Ni mwanadaawa, si nabii

Page 1

NI MWANADAAWA,

SI NABII

Usomaji wa Kihakiki wa Madhehebu ya Sheikh Muhammad bin Abdul Wahhab katika Ukufurishaji

‫داعية وليس نبيًا‬ ‫قراءة نقدية لمذهب الشيخ محمد بن عبد الوهاب في التكفير‬

Kimeandikwa na: Hasan bin Farhani al-Maliki

Kimetarjumiwa na: Sheikh Harun Pingili

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 1

1/20/2016 11:35:46 AM


‫ترجمة‬

‫داعية وليس نبيًا‬

‫قراءة نقدية لمذهب الشيخ محمد بن عبد الوهاب في التكفير‬

‫تأليف‬ ‫حسن بن فرحان المالكي‬

‫من اللغة العربية الى اللغة السوا حلية‬

‫‪1/20/2016 11:35:46 AM‬‬

‫‪15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 2‬‬


©Haki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: 978 - 9987 – 17 – 021 - 0 Kimeandikwa na: Hasan bin Farhani al-Maliki Kimetarjumiwa na: Sheikh Harun Pingili Kimehaririwa na: Alhaji Hemedi Lubumba Na: Ramadhani S. K. Shemahimbo Kimepangwa katika Kompyuta na: Al-Itrah Foundation Toleo la kwanza: Aprili, 2016 Nakala: 2000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. - 19701, Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 / 2127555 Barua Pepe: alitrah@yahoo.com Tovuti: www.ibn-tv-com Katika mtandao: www.alitrah.info

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 3

1/20/2016 11:35:46 AM


Yaliyomo Dibaji .......................................................................................viii Neno la Mchapishaji........................................................................ 1 Utangulizi......................................................................................... 3 Mas’ala za Utangulizi..................................................................... 4 Utafiti wa Kwanza: Katika Kukisoma Kitabu Kashfushub’ hat cha Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahabi.................................. 33 Kwanza: Yapaswayo Kuchunguzwa Katika Kitabu Kashfushub’hat.............................................................................. 35 Jambo la Kwanza Lipasalo Kuchunguzwa.................................... 36 Jambo la Pili Lipasalo Kuchunguzwa............................................ 40 Jambo la Tatu Lipasalo Kuchunguzwa.......................................... 44 Jambo la Nne Lipasalo Kuchunguzwa........................................... 47 Jambo la Tano Lipasalo Kuchunguzwa......................................... 50 Jambo la Sita Lipasalo Kuchunguzwa........................................... 54 Jambo la Saba Lipasalo Kuchunguzwa.......................................... 54 Jambo la Nane Lipasalo Kuchunguzwa......................................... 56 Jambo la Tisa Lipasalo Kuchunguzwa........................................... 57 Jambo la Kumi Lipasalo Kuchunguzwa........................................ 58 Jambo la Kumi na Moja Lipasalo Kuchunguzwa.......................... 59 Jambo la Kumi na Mbili Lipasalo Kuchunguzwa.......................... 59 Jambo la Kumi na Tatu Lipasalo Kuchunguzwa........................... 60 Jambo la Kumi na Nne Lipasalo Kuchunguzwa............................ 63 Jambo la Kumi na Tano Lipasalo Kuchunguzwa........................... 63 Jambo la Kumi na Sita Lipasalo Kuchunguzwa............................ 64

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 4

1/20/2016 11:35:46 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Jambo la Kumi na Saba Lipasalo Kuchunguzwa........................... 68 Jambo la Kumi na Nane Lipasalo Kuchunguzwa.......................... 71 Jambo la Kumi na Tisa Lipasalo Kuchunguzwa............................ 80 Jambo la Ishirini Lipasalo Kuchunguzwa...................................... 84 Jambo la Ishirini na Moja Lipasalo Kuchunguzwa........................ 84 Jambo la Ishirini na Mbili Lipasalo Kuchunguzwa....................... 85 Jambo la Ishirini na Tatu Lipasalo Kuchunguzwa......................... 85 Jambo la Ishirini na Nne Lipasalo Kuchunguzwa......................... 87 Jambo la Ishirini na Tano Lipasalo Kuchunguzwa........................ 89 Jambo la Ishirini na Sita Lipasalo Kuchunguzwa.......................... 91 Jambo la Ishirini na Saba Lipasalo Kuchunguzwa........................ 92 Jambo la Ishirini na Nane Lipasalo Kuchunguzwa........................ 94 Jambo la Ishirini na Tisa Lipasalo Kuchunguzwa......................... 95 Jambo la Thelathini Lipasalo Kuchunguzwa................................. 96 Jambo la Thelathini na Moja Lipasalo Kuchunguzwa................... 97 Jambo la Thelathini na Mbili Lipasalo Kuchunguzwa.................. 99 Jambo la Thelathini na Tatu Lipasalo Kuchunguzwa.................. 100 Kuhariri Mahali Penye Mzozo..................................................... 102 Utafiti wa Pili: ........................................................................... 105 Kuzisoma Kauli za Sheikh Katika Vitabu na Insha Nyingine, na ad-Durarus-Saniyyah ni Mfano Wake.................... 105 Mfano wa Kwanza...................................................................... 105 Mfano wa Pili............................................................................... 108 Mfano wa Tatu............................................................................. 109 Mfano wa Nne.............................................................................. 109 Mfano wa Tano............................................................................ 110 v

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 5

1/20/2016 11:35:46 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Mfano wa Sita ............................................................................. 111 Mfano wa Saba ........................................................................... 111 Mfano wa Nane ........................................................................... 112 Mfano wa Tisa ............................................................................ 113 Mfano wa Kumi .......................................................................... 117 Mfano wa Kumi na Moja ............................................................ 118 Mfano wa Kumi na Mbili ........................................................... 119 Mfano wa Kumi na Tatu ............................................................. 119 Mfano wa Kumi na Nne .............................................................. 119 Mfano wa Kumi na Tano ............................................................ 119 Mfano wa Kumi na Sita .............................................................. 120 Mfano wa Kumi na Saba ............................................................. 120 Mfano wa Kumi na Nane ............................................................ 121 Mfano wa Kumi na Tisa .............................................................. 122 Mfano wa Ishirini ........................................................................ 123 Mfano wa Ishirini na Moja ......................................................... 124 Mfano wa Ishirini na Mbili ......................................................... 124 Mfano wa Ishirini na Tatu ........................................................... 125 Mfano wa Ishirini na Nne ........................................................... 125 Mfano wa Ishirini na Tano .......................................................... 125 Mfano wa Ishirini na Sita ............................................................ 125 Mfano wa Ishirini na Saba .......................................................... 127 Mfano wa Ishirini na Nane ......................................................... 127 Mfano wa Ishirini na Tisa ........................................................... 128 Mfano wa Thelathini ................................................................... 129 Mfano wa Thelathini na Moja ..................................................... 130 vi

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 6

1/20/2016 11:35:46 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Mfano wa Thelathini na Mbili .................................................... 134 Mfano wa Thelathini na Tatu ...................................................... 134 Mfano wa Thelathini na Nne...................................................... 135 Mfano wa Thelathini na Tano..................................................... 135 Mfano wa Thelathini na Sita....................................................... 136 Mfano wa Thelathini na Saba..................................................... 136 Mfano wa Thelathini na Nane..................................................... 138 Mfano wa Thelathini na Tisa...................................................... 140 Mfano wa Arobaini...................................................................... 141 Sheikh Kujinasua Mbali na Ukufurishaji..................................... 142 Je Sheikh Zimepingana Kauli Zake............................................. 142 Utafiti wa Tatu: Mwendo Unaoendelea...................................... 150 Mawahabi Wakufurishana Wao kwa Wao.................................... 165 Miongoni mwa Mifano ya Wastani Katika Madrasa ya Kiwahabi................................................................................. 168 Utafiti wa Nne: Mahasimu wa Sheikh na Wapinzani Wake....... 170 Miongoni mwa Wapinzani Mashuhuri wa Uwahabi.................... 172 Tuhuma Zilizo Maarufu mno Walizozielekeza Wanazuoni kwa Sheikh Muhammad............................................ 181 Kiambatanisho............................................................................. 191 Hitimisho..................................................................................... 233 Utafiti Juu ya Kitabu Tawhiid cha Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahabi.................................................... 235

vii

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 7

1/20/2016 11:35:46 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬ DIBAJI

K

itabu hiki ni toleo la Kiswahili la taasisi ya Al Itrah Foundation. Chapisho lake limelenga kukidhi mahitaji ya kiroho ya zama hizi pamoja na Ubongo na fikra zinazokuwa za Muislam. Jitihada kubwa zimefanywa na Taasisi kuweka chapisho hili la Kiswahili katika msingi wa haki na wenye kukubalika katika Uislam. Unaombwa kwa Taadhima ukisome kitabu hiki katika malengo yaliyokusudiwa. Pia Unaombwa kuwasilisha kwetu maoni yako huru juu ya chapisho letu hili, jambo ambalo tutashukuru sana. Kutangaza ujumbe wa Uislam ni kazi ambayo inahitaji ushirikiano wetu sote. Taasisi inakuomba kuungana na kushirikiana kama ilivyoagizwa katika aya ya Qur’an: (Surat Saba’ 34:46). Na rehma za Allah ziwe juu yako. Wako katika Uislam Al Itrah Foundation Barua Pepe: alitrah@yahoo.com SMS: +255 778 300 140

viii

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 8

1/20/2016 11:35:46 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬ NENO LA MCHAPISHAJI

K

itabu ulichonacho mikononi mwako asili yake ni cha lugha ya Kiarabu kwa jina la, Da’iyatun wa laysa Nabiyyaa, kilichoandikwa na Hasan bin Farhani al-Maliki na kutarjumiwa kwa Kiswahili na Sheikh Harun Pingili. Mwandishi wa Kitabu hiki ametumia lugha ya upole sana, busara na hekima katika utafiti wake alioufanya juu ya vitabu na kauli za Sheikh Muhammad bin Abdul Wahhab na akafanya ukosoaji wa haki pale alipoona kuna makosa na kuunga mkono pale alipoona pana haki, bila ya kuongeza au kupunguza maneno wala kutia chumvi au chuki. Katika kitabu hiki amefanya utafiti juu ya kitabu Kashfu Shub’haat na baadhi ya kauli za Sheikh katika vitabu na insha nyingine, na “ad-Duraru ‘s-Saniyyah” - vyote vya Sheikh Muhammad bin Abdul Wahhabi. Huu ni ukosoaji wa kistaarabu ambao hauna nongwa ndani yake. Mwanachuoni huyu kaufanya kwa dhamira nzuri ili kuwaondolea watu taasubu na kuweka mambo hadharani ili kuacha kuwahukumu watu wengine kwa mambo wasiyoyajua. Hii pia ni moja kati ya kazi kubwa zinazofanywa na Taasisi ya Al-Itrah katika kuwahudumia kielimu wasomaji wake wazungumzaji wa Kiswahili. Na kwa maana hiyohiyo imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa lengo lake lilelile la kuwahudumia Waislamu, hususan wanaozungumza Kiswahili. Hivyo, ni matumaini yetu kwamba wasomaji wetu watanufaika vya kutosha kutokana na kitabu hiki, kwani tumekiona ni chenye 1

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 1

1/20/2016 11:35:46 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

manufaa sana, hususan wakati huu maendeleo makubwa ya elimu, sayansi na tekinolojia ambapo ngano na hekaya za zamani na upotoshaji wa historia hauna tena nafasi katika vichwa vya watu. Tunamshukuru mwandishi wa kitabu hiki Hasan bin Farhani al-Maliki kwa kazi kubwa aliyoifanya kwa ajili ya Umma huu wa Waislamu, Allah Azza wa Jallah amlipe kila kheri na amuingize Peponi kwa salama na amani insha’Allah. Halikadhalika tunamshukuru ndugu yetu Ustadh Sheikh Harun Pingili kwa kukitarjumi kwa Kiswahili kitabu hiki, insha’Allah na yeye Allah Azza wa Jallah amlipe kila la kheri hapa duniani na Akhera pia, bila kuwasahau na wale wote waliochangia kwa namna mmoja au nyingine mpaka kufanikisha kuchapishwa kwake. Allah awalipe wote malipo mema hapa duniani na Akhera pia. Mchapishaji| Al-Itrah Foundation

2

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 2

1/20/2016 11:35:46 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬ UTANGULIZI

S

ifa njema ni zake Allah, Swala na Salaam zimwendee Muhammad na Ali zake, na radhi za Mungu ziwafikiye swahaba wake miongoni mwa Muhajirina na Answari na ziwafikie pia wale waliowafuata kwa wema. Amma baada ya hayo:

Nilikuwa nimeandika kumbukumbu ndani ya nyaraka chache. Katika kukosoa kitabu KASHFU SHUB’HATI cha Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahabi miaka kadhaa iliopita, kisha nilianza wakati mwingine kupitia upya, kuongeza, kurekibisha na kukusanya mpaka nilipoona kuwa nimekusanya kiasi ambacho si kibaya, ambacho kinafaa kuutathmini utaratibu wa Sheikh katika kukufurisha. Kwa ajili hiyo nikaona ni vizuri hivi sasa kutawanya niliyoyakusanya na kuyachuja katika kitabu, baada ya kukithiri maswali kumhusu Sheikh na kuhusu utaratibu wake na wafuasi wake, na je kati yao kulikuwa na ukufurishaji wa kuwakufurisha Waislamu? Au ni uchafuzi wa mahasimu? au ni ufahamu mbaya wa maneno yake..................mpaka mwisho. Na kabla sijaingia katika kiini cha maudhui, ilikuwa hapana budi mas’ala fulani niyakunjue ndani ya utangulizi huu, ili kuondoa mkanganyiko na kuainisha lengo. Kisha baada ya hapo nigonge kiini cha maudhui ya Vitabu vya Sheikh na semi zake.

3

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 3

1/20/2016 11:35:46 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

MAS’ALA ZA UTANGULIZI SUALA LA KWANZA: Hivi Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahabi ni nani?

K

una utangulizi yapasa tuuainishe mwanzoni nao ni kuwa: Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahabi, Mungu amrehemu, ni mwanadaawa tu na mrekebishaji na wala sio Nabii.1 Hapana tofauti katika hili kwa upande wa nadharia, wala hapana tofauti katika hili - kwa wenye insafu - kwa upande wa utekelezaji pia, isipokuwa tofauti ipo katika makundi mawili ya watu: 1. Wapo wanaomkufurisha au wamuonao kuwa ni fasiki au wanaotilia shaka malengo yake. Hawa hawakubali kuwa yeye ni mwanadaawa na mrekebishaji. 2. Na wapo wanaozuwia kuchunguza (bali yachukuliwe kama yalivyo) yale aliyozalisha na kutathmini utaratibu wake, na wanakataa kumkosoa katika lile alilokosea. Na hawa wanakuwa ni wale waliompandisha kwenye daraja ya Manabii ambao ni maasumina (waliohifadhika na hawatendi kosa wala dhambi). Hivyo basi, kauli yetu kuwa yeye NI MWANA DAAWA, kwayo tunakusudia kumjibu yule anayemkufurisha au kumuona kuwa ni fasiki au mwenye kutilia shaka malengo yake kwa sura ya jumla. Na kauli yetu kuwa yeye SI NABII, kwayo tunakusudia kumjibu yule 1

  Yeye ni Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahhabi bin Sulayman bin Ali bin Mushraf atTamimiy, amezaliwa mwaka 1115 A.H. Na alifariki mwaka 1206 A.H. Daawa yake ilianza mwaka 1157 A.H. Baada ya kufariki baba yake, na alikuwa katika zama za Ibn Muammar (Amiri wa Uyeinah) na Muhammad bin Saudi, Amiri wa Deriyyah, kisha mwanawe Abdul-Azizi... na kwa ajili ya taarifa zaidi rejea Kiambatanisho ibara ya kwanza. 4

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 4

1/20/2016 11:35:46 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

anayefurutu ada kumhusu yeye. Na hao ndio waliokusudiwa katika kitabu hiki. Muhammad bin Abdul-Wahabi, Mungu amrehemu, ni mwenye fadhila juu yetu wote katika Mamlaka ya Kiarabu ya Saudia; bali juu ya Waislamu wengi duniani.2 Lakini sio jaizi kabisa tumfuate katika aliyokosea. Hali yake ni hali ya mwingine yeyote miongoni mwa wanadamu, miongoni mwa wanazuoni na wanadaawa na wanafunzi wa elimu. Ikiwa tunakubali kumkosoa Abu Hanifa, Shafii na walio mfano wao, basi vipi hatukubali kumkosoa Sheikh Muhammad bin Adil-Wahabi?! Hali yeye ni mchache kuliko wao (yaani Abu Hanifa, Shafii na wa mfano wao), kielimu na athari kwa ijmai ya wenye insafu miongoni mwa wanataaluma.

SUALA LA PILI: Sheikh Yupo Kati ya Ufurutu Ada wa Kumfuata na Ufurutu Ada wa Kumlaumu: Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahabi Mungu amrehemu, ni kama wengine walio mashuhuri. Watu kumhusu yeye wako katika aina mbili: Msemaji wa kufurutu ada katika kumlaumu na kumkejeli, na mfurutu ada katika kumsifu na kumhimidi. Na sisi tunajaribu kuhusu jambo hili kuchukua njia ya wastani. Ili tuwe miongoni mwa wenye insafu. Tuitambue haki yake na wema wake; na aliyonayo miongoni mwa makosa na udhaifu. Tuwatambue wenye haki na wala hatufanyi jamala katika 2

  Kama ambavyo ni insafu tuseme: kuwa mkazo wake - Mungu amrehemu - katika kuwakufurisha Waislamu umetuletea madhara na kwa Waislamu wengi duniani; Na dalili ya ufurutu ada wa Sheikhe wa kuwafanya Waislamu makafiri ni dhahiri kwa ambaye Mungu amemuokoa mbali na ushabiki wa kutokufuata haki. Mifano ya wazi itakuja katika kitabu hiki. Lakini kwa kuwa yeye ni binaadamu na si maasumu, basi makosa haya hayabatilishi fadhila zake, uwanadaawa wake na ijitihada yake, na mambo haya pia ni dhahiri katika sera zake na vitabuni mwake. 5

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 5

1/20/2016 11:35:47 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

kuipinga batili. Na katika hali mbili hizo tunamtarajia apate ujira na thawabu, na awe katika amani mbali na dhambi na adhabu. Hii ni pamoja na kuambatanisha matarajio haya na yale kwa kubainisha makosa haya kwa watu kwa dalili na uthibitisho. Ili wasiathirike nayo na kuwa nyuma ya wanaofurutu ada miongoni mwa wafuasi wake ambao kwa ushabiki wao wamemtendea uovu zaidi kuliko wema. Sawa makosa yake yawe katika itikadi, imani, au ­hukumu. Hii ni pamoja na kusalimu amri kuwa makosa katika itikadi yana athari mbaya mno kwa wafuasi wafurutu ada. Na hii leo wao ndio wenye ushindi juu ya wenye msimamo wa wastani, na wao ndio waliokusudiwa na somo hili la haraka la kutathmini. Wamefurutu ada katika kumkalidi na wamezuwia kuutathmini utaratibu wa Sheikh na wanapambana na kila mwenye kusoma kwa mtazamo mwingine unaokosoa baadhi ya yale aliyoyaandika Sheikh na kuyatawanya na kuyakazia; walighurika na usafi wa siku na zama, hivyo wakapania kwa juhudi kubwa, na wakawa wanaigawa dini kwenye makumi na robo, kwa hiyo wao wako kati ya kuanza na kurejea, kuvutia kwa mali na kufadhaisha, kuna kipindi wanaumaliza umri na dahari katika vitu vidogo, wanayafanya matawi hafifu kuwa ndio mizizi iliyo juu mbinguni, na juu yake wanajengea mtazamo wao ili kuyadharau makubwa yake, kama vile kuwakufurisha Waislamu na kuhalalisha damu zao. Basi hapo ndipo mahali ambapo fitna huwa madhubuti, na maafa hushika kasi ili mjinga aje na kauli yake, aseme: “Sisi tupo katika njia ya watu wetu wema waliotangulia, haturidhiki na kitu badala yao, wala haturidhiki na kingine kinyume nao. Wao ndio watu wetu wema waliotangulia na sisi tuna njia yetu iliyo wazi!” Hivyo watu pande zote mbili wanabaki katika upofu wa giza, na mbabaiko, wamejiambatanisha na ufurutu ada kwenye kingo mbili 6

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 6

1/20/2016 11:35:47 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

za njia iliyonyooka, wenye kuumaliza umri wao kati ya batili iliyoenea na haki isiyoshindwa. Hapo kale palisemwa: “Kuteleza kwa Mwanachuoni ni Kuteleza kwa Ulimwengu” Kwa minajili hiyo ni wajibu juu ya wenye elimu; wawe katika kiwango cha kubeba jukumu na ushujaa wa kubainisha makosa ya wakubwa kwa elimu na adabu na insafu; ufurutu ada wa wafuasi wao usiwazuwie kutambua fadhila zao, wala dhulma ya mahasimu wao isiwasukume kujihifadhi katika handaki na makosa yao na ukiukaji wao. La muhimu kwa mwanachuo mwenye insafu atendaye kwa ajili ya Allah ni kuwasukuma watu wawe na insafu katika mambo kama haya ili kuujua ukweli mtupu pindi anapowatathmini wanaofuatwa. Tumtambue mtu bila ya ufurutu ada au upunguzaji, tumjue kama alivyo kwa mema yake na maovu yake. Mtu hawi salama mbali na makosa na kuyang’ang’ania isipokuwa Manabii na Mitume.

SUALA LA TATU: Kuhusu Matumizi ya Istilahi “Uwahabi”: Na katika suala hili kuna mambo kadhaa: Jambo La Kwanza ni: Kuwa msomaji katika utafiti huu atakuta mimi ninatumia tamko UWAHABI, sio kwa maana ya tuhuma kama wafanyavyo mahasimu wao, au kuwa eti ni madhehebu mapya; bali nimelitumia kwa mtazamo wa kuwa ni nembo wanayoitumia Waislamu wengi kuhusu harakati ya kifikra ya daawa yenye historia yake na mambo mahsusi kwa ajili yake na tunzi zake na masheikhe wake. Jambo La Pili ni: Baadhi ya Mawahabi wameiridhia nembo hii na wamejiita hivyo wao wenyewe. 7

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 7

1/20/2016 11:35:47 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Jambo La Tatu: Si sharti kwamba Sheikh mwenyewe awe ndiye aliyeipa jina madhehebu yake, bali maimamu wengi wa madhehebu bali wote kulingana na ninavyojua hawakuzipa jina madhehebu zao. Watu ndio waliozipa majina madhehebu zao baada ya wao wenyewe kufariki dunia. Si Ahmad bin Hanbali aliyeipa jina madhehebu ya Hanbali, wala si Shafii aliyeiita madhehebu yake kwa jina lake, wala si Abu Hanifa aliyeipa jina madhehebu ya Hanafi, wala Maliki hakuyaita madhehebu yake kwa jina lake, wala si Ja’far as-Sadiq, aliyeipa jina Ithnaasharia au Imamiyah, wala si Zaydu bin Ali aliyeipa jina Zaidiya madhehebu yake, wala si Awzaiy wala si Tabariy, wala si Daudi Dhahiriy, wala si Abdullah bin Ibaadhi, wala si mwingine miongoni mwa maimamu wafuatwao wenye madhehebu aliyeiita madhehebu kwa jina lake. Na wala hayo majina hayakuitwa na wanafunzi wao mahsusi, bali majina yalikuja baadaye, kutokana na kufuatilia sifa za kila madhehebu.3

SUALA LA NNE: Sheikh Hakuwa Peke Yake Katika Elimu na Daawa: Baadhi ya wafuasi wa Sheikh wanadhania kuwa Sheikh alikuwa peke yake katika zama zake kielimu, na kwamba nchi ya Kiislamu ambayo haijaingia daawa yake ilikuwa ni nchi ya Kishirikina na ya Kikafiri, na kuwa wanazuoni wa nchi ile ni majahili hawajui kitu chochote katika dini. Na mfano wa hayo miongoni mwa itikadi za wafuasi wa Sheikh za kidhalimu, katika nchi za Waislamu na wanazuoni wa Kiislamu siku za Sheikh Muhammad. Na la kusikitisha ni 3

  Ili kupata maelezo zaidi kuhusu jina UWAHABI, rejea ifanywe kwenye Kiambatanisho, ibara ya pili. 8

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 8

1/20/2016 11:35:47 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

kuwa msingi huu wa kuwakufurisha Waislamu na kuizingatia nchi yao kuwa ni nchi ya kikafiri, na kuwa wanazuoni wao ni makafiri, nimeukuta katika maneno ya Sheikh mwenyewe - kama itakavyo kuja - na sisi pamoja na kuthamini kwetu athari ya Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahabi Mungu amrehemu, na mchango wake wa urekibishaji na wa daawa; ambao athari yake imepanuka na kuwafikia Waislamu wengi duniani, achilia mbali Waislamu wa ndani ya Bara Arabu ila ni kwamba mtafuta elimu ni wajibu atambue kuwa Sheikh na waliomfuata hawakuwa sahihi katika hili, na kwamba pamoja na Sheikh, katika karne tatu za mwishoni walikuwepo pia walinganiaji na wafanya marekibisho wengine, na kwa kupitia wanazuoni hao Mungu ameleta manufaa. Hivyo basi si sahihi kuzibomoa haki zao au kuwakufurisha Waislamu katika nchi zao, miongoni mwa hao ni Sheikh Shaha Waliyullah Dahlawiy, Sheikh Muhammad Hayati As-Sindiy, Sheikh at-Tahanuwiy al-Hindiy, na Allama Muhammad bin Ismail al-Amiri as-Swan’aniy. Na yeye alikuwa mjuzi zaidi kuliko huyo Sheikh Muhammad - na alikuwa wa wastani zaidi na mwenye athari ya kina na mwenye kukubalika mno kwa Waislamu wengine. Japokuwa Sheikh Muhammad - alikuwa na athari kubwa na mwenye harakati zaidi katika daawa.4 Na Muhammad bin Feyruzi wa Ahsa, mkuu wa mahanbali katika mji wa Ahsa, na wanazuoni wa Hijazi, kisha baada ya muda kidogo alikuja Imamu Shawkaniy al-Yamaniy baada ya Sheikh. Halafu katika karne ya mwisho walikuwepo wanazuoni na wanadaawa wenye athari kubwa za daawa kama tuonavyo katika daawa ya Sheikh Hasan al-Banna wa Misri na Allama Maududi wa Pakistani na Sehemu ya Bara la Asia, India, na Sheikh Jamaludini al-Qasimiy huko 4

  Ili kuwajua zaidi wanazuoni waliokuwa zama za Sheikh angalia kiambatanisho

ibara ya tatu.

9

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 9

1/20/2016 11:35:47 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Sham – Syria na al-Mahdiy Msudani huko Sudani, kuongeza juu ya hao wanazuoni wenye kutilia manani sana maarifa kuliko hima yao kwa umma, kama Sheikh Muhammad Abduh, na Jamaludini alAfghaniy na wengine wengi ambao rai zao katika mambo ambayo Sheikh anayahesabu kuwa ni shirki kubwa kwao wao ilikuwa si ukafiri. Kisha hatukatai kuwa hawa na wengine na khususan waliofuatwa, walikuwa na mchango mkubwa – Pamoja na yaliyoambatana na daawa hizi miongoni mwa makosa katika elimu au utendaji – katika kuufanya upya Uislamu na kuinua ari ya Waislamu na kusahihisha makosa sawa iwe katika imani au matendo. Na daawa za hawa warekibishaji zilikuwa daawa za Kiislamu kwa jumla. Na kuwa kwake daawa za Kiislamu haimaanishi kuwa hazikuwa na makosa. Na mas’ala hii haikutambuliwa na wengi miongoni mwa wafuasi ambao mwanga wa daawa hizi za marekibisho uliwatia kiwi wasiyaone baadhi ya makosa, ambayo yalifuatana na daawa zao. Kisha makosa haya yalikuwa na athari isiyokubalika kwa baadhi ya wanafunzi wa elimu, ambao waliwashabikia kupita kiasi hadi wakazuia kukosoa makosa yao. Na japo kinadharia waliendelea kutambua kuwa hao viongozi wao - wanazuoni walioshabikiwa hupatia na hukosea pia, lakini kiukweli hasa hautokuta tofauti kwa wafuasi wao kati ya mmoja miongoni mwao - hao wanazuoni walioshabikiwa - na Nabii 5. Na Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahabi Mungu amrehemu, sio wa pekee miongoni mwa hao wanazuoni, ni kama vile wafuasi wa Hasan al-Banna, walimshabikia kiasi cha kufurutu ada kumhusu yeye, na ndivyo walivyofanya wafuasi wa al-Mahdi kumhusu Mahdi (wa Sudani), na ndivyo walivyofanya waliomfuata Shawkani na Maududi na wengineo. Kwa hiyo walijitokeza wafuasi katika zama za Sheikh na baada yake waliofurutu ada kumhusu Sheikh, kufurutu 10

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 10

1/20/2016 11:35:47 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

kukubwa, walikuwa wanashabikia kila aliloandika ndani ya risala zake na fatuwa zake; bali na hukumu zake kuzihusu Hadithi, na rai yake kuhusu umma na dola na mtu binafsi na mengineyo.5 Kisha hawa – wafuasi wa Sheikh – wamefurutu ada katika ushabiki mpaka wameacha sehemu kubwa ya daawa ya Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahabi ambayo ilikuwa inakemea (kuwashabikia watu wema) kwani kufurutu ada kuwahusu watu wema ni miongoni mwa misingi mikubwa ambayo Sheikh, Mungu amrehemu, alikuwa anaikosoa. Kwa hiyo mas’ala hii ya msingi ni miongoni mwa mihimili ya itikadi kwa wafurutu ada miongoni mwa wafuasi wa Sheikh Muhammad, Mungu amrehemu.6 Na ufurutu ada wao umesaidia upande wa pili nao kufurutu ada, miongoni mwa masufi na Mashia na wafanya taklidi miongoni mwa watu wa madhehebu nne. Wamemshambulia Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahabi na kudhania kuwa ameleta dini mpya, au kuwa yeye ni matunda ya njama za Waingereza. Na kwamba yeye amedai unabii, na kuwa yeye anamchukia Nabii 5 na anamdhalilisha na mengine miongoni mwa uwongo na masingizio yaliyo batili.   Na miongoni mwa mifano ya kufurutu ada kumhusu Sheikh ni kauli ya baadhi yao kumhusu yeye: “Ni mwanachuoni wa kiungu na mkweli wa pili aliyejadidisha Daawa ya Kiislamu... ni wa pekee katika wanazuoni.” Tazama ad-Durarus-Saniyyah, Juz. 1, Uk. 29. Na Ibn Ubaydu katika kitabu Tadhkiratu Ulin-Nuha Wal-Irfani, Juz. 1, Uk. 173, amesema: “Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahhabi ambaye umma wa Muhammad umejionea fahari juu ya umma nyingine!” Na mtungaji amemuita kwa lakabu ya Sheikhul-Wujudi!! katika mashairi yake ndani ya kitabu Tadhkirah, Juz. 1, Uk. 33, nalo ni neno adhimu ambalo lau mtu mwingine angemuita Nabii 5 kwa jina hilo basi hao wanaomkalidi Sheikh wangekemea na huenda wangemkufurisha. 6   Bali sehemu kubwa ya Mas’ala za kijahiliya ambazo Sheikh ameandika kitabu kuzihusu ambacho ni wajibu wafurutu ada miongoni mwa wafuasi wake wao wenyewe warejee kukisoma, kwa masikitiko watakuta kiasi kikubwa kati ya yale yaliyomo humo wanayo wao wenyewe. (Rejea mifano yake katika Kiambatanisho ibara ya nne, utaona ni jinsi gani mas’ala hizo za kijahiliya zilivyothibiti miongoni mwa wafuasi wa Sheikh, Mungu amrehemu.) 5

11

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 11

1/20/2016 11:35:47 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Kwa hiyo ufurutu ada huu kutoka kwa mahasimu umesababisha kuendelea kwa ufurutu ada pinzani kutoka kwa baadhi ya wafuasi wa Sheikh ambao walimzingatia kila amkosoaye Sheikh kuwa ni hasimu wa daawa ya marekibisho na ni miongoni mwa mahasimu wa itikadi ya watangulizi wema, na huenda baadhi wanapindukia na kumuona huyu kuwa ni miongoni mwa mahasimu wa Uislamu! Na hili si jambo geni kwani kila mkuu wa dini katika wafuasi wake na mahasimu wake hujitokeza wafurutu ada; na hali hiyo huendelea ikiwa katika mahasimu na wafuasi hakutokuwa na watu wenye akili na insafu. Hivyo basi wafuasi wa Sheikh Muhammad wamekuwa wanazingatia kumpinga Sheikh ni kuupinga Uislamu wenyewe, ilihali hujuma yao kwa wanazuoni wa Waislamu na nchi za Waislamu na kuzituhumu kuwa ni nchi za kishirikina, tena shirki kubwa, hili kwao halizingatiwi kuwa ni uadui dhidi ya Uislamu. Na hiki ni kiini cha ufurutu ada ambacho Sheikh mwenyewe ­aliweka nadhiri ya kukilaumu na kujihadhari nacho na kupambana na watu wake kwa ulimi na upanga. Na mahasimu nao wanazingatia kwamba kumlinda na kutambua mema yake na maeneo yake yaliyo sahihi ni usaidizi wa kuubomoa Uislamu na kuieneza dini ya Makhawariji.

SUALA LA TANO: Jinsi Gani Wafurutu Ada Walivyouhodhi Uwahabi na ­Kuuhami? Kisha kuna jambo jingine inapasa kulifahamu kwa sababu ya umuhimu wake. Nalo ni kwamba kushika kasi kwa uhasama kati ya uwahabi na wapinzani wake na kuendelea uhasama huo mpaka hii leo, kumesaidia kuchomoza wimbi la ufurutu ada miongoni mwa 12

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 12

1/20/2016 11:35:47 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

wafuasi wa Sheikh, hivyo wamekuwa wao ndio wenye hamasa zaidi ya kujibu. Na wao kadiri muda unavyosonga mbele wamekuwa ndio wenye haki ya kutamka kwa jina la daawa, na kuhodhi haki ya kuihami itikadi ya watangulizi wema, na kufurutu ada katika kuwatuhumu wapinzani na katika kuyalinda na kuyatetea makosa ya Sheikh, kwa minajili hiyo yale aliyoyapigania Sheikh jana, leo yametelekezwa na mahasimu na wafuasi wake wote kwa pamoja bila tofauti, ila kwa yule ambaye Mola Wako amemrehemu.7 Na hili liko wazi zama zetu hizi, yakaribia kutokukuta ila ufurutu ada kumhusu Sheikh au ufurutu ada dhidi yake, au kumhusu Ibn Taymiya au dhidi yake. Na wafurutu ada wa pande zote mbili hawako tayari kufanya maongezi yaliyo tulivu yaliyo mbali na ushabiki. Na alama ya mtu mwenye kufurutu ada dhidi ya Sheikh ni kuwa hakubali ila kumsifu kwa kila ubaya, kama ambavyo alama ya mwenye kufurutu ada ya kumpendelea Sheikh – na hilo ndilo la muhimu kwetu katika risala hii – ni kuwa hakubali kumkosoa Sheikh na anaona kuwa ni dhambi 7

Ni kama hivyo wafurutu ada wa kiwahabi wamehodhi haki ya kuuhami uwahhabi kama walivyo hii leo, wamehodhi haki ya kumhami Sheikh kama muonavyo katika majibu ya haraka haraka na yenye kuchukiza ya baadhi ya ndugu ndani ya maandiko haya ya kumbukumbu, miongoni mwa wale wanaokaribia kumhesabu kuwa ameritadi yule anayemkosoa Sheikh! Na hali hii inashabihiana na ile ya Manawasibu wakiwemo wafurutu ada wa Kisunni, katika kuwajibu Shia na kutamka kwa jina la Usunni, na kisha wameanza kumkejeli Ali bin Abu Talib na Ahlulbayt wake kwa jina la Usunni! Na wanamsifu Muawiya na Yazid na wafuasi wao kwa jina la Usunni! Kama tufanyavyo katika risala zetu nyingi za chuo kikuu! Kisha imekuwa anayewakosoa anakuwa kwenye hatari ya kutuhumiwa kuwa ni Shia na Rafidhu! Kama ilivyo kwa mwenye kuwakosoa wafurutu ada wa kiwahabi yuko hatarini kutuhumiwa kuwa anahasimiana na daawa ya watangulizi wema, na huenda akatuhumiwa kuwa ni adui wa Uislamu na ni mwabudu makaburi! Haya yote hutokea kwa sababu ndogo; Nayo ni kwamba wafurutu ada ndio waliohodhi haki ya kutetea na kubainisha. Kwa hiyo anautetea usalafi yule ambaye si salafi, na anautetea Usunni yule aliye mchanganyiko kati ya Usunni na Unawasibu na Marjiah na Jebria. Na watetezi wanakuwa na kipaumbele cha kuongea kwa jina la madhehebu au harakati au kundi, na wanapata kutambulika kadiri zama zinavyokwenda, hivyo wao mwanzoni wanaridhika na ujirani, kisha inakuja hatua yao ya pili, nayo ni kuwatoa nje wenye nyumba wa asili! Na huu ni mwenendo wa kimaisha upo ndani ya madhehebu, makabila na vikundi. 13

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 13

1/20/2016 11:35:47 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

adhimu kumkosoa. Na aibu hizi zimeenea kwa aina zote za wafurutu ada, sawa wawe wafurutu ada wa kisalafi au wa kishia au wa mmoja wa maimamu wa nne.

SUALA LA SITA: Vipi Tutazuia Wimbi la Wafurutu Ada Kuuhodhi Uwahabi? Kwa kuwa sura yetu sisi - wanataaluma katika Mamlaka ya Saudi Arabia – imechafuka kwa sababu ya wafurutu ada kutawalia ­tathmini ya daawa ya Sheikh ikiwa ni pamoja na yanayoambatana na hili miongoni mwa ufurutu ada kumhusu Sheikh na daawa yake, imekuwa ni lazima kwetu kuangalia upya, na tuwazuie wafurutu ada kuongea kwa jina la wanataaluma katika Mamlaka ya Saudi Arabia, na tushirikiane nao katika kutathmini na kufanya rejea, kwa kuanzia mambo kadhaa: Jambo la Kwanza: Tujue ujuzi wa yakini kuwa zao lolote la mwanadamau – iwe kitendo au tunda la kifikra - lahitajia kila baada ya muda fulani lifanyiwe rejea na kutathminiwa, ili kuupa nguvu usahihi na kuepuka makosa, hakuna aibu katika hili, sio kisheria wala kiakili, bali hii ni alama ya kujiamini ndani ya nafsi, na kwamba fikra ya ukweli ndio inayokusudiwa kuchungwa na si watu. Jambo la Pili: Ni kuwa baadhi ya makosa ambayo Sheikh ameangukia humo, na wengi miongoni mwa wafuasi wake na hususan katika kukufurisha; yamewaingiza humo wanataaluma wengi, imma kwa kumkalidi au kwa kufurutu ada ndani ya Mamlaka ya Saudi Arabia na nje yake, na hali hiyo imejitokeza katika matukio ya utumiaji nguvu ya mwishoni, kwani dalili za kukufurisha ni zile zile, na jinsi ya utolewaji dalili ni ule ule na kaulimbiu ni zile zile. 14

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 14

1/20/2016 11:35:47 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Jambo la Tatu: Kukaa kimya kwa kila mwanataaluma ndani ya Mamlaka ya Saudi Arabia, bila kubainisha makosa hayo; japokuwa kuna haja ya dharura kabisa ya kufanya rejea, na kila mwenye uwezo afanye kupitia huko na kurejea huko kuwa ni wajibu juu ya kila mtu, na hilo ndilo limenifanya mimi niandike somo hili. Jambo la Nne: Ni haki ya kila mwanataaluma na kila mkazi ndani ya Mamlaka ya Saudi Arabia kuwasilisha lile aonalo kuwa litaondoa uendeleaji wa utumiaji nguvu na ukufurishaji, azitaje sababu za kweli, ajiweke mbali na majigambo ambayo hayatoidhuru ila nchi na wananchi wake kwa muda mrefu japo itaonekana kwetu kuwa yana maslahi ya karibu. Ni haki yetu kuihami dini yetu na nchi yetu isichafuliwe na fikra za kidhalimu au damu iliyohifadhika; kufanya hivyo tutakuwa tumeiinua heshima ya dini yetu na sisi wenyewe na nchi yetu; kwa kuwa sisi katika watu hatumfuati ila Muhammad 5 na kuwa sisi hatuzunguki ila kwenye: “Amesema Mwenyezi Mungu, amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu.� Na tuyasadikishe haya kwa vitendo, na kutaja mifano ya makosa ya tunaowatukuza na kuwathamini mfano wa Sheikh Muhammad, Ibn Taymiya, Ahmad bin Hanbal na wengine. Na japokuwa sisi kwa jumla ni matunda ya juhudi za Sheikh, Mungu amrehemu, ila sisi hatumfanyi Nabii Maasumu. Bali kauli zake tunaziweka chini ya utii wa hukumu za kisheria, wala hatumuweki juu ya sheria. Bali yeye na wanazuoni wote wanahukumiwa na sharia. Kila mmoja huchukuliwa kwa kauli yake na hujibiwa. Na kila mmoja hufanywa dalili kwa ajili ya usemi wake.... Na kila mmoja hakushuka kutoka mbinguni, na kila mmoja ni mwenye kuamriwa arejee kwenye dalili za kisharia sio kwenye kauli za watu. Huu ndio usalafi wa kweli. Hizi ni kanuni adhimu hutekelezwa juu ya wote, na ni wajibu wote waziheshimu na washikamane nazo. Na mwanachuoni ni wajibu ajue kuwa hii ndio itikadi yetu, haya ndiyo madhehebu 15

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 15

1/20/2016 11:35:47 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

yetu, hatuna madhehebu nyingine. Lakini kuhusu kanuni hizi maneno hayatoshi, hivyo hapana budi kutaja dalili za msimamo huu wa wastani. Na kwamba sisi tupo tayari kuwakosoa wanazuoni wetu, pamoja na kuwahifadhia upendo wao na kuwaombea dua na kuzithamini juhudi zao. Hakuna linalopingana kati ya mambo mawili haya ila kwa wafurutu ada wa pande mbili zote. Kwa hiyo yeyote aonaye kuwa upendo wetu kwao unazuia kuwakosoa basi yeye ni mfurutu ada katika kuwapendelea, na aonaye kuwa kuwakosoa kwetu kunazuia upendo wetu kwao basi yeye ni mfurutu ada dhidi yao. Hivyo upendo na kukosoa, kuthamini na kumchukulia mtu kwa makosa yake, yote hayo yanakwenda pamoja bila ya kupingana wala kuelemea upande mmoja dhidi ya mwingine, na Ibin Taymiyah amesema kuwa “Mtu huenda akawa apenda kwa upande fulani na akawa achukia kwa upande fulani.” Na mimi ninasema: Tunaweza kupenda kwa mtu baadhi ya kauli zake na matendo yake na vitu fulani kutoka kwake, na tukachukia kwa mtu huyo huyo kauli zake nyingine na matendo yake mengine. Huu ni uadilifu na ni sahihi, na ni ukweli tunaougusa nafsini mwetu pindi linapofanywa jaribio la kumtathmini mtu au kikundi cha watu au mkondo. Ama upendo wa moja kwa moja na chuki ya moja kwa moja kumchukia mtu, kauli zake, na matendo yake, huku ni kuingia katika upofu hali nuru ipo nyingi, na ni kujiingiza katika maangamizi hali waweza kujiepusha.

SUALA LA SABA: Je ni Sharti Kwamba Wafurutu Ada Waainishe Mtu wa ­Kurejea na Kukosoa?

16

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 16

1/20/2016 11:35:47 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Na hapa kuna swali linalojitokeza lenyewe nalo ni kuwa: Baadhi huenda wakasema: Maneno yako ni sahihi kwa upande wa nadharia, lakini usahihishaji na ukosoaji hatutaukubali ikiwa utafanywa na wewe au na fulani au fulani! Lakini tutaukubali ikiwa tu utafanywa na wanachuoni (wanaoaminika) katika daawa! Bali baadhi yao walisema - baada ya kutoka mswada wa kwanza - ambao ni sehemu ya kitabu hiki: “Huyu Zaydiya ni nani? hata aje kutufundisha itikadi?!� Na kwa Ajili ya Kujibu Nasema: Kwanza: Si sharti kwa atakaye kupitia upya apate shahada ya utakaso na ya usafi wa tabia njema, kutoka kwa waonao uzuri wa tabia, kuwa safi na utakaso, hivi vinakomea kwa wafuasi wao wanaowakalidi. Pili: Sio sharti kwamba mkosoaji wa madhehebu ni lazima awe mmoja wa wafuasi wa madhehebu husika; wafurutu ada wetu hao wanakosoa kila madhehebu na wao si wafuasi wa madhehebu husika! Tatu: Kujengea hoja juu ya utangulizi wenye makosa pia ni miongoni mwa alama za wafurutu ada. Hivyo basi hasimu wenu pamoja na kuzithamini kwake madhehebu zote za Kiislamu yakiwemo madhehebu ya Zaydiya, nayo ni miongoni mwa madhehebu za Ahlulbayt, isipokuwa yeye si mtu wa madhehebu hii, na kwa kuwa yeye anapenda na anaona bora abakie Sunni aliye huru, haambatani na madhehebu yoyote, na kujiambatanisha kwake na madhehebu ya Hanbali ni dharura itokanayo na malezi kwani ameleleka kutokana na madhehebu hiyo, vinginevyo ni bora kwa Mwislamu achukue kutoka kila madhehebu kile kilichoungwa mkono na dalili. Na hii ndio sunna ya kweli, ambayo juu yake kuna nadharia zote zinazokubalika 17

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 17

1/20/2016 11:35:47 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

ndani ya Usunni, japo itafunwe na ndimi na kalamu na kutemwa na nyoyo na matendo; Hili ni la kawaida kwa sababu vitendo huwa nyuma ya maneno, na utekelezaji huwa nyuma ya nadharia. Kwa hiyo watu wengi wanaishi kwa mwanga wa nadharia na uhaba wa utekelezaji. Na hapo kale Imamu Shafi aliwakabili waliokuwa wana shaka na Usunni wake kwa sababu tu ya kuwapenda kwake Ahlulbayti na kuwahami kwake, akasema: “Ikiwa kuwapenda Aali Muhammad ndio Rafdhu, basi vizito viwili (Qur’ani na Kizazi cha Mtume) viwe mashahidi kwamba hakika mimi ni Rafidhu!”

Na kuwa kwake mtu huyu – ambaye yeye ni shakhsia dhaifu amesoma historia na akaitilia manani na akaitambua haki ya Imamu Ali na Ahlulbayti wake, na kwa kiwango gani wao wamedhulumiwa na utamaduni wetu, na ameitambua dhulma ya Bani Umayya na ufedhuli wao, na kwa kadiri gani wao – Bani Umayya - wanalindwa na utamaduni wetu, mtu wa namna hiyo hatokuwa na jingine ila kukosoa na kuweka wazi kuwa huyu kapatia au kakosea. Na kukosoa uegemeaji huu wa upande mmoja na dhulma hii, si jambo mahsusi kwa ajili ya Zaydiya tu – bila kujali usahihi wa fikra au makosa yake - bali ni wajibu tuikatae dhulma sawa iwe imefanywa dhidi ya Ahlulbayti au Muutazilah au Jahamiya au Ashairah au Sufiyah au hata iwe imefanywa dhidi ya makafiri wanaoishi kwa amani. Na hao wote kwa kweli tumewadhulumu. Kisha si kwa kuwafuata Zaydiya au Ibaadhiya au Imamiya ndio maana yule (asiyejulikana kabisa)8 anasema yale ambayo ni sehemu ya itikadi za Zaydiya au ni sehemu ya yanayonasibishwa kwao kama kauli yao ya kwamba: Hawa wanne ni maasumina 8

Hapa anajikusudia yeye mwenyewe mwandishi kuwa ni mtu asiyejulikana kabisa, na hii inatokana na jinsi alivyokejeliwa baada ya mswada wake wa kwanza kutoka. – Mhariri. 18

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 18

1/20/2016 11:35:47 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

“Ali, Fatma, Hasan na Husein” au kuitanguliza kwao akili mbele ya nukuu,9 wala kutabaruku na watu wema,10 wala mengine yasiyokuwa hayo yaliyotajwa miongoni mwa ambayo husemwa kuwa ni misingi ya Zaidiya,11 ikiwa ni pamoja na yeye kukemea dhulma ya Muawiyya. Bali yeye anaona kuwa huku ni kufuata kwake nususi za kisheria ambazo anaamini usahihi wake katika vitabu vya kisunni ambavyo amevisoma na kujivunia bila kuamini kuwa   Na hili ndilo wasemalo Muutazila na Zaydiya, na kila mmoja wao anaona mwenzake amechukua kutoka kwake, kadhalika hilo wanalisema baadhi ya Ashairah, lakini kwa ajili ya insafu inapasa tuseme kuwa, makusudio ya vikundi hivi kuwa itangulizwe akili mbele ya nukuu sio ule unaovumishwa na Masalafi (Mawahabi), na ufafanuzi wa hili utakuwa mrefu, hivyo basi mwenye kutaka kutambua hilo afanye rejea kwenye vitabu vyao hao jamaa, au vitabu vilivyoandikwa kuwahusu wao na waandishi wa Kisunni wenye insafu, kama Dr. Ahmad Swabhiy (ameandika kuwahusu Muutazilah na Zaydiya), au Abdur Rahman Badawiy katika kitabu Madhahibul-Islamiyina. Au Dr. Ali Saamiy anNishar katika kitabu Nash’atul-Fikru al-Falsafiy Fil-Islami. Au Dr. Muhammad Ammara na wengine, mas’ala hii haipo kama wanavyoikuza Masalafi (Mawahabi). 10   Walio wengi miongoni mwa Ahlu Sunna (sio Masalafi (Mawahabi) wa wakati huu) walikuwa wanaona inafaa kutabaruku bali huyu hapa Imamu Dhahabi katika TarjumatulKarkhiy anaona kuwa udongo wa kaburi la al-Karkhiy ni mujarabu, ni dawa ya kupoza nguvu ya sumu. Hivyo hivyo Mahanbali waliotangulia walikuwa masufi, walikuwa wanaona inafaa kujipangusa na kaburi la Nabii 5 na mkomamanga wa mimbari ya msikiti wa Nabii 5 bali hii imethibiti kutoka kwa Ahmad Bin Hanbali mwenyewe, na wala Mahanbali waliotangulia hawakuwa mahasimu wa Usufi. Bali walikuwa mahasimu wa daraja ya kwanza wa Jahmiya (wanawakusudia Muutazilah) na Shia. Upindukiaji huu wote ni kwa sababu Khalifa wa Bani Abbasi Maamun alikuwa Shia Muutazilah, na kwamba yeye ndiyo sababu ya kufanyiwa mtihani Ahmad bin Hanbal, hivyo kadhia hii mwisho wake ni suala la mtu binafsi. Kisha Ibn Taymiya aliongeza uhasama na Masufi na akawaambatanisha Shia na Jahmiya (na amewaongeza hapa Muutazilah Ashairah!). Kisha umekuja uwahabi ukaongeza katika uhasama wafuasi wa madhehebu nne ambao hawaafikiani na Sheikh Muhammad, na ukaongeza mambo mawili makubwa: Kupanua wigo wa ukufurishaji na kufatiwa na uuaji, na Mawahabi wamekuwa wa pekee kwa kuzigawa nchi za Kiislamu kati ya nyumba za kufuru na nyumba za Kiislamu, kiasi kwamba hata Riyadh imekuwa ni nyumba ya kufuru na Deriya ni nyumba ya Kiislam, na watu wa miji hiyo wanasikia adhana ya swala katika miji yote miwili kwa wakati mmoja! 11   Hakika wengine wameshirikiana nao katika baadhi ya haya, kama kutabaruku na watu wema hii inakaribia kuwa ni rai ya jamhuri ya wenye elimu kama alivyonukuu alHafidhu Ibn Hajar. 9

19

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 19

1/20/2016 11:35:47 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

yasiyokuwa hayo yaliyotajwa miongoni mwa ambayo husemwa kuwa ni misingi ya Zaidiya,11 ikiwa ni pamoja na yeye kukemea dhulma ya vitabu hivyo – nakusudia vitabu vya ni maasumu visivyo Muawiyya. Bali yeye anaona kuwa huku ni kisunnikufuata kwake nususi za kisheria ambazo anaamini usahihi wake katika vitabu vya kisunni ambavyo na makosa. amevisoma na kujivunia bila kuamini kuwa vitabu hivyo – nakusudia vitabu Na kuhusu yeye kuikemea vya kisunnini maasumu visivyo na dhulma makosa.ya Muawiya, na hili pia haku-

lifanya kwa kuwafuata Zaydiya au Ibaadhi au Imamiya, bali anaona

Na kuhusu kuikemea ya Muawiya, hili pia hakulifanya kwa huku niyeye kufuata nususidhulma za kisharia ambazonaanaamini usahihi wake kuwafuata Zaydiya au Ibaadhi au Imamiya, bali anaona huku ni kufuata katika vitabu vya kisunni ambavyo amevisoma na anavitambua na nususi za kisharia anaamini usahihi wake katika vitabu vyavitabu kisunni anajivunia bilaambazo ya kuamini kuwa vitabu hivyo – nakusudia ambavyo amevisoma na anavitambua na anajivunia bila ya kuamini kuwa vya kisunni- ni maasumu visivyo na makosa. Kisha nususi hizo zinavitabu hivyo – nakusudia vitabu vya kisunni- ni maasumu visivyo na makosa. zokemea na kuiambatanisha na uovu, na zipouchafu katikana Kisha nususi dhulma hizo zinazokemea dhulma na na uchafu kuiambatanisha Kitabu cha Mwenyezi Mungu ambacho ndioambacho chimbuko la Waislamu uovu, zipo katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu ndio chimbuko la wote, kama ilivyokuja katikakatika kaulikauli YakeYake tukufu: Waislamu wote, kama ilivyokuja tukufu: Ç⎯tã 4‘sS÷Ζtƒuρ 4†n1öà)ø9$# “ÏŒ Ç›!$tGƒÎ)uρ Ç⎯≈|¡ômM}$#uρ ÉΑô‰yèø9$$Î/ ããΒù'tƒ ©!$# ¨βÎ) * ∩®⊃∪ šχρã©.x‹s? öΝà6¯=yès9 öΝä3ÝàÏètƒ 4 Ä©øöt7ø9$#uρ Ìx6Ψßϑø9$#uρ Ï™!$t±ósxø9$# “hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha uadilifu na hisani “Hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha uadilifu na hisani na kuwapa na kuwapa jamaa na anakataza uchafu na uovu na jamaa na anakataza uchafu na uovu na dhulma. Anawapa mawaidha dhulma. Anawapa mawaidha ili mpate kukumbuka.” ili mpate kukumbuka.” (Sura Nahli: 90). (Sura Nahli: 90).

Ikiwa huyu (asiyejua kabisa) hakuratibu ujira kwa ajili ya wala kwa ajili ya uovu kama mnavyofanya, ya udhalimu nukuu sio ule unaovumishwa nauchafu Masalafina (Mawahabi), na ninyi ufafanuzi wa hili utakuwa mrefu, hivyo basi mwenye kutaka kutambua hilo afanye rejea kwenye vitabu vyaoauhao maana yake sio kuwa yeye anafuata madhehebu ya Zaydiya jamaa, au vitabu vilivyoandikwa kuwahusu wao Imamiya au Dhahiriya au Jahmiya.12 na waandishi wa Kisunni wenye insafu, kama Dr. Ahmad Swabhiy (ameandika kuwahusu Muutazilah na Zaydiya), au Abdur

12 Rahman Badawiy kitabukuwa Madhahibul-Islamiyina. Ali Saamiy an-Nishar   Nataraji yeyotekatika asifahamu mimi kwa maneno Au hayaDr. namaanisha kuyalaumu katikamadhehebu kitabu Nash’atul-Fikru Dr. Muhammad Ammara miongoni mwa al-Falsafiy madhehebu Fil-Islami. za Kiislamu,Au si Jahmiya wala Zaydiya wala na wengine, mas’ala hii haipo kama wanavyoikuza Masalafi (Mawahabi). Muutazila, la hasha hapana. Hatuilaumu madhehebu moja kwa moja wala hatuisifu 10 Walio wengi mwa Ahlu wapo Sunnawafurutu (sio Masalafi (Mawahabi) wawa wakati huu) moja kwa miongoni moja, kila madhehebu ada na wenye msimamo wastani, walikuwa kutabaruku balihatuwalaumu huyu hapa Imamu Dhahabi katika Tarjumatulwenyewanaona ushabiki inafaa na wenye insafu, wala waja wema wa Mwenyezi Mungu. Karkhiy anaona kuwa udongo wa kaburi la al-Karkhiy ni mujarabu, dawa ya kupoza Kisha chuki hii kutoka kwa baadhi ya Masalafi kuzichukia madhehebuni nyingine si sheria nguvukulingana ya sumu. Hivyo hivyo Mahanbali waliotangulia walikuwa masufi, walikuwa na kipimo cha kisharia. Na ni wanazuoni wangapi Muutazilah, au Jahmi  na mkomamanga wanaona inafaa kujipangusa la Nabii wangapi waadilifu ni bora na kwakaburi Mwenyezi Mungu kuliko Sunni dhalimu, wa bali mimbari ni kipimo ya na kigezo cha kimadhehebu ndicho ambacho kinawafanya wafuasi wake wanajipa na msikiti wa Nabii  bali hii imethibiti kutoka kwa Ahmad Bin Hanbali mwenyewe, wala Mahanbali waliotangulia hawakuwa mahasimu wa Usufi. Bali walikuwa mahasimu wa daraja ya kwanza wa Jahmiya (wanawakusudia Muutazilah) na Shia. Upindukiaji huu 20 wote ni kwa sababu Khalifa wa Bani Abbasi Maamun alikuwa Shia Muutazilah, na kwamba yeye ndiyo sababu ya kufanyiwa mtihani Ahmad bin Hanbal, hivyo kadhia hii mwisho wake ni suala la mtu binafsi. Kisha Ibn Taymiya aliongeza uhasama na Masufi na akawaambatanisha Shia na Jahmiya (na amewaongeza hapa Muutazilah Ashairah!). Kisha 15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 20 umekuja uwahabi ukaongeza katika uhasama wafuasi wa madhehebu nne1/20/2016 ambao11:35:48 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Tatu: Sheikh Muhammad mwenyewe na kabla yake Ibn Taymiya na wengi miongoni mwa ambao (mtu) hujifaharisha nao, hawakungoja utakaso na kuepushwa na dosari kutoka kwa wanazuoni wa zama zao ili wapitie upya au wafanye rejea ukiachia mbali tathmini ya upitiaji upya huu na rejea hii. Bali Sheikh kwa mfano alikuwa anawaonesha wazi dalili na anawaomba dalili, pamoja na kuwa wao walikuwa wanamuona ni mchache kielimu, na ndivyo walivyofanya wanazuoni na wanadaawa zama zote. Ambalo ni wajibu kwa mrekibishaji ni auweke wazi ukweli pamoja na kuonesha dalili zake na aipinge batili bila ya kungoja upande wa pili uridhike au ukasirike; kwa kuwa dini sio kitu cha kuhodhiwa na kikundi fulani cha watu, bali ni ya wote. Kisha mtu atahesabiwa kwa dalili zake na uthibitisho wake na atapingwa kwa dalili na uthibitisho akiwa ni mtafuta haki. Nne: Usemi huu kuwa usahihishaji inabidi ufanywe na baadhi ya watu, ni batili. Usemi kama huo ulirudiwa na makafiri wa kikuraishi kwa usemi wao: “Na walisema: Kwa nini Qur’ani hii haikuteremshwa kwa mtu mkubwa katika miji miwili hii?” (Sura Zukhruf: 31). Jambo ambalo lilikuwa linawazuia makafiri wengi kufuata mwongozo ni kuwa wao hawakuridhika na nyumba ya Bani Hashim iwe ya unabii, na walikuwa wanataka udhihiri katika nyumba nyingine zenye dhamana ya maslahi ya makurayshi. Lakini Allah hakuwakubalia kwani Allah ndiye mjuzi mno wa mahali anapoweka ujumbe Wake. Na hii ni miongoni mwa mitihani ili abainike anayefuata haki na anayefuata kabila. Na warekebishaji wote katika muda wote wa historia hukabiliana na changamoto hii. Haki na kuisema ni wajibu juu ya kila Mwislamu, wala sio mahsusi kwa kundi moja miongoni mwa watu, wala kitongoji matumaini wao wenyewe na wanawachukia Waislamu wengine. Na kwa ajili ya taarifa zaidi khususan kuhusu Zaydiya angalia kiambatanisho ibara ya tano. 21

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 21

1/20/2016 11:35:48 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

miongoni mwa vitongoji. Sidhani kuna mtu mwenye akili mwenye dini miongoni mwa wanataaluma anaona uoni huu wa kijahili ambao Muhammad bin Abdullahi 5 ametumwa kuutengua, kabla hajaanza kuukosoa Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahabi Mungu amrehemu katika kitabu chake mashuhuri Masailu Ahlil-Jahiliyyah. Tano: Ajuaye nia za watu ni Mwenyezi Mungu, ni watu wangapi huaminiwa na baadaye hufanya khiyana. Na ni watu wangapi hudhaniwa dhana mbaya hali ni mtu bora mara elfu kwa ajili ya Uislamu ukimlinganisha na mtu anayeaminiwa, kwa minajili hiyo tuache upekuzi katika nia. Ajuaye nia za watu ni Mwenyezi Mungu, na sisi tuangalie kwenye dalili ipi iliyo karibu na Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna ya Mjumbe Wake 5. Sita: Halafu hao wa kuaminika wako wapi? Sisi tunawaona wamenyamaza kimya! Mpaka sasa hawajabainisha sababau za kweli za ufurutu ada, na wala hawajafanya rejea kwenye yale waliyozalisha Masalafi na Mawahabi. Pamoja na kuafikiana kwa Waislamu na makafiri kuwa zao hili lina mchango mkubwa katika ufurutu ada. Hatujawaona hao wanaoaminika wakibainisha makosa ambayo Ibn Taymiya ameingia, au Sheikh Muhammad au baadhi ya wanazuoni wa daawa. Mpaka wamedanganyika kwa ajili ya makosa hayo baadhi ya vijana na harakati ambazo zinaharakia kukufurisha na kuwatupia huo ukafiri wasio na makosa. Wala sitaki kupiga mifano kwa kuwa hayo yapo wazi kwa wote. Na sidhani kama baadhi ya wanaoaminiwa watatuacha sisi tubainishe ukweli, sembuse kushiriki katika hilo, kwa kuwa maslahi yao – siyo maslahi ya Uislamu – yanalazimu kumpinga kila mtoa nasaha na kuingiwa na shaka na njia yake na utaratibu wake. Wangali wanahitaji kupambana na nafsi na wakati mrefu mpaka wafikie daraja hii tuonayo kuwa ni dharura katika zama hizi kuliko wakati wowote uliopita. 22

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 22

1/20/2016 11:35:48 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Kwa hali yoyote hapana budi tuwe na ushujaa wa kuanza kukosoa makosa yetu na kufanya marekebisho ndani ya nyumba zetu. Na kutoona haya kufanya hivyo. Kwa kuwa suala ni la kidini sio werevu wa kisiasa wala sio kutafuta dunia.

SUALA LA NANE: Wafurutu Ada Wanakataza Ufurutu Ada! Ni miongoni mwa maajabu ya zama hizi, kuwa tunawakuta wafurutu ada wanakataza ufurutu ada na wanaupa ulinzi ukufurishaji wa kisalafi na wa kiwahabi, na wanalitakasa konyezo kwa upeo wote katika jambo hili la hatari, na wanaziegemeza sababu za ufurutu ada juu ya shabihi aliyoiandika Maududi na Sayyid Qutubi Mungu awarehemu, na wanasahau ukufurishaji wa wazi unaotokana na utamaduni wetu wa kisalafi na kiwahabi. Je hawaoni haya hao ambao wanajaribu kupanda farasi wawili wote kwa wakati mmoja! Kwa hiyo wanawapinga watu wanaokufurisha nao wanabakia katika kukufurisha! Wanawahujumu walioangukia katika shabihi ya kukufurisha na wanafurutu ada katika kuyalinda makosa ya Ibn Taymiya na maimamu wa daawa katika kukufurisha! Naam, huu sio mwisho wa ibara zinazopingana za wafurutu ada! Ndio tumekuwa tukiona wafurutu ada wakikataza ufurutu ada. Wanakemea wimbi la ukufurishaji la vijana ambao kupitia wao wamepotea, na kutoka katika mto wa maji yao wamekunywa, na katika bahari yao meli za ufurutu ada na msimamo mkali zimetia nanga. Hao wafurutu ada ambao wanakataza ufurutu ada wamekuwa wakipinga wimbi la matumizi ya nguvu ya ukufurishaji kwa dalili za wanazuoni ambao walikuwa wanampinga Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahabi! Wamekuwa wao kwa tendo lao hili kama 23

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 23

1/20/2016 11:35:48 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

kwamba wanampinga Sheikh Muhammad pamoja na ufurutu ada wao kumhusu yeye, na kuzuia kwao kukipitia upya alichozalisha na kutathmini utaratibu wake, kwa njia hii ambayo inakusanya pamoja kati ya vitu viwili vinavyopingana kwa hali ya juu mno. Na sisi tunawaambia: Ikiwa kupingana huku ni kwa sababu ya kutojua basi ni nani kati yetu ambaye hajitambui, na hakuna kinachozuia kujisahihisha na kuacha kufanya makosa. Na ikiwa kupingana kwao ni katika hali ya kujua na ni kwa sababu za kisiasa, basi Mungu ameharamisha kujigeuza rangi na kujitokeza na sura mbili; Nabii 5 amemlaumu mwenye nyuso mbili. Hivyo basi wataambiwa: Mkiwa mnawapinga hawa vijana wakufurishao; basi ni juu yenu jibu lenu liwe linalokinaisha kwa kuikosoa misingi walioifuata na kuishikilia, na wanazuoni ambao waliweka kanuni hizi za huu ukufurishaji na matumizi ya nguvu, dhidi ya wanazuoni na watawala wa zama zao. Na ikiwa mnamlinda Ibn Taymiya na Sheikh Muhammad na wanazuoni wa daawa na mnawaona wamepatia basi ni wajibu muwalinde hao vijana wakufurishaji, kwa kuwa wao ni wenye kuwafuata wanazuoni mliokataza kuwakosoa, na ni wenye kuchukua kutoka vitabu ambavyo mmewafundisha, na mumewausia kushikamana navyo, na mifano itakuja. Na mimi kwa himidi Yake Mungu - japo baadhi wamenidhania vibaya - sifanyi jamala kwa gharama ya ukweli; kwa ajili hiyo najikuta binafsi ni hasimu kifikra na wafurutu ada wa madhehebu mbalimbali na vikundi na mawimbi tofauti; na ninadai kuwa nina wajihi mmoja nazipinga shabihi za kukufurisha sawa aliyezisema awe hasimu au rafiki, mwenye nguvu au dhaifu, mwanafunzi wa elimu au mwanachuoni au mtu wa kawaida. Na kuzipinga kwangu shabihi hizi naona ni wajibu wa kidini pamoja na kuhifadhi haki ya Uislamu kwa wote na haki mahsusi 24

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 24

1/20/2016 11:35:48 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

ya Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahabi, kwa kumzingatia kuwa ndiye sababu ya jamii hii kubwa. Ambapo raia wa nchi hii wamekutana kutokea Kaskazini ya mbali mpaka Kusini ya mbali, na kutokea Mashariki ya mbali mpaka Magharibi ya mbali, kwa hiyo Sheikh akawa ndio sababu - baada ya tawfiki ya Mungu – kumaliza mgawanyiko wa vikundi na mizozo, pamoja na kutawanya elimu na daawa ili kuifanya imani iwe sahihi mbali na yaliyoambatanishwa nayo, na mbali na mambo ambayo imekutana nayo na kuambatanishwa nayo, miongoni mwa dosari na ngano za uwongo wa kijami. Hayo yote ni vitu tunavitambua na kuvithamimi, na tunampenda Sheikh kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kwa hivyo na tunamuombea. Lakini mema haya kugeuka kuwa kizuizi cha mtazamo wa kielimu katika kukosoa na kusahihisha dosari, hilo hapana! Hapana kheri kwetu ikiwa hamu yetu katika kumtakasa Sheikh na wanachuo wa daawa ni kubwa zaidi kuliko hamu yetu katika kuutakasa Uislamu wenyewe. Basi tutakuwa wafuasi waovu wa Uislamu endapo kujitoa kwetu muhanga kwa ajili ya Uislamu kutakuwa ni chini ya jinsi tunavyowatakasa watu fulani. Na vyovyote itakavyokuwa haki ya Sheikh juu yetu - Mungu amrehemu – bado haki ya kuutunza na kuulinda Uislamu ni kubwa zaidi, na ni bora zaidi tuutakase Uislamu mbali na mitizamo ya wanaofuatwa na utendaji wa wafuasi.

SUALA LA TISA: Vyanzo Vyetu Katika Kutambua Fikra ya Sheikh na Njia Yake: Hatukukutana na zama za Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahabi ili tuweze kuchukua ushuhuda wa watu kwa ajili yake au dhidi yake, lakini yeye ameturithisha vitabu na harakati au wimbi kubwa linalonadi kwa jina lake na kulingania kwa njia yake. Ama kuhusu 25

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 25

1/20/2016 11:35:48 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

wimbi la wanaharakati, kwa kweli tumeishi kati yao, na Mwenyezi Mungu ni shahidi kuwa wao kwa sura ya jumla, wanamdhulumu aliye kinyume na rai yao na wanafanya wawezavyo ili kumuweka mbali na kumtilia shaka na kumfanyia uadui. Na ni miongoni mwa mambo magumu kuthibitisha kiwango cha dhulma na ushabiki, kwa minajili hiyo hakuna kilichobakia katika kutathmini njia ya Sheikh isipokuwa matunda yake ya kielimu, miongoni mwa vitabu walivyochapisha wafuasi na kuvinasibisha na yeye na kuthibitisha kuwa vinatokana na yeye. Kama vile vitabu: At-Tawhidu, Kashfu-Shubuhati, Masailu AhlilJahiliyah au vingine miongoni mwa vitabu vya Sheikh na barua zake. Na hivi – vitabu – pamoja na haki na kheri tulizozikuta humo na dalili ya kuwa alikuwa na nia njema na daawa ya kweli, ila tu ni kuwa aliyevitunga ni mwanadamu anayejitahidi na ambaye hukosea, huridhia na hupatwa na ghadhabu na wakati mwingine hupigana na mwigine huwa katika amani, wakati mwingine husema wazi na wakati mwingine hufanya jamala. Kwa hiyo ni jambo la kawaida kabisa kukutana na hali ya kupingana katika kauli zake. Lakini sisi tujaribu kupata njia ya jumla, na tuachane na machache kwa ajili ya mengi na tuachane na shabihi kwa ajili ya yaliyo wazi, na tuachane na yaliyo na dhana ya kisiasa ndani yake na kushikamana na ya itikadi sahihi. Kwa minajili hiyo hakuna kizuizi kisheria wala kiakili kinachozuia kumtathmini Sheikh na kuijua njia yake katika ukufurishaji au katika jambo lingine kama lilivyo bila ya kupamba au kumdhulumu; Tulikusudialo ni kujibu swali hili rahisi nalo ni: Ni upi utaratibu wa Sheikh kifikra? Je! alikuwa anawakufurisha Waislamu kama wanavyotilia mkazo wapinzani wake? Au alikuwa anapambana na ukufurishaji kama wanavyoeneza wasaidizi wake? Basi ni upi ukweli ulio mwepesi na rahisi bila ya kujitakia ushindi wa 26

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 26

1/20/2016 11:35:48 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

kabla ili kumtakasa anayejilazimisha kumsifu au mwenye kutuhumu kidhalimu. Na mwisho ni kwamba kupatikana makosa kutoka kwa Sheikh au kwa mtu mwingine yeyote, sawa liwe kubwa au dogo, sawa makosa hayo yawe mengi au machache, liwe kosa la kifiqhi au la kiitikadi (la kiimani), ni jambo linalotazamiwa kutoka kwa yeyote yule, na ni jambo liwezekanalo kugunduliwa kumhusu kila akithirishaye utunzi, na hasa ukizingatia kwamba uhasama ndio unaoleta kudhulumiana. Mwenye kukataa hili atakuwa amefanya ufurutu ada ambao hatudhanii kama Sheikh mwenyewe angeuridhia, wala wenye ikhlasi miongoni mwa wanataaluma, bali daawa ya Sheikh yote inajikita katika kutangua ufurutu ada juu ya watu wema.13 Na kwa kumdhania mema yeye ni kwamba hata yeye hajitoi pindi anapokataza ufurutu ada juu ya watu wema. Kwa ajili hii kutokuukiri utangulizi mwepesi uliopita – lau ungetokea na umetokea kwa baadhi yao – yahesabika kuwa ni uangukaji kifudifudi hatari wa Masalafi unaoondoa juhudi ya Sheikh na kuitupa kwenye mavumio ya upepo, kati ya wapenzi wake na wafuasi wake kabla ya mahasimu wake na maadui zake. Kisha si katika uadilifu wala si katika insafu kukanusha ufurutu ada wa Mahanafi kumhusu Abu Hanifa na kukanusha ufurutu ada wa Madhwahiriya kumhusu Ibn Hazmi, achilia mbali ufurutu ada wa Masufi kwa Nabii 5 na ufurutu ada wa Shia kwa Imamu Ali....ilihali sisi Masalafi Mawahabi wa Saudi Arabia tunafurutu ada kumhusu Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahabi,14 kwa kuwa sisi tukifanya   Sheikh alikuwa anaona kuwakalidi ulamaa na kukataa kuwakosoa ni miongoni mwa namna za kuwafanya wao miungu badala ya Mwenyezi Mungu. Tazama ad-DurarusSaniyyah, Juz. 2, Uk. 9. 14   Miongoni mwa dalili za ufurutu ada huu kwa baadhi miongoni mwetu - na nisemapo: Sisi, basi mimi namkusudia kila aliyeleleka na elimu ya Sheikh katika vyuo, hotuba na darasa - kuwa baadhi humshangaa anayekosoa makosa yaliyomtokea Sheikh na 13

27

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 27

1/20/2016 11:35:48 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

hivi tutakuwa tumechangia kudhoofika kwa ukweli wa uwepo wetu mbele ya watu, na ukweli wetu katika kulaumu ufurutu ada juu ya watu wema kwa namna mahsusi.

