Maswali na mishkili elfu 6

Page 1

Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali Na Mishkili Elfu (Alfu Suaal wa Ishkaal)

Kuuliza na Kudadisi Kielimu katika Qur’ani ni Haramu Sehemu ya Sita

Kimeandikwa na: Sheikh ‘Ali al-Kuraani al-Aamili

Kimetarjumiwa na: Ustadh Abdallah Mohamed

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

B

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

©Haki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: 978 - 9987 - 512 - 55 - 3 Kimeandikwa na: Shaikh ‘Ali al-Kuraani al-Aamili Kimetarjumiwa na: Ustadh Abdallah Mohamed Kimehaririwa na:

Hemedi Lubumba Selemani Kimepangwa katika Kompyuta na: Hajat Pili Rajab Toleo la kwanza: April, 2011 Nakala: 1000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Nukushi: +255 22 2127555 Barua Pepe: alitrah@raha.com Tovuti: www.alitrah.org Katika mtandao: www.alitrah.info

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

YALIYOMO Mas’ala 97 Kila mwanafunzi wa dini wa Kisuni anastahili mijeledi na kutengwa kwa mujibu wa fatwa ya Umar..........................................................2

Mas’ala 98 Majini mashetani na wapenzi wao waikhofia Bismillahi.................5

Mas’ala 99 Kukanganywa kwa wapinzani wa Ahlul-Bayt juu ya masuala yote yanayohusiana na Bismillahi.............................................................7

Mas’ala 100 Kupagawa kwa wapinzani wa Ahlul Bayt juu ya kusoma Bismillahi kwa sauti .........................................................................................14

Mas’ala 101 Ahlul-Bayt wanapambana kwa ajili ya Bismillahi. Na Bismillahi ni Aya tukufu mno katika Qur’ani na sura ya Al-Hamdu ndio saba’u mathani............................................................................................17

Mas’ala 102 Kutia shaka kwao juu ya sura muawidhataynin na kutoamua kuwa hizo ni Qur’ani................................................................................23

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Mas’ala 103 Sura mbili za Hifdi na khali badala ya muawidhatayni alikuwa akiziswalia Umar.............................................................................32

Mas’ala 104 Fungua misahafu yenu muisahihishe au mkataeni Bukhari na Umar................................................................................................40

Mas’ala 105 Aya za Aisha zilizoliwa na wanyama

wafugwao nyum-

bani..................................................................................................45

Mas’ala 106 Jaribio la Umar la kugeuza Aya.......................................................48

Mas’ala 107 Riwaya zenu sahihi zinazopingana

kuhusu sehemu ya Qur’ani

iliyoshuka mwisho...........................................................................62

Mas’ala 108 Wamedai kwamba Qur’ani itaondolewa kutoka duniani, Al-Kaaba itavunjwa na Makka itaharibiwa.................................................... 76

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

NENO LA MCHAPISHAJI Kitabu kilichoko mikononi mwako, ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabu kwa jina la Alfu Suaal wa Ishkaal - sisi tumekiita Maswali na Mishkili Elfu kilichoandikwa na Shaikh ‘Ali al-Kuraani al-Aamili na tumekigawa katika mijalada sita, na hili ulilonalo sasa ni jalada la sita. Madhehebu ya Shia Ithnaasharia imekuwa ikishutumiwa na Waislamu wengine shutuma ambazo hazina msingi wala hazimo katika imani na itikadi zake. Shutuma hizi zimekuwa zikirudiwa mara kwa mara licha ya kutolewa majibu madhubuti na yakinifu na wanavyuoni wa zamani na wa sasa. Kutokana na kasumba hii, mwandishi wa kitabu hiki ameamua kukusanya maswali na mishkili elfu moja kutoka kwenye vitabu vya Kisunni na kutoa hoja kabambe kuzijibu shutuma hizo wanazozuliwa wafuasi wa madhehebu ya Shia. Katika kulitekeleza jukumu hili, mwandishi ametegemea rejea zao za msingi kutoka katika (vitabu vya) hadithi, tafsiri, fikihi na itikadi, na kauli za viongozi wao wakubwa kuanzia wa zamani hadi wa sasa. Sisi tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu. Katika wakati ambao maadui wa Uislamu na Waislamu wameamua kuungana ili kuubomoa Uislamu, na katika kutekeleza azma yao hii mbinu yao kubwa ni kutumia hitilafu zetu za kimadhehebu; hivyo, tunakitoa katika lugha ya Kiswahili ili wasomaji wetu wa Kiswahili wapate kufaidika na yaliyomo katika safu hii ya masomo na kuongeza ujuzi wao katika masuala ya kidini na ya kijamii.

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Tunamshukuru ndugu yetu, Abdallah Mohamed kwa kukubali kuchukua jukumu hili la kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwa kitabu hiki. Mchapishaji: Al-Itrah Foundation S. L. P. 19701 Dar-es-Salaam, Tanzania.

G

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

UTANGULIZI Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu. Kila sifa njema ni ya Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu. Rehema kamilifu zimfikie bwana wetu na Mtume wetu Muhammad na kizazi chake kitakatifu kitoharifu. Na daima laana ya Mwenyezi Mungu iwe juu ya madui zao wote. Wasiokuwa wafuasi wa madhehebu ya Ahlul-Baiti (a.s.) wametoa baadhi ya mishkeli na utata wao juu ya madhehebu ya haki na wafuasi wake, na wameendelea kurudia hilo ndani ya hotuba zao na vitabu vyao na hatimaye wakayajaza masoko mishkeli hiyo na utata huo, wakailundika kwenye tovuti huku wakisambaza vijitabu na mikanda kwa mahujaji na wafanya ziara huko Makka na Madina na kwenye miji mingine ya waislam. Wanavyuoni na wasomi wa Kishia kuanzia wa zamani hadi wa sasa wamejibu mishkeli hiyo na utata huo, hivyo tunamuomba Mwenyezi Mungu awalipe malipo bora mno kwa kitendo cha kuwatetea Ahlul-Baiti watoharifu waliodhulumiwa kwa ajili ya kutetea madhehebu yao ya haki. Maswali haya na mishkeli hii ya kielimu tumeiandika ili iwe ni majibu dhidi ya utata wanaouzusha juu yetu, na ili tuweze kuwazindua kuwa kilicho bora zaidi kwao ni kutatua kwanza mishkeli na migongano iliyosheheni ndani ya vitabu vyao vya rejea, ambavyo ndio msingi wa fikra za waandishi wao na watafiti wao katika fani ya akida, fiqhi na tafsiri zao, kwani ni bora kutengeneza nyumbani kabla ya kuanza kukosoa kwa jirani. H

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

(Pia kabla hujatoa kijiti kwenye jicho la mwenzako kwanza toa boriti kwenye jicho lako). Ndani ya mishkeli hii tumetegemea rejea zao za msingi katika Hadithi, tafsiri, fiqhi, akida na kauli za viongozi wao wakubwa kuanzia wa zamani hadi wa sasa. Ama katika kusanifu milango yake tumetegemea vitabu: Mawahabi na Tawhid, uandikwaji wa Qur’ani, akida za Kiisilamu na Aya za tukio la Ghadiri na nyinginezo. Ama mfumo tuliouchagua ni kuhariri suala husika kwa ibara nene inayothibitishwa kwa rejea zao, kisha suala hilo tunalitolea maswali na mishkeli, na hapo msomaji na mtafiti anapata wepesi. Kusudio langu na tawfiki ni kwa Mwenyezi Mungu, na ndiye aongozae kwenye njia sahihi. ‘Ali al-Kuraani al-Aamili Shawwal/Mfunguo mosi mtukufu 1423.

I

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

Mas’ala 97 Kila mwanafunzi wa dini wa kisunni anastahili mijeledi na kutengwa, kwa mujibu wa fatwa ya Umar Wanavyuoni wao wameafikiana juu ya kusihi kwa kadhiya ya Sabiigh Tamimi aliyekuwa kiongozi wa watu wake, akamuuliza Umar juu ya maana ya Aya za Qur’ani, Umar akakasirika, akaamrishwa apigwe kwa makole ya mtende mbichi kichwani kwake na mwilini mwake, mpaka itoke damu kichwani kwake na kuchuruzika mgongoni kwake na kupata majeraha. Kisha akaamrisha atiwe gerezani mpaka apone majeraha yake kisha arudiwe kupigwa kama mwanzo, kisha kuamriwa kuvaa vazi kama mfuko (taban) na kubebwa juu ya ngamia na kupelekwa kwa watu wake akizungushwa na pia katika koo zingine, na huku mtu akinadi kuwa Sabigh alikosea katika elimu akakalifisha yaliyotosha na yaliyofichwa, na anyimwe riziki yake na anavyopewa kutoka Baytul-mali na mtu yeyote asikae naye, asiuziane na mtu yeyote, akiumwa asitembelewe na akifa mtu yeyote asishuhudie jeneza lake. Janga la Sabigh lilipokewa na zaidi ya riwaya thelathini, na mafakihi wakasema ni sahihi... Katika hizo ni aliyopokea Darami Juz. 1, Uk. 54: “Kutoka kwa Suleiman bin Yasar kwamba mtu aitwaye Sabigh alikwenda Madina, akawa anauliza juu ya Aya mutashabih za Qur’ani, Umar akamwita kwake akaletwa akiwa amemuandalia makole ya mtende akamuuliza: “Ni nani wewe?” Akajibu: “Mimi ni Abdallah Sabigh.” Umar akachukua kole moja akampiga nalo, akasema: Mimi ni Abdallah bin Umar,” alimpiga mpaka akamtoa damu kichwani. Akasema: Eee Amirul-muminina, yatosha, kimeondoka kile kilichokuwa kichwani kwangu!”

2

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

Na imepokewa kutoka kwa Naafii’, huria wa Abdallah: “Umar akaagiza vikoto vya mtende akampiga navyo mpaka mgongo wake ukawa na alama, kisha akamwacha mpaka akapona, kisha akamrudia kisha akamwacha mpaka akapona, akamwita ili amrudie. Akasema Sabigh: “Ukiwa unataka kuniua basi niue kifo kizuri, na ukitaka kuniponya basi Wallahi nimepona.” Akamruhusu kwenye ardhi yake na akamuandikia Abu Musa Al-Ash’ari kwamba huyo asikae na mtu yeyote katika waislamu. Na katika Kanzul Ummali Juz. 2, Uk. 331: Akamsimamia akaendelea kumchapa mjeledi mpaka kilemba chake kikaanguka, akasema: “Naapa kwa yule ambaye nafsi ya Umar iko mikononi mwake, lau ningelikupata umenyoa basi ningelikupiga kichwa chako, mvalisheni nguo na mchukueni msobe msobe na mtoeni mpaka mumpeleke kwenye mji wake, kisha asimame mhutubu na aseme: “Sabigh alitaka ilimu na akaikosea.” na akaendelea kuwa dhalili kwa watu wake mpaka alipokufa ilhali alikuwa ni bwana wao (Ameipokea Ibnul Anbari katika Masahif, na Nasru Muqaddasi katika Al-Hujja, na Lalkani, na Ibn Asakir). Katika Al-Mughni cha Ibnu Quddama amesema katika Uk. 12, Juz. 80: “Dhahiri ya maneno ya Ahmad na Al-Kharqi ni kwamba haizingatiwi katika kuthibiti hukmu za toba kuanzia kukubali Ushahidi na kusihi uwalii katika ndoa ni kusuluhisha amali. Nayo ni moja ya kauli mbili za Shafi, na katika kauli nyingine huzingatiwa kuwa ni kutengeneza amali, na kwamba Umar alipompiga Sabigh aliamuru kuhamishwa mpaka ilipomfikia habari ya kutubu kwake, akaamuru mtu yeyote asiseme naye ila baada ya kupita mwaka. Nasi tuna kauli yake (a.s.): “Mwenye kutubu dhambi ni kama asiye na dhambi.” na kwamba msamaha hupatikana kwa kule kutubu, na pia hukmu, na kwamba toba ya shirki katika Uislamu haihitajii kuzingatiwa yaliyo kabla yake, nalo ni katika dhambi kubwa zaidi ya yote, hivyo lililo chini yake ni bora zaidi.”

3

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

Kisha Ibnu Quddama akavunja jengo lake la kifikhi la mwanzo, akasema: “Kilichotajwa kutoka kwa Umar juu ya haki ya Sabigh ilikuwa ni kwa sababu alitubu kutokana na bidaa, na toba yake ilikuwa ni kwa sababu ya kipigo na kuhamishwa. Inachukuliwa kuwa alidhihirisha toba ili kuficha. Hiyo ni kinyume na suala letu. Ametaja Kadhi kwamba mwenye kutubu kutokana na bidaa huzingatiwa kwa kule kupita mwaka, hiyo ni kutokana na Hadith ya Sabigh aliyoipokea Ahmad…. Na sahihi ni kuwa kutubu kutokana na bidaa ni kama kwingine tu, ila iwe toba kwa kitendo kinachofanana na kulazimisha kama kutubu kwa Sabigh, huhitaji muda ili idhihiri kwamba toba yake imetokana na ikhlasi, na si kwa kulazimishwa.” Na hivi wameoanisha mafakihi kwa Sabigh aliyedhulumiwa kuwa lazima upite kwake mwaka ili ijulikane kwamba yeye amejiepusha na aliokuwa akiwapenda katika watu wa bidaa’ na kumpenda aliyekuwa akimfanyia uadui katika Ahlu Sunna, lakini hakuwa na kikundi ila Ahlu Sunna na kama alikuwa na kikundi itajulikana vipi kuwa yeye aliwaepuka ilihali yeye amekatzwa kukaa nao na kuzungumza nao?

Maswali Vipi mnafafanua urahisishaji wa Umar katika kuisoma Qur’ani kwa aina saba za qiraa, na wakakati huo huo anaharamisha utafiti wa kielimu ndani ya Qur’ani na kuuliza kuhusu Aya zake? Je mwamuona kuwa Umar alikuwa amepatia aliyomfanyia Sabigh au alikosea? Kwa nini hamtekelezi hukmu ya Umar kwa wanafunzi wenu wanaouliza juu ya maana za Aya za Qur’ani, na kwenu wenyewe? Vipi toba ya shirki isihi kwa mtu kutangaza tu na isisihi kwa Sabigh ila 4

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

baada ya kupita mwaka? Kwa kipi mnafafanua uharamishaji wa Umar kuuliza na kutafiti kielimu katika Qur’ani, hivi hamchukulii kuwa sababu ya hilo ni uchache wa elimu yake? 11. BISMILLAHI AYA KUU KATIKA KITABU CHA MWENYEZI MUNGU, LAKINI WAMEIFICHA NA KUIKANUSHA

Mas’ala 98 Majini, mashetani na wapenzi wao waikhofia Bismillahi Bismillahi ilikuwa ni silaha kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kwa Mtume wake ya kuwafukuzia mashetani wa kikuraish, hivyo pale walipokuwa wakikusanyika mlangoni kwake ili wamtukane au wamuudhi alikuwa akipaaza sauti yake kwa Bismillahi, wakawa wanageuka wakikimbia. Katika Al-Kafi Juz. 8, Uk. 266 kutoka kwa Imam Sadiq (a.s.) amesema: “Wameificha Bismillahi Rahmani Rahiim Wallahi wameficha bora ya majina, alikuwa Mtume anapoingia nyumbani kwake na makurasish wakimkusanyikia, alikuwa akipaaza sauti, na makuraish hukimbia. Mwenyezi Mungu akateremsha: “Na unapomtaja Mola wako katika Qur’ani peke yake basi wao hugeuza migongo yao kwa chuki.” (Israi :46). Na katika Al-Kafi Juz. 2, Uk. 624 kutoka kwake (a.s.) amesema kumwambia Al-Mufaddhal bin Amru: “Ee Amru, jilinde na watu wote kwa Bismillahi na kwa Qul huwa llahu isome kwa upande wako wa kulia na wa kushoto na mbele yako na nyuma yako, na juu yako na chini yako, unapoingia kwa mfalme jeuri isome mara tatu unapomtazama, na ufumbe mkono wako wa kushoto usiufungue mpaka utokapo kwake.” 5

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

Katika mwaka wa nane wa Hijra Mtume (s.a.w.w.) aliwashtukiza mushrikina wa Makka kwa jeshi lenye wapiganaji elfu kumi, na kuwalazimisha kuacha silaha zao na kusalimu amri, na akawahiyarisha baina ya Uislamu na kuuwawa, wakasilimu hali ya kuwa hawajaridhika, akawasamehe na kuwaita kuwa ni walioachwa huru. Na baada ya ushindi wa Makka walioachwa huru wakawa wengi huko Madina, na wakafanya bidii wawe ni wengi na wenye nguvu, na hatimaye baada ya Mtume (s.a.w.w.) wakaweza kuchukua ukhalifa wake katika Saqifa. Lakini hofu yao dhidi ya Bismillahi ilibaki, yule aliyekuwa jana akimuudhi Mtume (s.a.w.w.) na anapomsomea Bismillahi anatetemeka viungo vyake na kukimbia, inakuwa ni vigumu kwake kustahamili kuisikia leo kutoka kwa Nabii (s.a.w.w.) katika msikiti wake wa Madina, kama ambavyo ni vigumu kwake kuisoma baada ya Mtume (s.a.w.w.) na kuidhihirisha waziwazi. Kuteswa na Bismillahi wale walioachwa huru kulidhihiri baada ya Mtumne (s.a.w.w.), kwani wao waliiharamisha kuisoma kwa sauti katika Swala, yaani waliiondoa kivitendo ndani ya Swala. Na hii ndio maana ya kauli ya Imam as-Sadiq (a.s.): “Wameificha Bismillahi Rahmani Rahiim, Wallahi wameficha bora ya majina...”. Na inaonekana wao walimkinaisha Abu Bakr na Umar kwa hili, wakaiacha. Imepokewa kutoka kwao kwamba wawili hao waliiacha katika Swala zao. Na imepokewa kutoka kwao kwamba waliisoma, na hiyo hapana budi itakuwa ni kabla ya kuthibitisha kuiondoa. Kisha wakaeneza maneno yao kuwa Mtume (s.a.w.w) alikuwa haisomi kwa sauti mpaka kufikia kusema kuwa Bismillahi si katika Aya za Qur’ani kama utakavyoona. Nawawi amesema katika Majmuu Juz. 3, Uk. 343: “Wamesema: Kwa sababu kuisoma kwa sauti kumefutwa. Amesema Said bin Jubayr: “Mtume alikuwa akiisoma Bismillahi kwa sauti huko Makka na watu wa 6

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

Makka walikuwa wakimwita Musaylamatu Rahman, wakasema: “Muhammad anamuomba mungu wa Yamama.’’ Mtume akaamuru kuificha. Kuanzia hapo hakuidhihirisha tena mpaka alipokufa. Wamesema: “Daru Qutni alipotunga kitabu Misri juu ya kudhihirisha walimuuliza akasema: “Haikusihi katika kudhihirisha sauti.” Wakasema: “Baadhi ya tabiina wamesema: Kudhihirisha sauti ni bidaa. Wamesema kwa kulinganisha na kujilinda. Tunaona kuwa wao wamekubali juu ya Mtume kusoma kwa sauti kwa huko Makka na wakadai kwamba wahyi umeifuta kwa sababu ya Musaylama kabla halijapatikana jina la Musaylama. Na baadhi ya tabiina ambao walisema kuwa kutoa sauti ni bidaa, basi ni yupi atakuwa si katika baadhi ya walioachwa. Ama kauli ya Daru Qutni ni taasubu na utakuja kujua kuwa watu wa Shafii na wengineo wamepokea Hadithi sahihi kutoka kwa Abu Hurayra na Anas huko Madina kwamba Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akiisoma kwa sauti!

Mas’ala 99 Kukanganywa kwa wapinzani wa Ahlul-Bayt juu ya masuala yote yanahohusiana na Bismillahi. Mafakihi wa madhehbu ya Ahlul-Bayt wamesema: “Bismillahi ni Aya kuu zaidi katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu, nayo ni Aya katika SuratulFat’ha na ni Aya ya Sura zote ila Sura ya Baraa’a. Na ameafiki katika hilo Shafii, Zahri, Ataau na Ibn Mubarak tu! Na ni mustahabbu kwetu kuisoma kwa sauti ya wazi, iwe ni katika Swala ya kusoma kwa sauti au ya kusoma kwa kunong’ona. (rejea kitabu Tadhkiratul Fuqahaa cha Allama Hilli Juz. 1, Uk. 114).

7

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

Ama wafuasi wa madhehebu mengine wamekanganywa na kila yanayohusiana na Bismillahi, wakahitilafiana kuwa: Je hiyo ni katika Qur’ani? Au imezidi ili kupambanua kati ya Sura? Je hiyo ni katika Qur’ani kwa kukata shauri au kwa njia ya kudhani? Je ni sehemu ya Sura ya Al-Hamdu au si sehemu? Je ni sehemu ya kila Sura au sio? Je inasomwa katika Swala au la? Je inasomwa kwa sauti au la? Kila moja kati ya mas’ala haya ina vipengele ambavyo wao wamehitilafiana pia kwavyo, mpaka rai na fatwa zao juu ya Bismillahi zimekuwa nyingi mno. Ukitaka dalili ya kila rai kutoka katika Hadith za Mtume utaikuta imeandaliwa, na zote ni zenye sanad sahihi, na dalili za wazi juu ya kuthibitisha au kukanusha, hakuna tofauti. Ama dhana na mapendekezo na utoaji hukumu, hayo ni mengi, na katika hayo kuna yale ambayo hayakuingiii akilini mwako. Mfano dalili zao juu ya Bismillahi kutokuwa ni Qur’ani kwa Hadith ya Mtume inayosema kuwa Mwenyezi Mungu ameigawanya Sura ya Al-Hamdu baina yake na mja wake. Abu Hanifa akasema: “Mtume (s.a.w.w) alianza mazungumzo kwa kuzisherehesha Aya za Sura ya Al-Hamdu kutoka Aya (Al-hamdu lillahi) si kwenye Bismillahi, hii ni dalili ya kuwa Bismillahi si katika Aya za Qur’ani. Na akatoa dalili kuwa kigawanyo ni lazima kilingane, inakuwa Al-Hamdu ina Aya sita, na pamoja na Bismillahi ina Aya saba, kwa hivyo haiwezi kugawanyika mara mbili sawa sawa, Na Bismillahi si Aya, na Sab’ul mathani si Sura ya Al-Hamdu.” As-Sarkhasi amesema katika Al-Mabsut Juz. 1, Uk. 15 akitetea rai ya Abu Hanifa: “Na mas’ala haya kwa hakika yanajengea kuwa Bismillahi si Aya katika mwanzo wa Sura ya Fat’ha, wala mwanzo wa Sura zingine kwetu, 8

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

kwa kuwa alikuwa akiihisabu Aya ya Iyyaka naa’budu wa iyyaka nastai’iinu, kuwa ni Aya…, Nasi tuna Hadith ya Abu Hurayra kutoka kwake kwamba Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akisema kuwa Mwenyezi Mungu amegawanya Swala baina yangu na mja wangu nusu mbili, mja anaposema alhamdu lillahi Rabbil a’aalamiina Mwenyezi Mungu husema: Mja wangu amenihimidi.... Kuanza na kauli ya Alhamdulillahi Rabbil a’aalamina ni dalili ya kuwa Bismillah si Aya katika mwanzo wa Sura ya Al-Fatiha. Kwani lau itakuwa ni Aya mwanzoni mwa Sura ya Fatiha basi mgawanyo wa nusu kwa nusu hauwezi kutimia, kwani itakuwa katika nusu ya kwanza kuna Aya nne ila nusu, ilihali imetajwa kugawanywa nusu mbili. Na masalafi wameafikiana kuwa Sura ya Kawthar ina Aya tatu, na tatu hizo ni bila ya Bismillahi. Na kwa kuwa daraja ya chini kabisa ya hitilafu ya Hadith na wanavyuoni ni kuleta shubha na Qur’ani haithibitiki kwa shubha, kwani njia yake ni ya yakini.” Ametoa fatwa Abu Hanifa na mfuasi wake Sarkhi kuwa, hainasibu kwa imamu wa madhehebu kama yeye na mfano wake na wala mtafutaji elimu achague Hadithi moja katika maudhui na kuifafanua kama anavyodhani, na kujengea madhehbu juu yake. Lakini ni kwa nini basi amezifumbia macho hadithi nyingi zilizo sahihi na zilizo sahihi na wazi? Imewapita kwamba: Mtume kuanza na Aya ‘Al-hamdu’ inaweza kuwa ni kule kusahau kwa mpokezi yale aliyoyasema (s.a.w.w.) kwenye Bismillahi, na hata kama itasihi kuwa alianza na hiyo ‘Al-hamdu’ basi hakuna dalili ya kuiua Bismilllahi na kuzipinga Hadith zinazothibitisha kuwa yenyewe ni sehemu ya Sura Al-Hamdu, nazo ni hadithi sahihi kwao! Imewapita kwamba: Kugawanya nusu mbili kati ya Mola na mja wake katika Sura Al-Hamdu ni kugawanywa kimaana na si kwa kimaneno, si kule kwa kuhesabu herufi na maneno. 9

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

Na Sarkhasi atuambie ni Salafi gani hao waliokusanyika katika kuihesabu Sura ya Kawthar kwenye Aya tatu. Ni kama yeye hajasoma hitilafu ya maneno ya waliohisabu, na rai za wengine zikajengeka juu ya misingi ya kuijumuisha Bismillahi na wengine juu ya kuiacha. Na wengine kuziunganisha baadhi ya Aya na kuzipambanua. Baya zaidi alilosema Sarkhani ni kauli yake: “Kwa kuwa daraja ya chini kabisa ya hitilafu ya Hadith na wanavyuoni ni kuleta shubha na Qur’ani haithibitiki kwa shubha.” Anasema maadam iko shaka japo ndogo juu ya kuwa Bismillahi ni katika Aya za Qur’ani katika Sura Al-Hamdu na mwanzo wa Sura zingine kutokana na hadithi au kauli ya mmoja wa wanavyuoni, basi kuwa kwake ni Qur’ani kumetetereka na hivyo isihisabiwe kuwa ni katika Qur’ani!!! Je yeye anaamini hivyo katika Sura za Muawidhtayni? Vyovyote itakavyokuwa, nimesikitika sana kwa kuwa nimepoteza wakati katika kufuatilia rai zao kuhusu Bismillahi, na sipotezi tena wakati wa msomaji, natosheka na mfano mdogo toka kwenye kitabu Al-Majmuu cha An-Nawawi, kwani naye pia amechafua kurasa nyingi katika maudhui hii kama wengine. Na hainipiti niashirie kwamba wapinzani wa Ahlul-Bayt pamoja na hitilafu yao na kugongana maoni yao juu ya Bismillahi lakini wameafikiana kuwa mwenye kupinga kuwa ni katika Qur’ani hahukumiwi kwa ukafiri, na mwenye kuithibitisha kwa upande wa dhana hahukumiwi kwa ukafiri, na mwenye kuthibitisha kwa upande wa kukata shauri kama akiwa ni katika ulamaa basi huyo huhukumiwa ni kafiri, na kama akiwa ni katika watu wa kawaida, baadhi yao wanamuhukumu kwa ukafiri na baadhi yao kwa uislamu! Bismillahi mwanzoni mwa Sura kwao si katika Qur’ani, na anayesema kuwa ni katika Qur’ani, husema nadhani, na sikati shauri Ibn Quddama amesema katika Al-Mughni Juz. 1, Uk. 522: “Imepokewa 10

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

kutoka kwa Ahmad kwamba hiyo si katika Sura Al-Hamdu wala si Aya katika sura nyingine na haipasi kuisoma katika Swala, nayo ni kauli ya Abu Hanifa, Malik, na Awzaai’, Abdallah bin Muubad Ar-Ramani. Na wamehitilafiana kutoka kwa Ahmad juu ya hilo ikasemwa kutoka kwake kuwa hiyo ni Aya pekee ilikuwa ikishuka kati ya Sura mbili ili kutenganisha kati ya sura. Na imepatikana kutoka kwake (Ahmad) kuwa hiyo ni katika kipande cha Aya katika Sura Namli. Vilevile Abdallah bin Maabad na Awzai wamesema: “Mwenyezi Mungu hakuteremsha Bismillahi ila katika Sura.

