Hija ya kuaga

Page 1

Hija ya Kuaga

Hotuba na Nasaha za Mtume (saww) Hotuba na Nasaha za Mtume (saww)

na Nasahaza za Mtume (saww) Hotuba Hotuba na Nasaha Mtume (saww)

Kimeandikwa na: Kimeandikwa Kimeandikwa na: SheikhJa’far Ja’farSubhani Subhani Sheikh Sheikh Ja'far Subhani Kimeandikwa na: Sheikh Ja’far Subhani Kimetarjumiwa na: Kimetarjumiwa na: Alhaji Hemedi Lubumba Kimetarjumiwa na:Selemani

Alhaji Hemedi Lubumba Selemani Kimetarjumiwa na: Alhaji Hemedi Lubumba Selemani

Alhaji Hemedi Lubumba Selemani Kimehaririwa na: Alhaji Ramadhani S K Shemahimbo

Kimehaririwana: na: Kimehaririwa Alhaji Ramadhani S1K Shemahimbo Alhaji Ramadhani S K Shemahimbo

Kimehaririwa na:

Alhaji Ramadhani 1 S K Shemahimbo 1


2 2 2 2


©Haki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION

ISBN: 978 - 9987 –17 -042 – 5

Kimeandikwa na: Sheikh Ja'far Subhani

Kimetarjumiwa na: Alhaji Hemedi Lubumba Selemani

Kimehaririwa na: Alhaji Ramadhani S K Shemahimbo

Kimepangwa katika Kompyuta na: Al-Itrah Foundation

Toleo la kwanza: Machi, 2014 Nakala: 1000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. - 19701, Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 / 2127555 Barua Pepe: alitrah@yahoo.com Tovuti: www.ibn-tv-com Katika mtandao: www.alitrah.info



YALIYOMO Neno la Mchapishaji........................................................................................... 01 Utangulizi............................................................................................................ 03 Idadi ya Hotuba Zake (saww) katika Hijja ya Kuaga......................................... 06 Hotuba Yake (saww) Mwezi Saba na Nane Dhulhaji......................................... 07 Maneno Yake Siku ya Arafa................................................................................ 08 Hotuba ya Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) Siku ya Arafa........ 13 Hotuba ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) Siku ya Kuchinja.................. 22 Hotuba Yake (saww) Aliyoitoa Katika Msikiti wa al-Khayfu........................... 29 Hotuba Yake (saww) Aliyoitoa Mbele ya Ka'ba................................................. 33 Hotuba ya Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) Aliyoitoa Ghadir Khum….................................................................................. 36

v



Hija ya Kuaga

NENO LA MCHAPISHAJI

K

ijitabu ulichonacho mikononi mwako ni mukhtasari wa khutba za Mtukufu Mtume (s.a.w.w) alizozitoa wakati wa hija yake mwisho, maarufu kama Hija ya kuaga (Hijatul-Wida). Mukhtasari huu umetolewa na Sheikh Ja'far Subhani katika moja ya mihadhara yake anayoindesha kwa ajili ya kuelemisha Ummah. Katika kijitabu hiki, Sheikh amekusanya takriban khutba sita ambazo Mtukufu Mtume alizitoa kwa mahujaji ikiwemo Hadithi maarufu aliyotoa akiwa Ghadir Khum wakati akirudi kuelekea Madina baada ya kumalizika kwa msimu wa ibada ya Hjja. Hizi ni khutba muhimu sana katika historia ya Uislamu, kwani ndizo zinazoelezea mustakabali wa Uislamu baada ya Mtume (s.a.w.w) kuondoka ulimwenguni hapa. Hivyo, ni muhumu sana kwa Waislamu wote kuzisoma, kuzielewa na kuzizingatia kwa vile zilikusudiwa kwa Waislamu wa zama zote ili wasije wakapotea kama alivyosisitiza mwenyewe Mtume (s.a.w.w) katika khutba zake hizi. Tumekiona kijitabu hiki ni chenye manufaa sana hususan wakati huu ambapo kuna upotoshaji mkubwa wa makusudi wa historia ya Uislamu. Lakini pia ni wakati ambao watu wameamka kielimu na upotoshaji huu hauna tena nafasi katika akili za watu kwani siku zote ukweli huelea, unapozama hapa huibukia pengine na hatimaye ukweli umedhihiri na uwongo umejitenga. Tunamshukuru ndugu yetu Alhaji Hemedi Lubumba ­Selemanikwa kazi kubwa aliyofanya kukileta kijitabu hiki katika lugha ya Kiswahili kutoka lugha yake ya asili ya Kiarabu. Pia shukurani ziwaendee wale wote ambao wameshiriki kwa namna moja au 1


Hija ya Kuaga

nyingine na kufanikisha kuchapishwa kwa kitabu hiki. Allah (swt) awalipe wote malipo mema ya hapa duniani na akhera pia. Mchapishaji Al-Itrah Foundation

2


Hija ya Kuaga

UTANGULIZI

M

namo mwaka wa kumi tangu Mtume ahamie Madina, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) aliazimia kwenda kufanya Hijja katika Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu, hivyo alitoka Madina kwenda Makka zikiwa ni siku tano kabla ya kuisha mwezi wa DhulQaadah, na alifika Makka siku ya mwezi nne Dhulhaji.1 Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) alikuwa amewahimiza Waislamu kwenda kufanya Hijja ndani ya mwaka huu, aliwaambia: "Atakaye kufanya Hijja basi aharakishe kwenda, kwani mtu anaweza kupatwa na ugonjwa, au kupotelewa na mnyama, au kupatwa na dharura."2 Baada ya Mwenyezi Mungu kumwamuru Nabii wake kuadhini na kutangaza Hijja, Mtukufu Mtume (saww) aliwaamuru waadhini wawatangazie Waislamu Hijja, na akawatumia ujumbe Ali bin Abu Talib (a.s.) na askari wake, na Abu Musa al-Ash'ariy na wafuasi wake huko Yemen, akiwataka waungane naye huko Makka Tukufu. Dhahiri ni kwamba mwanzo wa utangazaji wa habari hizi na kuwajulisha watu habari hizi ilikuwa ni mwanzoni mwa Dhul-Qaadah, Ibnu Is'haqa anasema: "Ilipowadia Dhul-Qaadah Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) alijiandaa kwa ajili ya Hijja na akawaamuru watu wajiandae kwa ajili ya Hijja hiyo."3 Mtukufu Mtume (saww) alitoka Madina na hali ni mwenye kuoga na ni mwenye kupaka mafuta, na walitoka pamoja naye wake zake wote. Na likamfuata kundi kubwa la Waislamu ambao walikuwa na hamu ya kufuatana naye toka Madina ili wapate heshima ya kusuhubiana naye. Imam Ja'far as-Sadiq (a.s.) anasema: "WakaAs-Siratun-Nabawiyyah ya Ibnu Hisham 4: 248. Musnad Ahmad bin Hanbal 1: 458. Sunan Ibnu Majah 2: 962. al-Muujamul-Kabir ya Tabarani 18: 296. as-Sunanul-Kubra ya Bayhaqiy 6: 463. 3 As-Siratun-Nabawiyyah ya Ibnu Hisham 4: 248. 1 2

3


Hija ya Kuaga

fahamu hilo waliokuwepo Madina, na pia watu wa vijijini na mabedui hivyo wakakusanyika, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) akahijji, na wao walikuwa wakimfuatisha wakimtazama na kufuata yale anayowaamrisha, au yeye anatenda kitu na wao wanatenda kitu hicho."4 Imepokewa kutoka kwa Jabir bin Abdillahi al-Ansariy kuwa alisema: "Walifika Madina watu wengi, wote wakitaka kuongozwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) na kutenda atendalo."5 Waislamu tangu mwanzo walitarajia safari hii ili wajifunze matendo ya ibada ya Hijja, hivyo kila tendo la kiibada alilotekeleza Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) ni sehemu ya Hijja ya Ibrahim (a.s.), na kila tendo aliloliacha ni sehemu ya matendo ya kijahiliya. Maandalizi haya, kungojea kwao, raghba yao, shauku yao, na wingi wao, vyote vinadhihirika wazi katika mwenendo wao kiasi kwamba walikwenda Makka kwa miguu na kwa vipando, umbali unaokaribia kilometa elfu moja kwenda na kurudi. Wanahistoria na wasimuliaji wa Hadithi wametofautiana juu ya idadi ya Waislamu katika tukio hilo, wapo wanaosema kuwa walikuwa ni watu laki moja na elfu ishirini.6Al-Maqriziy anapoelezea hotuba ya Mtukufu Mtume (saww) siku ya Arafa anasema: "Waliohudhuria katika hotuba hiyo ni takribani watu elfu arubaini."7Tabarasiy anasema: "Waliohijji pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) miongoni mwa watu wa Madina, wa vijijini na mabedui, walifikia watu elfu sabini au na zaidi."8 Baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) kumaliza Hijja alitoka Makka usiku wa mwezi kumi na nne Dhulhaji na kuelekea Madina, na akaingia Madina mwezi ishirini na tatu Dhulhaji. Ndani Al-Kafiy cha Kulayniy 4: 245. Tahdhibul-Ahkam cha Tusiy 5: 454. Sahih Muslim 2: 724. al-Maghaziy cha al-Maqriziy 2: 1088. 6 Tadhkiratul-Khawas: 30. 7 Imtaul-Asmai 2: 112. 8 Al-Ihtijaj cha Tabrasiy 1: 134. 4 5

4


Hija ya Kuaga

ya safari yake hii ya kurudi aliweza kusimama sehemu mbalimbali ambazo alipita, na Waislamu wakashuhudia kutoka kwake hotuba kadhaa za kupendeza na maelekezo ya kimalezi na kimaendeleo ya hali ya juu, ikiwa ni pamoja na nasaha za kielimu kiasi kwamba alikuwa akitekeleza kivitendo malengo ya Hijja aliyoyakusudia Mwenyezi Mungu toka ndani ya faradhi hii kubwa ya Kiislamu. Nasi ndani ya ujumbe huu mfupi tutagusia kwa ufupi na kwa muhtasari hotuba zake na maneno yake aliyoyatoa katika safari hii ya kihistoria, na tutaonesha misingi ya Uislamu, makusudio ya sheria na malengo yake yaliyomo ndani ya hotuba hizo. Ja'far Subhani.

5


Hija ya Kuaga

IDADI YA HOTUBA ZAKE (SAWW) KATIKA HIJJA YA KUAGA

W

aandishi wa Sira na wanahistoria kwa ujumla, wametofautiana juu ya idadi ya hotuba alizozitoa Mtukufu Mtume (saww) katika Hijja yake ya Kuaga. Al-Halbiy amesema ndani ya Sira yake: "Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) alitoa hotuba tano katika Hijja: Ya kwanza ni ya mwezi saba Dhulhaji huko Makka. Ya pili ni ya siku ya Arafa. Ya tatu ni ya siku ya kuchinja huko Mina. Ya nne ni ya mwezi kumi na moja huko Mina. Na ya tano ni ya siku ya kuondoka huko Mina."9 - Al-Maqriziy anasema: "Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) katika Hijja yake alitoa hotuba tatu."

9

As-Siratun-Nabawiyyah ya al-Halbiy 3: 333. 6


Hija ya Kuaga

HOTUBA YAKE (SAWW) MWEZI SABA NA NANE DHULHAJI

A

l-Waqidiy amesema ndani ya kitabu chake al-Maghaziy: "Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) alitoa hotuba baada ya Adhuhuri huko Makka siku moja kabla ya siku ya Tarwiyah (mwezi nane)."10 Al-Hakim an-Nisaburi anasema ndani ya Mustadrak yake: "Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) alikuwa akiwahutubia watu siku moja kabla ya siku ya Tarwiyah, akiwaeleza matendo yao ya Hijja."11 Na katika hadithi sahihi ya Muawiya bin Ammar kuna maelezo kutoka kwa Ja'far as-Sadiq (a.s.) kuwa: "Ilipofika siku ya Tarwiyah wakati wa kukengeuka jua Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) aliwaamuru watu kuoga na kuhirimia Hijja, nayo ndio kauli ya Allah aliyoiteremsha juu ya Nabii wake: "Fuateni mila ya baba yenu Ibrahim mwongofu."12 Mtukufu Mtume (saww) yeye na sahaba zake wakatoka huku wakihirimia Hijja mpaka wakafika Mina, wakaswali Dhuhri, Laasri, Maghribi, Isha na Alfajri, kisha akaondoka watu wakiwa pamoja naye."13

Al-Maghaziy 2: 1100. al-Mustadrak Alas-Sahihayni 1: 632. Na mfano wa habari hizo zinapatikana ndani ya as-Siratun-Nabawiyyah ya Ibnu Kathir 4: 337. Imtaul-Asmai cha al-Maqriziy 2: 117 – 118. Naylul-Awtar cha Shawkaniy 3: 307. Na As-Siratun-Nabawiyyah ya al-Halbiy 3: 227, 333. 12 (Sura Imran: 95) 13 Al-Kafiy cha Kulayniy 4: 246 – 247. 10 11

