Maeneo ya Umma na Mali Zake األماكن واألموال العامة
Kimeandikwa na: Jumuiya ya Maarifa na Utamaduni wa Kiislamu
Kimetarjumiwa na: Hemedi Lubumba (Abu Batul)
ترجمة
األماكن واألموال العامة
تأليف جمعية المعارف اإلسالمية الثقافية
من اللغة العربية الى اللغة السوا حلية
© Haki ya kunakili imehifadhiwa na: Al-Itrah Foundation
ISBN No: 978 - 9987 – 17 – 066 – 1
Kimeandikwa na: Jumuiya ya Maarifa na Utamaduni wa Kiislamu
Kimetarjumiwa na: Alhajj Hemedi Lubumba Selemani
Kimepangwa katika Kompyuta na: Al-Itrah Foundation
Toleo la kwanza: Juni, 2014 Nakala: 1000
Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. - 19701, Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 / 2127555 Barua Pepe: alitrah@yahoo.com Tovuti: www.ibn-tv-com Katika mtandao: www.alitrah.info
YALIYOMO Neno la Mchapishaji........................................................................1 Utangulizi.........................................................................................3 SURA YA KWANZA......................................................................4 MISIKITI.......................................................................................4 Utangulizi:..................................................................................4
Matumizi yaliyokatazwa na Uislamu:........................................5
Sheria mbalimbali zinazohusu msikiti:......................................6
Sala ya msikitini:........................................................................7
Haki ya kutangulia au kipaumbele:............................................8
Mali za Msikiti:..........................................................................9
Adabu za jumla za msikiti:.........................................................9
Hukumu za maeneo ya makaburi matukufu:............................ 11
SURA YA PILI..............................................................................13 BARABARA ZA UMMA.............................................................13 Utangulizi:................................................................................13
Ni nani mwenye haki ya unufaika na barabara?.....................13
Matumizi yasiyo ya kisharia:...................................................14
v
Maeneo ya Umma na Mali Zake
Haki ya jamii ni zaidi ya maslahi binafsi:................................14
Ama mambo yanayoruhusiwa ni:.............................................15
Watandaza biashara chini na hukumu ya wamachinga:...........16
Ni wakati gani barabara inakuwa ya umma?...........................17
Ni wakati gani inaruhusiwa kuzitumia barabara kwa matumizi binafsi?...............................................18
Hukumu za barabara za watu binafsi:......................................18
Miongoni mwa adabu za barabarani:.......................................18
SURA YA TATU...........................................................................20 WAKFU NA SADAKA................................................................20 Wakfu: ........................................................................................20
Vigawanyo vya Wakfu:............................................................20
Miongoni mwa hukmu za Wakfu:............................................21
Kuuza Wakfu makhsusi:...........................................................22
Sadaka:.....................................................................................23
Miongoni mwa hukumu za sadaka:..........................................23
Ni nani anayefaa kisharia kupewa sadaka?..............................23
SURA YA NNE.............................................................................24 vi
Maeneo ya Umma na Mali Zake
MALI ZA KISHARIA.................................................................24 Khumsi:....................................................................................24
Mzazi asiyetoa Khumsi:...........................................................25
Namna ya kutumia mali ya mtu asiyetoa Khumsi:..................25
Msaada:....................................................................................26 Manunuzi yatokanayo na mali ambayo haijatolewa Khumsi:.................................................................26 Zaka: ........................................................................................27
Miongoni mwa hukumu za mali ya Zaka:................................27
Zakatul-Fitri:............................................................................29
Miongoni mwa hukumu za Zakatul-Fitri:................................29
Mali ambayo mmiliki wake hajulikani:...................................30
Mfano wa mali hiyo:................................................................30
Hukumu ya bahatinasibu na Loto:...........................................31
SURA YA TANO...........................................................................33 MALI ZA DOLA..........................................................................33
Je dola inamiliki mali?.............................................................33
Wafanyakazi wa dola:..............................................................34
Kuharibu mali ya dola:.............................................................34
Kodi na ada:.............................................................................35 vii
Maeneo ya Umma na Mali Zake
بسم اهلل الرحمن الرحيم NENO LA MCHAPISHAJI
M
aeneo ya Umma na Mali Zake ni kitabu chenye maudhui yanayohusiana na matumizi na sheria za mahali, maneneo na mali za Umma kwa mujibu wa kanuni za Kiislamu. Kama tunavyosema wakati wote kwamba Uislamu ni dini na mfumo kamili wa maisha; haukuacha lolote linalomhusu mwanadamu kimwili au kiroho, bali umeweka sheria ya kuyaendesha maisha hayo (kiroho na kimwili). Katika kitabu hiki, Sheikh anazungumzia kwa mtazamo wa Kiislamu kuhusu mahali pa Umma, kama vile misikiti, mabustani, barabara na maeneo mengine kama hayo. Sisi kama wachapishaji, tunapenda kujulisha kitabu hiki kama kilivyo kwa wasomaji wetu na kuwashauri wayasome yaliyomo humu, wayafanyie kazi na kuyazingatia na kufaidika na hazina iliyomo ndani yake. Hii ni moja kati ya kazi kubwa zilizofanywa na Taasisi ya AlItrah katika kuwahudumia kielimu wasomaji wake wazungumzaji wa Kiswahili. Na kwa maana hiyo hiyo, imeamua kukichapisha kitabu hiki chenye manufaa makubwa kwa lugha ya Kiswahili kwa lengo lake lile lile la kuwahudumia Waislamu, hususan wanaozungumza Kiswahili. Tunamshukuru ndugu yetu Hemedi Lubumba (Abu Batul) kwa kufanikisha tarjuma ya kitabu hiki katika lugha ya Kiswahili, pia na 1
Maeneo ya Umma na Mali Zake
wale wote waliosaidia kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha toleo hili kuchapishwa na kuwa mikononi mwa wasomaji. Allah Mwenye kujazi awalipe wote malipo mema hapa duniani na huko Akhera pia. Amin! Mchapishaji Al-Itrah Foundation.
2
Maeneo ya Umma na Mali Zake
بسم اهلل الرحمن الرحيم UTANGULIZI
H
akika miongoni mwa mambo yasiyoachana na maisha ni watu kushirikiana katika mambo mengi, kama vile katika misikiti, masoko na barabara. Pia sheria za nchi huwashirikisha pamoja wakazi wa nchi moja, kwani sheria hizo hutekelezwa kwa wote kwa jumla. Watu wa dini moja huishi chini ya sheria moja bila kubagua baina yao, na wajibu alionao huyu miongoni mwao ndio alionao yule. Kuanzia hapa ndipo yakadhihiri mambo yenye sura ya ushirika, ambayo watu wa jamii moja hushirikiana katika pande zake zote. Uraia unawaleta pamoja kwa kuwa wao ni watoto wa nchi moja, na hapo wanatawaliwa na serikali moja na sheria moja. Dini moja inawaleta pamoja na hapo wanaungana katika wajibu za kisharia katika ibada mbalimbali na miamala tofauti. Kuanzia hapa ndipo mambo ya ushirika yakawa na umuhimu mkubwa hasa katika kuyanadhimu, hiyo ni kutokana na yanavyowakutanisha pamoja watu. Hiki kilichomo mikononi mwako ni sheria tukufu za kiislamu zinazohusu mambo ya ushirika. Tunamuomba Mwenyezi Mungu atuwafikishe wote kujua mipaka yake na sheria zake, hakika Yeye ni Msikivu Mwenye kujibu. Jumuiya ya Maarifa na Utamaduni wa Kiislamu.
3
Maeneo ya Umma na Mali Zake
بسم اهلل الرحمن الرحيم SURA YA KWANZA MISIKITI Utangulizi:
H
akika misikiti ndio makao makuu ya jukumu la kijamii ndani ya Uislamu. Yenyewe ndio vituo vya mafunzo ya wahanga, chimbuko la wanajihadi, mahali pa wanaibada na waswalihina, na ndio makutano ya waumini. Inatosha tujue kwamba hapo ndipo eneo la mja kukutana na Mola Wake na kuzungumza Naye kwa siri. Hapo ndipo panapotuwezesha kutazama kwa nuru ya elimu na hatimaye kuweza kuziona hima zetu na kuzihimiza nafsi zetu. Msikiti ni zawadi ya Mwenyezi Mungu kwetu na heshima aliyotutunuku, bila shaka ametuhusisha nayo kiasi kwamba ameifanya kuwa mapokezi ya kudumu kwa kila anayetaka kumtembelea nyumbani Kwake. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Imeandikwa ndani ya Taurati: ‘Hakika nyumba zangu aridhini ni misikiti. Uzuri ulioje kwa mja atakayejitoharisha nyumbani kwake kisha akanizuru nyumbani Kwangu. Ah! Hakika mwenye kutembelewa anapaswa kumkirimu mwenye kumtembelea. Ah! Wape habari njema wale wenye kwenda kwa miguu misikitini ndani ya giza, kuwa watapata nuru ing’aayo siku ya Kiyama.”’1 1
Mizanul-Hikma- Hadithi ya 8292, Chapa ya kwanza. 4
Maeneo ya Umma na Mali Zake
Uislamu umehimiza kujenga misikiti na kuiendea mara kwa mara, hivyo yenyewe ni sehemu zilizo wazi kwa ajili ya Waislamu wote, ni sehemu ya wao kukutana, na humo wanawasiliana na Muumba wao na kujielekeza Kwake kwa aina tofauti za dua, hivyo misikiti hii hata kama itajengwa kwa ajili ya kabila fulani au kundi fulani lakini si mahususi kwao tu, bali utakuwa ni wa Waislamu wote, mtu yeyote hana haki ya kumzuia mwislamu yeyote kuutumia au kuuingia.2 Hivyo misikiti ni maeneo ambayo Mwenyezi Mungu ameyaweka kwa ajili ya sala, dua, kisomo cha Qur’ani, mawaidha na nasaha. Na sala ndiyo ya kwanza kabla ya amali nyingine, hivyo kama eneo la kusalia litafinywa na eneo ambalo zinatekelezwa amali nyingine itakuwa ni wajibu kuliacha eneo hilo wazi kwa ajili ya sala.3
Matumizi yaliyokatazwa na Uislamu: 1.
