Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:25 PM
Huduma ya Afya katika Uislamu Kimeandikwa na: Jopo la Wataalamu la Taasisi ya Balagha
Kimetarjumiwa na: Al-H Hajj Hemedi Lubumba
Page A
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:25 PM
ŠHaki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: 978 - 9987 - 17 - 011 - 1
Kimeandikwa na: Jopo la Wataalamu la Taasisi ya Balagha
Kimetarjumiwa na: Al-Hajj Hemedi Lubumba Kimepangwa katika Kompyuta na: Hajat Pili Rajab Toleo la kwanza: Julai,2011 Nakala: 1000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Nukushi: +255 22 2127555 Barua Pepe: alitrah@raha.com Tovuti: www.ibn-tv.com Katika mtandao: www.alitrah.info
Page B
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:25 PM
Page C
YALIYOMO Afya na umbile la mwanadamu.........................................................3 Kuujali mwili na kuutunza.................................................................6 Maradhi ya Kisaikolojia na Athari zake katika Afya ya mwili.........21 Maradhi na kukamilika kwa Nafsi..................................................32 Maumivu na fidia.............................................................................41 Maradhi na Taklifu za Kisheria........................................................46 Mamlaka ya mgonjwa.....................................................................49 Matibabu na Mwanamke Ajinab.................................................... 52 Utabitu ni wajibu wa kutosheleza...................................................55 Kumtembelea mgonjwa...................................................................66
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:25 PM
Page D
Huduma ya Afya katika Uislamu
NENO LA MCHAPISHAJI Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya Kiswahili ya kitabu cha Kiarabu kiitwacho, ar-Ri’ayatu ‘s-Swihiyyah Fi ‘l-Islam kilichoandikwa na Jopo la Wataalamu la Taasisi a Balagha. Sisi tumekiita, Huduma ya Afya katika Uislamu. Afya ya mwili kwa mwanadamu ni kitu muhimu sana. Ili mwanadamu aweze kuyajenga maisha yake na kuwa bora kimwili, lazima awe na afya bora, na sio tu kwa ajili ya kuendesha maisha yake, bali pia bila afya nzuri mtu hawezi kutekeleza ibada zake sawasawa jinsi inavyotakiwa kuifanya. Hivyo, kama Uislamu ulivyo kwamba ni dini na ni mfumo kamili wa maisha, umeelezea kwa kina huduma ya afya, yaani mtu akiwa nini ili ajipatie afya njema. Waandishi wa kitabu hiki wameelezea mambo mbalimbali ambayo yanapaswa kufanywa kwa ajili ya afya ya mtu binafsi na ya jamii kwa ujumla. Katika maelezo yao wamezingatia Qur’ani Tukufu, Sunna pamoja na mafundisho ya Maimamu Watukufu. Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote, ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni mambo ambayo hayana nafasi tena katika akili za watu. Kutokana na ukweli huo, Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili. D
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:25 PM
Page E
Huduma ya Afya katika Uislamu Tunamshukuru ndugu yetu, Hemedi Lubumba kwa kukubali jukumu hili la kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake. Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa ni changamoto kubwa kwa wasomaji wetu. Mchapishaji: Al-Itrah Foundation
E
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
F
7/1/2011
4:25 PM
Page F
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:25 PM
Page 1
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:25 PM
Page 2
Huduma ya Afya katika Uislamu Kila sifa njema ni ya Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa viumbe vyote. Rehema na amani zimwendee Muhammad na aali zake watoharifu na Sahaba zake walio wema. Kanuni na taaluma za kibinadamu zimeamiliana na mwanadamu kwa msingi wa mahitaji ya kimwili pekee, hivyo zikajali na kutilia umuhimu masuala ya kimada tu na zimepuuzia mahitaji yake ya kiroho, jambo ambalo limefanya utatuzi wake ushindwe kuzaa matunda yoyote kwani kila wanapojaribu kutatua upande huu upande ule nao huharibika. Hiyo ni kwa sababu mwanadamu tangu mwanzo ni roho na mwili na bado ndivyo alivyo, na ukweli huo haujakanushwa ila na yule aliyejitenga, na bila shaka aliyekanusha hajabadili chochote katika ukweli wake halisi. Mkabala na mtazamo huo tunazikuta dini za kimapokezi – zisizokuwa Uislamu – kutokana na mageuzi na mabadiliko yaliyozifika katika historia zinaamiliana na mwanadamu kwa mtazamo mwingine usiokuwa sawa japokuwa ni kwa namna nyingine, pale walipopuuzia mahitaji ya mwanadamu ya kimwili na mahitaji yake ya kimada hivyo wakaifanya dini kuwa ni ibada tu za kiroho, na hatimaye wameyafunga mafanikio ya mtu kwenye hali ya kujitenga na dunia na kuacha ladha na yote aliyohalalisha Mwenyezi Mungu. Uislamu ulipambana na hali hizo zote mbili tangu pale tu ulipoteremka. Mwenyezi Mungu anasema: “Na uruhubani wameuzusha, sisi hatukuwaandikia” (Sura Hadid: 27). Kwani dini ilikuja ili kunadhimu maisha ya kweli ya mwanadamu, na mweka sheria ni Yule Mjuzi wa vile alivyoviumba Naye ni Mpole kwa waja wake. Hivyo hawezi kuipuuzia dunia na hali ameiumba kwa ajili ya waja wake. Amesema: “Sema: Ni nani aliyeharamisha mapambo ya Mwenyezi Mungu ambayo amewatolea waja wake na vitu vizuri vya riziki” (Sura Aaraf: 32). Kama ambavyo roho ina mchango mkubwa katika afya ya mwanadamu na usalama wa fikra zake, ndivyo hivyo hivyo mwili nao ulivyo na mchango 2
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:25 PM
Page 3
Huduma ya Afya katika Uislamu mkubwa kwa mwanadamu katika kutekeleza jukumu lake maishani, katika kujenga utu wake na kujenga jamii yake. Kwa ajili hiyo Uislamu umejali sana kanuni za afya ambazo zinawezesha sehemu kubwa ya ibada kutekelezwa na pia zinazohusu miamala mbalimbali. Kama ambavyo Uislamu umeweka sheria zinazohalalisha, zinazowajibisha na kuharamisha ili kudhamini usalama wa mtu na roho yake, pia una sheria nyingi zinazodhamini usalama wa mwili wa mwanadamu na kulinda afya yake. Anayesoma hazina adhimu ya Uislamu katika mchepuo huu na ule bila shaka atafikia ukweli kwamba dini hii ni dini ya wastani katika kila kitu ikiwemo mahitaji ya roho na mwili, dunia na Akhera. Tunafuraha katika maudhui hii kutoa uchambuzi tulionao ambao unakamilishwa na uchambuzi uliotangulia kuhusu Afya ya mwili katika Uislamu, tunataraji utarejea huko ili kufaidika zaidi. Taufiki ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Muasasatul-Balagha. AFYA NA UMBILE LA MWANADAMU Mwenywezi Mungu amesema ndani ya Kitabu Chake kitukufu:
“Ewe mwanadamu! Ni nini kikudanganyacho na Mola wako Mlezi Mtukufu. Aliyekuumba na kukutengeneza, kisha akakulinganisha sawa. Katika sura yoyote aliyoitaka amekutengeneza.” (Sura alInfitar: 6 – 8).
3
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:25 PM
Page 4
Huduma ya Afya katika Uislamu Akasema pia:
“Ndio sanaa ya Mwenyezi Mungu aliyekitengeneza kila kitu.” (Sura Namlu: 88). Akasema tena: “Bila shaka tumemuumba mtu katika hali nzuri sana.” (Sura Tini: 4). Imepokewa kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.w) - kwamba alisema: “Neema mbili hazithaminiwi: Amani na afya.” Kila kilichomo ndani ya ulimwengu huu kinathibitisha hekima na ufanisi wa muumba wake, na mwanadamu ni sehemu ya ulimwengu huu wa kimada, ameumbwa kutokana na udongo wa ardhi hii na umbile lake la kimwili limenadhimika kulingana na mpangilio wa kinidhamu wenye kushangaza. Mwili wa mwanadamu ni mfumo wa kipekee wa uhai katika ulimwengu wa viumbe, hufanya kazi ndani yake chembechembe hai, viungo na mashine kwa umakini na mpangilio makini. Asili katika mpangilio wa umbile ni afya, ukamilifu na ufanisi, kwa ajili hiyo imepokewa hadithi toka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwamba alisema katika kuitambulisha dosari: “Ni ile iliyozidi juu ya umbile.” Yaani kila kisichokuwa katika asili ya umbile ni dosari. Mwenyezi Mungu amemuumba mwanadamu hali kasalimika na dosari, maradhi na upungufu. Bali maradhi humpata mwanadamu kutokana na kuvurugika mpangilio wa mwili kwa sababu ya visababishi na viathiri vya nje kuvuruga mpangilio wa umbile, kwa ajili hiyo tunaiona Qur’ani Tukufu inamkumbusha mwanadamu neema za Mwenyezi Mungu juu yake, umakini uliopo kwenye sanaa, hekima na ufanisi uliopo katika viumbe. Tunalisoma hilo kwa uwazi katika kauli Yake: 4
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:25 PM
Page 5
Huduma ya Afya katika Uislamu
“Aliyekuumba na kukutengeneza, kisha akakulinganisha sawa.” (Sura al-Infitar: 6 ).
“Ndio sanaa ya Mwenyezi Mungu aliyekitengeneza kila kitu.” (Sura Namlu: 88).
“Bila shaka tumemuumba mtu katika hali nzuri sana.” (Sura Tini: 4). Hivyo kuanzia chembechembe hai hadi kiungo katika mwili wa mwanadamu kinafanya kazi kwa umakini na ufanisi ndani ya mipangilio na harakati zenye kuungana zilizokamilika. Chembechembe hai zina mpangilio wake makhususi katika mwili, kiungo kina mpangilio wake makhususi na mshipa una mpangilio wake makhususi, na yote ipo chini ya mpangilio mmoja na muungano mmoja wa kimajukumu uliokamilika, na pindi mpangilio wa mwili unapopatwa na mvurugiko au dosari ndipo mwanadamu huugua, ndio maana ugonjwa ukatambulishwa kuwa ni: Kutoka nje ya unyoofu makhususi wa mwanadamu.1
1 Muujamu Mufradati Alfadhil-Qur’ani cha ar-Raghib al-Isfihaniy. 5
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:25 PM
Page 6
Huduma ya Afya katika Uislamu
KUUJALI MWILI NA KUUTUNZA Miongoni mwa fikra na sheria ya Uislamu ni ulingano na uwiano na usawa kati ya mwili, akili, roho na nafsi. Kuujali kwake mwili na kutunza afya ya mwili ni kwa hali ya juu mno, kwa ajili hiyo umeuwekea mwili haki za kimaada ambazo umeziwajibisha juu ya mwanadamu mwenyewe, na juu ya dola na jamii pindi mtu binafsi mwenyewe anaposhindwa kuutekelezea mwili wake haki zake. Mwili una haki ya chakula, kinywaji, mavazi, tiba na makazi, achilia mbali mapumziko, usingizi na kinga. Qur’ani imezungumzia chakula, mlo na kujali mahitaji ya mwili, inathibitisha kwamba kupata usalama wa kichakula ni haki ya mwanadamu na kwamba ni sehemu ya mpangilio wa uwepo wa ulimwengu. Aya Tukufu imebainisha maana hii kwa maandiko yake ambayo yanazungumzia ardhi na riziki, Mwenyezi Mungu amesema: “Na akapima humo chakula chake katika hatua nne, ni sawa kwa waulizao.” (Sura Haa Mim: 10). Na katika sehemu nyingine ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu tunakuta ufafanuzi wa ukweli huu kwa Adam baba wa wanadamu wote, anasema Mwenyezi Mungu:
“Hakika hutakuwa mwenye njaa humo wala hutakuwa uchi. Na kwa hakika hutapata kiu humo wala hutapata joto.” (Sura Twaha: 18 – 19). Ameweka hayo yote na ameweka kanuni na mpangilio wa lazima ili kutimiza haja ya chakula kwa mwanadamu, kama vile sheria ya Zaka ambayo imefaradhishwa katika vyakula, ngano, shairi, tende, zabibu, kondoo na mbuzi, ng’ombe na ngamia, kama ambavyo pia imefaradhishwa katika pesa na ikawa ni sunna katika mbegu na matunda yaliyobakia.
6
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:25 PM
Page 7
Huduma ya Afya katika Uislamu Na Qur’ani ikawalaumu wale wanaolimbikiza dhahabu, fedha na mali huku wakiwakosesha wengine kustarehe na yale wenye haja nayo miongoni mwa chakula na vinywaji, na ikawaita mafakiri kwamba ni waliokoseshwa, ikawasifu wale ambao katika mali zao wametenga fungu kwa ajili ya kutatua matatizo ya waliokoseshwa, ikasema: “Na katika mali zao kuna haki ya mwenye kuomba na anayejizuia.� (Sura Dhariyat: 19). Na ili walafi na maadui wa ubinadamu wasichezee chakula cha tabaka fakiri Uislamu umeharamisha kulangua chakula, na umeipa dola, waamrishaji wa mema na kukataza mabaya na wenye kufanya kazi katika sekta ya uhasibu haki ya kuzuia ulanguzi na kumlazimisha mwenye kulangua kukipeleka sokoni chakula kilicholanguliwa ili bidhaa za chakula zipatikane, na bei zishuke kutokana na wingi wa chakula masokoni. Na katika kusoma maelekezo ya kiafya na umuhimu wa chakula tunagundua jinsi sheria na fikra ya Uislamu ilivyojali elimu ya chakula na malezi ya kiafya, hivyo tunakuta inahimiza kula vyakula na milo ambayo itawezesha mwili kukua katika hali ya afya na kuutimizia kinga imara dhidi ya magonjwa na dhidi ya sababu za udhoofu. Tunaweza kufupisha mfumo wa afya katika Uislamu na kujali kwake afya ya mwili kwa haya yafuatayo: Kwanza - Chakula bora: Uislamu umejali chakula bora na umewahimiza wazazi hasa mwanamke mjamzito na mwenye kunyonyesha kula baadhi ya vyakula ili kulinda afya ya mimba na kuipatia sifa ya uzuri. Na umetilia msisitizo katika kujali chakula cha mtoto kutokana na chakula kilivyo na athari katika afya ya mimba na usalama wa makuzi ya mwili na uzuri wa sura.
