Gender & IWT - report summary (Swahili)

Page 1

MUHTASARI WA RIPOTI

JINSIA NA BLASHARA HARAMU YA WANYAMAPORI KUPUUZWA NA KUTOZINGATIWAN

Ripoti hii inatoa ujumuishaji na tathmini ya kwanza ya mienendo ya kijinsia katika biashara haramu ya wanyamapori (IWT) ulimwenguni. Inaangazia utafiti unaozingatia jinsia, ushahidi kutoka eneo kazi na dhana zinazohusiana na uwindaji haramu, usafirishaji haramu na ulaji wa bidhaa za wanyamapori, pamoja na utawala na sera ya kimataifa. Kwa kutumia msingi huu wa ushahidi, inatoa “mfumo halisi wa kijinsia” wa kuongoza kuleta uchambuzi wa kijinsia katika mipango, sera na hatua za IWT kupitia uchunguzi wa kimfumo wa mienendo ya kijinsia kwa wahusika, visababishi, athari na ukabilianaji. Ripoti hii pia inabainisha mahitaji ya utafiti na inatoa mapendekezo kutoka viwango vya eneo hadi vya ulimwengu.

“Jinsia na Biashara Haramu ya Wanyamapori, Kupuuzwa na Kutozingatiwa” inapatikana Julai 2021. Mwandishi, Joni Seager Kwa maelezo zaidi, wasiliana na: Rob Parry-Jones, Msimamizi, Wildlife Crime Initiative, WWF International rparryjones@wwfint.org

1 KUSHINDWA KUZINGATIA JINSIA KATIKA MBINU ZETU ZA IWT NI KAMA “KUKABILIANA NA UHALIFU WA WANYAMAPORI HUKU MKONO MMOJA UKIWA UMEFUNGWA NYUMA YETU”. Inasababisha mapungufu makubwa katika kuelewa shughuli, michakato na fursa halisia za IWT kwa uingiliaji kati. Kinyume chake, kujumuisha uchambuzi wa kijinsia katika mbinu za IWT kunaboresha uwezekano wa kufanikiwa katika uhifadhi na inaweza kuwa kichocheo cha kukabiliana na ukosefu wa usawa wa kijamii. Kwa mfano katika eneo la Hifadhi ya Kitaifa ya Kafue nchini Zambia, ambapo baadhi ya wanawake waliotengwa wana fursa chache za kujipatia riziki na wanalazimika kutoa malazi na ngono kwa wawindaji haramu wa msimu, aibu na usiri hulinda utambulisho wa mwindaji haramu na sifa ya mwanamke.

1|muhtasari wa ripoti

Kushughulikia suala hili linalotokana na usawa wa kijinsia kunaweza kuimarisha sio tu juhudi za kukabiliana na uhalifu wa wanyamapori, lakini pia kunaweza kukabiliana na ukosefu wa usawa wa kijinsia ambao unaliwezesha. Kwa kuongezea, wakati jinsia haizingatiwi, hatua za kukomesha IWT zinaweza kukita mizizi ya tofauti na ukosefu wa usawa wa kijinsia, na hivyo kudhuru wanawake na uhifadhi – badala ya kufanya kazi kwa kupunguza IWT na wakati huo huo kuimarisha usawa wa kijinsia.

MUHTASARI UNAENDELEA


MUHTASARI WA RIPOTI

JINSIA NA BIASHARA HARAMU YA WANYAMAPORI KUPUUZWA NA KUTOZINGATIWA

2 TOFAUTI, KANUNI NA UKOSEFU WA USAWA WA KIJINSIA HUANZISHA NA KUBAINISHA IWT NA HATUA ZA KUKABILIANA NAYO. Kwa sababu IWT hufanyika katika ulimwengu unaodhibitiwa na utofautishaji wa kijinsia, wahusika, desturi, athari, shinikizo na matokeo ya IWT – na vile vile juhudi za kuikomesha au kuimaliza – “zina ujinsia ndani yake” pia. Wanawake na wanaume hushiriki tofauti katika sehemu zote za IWT, kuanzia uwindaji haramu hadi utumiaji na katika uundaji sera, na mara nyingi huwa na mitazamo tofauti. Gharama na manufaa ya uwindaji haramu, usafirishaji haramu na ulaji wanyamapori ni tofauti kwa wanaume na wanawake, jinsi ilivyo na gharama na manufaa ya kukomesha au kumaliza IWT. Tunahitaji kuelewa tofauti hizo ili kuweza kushughulikia IWT.