An-Nawawi amesema katika Majmuu, Juz. 3, Uk. 333: “Kisha je hiyo katika Al-Fatiha na nyinginezo ni Qur’ani kwa njia ya kukata shauri kama Qur’ani nyingine, au ni kwa njia ya hukmu kwa kuhitilafiana wanavyuoni kwayo? Kuna njia mbili zinazojulikana kwa watu wetu, amezieleza AlMuhamili na mwandishi wa Al-Hawi na Al-Bandiniji. Moja wapo ni kwa njia ya hukmu kwa maana ya kuwa haisihi Swala ila kwa kuisoma mwanzo wa Sura Al-Fatiha, na hawi ni mwenye kuisoma Sura nyingine kiukamilifu ila atakapoianza sura hiyo kwa Bismillahi. Na sahihi ni kuwa hiyo si kwa njia ya kukata shauri, kwani hakuna hitilafu kwa waislamu kwamba mwenye kuikanusha hakufurishwi, hivyo lau ingelikuwa ni Qur’ani kwa kukata shauri basi angekufurishwa kama yule mwenye kuzikanusha nyingine........ Imam wa haram mbili ameidhoofisha na wengineo kauli ya anayesema kwamba hiyo ni Qur’ani kwa yakini, akasema huu ni ujinga mkubwa wa anayesema hivyo, kwani anadai yakini ilihali hakuna kiyakinifu..... Na Malik, Abu Hanifa, Daud na Awzai wamesema: Bismillahi si Qur’ani mwanzoni mwa sura zote, si katika Sura Al-Fatiha wala nyingineyo. 11

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

Ahmad akasema, hiyo ni Aya katika mwanzo wa Sura Fatiha na si Qur’ani katika mwanzo wa Sura zingine. Na kutoka kwake kuna riwaya nyingine kuwa hiyo si katika Al-Hamdu pia! Na anayeikanusha mwanzoni mwa Sura Fatiha na Sura nyinginezo ametoa hoja kwamba, Qur’ani haithibitiki kwa dhana ila kwa tawaatur. Na pia katoa hoja kupitia hadithi ya Abu Hurayra kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) kuwa amesema: “Swala imegawanywa nusu mbili, kati yangu na mja wangu, ataposema mja Alhamdu lillahi Rabbil a’aalamiina…” mpaka mwisho wa Hadith. Na hapo hakutaja Bismillahi. (Ameipokea Muslim). Amesema katika Al-Majmuu Juz. 16, Uk. 235: “Na ya pili: Hiyo si katika maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, bali ilikuwa ni wahyi kutoka kwake, kwani kuna wahyi usiokuwa Qur’ani, kama ilivyopokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) kuwa amesema: “Jibril alikuja kwangu na kuniamuru kusoma Bismillahi kwa sauti na hiyo haikuwa Qur’ani na maneno kutoka kwa Mwenyezi Mungu.” Na amesema katika Uk. 337: “Na katika Sunan cha Al-Bayhaqi imepokewa kutoka kwa Ali na Abu Hurayra na Ibn Abbas na wengineo: “Kwamba Sura Al-Fatiha ndio sabu’ul mathaani nayo ni Aya saba, na Bismillahi ndio Aya ya saba..’’ Na katika Sunan cha Daru Qutni, imepokewa kutoka kwa Abu Hurayra amesema: Amesema Mtume (s.a.w.w): “Mnaposoma Al-hamdu, msome na Bismi llahi rahmani rahiim, kwani hiyo ni mama wa Qur’ani na ni mama wa Kitabu, na ni sabu’l mathaani na Bismi llahi rahmani rahiim ni moja ya Aya zake.” Akasema Daru Qutni: “Wapokezi wa isnad yake wote ni watu wakweli.” Hadithi hizi zinazopeana nguvu zinaleta dhana ya nguvu kuwa yenyewe ni Qur’ani kwa namna ilivyoandikwa. Kinachotakiwa hapa ni dhana na si 12

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

yakini, kinyume na alivyodhani Kadhi Abu Bakr Al-Baqalani alipoyashutumu madhehebu yetu akasema: “Qur’ani haithibiti kwa dhana.”, na Ghazali akamkanusha na kutoa dalili kwamba dhana inatosha kwa yale tuliyonayo.” Akasema katika Uk, 338: “Ama jibu la maneno yao kuwa Qur’ani haithibitiki ila kwa tawatur, kuna wajihi mbili: Ya kwanza, kwamba kuithibitisha kwake msahafuni ni tawatur. Pili: Tawatur ni sharti la kuthibitisha Qur’ani kwa njia ya yakini, ama inayothibitisha Qur’ani kwa njia ya hukmu inatosha dhana kama ilivyotangulia ufafanuzi wake, na Bismillahi ni Qur’ani kwa njia ya hukmu kwa usahihi na kauli ya watu wetu.” Amesema Seyyid Khui katika Al-Bayan Uk. 554: “Wenye kusema kuwa Bismillahi si sehemu katika Sura wametoa dalili kwa wajihi zifuatazo: Wajihi ya kwanza: Njia ya kuthibisha Qur’ani iwe ni kwa tawatur, hivyo kila chenye mzozo katika uthibitikaji wake basi hicho si katika Qur’ani. Na Bismillahi ni katika hizo zenye mzozo. Jibu lake: Kwanza: Bismillahi kuwa ni katika Qur’ani hilo limekuja kwa tawatir kutoka kwa Ahlul-Bayt (a.s.), wala hakuna tofauti katika tawatur iwe ni kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) au ni kutoka kwa Ahlul-Bayt wake watoharifu baada ya kuthibiti wajibu wa kuwafuata. Pili: Baadhi ya kikundi kusema kuwa Bismillahi si sehemu ya Qur’ani kwa shaka, hili halidhuru tawatur, ukiongezea kuwa kuna ushuhuda wa sahaba wengi kuwa hiyo ni katika Qur’ani. Tatu: Imekuja tawatir kwamba Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akiisoma Bismillahi anaposoma Sura ya Qur’ani, naye akiwa katika hali ya kubainisha, na hakubainisha kuwa yenyewe si katika Qur’ani, na hii ni dalili ya yakini kwamba Bismillahi ni katika Qur’ani. Ndio, kwa hii haithibiti kuwa 13

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

yenyewe ni sehemu ya Sura, inatosha kuthibitisha kutokana na riwaya zilizopita ukiachilia mbali riwaya nyingi zilizopokewa kutoka kwenye pande zote mbili. Na kuwa ni sehemu kunathibitishwa kwa habari isiyo tawatur lakini iliyo sahihi, na hakuna dalili ya kulazimu uthibitisho uwe kwa tawaatur katika hilo pia….” (Rejea pia, Al-Khilaf cha Sheikh Tusi Juz. 1, Uk. 332, Al-Muutabar cha Muhaqqiq A-Hilli Juz. 2, Uk. 179, Tadhkiratul Fuqahaa cha Allma Hilli Juz. 1, Uk. 114, Tafsir Suratul-Hamd cha Seyyid Muhammad Baqir AlHakim Uk. 139 na Tafsir Al-Qurtubi Juz. 1, Uk. 93).

Mas’ala 100 Kupagawa kwa wapinzani wa Ahlul-Bayt juu ya kusoma Bismillahi kwa sauti An-Nawawi amesema katika Al-Majmuu Juz. 3, Uk. 342: “Katika kitabu Khalaafiyyati cha Bayhaqi, kutoka kwa Jafar bin Muhammad amesema: ‘Aali Muhammad wamekongamana katika kusoma Bismi llahi rahmani rahiim kwa sauti.’ Abu Jafar Muhamad bin Ali akasema: ‘Haifai kuswali nyuma ya mtu asiyeisoma kwa sauti…”’ Nasema: Madam imethibiti kwenu kongamano la Ahlul-Bayt juu ya kusoma kwa sauti, na wengine wakahitilafiana nao, kwa nini hamuwafuati Ahlul-Bayt wa Mtume wenu? “Je anayeongoza kwenye haki ndiye mwenye haki zaidi ya kufuatwa, ama yule asiyeongoza ila aongozwe, mna nini nyinyi mwahukumu vipi?” (Yunus : 35). Katika Al-Mabsutu cha Sarkhasi. Juz. 1, Uk.51: “Malik alikuwa akisema: Mwenye kuswali hasomi Bismillahi kwa siri au kwa kutoa sauti, kwa mujibu wa Hadith ya Aisha kwamba Mtume alikuwa akifungua Swala kwa Alhamdu lillahi rabbil a’aalamiina.

14

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

Nasi tuna Hadith ya Anas amesema: ‘‘Niliswali nyuma ya Mtume na nyuma ya Abu Bakr na Umar walikuwa wakifungua Qur’ani kwa Bismi llahi rahmani rahiim. Na taawil ya Hadith ya Aisha ni kuwa Mtume alikuwa akisoma bila sauti, nayo ndio madhehebu yetu…. Shafii amesema: “Imam ataitoa kwa sauti katika Swala za kusoma kwa sauti, nayo ni kauli ya Ibn Abbas na Abu Hurayra. Na kutoka kwa Umar kuna riwaya mbili.” Akatoa hoja kwa Hadith ya Abu Hurayra kwamba Mtume alikuwa akiisoma kwa sauti, na Muawiya aliposwalisha Madina hakuitoa kwa sauti, watu wakampinga wakamwambia, umepunguza kitu katika Swala, Bismillahi iko wapi? Hiyo ikatoa dalili kuwa kusoma kwa sauti kulikuwa maarufu kwao. Nasi tuna Hadith ya Abdallah bin Mughaffal kutoka kwake kwamba alimsikia mtoto wake akiisoma kwa sauti katika Swala, akamkataza hilo akasema: “Ee Mwanangu, nakutahadharisha na kuzusha katika uislamu, mimi niliswali nyuma ya Mtume na nyuma ya Abu Bakr na Umar walikuwa hawasomi Bismillahi kwa sauti.’’ Na hivi ndivyo ilivyopokewa kutoka kwa Anas.” Na akasema Nawawi katika Majmuu Juz. 3, Uk. 332: “Ni wajibu kuanza na Bismi llahi rahmani rahiim kwa kuwa hiyo ni Aya yake. Na dalili yake ni alivyopokea Ummu Salam kwamba Mtume (s.a.w.w) alisoma Bismi llahi rahmani rahiim akaihisabu kuwa ni Aya. Na sahaba wameithibitisha kati ya yale waliyokusanya katika Qur’ani, na wakatoa dalili kuwa hiyo ni katika Aya yake, na ikiwa katika Swala inayosomwa kwa sauti, basi husomwa kwa sauti kama zinavyosomwa kwa sauti aya nyingine za AlFatiha. Ilivyopokewa kutoka kwa Ibn Abbas ni kwamba Mtume (s.a.w.w) aliisoma Bismi llahi rahmani rahiim kwa sauti, na kwamba inasomwa kuwa ni Aya ya Qur’ani kwa dalili kwamba inasomwa baada ya Au’udhu billahi , hivyo sunna yake ikawa ni kuisoma kwa sauti, kama aya nyingine15

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

zo za Al-Fatiha.’’ Je umeona mantiki ya watu wanaofanya kazi ili kutoa Fiqh ya kuwaridhisha watawala na majaribio yao mabaya ya kutoa dalili na kufafanua? Bismillahi kwao si katika Qur’ani, na yule anayekanusha kuwa si katika Qur’ani ni mwislamu kamili!!!! Na Bismilllahi ni Qur’ani kwa hukmu na dhana si kwa yakini, atayethibitisha kuwa ni Qur’ani kwa yakini basi yeye ni kafiri iwapo tu yeye ni katika ulamaa. Ama akiwa katika watu wa kawaida hapo kuna hitilafu. Na kuisoma katika Swala ni makruh kwa siri na kwa sauti, bali yajuzu kuisoma bila sauti na ni makruhu kwa kutoa sauti, bali ni mustahabu kuisoma kwa sauti, bali kutoka shakani zaidi ni kutokuisoma kabisa. Mpaka mwisho wa fatwa zao zenye kugongana! Na mwanzo wa msiba wao ni kwamba hivi sasa Bismilllahi iko hasa katika Qur’ani, na hili linahitaji ufafanuzi! Na ziko Hadith sahihi kwamba hiyo Bismillahi ni Aya, na Hadith sahihi kwamba si Aya, kwa hiyo ni Hadith zinazogongana. Miongoni mwazo ni kutoka kwa Anas pekee, ni Hadith sita kwa aina mbalimbali. Wao wanahitaji kuzihalalisha Hadith hizi zinazogongana! Kwa makuraish kusoma Bismillahi kwa sauti ni makruh, hilo linahitaji maelezo. Baadhi ya viongozi wameisoma na wengine hawakuisoma, wegine wameisoma kwa sauti na wengine hawakufanya hivyo.Wengine wamefanya kwa aina mbili. Na amali za wote ni sahih! Inahitaji fatwa ya kutegemea!

16

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

Kwa hivyo mafakihi hao wanaonelea kwamba hapana njia mbele yao ila wadhihirishe mantiki ya akili na kukubali vinyume viwili na viwili vinavyogongana, bali hata vingi ili wapate ufumbuzi wa tatizo.

Mas’ala 101 Ahlul-Bayt wanapambana kwa ajili ya Bismillahi. Na Bismillahi ni Aya tukufu mno katika Qur’ani, na Sura ya Al-Hamdu ndio Sabu’l mathaani Katika Tafsiri Al-Ayashi Juz. 1, Uk. 21: Kutoka kwa Imam Sadiq (a.s.) “Wana nini hao, Mungu awapige vita! Wametegemea Aya tukufu zaidi katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu wakadai kuwa ni bidaa anapoidhihirisha, nayo ni Bismillahi rahmaanir rahiim.” Na katika Wasa’ilus Shiia (Aali Bayt) Juz. 6, Uk. 59: Kutoka kwa Imam Hasan Al-Askari kutoka kwa baba zake, kutoka kwa Amirul muuminina (a.s.) amesema: “Bismillahi rahmaanir rahiim ni Aya katiika Sura al-Fatiha nayo ina Aya saba, inayotimiza saba ni Bismillahi rahmaanir rahiim.….” Aliambiwa Amirul muuminina, hebu tuambie kuhusu Bismillahi rahmaanir rahiim je hiyo ni katika Sura Fatihatul Kitab? Akasema: “Ndio. Mtume (s.a.w.w) alikuwa akiisoma na kuihesabu kuwa ni Aya katika AlHamdu na akisema: Fatihatul kitabu ni Sabu’l mathani.” Na katika Maa’anil Akhbar Uk. 121: “Ali (a.s.) alikuwa akiswalisha watu na akiisoma kwa sauti.’’ Al-Kulayni ametaja katika Al-Kafi Juz. 8 Uk. 58: “Ni khutba fasaha ya Ali (a.s.) kwa sanad sahihi kutoka kwa Ali bin Ibrahim kutoka kwa babake kutoka kwa Hamad bin Isa kutoka kwa Ibrahim bin Uthman, (Bin Umar Al-Yamani) kutoka kwa Sulaym bin Qays Al-Hilaly Imam Ali anasikia uchungu humo kwa kuwa haiwezekani kurekebisha upotofu waliouzusha 17

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

watawala katika akida ya Uislamu na sharia zake. Nasi tutatoa ushahidi zaidi ya mmoja: Amesema Al-Kulayni: “Alihutubu Amirul muuminina akamhimidi Mwenyezi Mungu na kumswalia Mtume kisha akasema: ‘Tambueni! Hakika ninachokihofia zaidi kwenu ni mambo mawili, kufuata matamanio na kuwa na mtarajio marefu. Ama kufuata matamanio kunazuia haki, na kuwa na mtarajio marefu kunasahaulisha Akhera… Ama fitna zilianza pale hawaa zilipofuatwa na hukmu kuzushwa, zikapingwa hukmu za Mwenyezi Mungu na watu kuwatawalisha watu wengine! Tambueni! Lau haki ingetakaswa kusingelikuwa na hitilafu, na lau batili ingelitakaswa basi asingehofiwa mwenye hoja, lakini huchukuliwa toka katika jambo hili fungu, na kutoka katika lile fungu, ndipo yakachanganywa pamoja na kuwekwa pamoja, hapo shetani anatawala vipenzi vyake na wale waliopata mema kutoka kwa Mwenyezi Mungu huokoka. Nimemsikia Mtume (s.a.w.w.) akisema: ‘Itakuwaje mtakapoiingia fitna ambapo mtoto atakua kwayo na mzee atazeeka kwayo, watu watapita ndani yake na kuifanya ni mwenendo, kikibadilishwa kitu kwao husemwa mwenendo umebadilishwa, na hakika watu wameleta mambo mabaya. Kisha balaa huzidi, vizazi kupokonywa, na fitna itawateketeza kama moto uteketezavyo kuni na kama linavyogonga jiwe la kusagia kwa uzito wake, na wanajifundisha kwa ajili ya asiyekuwa Mwenyezi Mungu na wanajifundisha pasi na amali, na wanaitafuta dunia kwa amali za Akhera.’ Kisha Ali (a.s.) akaelekea watu huku kando yake kukiwa na Ahlul-Bayt wake na wafuasi wake. Akasema: ‘Watawala wamenifanyia amali ambazo wampinga kwazo Mtume. Kwa kusudi wakimpinga, wakivunja ahadi zake wakibadilisha Sunna yake. Lau ningeliwalazimisha watu kuyaacha hayo na nikayageuza kuelekea mahali pake, na pale yalipokuwa wakati wa Mtume (s.a.w.w.) basi askari wangu wangefarikiana nikabaki pweke au na wafuasi wachache waliojua ubora wangu na faradhi za uimamu wangu kutoka kati18

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

ka Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna ya Mtume wake (s.a.w.w.). Mwaona lau ningeamuru Maqam Ibrahim nikairudisha mahali alipoiweka Mtume (s.a.w.w.) na nikarudisha Fadak kwa warithi wa Mtume (s.a.w.w.) na kuirudisha pishi ya Mtume kama ilivyokuwa, na nikairudisha nyumba ya Jafar kwa warithi wake na nikaivunja kutoka msikitini, na nikarudisha hukmu za dhulma zilizopitishwa na nikawatoa wanawake walio chini ya waume bila ya haki, nikawarudisha kwa waume zao, na nikaelekeza hukmu katika tupu na uzao, na nikawateka watu wa Bani Taghlab, na nikarudisha ardhi ya Khaybar iliyogawanywa. Na nikafuta vitabu vya kusajili watu wanachopewa na nikawapa watu kama alivyokuwa akifanya Mtume (s.a.w.w.) kutoa kwa usawa na nisifanye dola kati ya matajiri, nikaweka nafasi, na kuweka usawa kwa wanawake na nikatekeleza khumsi ya Mtume kama alivyoteremsha Mwenyezi Mungu na kuifaradhisha, na nikaurudisha msikiti wa Mtume kama ulivyokuwa nikafunga milango iliyofunguliwa, na kufungua iliyofungwa, nikaharamisha kupaka kwenye khuffa mibili, nikaadhibu kwa kupiga haddi kwa ulevi, nikaamuru kuhalalisha muta’a mbili, nikaamuru kupiga takbiri kwa majeneza takbira tano. Nikalazimisha watu kusoma Bismillahi rahmaanir rahiim kwa sauti, nikamtoa aliyeingia na Mtume katika msikiti wake (wakati wa milango yote kuelekea msikitini), aliyetolewa na Mtume (baada ya kufungwa milango), na nikamuingiza aliyetolewa (na watawala) baada ya mtume kati ya wale walioingizwa na Mtume, nikawachukua watu kwenye hukmu ya Qur’ani, na talaka juu ya Sunna nikachukua sadaka kwa aina na kwa mipaka yake, nikarudisha udhu, josho na Swala kwa wakati, sharia yake na mahali pake. Nikawarudisha watu wa Najran mahali pao, nikarudisha mateka wa Faris na watu wengine kwenye Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna ya Mtume wake; basi wangelifarikiana nami! Wallahi niliwaamuru watu wasiswali jamaa katika Swala mwezi wa Ramadhani ila za faradhi, na nikawafundisha kuwa kuswali kwao jamaa katika swala za suna ni bidaa, wakanadi askari wangu: ‘Enyi waislamu! 19

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

Sunna ya Umar imebadilishwa, anatukataza kuswali suna katika mwezi wa Ramadhani, nikahofia upinzani usisisimuke upande wa jeshi langu. Nilichopata katika umma huu ni mfarakano na kufuata maimamu wa upotovu na walinganiaji wa motoni! Hakuna watu wa nyumba ya Nabii yeyote yamewapata toka kwa umma wake kama yale yaliyotupata sisi baada ya Mtume wetu, na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kuombwa msaada juu ya waliotudhulumu na hakuna uwezo wala nguvu ila kwa Mwenyezi Mungu Mkuu, Mtukufu.’’ Na tumeshuhudia katika hutuba hiyo kauli yake: “Nikawalazimisha watu kusoma Bismillahi rahmaanir rahiim kwa sauti.’ Nayo ni katika yaliyobadilishwa na watawala baada yake. Inadhihiri katika riwaya ya Shafi ifuatayo kwamba, enzi za Muawiya watu wa Madina walikuwa wakiisoma Bismillahi rahmaanir rahiim kwa sauti kwa kufuata Sunna ya Mtume (s.a.w.w.), na waliojitokeza zaidi ni katika maanswari na Ahlul Bayt wake na wachache wao ni wale walioachwa huru, kwa sababu walikuja kuwa ni watawala au walihamia Sham. Hivyo watu wa Madina walizozana na Muawiya alipowaswalisha na hakusoma Bismillahi na wakamwambia: “(Kama ilivyo ndani ya kitabu Al-Ummu cha Shafi, Juz. 1, Uk. 129: ‘Ee Muawiya umeiba Swala yako, Bismillahi rahmaanir rahiim iko wapi? Akawaswalisha Swala nyingine humo akaisema ile waliyomuaibishia.’ Na katika Da’aalimul Islaam Juz. 1, Uk. 110: Jafar bin Muhmmad amesema: “Taqiyya ni dini yangu na ya mababa zangu ila katika mambo matatu; Kunywa pombe, kupaka juu ya khuffa mbili, na kutoisoma Bismillahi rahmaanir rahiim kwa sauti.’’ Na katika U’yuunul Akhbar Ridha, Juz. 1, Uk. 196: “Katika sifa za Imam Ridhaa (a.s.) amesema kuwa: “Yeye alikuwa akisoma Bismillahi kwa sauti, katika Swala zote za usiku na za mchana.’’ 20

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

Na katika Al-Kafi Juz. 3, Uk. 313: “Kutoka kwa Yahya bin Abi Umrani AlHamdani amesema: “Nilimuandikia Abu Jafar (Imam Al-Jawad (a.s.): Niwe ni fidia kwako! Wasemaje juu ya mtu aliyeanza kusoma Bismillahi rahmaanir rahiim katika Swala yake pekee katika Ummul Kitabi, na alipofika kwenye Sura isiyokuwa hiyo, akaiacha? Mfuasi wa bani Abbas amesema: Je hilo si jambo baya?” Akaandika kwa mkono wake: ‘Airudie mara mbili. Hata bila kupenda. Yaani hata bila kupenda huyo mfuasi wa bani Abbas.’’ Maswali juu ya kupambanua Bismillahi Je Bismillahi ni katika Qur’ani au imezidi ili kupambanua kati ya Sura? Je hiyo ni katika Qur’ani kwa yakini au kwa njia ya dhana? Je hiyo ni sehemu ya Surat Al-Hamdu au sio? Je ni sehemu ya Sura yoyote au la? Je imewekwa katika Swala au la? Je inasomwa kwa sauti au la, je mnawafiki kauli ya baadhi kama katika kitabu Al-Majmuu Juz. 3, Uk. 343: “Kwamba kusoma kwa sauti kumefutwa na kwamba haikusihi Hadithi kwayo. Na je ni bidaa? Je Hadith ya Abu Hurayra kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) kuwa alisema: ‘Mwenyezi Mungu amesema: ‘Swala baina Yangu na mja wangu imegawanyika nusu mbili, mja asemapo Alhamdu lillahi rabbil a’alamiina, Mwenyezi Mungu mtukufu husema, mja wangu amenihimidi, inajulisha kwamba Bismillahi si katika Qur’ani? Nini maoni yenu juu ya kauli ya Ibn Quddama katika Al-Mughni Juz. 1, Uk. 522: “Imepokewa kutoka kwa Ahmad kwamba hiyo si katika Surat Al-Fatiha, wala si Aya ya nyingineyo, wala haipasi isomwe katika Swala. Kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo, “Kwa hakika tumekupa Aya saba zisomwazo mara kwa mara…..(Al-Hijri : 87) mnaifafanua vipi. Ni zipi hizo kama si Surat Al-Fatiha? 21

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

Je mnashurutisha tawaatur katika kuthibitisha Aya ya Qur’ani? Je tawaatur kwenu iko wapi katika Bismillahi na Mua’widhatayni na Aya ya Khuzayma ambayo Zayd bin Thabit alisema kuwa haipatikani kwa mwengine! Imetangulia kauli ya Zayd katika Bukhari Juz. 8, Uk. 177: ‘Nikaifuatilia Qur’ani mpaka nikapata mwisho wa Sura ya Tawbah ikiwa na Abu Khuzayma Al-Answari sikuipata kwa mwingine yeyote.’’ Maadam imethibiti kwenu ijmai ya Ahlul-Bayt juu ya kusoma Bismillahi kwa sauti kwa nini hamchukui walichokongamana watu wa nyumba ya Mtume wenu, ambao aliwausia kuwafuata pamoja na Qur’ani akasema: ‘Mimi nawaachia vizito viwili: Kitabu cha Mwenyezi Mungu na AhlulBayt wangu? Mna maoni gani juu ya maneno ya Fakhru Razi katika Tafsiri yake Juz. 1 Uk. 105: Baada ya kunukuu riwaya ya Bayhaqi kuhusu kusoma kwa sauti Bismillahi, kutoka kwa Umar, Ibn Abbas, Ibn Umar na Ibn Zubayr, amesema: “Ama Ali (r.a.) alikuwa akisoma Bismillahi kwa sauti, hilo limethibiti kwa tawaatur, na atakayefuata dini ya Ali ameongoka, na dalili yake ni kauli ya Mtume (s.a.w.w.): ‘Ee Mola, izungushe haki na Ali popote azungukapo.’’’ Mna maoni gani juu ya kauli ya Fakhrud-Dini Razi Juz. 1, Uk. 106 kuhusu riwaya za Anas zinazogongana katika Bismillahi: “Pia ndani yake kuna tuhuma nyingine, ni kwamba Ali alizidisha sana katika kutoa sauti kwenye Bismillahi, ilipotawala dola ya Bani Umayya wakazidisha mno katika kuzuia hilo, ili kuondoa athari za Ali.’’ Kwa kitu gani mnafafanua asili ya mushkeli wa Bismillahi na mwenendo wa watawala kwayo, na kuhitilafiana mafakihi, na kupingana fatwa zao? Mnasemaje juu ya bidaa ya tarawehe, je inafaa kwa mmoja wa watawala wa sasa aanzishe kama hiyo?

