Kuwa Shujaa Parent's guide 1

Page 1

MWELEKEZO WA WAZAZI

O 1 0

3 0 F


“Natamani kujua jinsi ya kuzungumza na watoto wangu kuhusu HIV”

“Je, nikizungumza na watoto wangu kuhusu uhusiano wa kimapenzi, nitawafanya watake kuanza uhusiano huu mapema?”

“Mtoto wangu akiwa marafiki na watoto ambao wameambukizwa na virusi vya HIV, naogopa kwamba ataambukizwa.”

Tumempa mtoto wako kitabu cha ‘Kuwa Shujaa’ ili aweze kujifunza kuhusu HIV na Ukimwi; na pia, kuhakikisha kwamba atajifunza njia za kujikinga. Kando ya hayo, labda watoto wako wanajua mengi yatakayo saidia familia yenu kujikinga na kuhifadhi hali nzuri ya afya- Waulize!

Watoto wengi huchokozwa shuleni na watoto wengine ambao hawajui ukweli kuhusu HIV na Ukimwi. Nia ya kitabu hiki ‘Kuwa Shujaa’ ni kubadilisha tabia hizo. The production of this document was funded by UNITED STATES AGENCY FOR INTERNATIONAL DEVELOPMENT (USAID), through a cooperative agreement (623-A-00-09-00001-00) with the Population Council.


TO

MTO A P M E M NI TU

?

I K I H U B A WAKO KIT

KWA NI

Lengo la ‘KUWA SHUJAA’ ni kuhakikisha kuwa katika shule zote watu hawatengwi au kudhulumiwa kwasababu ya hali yao ya HIV. Kutimiza lengo hili, mtoto wako anatakikana: ...ajue ukweli kuhusu HIV / UKIMWI ...aelewe kuwa ujuzi kuhusu HIV na Ukimwi utamsaidia kujikinga ...aelewe umuhimu wa kujua hali yake ya HIV ili aweze kujitolea kupimwa ...awe na ukarimu na upendo akiwa anahusiana na wanafunzi walio na virusi vya HIV.

Tunahitaji usaidizi ili kuhakikisha kwamba shule ni pahali pasipo na hatari kwa wanafunzi wasio na virusi vya HIV, na pia wale walio na virusi vya HIV. Waweza kutupa usaidizi huu kwa kusoma mwelekezo huu na kuzungumza juu ya vitabu vya ‘KUWA SHUJAA’ na watoto wako.

Ndani ya mwelekezo kuna maswali ambayo utaweza kumuuliza mtoto wako kuhusu HIV. Haya maswali pia yatakusaidia kuzungumza na mtoto wako kuhusu HIV. Kando ya hayo, maswali haya yatamsaidia mtoto wako kulimulika swala hili la HIV katika mwangaza mpya..

ENDELEA KUSOMA ILI WEWE NAWE

UWE SHUJAA!!!

3


Watoto wanaweza kuwadhulumu na kuwachokoza wengine ambao wanaonekana kuwa na tofauti. Hawa watoto wanaochokozwa wanapitia mateso na uchungu mwingi, ilhali hawajatenda mabaya.

Kama wazazi, mnaweza kuwasaidia watoto wenu kuelewa kwamba kuwa marafiki na watu walioambukizwa na virusi vya HIV, sio jambo la kuogopa! Ukweli ni kwamba ni jambo la kujivunia, kwani linaonyesha kwamba wewe ni mtu mwenye elimu na busara, na hatimaye, wewe ni SHUJAA! MUULIZE MTOTO WAKO KAMA ANAWEZA KUFANYA URAFIKI NA MTU AMBAYE ANA VIRUSI VYA HIV. AKISEMA HAWEZI, MUULIZE “KWA NINI?” NA WEWE JE, UNA WASIWASI WOWOTE KULINGANA NA MTOTO WAKO KUWA RAFIKI WA MTU ALIYE NA HIV? KAMA UNAO WASIWASI, JIULIZE NI KWA NINI...KISHA SOMA UKWELI JUU YA UENEZAJI NA KUAMBUKIZWA NA VIRUSI VYA HIV...KUPATA HUU UJUZI KUTAKUONDOLEA WASIWASI.

a na kizw mbu kumbata a u k zi um hawe IV kwa k ushikilia ja Mtu o a H izwa, k y v i sa m virus eambuk wa dara umbani. ny a aliy ake, ku elea a kidond emb no w mko au kumt ukiwa n ika damu u u sh naye aenea t IV; a cho kina usi vya H nzi HIV in o wazi e p ir h na v wa kima kilic liye tu a husiano inga na ako m a k z y ia u mia wen kupit ila kutu e na m b ew w . a h wa kikis mmepim kuha

Katika hadithi hii, kijana mmoja alifikiri kuwa angeweza kutibu hali yake ya HIV kwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na bikira. Lakini HIV HAINA TIBA!

