MFUKO WA MAFAO YA KUSTAAFU WA GEPF
TAARIFA YA UENDESHAJI KWA MWAKA
2013 / 2014
TAARIFA YA UENDESHAJI KWA MWAKA 2013 / 2014
2
TAARIFA YA UENDESHAJI KWA MWAKA 2013 / 2014
TAARIFA MUHIMU Bodi ya Wadhamimi Bi. J.M. Shaidi Bw. A.S Kilima Bw. A.L. Mapunda Bi. F.S Kiongosya Bw. R.E. Chalamila Eng. D.L. Chamulesile Bw. O. M. Urassa Bw. C. W. Samanyi Bw. D.M. Msangi
Mwenyekiti Mjumbe Mjumbe Mjumbe Mjumbe Mjumbe Mjumbe Mjumbe Katibu
Kamati ya Ukaguzi ya Bodi Bw.O. M.Urassa Bi.F.S. Kiongosya Eng. D.L. Chamulesile Bw. A.S Kilima
Mwenyekiti Mjumbe Mjumbe Mjumbe
Anwani ya Ofisi (Makao Makuu) GEPF House Ghorofa ya nane na tisa, Barabara ya Ally Hassan Mwinyi S.L.P11492 Dar -es-Salaam Simu: +255 22 2927668/9 Ofisi za Mikoani Dodoma Ghorofa ya Kwanza S.L.P 1517, Dodoma. Simu:+255 26 2320151 Tanga Mtaa wa Uhuru, S.L.P 5071 Tanga. Simu:+255 27 2645218
TAARIFA YA UENDESHAJI KWA MWAKA 2013 / 2014
Jengo la Posta,
Jengo la Posta,
1
Mtwara Jengo la CWT Ghorofa ya Kwanza, Barabara ya TANU, S.L.P 1287 Mtwara Simu: +255 23 2334550 Mwanza Ghorofa ya Pili, Jengo la Alfa Barabara ya Nyerere S.L.P 2104 Mwanza Simu: +255 28 2540660 Iringa (Mafinga) Jengo la ofisi ya Kazi Wilaya Barabara ya Iringa-Mbeya S.L.P 359 Mafinga Simu: +255 26 2772491 Ilala Ghorofa ya nne, Jengo la Ushirika, Mtaa wa Lumumba S.L. P 11492 Dar Es Salaam Simu: +255 22 2181612 Kinondoni Ghorofa ya kwanza Jengo la Ubungo Plaza S.L.P 11492 Dar Es Salaam Simu: +255 22 2664790 Temeke Ghorofa ya nne Jengo la Mek one Plaza Bara bara ya Nyerere S.L.P 11492 Dar Es Salaam Simu: +255 22 2866296
2
TAARIFA YA UENDESHAJI KWA MWAKA 2013 / 2014
Arusha Ghorofa ya kwanza Jengo la Summit Block A Bara Bara ya Sokoine, S.L. P 10729 Arusha Simu/fax: +255 27 2507007 Mbeya Ghorofa ya kwanza Jengo la Delha Makutano ya Lupaway na Jamatin S.L. P 2423 Mbeya Simu/Fax: +255 25 2503666 Mabenki Benki ya NBC Limited S.L.P 9062 Dar-es-salaam Benki ya CRDB ( Jengo la Holland ) S.L.P 71960 Dar-es-Salaam Benki ya NMB S.L.P 9213 Dar-es Salaam Benki ya Posta Tanzania Bara Bara ya Ali Hassan Mwinyi - Jengo la Millenium Tower S.L.P. 9300 Dar-es-Salaam Wakaguzi wa Nje HLB MEKONSULT Limited Certified Public Accountants S.L.P 14950 Dar -es-salaam
Tafadhari tembelea moja ya Ofisi zetu au Wavuti / Tovuti; www.gepf.or.tz Barua pepe: info@gepf.or.tz
TAARIFA YA UENDESHAJI KWA MWAKA 2013 / 2014
3
Dira Kuwa Mfuko wa kwanza wa Hifadhi ya Jamii
MFUKO WA MAFAO YA KUSTAAFU WA
GEPF
Dhima Kutoa mafao ya Hifadhi ya Jamii yaliyo bora na yanayokidhi matarajio na huduma bora kwa wanachama
Misingi ya kazi zetu Misingi ya kazi zetu ni Uwajibikaji, Uadilifu, Kuwajali wanachama, Uwajibikaji wa pamoja katika kazi na kuwa wabunifu.