22

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

Mas’ala 102 Kutia shaka kwao juu ya Sura za Muawidhataynin na kutoamua kuwa hizo ni Qur’ani Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akitilia umuhimu maalum kwa wajuukuze Hasan na Husein na kuwalinda kupitia maneno ya Mwenyezi Mungu ili kuondoa husda na shari kwao. Alifanya hivyo ili kuweka nafasi yao ndani ya nyoyo za waislamu na kusisitiza kuwa wao ni kizazi kilichobaki na ni wajukuu zake na ni endelezo lake katika umma kama walivyokuwa Is’haq na Isma’il kuwa ni mabaki na endelezo la Ibrahim; na baada ya kushuka Muawidhatayn alikuwa akiwalinda kwazo. Hili ndilo kosa la Sura mbili hizo ambalo kwa ajili hiyo walizikanusha kutoka kwenye Qur’ani, wakaweka hivyo katika zinguo la Abdallah bin Mas’ud na Ubayya bin Ka’ab, na sasa hebu tuone: Ahmad amepokea katika Juz. 5, Uk. 135: “Kutoka kwa Zurr amesema: ‘Nilimwambia Ubayya, ndugu zako wanasema kuwa ziko katika msahafu na hakukanusha.’ Akaambiwa Sufyani: ‘Ni Ibn Mas’ud?’ Akasema: ‘Ndio.’Na katika msahafu wa Ibn Mas’ud hazimo. Alikuwa akimuona Mtume (s.a.w.w.) akiwalinda na Sura mbili hizo Hasan na Husein na hakumsikia akizisoma katika Swala yake, hivyo akadhania ni kinga tu na akadumu kwenye dhana yake, lakini wengine wakapata uhakika kuwa zenyewe ni sehemu ya Qur’ani ndipo wakaziweka humo.”’ Na amepokea kama hiyo Ibn Majah lakini hakuwataja Hasan na Husein, akasema katika Juz. 2, Uk. 1161: “Kutoka kwa Abi Said amesema: ‘Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akijilinda kwa audhu billahi na jicho la shetani kisha la binadamu, zilipoteremshwa Sura hizo akazitumia na kuacha zinginezo.’” (Ameitaja Tirmidhi Juz. 3, uk. 267, Kanzul Ummal Juz. 7, Uk.77. Na ametaja katika Kanzul Ummal Juz. 2, uk. 261, na Juz. 10 Uk. 108. kutoka kwa Umar bin Khatwab amesema: “Mtume (s.a.w.w.) alikuwa aki23

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

walinda Hasan na Husein akisoma:

Ama Bukhari amepokea taawidh ya Mtume kwa Hasan na Husein bila ya kusoma Sura mbili za Mua’wwidhatayni akasema katika Juz. 4, Uk. 119: “Kutoka kwa Ibn Abbas, amesema: ‘Mtume (s.a.w.w) alikuwa akiwalinda Hasan na Husein alikuwa akisema kwamba baba yenu alikuwa akitumia kuwalinda Ismail na Is’hak akisema:

(Ameipokea kama hiyo Ibn Majah Juz. 2, Uk. 1165. Abu Daud Juz. 2, Uk. 421, Tirmidhi Juz. 3, Uk. 267, Ahmad, Juz. 1, Uk. 236, na 270. Al-Hakim Juz. 3, Uk. 167, na Juz, 4, Uk. 416. Na akasema katika merejeo mawili, Ni sahihi kwa sharti la masheikh wawili na wao hawakuitaja). Bukhari amepokea idadi ya riwaya kutoka kwa Aisha lakini hakuwataja Hasan na Husein (a.s.) akasema katika Juz. 7, Uk. 24: “Kutoka kwa Masruq kutoka kwa Aisha kwamba Mtume alikuwa akiwalinda baadhi ya watu wa nyumbani kwake kwa kuwafuta kwa mkono wake wa kulia na akisema: ‘Allah ndiye Mola wa watu, ondoa ubaya na uponye, wewe ni mponyaji hakuna ponyo ila lako.’’’ Na katika Juz. 7, Uk. 26 amesema: “Mtume alikuwa akiwalinda baadhi yao kwa kuwafuta kwa mkono wake wa kulia, (akisema): ‘Ondoa ubaya Mola wa watu, ponya wewe ndiye mponyaji, hakuna ponyo ila lako.’’’ (Ameipokea kama hii Ahmad Juz. 6 Uk. 4 na 45…) Amepokea mwandishi wa Majmauz Zawaaid Juz. 5, Uk. 113 kwa riwaya kadhaa na moja wapo ni ufafanuzi mzuri, nao ni kutoka kwa Abdallah bin Mas’ud amesema: “Tulikuwa tumeketi na Mtume (s.a.w.w) mara Hasan na Husein wakapita nao ni wadogo, akasema: ‘Waleteni wanangu niwalinde kama alivyokuwa akiwalinda Ibrahim wanawe Ismail na Is’haq, akasema: 24

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

Ameitaja Tabrani, ndani yake kuna Muhammad bin Dhakuwani, akaithibitisha Shuuba na Ibn Habban na wakaidhoofisha jamaa, na wapokezi waliobaki ni wakweli.” Na kwa amali hii ya Mtume iliyokuwa ikirudiwa rudiwa, muawidhatayni zikafungana na bongo za maswahaba kwa Hasan na Husein, na kutokana na hizo mbili vikawapata (Hasan na Husein) aidha penzi au husda, kwa ajili hii baadhi yao walijaribu kuzifuta katika Qur’ani na kuweka mbadala, Sura mbili Hifdi na Khala’ alizokuwa Umar akizisoma Swalani. Riwaya za maerejeo ya Sunni, kuna zinazothibitisha kuwa (Muawidhatayni) ni Qur’ani, na kuna zenye shaka Riwaya zinazothibitisha kuwa ni Qur’ani ni kutoka kwa Uqba bin Amir AlJahni, amezipokea Bayhaqi kutoka kwake katika Sunan yake Juz. 2, Uk. 393: akasema: “Nilikuwa napeleka ngamia wa Mtume (s.a.w.w) akaniambia: ‘Ewe Uqba, je sikufundishi bora ya Sura mbili kuzisoma?’ Nikasema, kwanini! Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, akanisomea Qul audhu birabbil faalq na birabbi nnaasi, hakuniona nikipendezwa nazo, akaswalisha watu asubuhi na akazisoma akaniambia:’ ‘Ewe Uqba, umeonaje?’” Hivyo pia amesema Al-Alau bin Kathir. Na amesema Wahb kutoka kwa Muawiya kutoka kwa Alaa bin Harith, nayo ni sahihi zaidi. Kisha akapokea kwa riwaya nyingine ilikuja: ‘Hakuniona kufurahi sana kwa hizo.’ Kisha katika riwaya nyingine inayoonyesha kuwa Uqba ndiye aliyemuuliza Mtume juu ya hilo, na kwamba Mtume alitaka kutilia mkazo hilo akaswalisha nazo. Kutoka kwa Uqba bin Amir akasema: ‘Alimuuliza Mtume juu ya muawwidhatayni , Mtume akawasalisha nazo katika Swala ya Al-fajri.”’ 25

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

Lakini aliipokea Muslim Juz. 2, Uk. 200 kwa aina ya nguvu: “Kutoka kwa Uqba bin Amir akasema: Amesema Mtume (s.a.w.w.): ‘Hukuona Aya zilizoshuka usiku ambazo hazijaonekana kama hizo, ni Qul audhu birabbil falaq na birabbi nnaas. Mtume aliniambia: ‘Zimeshuka kwangu Aya hazijaonekana mfano wake nazo ni muawwidhatayni.”’ Tirmidhi naye amepokea katika Juz. 5, Uk. 122 na Juz. 4 Uk. 244 na akasema katika rejea mbili: “Hii ni Hadithi hasan, sahihi, kisha imepokewa kutoka kwa Uqba: ‘Ameniamuru Mtume nisome muawwidhatayni baada ya kila Swala.’ Akasema Hadith hii sahihi, hasan.” Haythami amepokea katika Majmauz Zawaaid Juz. 7, uk. 147 idadi ya riwaya katika kuthibitisha kuwa hizo ni katika Qur’ani. Na Shafi’i amesema katika Al-Ummu Juz. 7, Uk. 199: “Kutoka kwa Abdurahman bin Yazid amesema: ‘Nilimuona Abdallah akizikwangua Muawidhatayni katika msahafu, na akisema: ‘Msiichanganye na kisichokuwa yenyewe.’ Kisha Abdurahman akasema: ‘Na wao wanapokea kutoka kwa Mtume kuwa yeye alizisoma akiswalisha katika Swala ya Asubuhi, nazo zimeandikwa msahafuni, uliokusanywa wakati wa Abu Bakr, kisha ukawa kwa Umar, kisha kwa Hafsa, kisha watu wakakusanya kwa Uthman, nazo ni kutoka katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu nami napenda kuzisoma katika Swala zangu.”’ Nayo inajulisha kuwa mpokezi ambaye ni Mshami amesema kweli kuhusu kukusanywa Qur’ani mara tatu! Lakini ushahidi wake kwamba alimuona Ibn Mas’ud au alipokea kutoka kwake, ni mahali pa shaka. Na amesema Bukhari katika Tarikh yake, Juz. 5, Uk. 365: (1155: Abdurahman bin Yazid bin Jabir, Al-Azdi Ash-Shami, alimsikia Mak’huul na Bashar bin Abdallah na Abu Taa’mah, amesikia kutoka kwake Ibn Mubarak, amesema: “Hamad bin Malik, amekufa mwaka wa hamsini na nne. 26

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

Ibrahim bin Musa amesema: “Nimemsikia Isa bin Yunus akimtaja Said bin Abdul Aziz na akataja kheri na hakuwa Abdurahman bin Yazid ni katika watu aliokaa nao.” Walid amesema: “Kwa Abdurahman kulikuwa na kitabu alichokisikia na kulikuwa na kingine ambacho hakukisikia.” Na Yahya bin Bakir amesema: “Amekufa mwaka wa mia na hamsini na tatu.’’ Kwa nini Bukhari katika Sahih yake amekomea kwenye riwaya zenye kutia shaka ?!!! Bukhari amechagua kusimama katika safu za wenye kutia shaka katika muawidhatayni kuwa ni Qur’ani, pamoja na kuwa amepokea riwaya ya Uqba katika Tarikh yake Tarikhul Kabir Juz. 3, Uk. 353 lakini amerudi nyuma katika Sahih yake na kuweka anuani mbili za Muawidhatayni, lakini alitosheka na riwaya za kutia shaka zenye kutetemesha alizozipokea kutoka kwa Ubayya bin Ka’ab. Pamoja na kuwa alitunga Tarikh yake kabla ya Sahih yake kama ilivyo katika Tadhkiratul Hufadh Juz. 2, Uk. 555. Amesema katika Sahihi yake Juz. 6, Uk. 96: “Sura ya Qul au’udhu birabbil falaq ....Kutoka kwa Zurr bin Habish amesema: ‘Nilimuuliza Ubayy juu ya Muawidhatayni, akasema: Nilimuuliza Mtume, akasema: Niliambiwa, nikasema: Nasi tunasema kama alivyosema Mtume (s.a.w.w.)……Sura ya Qul audhu birabbin naas…Na ametuhadithia Asim kutoka kwa Zurr, amesema: ‘Nilimuuliza Ubayya bin Ka’ab, nikasema: ‘Abul Mundhir, ndugu yako Ibn Mas’ud anasema kadha wa kadha.’ Ubayya akasema: ‘Nilimuuliza Mtume (s.a.w.w.) akaniambia: Niliambiwa, na nikasema! Akasema: ‘Nasi twasema kama alivyosema Mtume (s.a.w.w.).”’ Kwa hivyo inakuwa Bukhari ameacha kutaja kuwa muawidhatayni ni katika Qur’ani, kwa kuacha kwake riwaya ya Al-Jahmi aliyoipokea katika Tarikh yake.

27

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

Ukisema kuwa: Kuna mahali kwingi hupatikana katika Sahihi Bukhari ametaja wazi wakati wa kutaja baadhi ya Aya katika Sura hizi mbili kwa yeye kusema: Amesema Mtukufu: “…..” Na hii inasisitiza kwamba yeye anaziona kuwa hizo ni katika Qur’ani. Amesema katika kitabu Al-Qadri: “Na kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: Qul au’udhu birabbil falaq min shari maa khalaq.” Na akasema katika kitabu At-Tibb: “Mlango wa sihri (uchawi) na kauli yake Mwenyezi Mungu: Na akasema katika Kitabu Tawhid: ‘’Kauli ya Mwenyezi Mungu ARABIC TXT. Jibu: Ni kwamba, Bukhari anajua hitilafu iliyoko katika Sura hizo mbili, kuwa ni katika Qur’ani au ni katika zilizozidi? Pamoja na hivyo amefanya kusudi katika kupokea riwaya za kushuku Sura hizo tu na kuacha zinazothibitisha kuwa ni katika Qur’ani, kwa nini aliacha Hadith sahih kwa sharti yake ambazo Al-Hakim amepokea baadhi yazo? Kwa ajili hiyo, maneno aliyoyataja kwa dhahiri ni kuwa yeye anaitakidi kuwa hizo ni Qur’ani. Lakini yanazidisha mushkil, kwani unapofika kwenye Hadith kwamba hizo ni katika Qur’ani unaziacha kwako na kwa ustadh wako Ibn Khuzayma zile Hadith za Al-Jahmi, kwani hujapokea kitu kati ya hizo! Na umepokea badala yake Hadith zinazosema kwamba hizo mbili ni wahyi, Jibril aliomfundisha Mtume (s.a.w.w.) ili awalindie Hasan na Husein lakini Jibril hakumwambia kuwa hizo ni katika Qur’ani! Tatizo kwa Bukhari ni kuwa yeye amekomea katika riwaya zinazokataa kuwa ni sehemu ya Qur’ani, pamoja na kujua kwake kuwa kuna Hadith zinazothibitisha kuwa ni sehemu yake. Naye anajua kuwa kushuku sehemu ya Sura katika Qur’ani ni kuikanusha Qur’ani yote, kwa sababu Qur’ani haithibitishwi kwa dhana bali kwa yakini!

28

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

Amesoma Bukhari kwa ustadh wake Ibn Khuzayma Sahihi yake Juz. 1, Uk. 266, humo mna: “Mlango wa kusoma muawidhatayni katika Swala ni dhidi ya kauli za anayedai kuwa muawidhatayni si katika Qur’ani…Ametuambia…..’’ na hapo akaiandika riwaya aliyoiacha Bukhari. Amesema Ibn Najim Al-Misri katika Al-Bahru Raiq Juz. 2, Uk. 68: “Yaliyotokea katika Sunan na zinginezo katika ziada ya Muawidhatayni wameyakanusha Imam Ahmad na Ibn Muin, na watu wengi wa ilimu hawakuchagua kama alivyosema Tirmidhi, na pia katika Sharh ya Minyatul Muswalli.” Ni nani hao waliodai kuwa Muawidhatayni si katika Qur’ani kwa Ibn Khuzayma? Je ni Shi’ah; na ni zipi Hadith zisemazo kuzidi kwa Muawidhatayni? Ila ni zile riwaya za Bukhari alizozipokea yeye na wengineo. Tofauti ni kuwa wengine wamepokea pamoja na zile zenye kuthibtisha kuwa hizo ni katika Qur’ani, lakini yeye amekomea kwenye zile riwaya zenye kushuku. Kisha kama kauli ya kudai kuwa zenyewe ni ziada haipo, ni kwa nini basi imam wenu Ahmad bin Hambali amehitaji kuipinga? Kauli hii si nyingine ni ile aliyoipokea Bukhari. Sahihi ni kuwa Bukhari ameingia katika mgongano ambapo imedhihiri katika baadhi ya maneno yake kwamba yeye anasema kuwa muawidhatayni ni sehemu ya Qur’ani, ambapo katika riwaya zake amekomea kwenye zile walizoshikamana nazo wale wenye kupinga ya kuwa hizo ni katika sehemu ya Qur’ani. Na mas’ala haya yako wazi kwa mafakihi wao, ambapo wamehitilafiana katika kumkufurisha anayezifanyia maskhara Aya za muawidhatayni

29

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

Akasema Ibn Najim katika Bahru Raiq Juz. 5, Uk. 205: “Hukufurishwa mtu anapokanusha Aya za Qur’ani au kuzifanyia maskhara ila Muawidhatayni, kwani katika kuzikanusha kuna hitilafu. Na sahihi ni kufru, na ikasemwa pia hapana, ikasemwa pia ikiwa ni mtu asiye na ilimu, basi hukufuru, lakini ikiwa mwanachuoni basi hapana. Ni nani hao waliosema ‘Hakufuru mwenye kuzifanyia maskhara Aya mbili hizo, na kwamba hizo ni Qur’ani hilo halijathibiti? Je hao ni Shi’ah?

Maswali Mnafahamu nini kutoka kwenye Hadith ya Bukhari ya Mtume kuwalinda Hasan na Husein, na kutoa andiko kuwa hiyo ni kama alivyokuwa Ibrahim akiwalinda wanawe Ismali na Is’haq? Amesema katika Juz. 4, Uk. 119: “Kutoka kwa Ibn Abbas amesema: ‘Mtume alikuwa akiwalinda Hasan na Husein na akisema: Baba yenu alikuwa akaliwalindia kwazo Ismail na Is’haq: ARABIC TXT Mwafahamu nini kutoka katika riwaya ya Aisha ya kuwalinda Mtume (s.a.w.w.) Hasan na Husein na kutowataja majina bali alisema: “Akitumia kuwalinda baadhi ya watu wake wa nyumbani, akiwalinda baadhi yake.’’ (Bukhari Juz. 7, Uk. 34 na 26). Ikiwa Hadith inayothibitisha kwamba muawidhatayni ni katika Qur’ani ni Hadith ya Jahni pekee yake, tawaatur mnayoihitajia iko wapi ili kuthibitisha Qur’ani yenu? Kwa kipi mnafafanua kukomea kwa Bukhari kwenye riwaya za kushuku kuwa Muawidhatayni ni Qur’ani, nayo ni sahihi katika majengeo yake na kwa ustadhi wake?

30

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

Na kwa nini ikawa kusoma Muawidhatayni katika Swala ni jambo lichukizalo kwa wafuasi wa ukhalifa, na wa kwanza kuzisoma wazi wazi alikuwa ni Ubaydullah bin Ziyad baada ya kiasi cha miaka arobaini kupita tangu kufa kwa Mtume (s.a.w.w.)? Hakuna sababu nyingine kwa watu wa kawaida ila ni kule kushakia kwao kuwa ni Qur’ani, au kule kusema kwao ni wahyi wa ziada. Amesema Ibn Shiba katika Muswannaf Juz. 7, Uk.: “Kutoka kwa Mughira kutoka kwa Ibrahim amesema: Wa kwanza kuzidhihirisha muawidhatayni katika Swala ni Ubaydullah bin Ziyad. Mna maoni gani juu ya fatwa ya Bukhari, Ibn Habban na wengineo waliojuzisha mwenye kuswali kujumuisha Sura nyingine asomapo muawidhatayni, kwa sababu hizo zinatiliwa shaka ya kuwa ni katika Qur’ani. Ibn Habban amesema katika Sahih yake Juz. 6, Uk. 201: “Ametaja kuwa ni mubaha kwa mtu kusoma Muawidhatayni, kwa kusoma Sura Qul huwa llahu, katika Witri.’’ Nini maoni yenu juu ya kauli ya Razi katika Al-Mahsul Juz. 8, Uk. 480: “Ibn Mas’ud amekanusha Muawidhatayni kuwa ni katika Qura’n kama kwamba hakushuhudia kusoma kwa Mtume (s.a.w.w.) kwazo, na wala hakuongoka kwa ufasaha wa muujiza uliomo ndani yake, au hakusadiki umma kwa kusema kuwa hizo ni katika Qur’ani, ikiwa watu hao hawakuwa hoja juu yake, basi ni bora wasiwe hoja juu yetu, sisi tunasameheka kwa kule kutokubali kauli yao.” Nini maoni yeni juu ya kauli ya Nawawi katika Sharhul-Muhaddhab: “Waislamu wamekongamana kuwa Muawidhatayni na Al-Fatiha ni katika Qur’ani na mwenye kukanusha kitu katika hizo huyo amekufuru. Na alichonukuu Ibn Mas’ud ni batili si sahihi. Alitanguliwa na Abu Muhammad bin Hazmi katika hilo, akasema katika Awaailul mahali: ‘Kilichonukuliwa kutoka kwa Ibn Mas’ud cha kukanusha kuwa Muawidhatayni ni katika 31

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

Qur’ani huo ni uongo batili.’ Pia Fakhru Razi mwanzoni mwa Tafsiri yake amesema: ‘Dhana iliyozidi ni kuwa nukuu hii ya kutoka kwa Ibn Mas’ud ni uongo, batili.’ Na kuzishutumu riwaya sahihi pasi na tegemeo hakukubaliki, bali riwaya hizo ni sahihi........ (Fat-hul Bari Juz. 8, Uk. 571). Je mnasema kuwa ni kafiri mwenye kukanusha Muawidhatayni na mwenye kukataza Zaka? Na je mnaafikiana na kauli ya Ibn Sabbagh: “Hakika Abu Bakr aliwapiga vita kwa ajili ya kutotoa Zaka, na hakusema kuwa walikufuru kwa hilo, kwa hivyo hawakukufuru kwa sababu ijmai haikuwa imetulia. Akasema: ‘Na sisi hivi sasa tunamkufurisha anayeipinga!’ Akasema: ‘Na pia kilichonukuliwa kutoka kwa Ibn Mas’ud kuhusu muawidhatayni kinamaanisha kuwa haikuthibiti kwa yakini kwake, kisha baadaye alipata itifaki!”’ (Fat-hul Bari Juz. 8, Uk. 572).

Mas’ala 103 Sura mbili za Hifdi na Khali’ badala ya Muawidhatayni alikuwa akiziswalia Umar Kisa cha Sura mbili za Hifdi na Khali’ zinazodaiwa kina uhusiano na kitendo chao cha kufuta Sura mbili za Muawidhatayni kwa upande mmoja, na kufuta kwao qunuti na dua za Mtume kwa viongozi wa kikuraishi kwa upande mwingine. Laana ya Mtume kwa viongozi wa kikuraishi katika Swala yake Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akiomba katika Swala zake akiwaapiza mafirauni wa kikuraishi akiwaita kwa majina yao na akiwalaani. Akiwamo Abu Sufiyan, Suhail bin Amru, Harith bin Hisham, Safwan bin Umayya na baadhi ya viongozi wa makabila ya waarabu, na aliendelea kufanya hivyo mpaka ushindi wa Makka na wale walaanifu kutangaza kusilimu kwao chini ya upanga, na hilo lilikuwa ni jambo zito sana kwao. Na katika Sahihi Muslim Juz 2, Uk. 134: Kutoka kwa Abu Hurayra: “Mtume wa Mwenyezi Mungu alikuwa akisema anapomaliza Swala yake, 32

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

akisha soma na kupiga takbir, na kuinua kichwa chake kwa ‘samia’ llahu liman hamidah rabbana lakal hamdu’ akisema huku akiwa amesimama: ‘Ewe Mola! Muokoe Walid bin Al-Walid, Salama bin Hisham, Iyash bin Rabia, na wanaoonewa katika waislamu, ee Mola tia nguvu zako kwa Mudhar. Ee Mola, mlaani Lihyaan, Raa’la, Dhakuwaan na waasi, wamemuasi Mungu na Mtume wake.’’’ Kisha Abu Hurayra akasema: “Kisha tumepata khabari kwamba Mtume aliacha iliposhuka Aya,

Lakini maneno ya Abu Hurayra ya mwisho yanaonyesha ni propaganda za utawala wa kikuraishi, kwa sababu Muslim yeye mwenyewe alipokea kutoka kwake baada ya hivyo kwamba alisema: ‘Wallahi nitawakurubisha katika Swala ya Mume.’ Akawa Abu Hurayra anasoma qunut katika Swala ya adhuhuri, ya Isha na ya Asubuhi. Na akiwaombea waislamu na kuwalaani makafiri.’’’ Utawala wa kikuraishi baada ya Mtume ulifanya juhudi kutibu tatizo hili, kwani baadhi ya waliolaaniwa na watoto wao mahuria waliishi Madina baada ya ushindi wa Makka, na kwa uzito wao Umar aliweza kuuvua ukhalifa kutoka kwa Bani Hashim na Maanswari. Imetajwa kwamba idadi ya wale ambao Mtume aliwatuma katika jeshi la Usama ilikuwa ni wapiganaji mia tisa, hii ina maana kuwa idadi yao ilikuwa ni maelfu. Makhalifa na wafuasi wao walitatua tatizo la waliolaamiwa kwa masuluhisho mbalimbali: Walipokea kuwa Mtume (s.a.w.w.) alikubali kosa lake na akamuomba Mwenyezi Mungu aijaalie laana yake kwao iwe ni Swala na ukaribu, Zaka na malipo, Zaka na rehema, ni kafara kwake siku ya Kiyama, msamaha, afya n.k…baraka, rehema, msamaha, na Swala kwani wao ni watu wangu. Kwa mujibu ya riwaya. 33

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

Amepokea Bukhari katika Juz. 7, Uk. 157: “Kutoka kwa Abu Hurayra, alimsikia Mtume (s.a.w.w.) akisema: ‘Ee Mola, Mwislamu yeyote niliyemtukana, basi ijaalie kwake hiyo iwe ni ukuruba wake Kwako siku ya Kiyama.’’’ Na akapokea Muslim Juz. 8, Uk. 26: “Kutoka kwa Abu Hurayra, alimsikia Mtume (s.a.w.w.) akisema: ‘Ee Mola, hakika Muhammad ni mwanaadamu, hukasirika, kama wanavyokasirika wanaadamu, nami nimechukua ahadi kwako hutoivunja, Mwislamu yeyote niliyemuudhi au kumtukana au kumpiga mjeledi ijaalie hiyo kwake ni kafara na ukuruba, umkurubishe Kwako siku ya Kiyama.’’’ Na amepokea Muslim riwaya zingine saba na marejeo yake yametaja riwaya nyingi kama hiyo. Miongoni mwa mbinu za utatuzi huo ni madai yao kwamba Mwenyezi Mungu ameteremsha kwake (s.a.w.w.) Aya kumkemea kuwalaumu, nayo ni kauli yake Mwenyezi Mungu:

“Wewe huna neno katika shauri hili awakubalie toba yao au awaadhibu, maana hakika wao ni madhalimu.” (Al-Imran: 128). Hakika utapata riwaya nyingi katika tafsri yao zikimtia makosa (s.a.w.w.) na kumlaumu kwa sababu aliapiza mataghuti wa kikuraishi kwa amri ya Mola Wake na akawalaani! Kama kwamba wamepata kilichowapotea kutoka katika Qur’ani dhidi ya Mtume (s.a.w.w.). Bukhari ameziwekea riwaya hizo milango minne, amepokea humo jinsi Mwenyezi Mungu alivyopinga maapizo ya Mtume wake kwa watu hao na akamkataza kuwalaani!

34

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

Katika riwaya zake nyingi Bukhari hakuwataja hao waliolaaniwa waheshimiwa kwa kuwalindia heshima yao. Amesema katika Juz. 5, Uk. 35: “Kutoka kwa Salim kutoka kwa babake kwamba alimsikia Mtume akisema wakati anapoinua kichwa chake kutoka rukuu katika rakaa ya mwisho ya Alfajiri akisema: ‘Eee Mola mlaani fulani na fulani na fulani.’ husema hivyo baada ya kusema samia’ llahu liman hamidah, rabbanaa lakal hamdu, Mwenyezi Mungu akateremsha

Na katiaka Juz. 5, Uk. 35 ni kuwa: “Mtume wa Mwenyezi Mungu alikuwa akimuombea mabaya Swaf’wan bin Umaiyyah, Suhaylu bin Amru na Harith bin Hisham, ndipo ikateremka Aya hiyo.” Natija ya riwaya zao ni kwamba: Aya imeshuka mara nyingi kwa ajili ya watu mbalimbali au vikundi, na katika nyakati tofauti, hivyo sababu za kushuka kwake zikafika ishirini kwa minasaba inayogongana katika mahali na wakati na watu waliolaaniwa! Miongoni mwa mbinu za utatuzi ni madai yao kwamba Jibril alikwenda kwa Mtume (s.wa.w.w.) naye alikuwa akikunuti na kuwalaani watu hao katika Swala. Akamkata qunuti yake na Swala yake na kumlaumu na kumfundisha badala ya laana (Sura mbili za Hifdi na Khala’) Al Bayhaqi amesema katika Sunan yake Juz. 2, Uk. 210: Kutoka kwa Khalid bin Abi Imran amesema: “Mtume alipokuwa akiwaapiza Mudhar (Yaani makuraishi), mara akaja Jibril, akamwashiria anyamaze, na akanyamaza, akasema: ‘Ee Muhammad Mwenyezi Mungu hakukutuma kuwa mtukanaji wala mwenye kulaani, bali amekutuma kuwa ni rehma hakukutuma kuwa ni mwenye kuadhibu, huna lako jambo, ni ima Mungu awakubalie toba au awaadhibu kwani wao ni madhalimu.’ kisha akamfundisha qunuti hii:

35

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

“Eee Mola, Sisi tunakuomba msaada, tunakuomba msamaha tunakuamini na kukunyenyekea, na tunamuacha anayekukufuru. Ee Mola, wewe tu tunakuabudu na kwako tu tunaswali na kusujudu na kwenda mbio, na tunataraji rehma yako na tunaogopa adhabu yako kali kwani adhabu yako ni yenye kuwapata makafiri.’’’ Kisha Bayhaqi akasema: “Hii ni mursal , imepokewa kutoka kwa Umar bin Khattab ile iliyo sahihi yenye muungano wa wapokezi.’’ Kisha akapokea kuwa Umar alikunuti baada ya rukuu akalaani makafiri wa Ahlul Kitab! Akasema: ‘

Ameipokea Abu Said bin Abdurahman bin Abza kutoka kwa babake, kutoka kwa Umar, akapinga hili sehemu nyingine. Na akakariri Al-Bayhaqi katika riwaya nyingi kuwa si nyingi zaidi ila riwaya za Suyuti katika Durrul manthuuri Juz. 6, Uk. 420 chini ya anuani, ‘Kutaja yaliyotajwa kuhusiana na Sura ya Khala’ na ya Hifdi’ Kisha mafakihi wao wakatoa fatwa kwa kupendekeza hili kisheria, katika Fat’hul a’ziz Juz. 4, Uk. 148 Juz. 4, Uk. 250: “Wamependekeza maimamu 36

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu miongoni mwao opokewa kutoka Juz. 1, Uk. 103, katika Majmuu’ qunut ya Umar.

Sehemu ya Sita

akiwa ni mwandishi wa Talkhis, aongeze ile qunut iliykwa Umar.” Na Malik akatoa fatwa katika Al-Midwana na Shafi’i katika Al-Ummu Juz. 7, Uk. 48, na Nawawi Juz. 3, Uk. 493, na wakaandika riwaya ya Bayhaqi na

Ni kawaida ziwe Sura mbili hizi ziko katika msahafu wa Umar uliokuwa kwa Hafsa na hakuueneza mpaka Marwan alipouchoma. Ibn Hazm anafedhehesha Sura mbili za Umar Alithubutu Ibn Hazm kutoa fatwa kwamba Sura mbili hizo ni katika maneno ya Umar na hazikupokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) akasema katika Al-Mahalli Juz. 4, Uk. 148: “Imekuja kutoka kwa Umar qunut nyingine sio hii, na yenye njia ya upokezi ndio tuipendayo sana. Ikisemwa: Umar hasemi ila lile aonalo limetoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Hapo tutawaambia: Riwaya ambayo tuna yakini kuwa imetoka kwa Mtume ni bora zaidi kuliko ile inayonasibishiwa kwa dhana, ambayo Mwenyezi Mungu na Mtume wake wameikataza. Mkisema kuwa si dhana, basi ingizeni katika Hadith yenu njia ya upokezi mseme: Kutoka kwa Umar kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.), na mkifanya hivyo mtakuwa mmesema uongo, na mkikataa basi mmehakikisha kuwa imetoka kwenu kauli ya kumzushia Mtume kwa kupitia dhana aliyoisema Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Dhana haisaidii chochote katika haki.’’ Na akasema katika Juz. 3, Uk. 91: “Ataomba anayeswali katika Swala yake katika sijda yake, na kisimamo chake, na kukaa kwake, anachopenda. Mtume aliwaapiza Asiyya, Raa’la na Dhakuwani na akamuombea AlWalid bin Al-Walid, Iyash bin Rabia na Salama bin Hisham, akiwataja kwa majina yao na Mtume hakukataza hili kamwe wala hakukatazwa.”

