i. ii.
Kusikiliza rufaa kutoka baraza la kata. Kusikiliza mashauri mbalimbali ya ardhi kwa mujibu wa sheria za ardhi pamoja na kusimamia utekelezajiwa maamuzi yake.
Baraza lina uwezo wa kusikiliza mashauri ya mali isiyohamishika yenye thamani isiyozidi shilingi za kitanzania milioni hamsini (50,000,000/-). Pia mashauri ya mali inayohamishika isiyozidi thamani ya shilingi za kitanzania milioni arobaini (40,000,000/-). Mtu ambaye hajaridhika na maamuzi ya baraza hili anaweza kukata rufaa katika mahakama kuu kitengo cha ardhi ndani ya siku sitini (60) tangu hukumu kutolewa.