SUALA LA KUMI: Njia ya Kutafiti, Na Sababu Yake: Sitorefusha kuelezea sababu na njia, humu nitafupisha kwa kusema: Ndiyo, sababu ya utafiti huu ilikuwa: Mimi nilifanya usomaji wa kukosoa kitabu Kashfu Shub’hati; kisha nikaongeza usomaji mwingine wa kukosoa kitabu chenye juzuu tano, ambacho ni Durarus-Saniyyah, kinachohusika na itikadi.15 Pamoja na kauli kadhaa kutoka katika insha nyingine za utafiti. Na nimechukua kutoka kitabu: Kashfushub’hat, yale yaliyo mazuri na nimetanabahisha yaliyomo katika vitabu viwili hivyo yanayopaswa kutupiwa jicho kulingana na jitihadi yangu. Kabla ya huharakia kusema: “Fulani amemhujumu Sheikh...fulani amemtia dosari Sheikh!...” kabla ya kuzidodosa dalili, kana kwamba Sheikh Mungu amrehemu, batili haiwezi kumjia mbele yake wala nyuma yake. Na hii kuharakisha kukanusha kabla ya kujitosheleza kwa nyudhuru kwa kuziangalia dalili ni haraka inayoaibisha, haifai, hususan kwa wanaomuunga mkono Sheikh kwa nguvu katika ukemeaji wa ufurutu ada kuwahusu watu wema na kuliita hilo kuwa ni ushirikina mkuu! 15   Hapa nilisema “itikadi” kulingana na uitaji ulioenea, vinginevyo sahihi isemwe “imani” hili ndilo tamko la kisharia, kinyume na “itikadi”, kwani hilo ni tamko maarufu la kubuni, na hakuna mzozo katika istilahi. Na nimezungumzia kwa upana katika kubatilisha uhalali wa tamko “itikadi” katika utangulizi wa kitabu changu Qiraatu Fii Kutubil-Aqaid, basi apendaye na arejee kitabu hicho. Na lau si Wafurutu ada kulichukua tamko hili “itikadi” kuwa ni silaha ambayo kwayo wanawatenganishia Waislamu, ikiwa ni pamoja na kulitumia baadhi ya Masalafi katika kuleta mizozo na kuzitelekeza Aya nyingi za Qur’ani tukufu zilizo wazi achilia mbali Sunnah, nisingelifanyia utafiti tamko hili kutaka kujua uhalali wake. Kwa kweli kwa wafurutu ada katika itikadi – wawe madhehebu yeyote ile – kipimo chao ni madhehebu sio sharia, hivyo kwao wao wafurutu ada lile linalokuzwa na madhehebu na uhasama wa waliopita ndio dini. 28

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 28

1/20/2016 11:35:48 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

miaka kadhaa nilikuwa nimekusanya katika rasimu yale yawezayo kuchunguzwa kukihusu kitabu Kashfushub’hat, na niliwapa ndugu watatu ili kutaka ushauri na kutoa maoni, hivyo mmoja wao aliisambaza labda ni kwa nia njema; ila ni kwamba alikanusha na kudai kuwa hakuisambaza. Huenda yeye – endapo itakuwa sahihi kuwa aliisambaza – alitaka kunidhuru, na amesahau hali yeye akiwa ni msomeshaji wa akida kuwa manufaa na madhara yapo mkononi mwa Mwenyezi Mungu, na vitimbi viovu havimfikii ila mhusika, na huenda lenye madhara likawa na manufaa, na huenda kitendo cha kuisambaza rasimu – kabla ya miaka kadhaa bila ya idhini yangu – ndicho kilichonishajiisha hivi sasa kuisambaza kazi hii kikamilifu usambazaji wa jumla, pindi nilipoona nguvu ya kukubaliwa nyaraka hizo zilizosambazwa pamoja na makosa yaliyopo humo. Na sasa huenda nami nashiriki kwa nasaha tulivu ya kielimu kwa kuifikisha kwa watu wote, baada ya kuwa hapo mwanzo nilinuia kuutoa utafiti huu katika hali ya sifa mahsusi kwa baadhi ya watu ninaowaheshimu miongoni mwa watu wa ukoo wa Sheikh, Mungu amrehamu. Na nasaha ya jumla ni bora kuliko mahsusi, hasa ikizingatiwa kuwa Sheikh ni alama maarufu na utaratibu wake unajulikana, na vitabu vyake viko wazi bayana, sio siri miongoni mwa siri. Nimebadilisha anwani ya nyaraka zilizosambazwa hapo kabla kutoka Qiraatu Fii Kashfushub’hat, na kuwa Daiyah Walaysa Nabiyah, na utafiti juu ya kitabu Kashfushubhat umekuwa ndio mlango wa kwanza wa kitabu hiki. Na kilikuwa kimetangazwa hapo mwanzo katika tovuti – bila ya idhini yangu – kwa anwani Naqdu Kashfushubhati! Nayo ni anwani nisiyoiridhia, na baada ya hapo nilikitangaza kwa anwani ya awali, kama pia ambavyo anwani hii

29

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 29

1/20/2016 11:35:48 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

haijawahi kuchapwa kabla ya sasa kama baadhi yao walivyodhania.16 Na usomaji wa kukosoa Kashfushubhat utakuwa kwa anwani hii ya mwisho Daiyah Walaysa Nabiyah. Hivyo Basi Kitabu Hiki Kitakuwa na Milango Mitano: Mlango wa kwanza: Utafiti juu ya kitabu Kashfushubhat, na hii ni pamoja na kitabu chake at-Tawhid ambacho ni miongoni mwa vitabu mashuhuri vya Sheikh, viwili hivyo vimekosolewa katika utafiti huu. Mlango wa pili: Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahabi katika vitabu vyake na insha zake, nazo ni mifano miongoni mwa kauli zake na rai zake ambazo ndani yake muna ukufurishaji. Mlango wa tatu: Je Sheikh usemi wake ulipingana? Na je aliacha ukufurishaji? Mlango wa nne: Mambo yalivyoendelea baada ya Sheikh. Je wafuasi wanaafikiana na rai ya Sheikh au hapana? Je walifanya rejea ya alichokizalisha au waliendelea na makosa yale yale na yaliyo sahihi miongoni mwake? 16

  La ajabu ni kwamba mimi wakati mwingine ninasitukizwa na aina fulani ya kuogopesha juu ya utafiti huu, au aina nyingine za utafiti na vitabu, na miongoni mwa mapya kuuhusu utafiti huu ni kwamba mtu mmoja mwenye cheo kikubwa kutoka Wizara ya Elimu siku moja aliniomba nakala moja iliyopigwa chapa, nilipompa habari kuwa kitabu hakijachapwa, akaanza kunihakikishia kuwa amepata habari kwa njia ilio sahihi kabisa kuwa Wizara ya Wakfu ya Dubai, huko Umoja wa Falme za Kiarabu imechapisha kitabu chako nakala 100000! Na hivi ni miongoni mwa vitisho vya wafurutu ada kwa wenye madaraka, wanakuja na wanayakuza mambo kwao na kuwajulisha kuwa mtu huyu nyuma yake kuna anayemuunga mkono na amemuwezesha kuchapa maelfu ya nakala, na kwamba ni mtu wa hatari sana na huenda ni mtu wa njama! .....mpaka mwisho! Na geni zaidi kuliko geni hili ni kuwa mimi husikia raha kwa habari kubwa kama hizi ambazo nazijua kunihusu mimi! Kwa kuwa mimi nahisi kuwa nimefanya kitu kikubwa kutoka katika hali ya kutokuwepo kitu! Fanya taswira kuwa mtu mmoja anaongea habari kukuhusu wewe kwa mkazo kabisa kuwa anajua ujuzi wa yakini kuwa wewe umepata ushindi kuiteka nchi iliyo nyuma ya mto! Na kuwa watu wa Samarkand wamekulaki kwa ngoma! Je habari hizi ngeni haziwi nzuri?! 30

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 30

1/20/2016 11:35:48 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Mlango wa tano: Kisimamo pamoja na mahasimu wa Sheikh na wapinzani wake na anaohitilafiana nao na walio katika mfano wao kati ya mwenye kuhujumu na mwenye msimamo wa wastani. Na tutasimama katika kiini cha mzozo kati yao na Sheikh na wafuasi wao, na jinsi gani kuelewana vibaya kulivyochukua nafasi kati ya makundi mawili? Kisha mwisho wa mas’ala hii hakuna hatari yeyote, kwa kuwa kiini cha utafiti huu ni kusema kuwa Sheikh Mungu amrehemu, alikosea katika kufikiri. Na kuitambua mas’ala hii kwa wenye insafu ni jambo rahisi na jepesi ilimradi tu dalili zake zikiwa sahihi, dini haitobomoka kwa hili wala jua halitochomoza upande wa Magharibi yake. Na mwisho ninataraji kuwa ndugu wanaoyatilia manani mambo haya, wataisoma kazi hii kwa insafu na kwa kuitafuta haki, chuki za wengine dhidi yenu zisiwafanye msiwe waadilifu, kuweni waadilifu, kwani uadilifu uko karibu mno na takuwa kama isemavyo Qur’ani. Haki ndio ipaswayo zaidi kufuatwa, kila mmoja huchukuliwa kutokana na kauli yake na hupingwa. Wala sizuii kudhihirisha yanayopaswa kuzingatiwa, bali mimi nayatafuta hayo kutoka kwa wanaopaswa, na nitamshukuru atakayenikidhia yapaswayo kuzingatiwa; lakini mimi ili kuyakubali ni kwa sharti yawe sahihi. Ama yatendwayo na baadhi kama vile kufanya jaribio la kuniingiza makosani na kuhofisha na kuzikataa nususi na mfano wa vitu kama hivyo; mtindo huu nadhani umekuwa wa kuchukiwa na ulioachwa na wenye insafu miongoni mwa wanafunzi wa elimu. Kwa minajili hiyo sikujishughulisha sana kuwafuatilia aina ya watu hawa.17 Lau tungefanya hivyo hatungekuwa tumefanya 17

Baadhi waligutuka na walifanya haraka kujibu kwa kuiboronga rasimu ya kwanza pamoja na kuambatanisha vitisho na jaribio la kukufurisha na kusema kuwa ni bidaa na uzushi, kama kawaida ya wafurutu ada wetu wanapohitilafiana na yeyote! Na miongoni mwa walioichukua rasimu na kuikosoa au waliorukia kuipinga, ni Sheikh Hamudu al-Uqalai (Mungu amrehemu amsamehe na amghufirie) na Sheikh Ali al-Khadhiri na 31

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 31

1/20/2016 11:35:48 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

kitu. Mungu amrehemu Mutanabbiu.18 Lau wangejua kuwa wao wananikidhia jema kwa kukosoa kwao hawangefanya! Kwa hakika mimi nimekuta kuwa fikra wameifikisha kwa watu wote. Kwa hiyo leo watu wanasoma na wanashangazwa, na kesho watafikiri na watatafiti, na baada yake watagundua! Ukweli umbali na malengo! Japo kukinaishwa nao kuchelewe, na kukithiri kuupotoshea umbo. Na himidi ni Yake Allah, na swala zimfikie mjumbe wa Mungu, Muhammad na Ahali wake.19 Hasan bin Farhani al-Malikiy Mwanzo niliziandika nyaraka hizi: 1 Sha’ban, 1421 A.H. Na kuipitia kwangu kwa mara ya mwisho ilikuwa: 28 Rabi’ Thani 1425 A.H. Sheikh Abdullahi as-Saad na wengine mfano wa Abdul-Karimu al-Hamidi, na Nasir al-Fahdi, na Rabiu Madkhaliy, na Swalihu al-Fawzani, na Abdul-Muhsin al-Ubaad. Na nilitosheka na kuwajibu watatu wa mwanzo katika bainisho zangu zilizosambazwa, na huenda nikawakusanya katika kitabu kijacho, ili mazungumzo yaingie katika jamii, kisha kwa kila ukinaifu wake, na kwa hali yeyote. Hivyo basi majibu yao wanajibiana wao kwa wao. Analolisokota mmoja wao mwingine hulipotoa, kwa kulikuza na kutishia, kwa kilio cha uchungu, na kusema uwongo na kulaumu, na tuhuma kwa jumla. Nao ni aibu ya zamani tunaijua kwa Wafurutu ada wanapoziona dalili zina nguvu, na bainisho zinazon’gaa na hatari iliyozunguka, na mwenye kwenda anakwenda, wanakimbilia kukithirisha majibu, ili kihifadhi kizazi kipya! Walivyodhania, haraka wanashindana; kwa ajili ya utashi uliorithiwa au tamaa; Huyu anaanzisha mahali, na yule anapata mahali! Wanasambaza vitabu, na wanatayarisha vikosi, handaki lao ni shubiri! Kila mmoja ananadi: Mimi ni mwonyaji niko bila kitu! Hawaachi kujikusanya vikundi, katika zama si zama zao, na mahali pamewaacha, na ulimwengu unaokuja upya umewaondoa nguo ya akili na maarifa. 18   Ndio msemaji:....jabali lingetopewa na dinari. 19   Baadhi ya ndugu wanaweza wakaona kuwa mimi aghlabu nafupisha katika kumswalia Nabii na ahali wake bila ya swahaba, sio kuzikana fadhila zao na wala sijilazimishi na tamko hili, bali ni kujaribu kukumbusha tamko ambalo tunalikariri siku zote katika kila Tashahhudi (Allahumma swali Alaa Muhammadin wa Alaa Aali Muhammad ) ndani ya swala. Katika tamko rasmi hakuna swala ya kuwaswalia swahaba kama tufanyavyo hii leo kufuata baadhi ya waliyoyazua Masalafi wa mwanzo, kisha hatujatosheka na swala kwa kuwaswalia swahaba wakubwa, tumechanganya na neno “wote”! Wema na waovu, ili aingiye al-Walid na Muawiya na muuaji wa Ammaar! 32

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 32

1/20/2016 11:35:48 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

UTAFITI WA AWALI KATIKA KUKISOMA KITABU KASHFUSHUB’HAT CHA SHEIKH MUHAMMAD BIN ABDUL-WAHABI Kwa nini iwe ni Kashfushubhat?! Nimejikita kwenye kitabu Kashfushubhat kama mfano tu miongoni mwa vitabu alivyoviandika Sheikh, kwa sababu kitabu hiki pamoja na udogo wake lakini kinajitofautisha kwa uwazi, na kinafundisha hoja na bainisho, na fikra zake ziko wazi, na kimeenea sana kati ya wengi miongoni mwa wanafunzi wa elimu na athari yake iko wazi kwao, nacho kwa umashuhuri ni kama kitabu chake kingine al-Tawhid. Mimi sintoyarukia sana mema ya kitabu, kwa sababu nne: Sababu ya Kwanza: Kwa kuwa mema ni machache ukilinganisha na taratibu za kitabu chote, kwa kuwa kinabubujika ufurutu ada katika kukufurisha, lakini ni kwa ibara ambazo nyingi si za wazi. Sababu ya Pili: Imetangulia kuwa nimeutaja ubora wa Sheikh na juhudi zake na kuwa ni mwanadaawa, kwa hiyo mema aliyoyaweza katika kitabu yanaingia ndani yake yenyewe katika sifa hii ya jumla ya jambo hili. Sababu ya Tatu: Utafiti huu lengo lake ni kubainisha yanayopaswa kuangaliwa miongoni mwa makosa ya kupigiwa 33

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 33

1/20/2016 11:35:48 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

mfano ambayo yamechangia kuenea kwa ukufurishaji katika baadhi ya vitabu vya Sheikh na baadhi ya vitabu vya baada yake kutoka kwa wanachuoni wa daawa. Hivyo wadhifa wa kazi hii ni kufichua siri ya kuwepo kwa huu ukufurishaji, ambao huenda usionekane katika rai ya mwanzo, na siri hii ilitokana na kuwa na shubha katika dalili, na si – nidhaniavyo – kwa utashi utokao kwa Sheikh au kupenda kukufurisha Waislamu. Japokuwa sighafiliki na hali ya kisiasa na uhasama wa kimadhehebu ulivyochangia, lakini ukufurishaji huo ulikuwa ni matokeo ya utumiaji dalili iliyo dhaifu au kukata shauri katika mambo ya dhana au kwa dalili isiyo sahihi kwa kuacha dalili thabiti au mfano wake. Na ubainifu utakuja kwa upana wake. Sababu ya Nne: Ni kuwa tofauti haiko katika kumsifu Sheikh na daawa yake na nia yake njema, wala si katika aliyoyafanya sawa iwe wito wake wa kuachana na shirki na imani potovu na bidaa. Katika hayo ni mahali mwafaka kwa wote, kwa uchache kati yangu na wanaohitilafiana na mimi kuhusiana na kuitathmini daawa ya Sheikh na utaratibu wake, kwa hiyo ndugu wanisamehe ikiwa sehemu kubwa ya kitabu hiki kinazungukia katika yale yapaswayo kuangaliwa, na si katika yale yaliyo katika mwafaka, kwa sababu tofauti bado ingalipo tokea siku za Muhammad mpaka hii leo, kati ya wenye ushabiki kwa ajili ya Sheikh au dhidi yake. Na aghlabu yao huacha kujikita kwenye kiini cha tofauti ambazo ni: Je Sheikh alipitiliza kiwango cha kuhadharisha shirki kiasi kwamba aliingiza katika shirki matendo ambayo sio shirki? Kwa ajili hiyo alifurutu ada katika kulitumia neno shirki kwa Waislamu? Je imemthibitikia kuwa anafurutu ada katika kukufurisha au hapana? Na ni ipi daraja ya ufurtu ada huu? 34

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 34

1/20/2016 11:35:48 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Je aliwakashifu waliotofautiana na yeye khususan Ahlus-Sunna na wasiokuwa wao, bali Mahanbali na wengineo kwa kuwanasibisha na ukafiri mkubwa unaomtoa mtu nje mbali na dini au hapana? Halafu endapo yatathibiti hayo je ni inaruhusiwa kwetu hii leo tukubaliane na hayo au hapana ?.... mpaka mwisho. Kwa minajili hiyo papohapo nilianza kutaja moja baada ya lingine miongoni mwa yale yapaswayo kuchunguzwa, hata ambalo ni dogo miongoni mwayo, kwa sababu ya dogo kufungamana na kubwa, na ili kuweka wazi, na kuambatanisha yale aliyoyaeleza kwa ujumla katika Kashfushubhat na aliyoyaeleza kwa uwazi na bayana katika vitabu vyake na insha zake nyingine.

KWANZA: YAPASWAYO KUCHUNGUZWA ­KATIKA KITABU KASHFUSHUB’HAT Haya yapaswayo kuchunguzwa nitayataja kwa utaratibu, na nitayataja maneno ya Sheikh kwenye mabano kisha nitajibu niyaonayo kuwa ni kosa au ni ufurutu ada. Na hususan yanayoambatana na ukufurishaji. Tambua kuwa kitabu kimechapishwa mara nyingi kwa kuhakikiwa na wanaonasibishwa na elimu na wala hawakutanabahisha kosa hata moja miomgoni mwa makosa haya yajayo. Na hii kwao imma ni wanaafikiana na makosa au ni kwa sababu ya kutolitambua kosa lenyewe, na kila moja kati ya hayo mambo mawili tamu mno ni chungu. Na kuafikiana huku kupo dhahiri kwa kila Msalafi anayeandika kumhusu Sheikh Muhammad, Mungu amrehemu, nalo ni miongoni mwa mambo makubwa ambayo yamenishajiisha kuandika kitabu hiki. Lau mmojawapo miongoni mwa wahakiki angetanabahisha baadhi ya makubwa kati ya yale yapaswayo kuchunguzwa nisingeandika kitabu hiki wala vilivyofatia kuihusu Kashfushubhat wala nyingine yeyote. 35

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 35

1/20/2016 11:35:48 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Na yenye kujitokeza sana kati ya yale yapaswayo kuchunguzwa katika Kashfushubhat – na huenda likatangulia ambalo lina umuhimu kidogo – ni haya yafuatayo:

JAMBO LA KWANZA LIPASALO ­KUCHUNGUZWA: Sheikh anasema katika kitabu al-Istihlal, Uk. 5: “Jua Mungu akurehemu kuwa Tawhidi ni kumpwekesha Mungu katika ibada, nayo ndiyo dini ya Mitume ambao Mwenyezi Mungu aliwatuma kwa waja Wake, na wa kwanza wao ni Nuhu D, Mungu aliwatuma kwa kaumu zao walipofurutu ada kuwahusu watu wema: Wadda na Suwaa na Yaghutha, na Yau'qa, na Nasra.”20 Nasema: Maneno haya mwanzo wake ni sahihi lakini mwisho wake kuna la kuchunguzwa na kuna mapungufu makubwa na ni kujenga itikadi ya kukufurisha; kwa kuwa Mwenyezi Mungu alimtuma Nuhu kwa kaumu yake ili awaitie kwenye ibada ya Mungu Mmoja na waache shirki, kwani wao walikuwa wanaabudu haya masamu, wala vitendo vyao havikuwa kufurutu ada kuhusu watu wema. Na neno hili “kufurutu ada” lina maana pana, na aghlabu lakusudiwa kukosea na bidaa, linapotumiwa bila ya kufungamanishwa na kitu, na huenda likafikia maana ya kufuru, na hii ni nadra. Hivyo basi kuubusu mkono huenda kukazingatiwa kuwa ni miongoni mwa kufurutu ada, na kutabaruku na watu wema huenda kukazingatiwa pia kuwa ni kufurutu ada, lakini haya na mengine huhesabika kuwa ni miongoni mwa makosa au bidaa wala sio miongoni mwa shirki. Na hata kama tukipanua wigo na kuvijumuisha vitendo hivi kuwa ni shirki bado vitakuwa ni shirki 20

Tazama Surat Nuh Aya ya ishirini na tatu: “Na wakasema: Msiwaache miungu Yenu; msimwache Wadda wala Suwaa wala Yaghutha, wala Yau’qa, wala Nasra.” – Mhariri. 36

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 36

1/20/2016 11:35:48 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

ndogo; na wala sio miongoni mwa shirki kubwa inayomtoa mtu nje ya Uislamu. Na Sheikh Muhammad, Mungu amrehemu, amesema maneno hayo ya mwanzo ili afanye dalili kuwa daawa yake ni mwendelezo wa daawa ya Mitume; ambao walitumwa au kama kwamba hawakutumwa ila kwa kaumu ya wafurutu ada tu! Au kuwa makosa yao makuu ni kufurutu ada juu ya watu wema! Na hili sio kweli, walikuwa wanamshirikisha Mungu na wanaabudu masanamu, na katika hili yatosha, lakini mahasimu wa Sheikh walikuwa wanamjibu kuwa hao ambao unaowaua na unaowakufurisha ni Waislaam; na uko uwezekano wakawepo miongoni mwa watu wao wa kawaida au wanachuo wao waliofurutu ada kuwahusu watu wema lakini hili halikuhalalishii wewe kuwakufurisha wala kuwauwa. Na ilipokuwa hii ndio hoja ya mahasimu wake, akaihudhurisha maana hii na akaikariri sana vitabuni mwake. Yampasa msomaji mtukufu atambue kuwa mimi niko pamoja na Sheikh, Mungu amrehemu, katika kukemea bidaa, fikra potovu, makosa, na matendo ambayo baadhi ya Waislamu wanayatenda kama vile ufurutu ada juu ya watu wema, kuyaadhimisha makaburi, kujipangusa juu yake, na mambo mengine yafuatanayo na vitu kama hivyo miongoni mwa dua, kuchinja au kutaka shifaa, tawasuli na mpaka mwisho. Lakini kukemea kwangu bidaa hizi na fikra potofu na huenda shirki katika baadhi ya hayo, hakunifanyi niwahukumu wayatendayo kuwa ni mshirki na kuwa wametoka nje ya mila ya Uislamu, sawa mhusika awe mjinga, yaani ametenda katika hali ya kutojua, au ajua, kwa sababu mjinga ujinga wake unatuzuia kumkufurisha, na mjuzi taawili yake inatuzuia kumkufurisha pia. Naam, inaweza ikasemwa, fulani ni mpotovu. Fulani ni mtu wa bidaa, fulani amepotoka. Tuhuma hizi pamwe na yaliyomo 37

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 37

1/20/2016 11:35:49 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

ndanimwe miongoni mwa ujumuishaji wa kidhalimu, lakini hatari yake ni ndogo. Ama kuvuka mpaka na kusema: Fulani kafiri; kufuru kubwa imtoayo nje ya mila ya Uislam! Hili ni zito miongoni mwa mazito ambayo Sheikh na wafuasi wake wamefanya kitu chepesi, wakati humo hukumu itafanyika na mtu atahojiwa kwa dhulma aitendayo; kwa hiyo si jaizi kwetu tumtuhumu yeyote kwa ukafiri ila kwa dalili iliyo dhahiri kwetu kutoka kwa Mwenyezi Mungu kulihusu jambo hilo; hususan Sheikh kulitumia neno shirki bila ya kulifunga, kufuru hiyo ni kufuru kuu imtoayo mtu nje ya Uislamu, kama itakavyokuja. Hii ni nukta miongoni mwa nukta kubwa zenye ihtilafu, nayo ni nukta adhimu bila shaka, lakini si sahihi kwa yeyote aufanye ukosoaji wangu wala wa mwingine kuwa ni kuwahalalishia hao ambao wanaitakidi itikadi hizi, au wanafanya upotovu huo kwenye makaburi ya Manabii, na watu wema na swahaba na wengine. Tunarejea na tunasema: Sheikh alikuwa anakabiliwa na mahasimu wake kuwa: “Hao unaowaua na kuwakufurisha ni Waislamu wanaoswali, wanaofunga na wanaohiji.” Hivyo jibu la hoja hii lilipasa kutoka kwake, na kwa kuwa ni hoja yenye nguvu basi ikajikita na kuwa hadhiri akilini mwa Sheikh, na kila alipotunga kitabu au kuandika insha zake alitilia mkazo katika mlango wa kutoa jibu kwa kuzuia kitendo, kama ambavyo iko dhahiri katika ibara ya mwanzo. Na alikariri kuonesha mema ya makafiri wa Kikurayshi na watu wa Musaylama21 Na wanafiki katika zama za unabii, na wafurutu 21

Musaylama bin Habib al-Hanafiy al-Mutanabiu al-Kadhabu. Alidai kuwa yeye ni nabii na alijitenga mbali na dola ya Kiislamu huko Najdi. Khalifa wa kwanza Abubakr asSwiddiqi K na Waislamu walifanikiwa kumuua na kuirudisha Najd kwenye dola ya Kiislamu. Katika hili, kuna tofauti kati ya uasi wa jamii kubwa ambayo inalazimu kujitenga mbali na makao makuu ya dola. Hivyo uasi wa aina hii ni wajibu kupambana nao na kuwaua kwa mujibu wa ijmai, sawa awe kafiri aliyeritadi au Mwislamu muovu. Amma kuhusu uasi wa mtu mmoja mmoja, katika hili kuna ufafanuzi na kuhitilafiana: Je afungwe au auliwe au atakiwe kutubu siku tatu au aachwe kama Nabii alivyowaacha 38

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 38

1/20/2016 11:35:49 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

ada ambao inasemekana kuwa Imamu Ali aliwachoma moto. Basi Sheikh alikariri kuwafanya kuwa wao ni bora kuliko Waislamu wa zama zake miongoni mwa wanazuoni na watu wa kawaida! Mpaka anathibitisha kuwa yeye hakuwaua ila watu ambao ubora wao ni mdogo mno ukiwalinganisha na makafiri wa Kikurayshi na wanafiki na watu wa Musaylama! Na hili ni kosa bila shaka, pamoja na baadhi ya mfanano uliopo katika ulinganishaji wake anaouandika kati ya hawa na wale lakini kuna tofauti kubwa aliyoiacha, jambo ambalo linaonesha jinsi mfupa wa hoja yenye nguvu kutoka kwa mahasimu wake ulivyomkwama. Ni bora ibara yake ingekuwa kama ifuatavyo: “Wa mwanzo wao ni Nuhu D ambaye Mungu alimtuma kwa kaumu yake – watu ambao walikuwa wanaabudu masanamu, na ibada hii ya masanamu mwanzo wake ulikuwa ni ufurutu ada juu ya watu wema mpaka ufurutu ada huu – baada ya muda mrefu – ukawa ibada mahsusi ya kumwabudu asiyekuwa Mungu. Mimi ninawaiteni mjiepushe mbali na ufurutu ada juu ya watu wema, ili msifikie walipofikia hao waliofurutu ada; mimi ninaogopa mambo kwenu au kwa dhuria zenu, usije ufurutu ada ukawa ibada mnayowaabudu watu wema kama vile: al-Badawiy, Abdulqadir Jaylani, Shadhliy na wengine...” Lau ibara ya Sheikh ingekuwa kama hivi au mfano wake ingekuwa sahihi mno na bora mno na mbali mno na ufurutu ada wa ukinzani au kudhulumu dalili. Zingatia hilo.

waliokufuru baada ya imani yao katika vita vya Tabuku. Na Mungu aliteremsha Aya kuwahusu pamoja na hayo Nabii 5 hakuwaua. Na huku ndiko ninakoelemea kuwa uasi wa mtu mmoja ambao haulazimu kujitenga mbali na umma na kujitenga mahali, malipo yao ni kulaumiwa na kupewa muda kama Qur’ani tukufu ilivyowalaumu walioritadi huko Tabuku, na Nabii ( s.a.w ) aliwapa muda hali ikiwa wao kwa maandiko ya Qur’ani walimdhihaki Mungu, Aya Zake, vitabu Vyake na Mitume Wake, na huku ni kuasi hasa lakini ni kuasi kwa mtu mmoja, na malipo yake ni kupewa muda si kuuliwa. 39

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 39

1/20/2016 11:35:49 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

JAMBO LA PILI LIPASALO KUCHUNGUZWA: Pia kauli yake katika kitabu chake al-Istihlal, Uk. 5 - 6: “Na mwisho wa Mitume ni Muhammad 5 naye ndiye aliyevunja sura za hao watu wema. Alimtuma kwa watu wafanyao ibada, watekelezao Hija na watoao sadaka na wanaomdhukuru Mungu.” Nasema: Hivi ndivyo Shekh, Mungu amsamehe, achoravyo picha nzuri na isiyo sahihi kuhusu makafiri wa kikurayshi ili juu yake ajenge fikra ya kuwakufurisha Waislamu wanaofanya ibada, wanaotekeleza Hija, watoao sadaka na wanaomdhukuru Mungu!! Na huu ni ulinganishaji ulio na tofauti kubwa kama ufafanuzi wa hilo ulivyotangulia na utakavyokuja. Kisha Sheikh ametaja sifa ambayo anaona ni kwa ajili yake Mtume aliwapiga makafiri na Sheikh aliwapiga Waislamu, amesema: “Lakini wao - anawakusudia makafiri wa kikurayshi – wanawafanya baadhi ya viumbe kuwa ni njia mbadala kati yao na Mungu!” kwa ibara hiyo anakusudia kuwa inaruhusiwa kisharia kuwaua na ni jaizi kwetu kuwaua kwa sababu ileile.22 22

Na haya ni miongoni mwa magumu ambayo hawezi kutanabahi aisomaye ibara hii hali yeye akiwa hazijui dalili zilizojificha za mifano ya nadharia kama hizi ambazo zinamwandaa msomaji wa kawaida kukubali kuwakufurisha Waislamu, na kwa mfano wa nadharia kama hizi Sheikh amewakinaisha jamii miongoni mwa wasiokuwa na uelewa wa hatari ya ukufurishaji na wala hawana uoni wa kitaaluma. Hivyo basi wakavamia Bara Arabu kwa kukufurisha na kuuwa. Ni sahihi kuwa baadhi huenda wakasema: Lau Sheikh Muhammad asingewakufurisha na kuwauwa usingeenea Uislamu ulio sahihi! Na tungebakia katika bidaa na fikra potofu mpaka zama zetu hizi! Dhana hii ni ya ghaibu, na huenda kauli hii ikapingwa na kauli nyingine, mtu anaweza kusema: Uislamu umeenea katika nchi nyingi za Kiislamu bila ya upanga, kwa kuwa sehemu kubwa za Afrika na Asia na katika nchi za Magharibi na Uchina Uislamu umeenea bila ya upanga. Lau Sheikh angewasiliana na wanazuoni na watu maalumu huenda wangeongoka katika imani sahihi bila ya madhara japo kuupokea kwao kungechelewa. Hii ikiwa tutakubali kuwa njia anayoiitia haina yaliyoingizwa. Na kuwa waliyokuwanayo wanazuoni wa wakati wake (wakati wa Sheikh) yote ni batili na katika hilo hakuna kuhitilafiana wala shaka. Huenda kama lingetimia hili daawa na wanadaawa wangekuwa salama mbali na tuhuma mbili kubwa zinazowathibitikia kwa 40

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 40

1/20/2016 11:35:49 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Subhanallah, makafiri wa Kikuraysh ambao hawasemi La Ilaha Ilallahu wala hawairidhii kauli hiyo, wala hawaamini siku ya Kiyama wala kufufuka wala pepo wala moto wala hawamwamini Nabii 5, na wanaabudia masanamu, wanauwa, wanadhulumu, wanakunywa pombe, wanazini, wanakula riba na wanafanya ya haramu, mfano wao uwe ni sawa na Waislamu wanaoswali, wanaofunga, wanaohiji, watoao Zaka, watoao sadaka, wanaojiepusha na haramu, watendao kwa maadili mema?! Hivi kweli unawafanya Waislamu kama waovu, mnahukumu vipi?! Hapana, hawako sawa, Waislamu sio kama makafiri hata kama wanazuoni wao watafanya taawili na watu wao wa kawaida wakawa hawajui, kwani taawili na kutojua ni milango miwili mipana na ni vizuizi vikubwa vinavyozuia kukufurisha. Lakini katika hali yoyote iwayo si sawa kuwalinganisha kati ya yule anayetekeleza nguzo za kauli na vitendo, nazo ni: Kukufurisha na Kuuwa. Tuhuma hizo mbili zimeendelea kuwa kikwazo kikubwa miongoni mwa vikwazo vya kufanikiwa daawa ya kiwahabi mpaka hii leo. Na zimewaletea madhara Waislamu kabla ya wengine, ni madhara makubwa hayawezi kuondolewa na maji ya bahari. Ndiyo, baadhi ya Waislamu wa leo na wa hapo kabla huenda wakapinga imani iliyo safi isiyo na doa wala bidaa, na Shetani humpambia mtu kuilinda batili, yote haya huenda ni kwa sababu ya uhasama wa uwahabi, kwa kuwa wao kulingana na rai yake (huyu Mwislamu) wanawakufurisha Waislamu na wanawaua bila dhulma yoyote walioitenda, wala kukata njia, wala hawakuritadi wazi wazi. Ni kama hivyo kila mmoja huenda akafanya dhana na dhana haina nafasi wakati wa kujadili jambo kisharia. Kwa mfano hukumu ya mwizi ni kukatwa mkono, hata mtu akileta dhana ya kuwa kumuuwa mwizi kutakuwa na athari zaidi ya kuzuia wizi kuliko kumkata mkono! Je kauli hii inafaa kisharia japo katika medani ya kiutendaji ni sawa?! Bila shaka hapana. Na miongoni mwa madhara ya kauli hii ya mfano ya mwisho ni kuwa pindi wengine watakapojua kuwa kundi fulani linamuuwa mwizi watalihofia kundi hili, na watalifanyia uadui kwa kuungana Waislamu na makafiri bila tofauti. Hii ndio siri ya kukithiri kwa maadui wa uwahabi, na huenda hasa kutoka kwa watu wasio na woga wala uchamungu. Lakini kukufurisha na kuuwa Waislamu kumewafanya wengine waone uhalali wa kufanya uadui huu kulingana na mtazamo wa baadhi ya wanachuoni kwa uchache. Hivyo basi kutambua hukumu ya kitu hakujumuishi matarajio ya baadaye kwa dhana ya kutokea kwake hapo baadaye. Kadhalika ikiwa mtu ni Mwislamu sio jaizi kumkufurisha na kumuua ili wengine waongoke kwa hofu, woga na kwa kukirihishwa! “Hivi wewe unawakirihisha watu ili wawe waumini?!� (Surat Yunus: 99). 41

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 41

1/20/2016 11:35:49 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Uislamu na anayezikanusha. Wala hawawi sawa yule anayemuamini Nabii 5 kuwa ni nabii na mjumbe, na anayemkadhibisha na anamdhania kuwa ni mchawi au kuhani. Wala hawawi sawa yule anayetawasali kwa Nabii 5 na anayetabaruku kupitia watu wema – hata ikiwa kufanya hivyo ni kosa – na yule anayempiga mawe Nabii 5 na anayewauwa watu wema. Hawawi sawa yule anayeamini Siku ya Kiyama, pepo na moto, na yule anayesema: Si chochote isipokuwa ni maisha yetu ya dunia tunakufa na tunaishi. Hawawi sawa yule asemaye: “Hapana Mungu ila Allah” na yule asemaye: “Amewafanya miungu kuwa ni Mungu mmoja.” Hapana, hawawi sawa yule anayeamini na anayekufuru. Hapana, hawawi sawa yule mwenye kuwasadiki mitume na mwenye kuwakadhibisha. Hapana, hawawi sawa yule wenye kuamini ufufuo na mwenye kuukufuru. Hapana, hawawi sawa yule aombaye shafaa ya Manabii na watu wema na yule aombaye shafaa kwa vitu visivyokuwa na uhai. Hapana, hawawi sawa yule aombaye shafaa ya manabii naye atambua kuwa wao ni waja wa Mungu, na anayeomba shafaa ya masanamu na anawajaalia kuwa ni washirika wa Mungu katika uungu. Hapana – Sheikhe wetu – Mungu akurehemu – Kuna tofauti kubwa kati ya hao na hawa. Na ninawaambia ndugu wanaohitilafiana na mimi katika mas’ala hii, kwamba: Wanachuoni wengi wa Kiislamu zama za Sheikh Muhammad na katika zama zetu hizi wanasema: ‘Yafaa kutabaruku na watu wema.23 na kutawasali kwao.’ Je hii leo 23

Bali wanachuoni wakubwa wa kisunni kama Ahmad bin Hanbal na Dhahbi na Ibn Hajar na wengine walikuwa wanaona kutabaruku inafaa. Rejea kwa mfano kitabu Fat’hulBariy, Juz. 3, Uk. 144, 254, 367, Chapa ya Sheikh Ibn Bazi, uone jinsi alivyotoa dalili alHafidhu Ibn Hajar kuwa inafaa kutabaruku. Ama Dhahbi rai zake ni nyingi, kwa mfano rejea: Wasifu maarufu wa al-Karkhiy katika al-Nubalau. Ama kuhusu Ahmad bin Hanbal, Mahanbali wanatambua kuwa yeye anaona kutabaruku na kujipangusa kwenye ngazi ya mimbari ya Nabii na kaburi tukufu inafaa. Rejea al-Ilal Watabaqaat. Na mimi binafsi sioni kuwa inafaa kutabaruku na hivyo vyote, lakini nampa 42

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 42

1/20/2016 11:35:49 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

sisi tunawakufurisha wote hao au tunawakosoa tu!? Bali natamani kama tungepewa dalili za ukosoaji na uthibitisho. Mkisema: Sisi tunawakufurisha kuwajibu ninyi wanachuoni wa wakati huu ndani ya Saudi Arabia na nje yake, mtatuhumiwa kwa ufurutu ada katika dini na kuwakufurisha Waislamu! Na ikiwa mtasema: ‘Hapana, sisi hatuwakufurishi’ mtakuwa mmemjibu Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahabi na ukufurishaji wake kwao, kwa sababu yeye alikuwa anawakufurisha wanachuoni na watu wa kawaida mfano wa wanachuoni na watu wa kawaida wa zama zetu. Hivyo wanaomkalidi Sheikh hawatoponyoka toka kwenye lazima hizi. Na hata kama watajikalifisha kutofautisha kati ya Waislamu miongoni mwa wanazuoni na watu wa kawaida wa leo; na wale waliokuwepo zama za Sheikh, bado tofauti baina ya makafiri wa Kikurayshi, na hao wanazuoni na watu wa kawaida ni bayana na dhahiri! Naam, kwa sababu kila alilokanusha na kupinga Sheikh Muhammad Mungu amrehemu, kuwa wasifanyiwe wanazuoni wa zama zake, kama vile: Kufanya tawasuli kwa waja wema au kutabaruku nao, au kutaka shifaa kupitia Nabii 5 au kuzuru makaburi, au aliloacha kulikanusha na kulipinga waziwazi juu ya watawala achilia mbali watu wa kawaida, bado yangalipo kwa ulamaa wa Misri, Sham, Hijazi, Yemen na Morocco, achilia mbali kwa watu wa kawaida wa maeneo hayo. Kwa hiyo ninyi endapo mtawakufurisha hao itawalazimu muwakemee wanazuoni wa Kisalafi wa Saudi Arabia ambao haudhuru mwenye kufanya. Na ijtihadi yake naithamini, japo simfuati. Kwa hiyo mimi kwa upande wa utekelezaji ninaafikiana kikamilifu na Sheikh Muhammad, ama upande wa utendeaji kazi hukumu kwa ninayehitilafiana naye mimi nahitilafiana na Sheikh pia. Na bila ya hizi nyudhuru baada ya kufahamu Waislamu watabakia katika kubughudhiana na kufarakana. 43

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 43

1/20/2016 11:35:49 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

wawakufurishi. Makemeo yenu yakiwafikia wanachuoni na wala wasiwakufurishe mtalazimika kuwakufurisha wanachuoni hao; kwa sababu miongoni mwa sheria za daawa ya Masalafi katika maandishi mengi ya wanazuoni wa daawa ni ‘Asiyemkufurisha kafiri au akawa na shaka na ukafiri wake yeye naye ni kafiri.”24

JAMBO LA TATU LIPASALO ­KUCHUNGUZWA: Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahabi anasema, Uk. 8: “Vinginevyo basi hao washirikina – anawakusudia makafiri wa Kikurayshi - wanashuhudia kuwa Mungu ni muumba pekee, hana mshirika, na kwamba hakuna anayeruzuku ila ni Yeye, wala anayehuisha ila ni Yeye, wala hakuna afishaye ila ni Yeye, na wala hakuna apangaye mambo ila ni Yeye, na kuwa mbingu zote na waliopo humo na ardhi saba na waliomo humo, wote ni waja Wake na wapo chini ya utumizi Wake na kahari Yake.” Kisha aliorodhesha Aya katika kuthibitisha hilo. Nasema: Hapa pia Sheikh amechora picha inayong’ara kuwahusu washirikina; wala hakutaja kukadhibisha kwao ufufuo, wala itikadi yao kuwa kinachowahilikisha ni dahari, wala kula kwao riba, na kuuwa kwao nafsi, kuwazika kwao mabinti, wala mengine yasiyokuwa hayo miongoni mwa dhulma na maovu, wala kusema chochote kuhusu kumsifu kwao Nabii 5 kwa sifa mbaya mno, na kumfanya kuwa muongo, kuwaadhibu kwao Waislamu na kuwauwa kwao Waislamu waliokuwa katika hali dhaifu. Hivyo Sheikh Muhammad amezichagua Aya zinazojulisha imani yao kwa sura ya jumla kuwa Mungu ndiye muumba mtoa riziki. 24

Na hili ndilo lililotokea katika mas’ala ya kuhukumu kwa asiyoyateremsha Mungu, nayo ni sheria iwezeshayo kuwakufurisha wanazuoni wanaokubali mazungumzo ya kitaifa, kwa hiyo mwenendo utaendelea, yote haya kwa sababu chimbuko halijazibwa, na njia iliyotumika haijafanyiwa rejea. 44

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 44

1/20/2016 11:35:49 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Wakati ambapo kukiri huku kulikofanywa na washirikina kumejibiwa na baadhi ya wanazuoni. Na wametaja kuwa washirikina walikiri hilo ili kukwamisha na kukatisha wala si katika mlango wa kukinai na kuamini. Lau wangekuwa wakweli katika kukiri kwao; wangetamka Shahada mbili na wangefanya yalazimianayo na kukiri huko miongoni mwa ibada za dhahiri; Kwa ajili hiyo Mwenyezi Mungu anamuamuru Nabii wake 5 awakumbushe lazima za utambuzi huu kama ilivyokuja katika kauli yake Mtukufu: “Hivi hamuogopi?!” “Hivi hamkumbuki?!” mpaka mwisho. Kama kwamba Mwenyezi Mungu anawalaumu kuwa wao ni waongo, na kuwa wao hawaamini kuwa Mwenyezi Mungu ni Muumba na ni mtoa riziki, kama ambavyo wakati huo huo hawawezi kusema kuwa masanamu ndiyo yaliyoumba mbingu na ardhi!! Kwa hiyo wakabakia njiapanda kati ya kutambua kauli hiyo na kufanya yaendayo kinyume nayo. Na jibu hili walilojibu baadhi ya wanazuoni endapo litakuwa dhaifu basi ni udhaifu mno kudhani kuwa makafiri wa Kikurayshi ni bora kuliko Waislamu – wa zama za Sheikh – kwa mambo mawili! La msingi: Si jaizi kwa Sheikh – Mungu amrehemu – wala si kwa mtu mwingine, kutaja yaliyo bora katika sifa za makafiri na kuyafumbia macho makosa yao, wakati huo huo aorodheshe na kutaja makosa ya Waislamu na kufumbia macho matukufu yao! Wala si jaizi tuwe tunazichagua Aya ambazo tunaweza kwazo kuwachanganya kifikra watu wa kawaida – japo si kwa makusudi – kwa sababu ndanimwe mna sifa njema kwa makafiri, na tuache Aya ambazo zinawashutumu na zibainishazo kufuru yao, dhulma zao, na kukadhibisha kwao ufufuo, mpaka mwisho. Sio jaizi tufanye yote haya kiasi kwamba tuhalalishe kwetu kuwauwa Waislamu wanaorukuu na kusujudu; kwa dhana zetu kuwa 45

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 45

1/20/2016 11:35:49 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

eti wao ni sawa na makafiri kabisa?! Eti na sisi tunafanya kazi ileile ya Nabii 5! Hii sio sahihi, na kulitambua kosa ni bora kuliko kung’ang’ania katika batili. Mwenye kufanya toba ya dhambi yake ni sawa na asiye na dhambi kabisa, na mwenye kuyaridhia maasi anakuwa sawa na aliyehudhuria kwenye tukio la maasi na kushiriki au yuko karibu na hali hiyo. Hivyo basi tumche Mungu wala nguvu na wingi visituhadae vikatupotosha mbali na dini yetu, wala tusighurike na kukithiri kwa wanaoinusuru batili kwa kusikia, ujinga, utashi wao na kwa dhulma. Kwa kuwa hao hawamiliki pepo wala moto. Na huenda Sheikh hivi sasa ni mwenye haja mno na dua zetu za kumuombea maghufira kuliko alivyo na haja ya kutaka sisi tutetee makosa aliyodumbukia, lakini sisi - kwa bahati mbaya – tunaghurika na kelele za wengi. Kisha kwa njia hii ya ajabu ya kulinganisha kati ya matukufu ya makafiri na makosa ya Waislamu! Tunaweza kusema: Inakuwaje sasa tunapigana na Mayahudi?! Hali wao katika usemi ni wakweli, na wanaheshimu uadilifu na wanagawa mali kwa usawa na wanamwamini Mungu, na wanaheshimu maeneo matakatifu, na wanaheshimu uhuru wa kujieleza ...mpaka mwisho! Na inakuwaje tunaacha kuwauwa Waislamu ambao wanadhulumu, wanaendesha miamala ya riba, wanasema uwongo, wanafanya kinyume na ahadi, wanafanya khiyana katika amana? Na ambao wanaruhusu kutawasuli na kutabaruku na watu wema?...mpaka mwisho! Vipi tutawapiga Mayahudi, hali wao wapo karibu mno na sisi kuliko washirikina wa Kikurayshi, na tuache kuwapiga ambao ni makafiri mno kuliko makafiri wa Kikuraishi na watu wa Musaylama kwa sifa mbili? Ni kama hivi, endapo tutataja mema yaliyopo kwa Mayahudi na kwa watu wa Musylama, na kujisahaulisha mabaya yao, na kisha tukigeuza suala upande wa Waislamu na tukayataja makosa yao na 46

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 46

1/20/2016 11:35:49 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

kuifumbia macho imani yao na matukufu yao; suala litageuka na kuwa katika mkanganyiko, na inakuwa kuwauwa Waislamu ni bora kuliko kuwauwa Mayahudi wavamizi.25 Amma ukichukua – ewe Mwislamu – sifa zote za hao na hao utatambua wapi utaliweka panga lako. Hali ni kama hiyo katika makafiri wa Kikurayshi au makafiri wa Kiarabu kwa jumla, ambao kwao wao amepelekwa Nabii 5. Ama ukiishia kwenye baadhi ya tabia njema, na baadhi ya makato waliyoyafanya au waliyokiri, utakuwa umetoka na picha nzuri kuwahusu wao ambayo Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahabi Mungu amrehemu, ameitoa. Ama ukizileta Aya zote zinazoongelea makafiri; utajua kuwa wanatofautiana sana na Waislamu mafasiki na madhalimu wao; sembuse wema wao na wanazuoni wao.

JAMBO LA NNE LIPASALO KUCHUNGUZWA: Anasema Sheikh katika Uk. 9: “Ukihakikisha kuwa wao wanakiri haya – anakusudia kuwa Mungu ni Muumba mtoa riziki – lakini bado hakuwaingiza katika Tawhidi aliyowalingania mjumbe wa Mwenyezi Mungu 5 utatambua kuwa Tawhidi ambayo waliikanusha ni Tawhidi ya ibada ambayo washirikina katika zama zetu hizi wanaiita Itikadi.” 25

Matokeo ya haya tumeyaona katika baadhi ya tovuti za Masalafi katika mtandao wa intaneti!! Ambapo Masalafi hawasikitiki kuuwawa kwa mashahidi wa Kipalestina, hao ndugu wafurutu ada walidhania kuwa suala liko sawa. Makafiri wanawauwa wafanyao bidaa! Kwa hiyo suala ni matofali yanavunjana – kulingana na ibara zao -. Na hapo mwanzo hao wafurutu ada walitangulia kuwalaumu mujahidina wa Bosnia na Chechnia kwa kuwa kati yao kuna usufi na umadhehebu. Mfano wa kauli za ajabu kama hizi ambazo wamepata yanayozihalalisha katika vitabu vya itikadi vya zamani na vya sasa. Lau ningependa kunakili kuwafanya kwao Mayahudi na Manaswara kuwa bora kuliko Waislamu wanaohitilafiana nao katika rai na madhehebu, nisingemaliza, na nimekwishataja kitu miongoni mwa haya katika kitabu Qiraatu Fii Kutubil-Aqaidi, mwenye kutaka afanye rejea huko. 47

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 47

1/20/2016 11:35:49 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Ninasema: Mungu amsamehe Sheikh Muhannad, katika tamko hili la wazi (la Sheikh) kuna ukufurishaji wa wazi wa kuwakufurisha wanazuoni wa Kiislamu waliokuwa katika zama zake au walio wengi miongoni mwao! Na ikiwa anawakusudia kila ambao wanalitumia neno ‘Itikadi’ kuviita vitabu vya theolojia, atakuwa amewakufurisha wanachuoni wote wa zama zake, na ikiwa anakusudia itikadi mahsusi (itikadi ya kisufi) atakuwa amewakufurisha baadhi ya wanachuoni, bila ya kuzingatia taawili zao, kwa kuwa taawili ni kizuizi kikubwa miongoni mwa vizuizi vinavyozuia ukufurishaji. Na ikiwa kusudi lake ni ya kwanza basi hiyo itakuwa ni miongoni mwa ukufurishaji wa kifichoficho ambao hawezi kuutambua kila msomaji. Hivyo kusudio la Sheikh linakuwa washirikina katika zama zake, ni wale ambao wana vitabu waviitavyo al-Iitiqad (Itikadi), na hili halipo katika umma wowote ila ni katika umma wa Waislamu. Kisha hoja ya Masufi ipo wazi kwa wengi miongoni mwa wanataaluma, nayo ni itikadi yao kuwa kuna baadhi ya nyakati na baadhi ya mahali ni madhanio ya kuteremkia rehema na kukubaliwa dua zaidi kuliko wakati na sehemu nyingine. Miongoni mwa nyakati hizo ni theluthi ya mwisho ya usiku, usiku wa Laylatul-Qadir, siku ya Arafa, usiku wa nusu ya Shaabani,....mpaka mwisho, sawa Hadithi kulihusu suala hili iwe sahihi au dhaifu, watu katika kuuzingatia usahihi wa Hadithi kuna mwenye msimamo mkali na kuna mwenye msimamo sahali. Na miongoni mwa mahali ambamo wanataraji kujibiwa dua ni katika misikiti, katika visimamo vya Hija huko Arafa, Mina, Muzdalifa, na Madina, na kwenye makaburi ya watu wema miongoni mwa Manabii au wafuasi wa Manabii. Na katika mas’ala ya mwisho sintofahamu ilijitokeza tokea zamani. Kuna anayeona hilo, anaamini kuwa: Huyu mtu ni mwema na kuwa roho yake inawasikia, hiyo ni kulingana na itikadi yao kuwa maiti wanasikia, na hii ni mas’ala ambayo watu wametofautiana, 48

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 48

1/20/2016 11:35:49 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

kwa hiyo wanaamini kuwa madamu yuko hai kaburini mwake au roho yake inawasikia basi matumaini ya kujibiwa kwenye kaburi lake yana uzito. Kwa minajili hiyo wanaomba kutoka kwake shafaa na dua na kuomba kukubaliwa dua yao. Sura hii ni halali kwa walio wengi miongoni mwa wanataaluma, bali Ibn Hazmi amenukuu ijmai juu ya suala hili, na tumekuta wanazuoni wa Kisalafi wamesema waziwazi kuhusu hilo, miongoni mwao ni Dhahbi na Shawkaniy. Kwa mujibu huo Mawahabi hapa wamekhalifu ijmai ya kunyamazia jambo,26 na hiyo ni haki yao kwa kuwa ijmai ya kunyamazia jambo sio hoja, lakini sio haki yao kuwakufurisha wanaoikubali ijmai ya kunyamazia jambo. Ili kujua kwa upana mas’ala hii rejea kiambatanisho ibara ya sita. Kisha katika maneno ya Sheikh Muhammad kuna lisemwalo kuwa hao wanawaabudu watu wema, na usemi huu si sahihi, kwani Waislamu wote wakiwemo Masufi, wanazuoni wao na watu wa kawaida hawamwabudu ila Mungu kinyume na washirikina miongoni mwa makafiri wa Kikurayshi na walio mfano wao; ambao wanasujudia masanamu. Na hii ikiwa si wazi hatutaweza kutofautisha kati ya mambo mengine yaliyo na utata zaidi, na miongoni mwa mambo yaliyo na utata, ni baadhi ya wanachuoni kumtuhumu Sheikh Muhammad na swahiba zake kuwa wao ni Makhawariji, kwa kuwa wao wanaona sifa za Makhawariji zimejikusanya kwao, kwa kuwa wao (Sheikh Muhammad na swahiba zake) wanawakufurisha Waislamu, na wanahalalisha damu zao, na kuwa wao watapatikana zama 26

Ijmai ya kunyamazia jambo ni kitendo cha Mujtahidu wa zama fulani kutoa kauli (fatwa) na kauli hiyo kuwafikia Mujitahidina wengine wa zama zake, lakini wao wanyamaze bila kuipinga wala kuiunga mkono kauli hiyo. Kuna tofauti kuhusu nguvu ya Ijmai hii kihoja: Wapo waonao kuwa Ijmai hii si hoja kwa kuwa kunyamaza kwa hao Mujtahidina wengine si dalili ya kukubali na kuunga mkono kauli, na hii ni rai ya Imam Shafi. Na wapo waonao kuwa ni hoja na ni Ijmai kweli ya kisharia, kwa kuwa kunyamaza kwa ulamaa katika jambo kama hilo kikawaida hutoa dhana na maana ya kuikubali kauli hiyo. Kiukweli ni kwamba kuna mjadala mzito baina ya maulamaa wa Kisuni kuhusiana na Ijmai hii – Mhariri. 49

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 49

1/20/2016 11:35:49 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

za mwisho, na watatokea upande wa Mashariki. Na baadhi ya wanazuoni wanaziambatanisha kwa Waislamu Aya zilizoteremka kuwahusu washirikina, na kuwa wao wanasoma Qur’ani ikiwa ni pamoja na Aya zenye amri na makatazo lakini hazivuki koo zao, hivyo ndio maana kisomo hiki hakijawazuia kuwaua Waislamu na kuhalalisha damu zao na kuwadhulumu licha ya kwamba maandiko ya Qur’ani yanakataza dhulma na haki kuivisha batili! Na kuwa alama yao (hao wenye sifa hizo) ni kunyoa vipara...mpaka mwisho. Hivyo basi ikiwa kuwafanya wao Mawahabi kuwa wako sawa na Makhawariji ni dhulma basi kuwafanya Waislamu kuwa wako sawa na makafiri wa Kikurayshi ni dhulma kubwa mno, na ni mbali sana na haki. Ikiwa Sheikh atakuwa anao udhuru katika kuwafanya makafiri wa Kikurayshi kuwa bora kuliko wanazuoni wa zama zake, basi awafanyaye wanachuoni wa daawa (Mawahabi) kuwa wako sawa na Makhawariji udhuru wake unakuwa bora zaidi; kwa kuwa Makhawariji – pamoja na haya – ni Waislamu kwa kauli yenye uzito, na wala Maswahaba hawakuwakufurisha, ilihali makafiri wa Kikurayshi hakuna mwenye shaka na ukafiri wao.

JAMBO LA TANO LIPASALO ­KUCHUNGUZWA: Usemi wake katika Uk. 9, katika kuyasifu mema ya Makurayshi na wengine:“Walikuwa wanamuomba Mungu Subhanahu usiku na mchana!! Halafu miongoni mwao kuna anayemuomba malaika kwa ajili ya mema yao na ukaribu wao kwa Mwenyezi Mungu ili wamuombee maghufira, au anamuomba mtu mwema mfano wa Laat! Au Nabii mfano wa Isa D na umekwishajua kuwa mjumbe wa Mwenyezi Mungu 5 aliwapiga vita kwa ajili ya shirki hii! Na aliwaitia kwe50

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 50

1/20/2016 11:35:49 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

nye kuifanyia ibada ikhlasi.....Mtume wa Mwenyezi Mungu 5 akawapiga vita ili dua yote iwe ya Mwenyezi Mungu na nadhiri yote na kuchinja viwe kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na kuomba msaada iwe kwa Mwenyezi Mungu, na ibada zote ziwe kwa ajili ya Mungu... mpaka mwisho”. Nasema: Makafiri hawakuwa wanamuomba Mwenyezi Mungu usiku na mchana! Bali walikuwa wanamtaja Habl, Laat, Uzza na Manaat. Lau wangekuwa wanamuomba Mwenyezi Mungu usiku na mchana Mwenyezi Mungu asingemkataza Nabii Wake asifanye ibada ya wanayemuomba, kama ilivyo katika kauli Yake Mtukufu: “Sema: Nimekatazwa kuwaabudu wale mnaowaomba badala ya Mwenyezi Mungu.” (Sura An’am: 56). Mwenyezi Mungu amesema kuielezea hali ya makafiri wakati wa umauti: “Basi ni nani dhalimu zaidi kuliko yule amzuliaye Mwenyezi Mungu uwongo au anayezikadhibisha Ishara Zake? Hao ndio itawafikia sehemu yao waliyoandikiwa; mpaka watakapowafikia wajumbe wetu ambao ni Malaika, kuwafisha, watasema: ‘Wako wapi mliokuwa mkiwaabudu badala ya Mwenyezi Mungu?’ Watasema wametupotea. Na watajishuhudia wenyewe kwamba wao walikuwa makafiri. (Sura A’arf: 37) Na amesema: “Hakika hao mnaowaabudu badala ya Mwenyezi Mungu ni waja mfano wenu. Hebu waombeni nao wawaitikie ikiwa nyinyi mnasema kweli.” (A’araf:194). Na amesema kuwahusu makafiri: “Na wale ambao wameshirikisha watakapowaona wale ambao wamewashirikisha watasema: Mola Wetu! Hawa ndio washirikishwa Wetu ambao tulikuwa tukiwaomba badala Yako. Ndipo wale watakapowatupia kauli: Hakika nyinyi ni waongo.” (an-Nahl: 86). 51

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 51

1/20/2016 11:35:49 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Na Aya nyingine nyingi ambazo sikupenda kuzifuatilia, nazo zinatoa habari kuhusu kinyume na alivyoelezea Sheikh, zinaonesha kuwa dua zao au zilizo nyingi miongoni mwazo au kwa uchache, zilikuwa zimeelekezwa kwa masanamu na wala sio kama asemavyo Sheikh kuwa wao “Wanamuomba Mwenyezi Mungu usiku na mchana”! Ukiongezea kuwa wao hawakuwa wanamuomba Mwenyezi Mungu kwa ikhlasi ila katika majanga. Lau wangekuwa wanamuomba Mwenyezi Mungu usiku na mchana kama Sheikh alivyowasifu, watawa miongoni mwa maswahaba wangetamani kuwa kama wao! Kwa hiyo hii ni picha miongoni mwa picha nyingi nzuri ambazo Sheikh anawasifu nazo makafiri wa Kikurayshi, sio kwa kuwapenda bali ili awalinganishe na Waislamu wa zama zake; akizuga kutokana na kulandana kwa hawa na wale! Halafu juu ya huu mlandano pungufu na juu ya ule uzugaji ajengee hoja ya kuwafanya kwake bora kuliko Waislamu, kisha juu ya yote hayo ajengee msingi wa uhalali wa kuwakufurisha kwake Waislamu na uhalali wa kuwaua.27 27

Na Sheikh Muhammad amewasifu makafiri mahali pengi, miongoni mwake ni kauli yake kuhusu makafiri wa Kikurayshi: “Walikuwa wanamtambua Mwenyezi Mungu na kumwogopa na kumtarajia.” Tazama ad-Durarus-Saniyah, 146 \1. Hii sio sahihi! Na miongoni mwayo kauli yake: “Walikuwa! – Anawakusudia makafiri wa Kikurayshi – wakitoa Zaka na wakihiji na wakifanya Umra na ibada, na walikuwa wanaacha vitu miongoni mwa vitu vya haramu kwa kumuogopa Mwenyezi Mungu!!” Tazama adDurarus-Saniyah, 118 \2. Katika maneno haya ndani yake mna la kuchunguzwa halijifichi kwa mwenye insafu. Aliwasifu wanafiki kwa lengo hili mahali pengi miongoni mwake, kauli yake: “Wanafiki katika zama za Mjumbe wa Mwenyezi Mungu 5 walikuwa wanapigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali zao na nafsi zao na walikuwa wanaswali pamoja na mjumbe wa Mwenyezi Mungu 5 swala tano na walikuwa wanahiji pamoja naye.” Tazama al-Durarus-Saniyah, 2\ 86. Nasema: Maneno yote yaliyopita – pamoja na makosa yaliyopo – yanaweza kukubaliwa isipokuwa kauli yake: “katika njia ya Mwenyezi Mungu.” Wanafiki hawafanyi haya kwa ajili ya Mwenyezi Mungu bali ni kwa malengo mengine, kuongeza ni kuwa wao hawatoi ila wakiwa wamekirihika, na hawaswali ila wakiwa wavivu, na walikuwa hawaswali pamoja na Nabii 5 swala ya Alfajri wala ya Isha... Sheikh katika mambo mengi 52

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 52

1/20/2016 11:35:49 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Na ambalo linapaswa kusahihishwa hapa ni kuwa Nabii 5 aliwapiga vita makafiri kwa mambo mengi, yaliyo muhimu katika miongoni mwa maovu yao ameacha kuyataja. Na itakujia mifano kama hii miongoni mwa kuwasifu makafiri wa Kikurayshi na kuwafanya bora kuliko Waislamu wa zama zake. Kama ambavyo Sheikh Mungu amsamehe, alivyowapamba na kuwasifu kwa lengo lilelile wale walioritadi kama vile Musaylama na swahiba zake. Akasema katika adDurarus-Saniyah 2\44: “Musaylama anashuhudia kwamba hapana Mungu isipokuwa Allah, na kuwa Muhammad ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, anaswali na kufunga.” Nasema: Hii sio sahihi, lau angekuwa anashuhudia kuwa Muhammad ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu hangedai unabii, na Nabii 5 alimkadhibisha. Kuongeza, Musaylama alikuwa na taratibu zake za ibada sio kama swala zetu na funga zetu. Na amesema kuwahusu Bani Hanifa, watu wa Musaylama katika ad-Durarus-Saniyah 9/387: “Wao mbele ya watu ni watu wabaya walioritadi na ni makafiri zaidi, pamoja na hayo wanashuhudia kuwa hapana Mungu isipokuwa Allah, na kuwa Muhammad ni mjumbe wa Mwenyezi Mungu. Wanaadhini wanaswali na wengi wao wanadhania kuwa Nabii 5 aliwaamuru hilo!!” Pia alisema kuwahusu watu wa Musaylama katika kitabu ad-Durarus-Saniyah, 9/383: “Walishuhudia kuwa hapana Mungu isipokuwa Allah, na kuwa Muhammad ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, lakini walimsadiki Musaylama kwa madai kuwa Nabii alimshirikisha katika unabii. Na hilo ni kwa sababu yeye aliweka mashahidi walioshuhudia hilo pamoja na yeye, kati yao akiwemo swahaba maarufu kwa elimu na ibada, anaitwa ar-Rihalu, walimsadiki walipomjua kuwa ni mwenye elimu na ibada.”!! Nasema: Kwa hiyo Bani Hanifa ni muhanga wa nadharia ya uadilifu wa Maswahaba ambao twakurubia kumkufurisha asiyeamini kuthibiti kwake kwa kila mmoja wao. Na hili ni dai la kuamini yanayopingana. Natija inakuwa: Mwenye kumfuata Musaylama atakuwa amekufuru, na mwenye kuurudi ushahidi wa swahaba atakuwa amekufuru! Na atakuwa amezikadhibisha Aya katika kuwafanya waadilifu kulingana na dhana ya wafurutu ada! Hivyo mnataka watu wa Musaylama wafanye nini? Wao kulingana na maelezo ya Sheikh ni miongoni mwa wafurutu ada wa Kisalafi katika suala la uadilifu wa Maswahaba! Je mnawataka wakanushe nadharia ya uadilifu wa Maswahaba au waamini unabii wa Musaylama?! Na Sheikh aliwasifu walioritadi ambao imesemwa kuwa Ali aliwachoma moto, akasema kuwahusu katika ad-Durarus-Saniyah 2\44: Walikuwa wanatamka tamko la shahada: Nashuhudia kuwa hapana Mungu isipokuwa Allah, na kuwa Muhammad ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu!! Nasema: Hii sio sahihi, kwa kuwa riwaya zenye nguvu zaidi zinasema kuwa watu hawa waliua na waliritadi kabisa. Na baadhi ya wafurutu ada wetu wanasema kuwa wao walidai uungu wa Ali. Hili likiwa sahihi lafikisha ujumbe wa uhakika wa kumpinga Sheikh kuwa hao – watu – hawatamki shahada mbili. Kwa ujumla Sheikh Mungu amsamehe, anawasifu vyema washirikina wa kweli, wawe makafiri au walioritadi au wanafiki, na anawashutumu Waislamu wa zama zake akiwatuhumu kwa ushirikina mkubwa mno kuliko ushirikina wa makafiri wa asili, na huu ni ufurutu ada wa kupindukia. 53

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 53

1/20/2016 11:35:49 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

hayo ni: Shirki mkongwe wa kumshirikisha Mungu, kuwatoa kwao Waislamu majumbani mwao, kuukana kwao unabii na kutenda kwao dhuluma...mpaka mwisho. Kwa minajili hiyo sababu za Sheikh Muhammad zina upungufu, na upungufu huu katika kuelezea sababu umeleta mauaji ya Waislamu ambao wanaswali, wanahiji na wanamdhukuru Mwenyezi Mungu. Kisha katika Qur’ani haijatajwa kuwa sababu ya Nabii 5 kuwapiga vita makafiri ni ili uchinjaji wote uwe kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na nadhiri zote na istighfari viwe ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu tu. Bali sababu kuu ni: Shirki mkuu na kuupinga unabii na kuwatoa Waislamu kwenye majumba yao...mpaka mwisho. Hivyo Sheikh huzitaja sababu ndogo ndogo zenye mlandano (au za kubabaisha kulingana na taabiri za wapinzani wake) ambazo hazikutajwa kwenye maandiko, zisizo za uhakika, na ambazo haitambuliki kwa yakini kuwa je ndio sababu hasa ya mapambano au hapana?! Na huacha sababu ambazo ni kubwa zilizoafikiwa katika Qur’ani tukufu kuwa hizo ndiyo sababu hasa za mapambano ya Nabii 5 na makafiri. Bali mwenye ufurutu ada miongoni mwa Makhawariji na makundi mengine amefurutu ada kwa kujikita katika haya yenye utata yenye mlandano na kuacha makubwa yaliyokatiwa shauri. Wanahalalisha damu ya Mwislamu kwa dhana na shubha mbali na dalili sahihi, au kwa dalili dhaifu. Kwa minajili hiyo wafurutu ada wamefurutu ada muda wote wa historia.

JAMBO LA SABA LIPASALO ­KUCHUNGUZWA: Kisha anaendelea katika Uk. 11 kwa kauli yake: “Hawakukusudia kuwa Mungu ndiye muumba mtoa riziki mpangaji, kwa kuwa wao wanajua kuwa hayo ni ya Mwenyezi Mungu peke yake kama nili54

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 54

1/20/2016 11:35:49 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

vyokwisha kutanguliza, bali wanamaanisha lile wanalomaanisha washirikina katika zama zetu hizi katika tamko Sayyid.” Nasema: Katika hili pia kuna kuwakufurisha Waislamu wa zama zake waziwazi, kwani watu wengi katika karne za mwishoni mpaka hii leo wamekuwa wakilitumia tamko ‘Sayyid’ kumaanisha mtu miongoni mwa Ahlulbayt. Na mara nyingine watu wa kawaida wa wakati wake na wakati wetu huu wamekuwa wakilitumia kumaanisha mtu wanayemdhania kuwa ana baraka;....... na kulitumia neno hili na kuitakidi hivyo sio kufuru wala si haramu. Naam, huenda ikawa makuruhu, ama Hadithi iliyokuja katika kulikataza, ina mzozo mkubwa, na ikumbukwe kuwa Umar alisema: ‘Sayyiduna Abubakri alimwacha huru Sayyiduna Bilal.’ Ikiwa baadhi ya watu wa Najdi au baadhi ya watu wa Hijazi, katika zama za Sheikh walikuwa wanalitumia neno Sayyid kwa mtu ambaye wanatabaruku kupitia kwake na kumuomba dua, basi kubwa linaloweza kusemwa kuhusiana na jambo hili ni kuwa hiyo ni bidaa. Nayo yaweza kuwa kubwa au yaweza kuwa ndogo kulingana na hali ya msemaji na anayeambiwa na uhusiano uliopo kati ya wawili hao, lakini sio kufuru. Kisha aliyoyasema Sheikh sio sahihi, eti washirikina wote walikuwa wanajua kuwa Mungu ndiye muumba, mtoa riziki...mpaka mwisho. Hilo linathibiti kwa baadhi ya makafiri sio wote; Kwa kuwa waliokuwa wakiamini dahari kwa mfano, walikuwa hawaamini hili kulingana na maandiko ya Qur’ani tukufu kuhusu kauli yao: “Hakuna kinacho tuangamiza ila ni wakati.”28 28

Kila aliyeandika kuhusu historia ya nyakati za jahilia amethibitisha kuwa dini za watu wa zama za jahilia zilikuwa nyingi, hivyo miongoni mwao ni wale waliokuwa wakiamini dahari. Na miongoni mwao ni waabudu masanamu – na wao ndio waliokuwa wengi - na miongoni mwao ni Ahlulkitabu, Majusi, wachawi na makuhani. Na miongoni mwao ni Ahnafu (waliobaki katika dini ya Nabii wa Mwenyezi Mungu Ibrahim D, na hawa walikuwa wachache, hata hivyo hawakuwa na ghera juu ya dini zao. Kwa hiyo Majusi hawakuwa wanaufanyia daawa umajusi wao wala waabudu masanamu hawakuwa wanafanya daawa kwa ajili ya sanamu zao. Kwa mujibu huo itikadi zinaweza kuingiliana, 55

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 55

1/20/2016 11:35:49 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

JAMBO LA NANE LIPASALO ­KUCHUNGUZWA: Kauli ya Sheikh katika Uk.11: “Nabii aliwajia akiwaitia neno la Tawhidi ambalo ni: Laa Ilaaha Ila Llahu” Nasema: Kulitamka peke yake japo kwa kudanganya au kujikinga - ili asiuliwe - kunamlinda mweye kulitamka, hawezi kuambiwa na kuitwa kafiri au kuuliwa, lakini cha kushangaza mwenye kulisema katika watu waliokuwa zama za Sheikh akiwa yu mkweli mwenye kutekeleza amri za dini halimzuwii kukufurishwa wala kuuliwa! Izingatiwe kwamba wanafiki zama za Nabii 5 walikuwa wanasema shahada mbili kwa ndimi zao tu, na Nabii alikuwa anajua hayo kutoka kwa walio wengi wao; lakini pamoja na hayo yote damu zao na mali zao zilihifadhika. Ama waliokuwa zama za Sheikh miongoni mwa Waislamu damu zao na mali zao hazikuhifadhiwa sio kwa shahada mbili wala kwa nguzo za Uislamu, ijapokuwa walikuwa wakweli katika hayo!

na hivyo inawezekana wote walikuwa wanakariri neno Allah na mmoja miongoni mwao akitambua kuwa ni muumba, lakini haamini kuwa ni mmoja tu, wala hamwabudu, wala hatekelezi amri Yake na wala haachi kutenda aliyoyakataza, wala hajui hili wala lile na wala haogopi kutenda dhulma na kutenda dhambi....mpaka mwisho. Na anayetaka kujua zaidi hali ya kidini ilivyokuwa kwa Waarabu kabla ya Uislamu, basi naafanye rejea vitabu vilivyotungwa kwa malengo hayo. Na huenda kilicho bora na mashuhuri miongoni mwavyo na chenye kukusanya zaidi ni kitabu al-Mufaswalu Fii TaarikhilArab Qablal-Islami cha Dkt. Jawad Ali, nacho kimechapwa, kikiwa na jalada kubwa kubwa kumi, ni chenye elimu ya kina kikitegemea vyanzo vilivyoandikwa na athari za nakshi zilizogunduliwa. Hivyo basi hapanabudi maneno yetu kuwahusu watu wa zama za jahilia yawe ya kielimu ili yachangie ufahamu wetu juu ya Qur’ani tukufu, ili tujue kundi gani Qur’ani inalikusudia kwa Aya hii au ile. 56

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 56

1/20/2016 11:35:49 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

JAMBO LA TISA LIPASALO KUCHUNGUZWA: Na anasema katika Uk.12: “Na ajabu ni kwa anayejidai kuwa ni Mwislamu, ilihali hajui tafsiri ya neno hili, ambayo waliijua majahili wa kikafiri, bali adhania (yaani anayejidai kuwa ni Mwislamu) kuwa hiyo (tafsiri yake) ni kutamka herufi zake tu bila ya moyo kuitakidi chochote katika maana zake.” Nasema: Aliyoyasema Sheikh siyo sahihi; hakuna Mwislamu hata mmoja asemaye kuwa maana ya Laa Ilaaha Ila Llahu ni kutamka tu bila ya kuitakidi kwa moyo. Waislamu wote wanachuoni wao na watu wao wa kawaida, wanamchukia Mwislamu asemaye asiyoyaamini. Bali hata watu wa kawaida wanaita hali hii kuwa ni unafiki, na wao humlaumu ambaye maneno yake yapo kinyume na vitendo vyake. Basi vipi Sheikh awe anadhania kuwa Waislamu katika zama zake wanasema inafaa utamke shahada mbili bila ya kuitakidi maana yake, tuseme Laa Ilaaha Ila Llahu na tumwabudu mwingine. Na tuseme Muhammadu Rasulullahi na tuamini kuwa yeye (Muhammad) ni mwongo?! Waislamu wa zama za Sheikh ni kama Waislamu wa hii leo katika nchi za Kiislamu, je inatufalia hii leo sisi tuseme kuwa wao wanasema: ‘Tunatamka Shahada mbili kwa tamko tu na tutaokoka japo tuwe tunaamini kinyume chake?!’ Naam, wanayo shubha na dalili ambazo kwazo wanajuzisha kutawassuli na kuomba shifaa na msaada na yaliyo mfano wa hayo, na hayo kwangu ni makosa bila ya shaka, na ninaafikiana na Sheikh juu ya hilo. Lakini wao wana shaka, bali wao hawaoni haya kuwa yanakinzana na shahada mbili. Na katika hayo wanavyo vitabu, dalili, hoja, na taawili hazina kadiri yenye uchache kwa kuzilinganisha 57

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 57

1/20/2016 11:35:49 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

na taawili za Mawahabi na hoja zao katika kuwakufurisha Waislamu! Na kuwafanya kuwa ni makafiri mno kuliko makafiri wa Kikurayshi kwa mambo mawili.29

JAMBO LA KUMI LIPASALO ­KUCHUNGUZWA: Kisha anasema katika Uk. 13: “Na mjuzi hodari miongoni mwao anamkusudia anayejidai kuwa ni Mwislamu katika wanazuoni wa Kiislamu! - anadhania kuwa maana yake ni haumbi wala haruzuku ila Allah!” Kisha Sheikh analifuatishia tamko hilo na pigo la kuvunja mgongo nalo ni “Hapana kheri kwa mtu mjinga ambaye makafiri ni wajuzi mno wa maana ya Laa Ilaaha Ila Llahu kuliko yeye.” Nasema: Jawabu limetangulia, kuwa wanazuoni wa Kiislamu katika zama zake hawaifasiri Shahada mbili kama Sheikh alivyosema hapa, – kama nijuavyo – inawezekana wakawa na upungufu katika kutafsiri maana ya Shahada mbili, na hata ukitokea upungufu huo lakini hawajuzishi kuielekeza ibada kwa asiyekuwa Mungu japo kwa dalili nyingine za Qur’ani ambazo zinawajibisha kuzielekeza ibada kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Naam, wana taawili kuwa kutabaruku na kutawassuli hakukinzani na shahada mbili, na hiki ni kitu kingine. Lakini aje mwanazuoni na adhanie kuwa Laa Ilaaha Na wengine wanang’ang’ania itikadi zao pamoja na makosa yaliyomo humo miongoni mwa taawili, nyudhuru, mfano wa ung’ang’aniaji wa Masalafi, mawahabi juu ya makosa yao bila kujali ufurutu ada na nyudhuru na uchokozi uliomo humo. Masufi na Mashia wanawatuhumu wanasihi wao kuwa wanafanya kwa ajili ya maslahi ya Mawahabi, ni kama Mawahabi wanavyowatuhumu wanasihi wao kuwa wanainusuru na kuitetea ibada ya kuabudu makaburi na kwamba wanatenda kwa ajili ya maslahi ya Masufi na Mashia, bali hiyo ni shirki kubwa mno. Na nadharia ya njama na shaka kuzihusu nia za wengine zitabaki zipo kwenye mazungumzo yetu madamu kuna ufurutu ada unaowakinza wawili hao kuwepo kwao katika mazungumzo haya.

29

58

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 58

1/20/2016 11:35:50 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Ila Llahu maana yake ni ‘Hapana Muumba ila Allah, na hapana mtoa riziki ila Allah’ na hivyo ni ruhusa kuielekeza ibada kwa ­mwingine asiye Mungu. Sidhani kuwa mwanachuo mwenye akili anasema hivi, na anayedhania hivyo basi ni juu yake kuleta dalili na ithbati.

JAMBO LA KUMI NA MOJA LIPASALO ­KUCHUNGUZWA: Amesema katika Uk.16, 15: “Maadui wa Tawhidi huenda wana elimu na hoja na ufasaha...” Nasema: Na huku ni kukiri kwake kuwa yeye anaongea kuwahusu wapinzani wake miongoni mwa wanazuoni wa zama zake huko Najdi na Hijazi na Sham, kuwa wao wanazo elimu na ufasaha, na kabla yake alikanusha kuwa wao wanajua maana ya Laa Ilaaha Ila Llahu!!

JAMBO LA KUMI NA MBILI LIPASALO ­KUCHUNGUZWA: Anasema katika Uk.17: “Mtu wa kawaida miongoni mwa wanatawhidi anawashinda elfu miongoni mwa wanazuoni wa hao washirikina!!” Nasema: Huu ni ukufurishaji wa wazi wa idadi kubwa ya wanazuoni, na kwa kawaida ni muhali kupatikana mfano wa idadi kubwa kama hii (elfu!) miongoni mwa wanazuoni makafiri katika mji mmoja; litambue hili kwa kuwa ni muhimu, nayo ni miongoni mwa dalili za wanaomtuhumu Sheikh kuwa anawakufurisha wasiomfuata! Na Sheikh na wafuasi wake wanasema: ‘Tunajikinga na Allah kuwakufurisha Waislamu.’ Hii ni kauli enezi lakini tatizo ni kwamba 59

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 59

1/20/2016 11:35:50 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Mwislamu kwao wao si yule Mwislamu anayezingatiwa na Waislamu wengine, kwa kuwa Mwislamu kwa mtazamo wa Sheikh na wanaomfuata ni yule mwenye masharti marefu na mapana yenye matawi mtawanyiko, yatakayomlazimu yeye na wanaomfuata kuhitilafiana na wanazuoni kwa sharti hizi kabla ya watu wa kawaida. Kwani (kwao wao) kutamka shahada mbili sio jambo limtoalo mtu kwenye ukafiri, kisha kuyatambua baadhi ya masharti pia hakumtoi mtu katika ukafiri. Kisha katika kutafsiri baadhi ya masharti hapana budi kumkalidi Sheikh katika tafsiri. Ni kama hivyo kiasi kwamba inakaribia masharti hayo, matawi yake na tafsiri yake kutotimia isipokuwa kwa anayemfuata na kumkalidi. Na hii ni kutia uzito ­katika yale ambayo Mwenyezi Mungu ameyafanya rahisi na mepesi. Kisha mchanganyiko wa kifikra na dhana haepukani navyo Mwislamu, hata swahaba wameongea kuwa wao wanakuta kuwa kama wangetupwa kutoka mbinguni ingekuwa kwao ni rahisi k­ uliko kutamka shahada mbili. Baadhi ya Tabiina wamewatambua makumi kadhaa ya maswahaba wanaohofia unafiki ndani ya nafsi zao. Hivyo basi fikra, dhana na maswali yenye kukanganya na makosa katika kufanya jambo ni jambo la kawaida bali yakaribia kwamba kila Mwislamu hutokewa na hali hiyo.