37

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

Maneno yake ya mwisho ni pigo lenye nguvu dhidi ya Sura mbili za Hifdi na Khala’ na ni kukadhibisha Hadith ya Shafi’i na Bayhaqi isemayo: “Ee Muhammad hakika Mwenyezi Mungu hakukutuma uwe ni mwenye kutukana wala kulaani.” Na wamezinasibisha Sura mbili za Umar kwa Ubayya bin Ka’ab Kwa ufafanuzi huu mfupi, umejua kuwa Sura mbili za Hifdi na Khala’ ni za Umar za kikuraish, na hazina uhusiano na maanswari wala Ubayya bin Kaa’ab! Na kwamba kila riwaya zinazonasibishwa kwake (Ubaya bin Ka’ab) ni kwa ajili ya kulitumia jina lake katika kuzitangaza. Zimepokewa ndani ya Durrul Manthuri Juz. 6 Uk. 420: ‘’Kutoka kwa Hammad amesema: ‘Tumesoma katika msahafu wa Ubayya bin Kaa’ab

(Ee Mola, sisi tunakuomba msaada na msamaha na tunausifia kwa kheri na hatukukufuru na tunajitoa na tunamuacha anayekufanyia uovu). Hammad akasema: ‘Aya hii ni Sura!”’ Na katika musahafu wa Ibn Abbas kuna kisomo cha Ubayya na cha Abu Musa na katika msahafu wa Hajr Na katika msahafu wa Ubayya na Abu Musa

Wakitaka kuzinasibisha na Ubayya mwenyewe tayari umeshaona jinsi walivyofanya. Na kama wakitaka kuzinasibisha na msahafu wake, ni kuwa mwanawe Muhammad alimkabidhi Uthman msahafu huo pale alipoufanya msahafu kuwa mmoja na haukuwa kwa mwingine yeyote. 38

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

Maswali Maana ya laana ni kufukuzwa kutoka kwenye rehma ya Mwenyezi Mungu mtukufu, vipi mtaleta taswira ya kwamba Mtume amlaani mtu kutoka upande wa nafsi yake bila ya idhini ya Mwenyezi Mungu au bila ya amri Yake? Vipi mtaleta taswira ya kwamba amri ya Mwenyezi Mungu itoke ya kumtoa mtu kwenye rehma yake kisha awe ni mtu mwema? Vipi akili zenu zinakubali kuwa Mwenyezi Mungu alieleza juu ya makuraishi kuwa wengi wao hawatoamini kisha mseme wao ni waumini? Amesema: Mwenyezi Mungu Mtukufu:”

(Yasin: 6-7). Vipi mnakubali yale ambayo Muslim ameyanasibisha kwa Mtume (s.a.w.w.), kwamba Mtume alikuwa akiudhi akitukana na akipiga kimaonevu bila ya haki? Angalia Sahihi Muslim Juz. 8 Uk. 36: “Kutoka kwa Abu Hurayra: ‘Nimemsikia Mtume (s.a.w.w.) akisema: ‘Ee Mola, hakika Muhammad ni mwanaadamu anakasirika kama anavyokasirika mwanaadamu na mimi nimechukua kwako ahadi hutoikhalifu, Mwislamu yeyote niliyemuudhi au kumtukana au kumpiga kwa mjeledi ijaalie kwake ni kafara na ukuruba wa kumkaribishia kwako Siku ya Kiyama.’’ Je mnakubali sababu za kuteremka Aya zinazogongana zilizopokewa na sahihi zenu katika sababu ya kuteremka kauli ya Mwenyezi Mungu:

39

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

“Wewe huna neno katika shauri hili awakubalie toba yao au awaadhibu, maana hakika wao ni madhalimu.’’ Je mnaikubali riwaya ya Bayhaqi ya kushuka Jibril na kumlaumu Mtume na kuikata Swala yake, au mnaafikiana na maneno ya Ibn Hazm ya kuikanusha? Je mnakubali kunasibishwa kwa Sura mbili za Al-Hifdi na Khala’ kwa Ubayya bin Kaa’b? Je mnatoa fatwa kuwa ni mustahabu kuleta qunut kwa Sura mbili za Umar?

SAHIHISHENI MISAHAFU YENU AU ZITIENI MAKOSA REJEA ZENU Mas’ala 104 Fungueni misahafu yenu muisahihishe au mkataeni Bukhari na Umar Umar alisimama mbele ya Mtume na akakataa kuandika wasia wake kwa umma wake, ili wasalimike na upotevu. Umar akasema: ‘’Kitabu cha Mwenyezi Mungu kinatutosha.’’ Mkasimama naye na mkapiga mayowe mbele ya Mtume wenu. Umar alisimama kwenye Saqifa akasema, sisi ni kabila la makuraishi, na Muhammad ni mkuraish, ni nani atakayeshindania nasi ufalme wa Muhammad? Mkasimama naye. Akavamia nyumba ya Ali na Fatima akawasha kuni mlangoni mwa nyumba, na kuwatishia kuwa wasipotoka na kuwabai ataichoma nyumba na waliomo akiwamo Ali, Fatima, Hasan na Husein na idadi ya muhajirina wakubwa na manswari wakiwa wamesimama pembeni mwa Ahlul-Bayt. 40

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

Mkasimama naye na mkasema aliyofanya ni haki! Kisha mkaichukua kutoka kwake dini yenu yote, mkamtii aliyosema na aliyoyafanya, bali mkamfanya ndio msingi wa dini yenu. Mkampenda ampendaye na kumfanyia uadui amkataaye! Mna nini mnamuepuka katika Aya za Kitabu cha Mwenyezi Mungu alizowafafanulia, na alikuwa akizisoma kwenye Swala zake na nje ya Swala zake. Kuanzia sasa tubuni kwa kule kumpinga imamu wenu, na kila mmoja wenu afungue msahafu wake na kuusahihisha kulingana na kisomo cha Umar: Sahihisheni Aya hii katika Suratu Jum-a’: Amesema Bukhari katika sahihi yake Juz. 6, Uk. 63: “Umar akasoma:’’

Katika Tarikhul Madina Ibn Shiba amepokea Juz. 2, Uk. 711: “Kutoka kwa Ibrahim kutoka kwa Kharsha bin Al-Hurr amesema: ‘Tuliona na Umar ubao umeandikwa

akasema: ‘Ni nani aliyekusomea hii?’ Nikasema ni Ubayya bin Ka’ab. Akasema: ‘Ubayya alikuwa ni msomaji sana wa zilizofutwa, hebu isome:

(Amepokea Bayhaqi katika Sunan yake Juz. 3, Uk. 227 na Suyuti katika Durrul Manthuri Juz. 6, Uk. 219).

41

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

Na sahihisheni Aya mbili katika Sura ya Al-Hamdu: Amesema Suyuti katika Durrul Manthur Juz. 1, Uk. 15: “Ametaja Wakii na Abu Ubayda na Said bin Mansur na Abdu bin Hamid na Ibn Al-Mundhir na Ibn Abi Daud na Ibn Abil Anbari na kila mmoja wao katika msahafu ana njia, kutoka kwa Umar bin Khatwab alikuwa akisoma:

(Amepokea Al-Baghawi katika Maalimu Tanzil Juz. 1, Uk. 42 na Raghib katika Muhadharat Juz. 2, Uk. 199. Na Ibn Jizyi katika Tas’hil, na wengineo na wengineo..). Na katika tafsir ya Ibn Kathir Juz. 1, Uk. 31: “Na kwa hili amepokea Abu Abdul Kasim bin Salam katika kitabu Fadhaailul Qur’ani kutoka kwa Abu Nuawiya, kutoka kwa Al-Aamash, kutoka kwa Ibrahim, kutoka kwa Aswad, kutoka kwa Umar bin Khattab alikuwa akisoma:

Na katika Fat’hul Bari Juz. 8, Uk. 122: “Na anatilia nguvu kisomo cha Umar

Ameitaja Abu Ubayd, na Said bin Mansur kwa isnad yake sahihi. Na sahihisheni Aya tatu katika Sura ya Baqara, Ali Imran na Taha: Amesema Bukhari katika Juz, 6, Uk. 72: “Kama alivyosoma Umar: Al Hayyul qiyam’ Bukhari amemtetea Umar katika Juz. 8, Uk. 18 kwamba maana ya neno qiyam ni sawa na ile ya neno qayyuum. Na katika Fat’hul Bari Juz. 8, Uk. 510: “Kauli yake kama alivyosoma Al hayyul qiyaam. Ametaja Abu Ubayda katika Fadhaailul Qur’ani kutoka kwa njia ya Yahya bin Abdurahman bin Hatib kutoka kwa babake kutoka 42

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

kwa Umar kwamba aliswali Swala ya Isha ya mwisho na akafungua sura Ali Imran akasoma:

Na ametaja Abu Daud katika Masahif kupitia njia za Umar kwamba alisoma hivyo.” Na sahihisheni katika msahafu wenu Aya katika Sura Nazia’ati: Nayo ni kauli yake Mwenyezi Mungu:

Iandikeni (Nakhira) kwa alif (mvute) Katika Durrul Manthuri ya Suyuti Juz. 6, Uk. 312 amesema: “Ametaja Said bin Mansur na Abdu bin Hamid kutoka kwa Umar bin Khattab kuwa alikuwa akisoma:

na pia katika Kanzul Ummali Juz. 2, Uk. 591. Katika Tarikh ya Ibn Muin Juz. 2, Uk. 121: “Nimemsikia Yahya bin Muin akisema: ‘Ametuhadithia Ghandar kutoka kwa Shu’bah kutoka kwa Sufiani kutoka kwa A’amash kutoka kwa Zayd bin Muawiya kutoka kwa Ibn Umar alikuwa akisoma herufi hii:

Maswali Mnachagua nini: Kusahihisha misahafu au kumtia makosa Bukhari na Umar? Nini maoni yenu juu ya kauli ya Umar na iliyopokewa kutoka kwa Ibn Mas’ud kwamba maana ya: 43

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

yaani kimbieni mbio. Na katika Majmauz Zawaaid Juz. 7, Uk. 124: “Kutoka kwa Ibrahim amesema: ‘Amesema Abdallah bin Mas’ud..lau ningeliisoma ‘kimbia’ basi ningekimbia mpaka vazi langu lianguke. Alikuwa akiisoma: yaani piteni.’ Amepokea Tabari, na Ibrahim hakumdiriki Ibn Mas’ud. Na wapokezi wake ni wakweli.” Nini maoni yenu juu ya fatwa ya Qurtbi kwamba mwenye kukanusha visomo vya Umar huyo si kafiri. Amesema katika Tafsiri yake Juz. 1, Uk. 83: “Wanayoeleza kutoka kwa Umar bin Khattab ni kwamba yeye alisoma:

ambapo kuna mifano mingi ya herufi kama hizi na wanavyuoni hawakuzinukuu kwamba kuswali kwazo ni halali wala kuwa zinapinga msahafu wa Uthman, kwani ni herufi ambazo lau mpingaji atazipinga kwamba hizo ni katika Qur’ani basi hajakuwa kafiri, na Qur’ani iliyokusanywa na Uthman kwa kuafikiana na maswahaba lau mtu ataikataa baadhi yake basi atakuwa kafiri, hukumu yake ni kama ya mwenye kuritadi, atakiwa aombe toba atubu au achinjwe. Nini maoni yenu juu ya waliopendekeza kisomo cha Umar kuliko cha msahafu uliopo hivi sasa, na kuhusu Ibn Hajar kumtia makosa Umar? Katika Fat’hul Bari Juz. 8, Uk. 530: “Abu Ubayda amesema katika kauli ya Mwenyezi Mungu: yaani nakhira na naakhira ni sawa. Al-Farau alisema hivyo hivyo, akasema hizo ni visomo viwili lakini kilicho kizuri zaidi ni naakhira. Kisha akategemeza sanad kutoka kwa Ibn Zubair kuwa alisema juu ya mimbari: ‘Watoto wana nini wanasoma nakhira ilihali ni naakhira.’ Nami nasema: Wasomaji wa jamhuri wamesoma bila ya kuvuta ‘nakhira’ na wamesoma kwa kuvuta watu wa mji wa Kufa lakini kwa kurithi toka kwa Asim. 44

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

Lau mngelikuwa na insafu mngeona kwamba mushkeli huu si visomo hivi vya Umar tu bali ni mengi kama vile katika rai zake na ushuhuda wake katika Aya na kisomo chake! Mtafanya nini inapothibiti kwenu kauli au kitendo cha Umar cha kwenda kinyume na Qur’ani iliyoko?

Mas’ala ya 105 Aya za Aisha zilizoliwa na wanyama wafugwao nyumbani Qur’ani ya waislamu wakaifanya ipungue mpaka siku ya Kiyama Kisa cha wanyama wa Aisha waliokula Aya kinaunganishwa na cha kuwanyonyesha watu wakubwa, ambacho ni yeye Aisha pekee aliyehusika nacho, akasema: “Yajuzu kwa mwanamke au kwa baadhi ya ndugu zake, amnyonyeshe mwanamume, na awe ni mwanawe wa kunyonya!” Wake wa Mtume wakampinga hilo lakini alisisitiza kauli yake hiyo, na akaongeza kuwa nyonyesho linalofanya kuwa mwanawe huyo ni mahram ni lile la mara tano, na sio la mara kumi na tano, au kumi! Na akadai kuwa imeshuka Aya inayotosheleza manyonyesho matano, na alikuwa akiisoma katika Qur’ani mpaka Mtume (s.a.w.w.) alipofariki, na hiyo ilikuwa imeandikwa pamoja na Aya zingine kwenye karatasi iliyokuwa chini ya kitanda chake. Akashughulishwa na kifo cha Mtume akaingia mnyama na akaila hiyo karatasi. Muslim amesema katika Juz. 4, Uk. 167: “Kutoka kwa Aisha, amesema: ‘Kati ya Qur’ani iliyoshuka ilikuwa ni: (ÚÔÑ ÑÖÚÇÊ ãÚáæãÇÊ íÍÑãä) (Manyonyesho kumi hufanya mahram), kisha zikafutwa na matano, hadi anapofariki Mtume (s.a.w.w.) zilikuwa bado zinazosomwa katika Qur’ani. (Amepokea Darmi Juz. 2, Uk. 157, Ibn Maja Juz. 1 Uk. 625, Musnad ya Shafi’i Uk. 416. Na akapokea baada ya hiyo kauli yake: ‘Ilishuka Aya ya rajm na kumnyonyesha mtu mzima mara kumi, na ilikuwa kwenye ukurasa chini ya kitanda changu, alipofariki Mtume (s.a.w.w.) tulikuwa tumeshughulishwa na kifo chake akaingia mnyama, akaila.”’ Aisha alikuwa akimtuma mtu anayetaka kumwona kuwa aende kwa dada 45

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

yake au mke wa kaka yake, amnyonyeshe mara tano, na hapo anakuwa maharim wake. na wapokezi wametaja majina ya wale watu ambao Aisha aliwatuma kwa ndugu zake wawanyonyeshe ili wapate kumwona yeye bila tatizo. Ahmad amesema katika Musnad yake Juz. 6, Uk. 271: “Aisha alikuwa akiamuru dada zake na mabinti wa dada zake wamnyonyeshe anayetaka kumuona Aisha japo kuwa ni mtu mzima, amnyonyeshe mara tano kisha huingia kwake! Ummu Salama na wakeze Mtume wengine wakakataa waingie kwao kwa manyonyesho hayo yeyote katika watu mpaka anyonye akiwa mdogo. Ama Maimamu wa Ahlul-Bayt wao wakasema: “Hakuna kunyonya baada ya muda wa kuachishwa, wala hakuna kunyonyesha kipindi cha chakula, hapana budi mtoto awe yu katika miaka ya kunyonya na anyonye kutoka kwa mama manyonyesho kumi na matano mfululizo, au anyonye kiasi cha kukua nyama za mwili wake na kukazana mifupa yake.

Maswali Mna maoni gani juu ya mtu mzima kunyonya kwa mwanamke asiyekuwa mahramu wake? Mna maoni gani juu ya alivyofanya Hafsa, Abdu Razak ametaja katika Muswannaf yake Juz. 7, Uk. 458 chini ya mlango wa kunyonya kwa mtu mzima, kiasi cha riwaya hamsini, ikiwamo hii: “Kutoka kwa Ibn Jarih amesema: ‘Nimemsikia Nafii huria wa Ibn Umar akieleza kuwa mwana wa Abu Ubayda mke wa Ibn Umar alimwambia kwamba, Hafsa binti Umar mke wa Mtume (s.a.w.w.) alimtuma kijana mtanashati kupitia baadhi ya mahuria wa Umar aende kwa dadake Fatima binti Umar, akamuamuru amnyonyeshe mara kumi, akafanya hivyo, basi akawa anaingia kwake baada ya kuwa ni mtu mzima.

46

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

Mna maoni gani juu ya fatwa ya Abdallah bin Umar kwamba kunyonya kwa mara ya kwanza kunajenga umaharimu? Suyuti amesema katika Durrul Manthuri Juz. 2, Uk. 1354: “Ametaja bin Abi Shiba, kutoka kwa Ibn Umar amesema: ‘Nyonyesho moja lafanya umaharim.”’ Mna maoni gani juu ya yale aliyopokea Bukhari katika Juz. 6, Uk. 125 “Kutoka kwa Masruq, kutoka kwa Aisha kwamba Mtume aliingia kwake ilihali kulikuwa na mtu, basi akawa kana kwamba uso wake umebadilika amechukizwa na hilo, Aisha akasema: ‘Huyo ni ndugu yangu.’ Mtume akasema: ‘Wachunguzeni ndugu zenu kwani kunyonyesha hutokana na njaa.’’’ Na katika Juz. 3, Uk. 150: “Mtume akasema: “Ni nani huyu?’ Aisha akasema: ‘Huyu ni ndugu yangu wa kunyonya.’’’ Mmesema kuwa Mtume aliugua na kufia na kuzikwa katika nyumba (yaani chumba) cha Aisha, na hapa Aisha anasema: “Na chini ya kitanda changu kulikuwa na karatasi, Mtume alipokufa tulishughulishwa na kifo chake, akaingia mnyama howa, akaila ile karatasi.” Hii inaonyesha kuwa kuugua na kufariki kwa Mtume hakukuwa kwenye chumba cha Aisha, ama sivyo asingeliingia mnyama alipokuwa mgonjwa au baada ya kufa kwake, mnasemaje? Katika riwaya ya Muslim Aisha anasema: “Akafariki Mtume nazo zikiwa ni kati ya Qur’ani zinazosomwa.” Na haya ni maelezo ya wazi kwamba Aya hizo zinazodaiwa hazikufutwa, na kuwa Qur’ani imebaki ikiwa pungufu, je mwamsadiki Aisha kwa kupungua Qur’ani? Mnakusanya vipi kati ya kauli ya Aisha iliyotangulia na ile kauli aliyoipokea Suyuti katika Durrul Manthuuri Juz. 2, Uk. 135, aliposema: “Ametaja Abdu Razaq kutoka kwa Aisha kuwa amesema: ‘Katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu kulikuwa na manyonyesho kumi kisha akayapunguza mpaka matano.”

47

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

Ibn Maja ametaja na pia Ibn Dharis kutoka kwa Aisha amesema: ‘‘Kati ya Qur’ani iliyoshuka kisha ikaondoshwa ilikuwa ni: (Hawi mtu maharim ila baada ya manyonyesho kumi au matano.)” Mnawalaumu Shi’ah kuwa katika rejea zao kuna riwaya zinazosema kuna upungufu katika Qur’ani, lakini bila shaka wanavyuoni wao wamejibu kwa matini na sanadi… Sasa ni huyu hapa Aisha anasema waziwazi kuwa Qur’ani imepungua, je mwamtia makosani? au mnazitia dosari sanad za riwaya zake? Mnataka Shi’ah wawakufurishe wanavyuoni wao ambao kutokana na shubha wanadai upungufu wa Aya katika Qur’ani au herufi moja, je mnafanya juu ya Umar, Aisha, Ash’ari na wengineo yale mnayoyataka kutoka kwetu, na je mnayafanya juu ya Bukhari, Muslim na wengineo? Nini maoni yenu juu ya wasifu wa Ibn Hazm kuhusu Hadithi za Aisha katika Al-Mahalli Juz. 10, Uk. 14: “Hadith hizi mbili ziko katika upeo wa usahihi wa wapokezi ni waaminifu, na hawezi mmoja kutoka nje ya hizo.” Kulingana na maneno ya Aisha, mnyama ndiye aliyesababisha Qur’ani ya waislamu iwe pungufu mpaka siku ya Kiyama, na hili ni kosa la kihistoria kwa haki ya umma na watu, je si wajibu wa masunni kuwachukia wanyama howa na mbuzi au waiharamishe nyama yao kwa kipimo cha nguruwe?

Mas’ala 106 Jaribio la Umar la kugeuza Aya Yamekuja maelezo rasmi juu ya elimu ya Kitabu ya Mwenyezi Mungu. Mfano: Maelezo ya kupewa Kitabu: Kwa maana ya kupewa umma wote, wakiwamo wale waliokikengeuka na kukipoteza, na hawakujua kutoka kwacho ila matamanio tu, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: 48

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

“Hakika dini mbele ya Mwenyezi Mungu ni Uislamu, na hawakuhitiafiana wale waliopewa Kitabu ila baada ya kuwajilia elimu kwa sababu ya hasadi baina yao. Na anayezikataa Aya za Mwenyezi Mungu, basi hakika Mwenyezi Mungu ni mwepesi wa kuhesabu.” (Aali Imran: 19) Kama ilivyotumika kwa maana ya kupewa hasa kwa manabii na mawasii wao pale aliposema Mwenyezi Mungu:

“Hao ndio wale tuliowapa Kitabu na hukmu na Utume, kama hawa wakiyakataa hayo, basi tumekwisha yawekea watu wasiyoyakataa. Hao ndio aliowaongoza Mwenyezi Mungu, basi fuata muongozo wao, sema, siwaombi malipo juu ya haya, hayakuwa haya ila ni mawaidha kwa walimwengu.” (Al-An’am: 89-90). Kurithishwa Kitabu: Pia imekuja kwa maana ya kiujumla, na kwa maana ya kimakhsusi, yamekusanywa hayo katika kauli yake Mwenyezi Mungu:

49

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

“Kisha tukawapa Kitabu wale tuliowachagua kutoka katika waja wetu, katika wao kuna katika wao aliyejidhulumu nafsi yake, na kuna walioshika njia ya kati na kati, na kuna miongoni mwao anayepita mbele katika kheri kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, hiyo ni fadhila kubwa.’’(Fatir : 32). Waliozama katika elimu: Amesema Mwenyezi Mungu:

“Yeye ndiye aliyekuteremshia Kitabu, ndani yake mna Aya waziwazi, hizo ni msingi wa kitabu, na kuna zingine za kufichikana (mutashabihaat), ama wale ambao ndani ya nyoyo zao kuna upotofu wanafuata zile zenye kufichikana katika hayo kwa ajili ya upotofu na kutaka kufasiri (watakavyo). Na hakuna ajuaye taawili yake ila Mwenyezi Mungu na waliozama katika elimu, wanaosema, tumekiamini kila kinachotoka kwa Mola wetu, na hawakumbuki ila wenye akili.” (AlImran: 7). 50

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

Ambaye ana elimu toka ndani ya Kitabu: Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Akasema (Suleiman): Enyi wakuu wa baraza! Ni nani kati yenu atakayeniletea kiti chake kabla hawajafika kwangu hali ya kuwa wamekwisha silimu? Akasema Ifriti katika majini: Mimi nitakuletea kabla hujasimama kutoka mahali pako, nami bila shaka nina nguvu, mwaminifu. Akasema yule ambaye alikuwa na elimu ya Kitabu: Mimi nitakuletea hicho hata kabla ya kupepesa jicho lako. Basi alipokiona kimewekwa mbele yake, alisema: Hii ni katika fadhila za Mwenyezi Mungu wangu ili anijaribu kama nitashukuru au nitakufuru. Anayeshukuru basi anashukuru kwa ajili ya nafsi yake na anayekufuru basi Mola wangu ni Mkwasi, Mkarimu.” (Namli: 38-40). Yule ambaye ana elimu ya Kitabu: Amesema Mwenyezi Mungu:

“Na wanasema makafiri, wewe si Mtume. Sema, Mwenyezi Mungu anatosha kuwa shahidi baina yangu na yenu na (pia) mwenye elimu ya Kitabu.’’ (Raad: 43). 51

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

Hadithi sahihi zimeonyesha kuwa waliozama katika elimu na walio na elimu ya Kitabu, baada ya Mtume wao ni Ahlul-Bayt watakatifu, na inaonyesha Hadith ya thaqalaini iliyoafikiwa na wote, nayo ni ile kauli ya Mtume (s.a.w.w.): “Mimi nakaribia kuitwa na kujibu mwito, nami nawaachia vizito viwili: Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu na kizazi changu. Kitabu cha Mwenyezi Mungu ni kamba iliyonyooka, kutoka mbinguni mpaka duniani, na kizazi changu Ahlul-Bayt wangu; na Mpole Mjuzi ameniambia kwamba viwilli hivyo havitatengana mpaka vinirudie kwenye hodhi, basi angalieni vile mtakavyoishi navyo baada yangu katika viwili hivyo. (Ahmad Juz. 3, Uk. 17 kwa sanad sahihi na wengineo…). Hakuna maana kwa Mwenyezi Mungu kumwambia Mtume wake kwamba hivyo havitatengana mpaka siku ya Kiyama ila kwamba kutakuwa katika wao Imam katika kila zama mwenye elimu ya Kitabu na atakuwa ni bora kuliko waziri wa Suleiman na wasii wake Asif bin Barkhiya ambaye ana elimu ya Kitabu. Mpaka kufikia hapa hakuna mushkil wala hitilafu, lakini una maoni gani kwa anayetaka kufanya kasra neno man katika kauli yake Mwenyezi Mungu akabadilisha kutoka kwenye ism mawsuul hadi kwenye harfu jar akafanya kasri neno i’ndahu na kilifanya i’ndihi Hapana budi useme kwamba kazi hii ni ya kishetani na ya kupotosha Qur’ani. Na utasema kuwa haisihi kwa kuwa maana ya jumla itakuwa

(Sema, Mwenyezi Mungu anatosha kuwa shahidi baina yangu na yenu ). Na akaifanya ‘min i’ndihi’ kuwa ni jumla mpya iko mbali na maudhui, 52

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

pamoja na kuwa Aya ni ya mwisho katika Sura ya Rad’d. Lakini mwenye kupomoka katika upotofu hajali maana dhaifu, lengo lake ni kukanusha kuwapo kwa watu wenye elimu ya Kitabu na hutaka kuiweka Aya mbali na Ali (a.s.). Na hivi ndiyo alivyosema Umar ‘wamin i’ndihi’ na kuinasibisha na Mtume (s.a.w.w.). Suyuti katika Durrul Manthur Juz. 4, Uk. 69 amesema: “Tamam ameeleza katika Fawaaid yake, na Ibn Mardawayhi kutoka kwa Umar kwamba Mtume (s.a.w.w.) alisoma akasema:

Na katika Kanzul-Ummal Juz. 2, Uk. 593 amesema: “Kutoka kwa Umar ni kuwa Mtume (s.a.w.w.) alisoma: Amepokea Daru Qutni katika Al-Ifrad na Tamam na Ibn Mardawayhi. Na katika Juz. 12, Uk. 589: “Kutoka kwa mtoto wa Umar amesema: ‘Amesema Umar, akataja kusilimu kwake, akataja ambapo alikwenda kwenye nyumba ili asilimu alimsikia Mtume akisoma: (Ibn Mardawayhi). Wanavyuoni wa kisunni wameona kuwa kisomo cha Umar…. hakifai Wafuasi wa Umar wameona kuwa kisomo chake ni dhaifu hakina wajihi hawakumtii, kwa hivyo katika msahafu uliopo sasa utaona: ARABIC TXT Muhtasari wa yale aliyosema Tabari katika Tafsiir yake Juz. 7, Uk. 118 ni: “Katika Aya hiyo kuna visomo viwili, kuna cha kusoma kwa fat-ha, hivyo herufi man inakuwa ni ismu mausuul. Na kingine ni kile cha kasra walichokuwa wakisoma waliotangulia, na kimepokewa kutoka kwa wale wenye kumchukia Ali (a.s.), watu kama Mujahid, Hasan Al-Basri, Sha’aba, Qatada, Harun na Dhahhak bin Muzahim, na akajiepusha na riwaya ya 53

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

kutoka kwa Umar licha ya kuwa Umar ameitegemeza kwa Mtume (s.a.w.w.). Tabari amesema: “Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) Hadith ya kusahihisha kisomo hiki na ufafanuzi huu, ila isnad yake inahitaji uangalifu, hiyo ni kutokana na yale aliyotuhadithia Al-Qasim, amesema: “Ametuhadithia Husein akasema: Ametuhadithia Ubbadu bin Al-Awaam kutoka kwa Haruna kiguru, kutoka kwa Zahri kutoka kwa Salim bin Abdallah kutoka kwa babake, kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) kwamba, yeye alisoma ARABIC TXT. Hadith hii haina asili kwa wapokezi wakweli katika wapokezi wa Zahri. Hivyo ikiwa hivyo ndiyo, na ikawa wasomaji wa miji minginne kuanzia wakazi wa Hijaz, Sham na Iraq walikuwa wakisoma kisomo kingine, nacho ni ARABIC TXT, basi maelezo ya maana ya kisomo cha wasomaji wa miji mingine ndio yaliyo awla na sawa kuliko yale ya wanaopinga, kwani kisomo cha wengi ndio chenye haki zaidi ya kuwa sawa.” Kwa hivyo Tabari alipendelea kisomo cha fat-ha kuliko cha Umar na waliomfuata miongoni mwa wasomaji wakubwa na wafasiri wa zamani, na akaiporomosha riwaya ya Zahri kwa sababu wanafunzi wa Zahri wakweli hawakuiamini! Lakini ameghafilika kuwa kisomo cha kasra hakikufungwa kwa njia ya Zahri, na kuwa wa kwanza kukizusha ni Umar na akakitegemeza kwa Mtume (s.a.w.w.). Ama Fakhru Razi yeye alikimbia katika vita vya kusoma kwa kasra na akatosheka katika Tafsir yake Juz. 19, Uk. 69 kwa kutaja kauli akijengea kisomo cha fat-ha na cha kasra wala hakupendelea chochote kati ya hivyo, 54

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

akasema: “Na Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye zaidi la sawa.’’ Na hivi ndivyo wafasiri wa kisunni walivyochagua usomaji wa fat-ha na wakalazimika wafuate njia nyingine ili kuiweka mbali Aya na Ali (a.s.), wakasema: “Makusudio ya Kitabu hapo si Qur’ani bali ni Tawrat na Injili. Na makusudio ya ARABIC TXT ni Abdallah bin Salaam au mwingine katika Ulamaa wa Kiyahudi na Kinaswara. Lakini mishkeli mitatu inawapinga bila Jawabu: Kwanza: Lau ingelikuwa Abdallah bin Salaam na wanavyuoni wa Kiyahudi na wa Kinaswara wana elimu ya Kitabu, basi daraja zao zingelikuwa juu zaidi kuliko lile la Asif bin Barkhiya aliyekileta kiti cha Balqis kutoka Yemen na ambaye alikuwa na elimu ya Kitabu. Pili: Vipi Mwenyezi Mungu awajaalie wanavyuoni wa Kiyahudi na Kinaswara mashahidi wa umma huu wa Kiislamu baada ya Mtume wake, ambapo lau utawauliza juu ya utume wa Mtume wetu wangeliukataa?! Tatu: Lau tungelikubali kama wana elimu ya Kitabu, je yuko wapi ambaye ana elimu ya Qur’ani kwenye umma wa Muhammad? Je haipatikani elimu ya Qur’ani baada ya Muhammad kwa yeyote? Au iko kwa fulani na fulani, sahaba ambaye alikuwa hajui maana ya Aya ARABIC TXT Nne: Said bin Jubayr amewaambia kwamba Aya imeshuka Makka, na Myahudi Abdallah bin Salaam amesilimu Madina vipi itamkusudia Aya kabla ya kusilimu?

