Ndoa ya Mutaa Dr.Kanju.qxd
7/15/2011
11:35 AM
Page A
NDOA YA MUTAA Kimeandikwa na: Sheikh Abdul Karim Bahbahani
Kimetarjumiwa na: Amiri Mussa Kea
Ndoa ya Mutaa Dr.Kanju.qxd
7/15/2011
11:35 AM
Page B
ŠHaki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: 978 - 9987 - 512 - 63 - 8
Kimeandikwa na: Sheikh Abdul Karim Bahbahani
Kimetarjumiwa na: Amiri Mussa Kea
Kimepangwa katika Kompyuta na: Hajat Pili Rajab
Toleo la kwanza: Augasti, 2009 Nakala: 1000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Nukushi: +255 22 2127555 Barua Pepe: alitrah@raha.com Tovuti: www.alitrah.org Katika mtandao: www.alitrah.info
Ndoa ya Mutaa Dr.Kanju.qxd
7/15/2011
11:35 AM
Page C
YALIYOMO Utangulizi..........................................................................................2
Dondoo ya Kwanza Ndoa ya Mut’aa katika Qur’an na Sunna..........................................4
Dondoo ya Pili Je! Ni kweli hukumu ya ndoa ya Mut’aa imefutwa..........................8
Dondoo ya Tatu Msimamo wa masahaba na Tabiina kuhusu ndoa ya Muta’a..........13 Je ndoa ya Mut’aa ni zinaa.............................................................18 Tija...................................................................................................19
Ndoa ya Mutaa Dr.Kanju.qxd
7/15/2011
11:35 AM
Page D
Ndoa ya Mutaa
NENO LA MCHAPISHAJI Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabu kwa jina la az-Zawaaju ‘l-Muwaqqat kilichoandikwa na Sheikh Abdul Karim Al-Bahbahani. Sisi tumekiita, Ndoa ya Mutaa. Kitabu hiki ni matokeo ya kazi ya kielimu iliyofanywa na mwanachuoni huyu wa Kiislamu - Sheikh Abdul Karim al-Bahbahani. Kumekuwepo na zogo kubwa katika miji yetu ya Kiislamu kuhusu suala hili la ndoa ya mutaa (mut‘ah) (ndoa ya muda); baadhi wanasema ni sahihi na wengine wanasema sio sahihi kwa kuifananisha ndoa hii na zinaa. Mwandishi wa kitabu hiki kwa kutumia Qur’ani Tukufu, Sunna na hoja za kiakili na elimu ameonesha kwa wazi kabisa kwamba ndoa hii ni halali, na kwamba ilikuwepo tangu zama za Mtukufu Mtume (s.a.w.) na ikaendelea wakati wa ukhalifa wa Abu Bakr na kipindi cha mwanzo wa ukhalifa wa Umar ambaye akaipiga marufuku. Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote. Kutokana na ukweli huu, Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili, ili kuongeza ujuzi wao katika masuala ya dini na ya kijamii. Tunamshukuru ndugu yetu, Sheikh Amiri Mussa Kea kwa kukubali jukumu hili la kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake. Mchapishaji: Al-Itrah Foundation S. L. P. 19701 Dar-es-Salaam, Tanzania. D
Ndoa ya Mutaa Dr.Kanju.qxd
7/15/2011
11:35 AM
Page E
Ndoa ya Mutaa
AHLUL-BAYT KATIKA QUR’ANII TUKUFU Mwenyezi Mungu anasema:
“Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu watu wa nyumba (ya Mtume) na (anataka) kukutakaseni sana sana”. (33:33)
AHLUL-BAYT KATIKA HADITHI Mtume (s.a.w.w) amesema: “Hakika mimi nawaachieni vizito viwili, Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi Changu, ndugu zangu wa karibu, iwapo mtashikamana navyo hamtapotea kamwe baada yangu”.1
1 Rejea: Sahih zote na Musnad zote. E
Ndoa ya Mutaa Dr.Kanju.qxd
7/15/2011
11:35 AM
Page F
NENO LA JUMUIYA Hakika mirathi ya Ahlul-Bait ambayo imehifadhiwa na kambi yao na wafuasi wao dhidi ya upotovu inaonyesha ni kambi iliyokusanya aina mbalimbali za taaluma za kiislamu. Kambi hii imeweza kulea nafsi mbalimbali zilizo tayari kunywa kutoka kwenye chemchemu hiyo, na kuupa umma wa kiislamu wanavyuoni wakubwa wenye kufuata nyayo za ujumbe wa Ahlul-Bait. Wanavyuoni waliokusanya vidodosa na maswali mbalimbali ya madhehebu na mitazamo tofauti ya kifikira kuanzia ndani ya desturi ya kiisilamu hadi nje ya desturi hiyo, huku wao wakitoa majibu na utatuzi makini juu ya maswali hayo ndani ya karne zote. Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bait imefanya hima kutetea tukufu za ujumbe wa Uislamu na ukweli wake ambao umechafuliwa na makundi, madhehebu na wanaharakati mbalimbali wenye chuki na Uislamu. Jumuiya imefuata nyayo za Ahlul-Bait na za wafuasi wa kambi yao njema ambayo imefanya hima kujibu madai yenye kuendelea na daima ikajaribu kubaki ndani ya msitari wa mapambano kwa kiwango kinachohitajika ndani ya kila zama. Hakika uzoefu ambao umehifadhiwa ndani ya vitabu vya wanavyuoni wa kambi ya Ahlul-Bait katika dhamira hii ni wa aina ya pekee, kwa sababu una akiba ya kielimu inayotegemea akili na hoja, huku ukijiepusha na matamanio na upendeleo uliokatazwa. Unazungumza na wasomi na wanafikra wenye fani maalumu, mazungumzo ambayo yanakubalika kiakili na yanapokewa na maumbile yaliyo salama.
