upendo wake, usiku wimbo wake uko nami: maombi kwa Mungu wa uzima wangu. 9 Ninamwambia Mungu Mwamba wangu, “Kwa nini umenisahau? Kwa nini niendelee kuomboleza, nikiwa nimeonewa na adui?” 10 Mifupa yangu inateseka kwa maumivu makali adui zangu wanaponidhihaki, wakiniambia mchana kutwa, “Yuko wapi Mungu wako?” 11 Ee nafsi yangu kwa nini unasononeka? Kwa nini unafadhaika hivyo ndani yangu? Weka tumaini lako kwa Mungu, kwa sababu bado nitamsifu, aliye afya ya uso wangu, Mwokozi wangu na Mungu wangu. 6
ZABURI 46 Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. 1
2
Kwa hiyo hatutaogopa, hata kama dunia ikiondolewa nayo milima ikiangukia moyoni wa bahari. 3 Hata kama maji yake yatanguruma na kuumuka, milima nayo ikitetemeka kwa mawimbi yake.
25
ZABURI
TUMAINI
ZABURI 56 Wakati ninapoogopa, nitakutumaini wewe. 4 Katika Mungu, ambaye neno lake ninalisifu, katika Mungu ninatumaini; sitaogopa. Mwanadamu apatikanaye na kufa, atanitenda nini? 3
8
Andika maombolezo yangu,
orodhesha machozi yangu katika gombo lako: je, haya hayapo katika kumbukumbu zako?
26
IRUB62AZ
7 Ee nafsi yangu, upumzike, kwa Mungu peke yake, tumaini langu latoka kwake. 5
Yeye peke yake ndiye mwamba wangu na wokovu wangu; ndiye ngome yangu, sitatikisika. 7 Wokovu wangu na heshima yangu viko kwa Mungu, ndiye mwamba wangu wenye nguvu na kimbilio langu. 6
8
Enyi watu, mtumainini yeye, wakati wote, mmiminieni yeye mioyo yenu, kwa kuwa Mungu ni kimbilio letu.
8
28
TUMAINI
1
ZABURI
Mungu uturehemu na kutubariki, na kutuangazia nuru za uso wako,
Mili njia zako zijulikane duniani, wokovu wako katikati ya mataifa yote. 3 Ee Mungu, mataifa na wakusifu, mataifa yote na wakusifu. 4 Mataifa yote na wafurahi na kuimba kwa shangwe, kwa kuwa unatawala watu kwa haki na kuongoza mataifa ya dunia. 2
Ee Mungu, mataifa na wakusifu, mataifa yote na wakusifu. 6 Ndipo nchi itatoa mazao yake, naye Mungu, Mungu wetu, atatubariki. 7 Mungu atatubariki na miisho yote ya dunia itamcha yeye. 5
ZABURI 67 ZABURI 68 Mwimbieni Mungu, liimbieni sifa jina lake, mwinueni juu yeye aendeshwaye juu ya mawingu, jina lake ni Bwana, furahini mbele zake. 4
Baba wa yatima, mtetezi wa wajane, ni Mungu katika makao yake matakatifu. 5
Sifa apewe Bwana, Mungu Mwokozi wetu, ambaye siku kwa siku hutuchukulia mizigo yetu. 19
Mungu wetu ni Mungu aokoaye, Bwana Mwenyezi hutuokoa na kifo. 20
EE MUNGU, TUNAKUSHUKURU, 1
tunakushukuru wewe, kwa kuwa jina lako li karibu; watu husimulia matendo yako ya ajabu. ZABURI 75
30
TUMAINI
ZABURI
ZABURI 84
Siku moja katika nyua zako ni bora kuliko siku elfu mahali pengine; 10
afadhali ningekuwa bawabu katika nyumba ya Mungu wangu kuliko kukaa katika mahema ya waovu. 11 Kwa kuwa Bwana ni jua na ngao, Bwana hutoa wema na heshima; hakuna kitu chema anachowanyima wale ambao hawana hatia. 12 Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote, heri ni mtu yule anayekutumaini wewe.
ZABURI 85 Nitasikiliza lile atakalosema Mungu aliye Bwana; anaahidi amani kwa watu wake, watakatifu wake, lakini nao wasirudie upumbavu. 9 Hakika wokovu wake uko karibu na wale wamchao, ili utukufu wake udumu katika nchi yetu. 10 Upendo na uaminifu hukutana pamoja, haki na amani hubusiana. 8
Uaminifu huchipua kutoka katika nchi, haki hutazama chini kutoka mbinguni.
11
Naam, hakika Bwana atatoa kilicho chema, nchi yetu itazaa mavuno yake. 13 Haki itatangulia mbele yake na kutengeneza njia kwa ajili ya hatua zake. 12
1
Ee Bwana, sikia na unijibu, kwa maana mimi ni maskini na mhitaji.
Linda maisha yangu, kwa maana nimejiweka kwako, wewe ni Mungu wangu, mwokoe mtumishi wako anayekutumaini. 3 Ee Bwana, nihurumie mimi, kwa maana ninakuita mchana kutwa. 4 Mpe mtumishi wako furaha, kwa kuwa kwako wewe, Ee Bwana, ninainua nafsi yangu. 2
5
Ee Bwana,wewe ni mwema na mwenye kusamehe, umejaa upendo kwa wote wakuitao.
6
Ee Bwana, sikia maombi yangu, sikiliza kilio changu unihurumie.
ZABURI 86
Katika siku ya shida yangu nitakuita, kwa maana wewe utanijibu. 8 Ee Bwana, katikati ya miungu hakuna kama wewe, hakuna matendo ya kulinganishwa na yako. 9 Ee Bwana, mataifa yote uliyoyafanya yatakuja na kuabudu mbele zako; wataliletea utukufu jina lako. 10 Kwa maana wewe ni mkuu na unafanya mambo ya ajabu; wewe peke yako ndiwe Mungu. 11 Ee Bwana, nifundishe njia yako, nami nitakwenda katika kweli yako; nipe moyo usiositasita, ili niweze kulicha jina lako. 12 Ee Bwana, wangu, nitakusifu kwa moyo wote; nitaliadhimisha jina lako milele. 13 Kwa maana upendo wako ni mkuu kwangu; umeniokoa kutoka 7
14
15
kwenye vilindi vya kaburi. Ee Mungu, wenye majivuno wananishambulia; kundi la watu wakatili linatafuta uhai wangu: watu wasiokuheshimu wewe. Lakini wewe, Ee Bwana, ni Mungu wa huruma na neema, si mwepesi wa hasira, bali ni mwingi wa upendo na uaminifu.
Nigeukie na unihurumie; mpe mtumishi wako nguvu zako, mwokoe mwana wa mtumishi wako wa kike. 17 Nipe ishara ya wema wako, ili adui zangu waione nao waaibishwe, kwa kuwa wewe, Ee Bwana, umenisaidia na kunifariji. 16
1
Nitaimba juu ya upendo mkuu wa Bwana milele; kwa kinywa changu nitajulisha uaminifu wako ujulikane kwa vizazi vyote. 2 Nitatangaza kuwa upendo wako unasimama imara milele na uaminifu wako umeuthibitisha mbinguni. 11
12
Mbingu ni zako, nayo nchi pia ni yako, uliuwekea ulimwengu msingi pamoja na vyote vilivyomo.
Uliumba kaskazini na kusini; Tabori na Hermoni wanaliimbia jina lako kwa furaha. 13 Mkono wako umejaa uwezo; mkono wako una nguvu, mkono wako wa kuume umetukuzwa.
14
15
Haki na hukumu ndio msingi wa kiti chako cha enzi; upendo na uaminifu vinakutangulia.
Heri ni wale ambao wamejifunza kukusifu kwa shangwe, wanaotembea katika mwanga wa uwepo wako, Ee Bwana. 16 Wanashangilia katika jina lako mchana kutwa, wanafurahi katika haki yako. 17 Kwa kuwa wewe ni utukufu na nguvu yao, kwa wema wako unatukuza pembe yetu. 18 Naam, ngao yetu ni mali ya Bwana, aliye Mtakatifu Pekee wa Israeli ni mfalme wetu.
Yeye akaaye mahali pa salama pake Yeye Aliye Juu Sana, atadumu katika uvuli wake Mwenyezi. 1
2 Nitasema kuhusu Bwana, “Yeye
ndiye kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu, ambaye ninamtumaini.” 3 Hakika yeye ataniokoa na mtego wa mwindaji na maradhi ya kuambukiza ya kuua. 4 Atakufunika kwa manyoya yake, chini ya mbawa zake utapata kimbilio, uaminifu wake utakuwa ngao na kinga yako. 5 Hutaogopa vitisho vya usiku, wala mshale urukao mchana, 6 wala maradhi ya kuambukiza yanayonyemelea gizani, wala tauni iharibuyo adhuhuri. 7 Ijapo watu elfu wataangukia kando yako, kumi elfu mkono wako wa kuume, lakini haitakukaribia wewe. 8 Utatazama tu kwa macho yako na kuona adhabu ya waovu. 9 Kama ukimfanya Aliye Juu Sana kuwa makao yako: naam, Bwana ambaye ni kimbilio langu; 10 basi hakuna madhara yatakayokupata wewe, wala maafa hayataikaribia hema yako. 11 Kwa kuwa atawaagiza malaika zake kwa ajili yako, wakulinde katika njia zako zote. 14 Bwana asema, “Kwa kuwa ananipenda nitamwokoa; nitamlinda kwa kuwa amelikubali Jina langu. 15 Ataniita, nami nitamjibu; nitakuwa pamoja naye katika taabu, nitamwokoa na kumheshimu. 16 Kwa siku nyingi nitamshibisha na kumwonyesha wokovu wangu.”
34
ZABURI
TUMAINI
ZABURI 103
7
Bwana ni mwenye huruma na rehema, si mwepesi wa hasira, amejaa upendo. 9 Yeye hatalaumu siku zote, wala haweki hasira yake milele, 10 yeye hatutendei kulingana na dhambi zetu wala hatupatilizi kwa kadiri ya maovu yetu. 11 Kama vile mbingu zilivyo juu sana juu ya dunia, ndivyo wema wake ulivyo mwingi kwa wanaomcha; 8
kama mashariki ilivyo mbali na magharibi, ndivyo Mungu alivyoziweka dhambi zetu mbali nasi. 12
Kama baba alivyo na huruma kwa watoto wake, ndivyo Bwana anavyowahurumia wale wanaomcha; 13
8
ZABURI
TUMAINI
ZABURI 105 Mshukuruni Bwana, liitieni jina lake, wajulisheni mataifa yale aliyoyatenda. 1
Mwimbieni yeye, mwimbieni yeye sifa, waambieni matendo yake yote ya ajabu.. 2
Utukufu kwa jina lake takatifu, mioyo ya wale wamtafutao Bwana na ifurahi. 3
4
Mtafuteni Bwana na nguvu zake, utafuteni uso wake siku zote.
35
36
ZABURI
TUMAINI
Kwa maana upendo wako ni mkuu, juu kuliko mbingu, uaminifu wako hufika mpaka angani. 5 Ee Mungu, utukuzwe, juu ya mbingu, utukufu wako na uwe duniani pote. 4
Utuokoe na kutusaidia kwa mkono wako wa kuume, ili wale uwapendao wapate kuokolewa. 6
ZABURI 108 Msifuni Bwana, enyi mataifa yote; mtukuzeni yeye, enyi watu wote. 1
Kwa kuwa upendo wake kwetu ni mkuu, 2
uaminifu wa Bwana unadumu milele. Msifuni Bwana.
ZABURI 117
ZABURI
TUMAINI
ZABURI 118 5
Wakati wa maumivu yangu makuu nilimlilia Bwana,
NAYE AKANIJIBU KWA KUNIWEKA HURU.
28
114
ZABURI 119
Nafsi yangu imechakazwa kwa huzuni, uniimarishe sawasawa na neno lako. 105 Neno lako ni taa ya miguu yangu na mwanga katika njia yangu.
Wewe ni kimbilio langu na ngao yangu,
NIMEWEKA TUMAINI LANGU KATIKA NENO LAKO.
37
38
7 ZABURI
TUMAINI
1
3
Nayainua macho yangu nitazame vilima, msaada wangu utatoka wapi? 2 Msaada wangu hutoka kwa Bwana, Muumba wa mbingu na dunia.
HATAUACHA MGUU WAKO UTELEZE, yeye akulindaye hatasinzia,
8
ZABURI
hakika, yeye alindaye Israeli hatasinzia wala hatalala usingizi. 5 Bwana anakulinda, Bwana ni uvuli wako mkono wako wa kuume, 6 jua halitakudhuru mchana, wala mwezi wakati wa usiku. 4
7
Bwana atakukinga na madhara yote, atayalinda maisha yako, 8 Bwana atakulinda unapoingia na unapotoka, tangu sasa na hata milele.
TUMAINI
39
40
TUMAINI
ZABURI 125
1
ZABURI
Wale wamtumainio Bwana ni kama mlima Sayuni, ambao hauwezi kutikisika wadumu milele.
Kama milima inavyozunguka Yerusalemu, ndivyo Bwana anavyowazunguka watu wake sasa na hata milele. 3 Fimbo ya waovu haitadumu juu ya nchi waliopewa wenye haki, ili kwamba wenye haki wasije wakatumia mikono yao kutenda ubaya. 4 Ee Bwana, watendee mema walio wema, wale walio wanyofu wa moyo. 5 Bali wale wanaogeukia njia zilizopotoka, Bwana atawafukuza pamoja na watenda mabaya. Amani iwe juu ya Israeli. 2
7 BWANA ATATIMIZA KUSUDI LAKE KWANGU, EE BWANA, UPENDO WAKO 8
wadumu milele: usiziache kazi za mikono yako.
38 1
8
ZABURI 13 Umbile langu halikufichika kwako, nilipoumbwa mahali pa siri. Nilipoungwa pamoja kwa ustadi katika vilindi vya nchi, 16 macho yako yaliniona kabla mwili wangu haujakamilika. Siku zangu zote ulizonipangia ziliandikwa katika kitabu chako kabla haijakuwapo hata moja. 15
17
TAZAMA JINSI GANI YALIVYO
ya thamani mawazo yako kwangu, Ee Mungu! Jinsi gani jumla yake ilivyo kubwa! Kama ningezihesabu, zingekuwa nyingi kuliko mchanga. Niamkapo, bado niko pamoja nawe. 18
ZABURI 142 Tazama kuume kwangu na uone, hakuna hata mmoja anayejihusisha nami. Sina kimbilio, hakuna anayejali maisha yangu. 4
EE BWANA, NAKULILIA WEWE, 5
nasema, “Wewe ni kimbilio langu, fungu langu katika nchi ya walio hai.”
8
TBWANA NI MWENYE NEEMA NA MWINGI WA HURUMA, si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa upendo.
Bwana ni mwema kwa wote, ana huruma kwa vyote alivyovifanya. Ee Bwana, vyote ulivyovifanya vitakusifu, watakatifu wako watakutukuza. 11 Watasimulia utukufu wa ufalme wako na kusema juu ya ukuu wako, 12 ili watu wote wajue matendo yako makuu na utukufu wa fahari ya ufalme wako. 13 Ufalme wako ni ufalme wa milele, mamlaka yako hudumu vizazi vyote. Bwana ni mwaminifu kwa ahadi zake zote na mwenye upendo kwa vyote alivyovifanya. 9
10
ZABURI 145 3
HANAWAPONYA WALIOVUNJIKA MIOYO
ana kuvifunga vidonda vyao. Huzihesabu nyota na huipa kila moja jina lake. Bwana wetu ni mkuu na mwenye uwezo mwingi, ufahamu wake hauna kikomo. 4
5
YOHANA
MA NGU JIA
Mambo kuyahusu kitabu hiki Umeshawai jiuliza kwamba huyu Yesu ni nani? Ushaskia watu wakimzungumzia ama labda kuimba kumhusu wakati wa krismasi au pasaka, ama pengine kuziona picha zake kwenye michoro. Vitabu vya historia hutuondolea shaka na vinadhibitisha ya kwamba kwa kweli aliishi na kupumua na akaacha alama kwenye ratba ya dunia. Lakini kwa kweli yeye ni nani?
Injili ya
NA ILELE
Kwenye hili jarida, tumehusisha hadithi yake Yesu kama vile ilivyo rekodiwa na mmoja ambaye aliishi na kutembea naye miaka elfu mbili iliyopita. Yohana alikuzwa katika jamii ya wavuvi katika mji mdogo, lakini mwishowe akawa mfuasi wa karibu wa Yesu. Alikaa naye katika mema na mabaya hadi mwisho,na akapata ufahamu kikamilifu wa mambo ya ajabu ambay Yesu Kristo alifanya kwa huo muda mdogo aliuoishi. Kwa wakati mwingine baadae, yohana aliketi chini na kuanza kuandika vitu vya ajabu alivyo kuwa akishuhudia. Lengo lake haswa lilikuwa haswa ni kuimiza ya kwamba kwa kweli yesu alikuwa mwana wa Mungu.Alitaka
kuwahakikishia wasomaji wake ya kuwa yeyote atakaye mwaamini yesu atapata uzima wa milele Hayo ni malengo makubwa na mawazo makubwa kuyaweka kichwani mwako. Lakini unaposoma habari za kwanza za maisha ya Yesu, hadithi hizo zitakugusa. Yesu wa kihistoria utakayekumbana naye ni tofauti na mtu mwingine yeyote ambaye vitabu vimemewahi kuandikwa kumhusu. Alishirikiana na watu kwa njia spesheli na alisema maneno makuu kujihusu yeye mwenyewe-maneno ambayo hutulazimu kufanya uamuzi kumhusu Yesu Kristo. Ikiwa haujawai kusoma hadithi hii yake Yesu Kristo, isome hadi mwisho sasa. Ni njia ya ajabu ambayo itabadili maisha yako
Yohana ni kitabu kimoja katika Agano Jipya, ambayo ni mkusanyiko wa maandiko yaliyotiwa pumzi na yaliandikiwa Kanisa la kwanza na kilitunzwa vyema kwa muda mrefu. Bibilia kamili yapatikana bure ukiweza kuipakua kupitia kifaa chako cha Android, iOS na Blackberry. Pakua NewLife app bure katika tovuti hii www.newlife.bible
«... pero a todos los que creyeron en él y lo recibieron, les dio el derecho de llegar a ser hijos de Dios». JUAN 1:12
YOHANA Neno Alifanyika Mwili 1 H apo mwanzo alikuwako Neno, huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. 2 Tangu mwanzo huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu. 3 V itu vyote viliumbwa kwa yeye, wala pasipo yeye hakuna cho chote kilichoumbwa ambacho kimeumbwa. 4 Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima na huo uzima ulikuwa nuru ya watu. 5 Nuru hung'aa gizani nalo giza halikuishinda. 6A likuja mtu mmoja aliyetumwa kutoka kwa Mungu, jina lake Yohana. 7 A likuja kama shahidi apate kuishuhudia hiyo nuru, ili kwa kupitia yeye watu wote waweze kuamini. 8 Yeye mwenyewe hakuwa ile nuru, bali alikuja kuishuhudia hiyo nuru. 9 Kwamba nuru halisi, imwangaziayo kila mtu ilikuwa inakuja ulimwenguni. 10 Huyo Neno alikuwako ulimwenguni na ingawa ulimwengu uliumbwa kwa yeye, haukumtambua. 11A likuja kwa walio wake, lakini wao hawakumpokea. 12 Bali wote waliompokea, aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake. 13 Hawa ndio waliozaliwa si kwa damu wala kwa mapenzi ya mwili au kwa mapenzi ya mtu, bali kwa mapenzi ya Mungu. 14 N eno alifanyika mwili, akakaa miongoni mwetu, nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba, amejaa neema na kweli. 15 Yohana alishuhudia habari zake, akapiga kelele akisema, “Huyu ndiye yule niliyewaambia kwamba, ‘Yeye ajaye baada yangu ni mkuu kuliko mimi, kwa kuwa alikuwako kabla yangu.’ ” 16 Kutokana na ukamilifu wake, sisi sote tumepokea neema juu ya neema. 17 K wa kuwa sheria ilitolewa kwa mkono wa Mose, lakini neema na kweli imekuja kupitia Yesu Kristo. 18 Hakuna mtu ye yote aliyemwona Mungu wakati wo wote, ila ni Mungu Mwana pekee, aliye kifuani mwa Baba ndiye ambaye amemdhihirisha.
1
Ushuhuda Wa Yohana Mbatizaji H uu ndio ushuhuda wa Yohana wakati Wayahudi walipotuma makuhani na Walawi kutoka Yerusalemu kumwuliza, “Wewe ni nani?” 20 Y ohana alikiri waziwazi pasipo kuficha akasema, “Mimi si Kristo *.” 19
TUMAINI
49
Nuru hung'aa gizani nalo
giza halikuishinda.
YOHANA 1:5
W akamwuliza, “Wewe ni nani basi? Je, wewe ni Eliya?” Yeye akajibu, “Hapana, mimi siye.” “Je, wewe ni yule Nabii?” Akajibu, “Hapana.” 22 Ndipo wakasema, “Basi tuambie wewe ni nani ili tupate jibu la kuwapelekea wale waliotutuma. Wewe wasemaje juu yako mwenyewe?” 23 A kawajibu kwa maneno ya Nabii Isaya, akisema, “Mimi ni sauti ya mtu aliaye nyikani, ‘Inyosheni njia ya Bwana.’ ” 24 Basi walikuwa wametumwa watu kutoka kwa Mafarisayo 25w akamwuliza, “Kama wewe si Kristo, wala si Eliya na wala si yule Nabii, kwa nini basi unabatiza?” 26 Yohana akawajibu, “Mimi ninabatiza kwa maji *, lakini katikati yenu yupo mtu msiyemjua. 27 Yeye ajaye baada yangu, sistahili hata kufungua kamba za viatu vyake.” 28 M ambo haya yote yalitukia huko Bethania, ng'ambo ya Mto Yordani, mahali Yohana alipokuwa akibatiza. 21
Yesu Mwana-Kondoo Wa Mungu Siku iliyofuata, Yohana alimwona Yesu akimjia akasema, “Tazama, MwanaKondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu! 30 Huyu ndiye yule 29
niliyewaambia ya kwamba, ‘Yuaja mtu nyuma yangu ambaye ni mkuu kuliko mimi kwa maana alikuwako kabla yangu.’ 31 M imi mwenyewe sikumfahamu, lakini sababu ya kuja nikibatiza kwa maji ni ili yeye apate kufunuliwa kwa Israeli.” 32 K isha Yohana akatoa ushuhuda huu: “Nilimwona Roho akishuka kutoka mbinguni kama hua, akakaa juu yake. 33 M imi nisingemtambua, lakini yeye aliyenituma nibatize kwa maji alikuwa ameniambia, ‘Yule mtu utakayemwona Roho akimshukia na kukaa juu yake, huyo ndiye atakayebatiza kwa Roho Mtakatifu.’ 34 M imi mwenyewe nimeona jambo hili na ninashuhudia kuwa huyu ndiye Mwana wa Mungu.” Wanafunzi Wa Kwanza Wa Yesu Siku iliyofuata, Yohana alikuwako huko tena pamoja na wanafunzi wake wawili. 36 A lipomwona Yesu akipita, akasema, “Tazama, Mwana-Kondoo wa Mungu!” 37 Wale wanafunzi wawili walipomsikia Yohana akisema haya, wakamfuata Yesu. 38 Yesu akageuka, akawaona wakimfuata akawauliza, “Mnataka nini?” Wakamwambia, “Rabi,” (maana yake Mwalimu), “Unaishi wapi?” 35
1:1 1Yn 1:2; Yn 17:5; Flp 2:6; Isa 55:11 1:2 Ufu 1:8; Mwa 1:1 1:3 Kol 1:16; Ebr 1:2 1:4 1Yn 5:20; Ufu 1:8; Yn 12:46 1:5 Yn 3:19 1:6 Mt 3:1 1:7 Yn 3:26; 5:33; Yn 3:15 1:8 Yn 1:20 1:9 1Yn 2:8; Isa 49:6 1:10 Yn 1:3; Ebr 1:2; 11; 3 1:11 Lk 19:14; Mdo 3:26; 13:46 1:12 Isa 56:5; Rum 8:15; Gal 3:26; 2Pet 1:4; 1Yn 3:1 1:13 Tit 3:5; Yak 1:18 1:14 1Yn 1:1-2; 4:2; Yn 14:6 1:15 Yn 1:32; 3:32; 5:33; Mt 3:11; Mk 1:7; Lk 3:16; Yn 1:27, 30; Yn 3:31; Yn 8:58; Kol 1:17 1:16 Kol 1:19; Kol 2:9 1:17 Kum 32:46 1:19 Yn 7:1; 10:24 1:20 Yn 3:28; Lk 3:15-16 1:20 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Mpakwa (au Aliyetiwa) mafuta 1:21 Kum 18:15; Mt 11:4 1:23 Mt 3:1; Isa 40:3 1:25 Mt 21:25 1:26 Mt 3:11; Mk 1:7, 8 1:26 Hapa tafsiri zingine zinasema ndani ya maji 1:27 Yn 3:26; Mdo 13:25 1:28 Yn 3:26; 10:40 1:29 Mwa 22:8; Ufu 5:6 1:30 Yn 15:27 1:31 Mal 3:1; Mt 3:6; Lk 1:17, 76, 77; 3:3, 4 1:32 Mt 3:16; Mk 1:10 1:33 Mk 1:4; Mt 3:11 1:34 Mt 4:3 1:35 Mt 3:1 1:36 Yn 1:29 1:38 Mt 23:7
50
TUMAINI
Yesu akawajibu, “Njoni, nanyi mtapaona!” Hivyo wakaenda na kupaona mahali alipokuwa anaishi, wakakaa naye siku ile, kwa kuwa ilikuwa yapata saa kumi. 40 A ndrea nduguye Simoni Petro, alikuwa mmoja wa wale wawili waliosikia yale Yohana aliyokuwa amesema, naye ndiye aliyemfuata Yesu. 41 K itu cha kwanza Andrea alichofanya ni kumtafuta Simoni nduguye na kumwambia, “Tumemwona Masiya” (yaani, Kristo). 42 Naye akamleta kwa Yesu. Yesu akamwangalia na kusema, “Wewe ni Simoni mwana wa Yohana. Utaitwa Kefa” (ambalo limetafsiriwa Petro *). 39
Yesu Awaita Filipo Na Nathanaeli Siku iliyofuata Yesu aliamua kwenda Galilaya. Akamkuta Filipo, akamwambia, “Nifuate.” 44 B asi Filipo alikuwa mwenyeji wa Bethsaida, mji alikotoka Andrea na Petro. 45 Filipo naye akamkuta Nathanaeli na 43
YOHANA kumwambia, “Tumemwona yeye ambaye Mose aliandika habari zake katika Torati na ambaye pia manabii waliandika kumhusu, yaani, Yesu wa Nazareti, mwana wa Yosefu.” 46 Nathanaeli akauliza, “Nazareti! Je, kitu cho chote chema chaweza kutoka Nazareti?” Filipo akamwambia, “Njoo uone.” 47 Yesu a lipomwona Nat ha naeli anakaribia, akanena habari zake akasema, “Tazama huyu ni Mwisraeli kweli kweli, hana hila ndani yake.” 48 Nathanaeli akamwuliza, “Umenifahamuje?” Yesu akamjibu, “Nilikuona ulipokuwa bado uko chini ya mtini, kabla hata Filipo hajakuita.” 49 Nathanaeli akamwambia, “Mwalimu, wewe ni Mwana wa Mungu! Wewe ni Mfalme wa Israeli!” 50 Yesu akamwambia, “Unaamini kwa kuwa nilikuambia nilikuona ulipokuwa
bado uko chini ya mtini? Basi utaona mambo makuu zaidi kuliko hilo.” 51 N dipo akawaambia, “Amin, amin nawaambia, ninyi mtaona mbingu ikifunguka na malaika wa Mungu wakipanda na kushuka juu ya Mwana wa Adamu.” Arusi Huko Kana S iku ya tatu kulikuwa na arusi katika mji wa Kana ya Galilaya, naye mama yake Yesu alikuwako huko. 2 Yesu pamoja na wanafunzi wake walikuwa wamealikwa arusini pia. 3 Divai ilipokwisha, mama yake Yesu akamwambia, “Wameishiwa na divai.” 4 Yesu akamwambia, “Mwanamke, nina nini nawe? Saa yangu haijawadia.” 5M ama yake akawaambia wale watumishi, “Lo lote atakalowaambia, fanyeni.” 6 Basi ilikuwapo huko mitungi sita ya kuhifadhia maji iliyotengenezwa kwa mawe kwa ajili ya kujitakasa kwa desturi ya Kiyahudi, kila mtungi ungeweza kuchukua vipipa viwili au vitatu *.