7


Hija ya Kuaga

MANENO YAKE SIKU YA ARAFA Yamepatikana maneno na hadithi nyingi kupitia muda aliokuwepo Arafa siku ya Arafa (mwezi tisa Dhulhaji), hapa tunataja baadhi tu: 1. Imeandikwa ndani ya kitabu Tahdhibul-Ahkam kwa njia yake kutoka kwa Saad bin Abdullah, kutoka kwa Muhammad bin Husain bin Abi al-Khatab, kutoka kwa Ahmad bin Muhammad bin Abi Nasri, kutoka kwa Muhammad bin Samaatul-Swayrifiy, kutoka kwa Samaatu bin Mahran, kutoka kwa Abu Abdillah Ja'far bin Muhammad as-Sadiq (a.s.) amesema: "Hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) alisimama huko Arafa watu wakawa wanakimbilia nyayo za ngamia wake na wakisimama pembeni yake, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) akamsogeza pembeni nao wakamfuata, ndipo Mtume akasema: 'Enyi watu! Hakika si sehemu tu ya nyayo za ngamia wangu ndio sehemu ya kusimama, lakini eneo lote hili ni sehemu ya kusimama.' Akaashiria sehemu ya kusimama. Na akasema tena: 'Eneo lote hili ni sehemu ya kusimama.' Ndipo watu wakatawanyika, na alifanya hivyo hivyo huko Muzdalifa..."14 2. Na katika hadithi nyingine sahihi ya Muawiya bin Ammar kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s.) ni kuwa alisema: "Kisha Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) aliondoka na watu wakiwa pamoja naye, Makuraishi walikuwa wakimiminika kutoka Muzdalifa huku wakiwazuia watu kumiminika kutoka hapo (Arafa), ndipo akaja Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) huku Makuraishi wakitaraji kuwa atatokea pale walipokuwa wakitokea (Muzdalifa), ndipo Mwenyezi Mungu akamteremshia kauli yake: 14

Tahdhibul-Ahkam cha Tusiy 5: 180. Man Layahdhuruhu al-Faqihu 2: 464. 8


Hija ya Kuaga

"Kisha miminikeni kutoka pale wanapomiminika watu, na muombeni Mwenyezi Mungu msamaha"15 yaani walipotokea Ibrahim, Ismail na Is'haqa (a.s.) na waliokuwa baada yao (Arafa). Makuraishi walipoona kuba la Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) limepita hadi Namra waliingiwa na kitu nyoyoni mwao kutokana na matarajio waliokuwa nayo ya kuwa atatokea sehemu yao (Muzdalifa), hapo aliweka hema lake na wao wakaweka mahema yao hapo, jua lilipokengeuka Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) alitoka pamoja na Makuraishi akiwa amekoga, akakata talbiya na akasimama msikitini, akawapa mawaidha watu, akawaamrisha na kuwakataza, kisha akaswali swala ya Adhuhuri na Laasiri kwa adhana moja na iqama mbili. Kisha alikwenda katika eneo lake la kusimama, watu wakawa wanakimbilia nyayo za ngamia wake na wakisimama pembeni yake, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) akamsogeza pembeni nao wakamfuata, ndipo Mtume akasema: 'Enyi watu! Hakika si sehemu tu ya nyayo za ngamia wangu ndio sehemu ya kusimama, lakini eneo lote hili ni sehemu ya kusimama.' Akaashiria kwa mkono wake sehemu ya kusimama, ndipo watu wakatawanyika, na alifanya hivyo hivyo huko Muzdalifa. Watu wakasimama mpaka jua likatua, kisha akaondoka na akawaamuru watu kutembea kwa utulivu na unyenyekevu mpaka alipofika Muzdalifa."16 3. Na katika kitabu al-Kafiy imepokewa hadithi mfano wa hiyo kutoka kwa Ali bin Ibrahim, kutoka kwa baba yake na kutoka kwa Muhammad bin Ismail, kutoka kwa al-Fadhlu bin Shadhan, kutoka kwa Ibnu Abi Umairi na Swaf'wan bin Yahya, kutoka kwa Muawiya bin Ammar, kutoka kwa Imam Ja'far as-Sadiq (a.s.).17 Sura al-Baqarah: 199. Al-Kafiy cha Kulayniy 4: 247.Tahdhibul-Ahkam cha Tusiy 5: 456. 17 Al-Kafiy cha Kulayniy 4: 463. 15 16

9


Hija ya Kuaga

4. Na riwaya ya Jabir iliyomo ndani ya kitabu Sahih Muslim inasema: "Akaamuru awekewe hema huko Namra. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) alikwenda huku Makuraishi wakiwa hawana shaka kuwa ni lazima atasimama al-Mash'aru al-Haram kama Makuraishi walivyokuwa wakifanya zama za Ujahiliyyah, lakini Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) alivuka hadi akafika Arafa, akakuta kawekewa hema huko Namra, akateremka hapo (Namra) na akabakia hapo mpaka jua lilipokengeuka, ndipo akaamuru aletewe ngamia wake al-Qas'wau. Akaondoka hapo mpaka Bat'nul-Wadi, akawahutubia watu....kisha akaadhini, akakimu na akaswali Dhuhri, kisha akakimu akaswali Laasri, na hakuswali swala nyingine yoyote baina ya Dhuhri na Laasri. Kisha Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) alipanda kipando chake mpaka akafika sehemu ya kusimama, akalielekeza tumbo la ngamia wake al-Qas'wau upande wa miamba na akaiweka njia ya watembea kwa miguu mbele yake,18 na akaelekea Kibla. Aliendelea kusimama mpaka jua lilipozama na wekundu kuondoka kidogo, mpaka umbo la jua likazama, akamweka Usamah nyuma yake....."19 5. Sheikh Tusiy amepokea kutoka Jamaah, kutoka kwa AbulMufadhali, kutoka kwa Abdullah bin Is'haqa bin Ibrahim bin Hammad al-Khatib al-Madainiy, amesema: Ametusimulia Uthman bin Abdullah bin Amru bin Uthman, amesema: Ametusimulia Abdullah bin Lahiatu kutoka kwa Abu Zubairi, amesema: Tumemsikia Jabir bin Abdullah akisema: "Mtume alipokuwa Arafa huku Ali (a.s.) akiwa amemwelekea, nasi tukiwa pamoja naye, Mtume alimwashiria Ali (a.s.) na kumwambia: 'Ewe Ali sogea karibu nami.' Akasogea karibu yake, akasema: 'Weka kitanga chako katika kitanga changu.' Akashika kitanga chake na kusema: 'Ewe Ali, mimi na wewe tumeumbwa kutokana na mti 18 19

An-Nihayyah 1: 333. Sahih Muslim 2: 726. Daaimul-Islam 1: 319. 10


Hija ya Kuaga

mmoja, mimi ndio shina lake na wewe ndio matawi yake, na Hasan na Husain ndio vijitawi vyake, na yeyote atakayeshikilia kijitawi miongoni mwa vijitawi vyake, Mwenyezi Mungu atamwingiza peponi kwa rehema zake."'20 6. Sheikh Tusiy amepokea kwa njia yake kutoka kwa Jabir bin Abdullah al-Ansariy kuwa hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) alitoa neno lake huko Arafa, licha ya kwamba neno hili limo kwa ujumla ndani ya hotuba yake mashuhuri, lakini tunalinukuu ili kutilia mkazo na kukamilisha. Kisha pia amepokea riwaya nyingine inayosisitiza kuwa neno hili alilitoa huko Mina: Jamaah ametupa habari kutoka kwa Abul-Mufadhali, amesema: Walitupa habari Abu Ja'far Muhammad bin Jarir Tabari kwa kusoma, na Ali bin Muhammad bin Hasan bin Kasi an-Nakhaiy, walisema: Ametusimulia Ahmad bin Yahya bin Zakariya alAwdiy as-Sufiy, amesema: Alitusimulia Hasan bin Husain – yaani al-Ar'niy – alisema: Amenisimulia Yahya bin Ya'la kutoka kwa Abdullah bin Musa at-Taymiy, kutoka kwa Abu Zubair, kutoka kwa Jabir bin Abdullah al-Ansariy, amesema: "Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) katika Hijja ya Kuaga huku goti langu likiwa limegusana na goti lake, akisema: 'Msirejee kwenye ukafiri baada yangu, mkaanza kuuwana ninyi kwa ninyi, hakika kama mtafanya hivyo basi mtakuja nitambua katika safu nyingine."21 7. al-Bayhaqiy amepokea kwa njia aliyoitaja, kutoka kwa Abdurahman bin Yaamur ad-Dayliy, amesema: Nilikuja kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) akiwa Arafa, likamfikia kundi la mal cha Tusiy: 611. Biharul-An'war 15: 20 na Juz. 65. Ameipokea pia Ibn al-MughazaA liy ndani ya al-Manaqib: 90 na 297, na katika at-Taraif: 111. Na pia kaipokea Ibnu Asakir ndani ya Tarikh Madinatud-Damashqi 42: 64 – 66. 21 Amal cha Tusiy: 503. Biharul-An'war 32: 294 na Uk. 363. Majmaul-Bayan cha Tabarasiy 9: 72. Tafsiru Furat: 280. 20

11


Hija ya Kuaga

Masahaba zake, wakamwamrisha mmoja wao akanadi: "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Hijja inatekelezwaje?" Akamwamuru mtu akanadi: "Hijja ni siku ya Arafa, atakayekuja usiku wa Arafa kabla ya swala ya Subhi bila shaka Hijja yake imetimia. Siku za Mina ni tatu: Lakini mwenye kufanya haraka katika siku mbili si dhambi juu yake." Kisha alifuata mtu mwingine naye akanadi kama hivyo."22

22

As-Sunanul-Kubra 7: 378. 12


Hija ya Kuaga

HOTUBA YA MTUKUFU MTUME WA MWENYEZI MUNGU (SAWW) SIKU YA ARAFA

I

kiwa ni wakati wa dhuha mwezi tisa Dhulhaji, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) alitulia katika hema lake alilowekewa huko Namra karibu na Arafa, akiwa ameshakoga na kujiandaa kwa ajili ya amali za siku hii. Baada ya jua kukengeuka Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) alitoka ndani ya hema lake na kwenda kuwahutubia watu.

Katika hadithi sahihi ya Muawiyya bin Ammar kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s.) anayozungumzia matendo ya ibada ya Hijja ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww), kuna ishara juu ya hotuba hii, amesema (a.s.): "Akawapa mawaidha watu na akawaamrisha na kuwakataza (lakini hakutaja hotuba yenyewe).23Hotuba hii imepokewa kwa muhtasari ndani ya Sahih Muslim na vyanzo vingine kwa mujibu wa riwaya ya Jabir.24 Hakika hotuba hii ni mashuhuri na maarufu ndani ya vitabu vya makundi mawili: Sunni na Shia, na katika medani ya fasihi ina hadhi kubwa kutokana na utamu wa maneno yake na ukubwa wa maana zake. Tofauti iliyopo kuhusu hotuba hii ni juu ya sehemu aliyoitolea na wakati aliotoa hotuba hii, je Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) alitoa hotuba hii huko Arafa au Mina? Na ilikuwa ni siku gani kati ya siku za Mina? 23 24

Al-Kafiy 4: 247. Tahdhibul-Ahkam 5: 456. Sahih Muslim 2: 726. Sunanu Abi Daud: 294 – 296. Sunan Ibnu Majah 2: 1022. as-Sunanul-Kubra cha al-Bayhaqiy 6: 14 – 19. al-Musannaf cha Ibnu Abi Shaybah 4: 423 – 426. 13


Hija ya Kuaga

Wapo waliyoitaja bila kutaja ni sehemu gani, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) alihutubia hotuba hii, mmoja wao ni Shaabatul-Harraniy ndani ya kitabu Tuhaful-Uquul25, mwingine ni al-Jahidh ndani ya kitabu al-Bayan Wat-Tibyan26, na Ibnu Abdu Rabbih al-Undlusiy ndani ya kitabu al-Aqdu al-Faridu27, bali wao wameitaja kwa anwani isemayo: "Hotuba ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) katika Hijja ya Kuaga." Na wapo wengine wameitaja na kusema kuwa ni hotuba ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) aliyoitoa huko Arafa, hao ni kama vile Ibnu Hisham ndani ya kitabu as-Siratun-Nabawiyyah, an-Nasai ndani ya as-Sunanul-Kubra,28 na Muslim ndani ya Sahih yake kama tulivyotaja, na wala hajataja hotuba yake (saww) ya huko Mina. Kundi la tatu ni wale walioitaja na kusema kuwa ni hotuba ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) aliyoitoa huko Mina, kama vile Bukhari ndani ya Sahih yake kutoka kwa Ibnu Abbas, amesema: "Hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) aliwahutubia watu siku ya kuchinja."29 Na pia al-Baghawi ndani ya kitabu MaswabihusSunnah,30 na hajataja hotuba yake (saww) ya huko Arafa. Na hakika al-Haythamiy ameitaja kwa njia kadhaa tofauti chini ya anwani: "Mlango wa Hotuba huko Hijja."31 Ibnu Kathir amepokea riwaya kadhaa kuhusu hotuba yake (saww) siku ya Iddi, na hotuba hii tukufu ameitaja Tabari na Ibnu Tuhaful-Uquul: 30 – 34. al-Bayan Wat-Tibyan: 228 27 al-Aqdu al-Faridu 4: 57 – 58. 28 as-Siratun-Nabawiyyah ya Ibnu Hisham 4: 250 – 252. Sunanul-Kubra 2: 421. 29 Sahih Bukhar 2: 231. Fat'hul-Bariy Fisharhi Sahihil-Bukhari 4: 2260. 30 Maswabihus-Sunnah 2: 272). 31 Majmauz-Zawaid 3: 585 – 599. 25 26

