Mama wa Waumini Mtazamo wa Kisharia katika Mwangaza wa Rejea za Shia Ithnaasharia
رؤية شرعية على ضوء مصادر الشيعة اإلمامية:أمهات المؤمنين
Kimeandikwa na: Husain Ali al-Mustafa
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 1
3/26/2016 12:31:34 PM
ترجمة
أمهات المؤمنين :رؤية شرعية على ضوء مصادر الشيعة اإلمامية
تأليف الشيخ حسين علي المصطفى
من اللغة العربية إلى اللغة السواحلية
3/26/2016 12:31:34 PM
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 2
©Haki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: 978 - 9987 – 17 – 048 – 7 Kimeandikwa na: Husain Ali al-Mustafa Kimetarjumiwa na: Abdul Karim Juma Nkusui Barua Pepe: abdulkarimjuma@yahoo.com Kimehaririwa na: Al-Haji Hemedi Lubumba Selemani Kimesomwa Prufu na: Al-Haji Ramadhani S. K. Shemahimbo Kimepitiwa na: Mujahid Rashid Kimepangwa katika Kompyuta na: Al-Itrah Foundation Toleo la kwanza: Agosti, 2016 Nakala: 2000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. - 19701, Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 / 2127555 Barua Pepe: alitrah@yahoo.com Tovuti: www.ibn-tv-com Katika mtandao: www.alitrah.info
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 3
3/26/2016 12:31:34 PM
Yaliyomo Dibaji ......................................................................................... vi Neno la Mchapishaji........................................................................ 1 1. Neno la msambazaji................................................................... 3 2. Utangulizi................................................................................... 5 3. Kukataza maneno machaf.......................................................... 7 4. Athari mbaya ya maneno mabaya............................................ 10 5. Nasaha...................................................................................... 11 6. Utukufu wa Mama za Waumini ni miongoni mwa utukufu wetu............................................................................. 13 7. Vita ya Ngamia na kilichofuatia katika vita ya maneno........... 23 8. Rai ya Makhawariji.................................................................. 25 9. Rai ya Muutazilah.................................................................... 25 10. Rai ya Ashair............................................................................ 26 11. Msimamowa Imamu Ali ď ‚.................................................... 27 12. Utukufu waMama wa Waumini na usafi wao.......................... 29 13. Ahlul-Bayti wanapokea kutoka kwaMama za Waumini.......... 40 14. Uhusiano waAhlul-Bayti na Mama za Waumini...................... 44
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 4
3/26/2016 12:31:34 PM
15. Katika Hadithi za Mtume wa Mwenyezi Mungu  pamoja na wake zake......................................................... 47 16. Fadhila za Imamu Ali katika ndimi za Mama za Waumini............................................................................... 50 17. Hitimisho katika fiqhi ya kutukana na kulaani......................... 56 18. Katika kutukana:...................................................................... 56 19. Katika kulaani:......................................................................... 56 20. Rejea ........................................................................................ 56
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 5
3/26/2016 12:31:35 PM
Mama wa Waumini
بسم هللا الرحمن الرحيم
DIBAJI
K
itabu hiki ni toleo la Kiswahili la taasisi ya Al Itrah Foundation. Chapisho lake limelenga kukidhi mahitaji ya kiroho ya zama hizi pamoja na Ubongo na fikra zinazokuwa za Muislam. Jitihada kubwa zimefanywa na Taasisi kuweka chapisho hili la Kiswahili katika msingi wa haki na wenye kukubalika katika Uislam. Unaombwa kwa Taadhima ukisome kitabu hiki katika malengo yaliyokusudiwa. Pia Unaombwa kuwasilisha kwetu maoni yako huru juu ya chapisho letu hili, jambo ambalo tutashukuru sana. Kutangaza ujumbe wa Uislam ni kazi ambayo inahitaji ushirikiano wetu sote. Taasisi inakuomba kuungana na kushirikiana kama ilivyoagizwa katika aya ya Qur’an: (Surat Saba’ 34:46). Na rehma za Allah ziwe juu yako. Wako katika Uislam Al Itrah Foundation Barua Pepe: alitrah@yahoo.com SMS: +255 778 300 140
vi
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 6
3/26/2016 12:31:35 PM
Mama wa Waumini
بسم هللا الرحمن الرحيم
NENO LA MCHAPISHAJI
K
itabu ulichonacho mikononi mwako asili yake ni cha lugha ya Kiarabu kwa jina la, Ummahatu ‘l-Mu’miniin kilichoandikwa na Husain Ali al-Mustafa. Kilichomsukuma mwandishi huyu kuandika kitabu hiki ni kutokana na fitna iliyojitokeza juu ya mmoja wa wake za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kuenezwa na wanafiki na maadui wa Uislamu. Waislamu wote bila kujali madhehebu zao wanawatambua wake wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kama Mama wa Waumini. Lakini wamejitokeza watu miongoni mwa Waislamu na madhehebu zao za upotofu kuwatuhumu Waislamu wenzao na utovu wa adabu ambapo kwa kweli ni wao ambao wamekosea adabu ya dini ya Allah pamoja na Mtume Wake (s.a.w.w.). Mwandishi wa Kitabu hiki anaelezea kwa undani kadhia hii kwa kutaja matukio muhimu ya kihistoria kwa ujumla. Sisi tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa makubwa kwa wasomaji wa lugha ya Kiswahili hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni vitu ambavyo havina nafasi tena katika akili za watu. Tunamshukuru mwandishi wa kitabu hiki Husain Ali al-Mustafa kwa kazi kubwa aliyoifanya kwa ajili ya Umma huu wa Waislamu, Allah Azza wa Jallah amlipe kila la kheri na amuingize Peponi kwa salama na amani insha’Allah. Halikadhalika tunamshukuru 1
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 1
3/26/2016 12:31:35 PM
Mama wa Waumini
ndugu yetu Ustadh Abdul Karim Juma Nkusui kwa kukitarjumi kwa Kiswahili kitabu hiki, insha’Allah na yeye Allah Azza wa Jallah amlipe kila la kheri hapa duniani na Akhera pia, bila kuwasahau na wale wote waliochangia kwa namna mmoja au nyingine mpaka kufanikisha kuchapishwa kwake. Allah awalipe wote malipo mema hapa duniani na Akhera pia. Mchapishaji Al-itrah Foundation
2
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 2
3/26/2016 12:31:35 PM
Mama wa Waumini
بسم هللا الرحمن الرحيم
NENO LA MTANGAZAJI
I
napotawala hali ya ubaguzi na kuenea mielekeo ya kasumba za kimadhehebu, na ummah kukumbwa na upepo wa fitina, hakika mengi miongoni mwa ukweli wa kidini na dhana zake hufukiwa na kufunikwa na pazia na giza, au hupatwa na upotoshaji na kupakwa matope. Jambo ambalo hutoa fursa ya kuvunja matukufu na kuwasha moto wa fitina ndani ya ummah Na haya ndio matatizo yanayoikabili medani ya Kiislamu leo hii, ambapo misingi ya umoja wa ummah na dhana za udugu wa kiimani, haki ya Mwislamu, uharamu wa damu yake, mali yake na heshima yake, na asili ya utukufu wa mwandamu na kuwaombea maghufira ndugu zetu waliotutangulia katika imani, yote hayo yamefunikwa, na mahala pake pamechukuliwa na mifarakano, mpasuko ndani ya umma, kukufurishana kwa zamu baina ya makundi yake, umwagaji wa damu, uvunjaji wa haki na ubaya wa kubadilishana wa kuvivunjia heshima vielelezo na shakhisiya za madhehebu na makundi mbalimbali, na kutumia lugha chafu, tuhuma na laana. Mbele ya hali hii mbaya na ya hatari, ni lazima maulamaa waelewa wa ummah wenye ikhilasi wabebe jukumu la kudhihirisha neno la haki na kudhihirisha msimamo sahihi wa kisharia katika mambo ambayo kumetokea ndani yake mkanganyiko na upotoshaji. Kwani mawili hayo ndio sababu ya kuchochea chuki na mifundo. Na miongoni mwa mambo hayo nyeti ambayo wanayatumia walinganiaji wa ubaguzi na fitina ni msimamo wa Mama wa Waumini, wake wa Mtume wa Mwenyezi Mungu 2. Ambapo imetoka 3
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 3
3/26/2016 12:31:35 PM
Mama wa Waumini
sauti ovu mbaya inayokosea adabu heshima ya Mtume wa Mwenyezi Mungu 2 na kuvunja utukufu wake na kukariri maneno ya wanafiki kwa kuelekeza tuhuma ya uongo na uzushi kwa mmoja wa Mama za Waumini baada ya wahyi wa Mwenyezi Mungu kutangaza kupinga na kukadhibisha na kuiepusha shakhisiya ya Mtume na ubaya wowote. Na ni wazi kwamba lengo la uongo huu mpya ni kumwagia mafuta juu ya moto wa fitina ya makundi katika ummah, kwa kuelezea maudhui kama udhihirisho wa wazi wa ikhitilafu baina ya Sunni na Shia, pamoja na kwamba kuhifadhi heshima ya Mtume wa Mwenyezi Mungu 2 na kuwatakasa Mama za Waumini ni msingi wa Qur’ani, wanauamini Waislamu wote Shia na Sunni. Na ameyazungumzia maudhui haya Allamah mhakiki Sheikh Hasan Ali al-Mustafaa, ambaye ni kati ya Maulamaa wa Qatif katika nchi ya kifalme ya Saudia. Amezungumzia hilo ndani ya kitabu chake kizuri Adabiyatu Taayushi Bainal-Madhahib, na kwa umuhimu wa maudhui haya na kwa kuwa medani inahitajia sana mada hii kuelezwa katika mtazamo wa kisharia wa asili, tumemuomba Allamah akubali kuchapishwa sehemu ya kitabu hicho (mlango wa Mama za Waumini), naye akakubali, na Mwenyezi Mungu amhifadhi. Na akafanya baadhi ya maboresho na kuongeza, na inatufurahisha kuyaleta mbele ya ummah ili kunusuru uelewa wa asili na kuchangia katika kutetea utukufu wa ujumbe na nafasi ya unabii na kuwatakasa Mama za Waumini na kuwakosesha fursa wabaguzi wachochezi. Tunataraji radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu naye ni Mbora wa wenye kutarajiwa. Na sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa viumbe.
4
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 4
3/26/2016 12:31:35 PM
Mama wa Waumini
بسم هللا الرحمن الرحيم
UTANGULIZI
H
akika ulimi ndio nyenzo yetu ya kufunguka kwa wengine, katika hisia zao, upole wao na huruma zao. Na katika mahitaji yao na majadiliano yao, na katika kuwalingania wengine yale tunayoyamini. Kama ambavyo ulimi ndio nyenzo ambayo kwayo tunamuomba Mola Wetu na kumlilia na kumtaja. Na ndio nyenzo ambayo inamnyanyua mwandamu kwa Mwenyezi Mungu na kumsaidia kufunguka Kwake na kwa watu: “Kwake hupanda neno zuri na amali njema huinua.” 1
Na katika mwangaza huu, Mwenyezi Mungu Mtukufu ametaka kwa watu wanapozungumza na wengine wayadurusu maneno yao. Na mtu ajue kwamba wenzake wana hisia na mawazo kama ambavyo yeye ana hisia na mawazo, na kwamba watu wanaheshimu nafsi zao kama ambavyo yeye anaiheshimu nafsi yake. Na kwamba wao hawataki yeyote awafanyie ubaya kama ambavyo yeye hataki yeyote amfanyie ubaya. Amesema Mwenyezi Mungu (swt): “Na semeni na watu kwa uzuri.”2 Kwa hiyo ilikuwa ni sifa ya Nabii 2 ambayo ameitilia mkazo Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Kitabu Chake Kitukufu, kwamba alikuwa na ulimi mzuri na moyo wa upole:
1 2
Suratul Fatir: 10 Suratul Baqarah: 83 5
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 5
3/26/2016 12:31:35 PM
Mama wa Waumini
َّفَبِ َما َرحْ َم ٍة ِمنَ ه ۖك َ ِب اَل ْنفَضُّ وا ِم ْن َحوْ ل ِ للاِ لِ ْنتَ لَهُ ْم ۖ َولَوْ ُك ْنتَ فَظًّا َغلِيظَ ْالقَ ْل “Kwa sababu ya rehema itokayo kwa Mwenyezi Mungu umekuwa laini kwao. Lau ungelikuwa mkali mwenye moyo mgumu bila shaka wangelikukimbia.” (Aali Imraan; 3:159).
6
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 6
3/26/2016 12:31:35 PM
Mama wa Waumini
بسم هللا الرحمن الرحيم
KUKATAZA MANENO MABAYA
U
islamu umezingatia maneno mazuri na kuyafanya yawe mazuri zaidi. Na imepokewa kutoka kwa Imamu Ali bin Husein Zainul-Abidin katika haki ya ulimi kwamba: “Ama haki ya ulimi: Ni kuuepusha na khanaa (nayo ni maneno mabaya, magumu na makali) na kuuzoeza katika kheri na kuuadabisha na kuudhibiti isipokuwa kwa ajili ya haja na manufaa ya dini na dunia. Na kuuepusha na ufedhuli mbaya, wenye uchache wa faida, ambao husalimiki na madhara yake na uchache wa faida yake. Na (ulimi) unahesabiwa kuwa ni shahidi wa akili na dalili yake, na anapambika mwenye akili kwa akili. Na uzuri wa mwenendo wa mtu uko katika ulimi wake na hakuna nguvu isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.”3
Katika sentensi hizi Imamu B anatia mkazo katika mambo yafuatayo:
3
a.
Kuulinda ulimi kutokana na mabaya - yaani maneno mabaya – kwa sababu ni katika yanayopelekea kuporomoka kwa mwanadamu na kudharauliwa kwake.
b.
Kuuzoeza ulimi katika maneno ya kheri na ambayo yana manufaa kwa watu na wala hayawadhuru.
c.
Kuulazimisha ulimi kusema kwa adabu na maneno mazuri, ambayo huinuliwa kwenda kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Risalatul- Huquq cha Imamu Ali bin Husein B 7
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 7
3/26/2016 12:31:35 PM
Mama wa Waumini
d.
Kuudhibiti ulimi - yaani kuhifadhi – na kunyamaza isipokuwa katika sehemu ya haja katika mambo ya kidini na kidunia.
e.
Kuuepusha na kuuzuia kutokuingia katika kauli mbaya ambayo haina faida kwake wala haina kheri kwa watu.
Na ni muhimu tujue kwamba mambo mengi katika hatima ya Akhera yanafungamana na harakati za ulimi katika dunia. Na imekuja katika sira ya Nabii 2 kwamba Maadhi bin Jabal alitaka wasia kutoka kwa Mtume 2 basi akamwamuru kuhifadhi ulimi wake, akamrudia tena katika hilo, akasema 2: “Hifadhi ulimi wako, una nini ewe Maadhi, watu watatupiwa motoni kutokana na ndimi zao.”4 Na katika baadhi ya nususi imekuja: “Watu watatupiwa motoni kutokana na matendo ya ndimi zao.”5 Na kwa hiyo tunaona Imamu Ali bin Husein B anatupa picha ya ukaribu ya hatari ya ulimi kupitia msimamo wa viungo kutoka kwake. Anasema kama ilivyo katika hadithi sahihi: “Hakika ulimi wa mwanadamu unaongoza viungo vyake vyote kila asubuhi, unasema: ‘Mmeamkaje?’ Vinasema: ‘Tuko salama maadamu utatuacha.’6 Na vinasema: ‘Allah Allah kwetu.’ Na vinaunasihi kwa kusema: ‘Hakika tutalipwa na kuadhibiwa kwa ajili yako.’”7 Ewe ulimi! Wewe ni siri ya malipo kama utasema maneno ambayo anayapenda Mwenyezi Mungu, na wewe ni siri ya adhabu kama utasema maneno ambayo hayapendi Mwenyezi Mungu. Jamiul-Ahaadith, Juz. 1, uk. 113. Yaani kama utatuacha na wala usilete maneno yanayomchukiza Mwenyezi Mungu au kwa maneno yanayotuchosha na kuhatarisha marejeo yetu, basi sisi tuko salama na mafanikio kwa sababu neno linaweza kukata mkono na kung’oa jicho na linaweza kuuwa mtu kabisa. 6 Sunanu Ibn Maajah, Juz. 2, uk. 1314. 7 Al-Kaafiy, Juz. 2, uk. 115 4
5
8
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 8
3/26/2016 12:31:35 PM
Mama wa Waumini
Na katika mambo ambayo Uislamu unayakataa na unaadhibu kwayo ni maneno mabaya katika kauli na uovu, nayo ni maneno ambayo yanaonewa haya na aibu kama vile maneno ambayo yanawakilisha ubaya na kuwa mbali na adabu na yenye kumdhalilisha mtu mwingine. Na tusikilize yaliyopokewa kutoka kwa Maimamu wa AhlulBayti G kuhusu hilo, na matokeo mabaya ambayo yanapatikana katika maneno mabaya na maovu katika dini na dunia. Kutoka kwa Amirul-Muuminina B amesema: “Alisema Mtume wa Mwenyezi Mungu 2: ‘Hakika Mwenyezi Mungu ameiharamisha pepo kwa kila mwenye maneno mabaya, muovu, mchache wa haya asiyejali aliyoyasema wala aliyoambiwa. Hakika kama utamdadisi hautamkuta isipokuwa mpuuzi au ni mshirika wa shetani.’ Akaambiwa: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu 2 je, katika watu kuna washirika wa shetani? Akasema 2: ‘Je, husomi kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na shirikiana nao katika mali na watoto.’” Amesema B: “Mtu mmoja alimuuliza Fakihi je katika watu kuna asiyejali aliyoambiwa? Akasema: ‘Mwenye kuwashutumu watu naye anajua kwamba wao hawatomwacha, basi huyo ni asiyejali aliyoyasema wala yaliyosemwa.”’8 Na kutoka kwa Imamu al-Baqir B amesema: “Hakika Mwenyezi Mungu anamchukia mwenye maneno mabaya mwenye kufanya uovu.”9 Na kutoka kwa Amru bin Nuuman al-Juufiy amesema: “Abu Abdillah B alikuwa na rafiki asiyeachana naye anapokwenda sehemu. Siku moja wakati alipokuwa anatembea pamoja naye wakiwa sambamba, nyuma yao kulikuwa na kijana mtumishi mwenyeji wa Sindi akitembea pamoja nao. Mtu yule aligeuka nyuma mara tatu akimwangalia kijana wake lakini hakumuona. Alipoangalia mara ya 8 9
Al-Kaafiy, Juz. 2, uk. 323 – 324. Al-Kaafiy Juz. 2, uk. 324. 9
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 9
3/26/2016 12:31:35 PM
Mama wa Waumini
nne akasema: ‘Ewe mtoto wa mzinifu ulikuwa wapi?’ Abu Abdillah B akanyanyua mkono wake akapiga uso wake kisha akasema: ‘Ametakasika Mwenyezi Mungu! Unamtuhumu mama yake?! Nilikuwa nakuona kuwa una uchamungu kumbe hauna uchamungu!’ Akasema: ‘Niwe fidia kwako, hakika mama yake ni mwenyeji wa Sindi mshirikina.’ Akasema B: ‘Je, hujajua kwamba kila umma una ndoa, hebu niondokee.’ Sikumuona akitembea naye hadi mauti yakatenganisha baina yao.”10
Athari Mbaya za Maneno Mabaya: Kutoka kwa Imamu al-Baaqir B amesema: “Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu 2: ‘Hakika maneno mabaya kama yangekuwa ni umbo basi lingekuwa ni umbo baya.”11Na kutoka kwa Imamu asSadiq B amesema: “Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu 2: ‘Hakika waovu miongoni mwa waja wa Mwenyezi Mungu ni ambaye inachukiza kukaa pamoja naye kutokana na ubaya wa maneno yake.’”12 Na kutoka kwake B amesema: “Ubaya unatokana na utovu wa adabu na mtovu wa adabu ataingia motoni.”13 Na kutoka kwake B hakika amesema: “Kulikuwa na mwanaume katika wana wa Israili, alimuomba Mwenyezi Mungu amruzuku mtoto kwa miaka mitatu. Alipoona Mwenyezi Mungu hamjibu akasema: ‘Ewe Mwenyezi Mungu; mimi niko mbali na wewe na hivyo hunisikii, au wewe uko karibu na mimi na hivyo hunijibu?’ Akamjia aliyemjia katika usingizi wake akamwambia: ‘Hakika wewe unamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu tangu miaka mitatu kwa ulimi mchafu, moyo wenye utovu wa adabu usio na uchamungu Al-Kaafiy Juz. 2, uk. 324. Al-Kaafiy Juz. 2, uk. 324. 12 Al-Kaafiy Juz. 2, uk. 320. 13 Al-Kaafiy Juz. 2, uk. 320. 10 11
10
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 10
3/26/2016 12:31:35 PM
Mama wa Waumini
na nia isiyokuwa ya kweli, hivyo ng’oa uchafu wako na moyo wako umuogope Mwenyezi Mungu, na nia yako iwe nzuri.’ Mtu yule akafanya hivyo kisha akamuomba Mwenyezi Mungu. Basi akapata mtoto.”14 Na katika hadithi nyingine imekuja: “Mwenye kumfanyia ubaya ndugu yake Mwislamu, Mwenyezi Mungu anamuondolea baraka ya riziki yake na anamtegemeza katika nafsi yake na anamharibia maisha yake.”15
Nasaha: Imamu Ja’far bin Muhammad as-Sadiq B alikuwa anawahadharisha wafuasi wake kutokana na maneno mabaya yasiyo na mazingatio kwa sababu katika hayo kuna kujiingiza katika matatizo mengi yanayotishia mwenendo mwema katika umma, kwa sababu baadhi ya watu wanaweza kuzungumza maneno ambayo yanaiingiza jamii katika fitina au yanayoiingiza katika vita. Anasema mmoja wa wafuasi wa Imamu as-Sadiq B, naye ni Abu Ali al-Jawaniy: “Nilimuona Abu Abdillahi B akimwambia huria wake anayeitwa Salim na hali ameweka mkono wake juu ya mdomo wake, akasema: ‘Ewe Salim hifadhi ulimi wako utasalimika, na wala usiwabebeshe watu juu ya shingo zetu.’”16 Na kwa hiyo imekuja katika Hadithi sahihi ya Abu Hamza, amesema: “Nilimsikia Abu Ja’far (Muhammad bin Ali B) anasema: ‘Hakika mashia wetu ni wakimya.’”17 Na imekuja katika hadithi ya kweli, Uthman bin Isa amesema: “Nilihudhuria kwa Abu Hasan B, mtu mmoja akamwambia niusie. Akamwambia: ‘Hifadhi uliAl-Kaafiy Juz. 3, uk. 325 - 326 Al-Kaafiy Juz. 2, uk. 326 16 Al-Kaafiy Juz. 2, uk. 113 17 Al-Kaafiy Juz. 2, uk. 113 14 15
11
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 11
3/26/2016 12:31:35 PM
Mama wa Waumini
mi wako utaheshimiwa na wala usiwaruhusu watu wakupelekeshe, utadhalilisha shingo yako.”’18 Unapoishi katika jamii hakika ni wajibu wako katika maneno yako yote utafakari matokeo ya mazuri na mabaya. Na ni juu yetu tubebe jukumu la ambalo tunahusiana nalo na ambaye tunahusiana naye. Tusiseme maneno katika matamanio ya nafsi zetu, au katika hasira zetu, au katika hamasa zetu, bali ni lazima tuseme maneno katika mpangilio wa akili zetu. Kwa sababu akili ndio ambayo inapanga maneno mazuri na mabaya, ya haki na ya batili, ya kheri na ya shari. Imekuja katika Sahih kutoka kwa Ahmad bin Muhammad bin Abi Naswir al- Bazantwiy, amesema: Amesema Abu Hasan Ridhaa B: “Miongoni mwa alama za kujua ni: Upole, elimu na kunyamaza; Hakika kunyamaza ni mlango miongoni mwa milango ya hekima, hakika kunyamaza kunachuma upendo, na hakika ni dalili ya kila kheri.”19 Mwanadamu ambaye anaishi katika zama yake, naye hafahamu mambo ya zama zake, huyo ni mwanadamu anayeishi katika upofu wa akili, na upofu wa roho, na upofu wa harakati katika maisha yake. Na huwenda tatizo kubwa katika wale wanaonekana katika chaneli za runinga za kidini, ingawa hatutuhumu nia zao, kwamba wao wanaishi nje ya zama yao na wanasoma vitabu ambavyo vimetungwa kabla ya karne nyingi, hawasomi hali ambayo jamii yao inaishi hivi sasa.
