MSAHAFU WA IMAM ALI Kimeandikwa na: Sayyid Abdul-Rahim al-Musawi
Kimetarjumiwa na Hemedi Lubumba Selemani
Š Haki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION
ISBN: 978 - 9987 - 512 - 62 - 1
Kimeandikwa na: Sayyid Abdur-Rahim al-Musawi Kimetarjumiwa na Hemedi Lubumba Selemani Kupangwa katika Kompyuta na: Al-Itrah Foundation Toleo la kwanza: Januari, 2014 Nakala:1000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 / 2127555 Barua Pepe: alitrah@yahoo.com Tovuti: www.ibn-tv-com Katika mtandao: w.w.w.alitrah.info
YALIYOMO Utangulizi.................................................................................. 2 Hatua ya Kwanza:.................................................................... .4 Hatua ya Pili...............................................................................5 Hatua ya tatu..............................................................................5 Mabingwa wa hatua ya kwanza.................................................5 Je, Mtume wa Allah aliikusanya Qur’ani yeye mwenyewe.......6 Jina ‘Msahafu wa Ali’ limetoka wapi?......................................7 Misahafu ya sahara iliyopewa majina ya kusanyaji wake, je inajitofautiana? na je kila mmoja una sifa ya pekee?.....................8 Ni lini Imam Ali (a.s) Aliukusanya Msahafu wake?.................9 Ni sifa zipi za pekee zenye kuutofautisha msahafu wa Ali dhidi ya mingine?..............................................................................10 Je, Imam alionyesha msahafu wake kwa watu?.......................11 Msahafu wa Imam Ali ulikwenda wapi?..................................12
NENO LA MCHAPISHAJI Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabu kiitwacho, Mus’hafu ’l-Imam Ali. Sisi tumekiita, Msahafu wa Imam Ali. Kitabu hiki ni matokea ya utafiti wa kielimu uliofanywa na wanazuoni wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bait (as). Wanazuoni hawa wamesukumwa na shutuma zinazotolewa na baadhi ya Waislamu wa madhehebu nyingine kwamba Mashia hawaamini Qur’ani hii tuliyonayo bali wana msahafu wao unaoitwa, Msahafu wa Imam Ali. Suala hili limeelezwa na kutolewa ufafanuzi wa kina katika vitabu vingi vilivyoandikwa na wanazuoni wa Kishia; na wanazuoni wa Jumuiya hii ni miongoni mwa wanazuoni hao na wanazidi kulitolea ufafanuzi suala hili ili watu waondokane na dhana na upotoshaji huu wenye nia ya kuwatenganisha Waislamu. Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote, ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni mambo ambayo hayana nafasi tena katika akili za watu.
Tunamshukuru ndugu yetu, Hemedi Lubumba Selemani (Lipumba) kwa kukubali jukumu hili la kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake. Mchapishaji: Al-Itrah Foundation
NENO LA JUMUIYA Hakika mirathi ya Ahlul-Bait ambayo imehifadhiwa na kambi yao na wafuasi wao dhidi ya upotovu inaonyesha ni kambi iliyokusanya aina mbalimbali za taaluma za kiislamu. Kambi hii imeweza kulea nafsi mbalimbali zilizo tayari kunywa kutoka kwenye chemchemi hiyo, na kuupa umma wa kiislamu wanavyuoni wakubwa wenye kufuata nyayo za ujumbe wa AhlulBait. Wanavyuoni waliokusanya vidodosa na maswali mbalimbali ya madhehebu na mitazamo tofauti ya kifikira kuanzia ndani ya desturi ya kiislamu hadi nje ya desturi hiyo, huku wao wakitoa majibu na utatuzi makini juu ya maswali hayo ndani ya karne zote. Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bait imefanya hima kutetea utukufu wa ujumbe wa Uislamu na ukweli wake ambao umechafuliwa na makundi, madhehebu na wanaharakati mbalimbali wenye chuki na Uislamu. Jumuiya imefuata nyayo za Ahlul-Bait na za wafuasi wa kambi yao njema ambayo imefanya hima kujibu madai yenye kuendelea na daima ikajaribu kubaki ndani ya msitari wa mapambano kwa kiwango kinachohitajika ndani ya kila zama. Hakika uzoefu ambao umehifadhiwa ndani ya vitabu vya wanachuoni wa kambi ya Ahlul-Bait katika dhamira hii ni wa aina ya pekee, kwa sababu una akiba ya kielimu inayotegemea akili na hoja, huku ukijiepusha na matamanio na upendeleo uliokatazwa. Unazungumza na wasomi na wanafikra wenye fani maalumu, mazungumzo ambayo yanakubalika kiakili na yanapokewa na maumbile yaliyo salama.
