Mukhtar

Page 1

1

MUKHTAR ‫ثورة المختار‬

SHUJAA ALIYELIPIZA KISASI DHIDI YA WAUAJI WA IMAM HUSAIN (AS) HAPO KARBALA (61-67 AH)

Kimeandikwa na: Dkt. Mahmood Husein Datoo BSc, PhD, MRAeS, MIMechE, MICE

Kimetarjumiwa na Umm Zahra Gulbanu Musa

Kimehaririwa na: Sh. Mulabba Saleh Lulat

Kimepitiwa na: Mbarak. A. Tila


‫‪2‬‬

‫ترجمة‬

‫ثورة المختار‬

‫تأ ليف‬ ‫محمود بن حسين داتو‬

‫من اللغة اإلنجليزية الى اللغة السوا حلية‬


3

Jaspal bhai, when you want LOGO write to me and will send you, I think I have sent you the logo of WF but if not we can send you again.

logo of WF Uchapishaji wa kitabu hiki umewezekana kupitia msaada mkubwa wa jumuiya ya kimataifa ya The World Federation of Khoja Shia Ithna Asheri Muslim Communities�.


4

© Haki ya kunakili imehifadhiwa na: Al-Itrah Foundation ISBN No: 978 - 9987 – 17 – 059 – 3

Kimeandikwa na: Mahmood Husein Datoo BSc, PhD, MRAeS, MIMechE, MICE

Kimetarjumiwa na Umm Zahra Gulbanu Musa Kimehaririwa na: Sh. Mulabba Saleh Lulat Kimepitiwa na: Mbarak. A. Tila Kimepangwa katika Kompyuta na: Al-Itrah Foundation Toleo la kwanza: Machi, 2014 Nakala: 1000

Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. - 19701, Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 / 2127555 Barua Pepe: alitrah@yahoo.com Tovuti: www.ibn-tv-com Katika mtandao: w.w.w.alitrah.info

Kwa Kushirikiana na: The World Federation of KSIMC, Islamic Centre, Wood Lane, Stanmore, Middlesex, HA7 4LQ, United Kingdom T: +44 (0) 20 8954 9881 | F: +44 (0) 20 8954 9034 E: secretariat@world-federation.org Registered Charity in the UK No. 282303.


5

Yaliyomo Neno la Mchapishaji………………………………………………………………….00 Mukhtar ni Nani?...................................................................................00 Mukhtar Aingia Jela Mara ya Kwanza………………………………………...00 Kufungwa na Kuachwa Huru Kumayl Hamadani ……………………………00 Kumayl Afanikiwa Kumpenyezea Mukhtar Kalamu na Karatasi …………..00 Kumayl Akutana na Abdullah bin Umar ……………………………………..00 Kumayl Akutana na Yazid…………………………………………………….00 Kuachwa huru kwa Mukhtar…………………………………………………..00 Ghasia Madina………………………………………………………………….00 Kifo cha Yazid………………………………………………………………….00 Mukhtar Apata Ruhusa Kutoka kwa Imamu Zaynul-Abidin (a.s)………….00 Watu Waliotubu (Tawwabun)…………………………………………………00 Ubaydullah bin Ziyad Aikimbia Basra……………………………………….00 Ubaydullah bin Ziyad Akiwa Mjini Damascus ………………………………00 Kazi Maalum ya Tawwabun…………………………………………………………00 Mukhtar Afungwa Jela Mara ya Pili na Aachwa Huru tena ………………...00 Abdullah bin Muti Ajaribu Kumfunga Jela Mukhtar ………………………..00 Mukhtar Aungana na Ibrahim bin Malik al -Ashtar………………………….00 Mukhtar Awa Gavana wa Kufa………………………………………………..00 Mukhtar Atawala Kufa…………………………………………………………00 Abdullah bin Muti Aungana na Jeshi la Musa’ab bin Zubair ………………00 Ibrahim Al-Ashtar Akamatwa na Kutoroka………………………………….00 Kudhibiti Mji wa Mosul……………………………………………………….00 Jaribio la Kumuua Mukhtar……………………………………………………00 Mukhtar Awafuata Wauaji wa Karbala……………………………………….00 Kumsaka Ubaydullah bin Ziyad………………………………………………00 Mukhtar Auwawa……………………………………………………………….00


6

‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬

NENO LA MCHAPISHAJI Kitabu ulichonacho mikononi mwako asili yake ni cha lugha ya Kiingereza kwa jina la, Mukhtar: How He Avenged the Karbala Perpetrators (61-67 AH). Kitabu hiki kimeandikwa na Dkt. Mahmood Husein Datoo. Maudhui ya kitabu hiki yanaelezea kuhusu mtu mashuhuri sana kwa jina la Mukhtar, ambaye aliishi mjini Kufa. Wakati wa masaibu ya Karbala alikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kula kiapo cha utii kwa Imam Husain (a.s.) kupitia kwa mwakilishi wake Muslim bin Aqil, lakini kwa bahati mbaya hakuwepo Karbala. Hata hivyo, baada ya Karbala, Mukhtar alikusanya jeshi kwa ajili ya kulipa kisasi kuuliwa kwa Imam Husain (a.s.), na alifanikiwa kuwaua takriban wale vinara wote walioshiri katika kumuua kikatili mjukuu kipenzi wa Bwana Mtume (s.a.w.w.). Msomaji wetu utakaposoma kwa makini na bila chuki yoyote na mawazo pandikizi utagundua mambo mengi aliyofanya bwana mkubwa huyu mwanaharakati. Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa makubwa hususan wakati huu wa sayansi na tekinolojia kubwa ambapo ngano, hadithi za kale na upotoshaji wa historia ni vitu ambavyo havina nafasi kwa watu wa sasa. Taasisi yetu ya Al-Itrah imeona ikichapishe kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili. Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa ni chenye manufaa makubwa kwao. Shukrani zetu za dhati ziwaendee ndugu zetu wa World Federation kwa mchango wao mkubwa uliowezesha kuchapishwa kwa kitabu hiki. Allah awalipe kila la kheri na awape tawfiki katika kazi hii ya tabligh. Aidha, tunamshukuru dada yetu Umm Zahra Gulbanu Musa kwa kufanikisha tarjuma ya kitabu hiki katika lugha ya Kiswahili, pia na wale wote waliosaidia kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha chapisho la toleo hili kuchapishwa na kuwa mikononi mwa wasomaji. Allah Mwenye kujazi awalipe wote malipo mema hapa duniani na huko Akhera pia. Amin! Mchapishaji: Al-Itrah Foundation


7

‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬

Mukhtar ni Nani? Jina lake kamili ni: Mukhtar Abu Ubaida Masood Thaqafi kutoka katika kabila la Banu Hawazin. Alizaliwa mwaka wa kwanza 1 A.H. Mama yake alikuwa akiitwa Husna, (riwaya nyingine zinasema aliitwa Hilya). Baba yake aliitwa Abu Ubaida Thaqafi. Alikuwa na dada yake mmoja jina lake Safia aliyekuwa ameolewa na Abdullah bin Umar, mtoto wa khalifa wa pili Umar bin Khatab. Dada yake mwingine alikuwa mke wa Umar bin Saad, kamanda mkuu wa jeshi la Yazid huko Karbala. Mmoja wa binti zake aliolewa na Imamu Zaynul-Abidin (as) na wakapata mtoto aliyeitwa Umar. Kutokana na kazi yake maalum iliyofanikiwa ya kulipiza kisasi cha maadui wa Imam Husayn (as), zilizuka habari nyingi za kupotosha kuhusu maisha yake kwa wakati ule, mfano watu walidai anatoka katika familia duni na hafai kuheshimika n.k… bali yeye anatoka katika kabila tukufu la Banu Hawazin, ambapo pia wanatoka watu watukufu kama: - Maimuna, mke wa Mtume Muhammad (saww) - Ummul Banin – mke wa Imam Ali (as) mama wa Hadhrat Abbas, - Laila – mke wa Imamu Husayn (as) mama wa Ali Akbar, - Labid – mshairi maarufu wa Arabuni, mtunzi wa mojawapo ya mashairi saba yaliyotundikwa kwenye Kaaba. Abu Ubaida Thaqafi alikuwa daima akitamani kupata mtoto wa kiume atakayefanya tendo tukufu na la kukumbukwa duniani humu. Kwa hiyo alioa tu pindi aliposhawishika juu ya mwenza sahihi atakayemzalia mtoto kama huyo. Hivyo aliota ndoto ya kumchagua msichana aliyeitwa Husna kutoka katika familia ya watu mashujaa, wa kabila lake. Wakati Husna alipokuwa na mimba ya Mukhtar, aliota ndoto mpanda farasi akishuka kutoka juu angani anampongeza ya kwamba atazaa mtoto shujaa. Na usiku uliofuata baada ya kuzaliwa Mukhtar, Husna akaota tena ndoto mpanda farasi yule yule akishuka na kumpongeza kwa kuzaliwa haswa mtoto huyo na kwamba mtoto atapokuwa mkubwa atakuwa mfuasi shupavu wa Mtume Muhammad (saww) na kizazi chake na atalipiza kisasi cha maadui na wauwaji wa Imam Husayn (as). Abu Ubaida, baba yake Mukhtar alikuwa ni kamanda wa jeshi lililoshambulia Iran kwa amri ya Khalifa Umar bin Khattab. Majeshi ya Iran yalikuwa na tembo ambao wanajeshi wa Abu Ubaida walikuwa hawajawahi kuwaona kamwe kabla ya hapo, kwa hiyo wakawaogopa, jambo ambalo liliwaathiri katika mapambano. Lakini Abu Ubaida akapambana kishujaa na kufanya mashambulizi kwenye maeneo ya adui. Abu Ubaida akafariki katika vita hivi mwaka 13 A.H, wakati Mukhtar ana umri wa miaka 12. Kwa hiyo kaka yake Abu Ubaida akawa kamanda na akashinda vita hivi na sehemu hiyo ikawa chini ya mamlaka yake. Hivyo Mukhtar alilelewa na mama yake na ami yake. Ami yake akachaguliwa na Khalifa Umar kuwa gavana wa Madayn. Wakati wa utawala wa Muawiya, baada ya suluhu baina ya Imam Hasan (a) na Muawiyah, ami yake Mukhtar akiwa bado gavana wa Madayn, alipewa uhamisho na kuwa gavana wa Mosul.


8

(Madayn ni mahali walipozikwa Salman Farsi, Jabir Abdullah Ansari na Hudhaifa Yamani. Pia hapo Madayn ndipo ilipo Take Kisra.)

Mukhtar Aingia Jela Mara ya Kwanza Pindi Muslim bin Aqil alipowasili Kufa mwaka wa 60 A.H, akiwa ametumwa na Imamu Husayn (as) kutoka Makka, alifikia nyumbani kwa Mukhtar. Mukhtar alikuwa mtu wa kwanza kutoa heshima kubwa kwa Muslim. Mukhtar akatoka nje ya mji wa Kufa, ili kuandaa jeshi kutoka katika wafuasi wa kabila lake, ambalo litamuunga mkono Muslim bin Aqil ambaye anamwakilisha Imamu Husayn (as). Baada ya Ubaydullah bin Ziyad kuwasili Kufa na baada ya matatizo yaliyotokea, Muslim bin Aqil akahamia nyumbani kwa Hani bin Urwa ambapo alifuatiliwa na baadaye kukamatwa na kuchinjwa hadharani kwa amri ya Ubaydullah bin Ziyad. Mukhtar alikuwa angali bado nje ya mji wa Kufa wakati Muslim bin Aqil anauawa; na wakati akiwa njiani yeye na watu wake wanarejea Kufa ndipo alipata habari za machafuko yanayoendelea mjini Kufa. Alikutana na wasafiri waliotoka Kufa na akapata habari ya kuchinjwa kwa Muslim bin Aqil. Alipigana pia na waliokua wanamzuia njiani waliotumwa na Ubaydullah bin Ziyad na kuwaua baadhi yao. Mukhtar alitawanya jeshi lake lililokuwa limekusanyika pamoja na kulinyang’anya silaha na kuchukua hatua ya kidiplomasia ya kujiunga na Umar Harith (Afisa wa serikali) aliyewekwa nje kidogo tu ya mipaka ya mji wa Kufa, na kuwahakikishia usalama watu ambao mwanzoni walimuunga mkono Muslim bin Aqil lakini sasa hawatasimama dhidi ya Ubaydullah bin Ziyad. Machifu wa Kufa waliitwa katika baraza ya Ubaydullah bin Ziyad na Mukhtar akiwa ni mmoja wao. Mojawapo ya riwaya inasema ya kwamba Mukhtar hakumsalimia Ubaydullah bin Ziyad na hivyo walinzi wake walimpiga hadi jicho lake likavia damu, bali habari nyingine zinasema Mukhtar alimsalimia lakini Ubaydullah alimdharau hivyo hakujibu salaam yake. Mukhtar aulizwa na Ubaydullah ni kwa sababu gani katoa kiapo cha utii kwa Muslim na kwa nini mwanzoni alimpokea na kumruhusu kufikia nyumbani kwake; kisha alimuuliza kwa nini alitawanya wafuasi wake baada ya kupata taarifa ya mauaji ya Muslim bin Aqil? Ndipo Umar Haris akatoa ushahidi kwamba Mukhtar alijisalimisha peke yake bila ya kuwa na wafuasi wowote. Wajane wa askari wazuia-njia waliouliwa na Mukhtar waliwasili kortini. Mukhtar akaulizwa kwa nini amewauwa askari wa Ubaydullah na sio askari mmoja bali kati ya ishirini hadi thelathini ikiwa kweli dhamira yake ilikuwa nzuri? Ndipo Ubaydullah akaamuru Mukhtar afungwe jela kwa kosa la kuwaua askari wake na pia kumpokea na kumsaidia Muslim Aqil. Mukhtar alifungwa katika gereza la chini ya ardhi pamoja na wafungwa wengine Mashia wapatao elfu nne au tano waliokuwa tayari ndani ya jela hiyo. (Ilikuwa ni dhamira ya Muslim bin Aqii kuwakomboa wafungwa hao). Jela hiyo ilikuwa ina urefu takriban wa futi 75 chini ya usawa wa ardhi. Mukhtar alifungwa pingu mikononi na kiunoni, miguu yake ikafungwa kwenye chuma la mzinga linalohitaji watu ishirini kulinyanyua. Jela hiyo ilikuwa ina giza sana chini ya ardhi, haina mwanga na ina hewa kidogo. Mukhtar aliamuriwa kukaa kwenye kona mbali ili asipate hewa mpya kutoka mlangoni. Chakula chake kilikuwa na lishe duni, na jela ilikuwa inalindwa usiku na mchana na askari arubaini kwa zamu.


9

Siku ya mauaji ya Ashura Mukhtar alikuwa ndani ya jela ya Kufa, lakini alitolewa kushuhudia kuwasili kwa vichwa vya mashahidi na walionusurika katika korti ya Ubaydullah bin Ziyad. Hapo ndipo alipojiapiza mwenyewe kwamba hatapumzika hadi atakapolipiza kisasi dhidi ya wahalifu wa Karbala. Ndani ya jela Mukhtar alikutana na Maytham Tammar, sahaba mkubwa na wa karibu wa Imam Ali (as), ambaye alifundishwa na Imam elimu ya kutabiri matukio yatakayotokea baadaye (ulumul balaya wal manaya). Maytham akamtabiria kuwa atafunguliwa na atatimiza nia yake ya kulipiza kisasi dhidi ya wauwaji na maadui wa Imam Husayn (as).

Kufungwa na Kuachwa Huru Kumayl Hamadani 1 Kumayl Hamadani (vyanzo vingine vimemwita Kathir Hamadani) alikuwa na umri wa miaka 70-80 katika mwaka wa 60 AH. Alikuwa mwalimu wa madrasa huko Kufa, aliyefundisha Qur’ani kwa watu wengi toka enzi za Imam Ali (as). Alikuwa mfuasi thabiti sana wa kizazi cha Mtume lakini alikuwa anaficha imani yake kama walivyokuwa wengine wengi kwa sababu za hali ya kisiasa ya wakati ule. Siku moja, akiwa anafundisha, Kumayl akapatwa na kiu (ukizingatia umri, hali ya joto ya mji wa Kufa na kazi yake ya kuongea kutwa), na alipopita muuza maji akanunua maji. Kabla hajayanywa akawakumbuka mashahidi wa Karbala, na kwa sauti kubwa, akawalaani wauaji wa Imam Husayn (as). Miongoni mwa watoto waliokuwepo darasani humo ni mtoto wa Sinan. Yeye alimpinga mwalimu wake na kusema kwamba wauaji walimfanyia fadhila Yazid na serikali yake. Baada ya masomo, kijana huyo akiwa njiani alijipiga mwenyewe na jiwe hadi akatokwa na damu na kisha akachana nguo zake. Alipofika nyumbani mama yake akamuuliza sababu ya kutoka damu, mtoto akasema mwalimu amempiga kwa sababu amempinga kwa tendo lake la kumlaani baba yangu Sinan na Yazid. Mama yake akakasirika na kumshitakia Sinan na kumtaka lazima alipize kisasi mara moja, na kusema vipi mwalimu huyu yupo chini ya serikali yetu kisha anafanya chuki dhidi yetu? Sinan mara moja alikwenda kwa Ubaydullah bin Ziyad na hatimaye Kumayl akaitwa. Kumayl akajitetea kwamba hakumdhuru mtoto yule, lakini Ubaydullah akachagua kumwamini mtoto yule na akamfunga Kumayl jela, ndani ya jela ile ile walimofungwa Mashia na Mukhtar. Kumayl akakutana na Mukhtar, Mukhtar akamwambia Kumayl kwamba alikuwa anasubiri kuja kwake yeye kama ilivyotabiriwa na Maytham Tammar. Kumayl alikuwa na hofu kwa kufungwa jela lakini Mukhtar akamtoa wasiwasi akamwambia kuwa ataachiwa huru na atamsaidia yeye (Mukhtar) kutoka jela kama alivyobashiri Maytham Tammar. Sasa, mmoja wa wapwa wa Kumayl aliyeitwa Bostan alikuwa ni yaya wa mjukuu wa Ubaydullah bin Ziyad (mtoto wa binti ya Ubaydullah), naye alimsihi sana binti yake Ubaydullah atumie umaarufu wake kufanya ami yake (Kumayl) atolewe gerezani kwa kosa la kusingiziwa kumpiga mtoto wa Sinan. Jioni hiyo, binti huyu alikwenda kwa baba yake Ubaydullah na akamwambia kuwa yaya wake ni mpwa wake Kumayl, na Kumayl ni mzee, dhaifu na mtu mwema ambaye watu wa mji wa Kufa wana deni la shukurani kwa mafunzo yake. Ubaydullah akakubali kumwacha huru siku itakayofuata, lakini binti yake akang’ang’ania aachiwe jioni hiyo hiyo, akasema atakwenda yeye mwenyewe huko jela kuwasilisha amri hiyo ili kuhakikisha anaachwa huru.

1

Huyu si yule Kumayl bin Ziyad maarufu wa Du’a Kumayl.


10

Kwa kuwa ilikuwa ni kawaida walinzi kubadilishana kwa ajili ya zamu ya usiku, na kwa kuwa katika jioni hiyo ilikuwa Kumayl aachiwe huru kama alivyoambiwa na Mukhtar kwa utabiri wa Maytham Tammar, Kumayl alikata tamaa, kwa sababu baada ya jioni kuingia na kubadilishana zamu milango ya jela haifunguliwi hadi kesho yake, lakini Mukhtar alimpa moyo na kumtaka aamini bishara ya Maytham. Na ni jioni hiyo hiyo, ambapo binti yake Ubaydullah alifika na amri ya kuachiwa huru kwa Kumayl. Kumayl akamuaga Mukhtar, ambapo Mukhtar akamuomba atafute njia ya kumletea kalamu na karatasi, Kumayl akamuahidi kufanya hivyo.

