JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA
“Uwajibikaji Unaanza na Wewe. Tushirikiane Katika Mapambano Dhidi ya Rushwa”
1
2
“Uwajibikaji Unaanza na Wewe. Tushirikiane Katika Mapambano Dhidi ya Rushwa”
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA
“Uwajibikaji Unaanza na Wewe. Tushirikiane Katika Mapambano Dhidi ya Rushwa”
i
ii
“Uwajibikaji Unaanza na Wewe. Tushirikiane Katika Mapambano Dhidi ya Rushwa”
Kumb na: PCCB/4/16/VOL.X
Mhe. Dkt John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1 barabara ya Barack Obama, IKULU, S.L.P. 9120, DAR ES SALAAM.
31 Machi, 2016
Mhe. Rais,
YAH: TAARIFA YA TAKUKURU YA MWAKA 2014/15
Tafadhali husika na somo tajwa hapo juu. Kwa mujibu wa kifungu cha 14 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba. 11 ya Mwaka 2007, ninayo heshima kubwa kuwasilisha kwako taarifa ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ya mwaka 2014/15. Taarifa hii imegawanyika katika maeneo makuu sita: Sehemu ya utangulizi; Sehemu ya kazi za Uchunguzi; Sehemu ya kazi za Utafiti na Udhibiti; Sehemu ya kazi za Elimu kwa Umma; Sehemu ya kazi za Uwezeshaji; Sehemu ya Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini na Majumuisho. Kwa pamoja maeneo hayo yanaonyesha hali halisi ya utendaji wa Taasisi kwa mwaka wa 2014/15 na matarajio yetu kwa mwaka 2015/16. Tunatarajia kuwa kwa kuendelea kuungwa mkono na Serikali ya Awamu ya Tano na azma yake ya Kupambana na tatizo la Rushwa na ufisadi pamoja na wananchi tutaweza kuinua zaidi kiwango chetu cha utendaji.
Wako Mtumishi Mtiifu,
Valentino Mlowola MKURUGENZI MKUU
“Uwajibikaji Unaanza na Wewe. Tushirikiane Katika Mapambano Dhidi ya Rushwa”
iii
VIFUPISHO VYA MANENO
Yaliyomo
DIRA, DHIMA NA MISINGI MUHIMU
vii ix
MUUNDO WA TAKUKURU x DIBAJI
xi
SURA YA KWANZA
1
UTANGULIZI 1 1.0
HISTORIA YA TAKUKURU
1
1.1
RUSHWA NA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA
2
1.2
RUSHWA NA MANUNUZI YA UMMA
2
1.3
RUSHWA NA UCHAGUZI
2
1.4
MAHUSIANO KATI YA TAKUKURU NA WADAU
2
1.5
MAMLAKA NA MAJUKUMU YA TAKUKURU
3
1.5.1
Mamlaka ya TAKUKURU
3
1.5.2
Majukukumu ya TAKUKURU
3
1.6
MPANGO MKAKATI WA TATU WA TAKUKURU (2014/15-2015/16)
3
SURA YA PILI
5
UCHUNGUZI 5 2.0 UCHUNGUZI
5
2.1
MATOKEO YA UCHUNGUZI NA MASHTAKA
5
2.1.1
Malalamiko ya vitendo vya rushwa yaliyopokelewa
5
2.1.2
Idadi ya majalada yaliyofanyiwa uchunguzi na kukamilika
6
2.1.3
Majalada yaliyopelekwa kwa DPP kuombewa kibali cha Mashtaka
7
2.1.5
Kesi Mpya
8
2.1.6
Idadi ya Kesi Zilizoamuliwa Mahakamani
9
2.1.7
Kiasi cha fedha/mali kilichookolewa
9
2.1.8
Mchanganuo wa Majalada ya Uchunguzi na Kesi kwa Tuhuma, Kisekta na Vifungu
vya Sheria
10
2.2
Ufuatiliaji wa fedha za miradi ya maendeleo katika Halmashauri
13
2.2.1
Manufaa yatokanayo na ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo
14
2.2.2
Sekta zilizofuatiliwa
14
2.2.3
Matokeo ya ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo na uelimishaji
15
2.2.4
Miradi ya Maendeleo
15
iv
“Uwajibikaji Unaanza na Wewe. Tushirikiane Katika Mapambano Dhidi ya Rushwa”
SURA YA TATU
18
UTAFITI NA UDHIBITI
18
3.0
KURUGENZI YA UTAFITI NA UDHIBITI
18
3.1
UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA UTAFITI NA UDHIBITI
18
3.1.1 Utafiti 18 3.1.2
Warsha na vikao vya wadau
19
3.1.3
Ufuatiliaji wa haraka wa kudhibiti vitendo vya rushwa
19
3.1.4
Ufuatiliaji wa utekelezaji wa maazimio ya kuziba mianya ya rushwa
19
3.1.5
Kutoa machapisho
22
SURA YA NNE
23
ELIMU KWA UMMA
23
4.0
ELIMU KWA UMMA
23
4.1
TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA KAZI ZA UELIMISHAJI UMMA
23
4.1.7 Machapisho
26
4.1.8
27
Makala za picha za video (video documentary)
4.1.9 Matangazo
27
4.1.10 Huduma za Maktaba:
27
4.1.11 Ziara za wageni (mahusiano na taasisi za ndani na nje ya Tanzania)
28
4.2
SHUGHULI ZA KIJAMII
28
4.2.1
Vikao vya Uelimishaji katika Serikali za Mitaa
28
4.3 MAFANIKIO
29
SURA YA TANO
30
UWEZESHAJI 30 5.0
UTAWALA NA USIMAMIZI WA RASILIMALI
5.1 Mafunzo
30 30
5.2
Vyeo 30
5.3
Usajili wa watumishi katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na Bima ya Afya
30
5.4
Ujenzi na ukarabati
31
5.5
Malipo ya pango
32
5.6
Watumishi waliochukuliwa hatua za kinidhamu
32
5.7
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
32
5.8 Manunuzi
32
5.9
32
Ukaguzi wa Ndani
“Uwajibikaji Unaanza na Wewe. Tushirikiane Katika Mapambano Dhidi ya Rushwa”
v
5.10
Fedha na Uhasibu
32
SURA YA SITA
34
MIPANGO, UFUATILIAJI NA TATHMINI
34
6.0
MIPANGO, UFUATILIAJI NA TATHMINI
34
6.1
Utekelezaji wa Mipango
34
6.1.1
Miradi inayofadhiliwa na wadau wa maendeleo (DPs)
34
6.1.1.5 Ufuatiliaji
36
6.1.1.6 Tathmini
36
SURA YA SABA
38
MAJUMUISHO
38
7.1 MAJUMUISHO
38
7.1.1 Uchunguzi
38
7.1.2
Utafiti na Udhibiti
39
7.1.3
Elimu kwa Umma
39
7.1.4 Changamoto
39
7.1.5 Matarajio
40
vi
“Uwajibikaji Unaanza na Wewe. Tushirikiane Katika Mapambano Dhidi ya Rushwa”
VIFUPISHO VYA MANENO 1
AfDB
-African Development Bank
2
ASDP
- Agriculture Sector Development Project
3
AU
-The African Union
4
AZISE
-Asasi zisizo za Kiserikali
5
BOQ
-Bill of Quantity
6
CAG
-The Controller & Auditor General
7
CIA
-Chief Internal Auditor
8
CSOs
-Civil Society Organizations
9
DFID
-Department for International Development
10
DMS
-Document Management System
11
DPP
-Director of Public Prosecution
12
GPSA
-Government Procurement Service Agency
13
HBF
-Health Busket Fund
14
ICT
-Information and Communications Technology
15
IPHRMS
-Integrated Payroll and Human Resource Management System
16
IPSAS
-International Public Sector Accounting Standard
17
ITV
-Independent Television
18
LGCBG
-Local Government Capital Building Grant
19
MKUKUTA
-Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kuondoa Umasikini Tanzania
20
MTEF
-Medium Term Expenditure Framework
21
NHIF
-National Health Insurance Fund
22
OPRAS
-Open Performance Review and Appraisal System
23
PETS
-Public Expenditure Tracking Survey
“Uwajibikaji Unaanza na Wewe. Tushirikiane Katika Mapambano Dhidi ya Rushwa”
vii
24
PMO-RALG -Prime Minister Office – Regional Administration and Local Government
25
PMU
-Procurement Management Unit
26
PPRA
-Public Procurement Regulatory Authority
27
QAIP
-Quality Assurance and Improvement Program
28
RWSSP
-Rural and Urban Water Supply and Sanitation Program
29
SADC
-The Southern African Development Community
30
SAFAC
-Southern Africa Forum Against Corruption
31
STACA
-Strengthening Tanzania Anti-Corruption Action
32
TACOSODE -Tanzania Council for Social Development
33
TAKUKURU
-Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
34
TAMISEMI
-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
35
TBC
-Tanzania Broadcasting Corporation
36
TEHAMA
-Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
37
TFDA
-Tanzania Food and Drugs Authority
38
TFF
-Tanzania Football Federation
39
TRA
-Tanzania Revenue Authority
40
UKIMWI
-Ukosefu wa Kinga Mwilini
41
UN
-The United Nations
42
UNCAC
-United Nations Convention Against Corruption
43
UNDP
-United Nations Development Program
44
WMA
-Weights and Measures Agency
viii
“Uwajibikaji Unaanza na Wewe. Tushirikiane Katika Mapambano Dhidi ya Rushwa”
DIRA, DHIMA NA MISINGI MUHIMU
DIRA YA TAKUKURU
“Kuwa chombo bora kinachofanya kazi zake kwa ufanisi na utimilifu huku kikiwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya rushwa nchini Tanzania ifikapo mwaka 2025”
DHIMA YA TAKUKURU
“Kupambana na rushwa kupitia uelimishaji umma, kuzuia, utambuzi, uchunguzi na mashtaka kwa kuwashirikisha wadau ili kuifanya rushwa itambulike kuwa ina madhara makubwa na isiyo na manufaa kwa jamii”
MISINGI MUHIMU
1. Kutoa huduma bora kwa kuzingatia haki na usawa; 2. Kuzingatia uadilifu na ukweli kwa kiwango cha juu; 3. Kufanya kazi kwa bidii, maarifa na kwa kushirikiana ili kutimiza malengo; 4. Kuzingatia uwajibikaji; 5. Kufanya kazi kwa kuzingatia maslahi ya umma; na 6. Kufanya kazi kwa heshima na uungwana.
“Uwajibikaji Unaanza na Wewe. Tushirikiane Katika Mapambano Dhidi ya Rushwa”
ix
MUUNDO WA TAKUKURU
x
“Uwajibikaji Unaanza na Wewe. Tushirikiane Katika Mapambano Dhidi ya Rushwa”
DIBAJI
T
aarifa ya utendaji kazi kwa mwaka 2014/2015 inalenga kutoa taswira ya utendaji wa TAKUKURU kwa kipindi cha kuanzia Julai 2014 hadi Juni 2015. Katika kipindi hiki wastani wa kiwango cha utendaji kazi wetu kimefikia asilimia 74.25. Mafanikio haya yamepatikana kutokana na kuboresha utoaji wa huduma zetu kwa umma kwa kutoa mafunzo kwa watumishi, kuimarisha mifumo ya utendaji na upatikanaji wa vifaa/vitendea kazi. Pamoja na mafanikio hayo tatizo la rushwa nchini na duniani kwa ujumla bado ni kubwa, hata hivyo TAKUKURU na Serikali kwa ujumla haijakata tamaa. Tunaamini kwamba bado kuna fursa nzuri ya kulitokomeza tatizo la rushwa nchini. Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli katika hotuba yake ya kwanza ya kuzindua Bunge jipya la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo tarehe 20 Novemba 2015 alieleza vipaumbele vya Serikali ya Awamu ya Tano kwa upande wa mapambano dhidi ya rushwa kuwa ni: Kuanzisha mahakama maalumu ya kusikiliza kesi za rushwa hususan ufisadi, kudhibiti matumizi mabaya ya Serikali na kusimamia Utawala Bora. Vipaumbele vingine alivyotaja ni pamoja na kupambana na urasimu, kutoa elimu bure, afya, maji, ajira na kupunguza pengo kati ya matajiri na masikini. TAKUKURU inaunga mkono dhamira ya Serikali kuanzisha mahakama ya kusikiliza makosa ya kesi za rushwa na ufisadi. Uamuzi huo ni utashi mkubwa kisiasa katika kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa na ni silaha kubwa kwetu inayoenda sambamba na mapendekezo yetu kwa Serikali. Nichukue fursa hii pia kutoa shukrani za pekee kwa Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuniamini na kuniteua kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU. Ninaahidi kuitumikia nafasi hii kwa kadri ya uwezo wangu wote niliopewa hivyo kukidhi matarajio ya wananchi na Serikali. Taasisi inaahidi kuendelea kufanya kazi kwa weledi, bidii na uadilifu kwa kushirikiana na wadau wengine kukabiliana na tatizo la rushwa na ufisadi nchini na kuunga mkono kauli mbiu ya Mheshimiwa Rais ya “Hapa Kazi Tu”. Tunawashukuru wananchi kwa kuendelea kutupatia ushirikiano kwa kutoa taarifa zinazotusaidia katika mapambano dhidi ya rushwa. Tunaishukuru pia Serikali kwa kututia shime katika mapambano haya kwa kutupatia vitendea kazi, rasilimali watu na fedha za kuendeshea ofisi. Mwaka ujao wa fedha tutapiga hatua kubwa zaidi katika kushughulikia changamoto zinazotukabili. Tunaamini kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko katika mapambano dhidi ya rushwa nchini hivyo kudumisha imani ya wananchi kwa Serikali yao na kuuhakikishia umma amani na utengamano kama Taifa moja.