Jaribio hili la Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bait limekuja kuwapa watafuta ukweli hatua mpya ya uzoefu wa thamani katika ulingo wa mazungumzo na maswali na kujibu hoja za utata zilizotolewa zama zilizopita au zinazotolewa leo kwa njia ya Tovuti, na hasa kwa kupewa nguvu na baadhi ya duru zenye chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu. Ikijiepusha na uchochezi uliyokatazwa, na ni yenye kuhangaikia kuzishauri akili zenye kufikiria na nafsi zenye kutafuta haki, ili ziweze kufikia kwenye haki ambayo inatolewa na Kambi ya AhlulBayt ulimwengu mzima, ndani ya zama ambazo akili inaerevuka na nafsi na roho zinaboreka kwa kasi ya pekee. Ni lazima tugusie kuwa mfululizo huu wa tafiti hizi umeandaliwa na Kamati maalumu toka jopo la wanachuoni watukufu, hivyo tunatoa shukurani njema kwa hawa wote na kwa wasomi na wahakiki kwa kila mmoja miongoni mwao kwa kupitia sehemu ya tafiti hizi na kutoa mchango wao wa thamani kuhusu tafiti hizi. Na sote tunategemea na kutaraji kuwa tutakuwa tumetoa kile tulichokiweza katika juhudi za kutekeleza baadhi ya wajibu tulionao mbele ya ujumbe wa Mtukufu Mola Wetu Mlezi ambaye alimtuma Mtume Wake na uongofu na dini ya haki ili aipe ushindi dhidi ya dini zote. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa shahidi.
Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bait Kitengo cha utamaduni
Msahafu wa Imam Ali
UTANGULIZI Maelezo yote ya Jemedari wa waumini Imam Ali bin Abi Talib (a.s.) yaliyomo ndani ya Nahjul-Balaghah, yanaafikiana kuwa Qur’ani hii iliyomo mikononi mwetu ndio kitabu ambacho Allah alikiteremsha kwa Mtume wake mwaminifu Muhammad hitimisho la manabii. Nacho ndicho kitabu ambacho Mwenyezi Mungu amechukua dhamana ya kukihifadhi na kukidumisha, kwa kuzingatia kuwa chenyewe ndicho dalili ya kudumu kwa utume ambao alikiteremsha ili kiuthibitishe na kuuimarisha. Nacho kimebeba uongofu wa Allah na dini timilifu ambayo ameiridhia kwa ajili ya waja wake, na iliyo hoja yake juu ya viumbe wake, mpaka siku ya Kiyama. Maneno yake yenye kudumu kuhusu Kitabu hiki chenye kudumu yameweka wazi kuwa, yeye (a.s.) anazungumzia Qur’ani hii iliyomo mikononi mwetu. Nayo ndio Qur’ani iliyoteremshwa juu ya Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.), na ikakusanywa ndani ya zama zake (a.s), na wakawa nayo waislam, kizazi baada ya kizazi, haijapungua herufi wala neno. Amesema (a.s.): “Tambueni kuwa Qur’ani hii ndio mnasihi asiyehadaa, kiongozi asiyepoteza na msaidizi asiyesema uongo. Na hakuna yeyote yule anayeketi na Qur’ani hii ila ni lazima atanyanyuka akiwa na ziada au upungufu: Ziada katika uongofu, au upungufu wa upotovu. “Na tambueni kuwa hakuna ukata wowote baada ya Qur’ani kwa yeyote yule, wala utajiri wowote ule kabla ya Qur’ani kwa yeyote yule. Hivyo ifanyeni dawa ya magonjwa yenu na itumieni juu ya matatizo 2
Msahafu wa Imam Ali yenu, kwani bila shaka ina tiba ya magonjwa makubwa, nayo ni ukafiri, unafiki, ujeuri na upotovu. Basi mwombeni Allah kwayo, na mwelekeeni Yeye kwa mapenzi yake.”1 Maelezo haya yaliyopatikana kutoka kwake kuhusu Qur’ani Tukufu iliyomo mikononi mwa waislamu katika zama zake hadi zama zetu hizi, ndio yenye kufasiri kauli yake (a.s.): “Na hakika kimeendelea kuwa pamoja nami. Sijaachana nacho tangu niliposuhubiana nacho.”2 Huu ndio msimamo wa Jemedari Imam Ali bin Abi Talib (a.s.) juu ya Kitabu cha Allah chenye kudumu. Lakini maadui wa Kitabu hiki cha Allah, ili kuwafarakisha waislamu, wametumia njia mbalimbali, na kati ya hizo ni: Kuwatuhumu Ahlul-Bait, ambao hasa ndio