Sadaqatul jariyah

Page 1

SADAQATUL JARIYAH SADAKA YENYE KUENDELEA

Kimeandikwa na: Kimeandikwa na: Al-Qazwini Muhammad Ibrahim Al-Muwahihd Muhammad Ibrahim Al-Muwahda Al-Qazuwiniy

Kimetarjumiwa na: Abdul-Karim J. Nkusui


©Haki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: 978 - 9987 - 17 - 005 - 0

Kimeandikwana: na: Kimeandikwa Muhammad IbrahimAl-Muwahda Al-MuwahihdAl-Qazuwiniy Al-Qazwini Muhammad Ibrahim Kimetarjumiwa na: Abdul - Karim J. Nkusui Kimepangwa katika Kompyuta na: Ukhti Pili Rajab Toleo la kwanza: Machi, 2014 Toleo la kwanza: Novemba, 2013 Nakala: 1000 1000 Nakala: Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 / 2127555 Barua Pepe: alitrah@yahoo.com Tovuti: www.ibn-tv.com Katika mtandao: www.alitrah.info Kwa kushirikiana na: Ahlul Bayt (‘a) Charitable Committee, Ahlul Bayt (‘a) Centre (ABC) S.L.P. – 7169, Arusha, Tanzania


YALIYOMO Sadaka ni nini?............................................................................................2 Hivyo ni kitu gani kinamnufaisha Mwanadamu.........................................4 Elimu yenye manufaa..................................................................................4 Sadaka yenye kuendelea..............................................................................6 Kuhuisha utajo wa Ahlul Bayt (a.s)............................................................8 Kufanya maombolezo ya Imam Husein......................................................9 Hadithi Tukufu kuhusiana na sadaka yenye kuendelea...........................16 Imam Ali na Sadaka yenye kuendelea......................................................22 Al-Imamul -Hussan na Sadaka yenye kuendelea......................................30 Imamul - Husein (a.s) na Sadaka yenye kuendelea...................................31 Imamu Zainul - Abidiyn (a.s) na Sadaka yenye kuendelea......................33 Al-Imamu Swadiq (a.s) na Sadaka yenye kuendelea................................34

Miongoni mwa athari za Sadaka duniani na Akhera Zinazima ghadhabu ya Mola Mlezi ..........................................................35 Huleta baraka ...........................................................................................36 Ni ponyo kwa mgonjwa ...........................................................................37 Inafuta Qudhwaa na Qadari ......................................................................37 Huongeza umri..........................................................................................38 Huondoa balaa...........................................................................................38

Ama Athari za Sadaka katika Akhera na kutajia baadhi yake Hutakasa maovu..............................................................................39 Huzuia Moto....................................................................................39 Zitakuwa kivuli siku ya Kiyama......................................................40 Katika adabu za Sadaka...................................................................40 Kuiona kuwa ni ndogo.....................................................................40 Kuifanya kwa siri.............................................................................40 Kuifanya haraka kuitoa....................................................................41


Neno la Mchapishaji Kitabu kilichoko mikononi mwako, ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabu, kwa jina la: "Sadaqatul Jariyah" Sisi tumekiita "Sadaka ya kuendelea" kilichoandikwa na: Jumuiya ya Maarifa na Utamaduni wa Kiislamu. Sadaka ni kitu ambacho kimekokotezwa sana katika Uislamu ambayo pamoja na Zaka lengo lake kubwa ni kwa ajili ya ustawi wa jamii. Zaka pia ni Sadaka, lakini tofauti na sadaka ambayo ndio mada ya kitabu hiki Zaka hutolewa na wenye mali mahususi kwa viwango maalumu na hutolewa wakati maalumu na kwa lengo hilohilo. Kuhusu sadaka ya kuendelea ambayo anwani ya kitabu hiki imekokotezwa sana na imepokewa hadithi kutoka kwa Mtukufu Mtume (saw) akisema: “Anapofariki mwanadamu matendo yake yote hukatika isipokuwa matatu; 1) Sadaka yenye kuendelea; 2) Elimu yenye manufaa na 3) Mtoto mwema mwenye kuwaombea wazazi wake”. Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu ambapo maadili ya Uislamu (yaani Amr Bil Ma’ruf na Nahi Anal Munkar) yamepuuzwa kwa kiasi cha kutisha. Kutokana na ukweli huo, Taasisi yetu ya 'Al-Itrah Foundation' imeona ikitoe kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili, kwa madhumuni yake yale yale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili. TunamshukuruSheikh AmiriAbdul-Karim Mussa Kea.kwa jukumu hili la kukifanyia Tunamshukuru Jumakukubali Nkusui. Kwa kukubali jukumu hili la tarjuma kitabu hiki. Vile vile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa kukifanyia ­tarjuma kitabu hiki. Vile vile tunawashukuru wale wote w ­ alioshiriki njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwa kitabu hiki. kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwa kitabu hiki. Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa ni chenye manufaa na Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa ni chenye manufaa ­na changachangamoto kubwa kwa wasomaji wetu. moto kubwa kwa wasomaji wetu. Mchapishaji: Al-Itrah Foundation Mchapishaji: Al-Itrah Foundation


“Mali na watoto ni mapambano ya maisha ya Dunia na mema yaliyobaki ni bora mbele ya Mola wako kwa malipo na ni mategemeo mema.” “Hakika sisi tunafufua wafu na tunaandika waliyoyatanguliza, athari zao na kila kitu tumekiandika katika kitabu kikuu.”


UTANGULIZI Vitendo anavyovifanya mwanadamu - ni sawa viwe vyema au viovu – vinagawanyika katika sehemu mbili:Kwanza : Vitendo vya muda maalumu na wakati maalumu Pili: Vitendo ambavyo vinabaki kwa muda mrefu vinavyovuka mipaka ya wakati Mfano: Unaweza kumlisha fakiri chakula na kuondoa njaa yake kwa masaa kadhaa kisha anarejea katika hali ya njaa tena. Na unaweza kumshtumu mwislam – Mungu apishe mbali hayo – na kujeruhi hisia zake kisha unamtaka radhi na kumuomba msamaha, kitendo cha awali ni chema kilichotokea kwako na una malipo kwa Mwenyezi Mungu na una daraja nyingi Kwake. Na cha pili ni kiovu kilichotokea kwako na utahisabiwa kwacho Siku ya Kiyama isipokuwa akikusamehe ndugu yako mwislamu, na ukamuomba Mola wako maghfira na akakusamehe. Hii ndio sehemu ya kwanza. Na unaweza kutoa sadaka kwa ajili ya kuchapisha kitabu cha dini kinachozungumzia juu ya Ahlul–Bayt na fadhila zao, Uimamu wao na utukufu wa shakhsiya yao, au kitabu kinachotatua tatizo la kijamiii - kama vile kutovaa hijabu na kutembea kichwa wazi – au kinacholingania kheri na kumtii Mwenyezi Mungu n.k. Kitabu hicho kikaenea mashariki na magharibi na kikaingia kila nyumba na kubadalisha maisha ya mamia bali maelfu ya watu na kuwaongoza katika njia ya sawa na kikabaki miaka na miaka.