Kumayl Afanikiwa Kumpenyezea Mukhtar Kalamu na Karatasi Baada ya kufunguliwa jela, Kumayl akaonywa na Ubaydullah bin Ziyad asirudie tena kosa la jinai la kumlaani Yazid na serikali yake. Kumayl akaahidi kuishi maisha ya kimya na kutoendelea kufundisha madrasah. Kumayl akafikiria mpango wa namna ya kuingiza kinyemela karatasi na kalamu huko jela kwa Mukhtar huku akitambua kuwa usiri ni suala muhimu, na ikiwa Ubaydullah atashuku chochote basi atabeba dhima ya kosa hilo, hivyo alimweleza mpango mzima mke wake, ambaye pia alikuwa mfuasi mkereketwa wa Ahlulbayt, na hivyo mke wake alimsaidia (vyanzo vingine vinasema alimtaliki mke wake ili kuzingatia usiri kamili wa harakati zake). Katika mikakati ya mpango huo ilikuwa ni pamoja na kufanya urafiki na mkuu wa jela, hivyo jioni hiyo akatayarisha chakula kizuri pamoja na pesa na kwenda nyumbani kwa mkuu huyo. Mkuu huyo alikuwa yupo kazini zamu ya usiku, Kumayl akamwambia mke wa mkuu huyo kuwa ameleta zawadi kwa mumewe kwa sababu aliweka nadhiri ya kufanya hivyo ikiwa ataachiwa huru. Hivyo asubuhi, Mkuu wa jela aliporudi, mkewe alimpa zawadi hizo. Mkuu wa jela akaelewa mara moja kwamba Kumayl anatafuta ihsani fulani. Usiku wa pili akafanya hivyo hivyo. Usiku wa tatu akamkuta Mkuu wa jela nyumbani. Akamuuliza Kumayl nia yake kwa kuwa hakuamini habari ya nadhiri, na mwishowe, Mkuu wa jela akakiri kwa mapenzi ya Ahlulbayt kwamba kama kweli Kumayl anataka kumsaidia Mukhtar, basi yeye yutayari kusaidia. Kumayl akafarijika akijua kwamba Mkuu wa jela anamuonea huruma Mukhtar. Kwa hivyo akamueleza nia yake ya kumpenyezea Mukhtar kalamu, karatasi na wino kinyemela, hivyo Mkuu wa jela akapanga mpango: -

Anasema katika jela kuna jumla ya walinzi 40 na yeye ndiye mkubwa wao, lakini walinzi wote wamechaguliwa kwa uangalifu, kila mmoja ana chuki na mwenzake, ili kudhibiti uzembe na kutowajibika katika ulinzi unaosababishwa na rushwa, kujuana, n.k. Walinzi wote wanaripoti moja kwa moja kwa Ubaydullah bin Ziyad. -

Mkuu wa jela akamshauri Kumayl aandae chakula kizuri na kitamu (kama jinsi mila ya Waarabu ilivyo), anunue matunda na badam (almonds). Katika tunda moja afiche kalamu, tunda lingine afiche karatasi nyembamba ndogo, na katika badam maalum afiche wino, matunda hayo yawekwe alama, ili Mkuu huyo atambue yapi yapelekwe kwa Mukhtar. -

Mkuu huyo akamwambia Kumayl: Utaleta chakula hicho nitakapokuwa kwenye zamu na ueleze nadhiri yako ya kuwalisha wafungwa baada ya wewe kufunguliwa jela. Nitakuonyesha hisia zangu za hasira na kukupiga kwa nguvu na ukatili, hadi walinzi wengine watakuonea


11

huruma (ambao watakwenda kinyume na matakwa yangu ya dhahiri, kama tunavyopingana siku zote) kama mwalimu mzee, dhaifu, mkweli ambaye ameamua kuleta chakula kizuri ili kutimiza nadhiri yake. Kwa kufanya hivyo itaonekana wazi mimi ni adui yako sipo pamoja na wewe. Walinzi wengine watakapokuruhusu kuingiza chakula, nitahakikisha Mukhtar anapata chakula kile kilichowekwa alama. Siku iliyofuata Kumayl akatayarisha chakula na kwenda jela, na kila kitu kikaenda kama kilivyopangwa. Mkuu wa jela akawaonya walinzi wa chini yake kuwa Ubaydullah anaweza kutopenda mzee huyo agawe chakula. Lakini walinzi hao hawakuona ubaya wowote hasa baada ya Mkuu huyo kumpiga Kumayl. Chakula kikaingizwa ndani ya jela na Mukhtar akapewa kile kilichotiwa alama, na akafanikiwa kukificha vizuri kwani mara tu akawasili hapo Ubaidullah na akiwa na walinzi binafsi takriban thelathini (vyanzo vingine vinasema kwamba Ubaydullah na walinzi binafsi wake waliwasili kabla tu ya chakula hicho kuingizwa ndani ya jela). Ubaydullah akatoa amri walinzi wote arobaini wa jela wapigwe vikali bila huruma kabisa. Baadaye walinzi pamoja na mkubwa wao, wakauliza kwa nini Ubaydullah amekuja ghafla na kuamuru waadhibiwe. Ubaydullah akasema anajua njama zao za kumpenyezea Mukhtar kalamu na karatasi. Akitegemea jema kwa dua, Mkuu wa jela akakanusha na akamtaka Ubaydullah aonyeshe kalamu na karatasi yoyote kwenye chakula kile. Walinzi wake wakafanya upekuzi makini kwenye vyakula vyote na hawakupata chochote, kwani Mukhtar alifanikiwa kukificha chakula kile, (riwaya nyingine zinasema hawakufikiria kutazama ndani ya matunda). Kwa kujibiwa dua ya mkuu wa jela, na baada ya kukosekana ushahidi wowote wa kuwepo kalamu na karatasi, Mkuu wa jela akamuuliza Ubaydullah amepataje habari zile za uongo. Ubaydullah akasema ni mtoto wa Mkuu wa jela ndiye aliyepeleka habari hizo. (Mtoto alisikia mazungumzo baina ya Kumayl na baba yake, lakini maelezo ya mwisho kuhusu kuficha wapi karatasi na kalamu hakuyasikia, kwani walikuwa wananong’ona kuhofia wasiwasikie watu waliokuwa wanaelekea msikitini kwa sala ya asubuhi. Mkuu wa jela akaeleza kuwa mtoto huyo sio wake wa kumzaa, bali alikuwa mtoto wa mitaani aliyetelekezwa, naye akamchukua na kumlea. Lakini katika jitihada zake za kumfundisha tabia njema na kumuadabisha, mtoto huyo alijenga chuki dhidi yake na kwa sababu hiyo akaleta ripoti za uongo na kumpotezea muda Ubaydullah bin Ziyad. Ubaydullah bin Ziyad akakasirika sana na akaamuru mtoto auawe mara moja. Ubaydullah bin Ziyad na walinzi wake wakaondoka, Kumayl akaenda nyumbani na Mukhtar akapata kalamu, karatasi na wino.

Kumayl Akutana na Abdullah bin Umar Mukhtar akiwa ndani ya jela ya mji wa Kufa, aliandika barua mbili: moja kwa dada yake Safia na nyingine kwa mume wa dada yake, Abdullah bin Umar wote wakiwa wapo Madina. Barua inaelezea kufungwa kwake jela na hali mbaya ya mateso ya jela hiyo, na akamuomba Abdullah bin Umar atumie umaarufu wake ili aweze kuachiwa huru. (Abdullah bin Umar, mtoto wa Khalifa Umar bin Khattab, alikuwa maarufu, anajulikana sana na alikuwa anaheshimiwa na watu na Makka, Syria, na Kufa).


12

Mukhtar alimpa barua zile Mkuu wa jela na yeye akazipeleka kwa Kumayl. Kumayl akafikiria njia ya kufika Madina bila ya Ubaydullah kukisia kuna njama yeyote kwani Ubaydullah alikuwa anajua wazi umaarufu wa Abdullah bin Umar (shemeji yake Mukhtar) kwa Yazid kwamba anaweza kumshinikiza amuachie huru Mukhtar, na kwa sababu hiyo, Ubaydullah hakutaka habari za kufungwa Mukhtar zijulikane. Kumayl akaamua kuondoka huku akiwa amepata baraka za Ubaydullah akihofia asije kukamatwa akiwa nje ya mji wa Kufa na hivyo akalazimika kurudishwa jela tena, vilevile ilikuwepo hali ya tahadhari katika mji wa Kufa, hivyo ilihitajika kibali cha kutoka nje ya mji. Kumayl alivaa Ihram yake akaenda kwenye hadhara ya Ubaydullah ambapo alisoma talbiya kwa sauti: Labaikallahuma Labaik… Ubaydullah akauliza nani anasoma talbiya wakati siyo msimu wa Hija? Akaambiwa ni Kumayl ambaye pia anataka kukuona. Kumayl akamwambia Ubaydullah bin Ziyad kwamba aliweka nadhiri kwenda Umrah baada ya kuachiwa huru. Lakini Ubaydullah akatia shaka, hasa alipokumbuka nadhiri ya kuwalisha wafungwa na hivyo kumuuliza ameweka nadhiri ngapi? Na akamuuliza kama nia yake ni kwenda Makka peke yake au na Madina pia. Kumayl hakuweza kusema Madina kwani angesema hivyo asingepewa kamwe ruhusa ya kuondoka. Akamjibu kwamba nia yake ni kutekeleza “Mukkamal Hajj” ikimaanisha kuzuru kaburi la Mtume huko Madina. Ubaydullah bin Ziyad hakuelewa maana ya jibu la Kumayl na anamruhusu kwa baraka zake kwa kuamini kwamba anamaanisha kwenda Makka pekee. Kumayl akaondoka Kufa lakini badala ya kwenda Makka akaenda moja kwa moja Madina kukutana na Abdullah bin Umar. Akafika hapo wakati chakula cha mchana chenye hadhi ya Abdullah bin Umar kimeandaliwa. Bi Safiya, mke wa Abdullah bin Umar, alikuwa akikataa kushiriki vyakula vya mchana vizuri kama kile kwa kukosa habari za kaka yake, Mukhtar. Kwa kusikia kwamba kuna msafiri kutoka mji wa Kufa, Bi Safiya akamhimiza mume wake kukutana naye ili huenda watapata habari za Mukhtar. Kumayl akajitambulisha kwa Abdullah bin Umar, kisha akatoa zile barua mbili kutoka kwa Mukhtar. Safiya aliposoma barua alihuzunika sana na akauliza habari zaidi kuhusu hali ya kaka yake Mukhtar moja kwa moja kutoka kwa Kumayl. Kumayl akamuelezea hali mbaya aliyonayo Mukhtar na jinsi Mukhtar anavyotarajia kuweza kuachiliwa haraka ili kulipa kisasi cha wauwaji wa Imam Husayn (as). Kutokana na huzuni na masikitiko yake, Bi Safiya akapandwa na hasira, akakata nywele za sehemu ya kichwa chake (kama ilivyokuwa mila ya wakati ule kwa kuashiria huzuni kubwa). Mabinti zake pia wakafanya vivyo walipoona huzuni ya mama yao. Safiya akamwambia mume wake Abdullah bin Umar aandike barua kwa Yazid huko Damascus, atoe amri ya kuachiwa Mukhtar kutoka jela. Abdullah bin Umar akakubali na Kumayl akajitolea kusafiri mara moja kwenda Damascus na kukabidhi barua kwa Yazid. Abdullah bin Umar alimpa Kumayl barua na mkoba uliokuwa na nywele za Safiya kama uthibitisho wa huzuni ya mkewe. Na barua ilisema: Mfungue Mukhtar kutoka jela ya mji wa Kufa, ama sivyo Abdullah bin Umar atatumia umaarufu wake kuhujumu serikali ya Yaziid katika sehemu zote ambazo yeye Abdullah bin Umar alikuwa na uwezo wa kufanya hivyo.

Kumayl Akutana na Yazid


13

Kumayl aliingia kwenye mipaka ya Syria na akaenda moja kwa moja hadi mji wa Damascus, na akapanga chumba katika nyumba ya mfanyabiashara mmoja wa duka . Kutokana na hali ya kisiasa ya wakati ule, Mashia walikuwa hawawezi kujitokeza, kwa hiyo Kumayl ilibidi awe m wangalifu ili isijulikane sababu ya yeye kuwepo Damascus. Alikuwa akipita kila siku kwenye Ikulu ya Yazid kwa matumaini ya uwezekano wa kuingia ndani, lakini alikuwa anazuiliwa na walinzi, iliendelea hivi kwa muda wa siku kumi na nane, alikuwa anahudhuria msikitini kila siku na a kiwaomba Waumini wenzie wamuombee dua ili haja zake - bila ya kuzitaja - zikidhiwe na kutimizwa. Siku ya kumi na nane, Imam wa msikiti (vyanzo vingine vinasema alikuwa ni yule bwana muuza duka aliyempangisha chumba) akamuuliza Kumayl sababu na lengo la ziara yake kwani kwa siku ya kumi na nane zilizopita amekuwa akijaribu kuingia Ikulu ya Yazid? Kumayl alikuwa mwenye hofu sana na ni baada ya kuthibitisha tu kwamba huyo Imam wa msikiti ana huruma na Mashia akamueleza kwamba ana ujumbe binafsi kwa Yazid kutoka kwa Abdullah bin Umar unaomuhusu Mukhtar huko Kufa. Imamu huyo akamwambia atamuelekeza njia ya kufika ndani ya Ikulu ya Yazid kwa kuwa lengo la ziara yake ni kulipiza kisasi dhidi ya wauwaji wa Imamu Husayn (as), na akasema vilevile kwamba angemuambia hivi Kumayl mapema kama angemuamini tangu mwanzo. Imamu wa msikiti akamwambia Kumayl: Ndani ya Ikulu ya Yazid kuna msaidizi wake wa ndani ambaye ni Shia, ambaye unapaswa kumuona huyo ili kuweza kukutana na Yazid. Tangu mauaji ya Karbala yalipotokea huyu msaidizi wake kila siku anavaa mavazi meusi, anaomboleza kila siku na hachukui mshahara kwa Yazid bali mapato yake anayapata kutokana na ufumaji. Unatakiwa umuone huyu kwani Yazid alimuahidi atatimiza haja yake moja katika maisha , haja ambayo hadi sasa bado hajamuomba. Na kama haja yako inahusiana na Imam u Husayn (as) bila shaka mtu huyu atamuomba Yazid aitimize haja hiyo. Swali: Kwa nini Yazid akubali Shia wa dhahiri kama huyo kubakia hapo pamoja naye? – Shahrbanu mke wa kwanza wa Imamu Husayn (as) alikuwa mtoto wa Mfalme aliyeletwa kutoka Iran baada ya ushindi wa vita, na alikuja na wafanyakazi wake na miongoni mwa wafanyakazi hao alikuwa ni Hinda. Zama za uhai wa Shahrbanu, Hinda alikuwa anaishi naye, lakini baada ya kufariki Shahrbanu, Imam Husayn (as) akawaruhusu wafanyakazi wote wa mkewe kuondoka isipokuwa mmoja tu aliyekuwa anamlea Imam Zaynul-Abidin (as) (ambaye alikuwa na umri wa chini ya miaka miwili kwa wakati ule). Hinda alikuwa mzuri sana na mrembo. Yazid alivutiwa naye sana, pamoja na kujua kwamba Hinda hampendi, Yazid akataka kumuoa lakini Hinda akakataa katakata. Akalazimishwa kuolewa na Yazid. (Ni yule yule Hinda aliyewazuru mateka wa Karbala katika jela ya Damascus na kugundua ya kwamba ni Ahlulbayt na sio waasi wa kawaida kama alivyosema Yazid). Hinda alikuwa na watumishi/wasaidizi wake na mmoja wao ndiye huyu ambaye Kumayl anatakiwa aonane na ye. Yazid alimchukua msaidizi huyu wa Hinda, na


14

akamuahidi kutimiza haja yake moja, yoyote ile kwa ajili ya mapenzi yake kwa Hinda. Kwa hiyo Kumayl alipaswa kumuona mtu huyu ndani ya kasri la Yazid na Imam akamuelewesha jinsi ya kuingia ndani ya Ikulu hadi kukutana na huyu msaidizi katika Ikulu ya Yazid. Kumayl alitakiwa apite vizuizi vingi vya usalama kwa kujiamini na kujifanya kama vile ni mwenyeji na anayefahamu njia yake. Imamu wa msikiti akamuelekeza Kumayl yafuatayo: -

Vaa kikamilifu mavazi meupe, kwani hayo ndiyo mavazi ya watu wenye ruhusa kuingia ndani ya Ikulu ya Yazid.

-

Ukifika Ikulu usisite kwenye lango kuu, (vyanzo vingine vinasema ni ilikuwa ni njia ya kuingilia ya pembeni ya yule muuza duka) bali endelea mbele kama vile unajua njia na ni mwenyeji unayekuja mara kwa mara. Ndani ya uwanja wa kwanza, kuna askari wa farasi wapatao elfu moja; tembea kwa kujiamini na usijibu swali lolote kutoka kwa walinzi hawa, kwa sababu watumishi walioruhusiwa huwa hawajibu lolote.

-

-

Ndani ya uwanja wa pili, patakuwa na askari wa farasi zaidi, tembea kwa kujiamini.

-

Ndani ya uwanja wa tatu, bado utakuta wapo wanafarasi wengi zaidi, tembea kwa kujiamini.

-

Ndani ya uwanja wa nne, kuna askari watano waliopanda farasi watakuwa wanalinda lango la kuingia katika uwanja wa ndani kabisa wa Yazid. Tembea kwa kujiamini.

-

Ndani ya ukumbi wa tano, watakuwepo askari wengi zaidi, tembea kwa kujiamini.

-

Ndani ya ukumbi wa sita, utakuta ofisi kuna watu wengi wanafanya kazi zao za utawala, tembea kwa kujiamini.

-

Katika ukumbi wa saba, kila upande, kuna chumba kirefu chembamba, kimesakafiwa kwa marumaru na dhahabu, glasi za vito vya thamani zimejazwa pombe. Utakuta watu watatu kila upande wamekaa wanastarehe. Hawa watu sita wanaitwa “Tashtiya� kwa kuwa walibeba binafsi yao wenyewe lile sinia lililowekwa juu yake kichwa cha Imam Husayn (a.s) hatimae kulifikisha kwa Yazid, kwa hiyo Yazid anawaruhusu kustarehe muda wote hapo kama malipo yao. Ukifika hapo tembea kwa kujiamini.

-

Ndani ya ukumbi wa nane, mara nyingine tena vipo vyumba virefu viwili kila upande, vimepambwa zaidi kuliko vile vya ukumbi wa saba. Hapo kila kitu kimepambwa kwa vito vya thamani na dhahabu. Hakutokuwepo na mtu pale, usisimame kutazama uzuri, kwani mtu yeyote anayesimama kushangaa ni kwamba ni mgeni anapita kwa mara ya kwanza. Kwa hiyo ataulizwa na walinzi wa usalama ambao wamejificha. Pita hapo kwa kujiamini.


15 -

Ndani ya ukumbi wa tisa, uko tupu usiyo na pambo lolote. Hii ni kuweka hali tofauti na ile ya kumbi nyingine zilizopambwa. Usisimame kwa kushangaa kwani hali hiyo ya tofauti, ni mtego kwa mgeni anayefika kwa mara ya kwanza. Tembea kwa kujiamini bila kusimama.

-

Ndani ya ukumbi wa 10, utakutana na mtu aliyevaa nguo nyeusi tupu, huyu ndiye huyo (msaidizi wa Hinda - mkewe Yazid) ambaye unatakiwa ukutane naye.

Siku iliyofuata Kumayl akaenda Ikulu ya Yazid akafuata maelekezo yote ya Imamu wa msikiti, akapita kumbi zote tisa hadi wa kumi akakutana na huyo mtu aliyevaa mavazi meusi. Huyu mtu akamsalimia Kumayl kwa kutaja jina lake na akamwambia alikuwa akisubiri kwa muda wa siku 18 kukutana naye. Kumayl mara akashikwa na wasiwasi akifikiri kwamba ni mtego na kwamba tambulisho wake umejulikana. Kumayl akamuuliza bwana huyu amejuaje jina lake na kwamba alikuwa yupo mjini humo Damascus kwa siku kumi na nane. Huyu mtu akamwambia: siku kumi na nane zilizopita, Imamu Husayn (as) alinijia katika ndoto akanijulisha kuwa mwalimu anayeitwa Kumayl anatoka Kufa atakuja na ombi lake ambalo napaswa kuliheshimu kwani linahusika na kulipiza kisasi kwa wahalifu wa Karbala. Pia Imamu Husayn (as) alinijia ndani ya ndoto usiku wa kuamkia leo na kunifahamisha kwamba utafika leo hii na pia nikufikishie shukrani zake kwako na kwangu pia kwa kazi inayofanyika. Wakati huo, watu wapatao mia moja walipita na harufu nzuri ya manukato na ubani mbalimbali ili kuinukisha hewa ya njia ya kuelekea bafuni ambako Yazid amepangiwa kwenda kuoga. Walifuatiwa na vijana waliovaa nguo za dhahabu. Hawa vijana walifuatiwa na walinzi mahsusi wa Yazid. Kisha Yazid akifuata kwa madaha akiwa amevalia taji la dhahabu, ameshika bakora ya dhahabu na kavaa viatu vya dhahabu vilivyopambwa na vito vya thamani. Msaidizi wa Hinda akaenda kwa Yazid na kumwambia kwamba wakati umefika sasa kwa ajili ya kutimiziwa ile haja yake moja (kama walivyoahidiana). Haja yenyewe ni kukutana na mtu aliyetokea Kufa ambaye ana ujumbe kutoka kwa Abdullah bin Umar kutoka Madina. Kumayl akakabidhi ile barua na mkoba uliokuwa na mikia ya nywele za Safia. Yazid akamuuliza Kumayl wewe ni nani? Wewe ni Shia? Je una chuki yoyote na watu waliomuua Imamu Husayn (as)? Kumayl akaogopa, lakini msaidizi wa Hinda akaingilia kati na kumsaidia kwa kusema kwamba maswali yote hayo hayana maana yoyote kwenye haja yake moja. Yazid akaagiza kalamu na karatasi na akamwandikia Ubaydullah Bin Ziyad huko Kufa hukumu ya kumwachia huru Mukhtar kutoka ndani ya jela mara tu atakapopokea amri hiyo. Barua akakabidhiwa Kumayl, Yazid akamwambia msaidizi wa Hinda ningekuwa radhi kukupa kiasi chochote cha pesa kama ingekuwa ndio haja yako, lakini kwa ahadi yangu juu mapenzi yangu kwa Hinda, pamoja na vitisho vya Abdullah bin Umar kuchochea ghasia katika milki yangu, nimelazimika kutoa hii hukumu ambayo naelewa itasababisha kuanguka kwa utawala wangu. Kumayl haraka akarejea chumbani kwake alipokuwa amepanga akakusanya vitu vyake akaenda moja kwa moja Madina kwa Abdullah bin Umar. Akamjulisha kuhusu amri aliyotoa Yazid lakini Abdullah bin Umar hakumwambia mkewe Safiya, kwa kuhofia iwapo kama Mukhtar hataachwa huru na Ubaydallah bin Ziyad, Safiya akaja kuvunjika moyo zaidi.


16

Kuachwa huru kwa Mukhtar Kumayl alisafiri kutoka Madina na kuelekea Kufa na njiani huku akiwa ana wasiwasi kwamba huenda Ubaydullah bin Ziyad alipata fununu jinsi mipango inavyoendelea, na hivyo amewatuma askari wake wamuue ili kumzuwia kufikisha hukumu ya kuachwa huru Mukhtar. Karibu na kuingia lango kuu la mji wa Kufa, Kumayl akajifunika kichwa chake (kama ilivyokuwa ada kujilinda na upepo wa jangwani), na kuendesha farasi wake kwa kasi kama vile kijana ili kuwakwepa maaskari kama wangelikuwa wamepewa amri ya kumsubiri mtu mzee. Hatimae Kumayl akafika kwenye hadhara ya Ubaydallah bin Ziyad na kukabidhi barua kutoka kwa Yazid. Ubaydallah alisoma hukumu iliyomtaka amwache huru Mukhtar hivyo akamwacha huru japokuwa alijua kumwacha huru kutasababisha kuanguka kwa utawala wake na kuuwawa, lakini alikuwa hana budi kutii amri ya Yazid. Mfua vyuma akaamuriwa akate nyororo alizofungwa Mukhtar. Akatibiwa majereha yake na daktari kisha akapelekwa kwa Ubaydullah Ziyad (inasemekana jicho lake moja lilipofuka akiwa kifungoni baada ya kupigwa na walinzi wa Ubaydallah kwa kukataa kumsalimu Ubaydallah mbele ya machifu wengine). Ubaydullah akamwamuru Mukhtar aondoke Kufa ndani ya siku tatu au atamfunga jela tena. Mukhtar akamshauri Kumayl kwamba ni vyema na yeye pia aondoke ndani ya mji wa Kufa kwa hiyo wote wakaondoka Kufa siku iliyofuata. Mukhtar akamwambia Kumayl mpango wake wa kuandaa jeshi la kulipa kisasi kwa wauwaji wa Karbala. Waliachana nje ya mji wa Kufa, Kumayl akaenda kwa watu wa kabila lake Bani Kanda na Mukhtar akaelekea Madina. Mukhtar aliwasili nyumbani kwa Abdullah bin Umar na akukutana na dada yake Safiya. (Kwa maoni yangu: Mukhtari ameachiwa huru mwishoni mwa mwaka 61 A.H./au mapema sana mwaka wa 62 A.H. kwani kama wasalimika wa Karbala wangekuwa wapo Madina baada ya Arobaini ya mwaka 62 A.H. kwa hakika Mukhtari angewatembelea). Kaka na dada walikuwa na furaha isiyo na kifani kwa kule kuungana tena. Furaha ya Safiya ilizidi kiwango hadi akazimia na hakupata fahamu tena, akafariki. Mukhtar akaondoka na akaanza kupanga mipango ya kulipa kisasi cha wauwaji wa Karbala, akaenda Makka kukutana na Abdullah bin Zubair. - Abdullah bin Zubair alikuwa ni miongoni mwa watu watatu mashuhuri waliokataa kumpa kiapo cha utii Yazid. Wengine ni Imamu Husayn (as) na Abdullah bin Umar. - Abdullah bin Zubair alikuwa Makka kwa nia ya kuchukua madaraka, kwa hiyo alikuwa anawachochea watu wa Madina na Makka kuasi dhidi ya Yazid kwa kisingizio cha huruma juu ya mauaji ya Imam Husayn (as) huku akijitangaza kwamba yeye ana uhusiano na Mtume Muhammad (saww) (ama kwa hakika alikuwa na uhusiano kupitia bibi Khadija kwani babu yake Abdullah bin Zubair alikuwa ni kaka yake na Bibi Khadija). Mukhtar akaona kuwa Abdullah bin Zubair pia anaonekana kama anataka kulipa kisasi cha wauwaji wa Imamu Husayn (as), hivyo akamtaka Abdullah bin Zubair waunde jeshi kulipiza kisasi cha wauwaji wa Imamu Husayn (as), lakini hakutoa ushirikiano. Mukhtar alipong’amua


17

kwamba hakuna msaada hapo, akaamua kuondoka Makka hadi Taif kwa watu wa kabila lake. Alikaa huko kwa mwaka mmoja huku akipanga namna ya kufanikisha mpango wake.