7
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:25 PM
Page 8
Huduma ya Afya katika Uislamu Tunaweza kuuona ukweli muhimu wa kielimu, nao ni kwamba kitendo cha Uislamu kutilia umuhimu sheria ya chakula si chini ya kitendo chake cha kutilia umuhimu sheria ya ibada na nidhamu ya jamii, hilo tunalikuta kwa uwazi kabisa katika riwaya na hukumu zake. Kati ya riwaya hizo ni ile iliyopokewa toka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.): “Chakula cha kwanza kwa mwanamke anayekaribia kujifungua kiwe ni tende laini, kwani hakika Mwenyezi Mungu alimwambia Mariam: ‘Na litikise kwako shina la mtende, litakuangushia tende nzuri, zilizoiva.’”2 Akasema tena: “Wanawake wanaokaribia kujifungua hawana tiba mfano wa tende laini, kwa sababu Mwenyezi Mungu alimlisha Mariam tende laini nzuri wakati wa uchungu wake.”3 Utafiti wa kielimu unaonyesha kwamba tende humtengenezea mwanadamu uwiano wa chakula kati ya sukari, protini, wanga, mafuta, madini na vitamini. Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Wanywesheni wanenu uji wa ngano na shairi udogoni mwao, kwani hakika (chakula) hicho huotesha nyama na kukomaza mifupa.”4 Imam Ali bin Musa ar-Ridha (a.s.) amesema: “Hakuna Nabii yeyote ila alimwombea mwenye kula shairi na kumbariki.”5 Imam Ja’far as-Sadiq (a.s.) amesema: “Mlisheni mwenye ugonjwa wa tumbo la kuachia mkate wa mchele, hakuna kitu kiingiacho katika tumbo la mwenye tumbo la kuachia chenye manufaa kushinda wenyewe.”6 2 Muujamu Mufradati Alfadhil-Qur’ani cha ar-Raghib al-Isfihaniy, Uk. 134. 3 Muujamu Mufradati Alfadhil-Qur’ani cha ar-Raghib al-Isfihaniy, Uk. 134. 4 Biharul-An’war Juz. 104, Uk. 105. 5 Biharul-An’war Juz. 17, Uk. 4. 6 Biharul-An’war Juz. 104, Uk. 5. 8
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:25 PM
Page 9
Huduma ya Afya katika Uislamu Imam Musa bin Ja’far (a.s.) amesema: “Nyama huotesha nyama.”7 Akasema tena: “Kuleni komamanga na maganda yake hakika husafisha utumbo.”8 Na kutoka kwa Ibrahim bin Abdul-Hamidi amesema: Nilimsikia AbulHasan akisema: “Jitahidini kula samaki, ukimla bila mkate atakutosheleza, na ukimla na mkate atakunufaisha.”9 Imam as-Sadiq (a.s.) amesema: “Nabii miongoni mwa Manabii wa Mwenyezi Mungu alimlalamikia Mwenyezi Mungu upungufu wa kizazi. Akasema: Kula nyama na mayai.” 10 Na pia amesema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alikuwa akila asali na kusema: Ina Aya nyingi toka katika Qur’ani.”11 Imam as-Sadiq (a.s.) alikuwa akisema: “Watu hawakupewa tiba mfano wa asali.”12 Na akisema: “Walisheni watoto wenu komamanga, kwani ndilo lililo jepesi zaidi kwa ujana wao.”13 Na pia akisema kuhusu mwanamke mjamzito anayekula pera: “Hakika mtoto atakuwa mwenye harufu nzuri na rangi ya kuvutia.”14 Na kuna maelekezo lukuki yanayousia kula matunda, mboga mboga na aina za nyama na mboga za majani, pia yanatoa wito wa kutilia umuhimu chakula cha mwili na kulinda uwiano wa chakula na mwili. 7 Biharul-An’war Juz. 104, Uk. 12. 8 Biharul-An’war Juz. 104, Uk. 16. 9 Biharul-An’war Juz. 104, Uk. 53. 10 Biharul-An’war Juz. 104, Uk. 57. 11 Biharul-An’war Juz. 104 Uk. 63. 12 Biharul-An’war Juz. 104 Uk. 73. 13 Biharul-An’war Juz. 104 Uk. 105. 14 Wasailus-Shia Juz. 7 Uk. 133, chapa ya Daru Ihyaut-Turathil-Arabiy 9
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:25 PM
Page 10
Huduma ya Afya katika Uislamu Pili: Kutokula baadhi ya vyakula: Uislamu umeharamisha baadhi ya vyakula, vinywaji na vitendo vyenye kudhuru afya ya mwili, na huenda mfano ulio kinara katika mfumo wa Uislam na sheria ya afya kwa ajili ya kulinda afya na kuhakikisha usalama wa kiafya ni kuharamisha kwake baadhi ya vyakula na vinywaji na vitendo vinavyodhuru mwili. Uislamu umeharamisha pombe, madawa ya kulevya, zinaa, kulawiti, kusagana, ukuwadi, damu, nyama ya nguruwe na mengineyo mengi, kama ulivyoharamisha kila ambalo asili yake ni kudhuru mwili, ikifuata kanuni isemayo: “Hakuna kudhuru wala kujidhuru,” Ambayo imepatikana katika kauli ya Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.). Katika jibu la Imam al-Baqir (a.s.) alilolitoa kwa mtu mmoja aliyemuuliza, tunapata ufumbuzi wa kielimu wa hekima ya uhalali na uharamu, muulizaji alisema: Kwa nini Mwenyezi Mungu aliharamisha pombe, mzoga, nyama ya nguruwe na damu? Akasema: “Hakika Mwenyezi Mungu hajaharamisha hayo kwa waja wake na akawahalalashia yasiyokuwa hayo kwa kutamani yale aliyowahalalishia na wala si kwa kutohitaji yale aliyowaharamishia, lakini aliumba viumbe na akajua yale yanayojenga miili yao na yanayowafaa wao, hivyo akawahalalishia na kuyaruhusu kwao, na akajua yanayowadhuru hivyo akawakataza hayo, kisha akahalalisha kwa yule aliye katika dhiki katika wakati ambao hakuna cha kuusaidia mwili wake ila hicho.” Hivyo kipimo cha uhalali ni “yale yanayojenga miili yao na yanayowafaa wao, hivyo akawahalalishia.” Na kipimo cha uharamu ni “yanayowadhuru hivyo akawakataza hayo.” Sayansi na uchunguzi wa kielimu umethibitisha kwamba magonjwa yaliyo hatari sana hivi sasa kwa afya ya mwanadamu sababu yake ni pombe, ngono ya kinyume na maumbile na ngono iliyo nje ya sheria, kama vile zinaa na mengineyo miongoni mwa aina za uharibifu wa kitabia. Na huenda janga la Ukimwi ndio janga baya mno lenye kutisha linalotishia maisha ya mwanadamu na ambalo sababu yake kuu ni ngono 10
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:25 PM
Page 11
Huduma ya Afya katika Uislamu zisizo za kisheria. Ama magonjwa yasababishwayo na pombe na madawa ya kulevya na yenye kuidhuru afya huzingatiwa kuwa ndio aina kubwa mno ya magonjwa na hatari zaidi kwa afya na usalama wa jamii. Magonjwa hayo hayaidhuru afya tu bali yanadhuru pia hali ya uchumi na usalama. Kesi nyingi za jinai za mauwaji na uporaji, ubakaji na ajali za barabarani sababu yake ni pombe na madawa ya kulevya. Ni mali nyingi kiasi gani hutolewa na dola na serikali katika kutatua bila mafanikio madhara yasababishwayo na pombe na madawa ya kulevya? Tatu: Kutofanya ubadhirifu: Uislamu umekataza kufanya ubadhirifu, na miongoni mwa vitendo hatari juu ya afya ya mwili ni kufanya ubadhirifu katika chakula, vinywaji na ngono. Maradhi mengi ya mwili sababu yake ni kuendekeza na kufuata matamanio ya mwili, ubadhirifu wa kupindukia katika kula na kunywa, kwa ajili hiyo Qur’ani imekataza kufanya ubadhirifu katika chakula na vinywaji na mengineyo. Mwenyezi Mungu amesema: “Kuleni na kunyweni wala msifanye ubadhirifu.” Mtume Mtukufu amesema: “Mwanadamu hakujaza chombo shari kushinda tumbo lake.” Kama alivyosema tena: “Utumbo ni nyumba ya magonjwa, na kujithamini ni kinara wa dawa.” Kwa sheria hizi za afya na kumwelimisha mwanadamu madhara ya ubadhirifu na kumkataza kufanya hivyo Uislamu umetoa wasia wa mbele kabisa wa kuilinda afya, nao ni wasia wa Kinga dhidi ya Maradhi, kwa kuifanyia kazi hekima mashuhuri: “Kinga ni bora kuliko tiba.” Nne: Kufuata kanuni za usafi: Kwa kuweka sheria ya tohara na kutoa wito wa usafi Uislamu unakuwa umeweka mfumo mpana wa kumuhami mwanadamu na mazingira dhidi ya uchafuzi na uchafu na vyanzo vya madhara ya kiafya. Tunaweza kufupisha 11
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:25 PM
Page 12
Huduma ya Afya katika Uislamu mfumo wa Uislamu katika sekta hii katika mambo mawili ya msingi, nayo ni: i. Uislamu umezingatia kwamba baadhi ya vitu ni najisi na ukalazimisha kujitenga navyo. Na najisi hizi ndio chanzo kikuu na kikubwa cha vijidudu na bakteria wa maradhi, kama vile haja kubwa na haja ndogo na kinyesi cha wanyama wengi, mizoga, damu, manii na vitu vingine vilivyonajisika kwa najisi hizo. Vinyesi hivyo na vitu hivyo hutengeneza chanzo cha uchafu na kupatwa na maradhi. Hivyo kwa kujitoharisha na kujikinga dhidi ya vitu hivyo tunakuwa tumejenga msingi muhimu katika kujikinga na maradhi na kuilinda afya. ii. Usafi: Usafi hutengeneza sura ya wazi miongoni mwa sura za mwanadamu aliyestaarabika ambaye anajali afya yake, akili yake na mwonekano wake. Uislamu umekuja ili kutimiza masilahi na kuondoa uharibifu, na kinara wa masilahi hayo ni kulinda afya ya mwanadamu na kuipa heshima akili yake na mwamko wake katika afya na ustaarabu. Hivi leo vipaumbele vya mwanadamu na tafiti zake za kielimu hasahasa huwa ni katika kuyalinda mazingira na kuyahifadhi dhidi ya uchafu na vyanzo vya uchafuzi ambavyo vimekuwa ni miongoni mwa matatizo ya sasa. Kwa kufuata mfumo wa Uislamu katika usafi na tohara unatuhakikishia ulinzi wa mazingira na kuhifadhi afya na kuokoka dhidi ya maradhi ambayo hutokana na kupuuza usafi na kueneza uchafu. Umekuja msisitizo juu ya usafi na wito wa kujiepusha na uchafu, tunalipata hilo wazi wazi katika ubainifu wa Qur’ani Tukufu:
“Mwenyezi Mungu hapendi kukutieni katika taabu, lakini anataka kukutakaseni na kutimiza neema yake juu yenu ili mpate kushukuru.” (Sura Maida: 6). 12
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:25 PM
Page 13
Huduma ya Afya katika Uislamu Tukiichunguza Aya hii ya tohara tunaikuta Qur’ani imezingatia kujitoharisha na uchafu ni kutimiza neema za Mwenyezi Mungu juu ya mwanadamu ambazo zinastahiki shukrani. Hiyo ni kwa sababu tohara ni moja ya vyanzo vya afya, na afya ni moja ya neema mbili ambazo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amemkumbusha kwazo mwanadamu: “Neema mbili hazithaminiwi: amani na afya.” Na katika maelekezo ya Nabii tunapata wito wa kujiepusha na uchafu na takataka, na kuhakikisha usafi katika mavazi, nyumba na mwili. Hayo yamekuja kwa kauli yake (s.a.w.w.): “Jisafisheni, hakika Uislamu ni msafi.” “Hakika Mwenyezi Mungu huchukia uchafu rafurafu.” “Ni mja mbaya aliyoje! Yule aliye mchafu.” Tano: Michezo: Michezo ni mkusanyiko wa vitendo na mazoezi ambayo hukuza uwezo wa mwanadamu na nguvu yake na kumhakikishia mwanadamu uwiano wa kimwili, kama vile kuogelea, upandaji wa ngamia, kutembea kwa miguu, mieleka na mengineyo miongoni mwa mazoezi mingine. Michezo kama hii ya kimazoezi hukuza nguvu za mwili katika kufanya kazi na uzalishaji, kama ambavyo huuongezea mwili uwezo wake wa kupambana na maradhi na mazingira ya afya ambayo huzorota kwa kuleta maradhi. Uislamu katika mfumo wake wa kiroho umesisitiza kuujali mwili na kuulinda mwili kwa mazoezi ili kukuza uwezo wa mwanadamu na nguvu zake, ili ujenge kizazi chenye miili imara na roho imara. Miongoni mwa kanuni hizo ni ile iliyokuja katika kauli ya Mwenyezi Mungu kuhusu jihadi na kutetea sheria, nchi na masilahi ya kisheria: “Na waandalieni nguvu muwezavyo, na kwa farasi waliofungwa..” (Surat Anfal: 60). Kanuni hiyo ambayo Mtukufu Mtume aliifasiri katika kauli zake nyingi na vitendo vyake, kama kauli ya Mtume: “Wafunzeni wanenu shabaha, uogeleaji na upandaji ngamia.” Na miongoni mwa tafsiri zake ni kushiriki kwake mwenyewe katika mashindano ya ngamia na mieleka, bali alikuwa akiweka zawadi kwa wenye kushinda katika mbio za ngamia na akiwashajiisha kufanya 13
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:25 PM
Page 14
Huduma ya Afya katika Uislamu hivyo. Mtume alishindana zaidi ya mara moja na akashinda kama ambavyo ngamia wake alishindwa mara moja. Na katika maadhishi ya Sharia ya Uislam tunapata hukumu makhsusi zinazohusu mashindano ya mbio, shabaha na zawadi ili kunadhimu mazoezi haya. Kama alivyoshiriki yeye mwenyewe (s.a.w.w.) katika mashindano na akahimiza kushiriki na akaweka zawadi kwa wenye kushinda pia aliingia katika shindano la mieleka pamoja na Rukana bin Yazid, na huyu alikuwa ni mwanamieleka mashuhuri lakini Mtume akamshinda. Kama alivyokuwa hodari wa mieleke, mbio za ngamia pia alikuwa anajua kuogelea, alijifunza hilo katika bwawa la Bani Adiy tangu angali mdogo. Na lililo wazi katika kanuni za sheria ya Uislamu ni kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) ni kigezo katika kila kitu, na pindi anapofanya kitu huwa kwa hali hiyo amethibitisha sheria kwa mwanadamu na mfumo wa matendo, maadamu tu kitendo hicho si makhususi kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Sita: Kujishughulisha na kuacha kujibwetesha: Mwenyezi Mungu anasema: “Yeye ndiye aliyefanya ardhi laini kwa ajili yenu, basi nendeni katika pande zake na kuleni katika riziki zake, na kwake ndio marejeo.” (Sura Mulki: 15). Katika Aya hii tukufu Qur’ani imemsisitizia mwanadamu kujituma ardhini kwa ajili ya kutafuta riziki na kipato cha halali, na kujituma ni kufanya harakati na kufanya kazi, na harakati na kazi ni vyanzo viwili muhimu vya uchangamfu na nguvu. Imekuja kauli kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Ibada ina sehemu sabini, iliyo bora kushinda nyingine ni kutafuta halali.” Na pia akasema: “Mwenyezi Mungu humchukia mja asiyejishughulisha mwingi wa kulala.”
14
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:25 PM
Page 15
Huduma ya Afya katika Uislamu Kazi haitoi faida za kiuchumi na kipato tu, bali pia humhakikishia mwanadamu faida ya afya, kwani kazi ni juhudi za mwili, hukuza uwezo wa mwanadamu na nguvu zake za kimwili, humpa afya, uhai na nguvu za mwili ambazo katika baadhi ya nyakati hushinda mazoezi na harakati za kimichezo. Kama ambavyo kazi ina athari chanya katika kuujenga mwili na kuupa kinga ya afya pia ina athari za kisaikolojia katika nafsi ya mwanadamu. Matatizo mengi ya kisaikolojia ya mwanadamu sababu yake ni kujibwetesha na kutojishughuliasha, na hivyo hali ya maradhi na machungu ya kisaikolojia hugeuka na kuwa machungu na maradhi ya kimwili. Na kama ambavyo kazi ni chanzo miongoni mwa vyanzo vya nguvu na uchangamfu wa kisaikolojia na kimwili, kujibwetesha na kutojishughulisha ni chanzo miongoni mwa vyanzo vya kudhoofika kwa mwili na kupotea nguvu zake. Saba: Kinga na tiba: Hakika sheria na maelekezo ambayo yanazungumzia afya, kinga, tiba na haki za mwili yanatengeneza uwanja mpana katika Fiqhi, elimu na mafunzo ya Uislamu. Kanuni na wasia wa Uislamu vimetilia mkazo mpaka kiwango cha wajibu kuujali mwili, kuilinda afya na kutibu maradhi, kwani maradhi hayatibiki ila kwa matibabu, kwa ajili hiyo Uislamu umezingatia kwamba matumizi ya mwanadamu ya mwaka anayoyahitajia katika kugharamia matibabu na huduma za afya kwa ajili yake mwenyewe na wanafamilia yake yamesameheka kodi ya wajibu ya Zaka na Khumsi. Na kwa ajili ya Uislamu kutilia mkazo matibabu na dawa sheria ya Uislamu imezingatia kwamba upatikanaji wa dawa, maabara na taasisi za tiba katika jamii ni wajibu wa kujitosheleza, kama ambavyo umezingatia matibabu kuwa ni wajibu wa mtu binafsi juu ya tabibu mtoa tiba ambaye yuko peke yake iwapo hapatikani mwingine. Ikiwa wajibu wa kuhakikisha maabara za tiba zinapatikana ni wajibu wa wanajamii wote basi kujitibu na kugharamia matibabu ya lazima ni wajibu kwa mtu binafsi ili aweze kujitibu na kumtibu yule ambaye kisheria matumizi yake yako juu yake, 15
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:25 PM
Page 16
Huduma ya Afya katika Uislamu kama vile mke, watoto wadogo, wazazi wawili wasioweza kujihudumia. Akiwa hana uwezo wa kufanya hivyo hupewa fungu toka katika mapato ya kisheria ili agharamie dawa na matibabu. Zaidi ya hapo ni kwamba dola inawajibika kuwatimizia wananchi wake wasiojiweza huduma ya matibabu na yote yanayoambatana na matibabu hayo. Uislamu katika wajibu wa matibabu umeanzia kwenye kanuni ya msingi katika kuifahamu afya, maradhi na tiba, na katika mtazamo wake wa kiitikadi na nadharia yake ya kifalsafa kuhusu uhai na maisha. Hivyo fikra ya Uislamu inaamini kuwa ulimwengu wote ni ulimwengu umesimama juu ya msingi wa kanuni ya sababu na falsafa ya uwepo wa uhusiano baina ya vitu, hivyo ulimwengu ni mnyororo wa sababu na matokeo, hivyo ugonjwa ni matokeo ya sababu na ila, na kwamba tiba huja kuondoa sababu hizo na ila hizo kupitia sababu nyingine na ila nyingine. Na kwamba uhusiano kati ya ugonjwa na tiba ni sehemu ya mpangilio wa mvutano uliopo katika ulimwengu wa mada na viumbe na katika wigo wa mwili wa mwanadamu. Ugonjwa katika hali zake nyingi ni sehemu ya mvutano huu, hivyo tiba huenda kulingana na mpangilio wa mvutano na kanuni ya sababu na kisababishwa. Fikra hii ya kielimu tunaisoma katika maelekezo ya kitabibu aliyoyatoa Mtukufu Mtume, na kutoka katika amri zake za kuamrisha tiba. Hakika kukimbilia kwenye matibabu kunaafikiana na imani ya Uislamu ambayo inakusanya baina ya kuamini kanuni ya sababu na mada na baina ya kumtegemea Mwenyezi Mungu. Hiyo ni kwa sababu ila na sababu za kimada hufuata nguvu za Mungu na msaada wake, hivyo sababu na ila kama alivyoeleza Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ni sehemu ya uwezo wa Mwenyezi Mungu. Hivyo umekuja msisitizo juu ya matibabu na kutumia dawa, na umekuja ufafanuzi wa uhusiano uliopo baina ya sababu za kimatibabu na uwezo wa Mungu. Imepokewa kutoka kwa Abu Huraira, kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) kwamba alisema: “Mwenyezi Mungu hakuleta ugonjwa ila aliushushia
16
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:25 PM
Page 17
Huduma ya Afya katika Uislamu tiba.”15 Na kutoka kwa Jabir bin Abdillah al-Ansariy amesema Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Kila ugonjwa una dawa, dawa ikiupata ugonjwa hupona kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.”16 Na imekuja katika habari kwamba: Hakika Musa bin Imran (a.s.) aliugua, wana wa Israil wakaingia kwake na wakautambua ugonjwa wake. Wakamwambia: Ungetumia dawa fulani ungepona. Akasema: Situmii dawa mpaka Mwenyezi Mungu anipe afya njema bila dawa. Ndipo Mwenyezi Mungu akampelekea wahyi: “Naapa kwa nguvu Zangu na utukufu Wangu, sikuponyeshi mpaka utumie dawa waliyokutajia.” Akawaambia: Nipeni dawa mliyoitaja. Wakampa dawa naye akapona. Akaingiwa na khofu nafsini mwake kwa hilo, ndipo Mwenyezi Mungu akampelekea wahyi: “Ulitaka kuvunja hikima yangu kwa tawakuli yako kwangu, basi ni nani asiyekuwa mimi aliyeweka katika mti wa Aqaqiri manufaa ya vitu!”17 Ahmad bin Hanbali ameandika katika Musnad yake kwamba Usama bin Sharik alisema: Nilikuwa kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ndipo wakaja mabedui na kusema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Tutumie dawa? Akasema: “Ndio enyi waja wa Mwenyezi Mungu tumieni dawa, hakika Mwenyezi Mungu hajaleta ugonjwa ila una tiba ila ugonjwa mmoja.” Wakasema ni upi? Akasema: “Ukongwe.”18 Kama alivyobainisha matibabu na utumiaji wa dawa pia alibainisha kwamba kila maradhi yana tiba isipokuwa ni kwamba sisi hatuijui, hivyo akawajibisha kufanya utafiti na kuitafuta ili kuigundua, hilo limekuja katika kauli yake (s.a.w.w.): “Hakika Mwenyezi Mungu hajaleta ugonjwa ila aliteremsha dawa yake, elimu yake ni toka katika Ujuzi Wake na hajaijua asiyeijua.” 15 Sahih Bukhar Juz. 7, Uk. 12. 16 Sahih Muslim, Mlango wa tiba. 17 Jamius-Saadat, chapa ya tatu, Juz. 3, Uk. 228. 18 Musnad Ahmad bin Hanbal, Mlango wa tiba. 17
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:25 PM
Page 18
Huduma ya Afya katika Uislamu Bali sheria ya Uislamu imezingatia kuficha maradhi na kutoyaeleza kwa tabibu ili ayatibu kwa ufanisi ni kuufanyia khiyana mwili, hivyo imepokewa Hadithi toka kwa Imam as-Sadiq (a.s.) kwamba: “Atakayemficha tabibu maradhi yake ameufanyia khiyana mwili wake.” Na ili kufafanua uhusiano uliyopo baina ya sababu za kimatibabu na baina ya uwezo wa Kimungu tusome aliyoyapokea Abu Khuzama, Hadithi ya Mtume ambayo alizingatia matibabu kuwa ni sehemu ya uwezo wa Mwenyezi Mungu. Alisema: Nikamwambia Mtume wa Mwenyezi Mungu: Unaona hirizi tunazotumia, dawa tunazotumia na kinga tunazoweka, je zinapingana na chochote katika uwezo wa Mwenyezi Mungu? Akasema: “Hayo ni sehemu ya uwezo wa Mwenyezi Mungu.”19 Hivyo ndivyo sheria ya tiba katika Uislamu inavyothibitisha wajibu wa kulinda mwili na kuupatia matibabu na usalama wa kiafya. Mafunzo haya ya kisheria na fikra hii ya kielimu vimeleta mfumo wa kielimu wa utafiti wa kitiba, na hivyo tiba ikaendelea sana mikononi mwa ulamaa wa kiislamu, na ikapanda hadi mustawa wa utafiti wa kielimu na mfumo wa kimaabara, zikagunduliwa nadharia za kitiba katika magonjwa, matibabu, mpangilio wa mwili na umbo lake. Nane: Utatuzi wa matatizo ya kisaikolojia: Uislamu umeweka mfumo wa afya ya kinafsi, kwani uhai wa mwanadamu katika sekta zake zote za kisiasa, uchumi, usalama, akida, afya ya mwili na ya kisaikolojia, mahusianio ya kijamii na kifamilia, zote zimekamilika na zinaathiriana zenyewe kwa zenyewe na kuathirika. Afya ya kisaikolojia ambayo ndio msingi wa wema wa mwanadamu na uovu wake huathiri hali ya mazingira yote ya mwanadamu. Ufakiri, ukosefu wa kazi, ugaidi wa kisiasa, ukosefu wa amani na matatizo ya familia, yote hayo ni sababu zinazoathiri afya ya saikolojia upande wa hasi na chanya. 19 Sahih Ibnu Majah, Mlango wa tiba. 18
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:25 PM
Page 19
Huduma ya Afya katika Uislamu Mfumo wa Uislamu ni mfumo wa kielimu uliokamilika ulioweka ufanisi katika sekta zake mbalimbali na katika utatuzi wake mbalimbali, na kwa namna ambayo unamhakikishia mwanadamu afya na utulivu wa nafsi. Zaidi ya hapo ni ule mfumo wake wa kimalezi katika sekta ya kuhifadhi usalama wa hali ya kisaikolojia dhidi ya mifundo na maradhi ya nafsi. Uislamu katika sehemu kubwa ya fikra zake na sheria yake umetilia umuhimu suala la kuihami hali ya kisaikolojia dhidi ya khofu, huzuni, hikdi, umimi, husuda na wivu kwa mwanamke. Kwa ajili hiyo umeichorea nafsi ya mwanadamu msitari wa kupita na mfumo wa kufuata ambao utaihami nafsi na maradhi ambayo huipata na kuiangamiza yenyewe na mwili wake. Tisa: Kutokomeza ufakiri: Ufakiri ni sababu hatari miongoni mwa sababu za maradhi na ukosefu wa afya bora ya kinafsi na kimwili. Pamoja na maendeleo ya kielimu na ya kiviwanda bado ufakiri umekuwa ni tatizo kubwa kwa mwanadamu, hiyo ni kwa sababu maendeleo ya kielimu na kiviwanda hayajachangia chochote katika kuutengeneza ubinadamu na tabia za mwanadamu, hivyo kila hali ya kiuchumi inavyokua kwa mwanadamu mjeuri ndivyo hali yake ya kinafsi inavyoporomoka na kumong’onyoka kimaadili, na hapo huzidisha dhulma, ulafi, kupenda mali na kuhodhi vyanzo vya mwanadamu dhaifu, jambo ambalo huwazidishia mafakiri tatizo na kupanuka uwanja wa ufakiri. Na huenda maradhi mabaya mno kati ya maradhi ya ufakiri ni uduni wa chakula na ukosefu wa chakula kinachowiana na afya ya mwanadamu. Mwili mahitaji yake ni protini, vitamini, wanga, sukari na mafuta, hivyo mwili unapokosa mahitaji ya kivyakula hupatwa na magonjwa mbalimbali na udhaifu wa kupambana na maradhi na hatimaye ni kuporomoka kwa afya na nguvu. Litakapotatuliwa tatizo la ufakiri tutaweza kuyatokomeza maradhi haya ya kifakiri. Kama ambavyo ufakiri moja kwa moja huleta maradhi yasababishwayo na chakula kutokana na uduni wa chakula pia 19
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:25 PM
Page 20
Huduma ya Afya katika Uislamu husababisha kudhoofika kwa taasisi na sera za kinga, upatikanaji wa maisha ya afya njema na kukosekana kabisa. Uislamu ulipoweka mfumo wake wa uchumi ulizingatia hali ya kumtimizia mwanadamu mahitaji yake ya chakula, makazi, mavazi na dawa, na kumwokoa mwanadamu na ufakiri. Na la kuzingatia katika mfumo wa uchumi wa Uislamu ni kwamba faradhi ya Zaka imejikita katika bidhaa za vyakula, kama vile ngano, tende, shairi, zabibu na wanyama, ukiongezea pesa, jambo ambalo huhakikisha uwepo wa usalama wa kichakula na husaidia kutokomeza maradhi yatokanayo na chakula duni. Kumi: Mapumziko na kulala: Mwili ni ala hai iliyojaa harakati, utendaji na uchangamfu, hivyo hupatwa na uchovu na mchoko, na kama hautapata mapumziko na maandalizi ya nishati ya harakati mpya hupatwa na maangamizi, mmong’onyoko na maradhi. Mwenyezi Mungu amekadiria mpangilio wa usingizi kuwa mapumziko ya fikra, nafsi na mwili, na ili kupangilia uhai wa mwanadamu. Kama ambavyo pia ameweka kwa namna ya uwiano ile kanuni ya kielimu ya kazi, kutoa juhudi na kupumzika, Mwenyezi Mungu amesema: “Na tukaufanya usingizi wenu ni mapumziko. Na tukaufanya usiku vazi. Na tukaufanya mchana kufufuka.” (Sura Nabai: 9 – 11). Kwa Aya hizi amegawa wakati baina ya mapumziko, kazi, harakati na uchangamfu. Na katika maelekezo ya Mtume (s.a.w.w.) kuna msisitizo wa kupunguza kuuchosha mwili, thamani ya mapumziko na kujiwekea udhibiti dhidi ya sababu za tamaa na ulafi ambazo humpelekea mwanadamu kuuchakaza mwili wake, fikra zake na nafsi yake. Kuuchakaza mwili ni sababu miongoni mwa sababu za kuyaharibu maisha ya mwanadamu na kudhoofika kwa nyama za mwili na zaidi ya hapo ni kuudhuru mwili. Kama ambavyo usingizi na mapumziko ni njia bora kati ya njia za kutibu misuli ya mwili na kuupa mwili fursa ya kuirejesha nishati yake. Maelekezo hayo 20
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:25 PM
Page 21
Huduma ya Afya katika Uislamu tunayakuta katika kauli ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Fanyeni wastani katika kutafuta, kwani hakika Roho Mtakatifu aliniambia: Nafsi haitakufa mpaka iwe imechukua riziki yake yote.� Kwa mpangilio huu na ugawaji huu wa wakati baina ya mapumziko, juhudi na kazi, Uislamu umeweka mfumo makini wa kielimu ili kuuhifadhi mwili, nafsi na fikra dhidi ya uchakavu na maradhi.