4
TAARIFA YA UENDESHAJI KWA MWAKA 2013 / 2014
YALIYOMO BARUA YA KUWASILISHA
6
TAARIFA YA MWENYEKITI
7
WAJUMBE WA BODI YA WADHAMINI
9
UONGOZI WA MFUKO
10
TAARIFA YA MKURUGENZI MKUU
11
MAPITIO YA UTENDAJI
13
Uandikishawaji wa Wanachama na ukusanyaji wa michango
13
Ulipaji Mafao kwa Wanachama
15
Uwekezaji na Mapato Yanayotokana na Uwekezaji
16
Vitegauchumi vyenye faida inayojulikana kabla ya kuwekeza
17
Uwekezaji katika Majengo
18
Uwekezaji katika Hisa
18
Thamani ya Mfuko
19
Riba kwa Wanachama
19
Huduma kwa Wanachama
20
Elimu kwa Umma
20
Rasilimali Watu
21
Misaada ya Kijamii
21
MATARAJIO YA BAADAE
22
TAARIFA YA UENDESHAJI KWA MWAKA 2013 / 2014
5
BARUA YA KUWASILISHA Mh. Saada Mkuya Salum (Mbunge), Waziri wa Fedha, 1 Mtaa wa Madaraka, S.L.P 9111 11468 DAR ES SALAAM.
Mh. Waziri, YAH: TAARIFA YA UENDESHAJI KWA MWAKA 2013/14 Ninayo furaha kuwasilisha taarifa ya uendeshaji wa Mfuko kwa kipindi kinachoishia tarehe 30 Juni 2014. Taarifa hii naiwasilisha kwako kwa mujibu wa kifungu Na. 36(4) cha Sheria ya Mfuko wa Mafao ya Kustaafu wa GEPF Namba 8 ya 2013. Taarifa hii inajumuisha hesabu za mwaka ulioishia mwezi Juni 2014. Wako katika ujenzi wa Taifa,
Joyce M. Shaidi MWENYEKITI WA BODI
6
TAARIFA YA UENDESHAJI KWA MWAKA 2013 / 2014
TAARIFA YA MWENYEKITI Ninayo furaha kuwasilisha taarifa ya uendeshaji wa Mfuko kwa kipindi cha mwaka unaoishia Juni 2014 kwa niaba ya Bodi ya Wadhamini ya GEPF. Katika kipindi hiki Mfuko ulibadili taratibu zake za kiuendeshaji kutoka mfumo wa akiba kuwa mfumo wa pensheni. Pamoja na mabadiliko haya, na kwa mujibu wa Sheria wanachama wa Mfuko chini ya sheria iliyokuwepo awali wanakuwa wanachama wa Mfuko Mpya unaojulikana sasa kama Mfuko wa Mafao ya Kustaafu wa GEPF (GEPF Retirement Benefits Fund) ambao umeanza rasmi mwezi Februari 2014. Kupitia mabadiliko haya, mafao yameongezwa kutoka matatu hadi sita ambayo ni pensheni kwa wastaafu, fao la warithi, fao la kuumia kazini, fao la kifo, fao la elimu na msaada wa mazishi. Kadhalika sheria imeruhusu Mfuko kuendelea kubuni na kutoa mafao ya muda mfupi, hivyo ni matarajio yetu kuendelea kubuni na kuongeza mafao mengine kulingana na mahitaji na uwezo wa Mfuko. Tunapojiunga na wenzetu ambao walianza kutoa mafao ya pensheni kabla yetu, napenda kuwahakikishia wanachama na wadau wote kwa ujumla kuwa tutaendelea na utoaji wa huduma bora. Mafao na huduma nyingine kwa wanachama vitatolewa kwa wakati na ni kusudio letu kuendelea kuongoza katika eneo hili. Ili kuhakikisha hatuyumbi katika huduma, Mfuko unakusudia kuwekeza zaidi katika teknolojia ya habari, elimu kwa watumishi wa Mfuko, kuanzisha vituo vya kutolea huduma na kuongeza matumizi ya mawakala. Kadhalika tutaendelea kufungua ofisi za mikoa kulingana na mahitaji na uwezo wa Mfuko. Lengo letu ni kufanya GEPF kuwa Chaguo la Kwanza katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii. Maendeleo ya Mfuko ni mazuri kwani tulifanikiwa kusajili wanachama wengi, kukusanya michango ya wanachama na kuwekeza katika vitegauchumi salama. Kielelezo cha mafanikio haya ni ukuaji wa Mfuko ambao ulifikia kiwango cha asilimia 33.77. Kwa kutumia namba halisi, thamani ya Mfuko iliongezeka na kufikia shillingi milioni 265,438.12 mwezi Juni 2014 kutoka shillingi milioni 198,433.08 mwezi Juni 2013. Maeneo mengine ni: wanachama ambao waliongezeka hadi kufikia 76,045 kutoka 59,042 sawa na ongezeko la asilimia 28.80, michango ya wanachama kutoka shillingi milioni 36,816.00 hadi 50,631.43 na mapato kutoka kwenye vitega uchumi kutoka shillingi bilioni 18.30 hadi shilingi bilioni 24.90. Riba kubwa katika masoko ya fedha, ongezeko la thamani ya hisa zetu katika makampuni ambayo Mfuko umewekeza na ongezeko la michango ya wanachama kwa pamoja vilichangia sana katika mafanikio yaliyopatikana. Maelezo ya kina kuhusu hali ya uendeshaji wa Mfuko yametolewa katika taarifa hii.