Ghasia Madina Mnamo mwaka 62 AH, baada ya msafara wa walionusurika kutoka Karbala kurejea Madina, kamati iliundwa ya kuchunguza mauaji ya Karbala. Kamati hii iliyokuwa na watu mashuhuri wa Madina ilimjumuisha Amir bin Zubair (kaka yake Abdullah bin Zubair) na Abdullah bin Hanzala. Kamati ilikwenda Damascus kuchunguza na ikatoa taarifa kuhusu tabia ya umaluuni ya Yazid kwamba ni mhuni wa kupindukia, mlevi, mcheza kamari, anakanusha wazi wazi Sharia za Kiislamu. Kamati ilipewa rushwa kubwa ili isitoe taarifa mbaya, lakini walikataa rushwa na wakatoa ripoti kama ukweli ulivyo. Mahitimisho ya kamati yalikuwa ni: Ni tendo la uovu na lisilosameheka kwa watu wa Madina kula kiapo cha utii na kuendelea kumtii Yazid. Watu wa Madina wakatangaza kujivua na kiapo cha utii kwa Yazid na wakatoa kiapo cha utii kwa Abdullah bin Hanzala, ambaye akawa sasa ndiye gavana wa Madina. Yazid aliposikia juu ya uasi uliofanyika Madina na kwamba Makka ipo chini ya Abdullah bin Zubair na maeneo mengineyo hayana utulivu, akatuma jeshi, kwanza lielekee mji wa Madina kisha baadaye Makka. Jeshi hilo lilikuwa linaongozwa na Muslim bin Aqaba. Huyu alikuwa mfuasi mtiifu na mkereketwa wa Yazid na adui mkubwa wa Ahlulbayt (a.s.). Yazid alimpa uhuru Muslim bin Aqaba afanye vyovyote atakavyo, ahakikishe tu miji ya Madina na Makka inarudi kuwa chini ya mamlaka ya Yazid, isipokuwa amri ilitolewa asimguse Imamu ZaynulAbidin (a.s) na familia yake ili kuepuka maafa mengine kama yaliyotokea Karbala. Ziada ya hilo, ikiwa itatokea Muslim Aqaba amekufa akiwa vitani, ukamanda wa jeshi hilo achukue Hasiin bin Numayr. Huyu alikuwa mkuu wa polisi wa mji wa Kufa aliyehusika na kumsaka na kumshika Muslim bin Aqiil na alihusika na kumwekea viziwizi njiani Imam Husayn (as) na kumzuia kuingia Kufa. Alikuwa miongoni mwa makamanda wa Karbala aliyeongoza vikosi vya walengamishale bingwa. Yeye ndiye aliyempiga Ali Akbar mkuki katili (vyanzo vingine vinasema ni Kurra bin Munqidh). Hivyo mnamo Dhulhaji mwaka wa 63 AH, Muslim bin Aqaba na jeshi lake wakaelekea Madina. Wakati huo watu wa Madina walikuwa wametoa kiapo cha utii kwa Abdullah bin Hanzala ambaye sasa ndiye gavana wao. Hali ilikuwa si shwari kwa wafuasi wengi wa Yazid. Watu waliwashambulia wale wote wanaofahamika kuwa ni wapenzi na watetezi wa Yazid. Marwan bin Hakam (aliyetoa ushauri kwa Walid, gavana wa enzi hizo wa Madina, kuwa asimuachie Imamu Husayn (as) kuondoka bila kutoa kiapo cha utii kwa Yazid), adui mkubwa wa Ahlulbayt na mfuasi mkubwa wa Bani Umayya, alishambuliwa na watu wa Madina. Marwan aliwapeleka wanawake wote wa nyumba yake kwa Imam Zaynul-Abidin (as) kwa ulinzi na kuwakinga na mashambulizi (hebu tazama kejeli hiyo katika mazingira hayo). Imam Zaynul-Abidin (as) bila kusita na kwa unyenyekevu na ukarimu akawapokea wote walioomba hifadhi kwake, wakiwemo hata maadui zake. (Inasemekana idadi ya wanawake waliopata hifadhi kwa Imam nyumbani na mashambani ilifikia mia nne, habari zingine zinasema walifikia elfu nne.) Marwan mwenyewe alikimbia kutoka Madina usiku kwa kuogopa kushambuliwa na watu. Wafuasi wa Yazid walitakiwa kuondoka Madina kwa usalama wao wenyewe. Nje ya mji wa Madina, Marwan akakutana na Muslim bin Aqaba na jeshi lake. Marwan akamshauri Muslim


18

kuwa pamoja na uasi unaoendelea Madina lakini hakuna jeshi la ulinzi, kwa hiyo sasa ni nafasi nzuri kuwashambulia. Muslim na jeshi lake wakaelekea Madina. Walipoingia kwenye viunga vya mji wa Madina watu wakatoka kuja kupigana na Muslim bin Aqaba, lakini hawakuwa na nguvu ya kupambana na jeshi hilo, idadi kadhaa ya watu wa Madina wakauawa. Muslim bin Aqaba akaingia ndani ya mji wa Madina mnamo mwezi 28 Dhulhaji 63 A.H. Watu wakakimbilia ndani ya msikiti wa Mtume (saww), kwani wote walijua kuwa wakikimbilia ndani ya msikiti na kwenye kaburi la Mtume watakuwa wote salama na hawatashambuliwa. Lakini maluuni huyu Muslim bin Aqaba hajali utakatifu wa Mtukufu Mtume, msikiti wake wala kaburi lake. Aliamrisha askari wake waingie msikitini na wakawauwa watu wote waliokuwemo ndani yake. Msikiti wa Mtume na kaburi lake vilidhalilishwa hadi kufikia ukomo, kunywa pombe ndani yake, kubaka, watu na wanyama wakauchafua kwa kujisaidia ndani yake. Umwagaji damu, mbwa waliwekwa kwenye mimbari ya Mtume wakaichafua. Hali hii ilidumu kwa siku tatu mfululizo usiku na mchana. Wakati huo huo hali ya vurugu na hatari ilienea mji wa Madina kwa siku tatu, jeshi hilo lilipewa uhuru kamili wa kupora, kuteka nyara, kubaka na kuuwa. (Ripoti zinaonyesha watoto 1,000 wanaharamu walizaliwa, hayo ni matokeo ya ubakaji kwa muda wa siku tatu). Mji mzima uliathirika isipokuwa nyumba ya Imamu Zaynul-Abidin (as). Baada ya ghasia hizo za laana, Muslim bin Aqaba akawataka watu wa Madina watoe tena kiapo cha utii kwa Yazid isipokuwa watu wa nyumba ya Imam Zaynul-Abidin (as). Hakuna aliyethubutu kukataa miongoni mwa watu wa kawaida. Baada ya kumweka madarakani gavana kibaraka hapo Madina, Muslim bin Aqaba na jeshi lake wakaelekea Makka. Humo njiani Muslim bin Aqaba akaugua na akafariki. Hivyo Hasiin bin Numayr akachukua ukamanda wa jeshi na wakaelekea Makka. Wakati huohuo hapo Makka, kabla tu hazijatokea ghasia zilizoudhalilisha mji wa Madina, Abdullah bin Zubair aliona kwamba hata Madina imemuasi na kumponyoka Yazid, akapata tamaa ya kutumia hali iliyokuwepo ili kuhujumu tawala zingine za karibu ziwe chini ya mamlaka yake. Kwa sababu hiyo, Abdullah bin Zubair akamwita Mukhtar ili aje kumsaidia kuimarisha nguvu za utawala wake. Mukhtar akakutana na Abdullah bin Zubair na akakubali kuungana naye kwa masharti mawili: 1. Iwapo Abdullah bin Zubair atasimamisha utawala, lazima Mukhtar atakwe ushauri katika maswala yote na asizuiwe kuonana na Abdullah bin Zubair. 2. Na kipaumbele cha kuasisi utawala wa Abdullah bin Zubair kiwe ni kulipa kisasi kwa wauwaji wa Karbala. Abdullah bin Zubair akakubaliana na sharti la kwanza na sasa akasema kwamba sharti la pili lilikuwa hasa ndiyo lengo lake (kwa kujitetea kwamba hapo mwanzo alikataa kumuunga mkono Mukhtari kwa vile maasi yalikuwa ndio yanaanza na kwamba mipango yao ingeweza kuwageukia). Abdullah bin Zubair, kwa ushujaa, ujasiri na uhodari wa kivita wa Mukhtar, alifanikiwa kuasisi utawala wake Makka na maeneo yanayoizunguka Makka (kwa maoni yangu: ni mwishoni mwa 63 A.H./ mwanzoni 64 A.H.). Baada ya kuona hali iliyoachwa huko Madina baada ya ghasia za laana zilizotokea, na kusikia Hasiin bin Numayr anaelekea Makka, Abdullah bin Zubair aliogopa na akakimbia kujificha milimani. Makka iliachiwa Mukhtar kuilinda. Mukhtar akaongoza jeshi kwenda nje ya Makka kujaribu kumzuia Hasiin bin Numayr na jeshi lake kuingia ndani ya mji wa Makka na al-Kaaba.


19

Mashambulizi ya kuishambulia Makka yalianza tarehe 4 Rabiul Awwal 64 A.H. (takriban miezi miwili baada ya mashambulizi ya Madina). Dhamira thabiti ya Mukhtar na watu wake waliozidiwa kwa idadi ilipungua nguvu, lakini hakusimamisha mapigano. Jeshi la Hasiin lilisonga mbele hadi ndani ya mji, walipokuwa masafa ya mbali na Kaaba, walitengeneza mabomu ya petrol na wakayatupa juu ya Kaaba. Kaaba ikaungua, Mukhtar na jeshi lake walifanikiwa kuwazuwia Hasiin na jeshi lake wasisogee karibu na Kaaba. Wakati huo Hasiin bin Numayr akapata habari kwamba Kiongozi wake, Kamanda mkuu wa majeshi, yaani Yazid amekufa huko Damascus tarehe 14 Rabiul Awwal 64 A.H. Hasiin bin Numayr na jeshi lake wakaondoka kuelekea Damascus kuona kinachoendelea na kusubiri amri mpya. Tarehe ya kukimbia kurudi nyuma ni siku chache baada ya mwezi 14 Rabil Awwal, kwani shambulizi la Makka lilianza mnamo mwezi 4 Rabil Awwal na kutoa fursa ya siku chache baada ya mwezi 14 Rabil Awwal kwa ajili ya taarifa hizo kuweza kufika Makka.

Kifo cha Yazid Baada ya matukio ya Karbala, Yazid hakupata utulivu wa akili wala usingizi mzuri. Alikuwa anahisi daima kiu isiyokatika, alikuwa anahisi joto wakati wote mwilini mwake. Madaktari wake wakamwambia ugonjwa wake hautibiki ila wakamshauri kwamba ili kutuliza hali yake ya wasiwasi na woga, awe anatoka anakwenda sehemu za wazi na kutumia muda wake kwenye jambo analopenda: uwindaji; ili kujipumbaza na kutuliza mawazo, kwa hiyo akawa kwa vipindi fulani anakwenda kuwinda porini. Yazid alielewa wazi kuwa ugonjwa wake huo usiotibika unatokana na uovu na ukatili aliomfanyia Imam Husayn (as) huko Karbala, kwani kila mara alikuwa akisikika akisema: ‘Husayn amenikosea nini mimi?’ Yazid alikwenda kuwinda kama kawaida yake, safari hii kwenye sehemu moja inayoitwa Harwan akiwa na wapambe wapatao 10. Ilikuwa ni tarehe 12 Rabiul Awwal 64 AH. Alimuona swala mmoja mzuri sana ambaye hajapata kumuona wa mfano wake. Akawaamrisha wapambe wake warudi nyuma yeye amuwinde peke yake. Alimfukuzia lakini hakuweza kumtega kila alipomvizia kwani swala huyo alikuwa akimchezea, hii iliendelea kwa muda wa siku mbili. Yazid alipokosa kurudi kwa wapambe wake wakaanza kumtafuta kwa siku mbili, hawakumuona hivyo wakaamua kurudi mjini, njiani wakati wakirudi waliona farasi wa Yazid akiwa na paja la Yazid limezingirwa ndani ya nguo wakajua kwamba Yazid ameuawa. Riwaya nyingine zinasema kwamba wapambe wake walipomtafuta waliuona mwili wake Yazid. Alikulihali wapambe wake wakarudi mjini Damascus kusimulia kisa hicho na wakiwa na farasi na paja (au mwili) wa Yazid kama ushahidi. Yazid akazikwa, na hadi leo hakuna dalili ya kaburi lake wala halijulikani liko wapi. Baada ya kifo cha Yazid ukhalifa akapewa mwanae aliyeitwa Muawiya ambaye alikataa hadharani madaraka hayo kutokana na aibu aliyoihisi kutokana na kukashifiwa ukhalifa huo na baba yake. Hata hivyo, alilazimishwa akubali, lakini hakutoka nje ya Kasri kwa sababu ya fedheha aliyoihisi. Baada ya muda wa siku kumi na nane (riwaya nyingine zinasema siku arobaini), Marwan bin Hakam akapanga mipango ya kumuua kwa kuhofia ukhalifa kuiponyoka familia ya Umayya (Bani Umayya).


20

Mukhtar Apata Ruhusa Kutoka kwa Imamu Zaynul-Abidin (a.s) Wakati huo katika mji wa Madina, walipopata habari ya kifo cha Yazid, gavana aliyewekwa na Muslim bin Aqaba akafukuzwa na watu wa Madina. Abdullah bin Zubair akachukua fursa hiyo kuimarisha nguvu zake Madina, na hivyo akamtuma Mukhtar kusimamia mambo ya Madina. Mukhtar akaenda Makka kwa Abdullah bin Zubair ili kufanya mipango ya kina ya kulipiza kisasi juu ya wauaji wa Karbala. Lakini Abdullah bin Zubair hakutoa ushirikiano mzuri, akasema kuwa huu sio wakati muafaka kulipiza kisasi, kwa hiyo wasubiri wakati muafaka. Mukhtar alisikitishwa sana na akamkumbusha Abdullah bin Zubair ahadi yake alipomuomba amsaidie ili asimike utawala wake. Pia akamkumbusha wajibu wa kimaadili wa kuwafurahisha Ahlulbayt (as), lakini Abdullah bin Zubair hakusikiliza. Abdullah bin Muti, rafiki wa Mukhtar na waziri mkuu wa Abdullah bin Zubair akamshauri Mukhtar aondoke Makka kwa usalama wa maisha yake, kwani vinginevyo Abdullah bin Zubair atamuua kama akiendelea kuwepo Makka. Abdullah bin Muti akampa pesa na usafiri ili kumsaidia aondoke Makka. Hivyo Mukhtar akiwa amebaki peke yake (baada ya Abdullah bin Zubair kumgeuka), akalazimika kuandaa mpango wa kulipiza kisasi kwa wauwaji wa Karbala. Kwa hilo kwanza akataka baraka za mpango wake kutoka kwa Imam wa zama zile, Imam Zaynul-Abidin (as). Mukhtar akaenda Madina kuonana na Muhammad bin Hanafiya ambaye alikuwa ana uhusiano mzuri naye. Akamuomba waende wote kwa Imam Zaynul-Abidin (as) ili kuomba ruhusa na kupata baraka zake juu ya mpango wake wa kulipiza kisasi kwa wauwaji wa Karbala. Muhammad Hanafiya alikuwa ni mdogo wake Imam Husayn (as) kwa mama mwingine. Kwa hiyo alikuwa ni ami yake na Imam Zaynul-Abidin (as). Muhammad Hanafiya na Mukhtar wakaenda kukutana na Imam Zaynul-Abidin (as), Muhammad Hanafiya akamueleza mpango wa Mukhtar anaotarajia kuutekeleza. Imam Zaynul-Abidin (as) akamwambia Muhammad Hanafiya: “kazi ya kulipa kisasi kwa wauwaji wa Imam Husayn (as) ni haki na wajibu kwa kila mmoja kutelekeza. Binafsi, siwezi kutekeleza jukumu hilo kwa sababu ya hali iliyopo ya kisiasa na kuangilia fursa na maslahi ya kueneza Uislamu. Kwa kuzingatia hayo, naliacha jambo hili katika mikono yako na unazo baraka zangu zote.� Wote Muhammad Hanafiya na Mukhtar wakabaini ruhusa isiyo bayana ya Imam Zaynul-Abidin (a), na kwamba kwa sababu ya hali ya kisiasa, Imam Zaynul-Abidin (as) hakuweza kutamka kwa uwazi, lakini akampa jukumu Muhammad Hanafiya. Muhammad Hanafiya akampa idhini Mukhtar na kuridhia mpango wake. Mukhtar kwa idhini ya Muhammad Hanafiya kama mwakilishi wa Imam Zaynul-Abidin (as), akaondoka na kwenda kutekeleza mpango wake. Watu Waliotubu (Tawwabun) Wakati wa utawala wa Ubaydullah bin Ziyad katika mji wa Kufa, wafuasi wa Ali (as) hawakudhihirisha imani yao kwa kuogopa hasira ya Ubaydullah bin Ziyad. Baada ya kupata taarifa za kifo cha Yazid, wafuasi wa Ali wakapata nguvu na kujiamini, wakatoka kwenda kushambulia kasri la Ubaydullah bin Ziyad, waliungwa mkono na watu wengine ambao si wafuasi wa Ali ambao walikuwa dhidi ya utawala wa Ubaydullah.


21

Wakati wa shambulio hilo Ubaydullah alikuwa yupo Basra, kwani alikuwa gavana wa Kufa na Basra na alikuwa akikaa katika kila mji kwa miezi sita. Hapo Kufa, Kasri la Ubaydullah lilitekwa na ile jela mbaya (aliyokuwa amefungwa Mukhtar na Mashia wengine wapatao 40005000) ilifunguliwa na wafungwa wote wakaachwa huru. Wafungwa wengi hawakujua kuhusu mauwaji yaliyotokea Karbala kwa sababu habari zilikuwa zimefichwa. Hawa wafungwa walipatwa na huzuni kubwa kwa kuwa hawakuweza kumfikia Imamu Husayn (as) wakati walikuwa wanahitajika zaidi ili wamsaidie. Walikutana nyumbani kwa Sulayman bin Surd Khuzai aliyekuwa na umri wa miaka kama tisini hivi. Alikuwa ni sahaba wa Mtume Muhammad (saww) na Imamu Ali (as). Sulayman akazungumza na Mashia akasema: “Tumemuangusha Imam wetu Husayn (as) kwani tulimwalika kisha tukashindwa kumsaidia kwa sababu moja au nyingine, lakini sasa tunaweza kusaidia kwa kulipiza kisasi kwa wauaji wa Karbala,” watu wakakubali. Sulayman bin Surd Khuzai akafanikiwa kukusanya watu wengine kwa ajili ya jambo hilo ambao idadi yao ikafikia watu elfu kumi na sita (16000); hili kundi likajulikana kama Tawwabun (watu wenye kujutia na kutubia). Sulayman Surd Khuzai bila kupingwa akachaguliwa kuwa kiongozi wa Tawwabun. Tawwabun walikuwa wanajua vizuri kwamba aghlabu ya wauwaji wa Karbala wapo ndani ya mji wa Kufa (watu kama Sinan, Shimri, Khuli, Umar bin Saad, Hurmala na wengineo). Lakini mkakati wao kwanza ulikuwa ni kumkamata mkubwa wao aliyepanga mauaji hayo ambaye ni Ubaydullah bin Ziyad. Pia wauwaji wa Karbala waliokuwa katika mji wa Kufa walikuwa na nafasi za juu na wenye ushawishi na mahusiano yenye nguvu na wananchi wa kawaida. Kwa sababu hiyo, Tawwabun waliona ni vyema wakasubiri hadi watakapojijenga na kupata nguvu ndipo watakapowasaka wauaji wa Karbala. Huko Makka, Abdullah bin Zubair, baada ya kusikia kwamba Ikulu ya Ubaydullah bin Ziyad imeshikwa na watu wa Kufa, akamtuma Abdullah bin Yazid Ansariy kwenda mji wa Kufa kuwa gavana wake pale. Gavana mpya alikuwa anaelewa vyema harakati za Tawwabun, lakini hakushughulika kuzizuia kwa kuwa hazikuwa zinaelekezwa kwa watu wa Kufa bali zilikuwa zinamlenga Ubaydullah bin Ziyad ambaye Abdullah bin Zubair alikuwa anamtaka aondoke madarakani. Ubaydullah bin Ziyad Aikimbia Basra Baada ya Yazid kufariki, ulikuwepo mgogoro wa kumpata mrithi, hasa pale mwanaye mkubwa Muawiya (wa pili) alipokataa kurithi madaraka ya Yazid, na haraka kuuawa kwa upinzani wake. Kwa hiyo nani sasa atachukua madaraka? Serikali ya Damascus iliwatizamia watu watatu: 1 - Umar bin Bashir Ansariy; alikuwa ni mmoja wa watu mashuhuri sana ndani ya duru za serikali ya Damascus. 2 - Khalid bin Yazid; mtoto wa Yazid wa miaka 12; kupitia yeye ufalme ungeendelea katika ukoo wao. 3 - Abdullah bin Zubair wa Makka – kwani tayari Makka na Madina ilikuwa chini ya milki yake. Marwan bin Hakam akatuma barua kwenda mji wa Kufa kwa Ubaydullah bin Ziyad kumjulisha kifo cha Yazid na akamtaka aende Damascus wazungumze na kujadili suala la mrithi wa kiti cha