Au anajenga – Mwenyezi Mungu apishe mbali - jengo la sinema kwa ajili ya kuonyesha filamu chafu, kusambaza uovu na ufisadi baina ya wanajamii, au kusambaza majarida ya uovu au kitabu cha kupotosha n.k. Haya yote yako katika sehemu ya pili. Ama ya kwanza – ambayo ni kuchapisha vitabu vya kidini mathalan – na kubaki karne nyingine na kuongoa mamia ya watu. Na hivyo kinakuwa ni kizuizi baina yako na moto na kuendelea kukufikia amali njema hali ya kuwa wewe uko akhera. Kama ambavyo kitendo cha pili cha kujenga jengo la sinema, kusambaza majarida na vitabu vya upotovu kwa mfano – na vitabu vinabaki muda mrefu vikieneza sumu na upotovu katika jamii - wewe utalipa gharama na fidia hali ya kuwa uko katika kaburi lako, utapata kichapo cha viboko vya moto kutoka kwa malaika wa adhabu vyenye kuumiza. Na kitabu hiki pamoja na udogo wake – kinazungumzia sadaka yenye kuendelea ambayo manufaa yake yananufaisha wakati wote kwa idhini ya Mola wake. Nimekiandika kwa kuitikia wito wa baadhi ya ndugu zangu watukufu ili kiwe ni hatua njema katika kuwapa watu moyo wa kuanzisha taasisi za kidini, markazi za kheri na kufanya vitendo vyema ambavyo ni vyenye manufaa na faida, na ambavyo vitaendelea kumpatia thawabu aliyevifanya. Namuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu anikubalie juhudi hii ndogo na aipokee kwa mapokezi mema na awape tawfiki ndugu zangu ambao wanalingania kheri na kuamrisha mema na kukataza maovu. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia dua na ni Mwenye kujibu maombi. Na wa kuwafikisha ni Mwenyezi Mungu, Kwake nimetegemea na Kwake narejea. Al-Qazwini Muhammad Ibrahim Al-Muwahhid al-Muwahda Al-Qazuwiniy 15 Sha’abani 15 Sha’abani 1414 1414 AH. AH. i


ii



Sadaka yenye kuendelea

Sadaka ni nini? Baadhi wanaweza kufikiri kwamba sadaka ni ile mali chache ambayo mwanadamu anaitoa kwa fakiri mwombaji aliyekaa kando ya njia au katika mlango wa msikiti. Lakini hii ndio maana pekee ya sadaka? Jawabu: Hapana, hakika sadaka inatokana na neno “taswidiyq� na maana ya hilo ni kumsadikisha Mwenyezi Mungu, Siku ya Kiyama, malipo makubwa na kutokuwa na shaka katika hilo abadani. Hii ndio maana ya sadaka. Hivyo kila kitendo kinachotokea kwako na kwa ajili ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ni sadaka, kwa sababu kinatokana na imani yako kwa Mwenyezi Mungu, maneno yake na ya Mitume Wake. Na miongoni mwa maana za sadaka zinazofahamika zaidi ni sadaka ya kimali, na zimepokelewa Aya nyingi za Qur’ani na hadithi nyingi tukufu vile vile. Tumeshasema kwamba sadaka ya mali inagawanyika sehemu mbili:Sadaka ya muda mfupi Sadaka yenye kuendelea Na mazungumzo yetu katika kitabu hiki yanajikita juu ya sadaka yenye kuendelea, isipokuwa sisi pia tutaelezea kuhusu sadaka ya mali ya muda mfupi, vile vile kuhusiana na athari nzuri zinazopatikana kwazo kama ilivyopokelewa katika hadithi tukufu.

2


Sadaka yenye kuendelea

Kitu gani kitakunufaisha baada ya kufa? Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww): “Anapokufa mwanadamu amali yake inakatika isipokuwa vitu vitatu: Elimu wanayonufaika watu kwayo Au sadaka yenye kuendelea Au mtoto mwema anayewaombea maghfira wazazi wake” Hakika watu – mara nyingi wanawaachia wanaokuja baada yao mali, utajiri, manyumba, ardhi n.k. Hivyo vinahamia kwa warithi wananeemeka kwavyo na wanavitumia wanavyotaka. Na mali hii wakati mwingine huwa ni majuto dhidi yao huko akhera na wakati mwingine huwa ni maangamio ambapo haiwanufaishi huko bali huwasimamisha mbele ya mahakama adilifu ya Mwenyezi Mungu kwa ajili ya hesabu. Alikufa mmoja wa matajiri – na mimi ninamfamu - akaacha utajiri mwingi sana kisha rafiki yake akamuona katika ndoto hali ya kuwa uso wake umeshakuwa mweusi akiwa amekaa katika chumba kilichoharibika na akiwa amevaa mavazi yaliyochakaa. Rafiki yake alipozinduka usingizini akamwendea mmoja wa maulamaa wa kidini na akamsimulia ndoto yake. Akamwambia: Hakika maana iko wazi. Hakika huyu mtu alipuuza akhera na hakutanguliza chochote kwa ajili ya maisha hayo yenye kubaki na kwa sababu hii anaishi katika gofu kama ilivyo hali ya mafakiri ambao wanaishi katika nyumba zilizochakaa na hawana tandiko isipokuwa mchaga. Mwenyezi Mungu alimruzuku mali duniani na hakuitoa katika twa’a ya Mwenyezi Mungu na kujichumia daraja zake, na kwa sababu hiyo uso wake umekuwa mweusi mbele ya Mwenyezi Mungu, anaishi maisha ya majuto na masikitiko. Na hii vile vile ni maana ya nguo zilizochakaa, hakika mavazi yanapokuwa mazuri ya fahari – basi huo ni uzuri wa 3


Sadaka yenye kuendelea mwanadamu, na yakiwa yamechakaa basi - aghalabu yanaonyesha ufakiri na kutokuwa na kitu, na mtu huyu ingawa alikuwa tajiri duniani – ila ni fakiri kesho akhera. Na katika hadithi inayotoka kwa Imamu Ali Amirul-Muumina (as) amesema: “Anapokufa mwanadamu watu wanasema: Ameacha nini? Na malaika wanasema: Ametanguliza nini?”