wabebaji wa Qur’ani, wenza wake, walinzi wake na wafasiri wa Aya zake kama zilivyofunuliwa kwa Mtume, kuwa wao wanadai kwamba kuna Qur’ani nyingine isiyokuwa hii waliyoihifadhi,3 huku wakidai kuwa kuna riwaya zinazogusia hilo. Ili kuuweka wazi ukweli ambao wadau wa haki wanaujua, na ambao maadui wanajaribu kuutokomeza, kuanzia hapa tutalichambua dai hili ili tufike kule zinakotuelekeza riwaya katika ulingo huu, na hilo ni kwa kupitia historia ya Qur’ani, kwa kuanzia tangu zama za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mpaka zama za Imam Ali (a.s.), ili tufikie kwenye ukweli wa kile kinachoitwa ‘Msahafu wa Imam Ali’ katika maelezo haya. 1Nahjul-Balagha, hotuba ya 176. pia rejea ensiklopedia ya maudhui za Nahjul-Balagha, ili humo uone kundi la maelezo yaliyopatikana toka kwa (a.s.) yakihusu hili. 2. Nahjul-Balagha, hotuba ya 122 3. Hii haimaanishi kuwa sahaba au Maimamu wa Ahlul-Bait (a.s.) hawana karatasi zinazohusu Qur’ani Tukufu, huenda karatasi hizo zina tafsiri zake na taawili yake, au sababu za kuteremka kwake, na mengineyo kama hayo yanayohusiana na Qur’ani Tukufu.3
Msahafu wa Imam Ali Hatuwezi kuichambua kadhia ya Msahafu wa Imam Ali (a.s.) ila baada ya kutambua historia ya ukusanywaji wa Qur’ani, kwa sababu Msahafu wa Imam Ali (a.s.) si chochote kingine bali ni ule ukusanywaji wa Qur’ani Tukufu na yale yanayoihusu uliyofanywa na Imam Ali (a.s.). Hakika uratibu wa Qur’ani na muda wa kukusanywa kwake, kupangilia Sura zake, kuiwekea irabu na nukta, kuigawa katika juzuu na mafungu, hayo yote hayakuwa tija ya kazi ya mtu mmoja, na wala haikukamilika ndani ya kipindi cha muda mfupi, bali kwa hakika ilipitwa na muda na zama nyingi, kuanzia zama za utume ikaendelea hadi zama za kuufanya msahafu mmoja, nazo ni zama za Uthman. Kisha ikaendelea mpaka zama za Al-Khalil bin Ahmad Al-Farahidiy, ambaye ndiye aliyemalizia kuiwekea irabu kama ilivyo sasa mikononi mwetu leo. Wanahistoria wanaona kuwa historia ya ukusanywaji wa Qur’ani imepitia hatua kuu tatu:
HATUA YA KWANZA: Kipindi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Qur’ani ilipokusanywa kimaandishi na kwa kuhifadhiwa vifuani, na ikaandikwa kwenye karatasi, magome ya miti, maganda ya mitende, mawe na mifupa ya ngamia. Zaid bin Thabit anasema: “Tulikuwa kwa Mtukufu Mtume wa Allah tukiandika, yaani tukiandika Qur’ani katika magome.”4
4. Al-Mustadrak Juz. 2 Uk. 611 4
Msahafu wa Imam Ali
HATUA YA PILI: Kipindi cha Abu Bakr, kwa kutoa nakala toka kwenye maganda ya mitende, magome na vifua vya watu.5
HATUA YA TATU: Kipindi cha Uthman bin Affan, pale Qur’ani ilipokusanywa kati ya gamba mbili, na watu wakalazimishwa juu ya kisomo kimoja, na kutokana na msahafu huo zikaandikwa nakala nyingine za misahafu aliyoipeleka miji mbalimbali, na ile mingine (isiyotokana na huo wa Uthman) ikachomwa moto.6
MABINGWA WA HATUA YA KWANZA Baadhi ya ulamaa wa Shia Imamiyya wanaona kuwa Qur’ani Tukufu ilikuwa imekusanywa tangu zama za Mtume wa Allah (s.a.w.w.), na kuwa hakuiacha dunia yake kwenda Akhera ila baada ya yale yaliyomo ndani ya kifua chake kuoana na yale yaliyomo ndani ya vifua vya mahafidhi, ambao kwa kweli walikuwa wengi. Na pia baada ya kuoana na yale yaliyomo ndani ya misahafu ya wale walioikusanya Qur’ani katika zama zake. Hilo linaashiriwa na riwaya nyingi, ikiwemo kauli yake (s.a.w.w.): “Atakayeisoma Qur’ani mpaka ikamkaa na kuihifadhi, basi Allah atamwingiza Peponi na atampatia shifaa ya watu kumi toka katika Ahlul-Baiti wake….” 7 Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akisimamia yeye mwenyewe yale 5. Al-It'qan Juz. 1, Uk. 202. Na Al-Mustadrak cha Al-Hakim Juz. 3, Uk. 656 6. Al-It’qan Juz. 1, Uk. 211. 7.Majmaul-Bayan Juz. 1 Uk. 75. Manahilul-Irfan Juz. 1, Uk. 234. Munad Ahmad Juz. 5, Uk. Mabahithu Uluumil-Qur’ani: 121. Hayatus-Sahaba Juz. 3, Uk. 26. Mustadrakul-Hakim Juz.3,Uk. 35. 5