Ndoa ya Mutaa Dr.Kanju.qxd
7/15/2011
11:35 AM
Page G
Jaribio hili la Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bait limekuja kuwapa watafuta ukweli hatua mpya ya uzoefu wa thamani katika ulingo wa mazungumzo na maswali na kujibu hoja za utata zilizotolewa zama zilizopita au zinazotolewa leo kwa njia ya Tovuti, na hasa kwa kupewa nguvu na baadhi ya duru zenye chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu. Ikijiepusha na uchochezi uliokatazwa, na ni yenye kuhangaikia kuzishauri akili zenye kufikiria na nafsi zenye kutafuta haki, ili ziweze kufikia kwenye haki ambayo inatolewa na Kambi ya Ahlul-Bayt ulimwengu mzima, ndani ya zama ambazo akili inaerevuka na nafsi na roho zinaboreka kwa kasi ya pekee. Ni lazima tugusie kuwa mfululizo huu wa tafiti hizi umeandaliwa na Kamati maalumu toka jopo la wanavyuoni watukufu, hivyo tunatoa shukurani njema kwa hawa wote na kwa wasomi na wahakiki kwa kila mmoja miongoni mwao kupitia sehemu ya tafiti hizi na kutoa mchango wao wa thamani kuhusu tafiti hizi. Na sote tunategemea na kutaraji kuwa tutakuwa tumetoa kile tulichokiweza katika juhudi za kutekeleza baadhi ya wajibu tulionao mbele ya ujumbe wa Mtukufu Mola wetu Mlezi ambaye alimtuma Mtume Wake na uongofu na dini ya haki ili aipe ushindi dhidi ya dini zote. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa shahidi.
Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bayt Kitengo cha utamaduni
Ndoa ya Mutaa Dr.Kanju.qxd
7/15/2011
11:35 AM
H
Page H
Ndoa ya Mutaa Dr.Kanju.qxd
7/15/2011
11:35 AM
Page 1
Ndoa ya Mutaa Dr.Kanju.qxd
7/15/2011
11:35 AM
Page 2
Ndoa ya Mutaa
UTANGULIZI Uislamu umefanya ndoa kuwa sheria katika aina mbili: Mosi: Ndoa ya daima, ambayo hii huzingatiwa kuwa ni jambo muhimu katika Uislamu, na aina hii ya ndoa ndiyo ya kwanza kuanzishwa na kufanywa kuwa sheria. Pili: Ndoa ya Muta’a, ambayo ina malengo na mikakati kabambe katika kuleta amani na utulivu katika jamii kwa kuepusha madhara, tabia mbaya na mambo machafu yatokanayo na Zinaa, iwapo mtu hataweza na kuwa vigumu kwake ndoa ya daima na hali malengo ya kimantiki na yanayokubalika kisheria yanamsukuma katika hilo. Kwa hakika ndoa ya Muta’a inashirikiana na ndoa ya daima katika kudhibiti matamanio na kuyaelekeza katika njia ya halali, kuhifadhi kizazi na kukinga mchanganyiko wa kifamilia, huleta heshima, hali kadhalika huepusha uasharati. Na inaachana nayo katika upande wa pili ambao haugusi kiini cha ndoa, hivyo katika ndoa ya Muta’a Akdi, Mahari na Eda, Muda huwa ni vyenye mipaka maalumu, na kuondoka wajibu wa matumizi na mirathi. Kwa hakika ndoa hii imethibiti kisheria kwa mujibu wa Qur’ani na Sunna za bwana Mtume (s.a.w.w.), hakuna hata mwislamu mmoja awezaye kusema ndoa hiyo haikuwepo zama za Mtume (s.a.w.w.), na mpingaji wa hilo hasemi lolote ila hukimbilia kusisitiza kuwa aliyekataza jambo hilo ni Khalifa wa pili Umar bin Khatwab, yeye ndiye aliyekataza na aliahidi kutoa adhabu kali kwa mwenye kuthubutu kufanya hivyo, na hatimaye Kambi ya Kisunni ikamfuata ikitegemea kanuni yake isemayo: “Matendo ya masahaba ni hoja,” na wapo waliosema kwamba hukumu ya ndoa hiyo imefutwa. 2
Ndoa ya Mutaa Dr.Kanju.qxd
7/15/2011
11:35 AM
Page 3
Ndoa ya Mutaa Kwa hivyo ili kuupa usahihi msimamo wake juu ya ndoa hiyo, yalizuka madai na hoja mbalimbali kwamba ndoa hiyo iliharamishwa tangu zama za Mtume (s.a.w.w), na kwamba Qur’ani imefuta hukumu ya Aya inayohalalisha ndoa hiyo. Katika kuweka bayana mchakato huu unaohusu suala muhimu la kisheria hapana budi kubainisha dondoo tatu, nazo ni: Dondoo ya Kwanza: Ndoa ya Muta’a katika Qur’ani na Sunna. Dondoo ya Pili: Je! ni kweli ndoa ya Muta’a imefutwa? Dondoo ya Tatu: Msimamo wa Masahaba na Tabiina (kizazi kilichokuja baada ya Masahaba) kuhusiana na ndoa ya Muta’a. ***
3
Ndoa ya Mutaa Dr.Kanju.qxd
7/15/2011
11:35 AM
Page 4
Ndoa ya Mutaa
DONDOO YA KWANZA Ndoa ya Muta’a katika Qur’ani na Sunna Waislamu wote wanakubaliana kwamba Mwenyezi Mungu ameiruhusu ndoa hii na kuifanya kuwa ni sheria katika Uislamu, pamoja na ihtilafu zilizopo baina ya wanachuoni wa Madhehebu ya kiislamu, lakini hakuna yeyote mwenye shaka juu ya hilo, bali huenda asili ya sheria hiyo ni jambo la msingi kama yalivyo mambo mengine ya msingi katika dini. Qur’ani tukufu inajulisha ruhusa ya jambo hilo, vivyo hivyo zimepokewa hadithi mutawatiri chungu nzima zinazothibitisha kuthibiti jambo hilo hata kwa yule ambaye anadai kwamba imefutwa. Qur’ani tukufu inasema:
“Ambao mmestarehe nao katika wao, basi wapeni mahari yao yaliyolazimu.” (Sura Nisai:24). Ubayy bin Kaab, Ibn Abbas, Said bin Jubeir, Ibn Mas’ud na Sady walikuwa wakisoma Aya hiyo kama ifutavyo: “Basi mtakapostarehe nao hadi muda maalum.” Twabari ameeleza hayo katika kitabu chake Tafsirul-Kabiir, aidha Zamakhshari ameeleza katika tafsiri yake Al-Kashaf kisomo hicho, hali kadhalika ameeleza Razi katika tafsiri yake, vilevile yameelezwa hayo katika kitabu Sharh Sahih Muslim cha Nawawi mwanzoni mwa mlango wa ndoa ya Muta’a.