Hivyo ni kitu gani kinamnufaisha mwanadamu akhera? Jawabu: Hakika hadithi tukufu ya Mtume (saww) iliyotajwa inatilia mkazo juu ya mambo matatu yanayobaki baada ya kufa mwanadamu, yanayodumisha jina lake, yanayohuisha utajo wake na yanaipelekea roho yake fungu la kheri, rundo la mema na daraja kubwa. Katika yafuatayo tunaashiria kwa ufafanuzi zaidi:-

Elimu yenye manufaa Na hiyo ni kama mfano wa kitabu ambacho kinakusanya – katika maandiko yake na kurasa zake – Elimu ya Muhammad na kizazi cha Muhammad miongoni mwa wanayonufaika watu kwayo na kuzipa nyoyo uhai. Kitabu kinahuisha nyoyo kama maji yanavyohuisha ardhi kame, kitabu kinachobaki na kuwa taa yenye kuwaka, taa yenye kuangaza kinaangaza njia kwa wenye kupotea, kuongoza majahili na kuwazindua walioghafilika. Ni vitabu vingapi vimeokoa watu kutokana na upotovu na kuwapeleka katika njia ya uongofu? Ni vitabu vingapi vimerekebisha dhamira za watu na kubadilisha mwelekeo wa maisha yao na kuyafanya kuwa mazuri zaidi? Ni vitabu vingapi vimesambaza tabia njema na adabu nzuri baina ya watu? Na ni vitabu vingapi vimerekebisha itikadi za watu na kuwapambanulia 4


Sadaka yenye kuendelea haki na batili? Kitabu hiki kinamdundulizia maiti malipo yenye kuendelea na thawabu za Mwenyezi Mungu zisizo na kikomo. Hakika baina yetu – hivi sasa kuna utunzi mwingi ambao maulamaa wetu watukufu (R.A) wameuandika na umekusanya maarifa, hukumu na mengineyo, navyo vinahuisha utajo wao na vinadumisha majina yao hao. Imekuja katika hadithi tukufu: “Mwenye kuacha karatasi yenye elimu basi itakuwa ni kinga baina yake na moto” Kitabu cha kidini kinampa mwenye kukiandika kinga kutokana na moto na kinatengeneza kizuizi imara baina yake na Jahannam. Na huenda miongoni mwa maana ya hadithi hii tukufu ni kwamba watu wanaongoka kwenye haki kwa sababu ya kitabu chake, hivyo wanamuombea rehema na maghfira, na hivyo anapata rehema ya Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu hubadilisha maovu yake kuwa mema na huko ndiko kufaulu kukubwa. Lakini wako wapi matajiri na wahazini wa mali? Anasema Imamu Ali (as): Wameangamia wahazini wa mali hali ya kuwa wako hai na Maulamaa ni wenye kubaki maadamu dunia ingalipo.” Na msomaji anaweza kusema mimi si miongoni mwa Maulamaa wala si miongoni mwa watunzi na waandishi, je nitanyimwa thawabu hizi? Jawabu: Hakika mbele yako kuna njia tatu unaweza kuzitumia, kwanza kuisajili nafsi yako na kuifanya idumu na kupata utajo mwema, na hii ni mojawapo. Kwa kuongezea ni kwamba unaweza kuchangia katika kuchapisha vitabu vya kidini vyenye kunufaisha na vile vile katika kuvisambaza ili ushirikiane na mtunzi katika kheri, malipo na thawabu. Na katika hadithi tukufu: “Yasiyowezekana yote basi hayaachwi yote.” 5


Sadaka yenye kuendelea

Sadaka yenye kuendelea Sadaka yenye kuendelea ni amali ya kheri yenye thawabu zenye kuendelea ambayo inabaki kama mti wenye matunda ambao unatoa matunda yake wakati wote kwa idhini ya Mola Wake Na Msikiti, Huseiniyah, taasisi, miradi ya kheri, maktaba, madrasa za kidini, nyumba za kulelea yatima na wazee ni miongoni mwa maana na tafsiri inayoonekana wazi, ya sadaka yenye kuendelea. Na katika ufafanuzi wa ziada na kukamilisha si vibaya kutaja maelezo mafupi kuhusu mambo haya.

1- Misikiti:Misikiti ni nyumba za Mwenyezi Mungu katika ardhi, na ni kati ya sehemu takatifu zaidi na tohara zaidi, nazo ni nyumba ambazo “Mwenyezi Mungu ameruhusu zijengwe na kutajwa humo Jina Lake, na humo wanamtukuza asubuhi na jioni watu ambao hawashughulishwi na biashara wala mali katika utajo wa Mwenyezi Mungu, kusimamisha swala, kutoa zaka wanaogopa siku ambayo humo macho na nyoyo vitageuzwa.’ Uislam unalingania kujenga Misikiti na kuiimarisha na kujaalia kuwa kuimarisha Miskiti ni kati ya alama za imani. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Hakika wanaimarisha Misikiti ya Mwenyezi Mungu wale waliomwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho.” (Sura Tawba: 18) 6


Sadaka yenye kuendelea Na imepokewa kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) kwa madhumuni yake kwamba: “Mwenye kujenga msikiti duniani Mwenyezi Mungu atampa kwa kila shibiri au kwa kila dhiraa mji peponi.”1 Na anasema Al–Imam Al-Baqir (as): “Mwenye kujenga msikiti hata kama ni mdogo sana kama vile shimo la mdudu Mwenyezi Mungu atamjengea nyumba peponi.”2 Shimo la mdudu ni sehemu ambayo anaifukua mdudu ndani ya ardhi ili atage humo. Shahidut-Thani anasema katika Sharhi ya Lumu’ah Uk, 214: “Na kufananishwa nayo ni upeo wa juu wa kupita kiasi katika udogo, kwani anaweza kutosheka tu na mchoro wake ambapo anaweza akanufaika kwa ule mchoro, na hilo ni daraja la chini la manufaa hata kama hakujenga ukuta na mfano wake.” Anasema Abu Ubaidah Al-Hadhai: “{Alipitia kwangu Abu Abdillah Aswadiq (as) kwenda Makka na hali nimekwishajenga msikiti wa mawe, nikasema nijaaliwe kuwa fidia yako je, nataraji kuwa hii itakuwa sawa na ile? Akasema (as) ndio.” Yaani natarajia msikiti huu mdogo – ambao unafanana na nyumba ya mdudu utakubaliwa mbele ya Mwenyezi Mungu na mimi nitakuwa na nyumba peponi? Hakika hadithi hii inaonyesha namna Uislam unavyowashajihisha watu kujenga misikiti na kuiimarisha vyovyote litakavyo kuwa jengo lake rahisi na la thamani ndogo, na vyovyote utakavyo kuwa mdogo. Hakika misikiti ni vituo vya msingi kwa ajili ya ibada, malezi, waadhi na kuongoza, na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) aliufanya msikiti wake wa Madina kuwa ni kituo cha harakati za Uislam, kufundisha hukumu, kufasiri Qur’ani, kupanga jeshi, kuandaa askari, kusaidia mafakiri na mengineyo kati ya mambo ya Kidini. 1 Wasailus Shi’ah, Juz: 2, uk. 486 2 Wasailus Shi’ah, Juz: 2, uk. 486