Valentino Mlowola MKURUGENZI MKUU
“Uwajibikaji Unaanza na Wewe. Tushirikiane Katika Mapambano Dhidi ya Rushwa”
xi
xii
“Uwajibikaji Unaanza na Wewe. Tushirikiane Katika Mapambano Dhidi ya Rushwa”
SURA YA KWANZA UTANGULIZI 1.0
HISTORIA YA TAKUKURU
Kabla ya mwaka wa 1975 shughuli za kuzuia rushwa zilifanywa na Wizara ya Mambo ya Ndani chini ya jeshi la polisi. Taasisi ya Kuzuia Rushwa iliundwa na Sheria namba 2 ya mwaka 1974 ambayo ilipitisha kuundwa kwa Kikosi cha Kuzuia Rushwa, baada ya kuifanyia marekebisho Sheria ya Kuzuia Rushwa Namba 16 ya mwaka 1971. Kikosi cha Kuzuia Rushwa kilianzishwa rasmi tarehe 15 Januari 1975 kwa tamko la Serikali Namba 17 la 1975. Mwezi Aprili, 2007 Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Namba 11 ya mwaka 2007 ambapo mswada ulisainiwa kuwa sheria na Mheshimiwa Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete tarehe 11 Juni 2007. Sheria mpya ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa imetungwa kwa shabaha ya kuanzisha na kuipa nguzu Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ili kuweza kushugulikia kikamilifu na kwa ufanisi mkubwa mapambano dhidi ya rushwa nchini. Sheria hii ilizingatia maendeleo ya kiuchumi na kijamii yaliyojitokeza nchini na duniani kote katika miaka ya hivi karibuni. Maendeleo haya ni pamoja na kuwepo mikataba ya kimataifa ya kupambana na rushwa katika kiwango cha Umoja wa Mataifa (UN), Umoja wa Afrika (AU), Jumuia ya Kiuchumi na nchi zilizo kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuia ya Afrika ya Mashariki (AU). Maendeleo haya yameleta mabadiliko mengi katika nyanja za teknolojia ya mawasiliano, mikataba, ushahidi, n.k, ambayo Sheria ya Kuzuia Rushwa ya mwaka 1971 ilionekana dhahiri kushindwa kupambana nayo. Aidha, Sheria iliyopita ilishindwa kukabiliana na changamoto ya ujio wa utandawazi na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ambavyo vimeifanya TAKUKURU kuweka mikakati mipya katika mapambano dhidi ya rushwa nchini. Sheria mpya imeboreshwa zaidi kwani pia imejumuisha vifungu madhubuti kwa ajili ya kuzuia, kuchunguza/kupeleleza na kupambana na vitendo vya rushwa ili kuipatia TAKUKURU uwezo wa kufanya shughuli zake kikamilifu na hivyo mambo mengi mapya ambayo hayakuwemo katika Sheria ya Rushwa ya mwaka 1971yaliongezwa. Mambo yaliyoongezwa katika Sheria mpya ni pamoja na msukumo mkubwa wa ushiriki wa wananchi na sekta binafsi katika mapambano dhidi ya rushwa nchini; wajibu wa wananchi kutoa taarifa kwa TAKUKURU kuhusiana na kufanyika au mpango wa kufanyika vitendo vya rushwa; mpango kabambe wa kuwalinda watu wanaotoa taarifa pamoja na mashahidi katika kesi za rushwa. Aidha, Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba 11 ya mwaka 2007 imeongeza idadi ya makosa ya rushwa toka manne (4) yaliyokuwepo katika sheria ya awali hadi kufikia ishirini na manne (24) ikiwa ni pamoja na rushwa ya ngono, ambalo ni kosa jipya na la aina yake. Vilevile Sheria hii inaeleza juu ya tatizo la rushwa jinsi lilivyo tishio kwa maendeleo kwa ujumla ikiwemo kidemokrasia, haki za binadamu, utawala bora, amani na usalama katika jamii.
“Uwajibikaji Unaanza na Wewe. Tushirikiane Katika Mapambano Dhidi ya Rushwa�
1
1.1
RUSHWA NA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA
Mwaka 1995 Serikali ilitunga Sheria ya maadili ya viongozi kwa lengo la kuhakikisha kuwa miiko ya uongozi inaheshimiwa na kulindwa kisheria. Kupitia Sheria hii na kwa kuzingatia ibala ya 132 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Sekretariati ya Maadili ya viongozi iliundwa kukabiliana na mmomonyoko wa maadili miongoni mwa viongozi na watumishi wa Umma.
1.2
RUSHWA NA MANUNUZI YA UMMA
Serikali ilitunga Sheria ya Manunuzi ya Umma Na 21 ya mwaka 2004 ili kutoa usimamizi madhubuti wa manunuzi ya Umma na kufuta Sheria Namba 3 ya mwaka 2001 iliyokuwa inatumika awali. Sheria hii inazingatia vipengele vya mikataba mbalimbali ya kimataifa katika kiwango cha Umoja wa Mataifa, Afrika na ule wa Jumuia ya Uchumi wa Nchi zilizo kusini mwa bara la Afrika (SADC). Kwa kiwango kikubwa, Sheria ya Manunuzi ya Umma Namba 21 ya mwaka 2004 iliendelea kuwa na vipengele vinavyozuia rushwa katika mchakato wa manunuzi ya Umma nchini. Mwaka 2011 Sheria hii ilifanyiwa marekebisho zaidi na kutungwa Sheria mpya ya manunuzi ya umma namba 9 ya mwaka 2011 na kanuni zake za mwaka 2013 ambayo inatamka ukiukwaji wa baadhi ya taratibu za manunuzi ya umma kuwa ni makosa ya rushwa.
1.3
RUSHWA NA UCHAGUZI
Sheria ya Uchaguzi Namba 6 ya mwaka 2010 imeweka vifungu vya kudhibiti matumizi ya fedha kuanzia mchakato wa uteuzi wa wagombea, kampeni, uchaguzi na baada ya uchaguzi. Sheria hii inatoa katazo la kuwabana watu wanaogeuza haki yao ya kupiga kura kuwa mradi au bidhaa ya kunufaika nayo kifedha kwa kuiuza wakati wa uchaguzi. Pia inalenga kuleta usawa katika michakato ya uchaguzi kati ya wagombea kwa kuwadhibiti wanasiasa wanaojinadi kwa kutumia fedha badala ya sera.
1.4
MAHUSIANO KATI YA TAKUKURU NA WADAU
Mahusiano mazuri kati ya TAKUKURU na ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) na Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) katika kufuatilia mianya ya rushwa kutokana na taarifa zao kuwasilishwa mapema TAKUKURU. Vilevile wadau mbalimbali kama Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Sekta Binafsi, Asasi za Kiraia na vyombo vya habari wanashirikiana kwa karibu na TAKUKURU katika mapambano dhidi ya rushwa katika maeneo yao. Aidha wadau wa maendeleo wakiwemo Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza (DFID) na wengineo wapo pamoja na TAKUKURU katika kuchangia mapambano dhidi ya rushwa nchini.
2
“Uwajibikaji Unaanza na Wewe. Tushirikiane Katika Mapambano Dhidi ya Rushwa”
1.5
MAMLAKA NA MAJUKUMU YA TAKUKURU
1.5.1 Mamlaka ya TAKUKURU Mamlaka ya TAKUKURU ni kuzuia na kupambana na rushwa kama ilivyoelekezwa katika Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba 11 ya mwaka 2007.
1.5.2 Majukukumu ya TAKUKURU Majukumu ya TAKUKURU yameainishwa katika kifungu cha 7 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kama ifuatavyo:
a)
Kurugenzi ya Uchunguzi i. Kupokea na kuchunguza malalamiko yanayohusiana na vitendo vya rushwa; ii. Kupitia taarifa za uchunguzi na kushauri hatua zinazostahiki kuchukuliwa; iii. Kusimamia mashtaka yanayohusiana na vitendo vya rushwa; iv. Kupitia Sheria mbalimbali ili kubaini mianya ya rushwa; v. Kutoa ushauri wa kisheria kwa Kurugenzi zote za TAKUKURU; na vi. Kukusanya taarifa za kiitelijensia zinazohusiana na rushwa.
b)
Kurugenzi ya Utafiti na Udhibiti i. Kufanya tafiti juu ya huduma mbalimbali zitolewazo na Serikali ili kubaini vitendo vya rushwa; ii. Kushauri njia za kuzuia na kuondoa vitendo vya rushwa; na iii. Kubaini maeneo yenye mianya ya rushwa kupitia tafiti na kushauri njia za kuziba mianya hiyo.
c)
Kurugenzi ya Elimu kwa Umma i. Kuishirikisha jamii katika mapambano dhidi ya rushwa; ii. Kutoa elimu juu ya rushwa; na iii. Kuandaa semina, warsha, midahalo na makongamano kuhusu vitendo vya rushwa
1.6
MPANGO MKAKATI WA TATU WA TAKUKURU (2014/15-2015/16)
Taasisi imeandaa Mpango Mkakati wa miaka miwili 2014/15-2015/16 ambao unatoa mwelekeo wa TAKUKURU wa kupambana na rushwa. Mpango Mkakati umeandaliwa kutokana na mafanikio ya mkakati uliotangulia 2011/122013/14 ambao unalenga kukabiliana na changamoto zilizoainishwa wakati huo. Aidha mkakati unatoa mfumo utakaotuwezesha kuendana na Dira ya Taifa 2025 na MKUKUTA II. Kwa hiyo unatoa sura ya Taasisi katika kutekeleza agenda za kitaifa za masuala ya Kupambana na Rushwa, Maadili na Utawala Bora kwa ujumla. Malengo na shabaha za Taasisi kama yalivyoelezwa katika Mpango Mkakati huu ni:
“Uwajibikaji Unaanza na Wewe. Tushirikiane Katika Mapambano Dhidi ya Rushwa�
3
a) Kupunguza maambukizi ya Virusi vya UKIMWI na UKIMWI kwa wafanyakazi wa TAKUKURU; b) Kupunguza rushwa miongoni mwa watumishi; c) Kuweka mazingira mazuri ya kufanyia kazi na vitendea kazi katika Taasisi; d) Kupambana na rushwa kupitia uchunguzi na uendeshaji wa mashtaka; e) Kuongeza uelewa wa jamii kuhusu athari za rushwa na utayari wa serikali katika kupambana nayo; f ) Kuzuia na kukabiliana na mianya ya rushwa katika jamii; g) Kuimarisha uwajibikaji na kukuza utawala wenye kujali matokeo; na h) Kuiwezesha Taasisi kuwa na rasilimali za kutosha kuendesha ofisi.
4
“Uwajibikaji Unaanza na Wewe. Tushirikiane Katika Mapambano Dhidi ya Rushwa�
SURA YA PILI UCHUNGUZI 2.0 UCHUNGUZI TAKUKURU inatekeleza jukumu lake la kuchunguza na kusimamia mashtaka ya vitendo vya rushwa kwa mujibu wa Sheria. Utekelezaji wa jukumu hili unaanza kwa kupokea na kuchunguza malalamiko yanayohusiana na vitendo vya rushwa. Vilevile hutokana na taarifa za ukaguzi zinazofanywa na vyombo vingine kama Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA). TAKUKURU inachukua hatua zinazostahili za kusimamia mashtaka yanayohusiana na vitendo vya rushwa, kutoa ushauri wa kisheria kwa masuala yanayohusu rushwa na kukusanya taarifa za kiintelijensia zinazohusu rushwa. Matokeo ya uchunguzi unaofanyika ni pamoja na kuokoa fedha za Serikali ambazo zingehujumiwa, kufungua kesi mahakamani kwa kibali cha DPP isipokuwa kesi za kifungu cha 15 na kusimamia mashtaka. Kazi zilizofanyika katika kipindi hiki ni pamoja na: i. Kufuatilia miradi ya maendeleo ambapo shilingi bilioni 7.0 ziliokolewa; ii. Kukamilisha majalada ya uchunguzi 667; iii. Kuwasilisha majalada 278 kwa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) ambapo majalada 172 yalipata kibali cha mashtaka; iv. Kufungua kesi mpya 314 ambapo kati ya kesi zilizotolewa uamuzi na mahakama, watuhumiwa katika kesi 132 walikutwa na hatia na kuhukumiwa kifungo au faini au vyote kwa pamoja.