2
1
1:40 Mt 4:18-22 1:41 Yn 4:25 1:42 Mwa 32:28; Mt 16:18 1:42 Petro kwa Kiyunani au Kefa kwa Kiaramu; maana yake ni Kipande cha mwamba 1:43 Mt 10:3; Yn 14:8-9; Mt 4:9 1:44 Yn 12:21 1:45 Yn 21:2; Lk 24:27; Mt 2:23; Lk 3:23 1:46 Yn 7:41-42, 52 1:47 Za 32:2; Rum 9:4-6 1:49 Mt 23:7; 4:3; 2; 2; 27:42 1:51 Mt 3:16; 8:20; Mwa 28:12 2:1 Yn 4:46; 21:2; Mt 12:46 2:4 Yn 19:26; Mt 8:26; 26:18; Yn 7:6 2:5 Mwa 41:55 2:6 Mk 7:3-4; Yn 3:25 2:6 Kipipa kimoja chenye ujazo wa lita 40; hivyo kila mtungi ulikuwa na ujazo wa lita 80 au 120
YOHANA 3:16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
YOHANA 7 Yesu akawaambia wale watumishi, “Ijazeni hiyo mitungi maji.” Nao wakaijaza ile mitungi mpaka juu. 8 Kisha akawaambia, “Sasa choteni hayo maji kidogo, mpelekeeni mkuu wa meza.” Hivyo wakachota, wakampelekea. 9 Yule mkuu wa meza akayaonja yale maji ambayo yalikuwa yamebadilika kuwa divai. Hakujua divai hiyo ilikotoka ingawa wale watumishi waliochota yale maji wao walifahamu. Basi akamwita bwana arusi kando 10 akamwambia, “Watu wote hutoa kwanza divai nzuri, kisha huleta ile divai hafifu wageni wakisha kunywa vya kutosha, lakini wewe umeiweka ile nzuri kupita zote mpaka sasa.” 11 Huu, ndio uliokuwa mwujiza wa kwanza Yesu aliofanya huko Kana ya Galilaya. Hivyo Yesu alidhihirisha utukufu wake na wanafunzi wake wakamwamini.
Yesu Atakasa Hekalu Baada ya hayo, Yesu pamoja na mama yake, ndugu zake na wanafunzi wake, walishuka mpaka Kapernaumu wakakaa huko siku chache. 13 I lipokaribia wakati wa Pasaka ya Wayahudi, Yesu alipanda kwenda Yerusalemu. 14 Huko Hekaluni aliwakuta watu wakiuza ng'ombe, kondoo na njiwa na wengine walikuwa wameketi mezani wakibadili fedha. 15 Akatengeneza mjeledi kutokana na kamba, akawafukuza wote kutoka kwenye eneo la Hekalu pamoja na kondoo na ng'ombe. Akazipindua meza za wale wabadili fedha na kuzimwaga fedha zao. 16 A kawaambia wale waliokuwa wakiuza njiwa, “Waondoeni hapa! Mnathubutuje kuifanya nyumba ya Baba yangu kuwa mahali pa biashara?” 17 Wanafunzi wake wakakumbuka kuwa imeandikwa: “Wivu wa nyumba yako utanila.” 18 N dipo Wayahudi wakamwuliza, “Unaweza kutuonyesha ishara gani ili kuthibitisha mamlaka uliyo nayo ya kufanya mambo haya?” 19 Y esu akawajibu, “Libomoeni hili Hekalu, nami nitalijenga tena kwa siku tatu!” 20 Wale Wayahudi wakamjibu, “Hekalu hili lilijengwa kwa muda wa miaka arobaini na sita, nawe wasema utalijenga kwa siku 12
tatu?” 21L akini yeye Hekalu alilozungumzia ni mwili wake. 22 B aada ya kufufuka kutoka kwa wafu, wanafunzi wake wakakumbuka yale aliyokuwa amesema. Ndipo wakayaamini Maandiko na yale maneno Yesu aliyokuwa amesema. 23 I kawa Yesu alipokuwa Yerusalemu kwenye Sikukuu ya Pasaka, watu wengi waliona ishara na miujiza aliyokuwa akifanya, wakamwamini. 24 Lakini Yesu hakujiaminisha kwao kwa sababu aliwajua wanadamu wote. 25 Hakuhitaji ushuhuda wa mtu ye yote kuhusu mtu, kwa kuwa alijua yote yaliyokuwa moyoni mwa mtu. Nikodemo Amwendea Yesu Usiku B asi palikuwa na mtu mmoja Farisayo, jina lake Nikodemo, mmoja wa Baraza la Wayahudi * lililotawala. 2 Huyu alimjia Yesu usiku akamwambia, “Rabi, tunajua kuwa wewe ni mwalimu uliyetumwa na Mungu, kwa maana hakuna mtu awezaye kufanya miujiza hii uifanyayo wewe, kama Mungu hayuko pamoja naye.” 3 Yesu a ka mjibu, “A min, a min nakuambia, mtu hawezi kuuona Ufalme wa Mungu asipozaliwa mara ya pili.” 4 Nikodemo akauliza, “Awezaje mtu kuzaliwa wakati akiwa mzee? Hakika hawezi kuingia mara ya pili kwenye tumbo la mama yake ili azaliwe!” 5 Yesu akamwambia, “Amin, amin nakuambia, hakuna mtu ye yote anayeweza kuingia katika Ufalme wa Mungu isipokuwa amezaliwa kwa maji na kwa Roho. 6 Mwili huzaa mwili, lakini Roho huzaa roho. 7 Kwa hiyo usishangae ninapokuambia huna budi ‘kuzaliwa mara ya pili.’ 8U pepo huvuma po pote upendapo. Mvumo wake unausikia lakini huwezi ukafahamu utokako wala uendako. Ndivyo ilivyo kwa kila mtu aliyezaliwa na Roho.” 9N ikodemo akamwuliza, “Mambo haya yanawezekanaje?” 10 Y esu akamwambia, “Wewe ni mwalimu mashuhuri wa Waisraeli, nawe huelewi mambo haya? 11 A min, amin ninakuambia, sisi tunazungumza lile tunalolijua na tunashuhudia lile tuliloliona. Lakini ninyi watu hamkubali ushuhuda wetu. 12 N imewaambia mambo ya duniani,
3
1
TUMAINI
51
nanyi hamkuniamini, mtaniaminije basi nitakapowaambia mambo ya mbinguni? 13 H akuna mtu ye yote aliyekwenda mbinguni isipokuwa yeye aliyeshuka kutoka mbinguni, yaani, Mwana wa Adamu. 14 Kama vile Mose alivyomwinua yule nyoka kule jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa juu. 15 Ili kila mtu amwaminiye awe na uzima wa milele. 16 “ Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. 17 K wa maana Mungu hakumtuma Mwanawe kuuhukumu ulimwengu, bali kwa yeye ulimwengu upate kuokolewa. 18 Ye yote amwaminiye hahukumiwi, lakini asiyeamini amekwisha kuhukumiwa, kwa sababu hakumwamini Mwana pekee wa Mungu. 19H ii ndiyo hukumu kwamba: Nuru imekuja ulimwenguni, nao watu wakapenda giza kuliko nuru kwa sababu matendo yao ni maovu. 20 K wa kuwa kila atendaye maovu huchukia nuru, wala haji kwenye nuru ili matendo yake maovu yasifichuliwe. 21 Lakini wale watendao yaliyo mema huja kwenye nuru, kusudi ionekane wazi kwamba matendo yao yametendeka katika Mungu.” Ushuhuda Wa Yohana Mbatizaji Kuhusu Yesu
22 B aada ya haya, Yesu na wanafunzi wake walikwenda katika nchi ya Uyahudi, nao wakakaa huko kwa muda na kubatiza. 23 Y ohana naye alikuwa akibatiza huko Ainoni karibu na Salimu kwa sababu huko kulikuwa na maji tele. Watu wazima wakamjia huko ili kubatizwa. 24 (Hii ilikuwa kabla Yohana hajatiwa gerezani). 25 M ashindano yakazuka kati ya baadhi ya wanafunzi wa Yohana na Myahudi mmoja kuhusu suala la desturi ya kunawa. 26 Wakamwendea Yohana wakamwambia, “Rabi, yule mtu aliyekuwa pamoja nawe ng'ambo ya pili ya Mto Yordani, yule uliyeshuhudia habari zake, sasa anabatiza na kila mtu anamwendea!” 27 Y ohana akawajibu, “Hakuna mtu ye yote awezaye kupata kitu cho chote isipokuwa kile tu alichopewa kutoka mbinguni. 28N inyi wenyewe ni mashahidi wangu kwamba
2:9 Yn 4:46 2:11 Mt 12:38; Yn 1:14; Kut 14:31 2:13 Yn 11:55; Kum 16:1-6; Lk 2:41 2:14 Mt 21:12; Mk 11:15; Lk 19:45 2:14 Mt 21:12, 13; Mk 11:15-17; Lk 19:45, 46 2:16 Lk 2:49 2:17 Za 69; 9 2:18 Mt 12:38 2:19 Mt 26:61; Mdo 6:14 2:21 1Kor 6:19 2:22 Lk 24:5-8; Yn 14:26 2:23 Yn 3:15 2:25 Kum 31:21; Mt 9:4 3:1 Yn 7:50; 19:39; Lk 23:13 3:1 Baraza la Wayahudi hapa ina maana ya Sanhedrin ambalo lilikuwa ndilo Baraza la juu kabisa la utawala wa Kiyahudi, lililoundwa na wazee 70 pamoja na Kuhani Mkuu 3:2 Yn 2:11; 9:16, 33; Mdo 2:22; 10:38 3:3 Yn 1:13; 1Pet 1:23 3:5 Tit 3:5 3:6 Yn 1:13; Mwa 5:3; Za 51:5 3:8 Mk 4:41; Mhu 11:5 3:9 Yn 6:52, 60 3:10 Lk 2:46 3:11 Yn 1:18; 7:16-17 3:12 Lk 22:67 3:13 Mit 30:4; Efe 4:8-10; Ebr 4:14; 9:24 3:14 Hes 21:8-9; Yn 8:28; 12:32 3:15 Mwa 15:6; Rum 3:22 3:16 Rum 5:8; Efe 2:4; Yn 6:29, 40; Yn 11:2526 3:17 Yn 17:8, 21; Yn 20:21; Isa 53:11; Rum 11:14 3:18 Yn 5:24; 1:18; 1Yn 4:9 3:19 Yn 1:4; Yn 8:12 3:20 Efe 5:11-13 3:22 Yn 4:2 3:23 1Sam 9:4; Mt 3:6 3:24 Mt 4:12; Mt 14:3 3:25 Yn 2:6 3:26 Mt 23:7; Yn 1:7 3:27 Ebr 5:4; 1Kor 4:7; Yak 1:17 3:28 Yn 1:20-23; 3:9; Mt 9:15; Flp 2:2; 2Yn 1:12 3:28 Yaani Masiya
52
nilisema, ‘Mimi si Kristo *, ila nimetumwa nimtangulie.’ 29 B ibi arusi ni wa bwana arusi. Lakini rafiki yake bwana arusi anayesimama karibu naye na kusikiliza kutoka kwake, hufurahi sana aisikiapo sauti ya bwana arusi. Kwa sababu hii furaha yangu imekamilika. 30 Y eye hana budi kuwa mkuu zaidi na mimi nizidi kuwa mdogo.” Yeye Aliyetoka Mbinguni “ Yeye ajaye kutoka juu yu juu ya yote, yeye aliye wa duniani ni wa dunia, naye huzungumza mambo ya duniani. Yeye aliyekuja kutoka mbinguni, yu juu ya yote. 32 Yeye hushuhudia yale aliyoyaona na kuyasikia, lakini hakuna ye yote anayekubali ushuhuda wake. 33 L akini ye yote anayekubali huo ushuhuda anathibitisha kwamba, Mungu ni kweli. 34 Yeye aliyetumwa na Mungu husema maneno ya Mungu, kwa kuwa Mungu humtoa Roho pasipo kipimo. 35 B aba anampenda Mwana, naye ametia vitu vyote mikononi mwake. 36Y e yote anayemwamini Mwana ana uzima wa milele, lakini yeye asiyemwamini Mwana hatauona uzima, bali ghadhabu ya Mungu itakuwa juu yake.” 31
Yesu Azungumza Na Mwanamke Msamaria
4
YOHANA
TUMAINI
M afarisayo wakasikia kwamba Yesu alikuwa anapata na kubatiza wanafunzi wengi zaidi kuliko Yohana, 2 i ngawa kwa kweli si Yesu mwenyewe aliyekuwa akibatiza, ila ni wanafunzi wake. 3 Bwana alipojua mambo haya, aliondoka Uyahudi akarudi tena Galilaya. 1
4W akati huo ilimlazimu apitie Samaria. kafika kwenye mji mmoja wa Samaria A uitwao Sikari, karibu na lile shamba ambalo Yakobo alimpa mwanawe Yosefu. 6 Huko ndiko kulikokuwa na kile kisima cha Yakobo. Naye Yesu alikuwa amechoka kwa kuwa alikuwa ametoka safarini. Akaketi karibu na hicho kisima. Ilikuwa yapata saa sita mchana. 7 Mwanamke mmoja Msamaria akaja kuteka maji, Yesu akamwambia, “Naomba maji ninywe.” 8 (Wakati huo wanafunzi wake walikuwa wamekwenda mjini kununua chakula.) 9 Yule mwanamke akamjibu, “Wewe ni Myahudi na mimi ni Msamaria. Yawezekanaje uniombe nikupe maji ya kuny wa?” Wayahudi walikuwa hawashirikiani kabisa na Wasamaria. 10 Yesu akajibu akamwambia, “Kama ungelijua karama ya Mungu, naye ni nani anayekuambia, Nipe maji ninywe, wewe ungelimwomba yeye, naye angelikupa maji yaliyo hai.” 11 Yule mwanamke akamjibu, “Bwana, wewe huna chombo cha kutekea maji na kisima hiki ni kirefu. Hayo maji ya uzima utayapata wapi? 12 Kwani wewe ni mkuu kuliko baba yetu Yakobo ambaye alitupatia kisima hiki, ambacho yeye pamoja na watoto wake na mifugo yake walikitumia?” 13 Y esu akamjibu, “Kila mtu anayekunywa maji ya kisima hiki, ataona kiu tena. 14 L akini ye yote anywaye maji nitakayompa, hataona kiu kamwe. Maji nitakayompa 5
Lakini ye yote anywaye maji nitakayompa, hataona kiu kamwe. Maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji yakibubujika uzima wa milele.
yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji yakibubujika uzima wa milele.” 15Y ule mwanamke akamwambia, “Bwana, tafadhali nipe maji hayo ili nisipate kiu tena na wala nisije tena hapa kuteka maji!” 16 Yesu akamjibu, “Nenda ukamwite mumeo, uje naye hapa.” 17 Yule mwanamke akajibu, “Sina mume.” Yesu akamwambia, “Umesema kweli kuwa huna mume. 18 Kwa maana umeshakuwa na wanaume watano na mwanaume unayeishi naye sasa si mume wako!” 19 Yule mwanamke akasema, “Bwana, naona bila shaka wewe ni nabii. 20B aba zetu waliabudu kwenye mlima huu, lakini ninyi Wayahudi mnasema ni lazima tukaabudu huko Yerusalemu.” 21 Y esu akamjibu, “Mwanamke, niamini, wakati unakuja ambapo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala huko Yerusalemu. 22N inyi Wasamaria mnaabudu msichokijua. Sisi Wayahudi tunamwabudu Mungu tunayemjua kwa sababu wokovu unatoka kwa Wayahudi. 23 L akini saa yaja, tena ipo, ambapo wale waabuduo halisi, watamwabudu Baba katika roho na kweli. Watu wanaoabudu namna hii, ndio Baba anawatafuta. 24 Mungu ni Roho na wote wanaomwabudu imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.” 25 Yule mwanamke akamwambia, “Ninafahamu kwamba Masiya (aitwaye Kristo) anakuja. Yeye akija, atatueleza mambo yote.” 26 Y esu akamwambia, “Mimi ninayezungumza nawe, ndiye Masiya.” 27 W akati huo wanafunzi wake wakarudi, wakashangaa sana kumwona akizungumza na mwanamke. Lakini hakuna aliyemwuliza, “Unataka nini kwake?” Au “Kwa nini unazungumza naye?” 28 Yule mwanamke akaacha mtungi wake, akarudi mjini akawaambia watu, 29 “ Njoni mkamwone mtu aliyeniambia kila kitu nilichotenda! Je, yawezekana huyu ndiye 3:29 Mt 22:2; 2Kor 11:2; Efe 5:25, 27; Ufu 21:9; Wim 5:1 3:30 2Sam 3:1 3:31 Yn 8:23; 1Yn 4:5 3:32 Yn 8:26; Yn 15:15 3:33 Rum 3:4; 1Yn 5:10 3:34 Isa 42:1; Mt 12:18 3:35 Mt 28:18; Yn 17:2 3:36 Yn 5:24; 6:47 4:1 Yn 3:22-26 4:2 1Kor 1:17 4:3 Yn 3:22 4:4 Lk 9:52 4:5 Mwa 48:22; Yos 24:32 4:7 Mwa 24:17; 1Fal 17:10 4:8 Yn 4:5, 30 4:9 Mt 10:5; Lk 9:52-53 4:10 Isa 55:1; Ufu 21:6 4:12 Yn 4:6; 8:53 4:13 Yn 6:58 4:14 Yn 6:35; Isa 12:3; Yn 7:38; Mt 25:46 4:15 Yn 6:34 4:19 Mt 21:11 4:20 Kum 11:29; Yos 8:33; Lk 9:53; 4:21; 4:20; Yn 5:28; 16:2; 1Tim 2:8 4:21 Yn 5:28; 16:2; Mal 1:11; 1Tim 2:8 4:22 2Fal 17:28-41; Isa 2:3; Rum 9:4-5 4:23 Yn 5:25; 16:32; Flp 3:3 4:24 Flp 3:3 4:25 Mt 1:16; Yn 1:41 4:26 Yn 8:24; 9:35-37 4:27 Yn 4:8
YOHANA Masiya *?” 30 Basi wakamiminika watu kutoka mjini wakamwendea Yesu. 31 W akati huo wanafunzi wake walikuwa wakimsihi, “Rabi, kula angalau cho chote.” 32 L akini yeye akawajibu, “Mimi ninacho chakula ambacho ninyi hamkifahamu.” 33 Basi wanafunzi wakaanza kuulizana, “Kuna mtu ambaye amemletea chakula?” 34 L akini Yesu akawajibu, “Chakula changu ni kufanya mapenzi ya Mungu ambaye amenituma na kuikamilisha kazi yake. 35 J e, ninyi hamsemi, ‘Bado miezi minne tuvune?’ Inueni macho yenu myaangalie mashamba jinsi mazao yalivyo tayari kuvunwa! 36 M vunaji tayari anapokea mshahara wake, naye anakusanya mazao kwa ajili ya uzima wa milele. Ili yeye apandaye na yeye avunae wafurahi pamoja. 37 Hivyo kule kusema, ‘Mmoja hupanda na mwingine huvuna,’ ni kweli kabisa. 38 Niliwatuma mkavune mazao ambayo hamkupanda, wengine walifanya kazi ngumu, nanyi mmevuna faida ya taabu yao.” Wasamaria Wengi Waamini W asamaria wengi kutoka katika mji ule wakamwamini Yesu kwa sababu ya ushuhuda wa yule mwanamke alipowaambia kwamba, “Ameniambia kila jambo nililotenda.” 40Hivyo wale Wasamaria walipomjia, wakamsihi akae kwao. Naye akakaa huko siku mbili. 41 Kwa sababu ya neno lake, watu wengi wakaamini. 42 W akamwambia yule mwanamke, “Sasa tunaamini, wala si kwa sababu ya maneno yako tu, bali kwa kuwa tumemsikia sisi wenyewe. Tumejua hakika kweli ya kwamba huyu ndiye Kristo, Mwokozi wa ulimwengu.” 39
Yesu Amponya Mwana Wa Afisa Baada ya zile siku mbili, Yesu aliondoka kwenda Galilaya. 44 (Basi Yesu mwenyewe alikuwa amesema kwamba nabii hapati heshima katika nchi yake mwenyewe.) 4 5 A l ipof i k a Ga l i laya , Waga l i laya walimkaribisha, kwani walikuwa wameona yale aliyoyatenda huko Yerusalemu wakati wa Sikukuu ya Pasaka. Kwa maana wao pia walikuwa wamehudhuria kwenye hiyo Sikukuu. 46 Hivyo Yesu akaja tena mpaka Kana ya Galilaya, kule alikokuwa amebadili maji kuwa divai. Huko kulikuwako na mtu mmoja 43
TUMAINI
53
afisa wa kifalme, ambaye mwanawe alikuwa mgonjwa huko Kapernaumu. 47 Huyo mtu aliposikia kwamba Yesu alikuwa amewasili Galilaya kutoka Uyahudi, alimwendea na kumwomba ili aje kumponya mwanawe, aliyekuwa mgonjwa karibu ya kufa. 48 Yesu akamwambia, “Ninyi watu msipoona ishara na miujiza kamwe hamtaamini.” 49 Yule afisa wa kifalme akamwambia, “Bwana, tafadhali shuka kabla mwanangu hajafa.” 50 Yesu akamjibu, “Enenda zako, mwanao yu hai.” Yule afisa akaamini yale maneno Yesu a l iyomwa mbia, a k aondok a akaenda zake. 51 Alipokuwa bado yuko njiani, akakutana na watumishi wake wakamwambia kwamba mwanawe yu mzima. 52 Akawauliza saa ambayo alianza kupata nafuu. Wakamwambia, “Jana yapata saa saba, homa ilimwacha.” 53 N dipo baba wa huyo mtoto akakumbuka kuwa huo ndio wakati ambapo Yesu alikuwa amemwambia, “Mwanao yu hai.” Kwa hiyo yeye, pamoja na wote wa nyumbani mwake wakamwamini Yesu. 54 Hii ilikuwa ishara ya pili ambayo Yesu alifanya aliporudi Galilaya kutoka Uyahudi.
7 Yule mgonjwa akamjibu, “Bwana, mimi sina mtu wa kuniingiza bwawani maji yanapotibuliwa. Nami ninapotaka kutumbukia bwawani, mtu mwingine huingia kabla yangu.” 8 Yesu akamwambia, “Simama, chukua mkeka wako na uende.” 9 Mara yule mtu akapona, akachukua mkeka wake, akaanza kutembea. Basi siku hiyo ilikuwa siku ya Sabato. 10 Kwa hiyo Wayahudi wakamwambia yule mtu aliyeponywa, “Leo ni Sabato, ni kinyume cha sheria wewe kubeba mkeka wako.” 11 Yeye akawajibu, “Yule mtu aliyeniponya aliniambia, ‘Chukua mkeka wako na uende.’ ” 12 Wakamwuliza, “Ni mtu gani huyo aliyekuambia uchukue mkeka wako uende?” 13 Basi yule mtu aliyeponywa hakufahamu ni nani aliyemponya, kwa sababu Yesu alikuwa amejiondoa katika ule umati wa watu uliokuwa hapo. 14 B aadaye Yesu akamkuta yule mtu aliyemponya ndani ya Hekalu na kumwambia, “Tazama umeponywa, usitende dhambi tena. La sivyo, lisije likakupata jambo baya zaidi.” 15 Yule mtu akaenda, akawaambia wale Wayahudi kuwa ni Yesu aliyemponya.