Kuingia Msikiti Mtukufu na Msikiti wa Mtume (s.a.w.w.) kwa mwenye janaba na mwenye hedhi, hata kama ni kwa namna ya kupita.
2.
Kuketi msikitini kwa mwenye janaba na mwenye hedhi, bali si ruhusa kuingia kwa namna yoyote ile. Ndio, inaruhusiwa kupita kwa kuingilia mlango mmoja na kutokea mlango mwingine.
3.
Kuweka kitu chochote msikitini kwa mwenye janaba na mwenye hedhi, hata kama ni kwa kutokea nje au katika hali ya kupita.
jwibatul-Istiftaat cha Sayyid Ali Khamenei Juz. 1, Uk. 113, Chapa ya kwanza ya A Darul-Islamiyyah. 3 Tahrirul-Wasilah cha Khomein Juz. 2, Uk. 214, Chapa ya Darul-Kutub al-Ilmiyyah. 2
5
Maeneo ya Umma na Mali Zake
4.
Matumizi yanayopingana na hadhi na heshima ya msikiti, kama vile michezo, kufanya mizaha kwa sauti ya juu au kwa vitendo, na kuongelea mambo yasiyofaa, na mengineyo miongoni mwa matendo ya kuchukiza.4
5.
Haijuzu kuinajisi misikiti, sawa iwe ni ardhi yake au ukuta wake au paa lake, bali ni wajibu kuharakisha kuitoharisha pindi inaponajisika, ila iwapo mtu hawezi peke yake kufanya haraka kuitoharisha. Bali ni kwamba iwapo ni mwenye kushughulishwa na sala na akawa amegundua kuwa msikiti umenajisika ni wajibu juu yake ikiwa wakati bado ungalipo, kukata sala na kuharakisha kwenda kutoharisha msikiti, ikiwa utoharishaji huo unalazimu kukatiza sala.
Sheria mbalimbali zinazohusu Âmsikiti: 1.
Iwapo kilichotandikwa msikitini kitanajisika basi kwa mujibu wa ihitiyati ni wajibu kukitoharisha.
2.
Kwa mujibu wa ihtiyat ni wajibu kutoipamba misikiti kwa dhahabu.
3.
Hairuhusiwi kuchora viumbe vyenye roho misikitini, kama vile mwanadamu na mnyama.5
4.
Ni haramu kuingiza najisi au kilichonajisika msikitini, kama kufanya hivyo ni kuukosea au kutokuuheshimu msikiti.6
jwibatul-Istiftaat cha Sayyid Ali Khamenei Juz. 1 Uk. 114, Chapa ya kwanza ya A Darul-Islamiyyah. 5 Tawdhihul-Masail cha Khomein Uk. 125. 6 Tawdhihul-Masail cha Khomein Uk. 125. 4
6
Maeneo ya Umma na Mali Zake
5.
Hairuhusiwi kuuza vifaa vya msikiti kama vile vyuma na mfano wake, bali ni wajibu kuvitumia katika msikiti huo huo. Na kama haiwezekani basi ni wajibu kuvitumia katika misikiti mingine. Na kama na hilo haliwezekani basi inaruhusiwa kuviuza na kutumia thamani yake katika kuamirisha msikiti ambao ulikuwa mmiliki wa vifaa hivyo.
Sala ya msikitini: Uislamu umetoa thawabu nyingi kwa mwenye kusali sala yake msikitini, hivyo ukubwa wa thawabu za sala inayosaliwa msikitini ni kwa utaratibu ufuatao:7
7 8
a.
Msikiti Mtukufu wa Makka.
b.
Msikiti Mtukufu wa Nabii (s.a.w.w.) huko Madina.
c.
Msikiti wa Kufa huko Iraq, uliyopo karibu na mji wa Najaf Tukufu. Pia msikiti wa al-Aqswa uliyopo katika mji wa Jerusalem huko nchini Palestina.
d.
Msikiti mkuu. Makusudio ya Msikiti mkuu ni ule ambao haukujengwa kwa ajili ya kundi maalumu au kwa ajili ya watu makhususi.8
e.
Msikiti wa kabila. Nao ni ule ambao umejengwa kwa ajili ya kundi maalumu.
Tahrirul-Wasilah cha Khomein Juz. 1, Uk. 151, Chapa ya Darul-Kutub al-Ilmiyyah. Ajwibatul-Istiftaat cha Sayyid Ali Khamenei Juz. 1, Uk. 116, Chapa ya kwanza ya Darul-Islamiyyah. 7
Maeneo ya Umma na Mali Zake
f.
Msikiti wa soko. Nao ni ule uliojengwa sokoni. Inafaa kuzingatiwa kuwa ubora wa sala ya msikitini si makhususi kwa wanaume tu.9
Haki ya kutangulia au kipaumbele: Misikiti ni sehemu inayokusudiwa na watu wote, hivyo yeyote atakayetangulia kufika sehemu yoyote msikitini kwa ajili ya sala au amali nyingine ambazo kikawaida hutekelezwa msikitini, kama vile kusoma Qur’ani, kusikia mawaidha na nasaha, haijuzu kwa wengine kumuondoa wala kumsumbua.10 Haki ya sehemu ya aliyeingia msikitini itaheshimiwa kwa kuweka tu kitu ambacho kikawaida hujulisha kwamba amezuia sehemu husika, kama pale atakapotandika msala, wala haitoshi kuweka turba au mswaki au tasbihi (yaani hivi havionyeshi kuwa ana haki na sehemu hiyo kwa kutangulia). Na lau ikitokea kwamba kuna mtu kaweka kitu kinachojulisha kuwa yeye kazuia sehemu hiyo, kisha akawa amekwenda kutekeleza jambo fulani na ukapita muda mrefu, basi haitakuwa lazima kujiepusha na sehemu hiyo, bali inaruhusiwa kwa mwingine kuitumia sehemu hiyo. Na kama mtu atasalia sehemu ambayo imezuiliwa na mtu mwingine aliyetangulia, basi kwa mujibu wa ihtiyat ni wajibu arudie sala yake sehemu nyingine.
Ajwibatul-Istiftaat cha Sayyid Ali Khamenei Juz. 1, Uk. 113, Chapa ya kwanza ya Darul-Islamiyyah. 10 Tahrirul-Wasilah cha Khomein Juz. 2, Uk. 215, Chapa ya Darul-Kutub al-Ilmiyyah. 9
8
Maeneo ya Umma na Mali Zake
Mali za Msikiti: Hairuhusiwi kutumia mali za msikiti katika mambo ambayo mali hizo hazikukusudiwa kutumika kwayo, hivyo maji yaliyowekwa kwa ajili ya udhu au kwa ajili ya matumizi ya wenye kusali, hairuhusiwi kuyatumia katika mambo mengine. Ikiwa maji yaliyopo msikitini ni wakfu makhususi kwa ajili ya anayetaka kusalia ndani ya msikiti husika, hairuhusiwi kwa yule asiyetaka kusalia msikiti huo kuyatumia maji hayo kwa udhu. Hivyo ili upate ruhusa ya kuyatumia kwa udhu ni lazima uwe na uhakika kwamba ni wakfu ya watu wote.11 Hairuhusiwi makafiri kuingia msikiti wowote ule, sawa uwe Msikiti Mtukufu au mwingineo.12 Na ni karaha kumsalia maiti msikitini isipokuwa ndani ya Msikiti Mtukufu huko Makka Tukufu.13
Adabu za jumla za msikiti: 1.
Kwenda msikitini hali umejinyunyuzia manukato na umevaa nguo nzuri kushinda zote ulizonazo, ili kwamba uwe katika sura nzuri pindi unapokutana na Mola Wako na ndugu zako.
2.
Kusafisha msikiti. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Atakayeondoa uchafu msikitini, Mwenyezi Mungu atamwandikia thawabu za aliyemwacha huru mtumwa. Na atakayeondoa humo kitu kinacholichukiza jicho, Mwenyezi Mungu atamwandikia rehema zake mara dufu.�14
Tawdhihul-Masail cha Khomein Uk. 35. Ajwibatul-Istiftaat cha Sayyid Ali Khamenei Juz. 1, Uk. 122, Chapa ya kwanza ya Darul-Islamiyyah. 13 Tawdhihul-Masail cha Khomein Uk. 82. 14 Wasailus-Shia Juz. 3, Uk. 511, Mlango wa 32, Hadithi ya 2. 11
12
9
Maeneo ya Umma na Mali Zake
3.
Kuweka mwanga msikitini usiku. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Atakayewasha taa yoyote katika msikiti wowote miongoni mwa misikiti ya Mwenyezi Mungu, Malaika na wabeba Arshi wataendelea kumuombea maghufira maadamu mwanga wa taa hiyo umo ndani ya msikiti huo.”15
4.
Kutofanya biashara msikitini. Imam as-Sadiq (a.s.) amesema: “Iepusheni misikiti yenu na biashara.”
