Dondoo za unyonyeshaji wa mtoto • Katika miezi sita ya mwanzo mpatie mtoto maziwa ya mama pekee (usimpe maji au vyakula vingine). • Maziwa ya mama humpatia mtoto maji na virutubishi vyote kwa ukuaji sahihi wa mwili na akili. • Baada ya miezi sita mtoto apewe chakula cha nyongeza chenye mchanganyiko wa makundi yote matano ya vyakula. Aendelee kun yonyeshwa maziwa ya mama hadi kufikia umri wa miaka miwili na au zaidi. • Wakati wa kunyonyesha mtoto akae kwa nafasi ambayo haitamuumiza shingo. • Hakikisha mwili wa mtoto umenyooka na umegusana na mwili wa mama. • Uso wa mtoto utazame ziwa na mdomo uachame vizuri ili kumuwezesha kunyonya ziwa na sio chuchu. • Afya ya mtoto ni jukumu la baba, mama na familia kwa ujumla! • Familia na jamaa zimsaidie mama kuhakikisha anapata muda na fursa ya kumnyonyesha mtoto kikamilifu.