55

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

Na hivi ndivyo tunaona kuwa kizazi kilichofuata katika wao katika kisomo cha Umar cha kasra hakikuondoa tatizo lao katika kuifafanua! Limebaki swali laelekezwa kwao: Ni nani aliyemjaalia Mwenyezi Mungu kuwa ni shahidi juu ya umma baada ya Mtume (s.a.w.w.)? Na ufafanuzi wao kuwa ni Abdallah bin Salaam au ni wengine katika ulamaa wa Kiyahudi unazidisha tatizo, haulitatui. Wala haiwachomoi kwa Ali (a.s.), kwani ni vipi wanakubali kuwa, mashahidi wenye mafungamano na Mwenyezi Mungu juu ya umma wa kiislamu ni ulamaa wote wa Kiyahudi au baadhi yao? La ajabu ni ile iliyopokewa na Tabari katika Tafsir yake Juz. 7, Uk. 118. Riwaya kutoka kwa Abi Swalih katika kauli yake ARABIC TXT Amesema: “Huyo ni mtu katika wanaadamu hakutajwa jina lake.” Abu Swalih ameogopa kusema kwamba ni Ali (a.s.) akasema ni mtu katika wanaadamu. Abdallah bin Salaam na nguzo za Kiyahudi Tunaporejea maisha ya Abdallah bin Salaam waliyedai kuwa ni shahidi kwa umma, tunampata kuwa bado kasumba yake ya kiyahudi iko katika damu yake. Imepokewa kutoka kwa Dhahabi kwamba alimuomba ruhusa Mtume (s.a.w.w.) kuwa aisome Qur’ani usiku mmoja na Tawrat usiku mwingine, Mtume akamruhusu. Amesema Dhahabi katika Tadhkiratul Hufaadh Juz. 1, Uk. 27: “Amesema Yusuf bin Abdallah bin Salaam kutoka kwa babake kwamba, alikwenda kwa Mtume (s.a.w.w.) akasema: ‘Mimi nimesoma Qur’ani na Tawrat.’ Akasema: ‘Hii soma usiku huu na hii soma usiku mwingine.’ Hii ikiwa sahihi basi kuna ruhusa ya kuisoma Tawrat na kuizingatia!” 56

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

Na juu ya hili yapasa waislamu wasome Tawrat iliyopotoshwa na waichapishe pamoja na Qur’ani!!! Imepokewa katika Majmauz-Zawaaid Juz. 9, Uk. 92 kuwa Abdallah bin Salaam na watoto wake walikuwa wenye kupewa chakula na Bani Umayya, akasema: “Kutoka kwa Abdul Malik bin Umayr kwamba Muhammad bin Yusuf bin Abdallah bin Salaam aliomba ruhusa kwa Hajjaj bin Yusuf, akaruhusiwa aingie akasalimia, akaamuru watu wawili waliokuwa wamekaa kitini wampe nafasi akae, wakampa nafasi akakaa. Hajjaj akamwambia: ‘Babako wallahi! Je wajua hadithi aliyomuhadithia babako Abdul Malik bin Marwan kutoka kwa babu yako Abdallah bin Salaam?’ Akajibu: ‘Ni Hadith gani hiyo Mwenyezi Mungu akurehemu?’ Akasema: ‘Hadithi ya wamisri walipomzingira Uthman?’ Akasema: ‘Ninaijua Hadithi hiyo. Abdallah bin Salaam alifika huku Uthman akiwa amezingirwa na wamisri, akaondoka akaingia kwake, wakampa nafasi akaingia, akasema: ‘Asalam Alayka ewe kiongozi wa waumini.’ akajibu: ‘Wa’alayka salaam. Ni kipi kilichokuleta ee Abdallah bin Salaam?’ Akajibu: ‘Nimekuja ili nithibiti mpaka nife shahidi, au Mwenyezi Mungu akufungulie…..’” Ni Hadithi ndefu, lakini amesema mwishoni mwake: “Ameipokea Tabari na wapokezi wake ni waaminifu.” Na maana ya hilo ni kuwa Maswahaba wote walikuwa dhidi ya Uthman na Abdallah bin Salaam yasemekana alikuwa ni katika wale waliothibiti kwa Uthman, lakini kama tujuavyo mayahudi ni watu wa kwanza kukwepa na kukimbia. Uthman aliuwawa na kubaki bila kuzikwa, lau Ibn Salaam angelikuwa amejitolea damu yake katika maisha yake, alikuwa wapi wakati wa kubeba jeneza na kumzika? Na kutokana na hilo tunajua sababu ya wao kumfanya Ibn Salaam kuwa ni mtu aliyepigana jihadi bega kwa bega na Mtume katika vita, bali ni mpiganaji wa vita vya Badr.

57

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

Amesema katika mstari wa pambizo za kitabu Tahdhibul Kamal Juz. 15, Uk. 75: “Ibnu Hajar amesema: ‘Abu Uruba amemtaja katika waliopigana Badr, na ni yeye pekee aliyesema hilo. Ama Ibn Saad yeye amemtaja katika tabaka la tatu la walioshuhudia vita vya Khandaq na vya baadaye. Na Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye zaidi.”’ (Tahdhibu Tahdhiib Juz. 5, Uk. 249). Mfano wa Hadith zilizowekwa katika tafsiri ya Aya Katika Majmauz Zawaaid Juz. 9, Uk. 92: Amesema Suyuti katika Durrul Manthuuri Juz. 4 Uk, 69: “Kauli ya Mwenyezi Mungu: ‘Na wanasema wale waliokufuru….’ Ameandika Ibn Mardawayhi kutoka kwa Ibn Abbas kuwa amesema: ‘Alikuja askofu kutoka Yemen kwa Mtume (s.a.w.w.), Mtume akamwambia: ‘Je unanipata mimi katika Injili kuwa ni Mtume wa Mwenyezi Mungu?’ akasema: ‘Hapana’. Mwenyezi Mungu akateremsha Aya: ‘Sema, anatosha Mwenyezi Mungu kuwa ni shahidi baina yangu mimi na baina yao na yule ambaye ana elimu ya Kitabu….’ Anasema: Ni Abdallah bin Salaam.”’ Lakini mzushi wa Hadith hakujua kuwa tukio la askofu wa Yemen lilikuwa Madina, ambapo Aya imeshuka Makka, na amesema Umar kwamba aliposilimu Makka alimsikia Mtume akiisoma kwa kasra. Kisha akanukuu Suyuti baadhi ya riwaya kutoka kwa Ibn Salaam akijifaharisha kwa nguo hii waliyomvisha makuraishi. Na kuiiba kutoka kwa Ali bin Abi Talib (a.s.) Amesema Suyuti: “Ametaja Ibn Jariri na Ibn Mardawayhi kwa njia ya Abdul Malik bin Umayr kwamba Muhammad bin Yusuf bin Abdallah bin Salaam amesema: ‘Amesema Abdallah bin Salaam: Mwenyezi Mungu ameteremsha Qur’ani ikinihusu mimi, nayo ni: ‘Sema, anatosha Mwenyezi Mungu kuwa ni shahidi baina yangu mimi na baina yao na yule ambaye ana elimu ya Kitabu….’ 58

7/2/2011

11:30 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

Imepokewa kutoka kwa Jundub amesema: ‘Alikuja Abdallah bin Salaam mpaka akanishika mkono wangu kwenye mlango wa msikiti, kisha akasema: ‘Je! mwajua kuwa mimi ndiye Aya ya “....Na yule ambaye ana elimu ya kitabu…” iliteremka kwake? Wakasema: ‘Ndio.’ Imepokewa kutoka kwa Abdallah bin Salaam kwamba yeye alikutana na wale waliotaka kumuua Uthman akawaambia je mnajua ni nani kwa ajili yake ilishuka Aya: “Sema, anatosha Mwenyezi Mungu kuwa ni shahidi baina yangu mimi na baina yao na yule ambaye ana elimu ya Kitabu….” Wakasema: ‘Kwa ajili yako.’ Na imepokewa kutoka kwa Mujahid kwamba yeye alikuwa akisoma: “Sema, anatosha Mwenyezi Mungu kuwa ni shahidi baina yangu mimi na baina yao na yule ambaye ana elimu ya Kitabu….” Akasema: ‘Mtu huyo ni Abdallah bin Salaam.’” Kisha Suyuti akapokea riwaya mbili zinazokadhibisha kuwa makusudio ya Aya awe ni Abdallah bin Salaam. Akasema: “Ametaja Said bin Mansur, Ibn Jarir, Ibn Mundhir, Ibn Hatim, na Nuhas katika Nasikh yake, kutoka kwa Said bin Jubayr kwamba aliulizwa juu ya kauli yake: “Na yule ambaye ana elimu ya Kitabu….” Je huyo ni Abdallah bin Salaam? Akasema: ‘Vipi iwe hivyo na Sura hii imeshuka Makka?’ Na kutoka kwa Shaaby amesema: ‘Hakikushuka kwa Abdalla bin Salaam, kitu chochote katika Qur’ani.’” Kisha akapokea tafsiri nyingine akaipanua ili iwakusanye watu wengi pamoja na Abdallah bin Salaam. Akasema: “Ametaja Abdu Razaq na Ibn Jarir, Ibn Mundhir na Qatada katika Aya hiyo, akasema: ‘Katika Ahlul Kitabu kulikuwa na watu wanaoshuhudia haki, na wanaoijua akiwamo Abdallah bin Salaam, Jarud, Tamim Dari na Salmanul Farsi.’’’ Kisha Suyuti akapokea tafsiri nyingine akajaalia mashahidi wa umma wa kiislamu wote ni Ahlul Kitab. (Ambao wanashuhudia dhidi ya huo umma). 59

7/2/2011

11:31 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

Akasema: “Ametaja Ibn Jarir kwa njia ya Al-Aufi, kutoka kwa Ibn Abbas: “...Na yule ambaye ana elimu ya Kitabu….” Akasema: ‘Wao ni Ahlul Kitab katika mayahudi na manaswara!”’ Kisha akapokea tafsiri nyingine aliyomfanya ni Jibril (a.s.) akasema: “Ametaja Ibn Abi Hatim kutoka kwa Said bin Jubayr kuhusu kauli yake Mwenyezi Mungu: “...Na yule ambaye ana elimu ya Kitabu….”, amesema, huyo ni Jibril.”’ Na katika tafsiri nyingine alimfanya ni Mwenyezi Mungu, akasema: “Ametaja Ibn Jarir na Ibnul Mundhir na Ibn Abi Hatim kutoka kwa Mujahid: “...Na yule ambaye ana elimu ya Kitabu….”, Akasema: ‘Huyo ni Mwenyezi Mungu.”’

Maswali Mna maoni gani juu ya jaribio la kipotosha Qur’ani? Ni nani huyo aliyejaaliwa kuwa shahidi na Mwenyezi Mungu wa umma juu ya utume wa Mtume wake? Nini maoni yako juu ya yale tuliyopokea kuwa shahidi huyu juu ya utume wa Nabii (s.a.w.w.) ni Ali (a.s.), na je mna mbadala wa maana katika maelezo asiyekuwa yeye anayeingia akilini? Amesema Al-Huwayzi katika maelezo ya Nuru Thaqalayni Juz. 2, Uk. 523: “Katika Aamali cha Saduq kwa isnad yake kwa Abu Said Al-Khidri, amesema: ‘Nilimuuliza Mtume (s.a.w.w.) kuhusu kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu “Sema, anatosha Mwenyezi Mungu kuwa ni shahidi baina yangu mimi na baina yao na yule ambaye ana elimu ya Kitabu….” Akasema: ‘Huyo ni ndugu yangu Ali (a.s.).’”

60

7/2/2011

11:31 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

Al-Ayashi amesema katika Tafsiir yake Juz. 2, Uk. 22: “Kutoka kwa Fudhayl bin Yasar, kutoka kwa Abi Jafar katika kauli yake: “...Na yule ambaye ana elimu ya Kitabu….” Akasema: ‘Imeshuka kwa Ali (a.s.) yeye ni mjuzi wa umma huu baada ya Mtume (s.a.w.w.).”’ Kutoka kwa Burayda bin Muawiya Al-Ujli amesema: “Nilimuuliza Abu Jafar juu ya Aya: “Sema, anatosha Mwenyezi Mungu kuwa ni shahidi baina yangu mimi na baina yao na yule ambaye ana elimu ya Kitabu….”, akasema: ‘Ni kwetu sisi, na Ali (a.s.) ni bora zaidi kwetu na wa mwanzo wetu na ni mbora wetu baada ya Mtume (s.a.w.w.).”’ Kutoka kwa Abdallah bin A’tai, amesema: “Nilimwambia Abu Jafar, huyu Ibn Abdillah bin Salaam anadai kuwa babake ndiye aliyetajwa na Mwenyezi Mungu katika Aya “Sema, anatosha Mwenyezi Mungu kuwa ni shahidi baina yangu mimi na baina yao na yule ambaye ana elimu ya Kitabu….” Akajibu: ‘Amesema uongo. Huyu aliyetajwa ni Ali (a.s.).”’ Kutoka kwa Abdallah bin Ajlan, kutoka kwa Abi Jafar amesema: “Nilimuuliza kuhusu kauli ya Allah “Sema, anatosha Mwenyezi Mungu kuwa ni shahidi baina yangu mimi na baina yao na yule ambaye ana elimu ya Kitabu….”. Akasema: ‘Hiyo imeshuka kwa Ali (a.s.) baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu na Maimamu baada yake, na Ali kwake yeye kuna Ummul Kitab.’’’ Ali bin Ibrahim Al-Qummi amesema katika Tafsiir yake Juz. 1, Uk. 367: “Amenihadithia baba yangu kutoka kwa Ibn Abi Umar kutoka kwa Ibn Adhina kutoka kwa Abu Abdillah (a.s.) amesema: “Yule ambaye ana elimu ya Kitabu….” ni Amirul-Mu’minin Ali (a.s.). Na akaulizwa juu ya yule aliye na elimu ya Kitabu ni mjuzi zaidi au yule aliyeipata toka katika elimu ya kitabu? Akasema: ‘Kiasi alichonacho yule aliyechukua toka kwa mwenye elimu ya kitabu mbele ya mwenye elimu ya kitabu, si chochote bali ni sawa na kiasi cha maji ya bahari anachochukua 61

7/2/2011

11:31 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

mbu kwa ubawa wake. Amirul-Mu’minin (a.s.) akasema: ‘Tambueni kuwa elimu ni ile aliyoshuka nayo Adam kutoka mbinguni mpaka duniani, na kwa manabii wote waliofadhilishwa mpaka kwa mwisho wa mitume, na katika kizazi cha mwisho wa manabii.’’’

Mas’ala 107 Riwaya zenu sahihi zinazopingana kuhusu sehemu ya Qur’ani iliyoshuka mwisho Mmepokea kutoka kwa Umar riwaya zinazogongana kuhusu Aya zilizoshuka mwisho, na kwamba Umar aliulizwa juu ya Aya ya riba na hakuzijua, akasema: “Mimi nina masikitiko kwa kuwa Aya hii ni Aya ya mwisho kushuka na Mtume alikufa na hakuieleza.” Kwa hivyo aliiepusha nafsi yake na akamtuhumu Mtume kuwa hakuifafanua kwa umma wake. Ahmad amesema katika Musnad yake, Juz. 1, Uk. 36: “Kutoka kwa Said bin Musayyib amesema: ‘Amesema Umar: Aya ya mwisho kushuka ni Aya ya riba, na Mtume amekufa na hakuifafanua.”’ (Amepokea mwandishi wa Kanzul Ummal katika Juz. 4, Uk. 186 kutoka kwa Ibn Rahabu Ibn Dhharis na Ibn Jarir, Ibn Mandhur, na Ibn Murdawayhi, na Bayhaqi katika AdDalaailu). Na katika Al-Mabsut Sarkhasi Juz. 2, Uk. 51 na Juz. 12, Uk. 114: “Umar amesema: ‘Aya ya riba ndiyo ya mwisho kushuka na Mtume amekufa kabla hajaifafanua.’’’ Suyuti amesema katika Al-Itqan Juz. 1, Uk. 101: “Ametaja Bukhari kutoka kwa Ibn Abbas amesema: ‘Aya ya mwisho kushuka ni ya riba.’ na Bayhaqi amepokea kama hivyo kutoka kwa Umar. Na amepokea Ahmad na Ibn Majah kutoka kwa Umar: ‘Ya mwisho kuteremka ni Aya ya riba.”’

62

7/2/2011

11:31 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

Na siku moja khalifa Umar hakujua maana ya neno ‘kalaalah’ akashindwa la kufanya akasema au aliambiwa kuwa hiyo ni Aya ya mwisho iliyoshuka na Mtume alikufa kabla hajaifafanua. Na katika Bukhari Juz. 5, Uk. 115: “Kutoka kwa Baraa amesema: ‘Sura ya mwisho kushuka kamili ni Baraa na Aya ya mwisho ni mwisho wa Sura ya Nisaa”’ (Amepokea pia katika Juz. 5 , Uk. 185, na katika Itqaan Juz.1, Uk. 101, na Musnad ya Ahmad Juz. 4, Uk. 298. Katika Bukhari Juz. 5, uk. 182: Amesema: “Nimemsikia Said bin Jubayr akisema: ‘Aya waliohitilafiana ndani yake watu wa Kufa nikaenda na akiwamo humo Ibn Abbas, nikamuuliza juu ya hilo, akasema: Aya hii “ARABIC TXT imeshuka mwisho na haikufutwa na chochote.’’’ Kama hiyo imepokewa katika Juz. 6, Uk. 15, na katika Durrul Manthuri Juz. 2, Uk. 196: “Ametaja Abdu bin Hamid, Bukhari, Muslim, Abu Daud, Nasai , Ibn Jarir na Tabrani kwa njia ya Said bin Jubayr amesema: ‘Watu wa Kufa wamehitilafiana katika kumuua Mwislamu, nikaenda, nayo ndiyo Aya ya mwisho kushuka, na haikufutwa kitu.’’ (Majmau Nawawi Juz. 18, uk. 345). Na katika Mustadrakul Hakim Juz. 2, Uk. 338: “Kutoka kwa Ubayya bin Ka’ab, amesema: ‘Ya mwisho kushuka katika Qur’ani ni Aya:’’ ARABIC TXT (Hakika amewajilia Mtume kutokana na nafsi zenu, ………’’ Hadith ya Shaa’ba kutoka kwa Yunus, bin Abid ni sahihi kwa sharti la masheikh wawili, na hawakuitaja.

63

7/2/2011

11:31 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

Na katika Durrul Manthuri Juz. 3, Uk. 295: “Ametaja Ibn Abu Shayba, Is’haq bin Rawih, Ibn Munii’ katika Musnad yake, Ibn Jarir, Ibnul Mundhir, Abu Sheikh, Ibn Murdawayhi, Al-Bayhaqi katika Ad-Dalaailu, kwa njia ya Yusuf bin Mahran kutoka kwa Ibn Abbas, kutoka kwa Ubayya bin Ka’ab amesema: ‘Aya ya mwisho kushuka kwa Mtume, na katika neno jingine, Ya mwisho kushuka katika Qur’ani ni: ARABIC TXT Na Ibn Dharis ametaja katika Fadhailul Qur’ani, na Ibnul Anbari, katika Masahif, na Ibn Mardawayhi, kutoka kwa Hasan, kwamba Ubayya bin Ka’ab alikuwa akisema: ‘Aya mbili zinazozungumzia ahadi na Mwenyezi Mungu ni hizi mbili: ARABIC TXT “ Amewajia Mtume kutoka kwenye nafsi zenu….” Na ametaja Abdallah bin Ahmad bin Hambali katika Zawaaidul Musnad, na Ibn Dharis katika Fadhail yake, Ibn Abi Daud katika Masahif, Ibn Abi Hatim, Abu Sheikh, Mardawayhi, Al-Bayhaqi katika Dalaailu, Al-Khatibu katika Talkhisul Mutashabiha kwa njia ya Abu A’aliya, kutoka kwa Ubayya bin Ka’ab, kwamba waliikusanya Qur’ani kwenye msahafu wakati wa ukhalifa wa Abu Bakr, watu walikuwa wakiandika na Ubayya akiwasomea, mpaka wakakomea katika Aya hii, katika Sura ya baraa ARABIC TXT wakadhani kuwa hii ndiyo Aya ya mwisho kushuka, Ubayya bin Ka’ab akasema: ‘Mtume alinisomea Aya mbili baada ya Aya hii ARABIC TXT.

Hii ndio ya mwisho kushuka katika Qur’ani.”’ 64

7/2/2011

11:31 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

Na katika Muslim, Juz. 8, uk. 243: “Kutoka kwa Ibn Abbas, Wajua kwamba sura ya mwisho iliyoteremshwa katika Qur’ani iliteremshwa yote? Nikasema, ndio, ni Sura ya Idhaa jaaa nasru llahi walfat-hu. Akasema: ‘Umesema kweli.”’ Na katika Mu’ujamul Kabir cha Twabarani Juz. 12, Uk. 19 “Kutoka kwa Abbas, amesema: ‘Aya ya mwisho kushuka ni ARABIC TXT”’. Na Aya hii ni ya 281 katika Suratul Baqarah! Huenda Suyuti aliona haya kutokna na Hadithi zenu nyingi zilizo sahihi, zinazozungumzia juu ya sehemu ya mwisho kushuka katika Qur’ani, ndipo akazikusanya kiujumla, hakuorodhesha ya kwanza wala ya mwisho, kama alivyoorodhesha kauli juu ya Aya iliyoshuka mwanzo, nasi tunaziorodhesha hapa kwa muhtasari: 1. Aya ya mwisho ni Aya ya riba, nayo ni Aya ya 278 katika Sura ya Baqarahh. 2. Aya ya mwisho ni Aya ya Kalaala , yaani urithi wa ndugu wasio karibu, nayo ni Aya ya 176 katia Sura ya Nisaa. 3. Aya ya mwisho ni Aya nayo niAya ya 281 katika Sura ya Baqarah.

ya

ARBIC

TXT

4. Aya ya mwisho ni Aya ya RABIC TXT Aya ya 128 katika Sura ya Tawbah.

nayo ni

5. Aya ya mwisho ni Aya ya ARABC TXT Aya ya 25 katika Sura ya Anbiyaa.

nayo ni

65

7/2/2011

11:31 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

6. Aya ya mwisho ni Aya ya Arabic txt 110. 7. Aya ya mwisho ni Aya ya ARABIC TXT Sura Nisaa.

Al-Kahf Aya ya

nayo ni ya 93

8. Sura ya mwisho ni Sura ya Tawbah. 9. Sura ya mwisho ni Sura ya Nasri Haya ndio yaliyokuja katika Itqan ya Suyuti Juz. 1, Uk. 101, kauli za maimamu wao na riwaya zao sahihi zimefikia mara mbili ya hapo kwa mtu anayefuatilia marejeo yao.

Maswali Kwa kipi mnafafanua migongano hii juu ya sehemu ya mwisho iliyoshuka katika Qur’ani na Mtume (s.a.w.w.) yuko kati yao na wote wapo? Je ni ujinga au ni vitendo vya kisiasa vilivyoathiri kila kilichotokea kwa masahaba wenu takriban? Vipi mnasema kuwa kila kilicho ndani ya Sahih Bukhari ni sahihi na kuna Hadith zinazogongana, je mgongano kwa mantiki yenu unafaa? Riba imetajwa katika Sura nne katika Qur’ani: Katika Aya mbili 275 na 276 za Baqarah, Aya 161 Suratun-Nisaa, Aya 39 Surat Rum, na Aya 130 Sura Al-Imran, na baadhi ya Sura hizi zimeshuka Makka na nyingine Madina, ni Aya ipi aliyoikusudia Umar? Kwa kipi mnafafanua kuwa Muawiya bin Abu Sufiani alijiingiza katika suala la Aya ya mwisho kuteremshwa, na akakanusha juu ya mimbari kuwa Aya ya ARABIC TXT si ya mwisho kushuka, na akatoa fatwa kuwa ya mwisho ni Aya ya 110 Sura ya Al-Kahf, na ilikuwa ni ya kum66

7/2/2011

11:31 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

funza adabu Mtume (s.a.w.w.). Katika Al-Kabir ya Tabarani Juz. 19, Uk. 392 “Kutoka kwa Umar bin Qaysi kwamba alimsikia Muawiya bin Abu Sufiani akisema juu ya mimbari kwamba ameivua Aya hii ya ARABIC TXT akasema: ‘Ilishuka siku ya Arafa siku ya Ijumaa.’ kisha akasema Aya ya mwisho kushuka ni: ARABIC TXT ili kumfundisha adabu Mtume (s.a.w.w.).