MARADHI YA KISAIKOLOJIA NA ATHARI ZAKE KATIKA AFYA YA MWILI Hakika miongoni mwa mambo yanayokubalika kimsingi ndani ya fikra za Uislamu ni kwamba kila kimoja kati ya roho, akili na nafsi kina umbo lake, mpangilio wake na kazi yake makhususi, kwamba vitu hivi huathiriana vyenyewe kwa vyenyewe na kuathiriwa. Katika somo letu hili fupi tutajaribu kutoa utambulisho mwepesi wa maradhi ya kisaikolojia na uhusiano wake na maradhi ya kimwili, na pia za maradhi hayo na ugumu wa utibikaji wake hata baada ya kuwa zimeanza nadharia za uchambuzi wa kisaikolojia na majaribio ya kutaka kugundua chanzo cha maradhi na tatizo la kisaikolojia. Pia tutabainisha hali za maradhi ambayo humsumbua mwenye maradhi ya kisaikolojia, na tutabainisha thamani ya kumwamini Mwenyezi Mungu na athari zake katika kuilinda nafsi ya mwabnadamu na tatizo hilo na maradhi hayo, na uwezo wake (huko kumwamini Mwenyezi Mungu) katika kuyatatua na kuyatibu maradhi hayo. Nafsi ya mwanadamu kama unavyoelekeza uchambuzi wa ulamaa wa kiislamu ni umbo lisilokuwa na sifa za kimaada, ni ni chombo chenye kujitergemea, na chombo hiki ni kama mwili, wakati mwingine huwa katika afya njema na hupata pia maradhi na hutibika. Hebu tumsikie mwanafalsafa wa maadili, Sheikh Muhammad Mahdi anNaraqiy mmoja wa ulamaa wa maadili wa kiislamu, hapa anazungumzia 21
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:25 PM
Page 22
Huduma ya Afya katika Uislamu nafsi, mwili na maadili, na yale yanayokisibu kila kimoja kati ya mwili na nafsi miongoni mwa maradhi na mvurugiko katika mpangilio wao. Amesema: “Tambua kwamba mwanadamu ana ndani na nje, roho na mwili, na kila kimoja kati ya hivyo viwili kina mambo yasiyooana nacho na yanayooana nacho, machungu na matamu, yenye kuangamiza na yenye kuokoa. Yasiyooana na mwili na ambayo ndio machungu yake ni maradhi ya kimwili, na yanayoona nao ni afya njema na ladha za mwili. Na elimu yenye dhamana ya kubainisha ufafanuzi wake na matibabu yake ni elimu ya tiba. Ama yasiyoona na roho na ambayo ndio machungu yake ni maadili machafu ambayo humwangamiza mwanadamu na kumsababishia mashaka, ama afya yake njema ni kurejea kwenye maadili mema ambayo yatampa wema na kumwokoa na kumfikisha karibu na watu wa Mwenyezi Mungu na walio karibu Kwake, elimu yenye dhamana ya kubainisha maadili machafu na kuyatibu ni elimu ya tabia njema. Kisha ni kwamba mwili ambao ni mada ni wenye kutoweka, na roho ambayo haina mada ni yenye kubakia.”20 Akasema tena: “Hakuna shaka kwamba nafsi haina mada na ni yenye kubaki baada ya kuachana na mwili.”21 Akafafanua kwa kusema: “Kutokuwa na mada kwa nafsi ni kule kwa asili na si sasa, kwa sababu sasa inahitaji mwili na nyenzo, hivyo utambulisho wake ni: Yenyewe ni chombo cha juu chenye kuutumikisha mwili katika haja zake, na chenyewe ndio mwanadamu mwenyewe. Viungo na nguvu ni nyenzo zake ambazo huzitegemea katika utendaji wake, na yenyewe ina majina mbalimbali kulingana na kigezo, huitwa roho kwa kuwa uhai wa mwanadamu huitegemea yenyewe, na huitwa akili kwa sababu huyadiriki mambo ya kiakili, na huitwa moyo kwa sababu ya kugeuka kwake katika 20 Jamius-Saadat Juz. 1, Uk. 5. 21 Jamius-Saadat Juz. 1, Uk. 5. 22
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:25 PM
Page 23
Huduma ya Afya katika Uislamu mawazo.”22 Hivyo ndivyo uchambuzi wa kifikra wa ulamaa wa kiislamu unavyochambua mambo yanayoambatana na nafsi ya mwanadamu, nayo ni: Hakika nafsi ya mwanadamu ni umbo lisilo na sifa za kimada, kama ambavyo nguvu kwa wazo la elimu ya fizikia inatofautiana na mada. Hakika nafsi ndio mwanadamu mwenyewe, na ndio huitwa “mimi”, mwanadamu asemapo: “mimi” hukusudia nafsi. Umbo hili lisilo na mada ambalo huhisi utamu na uchungu, hudiriki na kufikiri, huchukia na kupenda, hukhofu na kuhuzunika, hughadhibika na kuridhia, na hutaka na kukataa. Hakika mwili ni nyenzo ya kutekelezea mahitaji ya nafsi, kile ambacho nafsi inakitaka na kukipenda huenda kujitimizia kwa njia ya kubadili sura ya kifikra kwenda kwenye msimamo wa kutaka na tabia ya kimatendo. Hivyo hakika nafsi huathiri mwili kama ambavyo mwili huathiri nafsi, na kutoka katika unyenzo huu hisia nyingi na taswira nyingi hubadilika na kuwa hali za kimaradhi, kama vile huzuni, khofu, kupenda na kuchukia, na hivyo huathiri taathira ya mabadiliko na hapo mwili hupokea mabadiliko hayo mapokezi ya kifiziolojia, na baadhi ya wakati huacha athari zake za kimaradhi kwenye mwili. Hakika nafsi hupatwa na maradhi kama mwili unavyopatwa na maradhi, na maradhi ya nafsi ni kule kukengeuka msitari wa unyoofu ambao wanafalsafa wa maadili huuita msitari wa kati na uwiano, na hapo mwanadamu hupatwa na huzuni, khofu, hikdi na kuhisi upungufu. Na maradhi haya huleta mabadiliko kwa kubadilika na kuwa maradhi ya kimwili. Matokeo ya uchunguzi wa kielimu yamethibitisha kwamba asilimia kubwa ya maradhi ya kimwili sababu yake ni mabadiliko ya kisaikolojia, kama vile 22 Jamius-Saadat Juz. 1, Uk. 28 23
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:25 PM
Page 24
Huduma ya Afya katika Uislamu maradhi ya kisaga chakula, vidonda vya tumbo, usagaji mbaya wa chakula na uvimbe wa utumbo, kama pia maradhi ya mishipa, kutowiana kiwango cha sukari, maradhi ya maumivu ya kizazi na kuumwa kwa kichwa, na mengineyo. Maradhi mengi huanza kisaikolojia na baadaye hugeuka na kuwa maradhi ya kimwili. Taarifa na uchambuzi wa kisaikolojia unasisitiza kwamba maradhi mengi ya kimwili sababu zake ni maradhi ya kisaikolojia, na kwamba uhusiano kati ya hayo mawili mara nyingi ni wa kubadilishana kati ya mwili na nafsi katika afya njema na maradhi. Hebu sasa tusome yaliyopatikana katika ripoti ya afya inayozungumzia uhusiano wa maradhi ya kimwili na maradhi ya kisaikolojia. Imekuja humo: “Matokeo ya uchunguzi katika nchi za Kimagharibi ambazo humo imeenea elimu ya afya ya saikolojia na ambazo humo nyenzo za matibabu ya kisaikolojia zimeendelea, yanathibitisha kuenea sana kwa maradhi ya kisaikolojia na kiakili kwa watu. Mfano Marekani, matokeo yanaonyesha kwamba nusu milioni ya Wamarekani hupata matibabu katika hospitali kutokana na maradhi haya, kama ambavyo hospitali za Marekani hupokea kila mwaka wagonjwa wapya 150000 wa maradhi haya. Na baadhi ya matokeo yanaonyesha kwamba asilimia kumi ya Wamarekani wako kwenye hatari ya kupatwa na maradhi haya muda mchache tangu kuanza uhai wao.�23 “Ukweli ni kwamba matokeo waliyoyapata yanawafikiana kabisa na nadharia ya tiba ya kisasa inayohusu umuhimu wa kionjo cha saikolojia katika tiba ya kisasa. Matokeo ya kina yameonyesha kwamba asilimia thamanini ya wagonjwa wa maradhi mbalimbali katika miji yote ya Marekani maradhi yao sehemu kubwa hutokana na sababu za kisaikolojia. 23 Sayajmunda Farid Uk. 13. Huu ni utangulizi wa Dr. Muhammad Uthman Najatiy, Mtaalamu wa masuala ya saikolojia. 24
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:25 PM
Page 25
Huduma ya Afya katika Uislamu Hembu chunguza ni sababu zipi za msingi ambazo husababisha maradhi ya mishipa? Hakika miongoni mwa sababu za msingi za maradhi haya ni kuhisi dhambi, kosa, hikdi, khofu, mashaka, hasira, kubabaika, shaka, ghera na kuchoka. Na linalosikitisha ni kwamba wengi wanaojishughulisha na matibabu ya saikolojia wanaweza kufaulu katika kutibu sababu za mihangaiko ya kisaikolojia ambayo husababisha maradhi, lakini wanashindwa kutibu mihangaiko hii, kwa sababu wao katika matibabu yao hawakimbilii katika kupeleka imani ya kumwamini Mwenyezi Mungu katika nafsi za wagonjwa. Na juu ya hilo ni lazima tujiulize kuhusu mihangaiko hii na mabadiliko haya na sababu ambazo husababisha maradhi hayo, hiyo ndio mihangaiko yenyewe ambayo dini zimekuja kutukomboa nayo…..”24 Uchambuzi wa kisaikolojia wa sasa unaafikiana na uchambuzi wa ulamaa wa tabia njema wa kiislamu kuwa nafsi ya mwanadamu hupatwa na maradhi, na kwamba yenyewe hupatwa na hali ya afya njema na maradhi kama inavyoupata mwili. Mmoja wa maprofesa waliobobea katika elimu ya saikolojia anaandika ukweli huu kwa kusema: “Hakika siha ya saikolojia na maradhi ya kisaikolojia ni pande mbili za hali za kisaikolojia ambazo inapasa elimu ya siha ya kisaikolojia inapasa kutilia mkazo katika kuzisoma, kwa kuujua upande mmoja tutaweza kuzama kwa kina katika kuujua upande mwingine na kuweza kujua kiwango cha ukaribu wetu au umbali na pande zote mbili, nazo ni kama mikono miwili ya mizani moja, kwayo tunakuwa na uhakika wa maarifa yetu ya jinsi mwenendo unavyokuwa, unavyotikisika au kuchambuka ..…”25 Anaendelea kusema: “Na kwa upande wa kimatendo tunaweza kuzingatia uhai kuwa ni mnyororo wa mivutano ambayo mtu hufaula pale anapoishinda na hapo hujengeka siha ya kisaikolojia, au hushindwa na hapo huwa ni 24 Allahu Yatajala Fi Asril-Ilmi, Uk. 136, cha Dr. Paulo Artost Adolof. 25 Ilmus-Sihatun-Nafsiyah, Uk. 35 – 36, cha Dr. Mustafa Khalil Sharqawiy. 25
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:25 PM
Page 26
Huduma ya Afya katika Uislamu maradhi ya kisaikolojia. Na maana ya hilo ni kwamba siha ya kisaikolojia haiwezekani kuifahamu ila kwa mwangaza wa maradhi ya kisaikolojia. Na tunaweza kusema kwamba maradhi ya kisaikolojia uhalisia wake ni kule kushindwa kukusanya na kutimiza na kutekeleza sifa za mwenendo wa siha ya kisaikolojia, kama ambavyo kuyasoma maradhi ya kisaikolojia, kuyasimulia na kuchambua sababu zake kuna athari kubwa katika kuainisha sifa ambazo kwa mujibu wake unaweza kuhukumu na uwepo wa siha ya kisaikolojia.”26 Kisha anakomea kwenye kauli: “Kuna sehemu mbili za msingi, nazo ni ‘Sehemu ya siha ya kisaikolojia’ nayo inakusanya hali ya kutokuwa na maradhi ya kisaikolojia. Nayo ndio hali ya chini kabisa kati ya hali za sehemu hii, ambapo iliyo juu yake ni hali ya usalama wa kisaikolojia ambayo huwa katika kilele cha hali ya siha ya kisaikolojia. Na mkabala na sehemu hiyo ni ‘Sehemu ya maradhi ya kisaikolojia,’ nayo inakusanya hali ya mtikisiko na mabadiliko, hali ambayo huzingatiwa kuwa ni ya chini kabisa kati ya hali za maradhi ya kisaikolojia ni hali ya maradhi ya saikolojia ya mwili, kisha ni maradhi ya mishipa na mwisho ni ubongo, ambao huwakilisha hali mbaya zaidi ya ulemavu wa kiakili.”27 Hivyo ndivyo zinavyopatikana mbele yetu hali mbili zenye kukabiliana, nazo ni sura ya siha ya kisaikolojia na sura ya maradhi ya kisaikolojia, zinapambana juu ya nafsi ya mwanadamu na wala hakuna wema kwa mwanadamu ila kwa kujipatia siha ya kisaikolojia na nafsi kutokuwa na maradhi na mabadiliko ya kimaradhi. Na kama ambavyo ulamaa wa kiislamu wameweka wazi, hakika yale waliyoyaita tabia njema (hali za siha ya kisaikolojia) na kutokuwa na yale waliyoyaita tabia mbaya (hali za maradhi ya kisaikolojia) yenyewe ni miongoni mwa kanuni za msingi za kujenga utu wa kiislamu, hivyo 26 Ilmus-Sihatun-Nafsiyah, Uk. 46, cha Dr. Mustafa Khalil Sharqawiy. 27 Ilmus-Sihatun-Nafsiyah, Uk. 48, cha Dr. Mustafa Khalil Sharqawiy. 26
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:25 PM
Page 27
Huduma ya Afya katika Uislamu tunamkuta Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.) anatamka kwa sauti: “Hakika nimeletwa kuja kukamilisha tabia njema.”28 Na katika kauli nyingine anatuchambulia uchambuzi wa kielimu kwamba tabia mbaya huakisi maradhi juu ya nafsi, anasema: “Ambaye tabia yake ni mbaya ameiadhibu nafsi yake.”29 Kuiadhibu nafsi si kesho Akhera tu, bali ni hata katika adhabu ya mashaka na matatizo ya dhamiri miongoni mwa mashaka, ghamu, huzuni, hali ya umimi, ghera na husuda ambazo hujikita ndani ya kina cha nafsi na kumfikisha mwenye nayo kwenye moto wa daima. Imam Ali (a.s.) ametoa sura nzuri ya hali ya kisaikolojia kwa mwanadamu hasidi, naye ni yule mwenye umimi ambaye hawatakii wengine kheri, na huumia kuona wengine wanafanikiwa kushinda yeye, na hutamani ajitume ili kuwaepusha na mafanikio hayo na kuwakosesha kheri waliyonayo, hivyo huishi katika chuki, hasira na tamaa ya kuwaadhibu, ambaye mara nyingi hubadilika na kwenda katika hali za kujiuwa na kujinyonga, au kuwateta wengine au kuwashushia heshima zao na kujitahidi kuwaangusha. Amirul-Muuminina amesema kweli alipoisawiri picha hii kwa kusema: “Ole wako hasadi! Ni adilifu ilioje! Imemwanza mwenye nayo na hatimaye imemuuwa.”30 Matokeo ya uchunguzi na uchambuzi wa kisaikolojia yanaonyesha kwamba mashirika ya kijamii na mifumo ya kimalezi na nadharia za kunadhimu mwenendo wa mwanadamu zimeshindwa kutibu maradhi ya kisaikolojia na kumwokoa mwanadamu dhidi yake. Bali ripoti na matokeo ya uchunguzi vinathibitisha uwepo wa ongezeko la wapatwaji wa magonjwa ya kisaikolojia, na ukosefu wa siha ya kisaikiolojia ni matokeo ya maisha ya kimada yenye matatizo na yenye kumpa mashaka mwanadamu. Ugaidi wa 28 Kanzul-Ummal, Hadithi ya 5217. 29 Biharul-An’war: 78 Uk. 246. 30 Ghurarul-Hikam Wadurarul-Kalim. 27
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:25 PM
Page 28
Huduma ya Afya katika Uislamu kisiasa ni kwa sababu ya tofauti za mawazo au siasa, au utawala wa kidikiteta. Ukosefu wa amani wa mtu mmoja mmoja au wa jamii nzima katika nchi nyingi za ulimwengu ndio msiba mkubwa wa mwanadamu. Khofu ya kutokea vita na magomvi, kutokuwa na utulivu juu ya hali ya sasa na mustakbali, mashaka dhidi ya kudidimia kwa hali ya maisha, kuhisi ukosefu wa maana halisi ya maisha na kukata tamaa dhidi ya uwezo wa kipato cha kiuchumi, kukosekana maridhiano na uwelewano baina ya watu na jamii, kusambaratika kwa familia, kukosekana mapenzi, huruma na upendo, kutapakaa kwa hali ya kufukuzwa na upotevu, hisia za kudharauliwa na kutokuwepo mwenye kumjali mwanadamu aliyefukuzwa. Hali hizi zote zimekuwa miongoni mwa matatizo ya sasa na sumu za maendeleo ya kiuchumi ambayo yamemwingiza mwanadamu katika majuto na kusababisha kuenea kwa maradhi ya saikolojia ambayo yamemkosesha mwanadamu ladha ya maisha na raha yake. Hatuna kimbilio mbele wala mwokozi ila Uislamu, ambao mfumo wake umekusanya kinga ya nafsi na kumlinda na maradhi ya kisaikolojia kwa kumwamini Mwenyezi Mungu na ulimwengu wa Akhera, ukafanya kazi ya kuzitakasa nafsi na kuzisafisha dhidi ya hikdi na umimi, ukazihami na khofu na mashaka, kwa kusalimisha mambo kwa Mwenyezi Mungu na kuridhia maamuzi Yake na makadara Yake pindi mwanadamu anapokumbana na hali za kisaikolojia zisizo za kawaida, na ukaiwekea ngome nafsi dhidi ya kupatwa na maradhi ya kisaikolojia kwa kutumia malezi na kwa kuyatimiza mazingira ya kifamilia na kijamii na kisiasa na kikanuni, mazingira ambayo yatampa mwanadamu utulivu, upendo na heshima ya utu wake na kuuthamini. Na msingi wa kielimu ambao mfumo wa Uislamu unautegemea katika kuihami nafsi dhidi ya maradhi ya kisaikolojia ni kule kuamini kwamba umbile la mwanadamu ni umbile safi lililo salama dhidi ya maradhi ya kisaikolojia. Mwenyezi Mungu anasema:
28
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:25 PM
Page 29
Huduma ya Afya katika Uislamu
“Basi uelekeze uso wako kwa dini iliyo sawasawa ndio umbile Mwenyezi Mungu alilowaumba watu. Hakuna mabadaliko katika maumbile ya viumbe wa Mwenyezi Mungu, hiyo ndio dini iliyo haki lakini watu wengi hawajui.� (Sura Rum: 30). Bila shaka siha ya kisaikolojia inaonekana kwa kuhifadhi umbile hili na kulihami na uchafu na uendaji kinyume kwa kulizowezesha malezi mema ya maadili mema, na kuleta mazingira na hali ya kijamii ambayo itasaidia umbile hili kusafika na kubakia salama katika ukuaji na ukamilifu ulio mbali na maadili machafu na mabaya, baada ya kuwa Uislamu umeharamisha kumwogopa mwanadamu na kudharau utu wake, na umawetaka wazazi na wanafamilia na jamii kupendana na kusaidiana na kuheshimiana, na ukawajibisha kuleta amani ya kisiasa na kimaisha, na ukahimiza kwamba nafsi yenye kifundo ikimbilie kwa Mwenyezi Mungu na imtake msaada Yeye, kwa hayo mwanadamu atakuwa huru dhidi ya khofu, dharau na umimi. Na kanuni nyingine miongoni mwa kanuni za kuilinda nafsi na maradhi ya kisaikolojia ni kuamini Siku ya Mwisho na kutoweka kwa vitu vyote na kudumu kwa kheri na matendo mema, ili yawe msingi wa malipo na neema, na hivyo kuituliza nafsi na kuipa utulivu kwa kuisalimisha na mashaka na khofu, adui wa mwanadamu na sababu ya huzuni yake na adhabu ya nafsi yake katika maisha.