TAARIFA YA UENDESHAJI KWA MWAKA 2013 / 2014
7
Kwa niaba ya Bodi ya wadhamini napenda tena kutoa shukrani zangu za dhati kwa wanachama na wadau wengine kwa kuendelea kutuunga mkono. Napenda pia kuipongeza menejimenti na wafanyakazi wote wa Mfuko kwa kazi nzuri ambayo ndiyo imetufikisha hapa. Ombi langu kwao ni kuendelea kujituma na kutoa huduma bora kwa wanachama na wadau wetu. Mwisho kabisa napenda kuwahakikishia utayari wa Bodi katika kuhakikisha maslahi ya wanachama yanabaki kuwa kipaumbele cha Mfuko. Ahsanteni
Joyce M. Shaidi MWENYEKITI WA BODI
8
TAARIFA YA UENDESHAJI KWA MWAKA 2013 / 2014
WAJUMBE WA BODI YA WADHAMINI
Bi. Joyce Shaidi MWENYEKITI
Bi. Fatma Kiongosya MJUMBE
Bw. Oswald Urassa MJUMBE
Eng. Deonis Chamulesile MJUMBE
Bw. Ahmed Kilima MJUMBE
Bw. Alfred Mapunda MJUMBE
Bw. Charles Samanyi MJUMBE
TAARIFA YA UENDESHAJI KWA MWAKA 2013 / 2014
Bw. Renatus Chalamila MJUMBE
Bw. Daud Msangi KATIBU
9
UONGOZI WA MFUKO
Bw. Daud M. Msangi MKURUGENZI MKUU
Bw. Coster O. Mpagike
Bw. Hussein I. Kinduu
MKURUGENZI WA FEDHA NA UTAWALA
MKURUGENZI WA UKAGUZI WA NDANI
Bi. Anna T. Shayo
Bw. Edgar R. Shumbusho
MKUU WA KITENGO CHA SHERIA
10
MKUU WA KITENGO CHA TEHAMA
Bw. Anselim K. Peter
Bw. Festo L. Fute
MKURUGENZI WA UENDESHAJI
MKURUGENZI WA MIPANGO NA UWEKEZAJI
Bw. Charles G. Mnyeti
Bw. Aloyce B. Ntukamazina
MKUU WA KITENGO CHA UGAVI NA MANUNUZI
MKUU WA KITENGO CHA MASOKO
TAARIFA YA UENDESHAJI KWA MWAKA 2013 / 2014
TAARIFA YA MKURUGENZI MKUU Mwaka 2013/14 utakumbukwa kama mwaka ulipozaliwa GEPF Mfuko wa Mafao ya Kustaafu na kuanzishwa rasmi kwa utaratibu wa pensheni. Kabla ya hapo GEPF ulikuwa Mfuko wa Akiba ukihudumia wafanyakazi wa mikataba na wale wasio na stahili ya pensheni. Mabadiliko haya yalifikiwa baada ya kipindi kirefu cha majadiliano na wadau na hatimaye uandishi wa sheria ambayo ilipitishwa na Bunge mwezi Novemba 2013. Sheria hii ilitiwa saini na Mheshimiwa Rais mwezi Januari 2014 na kuchapishwa katika Gazeti la Serikali mwezi Februari 2014. Hadi tunafikia mwisho wa mwaka 2013/14, GEPF mpya ilikuwa na umri wa miezi mitano tu. Ninapowasilisha taarifa hii kwenu ninalazimika kuelezea umuhimu wa mabadiliko haya kwa wanachama. Jambo la kwanza sheria mpya inatoa fursa kwa wanachama kupata malipo endelevu yatakayolipwa kila mwezi. Utaratibu huu ambao haukuwepo wakati Mfuko ukiendeshwa kwa utaratibu wa akiba unajulikana kama utaratibu wa pensheni. Kwa maana nyingine, chini ya sheria mpya wanachama watahudumiwa na Mfuko kwa kipindi chote watakachoishi baada ya