Msahafu wa Imam Ali yanayoandikwa. Imepokewa kutoka kwa Zayd, amesema: “Nilikuwa nikiingia kwake nikiwa na kipande cha mfupa au gome, naanza kuandika huku yeye akinisomea imla. Ninapomaliza huniambia: ‘Isome.’ Basi nami nasoma, na kama kuna kosa husahihisha, na ndipo natoka kwenda nayo kwa watu.”8 Na imepokewa kuwa sahaba walikuwa wakihitimisha Qur’ani kuanzia mwanzo wake hadi mwisho wake, hadi (s.a.w.w.) akasema: “Hakika mwenye Qur’ani kwa kila hitimisho moja ana dua yenye kujibiwa mbele ya Allah.”9
JE MTUME WA ALLAH ALIIKUSANYA QUR’ANI YEYE MWENYEWE? Hakika kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kulikuwepo msahafu uliokusanywa. Katika hadithi ya Uthman bin Abil-A’sw ulipokuja ujumbe wa Thaqif kwa Mtume, amesema: “Nikaingia kwa Mtume wa Allah, nikamwomba msahafu uliokuwepo kwake, akanipa.”10. Bali Mtume wa Allah (s.a.w.w.) aliacha msahafu nyumbani kwake nyuma ya kitanda chake ukiwa umeandikwa katika magome ya mitende, hariri na mifupa, na alikuwa amemwamuru Ali (a.s.) auchukue na kuukusanya….” 11 Ama hatua ya pili ya ukusanyaji wa Qur’ani ambayo inasemekana kuwa ilikuwepo zama za Abu Bakr, ni kuwa habari kuhusu hatua hii ya ukusanyaji zinapingana, kama ambavyo hazihusiani kabisa na lile tunalozungumzia. Ama utata wa kuwa Imam Ali (a.s.) ana msahafu 8.Majmauz-Zawaid Juz. 1, Uk. 152. 9. Kanzul-Ummal Juz. 1. Hadithi ya 2280. 10.Majmauz-Zawaid Juz. 9, Uk. 371. Hayatus-Sahaba Juz. 3, Uk. 344. 11. Kanzul-Ummal Juz. 2. Hadithi ya 4792. 6
Msahafu wa Imam Ali wenye maandiko yasiyokuwa haya yaliyomo kwenye msahafu huu uliyomo mikononi mwa waislamu, ni utata usiyo na hoja wala msingi wowote wa ukweli na usahihi. Ndio, baadhi ya hadithi za Shia na Sunni zinaonyesha kuwa Imam Ali (a.s.) alijitenga na watu baada ya kifo cha Mtume wa Allah (s.a.w.w.) ili akusanye Qur’ani Tukufu, na msimamo wake huu ulitokana na amri ya Mtume wa Allah (s.a.w.w.), na (a.s.) alisema: “Sintovaa joho hadi niikusanye.” Na imepokewa kuwa hakuvaa joho ila kwa ajili ya Swala, mpaka alipoikusanya.12
JINA ‘MSAHAFU WA ALI’ LIMETOKA WAPI? Imamu Ali (a.s.) alikuwa na msahafu kama ilivyokuwapo misahafu mingine iliyokusanywa baadaye, kwa mfano msahafu wa Zayd, msahafu wa Ibnu Mas’ud, msahafu wa Ubayya bin Kaab, msahafu wa Abi Musa Al-Ash’ariy na msahafu wa Al-Miqdad bin Al-As’wad, kama ambavyo Aisha naye alivyokuwa na msahafu wake pia. Wakazi wa mji wa Kufa walikuwa wakisoma kwa kufuata msahafu wa Abdallah bin Mas’ud. Wakazi wa Basra walikuwa wakisoma kwa kufuata msahafu wa Abi Musa Al-Ash’ariy. Wakazi wa Sham walikuwa wakisoma kwa kufuata msahafu wa Ubayya bin Kaab. Na wakazi wa Damascus walikuwa wakisoma kwa kufuata msahafu wa Al-Miqdad. Lakini muda wa misahafu hii na usomaji wa kuifuata ulikoma zama za Uthman bin Affan, pale alipopeleka nakala yake na 12. Tazama At-Tabaqatil-Kubra Juz. 2 Uk. 338. Ansabul-Ashraaf Juz. 1 Uk. 587. Sharhu Bin Abil-Hadid Juz. 1 Uk. 27. Manahilul-Irfan Juz. 1 Uk. 247. Al-Itqan Juz. 1 Uk. 204. Kanzul-Ummal Juz. 2: 588: 4792 7
Msahafu wa Imam Ali akaichoma moto misahafu hiyo.13 Ama msahafu wa Imam Ali (a.s.) wenyewe aliuhifadhi yeye mwenyewe na watu wa nyumba yake, na wala hakumwonyesha yeyote mwingine. Hiyo ni ili ahifadhi umoja wa umma, kama itakavyobainika hapo baadaye.