Mas’ala ya 108 Wameunda naskhu za kisomo ili kuboresha kauli za maimamu wao za kuhusu kupotoshwa Wanavyuoni wa kiutawala waliunda neno la ‘kufutwa kisomo’ ili kuwatakasa maimamu wao na rejea zao kutokana na kauli ya kupotosha Qur’ani. Maana yake ni kwamba kila Aya ambazo zimedaiwa na maimamu wao kama Umar, Abu Musa, Aisha na wengineo kuwa ni katika Qur’ani zilikuwepo kisha ukafutwa usomwaji wake, zikaondolewa katika Qur’ani zikabaki hukmu zake. Lakini kufuta huko hakuponyeshi kila wayasemayo juu ya kupotoshwa Qur’ani, kama kauli ya Umar na wengineo, kwamba theluthi ya Qur’ani ilikwenda na kufariki kwa Mtume (s.a.w.w.) au zaidi, wala bidaa ya Umar katika herufi saba, fatwa yake katika kujuzu kubadilishwa maneno ya Qur’ani na mengineyo. Na hata Aya ambazo wamedai kuwa ni Qur’ani, kwani kufuta usomaji hakuondoi tatizo ila sehemu ndogo sana, mfano Aisha anasema kuwa Aya zilizoliwa na wanyama zilikuwa zikisomwa mpaka alipokufa Mtume (s.a.w.w.). Na hivyo anakataa kuwa iwe ni mansukh (yenye kufutwa) katika uhai wa Mtume na hata baada ya kufa kwake. 67

7/2/2011

11:31 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

Pia tunaona nassi (maandiko) ya Aya nyingi zinazodaiwa zinakataa kwao kwamba zimefutwa. Ibnul Jawzi amehesabu katika utangulizi wa kitabu chake Nawasikhul Qur’ani na akajaribu kuoanisha kufutwa kwa visomo na yale maneno ya maimamu wao kuhusu kupotosha. Akasema katika Uk. 33: “Kifungu cha kwanza: Zilizofutwa maandishi yake na hukmu yake. Na kimeletewa mfano kutoka kwa Abu Umama bin Sahal bin Hanif kwamba, watu katika maswahaba wa Mtume walimwambia kuwa kuna mtu katika wao alisimama usiku wa manane, akataka kuifunua Sura ambayo alikuwa ameihifadhi, hakuweza chochote ila Bismillahi rahmaanir rahiim, akaenda mlangoni kwa Mtume (s.a.w.w.) ili amuulize juu ya hilo. Akaja na mwingine na mwingine mpaka wakakusanyika wakaulizana: Kwa nini wamekusanyika? Wengine wakaambiana ni juu ya Sura ile. Akanyamaza saa nzima hawajibu kisha akasema: ‘Jana imefutwa.’ Na ikafutwa kutoka nyoyoni mwao, na kila kilichokuwamo ndani yake.’’ Na umepokewa mfano mwingine kutoka kwa Abu Musa Al-Ash’a’ri, amesema: “Iliteremka Sura kama Baraatun kisha ikaondolewa.’’ Akaihifadhi katika hiyo:

Na imepokewa kutoka kwa Mujahid, amesema: “Sura ya Ahzab ilikuwa kama ya Baqarah, au ndefu zaidi.” Na kutoka kwa Ubayya bin Kaa’ab naye amesema: “Imeshuka kwa Muhammad, nayo ni ndefu kama Baqarah au yazidi kidogo.’’ Na kutoka kwa Ibn Mas’ud, amesema: “Ilishuka Aya kwa Mtume na nikaiandika katika msahafu wangu, ikawa ilipofika usiku, mara karatasi ime68

7/2/2011

11:31 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

baki nyeupe! Nikamwambia Mtume (s.a.w.w.), naye akasema: ‘Je hujui kwamba hiyo ilifutwa jana usiku.’’’ Haiwezekani tuzisadiki riwaya hizi, kwani zilivyo hasa ni Hadith pwekesho, hazina uthibitisho mkubwa, vinginevyo zingepokewa na wengine. Kisha Ibnul Jawzi amesema: “Sehemu ya pili ya Aya ni zile zilizofutwa maandishi yake na kubaki hukmu yake, na akaioanisha na Aya ya Umar ARABIC TXT na Aya ya Umar nyingine ARABIC TXT. Zimetangulia kutajwa katika Bukhari na Muslim. Na akapokea kauli ya Umar: “Na Naapa kwa Mwenyezi Mungu, lau si mtu kusema kuwa Umar amezidisha katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu, basi ningeliiandika katika Qur’ani…hakika imeshuka na tumeisoma, ARABIC T XT: ‘Wazee wawili wa kike na wa kiume wakizini, basi wapigeni mawe,’ lau si kuambiwa Umar amezidisha katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu basi ningeliiandika kwa mkono wangu.’’ Kisha amepokea Ibnul Jawzi, kutoka kwa Ubayya bin Ka’ab, yeye amesema juu ya Suratul Ahzab: “Tulikuwa tukiisoma kama tunavyoisoma Sura ya Baqarah, na tulikuwa tukisoma ndani yake: ‘ARABIC TXT ‘Wazee wawili wa kike na wa kiume wakizini, basi wapigeni mawe mara moja ikiwa ni adhabu kutoka kwa Allah, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima.” Kisha ilipokewa kutoka kwa Umar kwamba alimwambia Abdurahman bin A’wf: “Je hukupata katika aliyoteremsha Mwenyezi Mungu kwetu ARABIC TXT lakini hatuioni, akasema: ‘Imefutwa katika zilizofutwa katika Qur’ani.’’’ 69

7/2/2011

11:31 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

Na amepokea kutoka kwa Hamida kwamba ilikuwa katika msahafu wa Aisha, ARABIC TXT Na kutoka kwa Anas: “ Mtume (s.a.w.w.) alimtuma mjomba wake na watu sabini wakauwawa siku ya Biir mauna. Akasema: Ikashuka kwetu ikawa ni katika tunayosoma, kisha ikafutwa nayo ni: ’ ARABIC TXT” Ibn Al-Jawzi amesema: “Hii ameitoa Bukhari peke yake.’’ Lakini haiwezekani kuzikubali riwaya za kifungu hiki pia kwa ajili ya mambo yafuatayo: Kwamba Hadith zote ni pwekesho, lau kama ni jambo sahihi habari yake ingelienea, na riwaya zake zingelikuwa nyingi kwa maswahaba na AhlulBayt. Aya zote zinazodaiwa ni dhaifu hazifanani chochote na Qur’ani! Aya ya Umar ARABIC TXT Umar aliifafanua kwamba itakapokuwa maamiri wa Bani Umayya na mawaziri wa Bani Makhzum! Amepokea Suyuti katika Durrul Manthuri Juz. 4, Uk. 371 riwaya hiyo ya Ibul Jawzi kutoka kwa Ibn A’uf na mwisho wake ni kama ifuatavyo: “Nikasema, ndio. Hii mpaka lini ewe Amirul-Mu’minin? Akasema: ‘Ni pale Bani Umayya watakapokuwa maamiri, na Bani Mughira kuwa mawaziri.’’’Akasema Suyuti: “Ameitaja Bayhaqi katika Dalail kutoka kwa Masruur bin Mukhrima.” Na sisi tunaafikiana na maana hii, kwa sababu imetoka katika Hadithi sahihi, kwetu na kwao, nayo inawajibisha waislamu kupigana jihadi na makuraish kwa maelezo ya Qur’ani, kama alivyopigana nao Mtume mwanzo wa kushuka na aliyesimamia hilo ni Ali (a.s.).

70

7/2/2011

11:31 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

Na katika Hadith zake katika rejea zao ‘Hadith ya fundi viatu’ aliyoipokea Tirmidhi Juz. 5, Uk. 298 na kuisahihisha humo kuna: “Ee watu wa Kuraish! Mtakoma au Mwenyezi Mungu atawaletea atakayewakata shingo zenu kwa upanga wake, juu ya dini, hakika amewafanyia mtihani nyoyo zao Mwenyezi Mungu kwa imani.’ Wakasema: ‘Ni nani huyo ee Mtume wa Mungu?’ Abu Bakr akasema: ‘Ni nani huyo ee Mtume wa Mungu? Umar akasema: ‘Ni nani huyo ee Mtume wa Mungu?’ Mtume akasema: ‘Huyo ni fundi viatu.’ Na Ali alikuwa amepewa kiatu chake cha sandali akishone.” (Amepokea Hakim Juz. 2, Uk. 138, na Juz. 4, Uk. 298, na kuisahihisha kwa sharti la Muslim).

Na katika Hadith zetu katika rejea zetu: Ni aliyopokea Al-Ayashi Juz. 2, Uk. 229: katika Tafsiir ya kauli yake Allah ‘ARABIC TXT Kutoka kwa Imam Sadiq (a.s.) amesema: “Mnasemaje juu ya hilo?’’ Wakasema: ‘Wao ni wawili kutoka kwa makuraishi wa Banu Umayya na Banu Mughira.’ Akasema: ‘Bali ni makuraishi wote. Mwenyezi Mungu amemwambia Mtume wake akasema: ‘Mimi nimewafanya bora makuraishi juu ya waarabu na kuwatimizia neema yangu ya kuwapelekea Mtume, wao wakazibadilisha neema Zangu, na kumkadhibisha Mtume Wangu.”’ Maneno ya jihadi ya mara ya kwanza au ya mara ya pili au jihadi juu ya kushuka kwake Qur’ani kisha juu ya maeelzo yake, ni maneno ya kiislamu yaliyothibiti kutoka kwa Mtume na kuambatana na itikadi ya Ahlul-Bayt, lakini hatuwafiki kuwa Aya ilishuka kwayo, kisha ikaondolewa kama inavyosema riwaya ya Umar. Nne: Riwaya za Aya hii inayodaiwa zinagongana, baadhi yao ni kuwa mwenye kudai Aya hii ni Umar, wengine Ibn Abbas, kama ile ya Suyuti, katika Durrul Manthur Juz. 5, Uk. 197. Na akataja mdahalo uliozuka baina 71

7/2/2011

11:31 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

ya Umar na Ibn Abbas, kana kwamba Umar haijui, au ana shaka nayo na Ibn Abbas anaithibitisha. Amesema Suyuti: “Ametaja Ibn Jarir na Ibn Mundhir, Ibn Mardawayhi na Ibn Abbas, kwamba Umar alimuuliza…Akasema Umar: ‘Ni nani aliyetuamuru kupigana nao jihadi? Akasema: ‘Bni Makhzum na Abdu Shams.’’ Upinzani huu unatia shaka katika asili ya kuwapo Aya hiyo kisha ifutwe! Tano: Hukmu katika kifungu cha pili kuwa maandishi yamefutwa lakini ikabaki hukmu, hata kama imefutwa au kuondolewa katika Qur’ani, lakini riwaya ya Ibnul Jawzi na ya Musawir bin Mukhrima (Katika Kanzul Ummal Juz. 2, Uk. 567 na nyingine) zinapinga hilo, na zinasema kuwa imeondolewa. Maana yake haikufutwa bali imeondolewa kusudi au kwa kusahau au kwa kupotea. Na hiyo si kufuta! Sita: Aya ya Aisha inayodaiwa, haina maana inayoingia akilini, mpaka ikubaliwe kuwa imeshuka na ikaondolewa. Nini maana ya kuwa Mwenyezi Mungu anafuatanisha Swala ya kumswalia Mtume wake, na kuwaswalia wanaoswali katika safu ya kwanza? Vipi hapo itasihi amalizie: ARABIC TXT Lau ingesihi nyongeza ya Aisha ingelazimu kusema kuwa, maana ya Aya ni makosa au dhaifu, mpaka Mwenyezi Mungu akalazimika kondoa katika Aya ile sehemu aliyoidai Aisha. Saba: Kwamba Aya ya Anas inayohusu wasomaji wa kisima cha Mauna ambao waliuawa na watu wa Najd: “Imetufikia watu wetu kwamba tumekutana na Mola wetu akaturidhia na sisi tukamridhia.” Hii ndiyo Aya peke katika Aya zinazodaiwa ambazo imekuja nassi ya riwaya yake kwamba ilikuwa katika inayosomwa katika Qur’ani kisha ikaondolewa au kufutwa. Ambapo imesihi riwaya yake kwenu. (Bukhari Juz. 3, Uk. 204, na 208, na Juz. 4, Uk. 35, na Juz. 5, Uk. 42, na zingine katika Sahih zenu). Hivyo 72

7/2/2011

11:31 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

yenyewe inakuwa ndio mfano pekee ulio sahihi kuhusu kufutwa kisomo na kubaki hukmu, lakini iko wapi hukmu yake iliyobakia? bali uko wapi ufasaha wa Aya za Qur’ani ndani ya Aya yenu hiyo. Kisha Ibnul Jawzi amesema: “Sehemu ya zilizofutwa maandishi yake na kuhitilafiana katika kubaki kwa hukmu yake: Na zimepokewa ndani yake Aya za Aisha ambazo zililiwa na mnyama, na kunakiliwa kauli zake mbali mbali katika kinachopasa kuharamisha kunyonya, je ni nyonyesho moja au matano au kumi! Akasema: ‘Wakaiawili kauli yake, nayo ni katika inayosomwa katika Qur’ani, hakika ishara juu ya kauli yake: ARABIC TXT (Na dada zenu wa kunyonya) wakasema: Lau ingelikuwa inasomwa baada ya kufa Mtume ingelinukuliwa kama kunukuliwa kwa msahafu, lau ingelibakia katika Qur’ani kitu hakijanukuliwa, ingejuzu hicho kisichonukuliwa kiwe ni chenye kufuta kilichonukuliwa, nayo ni muhali.” Kisha akasema: “Na katika zilizofutwa maandishi yake na kuhitilafiana katika hukmu ni aliyoipokea Muslim katika Ifrad yake, kutoka kwa Aisha kwamba alimsomea mwandishi wake ARABIC TXT na Aisha akasema: “Nimeisikia kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.).” Watu wamehitilafiana katika Swala ya Wusta, kwenye kauli tano, kwa idadi ya Swala tano. Tumelifafanua hilo katika tafsiri. Wamedhoofisha sehemu hii wale waliodai kuwa kufutwa kwake kuko wazi, kwani wao wamekubali kuwa kubaki hukmu yake kuna hitilafu, na ukweli ni kuwa hitilafu yao iko katika asili ya kuanzisha hukmu yake, si katika kubaki kwake, na maana yake ni kwamba katika wao yupo anayeshuku asili ya Aya mbili za Aisha katika manyonyesho, na Swala ya Asri.

73

7/2/2011

11:31 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

Nimegundua kwamba wao hawakupata utatuzi wa mgongano wa maneno ya Aisha: “Mtume alikufa nayo ni katika inayosomwa katika Qur’ani” ila ni wayafanye kuwa ni maneno kutoka kwenye Aya zingine. Mwisho, tunataja kilio cha Ibnul Munadi na Zarkashi juu ya Sura mbili za Hifd na Khalaa’ za Umar. Amesema katika Burhan Juz. 2, Uk. 37: “Ametaja imam mwana hadithi Abul Husein, Ahmad bin Jafar, Al-Munadi katika kitabu chake An-Nasikh wal-mansukh katika zilizoondolewa maandishi yake, katika Qur’ani na hazikuondolewa kutoka nyoyoni ni Sura mbili za qunut katika Witri.” Akasema: “Wala hakuna tofauti baina ya waliopita na walioko sasa kwamba zimeandikwa katika misahafu iliyonasibishwa na Ubayya bin Ka’ab na imetajwa kutoka kwa Mtume kwamba yeye alimsomea na zinaitwa Sura za Hifd na Khalaa’. Hapa kuna swali, nalo ni isemwe, nini hekima ya kuondoa kisomo na kubakisha hukmu, je kimebakishwa kisomo ili amali ikusanyike na hukmu yake na thawabu ya kusoma? Mwandishi wa Al-Funun amejibu, akasema: ‘Hivyo ni ili idhihiri kiasi cha utiifu wa umma huu katika kuharakisha kujitolea nafsi kwa njia ya dhana bila kutaka njia ya mkato, wanafanya haraka kwa kitu kilicho chepesi zaidi, kama alivyofanya haraka Khalil Ibrahim (a.s.) katika kumchinja mwanawe kwa ajili ya kuota ndoto tu, na kuota ni njia ya chini zaidi ya kupokea wahyi.” Utawaona wamefanya katika Hadith pwekesho (zisizo na mlolongo wa wapokezi) kuwa ni tegemeo la kisheria katika kuthibitisha kuwa ni Qur’ani zile ziada za Umar na Aisha na Abu Musa na wenye kuwafuata wao. Na mkusanyiko wake unafikia zaidi ya nassi ya Qur’ani ya hivi sasa na wakahukumu kuwa ilikuwa ni sehemu ya Qur’ani. Kisha wakavumbua bidaa ya kufuta kisomo ili kuwasafisha wenyewe na upotofu. Na pamoja na hayo, wamelia juu ya nassi hizo ambazo wamekunywa pendo lake kwa kuwapenda wenyewe na wakasema: ‘Ni katika zili74

7/2/2011

11:31 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

zoondolewa jina katika Qur’ani na hazikuondolewa nyoyoni.’ Kisha wakazua hekima na siri kuonyesha kwamba Mwenyezi Mungu ameteremsha zaidi ya Qur’ani hii, kisha akazifuta! Pamoja na haya yote ya kuongeza kwao yasiyokuwamo katika Qur’ani, utawaona wanasimama na kudai kuwa si Qur’ani Bismillahi na Muawidhatayni, kwa kuwafuata maimamu wao. Hebu shangaa juu ya mpango huu unaogongana!

Maswali Je mnaitakidi kuwa kufuta kisomo kunaponya Hadith zote za rejea zenu? Na kauli zote za maimamu na wanavyuoni wenu zinazosema kuwa Qur’ani imepotoshwa? Je yafaa kwa mwislamu aseme kuwa kifungu fulani ilikuwa siku fulani ni Aya ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu kisha kikafutwa, bila ya kuwa na dalili ya mambo hayo mawili? Vipi mmejaalia dalili ya kuinasibisha Aya na Qur’ani kuwa ni dalili ya kufutwa kwa minajili tu ya kukosekana bila ya kuwepo nassi ya kuifuta? Licha ya kuwepo nassi nyingi zinazoonyesha kwamba zimepotea na bado ni Qur’ani? Maadam mlikubali Hadith ya Umar ya Aya ya jihadi kwa mara ya pili, na mnasahihisha Hadith ya jihadi ya Ali (a.s.) kwa taawili ya Qur’ani, nini hukmu ya wale aliowapiga Ali? Na nini hukmu ya wale waliopinga kupigana wakiwa pamoja naye? Vipi liwe kabila la Bani Umayya, ambalo Mwenyezi Mungu alimuamuru Mtume wake na waislamu kulipiga vita, ndilo dola ya kiislamu yenye uadilifu, na viongozi wake wawe maimamu na makhalifa?

75

7/2/2011

11:31 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

Nini maoni yenu juu ya aliyopokea Al-Hakim Juz. 4, Uk. 487: “Kutoka kwa Abu Said Al-Khidri, amesema Mtume (s.a.w.w.): ‘Hakika Ahlul-Bayt wangu baada yangu katika umma wangu watauawa na kufukuzwa, na watu wanaotuchukia zaidi kwetu ni Bani Umayya na Bani Mughira na Bani Makhzum.’ Na hii ni Hadith yenye isnad sahihi, na hawakuitaja.” Na aliyopokea katika Majmauz Zawaaid Juz. 7, Uk. 44: “Kutoka kwa Ali juu ya kauli yake Allah: ‘Je huwaoni wale waliobadilisha neema ya Mwenyezi Mungu kuwa kufru…’ Akasema: ‘Hii iliteremka kwa wale waovu zaidi katika Bani Makhzum na Bani Umayya, na Mwenyezi Mungu akawaangamiza siku ya Badr. Ama Bani Umayya walineemeka hadi leo hii.’’’ Amepokea Tabrani katika Al-Awsat na ndani yake kuna Amru, na hakuipokea ila Abu Is’haq Sabii’ na watu wengine wakweli waliobaki.

Mas’ala 108 Wamedai kwamba Qur’ani itaondolewa kutoka duniani, Al-Kaaba itavunjwa na Makka itaharibiwa Mtume (s.a.w.w.) aliwalea waislamu kwa ahadi ya Mwenyezi Mungu kuwa Mwenyezi Mungu atawapa ushindi juu ya miji ya Kisra na Kaisari na kwamba wao ndiyo umma wa mwisho na bora, na kwamba Isa (a.s.) atawashukia na uletwao kwao Mahdi (a.s.) na ataujaza ulimwengu uadilifu. Na Mtume aliusia umma wake juu ya vizito viwili, Qur’ani na kizazi chake, na kwamba Mwenyezi Mungu alimwambia kuwa viwili hivyo vitabaki katika umma wake, na havitatengana mpaka vimrudie kwenye hodhi. Haya masisitizo ya Mtume (s.a.w.w.) yalikuwa kwenye ndimi za wengi hata washirikina, je maneno ya kuwa Uislamu utakwisha yalitoka wapi? Na Al-Kaaba itavunjwa? Na Makka itaharibiwa? Na kwamba makuraishi 76

7/2/2011

11:31 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

wote watatoweka, na kusibaki hata mmoja, na Qur’ani itaondolewa duniani! Ngano hizi zimetoka wapi na kuingia kwenye akili za waislamu na wakaziandika katika vitabu vyao kwamba ni katika Hadith zinazotukuzwa, je hizi si athari za mayahudi? Mayahudi walikuwa wanafanya kazi usiku na mchana kwa uwezo wao wote, pamoja na viongozi wa kikuraish, katika kumaliza mwito wa Mtume, bidii zao zikagonga mwamba na Mwenyezi Mungu akainusuru dini yake na Mtume wake (s.a.w.w.). Lakini waliendeleza kazi yao Mtume alipokuwa hai, na baada yake katika kuathiri elimu ya uislamu. Wale makasisi wao waliojidai kuudhihirisha Uislamu walikuwa na athari kubwa katika kuyaharibu mafunzo mengi ya kiislamu, hasa huyo Ka’abul-Akhbar alikuwa na nafasi maalum kwa Umar, Umar akimsadiki na kupokea kutoka kwake, akamwamini sana, akaweza kueneza kadri alivyoweza elimu zao na fikra zao. Na kwa kuwa ngano ya kuondoa Qur’ani inafungamana na ngano tulizozitaja katika chimbuko lake na lengo, imekuwa hapana budi kuipinga japo kwa muhtasari. Umar akipokea kutoka kwa Ka’abul Akbar kama muumini anavyopokea kwa Mtume wake Umar alikuwa akiitakidi kuwa vitabu vya mayahudi vilikuwa na elimu ya mustakbali, na Kaa’b alikuwa mtu maalum kwa hilo. Akawa akimuuliza mwenyewe je yeye ni mfalme wa kidunia au khalifa wa kisheria wa Mtume? Na akimuuliza juu ya hali yake na makazi yake Akhera na atakayehukumu baada yake, na tafsiri ya Qur’ani, na pia hukmu za kisheria.. n.k..

77

7/2/2011

11:31 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

Ka’ab alikuwa akimjibu kila swali kwa sharti Umar afurahi. Lakini matamshi ya Kaa’ab daima yalikuwa ni ya mwanachuoni anayeamini elimu yake. Katika Kanzul Ummal Juz. 12, Uk. 567: “Kutoka kwa Naim bin Hammad: ‘Umar alimuuliza Kaa’b: ‘Ee Ka’ab, waniona mimi ni khalifa au mfalme?’ Kaab akasema: ‘Khalifa. Wallahi wewe ni bora ya khalifa na wakati wako ndio ulio bora kuliko nyakati nyingine.’’’ Na katika Majmauz Zawaaid, Juz. 9, Uk. 65: “Kutoka kwa Umar bin Rabia kwamba Umar bin Khatwab alituma mtu aitwe Ka’ab kisha akasema: ‘Ee Ka’ab unaonaje sifa yangu?’ Akajibu: ‘Ni pembe ya chuma.’ Akamuuliza: ‘Ni nini pembe ya chuma?’ Akajibu: ‘Ni kiongozi ambaye haogopi lawama kwa jambo la Mwenyezi Mungu.’ Akasema ‘Kisha?’ Akajibu: ‘Kisha baada yako atakuja khalifa atakayeuawa na kikundi.’’’ Katika Durrul-Manthur Juz. 5, Uk. 347: “Ametaja Abdu Razaq na Abdu Hamdi kutoka kwa Qatada kwamba Umar alimuuliza: ‘Aden ni nini?’ Akamjibu: ‘Ni majumba ya dhahabu ya Peponi watayokaa manabii, wakweli na maimamu wa uadlilifu.’’’ Na katika Kanzul Ummal Juz. 12, Uk. 561: “Kutoka kwa Ibn Mubarak na Al-Harwi katika Al-Jaamii: “Amesema Umar bin Khatwab: ‘Ee Ka’ab nihadithie juu ya Pepo za Aden.’ Akasema: ‘Naam, ee Amirul muuminiina, ni majumba ya dhahabu, hatoyakaa ila nabii au shahid au hakimu mwadilifu.’ Umar akasema: ‘Ama utume umeshapita kwa watu wake, wakweli wamemsadiki Mwenyezi Mungu na Mtume wake, ama hukmu ya mwadilifu mimi nataraji kwa Mwenyezi Mungu sitahukumu ila kwa jambo ila liwe na uadilifu ndani yake, ama kufa shahid, Umar yuko wapi na hilo?’’’ Na katika Bughyatul Bahith Uk. 291: “Umar alisoma kwenye mimbari: ‘Pepo za Aden.’ akasema: ‘Je mnazijua hizo? Ni kasri liko Peponi lina milango elfu hamsini katika kila lango kuna Mahurul ayni elfu ishirini na 78

7/2/2011

11:31 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

tano, haingii humo ila nabii, furaha iliyoje kwako ee mtu wa kaburini.’ Akaashiria kaburi la Mtume (s.a.w.w.). ‘Au mweye kusadiki, furaha kwa Abu Bakr, au shahid, na mimi Umar ni shahid. Na yule aliyenitoa kutoka nyumbani kwangu hapo Huthma, anaweza kuuleta ushahidi.”’ Maneno haya yanaonyesha kuwa yeye alikuwa anatazamia kufa shahidi kama alivyomuahidi Ka’abul Akhbaar. Huthma ni sehemu yenye mawe karibu na Makka watu wa Umar walikaa huko wa Bani Adiyy baada ya kuiba ngamia na kufukuzwa Makka. Na amepokea Ibn Shiba katika Tarikhul Madina Juz. 3, Uk. 891: “Umar alipoingia kutoka Makka katika Hijja ya mwisho aliyohiji. Ka’ab alimwambia: ‘Ee Amirul-Mu’minin, Ahidi kwamba wewe utakufa katika mwaka wako.’ Akasema: ‘Umejuaje ee Ka’ab?’ Akamwambia: ‘Nimeona katika Kitabu cha Mungu.’ Akamwambia: ‘Ee Ka’ab je umeona kwa jina langu na nasaba yangu?’ Akajibu: ‘La, lakini nimeona sifa zako, sera yako, na amali zako na zama zako.’’’ Na katika mifano ya kuathirika Umar na Ka’ab ni kwamba yeye alimkinaisha kuwa nzige huzaliwa kutokana na pua ya papa! Umar alikuwa akipenda nzige na wakati mwingine akimla mkavu, katika Sunan ya Bayhaqi Juz. 9, Uk. 257: “Kutoka kwa Sanan bin Abdfillahi AlAnswari amesema: ‘Nilimuuliza Anas bin Malik juu ya nzige akasema: ‘Tulitoka pamoja na Mtume mpaka Khaybar na Umar bin Khattab ana kikoba ndani yake mna nzige, amekibeba nyuma yake, akawa anapinda mkono wake akichukua na kutupatia.’’’ Katika Uk. 258: ‘Kutoka kwa Said bin Musayyib, kwamba Umar na Ibn Umar, Miqdad bin Suwaid na Suhayb walikula nzige. Umar akasema: ‘Lau tungelikuwa na kikoba kimoja au viwili tuendelee kula.’’’ Umar alipendezwa na fatwa ya Ka’ab kwamba kuwinda nzige ni halali kwa mwenye kufanya ihram ya Hajj na Umra, kwa sababu kwao wao haram ni 79

7/2/2011

11:31 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

kuwinda vya bara, na nzige ni wa baharini, kwa sababu anazaliwa kutokana na pua ya papa, anamcheua (chafya) kutoka puani kwake mara moja kila baada ya miezi sita. Katika Muwatau ya Malik Juz. 1, Uk. 352: “Kutoka kwa Ataa bin Yasar kwamba Ka’abul- Akhbar alikwenda Sham akiwa katika msafara, walipofika katikati ya njia, walipata nyama ya mawindo, Ka’ab akatoa fatwa ya kuila, walipofika Madina kwa Umar watu wakamtajia hilo. Akasema: ‘Ni nani aliyewatolea fatwa?’ Wakasema ni Ka’ab. Akasema: ‘Mimi nimempa uongozi kwenu hadi mrejee.’ Kisha walipokuwa katikati ya njia ya Makka, walipita kwa mtu aliyekuwa na nzige, Ka’ab akafutu kwamba wachukue wale. Walipofika kwa Umar walimwambia hilo. Akasema: ‘Nini kilichokufanya ukafutu hivi?’ Akasema: ‘Hilo ni windo la baharini.’ Umar akasema: ‘Umejuaje?’ Akajibu: ‘Ee Amirul-Mu’minin, naapa kwa yule ambaye nafsi yangu iko mikononi wake! Nzige ni cheuo la chafya anayoitoa papa kila mwaka mara mbili.’’’ (Ameipokea Abdu Razaq Juz. 4 Uk. 435 na wengineo). Pamoja na siku zikapita upendo wa Umar ulizidi zaidi na hatimaye ikawa neno la msomi huyu aliye karibu na Umar, ni hadith kutoka kwa Mtume zikipitia isnadi ya Abu Hurayra, Ibn Abbas, Anas, Jabir na Khuzayma na wengineo kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.). Baadhi ya wapokezi wamepokea kwamba aliona papa akitoa nzige puani, kama ilivyo katika Tafsiir ya Ibn Kathir Juz. 2, Uk. 106 na zingine. Ibn Kathir amesema katika Tafsiir yake Juz. 2, Uk. 105: “Imepokewa kutoka kwa kikundi cha maswahaba kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) mfano wake, Amepokea Ahmad, Abu Daud, Tirmidhi na Ibn Maja kwa njia za Hammad bin Salma kuwa: Ametuhadithia Abul Muhzim, huyu ni Yazid bin Sufiani, nimemsikia Abu Hurayra akisema: ‘Tulikuwa na Mtume (s.a.w.w.) katika Hijja au Umra, wakaja nzige, tukawa tunawapiga na fimbo zetu, tunawaua wakaanguka mikononi mwetu, tukasema: Tunafanya nini na sisi 80