JAMBO LA KUMI NA TATU LIPASALO ­KUCHUNGUZWA: Anasema katika Uk, 19: “Na mimi nakutajia mambo miongoni mwa yale aliyoyataja Mwenyezi Mungu kitabuni Mwake ambayo ni jibu la maneno waliyoyafanya hoja dhidi yetu washirikina katika zama zetu hizi...!!” Nasema: Washirikina gani hao ambao wanazama mbizi kutoa dalili za Kitabu na za Sunna wakiwa na ufasaha, elimu na hoja ny60

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 60

1/20/2016 11:35:50 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

ingi...?! Je si wanazuoni wanaohitilafiana naye katika madai ya kuwakufurisha walio kinyume na yeye miongoni mwa wanazuoni na watu wa kawaida? Hapana shaka kuwa kauli hii ina ukufurishaji wa wazi wa kuwakufurisha wale wanaohitilafiana na yeye miongoni mwa wale tuwaitao mahasimu wa daawa au maadui wa Tawhidi, au maadui wa Uislamu!! Na hii ni dhulma, kwa kuwa Sheikh alikuwa anawajibu Waislamu, wala hakuwa anawajibu makafiri wala washirikina. Na hizi hapa insha zake na vitabu vyake hamna humo jina la mshirikina wala kafiri bali humo mna majina ya wanazuoni wa Kiislamu wa zama zake, kama Ibn Fairuzi, na Muridi at-Tamimiy na watoto wawili wa Sahim Sulayman na Abdullah, na Abdullah bin Abdul Latiif na Muhammad bin Sulayman al-Madaniy na Abdullah bin Daudi Az-Zubayriy, na alHadad al-Hadhramiy, na Sulayman bin Abdul-Wahab na Ibn Afaliq na al-Qadhiy Talib al-Humaidhiy, na Ahmad bin Yahya na Swalih bin Abdullah na Ibn Mutlaq, na wengine miongoni mwa wanazuoni ambao huitwa ‘Washirikina katika zama zetu’!! Na wanazuoni wa daawa ya Kiwahabi wameendelea kukufurisha au kuwafanya Waislamu kuwa ni wanabidaa baada ya Sheikh, imeendelea kuwepo idadi nyingine ya wanazuoni wa Kiislamu waliokufurishwa katika zama za dola ya Ukoo wa Kifalme wa Saudi wa pili, kama Ibn Salum na Uthman bin Sindi na Ibn Mansuri na Ibn Hamiid na Ahmad bin Dahlan al-Makiy na Daudi bin Jarjiis na wengine. Na katika karne ya kumi na nne Hijiria ukufurishaji wa Ma-Wahabi na kuwafanya wanazuoni wa Kiislamu kuwa ni wanabidaa30 uliendelea, kama al-Kawthariy, Abu Ghudah, Muhammad Hu30

Nimesema: ‘Kuwakufurisha na kuwafanya wanabidaa’ kwa sababu baadhi ya Mawahabi wanakufurisha, na baadhi yao wanaishia kuwafanya wanabidaa, na matokeo ni mamoja, kwa kuwa mwanabidaa kwao ni miongoni mwa watu wa motoni, ni katika kikundi cha kuangamia! Na kwao mfanya bidaa anapaswa auliwe baada ya kumtaka afanye toba. Na kwao bidaa ina maana pana zaidi kiasi kwamba inafikia kila aina ya upole na huruma unaofanywa juu ya Waislamu! 61

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 61

1/20/2016 11:35:50 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

sein Fadhlullah, ad-Dajawiy, Shaltut, Abu Zahra, al-Ghazaliy, alQardhwawiy, Tantawiy, al-Butiy, Abdullah al-Ghamariy, Ahmad al-Ghamariy, Habibur-Rahmani al-Aadhwamiy, al-Kabisiy, AbdulQadir al-Biihan, Abdur-Rahim at-Tahaniy, na wengineo. Lau tungependa tungewaita ‘Washirikina katika zama zetu.’ Na imeshasemwa!! Lakusikitisha ni kuwa hakuna linalotuzuia kuwakufurisha wengine na kuwafanya kuwa ni wafanya bidaa na kutowachokoza ila mambo mawili: Kwanza: Mamlaka ya dola. Pili kushindwa. Lau si haya mawili hatungembakisha yoyote ila tungempakazia ukafiri au bidaa inayokufurisha! Na tungemtaka afanye toba kisha kwa urahisi tungemuua! Kwa sababu watu wamezaliwa wakiwa huru. Ilihali lililo wajibu juu ya wanazuoni na wanafunzi wa elimu ni wawe wa kwanza kuzitambua haki za Mwislamu, na wachunge usia wa Nabii 5 alioutoa akiwa katika Hija yake ya kuaga: “Kwa hakika damu zenu, mali zenu na heshima zenu ni haramu kwenu kama ilivyo siku yenu hii katika nchi yenu hii katika mwezi wenu huu.” Huu ni usia wa mwisho wa Nabii 5 aliueneza akiwa na Waislamu zaidi ya mia moja elfu. Wanazuoni wanaujua kwa matamko yake na sanadi yake zaidi kuliko watawala. Ni miongoni mwa uzembe na ghushi dhidi ya dini wanazuoni kutozuia ukiukwaji wa usia huu mkubwa isipokuwa uzuiliwe na watawala.31

31

Watawala wa Kiislamu wengi wao hawaheshimu damu zilizohifadhiwa zisimwagwe bila haki, lakini wao kwa mkazo wamekuwa na uroho kidogo wa damu kuliko wanazuoni wengi na wanafunzi wa elimu, kwa sababu katika sheria za kimataifa na kanuni zake kuna mkazo wa kuhifadhi haki za binadamu zaidi kuliko vitabu vya itikadi wavisomavyo na kuvisomesha walio wengi miongoni mwa wanazuoni. 62

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 62

1/20/2016 11:35:50 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

JAMBO LA KUMI NA NNE LIPASALO ­KUCHUNGUZWA: Kauli yake katika Uk.12: “Ulilonitajia ewe mshirikina!! Kutoka katika Qur’ani au maneno ya Nabii 5 sijui maana yake...”32 Nasema: Huyu mshirikina ambaye anampa dalili ya Qur’ani na Sunna Sheikh na wafuasi wake ni nani?! Ni mshirikina gani huyu mpole?!

JAMBO LA KUMI NA TANO LIPASALO ­KUCHUNGUZWA: Na anasema katika Uk. 23: “Kwa hakika maadui wa Mwenyezi Mungu ni kama hivi! Wana kauli nyingi ambazo kwazo wanawazuia watu, miongoni mwazo ni kauli yao: ‘Sisi hatumshirikishi Mungu bali tunashuhudia kuwa haumbi wala hatoi riziki wala hanufaishi wala hadhuru isipokuwa Yeye Mungu peke Yake hana mshirika. Na tunashuhudia kuwa Muhammad amani iwe juu yake, hamiliki manufaa kwa ajili yake binafsi wala madhara sembuse Abdul-Qadir au mtu mwingine. Lakini mimi ni mwenye dhambi, na watu wema wana jaha kwa Mwenyezi Mungu, kwa hiyo namuomba Mwenyezi Mungu kupitia wao.’ Majibu yake ni yale yaliyotangulia, nayo ni kuwa wale aliowaua Mtume wa Mwenyezi Mungu 5 walikuwa wanakiri uliyoyataja na pia walikuwa wanakiri kuwa masanamu yao hayana mpango wa kitu chochote, ila wao walitaka jaha na uombezi kutoka kwao.” Nasema: Hii inajulisha kuwa Sheikh anaona yafaa kuwakufurisha na ni wajibu kuwaua hao ambao wanasema kauli iliyotangulia, 32

Hapa anamfundisha mmoja wa wafuasi wake amwambie anayehitilafiana naye hivi: “Na uliloniambia ewe mshirikina...!” Na hilo ni funzo la jumla la kukufurusha na kuwaita walio kinyume na yeye kuwa ni washirikina. 63

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 63

1/20/2016 11:35:50 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

na kuwa yeye anawazingatia kuwa ni washirikina kwa shirki kubwa; kama ile shirki ya makafiri wa Kikuraysh. Na huu ndio ukufurishaji wenyewe. Hali yao kubwa inayoweza kuzingatiwa kwao ni kuwa wao ni wafanya bidaa tu, na mfanya bidaa sio jaizi kumkufurisha sembuse kumuua, na wafanya bidaa wote waliouliwa muda wote wa historia walikuwa wanauawa katika mazingira ya kisiasa mtupu huyadiriki hayo mwenye kusoma historia.33

JAMBO LA KUMI NA SITA LIPASALO ­KUCHUNGUZWA: Kauli yake katika Uk. 24: “Hakika endapo atakiri – anamkusudia mtu aliye kinyume na utaratibu wa Sheikh – kuwa makafiri wanashuhudia kuwa ubwana au umiliki wote ni wa Mungu!! Na kuwa wao hawakutaka kutoka kwa waliyemkusudia ila ni uombezi lakini walikusudia atofautishe kati ya kitendo chao na kitendo chake kwa aliyoyataja miongoni mwa Swala zao na wema wao kinyume na makafiri, basi mkumbushe kuwa makafiri miongoni mwao kuna wanaowaomba watu wema na miongoni mwao kuna wanaowaomba mawalii...” Nasema: Makafiri hawaamini baadhi ya ubwana, wala uungu wote, wao wanayaabudu masanamu kwa dhati yake, na wala hawaishii kuomba uombezi tu bali kauli yao kuwa wanaamini baadhi ya ubwana wameisema ili kukata hoja na si kwa itikadi na imani, au ni kauli ya baadhi yao tu, kwa kuwa kwa uchache imethibiti kutoka kwa baadhi yao kuwa wanaamini Dahari wala hawaamini kufufuka. Ama kuhusu Waislamu, wao hawamsujudii yeyote asiyekuwa Mwenyezi Mungu, na wala hawamwabudu ila Mwenyezi Mungu, na 33

Kuhusu haya nimeyaongelea kwa upana katika kitabu cha al-Aqaidu hivyo basi mtu asidhanie kuwa Khalid al-Qasriy na al-Hajaju na walio mfano wao waliokuwa wanaiunguza Ka’aba na kuwaua watu wema kuwa wao waliwaua watu kwa kuipenda sana dini!! 64

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 64

1/20/2016 11:35:50 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

baadhi yao huenda wakawa wajinga au kufanya taawili kuwa watu wema miongoni mwao walio hai na walio kufa, inafaa kuwafanya wasila - njia - na kuomba uombezi wao kwa Mwenyezi Mungu na kumuomba Mwenyezi Mungu kwa jaha yao, na yakuwa wao endapo wakiwaombea watawanufaisha kwa idhini ya Mwenyezi Mungu sio kwa kujitegemea mbali na utashi wa Mwenyezi Mungu.34 Na hii ni tofauti sana na walivyo hao makafiri. Na tija ni kuwa kushabihiana kati ya makafiri na Waislamu wa hivi sasa - endapo tutaikubali hoja hiyo – kupo mbali mno kuliko kushabihiana kulikopo kati ya Makhawariji na wafuasi wa Sheikh. Hivyo basi kushabihiana kati yao katika kukufurisha na kunyoa vipara na kuhalalisha damu...mpaka mwisho ni kukubwa mno na ni kwa dhahiri mno. Hoja ya Makhawariji dhidi ya Ali D ipo karibu na hoja ya Mawahabi dhidi ya wanaopingana nao. Makhawariji wamesema ni wajibu 34

  Hata wafurutu ada wa ki-Sufi ambao wanasema kuwa walii anahuisha maiti, pamoja na kuwa kauli hii ni batili lakini hawasemi kuwa walii hufanya haya kwa kujitegemea mbali na Mwenyezi Mungu!! Na hali ni hiyo hiyo kwa wafurutu ada wa Kishia ambao wanasema kuwa Maimamu wana mamlaka katika mambo ya viumbe, na kwamba chembe chembe za ulimwengu zinatii amri yao, wao hawasemi kuwa haya hutokea kwa kujitegemea bila ya irada ya Mwenyezi Mungu, bali wafurutu ada miongoni mwa masufi na Shia wanadhania kuwa Mwenyezi Mungu amewatunukia mawalii na maimamu uwezo wa haya kwa idhini Yake, kama alivyowatunukia baadhi ya Manabii kama vile Nabii Isa D uwezo wa kuumba kutokana na udongo mfano wa umbo la ndege, na kumrejesha hai maiti na kumponesha aliyezaliwa kipofu na mwenye ukoma, lakini kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na kama alivyowatunukia baadhi ya mawalii kama vile swahaba wa Nabii Sulayman uwezo wa kuleta kitanda cha enzi cha Bilqisi katika muda wa kufumba jicho na kufumbua, yote haya ni kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Hivyo basi kauli hizi zote pamoja na kuwa ni batili hawazirejeshi ila kwenye uwezo wa Mwenyezi Mungu, katika idhini Yake, matakwa Yake, na kwa kuwatunukia sifa mahsusi baadhi ya waja Wake miongoni mwa Manabii na mawalii. Nao kuhusiana na hayo wana kauli nyingi na vitabu vingi vilivyotungwa na dalili nyingi zinazostaajabisha wameacha kushikamana na dalili yakinifu wamekimbilia kwenye dhana huku wakijikalifisha katika kutoa dalili ya kuthibitisha hayo, kama walivyojikalifisha Mawahabi katika kukufurisha japo kuna tofauti katika kiwango cha makosa. 65

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 65

1/20/2016 11:35:50 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

kuielekeza hukumu yote kwa Mwenyezi Mungu, na ikiwa iwe kwa ajili ya Mungu tu “Hakuna hukumu isipokuwa ya Mwenyezi Mungu tu.” Na hilo neno ni haki lakini limekusudiwa batili, mfano wa walivyodhania Mawahabi kwa kauli yao: “Hakuna uchinjaji isipokuwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu tu. Hakuna tawasuli isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu na hakuna kuomba msaada isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu.” Huu ni ukweli kwa mujibu wa asili ya neno lakini upo uwezekano wa kuwepo hali fulani katika utekelezaji zitokazo nje ya kauli hii jumuishi; na kwa uchache kabisa ni upo uwezekano wa kuwepo kwa utendaji wenye makosa ukilinganisha na kauli jumuishi zilizotangulia, unaotendwa na baadhi imma kwa taawili au kwa kutojua, kwa hiyo utendaji kama huu haumkufurishi mtendaji wake isipokuwa baada ya kutoweka vizuizi vya kumkufurisha na kuwepo kwa hoja. Na hakuna hoja itakayosimama baada ya hali ya kutojua na ya taawili, madamu asiyejua na afanyaye taawili anakiri kuwa ni Mwislamu, wala hakanushi suala lililokatiwa shauri na ijmai ya Waislamu, kama vile kuwa Swala ni wajibu na kuwatendea wema wazazi wawili, kutekeleza wajibu wa Zaka, kufunga Ramadhani,...au kuharamisha dhulma, uwongo, kughushi, na kuiua nafsi ambayo Mwenyezi Mungu ameharamisha kuiua...mpaka mwisho. Bali mwenye kuritadi wazi wazi peke yake wanazuoni hawakuafikiana kuwa ni wajibu kumuua, na Hadithi kuhusiana na hilo ni dhaifu, na utekelezaji wa Nabii 5 upo kinyume na hali hiyo.35 Basi itakuwaje tumfuate Sheikh katika maeneo finyu ambayo makosa yake humo ni zaidi kuliko kupatia kwake. Yakaribia hakuna mwanachuoni anayeafikiana naye katika hayo mabonde miongoni mwa wanazuoni waliotangulia na waliofuatia isipokuwa anayemkalidi. Na yaliyo dhahiri mno miongoni mwa hayo ni kuligawa Bara Arabu kwenye nchi ya ukafiri na nchi ya Uislamu, kwa sababu ya 35

Ufafanuzi juu ya hilo umetangulia huko nyuma. 66

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 66

1/20/2016 11:35:50 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

kuwepo bidaa huku na huko, na katika hili hajatanguliwa na yeyote si Ahmad bin Hanbali wala Ibn Taymiya wala mwingine mbali na wawili hao miongoni mwa wenye kupanua wigo wa ukufurishaji na bidaa. Katika wakati wao bidaa ilikuwa kama ilivyokuwa wakati wa Sheikh, kama ambavyo uwanja wa kukufurisha vitendo na kauli bali na watu haukuwa finyu, lakini pamoja na hayo wao hawakuugawa ulimwengu wa Kiislamu kwenye nchi ya ukafiri na nchi ya Uislamu, huu ugawanyaji ni miongoni mwa makubwa waliyojitenga nayo Mawahabi, hawajatanguliwa na mtu ila Maazariqa miongoni mwa Makhawariji.36 36

Al-Azariqah (Maazariqa): Ni nasaba ya Nafiu Bin al-Arzaq al-Hanafiy, na hawa ndio Makhawariji wakali mno, wamejitenga mbali na Makhawariji wengine kwa mambo kadhaa, miongoni mwa hayo ni: Kujiepusha na Makhawariji wa al-Qaadatu, na kumfanyia mtihani mwenye kwenda kwenye kambi ya walio kinyume, na kumkufurisha asiyehama kwenda kwao, na mwenye kubakia kwenye nchi ya ukafiri basi yeye ni kafiri. Na haya yote yapo katika uwahabi. Nao wana itikadi nyingine, lakini mwenye kufanya rejea itikadi za Makhawariji atajua kuwa wengi wao kati yao kuna wenye mtazamo wa wastani ambao hatuwezi kuukuta kwa baadhi ya Mawahabi na Masalafi, wala kwa Masunni walio wengi. Kama kauli yao kuwa: Ukhalifa ni haki ya kila ambaye ametimiza sharti za kufaa kuwa mtawala Mwislamu bila ya kuufanya makhsusi kwa Makuraishi. Na kujuzisha baadhi ya Makhawariji – kama vile watu wa Shabib – utawala wa mwanamke na ukadhi wake, na kuafikiana kwao – isipokuwa Najidat – kuwa Mungu hatomwadhibu mtenda dhambi kubwa adhabu ya daima. Na hii ni tofauti na tunayoyaeneza kutokana nao kwa itikadi ya baadhi miongoni mwao. Na walikuwa wanakubali udhuru wa ujinga wa mtu, na Najidat miongoni mwao walikuwa wanakubali udhuru wa ujinga wa mtu wakisema: ‘Dini ni mambo mawili: Moja ya hayo mawili ni kumtambua Mungu na kuwatambua Mitume Wake, kuharamisha damu za Waislamu zisimwagwe, na mali zao, na kuharamisha unyang’anyi, yaani kupora mali ya mtu. Na kukiri yaliyokuja kutoka kwa Mungu kwa ujumla wake. Haya ndiyo ya wajibu na katika yasiyokuwa hayo watu wana udhuru kwa kutoyajua mpaka hoja itakapowabainikia. Na atakayehalalisha kitu kwa njia ya ijitihadi ambacho huenda ni kitu haramu basi ni mwenye udhuru.’ Na Maibaadhi wanaiona nyumba ya walio kinyume na wao ni nyumba ya Kiislamu isipokuwa kambi ya kiaskari ya sulutani. Na hii ni kauli hafifu kuliko kauli ya Mawahabi. Na wanajuzisha ushahidi wa walio khilafu nao dhidi ya watu wao. Kwa hiyo mfano wa kauli kama hizi za Makhawariji ndani yake kuna wastani ambao baadhi yake hatuukuti kwa Masalafi, basi ni kwa nini kuwepo hali ya kuwafedhehesha na kuwalazimisha kauli ya baadhi yao na kuwabebesha makosa yetu katika kukufurisha na kuhalalisha damu za Waislamu? Ili kuielewa itikadi ya Makhawariji na hususan niliyonakili kutoka kwa Maazzariqah angalia kitabu: Maqalatul-Islamiyina cha al-Ash’ariy (1\167 ). 67

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 67

1/20/2016 11:35:50 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

JAMBO LA KUMI NA SABA LIPASALO ­KUCHUNGUZWA: Amesema katika Uk. 27: “Akisema - anamkusudia aliye kinyume na Sheikh – makafiri wanataka kutoka kwao – yaani sanamu -, na mimi nashuhudia kuwa Mwenyezi Mungu ndiye mnufaishaji mwenye kudhuru mwenye kupanga sitaki ila kutoka kwake, na watu wema hawana amri ya kitu chochote lakini nawakusudia nikitarajia kwa Mwenyezi Mungu uombezi wao, basi jibu ni: Hii ni kauli ya makafiri sawa kwa sawa!!” Nasema: Asemaye kauli iliyotangulia hakufurishwi; kwa sababu yeye ni mwenye kufanya taawili au mjinga, na Sheikh anamkufurisha, na kuafikiana kwake na makafiri ni katika kijisehemu kidogo ambacho hakimaanishi yuko sawa na makafiri, au ni kuwa wao wawili hukumu yao ni moja.37 Kwa maana endapo mtu ataapa kwa jina lisilokuwa la Mungu atakuwa ameshirikiana na makafiri katika kijisehemu kidogo, lakini hakufurishwi kwa sababu yake, lakini Sheikh ameghafilika na kitu kidogo mfano wa hiki; kwa hiyo akatumbukia katika dimbwi la kuwakufurisha Waislamu, kwa hiyo Sheikh kajikita kwenye Aya: “Hatuwaabudu wao ila twawatarajia watusogeze karibu ya Mungu.” ambayo humo kuna sifa moja tu miongoni mwa sifa za makafiri wa asili hasa. Au yenyewe ni kielelezo cha kukatikiwa kwao na kuuelezea udhuru wao usiokuwa na maana ambako hakuambatani na nia ya kweli. Na kughafilika kwake na Aya zilizobaki katika kuzielezea itikadi nyingine za makafiri za mkato na ni nyingi, katika hii kuna upungufu mkubwa katika kuleta maeneo ya tofauti kati ya makafiri na Waislamu. 37

Tambua kuwa sisi tunachukua kauli za hao kutoka kwa Sheikh mwenyewe hali yeye ni hasimu wao, kwani tunzi za wanazuoni waliomjibu hawakiri mfano wa nukuu hizi, lakini sisi tunazihoji kauli hizo kwa kuzichukulia kuwa kwake sahihi kwa msemaji wake. 68

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 68

1/20/2016 11:35:50 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Kisha kuomba uombezi kwa Nabii 5 na kwa watu wema pamoja na kuitakidi kuwa hao wote ni waja wa Mwenyezi Mungu na kuwa wao hawampi mtu kitu ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, haya yote si sawa na kusujudia masanamu, japo iwe nakisa au bidaa ndogo au kubwa. Kwa mujibu huo wapinzani wa Sheikh wanaweza kumlazimisha Sheikh amkufurishe mnywaji pombe, kwa kuwa yeye hainywi ila akiwa aipenda, na kupenda ni ibada na kukitoa kitu mbali na upendo wa Mwenyezi Mungu ni shirki na kama hivyo. Na endapo mtasema: Sisi hatupingi kuwapenda watu wema bali tunapinga kuwaabudu. Mtaambiwa: Hao hawawaabudu na ninyi mnaiita tawasuli yao kwa watu wema au kutabaruku kwao kuwa ni ibada, na wao hawawakubalii kuwa hii ni ibada, na wanazo dalili kuthibitisha hilo – pamoja na udhaifu wake – lakini zinazuia kuwakufurisha. Na hii ndio taawili ambayo wanazuoni wamesema kuwa inazuia kukufurisha. Endapo mtasema: Tawasul ni ibada. Watasema: Nini dalili yenu juu ya hilo? Mkisema: Wema waliotangulia hawakufanya. Watasema: Umar bin al-Khattab amefanya kwa Abbasi bin Abdul Mutalib. Mkisema Umar aliifanya kwa aliye hai sio kwa maiti. Watasema: Hivi ni jaizi kumwabudu aliye hai? Mkisema: Hapana. Watasema: Kwa nini mnaiita tawasuli kuwa ni ibada?! Hii ni dalili kuwa ninyi mwaviita vitu majina yasiyokuwa yao. hai.

Mkisema: Tawasuli kwa aliye kufa ni ibada kinyume na aliye

69

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 69

1/20/2016 11:35:50 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Watasema: Dalili yenu ya kutofautisha ni nini? Mkisema: Dalili yetu ni tendo la Maswahaba kwani wao walifanya hivi wala hawakufanya hivyo. Watakuambieni kwa kuwakubalieni: Wao – yaani swahaba - huacha kutenda jambo wala sio lazima liwe ni haramu sembuse kulizingatia kwenu - kuwa ni kufuru inayomtoa mtu nje ya Uislamu! Halafu sisi tuna dalili nyingi baadhi yao wamefanya Tawasuli kwa Nabii 5 akiwa amekwisha kufa, kama ilivyokuja katika Hadithi ya Uthman bin Haniif iliyo mashuhuri. Mkisema: Kwetu dalili hii ni dhaifu. Watakuambieni: Hadithi nyingi ambazo ninyi huzitolea dalili kwetu ni dhaifu, bali zenyewe ni dhaifu kwenye uhakiki, mfano wa Hadithi ya kumleta karibu nzi na Hadithi ya shirki ya Adam na Hawaa, na zisizo hizo miongoni mwa Hadithi dhaifu na ambazo ni za uzushi zilizo katika vitabu vyenu. Mkisema: Lililo bora ni kujiepusha na Tawasul ili kuepukana na shubha na kuhitilafiana. Watakwambieni: Lililo bora kuliko hilo ni kujiepusha kuwakufurisha Waislamu na kuwafanya makafiri wa Kikurayshi kuwa ni bora kuliko wao, kwa kuwa asili iliyo yakini ni Uislamu sio shirki, kwa hiyo hatutakiwi tuiache yakini na kushika linalodhaniwa. Mkisema: Hapanabudi kutilia mkazo hilo ili Waislamu waongoke na dini ya Mwenyezi Mungu na wajihadhari na bidaa hizo na upotovu. Watasema: Hapanabudi kuwajibuni ninyi ili wanafunzi wa elimu wajihadhari wasiingie katika kuwakufurisha Waislamu na kuhalalisha damu zao na mali zao. 70

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 70

1/20/2016 11:35:50 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Mkisema: Basi njooni ili tukifanye Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna ya Mjumbe Wake 5 kuwa ndio hakimu na tuachane na kuiga. Watakuambieni: Karibuni hapa ni kwenu, hili tulikuambieni muda mrefu, ninyi mlikuwa mkilikataa, mlikuwa mkituandalia maaskari, na hamkuacha kuwakufurisha wasiokuwa na makosa mpaka baadhi yenu wakawa wanawakufurisha baadhi, mkadhulumiana na hapo mkatambua kiwango cha dhulma yenu kwetu wakati uliopita. Na mlitambua baadhi ya tuliyokuwa tunayawasilisha yakiwa ni dalili ya kuwa sisi si makafiri. Kwa sababu ninyi mlitaja dalili za kuwajibu wanaokukufurisheni na sisi tulikuwa tukizikariri katika kuwajibuni ninyi mlivyokuwa mkitukufurisha. Kuwa kwenu na msimamo wa wastani katika zama za mwishoni yasikitisha sana kwamba ilikuwa ni kwa maslahi yenu binafsi na kujihami wala sio kuuhami upande wa sharia.

JAMBO LA KUMI NA NANE LIPASALO ­KUCHUNGUZWA: Ni kauli yake katika Uk. 33: “Wala Nabii 5 hamfanyii uombezi yeyote ila baada ya Mwenyezi Mungu kumpa idhini ya kufanya hivyo, kama alivyosema: ‘Wala hawatofanya uombezi ila kwa atakayemridhia.’ Na Yeye haridhii ila Tawhidi kama Mwenyezi Mungu alivyosema: ‘Na aitakaye dini isiyokuwa Uislamu hatokubaliwa.’ Wala Mwenyezi Mungu hatotoa idhini ila kwa wanatawhidi.” Nasema: Kwa mujibu huo inawezekana kusema yaliyosemwa na baadhi ya wapinzani wa Sheikh kuwa kwa mujibu wa maneno haya hatoingia peponi katika zama za Sheikh ila watu wa Uyeyna na Deriyyah! Katika maneno ya Sheikh yaliyotangulia ndani yake kuna ukufurishaji kwa kila anayeona yafaa kufanya Tawasul kwa watu 71

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 71

1/20/2016 11:35:50 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

wema au kuomba uombezi wao, nao ni jamhuri - yaani kundi kubwa - la wanazuoni wa Kiislamu na watu wao wa kawaida katika wakati ule na katika zama zetu pia. Na hapa nakumbuka ukweli wa neno alilosema mmoja wa wapinzani wa Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahabi Mungu awarehemu, aliposema ambayo hii ndiyo maana yake: “Nabii 5 alitoa habari kuwa siku ya Kiyama atakuja hali akijifaharisha na kaumu yake. Na kwa mujibu wa maneno ya huyu - anamkusudia Sheikh Muhammad –ni kwamba Nabii wetu 5 atakuja akiwa hana mtu mwingine yeyote ila kundi la watu miongoni mwa watu wa Uyeyna. Haya ameyataja Dkt. Abdul-Azizi bin Abdul-Latif katika kitabu chake Daawil-Munawiina. Dkt. Abdul-Azizi bin Abdul-Latif Mungu ampe tawfiki amejibu maneno yaliyotangulia kwa majibu ya jumla, wala hakutanabahi lazima za maneno ya Sheikh Muhammad hapa, alipouharamisha uombezi kwa watu wasiokuwa wafuasi wake ambao aliwaita wanatawhidi, kwa hoja ya kuwa wasiokuwa hao si Waislamu. Na anayeitaka dini isiyokuwa Uislamu hatokubaliwa. Hivyo Waislamu katika ulimwengu wa Kiislamu – isipokuwa wafusi wa Sheikh huko Najdi na sehemu zinazoambatana nayo – kwa mtazamo wa Sheikh wanakuwa: Wameitaka dini isiyokuwa Uislamu.38 Na suala hili lipo kwenye upeo wa juu kabisa wa ukufurishaji wa hatari. Kwa sababu katika ulimwengu wa Kiislamu bidaa na upotovu huu upo kwa muda mrefu. Ndani yake wakiwemo wanazuoni wafanyao taawili, watu wa kawaida wasiojua, lakini hali hiyo haituhalalishii sisi kusema kuwa ni makafiri, na aliowakuta Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahabi Mungu amrehemu, wao ni Waislamu wale wale ambao tuliwalilia kutokana na hujuma za watu wa msalaba huko Sham (Syria), na 38

Utakuja uthibitisho wa hili ukithibitishwa na fatwa za Sheikh na wengine miongoni mwa wanazuoni wa daawa. 72

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 72

1/20/2016 11:35:50 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

hujuma ya Maghol upande wa Mashariki, na kutokana na mbinyo wa wazungu huko Hispania. Ama kulingana na maneno ya Sheikh Mungu amrehemu, hakuna sababu ya kulia, kwani hao ni washirikina wafuatao dini isiyo Uislamu, basi kwa nini kulia?! Na ukufurishaji huu haukuwepo kwa Sheikh Ibn Taymiya, pamoja na makosa yaliyotokea kwake, kwani Ibn Taymiya alikuwa katika zama inayoshabihiana na zama za Sheikh Muhammad kwa kuenea ujinga kati ya watu wa kawaida na udhaifu wa wanazuoni, udhaifu wa kuwaita watu kwenye Tawhidi iliyo safi; lakini udhaifu wa hawa na ujinga wa wale hautuhalalishii sisi ila kuwasema kuwa wamezembea, na ni ujinga na ni dhambi na yatosha. Ama kuwaita wao makafiri kwa ukafiri umtoao mtu nje ya Uislamu; hiki ni kitu kingine kabisa. Kukufurisha mtu ni jambo kubwa mno na zito sana, na kuutoa umma huu wa Kiislamu nje ya dini ya Mwenyezi Mungu ni jambo baya mno na adhimu. Bali mabaki ya Makhawariji waliopo katika zama hizi za mwisho hayawakufurishi watu wa kawaida au kuhalalisha damu zao, kama alivyofanya Sheikh na wafuasi wake Mungu amrehemu kwa fatuwa zake kuwahusu wanazuoni na watu wa kawaida.39 Mungu amsamehe Sheikh na amghufirie, amepanda kheri nyingi lakini imeshabihiana na shari iliyoenea kwa msukumo wa hamasa. Ama kuhusu kheri ni kuimaliza kwake bidaa na upotovu mwingi, lakini yeye amepitiliza kiwango mpaka ameufikia ufurutu ada mbaya wa kulaumiwa, hivyo basi bidaa imetoweka umebaki ukufurishaji! Baadhi ya ndugu wanasema: Vipi tuikosoe njia ya Sheikh kwa fadhila zake, wakati baada ya fadhila za Mungu ndio imepatikana nchi hii kubwa ya Kiislamu?! 39

  Bali hivi hapa vitabu vya Maibaadhi vinawakemea Mawahabi kukufurisha! Endapo kuwatuhumu kwetu wao kutakuwa sahihi kwa kuwa wao ni Makhawariji, basi wao Makhawariji kutukemea kukufurisha ni dalili ya mambo matatu: Imma ni msimamo wa wastani wa Makhawariju au ni ufurutu ada mbaya wa uwahabi, au ni vyote viwili. 73

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 73

1/20/2016 11:35:50 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Tunasema: Bila shaka haya ni miongoni mwa mema makubwa ya Sheikh, na tumekwisha kuyataja kwenye utangulizi na wenye ikhlasi miongoni mwa watu hawatoyasahau. Huenda lau si daawa yake na kupigana kwake na Waislamu wa Bara Arabu40 hawangekuwa kitu kimoja kutokea Ghuba mpaka Bahari nyekundu, na kutokea Sham Kusini mpaka Yemeni. Lakini uzuri wa matokeo haimaanishi usahihi wa utangulizi, huenda matokeo yakawa mazuri pamoja na kujengewa kwake juu ya utangulizi pungufu, hili wanalitambua wanamantiki na wengine. Hivyo mapinduzi ya Khomeini kwa mfano, natija yake imekuwa nzuri kama vile kuondoa usekyula wa kimagharibi kwenye dola ya Iran, lakini natija hii haimaanishi kutomkosoa Khomeini na ufurutu ada wake, hali ni hivyo lau mmoja wa Makhawariji atafanikiwa kujenga dola, uzuri wa natija haumaanishi usahihi wa mgutuko. Hebu tubainishe hili kwa mfano wa wazi zaidi na tuseme: Lau mmoja kati ya viongozi au watawala akitoa amri ya kumuua mwizi badala ya kumkata mkono wake, bila shaka mikono itakatwa, na bila shaka wizi utapungua, na hapo itakuja zamu ya mwenye kumsifu mtawala huyu ili aisifu natija nzuri ambayo ni kupungua wizi au kutoweka kabisa...!! Lakini kitendo cha huyu mtawala hapa kilikuwa kinyume na maandiko ya kisheria (Qur’ani na Hadithi), na hapana budi siku moja kitendo chake hiki lazima kiwe na athari isiyokubalika, kwa sababu sharia ya Mwenyezi Mungu iko kamili na hakuna hukumu ya kisheria ila itakuwa kati ya kuzidisha kiwango na kupunguza chumvi. Vivyo hivyo lau mmoja miongoni mwa watawala akitoa amri ya kukatwa mkono kila atakayekiuka sheria ya usalama barabarani, au 40

  Ndiyo, hatumfuati Sheikh wala ulamaa wa daawa katika kuwakufurisha wakazi wa Bara Arabu wenye kwenda kinyume nao. Wote ni Waislamu na si makafiri wala si waabudu masanamu, si yule mwenye kufanya taawili katika kumpenda Nabii 5 na watu wema, wala si yule mwenye kufanya taawili katika kukufurisha na kuhalalisha damu. 74

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 74

1/20/2016 11:35:50 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

kuzidisha mwendo ulioidhinishwa kisharia, bila shaka kutakuwepo na udhibiti barabarani na vifo vitatoweka kwa kiwango kitakachozishangaza nchi zilizoendelea! Hapo itakuja zamu ya mwenye kumsifu mtawala huyu ili aisifu natija ya uamuzi huu!! Kwamba ulikuwa uamuzi wa hekima, na kuwa vifo vimepungua kutoka elfu sita kwa mwaka mpaka vifo kumi na tano tu!! Na kupungua idadi ya majeruhi na wasiojiweza kutoka laki moja kwa mwaka mpaka themanini na sita tu!! Lakini je, nini rai yenu kuhusu uhalali wa maamuzi haya kisheria na kikanuni? Na ni kitu gani yatasababisha baada ya muda mrefu?! Jibu ni maarufu kwa wenye akili miongoni mwa wanazuoni wa sharia na kanuni, na wanazuoni wa historia na wanazuoni wa elimu ya kijamii na kanuni. Na kadhalika sio jaizi kuwaua Waislamu kwa kuwepo tu bidaa na upotovu, kwa kuwa kuua sio jaizi ila kwa maandiko ya kisheria, kwa kuritadi kuliko dhahiri, au uvamizi njiani, au umalaya. Ama bila maandiko, kutenda hilo (kuua) ni baya zaidi kuliko hizo bidaa na upotovu. Na Sheikh Muhammad Mungu amrehemu, lau asingeua Waislamu, na akatosheka tu na kuwasiliana na wanachuoni kwa kuwaandikia barua na kuwahimiza wafanye daawa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, lau angefanya hivi huenda ingekuja natija ileile japo kwa kuchelewa, na tungekuwa kando na ukufurishaji na yaliyoambatana nayo katika zama zile mpaka zama zetu hizi ambazo wakufurishaji wanategemea fatwa za Sheikh na wanachuoni wa daawa katika kuwakufurisha Waislamu. Japokuwa Sayyid Qutub Mungu amrehemu ametuzidi katika kumkosoa kiasi kwamba sisi tumekuta maneno tata katika maneno yake, yamaanishayo ukufurishaji; lakini kwa Sheikh Muhammad 75

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 75

1/20/2016 11:35:50 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

tumeukuta ukufurishaji wa wazi na bayana katika maneno yake yaliyo bayana na wazi yasiyo tata.41 Tumemfanya Sayyid Qutub kondoo wa muhanga kwa kuwa yeye hana wa kumnusuru kwetu, na Sheikh anao wa kumnusuru! Na hii sio tabia ya mwanafunzi wa elimu ambaye husema ukweli japo uwe dhidi yake mwenyewe. Wala habebi majukumu ya wasio na hatia, hili pia haliafikiani na murua wa watu ambao wanakataa kuwatoa muhanga wanyonge kuwalinda wenye nguvu. Na muhtasari hapa ni kwamba huu ufurutu ada katika kukufurisha ndio uliyotufanya sisi tuzikosoe ibara za Sheikh pamoja na kutambua fadhila zake kwetu, lakini madhara yaliyo katika vitabu vyake japo baadhi wayaone kuwa ni kitu kidogo, ukweli ni kwamba wakati huohuo ni hatari sana, kwa kuzingatia hali kubwa na mbaya inayomzunguka Sheikh, Mungu amrehemu. Na tatizo kubwa tulionalo ni kuwa fatwa zetu hii leo kuhusu kukufurisha zinahitilafiana na Sheikh kabisa, lakini tunawalazimisha watu kuamini fatwa za Sheikh ambazo zina ufurutu ada katika kukufurisha, na kuziamini fatwa zetu ambazo Sheikh alikuwa anazizingatia kuwa ni tasa ikiwa hazizingatii kuwa ni kufuru, na ambazo zinaafikiana na fatwa za mahasimu wa Sheikh katika kujibu ukufurishaji!! Na huku ni kukusanya kati ya mambo yanayopingana.42 Lau sisi tungesema: ‘Sheikh alijitahidi katika kukufurisha lakini akakosea’ hali hii yote ya kupingana ingetoweka, hangekuwa ana  Na ikiwa kauli yake kuwa masheikh wake na masheikhe wao hawaijui dini ya Uislamu, pamoja na kuiona dini ya Amru bin Lahyi kuwa ndio bora kuliko dini ya Uislamu, na kwamba watu wengi katika zama zake huko Najdi na Hijazi walikuwa wanakanusha ufufuo, ikiwa maneno haya na mfano wake si katika ukufurishaji wa wazi bayana basi sijui ukufurishaji hasa ni nini? 42   Nakusudia kuwa fatwa za maulamaa wa wakati huu zinatoa jibu la kupinga ukufurishaji wa kushabihisha kwa hoja zilezile za mahasimu wa Sheikh ambazo kwazo walikuwa wanajibu kumpinga Sheikh, na iliyo wazi miongoni mwazo ni mas’ala ya utawala. 41

76

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 76

1/20/2016 11:35:50 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

pungukiwa na dini wala dunia wala cheo, kwani dini haitikisiki kwa kuwakosoa watu mfano wa Umar na Ali M basi vipi itatikisika kwa kumkosoa Ibn Taymiya au Ibn al-Qayyim au Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahabi?! Na kubainisha makosa ya Sheikh Muhmmad katika upade huu wa kukufurisha ni jambo lenye faida na ni dharura, kwa kuwa wimbi la usalafi kwa jumla na jamii ya Saudi Arabia hususan wanachuo wake na wanafunzi wa elimu, wameleleka katika fatwa za Sheikh na za ulamaa wa daawa ambao wanaelemea upande wa kuwakufurisha Waislamu, hivyo hapana budi waathirike walio wengi miongoni mwao kwa upande huu, bali taathiira imetanuka mpaka kwa Masunni wengi nje ya Saudia kutokana na harakati zetu za daawa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu! Mwenye kukisoma kitabu ad-Durarus-Saniyyah atalijua hili kikamilifu, bali katika kitabu hiki kuna juzuu mbili kubwa kubwa kwa anuani ya ‘Jihadi’ zote mbili zinazungumzia kuwapiga jihadi Waislamu, hakuna hata herufi moja izungumziayo kuwapiga jihadi Makafiri wa asili miongoni mwa Mayahudi na Manaswara na waabudiao sanamu, pamoja na kuwa baadhi ya nchi za Kiislamu kulikuwa na makafiri wa asili walioziteka. Na kulitokea hali ya kukufurishana kati ya wanazuoni wa daawa wenyewe kwa wenyewe pindi walipohitilafiana watoto wa Mfalme Faysal bin Turkiu, ambao ni Abdullahi na Suud, Mungu awarehemu. Hivyo kila Mfalme alikuwa na wanachuoni wanaolikufurisha kundi lingine. Kwa hiyo vurugu hii ya ukufurishanaji matokeo ya kawaida na natija mkataa ya njia ya Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahab Mungu amrehemu, ambaye amepanuka kifikra kiasi kwamba kila kikundi kimepata katika maneno yake linalotilia nguvu mtazamo wake. Bali harakati za Ikhwanu huko Najdi, na harakati za al-Haram, 77

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 77

1/20/2016 11:35:50 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

za watu wa milipuko huko al-Ulya, Mahya, Hamraa na al-Washim... ambao wanawafanya watu viziwi kwa kuwakufurisha, si ngeni kulingana na utamaduni wa eneo, bali endapo tutasema wao ni zao la njia ya Sheikh katika kukufurisha hatutakuwa tumekwenda mbali.43 Mwenye kutaka naafanye rejea vyanzo vya hayo makundi atayatambua haya kikamilifu.44   Bila ya kughafilika na sababu za nje kama vile kutenzwa nguvu na Wamarekani, na kuunga nguvu utawala wa Kizayuni, kisiasa, kijeshi na kiuchumi, hayo yamefanya Waislamu wachukizwe na kuomba ilhamu ya kumkufurisha aliyebakisha uhusiano wake na Marekani kana kwamba hawakuwatendea vibaya Waislamu hususan Palestina, Iraq, na kabla yake Sudani. Kwani sababu za nje zinashajiisha kuizingatia Magharibi yote na hususan Marekani kuwa ni adui. Na kughafilika na suala la kuukosoa ukufurishaji na machimbuko yake ya msingi inashajiisha Waislamu kuwadhulumu baadhi yao na kuwavuruga na kuzozana wao kwa wao, na kujenga mpasuko wa kisaikolojia na kijamii kati yao. 44   Kwa kuongezea ni kwamba makundi ya sasa kama vile al-Qaidah, Boko Haramu, alShabab, Daesh na mfano wa hayo miongoni mwa yale ambayo karne ya ishirini na moja imeshuhudia unyama wake, ni zao na tunda la fikra za Sheikh Muhammad bin AbdulWahabi, mwasisi wa Uwahabi. Kwa lugha nyingine ni kwamba fikra za Sheikh katika kuwakufurisha Waislamu bado zinafanyiwa kazi kivitendo, na ndio maana tunashuhudia mauaji ya kinyama yakifanywa na makundi haya dhidi ya Waislamu kwa jina la Uislamu. 43

Matakfiri wanapigana na Waislamu badala ya kupambana na Wazayuni. Kufufuliwa makundi ya kitakfiri katika miaka ya hivi karibuni ni tatizo lililopandikizwa na mabeberu katika ulimwengu wa Kiislamu. Mirengo hiyo habithi ya kitakfiri inatumikia malengo ya Marekani, madola ya kikoloni na utawala wa Kizayuni wa Israel hususan njama za makundi hayo za kujaribu kuwasahaulisha Waislamu suala muhimu zaidi la ulimwengu wa Kiislamu, yaani kadhia ya Palestina na Msikiti wa Aqsa. Hivyo kuanzisha mwamko wa kielimu, kimantiki na wa pande zote kwa ajili ya kung’oa mizizi ya mrengo unaowakufurisha Waislamu wengine, kuwazindua Waislamu kuhusu njama za siasa za kibeberu za kutaka kuhuisha mrengo huo na kulipa umuhimu mkubwa suala la Palestina ni miongoni mwa nyadhifa na wajibu mkubwa zaidi unaopaswa kupewa kipaumbele na maulamaa wa ulimwengu wa Kiislamu. Katika kuchunguza mrengo huu hatari unaokufurisha Waislamu wengine kuna ulazima wa kutiliwa maanani maudhui kuu ambayo ni kuanzisha mapambano ya pande zote dhidi ya mrengo uliohuishwa tena wa kitakfiri ambao ni mkubwa zaidi kuliko kundi moja tu linaloitwa Daesh, bali kwa hakika Daesh ni tawi moja la mti huo muovu. Mrengo wa kitakfiri na nchi zinazouunga mkono zinatumikia kikamilifu malengo ya mabeberu yaani Marekani, madola ya kikoloni ya Ulaya na utawala wa Kizayuni, kwa kutumia vazi la Kiislamu. Suala la kujaribu kupotosha harakati ya mwamko wa Kiislamu ni ushahidi 78

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 78

1/20/2016 11:35:51 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

wa kwanza wa kuthibitisha kwamba fikra ya kitakfiri inatumikia malengo ya mabeberu. Mwamko wa Kiislamu ni harakati iliyo dhidi ya Marekani, udikteta na vibaraka wa Marekani lakini makundi ya kitakfiri yamezuka ili kukabiliana na harakati hiyo adhimu iliyo dhidi ya ubeberu na kuifanya kuwa vita vya wenyewe kwa wenyewe na mauaji ya Waislamu kwa Waislamu. Msitari wa mbele wa mapambano ya Waislamu ni Palestina inayokaliwa kwa mabavu, lakini makundi ya kitakfiri yamegeuza mstari huo na kuingia kwenye mitaa na miji ya nchi za Iraq, Syria, Pakistan na Libya, na hiyo ni moja ya jinai kubwa sana zisizoweza kusahaulika zinazofanywa na makundi hayo ya kitakfiri. Kupotosha harakati ya mwamko wa Kiislamu ni kuitumikia Marekani, Uingereza na utawala wa Kizayuni pamoja na mashirika yao ya kijasusi. Ushahidi mwingine unaothibitisha kwamba vitendo vya makundi hayo vinatumikia malengo ya mabeberu ni kwamba wanaoendesha fikra hiyo ya kitakfiri hawasemi lolote dhidi ya utawala wa Kizayuni bali wanafikia hata kushirikiana na utawala huo dhidi ya Waislamu. Lakini hao hao utawaona wako mstari wa mbele katika vitendo vya kutoa pigo kwa nchi na mataifa ya Waislamu. Vitendo vya kuangamiza miundombinu yenye thamani kubwa ya nchi za Kiislamu vinavyofanywa na makundi hayo yanayoeneza fitna katika ulimwengu wa Kiislamu ni mfano mwingine unaothibitisha kwamba makundi hayo yanatumikia malengo ya maadui wa Uislamu. Hatua nyingine ya kihabithi zaidi ya makundi ya kitakfiri ni kupotosha sura halisi ya Uislamu ambayo ni dini ya upendo, ya kimantiki, ya kufanya mambo kwa kutumia busara na ya kuhurumiana, na kuonesha picha za jinai kubwa zinazofanywa na makundi hayo kama za kuchinja watu wasio na hatia, kupasua mwili na kutoa moyo wa Mwislamu na kuutafuna tafuna kwa meno mbele ya kamera tena kwa jina la Uislamu! Ushahidi mwingine wa kwamba makundi ya kitakfiri yanatumikia malengo ya mabeberu ni kutojali kwao hata kidogo jinai zilizofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika mashambulizi yake huko Ghaza na kuwaacha peke yao Wapalestina katika mashambulizi hayo ya Ghaza. Ushahidi mwingine ni namna makundi hayo ya kitakfiri yanavyopotosha hamasa na mwamko walioupata vijana wa ulimwengu wa Kiislamu baada ya kutokea mwamko wa Kiislamu katika ulimwengu huo, na inasikitisha kuona kuwa makundi hayo yanatumia vibaya hamasa hizo za vijana wa Kiislamu kwa ajili ya kuua Waislamu wengine wasio na hatia – Mhariri. Kabla ya hotuba ya Kiongozi Maudhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Hujjatul Islam Wal-Muslimin Alizadeh Mousavi, Katibu wa Kongamano la Mirengo ya Kufurutu Ada na Kitakfiri kwa Mtazamo wa Maulamaa wa Kiislamu ametoa ripoti fupi kuhusiana na namna kongamano hilo lilivyofanyika kwa ufanisi na kusema kuwa: Katika siku mbili za kongamano hilo, kuliundwa kamati mbalimbali za kitaalamu na kiistratijia na kuchunguza na kutafakari kwa kina mizizi ya makundi ya kitakfiri, masuala yao ya kisiasa na vilevile njia za kuweza kung’oa mizizi ya fikra nzima ya kitakfiri. Vilevile amegusia namna kulivyofanyika vikao vingine mbalimbali kabla ya kongamano hilo katika nchi za Syria na Pakistan na kuwasilishwa zaidi ya makala 700 kwa sekretarieti 79

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 79

1/20/2016 11:35:51 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Ni sawa kuwa Sheikh ana fadhila zake, ijtihadi yake, udhuru wake na mema yake kwa ajili ya nchi hii (Saudi Arabia). Hili ni miongoni mwa mambo ambayo tunatarajia kuwa atalipwa kwayo, lakini ukweli kuwa Waislamu wakufurishwa ndani ya vitabu vyake uko wazi, Mungu amrehemu. Lau tukijaribu kulipinga kosa hili la kuwakufurisha Waislamu na tukakiri uwepo wake ni lipi litalotudhuru?! Mtu miongoni mwa warekibishaji amejitahidi na akakosea, basi ni kwa nini jamii ya Saudi Arabia inabeba natija ya kosa hili hatari! Na kwa nini vita hii yote kwa anayejaribu kukosoa kosa la mrekibishaji, au iwapo mwanachuoni miongoni mwa wanachuoni amechukua jukumu la kufanya rejea ya kifikra ya kweli kuihusu njia aliyoitumia?!

JAMBO LA KUMI NA TISA LIPASALO ­KUCHUNGUZWA: Kauli ya Sheikh katika Uk. 36: “Endapo atasema: ‘Shirki ni kuabudu masanamu na sisi hatuabudu masanamu.’ Sema: Nini ibada ya masanamu? Unadhani kuwa wao wanaitakidi kuwa ile miti na mawe yanaumba na kuruzuku na kuratibu mambo wanayoyaomba! Qur’ani inalikadhibisha hili.” Nasema: Kuabudu masanamu ni kusujudu kwa ajili yake na kuswali kwa ajili yake na kuomba haja kwake pamoja na kuukufuru unabii. Ama Mwislamu haswali kwa ajili ya walii wala nabii na anakiri nguzo za Uislamu na nguzo za imani na anaamini kufufuka na hesabu, pepo na moto. ya kongamano hilo. Ameongeza kuwa: Kongamano hilo liliwakutanisha pamoja maulamaa 315 wa ulimwengu wa Kiislamu na kwamba makala 144 bora zilizoandikwa kwa lugha za Kifarsi na Kiarabu, zimekusanywa na kuchapishwa katika jildi nane za vitabu.– Mhariri. 80

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 80

1/20/2016 11:35:51 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Kisha katika maneno ya Sheikh kuna ibara inayoeneza kwa namna inayostaajabisha pindi aliposema katika Uk. 37: “Shirki ni kitendo chenu mnachokifanya kwenye mawe na majengo yaliyo kwenye makaburi na mengine.” Na alisema kuwa wao “Wanaomba hayo na wanachinja kwa ajili yake na wanasema kuwa: Yanatusogeza karibu na Mwenyezi Mungu! Na kutuombea kwa baraka zake.” Mimi nina shaka ya kuwepo kwa sura hii aliyoinakili Sheikh, hii endapo itakuwepo basi ni nadra sana. Ama kuitaka baraka kutoka kwenye udongo wa makaburi ya watu wema na mfano wake hayo mpaka hii leo ni bidaa wala sio kufuru,45 sembuse kuwa shirki kubwa inayomtoa mtu nje ya Uislamu kwa kila mwenye kuwa upande huo. Bali Dhahbi na baadhi ya wanachuoni walikuwa wanajuzisha na walikuwa wanasema: ‘Kaburi la fulani ni kinga mujarabu ya madhara.’ Je wao ni makafiri? Na wangali baadhi ya watu wa kawaida wanafanya haya maeneo tofauti, lakini hii haimaanishi kwa dharura kukufuru kwa mtendaji, basi vipi itakuwa wamekufuru wote waliopo pande hizo kwa hoja ya kuwa hawakukanusha au walikuwa na shaka ya ukafiri wa mtendaji au hawakuhama kutoka nchi ya kikafiri? Hili ni jambo lingine tofauti kabisa. Bali katika nchi au eneo mpaka hii leo hakukosi kuwepo mtu mmoja mmoja miongoni mwa wanaoamimi baraka ya baadhi ya makaburi, au wanaitakidi itikadi batili au ya kufuru kuhusu wachawi na makuhani, lakini hii haimaanishi kuwakufurisha watu ambao hawayafanyi haya kwa hoja ya kuwa mwenye kuwa na shaka ya ukafiri wa kafiri basi yeye ni kafiri, hususan ni kuwa sampuli hii ya watu ndio kundi kubwa la Waislamu katika zama zote, hali ikiwa Sheikh Muhammad Mungu amrehemu, alikuwa anawakufurisha kila walio kwenye eneo hilo ambalo vipo vitendo kama hivi, kwa hoja ya kuwa asiyekanusha yeye ni kama mtendaji. 45

Dhahbi anaona hayo ni jaizi. 81

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 81

1/20/2016 11:35:51 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Na inadhihiri kutoka katika maneno ya Sheikh Muhammad kuwa yeye akijua kutokea kwa tukio huko Hijazi au Asyir au Sadir basi hukumu ya ukafiri ataieneza kwa watu wa pande hizo zote, atawakufurisha na kuwapiga vita. Yeye huona kuwa kuwepo kwa kaburi ambalo baadhi ya watu hutabaruku nalo ni kama kuwepo kwa masanamu kabisa! Kwa mujibu huu miji yao ni nyumba za shirki hata kama kwa sauti zao wanainua adhana, wanaswali na wanafunga na wanatekeleza kanuni za dini na kumtaja Mwenyezi Mungu! Haya yote kwa Sheikh hayana thamani kwa kuwa yametokea kwa washirikina! “Na tukayageukia waliyoyatenda miongoni mwa amali tutakuwa tumeyafanya vumbi lenye kupeperushwa.” (Sura al-Furqan: 22). Na kupanuka huku kifikra na kuieneza pande zisizokuwa chini ya utii wa Sheikh ni hoja ya anayeziona harakati hizi kuwa ni za kisiasa kwa daraja la kwanza, kwa kuwa haiingii akilini kwa hao kuwa Sheikh alidhania kuwa watu wa Hijazi wako kwenye kuruhusu kuchinja kwa ajili ya waliomo makaburini au kuwaomba watu wa makaburini. Hili halitokuwa ila kwa wachache. Na historia ya Hijazi na al-Haramayni ni hii, na wasifu za wanazuoni wake na watu wao mashuhuri zipo wazi, kati yao hakuna anayesema kauli hii aliyoinakili Sheikh, si kabla ya Sheikh wala si katika zama zake wala baada yake, na mwenye kuwa na shaka na historia ya Najdi hatokuwa na shaka na historia ya Hijazi. Bali ujuzi wetu kuwa aliyoyanakili Sheikh kuihusu Hijazi ilikuwa ni kinyume na ukweli wa kihistoria ambao tunzi zote zilizotungwa kuihusu Hijazi zinashuhudia. Kwa hili tunathibitisha kuwa waliyoyanakili Mawahabi kuihusu Najdi pia yako kinyume na ukweli. Na watu wa itikadi muda wote wa historia wanaifanya siri historia na kuibana kwenye baadhi ya mas’ala, na kupitia usomaji pungufu wa historia wanajenga tafsiri zao za historia, matukio, mizozo, na 82

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 82

1/20/2016 11:35:51 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

kuuana, sawa iwe katika historia ya wakati uliopita au katika historia ya zama zao, kwa hiyo watu wa itikadi kutoka kila kundi wanajikinga kwa kupotosha ukweli wa kihistoria kwa kueneza ambalo linahudumia itikadi na mawazo wanayolingania.46 Ama kutabaruku na watu wema au na udongo wa makaburi yao, hii inawezekana ikawa sana katika watu wa kawaida na kwa baadhi ya wanazuoni wafanyao taawili, na miongoni mwao ni wanazuoni wakubwa ambao tunajifaharisha na usalafi wao mfano wa Dhahbi. Lau Dhahbi angekuwa zama za Sheikh je tungeona wajibu kumuua na kumkufurisha?! Khususan kuwa yeye alikuwa anaona jaizi kutabaruku na watu wema na udongo wa makaburi yao?! Mkisema: Ndio; mtakuwa mmejiengua na uhasama wenu utakuwa na wengine sio na sisi. Na mkisema: Hapana, mtakuwa mmeafikiana na sisi kuwa jambo hili halifai kukufurisha wala kuua. Naam, yawezekana kulikosoa na kulikemea bila ya kukufurisha wala upanga. 46

Miongoni mwayo ni tafsiri yao juu ya sababu za fitna na machafuko, ambapo wameirudisha kwa mtu wa simulizi za kubuni, jina lake Abdullah bin Sabaa, wameirejesha sababu hiyo kwake licha ya kuwa kwa mujibu wa ijmai ya wanahistoria wote ukimuondoa aliyeiweka hikaya hii batili, naye ni Seifu bin Umar, mtu huyu Abdullah bin Sabaa ni wa kubuni na hakuwahi kuwepo ulimwenguni. Na tafsiri ya Mahanbali ya kuzuka kwa vikundi vya falsafa vya wanazuoni wa Kiislamu kama vile Muutazila, kuwa hilo lilitokea kwa sababu ya tarjuma za vitabu vya falsafa ya Kigiriki. Wamesema hivyo licha ya kwamba sababu hii ni batili, kwa kuwa Muutazila ilidhihiri kabla ya tarjuma, ambayo ilikuwa katika zama za Maamun. Na miongoni mwa haya ni yale yanayonakiliwa na Uwahabi kuihusu Najdi na Hjazi na nchi nyingine miongoni mwa nchi za Kiislamu, kuwa zimerudi kuwa za kijahilia, zinaabudu masanamu, na ya kwamba shirki yake imevuka kiwango cha shirki ya Makurayshi. Kwa hiyo hii hali ya kujigeuza geuza rangi kihistoria kwa watu wa itikadi huwaambia watu ambao hawaijui historia, nao huwasadiki kuwa huu ndio ukweli na huwafuata katika njia iliyobaki. Mawahabi waliokuja mwishoni wamekiri kuwa Najdi haijawahi kuwa nchi ya shirki kabla ya daawa, na wametoa wasifu wa wanazuoni wa Najdi, na wanazuoni wa Hijazi na wakahukumu kuwa Najdi na Hijazi ni nchi za Kiislamu. Na yawezekana kufanya rejea haya mwanzoni mwa kitabu cha Sheikh Bassam chenye anwani ya “Wanachuoni wa Najdi katika karne nane.” Bali anuani ya kitabu inatosha, kwani Uwahabi haukujitokeza ila chini ya karne tatu kutokea nusu ya karne ya kumi na mbili Hijriya. 83

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 83

1/20/2016 11:35:51 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

JAMBO LA ISHIRINI LIPASALO ­KUCHUNGUZWA: Kauli yake katika Uk. 39: “Wanapiga kelele kama walivyopiga kelele ndugu zao waliposema: ‘Amewafanya miungu wote kuwa ni Mungu Mmoja tu? Hakika hili kweli ni jambo la ajabu.’” Nasema: Huu – usemi - ndani yake mna ukufurishaji kwa wanohitilafiana na yeye katika rai, ambao kuwaelekezea tuhuma hii sio sahihi kabisa. Kwa kuwa hakuna Mwislamu katika sura ya ardhi asemaye kauli hii, na hakuna Mwislamu aisomaye Aya hii kutoka katika maneno ya Makafiri kisha aseme mfano wa kauli yao.

JAMBO LA ISHIRINI NA MOJA LIPASALO KUCHUNGUZWA: Na anasema katika Uk. 39: “Ukitambua kuwa hili ambalo washirikina wa zama zetu huliita ‘Itikadi’ ni shirki ambayo Qur’ani iliteremshwa kuipiga vita, na Mtume wa Mungu 5 amepigana na watu dhidi yake, jua kuwa shirki ya watu wa mwanzo ni nyepesi kuliko shirki ya watu wa zama zetu kwa mambo mawili.” Nasema: Huu ni ukufurishaji wa dhahiri wa kuwakufurisha Waislamu waliokuwa katika zama zake isipokuwa waliokuwa katika njia yake, kwa kuwa halijui neno ‘Itikadi’ wala ‘vitabu vya Itikadi’ isipokuwa wateule miogoni mwa wanazuoni na wanafunzi wa taaluma ya dini wa zama zile. Ikiwa wale Waislamu wa zama za Sheikh shirki yao ni nzito zaidi kuliko ya makafiri wa Makurayshi basi vipi itakuwa kwa Waislamu wengine?!

84

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 84

1/20/2016 11:35:51 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

JAMBO LA ISHIRINI NA MBILI LIPASALO KUCHUNGUZWA: Na anasema katika Uk. 43: “Ambao Mtume wa Mwenyezi Mungu 5 aliwapiga vita walikuwa na akili sahihi zaidi na shirki nyepesi mno kuliko hawa.” Nasema: Huu ni ukufurishaji wa dhahiri.

JAMBO LA ISHIRINI NA TATU LIPASALO ­KUCHUNGUZWA: Anasema katika Uk.43: “Jua kuwa hawa wanayo hoja tata wanayoielekeza kwenye tuliyoyataja, nayo ni miongoni mwa hoja zao kubwa mno, basi hebu sikiliza jawabu lake kwa masikio yako, nalo ni kuwa wao wanasema: ‘Ambao Qur’ani ilishuka kwa ajili yao walikuwa hawasemi shahada: Hapana Mungu ila Allah. Walikuwa wanamkadhibisha Rasuli na kukanusha ufufuo, na walikuwa wanaikanusha Qur’ani na kuifanya kuwa ni uchawi. Na sisi tunashuhudia kwamba hapana Mungu ila Allah, na kwamba hakika Muhammadi ni Mtume Wake. Tunaisadiki Qur’ani na tunaamini ufufuo, tunaswali na tunafunga, basi vipi unatufanya sisi mfano wa hao?!’” Na Sheikh anaijibu hoja hii anasema: “Jibu ni: Wanachuoni wote hawahitilafiani kuwa mtu endapo atamsadiki Mjumbe wa Mwenyezi Mungu 5 katika jambo moja na akamkadhibisha katika jambo jingine, huyu mtu ni kafiri! Hajaingia katika Uislamu, hivyo endapo ataamini baadhi ya Qur’ani na kuikanusha baadhi yake! Ni kama aliyekiri tawhidi na akakanusha kuwa swala sio wajibu.” Kisha Sheikh alitaja vipengele kadhaa vya aina hii, aliendelea akisema: “Kwa kuwa Mwenyezi Mungu amesema waziwazi katika 85

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 85

1/20/2016 11:35:51 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Kitabu Chake kuwa mwenye kuamini baadhi ya kitabu na kuikufuru baadhi yake nyingine yeye ni kafiri wa kweli, na kuwa anastahiki yaliyotajwa, hivyo basi hoja hii imetoweka.” Nasema: Maneno ya Sheikh hapa ni ya ajabu na si ya kawaida kabisa! Kwa kuwa kuna tofauti kubwa kati ya anayekanusha kitu makusudi miongoni mwa aliyoleta Mtume, yule mwenye kukebehi na kukikanusha pamoja na itikadi yake kuwa Nabii alisema kitu hicho. Na ambaye ameacha baadhi ya aliyoyaleta Mtume 5 kwa taawili au kwa kutojua hili au amedhania kuwa limesitishwa kisharia au ilikuwa mahsusi kwa tukio au wakati, au limefungamana na kadhia maalum tu. Jambo la pili ni kwamba: Hao hawakukataa kitu kilichojulikana ndani ya dini kwa namna ya dharura kama mifano ambayo Sheikh ameitoa, mfano wa kuacha swala au kuacha kutoa Zaka au Hija au kuamini baadhi ya Qur’ani na kukufuru baadhi yake..... mpaka mwisho. Jambo la tatu ni kwamba: Lau Sheikh angefanya rejea vitabu vinavyohoji mas’ala za hitilafu za wanazuoni na huenda kilicho mashuhuri mno miongoni mwavyo ni kitabu Rafuul-Malaam cha Ibn Taymiya Mungu amrehemu, angeutambua udhuru wa walio tofauti na yeye, huenda kwao jambo fulani au katazo fulani halikuthibiti. Kulingana na hali hiyo sio jaizi kwake aseme: ‘Wao wanakanusha aliyoyaleta Rasuli 5’! Kwa kuwa wao wamefanya taawili sio wakanushaji. Ikumbukwe kuwa kuna tofauti kubwa kati ya ukanushaji uliojengeka kwa kejeli, na taawili inayotokana na dalili na hoja tata, au kuacha kwao amali kwa dalili waionayo kuwa ina udhaifu. Kwa hali hii haimaanishi kuwa wao wameamini baadhi ya kitabu na kukufuru baadhi yake nyingine! Au wameamini baadhi ya aliyoleta Mtume 5 na kuyakataa baadhi. 86

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 86

1/20/2016 11:35:51 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Na pia Sheikh hazingatii hali ya kutojua kitu kuwa inazuia kuvurumisha ukafiri kwa asiyejua. Ama kulingana na utaratibu wa Sheikh yawezekana kwa wanazuoni wanaohitilafiana wakufurishane kwa madai ya kila mmoja wao kuwa mwenzake amekataa kitu miongoni mwa aliyokuja nayo Mtume 5! Na kwa hili anakuwa kama aliyemkadhibisha Mtume 5 kwa jumla.! Na kadhalika..... Hali ikiwa usahihi sio hivyo. Upande wa pili haukubali kuwa eti yeye anakanusha kitu miongoni mwa aliyokuja nayo Mtume 5, bali atakwambia: Hili kwangu halijathibiti. Au atakwambia: Maana yake ni hivi au inapingwa na hili.47 Kisha kanuni yake inafaa kutumika na kila kundi miongoni mwa makundi ya Kiislamu, na huenda wanaohitilafiana nawe wakakupinga kwa jibu wakisema: Hao makafiri wa mwanzo ni ninyi wala si wengine, ninyi mnakufuru baadhi ya kitabu, kama vile: Kutokuheshimu kwenu damu ya Mwislamu na kuwa asikufurishwe, hivyo ninyi kwa hayo mnakubali baadhi ya kitabu na mnaikufuru baadhi nyingine!! Na wanatoa dalili juu ya hili kwa ukweli wakisema: Huu ukufurishaji na mauaji yatokanayo na kauli zenu tungali tunashuhudia athari zake katika siku hizi katika miji na katika nchi nyingi za Kiarabu.

JAMBO LA ISHIRINI NA NNE LIPASALO ­KUCHUNGUZWA: Kauli yake katika Uk. 48, na amekariri mfano wa hayo katika Uk. 57: “Hao Maswahaba wa Rasulillahi 5 waliwapiga vita Bani Han47

Kama msimamao mkali wa Ibn Abi Dhiibi dhidi ya Imamu Maliki alipoikanusha Hadithi ya ‘Wenyekuuziana kwa hiari.’ Ibn Abi Dhiibi amesema: ‘Aombwe (Maliki) kufanya toba waila shingo yake ikatwe?!’ Kwa hoja kuwa ameipinga Hadithi au ameacha kitu miongoni mwa aliyoleta Rasuli 5. Na huu ni upeo finyu mno wa Ibn Abi Dhiibi Mungu amrehemu, kwa kuwa Imamu Maliki hakuiacha Hadithi ila kwa sababu ya dosari aionayo au kwa kuwa umesitishwa, au mfano wake. Mungu awarehemu wawili wote. 87

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 87

1/20/2016 11:35:51 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

ifa hali walikuwa wamesilimu wakiwa pamoja na Nabii na wakiwa wanashuhudia kwamba hapana Mungu ila Allah, na kwamba hakika Muhammadi ni Mtume Wake. Walikuwa wanaswali na wanatoa adhana. Endapo watasema: ‘Hakika wao wanasema kuwa Musaylama ni nabii.’ Tutasema: Hili ndilo litakiwalo, ikiwa aliyemtukuza mtu mpaka daraja ya unabii 5 alichukuliwa kuwa amekufuru na mali yake na damu yake vikawa halali, na shahada mbili hazikumnufaisha wala Swala, basi vipi mwenye kumtukuza Shamsu au Yusuph au swahaba au Nabii na kumfikisha daraja ya Bwana wa mbingu na ardhi asiwe amekufuru...” Nasema: Maneno haya yana walakini nyingi za ajabu: Ya kwanza: Banu Haniifa waliritadi na waliachana na Uislamu kabisa na walimwamini mtu waliyemdhania kuwa ni nabii na waliacha amri za Nabii 5 kwa ajili ya amri zake makusudi. Na hao wanatofautiana na watu ambao hawawapendi watu wema ila ni kwa sababu tu ya hao wema wanampenda Nabii 5, au wanadhania hivyo, wala hawamtukuzi yeyote miongoni mwa watu wema zaidi ya daraja ya Nabii, wala hawamfikishi kwenye hili sembuse kumfanya mmoja katika watu wema kuwa katika daraja ya Allah Mtukufu, hili hawajalisema hao watu kabisa wala hajapata kulisema Mwislamu mwenye akili48 muda wote wa historia. Na Sheikh anaandamanisha pamoja vitu visivyoandamana pamoja, na kulingana na utaratibu wake huu yawezekana kumkufurisha anayetafuta kwa fulani riziki yake au anayeapa kwa jina la Nabii 5 au anayeapa kwa Ka’aba, au anayefurutu ada juu ya mmoja miongoni mwa watu wema au watu wengine. Naam, hili bila shaka ni kosa. Bali yawezekana kwa utaratibu huu tuwakufurishe wanaofurutu ada kumhusu Sheikh, ambao hawamkosoi na wala hawakubali kumkosoa; ambao wanatoa hoja kuwa yeye ni mjuzi mno 48

Kujiepusha na baadhi ya wafurutu ada wa Kishia na baadhi ya wafurutu ada wa Kisufi. 88

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 88

1/20/2016 11:35:51 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

wa sharia na huenda wakaipinga Hadithi sahihi au Aya tukufu kwa kumsalimisha yeye. Kwa mujibu huu uje useme: Hao wametukuza cheo cha Sheikh Muhammad na kukifikisha kwenye daraja ya unabii au uungu, kwa hiyo wao ni makafiri washirikina...mpaka mwisho. Huu ni utaratibu usio sahihi na mas’ala za kielimu hazichukuliwi kwa njia hii ya kiuhasama, bali zina njia zake zilizo maarufu kwa wenye insafu miongoni mwa watu wenye akili Waislamu na makafiri.

JAMBO LA ISHIRINI NA TANO LIPASALO KUCHUNGUZWA: Anasema katika Uk. 49, na amekariri mfano wa usemi huu katika Uk. 58: “Na pia husemwa, wale ambao Ali bin Abu Talibi aliwachoma moto wote walikuwa wanadai Uislamu, nao walikuwa ni miongoni mwa Maswahaba wa Ali K, walijifundisha elimu kutoka kwa maswahaba lakini walikuwa na imani kumhusu Ali K mfano wa itikadi iliyokuwepo kumhusu Yusuph na Shamsani na walio mfano wa wawili hao, basi vipi Maswahaba waliafikiana kuwa ni makafiri na wakawaua?!” Nasema: Wale ambao Ali K aliwachoma moto – endapo itasihi kweli kuwa aliwachoma moto49 - wao ni wale walioritadi am49

Kisa cha kuchomwa moto walio hai ni Ikrima tu huria wa Ibn Abbasi peke yake ndiye aliyekisimulia, na yeye hakushuhudia tukio la kisa hiki, bali alisema kuwa habari hii ilimfikia bwana wake Ibn Abbasi, hapo akasema - yaani Ibn Abbasi: “Lau ningekuwa mimi ningewaua kwa kuwa Nabii 5 alisema: ‘Mwenye kuibadili dini yake muuweni.’” Na Hadithi hii katika Bukhari imekuja kwa njia mbili kutoka kwa Ikrima wala Muslimu hakuiandika. Na Ikrima ameielazea kwa njia ya habari zilizomfikia wala hakuwa katika mji wa Kufa mahali pa tukio, bali yeye alikuwa Basra akiwa na bwana aliyekuwa anammiliki - Ibn Abbasi -. Na huenda habari iliwafika ikiwa na kasoro. Ama riwaya za walioshuhudia kwa macho zimetaja kuwa kaumu ya hao watu ilikuwa imeritadi na kwamba Ali aliwaua wala hakuwachoma moto, kisha baada ya kuwaua 89

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 89

1/20/2016 11:35:51 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

bao hawadai Uislamu kama Sheikh alivyosema, na halijathibiti lililo mashuhuri katika vitabu vya historia, kuwa wao walikuwa wanamfanya Ali ni Mungu, bali lililo sahihi katika Sahihi Bukhari ni kuwa walikuwa wameritadi au ni wazandiki. Haya matamko mawili yamekuja katika Bukhari, na endapo itakuwa sahihi riwaya iliyomo humo kuwa wao walikuwa na itikadi ya uungu wa Ali, basi hoja hii ni adhimu mno dhidi ya Sheikh, kwa sababu wao kwa mujibu huu hawadai Uislamu kama alivyosema Sheikh, kwa kuwa Waislamu hawasemi Ali ni Mungu, lakini wao hao wamemfanya Ali ni Mungu, na hii ni kufuru kwa ijmai ya Waislamu na kwa maandiko ya kisheria. alifanya mitaro kwa ajili yao na aliwatumbukiza humo na kuwafukisha kwa moshi kuzidisha mbinyo wa matwezo na kuhofisha matendo yao, kwa kuwa kabla ya kuwaua wao waliendelea kupokea posho iliyokuwa inatolewa kwa Waislamu kwa muda kadhaa japo walikuwa wameritadi. Hivyo basi huenda tendo hili la kuwafukishia moshi ndilo ambalo liliwachanganya baadhi ya walioshuhudia kuwa aliwachoma moto, vinginevyo Imamu Ali K mwenyewe ni miongoni mwa wenye hima sana ya kujilinda asiwaadhibu kwa moto, hususan yeye ni miongoni mwa marawi wa Hadithi “Haadhibu kwa moto isipokuwa Bwana wa moto.” Na haijakuja habari sahihi kuwa kuna swahaba aliwachoma moto watu wakiwa hai ila iliyomhusu Abubakri as-Swidiiq Mungu amuwiye radhi, alipomchoma moto murtadi al-Fujaat as-Salmiy. Yajulikana kuwa Sheikh Muhammad anadhania kuwa huyu al-Fujaat as-Salmiy alikuwa anatekeleza nguzo za Uislamu!! – na al-Fujaat as-Salmiy alitenda mabaya wakati aliporitadi. Na Khalid bin al-Walid aliwachoma moto walioritadi, lakini Khalid Mungu amuwiye radhi si katika maswahaba wenye uswahaba wa kisheria, yeye ni swahaba wa mambo mengi ya kukiuka utaratibu ambao baadhi yake Mtume 5 alijiepusha nao katika maisha yake kama katika kisa cha Bani Judhayma. Wala Khalid hahesabiki miongoni mwa mujtahid, bali yeye ni mtu wa upanga na ngao si mwanachuoni wala si mwanaelimu, Mungu amuwiye radhi na amsamehe. Na nimeeleza kwa upana katika kuzieleza njia za Hadithi na riwaya za kuchoma moto katika juzuu ya kwanza ya kitabu an-Naqdhu al-Kabir, kitabu ambacho ni jibu la kukikosoa kitabu Minhaju-Sunnah cha Ibn Taymiya Mungu amrehemu. Na nimwahidi msomaji kuwa utakuwa ukosoaji mkubwa kama jina lake lilivyo, wenye mkusanyiko wa kuburudisha, pamoja na uwastani na insafu inshaallah. Na mimi nina matumaini kuwa wakati ujao ni wa uwazi na uchambuzi wa utambuzi ambao ndani yake kuna insafu kwa wanaojibiwa na kukosolewa. Na ndani yake mna kuwaondolea dhulma waliodhulumiwa ambao wamedhulumiwa na vitabu vya theolojia vyenye ufurutu ada vilivyo na mchanganyiko na rai za Kikhawariji na Kinawasibu. 90

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 90

1/20/2016 11:35:51 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Kisha tunamuona Sheikh amechagua kuwa “Wao wamekuwa na itikadi kumhusu Ali kama itikadi za watu kumhusu Shamsani.” Na hili halijatokea kabisa kwa maana ya kwamba haijakuja katika riwaya za wale ambao inasemekana kuwa Imamu Ali aliwachoma moto, kuwa wao wanafurutu ada kumhusu yeye tu, ufurutu ada ule unaoambatana na kukiri nguzo za Uislamu!! Kwani wao waliuacha Uislamu wote. Je hivi Sheikh anataka kutubabaisha kuwa wale ambao Imamu Ali aliwaua ni kama hawa masufi na wanazuoni miongoni mwa Mahanbali na wengineo ambao wanachanganya katika ibada zao na aina fulani ya ufurutu ada juu ya watu wema kwa kuwafanya wasila na yaliyo mfano wa hayo.?!