MISAHAFU YA SAHABA ILIYOPEWA MAJINA YA WAKUSANYAJI WAKE, JE INATOFAUTIANA? NA JE KILA MMOJA UNA SIFA YA PEKEE? Wanahistoria wanaona kuwa misahafu hiyo ina tofauti kubwa kati yake yenyewe kwa yenyewe, upande wa utangulizaji wa Sura na ucheleweshaji. Mfano msahafu wa Ibnu Mas’ud wenyewe tunaukuta umeandikwa kwa kutanguliza Sura saba zilizo ndefu zaidi, kisha zenye Aya mia mbili, kisha zenye Aya mia moja, kisha zenye herufi, kisha Mumtahinat na hatimaye Mufaswilat. Ama msahafu wa Ubayya bin Kaab wenyewe tunaukuta umetanguliza Sura Al-Anfal na kuiweka baada ya Sura Yunus na kabla ya Sura al-Baraa. Na ametanguliza Sura Maryam, Shuaraa na Sura Haji kabla ya Sura Yusuf.14
13 Al-Masahif cha Al-Sijsitaniy: 11- 14. Al-Kamil Fitarikh Juz. 3, Uk. 55. Al-Burhan Juz. 1 Uk. 239 – 243. Juz. 6 Uk. 225 – 226. Sahih Bukhari. 14.At-Tamhid cha Muhammad Hadil-Maarifa Juz. 1, Uk. 312 8
Msahafu wa Imam Ali
NI LINI IMAM ALI (A.S.) ALIUKUSANYA MSAHAFU WAKE? Hakika aliyechukua jukumu la kuikusanya Qur’ani baada tu ya kifo cha Mtume (s.a.w.w.) na kwa usia wake (s.a.w.w.)15 ni Ali bin Abi Talib. Kwani alikaa nyumbani mwake akijishughulisha na ukusanyaji wa Qur’ani na kuiratibu kama ilivyoteremka. Ibnu Nadim amesema: “Hakika Ali aliona watu wamechanganyikiwa wakati wa kifo cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ndipo akaapa kutokulivaa joho lake mpaka atakapoikusanya Qur’ani.”16 Muhammad bin Sariin amepokea kutoka kwa Akrimah, amesema: “Mwanzoni mwa ukhalifa wa Abibakr, Ali alikaa nyumbani kwake akiikusanya Qur’ani.” Amesema: “Nikamwambia Akrimah: ‘Uratibu wa mwingine asiyekuwa yeye ulikuwa kama ilivyoteremka kwa kuanza iliyokuwa ya kwanza kisha iliyofuata?’ Akasema: ‘Lau kama majini na wanadamu wangekusanyika ili waiandike kwa utaratibu huu, wasingeuweza.”’ Ibnu Siriin amesema: “Nilitafuta kitabu hicho na nikaandika barua Madina nikikitafuta, lakini sikuweza kukipata.”17
15. Rejea Tafsiril-Qummiy: 745. Biharul-An’war Juz. 92, Uk. 47, hadithi ya 5 16. Al-Manaqib Juz. Uk. 40 17. Al-Manaqib Juz. Uk. 40. -Al-It’qan Juz. 1, Uk. 57. At-Tabaqat Juz. 2, Uk. 101. Al-Istiaab kwenye pambizo la Al-Iswaba Juz. 2, Uk. 253. AtTas’hiil Liuluumit-Tanziil Juz. 1, Uk. 4. Biharul-An’war Juz. 92, hadithi ya 27. Alaur-Rahman Juz. 1, Uk. 18. 9
Msahafu wa Imam Ali
NI SIFA ZIPI ZA PEKEE ZENYE KUUTOFAUTISHA MSAHAFU WA ALI DHIDI YA MINGINE? Baada ya kuthibiti kuwa kuna msahafu wa Imam Ali (a.s.) alioukusanya baada ya kifo cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), basi ni zipi hizo sifa za msahafu huo? Na je wenyewe unatofautiana na ile misahafu mingine iliyokusanywa baada ya msahafu wake? Wanasema: Hakika tofauti kati ya msahafu wa Imam Ali (a.s.) na misahafu mingine ambayo nayo yenyewe kwa yenyewe ilikuwa imetofautiana, ni kuwa wa kwake Imam Ali (a.s.) aliuratibu kwa kufuata utaratibu wa uteremkaji (wa Qur’ani). Kama ambavyo pia ulikuwa umejumuisha na kukusanya ufafanuzi na tafsiri za maudhui ya Aya, huku ukibainisha sababu zilizopelekea kuteremka Aya hizo, na pia maeneo zilipoteremkia. Amesema (a.s.): “Hakuna Aya yoyote iliyoteremka kwa Mtume ila alinisomea na kunifanyia imla, nami nikiiandika kwa hati yangu. Na alinifunza taawili yake na tafsiri yake, iliyofuta na iliyofutwa, muhkam na mutashabih yake. Na akaniombea kwa Mwenyezi Mungu anipe ufahamu wake na niihifadhi. Hivyo tangu aniombee hayo aliyoniombea sikuisahau Aya yoyote katika Kitabu cha Allah, wala elimu yoyote aliyonifanyia imla nami nikaiandika.”18 Na ni kama ambavyo ulikuwa umekusanya elimu mbalimbali za Qur’ani, mfano: Muhkam, mutashabih, mansukh, nasikh, tafsiri ya Aya na taawili zake. 19 18. Tafsirul-Burhan Juz. 1, Uk. 16, hadithi ya 14. 19.Al-Irshad War-Risalatus-Sarwiyyah cha Al-Mufid. Aaayanus-Shia Juz. 1, Uk. 89. Tarikhul-Qur’ani cha Al-Abyariy: 85. Haqaiqu Hammatu HawlalQur’ani Al-Karim: 153-158. 10
Msahafu wa Imam Ali