14


Hija ya Kuaga

Athiri pia.32 Na katika Kanzul-Ummal na at-Tabaqatul-Kubra hotuba hii imepokewa kwa riwaya kadhaa tofauti.33 Ibnu Majjah amepokea riwaya inayosema kuwa (saww) alitoa hotuba hiyo katika Hijja ya Kuaga, na nyingine inasema aliitoa huko Arafa, na ya tatu inasema aliitoa siku ya kuchinja baina ya Jamarati.34 Na katika baadhi ya riwaya imetajwa kuwa: Sura hii: "Itakapokuja nusura ya Mwenyezi Mungu na ushindi." (Sura Nasru: 1), ilimteremkia Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) akiwa katikati ya siku za Tashriq, hivyo akajua ni Hijja ya kuaga, akampanda mnyama wake, akamhimidi Mwenyezi Mungu na kumtukuza, kisha akasema: "Enyi watu, kila damu iliyomwagika zama za ujahiliya haina fidia."35 Kuna sehemu Ibnu Kathir kaitaja kwa anwani ya "Hotuba ya Mtume wa Mwenyezi Mungu huko Arafa" –kwa mujibu wa riwaya ya Muslim – na kuna sehemu nyingine kaitaja kwa anwani ya: "Hotuba ya Mtume wa Mwenyezi Mungu huko Mina" – kwa mujibu wa riwaya ya Bukhari.36 Al-Waqidiy ndani ya kitabu al-Maghaziy ameorodhesha vipengele vya hotuba hii ndani ya hotuba aliyoitaja kama "Hotuba ya Mtu l-Bidayah Wan-Nihayah 5: 185 – 189. Tarikhul-Umam Wal-Muluk 3: 150 – 152. alA Kamil Fitarikh 2: 302. 33 Kanzul-Ummal 5: 286 – 297. at-Tabaqatul-Kubra cha Ibnu Saad 2: 183 – 186. 34 Sunan Ibnu Majah 2: 1015 – 1016. 35 Al-Khiswal: 486. Biharul-An'war 74: 118. 36 As-Siratu an-Nabawiyyah cha Ibn Kathir Juz. 4, Uk. 387 – 392. Jamharat Khutabul-Arab Juz. 1, Uk. 155 – 158, Hotuba ya 13. Taarikh Ya'qubiy Juz. 2, Uk. 109 – 112. Sharhu Nahjul-Balagha cha Ibn Abil-Hadid Juz. 1, Uk. 126 – 127. As-Siratu an-Nabawiyyah cha Halbiy Juz. 3, Uk. 327. As-Sunan al-Kubra Juz. 7, Uk. 17, na Juz. 8, Uk. 111. DalailunNubuwwah cha Bayhaqiy Juz. 5, Uk. 441 – 442. Tafsirul-Qummiy Juz. 1, Uk. 171. Biharul-An'war Juz. 37, Uk. 836. 32

15


Hija ya Kuaga

me (saww) huko Makka siku ya kuikomboa Makka."37 Kadhalika kaitaja hivyo al-Maqriziy ndani ya kitabu Imtaul-Asmai.38 Tambua kuwa licha ya kuwepo tofauti baina ya wale walioitaja hotuba husika kwa muhtasari, wale walioitaja kwa urefu, au baina ya wale walioitaja kama hotuba ya Mtume katika Hijja ya Kuaga, au kwa anwani ya Hotuba yake huko Arafa, au kwa anwani ya hotuba yake huko Mina siku ya kuchinja, au katikati ya siku za Tashriq, lakini maelezo yake yote yanakaribiana kiujumbe na kimaana. Linalodhihiri wazi ni kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww)alitoa hotuba hii huko Arafa, lakini kutokana na umuhimu na ukubwa wa maana na ujumbe uliomo ndani ya hotuba hii, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) alirudia tena madhumuni yake na vipengele vyake katika matukio mengine, visimamo na sehemu nyingine katika siku ya kuchinja au mwezi kumi na moja, hivyo inahesabika kuwa ni hotuba kamili na neno timilifu na msingi imara wa umoja wa Waislamu na ni ubainifu wa mambo ya dini yao na dunia yao. Hata kama vyanzo tulivyovitaja vimetofautiana katika baadhi ya matamshi yake, lakini tofauti husika haidhuru maana na ujumbe, na yafuatayo ni maelezo ya hotuba yenyewe: "Himidi ni ya Mwenyezi Mungu, tunamhimidi Yeye, tunamtaka msaada Yeye, tunamuomba msamaha Yeye na tunatubu Kwake. Tunajilinda kwa Mwenyezi Mungu dhidi ya mabaya ya nafsi zetu na dhidi ya maovu ya matendo yetu. Aongozwaye na Mwenyezi Mungu hana wa kumpoteza, na apotezwaye hana wa kumuongoza. Nashahidilia kuwa hapana mungu isipokuwa Allah Mmoja wa pekee asiye na mshirika, na nashahidilia kuwa hakika Muhammad ni mja wake na Mtume wake. Enyi waja wa Mwenyezi Mungu! Nawausieni kumcha Mwenyezi Mungu na ninawahimiza kumtii Yeye katika 37 38

Al-Maghaziy 2: 836. Imtaul-Asmai 1: 392, na Juz. 2: 111 – 112. 16


Hija ya Kuaga

amali zenu, na ninamuomba Mwenyezi Mungu lile ambalo ni kheri. "Ama baad, enyi watu! Sikilizeni ninayowabainishia, kwani hakika mimi sijui kama nitaweza kukutana nanyi tena sehemu hii baada ya mwaka huu. Enyi watu! Hakika damu zenu na heshima yenu ni haramu juu yenu mpaka mtakapokutana na Mola wenu, kama ilivyo haramu katika siku yenu hii, ndani ya mwezi wenu huu na ndani ya mji wenu huu. Bila shaka nimefikisha, ewe Mwenyezi Mungu kuwa shahidi. "Yeyote mwenye amana basi aifikishe kwa muhusika, na hakika riba ya zama za Ujahiliyah imefutwa (imeharamishwa), na hakika riba ya kwanza kabisa ninayoanza kuifuta (kuiharamisha) ni riba ya Abbas bin Abdul-Mutalib. Na hakika umwagaji damu wa zama za Ujahiliyah umefutwa (umeharamishwa), na hakika damu ya kwanza ninayoanza kuifuta (kuiharamisha) ni damu ya Amir bin Rabiah bin al-Harith bin Abdul-Muttalib. Na hakika matendo ya Kijahiliyya yamefutwa (yameharamishwa) isipokuwa kuitunza Kaaba, huduma ya maji kwa mahujaji, na kumuuwa aliyeuwa kwa kukusudia, ama aliyeuwawa kwa namna inayofanana na makusudi ni yule aliyeuwawa kwa fimbo na jiwe, fidia yake ni ngamia mia moja, na kiasi chochote kitakachozidi kinazingatiwa kuwa ni miongoni mwa matendo ya Kijahiliyyah. "Enyi watu! Hakika shetani amekata tamaa ya kuabudiwa ndani ya ardhi yenu hii, lakini yupo radhi kutiiwa katika mengine yasiyokuwa hayo miongoni mwa matendo yenu mnayoyadharau. Enyi watu! Hakika kuakhirisha miezi ni kuzidi katika kukufuru, kwa hayo hupotezwa waliokufuru. Wanauhalalisha mwaka mmoja na kuharamisha mwaka mwingine, ili wafanye kuwa sawa idadi ya ile miezi aliyoitukuza Mwenyezi Mungu, kwa hivyo huhalalisha alivyoviharamisha Mwenyezi Mungu. Na hakika wakati huzunguka kama umbo lake tangu Mwenyezi Mungu alipoumba mbingu na ardhi, 17


Hija ya Kuaga

na hakika idadi ya miezi kwa Mwenyezi Mungu ni miezi kumi na mbili katika hukumu ya Mwenyezi Mungu tangu alipoumba mbingu na ardhi. Katika hiyo iko minne mitakatifu, mitatu imefuatana na mmoja uko peke yake: Dhul-Qaadah, Dhulhaji, Muharam na Rajab uliyopo baina ya Jumada na Shaaban. Bila shaka nimefikisha, ewe Mwenyezi Mungu kuwa shahidi. "Enyi watu! Hakika wake zenu wana haki juu yenu, nanyi mna haki juu yao. Haki yenu juu yao ni kwamba wasimlaze yeyote vitandani kwenu na wala wasimwingize ndani ya majumba yenu yeyote mnayemchukia isipokuwa kwa idhini yenu, na wala wasifanye uchafu (wasizini), kama watatenda lolote kati ya hayo basi hakika Mwenyezi Mungu amewapeni idhini ya kuwadhikisha, kuwahama vitandani na kuwapiga pigo lisilo na madhara, wakiacha na wakiwatiini ni juu yenu kuwalisha na kuwavisha kwa wema, kwani mliwachukua kwa amana ya Mwenyezi Mungu na mkahalalisha tupu zao kwa Kitabu cha Mwenyezi Mungu, hivyo mcheni Mwenyezi Mungu juu ya wanawake na wausieni kheri. "Enyi watu! Hakika waumini ni ndugu, na si halali kwa muumini kutumia mali ya nduguye isipokuwa kwa ridhaa yake. Bila shaka nimefikisha, ewe Mwenyezi Mungu kuwa shahidi. Msirejee kwenye ukafiri baada yangu mkaanza kuuwana ninyi kwa ninyi, kwani hakika mimi nimewaachieni lile ambalo kama mtashikamana nalo kamwe hamtapotea baada yangu: Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Kizazi changu Ahlul-Baiti wangu. Bila shaka nimefikisha, ewe Mwenyezi Mungu kuwa shahidi. "Enyi watu! Hakika Mola wenu ni Mmoja na hakika baba yenu ni mmoja, nyote mwatokana na Adam na Adam atokana na udongo, hakika aliye mbora kati yenu mbele ya Mwenyezi Mungu ni yule aliye mchamungu kuliko wote. Mwarabu hana ubora wowote 18


Hija ya Kuaga

juu ya asiyekuwa mwarabu isipokuwa kwa uchamungu, bila shaka nimefikisha." – Wakasema: Ndio. Akasema: "Aliyepo amfikishiye asiyekuwepo. Enyi watu! Hakika Mwenyezi Mungu amempa kila mrithi fungu lake kutoka katika mirathi, na mrithiwa hana ruhusa ya kuusia zaidi ya theluthi. Mtoto ni wa kitanda na mzinifu lake ni jiwe, na yeyote atakayejinasibisha na asiyekuwa baba yake, na yeyote atakayewatawala wasiokuwa watumwa wake, laana ya Mwenyezi Mungu, Malaika na watu wote iwe juu yake, na Mwenyezi Mungu hatakubali kutoka kwake toba yoyote wala fidia yoyote. Wasalam Alaykum Warahmatullahi." Hii ndio matini ya hotuba tukufu ya Mtume kama ilivyoandikwa ndani ya kitabu Tuhaful-Uquul. Hakika lililo wajibu juu yetu hapa ni kugusia nukta muhimu zilizopatikana ndani ya hotuba hii, nazo ni kama zifuatavyo: 1. Kumhimidi Mwenyezi Mungu, kumtukuza, kumsifu, kumuomba maghufira, kujilinda kwake na kutaja shahada mbili. 2. Kuwaasa waja wa Mwenyezi Mungu kumcha Mwenyezi Mungu, kutekeleza maamrisho yake na kujiepusha na maasi. 3. Kuwahimiza Waislamu kusikiliza maneno yake na kuyafahamu. 4. Kuharamisha kumwaga damu ya Waislamu, kuvunja heshima yao na ya mali yao, na kusisitiza kuheshimu amana. 5. Kuharamisha riba na visasi vya kijahiliyyah, na kufuta kabisa matendo ya kijahiliyyah. 19


Hija ya Kuaga

6. Kusisitiza baadhi ya hukumu, adhabu na fidia ndani ya sheria ya Kiislamu, na kuwafikishia watu sheria hizo. 7. Kubatilisha uakhirishaji wa miezi, kisha kutaja haki za wanawake, na kukataza kudhulumu kwa njia ya usia. 8. Kusisitiza msingi wa udugu wa Kiislamu. 9. Kulazimisha kushikamana na vizito viwili. 10. Kupinga ubaguzi, na kukiri kuwa ubora unaokubalika baina ya Waislamu ni ule utokanao na msingi wa uchamungu. Ukiachilia mbali hotuba hii imepokewa pia kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) alitoa hotuba fupi wakati wa kuzama jua akiwa Arafa. Vyanzo vyote vilivyopokea hotuba hiyo fupi vimekubaliana kuwa katika usiku huo wa Arafa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) aliuombea ummah wake maghufira na rehema, hivyo akakithirisha kuomba, ndipo Mwenyezi Mungu akamshushia wahyi kuwa hakika mimi nimeshatenda, isipokuwa kama watadhulumiana wao kwa wao.39 Pia katika baadhi ya vitabu imepokewa hotuba aliyoitoa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) huko Arafa kuhusu heshima ya hujaji mbele ya Mwenyezi Mungu, nasi tutaileta kwa ajili ya kukamilisha faida. Na inadhihiri mwanzoni mwa hotuba hii kuwa hotuba hii aliitoa usiku wa Arafa baada ya kusimama hapo, ilihali hotuba yake mashuhuri aliitoa baada ya kukengeuka jua huko Batni Irnah, nalo ni eneo jingine kabisa lililopo pembeni mwa Arafa. Imepokewa ndani ya kitabu Daaimul-Islam kuwa: Imepokewa kutoka kwa Ali (as) kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) ali39

As-Sunanul-Kubra 5: 118. Na 7: 257. 20


Hija ya Kuaga

pohiji Hija ya Kuaga, alisimama Arafa na akawageukia watu kwa uso wake na kusema: "Karibuni enyi wageni wa Mwenyezi Mungu. – Alisema mara tatu – ambao wanapoombwa hutoa, na hufidiwa kile watoacho, na huwekewa akiba huko Akhera mema elfu moja kwa kila dirhamu moja watoayo." Kisha akasema: "Enyi watu! Je niwapeni habari njema?" Wakasema: "Ndio, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu!" Akasema: "Unapofika usiku huu Mwenyezi Mungu hujifakharisha kwa Malaika kupitia watu ambao huwa hapa, husema: 'Enyi Malaika wangu, watazameni waja Wangu wanaume kwa wanawake, wamekuja Kwangu kutoka pande za dunia wakiwa wamejaa vumbi na mchoko, hivi mnajua wanachoomba?" Malaika husema: "Ewe Mola Wetu, wanakuomba maghufira." Mwenyezi Mungu husema: "Nawathibitishieni hakika mimi nimewasamehe wao. Na wanaondoka kutoka hapa wakiwa wamefutiwa dhambi zilizotangulia."40 Na imepokewa ndani ya kitabu al-Mustadrak kutoka ndani ya kitabu Lubil-Libab cha al-Qutbi ar-Rawandiy, kutoka kwa Mtukufu Mtume (saww) kuwa alisema: "Unapofika usiku wa Arafa Mwenyezi Mungu huwaambia Malaika Wake: 'Watizameni waja Wangu wanaume kwa wanawake,wakiwa wamejawa na vumbi na mchoko, wamenijia kutoka kila njia ya mbali licha ya kwamba hawajaona kwa macho rehema yangu (pepo) wala adhabu yangu (moto). Nawathibitishia enyi Malaika Wangu kuwa hakika mimi nimewasamehe wote, hujaji na asiye hujaji.' Haijaonekana siku yenye watu wengi wenye kutolewa motoni kama siku ya Arafa na usiku wake."41 Kisha Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) alikithirisha dua na maombi kwa Mwenyezi Mungu hapo Arafa, hakukomea kuomba yeye tu bali aliwahimiza pia Waislamu kuomba, kufanya dhikri na kurejea kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. 40 41