JAMBO LA ISHIRINI NA SITA LIPASALO ­KUCHUNGUZWA: Pia kauli yake katika Uk. 50 kuhusu Fatmiyina, ambao ni wana wa Abaydul-Qadahi ambao waliitawala Morocco na Misri katika zama za Bani Abbasi: “Walipodhihirisha kwenda kinyume na sharia katika vitu ambavyo ni kinyume na tulivyonavyo sisi, wanazuoni waliafikiana juu ya ukafiri wao na kuwapiga vita na kuihesabu nchi yao kuwa ni nchi ya vita, na Waislamu waliwashambulia mpaka wakazikomboa nchi za Waislamu zilizokuwa mkononi mwao.” Nasema: Na hili pia sio sahihi, kwani vita kati ya Ayubiyina na Fatmiyina ilikuwa ni ya kisiasa kabisa haikuwa na maingiliano yoyote na dini. Na katika siku hizo bidaa ilikuwa imeenea kila mahali katika dola ya Ayubiyina, na Fatmiyina na katika dola ya Bani Abbasi huko Iraq. Hali ya mambo katika ulimwengu wa Kiislamu siku hizo ilikuwa inashabihiyana na hali ya mambo katika ulimwengu wa Kiislamu zama za Sheikh kabisa! 91

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 91

1/20/2016 11:35:51 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Na Swalahudini alikuja kuwaunga mkono Fatmiyina wakiwemo watu wa Zanki, kisha aliteka mji. Na ilikuwa hapana budi Fatmiyina na Ayubiyina waitumikishe dini kama silaha katika vita kama wafanyavyo watawala wa Kiarabu hii leo, kwa hiyo suala sio geni, ni lazima kila dola idhihirishe kuwa vita yake dhidi ya wengine ni ya kidini na sio ya kisiasa, ili alifanye kundi kubwa la watu wa kawaida kuwa jeshi. Na dini imeanza kutumiwa kisiasa tokea siku za dola ya Bani Umayya, tokea zama za Muawiya, kama itakadiriwa mpaka wa toka lini?! Ama kuhusu Fatmiyina au Abidiyun - kwangu jina si muhimu – hawakukosa watetezi na wasambazaji wa mema yao, bali hata yule anayechukuliwa kuwa kiongozi mbaya zaidi kati ya viongozi wa Fatmiyina, ambaye alituhumiwa kwa uzandiki na ukafiri, pamoja na hayo hata naye baadhi ya ulamaa na wanahistoria wamemtetea.

JAMBO LA ISHIRINI NA SABA LIPASALO ­KUCHUNGUZWA: Kauli yake katika Uk. 51 kuhusu mlango wa hukumu ya murtadi, kwamba vitabuni mwa wanazuoni wametaja aina nyingi za murtadi: “Kila aina miongoni mwazo inakufurisha na kuhalalisha damu ya mtu na mali yake, mpaka wao wametaja vitu vidogo iwapo mtu atavifanya (atakuwa ameritadi), mfano wa neno asemalo kwa ulimi wake na halipo moyoni mwake au analisema kwa mzaha.” Nasema: Sio kila walilosema hao ni sahihi, hili ni jambo, kwa kweli wametaja vitu vingi, baadhi yake ni kuritadi kulingana na ijmai, na baadhi yake kuna kutoafikiana, na baadhi yake sio kuritadi kwa mujibu wa walio wengi, na hawakuafikiana katika kutaja mas’ala hizo, kama ambavyo mas’ala walizozisema zinahitilafiana kulingana na mas’ala ilivyo, na kulingana na msemaji, kama vile 92

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 92

1/20/2016 11:35:51 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

hali ya kutojua au taawili au kushurutishwa au kudharurika..... mpaka mwisho. Jambo la pili: Ulamaa katika zama za Sheikh walikuwa wanajua milango ya Fiqhi ambayo inazungumzia hukumu za mwenye kuritadi, na walikuwa wakiisoma na kuifundisha huko Makka na Madina na Hijaz, huko Ushayqar, Shaqrau na Riyadh, huko Sham, Yemen, Misri na Iraq, lakini hata hivyo hawakutoa fatwa za kuhalalisha mauwaji ya halaiki na umwagaji damu kiholela na uteketezaji mali za watu, fatwa anazozitoa Sheikh hapa. Bali ilikuwa hukumu inamhusu mtu binafsi yeye peke yake baada ya hoja na dalili kuthibiti. Jambo la tatu: Wanazuoni pindi watoapo hoja dhidi ya Sheikh kwa dalili ya kitu fulani miongoni mwa viliyosemwa na wanazuoni vitabuni mwao, yeye huharakia kuwatuhumu kuwa wanawafanya hao - wanazuoni - kuwa ni miungu kinyume na Mungu mmoja, na kuwa hiyo ndio shirki wenyewe!! Ama Sheikh ahitajiapo vitabu hivyo hunukuu kutoka humo alionalo kuwa ni ushahidi wa kauli yake, na endapo mwingine aliye khilafu na yeye atanukuu hoja kutoka humo Sheikh atamshitukiza na kauli yake kuwa hiyo ni shirki yenyewe kama ilivyotangulia na kama ifuatavyo, na kwamba wao wamewafanya wanazuoni hao kuwa ni miungu kinyume na Mungu mmoja. Kisha hatosheki kumhukumu amuonaye anatenda alionalo kuwa linakufurisha, bali akijua hali kadhaa zipo sehemu fulani, atalazimisha watu wa sehemu ile wote kuwa wameritadi na damu zao na mali zao kuzihalalisha, kwa hoja ya kuwa eneo lile kuna walionyamaza na walioritadi! Kwa hiyo mtendaji ameritadi na aliyenyamaza pia ameritadi! Na hii yahitilafiana kabisa na waliyosema wanazuoni chini ya mlango wa hukumu ya aliyeritadi, kwa kuwa wao hawawahukumu watu wote kwa tendo la baadhi, na wala hawaendi mbali ka93

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 93

1/20/2016 11:35:51 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

tika hukumu ya kuritadi kama afanyavyo Sheikh. Wala hawasemi kuwa huku ni kuritadi ila katika mambo yaliyo wazi aghlabu, wala hawazigawi nchi za Kiislamu kwenye mgao wa nchi za Kiislamu na za Kishirikina, naam baadhi ya wanazuoni wana ufurutu ada, wala makosa hayaachi kuwa katika kila mlango. Lakini hivi vitabu vya fiqhi ndani yake kuna msimamo wa wastani zaidi kuliko maeneo ya kuteleza, kinyume na vitabu vya itikadi, ni wajibu vifanyiwe rejea vitabu vyote vya kiitikadi, kifiqhi, na vya Hadithi, na tendo la kufanya rejea liendelee na mchujo ufanyike kukosoa na kuona kuwa hili ni sahihi, kwani elimu haisimami kwenye daraja maalum. Hivyo basi hukumu juu ya kauli au kitendo kuwa ni kuritadi haimaanishi kuwa ni hukumu juu ya mwenye kitendo, kwa kuwepo uwezekano wa kutendeka katika hali ya kutojua au kwa taawili. Basi itakuwaje kuwahukumu watu wa eneo lote sembuse sehemu kubwa ya ulimwengu wa Kiislamu kwa tendo la huyu na yule ambao hawajui au wamefanya taawili.

JAMBO LA ISHIRINI NA NANE LIPASALO KUCHUNGUZWA: Kisha Sheikh anasema katika Uk. 51 na 52: “Ambao Mwenyezi Mungu amesema kuwahusu: ‘Wanamuapa Mungu kuwa hawakusema, wamesema neno la kufuru na wamekufuru baada ya Uislamu wao.’ Je haujasikia Mwenyezi Mungu amewakufurisha kwa neno pamoja na kuwa kwao katika zama za Mjumbe wa Mwenyezi Mungu 5 na wanapigana jihadi pamoja naye na wanaswali na wanatoa Zaka, wanahiji na wanampwekesha Mwenyezi Mungu.” Nasema: Kwanza hao ni wanafiki. 94

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 94

1/20/2016 11:35:51 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Pili: Nabii 5 hakuhalalisha damu zao wala mali zao wala hakuwaua, bali alikataza hilo. Hili linatofautiana na tendo la Sheikh kwa aliowahukumu kuwa wameritadi miongoni mwa Waislamu si miogoni mwa wanafiki.

JAMBO LA ISHIRINI NA TISA LIPASALO ­KUCHUNGUZWA: Pia kauli yake katika Uk. 52: “Na kadhalika ambao Mwenyezi Mungu amesema kuwahusu ‘Sema: Ni Mwenyezi Mungu na Aya Zake na Mjumbe Wake mliokuwa mnawafanyia kejeli.’” Sheikh anasema:- “Hao ni wale ambao Mwenyezi Mungu amesema wazi kuwa wamekufuru baada ya imani yao hali wakiwa na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu 5 katika shambulio la Tabuku, walisema neno ambalo wao walisema kuwa wao walilisema hilo kwa njia ya mzaha! Basi zingatia hoja hii, nayo ni ule usemi wao: Mnawakufurisha Waislamu, watu wanaoshuhudia kwamba hapana Mungu isipokuwa Allah, wanaswali na wanafunga. Kisha zingatia jibu lake kwa kuwa ni miongoni mwa yenye manufaa zaidi yaliyomo katika nyaraka hizi.” Nasema: Kwanza: Wao walidai kuwa walilisema kwa njia ya mzaha: ‘Tulikuwa tukiingia kucheza tu’, lakini ukweli sio hivyo, hakika wao walikuwa wanamfanyia kejeli Mwenyezi Mungu, Malaika Wake, Vitabu Vyake na Mitume Wake kama ilivyokuja katika vyanzo vya kweli kabisa vya kihistoria, na miongoni mwa Mitume ni Nabii wetu Muhammad 5, na hata kama kejeli yao ikiishia kwa Nabii tu, bado kumfanyia kejeli yeye 5 ni kuifanyia kejeli sharia yenyewe na huu ni ukafiri na ni kuritadi. Pili: Kwa nini Sheikh hapa anawasadiki?! Kwa nini anawasadiki walipodhania kuwa wao walifanya hivyo kwa njia ya mzaha?! 95

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 95

1/20/2016 11:35:51 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Subhanallah, Mwenyezi Mungu anawakadhibisha katika Kitabu Chake kitukufu na anawaita wamfanyiao kejeli Mwenyezi Mungu, Aya Zake na Mitume Wake. Na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu 5 anawakadhibisha kwa hilo, wala haukubali udhuru wao; kwa kuwa habari kutoka kwa Mwenyezi Mungu zimemjia kuwa wao ni waongo katika udhuru wao wa madai yao kuwa walikuwa wanafanya mzaha na kucheza. Kisha anakuja Sheikh, Mungu amrehemu, anakubaliana na kauli yao ambayo Mwenyezi Mungu na Mtume Wake wamewakadhibisha nayo, na Sheikh anakiri kuwa wao wameisema kwa njia ya mzaha! Na kwa hii ametoa dalili kuwa: Kejeli kwa mzaha inamkufurisha mtendaji wake! Hivyo kauli yao imekuwa ya kusadikiwa kwa mtazamo wa Sheikh na maneno ya Mwenyezi Mungu na Mjumbe Wake katika kuwakadhibisha sio ya kuzingatiwa, basi angalia jinsi uwongo wa wanafiki ambavyo umekuwa hoja ya kuwakufurisha Waislamu!

JAMBO LA THELATHINI LIPASALO ­KUCHUNGUZWA : Kauli yake katika Uk. 53: “Na kauli ya watu miongoni mwa Maswahaba: ‘Tuwekee nasi mkunuzi.’” Nasema: Hao waliosema hilo si miongoni mwa Maswahaba wa uswahaba mahsusi wa kisharia; bali wao ni huria ambao Masalafi wanawatetea, walisema hilo siku ya Hunayni na walikuwa wachanga katika Uislamu wakiwa karibu na zama za ukafiri. Kisha katika kisa hiki kuna dalili kuwa jamii yeyote haikosi kuwa na watu wenye itikadi batili. Hii ni jamii ya Nabii 5 na ina anayeitakidi kama hili, kama vile huria, kwani hii aya inalingania kuwa na huruma na watu na kuwaongoza, Nabii 5 hakuwakufurisha kwa sababu ya kutojua kwao. 96

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 96

1/20/2016 11:35:51 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

JAMBO LA THELATHINI NA MOJA ­LIPASALO KUCHUNGUZWA: Kauli ya Sheikh katika Uk. 63: “Hatukatai kumuomba msaada kiumbe katika jambo analoweza kama ambavyo Mungu alivyosema katika kisa cha Musa: ‘Alimuomba msaada yule ambaye yu katika wafuasi wake dhidi ya adui yake.’ (al-Qasas: 15). Na kama vile mtu huomba msaada kwa wenzake vitani au mahali pengine katika vitu ambavyo kiumbe ana uwezo navyo, na sisi tumekataa uombaji msaada wa ibada wazifanyazo kwenye makaburi ya mawalii au katika hali yao ya ghaibu katika vitu ambavyo haviwezi ila Mwenyezi Mungu. Endapo litathibiti hilo, hivyo basi kutaka kwao uombezi kwa Manabii siku ya Kiyama wa kumtaka wamuombe Mungu, hili ni jaizi duniani na akhera. Na hivyo itakubidi uje kwa mtu mwema akae na wewe na umsikilize, maneno yako utamwambia: ‘Niombee Mungu’, kama walivyokuwa wakifanya Maswahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu 5 wakimuomba hivyo maishani mwake, ama baada ya umauti wake hapana, sivyo...” Nasema: Nini rai yako kwa atakayefanya t’awili kuwa kuomba msaada kwa Nabii 5 kwenye kaburi lake ni ruhusa kwa kuwa Nabii yuko hai kaburini mwake?! Hapana shaka mwenye kuwa na rai hii anao upande wa taawili bali katika hilo anayo Hadithi ya Uthman bin Haniif. Pia huenda akaja mwingine na kumwambia Sheikh: Kwa nini unaruhusu hili mtu aende kwa mtu mwema na amtake amuombee Mungu? Kwa nini humpi amri amuombe Mungu moja kwa moja? Je katika nasaha zako kwake ni kujuzisha kushabihiana na matendo ya makafiri katika kuwafanya hao njia kati yao na Mungu? Mungu hajasema: Mimi niko karibu najibu ombi la muombaji aniombapo?

97

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 97

1/20/2016 11:35:51 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Ni kama hivyo yawezekana kwa mwingine miongoni mwa mahasimu au wafuasi wafurutu ada kumbana Sheikh na akose maeneo ya kutokea mpaka amhukumu kuwa ni kafiri kama vile yeye alivyowabana wengine mpaka amewakufurisha. Naam, mwingine anaweza kumgeuzia kibao Sheikh katika mengi miongogni mwa maneno yake, miongoni mwayo ni kauli iliyotangulia ambayo kwayo yeye amewabana wengine, anaweza kumwambia: Nabii 5 ana mambo mahsusi, kwa kweli Mwenyezi Mungu aliwaamuru wanafiki wamwendee ili awaombee maghufira; kwa kuwa kwenda kwao kwake ni dalili dhahiri ya kutubia. Je ni kwa dalili gani wewe unamwingiza mtu mwema katika hivi vitu mahsusi vya kinabii, na unajuzisha mtu amjie na amtake amuombee?! Je hili Mwenyezi Mungu amelifanya sheria katika Kitabu Chake? Au Mjumbe Wake amelisema? Au limekuja na mmoja miongoni mwa maswahaba wake? Au limefanywa na watangulizi wema! Na hili lau lingekuwa sheria lingenukuliwa kwetu kwa kuwa ni miongoni mwa ambayo sababu za kulifanyia nukuu zipo?! Kisha ni kwa nini umeuwekea mabano ya mtu mwema uombaji wa dua? ‘Itakubidi uje kwa mtu mwema akae na wewe na umsikilize maneno yako...’ Nini tofauti kati ya hili na anayemwelekeza mtu kwenda kwa fulani amuombee?! Na matokeo hapa ni kwamba kwa mujibu wa utaratibu wa Sheikh ni kwamba anaweza mpinzani wake mkorofi kumgeuzia yeye Sheikh ukafiri, na ikiwa atatoa nyudhuru itakuwa ni jaizi kwa huyo mwingine naye kutoa nyudhuru mfano wa hizo. Sisi katika haya yote tunahimiza kuwa na ikhlaswi katika ibada ya Mungu na kuachana na mambo tata yatiayo aibu, kama tunavyotoa wito kuacha kufurutu ada katika kukufurisha.

98

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 98

1/20/2016 11:35:51 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

JAMBO LA THELATHINI NA MBILI ­LIPASALO KUCHUNGUZWA: Kisha Sheikh amehitimisha katika Uk. 66 kwa mas’ala kuu, nayo ni kuwa: “Tawhidi hapana budi iwe kwa moyo na ulimi na kutenda, endapo kitu katika hayo kikiingia dosari mtu hatokuwa Mwislamu..!!” Nasema: Na hili ndani yake muna utaratibu wa kuwakufurisha Waislamu wengine miongoni mwa wasiojua ukweli wa mambo yalivyo – na ya lazima aliyo yasema Sheikh, na - kwa utaratibu huu wafuasi wa Sheikh wanaweza kuwapima watu itikadi zao, matendo yao kwenye kila mji wanaoingia au wanao andikiana nao wakiwakuta na kujihifadhi au kosa watahalalisha kuwaua kwa kuwa wao (si Waislamu)!! Bali kwa kweli Sheikh hapa amejumuisha utiaji dosari katika amali na kuuhesabu kuwa ni miongoni mwa alama za ukafiri! Na kwa mujibu huo yawezekana kwa urahisi kumkufurisha Mwislamu kwa kufanya maasi?! Kwa hili na kwa yaliyo mfano wake mahasimu wake wamemtuhumu kuwa yeye ni miongoni mwa Makhawariji wanaomkufurisha Mwislamu kwa kutenda maasi. Na maudhui ya kutia dosari yana hitilafu kulingana na tofauti za maasi, lakini dosari ya moyoni haina athari katika hukumu za kidunia. Mjumbe wa Mwenyezi Mungu 5 alikuwa anawahesabu wanafiki kuwa ni Waislamu katika hali ya dhahiri pamoja na dosari za nyoyo zao, dosari ambazo tumezijua kwa maelezo ya Mwenyezi Mungu. Ama Sheikh hatosheki Mwislamu kudhihirisha Uislamu na kutamka kwake shahada mbili wala hatosheki na Swala wala Swaumu wala Zaka wala Hija, na amesema wazi kuwa yeye anawaua watu wanaoswali, wanaofunga, wanaokweda Hija, wanaotoa Zaka na wanaotamka shahada mbili! 99

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 99

1/20/2016 11:35:51 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Kisha utiaji dosari katika amali ni nini hasa? Je mtu kutenda moja kati ya dhambi kubwa kama kunywa pombe, kuiba na mengine ni miongoni mwa utiaji dosari katika amali? Je mwenye kutenda dhambi hiyo huwa ametoka nje ya Uislamu na si Mwislamu tena kwa mujibu wa dhahiri ya maneno ya Sheikh? Basi ni kwa nini tunawakanusha Makhawariji wanapowakufurisha watendao maasi? Na kwa nini tunawakanusha Muutazila na Zaydiya kwa kauli yao kuwa watendao dhambi kubwa watabaki milele motoni?! Na kwa nini tunawakanusha watu wengine wanapotutuhumu kuwa tunakwenda mbali sana katika kukufurisha na kuweka kaida kwa ajili hiyo?!

JAMBO LA THELATHINI NA TATU LIPASALO KUCHUNGUZWA: Sheikh amesema katika Uk. 70: “Hakumuengua mbali na ukafiri isipokuwa mwenye kulazimishwa.” Nasema: Ufupisho huu una angalizo, kwa kuwa mwenye kudharurika, mwoga, mwenye kufanya taawili, hawa haifai kuwakufurisha. Na hii yajulisha kwamba Sheikh hategemei sana mas’ala ya majina na hukumu, hivyo amepuuza vizuizi vyenye kujitokeza mno vinavyozuia kukufurisha, kama taawili na ujinga. Ama hoja yake kuwa Mwenyezi Mungu hakumuengua isipokuwa mlazimishwa katika kauli Yake “isipokuwa mwenye kulazimishwa” (Sura anNahlu:106 ), katika Aya hii ndio, ama katika Aya nyingine na katika Hadithi sahihi, huko kuna wenye udhuru wengine sio yule aliyelazimishwa tu.50 50

Nimetaja vizuizi hivi na dalili zake kwa mapana katika kitabu at-Takfiiru Wat-Tafjiiru Asbabu Wahlul, nacho ni kitabu ambacho kimetangulia kusambazwa katika insha tatu ndefu kwa anuani: Risala kwa ndugu yangu Abdul-Aziz al’-Mu’athamu, iliyotolewa katika gazeti la ar-Riyadh mwishoni wa mwaka 1416 A.H. Lakini kitabu hiki hakijachapishwa mpaka sasa. 100

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 100

1/20/2016 11:35:52 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Na hizi ni miongoni mwa aibu za utaratibu wa Sheikh. Yeye huitegemea Aya moja au Hadithi moja na kuziacha nyingine, hii ni dosari ya kitaaluma. Huenda akaja mwingine na kusema: Mwenyezi Mungu hakuharamisha isipokuwa haramu nne tu katika kauli Yake tukufu: ‘Alichoharamisha kwenu ni nyamafu, damu, nyama ya nguruwe na aliyechinjwa kwa njia isiyo ya Mwenyezi Mungu.’ (Sura al-Baqarah:172). Aseme: Kwa mujibu huu hakuna vitu vingine vilivyoharamishwa kama pombe, wizi, zinaa na vingine!! Huenda akasema hivyo na akasahau kuwa Mwenyezi Mungu ameharamisha pombe wizi na zinaa na vingine katika nasu nyingine na kwamba Aya iliyotangulia ni makhsusi kwa vyakula. Mambo yapasayo kuchunguzwa yaliyo dhahiri mno katika kitabu Kashfushubuhati yamekwisha, nayo ni mambo muhimu yapasayo kuchunguzwa - baadhi yako wazi zaidi kuliko baadhi – katika insha ndogo mashuhuri, nayo ni miongoni mwa maandishi yenye nguvu zaidi kati ya yale aliyoyaandika Sheikh, na ni miongoni mwa wanayojifaharisha nayo sana wafuasi wake kati ya yale aliyozalisha Sheikh. Kutokana nayo imebainika nidhaniavyo kuwa Sheikh Mungu amrehemu, amsamehe na amghufirie, amefurutu ada katika kukufurisha Waislamu ufurutu ada wa dhahiri. Hivyo basi tunasema: Amekosea, imetosha. Tunajiepusha na ufurutu ada wa kutoka kwa mahasimu wake na wafuasi wake, kwa kuwa kisharia haipasi tumhami Sheikh na makosa yake na tuubebeshe Uislamu, tudhanie ukufurishaji huu una dalili za maandiko ya kisheria, na kuwa ndiyo dini ya Mwenyezi Mungu. Njia hii ya kumtakasa Sheikh na makosa yake na kuubebesha Uislamu mizigo hiyo ndani yake ina khiyana dhidi ya dini yenyewe. Ni lazima dini ibakie juu ya kiwango tusichoweza kuambatanisha majaaliwa yake na majaaliwa ya tumpendaye miongoni mwa wanazuoni au watawala au wengineo. Dini sio ya kuho101

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 101

1/20/2016 11:35:52 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

dhiwa na yeyote. Usomaji si mmoja, wala hakuna maafikiano juu ya nasu zote upande wa usahihi wake na ufahamu. Lakini mwenye kuitwa Mwislamu; japo mnafiki na mwongo, damu yake, mali yake na heshima yake ni haramu kuguswa na ni wajibu haki zake kuhifadhiwa na kuheshimiwa, basi vipi itakuwa kwa aliyenasibika na Uislamu ilihali ni mkweli mwenye kutekeleza wajibu, mwenye kujiepusha mbali na dhambi kubwa, kisha baada ya haya tumuambatanishe na makafiri kwa sababu ya kufahamu dalili au kubumi hoja. Hili ni jambo hatari, lina matunda na natija mbaya. Na huu ubunifu wa kukufurisha inabidi msimamo kuuhusu uwe wazi katika hali na zama, tusifume leo kwa tamaa na kufumua kesho kwa mfadhaiko, tumche Mwenyezi Mungu kwa kuwa sisi iwapo tutaleta siasa katika kukiri ukweli, basi dini yetu itatoweka bila faida, na kwayo tukiila dunia hii leo kesho itatula sisi. Haya niyasemayo ni nasaha na kujisawazisha, kwa hili siutaki utukufu ardhini wala ufisadi, hakika Mwenyezi Mungu anaziona nia.

KUHARIRI MAHALI PENYE MZOZO Kuhitilafiana kukubwa kati ya Sheikh na wapinzani wake kunajificha katika nukta hii: Sheikh amejikita katika nadharia na wao wamejikita katika natija. Na mahasimu wa Sheikh si watu wa kawaida bali ni watu mahsusi wa zama zile, amekiri hilo Sheikh katika adDurarus-Saniyyah (2/62). Kwa mfano: Mahasimu wa Sheikh wanamtuhumu kuwa yeye anakanusha Shafaa. Na yeye anawajibu kuwa yeye hakanushi Shafaa, lakini wakati huohuo anaifunga Shafaa kwa wafuasi wake tu ambao anawaita wanatauhidi. Na anasema wazi kuwa Shafaa haiwi ila kwa Waislamu, yaani walio katika rai yake. Hivyo wao wamekosea katika kumtuhumu kuwa anakanusha asili ya Shafaa, na yeye 102

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 102

1/20/2016 11:35:52 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

amekosea kuifunga Shafaa kwa wafuasi wake tu. Wao wanaiangalia natija, na yeye anawabakisha katika utangulizi. Pia wanasema: Wewe unawakufurisha Waislamu. Na yeye anaapa kuwa hawakufurishi Waislamu na hamkufurishi ila aliyekufurishwa na Mwenyezi Mungu na Mtume Wake! Na siri ya mas’ala hii ni kuwa wao wanaiona natija ya kuwakufurisha kwake wao na wafuasi wao. Lakini yeye anategemea utangulizi kuwa wao sio Waislamu aslani! Na Waislamu ambao yeye hawakufurishi ni wanatauhidi, na wao hawamkubalii huu uwitaji wa mwisho, wa kwamba wanatauhidi ni wafuase wake tu.51 Na hili ndilo kubwa ambalo Sheikh na mahasimu wake wanazunguka wakiunguruma nalo, kila ncha imeshikamana na upande. Yeye anashikamana na utangulizi na wao wanapinga natija. Kwa ajili hiyo hakujapatikana kuelewana wala kuhariri mahali pa tofauti, na huenda lisitimie hilo maadamu kuna wafurutu ada kila upande, kila upande unavutia kwake na kudhulumu mwingine. Na hali hii inashabihiana na yanayojiri kati ya Sunni na Shia, Sunni kuwatuhumu Shia kuwa wanawakufurisha Maswahaba, na Shia wanasema sisi hatuwakufurishi Maswahaba, lakini inanakiliwa kutoka vitabuni mwao lijulishalo hivyo, kwani wao husema: ‘Hao si miongoni mwa 51

Angalia kwa njia ya mfano kauli yake katika kitabu Durarus-Saniyyah (1/63) – Akijihami kujiepusha na tuhuma za kuwakufurisha Waislamu - amesema: “Akisema msemaji wao – anawakusudia wampingao Sheikh:- Kuwa wao wanakufurisha kijumla! Tunasema: Subhanallah, utakatifu ni Wako, huu ni uwongo mkubwa!” Lakini Sheikh anakamilisha kwa linalotilia mkazo tuhuma kwa kauli yake: “Tunayemkufurisha ni yule anayeshuhudia kuwa Tawhidi ni dini ya Mwenyezi Mungu na ni dini ya Mjumbe Wake na kuwa daawa ya asiyekuwa Mungu ni batili, kisha baada ya haya anawakufurisha wanatawhidi na anawaita Makhawariji!” Nasema: Muafaka unakaribia kuwa ni wa tamko tu, kwa hiyo Sheikh kuwakufurisha kwake mahasimu na wapinzani kwa sababu ya kuuita kwao Uwahabi kuwa ni U-khawariji sio jaizi, bali endapo hasimu akiamua kutukufurisha haitokuwa jaizi sisi tumkufurishe. Hii ni njia ya Maswahaba, wao hawakumkufurisha aliyewakufurisha. Na Sheikh amelikiri hili mahali pengine, hivyo hili lahesabika miongoni mwa yanayopingana. 103

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 103

1/20/2016 11:35:52 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Maswahaba, hao ni walioritadi!!’ Na aliyeritadi sio swahaba kwa mujibu wa njia yetu na njia yenu!! Ninyi mnaweka sharti mtu kuwa swahaba ni lazima afe angali Mwislamu, na hao wamekufa hali si Waislamu, hivyo wao wako nje ya mzozo! Kwa hiyo tuhuma yenu dhidi yetu sio sahihi.’ Ni kama hivi wanaohasimiana wanazunguka kwenye duru iliyo tupu kwa kuwa wao hawakuhariri eneo la mzozo.

104

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 104

1/20/2016 11:35:52 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

UTAFITI WA PILI KUZISOMA KAULI ZA SHEIKH ­KATIKA VITABU NA INSHA NYINGINE: Na ad-Durarus-Saniyyah ni mfano wake Kwanza: Rai za Sheikh katika vitabu vingine mbali na Kashfushubhat: Kwa kuondoa maeneo machache kama risala ya Sheikh kwa watu wa Qaswim iliyomo ndani ya ad-Durarus-Saniyyah (1/34), tunakuta karibu katika kila kitabu cha Sheikh na insha zake, ndani yake kuna wasaa na ufurutu ada katika kukufurisha, hatuwezi kuwa na udhuru wa kukwepa makosa hayo ila kwa ung’ang’anizi, na imewahi kutokea hivyo! Lau tukichukua kitabu ad-Durarus-Saniyyah ambacho kimejumuisha vitabu na insha za Shekh, na kadhalika kitabu at-Tawhid ambacho ukosoaji wake utakuja baada ya viambatanisho, tutakuta yanayojulisha ufurutu ada katika ukufurishaji wa wazi katika maelezo mengi ya Sheikh, kati ya maelezo hayo nachagua mifano ijayo ya haraka haraka kutoka kitabu ad-Durarus-Saniyyah: Mfano wa Kwanza: Wanazuoni wa Najdi na Makadhi Wake Hawaujui Uislamu: Hii ni kauli ya wazi ya Sheikh Muhammad. Bali amewafanya hawajui: La ilaha ila llahu, wala hawajui tofauti kati ya dini ya Mu105

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 105

1/20/2016 11:35:52 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

hammad bin Abdullah, na dini ya Amri bin Lahyi aliyoiweka kwa ajili ya Waarabu! Na dalili ya kuthibiti hilo kutoka kwa Sheikh ni kauli yake kama ilivyo katika ad-Durarus-Saniyyah (10/51): “....Nimeitafuta elimu, na ninaamini aliyenijua alifikiri kuwa mimi nina maarifa na mimi katika wakati ule sikuwa najua maana ya: La ilaha ila llahu wala sikuwa naijua dini ya Uislamu kabla ya kheri hii ambayo Mwenyezi Mungu amenitunukia! Kadhalika masheikh wangu hakuna mtu miongoni mwao aliyejua hilo! Hivyo atakayedai miongoni mwa wanazuoni wa Aaridhu kuwa alijua maana ya La ilaha ila llahu! Au alijua maana ya Uislamu kabla ya wakati huu! Au akadai kutoka kwa masheikh wake kuwa yupo aliyejua hilo! Atakuwa amesema uwomgo na amezua! Na amewadanganya watu, na amejisifu kwa jambo asilokuwa nalo!” Kisha alisema maneno yanayoshabihiana na hayo katika adDurus-Saniyyah (10/57) kuwa wanazuoni ambao anaongea nao na masheikh wao na masheikh wa masheikh wao hawafahamu dini ya Uislamu: “Wala hawakupambanua kati ya dini ya Muhammad 5 na dini ya Amri bin Lahyi ambayo aliibuni kwa ajili ya Waarabu, bali dini ya Amri kwao ni dini sahihi!!” Nasema: Sina shaka kuwa - usemi huu - ndani yake kuna ukufurishaji wa wazi kwa wateule miongoni mwa wanazuoni na makadhi wa Najdi na masheikh wao na masheikh wa masheikh wao, basi itakuwaje kwa watu wa kawaida?! Na hili hatulikubali, hii leo vitabu vyote vya historia vinavyozungumzia eneo la Najdi vinataja wanazuoni na makadhi na wanafunzi wa elimu ya Kiislamu tokea zama za Ibn Adhiib katika karne ya tisa ya Hijiriyah, mpaka siku za Sheikh Muhammad katika karne ya kumi na mbili. Na wanazuoni wa historia wa wakati wa leo wametaja wasifu nyingi kuhusu wanazuoni wa Ashiqar, Shaqra, Burayda, Aniyza, Harimlaa, Uyayna, Riyadh, al-Kharaj, na Aflag, na wa miji mingine kabla ya Sheikh Muham106

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 106

1/20/2016 11:35:52 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

mad. Na kuna muafaka wa wakati uliopo kuwa hao sio makafiri wala sio waabudu masanamu. Naam yawezekana baadhi yao au wote wanaruhusu kutabaruku na watu wema, au daawa yao ilikuwa na udhaifu au baadhi ya bidaa, na haya ni mambo ambayo la juu kabisa liwezalo kusemwa kuyahusu ni kuwa hayo ni bidaa au ni makosa ya kiitikadi. Lakini kuwaita kuwa ni waabudu masanamu na kwamba wanaiona dini ya Amri bin Lahyi ni bora kuliko dini ya Muhammad Ibn Abdullah, haya ni maneno batili hawezi kuyakubali mwenye insafu, na sidhanii mwenye akili atathubutu kutamka maneno kama haya, na tunajitakasa kwa Mwenyezi Mungu tuwe mbali na kuwakufurisha Waislamu na tunamuomba Mungu amghufirie hili Sheikh la kuwakufurisha waziwazi wanazuoni wa Najdi Mungu awarehemu. Sheikh Ibn Hamid amewataja sana wanazuoni wa Najdi wa wakati wa Sheikh na kabla yake katika kitabu as-Suhubul-Waabilah.52 Na Sheikh Abdullahi al-Basaam53 ana kitabu Ulamau Najdi Khilal Thamania Qurun wala hakumtuhumu yeyote miongoni mwao kuwa alikuwa mfanya bidaa sembuse kuwa mwabudu masanamu na kuiona dini ya Amri bin Lahyi kuwa ndio bora! Na Sheikh Salehe alQaadhiy ametunga kitabu kuwahusu wanazuoni wa Najd, na hivyo hivyo Sheikh Bakar Abu Zayd54 katika kitabu chake Ulamaul-Hanabila na wengine. Na hatujakuta yeyote miongoni mwao au miongoni mwa wengine kati ya walioandika wasifu wa wanazuoni wa kabla ya Sheikh au wa zama zake ametaja kuwa mmoja wa hao wanazuoni alikuwa anaabudu masanamu au dini yake si Uislamu!! Na tunajikinga kwa Mwenyezi Mungu mbali na itikadi hii, huu ni mfano wa wazi miongoni mwa mifano ambayo inatilia mkazo kuwa Sheikh   Kimehakikiwa na Dr. Abdur Rahman al-Athimiyn.   Ni mwanachuo wa Kihanbali, naye ni mwanachama katika baraza la wanazuoni wakubwa. 54   Ni mwanachuo wa Kihanbali, naye ni mwanachama katika baraza la wanazuoni wakubwa. 52 53

107

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 107

1/20/2016 11:35:52 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

ameingia katika ukufurishaji na amekosea, Mungu amhurumie na amsamehe. Mfano wa Pili: Wanazuoni wa Kihanbali na Wengine Katika wanazuoni wa Zama za Sheikh Walikuwa Washirikina kwa Shirki Kubwa Imtoayo Mtu Nje ya Uislamu: Na miongoni mwa mifano ya kuwakufurisha watu maalumu katika maneno ya Sheikh ni kauli yake katika risala yake kwenda kwa Sheikh Sulayman bin Sahim al-Hanbaliy, kama ilivyo katika kitabu ad-Durarus-Saniyyah (1/31): “Tunakukumbusha wewe, kuwa wewe na baba yako mnafanya ukafiri na shirki na unafiki waziwazi !!.. Wewe na baba yako mnajitahidi kuifanyia uadui usiku na mchana dini hii!!... Wewe ni mtu mbishi mpotovu hali ukiwa unajua. Ni mwenye kuuchagua ukafiri kuliko Uislamu!! Na hiki kitabu chenu ndani yake kuna ukafiri wenu.” Na amesema kama ilivyo katika ad-Durarus-Saniyyah (1/78): “Ama kumhusu Ibn Abdul Latifu na Ibn Afaliq na Ibn Mutlaq, wao ni kidole cha shahada cha Tawhiidi... na Ibn Feyruzi yeye yuko karibu mno na Uislamu!” Nasema: Pamoja na kuwa huyu Muhammad bin Feyruz ni Mhanbali mwenye kumfuata Ibn Taymiya na Ibn al-Qayyim, na Sheikh amekiri kuwa yeye ni mtu miongoni mwa Mahanbali na anafuata maneno ya Ibn Taymiya na Ibn al-Qayyim, Subhanallah, ikiwa mtu huyu Mhanbali ambaye anamkalidi Ibn Taymiya na Ibn al-Qayyim hajaingia katika Uislamu mpaka hivi sasa!, basi itakuwaje kwa wengineo?!! 108

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 108

1/20/2016 11:35:52 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Bali Sheikh amesema wazi mahali pengine kuwa yeye ni kafiri: “Kafiri ukafiri mkubwa umtoao mtu nje ya Uislamu.”55 Ikiwa hii ndio hali ya Mhanbali amfuataye Ibn Taymiya na Ibn al-Qayyim basi vipi itakuwa hali ya wanazuoni wa Kimaliki, Kishafi, Kihanafi na Dhwahiriya, achilia mbali wanazuoni wa Kizaydia, Kiibaadhi, Kishia Imamiyyah, Kisufi na wengine wa kawaida?!! Mfano wa Tatu: Waislamu Huko Najdi na Hijazi Wanakanusha Ufufuo: Sheikh; Mungu amrehemu na amsamehe, anadhania kuwa wengi miongoni mwa watu wa Najd na watu wa Hijazi wanakanusha ufufuo, kama ilivyo katika ad-Durarus-Saniyyah (10/43). Nasema: Na hili ni miongoni mwa yanayojulikana kwa dharura kuwa ni batili na sio sahihi. Waislamu walio wengi, bali wote bali na Mayahudi wote na Manaswara pia, wanaamini Siku ya Ufufuo, sawa wale waliokuwepo katika zama zake au kabla yake au baada yake, ila tu ni kwamba watu wamepatwa na muda ambao bidaa na imani ya dhana imekithiri, nayo ni ya tangu zamani katika umma wa Kiislamu na ingali mpaka siku zetu hizi za leo, katika watu huyu na yule miongoni mwa Waislamu, wawe wengi au wachahe, ndani ya Bara Arabu na katika ulimwengu wa Kiislamu, lakini hili halimaanishi kuwa Waislamu walikuwa makafiri au kuwa wao wanakanusha kufufuka! Basi tofauti ilioje kati ya hili na lile. Mfano wa Nne: Kufuru Aikusudiayo Sheikh ni ile Imtoayo Mtu Nje ya Uislamu: Kufuru ambayo Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahabi anaivurumisha sio kufuru ndogo bali akusudialo kwa kufuru hiyo ni kufuru 55

Angalia ad-Durarus-Saniyyah (10/63). 109

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 109

1/20/2016 11:35:52 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

kubwa imtoayo mtu nje ya Uislamu. Na hili amelikariri sana katika vitabu vyake na katika insha zake, na miongoni mwayo ni kauli yake katika ad-Durarus-Saniyyah (10/63): “Bali ibara ni nyeupe na ni wazi katika kuwakufurisha mfano wa Ibn Feyruzi na Salehe bin Abdillah na walio mfano wa wawili hawa, ukafiri wa dhahiri unaomtoa mtu nje ya Uislamu, sembuse wasiokuwa wawili hao.” Nasema: Hawa ni wanazuoni wawili wa Kihanbali, na huu ndio ukufurishaji uliyo bayana na wazi katika utaratibu wa Sheikh Muhammad mwenyewe, basi vipi kwa wafuasi?! Mwenye insafu hatohitajia zaidi ya thibitisho kama hizi, hii ibara ya mwisho ina makosa mawili makubwa: La Kwanza: Kumkufurisha mwanazuoni maalumu Mwislamu mwenye kufanya taawili. La Pili: Ukufurishaji unaomtoa mtu nje ya Uislamu. Huu ukufurishaji unaomtoa mtu nje ya Uislamu, hatari yake haifichiki, nayo ni: Kuhalalisha damu, mali, na kuwateka dhuria. Kuzuia kurithiana na kuharamisha kuwaombea maghufira au kutoa sadaka kwa niaba yao, au kwenda Hija kwa niaba yao, na mengine miongoni mwa mambo makubwa. Baada ya hayo, Mwislamu mkweli hawezi ila ni kuishi pamoja nao maisha ya wanafiki, na afanye bidii ya dhimii mbele yake, hana njia ila ni kusikiliza kwa utii au kuwang’oa, anawaogopa asemapo ukweli, na anamwogopa Mwenyezi Mungu endapo atasema uwongo, anafishwa na Uislam na anaishi na unafiki. Mfano wa Tano: Kuwakufurisha Watu Maalumu Pia: Na Sheikh Mungu amrehemu, pindi Ahmad bin Abdulkariim alipokuwa kinyume na yeye, na huyu Ahmad ni mwanachuoni wa 110

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 110

1/20/2016 11:35:52 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Kihanbali, mwana wa Najdi, Sheikh alimtumia risala kama ilivyo katika ad-Durarus-Saniyyah (10/64): “Umeondoka kwa Ibn Ghanaam na mwingine na umejiepusha na mila ya Ibrahim na umefanya washuhudie juu ya nafsi yako kuwafuata kwako washirikina.” Nasema: Huu ni ukufurishaji mtupu hususan katika utaratibu wa Sheikh. Mfano wa Sita: Haram Mbili Tukufu (Makka na Madina) ni Nyumba za Ukafiri!! Ama nchi za washirikina kwa mujibu wa Sheikh Mungu amrehemu na amsamehe, ni kila nchi ambayo haijaingia chini ya utii wake au daawa yake, na wala hakuziengua kutoka humo Haram mbili takatifu (Makka na Madina)! Kwa mfano angalia Juz.10, uk. 75, 64, 77, 12, 86.56 Mfano wa Saba: Kuwakufurisha Shia Imamiya: Kuwakufurisha Shia Imamiya ni rahisi tukilinganisha na kuwakufurisha Mahanbali. Na Sheikh anasema kuwa mwenye kuwa na shaka na ukafiri wao yeye ni kafiri (10/369). Hii imenukuliwa kutoka kwa Muqadisiy na akathibitisha, hali ya kuwa Ibn Taymiya pamoja na ufurutu ada wake na chuki yake, ana maneno ya wazi kuwa hao (Shia Imamiya) ni watu wa bidaa, Waislamu sio makafiri, lakini Sheikh Mungu amrehemu anakusanya magumu. Mfano wa Nane: Kumkufurisha Mwenye Kumtukana Swahaba: 56

Yote haya yanapatikana katika ad-Durarus-Saniyyah, na kila uthibitisho katika mlango huu umechukuliwa kutoka kitabu ad-Durarus-Saniyyah isipokuwa niliyobainisha mahali pake. 111

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 111

1/20/2016 11:35:52 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Sheikh kumkufurisha mwenye kumtukana swahaba utakukuta katika ad-Durarus-Saniyyah (10/369). Na hii ipo katika vitabu vya akida vyenye ufurutu ada. Ila ni kwamba sio sahihi, Imamu Ali hakuwakufurisha Makhawariji hali wao walikuwa wanamkufurisha na kumtukana. Kadhalika Abu Bakr as-Swidiq; imethibiti kutoka kwake (Abu-Bakr) katika mlango wake uliomo katika Musnad Imam Ahmad kwa sanadi sahihi, kuwa alikataza na kuzuia kumuudhi mtu anayemtukana na kumtamkia kauli kali. Kisha kwa nini hawa wanajaalia kumtukana swahaba kuwa ni ukafiri, hali wao wanamuhami Muawiya, na hakika alikuwa anamtukana Ali bin Abu Talib? Na yeye ni nani? Je haikuthibiti kuhusu yeye (Muawiya) katika Sahih Muslim amri yake ya kumtukana Ali bin Abu Talib? Au ni kwamba heshima ya Imamu Ali ni halali kuvunjwa, na heshima ya huria (Muawiya) ndiyo yenye haki ya kulindwa? Kwa nini wamejaalia kumlinda Imamu Ali na kukemea dhulma kuihusu haki yake ni jambo linalohusu vitabu vya Mashia tu?57 Mna nini hivi ndivyo mnavyohukumu? 57

Ilihali wengi miongoni mwa wanazuoni wakubwa wa Kisunni wameandika na wametunga vitabu katika kuelezea fadhila za Imamu Ali D, miongoni mwao ni an-Nasaiy katika kitabu chake Khaswaisu Amiril-Muuminina Ali bin Abi Talib D, aliandika kikiwa ni jibu la kuwapinga watu wa Sham (Syria) - Damascus - ambao walikuwa ni Manawasibu, yaani wenye chuki binafsi dhidi ya Ahlulbayti G, ilikuwa ni mwanzoni mwa karne ya nne, na an-Nasaiy alipatwa na umauti wake kwa sababu ya kitabu hiki. Manawasibu wa Damascus walimtaka aandike kitabu kama hiki kuelezea fadhila za Muawiya! Akasema: “Sijui kumhusu yeye isipokuwa Hadithi hii: ‘Mungu asilishibishe tumbo lake.’” Walighadhibika wakaziponda korodani zake mpaka akafariki! Lawama ikawa kwao hasa katika kuwaua wanazuoni. Na miongoni mwa wanazuoni wa Kisunni ni Imamu al-Hafidhu Abu Abdillah al-Hakimu mtunzi wa kitabu al-Mustadrak, alikithirisha kutaja fadhila za Imamu Ali D na kumhami katika al-Mustadrak, mwanzoni mwa karne ya tano A.H. Manawasibu kama kawaida yao walimtaka awasilishe Hadithi zinazohusu fadhila za Muawiya, akasema: “Hainijii hadithi yoyote moyoni mwangu.” Wakamzingira nyumbani kwake huko Khurasani. Kadhalika Imamu Ibn Abdulbar, Imamu wa Masunni katika wakati wake. Alikuwa anamtetea sana Imamu Ali katika vitabu vyake, miongoni mwavyo ni al-Istiabu na al-Istidhkaru, katikati ya karne ya tano ya A.H., yeye hakusibiwa na makruhu, isipokuwa Masalafi wa hivi sasa wanamkosoa katika kueleza kwake kwa mapana jinsi walivyopambana Maswahaba kwa Maswahaba! Hali wao wanajua kuwa Ibn Taymiya ameeleza kwa mapana zaidi kuliko yeye, lakini kwa hili wanakusudia lile 112

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 112

1/20/2016 11:35:52 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Mfano wa Tisa: Kuwakufurisha Watu wa Makah na Madina. Na Madrasa ya Kiwahabi Inaendeleza: Sheikh kuwakufurisha kwake watu wa Makkah utakukuta katika (10/86), na (9/291), Sheikh amesema kuwa dini yao ndiyo ambayo Mjumbe wa Mungu alitumwa kwenda kuwaonya waachane nayo! Na baadhi ya Mawahabi wamezidisha kuwa: Kwa sababu wao ni waabudia makaburi! Na kwamba asiyewakufurisha basi yeye ni kafiri kama wao japo awe anawachukia na anaupenda Uislamu na Waislamu.58 alilosema kuhusu fadhila za Imamu Ali D na kulaumu dhulma za Bani Umayya. Kadhalika hii leo utawakuta wanajikita na kuelekeza mashambulizi yao kwa kila anayemhami Imamu Ali D na kukosoa dhulma za Bani Umayya na humtuhumu papohapo kuwa ni Rafidhi! Na makusudio hapa ni kwamba katika Masunni hakosi kupatikana mtu anayezieleza fadhila za Ahlulbayt na kuwalinda, isipokuwa Manawasibu aghlabu wanafanya juhudi kufisha utajo wao kama ilivyo hii leo, pamoja na kuvifanya mashuhuri vitabu vya Manawasibu kama vitabu vya Ibn Taymiya na Farau Hanbaliy na Muhibudin al-Khatibu na vitabu vingine vya Kisalafi na Rasailul-Jaamia katika maudhui ya Swahaba, hivyo vyote vina mchanganyiko wa chuki za Manawasibu zilizojificha! 58   Na baada ya ushindi wa Mawahabi kuiteka Makkah na Madina katika zama za Suudi mkubwa, ulazimishaji wa wanazuoni wa Makkah na Madina watie saini hati ya dhamana ulikamilika, hati ambayo ndani yake mna hukumu juu ya watu wa Makkah na Madina kuwa wao kabla ya ushindi walikuwa katika kufuru kubwa inayohalalisha damu na mali, na kuwa nchi nyingine za Waislamu zilizobaki siku zile ziko katika shirki mkubwa! Rejea ad-Durarus-Saniyyah (1/314-317) utazikuta hati mbili za dhamana, na kwa urahisi utatambua kuwa hati hizo zimetokana na kulazimishwa kwa vile matamko mawili ya hizo hati yamefanana, na kwa mkazo wake kuwakufurisha watu wa Haram mbili, na ya kuwa hao wanazuoni walikuwa dhidi ya Uwahabi kabla ya kutekwa Haram mbili. Na sababu ya kufurutu ada ya kupindukia ndani ya dola ya Suudia ya kwanza ni kuwa watawala walikuwa kama wanazuoni wa Kiwahabi, ni wafurutu ada. Ama katika dola mbili za Kisuudi ya pili na ya tatu alhamdulilahi wao sio Mawahabi lakini wao huenda hawaitambui hatari ya ufurutu ada wa kiwahabi. Kwa minajili hiyo wanasitukizwa na nguvu za ufurutu ada za wafurutu ada wa ndani ya Saudia, kwa kuwa wafurutu ada wamehodhi turathi yote ya Masalafi yenye ufurutu ada na kila turathi ya kiwahabi, na wamezidisha juu ya hayo harakati za safisha safisha ya kichama. Hivyo ukajikita katika nchi hii ufurutu ada wa zamani na mpya pamoja, na kujiweka kwenye makundi. Na ufumbuzi ni kufungua nafasi za kuzifanyia rejea njia hizi na vitabu, fikra na fatwa. 113

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 113

1/20/2016 11:35:52 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Itikadi hii imebakia kwa wafuasi wa Sheikh na madrasa yake mpaka ukatimia utekaji wa Haram mbili tukufu na wakawalazimisha wanazuoni wa Haramaini (Makka na Madina) waamini itikadi hii, wao, ndugu zao na wakazi wa miji miwili mitukufu, na hiyo ilikuwa mwaka 1225 A.H. Na utekaji wa Haramaini (Makka na Madina) na kuziambatanisha na mamlaka yao ulitimia katika zama za Suudi bin Abdul-Azizi bin Muhammad mwaka 1222 A.H. Na huyu Imamu Suudi si yule Mfalme wa zama hizi, Suudi bin Abdul-Azizi aliyekuwa mtawala baada ya Mfalme Abdul-Azizi, Mungu awarehemu wote. Hivyo Imamu Suudi bin Abdul-Azizi alikuwa mfurutu ada katika kukufurisha kama alivyokuwa Sheikh, Mungu awarehemu, naye ni miongoni mwa viongozi wa dola ya kwanza ya Suudi, ambayo maimamu wake wote walikuwa wanasiasa Mawahabi na wafurutu ada, Mungu awarehemu. Kinyume na dola mbili za Kisuudi, ya pili na ya tatu, wao ni wanasiasa tu, la muhimu kwao ni maslahi ya umma na mshikamano wa kitaifa, na wanauzuia Uwahabi usiambukize wananchi wengine, japokuwa baadhi yao hawakosi kuwa na uwahabi uliojificha, ambao huenda ukawasukuma kwenye utendaji wenye upendeleo mkubwa kwa uwahabi, bila kujua hatari ya upendeleo huu kwa muda mrefu. Vyovyote iwavyo, wanasiasa wangali bora sana kuliko wanadini ambao wanaitumia dini katika kuwakufurisha Waislamu na kukiuka haki zao. Katika uwahabi pia wako wenye akili nzuri na wenye insafu, lakini sisi tunazungumzia wale ambao ni ghalibu na ambayo tuyasomayo ambayo hayaepukani na ufurutu ada wa kupita kiasi. - Na hii ni nakala ya toba ya wanazuoni wa Makka na Madina ambao walilazimishwa kudhihirisha toba kwa ajili ya madhehebu zao walizokuwanazo hapo mwanzo (Madhehebu ya Kisunni) na kufuata kwao ufurutu ada wa kiwahabi ambao baada yake wamewakufurisha Waislamu wote.

114

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 114

1/20/2016 11:35:52 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

NAKALA YA WANAZUONI WA MAKKAH ­TUKUFU: Imeandikwa nakala hii ya ukufurishaji siku za Suudi bin AbdulAzizi bin Muhammad, naye ni kutoka madrasa ya Sheikh, ni miongoni mwa wanafunzi wake wenye ikhlasi Mungu amrehemu na amsamehe. Wanazuoni wa Makkah waliitia saini ndani yake mkiwa na: “Sisi wanazuoni wa Makkah tunashuhudia tukiwa wenye kuweka maandishi yetu na mihuri yetu katika hati hii: Kuwa dini hii ambayo kasimama nayo Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahabi Mungu amrehemu na ambayo Imamu wa Waislamu Suudi bin Abdul-Azizi kawaita watu kwayo, ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kukemea shirki ambayo ameitaja katika kitabu hiki, ni haki ambayo ndani yake hakuna shaka wala wasiwasi. Na kuwa yaliyotokea Makkah na Madina hapo mwanzo, pia Misri, Sham, na sehemu nyingine zisizokuwa hizo mbili miongoni mwa nchi mpaka sasa, miongoni mwa aina za shirki, ni ukafiri unaohalalisha damu na mali na unaowajibisha kubakia milele motoni. Na asiyeingia katika dini hii ambayo amesimama nayo Muhamad bin Abdul-Wahabi na anaifanyia kazi, anawapenda wenye kushikamana nayo na anawafanyia uadui maadui zake, huyo kwetu ni kafiri mwenye kumkana Mungu na Siku ya Kiyama. Na ni wajibu juu ya Imamu wa Waislamu (Suudi bin Abdul-Azizi) na Waislamu kumpiga vita na kumuua mpaka atubu kwa kujitoa katika aliyonayo na aitendee kazi dini hii.”59 59

ad-Durarus-Saniyyah (1/314). 115

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 115

1/20/2016 11:35:52 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Kisha alianza kutaja majina ya waliotia saini ambao walikuwa dhidi ya Uwahabi na dhidi ya Sheikh, hivyo kulazimishwa kupo wazi.

NAKALA YA MADINA TUKUFU: Na nakala ya Madina matamko na maana yake yanakaribiana na nakala ya Makkah, na miongoni mwayo: “.....na kwamba yaliyotokea Makkah na Madina hapo kabla, Sham, Misri na kwingineko miongoni mwa nchi mpaka sasa miongoni mwa aina za shirki zilizotajwa katika kitabu hiki, ni ukafiri unaohalalisha damu na mali. Na kila asiyeingia katika dini hii na kuitendea kazi na kuiamini, yeye ni kafiri mwenye kumkana Mungu na Siku ya Kiyama. Na ni wajibu juu ya Imamu wa Waislamu na Waislamu wote, kutekeleza faradhi ya jihadi na kuwapiga vita washirikina na wakaidi! Na kuwa atakayefanya kinyume na yaliyo kwenye maandishi haya miongoni mwa watu wa Misri, Sham, Iraqi, na kila walio katika dini yao! Ambayo waliyonayo hivi sasa, yeye ni kafiri mshirikina kwa msimamo wake!”60 Nasema: Nadhani baada ya hati hizi mbili inaonesha wazi: Kuwa madrasa ya Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahabi, katika maudhui ya ukufurishaji, yeye ni mfurutu ada sana mwenye kupitiliza kiasi. Haukuti maneno ya Sheikh au kurudi nyuma kwake au kujiepusha na makosa yake. Fanya rejea kama hizi, ambazo ni kwa maslahi ya Uislamu kwanza, pili kwa maslahi ya Waislamu. 60

Ad-Durarus-Saniyyah (1/316 – 317). 116

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 116

1/20/2016 11:35:52 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Kwa minajili hiyo unabaki uwahabi wa leo na vikundi vyake vikifaidika na fikra hii. Wanaendelea kukutana na sababu za kukufurisha toka pande za nje, na wanaendelea kuisifu madrasa ya Sheikh Muhammad, Mungu amrehemu, sifa zinazoendelea bila ya kufanya rejea hata kidogo, na bila ya kusita kuwafanyia uadui na kuwapiga vita wanaokosoa mambo kama haya. La kusikitisha ni kuwa wao wanaitumia dola hiyo hiyo kumpiga vita auwekae mkono wake kwenye ugonjwa, katika utamaduni wa mahali tulipo (Saudi Arabia), sawa chimbuko la ugonjwa liwe ni Usalafi au Uwahabi au harakati. Mfano wa Kumi: Kuwakufurisha Mabedui: Kuwakufurisha mabedui katika (10/113), 114), na (8/11,117,119). Kuwa wao ni makafiri mno kuliko Mayahudi na Wakristo, na kuwa wao hawana Uislamu hata kiasi cha unywele! Japo watamke shahada mbili, angalia ad-Durarus-Saniyyah (9/2,238 ). Yeyote miongoni mwa wanazuoni hajapata kumkufurisha bedui hapo kabla. Ni sahihi kuwa wao walikuwa ni wachache kielimu, na kuwa wao huenda walipitisha hukumu za kijadi za kimazoea ya kikabila, lakini hii sio kufuru imtoayo mtu nje ya Uislamu. Wao walikuwa wanaswali na wanafunga, japo katika wao kuna ujahili wa wazi. Na hali ya jangwani ilivyokuwa wakati wa Sheikh ni hali ileile ya jangwani iliyokuwa katika zama nyingine za Kiislamu.

117

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 117

1/20/2016 11:35:52 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Mfano wa Kumi na Moja: Kulikufurisha Kabila la Anzatu: Kulikufurisha kabila la Anzatu katika ad-Durarus-Saniyyah, (10/113). Kuwa wao hawaamini ufufuo! Mfano wa Kumi na Mbili: Kulikufurisha Kabila la al-Dhwafiir: Katika ad-Durarus-Saniyyah, (10/113). Kuwa wao hawaamini ufufuo! Mfano wa Kumi na Tatu: Kuwakufurisha Watu wa Uyayna na Dar’iyyah: Angalia katika ad-Durarus-Saniyyah (8/57 ) uone jinsi alivyowakufurisha wakazi wa Uyayna na Dar’iyyah ambao walikuwa na Ibn Sahim katika rai, na ambao walikuwa miongoni mwa wapinzani wa Sheikh. Mfano wa Kumi na Nne: Kulikufurisha Kundi Kubwa la Waislamu: Rejea ad-Durarus-Saniyyah (10/8) uone jinsi alivyolikufurisha kundi kubwa la Waislamu. Mfano wa Kumi na Tano: Kumkufurisha ibn Arabiy: Kuwa yeye ni kafiri mno kuliko Firauni na kwamba asiyemkufurisha yeye ni kafiri bali amemkufurisha mwenye kuwa na shaka na ukafiri wake! Katika ad-Durarus-Saniyyah (10/25). Na katika hili 118

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 118

1/20/2016 11:35:52 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

kuna kumkufurisha kila mwanazuoni wa kisufi na wengi miongoni mwa wanazuoni wa madhehebu nne kwa uchache. Ilihali yeye katika insha nyingine ya kipekee ya ajabu nayo ni Risala yake kwa watu wa Qaswim, amekanusha suala la yeye kuona Ibn Arabiy kuwa ni kafiri! Na hili lajulisha kuwa sio kila analokanusha Sheikh juu ya nafsi yake huwa ni sahihi, hii hapa risala yake ndani yake anakataa kuwa hakumkufurisha Ibn Arabiy, lakini sisi tunakuta katika vitabu vyake na risala zake makubwa zaidi ya hilo alilotuhumiwa, kwani hapa amekwenda mbali zaidi hadi amemkufurisha mwenye kuwa na shaka na ukafiri wa Ibn Arabiy! Bali nimekuta kiasi kikubwa cha aliyoyakanusha juu ya nafsi yake - nayo ni machache ukilinganisha na ambayo hakukanusha yapo katika vitabu vyake na risala zake! Kwa tamko au maana. Na hii inamaanisha yeye alikuwa na hali tofauti mara alikuwa anakufurisha na mara nyingine anaachana na ukufurishaji au kinyume. Au alikuwa anakanusha tuhuma hii kisiasa siyo kidini, na hasa risala yake kwa watu wa al-Qaswim ambayo mawahabi wa leo wanakithirisha kuitaja, ina vitu vingi ambavyo Sheikh amepita kiwango cha kukanusha na kuvisukuma mbali na nafsi yake, ilihali mengi kati ya hayo yapo katika vitabu vyake na risala zake ambazo wamezisahihisha wafuasi wake wenye msimamo wa wastani! Na hili linatia nguvu kuwa watu wa al-Qaswim ambao siku hizo alikuwa anatumai wangemuitikia walikuwa wanachukia ukufurishaji kwa kuathirika kwao na wanazuoni wa Iraqi. Huu ni ushahidi miongoni mwa shuhuda kuwa risala yake ya wastani kwa watu wa al-Qaswim ilikuwa ya kisiasa, utaratibu wake wote upo kinyume nayo. Hasa ukizingatia kwamba katika risala hiyo amepitiliza kukataa ukufurishaji kiasi cha kukataa humo kuwa hamkufurishi anayeabudu sanamu miongoni mwa Waislamu majahili! Na huu ni uongezaji chumvi mkubwa, kwani tumeona kuwa yeye anawakufurisha wanazuoni na mafukaha 119

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 119

1/20/2016 11:35:52 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

wa kihanbali wa Najdi ambao hawaabudu sanamu, si kwa ujahili wala taawili. Mfano wa Kumi na Sita: Kumkufurisha Anayeona Shida Kuwakufurisha Watamkao lailaha ila llahu: Kama ilivyo katika ad-Durarus-Saniyyah (10/139), nayo ni fatwa ngeni, kusudio lake ni kukata aina yoyote ile ya kuwatendea upole wapinzani. Na hii ni alama ya wanaitikadi wafurutu ada toka zamani. Wao wakihofia uchamungu wa wafuasi, huongeza ‘mwenye kuwa na shaka na hili ni kafiri, mwenye kusimama ni kafiri. Al-Waqifiyyah (wenye kusita) wao ni shari kubwa mno kuliko alJahamia. Kusita ni kuwa na shaka na hukumu ya Mwenyezi Mungu, na mwenye shaka ni kafiri.’ Baadhi ya watu wa kawaida wakati wa Sheikh walilitaja tatizo hili, kuwa wao wanaona shida kumkufurisha anayesema LA ILAHA ILALLAHU, nalo ni tatizo kubwa, lakini ufumbuzi wake ulikuwa kumkufurisha mwenye kuguswa na dhamira. Mfano wa Kumi na Saba: Kumkufurisha Anayewaita Wafuasi wa Sheikh Kuwa ni Makhawariji: Katika ad-Durarus-Saniyyah (1/63) anamkufurisha anayewaita wafuasi wa Sheikh kuwa ni Makhawariji na anasimama na mahasimu wao japo wawe wanatawhidi na wanakanusha daawa isiyo ya Mwenyezi Mungu. Nasema: Hivyo basi huu ni ushahidi kuwa sio kila watu wanaosimama pamoja na makabila yao wako dhidi ya Sheikh na wafuasi wake, kusimama kwao kunakuwa ni kwa sababu ya ujahili wa kutojua Tawhidi, na kwamba makabila yale na maeneo yale hayapi120

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 120

1/20/2016 11:35:52 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

gani na wanatawhidi, lakini inaonesha wao wanawafuata wanazuoni wao katika wajibu wa kujizuia kukufurisha na kuwa na hadhari ya kutomfuata Sheikh. Lau anayempinga Sheikh angekuwa mshirikina hangeshuhudia kuwa Tawhidi ni haki na kuikanusha daawa isiyokuwa ya Mwenyezi Mungu, kama ambavyo Sheikh mwenyewe ameshuhudia hilo kwa ajili yao. Hili ni jambo la kwanza. Jambo la pili ni kuwa katika mas’ala hii kupitiliza kiasi katika kukufurisha kuko wazi. Tumetangulia kusema kuwa Makhawariji wamemuita Ali na waliokuwa pamoja naye miongoni mwa Maswahaba kuwa ni makafiri, na hiyo ni tuhuma mbaya zaidi kuliko kuwatuhumu Mawahabi kuwa ni Makhawariji, pamoja na hayo Imamu Ali hakuwakufurisha wala waliokuwa pamoja naye miongoni mwa Muhajirina na Answari. Mfano wa Kumi na Nane: Katika Kila Mji Miomgoni Mwa Miji ya Najd Kuna Sanamu Liabudiwalo mbali na mungu: Sheikh Mungu amsamehe, amedhania kuwa kila mji miongoni mwa miji ya Najdi kuna sanamu ambalo watu wa mji huo wanaliabudu mbali na Mwenyezi Mungu, kama ilivyo katika ad-DurarusSaniyyah (10/193). Nasema: Usemi huu ni batili kwa kila mwenye maarifa angalau kidogo kuhusu historia ya Najdi. Na yawezekana Sheikh alikuwa hakusudii hapa sanamu la ukweli, inawezekana alikuwa anamaanisha masanamu ni wale wanazuoni miongoni mwa wanaofuatwa na watu wa madhehebu manne, au wale watu ambao watu hutabaruku kwao, na wanawadhania kuwa katika wao kuna wema. Ikiwa alikuwa anakusudia hivyo basi hii ni ufurutu ada katika uhasama. Na kutumikisha istiara - jambo ambalo mawahabi kwa kumkalidi Ibn Taymiya wanalipinga – si mahali pake, kwa kuwa huu ni ufujaji 121

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 121

1/20/2016 11:35:52 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

katika kutumia istiara na ni uenezi usio sahihi na ni kumbabaisha anayekutana na ibara kama hizi ilihali yeye ni mchanga. Mfano wa Kumi na Tisa: Kumkufurisha Razi, Mfasiri Mashuhuri: Sheikh katika ad-Durarus-Saniyyah (10/72, 273) kamkufurisha Razi, mfasiri mashuhuri. Bali Sheikh, Mungu amsamehe katika adDurarus-Saniyyah (10/355) amedhani kuwa huyu Razi ametunga kitabu kinachoona kuabudu nyota ni jambo zuri. Na amesema kuwa amenakili hii kutoka kwa Ibn Taymiya katika kitabu Iqtidhau Sirati Mustaqiim. Na nilifanya rejea ya kitabu kilichotajwa lakini sikugundua maneno haya. Na endapo haya yatakuwa sahihi kutoka kwa Ibn Taymiya bila shaka atakuwa amekosea, kwa kuwa Razi ni mwanachuoni Mwislamu hawezi kuona kuabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu ni jambo zuri.61 Inawezekana alitunga kitabu kuhusu faida za nyota na kuathiri kwao mimea, au alinakili maneno kutoka kwa wanajimu, hali akiwa yeye hasemi hayo wala haamini, na ndipo Ibn Taymiya au Shekh, Mungu amsamehe, akamnasibisha nayo, kisha sisi tunaponukuu maneno ya Ibn Taymiya au Sheikh Muhammad ndipo wafuasi wake wanasema: “Wananakili kutoka kwa Manawasibu na Makhawariji!” Kwa hakika Mwenyezi Mungu ameharamisha uwongo na dhulma yote, hivyo si sahihi tumtuhumu mmoja wa wanazuoni wakubwa wa Kiislamu tuhuma kubwa kama hizi ila kwa uthibitisho katashauri. 61

Dhahbi na as-Sabakiy na Ibn Khalkan na wengineo wamemsifia, na yeye ni mwanachuoni na mfasiri na mwana misingi ya sharia na mwanatheolojia wa Kiislamu, na ni tabibu. Anayo makosa kama wengine walivyo na makosa, lakini sio makosa ya kufuru kama asemavyo Sheikh, lau angekuwa anaona kuabudu nyota ni jambo zuri hao wangemlaumu au wangemkosoa au kwa uchache wangeusema ukafiri huu. Lau tutamkufurisha kila aliyekosea hatobaki na sisi mtu yeyote. 122

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 122

1/20/2016 11:35:52 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Mfano wa Ishirini: Kuyakufurisha Makundi Mbalimbali: Anayakufurisha makundi mbalimbali ambayo hakuna kinachowakusanya pamoja ila uhasama wa Sheikh, na kuwaona kuwa wanafanya shirki. Na tumekwishatambua upanuzi wa Sheikh katika kuelezea shirki na kuwa kiasi kikubwa cha anayoyakanusha yanaingia katika bidaa au shirki ndogo, na si kubwa. Na tumeshajua jinsi anavyomkufurisha mwenye kuwafanyia uadui walio washirikina (kwa rai yake) bila kuwakufurisha. Na anavyomkufurisha asiyeipenda wala kuichukia tawhidi. Na anavyomkufurisha asiyeijua shirki. Na anavyomkufurisha asiyejua tawhidi. Na anavyomkufurisha anayeifanyia kazi tawhidi lakini haijui kadiri yake! Na wala hamchukii mwenye kuiacha na wala hawakufurishi. (ad-Durarus-Saniyyah (2/22). Nasema: Yote aliyosema Sheikh ni sahihi lau angekusudia kwa shirki hiyo shirki kubwa ambayo imeafikiwa na wote kuwa ni shirki kubwa. Ama kuwalazimisha watu maana yake ya shirki na tawhidi, maana ambazo wanazuoni wengi wa zama zake hawaafikiani naye, hili linafanya jambo liwe la kuhitilafiana, kwa hiyo hapana budi kutofautisha kati ya shirki ndogo na shirki kubwa, na kati ya shirki na bidaa. Kisha ukufurishaji na kuua vinathibiti kwa ambao ni wenye shirki kubwa. Lakini hili halikutokea, tumeona kuwa mengi anayokanusha Sheikh ikiwa ni sahihi ukanushaji wake basi upeo wa juu kabisa wa makadirio ya mambo hayo ni bidaa na upotovu au ni shirki ndogo na si shirki kubwa. Ila ikiwa katika ardhi ya Arabuni kuna watu mmoja mmoja wanaohesabika, hili latarajiwa, lakini hili halihalalishi uhasama huu mkubwa miongoni mwa kukufurisha na kuua, vitendo ambavyo Sheikh na wafuasi wake wamevifanya maeneo yote. Kwa hiyo ukafiri anaowaudhi hao wengine miongomi mwa watendao bidaa na upotovu ni ukufurishaji mkubwa unaomtoa mtu nje ya Uislamu. Tanabahi kwa hili. 123

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 123

1/20/2016 11:35:53 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Mfano wa Ishirini na Moja: Kuwakufurisha Wengi Miongoni Mwa Watu wa Sham: Na kuwa wao wanamwabudu Ibn Arabiy, na kumkufurisha mwenye shaka na ukafiri wa Ibn Arabiy. Na ukufurishaji wa Sheikh kuwakufurisha wengi miongoni mwa watu wa Sham na kuwa wao wanamwabudu Ibn Arabiy upo katika ad-Durarus-Saniyyah (2/45). Wafuasi wa Ibn Arabiy hawamwabudu yeye, hata ikikutwa miongoni mwa wasiojua, mtu afanyae hivyo, haijuzu kueneza hukumu hiyo kwa wafuasi walio wengi. Ama kumkufurisha kwake mwenye kuwa na shaka na ukafiri wa wafuasi wa Ibn Arabiy utalikuta jambo hilo katika ad-Durarus-Saniyyah (2/45)(10/25). Mfano wa Ishirini na Mbili: Fiqhi Ndio Shirki Yenyewe: Nahofia kuwa nitakuwa nimekosea katika kuyafahamu maneno ya Sheikh hapa, kwa kuwa yeye katika risala yake kwa Ibn Isa ambaye alimlalamikia kuwa mafaqihi wanaona usiyoyaona; Sheikh ameitaja Aya tukufu “Wamefanya makuhani wao na watawa wao kuwa ni miungu badala ya Mwenyezi Mungu” Akasema: “Mjumbe wa Mwenyezi Mungu aliifasiri na maimamu baada yake kuwa ni hii ambayo mnaiita Fiqhi. Na hii ndiyo Mwenyezi Mungu aliyoiita shirki na kuwafanya miungu, na siijui tofauti kati ya watu wa tafsiri katika hilo!” haya ndio maneno yake katika ad-DuraruS-Saniyyah (2/59). Nasema: Hadithi ni Hadithi ya Adiy bin Hatim. Kuna mzozo mkubwa katika hadithi hiyo. Pili: Vipi vitabu vya fiqhi ambavyo hasimu amevitolea hoja viwe ndio shirki?! Ikiwa anakusudia kuwa mahasimu wake wanavifuata, yeye pia anafuata baadhi ya ufafanuzi wa mafaqihi katika mlango wa ‘mwenye kuritadi’. 124

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 124

1/20/2016 11:35:53 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Mfano wa Ishirini na Tatu: Watu wa Washmu ni Makafiri: Kuwakufurisha watu wa Washim miongoni mwa wanachuoni na watu wa kawaida, utakukuta katika ad-Durarus-Saniyyah (2/77). Mfano wa Ishirini na Nne: Watu wa Sadir ni Makafiri: Kuwakufurisha watu wa Sadir miongoni mwa wanazuoni na watu wa kawaida. Tazama ad-Durarus-Saniyyah (2/77). Mfano wa Ishirini na Tano: Anasema katika ad-Durarus-Saniyyah (1/43), katika risala yake kwenda kwa mmoja wa makadhi mashuhuri jina lake ni Abdullah bin Abdilatif: “Uzuri ulioje kwako ikiwa katika mwisho wa zama hizi utakuwa Faruqu wa dini ya Mwenyezi Mungu kama Umar K alivyokuwa hapo mwanzoni.� Nasema: Ni kama hivyo anaona kana kwamba wanaomkhalifu yeye si Waislamu ?! Mfano wa Ishirini na Sita: Wanatheolojia ni Makafiri: Amenakili katika ad-Durarus-Saniyyah (1/53) ijmai juu ya kuwakufurisha wanatheolojia. Tamko hili si sahihi, halitoi tamko hilo mwenye kujua maana ya neno al-Mutakalimu (mwanatheolojia), kwa kuwa likitumika moja kwa moja humaanisha wanazuoni wa Kiislamu watiliao manani suala la itikadi na hususan ni miongoni mwa Ashairah na Muutazilah, kwani mutakalimu (mwanatheolojia) Mwislamu, ni Mwislamu japo aingiye katika bidaa au kufuru kwa taawili. Na hata Ibn Taymiya naye ameingia - na yeye ni miongoni 125

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 125

1/20/2016 11:35:53 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

mwa mutakalimina (wanatheolojia) wa Kihanbali - katika mambo ambayo baadhi ya Masalafi wanayahesabu kuwa ni ukafiri. Mfano wa suala la mfululizo wa matukio na uzamani wa aina fulani wa ulimwengu, na kusahihisha Hadithi ambayo ni batili isemayo kuwa eti Mungu yupo katika umbo la kijana asiye na ndevu..... Mungu Mtukufu yu mbali na hayo. Hata hivyo yeye si kafiri kwa kuwa ameleta taawili, amedhania kuwa Hadithi hii batili iko sahihi, au usahihi wa fikra maalumu....mpaka mwisho.... Hivyo basi sio kila aliyeuangukia ukafiri huwa ukafiri umemuangukia. Yakaribia asisalimike mwanachuoni wala mtu wa kawaida katika kusema neno la kufuru, lakini hakufurishwi. Na Sheikh amenakili kutoka kwa Dhahbi, Daruqutniy, Bayhaqiy na kutoka kwa wengine kuwa wamewakufurisha Mutakalimuna (wanatheolojia), na hii ni nukuu batili, kwani hao watatu hata nao ni Mutakalimuna (wanatheolojia). Na kwa uchache tumetambua kutoka kwa baadhi yao kuwa hawawakufurishi Mutakalimuna (wanatheolojia). Tumeyajua hayo kumhusu Dhahbi kwa uchache, hiki hapa kitabu chake an-Nubalau kimejaa wasifu wa Mutakalimuna (wanatheolojia). Sikumbuki kama alimkufurisha yeyote miongoni mwao. Naam, huenda akamchukulia ni mfanya makosa na bidaa lakini hawakufurishi kama alivyonakili Sheikh Muhammad, bali yeye Dhahbi wakati mwingine huwatolea udhuru baadhi yao, wale wenye kutokewa na dosari kubwa, ambapo huwatolea nyudhuru nyepesi, kama vile kusema: “Huenda alilisema katika hali ya ulevi, huenda alisema hili naye akiwa hivi au vile...� Mwenye kutaka kufuatilia hili na arejee kitabu hiki. Bali Dhahbi anaona inafaa kutabaruku na udongo wa makaburi ya watu wema kama ilivyotangulia, na yeye kulingana na utaratibu wa Sheikh, ni kafiri ukafiri mkubwa unaomtoa nje ya Uislamu. Na mambo ambayo Sheikh anamtolea udhuru Dhahbi yawezekana kumtolea udhuru Ibn Sahim na Ibn Feyrouzi na Ibn Afaliq na wen126