4
Ndoa ya Mutaa Dr.Kanju.qxd
7/15/2011
11:35 AM
Page 5
Ndoa ya Mutaa Imam Ahmad bin Hanbali ameunga mkono hayo katika Musnad yake, Abu Bakr Jaswas katika kitabu Ahkamul Qur’ani, Abu Bakr Bayhaqi katika kitabu chake Sunanul Kubra, Kadhi Baydhawi katika Tafsiir yake, Ibn Kathiir katika Tafsiir yake, Jalalu Dini Suyutwi katika kitabu chake Durrul Manthuur, Kadhi Shawkani katika Tafsiir yake, Shahab Dini Aluusi katika Tafsiir yake, wote kwa pamoja wamethibitisha kwamba Aya hiyo imeteremshwa kuhusiana na ndoa ya Muta’a, sanad zote zaishia kwa Ibnu Abbas, Ubayya bin Kaab, Abdullah bin Mas’ud, Imran bin Haswin, Habib bin Abu Thabit, hao ni miongoni mwa Masahaba, aidha Said bin Jubeir, Qataada, Mujahid hao ni Tabiina (kizazi kilichokuja baada ya masahaba) na wote hao wamepokea kutoka kwa Ibnu Abbas. Na haiwezekani Aya hiyo kuifasiri na kuihusisha na ndoa ya daima, kama alivyoshadidia Mwandishi wa Tafsiri Al-Manaar, tunasema hivyo kwa sababu zifuatazo: Imeshakwishatangulia hapo kabla kwamba Masahaba walikuwa wakisoma aya hiyo hivi: “Basi mtapostarehe nao lazima wapeni malipo yao” (Sura Nisai: 24), na kuongezea hayo yale yaliyoelezwa kwa urefu na mapana katika kitabu Al-Wasat ambamo ipo ibara: “Mstarehe nao hadi muda maalum” na lengo lao ni kueleza na kubainisha maana husika, na maelezo hayo hayahusiani kabisa na ndoa ya daima bali yanahusiana na ndoa ya Muta’a. Kwa hakika neno Muta’a hata kama yafaa kutumika kwa ndoa ya daima isipokuwa kwa ndoa ya Muta’a ni dhahiri zaidi, kama vile neno Nikah linawezekana kutumika kwa ndoa ya Muta’a ila kwa ndoa ya daima ni dhahiri zaidi, kwa hivyo neno Muta’a kuwepo katika Aya hiyo inasaidia kulihusisha na ndoa ya Muta’a na sio ya daima, hata kama sio mashuhuri sana katika hilo.
5
Ndoa ya Mutaa Dr.Kanju.qxd
7/15/2011
11:35 AM
Page 6
Ndoa ya Mutaa Kwa mantiki hiyo kuna uwezekano mkubwa wa kuikubali dalili inayohusu jambo hilo, na kwa hivyo neno hilo linakuwa ni miongoni mwa maneno ambayo hutumika zaidi ya maana moja. 3. Kwa hakika Aya ya Muta’a imo ndani ya Suratun Nisaa ambayo imeanza kwa kutaja Nikah na ndoa ya daima, pamoja na hukumu zake katika Aya ya 3, 4, 20 na 23, na kama ingelikuwa makusudio ya Muta’a ni ndoa ya daima ingekuwa Aya hiyo inarudufu jambo ambalo limeshakwishaelezwa hapo mwanzoni mwa Sura. 4. Lau kama Muta’a ingelikuwa na maana ya ndoa ya daima basi kuna mantiki gani jambo hilo idaiwe ilifutwa?! Je! Makusudio yake ni kufutwa hukumu ya ndoa ya daima? Kwa hivyo dai la ufutwaji linahusiana na kuwepo Aya ya Muta’a (ndoa ya muda maalum na sio ya daima). Ama maandiko na hadithi mutawatiri zipo chungu tele, hapa tunataja baadhi ya hizo nazo ni: 1. Imepokewa kutoka kwa Jabir amesema: Tulikuwa tunafunga ndoa ya Muta’a …zama za Mtume (s.a.w.w) na zama za Abu Bakr … kisha Umar akaikataza ...2 2. Imepokewa kutoka kwa Ibnu Abbas amesema: “Hakika Muta’a ipo na haijafutwa.”3
Aya ya
“…Tumefunga ndoa ya Muta’a zama za Mtume (s.a.w.w) na zama za Abu Bakr na nusu ya zama za Umar bin Khatwab kisha akawakataza watu.”4 1 Rejea: Sahih zote na Musnad zote. 2 Sahih Muslim Juz. 4 uk. 131 chapa ya Mashkul, Musnad Ahmad Juz. 6, Uk. 405 na Fat’hu Baari Juz. 9, uk. 149. 3 Kashshaf Juz. 1 uk. 498 chapa ya Beirut, Ghadiir Juz. 6 kutoka Tafsir Khazin Juz. 1 Uk. 357. 4 Bidayat Mujtahid, Juz. 2, Uk. 58 na Al-Ghadiir, Juz. 6 Uk. 207 na 223. 6
Ndoa ya Mutaa Dr.Kanju.qxd
7/15/2011
11:35 AM
Page 7
Ndoa ya Mutaa Imepokewa kutoka kwa Hakim na Ibnu Jureh na wengineo wamesema: Ali (a.s) amesema: “Lau Umar asingelikataza ndoa ya Muta’a asingezini isipokuwa mtu muovu.”5 Imepokewa kutoka kwa Imran bin Haswin amesema: “Aya ya Muta’a imeteremshwa ndani ya Qur’ani na hakuna aya nyingine iliyoteremshwa kufuta hukumu yake, Mtume (s.a.w.w) alituamrisha kufanya hivyo, nasi tukawa tunafanya wakati wa Mtume (s.a.w.w) hadi alipofariki, akaja mtu mmoja kwa utashi wake binafsi akaikataza.”6 Tunahitimisha kwa kusema: Hakika amepokea Ibnu Jureh peke yake hadithi kumi na nane zenye kuhalalisha ndoa ya Muta’a7 achilia mbali hadithi chungu nzima zilizopokewa na wengineo. Kwa hivyo zipo hadithi nyingi na dalili mbali mbali zinazotilia mkazo yale yaliyoelezwa na Aya tukufu kuhusu uhalali wa ndoa ya Muta’a na kwamba hukumu ya ndoa hiyo ipo na itaendelea kuwepo, na kwamba katazo limetolewa na Umar na sio bwana Mtume (s.a.w.w), bali masahaba akiwemo mtoto wa Umar na kizazi kilichokuja baada ya masahaba walikiri na kuthibitisha kwamba ndoa hiyo ni halali hata kama Umar ameiharamisha.