29
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:25 PM
Page 30
Huduma ya Afya katika Uislamu Mwenyezi Mungu anasema:
“Jueni ya kwamba maisha ya dunia ni mchezo na upuuzi na pambo na kujifakharisha baina yenu, na tamaa ya kuzidiana katika mali na watoto. Kama mvua ambayo huwafurahisha wakulima mazao yake, kisha yanakauka ukayaona yenye rangi ya manjano, kisha yanakuwa yenye kuvunjika vunjika, na katika Akhera ni adhabu kali na msamaha wa Mwenyezi Mungu na radhi yake na maisha ya dunia siyo ila ni starehe idanganyayo tu. Uendeeni upesi msamaha wa Mola wenu Mlezi na Pepo ambayo upana wake ni kama upana wa mbingu na ardhi, iliyowekewa wale waliomwamini Mwenyezi Mungu na Mitume wake, hiyo ni fadhila ya Mwenyezi Mungu, humpa amtakaye na Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila kuu. Hautokei msiba katika 30
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:25 PM
Page 31
Huduma ya Afya katika Uislamu ardhi wala katika nafsi zenu ila huwamo Kitabuni kabla hatujauumba, kwa hakika hilo ni rahisi kwa Mwenyezi Mungu. Ili msihuzunike juu ya kitu kilichokupoteeni, wala msifurahi kwa alichokupeni. Na Mwenyezi Mungu hampendi kila ajivunaye, ajifakharishaye.” (Sura Hadiid: 20 – 23). Aya hizi tukufu zilizobarikiwa zimechukua jukumu la kutoa ufafanuzi wa maana ya uhai na kifo ili kumwelimisha mwanadamu na kumjengea fikra salama ya uhai na uhusiano wake salama, hivyo zikatoa taswira sahihi ya uhai kwa namna iliyo karibu na ufahamu wa mwanadamu na uwelewa wake, ili kung’oa vyanzo vya mashaka na huzuni ya nafsi iliyojikita katika khofu dhidi ya kupitwa na vitu na kuvipoteza, na katika khofu yake dhidi ya vile anavyotarajia kutokea na vile ambavyo amedumbukia. Pia Mwenyezi Mungu amefafanua ukweli wa uhai na akaushabihisha na uhai wa shamba, na anawataka kwamba wasiitii khofu dhidi ya kipato cha maisha na wala kisimpe mashaka. Kila kitu kimekadiriwa na kinakwenda kufuatana na makadara. Pia anamfafanulia mwanadamu kwamba kukimbilia kwa Mwenyezi Mungu ndio ufunguo wa furaha na utulivu, ili ajifungamanishe na Mwenyezi Mungu mbali na mashaka, hivyo anamwambia:
“Wale walioamini na zikatulia nyoyo zao kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu, sikilizeni kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu, nyoyo hutulia.” (Sura Ra’d: 28).
31
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:25 PM
Page 32
Huduma ya Afya katika Uislamu
MARADHI NA KUKAMILIKA KWA NAFSI Darasa na uchunguzi wa saikolojia ya maadili unasisitiza kwamba siha ya kisaikolojia ndio chanzo cha furaha ya mwanadamu, utulivu wa jamii na kulinda nidhamu yake. Hivyo jamii ambayo watu wake wanastarehe kwa siha ya kisaikolojia na kwa mwenendo sahihi hujenga nidhamu ya kijamii ambayo itakuwa nadra kuwa na makosa, mmong’onyoko, matatizo na migogoro ya kisiasa, kiuchumi na amani, na itasalimika na tabia za kiuadui. Mwanadamu kwa malezi mema, utashi, mazingira ya tiba na mazoezi ya kinafsi anaweza kuokoka na hali za kimaradhi, kama vile umimi, hikdi, kiburi, ujeuri, kujiona na ulafi. Na yenyewe kama ilivyoelezwa na Qur’ani Tukufu ipo katika hatari ya kupatwa na maradhi ya kiburi, dhulma na majivuno juu ya wengine. Ili sura hii iwe wazi kwako basi tusome sehemu tu ya ufafanuzi wa Qur’ani na uchambuzi wake. Mwenyezi Mungu amesema:
“Hautokei msiba katika ardhi wala katika nafsi zenu ila huwamo Kitabuni kabla hatujaumba, kwa hakika hilo ni rahisi kwa Mwenyezi Mungu. Ili msihuzunike juu ya kitu kilichokupoteeni, wala msifurahi kwa alichokupeni. Na Mwenyezi Mungu hampendi kila ajivunaye, ajifakharishaye.” (Sura Hadiid: 22 – 23).
32
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:25 PM
Page 33
Huduma ya Afya katika Uislamu
“Ama wale walioamini na kufanya vitendo vizuri, basi atawapa malipo yao na atawazidishia katika fadhila yake. Ama wale walioona unyonge na kufanya kiburi, basi atawaadhibu adhabu yenye kuumiza, wala hawatapata kiongozi wala msaidizi yeyote badala ya Mwenyezi Mungu.” (Sura Nisaa: 173).
“Kwa hakika wale wanaobishana katika Aya za Mwenyezi Mungu pasipo dalili yoyote iliyowafikia. Hamna nyioyoni mwao ila kiburi, lakini hawataufikia, basi jikinge kwa Mwenyezi Mungu, kwa hakika yeye ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.” (Sura Muumin / Ghafir: 56).
“Kwa hakika tumevifanya vilivyoko juu ya ardhi view mapambo yake, ili tuwajaribu ni nani katika wao mwenye vitendo vizuri zaidi.” (Sura Kahfi: 7).
33
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:26 PM
Page 34
Huduma ya Afya katika Uislamu
“…Na haukuwa uhai wa ulimwengu ila ni raha ya udanganyifu. Hapana shaka mtapata misukosuko katika mali zenu na nafsi zenu.” (Sura Aali Imran: 185 – 186).
“Na Ayubu, alipomwita Mola wake Mlezi ya kwamba imenigusa dhara nawe ndiye unayerehemu kushinda wote wanaorehemu. Basi tukamkubalia na tukamwondolea dhara aliyokuwa nayo na tukampa watu wake na mfano wa pamoja nao ni rehema kutoka kwetu, na ukumbusho kwa wafanya ibada.” (Sura Anbiyai: 83 – 84).
“Ambao anapotajwa Mwenyezi Mungu nyoyo zao hutetemeka, na wanaovumilia juu ya yale yanayowapata na wanaoshika Sala na katika vile tulivyowaruzuku wanatoa.” (Sura Hajji: 35).
“Ambaye ameniumba, naye ananiongoza. Naye ndiye anayenilisha na kuninywesha. Na ninapougua, basi yeye ananiponya” (Sura Shua’raa: 34
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:26 PM
Page 35
Huduma ya Afya katika Uislamu 78 – 80). Hivyo ndivyo Qur’ani inavyozungumzia mambo makubwa ya ulimwengu wa mwanadamu, tunaweza kutaja muhimu kati ya hayo: Hakika nafsi ya mwanadamu ipo katika hatari ya kupatwa na maradhi ya kisaikolojia, kama vile kiburi, majivuno, jeuri na kujidai, ambayo ni matokeo ya nguvu na kujiona amejitosheleza bila kumhitaji Mwenyezi Mungu wala watu, na ili kuficha hali ya kuhisi upungufu uliomo ndani ya kina cha akili ya ndani. Watu wengi miongoni mwa majeuri na wenye majivuno huhangaika na ugonjwa wa kuhisi upungufu, na kwa ajili hiyo bila kujua hukimbilia kwenye njia za kiburi. Hakika maradhi hayo ambayo hujiakisi kwenye maadili ya jamii hudhihirika kwenye muamala na mahusiano ya kibinadamu katika sura tofauti za kijamii na kisiasa. Na hakika maradhi haya ya kisaikolojia na kimaadili ndio msiba mkubwa wa mwanadamu na ndio chanzo cha taabu zake na adhabu yake duniani na Akhera, hivyo Qur’ani imelibainisha hilo kwa kusema:
“Wala usitembee katika ardhi kwa maringo, hakika wewe huwezi kuipasua ardhi, wala huwezi kufikia urefu wa milima.” (Sura Israil: 37).
“..Ama wale walioona unyonge na kufanya kiburi..” (Sura Nisaa: 173).
“..Hamna nyoyoni mwao ila kiburi.” (Sura Ghafir / Muumin: 56).
35
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:26 PM
Page 36
Huduma ya Afya katika Uislamu “Basi Adi walitakabari katika ardhi bila ya haki na wakasema: Ni nani aliye na nguvu zaidi kushinda sisi?” (Sura Fusilat/ Haa Miim: 15). Hivyo ndivyo mfundo ulivyo chanzo cha ukafiri, dhuluma na uharibifu wa kijamii, kisiasa na kiuchumi, kama ambavyo ndio chanzo cha utovu mwingine wa maadili ya mtu. Hakika kupatwa na maradhi aina mbalimbali ikiwemo maradhi ya kimwili ni moja ya njia za kimalezi na kimafunzo ambazo humhisisha mwanadamu udhaifu wake na haja yake ya kumtegemea Muumba wake, kama ambavyo huchukua nafasi ya adhabu kwa wakosaji, wajeuri na waovu. Kisha yenyewe ni somo na nasaha kwa wengine ambao hushuhudia muovu na jeuri na mwenye majivuno kauwawa kwa maradhi, yamemdhalilisha na kumkosesha afya na fursa ya kustarehe na maisha. Ulamaa wa theolojia na wanamaadili wa kiislamu wamezungumzia sana maradhi haya na athari zake katika kuikamilisha nafsi na kuifunza, hivyo wamegawa somo hilo sehemu mbili: Sehemu moja ni adhabu, kisasi, kuwaadabisha na kuwazuia wakosaji. Na sehemu nyingine ni mafunzo na kafara ya madhambi na kukuza hali ya ukamilifu kwa mwanadamu. Maradhi humfanya mwanadamu ahisi udhaifu mbele ya Muumba wake, ahisi uhitaji wake wa rehema zake, msamaha wake na hisani yake, na pia humhisisha upole na huruma kwa wengine, na humzuia na ujeuri, kiburi na kuwadhulumu wengine, hali ambazo huzalishwa na hali ya kujiona ana nguvu na ubora juu yao. Qur’ani tukufu imemtaka mwanadamu ambaye hajapatwa na masaibu na misukosuko ikiwemo maradhi, avute subira na kushukuru msiba na kupambana nayo kwa ushujaa na utashi imara na bila kukata tamaa ya kupona, kwani hakika ponyo imo mikononi mwa Mwenyezi Mungu, dawa na matibabu si chochote ila ni njia tu ya kupatia taufiki na utashi wa 36
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:26 PM
Page 37
Huduma ya Afya katika Uislamu Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapa wenye subira kitu mbadala badala ya matatizo na maradhi ya miili yao. Qur’ani imeonyesha mifano mingi tu ya majaribu ya maradhi ya kimwili, subira na kustahiki rehema na kitu mbadala. Imeonyesha maradhi yaliyomsibu Nabii Ayubu (a.s.), na imezungumzia kisa cha maradhi yake na urefu wa muda wa maradhi yake. Kutokana na uzoefu huu toka kwa Nabii mwanadamu hujifunza kuvuta subira juu ya maradhi, na kuelekea kwa Mwenyezi Mungu kwa dua ambayo humpeleka upande wa ukamilifu kwa nguvu ya nafsi, na husisitiza maana ya unyenyekevu, huja na mwelekeo kwa Muumba wa ulimwengu na mgawaji wa kheri na neema. Qur’ani imefichua ukweli uliokuwa mbali na watu wengi ambao huamiliana na matukio kwa muamala usio wa kina, hivyo hulitizama kila jambo ambalo linawaumiza na kuudhi nafsi zao au kwenda kinyume na utashi wao kuwa ni shari ambayo ni lazima kujiokoa nayo. Qur’ani inasahihisha makosa haya, na inasisitiza kwamba mengi kati ya mambo ambayo mwanadamu hudhani kuwa ni shari kwake kwa kweli ni kheri tupu kwake, na inaikataa fikira hii ambayo ni sawa na fikira ya mtoto mdogo anayeikana dawa kwa sababu ya uchungu wake. Kwa kupitia kanuni hii kuu ya kimafunzo na kimawazo Qur’ani inabainisha wazi hekima ya maradhi na falsafa yake katika maisha, inamfahamisha mwanadamu kwamba upatikanaji na uwepo wa maradhi ni dharura ya kimaumbile na ni dharura ya maisha ya mwanadamu. Qur’ani imebainisha ukweli huu kwa kusema: “Mmelazimishwa kupigana vita ingawa mwaichukia, huenda mkachukia kitu nacho ni kheri kwenu, na huenda mkapenda kitu nacho ni shari yenu. Na Mwenyezi Mungu anajua, na nyinyi hamjui.” (Surat al-Baqarah: 216).