18 19
Al-Kaafiy Juz. 2, uk. 113 Al-Kaafiy Juz. 2, uk. 113 12
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 12
3/26/2016 12:31:35 PM
Mama wa Waumini
UTUKUFU WA MAMA ZA WAUMINI NI MIONGONI MWA UTUKUFU WETU
K
wa masikitiko makubwa, kuna wengi miongoni mwa ambao wamezoea kulaani na kutukana matukufu ya wengine, na hili ni jambo haramu na lenye kupingwa, kwa sababu linaharibu mshikamano wa jamii ya Kiislamu na kuchochea fitina baina ya Waislamu. Na huwenda baadhi wanazidisha katika kuelekeza laana na dharau kwa baadhi ya vielelezo vya Kiislamu ambavyo ametuamuru Mwenyezi Mungu kuviheshimu, kama vile wake wa Nabii 2 na ambao amesema juu ya haki yao Mwenyezi Mungu Mtukufu: •
ۗ النَّبِ ُّي أَوْ لَ ٰى بِ ْال ُم ْؤ ِمنِينَ ِم ْن أَ ْنفُ ِس ِه ْم ۖ َوأَ ْز َوا ُجهُ أُ َّمهَاتُهُ ْم
“Nabii ni bora kwa waumini kuliko nafsi zao. Na wake zake ni mama zao.”20
Na Aya hii tukufu inaonyesha kwa dalili kubwa na muhimu na ya thamani, sehemu ambayo ameitaka Mwenyezi Mungu kwa wake za Nabii 2 katika ummah wa Kiislamu. Akawafanya ni mama wa waumini wanaume na waumini wanawake. Na kuchagua anwani ya Mama inamaanisha yale yanayopatikana katika maana ya umama miongoni mwa hisia, na yale yanayolazimishwa miongoni mwa wema, heshima na kuwa mbali na uasi. Na sio sahihi kusema kuwa kuwaelezea wake za Nabii 2 kuwa ni Mama wa waumini ilikuwa ni kubainisha uharamu wa kuwaoa tu, hivyo wao (r.a) wako katika daraja la mama ambaye inaharamishwa kumuoa. Na tunaweza kujibu hilo kwamba uharamu wa kuoa wake 20
Suratul-Ahzab; 33:6 13
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 13
3/26/2016 12:31:35 PM
Mama wa Waumini
za Nabii 2 umeshaelezwa kwa ubainifu wake na kwa njia ya wazi katika Aya nyingine, nayo ni kauli yake (swt):
ََّو َما َكانَ لَ ُك ْم أَ ْن تُ ْؤ ُذوا َرسُو َل ه للاِ َو اَل أَ ْن تَ ْن ِكحُوا أَ ْز َوا َجهُ ِم ْن بَ ْع ِد ِه أَبَدًا ۚ إِ َّن َّٰ َذلِ ُك ْم َكانَ ِع ْن َد ه •َظي ًما ِ للاِ ع “Na haiwafalii nyinyi kumuudhi Nabii wa Mwenyezi Mungu wala kuwaoa wake zake kabisa. Hakika hilo ni kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu.”21 Kwa kuongezea kwamba kuunganisha sentensi ‘na wake zake ni mama zao’ katika sentensi ‘Nabii ni bora kwa waumini kuliko nafsi zao’, sentensi ambayo imebeba jukumu la kubainisha nafasi ya Nabii kwa waumini, inatoa uwazi kwamba sentensi ‘na wake zake ni mama zao’ inabainisha nafasi ya wake za Nabii 2 katika ummah.
Amesema Fakihi mkubwa al-Fadhil al-Hindi (aliyefariki mwaka 1137 Hijiria): “Na miongoni mwa utukufu ni kwamba wake zake wamejaaliwa kuwa ni Mama za Waumini kwa tamko la Aya kwa maana ya: Kuharamisha kuwaoa kwa asiyekuwa yeye na kuwaheshimu pia.”22 Na amesema Fakihi mhakiki Sayyid Muhammad Bahrul-Ulumi (aliyefariki mwaka 1326 Hijiria): “Fahamu kwamba mama wako aina tatu: Mama wa nasaba, mama wa kunyonya na mama wa heshima na utukufu, na wao ni wake za Nabii 2, wao ni Mama za Waumini kwa kauli yake (swt): “Nabii ni bora kwa waumini kuliko nafsi zao na wake zake ni mama zao.”23 Na anasema Mwenyezi Mungu (swt) katika Aya nyingine:
ْ َض ْعنَ بِ ْالقَوْ ِل فَي ط َم َع َ يَا نِ َسا َء النَّبِ ِّي لَ ْستُ َّن َكأ َ َح ٍد ِمنَ النِّ َسا ِء ۚ إِ ِن اتَّقَ ْيتُ َّن فَ اَل ت َْخ الَّ ِذي فِي قَ ْلبِ ِه َم َرضٌ َوقُ ْلنَ قَوْ اًل َم ْعرُوفًا
Suratul- Ahzab; 33:53 Kashfu lithaam Juz. 7, uk. 39 . 23 Kwa lugha ya Faqihi Sayid Muhammad Bahrul-Ulumi Juz. 3, uk. 209. 21 22
14
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 14
3/26/2016 12:31:35 PM
Mama wa Waumini
“Enyi wake wa Nabii nyinyi si kama yeyote katika wanawake wengine kama mtamcha Mwenyezi Mungu. Basi msilegeze sauti, asije akaingia tamaa mwenye maradhi ya moyoni mwake. Na semeni maneno mema.” 24
Amesema Sheikh Tusi (aliyefariki mwaka 460 Hijiria): “Hakika amesema ‘kaahadin’ na wala hajasema ‘kawahidatin’; kwa sababu ahadan ni kukataa jumla kwa mwanaume na kwa mwanamke, mtu mmoja na wengi, yaani (nyinyi wake za Mtume) hafanani na nyinyi yeyote katika wanawake katika utukufu wa heshima, na utukufu wa daraja na nafasi yenu kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu 2, kwa sharti tu muogope adhabu ya Mwenyezi Mungu kwa kujiepusha na maasi Yake, na kutekeleza amri Zake. Hakika limewekwa sharti hilo la uchamungu ili wasitegemee uhusiano wao tu, hatimaye wakafanya maasi. Na kama si sharti hili wangehadaika katika maasi, na hilo halijuzu kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.”25 Aya baada ya kuashiria ubora wa hadhi yao na nafasi yao (r.a) kwa wanawake wengine kwa uchamungu imebainisha yale ambayo wao wanawajibika kuyatekeleza. Na miongoni mwayo ni kutolegeza sauti, na kutulizana katika nyumba na kutojiachia, kusimamisha Swala na kutoa Zaka. Na ambalo ni mahususi kwa wake za Nabii 2 katika mambo haya ni jambo la kwanza, yaani ubora wao kwa wanawake wengine waumini unapatikana kwa uchamungu. Ama mambo mengine ni taklifu ya kushirikiana baina ya waumini wote wanawake bila ya umahususi kwao. Na ushahidi juu ya hilo ni ule utajo wa kusimamisha Swala na kutoa Zaka, mambo yaliyothibiti wajibu wake katika haki ya mukalafu wote, uliotajwa kwa dharura wakati wa kueleza katazo la kulegeza sauti. Ikiwa ni pamoja na kutilia mkazo uharamu walioharamishiwa wanawake wote wa sauti nzuri 24 25
Suratul-Ahzab; 33:32 Tibyaanu fiy Tafsir al-Qur’ani, Juz. 8, uk. 338 na tazama: Zubdatu Tafaasir ya Fathullahi al-Kashaaniy Juz. 5, uk. 369. 15
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 15
3/26/2016 12:31:35 PM
Mama wa Waumini
na wa kuifanya iwe nyororo, kutokana na athari zilizomo humo za kuamsha na kuchochea matamanio. Hivyo kuweka sharti la uchamungu haimaanishi kwamba huu ubora ni wa namna ya uchamungu, kwa sababu Aya tukufu imewafadhilisha wake za Nabii 2 kwa wanawake wengine wakiwemo humo wachamungu, na ifahamike katika hilo kwamba nafasi yao ina sharti la uchamungu, nayo ni nafasi ya ubora mahususi kwao kwa hukumu ya kuwa kwao wake za Nabii 2. Na hakuna shaka kwamba Aya tukufu inatoa malezi kwa watu, inawalea katika kuamiliana pamoja na wake za Nabii 2 katika msingi wa nafasi hii ambayo unaipanda katika akili. Katika mantiki hii haijuzu kuwatukana mama za waumini (r.a) hata kama wamekosea, bali tunasema: Ni lazima kuwakirimu kwa kumkirimu Mtume wa Mwenyezi Mungu 2. Na kwa hiyo anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Haiwafalii kumuudhi Mtume wa Mwenyezi Mungu wala kuoa wake zake baada yake kabisa. Hakika hilo ni kubwa mno kwa Mwenyezi Mungu.�26 Na Aya tukufu imeanza kwa maelezo ya jumla ya yale ambayo anaudhika kwayo Mtume wa Mwenyezi Mungu 2, kisha ikafuatiliza kwa maelezo maalumu baada ya jumla, nayo ni kuoa wake zake Mtume2 kwa sababu hilo linakuwa na adha kubwa. Hivyo Mwenyezi Mungu akaharamisha kuoa wake zake 2 baada ya kufariki kwake. Na hii ni katika alama ya Mwenyezi Mungu kumtukuza Mtume wake na kuwajibisha uharamu wake akiwa hai au akifariki. Na kusema ni kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu ni kwa ajili ya kuogopesha na kuhofisha; kwa sababu ni kubwa katika uovu. Na sababu ya kitendo cha Mwislamu kuoa mmoja wa wake za Nabii 2 kuwa ni dhambi kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu, hakika ni kwa kuwa Mwenyezi Mungu amejaalia wake za Nabii 2 ni Mama za 26
Suratul-Ahzab: 53 16
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 16
3/26/2016 12:31:35 PM
Mama wa Waumini
Waumini, na hilo likapelekea kwamba mmoja wa Waislamu kuoa mmoja wao kuwa ni sawa na hukumu ya mtu kumuoa mama yake, na hilo ni kosa kubwa. Sheikh Mufid (aliyefariki mwaka 413 Hijiria) anasema: “Mwenyezi Mungu Mtukufu akabainisha kwamba mmoja kati ya Maswahaba wake kumchumbia mmoja kati ya wake za Nabii wake 2 jambo hilo ni kumkosea adabu na linamuudhi, na kwamba kufunguka kwao mbele yao kunamkera na kumuumiza, hivyo akawahifadhi kwa kumhifadhi na kumlinda yeye, akakataza kujifurahisha na mmoja wao au kumuuliza mmoja wao kitu isipokuwa nyuma ya pazia, na akakataza kukaa katika nyumba yake baada ya kutimiziwa haja miongoni mwa chakula na mengineyo, ili kisirefuke kikao chao humo na hatimaye wake zake wakajiliwaza kwao au wao wakaburudika kwa maneno yao.” 27 Na amesema Twabarisiy (aliyefariki mwaka 548 Hijiria): Yaani sio haki kwenu kumuudhi Mtume wa Mwenyezi Mungu 2 kwa kukhalifu amri zake kwa wake zake wala katika kitu chochote.”28 Na amesema Sheikh Muhammad Jawad Mughuniy (aliyefariki mwaka 1400 Hijiria): “Hukumu hii ni katika umahususi wa Mtukufu Mtume 2 peke yake, kwa sababu wake zake wako katika daraja la mama za waumini.”29Amesema Sayyid Muhammad Shiraziy (aliyefariki mwaka 1422 Hijiria): “’Na haiwafalii nyinyi’ enyi Waislamu ‘Kumuudhi Mtume wa Mwenyezi Mungu 2’ yaani sio haki kwenu kumuudhi kwa kukhalifu amri zake au kukusudia baya kwa wake zake baada ya kufariki kwake. Na huu ni utangulizi na maandalizi ya kauli yake (swt): ‘Na wala msioe wake zake.’ Yaani wake za Mtume 2. ‘Baada yake’ yaani baada ya kufariki kwake, ‘abadani’ hadi mwisho wa umri, wao sio kama wanawake wengine, amTafsirul-Qur’ani al-Majid, ya Sheikh al-Mufid, uk. 421 Majmaul-Bayaan, Juz. 8, uk. 177 29 Tafsir al-Kaashifu, Juz. 6, uk. 236. 27 28
17
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 17
3/26/2016 12:31:35 PM
Mama wa Waumini
bapo inapomalizika eda inajuzu kuwaoa, ‘hakika hilo kwenu’ yaani kuudhi na kuoa wake zake baada ya kufariki kwake ‘ni kubwa kwa Mwenyezi Mungu’ katika dhambi na kuasi.”30 Na amesema Sayyid Muhammad Husein Fadhlullahi (aliyefariki mwaka 1431 Hijiria): “Haiwafalii nyinyi kumuudhi Mtume wa Mwenyezi Mungu 2 katika nafsi yake na ahali zake kwa neno, kuangalia na kitendo. ‘Wala msioe wake zake baada yake abadani.’ Mwenyezi Mungu ameshaharamisha hilo kwa waumini, baada ya kuwafanya wake za Nabii ni Mama za Waumini, hivyo haijuzu kwao kuwaoa mama zao na katika hali ya jumla kwani hilo limehesabiwa ni katika madhambi makubwa mbele ya Mwenyezi Mungu: ‘hakika hilo ni kubwa kwa Mwenyezi Mungu.’ Na katika kauli yake (swt) ‘ni kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu, kuna kuhisisha ubaya wa kufanya mfano wa dhambi hii na ukubwa wake, jambo ambalo linamaanisha kushadidia linalofuata, kushadidia katika kukataza kifikiria, ukiachilia mbali kufanya mfano wa vitendo hivyo. Na katika hayo yote, na hakuna shaka, ni aina ya upambanuzi, umahususi na kumtukuza Nabii 2.31 Na amesema (swt):
ك ُح ْسنُه َُّن إِ اَّل َ َاج َولَوْ أَ ْع َجب َ َاَل يَ ِحلُّ ل ٍ ك النِّ َسا ُء ِم ْن بَ ْع ُد َو اَل أَ ْن تَبَ َّد َل بِ ِه َّن ِم ْن أَ ْز َو َّك ۗ َو َكانَ ه ْ َما َملَ َك للاُ َعلَ ٰى ُكلِّ َش ْي ٍء َرقِيبًا َ ُت يَ ِمين “Hawakuhalalikii wanawake (wengine) baada (ya hawa) wala kubadilisha kwa wake wengine ijapo uzuri wao utakupendeza; isipokuwa uliyemmiliki kwa mkono wako wa kuume. Na Mwenyezi Mungu ni mchungaji wa kila kitu.”32 Taqribul Qur’ani ilaa al-adhihaani Juz. 4, uk. 354 Min wahayi al-Qur’ani Juz. 18, uk. 340 – 341. 32 Suratul- Ahzab; 33:52. 30 22
18
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 18
3/26/2016 12:31:35 PM
Mama wa Waumini
Hakika Aya hii tukufu imemkataza Nabii 2 kubadilisha yeyote katika wake zake, na maana ya hilo ni kwamba ameamriwa kuwabakisha wote katika himaya yake. Na hilo linadhihirisha juu ya Mwenyezi Mungu kuwatukuza wote na kuwaridhia wao kuwa ni wake za Nabii Wake. Amesema Shahidithani (aliyefariki mwaka 965 hijiria): “Kuharamisha kubadilisha wake zake ambao walikuwepo kwake wakati wa kushuka aya hii ‘hawakuhalalikii wanawake baada ya hawa wala kubadili yeyote kati ya wanawake ijapo uzuri wao utakuvutia,’”33 vilevile inachukiza kuongeza juu yao. Inasemwa kwamba: Hiyo ilikuwa ni kuwalipa kwa uzuri wa kitendo chao pamoja naye, ambapo aliamriwa kuwapa hiyari ya wao kuachana naye au kuishi pamoja naye katika dhiki ya kidunia, wakamchagua Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na makazi ya Akhera.”34 Na amesema al-Fadhil al-Hindiy (aliyefariki mwaka 1137 Hijiria): “Na kuharamisha kubadili wake zake kwa kauli Yake (swt): ‘Wala usimbadilishe yeyote’ ni kuthibitisha kwamba wao wamemchagua yeye na makazi ya Akhera.”35 Na amesema Sheikh Muhammad Jawad Mughuniy (aliyefariki mwaka 1400 Hijiria): “Baada ya kuhalalisha Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa Nabii Wake aina za wanawake kama ilivyotangulia kuashiriwa, amewajibisha juu yake katika Aya hii kutosheka na ambao wako katika himaya yake, na walikuwa tisa na akaharamisha kwake kumtaliki yeyote miongoni mwao, na kuoa mke mwingine mahala pake japokuwa atamvutia. Na hayo ni malipo kwa wanawake wa Nabii kwa uzuri wa muamala wao pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu, na kumchagua kwao Mwenyezi Mungu na Mtume Suratul-Ahzab; 33:52. Masailiki al-Afuhaam, Juz. 7, uk. 73. 35 Kashifu Lithaami Juz. 8, Uk. 26 33 34
19
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 19
3/26/2016 12:31:35 PM
Mama wa Waumini
Wake 2 pale alipowapa hiyari baina ya talaka au kuvumilia katika dhiki pamoja na Mtume 2.”36 Na amesema Sheikh Nasir Makarimu Shiraziy: “Dhahiri ya maneno ‘baada’ ni kwamba kuoa ni haramu kwako baada ya haya. Na kwa kujengea juu ya haya hakika ‘baada’ ama inamaanisha ‘baada’, yaani usioe tena mke baada ya muda huu, au makusudio ni kwamba hakika wewe baada ya kuwapa hiyari wake zako, baina ya kubakia pamoja nawe na kuishi maisha mepesi katika nyumba yako, na ama kuondoka kwao, na wamekwishachagua kubaki pamoja na wewe kwa mapenzi yao, basi haipasi kuoa baada yao mwanamke mwingine. Na vivyo hivyo haiyumkini kwako kuacha baadhi yao na kuchagua mahala pao wake wengine. Na kwa maneno mengine usiongeze katika idadi yao wala usibadilishe waliopo miongoni mwao.”37 Aya hizi tukufu zinatengeneza msingi wa Qur’ani ili kuwatukuza Mama za Waumini (r.a) na yanayopatikana katika hayo miongoni mwa wajibu wa kuwaheshimu na kuhifadhi heshima yao ukiachilia mbali uharamu wa kuwatukana au kuwatuhumu. Amesema Sayyid Muhammad Baqir Hujatul-Islaam38 katika diwani yake: “Ewe mwekundu kukutukana ni haramu, kwa ajili ya jicho macho elfu moja yanaheshimiwa.” Aliulizwa Sayid Muhammad Husein Fadhlullahi swali hili: “Nini msimamo wenu katika kuwatukana Maswahaba M akiwemo Abu Bakri, Umar na Aisha?” Akajibu (r.m): “Mimi binafsi naharamisha kumtukana Swababa yeyote kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu amezungumzia juu ya Maswahaba kwa kauli Yake: Tafsir al-Mubiin uk. 558. Al-Amthal fiy Tafsiri al-Qur’ani, Juz. 13, uk. 321. 38 Faqihi Imamiy miongoni mwa wanafunzi wa Sheikh Ja’far Kaashif al-Ghitwaa aliyefariki 1260 Hijiria. 36 37
20
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 20
3/26/2016 12:31:36 PM
Mama wa Waumini
َُّم َح َّم ٌد َرسُو ُل ه ار ُر َح َما ُء بَ ْينَهُ ْم ۖ تَ َراهُ ْم ُر َّكعًا ِ َّللاِ ۚ َوالَّ ِذينَ َم َعهُ أَ ِش َّدا ُء َعلَى ْال ُكف َُّس َّجدًا يَ ْبتَ ُغونَ فَضْ اًل ِمنَ ه ۖ للاِ َو ِرضْ َوانًا “Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na walio pamoja naye wana nguvu mbele ya makafiri, na wanahurumiana wao kwa wao, utawaona wakirukuu na kusujudu wakitafu fadhila na radhi za Mwenyezi Mungu.’39
Hata kama tuna rai katika mas’ala ya uimamu na ukhalifa, lakini katika mas’ala ya kutukana nilishasema kwamba hii inaharamishwa kwa kila Mwislamu, na mimi naandika hili katika fatwa inayonijia, kwamba inaharamishwa kutukana Swahaba yeyote wakiwemo Makhalifa M. Na mimi nanukuu neno kutoka kwa Imamu Ali B alipokuwa njiani kwenda Swifin na akawasikia watu miongoni mwa watu wa Iraki wanawatukana watu wa Sham akawaambia: “Hakika mimi nachukia kwenu kuwa ni watukanaji, lakini nyinyi kama mngeelezea vitendo vyao na mkataja hali zao ingekuwa ni sahihi zaidi katika kauli na ingekuwa ni udhuru unaofaa. Na mkasema mahala pa kuwatukana: Ewe Mwenyezi Mungu hifadhi damu zetu na damu zao, na tengeneza baina yetu na baina yao na waongoze kutokana na upotovu wao ili wajue haki katika ujahili wao, na wajizuie kutokana na uovu na uadui katika maneno.” Na tamko hili lipo katika NahjulBalaghah. Na katika nyanja hii napenda kuzungumzia kuhusu njia ya Imam Ali B katika kuamiliana kwake pamoja na Makhalifa M ambao Shia wanaitakidi kwamba wao ndio ambao walimnyang’anya haki yake, katika barua yake kwa watu wa Misri alisema: “Sikufadhaishwa isipokuwa na kumiminika watu kwa Abu Bakri K wakimpa kiapo cha utiifu. Niliuzuia mkono wangu mpaka pale nilipoona kurejea kwa watu kwenye ukafiri wakiwa mbali na Uislamu, wakiwa wanalingania kuifuta dini ya Muhammad 2. Niliogopa kama sitonusuru 39