5.
Kutopaza sauti misikitini au kufanyia humo mijadala isiyofaa. Katika wasia wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa Abu Dhari, alimwambia: “Ewe Abu Dhari! Atakayemwitikia mwitaji wa Mwenyezi Mungu na akaamirisha vizuri misikiti ya Mwenyezi Mungu, thawabu zake kwa Mwenyezi Mungu zitakuwa ni kupata pepo.” Abu Dhari anasema: Nikasema: Ni vipi huamirishwa misikiti ya Mwenyezi Mungu? Akasema (s.a.w.w.): “Usipaze humo sauti wala kuzama katika mazungumzo yasiyofaa, usinunue humo wala kuuza, na acha kila la upuuzi maadamu ungalimo humo. Usipofuata haya basi usijemlaumu yeyote Siku ya Kiyama ila ujilaumu mwenyewe.”16
6.
Ni karaha kusoma mashairi msikitini. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Mtakapomsikia mtu akisoma mashairi msikitini mwambieni: Mwenyezi Mungu azibe kinywa chako. Hakika misikiti imewekwa kwa ajili ya Qur’ani.”17
Wasailus-Shia Juz. 3, Uk. 511, Mlango wa 34, Hadithi ya 1. Wasailus-Shia Juz. 3, Mlango wa 27. 17 Wasailus-Shia Juz. 3, Mlango wa 14, Hadithi ya 1. 15 16
10
Maeneo ya Umma na Mali Zake
7.
Ni makuruhu kulala msikitini.18
8.
Ni karaha mtu kwenda msikitini na hali kinywa chake chatoa harufu mbaya, kama ambavyo ni makuruhu mtu kutema mate msikitini.19
Hukumu za maeneo ya makaburi Âmatukufu: Maeneo ya makaburi matukufu ya Maimam maasumu (a.s.) nayo pia ni sehemu ambazo hukusudiwa na Waislamu kwa ajili ya sala, dua na ziara. Na bila shaka kuna riwaya zinazohimiza kuyazuru maeneo haya, na hukumu zake ni kama hukumu za misikiti, hivyo atakayetangulia kufika sehemu yoyote ya eneo la kaburi tukufu huyo ndio mwenye haki na eneo hilo kuliko mwingine, kama ilivyotangulia katika hukumu za msikiti, kama ambavyo pia kuzuia sehemu kutatimia kama kunavyotimia msikitini. Hairuhusiwi kwa mwenye janaba na mwenye hedhi kuingia kwenye maeneo matukufu ya makaburi ya Maimamu (a.s.). Na muradi wa maeneo hayo ni lile eneo ambalo husadikika kuwa ndio eneo la kaburi tukufu, yaani ni lile lililopo chini ya kuba. Ama jengo au uzio uliolizunguka kaburi wenyewe hauna hukumu ya utukufu na hivyo hakuna kizuizi chochote akitaka kuingia humo. Ndio, ikiwa sehemu hizo (za jengo au uzio) zimetolewa wakfu ya kuwa ni misikiti basi hairuhusiwi kwake kuingia. Ni haramu kuyanajisisha maeneo matukufu ya makaburi ya Maimamu (a.s.) kama ilivyo haramu kwenye misikiti, na ni wajibu kuharakisha kuyatoharisha iwapo itatokea kuwa yamenajisika. jwibatul-Istiftaat cha Sayyid Ali Khamenei Juz. 1, Uk. 114, Chapa ya kwanza ya A Darul-Islamiyyah. 19 Risalatu Tawdhihul-Masail cha Imam Khomeni Uk. 126. 18
11
Maeneo ya Umma na Mali Zake
Ni haramu makafiri kuingia maeneo matukufu ya Maimamu (a.s.) iwapo kuingia kwao kutalazimu kuyavunjia heshima, na kwa mujibu wa ihtiyat ni mustahabu kwamba wasiingie kabisa.20 Ni mustahabu kwa wale wanaoishi jirani na maeneo matukufu na sehemu za makaburi matukufu ya Maimam (a.s.) kuwahudumia na kuwatunza wale wanaokuja toka sehemu nyingine kwa ajili ya ziara na dua.
20
Tahrirul-Wasilah cha Khomein Juz. 2, Uk. 215, Chapa ya Darul-Kutub al-Ilmiyyah. 12
Maeneo ya Umma na Mali Zake
SURA YA PILI BARABARA ZA UMMA Utangulizi:
M
aisha ya jamii ya mwanadamu yanategemea baadhi ya mahitaji ambayo huitwa huduma za jamii, hivyo ni lazima kupatikane baadhi ya barabara na madaraja, mambo ambayo huwarahisishia wananchi harakati zao za usafiri. Na barabara hizi kikawaida si milki ya mtu binafsi, na kila mmoja ana haki ya kutumia barabara hiyo, na hakuna yeyote mwenye haki ya kuwazuia wengine wasitumie barabara hiyo au kuwabughudhi katika matumizi. Sheria ya Uislamu imekusanya kundi la kanuni ambazo ni taklifu na wajibu wa kisharia uliyopo juu ya bega la kila mwislamu, kanuni ambazo hunadhimu namna ya kutumia barabara katika jinsi ambayo haitasababisha mgongano baina ya watu, au kutofikiwa yale malengo yaliyokusudiwa katika ujenzi wa huduma hizo za jamii.
Ni nani mwenye haki ya unufaika na barabara? Kila mwananchi na kila mtu anayeishi juu ya ardhi hii ana haki ya kutumia huduma hizi za kijamii, kuanzia barabara, madaraja hadi mabustani, lakini bila kutoka nje ya makusudio yaliyokusudiwa ka13
Maeneo ya Umma na Mali Zake
tika upatikanaji wa huduma hizo, hivyo barabara itumike kwa ajili ya kupita, kwa sababu imejengwa kwa malengo hayo, na wala mtu asiitumie kama uwanja wa kuchezea mpira, kwa sababu itakuwa ni kinyume na malengo yaliyokusudiwa katika ujenzi wake. Hivyo barabara na madaraja vimejengwa kwa ajili ya kupita magari, na kila gari lina haki ya kupita juu ya barabara na madaraja hayo, wala hakuna tofauti baina ya mwananchi huyu na yule katika hilo. Na eneo la watembea kwa miguu lililojengwa kwa ajili ya watembea kwa miguu ni haki ya wote na kila mtembea kwa miguu ana haki ya kupita juu yake.
Matumizi yasiyo ya kisharia: Yeyote yule hana ruhusa ya kuhodhi sehemu yoyote ile ya maeneo haya ya umma kwa kujenga jengo au kuchimba shimo au kwa matumizi yoyote ambayo kikawaida hufanywa katika milki ya mtu binafsi, kama ambavyo pia yeyote yule hana ruhusa ya kuchukua sehemu yoyote ile ya barabara hata kama mkabala na kitendo hicho atatoa sehemu ya ardhi yake kwa ajili ya barabara.21
Haki ya jamii ni zaidi ya maslahi Âbinafsi: Maeneo haya ya umma yamejengwa ili yatumiwe na watu wote na lengo lake ni kurahisisha maisha ya watu na kuwaondolea shida na usumbufu, hivyo ruhusa ya kufanya kazi yoyote ndani ya maeneo haya iko chini ya sharti la kwamba matumizi yako yasiwabughudhi au kuzuia haki ya wengine kutumia maeneo hayo. Na mifano katika hilo ni mingi:22 21 22
Istiftiat cha Imam Khomein Juz. 2 Uk. 591, Chapa ya tano. Tahrirul-Wasilah cha Khomein Juz. 2 Uk. 187, Chapa ya Darul-Kutub al-Ilmiyyah. 14
Maeneo ya Umma na Mali Zake
a. Mabaraza ya ghorofani (balconies) ambayo huwekwa kwenye majumba katika namna ambayo huwa yamejitokeza hadi juu ya barabara, si ruhusa kuyajenga ikiwa yanapelekea kuzuia haki ya watumiaji wa barabara, hususan yale ambayo huwa chini zaidi toka usawa wa ardhi. b. Si ruhusa kuvuta bomba kwa juu kwa kulipitisha juu ya barabara ya umma ikiwa kufanya hivyo ni kero na usumbufu kwa watumiaji wa barabara. c. Ni ruhusa kutumia barabara na maeneo ya umma kwa ajili ya baadhi ya mambo chini ya miiko tutakayoitaja kwa ufafanuzi hapo baadaye, na miiko yote hiyo ni tofauti kabisa na sheria za miji ambazo zina ufafanuzi wake mahususi na ambazo hatutazigusia hapa, tukitaraji kwamba inshaallah tutaziandalia kitabu cha pekee.
Ama mambo yanayoruhusiwa ni: a. Kuweka matangazo ya biashara na mfano wake. b. Kulala ndani ya bustani za umma, kuketi humo na kusalia humo. c. Kutandaza bidhaa na kufanya biashara. d. Kuegesha magari na vyombo vya usafiri sehemu ambazo zimetengwa kwa ajili ya maegesho, na si kwenye sehemu ambazo uegeshaji huo utasababisha msongamano kwa watumiaji wa barabara. e. Wenye maduka kuweka bidhaa zao mbele ya maduka yao katika eneo la watembea kwa miguu, lakini kwa namna 15
Maeneo ya Umma na Mali Zake
ambayo haitakuwa kero kwa wapita njia. Ifahamike kwamba ruhusa ya hayo yote iko chini ya sharti la kwamba utumiaji huo usizuie haki ya wengine wala kuwa kero kwao, hivyo hairuhusiwi yafuatayo: 1.