Yesu Amponya Mtu Penye Bwawa La Bethzatha
Uzima Kupitia Mwana Kwa hiyo Wayahudi wakaanza kumsumbua, kwa sababu alikuwa anafanya mambo kama hayo siku ya Sabato. 17 Yesu akawajibu, “Baba yangu anafanya kazi yake daima hata siku hii ya leo, nami pia ninafanya kazi.” 18M aneno haya yaliwaudhi sana viongozi wa Wayahudi. Wakajaribu kila njia wapate jinsi ya kumwua, kwani si kwamba alivunja Sabato tu, bali alikuwa akimwita Mungu Baba yake, hivyo kujifanya sawa na Mungu.
5
B aada ya haya, kulikuwa na Sikukuu ya Wayahudi, naye Yesu akapanda kwenda Yerusalemu. 2 Huko Yerusalemu, karibu na mlango uitwao Mlango wa Kondoo, palikuwa na bwawa moja lililoitwa kwa Kiebrania Bethzatha *, ambalo lilikuwa limezungukwa na kumbi tano. 3 Hapa palikuwa na idadi kubwa ya wasiojiweza, yaani, vipofu, viwete, na waliopooza, wakingojea maji yatibuliwe 4 [kwa maana malaika alikuwa akishuka wakati fulani, akayatibua maji na yule aliyekuwa wa kwanza kuingia ndani baada ya maji kutibuliwa alipona ugonjwa wo wote aliokuwa nao]. 5 Mtu mmoja alikuwako huko ambaye alikuwa ameugua kwa miaka thelathini na minane. 6 Yesu alipomwona akiwa amelala hapo, naye akijua kuwa amekuwako hapo kwa muda mrefu, akamwambia, “Je, wataka kuponywa?” 1
16
Mamlaka Ya Mwana Wa Mungu Yesu akawaambia, “Amin, amin, nawaambia, Mwana hawezi kufanya jambo lo lote peke yake, yeye aweza tu kufanya lile analomwona Baba yake akifanya, kwa maana lo lote afanyalo Baba, Mwana pia hufanya vivyo hivyo. 20 Baba ampenda Mwana na kumwonyesha yale ambayo yeye Baba mwenyewe anayafanya, naye 19
4:29 Mt 12:23; Yn 7:26, 31 4:29 Masiya maana yake ni Mpakwa (au Aliyetiwa) mafuta 4:31 Mt 23:7 4:32 Ay 23:12; Mt 4:4 4:34 Mt 26:39; Yn 17:4; 19:30 4:35 Mt 9:37; Lk 10:2 4:36 Rum 1:13; Mt 25:46 4:37 Ay 31:8; Mik 6:15 4:39 Yn 4:29 4:42 Lk 2:11; 1Yn 4:14 4:44 Mt 13:57; Lk 4:24 4:45 Yn 2:23 4:46 Yn 21:1-11 4:47 Yn 4:3, 54; Lk 7:2 4:48 Dan 4:2-3; Ebr 2:4 4:53 Mdo 11:14 4:54 Yn 4:8; 2:11 5:1 Law 23:2; Kum 16:1; Yn 2:13 5:2 Neh 3:1; 12:39; Mdo 21:40; 26:14 5:2 Bethzatha ni neno la Kiebrania ambalo maana yake ni Nyumba ya mizeituni; mahali pengine limetajwa kama Bethesda kwa Kiaramu, yaani Nyumba ya huruma, na pengine kama Bethsaida, yaani Nyumba ya uvuvi 5:8 Mk 2:11; Lk 5:24 5:9 Mt 12:1-14; Yn 9:14 5:10 Yer 17:21; Mt 12:2 5:12 Lk 5:21 5:14 Mk 2:5; Yn 8:11; Yn 8:11 5:15 Yn 1:19 5:16 Mt 12:14 5:17 Yn 9:4; 14:10 5:18 Mt 12:14; Yn 10:30-33; Yn 19:7 5:19 Yn 8:28; 14:24 5:20 Yn 3:35; 14:12
54
TUMAINI
YOHANA atamwonyesha kazi kuu kuliko hizi ili mpate kushangaa. 21 Hakika kama vile Baba awafufuavyo wafu na kuwapa uzima, vivyo hivyo Mwana huwapa uzima wale anaopenda. 22 Wala Baba hamhukumu mtu ye yote, lakini hukumu yote amempa Mwana, 23 ili wote wamheshimu Mwana kama vile wanavyomheshimu Baba. Ye yote asiyemheshimu Mwana, hamheshimu Baba aliyemtuma. 24 “Amin, amin ninawaambia, ye yote anayesikia maneno yangu na kumwamini yeye aliyenituma, anao uzima wa milele, naye hatahukumiwa, bali amepita kutoka mautini, na kuingia uzimani. 25A min, amin nawaambia, saa yaja, nayo saa ipo, wafu watakapoisikia sauti ya Mwana wa Mungu, nao watakaoisikia watakuwa hai. 26 Kama vile Baba alivyo na uzima ndani yake, vivyo hivyo amempa Mwana kuwa na uzima ndani yake. 27 Naye amempa Mwanawe mamlaka ya kuhukumu kwa kuwa yeye ni Mwana wa Adamu. 28 “ Msishangae kusikia haya, kwa maana saa inakuja ambapo wale walio makaburini wataisikia sauti yake. 29 Nao watatoka nje, wale waliotenda mema watafufuka wapate uzima na wale waliotenda maovu, watafufuka wahukumiwe.
YOHANA 5:24 Amin, amin ninawaambia,
ye yote anayesikia maneno yangu na kumwamini yeye aliyenituma, anao uzima wa milele, naye hatahukumiwa, bali amepita kutoka mautini, na kuingia uzimani.
Shuhuda Kuhusu Yesu “Mimi siwezi kufanya jambo lo lote peke yangu. Ninavyosikia ndivyo ninavyohukumu, nayo hukumu yangu ni ya haki kwa kuwa sitafuti kufanya mapenzi yangu mwenyewe, bali mapenzi yake yeye aliyenituma. 31 “ Kama ningejishuhudia mimi mwenyewe, ushuhuda wangu si kweli. 32 Lakini yuko mwingine anishuhudiaye na ninajua kwamba ushuhuda wake ni wa kweli. 33 “ Mlituma wajumbe kwa Yohana, naye akashuhudia juu ya kweli. 34 Si kwamba naukubali ushuhuda wa mwanadamu, la, bali ninalitaja hili kusudi ninyi mpate kuokolewa. 35Y ohana alikuwa taa iliyowaka na kutoa nuru, nanyi kwa muda mlichagua kuifurahia nuru yake. 36 “Lakini ninao ushuhuda mkuu zaidi kuliko wa Yohana. Kazi zile nizifanyazo, 30
5:21 2Kor 1:9; Ebr 11:19; Yn 11:25 5:22 Amu 11:27; Mdo 10:42 5:23 Lk 10:16; 1Yn 2:23 5:24 Yn 3:18; 1Yn 3:14 5:25 Yn 16:32; 8:43-47 5:26 Yn 12:14 5:27 Mdo 10:42; 17:31 5:28 Yn 16:2 5:29 Dan 12:2; Mt 25:46 5:30 Isa 28:6; Mt 26:39; Yn 4:34 5:31 Yn 8:14 5:32 Yn 5:37; 8:18 5:33 Yn 1:7 5:34 1Yn 5:9 5:35 Dan 12:3 5:36 1Yn 5:9; Yn 14:11; 15:24; Yn 3:17; 10:25
YOHANA zinashuhudia juu yangu, zile ambazo Baba amenituma nizikamilishe, naam, ishara hizi ninazofanya, zinashuhudia kuwa Baba ndiye aliyenituma. 37 N aye Baba mwenyewe ameshuhudia juu yangu. Hamjapata kamwe kuisikia sauti yake wala kuona umbo lake, 38 w ala hamna neno lake ndani yenu, kwa sababu hamkumwamini yeye aliyetumwa naye. 39 Ninyi mnachunguza Maandiko mkidhani ya kuwa ndani yake mna uzima wa milele, maandiko haya ndiyo yanayonishuhudia Mimi. 40 Lakini mnakataa kuja kwangu ili mpate uzima. 41 “ Mimi sitafuti kutukuzwa na wanadamu. 42 Lakini ninajua kwamba hamna upendo wa Mungu mioyoni mwenu. 43 Mimi nimekuja kwa jina la Baba yangu, nanyi hamnipokei, lakini mtu mwingine akija kwa jina lake mwenyewe, mtampokea. 44 N inyi mwawezaje kuamini ikiwa mnapeana utukufu ninyi kwa ninyi, lakini hamna bidii kupata utukufu utokao kwa Mungu? 45 “ Lakini msidhani kuwa mimi nitawashtaki mbele za Baba, mshtaki wenu ni Mose, ambaye mmemwekea tumaini lenu. 46 Kama mngelimwamini Mose, mngeliniamini na mimi kwa maana aliandika habari zangu. 47 Lakini ikiwa hamwamini aliyoandika Mose, mtaaminije ninayoyasema?” Yesu Alisha Watu 5,000 B aada ya haya, Yesu alikwenda ng'ambo ya Bahari ya Galilaya, ambayo pia huitwa Bahari ya Tiberia. 2 Umati mkubwa wa watu uliendelea kumfuata, kwa sababu waliona ishara nyingi za miujiza alizofanya kwa wagonjwa. 3 K isha Yesu akapanda mlimani akaketi huko pamoja na wanafunzi wake. 4 P asaka ya Wayahudi ilikuwa imekaribia. 5Y esu alipotazama na kuuona ule umati mkubwa wa watu ukimjia, akamwambia Filipo, “Tutanunua wapi mikate ili watu hawa wale?” 6 Aliuliza swali hili kumpima, kwa maana alishajua la kufanya. 7 Filipo akamjibu, “Hata fedha kiasi cha dinari mia mbili *, hazitoshi kununua mikate ya kuwapa watu hawa kila mtu apate kidogo.” 8 M moja wa wanafunzi wake, aitwaye Andrea, ndugu yake Simoni Petro,
6
1
akamwambia, 9 “Hapa kuna mvulana mmoja mwenye mikate mitano ya shayiri na samaki wawili wadogo. Lakini hivi vitatosha nini kwa umati wote huu?” 10 Yesu akasema, “waketisheni watu chini.” Palikuwa na majani mengi katika eneo lile, nao watu wakaketi, palikuwa na wanaume 5,000. 11 N dipo Yesu akachukua ile mikate, akamshukuru Mungu na kuwagawia wale watu waliokuwa wamekaa kwa kiasi walichohitaji. Akafanya vivyo hivyo na wale samaki. Kila mtu akapata kadiri alivyotaka. 12 Watu wote walipokwisha kula na kushiba, akawaambia wanafunzi wake, “Kusanyeni vipande vilivyobaki vya ile mikate, kisipotee cho chote.” 13 Hivyo wakavikusanya wakajaza vikapu kumi na viwili kwa vipande vilivyobaki vya ile mikate mitano na samaki wale wawili wadogo. 14 B aada ya watu kuona mwujiza ule Yesu aliofanya, walianza kusema, “Hakika huyu ndiye Nabii ajaye ulimwenguni!” 15 Yesu akijua kwamba walitaka kuja kumfanya awe mfalme wao, kwa nguvu, akajitenga nao akaenda milimani peke yake. Yesu Atembea Juu Ya Maji I lipofika jioni, wanafunzi wake walitelemka kwenda baharini. 17 Wakaingia kwenye mashua, wakaanza kuvuka bahari kwenda Kapernaumu. Wakati huu kulikuwa tayari giza na Yesu alikuwa hajajumuika nao. 18 Bahari ikachafuka kwa sababu upepo mkali ulikuwa unavuma. 19W anafunzi walipokuwa wamekwenda mwendo wa karibu maili tatu au nne *, walimwona Yesu akitembea juu ya maji akikaribia mashua, wakaogopa sana. 20L akini Yesu akawaambia, “Ni mimi, msiogope.” 21 Ndipo kwa furaha wakamkaribisha kwenye mashua, na mara wakafika walikokuwa wanakwenda. 16
Watu Wanamtafuta Yesu S iku iliyofuata, wale watu waliokuwa wamebaki ng'ambo ya pili waliona kwamba palikuwepo na mashua moja tu na kwamba Yesu hakuwa ameondoka pamoja na wanafunzi wake, ila walikuwa wameondoka peke yao. 23 Lakini zikaja 22
TUMAINI
55
mashua nyingine kutoka Tiberia zikafika karibu na mahali pale walipokula mikate baada ya Yesu kumshukuru Mungu. 24 Mara wale watu wakatambua kwamba Yesu hakuwepo hapo, wala wanafunzi wake. Wakaingia kwenye mashua hizo, wakaenda Kapernaumu ili kumtafuta Yesu. Yesu Ni Mkate Wa Uzima W alipomkuta Yesu ng'ambo ya bahari wakamwuliza, “Rabi, umefika lini huku?” 26 Yesu akawajibu, “Amin, amin nawaambia, ninyi hamnitafuti kwa kuwa mliona ishara na miujiza, bali kwa sababu mlikula ile mikate mkashiba. 27 Msishughulikie chakula kiharibikacho, bali chakula kidumucho hata uzima wa milele, ambacho Mwana wa Adamu atawapa. Yeye ndiye ambaye Mungu Baba amemtia muhuri.” 28 Ndipo wakamwuliza, “Tufanye nini ili tupate kuitenda kazi ya Mungu?” 29 Y esu akawajibu, “Kazi ya Mungu ndiyo hii: Mwaminini yeye aliyetumwa naye.” 30 H ivyo wakamwuliza, “Utafanya ishara gani ya mwujiza, ili tuione tukuamini? Utafanya jambo gani? 31 B aba zetu walikula mana jangwani, kama ilivyoandikwa, ‘Aliwapa mikate kutoka mbinguni ili wale.’ ” 32 Yesu akawaambia, “Amin, amin nawaambia, si Mose aliyewapa mikate kutoka mbinguni, bali Baba yangu ndiye anawapa mkate wa kweli kutoka mbinguni. 33 Kwa maana mkate wa Mungu ni yule ashukaye kutoka mbinguni na kuupa ulimwengu uzima.” 34 W akamwambia, “Bwana, kuanzia sasa tupatie huo mkate siku zote.” 35 Y esu akawaambia, “Mimi ndimi mkate wa uzima. Yeye ajaye kwangu, hataona njaa kamwe na yeye aniaminiye, hataona kiu kamwe. 36 Lakini kama nilivyowaambia, mmeniona lakini bado hamwamini. 37W ale wote anipao Baba watakuja kwangu na ye yote ajaye kwangu, sitamfukuzia nje kamwe. 38 Kwa kuwa nimeshuka kutoka mbinguni si ili kufanya mapenzi yangu, bali mapenzi yake yeye aliyenituma. 39H aya ndiyo mapenzi yake yeye aliyenituma, kwamba, nisimpoteze hata mmoja wa wale alionipa, bali niwafufue siku ya mwisho. 25
5:37 Yn 8:18; Kum 4:12; 1Tim 1:17 5:38 1Yn 1:10; 2:4; Isa 26:10; Yn 3:17 5:39 Rum 2:17-18; Lk 24:27, 44; Mdo 13:27 5:40 Yn 6:44 5:41 Yn 5:44; 5:34; 1The 2:6 5:44 Rum 2:29 5:45 Yn 9:28; Rum 2:17 5:46 Mwa 3:15; Lk 24:27, 44 5:47 Lk 16:29-31 6:1 Mt 14:15; Mk 6:35; Lk 9:10, 12 6:2 Yn 2:11-13 6:3 Yn 6:15 6:4 Yn 11:55 6:5 Yn 1:43 6:7 Hes 11:21, 22 6:7 Dinari 200 ni sawa na mshahara wa kibarua wa siku 200; mshahara wa kibarua ulikuwa dinari moja kwa siku 6:8 Yn 1:40 6:9 2Fal 4:43 6:11 Mt 14:19 6:14 Yn 2:11; Kum 18:1518; Mt 21:11 6:15 Yn 18:36; Mt 14:23; Mk 6:46 6:16-21 Mt 14:22-33; Mk 6:45-52 6:19 Ay 9:8 6:19 Maili tatu au nne ni kama kilomita 5 au 6 6:20 Mt 14:27 6:22 Yn 6:2; 15:21 6:23 Yn 6:1, 11 6:25 Mt 23:7 6:26 Yn 2:11 6:27 Mt 25:46; Yn 4:14; Mt 8:20; 2Tim 2:19; Ufu 7:3 6:29 1Yn 3:23; 3:17 6:30 Yn 2:11; Mt 12:38 6:31 Hes 11:7-9; Neh 9:15; Za 105:40 6:32 Yn 6:49 6:33 Yn 3:13, 31 6:34 Yn 4:15 6:35 Yn 4:14; 6:48; 7:37 6:36 Yn 6:26, 29 6:37 Yn 17:2-6, 9, 24 6:38 Yn 3:17; 4:34 6:39 Isa 27:3; Yn 18:9
56
Kwa maana mapenzi ya Baba yangu ni kwamba kila mmoja amtazamaye, Mwana na kumwamini awe na uzima wa milele, nami nitawafufua siku ya mwisho.” 41 Wayahudi wakaanza kunung'unika kwa kuwa alisema, “Mimi ndimi mkate ulioshuka kutoka mbinguni.” 42W akasema, “Huyu si Yesu, mwana wa Yosefu, ambaye baba yake na mama yake tunawajua? Anawezaje basi sasa kusema, ‘Nimeshuka kutoka mbinguni’?” 43 Hivyo Yesu akawaambia, “Acheni kunung'unikiana ninyi kwa ninyi. 44 Hakuna mtu awezaye kuja kwangu kama asipovutwa na Baba aliyenituma, nami nitamfufua siku ya mwisho. 45 I meandikwa katika manabii, ‘Wote watafundishwa na Mungu.’ Ye yote amsikilizaye Baba na kujifunza kutoka kwake, huyo huja kwangu. 46H akuna mtu ye yote aliyemwona Baba isipokuwa yeye atokaye kwa Mungu, yeye ndiye peke yake aliyemwona Baba. 47 A min, amin nawambia, yeye anayeamini anao uzima wa milele. 48 Mimi ni mkate wa uzima. 49 Baba zenu walikula mana jangwani, lakini wakafa. 50 Lakini hapa kuna mkate utokao mbinguni, ambao mtu ye yote akiula, hatakufa. 51 M imi ni mkate wa uzima ule uliotoka mbinguni. Mtu ye yote akiula mkate huu, ataishi milele. Mkate huu ni mwili wangu, ambao nitautoa kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.” 52 N dipo Wayahudi wakaanza kuhojiana vikali wao kwa wao wakisema, “Mtu huyu awezaje kutupatia mwili wake tuule?” 53 H ivyo Yesu akawaambia, “Amin, amin nawaambia, msipoula mwili wa Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu. 54 Mtu ye yote aulaye mwili wangu na kunywa damu yangu, anao uzima wa milele. Nami nitamfufua siku ya mwisho. 55 Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli na damu yangu ni kinywaji cha kweli. 56 Ye yote alaye mwili wangu na kunywa damu yangu, atakaa ndani yangu nami nitakaa ndani yake. 57 Kama vile Baba aliye hai alivyonituma mimi, na kama nami ninavyoishi kwa sababu ya Baba, hivyo anilaye mimi ataishi kwa sababu yangu. 58 Huu ndio mkate ushukao kutoka mbinguni, si kama ule mkate baba zenu waliokula nao wakafa. 40
YOHANA
TUMAINI
Lakini yeye aulaye mkate huu ataishi milele.” 59 Yesu alisema maneno haya alipokuwa akifundisha katika sinagogi huko Kapernaumu. Wafuasi Wengi Wamwacha Yesu Wengi wa wafuasi wake waliposikia jambo hili wakasema, “Mafundisho haya ni magumu. Ni nani awezaye kuyapokea?” 61 Yesu alipojua kwamba wafuasi wake wananung'unika kuhusu mafundisho yake, akawaambia, “Je, jambo hili limewaudhi? 62 I ngekuwaje basi kama mngemwona Mwana wa Adamu akipaa kwenda zake huko alipokuwa kwanza? 63 Roho ndiye atiaye uzima, mwili haufai kitu. Maneno haya niliyowaambia ni Roho tena ni uzima. 64 L akini baadhi yenu hamwamini.” Kwa maana Yesu alifahamu tangu mwanzo wale ambao hawangemwamini miongoni mwao na yule ambaye angemsaliti. 65 A kaendelea kusema, “Hii ndiyo sababu niliwaambia kwamba hakuna mtu awezaye kuja kwangu isipokuwa amejaliwa na Baba yangu.” 66 T angu wakati huo wafuasi wake wengi wakarejea nyuma wakaacha kumfuata. 67 H ivyo Yesu akawauliza wale wanafunzi wake kumi na wawili, “Je, ninyi pia mnataka kuondoka?” 68 S imoni Petro akamjibu, “Bwana, tuondoke twende kwa nani? Wewe unayo maneno ya uzima wa milele. 69 T unaamini na kujua kuwa wewe ndiwe Kristo Mwana wa Mungu aliye hai.” 70 N dipo Yesu akajibu, “Je, sikuwachagua ninyi kumi na wawili? Lakini mmoja wenu ni ibilisi.” 71 ( Hapa alikuwa anasema juu ya Yuda, mwana wa Simoni Iskariote. Ingawa alikuwa mmoja wa wale kumi na wawili, ndiye ambaye baadaye angemsaliti Yesu.) 60
7
Kutokuamini Kwa Ndugu Zake Yesu
1 B aada ya mambo haya, Yesu alikwenda sehemu mbalimbali za Galilaya. Hakutaka kwenda Uyahudi kwa sababu Wayahudi huko walitaka kumwua. 2S ikukuu ya Vibanda ya Wayahudi ilikuwa imekaribia. 3 H ivyo ndugu zake Yesu wakamwambia, “Ondoka hapa uende Uyahudi ili wanafunzi Wako wapate kuona miujiza unayofanya. 4 Mtu anayetaka kujulikana hafanyi mambo yake kwa siri.