Daaimul-Islam 1: 293. Biharul-An'war 96: 49. Mustadrakul-Wasail 8: 36. Mustadrakul-Wasail 10: 32. 21


Hija ya Kuaga

HOTUBA YA MTUME WA MWENYEZI MUNGU (SAWW) SIKU YA KUCHINJA

B

aadhi ya waandishi akiwemo Bukhari na Nasaiy wameitaja hotuba ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) ya Siku ya Arafa kuwa ni hotuba ya Siku ya Kuchinja, kama ambavyo pia baadhi ya wanahistoria wameitaja hotuba nyingine kwa jina la hotuba ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) aliyoitoa huko Mina, na ujumbe wake unakaribiana na ule wa hotuba yake ya Arafa, lakini wao wameeleza kuwa ni hotuba yake aliyoitoa huko Mina. Miongoni mwa wanahistoria hawa ni Muhammad bin Saad ndani ya kitabu chake at-Tabaqat, amesema: "Alitupa habari Abdul-Wahab bin Atai, alisema: Alitupa habari Said bin Abu Arubah, kutoka kwa Qatadah, kutoka kwa Shahri bin Hawshab, kutoka kwa Abdurahman bin Ghanam, kutoka kwa Amru bin Kharijah, alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) alituhutubia huko Mina nami nikiwa chini ya shingo ya ngamia wake huku ngamia huyo akirudisha chakula tumboni mwake na mate yake yakidondokea begani mwangu, alisema: 'Hakika Mwenyezi Mungu amempa kila mwanadamu fungu lake toka katika mirathi, hivyo mrithi haruhusiwi kukhalifu usia. Tambueni hakika mtoto ni wa kitanda na mzinifu lake ni jiwe. Tambueni kuwa yeyote atakayejinasibisha na asiyekuwa baba yake, au kuwatawala wasiokuwa watumwa wake bila wao kuridhia, laana ya Mwenyezi Mungu, Malaika na watu wote itakuwa juu yake.'" Amesema pia: "Alitupa habari Sulayman bin Abdurahman adDamashqiy: Alitupa habari Walid bin Muslim: Alitupa habari Hisham bin al-Ghazi: Alinipa habari Nafiu kutoka kwa Ibnu Umar, kwamba Mtukufu Mtume (saww) alisimama baina ya nguzo tatu 22


Hija ya Kuaga

Siku ya Kuchinja katika Hija yake aliyohiji, akawaambia watu: "Ni siku gani hii?" Wakasema: "Ni Siku ya Kuchinja." Akasema: "Ni mji gani huu?" Wakasema: "Ni mji Mtakatifu." Akasema: "Ni mwezi gani huu?" Wakasema: "Ni mwezi Mtukufu." Akasema: "Hii ni siku ya Hija kubwa, hivyo damu zenu, mali zenu na heshima yenu ni haramu juu yenu kama ilivyo haramu juu ya mji wenu huu, ndani ya mwezi huu na katika siku hii." Kisha akasema: "Je nimefikisha." Wakasema: "Ndio." Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) akawa anasema: "Ewe Mwenyezi Mungu kuwa shahidi." Kisha akawaaga watu, ndipo wakasema: "Hii ni Hija ya kuaga." Ibnu Saad amepokea hotuba mfano wa hiyo kwa njia nyingine, amesema: Alitupa habari Khalfu bin Walid al-Azdiy: Alitupa habari Yahya bin Zakariya bin Abu Zaidah: Alinisimulia Abu Malik alAshjaiy: Alinisimulia Nubit bin Sharit al-Ashjaiy, alisema: Hakika mimi nilikuwa nimepanda mnyama mmoja pamoja na baba yangu katika Hijja ya Kuaga pindi Mtukufu Mtume (saww) alipoongea, ndipo nika simama nyuma ya kipando na nikaweka miguu yangu juu ya mabega ya baba yangu, nikamsikia Mtume akisema: "Ni siku gani iliyo tukufu zaidi?" Wakasema: "Ni Siku hii." Akasema: "Ni mwezi gani ulio mtukufu zaidi?" Wakasema: "Ni mwezi huu." Akasema: "Ni mji gani ulio mtukufu zaidi?" Wakasema: "Ni mji huu." Akasema: "Hakika damu zenu, mali zenu na heshima yenu ni haramu juu yenu kama ilivyo haramu katika siku yenu hii, katika mwezi wenu huu, katika mji wenu huu. Je nimefikisha?" Wakasema: "Ndio." Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) akasema: "Ewe Mwenyezi Mungu kuwa shahidi. Ewe Mwenyezi Mungu kuwa shahidi. Ewe Mwenyezi Mungu kuwa shahidi." Pia amesema: Alitupa habari Yunus bin Muhammad al-Muaddib: Alitupa habari Rabiat bin Kulthum bin Jabar: Alinisimulia baba yangu kutoka kwa Abu Ghadiyah ambaye ni mmoja kati ya Masahaba 23


Hija ya Kuaga

wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, alisema: "Alituhutubia Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) siku ya Aqabah, akasema: 'Enyi watu! Hakika damu zenu na mali zenu ni haramu juu yenu mpaka mtakapokutana na Mola Wenu, kama ilivyo haramu katika siku yenu hii, ndani ya mwezi wenu huu na ndani ya mji wenu huu. Je nimefikisha?' Tukasema: Ndiyo, akasema: 'Ewe Mwenyezi Mungu kuwa shahidi. Ah, msirudi katika ukafiri baada yangu, hatimaye mkaanza kuuwana ninyi kwa ninyi."' Kisha Ibnu Saad amesema: Alitupa habari Hashim bin al-Qasim: Alitupa habari Akrimah bin Ammar: Alinisimulia al-Harmas bin Ziyad al-Bahiliy, alisema: "Nilikuwa nimepanda mnyama mmoja pamoja na baba yangu Siku ya Kuchinja huku Nabii wa Mwenyezi Mungu akiwahutubia watu akiwa juu ya ngamia wake huko Mina." Na pia amesema: Alitupa habari Hisham Abul-Walid at-Tayalisiy: Alitupa habari Akrimah bin Ammar: Alinisimulia al-Harmas bin Ziyad al-Bahiliy, alisema: "Aliondoka Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) huku baba yangu Murdu akiwa nyuma yake katika ngamia wake, nami nikiwa mtoto mdogo, nikamuona Mtukufu Mtume (saww) Siku ya Kuchinja akiwahutubia watu huko Mina akiwa juu ya ngamia wake al-Adhbau." Ni wazi kuwa maana ya hotuba hii ni sawa na maana ya hotuba tuliyoitaja mwanzo, na ambayo tumeonesha kuwa aliitoa huko Arafa, na inawezekana aliitoa tena Mina. Na katika al-Muswannaf ya Ibnu Abi Shaybah imepokewa kwa njia mbili kutoka kwa Mujahid na Masruq kuwa Mtukufu Mtume (saww) aliwahutubia Siku ya Kuchinja. Na katika as-Sunanul-Kubra imepokewa kutoka kwa watu wawili wa Bani Bakri, wamesema: "Tulimuona Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) akihutubia, ilikuwa ni katikati ya siku za Tashriq, na 24


Hija ya Kuaga

sisi tulikuwa kwenye kipando chake, nayo ndio hotuba ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) aliyohutubia huko Mina." Pia amesema: Alitupa habari Ali bin Ahmad bin Abdan: Alitoa habari Ahmad bin Ubaydus-Swaffar: Alitusimulia Abu Muslim Ibrahim bin Abdullah. Na alitupa habari Abu Nasri Umar bin AbdulAziz bin Umar bin Qatadah an-Nuumaniy: Alitoa habari Abu Amru Ismail bin Nujid as-Sulmiy: Alitoa habari Abu Muslim Ibrahim bin Abdullah al-Basriy: Alitusimulia Abu Asim kutoka kwa Rabiat bin Abdurahman bin Hasnu al-Ghanawiy: Alinisimulia Sarau binti Nabhani – Alikuwa ni mtunza Nyumba katika zama za ujahiliyyah – alisema: "Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) akisema katika Hijja ya Kuaga: 'Hivi mnajua ni siku gani hii?' Na ilikuwa ni siku ile ambayo wao huiita kama Siku ya vichwa. "Walisema: 'Mwenyezi Mungu na Mtume Wake ndio wajuao zaidi.' Mtukufu Mtume (saww) akasema: 'Hii ni siku ya katikati ya siku za Tashriq. Hivi mnajua ni mji gani huu?' Walisema: 'Mwenyezi Mungu na Mtume Wake ndio wajuao zaidi.' Mtukufu Mtume (saww) akasema: 'Hii ni Mash'aru tukufu.' kisha akasema: 'Hakika sijui, lakini huenda nisikutane nanyi tena baada ya leo. Fahamuni kuwa hakika damu zenu, mali zenu na heshima yenu ni haramu juu yenu kama ilivyo haramu katika siku yenu hii na ndani ya mji wenu huu, mpaka mtakapokutana na Mola Wenu, na Yeye atawaulizeni kuhusu amali zenu, hivyo aliye karibu amfikishiye yule aliye mbali, je nimefikisha?' Tulipofika Madina hakuishi isipokuwa siku chache akawa amefariki (saww)." Kisha alisema: "Ameipokea Muhammad bin Sattar bin Bashar kutoka kwa Abu Asim kwa sanadi hii, alisema:'Alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) alituhutubia Siku ya vichwa."'42 42

As-Sunanul-Kubra 7: 330. 25


Hija ya Kuaga

Na katika Musnad Ahmad bin Hanbal imepokewa kutoka kwa Abu Nadhrah, amesema: "Alinisimulia mtu aliyesikia hotuba ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) katikati ya siku za Tashriq, aliposema: 'Enyi watu! Hakika Mola Wenu ni mmoja, na hakika baba yenu ni mmoja. Fahamuni kuwa mwarabu si mbora juu ya asiyekuwa mwarabu, wala asiyekuwa mwarabu si mbora juu ya mwarabu, mwekundu si mbora juu ya mweusi wala mweusi si mbora juu ya mwekundu, isipokuwa kwa takwa, je nimefikisha?' Wakasema: 'Mtume wa Mwenyezi Mungu amefikisha...mpaka mwisho wa hadithi."'43 Imepokewa ndani ya kitabu Daaimul-Islam kutoka kwa Imam Ja'far as-Sadiq (as) kutoka kwa Imam Ali (as) amesema: "Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) akitoa hotuba Siku ya kuchinja, nilimsikia akisema: 'Hii ni siku ya Thajju na Ajju: Thajju ni damu mnazomwaga humu, hivyo yeyote atakayekuwa na nia safi basi tone lake la kwanza litakuwa ni kafara ya kila dhambi. Ajju ni dua, hivyo muombeni Mwenyezi Mungu. Naapa kwa yule ambaye nafsi ya Muhammadi imo mikononi mwake, hatatoka yeyote sehemu hii bila kufutiwa dhambi zake isipokuwa yule mwenye madhambi makubwa mwenye kuendelea kutenda dhambi, ambaye haiamrishi nafsi yake kuacha kutenda dhambi hizo."' – Na kutokana na sentensi: "Sehemu hii" inaaminiwa kuwa hii ndio hotuba aliyoitoa hapo Mina Siku ya kuchinja katika Hijja ya kuaga, kama inavyoonesha sentensi hiyo. Lakini inawezekana aliitoa siku ya Iddul-Udh'ha huko Madina Tukufu katika moja ya miaka ya kazi yake, na makusudio ya "Sehemu hii" itakuwa ni sehemu waliosalia Iddi, alipotolea hotuba na walipokusanyika Waislamu. Lakini riwaya za al-Bayhaqiy zinatamka wazi kuwa aliitoa huko Mina Siku ya kuchinja katika Hijja ya kuaga. 43

usnad Ahmaf bin Hanbal 9: 127. Naylul-Awtar 5: 82, Mlango wa hotuba ya katikati M ya siku za Tashriq, Hadithi ya 3. 26


Hija ya Kuaga

Al-Bayhaqi amepokea kwa njia yake kutoka kwa Abubakrah kuwa alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) alituhutubia Siku ya kuchinja akasema: "Msirudie kuwa makafiri baada yangu mkaanza kukatana shingo ninyi kwa ninyi."Na kuna riwaya nyingine kwa njia yake kutoka kwa al-Harmasi bin Ziyad kuwa alisema: Nilimuona Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) akiwahutubia watu huko Mina Siku ya Udh'ha akiwa juu ya kipando chake, na mimi nilikuwa mdogo nikiwa nimenyanyuliwa na baba yangu. "Na kuna riwaya nyingine kwa njia yake kutoka kwa Abu Amamah, amesema nilimsikia Abu Amamah akisema: "Nilisikia hotuba ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) huko Mina Siku ya kuchinja."Na kuna riwaya nyingine kwa njia yake kutoka kwa Rafiu bin Umar na al-Mazniy, amesema: "Nilimuona Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) akiwahutubia watu huko Mina wakati wa dhuha akiwa juu ya baghala, huku watu wakiwa wamesimama na wengine wamekaa chini." As-Saduqu amepokea kwa njia yake kutoka kwa Abu Amamah kuwa alisema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) akisema: "Enyi watu! hakika hakuna Nabii baada yangu wala umma baada yenu ninyi, hivyo mwabuduni Mola wenu na salini Swala zenu tano, fungeni mwezi wenu na nendeni kuhiji katika Nyumba ya Mola Wenu, toeni zaka ya mali yenu kwa mapenzi ya nafsi zenu na watiini wenye mamlaka na jambo lenu, mkifanya hayo mtaingia katika pepo ya Mola Wenu."44 Riwaya hii hata kama haina dalili inayoonesha kuwa maneno haya yalitoka kwa Mtukufu Mtume (saww) katika Hijja yake ya mwisho (ya kuaga) lakini riwaya mbili nyingine zinaonesha hivyo, kwani Ahmad bin Hanbal ndani ya Musnad yake na pia al-Hakim ndani ya Mustadrak, wameongeza: "Abu Amamah anasema: 'Ni44