2.1
MATOKEO YA UCHUNGUZI NA MASHTAKA
2.1.1 Malalamiko ya vitendo vya rushwa yaliyopokelewa Mwaka 2014/15 TAKUKURU imepokea taarifa/malalamiko 4,675 yanazohusu vitendo vya rushwa kutoka vyanzo mbalimbali. Idadi hii ni pungufu ya malalamiko 394 ikilinganishwa na mwaka uliopita (Tazama kielelezo Na. 1). Upungufu huu unaweza kuwa umechangiwa na uelewa juu ya tofauti ya malalamiko yanayohusu vitendo vya rushwa na yale yasiyohusu rushwa. Uelewa huu wa wananchi umetokana na jitihada kubwa ya TAKUKURU ya kuwaelimisha wananchi kote nchini kupitia mbinu na vyombo mbalimbali vya habari, semina, makongamano, midahalo, maigizo n.k
“Uwajibikaji Unaanza na Wewe. Tushirikiane Katika Mapambano Dhidi ya Rushwa�
5
Kielelezo Na. 1: Malalamiko ya vitendo vya rushwa yaliyopokelewa
2.1.2 Idadi ya majalada yaliyofanyiwa uchunguzi na kukamilika Idadi ya majalada ambayo uchunguzi wake ulikamilika kwa kipindi cha mwaka 2014/15 ni 667 ikiwa ni ongezeko la majalada 60 ikilinganishwa na majalada yaliyokamilika mwaka 2013/14. Idadi kubwa ya majalada haya yanahusu na tuhuma za ubadhirifu wa miradi ya Serikali, pembejeo za kilimo, mishahara/malipo hewa, kukiuka taratibu za manunuzi na ubadhirifu wa fedha za umma. (Tazama kielelezo Na. 2)
6
“Uwajibikaji Unaanza na Wewe. Tushirikiane Katika Mapambano Dhidi ya Rushwa�
Kielelezo Na. 2: Idadi ya majalada yaliyofanyiwa uchunguzi na kukamilika
2.1.3 Majalada yaliyopelekwa kwa DPP kuombewa kibali cha Mashtaka Mwaka 2014/15, TAKUKURU ilifikisha kwa DPP majalada 278 kuomba kibali cha kufungua kesi mahakamani. Idadi hii ya majalada yaliyopelekwa kwa DPP ni pungufu kwa 83 ikilinganisha na mwaka uliotangulia, kati ya majalada hayo, 14 yalihusu kesi kubwa. (Tazama kielelezo Na. 3)
Kielelezo Na. 3: Majalada yaliyopelekwa kwa DPP
“Uwajibikaji Unaanza na Wewe. Tushirikiane Katika Mapambano Dhidi ya Rushwa�
7
2.1.4 Majalada yaliyorudi kutoka kwa DPP Mwaka 2014/15 majalada 172 yalirudi kutoka kwa DPP yakiwa na kibali cha mashtaka ikilinganishwa na majalada 261 yaliyopata kibali cha DPP mwaka 2013/2014. Aidha majalada 113 yalirudi yakiwa na maelekezo ya kufanyiwa uchunguzi zaidi ikilinganishwa na majalada 149 ya mwaka uliopita. Majalada manne (4) kati ya majalada yaliyorudi na kibali cha mashtaka ni ya kesi kubwa (Tazama kielelezo Na. 4).
Kielelezo Na. 4: Majalada yaliyorudi kutoka kwa DPP
2.1.5 Kesi Mpya Kesi mpya 314 zilifunguliwa katika mahakama mbalimbali kote nchini mwaka 2014/15 ikiwa ni pungufu ya kesi 18 ikilinganishwa na mwaka 2013/14. Kati ya kesi hizo, 9 zilikuwa za rushwa kubwa, 135 za kifungu cha 15 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa. Makosa ya kifungu hiki hayahitaji kibali cha DPP katika kufungua kesi mahakamani na 179 za vifungu vingine (Tazama kielelezo Na. 5).
8
“Uwajibikaji Unaanza na Wewe. Tushirikiane Katika Mapambano Dhidi ya Rushwa�
Kielelezo Na. 5: Idadi ya kesi mpya
2.1.6 Idadi ya Kesi Zilizoamuliwa Mahakamani Mwaka 2014/15 kesi zilizoamuliwa mahakamani ni 309 ambapo TAKUKURU imeshinda kesi 132 ikilinganishwa na kesi 104 zilizoshinda mwaka 2013/14. Hili ni ongezeko la 27% ikilinganishwa na mwaka 2013/14. Kesi zilizoshindwa ni kama inavyoonekana katika kielelezo namba 6.
Kielelezo Na. 6: Idadi ya kesi zilizoamuliwa Mahakamani
2.1.7 Kiasi cha fedha/mali kilichookolewa Kiasi cha fedha/mali zilizookolewa kwenye operesheni mbalimbali za TAKUKURU na katika ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo kwa mwaka wa fedha 2014/15 ni shilingi bilioni 7.0. (Tazama kielelezo Na.7).
“Uwajibikaji Unaanza na Wewe. Tushirikiane Katika Mapambano Dhidi ya Rushwa�
9
Kielelezo Na. 7: Kiasi cha fedha/mali kilichookolewa (Tsh. Bilioni)
2.1.8 Mchanganuo wa Majalada ya Uchunguzi na Kesi kwa Tuhuma, Kisekta na Vifungu vya Sheria 2.1.8.1 Mchanganuo wa Majalada ya Uchunguzi Kwa Tuhuma zinazoendelea kuchunguzwa Miongoni mwa tuhuma hizo ni ubadhirifu wa fedha za miradi ya maendeleo, ubadhirifu wa fedha za pembejeo za kilimo, hongo, rushwa katika utoaji wa zabuni mbalimbali. Tuhuma inayoongoza ni ya ubadhirifu katika miradi ya maendeleo yenye majalada 880 sawa na asilimia 39 ya majalada yaliyochunguzwa, inafuatiwa na hongo yenye majalada 379 sawa na asilimia 17, tuhuma zinazotokana na taarifa ya CAG yenye majalada 337 sawa na asilimia 15, mishahara/malipo hewa majalada 243 sawa na asilimia 11. Nyingine ni ubadhirifu katika pembejeo za kilimo ikiwa na majalada 170 sawa na asilimia 8, manunuzi/zabuni majalada 159 sawa na asilimia 7. Mwisho ni misitu na wanyamapori zenye majalada 57 sawa na asilimia 3 (Tazama Kielelezo Na.13).
10
“Uwajibikaji Unaanza na Wewe. Tushirikiane Katika Mapambano Dhidi ya Rushwa�
Kielelezo Na. 13: Mchanganuo wa Kituhuma kwa Majalada yanayoendelea na Uchunguzi
2.1.8.2 Mchanganuo wa Kisekta kwa Majalada yanayoendelea na Uchunguzi Katika mchanganuo huo, Serikali za Mitaa zinaongoza kwa kuwa na majalada 1271 sawa na asilimia 44 ikifuatiwa na elimu majalada 466 sawa na asilimia 16 afya majalada 312 sawa na asilimia 11 na kilimo na mifugo majalada 250 sawa na asilimia 9. Sekta nyingine ni ujenzi yenye majalada 138 sawa na asilimia 5, polisi majalada 64 na mahakama majalada 63 jumla majalada 127 sawa na asilimia 4, maliasili na utalii majalada 120 sawa na asilimia 4, ardhi majalada 75 sawa na asilimia 3, manunuzi majalada 51 sawa na asilimia 2 na Sekta binafsi yenye majalada 104 sawa na asilimia 4. (Tazama kielelezo Na. 14).
Kielelezo Na. 14: Mchanganuo wa Majalada Kisekta
“Uwajibikaji Unaanza na Wewe. Tushirikiane Katika Mapambano Dhidi ya Rushwa�
11
2.1.8.3 Mchanganuo wa Kesi zinazoendelea mahakamani Kituhuma Kesi zinazoendelea mahakamani zimegawanywa kwa kutegemea tuhuma. Tuhuma ya hongo ina kesi 211 Sawa na asilimia 41 ikifuatiwa na ubadhirifu miradi ya maendeleo yenye kesi 132 sawa na asilimia 26, tuhuma zinazotokana na ubadhirifu wa pembejeo za kilimo ni 44 sawa na asilimia 9, mishahara hewa kesi 44 sawa na asilimia 9, taarifa ya CAG yenye kesi 37 sawa na asilimia 7, manunuzi/zabuni yenye kesi 25 sawa na asilimia 5 na tuhuma za misitu/ wanyamapori kesi 16 sawa na asilimia 3 (Tazama kielelezo Na 15)
Kielelezo Na. 15: Mchanganuo wa kesi zilizopo Mahakamani Kituhuma
2.1.8.4 Mchanganuo wa kesi zinazoendelea mahakamani kisekta Hadi tunafunga mwaka 2014/15 kesi 557 zilikuwa zinaendelea mahakamani ambapo mchanganuo wake kisekta ni; Serikali za Mitaa inaongoza kwa kuwa na kesi 275 sawa na asilimia 50 ikifuatiwa na afya kesi 67 sawa na asilimia 12, elimu kesi 69 sawa na asilimia 12, polisi kesi 10 na mahakama kesi 25 jumla kesi 35 sawa na asilimia 6, kilimo, mifugo na ushirika kesi 37 sawa na asilimia 7, maliasili na utalii kesi 23 sawa na asilimia 4, ujenzi kesi 19 sawa na asilimia 3, ardhi kesi 9 sawa na asilimia 2 na Sekta binafsi kesi 23 sawa na asilimia 4 (Tazama kielelezo Na.16).
12
“Uwajibikaji Unaanza na Wewe. Tushirikiane Katika Mapambano Dhidi ya Rushwa�
Kielelezo Na. 16: Mchanganuo wa kesi zilizopo mahakamani kisekta
2.2
Ufuatiliaji wa fedha za miradi ya maendeleo katika Halmashauri
PETS (Public Expanditure Track Survey) kimsingi ni mfumo mzima wa kufuatilia fedha za umma zilizotolewa toka vyanzo mbalimbali kwa ajili ya miradi ya maendeleo katika mamlaka za Serikali za Mitaa na kupima kiasi gani ya fedha hizi kilipokelewa na kiasi ambacho hakikupokelewa au kimetumika kwa matumizi mengine ambayo hayakukusudiwa. Hapa Tanzania dhana ya PETS imewahi kutumiwa na mashirika yasiyo ya kiserikali kama HAKIELIMU na TACOSODE kwa kushirikisha jamii ya eneo husika na baadae kuandaa taarifa na kuitoa kwa jamii. Mashirika haya yalikabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo upatikanaji wa taarifa na nyaraka za raslimali kutoka kwenye mamlaka za serikali, vitisho toka watendaji wa mamlaka za serikali, kushindwa kuwachukulia hatua watendaji waliogundulika kutumia vibaya raslimali za umma na kutoweza kurejesha rasilimali zilizodhibitika kupotea kutokana na kutokuwa na mamlaka ya kisheria. Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba 11 ya mwaka 2007 kifungu namba 7 (a, c, na f ) na cha 8 inaipa TAKUKURU jukumu la kuchunguza na kushauri juu ya shughuli na taratibu katika Taasisi za Umma na binafsi ili kurahisha utambuzi na uzuiaji wa rushwa na kuongeza uwazi na ufanisi katika Taasisi husika, kushauri Taasisi za Umma na binafsi juu ya njia na namna ya kupambana na vitendo vya rushwa na kupendekeza mabadailiko na taratibu za kiutendaji ili kuleta ufanisi na kupunguza vitendo vya rushwa na kuchunguza tuhuma zote za rushwa na kuwafikisha mahakamani watuhumiwa. Kupitia utaratibu huu wa PETS TAKUKURU imefungua ofisi za waratibu wa Kanda (Zonal PETS Coordinators) kufuatilia fedha za miradi ya maendeleo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa ushirikiano na PMO-RALG nchini kote. Kazi ya ufuatiliaji inaanza kwa kupata tarifa za kumbukumbu za rasilimali zilizopangwa na kutumwa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kupitia Wizara ya Fedha pia kupata mipango ya manunuzi ya Mamlaka za Serikali za Mitaa zilizowasililishwa kwa Mamlaka ya Manunuzi ya Umma (PPRA) ili kuanzisha ufuatiliaji unaofahamika kama “fuatilia rasilimali (follow the resource)”.
“Uwajibikaji Unaanza na Wewe. Tushirikiane Katika Mapambano Dhidi ya Rushwa”
13
Ufuatilaji huu unafanyika katika maeneo ya elimu, afya, kilimo na mifugo, maji, ujenzi wa barabara na majengo. Lengo kubwa la PETS ni kuhakikisha kunakuwepo uwazi na uwajibikaji ili kuhakikisha thamani ya miradi inafikiwa. Utaratibu huu unajazia pale Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa hesabu za Serikali anapoishia na kwenda hadi kushuhudia kwenye maeneo miradi na huduma inapotolewa pia kukutana na wapokea huduma kupata mrejesho unaoweza kuonyesha kufanikiwa au kutofanikiwa kwa dhamira ya Serikali ya kutoa huduma.