7/2/2011

11:31 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

tuko kwenye ihram, tukamuuliza Mtume (s.a.w.w.), akasema: ‘Hapana ubaya kwa windo la bahari.’’’ Na katika Subulul Hudaa Juz. 9, Uk. 78: “Amepokea Abu Daud na akaifanya dhaifu. Na Ibn mardawayhi, na Bayhaqi kutoka kwa Abu Hurayra kwamba Mtume (s.a.w.w.) amesema: ‘Nzige ni katika windo la baharini.’’’ Na amepokea Ibn Maja kutoka kwa Anas, na Jabir, kwamba Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Nzige ni tawanyo la papa baharini.’’ Na lengo la Hadithi hizi ni kuhalalisha windo la nzige, kwa wenye kufanya ihram, na lau isingekuwa Ka’ab mwenyewe alikuwa ametoa fatwa juu ya nzige kuwa ni katika windo la bara na kuweka kafara ya dirhamu mbili kwa mwenye kufanya ihramu iwapo atawinda, na ikaenea hiyo, ingelifuzu kuhalalisha kwake. Ibn Quddama amesema katika Al-Mughni Juz. 3, Uk. 534: “Zimehitilafiana riwaya kuhusu nzige. Imepokewa kutoka kwake (s.a.w.w.) kuwa: “Ni katika windo la bahari.” Nayo ni madhehebu ya Abu Said. Amesema Ibnul Mundhir: ‘Amesema Ibn Abbas na Ka’ab: ‘Hiyo ni katika windo la bahari.’ Urwa amesema: ‘Ni tawanyo la papa.’ Na imepokewa kutoka kwa Abu Hurayra amesema: ‘Mtu kati ya watu wetu alikuwa akipiga nzige kwa fimbo yake naye yuko katika ihram, kukasemwa, hii haifai. Akatajiwa hilo Mtume (s.a.w.w.). Akasema: ‘Huyu ni katika windo la bahari.’ Na kutoka kwake kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) amesema: ‘Nzige ni katika windo la bahari.’ Amezipokea Abu Daud. Na imepkewa kutoka kwa Ahmad kwamba huyo ni katika windo la baharini, na kuna malipo. Na hii ni kauli ya wengi kutokana na iliyopokewa kuto81

7/2/2011

11:31 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

ka kwa Umar kuwa alimwambia Ka’ab kuhusu nzige wawili: ‘Utawafanyaje kwako?’ Akasema: ‘Dirhamu mbili.’ Akasema: ‘Dirhamu mbili ni bora kuliko nzige mia.’ Ameipokea Shafi’i katika Musnad yake.” Na wewe rejea maneno ya wafasiri wao na mafakihi wao yaliyo marefu katika tafsiri ya:

“Mmehalalishiwa kuvua mawindo ya baharini kwa faida yenu na kwa wasafiri, na mmeharamishwa mawindo ya bara maadam mko kwenye kuhiji, na mcheni Mwenyezi Mungu ambaye Kwake mtakusanya.’’ (Al-Maidah: 96). Ama mafakihi wa madhehebu ya Ahlul-Bayt wamekongamana kuwa nzige ni katika windo la bara, As-Saduq katika Man-laa Yahdhuruhul Faqiih amesema: “Alipita Abu Jafar, (Imam Al-Baqir) kwa watu, wakila nzige, akasema: ‘Subhanallah! Na nyinyi mnafanya ihram?’ Wakasema: ‘Hawa ni katika vya baharini.’ Akasema: ‘Mzamisheni majini basi!”’ (Amepokea katika Tahdhibul Ahkam Juz. 5, Uk. 363), na maana ya maneno ya Imam (a.s) lau kama nzige angelikuwa ni wa bahari kama mnavyodai, asingekufa mkimtosa majini, lakini atakufa, mzamisheni muone!) Na katika Tahdhib Juz. 5, Uk. 364: “Muawiya bin Ammar alimuuliza Imam Sadiq (a.s.): ‘Anapokuwa nzige yuko njiani na kuna watu wanafanya ihram, je watafanyaje?’ Akasema: ‘Watajiepusha watakavyoweza.’ Nikasema: ‘Je wakimuua?’ Akasema: ‘Hakuna kitu juu yao. Na samaki hapana ubaya kumla akiwa mbichi au ametiwa chumvi, na pia kila windo linalokuwa la baharini, linalofaa kulila. Mwenyezi Mungu amesema: “Mmehalalishiwa windo la bahari na kuleni starehe kwenu.’’” 82

7/2/2011

11:31 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

Na katika Masalikul Af-ham Juz. 2, Uk. 248: “Neno lake: Nzige katika maana ya kuwinda: Hakuna hitilafu kwetu, alizindua juu ya hitilafu ya Shafi’i aliposema kuwa ni katika windo la bahari kwa sababu huzaliwa na cheuo la samaki.” Ahlul-Bayt wanakataa elimu ya Ka’ab ya Kiyahudi Katika kitabu hiki kwenye mas’ala ya kwanza imetangulia kukataa kwa Ali (a.s.) katika kikao cha Umar ngano za Ka’ab ul-Akhbar Myahudi juu ya Mwenyezi Mungu kwamba Yeye kabla ya kuumba viumbe alikaa kwenye jiwe la Baytul Muqaddas…Akamwambia: “Watu wako wamekosa, wakapotosha kitabu, na wakafanya makosa. Ee Ka’ab, ole wako! Jiwe unalolidai halikusanyi utukufu Wake, wala halichukui utukufu Wake, wala kuenea ukuu Wake, na hewa uliyoitaja haipiti pambizo zake, lau jiwe na hewa ni za zamani basi zingekuwa zimemtangulia, na Mwenyezi Mungu hayuko kama wanavyosema walahidi au kama wanavyodhani wajinga, lakini alikuwapo na hakuwa mahali, ambapo akili hazimfikii, na kauli yangu kuwa ‘alikuwa’ ni kushindwa kwa kuwapo kwake, na yeye ni katika aliyoyafundisha, anasema Mwenyezi Mungu: “Amemuumba mwanadamu na akamfundisha kusema.” Na kauli ya kuwa ‘alikuwa’ ni katika aliyonifundisha ya kusema ili nitamke kwa hoja zake, na utukufu wake, alikuwa na ataendelea kuwa. Mola wetu ni Mwenye kuweza kwa anayoyataka, amekidhibiti kila kitu kisha akafanya alichokitaka bila ya fikra yenye kuzuka kwake...…” Hapa tutataja jibu la Imam Baqir (a.s.) kwa fikra za Ka’ab alizozieneza Umar kwa waislamu katika mafunzo ya waislamu! Katika Al-Kafi Juz. 4, Uk. 239: “Kutoka kwa Zurara amesema: ‘Nilikuwa nimekaa pembeni kwa Abu Jafar, naye aelekea Kibla. Akasema: ‘Ama kuiangalia ni ibada.’ Akaja mtu kutoka Bajila aitwaye Asim bin Umar, akamwambia Abu Jafar: ‘Ka’abul Akhbar alikuwa akisema kwamba AlKa’aba inasujudia Baytul Muqaddas, kila asubuhi.’ Abu Jafar akasema: 83

7/2/2011

11:31 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

‘Unasemaje juu ya aliyoyasema Ka’ab?’ Akasema: ‘Yamesema kweli maneno aliyosema Ka’ab.’ Abu Jafar akasema: ‘Umesema uongo, na Ka’ab pia amesema uongo nawe!’ Akakasirika. Akasema Zurara: Sijamuona akimuelekea mtu akimwambia ‘umesema uongo’ ila kwa Asim. Kisha akasema: ‘Hakuna sehemu ya ardhi aliyoiumba Mwenyezi Mungu aipendayo zaidi kuliko hiyo.’ Kisha akaashiria mkono wake upande wa AlKa’aba. ‘Na hakuna sehemu inayotukuzwa na Mola kama hiyo, kuna haram ya Mwenyezi Mungu ambayo ina miezi mitukufu, katika Kitabu chake, siku aliyoumba mbingu na ardhi, mara tatu mfululizo katika Hajj: Shawwal, Dhul Qaa’ada, na Dhul Hijja na mwezi mmoja wa Umra, nao ni Rajab.”’ Umar alisema: “Uislamu ni kama ngamia utazeeka na kufa Katika Musnad ya Ahmad Juz. 3, Uk. 463 Amesema: “Nilikuwa katika kikao ambacho alikuwako Umar bin Khatwab Madina, mtu mmoja akasema kumwambia mtu mmoja katika watu: ‘Ee fulani, umemsikia Mtume akiusifu vipi Uislamu?’ Akasema: ‘Nimemsikia akisema: ‘Uislamu ulianza kama gego kisha ukawa kijino kisha ukawa meno manne kisha meno sita kisha makubwa.’ Akasema Umar: ‘Hakuna baada ya meno makubwa ila ni upungufu.’’’ (Ameipokea katika Juz. 5, Uk. 52. na akasema katika Lisanul a’arb, kwamba mtu aliyemuuliza Umar ni A’laa bin Hadhrami. Na Ahllu Bayt wamesema: “Uislamu ni kama shamba, wanakula humo watu mwaka mmoja na wengine mwaka mwingine Saduq ametaja katika Khiswaal Uk. 475: “Kutoka kwa Jafar bin Muhammad, kutoka kwa baba zake, kutoka kwa baba zao kutoka kwa Ali (a.s.), Amesema: Amesema Mtume (s.a.w.w.): ‘Furahini, kisha furahini, (mara tatu), hakika mfano wa umma wangu ni kama mfano wa mvua, haijulikani mwanzo wake ni kheri au mwisho wake, hakika mfano wa umma wangu ni kama mfano wa shamba, watu wanakula mwaka na kisha wengine mwaka, huenda watu wa mwisho wakawa na bahari pana zaidi na 84

7/2/2011

11:31 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

yenye kina na yenye mazao bora zaidi. Vipi umma uangamie ilihali mimi ni wa kwanza wao, na wa kumi na mbili baada yangu ni katika watu wema wenye akili, na Masihi, Isa bin Maryam ni wa mwisho wake? Lakini wataangamia baina ya hivyo wanaokwenda ovyo, wao si katika mimi, nami si katika wao.’’’ (Ameipokea katika Kamalu Diin Uk. 269, na katika U’yuunul Akhbaari Ridhaa, Juz.2 Uk. 56). Wala hakuna nafasi ya kuanza kulinganisha kati ya aina hizi mbili za Hadithi na kuthibitisha ubatilifu wa maneno ya Umar. Madai ya Kaa’ab kwamba Al-Ka’aba itavunjwa na Makka kuharibika na asikae mtu yeyote Na katika Musnad ya Ahmad Juz. 2, Uk. 220: “Kutoka kwa Abdallah bin Amru amesema: Nimemsikia Mtume (s.a.w.w.) akisema: ‘Watakuja kuiharibu Al-Ka’aba katika mahabeshi, na kulipora pambo lake, na kuivua kutoka kwenye nguo yake, kama naiona hivi, iko wazi, ikipigwa na mitalimbo.”’ Na katika Musannif ya Abdu Razaq, Juz. 5, Uk. 136, kwa sanad sahihi kwao kutoka kwa Abu Hurayra, amesema: “Amesema Mtume (s.a.w.w.): ‘Zama za mwisho wa dunia, watadhihiri wahabeshi kwenye AlKa’aba.’’Akasema: ‘Nilidhani kuwa alisema ‘wataibomoa.’ Akasema Muamma: ‘Nimepata habari kutoka kwa baadhi yao kuwa Al-Ka’aba itavunjwa mara tatu, itainuliwa mara ya tatu au ya nne, basi faidikeni nayo.’’’ Amepokea Ahmad Juz. 1 Uk. 23: “Hadith ya Mtume kutoka kwa Umar kwamba alimsikia Mtume (s.a.w.w.) akisema: ‘Watu wa Makka watatoka kisha wasipite au asipite ila wachache kisha watajaa na watajenga kisha watatoka na wasirudi milele.’’’ (Na amesema kutoka kwa Majmauz Zawaid, Juz. 3, Uk. 298, amepokea Ahmad, Abu Ya’ala na pia Ibn Lahia’ na Hadithi yake ni hasan, na watu wake waliobaki ni watu wa Sahih).

85

7/2/2011

11:31 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

Ama Bukhari ameweka mlango katika Juz. 2, Uk. 159 wenye anuani ‘Mlango wa kuvunja Al-Kaaba’ Na humo akataja Hadith iliyotangulia ya Ahmad, lakini kutoka kwa Abu Hurayra. Kwa ufupi: Kutoka kwa Mtume, amesema: ‘Wataibomoa Al-Ka’aba wa kutoka Habashi.’ (Amepokea Muslim Juz. 8, Uk. 183) Kisha akapokea Bukhari Hadithi mbili zingine moja wapo ikiwa ya Ibn Abbas, kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Kama kwamba naona mtu mweusi akiing’oa jiwe baada ya jiwe.’’ Na Hadithi ya Aisha kutoka kwa Mtume, amesema: “Jeshi litaishambulia Al-Ka’aba kivita na watadidimizwa.” Na Hadith ya jeshi la kudidimizwa aliyoipokea Bukhari ni maarufu haina uhusiano na kuvujwa Al-Ka’aba. Wamepokea wakubwa wa maimamu wao toka kwa maswahaba wakubwa, kuwa ni katika alama za Mahdi (a.s.) na kwamba yeye atajilinda kwa Nyumba, na majeshi ya Sufyani yataikusudia na hapo Mwenyezi Mungu atawadidimiza katika Madina! Lau tungetaka kuoneyesha rejea zake, njia zake na kusahihishwa kwake kulikofanywa na ulamaa ingelifikia kitabu pekee zaidi ya kurasa mia, tumefupisha kwa kadiri katika Muujamu Hadithul Imam Mahdi Juz. 1, Uk. 442. Na katika riwaya sahihi kwao kama vile katika Ahmad Juz. 6, Uk. 316, Abu Daud Juz. 4, Uk. 107, Ibn Shiba Juz. 15, Uk. 45, Abdu Razaq Juz. 11, Uk. 371 na wengineo. “Itakuwepo hitilafu atakapokufa khalifa, ndipo atatoka mtu kutoka Madina na atakwenda Makka watu watataka kumtoa nyumbani kwake naye hataki, watambai baina ya nguzo na Maqam, ataletewa jeshi la kutoka Sham mpaka watakapofika Baydaa watadidimizwa. Ndipo watakuja watu wa Iraq, na wa Sham, watambai. Na zitatolewa hazina na mali kisha zitagawanywa na Uislamu utaenea ardhini kwa miguu yake. 86

7/2/2011

11:31 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

Na katika riwaya zake, katika rejea zetu kama katika Ghaybatu Tusi Juz. 269 na Al-Ikhtiswaas Uk. 255: Kutoka kwa Imam Baqir (a.s.): ‘Na ataletwa Sufyani mpaka Madina na Mahdi atamkimbia hadi Makka, kiongozi wa jeshi la Sufian itamfikia habari kwamba Mahdi amekwenda Makka, atatuma jeshi kumfuata, na hatompata mpaka ataingia Makka, akihofu huku akifuata sunna za Musa bin Imran (a.s.).’Akasema: ‘Kisha kiongozi wa Sufian atashuka Baydaa atanadi mwenye kunadi kutoka mbinguni: Ee Baydaa wamalize watu! Hapo watadidimizwa na hatoponyoka mmoja wao, ila watatu katika wao. Mwenyezi Mungu atazigeuza nyuso zao kwenye visogo vyao na wao ni majibwa, na kwa wao ndio ilishuka Aya: “Enyi mliopewa Kitabu, aminini tuliyoyateremsha mkisadikisha yaliyo kwenu kabla hatujazigeuza nyuso tukazirudisha nyuma ya migongo yake…”’ Akasema: ‘Na Qaim atakuwa wakati huo yuko Makka, akiwa ameegemeza mgongo wake kwenye Nyumba tukufu, akiomba, na atanadi: ‘Enyi watu! Sisi tunataka nusura ya Mwenyezi Mungu, na atakayetujibu, sisi ni AhlulBayt wa Mtume wenu, Muhammad (s.a.w.w.), nasi ni bora ya watu kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Muhammad (s.a.w.w.). Atakayebishana nami juu ya Adam, basi mimi ni bora ya watu kwa Adam, atakayehojiana nami kwa Nuh, basi mimi ni bora ya watu kwa Nuh. Atakayebishana nami juu ya Ibrahim, basi mimi ni bora ya watu kwa Ibrahim. Atakayebishana nami juu ya Muhammad (s.a.w.w.), basi mimi ni bora ya watu kwa Muhammad (s.a.w.w.). Na atakayehojiana nami kwa manabii mimi ni bora ya watu kwa manabii. Je Mwenyezi Mungu hasemi katika Kitabu chake: “Hakika Mwenyezi Mungu amemteua Adam na Nuh, na Ali Ibrahim na Ali Imran juu ya viumbe wote…” Mimi ni salio la Adam, na ni akiba ya Nuh na ni mteule kutoka kwa Ibrahim, na ni mteule wa Mtume Muhammad (s.a.w.w.). Atakayebishana nami juu ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu, basi mimi ni bora ya watu kwa Kitabu cha Mwenyezi Mungu. Atakayehojiana nami katika sunna za Mtume (s.a.w.w.), basi mimi ni bora ya watu kwa Sunna za Mtume (s.a.w.w.). Na atakayesikia maneno yangu haya leo amfikishie 87

7/2/2011

11:31 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

asiyekuwepo, na nawaomba kwa haki ya Mwenyezi Mungu, na haki ya Mtume wake (s.a.w.w.) na kwa haki yangu, hakika mimi kwenu nina haki ya walio karibu kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) ila wanapotunyima na wanapotuzuia wale waliyotudhulumu. Wametuficha na wakatudhulumu, wakatufukuza kutoka kwenye nyumba zetu sisi na watoto wetu, wakatuonea na kutuzuia kupata haki yetu, na watu wa batili wakatuzulia. Allah allah kwetu, msituache, mtunusuru Mwenyezi Mungu atawanusuru.’ Akasema: ‘Mwenyezi Mungu atamkusanyia maswahaba wake watu mia tatu na thelathini na tatu, na atamkusanyia bila ya miadi upepo kama upepo wa majira ya baridi, ee Jabir ni Aya aliyoitaja Mwenyezi Mungu katika Kitabu chake: “Popote mtakapokuwako, Mwenyezi Mungu atawaleta nyote, hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza juu ya kila kitu.’’ Na watambai kati ya nguzo na maqam na akiwa na ahadi kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amewarithisha watoto kutoka kwa mababa. Eee Jabir Qaim ni mtu kutoka kwa watoto wa Husein, Mwenyezi Mungu atamtengenezea jambo lake usiku, hilo si mushkil kwa watu ee Jabir, hawatokuwa na mushkili wa kuzaliwa kwake kunakotokana na Mtume (s.a.w.w.) na kurithi kwake wanavyuoni, mwanachuoni baada ya mwanachuoni, mishkeli zote hizi ni kwao, sauti kutoka mbinguni haiwatatizi ikiwa itanadiwa kwa jina lake na jina la babake na mamake. Kukanganywa kwa wafafanuzi wa Bukhari na wengineo juu ya Hadith ya kuvunjwa Al-Ka’aba Ibn Hajar katika Fat’hul Barri Juz. 3, Uk. 368 amesema: “Kutokana na Hadithi ya Aisha juu ya jeshi la kudidimizwa kuna ishara ndani yake kwamba vita vya Al-Ka’aba vitatokea. Vya kwanza Mwenyezi Mungu atawaangamiza kabla ya kuifikia, na vya pili vitawezekana, na dhahiri ni kwamba vita vya wale wenye kuharibu, vitachelewa kutokea (yaani vitakuwa vya pili).

88

7/2/2011

11:31 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

Kauli yake ‘kama naona..’ hiyo ni katika riwaya zote, kutoka kwa Ibn Abbas katika Hadith hii, na inadhihiri kwamba katika Hadithi kuna kitu kimefutwa, na inachukuliwa kuwa ni yale yaliyotokea katika Hadith ya Ali kwa Abu Ubayda katika Hadith gharib kutoka kwenye njia ya Abul Aa’liya, kutoka kwa Ali amesema: “Fanyeni wingi wa kutufu kwenye Nyumba hii, kabla hamjazuiwa kati yenu nayo, kama namuona mtu kutoka Uhabeshi, mwenye kipara, au alisema, amekaa juu yake, akiivunja. Kisha Ibn Hajar akasema: Imesemwa: ‘Hadith hii inapingana na kauli ya Mwenyezi Mungu “Je hamkuona kwamba sisi tumeijaalia sehemu tukufu yenye usalama.” na kwa sababu Mwenyezi Mungu aliifunga Makka kutokana na wenye ndovu, na hawakuweza kuivunja na wakati huo haikuwa na Kibla, vipi atawaruhusu mahabeshi baada ya kuwa ni Kibla cha waislamu? Nami najibu: Kwamba jambo hilo litatokea zama za mwisho kabla kusimama Kiyama, ambapo hapatabaki mmoja duniani asemaye Allah, Allah, kama ilivyothibiti kwenye Sahih Muslim: ‘Kiyama hakitosimama mpaka duniani iwe haisemwi Allah, Allah.’ Na kwa ajili hii ilitokea katika riwaya ya Said bin Sama’n: ‘Hakuna atakayeishi baada yake.’ Na kabla ya hapo ilitokea kushambuliwa katika vita vya watu wa Sham wakati wa Yazid bin Muawiya, kisha baada yake katika vita vingi, na vita vikubwa zaidi ni vya Maqaramitwa, baada ya miaka mia tatu…… na vyote hivyo havipingi kauli ya Mwenyezi Mungu “Je hamkuona kwamba sisi tumeijaalia sehemu tukufu yenye usalama.” Kwani hizi zilitokea mikononi mwa waislamu kwa kuandamana na kauli ya Mtume (s.a.w.w.): “Haitowastahili Nyumba hii ila watu wake.’’ Na yakatokea aliyoyasema Mtume nayo ni katika alama za utume wake. Na katika Aya hakuna kinachoonyesha kuendelea usalama uliotajwa. Na Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye zaidi.”

89

7/2/2011

11:31 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

Kwa hivyo Ibn Hajar amezipa uzito Hadith za Kuvunjwa Al-Ka’aba! Kisha katika Juzuu ya 13, Hadith Na. 68, ametaja Hadith ya Mtume kwamba Nyumba hiyo itabaki ilivyo hadi karibu na wakati wa Kiyama na kuja kwa Juju wa maajuju. Akajaribu kuwafikisha kati ya mbili hizo kwamba kuvunjwa kwa Al-Ka’aba kutakuwa kabla ya kuja kwa Juju wa maajuju, akasema: “Imetangulia katika Hijja kwamba itahijjiwa Al-Ka’aba baada ya kutoka Juju wa maajuju, na imetangulia Hadithi: ‘Kiyama hakisimami mpaka Nyumba (Al-Ka’aba) isihijiwe, na itaharibiwa na wahabeshi.’ Hivyo inapangika kutoka hapo kuwa wahabeshi watapoiharibu Nyumba hiyo watatokewa na kabila la Qahtani na kuwaangamiza, na waislamu kabla ya hivyo watahijji katika zama za Isa (a.s.) baada ya kutoka Juju wa maajuju na kuangamia kwao. Na kwamba ule upepo utakaochukua roho za waislamu utaanza na waliobakia baada ya Isa, na watakuja nyuma baada yake watu wa Yemen. Inawezekana hii ndio inayofasiri kauli yake: “Imani inachelewa.’’ Yaani itakuja nyuma baada ya kukosekana dunia nzima. Muslim ameitaja Hadith ya Qahtani baada ya Hadith ya kuharibu Al-Ka’aba, pengine ni ishara ya hii.” Huu ni mkanganyo kutoka kwa Ibn Hajar katika mfuatano wa Hadithi baada ya kudhihiri Mahdi (a.s.) na pia katika kusadikisha riwaya zake, kama ya Qahtani ambayo ameifanya kudhihiri kwake baada ya Mahdi na Isa (a.s.) licha ya kuwa riwaya zao katika rejea zao zinagongana, zingine zinasema atadhihiri kabla ya Mahdi, zingine baada ya Mahdi na zingine zinasema kuwa huyo ni Mahdi. Na nyingi ya hizo zimekatika hazina sanad. Na asili yake inavyoonekana zote ni kutoka kwa Ka’abu Myamani. Baadhi zinasema kuwa Qahtani au Mansur aliyeahidiwa ni Myamani, Waziri wa Mahdi, hii inawafikiana na Hadithi ya Ahlul-Bayt. Na inafahamika kutoka Hadithi ya Ibn Hammad katika Al-Fitani Uk. 237: “Kwamba asili ya riwaya ya Qahtani ni nyongeza ya baadhi ya Wayemeni 90

7/2/2011

11:31 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

ili ikabiliane na wa Hadithi za Mahdi (a.s.), akasema: ‘Ametuhadithia Ibn Lahia’ kutoka kwa Abdulrahman bin Qays bin Jabir As-Sadafi, kwamba Mtume (s.a.w.w.) amesema: ‘Kutakuwa katika Ahlul-Bayt wangu mtu akayeujaza ulimwengu uadilifu utapokuwa umejaa uonevu, kisha baada yake ni Qahtani na naapa kwa aliyenituma kwa haki, hakuna zaidi ya huyo tena.’’’ Ibn Hammad amepokea jibu la Abdallah bin Amr bin Al-Asi juu ya Wayamaani, akasema: “Enyi watu wa Yaman, mnasema kuwa atakayenusuriwa (msaidizi wa Mahdi) ni katika nyinyi, naapa kwa yule ambaye nafsi yangu iko mikononi kwake! Yeye huyo babake ni mkuraishi, lau ningelitaka nimuite kwa upeo wa juu zaidi ningelifanya hivyo.’’ Kinachohusu utafiti wetu huu ni kuwa Ibn Hajar amesahahu kwamba Hadith za kuvunja Al-Ka’aba kwao zinaeleza kuwa si baada yake, kisha vipi atahiji hapo baada ya hivyo? Katika Sahih ya Ahmad: “Kisha watakuja mahabeshi na kuiharibu sana kiasi ambacho haitajengwa tena milele!.” Pia ameipokea Al-Hakim Juz. 4, Uk. 452 na kuisahihisha kwa sharti la masheikh wawili, ndani yake imo: “Kisha watakuja mahabeshi na kuiharibu sana kiasi ambacho haitajengwa tena milele!.” Hapana budi kwa yule iliyothibiti kwake kwamba Al-Kaaba itahijiwa baada ya kutoka Juju wa Majuju aikadhibishe Hadith ya kuvunjwa kwa AlKa’aba, na hiyo ndio sahihi, au waseme kama alivyosema Abu Yaa’la Juz. 2, Uk. 278: “Nyumba itakuwa imebomoka na kutahijiwa mahali pake!’’ Na mwishowe tunagundua kuwa iko Hadith ya Mtume (s.a.w.w.) nyingine inayoamuru kuacha kupigana vita na wahabeshi, na kwamba atakayeitoa hazina ya Al-Ka’aba ni mtu kutoka uhabeshi. Lakini hakuna hata mtu wa Afrika wala mmoja wao wala wengineo atakayevunja Al-Ka’aba. Ahmad 91

7/2/2011

11:31 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

ameipokea na baadhi ya rejea zao, kama walivyopokea Isnadi ya karibu zaidi katika rejea zetu, lakini Bukhari na Muslim wameziacha, na wakapokea Hadith za kuvunjwa Al-Ka’aba. Katika Al-Mustadrak, Juz. 4, Uk. 453, Al-Hakim amesema: “Kutoka kwa Abdallah bin Umar kwamba Mtume (s.a.w.w.) alisema: ‘Waacheni wahabeshi, madam wamewaacha, kwani hakuna atakayezitoa hazina za Al-Ka’aba ila mhabeshi.’ Kisha Al-Hakim akasema: ‘Hii ni Hadithi yenye isnad sahihi na hawakuitaja masheikh wawili. Lakini wote wawili (Bukhari na Muslim) wameafikiana juu ya kutoa Hadithi ya Sufyani kutoka kwa Wathab bin Said kutoka kwa Zahri, kutoka kwa Said bin Al-Musayyib, kutoka kwa Abu Hurayra kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) kuwa amesema: “Watu watakaovunja Al-Ka’aba ni kutoka kwa mahabeshi.’’ (Rejea Musnad ya Ahmad Juz . 5, Uk. 371, Abu Daud Juz. 2, uk. 316, Nasai Juz, 45, Uk. 216, Al-Humayri Al-Qummi Uk. 82, na Biharul Anwar Juz. 18, Uk. 145). Ka’ab amesema: “Makuraish watatoweka kwenye mikono ya watu wa Yemen na kusibaki hata mmoja Hadith katika rejea za Sunni zimedai kuwa makuraishi watatoweka kwa mikono ya Wayemen, na kusibaki hata mmoja, na kuna Hadith zenye sanad sahihi kwa sharti la masheikh wawili. Na dhana kubwa ni kuwa ziliwekwa wakati wa Muawiya na baadaye wakati utawala wa Bani Umayya ulipozidi kwa waislamu na Wayemen wakahisi kama wanapunjwa na wanakandamizwa na makuraishi, licha ya kushiriki kwao kwa wingi katika ushindi mbalimbali, na kuwa wao ni wasimamizi wa jeshi la Bani Umayya. Na sina shaka kuwa asili ya uzushi wa Hadith hizi ni Ka’abul Akhbar, ili kuwakoroga Wayemen na kuhakikisha ndoto zake za kiyahudi!