Al-Khiswal: 322. 27


Hija ya Kuaga

limsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) akiwa juu ya ngamia akiwahutubia watu katika Hijja ya kuaga huku kaweka miguu yake juu ya ngazi ya kupandia mnyama. Nilimsikia akisema: "Hivi mnanisikia?" Akasema mtu mmoja aliyekuwa mwishoni kabisa mwa watu: "Unasemaje?" Akasema: "Mwabuduni Mola Wenu...." mpaka mwisho wa hadithi.45

45

Musnad Ahmad bin Hanbal 8: 274; al-Mustadrak Alas-Sahihayni 1: 547. 28


Hija ya Kuaga

HOTUBA YAKE (SAWW) ALIYOITOA KATIKA MSIKITI WA AL-KHAYFU

A

l-Kulayniy amepokea kutoka kwa jamaa zetu kadhaa, kutoka kwa Ahmad bin Muhammad bin Issa, kutoka kwa Ahmad bin Muhammad bin Abu Nasri, kutoka kwa Aban bin Uthman, kutoka kwa Ibnu Abi Ya'fur, kutoka kwa Abu Abdullah (a.s.) kuwa: "Hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) aliwahutubia watu katika msikiti wa al-Khayfu, alisema: 'Mwenyezi Mungu ampe uzuri mja ambaye ataisikiliza kauli yangu na kuielewa, akaihifadhi na kumfikishia yule ambaye hajaisikia, kwani huenda mwenye kubeba elimu si aalimu, na huenda mwenye kubeba elimu anaipeleka kwa aliye na elimu zaidi yake. Hakika Moyo wa Mwislamu haukosi mambo matatu: Kutenda amali kwa ikhlasi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kutoa nasaha kwa viongozi wa Waislamu na kushikamana na jamaa yao, kwani hakika ulinganio wao umewazunguka kwa nyuma. Waislamu ni ndugu, wanatoleana damu, na kwa dhima yao hupata heshima yule aliye mnyonge kati yao."' Kisha alisema: Na pia kaipokea hadithi mfano wa hiyo kutoka kwa Hammad bin Uthman, kutoka kwa Aban, kutoka kwa Ibnu Abi Ya'fur, lakini kwa nyongeza ya: "Na wao ni nguvu moja dhidi ya yule asiyekuwa wao." na ametaja katika hadithi yake kuwa alitoa hotuba hiyo katika Hijja ya kuaga huko Mina katika msikiti wa alKhayfu.46Ameipokea Sheikh Abu Abdullah al-Mufid katika al-Amal kwa sanadi nyingine ambayo kaitaja kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s.) kuwa alisema:"Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) alitoa hotuba huko Mina, akasema..."47Aliipokea pia Sheikh as-Saduq kutoka kwa 46 47

Al-Kafiy 1: 403. Al-Amal cha al-Mufid: 186; Biharul-An'war 2: 148. 29


Hija ya Kuaga

Muhammad bin Musa bin al-Mutawakil, amesema: "Ametusimulia Ali bin al-Husayni as-Saad Abady, amesema: Ametusimulia Ahmad bin Muhammad bin Khalid, kutoka kwa Ahmad bin Muhammad bin Abu Nasri al-Bazantiy, kutoka kwa Hammad bin Uthman, kutoka kwa Abu Abdullah (a.s.), na ameipokea kwa sanadi nyingine ndani ya al-Khiswal,48 na pia imepokewa ndani ya Jamharatu KhutabulArab49. Na ameipokea Ibnu Majah ndani ya as-Sunan kwa sanadi yake aliyoitaja kutoka kwa Jubair bin Mut'im, kuwa alisema: "Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) alisimama huko al-Khayfu alipotoka Mina, akasema: 'Mwenyezi Mungu ampe uzuri ..... – mpaka akasema - kwani hakika ulinganio wao umewazunguka kwa nyuma,"' ama sehemu ya mwanzo tu ya hadithi ameitaja ndani ya hadithi tofauti.50 Al-Fayruz Abad amesema: Alirejea nyumbani kwake karibu na msikiti wa al-Khayfu, akatoa hotuba nzito kiasi kwamba sauti yake iliwafikia watu wote waliokuwa ndani ya mahema yao, na hii ni miongoni mwa miujiza ya unabii.51 Na katika Sunnan Abu Daud ameipokea kwa njia yake kutoka kwa Abdurahman bin Muadh at-Taymiy, amesema: Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) alituhutubia tukiwa huko Mina, kiasi kwamba masikio yetu yalifunguka hadi tukaweza kusikia aliyokuwa akisema nasi tukiwa ndani ya majumba yetu. Alianza kuwafundisha ibada yao mpaka akafika katika kipengele cha kumpiga mawe shetani, akaweka vidole shahada vyake na kusema: "Ni kwa changarawe za kutupa kwa vidole shahada."Kisha aliwaamuru Muhajirina waAl-Amal cha as-Saduq: 431, al-Khiswal: 149. Jamharatu Khutabul-Arab 1: 151, hotuba ya Mtukufu Mtume (saww) huko al-Khayfu, namba 5. 50 Sunan Ibnu Majah 2: 1015. 51 Sunan Ibnu Majah1: 84 – 85. 48 49

30


Hija ya Kuaga

kateremka mpaka mbele ya msikiti, na akawaamuru Ansari wakateremka mpaka nyuma ya msikiti, kisha baada ya hapo watu wengine wakateremka.52 Na katika al-Kafiy imepokewa kutoka kwa Muhammad bin alHasan kutoka kwa baadhi ya rafiki zetu, kutoka kwa Ali bin al-Hakam, kutoka kwa al-Hakam bin Miskini, kutoka kwa mtu mmoja Mkuraishi wa Makka, amesema: Sufyan at-Thauriy alisema: "Nisindikize kwa Ja'far bin Muhammad (a.s.)." Nikaenda pamoja naye mpaka kwake, tukamkuta amempanda mnyama wake. Sufyan akamwambia: "Ewe Abu Abdullah! Tusimulie hadithi ya hotuba ya Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) aliyoitoa katika msikiti wa al-Khayfu," akasema: "Niache kwanza niende kwenye haja yangu kwani nimeshapanda kipando changu, nitakusimulia baada ya kurudi." Akasema: "Nakuomba kwa heshima ya ukaraba wako kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, nisimulie sasa." Akateremka na Sufyan akamwambia: "Amrisha niletewe wino na karatasi ili niweze kuiandika." Akaomba wino na karatasi kisha akamwambia: "Andika: Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu. Hotuba ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) aliyoitoa katika msikiti wa al-Khayfu: "Mwenyezi Mungu ampe uzuri mja ambaye ataisikiliza kauli yangu na kuielewa, ataihifadhi na kumfikishia yule ambaye haijamfikia. Enyi watu, aliyepo amfikishie yule asiyekuwepo hapa, kwani huenda mwenye kubeba elimu si aalimu, na huenda mwenye kubeba elimu anaipeleka kwa aliye na elimu zaidi yake. Hakika Moyo wa Mwislamu haukosi mambo matatu: Kutenda amali kwa ikhlasi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kutoa nasaha kwa viongozi wa Waislamu na kushikamana na jamaa yao, kwani hakika ulinganio wao umewazunguka kwa nyuma. Waislamu ni ndugu, wanatoleana damu, 52

Sunan Abi Daud: 303. Na mfano wa riwaya hiyo imo katika Tabaqatul-Kubra 2: 185. 31


Hija ya Kuaga

na kwa dhima yao hupata heshima yule aliye mnyonge kati yao." Sufyan akaandika kisha akamuonesha, na kisha Abu Abdullah (a.s.) akapanda mnyama wake na kuondoka.53 Al-Qummiy ameitaja hotuba hii tukufu na ameongeza mwishoni mwa hotuba: "Wasia wa Mtukufu Mtume kuhusu kushikamana na vizito viwili.54 Haiko mbali dhana hii kwa sababu yeye aliwaamuru Waislamu mara kadhaa na katika maeneo tofauti, kushikamana na vizito viwili.

53 54

Al-Kafiy 1: 403. Biharul-An'wari 47: 365. Tafsirul-Qummiy 2: 447. 37: 114. 32


Hija ya Kuaga

HOTUBA YA MTUME WA MWENYEZI MUNGU (SAWW) ALIYOITOA MBELE YA KA'BA

M

tume wa Mwenyezi Mungu (saww) alipomaliza Hijja yake alikwenda kuiaga Ka'ba tukufu, akashika kufuli la mlango na kunadi: "Enyi watu!" basi wakakusanyika waliokuwemo ndani ya Msikiti Mtukufu na waliokuwepo sokoni nyuma ya Ka'ba, akatoa hotuba nzito na kutaja machafuko yatakayotokea baada yake na uharibifu utakaowapata watu katika maadili yao, matendo yao na itikadi zao, na akataja alama za kutokea Kiyama. La budi kutaja hapa ni kwamba hotuba hii tukufu ina riwaya mbalimbali zenye kutofautiana na kupishana katika baadhi ya matamshi, lakini zinafanana katika mambo mengi. As-Suyut amepokea ndani ya ad-Durul-Manthur mwishoni mwa Aya tukufu:

َ‫ﻈﺮُونَ إِﻟﱠﺎ اﻟﺴﱠﺎﻋَﺔَ أَنْ ﺗَﺄْﺗِﻴَ ُﻬﻢْ ﺑَﻐْﺘَﺔً ۖ ﻓَﻘَﺪْ ﺟَﺎء‬ ُ ْ‫ﻓَﻬَﻞْ ﻳَﻨ‬ ْ‫ﻃﻬَﺎ ۚ ﻓَﺄَﻧﱠﻰٰ ﻟَ ُﻬﻢْ إِذَا ﺟَﺎءَﺗْ ُﻬﻢْ ذِآْﺮَا ُهﻢ‬ ُ ‫أَﺷْﺮَا‬ "Kwani wanangojea jingine isipokuwa iwafikie Saa kwa ghafla? Basi sharti zake zimekwishakuja. Na itapowajia kutawafaa wapi kukumbuka kwao?" (Surat Muhammad: 18) Amesema: Ameandika Ibnu Mardawayhi kutoka kwa Ibnu Abbas radhi za Mwenyezi Mungu ziwafikie, amesema: "Mtume alihiji 33


Hija ya Kuaga

Hijja ya kuaga kisha akashika kufuli la mlango wa Ka'ba na kusema: 'Enyi watu! je nikutajieni alama za Kiyama........mpaka mwisho."'55 – Na pia kaipokea Muhyid-Din Ibnu al-Arab katika kitabu Muhadharatul-Abrar Wamasamiratul-Akhbar akivusha riwaya kutoka kwa Abdullah bin Abbas kutoka kwa Mtukufu Mtume (saww).56 Ama ndani ya vitabu vya Shia Imamiyyah, imepokewa ndani ya Jamiul-Akhbar kwa kuvushwa kutoka kwa Jabir bin Abdullah al-Ansariy kuwa alisema: "Nilihiji pamoja na Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) Hijja ya kuaga, Mtukufu Mtume (saww) alipomaliza ibada za Hijja alizofaradhishiwa alikwenda kuiaga Ka'ba, akashika kufuli la mlango na kunadi kwa sauti ya juu: 'Enyi watu!' Wakakusanyika waliokuwemo msikitini na waliokuwepo sokoni, akasema: 'Sikieni, hakika mimi nasema yale ambayo yatatokea baada yangu....mpaka mwisho wake.57 Imeandikwa ndani ya Tafsirul-Qummiy mwishoni mwa Aya tukufu:

ۚ ‫ﻃﻬَﺎ‬ ُ ‫ﻈﺮُونَ إِﻟﱠﺎ اﻟﺴﱠﺎﻋَﺔَ أَنْ ﺗَﺄْﺗِﻴَ ُﻬﻢْ ﺑَﻐْﺘَﺔً ۖ ﻓَﻘَﺪْ ﺟَﺎءَ أَﺷْﺮَا‬ ُ ْ‫ﻓَﻬَﻞْ ﻳَﻨ‬ ٰ ‫ﻓَﺄَﻧﱠ‬ ْ‫ﻰ ﻟَ ُﻬﻢْ إِذَا ﺟَﺎءَﺗْ ُﻬﻢْ ذِآْﺮَا ُهﻢ‬ "Kwani wanangojea jingine isipokuwa iwafikie Saa kwa ghafla? Basi sharti zake zimekwishakuja. Na itapowajia kutawafaa wapi kukumbuka kwao?" (Surat Muhammad: 18). Amesema: Alinisimulia baba yangu, kutoka kwa Sulayman bin Ad-Durul-Manthur: 7: 412. Muhadharatul-Abrar Wamasamiratul-Akhbar: 1 / 60 – 62. 57 Jamiul-Akhbar: 395 – 397. Biharul-An'war: 52 / 262. 55 56