5 Tafsiir Tabari Juz. 5, Uk. 9, Tafsir Raazi Juz. 10, Uk. 50 na Durrul Manthuur Juz. 2, Uk. 140 bali waovu yaani kidogo. 6 Sahih Bukhari, Juz. 2, uk. 168 na Juz. 6, uk. 33, Sahih Muslim, Juz. 4, Uk. 48, Sunan Nisaai, Juz. 5, Uk. 155 na Musnad Ahmad, Juz. 4, Uk. 426 kwa sanadi sahihi. 7 Naylu Awtwar, Juz. 6, uk. 271 na Fat’hu Baari, Juz. 9, Uk.0. 7
Ndoa ya Mutaa Dr.Kanju.qxd
7/15/2011
11:35 AM
Page 8
Ndoa ya Mutaa
DONDOO YA PILI Je! Ni kweli Hukumu ya Ndoa ya Muta’a Imefutwa? Wanachuoni wengi miongoni mwa wanazuoni wakubwa wa Ahlu Sunna wamesema kwamba ndoa hiyo imefutwa, wamesema hayo ili kupasisha msimamo wa Umar bin Khatwab, baadhi yao wakasema: ‘’Hakika ndoa hiyo imefutwa na Qur’ani,’’ na wengine wakasema: “Hakika imefutwa na Sunna.” Kisha makundi hayo mawili yakatofautiana kama ifuatavyo: Ama kuhusu dai la kufutwa hukumu yake na Qur’ani wametumia Aya hizi:
‘’Isipokuwa kwa wake zao au kwa (wanawake) wale waliomilikiwa na mikono yao basi hao si wenye kulaumiwa, basi anayetaka kinyume cha haya, basi hao ndio warukao mipaka’’. (Surat Muuminuna: 6-7). Lakini Aya mbili hizo zimeteremshwa Makka, na Aya ya Muta’a ni Aya ambayo imeteremshwa Madina, ni dhahiri shahiri kwamba Aya iliyotangulia haiwezi kufuta hukumu ya Aya iliyokuja baada yake. Hakika Muta’a ni ndoa, na mwenye kustarehe naye ni mkewe, wala hakuna ukinzani kati ya Aya mbili hizo na Aya ya Muta’a hadi isihi kauli ya ufutaji. Ipo kauli inayosema kwamba Aya inayofuta Aya hiyo ni Aya ya Eda inayosema: “Basi waacheni katika wakati wa eda zao.” (Surat AtTalaq:1). Hakika amri ya Eda katika Aya hiyo inafuta hukumu ya ndoa ya 8
Ndoa ya Mutaa Dr.Kanju.qxd
7/15/2011
11:35 AM
Page 9
Ndoa ya Mutaa Muta’a ambayo haina talaka wala Eda. Jibu: Sio kweli kwamba ndoa ya Muta’a haina Eda, la hasha, bali ina Eda, ama talaka ni kweli haina talaka, na sisi tunathibitisha kwamba ndoa zipo za aina mbili: Ndoa ya daima na ndoa ya isiyo ya daima, kwa hivyo Aya ya talaka inahusu ndoa ya daima pekee na haihusiani na ndoa isiyo ya daima, kwa sababu uhusiano wa daima unahitaji ubainisho wa kutoendelea uhusiano huo kwa kutokea jambo ambalo husababisha kutoendelea kwake, ama uhusiano wa ndoa ya muda maalum (Muta’a) hauhitaji ubainifu huo, kwani uhusiano wake unaisha pindi muda waliokubaliana unapomalizika, kwa mantiki hiyo Aya ya talaka inahusu tu ndoa ya daima, wala haihusiani kabisa na ndoa ya muda hadi Aya hiyo ifute Aya ya Muta’a. Ipo kauli ya tatu inayosema: Aya ya Muta’a imefutwa na Aya ya Urithi (Mirathi), dalili hiyo inadai kwamba kutokana na ndoa hiyo haina urithi, hiyo ni sababu tosha ya kufutwa ndoa hiyo. Jibu la swali hilo halitofautiani na jibu la swali lililokwisha tangulia, vile vile tunaongezea katika kujibu hilo ni kwamba: Kutoweka kwa baadhi ya athari ya jambo fulani haina maana jambo husika limetoweka pia, kwa mfano: Mke asiyemtii mumewe hastahili kupewa huduma, pamoja na hivyo bado huwa mke halali na anastahili haki zingine zinazomhusu kila mke wa ndoa, au atakapoolewa mwanamke kati ya wale waliopewa kitabu na mwislamu hana urithi, pamoja na hivyo anabaki kuwa mke halali, ama haki na hukumu zingine zilizobakia ataendelea kustahili. Kwa hivyo kutokana na kukithiri madai ya kufutwa hukumu ya ndoa hiyo, bila shaka hiyo ni dalili tosha kuthibitisha kuwa madai hayo sio sahihi, na ufutwaji wa hukumu ya ndoa hiyo haujathibiti, hiyo ni dalili tosha kwamba ufutwaji huo haujatokea wala kuthibiti, nayo ni kutokana na kauli tofauti ya zama za ufutwaji wake nazo ni:
9
Ndoa ya Mutaa Dr.Kanju.qxd
7/15/2011
11:35 AM
Page 10
Ndoa ya Mutaa Ndoa hiyo ilikatazwa na Mtume (s.a.w.w) katika vita vya Khaybar. Hakika ndoa hiyo ilikatazwa mwaka wa Ukombozi. Jambo hilo liliruhusiwa lakini lilikatazwa wakati wa vita vya Tabuuk. Iliruhusiwa wakati wa Hijja ya kuaga kisha ikakatazwa. Iliruhusiwa kisha ikakatazwa, ikaruhusiwa kisha ikakatazwa, na ikaruhusiwa tena kisha ikakatazwa. Na ikasemwa kinyume na tofauti na hivyo.8 Kwa hakika upo ushahidi, dalili na vidokezo kadhaa wakadha vya kukata shauri ambavyo vinathibitisha kwamba ndoa hiyo haijafutwa, na miongoni mwa vidokezo hivyo ni mgongano uliyopo kati ya madai ya ufutwaji, kwa hakika Muslim ameandika katika kitabu chake Sahih mlango wa Muta’a kwa anwani: “Mlango wa ndoa ya Muta’a na ubainifu wake, ambayo iliruhusiwa kisha ikafutwa, na ikaruhusiwa kisha ikafutwa na uharamu wake utaendelea hadi siku ya Kiyama.”9 Qurtubi amenukuu katika kitabu chake cha Tafsiir yale aliyosema Ibnu Hajar kwamba: ‘’Hukumu ya ndoa hiyo ilifutwa mara mbili,” kisha akongeza kusema: ‘’Wapo wengine waliosema kwamba kulingana na baadhi ya hadithi ndoa hiyo ilihalalishwa mara saba.” Kisha akaorodhesha madai ya ufutwaji wa hukumu ya ndoa ya Muta’a, akasema: ‘’Sehemu saba hizo ilihalalishwa na kuharamishwa ndoa ya Muta’a.”10 8 Ahkamu Qur’ani Juz. 2, Uk. 184 – 195 mlango wa Muta’a chapa ya Darul-kutub ilmiya, Sahihi Muslim Juz. 9, Uk. 179 Sherh Nawawi mlango wa Ndoa ya Muta’a na Irshaad Saari Sherh Sahih Bukhari mlango 32, mlango wa Mtume (s.a.w.w) kukataza ndoa ya Muta’a hadithi ya 5115 na 5119. 