7


Sadaka yenye kuendelea Na utaona – katika mji wa Madina – Misikiti mingi ambayo masahaba waliijenga, tabiina na wengineo kwa kuongezea Misikiti ambayo aliijenga Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) kama vile Masjid Qubaa, Masjid Ghamamah, Masjid Imam Ali bin Abi Talib, Masjid Fatmatuz-Zahraa (as) na mskiti wa Salman Al-Farisiy (r.a) na mengineyo mingi kati ya misikiti. Hakika hii inaonyesha waislam kujali – tangu mwanzo wa Uislam kujenga misikiti, kuiimarisha kwake ili ibakie baada yao kuwa ni sadaka yenye kuendelea na watu wa kuiendeleza kwa ajili ya swala na ibada. Hivyo ni juu ya waislamu leo wazingatie jambo hili tukufu la kidini. Hivyo basi ni wajibu kwa waislamu - hivi leo – kujali jambo hili tukufu la dini hususan katika nchi na miji ambayo humo kuna misikiti michache na wajitengenezee kwa ajili ya nafsi zao hazina ya milele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.

2. Husainiya Husainiya ina nafasi tukufu na kubwa katika kufikisha ujumbe wa Kiislam na kueneza utamaduni wa kidini kwa njia bora zaidi na kwa namna kamilifu na nzuri zaidi. Na kwa maelezo ya haraka tunaashiria ambayo Husainiya inayafanya katika yafuatayo:-

Kuhuisha utajo wa Ahlul-Bait (a.s) Imekuja katika hadithi kutoka kwa Imamu Swadiq (as): “Mwenyezi Mungu amrehemu anayehuisha jambo letu, huisheni jambo letu, hakika mwenye kuhuisha jambo letu haufi moyo wake siku nyoyo zitakapokufa.”

8


Sadaka yenye kuendelea

Kufanya maombolezo ya Imamu Husein (as) Zimepokewa hadithi nyingi kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu na Ahali zake watoharifu katika kupendeza na umuhimu wa kufanya majlisi za maombolezo ya bwana wa vijana wa peponi Imamu Husein (as) ambaye aliuliwa kwa ajili ya kuutetea Uislam na kuhami misingi yake.

3. Kueneza mafunzo ya kidini Hakuna shaka kwamba elimu sahihi ni elimu ya Ahlul-Bait (as) kwani wao ndio warithi wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww), ni wabebaji wa elimu yake na katika nyumba yao imeshuka Qur’ani tukufu, wao ndio wafasiri wa Qur’ani bali wao ni Qur’ani yenye kuongea. Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) katika hadithi waliyoipokea Sunni na Shia – “Mimi ni mji wa elimu na Ali ni mlango wake, mwenye kutaka mji wa hekima basi auendee kupitia mlango wake.” Hizi Huseiniya humo hutolewa hotuba, mihadhara ya kidini yenye kujaa hadithi za Ahlul-Bait (as) na elimu yao na kupitia humo kunaenezwa utamaduni wa asili wa kidini ambao haujaguswa na mikono ya upotoshaji na udanganyifu.

4. Kupanda sifa njema Kupitia mimbari na hotuba zitolewazo katika Husainiya hupandwa katika nafsi upendo, fadhila, kujiamini, ushujaa, kutonyenyekea madhalimu na kuwa na msimamo katika kukabiliana na batili. Na mambo yote haya yanapatikana kupitia ubainifu aliofanya Imamu Husein (as) kwa kupinga batili na watu wake na kusimama dhidi ya uongozi potovu ambao ulieneza ufisadi katika ardhi. 9


Sadaka yenye kuendelea

5. Kuamrisha mema Husainiya zinazingatiwa kuwa ni vituo vya kuamrisha mema na kukataza maovu, na kuongoza watu katika yale ambayo humo kuna ridhaa ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na utii wake na kuwaonya kutokana na yale ambayo humo kuna hasira Yake na maasia yake. Ni watu wangapi ambao wameongoka katika haki kwa baraka za Husainiya hizi na majilisi za maombolezo ambazo zinafanywa humo? Ni wangapi waliokuwa wanafanya mambo ya haramu wametubia kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kupitia kusikiliza mihadhahara inayotolewa katika Husainiya? Ni wangapi ambao walikuwa wanaacha wajibu kama vile swala – wamerejea kwa Mwenyezi Mungu na wamekuwa miongoni mwa wenye kuswali kwa baraka za majilisi za Husainiya? Ni wanawake wangapi ambao walikuwa hawavai hijabu, waovu, wameongoka kwenye uchamungu na kuvaa hijabu kwa baraka za Husainiya, ni wangapi...? Ni wangapi‌..? n.k.

6. Kupambana na waovu Husainiya inapambana na makundi na mitandao miovu ambayo inavamia nchi za Kiislam baina ya wakati na wakati. Mitandao ambayo inabeba fikra zenye sumu na shubha zenye kupotosha ambazo zinalenga kuwapotosha vijana na kuwapotoa na mfumo sahihi wa Ushia. Kwa sababu hiyo utaona vyama, harakati na vikundi vipotovu vinapiga vita Husainiya tukufu kwa kila hila, tuhuma na mbinu mbalimbali. Wakati mwingine wanasema hakika kumlilia Husein ni bidaa! Na wakati mwingine wanasema, kwamba kauli ya Shia: Ewe Abu Abdillah ni Shiriki? Na mara nyingine wanasema: Hakika kulisha chakula kwa jina la Imamu Husein ni haramu! 10


Sadaka yenye kuendelea Na wakati mwingine wanasema kwa nini hamfanyi maombolezo kwa baadhi ya masahaba ambao waliuliwa? Na mara nyingi wawalingania watu wafunge siku ya Ashura na kuifanya kuwa ni siku ya sikukuu na furaha. Na mengi mengineyo anayoyataka shetani miongoni mwa kauli na hatua zenye kushindwa ambazo hazinenepeshi wala hazishibishi. Na haya kama yanaashiria jambo basi yanaashiria nafasi kubwa iliyonayo Husainiya katika kutekeleza haki, kuondoa batili na kuvua pazia la upotovu kwa matwaghuti ambao wanaharibu sifa nzuri ya dini na kupotosha hukumu zake na kuupiga vita Uislam kupitia jina la Uislam. Na haya ndio ambayo yamejaza nyoyo za maadui hofu na wasiwasi. Kwa sababu hii ni wajibu wa Shia kusaidiana katika kuasisi Husainiya nyingi zaidi katika sehemu mbalimbali na kuzihuisha katika kila nchi katika ulimwengu, kwani - hakika – ni miongoni mwa alama za wazi za usadikishaji wa sadaka yenye kuendelea ambayo inamridhisha Mwenyezi Mungu, Mtume wake na Mawalii wake. Na kwa kifupi ni kwamba Husainiya ni madrasa za kidini za malezi, zinafanya kazi ya kufundisha Qur’ani na tafsiri yake, historia sahihi, tabia njema, mawaidha na maelekezo. Mwenyezi Mungu azihuishe na awahuishe wale ambao wanafanya juhudi katika kuzijenga, kuziasisi, kuzishajihisha na kuziendesha.