Kama unafanya mambo haya jionyeshe kwa ulimwengu.” 5 H ata ndugu zake mwenyewe hawakumwamini. 6Y esu akawaambia, “Wakati wangu bado haujawadia, lakini wakati wenu upo siku zote. 7 U limwengu hauwezi kuwachukia ninyi, lakini unanichukia mimi kwa sababu ninawashuhudia kwamba matendo yao ni maovu. 8 Ninyi nendeni kwenye Sikukuu, lakini mimi sitahudhuria Sikukuu hii kwa sababu wakati wangu haujawadia.” 9 Akiisha kusema hayo, akabaki Galilaya. Yesu Kwenye Sikukuu Ya Vibanda Lakini ndugu zake walipokwisha kuondoka kwenda kwenye Sikukuu, yeye pia alikwenda lakini kwa siri. 11 Wayahudi walikuwa wakimtafuta huko kwenye Sikukuu na kuulizana, “Yuko wapi huyu mtu?” 12 Kulikuwa na minong'ono iliyoenea kumhusu Yesu katika umati wa watu, wakati wengine wakisema, “Ni mtu mwema.” Wengine walikuwa wakisema, “La, yeye anawadanganya watu.” 13 Lakini hakuna mtu ye yote aliyemsema waziwazi kumhusu kwa sababu ya kuwaogopa Wayahudi. 10
Yesu Afundisha Kwenye Sikukuu I lipokaribia katikati ya Sikukuu, Yesu alipanda kwenda Hekaluni na kuanza kufundisha. 15 Wayahudi wakastaajabia mafundisho yake wakasema, “Mtu huyu amepataje kujua mambo haya bila kufundishwa?” 16 Ndipo Yesu akawajibu, “Mafundisho yangu si yangu mwenyewe, bali yanatoka kwake yeye aliyenituma. 17 Mtu ye yote akipenda kufanya mapenzi ya Mungu, atajua kama mafundisho yangu yanatoka kwa Mungu au ninasema kwa ajili yangu mwenyewe. 18 Wale wanenao kwa ajili yao wenyewe hufanya hivyo kwa kutaka utukufu wao wenyewe. Lakini yeye atafutaye utukufu wa yule aliyemtuma ni wa kweli, wala hakuna uongo ndani yake. 19 Je, Mose hakuwapa ninyi sheria? Lakini hakuna hata mmoja wenu anayeishika hiyo sheria. Kwa nini mnataka kuniua?” 20 U le umati wa watu ukamjibu, “Wewe una pepo mchafu! Ni nani anayetaka kukuua?” 14
6:40 Mt 25:26 6:42 Lk 4:22; Yn 7:27, 28 6:45 Isa 54:13; 1Kor 2:13 6:46 Yn 1:18; 7:29 6:47 Mt 25:46 6:48 Yn 6:35, 51 6:49 Yn 6:3, 58 6:50 Yn 6:33 6:51 Ebr 10:10 6:52 Yn 9:16; 10:19 6:53 Mt 26:26; 8:20; 26:28 6:54 Yn 6:39 6:56 1Yn 2:24; 1Yn 3:24 6:57 Yn 3:17 6:58 Yn 3:36; 5:24 6:60 Yn 6:66; 6:52 6:61 Mt 13:57 6:62 Mk 16:19; Yn 17:5 6:63 2Kor 3:6 6:64 Yn 2:24-25 6:65 Mt 13:11 6:66 Yn 6:60 6:67 Mt 10:2 6:68 Mt 16:16 6:69 Mk 1:24; Lk 9:20 6:70 Yn 15:16-19; Yn 13:27; 17:12 6:71 Mt 26:14; Mt 10:4 7:1 Yn 1:19; 5:18; Mt 12:18 7:2 Law 23:34; Kum 16:16 7:3 Mt 12:46 7:5 Za 69:8; Mk 3:21 7:6 Mt 26:18 7:7 Yn 3:19-20; Yn 15:18-19 7:8 Yn 7:6; Mt 26:18; Yn 8:30 7:11 Yn 11:56 7:12 Yn 9:16; 10:19; Mt 21:46; Lk 7:16; Yn 6:14 7:13 Yn 19:38; 20:19 7:14 Mt 26:55 7:15 Mdo 26:24; Mt 13:54 7:16 Yn 3:11; 14:24 7:17 Za 25:14; Yn 8:23 7:18 Yn 5:41; 8:50-54 7:19 Kum 32:46; Mt 12:14 7:20 Mk 3:22; Yn 10:20
YOHANA
TUMAINI
57
YOHANA 7:37-38 Siku ile ya mwisho ya Sikukuu, siku ile kuu, wakati Yesu akiwa amesimama huko, akapaza sauti yake akasema, “Kama mtu ye yote anaona kiu na aje kwangu anywe. Ye yote aniaminiye mimi, kama maandiko yasemavyo, vijito vya maji ya uzima vitatiririka ndani mwake.” esu akawajibu, “Nimefanya mwujiza Y mmoja na nyote mkastaajabu. 22L akini kwa kuwa Mose aliwaamuru tohara (ingawa kwa kweli haikutoka kwa Mose bali kwa baba zenu wakuu), mnamtahiri mtoto hata siku ya Sabato. 23 Ikiwa mtoto aweza kutahiriwa siku ya Sabato kusudi sheria ya Mose isivunjwe, kwa nini mnanikasirikia kwa kumponya mtu mwili wake wote siku ya Sabato? 24 Acheni kuhukumu mambo kwa jinsi mnavyoona tu, bali hukumuni kwa haki.” 21
Je, Yesu Ndiye Kristo? dipo baadhi ya watu wa Yerusalemu N wakawa wanasema, “Tazameni, huyu si yule mtu wanayetaka kumwua? 26 Mbona yuko hapa anazungumza hadharani na wala hawamwambii neno lo lote? Je, inawezekana viongozi wanafahamu kuwa huyu ndiye Kristo *? 27 Tunafahamu huyu mtu anakotoka, lakini Kristo atakapokuja, hakuna ye yote atakayejua atokako.” 28 Ndipo Yesu, akaendelea kufundisha Hekaluni, akisema, “Ninyi mnanifahamu na kujua nitokako. Mimi sikuja kwa ajili yangu mwenyewe, bali yeye aliyenituma ni wa kweli na ninyi hamumjui. 29 Mimi namjua kwa kuwa nimetoka kwake, naye ndiye aliyenituma.” 30 N dipo wakatafuta kumkamata, lakini hakuna mtu ye yote aliyethubutu kumshika kwa sababu saa yake ilikuwa 25
bado haijawadia. 31 Nao watu wengi wakamwamini, wakasema, “Je, Kristo atakapokuja, atafanya miujiza mikuu zaidi kuliko aliyoifanya mtu huyu?” Walinzi Wanatumwa Kumkamata Yesu
Mafarisayo wakasikia watu wakinong'ona mambo kama hayo kuhusu Yesu, ndipo wao pamoja na viongozi wa makuhani, wakatuma walinzi wa Hekalu waende kumkamata. 33 Y esu akasema, “Mimi bado niko pamoja nanyi kwa kitambo kidogo, kisha nitarudi kwake yeye aliyenituma. 34 Mtanitafuta, lakini hamtaniona, nami niliko, ninyi hamwezi kuja.” 35 Wayahudi wakaulizana wao kwa wao, “Huyu mtu anataka kwenda wapi ambako hatuwezi kumfuata? Je, anataka kwenda kwa Wayunani ambako baadhi ya watu wetu wametawanyikia, akawafundishe Wayunani? 36Y eye ana maana gani anaposema, ‘Mtanitafuta lakini hamtaniona na huko nitakapokuwa ninyi hamwezi kuja?’ ” 32
Mito Ya Maji Ya Uzima Siku ile ya mwisho ya Sikukuu, siku ile kuu, wakati Yesu akiwa amesimama huko, akapaza sauti yake akasema, “Kama mtu ye yote anaona kiu na aje kwangu anywe. 38 Ye yote aniaminiye mimi, kama maandiko yasemavyo, vijito vya maji ya uzima vitatiririka ndani mwake.” 39 Yesu aliposema haya alimaanisha Roho 37
Mtakatifu ambaye wote waliomwamini wangempokea, kwani mpaka wakati huo, Roho alikuwa hajatolewa, kwa kuwa Yesu alikuwa bado hajatukuzwa. Mgawanyiko Miongoni Mwa Watu Waliposikia maneno hayo, baadhi ya watu miongoni mwa ule umati wakasema, “Hakika huyu ndiye yule Nabii.” 41 Wengine wakasema, “Huyu ndiye Kristo!” Lakini wengine wakauliza, “Je, Kristo kwao ni Galilaya? 42J e, Maandiko hayasemi kwamba Kristo atakuja kutoka katika jamaa ya Daudi na kutoka Bethlehemu, mji alioishi Daudi?” 43 Kwa hiyo watu wakagawanyika kwa ajili ya Yesu. 44 B aadhi yao walitaka kumkamata, lakini hakuna aliyethubutu kumgusa. 40
Kutokuamini Kwa Viongozi Wa Wayahudi
45 Hatimaye wale walinzi wa Hekalu wakarudi kwa viongozi wa makuhani na Mafarisayo waliokuwa wamewatuma ili kumkamata Yesu, wakaulizwa, “Mbona hamkumkamata?” 46 Wale walinzi wakajibu, “Kamwe hajanena mtu ye yote kama yeye anenavyo.” 47 Mafarisayo wakajibu, “Je, nanyi pia mmedanganyika? 48 Je, kuna kiongozi ye yote au mmoja wa Mafarisayo ambaye amemwamini? 49 Lakini huu umati wa watu wasiojua Sheria ya Mose, wamelaaniwa.”
7:31 Yn 11:45; Yn 12:11, 42; 2:11 7:33 Yn 16:5, 10, 17, 28 7:34 Yn 8:21; 13:33 7:35 Yak 1:1; Mdo 17:4; 1Pet 1:1 7:36 Yn 7:34 7:37 Law 23:36; Isa 55:1; Ufu 22:17 7:38 Isa 58:1; Yn 4:10 7:39 Yoe 2:28; Mdo 2:17, 33; Yn 20:22; 12:23; Yn 13:31-32 7:40 Mt 2:11; Yn 1:21 7:41 Yn 7:52; 1:21 7:42 Mt 1:1; Mik 5:2; Mt 2:5-6 7:43 Yn 9:16; 10:9 7:44 Yn 7:30 7:45 Yn 7:32 7:46 Mt 7:28 7:47 Yn 7:12 7:48 Yn 12:42
58
TUMAINI
YOHANA 50 Ndipo Nikodemo, yule aliyekuwa amemwendea Yesu siku moja usiku, ambaye alikuwa mmoja wao akauliza, 51“ Je, sheria zetu zinaturuhusu kumhukumu mtu kabla ya kumsikiliza na kufahamu alilotenda?” 52 Wakamjibu, “Je, wewe pia unatoka Galilaya? Chunguza nawe utaona kwamba hakuna nabii atokae Galilaya!” 53 [Kisha wakaondoka, kila mtu akarudi nyumbani kwake.
8
Mwanamke Aliyefumaniwa Akizini
Lakini Yesu akaenda katika Mlima wa Mizeituni. 2 A lfajiri na mapema Yesu akaja tena Hekaluni, watu wote wa ka kusany ika, a ka kaa a kaanza kuwafundisha. 3 Walimu wa sheria na Mafarisayo wakamleta mwanamke mmoja aliyefumaniwa akizini. Wakamsimamisha katikati ya umati wa watu wote. 4 Wakamwambia Yesu, “Mwalimu, huyu mwanamke amekutwa akizini. 5 Katika sheria, Mose alituamuru kuwapiga kwa mawe wanawake wa namna hii, mpaka wafe. Sasa wewe wasemaje?” 6W alimwuliza swali hili kama mtego ili wapate sababu ya kumshtaki. Lakini Yesu akainama akaanza kuandika ardhini kwa kidole chake. 7 W alipoendelea kumwulizauliza akainuka, akawaambia, “Kama kuna mtu ye yote miongoni mwenu ambaye hana dhambi na awe wa kwanza kumtupia jiwe.” 8 Akainama tena na kuandika ardhini. 9W aliposikia haya, wakaanza kuondoka mmoja mmoja, wakianzia wazee, hadi Yesu akabaki peke yake na yule mwanamke akiwa amesimama mbele yake. 10 Yesu akainuka na kumwambia, “Wako wapi wale waliokuwa wanakuhukumu kuwa mwenye hatia?” 11 Y ule mwanamke akajibu, “Hakuna hata mmoja Bwana.” Yesu akamwambia, “Hata mimi sikuhukumu. Nenda zako, kuanzia sasa usitende dhambi tena.”] 1
Yesu Nuru Ya Ulimwengu K isha Yesu akasema nao tena akawaambia, “Mimi ni nuru ya ulimwengu. Mtu ye yote akinifuata hatatembea gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.” 12
Ndipo mtaijua kweli nayo kweli itawaweka huru.
7:50 Yn 3:1 7:51 Kum 1:16, 17; 19:15 7:52 Yn 1:46; 7:41 8:1 Mt 21:1 8:2 Mt 26:55 8:5 Kum 22:22; Ay 31:11 8:6 Mt 22:15-18; 12:10 8:7 Kum 17:7; Eze 16:40; Rum 2:1, 22 8:9 Rum 2:22 8:11 Yn 3:17; 5:14 8:12 Yn 6:35; 12:35; Mit 4:18; Mt 5:14
YOHANA 13 M afarisayo wakamwambia, “Ushuhuda wako haukubaliki kwa kuwa unajishuhudia mwenyewe.” 14 Yesu a kawajibu, “Hata ka ma najishuhudia mwenyewe, ushuhuda wangu ni kweli kwa sababu najua nilikotoka na ninakokwenda. Lakini ninyi hamjui nilikotoka wala ninakokwenda. 15 Ninyi mnahukumu kwa kufuata vipimo vya kibinadamu, mimi simhukumu mtu ye yote. 16 Lakini hata kama nikihukumu, uamuzi wangu ni sahihi kwa sababu sitoi hukumu yangu, bali mimi pamoja na Baba aliyenituma. 17 Imeandikwa katika Sheria yenu kwamba, ushahidi wa watu wawili ni thabiti. 18 Mimi najishuhudia mwenyewe, naye Baba aliyenituma hunishuhudia.” 19 N dipo wakamwuliza, “Huyo Baba yako yuko wapi?” Yesu akawajibu, “Ninyi hamnifahamu mimi ni nani, wala hamumfahamu Baba yangu. Kama mngenifahamu mimi, mngemfahamu na Baba yangu.” 20 Yesu alisema maneno haya alipokuwa a k if undisha kati ka chumba cha hazina Hekaluni. Lakini hakuna mtu aliyemkamata kwa kuwa saa yake ilikuwa haijawadia. Yesu akasema, “ ‘Niendako mimi ninyi hamwezi kufika.’ ”
Yesu Atabiri Kifo Chake Mwenyewe
Yesu akawaambia tena, “Ninaenda zangu, nanyi mtanitafuta, lakini mtakufa katika dhambi zenu. Niendako ninyi hamwezi kuja.” 22 Ndipo wale Wayahudi wakasema, “Je, atajiua? Je, hii ndiyo sababu amesema, ‘Niendako Mimi ninyi hamwezi kuja’?” 23 A kawaambia, “Niny i mmetoka chini, mimi nimetoka juu. Ninyi ni wa ulimwengu huu, mimi si wa ulimwengu huu. 24 N iliwaambia kuwa mtakufa katika dhambi zenu, kwa maana msipoamini ya kwamba ‘Mimi Ndiye,’ mtakufa katika dhambi zenu.” 25 Wakamwuliza, “Wewe ni nani?” Naye Yesu akawajibu, “Mimi ndiye yule ambaye nimekuwa nikiwaambia tangu mwanzo. 26 N ina mambo mengi ya kusema juu yenu na mengi ya kuwahukumu. Lakini yeye aliyenituma ni wa kweli, nami nanena na ulimwengu niliyoyasikia kutoka kwake.” 21
27 Hawakuelewa kuwa alikuwa akiwaambia juu ya Baba yake wa Mbinguni. 28 K isha Yesu akawaambia, “Mtakapokwisha kumwinua juu Mwana wa Adamu, ndipo mtakapojua kuwa, ‘Mimi ndiye yule niliyesema na kwamba mimi sitendi jambo lo lote peke yangu bali ninasema yale tu ambayo Baba yangu amenifundisha. 29Y eye aliyenituma yu pamoja nami, hajaniacha, kwa kuwa siku zote nafanya mapenzi yake.’ ” 30W engi waliomsikia Yesu akisema maneno haya wakamwamini.
Wanafunzi Wa Kweli K isha Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, “Kama mkidumu katika maneno yangu, mtakuwa wanafunzi wangu kweli kweli. 32 Ndipo mtaijua kweli nayo kweli itawaweka huru.” 33 Wao wakamjibu, “Sisi tu wazao wa Abrahamu, nasi hatujawa watumwa wa mtu ye yote. Wawezaje kusema kwamba tutawekwa huru?” 34 Y esu akajibu, “Amin, amin nawaambia, kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi. 35M tumwa hakai nyumbani anakotumika siku zote, lakini mwana hukaa nyumbani daima. 36 H ivyo Mwana akiwaweka huru mtakuwa huru kweli kweli. 37 Ninajua ya kuwa ninyi ni wazao wa Abrahamu, lakini mnatafuta wasaa wa kuniua kwa sababu ndani yenu hamna nafasi ya neno langu. 38 Ninasema yale niliyoyaona mbele za Baba yangu, nanyi inawapa kufanya yale mliyosikia kutoka kwa baba yenu.” 31
Yesu Na Abrahamu akajibu, “Baba yetu ni Abrahamu.” W Yesu akawaambia, “Kama mngekuwa wazao wa Abrahamu mngefanya mambo yale aliyofanya Abrahamu. 40 Lakini sasa ninyi mnatafuta kuniua, mtu ambaye nimewaambia kweli ile niliyosikia kutoka kwa Mungu, Abrahamu hakufanya jambo la namna hii. 41 Ninyi mnafanya mambo afanyayo baba yenu.” Wakamjibu, “Sisi si watoto wa haramu, tunaye Baba mmoja ndiye Mungu.” 42 Yesu akawaambia, “Kama Mungu angekuwa Baba yenu, mngenipenda, kwa maana nilitoka kwa Mungu na sasa niko hapa. Sikuja kwa ajili yangu mwenyewe, ila yeye alinituma. 43 K wa nini hamwelewi 39
TUMAINI
59
ninayowaambia? Ni kwa sababu hamwezi kusikia nisemacho. 44 Ninyi ni watoto wa baba yenu ibilisi, nanyi mnataka kutimiza matakwa ya baba yenu. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo, wala hakushikana na kweli maana hamna kweli ndani yake. Asemapo uongo husema yaliyo yake mwenyewe kwa maana yeye ni mwongo na baba wa huo uongo. 45L akini kwa sababu nimewaambia kweli hamkuniamini! 46 Je, kuna ye yote miongoni mwenu awezaye kunithibitisha kuwa mwenye dhambi? Kama nawaambia yaliyo kweli, mbona hamniamini? 47 Yeye atokaye kwa Mungu husikia kile Mungu asemacho. Sababu ya ninyi kutosikia ni kwa kuwa hamtokani na Mungu.” Maelezo Ya Yesu Kuhusu Yeye Mwenyewe
48 Wayahudi wakamjibu Yesu, “Je, hatuko sahihi tunaposema ya kwamba wewe ni Msamaria na ya kwamba una pepo mchafu?” 49 Yesu akawajibu, “Mimi sina pepo mchafu, bali ninamheshimu Baba yangu, nanyi mnanidharau. 50 L akini mimi sitafuti utukufu wangu mwenyewe, bali yuko anayetaka kunitukuza, naye ndiye mwamuzi. 51 A min, amin nawaambia, mtu ye yote akilitii neno langu hataona mauti milele.” 52 Ndipo Wayahudi wakamwambia, “Sasa tumejua kwamba una pepo mchafu. Ikiwa Abrahamu alikufa na vivyo hivyo manabii, nawe unasema ‘Mtu akitii neno langu hatakufa?’ 53J e, wewe ni mkuu kuliko baba yetu Abrahamu ambaye alikufa na manabii ambao nao pia walikufa? Hivi wewe unajifanya kuwa nani?” 54 Yesu akawajibu, “Kama nikijitukuza utukufu wangu hauna maana. Baba yangu, huyo ambaye ninyi mnadai kuwa ni Mungu wenu, ndiye anitukuzaye mimi. 55 Ingawa hamkumjua, mimi ninamjua. Kama ningesema simjui, ningekuwa mwongo kama ninyi, lakini mimi ninamjua na ninalitii neno lake. 56 B aba yenu Abrahamu alishangilia kwamba angaliiona siku yangu, naye akaiona na akafurahi.” 57 Wayahudi wakamwambia, “Wewe hujatimiza hata miaka hamsini, wewe wasema umemwona Abrahamu?”
8:13 Yn 5:31 8:14 Yn 13:3; 16:28; Yn 7:28; 9:29 8:15 Yn 7:24; 3:17 8:16 Yn 5:30 8:18 Yn 5:37 8:19 Yn 16:3; 14:7; 1Yn 2:23 8:20 Mt 26:18, 55; Mk 12:41; Yn 7:30 8:21 Eze 3:18; Yn 7:34; 13:33 8:22 Yn 7:35 8:23 Yn 3:31; 17:14 8:24 Yn 4:26; 13:19 8:25 Yn 8:14 8:26 Yn 7:28; 3:32; Yn 15:15 8:28 Yn 3:14; 5:19 8:29 Yn 16:32; Isa 50:5; Yn 4:34 8:30 Yn 7:31 8:31 Yn 15:7; 2Yn 1:9 8:32 Gal 5:1, 13; Yak 2:12 8:33 Mk 3:9; Lk 3:8 8:34 Rum 6:16; 2Pet 2:19 8:35 Gal 4:30 8:36 Rum 8:2; Gal 5:1 8:37 Yn 7:19; 8:40 8:38 Yn 5:19, 30; Yn 14:10, 24 8:39 Lk 3:8; Gal 3:7 8:40 Yn 8:37; Yn 8:26 8:41 Isa 63:16; 64:8; Mal 1:6 8:42 1Yn 5:1; Yn 16:27; 7:28; 3:17 8:43 Yn 7:17 8:44 1Yn 3:8; 2Nya 18:21; Za 12:2 8:45 Yn 18:37 8:46 2Kor 5:21; 1Pet 2:22 8:47 Yn 18:37; 1Yn 4:6 8:48 Mt 10:5; Mk 3:22; Yn 7:20 8:50 Yn 7:20; 8:54; 10:20 8:51 Yn 11:26 8:52 Zek 1:5; Ebr 11:13 8:53 Yn 4:12 8:54 Yn 16:14; Yn 17:1-5 8:55 Yn 7:28-29; 15:10 8:56 Mwa 18:18; Mt 13:17; Ebr 11:13
60
TUMAINI
58 Yesu akawaambia, “Amin, amin nawaambia, kabla Abrahamu hajakuwako, ‘Mimi niko.’ ” 59 Ndipo wakaokota mawe ili kumpiga, lakini Yesu akajificha, naye akatoka Hekaluni.
Yesu Amponya Mtu Aliyezaliwa Kipofu
9
Yesu alipokuwa akipita, akamwona mtu aliyekuwa kipofu tangu kuzaliwa. 2W anafunzi wake wakamwuliza, “Rabi, ni nani aliyetenda dhambi, ni huyu mtu au wazazi wake hata azaliwe kipofu?” 3Y esu akawajibu, “Huyu mtu wala wazazi wake hawakutenda dhambi. Alizaliwa kipofu ili kazi za Mungu zidhihirishwe katika maisha yake. 4 Yanipasa kuzifanya kazi zake yeye aliyenituma wakati bado ni mchana, kwa kuwa usiku waja ambapo hakuna mtu awezaye kufanya kazi. 5 Wakati niko ulimwenguni, mimi ni nuru ya ulimwengu.” 6 Baada ya kusema haya, akatema mate ardhini, akatengeneza tope kwa mate na kumpaka yule mtu kipofu machoni. 7 K isha akamwambia, “Nenda ukanawe katika bwawa la Siloamu.” (Siloamu, maana yake ni aliyetumwa.) Ndipo yule kipofu akaenda, akanawa, naye akarudi akiwa anaona. 8M ajirani zake na wale wote waliokuwa wamemwona hapo awali akiombaomba wakaanza kuuliza, “Je, huyu si yule aliyekuwa akiketi akiombaomba?” 9 Wengine wakasema, “Ndiye.” Wengine wa kasema, “Siye, ba li wamefanana.” Lakini yeye akawaambia, “Mimi ndiye.” 10 Wakamwuliza, “Basi macho yako yalifumbuliwaje?” 11 Y eye akawajibu, “Yule mtu aitwaye Yesu alitengeneza tope, akanipaka machoni mwangu, naye akaniambia nenda ukanawe katika Bwawa la Siloamu, ndipo nikanawa nami nikapata kuona!” 12 Wale wakamwuliza, “Yeye huyo mtu yuko wapi?” Akawajibu, “Sijui.” 1
Mafarisayo Wachunguza Kuponywa Kwa Kipofu
13 Wakamleta kwa Mafarisayo yule mtu aliyekuwa kipofu hapo awali. 14 Basi siku hiyo Yesu alipotengeneza tope na kuyafungua macho ya huyo mtu ilikuwa Sabato. 15 Mafarisayo nao wakaanza
YOHANA kumwuliza alivyopata kuponywa. Naye akawaambia, “Alinipaka tope kwenye macho yangu, nikanawa na sasa ninaona.” 16 B aadhi ya Mafarisayo wakasema, “Huyu mtu hatoki kwa Mungu, kwa sababu hashiki Sabato.” Lakini wengine wakasema, “Awezaje mtu mwenye dhambi kufanya miujiza kama hii?” Wakagawanyika. 17 H ivyo wakamwambia tena yule mtu aliyekuwa kipofu, “Wewe ndiwe uliyefumbuliwa macho, wasemaje kuhusu mtu huyo?” Maana macho yako ndiyo yaliyofumbuliwa. Yeye akawajibu, “Yeye ni nabii.” 18 Wale Wayahudi hawakuamini ya kuwa mtu huyo alikuwa kipofu, akapata kuona, mpaka walipowaita wazazi wake. 19 Wakawauliza, “Je, huyu ni mtoto wenu, ambaye mnasema alizaliwa kipofu? Imekuwaje basi sasa anaona?” 20 Wazazi wake wakajibu, “Tunajua ya kuwa huyu ni mtoto wetu na ya kuwa alizaliwa kipofu. 21 Lakini sisi hatujui ni kwa jinsi gani kwamba sasa anaona, wala hatujui ni nani aliyemfungua macho yake. Mwulizeni, yeye ni mtu mzima na anaweza kujieleza mwenyewe.” 22 Wazazi wake walisema hivi kwa sababu waliwaogopa Wayahudi kwani walikuwa wamekubaliana kuwa mtu ye yote atakayemkiri Yesu kuwa ndiye Kristo * atafukuzwa kutoka katika sinagogi. 23 Kwa hiyo wazazi wake wakasema, “Yeye ni mtu mzima. Mwulizeni.” 24 H ivyo kwa mara ya pili wakamwita yule aliyekuwa kipofu, nao wakamwambia, “Mpe Mungu utukufu! Sisi tunafahamu kuwa mtu huyu aliyekuponya ni mwenye dhambi.” 25 Akawajibu, “Mimi sijui kama yeye ni mwenye dhambi. Lakini jambo moja ninalojua, nilikuwa kipofu na sasa ninaona.” 26 Wakamwuliza, “Alikufanyia nini? Aliyafumbuaje macho yako?” 27 A kawajibu, “Tayari nimekwisha kuwaambia, nanyi hamtaki kunisikiliza. Mbona mnataka kusikia tena? Je, ninyi nanyi mnataka kuwa wanafunzi wake?” 28 Ndipo wakamtukana na kusema, “Wewe ndiwe mwanafunzi wake, Sisi ni wanafunzi wa Mose. 29 Tunajua kwamba Mungu alisema na Mose, lakini kwa habari ya mtu huyu hatujui atokako.”
30 Yule mtu akawajibu, “Hili ni jambo la ajabu! Hamjui anakotoka, naye amenifungua macho yangu! 31 Tunajua ya kuwa Mungu hawasikilizi wenye dhambi, lakini huwasikiliza wote wanaomcha na kumtii. 32 Tangu kuumbwa kwa ulimwengu hatujasikia kwamba mtu amemponya ye yote aliyekuwa kipofu. 33 Kama huyu mtu hakutoka kwa Mungu, asingeweza kufanya lo lote.” 34 Wao wakamjibu, “Wewe ulizaliwa katika dhambi kabisa, nawe unajaribu kutufundisha?” Wakamfukuza atoke nje.