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 126

1/20/2016 11:35:53 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

gine katika aliowakufurisha Sheikh miongoni mwa wanazuomi wa Kihanbali katika zama zake. Bali Mahanbali wana vitabu vitatu kuhusu fadhila za kaburi la Ahmad bin Hanbali, na imetangulia kumesemwa kuwa Mahanbali waliotangulia takriban walikuwa Masufi, lakini ni wafurutu ada katika maudhui ya sifa na kuumbwa kwa Qur’ani na swahaba, wao humkufurisha mtu kwa tofauti ndogo aliyonayo dhidi ya utaratibu wao. Ama Daruqutniy, yeye ana vitabu ambavyo vimenasibishwa na yeye, wala hausihi mnasibisho huu, wameuweka baadhi ya Mahanbali, hivyo yawezekana nukuu ya Sheikh ni kutoka humo. Ama alBayhaqiy yeye ni Ashairah, na rai ya Sheikh kuwaelekea Ashairah ni kali inakaribia kukufurisha. Mfano wa Ishirini na Saba: Watu wa Ahsai Wanaabudu Masanamu: Na anasema katika ad-Durarus-Saniyyah (1/ 54): Kuwa watu wa Ahsai katika zama zake walikuwa wanaabudu masanamu!! Nasema: Hii sio sahihi. Mfano wa Ishirini na Nane: Watu wa Najdi Wanaabudu Jiwe na Mti: Na amesema katika risala yake kwa Ibn Abdulatif katika ad- Durarus-Saniyyah (1/53-54): Kuwa kwao kuna ibada ya masanamu “miongoni mwa watu na mawe,” na juu ya hayo amezidisha kuwa “hamjui yeyote miongoni mwa wenye elimu aliye kinyume na maelezo hayo” isipokuwa “anayemwamini Jibti na Taghuti.” Na kwamba wenye elimu katika mji wa Ibn Abdulatif “wamevaana na shirki kubwa” bali “wanailingania.” 127

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 127

1/20/2016 11:35:53 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Nasema: Haya yote ni uzidishaji chumvi, hakuna uhakika wala ukweli wa hayo, na ufurutu ada wa wanazuoni na makadhi wa Najdi, Hijazi, na hasa Waislamu katika zama za Sheikh ­Muhammad, endapo watapatikana basi ni mfano wa ufurutu wa wengine miongoni mwa wanazuoni na makadhi katika ulimwengu wa Kiislamu; katika zama zake na kabla yake na baada yake, na katika siku za Ibn Taymiya na Ahmad Bin Hanbal. Hivi hapa vitabu vyao na risala zao, na wao hawajanakili kutoka kwao ibada ya masanamu wala kulingania masanamu. Ama ufurutu ada juu ya masheikh na kutabaruku ni mambo ambayo inawezekana kukubali kuwekwa kwenye tabaka ambalo ndani yake mna bidaa na upotovu, na wala si kwenye tabaka la shirki kubwa imtoayo mtu nje ya Uislamu. Mfano wa Ishirini na Tisa: Kauli Yake Katika ad-Durarus-Saniyyah (1/73): “Mimi namkufurisha mwenye kuijua dini ya Rasuli kisha baada ya kuijua anaikashifu na kuwazuia watu wasiifuate, na kumfanyia uadui mwenye kutenda kwa mujibu wake...” Nasema: Maneno haya Sheikh huyakariri sana, nayo ni sahihi kinadharia, lakini kiukweli kwa “dini ya Rasuli” anakusudia aliyonayo yeye na wafuasi wake. Mahasimu wake miongoni mwa wanazuoni na makadhi na watu wa kawaida hawasemi kuwa wao wanaifanyia uadui dini ya Uislamu bali yeye anatambua kuwa wao wanatekeleza nguzo tano za Kiislamu na hawajawahi kuwa maadui wa dini ya Rasuli wala hawajawakataza watu kuifuata. Na wao wanajibu kwa hoja hiyohiyo wanasema: Kuwa miongoni mwa dini ya Rasuli ni tusimuue asemaye: LA ILAHA ILA LLAHU, kwa kuwa tamko hilo linahifadhi damu yake na mali yake. Na wanasema kuwa Sheikh Muhammad amelitambua hilo kisha amewakataza watu hilo na kuwa na 128

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 128

1/20/2016 11:35:53 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

uadui nalo, kwa minajili hiyo yeye ana uadui na dini ya Rasuli na anawakataza watu kuifuata. Ni kama hivyo hatujatoka kwenye mzunguko wa methali ya ­Kiarabu: “Mto umerudi na kumwaga maji yake kwenye chanzo chake.” Hivyo Sheikh na mahasimu wake wanakufurishana kwa kuwa wote wamepuuza vidhibiti na vizuizi vinavyozuia kumkufurisha mtu,62 na wote wanakata shauri katika mambo ambayo baadhi yake ni sahihi, na mengi kati yake ni yanayofanana, yaliyoingiliana ambayo ni vigumu kuyakatia shauri, lakini wote hawaamini uwiano katika mambo kama haya. Mas’ala moja ikiwa na uzito kwa mmoja wao ataihesabu kuwa ni katika dini ya Rasuli, na asiyeifuata anakuwa ni adui wa dini ya Rasuli! Na hii ni vurugu ya kielimu iliyochanganyikana na dhulama na kukufurishana na kupotoka katika uhasama. Na kukufurisha kunafika mbali zaidi kuliko kutukana na kulaumu, na huenda hali ya mambo kisiasa ikasaidia hilo, na uhasama wa kimadhehebu na ushabiki wa kizalendo, kikabila na kimadhehebu, Mungu awarehemu wote. Na sisi tunatakiwa tujifunze kutokana na makosa yaliyopita na tusiyarudie makosa hayo, kwani historia haina huruma, na kosa ambalo leo tunalisitiri, kesho yatakuwa makosa mawili, na Siku ya Kiyama yatakuwa matatu. Kosa limetokea, na kulifanyia ushabiki ni kosa la pili, na kuwapiga vita tuliowatanabahisha ni kosa la tatu, na kwa Mungu uhasama utajikusanya. Mfano wa Thelathini: Na Anaona Kuwa Itikadi Kuwahusu Watu Wema ni Zaidi ya Zinaa na Wizi: Na anaona kuwa itikadi kuwahusu watu wema sio kama zinaa na wizi bali hiyo ni ibada ya masanamu,63 na anairudiarudia sana maana   Ilihali wengi kati ya mahasimu wake hawamtuhumu kwa ukafiri mkubwa wala kuwa anaabudu masanamu, ila tu wanamtuhumu kuwa ni Khawariji. 63   ad-Durarus-Saniyyah (1/78). 62

129

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 129

1/20/2016 11:35:53 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

hii, ilihali neno itikadi kuwahusu watu wema ni neno lina maana enezi; inaingia ndani yake tawasuli na tabaruku na mfano wa hayo miongoni mwa mambo ambayo wamesema kuhusiana nayo wengi wenye elimu; na hususan tabaruku, na mimi sioni hili wala hili, na nimegombana na baadhi ya wanafunzi wa elimu miongoni mwa ambao wanaona tabaruku kuwa ni sawa, na nilishinda kwa kutumia rai ya Sheikh katika kuikanusha; ambayo naona ipo karibu na ukweli, lakini kukiri kwetu kuwa yuko katika haki katika kukanusha kwake itikadi hizi maana yake sio kukubali kumkufurisha asiyeafikiana naye miongoni mwa wanazuoni na watu wa kawaida, kwa kuwa kiasi kikubwa cha aliyoyakanusha Sheikh kwao aghlabu ni ijitihadi sahihi au yana sababu, au ni makosa na bidaa ndani yake kuna mkanganyiko na taawili na mfano wake na ufafanuzi wake umetangulia huko nyuma. Mfano wa Thelathini na Moja: Kuyakufurisha Makundi Kadhaa: Amesema katika ad- Durarus-Saniyyah (1/102) kuwa yeye anayakufurisha makundi haya yafuatayo:

• •

Mwenye kuijua dini ya Rasuli 5 na wala haifuati! Mwenye kumjua yeye na kumpenda lakini anamchukia mwenye kuingia katika Tawhidi na anampenda aliyebaki katika shirki! • Mwenye kuijua dini lakini anaitukana na anawasifu wanaomwabudu Yusufu, Ashqar na al-Khidhri! • Mwenye kusalimika na haya yote lakini hahami kutoka katika mji wake, mji wa kishirikina kwenda mji wa Tawhidi.64 Nasema: Katika hali hizi nne pia tunakutana na methali ya Kiarabu: “Mto unamwaga kwenye chimbuko lake.” Na jibu limetangulia 64

La kushangaza ni kuwa yeye Sheikh mahali pengine anakanusha kuwa yeye hamkufurishi asiyehamia kwake! Na hiki ni kigeugeu au kurejea kinyume na kauli ya kwanza. 130

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 130

1/20/2016 11:35:53 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

huko nyuma. Kuwa hawamkubalii Sheikh kuwa haki iko pamoja na yeye katika kila analosema. Au kuwa batili waliyonayo wao katika kila wasemalo, na linalomsababisha Sheikh kukanusha bidaa halimsababishi kumkufurisha mfanya bidaa, mjinga na wanaofanya taawili katika wanazuoni na walio wengi. Kisha vipi tutaweza kutia akilini ukweli kuwa kuna anayeijua Tawhidi na aipenda na anaifuata na anaingia ndani yake na anaacha shirki; kisha baada ya haya yote anamchukia aliyeingia katika Tawhidi na anampenda aliyebakia katika shirki?! Hii haiingii akilini. Hakuna mtu duniani aipendaye dini au madhehebu na kuwachukia watu wa dini ile au madhehebu ile isipokuwa ikiwa anawachukia kwa jambo anaona kuwa wao wamefanya kinyume na dini ile au madhehebu ile. Mfano, sisi Sunni huenda tukachukiana sisi kwa sisi kwa mahasimu wawili kudhania kuwa upande wa pili hawaitekelezi Sunna na kuwa wanaifanyia ubaya.65 Hakuna Mwislamu anayemchukia mwenye kuingia katika Uislamu wala Naswara amchukiye mwenye kuingia katika unaswara wala Shia amchukiye mwenye kuingia katika Ushia wala Msalafi amchukiye mwenye kuingia katika usalafi, hili ni tamko la ajabu sana. Naam, mtu anaweza kumuona yuko sawa katika baadhi ya anayoenda nayo; Nayo ni kama kukanusha bidaa na kulingania Tawhidi safi lakini asiende naye mpaka mwisho wa njia na awakufurishe. Kwa maana awe anajua kuwa katika kauli za Sheikh kuna ya haki na ya batili; basi yeye achukue ya haki na aiache ya batili, na Sheikh anamtaka ima akanushe yote ayasemayo au amfuate yote. Na hili halilazimu ila katika daawa ya Manabii ambao ni wajibu kuwafuata 65

  Kama alivyochukiana Sheikh na mahasimu wake hali ikiwa wote ni Waislamu na wote ni Ahlus-Sunna, na kama Imamu Maliki alivyochukiana na Ibn Is’haqa na hao wote ni Waislamu. Na kama hivyo uhasama mwingine wa watu wamoja hapana budi ufuatane na chuki lakini chuki hii haifai, isimsukume mwenye chuki kumkufurisha hasimu wake, ila kuwe na dalili iliyowazi yenye uthibitisho kutoka kwa Mungu s.w.t. 131

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 131

1/20/2016 11:35:53 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

katika kila wasemalo na kila wanaloamrisha na wanalokataza, ama watu wengine miongoni mwa Makhalifa, wanazuoni, watu wamefanya kinyume nao katika baadhi ya mambo, lakini hawakusibiwa na ukufurishaji wala uuaji kutoka kwao. Baadhi ya Maswahaba walikwenda kinyume na Imamu Ali D katika vita vyake dhidi ya Mabughati, na baadhi ya watu walimpiga vita, na watu wengine waliwafanya watu wamtelekeze, na wala hakuwaambia waliosimama bila ya kuingia naye katika vita wala waliomtelekeza wala waliompinga: Kuwa wao wameitukana dini ya Rasuli! Au wamewakataza watu ili wawe mbali na dini ya Rasuli, ilihali dini aifuatayo Ali bin Abu Talibi, Ammar bin Yasir ni safi mno na nadhifu mno kuliko dini aifuatayo Muhammad bin Abdul-Wahabi. Lau Imamu Ali angefuata mwenendo wa Sheikh basi angewakufurisha watu wa Jamal na watu wa Siffin na al-Haruriya kwa madai kuwa wao wanaipiga vita dini ya Rasuli! Ikiongezewa kuwa yeye alikuwa anamiliki Nususi makhsusi zaidi ya zile za kawaida ambazo kwazo anaweza kuzitegemea katika kuyakufurisha makundi haya.66 Sahihi kuwa imekuja habari kutoka kwa Imamu Ali D kwamba alikuwa anasema: “Sina lingine ila kuwapiga vita au kukufuru yaliyoteremshwa kwa Muhammad,” hilo alikuwa anajikusudia yeye mwenyewe, yaani lau asingewapiga vita Mabughat na Makhawariji angekuwa kana kwamba ameikufuru Aya tukufu: “Basi lipigeni 66

Miongoni mwa Nusus kuwahusu Makhawariju ni “Watatoka nje ya Uislamu kama utokavyo mshale kwenye utupaji.” Na miongoni mwa Nusus kukihusu kikundi cha pili, kikundi cha Muawiya ni: “Wanaitia kwenye moto.” Hivyo kwa nususi hizo ilikuwa inawezekana kwa Imamu Ali D – na aliokuwa pamoja nao miongoni mwa wana Badri na Ridhwan kuyakufurisha haya makundi mawili Makhawariji na Mabughat lau angeliitikia hamasa ya ndani kwa ndani na hali ya nje ya kivita. Alikuwa anaweza kusema mwenye kutoka nje ya Uislamu utokaji wa mshale kwenye utupaji hatorudi humo! Na mwenye kuitia kwenye moto si Mwislamu. Na al-Qasituna wao watakuwa kuni za Jehannam. Lakini Imamu Ali D na aliokuwa pamoja nao miongoni mwa wana Badri, walikuwa wachamungu mno kiasi cha kutoweza kuzitumia Nusus mahali pasipostahiki katika kuwakosoa Mabughat na Makhawariji na kuwajibisha kuwapiga vita. 132

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 132

1/20/2016 11:35:53 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

linalodhulumu mpaka lirejee kwenye amri ya Mwenyezi Mungu.� (Sura Hujurat: 9).67 Hivyo basi kufuru hapa inamaanisha kutoitikia amri za Aya hii, lakini yeye hakuwakufurisha Mabughati wala Makhawariji sembuse waliosimama bila ya kupigana pamoja na yeye na waliomtelekeza. Na udhuru wao ni utata uliojitokeza kwao japokuwa iwe anajua kuwa baadhi ya wakuu wao kama Muawiya hawakuwa na dhamira ila ni mpemda ufalme tu, lakini sera katika kuwapiga vita Mabughat ni lazima iwe kwa kuyatendea kazi matakwa yao ya dhahiri, na huu ndio ukamilifu wa uadilifu na hasimu, kwa kuwa kuitendea kazi nia na yanayotazamiwa sio njia ya kisharia, lau ingekuwa sharia Nabii 5 angewatendea wanafiki, na Imamu Ali D angemtendea Muawiya na Makhawariji. Na kwa ufupi ni kwamba ikiwa kupigana pamoja na Ali bin Abu Talib D si wajibu kwa mtu ambaye umemtokea mkanganyiko licha ya kuwepo dalili za jumla na makhsusi zilizo sahihi na nyeupe za 67

  Aya hii ni muhkam, baadhi ya wanazuoni wa Kihanbali miongoni mwa watu wa Sham waliompiga chenga Ali D, nao ni Ibn Taymiya, wamejaribu kwenda mbali na kudhania kuwa kimsingi Mungu hajaamuru kuwapiga vita kikundi hiki cha Mabughati. Na amesahau au kajisahaulisha kuwa pia sulhu haijaamuriwa kimsingi katika hiyo Aya! Bali aliamrisha baada ya mapigano! Je mwenye akili atasema kuwa sulhu kati ya makundi mawili sio sheria mpaka yapigane?! Ikiwa ameganda juu ya maana ya dhahiri ya tamko la Aya, basi na agande juu ya dhahiri ya kila Aya zote; na ikiwa anaona Sulhu kimsingi ni sheria japo kuwa haikutokea; itamlazimu aone kupigana na kikundi kiovu hata kama sulhu haijatokea. Ima abaki ameganda kwenye nusu ya Aya na kuiacha sehemu iliyobaki, na huko ni kupingana kunakojulisha hawaa. Sulhu inaweza kutimia bila ya kutanguliwa na vita, kama ambavyo uovu wa kijeuri unaweza kuwepo bila ya kutanguliwa na sulhu. Hilo linajulishwa na Nabii 5 kwani alikiita kikundi cha Muawiyya kuwa ni Mabughat kabla hapajatokea ila wito wake wa umoja. Hivyo ima hii iwe ndio sulhu iliyoamriwa katika Aya katika hali ambayo hasimu amekwisha kuwa Imamu kisheria, na ima uthibiti uovu wa kijeuri usiotanguliwa na sulhu. Na tukiweza kufaidika na kugundua kuwa sulhu ni sheria moja kwa moja nje ya Aya, tunaweza pia kufaidika na kugundua kwa urahisi kuwa kuwapiga vita Mabughat na wasambaratishaji wa umoja nje ya Aya, kwa hili na lingine imebainika kuwa kamba ni fupi, japo baadhi ya wanazuoni wa Sham wavumishe sauti kuizunguka! 133

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 133

1/20/2016 11:35:53 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

wajibu wa kupigana na Mabughat na Makhawarij, basi kupigana pamoja na Sheikh Muhammad na kuwakufurisha wanaomkhalifu si wajibu kabisa. Hivyo hivyo kumkufurisha kwake asiyehama na kuacha mji wake! Hili ni kosa pia, kwa kuwa Hijra kisharia ambayo ni wajibu na hukufurishwa atakayeacha kufanya akiwa mwenye kuweza, ilikuwa Hijra ya kwenda kwa Nabii 5, ama hijra baada yake 5 huwa wajibu kwa sharti, bila ya kukufurishwa mwenye kuacha, na huenda isiwe wajibu kwa maslahi mengine mfano wa zama zetu hizi, sio jaizi kwetu kuwakufurisha Waislamu wanaonyanyasika duniani ambao hawataki kuihama miji yao. Mfano wa Thelathimi na Mbili: Kauli Yake Kuwahusu Ashaira na Dhwahiria: Sheikh katika ad-Durarus-Saniyyah (1/112) amenakili kauli inayomaanisha kumkufurisha Ash’ariy na mwingine miongomi mwa wanaokataa sifa! Na Ibn Hazmi yeye anakanusha sifa moja kwa moja, na hoja zake utazikuta katika kitabu chake Alfaslu, zisomeni kabla hamjamkufurisha. Mfano wa Thelathini na Tatu: Kauli Zake Kuwahusu Ashaira, Muutazila na Wengine: Amesema katika ad-Durarus-Saniyyah, uk. 113: “Mwenye kusimamisha sifa – ni shari mno kuliko mshirikina!!” Na wasimamisha sifa kwa mujibu wa Masalafi wanaingia ndani yake Ashaira na Ibn Hazmi ambaye ni Dhwahiriyyah na kundi kubwa la Dwahiriyyah na wengi miongoni mwa Masufi, Shia, Mahanafi na wengi miongoni mwa wafuasi wa madhehebu nne isipokuwa mwenye kuwakalidi wafurutu ada wa kihanbali na Ibn Taymiya na Ibn alQayyim Mungu awarehemu. Na kanuni hiyo imewatoa wengi nje ya Uislamu. 134

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 134

1/20/2016 11:35:53 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Mfano wa Thelathini na Nne: Rejea ya Kumkufurisha Ibn Arabiy na Ibn al-Faridh: Kisha alisema katika ad-Durarus-Saniyyah, uk. (1/113) kuwa “Kumkataa Mola Mtukufu ndio madhehebu ya Ibn Arabiy na Ibn al-Faridh na kundi la watu ambalo hakuna ajuaye idadi yao ila Mungu.” Ilihali katika uk. 34 amesema hawakufurishi!! Akasema: “Wamesema kunihusu mimi kuwa mimi ninawakufurisha Ibn alFaridh wa Ibn Arabiy... Jibu langu juu ya mas’ala hizi nasema: Ewe Mungu utakatifu ni Wako, huu ni uzushi mkubwa.” Lakini amesema wazi katika uk. 14 kuwa yeye hamkufurishi mwenye kuabudu sanamu. Nasema: Vipi kwako inakuwa sahihi kwamba wao wanamkanusha Mola kisha hauwakufurishi?! Wala haumkufurishi anayeabudu sanamu?! Ilihali unawakufurisha wanaomwamini Mungu na Mtume Wake na atekelezaye nguzo za Uislamu na anayejiepusha mbali na yaliyoharamishwa pamoja na makosa yanayoambatana na hayo, sawa iwe katika itikadi au amali. Mfano wa Thelathini na Tano: Kuwahusu Ashaira Pia: Amesema katika ad-Durarus-Saniyyah, uk. (1/113) kuwa: “Anayekanusha sifa ni mwenye kukanusha hakika ya uungu.” Nasema: Na hii inamlazimu kuwakufurisha Ashaira na Ibn Hazmi na wengi miongoni mwa wafuasi wa madhehebu nne, na hali wao hawakanushi hakika ya uungu. Na alimtuhumu al-Ash’ariy na akamuita “Imamu wao mkubwa”, tazama uk. 114, akikusudia kuwa yeye ni imamu wa Muatila68 au 68

Al-Muatilah ni istilahi wanayoitumia Masalafi kuyaita makundi ambayo yanakunusha dhidi ya dhati ya Mwenyezi Mungu maana ya majina na sifa zilizotajwa katika nususi 135

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 135

1/20/2016 11:35:53 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

wa wanatheolojia, na mimi ni miongoni mwa anayemchukulia alAsh’ariy makosa makubwa hususan katika madai yake ya ijmai juu ya mambo yanayohitilafiwa. Na ninashajiisha jibu la kumpinga la haki kama tunavyoshajiisha jibu la kumpinga Ibn Taymiya la haki pia sio la batili, wote wawili ni Waislamu mafakihi wana elimu zao na mema yao, lakini tu wameingia katika baadhi ya makosa, sawa yawe makubwa au madogo, japokuwa makosa ya Ibn Taymiya ni makubwa mno kuliko makosa ya al-Ash’ariy. Mfano wa Thelathini na Sita: Kuwakufurisha Waislamu Wengi Katika Zama Zake: Kauli yake kuwahusu Waislamu waliokuwa katika zama zake, katika ad-Durarus-Saniyyah, uk.117: “Na wengi miongoni mwa watu wa zama hizi hawaijui Miungu iabudiwayo isipokuwa Hubal, Yaghuth, Yauqu, Nasra, Lata, Uzza na Manata!! Endapo fahamu yake itakuwa nzuri atatambua kuwa heshima zinazoabudiwa leo miongoni mwa wanadamu na miti, mawe, na mfano wake mfano wa Shamsani na Idirisa na Abu Hadiyda na mfano wa hao ni sehemu ya Miungu hiyo.” Nasema: Hakuna la kuongeza! Na katika tamko lifuatalo amewafanya Waislamu wengi kuwa ni makafiri!! Mfano wa Thelathini na Saba: Waislamu Wengi ni Makafiri Sana Kuliko Makafiri wa Kikuraysh: Na amesema katika ad-Durarus-Saniyyah, uk.120: “Shirki ya makafiri wa Kikurayshi ni hafifu kuliko shirki ya watu wengi hii leo.” na za matendo ya Mwenyezi Mungu, au wanaziletea maana nyingine, kama vile kundi la Jahmiyyah, Muutazila, Ashairah, Matridiyyah - Mhariri. 136

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 136

1/20/2016 11:35:53 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Na hawa watu makafiri kwa mtazamo wa Sheikh ndio walio wengi. Anasema katika ad-Durarus-Saniyyah, uk. 160: “Ukijua hili na ukijua ambayo waliyonayo watu wengi hii leo, utajua kuwa wao ni makafiri na washirikina wakubwa kuliko washirikina aliowapiga vita Nabii 5.” Na amesema katika ad-Durarus-Saniyyah, uk. 162: “Katika hao makafiri ni yule ambaye anahukumu kwa asiyoteremsha Mwenyezi Mungu.” Na hii ni nguzo na tegemeo ya wale ambao wanamkufurisha mtawala, aina hii imekumbana na ukosoaji kutoka kwa wanazuoni wa wakati huu, lakini la kusikitisha ni kwamba ukosaji huo ulifanyika kwa sababu za hali ya hewa ya kisiasa wala si kwa msukumo kutoka kwa wanazuoni kiasi cha kufanya maneno yao yawe na mashiko kwa vijana, hivyo hao vijana wanawaambia wanazuoni: “Ninyi mmekuwa ndio sauti ya mtawala, akiwachukia watu fulani mtawakufurisha, akiwakataza mnakatazika.” Kwa minajili hiyo hawawi na mashiko, lakini lau wangesimama toka zamani na kukemea ufurutu ada katika kukufurisha na kutoa jibu la kupinga ukufurishaji huo, wanazuoni wasingeangukia k­ wenye shida hii, hivyo hivyo watawala. Nasema haya ikiwa ni pamoja na kutaka sheria ya Uislamu itawale katika kila mambo yetu, lakini tunataka sheria itokayo kwenye Kitabu na Sunna sio kutoka kwenye fikra finyu za kimadhehebu wala kutoka kwenye uteuzi wa baadhi ya wanazuoni. Na hili lahitaji kuwa wazi kuihusu kila madhehebu ya Kiislamu pamoja na kufanya mazumgumzo na utafiti tulivu wa kina na darasa la kutosha. Mfano wa Thelathini na Nane: Madai Yake Kuwa Hamkufurishi isipokuwa...: Na amesema katika ad- Durarus-Saniyyah (1/234) kuwa yeye hamkufurishi ila: “Mwenye kufikiwa na daawa yetu kwa ukweli, na 137

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 137

1/20/2016 11:35:53 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

imemuwia wazi, na hoja imemdhihirikia na yeye akang’ang’ana kwa kiburi hali ni mpinzani.” Halafu hilo alilitolea mfano kwa kauli yake: “Kama ambavyo wengi tunaopambana nao leo wanang’ang’ana na shirki hiyo na wanakataa kutenda wajibu na wanajidhihirisha na matendo ya dhambi kubwa, yaliyo haramu..” Nasema: Japokuwa aliyenukuu ni mmoja wa pande mbili, na kwamba mmoja wa mahasimu wawili bado hatujasikia kauli yake, isipokuwa sisi tumeujua udhuru wake kupitia nukuu ya Sheikh aliponukuu kutoka kwao baadhi ya hoja kama ilivyotangulia. Ikiwa kwa hakika tumejua usafi wao kupitia toleo pungufu kutoka kwa hasimu wao, basi hili lajulisha kuwa wao wako katika kiwango kikubwa cha nguvu ya hoja! Kwa hiyo wao hali yao hivi sasa ni kwamba wapo bila ya vitabu wala dola wala vyuo vikuu wala mimbari wala propaganda au daawa. Lakini tumejua hoja zao kupitia ubainisho wa Sheikh Muhammad Mungu amrehemu, kuwa wao ni Waislamu waumini, walikuwa kama Waislamu wengine duniani katika ulimwengu wa Kiislam siku hizo. Kisha tunamwambia Sheikh na wanaomkalidi na kumfuata: Hawa hawakubaliani na ninyi kuwa hoja yenu inakubalika, kuwa ni ya wazi, na kuwa eti wao wamefanya kiburi na kung’ang’ania. Kwa uchache hawaoni kuwa daawa yenu ndiyo ya haki nyeupe isiyo na mchanganyiko, bali kuna wanaolikubali hilo na wanaolikanusha. Mfano wa watu kama hawa hoja haijawa wazi kwao, ili kuifikisha hoja haitoshi kuituma risala au kuiandika kwenye vipeperushi, kwa kuwa wao wanaona mfano wa hoja kama hizi ambazo risala inatosha ni makhsusi kwa Nabii 5 ambaye daawa yake yote ni haki tupu. Ama baada ya elimu kuwa na utata na ijitihadi kuwa nyingi, kufika daawa peke yake hakutoshi, na hasa yanawafikia kutoka kwa wanachuoni wao yatokayo kwa Sheikh miongoni mwa yale ya kuku138

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 138

1/20/2016 11:35:53 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

furishwa na kuhalalishwa damu. Na kuenea kwa haya kwao ni zaidi kuliko kujinasua kwake na ukufurishaji. Bali tumewakuta baadhi yao kama Ibn Sahim yuko kwenye kiwango cha juu cha uaminifu kitaaluma kuzihusu nukuu zake kwa Sheikh, kwa namna ambayo sisi tumeyakuta yanayosadikisha kauli zake kutoka katika vitabu vya Sheikh, japokuwa Sheikh ameviita vitendo vya Ibn Sahim kuwa ni uzushi mkubwa! Hili linawafanya wanaohitilafiana na ninyi waingiwe na shaka na wasiwasi, hawana ithibati na kujinasua kulikotanguliwa na kufahamu kwao vitabu kwa hati yenu ambavyo ndani yake mna yanayohitilafiana na kujinasua huku. Kwa haya na yaliyo mfano wake ni miongoni mwa nyudhuru za hawa za kutoitikia na kutoingia katika daawa hii, basi ni kwa nini mnawakufurisha? Ikizingatiwa kuwa wao wanavyo vitabu vya fiq’hi, na vitabu vya Ibn Taymiya na Ibn al-Qayyim ambavyo vinakataa ukufurishaji wa jumla licha ya ufurutu ada uliyomo humo, mfano wa hao wanaohitilafiana na Sheikh katika wanazuoni na hasa wa Kihanbali, na hususan watu wa Najdi miongoni mwao, tumepata hoja zao zinazoutosheleza upinzani wa Sheikh dhidi yao. Baada ya zama hizi za ushindi wa daawa ya Sheikh na propaganda kubwa kuihusu kwa upanga na kalamu, sasa jambo hili linapelekea wanazuoni wa zama za Sheikh Muhammad na wa kabla yake wa huko Najdi, kujionea fahari kubwa. Na inajulisha kuwa wao wamefikia daraja zenye nguvu kielimu. Basi Mungu awarehemu wote na amrehemu Sheikh na wafuasi wake, na awajumuishe katika msamaha Wake na ghufrani Yake. Lau tungewauliza, je hoja imewafikia kama alivyosema Sheikh? Jawabu lao lingekuwa: Sisi tunatekeleza nguzo za Uislamu kwa ushahidi wa Sheikh mwenyewe, lakini yeye pamoja na hivyo huyu Sheikh na wafuasi wake wametukufurisha na wameona halali kutuua mpaka tuiache miji yetu na tuhamie kwake na tuwaue Waislamu 139

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 139

1/20/2016 11:35:53 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

pamoja na yeye ambao Mwenyezi Mungu ameharamisha kuwaua. Mfano wa hoja fupi kama hizi zinatosha kuchelea kuwakufurisha na kuwaua, mwenye kuona haya haifai kuwakufurisha, japo huenda ikawa jaizi kuwaua kwa zinaa au kuvamia watu njiani au dhulma. Mfano wa Thelathini na Tisa: Kukiri Tawhidi Hakuhifadhi Damu Wala Mali: La ajabu ni kuwa Sheikh Mungu amrehemu, analeta dalili za ajabu katika ad-Durarus-Saniyyah (1/145), nayo ni kuwa makafiri hata wakikiri Tawhidi ya Mungu Mmoja bado hakuhifadhi damu zao na mali zao. Nasema: Juu ya kukubali kuwa kati yao hakuna Dahriyuna wala wanaokanusha siku ya mwisho na unabii, hakika Tawhidi yao haihifadhi mali zao endapo tu watakuwa hawajatamka shahada mbili, lakini endapo watafanya japokuwa kwa ulimi tu damu zao zitahifadhika na mali zao kama vile wanafiki. Ama Sheikh na wafuasi wake Mungu awarehemu, hawatosheki na kutamka kwa watu shahada mbili wala kutekeleza nguzo tano za Kiislamu, haya yoote hayahifadhi damu zao wala mali zao kwa mujibu wao. Na semi za Sheikh zinazopingana zinafikia kiwango cha kustajabisha, yeye mara anapindukia katika kueleza wingi wa idadi ya makafiri kama katika (1/106-160) kadhalika katika (1/266), aliposema kuwa shirki imeijaza ardhi katika zama zake, huku akisema katika (1/83) kuwa wengi katika umma wapo katika dini sahihi! Mfano wa Arobaini: Kumkufurisha Asiyejua Iwapo Atatamka Neno la Kufuru: Sheikh anaona yafaa kumkufurisha mwenye kutamka neno la kufuru hata ikiwa hajui maana yake! Au amedhania kuwa halimkufurishi, 140

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 140

1/20/2016 11:35:53 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

tazama (10/120). Na ametolea ushahidi hilo kwa kisa cha wanafiki wa Tabuk! Ilihali hakifai kukitolea ushahidi. Kwa kuwa hao walikuwa wanajua maana ya wanayoyasema na kuwa wanafanya mzaha, na udhuru wao ni uwongo, tanbihi imeshafanyika kuhusu jambo hili.

MUHTASARI: Ni kama hivi kwa jumla tunakuta njia au utaratibu wa Sheikh na wanazuoni wote wa daawa, ni kukufurisha na ufurutu ada katika hilo. Nadhani mifano iliyotangulia inatosha sana kwa anayetaka kufanya insafu. Na lugha hii katika kukufurisha ndiyo inayochukua nafasi kubwa kwa asilimia tisini katika maneno ya Sheikh na wafuasi wake katika kukufurisha au katika kinachoitwa mas’ala ya majina na sheria. Na kuna kiasi kidogo hakizidi asilimia tano ndicho kipo kinyume na njia au utaratibu huo. Huenda ikawa Sheikh alisema au wafuasi wake katika wakati wa utulivu wa nafasi, au kwa ajili ya siasa, au kitu mfano wa hayo. Kwa minajili hiyo ni jaizi kwa mwanasiasa kutumia hiki kidogo cha kulaumu ukufurishaji, lakini mwanafunzi wa elimu ya dini ni wajibu ajue alama ya jumla ya njia fulani au fikra. Asijaalie kiwango kidogo kuwa ndio kinachochukua nafasi kubwa au afanye kinyume cha suala. Au kwa uchache anukuu njia mbili kisha aone upande wenye uzito kuwa ni huu au ule. Kwa minajili hiyo nimeona ninukuu kiasi hicho kidogo ambacho hakizidi asilimia tano baada ya kidogo, ili uaminifu wa kielimu uwe karibu mno. Kwa sababu mimi nimeona waungao mkono huwa wananukuu kutoka hiki kidogo tu, na mahasimu wananukuu kutoka hiki kingi tu. Na jaribio la kuiweka kila sura wazi, na kubainisha kiwango cha uwiano kiwe kamili mno na cha kiadilifu mno.

141

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 141

1/20/2016 11:35:53 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

SHEIKH KUJINASUA MBALI NA ­UKUFURISHAJI: Pamoja na yote hayo tunamkuta Sheikh Mungu amrehemu, sana anajinasua mbali na ukufurishaji na kuusukuma mbali na yeye. Anasema: “Ama yaliyosemwa na maadui kunihusu kuwa ninakufurisha kwa dhana na kwa upendo, au namkufurisha asiyejua ambaye dalili haijathibitika, huu ni uzushi mkubwa, kwa hilo wanakusudia kuwachukiza watu wawe mbali na dini ya Mwenyezi Mungu na Mjumbe Wake.”69 Nasema: Hata pamoja na kujinasua huku, ibara hii ndani yake ina ukufurishaji wa ndani kwa ndani wa kumkufurisha anayepinga ukufurishaji wake! Kwa kuwa “Mwenye kukusudia kuwachukiza watu ili wawe mbali na dini ya Mwenyezi Mungu ni kafiri,” kulingana na njia ya Sheikh na njia ya mwingine. Hivyo basi ukufurishaji ikiwa haukujificha hata katika maeneo kama haya ya kujihami na tuhuma ya ukufurishaji basi ni lini na wapi utajificha?

JE SHEIKH ZIMEPINGANA KAULI ZAKE? Sheikh amejikanushia mambo kadhaa, mengi ya hayo aliyoyakanusha yapo katika fatwa zake, basi huenda kuyakanusha kwake ikawa ni kurejea, kugeuka, au mbinu. Miongoni mwa aliyoyakanusha ni: 1.

69

Anasema kuwa yeye habatilishi vitabu vya madhehebu manne. Tazama ad-Durarus-Saniyyah (1/34), (10/13), ilihali mahali pengine anaviita “ni shirki yenyewe hasa,” tazama ad-DurarusSaniyyah (2/59).

Ad-Durarus-Saniyyah (10/113). 142

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 142

1/20/2016 11:35:53 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

2.

Anasema kuwa yeye hasemi: Watu toka miaka mia sita hawana kitu! Tazama ad-Durarus-Saniyyah (9/34), (10/13). Na hili huenda hakulisema kwa maandishi, lakini anazo ibara za kuwatuhumu Waislamu wengi katika Najdi na Hijazi, toka karne tatu au nne, na huenda ikafahamika kutoka katika baadhi ya ibara ukufurishaji wake wa kuwakufurisha watu wa karne mbili za nyuma zaidi. Kwa vyovyote iwavyo si lazima aseme ibara iliyotangulia ndio ufurutu ada katika kukufurisha uthibiti, bali ukufurishaji uliothibiti humo watosha. Linakutosha koja linaloizunguka shingo! (Huo ni usemi wa Kiarabu).

3.

Anasema kuwa yeye hadai kuwa kaifikia daraja ya ijtihadi na kuwa ametoka kwenye taklidi, tazama ad-Durarus-Saniyyah (9/34), (10/13), ilihali hajatanguliwa na yeyote kwenye mambo yaliyotangulia kutajwa.

4.

Anasema kuwa yeye hasemi tofauti za wanazuoni ni balaa, tazama ad-Durarus-Saniyyah (9/34).(10/13).

5.

Anasema kuwa yeye hamkufurishi mwenye kufanya tawasuli ya watu wema, tazama ad-Durarus-Saniyyah (9/34), (10/13).

6.

Anasema kuwa yeye hamkufurishi al-Buswayriy kwa sababu ya kauli yake: ‘Ewe Mbora wa viumbe’, tazama ad-DurarusSaniyyah (9/34), (10/13). Na yeye anamkufurisha anayeitakidi yaliyo kinyume na yale aliyoyataja al-Buswayriy.

7.

Anasema kuwa yeye hasemi: “Lau angeweza angelibomoa Kuba la Mjumbe wa Mwenyezi Mungu. Na lau angeweza angechukua mizabu yake na angefanya mizabu ya mbao.” Tazama ad-Durarus-Saniyyah (9/34), (10/13). Kisa chao ni mashuhuri huko Madina. 143

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 143

1/20/2016 11:35:53 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

8.

Anasema kuwa yeye haharamishi ziyara ya kaburi la Nabii 5, tazama ad-Durarus-Saniyyah (9/34), (10/13).

9.

Anasema kuwa hajawahi kuharamisha kufaya ziyara ya kaburi la wazazi wawili, tazama ad-Durarus-Saniyyah (9/34), (10/13).

10. Anasema kuwa yeye hamkufurishi mwenye kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu, tazama ad-Durarus-Saniyyah (9/34), (10/13). 11. Anasema kuwa hamkufurishi Ibn al-Faaridh, tazama ad-Durarus-Saniyyah (9/34). 12. Anasema kuwa yeye hamkufurushi Ibn al-Arabiy, tazama adDurarus-Saniyyah (9/34 ), ilihali yeye mahali pengine anaona yeye ni kafiri mno kuliko Firaun! Bali anamkufurisha asiyemkufurisha na kundi lake! Angalia ad-Durarus-Saniyyah (10/2), (25/45). 13. Anasema kuwa yeye haunguzi dalili za kheri, tazama adDurarus-Saniyyah (9/80,34). Ukweli ni kwamba walipoingia Makka waliziunguza, ad-Durarus-Saniyyah (1/228). 14. Anasema kuwa yeye haunguzi bustani ya maua mazuri, tazama ad-Durarus-Saniyyah (9/34). Ukweli ni kwamba walipoingia Makka nayo pia waliiunguza, kwa madai kuwa inawaingiza watu kwenye shirki, tazama ad-Durarus-Saniyyah (1/228). 15. Anasema kuwa yeye hawakufurishi watu wote isipokuwa anayemfuata yeye, tazama ad-Durarus-Saniyyah (9/80). Hakulisema hili kwa tamko lake bali kwa maana yake na uthibitisho umetangulia. 144

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 144

1/20/2016 11:35:53 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

16. Anasema kuwa yeye hasemi kuwa ndoa za hao wasiomfuata sio sahihi, tazama ad-Durarus-Saniyyah (9/80), ilihali kwa mujibu wake wanakanusha kufufuliwa na wala hawatofautishi kati ya dini ya Muhammad bin Abdullahi na dini ya Amru bin Lahyi, na wao ni makafiri! Tazama ad-Durarus-Saniyyah (9/83). 17. Anasema kuwa yeye haanzi kuwapiga wengine wala hawaui ila kwa kuitetea nafsi na heshima, katika hali ya kuzuia ubaya kwa ubaya, zaidi ya hapo ni kuwaua wanaomtukana Mtume 5, tazama ad-Durarus-Saniyyah (9/83). Na ibara ya mwisho inaifutilia mbali ya kabla yake, hivyo yeye anaihesabu madhehebu yake ni dini ya Rasuli, na madhehebu ya mtu mwingine miongoni mwa Waislamu kuwa ni ukafiri mkubwa kuliko madhehebu ya Amri na makafiri wa Kikurayshi. 18. Anasema kuwa yeye hamkufurishi aabudiaye sanamu! Ambalo lipo juu ya kaburi la Abdul-Qadir wala aabudiaye sanamu ambalo lipo juu ya kaburi la al-Badawiy! Kwa sababu ya ujinga wa watu wanaoabudia hayo masanamu, tazama ad-DurarusSaniyyah (1/104). Lakini mahali pengine amewakufurisha wafanyao yaliyo chini zaidi ya haya, kisha yeye kizuizi cha ujinga hakitambui. Na anaandika kubatilisha kizuizi hiki, angalia adDurarus-Saniyyah, (10/369, 392). 19. Anasema kuwa yeye hamkufurishi asiyehamia kwake, tazama ad-Durarus-Saniyyah (1/104), ilihali ukweli ni kwamba yeye amekhalifu hili lakini kwa kuweka sharti zinazolifanya hili. Mfano: Mtu awe mwenye uwezo wa kudhihirisha dini yake! Na uwezo huu una sharti pia, nalo ni: Awakufurishe watu wa mji wake na wala asizibiwe na adha! Hivyo mto umerudi na kumimina kwenye chanzo chake! Kwani mji ambao mtu anaweza 145

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 145

1/20/2016 11:35:53 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

kuyatenda haya ni ule uliokwishakuwa wa Kiwahabi, wassalaam! Kwa sababu sisi tumeona yeye anaitakidi kuwa miongoni mwa dini ni kitu kadha na kitu kadha... miongoni mwa ambayo sio sahihi kisheria na wala hakuna anayeafikiana naye isipokuwa wanaomkalidi. Ikiwa mukalidu ataweza kuidhihirisha dini hii katika mji wake, inamaanisha kwa hukumu ya umbo la mwanzo itakuwa ni ukafiri mkubwa, kama walivyowafanyia wanazuoni wa al-Haramaini, na ikiwa mukalidu ataweza kuwakufurisha watu wa mji wake kabla ya daawa hii na asipatwe na adha, maana yake imeandaliwa ili kuupokea ujumbe mdogo wa watu kumi tu wa kikundi cha Mawahabi wa kabila walio jirani! Ili watu wajue itikadi na kukusanya Zaka kwa ajili ya hazina ya mali ya Waislamu na amri ya kunyoa vipara. 70 20. Anasema kuwa yeye hamkufurishi asiyewakufurisha walio kinyume naye na hapigani nao, tazama ad-Durarus-Saniyyah (1/104). Na tumeona yeye anafanya haya, yeye anarudia kusema kuwa, mwenye shaka na ukafiri wa makafiri basi yeye ni miongoni mwao. Na Waislamu katika zama zake wao kwa mtazamo wake ni makafiri mno kuliko makafiri wa Kikurayshi! 21. Anasema kuwa yeye hamkufurishi asiyeswali, tazama ad-Durarus-Saniyyah (1/102 ). Lakini wafuasi wake hii leo wanamkufurisha asiyeswali. Na jambo hili ni miongoni mwa wanayohitilafiana toka zamani, na Mahanbali wamekuwa ni miongoni mwa wanaotilia mkazo hili. 22. Anasema kuwa yeye hamkufurishi asiyeingia katika utii wake, tazama ad-Durarus-Saniyyah (10/128). Na imetangulia kuwa 70

Abdullah bin Isa amesema: “Imenifikia habari kuwa watu miongoni mwa watu wa Tuhama walinyoa vipara kwenye mwanga wa taa, na walikuwa karibu watu mia sita, katika usiku mmoja?! Na Sheikh Abdullah bin Muhammad bin Abdul-Wahabi amekiri kuwa “baadhi ya wanavijiji walioingia katika dini yetu walimuua asiyenyoa kipara kichwa chake... na asiyenyoa kichwa chake anakuwa murtadi.” Tazama Daawal-Munawiiyna, Uk. 184. 146

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 146

1/20/2016 11:35:54 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

yeye anawawekea sharti la kudhihirisha rai za Sheikh na kujiepusha mbali na mahasimu wake ambao anawaita mushirikina! 23. Anasema kuwa yeye hamhesabu jahili afanyaye shirki na kufuru kuwa ni kafiri mpaka imfikie hoja, na asemalo ni kuwa amali yake ni amali ya makafiri, tazama ad-Durarus-Saniyyah (10/136). Lakini yeye katika maandishi mengine amehukumu kuwa masheikh wake na masheikh wao na masheikh wa masheikh wao walikuwa wanaona dini ya Amri bin Lahyi ndio bora kuliko dini ya Nabii 5, na kuwa wengi miongoni mwa watu wa Najdi na Hijazi wako katika kukanusha ufufuo! Na aliwakufurisha wanazuoni wa Kihanbali na kuainisha majina yao, na mfano wa haya ndani yake kuna ukufurishaji mweupe kiasi kwamba inakuwa tabu kusadiki aliyoyasema katika mas’ala hizi. 24. Anasema kuwa anaoukataa ni Uislamu mtupu! Ambao hauchanganyiki na shirki wala bidaa, ama Uislamu ambao dhidi yake ni ukafiri haukanushi! tazama ad-Durarus-Saniyyah (10/16). Na mmeiona hukumu yake juu ya watu kuwa ni makafiri ukafiri unaomtoa kwenye Uislamu! Na kuwa washirikina wa Kikurayshi shirki yao ni nyepesi mno kuliko shirki ya washirikina wa zama zetu kwa mas’ala mbili! 25. Na Sheikh Abdur Rahmani bin Hasan Mungu amrehemu, amebainisha kuwa watu wa Sheikh Muhammad lau wangetoka makaburini mwao wangewaua! Akasema: “Lau wangetushinda watu wa Deriyya wangetuua”, tazama ad-Durarus-Saniyyah (16/6), na huu ni ushahidi mkubwa juu ya ufurutu ada katika kukufurisha na kuua. Ikiwa watu wa zama za Abdur Rahmani bin Hasan wanastahiki kukufurishwa na kuuawa kwa mujibu wa 147

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 147

1/20/2016 11:35:54 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

njia ya Sheikh Muhammad, licha ya kuwa wao nao ni wafurutu ada pia katika kukufurisha na kuua, basi itakuwa vipi - Mungu Wangu – kwa Waislamu wengine?!! Khususan ukizingatia kuwa Abdur Rahman bin Hasan alikuwa mkali katika kutetea haki, alifarikiana na Amir Faysal bin Turkiy kwa sababu huyu wa mwisho alitaka mmoja wa askari wake aadhibiwe katika zizi na alizuia asiadhibiwe sokoni, Abdur Rahman bin Hasan akasema: “Salamun Alaykum” na akatengana naye, na Faysal bin Turkiy hakumrudisha isipokuwa kutoka Houtta! Na wala hakurejea mpaka yule askari alipoadhibiwa sokoni. Na ikiwa hii ndio hali ya zama zake na anaona kuwa Sheikh Muhammad atahalalisha kuuliwa kwao na kukufurishwa basi itakuwaje kwa Waislamu waliobaki? Na hili linajulisha kuwa Sheikh Muhammad, Mungu amrehemu na wafuasi wake walikuwa wanakufurisha na wanaua kwa sababu ndogo tu.

MUHTASARI: Kupitia usomaji wangu wa vitabu vikubwa vya Sheikh na risala zake, nimekutana na mpingano mkali. Huwa anakanusha kitu kilichothibiti, na anawatuhumu watu wengine kuwa wamesema uwongo kwa hilo. Lakini pia tunakuta mengi kati ya yale anayojaribu kujinasua mbali nayo yapo katika vitabu vyake, na hili linatujulisha juu ya nguvu ya wapinzani wake na usahihi wa machukulio yao, kama ambavyo yatujulisha sisi kuwa Sheikh ama anasahau, au anajiepusha kisiasa, au waliopiga chapa vitabu vyake katika ahadi za mwisho – hali wao wakiwa Mawahabi wa Saudia – wamemsingizia. Lakini haya yote yanatoweka ninapokuta kuwa maeneo ambayo kuna maelezo ya kujaribu kujiepusha mbali na ukufurishaji pia nayo yanabeba ukufurishaji, lakini ni ukufurishaji uliojificha, kama tulivyotangulia kufafanua katika kuhariri mahali penye tofauti mwisho wa utafiti wa kwanza. 148

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 148

1/20/2016 11:35:54 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Na tatizo hapa ni kwamba ukija na kauli ya Sheikh ambayo ndani yake kuna msimamo wastani, mpinzani wako anaweza kuleta kauli kumi ndani yake mna ufurutu ada. Na ukimtaka awe na dhana njema na azichukue kauli za wastani za Sheikh kwa uchache wake katikati ya rundo la ukufurishaji, atakwambia tunachukua ile bayana na iliyofululiza na tunaacha nadra. Na hapa ufurutu ada utashinda, na hii ni adhabu ya anayeridhika kuhukumiwa na Sheikh; badala ya kuhukumiwa na nususi za kisharia.

149

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 149

1/20/2016 11:35:54 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

UTAFITI WA TATU MWENDO UNAOENDELEA

W

amekuja wanafunzi wa Sheikh na wanaomfuata, Mungu awarehemu na awasamehe, ili waendeleze ukufurishaji, hivyo wakasema amekufuru yule mwenye kuafikiana na watu wa mji wake katika dhahiri japokuwa anaona wamo makosani na anampenda Sheikh katika hali yake ya batini. Na wameyakufurisha makabila ya Qahtan na al-Ajman. Na pia wamewakufurisha watu wa Hail, na atokaye kwenda miji mingine nje ya miji ya daawa ikiwa anaamini kuwa watu wa miji ile ni Waislamu. Na wamemkufurisha Ibn Arabiy na Ibn al-Faridh, japokuwa hawa wawili hawakukufurishwa na Mawahabi tu, lakini kwa hawa wawili kuwafanya wanabidaa ndio laiki na salama mno kwao. Na wamewakufurisha watu wa Makka na Madina. Na wameikufurisha dola ya Uthmaniyyah, bali wamemkufurisha asiyeikufurisha! Na wamewakufurisha Maibaadhi na vikundi vingi vya Kiislamu, ikiwa ni pamoja na kuwa na rai zenye ufurutu ada dhidi ya mfumo wa elimu, mwanamke na mambo ya maisha ya kisasa. Na hapa nitaugawa mwendelezo katika sehemu mbili: Ya kwanza: Kauli za madrasa ya Sheikh katika kutilia mkazo njia ya Sheikh katika kukufurisha: Ya pili: Rai zao zenye ufurutu ada kuyahusu mambo mapya, na yenye kujitokeza mno ni elimu ya kisasa. SEHEMU YA KWANZA: Nayo ni mahsusi kwa vitendo vya kutilia mkazo ufurutu ada wa Sheikh Mungu amrehemu, vitendo 150

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 150

1/20/2016 11:35:54 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

vinavyofanywa kwa njia ya ufurutu ada na wale waliokuja nyuma yake miongoni mwa Mawahabi, mifano ya vitendo hivyo ni: 1.

Kumkufurisha mwenye kuafikiana na watu wa mji wake, kama vile Hijazi, Yemen au Shaam, hata kama kwa dhahiri na kwa batini ni mpenzi wa Uwahabi na ni mwenye chuki na kaumu yake. Haya yamekuja katika kitabu ad-Durarus-Saniyyah (8/121), ameyasema hayo Sheikh Sulayman bin Abdullah bin Muhammad, Mungu amrehemu.

2.

Ama kumkufurisha msafiri aendaye nje ya mji wa daawa na ikiwa anaitikadi Uislamu wa miji mingine, utalipata hilo katika kitabu ad-Durarus-Saniyyah (8/424). Hili amelisema Hamdu bin Abdul-Azizi.

3.

Ama kumkufurisha Ibn Arabiy na Ibn al-Faridh na kuwa wao ni makafiri mno kushinda watu wote wa ardhini, hilo limo katika kitabu ad-Durarus-Saniyyah (8/366). Hili ni la Sheikh AbdulLatiif bin Abdur Rahman Mungu amrehemu.

4.

Ama kubainisha kuwa Makka na Madina ni miji ya ukafiri na imejitenga mno na Uislamu, hilo utalipata katika kitabu ad-Durarus-Saniyyah (9/285).

5.

Ama kuikufurisha dola ya Uthmaniyyah, hilo utalipata katika kitabu ad-Durarus-Saniyyah (10/429), na kwamba asiyeikufurisha ni kafiri! Haijui maana ya La ilaha illa llahu! Na kwamba atakayewasaidia atakuwa ameritadi waziwazi! Hilo amelisema Sheikh Abdullah bin Abdur Rahman al-Babatini Mungu amrehemu.

6.

Ama kulikufurisha kabila la Qahtan, hilo utalipata katika kitabu ad-Durarus-Saniyyah (10/503), kwa sababu ya kupeleka mash151

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 151

1/20/2016 11:35:54 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

taka kwenye hukumu za kikabila, na hili ni kwa mujibu wa Ibn Sahman. 7.

Ama kulikufurisha kabila la al-Ajman, hilo utalipata katika kitabu ad-Durarus-Saniyyah (10/503), kwa sababu ya kupeleka mashtaka yao kwenye hukumu za kikabila, pia kwa mujibu wa Ibn Sahman.

8.

Ama kuwakufurisha watu wa Hayil, hilo utalipata katika kitabu ad-Durarus-Saniyyah (9/292,291), na kwamba kuwapiga jihadi wao ni jihadi bora.

9.

Kuwakufurisha Maibaadhi, hilo utalipata katika kitabu adDurarus-Saniyyah (10/431,438 ), kwa mujibu wa Abdullah bin Abdul-Latif Mungu amrehemu.

10. Kumkufurisha aliyeingia katika daawa na akadai kuwa baba zake wamekufa wakiwa Waislam! Huambiwa afanye toba, akitubu kheri yake vinginevyo hukatwa shingo yake! Na mali yake huwa ngawira ya Waislamu! Tazama katika kitabu adDurarus-Saniyyah (10/143). Na ikiwa alipata kuhiji ni wajibu juu yake ahiji tena kwa kuwa Hija yake ya kabla ya kujiunga na daawa ilikuwa ndani ya siku zake za shirki, na miongoni mwa sharti za Hija ni Uislamu! Tazama katika kitabu ad-DurarusSaniyyah (10/138). Haya ni kwa mujibu wa watoto wa Sheikh na Hamad Bin Naasir Mungu awarehemu wote na afumbiye macho makosa yao, awabadilishiye mambo yao kwa kuyafidia kwa yale waliyoyafanya kiusahihi, na awaghofiriye wao na sisi. 11. Kuwakufurisha Jahmiyyah, tazama katika kitabu ad-DurarusSaniyyah (10/430). Kuwa wao ni mazindiki walioritadi kwa Ijmai. Haya ni kwa mujibu wa baadhi ya Mawahabi. Inapaswa 152

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 152

1/20/2016 11:35:54 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

ieleweke kuwa wao wanawaingiza Ashairah kwenye Ujahmiyyah! Na wanazuoni wengine katika wanazuoni wa daawa wamekuwa na msimamo wa wastani, tazama katika kitabu adDurarus-Saniyyah (10/373) wametaja tofauti iliyopo katika kuwakufurish na kuwa hukumu ya Uislamu wao sio ijmai. Na hii ni hafifu mno kuliko anayedai ijmai juu ya ukafiri wao. 12. Kumkufurisha anayeuita Uwahabi kuwa ni Ukhawariji, tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (10/182), hii ni kwa mujibu wa Sheikh Abdullah bin Muhammad, pamoja na kuwa yeye ni miongoni mwa wenye msimamo wa wastani. Na hili hapa ni jibu la anayeleta bidaa ya kukufurisha! Kwamba Ali K na waliokuwa pamoja naye miongoni mwa Maswahaba hawakuwakufurisha Makhawariji ilihali Makhawariji waliwakufurisha wao. Sheikh amekiri kuwa “Haijuzu kumkufurisha anayetukufurisha.� Tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (10/24). 13. Sheikh Abdul-Latif bin Abdur Rahman anaona kuwa swala ya Ahmad nyuma ya Jahmiyyah ni miongoni mwa dalili za wazi mno juu ya ukafiri wao. Tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (10/420) Hii ni dalili ya ajabu, ya pekee, inaniwia vigumu kuifahamu! 14. Mwenye kusema La ilaha ila llahu katika hali ya vita huuliwa wala asiachwe kama alivyofanya Usamah bin Zaydi, kwa kuwa mtu wa Usamah hakupata kuisema kabla yake na wao wanaisema kabla ya hivyo!! Tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (9/239). 15. Kumkufurisha aliyefikiwa na daawa (ya Kiwahabi) na hakusilimu (japo ni Mwislamu). Tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (9/245). 153

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 153

1/20/2016 11:35:54 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

16. Kumkufurisha asiyewakufurisha watu wa Makkah. Tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (9/291). 17. Kuwakufurisha Ashairah na kwamba wao hawajui maana ya shahada mbili. Tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (1/264, 362, 324, 312, 320). 18. Kuwakufurisha Muutazilah. Tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (1/357). 19. Kuwakufurisha Makhawariji na kuwa wao wametoka nje ya Uislamu. Tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (10/177), hii ni kwa mujibu wa Abdullahi Ibn Sheikh. 20. Kuwakufurisha wanaozuia Zakka na kwamba wao wametoka nje ya Uislamu. Tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (10/177), hii ni kwa mujibu wa Abdullah Ibn Sheikh. 21. Kuwakufurisha watu Haramaini, Misri, Shaam,Yemen, Iraq, Najran, Hadhramaut, na Musal na Makurdi (1/385, 380). 22. Sheikh Ibn Hamid Mungu amrehemu, amehadithia kuhusu kugeuka wengi mbali na dini ya Uislamu na kuwapenda kwao waabudu masanamu na maadui wa Sharia miongoni mwa makafiri, Manaswara na Rafidh. Tazama kitabu ad-DurarusSaniyyah (15/471). Na kuwa haya yameenea vijijini, mijini na majangwani isipokuwa mabaki miongoni mwa ambao imani zao zimejikita kwenye Tawhidi. Tazama kitabu ad-DurarusSaniyyah (15/471). 23. Na kuwa kila Mwislamu awapendae makafiri, washirikina, Mayahudi na Manaswara wala hakanushi shirki yao na anaona 154

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 154

1/20/2016 11:35:54 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

vitendo vyao kuwa ni vizuri au ana shaka na ukafiri wao, yeye ni kafiri hata kama anaijua Tawhidi na anazifanyia kazi sharia za dhahiri za Kiislamu. Tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (15/475). 24. Kisha alizitaja aina za kujishabihisha na makafiri na kutegemea na akataja miongoni mwazo “kuvaa na kuwatembelea, kulainisha lugha na kukodolea macho kwenye mazuri yao, kukaa karibu nao na kuwatumia katika nyadhifa mbalimbali, kuingia kwao na kuwa na bashasha nao au kuonesha tu kitu cha bashasha na ukunjufu, kuwaheshimu kwa jumla na kuwasaidia japo kwa kitu hafifu, kuvaa mavazi yao, kukaa nao katika majumba yao na kuelemea kidogo kwao basi sikwambii kuhusu kuketi nao na kula nao na kulainisha maneno na kuwakaribia katika kikao.” Tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (15/476 - 482). 25. Kisha anasema: “Ukifahamu yaliyotangulia itakubainikia kupotoka kwa wengi miongoni mwa watu wa zama hizi na kuritadi kwao waziwazi.” Kwa hiyo mwenye kuwaheshimu au kuwasifu au kuishi nao au hakutangaza kujiepusha nao “huku ni kuritadi kwa mwenye kufanya hayo! Ni wajibu zitekelezwe dhidi yake hukumu za walioritadi! Kama kijulishavyo Kitabu na Sunna, na ijmai ya umma wa kufuatwa.” Tazama kitabu adDurarus-Saniyyah (15/479). 26. Na kwamba “Ni haramu kusafiri kwenda nchi za washirikina kwa ajili ya biashara ila akiwa Mwislamu huyo ni mwenye nguvu mwenye kizuizi ambacho kwacho anaweza kudhihirisha dini yake na kuwakufurisha na kuiaibisha dini yao, kuwaponda, kujiepusha nao, na kuwadhihirishia bughudha na uadui. Hivyo wasianze kuwatolea salamu, na wakikutana nao njiani wawa155

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 155

1/20/2016 11:35:54 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

bane na kuwadhihaki na wawabainishie kuwa wao ni makafiri! Na kuwa yeye ni adui wao, walijue hilo kwake! Ikiwa hakuyapata haya basi hajawa mwenye kuidhihirisha dini.71 Halizingatiwi tendo la swala tu ndio kuidhihirisha dini wala kuwatenga na kujiepusha na walichochinja.” Tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (15/482 – 491). 27. Na kuwa ambao wanawatumikisha watumishi makafiri majumbani mwao na maofisini mwao na shughulini mwao....pamoja na hayo wao ni wenye kuacha wajibu nyingi, watendaji wa haramu nyingi, hawazijui shahada mbili ila matamko, wao ni kama hao makafiri wameritadi. “Na mwenye shaka na kuritadi kwao mbali na Uislamu basi yeye haijui dini wala hajanusa harufu ya elimu yenye manufaa.” Tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (15/486). Na kwamba utumikishaji kama huu “Ni haramu kwa tamko la Kitabu na Sunna na ijmai ya wema waliotangulia katika umma huu.” Tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (15/486). Nasema: Baada ya ufurutu ada huu ambao sijapata mfano wake, wanazuoni wengi na walinganiaji wanazitaja sababu za kukufurisha na utumiaji nguvu za Sayyid Qutub na Maududiy na UkhwanulMuslimuna na Hizbu Tahriri! Sahihi kwamba katika hawa kuna ufurutu ada upande wa siasa, lakini haufikii ufurutu ada wa Kiwahabi katika pande zote, kisiasa, kiitikadi, kifikihi, kitaaluma na kijamii. Insafu ni dini. Zingatieni ibara zilizopita na angalieni je kumebakia kitu ambacho kipo kwenye itikadi na sera za kundi la al-Qaida na vikundi vya jihadi am71

Sehemu kubwa ya haya ni makhususi kwa makafiri walio vitani dhidi ya Waislamu, sio kwa Waislamu wala Ahludhima wala walio katika ahadi, basi vipi ikiwa tunajua washirikina wanaokusudiwa katika ibara hizi - inavyoonesha - ni Waislamu waishio katika dola zilizo jirani?! Kwani watumiapo kwa neno ‘washirikina’ mutlaka, aghlabu huwa hawawakusudii makafiri wa asili bali mara nyingi wanawakusudia Waislamu wengi kwa jumla, na nadra haina hukumu. 156

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 156

1/20/2016 11:35:54 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

bacho hakijasemwa na Mawahabi? Bali kinyume chake ni sahihi. Kwani al-Qaida na makundi ya jihadi havisemi yote haya. Wala sijui kama wao wanazigawa nchi za Waislamu kwa mgao wa nchi za Kiislamu na nchi za Kikafiri, bali miongoni mwa sababu kubwa za kuzuka kwao ni kwamba wao wanaona kuwa makafiri wameonesha uadui dhidi ya nchi za Waislamu, kwa hiyo wao wanaukubali Uislamu wa umma wa Kiislam, na kukufurisha kwao ni juu ya watawala, ilihali Uwahabi unamkufurisha anayekwenda kinyume nao, sawa wawe watawala au watawaliwa, na unawajibisha kumtii amiri wake wa kiwahabi juu ya Waislamu wote, kama tulivyoona katika bainisho la kulazimishwa wanazuoni wa Makkah na Madina, na hili ni miongoni mwa mambo makubwa ya kipekee waliyonayo, na dini si mchezo wa kisiasa. Hivyo basi ni dhahiri kabisa kuwa katika wanazuoni wa kiwahabi kulikuwa na ambaye yuko wazi na mbele mno katika kukufurisha na kuhalalisha damu kuliko kundi la al-Qaida na vikundi vya jihadi katika ulimwengu wa Kiislamu. Kimsingi walengwa wa kukufurishwa na kuuliwa kwa mtazamo wa kiwahabi ni Waislamu. Hivyo basi pamoja na kukemea kwangu kwa tashdidi ufurutu ada wa namna yoyote ile, uwe kutoka upande wowote ule, lakini dhamiri yangu na tabia yangu inakataa kumtendea ukatili aliye na idadi dhaifu mno na chache ya ukufurishaji na nimsahau aliye na idadi kubwa na mkufurishaji mkubwa mwenye chimbuko la zamani mno na mwenye kufuatwa na wengi. Elimu ni lazima iwe lengo lake ni ukweli peke yake, kisha baada ya hivyo, ukweli hautomdhuru ila asiyependa ukweli. SEHEMU YA PILI: Mifano ya misimamo ya waliokuja nyuma kuhusu mifumo ya elimu. Hapa nitataja fatwa zao zilizo na ufurutu ada kuihusu elimu ya wakati uliopo, na iliyo mashuhuri ni sekyula. Kabla ya haya napenda nibainishe sababu ya hujuma yao dhidi ya 157

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 157

1/20/2016 11:35:54 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

elimu ya kisasa kwa kadiri nidhaniavyo, ni hofu yao kuwa itaisonga elimu ya kisharia ambayo wanaitumia ili kunusuru ufurutu ada wa kiwahabi, vinginevyo hakuna yeyote katika Waislamu ambaye hapendi ienee elimu ya kisharia, lakini mtu kuiharibu sura ya dini kwa ufurutu ada, na kisha aseme hii ndiyo elimu ya sharia, hiki ni kitu kingine. Vyovyote itakavyokuwa, nitataja sampuli bila ya kutaja majina ya waliosema hayo ili kutojiingiza matatani, kwa sababu ndani yake kuna rai kali mno, na kwa kuwa lengo ni kuikosoa fikra sio watu, kwa hiyo miongoni mwa hiyo mifano ni kauli ya baadhi yao: 1.

Walimu ambao Wizara ya Elimu inawatumia katika dola za Kiarabu ni makafiri. Tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (16/5), na ni mazandiki. Tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (16/12).

2.

Na aliendelea na ukufurishaji mpaka kwa watu maalumu, hivyo akawakufurisha baadhi ya wanazuoni akiwemo Dkt. Fawziy as-Shiibiy, na alimtuhumu kuwa yeye ni mwanadaawa mkubwa wa ukafiri na uzandiki. Tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (16/12).

3.

Kuwa walimu hao wanaokuja kutoka dola za Kiarabu wamekuja kwa ajili ya mti wa La ilaha ila llahu ambao Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahabi ameuleta.72 Wao wamekuja ili waung’oe kutoka nchi hii. Tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (16/8).

Pamoja na yaliyomo humo miongoni mwa ufurutu ada wa wazi juu ya Sheikh Muhammad, kwani mti wa La ilaha ila llahu aliuleta Nabii 5, lakini pia wamemtangulia Manabii wengine D. Laiti ibara ingekuwa: “Mti ambao ameumwagia maji Muhammad bin Abdul-Wahabi,” ingekuwa laiki kwa nafasi ya Nabii 5 na laiki kwa nafasi ya Sheikh Muhammad, katika hili pia kuna kufumbia macho. Ama kunyanyua hadhi ya Sheikh Muhammad kwa gharama ya Nabii 5, hilo hapana na hapana mara elfu.

72

158

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 158

1/20/2016 11:35:54 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

4.

Kuwa mti huu umetoweka katika nchi hizo.73 Tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (16/8).

5.

Kuwa walimu hawa ni miongoni mwa vifaranga vya wazungu na waabudu mawalii na waachao swala na ibada nyingine za Kiislamu. Tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (16/100).

6.

Kuwa mwenye kusafiri kwenda nchi za jirani kusoma au kufanya biashara au jambo lingine inapasa ahamwe mpaka toba itakapodhihiri. Tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (15/462).

7.

Na ilikuwa mwananchi ajae kutoka nchi hizo hutoswa ndani ya maji akiwa na nguo zake baada ya swala ya Ijumaa ili ajizuiye kufanya safari kwenda nchi za washirikina. Tazama kitabu adDurarus-Saniyyah (15/462).

8.

Na katika fatwa zao ni kuharamisha na kukataza elimu zote zisizo za kisharia kama uchoraji, stadi za kazi, riadha na michezo. Tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (16/15).74

73

74

Na huu ni ukufurishaji ulio bayana wa kuwakufurisha Waislamu walio katika

dola ambazo wizara ya elimu ilikuwa inawaleta kutoka dola hizo, kama vile Misri, Syria, Jordan, Sudan, Palestina na Morocco ya Kiarabu na nyinginezo.

Na miongoni mwa madhara na matokeo ya fatwa na itikadi potofu kama hizi za Kiwahabi na Kisalafi ni kuzuka na kuasisiwa kwa kundi la Boko Haram. Hili ni kundi la Mawahabi Masalafi wenye itikadi kali Kaskazini mwa Nigeria; lina mwelekeo wa kijihadi na kutumia mbinu za ufurutu ada na mabavu. Jina “Boko Haram” linatokana na lugha ya Kihausa likimaanisha “vitabu ni haramu” yaani “Elimu ya Sekyula ni Haramu au dhambi”. Boko Haram ilianzishwa na Yusuf Mohamed mwaka 2002 na inalenga kuanzisha Dola la Kiislamu katika Nigeria ambako sharia itakuwa ndio sheria ya pekee. Imekadiriwa ya kwamba mapigano yaliyoanzishwa na Boko Haram au kutekelezwa dhidi yake yamesababisha vifo vingi. Rais wa Nigeria Jonathan Goodluck alidai Mei 2014 kuwa kundi lilisababisha vifo vya watu 12,000 na majeruhi 8,000. Baada ya kushambulia shule, vituo vya polisi, makanisa na ofisi za serikali kundi lilitoa tamko mwaka 2012 kuwa linawapa Wakristo wote nafasi ya siku 3 kuondoka Kaskazini mwa Nigeria au watauawa. Tangu tangazo lile mashambulio yameongezeka. Hawashambulii Wakristo na 159

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 159

1/20/2016 11:35:54 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

9.

Na kukataza Haki, maumbile na upigaji picha. Tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (16/10).

10. Na kukataza elimu za kisasa. Tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (16/50). 11. Na kukataza kuwasomesha mabinti. Tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (17/50). 12. Na kwamba elimu za sekyula ni chanzo cha ukafiri. Tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (15/489). Na alikwishabainisha mwandishi wa makala husika kuwa ni: uchoraji, stadi za kazi, mazoezi ya viungo, na michezo. Tazama kitabu ad-DurarusSaniyyah (16(2)/15). 13. Na kuwa kumwelimisha mwanamke kunasababisha kujiremba na kuraruka kwa hijabu na kuwa wazi muundi, mapaja, kichwa na kifua. Tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (16/74), na kufungua madanguro, maeneo ya sinema, kucheza ngoma na utovu wa nidhamu. Tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (16/81). 14. Na nasaha kwa kila muumini, ni kwamba asimwingize mwanawe au binti yake kwenye shule hizi ambazo dhahiri yake ni rehema na batini yake ni balaa na fitina na mwisho wake ni wanawake kuishi bila hijabu na kupotoka. Tazama kitabu adDurarus-Saniyyah (16/74). polisi pekee lakini pia idadi kubwa ya Waislamu ambao ndio wakazi wengi Kaskazini. Mnamo Aprili 2014 kundi la Boko Haram lilishambulia mji wa Chibok katika jimbo la Borno, likaweka moto na kuharibu nyumba 170 na kuingia shule ya sekondari walipokamata wasichana zaidi ya 200. Tarehe 6 Mei 2014, wasichana wengine 8 walitekwa na watu wenye silaha wanaofikiriwa kuwa wa kundi hilohilo. Kiongozi wa Boko Haram, Shekau alitishia kuwauza mabinti kama watumwa. Tarehe 12 Mei 2014 video ya Boko Haram ilidai kuwa mabinti wote wameongokea Uislamu na watashikwa hadi wafungwa wa Boko Haram waliomo mkononi mwa serikali watakapoachiwa na kuwekwa huru – Mhariri. 160

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 160

1/20/2016 11:35:54 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

15. Kuwa kufungua shule za wasichana ni msiba mkuu na maangamizi makubwa. Tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (16/78, 83). 16. Na walipinga kwa kiongozi mkuu wa elimu ya wasichana azma yake ya kuwaelimisha mabinti hesabu, uinjinia na jografia. Tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (16/79). 17. Kuwa wanaotangaza kumwelimisha mwanamke wao ni vifaranga wa wazungu. Tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (16/81). 18. Kuwa wao wanapenda shari na wanaichukia kheri na watu wake na wanawafuata makafiri na kujishabihisha na Majusi. Tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (16/81). Na kuwa wao wanajaribu kuwatoa mabinti nje ya nyumba zao ili waweze kustarehe nao kwa hila ya kuelimisha. Tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (16/82). 19. Kuwa haridhiki na shule hizi ila asiyekuwa na ghera wala ujanadume wala dini na aghlabu watu hawa ni walinganiaji wa upotovu. Tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (16/84). 20. Kuwa watu wa nchi hizi wameshabihiana na Makhawariji miongoni mwa makafiri na vifaranga vyao katika mambo mengi yaliyo haramu. Waliyataja miongoni mwao ni maeneo ya starehe na burudani na runinga. Tazama kitabu ad-DurarusSaniyyah (15/31). 21. Na wameharamisha kwa watoto na wengine kucheza mpira na kwamba mchezo huo umeingia kwa Waislamu kutoka Magharibi wala haukuwepo zama za makhalifa waongofu wala zama 161

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 161

1/20/2016 11:35:54 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

za wafalme wa Kiislamu. Tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (15/200, 204). Na kuwa hayo ni miongoni mwa kujishabihisha na maadui wa Mwenyezi Mungu, tazama kitabu ad-DurarusSaniyyah (15/206). Wala hayatendwi hayo ila na wapumbavu, tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (15/206). Na kwamba miongoni mwa yanayojulisha kuwa huko ni kujishabihisha na makafiri ni kuwa matendo yao yanaafikiana na matendo ya Wamarekani, ikiwa ni pamoja na kuweka magoli ya mpira.75 Tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (15/206). Na kuwa huku ni miongoni mwa kujishabihisha na makafiri, kisha alileta Hadithi “Mwenye kujishabihisha na kaumu ya watu naye ni miongoni mwao.” Na kwamba kufanya hivyo ni miongoni mwa uovu unaopasa kubadilishwa, tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (15/206). Na kwamba ni miongoni mwa uchafu, tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (15/207). Na walitaja sababu za kuharamishwa mpira kuwa ndani yake mna maringo, na Mwenyezi Mungu amesema: “Usitembee ardhini kwa maringo.”76 Tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (15/210 ). Na kwamba mchezo huo wa mpira ni miongoni mwa lahawi iliyo batili, tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (15/213 ). Na ni miongoni mwa upotovu, tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (15/214 ). Na kwamba ni shari mno kuliko sataranji, tazama kitabu adDurarus-Saniyyah (15/215 ), na mcheza sataranji ni ufasiki, tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (15/214 ).  Anakusudia kwamba kwa Waislamu kuna miamba mitatu inayotengeneza goli, na kwa makafiri pia ni hiyo hiyo miamba mitatu, jambo ambalo linatilia nguvu hali ya kujishabihisha na makafiri. Na nimejitahidi kufikiria aina nyingine ya goli inayoweza kuwa tofauti na magoli haya mbali na yanayotumiwa na makafiri lakini sijapata. 76   Huu ni utumiaji wa Nususi za kisheria usio wa kiadilifu ili kuzifanya dalili ya uharamu, hii ni alama ambayo aghlabu ipo juu ya dalili za wanazuoni wengi, Mungu awasamehe. Asili katika vitu ni uhalali wala si haramu, na yakuwa kukosea katika kuhalalisha ni bora kuliko kukosea katika kuharamisha, kwa kuwa asili ndio rahisi kuhalalisha na kurahisisha, na si kuchukiza na kufukuza. 75

162

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 162

1/20/2016 11:35:54 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

22. Kuwa runinga ni chombo balaa na shari na ni sababu ya kila ovu na ukosefu wa haya na staha, tazama kitabu ad-DurarusSaniyyah (15/243 ). Na kwamba mwenye kuona uhalali wa runinga Shetani ametupia zubda yake kwenye nyoyo zenye giza, tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (15/236 ). Na wamefuata utashi wa nafsi zao na wao ni watu waliopotea kabla na wamepotea mbali na njia iliyo sawa, tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (15/236). 23. Ama kuhusu muziki, wamepitiliza katika kuharamisha, wameharamisha pia hata kusikiliza dufu bali sauti za santuri, tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (14/536). 24. Wamepitiliza katika kuharamisha tumbaku mpaka wameifikisha daraja ya pombe na kuwa tumbaku ni kileo kama pombe, tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (15/59, 72). Na wametoa fatwa kuwa mvuta sigara apigwe mijeledi themanini kama mnywa pombe kabisa, tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (15/ 93). 25. Na wamepitiliza katika kuharamisha picha, umbo zake zote na aina zake zote, yenye kivuli na isiyo na kivuli, na wameifanya kuwa ndio asili ya shirki, tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (15/295). 26. Na kuwa vazi la askari ni haramu pia, kwa kuwa ni miongoni mwa kujishabihisha na makafiri, mwenye kujishabihisha na kaumu naye ni miongoni mwao, tazama kitabu ad-DurarusSaniyyah (15/373), kwa kuwa linashabihiyana na vazi la wazungu washirikina, tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (15/365). 27. Vivyo hivyo chepeu, tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (15/367). 163

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 163

1/20/2016 11:35:54 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

28. Na suruwali, tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (15/367). 29. Na mwenye kukusanya kati ya mavazi haya hapana tofauti kati yake na wazungu. (15/367). 30. Na kuwa mavazi haya ni njama kutoka kwa wanaopenda kuufanyia vitimbi Uislamu, tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (15/366). 31. Na kuzikiri ni miongoni mwa kuzikiri kauli mbiu za kikafiri na kishirikina, tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (15/366). 32. Kadhalika kupiga miguu ardhini na maamkizi ya kiaskari, tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (15/363), na kwamba upigaji miguu huu unashabihiana na upigaji wa punda na nyumbu miguu yao wanapohisi kitu kinatambaa miguu yao! Hivyo ndani yake mna ushabihianaji wa jinsia mbili, tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (15/379). 33. Ama upigaji kofi utokao kwa wanaume ni miongoni mwa maovu mabaya mno, tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (15/396). Na kuwa hiyo ni miongoni mwa matendo ya kaumu Luut ambayo kwayo wamehiliki, na ni miongoni mwa kujishabihisha na maadui wa Mwenyezi Mungu, tazama kitabu ad-DurarusSaniyyah (15/397). 34. Na kupiga makofi ni miongoni mwa mambo mahsusi ya wanawake, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu 5 amewalaani wanaojishabihisha na wanawake miongoni mwa wanaume, tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (15/399). 35. Na mwanaume kupiga makofi ni miongoni mwa kujifanya mwanamke, tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (15/404). Na hilo ni katika madhambi makuu, tazama kitabu ad-DurarusSaniyyah (15/399). 164

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 164

1/20/2016 11:35:54 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Nasema: Hii ni mifano ya haraka haraka tu miongoni mwa fatwa za wanazuoni wa wakati huu katika madrasa ya Sheikh Muhammad Mungu amrehemu, ufurutu ada wao uko dhahiri katika uharamishaji wa yaliyo halali lakini hata ya dharura. Ikiwa agizo la kisiasa na la kimalezi limetelekeza mambo haya kwa maslahi ya waja na nchi, basi ni kwa nini haufanyiki utelekezaji huu wa kuacha kuwakufurisha Waislamu, kukufurisha ambako kungali kunaendelea katika risala na hotuba na fatwa, au kwa uchache ufanyike msamaha kwa apendaye kuufanyia rejea mfumo wa kifikra wa eneo hili (Saudia), au je kwenda kinyume na wanazuoni katika uharamishaji mpira au kuwaelimisha mabinti kunahesabika ni kuchelewa au kurudi nyuma, ama kuwatii wao katika kukufurisha Waislamu kwahesabiwa kuwa ni ijtihadi inayokubalika, na kuwa sisi hatujiingizi katika elimu, na utukufu unabakia kwa kila mbeba ufurutu ada mpaka kwa mwenye ufurutu ada zaidi kuliko yeye.