7. Maktaba Hakika madhehebu ya Shia yanasifika kwa hazina kubwa mno ya kifikra, mizizi yake inatokana na chemchem za elimu ya kiungu chimbuko la Utume, Uimamu, mashukio ya wahyi, nao ni Muhammad na kizazi cha Muhammad (as). 11


Sadaka yenye kuendelea Na hazina hii kubwa ya kifikra ndio ambayo imehifadhi – baada ya matakwa ya Mwenyezi Mungu Mtukufu - madhehebu ya Shia - muda wote wa karne zilizopata, pamoja na vikwazo vilivyoipata madhehebu hii ya haki miongoni mwa majaribio ya kuyazima na kuyakandamiza. Pamoja na vikwazo vilivyoipata hazina hii miongoni mwa kuchomwa moto vitabu na kuzamishwa baharini na kuvunjwa maktaba. Ni maktaba ngapi za umma ambazo aliziunguza moto Salahu diyn AlAyubiy katika nchi ya Misri na Halab?!! Na ni nyaraka ngapi tukufu za kidini ambazo aliamuru zitupwe katika mto Nile hadi maji yake yakabadilika rangi kwa wiki kadhaa? Na wala usiulize kuhusu maktaba za kidini zingine ambazo wakoloni waliziteketeza kwa moto huku na kule, ni nyingi mno. Kati ya hizo ni maktaba ya mrekebishaji mtukufu na mwanazuoni mtukufu As-Sayyid AbdulHusein Sharafu Diyin (r.a) ambayo ilikuwa inakusanya vitabu vya thamani na utunzi mwingi, ambapo walichoma nyumba yake katika jaribio la kutaka kumuuwa, na kuishambulia nyumba yake Kusini mwa Lebanoni. Vyovyote iwavyo – pamoja na majaribio yote hayo ya chuki, hakika Shia bado wangali wanasifika kwa hazina kubwa ya kifikra, wanasifika kwa elimu waliyoirithi kutoka kwa Ahlul–Bait ambao Mwenyezi Mungu amewaondolea uchafu na akawatakasa kabisa. Hakika maktaba ndio ambazo zinakusanya hazina hii na zinahifadhi rejea za Kidini na vitabu vingi vya thamani ambavyo wamevitunga Maulamaa wetu wema (r.a). Hivyo wajibu wetu wa kidini unatutaka tuchangie katika kuanzisha maktaba za umma, kushajihisha na kupata mwanga kwa yale zilizoyakusanya miongoni mwa elimu na maarifa. Anasema Al-Imamu Ali, Amirul-Muuminina (as): “Thamani ya mtu ni kile anachokifanya vizuri.” Haya, na mazungumzo juu ya miradi ya kheri na sadaka zenye kuendelea hayaishii katika wigo huu, uwanja ni mpana na 12


Sadaka yenye kuendelea maelezo ni mengi. Lakini sisi tunatosheka na kiasi hiki kwa kutaraji kuwa utafiti huu utakuwa umeleta changamoto na athari nzuri na kubwa katika nyoyo za waumini wa kiume na wakike na kuwasukuma kupiga hatua pana katika nyaja hizi ili sadaka hizi - zibaki baada yao – ni taa zenye kuwaka ziangazie kaburi zao, zinyanyue daraja zao na kuongeza mema yao Inshaallaah.

Mtoto mwema Hakika mtoto anaweza kuwa mwema na muumini na wakati mwengine anaweza kuwa muovu na mpotovu, akiwa ni yule wa kwanza basi atawafanyia wema wazazi wake katika maisha yao na atawaombea maghfira baada ya mauti yao na atawakumbuka kwa mema na kuzipelekea roho zao zawadi za kheri na amali njema. Imekuja katika hadithi tukufu kwamba maiti anafurahi kwa kheri ambazo zinatolewa zawadi kwa roho yake kama mwanadamu aliye hai anavyofurahi kwa kupewa zawadi. Na mtoto mwema anaweza kuwa ni sababu ya kuondolewa adhabu kwa wazazi wake wawili au mmoja wao kama ilivyokuja katika hadithi kwamba Nabii Issa (as) alipita katika kaburi, akaona kuwa mwenye kaburi hiyo anaadhibiwa kisha akapita tena katika mwaka mwingine akaona adhabu imeshaondolewa kwake akasema: Ee Mola wangu nilipita katika kaburi hili mwaka wa kwanza naye anaadhibiwa na nikapita tena mwaka huu nikakuta haadhibiwi? Mwenyezi Mungu akampa wahyi: Ewe Roho ya Mwenyezi Mungu mtoto mwema amemdiriki basi akamtengenezea njia yake, amemsitiri yatima basi nikamsamehe kutokana na yale aliyoyafanya mtoto wake.3 Na katika hadithi hii tukufu kuna kushajihisha kukubwa kwa wazazi wawili kuzingatia malezi ya watoto wao ili wafurahike kwao na ili Mwenyezi Mungu awaghufirie kwa wema wa watoto wao. Na imepokewa kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) kwamba amesema: “Miongoni mwa 3 Wasilus-Shiah, Juz. 11, uk. 561