kustaafu. Halikadhalika sheria inatoa fursa Mfuko kutoa mafao ya muda mfupi na muda mrefu kwa wanachama wake. Kutokana na fursa hii, ni kusudio letu na matarajio yetu kuanzisha mafao zaidi ya muda mfupi ili kuwasaidia wanachama wetu kugharamia mahitaji yao ya sasa bado wakiwa katika ajira. Maendeleo ya Mfuko kwa kipindi cha taarifa hii yameendelea kuwa mazuri kwani Mfuko umekuwa na ukuaji katika takribani maeneo yote ya uendeshaji. Wanachama na mali za Mfuko kwa ujumla vimeongezeka kwa kiwango kikubwa. Ukuaji huu unathibitishwa na na takwimu zilizotolewa katika taarifa hii na katika taarifa ya Mwenyekiti. Ubora wa huduma zetu kwa wanachama umeongezeka na malengo yaliyowekwa kwa mwaka yamefikiwa. Tumeanza kutekeleza majukumu yetu kama Mfuko wa Pensheni kwa kuandaa Mpango Kazi wa miaka mitatu ili kuonyesha vipaumbele, malengo na kuelekeza namna ya kuwekeza rasilimali za Mfuko. Zoezi hili lilikamilika Julai 2014. Malengo makuu ya Mpango ni kuongeza ubora wa huduma kwa wanachama, kupanua wigo wa wanachama, kuongeza mapato ya uwekezaji na kuongeza ufanisi katika utoaji huduma kwa wanachama. Nina kila sababu ya kuwahakikishia wanachama wetu na
TAARIFA YA UENDESHAJI KWA MWAKA 2013 / 2014
11
wote wanaopenda kujiunga na GEPF hali bora kupitia sheria mpya. Huu ni wakati muafaka wa kuifanya GEPF chaguo lako namba moja. Kwa niaba ya Bodi ya Wadhamini, Menejimenti na watumishi wote napenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa kuendelea kutuunga mkono kwani bila wao mafanikio yote niliyoeleza yasingepatikana. Kadhalika naishukuru Bodi ya Wadhamini kwa kutuongoza vizuri na utayari walionao katika kuhakikisha wanaifanya GEPF chaguo lako namba moja. Kwa upande wa watumishi wa Mfuko natoa wito waendelzee juhudi na kujituma kazini huku wakizingatia misingi tuliyojiwekea kama Mfuko. Ninawashukuru kwa mchango wao mkubwa ambao ndiyo msingi wa mafanikio yaliyopatikana.
Daud M Msangi MKURUGENZI MKUU
12
TAARIFA YA UENDESHAJI KWA MWAKA 2013 / 2014
MAPITIO YA UTENDAJI Uandikishawaji wa Wanachama na ukusanyaji wa michango Skimu ya Lazima Mfuko ulipata mafanikio makubwa kwa upande wa usajili wa wanachama na ukusanyaji wa michango. Usajili uliongezeka kwa asilimia 28.8 wakati makusanyo yaliongezeka kwa asilimia 37.52. Kuongezeka huko kwa wanachama na michango kulitokana na hatua mahsusi za kuutangaza Mfuko na hivyo kuwavutia wanachama wengi kujiunga. Kuongezeka kwa mishahara, katika sekta ya umma pia kulichangia sana ukuaji huu. Jedwali namba 1 linaonyesha hali halisi kuanzia mwaka 2009/10.