MAWAHABI WAKUFURISHANA WAO KWA WAO Kutokana na matokeo ya mkazo wa Sheikh katika ukufurishaji, ni kwamba wafuasi wake hawakubaki nyuma baada yake isipokuwa miaka michache wakawa wanakufurishana wao kwa wao, baadhi yao wakawachukua mateka wanawake wa wenzao. Angalia kitabu ad-Durarus-Saniyyah (8/329 ), (9/35, 33, 22), kuhusu hili la kukufurishana wao kwa wao kuna mifano mashuhuri, sisi tutatosheka na mifano miwili tu: MFANO WA KWANZA: Sheikh Abdul-Latif bin Abdur Rahman ametoa fatwa akijiepusha mbali na Amiri Abdullah bin Faysal kwa sababu ya kuomba kwake msaada kwa dola ya Uthmaniya (ya kikafiri kwa mtazamo wake). Na Amiri huyo alipoiteka Riyadh, 165

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 165

1/20/2016 11:35:54 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Sheikh Abdul-Latif alimpa kiapoa cha utii, na alimuona kuwa amesilimu upya na Uislamu unafutilia mbali yaliyokuwa kabla. Tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (9/22). Na mara nyingine alisema: Kuwa kumkufurisha kwake hakujathibiti kwake, tazama kitabu adDurarus-Saniyyah (9/33).77 Na kabla ya hapo alimkufurisha Suudi bin Faysal na jeshi lake kwa kuomba kwao msaada kwa makafiri pia, tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (8/392 ), kisha alidharurika kumhesabu kuwa ni Mwislamu na kumpa kiapo cha utii alipopata ushindi. Ni kama hivyo mizaha, mara ni wajibu kupigana jihadi na huyu na kumkufurisha, kisha ni wajibu kumpa kiapo cha utii na kupigana jihadi nyuma yake dhidi ya Amiri mwingine ambaye tulikuwa tukitoa fatwa za usahihi wa Uislamu wake na kupigana jihadi nyuma yake. Na Amiri mwingine hakosi wanazuoni wanaokufurisha pia! Kisha huko hakuna ila fatwa ya ukafiri au imani tu; kwa kuwa watu wameizoea lugha hii, wala hawajasikia kuwapiga vita wazinzi madhalimu na wachokozi, kwa hiyo tumpigae vita basi ni murtadi kafiri mshirikina kama kufuru ya Firauni na Ibilisi! Na tunayepigana nyuma yake basi yeye ni muumini kama imani ya Manabii na wakweli na yeye ni sultani wa Mwenyezi Mungu ardhini! 77

  Na Sheikh Abdul-Latif Mungu amrehemu, ni muweza zaidi katika jaribio lake la kuzuia fitina, kuzihifadhi nafsi, heshima, na mali lakini yeye, Mungu amrehemu anatetea kila msimamo anaouchukua kwa sharia, kwa hiyo ni wajibu kumpiga vita Suudi bin Faysal kwa sharia! Na ni wajibu kumnusuru kwa sharia! Na ni wajibu kumpiga jihadi ndugu yake Abdllahi bin Faysal kwa sharia! Na ni wajibu kumnusuru kwa sharia! Na ni wajibu kuwapiga vita mafisadi kwa sharia! Na ni wajibu kuwatii mafisadi kwa sharia! Kwa sababu wao ndio washindi! Na kama hivyo...( Rejea ad-Durarus-Saniyyah 9/34 na ya baada yake). Sharia hii imetudhoofisha kabisa katika mfano wa utumikishaji huu. Na nilikuwa natamani Sheikh asingeubebesha Uislamu misimamo hii yote inayopingana. Na kwa bahati mbaya ni kwamba usalafi unasumbuliwa na maradhi haya ya kupingana na udhabidhabina tangu zamani kiasi kwamba msomaji ataingiza fikrani kuwa Msalafi huyu anakusudia kuutiisha Uislamu katika lile alitakalo yeye binafsi! Linaloafikiana na utashi wake ndilo litakiwalo kisharia bali ndio Tawhidi halisi, na analolichukia au asilolielewa ndio la kulaumiwa kisharia! Bali ni kufuru na kuritadi!! 166

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 166

1/20/2016 11:35:54 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

MFANO WA PILI: Kurushiana tuhuma za ukafiri kati ya wanazuoni wanaomuunga mkono mfalme Abdul-Azizi Mungu amrehemu, na jamaa wa Faysal ad-Duweyshi. Sina shaka kuwa ad-Duweyshi na wenzake ni wenye makosa, lakini kosa lao sio kufuru imtoayo mtu nje ya Uislamu, lahasha si hivyo. Bali wao ni Waislamu waliotoka nje ya utii wa amri, na hii ndio iitwayo uasi. Ama wanazuoni wanaomuunga mkono mfalme Abdul-Azizi Mungu amrehemu, wao walitoa fatwa ya kumkufurisha ad-Duweishi na Ajamani na kuthibitisha kuritadi kwao! Fatwa imekuja kutoka kwa wanazuoni kadhaa, miongoni mwao ni Muhammad bin Abdul-Latif, na Muhammad bin Ibrahim, na Sulayman bin Sahman, na Swaleh bin Abdul-Azizi, na wanazuoni wengi wa al-Aaridh, tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (9/209). Na walitilia mkazo kuwa hapana shaka kuhusu ukafiri wao na kuritadi kwao... na kuwa miongoni mwa dalili kubwa ya kuritadi kwao ni madai yao kuwa wao hawakuwa chini ya mamlaka ya Ibn Suudi ila kwa kulazimishwa! Na kuwa wao ni miongoni mwa raia wa Uturuki. Nasema: Mfalme Abdul-Azizi, Mungu amrehemu, alikuwa anaridhika nao bila ya kuwakufurisha Waislamu, ilikuwa wanachuoni hawa wanaweza kumhesabu ad-Duweyshi na wafuasi wake kuwa ni madhalimu, na madhalimu ni wajibu kuwapiga vita mpaka warejee kwenye haki, na warudi kwenye jamaa. Na sisi hii leo kwa kauli moja hatusemi hao wameritadi bali tunasema wamefanya makosa kwa kumkiuka kwao mtawala, kila utunzi hii leo unaoongelea mapinduzi ya ad-Duweyshi, Jahimani na wengineo unaongelea kwenda kinyume na amri ya Amiri, na hii kwa mafakihi kwa ijmai huitwa uasi, wala haiitwi kufuru wala uritadi. NA WAKATI ULIOPO: Wote wanajua kuwa Mawahabi baada ya tatizo la pili la Ghuba (vita ya kuikomboa Kuwait), Uwahabi uligawanyika makundi manne, wanachukiana wao kwa wao, wanatwis167

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 167

1/20/2016 11:35:55 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

hana wao kwa wao tuhuma mbaya, kiasi kwamba hali hii ilijitokeza vitabuni na katika makala, na mapambano yangali ni makali, bali suala limefikia kufanyiana uadui kimwili katika baadhi ya hali, lau si kuhofia mateso ya dunia wangeuana wao kwa wao. Msomaji hana budi ila ni kuingia katika makongamano ya kisalafia na ataona kukufurishana na kuitana kwao wanabidaa wao kwa wao, wala hakuna tofauti kati ya sifa mbili hizo (ukafiri na bidaa) kwa wafurutu ada kwa kuwa sifa mbili hizo zote kwao zinawajibisha moto.

MIONGONI MWA MIFANO YA WASTANI ­KATIKA MADRASA YA KIWAHABI: Tulisema kuwa ni katika insafu kutaja sura nyingine japo ziwe hafifu, na imetangulia hapo kabla, nimeorodhesha kauli za wastani, lakini yasikitisha ni chache mno, na zina hali isiyo wazi na ya kupingana. Lakini baadhi ya Mawahabi waliishi Misri baada ya kuanguka kwa Dariyya na walichuma baadhi ya maarifa yaliyopanua uwelewa wao. Na tulikuta baadhi ya misimamo ya wastani halisi isiyochangamana na giza katika fatwa zao. Huyu hapa Sheikh Abdullah bin Muhammad bin Abdul-Wahabi anaona kuwa: “Waliyonayo wahakiki miongoni mwa wenye elimu ni: kutowakufurisha watendao bidaa kama Makhawariji, Marafidhi (Shia), al-Qadiria na Murjia, kwa sababu kukufurisha hakui ila kwa kukataa la dharura katika dini au kutenda kitu ambacho imeafikiwa kuwa chamkufurisha mwenye kukitenda”. Tazama kitabu ad-Durarus-Saniyyah (10/244). Na hii ni rai ya wastani, ipo kinyume na aliyonayo baba yake Sheikh Muhammad na wengi miongoni mwa wanazuoni wa Kiwa168

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 168

1/20/2016 11:35:55 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

habi mpaka hii leo. Anacho kitabu kuhusu Sira ya Mtume 5 amekwenda humo mwenendo wa wastani, na alimsifu Ammar Bin Yasir na kumfanya kuwa ni mizani ya haki katika vita vile. Na huo ni msimamo wa wastani sijawaona nao Mawahabi ukimuondoa Sheikh Ibn Bazi Mungu amrehemu. Katika Uwahabi kuna chuki dhidi ya Ahlulbayt kwa sababu mbili: Kwanza kwa kuiga, yaani kwa kumfuata Ibn Taymiya na wafurutu ada wa kihanbali. Pili kwa uhasama wa kihistoria tangu siku ya kuanza kwake, dhidi ya Shia upande wa Mashariki, Magharibi Kaskazini, na Kusini.

169

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 169

1/20/2016 11:35:55 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

UTAFITI WA NNE MAHASIMU WA SHEIKH NA ­WAPINZANI WAKE

K

ama ilivyotokea dhulma na ukufurishaji kutoka kwa Sheikh na kwa wafuasi wake dhidi ya wapinzani wao, wapinzani nao wamewadhulumu wao isipokuwa wachache. Walimtupia Sheikh tuhuma kubwa, mfano ya kudai unabii na kumpunguzia hadhi Nabii 5. Wanagawanyika wapinzani wa Sheikh na wa daawa ya uwahabi katika vikundi vitatu: KIKUNDI CHA KWANZA: Waliopitiliza kulaumu na wakaukufurisha Uwahabi na walimkufurisha Sheikh na Mawahabi. Makosa ya kikundi hiki hayajifichi kwa mwenye insafu. Hii kaumu ni Waislamu wenye dini lakini ufuasi, na uhasama wa kimadhehebu na wa kisiasa uliwasukuma kuwakufurisha wengine, na aliyetumbukia katika ukufurishaji kwa taawili hakufurishwi, hivyo basi walioukufurisha Uwahabi au Sheikh Muhammad wameingia walipokuwa wanapahadhari kwa namna wasioijua, kwa kuwa wao ikiwa watatoa udhuru kuhusu baadhi ya wanayoyakanusha kama vile ufurutu ada katika usufi au ushia na kuwa hao wanayo taawili na katika wao kuna ujinga, hali ni hiyo hiyo kwa Mawahabi ambao hawawi salama mbali na ujinga na taawili. Ama kuutuhumu uwahabi kuwa umetengenezwa na Uingereza, kulingana na muswada wa mtu mmoja Mwingereza ulio mashuhuri katika mtandao wa intanet ni batili. Mwingereza huyo ambaye alina170

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 170

1/20/2016 11:35:55 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

sibishwa na muswada huo jina lake ni Hamfrey, humo amedai kuwa alikutana na Sheikh huko Basra na kwamba alimuongoza mpaka Najd.... hii ni miongoni mwa uzushi batili ulio wazi, kwa sababu kadhaa, na zilizo muhimu ni: YA KWANZA: Sheikh na maimamu wa Aali Suudi (Muhammad na mwanawe Abdul-Azizi) waliendelea kuipiga vita Riyadh, Dukhna na Manfuha, na miji ile ya karibu na Dariyya zaidi ya miaka ishirini. Lau wangekuwa na usaidizi wa Uingereza wasingebaki katika vita na miji ile na vitongoji vya karibu ila siku chache au miezi kadhaa kwa makadirio ya mbali. PILI: Muswada wa yule Mwingereza aitwae Hamfrey sio sahihi.... TATU: Kuwa lugha ya Sheikh katika vitabu vyake na risala zake zinabainisha kwa asiye na ushabiki kuwa huyu mtu ni mkweli kwa alionalo kuwa ni haki si mfuasi wa mtu yeyote. Na alikuwa anaomba maapizano na hatoyaomba Mwislamu ila akiwa anaamini asemayo. Vitabu vyake vyote na risala zake na sera yake zajulisha kuwa huyu mtu ni mkweli katika daawa yake, lakini ukweli wake katika daawa haumaanishi usahihi wake katika maudhui ya kukufurisha. KIKUNDI CHA PILI: Wameona Uwahabi ni bidaa na hawakuwafurisha Mawahabi, lakini wao hawakutambua mema yao, na huu ni ushabiki, ni sahihi kuwa kaumu hii wamefanya bidaa katika vitu kama vile kukufurisha, lakini wao wamehuisha miji mingi ya alJazira kutoka kwenye ulegevu wa kidini, bidaa na itikadi za dhana, na walidhihirisha nembo za kidini na walikuwa sababu ya kuimarika dola iliyokusanya mparaganyiko wa makabila katika eneo kubwa la Rasi ya Uarabu, wala mwenye insafu hawezi kukanusha kuwa umoja wa haya makabila chini ya bendera moja ni bora kuliko mtawanyiko wao, japo baadhi yao yawadhulumu wengine. 171

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 171

1/20/2016 11:35:55 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

KIKUNDI CHA TATU: Wametambua haki waliyonayo Mawahabi na athari waliyoizusha, lakini waliwakubali na waliwachukulia kuwa wametenda makosa ya kupanua wigo wa kukufurisha na kuua na hawakuwakufurisha au kuwafanya wanabidaa. Na sehemu hii ya mwisho kwa hakika sio miongoni mwa mahasimu wa Mawahabi na wala sio wapinzani wao katika kukemea bidaa na itikadi za dhana, na ilikuwa ni wajibu juu ya Mawahabi wafanye kazi ya kuwapata hawa na kuwahesabu kuwa ni Waislamu. Lakini yasikitisha Mawahabi wengi walikuwa wanaikufurisha sehemu hii ya mwisho.

MIONGONI MWA WAPINZANI MASHUHURI WA UWAHABI NI: 1.

Suleyman bin Sahim al-Hanbaliy An-Najdiy (1130 -1181A.H), fakihi wa watu wa Riyadh, jina lake kamili ni Sulayman bin Ahmad bin Sahim. Baba yake alikuwa fakihi pia na miongoni mwa wapinzani wa Sheikh Muhammad, naye ni wa kabila la Anzah. Alikuwa fakihi wa kihanbali mbora, mchimbuaji. Alitoka kwenda mji wa Zubayr baada ya Mawahabi kuiteka Riyadh na alifariki dunia huko. Na Sheikh Muhammad bin AbdulWahabi alimkufurisha, kufuru kubwa inayomtoa nje ya Uislamu! Na huenda Sheikh alifanya vibaya katika kumlaumu hadi akamwita Albahim, na huku ni kupita kiasi katika kulaumu.

2.

Sulayman bin Abdul-Wahabi at-Tamiimiy an-Najdiy (1208 A.H.), Ni ndugu wa Sheikh Muhammad kwa baba na mama, na alikuwa mjuzi zaidi kuliko yeye Sheikh Muhammad. Na yeye ni fakihi wa kihanbali miongoni mwa makadhi wa Najdi na wanazuoni wao, na ni mtu mwadilifu miongoni mwao. Alizaliwa Uyayna, na alijielimisha huko Hariymla wakati wa 172

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 172

1/20/2016 11:35:55 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

baba yake, na alitawalia ukadhi wa Hariymla, na alikwenda Sadiyr baada ya kuangukia Hariymla mkononi mwa Uwahabi. Naye alikuwa na wafuasi huko Uyayna na Dariyya, na alikuwa anawasiliana nao ili kuwakinaisha waachane na Sheikh Muhammad na kukufurisha, basi wafuasi wa Sheikh Muhammad walikuwa kila wakimfuma mshenga wake wanamuua hapohapo! Eti kwa sababu amekuja kutoka nchi ya vita kulingana na mtazamo wao. Alihamia Sadiyr baada ya kuanguka Hariymla, alibaki mpinzani dhidi ya nduguye zaidi ya miaka arobaini, toka mwaka 1157 A.H., mpaka mwaka1190 A.H, kisha baada ya kuenea dola ya daawa mpaka katikati ya Najd alikuja na msafara wa Zulfiy akiwa hapendi, na alibakia Dariyya akiwa na itikadi yake karibu miaka ishirini, yeye hakufa ila baada ya kifo cha nduguye kwa miaka miwili. Baadhi walivumisha kutokana na yeye, lakini haikuwa sahihi, naye ni mfano wa hali ya juu wa mwanachuoni mwenye kujiheshimu kwa elimu yake ambaye hasukumwi na ukaribu au umbali kubadili analolifanyia dini yake kwa Mungu, na anavuta subira juu ya aonalo kuwa ni haki japo awe kwenye mabano ya mdomo wa simba. Na ndugu Sheikh Suudi Sarhan anao utafiti mzuri kuhusiana na tofauti za ndugu wawili (Muhammad na Sulayman). Na Sheikh al-Bassam ameripoti katika kitabu chake, ‘Wanazuoni wa Najd,’ kuwa Sheikh Suleyman bin Abdul-Wahabi hakuitelekeza madhehebu yake katika kumpinga Sheikh, lakini sauti yake ilihafifishwa, na aliombewa asiuliwe kwa kuwa ni ndugu wa Sheikh, vinginevyo yeye katika madhehebu yao ni kafiri ukafiri mkubwa unaotoa nje ya Uislamu, kwa kuwa kulingana na adabu za Kiwahabi anaitukana dini ya Rasuli! Na yeye anacho kitabu Aswawaiqul-Ilahiyah katika kumjibu ndugu yake, nalo ni miongoni mwa majibu yenye nguvu yaliyopata kuandikwa kuwajibu Mawahabi, wapinzani wa 173

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 173

1/20/2016 11:35:55 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

uwahabi walikipa umuhimu hivyo walikichapisha mara nyingi huko India, Misri na Uturuki. Nacho mpaka hii leo chahesabiwa miongoni mwa majibu yenye nguvu mno dhidi ya Mawahabi, kwa kuwa huyu mtu ni Muhanbali na ni ndugu bali ni wa baba mmoja mama mmoja na Sheikh, anaijua Najdi na hali ya Najdi, hivyo basi hatuhumiwi kuwa na chuki ya utaifa wala kabila wala nchi, na nimesoma kitabu chake cha kumjibu Sheikh naye ni mwenye uwezo kielimu na ni mtulivu wa nafsi na ni mwenye hoja zenye nguvu Mungu amrehemu na awe radhi naye. 3.

Muhammad bin Abdur Rahman bin Afaliq Hanbaliy Ahsa (1100 -1164 A.H ). Ni miongoni mwa wanazuoni wakubwa wa Ahsa. Alikuwa fakihi mwenye fadhila mwenye elimu kubwa kwa viwango vya zama zake, na ana vitabu vya fikihi na elimu ya sayari. Na alikuwa sababu ya kumtoa Uthman bin Muammar Amiri wa Uyayna mbali na Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahabi pamoja na kuwa Sheikh Muhammad alikuwa kwa Ibn Muammar, lakini nguvu za hoja za Ibn Afaliq zilimsukuma Ibn Muammar aachane na Sheikh na asimnusuru. Na kuwa Ibn Afaliq alikuwa anaweza kwa barua kutoka Ahsa kumkinaisha Ibn Muammar kwa sababu ya udhaifu wa hoja za Sheikh ambaye ni mkwewe. Na hili linatujulisha sisi jinsi Ibn Afaliq alivyojengeka kwa nguvu za kielimu, Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahabi alimkufurisha huyu kufuru kubwa inayomtoa nje ya Uislamu.

4.

Abdullahi al-Muwaysi (1175 A.H ), ni fakihi wa watu wa Hurmah katikati ya Najdi, na jina lake ni Abdullah bin Isa at-Tamiimiy (1175 A.H.), ambaye ni mashuhuri kwa jina la al-Muwaysi. Na al-Muwaysi ni miongoni mwa Masheikh watukufu wa watu wa Najdi. Alisoma kwa wanazuoni wa Najdi halafu alisafiri 174

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 174

1/20/2016 11:35:55 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

kwenda Sham (Syria) na alisoma kwa Allamah as-Safariniy, na as-Safariniy ana usia mahsusi kwa Sheikh al-Muwaysi, na yeye ni miongoni mwa wanazuoni watukufu wa Najdi kwa mujibu wa Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahabi, naye ndiye ambaye aliweza kumkinaisha Abdullahi bin Sahim aache kumuunga mkono Sheikh Muhammad na hali alikuwa miongoni mwa waungaji mkono wake. Kwa minajili hiyo Sheikh alimghadhibikia na kumkufurisha. Sheikh al-Basam alileta dondoo za majibu ya huyu Ibn Isa dhidi ya Sheikh Muhammad katika kitabu Ulamau Najd (4/365), katika majibu yake mna nguvu za dhahiri za kupinga ukufurishaji aliokuwanao Sheikh Muhammad, kwa hiyo Sheikh Muhammad alimtuhumu kuwa ni miongoni mwa wazuiaji dini ya Rasuli! Na alimkufurisha na kumtoa nje ya Uislamu! Na hili ndilo tulikanushalo dhidi ya Sheikh Muhammad Mungu amrehemu kuwa yeye humkufurisha kila asiyeafikiana naye na humtuhumu kuwa ni adui wa dini ya Rasuli, ilihali si jaizi kwa mtu yeyote kuhodhi binafsi dini ya Rasuli kwa madai na tafsiri na awakufurishe watu kwa kujengea juu ya tafsiri yake peke yake. 5. Abdullahi

bin Ahmad bin Sahim (1175 A.H ), ni fakihi wa watu wa Majmaa huko Qaswim, alikuwa fakihi na ni Mhanbali na kadhi wa miji yote ya Sadir. Hakuwa na uadui mkubwa na Uwahabi lakini alikuwa anaupinga ufurutu ada wa Uwahabi katika kukufurisha. 5.

Abdullahi bin Muhammad bin Abdul-Latif wa Ahsa, naye ni miongoni mwa masheikh wa Sheikh Muhammad na ni miongoni mwa wapinzani wake wakali dhidi ya daawa yake.

6.

Muhammad bin Abdullahi bin Feyruz wa Ahsa (1216 A.H ), na Aali Feyruzi ni Matamimu miongoni mwa Wahbat ambao ni 175

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 175

1/20/2016 11:35:55 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

kabila la Sheikh Muhammad. Ibn Feyruzi huyu na baba yake na babu yake ni miongoni mwa wanazuoni wa kihanbali, na alikuwa mjuzi katika kuhifadhi na werevu, kiasi kwamba ilisemekana alikuwa anafanya imla ya Sahihi Bukhari akiwa ameihifadhi. Na alikuwa anasimamia mambo ya wanafunzi wake, na aliwadhamini karibu wanafunzi hamsini. Alikwenda Basra akiwa na wapambe na wanafunzi wake baada ya Mawahabi kuiteka Ahsa katika zama za Abdul-Azizi bin Muhammad, watu wa Basra watukufu miongoni mwao wakiwemo wanazuoni walimpokea mapokezi makubwa, hivyo siku ilikuwa ya kushuhudiwa kwa mujibu wa ibara ya Sheikh Basam. Na alibaki huko akisoma elimu ya sharia, na ulikamilika upanuzi wa msikiti wa Basra baada ya kufika kwake huko kwa sababu ya kukithiri wahudhuriaji huko. Watawala na masultani walikuwa wanamuomba yeye kuwateua makadhi na walimu, baada ya kifo chake alibebwa juu ya vichwa kutoka Basra mpaka mji wa Zubair ambako ndiko alikozikwa pembezoni mwa kaburi la Zubair bin Awam. Watu wa nchi mbalimbali wa madhehebu nyingine walimfanyia wasifu, na alikuwa na heshima kubwa kwa Sultani wa utawala wa Uthmaniyyah. Alikuwa anampinga Sheikh Muhammad kwa nguvu, na upinzani wake ulikuwa na umashuhuri na athari kwa ajili ya heshima yake kubwa katika fani mbalimbali za elimu za kisharia. Na Sheikh alikuwa anamkufurisha kufuru kubwa imtoayo nje ya Uislamu! Na kumhesabu mwanachuoni mkubwa mwerevu kama huyu kuwa ni kafiri mkubwa kunatufanya tutambue kuwa Sheikh Muhammad amefanya ufurutu ada katika ukufurishaji. 7.

Muhammad bin Ali bin Salum (1246 A.H ), lakabu yake ni Fardhiy. Ni miongoni mwa wazaliwa wa Sadir, miongoni mwa ma176

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 176

1/20/2016 11:35:55 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

fakihi wa Kihanbali, alikimbilia Basra kuwaogopa Mawahabi, akiwa na Sheikh wake Ibn Feyruzi wa Ahsa. 8.

Uthman bin Mansur an-Nasriy (1282 A.H) ni katika watu wa Sadir, alisoma huko Najdi na Irak. Walimsifu ndani ya al-Jazira na nje yake, na anao ufafanuzi wa kitabu Tawhid cha Sheikh Muhammad, lakini yaonesha kuwa ni ufafanuzi ambao hakumfuata humo Sheikh katika kila alilosema. Alikuwa kadhi wa Sadri, kisha Hail katika siku za Turki bin Abdullahi na Faysal bin Turkiy. Na hii ni miongoni mwa dalili zetu kuwa dola ya pili ya Saudia haikuwa ya kiwahabi au ni kuwa iliachana na uwahabi. Na Sheikh alikuwa na rai kali kuuhusu uwahabi.

9.

Yeye anawaona wao ni katika Makhawariji. Na anavyo vitabu kupinga ufurutu ada wa daawa hii, miongoni mwavyo ni Jalaul-Ghummah Ani Takfiri Hadhihil-Ummah, kwa minajili hiyo wanazuoni wa kiwahabi moja kwa moja walimwita kafiri na kumwelekezea lawama mbaya dhidi yake, na miongoni mwa hao ni Sheikh Abdur Rahman bin Hasan na mwanawe Abdul-Latif, zikaja tuhuma zao kwa Sheikh huyu kadhi wa kihanbali mwana wa Najdi kuwa yeye: “Anaitusi dini ya Mungu na kumsemea uwongo Mwenyezi Mungu na Mjumbe Wake na kuzuia njia ya Mwenyezi Mungu na kuifayia uadui dini ya Mwenyezi Mungu.�

10. Na hizi ni miongoni mwa dhulma za uwahabi hadi hii leo. Kila anayehitilafiana nao wanapanda na tuhuma zake mpaka mbinguni na wanamtuhumu na tuhuma nzito kama vile kuwa anaitukana dini na kumtukana Mwenyezi Mungu na Mjumbe Wake na kuizuia dini ya Rasuli. Tunajilinda kwa Mwenyezi Mungu dhidi ya dhulma ya uhasama, hususan dhidi ya wafurutu ada. 177

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 177

1/20/2016 11:35:55 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

11. Uthman bin Sindi al-Basriy (1250 A.H), ni fakihi wa Basra, aona kuwa Mawahabi wawakufurisha Waislamu walio juu ya ardhi hii kwa jumla! Na alistaajabishwa na Dkt. Abdul-Azizi Abdul-Latif vipi alijaalia jambo hili kuwa miongoni mwa yaliyozushwa na Uthman bin Sindi! Hivyo ukweli wa baadhi ya maandishi ya kiwahabi yanayotegemewa kimadhehebu uko hivi, japo halikusemwa hilo kwa tamko la ibara, mifano imetangulia. 12. Muhammad bin Sulayman al-Kurdiy (1194 A.H), Alikulia Sham, naye alikuwa ni mufti wa Kishafi huko Madina tukufu baada ya kuiendea, na alikuwa miongoni mwa wapinzai wa daawa ya kiwahabi na anayo majibu ya kumpinga Sheikh aliyoyaita Masailu Waajwiba Waraddu Alal-Khawariji. Ni wazi kutokana na anwani hiyo kuwa anamtuhumu Sheikh Muhammad na uwahabi kuwa wao ni Makhawariji, kwa sababu ya ufurutu ada wao katika kukufurisha, lakini kupandikiziana vijisifa sio sawa. Kisha ieleweke kuwa Uwahabi haukufurishi kwa maasi isipokuwa unakufurisha kwa mambo ya ndani ya imani, na aghlabu ni yale yenye uzito. Kwa minajili hiyo wao sio Makhawariji kwa maana ya moja kwa moja, lakini wao wameafikiana na Makhawariji katika baadhi ya mas’ala na wamehitilafiana nao katika mengine. 13. Muridu bin Ahmad Tamimi (1171 A.H), ni miongoni mwa wanazuoni wakubwa wa Najd. Alisoma Najd na Sham, na alitawalia ukadhi huko Harimla, naye ndiye aliyesafiri mpaka Sanaa na alikutana na Allamah mtukufu Muhammad al-Amiriy as-Swan’aniy, na ndiye mwenye kitabu Subulus-Salam. Na Allamah mtukufu Muhammad al-Amiriy as-Swan’aniy alikuwa amemsifu Sheikh Muhammad na daawa yake katika 178

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 178

1/20/2016 11:35:55 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

kaswida. Sheikh Muridu alimkinaisha ajiepushe na kaswida ile baada ya kumuonesha vitabu vya Sheikh mwenyewe. Basi Allamah mtukufu Muhammad al-Amiriy as-Swan’aniy aliona ndani yake kuna ukufurishaji wa kuwakufurisha Waislamu, hivyo akabadili msimamo dhidi ya kaswida yake ile kwa kuitangua kwa kaswida nyingine ambayo Mawahabi walijaribu kuitilia shaka. Na miongoni mwa aliye mashuhuri mno kati yao ni Ibn Sahman katika kitabu chake Tabriatul-Imamayni al-Jalilayni, kwa kuzingatia heshima kubwa ya kielimu aliyokuwa nayo Allamah mtukufu Muhammad al-Amiriy as-Swan’aniy. Lakini kaswida ipo thabiti, nayo ipo katika diwani ya Allamah mtukufu Muhammad al-Amiriy as-Swan’aniy. Basam ameithibitisha na Hamadul-Jasiru na wengineo. Mawahabi walimuua fakihi huyu katika mji wa Raghbat mwaka 1171 A.H. 14. Seifu bin Ahmad al-Atiqiy (1189 A.H), alizaliwa Hurmat na alihamia Ahsa, alikuwa fakihi mwenye heshima. 15. Swalih bin Abdullah Swaigh (1183 A.H), ni fakihi wa Anizat, na ni kadhi wa hapo Anizat. Alikuwa ameshaijibu kaswida ya Allamah mtukufu Muhammad al-Amiriy as-Swan’aniy ambayo humo alikuwa anamsifu Sheikh, na alimsuta Allamah mtukufu Muhammad al-Amiriy as-Swan’aniy kuwa kumuunga mkono kwake Sheikh Muhammad kwa kuwa ni Zaydiya. Na huenda anakusudia kuwa njia ya Zaydiya inaelemea kwenye mageuzi dhidi ya hali ya mambo iliyopo, na imefichika kwake kuwa Zaydiya maoni yao sio kukufurisha, wala mageuzi ya kiupofu bila ya udhibiti wala masharti. Na mradi wa kisiasa ni wa uadilifu, kama ambavyo Allamah mtukufu Muhammad alAmiriy as-Swan’aniy ni mujtahidu wa kisunni, lakini bila ya 179

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 179

1/20/2016 11:35:55 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

sanamu wala kushabihisha. Lakini hapa la muhimu kwetu ni muundaji alikuwa Hanbali mtu wa Najd mpinzani wa Sheikh. 16. Ahmad bin Ali al-Basriy al-Qabaniy, ni msunni wa Irak, ametunga kitabu Faslul-Khitabi Firadi Dhwalalatu Muhammad bin Abdul-Wahabi, kumjibu Muhammad bin Abdul-Wahabi. Na kitabu hicho Dkt. Abdul-Azizi Abdul-Latif amekisifu kuwa ni jalada kubwa. 17. Abdullah bin Daudi Zubairiy (1225 A.H) ni msunni wa Iraq, kutoka mji wa Zubair, amesoma huko Zubair na Ahsa, ameandika kitabu as-Swawaiqu Waruduud, kuwajibu Mawahabi, amepata heshima kutoka kwa baadhi ya wanazuoni wa kisunni wa Iraq, Sham, na Hadhramaut. Na Ibn Hamidi al-Hanbaliy al-Makiy mwenye kitabu Subulul-Wabilah Ala DhwaraihilHanabilah amemsifu. 18. Alawi bin Ahmad al-Hadadu al-Hadhramiy (1232 A.H), ni miongoni mwa wanazuoni wakubwa wa kisunni wa Hadhramaut, na ana vitabu vingi katika kuwajibu Mawahabi. 19. Umar bin al-Qasim bin Mahjub at-Tunisiy (Muujamul-Mualifina). 20. Muhammad bin Abdullah bin Kiiran al-Maghribiy (1227 A.H), ni miongoni mwa wanazuoni wa Faas huko Morocco. 21. Muhammad bin Abdullah bin Hamiid (1215 A.H), ni Imamu wa mahanbali huko Makkah Tukufu, mwenye kitabu SubululWabilah, na alikuwa msomeshaji wa fikihi ya kihanbali huko Makkah.

180

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 180

1/20/2016 11:35:55 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

22. Abdul-Azizi bin Abdur Rahman bin Udwan (1179 A.H), miongoni mwa wanazuoni wa al-Washim. 23. Hasan bin Ummar as-Shatiy ad-Damashqiy (1274 A.H), ni miongoni mwa wanazuoni wa Damascus. Naye ni fakihi wa kihanbali mashuhuri.

TUHUMA ZILIZO MAARUFU MNO ­WALIZOZIELEKEZA WANAZUONI KWA SHEIKH MUHAMMAD: 1.

Kukufurisha: Na hii ni tuhuma yenye nguvu mno na sahihi kabisa na itoshelezayo na ni hatari mno kati ya tuhuma ambazo mahasimu wa Sheikh Muhammad wanazielekeza kwake na kwa wafuasi wake, kiasi kwamba hata wale walio wakali sana katika kumhami Sheikh na da’awa yake miongoni mwa wanazuoni wa Kisalafi hawakuweza ila kukiri kuwepo kwa tuhuma hizi. Kwa mfano Shawkaniy, na yeye upande wa Tawhidi ni Msalafi kwa mujibu wa Mawahabi wenyewe. Yeye pamoja na ushabiki wake wa kuipendelea daawa ya kiwahabi na kuisifu kwake mno na kumsifu kwake Sheikh Muhammad, hakuweza ila kusema: “Lakini wao wanaona asiyeingia katika dola ya Bwana wa Najd, akiwa mtekelezaji wa amri yake, yuko nje ya Uislamu.” Rejea kitabu al-Badru Taaliu (2/5).

Kadhalika Mansur al-Hazimiy, naye ni Msalafi, pamoja na kumsifu kwake Sheikh Muhammad ila yeye amemchukulia kwamba amefanya makosa katika mambo mawili: Kwanza: Kwa kuwakufurisha watu wote walio ardhini kwa uzushi tu. Pili: Kwa kumwaga damu iliyohifadhiwa bila ya hoja wala uthibitisho. Tazama kitabu Abjadul-Ulumi (3/194). 181

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 181

1/20/2016 11:35:55 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Kadhalika Sheikh Msalafi Muhammad Swidid Hasan Khaan, alitangaza kujiepusha kwa watu wa Hadith dhidi ya Uwahabi kwa sababu wao hawajui ila kumwaga damu. Angalia: Daawal-Munawiina, Uk.160.78 Na miongoni mwa wasioelemea upande wowote ambao walisema Mawahabi wanakufurisha, ni Sheikh mwanahadithi Anwar Shaha Kashmiriy, yeye anaona Mawahabi wanafanya haraka katika kumhesabu mtu kuwa ni kafiri. Angalia kitabu Daawal-Munawiina, uk. 160. Ama walio kinyume na uwahabi kauli zao katika hili ni nyingi sana. Nitafanya ufupi humu kwa mifano ya kauli za Ahlus Sunna nikianzia na kauli za Mahanbali miongoni mwao: Huyu hapa Sheikh wa Kisunni Mhanbali Ibn Afaliq anasema kuhusu Sheikh Muhammad kuwa yeye: “Ameapa yamini mbaya: Kuwa yahudi na washirikina wako na hali nzuri kuliko umma huu.”79   Dkt, Abdul-Azizi Abdul-Latif ametoa udhuru kuwa vyanzo vyake katika hilo ni vya kikristo! Mtukufu Dkt. amejisahaulisha kuwa umwagaji damu wa Mawahabi upo katika vyanzo vya kiwahabi vyenyewe. Huyu Ibn Ghannaam anataja katika kitabu chake cha historia zaidi ya hujuma 300, ibara zake zote zinasema: Katika mwaka huu Waislamu waliwashambulia makafiri...(Mashambulizi haya ni kutoka kwa Mwislamu dhidi ya Waislamu katikati ya Najdi, Hijazi na Ahsa ......)! Kisha Wakristo huandika habari za Mawahabi kutoka kwa Waislamu, hata hivyo Wanajd hawakuwa Wakristo. Kisha Dkt. Na wengine wanaouhami Uwahabi tunawakuta katika natija hawaikubali nukuu ila kutoka kwa Mawahabi, wala hawazikubali riwaya za wanazuoni wa ki-Sunni miongoni mwa wale wanaohitilafiana na Mawahabi, kana kwamba wao wanatulazimisha sisi kufahamu yaliyojiri kulingana na wasemavyo Mawahabi tu! Kama kwamba Waislamu wengine ni makafiri wa kikureshi mbele ya Nabii 5. Na hii ni ufurutu ada na kupitiliza. Hivyo Waislamu walio kinyume na uwahabi mwishowe ni wakweli katika kuwatuhumu Mawahabi kwa kukufurisha na kuua. Haya tumeyaona yamethibiti kutoka katika maneno ya Sheikh mwenyewe na maneno ya wafuasi wake kwa kiasi ambacho hatuwezi kumtupia lawama mkristo wala myahudi. 79   Daawal-Munawiina cha Dr. Abdul-Azizi Abdul-Latif, uk.164, Chapa ya kwanza – Nayo ni risala ya chuo kikuu cha Imamu Muhammad bin Suud al-Islamiya huko Riyadh – Chapa ya Darul-Watan,1412 A.H.. 78

182

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 182

1/20/2016 11:35:55 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Nasema: Na hili lipo wazi katika kauli ya Sheikh kuwa washirikina wa zama zetu (kwa usemi huo anawakusudia Waislamu waliohitilafiana na yeye) ni makafiri mno kuliko makafiri wa Kikuraishi kwa mambo mawili, na ni wazi kuwa makafiri wa Kikuraishi ni wenye kufuru mno kuliko Ahlulkitab. Hatujamkuta Dkt. Abdul-Aziz AbdulLatif katika kitabu chake Daawal-Munawiina akimkusanya Sheikh Ibn Afaliq kwa kauli hii na mfano wake katika jumla ya waongo. Itawezekanaje wakati kauli za Sheikh ziko bayana katika hili kama ilivyotangulia katika kukikosoa kitabu chake Kashfushubhat. Na huyu hapa Sheikh wa Kisunni Mhanbali Suleyman Ibn Sahim anasema kumhusu Sheikh Muhammad: “Na asiyeafikiana naye kwa kila alilosema na kushuhudia kuwa hiyo ndio haki, anakata shauri kuwa ni kafiri! Na anayeafikiana naye na kumsadiki kila alilosema, atasema: Wewe ni mwanatauhidi, japo awe muovu kabisa.”80 Na huyu hapa Sheikh wa Kisunni Mhanbali Msalafi wa Najdi, Uthman bin Mansur, ni miongoni mwa makadhi wa utawala wa Aali Suud katika dola ya Saudia ya pili.81 Anasema: “Mwenyezi Mungu 80 81

Rejea iliyotangulia, uk. 160.   Hizi ni sifa sita za kisalafi katika mtiririko mmoja! Sheikh Msunni, Msalafi, Mhanbali, Mwenyeji wa Najdi, na Kadhi aliyefanya kazi na watawala wa Aali Suud, na hii ni sifa ya saba. Na Basaam na Bakari Abu Zayd na Swalih al-Qadhi walitaja wasifu wake na waliridhika naye na walimsifu, na hii ni sifa ya nane. Lakini wafurutu ada wa kiwahabi mwishowe hawakubali katika uwahabi wala usalafi ila kauli ya anayesifu tu, wao hadi hii leo katika kumhami Sheikh Muhammad wanazitoa kama ushahidi kauli za al-Qaswimiy ambaye jambo limemfikisha kwenye ulahidi, wala hawamleti Msalafi Mhanbali katika kumpinga Sheikh Muhammad, hivyo basi natija yao ni kutofanikiwa. Hivyo wao ni kama wanasema: Tutachukua kauli za wanaosifu na anayetakasa japo awe muovu au kafiri au Yahudi au Mkristo, na tutamtuhumu kila anayekosoa japo awe ni miongoni mwa waja wema wa Mwenyezi Mungu na wajuzi mno na wanyenyekevu mno kwa Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo wao wanazuia kunakili kutoka kwa Waislamu na kwa wasio Waislamu. Ama kuhusu wasio Waislamu inatosha wadai kuwa si Mwislamu. Ama Mwislamu wanasema yeye ni mtu wa bidaa. Na tukinukuu kutoka kwa Sunni husema: Huyu yuko mbali na daawa na si mtu wa Najd. Na tukinukuu kutoka kwa Mhanbali na mtu wa Najd, husema huyu ni miongoni mwa mahasimu wa Sheikh na wanaomhusudu! Hivyo hawakubakisha mbele yetu ila kunukuu kutoka kwa Sheikh na kwa wafuasi wake. 183

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 183

1/20/2016 11:35:55 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

amewapa mtihani watu wa Najd bali wa Rasi ya Uarabu kwa kuwepo mwenye kutoka dhidi yao na kufanya juhudi kuukufurisha umma huu mahsusi na umma wote kwa ujumla wake...kwa uzushi ambao Mwenyezi Mungu hajauteremshia dalili.”82 Na amesema: “Lakini mtu huyu - anamkusudia Sheikh Muhammad – amejaalia kufanya utii kwake yeye kuwa nguzo ya sita miongoni mwa nguzo za Uislam.”83 Na kadhalika Sheikh Suleyman bin Abdul-Wahabi ni ndugu wa Sheikh, anasema: “Nguzo za Uislamu ni ngapi ewe Muhammad bin Abdul-Wahabi?” Akasema: “Ni tano.” Akasema:”Wewe umezifanya ziwe sita, ya sita asiyekufuata si Mwislamu, hii kwako ni nguzo ya sita miongoni mwa nguzo za Uislam.”84 Nasema: Hapa usemi wa Sheikh Suleyman ni lazima ya usemi, vinginevyo Sheikh Muhammad hasemi hivyo, lakini ni natija ya masharti yake magumu ya kuthibiti Uislam. Na Zahawi anasema: “Lau muulizaji atauliza madhehebu wanayoifuata Mawahabi ni madhehebu gani? Na lengo lake ni nini? Tutasema katika kujibu maswali mawili haya: Ni kuwakufurisha Waislamu wote, na hilo jibu kwa ufupi wake litakuwa ni kitambulisho tosha cha madhehebu yake, (ya uwahabi).”85 Na anasema Sheikh Ahmad Zeyni Dahlani: “Hawaitakidi mtu kuwa ni mwanatauhidi ila mwenye kuwafuata wayasemayo.”86 Na tumefanya hivyo katika utafiti huu na tumethibitisha kuwepo kwa ukufurishaji katika kauli za Sheikh sembuse wafuasi, kimebaki nini baada ya yote hayo? Ijulikane kuwa wao wanajihalalishia wao binafsi kunakili kutoka kwa wauza vitabu na wauzao dhamiri na walioghafilika na makafiri, kwa minajili hiyo sisi humu hatuongei na wafurutu ada hukumu yao iliyotangulia yajulikana kwetu tokea mwanzo. 82   Daawal-Munawiina, uk. 166. 83   Daawal-Munawiina, uk. 166. 84   Daawal-Munawiina, uk. 166. 85   Daawal-Munawiina, uk. 167. 86   Daawal-Munawiina, uk. 166. 184

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 184

1/20/2016 11:35:55 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Na Sayyid Msunni al-Hadad al-Hadhramiy anasema: “Mtu akitaka kuingia katika dini yake anamwambia: ‘Shuhudia mwenyewe binafsi kuwa ulikuwa kafiri. Na shuhudia kuwa wazazi wako wawili walikufa wakiwa makafiri. Na shuhudia kuwa mwanachuoni fulani na fulani wao ni makafiri’...akishuhudia hivi atamkubali waila atamuua.”87 Kisha Sayyid al-Haddad anamalizia juu ya kitendo hiki cha Mawahabi kwa kauli yake: “Vipi hautosheki na walio hai kwa kuwafanya washirikina mpaka umevuka mpaka kwa maiti wa Kiislamu wa miaka mingi unasema: Wapotovu wenye kupotosha, umefikia hata kuainisha watu miongoni mwa wanazuoni wahakiki wakubwa...” Na Sheikh Msunni Hasan Shatiy ad-Damashqiy amesema: “Duru ya daawa ya kiwahabi ni juu ya kuwakufurisha Waislamu.”88 Ni kama hivi kila walio kinyume na Sheikh sawa wawe katika Ahlu Sunna, Ashairah au miongoni mwa waliotangulia zamani kama vile Shawkaniy, as-Swan’aniy na Uthman bin Mansur – lakini baadhi yao ni wana chuki naye – wanakiri kuwa Sheikh Muhammad na wafuasi wake wanafanya ufurutu ada katika kuwakufurisha Waislamu kati ya wanazuoni na watu wa kawaida, na hili ndilo tulilolikuta katika vitabu vyake. Na tunavikuta vikundi vingine vya wasio Ahlu Sunna kama Shia na Ibaadhi wanaafikiana na Ahlus Sunna kuwa Sheikh Muhammad na wafuasi wake wamefanya ufurutu ada katika kukufurisha. Huyu   Rejea iliyotangulia, uk. 165. Na Dkt. Abdullah bin Muhamad Abu Daahish katika kitabu chake ‘Athari ya Daawa ya Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahhabi Kusini mwa Rasi ya Arabu,’ Nayo ni insha yake ya udaktari wake katika chuo kikuu cha Imamu, ametaja visa vinavyotilia mkazo maneno ya Sayyid Alawi al-Haddad au kwa uchache kuwa walifanya hivi baadhi ya Mawahabi, kwa minajili hiyo, hii siyo (ubunifu wake kama alivyosema Dkt. Abdul-Azizi Abdul-Latif. 88   Rejea iliyotangulia. 87

185

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 185

1/20/2016 11:35:55 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

hapa Muhammad Jawadi Maghniyyah – na yeye ni Shia Imamiyya – anasema: “Hapana shaka kuwa wao wanaposema ‘mwanatauhidi’ wanawakusudia Mawahabi wao wenyewe, na wanaposema ‘mushrikina’ wanawakusudia Waislamu wote bila ya kumtoa yeyote.”89 Na hili wameliafiki mfano wa Shawkaniy, naye ni Msalafi anao utunzi kadhaa katika kuharamisha kujenga juu ya makaburi na kutoa wito wa Tawhidi iliyo safi na kukemea bidaa. Isipokuwa alikuwa hawakufurishi Waislamu wala halienezi tendo la baadhi kwa wote, wala hamkufurishi jahili wala mwenye kufanya taawili. Juu ya hili ndio msimamo wa kila mwanachuoni wa Kiislamu ila baadhi ya wafurutu ada wa Kihanbali na baadhi ya wafurutu ada wa Kishia na baadhi ya wafurutu ada wa Kikhawariji, kwa hakika wao wanawakufurisha wanaohitilafiana nao katika itikadi. Lakini inabidi nifanye angalizo kuhusu suala moja nalo ni: Ukufurishaji wa kiwahabi kuna wakati huwa dhaifu katika hali ya udhaifu, na kuna wakati huwa na nguvu wakati wa nguvu, ni katika mlango wa taqiya na siasa wala si katika mlango wa itikadi na insafu au hata kupingana, hali hii ndio inayonidhihirikia na Mwenyezi Mungu ndiye Mjuzi mno. Na wakati mwingine hukimbilia kuzuga na kuhadaa mfano wa usemi wa baadhi yao: “Sisi hatuwakufurishi Waislamu, hii ni tuhma batili, Mungu atulinde na kumkufurisha Mwislamu! Tuwakufurishao ni washirikina na wanaoitukana dini ya Rasuli.” Kauli hii ni ya mtu anayehadaa, kwa kuwa sehemu ya pili ya kauli hii atahadaika asiyewajua, na kauli hii inakusanya kati ya propaganda na kukufurisha. Hili hulijua mwenye kuzowea kusoma tunzi zao ili aelewe siri ya tofauti kati yao na Waislamu, na ili aainishe mahali mwa tofauti, na atakuta mahali pa tofauti ni kuwa Mwislamu miongoni mwa wapinzani wao kwao wao ni mshirikina! Kwa mujibu huo mmoja 89

Daawal-Munawiina, uk. 168. 186

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 186

1/20/2016 11:35:55 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

miongoni mwao anaweza kuapa yamini hamsini kuwa yeye hawakufurishi Waislamu! Naye huwa hakusudii ila Waislamu kulingana na ubainifu wao na utambulisho wao wenye makosa. Hii ikiwa tutaitoa miaka ya udhaifu na tofauti kati ya watawala wa Dola ya pili ya Suudia, au katika siku hizi ambazo wanakabiliwa na mbinyo kutoka serikalini wa kukosoa njia ya ukufurishaji, hapa jambo hili linaweza kuwa tofauti, kuongezea baadhi yao pia hawana maoni ya kukufurisha. Lakini maneno yetu ni kulingana na turathi ya mwanzo ya kiwahabi na matendo ya mwanzo. Maneno yetu ni kwa uenezi sio kwa kuengua kuhukumiwako na hali ya mbinyo au tofauti au siasa au hadaa. 2.

Kudai Unabii: Na tuhuma hii kwa ujumla wake ni kuwa yeye amedai unabii kwa lugha ya hali ilivyo na sio kwa tamko. Na hii ni tuhuma ya kidhalimu, lakini ni miongoni mwa insafu ikiwa tutasema: Wao hawakuiita hivyo moja kwa moja, wala hawakusudii kuwa yeye amedai unabii wazi bayana, lakini yeye kwa mtazamo wao, amejiweka yeye na wafuasi wake kwenye daraja ya Nabii 5 na Maswahaba zake. Na Waislamu wengine amewateremsha kwenye bonde la ukafiri. Lakini baadhi yao wameongeza juu ya hilo kuwa yeye alikuwa ana mazoea ya kusoma sera za walioritadi kama Musaylama na al-As’wadi na al-Ansiy, na hii ni tuhuma ya ziada kuwa anakusudia kujifanya nabii. Vyovyote iwavyo hii ni tuhuma batili ya kidhalimu japo iwe ya kiwango kidogo kuliko tuhuma ya Sheikh kuwatuhumu wao kwa ukafiri mkubwa na kuifanyia uadui dini ya Rasuli.

Na waliorudia rudia tuhuma ya kudai unabii kumhusu Sheikh Muhammad kwa ufafanuzi uliopita ni Muhammad bin Abdur Rahman bin Afaliq, Ahmad al-Qubaniy, Sayyid Alawi al-Haddad alHadhramiy, Sheikh Hasan Umar as-Shatiy ad-Damashqiy, Sheikh 187

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 187

1/20/2016 11:35:55 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Ahmad Zayni Dahlani, Jamil Zahawi, Abdul-Qadir al-Iskandraniy, Mukhtar Ahmad Basha al-Muayidu as-Samhudiy, Muhammad Tawfiiq na mshairi Abdur Rahman bin Umar al-Ahsaiy na Sheikh Yusuf an-Nabhaniy.... Na wamepaza sauti wanazuoni wa daawa katika kujibu madai hayo, na aliyekuwa mashuhuri mno katika wao ni ulimi wa daawa Sulayman bin Sahman na Fawzan na wengine. Na walirefusha katika kujibu lakini hawakujibu kiini cha hoja hii, nayo ndiyo walilolitaka baadhi yao waliposema “kwa lugha ya hali ilivyo�. Kwa kweli hao mahasimu wa Sheikh wanakusudia kwa ibara fupi ya kisasa kuwa Sheikh ameuhodhi Uislamu, na amewajaalia walio kinyume na yeye kuwa ni washirikina, na ameifanya dini yake kuwa ndiyo dini ya Rasuli na mwenye kuwa kinyume na yeye kuwa ameitukana dini ya Rasuli. Na mwenye kusema kuwa Mawahabi ni Makhawariji ameitukana dini ya Rasuli. Na tuhuma hii ni sahihi kwa kiwango cha mbali cha kusikitisha, lakini hamtuhumu Sheikh kuwa alifanya hilo makusudi. Mifano mingi imepita ikiwa katika ukali katika kujitakasa binafsi na madhehebu ambayo humo imechipuka fikra ya kumkufurisha mpinzani. Hili ndilo ambalo limeduwaza akili za wapinzani wake, sio wenye chuki miongoni mwao, na ndio iliyowasukuma kusema kuwa Sheikh amejiweka binafsi mahali pa Nabii 5 na kuwaweka wapinzani wake mahali pa makafiri wa Kikurayshi bali zaidi. Hili kwa mtazamo wao ni kudai unabii kwa ulimi wa hali ilivyo. Na huku bila shaka ni kuvuka kwao kiwango katika ibara, lakini hailazimu kukufurishwa. Kinyume na Mawahabi wanavyowakufurisha wao, hili liko wazi. Na sisi tunaepukana na dhulma ya wao kwa wao, na tunasema makundi mawili yote ni Waislamu, na kuwa katika wao kuna dhalimu na anayedhulumiwa, mshambuliaji na anayeshambuliwa. Na katika kila kikundi kuna haki na batili, na uadilifu 188

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 188

1/20/2016 11:35:55 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

na tuwachukulie Mawahabi kuwa wana kosa la ufurutu ada katika kukufurisha, na tuwachukulie wao kuwa wana kosa la ufurutu ada katika kutuhumu na kuhalalisha hali iliyopo na yaliyo kwa baadhi ya watu miongoni mwa bidaa na upotovu. 3.

Kumfanya Mungu kuwa ana mwili na anashabihiana na v­ iumbe:

Tuhuma za mahasimu wa Sheikh dhidi yake katika jambo hili si mahali pake, kwa kuwa hakuna katika maneno ya kiwahabi kitu hata kidogo cha kumuona Mungu kuwa ana mwili na anashabihiana na viumbe, mfano kama huu huenda ukawepo katika maneno ya Masalafi wengi, khususan wanaomfuata Ibn Taymiya na Ibn al-Qayyim, kwa kuwa maudhui ya sifa si miongoni mwa ayatiliayo umuhimu Sheikh wala uwahabi uliotangulia, bali hima yao ilielekea kwenye Tawhidi. Tuhuma hii ni kama jaribio la wanazuoni wa zama zake kumchafua mbele ya macho ya wanazuoni wa zama zao, na aghlabu ni wanatheolojia wa Ashairah, Matridiyah, Zaidiyah au Imamiyah. Na sifa kwa wanatheolojia ni maudhui yenye hisia kali sana, kwa ajili hiyo inakuwa kana kwamba lengo la tuhuma hizi ni kukithirisha tuhuma, bali Sheikh na wafuasi wake ni mahafifu katika kumshabihisha Mungu na viumbe endapo katika wao kutakuwa na itikadi hiyo, ukiwalinganisha na Ibn Taymiya na Mahanbali waliotangulia. Na Sheikh huenda alitaja kitu cha kifikihi au sifa au historia kwa kukalidi au alikitaja kwa kuonesha, au alifupisha kwa kuandika, hivyo hahesabiwi kuwa kafanya kosa kwa kunakili kosa alilokosea aliyemtangulia, khususan kwamba maudhui ya kumsawiri Mungu kuwa ni mwili japo ni maudhui ya hatari lakini hayarejeshi adha kwa walio kinyume naye. Bali waliotilia umuhimu maudhui ya sifa na kuangukia katika kumshabihisha Mungu na viumbe na kuhamasika nayo ni Mawahabi waliokuja nyuma, wakiwa wameathirika na vitabu vya Masalafi vilivyochapishwa, kama vile Daramiy, Abdullahi 189

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 189

1/20/2016 11:35:56 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

bin Ahmad na kitabu al-Ibanah cha Ibn Battah na Usulul-Iitiqadi cha al-Alkaiy, na as-Shariat cha al-Ajiriy na Sunnah cha al-Khilal na vilivyo mfano wake, kwani ndani ya vitabu hivi mna kumsawiri Mungu kuwa ni mwili na kumshabihisha na viumbe. 4.

Kukanusha karama za Mawalii: Sheikh hazikanushi, lakini anatofautiana na wanazuoni wa zama zake kwa kufuata kutofautiana kwa Ibn Taymiya na wanazuoni wa zama zake katika mlango huu. Na mimi hapa naelemea kwenye rai ya Sheikh na ya Ibn Taymiya na ya walio pamoja na wawili hao, hasa katika maudhui ya karama, kwa kuwa Masufi na wengine wamepitiliza kiasi sana humo. Na visa vingi katika mlango huu havina ithbati... na kujihadhari na upitilizaji kiasi ni bora kuliko kuangamia humo.

Kwa kweli wametuhumiwa wanazuoni wa kiwahabi tuhuma nyingi, lakini nyingi katika hizo sio sahihi au ni mahali panafaa kufikiriwa, isipokuwa katika mas’ala mbili, kukufurisha kisha kuua kulikojengeka juu ya msingi wa ukufurishaji. Tuhuma hizi mbili ni thabiti na zipo wazi, kwa mwenye kutaka insafu. Lakini hili halitufanyi tupuuze mema yao na mabadiliko ya baadhi yao, na kulazimika kwa kikundi cha tatu kukufurisha wakati walipopata nguvu na Mawahabi kuitawala Saudia, na hatimaye kuingia katika hali ya kulazimisha, kama tulivyoona katika ubainisho wa wanazuoni wa Makka na Madina. Wala halitufanyi tupuuze kusoma maendeleo ya kiwahabi na kujua kuathirika kwao na hali ya mambo, kuacha kwao au kulegeza kwao ukufurishaji katika miaka migumu. Ili kuyaelewa haya yote yahitaji wakati na juhudi nyingine.

190

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 190

1/20/2016 11:35:56 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

KIAMBATANISHO IBARA YA KWANZA: Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahabi, japokuwa maneno mengi yamesemwa kumhusu, wasifu na kutiwa dosari, ila tu ni wazi kuwa amejitahidi, na alikuwa mwenye ikhlasi katika daawa yake. Alikuwa mwenye azma kali, kwa hakika ameleta kheri nyingi lau madarasa yake ingejiepusha na kasoro za daawa yake na kupanua nafasi ya kuyapitia aliyoyazalisha. Sheikh Muhammad hakuwa mtaka mamlaka ya dola, lakini aliitumia mamlaka ya dola kuihudumia daawa, kiasi kwamba nimegundua kupitia usomaji wangu wa sera yake kwamba daawa yake na hamasa yake kubwa vilipatwa na majibu makali kwa sababu ya kuenea kwa baadhi ya bidaa na imani potovu katika zama zake. Na alizidisha ukali kutokana na yale aliyoyaona miongoni mwa ubaridi wa wanazuoni wa wakati wake katika kuzikemea bidaa na itikadi potovu. Na huenda alipata kuona au kusoma baadhi ya ujuzishaji wa hayo na taawili zinazoona itikadi potovu hizi na bidaa hizo kuwa ni matendo mema. Hii pia iliathiri sana utu wake thabiti, akawa hakubali kufanya insafu katika ufumbuzi, wala uombaji radhi usiomkinaisha. Hili likamsukuma kufanya pupa katika kuyaona matokeo ya haraka, hivyo basi alikurupuka kufanya daawa kwa hamasa na ujahili na kung’ang’ania, pamoja na uchache wa elimu na wingi wa uchamungu. Na vinapokutana hivyo viwili huwa vina athari kubwa katika matendo ya mtu, kwani huwa anazidisha ukali na ufurutu ada kwenye alitakalo khususan endapo mambo yatamuelekea. Na kwa kupitia usomaji vitabu vya Sheikh Muhammad nimegundua kuwa sio mwanazuoni yule mhakiki mdodosaji wa kina. Alikuwa na udhaifu ulio dhahiri katika Hadithi na historia, na ni kwa 191

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 191

1/20/2016 11:35:56 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

mawili hayo hupatikana uelewa wa mwanazuoni Mwislamu. Kwa minajili hiyo akawa anakusanya kila aina ya mkazo wa kuyatolea hukumu mambo kuwa ni shirki au ni bidaa, akiyatolea ushahidi kwa nususi sahihi zilizo katika sura ya jumla na nususi zilizo wazi katika udhaifu, na amekithirisha kujengea hoja hukumu za kukufurisha wazi wazi juu ya Hadithi dhaifu au athari iliyozushwa, au wakati mwingine anatumia ulinganisho, yaani kulinganisha hukumu isiyo na maandiko na hukumu iliyo na maandiko. Na wakati wa nia njema na ibada ya nguvu na himma jabali laweza kusukumwa. Na mara nyingi utamkuta anatia chumvi na kutojali katika kuzibebesha nususi za kisheheria yale yasiyobebwa na nususi hizo, miongoni mwa ukufurishaji au kumfanya mtu kuwa ni mtenda bidaa. Na yeye hukazia neno la shirki sana, na wala hachungi vithibitisho vya ukufurishaji. Kwa rai yake hutoa ushahidi kwa kauli zisizo za kawaida na natija zilizo ngumu na matamshi yamponyokayo yeye binafsi. Kisha anawakusanyia hayo watu wa kawaida, wafuasi au wanazuoni walio chini yake. Hivyo basi humfanya msomaji mwenye uelewa wa juujuu miongoni mwao; na hao ndio walio wengi miongoni mwa wafuasi wake, adhanie kuwa hii ni elimu kubwa na kuwa wanazuoni katika wakati wake wameufanyia khiyana uaminifu wao, wala hawakuwahadharisha kuwa mbali na shirki, na kuwa eti watu wameurudilia ujahilia wao wa mwanzo, na ni kuwa katika siku hizo hakuna tofauti kati ya wanaoswali, wanaofunga na wale wanaoabudu Laat na Uzza. Kwa minajili hiyo walikurupuka na kuwa pamoja na yeye bila kumgeukia mwingine, kwa kuwa yeye amewahadharisha wawe mbali na wanazuoni na watu wa kawaida bila tofauti. Hivyo akadhania kuwa wanazuoni ni kama wanazuoni wa wana wa Israeli, wamewafanya wanazuoni wao na marabi wao kuwa miungu. Hivyo mabedui walimfuata wakazitumia panga zao kumwaga damu wakiwa na tamaa, ndimi zao katika kukufurisha zikiwa na ki192

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 192

1/20/2016 11:35:56 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

tata! Hali ya mambo iliwasaidia na zama ziliwaelekea, kama vile kudhoofu kwa dola ya Uthmaniyyah na kufarakana kwa maamiri huko Najdi. Na kumdharau jirani mwenye nguvu, kwa vile waliwadhania kuwa ni mawingu ya kiangazi yatatoweka punde tu. na uasi wa mabedui ulikuwa umezingirwa, na katikati ya Najdi ni eneo kame, mpaka walipoweza kuiteka Najdi yote. Wakawafanya watu wawe kulingana na itikadi yao katika kila mji wanaoufuata wao. Kisha walijitawanya wakiiteka miji Mashariki na Magharibi, na ilikuwa yatazamiwa, baada ya mambo kutulia na uwepo wa kisiasa kujipanga, urejeleaji wa yaliyopita ufanyike na kuachana na ufurutu ada na kuunusuru msimamo wa wastani, kwani lengo limetimia na hoja imefika. Lakini la kushangaza ni kwamba ufurutu ada huu uliendelea, na ari ilihamia kwenye uenezaji wa fikra hii na kujizatiti kwenye handaki hilo, na kuendelea kulaumu ambayo yapo kinyume na yeye miongoni mwa usomaji na ijtihadi, bali umefanyika uungaji mkono wa kujifaharisha nayo na kuachana na nyingine. Na alifungua vituo Mashariki ya nchi na Magharibi yake, mrindimo ukawa kuwagawa Waislam; mshirikina na mwanatawhidi, mpaka mgawanyiko ulipoanza kati ya dola na daawa, pindi Mawahabi wa asili waliolewa uasi na ukufurishaji wa kiwahabi na kisalafi kuwa yale ambayo kwayo wanawakufurisha Waislamu miomgoni mwa mambo ya kina yapo pia kwa wengi miongoni mwao. Ndani ya dola ambayo wao wanaizingatia kuwa ni ya kisalafi, kwa hiyo waliikufurisha nayo. Inanidhihirikia kuwa dola ilikuwa inategemea nadharia nyingine ya Kisalafi, nayo ni “utii japo aupige mgongo wako na achukue mali yako.” Dola haikung’amua kuwa mambo ya kisalafi ni mengi, na mambo ya kiwahabi ni mengi. Na heri yote iko katika uadilifu na kuwa katika hali ya wastani, kwa hiyo usilihukumu kundi, kuwa ndiyo bora juu ya makundi na madhehebu zote. Ilikuwa yatazamiwa kwamba dola itazitambua madhehebu na 193

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 193

1/20/2016 11:35:56 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

makundi ya amani, na wasiridhishwe wachache kwa minajili ya kuwadhulumu walio wengi. Hivyo basi kuna Usalafi wa utii na Uwahabi wa uasi, na utii ni zaidi katika Usalafi, kama ambavyo uasi ni zaidi katika Uwahabi. Na wanakutana katika ukufurishaji na uwekaji mbali na kutowatambua wengine. Na kadiri siku zinavyokwenda, chini ya joho la Uwahabi wamejitokeza Ikhwanu, wafuasi wa Duweish,90 kisha chini ya joho la Usalafi wakajitokeza jamaa wa Juhayman.91 Kisha   Faysal bin Sultan bin Hamidiy Duweish, alizaliwa October 1882 na alifariki mwaka 1931. Yeye ni Sheikh wa kabila la Matwila na kiongozi wa kundi la Ikhwani na ni kiongozi wa mji wa Ar’twawiyyah. Alitawalia kiti cha usheikh katika zama za uhai wa mzazi wake Sultani bin Hamidiy Duweish, na akaishi katika mji wa Ar’twawiyyah mnamo mwaka 1915, na akashiriki katika vita vingi vya kuunda nchi ya Saudia, akiwa sambamba na Mfalme Abdul-Aziz na akafanikiwa kuweza kutawala baadhi ya maeneo ya nchi hiyo – Mhariri. 91   Juhayman bin Muhammad bin Seif ad-Dhani al-Hafi ar-Ruqiy al-Utaybiy, alizaliwa Septembar 16, mwaka 1936, sawa na Rajabu mosi mwaka 1355 A.H. Na alifariki Juni 9, mwaka 1980. Alifanya kazi katika Jeshi la Ulinzi la Saudia karibuni miaka kumi na nane. Alijifunza falsafa ya dini katika Chuo Kikuu cha Ummul-Qura huko Makka, na baadaye akahamia Chuo Kikuu cha Madina Tukufu. Na alipokuwa Madina ndipo alipokutana na Muhammad bin Abdullah al-Qahtwaniy, mmoja kati ya wanafunzi wa Sheikh AbdulAziz bin Baz. Na ifahamike kwamba mke wa Juhayman ni dada wa Muhammad alQahtwaniy, na kwa kukutana hawa wawili ndipo linapoanzia tukio mashuhuri la Muharramu mosi ya mwaka 1400 A.H. Baadhi ya Waislamu wanaamini kwamba kila baada ya miaka mia moja lazima atajitokeza atakayekuja kuirudisha dini katika hali yake halisi, na katika hilo wanategemea kauli inayonasibishwa na Mtume kuwa alisema: “Kila mwishoni mwa miaka mia moja Mwenyezi Mungu atamleta mtu atakayeurudishia umma wangu dini yao katika uhalisia wake.” Hii ni kama wanavyoamini Waislamu wengi kuja kwa Mahdi D ambaye kwa mujibu wa Mtukufu Mtume: “Jina lake ni sawa na jina la Mtume, naye ni kutoka katika kizazi cha Fatuma J, naye ndiye atakayeujaza ulimwengu uadilifu na wema baada ya kuwa umejaa dhulma na uharibifu.” Na kwamba kituo chake cha kwanza atakachoanzia jukumu lake na harakati yake ya kuweka mambo sawa itakuwa ni katika Msikiti Mtukufu wa Makka. Hivyo kutokana na mwafikiano huo wa nadharia hizo mbili, Juhayman alitumia fursa yake mwanzoni mwa karne mpya ya Hijiriya, yaani mwaka 1400 A.H. alipomshirikisha katika mpango wake huo shemeji yake aliyeitwa Muhammad bin Abdullah, wakaenda mpaka Msikiti Mtukufu wa Makka na kisha akamtangaza Muhammad bin Abdullah kuwa 90

194

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 194

1/20/2016 11:35:56 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

kutokana makundi hayo wakajitokeza wenye misimamo mikali na ukufurishaji waliopo sasa. Hivyo basi dola imedhihirikiwa kuwa mambo ni magumu na yenye kusongamana na si kama wanavyofafanua Mawahabi wa ufalme. Kwamba kheri yote iko katika Usalafi na Uwahabi, hivyo matumaini haya sasa yamedhihirika kuwa si sahihi, kwa sababu mwenye kuufanyia rejea ukufurishaji wa Masalafi na ukubwa wake na kutawanyika kwake na matawi yake atatambua kwa yakini kuwa pindi Msalafi ahitajiapo kukufurisha wakati wowote na mahali popote, hili kwake ni jepesi kuliko kutema mate yake au kumeza mate yake, na ni jambo lililo karibu mno kwake kuliko mshipa wake wa damu. Na hawa waliokufurishwa japokuwa wana makosa yao mabaya lakini ni wenye kufukuzwa na ukufurishwaji wa Waislamu ufanywao na Masalafi pamoja na uasi wa Mawahabi dhidi ya wandiye Mahdi anayengojewa aliyetabiriwa na Mtume 5. Tukio hili lilitokea alfajiri ya Muharam mosi mwaka 1400 A.H. sawa na Novembar 20, mwaka 1979. Juhayman na jamaa zake waliingia katika Msikiti Mtukufu wa Makka ili kuswali Swala ya Alfajiri huku wakiwa wamebeba jeneza kwa ajili ya kuswalia swala ya maiti baada ya Swala ya Alfajiri. Na baada tu ya kumalizika kwa Swala ya Alfajiri alisimama Juhayman na shemeji yake mbele ya hadhira iliyokuwemo msikitini na akawatangazia watu habari za Mahdi anayengojewa na jinsi atakavyowakimbia maadui wa Mwenyezi Mungu na kukimbilia katika Msikiti Mtukufu wa Makka. Kisha akamtambulisha shemeji yake Muhammad bin Abdullah al-Qahtwaniy kuwa ndio Mahdi anayengojewa atakayeirudisha dini katika hali yake halisi. Juhayman na jamaa zake walitoa kiapo cha utii kwa Mahdi wao Muhammad bin Abdullah al-Qahtwaniy, na wakawataka watu waliokuwemo msikitini wampe kiapo cha utii, wakafunga milango ya msikiti na hadhira iliyokuwemo humo ikajikuta imo kizuizini ndani ya msikiti. Baadhi ya mashuhuda wanasema walikuwa imara na waliojipanga kiasi kwamba waliweza kuwaangusha kutoka katika minara askari wa Serikali, na waliokuwa nje walishuhudia moshi wa majibizano ya risasi, na inasemekana watu walibakia ndani ya msikiti kwa muda wa siku tatu, na baada ya hapo ndipo Juhayman akawaachia baadhi yao hasa wale waliokuwa wameandamana na wanawake na watoto. Na inatajwa kwamba baadaye vikosi vya jeshi vilitumia maji na umeme katika kudhoofisha nguvu na mpango wa Juhayman na baada ya mapambano makali waliweza kufariki wengi kati ya wafuasi wa Juhayman ikiwa ni pamoja na Muhammad bin Abdullah al-Qahtwaniy (Mahdi wao) – Mhariri. 195

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 195

1/20/2016 11:35:56 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

shirikina na makafiri katika Rasi ya Uarabu. Lakini baadhi ya Mawahabi – iwe wanajua au hawajui – wameona kuwa maslahi yapo katika kuachana na mengi aliyoyakubali Sheikh Muhammad miongoni mwa ukufurishaji na uasi, hivyo wawe pamoja na kundi linalokubaliana na Mfalme kupitia nadharia hasi ya Kisalafi ambayo ilianza katika njia ya Ibn Umar ya kwamba “Sisi tuko pamoja na atakayeshinda.” Hivyo basi pande mbili zinagongana kwenye mlango wa dola, ile inayokubali na ile inayokufurisha. Hawa wataka kutoka bila ya kurudi na hawa wataka kuingia bila ya kutoka. Huyu ni Msalafi anayeufuata usalafi unaobomoa kwa kukufurisha na kuua. Na huyu ni Msalafi aliyeuchagua usalafi wa kutii kiupofu, na njia hizi zote mbili ziko kati ya kukufurisha na upingaji. Uzuri ulioje wa kujitegemea na kuwa huru, ukweli katika usemi, kuyanusuru maarifa na elimu, kuzihifadhi haki na kuzidai, kumheshimu mwanadamu na uzamaji mbizi kwa ajili ya maarifa, na kuingiliana na ulimwengu katika mambo ambayo yanaleta manufaa, na kuachana na usomaji wa juu juu wa dini hii adhimu. Lakini hapana, na hapana mara elfu, umwagaji damu, utumiaji nguvu, dhulma, na ufinyu wa upeo, kuzipoteza haki, ufurutu ada katika dini, khususan muasi hamiliki mradi adilifu wa kisiasa isipokuwa kumtesa mnyonge. Na mfano wa Taleban hauko mbali na sisi, lau si dola ya Saudia katika siku za Mfalme Abdul-Aziz, kujichukulia binafsi maendeleo mfano wa Taleban ungekuwa kwetu Saudia. Lakini aliyoyafanya Mfalme Abdul-Aziz yalikuwa hafifu mbele ya mapambano ya uchelewaji wa kijamii yaliyofanywa siku za Abdunasir, kisha mbele ya mzozo wa Sunni na Shia uliojitokeza zama za Khomein, na katika hali mbili hizo, inadhihiri kuwa dola ya Saudia iliona kuna la kufaidika la kuwa na Masalafi pinzani ndani ya nchi na Masalafi wakubalikao nje ya nchi. Hii ilikuwa sawa kisiasa kwa 196

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 196

1/20/2016 11:35:56 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

kiwango cha jiwe moja ndege wawili, na ni kosa la kisheria kwa kiwango cha mikakati. Na hii leo baada ya dola kufichukiwa na ambayo hayakuwa hapo kabla, inaomba maarifa yaenezwe kwanza, hivyo taarifa na maarifa ni lazima vyenyewe viwe ndiyo lengo, bila swali: Tutapata faida gani na haya maarifa au taarifa hizi? Maarifa hayafanyi hiyana, endapo yatakuhuzunisha saa moja yatakufurahisha dahari, nayo ni msingi wa ustawi na maendeleo, nayo ni dhamana ya mikakati ya utulivu, ustawi na kupiga hatua mbele. Kwa hiyo maarifa yana mamlaka juu ya akili, nyoyo na harakati za matendo. Na huu usalafi na uwahabi na umadhehebu ambao haumkubali mwingine asiye wa madhehebu hayo unatoa mchango wa kuyadhulumu maarifa na kuyapiga vita, na kuwanyima maarifa watu. Kwa minajili hiyo tunakuta yanayotokea katika mfumo wa elimu kwetu sana hububujikia kwenye kuwafanya watu wawe majahili, na hilo lasikitisha. Natija yake ya mwisho ni huu utumiaji nguvu wa kiupofu, na hii ni kawaida. Hivyo hatutumainii kutoka kwenye wimbi la ufurutu ada hali ya wao kuzitambua haki za wasio Waislamu ikiwa haki za Waislamu hawazitambui. Hatuwatumainii kumtendea uadilifu kafiri aliyesalimu amri ikiwa mfumo wa elimu kwa sura ya jumla na vyuo vikikuu na hotuba, mawaidha, tunzi, fatwa, vyote vyazunguka kuelezea wajibu wa kuvunja na kutoheshimu haki za Waislamu. Endapo huku kuwafanya watu majahili kutaendelea kuwa ndio mapatano, hatudhanii kuwa itatoweka kwa fatwa tuitoayo kati ya lundo la taka la karne na karne.