34


Hija ya Kuaga

Muslim bin al-Khashab, kutoka kwa Abdullah bin Jarij al-Makkiy, kutoka kwa Atau bin Abu Rabah, kutoka kwa Abdullah bin Abbas, amesema: "Tulihiji pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu Hijja ya kuaga, akashika kufuli la mlango wa Ka'ba, kisha akatuelekea kwa uso wake na kusema: 'Je niwatajie alama za Kiyama?' Na mtu aliyekuwa karibu yake zaidi siku hiyo ni Salman rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, akasema: 'Ndiyo ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu.' Akasema: 'Hakika miongoni mwa alama za Kiyama ni watu kuipuuza Swala na kufuata matamanio, na kuelemea kwenye matamanio, kuwatukuza wenye mali na kuuza dini kwa thamani ya dunia, wakati huo moyo wa muumini utayeyuka ndani ya tumbo lake kama chumvi inavyoyeyuka ndani ya maji, hiyo ni kutokana na maovu anayoyaona lakini hawezi kuyaondoa.' Salman akasema: 'Je yatatokea kweli haya ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?!' akasema: 'Ndiyo ewe Salman, naapa kwa yule ambaye nafsi yangu imo mikononi Mwake, hakika wakati huo watu watatawaliwa na viongozi madhalimu na mawaziri waovu, wajuzi madhalimu na watunza hazina wasiokuwa waaminifu.' Salman akasema: ' 'Je yatatokea kweli haya ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?!' akasema: 'Ndiyo ewe Salman, naapa kwa yule ambaye nafsi yangu imo mikononi Mwake, hakika wakati huo mabaya yataonekana mema, na mema yataonekana mabaya, asiye mwaminifu ataaminiwa na mwaminifu ataonekana si mwaminifu, muongo atasadikishwa na mkweli atapingwa....mpaka mwisho wa hotuba tukufu."'58

58

afsirul-Qummiy 2: 303 – 307. Biharul-An'war 6: 305 – 309. Tafsirul-Burhan 4: 183 T mwishoni mwa Aya tukufu: 35


Hija ya Kuaga

HOTUBA YA MTUKUFU MTUME (SAWW) ALIYOITOA GHADIR KHUM

B

aada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) yeye na Waislamu kutimiza Hijja yao na kumaliza ibada zao walitoka Makka tukufu wakati wa dhuha siku ya mwezi kumi na nne Dhulhaji na kuelekea Madina tukufu. Msafara wa Mtukufu Mtume (saww) ulikuwa ukitembea kuelekea Madina kituo baada ya kituo, hatua baada ya hatua, mpaka ilipopita siku ya mwezi kumi na tano, mwezi kumi na sita na mwezi kumi na saba. Ilipofika dhuha ya siku ya mwezi kumi na nane, msafara ulipofika karibu na Juhfa eneo la Ghadir Khum, ukiwa umbali wa kilometa 185 toka Makka, na kabla mahujaji hawajaachana kwa kuchukua njia zao zinazowafikisha katika miji yao, alinadi mnadi wa Mtukufu Mtume (saww): "Swala ya pamoja." –Hili ni tamko la kuwaita watu wakusanyike pamoja. Mahujaji wakashtuka kutokana na wito huu kwani muda huu haukuwa ni wakati wa kuteremka na kupumzika, na sehemu hii haikuwa na eneo la kuteremkia na kupumzikia, hivyo msafara ulisimama na waliokuwa nyuma wakaungana na msafara na wakarudi nyuma wale waliokuwa wametangulia.Wakakusanyika wakati wa joto kali ili wasikilize habari muhimu, kiasi kwamba wengi wao waliweka nguo juu ya vichwa vyao ili kuzuia joto la jua, na wengine waliweka chini ya nyayo zao kwa kuzuia joto la changarawe. Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) aliwaswalisha Waislamu swala ya Dhuhri kisha wakamtengenezea Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) mimbari ndefu kutokana na matandiko ya ngamia, kisha maelfu ya watu wakawa na masikio yenye kusikiliza maneno yake (saww), ili wasikilize na kuelewa maneno ya mhutubu wa Mwenyezi Mungu. Alipanda mimbari, akafungua kinywa chake 36


Hija ya Kuaga

kizuri na akazungumza maneno ambayo kwayo aliwafikishia Waislamu yale aliyoamrishwa na Mwenyezi Mungu kuyafikisha. Nasi hapa tunaileta hotuba tukufu kutoka ndani ya kitabu alManaqib cha Ibnu al-Maghazaliy as-Shafiy kwa njia aliyoitaja yeye, amesema: Kisha Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) akasema: "Kila himidi njema ni ya Mwenyezi Mungu, tunamhimidi Yeye na kumtaka msaada Yeye, tunamwamini Yeye na tunamtawakali Yeye, na tunajilinda kwa Mwenyezi Mungu kutokana na mabaya ya nafsi zetu na mabaya ya matendo yetu. Ambaye hapana wa kumuongoa yule aliyempoteza Yeye wala hapana wa kumpoteza yule aliyemuongoa Yeye. Na nashahidilia kwamba hapana mungu isipokuwa Allah, na hakika Muhammadi ni mja Wake na Mtume Wake. Ama baad, enyi watu! Nabii hakuwa na umri isipokuwa nusu ya umri wa Nabii aliyekuwa kabla yake, na hakika Issa bin Mariyam aliishi pamoja na watu wake miaka arubaini, na mimi nimeshafika katika ishirini, hivyo fahamuni kuwa ni karibu nitatengana na ninyi, fahamuni kuwa hakika mimi ni mwenye kuulizwa na ninyi ni wenye kuulizwa, je nimewafikishia? Mtasema nini?" Alisimama kutoka kila upande mtu mmoja mwenye kujibu: "Wanasema: Tunashahidilia kuwa hakika wewe ni mja wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na umefikisha ujumbe Wake na kupigana katika njia yake, umetangaza amri Yake na umemwabudu mpaka ulipofikwa na yakini. Tunamuomba Mwenyezi Mungu akulipe kwa niaba yetu malipo mazuri kushinda yale aliyowahi kumlipa Nabii yeyote kwa niaba ya umma wake." Mtume akasema: "Si mnashahidilia kwamba hapana mungu isipokuwa Mmoja asiye na mshirika, na kwamba Muhammadi ni mja Wake na Mtume Wake, na kwamba hakika pepo ni haki, na hakika moto ni haki, na mnaamini Kitabu chote?" Wakasema: "Ndiyo." Aka37


Hija ya Kuaga

sema: "Hakika mimi nashahidilia kuwa nimewasadiki nanyi mmenisadiki, basi fahamuni kuwa mimi nitawatangulia na ninyi mtanifuata na mtanikuta katika hodhi yangu, mtakaponikuta nitawaulizeni kuhusu vizito vyangu viwili, mliamiliana navyo vipi baada yangu?" Anasema: Tukapigwa na butwaa ni vipi hivyo vizito viwili, mpaka aliposimama mtu mmoja kutoka kwa Muhajirina, akasema: "Naapa kwa haki ya baba yangu na mama yangu na wewe ewe Nabii wa Mwenyezi Mungu, ni vipi hivyo vizito viwili?" Akasema: "Kikubwa kati ya hivyo viwili ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu, nayo ni kamba ambayo ncha moja imo mikononi mwa Mwenyezi Mungu na nyingine imo mikononi mwenu, hivyo ishikilieni, wala msipotee. Na kidogo kati ya vizito hivyo viwili ni kizazi changu ambacho kilipokea Kibla yangu na kuitikia wito wangu, hivyo msiwauwe, msiwadhulumu wala msikae mbali nao, kwani hakika mimi nilimuomba Mpole Mwingi wa habari naye akanipa wao. Mwenye kuwanusuru wao ni mwenye kuninusuru mimi, mwenye kuwatelekeza wao ni mwenye kunitelekeza mimi, mwenye kuwapenda wao ni mwenye kunipenda mimi na mwenye kuwafanyia uadui wao ni mwenye kunifanyia uadui mimi. Fahamuni kuwa hakuna umma uliyohiliki kabla yenu isipokuwa ni pale walipofuata matamanio yao, walipomdhulumu Nabii wao na walipomuua yule mwenye kusimamisha uadilifu." Kisha aliushika mkono wa Ali bin Abu Talib akaunyanyua juu na kusema: "Yeyote ambaye mimi nina mamlaka naye basi huyu Ali ni mwenye mamlaka naye. Yeyote ambaye mimi ni mtawala wake basi huyu Ali ndiye mtawala wake. Ewe Mwenyezi Mungu mpende mwenye kumpenda na mfanyie uadui mwenye kumfanyia uadui." alisema hayo mara tatu.59 Kisha Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu alimvisha Ali 59

l-Manaqib ya Ibnu al-Maghazaliy: 16, amenukuu kutoka kwa al-Umdah cha Ibnu A Batriq: 104. 37: 184. Na al-Amaal cha Tusiy: 227. 38


Hija ya Kuaga

(a.s.) kwa mkono wake mtukufu taji kwa kilemba chake mbele ya kundi kubwa la Waumini na kuning'iniza ncha zake mabegani mwake, kisha aliwaamuru Ansari na Muhajirina waje kumsalimu Ali na kumpongeza kwa fadhila hii adhimu ya kutawazwa kuwa Amiri wa Waumini. Walijitokeza watu wazito kati ya Waislamu60 wakamsalimu na kumpongeza61 kwa kuwa Amiri wa Waumini. Yeyote atakayerejea vyanzo vingi vya historia na vitabu vya hadithi atakuta kuwa hotuba hii imechukua kurasa nyingi, na waandishi wamegusia pande zake mbalimbali, miongoni mwao ni Tabari ambaye ameandika kitabu ambacho kimekusanya hadithi za Ghadir Khum katika mijalada miwili mikubwa.62 Sheikh Sulayman al-Hanafiy al-Qunduziy amesema ndani ya kitabu chake Yanabiul-Mawaddah kuwa: Imesimuliwa kutoka kwa Abul-Maaliy al-Juwayniy mwenye lakabu ya Imamul-Haramayni kuwa Ustadh Abu Hamid al-Ghazaliy alisema: "Niliona mjalada huko Baghdad ukiwa mikononi mwa wana habari, ukiwa na riwaya mbalimbali za Ghadir Khum, ukiwa umeandikwa: Mjalada wa ishirini na nane wa njia za kauli yake (saww): Yeyote ambaye mimi nina mamlaka naye basi huyu Ali ni mwenye mamlaka naye. Na unafuata 60

Ameandika Tabaraniy ndani ya kitabu al-Wilayah (214 – 216) hadithi kwa njia yake kutoka kwa Zaid bin Arqam kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu alisema baada ya hotuba yake: "Enyi watu, semeni: Tumekupa ahadi juu ya hilo kutoka ndani ya nafsi zetu….Mpaka akasema: Semeni niliyowaambia na msalimuni Ali kwa kupata uamiri juu ya Waumini. Na semeni: Kila himidi njema ni ya Mwenyezi Mungu aliyetuongoza katika hili… - Zayd bin Arqam amesema: Ndipo watu wakaharakisha kusema: Ndiyo tumesikia na tumetii amri ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa nyoyo zetu.

Mtu wa kwanza kumpa Ali mkono wa pongezi ni Abu Bakri, Umar, Uthman, Talha, Zubair, na Muhajirina na Ansari wengine, na ndipo watu wengine wakaendelea kumpa mkono wa pongezi mpaka akawa ameswali Dhuhri mbili wakati mmoja, zoezi hilo likaendelea mpaka akaswali Ishaa mbili wakati mmoja. 61 Musnad Abi Daud: 23; Kanzul-Ummal 15: 482. ar-Riyadh an-Nadhrah 3: 180. FaraidusSamtwayn 1: 75. al-Fusulul-Muhimmah: 41. as-Siyratul-Halabiyyah 3: 341. 62 Al-Bidayah Wan-Nihayah 11: 157. 39


Hija ya Kuaga

mjalada wa ishirini na tisa.63 Matini ya hotuba hii tukufu inatofautiana katika riwaya zinazoizungumzia, lakini zote zinajumuisha kauli ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) alipolihutubia kundi hili kubwa kwa kusema: "Je mimi si nina mamlaka juu yenu kuliko nafsi zenu wenyewe?" Wakasema: "Ndiyo." akamshika mkono Ali bin Abu Talib (a.s.) na kuunyanyua juu mpaka ukaonekana weupe wa makwapani mwake, kisha akasema: "Yeyote ambaye mimi nina mamlaka juu yake basi huyu Ali ni mwenye mamlaka juu yake. Ewe Mwenyezi Mungu mpende mwenye kumpenda, mfanyie uadui mwenye kumfanyia uadui, mnusuru mwenye kumnusuru na mtelekeze mwenye kumtelekeza." Na katika kitabu al-Ihtijaj, Rawdhatul-Waidhina, al-Adadu alQawiyyah, na al-Yaqin,64 waandishi wametaja humo hotuba ndefu sana ya Mtukufu Mtume (saww) katika tukio hili kuu. Baadhi ya waandishi wametaja maelezo ya kati kwa kati ya hotuba hii, si mafupi wala si marefu, mfano wao ni Ibnu al-Maghazali (483 A.H) ndani ya kitabu chake al-Manaqib, kama ilivyotangulia. Na pia Ibnu al-Athir ndani ya Usudul-Ghabah,65 Sheikh Ahmad AbulFadhli bin Muhammad Bakthiri al-Makiy as-Shafiiy (aliyefariki mwaka 1047 A.H.) ndani ya kitabu Wasilatul-Aamal Fiaddi Manaqibul-Aal,66 na Sheikh al-Amiliy katika kitabu Dhiyaul-Alimina kutoka katika kitabu al-Wilayah cha mwanahistoria Tabari,67 na al-Mutaqiy al-Hindiy ndani ya kitabu Kanzul-Ummal,68 na al-HuYanabiul-Mawaddah 1: 113 – 114. Al-Ihtijaj 1: 133 – 162. Rawdhatul-Waidhina: 89 – 101. al-Adadu al-Qawiyyah: 169; al-Yaqin 343 – 361. 65 Usudul-Ghabah 3: 33 – 34. 66 Wasilatul-Aamal Fiaddi Manaqibul-Aal: 116 – 118. 67 Amesema Ibnu Kathir katika kitabu chake cha historia Juz. 11: 146 katika wasifu wa Tabari: Hakika mimi niliona ana kitabu ambacho kakusanya humo hadithi za Ghadir Khum katika mijalada miwili mikubwa. Tazama al-Ghadir cha al-Amin 1: 424 – 426. 68 Kanzul-Ummal 13: 104 – 105. 63 64

