Afya ya mtoto ni jukumu la baba, mama na familia kwa ujumla!
FAHAMU JINSI YA KUMNYONYESHA
MTOTO
Uzalishwaji wa maziwa ya kutosha yenye virutubisho unategemea upatikanaji wa makundi matano ya vyakula katika mlo wa mama.Wanaume wahakikishe upatikanaji wa vyakula nyumbani. VIRUTUBISHI VILIVYOMO KWENYE MAZIWA YA MAMA. Virutubishi vilivyomo kwenye maziwa ya mama vinauwiano sahihi kwa ukuaji na maendeleo ya mtoto.
NA UMUHIMU WAKE
Punguza vifo vya mama na mtoto kwa kuboresha afya yao!
Huyeyushwa kiurahisi na hufyonzwa na mwili wa mtoto kwa ufanisi. Virutubishi vilivyomo katika maziwa ya wanyama Figo za mtoto mchanga haziwezi kutoa mabaki ya ziada mwilini yatokanayo na maziwa ya wanyama KUMBUKA Madhara yatokanayo na ukosefu wa lishe katika kipindi cha miaka miwili ya awali ya mtoto hayawezi kutibika au kurekebishika hata hapo baadaye!
World Vision Tanzania ENRICH Project Singida Regional Commissioner Office Compound P.O.Box 1573. Singida mwivano_malimbwi@wvi.org www.wvi.org/tanzania World Vision Tanzania twitter: wv_tanzania
UNYONYESHAJI WA MTOTO MIEZI SITA YA MWANZO Katika miezi sita ya mwanzo mpatie mtoto maziwa ya mama pekee (usimpe maji au vyakula vingine).
mara baada ya kujifungua, kuchangia katika kupanga uzazi na hupunguza uwezekano wa kupata saratani ya mfuko wa uzazi na matiti.
Uso wa mama utazamane na mtoto. Kunyonyesha sio tu kwa ajili ya mtoto kupata maziwa bali upendo!
JINSI YA KUMPAKATA MTOTO WAKATI WA KUMNYONYESHA
KUMBUKA Ziwa lisipokaa vizuri kwenye kinywa cha mtoto humsababishia tumbo kujaa gesi na hivyo kupata maumivu makali ya tumbo (mila na desturi huita chango) na hivyo kulia mara kwa mara.
Humpatia maji na virutubishi vyote kwa maendeleo na ukuaji wa mwili na akili. Maziwa ya mama katika miezi sita ya mwanzo hupunguza vifo vitokanavyo na ugonjwa wa kuhara. Humpatia mtoto kinga dhidi ya magonjwa na humpunguzia uwezekano wa kupata utapiamlo hususani udumavu, uzito pungufu na ukondefu. Baada ya Miezi Sita Baada ya miezi sita mtoto apewe chakula cha nyongeza chenye mchanganyiko wa makundi yote matano ya vyakula. Mtoto asipewe vyakula au vinywaji kama soda, kahawa, chai na juisi za kusindikwa kwani kemikali zake hazina virutubishi vyovyote kwa ukuaji wake. Aendelee kunyonyeshwa maziwa ya mama hadi kufikia umri wa miaka miwili au zaidi. Faida za kunyonyesha kwa mama Kunyonyesha maziwa ya mama hulinda afya ya mama anayenyonyesha kwa kupunguza uwezekano wa kutokwa na damu nyingi
USHIRIKI WA FAMILIA KATIKA AFYA YA MAMA NA MTOTO. Kipindi cha Unyonyeshaji
Wakati wa kunyonyesha mtoto akae kwa nafasi ambayo haitamuumiza shingo Hakikisha mwili wa mtoto umenyooka na umegusana na mwili wa mama Uso wa mtoto utazame ziwa na mdomo uachame vizuri ili kumuwezesha kunyonya ziwa na sio chuchu Mama hakikisha unamshika mtoto mwili mzima na sio kichwa pekee.
Familia na jamaa zimsaidie mama kuhakikisha anapata muda na fursa ya kumnyonyesha mtoto kikamilifu.