Jedwali 1: Makusanyo ya michango na uandikshwaji wa wanchama Mwaka 2009/10 2010/11 2011/12 2012/13 2013/14
Idadi ya Wanachama 35,279 41,879 52,670 59,042 76,045
Ongezeko 18.71% 25.77% 12.10% 28.80%
Michango(millioni) 16,321.46 25,711.90 30,149.13 37,299.76 52,169.48
Ongezeko 57.39% 17.26% 23.70% 39.90%
Mhimili 1: Kukua kwa wanachama pamoja na michango
TAARIFA YA UENDESHAJI KWA MWAKA 2013 / 2014
13
Skimu ya Hiari Mfuko uliendelea na utekelezaji wa skimu ya hiari (Mpango wa Hiari wa Kujiwekea Akiba ya Uzeeni) kwa mwaka 2013/14. Huu ulikuwa ni mwaka wa tatu wa utekelezaji wa Mpango huu. Mfuko ulijielekeza zaidi kuelimisha wanachama na wananchi kwa ujumla kupitia kwenye warsha, semina, na aina nyingine za uelimishaji ili kuutangaza Mpango huu. Kupitia uelimishaji wa umma wanachama wapya 15,204 walijiunga na Skimu hii hivyo kuongezeka hadi kufikia wanachama 33,003 mwezi Juni 2014. Halikadhalika makusanyo ya michango yaliongezeka na kufikia shilingi 3,101.25 million kwa mwaka wa 2013/14. Mhimili Namba 2 unaonyesha hali ya ukusanyaji wa michango. Mhimili 2: Ukusanyaji Michango kutoka 2009-2010 hadi 2013-2014 (TZS 000,000)
Ulipaji Mafao kwa Wanachama Ulipaji mafao kwa wanachama ni miongoni mwa kazi muhimu za Mfuko. Kiasi cha shilingi milioni 13,586.26 kililipwa kwa wanachama walioondoka kwenye Mfuko ikiwemo waliostaafu na waliohamia Mfuko wa Pensheni wa Watumishi wa Umma baada ya taratibu za ajira zao kubadilika na kuwa pensheni. Kumekuwepo na ongezeko la malipo mwaka hadi mwaka kama inavyoonyeshwa katika jedwali namba 2 hata hivyo malipo haya yameendelea kubaki katika viwango vinavyokubalika. Kama ilivyo katika jedwali hili, kiasi kilicholipwa mwaka 2013/14 ni asilimia 26.00 ya makusanyo yote ya mwaka hivyo Mfuko ulibaki na asilimia 74.00 ya makusanyo kwa ajili ya uwekezaji. Hiki ni kipimo cha Mfuko wenye afya nzuri unaoonyesha vyanzo vya uhakikika wa mapato kupitia michango ya wanachama na vitegauchumi vya Mfuko.
14
TAARIFA YA UENDESHAJI KWA MWAKA 2013 / 2014
Jedwali 2: Malipo ya Mafao (TZS. Milioni) Mwaka Mafao Ukuaji kwa mwaka
2009/10
2010/11
2011/12
2012/13
2013/14
16,321.46 3,323.66
25,711.90 3,675.46
30,149.13 5,247.25
37,299.76 9,536.60
52,169.48 13,586.29
Asilimia ya Makusanyo kwenye Mafao
20.4%
14.3%
17.4%
25.6%
26.0%
Mfuko utaendelea kuhakikisha makusanyo ya michango hayazidi mafao yatolewayo na Mfuko ili kuweza kuhakikisha fedha kwa ajili ya uwekezaji zinapatikana. Azma hii itafanikiwa kwa kuendelea kuongeza wigo na wingi wa wanachama wanaosajiliwa kila mwaka sambamba na kujenga mahusiano bora na waajiri ili michango iwasilishwe kwa wakati. Uwekezaji na Mapato Yanayotokana na Uwekezaji Katika mwaka 2013/14 Mfuko uliendelea kuwekeza katika maeneo makubwa manne ambayo ni maeneo yenye faida inayojulikana kabla ya kuwekeza, hisa za makampuni, majengo (ardhi) na uwekezaji wa pamoja. Kiasi cha shilingi milioni 242,376.80 kiliwekezwa na kuuingizia Mfuko mapato ya shilingi milioni 24,899.81. Kiasi hiki kikijumlishwa na mapato yaliyotokana na kukua kwa thamani ya hisa za makampuni, mapato yalifikia shilingi milioni 36,511.93 ambyo ni sawa na asilimia 15.06 ya fedha zilizowekezwa. Jedwali Namba 3 linaonyesha uwekezaji ulikua kwa asilimia 34.99 kwa mwaka 2013/14 ukilinganisha na uwekezaji uliofanyika mwaka 2012/13. Jedwali 3: Hali ya Uwekezaji Mwaka 2013/14 (TZS. Milioni) Aina ya uwekezaji
Amana za Serikali Amana za Mabenki Hisa Hati Fungani Mikopo kwenye Makampuni Mikopo Serikalini Uwekezaji wa pamoja Majengo Jumla Thamani ya Mfuko (Juni 2014)
Ukuaji
2012/13 TZS (000,000) 80,788.96 57,316.00 10,308.45 4,583.33 1,650.00 10,029.35 1,011.72 13,864.62 179,552.60