197

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 197

1/20/2016 11:35:56 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

IBARA YA PILI: ISTILAHI YA UWAHABI: Japokuwa neno Uwahabi sio wasifu wa dosari wala uzuri, sio dosari hata kama Uwahabi ukilitambua kuwa laashiria madhehebu, kwani madhehebu itegemeayo dalili zilizo sahihi jina jipya halitoidhuru wala watu kuipa jina hilo, na wala sio sharti madhehebu kuwa madhehebu iwe ilikuwa katika karne tatu za mwanzo, kama ambavyo harakati au madhehebu ambayo inajengea fikra zake na kazi zake juu ya dalili dhaifu; kuitwa majina mazuri hakutolinufaisha japo liwe katika karne ya mwanzo, linalozingatiwa ni usahihi wa elimu na usafi wa imani na wema wa matendo, hakuzingatiwi jina wala kutamani. Nastaajabishwa na wanaokariri miongoni mwa wanaofuata kuwa tamko Uwahabi walioliweka ni mahasimu, na wanazunguka katika jina ilihali jina ni kitu kipo nje ya mzozo wa jambo husika. Jambo la pili ni kwamba kwa hakika wanazuoni wa daawa walikuwa wanaruhusu kutumia jina Uwahabi na walikuwa wanalirudiarudia vitabuni mwao bila ya hofu ya kutuhumiwa kuwa ni madhehebu, bali wakati mwingine walitunga vitabu na insha za itikadi ya kiwahabi na daawa yao bila tatizo lolote. Na miongoni mwa wanazuoni wa daawa ambao walitumia istlahi ya Uwahabi ni Sulayman bin Sahman, na kabla yake ni Muhammad bin Abdul-Latif, utazipata habari hizi katika kitabu ad-Durarus-Saniyyah (8\433), na wengine mbali na wawili hao. Kadhalika wanaouhami uwahabi kama Sheikh Hamidu al-Faqiy na Muhammad Rashid Ridhwa na Abdullahi al-Qaswimiy, na Sulayman ad-Dakhili na Ahmad bin Hajar Abu Twamiy na Mas’udi an-Nadwiy na Ibrahim bin Abidi mwenye kitabu at-Tadhkirah, na wengineo. Wote walikuwa wanalitumia neno Uwahabi, pamoja na kuwa Sheikh Hamidi al-Faqiy Mungu 198

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 198

1/20/2016 11:35:56 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

amrehemu, alijaribu kutilia shaka nia ya kila aliyeitumia Istilahi hii na alipendekeza iitwe ad-Daawatul-Muhammadiyyah, kwa kuwa jina hilo linanasibishwa na Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahabi! Na wala si baba yake Abdul-Wahabi. Na walimfuata miongoni mwa waliokuja nyuma kama Sheikh Swalih al-Fawzani katika kumkanusha Abu Zahra na wengineo. Na ombi la al-Faqiy na al-Fawzani kututaka tuuite Uwahabi adDaawatul-Muhammadiyyah badala ya Uwahabi, kwa sababu Sheikh jina lake ni Muhammad, pendekezo hili la wawili hawa ni la pekee na la ajabu. Kwa sababu ndogo nayo ni kwamba madhehebu nyingi zilizo mashuhuri haziitwi kwa majina ya wenye madhehebu, bali huitwa kwa majina ya baba zao au babu za wenye madhehebu. Kwa mfano madhehebu ya Hanbali imenasibishwa na Hanbali na Hanbali huyu ni babu wa Ahmad bin Hanbali. Jina lake ni Ahmad bin Muhammad bin Hanbal, na Sheikh al-Fawzani au Sheikh al-Faqiy Mungu awarehemu na waliowafuata hawapingi Mahanbali kuitwa kwa jina hili, wala madhehebu ya Hanbali hawayaiti madhehebu ya Ahmad. Kadhalika madhehebu ya Shafi, imenasibishwa na Shafi, na huyu Shafi ni babu wa nne wa Imam Shafi kwani Imam Shafi jina lake ni Muhammad bin Idris bin Abbas bin Uthman bin Shafi. Basi ni kwa nini madhehebu ya Shafi hawayaiti kuwa ni madhehebu ya Muhammad! Kadhalika Hanafi. Madhehebu hiyo imenasibishwa na Abu Hanifa, na Hanafi sio jina la mwenye madhehebu, bali jina lake ni an-Nu’man bin Thabiti, na kadhalika Ashairah walionasibishwa na Abul Hasan al-Ash’ariy, kwani Ash’ariy ni babu wa zama za jahiliya wa hapo zamani wa kila mtu wa kabila la Ashairah, ambao miongoni mwao ni Abul Hasan, naye ni: Ash’ari bin Adad bin Zaidi bin Yashjub bin Arib bin Zaid bin Kahlan bin Sabaa. Huyu ni babu wa kabila ya Ashairah, ambaye kati yake na Abul Hasan al-Ash’ariy mwenye madhehebu kuna makumi ya mababa. Hivyo hivyo Ibaadhi 199

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 199

1/20/2016 11:35:56 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

ni nasaba ya Abdullah bin Ibadhi,...na ni kama hivyo, si rahisi kuikuta madhehebu inaitwa kwa jina la mwenye madhehebu ila kwa nadra kama vile madhehebu ya Maliki iliyonasibishwa na Maliki bin Anas, na madhehebu ya Zaidiyah ya Zaydu bin Ali, na madhehebu ya Ja’fariyah ya Ja’far as-Sadiq. Hivyo utumiaji wa jina Uwahabi juu ya madhehebu ya Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahabi haupo mbali na ukweli kuliko wafuasi wa Ahmad bin Muhammad bin Hanbali kuwaita Mahanbali. Kisha Sheikh Swalih al-Fawzani kwa mfano hutumia jina asSururiyyah kuwaita wafuasi wa Muhammad bin Surur bin Tayif Zaynul-Abidina. Kwa nini hawaiti Muhammadiyyah? Pia tunasikia kutoka kwa Masalafi wa leo wakivurumishiana majina kama vile Jamiyina, Mudikhiliyina, Baziyina, Albaniyina, na Qutubiyina na Banaiyina...mpaka mwisho.

IBARA YA TATU: WAFURUTU ADA KUMHUSU SHEIKH WAPO KINYUME NA ALIYOYAKATAZA: Na miongoni mwa dalili za hayo ni kwamba mengi kati ya yale aliyoyakataza Sheikh katika vitabu vyake, ikiwa ni pamoja na suala la ufurutu ada kuwahusu watu wema, ambalo ndilo mashuhuri kati ya hayo aliyoyakataza, leo hii linatendwa na wao wenyewe kwa kufurutu ada juu ya Sheikh mwenyewe. Kama ambavyo wao hawakufaidika na insha nyingi alizoziandika kukataza kufuata kibubusana kuipuuza haki, hivyo ushabiki wao kumhusu Sheikh umebaki mtupu bila ya kujiepusha na mengi miongoni mwa anayokataza. Na hebu tuchukue mfano wa hayo, nayo ni yale mas’ala ya kijahiliya ambayo Sheikh Muhammad ametaja kuwa Nabii 5 alikuja kuyaba200

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 200

1/20/2016 11:35:56 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

tilisha, na yalikuwa ndio sababu ya msingi ya makafiri wa Kikuraishi kutoikubali haki. Na mambo hayo hii leo tunayaona wazi kabisa kwa wafurutu ada miongoni mwa wafuasi wa Sheikh, na miongoni mwayo pamoja na kufupisha na kufanya muhtasari ni:1.

Usemi wa Sheikh kuwa: “Dini yao – anawakusudia watu wa zama za jahiliya - imejengeka juu ya kanuni ambazo iliyo kuu zaidi ni kukalidi (kufuata). Na huo ndio msingi mkuu wa makafiri wote, wa mwanzo wao na wa mwisho wao.

Nasema: Suala la kukalidi kibubusa liko dhahiri mno kwa wafurutu ada wetu kuliko tuwezavyo kulitolea mfano, khususan katika itikadi. Kwani wao wanaziweka kauli za wanazuoni katika itikadi kwenye nafasi ya maandiko ya kisheria kiukamilifu kama si zaidi. Yamtosha mmoja wao katika kuleta dalili aseme: Amesema Imamu Ahmad...au Amesema Sheikhul-Islamu Ibn Taymiya...au amesema Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahabi... anakuwa kana kwamba analeta dalili mkataa iliyothibiti ya kisheria! Na hii ni dosari kubwa mno sioni anayeitilia manani isipokuwa wanazuoni wachache mno wa hapo zamani na sasa sembuse wengine. Bali hata wanaowakemea wanaokalidi walikemealo kwao ni kukalidi katika fikihi na wanajiepusha kukemea kukalidi katika itikadi, na hilo la kukalidi katika itikadi ni umizo kubwa kwa umma kuliko kukalidi katika fikihi, kwa sababu wanafikihi wanakubali kuishi na wenzao, ama wanaokalidi katika itikadi wao huzirithi kauli za kumkufurisha asiye na rai kama hii au ana rai ile. Na wanamrithisha atakayekuwa baada yao. Na huenda Ibn Hazmi na al-Muqbiliy ni miongoni mwa wachache waliokemea suala la kukalidi katika itikadi, na al-Muqbiliy ni mwenye nguvu mno kati ya hao watu wawili katika upande huu na ni mtu wa wastani mno na mchache wa kuwa na maneno yanayopingana, na maarifa yake ya itikadi za madhehebu za Kiislamu ni ya kina kirefu mno. 201

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 201

1/20/2016 11:35:56 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

2.

Kauli ya Sheikh: “Na taratibu zao kubwa - anawakusudia watu wa zama za jaahiliya - ilikuwa ni kughururika na wingi! Na wanautolea dalili ili kuthibitisha usahihi wa kitu kuwa sahihi, na wanaleta dalili juu ya kuwa kitu batili kwa ugeni wake na uchache wa watu wake!”

Nasema: Na hili liko dhahiri kwa wengi miongoni mwa wafurutu ada wetu miongoni mwa wanaomkalidi Sheikh na miongoni mwa Masalafi pindi wanapokuwa na wingi na nguvu, na wanapotambua unyonge na uchache wanarudi chini! (furaha kwa wageni)! 3.

Na miongoni mwa aliyoyataja Sheikh ni: “Kuwafanya waliotangulia kuwa ni hoja mfano wa kauli yake Mtukufu akiielezea hoja ya Firaun: ‘Basi itakuwaje kuhusu watu wa karne zilizopita?’”

Nasema: Haya pia yapo katika wafurutu ada wetu pia, mfano wa kauli ya baadhi ya wafurutu ada wa kisalafi pindi unapowaongoza kwa kuwaonesha baadhi ya makosa yao husema: ‘Nani amekutangulia kwenye hili?’ ilihali hawaulizi nani aliyewatangulia katika makosa yao. Na miongoni mwayo ni vitu vingi tumevitaja katika baadhi ya tafiti na katika kitabu cha itikadi. 4.

Miongoni mwa aliyoyataja Sheikh ni: “Kuwafanya watu waliopewa kipaji cha nguvu ya ufahamu na matendo kuwa ndiyo dalili.”

Nasema: Kadhalika baadhi ya wanaomkalidi Ibn Taymiya huo ndio mwenendo wao, kwa mfano pindi wanaposema: ‘Wewe ni nani hata umkosoe! Yeye ni mwenye uwerevu, mantiki na falsafa,’ na kadhalika na kadhalika. Mpaka mwisho.

202

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 202

1/20/2016 11:35:56 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

5.

Na miongoni mwa hayo Sheikh amesema: “Kutoa dalili kuwa kitu fulani ni batili kwa kuwa hawajakifuata ila wanyonge!”

Nasema: Na hili linafanywa hii leo na baadhi ya wafurutu wanaomkalidi Sheikh, pindi wanaposema: ‘Hawawafuati hao isipokuwa wachache miongoni mwa wasio na uzito wala hawana shahada wala madaraka...’ Kadhalika unapowahadithia kuhusu mmoja wa wanazuoni au watafiti, watakuwahi: ‘Yeye hajulikani na yeyote wala wanawazuoni hawajamtaja kwa habari yeyote!’ 6.

Miongoni mwa aliyoyasema Sheikh ni: “Kufurutu ada kuwahusu wanazuoni na watu wema.”

Nasema: Hili mifano yake ni mingi, lau mtu mwenye insafu atasoma wanayoyaandika wafurutu ada kumhusu Imamu Ahmad, Ibn Taymiya, na Sheikh Muhammad, atafikiria kuwa wao wanawazungumzia viumbe wasio wa kawaida, si miongoni mwa Majini wala Watu wala Malaika. Huyu anajua uteremkaji wa jambo kati ya tabaka za mbingu na ardhi, na yule anamkaripia Munkar wa Nakir, na huyu anatoa habari ya ujio wa Tatar kabla hawajatoka maeneo yao. Kisha baada ya haya yote tunawakuta hao wafurutu ada ambao wanaikubali mizaha hii yote ni miongoni mwa watu wakali mno kukemea ufurutu ada na wafurutu ada. (Rejea tuliyoandika kuhusu ufurutu ada katika kitabu cha al-Aqaid. 7.

Miongoni mwa aliyoyataja Sheikh ni: “Mtu kufuata utashi wa nafsi yake, dhana, na kupuuza aliyowaletea Mwenyezi Mungu.”

Nasema: Haya ndiyo wafanyayo baadhi ya wafurutu ada wetu hii leo. Umleteapo dalili ya kisheria atakujibu kuwa Ibn Taymiya au Ibn al-Qayyim anaona hivi na hivi, na kuwa wanazuoni wanasema hivi na hivi. Laiti msemaji wa kauli hizi angekuwa katika watu wa 203

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 203

1/20/2016 11:35:56 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

kawaida suala lingekuwa jepesi lakini tunakuta usia wa wanazuoni wanaokalidi upo kati ya watafuta elimu wenye uwezo. Wao ndio wa kwanza wanaojua kuwa walio bora miongoni mwa wanazuoni wanamfuata aliye na uchache wa elimu na mwenye ushabiki mwingi, vinginevyo basi sisi tunatambua kuwa katika jopo la wanazuoni wakubwa kwa mfano, kuna wanazuoni wenye haki lakini hawana sauti na wao ni wenye kufuata, wenye kunyenyekea kwa wanazuoni wengine, hawana hadhi ya kuhakiki wala insafu. Na hapa elimu inakuwa imekamatwa pindi watu wanapowafanya majahili kuwa viongozi, hapo wanapotosha na wanapotea. 8.

Na miongoni mwa aliyoyataja Sheikh ni: “Udhuru wao wa kutofuata aliyowaletea Mwenyezi Mungu ni kutokuwa na elimu, ‘nyoyo zetu zimefunikwa.’”

Nasema: Na hili nimeliona kwa mmoja wao tulipoongea akasema: “Umetuzingatia sisi wapumbavu hatufahamu!” 9.

Na miongoni mwa aliyoyataja Sheikh: “Kunasibisha batili yao kwa Manabii.”

Nasema: Na hili lipo kwa wafurutu ada wa Kisalafii na Mawahabi, wananasibisha ukufurishaji kwa Mwenyezi Mungu na Mjumbe Wake. 10. Miongoni mwa aliyoyataja Sheikh ni: “Kupingana kwa maneno yao katika kuhusiana na nasaba yao, hivyo huwa wanadai wana nasaba na Nabii 5 na wanaacha wafuasi wake.” Nasema: Na hili pia lipo kwa baadhi ya wafurutu ada wetu pindi unapomwambia mmoja wao kuwa Nabii 5 amesema hivi, watatoa udhuru kuwa baadhi ya wanazuoni wamesema hivi, na kuwa wao wanafahamu zaidi Hadithi kuliko sisi! Hali ikiwa endapo 204

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 204

1/20/2016 11:35:56 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

maudhui ipo nzuri upande wao wanaiweka mbele kauli ya Maliki. “Kila mtu huchukuliwa kutokana na kauli yake na hurejeshwa kwa mwenye kaburi hili.” 11. Na miongoni mwa aliyoyataja Sheikh ni: “Kuwaharibia sifa baadhi ya watu wema kwa tendo la baadhi ya watu wenye nasaba nao.” Nasema: Na hili lipo kwa baadhi ya Wafurutu ada wetu, kama vile kebehi yao kwa Usufi kwa tendo la baadhi, na kebehi yao kwa Shia kwa tendo la baadhi, bali kabla ya hivyo kebehi yao kwa Imamu Ali au Ja’far as-Sadiq kwa tendo la baadhi ya Shia, kiasi kwamba mtu mmoja miongoni mwa Wafurutu ada wa Kisalafi hudhania kuwa eti Ali K alipigana kwa ajili ya madaraka sio kwa ajili ya dini. Na mwingine anathubutu kusema waziwazi kuwa Ja’fari as-Swadiq ni Masoni mwongo! – Tunajikinga kwa Mwenyezi Mungu na hayo –. Na sisi hapa hatumtakasi yeyote kuwa yuko mbali na makosa, si Abubakri wala si Ali wala Ja’far as-Sadiq wala Shafi, wote ni wanadamu wana makosa yao kama walivyo wengine, lakini haifai tuwatuhumu Ahlalbayt kuwa ni watendao batili na tuwaachie Shia kuwatetea! As-Sadiq kwa mfano, Mungu apishe mbali, kamwe hawezi kuwa Masoni au mwongo kama adhaniavyo Jabhani, la kushangaza kwa waadilifu wetu ni kunyamaza kwao kimya bila kuwapinga hao, ilihali hawajizuwii kumpinga amkosoaye Ibn Taymiya au Barbahariy au Sheikh Muhammad. Na huu ni mpingano wa misimamo na ni dalili ya kuathirika kwetu na radiamali au woga wetu wa kutuhumiwa na mwanadamu na kujiamini kwetu na tuhuma za Bwana wa wanadamu. 12. Miongoni mwa aliyoyasema Sheikh ni: “Yamewaghuri maisha ya dunia wamedhania kuwa miongoni mwa ayatoayo Mwenyezi Mungu ni dalili ya kuridhika Kwake.” 205

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 205

1/20/2016 11:35:56 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Nasema: Na hili pia lipo katika baadhi ya Wafurutu ada wetu pindi wanapotoa hoja dhidi ya aliye kinyume na wao kwa kauli yao: ‘Je huoni kuwa Mwenyezi Mungu ametuneemesha kwa mali na cheo.’ Lakini endapo watu wengine kinyume na wao wakipata daraja na mali wanasema: ‘Mungu amewapa hii dunia ili wapate hasara Siku ya Kiyama.’ Hili limeenea kwa wafurutu ada wote, na endapo watasibiwa na makuruhu husema: ‘Haya ni majaribu! kwani Mwenyezi Mungu anapoipenda kaumu ya watu huipa majaribu.’ Na endapo mahasimu wao watasibiwa na makuruhu watasema: ‘Hii ni adhabu ya Mwenyezi Mungu, na inayomngoja ni kubwa mno.’ Na hii yote ni katika kujiweka nafasi ya Mwenyezi Mungu, kwani hapana yeyote ajuae siri ya makuruhu hii au neema hii isipokuwa Yeye. La wajibu kwa Mwislamu endapo atapata heri au amepatwa hasimu wake, basi asikate shauri juu ya kitu chochote kuwa eti ni kwa ajili hii au ile, bali awe na matarajio kwa ajili yake na aogope kwa ajili ya nafsi yake, na hivyo hivyo atarajie kwa ajili ya Waislamu na aogope kwa ajili yao japo wawe miongoni mwa mahasimu wake wakali mno. 13. Na miongoni mwa aliyoyataja Sheikh ni: “Kuacha kuingia kwenye jambo la haki endapo wanyonge watakuwa wamelitangulia, kwa kibri na kujisikia.” Nasema: Hili mfano wake umetangulia. 14. Miongoni mwa aliyoyataja Sheikh ni: “Kutoa dalili ya kuwa haki ni batili kwa kuitangulia wanyonge kama vile hali ya washirikina waliosema: ‘Lau ingekuwa ni kheri basi wasingetutangulia.’” Nasema: Kimetangulia kitu miongoni mwa hiki. 15. Miongoni mwa aliyoyataja Shekh ni: “Wao hawazingatii chochote katika haki isipokuwa ile ambayo ipo na watu wao.” 206

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 206

1/20/2016 11:35:56 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Nasema: Hili katika wafurutu ada wetu ni miongoni mwa mambo yaliyo wazi mno. Uwaleteapo dalili watasema: ‘Haya hatujayasikia kwa masheikh zetu na wala hayapo katika vyanzo vyetu.’ Ilihali haki sio sharti yote iwe imetajwa na sisi. Na hapo zamani wafurutu ada walizipiga vita elimu zenye faida katika mlango huu, mfano elimu ya mantiki. 16. Miongoni wa aliyoyataja Sheikh ni: “Wao pamoja na hayo hawayafanyii kazi yasemwayo na watu wao.” Nasema: Na hili pia lipo kwa wafurutu ada wetu, wao hawajui kuwa Ibn Taymiya hawakufurishi Jahmiya wala Rafidha - yaani Shia! Na kuwa haifai mtu akate shauri kuwa kundi fulani ndilo litakalookoka na kundi fulani ni lenye kuangamia, kwa kuwa hivyo ni katika kujiweka nafasi ya Mwenyezi Mungu. Wala baadhi yao hawajui kuwa baadhi ya Mahanbali wa zamani walikuwa wanamkufurisha Abu Hanifa! Na kuwa Ahmad bin Hanbal alikuwa hakufurishi kwa kutabaruku na kaburi la Nabii (s) na mimbari yake. 17. Miomgoni mwa aliyoyataja Sheikh ni: “Kuikataa kwao haki ikiwa iko pamoja na ambaye hawampendi! Nasema: Na hili liko dhahiri kwa baadhi ya wafurutu ada wetu, utawakuta wanakupinga na haki yako ikiwa ataisema fulani, lakini wakijua kuwa fulani miongoni mwa wampendae ameisema kauli hii,mambo yatawawia mepesi, na watasema kuwa ni sawa na nyoyo zao zitatulia tuli. 18. Miongoni mwa aliyoyasema Sheikh ni: “Kukanusha kwao yale waliyokiri kuwa ni katika dini yao.” Nasema: Na huu ni kama ukanushaji wa baadhi ya wafurutu ada wetu kuwa ni katika dini yetu kuilamu dhulma na ujeuri na 207

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 207

1/20/2016 11:35:56 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

kwamba hapana hoja isipokuwa katika kauli ya Mwenyezi Mungu na Mjumbe Wake, na kuwa utaratibu wa kumthamini mpokezi katika Hadithi unaweka wazi kuwa katika vyanzo vyetu vya itikadi kuna Hadithi kadhaa zimewekwa na mfano wa hayo.... 19. Na miongoni mwa aliyoyataja Sheikh ni: “Kila dhehebu linajigamba kuwa ndilo lenye kufanikiwa, Mwenyezi Mungu akawakadhibisha kwa kauli yake: ‘Leteni uthibitisho wenu mkiwa mnasema kweli.’” Nasema: Na hii ni wazi katika ukataji shauri wa wafurutu ada wetu kuwa wao ndio wao tu waliofaulu na wengine miongoni mwa vikundi vya Kiislamu ambao hawawafuati wao kulingana na uoni wao ni wenye kuangamia na ni watu wa motoni! Lakini baadhi wanajirudi na kusema kuwa wengine miongoni mwa Waislamu wenye kuhiliki, kwa maoni yao, upo uwezekano wa wao kutoka motoni kwa njia ya uombezi, lakini yabakia kuwa tazamio hafifu. 20. Na miongoni mwa aliyoyataja Sheikh ni: “Kuabudu kwa kuharamisha halali.” Nasema: Halali nyingi zilioje ambazo wafurutu ada wa kiwahabi wanaziharamisha. Imetangulia kusemwa kuwa uharamishaji wao ulifikia kuharamisha hata kujielimisha, katika baadhi ya nyakati, na lau si serikali kuzilazimisha halali zilizo nyingi kwa nguvu, hangeweza yeyote kuwakinaisha japo angeleta dalili za kisheria zilizo wazi mno, kwa kuwa wao hawakinai ila na kile kilichosemwa na kikundi chao. 21. Miongoni mwa aliyoyataja Sheikh ni: “Ufanyaji ibada kwa kuwafanya wanazuoni na watawa au masufi kuwa miungu mbali na Mwenyezi Mungu.” 208

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 208

1/20/2016 11:35:56 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Nasema: Haya ni maneno ya Sheikh Muhammad. Alikuwa anajariibu kuwapinga awaonao kuwa wanakalidi, wanaipinga haki ambayo Sheikh ameileta kwa kuwataja wanazuoni wengine waliosema kinyume na yeye, Japokuwa ibara ya Sheikh ndani yake mna ukali, lakini je hamuoni kuwa hali ile ambayo Sheikh alikuwa anailalamikia imerejea, mara hii wao ndio wanaokalidi na wanakataa kufanya rejea. 22. Na miongoni mwa aliyoyataja Sheikh ni: “Kuipinga sheria ya Mwenyezi Mungu kwa makadara yake. Nasema: Hili lipo kwa wafurutu ada wetu. Wao husema: Mwenyezi Mungu amemuwezesha al-Hujaj kuwa mtawala juu ya watu wa Iraq, wala hawasemi Mwenyezi Mungu amemuwezesha Mmarekani kuwadhibiti Taliban. Hivyo wao hutolea hoja makadara ya Mwenyezi Mungu katika wanalolipenda miongoni mwa majanga ya wengine, na wanayakanusha makadara katika wanalolichukia miongoni mwa majanga yao. 23. Na miongoni mwa aliyoyataja Sheikh ni ushabiki wa kimadhehebu. Ushabiki ni ung’ang’anizi wa mtu itikadi yake au mawazo yake kwa dhana ya kuwa yenyewe peke yake ndio saihi. 24. Nasema: Katika hili mifano ipo wazi. 25. Na miongoni mwa aliyoyasema Sheikh ni: “Kuliondoa neno mahali pake.” Nasema: Haya ni miongoni mwa mambo yaliyo wazi mno kwa wafurutu ada wetu, kwani kuliondoa neno mahali pake siupati mfano wake katika kundi miongoni mwa vikundi au mpinzani isipokuwa baadhi ya wafurutu ada wa Kishia.

209

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 209

1/20/2016 11:35:56 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

26. Na miongoni mwa aliyoyataja Sheikh ni: “Kuwapandikizia wapinzani majina batili.” Nasema: Na hili pia kwa wafurutu ada wetu ni miongoni mwa mambo yaliyo wazi mno, kama vile kumuona kwao kila anayemhami Imamu Ali dhidi ya dhulma zao au kuulaumu uasi kuwa ni Shia na ni Rafidh, na kumuona kwao anayekanusha mwili na mfanano kwa Mwenyezi Mungu kuwa yeye ni Jahmia, na kumuona kwao aukosoaye utaratibu wa kiwahabi katika kukufurisha kuwa yeye ni Marjaiyya na ni mwanamakaburi. 27. Ni miongoni mwa aliyoyataja Sheikh ni: “Kuikadhibisha haki.” Nasema: Hili lipo wazi kwa wafurutu ada wetu kwa kukadhibisha kwao kila haki isemwayo na wapinzani wao na kutokuwa na dalili katika kukataa kwao. 28. Miongoni mwa aliyoyataja Sheikh ni: “Kumzulia Mwenyezi Mungu uwongo.” Nasema: Ni mfano wa kauli za baadhi ya wafurutu ada wetu wa zamani na wa hivi sasa, kuwa Mwenyezi Mungu amemsifu kila aliyemuona Nabii 5 na kwamba Mwenyezi Mungu amewaahidi wote pepo. Ilihali miongoni mwao kuna aliyeritadi, na mwingine ni mnafiki, na mwingine ni mwenye mwenendo mbaya. Na tumethibitisha kuwa kauli hii ni kauli ya kuelezea kumhusu Mwenyezi Mungu bila ya elimu na kuzifanyia taawili mbaya Aya tukufu ambazo hazikushuka ila kwa ajili ya kuuelezea ubora wa Muhajirina na Answari na walio katika hukumu yao. Kisha mwenye kutenda mema anaingia katika waliofuata kwa kutenda mema. Ili kuyapata haya kwa upana zaidi unaweza kurejea kitabu as-Suhbatu WasSwahabah.

210

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 210

1/20/2016 11:35:56 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

29. Na miongoni mwa aliyoyataja Sheikh ni: “Wao wakishindwa na hoja hukimbilia kuwalalamikia wafalme kama alivyosema: ‘Wamuacha Musa na kaumu yake wafanye ufisadi katika nchi. (Sura Aarafu:127)’” Nasema: Hili ni dhahiri sana kwa wafurutu ada wetu, kwani wao huomba msaada kwa dola pindi hoja yao inapokuwa dhaifu ili kuwakomesha mahasimu wao na kuwazuia kueneza itikadi yao na kuzuia vitabu vyao visiingie nchini, na kuwazuia kusafiri. Na huenda wakaomba kuwatokomeza kimwili baadhi ya wapinzani wao ili kuzuia ufisadi katika nchi! Na kukihami kizazi! 30. Na miongoni mwa aliyoyataja Sheikh ni: “Kuwavurumishia kwao watu wema masingizio ya kuwa wanaidogesha dini ya Mfalme.” Nasema: Ni kama kauli ya baadhi ya wafurutu ada wetu kuwa mwenye kwenda kinyume na itikadi ya kisalafi kwa hakika moyo wake umedhamiria kujitoa nje ya mamlaka ya mtawala! Na hili si lazima kwa kuwa kaumu fulani kati ya makundi yote ilishawahi kutoka wakiwemo Mahanbali hapo zamani, na sasa Mawahabi, kwa hiyo mas’ala hii sio jaizi kuizidisha. Na tulikwishasema maneno haya kabla ya matukio ya utumiaji nguvu na ukufurishaji wa hivi mwishoni katika dola ya kifalme (Saudia), na kwa kuainisha nilikuwa nimelitaja hili ndani ya kitabu al-Aqaidu katika faslu ya Mahanbali na Siasa. Na wakati huo dola ya kifalme (Saudia) ilikuwa ni miongoni mwa dola tulivu mno iliyo mbali mno na utumiaji mabavu, lakini mimi nilikuwa najua kuwa njia ya Masalafi Mahanbali na ya Mawahabi ni njia au utaratibu unaobeba ndani yake mfarakano, kwa kuwa unalingania kumchukia Mwislamu kwa tofauti ndogo mno basi itakuwaje kwa wanaloliona kuwa ni ukafiri wa mtawala na serikali? Mtu tuliyemuona akimkufurisha mtu mfano wa Imamu 211

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 211

1/20/2016 11:35:56 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Abu Hanifa na Allamah Ibn Fayruzi si ajabu kumuona akimkufurisha fulani na fulani. 31. Na miongoni mwa aliyoyataja Sheikh ni: “Kuwavurumishia kwao tuhuma ya kubadili dini.” Nasema: Na hili liko wazi katika majibu ya wafurutu ada wetu, kwani kila jibu lao kwa wapinzani wao miongoni mwa Waislamu huwavurumishia humo madai ya kubadili dini.” 32. Na miongoni mwa aliyoyataja Sheikh ni: “Kuacha kwao wajibu kwa woga.” Nasema: Kama uachaji wa baadhi ya wafurutu ada wetu kukiri kuwa Imamu Ali yuko sahihi, kwa woga tu! Na kuacha kwao kuwalaumu madhalimu kwa woga tu! Na kuacha kwao kuwahesabu Waislamu wasio wao kuwa ni wenye kufanikiwa, kwa woga tu. 33. Na miongoni mwa aliyoyataja Sheikh ni: “Ibada yao ya kuacha vya halali katika riziki.” Nasema: Hili limetangulia. 34. Na miongoni mwa aliyoyataja Sheikh ni: “Kuwaitia kwao watu kwenye upotovu bila ya elimu.” Nasema: Hili kwa wafurutu ada wetu liko dhahiri; kama vile wito wao wa kukufurisha na kubidaisha, yaani kuwaita watu kuwa ni wafanya bidaa bila ya elimu, wakiwa na hali ya kutojua kwao vidhibiti vya ukufurishaji, yaani bila kujua maeneo ambayo anaweza kusemwa mtu kuwa anafanya bidaa. Na hii leo wamefanya vyema Mawahabi wa jumba la kifalme katika kuchunga kwao maeneo ya kukufurisha na yanayozuia ukufurishaji, kwa sababu dola imewataka wafanye hivyo, na ni vizuri ilivyofanya - yaani dola - na walivyo212

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 212

1/20/2016 11:35:57 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

fanya, na ujira utakuwa kulingana na nia ilivyo, lakini ni juu ya dola ikamilishe kitu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, nacho ni iwaombe wanazuoni kuchunga vigezo vya kumfanya mtu mwana bidaa pia, kwa kuwa katika wanazuoni pia kuna wafurutu ada. Wao humbughudhi sana wamdhaniaye kuwa ni mfanya bidaa kuliko bughudha yao kwa Myahudi na Mkiristo. Na fatwa zao haziishii katika kulaumu na kumbughudhi atendaye bidaa. Na hao wanabidaa kulingana na mtazamo wao ni kila asiyekuwa wao, na hii leo kwa fatwa za wafurutu ada na mihadhara yao, mikutano yao na hotuba zao makafiri wamepata haki zao. Hilo ni jambo jema, lakini imebaki haki za Waislamu, hivyo basi ni wajibu juu ya dola iwaite wanazuoni na kuwaomba wachunge vidhibiti vya kumhesabu mtu kuwa ni mfanya bidaa. Kwa mfano kuna vizuizi kadhaa kama vile ujinga, na taawili katika mas’ala ya ukafiri, basi vizuizi hivyo hivyo inabidi vitumike katika mas’ala ya bidaa. Na mwanachuoni Albaniy anayo insha nzuri ya ulazimiano huu. Yajulikana kuwa hayupo Mwislamu aghlabu ila atakuwa na mchanganyiko wa bidaa na Sunna. Na hili ndilo alilokiri Ibn Taymiya mwenyewe. Na Mwenyezi Mungu ametukataza kujitakasa wenyewe binafsi, hivyo kujitakasa mtu mwenyewe ni haramu kisheria na ni wajibu kimadhehebu. Na sheria ndiyo yapaswa itangulizwe kabla ya madhehebu kwa nadharia ya ijmai, japo kuwe na tofauti katika utekelezaji wake. 35. Na miongoni mwa aliyoyasema Sheikh ni: “Madai yao kwamba wanampenda Mwenyezi Mungu ilihali wanaacha sheria Yake.” Nasema: Miongoni mwa sheria za Mwenyezi Mungu ni: Usimkufurishe Mwislamu, wala usimsengenye, wala usifanye kiburi, wala usiseme uwongo kwa watu, wala usihalalishe uvunjwaji wa heshima za Waislamu, wala usijifaharishe kwa nasaba au eneo, na yasikitisha haya kwamba yapo kwa wafurutu ada wetu. 213

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 213

1/20/2016 11:35:57 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

36. Miongoni mwa aliyoyataja Sheikh ni: “Vitimbi vikubwa.” Nasema: Hili wanalifanya sana wafurutu ada wetu, khususan mahali palipo mbali na uangalizi wa vyombo vya dola, khususan katika vyuo vikuu vya Kiislamu, vitimbi vyao ni vikubwa vikubwa! Wanawafanyia vitimbi baadhi ya wanafunzi walio na uelewa wa juu juu. 37. Na miongoni mwa aliyoyataja Sheikh ni: “Viongozi wao ima ni mwanazuoni muovu au ni mwanaibada asiye na elimu.” Nasema: Kauli ya Sheikh iliyotangulia ina ukali wa kutotenda haki, ukali nisiouridhia. Lakini nawaona wafurutu ada wetu wanakimbilia kwa baadhi ya Masheikh miongoni mwa wale wasiomuogopa Mwenyezi Mungu katika haki za wengine. Au miongoni mwa wasiofahamu maudhui ambayo ndio chanzo cha tofauti, wanatoa fatwa ili lije jibu la upotovu. Na mkweli Sheikh Abdullah bin Bijadi al-Utaybiy ana makala inayohusu stadi ya fatwa, natamani kama angeikamilisha na kuisambaza katika uchunguzi mwepesi. 38. Na miongoni mwa aliyoyataja Sheikh ni: “Kujipa matumaini ya uwongo.” Nasema: Kama wanavyojipa matumaini wao kuwa watakuwemo ndani ya pepo ya Firdausi, na wasiokuwa wao watakuwa ndani ya moto wa Jahannam. Hayo ni matamanio yao, si ruhusa kujiweka nafasi ya Mwenyezi Mungu. Na wakikataa tunawaambia: Leteni dalili yenu ikiwa mnasema kweli.” 39. Na miongoni mwa aliyoyataja Sheikh ni: “Madai yao kuwa wao ni Mawalii wa Mwenyezi Mungu na si watu wengine.” Nasema: Mwenye kudai kuwa yeye na kundi lake ndio waliookoka na wengineo wameangamia, bila shaka atakuwa ameafiki214

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 214

1/20/2016 11:35:57 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

ana na kauli ya Sheikh. Na wanaoongoza katika kauli hiyo ni wafuasi wake. 40. Na miongoni mwa aliyoyataja Sheikh ni: “Kujifaharisha kwa nasaba.” 41. Na miongoni mwa aliyoyataja Sheikh ni: “Kukebehi nasaba za wengine.” Nasema: Mifano ya nukta hizi mbili ipo wazi kwa wafurutu ada wetu, pamoja na kuwa ni kujifaharisha bila ya elimu. Na kujifaharisha kwa daraja na nasaba hutegemea lengo lake. Endapo lengo lake litakuwa ni kuhimiza mema basi ni jambo jema, na endapo itakuwa ni kujiongezea utukufu kuliko watu wengine, hii ni mbaya. Kumponda mtu kinasaba ni kitendo kiovu kwa hali yoyote, lakini mwenye kujinasibisha na wasio ahali wake, ni lazima kulibainisha hilo kwa wenye nasaba, kwa sababu ni haramu. Na kigezo cha ubora katika sheria ni takwa, na takwa imekuwa neno, na kwa Mwenyezi Mungu ni kipimo. 42. Na miongoni mwa aliyoyataja Sheikh ni: “Ambalo hawanabudi nalo wao ni mtu kulishabikia kundi lake na kumnusuru aliye humo dhalimu au mdhulumiwa.” 43. Na miongoni mwa aliyoyataja Sheikh ni: “Kumhukumu mtu kwa kosa la mwingine. 44. Na miongoni mwa aliyoyataja Sheikh ni: “Mtu kulitoa dosari alilonalo mtu mwingine.” 45. Na miongoni mwa aliyoyataja Sheikh ni: “Ni dunia kuwa tukufu ndani ya nyoyo zao.” 215

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 215

1/20/2016 11:35:57 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

46. Na miongoni mwa aliyoyataja Sheikh ni: “Kuwazulia kwao wafuasi wa Mitume kuwa hawana ikhlasi na ni wenye kuitaka dunia.” Nasema: Na nukta hizi zipo kwa baadhi ya wafurutu ada wetu kwa kumhukumu kwao mtu kwa kosa la mtu mwingine, na ushabiki kwa ajili ya kundi au kabila au eneo na kuwashambulia kwao waumini kuwa ni wapenda dunia na wao ni wenye pupa mno na dunia. 47. Na miongoni mwa aliyoyataja Sheikh ni: “Haki kuivisha batili.” Nasema: Hili ni miongoni mwa mambo yaliyo wazi mno kwa wafurutu ada wetu. Endapo mmoja wetu atasema kauli wataivisha vazi lisilo lake, watamtanguliza ili baadhi ya watu wamtolee fatwa. Na mas’ala hii ni miongoni mwa alama za wazi mno katika wafurutu ada wetu, nayo ni alama ya jumla kwa wafurutu ada wa makundi ya Kiislamu. 48. Na miongoni mwa aliyoyataja Sheikh ni: “Kuificha haki japokuwa inajulikana.” Nasema: Na hili lipo kwa baadhi ya wafurutu ada wetu na walio na msimamo wa wastani. Na katika hilo wanarudia rudia kauli ambayo ni sahihi lakini haipo mahala pake, kwa mfano: “Sio kila lijulikanalo husemwa!” Na: “Wahadithie watu wanayoyajua!” Na “Kwenda kwa daraja katika daawa!” Na yasiyo hayo miongoni mwa nyudhuru ambazo kwazo wanasitisha kutekeleza wajibu wa kukanusha yaliyo ndani ya vitabu miongoni mwa ukufurishaji, kudharau haki za Mwislamu, kama ambavyo unatimia ufichaji wa elimu iliyo sahihi, na kujipendekeza na kitu batili kwa kuzitumia kauli kama hizi ambazo wanaziteremsha mahali pasipokuwa pake, na ikiwa 216

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 216

1/20/2016 11:35:57 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

wamekwisha ziteremsha Aya tukufu mahali zisipoteremshiwa vitu vingine ni zaidi. 49. Na miongoni mwa aliyoyasema Sheikh ni: “Kuzungumzia juu ya Mwenyezi Mungu (s.a) bila ya elimu.� Nasema: Hili liko kwao kwa wingi mno, kwani wao huwa wanarudiarudia kuwa Mungu ametaka kadha na amefanya kadha kwa ajili ya kadha... na ameharamisha kadha na ameruhusu kadha..mpaka mwisho.

IBARA YA TANO: ZAYDIYYAH: Kwa kuzingatia juhudi yangu nyenyekevu katika kufichua dhulma ya wafurutu ada dhidi ya Ahlulbayt, Masalafi wamekithirisha kuninasibisha na Zaydiyyah! Lau hii ingekuwa haki ningetangaza, kwani Zaydiyyah ni bora mara nyingi kuliko ufurutu ada wa Kisalafi upande wa kielimu, uchamungu, kihistoria, na nasaba. Kwa hali yeyote iwayo Zaydiyyah ni madhehebu kama zilivyo madhehebu nyingine, waweza kuchukua kutoka kwao na kuacha. Na wao ni miongoni mwa vikundi vilivyodhulumiwa na wafurutu ada wa Kisalafi. Na katika Zaydiyyah wapo wanazuoni na watu bora na wajinyimao matukufu ya dunia hii kwa ajili ya Akhera, na wana ubora mkubwa katika historia ya Uislamu kifikra na kisiasa. Pindi ninapoutambua Uislamu wao na ubora wao au Uislamu na ubora wa Ushafi, Uhanafii, Umaliki na Udhahiria haimaanishi kuwa tunanasibika na mmoja wapo miongoni mwa madhehebu hizi. Yajulikana kuwa kunasibika na mojawapo miongoni mwa madhehebu nne au na ya Zaydiyyah au na Dhahiriyyah au 217

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 217

1/20/2016 11:35:57 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Ja’fariyyah au Ibaadhi sio haramu kisheria wala sio aibu kikabila kiasi kwamba hao wafurutu ada walaumu, bali lau suala lingekuwa kama walifanyiavyo taswira hao jamaa ingekuwa kujinasibisha na madhehebu ya mtu miongoni mwa watoto wa Mtume wa Mungu 5 ambao wao ni wabora miongoni mwa wabora, na ambao tunawaswalia katika kila tashahudi, ingekuwa ni bora kuliko kujinasibisha na madhehebu ya mtu kutoka ukoo wa Bakri Wail au Bani Tamimu au al-Aswabihu. Halafu ni kwamba Mazaidiyyah khususan waliotangulia miongoni mwao, walikuwa maimamu wa Ahlus Sunna. Hivyo Imamu Zaydi bin Ali Mungu amrehemu, na kadhalika An-Nafsuz-Zakiyyah wengi kati ya watetezi wao walikuwa ni watu wa Hadithi na fikihi katika zama zao, bali watatu miongoni mwa maimamu wanne: ‘Abu Hanifa na Maliki na Shafi’ walikuwa miongoni mwa wafuasi wa maimamu wa Zaydiyyah katika zama zao, kwani Abu Hanifa alikuwa miongoni mwa wafuasi na wanafunzi wa Zaydi bin Ali. Kisha hao watatu ni miongoni mwa wafuasi wa Nafsuz-Zakiya baada yake ambaye Mansur alimtilia sumu kwa sababu ya hili. Na kadhalika Imamu Maliki alikuwa anatoa fatwa ya kutoka pamoja na NafsuzZakiyyah kwenda kwenye mapigano, na kwa ajili hiyo alifungwa jela kwa sababu ya fatwa yake isemayo: “Mwenye kulazimishwa hana kiapo cha utii.” Na Shafi alikuwa pamoja na mmoja wa maimamu wa Zaydiyyah huko Yemen; na ilikaribia Rashidi amuue kwa ­kustukiza. Na pamoja nao pia walikuwa wanazuoni wakubwa miongoni mwa Ahlus Sunna, wana Hadithi na wanafikihi wakubwa kama vile ­Mansur bin al-Muutamar na Salman bin Kuhayl na Sufiani Thawriy. Na huyu baada ya kuuliwa Ibrahim bin Abdullahi Zaydiy alikuwa akisema: “Sidhani kama swala itakubaliwa ila kuiswali ni bora kuliko kuiacha.” Na hii yajulisha kuathirika kwake na kujilaumu kwake. 218

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 218

1/20/2016 11:35:57 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Na miongoni mwa watetezi wao ni Aamashu, Ubaadu bin Awwamu, Yazidi bin Harun, na Hasim bin Bashir, huyu ni Sheikh wa mwanzo wa Imamu Ahmad. Na Awwamu bin Haushab, Mus’ir bin Kuddam, Shuubatu bin Hujaj Amirul-Muuminina katika Hadithi, huyu alikuwa anasema kupigana vita na Mazaydiyyah ni Badru ndogo. Na Hasan bin Sa’adu al-Faqiihu, Yazid bin Abiy Ziyad, Muhammad Ibn Abi Layla, Qaysu bin Rabii, Abu Amru bin Alaau, mtaalamu wa Lugha na msomaji mashuhuri, Salaam al-Hadhai, Abu Daudi al-Dhwahiry, Fitru bin Khalifa, Isa bin Abi Is’haqa al-Sabi’i, na ndugu yake Yunusu, na Abu Khalidi al-Ahmar, Abdullah bin Ja’far baba wa Ali bin al-Madiniy, na Usaama bin Zaydi, huyu ni yule msimuliaji wa hadithi na si yule swahaba. Na Mualim bin Saidi, Khalifatu bin Hasan, Is’haqa bin Yusufu al-Azraqu, Asbaghu bin Zayd, Hishamu bin Hassan, Swalihu alMuruziy, Hajaju bin Bashir, Abul-Awwamu al-Qatan, Abdu Rabbih bin Zayd, Abdul-Hamidi bin al-Muhbaqu, al-Hakamu bin Musa, Imran bin Shabibi, Ubadu bin Mansur, Khalidu bin Abdullahi al-Wasitiy, huyu si yule al-Qasriy ambaye ni mashuhuri kwa dhulma. Na Yunusu bin Arqam, al-Mufadhalu al-Dhwabiy, Umar bin Awni, Muammal bin Ismail, Hasan bin Swalihu bin Hay na ndugu yake Ali bin Swalihu, bali hawa wawili walikuwa Mazaydiyyah. Na wengine wengi miongoni mwa wanataaluma na ubora, na fikihi. Kwa anayetaka anaweza kurejea kitabu Taarikhu at-Tabary, faslu inayozungumzia mwaka 122 na mwaka 145 A.H. Au arejee kitabu Maqtalu Twalibiina cha Asfahaniy, na vitabu vingine, ndani yake kuna riwaya zinazotaja Ijmai ya wanahadithi na wanafikihi zinazoonesha jinsi walivyokuwa wakiwatetea Mazaydiyyah katika zama zile na wala hawamuengui yeyote isipokuwa mmoja mmoja (kulingana na tabia zake binafasi). 219

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 219

1/20/2016 11:35:57 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Hivyo basi kujiunga na madhhebu ya Zaydiy laiti ningependa kujiunga nayo ningefanya hivyo. Hakuna linalonizuia ila ni kuwa mimi siijui madhehebu hii kwa ufafanuzi, na njia yake katika kuidondosha Hadithi na kuiona kuwa inafaa na kuzikubali riwaya. Na hata nikijiunga nayo basi wamekwishajiunga nayo au kuinusuru watu waliyo bora na wenye elimu zaidi kuliko mimi, bali aliye na elimu zaidi na mbora kuliko Ahmad bin Hanbali na Ibn Taymiya na Muhammad bin Abdul-Wahabi, sembuse al-Barbahariy na Ibn Battat na Abi Ya’ali na walio mfano wao. Nimekanusha kujiunga na madhehebu ya Zaydiyyah kwa sababu zile zilizopita, na kwa kuwa mimi najitambua binafsi kuwa mimi kiukweli ni Sunni wa kuzaliwa na wa vyanzo na utendaji wa ibada. Hivyo basi Swala zangu na funga zangu, Hija na kuacha kwangu kujiingiza katika undani wa itikadi, yote haya ni kulingana na utaratibu wa kisunni, hii ni kutokana na utafiti wa dalili. Hii haimaanishi kuwa mimi nikiigundua haki ipo kwa Zaydiyyah au ipo kwa wengine niikanushe kwa kutaka utakaso kutoka kwa wafurutu ada! Na laiti kupitia elimu ningekusudia kupata utakaso wa watu na kupata utukufu nisingekuwa katika uhasama huu zaidi ya miaka kumi na tano, na ningejua kwa urahisi jinsi ya kujipendekeza kwa wafurutu ada na niwakufurishe Waislamu na nijinyanyue juu ya waja wa Mwenyezi Mungu ili niufikie utukufu na mali na cheo kama wafanyavyo baadhi yao kwa urahisi pia! Ni sahihi kuwa baadhi ya Mazaydiyyah wana ufurutu ada na kumhesabu mtu kuwa ni mfanyabidaa na kujinyanyua juu ya watu kama ilivyo hali hiyo katika baadhi ya watu wa madhehebu nyingine, lakini sijui ni kwa kitu gani wafurutu ada wa Kisalafi wanajifakharisha mbele ya Mazaydiyyah ilihali hawana nasaba ya kisharifu kama walivyo wenzao, wala hawana kiwango makini cha uchamungu, wala hawana akili ya wazi, wala hawana uchaji wa kujinyima 220

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 220

1/20/2016 11:35:57 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

matukufu ya dunia, wala hawana mapambano kama yao kwa ajili ya uhuru na uadilifu wala historia kama yao ya kishujaa?! Sioni sababau ya kebehi hii ya Masalafi dhidi ya Mazaydiyyah isipokuwa ni kutojielewa kabla ya kutomwelewa mwingine. Na kwa kawaida watu huwa ni maadui wa wasilolijua, kiasi kwamba hata wafurutu ada wa Kisalafii wanalihesabu neno Zaydiyyyah kuwa ni aibu na tusi?! Kwa kweli suala ni la kustaajabisha! Kana kwamba wanaojifaharisha miongoni mwa wafurutu ada wa Kisalafi wanalingana na Mazaydiyyah kielimu, utambulisho, akili, ubora, historia na nasaba!

IBARA YA SITA: Mambo mengi ambayo kwayo Sheikh na wafuasi wake huwakufurisha Waislamu si yenye kukufurisha, bali wengi wa wanazuoni wa Kiislamu wanaona kuwa ni jaizi, bali Mahanbali wao wenyewe pamoja na mkazo wao katika mambo wanaona hili ni jaizi, kama Imamu Ahmad bin Hanbali, na Ibrahimu al-Harbiy ambaye ni Mhanbali na Abdullahi bin Ahmad bin Hanbali...na wanazuoni waonao kuwa hili ni jaizi kwa wengine ni bora. Itakuwa vyema kama nitathibitisha baadhi ya yaliyopita:

KWA MFANO: 1.

Kutabaruku na makaburi na kuyagusa Sheikh anajaalia kuwa ni shirki kubwa. Lakini kwa mtazamo wa Imamu Ahmad bin Hanbali imamu wa madhehebu si vibaya. Katika kitabu: alIlalu Wamaarifatur-Rijali (2/492) cha Abdullahi bin Hanbal amesema: “Nilimuuliza - anakusudia baba yake - kuhusu mtu anayegusa mimbari ya Nabii 5 na anatabaruku kwa kuigusa na 221

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 221

1/20/2016 11:35:57 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

anaibusu na pia analifanyia hivyo kaburi au mfano wa hivi, kwa kufanya hivyo anataka kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu? Akasema (Ahmad bin Hanbali): Si vibaya kufanya hivyo!”

KWA HIYO SHEIKH NA WAFUASI WAKE HAPA, WANA CHAGUZI NYINGI:

Imma waseme: Kuwa hili si sahihi kwa Ahmad, kwa hiyo itawalazimu kumkadhibisha Abdullah bin Ahmad, na kuvitupilia mbali vitabu vya Ahmad bin Hanbali ambavyo Abdullah amekuwa wa pekee kuelezea riwaya zake kama Musnadu na Fadhail, na al-Ilalu. Na hili hawaliwezi. Imma waseme kuwa Ahmad bin Hanbali Mungu amrehemu, kwa kauli hii yeye ni mshirikina kwa shirki kubwa inayomtoa mtu kwenye Uislamu! Na hili hawatolisema wala hawana haki wala hawawezi.

Imma waseme: Kuwa hii si shirki, na kwamba mwenye kufanya hivyo hakufurishwi, na hapa inawalazimu wawahesabu aliowakufurisha Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahabi na wafuasi wake kuwa ni Waislamu, kwa kuwa upeo wa tunalojua kutoka kwao ni kuwa wao wanaona inafaa kutabaruku na kugusa makaburi ya watu wema na mawalii, na yasiyo hayo ni madai ya mahasimu wao Mawahabi. Kwa hiyo ikiwa tofauti ni kubwa kati ya Imamu Ahmad na Sheikh Muhammad, mmoja wao anasema: “Si vibaya”, na mwingine anasema: “Ni shirki kubwa”, hii ni tofauti kubwa mno, ambayo baada yake haitokuwa sahihi Sheikh Muhammad na wanaomkalidi waseme kuwa wao wapo kwenye njia ya Ahmad bin Hanbali katika itikadi. 222

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 222

1/20/2016 11:35:57 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Kisha wanazuoni waliokuwa katika zama za Sheikh huenda wakaona kutabaruku na makaburi ya watu wema kwa uoni huu, wala hawaoni hii kuwa ni ibada ya kumwabudu asiyekuwa Mungu wala sio shirki, bali huenda wakawa na rai ya Ahmad bin Hanbali kuwa hii sio haramu wala makuruhu aslan. Na hoja ya Ahmad bin Hanbali na wengine miongoni mwa wanazuoni ambao Mawahabi wamekuwa kinyume nao, ambao ni jamhuri ya wanazuoni wa Kiislam, wapo katika kauli hii kuwa: “Si vibaya au ni ruhusa au ni yenye kuagizwa,� kwa kuwa baadhi ya Maswahaba kama vile Abu Ayyubu al-Answari na Ibn Umar walikuwa wanafanya mfano wa haya kwenye mimbari au kaburi wakiwa katikati ya Maswahaba wala yeyote hakuwahi kuwakanusha, na hii ni miongoni mwa yanayojulisha kuwa hii ni Ijmai ya kunyamazia. Endapo msemaji atasena: Kuna tofauti kati ya kaburi la Nabii 5 kwa kuwa katika udongo wake mna baraka, amma asiyekuwa yeye hapana...! Tunasema: Sheikh hili analijaalia kuwa ni ibada, na sio jaizi kuwaabudia Manabii, na yeye anarudiarudia kuwa mwenye kumwabudu Nabii au walii huyo ni mshirikina. Na yeye katika kauli hii ni mkweli, lakini si mkweli kuwa atakayetabaruku na Nabii atakuwa amefanya shirki. Kuna tofauti kubwa sana kati ya kauli ya Sheikh ya jumla ambayo kila Mwislamu anaafikiana naye, lakini yeye ni mwenye makosa katika kuingiza sura nyingi na kuzitumia pamoja na shirki, nazo zikiwa si shirki aslan, sio kubwa wala si ndogo. Hahalalishi kuabudiwa Manabii, na wote wanaafikiana na yeye katika utangulizi huu, kwani hili halina mjadala. Mjadala na ukanushaji upo tu katika kuijaalia tabaruku na tawasuli kuwa ni shirki kubwa, ilihali Maswahaba miongoni mwa watu wa Badri na walioridhiwa wamefanya hivyo, wala yeyote miongoni mwa Maswahaba hakukemea wala Tabiina. 223

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 223

1/20/2016 11:35:57 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Kwa mujibu huo mnalazimika kumkufurisha Abu Ayyubu alAnswariy, Ibn Umar, na Ahmad bin Hanbali, bali na kuwakufurisha Maswahaba ambao hawakuwakemea kwa hili, pamoja na kuthibitisha kuwa katika zama za Maswahaba mwanatauhidi alikuwa ni Marwan bin al-Hakam tu! Ni yeye pekee ndiye aliyemkemea Abu Ayyubu kuweka shavu lake juu ya kaburi tukufu. Na hapa kuna nukta: Nayo ni kuwa mimi nakuta mambo yetu yote mmiminiko wake ni kwa Bani Umayya! Hata katika mfano wa mikazo ya kiitikadi ambayo tunakutana nayo, ni kutoka kwa alWazau bin al-Wazau Marwan bin al-Hakam. Na mkazo wa kifikihi katika kuunganisha nywele za wanawake na rakaa mbili baada ya al-Asri na kuswali Swala kamili katika Hija, tunavikuta kwa Muawiya ambaye ni kichwa cha pote la kidhalimu katika zama za ukhalifa ongofu, na wawili hawa ni miongoni mwa waja wa Mwenyezi Mungu watelekezaji mno wa uadilifu, hisani na haki, na ni miongoni mwa wakiukaji mno wa aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu miongoni mwa umwagaji damu, kulaani, kupora mali mpaka mwisho. Na Wafurutu ada wa Kisalafi na wa Kiwahabi wanakwenda na sera yao kiatu kwa kiatu, hawana umuhimu na uadilifu wala haki ya mwanadamu wala kuondoa dhulma wala kupunguza athari isipokuwa iliyokuja ghafla, au kwa nadra, au kujilinganisha na wengine. Wao Bani Umayyah ndio chaguo lao la kwanza katika mambo haya ambayo kwayo wamewaparaganya waja wa Mwenyezi Mungu kati ya mshirikina na mwanatawhiidi, mwongofu na mpotovu. 2.

Ibrahim al-Harbiy Mhanbali, naye ni miongoni mwa wanafunzi wakubwa wa Ahmad bin Hanbali, amesema: “Kaburi la Maarufu al-Karakhiy ni kimbilio mujarabu.� Angalia Siyaru Aalamun-Nubalau cha ad-Dhahabi (9/343). 224

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 224

1/20/2016 11:35:57 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Na ad-Dhahabi amekiri hilo bali Dhahabi amezidisha akifafanua hili kwa kauli yake: “Anakusudia kujibiwa dua ya mwenye dharura kwenye hilo kaburi, kwa sababu ni maeneo yaliyobarikiwa, na dua hujibiwa kwenye maeneo hayo, kama ambavyo dua wakati wa usiku wa manane huwa na matumaini ya kujibiwa, na mwishoni mwa Swala za wajibu, na katika misikiti.” Nasema: Kwa muktadha huu lau Ahmad bin Hanbali, Ibrahimu al-Harbiy, na Dhahbi wangekuwepo zama za Sheikh Muhammad, kwa kauli zao za mwanzo wangekuwa makafiri, ukafiri mkubwa umtoao mtu kwewnye Uislamu. Lau ningeorodhesha majina ya wanazuoni wanaoona muono uliopita na mfano wake miongoni mwa ambayo Uwahabi unayafanya kuwa ni shirki kubwa, nafasi ingekuwa ndefu na yangekuwa marefu. Na ukweli wa tofauti ni kwamba Sheikh hakuainisha maana ya kisheria ya istilahi nyingi ambazo anazitumia mfano wa Shirki, Ibada, Kuomba msaada, Dua, Tawhidi, na Imani, bali na hata Uislamu. Kwa hiyo utamkuta anajinusuru kwa kiarifisho kigumu cha istilahi hii au ile kisha anawasukuma watu kwa bakora yake ili awafanye walengwa katika ubainisho huu na kumkufurisha anayekweda kinyume naye. Na huenda akalingana na aliyetangulia kama Ibn Taymiya na Ibn al-Qayyim au baadhi ya wanalugha katika kutoa ubainisho mgumu na maana ya jambo husika, lakini hampati atakayeafikiana naye katika kuuteremsha ubainisho huu mgumu kwenye ukweli wa Waislamu, kwa kuwa kwanza ubainisho huo ni wa dhana, pili kwa kuwa kuna vizuizi..... na kwa kuwa ..... na kwa kuwa.... mpaka mwisho. Kwa mfano neno Ibada, ikiwa ubainisho wake tutarejea kwa Sheikh bali na kwa wanazuoni wa lugha tutaukuta unazunguka kwenye maana moja, nayo ni: “Kunyenyekea na kujidhalilisha.” Lakini 225

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 225

1/20/2016 11:35:57 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

je tunaitekeleza moja kwa moja maana hii kwa mwenye kumnyenyekea Sultani dhalimu, au akajidhalilisha kwa wazazi wake wawili au kwa mpenzi wake. Je tunaweza kusema hawa wanamwabudu asiyekuwa Mungu?! Hapana, kwani Mungu ameamuru kunyenyekea na kujidhalilisha kwa wazazi wawili, “Wateremshie bawa la unyenyekevu kutaka huruma.” Je unyenyekeaji huu na kujidhalilisha huku ni ibada ya kuwaabudu wao? Na Mwenyezi Mungu ameeleza kuwahusu waumini akiwasifu kwa kauli yake: “Wanakuwa dhalili kwa Waumini wenzao.....”Je hivi waumini wanawaabudu waumini? Na amesema kuwahusu wazazi wa Yusufu na ndugu zake: “Waliporomoka kwa ajili yake kusujudu.” Je kwa hili walimwabudu? Je Mungu hakumtuma kila Nabii – kama Sheikh Muhammad asemavyo – kwenda kueneza tawhidi ya Uungu? Vipi sasa Nabii Yakubu mzazi wa Yusufu ambaye naye ni Nabii asujudu?! Je kwa sijda hii alikuwa mshirkina? Hivi tutasema kuwa Mungu anawalaumu Manabii kwa kukosea kuhukumu kati ya watu wa kondoo jike wala hawalaumu kwa shirki kubwa? Tunajilinda kwa Mwenyezi Mungu ili tuwe mbali na kauli hii. Hivyo basi kuna tofauti kubwa kati ya anayelinyenyekea sanamu au mtu akiwa ana itikadi ya uungu kwa mtu au sanamu hilo, na anayenyenyekea kwa kumheshimu au kumpenda au hofu au kwa tamaa akiwa na itikadi kumhusu mtu huyo kuwa ni mtu tu na uungu ni wa Mungu peke Yake. Makafiri wa Kikuraishi walikuwa wanadhania kuwa masanamu ni miungu, na kuwa yanadhuru na kunufaisha na yanaruzuku na kuombea, sawa Mungu ameidhinisha au hakuidhinisha. Na kwamba yenyewe yanastahiki ibada, na kwamba haifanywi ila kwa ajili yao, kwa hiyo ibada zao zote, dua zao, matarajio yao, chinja zao na nadhiri zao vilikuwa kwa ajili yao...wala Mungu hapati chochote katika matarajio yao, hofu zao na ibada zao. Mungu kwao anakuwa ni jina 226

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 226

1/20/2016 11:35:57 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

tu, chake ni kuumba tu. Na hili halikuwa kwa Waislamu waliouawa na Mawahabi hali wao wakiwa wanaswali Ijumaa ndani ya msikiti wa Uyaina kwa mujibu wa Mawahabi wenyewe. Je hawa walikuwa wanatekeleza swala ya Hubal, Laatu na Manatu?!. Kwa hiyo Waislamu wao wanatambua kuwa Mwenyezi Mungu peke Yake ndiye ambaye mkononi Mwake mna kila kitu, lakini wao pindi wanapomnyenyekea binadamu au kumuomba kwao uombezi wake hawasemi hivyo wakiwa wanaitakidi katika hao uungu. Na hii ni tofauti kubwa kati ya ibada ya kishirikina ambayo inajaalia anayeombwa ni Mwenyezi Mungu, na miongoni mwa matendo mengine sawa yawe yanayoruhusiwa au yanayokatazwa, ambayo yanajaalia anayeombwa kuwa ni mtu ambaye Mwenyezi Mungu amemtunukia uombezi au baraka, vinginevyo hamiliki kitu chochote mwenyewe binafsi isipokwa kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu na rehema Zake na uungaji wake mkono na idhini Yake na kuwa maombi yote ni ya Mwenyezi Mungu. Ni kama hivyo katika Aya nyingi ambazo kwazo Sheikh hutolea dalili, huwa hazitaji Aya nyingine ambazo zinazuia ufahamu wake mkali wa Aya hizi au zile.

IBARA YA SABA: Hadithi zinazoitia dosari Najdi, kati ya Iraki na Najdi: Tulikwishasema kuwa ni rahisi mno mahasimu wa Mawahabi kuthibitisha kuwa wao Mawahabi ni Makhawariji kuliko Mawahabi kuthibitisha kuwa makafiri wa Kikuraishi ni bora kuliko Waislamu wa zama zao, na miongoni mwa Hadithi ambazo wamezitolea dalili mahasimu wa Mawahabi katika kuwatia dosari Mawahabi ni Hadithi: “Kutakuwepo na matetemeko na fitina, na huko kutajitokeza 227

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 227

1/20/2016 11:35:57 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

pembe la Shetani.� Hadithi ambayo Mawahabi wameitolea tafsiri kuwa makusudio yake ni Najdi ya Iraki. Na wa mwanzo kuitolea tafsiri hiyo ni Masalafii waliotangulia ili kuwabughudhi Shia, watu wa rai, na Muutazila. Zifuatazo ni dalili zenye kuthibitisha kuwa Najdi iliyokusudiwa katika Hadithi ni Najdi ya hivi sasa, na hii haimaanishi ubaya wa kila mtu wa Najdi na wala wa kila zama za Najdi, bali hii haimaanishi kuwa ni mkataa wa kusihi Hadithi japokuwa ipo katika Sahih mbili Bukhari na Muslim, kwa kuwa ni Hadithi ya wapokezi wachache (Aahad). Miongoni mwa hoja za aonaye Najdi ya Hadithi ni hii Najdi maarufu leo hii ni: 1. Itajwapo Najdi kwa sura ya jumla haitokuwa na maana ila ni Najdi iliyo maarufu katikati ya Rasi ya Uarabu, mfano tuitajapo Hijazi kwa sura ya jumla huwa ni Hijazi maarufu iliyopo pwani ya Bahari Nyekundu ambayo inachukua sehemu yote ya Bahari Nyekundu, na inajumuisha eneo linaloiingiza Makka na Madina na Jiddah..., na wala sio kila ambacho kipo kati ya bahari na jabali kinakuwa ni Hijazi kwa upande wa uwelewa wa kijamii, japokuwa hili ni jaizi upande wa kilugha. Kwa minajili hiyo itajwapo Najdi kwa sura ya jumla itaelekea kwenye maana iliyo maarufu kijamii kama ambavyo tusemapo Hijazi kwa sura ya jumla huelekea kwenye maana iliyo maarufu kijamii, na maana maarufu kijamii hutangulizwa kuliko weko la kilugha kwa mujibu wa ijmai. Ama Najdi kulingana na weko la kilugha ni sahihi huingiza kila ardhi iliyoinuka, kadhalika Hijazi kilugha huingiza kila kilichozuiliwa kati ya bahari na jabali. 2.

Na miongoni mwa linalojulisha kuwa sio Iraki bali ni Najdi hii iliyo maarufu hii leo ni kuwa kuna vituo (Miqat) viwili vya kuhirimia miongoni mwa vituo vya Hija, kituo cha watu wa 228

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 228

1/20/2016 11:35:57 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Najdi na kituo cha watu wa Iraki. Lau ingekuwa Najdi na Iraki ni kitu kimoja ingesemwa kituo cha Najdi ya mwanzo na Najdi ya pili, kama isemwavyo katika mipaka ya Kiislamu kutoka Arminia ya kwanza na ya pili, na ya tatu na ya nne. 3.

Na miongoni mwa dalili za udhaifu wa tafsiri hii ni kuwa Mashariki ya Madina ndio Najdi ya hivi sasa, na katika Hadithi imekuja kuwa Nabii 5 aliashiria kwa mkono wake upande wa Mashariki, na ilikuwa siku aliyoashiria anahutubia msikiti wa Nabii. Hivyo Mashariki ya Madina ndio Najdi maarufu, na wala sio Iraki. Na atakaye kuhakiki na aikunjue ramani ya Arasi ya Uarabu na ajisaidie kwa msaada wa ukanda ambao hawakuuweka Mawahabi wala wapinzani wao, kwa kuwa unapita Kusini mwa Madina na Kusini mwa Riyadh, lau utachukua msitari ulionyooka kwenye ile ramani na kwayo ukaelekea kutoka Mashariki ya Madina haitokosa Dariya au al-Bat’hau au iliyo kati ya hizo mbili!

Ikithibiti kuwa Nabii aliashiria kwa mkono wake upande wa Mashariki na Hadithi imo katika Sahihi mbili, na akasema kule kutatokea mtetemeko na fitina, kutachomoza pembe la Shetani. Na Mashariki ya Madina ndiyo katikati ya Najdi ambayo ni maarufu, basi hiyo ndiyo iliyokusudiwa wala sio katikati ya Iraki, na hii haimaanishi dosari kwa Najdi yote, na wala sio kuilaumu Najdi ya zama zote, kama ambavyo kuisifu Madina hakumaanishi kumsifu kila mtu wa Madina, bali zingatio ni aghlabia au kwa muda fulani mbali na mwingine. Au ni kuwa lawama ni kwa ajili ya kuuacha Uislamu. Kwa hiyo toleo hili ni bora kuliko ile tafsiri ya kujikusuru tunayoitoa dhidi ya Muutazila na Ashairah pindi tunapoona wao wanazungumzia sifa, na hii ni dalili ya kuichukia kwao Hadithi na dalili ya kuipiga vita kwao Sunna. 229

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 229

1/20/2016 11:35:57 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

4.

Kudhihiri elimu huko Iraki na si Najdi, kwani wengi miongoni mwa wanahadithi na maimamu wa fikihi na lugha ni Wairaki. Na hili linatilia mkazo kuwa Iraki kuna kheri na elimu na maendeleo ya Kiislamu kwa alama zake mbalimbali ambazo hazipo Najdi, wala nchi za Kiislamu zilizobaki, kwani maimamu wa Waislamu katika Hadithi, fikihi, tafsiri, lugha, na mantiki ni Wairaki. Endapo tutaiona ni sahihi Hadithi iliyomo katika Sahih mbili katika kuilaumu Najdi, basi ni bora lawama hiyo kuinasibisha na Najdi hii iliyo mashuhuri kuliko kuigandisha lawama hii kwenye Najdi ya lugha.92

Kwa mujibu huu ni kwamba pembe la Shetani limetokeza huko Najdi, huenda makusudio yake ni Musaylama al-Kadhabu, akafuatiwa na Makhawariji, nao wakafuatiwa na Qaramitwa. Basi ni kwa nini kuwepo na hamasa hizi zote katika kuipinga dalili ya Hadithi. Je hawahofii hawa watafanya taawili kwamba kung’ang’ania huku katika kuipinga Hadithi kusije kuwa miongoni mwa tetemeko na fitna na miongoni mwa upambaji wa Shetan?! Kisha imetangulia tumesema kuwa kulilaumu eneo na kulisifu lingine huwa kwa sababu mahsusi au kulingana na aghlabia au   Sisi kundi la Masalafi tumerithi kuilaumu Iraki kutoka kwa mahasimu wao ambao ni Manawasibu wa Sham ( Syria). Mengi yaliyoje tumeyarithi kutoka kwao, kwani hotuba za Hujaj na Ziyad zingali zinarudia rudia masikioni, kwa kuwa baadhi ya wapokezi wa Hadithi wamepotosha baadhi ya matamshi ya Hadithi na kubadilisha neno ‘upande wa Mashariki’ ambalo lipo katika Sahih mbili kwa neno ‘upande wa Iraki’ ili kukazania katika kuilaumu Irak na uadui wao. Dola ya Bani Umayya ilikuwa na athari yake kubwa katika kuilaumu Iraki kiasi kwamba wameathirika na hayo baaadhi ya mafakihi na watu walio bora, kiasi kwamba hata Imamu Maliki anazo Hadith kwazo anajaalia Hadithi za watu wa Iraki ni kama Hadithi za Ahlulkitabu: “Msiwasadiki wala msiwakadhibishe.” Huyu ni Maliki akiwa katika nafasi yake, basi itakuwaje kwa watu wenguine... Lakushangaza ni baadhi ya Mahanbali kama Ibn Taymiya, naye ni mtu wa Sham anakwenda mbali mno katika kuilaumu Iraki akiikariri kauli ya Imamu Maliki aliyetangulia bila ya kuangalia usahihi wake ni wa umbali gani. Na lau mtu angemwambia Ibn Taymiya: “Vyema, basi Imamu Ahmad bin Hanbali ni Mwiraki, kwa muktadha huu msimsadiki wala msimkadhibishe.” Wangeshikwa na butwaa...!

92

230

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 230

1/20/2016 11:35:57 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

mfano wa hayo. Hata tukikubali kuwa Najdi ilaumiwayo ni Iraki je, Iraki hakuna watu walio bora na wema wa wakati uliopita na hivi sasa? Je Maswahaba wengi na Tabiina, mafakihi na wanahadithi hawakuwepo Iraki? Miongoni mwa Maswahaba walioishi huko Iraki ni Ali bin Abu Talib, Hudhayfa bin al-Yammani, Ammar bin Yasir, Amran bin Haswin, Saad bin Abi Waqas na walio mfano wao, bali waliingia Kufa pamoja na Ali bin Abu Talibi miongoni mwa Maanswar mia nane. Kisha baada ya tabaka hili lilifuatia tabaka la wanazuoni wakubwa wa Taabiina, kama vile Uwaysu al-Qarniy ambaye ni Tabiina bora, Alqamatu bin Qays, Ubaidatu as-Salmaniy, na Abu Abdur Rahman as-Salmiy, na Abdur Rahman bin Abi Layla, na Shariihu bin al-Harith Kadhi wa umma, na Rabiu bin Hathiim na Suwaydu bin Ghaflat, na al-Harithu al-Aawam na Abu Wailu, Wazaru bin Habiish, na al-Aswadu bin Yazid, na Saadu bin Jubair. Kisha Ibrahimu Nakh’iy na walio katika tabaka lake kama Shaabi na Salim bin Abi Ja’ad, al-Hakam bin Utaybah, Salmatu bin Kuhayl, Hammad bin Abi Sulaymam Imamu wa Watu wa rai, Abu Is’haqa Sabi’iy. Kisha Abu Hanifa na tabaka lake kama vile Aamashu na Ibanu bin Taghlabu na Aaswimu bin Abi Najudi msomaji mashuhuri wa Qur’ani, na Mansur bin al-Muutamar na Mus’ar bin Kudam, na Hasan bin Swalihu bin Hay, na Sufian Thauriy, na Imamu Zufar, na Kadhi Abu Yusufu, na Muhamad bin Hasan Shaybaniy. Kisha Wakiiu na tabaka lake kama vile Abu Muawiya Dharir na Ibn Fudhailu na Hafsa bin Ghiyath na Abu Bakr bin Iyashu, na Abu Naimu al-Fadhlu bin Dikiyn, na Ubaydullahi bin Musa al-Abisiy Sheikh wa Bukhariy na tabaka lake. Kisha sehemu kubwa ya Watu wa Hadithi ni kutoka Kufa achilia mbali sehemu nyingine za Iraki kama vile Basra na Baghdadi na Wasitu na Ahwazi na Mousel... . Na Iraki kuna wasiokuwa watu wa Kufa kama vile al-Hasan al-Baswriy na Ibn Siyrin, Qutadah, Ahmad bin Hanbal, al-Khatibu 231

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 231

1/20/2016 11:35:57 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

al-Baghdadiy, Ibn al-Jawziy na walio mfano wao. Na miongoni mwa wanalugha ni Sibawayhi na Abu Amru bin al-Alai, al-Akhfashu. Na miongoni mwa washairi: al-Mutanabiy na al-Bahtariy na Abi Tamaam...mpaka mwisho. Ilihali Maswahaba na Tabiina hawajakanyaga katikati ya Najdi isipokuwa waliokwenda kupigana na walioasi kwa kuwaengua wachache kama vile Thamamatu bin Athali, na wala hawakujitokeza huko wenye elimu walio mashuhuri isipokuwa Yahya bin Abi Kathiir Taiy miongoni mwa masheikh wa Muamar na tabaka lake, naye pamoja na hayo hasikiki isipokuwa kwa watu mahsusi, halafu muda mkubwa wa ujahili uliendelea, na huenda hali zake nzuri ni katika vipindi vile vilivyokuwa kabla ya Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahabi. Katika muda huo kulikuwa na idadi kubwa ya Makadhi na wanazuoni. Pamoja na hayo Mawahabi walizilaumu vibaya sana zama zile na waliwakufurisha watu wa kawaida kama walivyowalaumu watu mahsusi. Na waliwajaalia kuwa ukafiri wao ni mbaya zaidi kuliko ukafiri wa makafiri wa Kikuraishi. Ikiwa hii ndiyo hali yake nayo ikiwa katika hali zake nzuri mno basi yenyewe ina nafasi bora ya kunasibishwa na Hadithi hiyo kuliko Iraki ambayo humo wametoka nusu ya wanazuoni wa Umma. Na mwenye shaka na afanye upembuzi wa idadi ya Wairaki miongoni mwa wanachuoni, awaweke kwenye sahani moja ya mizani na awalinganishe na umma miongoni mwa Wahijazi, Washam, Wamisri, Wamorocco, Wahispania, Wayemeni, Waajemi kutoka Khurasani, Nisaburi, Isfahani, Kazwini, Sajistani, Bukhari na Samarqandi, na Wanazuoni wa kutoka Jaylani, Daylama na Muruzi. Kisha arudie kuisoma Hadithi na angalie je ni bora kuinasibisha Hadithi ya Najdi na Iraq au na Najdi hii iliyo mashuhuri leo ya Saudia? Na mimi nina utafiti haujakamilika wenye anuani ‘Uungwana wa Wairaki,’ humo nimeorodhesha fadhila za nchi hii tukufu na alama 232

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 232

1/20/2016 11:35:57 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

zake na athari zake kuhusu maendeleo ya Kiislamu ambao unaponya moyo wa kila mwenye insafu.., wala hailaumu Iraki na watu wake isipokuwa asiyeijua Iraki na hajijui yeye mwenyewe.