37
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:26 PM
Page 38
Huduma ya Afya katika Uislamu Kama alivyobainisha falsafa ya adhabu za mahakama ya kiislamu kwa kusema: “Na mnao uzima katika kisasi, enyi wenye akili ili msalimike.” (Surat al-Baqarah: 179). Ijapokuwa kupigana vita na adhabu za kimahakama ni vitu vyenye maumivu na kuchukiwa na nafsi lakini bado ni moja ya njia za upatikanaji wa usalama na amani katika jamii ya mwanadamu. Hivyo hivyo viwili ni miongoni mwa vyanzo muhimu kabisa vya furaha na utulivu. Na kwa msingi wa kanuni hii inapatikana hikima ya maradhi ya kimwili ambayo huwa kizuizi cha maradhi ya kisaikolojia na nyenzo ya kuelimisha na kuadabisha. Hivyo tunakuta uwazi wa hikima ya maradhi unaonekana katika hadithi na maelezo ya Mtume (s.a.w.w.), huku mwingine ukija toka kwa Maimamu wa nyumba ya Mtume (a.s.) ambao unazungumzia maradhi kama moja ya nyenzo za majaribu na mitihani, na mwingine ukizungumzia maradhi kama moja ya njia ya ukamilifu na kusafisha moyo wa mwanadamu dhidi ya maradhi ya kisaikolojia. Katika kundi la kwanza tunasoma kauli ya Mtume (s.a.w.w.): “Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema: Hakuna mja nitakaye kumuingiza peponi ila ni lazima nitamjaribu kwa maradhi mwilini kwake, hiyo huwa ni kafara ya dhambi zake, na la sivyo humbana katika riziki yake, hiyo nayo huwa ni kafara ya dhambi zake, la sivyo humkazia kifo mpaka anijie na hali hana dhambi, kisha humwingiza peponi.”31 Imam as-Sadiq (a.s.) akasema: “Muumini hapitiwi na siku arubaini bila Mwenyezi Mungu kumjaribu, ima kwa maradhi katika mwili wake na ima kwa msiba ambao Mwenyezi Mungu atamlipa kwawo.”32
31 Mishkatul-An’war Uk. 291. 32 Mishkatul-An’war Uk. 292. 38
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:26 PM
Page 39
Huduma ya Afya katika Uislamu Na akasema tena: “Bila shaka mja hupata cheo mbele ya Mwenyezi Mungu, lakini hakipati ila kwa moja ya sifa mbili: Ima kwa kuondokewa na mali yake au kwa maradhi katika mwili wake.”33 Imam Ali Ibni Husain Sajjad (a.s.) anazungumzia maradhi kwa kusema: “Mimi nachukia mtu kupewa afya njema duniani bila kupatwa na kitu kati ya misiba yake.”34 Mtume (s.a.w.w.) anafafanua kiwango cha mafunzo na athari za kimarekebisho za maradhi ya kimwili na pale mwanadamu anaposibiwa na majaribu ya maradhi. Anafafanua athari za maradhi kwa mujibu wa maadili na tiba ya hali za kisaikolojia za mgonjwa, na jinsi harakati za kisaikolojia zinavyokua kupita na kushinda athari nyingine za kimarekebisho ambazo huachwa na matendo mengine mema pindi utakapoamua kuzilinganisha na jinsi maradhi yanavyoacha athari za kina na mabadiliko ya kina ndani ya nafsi. Hayo yote anayafafanua Mtume kwa hikima yake pale anapoongea na masahaba zake kwa kusema: “Anayependa kwamba awe na afya njema basi asiugue.” Tukabutwaa na kusema: Ewe Nabii wa Mwenyezi Mungu tueleze hilo litawezekanaje? Akasema: “Hivi mnapenda muwe kama punda aliyepotea?” wakasema hapana ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu. Akasema: “Hivi hampendi kuwa watu wa majaribu na kafara. Naapa kwa yule Ambaye nafsi yangu imo mikononi mwake, hakika Mwenyezi Mungu hamjaribu muumini kwa majaribu yoyote aliyompa ila ni kwa ajili ya kumkirimu, hakika Mwenyezi Mungu anakuwa amemweka nafasi ambayo amali yake yoyote isingeweza kumfikisha hapo bila ya kufikwa na majaribu ambayo yameweza kumfikisha nafasi hiyo.”35 Na tunasoma ufafanuzi wa kina wa Imam Muhammad al-Baqir (a.s.) wa hikima za maradhi na athari zake ambazo hufanya kazi ya kuiimarisha nafsi na kusahihisha mwenendo wake wa kimaadili, na kutibu hali yake ya 33 Mishkatul-An’war Uk. 298. 34 Mishkatul-An’war Uk. 295. 35 Mishkatul-An’war Uk. 301. 39
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:26 PM
Page 40
Huduma ya Afya katika Uislamu kimaradhi, yeye anafafanua kwamba maradhi ya kimwili hutibu maradhi ya kisaikolojia. Ufafanuzi huo umeletwa ndani ya maandiko yafuatayo: “Mwili usipougua huwa shari mbaya mno, na wala mwili wenye shari hauna kheri.”36 Hivyo ndivyo maandiko ya Qur’ani na Sunna yanavyotoa utatuzi wa kimatendo wa kadhia hatari sana inayomkabili mwanadamu katika maisha yake, nayo ni kadhia ya maradhi ya kimwili na kisaikolojia, na ili kujua kwa undani kuhusu suala zito katika kadhia hii, ni kwamba nyingi kati ya hali za maradhi ya kimwili ndio tiba ya maradhi ya kisaikolojia. Na kwamba maradhi ya muumini ambayo humpata toka kwa Yeye Mwenyezi, huwa si kwa uzembe wake, bali hata maradhi ambayo humfika mwanadamu kwa sababu ya uzembe wake bado humpa uzoefu wa kinga ya maradhi, na humhisisha neema ya siha njema aliyoweza kumneemesha, hivyo maradhi kama maandiko yasemavyo ni malezi kwa mwanadamu mwislamu muumini, na ni kukuza harakati za ukamilifu wa nafsi yake kutokana na subira dhidi ya maumivu, kuimarisha utashi, kuridhia makadara ya Mwenyezi Mungu na majaliwa yake, kupambana na chembechembe hai za kiburi, ujeuri na majivuno. Baada ya hapo hayo huwa ni kafara ya madhambi, kwani maradhi yanayomfika muumini kwa makadara ya Mwenyezi Mungu huwa ni maumivu, na maumivu haya yana fidia yake toka kwa Mwenyezi Mungu. Fidia hii ni maghfira, na msamaha mzuri. Hii haimaanishi kwamba mwanadamu ajitafutie maradhi na asipambane nayo, bali ni kwamba Uislamu umemwajibisha mwanadamu kujilinda dhidi ya kila aina ya madhara na ukaharamisha kujidhuru, kama ambavyo pia umewajibisha kujitibu na maradhi ambayo hayaondoki ila kwa tiba. Hivyo sheria ya Uislamu imezingatia kwamba gharama za matibabu ya mke ni sehemu ya matumizi yaliyo wajibu juu ya mume. Bali pia umetueleza kwamba kuficha maradhi na kutokwenda kwa tabibu ili ayafanyie uchunguzi na kuyatibu ni kuu36 Mishkatul-An’war Uk. 280. 40
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:26 PM
Page 41
Huduma ya Afya katika Uislamu fanyia khiyana mwili. Imam Ali (a.s.) amesema: “Mwenye kuwaficha matabibu maradhi yake bila shaka ameufanyia khiyana mwili wake.” Maelekezo ya Uislamu yanaamiliana na hali za kisaikolojia za mgonjwa kwa kumpa utatuzi wa kielimu wenye manufaa, kati ya huo ni kwamba baadhi ya wagonjwa huhisi makosa na uzembe mbele ya nafsi zao, muumba wao na jamii yao, isipokuwa ni kwamba baada tu ya maradhi kuondoka na afya kuboreka haraka sana husahau mawaidha haya na kusahau fadhila za Mwenyezi Mungu juu yao, hivyo maelekezo hayo yanaamiliana nao kwa kuwapa mwamko, ukumbusho na kusahihisha mienendo yao na tabia zao ili kuweza kuwavua toka kwenye tatizo hili la kimaadili. Maelekezo hayo unayapata katika kauli ya Sayidina Ali (a.s.): “Usiwe anayetarajia Akhera bila matendo, akiugua hushinda katika majuto, na akipata afya njema hujiaminisha kwa kusahau. Anajivuna anapopewa afya njema na anakata tamaa anapojaribiwa kwa maradhi.”
MAUMIVU NA FIDIA Hakika miongoni mwa neema za Mwenyezi Mungu na ukarimu Wake mkubwa ni mwanadamu kuhisi maumivu na raha na kupatikana raha na maumivu, hali ambayo ni msukumo wa asili wa mwenendo wa mwanadamu. Mwanadamu kwa asili yake hupokea lile linalompa raha na huliepuka lile linalomletea maumivu, hivyo yeye huchukia maumivu na hupenda raha. Allama al-Hilli alitambulisha maumivu na raha kuwa ni: “Maumivu ni kudiriki usiyoyataka, na raha ni kudiriki unayoyataka.”37
37 Kashful-Murad Fisharhi Tajridul-Iitiqad Uk. 295 – 296. 41
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:26 PM
Page 42
Huduma ya Afya katika Uislamu Akasema tena: Jua kwamba raha na maumivu hufuata hali ya kiafya, raha ni kustawi kwa hali ya kiafya, na maumivu ni kudorora kwa hali ya kiafya, na maana hizi mbili zinasihi kwenye miili.�38 Wataalamu wa elimu ya saikolojia wakatambulisha maumivu kwamba ni: Kuhisi hatari, hivyo maumivu ni kengele ya kumzindua na kumhisisha mwanadamu uwepo wa hatari inayomtishia usalama, na hali hii ndio aliyoieleza Allama al-Hilli kwa kusema: ni kudiriki usiyoyataka. Na maumivu jinsi yalivyo hugawanywa sehemu mbili, nazo ni: Maumivu ya kimwili na maumivu ya kisaikolojia. Kila kimoja kati ya vigawanyo hivyo kina sifa zake makhususi, athari na matokeo yake. Kama ambavyo maumivu ya kisaikolojia yanaathiri utendaji wa mwili, harakati zake na uwezo wake, ni hivyo hivyo kwamba maumivu ya kimwili huiathiri nafsi na aghlabu kuiachia sura yenye kuumiza. Maumivu ya kisaikolojia hubadilika na kuwa maumivu ya kimwili, na maumivu ya kimwili hubadilika na kuwa maumivu ya kisaikolojia. Basi kutokana na kuamini na kukubali kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye hikima, hafanyi kitu ila kwa hikima na chenye masilahi kwa waja wake duniani na akhera, ijapokuwa hikima hiyo hawataiona, na kwamba vitendo vyake vina shabaha na lengo maalumu, basi kutokana na hayo yote tunaamini kwamba maradhi yanayomsibu mwanadamu toka kwa Mwenyezi Mungu yana lengo, shabaha na hikima inayorudi kwa mwanadamu mwenyewe. Hikima hii na shabaha hii inapatikana katika: Mwenyezi Mungu anaweza kumpa maradhi mwanadamu kutokana na huruma Yake juu yake ili kumwondolea madhara yaliyo makubwa kushinda maradhi hayo, na kwamba bila maradhi hayo basi mwanadamu huyo angedumbukia ndani ya hatari kubwa zaidi na madhara makubwa zaidi. Mwenyezi Mungu anaweza kumpa maradhi mwanadamu kutokana na huruma Yake juu yake ili kumtimizia manufaa na masilahi yanayomrudia 38 Kashful-Murad Fisharhi Tajridul-Iitiqad Uk. 295.. 42
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:26 PM
Page 43
Huduma ya Afya katika Uislamu yeye mwenyewe au kumrudia mtu mwingine. Mwenyezi Mungu anaweza kumpa maradhi mwanadamu kwa ajili ya kumwadhibu kutokana na kustahili kufanyiwa hivyo. Na kutokana na uadilifu wa Mwenyezi Mungu kwa uadilifu wake humpa mwanadamu huyu fidia ya yale maumivu ya kimwili au kisaikolojia yaliyompata katika hali mbili za mwanzo. Ama maumivu yanayomsibu mwanadamu katika hali ya tatu yenyewe huwa ni adhabu na wala hayana fidia, hivyo ulamaa wa theolojia ya kiislamu wamezungumzia maumivu kama walivyozungumzia maradhi na mengineyo yanayomfika mwanadamu kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na fidia anayostahiki aliyefikwa na hayo. “Katika fidia, Shia Imamia wanaona kwamba maumivu anayoyaweka Mwenyezi Mungu kwa mwanadamu huwa ni ima ni kwa ajili ya kisasi na kumwadhibu, naye hustahiki hilo. Mwenyezi Mungu anasema: “Na kwa hakika mmekwishawajua wale walioasi miongoni mwenu katika sabato, basi tukawaambia: Kuweni manyani madhalili.” (Surat alBaqarah: 65). Na akasema: “Je hawaoni kwamba wanajaribiwa kila mwaka mara moja au mara mbili? Kisha hawatubu wala hawakumbuki.” (Sura Tawba: 126). Maumivu haya hayana fidia. Na ima huwa kwa namna ya hisani, na bila shaka hufanywa hisani hiyo na Mwenyezi Mungu kwa sharti mbili: Kwanza ni lazima iwe ina masilahi fulani kwake mwenyewe yule mwenye kupatwa na maumivu au kwa mwingine, na hiyo ni aina ya huruma yake, kwani bila masilahi hayo kitendo hicho kingekuwa ni mchezo, na Mwenyezi Mungu ametakasika na kila aina ya mchezo. Pili mkabala na maumivu hayo kuwepo fidia yenye thamani kushinda maumivu, ambayo ataipata yule aliyefikwa na maumivu, kiasi kwamba la aliyepatwa na maumivu ataonywesha maumivu na fidia na akaombwa achague basi atachagua fidia, la sivyo itakuwa ni dhuluma na 43
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:26 PM
Page 44
Huduma ya Afya katika Uislamu uonevu toka kwa Mwenyezi Mungu juu ya mja wake, kwani kumuumiza mwanadamu na kumwadhibu bila dhambi yoyote wala faida ni dhuluma na uonevu, na jambo hilo ni muhali kwa Mwenyezi Mungu.”39 Allama al-Hilli amesema: “Hizi ni aina ambazo kwazo Mwenyezi Mungu hustahiki kutoa fidia: Kwanza: Anaposhusha maumivu kwa mja, kama vile maradhi na mengineyo. Tayari tumeshabainisha kwamba fidia ni lazima kwa sababu bila fidia hiyo itakuwa ni dhuluma. Tatu: Kumshushia huzuni, kwa Mwenyezi Mungu kumwekea sababu za huzuni, kwani huzuni katika akili ni sawa na madhara mengine, hiyo ni bila kujali kwamba huzuni hiyo ni alama ya dharura ya kuteremka msiba au kufikwa na maumivu, au ni dhana inayoonyesha alama za kufikwa na madhara au kupitwa na manufaa. Hivyo kwa sababu huzuni hiyo imetoka kwake Mwenyezi Mungu basi na fidia huwa ni juu yake. Ama huzuni inayopatikana kwa mwanadamu mwenyewe bila kutoka kwa Mwenyezi Mungu, kwa mfano yeye mwenyewe afanye utafiti na kwa kutokana na ujinga wake aone kwamba kafikwa na madhara au kapitwa na manufaa, basi fidia si juu ya Mwenyezi Mungu.”40 Hivyo ndivyo somo la theolojia ya kiislamu linavyotuletea uhusiano uliopo baina ya uadilifu wa Mwenyezi Mungu na hikma yake na baina ya yale yanayomsibu mwanadamu katika maradhi ya mwili au huzuni ya nafsi. Na linatufafanulia kwamba maumivu yatokayo kwa Mwenyezi Mungu kwa hisani yake ni kitu kizuri, kwa sababu yanamnufaisha mwanadamu kwa kuwa huwa yana masilaha ya kidunia na fidia ya kiakhera. Ama yale yanayomsibu mwanadamu kwa uzembe wake au dhana zake za kimaradhi na hatimaye kujawa na huzuni na mfundo, hayo hayana fidia. 39 Dalailus-Didqi cha Shaikh Muhammad Hasan Mudhaffar, Juz. 1 Uk. 361. 40 Kashful-Murad Fisharhi Tajridul-Iitiqad Uk. 360. 44
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:26 PM
Page 45
Huduma ya Afya katika Uislamu Zimepatikana riwaya nyingi zikizungumzia athari za huzuni na mifundo na mashaka katika kuitakasa nafsi na kuitengeneza na kuisafisha dhidi ya kila aina ya uchafu. Zaidi ya hapo ni kule kustahiki malipo na fidia juu ya huzuni hizo. Mtume anasema: “Madhambi ya mja yanapokithiri na akawa hana amali yakuweza kumfutia madhambi hayo, basi Mwenyezi Mungu humjaribu kwa huzuni ili iweze kumfutia.”41 Pia amesema: “Mwislamu hapatwi na mchoko wala mnyong’onyeo, mashaka wala huzuni, udhia wala mfundo, hata mwiba unaomchoma ila ni lazima Mwenyezi Mungu amfutie makosa yake kwa mwiba huo.”42 Abdullah (r.a.) amesema: “Nilimtembelea Mtume wakati wa maradhi yake naye akiwa ana homa kali. Nikasema: Hakika wewe una homa kali sana, hiyo ni kwa sababu wewe una malipo mawili. Akasema: “Ndio, hakuna mwislamu atakayepatwa na udhia ila ni lazima Mwenyezi Mungu atamfutia makosa yake kama yanavyopukutika majani ya mti.”43 Hivyo ndivyo Mtume (s.a.w.w.) anavyobainisha kwamba maradhi ya muumini huwa ni kafara ya madhambi yake, kama ambavyo maumivu ya kisaikolojia kama vile mashaka, mfundo na huzuni nayo huwa ni kafara ya dhambi, hivyo ni juu ya mwislamu awe na subira juu ya yale maradhi na matatizo yanayompata katika mwili wake na nafsi yake. Hivyo Qur’ani imezungumzia malipo ya wale wenye kuvuta subira dhidi ya maradhi na matatizo, ikatoa hali ya Nabii Ayubu kama mfano halisi wa aina hiyo ya subira. Mwenyezi Mungu akasema: “Na Ayubu, alipomwita Mola wake Mlezi ya kwamba imenigusa dhara nawe ndiye unayerehemu kushinda wote wanaorehemu.” (Sura Anbiyai: 83). Kama ambavyo 41 Mishkatul-An’war Uk. 281. 42 Sahih Bukhari Juz. 7, Uk. 2. 43 Sahih Bukhari Juz. 7, Uk. 3. 45
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:26 PM
Page 46
Huduma ya Afya katika Uislamu imezungumzia nafasi ya subira katika kuimarisha utashi na azma katika kupambana na matatizo na hatari. Mwenyezi Mungui akasema:
“Na subiri juu ya yale yanayokupata, hakika hayo ni katika mambo yanayoazimiwa.” (Sura Luqman: 16).
“Enyi mlioamini! Ombeni msaada kwa subira na Sala, bila shaka Mwenyezi Mungu yu pamoja na wenye kusubiri.” (Surat al-Baqarah: 153).
“Na uwakumbushe siku za Mwenyezi Mungu. Hakika katika hayo mna mazingatio kwa kila mwenye kusubiri akashukuru.” (Surat Ibrahim: 5).
MARADHI NA TAKLIFU ZA KISHERIA Sheria ya Uislamu imeainisha taklifu za kiibada zilizo wajibu juu ya mwanadamu awapo katika hali ya afya njema na awapo katika hali ya maradhi, imezingatia katika hali zote mbili nguvu za mwanadamu na uwezo wake. Hivyo Qur’ani, Sunna ya Nabii na somo la sheria ya Uislam vimezungumzia taklifu ya mgonjwa na hukumu zinazomhusu kwa kufuata msingi wa majukumu na malipo katika akida ya Uislamu inayofungamana
46
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:26 PM
Page 47
Huduma ya Afya katika Uislamu na uadilifu wake na huruma yake juu ya waja wake. Mwenyezi Mungu amefafanua kanuni kuu ya majukumu kwa kusema:
“Mwenyezi Mungu haikalifishi nafsi yoyote, ila iliwezalo” (Sura alBaqarah: 286).
“Mwenyezi Mungu hamkalifishi mtu yeyote ila kwa kadiri alivyompa” (Surat Talaaq: 7).
“Wala hakuweka juu yenu uzito katika dini” (Sura Hajji: 78).
“Mwenyezi Mungu anataka kuwapunguzieni, na ameumbwa mwanadamu hali ya kuwa ni dhaifu.” (Sura Nisai: 28). Kwa msingi wa kanuni hii Mwenyezi Mungu anasema:
“Na ambaye alikuwa katika nyinyi ni mgonjwa au yuko safarini basi yampasa idadi yake katika siku nyingine. Na wale waiwezayo kwa mashaka yawapasa fidia kumlisha masikini.” (Surat al-Baqarah: 184).