13


Sadaka yenye kuendelea furaha ya mtu ni kuwa na mtoto mwema.”4 Na Imam Ja’fari Swadiq (as) amesema. “Urithi wa Mwenyezi Mungu kwa mja wake muumini ni mtoto mwema anayemuombea maghfira.”5 Malezi mazuri ili wawafanyie wao wema na ili Mwenyezi Mungu awaghafirie wao kutokana na wema wa watoto wao. Na imepokewa kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) kwamba anasema “Miongoni wa furaha ya mtu ni kuwa na mtoto mwema.”6 Na amepokea Is’haq bin Ammar kutoka kwa Imamu Ja’far Swadiq (as) kwamba mtu alimwambia: “Hakika mimi nilikuwa sitaki kuwa na mtoto basi siku moja nilisimama Arafah, basi pembezoni mwangu pakawa na kijana anaomba na huku analia. Anasema Mola wangu, wazazi wangu, wazazi wangu, basi akanipa raghiba ya kuwa na mtoto kwa kusikia hayo.”7 Soma hadithi hii, ni utukufu ulioje! Anasema bwana wetu, na kiongozi wetu Amirul-Muuminina Ali bin Abi Talib (as): Sikumuomba Mola wangu mtoto mweupe wa uso, wala sikumwomba mtoto mwenye umbo zuri lakini nilimuomba Mola wangu watoto wenye kumtii Mwenyezi Mungu, wenye kumwogopa Mwenyezi Mungu ili nitakapomtazama hali yakuwa ni mwenye kumtii Mwenyezi Mungu macho yangu yanaburudika.”8 Na kwa maana hii imekuja ishara katika Qur’ani tukufu – katika kisa cha Nabii Ibrahim (as): ”Mola wangu nipe miongoni mwa wema.”9 Na katika kisa cha Nabii Zakaria (as): Hapo Zakaria alimuomba Mola Wake akasema; Mola Wangu nipe kutoka kwako kizazi chema, hakika wewe ni mwenye kusikia dua.”10 4 Biharul-Anwar Juz. 105, uk. 97 5 Biharul-Anwar, Jz. 105, uk. 90 6 Wasailus Shiah, Juz. 15, uk. 95 7 Biharul Anwar, Juz. 104, uk. 98 8 Biharul Anwar, Juz. 104, uk. 98 9 Suratu Swafaat: 100 10 Surat Al Imran: 38

14


Sadaka yenye kuendelea Na imepokewa kutoka kwa Mustafa (saww) kwamba amesema: ”Mtoto mwema ni harufu miongoni mwa harufu nzuri za peponi.” Hivyo ni wajibu wa wazazi wawili kujitahidi kadri ya uwezo wao kwa ajili ya kuwalea watoto wao katika wema, imani, swala, ibada, maadili mema na adabu. Na mimi naapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba runinga, Sinema, majarida ya ufisadi na ziara za kujiburudisha katika nchi za kigeni haziongezi kwa watoto isipokuwa ufisadi, upotovu, kumomonyoka kwa maadili na hatimaye kuporomoka. Na hakika njia ya sawa inapatikana katika Misikiti, Husainiya majlisi za maulamaa wa kidini, kujisomea vitabu vya dini na kuepukana na marafiki waovu na mfano wa hayo. Na hakika wazazi ambao wanawaacha watoto wao bila ya malezi na mafunzo na wanawapa uhuru wa kwenda watakako na kuwaacha wakae na yeyote yule wanayemtaka na kusafiri popote watakapo watakuja kujuta majuto makubwa siku ambayo majuto hayatafaa abadani. Hakika mtoto muovu ni aibu kwa wazazi, bali kwa familia na jamii yote. Imepokewa kutoka kwa Imamu Ali (as) kwamba amesema: “Mtoto muovu anavunja heshima na kuwafedhesha wazazi.”11 Na amesema (as): “Na kati ya misiba mikubwa ni kuacha mtoto muovu.”12 Ndio, hakika mtoto muovu anaharibu heshima ya familia na kuvunja heshima yake katika jamii, kwa kuongezea kwamba yeye ni msiba mkubwa mno katika nyoyo za wazazi. Nahitimisha maneno yangu – hapa – kwa hadithi hii: Anasema Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) maangamio ya watoto wa akhiri zamani ni kutokana na wazazi wao. Akaambiwa: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu kutokana na wazazi wao washirikina? Akasema hapana, kutokana na wazazi wao waislam wasiowafundisha mambo ya wajibu, na wao wanapojifunza wanawazuia.” 11 Ghurarul-Hikam wa Durah Kalim 12 Ghurarul-Hikam wa Durah Kalim

15


Sadaka yenye kuendelea

Hadithi Tukufu Kuhusiana na Sadaka Yenye Kuendelea Ewe msomaji mtukufu zifuatazo ni baadhi ya hadithi tukufu zilizopokelewa kutoka kwa Ma’asumina (as) kuhusu sadaka yenye kuendelea, na mambo mengine mema ambayo yanaongezea malipo na thawabu kwa mwanadamu vyovyote muda utakavyorefuka na miaka kuzunguka.

1. Jambo jema Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) Mwenye kuanzisha jambo jema na kufanywa baada yake atakuwa na malipo yake na mfano wa malipo yao bila ya kupungua chochote katika malipo yao. Na mwenye kuanzisha jambo baya na likafanywa baada yake atapata madhambi yake na mfano wa madhambi yao bila ya kupungua chochote katika madhambi yao.13 Ewe msomaji mtukufu hakika hadithi hii tukufu imekusanya baina ya kuraghiribisha na kuhofisha kwa wakati mmoja. Ama kuraghiribisha na kushajihisha ni kwa yule mwanadamu ambaye anaacha athari njema, ada na utamaduni mzuri katika jamii ambao wanaufuata watu na kurithishana kizazi baada ya kizazi. Mtu huyu atapata malipo yake na malipo ya kila atakayefuata mwendo wake katika njia yake na uongofu wake. Na nilishamuona mmoja wa maulamaa wa kidini na marjaa wa waislamu aliingia katika mji kati ya miji akakuta watu wamejishughulisha na dunia na matamanio yake, wako mbali na mambo ya kiroho na athari zake na wanatumia muda wao mwingi katika upuuzi na pumbao. Hakufanya jingine ila aliwalingania kufanya majilisi za Imam Husein (a.s.) kwa kila wiki katika nyumba zao na akawashajihisha juu yake na akawaeleza uzuri 13 Kanzul-Umal cha Al-Muttaqiy

16


Sadaka yenye kuendelea wake, faida zake na athari zake za kidini na kijamiii na yanayopatikana humo miongoni mwa baraka na kheri, malipo na thawabu. Yeye binafsi alifanya majlisi za Imamu Huseini nyumbani kwake kila wiki na alikuwa anahudhuria Majilisi za Imamu Husein zinazofanywa huku na kule na amevumilia kwa ajili ya hilo mengi, mengi mno. Baada ya muda majlisi za Imam Huseini zikawa zinafanywa hapa na pale, katika nyumba hii na ile, kwa wingi hadi ikawa ni vigumu kuhudhuria wote majlisi zote katika usiku mmoja. Na jambo hili lingali linaendelea hadi wakati wa kuandika kitabu hiki. Ndio, huu ni mfano wa jambo jema. Ama kuhofisha na kuogopesha ni kwa yule ambaye analeta bidaa na mambo mabaya katika jamii, na watu wakayafuata kutokana na ujahili na upumbavu, hakika anabeba dhambi yake na dhambi ya anayeifanya hadi Siku ya Kiyama na mifano iko mingi katika historia, ya viongozi ambao wameharamisha halali ya Mwenyezi Mungu na wakahalalisha haramu ya Mwenyezi Mungu na wakaingiza katika dini ambayo hayapo katika dini na ingali mambo hayo maovu yanaendelea kwa wafuasi wao hadi sasa.