2.2.1 Manufaa yatokanayo na ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo Kazi hii imeleta mafanikio yafuatayo:a) Husaidia fedha za miradi kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa; b) Huwezesha kupatikana kwa huduma bora za jamii zinazokidhi na kwa wakati; c) Hujenga mazingira ya wasimamizi wa miradi kufuata sheria, kanuni na taratibu katika kutoa zabuni na kusimamia utekelezaji wa miradi; d) Huinua na kuimarisha uchumi wa Taifa na pato la kila mwananchi; e) Hurahisisha utekelezaji wa majukumu ya Serikali na jamii kwa ujumla na kuwezesha kufikia malengo yaliyowekwa na Serikali; f ) Husaidia wananchi kujenga imani kwa serikali na kutoa ushirikiano katika shughuli nyingine za maendeleo; na g) Huwajengea uwezo wananchi kuweza kuhoji na kuchukua hatua za kutoa taarifa na baadae kuweza kutoa ushahidi wa ubadhirifu, rushwa na matumizi mabaya ya madaraka;
2.2.2 Sekta zilizofuatiliwa TAKUKURU iliainisha maeneo machache ya kufuatilia matumizi ya fedha za Umma katika mamlaka za Serikali za Mitaa. Maeneo hayo ni kama ifutavyo;
a) Elimu Katika sekta hii miradi iliyokaguliwa ilikuwa ni ujenzi wa madarasa, ofisi za utawala, ofisi za walimu, utengenezaji wa madawati, ujenzi wa vyoo, maabara na ujenzi wa nyumba za watumishi wa idara ya elimu. Chanzo kikubwa cha fedha katika sekta hii ni ruzuku ya Serikali kuu kupitia mipango ya maendeleo ya elimu ya msingi na sekondari (MMEM na MMES)
b) Maji Miradi ya maji iliyokaguliwa ni ujenzi wa miundombinu ya maji ikiwa ni ujenzi wa visima, matanki,vituo vya kusambazia maji, uchimbaji wa mitaro, ulazaji wa mabomba, malambo ya kunyweshea mifugo na ujenzi wa nyumba za mashine za kusukuma maji ( pump houses). Wakati wa ukaguzi baadhi ya miradi ilikuwa imekamilika na maji yalikuwa yanatoka na baadhi ujenzi wake ulikuwa unaendelea. Tatizo linalojitokeza katika miradi hii ni kutokukamilika kwa wakati na sababu kubwa ikiwa ni kutotolewa kwa fedha za ujenzi kwa wakati. Chanzo kikubwa cha fedha katika miradi hii ni mfuko unaofadhiliwa na Wadau wa Maendeleo kupitia mpango wa Usambazaji maji na ukusanyaji na uteketezaji majitaka mijini na vijijini (Rural and Urban Water Supply and Sanitation Program “RWSSP”)
14
“Uwajibikaji Unaanza na Wewe. Tushirikiane Katika Mapambano Dhidi ya Rushwa”
c)
Ujenzi wa barabara na majengo ya utawala
Katika sekta hii kulikaguliwa ujenzi/matengenezo ya barabara na majengo ya utawala. Barabara zilikuwa zimefanyiwa matengenezo ya kawaida ikiwa ni kuchongwa, kufyeka, kutengeneza mifereji, kujenga makalvati/madaraja, vituo vya mabasi na matengenezo ya sehemu korofi. Majengo ya utawala yanayohusisha ofisi za wakurugenzi watendaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, ofisi za Kata, Vijiji na Vitongoji. Chanzo kikubwa cha fedha katika miradi hii ni Mfuko wa barabara (Road Fund) na DFID kwa barabara na kwa majengo ni ruzuku toka Serikali Kuu na vyanzo vya ndani vya Mamlaka za Serikali za Mitaa.
d) Afya Miradi iliyokaguliwa katika sekta hii ni ujenzi wa hospitali za wilaya, vituo vya afya, zahanati, wodi, vyumba vya kuhifadhia maiti na upasuaji, vichomea taka zitokanazo na shughuli za tiba na nyumba za watumishi wa idara ya afya, pia usambazaji wa madawa na chanjo. Chanzo kikubwa cha fedha katika miradi hii ni MMAM (Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi) na Mfuko wa Afya (Health Busket Fund “HBF”)
e)
Kilimo na ufugaji
Ufuatiliaji ulifanyika katiika maeneo ya ujenzi wa masoko, maghala ya mazao, ununuzi wa mashine za kutotoa vifaranga, mashine za kutengeneza chakula cha kuku, vituo vya mafunzo ya wakulima, ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji ikiwemo mabwawa na mifereji ya kusambaza maji mashambani. Chanzo kikubwa cha fedha za miradi hii ni kutoka mpango wa Kilimo wa Wilaya (District Agriculture Develoment Programs “DADPS”) na (Agriculture Sector Development Project “ASDP”) na Ruzuku ya kujenga uwezo wa Mamlaka za Serikali za Mitaa (Local Government Capital Building Grant “LGCBG”)
2.2.3 Matokeo ya ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo na uelimishaji Ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini umekuwa na matokeo yafuatavyo:a) Miradi ilifuatiliwa na mapungufu yaliyobainika hatua za uchunguzi na udhibiti zilichukuliwa; b) Elimu kuhusu mianya ya rushwa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo na utoaji wa huduma ilitoplewa kwa mamlaka, watendaji na wananchi; na c) Mbinu zinazotumika na mianya ya ubadhirifu, rushwa, uchepushaji na matumizi mabaya ya madaraka katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo na huduma zilibainika.
2.2.4 Miradi ya Maendeleo Katika kipindi hiki TAKUKURU ilipanga kufanya ukaguzi wa miradi 150 katika mamlaka za Serikali za Mitaa, vikao vya uelimishaji 12 na kongamano nne. Madhumini ya kazi hizi ni kuiwezesha TAKUKURU kupata taarifa za ubadhirifu, rushwa, uchepushaji na matumizi mabaya ya madaraka katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Katika kutekeleza jukumu hili miradi ya maendeleo 1,796 yenye thamani ya shilingi 262.818 bilioni ilifuatiliwa ambapo miradi 279 sawa na asilimia 15.53 ya miradi yote iliyofuatiliwa
“Uwajibikaji Unaanza na Wewe. Tushirikiane Katika Mapambano Dhidi ya Rushwa”
15
ilibainika kuwa na kasoro zinazoashiria kuwepo kwa rushwa au ubadhilifu ikiwa na thamani ya shilingi 40.422 bilioni sawa na asilimia 15.38 ya fedha zilizotumika. Miradi 209 kati ya iliyobainika kuwa na kasoro ilipendekezwa kufunguliwa majalada kwa ajili ya uchunguzi au udhibiti. Baadhi ya mapungufu yaliyobainika katika ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo ni:a) Ujenzi duni unaonekana kupitia nyufa kwenye majengo, madaraja, kalvati, mitaro ya barabara, njia za waenda kwa miguu, kingo za malambo na mabwawa ya maji muda mfupi baada ya ujenzi kukamilika. Mfano ujenzi wa tuta la kuzuia maji ya umwagiliaji kijiji cha Chemichemi katika Halmashauri ya Moshi. b) Matumizi ya vifaa hafifu vya ujenzi kama mbao za mpodo badala ya mninga/mkangazi. Kuweka kifusi barabarani badala ya changarawe, matumizi ya mabomba hafifu ya kusambaza maji ambayo hupasuka muda mfupi baada ya mradi kukamilika; c) Ujenzi usiokamilika na umaliziaji hafifu wa majengo hasa upande wa rangi, dari, kukosekana kwa nyavu za kuzuia mbu kwenye nyumba za watumishi wa vituo vya afya na shule za misingi na sekondari; d) Kuibuka utata wa maelezo baina ya wadau wa miradi hasa ya kilimo na ufugaji. Watendaji wanatoa taarifa tofauti na zile zilizotolewa na wananchi wanaoendelea na mradi. Mfano wanakijiji wa vijiji vya Mbulizaga na Mkwaja katika Halmashauri ya Wilaya ya Pangani walidai kupokea ng’ombe 10 kwa kila kijiji lakini taarifa ya Mkurugenzi Mtendaji inaonesha kila kijiji kilipokea ng’ombe 20; e) Gharama za miradi kuhusisha nguvu za wananchi ambazo hesabu zake hulipwa tena kwa wakandarasi kama vifaa walivyonunua katika ukamilishaji wa miradi; f ) Fedha kuonekana kutumika katika ujenzi wa miradi au utoaji huduma wakati hakuna ujenzi uliofanyika au huduma iliyotolewa. Mfano Shule ya Msingi Gehandu na Gisambalang Wilaya ya Hanang na Shule ya Msingi Mdunku wilaya ya Kiteto ambapo taarifa ya Afisa Elimu inaonesha madarasa na vyoo vimekamilika na vinatumika wakati kuna msingi tu na wanafunzi wanajihifadhi vichakani. g) Baadhi ya miradi iliyotekelezwa kwa lengo la kutoa huduma kwa wananchi kwa ajili ya kuondoa kero kushindwa kutimiza lengo. Mfano Josho la kijiji cha Linyala Wilaya ya Nkasi halitunzi maji hivyo mifugo iliogeshwa siku moja tu ya ufunguzi na josho halitumiki tena; h) Miradi mingine inaonesha kutumia fedha za vyanzo viwili tofauti na kila chanzo kutoa fedha zote za kukamilisha mradi kwa maana hiyo kunakuwepo matumizi ya fedha za miradi miwili kwenye mradi mmoja. Mfano matundu ya vyoo vya shule za msingi Buguruni, Kimanga, Ulongoni ni hewa kwani vyoo vilikuwepo na vilijengwa kwa msaada wa shirika lisilo la kiserikali la PLAN International, lakini ufuatiliaji ulibaini kuwa ujenzi huo ulitumia fedha za Mpango Maalumu wa Elimu ya Mshingi (MMEM) toka Manispaa ya Ilala; i) Baadhi ya miradi fedha zake kubadilishwa matumizi na kutekeleza miradi mingine ambayo ilipangiwa fedha kipindi cha nyuma lakini fedha zake hazijulikani zilienda wapi. Mfano ujenzi wa darasa sekondari ya Tema Wilaya ya Hai kubadilishwa kuwa maabara bila nyaraka za zabuni kubadilishwa;
16
“Uwajibikaji Unaanza na Wewe. Tushirikiane Katika Mapambano Dhidi ya Rushwa”
j)
Miradi kutekelezwa katika maeneo ambayo hayafai kimazingira mfano soko la Kigogo Fresh Kata ya Pugu Wilaya ya Ilala limejengwa mahali ambapo mvua ikinyesha kunageuka bwawa la maji machafu; na k) Kuna ushirikishwaji mdogo wa wananchi katika kupanga na kusimamia miradi ya maendeleo na huduma zinazotolewa.
Kielelezo Na. 17: Miradi ya Maendeleo iliyofuatiliwa Utekelezaji wa malengo ya kazi za uchunguzi katika kipindi hiki ulifanyika kwa kiwango cha wastani cha asilimia 40.95. Aidha kutokana na operesheni mbalimbali za TAKUKURU kiasi cha shilingi bilioni 7.0 kiliokolewa katika kipindi hiki. Kiwango hiki kimefikiwa kutokana na changamoto zilizoikabili TAKUKURU katika kipindi hiki ikizingatiwa kuwa ulikuwa ni mwaka wa Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani.
“Uwajibikaji Unaanza na Wewe. Tushirikiane Katika Mapambano Dhidi ya Rushwa�
17
SURA YA TATU UTAFITI NA UDHIBITI 3.0
KURUGENZI YA UTAFITI NA UDHIBITI
Katika kifungu cha 7(a) na 7(c) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba 11 ya Mwaka 2007, TAKUKURU imepewa jukumu la kutathmini mifumo na taratibu zinazoongoza utendaji wa taasisi za umma na binafsi ili kubaini mianya ya rushwa na kuzishauri Taasisi hizo namna bora ya kuzuia rushwa na kusimamia utekelezaji wa mifumo na taratibu zilizorekebishwa. TAKUKURU imeendelea kutekeleza jukumu hilo la kuzuia rushwa kwa kuimarisha mifumo na kuandaa mapendekezo ya utafiti (research proposals); kufanya tafiti katika sekta mbalimbali; kuandaa na kufanya warsha na vikao vya wadau kujadili matokeo ya utafiti; kuweka mikakati ya kudhibiti mianya ya rushwa na kufanya ufuatiliaji wa haraka (quick wins). Lengo ni kuzuia rushwa katika mifumo ya utendaji na utoaji huduma za jamii.
3.1
UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA UTAFITI NA UDHIBITI
3.1.1 Utafiti Tafiti tano zilifanyika mwaka 2014/15 ambapo hadi kufikia Juni 30, 2015, tafiti tatu zilikamilika na mbili zilikuwa zinaendelea. Tafiti zilizokamilika ni Mianya ya Rushwa katika Sekta ya Mafuta na Gesi (Oil and Gas sector Corruption vulnerability analysis), Mianya ya rushwa katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2014 na Utafiti wa Msingi wa hali ya rushwa katika shughuli za Wakala wa Vipimo Nchini (Weights and Measures Agency Corruption Baseline Survey). Tafiti ambazo bado zilikuwa zinaendelea kufanyika ni Minya ya Rushwa katika Mfumo wa Misamaha ya Kodi (Corruption Loopholes in Tax Exemption System) na Mianya ya Rushwa katika Sekta ya Maji (hatua ya ukusanyaji wa taarifa). Aidha, katika kipindi cha mwaka 2014/15 TAKUKURU iliratibu kufanyika kwa tafiti mbili pamoja na uandaaji wa mwongozo wa kuzuia rushwa katika manunuzi ya umma. Kazi hizi zilifanywa na Washauri Elekezi. Tafiti hizo zilifanyika katika ujenzi wa miundombinu ya barabara na katika sekta zinazolalamikiwa zaidi kwa rushwa (Corruption Review in High Risk and High Impact Sectors) yaani Mahakama, Ardhi na Polisi. Taarifa za kazi za utafiti kuhusu Mianya ya Rushwa katika Sekta ya Mafuta na Gesi, Mianya ya rushwa katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2014 na Utafiti wa Msingi wa hali ya rushwa katika shughuli za Wakala wa Vipimo Nchini ziliwasilishwa kwa wizara na Taasisi husika kwa ajili ya utekelezaji wa mapendekezo na maazimio yaliyotolewa. Kwa ulinganifu, katika mwaka 2014/15 kulikuwa na ongezeko la asilimia 25 ya kazi za utafiti zilizofanywa na TAKUKURU na asilimia 50 ya kazi zilizofanywa na Washauri Elekezi ikilinganishwa na kazi kama hizo zilizofanyika katika mwaka 2013/14.
18
“Uwajibikaji Unaanza na Wewe. Tushirikiane Katika Mapambano Dhidi ya Rushwa�
Kielelezo Na. 18: Ulinganifu wa kazi za utafiti zilizofanywa mwaka 2013/14 na 2014/15
3.1.2 Warsha na vikao vya wadau Katika utekelezaji wa majukumu ya kuzuia rushwa, ushirikishwaji wa wadau ni muhimu ili kuwa na uelewa wa pamoja wa mianya ya rushwa iliyopo na kujenga umiliki (ownership) wa mikakati ya kuzuia rushwa katika Taasisi inayokusudiwa kuimarishwa mifumo yake. Ushirikishwaji huu hufanyika kwa njia ya warsha na kwa kufanya vikao na wadau kwa lengo la kujadili mianya ya rushwa iliyobainika na kuweka mikakati endelevu ya kuziba mianya hiyo. Jumla ya warsha/ vikao 363 vimefanyika kwa kipindi cha mwaka 2014/15 katika idara/sekta mbalimbali.