22

Yazid. Barua ilipowasili Kufa, Ubaydullah kwa wakati huo alikuwa yuko Basra kwa kipindi cha mzunguko wa miezi sita kati ya Kufa na Basra huku mwanae Umar akikaimu nafasi yake huko Kufa. Umar akapeleka barua ya Marwan bin Hakam Basra na habari za vurugu zilivyooenea ndani ya Kufa kufuatia habari za kifo cha Yazid kujulikana wazi kwa wakazi wa Kufa. Ubaydullah akawaita watu wa Basra kwenye mkutano wa hadhara. Akawajulisha kuhusu kifo cha Yazid (riwaya nyingine zinasema hakuwajulisha) na akawambia anaondoka Basra kuelekea Damascus haraka iwezekanavyo kwa kuwa huko kuna vurugu. Akawaonya kwamba anamuacha makamu wake na wasifanye vurugu kipindi hayupo na makamu wake atasimamia maswala yote, mtu yeyote atakayempinga atauawa pamoja na familia yake pia. Ubaydullah akauliza kama kuna watu wanaoweza kumfikisha kwa haraka na usalama huko Damascus kwa malipo ya ujira mkubwa. Umar Jaru (chanzo kingine kinasema Umar Harith) alikuwa kiongozi mzoefu na mtaalamu wa safari za jangwani, ilikuwa ni kazi yake kuisindikiza misafara ya biashara na watu kutoka sehemu moja hadi nyingine; alikuwa na watoto watano, (riwaya nyingine zinasema alikuwa na watoto wa kiume ishirini na moja), na wote walikuwa na uzoefu wa safari za jangwani na uongozaji, na kila mtoto alikuwa na wasaidizi wapatao thelathini. Umar Jaru na kundi lake wakamsindikiza Ubaydullah bin Ziyad kwenda Damascus; Ubaydullah akafungasha pesa zote na vito vya thamani kutoka katika Ikulu yake na akasafirisha kwa njia tofauti na ile aliyokuwa anasafiria, akihofia kuvamiwa na kunyang’anywa njiani. Msafara wa Ubaydullah bin Ziyad na Umar Jaru ulikuwa na ngamia mia moja waliobeba watu, mizigo, na maji, wengi wa ngamia hao walibeba maji kwa ajili ya akiba ya safari ndefu iliyokuwa mbele yao. Kwa hiyo Ubaydullah bin Ziyad akaondoka kuelekea Damascus. Sulayman bin Surd na wale Tawwabun wapatao elfu nne na mia tano ambao walikuwa nje ya mji ya Kufa, wakapata habari kuhusu msafara wa Ubaydullah bin Ziyad unaoelekea Damascus. Tawwabun kwa hiyo wakajipanga katika njia panda ya kutoka Basra kuelekea Damascus. Kikundi cha msafara cha Umar Jaru walikuwa wazoefu na waelekezaji wataalamu hivyo walikuwa wanatanguliza watu kuangalia kama kuna hatari ya kuvamiwa, wakaripoti kuwa kuna jeshi kubwa limesimama kuzuia njia ya kuelekea Damascus na wamebeba mabango ambayo yameandikwa ‘Wafuasi wa njia ya Husayn.’ Wakatoa habari kwa Umar Jaru ambaye akamuuliza Ubaydullah bin Ziyad ni kwa nini kuna jeshi kama hilo lililofunga njia yetu? Ubaydullah bin Ziyad akawa lazima akiri kuhusu kifo cha Yazid na kwamba anakwenda Damascus kwa ajili ya kushawishi suala la urithi wa Yazid, na jeshi lililo mbele yao ni la Tawwabun ambao wanamsaka yeye bin Ziyad. Kwa hiyo Ubaydullah bin Ziyad akamuahidi kuwa atampa pesa nyingi zaidi iwapo atamfikisha hai salama Damascus. Umar Jaru akaja na mpango mmoja ambao Ubaydullah bin Ziyad kwanza aliukataa lakini baadaye alikubali ili kunusuru maisha yake, mpango huo ni kumfunga Ubaydullah bin Ziyad kwenye tumbo la ngamia kisha kumficha kwa mifuko iliyojaa maji iliyokuwa inaninginia pembezoni mwa tumbo la ngamia ambaye atakuwa katikati ya ngamia wengine waliobeba maji. Hivyo uwezekano wa kuonekana alipojificha Ibn Ziyad utakuwa mgumu.


23

Sulayman bin Surd Khuzai na Tawwabun wakawasili. Sulayman akamwambia Umar Jaru kwamba hawana nia ya kumpora chochote alichonacho wao wanamtafuta Ubaydullah bin Ziyad ambaye Umar Jaru alikuwa anamsindikiza kumpeleka Damascus. Umar Jaru akakanusha akasema sio kweli yeye anasafirisha mizigo tu na kwamba bin Ziyad hayupo pamoja nao. Umar Jaru akampa ruhusa aikague mizigo. Tawwabun wakakagua mizigo lakini hawakufikiria hata kidogo kuangalia chini ya tumbo la ngamia ingawa waliwatawanya baadhi ya ngamia waliobeba maji. Sulayman Surd na watu wake wakarudi Kufa, wakidhani Ubaydulla Ziyad ametega mtego wa ujanja na amefanikiwa kuwaponyoka. Baada ya masafa kiasi, Ubaydullah bin Ziyad akafunguliwa na akafika Damascus bila upinzani wowote. Ubaydullah bin Ziyad Akiwa Mjini Damascus Alipowasili Damascus, Ubaydullah bin Ziyad akakutana na Marwan bin Hakam kujadili suala la urithi wa kiti cha Yazid. Marwan akamjulisha juu ya wale wagombea watatu; Umar Bashir alAnsariy, Khalid bin Yazid na Abdullah bin Zubayr. Marwan akamwambia bin Ziyad kwamba itifaki hapo Ikulu ya Damascus wamekubaliana Umar bin Bashir Ansariy ndiye apewe kiti cha ukhalifa. Ubaydullah alikuwa kinyume na hili, hamtaki Khalid bin Yazid (mtoto wa Yazid wa miaka 12) awe Khalifa kwani huyu atawasaliti kama baba yake alivyofanya; Ubaydullah akasema, Yazid aliamrisha kwa maandishi wasimuache hai Imam Husayn (as) kwa gharama yeyote lakini baada ya Karbala Yazid akakanusha kwamba hakutoa amri yeyote ya mauaji ya Karbala bali yalifanywa na Ubaydullah na Shimr na wengineo na huu usaliti ulimuudhi Ubaydullah bin Ziyad. Ubaydulla bin Ziyad akamtaka Marwan Hakam awe Khalifa kuliko kuitoa ofisi kwa mtu mwingine yoyote; Marwan kwanza alikataa akasema kwamba watu hawatamuunga mkono, lakini Ubaydullah akaahidi kuwa atamuunga mkono na kufanya watu wamkubali na kuwa na imani naye; pia atampa hazina alizokuja nazo kutoka Kufa pamoja na hazina zingine za Yazid zilizofichwa ambazo anazijua zilipo ili zitumike kuwahonga watu maarufu ili wamuunge mkono na wamkubali Marwan Hakam kwa sharti ya kumchagua Ubaydullah awe ndiye kamanda mkuu wa jeshi. Marwan bin Hakam akakubali na Ubaydullah bin Ziyad kwa haraka akatoa kiapo cha utii kwa Marwan bin Hakam. Ubaydallah bin Ziyad akamuonyesha Marwan hazina zilizofichwa za Yazid ambazo zikawa chini ya usimamizi wa Marwan. Ubaydallah bin Ziyad akaanza desturi yake ya kuwalazimisha watu watoe kiapo cha utii kwa Marwan bin Hakam iwapo watakataa watakabiliwa na adhabu kali na kuuwawa. Katika hali hiyo ya adhabu, Zufar bin Haris alifanikiwa kutoroka Damascus na kukimbilia mji ulioitwa Qarqisia mji ulio katikati baina ya Damascus na Kufa. Kutokea Qarqisia Zufar bin Haris aliyekuwa ni mfuasi wa Abdullah bin Zubair huko Makka na alikuwa dhidi ya Ubaydullah bin Ziyad alijaribu bila mafanikio kudhoofisha uwezo na ushawishi wa Marwan bin Hakam na Ubaydallah bin Ziyad huko Damascus. Ubaydullah bin Ziyad akamshauri Marwan bin Hakam amuoe mjane wa Yazid mama yake Khalid, ili aimarishe nguvu zake. Baada ya kuimarisha nguvu zake Damascus, Ubaydallah bin Ziyad alikwenda kumsaka Sulayman bin Surad na kikundi chake cha Tawwabun. Kazi Maalum ya Tawwabun


24

Wakati ambapo Tawwabun hawakufanikiwa kumpata Ubaydullah bin Ziyad, katika msafara wa Umar Jaru, Sulayman bin Surd na watu wake wapatao elfu nne na mia tano walirudi Kufa wakaongeza askari wengine waliofikia idadi ya elfu kumi na sita. Mnamo tarehe 1 Muharram 65 AH, Tawwabun chini ya uongozi wa Sulayman bin Surd walipiga kambi huko Nukhaylah nje kidogo ya mji wa Kufa. Sulayman akaona askari waliohudhuria ni elfu tatu (3000) tu kati ya elfu kumi na sita (16000) waliojisajili; kwa hiyo akarudi Kufa akiwa na ujumbe wa ‘Wafuasi wa njia ya Husayn.’ na akafanikiwa kupata askari wengine elfu moja na miatano (1500) ikafikia idadi ya askari elfu nne na miatano (4500). Kabla hawajaondoka kwa bidii ya kumuwinda Ubaydullah bin Ziyad, Tawwabun wakaelekea kwanza Karbala wakafanya kikao cha maombolezo na ziara usiku na mchana. Baadaye waliondoka kuelekea Damascus, na wakati huo huo Ubaydullah bin Ziyad akaondoka Damascus kuelekea Kufa. Tawwabun waliwasili Qarqisiya usiku, wakamkuta Zufar bin Haris (ambaye alikuwa amemkimbia Ubaydullah bin Ziyad huko Damascus) alikuwa sasa ndiye mtawala wa Qarqisiya. Sulayman akamtuma naibu wake Musayyab bin Najaba amtaarifu Zufar kwamba hawakuja kwa nia ya kuivamia Qarqisiya, lakini wao wanapita njia wanamtafuta Ubaydallah bin Ziyad. Zufar akafurahi kusikia kwamba Ubaydullah anawindwa na akawaamuru wenye maduka kufungua maduka yao usiku na kuwapa bidhaa Tawwabun bure bila malipo. Jeshi la Ubaydullah bin Ziyad lilikuwa jumla na askari 300,000 wenye nguvu wakiwemo kundi la askari waliotangulia wapatao 100,000. Ama Tawwabun walikuwa na askari 4500 tu. Majeshi ya pande mbili yalikutana eneo linaloitwa Aynul-Warda na yakaanza mapambano. Katika mzunguko wa kwanza wa vita ambao ulichukua siku mbili ilikuwa ni baina ya Tawwabun na kikosi cha mbele cha Ubaydullah bin Ziyad. Duru ya pili ya mapigano, ilikuwa ni baina ya Tawwabun na jeshi lote la Ubaydulla bin Ziyad, ambavyo vilidumu kwa siku saba. Katika kikosi cha Sulayman alibakiwa na askari 75, miongoni mwao wakiwemo makamanda 5 ambao watachukua cheo cha ukamanda mkuu iwapo kamanda wao atauliwa, nao ni Sulayman bin Surd, Musayab bin Najaba, Abdulla bin Saad, Abdulla bin Walin na Rufa bin Shadad. Katika usiku wa mwisho wa vita, baadhi ya Tawwabun waliazimia bora waache mapambano kutokana na idadi yao ndogo ya askari ambao walikuwa wamechoka, wameumia na wenye kiu (Kwani jeshi la Ubaydullah bin Ziyad lilizuia wasipate maji), ukilinganisha na jeshi lililobaki la Ziyad la watu wapatao 150,000 lenye nguvu na zana. Lakini Sulayman akaliambia jeshi lake kuwa nia yao ni kulipiza kisasi cha mauaji ya Imam Husayn (as), na kama haitawezekana ni bora kufa katika mapambano kuliko kukimbia. Baada ya swala, usiku, Sulayman akaona ndani ya ndoto yumo ndani ya mabustani mazuri yaliyojaa miti na maua mazuri na katikati kuna nyumba nzuri ya dhahabu. Mwanamke aliyejihifadhi vizuri akatoka nje ya kasri hilo, Bi Khadija (as) akawasilisha salam kutoka kwa Mtume na Ahlu Kisaa na kwamba Imamu Husayn anawapa hongera Tawwabun kwa kazi yao nzuri mpaka kufikia hapo, na akamfahamisha Sulayman kwamba atauawa siku inayofuata. Bi Khadija (as) akachukua chungu cha maji akampa Sulayman apake majeraha yao ili ayatibu na kuendelea na vita kesho yake.


25

Sulayman alipoamka akaona kile chungu cha maji karibu yake na akaswali swala ya shukurani. Akawapaka askari wake waliobakia ambao walikuwa wamelala maji yale kwenye majeraha yao. Maji ya mbinguni yakawaponya majeraha yote na uchovu wote ukaisha. Wakati anaendelea kusali chungu kikatoweka na wote walipoamka Sulayman akawafahamisha muujiza uliotokea. Siku iliyofuata, Tawwabun wakapigana kwa uthabiti na ushujaa dhidi ya askari 150,000 wa Ubaydullah ambao walitarajia upinzani dhaifu. Adhuhuri, Sulayman akauawa, Musayab bin Najaba akachukua ukamanda naye akauawa, Abdullah bin Saad naye akachukua ukamanda akauawa, Abdullah bin Walin naye akachukua ukamanda akauawa, mwishowe Rufa bin Shadad akachukua ukamanda na huku wamebaki Tawwabun 10 tu, wakakimbilia Kufa ili kupata askari wengine. Kwa kuona wameshinda vita kwa mara ya pili na wamewapiga vibaya Tawwabun, Ubaydullah bin Ziyad akaenda Basra. Mukhtar Afungwa Jela Mara ya Pili na Aachwa Huru tena Wakati huo huo Mukhtar baada ya kupata ruhusa kutoka kwa Muhamad Hanafiya kwa niaba ya Imamu Zaynul-Abidin (as) aliondoka Makka kuelekea Kufa. Alipofika njia panda ya Qarqisiya, akageuza njia na kuelekea Karbala kwa ajili ya kumzuru Imam Husayn (as), ambapo akatoa ahadi kwa Imam Husayn (as) kwamba atalipiza kisasi dhidi ya wahaini wa Karbala. Kisha akaingia mji wa Kufa na akatangaza bayana kuwasili kwake ili watu wote wa Kufa akiwemo gavana Abdullah bin Yazid Ansariy na wauaji wote wa Karbala watambue kuwepo kwake. Ilikuwa ni wakati ule Sulayman bin Surd alipokuwa anaandikisha askari wapya katika mji wa Kufa ndipo Mukhtar aliwasili kutoka Karbala; wakakutana na kujadili mbinu za vita; Tawwabun lengo lao la awali kabisa lilikuwa ni kumkamata Ubaydullah bin Ziyad, wakati Mukhtar lengo lake ni kulipiza kisasi dhidi ya wauaji wa Karbala waliomo ndani ya mji wa Kufa kwani wengi wao walikuwa bado wanaishi hapo Kufa. Mukhtar alipowasili Kufa, wauaji wa Karbala ambao ni wenyeji wa hapo Kufa wakaogopeshwa na dhamira yake aliyoitangaza ya kuwasaka wauwaji hao, wakati hapo mwanzoni hawakuwa na hofu ya haraka kutoka kwa Tawwabun. Wauaji hao wenyeji wa Kufa walikuwa wana nafasi za juu na walikuwa watu maarufu katika mji wa Kufa. Kwa hiyo wakamshauri gavana Abdullah bin Yazid Ansariy amfunge jela Mukhtar ili asiwasababishie wao matatizo yoyote yale. Kwa shinikizo la watu hao maarufu wa Kufa, Abdullah bin Yazid Ansariy akamfunga jela Mukhtar, kwa hiyo Mukhtar sasa akawa anatumikia kifungo chake cha mara ya pili. Rufa’ bin Shadad (kutoka miogoni mwa Tawwabun) alipowasili Kufa alipata habari za kufungwa jela Mukhtar. Tofauti na mwanzo alipofungwa jela na Ubaydullah bin Ziyad hivi sasa Mukhtar aliruhusiwa kutembelewa na ndugu na jamaa, pia hakufungwa kwa pingu na barua zilikuwa zinaruhusiwa kuingia na kutoka. Mukhtar alipopata habari kuwa Tawwabun wameshindwa vibaya na za kurejea kwa Rufa’, akamwandikia barua asife moyo amsubiri Mukhtar akiachiwa waje wapange mipango. Rufa’ akaenda kule jela akiwa na mpango wa kumtoa Mukhtar jela kwa nguvu. Mukhtar akamkataza asitende kinyume na sheria na akamhakikishia juu ya kuachiwa kwake kwa njia rasmi hivi karibuni tu. Mukhtar akamtuma mmoja wa watu wake aende Madina amjulishe Abdullah bin Umar (yaani shemeji yake) juu ya hali ilivyo.


26

Abdullah bin Umar akamwandikia Abdullah bin Yazid Ansariy, gavana wa Kufa, akimwelezea uhusiano wake na Mukhtar na akataka amwache huru haraka iwezekanavyo. Baada ya kupata barua hiyo na kwa kutambua ushawishi mzito wa Abdullah bin Umar akamwacha huru baada ya kufikiria kuwa kumfunga ilikuwa sio amri ya mkubwa wake Abdullah bin Zubair bali ni shinikizo la wauaji wa Karbala waliokuwa wanaishi Kufa. Hivyo kumuachia Mukhtari sio kufunja amri yoyote kutoka kwa Abdullah bin Zubayr. Wauaji wa Karbala hawakukubali kuachiwa huru Mukhtar kwa kuhofia maisha yao. Abdullah bin Yazid Ansariy akajikuta anavutwa baina ya amri ya Abdullah bin Umar na msukumo wa wenyeji hawa. Hatimaye akaamua kumfungua jela kwa masharti kadhaa kwa ajili ya uhuru wake. Gavana Abdullah bin Yazid Ansariy akamwita Mukhtar na akamtaka atoe ahadi kwamba hatofanya vurugu na kwenda kinyume na yeye gavana, na akifanya vurugu yeyote basi fidia yake itakuwa kafara ya wanyama elfu moja na kuwaacha huru watumwa wake wote. Mukhtar akaahidi mbele ya mashahidi kukubaliana na masharti hayo na akafunguliwa kutoka jela. Mukhtar alitambua kuwa kafara ya mifugo elfu moja na kuwaachiwa huru watumwa wake ilikuwa ni jambo lenye umuhimu mdogo sana ukilinganisha na kuwasaka wale wauaji wa Karbala. Chanzo kimoja kinasema kwamba Mukhtar alifungwa jela tena kwa mara ya tatu na akafanikiwa kujipatia uhuru wake kwa mara nyingine tena. Abdullah bin Muti Ajaribu Kumfunga Jela Mukhtar Abdullah bin Zubair huko Makka akamchagua Abdullah bin Muti kuwa gavana badala ya Abdullah bin Yazid Ansariy. Huyu Abdullah bin Muti alikuwa ni waziri wake mkuu hapo Makka. Abdullah bin Zubair alifikiri kwamba kwa kumchagua Abdullah bin Muti kama gavana wa Kufa, Mukhtar hataweza kuanzisha upinzani kutokana na urafiki wake na Abdullah bin Muti. Abdullah bin Muti ni yule ambaye aliingilia kati kwa ajili ya Mukhtar baada ya Abdullah bin Zubair kuimarisha nguvu zake kwa msaada wa Mukhtar, akavunja ahadi yake ya kumsaidia Mukhtar kulipiza kisasi dhidi ya wauaji wa Karbala. Ni Abdallah bin Muti kwa wakati ule alipokuwa waziri mkuu ndiye alijaribu bila mafanikio kumshawishi Abdullah bin Zubair abadilishe uamuzi wake wa kutomruhusu Mukhtar kwenye baraza yake kwa majadiliano yoyote yale. Kwa hiyo Abdullah bin Muti akamshauri Mukhtar kuondoka Makka kwa ajili ya usalama wa maisha yake, na akampa fedha na usafiri aondoke nje ya mji wa Makka. Baada ya kusimikwa gavana mpya wauaji wa Karbala wakaenda kwa Abdullah bin Muti na kumshauri amfunge jela Mukhtar, kwani iwapo ataachwa huru atatekeleza tishio lake la kulipiza kisasi dhidi ya wauaji hao wa Karbala ambao ni watu maarufu wanaojulikana wenye vyeo ndani ya mji wa Kufa. Na iwapo hao watu maarufu watatishwa hiyo itasababisha kupinduliwa kwake yeye Abdullah bin Muti mwenyewe. Abdulla bin Muti akawaambia kuwa hawezi kumfunga jela Mukhtar bila ya kufanya kosa lolote, na isitoshe yeye ni rafiki yake mpenzi. Lakini Abdullah bin Muti akajikuta analazimishwa sana


27

achukue hatua dhidi ya Mukhtar. Wakati Abdullah bin Muti alipoingia Kufa Mukhtar kwa makusudi aliondoka ndani ya mji wa Kufa kwa kisingizio cha kumkwepa Abdullah bin Muti. Abdullah bin Muti mwishowe akaamua kumfunga jela Mukhtar. Ayaz bin Mazarib kamanda mkuu wa polisi wa Kufa akamshauri Abdullah bin Muti kuwa: “Njia nzuri ya kumkamata ni kumuongopea aje binafsi Ikulu kukutana na wewe kama rafiki yake. Ujumbe upelekwe kwa Mukhtar na watu wawili ambao hawashirikiani na wewe, wawe kama wajumbe wasiopendelea upande wowote, hii itamfanya Mukhtar asiwe na shaka yeyote.” Zaida bin Qudama na Husayn bin Abdullah wakachaguliwa kwenda nyumbani kwa Mukhtar wakiwa na ujumbe kuwa Abdullah bin Muti anamwita kwa majadiliano kuhusu mambo muhimu ya dola na anahitaji ushauri wa Mukhtar. Hawa wajumbe walipofika nyumbani kwa Mukhtar wakamkuta anasoma Qur’ani, na hili likamsukuma Zaida asipende kuona Mukhtar anaingizwa katika mtego wa kukamatwa, kwa hiyo wakafikisha taarifa bandia ya Abdullah bin Muti (yenye mtego). Lakini pia Zaida akaongelea juu ya miujiza ya Qur’ani, na akasoma aya moja ambayo kwa dhahiri inamuonya wazi Mukhtar kuwa kuna hatari mbele. Zaida akatoa ujumbe huu kwa fumbo ili kujilinda asipate matatizo kwa Abdullah bin Muti kwani vinginevyo mwenzake Husayn bin Abdullah angemshitaki. Mukhtar alipopata ujumbe huo akajisingizia ugonjwa na akawaambia wakamwambie Abdullah bin Muti kuwa sasa hivi anajisikia mgonjwa lakini akipata ahueni atakwenda kumuona Abdullah Muti. Wajumbe wawili hao wakaondoka, njiani Husayn bin Abdullah akamwambia Zaida bin Qudama kwamba ule ujumbe uliompa Mukhtar nimeufahamu, lakini siwezi kumwambia Abdullah bin Muti kwani nilisikia hadithi kwa watu waliomsikia Mtume (saww) ikisema kwamba Mukhtar atalipiza kisasi kwa wauaji wa Imam Husayn (as) na bora niwe pamoja na Mukhtar kuliko kuwa pamoja na Abdullah bin Muti. Mukhtar akaelewa ya kuwa haitachukua muda mrefu kabla Abdullah bin Muti hajafanya jaribio jingine la kumuweka jela, hivyo ilikuwa ni muhimu kuharakisha mpango wake. Kutokana na haraka akaona kuwa mpango hautawezekana hadi atakapompata mwenzake shujaa ambaye ni madhubuti katika dhamiri ya kulipiza kisasi dhidi ya wauaji wa Karbala kama yeye mwenyewe. Mukhtar Aungana na Ibrahim bin Malik al-Ashtar Mukhtar alifanya ijulikane ndani ya mji wa Kufa na nje kuwa anamtafuta mwenza wa kushirikiana naye kulipiza kisasi dhidi ya wauaji wa Imam Husayn (as). Mtu huyo awe shujaa, jasiri, mwenye nguvu, Shia, mwenye shauku ya kujitolea kwa dhati ya kuona kwamba wauaji wa Karbala wanalipizwa kisasi. Mtu kama huyu anahitajika kukinzana na nguvu, umashuhuri na madaraka ya wauaji wa Karbala ambao wanaishi ndani ya mji wa Kufa. Mtu mwenye sifa hizo ni Ibrahim bin Malik al-Ashtar mtoto wa Malik al-Ashtar ambaye alikuwa Shia imara, na mfuasi mtiifu wa Imamu Ali (as). Kawaida watu walikuwa wakimfuata Mukhtar, lakini kwa Ibrahim ni yeye Mukhtari ndiye aliyemfuata mwenyewe Ibrahim na kumwambia ni mara yake ya kwanza kwenda kwenye nyumba ya mtu na kumtaka ajiunge naye.