Suratul-Fath; 48:29. 21
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 21
3/26/2016 12:31:36 PM
Mama wa Waumini
Uislamu na watu wake kwa kuona dosari humo au mmong’onyoko juu yangu, itakuwa ni msiba mkubwa zaidi kuliko kuukosa ukhalifa wenu ambao ni starehe ya siku chache. Hutoweka kilichokuwa kama yanavyotoweka mazigazi au kama yanavyotawanyika mawingu. Nikasimama katika matukio yale mpaka batili ilitoweka na kuyeyuka, na dini kubaki katika amani na salama.” Kwa hiyo sisi tunaamiliana pamoja na Makhalifa M katika mas’ala ya ukhalifa kama alivyoamiliana Imamu Ali bin Abutalib B ambaye alikuwa ni mwenye kufunguka kwao na alikuwa anawasaidia na anawashauri kwa kila lenye maslahi kwao. Na kuna hadithi kutoka kwa Imam Ja’far as-Sadiq B humo anawahutubia baadhi ya Waislamu Shia: “Ni mepesi yaliyoje yale waliyoyaridhia watu kwenu. Zuieni ndimi zenu kwao.” Ama Mama za Waumini, sisi tunaharamisha kuwatukana na tunasema kwamba ni lazima kuwakirimu kwa kumkirimu Mtume wa Mwenyezi Mungu 2, hivyo sisi tunaharamisha kuwatukana Mama za Waumini na kuwakosea adabu, kama ambavyo tunaharamisha kutukana Maswahaba M na tumekwishatoa fatwa katika hilo na imekwishaenea katika ulimwengu.”40
40
JaridatuI-Kaadhi la 28 Swafar 1429 Hijiria sawa na 6/3/ 2008 22
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 22
3/26/2016 12:31:36 PM
Mama wa Waumini
VITA VYA NGAMIA NA YALIYOFUATIA MIONGONI MWA VITA VYA MANENO:
H
akika kila mtu isipokuwa maasum anakabiliwa na kukosea na kujadiliwa hata kama mkosaji ni mke wa Nabii 2, lakini inapasa kudokeza hapa kwamba kuthibitisha kosa la baadhi ya misimamo ya wake wa Nabii ni jambo moja na kuwadharau, kuwakosea adabu na kutowaheshimu ni jambo jingine, ambapo hakuna mafungamano baina yake. Ama katika yanayohusiana na kosa la mama wa waumini Aisha O kuhusu kutoka kwake katika vita vya Jamal, amekwishataja Sheikh Nasirudini Albani (aliyefariki mwaka 1420 Hijiria) baada ya kujadili hadithi ya Hauab: “Nani kati yenu atabwekewa na mbwa wa Hauab,” kwamba hadithi hii sanadi yake ni sahihi na hakuna tatizo katika matamko yake, na akasema: “Na hitimisho la maneno ni kwamba hakika sanadi ya hadithi ni sahihi na hakuna tatizo katika matini yake kinyume na dhana ya Ustadh alAfghaaniy. Hakika lengo la yaliyomo humo ni kwamba Aisha O alipoijua Hauab, ilikuwa ni juu yake kurejea! Na hadithi inaonyesha kwamba hakurejea! Na haya ni ambayo hayapasi kunasibishwa kwa Mama wa waumini Aisha O. Na jawabu letu katika hilo ni kwamba sio yote yanayotokea miongoni mwa ukamilifu yananasibiana nao, ambapo hakuna umaasumu isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu peke Yake. Na Sunni haipasi kwake kuchupa mpaka kwa anayemheshimu hadi kumnyanyua katika daraja ya Maimamu masumina wa Kishia! Na hakuna shaka kwamba kutoka kwa Bibi Aisha ilikuwa ni kosa katika asili na kwa hiyo alitaka kurejea alipojua kutimia kwa utabiri wa Nabii 2 – katika Hauab – lakini Zuberi K alimkinaisha asirejee kwa kauli yake: “huwenda Mwenyezi Mungu atasuluhisha 23
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 23
3/26/2016 12:31:36 PM
Mama wa Waumini
kupitia kwako baina ya watu.” Na hatuna shaka kwamba alikosea katika hilo vilevile. Na akili inahukumu bila ya shaka kwamba hakuna njia katika kusema kwamba moja ya pande mbili zilizopigana ilikosea, ambapo humo kulitokea mamia ya waliouliwa, na hakuna shaka kwamba Bibi Aisha O ndiye aliyekosea kwa sababu nyingi na dalili zilizo wazi na miongoni mwazo ni kujutia kwenda kwake vitani. Na Bibi Aisha O alidhihirisha kujuta kwake kama alivyopokea Ibn Abdul-Bar katika kitabu al-Istiaab, kutoka kwa Abu Bakri Atiiq - naye ni Abdullahi bin Muhammad bin Abdu Rahman bin Abu Bakri as-Sidiq amesema: Bibi Aisha alimwambia Ibn Umar: Ewe baba Abdurahman, nini kilikukataza kunizuia katika kutoka kwangu? Akasema: Niliona mwanaume ameshakushinda – yaani Zuber. – Akasema: Ama Wallahi kama ungenikataza nisingetoka.” Albani ameendelea mpaka aliposema: “Na amesema vilevile Ismail bin Abi Khalid kutoka kwa Qais, amesema: Alisema Aisha na alikuwa anaizuia nafsi yake isizikwe katika nyumba yake, akasema: ‘Hakika mimi nimezua jambo baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, nizikeni pamoja na wake zake.’ Na hivyo alizikwa Baqii. Nasema: tukio analomaanisha ni kwenda kwake katika Vita vya Ngamia. Hakika yeye alijutia hilo na akatubia kutokana na hilo.”41 Yamemalizika maneno ya Albani. Na tumenukuu maneno ya Albani kwa kirefu ili tujue kwamba aliyoyafanya Mama wa waumini Aisha O katika uamuzi wake wa kwenda katika vita na kutoka kwake kwenda Basra ni uamuzi wa makosa na ni wenye kuangamiza. Na sisi hapa hatuhukumu nia, na kuzungumzia tusiyoyajua. Katika kuelezea balaa ya vita hivi, wanahistoria wametaja lile alilopokea Tabariy na wengineo kutoka kwao, kwamba wao wamesema: “Siku ya vita vya Ngamia tulirushiana mishale hadi ikamalizika 41
Silsilatu al-Hadiithi Sahiha Juz. 1, uk. 767-775 hadithi ya 474. 24
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 24
3/26/2016 12:31:36 PM
Mama wa Waumini
na tulipigana kwa mikuki hadi ikaingia katika vifua vyetu na vifua vyao, hadi kama angerushwa farasi basi angeruka.” Na baadhi yao walisema: “Sikupita katika nyumba ya Walid katu isipokuwa nilikumbuka vita vyao pindi nisikiapo sauti za waimbaji wakipiga ngoma ndani ya nyumba yake.”42 Na ilikuwa ni lazima kutokana na hayo, Waislamu wafarikiane na kugawanyika katika makundi na madhehebu. Hivyo wakawa ni Alawiya, Uthmaniya, Khawariji, Bakriy na mengineyo yasiyokuwa hayo miongoni mwa makundi yenye kuhasimiana. Wakati mwingine baina yao vinapiganwa vita vya umwagaji damu, na mara nyingine vita vya maneno.43 Na ni juu yetu tusimame kidogo hapo ili kueleza rai za madhehebu za Kiislamu katika mas’ala haya. Rai ya Makhawariji: Makhawariji wamesema: Hakika Aisha, Twalha na Zuberi walikufuru kwa kumpiga vita kwao Ali. Na wakasema: Hakika Ali siku hizo alikuwa katika haki lakini yeye alikufuru baada ya tukio la mahakimu wawili.44 Na wakamlaani Ali kwa kuacha kuchukua ngawira ya mali zao na kuwateka watoto wao na wake zao.45 Rai ya Muutazilah: Limesema kundi katika Muutazila kwamba makundi yote mawili ya watu wa vita vya Ngamia ni mafasiki, na kwamba wao ni wenye Tarikhu Twabariy Juz. 5, uk. 218; al-Uqud al-Farid, Juz. 4, uk. 32, na ( Darul-Walid) ni sehemu ya Basra humo walikuwa wanakutana wafua nguo na mikuki yake. 43 Al-Uthmaniya ya al-Jahidh uk. 155 – 250, na Naqid al-Uthmaniya ni ya Abu Ja’far alAskaafiy katika Sharih Nahjul- Balaghah Juz. 2, uk. 159. 44 Tabswiru uk. 41; al-Milal wa Nihali cha Shaharstaniy Juz. 1, uk. 185 na al-Faswil Baina al-Milal wa Nihali ya Ibnu Hazim Juz. 4, uk. 153, na al-Firaq Baina al-Fariq cha alBaghidaadiy uk. 55 - 56 45 Al-Milalu wa Nihal Juz. 1, uk. 176, Tabswira uk. 27, na al-Furaq Baina al-Firaq uk. 58 42
25
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 25
3/26/2016 12:31:36 PM
Mama wa Waumini
kudumu katika moto.46 Na wengine miongoni mwao wamesema: Hakika moja ya makundi mawili ni fasiki na wala hakuna shaka, na daraja ya chini kabisa ya makundi mawili haya ni kutokukubaliwa ushahidi wake.47 Na kwamba kama wangeshuhudia wote juu fungu la mbogamboga, basi usingekubaliwa 48ushahidi wao. Na limesema kundi la tatu miongoni mwao: Watu wote wa vita vya Ngamia ni wenye kuangamia isipokuwa yule ambaye imethibiti kutubia kwake, na vile vile Twalha na Zuberi. Ama Aisha hakika yeye alikiri kosa kwa Ali siku ya vita vya Ngamia na akamuomba msamaha.49 Na amepokea al-Jahidh kutoka kwa baadhi ya Masalafi kwamba: Hakika walikuwa wanapokumbuka siku ya vita vya Ngamia husema: “Wameangamia wafuasi na wamefaulu viongozi.�50 Rai ya Ashairah: Na wamesema wengi miongoni mwa Ashairah: Hakika watu wa vita vya Ngamia walikosea, lakini ni kosa linalosameheka, kama vile kosa la mwenye kujitahidi katika baadhi ya mambo ya matawi na wala hailazimu kwake kukufuru, ufasiki, kujiepusha naye wala uadui.51 Na wamesema baadhi yao: Hakika Aisha na Twalha walitubia kosa.52 Tabswira uk. 42, kutoka kwa Amru bin Ubaid. Al-Milalu wa Nahal Juz. 1, uk. 65 kutoka kwa Waaswil bin Atwai, na al-Faswil Juz. 4, uk. 153 na Tabswira uk. 51 48 Tabswira uk. 41, Lubaab uk. 152, Na Amru bin Ubaid al-Muutaziliy al-Baswariy na alikuwa ni Qadiriya, na anasema kwamba kama wangeshuhudia Ali, Twalha na Zubri katika jambo, hautokubaliwa ushahidi wao. 49 Sharih Nahjul-Balaghah, Juz. 3 uk. 396 na katika Juz. 2, uk. 448 anaashiria ishara ya haraka katika hayo. 50 Al-Uthamiya, uk. 246. 51 Sharhi Nahjul- Balaghah Juz. 3, uk. 266 52 Tabswira uk. 41 46 47
26
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 26
3/26/2016 12:31:36 PM
Mama wa Waumini
Na wamesema wasiokuwa wao: Hakika wao walifanya ijitihadi na hivyo hakuna kosa juu yao na wala hatuhukumu katika kukosea kwao na juu ya kosa la Ali na wafuasi wake.53 Msimamo wa Imam Ali B: Hakika kauli njema na nzuri kwa mama wa waumni Aisha O ni ambayo aliisema juu yake Imamu Ali B, ambapo alisema: “Mwenye kuweza wakati huo kuifunga nafsi yake kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na afanye hivyo. Na kama mtanitii hakika mimi kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu nitawachukueni kwenye njia ya peponi, japo kwamba ni njia ya matatizo sana na yenye ladha chungu. Ama kuhusu fulani (bibi Aisha) ameshikwa na rai ya kike na kijicho kinatokota kifuani mwake kama jiko (tanuri) la mfua chuma. Lau angeambiwa amfanyie kebihi mtu mwingine kwa kiwango alichonifanyia asingefanya. Naye bado kwangu mimi ana heshima yake ya mwanzo na hesabu (yake) ni kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.”54 Nini Maana ya Heshima Yake ya Mwanzo? Sidhani kwamba Imamu B alikusudia isipokuwa ni kwamba yeye ni mke wa Nabii 2 na kwamba yeye ni mama wa waumini. Na kwa sababu hii alisema katika hotuba nyingine: “Walitoka wakiikokota heshima ya Mtume wa Mwenyezi Mungu 2 kama anavyokokotwa kijakazi wakati anaponunuliwa, wakaelekea naye Basra wakaacha wake zao katika nyumba zao na wakamtoa nje mke wa Mtume wa Mwenyezi Mungu 2 kwa ajili yao na kwa wasiokuwa wao.”55 Ali B amemwita heshima ya Mtume wa Mwenyezi Mungu 2 na heshima ni sehemu ambayo inaharamishwa kuisogelea na kuiAl-Milalu wa Nihal, Juz. 1, uk. 144 na al-Faswil Juz. 4, uk. 153. Nahjul- Balaghah, hotuba ya 154 55 Nahjul-Balghah, hotuba ya 172 53 54
27
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 27
3/26/2016 12:31:36 PM
Mama wa Waumini
karibia, na kwamba yeye bado angali ni mke wa Mtume 2 hata baada ya kufariki kwake. Na Imamu B anaamiliana kulingana na matamko ya Kitabu na Sunnah, je, inajuzu kurefusha ulimi humo, kumtukana, kumpuuza na kumtuhumu? Kisha Amirul-Muuminina alikwenda kwake yeye binafsi hadi akasimama mbele yake na akapiga haudaji kwa fimbo na akasema: Ewe chekundu! Je, Mtume wa Mwenyezi Mungu 2 alikuamuru hili la kutoka dhidi yangu? Je, hajakuamuru kutulizana katika nyumba yako? Wallahi hawajakutendea haki wale waliokutoa katika nyumba yako, ambapo wao waliwahifadhi wake zao na wakakutoa wewe.� Kisha hakika yeye B alimwamuru ndugu yake Muhammad ampeleke katika nyumba ya Amina binti al-Harith Ibn Twalha al-Twalahatiy.�56
56
Waaqitu al-Jamali, Dhwamin bin Shaqan al-Madsaniy uk. 136, Kifayatu al-Athari cha Khazaaz uk. 181 28
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 28
3/26/2016 12:31:36 PM
Mama wa Waumini
UTUKUFU WA MAMA ZA WAUMINI NA USAFI WAO
M
aulamaa wa Kishia wamekataza kabisa tuhuma yoyote ya uchafu inayomgusa mke yeyote kati ya wake za Manabii, sasa itakuaje kuhusu wake wa hitimisho la Mitume 2? Anasema Sharifu al-Murtadhaa (r.m) - baada ya kunukuu rai ya baadhi ya wafasiri kwamba, hakika makusudio ya hiyana ni hiyana inayohusiana na zinaa na maovu, yeye amesema: “Na kwa hakika Manabii E ni wajibu watakaswe na mfano wa hali hii; kwa sababu inaaibisha, inafedhehesha na kuwashushia hadhi, na Mwenyezi Mungu amewaepusha Manabii wake E na ambayo ni madogo zaidi kuliko hayo, kwa kuwatukuza na kuwaheshimu, na kupinga kila kinachowafanya wasikubalike.”57 Na amesema Sheikh Tusi (r.m) katika Tafsiir yake: “Na hakuwahi kuzini mke yeyote wa Nabii katu, kutokana na yaliyomo katika tendo hilo ikiwa ni pamoja na kuwakimbiza watu kwa Mtume. Kwa hiyo yeyote anayenasibisha zinaa kwa wake wa Nabii basi ameshakosea kosa kubwa sana.”58 Na amesema Sheikh Tabarasiy katika kisa cha mtoto wa Nuhu B: “Hakika hakuwa ni mtoto wake halisi bali amezaliwa katika kitanda chake. Amesema B: Hakika yeye ni mtoto wangu katika dhahiri ya mambo, Mwenyezi Mungu akamfahamisha kwamba mambo ni kinyume na dhahiri na akamtanabahisha juu ya hiyana ya mke wake, hii ni kutoka kwa Hasan na Mujahidi. Na mtazamo huu uko mbali ambapo humo kuna yanayopinga Qur’ani kwa sababu Mwenyezi 57 58
Tanuwihil-Anbiyai uk. 44 Tibiyaanu fiy Tafsiril-Qur’ani, Juz. 1, uk. 52 katika maelezo ya aya 10 ya Surati Taharim. 29
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 29
3/26/2016 12:31:36 PM
Mama wa Waumini
Mungu Mtukufu anasema: “Na Nuhu akamwita mtoto wake.”59 Bali ni kwa sababu Manabii ni wajibu watakaswe kutokana na hali hii, kwa sababu ni aibu na dosari, na Mwenyezi Mungu ameshawatakasa Manabii Wake na yaliyo duni kuliko hayo, kwa kuwaheshimu na kuwatukuza kutokana na yanayopelekea wasikubalike.”60 Na amesema katika Aya ya uzushi katika kauli yake (swt): “Msiidhanie kuwa ni shari kwenu bali ni kheri kwenu.” Yaani msidhani huzuni ya uzushi kuwa ni shari kwenu bali ni kheri kwenu, kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu anamuondolea Aisha O hatia na kumlipa kwa subira yake na kuvumilia kwake na kuwalazimu watu wa uzushi kwa yale waliyostahiki katika dhambi ambayo wameifanya katika jambo lake.”61 Na amesema Sheikh Muhamaad Swalih al-Mazandaraaniy (aliyefariki mwaka 1081 Hijiria): “Na makusudio ya hiyana sio uasherati na zinaa; ambapo hajazini katu mke wa Nabii.”62 Na amesema Sayyid Abdul-Husein Sharafudin (aliyefariki mwaka 1377 Hijiria): “Miongoni mwa pande alizotegemea Musa Jarullahu katika kuwakufurisha Shia Imamiya: Ni kwamba ‘wao wanamsema vibaya Aisha O na wanazungumza juu ya haki yake katika jambo la uzushi yasiyofaa katika heshima yake,’ hadi mwisho wa uongo na uzushi wake. Jawabu ni kwamba: Hakika yeye (Aisha) kwa Shia Imamiya katika jambo lilelile ni msafi, twahara na heshima ya hali ya juu. Amehifadhika na ana daraja ya juu, ametukuzwa na ana nafasi ya juu kuliko kutenda kisichokuwa usafi. Na haiwezekani katika haki yake isipokuwa heshima na kuhifadhika. Na vitabu vya Suratu Hud: 11 Majimaul-Bayaan fiy Tafsiri al-Qur’an Juz. 5, uk. 310- 316 katika maelezo ya aya ya 10 katika suratu Taharim. 61 Majimaul-Bayaan fiy Tafsiri al-Qur’an Juz. 7 Uk. 230 katika maelezo ya aya ya 11 katika Sura Nuur. 62 Sharih Usulu al-Kafiy Juz. 10, uk. 107 59 60
30
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 30
3/26/2016 12:31:36 PM
Mama wa Waumini