2 . Mambo matatu Imamu Ali anasema: Hakimfuati mtu chochote baada ya kufa isipokuwa:1. Sadaka yenye kuendelea 2. Au elimu ya sawa 3. Au dua ya mtoto mwema

3. Nini kinamfuata mtu baada ya kufa kwake? Muawiya Bin Amaar alimuuliza Imamu Swadiq (as) nini kinamfuata mtu baada ya kufa kwake? Akasema: (a) Jambo zuri litakalofanywa baada ya kufa kwake hivyo atakuwa na malipo ya mfano wa mwenye kulifanyia kazi bila ya kupungua chochote katika malipo yao. 17


Sadaka yenye kuendelea (b) Sadaka yenye kuendelea baada yake (c) Mtoto mwema anayewaombea wazazi wake baada ya kufariki kwao, na kuhiji, kutoa sadaka na kuacha mtumwa kwa niaba yao, na kuswali na kufunga kwa niaba yao.14

4. Mambo sita Kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) amesema: Hakika kati ya yanayomfuata muumini miongoni mwa amali zake na wema wake baada ya kufa kwake ni:1. Elimu aliyoifundisha na kuisambaza 2. Mtoto mwema aliyemwacha hai 3. Au msikiti alioujenga 4. Nyumba aliyoijenga kwa ajili ya wapita njia walioharibikiwa 5. Kisima alichokichimba 6. Au sadaka aliyoitoa katika mali yake katika uhai wake na siha yake itamfuata baada ya kufa kwake.15 Na katika hadithi nyingine - Kutoka kwa Imamu Swadiq (as) amesema: Mambo sita anayonufaika nayo muumini baada ya kufa kwake ni:1. Mtoto mwema anayemuombea maghfira 2. Msahafu anaosoma 3. Kisima alichokichimba 4. Mti wa (matunda) aliopanda 5. Sadaka yenye kuendelea 6. Jambo zuri alilolianzisha linalofanyiwa kazi baada yake.16 14 Wasa’ilus-Shiah, Juz. 6 uk. 292 15 Tarihiybu Watarighiyb Juz: 1 uk: 99 cha Ibnu Majid na Baihaqiy 16 Biharul-Anwar, Juz. 17, uk. 257

18


Sadaka yenye kuendelea

Sahaba huyu alitoa sadaka bustani yake katika njia ya Mwenyezi Mungu: Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) alikuwa anawafundisha watu kufanya amali kwa ajili ya akhera na kuchuma pepo ambayo upana wake ni sawa na upana wa mbingu na ardhi kwa sababu ni yenye kubaki na yenye manufaa zaidi kwa mwanadamu kuliko dunia yenye kuondoka na ambayo itaisha na kumalizika, na kumalizika kilichomo humo. Na mazungumzo yake (saww) yalikuwa yanapenya katika nyoyo zilizoamini na kuacha humo athari nzuri, haya ndio utakayoyafahamu katika kisa kifuatacho: Imepokewa kutoka kwa Imamu Muhammad Al-Baqir kutoka kwa baba zake watukufu (as) kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) alipita kwa mtu akiwa anapanda miti katika bustani yake akasimama kwake akasema: “Je, nikuonyeshe mti imara zaidi, wenye kutoa matunda haraka zaidi na wenye athari nzuri na msafi zaidi?” Akasema: “Ndio, nionyeshe, baba yangu na mama yangu wawe fidia kwako Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu.” Akasema (saww): “Unapoamka asubuhi na wakati wa jioni sema: Subhanallah wal-Hamdulillahi walaa ilaha iIa’llaahu wallahu Akbaru, hakika hayo ukiyasema – utapata – kwa kila tasibihi miti kumi peponi na aina za matunda. Hayo ni kati ya maneno mema yenye kubakia.” Ni dhahiri kwamba yule mtu alifahamu kwa meneno ya Mtume (saww) kwamba ni wajibu wake kufanya amali ya kheri kwa ajili ya mema yenye kubakia na kuimarisha bustani kwa ajili ya sadaka yenye kuendelea itakayobakia kwa ajili yake, vinginevyo bustani – na yaliyomo humo kati ya miti na matunda – itahama kutoka kwake na kwenda kwa mwingine baada ya kufa kwake. Alipofahamu maana hii alifanya haraka na kuchukua maamuzi ambapo inaonyesha juu ya Imani yake katika malipo na upeo wa kuwa kwake huru katokana na nafsi inayoamrisha maovu, pupa na tamaa na kwa ajili hiyo alisema: “Nakushundisha ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu hakika busta19


Sadaka yenye kuendelea ni yangu ni sadaka kwa ajili ya mafakiri miongoni mwa Ahlus-Sufah.

Mtukufu Mtume (saww) na sadaka yenye kuendelea Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww), naye ni bwana wa mawalii wa Mwenyezi Mungu na Manabii Wake, alikuwa ni kati ya wale wanaoshidana katika amali njema ambazo Mwenyezi Mungu anazipenda. Na vipi isiwe hivyo naye ndiye kigezo chema ambacho Qur’ani tukufu imesema juu yake: “Hakika mnacho kigezo chema kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu.” Na katika jumla ya hatua njema ambazo alikuwa anazifanya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) na kuwashajihisha waislam kuzifanya ni sadaka kwa vigawanyo vyake vyote, sadaka yenye kuendelea na nyinginezo. Ni ardhi ngapi ambazo amezitoa wakfu katika njia ya Mwenyezi Mungu? Na ni mali ngapi ambazo aliwapa watu wengine badala ya kupendelea nafsi yake? Ameacha mifano ambayo imetajwa katika vitabu ambavyo vinazungumzia maisha yake (saww) na sira yake na ifuatayo ni baadhi yake. 1. Imam Ja’fari Swadiq (as) amesema Mtume wa Mwenyezimungu (saww) alitoa Sadaka mali yake akaifanya waqfu, na alikuwa anatoa humo matumizi ya wageni wake.17 2. Imepokewa kwamba alichinjwa kondoo nyumbani kwake Mtume (saww) wakagawa nyama yake katika nyumba za mafakiri na masikini, Nabii akamwambia Aisha: Nini kimebaki? Akasema haijabaki ila ubavu wake. Akasema (saww) yote imebakia isipokuwa ubavu wake.18 Na hii ni ishara ya kauli yake (swt): Yaliyopo kwenu yanamalizika na yaliyopo kwa Mwenyezi Mungu ni yenye kubaki,” kwa sababu aliyoyatoa kwa mafakiri na vilema ni yenye kubaki yamehifadhiwa kwa Ambaye 17 Mustadrakul Wasail, Juz. 14, uk. 46 18 Kanzul-Umal, cha Al Muttaqiy

20


Sadaka yenye kuendelea hapotezi malipo ya watu wema.