Kuweka matangazo ya biashara ambayo yatawazuia watu kutumia barabara au kuwanyima raha ndani ya mabustani.
2.
Kutandaza bidhaa na kuanzisha maeneo ya biashara bila kujali na kuheshimu haki ya wapitanjia.
3.
Kuegesha magari katika namna ambayo itawazuia watu kuendelea na harakati zao au itakayokuwa kero kwao, kama wafanyavyo baadhi ya watu ambao huegesha magari yao kwenye maeneo ya watembea kwa miguu, kiasi kwamba huzuia harakati na shughuli za watembea kwa miguu au huwazuia kabisa kupita.
Watandaza biashara chini na hukumu ya wamachinga: Baadhi ya wafanyabiashara hutegemea barabara ili kuzitangaza bidhaa zao na kuziuza, na suala hilo laruhusiwa kisharia iwapo tu kufanya hivyo hakuzuii haki ya wapita njia. Baadhi hufikia hata kuwa na sehemu mahususi na kuitumia kila siku, lakini hali hii haimpi haki itakayomwezesha kuwazuia wengine kuitumia sehemu hiyo kibiashara au kwa matumizi mengine. Kipimo cha kisharia katika hali hiyo ni kutangulia, hivyo atakayetangulia kuweka bidhaa zake sehemu hiyo ndiyo mwenye haki na sehemu hiyo na wala wengine hawaruhusiwi kumzuia. Bali ni kwamba hata kama atakuwa ame16
Maeneo ya Umma na Mali Zake
zoea kukaa sehemu hiyo miaka nenda rudi, bado hali hiyo haimpi haki ya kumiliki sehemu hiyo. Amirul-Muuminin (a.s.) amesema: “Soko la Waislamu ni sawa na msikiti wao, yule atakayetangulia kufika sehemu yoyote ndiyo mwenye haki na sehemu hiyo mpaka usiku.�23 Imekuwa ni kawaida kwa wafanyabiashara wadogo wadogo kuweka hema linalowasaidia kuzuia joto au mvua na hata baridi, hakuna kizuizi katika kufanya hivyo, kwa sharti tu la kufuata vigezo na masharti yaliyotangulia. Ndio, haruhusiwi kujenga jengo lisilohamishika, hiyo ni kwa sababu barabara si milki yake binafsi.24
Ni wakati gani barabara inakuwa ya umma? Ili barabara iwe miongoni mwa maeneo ya umma ni lazima litimie jambo moja kati ya mambo yafuatayo: 1. Ukithiri upitaji wa wapita njia juu ya ardhi ya wazi ambayo si milki ya yeyote yule. 2. Mtu au kundi la watu lijitolee sehemu ya ardhi yao ili iwe barabara ya umma yenye lango la kuingilia na lango la kutokea. 3. Watu waanzishe kijiji au mji na waweke barabara za ndani katika ramani yao.25
Al-Kafiy ya Kulayniy Juz. 3, Uk. 662, Chapa ya tatu ya Darul-Kutub al-Islamiyyah. Tahrirul-Wasilah cha Khomein Juz. 2, Uk. 188, Chapa ya Darul-Kutub al-Ilmiyyah. 25 Tahrirul-Wasilah cha Khomein Juz. 2, Uk. 188, Chapa ya Darul-Kutub al-Ilmiyyah. 23 24
17
Maeneo ya Umma na Mali Zake
Ni wakati gani inaruhusiwa kuzitumia barabara kwa matumizi binafsi? Ikitokea mji kuharibika kiasi kwamba barabara zake zikawa hazipitiki wala watu hawazikusudii kuzipita basi wakati huo zinakuwa sawa na maeneo ya umma, hivyo anaruhusiwa mtu yeyote kuzitumia kwa matumizi yake binafsi na hata kuziendeleza. Ndio, ikiwa barabara imepatikana kwa njia ya kujitolea, yaani imetolewa na watu maalumu basi haruhusiwi yeyote yule kuitumia kwa matumizi binafsi.26
Hukumu za barabara za watu binafsi: Katika baadhi ya vijiji hupatikana barabara za watu binafsi, na tofauti yake na barabara za umma ni kwamba hizi za watu binafsi ni eneo mahususi la kupita kuelekea kwenye baadhi ya nyumba, na barabara hizi huwa ni milki ya wenye nyumba hizo zinazozunguka barabara hiyo, hivyo wenye nyumba hizi wanaruhusiwa kuziba barabara hiyo au kummilikisha mmoja wao sehemu fulani ya barabara hiyo, kwa sharti tu la kuwepo ridhaa ya wote wenye nyumba katika barabara hiyo.27
Miongoni mwa adabu za barabarani: 1.
26 27
Ni mustahabu kwamba mwenye kutembea kwa miguu barabarani akikuta kitu chochote chenye kuwaudhi watu akiondoe. Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.)
Tahrirul-Wasilah cha Khomein Juz. 2, Uk. 1189, Chapa ya Darul-Kutub al-Ilmiyyah. Tahrirul-Wasilah cha Khomein Juz. 2, Uk. 186, Chapa ya Darul-Kutub al-Ilmiyyah. 18
Maeneo ya Umma na Mali Zake
amesema: “Isa bin Mariam (a.s.) alipita kaburini akakuta mhusika wa kaburi akiadhibiwa, kisha alipita mwaka uliofuata akakuta haadhibiwi, Isa akasema: ‘Ewe Mola! Nilipita katika kaburi hili mwaka uliopita nikamkuta mhusika akiadhibiwa, na nimepita mwaka huu nimemkuta haadhibiwi.’ Mwenyezi Mungu akamfunulia wahyi: ‘Ewe Roho wa Mwenyezi Mungu! Aliacha nyuma mtoto mwema, naye akatengeneza barabara na kumtunza yatima, hivyo nikamsamehe kwa sababu ya amali aliyotenda mwanaye.”’28 2.
Kujiepusha na kila kinachoondoa heshima kama vile kula barabarani na kutafunatafuna ubani. Abu Ja’far (a.s.) amesema: “Kurusharusha vijiwe na kutafuna ubani vikaoni na barabarani ni miongoni mwa matendo ya watu wa Luti.”29
3.
Kujiepusha kujichanganya na jinsia ya pili na kulinda heshima na staha. Abu Hasan (a.s.) amesema: “Haipasi mwanamke kutembea katikati ya barabara, lakini yeye atembee pembezoni mwa ukuta.”30
Biharul-An’war Juz. 110 Uk. 107. Wasailus-Shia Mlango wa 36 katika milango ya hukumu za misikiti, Hadithi ya 3. 30 Wasailus-Shia Mlango wa 97 katika milango ya vitangulizi vya ndoa, Hadithi ya 3. 28 29
19
Maeneo ya Umma na Mali Zake
SURA YA TATU WAKFU NA SADAKA Wakfu:
W
akfu ni mtu kuzuia mali na kuruhusu matumizi yake (kwa maana ya kuondoa vizuizi katika matumizi), yaani mali inatoka katika milki ya mtu binafsi na kuwa milki ya upande uliowekewa wakfu hiyo. Hivyo haruhusiwi yeyote kuiuza na kuitoa nje ya wakfu, (na hii ndio maana ya kuizuia mali). Ama manufaa na faida zitokanazo na mali hiyo ni milki ya upande uliowekewa wakfu, (na hii ndio maana ya kuondoa vizuizi katika matumizi), hivyo wanaruhusiwa kuitumia kama kusudio la wakfu husika lilivyoelekeza. Wakfu ni miongoni mwa mambo ambayo Uislamu umehimiza sana, Imam as-Sadiq (a.s.) amesema: “Hakuna kitu kinachompelekea mtu malipo baada ya kifo chake ila mambo matatu: Sadaka aliyoitoa enzi za uhai wake na ikaendelea kuwepo baada ya kifo chake, mwenendo mwema aliouanzisha na ukaendelea kufanyiwa kazi baada ya kifo chake, na mtoto mwema anayemwombea dua.�31
Vigawanyo vya Wakfu: Wakfu umegawanyika sehemu kuu mbili: 1.
31
Wakfu wa jumla: Nao ni ule wakfu unaotolewa kwa ajili ya umma, kama vile msikiti, Husainiyyah, eneo la makaburi, shule na mfano wake.
Wasailus-Shia Juz. 13, Uk. 292. 20
Maeneo ya Umma na Mali Zake
2.
Wakfu makhsusi: Nao ni ule unaotolewa kwa ajili ya upande maalumu, kama vile wakfu unaotolewa kwa ajili ya watoto na wajukuu.32
Miongoni mwa hukmu za Wakfu: a.
Hairuhusiwi kuugeuza Wakfu, kwa maana ya kwamba kama mali hiyo ya Wakfu ni nyumba basi hairuhusiwi kuifanya eneo la biashara. Ndio, ikiwa kilichotolewa Wakfu si nyumba yenyewe kama nyumba, bali ni manufaa yatokanayo na nyumba hiyo, kwa mfano muweka Wakfu aseme: “Nimetoa Wakfu manufaa ya nyumba hii kwa wapigania njia ya Mwenyezi Mungu.� Hapo inaruhusiwa kuigeuza nyumba ikiwa haina manufaa yoyote.33
b.
Hairuhusiwi kwa hali yoyote ile kuuza Wakfu wa umma, kama vile msikiti, Husainiyyah na eneo la makaburi, kama ambavyo pia si ruhusa kukodisha au kutumia kwa matumizi ambayo hayakukusudiwa.34
c.