28

Ibrahim akakubali kujiunga pamoja na Mukhtar kwa sharti kuwa Ibrahim atakuwa kamanda mkuu wa jeshi, na hilo sio kwa sababu ya tamaa ya madaraka, bali kuhakikisha kwamba hatumii kipaji chake, ushujaa, na ujasiri wake ili mtu mwingine apate madaraka. Kwani jeshi likiwa chini ya amri yake ataweza kuhakikisha kwamba matumizi mabaya hayatokei. Mukhtar akamuonyesha Ibrahim mamlaka aliyopewa na Muhamad Hanafiya kama wakili wa Imam Zainul-Abidin (as). Kwa kuona maandishi hayo, Ibrahim na kabila lake haraka wakatoa kiapo cha utii kwa Mukhtar; ama riwaya nyingine inasema Ibrahim aliomba muda wa siku chache ili atoe uamuzi, kwani anawatuma wajumbe wake Madina kumuona Muhamad Hanafiya na kuthibitisha maandishi ya Mukhtar. Waliotumwa wakarejea Kufa ili kutoa taarifa kwa Ibrahim. Kwa mujibu wa riwaya moja, walipowasili Qadisiya walikutana na Khayr kutoka familia ya Mukhtar. Akapewa taarifa kutoka Madina na haraka akakimbilia kwa Mukhtar kumuelezea uthibitisho wa Muhammad Hanafiya na baraka zake, ambapo Mukhtar akaswali swala ya kushukuru. Ama taarifa nyingine inasema walikwenda moja kwa moja kwa Ibrahim na kumtaarifu uthibitisho wa Muhammad bin Hanafiya. Pamoja na kuwa na yakini, Ibrahim hakumpa jibu Mukhtar mara moja, ilipokuwa hakuna majibu ya haraka kutoka kwa Ibrahim, Mukhtar anachukulia kwamba Muhammad Hanafiya alidhani hakuidhinisha ujumbe huo kwa hiyo Ibrahim amekataa. Baada ya siku kadhaa, Mukhtar akagundua kwamba ilikuwa kinyume na hivyo na akamuendea Ibrahim ambaye alikubali mara moja kujiunga naye. Mukhtar Awa Gavana wa Kufa Mukhtar na Ibrahim wakaamua kuwa njia nzuri ya kuwakamata wauaji wa Karbala waliomo ndani ya mji wa Kufa, ambao ukizingatia kwamba ni watu mashuhuri na wenye madaraka, ni kuchukua udhibiti wa serikali, na hii maana yake ni kuvamia kasri ya gavana (Abdullah bin Muti). Mpango ukakubaliwa kwamba usiku wa Alhamisi tarehe 14 Rabiul Awwal 66 AH wafuasi wote wa Mukhtar na Ibrahim watatoka majumbani kwao na waizunguke Ikulu ya Abdullah bin Muti ili wamuondoe madarakani. Alama itakuwa kuwasha mwenge juu ya paa ya nyumba ya Mukhtar na sauti ya ngoma ya kuashiria vita, baada ya kuona mwenge huo wa kwanza, mienge kwa mfululizo itawashwa juu ya mapaa ya nyumba za wafuasi ili kusambaza ishara hiyo. Kila kundi la wafuasi wachukue bango linalosomeka ‘Tokeni enyi wafuasi wa njia ya Husayn’, pia wakaonywa wasidanganywe na hila za maadui kwa hiyo mtu yeyote asitoke nje ya nyumba yake kabla ya makubaliano yao ya Alhamisi usiku. Ayaz bin Mazarib mkuu wa polisi wa Kufa akapata habari kuwa siku chache zilizopita muda wa usiku Ibrahim na kundi la watu wamekuwa wanakutana nyumbani kwa Mukhtar; akashuku kwamba kuna mpango unaoendelea na hivyo akapeleka habari kwa Abdullah bin Muti mnamo tarehe 13 Rabiul Awwal, usiku mmoja kabla mpango wa mapinduzi haujafanyika. Usiku huo huo Abdullah bin Muti alipopata taarifa kutoka kwa Ayaz, akaamuru viwekwe vituo vya ukaguzi katika wilaya zote (takriban kumi) za mji wa Kufa. Katika siku hizo kulingana na mipangomiji, miji, wilaya, kata, mitaa na hata koo mbalimbali zilikuwa na mipaka, kulikuwa na barabara moja kutoka wilaya moja hadi nyingine. Hii iliruhusu


29

kuhakikisha kwamba kulikuwa na upitikaji huru wa eneo husika, lakini kwenda eneo moja hadi lingine ilibidi kupita katika hiyo barabara inayounganisha, utaratibu huu ulikuwa ni kwa ajili ya usalama dhidi ya uvamizi wa maadui wa mara kwa mara uliokuwepo zama zile., kwa hiyo walinzi walitawanywa kwenye barabara kuu hizo zinazounganisha ili kudhibiti harakati za watu wanaotoka sehemu moja hadi nyingine. Ibrahim na kundi lake wakatoka sehemu yao na wakaelekea nyumbani kwa Mukhtar katika wilaya nyingine ili kukamilisha mipango ya mashambulizi ya kesho yake usiku. Njiani, kwenye kituo cha ukaguzi, wakapambana na Ayaz bin Mazarib ambaye ni kamanda mkuu wa polisi, na ili waweze kupita Ibrahim akafanikiwa kumuua Ayaz. Askari wa Ayaz wakafanikiwa kutoroka na kutoa taarifa kwa Abdullah bin Muti. Ibrahim na kundi lake walikabiliana na vituo vingi vya ukaguzi na baada ya mapambano walifanikiwa kufika nyumbani kwa Mukhtar. Ibrahim akamjulisha Mukhtar kuhusu viziwizi na jinsi walivyopambana na kumuuwa Ayaz. Kwa sababu hiyo, wakasogeza mpango wao wa mashambulizi kwa usiku mmoja kabla ili kufanikiwa. Vinginevyo wasipowahi, ikifika asubuhi, Abdullah bin Muti ataweza kudhibiti mapinduzi ikiwa atatambua kuna mapinduzi yanayotengenezwa. Mukhtar akawasha mwenge wa moto juu ya paa la nyumba yake kisha akapiga ngoma za kuashiria vita, lakini hakupata muitikio wowote, hii ni kwa sababu watu toka mwanzo walionywa wasitoke ikiwa kuna ishara yoyote kabla ya muda uliopangwa. Kwa hiyo wakadhani kwamba hiyo pengine ni njama za maadui, kwani mwito uliotarajiwa ulikuwa umepangwa kufanyika usiku wa kesho yake. Kwa hiyo Abdullah bin Muti akafikiri Mukhtar na Ibrahim wamekusanya jeshi kubwa ili kumuondoa madarakani. Lakini kwa hakika walikuwa na jeshi dogo tu usiku huu, kwani mpango wa mashambulizi ulikuwa ni usiku wa kesho yake. Rashid, mtoto wa Ayaz bin Mazarib, akapata habari ya kifo cha baba yake akaenda kwa Abdullah bin Muti huku analia. Abdullah bin Muti akamwambia hakuna haja ya kulia, ni bora alipize kisasi cha kuuawa baba yake. Abdullah bin Muti akampa kikosi cha askari ili akapigane dhidi ya Mukhtar na Ibrahim. Abdullah bin Muti akamtuma Shabath bin Rabi (alikuwa ni mmojawapo kati ya makamanda waliokuwepo Karbala) akapewa askari elfu moja (1000) ili kupambana na Mukhtar na kumuua. Shabath bin Rabi akashauri ni bora kusubiri hadi mchana ndipo mashambulizi yataleta tija. Abdullah bin Muti akakataa kwani hakutaka kufanya kosa, kwa kuhofia Mukhtar anaweza kuanza mashambulizi usiku huo. Kituo cha ukaguzi katika wilaya alipokuwa anaishi Mukhtar kilikuwa chini ya kamanda Hijab bin Hurr akiwa na askari wapatao 700. Walipoona jeshi la Shabath bin Rabi linaelekea nyumbani kwa Mukhtar, wakadhani ni kikosi cha kumsaidia Mukhtar, hawakuwatambua kwa sababu ilikuwa ni usiku na kila mmoja alitaka kufanya shambulizi la kushtukiza. Hivyo wakaanza kupigana wenyewe kwa wenyewe kila upande ukapoteza nusu ya askari wake; wale makamanda wote wawili, kila mmoja akidhani amewafukuza maadui, wakapeleka taarifa kwa Abdullah bin Muti usiku huo huo, hivyo wakatambua makosa yao. Hii ikasababisha kituo cha ukaguzi cha njia ya kuelekea nyumbani kwa Mukhtar kuachwa bila ulinzi. Mukhtar na Ibrahim wakajua yaliyojiri huko nje, na kwa muono wa jinsi hali halisi ilivyokuwa, hiyo wakaamua kutoka na kwenda wilaya nyingine kuwaita wafuasi wao. Mukhtar alitakiwa kuwafikishia ujumbe wafuasi wake wapatao 1400 kutoka wilaya ya Sakariya, na Ibrahim


30

akaenda wilaya nyingine kuwajulisha wafuasi wao juu ya mabadiliko ya mpango wao. Mukhtar akashauriwa asithubutu kujitokeza haraka kwani watamtambua. Mtu mmoja akiitwa Bashir akajitolea kwenda Sakariya. Akavaa nguo zilizochanika chanika na alipofika kwenye kituo cha ukaguzi cha Sakariya akasimamishwa na kuulizwa alifikaje hapo wakati kumetolewa amri ya kutotembea? Akasema kuwa yeye ni msafiri ametoka nje ya Kufa na amekuja kukutana na ndugu yake na alipofika njiani akaporwa na watu wa Mukhtar na wakamuibia mzigo wake, na akamlani Mukhtar na jeshi lake, kulaani huku kukapendwa na baadhi ya walinzi na wakamruhusu kuingia. Bashir alipoingia wilaya ya Sakariya akamjulisha kiongozi wa wilaya mabadiliko yaliyotokea kutokana na matukio. Kuogopa isiwe ni mtego, kiongozi huyo akamuuliza Bashir maswali kwa kina ili kuthibitisha utambulisho wake, na kumuuliza juu ya neno la siri la mawasiliano ambalo jibu lake ni watu wa karibu tu ya Mukhtar wangeweza kulitoa. Kiongozi huyo aliporidhika naye akawaamuru watu wa Sakariya watoke na kupigana kwenye vituo vya ukaguzi, wakiwa njiani kuelekea sehemu walipokubaliana kukutanika. Na baadhi yao wakaenda wilaya nyingine kueneza habari za mabadiliko ya mpango. Ibrahim naye akaelekea kwenye vituo mbalimbali vilivyokuwa vinaongozwa na wauaji maarufu wa Karbala, na kuwaondoa walinzi wakuu ambao ama waliuawa au kutoroka. Kwa mfano kwenye kituo cha kwanza Umar bin Hajjaj alikuwa na askari wapatao 500. Ibrahim alimuua Umar bin Hajjaj na baadhi ya askari wake, na wengi walikimbia. Kwenye kituo cha pili, Ibrahim alimuuwa Zahr Qays, Ibrahim aliendelea mbele kutoka wilaya moja hadi nyingine, lakini majeshi yake ya mwanzo ya watu wapatao 500 yaliendelea kupungua kutokana na mapigano, wakati huo huo majeshi ya upande wa adui yakawa yanaongezewa nguvu. Wakati huo huo habari zikaenea miongoni mwa wafuasi wa Mukhtar kuhusu kubadilika kwa mpango kwa hiyo wote wakatoka na kukutana kwenye Ikulu ya gavana. Ibrahim alikuwa katika pilikapilika ya kuwahamasisha watu na katika baadhi ya nyakati akakutana na watu waliobeba mabango yaliyoandikwa ‘‘Tokeni enyi wafuasi wa njia ya Husayn,’’ ambao wanamjulisha Ibrahim kwamba wana habari ya mabadiliko kwa sababu watu kutoka Sakariya walifika kwenye wilaya zao kuwafahamisha kuhusu hayo mabadiliko. Mukhtar Atawala Kufa Wakati wa alfajiri Mukhtar akamtuma mpelelezi aitwaye Said ili akatathmini hali ya Abdullah bin Muti. Alimletea taarifa kwamba Abdullah bin Muti na majeshi yake wamekusanyika nje ya msikiti karibu na Ikulu. Ilikuwa ni alifajiri ya Alhamisi, tarehe 13 Rabiul Awwal 66 AH, wakati pande zote mbili zilikuwa zimejitayarisha kwa vita huku ngoma za kuashiria vita zikipigwa kila mahali. Wakati vita baina ya pande mbili hizo inaendelea Abdullah bin Muti alikimbilia kwenye sehemu inayohusiana na usalama huko Ikulu huku akilindwa na walinzi wake. Mukhtar hakufanya jaribio lolote la kuivamia Ikulu, lakini akachagua sera ya kusubiri na kutizama. Baada ya siku tatu Ikulu ikawa na upungufu wa chakula, na Abdullah bin Muti akatuma barua kwa Mukhtar. Katika barua hiyo Abdullah bin Muti akamwambia Mukhtar: “Nakumbusha urafiki wetu, juu ya tulivyofanya kazi pamoja kusimika utawala wa Abdullah bin Zubair katika mji wa Makka na Madina, nilijaribu kutumia umaarufu wangu kumshawishi Abdullah bin Zubair kutimiza ahadi


31

yake ya kulipiza kisasi cha wauaji wa Karbala. Na pia kumbuka kwamba niliokoa maisha yako kwa kukupa usafiri na pesa ukaondoka Makka. Basi kwa kuwa nilisalimisha maisha yako wakati huo, na wewe unapaswa kusalimisha leo maisha yangu na niache huru niondoke zangu.” Mukhtar akamjibu kuwa: “Nakumbuka fadhila zako na deni lako, lakini kwa ukumbusho wako kwa kiburi na kujigamba, umebatilisha yale mema uliyonitendea. Hata hivyo nilikupa siku tatu za kutofanya vita dhidi yako. Tangu umekuwa gavana hapa, umechukua ushauri kutoka tu kwa maadui wa Ushia, lakini kama ungeshirikiana na mimi tungelikuwa tumekwishalipa kisasi kwa wauaji wa Karbala. Huna nia ya kunisaidia katika kazi hii na vitendo vyako vimekwisha sababisha vifo vya wafuasi wangu na Mashia.” Abdullah bin Muti sasa akajibu kwa unyenyekevu: “Kwa sasa nahitaji huruma yako, kwani mimi sikuhusika kwa namna yoyote katika mauaji ya Karbala. Tafadhali nisamehe kwa vitendo vyangu katika kushirikiana na upande wa maadui zako. Niache angalau niondoke katika mji wa Kufa nikiwa hai, sitakuletea matatizo tena.” Mukhtar akaomba ushauri kwa Ibrahim akamuelezea urafiki uliokuwepo baina yake na Abdullah bin Muti. Ibrahim akamwambia atamuunga mkono Mukhtar katika uamuzi wowote ambayo atakaoamua, Mukhtar akaamua kumwachia Abdullah Muti akiwa hai na akamtumia ujumbe kuwa anamruhusu kuondoka Ikulu usiku huo. Usiku Abdulla Muti akavaa nguo za kike akaondoka Ikulu na Mukhtar akamwambia kuwa kwa uhuru huo ameshalipa deni lake la wakati yeye alivyookoa maisha yake. Abdullah Muti akutorokea kwenye giza la usiku akitafuta hifadhi lakini hakupata mtu aliyekuwa tayari kumhifadhi; mwishowe mtu aitwaye Abu Musa al-Asha’ari alikubali kumpa hifadhi. Abdullah bin Muti sasa hakuwa na pesa wala usafiri kwa hiyo Mukhtar akampatia vyote, pesa na usafiri ili kumuwezesha aondoke hai katika mji wa Kufa. Mukhtar akamtumia ujumbe kuwa kwa kufanya hivyo ameshalipa kikamilifu deni alilokuwa anamdai wakati Abdullah bin Muti alipomuwezesha Mukhtar kumkimbia Abdullah bin Zubayr hapo Makka kwa kumpa usafiri na pesa. Baada ya Aballah bin Muti akafanikiwa kutoroka Kufa akiwa hai, na sasa Mukhtar akawa gavana wa Kufa. Alipoingia madarakani akawaita watu kwenye mkutano wa hadhara, akawajulisha watu nia yake ya kuchukua madaraka ni kulipiza kisasi dhidi ya wauaji wa Karbala. Kwa hiyo hatawabughudhi wala kuwadhuru watu wasio na hatia pia hatavumilia unyanyasaji wa baadhi ya watu kwa wengine, atatawala kwa haki na kufuata sharia za Kiislamu. Hatua za haraka za Mukhtar zilikuwa ni kuwatendea watu ubinadamu. Akawafungua jela wafungwa, akawasaidia masikini kuishi katika nyumba bora na wagonjwa kupata matibabu mazuri. Akawatambua na akahakikisha Bani Hashim waliomo Kufa wanahudumiwa vizuri baada ya miaka mingi ya mateso na kwamba sasa wanalipwa kwa haki lile fungu la masharifu katika Khums. Mapinduzi ndani ya Kufa yalitokea mnamo Rabiul Awwal 66 A.H na baada ya Hijja ya mwaka huo yaani Dhulhaji 66 A.H, Minhal al-Kufiy alikwenda Madina na kukutana na Imamu ZaynulAbidin (as). Imam Zaynul-Abidin (as) akamuuliza kuhus hali ilivyo huko Kufa. Minhal akajibu kwamba kwa Mukhtar kuwepo madarakani wauaji wa Karbala wanasakwa na kuuawa. Taarifa hii ilimfariji na kumfurahisha sana Imam Zaynul-Abidin (as).


32

Abdullah bin Muti Aungana na Jeshi la Musa’ab bin Zubair Abdullah bin Muti akawasili Basra ambapo Musa’ab bin Zubair (ndugu yake Abdullah bin Zubair) alikuwa gavana wa mji huo. Kwa kuwa Musa’ab alikuwa hamtaki Mukhtar awepo madarakani akamshawishi Abdullah bin Muti apigane dhidi ya Mukhtar kulipiza kisasi dhidi yake, kwa hiyo wakaamua waungane wapigane na Mukhtar na kundi lake. Musa’ab akamtanguliza Abdullah bin Muti aende mbele na kikosi cha jeshi na akamwambia kuwa atamfuata na nyongeza ya majeshi baada ya siku chache kwani anamalizia kuweka mambo yake sawa hapo Basra. Jeshi la Abdullah bin Muti, likaenda kupambana na Ibrahim na jeshi lake lililokuwa nje ya mipaka ya Kufa, kwa kuwa walikuwa ndio mstari wa mbele kulinda mji wa Kufa. Majeshi ya Abdullah bin Muti na Ibrahim yakakutana katika mji wa Nahrawan, na mapigano yakafuatia ambapo upande wa Abdullah bin Muti ukapata hasara kubwa. Usiku, Abdullah bin Muti akamtuma mpelelezi ili kutathmini hali ya jeshi la Ibrahim. Mpelelezi huyo akakamatwa na kuhojiwa na Ibrahim, akasema aliingizwa ndani ya jeshi huko Basra na wala hataki kujihusisha katika vita vyovyote. Ibrahim akamwambia madhumuni ya jeshi lake ni kulipiza kisasi dhidi ya wauwaji wa Karbala. Baada ya kujua ukweli ule, yule jasusi akabadili nia yake na akajiunga na Ibrahim. Akamwambia yuko tayari kumpeleka kwenye kambi ya Abdullah bin Muti ili kumvamia na kumuua. Ibrahim akajibadilisha na akafuatana na yule mpelelezi hadi kwenye hema la Abdullah bin Muti. Walinzi wakawasimamisha na wakamuuliza huyo anayefuatana naye ni nani. Mpelelezi huyo akadai ni rafiki yake lakini walinzi wakakataa kumwingiza bila ruhusa ya Abdullah bin Muti. Walinzi wakaenda kwenye hema la Abdullah bin Muti kutaka ruhusa, wakati huo alikuwa anaanza kusinzia akawambia wawaruhusu waingie kwani alikuwa anasubiri kwa hamu habari za upelelezi juu ya Ibrahim na jeshi lake. Hadi wanafika hemani, Abdallah bin Muti alikuwa ameshalala. Ibrahim akiwa tayari anataka kutoa upanga wake kumpiga, kelele zilisikika kutoka nje ya hema, hivyo Ibrahim akashindwa kumuua. Huyo alikuwa ni Musa’ab bin Zubair akiwasili na jeshi lake kuja kuongezea nguvu upande wa Abdullah bin Muti. Ibrahim akafanikiwa kuondoka na mpelelezi huyo bila kutambulika. Siku iliyofuata vita ikaanza, na Ibrahim akafanikiwa kumuua Abdullah bin Muti katika mapigano, Musa’ab bin Zubair akakimbia kurejea Basra. Ibrahim Al-Ashtar Akamatwa na Kutoroka Alipowasili Basra Musa’ab bin Zubair akamwandikia kaka yake Abdullah bin Zubair ambaye yupo Makka namna alivyoshindwa na jeshi la Ibrahim na kuuawa kwa Abdullah bin Muti. Abdullah bin Zubair akajibu kuwa anakabiliwa na matatizo kwa hiyo hawezi kutuma jeshi la kumsaidia. Kisha Musa’ab akamwandikia barua Abdul Malik bin Marwan bin Hakam ambaye alikuwa gavana wa Damascus, na akapata majibu mazuri. Abdul Malik akatuma jeshi la watu elfu sabini (70,000) chini ya ukamanda wa Amir bin Rabia kwenda Kufa kupambana na jeshi la Mukhtar na Ibrahim. Amir bin Rabia na jeshi lake likawasili na kuweka kambi nje ya mji wa Kufa.