Shia Imamiya vya zamani na vya sasa ni ushahidi mwadilifu kwa ninayoyasema: Kwamba Msingi wao katika umaasumu wa Manabii unazuia kabisa waliyoyasema watu wa uzushi, na kanuni zao zinazuia kutokea kwake kiakili, na hivyo amesema Fakihi wa Ummah na mwaminifu wake Ustadhi wetu mtukufu Sheikh Muhammad Twaha an-Najafiy,63 Mwenyezi Mungu amtukuze, akiwa katika mimbari ya kufundishia kwamba, ni wajibu atakaswe kutokana na malengo ya uzushi, kwa kufanyia kazi ambayo yako huru katika hukumu ya akili miongoni mwa wajibu wa kuwatakasa Manabii na dosari ndogo. Na ulazima wa kutakasa heshinma yao kutokana na kosa dogo kabisa. Hivyo sisi Wallahi hatuhitaji dalili katika kumtoa hatiani, wala haturuhusu juu yake wala kwa asiyekuwa yeye miongoni mwa wake za Manabaii na Mawasii yote yaliyo katika aina hii.”64 Na amesema Sheikh Muhmaad Jawad Mughuniya (aliyefariki mwaka 1400 Hijiria): “Hakika Waislamu wanaitakidi kwamba hajazini mke yeyote wa Nabii katu.”65 Na amesema Sheikh Nasir Makarimu Shiraziy – katika kisa cha mke wa Nuhu na mke wa Luti: “Na kwa vyovyote vile hakika hawa wake wawili waliwafanyia hiyana heikh Muhammad Twaha bin Sheikh Mahdiy Najaf. Alizaliwa mwaka 1241 hijiria kaS tika mji wa Najaf tukufu, alikuwa na elimu pana katika elimu ya dini na fasihi. Mwenye maarifa mapana katika historia, lugha, hekima na mashairi ya Waarabu n.k. Isipokuwa alikuwa juu zaidi katika Fiqihi na Usuli, Hadith, Ilimu rijali, na akabobea kwayo na akahesabiwa katika safu ya wajuzi wa zama zake na watambuzi. Alisoma kwa Sheikh Murtadhaa al-Answaariy, Sheikh Jawadi Najaf, Sayid Husein al-Kuhu Kumariy na wengineo. Miongoni mwa wanafunzi wake ni: Sayid Abdul-Husein Sharafu Dyin al-Musawiy al-Amiliy, Sheikh Muhammad Muhsin al-Maarufu kwa jina la Aghaa Buzurghi Twaharaaniy, Sheikh Hasan mtoto wa mwenye Jawahiri, Sheikh Murtadhaa Kaashifu alGhitwaa, Sheikh Haadi Kaashifu al-Ghitwaa, Sayid Muhammad Said al-Habubiy, Sayid Muhsin al-Amin al-Amiliy, Sheikh Abdul-Husein al-Baghidaadiy, Sheikh Muhammad Jawad al-Balaghiy, Sayid Ridhwa al-Hindiy, Sayyid Swalih al-Hilliy, Sayyidi Mahdiy al-Hakim, Sheikh Husein Mughuniya, Sayyid Hasan Swadir na wengineo. Alijulikana kwa uchamungu, wema, zuhudi, ibada, tabia njema, unyenyekevu, nia nzuri na usafi wa moyo. Alifariki mwaka 1323 Hijiria. 64 Al-Fusulu al-Muhimamatu fiy Taalifi al-Ummati uk. 156. 65 Tafsiru al-Kaashif Juz. 7, uk. 268 63
31
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 31
3/26/2016 12:31:36 PM
Mama wa Waumini
Manabii wawili watukufu kati ya manabii wa Mwenyezi Mungu. Na hiyana hapa haimaanishi kupotoka katika njia kuu ya heshima na usafi, kwa sababu wao ni wake za Manabi wawili, na wala haiwezekani mke wa Nabii kufanya hiyana kwa maana hii ya hiyana. Imekuja kutoka kwa Mtume 2: “Hajazini mke yeyote wa Nabii katu.”66 Na amesema Sayyid Muhammad Husein Fadhlullahi (aliyefariki mwaka 1431 Hijiria):
َّب ه وط ۖ َكانَتَا تَحْ تَ َع ْب َدي ِْن ِم ْن ٍ ُوح َوا ْم َرأَتَ ل َ ض َر َ ٍ ُللاُ َمثَ اًل لِلَّ ِذينَ َكفَرُوا ا ْم َرأَتَ ن صالِ َحي ِْن َ ِعبَا ِدنَا “Mwenyezi Mungu amepiga mfano wa ambao wamekufuru, mke wa Nuhu na mke wa Luti, walikuwa chini ya waja wetu wawili kati ya waja wetu wema.67 Walikuwa ni wake wawili wa Manabii wawili kati ya Manabii wa Mwenyezi Mungu nao ni Nuhu na Luti E, wakawafanyia hiyana katika misimamo yao dhidi ya ujumbe, ambapo walifuata kaumu yao katika ukafiri na hawakuenda sambamba na mazingira ya nafasi yao ya wake za Manabii, ambayo inawalazimisha kuwa kati ya waumini wa mwanzo wa ujumbe, kwa sababu wao wanajua kutokana na msimamo wa waume zao, amana yao, ukweli wao na juhudi yao, yale wasiyoyajua wengine.
Hivyo haubakii kwao udhuru wowote katika kupotoka katika njia ya ujumbe wa Mtume, lakini tatizo ni kwamba wao hawakuwa makini katika mas’ala ya kufuata kiimani na kushikamana kivitendo. Hawakuangalia mas’ala kwa mtazamo wa kuwajibika, bali waliishi katika hali ya kasumba ambayo inawafungamanisha na mila ya kaumu yao. Hivyo wakawa wanatoa siri za Manabii, jambo ambalo linaweza kuharibu maslahi ya ujumbe na Mtume. Na katika nyenendo zao walikuwa mbali na mantiki ya misingi ya kiroho ya kiimani 66 67
Al-Athal fiy Tafsir al-Qur’an, Juz. 18, uk. 294. Suratu Tahrim: 10 32
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 32
3/26/2016 12:31:36 PM
Mama wa Waumini
kwa kubakia katika mantiki ya kipagani ambayo inafanya nyumba ya ndoa ya unabii kuzunguka katika duara la kijahilia sambamba na duara la imani. Na huenda upotovu wa mtoto wa Nuhu ulikuwa unatokana na kuathirika na mama yake na inasemwa: Hakika mke wa Luti alikuwa anawapa habari kaumu yake juu ya wageni ambao wanamtembelea mume wake ili wafanye uadui dhidi yao, hivyo hiyana yao ilikuwa katika msimamo na nafasi.”68 Na kwa hiyo amesema mfasiri mkubwa Sayyid Muhmammad Husein Tabatabaiy (aliyefariki mwaka 1402 Hijiria) katika tafsiri ya kauli yake (swt): ‘Mambo ya uhabithi ni ya mahabithi, na mahabithi ni wa mambo ya uhabithi. Na mema ni ya walio wema na walio wema ni wa mema.’ 69 Tunasema: Hakika kupenya uasherati kwa mke wa Nabii kunazikimbiza nyoyo mbali na yeye, hivyo ni wajibu Mwenyezi Mungu kutakasa upande wa wake za Manabii kutokana na uchafu wa zinaa na uasherati, vinginevyo daawa ingechafuka. Na inathibiti kwa hoja hii ya kiakili heshima yao ya kiuhalisia, na sio kwa dhahiri tu, Nabii 2 anajua zaidi hoja hii kuliko sisi, namna gani inajuzu kwake kuingiwa na shaka katika jambo la mke wake kwa kutuhumiwa na mwenye kutuhumu au kusambaa uzushi.”70 Na kwa kufafanua maneno yake (r.m) anasema: Hakika kauli ya kufanya uasherati wake za Nabii 2 – sawa iwe kwa kuzini au njia nyingine – ni kati ya mambo ambayo yanakimbiza nyoyo za watu kutoka kwa Nabii Mtukufu 2, hivyo ni wajibu – katika hekima ya kiungu – Mwenyezi Mungu kuutakasa upande wa wake wote wa Manabii kutokana na uchafu wa zinaa na uasherati, bali kwa kila ambalo linagusa heshima ya wake za Manabii. Na kama Mwenyezi Mungu asingefanya hivyo, daawa ya kiungu ingekuwa ni upuuzi na mchezo. Na inathibiti – kwa hoja hii ya kiakili – utukufu wao kwa Min Wahyi al-Qur’an, Juz. 22, uk. 328 – 329. Suratu Nur: 26 70 Mizanul-Hikimati fiy Tafsir Qur’an, Juz. 15, uk. 103 68 69
33
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 33
3/26/2016 12:31:36 PM
Mama wa Waumini
dhahiri na kwa uhalisia, na hakuna shaka kwamba Nabii 2 anajua zaidi hoja hii kuliko sisi, na ametakasika 2 hawezi kuwa na shaka na mke wake. Na vilevile tunasoma kuhusu mwanachuoni kati ya maulamaa wetu wa karne ya tano hijiria, kwamba aliandika kitabu kuhusu jambo hili na akakiita Tanziihi Aisha (kumtakasa Aisha). Anasema Imamu Abul-Qasimu Khui (r.m) akinukuu kutoka katika kitabu alFaharasti cha Thiqatur-Rijaliy Muntajabud-Diyn: “Amesema Muntajabud-Diyn katika kitabu chake al-Faharasti: ‘Sheikh Al-Waidh Nasirud-Diyn Abdul-Jalili bin Abil-Husein bin al-Fadhil al-Qazuwiniy, ni mwanachuoni, mfasaha, mwenye dini…. ana kitabu kinachoitwa Tanzihi Aisha.”71 Ndio, imepokewa katika Tafsir ya Ali bin Ibrahimu al-Qummiy, Juz. 2, uk. 377, kwamba: “Hakika Aisha alipotoka kwenda Basra kumpiga vita Amirul-Muuminina B katika vita vya Ngamia alidanganywa na Twalha na akamwambia: “Si halali kwako kutoka bila ya kuwa na mahram. Hivyo akaiozesha nafsi yake kwake.”72 Na amesema al-Majilisiy (aliyefariki mwaka 1111 Hijiria) – katika kuelezea yaliyokuja katika Tafsir al-Qummiy: “Kauli hiyo ina uovu mkubwa na mshangao wa ajabu, ni mbali sana kutokea mfano wake kutoka kwa Sheikh wetu Ali bin Ibrahim, bali tunadhani ni katika ziada ya asiyekuwa yeye; Kwa sababu tafsiri iliyopo sio yote imetoka kwake (r.m) bali humo kuna nyongeza nyingi kutoka kwa asiyekuwa yeye. Vyovyote iwavyo maneno haya Waislamu wote wanayapinga Shia na Sunni, na wote wanaitakidi kutakasika kwa wake za Nabii 2 katika yaliyotajwa. Ndio, baadhi yao wanaitakidi Muujam Rijaalil, Hadithi Juz. 9, uk. 265 namba 6252, Amalul-Amil, Juz. 2, uk. 143. Aayaan Shiatu Juz. 7, uk. 434. 72 Tafsir al-Qummiy, Juz. 2, uk. 377. 71
34
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 34
3/26/2016 12:31:36 PM
Mama wa Waumini
kuwa mmoja wao aliasi kwa kumkhalifu kwake Amirul-Muuminina Ali B.”73 Na katika mjadala uliofanywa na runinga ya Misri pamoja na Marjaa aliyefariki Sayyid Muhammad Fadhlullahi (r.m) juu ya Swali: Sunni wanawalaumu Shia kwa kuwatukana na kuwalaani kwao baadhi ya Maswahaba na Bibi Aisha, nini msimamo wa Shia wa kisharia katika hilo? Alijibu kwa kusema: - “Sisi tunaharamisha kabisa, na huu ndio msimamo wetu katika fatwa zote ambazo tunazijibu kwa wenye kuuliza. Tunaharamisha kuwakosea adabu Maswahaba na kuwatukana, kama ambavyo tunaharamisha kumkosea adabu Aisha, pamoja na kwamba sisi tunaitakidi kwamba yeye alikosea katika kushiriki kwake katika vita dhidi ya Imam Ali B. Na Imam Ali B alimheshimu alipomtaka arejee Madina kwa heshima na taadhima. Na sisi pia tunamtoa hatiani Aisha na kadhia ya uzushi; kwa sababu Mwenyezi Mungu amemtakasa katika hilo, na wala haijuzu sisi kumtuhumu yeye wala kumtuhumu yeyote katika wake za Nabii 2 katika maudhui haya, kwa sababu kuna riwaya inayosema hakika kadhia ilitokea kwa Maria mke wa Nabii 2. Na vyovyote iwavyo, sisi tunapinga ukosefu wowote wa adabu kwa Swahaba.”74 Na kutokana na msimamo huu haiujuzu kuwagusa kwa kuwatukana mama za waumini au kuwadharau au kuwashutumu, kwa kumheshimu Mtume wa Mwenyezi Mungu 2. Kisimamo Pamoja na Wanaotukana: Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Surat Nuur:
ت لُ ِعنُوا فِي ال ُّد ْنيَا َو آْال ِخ َر ِة َ ْإِ َّن الَّ ِذينَ يَرْ ُمونَ ْال ُمح ِ ت ْال ُم ْؤ ِمنَا ِ ت ْالغَافِ اَل ِ صنَا َظي ٌم يَوْ َم تَ ْشهَ ُد َعلَ ْي ِه ْم أَ ْل ِسنَتُهُ ْم َوأَ ْي ِدي ِه ْم َوأَرْ ُجلُهُ ْم بِ َما َكانُوا ِ َولَهُ ْم َع َذابٌ ع 73 74
Biharul-Anwar, Juz. 22, uk. 240 ovuti ya al-Allamma al-Marjii Sayid Muhammad Husein Fadhilullahi, na katika kisa T cha uzushi, tazama: Min Wahyi al-Qur’an, Juz. 16, uk. 245 – 265. 35
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 35
3/26/2016 12:31:36 PM
Mama wa Waumini
َّق َويَ ْعلَ ُمونَ أَ َّن ه َّيَ ْع َملُونَ يَوْ َمئِ ٍذ يُ َوفِّي ِه ُم ه َّ للاُ ِدينَهُ ُم ْال َح ُّ للاَ هُ َو ْال َح ُ ِق ْال ُمب ين ُ َت ۖ َوالطَّيِّب ُ َْال َخبِيث ت ِ ات لِلطَّيِّبِينَ َوالطَّيِّبُونَ لِلطَّيِّبَا ِ ات لِ ْل َخبِيثِينَ َو ْال َخبِيثُونَ لِ ْل َخبِيثَا ٌ ك ُمبَ َّرءُونَ ِم َّما يَقُولُونَ ۖ لَهُ ْم َم ْغفِ َرةٌ َو ِر ْز ق َك ِري ٌم َ ِۚ أُو ٰلَئ “Hakika wanaowasingizia wanawake wanaoheshimika, walioghafilika, walio waumini, wamelaaniwa duniani na akhera na watapa adhabu kubwa. Siku ambayo zitawashuhudia ndimi zao na mikono yao na miguu yao kwa waliyokuwa wakiyatenda. Siku hiyo atawatekelezea sawa malipo yao ya haki na watajua kwamba Mwenyezi Mungu ndiye haki iliyo wazi. Mambo ya uhabithi ni ya mahabithi na mahabithi ni wa mambo ya uhabithi. Na mema ni ya walio wema na walio wema ni wa mema. Hao wameepushwa na wanayoyasema; Wao watapata msamaha na riziki ya ukarimu.” (an-Nur; 24:23-26)
Kati ya mwonekano mbaya wa runinga za fitina na matusi na kucheza shere ambazo zinadai kwamba zinalingania dini, ni dharau kubwa wanazozirusha, bali iliyo wazi kwa mke wa Mtume 2 Bibi Aisha hadi imepelekea kubadili maneno katika maweko yake na kutoa maana nyingine ambayo inatamka kwa lugha ya matamanio na sio kwa haki aliyoikusudia Mwenyezi Mungu katika Kitabu kitukufu; aliposema (swt) kumtoa hatiani Bibi Aisha Mama wa Waumini. Na miongoni mwa mwonekano wa sababu hizi ni kwamba madai yao hayana mashiko katika mashahidi, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
َّك ِع ْن َد ه َللاِ هُ ُم ْال َكا ِذبُون َ ِفَإِ ْذ لَ ْم يَأْتُوا بِال ُّشهَدَا ِء فَأُو ٰلَئ “…..na kwa kutoleta mashahidi, basi hao mbele ya Mwenyezi Mungu ni waongo.” (an-Nur; 24:13). Na kama kilichokusudiwa katika kuondolewa tuhuma hiyo ni dhahiri tu basi asingesema: “mbele ya Mwenyezi Mungu” bali angetosheka na kauli yake: “Hao ndio waongo.” Kwa 36
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 36
3/26/2016 12:31:36 PM
Mama wa Waumini
sababu madai ambayo hayajikiti katika kanuni imara hayana thamani ya kivitendo katika hesabu za ukweli, na hususan kwamba yagusa heshima ya waumini na utu wao, ambayo yanamfanya mtoa habari kuwa ni mtu dhalimu katika maneno yake ambayo hayawakilishi shari inayotembea katika shakhisiya yake, kwa sababu anajua kwamba maneno yake hayathibitishi madhumuni yake na haibaki kwayo isipokuwa kuchafua sura na kuchochea uharibifu katika safu za Waumini.”75
Kudhihirisha kuwatuhumu ni kukhalifu sharia ya Mwenyezi Mungu, nako kuko katika hukumu ya sharia ya Mwenyezi Mungu iliyoteremshwa kuhusu watu wa uzushi. Na anastahili aliyowaahidi Mwenyezi Mungu katika mwisho wa Aya iliyokuja baada ya Aya hii, nayo ni:
ت لُ ِعنُوا فِي ال ُّد ْنيَا َو آْال ِخ َر ِة َ ْإِ َّن الَّ ِذينَ يَرْ ُمونَ ْال ُمح ِ ت ْال ُم ْؤ ِمنَا ِ ت ْالغَافِ اَل ِ صنَا َظي ٌم ِ َولَهُ ْم َع َذابٌ ع “Hakika wanaowasingizia wanawake wanaoheshimika, walioghafilika, walio waumini, wamelaaniwa duniani na akhera na watapata adhabu kubwa.” (an-Nur; 24:23)
Na miongoni mwa sababu za kuepushwa na tuhuma hiyo, ambazo amezitaja Mwenyezi Mungu ni Aya ya kulaaniana ambayo imejaalia haki ya mume ambaye anamtuhumu mke wake na wala hana shahidi ila yeye mwenyewe;
َوالَّ ِذينَ يَرْ ُمونَ أَ ْز َوا َجهُ ْم َولَ ْم يَ ُك ْن لَهُ ْم ُشهَدَا ُء إِ اَّل أَ ْنفُ ُسهُ ْم فَ َشهَا َدةُ أَ َح ِد ِه ْم أَرْ بَ ُع َّاللِ ۙ إِنَّهُ لَ ِمنَ الصَّا ِدقِينَ } َو ْالخَا ِم َسةُ أَ َّن لَ ْعنَتَ ه َّت بِ ه َللاِ َعلَ ْي ِه إِ ْن َكانَ ِمن ٍ َشهَادَا َْال َكا ِذبِين 75
Min Wahyil-Qur’an. 37
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 37
3/26/2016 12:31:36 PM
Mama wa Waumini
“Na wale wanaowasingizia wake zao na hawana mashahidi ila nafsi zao, basi ushahidi wa mmoja wao utakuwa kushuhudia mara nne kiapo cha Mwenyezi Mungu ya kwamba hakika yeye ni katika wasema kweli. Na mara ya tano kwamba laana ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake ikiwa ni niongoni mwa waongo.” (an-Nur; 24:6-7)
Hapa ndipo linakuja swali chungu: Je, nyinyi mnamtuhumu Mama wa Waumini kwa uzushi huu kwa kujua au bila ya kujua? Kama mnamtuhumu bila ya elimu basi nyinyi ni katika watu wa uzushi, na mnastahili ambayo yametangulia kutajwa katika Aya, na mkidai kuwa nyinyi mmeyasema kwa kujua je, Mtume wa Mwenyezi Mungu 2 alijua mliyoyajua au hakujua? Kama mtasema: Hakuyajua, namna gani mmejua ambayo hakuyajua yeye? Na mkisema alijua tunawambia: Namna gani aliyajua na wala hakuwalaani na hakuwapa talaka bali, aliwaacha hadi mwisho wa uhai wake? Je, hamuoni kwamba katika tuhuma hii kwa sifa mbaya ni kumkosea adabu Mtume 2, na namna gani Mwenyezi Mungu aliridhia kwake kuwabakisha pamoja na hayo. Na hivyo kwa nini Mwenyezi Mungu alisema katika kubainisha sababu za kumtoa hatiani:
ُ َت ۖ َوالطَّيِّب ُ َْال َخبِيث ت ِ ات لِلطَّيِّبِينَ َوالطَّيِّبُونَ لِلطَّيِّبَا ِ ات لِ ْل َخبِيثِينَ َو ْال َخبِيثُونَ لِ ْل َخبِيثَا ٌ ك ُمبَ َّرءُونَ ِم َّما يَقُولُونَ ۖ لَهُ ْم َم ْغفِ َرةٌ َو ِر ْز ق َك ِري ٌم َ ِۚ أُو ٰلَئ Mambo ya uhabithi ni ya mahabithi na mahabithi ni wa mambo ya uhabithi. Na mema ni ya walio wema na walio wema ni wa mema. Hao wameepushwa na wanayoyasema; Wao watapata msamaha na riziki ya ukarimu.” (an-Nur; 24:26)
Ikiwa Mtume wa Mwenyezi Mungu 2 anajua kwamba yeye sio msafi kwa nini amwaache kwake hadi mwisho wa uhai wake baada ya kusikia Aya hii? Au kuna Aya inayopinga Aya hii aliyoi38
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 38
3/26/2016 12:31:36 PM
Mama wa Waumini
teremsha Mwenyezi Mungu juu yao baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu 2 na amewafanya nyinyi ni mahususi wa kuijua Aya hiyo bila ya walimwengu wengine? Tunajikinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na vitendo na kauli mbaya
َان َو اَل تَجْ َعلْ فِي قُلُوبِنَا ِغ ّاًل لِلَّ ِذين ِ َربَّنَا ا ْغفِرْ لَنَا َولإِ ِ ْخ َوانِنَا الَّ ِذينَ َسبَقُونَا بِالإْ ِ ي َم ٌ ك َر ُء وف َر ِحي ٌم َ َّآ َمنُوا َربَّنَا إِن “Mola Wetu! Tughufirie sisi na ndugu zetu waliotangulia katika imani, wala usijaalie ndani ya nyoyo zetu undani kwa walioamini. Mola Wetu! Hakika Wewe ni Mpole Mwingi wa rehema.” (al-Hashr; 59:10).