HITIMISHO Nafupisha kama ifuatavyo: 1.

Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahabi Mungu amrehemu ni Sheikh mwanafiqihi, ni Sheikh wa Kihanbali, tunamtukuza na tunamheshimu na tunathamini bidii yake ya kutaka uwepo wa Tawhidi halisi, na tunashukuru juhudi yake ambayo matunda yake ni kuunganisha umoja wa nchi hii kubwa, na tunamshukuru kwa daawa ya kuichuja tawhidi ili kuinasua itokane na yale yaliyochanganywa kwa watu wengi wa kawaida. Na hii haimaanishi kuwa Sheikh alipatia katika mas’ala ya ukufurishaji.

2.

Sheikh Muhammad pamoja na makosa yake katika ukufurishaji, lakini yuko mbali na tuhuma nyingi zilizoelekezwa kwake, kama madai ya unabii au kumpunguzia hadhi Nabii 5, au kuwa yeye anajitakia ukubwa binafsi. Na ni kwamba yeye kwa jumla amepatia ukiondoa ufurutu ada wake katika ukufurishaji na yaliyoambatana nayo miongoni mwa kuhalalisha damu zilizohifadhika.

3.

Ukufurishaji ndio njia ya Sheikh iliyotanda na ya msingi kwa Sheikh Muhammad, na huhitilafiana na njia hii katika baadhi ya fatwa chache kwa ajili ya hali ya kisiasa au ni kurudi nyuma au yaweza ikawa ni ibara ya jumla iliyobeba ukufurishaji na uzubaishaji wa kujiepusha na ukufurishaji. 233

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 233

1/20/2016 11:35:57 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

4.

Ukufurishaji katika njia ya Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahabi Mungu amrehemu uko thabiti katika tunzi zake na risala zake, na katika wanayonukuu wapinzani wake, na wanahistoria kwenye ngazi hiyo.

5.

Uwahabi rasmi wa leo haupo katika njia ya Sheikh katika kukufurisha, na wamebakia katika njia yake jamaa wa kileo wakufurishao, na baadhi ya Masalafi wa Saudia ambao wako nje ya utawala.

6.

Miongoni mwa vitu ambavyo utaratibu wa Sheikh Muhammad unavijaalia kuwa ni shirki kubwa ni vile ambayo vinaruhusiwa kwa mtazamo wa wengi miongoni mwa maimamu wa kihanbali kama Ahmad bin Hanbali na Ibrahimu bin al-Harbiy na wengine wasiokuwa hao wawili.

7.

Kujiepusha kuwakufurisha Waislamu na kulikosoa hilo ni wajibu iwe wazi safi bila kuomba kwa yeyote, kwa sababu ya ile athari mbaya iliyomo kwa mtu mmoja mmoja na kwa jamii.

8.

Nausia kufungua nafasi ya kuidurusu fikra ya kiwahabi kwa kuwa ni zao la mtu mwanadamu ambalo hukabiliwa na makosa na usahihi kama mazao mengine ya kimadhehebu na ya kifikra, na utimie utoaji wa nafasi kwa vitabu vyenye mwelekeo wa kuifanyia rejea fikra ya Sheikh, kufuata muongozo wa vitabu ambavyo vinahoji vikundi na madhehebu nyingine, na kufuata vitabu ambavyo vinafanya ufurutu ada kwa ajili ya Sheikh.

9.

Pamoja na haya yote ni wajibu nyoyo ziungane hata baada ya kuwepo ukosoaji na ghadhabu ya kielimu, kwani kuhitilafiana rai haifai kuharibu msingi wa udugu wa Kiislamu.

234

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 234

1/20/2016 11:35:57 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

10. Wananchi wote wa nchi hii haifai awasemee ila yule anayewawakilisha, na wala halitowawakilisha kundi wala madhehebu, kutokana na ukweli wa kuwepo aina nyingi na kuhitilafiana kwingi. Kwa ajili hiyo ni wajibu juu ya dola – hiyo ni kwa mujibu wa uadilifu – isifanye hotuba za ndani ziishie kwa kikundi kimoja mbali na kingine, na hotuba rasmi za kidini zisisumbue madhehebu za Kiislamu zilizopo ndani ya nchi na nje yake. Ama hotuba isiyo rasmi ni vigumu kuidhibiti. Na uadilifu ambao ni wajibu juu ya kila dola kuutekeleza ni kila madhehebu iwe na darasa zake, vitabu vyake, mimbari zake, misikiti yake masomo yake na madrasa zake za kielimu, bila ya yeyote kumchokoza yoyote. Na mwenye kuhimiza miongoni mwao matumizi ya nguvu au kuukufurisha upande mwingine itabidi kutoa fursa kwa upande wa pili ya kujibu na kujihami binafsi dhidi ya dhulma ya wakufurishaji, haya yakiwa makadirio madogo. Hii haimaanishi kuacha mazungumzo ya lile ambalo ni jema, wala mjadala wa kidugu wala ukosoaji wa kielimu utakiwao. Sifa njema ni za Mwenyezi Mungu, Bwana wa ulimwengu, na rehema na amani zimfikie Bwana wetu Muhammad na ziwafikie Aali zake watoharifu na ziwafikie Maswahaba wake miongoni mwa Muhajirina na Answari na waliowafuatia kwa hisani.

UTAFITI JUU YA KITABU TAWHIDI ­CHA SHEIKH MUHAMMAD BIN ABDUL-WAHABI Utangulizi: Kitabu hiki kidogo na kitabu Kashfu-Shubuhati ni miongoni mwa vitabu vya Sheikh Muhammad bali huenda ni vitabu vyake 235

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 235

1/20/2016 11:35:58 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

mashuhuri mno kwa ujumla.93 Kwa hakika Sheikh alivitunga mwanzoni mwa daawa kwa hiyo ni vya mwanzo miongoni mwa alivyotunga Sheikh. Kitabu hiki kimechangia katika kunyanyua daraja ya ufurutu ada miaka ya mwishoni, kwa kuwa insha yake ilipitishwa kuwa kitabu cha kiada katika kila ngazi ya elimu katika ufundishaji kwetu sisi katika dola ya kifalme (Saudia). Kwa hiyo ni kitabu cha kiada katika elimu kutoka darasa la kwanza shule ya msingi mpaka darasa la tatu sekondari, pamoja na nyongeza ya maudhui ya tamaduni katika masomo ya Sekondari tu. Ama katika masomo ya Sekondari hatua ya juu, kitabu pamoja na kuwekewa nyongeza ya ufafanuzi na kubadilisha baadhi ya anuani kwa namna ambayo itakuwa na utulivu 93

 Na nakala ninayoitegemea ni ile iliyochapishwa na Wizara ya mambo ya Kiislamu, Chapa ya mwaka 1422 A.H. Na nakala hiyo ina kurasa 108 katika sehemu ndogo, na ni kwa gharama ya tajiri mashuhuri Sulayman bin Abdul-Azizi ar-Rajihiy. Na katika nakala hiyo kuna upande wa kiserikali na upande wa umma, pamoja na kuwa ndani ya kitabu kuna ufurutu ada wa ukufurishaji. Na laiti serikali na matajiri wangeishia kutawanya vitabu vyenye msimamo wa kati visivyoelemea upande mmoja, kama vile msahafu mtukufu, Sahihi mbili na kitabu al-Ummu cha Shafi, na kitabu al-Istidhkari cha Ibn Abdulbari na mfano wa hivyo, ingekuwa bora, bali hata vitabu vya kimadhehebu kama al-Mughniy cha fikihi ya kihanbali na Sunanul-kubra cha al-Bayhaqiy katika fikihi ya Shafi, na al-Inaya katika fiqihi ya Hanafi, na al-Mudawanatu cha fikihi ya Maliki, ingekuwa bora kuliko kutawanya vitabu vilivyozama katika madhehebu ambavyo athari yake kubwa ni kuzidisha ufurutu ada na kuufarakisha umoja wa Waislamu na kuzidisha mzozo wao. Mfano wa vitabu vya Ibn Taymiya na vitabu vya Sheikh Muhammad Mungu awarehemu hao wawili. Vitabu hivi vinapanda mfarakano kuliko vipandavyo kheri. Inakaribia kwamba hautaingia nyumba (ya Msuudia) ila utakuta humo tofauti imezagaa na hali ya kuhamana, kubughudhiana, kwa kuwa vinakazania mambo ya tofauti kisha vinainusuru rai ya msimmo mkali katika mambo haya, kisha vinaainisha kuwa usipofuata msimamo huu wa ukufurishaji au wa kuwafanya watu ni wanabidaa ni dhambi pamoja na kuwajibisha kuhama na bughudha kwa asiyeafikiana nao katika rai hii, kwa kuwa rai hiyo yenyewe – kulingana na rai yao - ndio Uislamu wenyewe! Nayo ndio maandiko, na ndio haki ya moja kwa moja!... Ni jambo la kawaida kutokea tofauti na mfarakano kati ya watu wa nyumba moja. Kisha baada ya haya tunasema: Tusichangie kueneza ufurutu ada na tusishangazwe na tuhuma za watu wengine kwetu miongoni mwa Waislamu na makafiri. 236

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 236

1/20/2016 11:35:58 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

mwingi, lakini bado ni kilekile na kwa anuani ileile ya Kitabu cha tawhidi ambayo ni haki ya Mungu kwa waja, ama katika hatua ya shule ya msingi ni muhtasari wake. Na tumetaabika katika kutahadharisha maudhui hii toka zamani, lakini Wizara ya Malezi na Mafunzo Saudia yaonesha haina mamlaka katika kubadilisha kitabu cha kiada au kuunda kamati ya utungaji ya kiadilifu ya kisheria inayojitegemea, kwa sababu lalamiko moja tu la wanachuoni kwenye mamlaka za kisiasa linatosha kuifuta kamati hii na kuiweka sawa. Kwa minajili hiyo Wizara ya Malezi na Mafunzo inajitahidi kuwakinaisha baadhi ya wanazuoni na kuonesha vitabu vya kiada kwao kila baada ya muda, ili kupata mwafaka wa marekibisho yanayofaa...........Na kila mwenye kupendekeza au kujaribu kukosoa kitabu cha kiada cha Tawhidi japo iwe ukosoaji mdogo mno basi atakuwa kwenye hatari ya kuadhibiwa vikali! Vyovyote iwavyo hebu turudi kwenye kitabu Tawhid. Kitabu hiki kina kurasa 112 kwenye umbile dogo kikiwa na milango 65. Hapa nitataja mfano wa yawezayo kuzingatiwa, kwa sababu ya kuambatana kwake sana na fikra ya Sheikh Muhammad na utaratibu wake, na kwa kuwa ni cha kwanza miongoni mwa vitabu vyake alivyotunga, na kuwa hicho, pamoja na Kashfushubuhati ni vitabu mashuhuri mno vya kiwahabi pasi na mpaka. Ijulikane kuwa mimi sijakamilisha usomaji wa kitabu usomaji wa kukosoa, ninatumai kutakuwa na fursa bora ya kukamilisha usomaji huu.

LA KWANZA LIPASALO KUCHUNGUZWA: Sheikh ameanza kitabu katika uk. 5 kwa kutaja Aya zinazoelezea wajibu wa kumwabudu Mungu peke Yake bila kumshirikisha na chochote. Hili halina tofauti kati ya Waislamu. Laiti kitabu king237

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 237

1/20/2016 11:35:58 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

ekuwa kimeelekezwa kwa washirikina wanaomwabudu asiyekuwa Mungu hilo lingekuwa sahihi. Lakini waliokusudiwa – yasikitisha – ni walio kinyume na yeye miongoni mwa Waislamu, ambao wanafanya baadhi ya mambo ambayo tunayaona kuwa ni ushirikina, nayo kiukweli yapo miongoni mwa mambo yaliyo na uhitilafiano au yapo katika utendaji wenye makosa watendayo baadhi yao, sawa yawe yanaruhusiwa kisharia au ni bidaa au ni shirki ndogo. Ama shirki kubwa ipo kwa kiwango kidogo mno kama si kutokuwepo kabisa..... Kisha hitilafu hizi, upotovu, na bidaa sio mahsusi kwa zama zetu, bali zenyewe ni za tangu zamani. Na hii haimaanishi kwamba haipasi kukososa, kubainisha na kuhadharisha dhidi ya matendo hayo, bali ni wajibu kujiepusha na ufurutu ada katika kukemea hayo ili isifikie kiasi cha kuwakufurisha Waislamu. Upeo wa jambo ulivyo katika suala hili ni tujue kuwa: Jamii ya Kiislamu haitokosa kuwa na fikra zisizo za kawaida, kwa baadhi ya watu wake, huyu au yule. Hili ni jambo la kawaida katika kila umma na kila taifa, lakini tusizifanye hitilafu hizi kuwa ndio halalisho la kuwadhuru wengine na tupitilize kiwango katika kuhasimiana hadi tufikie kuomba msaada kutoka mamlaka ya dola na kwa usalama wa taifa, hotuba, matangazo na mimbari. Hakika upitilizaji huu katika kujinusuru katika mambo ambayo mengi kati ya hayo watu wamehitilafiana, hiyo ndio bidaa na dhulma.

LA PILI LIPASALO KUCHUNGUZWA: Kisha Sheikh aliitaja athari kutoka kwa Ibn Mas’ud isemayo: “Anayetaka kuangalia usia wa Muhammad 5 ambao una hitimisho basi naasome kauli Yake Mtukufu:

238

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 238

1/20/2016 11:35:58 AM


hayo watu wamehitilafiana, hiyo ndio bidaa na dhulma. lA PIlI lIPASAlo KUChUNGUZWA: Kisha Sheikh aliitaja athari kutoka kwa Ibn Mas’ud isemayo: “Anayetaka NI MWANADAAWA, SI NABII kuangalia usia wa Muhammad  ambao una hitimisho basi naasome kauli Yake Mtukufu: ..... $\↔ø‹x© ⎯ÏμÎ/ (#θä.Îô³è@ ωr& ( öΝà6øŠn=tæ öΝà6š/u‘ tΠ§ym $tΒ ã≅ø?r& (#öθs9$yès? ö≅è% * çνθãèÎ7¨?$$sù $VϑŠÉ)tGó¡ãΒ ‘ÏÛ≡uÅÀ #x‹≈yδ β ¨ r&uρ

‘Sema: Njooni niwasomee aliyowaharamishia Wenu: ‘Sema: Njooni niwasomee aliyowaharamishia MolaMola Wenu: Kwamba Kwamba msimshirikishe na chohote mpaka kauli Yake msimshirikishe na chohote - mpaka kauli Yake tukufu - Na kwa tukufu Na kwa hakika hii ndiyo njia yangu iliyonyooka.’” hakika hii ndiyo njia yangu iliyonyooka.’” (6:151, 153). (6:151-152).

Ni kama hivi Sheikh hakutaja nususi za Aya hizi mbili, wala Ni hakutaja kama hivichimbuko Sheikh hakutaja Ayala hizi mbili,kwetu wala nihakutaja la athari,nususi lakini za hapa muhimu Aya chimbuko la athari, lakini hapa la muhimu kwetu ni Aya tukufu bila kujali tukufu bila kujali kuwa riwaya hiyo ya usia wa Nabii 5 ni sahihi kuwa riwaya hiyo ya usia wa Nabii  ni sahihi au hapana. Yatosha au hapana. Yatosha kuwa Mwenyezi Mungu ameyaita makatazo kuwa na Mwenyezi Mungu ameyaita makatazo na amri zilizopo Aya ya 151 – 152 za amri zilizopo Aya ya 151, 153 za Sura al-An’am kuwa ni njia yake Sura al-An’am kuwa ni njia yake iliyonyooka. Na Aya mbili hizo baada ya iliyonyooka. Nahumo Aya mbili hizo baada ya kuzirejelea tunakuta humo kuzirejelea tunakuta yafuatayo: yafuatayo: 1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9.

Katazo la shirki. Katazo la shirki. Amri1. ya kuwatendea hisani wazazi wawili. Katazo la kuwaua watoto kuhofia umasikini. 2. Amri ya kuwatendea hisani wazazi wawili. Katazo la kutenda maovu yaliyo wazi katika hayo na yaliyofichika. 3. laKatazo la kuwaua kuhofia umasikini. Katazo kuua nafsi ambayowatoto Mwenyezi Mungu ameharamisha isipokuwa kwa haki. 4. Katazo la kutenda maovu yaliyo wazi katika hayo na yaliKatazo la kula mali ya yatima. yofichika. kipimo na mizani kwa uadilifu. Amri ya kukamilisha Amri5. ya kuwa na la kauli ya kiadilifu japo wawe ndugu wa karibu. Katazo kuua nafsi ambayo Mwenyezi Mungu ameharaAmri ya kutekeleza ahadi. misha isipokuwa kwa haki.

Sheikh 6. amefanya vyema kukataza iwe ndogo au kubwa, pamoja na Katazo la kula mali yashirki yatima. hayo tujihadhari na mambo mengi ambayo ameyaingiza katika shirki na wala 7. Lakini Amrilau ya tukiyaacha kukamilishahayo kipimo na mizani kwa sio shirki. tutazikuta baadhi yauadilifu. amri za Aya hii zimetelekezwa kikamilifu na Mawahabi wenyewe mfano ‘Katazo la kumuua 8. Amri ya kuwa na kauli ya kiadilifu japo wawe ndugu wa mtu ambayekaribu. Mwenyezi Mungu ameharamisha kumuua isipokuwa kwa

9.

149 Amri ya kutekeleza ahadi. 239

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 239

1/20/2016 11:35:58 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Sheikh amefanya vyema kukataza shirki iwe ndogo au kubwa, pamoja na hayo tujihadhari na mambo mengi ambayo ameyaingiza katika shirki na wala sio shirki. Lakini lau tukiyaacha hayo tutazikuta baadhi ya amri za Aya hii zimetelekezwa kikamilifu na Mawahabi wenyewe mfano ‘Katazo la kumuua mtu ambaye Mwenyezi Mungu ameharamisha kumuua isipokuwa kwa haki.’ Mawahabi wamewaua Waislamu wengi bila ya haki, mpaka uuaji wao umefikia kuwaua wakati wakitekeleza wajibu wa Swala ndani ya misikiti. Kama ambavyo hawakufanya uadilifu katika kumhesabu mtu kuwa ni kafiri kwa ukafiri umuondoao kwenye Uislamu, sawa mtu huyo awe ni miongoni mwa wanazuoni au miongoni mwa watu wa kawaida wa zama zao, miongoni mwa Mahanbali na Masunni sembuse wasiokuwa hao. Pia wametelekeza amri ya ‘Kuwa na uadilifu katika kauli japo iwe kwa ndugu wa karibu.’ Kwani yapasa tuutambuwe ukweli pindi tuzionapo dalili za kutosha za kuthibiti kwake. Na Sheikh na pia wafuasi wake wanakazania usia wa mwanzo katika Aya hii nao ni kukataza shirki, japokuwa shirki ni ndogo au haipo kabisa katika umma wa Kiislamu, huku wakipindukia katika kuingiza ambayo si shirki katika shirki, ilihali wanaacha kwa kupindukia pia amri na makatazo mengine katika Aya hii hii, japokuwa kuna sababu ya kuzitekeleza amri hizo ambazo zipo bayana, achilia mbali kuwa ni wajibu kutekeleza amri na makatazo yote yaliyomo katika Qur’ani tukufu. Na ambalo wanalipuuza zaidi na kulitelekeza japo ni la muhimu sana ni uharamu wa kumwaga damu na kuvunja heshima. Hapana uharamu wa kumwaga damu za Waislamu kwao. Wala hapana uadilifu katika kauli na hukumu katika kuwahukumu walio kinyume nao miongoni mwa Waislamu wanazuoni na watu wa kawaida, Mungu awarehemu na awasamehe.

240

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 240

1/20/2016 11:35:58 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

LA TATU LIPASALO KUCHUNGUZWA: Kisha Sheikh katika uk. 5 ametaja athari ya Muadhi bin Jabal ambaye kumhusu yeye kuna kauli ya Nabii 5: “Ewe Muadhi, wajua nini haki ya Mwenyezi Mungu juu ya waja na haki ya waja kwa Mwenyezi Mungu?..... Haki ya Mwenyezi Mungu juu ya waja ni wamwabudu wala wasimshirikishe na kitu. Na haki ya waja kwa Mwenyezi Mungu asimuadhibu asiyemshirikisha na kitu....” Nasema: Kwanza: Hapa kuna falsafa kubwa kuhusiana na kuzitolea hoja hadithi za Nabii 5 ambazo dhahiri yake zinapingana na Qur’ani tukufu. Hapa sitaki kuingia humo wala sisemi kuwa hadithi ya Muadhi ni miongoni mwa hizo, ila ni kwamba suala vyovyote litakavyotufikia, kutoifanyia kazi Hadithi ya wapokezi wachache (Aahad) kwa kuwa kuthibiti kwake ni kwa dhana, inabaki ni rahisi kuliko kutozifanyia kazi Aya tukufu ambazo kuthibiti kwake na kuwa kwake dalili ni mkataa kama itakavyokuja. Na Sheikh Muhammad Mungu amrehemu pia wimbi la kiwahabi, kutokana na dhahiri tuisomayo na kuifahamu kutokana nao ni kwamba wanawafahamisha watu Hadithi hii kuwa: Mwislamu ikiwa hakufanya shirki Mungu hatomwadhibu, na shirki hapa wanamaanisha vitu viwili: Shirki ya asili na matendo mengine waliyoyaambatanisha na shirki, ambayo ndani yake kuna kuhitilafiana. Na hii kwanza ni kosa la kiutaratibu litokanalo na kuifuata dalili ya dhana au kufuata dalili moja na kutozitilia manani dalili zingine zenye nguvu zaidi na nzito kuliko zingine, nao ni msiba ulioenea katika Waislamu sio mahsusi kwa uwahabi. Hivyo basi sio jaizi kuifanya hoja Hadithi inayopingana na nususi za Qur’ani hata ikiwa sahihi, au ni wajibu juu yetu kwa uchache tuusahihishe ufahamu wetu wa Hadithi. Ama tuilete Hadithi kisha 241

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 241

1/20/2016 11:35:58 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

tuifahamu ufahamu pungufu twende yake kuliko zingine,dhahiri nao niyake msiba ulioenea katikahalafu Waislamu sionyuma mahsusi kwa ilihali tukiwa hatung’amui umuhimu wa kuijua mipaka ya maana uwahabi. yake, ile isiyohitilafiana au kupingana na ile maana ambayo ni sahihi

Hivyo basi sio jaizi kuifanyaKisha hoja tuki Hadthi inayopingana nakinyume nususi zakatika Qur’ani zaidi kuliko yenyewe. halifu na kwenda hatahuu ikiwa sahihi, wa au niharaka wajibukiwango juu yetukikubwa kwa uchache tuusahihishe ufahamu mwendo cha Aya za Qur’ani na wetu wa Hadithi. Ama tuilete Hadithi kisha tuifahamu dhahiri yake ufahamu Hadithi za Nabii na mkataa za Kiislamu. Hakika kufanya hivyo ni pungufu halafu twende nyuma yake ilihali tukiwa hatung’amui umuhimu wa ujinga au utashi potovu unaotuingiza katika kupingana na kuijua mipaka ya maana yake,wailenafsi isiyohitilafiana au kupingana na ile maana kutuwezesha na makosa yanayofuatia, kufanya ambayo ni sahihi sisi zaidikujitakasa kuliko yenyewe. Kisha tukhalifu na katika kwenda kinyume taswira kuhukumu au katika utendaji. katika huu au mwendo wa haraka kiwango kikubwa cha Aya za Qur’ani na Hadithi za Nabii na mkataa za Kiislamu. Hakika kufanya hivyo ni ujinga au Ibada wa Katika – Endapo lakenalitakuwa sahihisisi utashi potovu nafsi Hadithi unaotuingiza katika tamko kupingana kutuwezesha ni kumtii Mungu yanayofuatia, katika amri kuu zakufanya Kiislamu na makatazo yakeau kujitakasa na makosa katika taswira au kuhukumu makuu, si jaizi tuifahamu Hadithi – sawa iwe hii au nyingine – katika utendaji.

ufahamu uliotengwa na Aya na Hadithi zilizothibiti, khususan ni

Ibada Katika hadithi – Endapo tamko lake litakuwa sahihiyake ni kumtii Mungu kuwa Hadithi hii tukiichukua kulingana na dhahiri ingekuwa katika amri kuu na za Qur’ani Kiislamutukufu na makatazo yake wa makuu, jaiziiwe tuifahamu inapingana upinganaji wazi,si lau mtu Hadithi – sawa iwe hii au nyingine – ufahamu uliotengwa na Aya na Hadithi hamshirikishi Mungu na kitu lakini mtu huyu anaua nafsi, yaani zilizothibiti, khususan ni kuwa Hadithi hii tukiichukua kulingana na dhahiri watuinapingana ambao ni na haramu kuuliwa je tutamwambia: yakeanaua ingekuwa Qur’ani tukufu upinganaji wa wazi,‘Kuwa lau iwena mtu matumaini madamu wewe haumshirikishi Mungu na kitu, hatokuahamshirikishi Mungu na kitu lakini mtu huyu anaua nafsi, yaani anaua watu dhibu kwa kuwaua watu, kuwadhulumu na kula mali zao??’ Laambao ni haramu kuuliwa je tutamwambia: ‘Kuwa na matumaini madamu wewe haumshirikishi Mungu na kitu, hatokuadhibu kwa kuwaua hasha! bali tutamwambia: Qur’ani tukufu kabla ya Hadithi hii watu, ya kuwadhulumu na kula mali zao??’ kuwa Lahasha! bali tutamwambia: Qur’ani wapokezi wachache inabainisha mwenye kuiua nafsi ambayo tukufu kabla ya Hadithi hii ya wapokezi wachache inabainisha kuwa mwenye ni haramu kuuawa ameahidiwa moto kama ilivyokuja katika kauli kuiua nafsi ambayo ni haramu kuuawa ameahidiwa moto kama ilivyokuja Yake Mtukufu: katika kauli Yake Mtukufu: Ïμø‹n=tã ª!$# |=ÅÒxîuρ $pκÏù #V$Î#≈yz ÞΟ¨Ψyγy_ …çνäτ!#t“yfsù #Y‰ÏdϑyètG•Β $YΨÏΒ÷σãΒ ö≅çFø)tƒ ⎯tΒuρ

∩®⊂∪ $VϑŠÏàtã $¹/#x‹tã …çμs9 £‰tãr&uρ …çμuΖyès9uρ

mwenye kumuua muumini kwa kukusudia, “Na“Na mwenye kumuua muumini kwa kukusudia, basi malipobasi yake ni malipo yake ni Jahannam, ni mwenye kudumu Jahannam, ni mwenye kudumu humo; na Mwenyezihumo; Munguna amMwenyezi Mungu amemghadhibikia na amemlaani na amemwandalia adhabu kubwa.” 242 (Sura Nisai: 93). Je tuiache Aya hii iliyo wazi kwa ajili ya nukuu ya orodha ya marawi wa Hadithi - yaani wapokezi wa Hadithi – ilihali tukiwa hatuna dhamana ya huyu kusahau au yule kuelewa makosa? 15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 242 1/20/2016 11:35:58 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

emghadhibikia na amemlaani na amemwandalia adhabu kubwa.” (Sura Nisai: 93).

Je tuiache Aya hii iliyo wazi kwa ajili ya nukuu ya orodha ya marawi wa Hadithi - yaani wapokezi wa Hadithi – ilihali tukiwa hatuna dhamana ya huyu kusahau au yule kuelewa makosa? Kisha Sheikh mwenyewe binafsi na wimbi la kiwahabi hawatosheki na mtu kumwabudu Mungu na hamshirikishi na kitu bali wanamkufurisha asiyehama kwenda kwao ikiwa hawezi kukataza maovu nchini mwake, na wanamkufurisha asiyeafikiana nao juu ya kuwakufurisha Waislamu na wanamuua. Na wamemkufurisha awaitaye kuwa wao mawahabi ni Makhawariji, wamemuua na kumfanya kuwa ni mwenye kuitukana dini ya Rasuli! Umetangulia uthibitisho kwa ushahidi juu ya haya na mfano wake. Hivyo basi wao kwa upande wa utekelezaji wamekwenda mbali zaidi kuiita shirki bila mipaka na hukumu bila mipaka na kisha kuutumia upanga bila mpaka.

LA NNE LIPASALO KUCHUNGUZWA: Kisha Sheikh katika uk. 6 ametaja mas’ala kadhaa akiyadondoa kutoka katika Hadithi hii, miongoni mwayo ni: 1. Ibada ni tawhidi kwa kuwa kuna uhasama humo: Nasema: Huku ni kuifupisha ibada kwenye baadhi tu ya sehehmu yake, kwa kuwa walio kinyume na Sheikh walikuwa wanasema: “Sisi hatuabudu ila Mungu basi ni kwa nini mnatukufurisha?” Yeye akawa anawaambia kauli ile iliyotangulia, kwa kuwa anaiwekea wigo ibada katika Tawhidi, kisha anaiwekea Tawhidi wigo wa orodha ndefu ya sharti za La ilaha ila llahu na vinavyoitengua, kwa 243

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 243

1/20/2016 11:35:58 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

namna ambayo inakuwa vigumu kwa mpinzani wake abakie kuwa Mwislamu isipokuwa kama atafuata rai yake na ijtihadi yake katika utambulisho wa Tawhidi na shirki yenye mkazo. Mwanzo wa jambo mtafuta elimu atamdhania kuwa yuko sahihi. Kwa minajili hiyo tunawakuta baadhi ya wanazuoni kama vile al-Amir as-Swan’aniy na as-Shawkaniy wanashuhudia kuwa asemayo Sheikh Muhammad ni sahihi! Kwa kuwa Sheikh na wafuasi wake baada yake pindi wanapowaandikia wanazuoni hawa wanawaambia: ‘Sisi tunalingania ibada ya Mungu peke Yake na kuacha shirki!’ Kwa hiyo wanazuoni wengine hawatokuwa na wanalomiliki ila ni kusema: ‘Hii ni dini ya Mwenyezi Mungu na sisi tu pamoja na ninyi.’ Na huenda wakamuandikia Sheikh au wafuasi wake, na huenda wakasifu kwa mashairi na kwa semi za kawada..... Lakini lau hao wanazuoni wangejua kuwa neno Tawhidi hapa kwa Mawahabi lina masharti marefu, mapana likifuatiwa na vitanguzi vingi ambavyo si sahihi, hawangemuunga mkono Sheikh. Kwa minajili hiyo tunamkuta al-Amiri as-Swan’aniy anarudi nyuma na kutengua sifa alizomsifu Sheikh na kisha anamkosoa ukosoaji mkali pindi Muridu at-Tamiimiy94 alipomjulisha juu ya vitabu vikubwa vya Sheikh na vilivyo na ufafanuzi wa mafumbo yaliyomfikia as-Swan’aniy. Na tofauti ya wanazuoni na Sheikh si katika daawa ya Tawhidi na kukataza shirki. Hili ni jambo ambalo Mwislamu wa kawaida hawi na rai tofauti sembuse wanazuoni wa zama zake katika Najdi na Hijazi, Iraki naYemen. Tofauti yao na yeye ni katika orodha hii ndefu ya masharti na vitanguzi ambavyo Sheikh anavifanya kuwa ni sharti katika Tawhidi na kusalimika na shirki. Tukifahamu hili vyema tutakuwa tumetambua sababu ya upinzani wa wanazuoni dhidi yake na utii wa watu wa kawaida kwake. 94

Mawahabi walimuua katika mwaka 1171 A. H. 244

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 244

1/20/2016 11:35:58 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Na Sheikh amelalamika kuwa wapinzani wake ni miongoni mwa wanazuoni na watu mahsusi na si katika watu wa kawaida (uthibitisho utakuja). Hiyo ni kwa kuwa watu wa kawaida waisikiapo Hadithi japo iwe dhaifu, au kauli ya mwanachuoni japo iwe kibutu wanakuwa na itikadi na yaliyomo humo, kama vile mvuto au tishio, na watatoka na kuwaua Waislamu kwa marefu na mapana kwa sababu wanachuoni wao wamewaambia kuwa hao ni washirikina wa shirki kubwa kuliko shirki ya Abu Jahli,95 kama alivyokuwa anafanya Sheikh katika kuwaelezea wapizani wake miongoni mwa wanazuoni Mungu amsamehe. Kisha ikiwa Sheikh anakusudia kuwa uhasama kati ya Manabii na watu ulikuwa katika Tawhidi tu, hii sio sahihi, na huku ni kuifupisha risala kwenye baadhi ya yale yaliyohitajika, bali kulikuwa na dhambi nyingi watu walikuwa wanazifanya na Mitume waliwakataza, kama vile dhulma, kupunguza katika kipimo cha mizani, kuiua nafsi ilio haramu kuuliwa. Na Sheikh Muhammad ametunga kitabu Masailul-Jahiliyah, ambamo humo ametaja maswala zaidi ya sabini ambayo Mtume 5 aliwakhalifu watu wa zama za Jahiliyyah. Hiyvo kila ambalo Qur’ani tukufu imelikataza kwa uchache lilikuwa kwa baadhi ya makafiri. Ama Sheikh akikusudia kuwa uhasama kati yake na wanachuoni wa zama zake ulikuwa katika Tawhidi tu, hili pia sio sahihi, kwani walikuwa wanahasimiana naye katika mas’ala mawili makuu: Kukufurisha na kuua. Basi ilivyo ni kwamba Sheikh kuifupisha ibada katika Tawhidi tu ni kosa, na kauli yake kuwa uhasama ulikuwa katika Tawhidi tu ni kosa lingine. Lakini makosa haya mawili hangeyagundua mbumbumbu na bedui, ndio maana walikuwa na hamasa kubwa 95

Tutaonesha jinsi Sheikh alivyomzungumzia mmoja wa wanazuoni wa Kihanbali katika zama zake kuwa yeye ni kafiri mno kuliko Abu Jahli! Na sana amekariri kuwa watu huko Najdi na Hijazi katika zama zake shirki yao ilizidi shirki ya makafiri wa Kikuraishi kwa mawili! 245

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 245

1/20/2016 11:35:58 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

ya kuwaua Waislamu kwa kuwa wao walidhania kama Sheikh alivyosema kuwa mahasimu wao ni washirikina wa shirki kubwa kuliko shirki ya makafiri wa Kikuraishi! 2.

Asiyefanya Tawhidi hajamwabudu Mwenyezi Mungu..:

Hili kwa upande wa nadharia ni sahihi, lakini kuhitilafiana kati ya Sheikh na wanazuoni wa zama zake huko Najdi, Hijazi na mahali pengine si katika hili, bali kuhitilafiana ni katika maana ya Tawhidi ambayo Sheikh ameiwekea masharti marefu ya dhana au yaliyo na makosa au aliyohitilafiana na mtu mwingine miongoni mwa wanazuoni. Na asiyeileta Tawhidi hiyo yenye masharti basi huyo kwa Sheikh ni mshirikina na kwa wanazuoni wengine ni Mwislamu. Hivyo yeye ameiondoa tofauti mahali pake na kuiweka mahali ambapo si wanapohitilafiana, ndani ya hilo kuna kuisitiri baadhi ya mitazamo kuhusu kilichomsukuma! Je ni hamasa au ijtihadi na nia njema, au uhasama uliofikisha kwenye kudhulumiana! 3.

I bada ya Mungu haipatikani ila kwa kumkufuru ­Twaghuti:

Nasema: Hii ni sahihi lakini si mahali pa uhitilafiano, kwa kuwa walio kinyume na Sheikh hawajasema: ‘Sisi tunamwamini Mungu na Twaghuti.” Ila ni kuwa Sheikh amejitahidi kuvisifu vitu kuwa ni Twaghuti ilihali wala haviko hivyo, kama vile tawassul, na mazoezi ambayo aghlabu ni makosa. Na walio kinyume naye wanasema: “Haya yapo kati ya yaliyoruhusiwa, makuruhu, haramu, na si sahihi tuseme kuwa hayo ni Twaghuti, kisha juu ya hayo turatibu kuwa asiyeyaona hayo kuwa ni shirki ni mwenye kuamini Twaghuti na ni wajibu kumuua.” 246

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 246

1/20/2016 11:35:58 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Bila shaka ninyi mwaona kuwa maneno katika sura yake ya jumla hapana uhitilafiano isipokuwa hitilafu pindi haya maneno yaliyo katika sura yake ya jumla yanapowekwa kwa asiyestahiki. Kutokea hapo ndipo huanza hitilafu kati ya Sheikh na wanazuoni wa Najdi wa zama zake, kisha kati yake na wanazuoni wa Hijazi na Iraq ... kisha hii leo kati yetu (Mawahabi) na ulimwengu wote! 4.

Twaghuti ni jumla ya kila kinachoabudiwa kinyume na Mwenyezi Mungu:

Nasema: Na hii ni sahihi, lakini kuna mambo, miongoni mwayo ni maana ya Ibada. Je natija ya ujahili au taawili inakuwa ni ibada ya kumwabudu asiyekuwa Mungu? Kwa mujibu huo sio jaizi tuwakufurishe wanaokalidi kwa madai kuwa wao wamewafanya wanazuoni wao miungu kinyume na Mungu, kama awafanyavyo Sheikh wale wanaowakalidi wanazuoni wanaohitilafiana na yeye. Lau hilo lingekuwa jaizi ingekuwa jaizi kwangu nimkufurishe mwenye kunikanusha juu ya utafiti huu kwa kuwa mimi nitamtuhumu kuwa amemfanya Sheikh Muhammad mungu kinyume na Mungu Mmoja! Hivyo basi utumiaji wa jumla katika baadhi ya nususi hauchukuliwi kama ilivyo dhahiri yake bali hukusanywa na nususi zingine zinazohadharisha kumkufurisha Mwislamu na zinazochunga vizuizi vya kukufurisha, kama ujinga, taawili, kukirihishwa na kudharurika. Lau ingekuwa jaizi kwa kila mwenye kuleta rai amtuhumu asiyemfuata kuwa anawaabudia wanazuoni wengine hangebaki Mwislamu katika sura ya dunia ila tungemtuhumu kwa ukafiri na ibada ya kumwabudu asiyekuwa Mungu Mmoja. Jambo la pili: Ni kuwa walio kinyume na Sheikh ambao Sheikh ameandika kitabu hiki (Tawhid) kutoa hoja dhidi yao, wanazozana naye kuwa baadhi ya mambo ambayo anaona na kudai kuwa ni kum247

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 247

1/20/2016 11:35:58 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

wamini Twaghuti hayapo hivyo bali hayo ni kati ya yale yanayoruhusiwa kisharia na ambayo ni makuruhu, au ambayo ni haramu au ambayo ni bidaa. Na ikiwa watamkubalia kuwepo kwa kitu miongoni mwa shirki kuu katika umma hawatomkubalia kuwa ni shirki iliyoenea kama asemavyo yeye, kwani yeye anadhani kuwa shirki imeenea ardhi yote! Watu wamerudi kuabudu Lata na Uzza. Na kuwa hapana mji miongoni mwa miji ya Najdi ila sanamu linaabudiwa kinyume na Mungu Mmoja! Na kuwa shirki kuu imegubika Rasi ya Arabu. Na kuwa watu wengi katika zama zake huko Najdi na Hijazi wanakanusha ufufuo. Na mengine miongoni mwa mambo makubwa ambayo alikuwa akiyachukulia kwa ujumla wake, umetangulia udhibiti wake. Hivyo wao wakisalimu amri kuwepo kwa shirki kuu wao wanaiona kuwepo kwa watu mmoja mmoja na wala sio kwa wote. Ni kama ilivyo, leo hatuoni kuwa ni jambo lina umbali kutokea shirki kuu katika miji ya Waislamu lakini ikiwa lipo basi ni kwa watu mmoja mmoja. Kwa wachache na wala sio enevu wala hatuwezi kumfuata anayesema kuwa shirki imeenea kwa Waislamu. 5.

Mas’ala hii Maswahaba wengi hawaijui:

Nasema: Ikiwa Sheikh anaposema ‘mas’ala hii’ anakusudia Hadithi yenyewe, kuwa Maswahaba wengi hawaijui kwa kuwa Nabii 5 alimuamuru Muadhi kuificha, hili ni sahihi, na ikiwa anakusudia kuwa mas’ala ambazo zimo ndani ya Hadithi hii hawazijui Maswahaba wengi, hili sio sahihi. Bali dosari hii ni dosari ya matini ya Hadithi, kwa kuwa si jaizi kwa Nabii awafiche Maswahaba wake mas’ala miongoni mwa mas’ala muhimu! Halafu ikiwa Maswahaba wengi hawaijui mas’ala hii basi vipi Sheikh anataka aijue kila Mwislamu katika zama zake?! Na asiyeijua anaweza kuwa chini ya nyundo ya ukufurishaji... Kisha vipi tunakariri kuwa Maswahaba 248

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 248

1/20/2016 11:35:58 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

ni wajuzi zaidi kuliko sisi na hali sisi tunadhania kuwa wengi wao hawaijui mas’ala muhimu walioijua watu wa Daraya?! 6.

Yafaa kuificha elimu kwa maslahi:

Anakusudia Nabii alimuamuru Muadhu kuificha Hadithi hii, lakini vipi Sheikh Muhammad ameijaalia kuwa ndio mwanzo wa daawa yake? Kisha hivi Sheikh anaona wapinzani wake ni Waislamu lakini yeye anaificha hii kwa maslahi?! Kwa sababu watu hawatohamasika kuwaua endapo atawahesabu kuwa ni Waislam?! Kisha ikiwa Nabii aliwahofia Maswahaba wasije wakazozana hivyo akaificha, kwa nini sasa Sheikh amejaalia kuwa Hadithi ambayo watu wengi ni lazima waijue na waitegemee?! Lau Nabii 5 angekuwa anataka kutokana na maana ya Hadithi lile alilolifahamu Sheikh angeamuru ifichwe ili watu wasiijue na si ili waitegemee. Hili limetubainishia sisi upeo wa kupotoka kwa ufahamu wa Sheikh katika kuifahamu Hadithi hii, kwa kuwa ameifupisha ibada iliyotajwa katika Hadithi kwenye Tawhidi kisha ameiwekea Tawhidi masharti na vitanguzi vingi kwa namna ambayo Hadithi inazuia wito wa kutegemea na kuwa kwenye wito wa kufeli. Kisha kuhusiana na Hadithi ni kama tulivyosema, ima iwe inakhalifu Qur’ani au inaafikiana na Qur’ani. Ikiwa inaafikiana na Qur’ani itakuwa wajibu tuifasiri kwa tafsiri ambayo haiendi kinyume na yaliyomo katika Qur’ani tukufu. Kwa hiyo tusiiwekee wigo risala katika Tawhidi na wala tusiiwekee Tawhidi masharti kwa namna ambayo haiingii humo ila rai ya kuwakufurisha Waislamu. Na ikiwa inakhalifu Qur’ani tukufu itakuwa wajibu kumtakasa Nabii na kumweka mbali nayo, na tusimbebeshe mawazo ya watu na kauli zao za kimdomo kutoka kwa baadhi yao, na yanayoweza kuambatana na nukuu hii ya mdomo miongoni 249

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 249

1/20/2016 11:35:58 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

mwa mapungufu kwa sababu moja tu, nayo ni kuwa wasimulizi sio maasumina mbali na dhana, kukosea, na kusahau. Anaweza mmoja wao akasahau tamko moja linalobadilisha maana ya Hadithi au kuathiri katika maana yake kwa namna ambayo linaondoa kuafikiana kwake na maandiko ya Aya za Qur’ani tukufu. Kwani kati ya Muadhi bin Jabal msimulizi aliyeisikia Hadithi moja kwa moja na kati ya Bukhari na Muslim zimepita zama karne mbili, hatuna dhamana inayozuia kwamba katika nyakati za nukuu za Hadithi hapawezi kutokea dhana, kosa wala kusahau kutoka kwa mmoja wa wasimulizi, hata kama wanaaminika kwa ujumla. Mara ngapi tumewaona watu katika zama zetu hizi ambao hatuna shaka na kuaminika kwao na kuwa ni watu wema, hata hivyo wanafikwa na dhana katika nukuu kutoka kwa mtu mmoja, basi itakuwaje nukuu kutoka kwa mtu naye kutoka kwa mwingine, naye kutoka kwa mtu wa tatu, naye kutoka kwa wa nne..? Mimi hapa sisemi tuzikatae Hadithi, ila itakapobainika kuhitilafiana kwake na Qur’ani tukufu. Na watu wa Hadithi kinadharia wanakiri katika vitabu vyote vya istilahi za Hadithi kuwa Hadithi inaweza kuwa na sanadi sahihi lakini matini yake ni batili endapo itakuwa kinyume na Qur’ani tukufu na haiwezekani kukusanywa pamoja. Ama Muutazilah nao ni madhehebu ya Kiislamu itumikishayo sana akili wanasema: “Endapo Hadithi itakhalifu Qur’ani hatutohitajia kujikusuru kukusanya bali kuikataa kunatimia na Qur’ani inatangulizwa. Na kuamini kwa yakini kuwa Marawi wamekosea katika nukuu na kwamba huu sio usemi wa Nabii 5 kwa kuwa Nabii hasemi kinyume na Qur’ani tukufu.” Hivyo basi ni sawa tuwe tumeona sanadi ya Hadithi ni sahihi pamoja na matni yake, au tumeikataa kabisa, bado sio jaizi kuifahamu peke yake huku tukizipuuza nususi zenye nguvu khususan nususi za Qur’ani tukufu.

250

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 250

1/20/2016 11:35:59 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

7.

I nafaa kuwahusisha baadhi ya watu na elimu mbali na wengine:

Nasema: Hili kwa watu wa Hadithi ni mahali pa kuchunguzwa, kwa kuwa haifai kuuficha umma elimu unayoihitaji, bali inafaa kuuficha elimu ambayo hauihitajii. Na hivi ni miongoni mwa vitu wamevichukua dhidi yao wale wanaowakosoa watu wa Hadithi. Utafiti wahitajika. 8.

Utukufu wa mas’ala hii:

Nasema: Na hii ni miongoni mwa dosari za matini ya Hadithi hii. Nabii 5 hatouficha umma kitu kitukufu kisha aamuru kukificha. Nabii 5 ni mubalighu na mfikishaji kwa watu wote. Na Uislamu hauna usiri; bali ni dini ya uwazi, na ni kwenye mlango huu madhehebu ya Baatniya imeingia na ikadhania iliyoyadhania. Na baadhi ya Masalafi wanakwenda kinyume na usemi huu, na wanadhania kuwa ni kafiri yule mwenye kudhania kuwa Nabii 5 ameuficha umma jambo.

LA TANO LIPASALO KUCHUNGUZWA: Sheikh ameweka mlango wa kwanza uk. 9: “Mlango wa ubora wa Tawhidi na dhambi ambazo inaziondoa.” Na ameleta Hadithi nyingi na miongoni mwazo ni Hadithi ya Ubadatu bin Swamit: “Mwenye kushuhudia kwamba hapana Mungu isipokuwa Allah, na kwamba Muhammadi ni mtumwa Wake na mjumbe Wake, na kuwa Isa ni mtumwa wa Mungu na mjumbe Wake, na ni neno Lake aliloliweka kwa Mariam, na ni roho kutoka Kwake. Na kwamba hakika pepo ni kweli na moto ni kweli, Mungu atamuingiza peponi kwa amali aliyoitenda.” 251

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 251

1/20/2016 11:35:59 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Nasema: Hapa nitataja mfano wa utangulizi katika kuzikosoa Hadithi. Watu wengi wa Hadithi hawako katika mtindo huo upande wa utekelezaji japo wapo katika mtindo huo upande wa nadharia. Na kutofautiana huku kati ya nadharia ya watu wa Hadithi na utekelezaji wao ni jambo lionekanalo kirahisi kwa mwenye kumiliki mambo matatu: La kwanza: Kuitambua nadharia ya watu wa Hadithi. Na ujuzi wa mas’ala hii ni mwingi khususan kati ya wanafunzi wa elimu ya Hadithi. Pili: Kulinganisha na kupima mazao ya watu wa Hadithi (vitabu vya hadithi) kwenye nadharia ambayo wameiweka wao wenyewe. Hili kutokea kwake ni kwa nadra isipokuwa katika Hadithi ambazo ni mashuhuri kwa udhaifu, au zitoleazo ushahidi rai za mahasimu wa watu wa Hadithi. Baadhi yao kama vile Daruqutniy, Albaniy na Ahmad al-Ghumariy ndio wamekwenda kinyume na udhaifu huu wa kutotabikisha au kutolinganisha nadharia na mazao yake, hivyo wakazidhoofisha Hadithi zilizomo katika Sahih mbili au mojawapo, kwa kuona haya na kutaradadi. Tatu: Ushujaa wa kielimu kwa namna ambayo mwanafunzi wa elimu haogopi lawama ya mwenye kulaumu wala chukio la yeyote miongoni mwa watu wanaomchukulia yeye kuwa ni mtu wa bidaa au upotovu au ukafiri, bali yampasa awe na ikhlasi katika nia yake kwa ajili ya Mungu kisha kwa ajili ya ukweli, kisha atangaze haki aionayo. Elimu iko sehemu mbili, sehemu ni kile kinachojulikana, na sehemu nyingine ni ushujaa wa kukitoa kinachojulikana. Kisha nasema: Hadithi ya kwanza aliyoileta Sheikh imo katika Sahihi Bukhariy lakini sio sahihi kuinasibisha na Nabii 5 kwa sababu ambazo tutazitaja hapa: 252

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 252

1/20/2016 11:35:59 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Kwanza dhahiri ya Hadithi hii iko kinyume na Qur’ani tukufu wazi wazi kabisa... Lau Mwislamu atashuhudia mambo haya (yaliyotajwa katika shahada mbili), halafu akawa na mwenendo mbaya akadhulumu, akaua watu, akaiba, akazini, akala mali ya yatima, akaacha swala na zaka, Hija na swaumu, akafanya mambo mabaya na yaliyo haramu, na akafanya dhambi kubwa mfano wa haya, Qur’ani tukufu imeweka wazi kuwa huyu ataingia motoni sio peponi. Kwa minajili hiyo ndio maana nimetangulia kusema kuwa sisi tumeifanya Qur’ani yenye kuhamwa... Qur’ani imekuwa ni ya mwisho tutoapo dalili, na tunaziamini kuliko Qur’ani riwaya zilizonasibishwa na Nabii 5 ambazo upo uwezekano katika marawi wake kuna aliyeielewa kimakosa na mwenye kusahau na mwingi wa kukosea, hii ni ikiwa tu amesalimika na kukusudia kusema uwongo kwa ajili ya maslahi au siasa au madhehebu au rai. Wala hatutahitajia katika Hadithi kama hii kuangalia sanadi. Inatosha kuzikumbuka tu Aya tukufu ambazo zinamtishia moto mwenye kutenda madhambi makubwa. Kisha tunaiangalia Hadithi ikiwa kutokana nayo hailazimu kujiepusha mbali na madhambi makubwa, basi kunasibisha tamko lake hili kwa Nabii ni nasibisho batili japo Hadithi iwe katika Sahihi Bukhariy.

KUIKOSOA SANAD YA HADITHI: Kwanza: Hadithi ni ya mtu wa Sham, na watu wa Sham walikuwa miongoni mwa Murjiah wabaya mno, na Hadithi inaafikiana na itikadi za Murjiah. Pili: Ameieleza Hadithi hii Bukhariy katika Sahih yake kutoka kwa Swadaqatu bin al-Fadhlu, huyu ni mtu wa Khurasani, Msalafi mwaminifu. Ametuhadithia Walidi bin Muslim ad-Damashqiy 253

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 253

1/20/2016 11:35:59 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

mfuasi wa Bani Umayyah, muongo, naye ndio dosari ya Hadithi hii kama ufafanuzi utakavyokuja. Ametuhadithia kutoka kwa al-Awzaiy Imamu wa watu wa Sham, ambaye Hadithi zake nyingi ni dhaifu96 japokuwa yeye ni mwaminifu. Amenihadithia Umairu bin Hanii, huyu ni mtu wa Damascus na hakuna yeyote miongoni mwa watu wanaokubalika aliyemtaja kuwa ni mwaminifu. Ibn Abil-Hiwariy aliikataa riwaya ya al-Awzaiy kutoka kwake na alisema kuwa yeye anamchukia, na huyu Umairu alikuwa pamoja na watu wa Sham wahimizaji wa Yazidi bin Walidi ambaye ni mwadilifu mno katika Bani Umayya baada ya Umar Bin Abdul-Azizi, na aliuliwa kwa sababu hiyo! Na hii yamaanisha kuwa yeye alikuwa anasimama pamoja na Walidi bin Yazidi ambaye ni fasiki mno katika Bani Umayya! Wala sioni kuwa ni vigumu kuwa yeye ndiye aliyeiweka Hadithi hii ili kujilinda mbali na Walidi ambaye alikuwa amepitiliza katika maasi, lakini Hadithi hii inamfanya Walid anastahiki pepo kwa milango yake minane. Amesema: Amenihadithia Junadatu bin Abi Umayya, naye ni mtu wa Sham, na watu wa Sham hawakuwa watu wa Hadithi. Kisha yeye ni mtu wa Zahran, na wengi waliojishughulisha na Hadithi miongoni mwa watu wa Zahran huwa kati yao kuna la kuchunguzwa. Wao hukithirisha riwaya katika wasiyoyajua. Kisha yeye alikuwa miongoni mwa wasaidizi wa Muawiya na alimpa utawala wa eneo la Bahari! Na Muawiya alikuwa anapoighadhibikia kaumu ya watu huwahujumu kupitia Bahari. Na wakati mwingine Safina 96

Ahmadi alipoulizwa kumhusu alisema: “Hadithi dhaifu na rai dhaifu.’ Hayo aliyasema Dhahbi katika an-Nubalau katika wasifu wa al-Awzaiy ninavyo kumbuka, au katika wasifu wa Maliki. Wala Ahmad hakusudii kuwa al-Awzaiy ni dhaifu bali Hadithi zake ndio dhaifu. Na kuna tofauti kati ya haya mambo mawili, tusemapo: Hadithi yake ni dhaifu inamaanisha kuwa huwa anachukua kutoka kwa watu dhaifu au hutoa hoja kupitia Hadithi zisizo na sanadi na kazi za watu wa nchi yake... Hivyo udhaifu ni wa mtu mwingine, na yeye ni mnukuu wa udhaifu. Na pindi tusemapo yeye ni dhaifu, hii inamaanisha kuwa yeye ni chimbuko la udhaifu. 254

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 254

1/20/2016 11:35:59 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

hupinduka! Na hili halikuwa linatimia ila kwa ujuzi wa mtu huyu! Hivyo yeye alikuwa ni mahali anapopaamini Muawiya, na Muawiya hakumwamini ila aliye mtuhumiwa. Kutoka kwa Ubadatu bin Swamit, huyu ni Swahaba mkubwa aliyepigana Badru. Alikuwa katika ugomvi na Muawiya kwa ajili ya dhambi kama vile riba na kuuza pombe, hata kama atakuwa ni mwelezaji wa Hadithi hii hatotaja dhulma za Muawiya, atazifanyia udhuru kwa sababu yeye anadhihirisha imani katika mambo yote yaliyopita. Mungu amemtakasa Ubadatu bin Swamiti mbali na kueleza mfano wa Hadithi kama hii sembuse Rasuli 5. Tatu: Dosari kuu ya Hadithi hii ni Walidi bin Muslim. Yeye ni mtu wa Sham Damascus, ni miongoni mwa wapenzi wa Bani Umayya, na watu wa Sham hawakuwa watu wa Hadithi wala hawana umuhimu nazo. Kisha kuwa kwake huria wa Bani Umayya ni mahali pakudhaniwa kuwa yeye alikuwa ni Murjia. Kwa kweli Bani Umayya wamefanya vya kutosha kueneza itikadi ya jaala na majaliwa, na ya Irjai huko Sham. Na la muhimu zaidi kuliko haya yote na miongoni mwa yanayojulisha kuwa ni dosari ya Hadithi hii, ni kuwa yeye ni mtuhumiwa wa uwongo katika sanad, na yeye anaelezea Hadithi kutoka kwa waongo na walio dhaifu, kati yake na al-Awzaiy. Kisha pindi anapoelezea Hadithi anafuta majina yao na wakati mwingine anawafuta masheikh wa al-Awzaiy madhaifu, na mahali pao anawaweka wanaoaminika kwa kuwa yeye kwa dhana zake anamtakasa al-Awzaiy asionekane kuwa ameelezea Hadithi kutoka kwa madhaifu kama hawa na waongo kama wale. Na ametuhumiwa kuwa yeye ameiharibu Hadithi ya al-Awzaiy. Na hebu tuache waliyoyasema humo miongoni mwa uaminishaji wa jumla na tutaje waliyoyataja humo miongoni mwa dosari zake mahususi, Imamu Ahmad amesema: “Yeye ni mwenye makosa mengi.” “Na alikuwa mrushaji sana wa Hadithi.” 255

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 255

1/20/2016 11:35:59 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Mkazi mwenzake na mtu wa zama zake; Abu Mas’har ambaye ni mtu wa Damascus na ni mtu wa Sham, alisema: “Walidi alikuwa anachukuwa kutoka kwa Ibn Abiy Safar Hadithi za al-Awzaiy, na Ibn Abiy Safar ni mwongo, naye anasema katika hizo Hadithi kuwa: al-Awzaiy amesema.” Pia Abu Mas’har amesema: “Walidi bin Muslim alikuwa anahadithia Hadithi za al-Awzaiy azichukuazo kutoka kwa waongo kisha anaondoa majina yao.” Haythami bin Kharija alimwambia Walidi bin Muslim: “Kwa hakika umeiharibu Hadithi ya al-Awzaiy...” Kisha alimwambia vipi ilitokea hivyo, kuwa al-Awzaiy anaelezea Hadithi kutoka kwa madhaifu kutoka kwa watu mfano wa Zuhriy na Nafiu, kisha anakuja Walidi anawaondoa hao madhaifu kutoka kwenye sanadi. Walidi akasema kwa baridi ikiwa ni jibu la tuhuma hii ya hatari: “al-Awzaiy amejiona bora si wa kuelezea Hadithi kutoka kwa watu mfano wa hao.” Kisha Haythami alisema kuwa Walidi hakutilia manani nasaha yake. Daruqutni amenena kuwa: “Walidi bin Muslim anarusha Hadithi na anaelezea kutoka kwa al-Awzaiy Hadithi, ambazo kwa al-Awzaiy ni kutoka kwa masheikh madhaifu kutoka kwa masheikh ambao alAwzaiy aliwadiriki watu mfano wa Nafiu na Atau na Zuhriy, hivyo yeye Walidi huyadondosha majina ya madhaifu na kuifanya riwaya hiyo kuwa ni kutoka kwa al-Awzaiy kutoka kwa Nafiu, na kutoka kwa al-Awzaiy kutoka kwa Atau na Zuhriy...” Abu Daudi amesema: “Walidi bin Muslim ameelezea kutoka kwa Maliki Hadithi kumi ambazo hazina asili.” Nasema: Hiyo ni pamoja na kuwa yeye ni mtu wa Sham na Maliki ni wa Madina Mhijazi, vipi lau Maliki angekuwa wa Sham? Ni ngapi atazielezea kutoka kwake miongoni mwa Hadithi batili? Pia Abu Daudi amesema: “Baqiyat 256

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 256

1/20/2016 11:35:59 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

ana hali nzuri kuliko Walidi bin Muslim.” Na huyu Baqiyat alikuwa bingwa wa kubadili Hadithi kuliko wengine. Na al-Hafidh Ibn Hajar amesema: “Mwaminifu lakini ni mwenye kubadili Hadithi mno na kusawazisha.” Na amemuorodhesha katika kitabu cha wanaobadili Hadithi katika tabaka la nne miongoni mwao, nalo ni lile ambalo amekubali kuwa hatolei hoja kitu katika Hadithi zao ila kwa kile walichokieleza wazi kwa kusikia, kwa sababu ya kukithiri uwongo wao kutoka kwa madhaifu na wasiojulikana.” Nasema: Hadithi hii Walidi ameirefusha kwa kuongeza wasimuliaji, kwa hiyo kuna dhana ya kwamba imegeuzwa na kubadilishwa, wala haichukuliwi Hadithi kutoka kwa Walidi ila ile aliyoieleza wazi kwa kuhadithiwa. Dhahbi, japokuwa amekiri kuwa ubadilishaji wake (Walidi) wa hadithi ni mbaya, lakini amejaribu kumlinda Walidi na kumtetea dhidi ya ubadilishaji wa Hadithi, kwa madai yaliyoenea kwa waliokuja mwisho miongoni mwa wanahadithi kuhusu kila dhaifu aliyepokea Hadithi ndani ya Bukhari au Muslim, akasema: “Bukhari na Muslim wote wawili wamemfanya kuwa ni hoja, lakini wawili hao wanaitakasa Hadithi yake na wanajiepusha na yanayokataliwa kwa ajili yake.” Nasema: Ama madai ya kwamba Bukhari na Muslim wamemfanya kuwa ni hoja japokuwa kuna hizi dosari, hiyo ni dalili kwetu kuwa kuikosoa nidhamu ya ki-Hadithi ina uhalali wake ili kuuhami upande wa Nabii 5 asije kunasibishiwa asilolisema. Ama dhana ya Dhahbi kuwa Bukhari na Muslimu wanazitakasa Hadithi zake na kuiacha ambayo haikubaliki miongoni mwazo haya ni madai yanavunjwa na kuwepo kwa Hadithi hii yenyewe inayopingana na Qur’ani tukufu. Ni sahihi kuwa Bukhari na Muslim ni miongoni 257

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 257

1/20/2016 11:35:59 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

mwa wabora waliotunga katika Hadithi zilizo sahihi lakini akili ya Qur’ani - ikiwa ibara itakuwa sahihi – imekosekana kabisa miongoni mwa watu wa Hadithi, ndio maana wanaieleza Hadithi kama hii...­ ambayo madhumuni yake hayasemi Mwislamu yeyote si mwanahadithi wala Muutazilu wala Wahabi wala walio kinyume nao. Halafu vipi tukate shauri kuwa Bukhari na Muslim kuwa wanachuja kabisa uchafu na tusahau kuwa wao wanaweza wakakabiliwa na wazo na wakadhania kuwa Hadithi fulani ni miongoni mwa Hadithi sahihi za fulani, ilihali haiko hivyo! Hapana budi kuwe na uthibitisho.

MUHTASARI: Hadithi hii ambayo Bukhari ameieleza lakini Muslim kajiepusha nayo ni Hadithi batili sio sahihi kuinasibisha na Nabii 5 kwa sababu ya kuhitilafiana kwake kiasili na Qur’ani tukufu na udhaifu wake wa sanad. Halafu wote ambao Sheikh anawakufurisha wanashuhudia shahada mbili na wanaamini vipengele vyote vilivyo katika Hadithi hii. Na kama mtu huyu atakuwa mwenye kulazimiana na sharti zao katika kuthibiti Tawhidi, lakini yeye anazifanyia taawili sifa au aona inafaa kutabaruku na kutawasuli kwa watu wema, au anaona kuwa Ali ni bora kuliko Abu Bakri au mfano wa haya; wanamfanya kuwa ni mwanabidaa na kumtuhumu kuwa ni Jahmiyyah au ni afanyaye shirki au ni Rafidhu, kwa hiyo vipengele vilivyotajwa katika Hadithi hii hawalazimiani navyo, na kuifunga dini kwenye hivyo ni makosa, kwa sababu hivyo vinaambatana na imani ya tamko la ulimi na la kimoyo na si kitendo. Na hii ni Irjau ambayo hao wanailaumu lawama kali, bali baadhi ya Masalafi wa zama hizi wametoa udhuru kuhusu Mahanbali kumkufurisha Abu Hanifa kwa kudhania kwao kuwa ndani ya yeye kuna aina fulani ya Irjau. Na Irjau ya Ahlus 258

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 258

1/20/2016 11:35:59 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

sunna wa Iraki ilikuwa inamaanisha kujiepusha mbali na kukufurisha kwa jumla... sio kama Irjau ya watu wa Sham ifuatayo mamlaka na ni yenye kuihalalisha. Na Irjau ya watu wa Kufa ambao miongoni mwao ni Abu Hanifa, ni yenye nafuu sana kuliko Irjau ya watu wa Sham, wao ni Murjiah wa asili, kwani Irjau yao ni mbaya zaidi.

MWISHO: Huu ni mfano wa kukosoa kitabu Tawhid cha Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahabi Mwenyezi Mungu amrehemu. Ukosoaji huu sijaukamilisha, na sikutaka kibakie rehani ndani ya mahabusu tano! Nikasema ninasambaza kiasi kilichokamilika kwa sababu ya faida iliyo humo, na kwa ajili ya kuondoa dhana ya baadhi ya watu kuwa kitabu cha Tawhid cha Sheikh Muhammad hakijiwi na batili mbele yake wala nyuma yake.97 Na huenda nikapata katika wasomaji atakayenishajiisha nikitimize, kwa sababu mimi niko katika fikra mtawanyiko katika utafiti huu na huenda nisiweze kukamilisha utafiti mmoja wapo. Mungu amsamehe Sheikh Muhammad na wafuasi wake na awasamehe wapinzani wake miongoni mwa wanazuoni wa Kiisla97

  Na wao wanakifanyia hivi kila kitabu wakionacho kinaunga mkono lile walilonalo, miongoni mwa ufurutu ada au ukufurishaji au chuki binasi dhidi ya Ahlulbayti au kumfanya Mungu kuwa ni mwili. Kama walivyokifanyia sifa kubwa kitabu as-Sunnah cha al-Barbahariy japokuwa kina ufurutu ada mkubwa. Na wamekifanyia hivyo kitabu Minhajus-Sunnah cha Ibn Taymiya japokuwa kina chuki binasi dhidi ya Ahlulbayti ya kufadhaisha ambayo imedhihiri katika kitabu hiki. Na wamevifanyia hivyo vitabu vya Itikadi vya kihanbali vya zamani kwa kuwa ndani yake mna U-Hashawiy na kumfanya Mungu kuwa ni mwili. Na wamevifanyia hivi vitabu vya Sheikh Muhammad kwa kwenda kwake mwendo wa ukufurishaji. Na natija ikawa ni kuwa mbali na maamuzi ya kisharia iliyo nyoofu, na kuvifanya vitabu hivyo ndio rejea katika kuwahukumu watu. Kwa hiyo Waislamu wasio wao wamekuwa kati ya aliye kafiri na aliyeritadi, aliyeukana Uislamu na mpotevu. Na wao wanadhania kuwa wanatenda mema. Na ushirikiano wao huu pamoja na kuwepo kwa anayewasikiliza kwa nguvu katika jamii yetu ni ushahidi wa hatia. 259

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 259

1/20/2016 11:35:59 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

mu na watu wa kawaida na awajumuishe wote katika rehma Yake. Na Mungu amrehemu Muhammad na Aali Muhammadi kama alivyomrehemu Ibrahim na Aali Ibrahim kwani yeye ni Msifika Mtukufu. Ameandika: Hasan bin Farhan al-Makki Siku ya Jumanne, 11 Jamadul-Awwal, 1425 A.H. Riyadh, Saudi Arabia.

260

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 260

1/20/2016 11:35:59 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

Orodha Ya Vitabu Vilivyo ­Chapishwa Na Al-Itrah Foundation 1. i) Qur’ani Tukufu — Pamoja na Tarjuma ya Kiswahili ii) Qur’an Al-Kariim — Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Thelathini 2. Uharamisho wa Riba 3. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza 4. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili 5. Hekaya za Bahlul 6. Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) 7. Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (a.s.) 8. Hijab vazi Bora 9. Ukweli wa Shia Ithnaashari 10. Madhambi Makuu 11. Mbingu imenikirimu 12. Abdallah Ibn Saba 13. Khadijatul Kubra 14. Utumwa 15. Umakini katika Swala 16. Misingi ya Maarifa 17. Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia 18. Bilal wa Afrika 19. Abudhar 20. Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu 21. Salman Farsi 22. Ammar Yasir 23. Qur’an na Hadithi 24. Elimu ya Nafsi 25. Yajue Madhehebu ya Shia 26. Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur’an Tukufu 261

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 261

1/20/2016 11:35:59 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

27. Al-Wahda 28. Ponyo kutoka katika Qur’an 29. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii 30. Mashukio ya Akhera 31. Al Amali 32. Dua kwa Mujibu wa Ahlulbayt (a.s) 33. Udhuu kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna 34. Haki za wanawake katika Uislamu 35. Mwenyezi Mungu na sifa zake 36. Kumswalia Mtume (s) 37. Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) 38. Adhana 39. Upendo katika Ukristo na Uislamu 40. Qur’ani na Kuhifadhiwa Kwake 41. Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu 42. Kupaka juu ya khofu 43. Kukusanya Sala Mbili 44. Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara 45. Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya 46. Kusujudu juu ya udongo 47. Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s) 48. Taraweheas 49. Malumbano baina ya Sunni na Shia 50. Kupunguza Swala safarini 51. Kufungua safarini 52. Umaasumu wa Manabii 53. Qur’an Yatoa Changamoto 54. as-Salaatu Khayrun Mina -’n Nawm 55. Uadilifu wa Masahaba 56. Dua e Kumayl 57. Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu 262

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 262

1/20/2016 11:35:59 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

58. Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake 59. Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata 60. Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mtume Muhammad (s) 61. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza 62. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili 63. Kuzuru Makaburi 64. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza 65. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili 66. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu 67. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne 68. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano 69. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita 70. Tujifunze Misingi Ya Dini 71. Sala ni Nguzo ya Dini 72. Mikesha Ya Peshawar 73. Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu 74. Ubora wa Imam ‘Ali na Ushia ndio njia iliyonyooka 75. Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake 76. Liqaa-u-llaah 77. Muhammad (s) Mtume wa Allah 78. Amani na Jihadi Katika Uislamu 79. Uislamu Ulienea Vipi? 80. Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) 81. Dhana ya Ndoa ya Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) 82. Urejeo (al-Raj’ah) 83. Mazingira 84. Utokezo (al - Badau) 85. Hukumu ya kujenga juu ya makaburi 86. Swala ya maiti na kumlilia maiti 87. Uislamu na Uwingi wa Dini 88. Mtoto mwema 263

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 263

1/20/2016 11:35:59 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

89. Adabu za Sokoni Na Njiani 90. Johari za hekima kwa vijana 91. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza 92. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili 93. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu 94. Tawasali (AT- TAWASSUL) 95. Imam Mahdi katika Usunni na Ushia 96. Hukumu za Mgonjwa 97. Sadaka yenye kuendelea 98. Msahafu wa Imam Ali 99. Maimamu wa Ahlul Bait – Ujumbe na Jihadi 100. Idi Al-Ghadir 101. Kusoma sura zenye Sijda ya wajibu 102. Hukumu zinazomuhusu mkuu wa kazi na Mfanyakazi 103. Huduma ya Afya katika Uislamu 104. Sunna za Nabii Muhammad (saww) 105. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza) 106. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili) 107. Shahiid Mfiadini 108. Mwanamke Na Sharia 109. Ujumbe -Sehemu ya Kwanza 110. Ujumbe - Sehemu ya Pili 111. Ujumbe - Sehemu ya Tatu 112. Ujumbe - Sehemu ya Nne 113. Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu 114. Hadithi ya Thaqalain 115. Ndoa ya Mutaa 116. Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza 117. Ukweli uliopotea sehemu ya Pili 118. Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu 119. Ukweli uliopotea sehemu ya Nne 264

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 264

1/20/2016 11:35:59 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

120. Ukweli uliopotea sehemu ya Tano 121. Mkutano wa Maulamaa wa Baghdad 122. Safari ya kuifuata Nuru 123. Fatima al-Zahra 124. Myahudi wa Kimataifa 125. Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi 126. Visa vya kweli sehemu ya Kwanza 127. Visa vya kweli sehemu ya Pili 128. Elimu ya Ghaibu ya Maimamu 129. Mwanadamu na Mustakabali wake 130. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Kwanza) 131. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Pili) 132. Khairul l’Bariyyah 133. Uislamu na mafunzo ya kimalezi 134. Vijana ni Hazina ya Uislamu 135. Adhana ni Ndoto au ni Wahyi? 136. Tabaruku 137. Saada Kamili – Kitabu cha Kiada cha Maadili 138. Vikao vya furaha 139. Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje? 140. Visa vya wachamungu 141. Falsafa ya Dini 142. Kuhuzunika na Kuomboleza 143. Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah 144. Mjadala wa Kiitikadi 145. Kuonekana kwa Allah 146. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza) 147. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili) 148. Ndugu na Jirani

265

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 265

1/20/2016 11:35:59 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

149. Ushia ndani ya Usunni 150. Maswali na Majibu 151. Mafunzo ya hukmu za ibada 152. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 1 153. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 2 154. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 3 155. Abu Huraira 156. Vipengee kadhaa katika Swala ya Jamaa na Msikiti. 157. Mazingatio kutoka katika Qur’an - Sehemu ya Kwanza 158. Mazingatio kutoka kaitka Qur’an - Sehemu ya Pili 159. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya kwanza 160. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya Pili 161. Shia na Qur’ani – Majibu na Maelezo 162. Falsafa ya Mageuzi ya Imam Husein (a.s) 163. Amali za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani 164. Elimu ya Tiba za Kiislamu - Matibabu ya Maimamu 165. Uislamu Safi 166. Majlisi za Imam Husein Majumbani 167. Je, Kufunga Mikono 168. Uislam wa Shia 169. Amali za Makka 170. Amali za Madina 171. Asili ya Madhehebu katika Uislamu 172. Sira ya Imam Ali kuhusu Waasi 173. Ukweli uliofichika katika neno la Allah 174. Uislamu na Mifumo ya Uchumi 175. Umoja wa Kiislamu na Furaha 176. Mas’ala ya Kifiqhi 177. Jifunze kusoma Qur’ani 178. as-Sahifatul Kamilah as-Sajjadiyyah 179. Hayya ‘Alaa Khayri’l-’Amal Katika Adhana 266

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 266

1/20/2016 11:35:59 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

180. Ukweli kuhusu Funga ya Siku ya Ashura 181. Dua za Miezi Mitatu Mitukufu (Rajabu, Shaabani na Ramadhani) 182. Uadilifu katika Uislamu 183. Mahdi katika Sunna 184. Maswali Ya Uchunguzi Kuhusu Uislam 185. Kazi na Bidii ni njia ya maendeleo 186. Abu Talib – Jabali Imara la Imani 187. Ujenzi na Utakaso wa Nafsi 188. Vijana na Matarajio ya Baadaye 189. Historia maana na lengo la Usalafi 190. Ushia – Hoja na Majibu 191. Mateso ya Dhuria wa Mtume (saww) 192. Maombolezo – Msiba wa Bwana wa Mashahidi (a.s.) 193. Shahidi kwa Ajili ya Ubinadamu 194. Takwa 195. Upotoshaji Dhahiri katika (Turathi) Hazina ya Kiislamu 196. Amirul Muuminina (as) na Makhalifa 197. Tawheed Na Shirki 198. Kuvunja hoja iliyotumika kutetea Uimamu wa AbuBakr 199. Adabu za vikao na mazungumzo 200. Hija ya Kuaga 201. Uwazi baina ya Maslahi na Vikwazo 202. Fadhila za watukufu watano katika Sahih Sita 203. Mdahalo baina ya Mwanachuoni wa Kisunni na Kishia (Al- Muraja’aat) 204. Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (as) 205. Imam Husain ni Mfumo wa Marekebisho na Mageuzi 206. Mtazamo kuhusu msuguano wa Kimadhehebu 207. Nchi na Uraia – Haki na wajibu kwa Taifa 208. Mtazamo wa Ibn Taymiyyah juu ya Imam Ali (as) 209. Uongozi wa Kidini – Maelekezo na Utekelezaji wa Kijamii 210. Maadili ya Ashura 267

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 267

1/20/2016 11:35:59 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

211. Mshumaa – Shahidi na Kifo cha Kishahidi 212. Mizani ya Hekima – Hadithi za Ahlul Bait (as) – Sehemu ya Kwanza 213. Imam Ali na Mambo ya Umma 214. Imam Ali na Mfumo wa Usawa 215. Uimamu na Tamko la Kutawazwa 216. Mfumo wa Wilaya 217. Vipi Tutaishinda Hofu? 218. Kumswalia Mtume ni Ufunguo wa Utatuzi wa Matatizo 219. Maeneo ya Umma na Mali Zake 220. Nahju ‘L-Balagha – Majmua ya Khutba, Amri, Barua, Risala, Mawaidha na Semi za Amirul-Muuminin Ali bin Abu Talib (a.s.) 221. Mukhtar – Shujaa aliyelipiza kisasi dhidi ya wauaji wa Imam Husein (as) hapo Karbala 222. Mazingatio Katika Swala 223. Imam Hasan na Mfumo wa Kujenga Jamii 224. Vyakula Na Vinywaji 225. Kuelewa Rehema ya Mwenyezi Mungu 226. Imam Mahdi na Bishara ya Matumaini 227. Mtazamo Mpya - Wanawake katika Uislamu 228. Shia Na Sahaba - Majibu na Maelezo 229. Majanga Na Jukumu la Jamii 230. Shia Na Hadith - Majibu na Maelezo 231. Upotofu Ndani ya Kitabu cha Mitaala kwa Shule za Sekondari 232. Ugaidi Wa Kifikra Katika Medani Ya Kidini 233. Yafaayo kijamii 234. Uswalihina Dhahiri Na Batini Yake 235. Mkakati wa Kupambana na Ufakiri 236. Mwanamke Katika Harakati Za Mageuzi 237. Jihadi 238. Hija Katika Maneno Na Ujumbe Wa Imam Khomeini (R.A) 239. Tiba Ya Maradhi Ya Kimaadili

268

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 268

1/20/2016 11:35:59 AM


NI MWANADAAWA, SI NABII

240. Yusuf Mkweli 241. Taqiyya Kwa Mujibu Wa Sheria Ya Kiislamu 242. Imam Mahdi (A.S) Imam Wa Zama Hizi Na Kiongozi Wa Dunia 243. Talaka Tatu 244. Safari Ya Kuelekea Kwa Mwenyezi Mungu 245. Hotuba Za Kisslamu Juu Ya Haki Za Binadamu 246. Mashairi Ya Kijamii 247. Ngano Ya Kwamba Qur’ani Imebadilishwa 248. Wito Kwa Waumini: “Enyi Mlioamini” 249. Imam Husain (a.s) ni Utu na Kadhia 250. Imam Husain ni Kielelezo cha Kujitoa Muhanga na Fidia

269

15_15_Mwana Dawaa _20_Jan_2016.indd 269

1/20/2016 11:35:59 AM


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.