40


Hija ya Kuaga

muwayni ndani ya Faraidus-Samtwayni69, na Ibnu as-Swabaghu al-Malikiy ndani ya kitabu al-Fusulul-Muhimmah70, na Ibnu Kathir katika al-Bidayah Wan-Nihayah71, na Ibnu Hajar katika as-Swawaiqul-Muhriqah,72 na al-Halabiy katika as-Siratun-Nabawiyyah73, na al-Haythamiy katika Majmauz-Zawa'id74, na al-Qarmaniy katika Akhbarud-Duwal75. Baadhi ya wanahadithi na wapokezi wamepokea nukta muhimu tu katika hotuba hii, nayo ni kauli ya Mtume wa Mwenyezi Mungu: "Yeyote ambaye mimi nina mamlaka juu yake basi huyu Ali ni mwenye mamlaka juu yake." Baada ya Mtume kutoa hotuba hii tukufu, mshairi mashuhuri Hassan bin Thabit alimwambia Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww): "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, nipe ruhusa nisome beti kadhaa kuhusu Ali ambazo utazisikia." Mtume wa Mwenyezi Mungu akasema: "Soma kwa baraka za Mwenyezi Mungu." Hassan bin Thabit akasoma shairi lake maarufu: "Amewaita Nabii wao siku ya Ghadir Khum, msikilize Nabii mwenye kunadi. Akasema: Ni nani mwenye mamlaka nanyi na Nabii wenu? Wakasema tena bila kusita: Mola Wako ndiye mwenye mamlaka nasi na wewe Nabii wetu, na kamwe hutakutana na uasi kutoka kwetu katika suala la mamlaka. Ndipo akamwambia: Simama ewe Ali, hakika mimi nimekuridhia kuwa Imam na kiongozi baada yangu. Yeyote ambaye mimi nina mamlaka juu yake basi huyu Ali ni mwenye mamlaka juu yake. Hivyo kuweni wafuasi wake wa Faraidus-Samtwayni 1: 62 – 78. al-Fusulul-Muhimmah: 40. 71 al-Bidayah Wan-Nihayah 5: 197 – 205. Na Juz. 7: 328 – 331. 72 as-Swawaiqul-Muhriqah: 42 – 49. 73 as-Siratun-Nabawiyyah 3: 336 – 337. 74 Majmauz-Zawaid 9: 259. 75 Akhbarud-Duwal: 102. 69 70

41


Hija ya Kuaga

kweli wenye mapenzi kwake. Hapo aliomba: Ewe Mwenyezi Mungu mpende ampendaye na kuwa adui wa yule mwenye kumfanyia uadui Ali." Allamah al-Amini amepokea beti hizi sita ndani ya kitabu chake al-Ghadir76 kutoka kwa wanazuoni kumi na wawili wa Kisunni, na kutoka kwa wanazuoni ishirini na mbili wa Kiimamiyyah, na ameinukuu kutoka katika kitabu cha Sulaymani bin Qays al-Hilaliy na kutoka kwa al-Mawla Muhsin al-Faydhu al-Kashaniy katika kitabu Ilmul-Yaqin77, kwa ziada ya beti nne, amesema baada ya ubeti wa kwanza: "Jibril alikuja kwa amri ya Mola Wake, kwamba hakika wewe ni maasumu hivyo usisite. Wafikishie aliyoteremsha Mola Wao kwako, wala usikhofu maadui. Akasimama wakati huo huku kaushika mkono wa Ali kwa mkono wake na kuuinua juu, na kumtangaza kwa sauti ya juu." Baada ya ubeti wa sita ameongeza: "Ewe Mola mnusuru mwenye kumnusuru, kwa kumnusuru kwao Imam mwenye kuongoza kama mbalamwezi yenye kung'aa ndani ya usiku wenye giza." Kisha Allamah Amin akasema: "Na kinachomdhihirikia mtafiti ni kuwa Hassan alikamilisha beti hizi kwa kaswida ambayo ilibeba muhtasari wa fadhila za Amirul-Muuminin (as).78 Mwisho wa mazungumzo yetu kuhusu hotuba hii muhimu, na ili tuondoe shaka inayoweza kuenea ndani ya nafsi za baadhi ya watu, tunataja sehemu fulani ya wapokezi wake miongoni mwa Sahaba na Tabiina, na vitabu vilivyotungwa kuhusu hadithi ya Ghadir, tunasema: Mosi: Hadithi ya Ghadir imepokewa kutoka kwa Masahaba mia moja na ishirini, miongoni mwao ni: Al-Ghadir 2: 65. Ilmul-Yaqin: 343 – 361. 78 Al-Ghadir 1: 73. 76 77

42


Hija ya Kuaga

1. Abu Bakr bin Abu Quhafah at-Taymiy (Aliyefariki mwaka 13 A.H) 2. Abu Huraira ad-Dawaiy (Aliyefariki mwaka 57 - 59 A.H) 3. Abu Layla al-Ansariy. Huyu alifariki katika vita vya Sufin akiwa pamoja na Ali (as) mwaka 37 A.H. 4. Abu Zainab bin Awfi al-Ansariy. 5. Abu Fadhalah al-Ansariy. Huyu ni mwanabadri alifariki katika vita vya Sufin akiwa pamoja na Imam Ali (a.s.). 6. Abu Qudamah al-Ansariy. 7. Abu Umrah bin Amru bin Muhaswin al-Ansariy. 8. Abul-Haytham bin at-Tihan. Huyu alifariki katika vita vya Sufin akiwa pamoja na Ali (as) mwaka 37 A.H. 9. Abu Rafiu al-Qibtwiyyu. 10. Abu Dhuaybu Khuwaylidu – au Khalid – Ibnu Khalid bin Muhrith al-Hadhliy. Pili: Imepokewa pia na Tabiina themanini na mbili, hapa tunawataja baadhi yao: 1. Abu Rashid al-Habraniy as-Shamiy. Jina lake ni Akhdhar, Nuuman. 2. Abu Salmah Abdullah bin Abdurahman bin Awfi Az-Zahriy alMadaniy (Aliyefariki mwaka 94 A.H). 43


Hija ya Kuaga

3. Abu Sulayman mwadhini. 4. Abu Swalih as-Samman, Dhakwan al-Madaniy (Aliyefariki mwaka 101 A.H). 5. Abu An'fawanah al-Maziniy. 6. Abu Abdurahim al-Kindiy. 7. Abul-Qasim al-Asbagh bin Nubatah at-Tamimiy al-Kufiy. 8. Abu Layla al-Kindiy. 9. Iyasi bin Nudhayru. 10. Jamil bin Ammarah. Tatu: Pia imeungwa mkono na kupokewa na ulamaa, mahafidhi na wanahistoria mia tatu na sitini, hapa tunataja baadhi yao: 1. al-Hafidhu Abu Issa at-Tirmidhiy (Aliyefariki mwaka 279 A.H).79 2. al-Hafidh Abu Ja'far at-Tahawiy (Aliyefariki mwaka 279 A.H).80 3. al-Hafidh Ibnu Abdul-Barri al-Qurtubiy (Aliyefariki mwaka 463 A.H).81 4. al-Faqihi Abul-Hasan bin al-Maghazaliy as-Shafiiy (Aliyefariki mwaka 483 A.H).82 Sunanu Tirmidhi 5: 591. Mushkilul-Athar 2: 308. 81 Al-Istiab 2: 373. 82 Manaqib Ali bin Abi Talib: 27, Namba 39. 79 80

44


Hija ya Kuaga

5. Hujatul-Islam Abu Hamid al-Ghazaliy (Aliyefariki mwaka 505 A.H).83 6. al-Hafidh Abul-Faraj bin al-Jawziy al-Hanbaliy (Aliyefariki mwaka 597 A.H). 7. Abul-Mudhaffar – mjukuu wa Ibnu al-Jawziy al-Hanafiy (Aliyefariki mwaka 654 A.H).84 8. Ibnu Abul-Hadid al-Mu'utaziliy (Aliyefariki mwaka 655 A.H).85 9. al-Hafidh Abu Abdullah al-Kunjiy as-Shafiiy (Aliyefariki mwaka 658 A.H).86 10. Sheikh Abul-Makarim Alaud-Din as-Samnaniy (Aliyefariki mwaka 736 A.H).87 11. Shamsud-Din ad-Dhahbiy as-Shafiiy (Aliyefariki mwaka 748 A.H).88 12. Shamsud-Din al-Jazriy as-Shafiy (Aliyefariki mwaka 833 A.H).89 13. al-Hafidh Ibnu Hajar al-Asqalaniy (Aliyefariki mwaka 852A.H).90 14. Jamalud-Din Abul-Mahasin Yusuf bin Swalahud-Din alSirul-Aamiliina: 21. Tadhkiratul-Khuwas: 29. 85 Sharhu Nahjul-Balaghah 9: 166. 86 Kifayatut-Twalibu: 60 – 61. 87 al-Ur'watu Liahlil-Khul'wah: 422. 88 Talkhisul-Mustadrak 3: 613. 89 Asnal-Matalib: 48. 90 Fat'hul-Bari 7: 74. 83 84

45


Hija ya Kuaga

Hanafiy.91 15. Nurud-Din al-Harawiy at-Taziy al-Hanafiy (Aliyefariki mwaka 101 A.H).92 16. Zaynud-Din al-Manawiy as-Shafiiy (Aliyefariki mwaka 1031 A.H).93 17. Nurud-Din al-Halabiy as-Shafiiy (Aliyefariki mwaka 1044 A.H).94 18. as-Sayyid Muhammad al-Barzanjiy as-Shafiiy (Aliyefariki mwaka 1103 A.H).95 19. as-Sayyid Ibnu Hamza al-Haraniy ad-Damashqiy al-Hanafiy (Aliyefariki mwaka 1120 A.H).96 20. Mirza Muhammad al-Badkhashiy.97 21. Mufti wa Sham al-Amadiy al-Hanafiy ad-Damashqiy (Aliyefariki mwaka 1171 A.H).98 22. Abul-Irfan as-Swabban as-Shafiiy (Aliyefariki mwaka 1206 A.H).99 al-Muutaswar Minal-Mukhtasar 2: 301. al-Mirqat Fii Sharhil-Mishkat 10: 464. 93 Faydhul-Qadir 6: 218. 94 as-Siratul-Halabiyyah 3: 274. 95 an-Nawaqidh Lir-Rawafidh: Ukurasa wa 8. 96 al-Bayan Wat-Taarif 3: 75. 97 Nazarul-Abrar: 54. 98 as-Swalatul-Fakhirah: 49. 99 Is'afur-Raghibin Fii Hamish Nurul-Abswar: 153. 91 92

46


Hija ya Kuaga

23. Mahmudu al-Alusiy al-Baghdadiy (Aliyefariki mwaka 1270 A.H).100 24. Sheikh Mahmud al-Hut al-Bayrutiy as-Shafiiy (Aliyefariki mwaka 1276 A.H).101 25. al-Mawlawiy Waliyullah al-Luk'hanawiy.102 26. al-Hafidh al-Muasir Shihabud-Din al-Ghamariy al-Maghrib103 27. Sheikh Abdul-Aziz Muhammad bin as-Sidiq al-Maghribiy.104 Nne: Walioandika kuhusu hadithi ya Ghadir: Ifuatayo ni orodha ya majina ya baadhi ya wale walioandika kuhusu hadithi ya Ghadir, jina la mwandishi na kitabu chake au risala yake. Nilazima tukumbushe hapa kuwa hatudai kuwa tutataja vitabu vyote vilivyoandikwa kuhusu suala hili, kwa sababu halitawezekana kwa sasa, Inshaallah: 1. Abu Ja'far Muhammad bin Jarir bin Yazid bin Khalid Tabariy al-Aamiliy (Aliyefariki mwaka 310 A.H), ana kitabu kiitwacho al-Wilayah Fii Turuqi Hadithil-Ghadir. 2. Abul-Abbas Ahmad bin Muhammad bin Said al-Hamadaniy, al-Hafidh maarufu kwa jina la Ibnu Aqadah (Aliyefariki mwaka 333 A.H), ana kitabu kiitwacho al-Wilayah Fii Turuqi HadithilGhadir. Ruhul-Maan 6: 195. Asnal-Matwalib: 461. 102 Mir'atul-Muuminin Fii Manaqib Ahli Bayti Sayyidil-Mursalin: 40. 103 Tashniful-Adhaan: 77. 104 Majallatul-Muusim: 74, M 2 – 1190 M, Maadhimishi ya Ghadir, London. 100 101