39
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 39
3/26/2016 12:31:36 PM
Mama wa Waumini
AHLUL-BAYT WANAPOKEA KUTOKA KWA MAMA ZA WAUMINI
T
unapokuja katika Hadithi iliyopokewa kutoka kwa Maimamu wa Ahlul-Bayt E katika uhalisia wa kivitendo na katika nyanja ya kusambaza Hadithi hatuoni dharau kutoka kwa Maimamu wa Ahlul-Bayt E katika kupokea kutoka kwa Mama za waumini (r.a), bali imekuja katika rejea za Kishia sehemu kubwa katika riwaya hizi na miongoni mwazo katika njia ya mfano ni: i.
Amesema Suduqu: Alitusimulia Muhammad Abdusi bin Ali bin Abbas al-Jarjaaniy katika nyumba yake huko Samarkand, alisema: Alitupa habari Abul- Abbasi Ja’far bin Muhammad bin Maruzuq as-Saraaniy, alisema: Alitusimulia Abdullah bin Said Twaiy, alisema: Alitusimulia Ubaad bin Suhaib kutoka kwa Hisham bin Hayaan, kutoka kwa Hasan bin Ali bin Abu Talib B, alisema: Amesema Aisha – katika mwisho wa hadithi ndefu katika nusu ya usiku: “Hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu 2 amesema: ‘Katika usiku huu aliteremka kwangu kipenzi changu Jibril B akaniambia: Ewe Muhammad! Uamuru ummah wako inapofika nusu ya usiku aswali mmoja wao rakaa kumi, katika kila rakaa asome Alhamdu na Qul-huwallahu Ahadi mara kumi, kisha asujudu na aseme katika sijida yake: Allahumma Laka Sajada Sawaadiy Wajananiy wa Bayaadhiy, Yaa Adhiym Kuli Adhiym Ighfir Dhambiya al-Adhiym wa Innahu Laa Yaghfir Ghairuka Yaa Adhiym.” Akifanya hivyo Mwenyezi Mungu anamfutia makosa sabini na mbili elfu (72,000) na anamwandikia mema mfano wake, na Mwe40
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 40
3/26/2016 12:31:36 PM
Mama wa Waumini
nyezi Mungu Mtukufu anawafutia wazazi wake makosa sabini elfu (70,000).76 ii. Amesema Sheikh Tusiy: Na kutoka kwake kutoka kwa Saad bin Isma’il kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Ismail bin Isa, amesema: Nilimuuliza Imam Ridha B kuhusu mwanaume aliyepatwa na janaba katika mwezi wa Ramadhani na akalala hadi asubuhi, kuna nini juu yake? Akasema: Hili halimdhuru, na wala hafungui. Hakika baba yangu B amesema: Aisha amesema: Hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu 2 aliamka na janaba ya jimai na sio ya kujiotea akasema: Hafungui na wala hakuna tatizo…” 77 iii. Sheikh Tusiy amesema: Na kutoka kwake, kutoka kwa Abu Ali al-Ash’ariy kutoka kwa Muhammad bin Abdil-Jabar, kutoka kwa Swaf’wan, kutoka kwa Ayadh bin Qasim, kutoka kwa Abu Abdillah B amesema: Aisha alimwambia Mtume wa Mwenyezi Mungu 2: Hakika watu wa Barirah wametoa sharti la ufuasi wao. Mtume wa Mwenyezi Mungu 2 akasema: Ufuasi ni kwa aliyeacha huru.”78 iv. Sheikh Suduqu amesema: Ametusimulia Muhammad bin Ali Majluwaihi amesema: Alitusimulia Muhammad bin Yahya al-Atwaar, alisema: Alitusimulia Muhammad bin Ahmad bin Yahya bin Imraan al-Ash’ariy, alisema: Alitusimulia Abu Is’haaq Ibrahim bin Hisham kutoka kwa Muhammad bin Umar kutoka kwa Musa bin Ibrahim, kutoka kwa Abu Hasan Musa bin Ja’far, kutoka kwa baba yake B kutoka kwa babu yake B, alisema: Alisema Ummu Salama kwamba alimwambia Mtume wa Mwenyezi Mungu Fadhail al-Ashuhur Thalathati, uk. 65, Hadithi ya 47. Tahadhibu al-Ahkaami, Juz. 4, uk. 210, Hadithi ya 610. 78 Tahadhibu al-Ahkaami, Juz. 8, uk. 250, Hadithi ya 907. 76 77
41
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 41
3/26/2016 12:31:37 PM
Mama wa Waumini
2: Naapa kwa baba yangu na mama yangu, mwanamke anakuwa na waume wawili, wanakufa na wanaingia peponi, je atakuwa ni wa yupi? Akasema: Ewe Ummu Salama atapewa hiyari ya kuchagua mzuri zaidi wa tabia na mbora zaidi kwa mke wake. Ewe Ummu Salama hakika tabia njema hutembea na kheri ya dunia na Akhera.”79 v.
Al-Bariqiy amesema: Kutoka kwake, kutoka kwa Ja’far bin Muhammad, kutoka kwa Ibn al-Qudaahi, kutoka kwa Abu Abdillahi, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Ali bin Husein B, kutoka kwa Zainabu binti wa Ummu Salama, kutoka kwa Ummu Salama, amesema: Hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu 2 alikuja na mkono wa mbuzi, akala kisha ikaadhiniwa kwa ajili ya swala ya Alasiri, akaswali na hakugusa maji.”80
vi. Sheikh Suduqu amesema: Alitusimulia Sheikh mtukufu Abu Ja’far bin Muhammad bin Ali bin Husein bin Musa bin Babawaihi al-Qummiy (r.m), alisema: Alitusimulia baba yangu B, alisema: Alitusimulia Saidi bin Abdillahi, alisema: Alitusimulia Abu Abdillahi al-Baraqiy kutoka kwa baba yake Muhammad bin Khalid, kutoka kwa Abu alBakhitariy Wahab bin Wahab, kutoka kwa as-Sadiq Ja’far bin Muhammad, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa baba zake E, kutoka kwa Ummu Salama. Hakika siku moja aliamka analia, akaulizwa: Una nini? Akasema: “Hakika ameuliwa mwanangu Husein B, sijamuona Mtume wa Mwenyezi Mungu tangu afariki isipokuwa usiku wa leo, nikamwambia: Naapa kwa baba yangu na mama yangu una nini mbona nakuona ni mwenye huzuni? Akasema: ‘Tangu 79 80
Amaaliy Suduqu, uk. 588, Hadithi ya 811. Al-Mahaasin, Juz. 2, uk. 423, Hadithi 239. 42
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 42
3/26/2016 12:31:37 PM
Mama wa Waumini
usiku sikuacha kuchimba kaburi la Husein na makaburi ya wafuasi wake.’�81
81
Amaaliy Suduqu, uk. 202, Hadithi 217. 43
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 43
3/26/2016 12:31:37 PM
Mama wa Waumini
UHUSIANO WA AHLUL-BAYT NA MAMA ZA WAUMINI
U
husiano wa Ahlul-Bayti E na mama za waumini (r.a) ulikuwa umeimarika kwa upendo na uelewano na muamala mzuri, na zimetuhifadhia riwaya za Ahlul-Bayt E mkusanyiko wa misimamo hiyo mizuri: i.
82
Amepokea al-Humairiy katika Qurubu-Asanid kwamba: Hakika Ali bin Abutalib B amesema: “Niliingia sokoni nikanunua nyama kwa dirhamu moja na nafaka kwa dirhamu moja, nikampelekea Fatimah, hadi alipomaliza kutengeneza mikate na kupika akasema: Ungemwita baba yangu, nikatoka nikamkuta amejipumzisha naye anasema: ‘Najikinga kwa Mwenyezi Mungu na njaa yenye kuumiza,’ nikasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu tunacho chakula. Akaniegemea na tukaondoka kuelekea kwa Fatimah, tulipoingia akasema: ‘Lete chakula chako ewe Fatimah.’ Anasema Fatimah: Nikampelekea zabibu na vipande vya mkate, akafunika mikate na akasema: ‘Ewe Mwenyezi Mungu tubariki katika chakula chetu.’ Kisha akasema: ‘Mgawie Aisha,’ nikamgawia, kisha akasema: ‘Mgawie Ummu Salama’ nikamgawia, hakuacha kuwa anagawa hadi nikapeleka vipande vya mikate na mchuzi kwa wake zake, akasema: ‘Mgawie baba yako na mume wako’ kisha akasema: ‘chukua na ule na toa zawadi kwa jirani zako’, nikafanya hivyo na ikabakia kwao kwa siku kadhaa wakila.”82
urbul-Isnaad, uk. 326; al-Kharaiji Juz. 1, uk. 179; Biharul-Anwar, Juz. 17, uk. 232 na Q Juz. 18, uk. 30. 44
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 44
3/26/2016 12:31:37 PM
Mama wa Waumini
ii. Amepokea Kulainiy kwa sanadi yake kutoka kwa Yaqub bin Salim, kutoka kwa Muhammad bin Muslim, kutoka kwa Abu Abdillahi B, kuhusu mwanaume anapompa hiyari mke wake. Amesema: “Hakika hiyari ni yetu na sio kwa yeyote. Hakika alitoa hiyari Mtume wa Mwenyezi Mungu 2 kwa nafasi ya Aisha, basi wakamchagua Mwenyezi Mungu na Mtume wake na hawakuwa na hiyari ya kumchagua asiyekuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu 2.”83 Na Sheikh al-Majilisiy amefafanua kwamba: “Ni hadithi yenye kuaminika.” Kisha akasema: “Kauli yake B: ‘Kwa nafasi ya Aisha’ yaani hawakutalikiwa awali, bali walipewa uhuru wa kuchagua. Kwa sababu alikuwa anampenda Aisha kwa uzuri wake, na alikuwa anajua kwamba wao hawatamchagua asiyekuwa yeye 2 kwa kuharamishwa waume kwao na nyinginezo miongoni mwa sababu.”84 Na kwa hiyo Mama za Waumini walikuwa wanatoa zawadi ya siku zao kwa bibi Aisha baada ya kushuka Aya ya hiyari.”85 iii. Na Maimamu E wamewaita mabinti zao baadhi ya majina ya Mama za Waumini, miongoni mwao ni: - Imamu Musa bin Ja’far al-Kadhim B aliita mabinti zake watatu: Aisha, Ummu Salama na Maimuna.”86 - Imamu Ali bin Musa Ridha B ana binti anayeitwa Aisha.87 - I mamu Muhammad bin Ali al-Jawad B ana binti jina lake ni Maimuna. Al-Kaafiy, Juz. 6, uk. 139. Miriatul-Uquul, Juz. 21, uk. 233. 85 Ilaamul-Waraa, uk. 488; Majmaul-Bayaan, Juz. 8, uk. 366; Biharul-Anwar, Juz. 22, uk. 182 na 205. 86 Al-Irishad, uk. 323; Ilaamu al-Waraa, uk. 301; Biharul-Anwar, Juz. 48, uk. 320. 87 Kashiful-Ghumah, Juz. 3, uk. 113; Biharul-Anwar, Juz. 49, uk. 222. 83 84
45
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 45
3/26/2016 12:31:37 PM
Mama wa Waumini
- Imamu Ali bin Muhammad al-Hadiy B ana binti jina lake ni Aisha.88 Na Misri kuna sehemu kubwa humo kuna kaburi linalonasibishwa na Aisha binti wa Imamu Ja’far as-Sadiq B, naye ni dada wa Is’haq al-Mu’utaman, mtoto wa Imamu as-Sadiq B na mume wa bibi Nafisa, mjukuu wa Imamu Hasan B.
88
Al-Irishad, uk. 314; Ilaaamul-Waraa, uk. 349; al-Bihaarul-Anwar, Juz. 50, uk. 231. 46
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 46
3/26/2016 12:31:37 PM
Mama wa Waumini
KATIKA HADITHI YA MTUKUFU MTUME WA MWENYEZI MUNGU PAMOJA NA WAKE ZAKE
K
atika kusoma kwetu hazina ya Ahlul-Bayti E tunawaona hawakuzuia sehemu kubwa miongoni mwa riwaya ambazo Mtume wa Mwenyezi Mungu 2 alizizungumza akiwa katika nyumba za wake zake Mama za Waumini, na hususam katika nyumba ya Bibi Aisha, na katika jumla ya hadithi hizo ni: i.
Katika hadithi Sahih ya Abi Baswir kutoka kwa Abu Ja’far B amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu 2 alikuwa kwa Aisha katika usiku wake, akasema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, kwa nini unataabisha nafsi yako ilihali Mwenyezi Mungu ameshakusamehe madhambi yaliyotangulia na yajayo?” Akasema: “Ewe Aisha! Je haipasi mimi kuwa mja mwenye kushukuru?!”89
ii. Katika hadithi Sahihi ya Zurarah kutoka kwa Abu Ja’far B amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu 2 alimwambia Aisha: “Ewe Aisha hakika maneno mabaya kama yangekuwa ni umbo basi yangekuwa ni umbo baya.”90 iii. Katika hadithi yenye kuaminika ya Abu Baswir kutoka kwa Abu Abdillah B amesema: “Hakika Nabii 2 wakati mmoja alipokuwa kwa Aisha, mtu mmoja alimuomba ruhusa ya kuingia ndani, Mtume wa Mwenyezi Mungu 2 akasema: “Ndugu mbaya katika ukoo.” Aisha akasimama akaingia ndani ya nyumba, Mtume wa Mwenyezi Mungu 89 90
Al-Kaafiy, Juz. 2, uk. 695. Al-Kaafiy, Juz. 2, uk. 325. 47
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 47
3/26/2016 12:31:37 PM
Mama wa Waumini
akamruhusu mtu huyo, alipoingia akamwelekea kwa uso wake na mwili wake akizungumza naye hadi alipomaliza na kutoka kwake, Aisha akasema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ulipokuwa unamtaja huyu mtu kwa uliyoyataja kwake, ulimwelekea kwa uso wako na mwili wako.” Hapo Mtume wa Mwenyezi Mungu 2 akasema: “Hakika miongoni mwa waja wa Mwenyezi Mungu waovu ni yule ambaye kunachukiza kukaa naye kutokana na ubaya wake.”91 iv. Katika hadithi sahihi ya Zurarah kutoka kwa Abu Ja’far B amesema: “Myahudi aliingia kwa Mtume Mwenyezi Mungu 2 na Aisha yuko naye akasema: “Maangamio yawe juu yenu.” Mtume wa Mwenyezi Mungu akasema: “Na juu yenu.” Kisha akaingia mwingine akasema mfano wa hayo na Mtume akamjibu kama alivyomjibu sahibu yake, kisha akaingia mwingine akasema mfano wa hayo na Mtume wa Mwenyezi Mungu akamjibu kama alivyowajibu sahiba zake. Aisha O akakasirika akasema: “Na maangamio yawe juu yenu na ghadhabu na laana enyi Mayahudi, enyi ndugu wa manyani na nguruwe.” Mtume wa Mwenyezi Mungu akamwambia: “Ewe Aisha hakika maneno mabaya kama yangekuwa ni umbo basi yangekuwa ni umbo baya. Hakika upole haujawekwa kwenye kitu katu isipokuwa unakizidishia uzito, na haukuondolewa kwenye kitu katu isipokuwa unakifanya kiwe kibaya.” Akasema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu je, hujasikia kauli yao: Maangamio yawe juu yako?” Akasema: “Nimesikia, je, hujasikia niliyowajibu, nilisema na juu yenu. Anapowasalimia Mwislamu semeni: amani iwe juu yenu, na anapowasalimia kafiri semeni: Na juu yako.”92 91 92
Al-Kaafiy, Juz. 2, uk. 326. Al-Kaafiy, Juz. 2, uk. 648. 48
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 48
3/26/2016 12:31:37 PM
Mama wa Waumini
v.
93
Amepokea Mus’adah bin Swadaqah kutoka kwa Abu Abdillahi B amesema: Nilimsikia anasema na aliulizwa kuhusu kuoa katika Shawwal na akasema: “Hakika Mtume alimuoa Aisha O katika mwezi wa Shawal. Na hakika watu wa zama ya mwanzo walichukia kufanya hilo katika mwezi wa Shawal, na hiyo ni kwa sababu ugonjwa wa tauni ulikuwa unatokea kwa mabinti na vijakazi, basi wakauchukia mwezi huo kwa hilo na sio kwa jinginelo.”93
Al-Kaafiy, Juz. 54, uk. 266. 49
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 49
3/26/2016 12:31:37 PM
Mama wa Waumini
FADHILA ZA IMAM ALI B KATIKA NDIMI ZA MAMA ZA WAUMINI
M
apenzi ya kumpenda Imamu Ali B katika nyoyo za Mama za Waumini yalikuwa ni makubwa, na nafasi yake kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu 2 ina athari katika kusambaza fadhila zake kwa hadithi nyingi kutoka kwa Maswahaba watukufu. Na Mama za Waumini (r.a) walikuwa ni watu wanaojali sana kusambaza fadhila za Amirul-Muuminina B, na miongoni mwa fadhila hizo ni zile ambazo kazipokea Mama wa Waumini Aisha katika haki ya Imamu Ali B, kama ilivyokuja katika rejea za Kishia: i.