Upofu Wa Kiroho Yesu aliposikia kuwa wamemfukuzia nje yule mtu aliyemfumbua macho, alimkuta akamwuliza, “Je, unamwamini Mwana wa Adamu?” 36 Yule mtu akamjibu, “Yeye ni nani ili nipate kumwamini, niambie ili nipate kumwamini.” 37 Y esu akamjibu, “Umekwisha kumwona, naye anayezungumza nawe, ndiye.” 38 Y ule mtu akasema, “Bwana, naamini.” Naye akamwabudu. 39 Y esu akasema, “Nimekuja ulimwenguni humu kwa ajili ya kuhukumu, ili wale walio vipofu wapate kuona, nao wale wanaoona, wawe vipofu.” 40 B aadhi ya Mafarisayo waliokuwa karibu naye wakamsikia na kumwambia, “Je, kweli sisi ni vipofu?” 41 Yesu akawajibu, “Kama mngekuwa vipofu kweli, msingekuwa na hatia ya dhambi, lakini kwa kuwa mnasema, ‘Tunaona,’ basi mna hatia. 35
Mchungaji Mwema “Amin, amin nawaambia, yeye asiyeingia katika zizi la kondoo kwa kupitia kwenye lango, lakini akwea kuingia ndani kwa njia nyingine, ni mwivi na mnyang'anyi. 2 Yeye anayeingia kwa kupitia kwenye lango ndiye mchungaji wa kondoo. 3 Mlinzi humfungulia lango na kondoo huisikia sauti yake. Huwaita kondoo wake kwa majina yao na kuwatoa nje ya zizi. 4 A kiisha kuwatoa wote nje, hutangulia mbele yao na kondoo humfuata kwa kuwa wanaijua sauti yake. 5 Lakini kondoo hawatamfuata mgeni bali watamkimbia, kwa sababu hawaijui sauti ya mgeni.” 6 Yesu alitumia mfano huu,
10
1
8:58 Yn 1:2; 17:5, 24; Kut 3:14; 6:3 8:59 1Sam 30:6; Yn 11:8; 12:36 9:1 Mdo 3:2; 14:8 9:2 Lk 13:2; Mdo 28:4; Eze 18:20; Kut 20:5; Ay 21:19 9:3 Yn 11:14 9:4 Yn 1:9; 12:35 9:5 Yn 8:12 9:6 Mk 7:33; 8:23 9:7 2Fal 5:10; Lk 13:4; Isa 35:5; Yn 11:37 9:8 Mdo 3:2-10 9:11 Yn 9:6, 7 9:14 Mt 12:1-14; Yn 5:9 9:16 Mt 12:2; Yn 7:43; 10:19 9:17 Mt 21:11; Yn 4:19 9:18 Yn 1:19 9:22 Yn 7:13; Lk 6:22; Yn 16:2; 12:42 9:22 Yaani Masiya 9:23 Yn 9:21 9:24 Yos 7:19 9:27 Yn 9:15 9:28 Yn 5:45 9:29 Yn 8:14 9:30 Yn 3:10 9:31 Za 66:18; Yak 5:16-18 9:33 Yn 3:2 9:34 Isa 66:5 9:35 Mt 14:33; 16:16; Mk 1:1; 1Yn 5:13 9:36 Rum 10:14 9:37 Yn 4:26 9:38 Mt 28:9 9:39 Yn 5:22; 3:19; Yn 12:47; Lk 4:18; Mt 13:13 9:40 Rum 2:19 9:41 Yn 15:22-24 10:1 Yn 10:8, 10 10:2 Mk 6:34; Yn 10:11, 14 10:3 Yn 10:4, 5, 14 10:4 Yn 10:3 10:5 Yn 10:27 10:6 Yn 16:25; Yn 16:25
YOHANA lakini wao hawakuelewa hayo aliyokuwa akiwaambia. 7 Kwa hiyo Yesu akasema nao tena akawaambia, “Amin, amin nawaambia, mimi ndimi lango la kondoo. 8 Wote walionitangulia ni wevi na wanyang'anyi, lakini kondoo hawakuwasikia. 9 M imi ndimi lango, ye yote anayeingia zizini kwa kupitia kwangu ataokoka, ataingia na kutoka, naye atapata malisho. 10 Mwivi huja ili aibe, kuua na kuangamiza. Mimi nimekuja ili wapate uzima kisha wawe nao tele. 11 “Mimi ndimi mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo. 12M tu wa kuajiriwa ambaye kondoo si mali yake, amwonapo mbwa mwitu anakuja, hukimbia na kuwaacha kondoo na mbwa mwitu hulishambulia kundi na kulitawanya. 13 Yeye hukimbia kwa sababu ameajiriwa wala hawajali kondoo.
14 “ Mimi ndimi mchungaji mwema. Ninawajua kondoo wangu nao kondoo wangu wananijua. 15 Kama vile Baba anavyonijua mimi, nami ninavyomjua Baba, nami nautoa uhai wangu kwa ajili ya kondoo. 16 Ninao kondoo wengine ambao si wa zizi hili, inanipasa kuwaleta, nao wataisikia sauti yangu, hivyo patakuwa na kundi moja na mchungaji mmoja. 17B aba yangu ananipenda kwa kuwa ninautoa uhai wangu ili niupate tena. 18H akuna mtu aniondoleaye uhai wangu, bali ninautoa kwa hiari yangu mwenyewe. Ninao uwezo wa kuutoa uhai wangu na pia ninao uwezo wa kuutwaa tena. Amri hii nimepewa na Baba yangu.” 1 9 Kw a ma neno hay a Way a hud i waligawanyika. 20 Wengi wao wakasema, “Huyu amepagawa na pepo mchafu, naye amechanganyikiwa.” 21 W engine wakasema, “Haya si maneno ya mtu mwenye pepo mchafu. Je, pepo mchafu aweza kufungua macho ya kipofu?”
TUMAINI
61
Yesu Akataliwa Na Wayahudi Wakati huo ilikuwa Sikukuu ya Kuwekwa wakfu kwa Hekalu, * nao ulikuwa wakati wa majira ya baridi. 23 Naye Yesu alikuwa akitembea ndani ya Hekalu katika ukumbi wa Solomoni. 24 Wayahudi wa ka m kusa ny i k ia wa ka mw u liza, “Utatuweka katika hali ya mashaka mpaka lini? Kama wewe ndiye Kristo * tuambie waziwazi.” 25 Y esu akawajibu, “Nimewaambia, lakini hamwamini. Mambo ninayoyatenda kwa jina la Baba yangu yananishuhudia. 26 L akini hamwamini, kwa sababu ninyi si wa kundi la kondoo wangu. 27 Kondoo wangu huisikia sauti yangu nami nawajua, nao hunifuata, 28 nami ninawapa uzima wa milele, hawataangamia kamwe wala hakuna mtu atakayewapokonya kutoka katika mikono yangu. 29 B aba yangu aliyenipa hawa ni mkuu kuliko wote na hakuna awezaye kuwapokonya kutoka 22
10:7 Za 118:20; Yn 14:6; Mt 7:13; 14 10:8 Yer 23:1-2; Eze 34:2 10:9 Za 118:20; Yn 14:6; 1Kor 3:15 10:10 Yn 1:4; 3:15, 16; 5:40; 20:31; Za 65:11; Rum 5:17 10:11 Za 23:1; Mt 2:6; Yn 15:13; 1Yn 3:16 10:12 Zek 11:16-17 10:14 Kut 33:12; 2Tim 2:19 10:15 Mt 11:27; Yn 15:16 10:16 Isa 56:8; Mdo 10:34-35; Yn 17:20-21; Efe 2:11-19; Eze 34:23; 1Pet 2:25 10:17 Isa 53:7, 8, 12; Ebr 2:9 10:18 Mt 26:53; Flp 2:8; Ebr 5:8 10:19 Yn 6:52 10:20 Mk 3:22; Yn 7:20; 2Fal 9:11 10:21 Mt 4:24; Kut 4:11; Yn 9:32-33 10:22 Sikukuu ya Kuwekwa wakfu kwa Hekalu ni Hanukkah kwa Kiebrania 10:23 Mdo 3:11; 5:12 10:24 Yn 1:19; Lk 22:67 10:24 Yaani Masiya 10:25 Yn 4:26; 4:11 10:26 Yn 8:47 10:27 Yn 10:4, 14 10:28 Yn 6:39 10:29 Yn 17:2, 6, 24; 14:28
YOHANA 10:11
Mimi ndimi mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo.
62
YOHANA
TUMAINI
mikononi mwake. 30 Mimi na Baba yangu tu umoja.” 31 K wa mara nyingine Wayahudi wakainua mawe ili wampige nayo, 32 lakini Yesu akawaambia, “Nimewaonyesha miujiza mingi mikubwa kutoka kwa Baba yangu. Ni ipi katika hiyo mnataka kunipiga mawe?” 33 W ayahudi wakamjibu, “Hatukupigi mawe kwa sababu ya mambo mema uliyotenda, bali ni kwa kuwa umekufuru. Wewe ingawa ni mwanadamu unajifanya kuwa Mungu.” 34 Y esu akawajibu, “Je, haikuandikwa katika Torati ya kwamba, ‘Nimesema kuwa, ninyi ndinyi miungu?’ 35 K ama aliwaita ‘miungu,’ wale ambao neno la Mungu liliwafikia, nayo Maandiko hayawezi kutanguka. 36 Je, mwawezaje kusema kwamba, yule ambaye Baba amemweka wakfu na kumtuma ulimwenguni anakufuru kwa sababu nilisema ‘Mimi ni Mwana wa Mungu?’ 37 I kiwa sifanyi kazi za Baba yangu, basi msiniamini, 38l akini ikiwa nazifanya kazi za Mungu, hata kama hamniamini mimi ziaminini hizo kazi, ili mpate kujua na kuelewa kwamba Baba yu ndani yangu, nami ndani yake.” 39 Ndipo wakajaribu kumkamata kwa mara nyingine, lakini akaponyoka kutoka mikononi mwao. 40 A kaenda tena ng'ambo ya Mto Yordani mpaka mahali pale ambapo Yohana alikuwa akibatiza hapo awali, naye akakaa huko. 41 W atu wengi wakamjia, nao wakawa wakisema, “Yohana hakufanya mwujiza wo wote, lakini kila jambo alilosema kumhusu huyu mtu ni kweli.” 42 N ao wengi wakamwamini Yesu huko.
kutukuzwa kutokana na ugonjwa huu.” 5 Pamoja na hivyo, ingawa Yesu aliwapenda Martha, Maria na Lazaro ndugu yao, 6b aada ya kusikia kwamba Lazaro ni mgonjwa, aliendelea kukawia huko alikokuwa kwa siku mbili zaidi. 7 Ndipo akawaambia wanafunzi wake, “Haya na turudi Uyahudi.” 8W anafunzi wake wakamwambia, “Rabi, Wayahudi walikuwa wanataka kukupiga mawe, nawe unataka kurudi huko?” 9 Yesu akawajibu, “Si kuna saa kumi na mbili za mchana katika siku moja? Wala watembeao mchana hawawezi kujikwaa kwa maana wanaona nuru ya ulimwengu huu. 10 L akini wale watembeao usiku hujikwaa kwa sababu hakuna nuru ndani yao.” 11 B aada ya kusema haya, Yesu akawaambia, “Rafiki yetu Lazaro amelala, lakini nakwenda kumwamsha.” 12 Wanafunzi wakamwambia, “Bwana, kama amelala usingizi ataamka.” 13 Hata hivyo, Yesu alikuwa anazungumzia kuwa Lazaro amekufa, lakini wanafunzi wake hawakuelewa, walidhani kwamba anasema Lazaro amelala usingizi tu. 14 Kwa hiyo Yesu akawaambia waziwazi, “Lazaro amekufa. 15 Hata hivyo nafurahi kwa kuwa sikuwepo huko kabla ya Lazaro kufa, ili mpate kuamini. Lakini sasa twendeni kwake.” 16 Tomasi aliyeitwa Pacha akawaambia wanafunzi wenzake, “Sisi nasi twendeni tukafe pamoja naye.”
Kifo Cha Lazaro Basi mtu mmoja jina lake Lazaro alikuwa mgonjwa. Yeye alikuwa akiishi Bethania kijiji cha Maria na Martha dada zake. 2 Huyu Maria, ambaye Lazaro kaka yake alikuwa mgonjwa, ndiye yule ambaye alimpaka Bwana mafuta na kuifuta miguu yake kwa nywele zake. 3H ivyo hawa dada wawili walituma ujumbe kwa Yesu kumwambia, “Bwana, yule umpendaye ni mgonjwa.” 4 L akini Yesu aliposikia hayo, akasema, “Ugonjwa huu hautaleta mauti bali umetokea ili kudhihirisha utukufu wa Mungu, ili Mwana wa Mungu apate
Yesu Ndiye Ufufuo Na Uzima Yesu alipowasili huko alikuta Lazaro amekwisha kuwako kaburini siku nne. 18 B asi Bethania ulikuwa karibu na Yerusalemu umbali wa karibu maili mbili *, 19 Wayahudi wengi walikuwa wamekuja kuwafariji Martha na Maria kwa ajili ya kufiwa na ndugu yao. 20 M artha aliposikia kwamba Yesu anakuja, alitoka kwenda kumlaki, ila Maria alibaki nyumbani. 21 Martha akamwambia Yesu, “Bwana, kama ungalikuwa hapa, ndugu yangu hangalikufa. 22 Lakini sasa ninajua kuwa cho chote utakachomwomba Mungu, atakupa.”
11
1
17
23 Yesu akamwambia, “Ndugu yako atafufuka.” 24 Martha akamjibu, “Ninajua ya kuwa atafufuka wakati wa ufufuo wa wafu siku ya mwisho.” 25 Yesu akamwambia, “Mimi ndiye huo ufufuo na uzima. Yeye aniaminiye mimi, hata akifa atakuwa anaishi 26 na ye yote aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je, unasadiki haya?” 27 M artha a kamwambia, “Ndiyo Bwana, ninaamini ya kuwa wewe ndiwe Kristo *, Mwana wa Mungu, yeye ajaye ulimwenguni.”
Yesu Alia B aada ya kusema haya Martha alikwenda, akamwita Maria dada yake faraghani na kumwambia, “Mwalimu yuko hapa anakuita.” 29 Maria aliposikia hivyo, akaondoka upesi akaenda mpaka alipokuwa Yesu. 30 Yesu alikuwa hajaingia kijijini, bali alikuwa bado yuko mahali pale alipokutana na Martha. 31W ale Wayahudi waliokuwa pamoja na Maria nyumbani wakimfariji walipoona ameondoka haraka na kutoka nje, walimfuata wakidhani ya kwamba alikuwa anakwenda kule kaburini kulilia huko. 32 M aria alipofika mahali pale Yesu alipokuwa, alipiga magoti miguuni Pake na kusema, “Bwana, kama ungalikuwa hapa, ndugu yangu hangalikufa.” 33 Yesu alipomwona Maria akilia na wale Wayahudi waliokuja pamoja naye pia wakilia, Yesu alisikia uchungu moyoni, akafadhaika sana. 34 Akauliza, “Mmemweka wapi?” Wakamwambia, “Bwana, njoo upaone.” 35 Yesu akalia machozi. 36 N dipo Wayahudi wakasema, “Tazama jinsi alivyompenda Lazaro!” 37 L akini wengine wakasema, “Je, yule aliyefungua macho ya kipofu, hakuweza kumfanya na huyu asife?” 28
Yesu Amfufua Lazaro Yesu kwa mara nyingine akiwa amefadhaika sana, akafika penye kaburi. Hilo kaburi lilikuwa pango ambalo jiwe lilikuwa limewekwa penye ingilio lake. 39 Yesu akasema, “Liondoeni hilo jiwe.” 38
10:30 Kum 6:4; Yn 17:21-24 10:31 Yn 8:59 10:33 Law 24:16; Mt 26:63-66 10:34 Rum 3:19; 1Kor 14:21; Za 82:6 10:35 Rum 13:1; Mt 5:17, 18 10:36 Yer 1:5; Yn 6:69; 3:17 10:37 Yn 15:24 10:38 Yn 14:10-11; Yn 20:17-21 10:39 Yn 7:30; Lk 4:30; Yn 8:59 10:40 Yn 1:28 10:41 Yn 2:1; Yn 1:26-34 10:42 Yn 7:31 11:1 Mt 21:17; Lk 10:38 11:2 Mk 14:3; Lk 7:3811:3 Yn 11:5, 36 11:4 Yn 11:40 11:6 Yn 10:40 11:7 Yn 10:40 11:8 Mt 23:7; Yn 8:59; Yn 10:31 11:9 Yn 9:4; 12:35 11:10 Yn 12:35 11:11 Mt 9:24; Lk 8:52 11:13 Mt 9:24 11:16 Mt 10:3; Mdo 1:13 11:17 Yn 11:6, 39 11:18 Yn 11:1; Mt 21:17 11:18 Maili mbili ni kama kilomita tatu 11:19 Yn 11:31; Ay 2:11 11:20 Lk 10:3842 11:21 Yn 11:32, 37 11:22 Yn 11:41, 42 11:24 Dan 12:2; Mdo 24:15 11:25 Yn 1:4 11:26 Yn 3:15; Mt 25:46 11:27 Lk 2:11; Mt 4:3; 16:16; Yn 6:14 11:27 Yaani Masiya 11:28 Mt 26:18; Yn 13:13 11:30 Yn 11:20; Yn 13:13 11:31 Yn 11:19; 8:59 11:32 Yn 11:21; 5:18 11:33 Yn 11:38; Yn 12:27; 13:21 11:35 Lk 19:41 11:36 Yn 11:3 11:37 Yn 9:6, 7; Yn 11:21, 32 11:38 Yn 11:33; Mt 27:60; Lk 24:2; Yn 20:1 11:39 Yn 11:17
YOHANA Martha ndugu yake yule aliyekuwa amekufa akasema, “Lakini Bwana, wakati huu atakuwa ananuka kwani amekwisha kuwako kaburini siku nne.” 40 Yesu akamwambia, “Sikukuambia kwamba kama ukiamini utauona utukufu wa Mungu?” 41 Kwa hiyo wakaliondoa lile jiwe kutoka penye kaburi. Yesu akainua macho yake juu akasema, “Baba, ninakushukuru kwa kuwa wanisikia. 42N inajua ya kuwa wewe hunisikia siku zote, lakini nimesema haya kwa ajili ya umati huu uliosimama hapa, ili wapate kuamini ya kuwa wewe umenituma.” 43 Baada ya kusema haya, Yesu akapaza sauti yake akaita, “Lazaro, njoo huku!” 44 Yule aliyekuwa amekufa akatoka nje, mikono yake na miguu yake ikiwa imeviringishiwa vitambaa vya kitani na leso usoni pake. Yesu akawaambia, “Mfungueni, mwacheni aende zake.” Shauri La Kumwua Yesu Hivyo Wayahudi wengi waliokuwa wamekuja kumfariji Maria, walipoona yale Yesu aliyoyatenda wakamwamini. 46 Lakini baadhi yao wakaenda kwa Mafarisayo na kuwaambia mambo Yesu aliyoyafanya. 47 Kwa hiyo viongozi wa makuhani na Mafarisayo wakaita mkutano wa baraza, wakaulizana, “Tufanyeje? Huyu mtu anafanya ishara nyingi. 48 Kama tukimwacha aendelee hivi, kila mtu atamwamini, nao Warumi watakuja na kupaharibu mahali petu patakatifu na taifa letu.” 49 M moja wao, aliyeitwa Kayafa, ambaye alikuwa Kuhani Mkuu mwaka huo akasema, “Ninyi hamjui kitu cho chote! 50 H amjui kwamba ni afadhali mtu mmoja afe kwa ajili ya watu, kuliko taifa lote liangamie?” 51 Hakusema haya kutokana na mawazo yake mwenyewe bali kama Kuhani Mkuu mwaka huo, alitabiri kuwa Yesu angelikufa kwa ajili ya Wayahudi, 52 wala si kwa ajili ya Wayahudi peke yao, bali pia kwa ajili ya watoto wa Mungu waliotawanyika, ili kuwaleta pamoja na kuwafanya wawe wamoja. 53 H ivyo tangu siku hiyo wakawa wanafanya mipango ili wamwue Yesu. 45
TUMAINI
63
Yesu akamwambia, Mimi ndiye huo ufufuo na uzima. Yeye aniaminiye mimi, hata akifa atakuwa anaishi
YOHANA 11:25
54 Kwa hiyo Yesu akawa hatembei hadharani miongoni mwa Wayahudi, bali alijitenga akaenda sehemu iliyo karibu na jangwa kwenye kijiji kiitwacho Efraimu. Akakaa huko na wanafunzi wake. 55 Basi Pasaka ya Wayahudi ilipokuwa imekaribia, watu wengi walitoka vijijini wakaenda Yerusalemu kabla ya Pasaka ili wakajitakase. 56W atu wakawa wanamtafuta Yesu, nao waliposimama kwenye eneo la Hekalu waliulizana, Je, mtu huyu hatakuja kamwe kwenye Sikukuu? 57 Viongozi wa makuhani na Mafarisayo walikuwa wametoa amri kuwa ye yote atakayejua mahali Yesu aliko, lazima atoe taarifa ili wapate kumkamata.
12
Maria Ampaka Yesu Mafuta Huko Bethania
1 Siku sita kabla ya Pasaka, Yesu alikwenda Bethania mahali ambako Lazaro aliyekuwa amefufuliwa na Yesu alikuwa anaishi. 2 W akaandaa karamu kwa heshima ya Yesu. Martha akawahudumia wakati Lazaro alikuwa miongoni mwa waliokaa mezani pamoja na Yesu. 3 Kisha Maria akachukua chupa ya painti moja * yenye manukato ya nardo * safi ya thamani kubwa akayamimina miguuni mwa Yesu na
kuifuta kwa nywele zake. Nyumba nzima ikajaa harufu nzuri ya manukato. 4N dipo Yuda Iskariote mwana wa Simoni, mmoja wa wale wanafunzi ambaye ndiye atakayemsaliti Yesu, akasema, 5 “Kwa nini manukato haya hayakuuzwa kwa dinari 300 * na fedha hizo wakapewa maskini?” 6 Yuda alisema hivi si kwa kuwa aliwajali maskini, bali kwa kuwa alikuwa mwivi, kwani ndiye aliyekuwa akitunza mfuko wa fedha akawa anaiba kile kilichowekwa humo. 7Y esu akasema, “Mwacheni. Aliyanunua manukato hayo ili ayaweke kwa ajili ya siku ya maziko yangu. 8 Maskini mnao siku zote lakini mimi hamko pamoja nami siku zote.” Shauri La Kumwua Lazaro U mati mkubwa wa Wayahudi walipojua kwamba Yesu alikuwa huko Bethania, walikuja si tu kwa ajili ya Yesu, lakini pia kumwona Lazaro ambaye Yesu alikuwa amemfufua. 10 Kwa hiyo viongozi wa makuhani wakafanya mpango wa kumwua Lazaro pia, 11 k wa kuwa kutokana na habari za kufufuliwa kwake Wayahudi wengi walikuwa wanamwendea Yesu na kumwamini. 9
11:40 Yn 11:23-25 11:41 Yn 17:1; Mt 11:25 11:42 Yn 12:30; Yn 3:17 11:43 Lk 7:14 11:44 Yn 19:40; 20:7 11:45 Yn 11:19; Yn 2:23; 14 11:47 Yn 2:11 11:49 Lk 3:2; Yn 18:14; Mdo 4:6 11:50 Yn 18:14 11:51 Mwa 50:20; Kut 28:30; Hes 27:21 11:52 Isa 49:6; Yn 10:16 11:53 Mt 12:14 11:54 Yn 7:1 11:55 Kut 12:13, 23, 27; Mk 14:1; 2Nya 30:17-18 11:56 Yn 7:11; Yn 17:7 12:1 Yn 11:55; Mt 21:17 12:2 Lk 10:38-42 12:3 Yn 11:12 12:3 Painti moja ni kama nusu lita 12:3 Nardo ni aina ya mafuta yaliyokuwa yanatengenezwa kutokana na mimea yenye mizizi inayotoa harufu nzuri 12:4 Mt 10:4 12:5 Dinari 300 ni sawa na mshahara wa kibarua wa siku 300 12:6 Yn 13:29 12:7 Yn 19:40 12:8 Kum 15:11 12:9 Yn 11:43, 44 12:10 Lk 16:31 12:11 Yn 11:45; 12:18
64
Kuingia Kwa Yesu Yerusalemu Kwa Ushindi
12 S iku iliyofuata umati mkubwa uliokuwa umekuja kwenye Sikukuu walisikia kwamba Yesu angekuja Yerusalemu. 13B asi wakachukua matawi ya mitende wakatoka kwenda kumlaki, huku wakipaza sauti wakisema, “Hosana *!” “Amebarikiwa yeye ajaye kwa Jina la Bwana!” “Amebarikiwa Mfalme wa Israeli!” 14 Yesu a k a m k uta mwa na-pu nda akampanda, kama ilivyoandikwa, 15 “Usiogope, Ewe binti Sayuni; tazama, Mfalme wako anakuja, amepanda mwana-punda!” 16 Wanafunzi wake Yesu mwanzoni hawakuelewa mambo haya, lakini Yesu alipotukuzwa, ndipo walipokumbuka kuwa mambo haya yalikuwa yameandikwa kwa ajili yake na alitendewa yeye. 17 Wale waliokuwepo wakati Yesu alipomwita Lazaro kutoka kaburini na kumfufua kutoka kwa wafu, waliendelea kushuhudia. 18N i kwa sababu pia walikuwa wamesikia kwamba alikuwa ametenda mwujiza huu ndiyo maana umati wa watu ukaenda kumlaki. 19 Hivyo Mafarisayo walipoona hayo wakaambiana, “Mnaona, hamwezi kufanya lo lote. Angalieni, ulimwengu wote unamfuata yeye!”