MUULIZE MTOTO WAKO KAMA ANAJUA MBINU ZOZOTE ZA KUTIBU HIV. AKIKUPA MBINU YOYOTE, MWELEZEE KWA UTARATIBU, KWAMBA HIV HAINA TIBA.

4

MUULIZE MTOTO WAKO FIKRA ZAKE KUHUSU KIJANA ALIYEJARIBU KUMBAKA IMANI. JE, KAMA ANGEWEZA KUMBAKA, NI NINI KINGEFANYIKA? JE, HUYU KIJANA ANGEFUATA UTARATIBU GANI ILI KUTOKUWA NA HOFU ZAIDI KUHUSU HALI YAKE YA HIV?


’ ? O D U O Y D L U O W ‘WHAT

i

nafunz esha wa kuwawez i kupata n a ia p iz HIV, na wa kuig u u s u u h h u o k z che aida a HIV. Nia ya m mzo ya f ukizwa n mazungu alioamb w e l a kuwa na w za ya hisia fahamu Muulize mtoto wako juu ya mchezo huo wa kuigiza. Alikua nani katika huu mchezo? Je, mchezo huu ulibadilisha maoni yake kuhusu HIV?

Unajua mtu yeyote ambaye ana HIV? Una hisia gani kumhusu? Una ukarimu na roho ya usaidizi? Kwa nini usimuulize juu ya kuishi na hali hiyo ya HIV? Waweza kupata ujuzi wa faida ambao unaweza kuutumia katika mazungumzo zaidi na watoto wako.

Tunajua kwamba kuna mambo mengi ambayo watoto wanahofia kuuliza wakubwa wao. Kwasababu hiyo tumekupa sampuli ya vituo vingi vya VCT ambavyo vinahusika na vijana. Katika vituo hivi wanaweza kupata majibu yoyote wanayoyahitaji. Endelea basi kuangalia mienendo ambayo tumekupa ili kujua jinsi ya kuzungumza na watoto wako iwapo unasikia haya?

TRUE OR FALSE Katika sekta hii, tutazungumza kuhusu mambo yanayotajwa juu ya HIV na Ukimwi ambayo sio ya ukweli. Jaribu kusoma na kufanya huu mtihani na mtoto wako! Je, mtapita?

FACT

Mara nyingi ujuzi ni kinga dhidi ya kifo… zungumza na mtoto wako umpe ujuzi wowote ulio nao kuhusu HIV ili ajikinge!

BOX:

idia kusa weza nea kwa a n a w a ue Watu ha k push mo c wa kujie enzi kiko p k a , ifike a kim ia HIV k usiano w wa; na p . a iz h j k u u o a b m n m a no p alioa na w mia sinda tu kuto

5


Katika hadithi hii, Malkia anamsaidia rafiki yake kufanya uamuzi wa kutokuwa na uhusiano wa kimapenzi. Anampa huu usaidizi kutokana na ujuzi alioupata katika kituo cha VCT.

Je, umewahi kuenda kituo cha VCT? Walikupa mawaidha gani? Unaweza kumpa mtoto wako mawaidha haya? Muulize mtoto wako kama amewahi kuenda kituo cha VCT. Akisema ndio, mpe sifa na umuulize alijifunza nini alipoenda huko.

Wazazi wengi wakifikiria kuongea na watoto wao juu ya uhusiano wa kimapenzi, wanatatizika sana. Kwasababu ya jambo hili, watoto wengi hupata kujifunza kuhusu uhusiano huu, kutoka kwa vijana wenzao na kujaribu jaribu kama vipofu. Mara nyingi, majibu wanayoyapata ni ya kuchanganyisha na sio ya ukweli. Yanayofuata ni maelezo ya kukusaidia kuongea na mtoto wako kuhusu uhusiano wa kimapenzi...