Amesema Tusiy: Abu Abbasi, amesema: Ametusimulia Muhammad bin Ahmad bin Hasan al-Qatawaniy, amesema: Ametusimulia Ubaad bin Thabiti amesema: Ametusimulia Ali bin Swalih kutoka kwa Abi Is’haq as-Shaibaniy, amesema: Amenisimulia Yahya bin Abdul-Malik bin Abi Ghaniyah na Ubaad bin Rabi’i, na Abdillahi bin Abi Ghaniyah, kutoka kwa Is’haq as-Shaibaniy, kutoka kwa Jami’i bin Umair, amesema: “Niliingia pamoja na mama yangu kwa Aisha nikamtajia Ali B, akasema: ‘Sijaona mwanaume aliyekuwa anapendwa zaidi na Mtume wa Mwenyezi Mungu 2 kuliko yeye, na sijaona mwanamke aliyekuwa anapendwa zaidi na Mtume wa Mwenyezi Mungu 2 kuliko mke wake J.’”94
ii. Sheikh Suduqu: Ametusimulia Ahmad bin Hasan al-Qatwan amesema: Ametusimulia Ahmad bin Yahya bin Zakaria al-Qatwan amesema: Ametusimulia Bikir bin Abdillahi, 94
Amaaliy Tusiy, uk. 249, Hadithi 440; Biharul-Anwar Juz. 37, uk. 40. 50
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 50
3/26/2016 12:31:37 PM
Mama wa Waumini
amesema: Ametusimulia Tamim bin Bahalul, amesema: Ametusimulia Abdillahi bin Swalih bin Abi Salama Naswaibainiy, amesema: Ametusimulia Abu Awanah kutoka kwa Abi Bishir, kutoka kwa Said bin Jubair, kutoka kwa Aisha O, amesema: “Nilikuwa kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu 2 mara akaja Ali bin Abutalib, Mtume akasema: ‘Huyu ni bwana wa Waarabu.’” Nikasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, wewe si ndio bwana wa Waarabu? Akasema: ‘Mimi ni bwana wa kizazi cha Adam na Ali ni bwana wa Waarabu.’ Nikasema: Na bwana ni nani? Akasema: ‘Ni ambaye imefaradhishwa kumtii kama ilivyofaradhishwa kunitii mimi.”’ 95 iii. Amesema Abu Ja’far Muhammad bin Suleiman al-Kufiy: Ametusimulia Khidhri bin Abaan, amesema: Amenisimulia Yahya bin Abdul-Hamid kutoka kwa Abi Awanah, kutoka kwa Ja’far bin Ayaasi, kutoka kwa Said bin Jubair, kutoka kwa Aisha O, amesema: “Nilikuwa nimekaa kwa Nabii 2 mara akaja Ali, Mtume akasema: ‘Huyu ni bwana wa Waarabu.’ Nikasema: Naapa kwa baba yangu na mama yangu, wewe si ndio bwana wa Waarabu? Akasema: ‘Mimi ni bwana wa walimwengu na huyu ni bwana wa Waarabu.’”96 iv. Amesema Ibn al-Batwariq na kwa sanadi iliyotangulia, amesema: Ametupa habari Abul-Hasan Ahmad bin al-Mudhwafar bin Ahmad al-Atwaar, mwanafikihi wa Kishafii – kwa kumsomea kwangu naye akakiri kwayo – nikasema: Amekupeni habari Abu Muhammad bin Abdul-Aziz bin Muhammad bin Uthman al-Maziniy, mwenye jina la Ibn Saqaai al-Hafidh al-Wasitwiy, amesema: Ametusimulia maaliy Suduqu, uk. 94, Hadithi 71; Maanil-Akhbar, uk. 103; Raudhwatul-Waaidhin, uk. A 101; Biharul-Anwar, Juz. 38, uk. 93 na 110. 96 Manaaqib Amirul-Mu’minina, uk. 512, Hadithi 1011. 95
51
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 51
3/26/2016 12:31:37 PM
Mama wa Waumini
Muhammad bin Ali bin Ma’amar al-Kufiy amesema: Ametusimulia Hamdani bin al-Maaniy, amesema: Ametusimulia Waki’i kutoka kwa Hisham bin Uruwa kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Aisha, amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu 2: “Kumtaja Ali ni ibada.”97 v.
Amesema Abu Ja’far Muhammad bin Suleiman al-Kufiy: Ametusimulia Khidhri bin Ibaana amesema: Abu Naim al-Fadhil bin Dakin, amesema: Ametusimulia Sahariki kutoka kwa Aamashi kutoka kwa Jamii bin Umair, kutoka kwa shangazi yake, amesema: Nilimwambia Aisha: “Ni nani alikuwa anapendwa zaidi na Mtume wa Mwenyezi Mungu 2 kati ya watu?” Akasema: “Fatimah.” Nikasema: Bali nakuuliza kuhusu wanaume? Akasema: “Mume wake.”98
vi. Amesema Sheikh Suduqu: Ametupa habari Ahmad bin AsSwalti, amesema: Ametupa habari Ahmad bin Muhammad, amesema: Ametusimulia Yaaqub bin Yusufu al-Dhwabniy, amesema: Ametusimulia Ubaidullahi bin Musa, amesema: Ametusimulia Ja’far al-Ahmar kutoka kwa Shaibaniy kutoka kwa Jamii bin Umair, amesema: Shangazi yangu alimwambia Aisha O na mimi nasikiliza: “Umeonaje kutoka kwako kwenda kumpiga vita Ali B?” Akasema: “Tuachane na hayo, hakika hapakuwa na mwanaume anayependwa zaidi na Mtume wa Mwenyezi Mungu 2 kuliko Ali, wala mwanamke aliyekuwa anapendeza zaidi kwake kuliko Fatima J.”99 Al-Umdatu, uk. 360; al-Biharu, Juz. 38, uk. 199. Maanaqib al-Imamu Ali, uk. 194, Hadithi 666; Kashiful-Ghummah, Juz. 1, uk. 244; alBiharul-Anwar, Juz. 32, uk. 272 na Juz. 38, uk. 313, na Juz. 40, uk. 152. 99 Ammaliy Suduqu, uk. 332, Hadithi 663; Bisharatu al-Mustafaa cha Twabariy, uk. 369; Biharul-Anwar Juz. 32, uk. 268. 97 98
52
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 52
3/26/2016 12:31:37 PM
Mama wa Waumini
vii. Na ameongeza Sheikh Suduqu kwamba yeye alisema: “Wallahi kama mimi ningekuwa na watoto ishirini wa kiume kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu na wote ni kama mfano wa Abdurahman bin Harithi bin Hisham na wote wakafa au wakauliwa mashahidi ingekuwa ni kwepesi kwangu kuliko kutoka kwangu dhidi ya Ali, na kutoka kwangu ambapo nilikwenda, mashitaka yangu ni kwa Mwenyezi Mungu na sio kwa mwingine.”100 viii. Amesema Sheikh Suduqu: Ametusimulia Yaaqub bin Yusuf bin Yaaqub al-Faqihi, Sheikh wa wenye rai, amesema: Ametusimulia Ismail bin Muhammad as-Swafaar al-Baghidadiy, amesema: Ametusimulia Muhammad bin Ubaid bin Utuba al-Kindiy, amesema: Ametusimulia Abdur-Rahman bin Shariki, amesema: Ametusimulia baba yangu kutoka kwa Aamash kutoka kwa Atwau, amesema: Nilimuuliza Aisha kuhusu Ali bin Abutalib B akasema: “Huyo ni mbora wa watu na wala hana shaka naye isipokuwa kafiri.”101 ix. Amesma Sheikh Suduqu: Na kwa sanadi hii kutoka kwa Ibrahim bin Muhammad Athaqafiy amesema: Ametupa habari Ismail bin Abaana al-Azidiy amesema: Ametusimulia Abdillah bin Kharashi Shaibaniy kutoka kwa al-Awaam bin Haushab kutoka kwa Tamim, amesema: “Niliingia kwa Aisha akatusimulia kwamba yeye alimuona Mtume wa Mwenyezi Mungu 2 amemwita Ali, Fatima, Hasan na Husein akasema: ‘Eee Mwenyezi Mungu hawa ni AhlulBayti wangu, waondolee uchafu na uwatakase kabisa.’”102 Ilalu Sharaaiu, Juz. 1, uk. 222; Biharul-Anwar, Juz. 44, uk. 34. Amaaliy Suduqu, uk. 135, Hadithi ya 130, al-Biharul-Anwar, Juz. 38, uk. 5. 102 Amaaliy Suduqu, uk. 559, Hadithi ya 747. 100 101
53
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 53
3/26/2016 12:31:37 PM
Mama wa Waumini
x.
Amesema Sheikh Suduqu: Ametusimulia Ahmad bin Hasan al-Qatwaan, amesema: Ametusimulia Ahmad bin Yahya bin Zakaria al-Qatwaan, amesema: Ametusimulia Bikir bin Abdillah bin Habib amesema: Ametusimulia Tamim bin Bahalul, amesema: Ametusimulia Abdillah bin Swalih bin Abi Salama Naswaibainiy, amesema: Ametusimulia Abu Awanah kutoka kwa Abi Bishir, kutoka kwa Saidi bin Jubair kutoka kwa Aisha, amesema: “Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu 2 anasema: ‘Mimi ni bwana wa mwanzo na wa mwisho, na Ali bin Abutalib ni bwana wa Mawasii naye ni ndugu yangu, mrithi wangu na khalifa wangu katika ummah wangu. Uongozi wake ni faradhi na kumfuata kwake ni fadhila, na kumpenda kwake ni wasila kwa Mwenyezi Mungu. Kundi lake ni kundi la Mwenyezi Mungu na wafuasi wake ni wenye kumnusuru Mwenyezi Mungu, na wenye kumpenda ni mawalii wa Mwenyezi Mungu, na maadui zake ni maadui wa Mwenyezi Mungu. Yeye ni Imamu wa Waislamu na ni mtawala wa Waumini na ni kiongozi wao baada yangu.”’103 xi. Amesema Sheikh Suduqu: Ametusimulia al-Hasan bin Ahmad bin al-Walid Thaqafiy amesema: Ametusimulia Ahmad bin Alawiyah al-Isbahaaniy kutoka kwa Ibrahim bin Muhammad Thaqafiy: Ametusimulia Abu Naim al-Fadhil bin Dakin amesema: Ametusimulia Zakaria bin Abi Zaidah amesema: Ametusmulia Farasi kutoka kwa Shaabiy, kutoka kwa Masuruqu, kutoka kwa Aisha, amesema: “Fatima J alikuja akitembea kana kwamba mwendo wake ni mwendo wa Mtume wa Mwenyezi Mungu 2. Nabii 2 akasema: ‘Karibu binti yangu.’ Akamkalisha kuliani kwake au kushotoni kwake kisha akaongea naye kwa siri. 103
Amaaliy Suduqu, uk. 679, Hadithi ya 924. 54
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 54
3/26/2016 12:31:37 PM
Mama wa Waumini
Akalia, na kisha akaongea naye kwa siri, akacheka. Nikamwambia: ‘Umeongea na Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa siri ukalia kisha akaongea nawe kwa siri ukacheka, sijaona siku kama leo furaha iliyo karibu na huzuni kama furaha yako.’ Nikamuuliza juu ya aliyosema, akasema: ‘Sikuwa ni mwenye kutoa siri ya Mtume wa Mwenyezi Mungu 2.’ Alipofariki Mtume nikamuuliza, akasema: ‘Hakika alininong’oneza kwa siri akasema: Hakika Jibril alikuwa ananisomea Qur’ani yote kila mwaka mara moja lakini amenisomea mara mbili katika mwaka huu na sioni isipokuwa kifo changu kimeshakaribia, na hakika wewe ni wa mwanzo kunifuata katika Ahlul-Bayt wangu, na mimi ni mtangulizi bora kwako. Nikalia, kisha akasema: Je, huridhii wewe kuwa ni bibi wa wanawake wa ummah huu? Au wanawake wa waumini? Basi nikafurahi kwa ajili ya hilo.’”104
104
Amaaliy Suduqu, uk. 692, Hadithi ya 948. 55
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 55
3/26/2016 12:31:37 PM
Mama wa Waumini
HITIMISHO KATIKA FIQHI YA KUTUKANA NA KULAANI Kuhusu kutukana:
S
isi tunajua kwamba katika tabia kuna mistari mibaya nayo ni tabia ambayo Mwenyezi Mungu haitaki kwa mwanadamu kujipamba nayo. Na kuna mistari mizuri anayoitaka Mwenyezi Mungu kwake kujipamba nayo. Na tukitafakari katika maneno yaliyopokewa kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu 2: “Hakika nimetumwa kuja kukamilisha tabia njema,”105 hakika sisi tunafahamu kwamba Uislamu wote ni harakati ya tabia. Tabia inajumuisha fiqhi, manhaji na mbinu. Na miongoni mwa tabia mbaya ambayo Mwenyezi Mungu ametia msisitizo juu yake katika Kitabu chake kwa kuikataza ni matusi. Kwanza: Zimepokewa nususi nyingi za Kiislam katika kuharamisha kutukana: Katika Qur’ani Tukufu: Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu, Naye anaelekeza maneno kwa Waislamu:
َّللاِ فَيَ ُسبُّوا ه َّون ه ك َزيَّنَّا َ ِللاَ َع ْد ًوا بِ َغي ِْر ِع ْل ٍم ۗ َك ٰ َذل ِ َو اَل تَ ُسبُّوا الَّ ِذينَ يَ ْد ُعونَ ِم ْن ُد لِ ُكلِّ أُ َّم ٍة َع َملَهُ ْم “Wala msiwatukane ambao wanaoomba asiyekuwa Mwenyezi Mungu, wasije wakamtukana Mwenyezi Mungu kwa jeuri bila ya kujua. Kama hivyo ndivyo tumewapambia kila umma vitendo vyao…..”106 usnad Ridhwa, uk. 131; Sunan al-Baihaqiy, Juz. 10, uk. 20571; Musnad Shihaab, M Juz. 2, uk. 195, Hadithi ya 1165. Kanzul-Umaal, Juz. 3, uk. 9, Hadithi ya 5217. JamiulAhadith, Juz. 3, uk. 193, Hadithi ya 8105. 106 Suratul-An’am: 108 105
56
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 56
3/26/2016 12:31:37 PM
Mama wa Waumini
Mwenyezi Mungu hakuharamisha matusi kwa washirikina kwa sababu wao hawastahiki matusi kwa shiriki yao na kufuru yao na dhulma yao kwa Uislamu, na watu wake wanastahili kila sifa ambayo inafanana na matusi, lakini Mwenyezi Mungu Mtukufu amewataka Waislamu wachukue sababu za kijamii kwa ajili ya kuhifadhi matukufu ya Kiislamu ambayo yanatukanwa na hawa kwa kuzingatia kwamba kitendo hicho kinasababisha kisasi. Wewe unapotukana matukufu ya wengine hakika wao kwa kitendo hiki cha kibabe ambacho unakielekeza kwao, wao watakurejeshea ubabe mfano wake na kutukana matukufu yako. Kwa sababu wao hawajui utukufu wa Mwenyezi Mungu na kutukana kwenu matukufu yao hakuwafanyi wafunguke kwa Mwenyezi Mungu, bali kutukana huku ni kitendo kibaya, kinasababisha kitendo kibaya kinachofanana nacho au kibaya zaidi kuliko hicho. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu anaelezea mas’ala haya kwa kauli yake: hivyo ndivyo tulivyoupambia kila umma vitendo vyao. Lakini nyinyi kama mnaona kwamba hakika kitendo chenu ni kitendo sahihi, hakika wengine wanaona kitendo chao ndio kitendo sahihi, na matusi sio njia ambayo inawathibitishia wengine uharibifu wa kitendo chao, bali hakika wewe unawafanya wawe na kasumba zaidi. Na kauli yake (swt): “Na jiepusheni na kauli ya uongo.”107 Na ni uongo upi mkubwa zaidi kuliko huu? Hakika ni kati ya uwazi wa ukweli wake. Katika Sunna: i.
107
Hadithi sahihi ya Abdur-Rahman bin al-Hajaji, kutoka kwa Abil-Hasan Musa B, kuhusu watu wawili wanaotukanana, amesema: “Mwenye kuanza kati yao ni dhalimu zaidi na
Suratul-Haji: 30 57
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 57
3/26/2016 12:31:37 PM
Mama wa Waumini
dhambi yake na ya sahiba wake ni juu yake maadamu hajaomba msamaha kwa aliyedhulumiwa.”108 ii. Katika hadithi sahihi ya Abu Baswir, kutoka kwa Abu Ja’far B, amesema: “Hakika mwanaume kutoka kwa Bani Tamim alimwendea Nabii 2 akasema: ‘Niusie.’ Ikawa kati ya aliyomuusia ni: Usiwatukane watu na kuchuma uadui baina yao.”109 Na tunaona katika hadithi hii kwamba watu katika zama za Nabii 2 hawakuwa wote ni Waislamu na kwa hiyo Nabii 2 alitaka kubainisha kwamba matusi ni moja ya wasila wa kuchuma uadui kwa sababu wewe unapotukana mtu, hakika unadharau utu wake na unavunja heshima yake, na unachochea katika nafsi yake vikwazo ambavyo vitageuka kuwa ni uadui. Na Mwenyezi Mungu anataka kwa Waislamu wabadilishe uadui wa maadui zao kuwa urafiki, badala ya kuwageuza marafiki kuwa maadui. Mema na maovu hayawi sawa, zuieni uovu kwa lililo jema zaidi. Mara yule ambaye baina yako na yeye pana uadui, atakuwa kana kwamba ni rafiki mkubwa.”110
َّفَبِ َما َرحْ َم ٍة ِمنَ ه ۖك َ ِب اَل ْنفَضُّ وا ِم ْن َحوْ ل ِ للاِ لِ ْنتَ لَهُ ْم ۖ َولَوْ ُك ْنتَ فَظًّا َغلِيظَ ْالقَ ْل “Kwa rehema itokayo kwa Mwenyezi Mungu, umekuwa laini kwao. Lau ungelikuwa mkali mwenye moyo mgumu bila shaka wangelikukimbia…..”111
iii. Katika hadithi inayokubalika ya Abu Baswir kutoka kwa Abu Ja’far B amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu 2: “Kumtukana muumini ni ufasiki, kumpiga Al-Kaafiy, Juz. 2, uk. 268. Rejea iliyotangulia 110 Suratu Fuswilat: 34 111 Aali-Imran: 159 108 109
58
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 58
3/26/2016 12:31:37 PM
Mama wa Waumini
vita ni ukafiri, kumsengenya ni maasi na uharamu wa mali yake ni kama ulivyo uharamu wa damu yake.”112 Mtume wa Mwenyezi Mungu 2 alikusanya katika vipengele hivi uhusiano wa muumini kumheshimu muumini. - Kumtukana kwake ni ufusuka: Kwa sababu Mwenyezi Mungu ameharamisha kumtukana muumini ukimtukana muumini basi umeshafanya maasi kati ya maasi ya kumuasi Mwenyezi Mungu na kwa hiyo umeshachuma sifa ya ufuska, kwa sababu ufasiki ni kuvuka mpaka ambao Mwenyezi Mungu amewataka watu wasiuvuke. - Na kumpiga vita: Yaani kuhalalisha kumpiga vita bila ya kuwa na sababu ya kisharia ya kupigana. - Na kula nyama yake ni maasi: Nayo ni kinaya ya kumsengenya, na uharamu wa mali yake ni kama ulivyo uharamu wa damu yake. iv. Katika hadithi sahihi, Abdur-Rahmani amesema: Nilimuuliza Abu Abdillah B juu ya mtu aliyemtukana mtu bila ya kosa alilolifanya, je, anapigwa mjeledi? Akasema: “Ataadhibiwa kwa kuchapwa viboko.” v.