3 UPUUZAJI WA JINSIA UNAONYESHA PICHA ISIYO WAZI. Wanaume na wanawake huingiliana na mazingira yao na maliasili kwa njia tofauti, na kawaida wana maarifa na uzoefu tofauti wa mazingira. Kwa mfano, katika baadhi ya jamii za pwani, wanawake wamepigwa marufuku kufanya uvuvi baharini, lakini hutumia wakati wakikusanya rasilimali kando ya pwani. Kukusanya maelezo kuhusu wanaume pekee (au wanawake pekee) hutoa maarifa yasiyo na manufaa na yanayoegemea upande mmoja. Hadi leo, maarifa ya IWT aidha yanapuuza jinsia au yanaegemea sana jinsia, bila uegemeaji huo kutambuliwa sana.

4 UNYANYASAJI WA KIJINSIA NA UKOSEFU WA USAWA WA KIJINSIA NDIZO HURAHISISHA IWT KATIKA MAMBO MENGI YA SHUGHULI MUHIMU. Mifano kadhaa ipo ya unyanyasaji wa kingono, ukahaba wa wanawake na usafirishaji wa kingono inayowezesha shughuli za kibinafsi na za kibiashara za IWT kwenye viwango vya eneo na vya ulimwengu. Kuangazia njia ambazo unyanyasaji wa kijinsia hutumika katika IWT hufungua njia za kukabiliana na kubadilisha mienendo hii.

2|muhtasari wa ripoti

5 KUSHUGHULIKIA JINSIA HUNUFAISHA WANAUME PIA. Kujumuisha uzingatiaji wa jinsia ni pamoja na kushughulikia kanuni zilizokita mizizi kuhusu wanaume na uume. Ni kawaida kwa wanaume kushinikizwa kufanya uwindaji haramu, na wanawake au wanaume wazee, kupitia uaibishaji wa uume. Dhana kwamba wanaume wanafaa zaidi kwa kazi ya mlinzi mwenye silaha huwaweka katika hatari kubwa. Utekelezaji wenye uume mwingi mara nyingi huathiri vibaya uhusiano na wanajamii ambao wanaweza kuwa washirika; pia unaongeza uwezekano kwamba utekelezaji utakuwa wa vurugu, na unaweza kuhusisha unyanyasaji wa kijinsia.

6 KAZI NA UTEKELEZAJI JUMUISHI WA WALINZI KWA KAWAIDA HUWA NA UFANISI ZAIDI. Kuna ushahidi madhubuti kwamba wanawake wana uwezekano mkubwa kuliko wanaume kutumia njia zisizo za vurugu na za majadiliano katika kusuluhisha mizozo.

7 KUWASHIRIKISHA WANAWAKE INANUFAISHA USAWA WA JINSIA NA UHIFADHI. Usawa wa kijinsia unahusishwa na ustawi wa kijamii na mazingira: wakati ukosefu wa usawa wa kijinsia uko juu, kwa kawaida ndivyo uharibifu wa mazingira unavyokuwa juu. Miundo ya kijamii na kiuchumi ambayo inakuza usawa wa kijinsia – maamuzi na ushiriki jumuishi, utambuzi wa athari nzuri za utofauti, raia wanaoshirikishwa na kuwezeshwa, utambuzi wa haki za kibinadamu ulimwenguni – pia ni masharti ya uendelevu wa kimazingira.