9 Sahih Muslim Juz. 2, Uk. 130 chapa ya Darul-Fikr Beirut. 10 Tafsir Qurtubi Juz. 5, Uk. 130 – 131. 10
Ndoa ya Mutaa Dr.Kanju.qxd
7/15/2011
11:35 AM
Page 11
Ndoa ya Mutaa Ibnu Qaym Jauzi amesema: ‘’Ufutwaji huu hauna mfanowe katika sheria, bila shaka hilo halijawahi kutokea katika sheria za dini mfano wa jambo hilo.”11 Hebu tujiulize inakuwaje madai hayo yajitokeze baada ya zama za masahaba? Kwa nini Umar bin Khatwab hakutolea ushahidi angalau hadithi moja kwa kitendo chake cha kuharamisha ndoa hiyo?! Ni dhahiri shahiri kwamba lau angelikuwa na dalili na ushahidi unaokataza hilo bila shaka angeliutoa na hatimaye kuwa hoja yake, naye alimpinga Abu Bakr kwa uamuzi wake wa kutangaza vita dhidi ya wale ambao waliokataa kutoa Zaka, alitoa ushahidi wa hadithi mbali mbali zinazokataza kuua watu ambao hutoa shahada mbili, kwa nini kuhusu jambo hili hakushikamana na Sera na Sunna za bwana Mtume (s.a.w.w) zenye kukataza jambo hilo kama inavyodaiwa?! Au wale wenye kudai hivyo ni wajuzi zaidi wa Sera na Sunna za Mtume (s.a.w.w) kuwashinda masahaba akiwemo Umar bin Khatwab mwenyewe. Khalifa wa pili hakutosheka kwa hayo, bali aling’ang’ania na kubakia na msimamo wake huo pamoja na kupingwa vikali na waislamu, kwani wao walikuwa wakifunga ndoa hiyo zama za Mtume (s.a.w.w) na zama za Abu Bakr, na kama kungelikuwa na ufutwaji wa ndoa hiyo basi ingelidhihiri na kuthibiti hilo. Kisha madai yote hayo yanapingana na maneno ya Khalifa wa pili pale aliposema: “Muta’a mbili zilikuwako wakati wa Mtume (s.a.w.w): Mut’atulNisaa na Mut’atul-Hajji, na mimi nazikataza na natoa adhabu kwa atakayefanya.”12 11 Zaad Maad Juz. 2, Uk. 204. 12 Sherh Maani Aathar Juz. 2, Uk. 146 cha Ahmad bin Muhammad bin Salma Azadi. 11
Ndoa ya Mutaa Dr.Kanju.qxd
7/15/2011
11:35 AM
Page 12
Ndoa ya Mutaa Na lau ingelikuwa ipo dalili au ushahidi ambao umefuta jambo hilo asingelinasibisha jambo hilo kwake yeye mwenyewe. Kwa mantiki hiyo madai ya kufutwa ndoa hiyo yanapingana na maneno ya Khalifa wa pili. Vile vile lipo tukio lingine ambalo linakosoa hekaya ya ufutwaji wa jambo hilo, Twabari ameeleza katika kitabu chake Tarikh Twabari kuhusiana na matukio ya mwaka 23 A.H kwamba Imran bin Suwada siku moja aliingia kwa Umar bin Khatwab akamweleza mambo ambayo ni gumzo kwa watu kutokana na yale ambayo yeye amezusha, na wao kabisa hawakubaliani naye, kati ya hayo ni uharamishaji wake wa ndoa ya Muta’a, akamwambia hivi: “Wanasema kwamba hakika wewe umeharamisha ndoa ya Muta’a ambayo imeruhusiwa na Mwenyezi Mungu, tulikuwa tukifunga ndoa ya Muta’a kwa gao la tende.” Umar bin Khatwab akasema: “Hakika Mtume (s.a.w.w.) alihalalisha ndoa hiyo wakati wa dharura kisha watu wakarejea katika hali ya kawaida, kisha sijui kama yupo aliyerudia jambo hilo na kulitendea kazi, na hivi sasa mwenye kutaka kufanya hivyo basi na afanye iwe kwa gao la tende au kwa kitu kingine, na watatengana kwa talaka tatu, hapo nitakuwa nimepatia.’’13 Katika mazungumzo hayo kwa mara nyingine Khalifa wa pili anatilia mkazo kwamba katazo na haramisho la ndoa ya Muta’a ni msimamo wake binafsi, hiyo ni rai yake na asilan jambo hilo halijakatazwa na Mtume (s.a.w.w.). Na Ijitihadi ambayo ameieleza katika mazungumzo yake sio timilifu, ni dhahiri hilo ni batili kutokana na kudai kwamba Mtume (s.a.w.w) alihalalisha wakati wa dharura, na kwa hivyo kauli yake hiyo inajulisha kwamba ndoa hiyo ni halali tu wakati wa dharura, ikiwa ni hivyo basi kwa nini ameiharamisha moja kwa moja na kuahidi kutoa adhabu kwa mwenye 13 Tarikh Twabari, Juz. 5, Uk. 32. 12
Ndoa ya Mutaa Dr.Kanju.qxd
7/15/2011
11:35 AM
Page 13
Ndoa ya Mutaa kufanya hivyo bila kutenga na kuruhusu wakati wa dharura? ikiwa aliruhusu wakiwa safarini basi hilo ni jambo na dharura ni jambo jingine.