3.1.3 Ufuatiliaji wa haraka wa kudhibiti vitendo vya rushwa TAKUKURU imefanya ufuatiliaji wa haraka (quickwins) kudhibiti vitendo vya rushwa katika maeneo mbalimbali kwa lengo la kutatua kero za wananchi. Ufuatiliaji wa aina hii hufanyika kwa kukusanya taarifa za kero husika na kuzitatua kwa kushirikisha wadau kwa njia ya haraka inayoleta matokeo kwa muda mfupi. Katika mwaka 2014/15, dhibiti 519 zimefanyika katika mikoa na wilaya zote nchini (Kilelezo Na 19)
3.1.4 Ufuatiliaji wa utekelezaji wa maazimio ya kuziba mianya ya rushwa TAKUKURU ina jukumu la kuratibu utekelezaji wa maazimio na mikakati iliyowekwa ili kuziba mianya ya rushwa. Ufuatiliaji hufanyika baada ya muda wa utekelezaji wa mikakati husika uliokubalika na wadau. Dhumuni la ufuatiliaji huu ni kupata taarifa ya utekelezaji wa maazimio yaliyokubaliwa na kupima mafanikio yaliyopatikana katika udhibiti wa mianya ya rushwa. Katika kipindi cha mwaka 2014/15, kazi 261 za ufuatiliaji zilifanyika na taarifa za utekelezaji kuandaliwa. Ufuatiliaji huu ulifanywa katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Polisi, TAMISEMI, Maliasili na Utalii, Magereza, Maji, Elimu, Kilimo na Mifugo, Ardhi, Afya, Ujenzi, Uhamiaji, Uchukuzi, Fedha, Mahakama na Misitu kama mchanganuo unavyoonesha hapo chini:
“Uwajibikaji Unaanza na Wewe. Tushirikiane Katika Mapambano Dhidi ya Rushwa�
19
Jedwali Na 1: Mchanganuo wa kazi za udhibiti kisekta NA. 1 2 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17 18 19 20 21 22 23 24 25 26 27
20
SEKTA Nishati na Madini Polisi TAMISEMI Maji Elimu Kilimo na Mifugo Ardhi Afya Maliasili Ushirika Sekta Binafsi TRA Mahakama NGO’s Ujenzi Mifuko ya Jamii Uhamiaji Benki Ulinzi na Usalama Taasisi za dini Bima Vizazi na Vifo (RITA) Usafirishaji Mfuko wa Maendeleo (WDF) Manunuzi ya umma Viwanda na biashara JUMLA
UDHIBITI 9 40 156 22 27 27 37 72 15 8 11 6 31 1 10 16 2 2 1 0 3 3 11 1
WARSHA/VIKAO 7 16 128 15 15 17 33 49 14 6 6 3 11 1 4 10 2 3 1 0 3 3 6 1
UFUATILIAJI 5 9 102 11 6 15 18 26 13 2 5 0 16 1 3 5 2 2 1 0 1 1 7 2
0 8 519
1 7 363
0 8 261
“Uwajibikaji Unaanza na Wewe. Tushirikiane Katika Mapambano Dhidi ya Rushwa”
Kielelezo Na 19: Mchanganuo wa kazi za Utafiti na Udhibiti
Aidha, utendaji wa TAKUKURU katika eneo la Utafiti na Udhibiti ulipanda kwa mwaka 2014/15 ikilinganishwa na kazi zilizofanyika mwaka 2013/14. Ongezeko la kazi hizi ni kama ilivyoainishwa katika kielelezo Namba 20 hapo chini.
Kielelezo Na. 20: Mlinganisho wa kazi za Utafiti na Udhibiti
“Uwajibikaji Unaanza na Wewe. Tushirikiane Katika Mapambano Dhidi ya Rushwa�
21
3.1.5 Kutoa machapisho Machapisho mbalimbali hutolewa na TAKUKURU kwa lengo la kuwaarifu wadau na wananchi kwa ujumla juu ya kazi za kuimarisha mifumo zilizofanyika. Katika kipindi cha mwaka 2014/15, jumla ya nakala 2000 za taarifa ya utafiti wa rushwa katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2014 na nakala 1000 za “investigation manual in Public Procurement” zilichapwa na kusambazwa kwa wadau. TAKUKURU itaendeleza ushirikiano na taasisi za kitafiti za kupambana na rushwa ndani na nje ya nchi ili kuongeza ufanisi, kujenga uhusiano mzuri na wadau na kuendelea kuwaelimisha juu ya wajibu wao katika mapambano dhidi ya rushwa, kuwahimiza wadau wajibu wao wa kutekeleza mapendekezo na maazimio ya kuziba mianya ya rushwa yaliyokubaliwa kwa wakati. Kazi za utafiti na udhibiti zilizofanyika kwa kipindi cha mwaka 2014/15 ni hatua katika kuboresha mifumo ya utendaji katika sekta zilizofanyiwa kazi. Matokeo ya uimarishaji wa mifumo hiyo ni kuongeza uwazi na uwajibikaji zaidi katika Taasisi ili kutoa huduma bora kwa wananchi. Jukumu la kuzuia rushwa kwa kuimarisha mifumo ni suala mtambuka na endelevu linalohitaji mbinu mbalimbali ili kufikia malengo yaliyokusudiwa. Kwa upande mwingine, mwitikio bora wa Taasisi na sekta zilizohusika unatarajiwa kuzuia vitendo vya rushwa kwa Taasisi husika kwa kujisahihisha zenyewe. Aidha, matokeo mazuri ya utekelezaji wa majukumu ya Utafiti na Udhibiti yanaweza kuwa ni kichocheo kikubwa katika kuelimisha umma na uchunguzi wa vitendo vya rushwa. Ili kufikia matarajio hayo ni muhimu kuwa na usimamizi bora wa kazi za utafiti na udhibiti. Mapambano dhidi ya rushwa hayawezi kufikiwa endapo mzizi wa tatizo haujajulikana na hususan rushwa inayotokana na udhaifu wa mifumo, sheria, taratibu, kanuni na sera katika sekta ya umma. Ili kuyafahamu mapungufu hayo, Taasisi haina budi kuimarisha hatua mbalimbali za uzuiaji wa rushwa kwa kufanya tafiti za kisayansi ili kubaini mianya ya rushwa iliyopo hatimaye kupanga mikakati ya kuidhibiti kwa kushirikiana na wadau katika maeneo husika. Utafiti na udhibiti una gharama; fedha, rasilimali watu waliobobea na vitendea kazi ili kupata matokeo bora. Ni matarajio yetu kuwa Serikali itaendelea kuimarisha eneo hili.
22
“Uwajibikaji Unaanza na Wewe. Tushirikiane Katika Mapambano Dhidi ya Rushwa”
SURA YA NNE ELIMU KWA UMMA 4.0
ELIMU KWA UMMA
Kwa mujibu wa kifungu cha 7(b) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba 11 ya Mwaka 2007, TAKUKURU inalo jukumu la kuanzisha na kustawisha ushirikiano na ushiriki wa umma katika mapambano dhidi ya rushwa. Aidha, dhima ya Idara ya Elimu kwa Umma ni “kuishirikisha jamii katika mapambano dhidi ya rushwa”. Ili kutekeleza jukumu na dhima hiyo, TAKUKURU inatumia njia mbalimbali kusudi kila kundi/mdau afikiwe. Kwa vijana walioko vyuoni na shuleni huhamasishwa kuanzisha klabu za wapinga rushwa na kufanya shughuli mbalimbali za kupambana na rushwa. Elimu inayotolewa hulenga kuifahamisha jamii juhudi za Serikali katika mapambano dhidi ya rushwa, madhara ya rushwa, umuhimu na faida za jamii kushiriki katika mapambano haya. Aidha, elimu hutolewa kupitia ofisi za Makao Makuu, Mikoa, Wilaya na Vituo maalum.
4.1
TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA KAZI ZA UELIMISHAJI UMMA
Tathmini ya utekelezaji wa malengo yaliyowekwa kwa kuzingatia vigezo vilivyomo katika Mpango Mkakati wa TAKUKURU 2014/15 – 2015/16 na mengineyo ni kama inavyofafanuliwa hapa chini;
4.1.1 Mafunzo/Semina Mafunzo/Semina 2,945 zimefanyika kati ya 2,880 zilizopangwa ambapo wadau 190,367 walifikiwa. Idadi hii ni pungufu ikilinganishwa na semina 2,959 zilizotolewa mwaka 2013/14 kama kielelezo Namba 21 kinavyoonesha. Aidha mafunzo/semina 1,400 kati ya hizi ziliwafikia watumishi wa sekta ya umma wakiwemo Wizara, Idara na Wakala za Serikali, Idara za Halmashauri, Askari Polisi, Magereza na Mgambo, Watendaji wa Vijiji na Kata, Madiwani, Wajumbe wa Mabaraza ya Maendeleo ya Kata na Mabaraza ya Ardhi, Walimu wa shule za msingi na sekondari, wakufunzi wa vyuo, wafanyakazi wa Mahakama na wajumbe wa Kamati za Uadilifu. Semina 716 zilihusisha wadau wa sekta binafsi ambao ni Taasisi za dini, wazalishaji/wafanyabiashara, wanahabari, asasi zisizo za kiserikali, vikundi vya sanaa, wasanii, wanasiasa, vikundi vya wazee, wanamichezo, vyama vya ushirika, vikundi vya kijamii na wananchi. Mafunzo/semina 817 ziliendeshwa kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu, shule za sekondari na msingi.
4.1.2 Mikutano ya hadhara/mijadala ya wazi Mikutano ya hadhara/mijadala ya wazi 1,920 imefanyika kati ya 1,920 iliyopangwa ambapo wadau 208,075 walishirikishwa. Hii ni sawa na ongezeko la asilimia 30 ikilinganishwa na mikutano iliyofanyika mwaka 2013/14 (rejea kielelezo Na 21). Ongezeko hili limesababishwa na juhudi kubwa ya uelimishaji uliofanyika kabla na wakati wa uchaguzi wa Serikali za mitaa. Mikutano ya hadhara/mijadala 227 kati ya hiyo ilihusisha sekta za umma na 1,693 sekta binafsi.
“Uwajibikaji Unaanza na Wewe. Tushirikiane Katika Mapambano Dhidi ya Rushwa”
23
4.1.3 Kufungua na Kuimarisha Klabu za wapinga rushwa (a)
Kufungua klabu za wapinga rushwa
Klabu za wapinga rushwa 562 zenye wanachama 47,716 zimefunguliwa. Idadi hii imepungua kwa idadi ya klabu 1,874 ikilinganishwa na zilizofunguliwa mwaka 2013/14 (rejea kielelezo Na 21), upungufu huu umetokana na klabu nyingi kuwa zimeshafunguliwa katika kipindi kilichopita. Aidha kati ya klabu 562; klabu 506 ni za shule za msingi zenye wanachama 41,553, klabu 43 za sekondari zenye wanachama 4,152 na klabu 13 za vyuo zenye wanachama 2,011 zimefunguliwa.
(b)
Kuimarisha klabu za wapinga rushwa
Klabu 2,439 zenye wanachama 154,541 ziliimarishwa nchini kote kwa njia zifuatazo: (i) Midahalo 71 iliyoshirikisha wanachama 4,629 wa shule za sekondari na vyuo. (ii) Matamasha 8 na shindano 1 yaliyoshirikisha wanafunzi 572. (iii) Kazi mradi 263 zilihusisha wanafunzi 2,052 wa shule za sekondari na vyuo. (iv) Semina/Mafunzo 2,053 kwa wanachama 140,398. (v) Mikutano ya hadhara/mijadala ya wazi 43 kwa wanachama 6,890. Idadi ya klabu zilizoimarishwa imeongezeka kwa asilimia 25 ikilinganishwa na idadi ya mwaka 2013/14 (rejea kielelezo Na. 21)
24
“Uwajibikaji Unaanza na Wewe. Tushirikiane Katika Mapambano Dhidi ya Rushwa�
Kielelezo 21: Uwiano wa njia za uelimishaji kwa mwaka 2013/14 na 2014/15
4.1.4 Uandishi wa habari na makala Habari na makala 264 kati ya 240 zilizopangwa ziliandaliwa na mikoa na wilaya na kuwasilishwa Makao Makuu kwa mapitio na kutumika katika jarida au wavuti ya TAKUKURU. Habari/makala 34 kati ya 264 zimetumika katika kuandaa jarida la TAKUKURU, 7 zimetumika katika wavuti na 223 zimerejeshwa kwa waandishi ili ziboreshwe.
4.1.5 Maonesho Ofisi za TAKUKURU za mikoa na wilaya zilishiriki katika maonesho 183 kati ya 121 yaliyopangwa na kuwafikia wadau 105,601. Maonesho hayo ni pamoja na Nane Nane, Wiki ya Sheria, Siku ya Serikali za Mitaa, Siku ya Kimataifa ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa na Siku ya Ukimwi Duniani. Mengine ni Uwekezaji, Siku ya Chakula Duniani, Mbio za Mwenge wa Uhuru na Wiki ya Vijana Kitaifa.