JE IMAM ALI ALIONYESHA MSAHAFU WAKE KWA WATU? Ndio, baada ya kuukusanya alikuja nao mbele ya watu na kusema: “Mimi tangu Mtume wa Allah (s.a.w.w.) alipofariki nilikuwa nikishughulishwa na kumwosha na kumwandaa kwa mazishi, kisha ukusanyaji wa Qur’ani mpaka nilipoikusanya yote. Na hakuna Aya yoyote ya Qur’ani ambayo Allah ameiteremsha kwa Nabii wake ila bila shaka nimeikusanya.”20 Hapo Imam Ali (a.s.) akawaonyesha watu msahafu wake na akabainisha sifa zake za pekee, ndipo akasimama mtu mmoja kati ya mabwana wa kaumu ile, akautazama kwa kuuchunguza, akasema: “Ewe Ali! Urudishe hatuna haja nao.”21 Imam Ali (a.s.) akasema: “Naapa wallahi, kamwe baada ya siku yenu hii hamtouona tena. Hakika nilipoukusanya ilikuwa ni wajibu wangu nikuelezeni ili muusome.”22
KWA NINI IMAM ALI HAKUUTOA MSAHAFU WAKE ZAMA ZA KHALIFA UTHMAN? Ndani ya kipindi cha utawala wa Uthman misahafu ilitofautiana na kuzusha kelele kati ya waislamu, ndipo Talha akamwomba Imam Ali (a.s.), lau awatolee watu msahafu wake ambao aliukusanya baada ya kufariki Mtume wa Allah (s.a.w.w.), akasema: “Ni kipi kikuzuiacho 20. Al-Ihtijaj cha Tabarasiy: 82. 21. Kitabu Salim bin Qaysi: 72. Al-Manaqib Juz. 1, Uk. 40-41. Al-Ihtijaj cha Tabarasiy: 82. Biharul-An’war Juz. 92, Uk. 51, hadithi ya 18.22. Tafsurus-Swafiy Juz. 1, Uk. 36. 11
Msahafu wa Imam Ali kuwatolea watu Kitabu cha Allah?” Kwanza Imam hakumjibu, ndipo Talha akakariri swali lake, akasema: “Nakuona Abil Hasan hujanijibu swali nililokuuliza kuhusu Qur’ani. Kwa nini usiutoe kwa watu?” Ndipo Ali (a.s.) akaweka wazi sababu ya kutokumjibu Talha akihofia umoja wa umma usifarakane, akasema: “Ewe Talha! Makusudi kabisa nimejizuia kukujibu, hebu nieleze kuhusu ile waliyoiandika kaumu, je yote ni Qur’ani, au humo mna yasiyokuwa Qur’ani?” Talha akasema: “Bali yote ni Qur’ani.” Akasema (a.s.): “Mkichukua yaliyomo humo mtaokoka dhidi ya moto, na mtaingia peponi…”23
MSAHAFU WA IMAM ALI ULIKWENDA WAPI? Riwaya zinaonyesha kuwa Imam Ali (a.s.) aliukabidhi msahafu huo kwa Maimamu wa baada yake, wakirithishana mmoja baada ya mwingine, huku wakiwa hawamwonyeshi mwingine yeyote yule.24 Kama ambavyo habari na mazungumzo kuhusu msahafu huo havikuwa siri kwa ulamaa wengine. Ibnu Nadim amesema: “Ndio msahafu wa kwanza ambao humo ilikusanywa Qur’ani. Na msahafu huu ulikuwepo kwa Ali Jafar.” Na katika kauli yake nyingine amesema: “Walikuwa wakirithishana wana wa Hasan.”25 Kisha Ibnu Siriin amefuatilia mwisho wa msahafu huu huko Madina, lakini hakufanikiwa kuupata. Na ameeleza waziwazi wasifu wa msahafu huu kwa kauli yake: “Natamani lau ningekipata kitabu hicho, 23. Salim bin Qaysi: 110. Biharul-An’war Juz. 92 Uk. 42, hadithi ya 1. 24. Biharul-An’war Juz. 92 Uk. 42, hadithi ya 1 25. Al-Fahras cha Ibnu Nadiim: 47-48. 12
Msahafu wa Imam Ali kilikuwa na elimu.”26 Hivyo muhtasari wa kadhia ya Msahafu wa Imam Ali ni kama ifuatavyo: Hakika Imam alikusanya Qur’ani baada tu ya kifo cha Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.), na Sura zake na Aya zake zilikuwa ni zilezile zilizomo mikononi mwa waislamu leo hii. Ulikuwa umeratibiwa kwa utaratibu wa kufuata jinsi Sura zilivyoteremka, huku pembezoni mwake mkiwa na sababu zilizopelekea kuteremka. Isipokuwa msimamo wa baadhi ya sahaba dhidi ya msahafu wake, ulikuwa ni wa kisiasa. Hivyo kuanzia hapa ni bora tukauzingatia kuwa ulikuwa ni nakala nyingine ya Qur’ani Tukufu iliyobeba Sura zake na Aya zake, na wala si Qur’ani nyingine iliyo tofauti na hii tuliyonayo sasa. Baada ya hapo maadui wakaja ili waseme kuwa: Shia Imamiya wanadai kuwa Imam Ali (a.s.) ana msahafu, kwa maana ya Qur’ani nyingine tofauti na hii iliyomo mikononi mwa waislamu. Wamefanya hivyo kwa lengo la kufanya dhulma na kutamani kuifarakisha safu ya umma wa kiislamu.27
26. At-Tabaqat Juz. 2 Uk. 101. Al-It’qan Juz. 1 Uk. 57. 27. Fuatilia kitabu Shia Was-Sunnah cha Ihsan Ilahiy Dhahiir: 88, na wengineo waliofuata mwenendo wake. 13
Msahafu wa Imam Ali
ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION 1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9. 10. 11. 12. 13. 14. 15. 16. 17. 18. 19. 20. 21. 22.
