item 3b ni redio ilio na fm, a.m. frequency, nani atainunua kwa mia mbili? chief ameipata kwa mara ya kwanza, ya pili na ya tatu!
BOYIE aweka chief kwa noma
...liiii... ...liii..
sob sob
habari mama, una shida gani?
sob sob
vitu zangu ndizo zinauzwa kwa auction!
3
mambo yaliharibika baada ya mume wangu kufariki. Watu walinitumia SMS wakiniambia nihame sababu mimi si mwenyeji
“mume wangu alikuwa na deni kubwa...
“AUCTIONEERS WALICHUKUA VITU VYA NYUMBA NA KUTUHAMISHA KWA SHAMBA YETU...
“niliuliza chief usaidizi na akakataa na kusema hasaidii watu wa kabila yetu...
“NILIPOKUWA MSICHANA NILIKUWA NATAKA KUWA NA SALON. LAKINI SINA MBELE WALA NYUMA. SINA PESA ZA KUJIENDELEZA...”
Siskii kama niko safe hapa na ni lazima nihame
USIJALI MAMA NITAAMBIA RAFIKI YANGU ALIYE NA KIPINDI YA KUENDELEZA VIJANA KWA REDIO yaani shujaaz fm NA ATAWEZA KUKUSAIDIA.
4
hii ni shujaaz fm na kijana wenu djb! niaje mafans? nimepata sms kutoka kwa rafiki yangu ambaye mali yake yote iliuzwa na auctioneers!!! amepoteza mali yake yote!
big-ups kwa mafans wanaonitumia ideas poa za kujiendeleza kama vijanaa...
nitumie ideas za kusaidia friend ya mine on 3008.
Ni responsibility yetu kama community kusaidiana hata kama ni watu wa community ingine
big-ups kwa fan aliyenitumia sms na kuniambia ana idea ya kusaidia friend ya mine ya kujiendeleza. nitawa-connect mara hiohio!
natafuta mama teresa.
ni mimi.
5
MImi ni kiongozi wa District peace commitee na ninataka kukusaidia. niliskia story yako kutoka kwa redio na nikaona naweza kukuSAIDIA twende nikuambie njiani.
unajua nimezoea kufanya kibarua ya kuosha na kupata 50 bob kila siku. lakini haitoshi kutuchunga mimi na watoto...
nashukuru sana.
mume wangu alikufa, mali yangu ikachukuliwa na auctioneers na hata chief alikuwa anawaangalia wakifanya haya yote. nilimuuliza anisaidie akakataa kwa sababu ya kabila yangu.
yaani chief hakusaidia? pole, sikujua kuwa maisha yako magumu HIVO
so, ulikuwa unataka kunisaidia kivipi?
hapana NA SIKUMALIZA MASOMO YANGU, SINA PESA ZA KUFUNGUA ACCOUNT NA KUNUNUA FORM.
unajua juu ya women’s fund?
HaUHITAJI VITU HIVYO VYOTE. KUPATA FORM NI BURE, NA HAWATAKUULIZA JUU YA MASOMO YAKO. TWENDE KWA OFISI YA WOMEN’S FUND ILI UPATE UJUMBE.
ndio hii women’s fund office. twende uongee na wao ili waweze kukusaidia.
6
hakikisha ujaze hizo forms na uzirudishe kwa women’s fund office
asante sana. sikufikiria ingekuwa rahisi hivi ku-apply women’s fund.
asante pia. all the best.
munch!
!
h krunc
sasa huyo mama hata hana kikombe! unadhani watoto wake wanaishi wapi na wamefukuzwa kwa nyumba YAO?
MUME WANGU! Kwanini hungesaidia huyo mama ILI ASIFAGILIWE na auctioneers?!? wewe ni mkabila! niliskia HIYO STORY KWA show ya kijana dj b na ikanisumbua sana!
NILIFIKIRI KAZI YAKO NI KUCHUNGA WANANCHI KUTOKANA NA MAOVU! YAANI CHEO YAKO INAKUKUBALISHA KUFANYA HIVO?
NAJUA HAYA YOTE NILIOSEMA HUJASKIA LAKINI LAWAMA NI KWAKO!!!
7
SASA ALIKUWA AKIONGEA JUU YA NINI? NIKIPATA HUYO DJ B NITAMFUNGIA STATION AACHE MAKELELE MINGI!!
!! ! U U U KU ASANTE BOYIE KWA KUNISAIDIA! NILI-SAIDIWA NA MAMA MWINGINE KUPATA WOMEN’S FUND.
SAWA, LAKINI NILIKUWA NATAKA KUMSHUKURU IN PERSON.
NITAAMBIA RAFIKI YANGU DJ B KUWA ALIKUSAIDIA.
Women’s Fund Mwaka wa 2007, serikali ilianzisha womens fund ili kusaidia wanawake kujiendeleza kiuchumi watajitegemee kifedha na kuwa more confident na kuparticipate kwa maendeleo ya nchi. Kila constituency imepewa 1 million shillings ili wanawake waweze ku-apply na kuipata. Womens fund inasaidia ku-build capacity ya wamama wanao omba loans, kwa kusaidia ku-market bidhaa zao na
8
kuwa-link na companies. Ni wanawake wachache wame-apply kupata women’s fund juu hawajui requirements za ku-apply sababu, hawana mali yao, na kuona ikiwa process refu ya ku-apply loans. Kuna aina mbili za womens fund loans: 1. C-WES loan “Tuinuke Loan”. 0% interest. Unaweza pata loan ya up to 50,000 bob na kurudisha malipo within 12 months (Unaanza kulipa loan baada ya 3 months za kupata loan). Hii loan inapewa tu kwa groups, si individuals. Enda kwa CWES office ilio karibu ili kupata more info. 2. Financial intermediaries Registered group ama individual anaweza-apply. Hizi hupewa na banks na saccos zilme-authorize-iwa na womens fund.
Interest ni 8 %. Unaweza pata loan ya up to Ksh.500,000. Malipo ya loan yanaanza kurudiswa within 36 months. Ili ku-apply kwa womens fund unahitaji 1. Kuwa 18yrs and above. 2. Kuwa from registered group ilio na more than 10 members kwa zaidi ya 3 months. Unaweza pata loan kutoka kwa Constituency Women Empowerment Scheme (CWES) inayomanage-iwa na District Gender and Social Development Officer kwa kila district. 3. Kuwa na account ya bank au sacco. 4. Men wanaweza apply kama wana 30% representation kwa group ya wamama. Hizi loans ni revolving na lazima watu warudishe malipo ili wengine waibenefit. Securities za CWES loan ni kama household items na business stocks. Tumia DJ B views na opinions juu ya hii storo ya womens funds on 3008.