33

Lilikuwepo kundi la wauaji kumi na nne waliokuwa wamepandikizwa ndani ya jeshi la Mukhtar ili wakipata nafasi nzuri wamuue Mukhtar. Amir bin Rabia akatuma mpelelezi aende ndani ya jeshi la Mukhtar na apeleke amri ya maandishi kwa hili kundi pandikizi kwamba sasa limuue Mukhtar. Jasusi huyu alitumwa kwa kisingizio kuwa amefukuzwa kutoka katika jeshi lake, akavaa nguo zilizochanika chanika, akieleza kwamba Amir bin Rabia alitaka kumuua lakini akafanikiwa kukimbia na hivyo anaomba apewe hifadhi na Mukhtar. Mukhtar akamuonea huruma huyu jasusi akampa nguo mpya na pesa kisha akamwacha huru. Jasusi huyo akaathirika na wema na ukarimu wa Mukhtar hivyo akamuonyesha ile barua ya amri aliyopewa na Amir bin Rabia na akamweleza juu ya hao mapandikizi 14 waliomo ndani ya jeshi la Mukhtar. Mapandikizi hao wakatambuliwa na kuuwawa. Yule jasusi akashauri mpango kwa Mukhtar kuwa atamchukua Mukhtar, akiwa amejibadilisha, kurudi naye kwa Amir bin Rabia. Wakifika huko, jasusi atamwambia Amir kwamba ile amri ameifikisha na kwamba mmoja kati ya hao mapandikizi yuko kitambo kidogo amekuja kuhakiki mwenyewe amri hiyo kwa Amir bin Rabia. Pia kwamba huyu pandikizi hatokwenda moja kwa moja kambini bali Amir amfuate kule, kwa udanganyifu huu Amir bin Rabia atakuja peke yake na hapo itakuwa rahisi kumshambulia. Mukhtar akakataa mpango huo na kuwaambia kwamba itakuwa rahisi kwa maadui kumtambua mara moja. Ama Ibrahim akapendezwa na mpango huo na siku inayofuata, yeye na yule jasusi wakaondoka na kwenda kuingia katika kambi ya Amir bin Rabia bila ya Mukhtar kujua. Yule jasusi na Ibrahim wakasimamishwa na walinzi wa Amir bin Rabia, wakamtambua yule jasusi kuwa ni miongoni mwa watu wao, lakini hawakumtambua aliyefuatana naye yaani Ibrahim. Kwa hiyo wote wawili wakakamatwa wakapelekwa kwa Amir bin Rabia. Amir bin Rabia akamtambua Ibrahim mara moja, pamoja na kujigeuza kwake, na akaamuru auawe, lakini msaidizi wake akamshauri amfunge jela usiku huo ili watu asubuhi washuhudie kuuawa kwa mtu huyu shujaa. Ibrahim na yule jasusi wakafungwa jela ambako walifungwa pingu na minyororo iliyokuwa imepigiliwa misumari chini tayari kwa kuuawa asubuhi yake. Yule mlinzi akasinzia akapata ndoto akamuona Imam Husayn (as), na matokeo yake akapata huruma kwa wale wafungwa, hivyo basi hakutaka kuhusika na kuendelea kumfunga jela Ibrahim. Kwa hiyo mlinzi huyo akafungua minyororo yote na pingu akawaacha huru Ibrahim na yule jasusi na akawaambia wakimbie mbali sana na haraka iwezekanavyo. Baada ya muda, mlinzi akapiga king’ora na kusema kwamba alipokagua jela alikuta wafungwa wametoroka. Ibrahim na jasusi wakaendelea kukimbia lakini kila mmoja akachukua njia yake ili kufuta dalili za mwelekeo wao. Ibrahim aliendelea kukimbia hadi asubuhi akakutana na jeshi linalomsaka, na hivyo akajificha juu ya mti mrefu. Hapo alimuona askari wa cheo cha juu kutokana na sare yake anakuja kupumzika chini ya mti huo huku anawalaani Mashia. Ibrahim akapata hasira, akashuka chini kutoka juu ya mti akamkabili na kumuona tu kwamba ni yule askari mwenye sifa mbaya kutoka katika jeshi la Syria aliyekuwa na Amir bin Rabia. Ibrahim akamuua na akamkata kichwa, akakichukua kichwa chake akar udi nacho hadi mji wa Kufa.


34

Wakati huo Mukhtar alikuwa na wasiwasi juu ya Ibrahim kwani aliondoka bila kuacha ujumbe wowote na alikuwa bado hajarudi kwa muda wa siku tatu. Mukhtar akaandaa jeshi la watu elfu thelathini (30,000) ili waende kumtafuta na kumsaidia Ibrahim. Jeshi likiwa tayari kuondoka, mara Ibrahim akaingia akiwa na kichwa cha kamanda aliyemkabili chini ya mti, na akamweleza Mukhtar yote yaliyotokea. Muda si mrefu akawasili yule jasusi akiwa na kichwa cha mmoja wa askari muuaji (kutoka kikosi cha Amir bin Rabia) ambaye aliyepambana naye katika mapigano. Mukhtar na Ibrahim walifurahi kwamba wameweza kuwaua watu wawili waovu wenye sifa mbaya, lakini Ibrahim akasema lazima aende kumsaidia yule mlinzi aliyemuokoa kwani bila shaka wakati huu atakuwa katika matatizo. Kabla Ibrahim hajaweza kuondoka, wakamuona yule mlinzi anakuja na akawaelezea jinsi alivyofanikiwa kutoroka: baada ya kumwacha huru Ibrahim na kutoa tahadhari ya kuashiria kutoroka kwa wafungwa, kwa kawaida Amir bin Rabia alimshuku moja kwa moja kwa usaliti, lakini mlinzi huyo akatunga uongo kuwa mhusika ni mshauri wake Amir bin Rabia, yule aliyemtaka aahirishe kuuawa kwa Ibrahim hadi asubuhi ya siku iliyofuata, huyo ndiye aliyehusika na kutoroka kwa Ibrahim. Huyu mlinzi alikuwa anafahamu wazi kuwa Amir bin Rabia si mtu hatari kama alivyo mshauri wake ambaye alielekeza kila kitu. Hivyo ilikuwa ni jambo lenye manufaa kummaliza mshauri huyu ambaye ni tishio kubwa kwa Mukhtar na Ibrahim. Amir hakuweza kujimiliki mbele ya uhaini kama huu wa mshauri wake, akaamrisha auawe, pamoja na yeye kulalamika na kuapa kwamba hahusiki. Ibrahim akachukua jeshi lake na kwenda kumaliza vita na Amir bin Rabia, na hatimaye wakarejea na ushindi. Kudhibiti Mji wa Mosul Ibrahim akamshauri Mukhtar kwamba kabla ya kuanza kazi ya kuwatafuta wauaji wa Karbala kwa bidii zote, kwanza wanatakiwa washike maeneo yanayowazunguuka na kuyaweka chini ya amri yao ili kuimarisha serikali yao. Mosul ilikuwa ni sehemu muhimu kimkakati hivyo wakaamua juu ya mbinu ya kufanya mji huu uwe chini ya udhibiti wao. Wakati huo Mosul ilikuwa inatawaliwa na Muhammad Ash’ath ambaye alikuwa adui mkali wa Ushia. Baba yake, Ash’ath bin Qays alisababisha matatizo makubwa kwa Imam Ali (as) na dada yake, Ju’dah binti Ash’ath ambaye alikuwa mke wa Imam Hasan (as) ndiye aliyemuua Imam kwa sumu. Hivyo Mukhtar na Ibrahim walikuwa wanatambua upinzani wataokabiliana nao dhidi ya Muhammad bin Ash’ath. Hivyo mpango ulikuwa kwanza ni kuwaita watu mashuhuri wa Kufa pamoja na makamanda wa jeshi wa vikosi vilivyokuwepo Karbala ambao wengi wao walikuwa wanaishi mjini Kufa. Mukhtar akawaita watu hawa na akawajulisha kwamba kauli zake na hotuba zake za awali kwamba anataka kulipiza kisasi dhidi ya wauaji wa Imam Husayn (as) ilikuwa tu ni mbinu ili apate madaraka. Na kwa kuwa ameshayapata, hima yake ni kuyahifadhi na kukusanya mali. Akawapa pesa nyingi na zawadi ili kuwakinaisha kuhusu ulafi wake wa utajiri na akaahidi kugawana nao ngawira yoyote ya zaida kutokana na vita. Baada ya siku chache Mukhtar akamwita mtoto wa Mohamed Ashath, Abdurahman bin Muhammad bin Ash’ath aliyekuwa anaishi Kufa na kumfanyia takrima kama Mfalme na kumpa pesa na zawadi nyingi na kumueleza kama alivyowaeleza watu wa Kufa wengineo. Baada ya siku kadha kupita, tena Mukhtar akamuita Abdurahman bin Muhammad bin Ash’ath, akamtuma apeleke ujumbe binafsi kwa baba yake, Muhammad bin Ash’ath katika mji wa Mosul. Ujumbe


35

huo ulikuwa unasema hivi: “Muhammad bin Ash’ath atoe kiapo cha uti kwa Mukhtar na malipo yake atampa ugavana wa Madain, jimbo ambalo ni kubwa na lenye nguvu kuliko Mosul.” Abdurahman akasafiri hadi Mosul na akakutana na baba yake na akampa ujumbe wa Mukhtar. Muhammad bin Ash’ath akastaajabu jinsi gani mwanaye anaweza kuleta ujumbe kama huo. Lakini mwanaye akamthibitishia kuwa Mukhtar amebadilika akamuonyesha ushahidi wa zawadi na pesa alizowapa yeye pamoja na wauaji wa Karbala wanaoishi Kufa. Muhammad bin Ash’ath akawataka ushauri washauri wake na wakamjibu kwamba aliyoahidiwa ni mazuri sana na hayafai kuyakataa kwa sababu mbili: Kwanza Madain kwa kweli ni jimbo kubwa zaidi lakini ya pili na muhimu zaidi ni kwamba kama Ubaydullah bin Ziyad yupo njiani kuja Mosul kuimarisha nguvu za utawala wa Abdul Malik bin Marwan (ambaye ni mtawala mpya wa Damascus), hivyo Mukhtar na Ibrahim watakuwa wanamtafuta Ubaydullah bin Ziyad hata ndani ya Mosul kwa kuungwa mkono au bila kuungwa mkono na Muhammad bin Ash’ath, na bila kutaka ataburuzwa na kuingizwa katika vita hivi. Hivyo Muhammad bin Ash’ath akachukua askari elfu nne (4000) na akaondoka Mosul kuelekea kwa Mukhtar katika mji wa Kufa. Watu wa Mosul wakapandwa na ghadhabu kuona gavana anakimbia na pesa zao zote walizolipa kama kodi. Wakamkabili Muhammad na kupigana na jeshi lake mpaka wakarejesha pesa zao zote. Bila pesa wala mamlaka, sasa Muhammad bin Ash’ath akajikuta analazimika kukubali ahadi (ofa) ya Mukhtar. Alipowasili mji wa Kufa Mukhtar akampokea kwa ukarimu na akampa pesa nyingi na nyumba huku akimuahidi kwamba baada ya muda mfupi atafanya matayarisho ya kumpeleka kuwa gavana wa Madain. Mukhtar akamchagua mtu aitwaye Abdurahman kuwa gavana mpya wa Mosul (sio mtoto wa Muhammad bin Ash’ath bali majina yanafanana). Wakati huo huo Abdul Malik bin Marwan kutoka Damascus akamtuma Hasin bin Namir pamoja na jeshi katika mji wa Mosul kumng’oa Abdurahman. Kikosi cha Hasin bin Namir kilikuwa ni cha kutangulia na baadae kifuatiwe na majeshi ya kuongeza nguvu yakiongozwa na Ubaydullah bin Ziyad mwenyewe, ambaye alikuwa anashughulika kusimika na kuimarisha utawala wa Abdul Malik hapo Damascus. Baada ya kusikia ujio wa Hasin, Abdurahman akakimbia kutoka Mosul hadi Tikrit na akatuma barua kwa Mukhtar kuwa hawezi kukabiliana na jeshi la Hasin bin Namir na kuwa apeleke gavana mwingine. Huko Kufa Zayd, ambaye alikuwa ni mzee na mgonjwa, alikuwa yuko tayari kusafiri kuelekea Mosul kukabiliana na Hasin bin Namir. Hii ni kwa sababu Zayd alikuwa amedhamiria kulipa kisasi dhidi ya Hasin bin Namir ambaye alimpiga mkuki uliomsababishia kifo Ali Akbar. Zayd na vikosi vyake wakaondoka kuelekea Mosul kukabiliana na Hasin Namir na wakati huo huo Ubaydullah bin Ziyad na jeshi lake wakaondoka Damascus kuelekea Mosul kumsaidia Hasin bin Namir. Majeshi ya pande mbili yalikutana njiani kuelekea Mosul na vita ikaanza hapa. Zayd akafariki kwa ugonjwa wake na jeshi lake likashindwa, huku Ubaydulla bin Ziyad akielekea Mosul akiwa mshindi. Huko Kufa Mukhtar akapata habari za vita hivyo na kushindwa kwa Zayd. Mukhtar na Ibrahim wakaweka mikakati ya kivita kwa kuamua kwamba badala ya kuwafuata wauaji wa Karbala sasa ni nafasi nzuri kumkamata Ubaydullah bin Ziyad huko Mosul kwani hata hivyo Ubaydullah bin Ziyad ndiye mhusika mkuu aliyepokea na kutekeleza amri ya Yazid ya mauaji ya


36

Karbala. Jeshi kubwa likakusanywa kwa kutumia pia majeshi ya akiba ili kuelekea Mosul chini ya kamanda mkuu Ibrahim kwa nia ya kummaliza kabisa Ubaydullah bin Ziyad. Ibrahim akapata wasiwasi hasa kwamba pamoja na majeshi yote ya akiba kuwa yametoka nje ya Kufa, Mukhtar amebaki bila ulinzi, na huku akiwa na maadui wengi ndani ya Kufa. Kwa hiyo wakaona njia nzuri ni kuwataka watu mashuhuri wa Kufa na wauaji wa Karbala wawatoe wasaidizi wao wa nyumbani kwenda kusaidia kwenye Ikulu ya Mukhtar kwa kisingizio cha kumlinda Mukhtar, ili kupunguza uwezekano wa wauaji hawa kufanya mashambulizi ya ghafla. Wauaji wakakubali mpango huo kwa kuwa walikuwa na dhamira toka awali ya kupata habari za kuaminika juu ya harakati za Mukhtar. Ibrahim pamoja na jeshi kubwa lililokusanyika likiwemo na la akiba wakaelekea katika mji wa Mosul ili kukabiliana na Ubaydullah bin Ziyad. Jaribio la Kumuua Mukhtar Baada ya Mukhtar kuachwa bila ulinzi, Shabath bin Rabi aliyekuwa mmojawapo wa makamanda wa Karbala na pia aliyetumwa na Abdulla bin Muti ili kupigana na jeshi la Mukhtar usiku wa mapinduzi katika mji wa Kufa, alikwenda kwa Umar bin Saad akamwambia kuwa huu ndio wakati mzuri wa kumuua Mukhtar, kwa sababu hana ulinzi, na wakaona kwamba kama Ibrahim akirudi na ushindi, Mukhtar atakuwa na nguvu nyingi zaidi, na tena itakuwa vigumu kumuua. Umar bin Saad akawaita viongozi wa vikosi vya jeshi waliokuwa Karbala kutaka ushauri wao. Wote walikwenda kwa Muhammad bin Ash’ath (wakati huo alikuwa yupo katika mji wa Kufa), ili kupata ushauri na ridhaa. Muhammad bin Ash’ath akakataa mpango huo kwa kudhani kuwa Mukhtar lazima atakuwa na kikosi cha akiba kisichotangazwa kinachomlinda. Muhammad bin Ash’ath pia akawashauri kuwa wasimshambulie Mukhtar, kwa sababu ana maadui wengi wenye nguvu ambao wanamuwinda kumuua kama Ubaydullah bin Ziyad, Abdullah bin Zubair, Abdul Malik na Musa’ab bin Zubair, na hivyo haitachukua muda kwa watu hawa kumkamata na kummaliza Mukhtar. Umar bin Saad na kundi la watu wakaamua kuhakiki kama Mukhtar analo jeshi la akiba lisilofahamika. Mpango ukawa ni mmoja wao aende kwa Mukhtar amwambie kuwa ugavana wake ni batili na hatambuliwi na Abdullah bin Zubair na kwamba watu wa Kufa wanataka kutoa kiapo cha utii kwa Abdullah bin Zubair. Iwapo Mukhtar atajibu kwa upole, atakuwa anaogopa kusababisha uhasama na yeyote yule kwa wakati huo, ikimaanisha kuwa hana ulinzi wowote wa akiba. Kama akijibu kwa kujiamini basi atakuwa na akiba ya ulinzi. Hivyo walisubiri siku tatu baada ya Ibrahim kuondoka mji wa Kufa (kwani itakuwa vigumu kwa Mukhtar kumuita kwa haraka Ibrahim arudi), ndipo Shabath bin Rabi akaenda kwa Mukhtar akamwambia kuwa watu wa Kufa hawataki ugavana wake na kwamba aondoke Ikulu. Mukhtar akamuuliza watu hao wanachokipinga ni nini? Shabath bin Rabi akasema kwa mfano hawafurahishwi kwa Mukhtar kuwaweka watumishi wao wa nyumbani ndani ya Ikulu yake. Mukhtar akamwambia yuko tayari wao waje wawachukue watumishi hao na kwamba Mukhtar atawapa ruhusa waondoke. Shabath bin Rabi akawaarifu kundi lake kuwa Mukhtar amejibu kwa upole, hivyo inaonyesha kuwa hana jeshi la akiba la kumsaidia na kumlinda. Muhammad bin Ash’ath naye akaridhika sasa kuwa Mukhtar hana jeshi lililofichwa la kumlinda, kwa hiyo akakubaliana na wauaji kuwa sasa ni wakati mwafaka kuanza kumshambulia Mukhtar,


37

usiku huo Umar bin Saad na kundi lake wakawaita wafuasi wao wakutane nje ya Ikulu ya Mukhtar na huku wakitumaini watu wao waliomo ndani ya Ikulu watakuwa upande wao. Wakati huo Mukhtar aliwaita wasaidizi na kuwaambia kuwa mabwana wao wanawataka warejee na kuwa yeye yuko tayari kuwaachia waondoke. Watu wale wakakataa kuondoka na wakasema kwa vile wamefanikiwa kutoka mikononi mwa mabwana zao, hawatarejea kwao tena bali wataendelea kubaki na Mukhtar. Mukhtar akawaambia kubaki kwao inaweza ikamaanisha kupigana hadi kufa, wakasema wanakubali na wapo tayari. Mukhtar akamtuma msaidizi wake aitwae Khayr kwa Ibrahim akiwa na ujumbe usemao: “Mahali popote ulipo, jambo lolote unalofanya, na kwa mazingira yoyote yale, wacha kila kitu na njoo moja kwa moja haraka Kufa kwani hapa hali imekuwa mbaya na maisha yangu yapo hatarini, ninahofia kwamba kama nitauawa, basi wauaji wa Imam Husayn hawatalipiziwa kisasi.” Ibrahim alipopata barua akarudi haraka na jeshi lake. Hakupumzika vya kutosha yeye na jeshi lake na farasi wake ila kidogo tu, kwa hiyo safari ya siku tatu ya kurejea akaifanya kwa siku moja. Muhammad bin Ash’ath, Umar bin Saad na kundi lake walikuwa tayari wameizunguka Ikulu ya Mukhtar. Mukhtar akajaribu kuzuia mashambulizi; yeye binafsi akatoka kupigana lakini akazidiwa sana kwa idadi na jeshi la maadui. Wakati huu Ibrahim na jeshi lake wakawasili, hawakutarajiwa na maadui kurudi kwa siku mbili nyingine (sababu safari ilikuwa ina siku tatu kabla ya Shabath bin Rabi kumkabili Mukhtar) na kuwasili kwa ghafla kwa Ibrahim na jeshi lake kuliwashitukiza maadui. Ibrahim na jeshi lake walikuwa wamechoka kwa safari ya kurudi nyumbani kwa haraka lakini wakapigana na maadui. Ibrahim akamtaka Muhammad bin Ash’ath abarizi kwa vita ya mtu mmoja kwa mmoja lakini akaogopa na akakataa, kwa sababu ya woga hakuna hata mmoja katika jeshi la adui aliyekuwa tayari kumkabili Ibrahim. Muhammad bin Ash’ath na watu wachache wakafanikiwa kutoroka wakakimbilia mji wa Qadisiya. Ibrahim na baadhi ya wanajeshi wake wakawafukuza. Muhammad bin Ash’ath akakimbilia katika nyumba moja akawekwa chini ya ulinzi kwa muda, wakati huo huo Ibrahim akirejea kwa haraka Kufa kwa Mukhtar. Usiku huo Muhammad bin Ash’ath akajigeuza na kujifanya kama mwanamke, akavaa mavazi ya kike akapanda punda na akaondoka kupitia mlango wa nyuma bila kushambuliwa na kukimbilia Mosul. Njiani akakutana na Ubaydullah bin Ziyad akamueleza yote yanayoendelea. Mukhtar Awafuata Wauaji wa Karbala Ibrahim aliporudi Kufa, Mukhtar akaamua kwanza amuache Ubaydullah bin Ziyad kwa muda, kwani hilo linamshughulisha sana bila mafanikio ya haraka. Mukhtar akamwambia Ibrahim kuwa sasa ni wakati mwafaka kuwasaka watu walioshiriki katika mauaji ya Karbala. Na hivi sasa watashitukizwa kwa kuwa wanadhani lengo letu la kwanza ni kumkamata Ubaydullah bin Ziyad. Mukhtar akamwita mmoja wa makamanda wake mahiri aliyeitwa Abdullah bin Kamil akampa mamlaka kamili na amri ya kwamba: “Zingira na zuia kabisa mji wa Kufa, na kwamba hakuna mtu yoyote awezaye kutoka au kuingia ndani ya mji wa Kufa, bila kupitia kwa askari wetu.”