MUHTASARI UNAENDELEA


MUHTASARI WA RIPOTI

JINSIA NA BIASHARA HARAMU YA WANYAMAPORI KUPUUZWA NA KUTOZINGATIWA

8 MASHIRIKA YA UHIFADHI YANAYOKABILIANA NA IWT YANA FURSA YA KUWA VIONGOZI KATIKA KUFANYA MABADILIKO MAZURI YA KIJINSIA.. Kwa kuonyesha kujitolea kwa uwezeshaji wa wanawake na ujumuishaji wa kijinsia katika miradi na mipango yao, mashirika yanaweza kuwa washawishi wakubwa katika kubadilisha kanuni kandamizi na haribifu – haswa katika maeneo duni, vijijini. Kuhakikisha manufaa ya miradi ya uhifadhi yanasambazwa kwa njia zinazosaidia usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake inaboresha matokeo ya uhifadhi na wakati huo huo inasaidia maendeleo ya kijamii. Usawa wa kijinsia, utofauti na ujumuishaji pia hufanya kazi ya mashirika ya uhifadhi iwe rahisi na yenye ufanisi zaidi, na hivyo kuboresha mtazamo, upangaji na matokeo ya shirika.

9 UJUMUISHAJI WA JINSIA KATIKA KAZI ZA IWT UNAONYESHA AZIMA – NA WAJIBU – WA KIWANGO CHA JUU.

11 UTAFITI NA UCHAMBUZI WA JINSIA UNAHITAJIKA ZAIDI KATIKA SEHEMU ZOTE ZA KAZI ZA KUKABILIANA NA IWT. Sehemu kubwa ya ushahidi uliopo hutegemea tafiti chache tu. Mitindo ya nguvu na utofautishaji ambao hudhihirika kupitia jinsia pia inahusu vitambulisho vingine kama vile mbari/kabila, hadhi au dini, miongoni mwa zingine. Kuna uchambuzi mdogo sana wa mienendo hiyo kuhusiana na IWT.

12 UCHAMBUZI WA JINSIA NI ZANA, SI NJIA YA MKATO. Hautasuluhisha matatizo ya biashara isiyo endelevu na yenye vurugu ya wanyamapori. Lakini unachangia suluhisho kwa kushirikisha uelewa mpana wa matatizo, suluhisho na sera ambazo hazijatumiwa mahali pengine. Pia unawezesha mashirika ya IWT kuainisha kazi zao na ahadi za haki za binadamu na utofauti ambazo tayari zimeshafanywa katika sekta ya uhifadhi.

Usawa wa kijinsia umeamrishwa katika sheria nyingi za kitaifa na sera za shirika, na ajenda za usawa wa kijinsia zinazidi kuwa maarufu katika ahadi za sera za ulimwengu, ikiwa ni pamoja na Malengo ya Ukuzaji Endelevu. Wafadhili, wa kibinafsi na wa kiserikali, wanazidi kutarajia uchambuzi wa kijinsia kufanywa na kutekelezwa katika mipango wanayoiunga mkono. Hata hivyo, huluki zinazoongoza katika uwanja wa IWT hazizingatii hili: hakujakuwa na wito wowote katika kukabiliana na IWT kwa kuzingatia jinsia kutoka kwa washirika kama vile CITES au katika matamko mengine mbalimbali ya Umoja wa Mataifa au yanayoongozwa na serikali dhidi ya IWT.

10 UTUMIAJI WA WANYAMAPORI UNAJUMUISHA SANA JINSIA, KATIKA VIWANGO VYA CHINI NA JUU. Wanaume na wanawake hutumia na kununua bidhaa tofauti za wanyamapori, kwa madhumuni tofauti: mara nyingi wanawake ndio wanunuzi wa msingi wa bidhaa za dawa za wanyamapori; wanaume hutumia matumizi ya wanyamapori kama njia ya kuimarisha mitandao jamii ya kiume na mahusiano ya kibiashara. Jitihada za kupunguza mahitaji zitaongezwa kwa kuzingatia tofauti kama hizo za kijinsia.

3|muhtasari wa ripoti

“Jinsia na Biashara Haramu ya Wanyamapori, Kupuuzwa na Kutozingatiwa” inapatikana Julai 2021. Mwandishi, Joni Seager Kwa maelezo zaidi, wasiliana na: Rob Parry-Jones, Msimamizi, Wildlife Crime Initiative, WWF International rparryjones@wwfint.org

MWISHO


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.