TZS (000,000) 101,311.45 86,953.00 20,848.41 1,000.00 1,100.00 9,439.71 1,117.81 20,970.42 242,376.80 265,438.12 34.99%
TAARIFA YA UENDESHAJI KWA MWAKA 2013 / 2014
2013/14 Ukuaji mpaka Juni 2014 38.17% 32.76% 7.72% 0.38% 0.41% 3.56% 0.42% 7.90%
Matakwa ya sera 20.0 - 60.00% 35.00% 10.00% 35.00% 10.00% 10.00% 25% 25.00%
15
Muhimili 2: Mgawanyo wa Vitegauchumi ( 30 Juni 2014)
0.42% 0.41%
7.90%
3.56%
0.38% AmanaSecurites za Serikali Gvt Amana Deposits za mabenki Bank
7.85%
38.17%
Hisa Equity
Corp. bonds Hati fungani Loans Mikopo Loan Govt Mikopo to ya Serikali Uwekezaji wa pamoja Coll. Scheme
32.76%
Property Ardhi na Majengo
Vitegauchumi Vyenye faida inayojulikana kabla ya kuwekeza Kundi la vitegauchumi hivi linajumuisha amana za mabenki, hati fungani, amana za serikali na mikopo. Kufikia Juni 2014 Mfuko ulikuwa umewekeza jumla ya shilingi milioni 199,804.16 ikilinganishwa na shilingi milioni 154,365.64 zilizowekezwa mwaka uliopita 2012/13. Kiasi hicho ni asilimia 82.44 ya fedha zote zilizowekezwa katika mwaka huo ambazo zilikuwa shilingi milioni 242,376.80 na kiasi cha asilimia 17.56 kilichosalia kiliwekezwa katika vitegauchumi vingine ikiwemo ununuzi wa hisa na uwekezaji katika majengo. Jedwali Namba 3 hapo juu linaonyesha mgawanyo wa uwekezaji katika vitegauchumi mbalimbali. Mapato yaliyokusanywa kutokana na uwekezaji wa aina hii yalikuwa shilingi milioni 24,009.44 ambayo ni sawa na silimia 96.1 ya mapato yote yaliyopatikana mwaka huu. Kiasi cha shilingi milioni 970.37 pekee sawa na asilimia 3.9 ndicho kilipatikana kutoka katika vyanzo vingine ikiwemo gawio kutokana na hisa za makampuni yaliyoodhoreshwa kwenye soko la mitaji na vipande vya Mfuko wa Umoja.
16
TAARIFA YA UENDESHAJI KWA MWAKA 2013 / 2014
Jedwali 4: Mapato yanayotokana na Uwekezaji Aina ya uwekezaji Amana za Serikali Amana za Mabenki Gawio Hati fungani Riba ya Mikopo Riba ya Mikopo ya Serikali Uwekezaji wa pamoja Jumla Ukuaji
(TZS 000’000)
2009/210 4,268.51 2,525.21 296.75 226.47 376.67 0
2010/11 4,301.72 3,355.07 292.4 411.31 265.3 1,183.30
2011/12 5,891.25 3,952.36 553.42 615.38 278.81 46.60
2012/13 8,410.99 7,926.32 633.80 586.53 340.76 109.05
7,693.62
9,809.30 27.5%
11,538.15 17.65%
18,253.99 58.21%
2013/14 13,066.72 9,999.21 883.11 356.55 466.74 120.22 87.26 24,979.81 36.80%
Uwekezaji katika Majengo Hadi kufikia mwezi Juni 2014 uwekezaji katika majengo ulifikia kiasi cha shilingi milioni 20,970.42. Kiasi hiki ni sawa na ongezeko la asilimia 51.25 kutoka shilingi milioni 13,864.62 zilizowekezwa mwaka 2012/13. Ongezeko hili linatokana na malipo yaliyolipwa kwa Mkandarasi wa jengo la ofisi (GEPF House). Jengo hili lilikabidhiwa rasmi kwa Mfuko mwezi November 2013 na ofisi za Mfuko kuhamishiwa hapo mwezi Januari 2014. . Uwekezaji katika majengo kwa ujumla wake ulifikia asilimia 7.90 ya thamani ya Mfuko. Uwekezaji mwingine uliofanya katika majengo ni ununzi wa ekari 50 za ardhi katika eneo la Kijaka-Kimbiji Kigamboni Dar-es-salaam na ekari 40.54 za ardhi katika eneo la Njedengwa Dodoma. Maeneo haya yote ni kwa ajili ya kujenga nyumba za gharama nafuu ili kuwauzia wananchi kwa ujumla. Uwekezaji katika Hisa Uwekezaji katika hisa unajumuisha hisa katika makampuni yaliyoorodheshwa katika Soko la Mitaji la Dar-es-salaam (DSE). Hadi kufikia tarehe 30 Juni 2014, uwekezaji katika hisa ulikuwa umefikia shilingi milioni 20,848.41 kutoka shilingi milioni 10,308.45. Ongezeko hili ambalo ni sawa na asilimia 102.25 lililotokana na kupanda kwa thamani za hisa ambazo lilileta faida ya shilingi milioni 15,550.89 ikilinganisha na gharama za ununuzi wa hisa zote. Jedwali namba 5 linaonyesha mgawanyo wa hisa zinazomilikiwa na Mfuko hadi kufikia mwezi juni 2014.