Yesu Anatabiri Kifo Chake Basi palikuwapo Wayunani fulani miongoni mwa wa le wa liokuwa wamekwenda kuabudu wakati wa Sikukuu. 21 Hawa wakamjia Filipo, ambaye alikuwa mwenyeji wa Bethsaida huko Galilaya, wakiwa na ombi, wakamwambia, “Tungependa kumwona Yesu.” 22 Filipo akaenda akamweleza Andrea, nao wote wawili wakamwambia Yesu. 23 Yesu akawajibu, “Saa imewadia ya Mwana wa Adamu kutukuzwa. 24 Amin, amin nawaambia, mbegu ya ngano isipoanguka ardhini na kufa, hubakia kama mbegu peke yake. Lakini ikifa huzaa mbegu nyingi. 25 Mtu ye yote anayependa maisha yake atayapoteza, naye ayachukiaye maisha yake katika ulimwengu huu atayaokoa hata uzima wa milele. 26 Mtu ye 20
YOHANA
TUMAINI
yote akinitumikia lazima anifuate, nami mahali nilipo ndipo mtumishi wangu atakapokuwa. Mtu akinitumikia, Baba yangu atamheshimu. 27 “Sasa roho yangu imefadhaika sana. Niseme nini? ‘Baba, niokoe na saa hii.’ Lakini, ni kwa kusudi hili nimeufikia wakati huu. 28 Baba, litukuze jina lako.” Ndipo ikaja sauti kutoka mbinguni, “Nimelitukuza, nami nitalitukuza tena.” 29 U le umati wa watu uliokuwa mahali pale uliisikia nao ukasema, “Hiyo ni sauti ya radi,” wengine wakasema, “Malaika ameongea naye.” 30 Y esu akawaambia, “Sauti hii imesikika kwa faida yenu, wala si kwa faida yangu. 31 S asa ni saa ya hukumu kwa ajili ya ulimwengu huu, sasa mkuu wa ulimwengu huu atatupwa nje. 32 L akini mimi, nikiinuliwa kutoka katika nchi, nitawavuta watu wote waje kwangu.” 33 Y esu aliyasema haya akionyesha ni kifo gani atakachokufa. 34 U le umati wa watu ukapiga kelele ukasema, “Tumesikia kutoka katika Torati kwamba ‘Kristo * adumu milele,’ wewe wawezaje kusema, ‘Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa juu?’ Huyu ‘Mwana wa Adamu ni nani?’ ” 35 N dipo Yesu akawaambia, “Bado kitambo kidogo nuru ingalipo pamoja nanyi. Enendeni maadamu mna nuru, msije mkakumbwa na giza. Mtu anayetembea gizani hajui anakokwenda. 36W ekeni tumaini lenu katika nuru hiyo ili mpate kuwa wana wa nuru.” Baada ya kusema haya, Yesu aliondoka, akajificha wasimwone. Wayahudi Waendelea Kutokuamini H ata baada ya Yesu kufanya miujiza hii yote mbele yao, bado hawakumwamini. 38 H ii ilikuwa ili kutimiza lile neno la nabii Isaya lililosema: “Bwana, ni nani aliyesadiki ujumbe wetu na mkono wa Bwana amefunuliwa nani?” 39 Kwa hivyo hawakuamini, kwa sababu Isaya anasema mahali pengine: 40 “Amewafanya vipofu na kuifanya mioyo yao kuwa migumu, ili wasiweze kuona kwa macho yao, 37
wala kuelewa kwa mioyo yao, wasije wakageuka, nami nikawaponya.” 41 I saya alisema haya alipoona utukufu wa Yesu na kunena habari zake. 42 L akini wengi miongoni mwa viongozi wa Wayahudi walimwamini, lakini kwa sababu ya Mafarisayo hawakukiri waziwazi kwa maana waliogopa kufukuzwa katika masinagogi. 43 Wao walipenda sifa za wanadamu kuliko sifa zitokazo kwa Mungu. Amwaminiye Yesu Hatabaki Gizani
Yesu akapaza sauti akasema, “Ye yote aniaminiye, haniamini mimi peke yangu, bali yeye aliyenituma. 45 Ye yote anionaye mimi, amemwona yeye aliyenituma. 46 M imi nimekuja kama nuru ulimwenguni, ili kwamba kila mtu aniaminiye asibaki gizani. 47“ Mimi simhukumu mtu ye yote anayesikia maneno yangu na asiyatii, kwa maana sikuja kuuhukumu ulimwengu, bali kuuokoa. 48 Y uko amhukumuye yeye anikataaye mimi na kutokuyapokea maneno yangu, yaani, yale maneno niliyosema yenyewe yatamhukumu siku ya mwisho. 49 Kwa maana sisemi kwa ajili yangu mwenyewe, bali Baba aliyenituma aliniamuru ni nini cha kusema na jinsi ya kukisema. 50N ami ninajua amri zake huongoza hadi kwenye uzima wa milele. Hivyo lo lote nisemalo, ndilo lile Baba aliloniambia niseme.” 44
Yesu Awanawisha Wanafunzi Wake Miguu
13
1 I likuwa mara tu kabla ya Sikukuu ya Pasaka. Yesu alijua ya kuwa wakati wake wa kuondoka ulimwenguni ili kurudi kwa Baba umewadia. Alikuwa amewapenda watu wake waliokuwa ulimwenguni, naam, aliwapenda hadi kipimo cha mwisho. 2W akati alipokuwa akila chakula cha jioni na wanafunzi wake, ibilisi alikuwa amekwisha kutia ndani ya moyo wa Yuda Iskariote, mwana wa Simoni, wazo la kumsaliti Yesu. 3Y esu akijua ya kwamba Baba ameweka vitu vyote chini ya mamlaka yake na kwamba yeye alitoka kwa Mungu na alikuwa anarudi kwa Mungu, 4 hivyo aliondoka chakulani, akavua vazi lake la nje, akajifunga kitambaa kiunoni. 5 K isha akamimina maji kwenye
12:12 Mt 21:8; Mk 11:8; Lk 19:35, 36 12:13 Za 118:25-26; Yn 1:49 12:13 Kiebrania kusema Okoa, basi likawa neno la shangwe 12:14 Mt 21:7 12:15 Zek 9:9 12:16 Lk 18:34; Yn 7:39 12:17 Yn 11:42 12:18 Yn 12:11; 19:37 12:19 Yn 11:47, 48 12:20 Yn 7:35; Mdo 11:20 12:21 Mt 11:21; Yn 1:44 12:23 Yn 13:32; 17:1 12:24 1Kor 15:36 12:25 Mk 8:35; Lk 14:26 12:26 Flp 1:23 12:27 Mt 26:38, 39; Lk 12:50; Yn 13:21; Lk 22:53; Yn 18:37 12:28 Mt 3:17 12:29 Lk 22:43 12:30 Kut 19:9 12:31 Yn 16; 11; Efe 2:2; 1Yn 5:19 12:32 Isa 11:10; Yn 3:14; 6:44 12:33 Yn 18:32; 21:19 12:34 Za 110:4; Isa 9:7; Mt 8:20; Yn 3:14 12:34 Yaani Masiya 12:35 Yn 1:9; 8:12; 9:5; Yer 13:16; Efe 5:8; 1Yn 2:11 12:36 Lk 16:8; Efe 5:8; 1The 5:5; 1Yn 2:9, 10, 11; Yn 8:59; 11:54 12:37 Yn 2:11 12:38 Isa 53:1; Rum 10:16 12:39 Isa 6:9, 10; Mt 13:14, 15 12:40 Isa 6:10; Mt 13:13, 15 12:41 Isa 6:1-4; Lk 24:27 12:42 Yn 7:48; 9:22 12:43 Yn 5:44; Rum 2:29 12:44 Mt 10:40; Yn 5:24 12:45 Yn 14:9 12:46 Yn 3:19; Yn 8:12 12:47 Yn 3:17 12:48 Yn 5:45 12:49 Yn 14:31 12:50 Yn 8:26, 28 13:1 Yn 11:55; 12:33; 16:28 13:2 Lk 22:3 13:3 Mt 28:18; Yn 8:42; 17:8 13:4 Mt 11:29; 20:29; Lk 12:37 13:5 Lk 7:44
YOHANA sinia na kuanza kuwanawisha wanafunzi wake miguu na kuikausha kwa kile kitambaa alichokuwa amejifunga kiunoni. 6 A lipomfikia Simoni Petro, Petro a ka mwa mbia, “Bwa na, je, wewe utaninawisha mimi miguu?” 7 Yesu akamjibu, “Hivi sasa hutambui lile nina lofanya, la k ini baadaye utaelewa.” 8 P etro akamwambia, “La, wewe hutaninawisha miguu kamwe.” Yesu akamjibu, “Kama nisipokunawisha, wewe huna sehemu nami.” 9 Nd ipo Si moni Pet ro a k ajibu, “Usininawishe miguu peke yake, bali pamoja na mikono na kichwa pia!” 10 Yesu akamjibu, “Mtu aliyekwisha kuoga anahitaji kunawa miguu tu, kwani mwili wake wote ni safi. Ninyi ni safi, ingawa si kila mmoja wenu.” 11 Kwa kuwa yeye alijua ni nani ambaye angemsaliti, ndiyo sababu akasema si kila mmoja aliyekuwa safi. 12 Alipomaliza kuwanawisha miguu yao, alivaa tena mavazi yake, akarudi alikokuwa ameketi, akawauliza, “Je, mmeelewa nililowafanyia? 13 Ninyi mnaniita mimi ‘Mwalimu’ na ‘Bwana,’ hii ni sawa, maana ndivyo nilivyo. 14 Kwa hiyo, ikiwa mimi niliye Bwana wenu na Mwalimu wenu nimewanawisha ninyi miguu, pia hamna budi kunawishana miguu ninyi kwa ninyi. 15 M imi nimewawekea kielelezo kwamba imewapasa kutenda kama vile nilivyowatendea ninyi. 16 A min, amin nawaambia, mtumishi si mkuu kuliko bwana wake, wala anayetumwa si mkuu kuliko yule aliyemtuma. 17 S asa kwa kuwa mmejua mambo haya, heri yenu ninyi kama mkiyatenda. 18 “ Sisemi kuhusu ninyi nyote. Ninawajua wale niliowachagua. Lakini ni ili maandiko yapate kutimia, ‘Yeye aliyekula chakula changu, ameinua kisigino chake dhidi yangu.’ 19 “Ninawaambia mambo haya kabla hayajatukia, ili yatakapotukia mpate kuamini ya kuwa Mimi ndiye. 20 A min, amin, nawaambia, ye yote anayempokea yule niliyemtuma, anipokea mimi, naye anipokeaye mimi ampokea yeye aliyenituma mimi.”
Yesu Anatabiri Kusalitiwa Kwake B aada ya kusema haya, Yesu alifadhaika sana moyoni, akasema, “Amin, amin, nawaambia, mmoja wenu atanisaliti.” 22 Wanafunzi wake wakatazamana bila kujua kuwa alikuwa anamsema nani. 23 M moja wa wanafunzi wake, ambaye Yesu alimpenda sana alikuwa ameegama kifuani mwa Yesu. 24 Simoni Petro akampungia mkono yule mwanafunzi akamwambia, “Mwulize anamaanisha ni nani.” 25 Y ule mwanafunzi akiwa amemwegemea Yesu akamwuliza, “Bwana tuambie ni nani?” 26 Yesu akajibu, “Ni yule nitakayempa hiki kipande cha mkate baada ya kukichovya kwenye bakuli.” Hivyo baada ya kukichovya kile kipande cha mkate, akampa Yuda, mwana wa Simoni Iskariote. 27 M ara tu baada ya kukipokea kile kipande cha mkate, Shetani akamwingia. Yesu akamwambia Yuda, “Lile unalotaka kulitenda litende haraka.” 28 Hakuna hata mmoja wa wale waliokuwa ameketi nao chakulani aliyeelewa kwa nini Yesu alimwambia hivyo. 29 Kwa kuwa Yuda alikuwa mtunza fedha, wengine walifikiri Yesu alikuwa amemwambia akanunue vitu vilivyohitajika kwa ajili ya Sikukuu, au kuwapa maskini cho chote. 30M ara tu baada ya kupokea ule mkate, Yuda akatoka nje. Wakati huo ulikuwa ni usiku.
TUMAINI
65
21
Yesu Atabiri Petro Kumkana B aada ya Yuda kutoka nje, Yesu akasema, “Sasa Mwana wa Adamu ametukuzwa, naye Mungu ametukuzwa ndani yake. 32 Ikiwa Mungu ametukuzwa ndani ya Mwana, Mungu atamtukuza Mwana ndani yake mwenyewe naye atamtukuza mara. 33 “ Watoto wangu, mimi bado niko pamoja nanyi kwa kitambo kidogo. Mtanitafuta na kama vile nilivyowaambia Wayahudi, vivyo hivyo sasa nawaambia na ninyi. Niendako, ninyi hamwezi kuja. 34 “ Amri mpya nawapa: Mpendane kama mimi nilivyowapenda ninyi, vivyo hivyo nanyi mpendane. 35 Kama mkipendana ninyi kwa ninyi, kwa njia hii, watu wote watajua kuwa ninyi ni wanafunzi wangu.” 36 Simoni Petro akamwuliza, “Bwana, unakwenda wapi?”
YOHANA
12:44, 46
31
13:6 1Pet 5:5 13:7 Yn 13:12 13:8 Yn 3:5; 1Kor 6:11; Efe 5:26; Tit 3:5; Ebr 10:22 13:10 Yn 15:3 13:11 Mt 10:4 13:13 Mt 26:18; Yn 11:28; Mdo 10:36 13:14 1Pet 5:5 13:15 Mt 11:29; 1Tim 4:12 13:16 Mt 10:24; Lk 6:40 13:17 Lk 11:28; 1:25 13:18 Za 41:9; Mt 26:23 13:19 Yn 14:29; 16:4; Yn 4:26; 8:24 13:20 Mt 10:40; Lk 10:16 13:21 Yn 12:27; Mt 26:21 13:23 Yn 20:2; Yn 21:7, 20 13:25 Mt 26:22; Yn 21:20 13:26 Mt 10:4 13:27 Lk 22:3 13:29 Yn 12:6 13:30 Lk 22:53 13:31 Yn 7:39; 12:23; Yn 17:4; 1Pet 4:11 13:32 Yn 17:1 13:33 Yn 7:33, 34 13:34 1Yn 2:7-11; 3:11; Law 19:18; 1The 4:9; Efe 5:2; 1Yn 4:10, 11; 2:14 13:35 Yn 3:14; Yn 4:20 13:36 Yn 16:5; 14:2; 21:18, 19; 2Pet 1:4
Yesu akapaza sauti akasema, “Ye yote aniaminiye, haniamini mimi peke yangu, bali yeye aliyenituma. Mimi nimekuja kama nuru ulimwenguni, ili kwamba kila mtu aniaminiye asibaki gizani.
66
YOHANA
TUMAINI
YOHANA 14:6 Yesu akawaambia, “Mimi ndimi njia na kweli na uzima. Mtu hawezi kuja kwa Baba isipokuwa kwa kupitia kwangu.
Yesu akamjibu, “Ninakokwenda huwezi kunifuata sasa, lakini utanifuata baadaye.” 37 Petro akamwuliza tena, “Bwana, kwa nini siwezi kukufuata sasa? Mimi niko tayari kuutoa uhai wangu kwa ajili yako.” 38 Y esu akamjibu, “Je, ni kweli uko tayari kuutoa uhai wako kwa ajili yangu? Amin, amin nakuambia, kabla jogoo hajawika, utanikana mara tatu.” Yesu Awatia Moyo Wanafunzi Wake
14
Yesu akawaambia, “Msifadhaike mioyoni mwenu, mnamwamini Mungu, niaminini na mimi pia. 2N yumbani kwa Baba yangu kuna makao mengi. Kama sivyo, ningeliwaambia. Nakwenda kuwaandalia makao. 3 Nami nikienda na kuwaandalia makao, nitarudi tena na kuwachukua mkae pamoja nami, ili mahali nilipo, nanyi mpate kuwepo. 4 Ninyi mnajua njia ya kufika ninakokwenda.” 1
Yesu Ndiye Njia Ya Kwenda Kwa Baba
Tomasi akamwam bia, “Bwana, sisi hatujui unakokwenda, tutaijuaje njia?” 6Y esu akawaambia, “Mimi ndimi njia na kweli na uzima. Mtu hawezi kuja kwa Baba isipokuwa kwa kupitia kwangu. 7 Kama mngenijua mimi, mngemjua na Baba pia. Tangu sasa, mnamjua Baba yangu, tena mmemwona.” 8F ilipo akamwambia, “Bwana, tuonyeshe Baba yako yatosha.” 5
9 Yesu akamjibu, “Filipo, nimekaa nanyi muda huu wote hata usinijue? Mtu ye yote aliyeniona mimi, amemwona Baba. Sasa wawezaje kusema, ‘Tuonyeshe Baba?’ 10 Je, huamini ya kuwa mimi niko ndani ya Baba, naye Baba yuko ndani yangu? Maneno ninayowaambia siyasemi kwa ajili yangu mwenyewe, bali Baba akaaye ndani yangu ndiye atendaye hizi kazi. 11 Nisadiki mimi kwamba niko ndani ya Baba na Baba yuko ndani yangu, la sivyo, niaminini kwa sababu ya zile kazi nizitendazo. 12 A min, amin nawaambia, ye yote aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo yeye atazifanya, naam na kubwa kuliko hizi atazifanya, kwa sababu mimi ninakwenda kwa Baba. 13 Nanyi mkiomba lo lote kwa Jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba apate kutukuzwa katika Mwana. 14 Kama mkiniomba lo lote kwa Jina langu nitalifanya.
Yesu Aahidi Roho Mtakatifu “ Kama mnanipenda, mtazishika amri zangu. 16 Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine akae nanyi milele. 17H uyo ndiye Roho wa kweli ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa sababu haumwoni wala haumjui. Ninyi mnamjua kwa kuwa yuko pamoja nanyi naye anakaa ndani yenu. 18S itawaacha ninyi yatima, naja kwenu. 19B ado kitambo kidogo ulimwengu hautaniona tena, ila ninyi mtaniona, kwa kuwa mimi ni hai, ninyi nanyi mtakuwa hai. 20 Wakati huo mtajua ya kuwa mimi niko ndani ya Baba na ninyi mko ndani 15
yangu na mimi niko ndani yenu. 21 Y e yote mwenye amri zangu na kuzishika ndiye anipendaye, naye anipendaye atapendwa na Baba yangu, nami nitampenda na kujidhihirisha kwake.” 22 N dipo Yuda, siyo Iskariote, akamwambia, “Bwana, itakuwaje kwamba utajidhihirisha kwetu na si kwa ulimwengu?” 23 Yesu akamjibu, “Mtu ye yote akinipenda atalishika neno langu na Baba yangu atampenda, nasi tutakuja kwake na kufanya makao yetu kwake. 24 Mtu ye yote asiyenipenda hayashiki maneno yangu na maneno niliyowapa si yangu bali ni ya Baba aliyenituma. 25 “Nimewaambia mambo haya yote wakati nikiwa bado niko pamoja nanyi. 26 L akini huyo Msaidizi, yaani, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atamtuma kwenu kwa Jina langu, atawafundisha mambo yote na kuwakumbusha yote niliyowaambia. 27 A mani nawaachia, amani yangu nawapa, amani hii niwapayo si kama ile ulimwengu utoayo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiogope. 28 “Mlinisikia nikisema, ‘Ninakwenda zangu, lakini nitarudi tena.’ Kama kweli mngelinipenda mngelifurahi kwa kuwa nakwenda kwa Baba, kwani Baba ni mkuu kuliko mimi. 29 Nimewaambia mambo haya kabla hayajatukia, ili yatakapotukia mpate kuamini. 30 Sitasema nanyi zaidi, kwa sababu yule mkuu wa ulimwengu huu anakuja, naye hana kitu kwangu, 31 lakini ulimwengu upate kujua kuwa ninampenda Baba, nami hufanya vile vile kama Baba alivyoniamuru. “Haya inukeni; twendeni zetu. Yesu Mzabibu Wa Kweli “Mimi ndimi mzabibu wa kweli na Baba yangu ndiye mkulima. 2K ila tawi ndani yangu lisilozaa matunda, Baba yangu hulikata, nalo kila tawi lizaalo, hulisafisha ili lipate kuzaa matunda zaidi. 3 Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililonena nanyi. 4 K aeni ndani yangu, nami nikae ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa matunda lisipokaa ndani ya mzabibu, vivyo hivyo ninyi msipokaa ndani yangu hamwezi kuzaa matunda.
15
1
13:37 Mt 26:33, 34, 35; Mk 14:29, 30, 31; Lk 22:33, 34 13:38 Yn 18:27 14:1 Yn 14:27; Yn 3:19; Za 4:5; Mk 11:22 14:2 Yn 13:33, 36; 16:5 14:3 Yn 12:26 14:5 Yn 11:16 14:6 Efe 2:18; Ebr 10:20; Yn 1:25; Mdo 4:12 14:7 Yn 8:19; 1Yn 2:23 14:8 Yn 1:43 14:9 Isa 9:6; Kol 1:15 14:10 Yn 14:20; 10:38; 17:21, 23; 5:19; 7:16 14:11 Yn 5:36; 10:38 14:12 Mt 21:21; Lk 10:17 14:13 Mt 7:7 14:15 Za 103:18 14:16 Yn 15:26; 16:7 14:17 1Yn 4:6; 5:6; 1Kor 2:14 14:18 Mt 16:27 14:19 Yn 7:33, 34; 16:16; Yn 6:57 14:20 Yn 17:21 14:21 Yn 14:15; Kum 7:13; Yn 16:27 14:22 Lk 6:16; Mdo 1:13; 10:41 14:23 Rum 8:10; Yn 14:15 14:24 Yn 5:19 14:26 Yn 15:26; 16:7; Mdo 2:33; Yn 16:13; 2:22; 1Yn 2:20, 27 14:27 Hes 6:26; Lk 2:14 14:28 Mt 16:27; Yn 5:18; 10:29; Flp 2:6 14:29 Yn 13:19; 16:4 14:30 Yn 12:31 14:31 Yn 10:18; 12:49 15:1 Za 80:8-11 15:2 Mt 3:10; Za 92:14; Mt 3:8; 7:20; Gal 5:22; Efe 5:9; Flp 1:11; Yn 16:6 15:3 Yn 17:17; Efe 5:26 15:4 Yn 6:56; 2:6
YOHANA 14:27
YOHANA “Mimi ni mzabibu, ninyi ni matawi. Akaaye ndani yangu, nami ndani yake, huyo huzaa sana, maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya jambo lo lote. 6 Mtu ye yote asipokaa ndani yangu, hutupwa nje kama tawi na kunyauka. Matawi kama hayo hukusanywa na kutupwa motoni, yakateketea. 7 Ninyi mkikaa ndani yangu na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni lo lote mtakalo, nanyi mtatendewa. 8K wa hiyo Baba yangu hutukuzwa, kwa vile mzaavyo matunda mengi, nanyi mtakuwa wanafunzi wangu. 9 “Kama vile Baba alivyonipenda mimi, hivyo ndivyo mimi nilivyowapenda ninyi. Basi kaeni katika pendo langu. 10 M kizishika amri zangu mtakaa katika pendo langu, kama mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake. 11 Nimewaambia mambo haya ili furaha yangu iwe ndani yenu na furaha yenu iwe kamili. 12 A mri yangu ndiyo hii: Mpendane kama mimi nilivyowapenda ninyi. 13 Hakuna mtu mwenye upendo mkuu kuliko huu, mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake. 14 Ninyi ni rafiki zangu mkifanya ninayowaamuru. 15S iwaiti ninyi watumishi tena, kwa sababu watumishi hawajui bwana wao analofanya, bali nimewaita ninyi rafiki, kwa maana nimewajulisha mambo yote niliyoyasikia kutoka kwa Baba yangu. 16 Si ninyi mlionichagua, bali mimi ndiye niliyewachagua ninyi na kuwaweka mwende mkazae matunda na matunda yenu yapate kudumu, ili lo lote mtakalomwomba Baba katika Jina langu, awape. 17A mri yangu ndiyo hii: Mpendane. 5
Ulimwengu Wawachukia Wanafunzi
“ Kama ulimwengu ukiwachukia ninyi, kumbukeni kwamba ulinichukia mimi kabla yenu. 19 Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungeliwapenda kama vile unavyowapenda walio wake. Kwa sababu ninyi si wa ulimwengu, lakini mimi nimewachagua kutoka katika ulimwengu, hii ndiyo sababu ulimwengu unawachukia. 20 Kumbukeni lile neno nililowaambia, ‘Hakuna mtumishi aliye mkuu kuliko 18
15:5 1Kor 12:12, 27; 2Kor 3:5 15:6 Mt 3:10; 13:40; Eze 15:4; Yn 15:2 15:7 Mk 11:24; Yn 6:56; Mt 7:7 15:8 Mt 5:16; Yn 8:31 15:9 Yn 17:23, 24, 26 15:10 Yn 14:15 15:11 Yn 3:29 15:12 Yn 13:34; 1Yn 3:11; Mk 12:30 15:13 Mwa 44:33; Rum 5:7, 8 15:14 Mit 18:24; Mt 12:50 15:15 Yn 8:26 15:16 Yn 6:70; 13:18 15:17 Yn 15:12 15:18 Isa 66:5 15:19 Yn 15:16; 17:14 15:20 Yn 13:16; 2Tim 3:12
TUMAINI
67
Amani nawaachia, amani yangu nawapa, amani hii niwapayo si kama ile ulimwengu utoayo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiogope.
68
bwana wake.’ Kama wamenitesa mimi, nanyi pia watawatesa, kama wamelishika neno langu, watalishika na neno lenu pia. 21 Watawatendea ninyi haya yote kwa ajili ya Jina langu, kwa sababu hawamjui yeye aliyenituma. 22 Kama sikuja na kusema nao wasingalikuwa na hatia ya dhambi. Lakini sasa hawana udhuru kwa ajili ya dhambi zao. 23 Ye yote anayenichukia mimi, anamchukia pia na Baba yangu. 24 K ama sikuwa nimefanya miujiza ambayo haijapata kufanywa na mtu mwingine ye yote, wasingalikuwa na hatia ya dhambi. Lakini sasa wameiona miujiza hii na bado wakatuchukia mimi na Baba yangu. 25 Lakini hii ni kutimiza lile neno lililoandikwa kwenye Torati kwamba ‘Walinichukia pasipo sababu.’ 26 “Lakini atakapokuja huyo Msaidizi nitakayemtuma kwenu kutoka kwa Baba, yaani, huyo Roho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia mimi. 27 Ninyi nanyi itawapasa kushuhudia kwa sababu mmekuwa pamoja nami tangu mwanzo. 1 “ Nimewaambia mambo haya yote ili msije mkaiacha imani. 2 Watawatenga na masinagogi. Naam, saa yaja ambayo mtu ye yote atakayewaua atadhani kwa kufanya hivyo anamtumikia Mungu. 3 Nao watawatenda haya kwa sababu hawamjui Baba wala mimi. 4 L akini nimewaambia ninyi mambo haya, ili saa hiyo ikiwadia mpate kukumbuka ya kuwa nilikuwa nimewaambia. Sikuwaambia mambo haya tangu mwanzo kwa sababu nilikuwa pamoja nanyi.
