Kipeperushi cha tawla

Page 1

Chama cha Wanawake Wanasheria Tanzania (TAWLA) kilianzishwa mnamo mwaka 1989 na kusajiliwa rasmi mwaka 1990 chini ya sheria ya vyama vya hiari sura ya 337 kama sheria zilivyorekebishwa mwaka 2002. Chama kilianzishwa kwa lengo la kuwaleta pamoja na kuwawezesha kujiendeleza kitaaluma wanawake wanasheria. Lengo kuu la chama hiki ni kutetea haki ya usawa wa kijinsia,utu na haki kwa kufanya uchemuzi wa mabadiliko ya sheria na sera ambazo ni kandamizi, kuhamasisha jamii na kutoa elimu kwa umma kupitia vyombo vya habari.


TAWLA inahamasisha jamii kuheshimu na kutetea haki za binadamu.

TAWLA imejitoa zaidi katika kuwaendeleza wanachama wake kitaaluma pamoja na kutetea haki za wanawake na watoto na utawala bora.

• • • • •

Uwazi Kujitoa Uadilifu Mikanganyiko Fani

1. Huduma ya msaada wa kisheria Shirika linatoa huduma ya ushauri wa kisheria na kuwawakilisha wanawake na watoto mahakamani, tumeanzisha na tunasimamia vituo vya msaada wa sheria katika mikoa ya; Arusha, Dodoma, Tanga, Mwanza na Dar es Salaam kwa wanawake na watoto walio katika mazingira magumu. 2. Kuongeza uelewa/ufahamu Kueneza uelewa wa haki za binadamu, haki ya afya ya uzazi, haki ya kumiliki mali, utawala bora na ukatili wa kijinsia kupitia semina za mafunzo, machapisho, uragabishi na utetezi na kusambaza taarifa juu ya sheria mbalimbali za nchi na mikataba ya kimataifa. 3. Tafiti za sheria na utetezi. Kufanya tafiti kuhusu sera na sheria ili kutetea mabadiliko na kuhamasisha sheria zinazolinda masuala ya jinsia na makundi yaliyo katika mazingira magumu. Tumefanya tafiti katika mambo mbalimbali mfano ardhi, afya ya uzazi, haki za watoto,katiba na kupelekea kuwepo kwa mswada wa jinsia na makundi yaliyosahaulika kama vile Sheria ya ardhi 1999, sheria ya mtoto 2009 na sheria ya makosa ya kujamiiana ya mwaka 1998.


Tangu kuanzishwa kwake chamakimefanikiwa; • Kutoa msaada wa kisheria kupitia vituo na huduma ya simu bila malipo kupitia namba 0800751010/0800110017 kwa zaidi ya wanawake milioni 5, kupitia vituo vilivyopo Dar es Salaam, Tanga, Arusha na Dodoma. • Tumeweza kuihamasisha jamii juu ya masuala ya kisheria kupitia machapisho mbalimbali, vyombo vya habari, michezo ya kuigiza na mafunzo. • Kutetea mabadiliko ya sheria kandamizi ili kuwalinda wanawake na watoto • Kuchangia uteuzi na ushiriki wa wanawake katika vyombo vya maamuzi. Tumeweza kuwatumia mawakili 173 katika kusaidia kuwawakilisha wanawake. • Kuwapa elimu wasaidizi wa msaada wa kisheria 402 katika wilaya 18 za Tanzania bara ambao wameweza kuwafikia watu 10,500 kwa mwaka 2014. • Tuna mahusiano mazuri ya kiutendaji na wadau mbalimbali wakiwepo asasi zisizo za kiserikali, wadau wa maendeleo, serikali kuu na serikali za mitaa.

TAWLA imegawanyika katika sehemu kuu tatu: 1. Mkutano mkuu wa wanachama:Hujumuisha wanachama wote na ndio chombo cha juu katika chama. 2. Baraza kuu Hili linaundwa na viongozi saba (7) wa chama ambao ni:i. Mwenyekiti wa chama, makamu mwenyekiti, Katibu, Mweka hazina na wajumbe wengine watatu 3. Sekretarieti Hawa ni watendaji wakuu wa shughuli za kila siku za chama wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji.

TAWLA inawaalika wanawake wanasheria wote kujiunga na chama ikiwa tu watazingatia I. Kulipa ada ya usajili. II. Kulipa ada ya mwaka.



Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.