TAARIFA YA UENDESHAJI KWA MWAKA 2013 / 2014
17
Jedwali 5: Uwekezaji katika hisa No
Jina la Kampuni
Jumla ya hisa
Gharama (TZS Mil.)
Uhalisia wa soko (TZS mil)
Faida/Hasara (TZS mil.)
1
Kampuni ya Sigara Tanzania
207,674
357.81
2,325.95
1,968.14
2
Kampuni ya Bia Tanzania
900,000
1,650.12
8,910.00
7,686.00
3
Kampuni ya Saruji Tanga
221,617
170.9
531.89
360.99
4 5 6
Benki ya CRDB Benki ya NMB Kampuni ya Swissport Kampuni ya Saruji ya Twiga JUMLA
6,226,612 986,778 301,957
1,155.15 795.83 168.32
1,992.52 3,937.24 797.16
837.37 3,141.41 628.84
1,014,505
1,425.51
2,353.65
928.14
9,859,143
5,724.00
20,848.41
15,550.89
7 Â
Thamani ya Mfuko Thamani ya Mfuko imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka ambapo katika mwaka ulioishia mwezi Juni 2014, thamani ya Mfuko iliongezeka kutoka shilingi milioni 198,433.08 hadi kufikia shilingi milioni 265,438.12. Ongezeko hili ni sawa na asilimia 33.77. Kukua huku kwa Mfuko kumechangiwa na kuongezeka kwa makusanyo ya michango ya wanachama na kuongezeka kwa mapato yanayotokana na vitegauchumi. Sambamba na mapato mazuri, uwekezaji wote ulifanywa kwa kuzingatia taratibu kama zilivyowekwa na Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii. Riba kwa Wanachama Mabadiliko ya uendeshaji wa Mfuko kutoka Mfuko wa Akiba kuwa Mfuko wa Pensheni yanaelekeza mwanachama anayestaafu alipwe pensheni kila mwezi. Hata hivyo Mfuko una wanachama wa mpango wahiari wa kujiwekea akiba ambao wataendelea kulipwa riba kutokana na michango yao. Wengi wa wanachama hawa hawakidhi vigezo vya kulipwa pensheni hivyo wanasalia katika utaratibu wa akiba. Pamoja na wanachama wa mpango wa hiari kuna baadhi ya wanachama walioko katika mpango wa lazima ambao hawatakidhi kulipwa pensheni hivyo nao pia watalipwa michango yao pamoja na riba. Katika mwaka wa 2013/14 Bodi ya Wadhamini imetangaza riba la asilimia 7.5. Kiasi hiki kinatolewa ili kulinda thamani ya michango ya wanachama. Jedwali Namba 7 linaonyesha jinsi riba imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka tokea 2009/10. Jedwali 6: Riba kwa wanachama Kipindi Kiasi cha riba
18
2009/10 5.20%
2010/11 6.00%
2011/12 6.50%
2012/13 6.65%
2013/14 7.50%
TAARIFA YA UENDESHAJI KWA MWAKA 2013 / 2014
Huduma kwa Wanachama Mfuko umeendelea kutoa huduma bora kwa wanachama kwa kupunguza muda wa kuwahudumia wateja ikiwemo kulipa mafao na kushughulikia shida zao nyingine. Ili kufanikisha hili Mfuko uliongeza wafanyakazi na vitendea kazi katika ofisi ya makao makuu na ofisi za mikoa. Ofisi za mikoa pia zilipewa mamlaka ya kuanza kulipa mafao ya wanachama tofauti na ilivyokuwa hapo awali ambapo malipo yote yalikuwa yanafanyika makao makuu. Aidha muundo wa Mfuko umeboreshwa kwa lengo hilo hilo la kuongeza ufanisi katika kutoa huduma. Mpango wa Miaka Mitatu wa Mfuko umezingatia muundo mpya wa Mfuko ambao pamoja na mambo mengine kimeanzishwa Kitengo cha Masoko kinachojitegemea na idara ya huduma kwa Mteja.