16
Kazi Ya Roho Mtakatifu
“ Sasa mimi ninakwenda kwake yeye aliyenituma, lakini hakuna hata aniulizaye, ‘Unakwenda wapi?’ 6 Kwa sababu nimewaambia mambo haya, mioyo yenu imejawa na huzuni. 7 Lakini amin nawaambia, yafaa mimi niondoke kwa kuwa nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu, lakini nikienda nitamtuma kwenu. 8 N aye atakapokuja, atauthibitishia ulimwengu kuhusu dhambi, haki na hukumu. 9 Kwa habari ya dhambi, kwa sababu hawaniamini mimi, 10 kwa habari ya haki, kwa sababu ninakwenda kwa 5
YOHANA
TUMAINI
Baba, nanyi hamtaniona tena, 11k wa habari ya hukumu, kwa sababu yule mkuu wa ulimwengu huu amekwisha kuhukumiwa. 12 “ Bado ninayo mambo mengi ya kuwaambia, lakini hamwezi kuyastahimili sasa. 13 Atakapokuja huyo Roho wa kweli atawaongoza awatie katika kweli yote. Yeye hatanena kwa ajili yake mwenyewe, bali atanena yale yote atakayosikia, naye atawaonyesha mambo yajayo. 14 Atanitukuza mimi, kwa maana atayachukua yaliyo yangu na kuwajulisha ninyi. 15V yote alivyo navyo Baba ni vyangu. Ndiyo maana nimesema Roho atachukua yaliyo yangu na kuwajulisha ninyi. 16 “ Bado k itambo k idogo nany i hamtaniona na tena bado kitambo kidogo nanyi mtaniona.” Huzuni Itageuka Kuwa Furaha Baadhi ya wanafunzi wakaulizana, “Ana maana gani asemapo, ‘Bado kitambo kidogo nanyi hamtaniona na tena bado kitambo kidogo nanyi mtaniona?’ Naye ana maana gani asemapo, ‘Kwa sababu ninakwenda kwa Baba?’ ” 18 Wakaendelea kuulizana, “Ana maana gani asemapo, ‘Kitambo kidogo?’ Hatuelewi hilo analosema.” 19 Yesu akatambua kuwa walitaka kumwuliza juu ya hilo, hivyo akawaambia, “Je, mnaulizana nina maana gani niliposema, ‘Bado kitambo kidogo nanyi hamtaniona na tena bado kitambo kidogo nanyi mtaniona?’ 20 Amin, amin nawaambia, ninyi mtalia na kuomboleza, lakini ulimwengu utafurahi. Ninyi mtahuzunika, lakini huzuni yenu itageuka kuwa furaha. 21 M wanamke anapokuwa na utungu wa kuzaa huwa na maumivu kwa sababu saa yake imewadia. Lakini mtoto akiisha kuzaliwa, yule mwanamke husahau maumivu hayo kwa sababu ya furaha ya kuzaliwa mtoto ulimwenguni. 22 Hivyo ninyi mna maumivu sasa, lakini nitawaona tena, nayo mioyo yenu itafurahi na furaha yenu hakuna awaondoleaye. 23 K atika siku hiyo hamtaniuliza neno lo lote. Amin, amin nawaambia, kama mkimwomba Baba jambo lo lote kwa Jina langu, yeye atawapa. 24 Mpaka sasa hamjaomba jambo lo lote 17
kwa Jina langu. Ombeni nanyi mtapewa, ili furaha yenu ipate kuwa kamili. Amani Kwa Wanafunzi “Nimewaambia mambo haya kwa mafumbo. Saa yaja ambapo sitazungumza nanyi tena kwa mafumbo bali nitawaeleza waziwazi kuhusu Baba. 26 S iku hiyo mtaomba kwa Jina langu. Wala sitawaambia kwamba nitamwomba Baba kwa ajili yenu, 27 k wa maana Baba mwenyewe anawapenda, kwa sababu mmenipenda mimi na mmeamini kwamba nimetoka kwa Mungu. 28 Nilitoka kwa Baba na kuja ulimwenguni, sasa naondoka ulimwenguni na kurudi kwa Baba.” 29 Ndipo wanafunzi wake wakasema, “Sasa unazungumza waziwazi, wala si kwa mafumbo. 30 Sasa tumejua kwamba wewe unajua mambo yote, wala hakuna haja ya mtu kukuuliza maswali. Kwa jambo hili tunaamini kwamba ulitoka kwa Mungu.” 31 Yesu akawajibu, “Je, sasa mnaamini? 32 S aa inakuja, naam, imekwisha kuwadia, mtakapotawanyika kila mmoja kwenda nyumbani kwake na kuniacha peke yangu. Lakini mimi si peke yangu kwa sababu Baba yu pamoja nami. 33 Nimewaambia mambo haya, ili mpate kuwa na amani mkiwa ndani yangu. Ulimwenguni mtapata dhiki. Lakini jipeni moyo, kwa maana mimi nimeushinda ulimwengu.” 25
Yesu Ajiombea Mwenyewe 1 B aada ya Yesu kusema haya, alitazama kuelekea mbinguni akawaombea na kusema: “Baba, saa imewadia. Umtukuze Mwanao, ili Mwanao apate kukutukuza wewe. 2K wa kuwa umempa mamlaka juu ya wote wenye mwili ili awape uzima wa milele wale uliompa. 3 Nao uzima wa milele ndio huu, wakujue wewe uliye Mungu wa pekee, wa kweli na Yesu Kristo uliyemtuma. 4 Nimekutukuza wewe duniani kwa kuitimiza ile kazi uliyonipa niifanye. 5 Hivyo sasa, Baba, unitukuze mbele zako kwa ule utukufu niliokuwa nao pamoja na wewe kabla ulimwengu haujakuwako.
17
15:21 Isa 66:5; Yn 16:3 15:22 Rum 1:20; 2:1 15:23 1Yn 2:23 15:24 Yn 5:36 15:25 Za 69:4; 109:3 15:26 Yn 14:15; 16:7; Yn 14:17; 1Yn 4:4 15:27 Lk 24:48; 1:21; 1Yn 4:14 16:1 Yn 15:1827; Mt 11:16 16:2 Yn 12:42; Isa 66:5; Ufu 6:9 16:3 Yn 17:25; 1Yn 3:1 16:4 Yn 14:29 16:5 Yn 16:10, 17, 28; 7:33; 13:36; 14:5 16:6 Yn 6:22; 14:1 16:7 Yn 14:16, 26; Yn 15:26 16:8 1Kor 14:24; Ebr 4:12 16:9 Yn 15:22 16:10 Rum 1:17; 1Pet 3:18 16:11 Yn 12:31 16:12 1Kor 3:2 16:13 Yn 14:17; Za 25:5 16:15 Yn 17:10 16:16 Yn 7:33; 16:22; 14:18-24 16:17 Yn 16:16; 16:5 16:20 Mk 16:10; Yn 20:20 16:21 Mik 4:9; 1The 5:3 16:22 Isa 60:14; Lk 24:41, 52; Yn 14:1, 27; Mdo 2:46; 13:52; 1Pet 1:8 16:23 Mt 7:7; Yn 15:16 16:24 Yn 3:29; 15:11 16:25 Yn 10:6 16:26 Yn 16:23, 24 16:27 Yn 14:21, 23 16:28 Yn 5:10, 17; 13:3 16:29 Yn 16:25 16:30 1Fal 17:24; Yn 16:27; 13:3; 2:25 16:32 Yn 16:2, 25; Mt 26:31; Mt 26:56; Yn 8:16, 29 16:33 Yn 14:27; Yn 15:18-21; 1Yn 5:4; Ufu 21:7 17:1 Yn 11:41; 12:23; Yn 13:31, 32 17:2 Dan 7:14; Yn 6:37, 39 17:3 Flp 3:8; Yn 17:8, 18, 21, 23, 25; 3:17 17:4 Yn 13:31; 19:30 17:5 Flp 2:6; Yn 1:2
YOHANA Yesu Awaombea Wanafunzi Wake “ Nimewajulisha jina lako wale ulionipa kutoka katika ulimwengu. Walikuwa wako, ukanipa mimi, nao wamelitii neno lako. 7 Sasa wamejua ya kuwa vyote ulivyonipa vimetoka kwako, 8 k wa kuwa maneno yale ulionipa nimewapa wao, nao wameyapokea na kujua kwamba kweli nimetoka kwako, nao wameamini kuwa wewe ulinituma. 9 Ninawaombea wao. Mimi siuombei ulimwengu, bali nawaombea wale ulionipa kwa sababu wao ni wako. 10 Wote walio wangu ni wako na walio wako ni wangu, nami nimetukuzwa ndani yao. 11 Mimi sasa simo tena ulimwenguni, lakini wao bado wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba Mtakatifu, uwalinde kwa uweza wa jina lako ulilonipa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo wamoja. 12 N ilipokuwa pamoja nao, niliwalinda, wakawa salama kwa lile jina ulilonipa. Hakuna hata mmoja aliyepotea, isipokuwa yule aliyekusudiwa, ili Maandiko yapate kutimia. 13“ Lakini sasa naja kwako, nami ninasema mambo haya wakati bado nikiwa ulimwenguni, ili wawe na furaha yangu kamili ndani yao. 14 Nimewapa neno lako, nao ulimwengu umewachukia kwa kuwa wao si wa ulimwengu kama mimi nisivyo wa ulimwengu huu. 15 Siombi kwamba uwaondoe ulimwenguni, bali uwalinde dhidi ya yule mwovu. 16 Wao si wa ulimwengu huu, kama vile mimi nisivyo wa ulimwengu. 17U watakase kwa ile kweli, neno lako ndilo kweli. 18 K ama vile ulivyonituma mimi ulimwenguni, nami nawatuma vivyo hivyo. 19 K wa ajili yao najiweka wakfu ili wao nao wapate kutakaswa katika ile kweli. 6
Yesu Awaombea Wote Wamwaminio
“Siwaombei hawa peke yao, ba li nawaombea na wa le wote watakaoniamini kupitia neno lao 21 i li wawe na umoja kama vile wewe Baba ulivyo ndani yangu na mimi nilivyo ndani yako, wao nao wawe ndani yetu, ili ulimwengu upate kuamini ya kuwa wewe ndiye uliyenituma mimi. 22U tukufu ule ulionipa nimewapa wao, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo wamoja. 23 M imi ndani yako na wewe ndani yangu, ili wawe wamekamilika katika umoja na ulimwengu upate kujua ya kuwa umenituma, nami nimewapenda wao kama unavyonipenda mimi. 20
“ Baba, shauku yangu ni kwamba, wale ulionipa wawe pamoja nami pale nilipo, ili waweze kuuona utukufu wangu, yaani, utukufu ule ulionipa kwa kuwa ulinipenda hata kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu. 25“ Baba Mwenye Haki, ingawa ulimwengu haukujui, mimi ninakujua, nao wanajua ya kuwa umenituma. 26 Nimefanya jina lako lijulikane kwao nami nitaendelea kufanya lijulikane, ili kwamba upendo ule unaonipenda mimi uwe ndani yao na mimi mwenyewe nipate kuwa ndani yao.” 24
Yesu Akamatwa Yesu a lipoma liza kuomba, akaondoka na wanafunzi wake wakavuka Bonde la Kidroni. Upande wa pili palikuwa na bustani, yeye na wanafunzi wake wakaingia humo. 2B asi Yuda, yule aliyemsaliti alipafahamu mahali hapo kwani Yesu alikuwa akikutana humo na wanafunzi wake mara kwa mara. 3 Hivyo Yuda akaja bustanini, akiongoza kikosi cha maaskari wa Kirumi na baadhi ya maafisa kutoka kwa viongozi wa makuhani na Mafarisayo, wakiwa wamechukua taa, mienge na silaha. 4 Yesu akijua yale yote yatakayompata, akajitokeza mbele yao akawauliza, “Mnamtafuta nani?”
18
1
TUMAINI
69
Wao wakamjibu, “Yesu wa Nazareti.” Yesu akawajibu, “Mimi ndiye.” Yuda, yule aliyemsaliti alikuwa amesimama pamoja nao. 6 Yesu alipowaambia, “Mimi ndiye,” walirudi nyuma na kuanguka chini! 7 A kawauliza tena, “Mnamtafuta nani?” Nao wakamjibu, “Yesu wa Nazareti.” 8 Yesu akawaambia, “Nimekwisha kuwaambia kuwa, mimi ndiye; kwa hiyo kama mnanitafuta mimi, waacheni hawa watu waende zao.” 9 Hii ilikuwa ili litimie lile neno alilosema, “Sikumpoteza hata mmoja miongoni mwa wale ulionipa.” 10 Simoni Petro aliyekuwa na upanga akaufuta na kumkata sikio la kuume mtumishi wa Kuhani Mkuu. Jina la mtumishi huyo aliitwa Malko. 5
17:6 Yn 17:26; 1:18 17:8 Yn 8:26; 1:18 17:9 Lk 22:32 17:10 Yn 16:15 17:11 Yn 13:1; 17:13; 7:33; 17:21-23; Za 133:1; Yn 10:30 17:12 Yn 6:39; 6:70 17:13 Yn 3:29 17:14 Yn 15:19; 8:23; 1Yn 3:13; Yn 17:16 17:15 Mt 5:37 17:16 Yn 17:14 17:17 2Sam 7:28; Yn 15:3; 1Fal 17:24 17:18 Yn 17:3, 8, 21, 23, 25; 20:21 17:19 Yn 17:17; 1Kor 1:2, 30; 1The 4:7; Ebr 10:10 17:20 Yn 17:9 17:21 Gal 3:28; Rum 12:5; Yn 10:38; 14:11 17:22 Yn 14:20; 1Yn 1:2; 3:24 17:23 Yn 3:17; 16:27; Kol 3:14 17:24 Yn 12:26; 1:14; Mt 25:34; Yn 1:2 17:25 Yn 15:21; 16:3; Yn 3:17; 7:29 18:1 2Sam 15:23; Mt 21:1; 26:36 18:2 Lk 21:37; 22:39 18:3 Mt 26:47; Mk 14:43; Lk 22:47; Mdo 1:16 18:4 Yn 6:64; 13:1; 11; 19:28 18:5 Mk 1:4 18:7 Yn 18:4 18:9 Yn 6:39; 17:12 18:10 Mt 26:51; Mk 14:47; Lk 22:49, 50
Nimewaambia mambo haya, ili mpate kuwa na amani mkiwa ndani yangu. Ulimwenguni mtapata dhiki. Lakini jipeni moyo, kwa maana mimi nimeushinda ulimwengu.”
YOHAN 16:33
70
YOHANA
TUMAINI
Kwa kusudi hili nilizaliwa na kwa ajili ya hili nilikuja ulimwenguni ili niishuhudie kweli.
ubaya niliousema. Lakini kama nimesema yaliyo kweli, mbona umenipiga?” 24 N dipo Anasi akampeleka Yesu kwa Kuhani Mkuu Kayafa, akiwa bado amefungwa. Petro Amkana Yesu Tena Wakati huo Simoni Petro alikuwa amesimama akiota moto. Baadhi ya wale waliokuwepo wakamwuliza, “Je, wewe si mmoja wa wanafunzi wake?” Petro akakana, akasema, “Mimi sio.” 26 M moja wa watumishi wa Kuhani Mkuu, ndugu yake yule mtu ambaye Petro alikuwa amemkata sikio, akamwuliza, “Je, mimi sikukuona kule bustanini ukiwa na Yesu?” 27 Kwa mara nyingine tena Petro akakana, naye jogoo akawika wakati uo huo. 25
Yesu Apelekwa Kwa Pilato dipo Wayahudi wakamchukua Yesu N kutoka kwa Kayafa na kumpeleka kwenye jumba la kifalme la mtawala wa Kirumi *. Wakati huo ilikuwa ni alfajiri, ili kuepuka kuwa najisi kwa taratibu za ibada, Wayahudi hawakuingia ndani kwa sababu ya sheria za Kiyahudi. Wangehesabiwa kuwa najisi kama wangeingia nyumbani mwa mtu asiye Myahudi na wasingeruhusiwa kushiriki katika Sikukuu ya Pasaka. 29 Hivyo Pilato akatoka nje walikokuwa akawauliza, “Mmeleta mashtaka gani kumhusu mtu huyu?” 30 Wao wakamjibu, “Kama huyu mtu hakuwa mhalifu tusingemleta kwako.” 31 Pilato akawaambia, “Basi mchukueni ninyi mkamhukumu kwa kufuata sheria zenu.” Wayahudi wakamjibu, “Sisi haturuhusiwi kutoa hukumu ya kifo kwa mtu ye yote.” 32 W alisema hivyo ili yale maneno aliyosema Yesu kuhusu kifo atakachokufa yapate kutimia. 33 Kwa hiyo Pilato akaingia ndani akamwita Yesu, akamwuliza, “Wewe ndiye mfalme wa Wayahudi?” 34 Y esu akamjibu, “Je, unauliza swali hili kutokana na mawazo yako mwenyewe au uliambiwa na watu kunihusu mimi?” 35 Pilato akamjibu, “Mimi si Myahudi, ama sivyo? Taifa lako mwenyewe na viongozi wa makuhani wamekukabidhi kwangu. Umefanya kosa gani?”
YOHANA 18:37 28
11 Yesu akamwambia Petro, “Rudisha upanga wako kwenye ala yake. Je, hainipasi kukinywea kikombe alichonipa Baba?”
Yesu Mbele Ya Kuhani Mkuu H ivyo wale maaskari wakiwa pamoja na majemadari wao na maafisa wa Wayahudi, wakamkamata Yesu na kumfunga. 13K wanza wakampeleka kwa Anasi, mkwewe Kayafa, aliyekuwa Kuhani Mkuu mwaka ule. 14K ayafa ndiye aliyekuwa amewashauri Wayahudi kwamba imempasa mtu mmoja kufa kwa ajili ya watu. 12
Petro Anamkana Yesu Simoni Petro pamoja na mwanafunzi mwingine walikuwa wakimfuata Yesu. Huyu mwanafunzi mwingine alikuwa anafahamika kwa Kuhani Mkuu, hivyo aliingia ndani ya ukumbi pamoja na Yesu. 16 L akini Petro alisimama nje karibu na lango, ndipo yule mwanafunzi mwingine akazungumza na msichana aliyekuwa analinda lango, akamruhusu Petro aingie ndani. 17 Y ule msichana akamwuliza Petro, “Je, wewe pia si mmoja wa wanafunzi wa mtu huyu?” 15
Petro akajibu, “Mimi sio.” 18 W ale watumishi na maaskari walikuwa wamesimama wakiota moto wa makaa kwa sababu palikuwa na baridi, Petro naye alikuwa amesimama pamoja nao akiota moto.
Kuhani Mkuu Amhoji Yesu Wakati huo Kuhani Mkuu akawa anamwuliza Yesu kuhusu wanafunzi wake na mafundisho yake. 2 0 Ye su a k a mjibu , “Ni mek uw a nikizungumza waziwazi mbele ya watu wote. Siku zote nimefundisha katika masinagogi na Hekaluni mahali ambapo Wayahudi wote hukusanyika. Sikusema jambo lo lote kwa siri. 21 Mbona unaniuliza mimi maswali? Waulize wale walionisikia yale niliyowambia. Wao wanajua niliyosema.” 22 A lipomaliza kusema hayo, mmoja wa maaskari aliyekuwa amesimama karibu naye, akampiga Yesu kofi usoni, kisha akasema, “Je, hivyo ndivyo unavyomjibu Kuhani Mkuu?” 23 Yesu akamjibu akasema, “Kama nimesema jambo baya, shuhudia huo 19
18:11 Mt 20:22 18:12 Yn 18:3 18:13 Yn 18:24; Mt 26:3 18:14 Yn 11:49-51 18:15 Mt 26:3; 26:58; Mk 14:54 18:16 Mt 26:69; Mk 14:66; Lk 22:54 18:17 Yn 17:25 18:18 Yn 21:9; Mk 14:54, 67 18:20 Mt 4:23; 26:55; Yn 7:26 18:22 Yer 20:2; Mdo 23:2; Mt 16:21 18:23 Mt 5:39; Mdo 26:3 18:24 Yn 18:13; Mt 26:3 18:25 Yn 18:18; 18:17; Mt 26:69, 71; Mk 14:69; Lk 22:58 18:26 Yn 18:1; 10 18:27 Yn 13:38 18:28 Mt 27:2; Yn 18:33; 19:9; 11:55 18:28 Jumba la mfalme la mtawala wa Kirumi lilikuwa linaitwa Praitorio 18:32 Mt 20:19; 26:2 18:33 Mt 27:11; Yn 19:9; Lk 23:3; Mt 2:2 18:34 Mt 16:13 18:35 Yn 1:11; Mt 21:39
YOHANA 36 Yesu akajibu, “Ufalme wangu si wa ulimwengu huu. Ufalme wangu ungekuwa wa ulimwengu huu wafuasi wangu wangenipigania ili nisitiwe mikononi mwa Wayahudi. Lakini kama ilivyo ufalme wangu hautoki hapa ulimwenguni.” 37 Pilato akamwuliza, “Kwa hiyo wewe ni mfalme?” Yesu akajibu, “Wewe wasema kwamba mimi ni mfalme. Kwa kusudi hili nilizaliwa na kwa ajili ya hili nilikuja ulimwenguni ili niishuhudie kweli. Mtu ye yote aliye wa kweli husikia sauti yangu.” 38 P ilato akamwuliza Yesu, “Kweli ni nini?” Baada ya kusema haya Pilato akaenda nje tena akawaambia wale viongozi wa Wayahudi waliomshtaki Yesu, “Sioni kosa lo lote alilotenda mtu huyu. 39 Lakini ninyi mna desturi yenu kwamba wakati wa Pasaka nimwachie huru mfungwa mmoja mnayemtaka. Je, mnataka niwafungulie huyu ‘Mfalme wa Wayahudi?’ ” 40 Wao wakapiga kelele wakisema, “Si huyu mtu bali tufungulie Baraba!” Basi Baraba alikuwa mnyang'anyi.