Ikiwa msikitini mna baadhi ya misahafu iliyoharibika inaruhusiwa kuitengeneza na kuiwekea gamba na kisha kuirudisha msikitini, wala haihitaji kupata idhini ya Marjaa katika hilo.
d.
Iwapo mtu itaiharibu mali ya Wakfu atalazimika kulipa, atatoa thamani ya kile kilichoharibika na kinunuliwe kingine. Na kama alikuwa akijinufaisha na mali ya Wakfu,
Tahrirul-Wasilah cha Khomein Juz. 2 Uk. 62, Chapa ya Darul-Kutub al-Ilmiyyah. Tahrirul-Wasilah cha Khomein Juz. 2 Uk. 71, Chapa ya Darul-Kutub al-Ilmiyyah. 34 Tahrirul-Wasilah cha Khomein Juz. 2 Uk. 69, Chapa ya Darul-Kutub al-Ilmiyyah. 32 33
21
Maeneo ya Umma na Mali Zake
kama vile nyumba iliyowekwa Wakfu au eneo la biashara, ni wajibu juu yake kulipa malipo ya muda wote aliotumia mali hiyo ya Wakfu.35
Kuuza Wakfu makhsusi: Inaruhusiwa kuuza mali za Wakfu makhsusi iwapo tu itajitokeza moja ya sura zifuatazo: Sura ya kwanza: Iwapo mali ya Wakfu itaharibika katika jinsi ambayo haiwezekani tena kunufaika nayo, na wala haiwezekani kuirudisha katika hali yake ya mwanzo, basi hapo inaruhusiwa kuiuza, na ni lazima kununua mfano wake badala yake, kama haiwezekani kununua mfano wake basi inunuliwe ile iliyo karibu mno na asili.36 Sura ya pili: Iwapo mali iliyowekwa Wakfu itapatwa na uharibifu na ikawa inawezekana kunufaika nayo, lakini manufaa machache mno.37 Sura ya tatu: Iwapo aliyetoa Wakfu aliweka sharti la kuuzwa mali hiyo kama itatokea sura fulani, basi hapo litafuatwa sharti la aliyeweka Wakfu.38 Sura ya nne: Iwapo itajitokeza hali ya kutoelewana baina ya wale waliowekewa Wakfu, kiasi kwamba haiwezekani kuzuia mapigano baina yao au uharibifu wa mali zao.39
Tahrirul-Wasilah cha Khomein Juz. 2, Uk. 70, Chapa ya Darul-Kutub al-Ilmiyyah. Tahrirul-Wasilah cha Khomein Juz. 2, Uk. 70, Chapa ya Darul-Kutub al-Ilmiyyah. 37 Tahrirul-Wasilah cha Khomein Juz. 2, Uk. 71, Chapa ya Darul-Kutub al-Ilmiyyah. 38 Tahrirul-Wasilah cha Khomein Juz. 2, Uk. 71, Chapa ya Darul-Kutub al-Ilmiyyah. 39 Tahrirul-Wasilah cha Khomein Juz. 2, Uk. 71, Chapa ya Darul-Kutub al-Ilmiyyah. 35 36
22
Maeneo ya Umma na Mali Zake
Sadaka: Nayo ni sunna iliyosisitizwa sana, Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Hakika Mwenyezi Mungu hakuna mungu isipokuwa Yeye, kupitia sadaka huondoa maradhi, janga la moto, gharika, kubomokewa na nyumba na uwendawazimu, na hufunga milango saba ya mabalaa. “40
Miongoni mwa hukumu za sadaka: 1.
Si ruhusa mtu akitoa sadaka kuirudia sadaka hiyo na kumpokonya fakiri baada ya fakiri kuipokea, hata kama aliyepewa ni mtu baki, yaani si katika ndugu zake wa damu.41
2.
Hashimiyya anaruhusiwa kupokea sadaka ya sunna hata kama inatoka kwa asiyekuwa Hashimiyya.42
Ni nani anayefaa kisharia kupewa sadaka? Inaruhusiwa kumpa sadaka fakiri na hata tajiri, Shia na hata asiyekuwa Shia, bali hata mkiristo au yahudi ambaye anaishi katika nchi ya Waislamu, yule mwenye kuishi nao kwa amani, mwenye kufuata masharti ya Uislamu. Si ruhusa kumpa Nasibiy sadaka wala kafiri mwenye kuwapiga vita Waislamu. Tahrirul-Wasilah cha Khomein Juz. 2, Uk. 90, Chapa ya Darul-Kutub al-Ilmiyyah. Tahrirul-Wasilah cha Khomein Juz. 2, Uk. 80, Chapa ya Darul-Kutub al-Ilmiyyah. 42 Tahrirul-Wasilah cha Khomein Juz. 2, Uk. 81, Chapa ya Darul-Kutub al-Ilmiyyah. 40 41
23
Maeneo ya Umma na Mali Zake
SURA YA NNE MALI ZA KISHARIA Khumsi:
M
wenyezi Mungu amesema: “Na jueni kwamba chochote mlichopata ghanima, basi Khumsi yake ni ya Mwenyezi Mungu na Mtume na jamaa na mayatima na masikini na msafiri. Ikiwa nyinyi mmemwamini Mwenyezi Mungu na tuliyoteremsha kwa mja Wetu siku ya upambanuzi, siku yalipokutana majeshi mawili. Na Mwenyezi Mungu ni muweza juu ya kila kitu.” (Sura An’fal: 41) Khumsi ni kodi ya mali, Mwenyezi Mungu ameifaradhisha kwenye mali za matajiri, na ameigawa mali ya Khumsi mafungu mawili: Fungu moja huitwa fungu la Imam maasum, yaani al-Hujjah ibnu Hasan al-Mahdi (a.s.). Na fungu lingine ni fungu la masharifu, yaani wale ambao kinasaba ni Bani Hashim, kwa sharti wawe mafakiri.43 Hivyo ni lazima mwanadamu anapotaka kutumia mali ya Khumsi kuchukua idhini toka kwa Marjaa, sawa iwe ni katika fungu la Imam (a.s.) au fungu la masharifu.44 Si ruhusa kutumia mali ambayo inawajibika kutolewa Khumsi, kwa sababu sehemu ya mali hii ambayo ni kile kiwango cha Khumsi si milki ya mtumiaji, bali lau ikitokea kutaka kuitumia ni wajibu juu yake kuchukua dhamana ya kulipa, ila tu kama atakuwa amepata idhini ya Marjaa au mwakilishi wake. 43 44
Tahrirul-Wasilah cha Khomein Juz. 1, Uk. 334, Chapa ya Darul-Kutub al-Ilmiyyah. Ajwibatul-Istiftaat cha Sayyid Ali Khamenei Juz. 1, Uk. 300, Chapa ya kwanza ya Darul-Islamiyyah. 24
Maeneo ya Umma na Mali Zake
Mzazi asiyetoa Khumsi: Baadhi ya vijana kutokana na matatizo fulani hujikuta wakiishi na wazazi wao ambao hawaheshimu sheria ya kutoa haki za kisharia ambazo ni Khumsi na Zaka, hivyo hapa mtoto huwa mbele ya hali fulani, nazo ni: Kwanza: Huenda akawa mtu huyu hana yakini ya kuwa mzazi wake ameshakuwa na dhima ya wajibu wa kutoa Khumsi. Hapa mtoto anaruhusiwa kutumia mali ya mzazi wake na wala si wajibu juu yake kuchunguza na kufanya tahakiki. Pili: Huenda ana yakini ya kuwa mzazi wake ana dhima ya wajibu wa kutoa Khumsi, na yeye mwenyewe (mtoto) ana uwezo wa kujiepusha kutumia mali hii bila kujisababishia matatizo. Hapa ni wajibu juu yake kujiepusha kutumia mali hiyo. Tatu: Huenda ana yakini ya kuwa mzazi wake ana dhima ya wajibu wa kutoa Khumsi, lakini yeye (mtoto) hana uwezo wa kujiepusha kutumia mali hiyo, bali akifanya hivyo atajiletea matatizo. Hapa anaruhusiwa kuitumia mali hiyo, lakini ana dhamana ya wajibu wa kulipa kiwango cha Khumsi stahiki kilichopo kwenye mali anayoitumia.
Namna ya kutumia mali ya mtu Âasiyetoa Khumsi: Ni ruhusa kutumia mali ya tajiri ambaye hatoi Khumsi iwapo tu hauna yakini kuwa ana mali ambayo inawajibika kutolewa Khumsi naye hajatoa. Lakini kama utajua kwa yakini kwamba ana mali ambayo haijatolewa Khumsi licha ya kuwajibika kutolewa Khumsi, 25
Maeneo ya Umma na Mali Zake
hapa hauruhusiwi kuitumia isipokuwa kama kuacha kwako kuitumia kutakuletea matatizo, basi hapa unaruhusiwa kutumia kwa sharti la kuchukua dhamana ya kulipa haki ya mafakiri.
Msaada: Lau msamaria mwema atatoa msaada toka ndani ya mali ambayo inapasa kutolewa Khumsi, hairuhusiwi kutumia kile kiwango cha Khumsi, hivyo ni wajibu kumrejeshea Marjaa au mwakilishi wake kile kiwango cha Khumsi.