92

7/2/2011

11:31 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

Hakika Mwislamu yeyote anajua kuwa umma wa Muhammad na AhlulBayt wake watabaki mpaka siku ya Kiyama, Mtume aliusia kwa kizazi chake na Qur’ani na akasema kuwa havitatengana hadi vimfikie kwenye hodhi, na akawaahidi watu kuwa Mwenyezi Mungu atamleta Mahdi (a.s.) zama za mwisho ili kuijaza ardhi uadilifu baada ya kujaa dhulma na uonevu…. Na riwaya ifuatayo inaonyesha nafasi ya Ka’ab na jinsi maneno yake yakawa ni Hadith ya Mtume iliyopokewa na Abu Hurayra na wengineo! Naim katika kitabu chake Al-Fitan Uk. 239 amesema: “Ametuhadithia Baqiyya na Abdul Quddus, kutoka kwa Abu Bakr kutoka kwa masheikh, kutoka kwa Ka’ab amesema: ‘Watu wa Yemen, watakapompiga vita mwenye Baytul Muqaddas, watawaelekea makuraishi na kuwaua na kusibaki katika wao hata mmoja, mpaka kiatu katika viatu vyao vionekane, isemwe kuwa hiki ni kiatu cha mkuraishi.”’ Na unapoona maneno ya Ka’abul Akhbari yanapogeuka kuwa Hadith ya Mtume usistaajabu! Abu Hurayra alikuwa anavutiwa na Ka’ab, kama Umar, na akipokea kutoka kwake, pamoja na kuwa Ka’ab hakumuona Mtume. Ulamaa wa jeraha na nyoofu wamesema kuwa Abu Hurayra alikuwa akikanganywa na Hadith na kuzinasibisha Hadith za Mtume kwa Ka’ab. Katika An-Nihaya cha Ibnu Athir Juz. 8, Uk. 117: “Yazid bin Harun amesema: ‘Nimemsikia Shuuba akisema: Abu Huraira alikuwa akipokea anayoyasikia kutoka kwa Ka’ab na aliyoyasikia kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) na hapambanui hii na hii! Ibnu Asakir pia ametaja hilo.”’ Kama ilivyogeuka maneno ya Ka’ab juu ya kutoweka kwa makuraish, kuwa ni maneno ya Mtume (s.a.w.w.)!

93

7/2/2011

11:31 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

Katika Musnad ya Ahmad Juz. 8, Uk. 336: “Kutoka kwa Abu Hurayra amesema: ‘Mtume (s.a.w.w.) amesema: Kabila litakalotoweka haraka zaidi katika makabila ya waarabu ni makuraishi, itafikia apite mwanamke aone kiatu na aseme hiki ni kiatu cha makuraishi.’’’ Na katika Muswannifu ya Ibn Abu Shiba Juz. 8, uk. 693: “Abu Hurayra amesema: ‘Wallahi lau mngeliyajua ninayoyajua, mngelicheka sana na kulia kidogo, na lau mngeliyajua ninayoyajua, mngelia sana na kucheka kidogo. Wallahi kutatokea mauaji ya makuraishi katika eneo hili mpaka aje mfagiaji aone ndani yake mna kiatu cha kikuraishi.’’’ (Rejea riwaya yake pia katika Musnad ya Ibn Rahuba Juz. 1, Uk. 390 na Ahaad wal mathaani cha Dhahhak Juz. 4, Uk. 135). Na katika Sahih ya Ibn Habbani Juz. 15, Uk. 266, kutoka kwa Abu Hurayra: “Mwanzo wa kabila kutoweka katika waarabu ni makuraishi, naapa kwa yule ambaye nafsi yangu iko mikononi mwake, itafikia mtu apite kwenye kiatu kimetupwa njiani atakichukua kwa mkono wake na aseme: ‘Hiki kilikuwa ni kiatu cha mkuraishi katika watu.’’’ (Ameipokea katika Kanzul Ummali Juz. 11 Uk. 248 na Juz. 12 Uk. 23na Juz. 14 Uk. 253). Madai yao kuwa Qur’ani itaondolewa kutoka ardhini na kutoka nyoyoni Ilitangulia hapo awali Hadith ya kuondolewa Qur’ani duniani na kutoweka msahafu wote, na kuondolewa nyoyoni mwa waislamu, hayo yalikuwa tu ni mawazo ya Ka’abul Akhbaari juu ya hatima ya janga la waislamu, ambazo alizinukuu Abu Hurayra, Umar, Abdallah bin Umar, Abdallah bin Amru bin Al-Asi na wengineao. Na ikiwa wengi wao hawakuyategemeza kwa Mtume, lakini ndugu zao waliyategemeza kama ilivyotangulia. Na walizipokea kama Hadith tukufu, kisha wakapokea kutoka kwa Abdallah bin Mas’ud, Hadithi alizosema 94

7/2/2011

11:31 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

Ibnul Jawzi kuwa ni hasan, hivyo kauli za Ka’ab kwa Ibnul Jawzi zilichukuliwa kuwa na nguvu ya Hadith ya Mtume (s.a.w.w.) iliyo sahihi. Ametaja Ibn Shayba katika Musannif yake, Juz. 7, Juk. 192 Mlango aliouita ‘Kuiondoa Qur’ani na kwenda nayo usiku’ na akapokea humo kuwa Abdallah bin Umar alisema: “Mtakuwaje nyinyi kitakapoondolewa Kitabu cha Mwenyezi Mungu?” Na akasema: “Hii Qur’ani mliyo nayo mikononi mwenu inakaribia kuvuliwa kutoka kwenu.” Akasema: ‘Nikasema, vipi itavuliwa kwetu na Mwenyezi Mungu amefanya madhubuti katika nyoyo zetu, na tumeidhibiti kwenye misahafu yetu.’ Akasema: “Itachukuliwa usiku mmoja na kondolewa yaliyomo nyoyoni, na kuondolewa yaliyomo misahafuni, na watu watakuwa mafukara.” Kisha akasoma: “Na tukitaka tutawaondolea yale tuliyowapa wahyi kwako kisha hutapata wa kukutetea.” Na Suyuti amepokea baadhi ya hizo katika Durrul Manthuri Juz. 1, Uk. 135 akasema: “Ametaja Al-Azraqi kutoka kwa Abdallah bin Amru bin AlAsi akasema: ‘Mwenyezi Mungu ataivua Qur’ani vifuani mwa watu na jiwe jeusi (Hajarul aswad) kabla ya siku ya Kiyama.’’’ Na ametaja Al-Azraqi, kutoka kwa Mujahid amesema: “Mtakuwaje nyinyi kitakapoondolewa Kitabu cha Mwenyezi Mungu nyoyoni mwenu na ikafuata Nguzo kuondolewa?” Na ametaja Al-Azraqi kutoka kwa Uthman bin Sanaj amesema: “Imenifikia habari kwamba Mtume (s.a.w.w.) amesema: ‘Ya kwanza kuondolewa ni nguzo, na Qur’ani na ndoto za Mtume wakati wa kulala.’’’ Ibn Abi Shiba na Tabrani wametaja kutoka kwa Abdallah bin Amru amesema: “Hijini Nyumba hii na mlishike jiwe hili, wallahi litaondoka au lipatwe na jambo kutoka mbinguni, ikiwa ni mawe mawili yaliyoanguka kutoka Peponi likaondolewa moja basi na litaondolewa jingine, na ninayoyasema yasipotokea kama ninavyosema, basi atakayepita kaburini kwan95

7/2/2011

11:31 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

gu na aseme, hili ni kaburi la Abdallah bin Amru muongo!’’ Na Suyuti amesema katika Juz. 4, Uk. 201: “Na ametaja Muhammad bin Nasr katika kitabu swalaa kutoka kwa Abdallah bin Amru bi Al-Asi amesema: ‘Kiyama hakisimami mpaka iondolewe Qur’ani kwa yule aliyeteremshiwa na mvumo kuzunguka Arshi, kama mvumo wa nyuki. Itasema: ‘Nasomwa lakini sifanyiwi amali.’ Na Muhammad bin Nasr ametaja kutoka kwa Layth bin Sad amesema: ‘Itaondolewa Qur’ani ambapo watu watavielekea kuvikubali vitabu na kuviangukia na kuacha Qur’ani.’’’ Na amepokea Al-Haythami katika Mawridu Dhaman Uk. 471 chini ya anuani: Qabdhu ruuh kulli muminin warafi’l Qur’ani’ katika Hadith kutoka kwa Abu Hurayra kutoka kwa Mtume imekuja: “Kiyama hakisimami mpaka uje upepo mwekundu kutoka upande wa Yemen na Mwenyezi Mungu kwao ataichukua kila roho, inayoamini Mungu na siku ya mwisho, na kitachukuliwa Kitabu cha Mungu na kupelekwa mbinguni isibaki duniani katika hiyo hata Aya moja.’’ Na katika Kanzul Ummali Juz, 14, Uk, 233: “Kutoka kwa Daylami kutoka kwa Abdallah bin Amru bin Al-Asi, amesema: ‘Hakisimami Kiyama mpaka irejee Qur’ani ilipotoka, na itakuwa na mvumo pembeni mwa Arshi kama wa nyuki na Mwenyezi Mungu Mtukufu atasema: ‘Una nini?’ Itasema: ‘Kwako wewe nimetoka, na kwako narudi nasomwa lakini sifanyiwi amali.’ na hapo itaondolewa iinuliwe Qur’ani.” Na katika Juz. 14, Uk. 223: Kutoka kwa As-Sajzi kutoka kwa Umar: “Hakisimami Kiyama mpaka iondolewe nguzo na Qur’ani.’’ Na katika Juz. 14, uk. 211: “Kitu cha kwanza kuondolewa ni Nguzo, na Qur’ani na ndoto za Mtume usingizini.’’ Na katika Al-Jamius Saghiir ya Suyuti, Juz. 1, Uk. 435: ‘’Cha kwanza kuondolewa ni Nguzo, na Qur’ani na ndoto usingizini.’’ 96

7/2/2011

11:31 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

Na katika Tafsiir ya Thaa’labi Juz. 3, Uk. 539: “Qurtubi amesema katika Tadhkira yake na kataja kutoka kwa Amru bin Dinar Al-Khadhri na Ilyas (a.s.) Hayyan: ‘Itakapoondolewa vitu viwili vitakufa.’ Qurtubi amesema: Hii ndio sahihi.’’ Ibnul Jawzi amesema katika Zadil Maysir Juz. 5 uk. 59: “Kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Tukitaka tutawaodndolea yale tuliyowaletea wahyi kwako kisha hupati wa kukutetea.” Na imepokewa kutoka kwa Abdallah bin Mas’ud amesema: ‘Itapandishwa Qura’ni katika usiku mmoja, atakuja Jibril katikati ya usiku ataiondoa kutoka vifuani mwao, na majumbani mwao, watakuwa hawaisomi Aya wala hawaihisi.’’’ Abu Sulaiman Damishqi akajibu kupinga usahihi wa Hadith hii kwa kauli ya Mtume (s.a.w.w.): “Hakika Mwenyezi Mungu haichukui elimu kwa kuing’oa.’’ Na Hadith ya Ibn Mas’ud iliyopokewa kwa njia za hasan inachukuliwa kuwa Mtume alikusudia elimu zingine siyo ya Qur’ani, kwani elimu inaendelea kupungua mpaka kuondoka kwa Qur’ani kuwe ni jambo la mwisho.’’ Kuzipinga riwaya zinazosema kuwa Qur’ani itaondolewa Hadith zinazotoka kwa Ahlul-Bayt zimeonyesha kubatilika kwa maneno ya kuondolewa Qur’ani, na pia Hadith inayoshiriki katika rejea za pande mbili kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) kwamba: “Hakika Mwenyezi Mungu haichukui elimu kwa kuing’oa.’’ Ametaja Ibul Jawz kuwa Abu Sulayman Damishqi alitumia hadithi hiyo kujibu usahihi wa Hadith ya Ibn Mas’ud juu ya kuondolewa kwa Qur’ani. Ama Hadith zetu hasa ni kuwa: Katika kitabu‘Man laa yahdhuruhul faqiih’ Juz. 2, Uk. 158: “Kuna mtu alimuuliza Imam Sadiq (a.s.): ‘Niambie juu ya usiku wa Laylatul-Qadri ulikuwa au uko kila mwaka?’ Akajibu: ‘Lau ingeondolewa Laylatul-Qadri, basi ingeondolewa Qur’ani.’’’ 97

7/2/2011

11:31 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

Na katika Baswair Darajaat Uk. 134: “Kutoka kwa Imam Sadiq (a.s.) amesema: ‘Hakika elimu iliyoshuka na nabii Adam haikuondolewa, elimu hurithishwa, na hafi kwetu mwanachuoni ila humwachie mtu wake anayeijua elimu yake au kiasi anachopenda Mwenyezi Mungu.’’’ Ama aliyopokea Al-Jazairi katika Nurul Burhan Juz. 2, Uk. 15: “Kati ya swali la Ash’ath bin Qays kwa Amirul muuminna ni, vipi itachukuliwa kodi kwa mmajusi na hawakuteremshiwa Kitabu na kupelekewa Mtume?’’ Akasema: ‘Kwa nini! Ee Ash’ath Mwenyezi Mungu aliwateremshia kitabu na kuwapelekea Mtume hata walikuwa na mfalme, alilewa usiku mmoja akamwita binti yake kitandani kwake na akafanya maasi, kulipokucha watu wake wakaambiana, watu wakaja mlangoni kwake wakasema: ‘Ewe mfalme, umeichafua dini yetu, na umeiangamiza, toka tukutakase na tukupige hadi.’ Akawaambia: ‘Kusanyikeni musikilize maneno yangu, ikiwa sina la kujitetea kwa niliyoyafanya basi nawaachia nyinyi.’ Wakakusanyika na ndipo akasema: ‘Je mnajua kwamba Mwenyezi Mungu hakuumba kiumbe aliyekuwa ametukuzwa zaidi kuliko baba yetu Adam na mama yetu Hawa?’ Wakasema: ‘Umesema kweli ee mfalme.’ Akasema: ‘Je si aliwaoza wanawe wa kiume kwa wanawe wa kike na wa kike kwa wa kiume?’ Wakasema: ‘Umesema kweli. Hii ndio dini.’ Basi Wakashikamana juu ya hilo. Hapo ndipo Mwenyezi Mungu akaifuta elimu vifuani mwao, na kuwaondolea kitabu, wao ni makafiri, wataingia motoni bila hesabu.’’ Hii ndio imesihi kwa majusi lakini hakuna dalili ya kuondolewa Qur’ani kwa umma huu.’ Ibn Shaba Al-Hurrani katika Tuhaful U’quul amepokea Uk. 37: “Kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) amesema: ‘Elimu haiondolewi kwa kung’olewa kwa watu lakini kwa kuondolewa Wanavyuoni, mpaka kusibaki mwanachuoni ndipo watu wataweka viongozi wajinga, wataulizwa na watoe fatwa bila ya kujua, watapotea na watapoteza.’’’ 98

7/2/2011

11:31 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

Kadhi Al-Maghribi amepokea katika Daaimul Islam katika Juz.1 uk. 96 kwa maneno: “Elimu haiondolewi kwa kung’olewa kwa watu lakini kwa kuondolewa Wanavyuoni, mpaka kusibaki mwanachuoni ndipo watu wataweka viongozi wajinga wataulizwa na watoe fatwa bila ya kujua, watapotea na watapoteza.’’ Na Imepokewa kutoka kwa Ali (a.s.) kuwa amesema: “Jifundisheni elimu kabla haijaondolewa, ama mimi sisemi hivi.. ( akainua mkono wake), lakini itakuwa mwanachuoni katika kabila atakufa na aondoke na elimu yake, na kutakuwa na mwingine kabila nyingine afe na kuondoka na elimu yake. Itakapokuwa hivyo watu watawachukua wajinga kuwa ndio wanatoa fatwa kwa rai zao, na kuacha athari. Watapotea na watapoteza na hapo umma huu utaangamia.’’ Na katika Mustadrak Juz. 17 Uk. 308: “Kutoka kwa Imam Ali Al-Askari (a.s.) kutoka kwa baba zake, kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) amesema: ‘Mwenyezi Mungu haiondoi elimu kuing’oa kwa watu bali atawachukua Wanavyuoni. Asiposhuka mwanachuoni kwenye dunia huletewa wanotafuta takataka za dunia na mambo ya haram ya ulimwengu na wenye haki watanyimwa wapewe wasio wa haki, na watu watawachukua wajinga kuwa viomgozi, wataulizwa, na watatoa fatwa bila ya kuwa na elimu, watapotea na watapoteza.”’ (Amepokea Al-Mufid katika Amali Uk. 20 kutoka kwa Al-Karajiki katika Kanzul Fawaaid, na Ibn Shahrashub katkka Al-Manaqib Juz. 3, Uk. 92 na Ibn Abul Jamhur Al Ahsai katika Ghawailu Laly Juz. 40, uk. 62 na Shahid wa pili katika Mun-tatul Murid na wengineo). Na amepokea katika rejea zao Bukhari Juz. 1, Uk. 33: Kutoka wa Abdallah bin Amru bin Al-Asi amesema: “Nimemsikia Mtume (s.a.w.w.) akisema: ‘Mwenyezi Mungu haiondoi elimu kwa kuing’oa kutoka kwa watu, lakini huondoa kwa kuwaondoa wanavyuoni mpaka kusibaki mwanachuoni hata mmoja, hapo watu watawafanya wajinga wao kuwa viogozi, watawauliza 99

7/2/2011

11:31 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

nao watatoa fatwa bila ya kuwa na elimu, watapotea na watapoteza.’’’ (Mfano wake amepokea Muslim Juz. 8, Uk. 60, na Ibn Majah Juz. 1, Uk. 20, Tirmidhi Juz. 4, Uk. 139 na Daramu Juz. 1, Uk. 77, na wengineo. Na akasema katika Fat’hul Bari Juz. 1, Uk. 175 kauli yake: “elimu kaichukuliwi kwa kuing’oa.” Yaani ni kuwa imefutwa kutoka vifuani mwao na hiyo ilikuwa ni Hadith ya Mtume katika Hijja ya kuaga kama alivyopokea Ahmad na Tabrani kutoka katika Hadith ya Umama akasema: ‘Ilipokuwa wakati wa Hijja ya kuaga, Mtume (s.a.w.w.) alisema: ‘’Ichukueni elimu kabla haijachukuliwa au kuondolewa.’ Bedui akauliza: ‘Vipi itaondolewa?’ Akajibu: ‘Ehe, kuondolewa elimu ni kuondolewa wenye nayo.’ Akasema mara tatu.” Na kwa ajili hii hapana budi tuziweke katika kundi moja zile Hadith za kuondolewa Qur’ani na kuzifuta vifuani pamoja na ngano za Ka’ab, kama vile kuondoka kwa Uislamu na umma wake, kuvunjwa Al-Ka’aba (Mungu ailinde!) na kubomolewa Makka (Mungu ailinde!).

Maswali Kwa rai yenu, ni ipi sabau ya Umar kumuamini sana Ka’abul Akhbaar? Je alikuwa akiamini kuwa huyo Ka’ab alikuwa anajua mambo ya ghaibu? Nini maelezo yenu juu ya Ka’ab kujua kuwa Umar atauwawa mwaka ule (Ka’ab alimwendea akamwambia: ‘Ewe Amirul-Mu’minin, toa ahadi kwamba wewe utakufa katika mwaka huu.’ Umar akasema: ‘Umejuaje ee Ka’ab?’ Akajibu: ‘Nimeyapata katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu!”’ Je mnaitakidi kuwa nzige huzaliana kutokana na pua ya papa, na kwamba ni windo la baharini? Mna maoni gani juu ya kauli ya Ka’ab kuwa Al-Ka’aba inaisujudia Baytul Muqaddas? 100

7/2/2011

11:31 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

Mna maoni gani juu ya maneno ya Umar kwamba Uislamu ni kama ngamia, lazima uzeeke na kutoweka? Je Hadith hii imeswihi kwenu?: “Hakika mfano wa umma wangu ni kama mfano wa bustani imelisha watu kwa mwaka na ikalisha watu kwa mwaka.” Au maana yake? Mnasemaje juu ya Hadith zenu sahihi kwamba Al-Ka’aba itavunjwa mwishowe kisha isijengwe, na Makka itaharibiwa mwishowe na isikaliwe? Mna maoni gani juu ya aliyopokea Suyuti Juz. 1, Uk. 136 katika Durrul Manthuuri akasema: “Ametaja Al-Bazaz katika Musnad yake na Ibn Khuzayma, Ibn Habban, Tabrani na Hakim, na kuisahihisha kutoka kwa Ibn Umar, amesema Mtume (s.a.w.w.): “Itumieni Nyumba hii kwani imevunjwa mara mbili na itaondolewa mara ya tatu?’’ Mna maoni gani juu ya Bukhari kuzikata Hadith? Je Hadith ya kuwa makuraish watatoweka imesihi kwenu? Mna maoni gani juu ya Hadith sahihi zenu kuwa Qur’ani itapelekwa mbinguni na nakala zote zitakosekana na watu watasahau walichokihifadhi? Mtakusanya vipi kati ya hadithi ya vizito viwili iliyo mutawatir na kwamba Qur’ani na kizazi chake havitatengana mpaka vimuendee Mtume (s.a.w.w.) kwenye hodhi lake; na yale maneno yaliyotangulia hapo awali mfano: Kutoweka makuraish, kuvunjwa Al-Ka’aba na kuondolewa Qur’ani? Vipi mnakusanya baina ya Hadithi zenu sahihi na hasan juu ya kuondolewa Qur’ani; na ile Hadith yenu sahihi: “Elimu haiondolewi kwa kung’olewa.’’?

101

7/2/2011

11:31 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

Nini maelezo yenu juu ya kuwapo Hadith za majanga ya waislamu na kuisha kwao katika rejea zenu’ na rejea za Shi’ah kutokuwa na hadithi hizo? Mwisho wa du’a zetu ni kumshukuru Mwenyezi Mungu Bwana Mlezi wa walimwengu.

102

7/2/2011

11:31 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION 1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9. 10. 11. 12. 13. 14. 15. 16. 17. 18. 19. 20. 21. 22. 23. 24. 25. 26.

Qur'an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Thalathini Uharamisho wa Riba Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili Hekaya za Bahlul Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.) Hijab vazi Bora Ukweli wa Shia Ithnaashari Madhambi Makuu Mbingu imenikirimu Abdallah Ibn Saba Khadijatul Kubra Utumwa Umakini katika Swala Misingi ya Maarifa Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia Bilal wa Afrika Abudharr Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu Salman Farsi Ammar Yasir Qur'an na Hadithi Elimu ya Nafsi Yajue Madhehebu ya Shia Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur'an Tukufu 103

7/2/2011

11:31 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu 27. 28. 29. 30. 31. 32. 33. 34. 35. 36. 37. 38. 39 40. 41. 42. 43. 44. 45. 46. 47. 48. 49. 50. 51. 52. 53. 54. 55. 56. 57.

Sehemu ya Sita

Al-Wahda Ponyo kutoka katika Qur'an. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii Mashukio ya Akhera Al Amali Dua Indal Ahlul Bayt Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna. Haki za wanawake katika Uislamu Mwenyeezi Mungu na sifa zake Amateka Na Aba'Khalifa Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) Adhana. Upendo katika Ukristo na Uislamu Nyuma yaho naje kuyoboka Amavu n’amavuko by’ubushiya Kupaka juu ya khofu Kukusanya swala mbili Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Kusujudu juu ya udongo Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s) Tarawehe Malumbano baina ya Sunni na Shia Kupunguza Swala safarini Kufungua safarini Umaasumu wa Manabii Qur’an inatoa changamoto as-Salaatu Khayrun Mina -'n Nawm Uadilifu wa Masahaba Dua e Kumayl Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu 104

7/2/2011

11:31 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu 58. 59. 60. 61. 62. 63. 64. 65. 66. 67. 68. 69. 70. 71. 72. 73. 74. 75. 76. 77. 78. 79. 80. 81. 82. 83. 84. 85. 86.

Sehemu ya Sita

Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mitume Muhammad (s) Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili Kuzuru Makaburi Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita Tujifunze Misingi Ya Dini Sala ni Nguzo ya Dini Mikesha Ya Peshawar Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu Ubora wa Imam 'Ali Juu ya Maswahaba Na Ushia ndio njia iliyonyooka Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake Liqaa-u-llaah Muhammad (s) Mtume wa Allah Amani na Jihadi Katika Uislamu Uislamu Ulienea Vipi? Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) Urejeo (al-Raja’a ) Mazingira Utokezo (al - Badau) Sadaka yenye kuendelea Msahafu wa Imam Ali 105

7/2/2011

11:31 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

87. 88. 89. 90. 91. 92. 93. 94. 95.

Uislamu na dhana Mtoto mwema Adabu za Sokoni Johari za hekima kwa vijana Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu Tawasali Imam Mahdi katika Usunni na Ushia

96.

Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu

97.

Hukumu ya kujenga juu ya makaburi

98.

Swala ya maiti na kumlilia maiti

99.

Shiya na Hadithi (kinyarwanda)

100.

Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu

101.

Hadithi ya Thaqalain

102

Fatima al-Zahra

103.

Tabaruku

104.

Sunan an-Nabii

105.

Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza)

106.

Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili)

107.

Mahdi katika sunna

108.

Kusalia Nabii (s.a.w)

109.

Ujumbe -Sehemu ya Kwanza

110.

Ujumbe - Sehemu ya Pili

111.

Ujumbe - Sehemu ya Tatu

112.

Ujumbe - Sehemu ya Nne

113.

Ngano ya kwamba Qur’ani imebadilishwa 106

7/2/2011

11:31 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

114.

Iduwa ya Kumayili

115.

Maarifa ya Kiislamu.

116.

Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza

117.

Ukweli uliopotea sehemu ya Pili

118.

Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu

119.

Ukweli uliopotea sehmu ya Nne

120.

Ukweli uliopotea sehmu ya Tano

121.

Johari zenye hekima kwa vijana

122.

Safari ya kuifuata Nuru

123.

Idil Ghadiri

124.

Myahudi wa Kimataifa

125.

Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi

126.

Visa vya kweli sehemu ya Kwanza

127.

Visa vya kweli sehemu ya Pili

128.

Muhadhara wa Maulamaa

129.

Mwanadamu na Mustakabali wake

130.

Imam Ali binamu ya Mtume Sehemu ya Kwanza

131.

Imam Ali binamu ya Mtume Sehemu ya Pili

132.

Khairul Bariyyah

133.

Uislamu na mafunzo ya kimalezi

134.

Vijana ni Hazina ya Uislamu.

135.

Yafaayo kijamii

136.

Kusoma sura zenye Sijda ya wajibu

137.

Taqiyya

138.

Vikao vya furaha

139.

Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje? 107

7/2/2011

11:31 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

140.

Uislamu na Mazingatio Sehemu ya Kwanza

141.

Uislamu na Mazingatio Sehemu ya Pili

142.

Azadari-Kuhuzunika na Kuomboleza

143.

Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah

144.

Mtazamo Mpya - Wanawake katika Uislamu

145.

Kuonekana kwa Allah

146.

Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza)

147.

Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili)

148.

Ndugu na Jirani

149.

Ushia ndani ya Usunni

150.

Maswali na Majibu

151.

Mafunzo ya hukmu za ibada

152

Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisusunni No 1

153.

Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisusunni No 2

154.

Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisusunni No 3

155.

Abu Huraira

156.

Kati ya Alama kuu za dini ni swala ya Jamaa na Adabu za Msikiti na Taratibu zake.

157.

Uadilifu katika Uislamu

108

7/2/2011

11:31 AM

Pag


Maswali na Mishkel. sehemu ya sita. By Lubumba PROOFREAD BY SHEMAHIMBO 17-4-09.qxd

Maswali na Mishkili Elfu

Sehemu ya Sita

BACK COVER Madhehebu ya Shia Ithnaasharia imekuwa ikishutumiwa na Waislamu wengine shutuma ambazo hazina msingi wala hazimo katika imani na itikadi zake. Shutuma hizi zimekuwa zikirudiwa mara kwa mara licha ya kutolewa majibu madhubuti na yakinifu na wanavyuoni wa zamani na wa sasa. Kutokana na kasumba hii, mwandishi wa kitabu hiki ameamua kukusanya maswali na mishkili elfu moja kutoka kwenye vitabu vya Kisunni na kutoa hoja kabambe kuzijibu shutuma hizo wanazozuliwa wafuasi wa madhehebu ya Shia. Katika kulitekeleza jukumu hili, mwandishi ametegemea rejea zao za msingi kutoka katika (vitabu vya) hadithi, tafsiri, fikihi na itikadi, na kauli za viongozi wao wakubwa kuanzia wa zamani hadi wa sasa. Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Nukushi: +255 22 2127555 Barua Pepe: alitrah@raha.com Tovuti: www.alitrah.org Katika mtandao: www.alitrah.info

109

7/2/2011

11:31 AM

Pag


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.