Qur'an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Thelathini Uharamisho wa Riba Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili Hekaya za Bahlul Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.) Hijab vazi Bora Ukweli wa Shia Ithnaashari Madhambi Makuu Mbingu imenikirimu Abdallah Ibn Saba Khadijatul Kubra Utumwa Umakini katika Swala Misingi ya Maarifa Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia Bilal wa Afrika Abudharr Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu Salman Farsi Ammar Yasir 14
Msahafu wa Imam Ali 23. 24. 25. 26. 27. 28. 29. 30. 31. 32. 33. 34. 35. 36. 37. 38. 39 40. 41. 42. 43. 44. 45. 46. 47. 48. 49. 50.
Qur'an na Hadithi Elimu ya Nafsi Yajue Madhehebu ya Shia Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur'an Tukufu Al-Wahda Ponyo kutoka katika Qur'an. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii Mashukio ya Akhera Al Amali Dua Indal Ahlul Bayt Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna. Haki za wanawake katika Uislamu Mwenyeezi Mungu na sifa zake Kumswalia Mtume (s) Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) Adhana. Upendo katika Ukristo na Uislamu Tiba ya Maradhi ya Kimaadili Maana ya laana na kutukana katika Qur'ani Tukufu Kupaka juu ya khofu Kukusanya swala mbili Bismillah ni sehemu ya Qur'ani na husomwa kwa Jahara Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Kusujudu juu ya udongo Kusherehekea Maulidi Ya Mtume (s) Tarawehe Malumbano baina ya Sunni na Shia Kupunguza Swala safarini 15
Msahafu wa Imam Ali 51. 52. 53. 54. 55. 56. 57. 58. 59. 60. 61. 62. 63. 64. 65. 66. 67. 68. 69. 70. 71. 72. 73. 74. 75. 76.
Kufungua safarini Umaasumu wa Manabii Qur'an inatoa changamoto as-Salaatu Khayrun Mina -'n Nawm Uadilifu wa Masahaba Dua e Kumayl Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mtume Muhammad (s) Nahju'l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza Nahju'l-Balaghah - Juzuu ya Pili Kuzuru Makaburi Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita Tujifunze Misingi Ya Dini Sala ni Nguzo ya Dini Mikesha Ya Peshawar Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu Ubora wa Imam 'Ali Juu ya Maswahaba Na Ushia ndio njia iliyonyooka Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake Liqaa-u-llaah 16
Msahafu wa Imam Ali 77. 78. 79. 80. 81. 82. 83. 84. 85. 86. 87. 88. 89. 90. 91. 92. 93. 94. 95. 96. 97. 98. 99. 100. 101. 102 103. 104.
Muhammad (s) Mtume wa Allah Amani na Jihadi Katika Uislamu Uislamu Ulienea Vipi? Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) Urejeo (al-Raja'a ) Mazingira Utokezo (al - Badau) Hukumu ya kujenga juu ya makaburi Swala ya maiti na kumlilia maiti Uislamu na Uwingi wa Dini Mtoto mwema Adabu za Sokoni Johari za hekima kwa vijana Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu Tawasali Imam Mahdi katika Usunni na Ushia Hukumu za Mgonjwa Sadaka yenye kuendelea Msahafu wa Imam Ali Ngano ya kwamba Qur'ani imebadilishwa Idil Ghadiri Kusoma sura zenye Sijda ya wajibu Hukumu zinazomuhusu mkuu wa kazi na Mfanyakazi Huduma ya Afya katika Uislamu Sunan an-Nabii 17
Msahafu wa Imam Ali 105. 106. 107. 108. 109. 110. 111. 112. 113. 114. 115. 116. 117. 118. 119. 120. 121. 122. 123. 124. 125. 126. 127. 128. 129. 130.
Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza) Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili) Shahiid Mfiadini Kumswalia Nabii (s.a.w) Ujumbe - Sehemu ya Kwanza Ujumbe - Sehemu ya Pili Ujumbe - Sehemu ya Tatu Ujumbe - Sehemu ya Nne Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu Hadithi ya Thaqalain Maarifa ya Kiislamu Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza Ukweli uliopotea sehemu ya Pili Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu Ukweli uliopotea sehemu ya Nne Ukweli uliopotea sehemu ya Tano Safari ya kuifuata Nuru Fatima al-Zahra Myahudi wa Kimataifa Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi Visa vya kweli sehemu ya Kwanza Visa vya kweli sehemu ya Pili Muhadhara wa Maulamaa Mwanadamu na Mustakabali wake Imam Ali ('a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Kwanza) Imam Ali ('a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Pili) 18
Msahafu wa Imam Ali 131. 132. 133. 134. 135. 136. 137. 138. 139. 140. 141. 142. 143. 144. 145. 146. 147. 148. 149. 150. 151. 152 153. 154.