Manunuzi yatokanayo na mali ambayo haijatolewa Khumsi: Mtu akinunua ardhi au nyumba kwa mali ambayo haijatolewa Khumsi licha ya kuwa inawajibika kutolewa Khumsi, kile kiwango cha Khumsi kitategemea ruhusa ya Marjaa au mwakilishi wake, hivyo si ruhusa kusalia ndani ya eneo hilo iwapo haijapatikana ruhusa ya kutumia kile kiwango cha Khumsi. Mtu haruhusiwi kutoa Khumsi kwa kuwapa mafakiri ambao matumizi yao ni wajibu ulio juu yake, hivyo si ruhusa kwa mtu mwenye Khumsi kuwapa Khumsi wazazi wake au wanawe na mke wake, maadamu tu ana miliki mali inayomwezesha kuwatimizia matumizi yao.45 Ndio, mtoto anaruhusiwa kumpa mzazi wake Khumsi ili atoe matumizi kwa mkewe iwapo tu mke huyo si mama mzazi wa mtoa Khumsi (mama wa kambo), lakini ni baada ya kuchukua idhini toka kwa Marjaa au mwakilishi wake. 45
jwibatul-Istiftaat cha Sayyid Ali Khamenei Juz. 1 Uk. 304, Chapa ya kwanza ya A Darul-Islamiyyah. 26
Maeneo ya Umma na Mali Zake
Kwa mujibu wa ihtiyat ni wajibu kutokumpa fakiri kiasi kinachozidi matumizi yake ya mwaka.46 Na iwapo mtu atafikiwa na mali ya Khumsi ili aitumie katika matumizi yake na akawa kweli yeye ni miongoni mwa mifano halisi ya wanaostahiki, ni ruhusa kwake kuitumia.
Zaka: Ni kodi ya mali, Mwenyezi Mungu ameifaradhisha juu ya aina maalumu za mali, na amefanya kinachopatikana humo kiwe cha mafakiri, na ameigawa mali hiyo katika mafungu mbalimbali. Zaka ni miongoni mwa ibada kama Khumsi, yaani ni matendo yanayohitaji niya ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Miongoni mwa hukumu za mali ya Zaka:
46 47
1.
Mtu haruhusiwi kuwapa Zaka watu ambao matumizi yao ni wajibu ulio juu yake, kama vile mke, watoto na wazazi wawili, hii ni kama akitaka kuwapa mali kwa anwani ya ufakiri. Ama ikiwa ni kwa anwani nyingine kama vile anwani ya njia ya Mwenyezi Mungu, kwa mfano mzazi akataka kumpa Zaka mwanaye ambaye ni miongoni mwa wanafunzi, anaruhusiwa kumpa.47
2.
Asiyekuwa Hashimiyyah haruhusiwi kumpa Zaka Hashimiyyah. Na Hashimiyyah ni kila ambaye nasaba yake inagota kwa Hashim babu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), hivyo in-
Tahrirul-Wasilah cha Khomein Juz. 1 Uk. 335, Chapa ya Darul-Kutub al-Ilmiyyah. Tahrirul-Wasilah cha Khomein Juz. 1, Uk. 310, Chapa ya Darul-Kutub al-Ilmiyyah. 27
Maeneo ya Umma na Mali Zake
awajumuisha watoto wote wa Abdul-Mutalib, kuanzia watoto wa Abbasi hadi wa Abu Talib (r.a).48 3.
Katika zama hizi ambazo Imam wa zama hizi yu ghaibu ni bora kumkabidhi Zaka Marjaa, ijapokuwa si wajibu kufanya hivyo. Ndio, lau kama Marjaa atatoa hukumu ya kumkabidhi yeye kwa kuwa hilo (la kumkabidhi yeye) ndilo lenye maslahi na Uislam na Waislamu, basi ni wajibu kumkabidhi.49
4.
Lau mtu ataharibu mali ya Zaka, ni wajibu juu yake kulipa, sawa aliyeharibu awe ni yule mmiliki mwenyewe au mtu mwingine.
5.
Ni ruhusa kusafirisha Zaka kutoka nchi yake kupeleka nchi nyingine, lakini gharama za usafirishaji ni juu ya msafirishaji mwenyewe na si kutoka ndani ya mali ya Zaka, hivyo akisafirisha mali ya Zaka kwa njia ya benki, makato ya benki hayapasi kuchukuliwa toka kwenye mali ya Zaka bali ni kutoka kwa yule aliyeikabidhi benki.50
6.
Lau mtu atampa mtu mwingine Zaka ili aitumie kwenye sehemu ambazo Zaka inastahiki kutumiwa, na huyo aliyepewa akawa ni moja ya sehemu hizo, basi anaruhusiwa kuimiliki.51
7.
Ikiwa mtu ana wajibu wa kutoa Zaka, na mauti yake yakawa yamekaribia ni wajibu juu yake kukabidhi wasia unaoelekeza kuwa Zaka hiyo itolewe toka kwenye mali zake atakazoziacha, na hapa ni wajibu juu ya warithi wake au kabidhi
Tahrirul-Wasilah cha Khomein Juz. 1, Uk. 311, Chapa ya Darul-Kutub al-Ilmiyyah. Tahrirul-Wasilah cha Khomein Juz. 1, Uk. 313, Chapa ya Darul-Kutub al-Ilmiyyah. 50 Tahrirul-Wasilah cha Khomein Juz. 1, Uk. 314, Chapa ya Darul-Kutub al-Ilmiyyah. 51 Tahrirul-Wasilah cha Khomein Juz. 1, Uk. 315, Chapa ya Darul-Kutub al-Ilmiyyah. 48 49
28
Maeneo ya Umma na Mali Zake
wasii wake kutoa Zaka, kwani hapa inakuwa sawa na madeni yake mengine.52 8.
Lau mtu akimkabidhi mtu Zaka kwa kujua kuwa ni mmoja wa wale wanaostahiki Zaka, kisha baadaye akabaini kuwa si mstahiki wa Zaka, ni juu ya mtoaji kumuomba amrejeshee Zaka hiyo, na kama itaharibika ni wajibu juu ya mtoaji kulipa mali hiyo ya Zaka.
9.
Mtu akishatenga kiwango cha Zaka anaruhusiwa kutumia mali iliyobaki iliyopo kwake, kadhalika akishatoa Zaka toka kwenye mali yake ya mwisho.
Zakatul-Fitri: Hujulikana kama Zaka ya mwili, nayo ni ile ambayo ni wajibu juu ya kila mwislamu kuitoa siku ya Idil-Fitri.
Miongoni mwa hukumu za ÂZakatul-Fitri:
52
1.
Si ruhusa kwa asiyekuwa Hashimiyyah kumpa Zaka Hashimiyyah.
2.
Katika Zaka hii ni lazima ipatikane nia ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu.
3.
Iwapo ndani ya nchi husika anapatikana anayestahiki Zakatul-Fitri si ruhusa kusafirisha Zaka hiyo kwenda nchi nyingine baada ya kuitenga.
Tahrirul-Wasilah cha Khomein Juz. 1, Uk. 314, Chapa ya Darul-Kutub al-Ilmiyyah. 29
Maeneo ya Umma na Mali Zake
4.
Mtu anaruhusiwa yeye mwenyewe kumpa Zakatul-Fitri mstahiki, wala haihitaji kupata idhini ya Marjaa.
5.
Anayestahiki kupewa Zakatul-Fitri ni yule anayestahiki kupewa Zaka ya mali. Bora zaidi ni wapewe mafukara walio waumini, ndio, uadilifu si kigezo katika mgao wa ZakatulFitri.
6.
Si ruhusa kumpa Zakatul-Fitri yule atakayeitumia katika maasi.53
Mali ambayo mmiliki wake Âhajulikani: Kila mali ambayo inajulikana kuwa ina mwenyewe lakini hajulikani ni nani, na wala haiwezekani kumpata mwenyewe, huingia chini ya hukumu ya mali ambayo mmiliki wake hajulikani, hivyo hukumu ya mali ya jinsi hii ni kutolewa sadaka baada ya kuomba idhini toka kwa Marjaa.