DONDOO YA TATU Msimamo wa Masahaba na Tabiina Kuhusu Ndoa ya Muta’a Dalili nyingine ambayo inathibitisha kwamba ndoa ya Muta’a haijafutwa ni ile hali ya kuenea na kuwa mashuhuri kwa masahaba, tabiina pamoja na wanavyuoni hadi zama za kudhihiri kwa madhehebu manne katika karne ya tatu na nne Hijriya. Na ushahidi wa hayo ni kutokana na yale yaliyoelezwa na Bukhari na Muslim katika sahih zao, hadithi zilizopokewa kutoka kwa Salama bin Akuu, Jabir ibn Abdillah Answari, Abdullah bin Mas’ud, Ibn Abbas, Sabra bin Ma’abad, Abu Dharr Ghaffari, Imran bin Haswin na Akuu bin Abdillah Aslama.14 Muslim ameeleza kutika mlango wa Muta’a hadithi chungu nzima kutoka kwa Jabir bin Abdillah Answar na Ibnu Zubeir kwamba hao wawili walifunga ndoa ya Muta’a zama za Mtume (s.a.w.w) na pia zama za Abu Bakr, waliendelea hivyo hadi Umar bin Khatwab alipoikataza. Na katika Sahihi Bukhari15 amesema: “Aya ya Muta’a imeteremshwa na imo ndani ya Qur’ani tukufu, na tukaitendea kazi zama za Mtume (s.a.w.w) na wala haijashushwa Aya nyingine inayoharamisha hilo, aidha Mtume 14 Sahih Muslim Juz. 9, Uk. 179 – 189 Sharh Nawawi, Sahih Bukhari kitabu tafsir mlango wa 33 na hadithi 4156 na kitabu Nikah mlango wa 32 hadithi 4724 na kitabu Al-Itiswamu mlango wa 28 hadithi 6819. 15 Sahih Bukhari, Juz. 5, Uk. 185 chapa ya Darul-Fikr. 13
Ndoa ya Mutaa Dr.Kanju.qxd
7/15/2011
11:35 AM
Page 14
Ndoa ya Mutaa (s.a.w.w.) hakuikataza hadi alipofariki, kisha akaja mtu mmoja kwa utashi wake binafsi akaamua kuikataza.” Vilevile kutokana na uharamishaji huo alipingwa vikali na masahaba wakubwa kama vile Imam Ali (a.s), Abdullah bin Abbas, Jabir bin Abdillah Answar, Abdullah bin Umar na Abdullah bin Mas’ud. Hali kadhalika wapo wanavyuoni wa Ahlu Sunna walioishi karne ya kwanza na ya pili Hijiria walitoa fatwa juu ya uhalali wa ndoa hiyo, na hawakuishia tu kutoa fatwa bali walifunga ndoa hiyo, kwa mfano Abdul Malik bin Jureh aliyekufa mwaka 149 A.H. Ibnu Hazmi katika kitabu Al-Muhalla amesema: “Kwa hakika uhalali wa ndoa hiyo umethibitishwa na bwana Mtume (s.a.w.w) na watu chungu nzima, na kati yao ni masahaba, kama vile Asmau bint Abi Bakr, Jawiya bin Abi Sufyan, Amru bin Harith, Abu Said Khudri, Salama na Ma’abad watoto wa Umaiya bin Khulfu, vivyo hivyo Jabir bin Abdillah amepokea kutoka kwa kundi la masahaba kwamba walifunga ndoa hiyo zama za Mtume (s.a.w.w.) na zama za Abu Bakr hadi zama za mwisho za ukhalifa wa Umar bin Khatwab …”. Ifuatayo ni orodha ya baadhi ya masahaba pamoja na tabiina (kizazi kilichokuja baada ya Masahaba) ambao wamethibitisha uhalali wa ndoa hiyo, aidha walikanusha vikali madai ya ufutwaji wa hilo, nao ni: 1. Imran bin Haswin. 2. Abdullah bin Umar. 3. Salama bin Umayya. 4. Ma’abad bin Umayya. 5. Zuheir bin Awwam. 14
Ndoa ya Mutaa Dr.Kanju.qxd
7/15/2011
11:35 AM
Page 15
Ndoa ya Mutaa 6. Khalid bin Muhajir. 7. Ubayy bin Kaa’b. 8. Rabia bin Umayya. 9. Samiir (katika kitabu Al-Iswaba Samrat Ibnu Jundub). 10. Sadu. 11. Mujahid. 12. Ibnu Ausi Madani. 13. Anas bin Malik. 14. Muawiya bin Abu Sufyan. 15. Ibnu Jureh. 16. Nafiu. 17. Swabib bin Abu Thabit. 18. Hakim bin Utayba. 19. Jabir bin Yazid. 20. Barau bin Azib. 21. Sahal bin Saad. 22. Mughiira bin Shuuba. 15
Ndoa ya Mutaa Dr.Kanju.qxd
7/15/2011
11:35 AM
Page 16
Ndoa ya Mutaa 23. Salama bin Akuu. 24. Zayd bin Thabit. 25. Khalid bin Abdullah Answari 26. Yuula bin Umayya. 27. Swafwan bin Umayya. 28. Amru bin Hawshab. 29. Amru bin Dinar. 30. Ibnu Jarir. 31. Said bin Habib. 32. Ibrahim Nakhai. 33. Hasan Baswari. 34. Ibnu Masiib. 35. Aamish. 36. Rabii bin Maysara. 37. Abu Zuhari. 38. Malik bin Anas. 39. Ahmad bin Hanbali, katika baadhi ya hali. 40. Abu Haniif, kwa mujibu wa baadhi ya rejea.16 16 Ghadiir, Juz. 6, Uk. 220, Zawaaju Muwaqqat fil Islam uk. 123, Al-Mut’atu cha Fakiik na Ahkamu Shar iya fil-Ahwaal Shakhswiyya Juz.. 1, Uk. 28. 16
Ndoa ya Mutaa Dr.Kanju.qxd
7/15/2011
11:35 AM
Page 17
Ndoa ya Mutaa Hayo huongezewa na yale yaliyosemwa na Abu Amru: “Hakika masahaba wa Ibnu Abbas miongoni mwa watu wa Makka na Yemen, wote walikuwa wakifunga sana ndoa hiyo na walikuwa wakiiona kuwa ni halali…..” Qurtubi katika Tafsiir yake17 amesema: “Watu wa Makka walikuwa wakifanya hivyo sana.”Raazi katika Tafsiir yake18 amesema: …. “Miongoni mwao alikuwa ni Sawwad, amesema: ‘Ndoa hiyo iliruhusiwa na ikaendelea kubaki hivyo.’” Abu Hayan katika Tafsiir yake baada ya kunukuu hadithi ambayo inahalalisha ndoa hiyo akasema: “Hiyo ni Ijmaa (makubaliano ya wanavyuoni) miongoni mwa Ahlul Bayt (a.s) na Tabiina.19” Na mwenye kutaka ufafanuzi zaidi kuhusiana na kadhia hiyo katika nyanja za kisheria, historia na hadithi, basi ni vema arejee kitabu kiitwacho Maalim20 cha Allama Sayyid Murtadha Al-Askari. Na iwapo dai la kwamba ndoa hiyo ilifutwa na Mtume (s.a.w.w.) litasadikika, basi uharamisho utakuwa katika muktadha wa hukumu ya kiongozi kwa muda fulani, na sio sheria ya daima, na mfano wa hilo yanafanana na yale yaliyotokea zama za Mtume (s.a.w.w) ambapo aliharamisha ulaji wa nyama ya punda wafugwao katika mwaka ambao ilitokea vita vya Khaybar, kwani hukumu hiyo ilikuwa ni ya muda maalum na haikuwa sheria ya daima.