Mambo ya muhimu ya kuwajulisha watoto wako kuhusu Uhusiano wa Kimapenzi, na Hisia za Kimapenzi Uhusiano wa kimapenzi ni jambo la kawaida kati ya watu wawili ambao wameahidiana kuwa pamoja. Sio vizuri kuwa na uhusiano huu kabla hujakomaa kimwili na kiakili. Watu wakiendelea kuwa, miili yao pia hubadilika. Mwili huonekana kama wa mtu mkubwa na sio wa mtoto. Haya mabadiliko ni ya kawaida, na hulingana na mtu mwenyewe. Kila mtu ana wakati wake binafsi wa mabadiliko haya kutokea. Hata hivyo, haimaanishi kwamba umekuwa tayari kuwa na uhusiano wa kimapenzi kwa sababu una mwili wa mtu mkubwa, lazima akili nayo iwe imekomaa. Mwili ni wako na uamuzi kuhusu wakati wa kuwa na uhusiano wa kimapenzi, pia ni wako. Usimkubali mtu yeyote akutolee uamuzi huo, hakikisha kwamba wewe uko tayari. Tafuta mtu mwenye umri wa kukushinda ili uongee naye kuhusu uhusiano wa kimapenzi. Kila mtu anaweza kuambukizwa virusi vya HIV. Lazima ujikinge dhidi ya uhusiano wowote wa kimapenzi usiokufaa‌ Wanafunzi wa umri mkubwa zaidi wanatakikana wajue ugonjwa wa zinaa ni ugonjwa wa aina gani, na pia waelewe kwamba mtu akiwa na ugonjwa wa zinaa, anaweza kuambukizwa na virusi vya HIV kwa urahisi zaidi.

Je, unajua kama mtoto wako ameanza kufanya uhusiano wa kimapenzi? Ukitaka kumsaidia usimkemee au kumuadhibu, la muhimu ni kumpa ujuzi na mawaidha yote anayohitaji ili kufanya uamuzi utakaofaa afya yake.

6


Najua ni jambo gumu kuzungumza na watoto wako kuhusu HIV, Ukimwi, na Uhusiano wa Kimapenzi...yafuatayo ni maelezo yatakayokupa roho na mwenendo wa kuzungumza na watoto wako kuhusu maneno magumu...

1. ANZA MAZUNGUMZO: Jaribu kulinganisha mazungumzo yako na mambo ya kawaida ambayo mtoto wako huona au kusikia. Inawezekana kuwa ameona jambo hili kwa kipindi televisheni au labda amesoma jambo hili katika kitabu cha KUWA SHUJAA. Waulize “Je, umepata mafunzo yoyote kuhusu HIV au Ukimwi?” au “Neno HIV lina maana gani kwako?”

2. SEMA UKWELI: Ongea na mtoto wako kulingana na umri wake. Hakikisha kwamba unawapa ukweli ukiwa unaongea nao.

3. WAKOSOE MAPEMA: Fikra za watoto kuhusu HIV na Ukimwi mara nyingi ni za kuchanganyikiwa na kutatanisha. Kwasababu hii, ni muhimu kuwakosoa mapema.

4. JENGA HISIA ZA KIBINAFSI: Kuwasifu watoto wetu wakifanya mambo mazuri na pia kujua wanapenda kufanya vitu gani ni njia moja ya kuwafundisha kujipenda. Jambo hili ni muhimu kwasababu watoto wakiwa na mapenzi ya kibinafsi hawatafuti sana mapenzi kutoka nje. Pia hawatajaribu sana kupendeza vijana wenzao na kupotea katika uhusiano wa kimapenzi kabla hawajakomaa. Kando na hayo, wasiwasi wa kuongea nawe kuhusu hisia zao utapotea.

5. GUNDUA UKWELI WEWE MWENYEWE: Utaweza kuikinga familia yako ukijua ukweli kuhusu HIV na Ukimwi. Enda VCT, gundua hali yako, kisha jifunze njia ambazo unaweza kutumia kuikinga familia yako na kuhifadhi hali yao ya afya.

7


Naweza ongea na wewe kuhusu mpenzi wangu?

i

Naogopa kujua hali yangu ya ukimwi. Naweza ongea na wewe kuihusu?

Nimepimwa na nimepatikana na virusi vya ukimwi. Ni wapi nitapata usaidizi?

Nilibakwa. Nichukue hatua gani?

Unahitaji kujua zaidi...kushauriwa... ama mahala salama kupimwa? Tutembelee:

KNH Youth Centre Tower Block, Ground Floor Kenyatta National Hospital Hospital Road, Nairobi. Tel: 020-2726300-9

kuwa shujaa production charles j ouda | bridget deacon | fatima aly jaffer design salim busuru art salim busuru | eric muthoga | noah mukono | kevin mmbasu stories grace irungu | daniel muli | peter kades published by well told story: www.wts.co.ke


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.