Mfano wa mali hiyo: Miongoni mwa mifano ya mali ambayo mmiliki wake hajulikani ni yule mnyama anayeingia ndani ya nyumba ya mtu na mwenye mnyama hajulikani. Pia lau kama mtu atanunua kitu kutoka kwa mtu, kisha baadaye akagundua kuwa muuzaji alikipata kwa dhulma na unyang’anyi, yaani ilikuwa ni mali ya wizi, na mwenyewe aliyeibiwa hajulikani. Pia miongoni mwa mifano ni mali itokanayo na michezo ya bahati nasibu na Loto. 53
Tahrirul-Wasilah cha Khomein Juz. 1, Uk. 320, Chapa ya Darul-Kutub al-Ilmiyyah. 30
Maeneo ya Umma na Mali Zake
Hukumu ya bahati nasibu na Loto: Si ruhusa kucheza bahati nasibu, Loto na michezo ya jinsi hiyo ya kubahatisha. Nayo ni ile michezo ambayo shirika (au kampuni au mtu) au nchi inauza tiketi kwa thamani fulani, na mnunuzi anabakia na namba, kisha inafanyika droo ya kuchagua kwa njia ya kubahatisha au njia nyingine za uchaguzi, namba itakayoshinda na kupata zawadi. Si ruhusa kucheza michezo hiyo kama ambavyo pia mwenye kushinda kwa bahati nasibu haruhusiwi kupokea zawadi. Imam Khamenei anasema: “Si ruhusa kuuza na kununua tiketi za bahati nasibu, wala mshindi kumiliki zawadi, na wala hapasi kuipokea.”54 Baadhi ya watu hudhani kwamba mshindi wa zawadi atatoa sehemu ya Khumsi ya zawadi hiyo na hivyo kuhalalisha sehemu iliyobaki na suala litakomea hapo. Ukweli ni kwamba suala haliko hivyo, kwani hakika mali itokanayo na michezo ya Loto na bahati nasibu ni sawa na mali ya kamari, hivyo asilani si ruhusa kuichukua. Imam Khamenei anasema katika moja ya fatwa zake: “Hakuna biashara kwenye tiketi za bahati nasibu, bali zenyewe ni njia anayoitumia msambazaji na muuzaji wake kuchukulia mali toka kwa mnunuzi, kama ambavyo zenyewe ni njia anayoitumia mnunuzi kupata zawadi yake, hivyo ni kama njia ya kamari, hivyo si ruhusa kuziuza wala kuzinunua, wala si halali kwake ile zawadi anayoipata huyo mwenye tiketi hiyo.”55 jwibatul-Istiftaat cha Sayyid Ali Khamenei Juz. 2, Uk. 54, Chapa ya kwanza ya A Darul-Islamiyyah. 55 Ajwibatul-Istiftaat cha Sayyid Ali Khamenei Juz. 2, Uk. 55, Chapa ya kwanza ya Darul-Islamiyyah. 54
31
Maeneo ya Umma na Mali Zake
Baadhi ya mashirika ya misaada ya kibinadamu yanaweza kuchangisha misaada ili kutoa misaada ya kibinadamu kama vile kulea mayatima na kuwasaidia wasio na kitu, na mkabala na uchangishaji huo yakatoa tiketi zenye namba, tiketi ambazo yatachagua mojawapo kwa njia ya droo na hatimaye mwenye namba kujishindia kiasi fulani cha mali, ili kushajiisha matendo ya kheri. Katika hali kama hii je kitendo hiki kinaruhusiwa? Na ni ipi hukumu ya mali ambayo ameshinda mmoja wa wachangiaji? Katika hali hii kitendo chenyewe ni halali, lakini kwa sharti la msingi kwamba kiwe kimekusudiwa kushajiisha uchangiaji katika njia ya Mwenyezi Mungu. Imam Khamenei (a.s.) amesema: “Hakuna ubaya kugawa karatasi za kuombea michango kwa ajili ya mambo ya kheri, na inaruhusiwa kuwashajiisha wachangiaji, kuwatia mori na kuwahimiza kuchangia kwa kuahidi kumpa zawadi yule ambaye jina lake litashinda katika droo, kwa sharti kwamba kusudio la wachangiaji liwe ni kushiriki katika matendo ya kheri.�56
56
jwibatul-Istiftaat cha Sayyid Ali Khamenei Juz. 2 Uk. 55, Chapa ya kwanza ya A Darul-Islamiyyah. 32
Maeneo ya Umma na Mali Zake
SURA YA TANO MALI ZA DOLA Ni wazi kwamba dola yoyote iwe ndogo au kubwa inamiliki baadhi ya mali, vitu na ardhi. Ni ipi hukumu ya kisharia kuhusu miliki hizi? Je zile dola zisizokuwa za kiislamu zinahesabika kuwa ni wamiliki wa ardhi hivi sasa? Na je mtu anayeishi humo anaruhusiwa kutumia mali hizo vyovyote atakavyo yeye? Na je ikitokea mathalani mtu kuharibu barabara au nguzo ya umeme, je ni wajibu juu yake kulipa badala? Maswali haya tutayajibu ndani ya anwani zifuatazo:
Je dola inamiliki mali? Ni kinyume na wanavyodhani baadhi ya watu kuwa dola haimiliki chochote katika ardhi na barabara, ukweli ni kwamba sheria inatambua kuwa mali za dola – hata kama si ya kiislamu - ni milki ya dola yenyewe, na ina haki ya kuzitumia kwa jinsi inavyoona inafaa, kwa kuwa ni milki yake binafsi. Imam Khamenei anasema: “Mali za dola, hata kama si ya kiislamu, kisharia ni milki ya dola, na katika kuamiliana nazo ni kwa mujibu wa muamala wa milki ambayo mmiliki wake anajulikana. Na katika ruhusa ya kuzitumia ni lazima kupata idhini kutoka kwa mhusika ambaye ndiye mwenye mamlaka ya kutoa idhini ya matumizi katika mali hizi.”57 57
jwibatul-Istiftaat cha Sayyid Ali Khamenei Juz. 2 Uk. 322, Chapa ya kwanza ya A Darul-Islamiyyah. 33
Maeneo ya Umma na Mali Zake
Wafanyakazi wa dola: Ikiwa mali za dola ni milki ya dola basi ni lazima kuheshimu umiliki wake, hivyo si ruhusa kwa hali yoyote ile kuharibu mali ya dola, hususan kwa wale wanaofanya kazi katika vyombo vya dola, kuanzia wale wa maofisini hadi wale wa nje ya ofisi, hivyo si ruhusa kutumia mali hizi za umma kwa matumizi yao binafsi, isipokuwa baada ya kupata idhini ya wenye kuwajibika na mali husika. Imam Khamenei anasema: “Viongozi, mabosi na hata wafanyakazi wa kawaida hawaruhusiwi kutumia chochote kile toka kutoka katika mali za dola kwa matumizi yao binafsi, isipokuwa watakapopata ruhusa ya kisharia kutoka upande unaohusika.�58
Kuharibu mali ya dola: Kwa kuwa mali ya dola ni mali ambayo mmiliki wake anajulikana, basi atakayeharibu miliki za dola ni lazima alipe mali hiyo. Kwa mfano mtu ataharibu barabara ni wajibu juu yake kuitengeneza, na kama mtu atatumia kitu na akakiharibu au kukiua, basi ni lazima ailipe dola. Imam Khamenei anasema: “Katika wajibu wa kuheshimu mali ya mtu na uharamu wa kutumia mali ya mtu bila idhini yake, hakuna tofauti katika hayo mawili baina ya miliki za watu binafsi na miliki za dola, sawa iwe ni dola ya kiislamu au si ya kiislamu, sawa iwe ni ndani ya nchi ya kikafiri au nchi ya kiislamu, katika hayo hakuna tofauti, na sawa mmiliki wa mali awe ni mwislamu au ni kafiri, hakuna tofauti. Kwa jumla ni kwamba si ruhusa kisharia kufaidika 58
jwibatul-Istiftaat cha Sayyid Ali Khamenei Juz. 2, Uk. 323, Chapa ya kwanza ya A Darul-Islamiyyah. 34
Maeneo ya Umma na Mali Zake
na kutumia mali ya mtu bila idhini yake, na kufanya hivyo ni wizi na ni haramu na kunawajibisha kulipa.”59
Kodi na ada: Hakika dola huwataka wananchi wake kulipa ada mkabala na huduma zinazotolewa na dola husika, kama vile huduma ya maji, umeme na simu. Je, ni wajibu juu ya wananchi kulipa ada hizi wanazotozwa na dola? Na je mukalafu anaruhusiwa kuliibia shirika la maji au shirika la umeme kwa kutumia huduma zao kinyume na kanuni? Hakika sharia tukufu haijamruhusu mwanadamu kukimbia kulipa ada hizi za dola mkabala na huduma za maji, umeme na nyinginezo zinazotolewa na dola. Imam Khamenei anasema: “Ni wajibu kwa kila aliyetumia maji na umeme toka kwenye mradi wa serikali wa maji na umeme kuilipa dola ada ya huduma hiyo, hata kama si dola ya kiislamu.”60 Pia wananchi hawaruhusiwi kujipangia kiasi watakachoilipa dola, bali ni wajibu kulipa kulingana na viwango vya serikali na si kulingana na matakwa ya mtu na makisio yake binafsi. Imam Khamenei anasema: “Ada za serikali na kodi za serikali ni wajibu zilipwe kulingana na viwango vya dola.”61 Na mwisho wa maombi yetu ni kumshukuru Mwenyezi Mungu Mkuu wa enzi. jwibatul-Istiftaat cha Sayyid Ali Khamenei Juz. 2, Uk. 322 - 323, Chapa ya kwanza ya A Darul-Islamiyyah. 60 Ajwibatul-Istiftaat cha Sayyid Ali Khamenei Juz. 2, Uk. 334, Chapa ya kwanza ya Darul-Islamiyyah. 61 Ajwibatul-Istiftaat cha Sayyid Ali Khamenei Juz. 2, Uk. 334, Chapa ya kwanza ya Darul-Islamiyyah. 59
35
Maeneo ya Umma na Mali Zake
ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION 1. Qur’an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Thelathini 2.
Uharamisho wa Riba
3.
Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza
4.
Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili
5.
Hekaya za Bahlul
6.
Muhanga wa Imamu Husein (A.S.)
7.
Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.)
8.
Hijab vazi Bora
9.
Ukweli wa Shia Ithnaashari
10.
Madhambi Makuu
11.
Mbingu imenikirimu
12.
Abdallah Ibn Saba
13.
Khadijatul Kubra
14. Utumwa 15.
Umakini katika Swala
16.
Misingi ya Maarifa
17.
Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia 36
Maeneo ya Umma na Mali Zake
18.
Bilal wa Afrika
19. Abudharr 20.
Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu
21.
Salman Farsi
22.
Ammar Yasir
23.
Qur’an na Hadithi
24. Elimu ya Nafsi 25. Yajue Madhehebu ya Shia 26.
Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur’an Tukufu
27. Al-Wahda 28.
Ponyo kutoka katika Qur’an
29.
Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii
30.
Mashukio ya Akhera
31.
Al Amali
32.
Dua Indal Ahlul Bayt
33.
Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna.
34.