Katika hadithi inayokubalika ya Is’haqa bin Ammaar kutoka kwa Ja’far B, amesema: “Hakika Ali B alikuwa anaadhibu kwa kusema uongo na wala hakuwa anapiga mijeledi isipokuwa katika uongo ulio wazi, kwa kusema: Ewe mzinifu, ewe mtoto wa zinaa au wewe sio wa baba yako.”113
vi. Katika hadithi Sahihi ya Muhammad bin Muslim: Nilimwambia Abu Ja’far B: Unaonaje, kama mtu ikimtukana Nabii 2 hivi sasa anauliwa? Akasema: “Kama hauogopi madhara kwa nafsi yako basi muuwe.”114 Al-Kaafiy, Juz. 2, uk. 268. Al-Kaafiy, Juz. 7, uk. 240. 114 Tahdhiibu, Juz. 10, uk. 88. 112 113
59
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 59
3/26/2016 12:31:37 PM
Mama wa Waumini
Pili: Sayyid Khui anasema: Dhahiri kijamii na kilugha, dharau na kuaibisha inazingatiwa katika maana ya kutukana, na kwamba kutukana ni dharau na kejeli kwa mwenye kutukanwa, na kwamba inaungana na shutuma. Na kwa hili yanaingia humo kila yanayopelekea dharau kwa mwenye kutukanwa na kumvunjia heshima, kama vile kumsingizia na kumsifu kuwa ni muovu, si chochote, punda, mbwa, nguruwe, kafiri, murtadi, mwenye mbalanga, ukoma, chongo na mengineyo miongoni mwa maneno yanayopelekea dharau na kejeli, na hivyo haitimii dhana yake ila kwa kukusudia kuvunja heshima. Ama majibu ya mwenye kutukanwa hayazingatiwi humo.”115 Tatu: Katika kupitia kwetu riwaya na, hususan wakati tunaposoma kauli ya Mtume 2: “Kumtukana muumini ni ufuska na kumpiga vita ni ukafiri” tunagundua kwamba muumini kumtukana ndugu yake hilo linampa sifa ya ufasiki kwa sababu fasiki ni yule anayetoka katika njia ya sawa. Na Mwenyezi Mungu anataka neno zuri liwe ndio njia ya sawa na sio neno la kushutumu ambalo linawakilisha kutoka katika njia hii, bila kujali kwamba shutuma inabeba maana iliyopo katika shutuma au matusi, kadhia sio kwamba huyu anastahiki au hastahiki lakini njia kwa tabia yake ni ya kimakosa hata kama mkosaji anastahiki kushutumiwa au matusi, kana kwamba anataka kusema kwamba ni juu yako usitatue kosa kwa kosa na tusi kwa tusi, ni lazima kwa Mwislamu aishi pamoja na Mwislamu mwingine maisha ya salama. “Mwislamu ni ambaye wanasalimika Waislamu kutokana na ulimi wake na mkono wake.”116 Ambaye Waislamu hawakusalimika kutokana na mkono wake na ulimi wake basi sio Mwislamu katika maana, ingawa kwa umbo ni Mwislamu. Nne: Inaweza kusemwa kuwa hakuna uharamu wa kutukana iwapo mtu atatukanwa, maadamu tu hajavuka mpaka, na kwamba 115 116
Misbahul-Faqaha, Juz. 1, uk. 434. Al-Kaafiy, Juz. 2, uk. 234; Raudhatul-Mutaqina Juz. 7, uk. 269. 60
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 60
3/26/2016 12:31:38 PM
Mama wa Waumini
dhambi ni kwa aliyeanza miongoni mwao. Amesema mhakiki alArdabiliy (r.m) – katika aya za Sharia baada ya kutaja baadhi ya Aya zinazoonesha kuwa zinaruhusu kufanya uadui kama ule uliofanyiwa: “Zinaonyesha kwamba inaruhusiwa kufanya kisasi katika nafsi, viungo na majeraha, bali inaruhusiwa kulipiza kisasi kabisa hata cha aliyepigwa na aliyeshutumiwa kwa mfano wa kitendo alichofanyiwa…. na mwisho inaonyesha kutoruhusiwa kuvuka mpaka katika aliyofanyiwa na kuharamisha dhulma na kuvuka mpaka.”117 Na vilevile amesema Sheikh al-Majilisiy kwamba kinachofanywa na aliyedhulumiwa ni dhambi ila sharia imeacha kumwadhibu na imejaalia adhabu kwa mwenye kuanza! Amesema (r.m) hakika dhambi ya matusi ya wenye kutukanana ni juu ya aliyeanza. Dhambi ya kuanza kwake ni kwa sababu kutukana na ufusuka ni haramu, kwa hadithi “Kumtukana muumini ni ufasiki na kumpiga vita ni ukafiri.” Ama dhambi ya kutukana ya mwenye kujibu ni kwa sababu aliyeanza ndio mwenye kumbebea mwenye kujibu, lakini kinachotokea kwake ni tusi ambalo kwalo anapata dhambi, isipokuwa sharia imeondosha kwake adhabu na ikaijaalia kwa aliyeanza kwa sababu iliyotangulia. Na imeondosha kwake maadamu hatovuka mpaka, akivuka mpaka basi atakuwa ni mwanzilishi kwa kiasi kilichozidi.”118 Na inadhihiri kwa wa kwanza miongoni mwao (mwenye kujibu) kuwa hatokuwa na dhambi kwa dalili ya Aya zinazoruhusu uadui unaofanana (wa kisasi), na kwa wa pili miongoni mwao (mwanzilishi) kuwa ametenda haramu, sharia imejaalia dhambi ya kutukanana juu ya mwanzilishi, na Sayyidi Khui (r.m) ameichagua rai hii katika Misbahul–Faqaha.119 Zubdatul-Bayaan, uk. 670. Mir’atul-Uqul, Juz. 10, uk. 265. 119 Misbahul-Faqaha, Juz.1, uk. 434. 117 118
61
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 61
3/26/2016 12:31:38 PM
Mama wa Waumini
Na la juu zaidi ambalo inawezekana kulifanya dalili juu ya hilo ni mambo yafuatayo: 1.
Kauli yake (swt):
َّفَبِ َما َرحْ َم ٍة ِمنَ ه ۖك َ ِب اَل ْنفَضُّ وا ِم ْن َحوْ ل ِ للاِ لِ ْنتَ لَهُ ْم ۖ َولَوْ ُك ْنتَ فَظًّا َغلِيظَ ْالقَ ْل َّفَ َم ِن ا ْعتَد َٰى َعلَ ْي ُك ْم فَا ْعتَ ُدوا َعلَ ْي ِه بِ ِم ْث ِل َما ا ْعتَد َٰى َعلَ ْي ُك ْم ۚ َواتَّقُوا ه... للاَ َوا ْعلَ ُموا َّأَ َّن ه َللاَ َم َع ْال ُمتَّقِين “Na piganeni nao mpaka kusiwe na fitina, na dini iwe ya Mwenyezi Mungu peke Yake. Na wakikoma, basi usiweko uadui ila kwa dhalimu. …..Basi anayewachokoza, nanyi mlipizeni kwa kadri ya alivyowachokoza. Na mcheni Mwenyezi Mungu na jueni kwamba Mwenyezi Mungu yupo pamoja na wanaomcha.”120
Lakini Aya haihusiani na hayo, vinginevyo ingeruhusiwa ‘kutukana’ mkabala na ‘tusi ulilotukanwa’ kwa kutokuwa na tofauti baina yake. Na kauli ya kutohusika kwake ni kwa dalili maalumu kama ulivyoona, na hali ni hiyo hiyo ingelazimu ‘kusengenya’ mkabala na ‘utesi uliosengenywa’ na ‘kutuhumu’ mkabala na ‘tuhuma uliyotuhumiwa.’ Na kufanya hivyo ni jambo la ajabu. Na vivyo hivyo hakika tafsiri ya Aya mbili zilizotangulia haiwezi kutumika kwa ujumla katika sehemu zote. Na hilo linaungwa mkono na yaliyokuja katika hadithi sahihi ya Mu’awiya bin Ammar, amesema: “Nilimuuliza Abu Abdillah B kuhusu mwanaume aliyemuuwa mtu nje ya Eneo Takatifu, kisha akaingia ndani ya Eneo Takatifu? Akasema: ‘Hauliwi, hapewi chakula wala maji, hauziwi wala hapewi nguo hadi atoke katika Eneo Takatifu na kufanyiwa kisasi.’ Nikasema: Unasemaje juu ya mtu aliyeuwa katika Eneo Takatifu au aliyeiba? Akasema: ‘Anaadhibiwa katika Eneo Takatifu hali ya 120
Suratul- Baqarah: 193 – 194. 62
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 62
3/26/2016 12:31:38 PM
Mama wa Waumini
kuwa dhalili, kwani yeye hakuchunga utukufu wa Eneo Takatifu, na ameshasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Basi anayewachokoza nanyi mlipizeni kwa kadri ya alivyowachokoza. Haya ni ndani ya Eneo Takatifu. Hakuna uadui ila kwa madhalimu.’” 121 Labda isemwe kwamba kauli yake B: “Haya ni ndani ya Eneo Takatifu” haionyeshi umahususi wa Aya katika sehemu iliyotajwa na kuitumia katika sehemu isiyokuwa ya kuuwa ni jambo sahihi, na ni jambo liko mbali sana Aya kutohusika na sehemu nyingine ambazo hazikutajwa katika riwaya. 2.
Yaliyopita katika sahihi ya Abdur-Rahman bin al-Hajaji kutoka kwa Abul Hasan Musa B katika watu wawili wanaotukanana, amesema: “Mwenye kuanza miongoni mwao ni dhalimu zaidi, na dhambi yake na dhambi ya sahiba yake ni juu yake, maadamu hajaomba msamaha kwa aliyedhulumiwa.”122
Na riwaya imenukuliwa katika njia mbili: i.
Katika mojawapo: “Dhambi yake na dhambi ya sahiba wake ni juu yake maadamu hajaomba msamaha kwa aliyedhulumiwa.”
ii. Katika riwaya nyingine kuna tofauti katika chanzo cha sanadi ya hadithi na matini yake “maadamu mwenye kudhulumiwa hajavuka mpaka” na dhahiri yake ni kwamba hakuna dhambi juu yake kama hajavuka mpaka na kuafikiana na Aya za kufanya uchokozi unaofanana. Ni dhahiri kwamba hizo si riwaya mbili, bali tofauti baina yake inatokana na tofauti ya tamko baada ya kuungana mpokezi na aliye121 122
Suratul- Baqarah: 193. al-Kafiy, Juz. 2, uk. 168. 63
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 63
3/26/2016 12:31:38 PM
Mama wa Waumini
pokea kutoka kwake B na madhumuni, na kuwepo tofauti ni katika sanadi tu. Hivyo kuitumia kama dalili ni jambo lenye mushkeli kwa kuwa haijathibiti matini ya pili, na hususan kwamba sanadi ya kwanza ni yenye nguvu zaidi. Na hoja yake vilevile ni tatizo; kwa kuwa kuna uwezekano ikawa ni miongoni mwa aina za “Mwenye kuanzisha sunna mbaya basi ni juu yake dhambi za mwenye kuitenda bila ya kupungua chochote katika dhambi zao.” Hususan kwa dalili ya kauli yake: “Ni dhalimu zaidi.” Na mambo mawili yanaunga mkono rai iliyochaguliwa: Mojawapo: Imepokewa katika hukumu ya kuadhibu katika mas’ala ya wenye kutukanana: Kutoka kwa Abu Mukhalad Siraji kutoka kwa Abu Abdillah B, amesema: “Amirul-Muuminina B alihukumu kati ya mwanaume aliyemwita mwenzake: ‘Mtoto wa kichaa’, na mwenzake akasema: ‘Wewe ndiye mtoto wa kichaa!’ Aliamuru wa kwanza amchape sahiba yake mijeledi 20 na akamwambia: Jua kwamba yeye pia anastahili mfano wake mijeledi 20, alipomchapa akampa aliyechapwa mjeledi akampiga kwa kosa waliloadhibiwa kwalo.”123 Hakika inaonesha dhambi ya pande mbili, isipokuwa inakuwa ni tatizo kuikubali kwa kutosihi sanadi yake. Na vilevile imepokewa katika hukumu ya wenye kusingiziana kwa kuwaondolea kosa wote wawili na kuthibiti adhabu kwa wote wawili, mfano wa aliyoyapokea Abdullahi bin Sanan – katika hadithi sahihi – amesema: Nilimuuliza Abu Abdillah B kuhusu watu wawili, kila mmoja amemsingizia mwenzake? Akasema: ‘Wanatiwa hatiani na wanaadhibiwa wote wawili.’”124 Na kwa madhumuni yake mafakihi wametoa fatwa kadhaa bila kikwazo. La pili: Kumkabili mtu kwa mfano wa kitendo chake inaweza kuwa kwa maudhi peke yake, hivyo inaruhusiwa kufanya hivyo kwa 123 124
Al-Kaafiy, Juz. 7, uk. 242. Al-Kaafiy, Juz. 7, uk. 240.
64
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 64
3/26/2016 12:31:38 PM
Mama wa Waumini
dalili ya kisasi na nyinginezo. Na namna nyingine ya kukabiliana naye yenyewe ilivyo inaweza kuwa ni jambo lililoharamishwa, na katika mfano wa jambo kama hilo si ruhusa kutenda jambo hilo, kwa sababu ni katika kauli ya uongo na lenyewe lilivyo ni jambo baya, kama vile kusengenya kwa kulipiza kusengenya alikosengenywa, na kutuhumu kwa kulipiza tuhuma aliyotuhumiwa. Na kigezo ni kwamba ruhusa ya kulipiza kitendo ipo katika mambo yanayohusu haki za watu, wala ulipizaji huo hauna nafasi katika upande wa haki ya Mwenyezi Mungu, kama vile kusengenya, tuhuma, kutukana na kuchoma nyumba ya mwingine kwa kulipiza kitendo cha kuchomewa nyumba yake, kutokana na ubaya uliyomo humo. Na amesema Mwenyezi Mungu (swt):
َصرُونَ َو َجزَا ُء َسيِّئَ ٍة َسيِّئَةٌ ِم ْثلُهَا ۖ فَ َم ْن َعفَا َ ََوالَّ ِذينَ إِ َذا أ ِ صابَهُ ُم ْالبَ ْغ ُي هُ ْم يَ ْنت ََّوأَصْ لَ َح فَأَجْ ُرهُ َعلَى ه ك َ ِص َر بَ ْع َد ظُ ْل ِم ِه فَأُو ٰلَئ َ َللاِ ۚ إِنَّهُ اَل ي ُِحبُّ الظَّالِ ِمينَ َولَ َم ِن ا ْنت ْ َيل إِنَّ َما ال َّسبِي ُل َعلَى الَّ ِذينَ ي ض َ َّظلِ ُمونَ الن ٍ َِما َعلَ ْي ِه ْم ِم ْن َسب ِ ْاس َويَ ْب ُغونَ فِي أْالَر ِّ بِ َغي ِْر ْال َح ك لَهُ ْم َع َذابٌ أَلِي ٌم َ ِق ۚ أُو ٰلَئ “Na ambao wanapofanyiwa ujeuri hujitetea. Na malipo ya uovu ni uovu mfano wa huo. Lakini mwenye kusamehe na akasuluhisha, basi huyo malipo yake yapo kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye hapendi wenye kudhulumu. Na wanaojitetea baada ya kudhulumiwa, hao hapana njia ya kuwalaumu. Hakika hapana njia ni ya kuwalaumu. Bali njia ya lawama ipo tu kwa wale wanaowadhulumu watu, na wanafanya jeuri katika ardhi bila ya haki. Hao watapata adhabu iliyochungu.”125
Tano: Maeneo yaliyoondolewa katika hukumu hii: 1. 125
Mwenye kujidhihirisha kwa ufuska: Kwa sababu hakuna utukufu kwake, katika hadithi hasan ya Haruna bin al-Ja-
Suratu Sharaa: 39 – 42. 65
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 65
3/26/2016 12:31:38 PM
Mama wa Waumini
ham kutoka kwa as-Sadiq B, amesema: Fasiki akidhihirisha ufasiki wake basi hakuna uharamu kwake wala ubaya wa kumsengenya.”126 2.