47


Hija ya Kuaga

3. Abubakri Muhammad bin Umar bin Muhammad bin Salim atTamiymiy al-Baghdadiy maarufu kwa jina al-Juabiy (Aliyefariki mwaka 355 A.H), ana kitabu kiitwacho Man'rawa Hadith Ghadir Khum. 4. Abu Talib Abdullah bin Ahmad bin Zaydu al-Anbariy, al-Wasitiy (Aliyefariki mwaka 356 A.H), ana kitabu kiitwacho Turuqu Hadithil-Ghadir. 5. Abughalib Ahmad bin Muhammad bin Muhammad ar-Raziy (Aliyefariki mwaka 368 A.H), ana juzuu zima kuhusu hotuba ya Ghadiri. 6. Abul-Mufadhal Muhammad bin Abdullah bin al-Mutalib asShaybaniy (Aliyefariki mwaka 372 A.H), ana kitabu Man'rawa Hadith Ghadir Khum. 7. al-Hafidh Ali bin Umar ad-Dar'qutuniy al-Baghdadiy (Aliyefariki mwaka 385 A.H), al-Kunjiy as-Shafiiy amesema ndani ya kitabu chake al-Kifayah wakati wa kutaja Hadithi Ghadiri: al-Hafidh ad-Dar'qutuniy amekusanya njia zake ndani ya juzuu moja. 8. Sheikh Muhsin bin Husain bin Ahmad an-Nisaburiy al-Khazaiy, ana kitabu Hadithul-Ghadir. 9. Ali bin Abdurahman bin Issa bin Ur'wah bin al-Jarah al-Qananiy (Aliyefariki mwaka 413 A.H), ana kitabu kiitwacho Turuqu Khabaril-Wilayah. 10. Abu Abdullah al-Husain bin Ubaydullah bin Ibrahim al-Ghadhairiy (Aliyefariki mwaka 411 A.H), ana kitabu kiitwacho Yawmul-Ghadir. 48


Hija ya Kuaga

11. al-Hafidh Abu Said Masuud bin Nasir bin Abu Zaydu as-Sajistaniy (Aliyefariki mwaka 477 A.H), ana kitabu kiitwacho adDirayah Fii Hadithil-Wilayah. 12. Abul-Fat'hi Muhammad bin Ali bin Uthman al-Karajikiy (Aliyefariki mwaka 411 A.H), ana kitabu kiitwacho Iddatul-Baswir Fii Hujaji Yawmil-Ghadir. 13. Ali bin Bilal bin Muawiya bin Ahmad al-Mahlabiy, ana kitabu kiitwacho Hadithul-Ghadir. 14. Sheikh Mansuri al-Laiy ar-Raziy, ana kitabu kiitwacho HadithulGhadir. 15. Sheikh Ali bin Hasan at-Twatwiriy al-Kufiy, ana kitabu kiitwacho Fadhailu Amiril-Muuminin, na kingine kinaitwa KitabulWilayah. 16. Abul-Qasim Ubaydullah bin Abdullah al-Haskaniy, ana kitabu kiitwacho Duatul-Hudat Ila Adai Haqil-Muwalat, katika kitabu hiki ameitaja hadithi ya Ghadir. 17. Shamsud-Din Muhammad bin Ahmad ad-Dhahbiy (Aliyefariki mwaka 748 A.H), ana kitabu kiitwacho Turuqu Hadithil-Ghadir. 18. Shamsud-Din Muhammad bin al-Jazriy ad-Damashqiy alMaqriy as-Shafiiy (Aliyefariki mwaka 833 A.H), na ametenga risala maalumu inayoitwa Ithbat Tawaturi Hadithil-Ghadir. 19. al-Mawla Abdullah bin Shah Mansuri al-Qaz'winiy at-Tusiy, ana kitabu kiitwacho ar-Risalah al-Ghadiriyyah. 20. as-Sayyid Sibtul-Hasan al-Jayisiy al-Hindiy al-Luk'hanawiy, ana kitabu kiitwacho Hadithul-Ghadir kwa lugha ya Kiurdu chapa ya India. 49


Hija ya Kuaga

21. as-Sayyid Mira Hamid Husain Ibnu as-Sayyid Muhammad Qaliy al-Musawi, al-Hindiy al-Luk'hanawiy (Aliyefariki mwaka 1306 A.H), ametaja Hadithi Ghadir, njia zake, utawaturi wake na maana yake, ametaja ndani ya mijaladi miwili mikubwa ndani ya kurasa elfu moja na thamanini, nayo ni sehemu ya mijalada ya kitabu chake kikubwa al-Aqabat. 22. as-Sasyyid Mahdi Ibnu As-Sayyid Ali al-Gurayfi al-Bahraniy an-Najafiy (Aliyefariki mwaka 1343 A.H), ana kitabu kiitwacho Hadithul-Wilayah Fii Hadithul-Ghadir. 23.

al-Hajji Sheikh Abbas bin Muhammad Qummiy(Aliyefariki mwaka 1359 A.H).

Ridha

al-

24. as-Sayyid Murtaza Husain al-Khatib al-Fat'huburiy al-Hindiy, ana kitabu kiitwacho Tafsirut-Takmil kuhusu Aya: Leo nimewakamilishia dini yenu. Iliyoteremka katika tukio la Ghadir. 25. Sheikh Muhammad Ridha Ibnu Sheikh Tahir Aal Farajullah anNajafiy, ana kitabu kiitwacho al-Ghadir Fil-Islam. 26. al-Allamah Sheikh Abdul-Husain bin Ahmad al-Amini an-Najafi (Aliyefariki mwaka 1390 A.H), ana kitabu kiitwacho al-Ghadir Fil-Kitab Was-Sunnah Wal-Adab, katika juzuu kumi na moja. Haya ndiyo tuliyoweza kumuonesha msomaji kuhusu hotuba za Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) katika Hijja ya kuaga, bila shaka tutakuwa tumesaidia na kuchangia katika kuchora na kutoa picha halisi ya zile juhudi na mihanga aliyoitoa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) katika njia ya kuuongoza umma wake na kuweka wazi mafunzo ya dini ya Uislamu kwa ajili ya vizazi vyote vya umma wa Kiislamu. 50


Hija ya Kuaga

Tunamuomba Mwenyezi Mungu atuafikishe tuweze kufuata Sunnah yake na aturuzuku uombezi wake huko Akhera na tuweze kumzuru hapa duniani. Shukrani zote ni za Mwenyezi Mungu na kila himidi njema ni Yake kwa kutuwafikisha kutenda mema. Wassalam Alaykum Warahmatullah Wabarakatuhu.

51


Hija ya Kuaga

ORODHA YA VITABU VILIVYO ­CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION 1. Qur'an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Thelathini 2.

Uharamisho wa Riba

3.

Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza

4.

Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili

5.

Hekaya za Bahlul

6.

Muhanga wa Imamu Husein (A.S.)

7.

Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.)

8.

Hijab vazi Bora

9.

Ukweli wa Shia Ithnaashariyyah

10. Madhambi Makuu 11. Mbingu imenikirimu 12. Abdallah Ibn Saba 13. Khadijatul Kubra 14. Utumwa 15. Umakini katika Swala 16. Misingi ya Maarifa 52


Hija ya Kuaga

17. Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia 18. Bilal wa Afrika 19. Abudharr 20. Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu 21. Salman Farsi 22. Ammar Yasir 23. Qur'an na Hadithi 24. Elimu ya Nafsi 25. Yajue Madhehebu ya Shia 26. Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur'an Tukufu 27. Al-Wahda 28. Ponyo kutoka katika Qur'an. 29. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii 30. Mashukio ya Akhera 31. Al Amali 32. Dua Indal Ahlul Bayt 33. Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna 34. Haki za wanawake katika Uislamu 35. Mwenyeezi Mungu na sifa zake 36. Kumswalia Mtume (s) 37. Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) 38. Adhana 53


Hija ya Kuaga

39

Upendo katika Ukristo na Uislamu

40. Tiba ya Maradhi ya Kimaadili 41. Maana ya laana na kutukana katika Qur'ani Tukufu 42. Kupaka juu ya khofu 43. Kukusanya swala mbili 44. Bismillah ni sehemu ya Qur'ani na husomwa kwa Jahara 45. Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya 46. Kusujudu juu ya udongo 47. Kusherehekea Maulidi Ya Mtume (s) 48. Tarawehe 49. Malumbano baina ya Sunni na Shia 50. Kupunguza Swala safarini 51. Kufungua safarini 52. Umaasumu wa Manabii 53. Qur'an inatoa changamoto 54. as-Salaatu Khayrun Mina -'n Nawm 55. Uadilifu wa Masahaba 56. Dua e Kumayl 57. Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu 58. Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake 59. Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata 60. Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mtume Muhammad (s) 54


Hija ya Kuaga

61. Nahju'l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza 62. Nahju'l-Balaghah - Juzuu ya Pili 63. Kuzuru Makaburi 64. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza 65. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili 66. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu 67. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne 68. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano 69. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita 70. Tujifunze Misingi Ya Dini 71. Sala ni Nguzo ya Dini 72. Mikesha Ya Peshawar 73. Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu 74. Ubora wa Imam 'Ali Juu ya Maswahaba Na Ushia ndio njia iliyonyooka 75. Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake 76. Liqaa-u-llaah 77. Muhammad (s) Mtume wa Allah 78. Amani na Jihadi Katika Uislamu 79. Uislamu Ulienea Vipi? 80. Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) 81. Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s)

55


Hija ya Kuaga

82. Urejeo (al-Raja'a ) 83. Mazingira 84. Utokezo (al - Badau) 85. Hukumu ya kujenga juu ya makaburi 86. Swala ya maiti na kumlilia maiti 87. Uislamu na Uwingi wa Dini 88. Mtoto mwema 89. Adabu za Sokoni 90. Johari za hekima kwa vijana 91. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza 92. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili 93. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu 94. Tawasali 95. Imam Mahdi katika Usunni na Ushia 96. Huduma ya Afya katika Uislamu 97. Sunan an-Nabii 98. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza) 99. Shahiid Mfiadini 100. Ujumbe -Sehemu ya Kwanza 101. Ujumbe - Sehemu ya Pili 102. Ujumbe - Sehemu ya Tatu 103. Ujumbe - Sehemu ya Nne 56


Hija ya Kuaga

104. Kumswalia Nabii (s.a.w) 105. Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu 106. Hadithi ya Thaqalain 107. Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza 108. Ukweli uliopotea sehemu ya Pili 109. Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu 110. Ukweli uliopotea sehemu ya Nne 111. Ukweli uliopotea sehemu ya Tano 112. Safari ya kuifuata Nuru 113. Fatima al-Zahra 114. Myahudi wa Kimataifa 115. Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi 116. Visa vya kweli sehemu ya Kwanza 117. Muhadhara wa Maulamaa 118. Mwanadamu na Mustakabali wake 119. Imam Ali ('a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Kwanza) 120. Imam Ali ('a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Pili) 121. Khairul Bariyyah 122. Uislamu na mafunzo ya kimalezi 123. Vijana ni Hazina ya Uislamu. 124. Yafaayo kijamii 57


Hija ya Kuaga

125. Tabaruku 126. Taqiyya 127. Vikao vya furaha 128. Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje? 129. Visa vya wachamungu 130. Falsafa ya Dini 131. Kuhuzunika na Kuomboleza - Azadari 132. Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah 133. Kuonekana kwa Allah 134. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza) 135. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili) 136. Ushia ndani ya Usunni 137. Maswali na Majibu 138. Mafunzo ya hukmu za ibada 139. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 1 140. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 2 141. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 3 142. Abu Huraira 143. Vipengee kadhaa katika Swala ya Jamaa na Msikiti. 144. Mazingatio kutoka katika Qur'an - Sehemu ya Kwanza 145. Mazingatio kutoka kaitka Qur'an - Sehemu ya Pili 146. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya kwanza 58


Hija ya Kuaga

147. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya Pili 148. Qur'ani Tukufu – Pamoja na Tarjuma ya Kiswahili 149. Falsafa ya Mageuzi ya Imam Husein (a.s) 150. Amali za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani 151. Elimu ya Tiba za Kiislamu - Matibabu ya Maimamu 152. Uislamu Safi 153. Majlisi za Imam Husein Majumbani 154. Uislam wa Shia 155. Amali za Makka 156. Amali za Madina 157. Asili ya Madhehebu katika Uislamu 158. Sira ya Imam Ali kuhusu Waasi 159. Ukweli uliofichika katika neno la Allah 160. Uislamu na Mifumo ya Uchumi 161. Umoja wa Kiislamu na Furaha 162. Mas'ala ya Kifiqhi 163. Jifunze kusoma Qur'ani 164. As-Sahifatul Kamilah as-Sajjadiyyah 165. Hayya 'Alaa Khayri'l-'Amal Katika Adhana 166. Ukweli kuhusu Funga ya Siku ya Ashura 167. Dua za Miezi Mitatu Mitukufu (Rajabu, Shaabani na Ramadhani) 168. Uadilifu katika Uislamu

59


Hija ya Kuaga

169. Mahdi katika Sunna 170. Kazi na Bidii ni njia ya maendeleo 171. Abu Talib – Jabali Imara la Imani 172. Ujenzi na Utakaso wa Nafsi 173. Vijana na Matarajio ya Baadaye 174. Usalafi – Historia yake, maana yake na lengo lake 175. Ushia – Hoja na Majibu 176. Mateso ya Dhuria wa Mtume (saww) 177. Maombolezo – Msiba wa Bwana wa Mashahidi (a.s.) 178. Shahidi kwa Ajili ya Ubinadamu 179. Takwa 180. Amirul Muuminina ('as) na Makhalifa 181. Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.) 182. Kuelewa Rehma ya Mwenyezi Mungu 183. Mtazamo kuhusu msuguano wa kimadhehebu 184. Upotoshaji Dhahiri katika Turathi (Hazina) ya Kiislamu 185. Nchi na Uraia – Haki na wajibu kwa Taifa 186. Mtazamo wa Ibn Taymiyyah kwa Imam Ali (a.s.) 187. Uongozi wa kidini – Maelekezo na utekelezaji wa Kijamii 188. Huduma ya Afya katika Uislamu 189. Historian a Sira za Viongozi Waongofu – Sehemu ya Pili 190. Uwazi baina ya Maslahi na Vikwazo

60


Hija ya Kuaga

KOPI NNE ZIFUATAZO ZIMETAFSIRIWA KWA LUGHA KINYARWANDA 1. Amateka Na Aba'Khalifa 2. Nyuma yaho naje kuyoboka 3. Amavu n'amavuko by'ubushiya 4. Shiya na Hadithi

61


MUHTASARI

62


MUHTASARI

63


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.