Khairul Bariyyah Uislamu na mafunzo ya kimalezi Vijana ni Hazina ya Uislamu. Yafaayo kijamii Tabaruku Taqiyya Vikao vya furaha Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje? Visa vya wachamungu Falsafa ya Dini Kuhuzunika na Kuomboleza - Azadari Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah Mtazamo Mpya - Wanawake katika Uislamu Kuonekana kwa Allah Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza) Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili) Ndugu na Jirani Ushia ndani ya Usunni Maswali na Majibu Mafunzo ya hukmu za ibada Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 1 Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 2 Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 3 Abu Huraira
19
Msahafu wa Imam Ali 155. 156. 157. 158. 159. 160. 161. 162. 163. 164. 165. 166. 167. 168. 169. 170. 171. 172. 173. 174. 175. 176. 177. 178. 179. 180. 181.
Vipengee kadhaa katika Swala ya Jamaa na Msikiti. Mazingatio kutoka katika Qur'an - Sehemu ya Kwanza Mazingatio kutoka kaitka Qur'an - Sehemu ya Pili Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya kwanza Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya Pili Qur'ani Tukufu - Pamoja na Tarjuma ya Kiswahili Falsafa ya Mageuzi ya Imam Husein (a.s) Amali za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani Elimu ya Tiba za Kiislamu - Matibabu ya Maimamu Uislamu Safi Majlisi za Imam Husein Majumbani Mshumaa Uislam wa Shia Amali za Makka Amali za Madina Asili ya Madhehebu katika Uislamu Sira ya Imam Ali kuhusu Waasi Ukweli uliofichika katika neno la Allah Uislamu na Mifumo ya Uchumi Umoja wa Kiislamu na Furaha Mas'ala ya Kifiqhi Jifunze kusoma Qur'ani As-Sahifatul Kamilah as-Sajjadiyyah Hayya 'Alaa Khayri'l-'Amal Katika Adhana Ukweli kuhusu Funga ya Siku ya Ashura Dua za Miezi Mitatu Mitukufu (Rajabu, Shaabani na Ramadhani) Uadilifu katika Uislamu 20
Msahafu wa Imam Ali 182. 183. 184. 185. 186. 187. 188. 189. 190. 191. 192. 193. 194. 195. 196. 197. 198. 199. 200. 201.
Mahdi katika Sunna Jihadi ya Imam Hussein ('as) Kazi na Bidii ni njia ya maendeleo Abu Talib - Jabali Imara la Imani Ujenzi na Utakaso wa Nafsi Vijana na Matarajio ya Baadaye Usalafi - Historia yake, maana yake na lengo lake Ushia - Hoja na Majibu Mateso ya Dhuria wa Mtume (saww) Maombolezo - Msiba wa Bwana wa Mashahidi (a.s.) Shahidi kwa Ajili ya Ubinadamu Takwa Amirul Muuminina ('as) na Makhalifa Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.) Kuelewa Rehma ya Mwenyezi Mungu Mtazamo kuhusu msuguano wa kimadhehebu Upotoshaji Dhahiri katika Turathi (Hazina) ya Kiislamu Nchi na Uraia - Haki na wajibu kwa Taifa Mtazamo wa Ibn Taymiyyah kwa Imam Ali (a.s.) Uongozi wa kidini - Maelekezo na utekelezaji wa Kijamii
KOPI NNE ZIFUATAZO ZIMETAFSIRIWA KWA LUGHA KINYARWANDA 1. 2. 3. 4.
Amateka Na Aba'Khalifa Nyuma yaho naje kuyoboka Amavu n'amavuko by'ubushiya Shiya na Hadithi 21
Msahafu wa Imam Ali
BACK COVER Kumekuwepo na shutuma nyingi zinazotolewa na baadhi ya Waislamu na kuzielekeza kwa Mashia. Moja ya shutuma hizo ni hii inayoitwa “Msahafu wa Imam Ali.” Suala hili limeelezwa na kutolewa ufafanuzi wa kina katika vitabu vingi vilivyoandikwa na wanazuoni wa Kishia; na wanazuoni wa Jumuiya hii ni miongoni mwa wanazuoni hao na wanazidi kulitolea ufafanuzi suala hili ili watu waondokane na dhana na upotoshaji huu wenye nia ya kuwatenganisha Waislamu. Wanachuoni hawa wamesema zamani na wanaendelea kusema sasa kwamba Qur’ain hii tuliyonayo mikononi mwetu ni ileile aliyoicha Mtukufu Mtume (saw) na si nyingine na si vinginevyo. Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 / 2127555 Barua Pepe: alitrah@yahoo.com Tovuti: www.ibn-tv-com Katika mtandao: w.w.w.alitrah.info
22
Msahafu wa Imam Ali
23