47
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:26 PM
Page 48
Huduma ya Afya katika Uislamu “Si vibaya kwa kipofu, wala si vibaya kwa kilema, wala si vibaya kwa mgonjwa..” (Sura Nuru: 61). Kama ambavyo Qur’ani tukufu inavyozungumzia kanuni ya msingi ya taklifu, ikabainisha kwamba miongoni mwa masharti ya mtu kuwajibikiwa na kitu kisheria na kupata malipo yake ni kuwa na uwezo wa kutekeleza kitu hicho, sawa iwe uwezo huo unaohitajika ni wa kimwili au kimali au kinafsi. Kama pia ilivyobainisha pia kwamba waja wameondolewa uzito, na Mwenyezi Mungu hamkalifishi mwanadamu taklifi ambayo itamsababishia uzito, bali Mwenyezi Mungu kwa upendo Wake, huruma Yake na rehema Zake amewasahilishia waja na kuwarahisishia njia ya kufika Kwake. Hivyo taklifi za kiibada kama tohara, Sala, Saumu, Hija na Jihadi zimetegemea uwezo wa kimwili. Kanuni hii inaelezea uadilifu wa Mwenyezi Mungu, upendo Wake na huruma Zake kwa viumbe. Tunaposoma maandishi ya kifiqhi tunaona sheria ya Uislamu imetofautisha baina ya mtu mgonjwa na mzima katika taklifu. Kwa mfano sheria ya Uislamu imemwajibisha mtu mwenye afya njema ya kawaida kuoga josho la hadathi kubwa, kama vile janaba, hedhi na nifasi, kama ilivyomwajibisha kuchukua wudhu kwa ajili ya Sala. Ama mgonjwa ambaye kuoga kunamdhuru au kuchukua udhu kunamdhuru yeye amesamehewa na taklifu hizo, na ni juu yake kuchukua tohara kwa njia mbadala nayo ni kutayamamu, atayamamu kwa udongo badala ya kuoga au udhu kwa maji. Mgonjwa ambaye saumu inamdhuru basi saumu yake haisihi, na ni juu yake kutokufunga na alipe baada ya kupona maradhi yake, au atoe fidia, nayo ni kiwango maalumu cha chakula, atatoa fidia ya kila siku moja kati ya siku alizoshindwa kufunga kwa sababu ya maradhi kwa kuwapa chakula hicho mafukara. Mgonjwa ambaye hawezi kutekeleza Sala katika hali ya kusimama wima ataitekeleza akiwa amekaa chini, na akishinda hali hiyo basi ni huku akiwa amelala.
48
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:26 PM
Page 49
Huduma ya Afya katika Uislamu Na ambaye hawezi kuhiji wala kupigana jihadi kwa sababu ya matatizo ya kimwili basi wajibu na taklifu hiyo huwa imemvuka na husamehewa majukumu hayo. Kama ambavyo tunaikuta kanuni ya hakuna kudhuru wala kujidhuru ni hukumu yenye kuhusika na taklifu zote, inahusika na kila taklifu inayosababisha madhara ya kimwili kwa mwanadamu, na kwa kufuata kanuni hii basi kila taklifu inayosababisha madhara ya kimwili kwa mtu huwa imemvuka mtu huyo mhusika.
MAMLAKA YA MGONJWA Hakika baadhi ya maradhi yanayomsibu mwanadamu ni maradhi hatari yanayopelekea kukatisha uzima wake na maisha yake na wala hawezi kupona maradhi hayo. Wanafiqhi huyaita maradhi kama haya kwa jina la ‘maradhi ya kifo’. Kanuni ya Uislamu huamiliana na matumizi ya mali za wagonjwa wa namna hiyo, ili kuihifadhi na kuiweka chini ya vizuizi maalumu, hivyo mgonjwa huzuiliwa kutumia mali kwa matumizi ambayo yatawadhuru warithi baada ya kifo chake. Hiyo ni kwa sababu baadhi ya matumizi yake katika mali yatawadhuru warithi kwa sababu za kisaikolojia ambazo huzikimbilia baadhi ya wale waliopatwa na maradhi ya kifo, wale waliokata tamaa ya kupona, kama vile kwa sababu ya kuwapenda baadhi ya jamaa huwapendelea kuliko wengine, au kwa sababu ya kuwachukia hutamani na kutaka kuwanyima haki yao ya mirathi. Lakini tambua kwamba kanuni za Uislamu zinazoamiliana na mgonjwa wa namna hii haziangalii nia ya mgonjwa katika hali hii, bali huangalia matumizi ya kimali je yanawadhuru warithi au la. Miongoni mwa matumizi ambayo hukimbilia wale wenye kupatwa na maradhi haya ya kifo ni: Kutoa au kuomba talaka ili kumnyima mke au mume mirathi. Kutoa zawadi, kifutajasho, kisuluhishi, kijivuo, wakfu, sadaka na mfano wake miongoni mwa matumizi ya kimali ya kisheria, matumizi ambayo 49
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:26 PM
Page 50
Huduma ya Afya katika Uislamu yatahamishia umiliki wa mali yake kwa watu wengine bila fidia wala mbadala, na hatimaye kuwasababishia madhara warithi. Kabla hatujafafanua hukumu inayohusu hali hiyo ya maradhi ya kifo, hatuna budi kutaja kwamba sheria ya Uislamu haijamruhusu mtu yeyote, sawa awe mgonjwa au mzima, kukabidhi wasia uliozidi theluthi ya mali yake, ila pale tu warithi watakapoafikiana na kukubali ule wasia ambao ni ziada iliyo juu ya theluthi, la sivyo ile ziada haitokubalika kisheria. Hapa tunanukuu hukumu kwa mujibu wa sheria ya Uislamu juu ya matumizi ya mali ya mgonjwa yanayowadhuru warithi, hebu tuone sheria inasema nini: Lau aliyepatwa na maradhi ya kifo atatoa tamko la kuwepo kwa deni juu yake au amana ya mtu kwake, sawa huyo mwenye deni na amana awe ni mmoja wa warithi wake au la, basi ufanyiwaji kazi wa tamko hilo utategemea kuthibiti kwa ukweli wake, kukiwa kuna vielelezo vinavyoonyesha kwamba tamko hili limetoka kwake ili kuwanyima warithi haki yao, au ili kumpendelea mtu huyo na ukweli ni kwamba hakuna deni lolote lililo juu yake wala amana yoyote ya mtu huyo iliyo chini ya dhima yake, basi tamko hilo halifanyi kazi ila kwa kadiri ya theluthi ya mali yake. Ama ikiwa hakuna vielelezo vinavyoonyesha uwongo wa tamko lake basi tamko lake litafanya kazi na matumizi yake hayo ni sahihi. Na vinapokosekana vielelezo vya kuthibitisha ukweli wake wala kukanusha tamko lake basi tahadhari ya mkazo ni kutolitekeleza tamko katika ile ziada iliyozidi juu ya theluthi.44 Bora zaidi ni warithi kujadiliana na huyo aliyetamkwa kwenye tamko. Akitoa zawadi mali au kuitoa wakfu au akaitumia katika aina yoyote ya matumizi yasiyokuwa na mbadala na ambayo yanawadhuru warithi, ikiwa matumizi haya yanazidi theluthi ya mali yake hayatatekelezwa ila baada ya warithi kuafikiana na hilo. Ama baadhi wakiafiki na wengine kutoafiki basi 44 Tahrirul-Wasila cha Ima Khomeini, Juz. 2, Uk. 23.
50
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:26 PM
Page 51
Huduma ya Afya katika Uislamu ile ziada iliyo juu ya theluthi itatekelezwa kwa kadiri ya uwafiki wa warithi hawa baadhi. Iwapo aliyepatwa na maradhi ya kifo atamtaliki mkewe talaka rejea au isiyokuwa na rejea bado mke atakuwa na haki ya kurithi mpaka upite muda wa mwaka mzima, iwapo atakufa kabla ya mwaka mzima tangu kutoa talaka. Lakini iwapo atafariki baada ya mwaka mzima tangu talaka itolewe, mke hatokuwa na haki ya mirathi. Hiyo ni kwa sharti kwamba talaka hiyo isiwe imeombwa na mke mwenyewe, na wala isiwe ya Khluu na Mubarati, na pia asiwe amepona maradhi haya ya kifo, na asiwe ameolewa baada ya eda kuisha, hivyo iwapo ataolewa basi hana mirathi, kama ambavyo iwapo talaka ni ya kuomba yeye mwenyewe basi hana mirathi ila iwapo atafariki ndani ya kipindi cha eda katika talaka rejea. Hukumu hii inamhusu mgonjwa wa maradhi ya kifo na hata yule asiyekuwa katika maradhi hayo, kama ambavyo pia mume atamrithi mkewe iwapo atafariki ndani ya eda hii, hiyo ni kwa sababu aliyetalikiwa talaka rejea huzingatiwa kuwa ni mke maadamu tu bado yumo ndani ya eda.45 Miongoni mwa hukumu zilizomo ndani ya sheria ya Uislamu ni kwamba mwamnamke anastahiki mahari kamili toka kwa mumewe iwapo atajamiiana naye, na anastahiki nusu ya mahari iwapo atatalikiwa, au atafariki au kufariki mumewe kabla ya kujamiiana naye. Lakini iwapo mmoja atafariki kabla ya kujamiiana basi aliyebaki hai atamrithi mwenzake, kujamiina si sharti katika kustahiki mirathi. Lakini hukumu hii haifanyi kazi iwapo mume atapatwa na maradhi ya kifo. Kwani iwapo mume huyu atafariki katika maradhi ya kifo, sawa iwe kwa maradhi haya au kwa sababu nyingine kama vile matukio ya ghafla na maradhi mengine, basi hapo ndoa huwa imevunjiaka, na mke huwa hana mirathi wala mahari. Ama akifariki baada ya kujamiiana naye, hapo mahari huthibiti na mirathi pia.46 45 Min’hajus-Salihin cha Sayyid Muhsin al-Hakim, Juz. 2, Uk. 316. 46 Min’hajus-Salihin cha Sayyid Muhsin al-Hakim, Juz. 2, Uk. 316.
47 Min’hajus-Salihin cha Sayyid Muhsin al-Hakim, Juz. 2, Uk. 316. 51
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:26 PM
Page 52
Huduma ya Afya katika Uislamu Iwapo aliyepatwa na maradhi ya kifo atafunga ndoa na mwanamke, kisha akafariki kabla hajajamiina naye basi mwanamke huyo hatokuwa na eda ya kufiwa na mume.47
MATIBABU NA MWANAMKE AJINABI Ili sheria ya Uislamu ihifadhi heshima ya mwanamke na utukufu wake, na ili ing’oe mizizi ya uharibifu na ukiukaji wa maadili ikiwa ni miongoni mwa vitu vinavyochochea vitendo vya ngono, Uislamu uliwajibisha sitara juu ya mwanamke. Ukaweka hukumu na maelekezo makhususi juu ya hilo, ambayo yanahusu kumtizama mwanamume ajinabi au kumgusa mwanamke ajinabi. Nasi tukiwa tunazungumzia hukumu za kumgusa na kumtazama mwanamke ni lazima tufafanue kwamba hakika sheria ya Uislamu ambayo inatatua suala na maudhui hii, imetofautisha hukumu ya mukallafu kulingana na mazingira halisi na hali iliyopo. 1. Katika hali ya kawaida ya mwanadamu: Sheria ya Uislamu imeharamisha mwanamume kumtizama au kumgusa mwanamke ajinabi awapo katika hali ya kawaida, ila mtazamo wa kwanza usio wa kumtamani. Ama iwapo atataka kumuoa basi anaruhusiwa kumtizama usoni na mikononi, na amtizame akiwa katika hali ya kutembea na kusimama. Kama Uislamu ulivyoharamisha kwa mwanamume ajinabi kumtizama mwanamke ajinabi pia umeharamisha mwanamke ajinabi kumtizama mwanamume ajinabi au kumgusa katika hali ya kawaida. Kwa msingi wa kanuni hii ya kisheria hairuhusiwi kisheria mwanamke kumgusa mwanamume ajinabi au kuutazama mwili wake kwa lengo la kumtibu, kama ambavyo hairuhusiwi kisheria kwa mwanamume kuugusa mwili wake au kumtizama kwa lengo la kumtibu pindi anapokuwepo na kupatikana tabibu wa jinsia yake, mwanamume kwa mwanamume na mwanamke kwa mwanamke.
52
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:26 PM
Page 53
Huduma ya Afya katika Uislamu Mara nyingi mwanamke au mwanamume hutokewa na maradhi na hali hakuna tabibu wa jinsia yake au aliye maharimu wake, basi wakati huo inaruhusiwa kisheria kwa kila mmoja kumtizama mwenzake au kumgusa kwa lengo la kumtibu, kwa sababu tu ya dharura hii bila kumtamani. Na kama kitendo kimoja kati ya kumtizama na kumgusa kitatosha kusaidia kumtibu, basi hairuhusiwi kisheria kutekeleza na cha pili, kwa mfano iwapo matibabu yanaweza kukamilika kwa kumtizama tu, basi haijuzu kumgusa, na hivyo hivyo kinyume chake.
UTABIBU NI WAJIBU WA KUTOSHELEZA Miongoni mwa mambo ambayo yanayopatikana tu katika sheria ya Uislamu kutokana na utukufu wa malengo yake ya kimaendeleo, na mtizamo wake wa kibinadamu na kimaadili kwenye majukumu ya kijamii na kwenye thamani ya mali, ni kuweka sheria zinazohusu afya. Tunaweza kufahamu utukufu huu wa kimaendeleo wa kiislamu katika sekta hii ya sheria kwa kutizama yale yaliyojaa katika masomo ya fiqhi katika mlango wa tiba. Na ili kuonyesha uhusiano uliyopo kati ya maudhui ya maradhi na matibabu au kati ya wajibu wako mbele ya maradhi na usalama wa kiafya, tutaonyesha baadhi ya hukumu na hatua ambazo zimethibitishwa na wanafiqhi katika sekta hii. Wanafiqhi wamegawa wajibu wa kisheria sehemu mbili: Wajibu binafsi wa kila mmoja: Nao ni ule wajibu ambao maelekezo na majukumu yanaelekezwa kwa kila aliye mukalafu, kwa sura ya mtu mmoja mmoja, kama vile sala na saumu. Wajibu wa kutosheleza: Nao ni ule wajibu ambao maelekezo huelekezwa kwa mtu kwa sura ya kundi, na hutakiwa kuutekeleza bila kujali ni nani atakayeutekeleza, na inatosha iwapo baadhi ya walengwa watatekeleza amri hiyo, na hapo wajibu ule huwaondokea waliobaki, kama vile kumtetea aliyedhulumiwa, kumwokoa aliye katika vitisho vya hatari, 53
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:26 PM
Page 54
Huduma ya Afya katika Uislamu kumzika maiti na kumtibu mgonjwa, na mengineyo. Fikra na sheria ya Uislamu vimetilia umuhimu sana majukumu ya kijamii ambayo huleta manufaa na kutimiza mahitaji ya wanajamii na jumuia zake, hivyo ikayafanya mambo hayo kuwa ni wajibu wa kutosheleza, kama vile uhandisi, utabibu na fani nyinginezo za kielimu zinazohitajika kijamii. Hebu hapa tunukuu maandiko ya kifiqhi yanayotufafanulia wajibu wa tiba juu ya mtabibu, wajibu wa kutosheleza. Katika maandiko hayo imeandikwa: “Pia inajuzu kuchukua malipo lau akimuajiri kwenye wajibu mwingine usiokuwa wa kiibada, kama vile kumwandikia dawa mgonjwa, au kumtibu au mfano wa hayo, bila shaka inasihi. Na pia kama atamwajiri katika mambo ambayo yanahitaji utawala, kama vile baadhi ya taaluma zinazohusu kilimo, viwanda, utabibu……”48 Sheria hii inamaanisha kuhakikisha uwepo wa yale yanayohitajika na jamii miongoni mwa matabibu, dawa, vifaa vya tiba, taasisi za uchunguzi wa tiba na vyuo vya tiba, na kila kinachotakiwa katika kutimiza wajibu huu kwa namna ya wajibu wa kutosheleza. Lakini kutoa matibabu huwa ni wajibu binafsi wa kila mmoja juu ya tabibu iwapo hakuna wa kutimiza hilo ila yeye tu, na hapo huwa ndiye mwenye dhamana na uhai wa mgonjwa, hivyo iwapo akimwacha bila kumtibu kisha akafa kwa sababu ya kuacha kwake, basi yeye ndiye mhusika wa kifo hicho. Ijapokuwa ni wajibu wa kutosheleza lakini tabibu ana haki ya kuomba malipo yanayooana na matibabu, kama maandiko ya fiqhi yaliyotangulia yalivyoeleza. Lakini analazimika kumtibu bila malipo mgonjwa ambaye uhai wake unategemea matibabu haya, hiyo ni iwapo mgonjwa hana uwezo wa malipo hayo, na kama atamwacha bila kumtibu kwa sababu ya kushindwa kulipia matibabu, basi yeye ndiye mwenye kuwajibika iwapo atafariki, 48 Min’hajus-Salihin cha Sayyid Muhsin al-Hakim, Juz. 2, Uk. 120. 54
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:26 PM
Page 55
Huduma ya Afya katika Uislamu kama ambavyo yeye ndiye mwenye kuwajibika na madhara yoyote yatakayomfika mgonjwa kwa sababu ya yeye tabibu kushindwa kutekeleza jukumu lake. Hebu tunukuu maandiko ya kifiqhi yanayobainisha wajibu wa tabibu na ulazima wa kuwajibika iwapo atamsababishia mgonjwa madhara kwa sababu ya kushindwa kutekeleza majukumu yake: “Na pia tabibu aliyehusika kutoa matibabu yeye mwenyewe ni mwenye dhamana ya uharibifu iwapo utatokea..”49 yaani ndiye mwenye kuwajibika na madhara yoyote yatakayompata mgonjwa kutokana na kutotekeleza jukumu lake katika njia ya kutoa matibabu, au kwa sababu ya mtabibu asiye na ujuzi na ugonjwa huo kujitwika kazi hiyo. Tunaweza kufahamu thamani ya utabibu, malipo yake na thawabu zake kupitia maelezo ya Uislamu ambayo yanalingania huruma na msaada, kupunguza maumivu ya watu, kutoa msaada wa hali na mali kwa wengine na kuwaondolea adha na madhara, thawabu ambazo anastahiki kuzipata tabibu mwenye nia safi na utashi safi, yule mwenye kuwapunguzia watu maumivu na mwenye kuilinda afya yao.
DUA NA PONYO
“Ambaye ameniumba, naye ananiongoza. Naye ndiye anayenilisha na kuninywesha. Na ninapougua, basi yeye ananiponya” (Sura Shua’raa: 78 – 80).
49 Min’hajus-Salihin cha Sayyid Muhsin al-Hakim, Juz. 2, Uk. 120 55
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:26 PM
Page 56
Huduma ya Afya katika Uislamu
“Na tunateremsha Qur’ani ambayo ni ponyo na rehema kwa wenye kuamini, wala hayawazidishii madhalimu ila hasara tu.” (Sura Israil: 82).
“Muombeni Mola wenu Mlezi kwa unyenyekevu na kwa siri, hakika yeye hawapendi warukao mipaka.” (Sura Aaraf: 55).
“Na Mola wenu Mlezi husema: Niombeni nitakujibuni. Kwa hakika wale wajivunao kufanya ibada yangu, wataingia Jahannam wakifedheheka.” (Sura Muumin: 60).
“Wale walioamini na zikatulia nyoyo zao kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu, sikilizeni, kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu, nyoyo hutulia.” (Sura Ra’d: 28).