Watu wa shaka na bidaa, na yanaonyesha juu yake aliyoyapokea Daud bin Sarhaan kutoka kwa Abu Abdillahi B amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu 2: “Mnapoona watu wa shaka na bidaa baada yangu basi dhihirisheni kujiepusha nao na zidisheni kuwatukana.”127 3. Ambayo kijamii haathiriki kwayo mwenye kutukanwa, kwamba kusiwe na upungufu katika haki yake, kama vile kauli ya mzazi kwa mtoto wake katika baadhi ambayo yanatendeka baina yao, au anaweza kuwa na ufahari hivyo kama vile kauli ya mwalimu wake kumsema juu ya tabia hiyo. 4. Ambayo yapo katika anwani ya kuadabisha kama vile mzazi kumwadabisha mtoto wake kwa maslahi yanayomruhusu kumchapa. 5. Ambayo yanatendwa kwa ajili ya kukataza uovu, ikiwa kufanya hivyo ndio njia pekee ya kuzuia uovu husika, basi inajuzu kwa hoja zake. Lakini badhi yake hayaepukani na tafakari: Kwanza: Hakika fasiki mwenye kujidhihirisha kwa ufasiki wake kutokuwa tu na utukufu wowote si sababu inayotosha kutoa ruhusa ya kumtukana, maadamu kutukana huko hakuingii katika anwani ya kuamrisha mema na kukataza maovu, wala hairuhusiwi kuwa kigezo cha kutoharamisha kumsengenya kwake. Pili: Hakika kutukana watu wa bidaa vilevile inaingia katika anwani hii, ima wao ni katika wenye kudhihirisha ufasiki au kuwatukana kunaingia katika upande wa kukataza maovu. 126 127
Amaaliy Suduqu, uk. 93, Hadithi ya 78. Al-Kaafiy, Juz. 2, uk. 375. 66
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 66
3/26/2016 12:31:38 PM
Mama wa Waumini
Tatu: Hakika kumtukana asiyeathirika na matusi husika ni jambo liko nje ya anwani yake, kwa sababu haiwi ni upungufu, maudhi na dharau kwake, hivyo haiwi mbali kuruhusiwa kwake, ikiwa haijawa ni yenye kuingia chini ya anwani ya kauli ya uongo. Ama ikiwa ni katika upande wa kutojali kwake aliyosema na yaliyosemwa, inakuwa ni tatizo yeye kutojumuishwa na ujumla wa hadithi zilizotangulia. Nne: Kujuzu kumtukana kwa kigezo cha kutia adabu au kukataza maovu hakika inasihi ikiwa tu halikuwezekana hilo kwa njia nyingine isiyojumuisha matusi. Kuhusu kulaani: Katika hadithi inayokubalika kutoka kwa Abu Hamza al-Thumaliy amesema: Nilimsikia Abu Ja’far B anasema: “Hakika laana inapotoka katika kinywa cha mtamkaji wake inasitasita baina yao wawili, kama itapata pakwenda inakwenda, vinginevyo inarejea kwa mwenyewe.”128 Kama yule mwenye kumlaani mke wake au jirani yake au rafiki yake, hakika laana ni yenye uelewa, inafahamu mapito yake vizuri inasimama njiani ikijiuliza: Je, ambaye amelaaniwa anastahili laana au hastahili, kama ikipata mapito inaendelea katika njia yake vinginevyo inareja kwa mwenye kulaani. Na kwa masikitiko makubwa, mantiki ya wenye kukufurisha yanapata nafasi kwa wengi miongoni mwa watu, hakika wao wanasema: Hakika wengine wanatukufurisha na wanatudhalilisha na wanatutia ufasiki, hivyo ni lazima tukabiliane na mfano wa hayo, kufuru kwa kufuru, upotovu kwa upotovu, ufasiki kwa ufasiki, na chuki mukabala wa chuki. Hata baadhi ya Waislamu katika upande huu au ule wamekuwa wanasema kama walivyokuwa Mayahudi wanasema juu ya washirikina “hao wameongoka zaidi katika njia 128
Al-Kaafiy, Juz. 2, uk. 360. 67
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 67
3/26/2016 12:31:38 PM
Mama wa Waumini
ya haki kuliko walioamini.”129 Hadi tumefika kuwa na chuki binafsi dhidi ya uhalisia wa Uislamu, hadi Mwislamu anawaambia Waislamu wengine kuwa, hakika makafiri wameongoka zaidi kuliko wao, wakati ambapo hakika Mwislamu vyovyote atakavyofikia katika upotovu, haiwezekani kafiri akawa ni bora zaidi kuliko yeye, kwa sababu Uislamu na imani viwili hivyo ndio msingi katika hilo. Na katika matatizo haya yaliyorundikana ndipo linakuja lile linaloitwa vita vya istilahi na uelewa. Anasema mwenye kasumba kutoka kila upande: Hakika kutukana ni jambo moja na laana ni jambo jingine, sisi hatutukani lakini tunalaani. Tunasema: Ni sahihi kwamba kuna tofauti katika maana ya kilugha baina ya maneno mawili hayo, lakini yote katika manhaji ni sawa, pamoja na kuwepo tofauti kati ya laana na kutukana kulingana na maana, ila kwa hakika matokeo mabaya ambayo yanabebwa na laana ni matokeo yale yale mabaya ambayo yanabebwa na matusi. Kama ambavyo wewe unapotukana matukufu ya wengine, hakika wengine pia watatukana matukufu yako kwa sababu ambayo ameitaja Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kauli yake: “Kama hivyo tumewapambia kila umma vitendo vyao.”130 Vivyo hivyo laana unapolaani wanayoyaheshimu wengine na kuyatukuza hakika wao wanaweza kulaani unayoyaheshimu na kuyatukuza. Na kwa maneno mengine: Hakika sababu ambayo ni kauli yake (swt): “Kama hivyo tumewapambia kila umma vitendo vyao,” hata kama imekuja katika mas’ala ya kutukana,131 lakini sababu ni Suratu Nisaa: 50 Suratul-An’am: 108 131 Amesema Mwenyezi Mungu: wala msiwatukane wale wanaomuomba asiyekuwa Mwenyezi Mungu kinyume cha Mwenyezi Mungu na hivyo wakamtukana Mwenyezi Mungu kwa uadui na bila ya elimu, vivyo hivyo tuwameupambia kila umma vitendo vyao kisha kwa Mola wao watarejea na kuwaambia waliyokuwa wanayafanya – Suratul-An’am: 108. 129 130
68
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 68
3/26/2016 12:31:38 PM
Mama wa Waumini
ya jumla na kwa hiyo inasambaza hukumu katika kila sehemu ambayo humo imepatikana sababu, na haya ndio yaliyokubaliwa katika elimu ya Misingi ya Fiqhi, ya kwamba sababu inakuwa ni maalumu na ya jumla. Kama ambavyo kupokewa laana katika Qur’ani tukufu haimaanishi kwamba inapingana na ambayo tumeyataja, hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu amelaani mwelekeo na msingi wa wenye kwenda humo. Kilichopokewa hapa ni utukufu wa mtu au wa kitu, kwa anwani yake ambayo inatengeneza utukufu kwa kundi hili au lile. Na katika Nyanja hii tunakuta kwamba Imamu Ali B pamoja na kwamba alikuwa katika vita na Muawiya kwa sababu ya uasi wa mwisho dhidi ya ukhalifa wa kisharia, na kuchezea kwake amani ya Waislamu na mali zao, jambo ambalo lilikuwa linaweza kupelekea kuondoa uhalisia wa Uislamu kabisa, na baada ya kumwandikia barua nyingi za nasaha na za kumkinaisha na mfano wa hayo, na akabakia katika hali ya uasi na ukaidi na akaandaa jeshi lake, Imamu alikwenda kupigana naye. Pamoja na hivyo tunakuta matukio mawili yanaashiria kwenye lengo kubwa la Uislamu ambalo alikuwa analiendea Imamu Ali B, nalo ni kwamba jeshi lake liwe la Kiislamu na kubeba jukumu la ujumbe. Hapigani kwa msingi wa chuki na bughudha wala hafikirii katu namna ya kumuuwa hasimu, bali anafikiri namna gani atawaongoa. Tukio la kwanza: Ambayo yananukuliwa katika Nahjul-Balaghah, kwamba watu walichelewa kupewa idhini ya kupigana, na akawasikia wanaulizana juu ya sababu ya hilo. Je, yeye anachukia mauti, ambapo alishakuwa mzee na mtu anapokuwa kijana yanakuwa pamoja naye mambo mawili: Pupa na matarajio makubwa. Au Imamu amepata shaka katika uhalali wa vita na hivyo amechelewa kutoa idhini? Akawaambia B: “Ama kauli yenu kuwa: Yote haya yanatokana na kuyachukia mauti? Naapa kwa jina la Mwenyezi 69
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 69
3/26/2016 12:31:38 PM
Mama wa Waumini
Mungu mimi sijali nimeingia kwenye mauti au mauti yamenijia. Ama kauli yenu ya kwamba nimepata shaka juu ya kuwapiga katika vita watu wa Shamu! Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kwamba sijawahi kuacha vita hata siku moja ila ikiwa mimi nina matumaini kuwa kundi la watu likutane na mimi na liongoke kwa mimi, liangaze kwa mwanga wangu japo kwa mtazamo finyu. Na hilo linanipendeza mno kuliko niliuwe kundi la watu hali likiwa ndani ya upotovu, japo kuwa linarejea na dhambi zake.”132 Tukio la pili: Aliposikia B baadhi ya watu miongoni mwa wafuasi wake wanawatukana watu wa Sham wanaowakilishwa na jeshi la Muawiya wakati huo, alisimama akahutubia na akawaambia: “Hakika mimi nachukia kwenu kuwa watukanaji, lakini nyinyi lau mngeelezea vitendo vyao na kuzitaja hali zao, ingekuwa ni sahihi zaidi katika usemi, na udhuru uliofika mahali husika. Na mngesema hivi badala ya kuwatukana: “Ewe Mwenyezi Mungu zihifadhi damu zetu na damu zao na tupatanishe baina yetu na wao na waongoze ili waepukane na upotovu wao, mpaka aitambue haki asiyeijua, na arejee kwenye upotovu na uadui mwenye kuzoea hivyo.”133 Tamko hili linakubainishia utukufu wa moyo wa Kiislamu uliopo kwa Imamu Ali B kinyume na moyo wa kasumba na mfarakano uliopo kwa Waislamu wa leo. Hayo ni pale aliposema: “Na mkasema badala ya matusi yenu kwao: “Ewe Mwenyezi Mungu zihifadhi damu zetu na damu zao na upatanishe baina yetu na wao na waongoze ili waepuke upotovu wao.” Yaani moyo wenu kuwa ni moyo ambao unatafuta ambayo yanawezekana kukusanya baina ya Waislamu na kuwaonyesha wao ukweli kwa mbinu ambazo zinakubalika katika akili za wengine. Hakika tofauti baina yetu na baina ya Imamu Ali B ni kwamba 132 133
Nahjul- Balghah, Hotuba ya 55. Nahjul-Balaghah, Hotuba ya 206 70
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 70
3/26/2016 12:31:38 PM
Mama wa Waumini
Imam Ali alikuwa anaishi kwa kuuonea uchungu Uislamu, na sisi tunaishi na kasumba, hii ndio tofauti ambapo anasema: “Niliogopa nisiponusuru Uislamu na watu wake kuona humo pengo au mvunjiko. Na msiba wake kwangu ni mkubwa zaidi kuliko uongozi wenu ambao hakika ni manufaa ya siku chache tu, yataondoka kwayo yaliyokuwepo, kama yanavyoondoka mazigazi au kama yanavyotawanyika mawingu.”134 Na mjukuu wake, Imamu Ja’far as-Sadiq B alikuwa anawaambia wafuasi wake, na wao ni kigezo chetu: “Ni wepesi ulioje waliyoridhia watu kwenu. Zuieni ndimi zenu kwao.”135 Yaani msitukane na kulaani ili muweze kufunguka katika uhalisia wa kijamii ulio tofauti, na unaovutia watu katika njia hii iliyonyooka kwenu. Lakini sisi kulingana na uhalisia uliopo, sawa yale wanayoyabeba Waislamu Sunni dhidi ya Mashia, au ambayo wanayabeba Waislamu Mashia dhidi ya Sunni, daima tunazungumzia ambayo yanawachochea wao dhidi yetu na wao wanazungumzia juu ya ambayo yanatuchochea sisi dhidi yao, na wakati huo mas’ala yanakuwa ni hamasa na kisasi. Na mas’ala yanaweza kufikia kwenye kukufurishana na kupotoshana, na kumalizikia kwenye mapigano na umwagaji wa damu. Na hususan sisi tunaona katika nyakati hizi ngumu ambazo zinawazunguka Waislamu, mabeberu wa kiulimwengu wanajaribu kuukwaza uhusiano baina ya Waislamu na wanajitahidi kuleta fitina ya mfarakano wa makundi hapa au vita vya kimadhehebu pale. Na kati ya mambo ambayo yanasambaratisha umoja na kupanda chuki ni kujionyesha, mabishano na ugomvi, wepesi wa kulaumu, wingi wa kukosoa na ushauri. Amesema Shahidithani (aliyefariki mwaka 965 Hijiria): “Ria kilugha ni majadiliano ya kujifakharisha wakati wa majadiliano. Na 134 135
Nahjul-Balaghah, Barua ya 62. Al-Kaafiy, Juz. 8, uk. 341. 71
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 71
3/26/2016 12:31:38 PM
Mama wa Waumini
makusudio yake hapa ni majadiliano katika jambo la kidunia au kidini kwa lengo la kuthibitisha ushindi au ubora, kama inavyotokea kwa wengi miongoni mwa wenye kusifika kwa elimu. Na aina hii ni haramu hata nje ya itikafu, na umepokewa msisitizo wa uharamu wake katika nususi. Na jambo hilo kuingizwa katika mambo yaliyoharamishwa katika itikafu, ima ni kwa sababu ya ujumla wa dhana yake au ni kwa ziada ya uharamisho wake katika ibada hii.”136 Na katika hadithi hasan ya Umar bin Yazidi kutoka kwa Abu Abdillahi B amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu 2: “Jibril hakunijia isipokuwa alisema: Ewe Muhammad ogopa chuki za watu na uadui wao.”137 Na kutoka kwa Mas’adatu bin Swadaqatu kutoka kwa Abu Abdillahi B amesema: Amesema AmirulMuuminina B: “Jihadharini na ria na ugomvi, hakika hayo mawili yanatia ugonjwa katika nyoyo za ndugu na kwayo unamea juu yake unafiki.”138
Masaliku al-Ifahaam, Juz. 2, uk. 109. Al-Kaafiy, Juz. 2, uk. 300. 138 Al-Kaafiy, Juz. 2, uk. 300. 136 137
72
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 72
3/26/2016 12:31:38 PM
Mama wa Waumini
Orodha Ya Vitabu Vilivyo Chapishwa Na Al-Itrah Foundation 1. i) Qur’ani Tukufu – Pamoja na Tarjuma ya Kiswahili ii) Qur’an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Thelathini 2. Uharamisho wa Riba 3. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza 4. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili 5. Hekaya za Bahlul 6. Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) 7. Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (a.s.) 8. Hijab vazi Bora 9. Ukweli wa Shia Ithnaashari 10. Madhambi Makuu 11. Mbingu imenikirimu 12. Abdallah Ibn Saba 13. Khadijatul Kubra 14. Utumwa 15. Umakini katika Swala 16. Misingi ya Maarifa 17. Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia 18. Bilal wa Afrika 19. Abudhar 20. Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu 21. Salman Farsi 22. Ammar Yasir 23. Qur’an na Hadithi 24. Elimu ya Nafsi 25. Yajue Madhehebu ya Shia 26. Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur’an Tukufu 73
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 73
3/26/2016 12:31:38 PM
Mama wa Waumini
27. Al-Wahda 28. Ponyo kutoka katika Qur’an 29. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii 30. Mashukio ya Akhera 31. Al Amali 32. Dua kwa Mujibu wa Ahlulbayt (a.s) 33. Udhuu kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna 34. Haki za wanawake katika Uislamu 35. Mwenyezi Mungu na sifa zake 36. Kumswalia Mtume (s) 37. Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) 38. Adhana 39. Upendo katika Ukristo na Uislamu 40. Qur’ani na Kuhifadhiwa Kwake 41. Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu 42. Kupaka juu ya khofu 43. Kukusanya Sala Mbili 44. Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara 45. Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya 46. Kusujudu juu ya udongo 47. Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s) 48. Taraweheas 49. Malumbano baina ya Sunni na Shia 50. Kupunguza Swala safarini 51. Kufungua safarini 52. Umaasumu wa Manabii 53. Qur’an Yatoa Changamoto 54. as-Salaatu Khayrun Mina -’n Nawm 55. Uadilifu wa Masahaba 56. Dua e Kumayl 57. Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu 74
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 74
3/26/2016 12:31:38 PM
Mama wa Waumini
58. Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake 59. Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata 60. Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mtume Muhammad (s) 61. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza 62. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili 63. Kuzuru Makaburi 64. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza 65. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili 66. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu 67. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne 68. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano 69. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita 70. Tujifunze Misingi Ya Dini 71. Sala ni Nguzo ya Dini 72. Mikesha Ya Peshawar 73. Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu 74. Ubora wa Imam ‘Ali na Ushia ndio njia iliyonyooka 75. Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake 76. Liqaa-u-llaah 77. Muhammad (s) Mtume wa Allah 78. Amani na Jihadi Katika Uislamu 79. Uislamu Ulienea Vipi? 80. Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) 81. Dhana ya Ndoa ya Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) 82. Urejeo (al-Raj’ah) 83. Mazingira 84. Utokezo (al - Badau) 85. Hukumu ya kujenga juu ya makaburi 86. Swala ya maiti na kumlilia maiti 87. Uislamu na Uwingi wa Dini 88. Mtoto mwema 75
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 75
3/26/2016 12:31:38 PM
Mama wa Waumini
89. Adabu za Sokoni Na Njiani 90. Johari za hekima kwa vijana 91. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza 92. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili 93. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu 94. Tawasali (AT- TAWASSUL) 95. Imam Mahdi katika Usunni na Ushia 96. Hukumu za Mgonjwa 97. Sadaka yenye kuendelea 98. Msahafu wa Imam Ali 99. Maimamu wa Ahlul Bait – Ujumbe na Jihadi 100. Idi Al-Ghadir 101. Kusoma sura zenye Sijda ya wajibu 102. Hukumu zinazomuhusu mkuu wa kazi na Mfanyakazi 103. Huduma ya Afya katika Uislamu 104. Sunna za Nabii Muhammad (saww) 105. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza) 106. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili) 107. Shahiid Mfiadini 108. Mwanamke Na Sharia 109. Ujumbe -Sehemu ya Kwanza 110. Ujumbe - Sehemu ya Pili 111. Ujumbe - Sehemu ya Tatu 112. Ujumbe - Sehemu ya Nne 113. Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu 114. Hadithi ya Thaqalain 115. Ndoa ya Mutaa 116. Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza 117. Ukweli uliopotea sehemu ya Pili 118. Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu 119. Ukweli uliopotea sehemu ya Nne 76
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 76
3/26/2016 12:31:38 PM
Mama wa Waumini
120. Ukweli uliopotea sehemu ya Tano 121. Mkutano wa Maulamaa wa Baghdad 122. Safari ya kuifuata Nuru 123. Fatima al-Zahra 124. Myahudi wa Kimataifa 125. Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi 126. Visa vya kweli sehemu ya Kwanza 127. Visa vya kweli sehemu ya Pili 128. Elimu ya Ghaibu ya Maimamu 129. Mwanadamu na Mustakabali wake 130. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Kwanza) 131. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Pili) 132. Khairul l’Bariyyah 133. Uislamu na mafunzo ya kimalezi 134. Vijana ni Hazina ya Uislamu 135. Adhana ni Ndoto au ni Wahyi? 136. Tabaruku 137. Saada Kamili – Kitabu cha Kiada cha Maadili 138. Vikao vya furaha 139. Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje? 140. Visa vya wachamungu 141. Falsafa ya Dini 142. Kuhuzunika na Kuomboleza 143. Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah 144. Mjadala wa Kiitikadi 145. Kuonekana kwa Allah 146. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza) 147. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili) 148. Ndugu na Jirani
77
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 77
3/26/2016 12:31:38 PM
Mama wa Waumini
149. Ushia ndani ya Usunni 150. Maswali na Majibu 151. Mafunzo ya hukmu za ibada 152. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 1 153. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 2 154. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 3 155. Abu Huraira 156. Vipengee kadhaa katika Swala ya Jamaa na Msikiti. 157. Mazingatio kutoka katika Qur’an - Sehemu ya Kwanza 158. Mazingatio kutoka kaitka Qur’an - Sehemu ya Pili 159. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya kwanza 160. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya Pili 161. Shia na Qur’ani – Majibu na Maelezo 162. Falsafa ya Mageuzi ya Imam Husein (a.s) 163. Amali za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani 164. Elimu ya Tiba za Kiislamu - Matibabu ya Maimamu 165. Uislamu Safi 166. Majlisi za Imam Husein Majumbani 167. Je, Kufunga Mikono 168. Uislam wa Shia 169. Amali za Makka 170. Amali za Madina 171. Asili ya Madhehebu katika Uislamu 172. Sira ya Imam Ali kuhusu Waasi 173. Ukweli uliofichika katika neno la Allah 174. Uislamu na Mifumo ya Uchumi 175. Umoja wa Kiislamu na Furaha 176. Mas’ala ya Kifiqhi 177. Jifunze kusoma Qur’ani 178. as-Sahifatul Kamilah as-Sajjadiyyah 179. Hayya ‘Alaa Khayri’l-’Amal Katika Adhana 78
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 78
3/26/2016 12:31:38 PM
Mama wa Waumini
180. Ukweli kuhusu Funga ya Siku ya Ashura 181. Dua za Miezi Mitatu Mitukufu (Rajabu, Shaabani na Ramadhani) 182. Uadilifu katika Uislamu 183. Mahdi katika Sunna 184. Maswali Ya Uchunguzi Kuhusu Uislam 185. Kazi na Bidii ni njia ya maendeleo 186. Abu Talib – Jabali Imara la Imani 187. Ujenzi na Utakaso wa Nafsi 188. Vijana na Matarajio ya Baadaye 189. Historia maana na lengo la Usalafi 190. Ushia – Hoja na Majibu 191. Mateso ya Dhuria wa Mtume (saww) 192. Maombolezo – Msiba wa Bwana wa Mashahidi (a.s.) 193. Shahidi kwa Ajili ya Ubinadamu 194. Takwa 195. Upotoshaji Dhahiri katika (Turathi) Hazina ya Kiislamu 196. Amirul Muuminina (as) na Makhalifa 197. Tawheed Na Shirki 198. Kuvunja hoja iliyotumika kutetea Uimamu wa AbuBakr 199. Adabu za vikao na mazungumzo 200. Hija ya Kuaga 201. Uwazi baina ya Maslahi na Vikwazo 202. Fadhila za watukufu watano katika Sahih Sita 203. Mdahalo baina ya Mwanachuoni wa Kisunni na Kishia (Al- Muraja’aat) 204. Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (as) 205. Imam Husain ni Mfumo wa Marekebisho na Mageuzi 206. Mtazamo kuhusu msuguano wa Kimadhehebu 207. Nchi na Uraia – Haki na wajibu kwa Taifa 208. Mtazamo wa Ibn Taymiyyah juu ya Imam Ali (as) 209. Uongozi wa Kidini – Maelekezo na Utekelezaji wa Kijamii 210. Maadili ya Ashura 79
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 79
3/26/2016 12:31:38 PM
Mama wa Waumini
211. Mshumaa – Shahidi na Kifo cha Kishahidi 212. Mizani ya Hekima – Hadithi za Ahlul Bait (as) – Sehemu ya Kwanza 213. Imam Ali na Mambo ya Umma 214. Imam Ali na Mfumo wa Usawa 215. Uimamu na Tamko la Kutawazwa 216. Mfumo wa Wilaya 217. Vipi Tutaishinda Hofu? 218. Kumswalia Mtume ni Ufunguo wa Utatuzi wa Matatizo 219. Maeneo ya Umma na Mali Zake 220. Nahju ‘L-Balagha – Majmua ya Khutba, Amri, Barua, Risala, Mawaidha na Semi za Amirul-Muuminin Ali bin Abu Talib (a.s.) 221. Mukhtar – Shujaa aliyelipiza kisasi dhidi ya wauaji wa Imam Husein (as) hapo Karbala 222. Mazingatio Katika Swala 223. Imam Hasan na Mfumo wa Kujenga Jamii 224. Vyakula Na Vinywaji 225. Kuelewa Rehema ya Mwenyezi Mungu 226. Imam Mahdi na Bishara ya Matumaini 227. Mtazamo Mpya - Wanawake katika Uislamu 228. Shia Na Sahaba - Majibu na Maelezo 229. Majanga Na Jukumu la Jamii 230. Shia Na Hadith - Majibu na Maelezo 231. Upotofu Ndani ya Kitabu cha Mitaala kwa Shule za Sekondari 232. Ugaidi Wa Kifikra Katika Medani Ya Kidini 233. Yafaayo kijamii 234. Uswalihina Dhahiri Na Batini Yake 235. Mkakati wa Kupambana na Ufakiri 236. Mwanamke Katika Harakati Za Mageuzi 237. Jihadi 238. Hija Katika Maneno Na Ujumbe Wa Imam Khomeini (R.A) 239. Tiba Ya Maradhi Ya Kimaadili
80
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 80
3/26/2016 12:31:38 PM
Mama wa Waumini
240. Yusuf Mkweli 241. Taqiyya Kwa Mujibu Wa Sheria Ya Kiislamu 242. Imam Mahdi (A.S) Imam Wa Zama Hizi Na Kiongozi Wa Dunia 243. Talaka Tatu 244. Safari Ya Kuelekea Kwa Mwenyezi Mungu 245. Hotuba Za Kisslamu Juu Ya Haki Za Binadamu 246. Mashairi Ya Kijamii 247. Ngano Ya Kwamba Qur’ani Imebadilishwa 248. Wito Kwa Waumini: “Enyi Mlioamini” 249. Imam Husain (a.s) ni Utu na Kadhia 250. Imam Husain ni Kielelezo cha Kujitoa Muhanga na Fidia
81
04_16_Mama za waumini_26_March_2016.indd 81
3/26/2016 12:31:38 PM