17 Jaamiu Ahkamul Qur’an, Juz.. 5, Uk. 132. 18 . Tafsir Kabiir Juz. 3 uk. 200 cha Fakhru Raazi. 19 Ghadiir Juz. 6, Uk. 222 amenukuu kutoka katika kitabi Al-Itiaab na wengineo. 20 Mualimu Madrasatain Juz.. 2, Uk. 232 – 280. 17
Ndoa ya Mutaa Dr.Kanju.qxd
7/15/2011
11:35 AM
Page 18
Ndoa ya Mutaa Na lau sisi tutasalimu amri na kukubaliana na madai ya ufutwaji na uharamisho wa ndoa hiyo, sasa tujaalie watu wawili walikuwa wamefunga ndoa hiyo na wakawa katika mahusiano ya mume na mke kisha wakatengana, kisha ukapita muda fulani je! ni ipi hukumu ya mahusiano hayo? Je! hukumu yake ni haramu na walikuwa wakifanya zinaa? Jibu: Hakuna shaka kuhukumu kwamba mahusiano yao yalikuwa ya haramu, hilo ni dai lisilo na dalili, na kukiri kwamba mahusiano yao yalikuwa halali kwa hakika hilo linaafikiana na ukweli ambao Ahlul Bayt (a.s) wanaukubali na kushikamana nao.
JE! NDOA YA MUTA’A NI ZINAA? Kuhusu kauli isemayo kwamba ndoa ya Muta’a inalingana na zinaa, au ndoa hiyo ni zinaa, huko ni kwenda kombo hata kama tutajaalia ilifutwa, kwa sababu hilo linapelekea kusema kwamba Mwenyezi Mungu aliruhusu zinaa kisha akaiharamisha, je! yupo mwislamu yeyote anayekubali hilo? Kama ilivyokwishatangulia hapo kabla kwamba ndoa ya Muta’a ni ndoa halali kama vile ndoa ya daima, ina masharti na vigezo kadhaa wakadha kama vile: Ifanywe Aqdi, mahari na ubainishwe muda, ama vidokezo vinavyozingatiwa ni kama vile: Akili, kubalehe, kisiwepo kizuizi cha nasaba na sababu ya kunyonya pamoja na mambo mengine. Ama Zinaa haina Aqdi, hakuna uhusiano wa mke na mume, hakuna Eda, mtoto hanasibishwi kwa baba na wala hamrithi, kwa hivyo kitendo cha kuifananisha ndoa hiyo na uzinifu ni kauli iliyo batili, na mwenye kusema hivyo ni mbishi na mpenda malumbano. Ndio, huenda ikasemwa: Kuruhusu ndoa hiyo ni kuwapa nafasi watu waovu kuutumia mwanya huo kufanya mambo yasiyofaa. 18
Ndoa ya Mutaa Dr.Kanju.qxd
7/15/2011
11:35 AM
Page 19
Ndoa ya Mutaa Jibu: Kwa hakika dunia imejaa mambo mazuri pamoja na hivyo waovu huyatumia vibaya, na utatuzi wa mambo kama hayo sio kuharamisha, bali zitafutwe mbinu na njia muafaka ambazo zitasaidia kwa upande mmoja mambo mazuri yaendelee vizuri na kuepusha kutotumiwa vibaya na waovu kwa upande mwingine, kwa hivyo kiongozi wa juu wa kiroho wa kiislamu anaweza kuweka masharti kuhusiana na jambo hilo, masharti ambayo huenda sanjari na wakati, masharti ambayo huzingatia zama na mahala husika, ili kuinusuru sheria hii na mafisadi na watu waovu.
TIJA Hivyo ndivyo ilivyobainika kwetu kwa mujibu wa maandiko, Aya za Qur’ani tukufu, Sunna sahihi za Mtume (s.a.w.w.), maandiko mbalimbali, ushuhuda wa maneno na vitendo vya masahaba na tabiina, hali kadhalika kulingana na Ijimaa ya wanazuoni kuhusiana na kukiri uhalali wa ndoa hiyo, aidha kutothibiti dalili inayojulihsha kufutwa kwa jambo hilo, vile vile masahaba na tabiina walipinga vikali kuzuiwa na kukatazwa suala hilo, hasa hasa Ahlul Bayt (a.s) akiwemo Ali bin Abu Twalib (a.s) ambaye ni kiongozi wa mawasii na mawalii, wanawe watoharifu waliohifadhika na dhambi, wanazuoni wakubwa pamoja na wafuasi wao kizazi hadi kizazi, bila shaka hiyo ni dalili tosha ya kusihi hilo, na hakuna nguvu ya hoja nzito zaidi kuliko hiyo. Kwa mantiki hiyo ndoa ya Muta’a ni ndoa sahihi na halali kwa mujibu wa Qur’ani tukufu na Sunna za Mtume (s.a.w.w), kama vile ilivyo ndoa ya daima katika sheria ya kiislamu, kwa hivyo hukumu ya ndoa hiyo hutofautiana kidogo na hukumu za ndoa ya daima kama tulivyoeleza kinaga ubaga hapo kabla. Ama kuhusu yale yaliyopokewa kutoka kwa Umar bin Khatwab kuhusiana na ukatazaji na uharamisho pamoja na yale yaliyoelezwa ili kuthibitisha kwamba ndoa hiyo imefutwa sio sahihi, na hukumu aliyoitoa Umar bin Khatwab ya kuharamisha jambo hilo haikustahili na haikubaliki hata kido19
Ndoa ya Mutaa Dr.Kanju.qxd
7/15/2011
11:35 AM
Page 20
Ndoa ya Mutaa go, kama walivyoeleza na kupinga wazi wazi masahaba na tabiina. Mwisho tunapenda kuchukua nafasi hii adhimu kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa uwezo na tawfiki yake kutuwezesha kubainisha haya machache, aidha tunamuomba atujaalie kufuata yale ayapendayo na anayoyaridhia.