56
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:26 PM
Page 57
Huduma ya Afya katika Uislamu “Na waja wangu watakapokuuliza juu yangu basi hakika mimi nipo karibu, nayaitikia maombi ya mwombaji anaponiomba, basi waniitikie na waniamini, ili wapate kuongoka. (Surat al-Baqarah: 186). “Na Ayubu, alipomwita Mola wake Mlezi ya kwamba imenigusa dhara nawe ndiye unayerehemu kushinda wote wanaorehemu. Basi tukamkubalia na tukamwondolea dhara aliyokuwa nayo na tukampa watu wake na mfano wa pamoja nao ni rehema kutoka kwetu, na ukumbusho kwa wafanya ibada.” (Sura Anbiyai: 83 – 84). Maradhi ni jina la kuvurugika mpangilio wa mwili au nafsi na kuharibika utendaji wake, na ili mwili na nafsi virudi kwenye hali yake ya afya na mazingira ya kawaida ni lazima kuondoa uvurugikaji huo na uharibikaji huo. Kazi hii ya kuondoa ndio huitwa tiba. Tiba ya mwili ina vifaa na njia mbalimbali za kielimu, hivyo maradhi ya kimwili hutibiwa kwa njia ya vyakula, dawa za kemikali au za asili, mazoezi ya kawaida, utumiaji wa miyonzi, upasuaji, uondoaji wa kiungo au kukibadili au kuitoa ile sehemu yenye kudhuru, na mengineyo. Na suala la kuathiriana kati ya mwili na nafsi ni mambo yenye ukweli wa kielimu uliothibitishwa na uchunguzi wa kitiba, hivyo maradhi mengi ya mwili sababu yake ni maradhi na hali za kisaikolojia, kama ambavyo maradhi mengi ya kisaikolojia sababu yake ni maradhi ya kimwili. Hivyo matabibu wanasisitiza kwamba maradhi ya mapafu, mgandamizo wa damu, vidonda vya tumbo, kichwa, kisukari, moyo na mengineyo miongoni mwa maradhi yamsumbuayo mwanadamu, chanzo chake ni hali na mabadiliko ya kisaikolojia, kisha ni kwamba yaligeuka na kuwa maradhi ya kimwili. Amatekasika Mwenyezi Mungu ambaye alimuumba vilivyo mwanadamu, mwili na nafsi vina uwezo wa kuandaa mazingira ya kawaida na kubadili hali ya kimaradhi. Mwili unamiliki uwezo wa kujitengeneza wenyewe kwa 57
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:26 PM
Page 58
Huduma ya Afya katika Uislamu kutumia nguvu ya asili au kwa msaada wa chakula au dawa, viharakishi na vifaa vyenye kusaidia kuurudishia mwili mpangilio wa kawaida. Kama ambavyo mwili unaweza kuandaa mazingira ya kawaida ya mwili, yaani ile ghali ya afya, kwa kutumia nguvu ya asili na kwa msaada wa tiba, ndivyo hivyo hivyo nafsi nayo inaweza kubadili na kugeuza kwa kuleta mazingira mengine. Hakika miongoni mwa nyenzo muhimu za kutibia maradhi ya kisaikolojia, ni kazi ya uchambuzi wa kisaikolojia na kugundua sababu za mabadiliko ya hali za kisaikolojia, na kujitahidi kuweza kuzidhibiti. Na hakika miongoni mwa njia bora kabisa za kuyadhibiti maradhi ya kisaikolojia ni kumwelimisha mgonjwa na kumfahamisha hali ya ugonjwa baada ya kuufafanua, na pia kuondoa mafundo ya ugonjwa na kuinua hali yake ya kisaikolojia, na kuweza kulipokea tatizo kama hali ya kawaida, au kama hali ya kawaida inayoweza kuondoka kupitia tiba ya kimada au kisaikolojia. Njia zote hizo za matibabu, sawa ziwe za kutibu maradhi ya kisaikolojia au ya kimwili, zote zinategemea msaada wa mwili na nafsi katika kuandaa mazingira ya asili yake ya kawaida. Hivyo mtu anapomwelekea Mwenyezi Mungu kwa dua na moyo wenye ikhlasi, akatenda mema, kama kutoa sadaka, kutekeleza nadhiri na kuomba maghufira, basi rehema humwelekea yeye, na hapo Mwenyezi Mungu huruhusu mwili na nafsi viandae mazingira yake ya asili yake ya kawaida, kwani utashi wa Mwenyezi Mungu wenye kutawala na kutiisha vitu vyote ndio sababu yenywe nguvu yenye kutawala ulimwengu huu ambao huenda kulingana na utashi Wake na matakwa Yake. Kumwamini Mwenyezi Mungu na kumtegemea yeye ndio sababu kubwa ya kuitengeneza nafsi na kuitibu na maradhi yake, kwa sababu hali hiyo ya imani ina uwezo wa kuiokoa na mashaka, khofu, huzuni, hasira na hali ya mihangaiko ya kinafsi. 58
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:26 PM
Page 59
Huduma ya Afya katika Uislamu Hivyo Mwenyezi Mungu amembainishia wazi mwanadamu kwamba miongoni mwa Aya za Qur’ani zimo zilizo ponyo la nyoyo na kisafisho cha nafsi dhidi ya hali za khofu, mashaka, na hali mbalimbali ambazo husababisha maradhi ya kisaikolojia. Mwenyezi Mungu akasema: “Na tunateremsha Qur’ani ambayo ni ponyo na rehema kwa wenye kuamini.” (Sura Israil: 82). Na akasema: “Sikilizeni kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu, nyoyo hutulia.” (Sura Ra’d: 28). Nafsi inapopona maradhi yake ndipo mwili nao unapopona maradhi yake makubwa ya kimwili. Hivi ndivyo dua inavyokuwa sababu ya kupata ponyo: Kwanza: Ni kutokana na uwezo wake wa kutengeneza hali ya kisaikolojia kwa mgonjwa kutokana na kumpa mgonjwa hali ya kumtegemea Mwenyezi Mungu na kuridhia majaaliwa yake na makadara yake, hivyo imani hii inamwokoa na hali ya mfundo, hasira, na mihemuko mingine ya kisaikolojia, na hapo athari za imani zinaakisi hali ya kiafya ya mwili na kutoa matokeo mazuri. Hivyo ndivyo kumwamini Mwenyezi Mungu kunavyoisaidia nafsi kurejesha hali yake ya kawaida na kuathiri hali ya mwili, kwa njia hiyo dua inaingia kama tiba ya kielimu na sababu yenye kuathiri mfumo wa utendaji wa mwili kwa kutoa athari za kawaida. Pili: Hakika uumbaji na mambo yote yapo chini ya Mwenyezi Mungu naye ndiye muweza wa kutenda alitakalo: “Ufalme umo mikono mwake naye ni Muweza wa kila kitu.” Hivyo hutoa ponyo na uokovu kwa mgonjwa, na hapo mwili hurudi kwenye hali yake ya kawaida kama alivyouumba ukiwa salama katika maumbile yake, harakati zake na utendaji wake. Mwenyezi Mungu ametuambia kwamba hujibu maombi ya mwenye kumuomba pindi anapomuomba, na kwamba Yeye ndiye anayemiliki ponyo, na Yeye ndiye ambaye rehema Zake zilimfunika Nabii Ayubu (a.s.) baada ya kupatwa na maradhi na kumchosha, hapo akamjibia dua yake na akamrudishia afya njema na usalama. 59
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:26 PM
Page 60
Huduma ya Afya katika Uislamu Kuna habari na riwaya zimepokewa kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwamba alikuwa akiwakinga Hasan na Husain kwa kuwasomea Surat Nasi na Surat al-Falaqi. Kama ambavyo alikuwa akiomba dua ya kutaka ponyo dhidi ya maradhi na akisisitiza kumwombea dua mgonjwa. Ali (a.s.), Fatima binti wa Mtume (s.a.w.w.) na Fidha mtumishi wa Fatima (a.s.) waliweka nadhiri ya kufunga siku tatu ili kuomba ponyo la ugonjwa uliowasibu Hasan na Husein, na hapo Mwenyezi Mungu akawaneemesha na ponyo, na ndipo wakatoa sadaka ile futari yao kwa muda wa siku tatu, na hapo Mwenyezi Mungu akateremsha Surat Dahri akiwapongeza Ali, Fatuma, Fidha, Hasan na Husain (a.s.). Ili kukamilisha faida hebu tunukuu baadhi ya dua za Mtukufu Mtume zinazohusu tiba ya maradhi, ili dua hizo ziwe njia ya kuomba fadhila na rehema toka kwa Mola Mlezi na ziwe sababu ya kupona. Al-Kaf’amiy amepokea kutoka kwa al-Mujahidi kwamba: Anayetafuta tiba ya ugonjwa alionao, basi aseme kwenye sijida yake ya pili katika rakaa zake mbili za mwanzo za sala ya usiku: “Ewe Mtukufu! Ewe Adhimu! Ewe Rahman! Ewe Rahimu! Ewe Msikivu wa dua! Ewe Mwenye kutoa kheri! Msalie Muhammadi na aali Muhammadi, na nipe toka katika kheri ya dunia na Akhera yale uyaridhiayo wewe, na niepushie toka katika shari ya dunia na Akhera uyachukiayo wewe, na niondolee ugonjwa huu (taja ugonjwa) kwani bila shaka umenizidia na umenihuzunisha.” Ataomba dua mara kwa mara bila shaka insha’allah atapatwa na afya haraka iwezekanavyo. Imepokeawa dua ya maradhi yote kutoka kwa Imam Ridha (a.s.): “Ewe Mteremshaji wa ponyo na muondoaji wa ugonjwa! Msalie Muhammadi na aali zake, na niteremshie ponyo kwenye ugonjwa wangu.” Sayyid Ibnu Taus katika kitabu al-Muhji amepokea kutoka kwa Ibnu Abbasi kwamba alisema: Nilikuwa nimeketi kwa Ali (a.s.) na ndipo alipoingia mtu aliyesawijika rangi, akasema: Ewe Amirul-Muuminina! 60
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:26 PM
Page 61
Huduma ya Afya katika Uislamu Mimi ni mtu mwenye maradhi, mwingi wa magonjwa na maumivu, naomba unifundishe dua itakayonisaidia katika maradhi yangu. Ali (a.s.) akasema: “Nitakufundisha dua ambayo Jibril (a.s.) alimfunza Mtume (s.a.w.w.) walipougua Hasan na Husain (a.s.), nayo ni: ‘Ilahi! Kila unineemeshapo neema yoyote, hupunguka shukurani yangu kwako juu ya neema hiyo, na kila unaponijaribu kwa mtihani wowote, hupunguka subira yangu kwenye mtihani huo. Ewe ambaye hupunguka shukurani yangu juu ya neema yake lakini haninyimi! Na ewe ambaye hupunguka subira yangu kwenye mtihani wake lakini hanitelekezi! Na ewe ambaye aliniona nikiwa katika maasi lakini hajanifedhehesha! Na ewe ambaye aliniona nikiwa katika makosa lakini hajaniadhibu kwayo! Msalie Muhammadi na aali Muhammadi na nighufirie dhambi zangu na niponye maradhi yangu, hakika wewe ni Muweza wa kila kitu.”’ Ibnu Abbasi amesema: Baada ya mwaka nikamwona mtu yule akiwa na uso wa kupendeza wenye kung’aa wekundu, akasema: Sikuwahi kuiomba na hali ni mgonjwa ila nilipona, wala nikiwa na maradhi ila yalipona, na sikuwahi kuingia kwa mtawala ila alipunguza ujeuri wake, na sikuwahi kuisoma ila Mwenyezi Mungu alinikinga naye.” Imam as-Sadiq (a.s.) amesema: Mwenye ugonjwa ausomee dua hii mara arubaini kila siku asubuhi: “Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu. Kila sifa njema ni ya Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa viumbe wote. Anatutosha Mwenyezi Mungu naye ndio mtegemewa bora. Ametukuka Mwenyezi Mungu muumbaji bora kushinda wote. Hakuna ujanja wala nguvu ila kwa msaada wa Mwenyezi Mungu Mtukufu Adhimu.” Imam as-Sadiq amesema: Weka mkono wako juu ya eneo lenye maumivu na useme mara tatu: “Allahu, Allahu, Allahu ni Mola wangu Mlezi kweli, simshirikishi na chochote. Ewe Mwenyezi Mungu! Wewe ndiye Mmiliki wake na kila lililokubwa basi yaondowe (maumivu) na unifariji dhidi yake.” 61
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:26 PM
Page 62
Huduma ya Afya katika Uislamu Imam as-Sadiq amesema: Ni kwa ajili ya maumivu yote: “Kwa jina la Mwenyezi Mungu na kwa msaada wa Mwenyezi Mungu, ni neema ngapi za Mwenyezi Mungu zimo ndani ya mishipa tulivu na isiyo tulivu, juu ya mja mwenye shukurani na asiye na shukurani.” Na sema mara tatu: “Ewe Mwenyezi Mungu! Niondolee matatizo yangu na niharakishie afya yangu na niondolee dhara langu.” Imam as-Sadiq amesema: Hakika Ali aliugua, Mtume akamjia na kumwambia: “Sema: “Ewe Mwenyezi Mungu! Hakika mimi nakuomba kuharakishiwa afya yako, subira juu ya mtihani wako na kutoka kwenye dunia kwenda kwenye rehema yako.” Na Shahidi (r.a.) alikuwa akimshika mgonjwa mkono wa kulia na kusoma: “Ewe Mwenyezi Mungu! Mwondolee maradhi na magonjwa, na mrudishe kwenye siha na ponyo, na mwendelezee kwa kumpa kinga bora na mrudishe kwenye afya njema, na fanya maradhi yaliyomsibu nyongeza ya uhai wake na kafara ya makosa yake. Ewe Mwenyezi Mungu na msalie Muhammadi na aali Muhammadi.” Imepokewa ndani ya kitabu al-Mujtaba Minaduail-Mujtaba kwamba utamsomea mgonjwa: “Ewe Mwenyezi Mungu! Hakika wewe umesema ndani Kitabu chakio kilichoteremshwa juu ya Nabii wako uliyemtuma: Hakuna msiba wowote uliowapata ila ni kwa sababu ya yale yaliyochumwa na mikono yenu, na anasamehe mengi, ewe Mwenyezi Mungu msalie Muhammadi na aali Muhammadi na yaweke maradhi haya miongoni mwa yale mengi unayosamehe na kuponya. Tulia ewe maumivu na ondoka sasa hivi toka kwa mja huyu dhaifu, nimekutuliza na kukuondoa kupitia ambaye vimetulia kwa ajili yake vilivyomo usiku na mchana, naye ni Msikivu Mjuzi.” 62
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:26 PM
Page 63
Huduma ya Afya katika Uislamu Ali (a.s.) amesema: Ni kinga ya kila maumivu ya mwili, atakayeyasema hatodhuriwa na maumivu, nayo ni: “Najilinda kwa nguvu ya Mwenyezi Mungu na uwezo wake juu ya vitu vyote. Nailinda nafsi yangu kwa Jabari wa mbinguni na ardhini. Nailinda nafsi yangu kwa ambaye jina lake halidhuriwi na ugonjwa wowote. Nailinda nafsi yangu kwa ambaye jina lake ni baraka na ponyo.” Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema: “Mkiwaona waliopatwa ni mitihani, muhimidini Mwenyezi Mungu na wala msiwasikilizishe kwa kufanya hivyo kutawahuzunisha.” Imam al-Baqir (a.s.) amesema: “Ukimuona aliyepatwa na mtihani, sema mara tatu bila yeye kusikia: Kila sifa njema ni ya Mwenyezi Mungu ambaye amenipa afya njema dhidi ya yale aliyomjaribu, na lau angelitaka angefanya.” Dua wakati unapopatwa na msiba: “Na wape habari ya furaha wenye kusubiri. Ambao ukiwafikia msiba, husema: Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu na sisi tu wenye kurejea kwake. Hao juu yao ziko baraka na rehema kutoka kwa Mola wao Mlezi, nao ndio wenye kuongoka. Kila sifa njema ni ya Mwenyezi Mungu ambaye hajafanya msiba wangu ni katika dini. Na kila sifa njema ni ya Mwenyezi Mungu ambaye lau angelitaka msiba wangu uwe mkubwa kushinda ulivyo angefanya, na kila sifa njema ni ya Mwenyezi Mungu juu ya jambo ambalo alitaka liwe na likawa.” Dua ya kuondoa mashaka na huzuni: “Ewe Ambaye Kwake hufunguka mafundo yachukizayo. Ewe Ambaye kupitia Kwake makali ya shida huwa butu. Ewe Ambaye huombwa ubaridi wa kuifikia faraja. Magumu yamedhalilika mbele ya nguvu Zako, kwa huruma Zako sababu zimepatikana, kwa nguvu Zako hukumu zimepita na kwa utashi Wako vitu vimekwenda kama ilivyotakiwa. Kwa utashi Wako bila kauli Yako vimewajibika na kwa utashi Wako bila katazo Lako vime63
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:26 PM
Page 64
Huduma ya Afya katika Uislamu jizuia. Wewe ndiye wa kuombwa wakati wa jambo muhimu na ndio kimbilio la wakati wa shida. Haiondoki isipokuwa ile uliyoiondoa na wala haitatuki isipokuwa ile uliyoitatua. Tayari ewe Mola wangu Mlezi yameshaniteremkia yale ambayo uzito wake umenielemea na limenishukia jambo ambalo uzito wake umenishinda. Kwa nguvu Zako umelishusha juu yangu na kwa mamlaka Yako umelielekeza kwangu. Hivyo basi hakuna wa kuondoa ulilolileta, kuzuia ulilolielekeza, wa kufungua ulichofunga wala wa kufunga ulichokifungua, kukifanya chepesi kile ulichokifanya kizito, wala wa kumsaidia uliyemtelekeza. Hivyo msalie Muhammad na Aali zake na nifungulie ewe Mola wangu Mlezi mlango wa faraja kwa rehema Zako. Vunjilia mbali mamlaka ya usumbufu kwa nguvu Zako. Nipe mtazamo mzuri kwa malalamiko yangu. Nionjeshe utamu wa matendo kupitia yale niliyokuomba. Nipe faraja njema na rehema kutoka Kwako. Na nijaalie mwanya wa kupenya upesi kutoka Kwako. Usinifanye nijishughulishe na mengine na kuacha kutekeleza wajibu Wako na Sunna Yako. Nimedhikika kutokana na yale yaliyonishukia Ee Mola Wangu Mlezi! nimejawa na huzuni kwa kuyabeba yale yaliyoniteremkia, na Wewe ndiye Mwenye uwezo wa kuondoa yaliyonifika na kuyaweka mbali niliyoangukia, hivyo nifanyie hayo ingawa sistahiki kupata hayo kutoka Kwako ewe bwana wa Arshi adhimu na Mwenye neema uliye Mkarimu, Wewe ni Muweza ewe Mwenye huruma kushinda wote wenye huruma. Amina ewe Mola Mlezi wa viumbe wote.� Dua ya kuondoa matatizo: “Ewe nguzo ya asiyekuwa na nguzo! Ewe akiba ya asiyekuwa na akiba! Ewe egemeo la asiyekuwa na egemeo! Ewe hirizi ya asiyekuwa na hirizi! Ewe hirizi ya wanyonge! Ewe mwenye matarajio makubwa! Ewe 64
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:26 PM
Page 65
Huduma ya Afya katika Uislamu mwokozi wa aliyezama! Ewe mwokozi wa aliyehiliki! Ewe mwema! Ewe mtenda mazuri! Ewe mneemeshaji! Ewe mtenda fadhila! Wewe ndiye ambaye umesujudiwa na giza la usiku, nuru ya mchana, mwanga wa mwezi, mionzi ya jua, mvumo wa miti na sauti ya maji. Ewe Mwenyezi Mungu! Ewe Mwenyezi Mungu! Ewe Mwenyezi Mungu! Hakuna mungu ila Wewe Mmmoja wa pekee usiye na mshirika. Ewe Mola wangu ewe Mwenyezi Mungu! Msalie Muhammadi na aali Muhammadi na nitendee mimi yale uyatakayo, nitendee mimi kadha wa kadha. (Hapo utataja haja yako).” Dua nyingine kutoka kwenye kitabu Kunuzun-Najah, Mtume (s.a.w.w.) alimfunza bintiye Fatima (a.s.) dua hii, nayo ni: “Ewe Mjuzi wa ghaibu na siri! Ewe Mwenye kutiiwa! Ewe Mwenye nguvu! Ewe Mjuzi! Ewe uliyeyashinda makundi kwa ajili ya Muhammadi! Ewe uliyemtega Firaun kwa ajili ya Musa! Ewe uliyemwokoa Isa toka mikononi mwa madhalimu! Ewe uliyemwokoa Nuhu na gharika! Ewe mwenye kutenda kila kheri! Ewe mwenye kuongoza kuelekea kwenye kila kheri! Ewe mwenye kujilisha kila kheri! Ewe mwenye kuamuru kila kheri! Ewe muumba wa kheri! Wewe ndiye Mwenyezi Mungu hakuna mungu ila Wewe, nimetamani kwako yale ambayo wewe umeshayajua, basi nijibu kwa fadhila zako, ewe Mwenyezi Mungu! Ewe Mwingi wa rehema.”