38

Kwa jeshi kufanikiwa kudhibiti vyema mji wa Kufa, Mukhtar na Ibrahim wakatoa amri wakamatwe watu wote waliohusika katika mauaji ya Karbala na wapelekwe Ikulu. Kama alivyofikiria Mukhtar, wauaji wa Karbala wakapata mshituko kwani hawakutarajia watazingirwa katika mji wa Kufa, walidhani Mukhtar na Ibrahim wapo katika pilikapilika za kumsaka Ubaydullah bin Ziyad. Walikamatwa watu waliohusika na mauwaji ya Karbala na kupelekwa Ikulu, Mukhtar na IbrahimWaliwataka waeleze ni nini walikifanya kule, kwa njia hii watu wasio na hatia hawakuadhibiwa dhabu ya kifo na pia hivi ndivyo zilivyopatikana habari za uhakika za ukatili walioufanya Karbala nyingi zaidi moja kwa moja kutoka kwenye vinywa vya wauwaji wenyewe. Na pia udhuru wa kwamba “Nilikuwa chini ya amri,”haukukubaliwa na Mukhtar kwani watu walikuwa na nafasi ya kuacha upande muovu na kujiunga na upande wa haki kama alivyofanya Hurr na wengine wachache. Watu wawili wa mwanzo kukamatwa ni Abdullah bin Asad na Malik bin Bashir. Abdullah alikuwa miongoni mwa watu waliounguza mahema na kumpora Imam Husayn (as) kilemba chake baada ya kufariki. Mukhtar akaamrisha Abdullah bin Asad akatwe mikono yake na miguu yake na ikamfanya atapetape kwa maumivu na kufa. Ama Malik bin Bashir alikuwa ndiye alimpora Imam Husayn (as) upanga wake, Mukhtar akaamuru auwawe kwa njia hiyo hiyo. Aliyefuatia kukamatwa ni Nafii bin Malik. Alikuwa mmojawapo wa makamanda wa Umar bin Saad aliyekuwa kiongozi wa askari waliokuwa wanalinda kingo za mto Furati na kuhakikisha upande wa Imam Husayn (as) haupati hata tone la maji. Ni yeye ndiye aliyeamrisha mfuko wa maji wa Sayyidna Abbas utobolewe kwa mshale, Mukhtar akaamuru Nafii auawe. Baada ya siku chache wengi wa wauaji wa Karbala walikamatwa na wakasailiwa na wenye hatia kuuawa kwa amri ya Mukhtar. Abdullah bin Kamil alikuwa sasa anawatafuta wauaji wakuu kama Khuuli, Sinan, Hurmula, Shimr na Umar bin Saad. Abdullah bin Kamil na watu wake walikwenda kupekua nyumbani kwake Khuuli lakini hawakumkuta. Khuuli alikuwa na wake wawili; mmoja mwenyeji wa Kufa na mwingine anatoka Syria. Huyu mke Msyria ambaye alikuwa dhidi ya Shia alipoulizwa akasema Khuuli yupo nje ya mji wa Kufa. Ama huyu mke mwingine mwenyeji wa mji wa Kufa alikuwa ni Shia akasema kama mwenzake lakini kwa uangalifu wa tahadhari akaonyesha kidole chake kuashiria kwenye dari (riwaya nyingine kwenye choo sehemu ya chini). Kwa hiyo msako zaidi ukaendelea na kumkuta amejificha sehemu ya siri ndani ya dari. Abdullah bin Kamil akamchukua Khuuli na wake zake wawili hadi kwa Mukhtar. Khuuli akafungwa jela wakati wake zake wakihojiwa kwanza na Mukhtar: Akamuuliza yule mke mwenyeji wa Kufa kwa nini ameonyesha alipojificha Khuuli. Akajibu kuwa yeye ni Shia, na kwamba siku moja, yule mwanamke Msyria alikuja kwake akiimba na kucheza na akisema kuwa ana furaha sana kwa kuwa Khuuli ameleta kichwa cha Imam Husayn (as) na kukiweka kwenye sehemu wanayokokea moto, na kwamba yeye mwanamke wa Kufa alikichukua kichwa hicho kutoka kwenye jiko na kuanza kuomboleza na kukihuzunikia juu yake. Kisha Mukhtar akamhoji yule mke Msyria na akakubali madai ya matendo yake na akasema Yazid alikuwa ni Khalifa wake. Mukhtar akaamrisha mwili wake ukatwekatwe. Yule mwanamke mwenyeji wa Kufa akapewa pesa na kuachwa huru. Khuuli akaletwa mahakamani, na baada ya kujitetea mwanzoni kwamba ‘Nilikuwa ninatii amri tu,’ na kadhalika, kisha akakiri alifanya


39

yafuatayo miongoni mwa madhambi aliyofanya: “Alikuwa kiongozi wa kikosi cha wapiga mishale, na yeye ndiye alitoa amri ya kupiga mishale kama mvua, akamvua Sukaina hijabu yake, akamvuta hereni kutoka katika tundu za masikio yake, akampiga Imam Zaynul-Abidin (as) kwa fimbo huku akiwa katika hali ya kuzimia na akamburuza chini kutoka kwenye kitanda, na aliiba mablanketi aliyokuwa amefunikwa Imamu mgonjwa, na alimvua hijabu bibi Zaynab na hereni zake.” Mukhtar akaamrisha Khuuli akatwe miguu na mikono kisha atupwe akiwa hai ndani ya moto aungue hadi afe. Kisha wakafuatwa viongozi kumi waliomkanyaga kanyaga Imam Husayn (as) na farasi nao wakakamatwa. Wakahojiwa kisha wakafungwa wakalazwa chini kisha wakakanyagwa kanyagwa na farasi hadi wakafa. Wahalifu wa Karbala wengine wengi waliletwa mbele ya Mukhtar na kuhojiwa na waliokutwa na hatia waliuliwa. Kwa muda mfupi, pamoja na msako kuendelea kuna wahalifu ilishindikana kuwakamata kwa sababu watu maarufu na wenye nguvu wa Kufa walikuwa wanawalinda kwa kuwapa hifadhi ndani ya nyumba zao. Mukhtar akatoa amri wakamatwe wahalifu hata kama wakiwa katika nyumba za watu mashuhuri na wenye nguvu. Abdullah bin Kamil akapata habari kuwa Hakim bin Tufail muuwaji wa Saydina Abbas yupo chini ya ulinzi wa Adi bin Hakim at-Tai, mtu maarufu na mwenye nguvu sana katika mji wa Kufa. Abdullah bin Kamil alikwenda na watu wake hadi nyumbani kwa Adi at-Tai na akamkamata Hakim bin Tufail, wakati huo Adi at-Tai hakuwepo nyumbani lakini akapata habari ya kukamatwa kwa Tufail. Adi at-Tai akaenda moja kwa moja kwa Mukhtar kwa kutaka aachiwe Hakim bin Tufail kwa kudai kuwa yupo chini ya ulinzi wake na hifadhi yake, wakati huo huo Abdullah bin Kamil aliingia na kichwa cha Hakim bin Tufail na akaeleza kwamba njiani watu waliposikia kuwa muuwaji wa Saydina Abbas amekamatwa walishindwa kuzuia hasira zao na mara moja tu wakamuua. Habari nyingine zinasema kwamba, watu walipojua kwamba kama Hakim bin Tufail atafika kizimbani akiwa hai (hususan wakati Adi at-Tai tayari yupo mahakamani kupinga kukamatwa kwa Hakim bin Tufail) basi kuna uwezekano kwamba atasamehewa, kwa sababu ya shinikizo ambamo Mukhtar atakuwemo chini ya umaarufu mkubwa wa Adi at-Tai, hivyo watu wakaamua kumuua. Baada ya kuona kuwa hakuna msaada wowote licha ya kuingilia kati kwa mtu maarufu kama Adi at-Tai, wale wauaji wakuu wote (kama Shimr, Sinan, Hurmula, Umar bin Saad) waliobakia wakapatwa na hofu sana kuhusu maisha yao. Sinan akafanikiwa kutoroka kutoka mji wa Kufa hadi katika mji wa Zihad ambapo aliwaomba watu wampe hifadhi lakini watu wakakataa kwa kuogopa kuwa Mukhtar akijua kama wauaji wamepewa ulinzi na wao maisha yao yatakuwa hatarini, kwa hiyo Sinan akaondoka. Baada ya kuondoka watu wengine wakapinga kutokupewa hifadhi Sinan, kwa hiyo wakamfuata ili wamrudishe katika mji wao. Sinan alipoona watu wanamkimbilia, akafikiri kuwa ni askari wa Mukhtar hivyo akaanza kuwarushia mishale, watu hawa wakakasirika kwa sababu walitaka kumpa hifadhi, na yeye anadiriki kuwashambulia, kwa hiyo watu wakamrudishia mishale na kisha wakamkamata na kumpeleka kwa Mukhtar. Sinan alifikishwa katika hadhara ya Mukhtar na kukiri kwamba miongoni mwa madhambi aliyoyafanya ni: “Alijaribu kuiba mkanda wa Imam Husayn (as) muda mchache kabla hajafariki, lakini Imam Husayn (as) akawa anauzuia kwa mikono yake, mkanda huu alishonewa na mama yake Bibi Fatima (as), hivyo yeye Sinan alimkata Imam Husayn (as) mikono ili aupate mkanda ule.” Mukhtar akatoa amri kwamba vidole vya Sinan vikatwe kimoja kimoja, kisha akatwe


40

viwiko vya mikono kisha mikono yote, kisha miguu na kisha atupwe ndani ya moto aunguwe hadi afe. Wauwaji wakuu wengine sasa walikuwa wanatetemeka kwa hofu kubwa na kuogopa hasa baada ya kuona tukio la Hakim bin Tufail na Sinan, kwa hiyo wakakutana wauaji wote na kupanga mpango wa kutoroka kutoka mji wa Kufa. Shimr alijaribu kutoroka lakini alishikwa na kuuliwa. Hurmula akakamatwa na kuletwa katika hadhara ya Mukhtar. Hurmula akakiri kuwa miongoni mwa ukatili alioufanya ni: “Alitoboa kwa mshale mfuko wa maji alioubeba Sayyidna Abbas, alimdunga Ali Asghar kwenye shingo yake teke mshale wenye ncha tatu uliomuua, pia alimpiga mshale Imam Husayn (as) kwenye paji la uso katika dakika zake za mwisho za uhai wake, hii ikasababisha Imam Husayn (as) kuanguka chini.” Mukhtar akaamrisha mikono yake na miguu ikatwe na apigwe na mishale hadi afe. Umar bin Saad anasema tangu mwanzo alikwenda kutafuta hifadhi kwa Abdullah bin Ju’da alHubayra ambaye alikuwa ni rafiki wa karibu wa Imam Ali (as) na hivyo Mukhtar angeheshimu ulinzi huo. Pindi Abdullah bin Ju’da al-Hubayra alipoingilia kati kwa ajili ya Umar bin Saad, Mukhtar (akiwa na mpango kichwani mwake) alikubali kwa shingo upande msamaha wa Umar bin Saad kwa sharti kwamba asijihusishe na uhalifu wowote na wala asiondoke nje ya mji wa Kufa. Hata hivyo, baadaye Mukhtar alimuamuru Abdullah bin Kamil kumkamata muuaji wa Karbala, ambaye sifa zake zinaafikiana na Umar bin Saad, lakini bila kumtaja kwa jina lake. Mmoja katika jamaa zake Umar bin Saad aliyekuwa katika hadhara ile kwa wakati ule akasikia maelezo ya Mukhtar na akamtumia ujumbe Umar bin Saad kuwa akimbie kwani imeshatolewa amri ya kukamatwa kwake. Umar bin Saad akamtafuta mtu ambaye atamsaidia kumtorosha kutoka katika mji wa Kufa kwa siri. Mtu mmoja akamshauri kwamba kuna jamaa mmoja katika Bani Tamim ambaye ni mhandisi aliyehusika na mpango-mji wa Kufa, yeye anaweza kumtoa Umar bin Saad nje ya mji. Huyu mhandisi akafuatwa lakini hakuambiwa sababu wala utambulisho wa mtu anayetaka kuondoka nje ya mipaka ya Kufa. Huyu mhandisi akampeleka kwenye mipaka ya mji wa Kufa, kule watu wakamshauri Umar bin Saad bora arudi Kufa kwani kukimbia atakuwa anavunja mkataba wa ahadi yake na yule anayemuhifadhi (ya kubaki ndani ya Kufa), na hivyo kumpa mwanya Mukhtar kumsaka na kumkamata. Huyu mhandisi akatambua ujanja uliofanywa juu yake na akasema kuwa atamuarifu Mukhtar, kwa hiyo Umar bin Saad kwa shingo upande akarudi Kufa na kwa mhifadhi wake yaani Abdullah bin Ju’da al-Hubayra. Lakini al-Hubayra naye sasa akakataa kuendelea kumhifadhi Umar bin Saad kwa sababu amevunja ahadi yake ya kutokimbia kutoka mji wa Kufa. Baada ya Mukhtar kupata taarifa za yote yaliyotokea, alikwenda kwa Abdullah bin Ju’da alHubayra na kumwambia kuwa Umar bin Saad sasa anaweza kukamatwa kwa vile kuna uvunjaji wa ahadi kwamba Umar bin Saad hatajaribu kutoroka katika mji wa Kufa. Umar bin Saad sasa akabuni ujanja mwingine ili asiuawe, alikwenda kwa mmoja wa wake zake ambaye alikuwa dada yake Mukhtar na akamtaka aingilie kati kumsaidia. Akamjibu kuwa hajamuona Mukhtar kwa muda mrefu kutokana na vitendo vya Umar bin Saad, lakini Umar bin Saad akamsihi na kumuomba ajaribu kumtetea. Dada yake Mukhtar alikwenda kwa Mukhtar lakini Mukhtar akashangaa kumuona kwani hawakuwa na mawasiliano wakati alipokuwa bado ni mke wa Umar


41

bin Saad, Mukhtar akamwambia dada yake kuwa anapaswa kuona aibu kuendelea kuwa mke wa Umar Saad. Dada yake akajibu kuwa alikuwa anafikiria kumuua Umar bin Saad kwani alikuwa adui dhidi ya Mashia na mfuasi wa Ubaydullah bin Ziyad, lakini wakati huo Mukhtar alikuwa yupo jela kwa amri ya Ubaydullah bin Ziyad na iwapo angemuua mume wake, basi Ubaydullah bin Ziyad asingelimsamehe na asingelimuacha huru Mukhtar hata kwa mapendekezo ya Abdullah bin Umar. Mukhtar akamshauri dada yake asirudi tena kwa Umar bin Saad kwani ni punde tu atakamatwa. Umar bin Saad aliyekuwa kamanda mkuu huko Karbala, na kiongozi wa ukatili wote uliofanyiwa kizazi cha Mtume akakamatwa, na Mukhtar akaamrisha kwa mujibu wa sheria za kisasi naye apewe mateso angalau yanayolingana na aliyoamuru huko Karbala, 2 kucha zake zikang’olewa, Mukhtar binafsi akamtoboa macho yake kama yeye alivyotoboa jicho la Abbas na akakata kipande cha nyama kutoka kwenye paja lake na kisha Mukhtar akawaita wapiga mikuki ili wamchome Umar bin Saad hadi afariki kama walivyomjaza Imam mikuki na mshale kama nungunungu. Kumsaka Ubaydullah bin Ziyad Mukhtar sasa akajizatiti juu ya kumkamata Ubaydullah bin Ziyad kwa kuwa yeye ndiye aliyekuwa mpangaji msanifu wa mauaji ya Karbala. Pamoja na Ubaydullah bin Ziyad pia walikuwapo Hasin Namir na Shabath bin Rabi. Mukhtar akamwambia Ibrahim akusanye jeshi na aelekee Mosul ili kumkamata Ubaydullah bin Ziyad, kwa hiyo wakaagwa kwa wingi mno na watu wa Kufa kwani wote walikuwa wakiomba ushindi upatikane na akamatwe Ubaydullah bin Ziyad. Njiani kuelekea Mosul Ibrahim alipigana na maadui wa Shia waliokuwa wanatamani Ubaydullah bin Ziyad apate ushindi dhidi ya Mukhtar. Ibrahim alijitayarisha kwa vita dhidi ya upande wa Ubaydullah bin Ziyad na aliweka kambi yake maili 15 kutoka mji wa Mosul karibu na mji mdogo wa Mawari ambao alikuwepo Nasiben, huyu alikuwa ni chifu wa kabila la Hanzala, alifurahi sana kumuona kwani mtawala huyu alikuwa ni mpenzi wa Mashia. Nasiben akamwambia Ibrahim kuwa masaa mawili yaliyopita Ubaydullah bin Ziyad alipita katika mji huo na akamuomba Nasiben aihifadhi familia yake katika usalama kwani yeye Ubaydullah bin Ziyad anakwenda kupigana vita na Ibrahim na hataki familia yake ipate madhara. Nasiben ambaye pia alipendelea kuona maovu ya Karbala yakilipiziwa kisasi akampeleka Ibrahim katika nyumba alimoihifadhi familia ya Ubaydullah bin Ziyad. Ibrahim akaamrisha wote watoke nje. Akamuua kijana mkubwa wa miaka ishirini ili kulipiza kisasi cha watoto wa Imam Husayn (as). Jeshi la Ibrahim kwa mara moja likawauwa askari wake wote waliobakia. Nasiben akapanga kumpeleka Ibrahim katika hema la Ubaydullah bin Ziyad ambapo itakuwa rahisi kumuua ili kuepuka umwagaji mkubwa wa damu. Nasiben akaenda na Ibrahim (huku akiwa amejigeuza) hadi kwenye hema la Ubaydullah bin Ziyad. Nasiben akamwambia kuwa amekuja kumjulisha Ubaydullah bin Ziyad hali ya familia yake, Ubaydullah bin Ziyad 2

Qur’ani 16: 126


42

akamruhusu aingie na mwenzie (Ibrahim ambaye alikuwa amejibadilisha). Nasiben akawa anaongea na Ubaydullah bin Ziyad ili ampe nafasi Ibrahim ya kumshambulia. Nasiben akamwambia Ibn Ziyad kwamba tangu aondoke, yeye amesikia kuwa Ibrahim yupo njiani naye, Nasiben ana hofu juu ya familia ya Ubaydullah bin Ziyad, Ubaydullah bin Ziyad akasema kuwa atatuma majeshi ya ziada kuilinda nyumba waliomo familia yake. Nasiben akaona Ibrahim hakufanya jaribio la shambulio lolote hivyo akaamua waondoke, Ibrahim akamwambia ilikuwa haiwezekani kumshambulia Ubaydullah bin Ziyad bila walinzi wa nje kuja kwa haraka kumsaidia na kumuokoa, kwa hiyo jaribio hilo lilikuwa sawa na kujiua. Ibrahim akarudi kwenye kambi yake, na pande zote mbili zikawa zinajitayarisha kwa vita inayofuata. Kesho yake vita ikaanza na ikaendelea kwa muda wa siku tatu. Miongoni mwa watu waliouliwa baada ya vita ya siku tatu ni Hasin bin Namir ambaye alikuwa ni mmoja wa makamanda wa Karbala na ndiye aliyemuumiza vibaya Ali Akbar. Siku ya nne ya vita ilikuwa ni tarehe 10 Muharram 67 AH. Mahali ilipopiganiwa vita hii ni kwenye ukingo wa mto Tigris karibu na mji wa Mosul. Vita iliendelea na matokeo yake yalikuwa: Ubaydullah bin Ziyad alipoteza watu 80,000 akabaki na jeshi la watu 20,000 ambao walirudi nyuma. Ibrahim alipoteza askari 7000 ambapo jumla alikuwa na askari 24,000. Kuuawa kwa Ubaydullah bin Ziyad kunaelezwa na riwaya mbili. Riwaya ya kwanza inasema Ibrahim alimuona mtu anakimbia kwa haraka na farasi, akamkimbiza na akakumbwa na harufu ya ambari na miski, ni Ubaydullah bin Ziyad pekee ndiye anaweza kujipaka manukato wakati wa vita; (Ubaydullah bin Ziyad alipoweka kichwa cha Imam Husayn (as) juu ya miguu yake, tone ya damu kutoka kwenye kichwa cha Imam Husayn (as) lilidondokea juu ya paja la Ubaydullah bin Ziyad lililosababisha donda ndugu ambalo lilikuwa linatoa harufu mbaya, kwa hiyo Ubaydullah bin Ziyad alikuwa anatumia marashi makali ili kupunguza harufu mbaya ya donda hilo). Hivyo Ibrahim akabaini kuwa ni Ubaydullah bin Ziyad ambaye anakimbia, haraka akamuua. Baada ya kumalizika vita Ibrahim na watu wake walikwenda kuthibitisha na wakakuta kweli ni Ubaydullah bin Ziyad na hivyo akamkata kichwa chake. Riwaya ya pili inasema kuwa Ibrahim na Ubaydullah bin Ziyad walipigana vita ya mtu mmoja kwa mmoja, na Ubaydullah bin Ziyad akakamatwa akiwa mzima. Akavunjwa miguu yake miwili, magoti yakavunjwa, maungio ya nyonga yakavunjwa, mikono ikakatwa, kichwa kikanyolewa, macho yakachopolewa, midomo ikakatwa, mashavu yakakatwa, kisha nyama yake akalishwa yeye mwenyewe kinywani mwake na baadaye akapigwa mikuki mingi kwa nguvu sana hadi kufa huku mwili wake ukiwa vipande vidogo vidogo. Na hatimaye Ibrahim na jeshi lake wakaenda katika mji wa Mosul wakiwa washindi na kukaribishwa kwa furaha na wakazi wa mji huo. Ibrahim akatuma kichwa cha Ubaydulah bin Ziyad kwa Mukhtar katika mji wa Kufa. Mukhtar akakitendea kichwa cha Ubaydullah kama vile Ubaydullah alivyokitendea kichwa cha Imam Husayn (as). Alikipandisha juu ya ncha ya mkuki na kukitembeza mji mzima, na akaweka kichwa cha Ubaydullah siku tatu kwenye ule ule mlango wa uwanja kilipowekwa kichwa cha Imam Husayn (as) ili watu wote wakishuhudie. Watu walioshuhudia wanasema kwa muda wa siku hizo, walimuona nyoka akimtambaa kutoka mdomoni kupitia puani huku akimdonoa nyama yake. Mukhtar akakituma kichwa cha Ubaydullah kwa Muhammad Hanafiya mjini Makka.