19
Yesu Ahukumiwa Kusulibiwa
1 N dipo Pilato akamtoa Yesu akaamuru apigwe mijeledi. 2 Askari wakasokota taji ya miiba wakamvika Yesu kichwani. Wakamvalisha joho la zambarau. 3 Wakawa wanapanda pale alipo tena na tena, wakisema, “Salamu! Mfalme wa Wayahudi!” Huku wakimpiga makofi usoni. 4P ilato akatoka tena nje akawaambia wale waliokusanyika, “Tazameni, namkabidhi Yesu kwenu kuwajulisha kwamba mimi sikumwona ana hatia.” 5 Kwa hiyo Yesu akatoka nje akiwa amevaa ile taji ya miiba na lile vazi la zambarau. Pilato akawaambia, “Tazameni, huyu hapa huyo mtu!” 6W ale viongozi wa makuhani na maafisa walipomwona, wakapiga kelele wakisema, “Msulibishe! Msulibishe!” Pilato akawaambia, “Mchukueni ninyi mkamsulibishe, mimi sioni hatia juu yake.” 7 Wayahudi wakamjibu, “Sisi tunayo sheria na kutokana na sheria hiyo, hana budi kufa kwa sababu yeye alijiita Mwana wa Mungu.” 8 Pilato aliposikia haya, akaogopa zaidi. 9 A kaingia tena ukumbini akamwuliza
Yesu, “Wewe umetoka wapi?” Lakini Yesu hakumjibu. 10 Pilato akamwambia, “Wewe unakataa kuongea na mimi? Hujui ya kuwa nina mamlaka ya kukuachia huru au kukusulibisha?” 11 Ndipo Yesu akamwambia, “Wewe hungekuwa na mamlaka yo yote juu yangu kama hungepewa kutoka juu. Kwa hiyo yeye aliyenitia mikononi mwako ana hatia ya dhambi iliyo kubwa zaidi.” 12 Tangu wakati huo, Pilato akajitahidi kutafuta njia ya kumfungua Yesu, lakini Wayahudi wakazidi kupiga kelele wakisema, “Ukimwachia huyu mtu, wewe si rafiki wa Kaisari. Mtu ye yote anayedai kuwa mfalme anampinga Kaisari.” 13 P ilato aliposikia maneno haya akamtoa Yesu nje tena akaketi katika kiti chake cha hukumu, mahali palipoitwa Sakafu ya Jiwe, kwa Kiebrania paliitwa Gabatha *. 14 B asi ilikuwa siku ya Maandalio ya Pasaka, yapata kama saa sita hivi. Pilato akawaambia Wayahudi, “Huyu hapa mfalme wenu!” 15 Wao wakapiga kelele, “Mwondoe! Mwondoe! Msulibishe!” Pilato akawauliza, “Je, nimsulibishe mfalme wenu?” Wale viongozi wa makuhani wakamjibu, “Sisi hatuna mfalme mwingine ila Kaisari.” 16 Ndipo Pilato akamkabidhi Yesu kwao ili wamsulibishe. Kusulibiwa Kwa Yesu Kwa hiyo maaskari wakamchukua Yesu. 17 Yesu akiwa ameubeba msalaba wake, akatoka kuelekea mahali palipoitwa, Fuvu la Kichwa (ambapo kwa Kiebrania ni Golgotha). 18H apo ndipo walipomsulibisha. Pamoja naye walisulibisha watu wengine wawili, mmoja upande wa kushoto na mwingine upande wa kuume wa Yesu. 19 Pilato akaamuru tangazo liandikwe na liwekwe juu kwenye msalaba wa Yesu: “YESU WA NAZARETI, MFALME WA WAYAHUDI.” 20 Kwa kuwa mahali hapo aliposulibiwa palikuwa karibu na mjini, Wayahudi wengi walisoma maandishi haya yaliyokuwa yameandikwa kwa lugha za Kiebrania, Kiyunani na Kilatini. 21V iongozi wa makuhani wa Wayahudi wakapinga,
TUMAINI
71
wakamwambia Pilato, “Usiandike, ‘Mfalme wa Wayahudi,’ bali andika kwamba, mtu huyu alisema, ‘Mimi ni mfalme wa Wayahudi.’ ” 22 Pilato akawajibu, “Nilichokwisha kuandika, nimeandika!” Mavazi Ya Yesu Yagawanywa Askari walipokwisha kumsulibisha Yesu, walichukua nguo zake wakazigawa mafungu manne, kila askari fungu lake. Ila walikubaliana wasilichane lile vazi lake kwa maana lilikuwa halina mshono bali limefumwa tangu juu hadi chini. 24 W akaambiana, “Tusilichane ila tulipigie kura ili kuamua ni nani alichukue.” Hili lilitukia ili Maandiko yapate kutimizwa yale yaliyosema, “Waligawana nguo zangu na mavazi yangu wakayapigia kura.” Hayo ndiyo waliyoyafanya wale askari. 25 Wakati huo huo karibu na msalaba wa Yesu walikuwa wamesimama: Maria mama yake, Maria dada wa mamaye, yaani, mke wa Klopa na Maria Magdalene. 26 Y esu alipomwona mama yake mahali pale pamoja na yule mwanafunzi aliyempenda wamesimama karibu, akamwambia mama yake, “Mwanamke, huyo hapo ndiye mwanao,” 27 K isha akamwambia yule mwanafunzi, “Nawe huyo hapo ndiye mama yako.” Tangu wakati huo yule mwanafunzi akamchukua mama yake Yesu nyumbani kwake. 23
Kifo Cha Yesu aada ya haya, Yesu hali akijua kuwa B mambo yote yamemalizika, alisema ili kutimiza Maandiko, “Naona kiu.” 29 Hapo palikuwa na bakuli lililojaa siki. Kwa hiyo wakachovya sifongo kwenye hiyo siki, wakaiweka kwenye ufito wa mti wa hisopo, wakampelekea mdomoni. 30 B aada ya kuionja hiyo siki, Yesu akasema, “Imekwisha.” Akainamisha kichwa chake, akakata roho. 28
Yesu Achomwa Mkuki Ubavuni wa kuwa ilikuwa siku ya Maandalio K ya Pasaka, Wayahudi hawakutaka miili ibaki msalabani siku ya Sabato, hasa kwa 31
18:36 Mt 3:2; 26:53; Lk 17:21; Yn 6:51 18:37 Yn 3:32; 8:47; 1Yn 4:6 18:38 Lk 23:4-6 18:39 Mt 27:15; Mk 15:6; Lk 23:19 18:40 Mdo 3:14 19:1 Kum 25:3; Mt 27:26 19:3 Mt 27:29; Yn 18:22 19:4 Yn 18:38; 19:6; Lk 23:4 19:5 Yn 19:2 19:6 Mdo 3:13; Yn 19:4; Lk 23:4 19:7 Law 24:16; Mt 26:63-66; Yn 5:18 19:9 Yn 18:33; Mk 14:61 19:11 Rum 13:1; Yn 18:28-30; Mdo 3:13 19:12 Lk 23:2 19:13 Mt 27:19; Yn 5:2 19:13 Gabatha ni neno la Kiebrania ambalo maana yake ni Sakafu ya jiwe; ni mahali pa wazi palipoinuliwa ambako palitumika kama mahakama 19:14 Mt 27:62; Mk 15:25 19:15 Yn 19:6 19:16 Mt 27:26; Mk 15:15 19:17 Mwa 22:6; Lk 14:27; 23:33; Yn 5:2 19:18 Lk 23:32 19:19 Mk 1:24; 14:21 19:20 Ebr 13:12 19:21 Yn 19:14 19:23 Mt 27:35; Mk 15:24; Lk 23:34 19:24 Yn 19:28, 36, 37; Mt 1:22; Za 22:18 19:25 Mk 15:40, 41; Lk 23:49; Mt 12:46; Yn 13:23 19:26 Mt 12:46; Yn 13:23 19:27 Yn 1:11; 16:32 19:28 Za 69:21; Yn 19:30; 13:1; 19:24, 36, 37; Mt 1:22 19:29 Za 69:21; Mt 27:48 19:30 Lk 12:50 19:31 Yn 19:42; Mk 15:42; Kum 21:23
72
YOHANA
TUMAINI
kuwa hiyo Sabato ingekuwa Sikukuu. Wakamwomba Pilato aamuru miguu ya wale waliosulibiwa ivunjwe ili wafe haraka miili iondolewe kwenye misalaba. 32 Kwa hiyo maaskari wakaenda wakavunja miguu ya mtu wa kwanza aliyesulibiwa pamoja na Yesu na yule mwingine pia. 33 Lakini walipomkaribia Yesu, wakaona ya kuwa amekwisha kufa, hivyo hawakuvunja miguu yake. 34 Badala yake mmoja wa wale maaskari akamchoma mkuki ubavuni na mara pakatoka damu na maji. 35 Mtu aliyeona mambo hayo ndiye aliyetoa ushuhuda, nao ushuhuda wake ni kweli. Anajua kuwa anasema kweli, naye anashuhudia ili pia nanyi mpate kuamini. 36 Kwa maana mambo haya yalitukia ili Maandiko yapate kutimia, yale yasemayo, “Hakuna hata mfupa wake mmoja utakaovunjwa.” 37 Tena Maandiko mengine yanasema, “Watamtazama yeye waliyemchoma kwa mkuki.” Maziko Ya Yesu Baada ya mambo haya, Yosefu wa Arimathaya, aliyekuwa mfuasi wa Yesu, ingawa kwa siri kwa sababu ya kuwaogopa Wayahudi, alimwomba Pilato ruhusa ili kuuchukua mwili wa Yesu. Pilato alimruhusu, hivyo akaja, akauchukua. 39 Naye Nikodemo, yule ambaye kwanza alimwendea Yesu usiku, akaja, akaleta mchanganyiko wa manemane na manukato, yenye uzito wa zaidi ya kilo thelathini *. 40 Wakauchukua mwili wa Yesu, wakauviringishia sanda ya kitani safi pamoja na yale manukato, kama ilivyokuwa desturi ya Wayahudi. 41 Basi palikuwa na bustani karibu na mahali pale aliposulibiwa, nako ndani ya ile bustani palikuwa na kaburi jipya, ambalo hajazikiwa mtu bado. 42 Kwa hiyo, kwa kuwa ilikuwa siku ya Wayahudi ya Maandalio, nalo kaburi hilo lilikuwa karibu, wakamzika Yesu humo. 38
Kufufuka Kwa Yesu A lfajiri na mapema siku ya kwanza ya juma, kulipokuwa kungali giza bado, Maria Magdalene alikwenda kaburini na kukuta lile jiwe limeondolewa penye ingilio. 2 Hivyo akaja kwa Simoni Petro
20
1
pamoja na yule mwanafunzi mwingine ambaye Yesu alimpenda akikimbia na kusema, “Wamemwondoa Bwana kaburini na hatujui walikomweka!” 3 Petro na yule mwanafunzi mwingine wakaondoka mara kuelekea kaburini. 4 Wote wawili walikuwa wanakimbia, lakini yule mwanafunzi mwingine akakimbia mbio zaidi kuliko Petro, akatangulia kufika kaburini. 5 Alipofika, akainama na kuchungulia mle kaburini, akaona vile vitambaa vya kitani vilivyokuwa sanda mle ndani, lakini hakuingia. 6 Ndipo Simoni Petro akaja, akimfuata nyuma akaenda moja kwa moja hadi ndani ya kaburi. Naye akaona vile vitambaa vya ile sanda vikiwa pale chini 7 na kile kitambaa kilichokuwa kichwani mwa Yesu. Kitambaa hicho kilikuwa kimekunjwa mahali pa peke yake, mbali na vile vitambaa vya kitani vya ile sanda. 8 K isha yule mwanafunzi aliyetangulia kufika kaburini naye akaingia ndani, akaona, akaamini, 9 (kwa kuwa mpaka wakati huo walikuwa bado hawajaelewa yale maandiko kwamba ilikuwa lazima Yesu afufuke kutoka kwa wafu). 10 Kisha hao wanafunzi wakaondoka wakarudi nyumbani kwao. Yesu Anamtokea Maria Magdalene
L akini Maria Magdalene akasimama nje ya kaburi akilia. Alipokuwa akilia, akainama, kuchungulia mle kaburini, 12 naye akaona malaika wawili wamevaa mavazi meupe, wameketi pale mwili wa Yesu ulipokuwa umelazwa, mmoja upande wa kichwani na mwingine upande wa miguuni. 13 Wakamwuliza Maria, “Mwanamke, mbona unalia?” Akawaambia, “Nalia kwa kuwa wamemchukua Bwana wangu na sijui walikomweka.” 14 Baada ya kusema hayo, akageuka, akamwona Yesu amesimama, lakini hakumtambua. 15 Yesu akamwambia, “Mwanamke, mbona unalia? Unamtafuta nani?” Maria akidhani ya kuwa aliyekuwa anaongea naye ni mtunza bustani, kwa hiyo akamwambia, “Bwana, kama ni wewe umemchukua, tafadhali nionyeshe ulikomweka, nami nitamchukua.” 11
Yesu akamwita, “Maria!” Ndipo Maria akamgeukia Yesu na kusema naye kwa Kiebrania, “Rabboni!” (Maana yake Mwalimu). 17 Yesu akamwambia, “Usinishike, kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini nenda kwa ndugu zangu ukawaambie, ‘Ninapaa kwenda kwa Baba yangu ambaye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu ambaye ni Mungu wenu.’ ” 18 Kwa hiyo Maria Magdalene akaenda kuwatangazia wanafunzi wa Yesu akisema, “Nimemwona Bwana!” Naye akawaambia kwamba amemweleza mambo hayo yote. 16
Yesu Awatokea Wanafunzi Wake Ikawa jioni ya ile siku ya kwanza ya juma, wanafunzi wake walipokuwa pamoja, milango ikiwa imefungwa kwa kuwaogopa Wayahudi, Yesu aliwatokea, akasimama katikati yao, akasema, “Amani iwe nanyi.” 20 Baada ya kusema haya, akawaonyesha mikono yake na ubavu wake. Wanafunzi wake wakafurahi sana walipomwona Bwana. 21 Yesu akawaambia tena, “Amani iwe nanyi! Kama vile Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawatuma ninyi.” 22 Naye alipokwisha kusema haya, akawavuvia, akawaambia, “Pokeeni Roho Mtakatifu. 23 M kimwondolea mtu ye yote dhambi zake, zitaondolewa na ye yote mtakayemfungia dhambi zake, zitafungiwa.” 19
Yesu Anamtokea Tomasi Lakini Tomasi, aliyeitwa Didimasi, yaani, Pacha, mmoja wa wale kumi na wawili, hakuwa pamoja nao Yesu alipokuja. 25H ivyo wale wanafunzi wengine wakamwambia, “Tumemwona Bwana.” Lakini yeye akawaambia, “Nisipoona zile alama za misumari mikononi mwake na kuweka kidole changu kwenye hizo alama za misumari na mkono wangu ubavuni mwake, sitaamini.” 26 Baada ya siku nane, wanafunzi wake walikuwa tena pamoja ndani ya nyumba, naye Tomasi alikuwa pamoja nao. Ndipo Yesu akaja milango ikiwa imefungwa na kusimama katikati yao akasema, “Amani iwe nanyi.” 27 K isha akamwambia Tomasi, “Weka kidole chako hapa na uone mikono 24
19:32 Yn 19:18 19:34 Zek 12:10; Ufu 1:7; 1Yn 5:6, 8 19:35 Lk 24:48; 15:27; Lk 21:24 19:36 Yn 19:24, 28, 37; Mt 1:22; Kut 12:46; Hes 9:12; Za 34:20 19:37 Zek 12:10; Ufu 1:7 19:39 Yn 3:1; 7:50 19:39 Zaidi ya kilo 30; tafsiri nyingine zinasema ratili 100, na nyingine ratili 75, ambazo ni kama kilo 34 19:40 Ebr 13:12 20:1 Lk 8:2; Yn 19:25; Mt 27:60, 66 20:2 Yn 13:23 20:3 Lk 24:12 20:5 Yn 20:11; 19:40 20:7 Yn 11:44 20:8 Yn 20:4 20:9 Mt 22:29; Yn 2:22; Lk 24:26; Mdo 2:24 20:11 Yn 20:5 20:12 Mk 16:5; Mdo 10:30 20:13 Yn 20:2, 15 20:14 Mt 28:9; Mk 16:9; Lk 24:16; Yn 21:14 20:15 Yn 20:13 20:16 Yn 5:2; Mt 23:7 20:17 Mt 28:10; Yn 7:33; Mt 28:10 20:18 Yn 20:1; Lk 24:10, 22, 23 20:20 Lk 24:36-39, 40; Yn 19:34; 16:20, 22; Lk 24:39, 40; Yn 19:34; Yn 16:20 20:21 Yn 20:19; Yn 3:17; Mt 28:19; Yn 17:18 20:22 Mdo 19:2; Gal 3:2; Yn 7:39; Mdo 2:38; 8:15; 17; 19:2; Gal 3:2 20:23 Mt 16:19; 18:18 20:24 Yn 11:16 20:25 Mk 16:11 20:26 Yn 14:27; 20:21 20:27 Yn 20:25; Lk 24:40
YOHANA yangu, nyosha mkono wako uguse ubavuni mwangu. Usiwe na shaka, bali uamini tu.” 28 Tomasi akamwambia, “Bwana wangu na Mungu wangu!” 29 Yesu akamwambia, “Umeamini kwa kuwa umeniona? Wamebarikiwa wale ambao hawajaona lakini wameamini.” Kusudi La Kitabu Hiki
30 Yesu alifanya miujiza mingine mingi mbele za wanafunzi wake, ambayo haikuandikwa katika kitabu hiki. 31 L akini haya yameandikwa ili mweze kuamini ya kuwa Yesu ndiye Kristo *, Mwana wa Mungu na kwa kumwamini mpate uzima katika jina lake.
Yesu Awatokea Wanafunzi Saba
21
1 Baada ya haya Yesu akawatokea tena wanafunzi wake kando ya Bahari ya Tiberia *. Yeye alijionyesha kwao hivi: 2 S imoni Petro, Tomasi aitwaye Didimasi, yaani Pacha, Nathanaeli wa Kana ya Galilaya, wana wa Zebedayo na wanafunzi wengine wawili walikuwa pamoja. 3 S imoni Petro akawaambia wenzake, “Mimi nakwenda kuvua samaki.” Nao wakamwambia, “Tutakwenda pamoja nawe.” Wakatoka, wakaingia ndani ya mashua, lakini usiku ule hawakupata cho chote. 4 Mara baada ya kupambazuka, Yesu akasimama ufuoni, lakini wanafunzi hawakumtambua kwamba alikuwa Yesu. 5 Yesu akawaambia, “Wanangu, je, mna samaki wo wote?” Wakamjibu, “La.” 6A kawaambia, “Shusheni nyavu upande wa kuume wa mashua yenu nanyi mtapata samaki.” Wakashusha nyavu na tazama wakapata samaki wengi mno hata wakashindwa kuvutia zile nyavu zilizojaa samaki ndani ya mashua. 7Y ule mwanafunzi aliyependwa na Yesu akamwambia Petro, “Huyu ni Bwana!” Simoni Petro aliposikia haya, akajifunga nguo yake kwa kuwa alikuwa uchi, naye akajitosa baharini. 8 Wale wanafunzi wengine wakaja kwa ile mashua huku wakikokota ule wavu uliyojaa samaki, maana hawakuwa mbali na nchi kavu, ilikuwa yapata dhiraa 200 *. 9 Walipofika
pwani, wakaona moto wa makaa na samaki wakiokwa juu yake na mikate. 10 Yesu akawaambia, “Leteni baadhi ya hao samaki mliovua sasa hivi.” 11 Simoni Petro akapanda kwenye mashua na kuukokota ule wavu pwani. Ulikuwa umejaa samaki wakubwa 153. Ingawa samaki walikuwa wengi kiasi hicho, ule wavu haukuchanika. 12 Yesu akawaambia, “Njoni mpate kifungua kinywa.” Hakuna hata mmoja wao aliyethubutu kumwuliza, “Wewe ni nani?” Kwa sababu walijua ya kuwa ni Bwana. 13 Yesu akaja, akachukua ule mkate, akawapa na vivyo hivyo akawagawia pia wale samaki. 14 H ii ilikuwa mara ya tatu Yesu kuwatokea wanafunzi wake tangu afufuke kutoka kwa wafu. Yesu Amwuliza Petro Kama Anampenda
15 W alipokwisha kula, Yesu akamwuliza Simoni Petro, “Je, Simoni mwana wa Yohana, unanipenda kweli kuliko hawa?” Yeye akamjibu, “Ndiyo Bwana, wewe unajua ya kuwa ninakupenda.” Yesu akamwambia, “Lisha wana-kondoo wangu.” 16 Yesu akamwambia tena, “Simoni, mwana wa Yohana, wanipenda?” Petro akamjibu, “Ndiyo Bwana, wewe unajua ya kuwa ninakupenda.” Yesu akamwambia, “Chunga kondoo zangu.” 17 Kwa mara ya tatu Yesu akamwuliza Petro, “Simoni mwana wa Yohana, unanipenda?” Petro akahuzunika sana kwa kuwa Yesu alimwuliza mara ya tatu, “Unanipenda?” Akamjibu, “Bwana, wewe unajua yote, unajua ya kuwa ninakupenda.” Yesu akamwambia, “Lisha kondoo zangu. 18 Amin, amin nakuambia, ulipokuwa kijana ulivaa na kwenda unakotaka, lakini utakapokuwa mzee utanyosha mikono yako na mtu mwingine atakuvika na kukupeleka usipotaka kwenda.” 19 Yesu alisema haya ili kuashiria ni kifo cha aina gani Petro atakachomtukuza nacho Mungu. Kisha Yesu akamwambia Petro, “Nifuate!” 20 P etro akageuka akamwona yule mwanafunzi aliyependwa na Yesu akiwafuata. (Huyu ndiye yule mwanafunzi aliyeegama kifuani mwa Yesu walipokula
TUMAINI
73
YOHAN 20:31
Lakini haya yameandikwa ili mweze kuamini ya kuwa Yesu ndiye Kristo , Mwana wa Mungu na kwa kumwamini mpate uzima katika jina lake.
naye chakula cha mwisho na kuuliza, “Bwana, ni nani atakayekusaliti?”) 21 Petro alipomwona huyo mwanafunzi, akamwuliza Yesu, “Bwana na huyu je?” 22 Yesu akamjibu, “Ikiwa nataka aishi mpaka nitakaporudi, inakuhusu nini? Wewe inakupasa unifuate!” 23 K wa sababu ya maneno haya ya Yesu, uvumi ukaenea miongoni mwa ndugu kwamba huyu mwanafunzi hangekufa. Lakini Yesu hakusema kuwa hangekufa. Yeye alisema tu kwamba, “Ikiwa nataka aishi mpaka nitakaporudi, inakuhusu nini?” 24 H uyu ndiye yule mwanafunzi anayeshuhudia mambo haya na ndiye ambaye ameandika habari hizi. Nasi tunajua ya kuwa ushuhuda wake ni kweli. 25 L akini kuna mambo mengine mengi ambayo Yesu alifanya. Kama yote yangeliandikwa, nadhani hata ulimwengu wote usingekuwa na nafasi ya kutosha kuweka vitabu vyote ambavyo vingeandikwa. Amen.
20:28 Yn 1:1; 20:29; Yn 3:15; 1Pet 1:8 20:29 Yn 3:15; 1Pet 1:8 20:30 Yn 21:25; Yn 2:11; 21:25; Mt 4; 3; 25:46 20:31 Yn 3:15; 19:35; Mt 4:3; 25:46 20:31 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Mpakwa (au Aliyetiwa) mafuta 21:1 Yn 21:14; Yn 20:19, 26 21:1 Yaani Bahari ya Galilaya 21:2 Yn 11:16; 1:4; Yn 2:1; Mt 4:21 21:3 Lk 5:5 21:4 Lk 24:16; Yn 20:14 21:5 Lk 24:41 21:6 Lk 5:4-7 21:7 Yn 13:23 21:8 Dhiraa 200 ni kama mita 90 21:9 Yn 18:18; 21:10, 13 21:12 Mdo 10:41 21:13 Yn 21:9 21:14 Yn 20:19, 26 21:15 Lk 24:41 21:16 2Sam 5:2; Mt 2:6 21:17 Yn 2:24, 25; 16:30 21:19 Yn 12:33; 18:32 21:20 Yn 16:22; Yn 21:7; 13:23 21:22 Mt 16:27, 28; 25:31; 1Kor 4; 5; 11:26; Ufu 2:25; 3:11; 22:7, 20 21:23 Mdo 1:16 21:24 Yn 15:27; 19:35 21:25 Yn 20:30
MUNGU ANAKUPENDA Mungu hakwambii tu anakupenda bali amedhirisha upendo wake kwako kwa kumtuma mwanawe wa pekee kuishi maisha mema nasi na hata kufa nasi Maana Mungu aliupenda ulimwengu hivi hata akamtoa Mwana wake wa pekee, ili kila amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Y0HANA 3:16 WOTE NI WATENDA DHAMBI Mungu ni mukamilifu na anastahili heshima, bali sisi tumepungukiwa na ni watenda dhambi. Watu wote wametenda dhambi na wametindikiwa utukufu wa Mungu. WARUMI 3:23 Kama Maandiko Matakatifu yasemavyo: “Hakuna hata mmoja aliye mwadilifu!” WARUMI 3:10
MPANGO WA MUNGU KUTUOKOA Sote twapaswa kufa na kutenganishwa na Mungu kwasababu tumetenda dhambi—lakini Mungu ana mpango! Alimtuma Mwanawe kama kipawa cha bure kwetu sisi, ili wote watakaoamini na kumkubali Mwanawe waweza kusamehewa! Mwana wa Mungu ni Yesu Kristo, ambaye aliishi, akafa na alifufuka kwa uhai kwa ajili yako. Mungu amekutengenezea njia ili umujue na ‘’njia’’ hii ni Yesu. Kwa maana mshahara wa dhambi ni kifo; lakini zawadi anayotoa Mungu ni uzima wa milele katika kuungana na Kristo Yesu, Bwana wetu. WARUMI 6:23 Lakini wale wote waliompokea na kumwamini, hao aliwapa uwezo wa kuwa watoto wa Mungu. YOHANA 1:12
Mimi niliwakabidhi ninyi mambo muhimu sana ambayo mimi niliyapokea: kwamba Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu kufuatana na Maandiko Matakatifu; kwamba alizikwa, akafufuka siku ya tatu kama ilivyoandikwa; 1 WAKORINTHO 15:3-4
JAWABU LAKO Wakati unapogundua ya kwamba umemkosea,hatua ya kwanza ni kuomba msamaha. Kiri ya kwamba umemkosea na amini ya kuwa amekusamehe na kukuokoa toka kwa matokeo ya dhambi kwa ajili ya yale ambayo mwanawe wa pekee amekutendea. Lakini tukiziungama dhambi zetu, basi Mungu ni mwaminifu na mwadilifu, naye atatusamehe dhambi zetu na kututakasa na uovu wote. 1 YOHANA 1:9 Maana Maandiko Matakatifu yasema: “Kila mtu atakayeomba kwa jina la Bwana, ataokolewa.” WARUMI 10:13
DH A MIR A YA NGU ‘Mungu,najua ya kwamba mimi ni mtenda dhambi na ninaamini ya kuwa mwanao wa kipekee yesu kristo alinifia pale msalabani na kufufuka toka kwa wafu kwa ajili yangu. Natoka kwenye dhambi zangu na kukiri ya kwamba Yesu ndiye Bwana na mwokozi wangu.’’ __________________________________________ JINA
LIPI LINGINE? Baada ya kumkubali Yesu kama mwokozi wako, tuna kuimiza ukatafute kanisa lililoko karibu nawe ili ukaweze kushiriki. Unapo endelea kutafuta kanisa, zidi kuomba akaweze kukupa kanisa ambalo litakusaidia kukuwa kama Mkristo na kujua zaidi kumhusu Mungu na Biblia pia. Lakini endeleeni kukua katika neema na katika kumjua Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo. 2 PETRO 3:18
_________________________________________ TAREHE
MUNGU HAWEZI KUKUACHILIA Mungu sio kama mwanadamu ambaye atakupenda tu wakati unapo tenda mema. Mungu anataka uamini ya kuwa anakushikilia zaidi ya jinsi ambavyo wewe ungeweza. Mungu ni mwaminifu na amekukubali wewe kama mwanawe na katu hatowacha kukupenda na kukujali. Kama ukikiri kwa kinywa chako kwamba Yesu ni Bwana na kuamini moyoni mwako kwamba Mungu alimfufua kutoka wafu, utaokoka. WARUMI 10:9 “Kweli nawaambieni, anayesikia neno langu, na kumwamini yule aliyenituma, anao uzima wa milele. Hatahukumiwa kamwe, bali amekwisha pita kutoka kifo na kuingia katika uzima. YOHANA 5:24 Lakini hizi zimeandikwa ili mpate kuamini kwamba Yesu ni Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mpate kuwa na uzima kwa nguvu ya jina lake. YOHANA 20:31
NewLife CHUNGUZA HAYA MASWALI! Swali kama: “Je, ni nini dhamira na lengo katika maisha yangu?’’ “Wakati nitakapo aga,ni kipi kitakachotendeka?’’ “Mungu ananipenda kweli?’’ Swali lingine la kuchunguza ni:
“NI KIPI AMBACHO NAAMINI KATIKA YESU?’’ Pakua app ya NewLife kwenye simu yako rununu ili kuchunguza zaidi maswali haya na mengineyo Ni rahisi kutumia. Anza na “Mraba wa kwanza”na ujue mada kama”Uwepo wake Mungu,” “Madhumuni ya Maisha” na “Ukweli Ni Upi?” Au waweza enda moja kwa moja kwa “Nielezee Zaidi” kifungu ambapo utapata mada kama ya Yesu Kristo, imani, dhambi na maombi.
Inapatikana katika lugha nyingi.
Pakua bure kwenye WWW.NEWLIFE.BIBLE
G6002 • KISWAHILI • KENYA 2021
www.sharewordglobal.com
Na kwa kupitia kwenye app hii, waweza kujisomea Biblia kwa njia na lugha rahisi popote ulipo.