4.1.6 Vipindi vya Redio, Televisheni na Magazeti Taarifa kwa vyombo vya habari, vipindi vya redio na televisheni 334 kati ya 110 vilivyopangwa, vilirushwa kupitia magazeti na vituo mbalimbali vya televisheni na redio. Vipindi 14 vilirushwa katika televisheni za TBC1, ITV, Geita Cable, Abood Tv na Bukoba Tv na vipindi 201 vilirushwa kupitia vituo vya redio. Aidha taarifa 97 zilitolewa kupitia vyombo vya habari na mikutano 22 na waandishi wa habari ilifanyika kwa lengo la kuelimisha au kuarifu umma juu ya harakati za mapambano dhidi ya rushwa kitaifa na kimataifa. Kampeni ya ACHA iliyolenga kudhibiti rushwa katika Uchaguzi Mkuu 2015 na kuwasaidia wapiga kura kuchagua viongozi wao kwa sera na si kwa rushwa. Kampeni hii ilirushwa kupitia vyombo vya habari vya Clouds.
“Uwajibikaji Unaanza na Wewe. Tushirikiane Katika Mapambano Dhidi ya Rushwa�
25
Jedwali namba 2: Uwiano wa vipindi vya redio na televisheni vilivyorushwa Na.
Stesheni
Idadi ya vipindi 23 17 13 12 6 5 4 4 4 3 3 3 3 3 3 3 2 2 2 2 2 2 2 2
Na.
1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17 18 19 20 21 22 23 24
Huruma Fm Redio Best Fm Sibuka Fm Redio Boma Fm CG Fm Tripple A Redio Ruangwa Redio Kwizera Kasibante Fm Ushindi Redio Jogoo Fm Furaha Fm Redio Ulanga Fm Redio Pride FADECO Fm Wapo redio Kings Fm Redio chemchem Fm Redio Habari njema Karagwe Fm Dodoma Fm Redio Pambazuko Fadhila Fm Redio One
25 26
Stesheni
Idadi ya vipindi 1 1 54 1 1 1 1 1 1 1 1 1 1 1 1 1 1 1 1 1 1 1 1 4
27 28 29 30 31 32 33 34 35 36 37 38 39 40 41 42 43 44 45 46 47 48 49 50
Uplands Redio Highland Fm TBC Taifa Redio Manyara Ice Fm Kitulo Fm Radio Info Redio Terrat Redio Jamii Fm HHC Alive Redio Vision Kyela Fm Hai fm Nkasi Fm Mpanda Fm Redio 5 Fm Redio Abood BTV Fm Faraja Fm Uvinza Fm Nuru Fm Mashujaa Fm Singida Fm Bukoba Tv
ITV
1
51
Geita Cable
9
TBC1
3
52
Abood Tv
1
3.1.7 Machapisho Aina 7 za machapisho yanayoelimisha zilichapwa na kusambazwa kati ya aina 5 zilizolengwa; vyeti vya wanaklabu, vipeperushi, majarida, mabango, fulana, kofia, kalenda za mezani na za ukutani.
26
“Uwajibikaji Unaanza na Wewe. Tushirikiane Katika Mapambano Dhidi ya Rushwa”
Kielelezo Na 22: Uwiano wa machapisho yaliyochapwa kwa kipindi cha 2013/14 na 2014/15
4.1.8 Makala za picha za video (video documentary) Makala za picha za video (video documentaries) 15 ziliandaliwa kati ya 8 zilizopangwa kwa ajili ya kuitangaza TAKUKURU kupitia televisheni na kuweka kumbukumbu kwa matumizi ya ofisi.
4.1.9 Matangazo Matangazo 6 kati ya 4 yaliyopangwa yenye ujumbe wa kukemea vitendo vya rushwa katika elimu, afya, maendeleo na uzalendo yaliandaliwa na kurushwa. Aidha matangazo 5 ya video (TV spot) kuhusu rushwa katika uchaguzi yamehaririwa.
4.1.10 Huduma za Maktaba: Maktaba ya TAKUKURU inatumika kupata rejea muhimu za majukumu makuu tunayotekeleza na kuwahudumia watumishi na wananchi wengine wanaoruhusiwa kuitumia. Katika kipindi cha mwaka 2014/2015 huduma za ukutubi na kujiimarisha zilifanyika ambapo watumishi walihudumiwa mara 7,083. Kutokana na kazi zilizotekelezwa, jumla ya wananchi wapatao 706,300 wamefikiwa. Idadi hii haihusishi wananchi waliofikiwa kupitia vituo vya redio, televisheni, magazeti na machapisho kwani ni vigumu kuipata.
“Uwajibikaji Unaanza na Wewe. Tushirikiane Katika Mapambano Dhidi ya Rushwa�
27
4.1.11 Ziara za wageni (mahusiano na taasisi za ndani na nje ya Tanzania) Kushirikiana na Taasisi za ndani na nje ya nchi zinazojihusisha na mapambano dhidi ya rushwa ni wajibu wa TAKUKURU kwa mujibu wa kifungu cha 7(d). Taasisi imepokea na kukutana na wageni mbalimbali wanaofika nchini na TAKUKURU kwa lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu. Ziara hizi zinasaidia kueleza mafanikio katika mapambano dhidi ya rushwa nchini na kuitangaza TAKUKURU nje ya mipaka. Katika kipindi hiki TAKUKURU ilipokea Ujumbe wa Taasisi 22. Baadhi ya wageni hao walitoka Botswana, Lesotho, Zaire, Malawi, Mauritius, Zambia na China.
4.2
SHUGHULI ZA KIJAMII
Shughuli za kijamii 17 zimefanyika katika baadhi ya mikoa na wilaya nchini. Shughuli hizi ni kutoa misaada kwa watoto yatima, wanaoishi katika mazingira magumu na wagonjwa. Kuwatembelea/kuwafariji wagonjwa na wazee wenye ukoma. Kushiriki katika tamasha la mpira wa miguu, kufanya usafi katika maeneo mbalimbali na kupanda miti. Shughuli kama hizi hufanywa na watumishi wa TAKUKURU kwa lengo la kujenga mahusiano mazuri na jamii wanayoitumikia ili waunge mkono juhudi za Serikali katika vita dhidi ya rushwa.
4.2.1 Vikao vya Uelimishaji katika Serikali za Mitaa Vikao 50 vya uelimishaji wadau vilifanyika vikiwa na nia ya kutoa elimu kuhusu madhara ya rushwa katika miradi ya maendeleo pia wajibu wa wananchi katika kusimamia miradi ya maendeleo. Aidha na kongamano moja lilifanyika Mkoa wa Temeke na kuibua changamoto nane ambapo maazimio ya kuzikabili changamoto yalifikiwa. Wadau 892 walifikiwa katika uelimishaji huu wa miradi ya maendeleo yakiwamo makundi ya wananchi kupitia mikutano ya hadhara, Wakuu wa Idara za Mamlaka za Serikali za Mitaa kupitia vikao vya tathmini za ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo, watendaji wa kata kupitia kongomano na wajumbe wa kamati za maendeleo za Kata za kisekta kupitia semina.
PICHA NA 1: Wananchi wa kijiji cha Kironge Halmashauri ya wilaya Mafia Mkoa wa Pwani wakisikiliza mada ya umuhimu wa wananchi kushiriki katika ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo toka kwa mratibu wa PETS Ndg Ali Mfuru (aliyesimama katikati)
28
“Uwajibikaji Unaanza na Wewe. Tushirikiane Katika Mapambano Dhidi ya Rushwa”
4.3 MAFANIKIO Mafanikio ni mengi, hapa tumetaja baadhi. (i) (ii)
Kampeni ya “ACHA” imesaidia kuwafikia wananchi wengi kupitia kituo cha Clouds Media. Uelewa wa wananchi kuhusu rushwa umeongezeka kiasi cha kuwa na uthubutu wa kuhoji mambo mbalimbali kupitia vyombo vya habari na mikutano ya hadhara. Elimu imewasaida wananchi kujua taarifa zinazohusu rushwa. (iii) Baadhi ya vijana hasa wa klabu za wapinga rushwa waliomaliza vyuo au shule na kuajiriwa, wameendelea kushiriki mapambano dhidi ya rushwa kwa mfano kwa kujitolea kutoa elimu kwa jamii kama walivyofanya wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu 2015, kutoa taarifa TAKUKURU. Hii ni ishara kwamba program hii inajenga uadilifu na uzalendo.
“Uwajibikaji Unaanza na Wewe. Tushirikiane Katika Mapambano Dhidi ya Rushwa”
29
SURA YA TANO UWEZESHAJI 5.0
UTAWALA NA USIMAMIZI WA RASILIMALI
Kurugenzi ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu ina jukumu kubwa la kuwezesha rasilimali watu na rasilimali nyingine kama watu na fedha, zinapatikana kwa wakati na muda muafaka. Katika kutekeleza jukumu hili kazi zifuatazo zilifanyika katika kipindi cha mwaka 2014/15.
5.1 Mafunzo Katika kipindi cha mwaka 2014/15 watumishi 432 wa kada mbalimbali sawa na asilimia 21 ya watumishi wote, walihudhuria mafunzo ya muda mrefu na mfupi ndani na nje ya nchi ili kuwajengea uwezo wa kuwawezesha kufanya kazi kwa ufanisi.
5.2 Vyeo Watumishi 526 wenye sifa na vigezo stahiki walipandishwa vyeo kwa mujibu wa Muundo wa Utumishi wa TAKUKURU na Ikama ya mwaka 2014/15 ili kuongeza tija na morali ya kufanya kazi kwa bidii. Kati ya hao, Maafisa Uchunguzi walikuwa 217 sawa na asilimia 41 ya waliopandishwa vyeo na wachunguzi wasaidizi walikuwa 309 sawa na asilimia 59.
5.3
Usajili wa watumishi katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na Bima ya Afya
Hadi kufikia mwezi Juni, 2015 asilimia 97 ya watumishi wote walikuwa wamesajiliwa katika mifuko mbalimbali ya hifadhi ya jamii. Vilevile, asilimia 99 ya watumishi wote walisajiliwa katika Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na kupata vitambulisho ili waweze kunufaika na huduma zitolewazo na Mfuko huo. Kwa watumishi ambao bado hawajasajiliwa Taasisi imeendelea kuwakumbusha na kuwahimiza kujisajili.
30
“Uwajibikaji Unaanza na Wewe. Tushirikiane Katika Mapambano Dhidi ya Rushwa�
Kielelezo Na. 23: Usajili wa watumishi katika Mifuko ya Hifadhi za Jamii
5.4
Ujenzi na ukarabati
Katika kipindi cha mwaka 2014/15, TAKUKURU ilijenga majengo 3 ya ofisi za Kigoma, Newala na Mkinga. Vile vile Taasisi iliendelea kufanya ukarabati wa ofisi zake ili kuboresha mazingira ya kufanyia kazi kwa watumishi. Ofisi 5 zilifanyiwa ukarabati mkubwa, Ukarabati/matengenezo madogo madogo kwa majengo yanayomilikiwa na Taasisi ni wa kudumu ili kuhakikisha majengo yanaendelea kubaki katika hali nzuri wakati wote.
PICHA NAMBA 2: Jengo la ofisi ya TAKUKURU lililokamilika kujengwa mwaka 2014/15 - Wilaya ya Newala Mkoa wa Lindi.
“Uwajibikaji Unaanza na Wewe. Tushirikiane Katika Mapambano Dhidi ya Rushwa�
31
5.5
Malipo ya pango
Katika kipindi cha mwaka 2014/15 Taasisi ilifanya malipo ya pango kwa majengo 78 yanayotumiwa na ofisi za mikoa na wilaya ambapo kiasi cha shilingi 366,653,998.50 kilitumika. Taasisi imekuwa ikilipa kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya pango la ofisi kutoka fedha za kuendesha ofisi kwa kuwa haipati fedha za maendeleo. Hadi kufikia Juni, 2015, Taasisi imeendelea kulipia kodi kwa ajili ya ofisi 3 za mkoa, 68 za wilaya na 7 za vituo maalum.
5.6
Watumishi waliochukuliwa hatua za kinidhamu
Katika kipindi cha mwaka 2014/15, watumishi 45 walichukuliwa hatua za kinidhamu ambapo watumishi 10 walifukuzwa kazi kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo, utoro kazini, ukosefu wa nidhamu na utendaji mbovu. Pia katika kipindi hicho watumishi 35 walipewa onyo kutokana na makosa mbalimbali ya kiutendaji na nidhamu.
5.7
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kina jukumu la kuimarisha mifumo ya kompyuta iliyopo ili kuboresha mazingira ya utendaji kazi kwa kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano. Katika kipindi cha mwaka 2014/15 kitengo hiki kimeendelea kuboresha mifumo ya upashanaji habari iliyokuwepo na ambayo tayari ilikuwa imeanzishwa kwa kuimarisha miundombinu ya mawasiliano na kupanua wigo wa mtandao wa Taasisi na kuwezesha kurugenzi, vitengo na mikoa katika matumizi ya mifumo iliyopo. Pia kitengo hiki, kwa kipindi husika kimeendelea kusimamia mifumo ya taarifa ya Taasisi na kuimarisha usalama wa miundombinu ya mawasiliano na mifumo.
5.8 Manunuzi Taasisi inacho Kitengo cha Manunuzi chenye jukumu la kusimamia manunuzi na ugavi katika. Katika kipindi cha mwaka 2014/15 kupitia kitengo hiki TAKUKURU ilifanya manunuzi yenye thamani ya shilingi 2,440,370,825.33. Aidha, katika kipindi hiki, kitengo kilisambaza vifaa mbalimbali vilivyonunuliwa katika ofisi za Makao Makuu, mikoa na wilaya kwa mujibu wa mpango wa manunuzi na usambazaji.