Wajumbe wa Bodi, Menejimenti na baadhi ya wafanyakazi katika picha ya pamoja wakati wa kujadili Mpango kazi wa Mfuko wa Miaka mitatu.
Elimu kwa Umma Programu za kuongeza uelewa wa wanachama, waajiri na wadau wengine kwa ujumla juu ya Mfuko ziliendelea kutekelezwa. Njia mbalimbali zilitumika kutoa elimu ikiwemo matumizi ya dawati la huduma kwa wateja, tovuti ya Mfuko, semina, washa na matangazo redioni na kupitia television. Programu hii ilichangia kiasi kikubwa sana katika usajili wa wanachama wapya. Rasilimali Watu Muundo wa uongozi wa Mfuko uliimarishwa ili kuleta tija na kuongeza weledi. Katika kipindi cha mwaka huu vitengo viwili vilipandishwa hadhi (kitengo cha ukaguzi wa ndani na kitengo cha technolojia ya habari) na kuwa kurugenzi kamili na kuanzishwa kwa kitengo cha masoko. Kadhalika iliyokuwa idara ya shughuli na masoko majukumu yake yalibadilishwa kwa kuondoa huduma za
TAARIFA YA UENDESHAJI KWA MWAKA 2013 / 2014
19
masoko na kuanzisha kitengo cha huduma kwa wateja. Wafanyakazi waliendelea kupewa mafunzo ili kuwaongezea ujuzi katika sehemu zao za kazi. Hadi kufikia tarehe 30 Juni 2014 Mfuko ulikuwa na jumla ya wafanyakazi 84 kutoka wafanyakazi 77 waliokuwepo mwezi Juni 2013. Wafanyakazi wengi waliajiriwa katika mwaka wa fedha wa 2013/14 mahsusi kwa ajili ya kuboresha huduma za Mfuko. Mfuko uliendelea kuwapeleka wafanyakazi katika mafunzo ya ndani na ya nje na kuendelea kuwasaidia wale walioonyesha juhudi binafsi za kusoma baada ya muda wa kazi. Misaada ya Kijamii Mfuko uliendelea kutoa misaada katika jamii zenye uhitaji ikiwa ni sehemu ya huduma za kijamii kama zilivyoanishwa katika majukumu ya Mfuko. Misaada hii inasaidia pia kujenga muonekano mzuri wa Mfuko miongoni mwa Jamii. Mfuko ulitoa misaada mbalimbali katika maeneo ya elimu kwa baadhi ya wanafunzi waliokosa ada za shule, kusaidia watoto wenye ulemavu katika vituo mbali mbali vya watoto wasiojiweza na maeneo mengine yenye manufaa kwa Taifa.
Meneja wa Masoko Ndugu Aloyce Ntukamazina akitoa msaada wa vifaa vya kusomea kwa watoto wenye ulemavu wa ngozi katika shule ya msingi ya Matumaini iliyoko eneo la Kurasini. Mtoto Maria Mwingira akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya watoto wenzake.
MATARAJIO YA BAADAE Mabadiliko ya Mfuko kutoka kwenye utaratibu wa akiba na kuwa pensheni yameongeza ushindani miongoni mwa Mifuko. Ushindani huu ni changamoto kubwa kwa Mfuko hasa ikizingatiwa kuwa baadhi ya Mifuko ina ofisi nchi nzima wakati GEPF ina ofisi katika mikoa nane (8) tu. Ili kupambana na ushindani huu, katika kipindi kijacho Mfuko utaendelea kupanua uwepo wake kwa kufungua ofisi zaidi mikoani, kuandaa na kutekeleza mpango mkakati wa masoko na kuongeza ubora wa huduma kwa wanachama. Uwekezaji katika rasilimali watu na matumizi ya teknolojia ya habari katika kazi za kila siku vitapewa kipaumbele ili kupunguza matumizi ya karatasi na kuongeza ufanisi. Kadhalika Mfuko utaongeza matumizi ya wakala kusaidia ukusanyaji wa michango na kuutangaza Mfuko.
20
TAARIFA YA UENDESHAJI KWA MWAKA 2013 / 2014