Haki za wanawake katika Uislamu
35.
Mwenyezi Mungu na sifa zake
36.
Kumswalia Mtume (s)
37.
Nafasi za Ahlul Bayt (a.s)
38. Adhana 37
Maeneo ya Umma na Mali Zake
39
Upendo katika Ukristo na Uislamu
40.
Tiba ya Maradhi ya Kimaadili
41.
Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu
42.
Kupaka juu ya khofu
43.
Kukusanya swala mbili
44.
Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara
45.
Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya
46.
Kusujudu juu ya udongo
47.
Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s)
48. Tarawehe 49.
Malumbano baina ya Sunni na Shia
50.
Kupunguza Swala safarini
51.
Kufungua safarini
52.
Umaasumu wa Manabii
53.
Qur’an inatoa changamoto
54. as-Salaatu Khayrun Mina -’n Nawm 55.
Uadilifu wa Masahaba
56. Dua e Kumayl 57.
Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu
58.
Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake
59.
Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata
60. Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mtume Muhammad (s) 38
Maeneo ya Umma na Mali Zake
61.
Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza
62.
Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili
63. Kuzuru Makaburi 64.
Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza
65.
Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili
66.
Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu
67.
Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne
68.
Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano
69.
Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita
70.
Tujifunze Misingi Ya Dini
71.
Sala ni Nguzo ya Dini
72.
Mikesha Ya Peshawar
73.
Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu
74. Ubora wa Imam ‘Ali Juu ya Maswahaba Na Ushia ndio njia iliyonyooka 75.
Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake
76. Liqaa-u-llaah 77.
Muhammad (s) Mtume wa Allah
78.
Amani na Jihadi Katika Uislamu
79.
Uislamu Ulienea Vipi?
80.
Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s)
81.
Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s)
39
Maeneo ya Umma na Mali Zake
82. Urejeo (al-Raja’a ) 83. Mazingira 84.
Utokezo (al - Badau)
85.
Hukumu ya kujenga juu ya makaburi
86.
Swala ya maiti na kumlilia maiti
87.
Uislamu na Uwingi wa Dini
88.
Mtoto mwema
89.
Adabu za Sokoni
90.
Johari za hekima kwa vijana
91.
Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza
92.
Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili
93.
Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu
94. Tawasali 95.
Imam Mahdi katika Usunni na Ushia
96.
Hukumu za Mgonjwa
97.
Sadaka yenye kuendelea
98.
Msahafu wa Imam Ali
99.
Ngano ya kwamba Qur’ani imebadilishwa
100. Idil Ghadiri 101. Kusoma sura zenye Sijda ya wajibu 102 Hukumu zinazomuhusu mkuu wa kazi na Mfanyakazi 103. Huduma ya Afya katika Uislamu 40
Maeneo ya Umma na Mali Zake
104. Sunan an-Nabii 105. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza) 106. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili) 107. Shahiid Mfiadini 108. Kumsalia Nabii (s.a.w) 109. Ujumbe -Sehemu ya Kwanza 110. Ujumbe - Sehemu ya Pili 111. Ujumbe - Sehemu ya Tatu 112. Ujumbe - Sehemu ya Nne 113. Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu 114. Hadithi ya Thaqalain 115. Ndoa ya Mutaa 116. Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza 117. Ukweli uliopotea sehemu ya Pili 118. Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu 119. Ukweli uliopotea sehemu ya Nne 120. Ukweli uliopotea sehemu ya Tano 121. Mkutano wa Maulamaa wa Baghdad 122. Safari ya kuifuata Nuru 123. Fatima al-Zahra 124. Myahudi wa Kimataifa 125. Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi 41
Maeneo ya Umma na Mali Zake
126. Visa vya kweli sehemu ya Kwanza 127. Visa vya kweli sehemu ya Pili 128. Elimu ya Ghaibu ya Maimamu 129. Mwanadamu na Mustakabali wake 130. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Kwanza) 131. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Pili) 132. Khairul Bariyyah 133. Uislamu na mafunzo ya kimalezi 134. Vijana ni Hazina ya Uislamu 135. Yafaayo kijamii 136. Tabaruku 137. Taqiyya 138. Vikao vya furaha 139. Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje? 140. Visa vya wachamungu 141. Falsafa ya Dini 142. Azadari-Kuhuzunika na Kuomboleza 143. Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah 144. Mtazamo Mpya - Wanawake katika Uislamu 145. Kuonekana kwa Allah 146. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza) 42
Maeneo ya Umma na Mali Zake
147. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili) 148. Ndugu na Jirani 149. Ushia ndani ya Usunni 150. Maswali na Majibu 151. Mafunzo ya hukmu za ibada 152. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 1 153 Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 2 154. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 3 155. Abu Huraira 156. Vipengee kadhaa katika Swala ya Jamaa na Msikiti. 157. Mazingatio kutoka katika Qur’an - Sehemu ya Kwanza 158. Mazingatio kutoka kaitka Qur’an - Sehemu ya Pili 159. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya kwanza 160. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya Pili 161. Qur’ani Tukufu – Pamoja na Tarjuma ya Kiswahili 162. Falsafa ya Mageuzi ya Imam Husein (a.s) 163. Amali za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani 164. Elimu ya Tiba za Kiislamu - Matibabu ya Maimamu 165. Uislamu Safi 166. Majlisi za Imam Husein Majumbani 167. Je, Kufunga Mikono 168. Uislam wa Shia 43
Maeneo ya Umma na Mali Zake
169. Amali za Makka 170. Amali za Madina 171. Asili ya Madhehebu katika Uislamu 172. Sira ya Imam Ali kuhusu Waasi 173. Ukweli uliofichika katika neno la Allah 174. Uislamu na Mifumo ya Uchumi 175. Umoja wa Kiislamu na Furaha 176. Mas’ala ya Kifiqhi 177. Jifunze kusoma Qur’ani 178. As-Sahifatul Kamilah as-Sajjadiyyah 179. Hayya ‘Alaa Khayri’l-’Amal Katika Adhana 180. Ukweli kuhusu Funga ya Siku ya Ashura 181. Dua za Miezi Mitatu Mitukufu (Rajabu, Shaabani na Ramadhani) 182. Uadilifu katika Uislamu 183. Mahdi katika Sunna 184. Maswali Ya Uchunguzi Kuhusu Uislam 185. Kazi na Bidii ni njia ya maendeleo 186. Abu Talib – Jabali Imara la Imani 187. Ujenzi na Utakaso wa Nafsi 188. Vijana na Matarajio ya Baadaye 189. Usalafi – Historia yake, maana yake na lengo lake 190. Ushia – Hoja na Majibu 44
Maeneo ya Umma na Mali Zake
191. Mateso ya Dhuria wa Mtume (saww) 192. Maombolezo – Msiba wa Bwana wa Mashahidi (a.s.) 193. Shahidi kwa Ajili ya Ubinadamu 194. Takwa 195. Upotoshaji dhahiri katika Turathi (Hazina) ya Kiislamu 196. Amirul Muuminina (‘as) na Makhalifa 197. Uongozi na Utawala katika Mwenendo wa Imam ‘Ali (‘a) 198. Kuvunja hoja iliyotumika kutetea Uimamu wa AbuBakr 199. Adabu za vikao na mazungumzo 200. Hija ya Kuaga 201. Uwazi baina ya Maslahi na Vikwazo 202. Fadhila za watukufu watano katika Sahih Sita 203. Mdahalo baina ya Mwanachuoni wa Kisunni na Mwanachuoni wa Kishia (Al-Muraja’aat) 204. Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (as) 205. Mjadala wa Kiitikadi 206. Mtazamo kuhusu msuguano wa Kimadhehebu 207. Nchi na Uraia – Haki na wajibu kwa Taifa 208. Mtazamo wa Ibn Taymiyyah juu ya Imam Ali (as) 209. Uongozi wa Kidini – Maelekezo na Utekelezaji wa Kijamii 210. Maadili ya Ashura 211. Mshumaa – Shahidi na Kifo cha Kishahidi
45
Maeneo ya Umma na Mali Zake
212. Mizani ya Hekima – Hadithi za Ahlul Bait (as) – Sehemu ya Kwanza 213. Imam Ali na Mambo ya Umma 214. Imam Ali na Mfumo wa Usawa 215. Mwanamke na Sharia 216. Mfumo wa Wilaya 217. Vipi Tutaishinda Hofu? 218. Kumswalia Mtume ni Ufunguo wa Utatuzi wa Matatizo
219. Mahali na Mali za Umma 220. Nahjul-Balagha – Majmua ya Khutba, Amri, Barua, Risala, Mawaidha na Semi za Amirul-Muuminin Ali bin Abu Talib (a.s.) 221. Mukhtar – Shujaa aliyelipiza kisasi dhidi ya wauaji wa Imam Husein (as) hapo Karbala 222. Uimamu na Tamko la Kutawazwa 223. Imam Husain ni Mfumo wa Marekebisho na Mageuzi 224. Saada Kamili – Kitabu cha Kiada cha Maadili 225. Maeneo ya Umma na Mali Zake
46
Maeneo ya Umma na Mali Zake
KOPI NNE ZIFUATAZO ZIMETAFSIRIWA KWA LUGHA KINYARWANDA 1.
Amateka Na Aba’Khalifa
2.
Nyuma yaho naje kuyoboka
3.
Amavu n’amavuko by’ubushiya
4.
Shiya na Hadithi
47
Maeneo ya Umma na Mali Zake
ORODHA YA VITABU VILIVYO ÂCHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION KWA LUGHA YA KIFARANSA 1.
Livre Islamique
48