5.9
Ukaguzi wa Ndani
Taasisi inacho Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani chenye jukumu la kufanya ukaguzi wa ndani wa Taasisi. Katika kipindi cha mwaka 2014/15, kitengo hiki kimeendelea kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria ya Fedha ya Umma Na. 6 ya mwaka 2001 ambapo kwa kipindi hicho kazi 13 za ukaguzi zilifanyika.
5.10 Fedha na Uhasibu Taasisi inacho Kitengo cha Fedha na Uhasibu chenye jukumu la kusimamia na kuwezesha rasilimali fedha kupatikana kwa wakati. Katika mwaka wa fedha 2014/15, kitengo hiki kiliendelea kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria ya Fedha ya mwaka 2001 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2004 na kuhakikisha bajeti iliyoidhinishwa na Bunge kwa TAKUKURU kwa ajili ya mishahara na fedha za ndani inatumika kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za Fedha.
32
“Uwajibikaji Unaanza na Wewe. Tushirikiane Katika Mapambano Dhidi ya Rushwa�
Pamoja na changamoto mbalimbali zilizojitokeza katika kutekeleza kazi za Kurugenzi ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu na vitengo kama vilivyoainishwa hapo juu, tathmini ya matokeo ya kazi zilizofanyika ilikuwa kama ifuatavyo; Kurugenzi ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu ilitekeleza majukumu yake kwa asilimia 88.05, Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano asilimia 81.38, Kitengo cha Manunuzi asilimia 92.83, Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani asilimia 69.63 na Kitengo cha Fedha na Uhasibu asilimia 97.43.
“Uwajibikaji Unaanza na Wewe. Tushirikiane Katika Mapambano Dhidi ya Rushwa�
33
SURA YA SITA MIPANGO, UFUATILIAJI NA TATHMINI 6.0
MIPANGO, UFUATILIAJI NA TATHMINI
Mipango thabiti ni muhimu kwa ustawi na maendeleo ya Taasisi yoyote. Ili kuleta matokeo makubwa TAKUKURU inapanga mipango yake ya utekelezaji kwa kuzingatia miongozo ya Serikali, Sera, Bajeti na Sheria.
6.1 a) b)
c) d)
e)
f )
Utekelezaji wa Mipango Mpango kazi wa Taasisi wa mwaka 2015/16 umeandaliwa na tayari utekelezaji wake umeanza Julai 2015 kwa kuzingatia ilani ya uchaguzi, Mpango Mkakati wa TAKUKURU na bajeti iliyopitishwa na Serikali. Taasisi ilishiriki vikao vyote vya maandalizi ya bajeti ikiwa ni pamoja na kikao na Kamishna wa bajeti, kikao na Kamati ya Bunge, maandalizi ya hotuba ya Waziri wa Utawala Bora na vikao vya Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aidha “Medium Term Expenditure Framework “(MTEF) mwaka 2015/16 iliandaliwa na kuwasilishwa Hazina na Ikulu. Taasisi iliandaa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi kwa kipindi cha mwaka 2013/14 pamoja na mpango wa utekelezaji wa mwaka 2014/15 na kuwasilisha Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Ikulu. Taasisi kupitia ufadhili wa “Department For International Development” (DFID) imeweza kutekeleza kazi mbalimbali zinazohusiana na mafunzo, uchunguzi hasa wa rushwa kubwa, utafiti katika maeneo ya maliasili, gesi, reli pamoja na uelimishaji umma kupitia baluni. Uratibu wa mradi unaofadhiliwa na “African Development Bank” (AfDB) uliendelea kufanyika ambapo wazabuni wanaendelea na kazi. Miongoni mwa kazi zilizopangwa kukamilika ni pamoja na utafiti katika miundo mbinu ya barabara, mafunzo maalumu kwa wachunguzi na uandaaji wa Mwongozo wa uzuiaji na uchunguzi wa rushwa katika manunuzi (prevention and investigation manual in procurement). Taarifa zinazohusiana na miradi ya AfDB, DFID ziliandaliwa na kuwasilishwa kadri zilivyohitajika na wadau mbalimbali ikiwemo Ikulu.
6.1.1 Miradi inayofadhiliwa na wadau wa maendeleo (DPs) TAKUKURU ilitekeleza miradi iliyofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na “Department For Iternational Development” (DFID) ifuatayo:
6.1.1.1 Miradi iliyofadhiliwa na DFID a) b) c)
34
Vipindi vya Radio na Televisheni kwa ajili ya kuhamasisha na kuelimisha umma viliandaliwa na kurushwa. Uchunguzi wa majalada yatokanayo na taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), malalamiko ya wananchi na tuhuma za awali za rushwa ulifanyika. Mfumo wa kielektroniki wa utunzaji wa takwimu za TAKUKURU umeanzishwa na umeanza kutumika ili kutuwezesha kuwa na takwimu sahihi
“Uwajibikaji Unaanza na Wewe. Tushirikiane Katika Mapambano Dhidi ya Rushwa”
d)
Mafunzo ya namna ya kuutumia mfumo huo yametolewa, waliopata mafunzo ni
e) f )
IC, makao makuu mikoani pamoja na wilayani. Kuunganisha wilaya na mikoa na mfumo wa mawasiliano ya ndani ya Taasisi Ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za miradi ya maendeleo katika mamlaka za Serikali za Mitaa ulifanyika.
pamoja na wakurugenzi, wakuuu wa vitengo na wakuu wa sehemu, maafisa wa
6.1.1.2 Miradi iliyofadhiliwa na AfDB a) b)
Mwongozo wa uzuiaji na uchunguzi wa rushwa katika manunuzi – Mzabuni aliwasilisha taarifa ya mwisho. Zabuni ya utafiti wa rushwa katika barabara imetolewa na mzabuni anaendelea na kazi.
6.1.1.3 Miradi ya wafadhili iliyotekelezwa 2014/15 Miradi ya wafadhili iliyotekelezwa katika kipindi hiki ni ya DFID nayo ni; a) b) c) d)
Kufanya Uchunguzi wa majalada yatokanayo na taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), malalamiko ya wananchi na tuhuma za awali za rushwa na kuharakisha upatikanaji wa majalada yaliyokamilika; Kuunganisha wilaya na mikoa na mfumo wa mawasiliano ya ndani ya Taasisi; Kuandaa vipindi (documentary) vya kuhabarisha umma matukio na kashfa za rushwa na kuvitangaza kwenye radio, runinga na kwa kutumia baluni; na Ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za miradi ya maendeleo katika mamlaka za Serikali za Mitaa.
6.1.1.4 Mpango wa utekelezaji mwaka 2015/16 i. ii.
iii. iv. v. vi.
vii. viii. ix.
Kuendelea kuchunguza tuhuma 2,783 zilizopo na mpya zitakazojitokeza; Kukamilisha uchunguzi maalum unaoendelea katika vocha za pembejeo za kilimo, maliasili na tuhuma zilizobainishwa na taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali; Kukamilisha chunguzi za tuhuma kumi (10) za rushwa kubwa (Grand corruption) kama ilivyopangwa katika mpango Mkakati wa Taasisi; Kuendelea kuendesha kesi 659 zilizopo mahakamani na zitakazoendelea kufunguliwa kutokana na kukamilika kwa chunguzi mbalimbali; Kufuatilia na kudhibiti vitendo vya rushwa katika mchakato wa uchaguzi Mkuu wa 2015 katika hatua zote; kabla ya uchaguzi, wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi; Kuendelea kutoa elimu kuhusu rushwa kwa wananchi, watumishi wa Serikali na makampuni binafsi na kuendeleza ushirikiano na Asasi za Kiraia katika mapambano dhidi ya rushwa; Kuendelea kutoa Elimu kwa wananchi kuhusu Rushwa katika Uchaguzi Mkuu wa 2015; Ufunguzi na uimarishaji wa klabu za wapinga rushwa katika shule za Msingi, Sekondari na vyuo vya elimu ya juu ili kuendelea kujenga jamii inayochukia rushwa; Kuwajengea uelewa wa masuala ya rushwa Asasi za Kiraia (CSOs) na wanahabari ili washiriki kikamilifu kuwajengea uwezo wananchi wa kudhibiti rushwa;
“Uwajibikaji Unaanza na Wewe. Tushirikiane Katika Mapambano Dhidi ya Rushwa”
35
x.
Kuendelea kuimarisha mifumo ya utendaji dhidi ya mianya ya rushwa kwa kufanya utafiti na udhibiti katika sekta za nishati na mazingira. xi. Kushirikisha wadau kuweka mikakati ya kudhibiti mianya ya rushwa na kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa mikakati hiyo; xii. Kuendelea kufuatilia miradi ya maendeleo katika Serikali za Mitaa ili kuongeza ufanisi na kuhakikisha thamani halisi ya fedha; xiii. Kuimarisha kitengo cha Ufuatiliaji na Urejeshaji wa mali za umma (Asset Tracing and Asset Recovery), Maabara ya uchunguzi na ofisi za waratibu wa kanda wa Ufuatiliaji wa Matumizi ya fedha za umma katika miradi ya maendeleo kwenye Serikali za Mitaa kwa kutoa mafunzo kwa watumishi; xiv. Kufanya mafunzo maalum ya weledi kwa watumishi ili kuboresha utendaji kazi na kuongeza ufanisi; xv. Kuanza ujenzi wa jengo la ofisi la Makao Makuu ya Bodi ya Ushauri ya Masuala ya Rushwa ya Umoja wa Afrika baada kukamilika kwa mchakato wa umiliki wa kiwanja na kumpata Mkandarasi wa ujenzi; xvi. Kufanya tafiti (survey) nne za kupata taarifa za kuanzia (baseline data) za viashiria vya kupima kiwango cha rushwa na mafanikio ya mapambano dhidi ya rushwa nchini.
6.1.1.5 Ufuatiliaji Katika kipindi cha Julai, 2014 hadi Juni, 2015 Taasisi iliendelea kutekeleza majukumu yake mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufanya Ufuatiliaji na Tathmini kwa Kurugenzi, Vitengo/ Sehemu, Wakuu wa TAKUKURU Mikoa na Wilaya pamoja na kuhudhuria vikao vya Wadau wa Maendeleo na kusimamia upatikanaji wa rasilimali fedha toka DFID, AfDB, UNDP na kuandaa taarifa ya mwaka 2014/15. Mafanikio yameendelea kuonekana kutokana na uwepo wa mfumo wa ufuatiliaji ambao unafanyika kipitia taarifa za kila mwezi, robo mwaka, miezi sita na mwaka pamoja na maafisa wa ufuatiliaji na tathmini kutembelea ofisi za mikoa kuona hali halisi ya utekelezaji wa shughuli zetu na kufanya uchambuzi wa kina na kutoa ushauri katika maeneo ambayo yalibainika kuwa na mapungufu.
6.1.1.6 Tathmini Tathmini ya utekelezaji wa malengo ya Mpango Mkakati imekuwa ikifanyika kila mwezi, robo mwaka, nusu mwaka na mwaka mzima. Taarifa ya tathmini hizi ya kila kipindi imekuwa ikiandaliwa na uchambuzi kufanyika kuonesha mtiririko wa utendaji na kutoa maoni juu ya yale ya kujifunza na kusahihisha kutokana na hali ya utendaji ilivyo. Tathmini hii inahusisha Kurugenzi, Vitengo, Sehemu, Kanda, Mikoa, Wilaya na Vituo maalum. Maoni yamewasilishwa kwa uongozi kwa lengo la kutumia taarifa hizo kuboresha utendaji wa kazi. Utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Taasisi kwa mwaka wa pili 2014/2015 umefanyika katika kiwango kizuri na umetoa matokeo mazuri. Malengo na shabaha tulizojiwekea vimezingatiwa katika utekelezaji na upimaji wa matokeo. Ufuatiliaji na uhakiki umefanyika kubaini mapungufu na marekebisho yamefanyika. Vilevile tathmini kwa watumishi na kila ofisi imefanyika, hivyo ni matumaini yetu mwaka 2015/2016 utakuwa na matokeo makubwa zaidi kwani Taasisi
36
“Uwajibikaji Unaanza na Wewe. Tushirikiane Katika Mapambano Dhidi ya Rushwa�
imewekeza zaidi na mengi yamefanyika mwaka uliopita ya kuongeza uwezo na ufanisi katika utendaji wetu. Kila mtumishi anaelewa ili kuwa na utendaji wenye kujali matokeo ni muhimu kuwa na mfumo mzuri wa Mipango, Bajeti, Takwimu, Ufuatiliaji na Tathmini.
6.1.1.7 Takwimu Katika kuboresha mfumo wa utendaji wa kazi zetu tumezingatia mfumo wa takwimu wa Taasisi ulioanzishwa ambao unauwezo wa kutoa takwimu sahihi kwa wakati na hali halisi ya muelekeo wa utekelezaji wa kila ofisi katika kipindi husika. Hii itatuwezesha kuleta mabadiliko katika kutekeleza majukumu ya TAKUKURU kwa ufanisi zaidi kwani takwimu sahihi huifanya menejimenti kuwa na maamuzi sahihi. Siku zote tutatanguliza maslahi ya Taifa kwanza kwa kufanya kazi kwa kujituma zaidi kabla ya kufikiria maslahi yetu binafsi. Mipango, Takwimu, Ufuatiliaji na Tathmini ni kiungo kikubwa katika utekelezaji na uratibu wa shughuli za Taasisi. Mipango madhubuti na takwimu sahihi zinaisaidia menejimenti kuwa na maamuzi sahihi na kuwa na mikakati inayoiwezesha kufikia malengo.