43

Wakati huo Imam Zaynul-Abidin (as) alikuwa yupo Makka, na Muhammd Hanafiya akakipeleka kwa Imam Zaynul-Abidin (as), ilikuwa ni tarehe 9 Rabiul Awwal 67 AH. Mukhtar Auwawa Wakati Musa’ab bin Zubair pamoja na Abdullah bin Muti waliposhindwa dhidi ya Ibrahim bin Malik al-Ashtar, Musa’ab bin Zubair alikimbilia katika mji wa Basra, Muhammad bin Ash’ath akaungana naye huko Basra. Mukhtar nia yake ilikuwa ni Muhammad bin Ash’ath akamatwe lakini hakuwa na ugomvi na Musa’ab bin Zubair. Mukhtar akatuma barua kwa Musa’ab bin Zubair amrejeshe Muhammad bin Ash’ath ahukumiwe la sivyo itatokea vita. Musa’ab bin Zubair akajibu kwamba hawezi kumsalimisha Muhammad bin Ash’ath na akamwandikia ndugu yake Abdullah bin Zubair, mtawala wa Makka, kwamba anahitaji msaada kupambana na jeshi la Mukhtar pindi litakapokuja. Abdullah bin Zubair akatuma majeshi ya msaada yapatayo 15,000 chini ya kamanda aitwaye Muhlab, mmoja wa magavana wa jimbo waliokuwa chini ya utawala wake. Muhlab akamshauri Musa’ab bin Zubair asubiri kwa muda kwani Abdul Malik kutoka Damascus atalipiza kisasi kwa Ibrahim, na bila Ibrahim Mukhtar atakamatwa kwa urahisi. Musa’ab bin Zubair hakukubaliana na wazo hilo lakini akamwandikia Ibrahim kuwa atampa pesa na madaraka makubwa iwapo atajiunga na Musa’ab bin Zubair dhidi ya Mukhtar. Bila shaka Ibrahim akakataa na akamjulisha Musa’ab bin Zubair kuwa hayupo tayari kufanya hivyo pia akampelekea ujumbe Mukhtar akimjulisha yanayojiri na kwamba Musa’ab bin Zubair anafanya matayarisho ya vita. Musa’ab akaweka kambi yake ya jeshi nje kidogo tu ya mji wa Basra. Mukhtar akaweka kambi yake ya jeshi nje ya mji wa Kufa huku akimsubiri Ibrahim aliyemuomba aje ajiunge pamoja naye. Ibrahim akajibu hawezi kuja kwani Abdul Malik ameuzunguka mji wa Mosul na anaelekea katika mji huo akiwa na askari 40,000. Ibrahim akamshauri Mukhtar asiondoke ndani ya mji wa Kufa bali apeleke msaidizi aongoze jeshi dhidi ya Musa’ab bin Zubair, kwa njia hii mji wa Kufa utakuwa umedhibitiwa chini ya Mukhtar na mji wa Mosul utakuwa umedhibitiwa chini ya ulinzi wa Ibrahim. Mukhtar akamchagua Ahmad bin Shomit na Abdullah bin Kamil kuwa makamanda wake akawatuma kuelekea katika mji wa Basra. Wakati huo huo Mukhtar akarejea katika mji wa Kufa, hii ilikuwa katika mwezi Jamadil Awwal 67 AH. Masa’ab na jeshi lake pia wakaelekea mbele na pande zote mbili zikapiga kambi karibu na mji wa Madar, takriban robo tatu ya masafa ya njia kutoka katika mji wa Kufa kuelekea katika mji wa Basra. Siku iliyofuata vita vikaanza, Ahmad bin Shomit katika mizunguko miwili akapata ushindi kwa kuwaua maadui na kuweza kulirudisha nyuma jeshi la Musa’ab bin Zubair. Musa’ab akamtuma jasusi aende kutathmini idadi ya askari katika jeshi la Mukhtar na iwapo Mukhtar mwenyewe yupo. Jasusi akaleta taarifa kuwa idadi ya askari ni wachache na Mukhtar hayupo pamoja nao, habari ikamfariji Musa’ab bin Zubair. Abdullah bin Kamil akaingia kwenye medani ya vita na akaweza kutia hasara majeshi ya Musa’ab bin Zubair. Muhammad bin Ash’ath akaumia na kukimbia kutoka katika uwanja wa vita. Ahmad bin Shomit na kikosi chake


44

wakarudi kwenye uwanja wa mapambano. Musa’ab bin Zubair akamkusudia Ahmad bin Shomit na akaamuru wamzunguke na kumshambulia kwa pamoja, kisha wakamuua. Abdullah bin Kamil na watu wake wakavunjika moyo kwa kuuawa Ahmad bin Shomit, lakini wakaendelea kupigana kishujaa ingawa Musa’ab bin Zubair alianzisha mashambulizi pande mbili; kwa mbele na kwa nyuma ambayo yalimpa ushindi. Abdullah bin Kamil na watu wake wakarudi Kufa wakiwa wameshindwa. Musa’ab bin Zubair aliposhinda vita akaelekea katika mji wa Kufa huku akijiamini. Watu wa Kufa wakawa na huzuni ya kushindwa na kufariki kwa Ahmad bin Shomit licha ya kuliwazwa na kuhamasishwa na Mukhtar. Musa’ab bin Zubair akamtumia barua Mukhtar akimtaka ajisalimishe. Mukhtar na makamanda wake waliopo katika mji wa Kufa wakakataa kujisalimisha wakaamua kuendelea kupigana. Mukhtar akajibu kuwa hawatajisalimisha, akachukua jeshi la watu wapatao elfu ishirini akapiga kambi mpakani mwa mji wa Kufa mahali pakiitwa Harura, na hapo pande zote mbili zikawa tayari kwa ajili ya vita. Mukhtar akapanga mtego ili kupunguza idadi ya askari wa Musa’ab bin Zubair. Mtego wenyewe ni kuwa Mukhtar atakuwa analumbana na anaongea kwa sauti ya juu na mmoja wa makamanda wake aitwae Muhammad bin Saad, kuwa aende mara moja kushambulia upande wa Musa’ab bin Zubair, na Muhammad bin Saad ajifanye kuwa anakataa na amuache Mukhtar na kuondoka na kundi la jeshi lake, mpango ulikuwa Musa’ab akipata taarifa za kutokubaliana na kutengana, atamfuata Muhammad bin Saad, ambapo Mukhtar atashambulia kwa kushtukiza kutokea nyuma. Siku iliyofuata mpango ulikwenda katika utekelezaji na Musa’ab bin Zubair akaangukia ndani ya mtego na akatuma mmoja wa makamanda wake aitwae Rabia na askari wapatao 5000 ili kumshambulia Muhammad bin Saad. Wakavamiwa kutokea nyuma na askari wa Mukhtar na wote wakauawa. Vita vikali vikaendelea baina ya pande hizi mbili lakini hakuna upande uliopata ushindi wa kuridhisha. Siku ya pili vita ikaendelea, katika siku ya tatu Mukhtar mwenyewe akaingia vitani kupigana, Muhammad bin Ash’ath akauawa, Musa’ab bin Zubair akaanzisha mashambulizi makali dhidi ya askari wa Mukhtar, Mukhtar akapoteza idadi ya watu na kurudi nyuma kuelekea Kufa, na ni askari takriban 6000 ndio waliokuwa wamebaki katika jeshi lake. Musa’ab bin Zubair akawafuata na kuuzingira mji wa Kufa pamoja na mipaka yake. Ilikuwa hakuna mahitaji yanayoweza kuingia hivyo watu wakavunjika moyo, na wakakataa kuitika mwito wa Mukhtar wa kuendelea kupigana, wakaona ni bora wajisalimishe kwa Musa’ab bin Zubair kuliko kuendelea kupigana na kuwa na maisha magumu. Musa’ab bin Zubair aliposikia kuhusu kuvunjika moyo na uasi wa watu wa Kufa akaingia katika mji wa Kufa kwa nia ya kuizingira Ikulu ya Mukhtar. Abdullah bin Hatim alikuwa ni chifu wa palepale Kufa, akaja na askari 4000 shujaa wakaweza kupunguza mashambulizi ya Musa’ab bin Zubair ili asiweze kuingia katika wilaya ya Kanasa iliopo ndani ya mji wa Kufa. Wakawaua askari 1000 wa Musa’ab bin Zubair na baadaye Abdullah bin Hatim na askari wake wote wakauawa. Katika Ikulu ya gavana, Mukhtar alibaki tu na idadi ndogo sana ya rafiki zake wa karibu takribani watu thelathini ambao walikuwa tayari kumhami Mukhtar. Walipigana kwa ushujaa


45

mpaka wote wakauliwa. Ama wale elfu sita waliorejea Kufa, walimsaliti Mukhtar lakini baadae wote waliuliwa kwa amri ya Musa’ab bin Zubair. Mukhtar akaendelea kupigana vikali na jeshi lake lote likauliwa hadi akabaki yeye peke yake wakamuua na kumkata kichwa. Ilikuwa ni tarehe 15 Ramadhan 67 AH. (Mukhtar aliingia madarakani tarehe 14 Rabiul Awwal 66 AH kama gavana wa Kufa kwa lengo la kulipa kisasi dhidi ya wauaji wa Karbala). Mukhtar alizikwa nyuma ya kaburi la Muslim bin Aqil katika mji wa Kufa, kaburi lake limepakana na msikiti wa Kufa, na ni mahali ambapo watu huwa wanakwenda kuzuru na kutoa heshima zao. Taarifa zinasema kwamba Mukhtar aliweza kuwafikisha kwenye haki wauaji 18,000 wa Karbala na kuhukumiwa wakati wa Ugavana wake. Musa’ab bin Zubair alipeleka kichwa cha Mukhtar kwa Abdullah bin Zubair huko Makka. Historia inaarifu kuwa baadaye na yeye akauliwa na majeshi ya Abdul Malik bin Marwan bin alHakam gavana wa Damascus, kichwa cha Musa’ab bin Zubair nacho kikapelekwa kwa Abdul Malik aliyekuwepo kwa wakati huo ndani ya Ikulu ya gavana hapo katika mji wa Kufa. Mzee mmoja aliyekuwa katika baraza ya Ikulu ya Kufa aliyeshuhudia yaliyokuwa yakiendelea akasema: katika baraza hii hii ya Kufa niliona kichwa cha Imam Husayn (as) kikiletwa mbele ya Ubaydullah bin Ziyad, na kichwa cha Ubaydullah bin Ziyad kikiletwa mbele ya Mukhtar, na kichwa cha Mukhtar kikiletwa mbele ya Musa’ab bin Zubair, na sasa kichwa cha Musa’ab bin Zubair mbele ya Abdul Malik. Abdul Malik aliposikia hivi akaona kuwa uwanja ule ndani ya Ikulu ya Kufa ni ishara mbaya akatoa amri Ikulu ya gavana ichomwe moto. MWISHO ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION `1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9. 10. 11. 12.

Qur'an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Thelathini Uharamisho wa Riba Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili Hekaya za Bahlul Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.) Hijab vazi Bora Ukweli wa Shia Ithnaashari Madhambi Makuu Mbingu imenikirimu Abdallah Ibn Saba


46 13. 14. 15. 16. 17. 18. 19. 20. 21. 22. 23. 24. 25. 26. 27. 28. 29. 30. 31. 32. 33. 34. 35. 36. 37. 38. 39 40. 41. 42. 43. 44. 45. 46. 47. 48. 49. 50. 51. 52. 53. 54.

Khadijatul Kubra Utumwa Umakini katika Swala Misingi ya Maarifa Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia Bilal wa Afrika Abudharr Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu Salman Farsi Ammar Yasir Qur'an na Hadithi Elimu ya Nafsi Yajue Madhehebu ya Shia Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur'an Tukufu Al-Wahda Ponyo kutoka katika Qur'an Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii Mashukio ya Akhera Al Amali Dua Indal Ahlul Bayt Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna. Haki za wanawake katika Uislamu Mwenyezi Mungu na sifa zake Kumswalia Mtume (s) Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) Adhana Upendo katika Ukristo na Uislamu Tiba ya Maradhi ya Kimaadili Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu Kupaka juu ya khofu Kukusanya swala mbili Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Kusujudu juu ya udongo Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s) Tarawehe Malumbano baina ya Sunni na Shia Kupunguza Swala safarini Kufungua safarini Umaasumu wa Manabii Qur’an inatoa changamoto as-Salaatu Khayrun Mina -'n Nawm


47 55. 56. 57. 58. 59. 60. 61. 62. 63. 64. 65. 66. 67. 68. 69. 70. 71. 72. 73. 74. 75. 76. 77. 78. 79. 80. 81. 82. 83. 84. 85. 86. 87. 88. 89. 90. 91. 92. 93. 94. 95. 96.

Uadilifu wa Masahaba Dua e Kumayl Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mtume Muhammad (s) Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili Kuzuru Makaburi Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita Tujifunze Misingi Ya Dini Sala ni Nguzo ya Dini Mikesha Ya Peshawar Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu Ubora wa Imam 'Ali Juu ya Maswahaba Na Ushia ndio njia iliyonyooka Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake Liqaa-u-llaah Muhammad (s) Mtume wa Allah Amani na Jihadi Katika Uislamu Uislamu Ulienea Vipi? Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) Urejeo (al-Raja’a ) Mazingira Utokezo (al - Badau) Hukumu ya kujenga juu ya makaburi Swala ya maiti na kumlilia maiti Uislamu na Uwingi wa Dini Mtoto mwema Adabu za Sokoni Johari za hekima kwa vijana Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu Tawasali Imam Mahdi katika Usunni na Ushia Hukumu za Mgonjwa


48 97. 98. 99. 100. 101. 102 103. 104. 105. 106. 107. 108. 109. 110. 111. 112. 113. 114. 115. 116. 117. 118. 119. 120. 121. 122. 123. 124. 125. 126. 127. 128. 129. 130. 131. 132. 133. 134. 135. 136. 137. 138.

Sadaka yenye kuendelea Msahafu wa Imam Ali Ngano ya kwamba Qur’ani imebadilishwa Idil Ghadiri Kusoma sura zenye Sijda ya wajibu Hukumu zinazomuhusu mkuu wa kazi na Mfanyakazi Huduma ya Afya katika Uislamu Sunan an-Nabii Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza) Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili) Shahiid Mfiadini Kumsalia Nabii (s.a.w) Ujumbe -Sehemu ya Kwanza Ujumbe - Sehemu ya Pili Ujumbe - Sehemu ya Tatu Ujumbe - Sehemu ya Nne Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu Hadithi ya Thaqalain Ndoa ya Mutaa Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza Ukweli uliopotea sehemu ya Pili Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu Ukweli uliopotea sehemu ya Nne Ukweli uliopotea sehemu ya Tano Mkutano wa Maulamaa wa Baghdad Safari ya kuifuata Nuru Fatima al-Zahra Myahudi wa Kimataifa Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi Visa vya kweli sehemu ya Kwanza Visa vya kweli sehemu ya Pili Elimu ya Ghaibu ya Maimamu Mwanadamu na Mustakabali wake Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Kwanza) Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Pili) Khairul Bariyyah Uislamu na mafunzo ya kimalezi Vijana ni Hazina ya Uislamu Yafaayo kijamii Tabaruku Taqiyya Vikao vya furaha


49 139. 140. 141. 142. 143. 144. 145. 146. 147. 148. 149. 150. 151. 152. 153 154. 155. 156. 157. 158. 159. 160. 161. 162. 163. 164. 165. 166. 167. 168. 169. 170. 171. 172. 173. 174. 175. 176. 177. 178. 179. 180.

Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje? Visa vya wachamungu Falsafa ya Dini Azadari-Kuhuzunika na Kuomboleza Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah Mtazamo Mpya - Wanawake katika Uislamu Kuonekana kwa Allah Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza) Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili) Ndugu na Jirani Ushia ndani ya Usunni Maswali na Majibu Mafunzo ya hukmu za ibada Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 1 Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 2 Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 3 Abu Huraira Vipengee kadhaa katika Swala ya Jamaa na Msikiti. Mazingatio kutoka katika Qur’an - Sehemu ya Kwanza Mazingatio kutoka kaitka Qur’an - Sehemu ya Pili Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya kwanza Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya Pili Qur’ani Tukufu – Pamoja na Tarjuma ya Kiswahili Falsafa ya Mageuzi ya Imam Husein (a.s) Amali za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani Elimu ya Tiba za Kiislamu - Matibabu ya Maimamu Uislamu Safi Majlisi za Imam Husein Majumbani Je, Kufunga Mikono Uislam wa Shia Amali za Makka Amali za Madina Asili ya Madhehebu katika Uislamu Sira ya Imam Ali kuhusu Waasi Ukweli uliofichika katika neno la Allah Uislamu na Mifumo ya Uchumi Umoja wa Kiislamu na Furaha Mas’ala ya Kifiqhi Jifunze kusoma Qur’ani As-Sahifatul Kamilah as-Sajjadiyyah Hayya ‘Alaa Khayri’l-’Amal Katika Adhana Ukweli kuhusu Funga ya Siku ya Ashura


50 181. 182. 183. 184. 185. 186. 187. 188. 189. 190. 191. 192. 193. 194. 195. 196. 197. 198. 199. 200. 201. 202. 203. 204. 205. 206. 207. 208. 209. 210. 211. 212. 213. 214. 215. 216. 217. 218. 219. 220.

Dua za Miezi Mitatu Mitukufu (Rajabu, Shaabani na Ramadhani) Uadilifu katika Uislamu Mahdi katika Sunna Maswali Ya Uchunguzi Kuhusu Uislam Kazi na Bidii ni njia ya maendeleo Abu Talib – Jabali Imara la Imani Ujenzi na Utakaso wa Nafsi Vijana na Matarajio ya Baadaye Usalafi – Historia yake, maana yake na lengo lake Ushia – Hoja na Majibu Mateso ya Dhuria wa Mtume (saww) Maombolezo – Msiba wa Bwana wa Mashahidi (a.s.) Shahidi kwa Ajili ya Ubinadamu Takwa Mwonekano wa Upotoshaji katika Hazina ya Kiislamu Amirul Muuminina (‘as) na Makhalifa Uongozi na Utawala katika Mwenendo wa Imam ‘Ali (‘a) Kuvunja hoja iliyotumika kutetea Uimamu wa AbuBakr Adabu za vikao na mazungumzo Hija ya Kuaga Uwazi baina ya Maslahi na Vikwazo Fadhila za watukufu watano katika Sahih Sita Mdahalo baina ya Mwanachuoni wa Kisunni na Mwanachuoni wa Kishia (AlMuraja’aat) Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (as) Upotoshaji dhahiri katika Turathi (Hazina) ya Kiislamu Mtazamo kuhusu msuguano wa Kimadhehebu Nchi na Uraia – Haki na wajibu kwa Taifa Mtazamo wa Ibn Taymiyyah juu ya Imam Ali (as) Uongozi wa Kidini – Maelekezo na Utekelezaji wa Kijamii Maadili ya Ashura Mshumaa – Shahidi na Kifo cha Kishahidi Mizani ya Hekima – Hadithi za Ahlul Bait (as) – Sehemu ya Kwanza Imam Ali na Mambo ya Umma Imam Ali na Mfumo wa Usawa Kuvunja Hoja Iliyotumika Kutetea Uimamu wa Abu Bakr Mfumo wa Wilaya Vipi Tutaishinda Hofu? Kumswalia Mtume ni Ufunguo wa Utatuzi wa Matatizo Maeneo ya Umma na Mali Zake Nahjul-Balagha – Majmua ya Khutba, Amri, Barua, Risala, Mawaidha na Semi za Amirul-Muuminin Ali bin Abu Talib (a.s.)


51 221.

Mukhtar – Shujaa aliyelipiza kisasi dhidi ya wauaji wa Imam Husein (as) hapo Karbala

KOPI NNE ZIFUATAZO ZIMETAFSIRIWA KWA LUGHA KINYARWANDA

1. 2. 3. 4.

Amateka Na Aba'Khalifa Nyuma yaho naje kuyoboka Amavu n’amavuko by’ubushiya Shiya na Hadithi

ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION KWA LUGHA YA KIFARANSA

1.

Livre Islamique

BACK COVER Mukhtar: Mtu aliyelipa kisasi kwa kupigana na kuwaua wale vinara wote walioshiriki katika mauaji ya mjukuu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) Imam Husain (a.s.) pale Karbala. Jina lake kamili ni: Mukhtar Abu Ubaida Masuud Thaqafi kutoka katika kabila la Banu Hawazin. Alizaliwa mwaka wa kwanza wa Hijria. Mama yake alikuwa akiitwa Husna, (riwaya nyingine zinasema aliitwa Hilya). Baba yake aliitwa Abu Ubaida Thaqafi. Alikuwa na dada yake mmoja jina lake Safia aliyekuwa mke wa Abdullah bin Umar, mtoto wa khalifa wa pili, Umar bin Khattab. Dada yake mwingine alikuwa mke wa Umar bin Saad, kamanda wa jeshi la Yazid katika Karbala. Mmoja wa binti zake aliolewa na Imam Zaynul Abidin (a.s.) na wakapata mtoto aliyeitwa Umar. Kutokana na kazi yake maalumu iliyofanikiwa ya kulipiza kisasi cha maadui wa Imam Husain (a.s.), zilizuka habari nyingi za kupotosha kuhusu maisha yake kwa wakati ule, kwa mfano, watu


52

walidai alitoka katika familia duni isiyostahiki kuheshimika, n.k., bali yeye alitoka katika kabila tukufu la Banu Hawazin, ambapo pia walitoka watu watukufu kama utakavyoona ndani ya kitabu hiki. Kimetolewa na kuchapishwa na: Al-Itrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 / 2127555 Barua Pepe: alitrah@yahoo.com Tovuti: www.ibn-tv-com Katika mtandao: w.w.w.alitrah.info Kwa Kushirikiana na: The World Federation of KSIMC, Islamic Centre, Wood Lane, Stanmore, Middlesex, HA7 4LQ, United Kingdom T: +44 (0) 20 8954 9881 | F: +44 (0) 20 8954 9034 E: secretariat@world-federation.org Registered Charity in the UK No. 282303.


53


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.