65
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:26 PM
Page 66
Huduma ya Afya katika Uislamu
KUMTEMBELEA MGONJWA Mwenyezi Mungu amesema:
“Enyi watu! Kwa hakika tumekuumbeni kutokana na mwanaume na mwanamke, na tumekufanyeni mataifa na makabila ili mjuane, hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni aliye mcha Mungu zaidi katika nyinyi, kwa hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye khabari.� (Sura Hujrat: 13). Hakika kuisoma jamii ya kiislamu au namna Uislamu unavyoinadhimu jamii ya kibinadamu kunatuonyesha misingi na viunganishi imara ambavyo Uislamu umetumia kujengea mahusiano ya kijamii na heshima ya mwanadamu na utukufu wake. Hakika maadili, kanuni, maelekezo, ibada na fikra za kiitikadi, yote hayo yanachangia katika kujenga umbile la kijamii na kulinadhimu kwa misingi ya upendo, kusaidiana na kuheshimu hisia za mwanadamu, na kusisitiza maana ya ushirikiano wa ubinadamu na upendo na kuleta hisia za huruma. Kitendo cha Uislamu kujali sana suala la maingiliano na muamala wa kijamii na kusisitiza kuendelea kwa mwenendo huu kinaakisi kwetu thamani ya maisha ya kijamii na jinsi ulivyojali jamii na adabu zake. Uzoefu wa kihistoria na kimaendeleo umethibitisha kwamba misingi na viunganishi vya kimali vyenyewe pekee havijengi jamii yenye mshikamano na wala haviimarishi jamii ya kibinadamu iliyo imara. Na bila shaka kusoma na kuchambua jamii ya kimali tuliyonayo sasa kunatufichulia kiwango cha matatizo ya kisaikolojia na kijamii, ukosefu wa huruma, 66
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:26 PM
Page 67
Huduma ya Afya katika Uislamu kutokuwepo kwa roho ya kibinadamu katika mahusiano na mafungamano, na pia jinsi mwanadamu anavyohisi mashaka, huzuni, mchoko, unyonge, kutokuwa na maana, ugeni na upweke katika jamii hii. Ni jambo lililo wazi katika masomo ya saikolojia, maadili na maisha ya hisia, kwamba jambo la kwanza analolihitaji mwanadamu kabla ya haja zote na lenye athari kubwa katika kumletea furaha ni kushibisha upande wa kisaikolojia na wa huruma, ushibishaji salama. Bali ni kwamba furaha ya kweli kwake ni utulivu wa kisaikolojia na hisia za ndani ambazo huonekana katika hali ya kuridhia, upendo na utulivu. Mwanadamu katika baadhi ya hatua za maisha yake anahisi haja ya kujaliwa na wenzake na kupata huruma yao kushinda anavyohisi katika hatua nyingine. Katika hatua ya utoto, uzee, udhaifu, maradhi na matukio ya kuumiza, mwanadamu huhitaji kusaidiwa na msaada wa huruma, kujaliwa na wengine na huduma yao kwake kushinda anavyohitajia mambo hayo katika wakati na mazingira mengine. Na kwa kweli kukosekana kwa huduma hii toka kwa wenzako huathiri vibaya hali ya mwanadamu huyu na hatimaye huakisi uhusiano wake na nafsi yake na jamii yake. Hakika hisia hatari zaidi ambayo huleta uadui kwa watu wengi ni kule mwanadamu kuhisi kutengwa na wenzake na kutoheshimu utu wake. Misimamo kama hii kutoka kwa wenzake na mfano wa hisia kama hizi hutengeneza hali ya maradhi inayoongeza mahangaiko yake na taabu zake, kwa ajili hiyo Uislamu umelingania kusaidiana na huruma, kumjulia hali asiyekuwepo na ukahimiza kutembeleana na ukasisitiza kumtembelea mgonjwa, undugu, ujirani mwema na kuwa na ndugu na marafiki, ili kwamba wanajamii waingie katika mnyororo wa mahusiano ya kiupendo na ubinadamu ambayo yatatoa roho ya kusaidiana na kujaliana, na yatapandikiza hisia za upendo na kuhehimu utu wa mtu, jambo ambalo litasaidia sana kujenga maadili mema na kuondoa hali za upotofu na mkengeuko.
67
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:26 PM
Page 68
Huduma ya Afya katika Uislamu Hakika kumzuru mgonjwa hupandikiza ndani ya nafsi yake hisia za kupendwa na wenzake na hupunguza machungu ndani ya nafsi yake, na humhisisha huduma toka kwa ndugu zake, watu wake, marafiki zake na jamii yake. Mara nyingi anachokianza mgonjwa aliyepatwa na maradhi makubwa, au ya muda mrefu au yaliyo hatari zaidi kwa uhai wake, mara nyingi baada ya kupona huanza mwenendo mpya na mahusiano mengi mazuri ya kibinadamu na yaliyo sahihi, hususan anapompata mwenye kumsaidia kwa tiba na ponyo, kwa kumpunguzia maumivu ya kihali na mali. Hivyo tunaikuta Qur’ani tukufu inasisitiza kujuliana hali, kusaidiana na kushirikiana baina ya wanajamii. Katika wosia wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na maimamu waongofu, tunasoma maelekezo na mwongozo wa thamani katika maudhui hii. Hapa tutataja zile riwaya zilizopatikana kuhusu kumtembelea mgonjwa na kuhurumiana naye. Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Mwislamu akimtembelea ndugu yake kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu husema: Umepata mema na umepata makazi peponi.”50 Imam as-Sadiq (a.s.) amesema: “Watembeleeni wagonjwa wenu na waombeeni dua.”51 Al-Barau bin Azib amesema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alituamuru mambo saba na alitukataza mambo saba: Alituamuru kumtembelea mgonjwa, kusindikiza jeneza, kumwombea dua mwenye kutoa chafya, kuitikia salamu, kumvua na tuhuma yule mwenye kuapa, kuitikia mwaliko, na kumsaidia mdhulumiwa. Alitukataza kutumia vyombo vya madini ya fedha, kuvaa pete ya dhahabu, hariri……”52
50 Musnad Ahmad bin Hanbal Juz. 2, Uk. 326. 51 Mishkatul-An’war Uk. 280. 52 Musnad Ahmad bin Hanbal Juz. 4, Uk. 284. 68
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:26 PM
Page 69
Huduma ya Afya katika Uislamu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Hakika mwenye kumtembelea mgonjwa huzama ndani ya rehema, anapoketi humfunika.”53 Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Hakuna mtu anayemtembelea mgonjwa na kuketi kwake ila hufunikwa na rehema toka kila upande muda wote atakaokaa kwake. Na atokapo kwake huandikiwa malipo ya funga ya siku nzima.”54 Kama ambavyo wosia na maelekezo ya Uislamu umesisitiza kumtembelea mgonjwa ndivyo hivyo hivyo umesisitiza kumkirimu mgonjwa na kumpelekea zawadi, ili kumhisisha furaha na upendo wa mwenye kumtembelea. Tunaposoma msimamo wa Imam Ja’far as-Sadiq (a.s.) tunaona harakati hizi za kimaadili na ambazo zimesisitizwa. Mfanyakazi wa Imam Ja’far as-Sadiq (a.s.) amesema: “Mmoja wa wafuasi wake aliugua tukatoka kwenda kumtembelea nasi tukiwa na kundi la wafuasi wa Ja’far, ghafla tukakutana na Ja’far njiani, akatuambia: ‘Mnaelekea wapi?’ tukasema tunakwenda kumtembelea fulani. Akatwambia: ‘Simameni.’ Tukasimama, ndipo akatuambia: ‘Je mmoja wenu ana tufaha, pera au manukato au udi?’ tukasema hatuna chochote. Akasema: ‘Hivi hamjui kwamba mgonjwa hupata raha kwa kila anachopelekewa.”55 Hakika riwaya hii inatufichulia alama ya utamaduni wa kiislamu ambao unajali sana upande wa nafsi na kuingiza furaha moyoni mwa mgonjwa, ukiachia mbali ile faida na manufaa ya kimada anayoyapata. Hivyo utaona inasisitiza kumpelekea mgonjwa zawadi za matunda yenye rangi nzuri na manukato mazuri. Kama ambavyo inavyosisitiza udi na harufu nzuri kama alama ya kuonyesha thamani ya uzuri na hisia za kisaikolojia ambazo huachwa na zawadi ndani ya nafsi ya mgonjwa. 53 Kanzul-Ummal Juz. 9, Hadithi ya 25169. 54 Kanzul-Ummal Juz. 9, Hadithi ya 25184. 55 Mizanul-Hikma Uk. 129. 69
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:26 PM
Page 70
Huduma ya Afya katika Uislamu Na miongoni mwa mambo muhimu ya kisaikolojia ambayo yametiliwa umuhimu na adabu za kijamii za Uislamu ni kumsikilizisha mgonjwa maneno mazuri, kumuombea dua apone na kumsisitiza kuvuta subira, jambo ambalo huingiza ndani ya nafsi yake hisia za upendo na hisia za kujaliwa na wenzake, na hivyo kuongeza ari yake katika kupambana na maradhi na kupata matumaini na matarajio au kuyaimarisha ndani ya nafsi yake. Hakika Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anatuelekeza kwenye muamala huu wa kuamiliana na mgonjwa, anasema: “Hakika miongoni mwa namna za mmoja wenu kutimiza hali ya kumtembelea ndugu yake ni aweke mkono wake juu yake, na amuulize alivyoamka na alivyoshinda.”56 Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alimtembelea sahaba mtukufu Salman, akasema: “Ewe Salman! Mwenyezi Mungu auponye ugonjwa wako, akughofirie dhambi zako na akuafu katika dini yako na mwili wako mpaka wakati wa kifo chako.”57 Uislamu katika maadili yake na adabu zake na misingi ya mahusiano yake unapambika kwa heshima na kuheshimu adabu za kijamii, na kuuheshimu upendo wa nafsi ya mwanadamu, hivyo umetaka tupunguze muda wa kumtembelea mgonjwa na kutokurefusha kikao kwa mgonjwa, hiyo ni ili kumpa muda wa kupumzika kimwili na kimawazo na kumpa usalama wa kiafya yule mwenye kumtembelea. Kwani hakika baadhi ya watembeleaji humuudhi mgonjwa kwa sababu ya kurefusha ziara na kikao na kukithirisha mazungumzo, hivyo imekuja katika maelekezo ya Mtukufu Mtume kwamba alisema: “Mtembeleaji mgonjwa aliye bora kushinda wote ni yule mwenye kuhafifisha.”58 Na pia alisema: “Kumtembelea mgonjwa ni kwa kadiri ya mpito wa ngamia.”59 56 Kanzul-Ummal Juz. 9, Hadithi ya 25195. 57 Kanzul-Ummal Juz. 9, Hadithi ya 25200. 58 Kanzul-Irfan, Hadithi ya 25139. 59 Kanzul-Irfan, Hadithi ya 25155. 70
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:26 PM
Page 71
Huduma ya Afya katika Uislamu Bali msisitizo wa kufupisha ziara na kupunguza muda wa kukaa kwa mgonjwa unaongezeka pale mgonjwa anapokuwa hapendi kuzongwa, Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Hakika kumtembelea mgonjwa kuliko na malipo makubwa na kule kwa muda mfupi.”60 Na amesema: “Aliye na malipo makubwa kwa Mwenyezi Mungu kushinda wote wenye kumtembelea mgonjwa ni yule ambaye anapomtembelea ndugu yake mgonjwa hupunguza kikao, ila iwapo mgonjwa atapenda hilo au kulitaka, na akawa amemwomba kufanya hivyo.”61 Hivi ndivyo zinavyokamilika kanuni na misingi ya adabu za kijamii katika kumtembelea mgonjwa, adabu ambazo zinaoana na hali za kisaikolojia na kinafsi na ambazo zinatoa matokeo bora ya kijamii kiasi kwamba zinapandikiza upendo, kujuliana hali na hisia za roho ya undugu na kusaidiana. Na mwisho wa dua zetu ni kumshukuru Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa viumbe wote.
60 Kanzul-Irfan, Hadithi ya 25149. 61 Mizanul-Hikma: Mgonjwa. 71
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:26 PM
Page 72
Huduma ya Afya katika Uislamu
ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION 1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9. 10. 11. 12. 13. 14. 15. 16. 17. 18. 19. 20. 21. 22. 23. 24.
Qur'an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Thalathini Uharamisho wa Riba Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili Hekaya za Bahlul Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.) Hijab vazi Bora Ukweli wa Shia Ithnaashari Madhambi Makuu Mbingu imenikirimu Abdallah Ibn Saba Khadijatul Kubra Utumwa Umakini katika Swala Misingi ya Maarifa Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia Bilal wa Afrika Abudharr Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu Salman Farsi Ammar Yasir Qur'an na Hadithi Elimu ya Nafsi 72
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:26 PM
Huduma ya Afya katika Uislamu 25. 26. 27. 28. 29. 30. 31. 32. 33. 34. 35. 36. 37. 38. 39 40. 41. 42. 43. 44. 45. 46. 47. 48. 49. 50. 51. 52. 53. 54. 55.
Yajue Madhehebu ya Shia Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur'an Tukufu Al-Wahda Ponyo kutoka katika Qur'an. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii Mashukio ya Akhera Al Amali Dua Indal Ahlul Bayt Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna. Haki za wanawake katika Uislamu Mwenyeezi Mungu na sifa zake Amateka Na Aba'Khalifa Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) Adhana. Upendo katika Ukristo na Uislamu Nyuma yaho naje kuyoboka Amavu n’amavuko by’ubushiya Kupaka juu ya khofu Kukusanya swala mbili Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Kusujudu juu ya udongo Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s) Tarawehe Malumbano baina ya Sunni na Shia Kupunguza Swala safarini Kufungua safarini Umaasumu wa Manabii Qur’an inatoa changamoto as-Salaatu Khayrun Mina -'n Nawm Uadilifu wa Masahaba 73
Page 73
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:26 PM
Huduma ya Afya katika Uislamu 56. 57. 58. 59. 60. 61. 62. 63. 64. 65. 66. 67. 68. 69. 70. 71. 72. 73. 74. 75. 76. 77. 78. 79. 80. 81. 82. 83. 84.
Dua e Kumayl Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mitume Muhammad (s) Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili Kuzuru Makaburi Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita Tujifunze Misingi Ya Dini Sala ni Nguzo ya Dini Mikesha Ya Peshawar Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu Ubora wa Imam 'Ali Juu ya Maswahaba Na Ushia ndio njia iliyonyooka Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake Liqaa-u-llaah Muhammad (s) Mtume wa Allah Amani na Jihadi Katika Uislamu Uislamu Ulienea Vipi? Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) Urejeo (al-Raja’a ) Mazingira Utokezo (al - Badau) 74
Page 74
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:26 PM
Huduma ya Afya katika Uislamu 85. 86. 87. 88. 89. 90. 91. 92. 93. 94. 95.
Sadaka yenye kuendelea Msahafu wa Imam Ali Uislamu na dhana Mtoto mwema Adabu za Sokoni Johari za hekima kwa vijana Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu Tawasali Imam Mahdi katika Usunni na Ushia
96.
Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu
97.
Hukumu ya kujenga juu ya makaburi
98.
Swala ya maiti na kumlilia maiti
99.
Shiya na Hadithi (kinyarwanda)
100.
Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu
101.
Hadithi ya Thaqalain
102
Fatima al-Zahra
103.
Tabaruku
104.
Sunan an-Nabii
105.
Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza)
106.
Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili)
107.
Mahdi katika sunna
108.
Kusalia Nabii (s.a.w)
109.
Ujumbe -Sehemu ya Kwanza
110.
Ujumbe - Sehemu ya Pili
111.
Ujumbe - Sehemu ya Tatu 75
Page 75
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
Huduma ya Afya katika Uislamu 112.
Ujumbe - Sehemu ya Nne
113.
Ngano ya kwamba Qur’ani imebadilishwa
114.
Iduwa ya Kumayili.
115.
Maarifa ya Kiislamu.
116.
Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza
117.
Ukweli uliopotea sehemu ya Pili
118.
Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu
119.
Ukweli uliopotea sehmu ya Nne
120.
Ukweli uliopotea sehmu ya Tano
121.
Johari zenye hekima kwa vijana
122.
Safari ya kuifuata Nuru
123.
Idil Ghadiri
124.
Myahudi wa Kimataifa
125.
Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi
126.
Visa vya kweli sehemu ya Kwanza
127.
Visa vya kweli sehemu ya Pili
128.
Muhadhara wa Maulamaa
129.
Mwanadamu na Mustakabali wake
130.
Imam Ali binamu ya Mtume Sehemu ya Kwanza
131.
Imam Ali binamu ya Mtume Sehemu ya Pili
132.
Khairul Bariyyah
133.
Uislamu na mafunzo ya kimalezi
134.
Vijana ni Hazina ya Uislamu.
135.
Yafaayo kijamii
136.
Kusoma sura zenye Sijda ya wajibu
137.
Taqiyya 76
4:26 PM
Page 76
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:26 PM
Huduma ya Afya katika Uislamu 138.
Vikao vya furaha
139.
Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje?
140.
Uislamu na Mazingatio Sehemu ya Kwanza
141.
Uislamu na Mazingatio Sehemu ya Pili
142.
Azadari-Kuhuzunika na Kuomboleza
143.
Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah
144.
Mtazamo Mpya - Wanawake katika Uislamu
145.
Kuonekana kwa Allah
146.
Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza)
147.
Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili)
148.
Ndugu na Jirani
149.
Ushia ndani ya Usunni
150.
Maswali na Majibu.
151.
Mafunzo ya hukmu za ibada
152.
Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisusunni No 1
153
Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisusunni No 2
154.
Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisusunni No 3
155.
Abu Huraira
156.
Kati ya Alama kuu za dini Swala ya Jamaa.
157.
Mazingatio kutoka katika Qur’an sehemu ya Kwanza
158.
Mazingatio kutoka kaitka Qur’an sehemu ya Pili
159.
Mazingatio kutoka katika Uislamu sehemu ya kwanza
160.
Mazingatio kutoka katika Uislamu sehemu ya Pili
161.
Hukumu zinazomuhusu mkuu wa kazi na Mfanyakazi
162.
Falsafa ya mageuzi ya Imam Husein (a.s)
163.
Huduma ya Afya katika Uislamu 77
Page 77
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
Huduma ya Afya katika Uislamu 164.
Hukumu za Mgonjwa
165.
Falsafa ya Mageuzi ya Imam Husein
166.
Uislamu Safi
167.
Majlis ya Imam Husein
168.
Mshumaa
169.
Tiba ya Maradhi ya Kimaadili
170.
Uislam wa Shia
78
4:26 PM
Page 78
Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba
final.qxd
7/1/2011
4:26 PM
Page 79
Huduma ya Afya katika Uislamu
BACK COVER Afya ya mwili kwa mwanadamu ni kitu muhimu sana. Ili mwanadamu aweze kuyajenga maisha yake na kuwa bora kimwili, lazima awe na afya bora, na sio tu kwa ajili ya kuendesha maisha yake, bali pia bila afya nzuri mtu hawezi kutekeleza ibada zake sawasawa jinsi inavyotakiwa kuifanya. Hivyo, kama Uislamu ulivyo kwamba ni dini na ni mfumo kamili wa maisha, umeelezea kwa kina huduma ya afya, yaani mtu akiwa nini ili ajipatie afya njema. Waandishi wa kitabu hiki wameelezea mambo mbalimbali ambayo yanapaswa kufanywa kwa ajili ya afya ya mtu binafsi na ya jamii kwa ujumla. Katika maelezo yao wamezingatia Qur’ani Tukufu, Sunna pamoja na mafundisho ya Maimamu Watukufu. Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote, ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni mambo ambayo hayana nafasi tena katika akili za watu. Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Nukushi: +255 22 2127555 Barua Pepe: alitrah@raha.com Tovuti: www.ibn-tv.com Katika mtandao: www.alitrah.info
79