“Uwajibikaji Unaanza na Wewe. Tushirikiane Katika Mapambano Dhidi ya Rushwa�
37
SURA YA SABA MAJUMUISHO 7.1 MAJUMUISHO Wote tunatambua kwamba rushwa ni kikwazo cha maendeleo ya Taifa na utoaji wa haki nchini. Kwa maana hiyo, isipodhibitiwa, madhara yake kwa jamii lazima yatakuwa ni makubwa. Tathmini iliyofanywa mwaka 2009 na Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Kupambana na Rushwa (United Nations Convention Against Corruption 2003 – UNCAC) kwa kushirikiana na Serikali za Uingereza na Uholanzi kuhusiana na mapambano dhidi ya rushwa nchini imeonyesha kwamba, Tanzania ni Nchi inayopambana na rushwa kwa dhati. Aidha, Tanzania ndiyo nchi pekee Barani Afrika iliyo kamilisha mchakato wa tathmini hiyo ya Shirika la Umoja wa Mataifa. Rushwa katika nchi yetu iko zaidi katika utoaji huduma kwa jamii na utoaji kandarasi na mikataba. Vilevile, maeneo yanayoongoza kwa rushwa ni katika chaguzi hasa za ndani za vyama vya siasa, taasisi na asasi ambazo uongozi unapatikana kwa njia za uchaguzi, hususan uchaguzi mkuu.
7.1.1 Uchunguzi Mwaka 2014/15 taarifa ya Taasisi katika eneo la uchunguzi imekuwa na matokeo ambayo takwimu zinaonyesha mwenendo wa malengo mengi umeshuka. Malalamiko yamepungua toka 5,069 mwaka 2013/14 hadi 4,675 mwaka 2014/15, idadi ya majalada yaliyofanyiwa uchunguzi na kukamilika iliongezeka kwa kiasi kidogo toka 607 mwaka 2013/14 hadi 667 mwaka 2014/15, majalada yaliyopelekwa kwa DPP yalipungua toka 361 mwaka 2013/14 hadi 278 mwaka 2014/15, majalada yaliyorudi toka kwa DPP na kibali cha mashtaka yalipungua toka 261 mwaka 2013/14 hadi 172 mwaka 2014/15. Aidha, idadi ya kesi mpya ilipungua toka 332 mwaka 2013/14 hadi 314 mwaka 2014/15, kesi zilizoshinda zimeongezeka toka 89 mwaka 2013/14 hadi 177 mwaka 2014/15 na kiasi cha fedha kilichookolewa kilishuka toka shilingi 38.96 bilioni mwaka 2013/14 hadi shilingi 7.0 bilioni mwaka 2014/15. Ubadhirifu katika miradi ya maendeleo ambao ni asilimia 26 ya kesi zilizopo mahakamani inaonyesha kiasi gani eneo hili linahitaji kushughulikiwa kwa karibu ili kukomesha ubadhirifu huo. Hivyo, Taasisi inajipanga kwa kufanya maboresho makubwa ili kuweza kuleta mabadiliko chanya katika uchunguzi na maeneo mengine muhimu. Serikali na wananchi watarajie mabadiliko yenye tija katika uchumi na ustawi wa jamii yatakayoletwa na mapambano dhidi ya rushwa nchini.
38
“Uwajibikaji Unaanza na Wewe. Tushirikiane Katika Mapambano Dhidi ya Rushwa”
7.1.2 Utafiti na Udhibiti a)
b)
c) d)
e)
Tafiti tano zilifanyika ambapo hadi kufikia Juni 30, 2015, tafiti mbili zimekamilika na tatu zilikuwa zinaendelea. Tafiti hizo zilifanyika katika maeneo ya nishati, uchaguzi, maji na fedha. Aidha, katika kipindi cha 2014/15 TAKUKURU kupitia mshauri elekezi ilifanya tafiti mbili na kuanda mwongozo wa kuzuia rushwa katika manunuzi ya umma. Katika utekelezaji wa majukumu ya kuzuia rushwa, ushirikishwaji wa wadau ni muhimu ili kuwa na uelewa wa pamoja wa mianya ya rushwa iliyopo na kujenga umiliki (ownership) wa mikakati ya kuzuia rushwa ndani ya Taasisi inayokusudiwa kuimarishwa mifumo yake. Ushirikishwaji huu hufanyika kwa njia ya warsha na vikao na wadau vya kujadili matokeo ya kazi 363 za udhibiti zilizofanywa na kuweka mikakati endelevu ya kuziba mianya hiyo; Katika mwaka 2014/15, kazi 519 za udhibiti wa haraka wa kero za wananchi zilifanyika katika mikoa na wilaya zote nchini; Ili kupata taarifa za utekelezaji wa maazimio yaliyokubaliwa na kupima mafanikio yaliyopatikana katika udhibiti wa mianya ya rushwa, kazi 260 za ufuatiliaji zilifanyika na taarifa za utekelezaji kuandaliwa. Katika kutoa na kusambaza taarifa za kazi za utafiti na udhibiti, machapisho mbalimbali huandaliwa na hutolewa na TAKUKURU. Jumla ya nakala 3000 za machapisho kuhusu uchaguzi wa Serikali za mitaa, na mwongozo wa uchunguzi katika mananuazi ya umma yaliandaliwa na ksambazwa kwa wadau.
7.1.3 Elimu kwa Umma a)
TAKUKURU imeendelea kutoa elimu ya rushwa kwa jamii kwa kutumia vyombo vya habari, machapisho na shughuli nyingine za kijamii katika ngazi ya Kitaifa, Mkoa na Wilaya. Aidha, semina 2,933 zilitolewa katika kipindi hiki ambapo wadau 190,367 walifikiwa; b) Klabu za Wapambanaji wa Rushwa 2,434 zenye Wanachama 154,541 ziliimarishwa kote nchini na pia klabu 562 mpya zenye wanachama 47,716 zimefunguliwa katika Shule za sekondari nchini kote kwa kipindi cha kuanzia mwezi Julai, 2014/15 hadi Juni, 2014/15.
7.1.4
Changamoto
i)
Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11/2007 kutoa adhabu ndogo kwa makosa ya rushwa ambapo adhabu zinazotolewa hazilingani na hasara ambayo wala rushwa wamesababisha kwa Taifa. Kwa mujibu wa Sheria hii adhabu ya juu kabisa ni kifungo cha miaka saba jela au faini ya shilingi milioni kumi na tano;
ii)
Baadhi ya watumishi wa Serikali kuhukumiwa mahakamani na kukutwa na hatia lakini bado wanaendelea na kazi;
“Uwajibikaji Unaanza na Wewe. Tushirikiane Katika Mapambano Dhidi ya Rushwa”
39
iii)
Mapungufu katika Sheria za Utumishi kuruhusu mwajiri kutolazimika kumsimamisha kazi mtumishi aliyefikishwa mahakamani.
iv)
Baadhi ya wananchi kukosa moyo wa kizalendo katika kutetea maslahi ya Taifa kwa kushirikiana na TAKUKURU hasa suala la kutoa taarifa za rushwa na ushahidi mahakamani dhidi ya watuhumiwa;
v) vi) vii) viii) ix)
Upungufu wa fedha za kufanya chunguzi mbalimbali kutokana na ufinyu wa bajeti; Kukosekana kwa vyumba vya kutosha vinavyofaa kwa kazi ya chunguzi kubwa; Kukosekana kwa Sera ya Taifa ya mapambano dhidi ya rushwa; Baadhi ya wadau kutotekeleza maazimio ya kudhibiti mianya ya rushwa kwa wakati; Kukosekana kwa Sheria ya kusimamia utekelezaji wa maazimio ya kuziba/kudhibiti mianya ya rushwa; Upatikanaji wa nyaraka za migawo ya fedha za miradi kwa wakati kutoka Wizara ya Fedha. Mara nyingi nyaraka hizi huwekwa kwenye wavuti miezi mitatu au sita baada ya fedha kupelekwa kwenye Halmashauri; Baadhi ya Halmashauri zimekuwa haziwasilishi mipango ya manunuzi ya umma ya mwaka kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Manunuzi ya Umma (PPRA) hivyo kukwamisha kazi za ukaguzi; Rasilimali watu ni chache katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku;
x)
xi) xii)
xiii) Uelewa mdogo wa mahakimu kuhusu makosa ya rushwa yaliyomo katika Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na.11/2007; xiv) Kutotambuliwa kisheria kwa wataalamu wa TAKUKURU wanaoshughulika na maabara ya utambuzi wa makosa ya mtandao wa kompyuta; xv) Vifaa vya ununuzi kununuliwa hutoka nje ya nchi na hivyo mfumuko wa bei uliosababishwa na kushuka thamani ya shilingi ya Tanzania umeathiri bajeti yetu ya manunuzi ya mwaka na xvi) Kukosekana kwa majengo ya ofisi na nyumba za kuishi watumishi waandamizi
7.1.5 Matarajio (i)
Kutumia weledi katika kazi za kiuchunguzi ili kupata matokeo yanayotarajiwa;
(ii)
Serikali na wadau wengine kuona umuhimu wa kuanzisha mahakama itakayoshughulikia makosa ya rushwa ili kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi;
(iii)
Kudhibiti mianya ya rushwa katika mapato ya Serikali na matumizi mabaya ya mapato hayo na ya ofisi za umma au mamlaka;
(iv)
Kuwa na Sera ya Taifa ya mapambano dhidi ya Rushwa;
(v) Kuendelea kuiboresha maabara ya utambuzi wa makosa ya rushwa kwa njia ya mawasiliano ya computer; (vi)
40
Kuboresha maslahi ya watumishi;
“Uwajibikaji Unaanza na Wewe. Tushirikiane Katika Mapambano Dhidi ya Rushwa�
(vii) Kuratibu Mpango wa Mawasiliano (PCCB Communication Strategy) ili kuwa na njia bora za kuelimisha umma na kubadili mtazamo wa jamii juu ya mapambano dhidi ya rushwa; (viii) Kuendelea kuwatumia wataalam mbalimbali wa ndani na nje ya TAKUKURU ili maafisa wapewe mafunzo ya mara kwa mara kuboresha utendaji wao wa kazi; (ix)
Kuendelea kutumia vyombo vya habari kufikisha elimu ya mapambano dhidi ya rushwa kwa kulenga makundi mbalimbali ya jamii;
(x)
TAKUKURU kushirikiana na Wizara ya Fedha kupitia makubaliano (MoU) yatakayowezesha kupatikana kwa wakati nyaraka za kutuma rasilimali fedha kwenye Halmashauri zote mapema ili ufuatiliaji ufanyike kuanzia mchakato wa manunuzi wa miradi na huduma kama njia ya kuzuia kuliko ilivyo sasa (pro-active rather than post-mortem)
(xi) TAKUKURU kushirikiana na PPRA katika kuwezesha kupatikana kwa mipango ya manunuzi ya mwaka (Annual Procurement Plans) ili ufuatiliaji wa miradi uanze ngazi ya mchakato wa manunuzi hadi utekelezaji wa miradi au utoaji wa huduma. (xii)
TAKUKURU kushirikiana na PPRA kutumia nyenzo zinazotumiwa na mamlaka hii (Corruption Red Flags Checklist and Value for Money Audit) kuweza kubaini uchepushaji, ubadhirifu, rushwa na matumizi mabaya ya madaraka kwa watendaji kupitia matumizi ya raslimali.
(xiii) Kushirikisha bodi za uweledi kama CRB, ERB, PSPBT, NBAA na AQSRB katika kuchukua hatua dhidi ya watalaam ambao kazi zao zilisababisha raslimali za umma kupotea kupitia utekelezwaji wa miradi isiyokidhi thamani ya fedha. (xiv) Kuendelea kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango kuona namna ya kuongeza wigo wa bajeti ya Taasisi. (xv) Kuendelea kushirikiana na taasisi nyingine za Serikali kama vile Idara kuu ya Utumishi na Wakala wa Serikali Mtandao, ili kufaidika na fursa za mafunzo na vifaa vya TEHAMA na punguzo la gharama za mtandao kwa kuzingatia mzigo ambao TAKUKURU inabeba kutokana na mapana ya kimuundo. Mafanikio yote tuliyoyapata yasingeweza kufikiwa bila mchango wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na wadau wa Maendeleo ambao wameweza kutusaidia kwa misaada mbalimbali. Tunaishukuru Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza (DFID) na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa kutuwezesha kufanikisha malengo yetu. Hata hivyo Taasisi kufanya maboresho makubwa kuongeza ufanisi wa shughuli zake ili kuleta matokeo makubwa zaidi ya hayo na Serikali na wananchi watarajie mabadiliko yatakayotokana na mapambano dhidi ya rushwa kupitia huduma bora na ongezeko la mapato.
“Uwajibikaji Unaanza na Wewe. Tushirikiane Katika Mapambano Dhidi ya Rushwa�
41
Notes
42
“Uwajibikaji Unaanza na Wewe. Tushirikiane Katika Mapambano Dhidi ya Rushwa”
Notes
“Uwajibikaji Unaanza na Wewe. Tushirikiane Katika Mapambano Dhidi ya Rushwa”
43
Notes
44
“Uwajibikaji Unaanza na Wewe. Tushirikiane Katika Mapambano Dhidi ya Rushwa”
“Uwajibikaji Unaanza na Wewe. Tushirikiane Katika Mapambano Dhidi ya Rushwa”
45
“Uwajibikaji Unaanza na Wewe. Tushirikiane Katika Mapambano Dhidi ya Rushwa”
16 Mtaa wa Urambo, S.L.P 4865, DAR ES SALAAM. TANZANIA, Simu: + 255 22 2150043-6, Nukushi: +255 22 2150047 Baruapepe: dgeneral@pccb.go.tz, Wavuti: www.pccb.go.tz Simu ya bure ya dharura: 113
46
“Uwajibikaji Unaanza na Wewe. Tushirikiane Katika Mapambano Dhidi ya Rushwa”