Alhamdu Lillahi Rabbil Alamiina.
20
Ndoa ya Mutaa Dr.Kanju.qxd
7/15/2011
11:35 AM
Page 21
Ndoa ya Mutaa
ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION: 1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9. 10. 11. 12. 13. 14. 15. 16. 17. 18. 19. 20. 21. 22. 23. 24. 25. 26.
Qur'an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Ishirini na Nne Uharamisho wa Riba Uharamisho wa uwongo Juzuu ya kwanza Uharamisho wa uwongo Juzuu ya pili Hekaya za Bahlul Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.) Hijab vazi Bora Ukweli wa Shia Ithnaashari Madhambi Makuu Mbingu imenikirimu Abdallah Ibn Saba Khadijatul Kubra Utumwa Umakini katika Swala Misingi ya Maarifa Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia Bilal wa Afrika Abudharr Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu Salman Farsi Ammar Yasir Qur'an na Hadithi Elimu ya Nafsi Yajue Madhehebu ya Shia Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur'an Tukufu 21
Ndoa ya Mutaa Dr.Kanju.qxd
7/15/2011
11:35 AM
Page 22
Ndoa ya Mutaa 27. 28. 29. 30. 31. 32. 33. 34. 35. 36. 37. 38. 39 40. 41. 42. 43. 44. 45. 46. 47. 48. 49. 50. 51. 52. 53. 54. 55. 56. 57. 58. 59.
Al-Wahda Ponyo kutoka katika Qur'an. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii Mashukio ya Akhera Al Amali Dua Indal Ahlul Bayt Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna. Haki za wanawake katika Uislamu Mwenyeezi Mungu na sifa zake Amateka Na Aba'Khalifa Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) Adhana. Upendo katika Ukristo na Uislamu Nyuma yaho naje kuyoboka Amavu n’amavuko by’ubushiya Kupaka juu ya khofu Kukusanya swala mbili Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Kusujudu juu ya udongo Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s) Tarawehe Malumbano baina ya Sunni na Shia Kupunguza Swala safarini Kufungua safarini Umaasumu wa Manabii Qur’an inatoa changamoto as-Salaatu Khayrun Mina -'n Nawm Uadilifu wa Masahaba Dua e Kumayl Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata 22
Ndoa ya Mutaa Dr.Kanju.qxd
7/15/2011
11:35 AM
Page 23
Ndoa ya Mutaa 60. 61. 62. 63. 64. 65. 66. 67. 68. 69. 70. 71. 72. 73. 74. 75. 76. 77. 78. 79. 80. 81. 82. 83. 84. 85. 86. 87. 88. 89. 90. 91.
Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mitume Muhammad (s) Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili Kuzuru Makaburi Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu Maswali na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne Maswali na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita Tujifunze Misingi Ya Dini Sala ni Nguzo ya Dini Mikesha Ya Peshawar Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu Ubora wa Imam 'Ali Juu ya Maswahaba Na Ushia ndio njia iliy onyooka Shia asema haya, Sunni asema haya, Wewe wasemaje? Liqaa-u-llaah Muhammad (s) Mtume wa Allah Amani na Jihadi Katika Uislamu Uislamu Ulienea Vipi? Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) Urejeo (al-Raja’a ) Shahidi kwa ajili ya Ubinadamu Utokezo (al - Badau) Kuanzia ndoa hadi kuwa wazazi Myahudi wa Kimataifa Uislamu na dhana Mtoto mwema Adabu za Sokoni Johari za hekima kwa vijana Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili 23
Ndoa ya Mutaa Dr.Kanju.qxd
7/15/2011
11:35 AM
Page 24
Ndoa ya Mutaa 92. 93. 94.
Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu Tawasali Imam Mahdi katika Usunni na Ushia
95.
Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu
96.
Hukumu ya kujenga juu ya makaburi
97.
Swala ya maiti na kumlilia maiti
98.
Shiya na Hadithi (kinyarwanda)
99.
Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu
100.
Hadithi ya Thaqalain
101.
Fatima al-Zahra
102.
Tabaruku
103.
Sunan an-Nabii
104.
Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza)
105.
Idil Ghadiri
106.
Mahdi katika sunna
107.
Kusalia Nabii (s.a.w)
108.
Ujumbe -Sehemu ya Kwanza
109.
Ujumbe - Sehemu ya Pili
110.
Ujumbe - Sehemu ya Tatu
111.
Ujumbe - Sehemu ya Nne
112.
Shiya N’abasahaba
113.
Safari ya kuifuata Nuru
114.
Ukweli uliopotea sehemu ya Pili
115.
Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu
116.
Ukweli uliopotea sehemu ya Nne
117.
Ukweli uliopotea sehmu ya Tano
24
Ndoa ya Mutaa Dr.Kanju.qxd
7/15/2011
11:35 AM
Page 25
Ndoa ya Mutaa
BACK COVER Kitabu hiki ni matokeo ya kazi ya kielimu iliyofanywa na mwanachuoni huyu wa Kiislamu - Sheikh Abdul Karim al-Bahbahani. Kumekuwepo na zogo kubwa katika miji yetu ya Kiislamu kuhusu suala hili la ndoa ya mutaa (mut‘ah) (ndoa ya muda); baadhi wanasema ni sahihi na wengine wanasema sio sahihi kwa kuifananisha ndoa hii na zinaa. Mwandishi wa kitabu hiki kwa kutumia Qur’ani Tukufu, Sunna na hoja za kiakili na elimu ameonesha kwa wazi kabisa kwamba ndoa hii ni halali, na kwamba ilikuwepo tangu zama za Mtukufu Mtume (s.a.w.) na ikaendelea wakati wa ukhalifa wa Abu Bakr na kipindi cha mwanzo wa ukhalifa wa Umar ambaye akaipiga marufuku. Fuatana mwandishi wa kitabu hiki ili uweze kuifahamu vilivyo ndoa hii na kuondokana na dhana potofu iliyojengewa juu yake. Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Nukushi: +255 22 2127555 Barua Pepe: alitrah@raha.com Tovuti: www.alitrah.org Katika mtandao: www.alitrah.info
25