Fatmaz-Zahraa (as) na sadaka yenye kuendelea Bibi Fatma, Bibi wa wanawake wa ulimwenguni ambaye Mtume (saww) alimuita “Aswidiyqah”19 - Imam swadiq (as) amesema: “Naye ndio Aswidiyqatul-Kubra (Msadikishaji mkuu ).” 20 Umeshajua maana ya Swidiyq kwamba ni msadikishaji wa yote ambayo ameamrisha Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, haimwingii shaka, na ambaye amali yake inasadikisha kauli yake. Na Aswidiqaal Fatmatuz-Zahraa (as) alikuwa na sadaka yenye kuendelea na Wakfu za kheri alizotoa katika njia ya Mwenyezi Mungu na kati ya hizo ni bustani saba alizozitoa wakfu kwa Bani Hashim, Bani Abdul-Mutalib na akajaalia uongozi wake kwa Imam Ali (as) kama ilivyokuja katika hadithi ifuatayo. Kutoka kwa Abi Baswir kwamba Imamu Baqir (as) alimwambia: Je, nikusomee wasia wa Fatma (as)? Nikasema ndio. Akatoa mfuko au kipande cha ngozi humo akatoa kitabu akasoma: Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu, haya ndio aliyousia Fatma binti wa Muhammad (saww), ameusia bustani zake saba Al-a’awaf, dalal, baraqah, Al Maithab, al Husnaa, As swafiyah, Mishrab na Ummu Ibrahim kwa Ali bin Abi Twalib, akiondoka Ali ni kwa Hasan, akiondoka Hasan ni kwa Husein, akiondoka Husein basi kwa mkubwa anayefuatia kisha kwa mkubwa katika kizazi changu. Mwenyezi Mungu ameshuhudia juu ya hilo na Miqidad bin Al-Aswad, Zubeir Al-Awaam, na akaandika Ali bin Abi Talib.21 Unaweza kuuliza vipi bustani hizi zimefika kwa bibi Fatma Zahraa (as)? Jawabu: Ametaja Samhudiy22 kwamba Mukhayraqi al-Yahudiy - na 19 Riyadhu Nadhar, Juz. 2, uk. 202 20 Biharul Anwar, Juz. 43, uk. 105 21 Mustadrakul Wasail, Juz. 14, uk. 50 na 59

21


Sadaka yenye kuendelea alikuwa kati ya wachungaji wa kiyahudi wa Bani Nadhir – alisilimu na aliuliwa siku ya Uhdi, aliusia bustani zake saba kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu na kizazi chake, na Nabii alizitoa wakfu - mwaka wa saba Hijiria – hususan kwa Fatma (as) na alikuwa anazitumia kwa ajili ya wageni wake na katika haja zake.

Imam Ali na sadaka yenye kuendelea Imam Ali (as) Amirul-Muuminina, Imamu wa maimamu, mkuu wa wakuu na mbora wa masahaba wote, Imam Ali ndugu wa Mtumne wa Mwenyezi Mungu, na khalifa wake, msaidizi wake, wasii wake, mlango wa elimu yake, msiri wake, mbeba bendera yake na anayependeza mno kwake. Imam huyu mtukufu maisha yake matukufu yamejaa kadhia nyingi za sadaka na vigawanyo vyake vyote. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) alishampa lakabu ya ”As-Sidiyq” nayo ni tamko linaloonyesha juu ya usadikishaji wake ulio kamili na wenye kuendelea kwa Mwenyezi Mungu na kwa Mtume Wake kutoa kwake katika njia ya Mwenyezi Mungu, msaada wake kwa mafakiri na maskini, kupendelea kwake wengine badala ya nafsi yake na ahali zake kama alivyosema Mwenyezi Mungu (swt): ”Na wanawapendelea wengine kuliko nafsi zao ingawa wao wanahitaji.”23 Na imepokewa kwamba aya hii imeshuka kwa ajili yake na hiyo ni pale mtu alipokuja kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu akamshitakia njaa, Mtume akaagiza (chochote) katika nyumba za wake zake wakasema: Hatuna chochote isipokuwa maji. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) akasema nani atakuwa na mtu huyo usiku wa leo? Ali bin Abi Talib akasema: Mimi ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, akamwendea Fatma (as) akamwambia una kitu gani ewe binti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu? Akasema: Hatuna isipokuwa chakula cha jioni tu,24 lakini tutampa mgeni wetu. Akasema (as) Ewe binti wa 22 Kitabu Tarikhul Madinah, Juz. 2, uk. 152 23 Suratul Hashir: 9

22


Sadaka yenye kuendelea Muhammad, walaze watoto na uzime taa. Ali alipoamka asubuhi akaenda kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu na akampa habari, haukupita muda Mwenyezi Mungu akateremsha: ”Na wanawapendelea wengine ingawa wao wenyewe wanakihitaji na wenye kushinda uroho wa nafsi yake basi hao ndio wenye kufaulu”25 Na katika yafuatayo tunataja baadhi ya mifano ya sadaka zenye kuendelea za Imamu Ali bin Abi Talib (as).

1. Aynu Yanbu’u Imepokewa kutoka kwa Imamu Swadiq (as) kwamba yeye amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) aligawa pato na ngawira, basi Ali akapata ardhi, na akachimba kisima humo na yakatoka humo maji yenye kububujika kama shingo za ngamia basi akayaita “Aynu yanbu’u,” chemchem yenye kububujika, kisha akasema (as) hii ni sadaka isiyo chini ya mwanzilishi, ni kwa ajili ya mahujaji wa nyumba ya Mwenyezi Mungu tukufu na wapita njia, haiuzwi, haitolewi zawadi wala hairithiwi, atakayeiuza au kuitoa zawadi basi laana ya Mwenyezi Mungu, malaika Wake na watu wote, Mwenyezi Mungu asimkubalie aslani. Ardhi hii ilikuwa katika njia ya mahujaji, kwa sababu hiyo Imam aliifanya kuwa ni wakfu kwa ajili ya mahujaji na kwa kila anayepitia katika ardhi hiyo. Chemchem hii ilikuwa ni sadaka yenye kuendelea, kwa miaka mingi mahujaji wanapitia hapo na wanafaidika kwa maji yake matamu na mazuri ambayo yamechimbwa kwa mikono mitukufu ya Imamu Ali (as).

2. Nyumba katika eneo la Bani Zariyq 24 Na katika nukuu nyingine “hatuna ila watoto tu” 25 Tafsir ya Nuru Thaqalain na Amali ya Tuusi

23


Sadaka yenye kuendelea Katika mji mtukufu wa Madina kulikuwa na eneo katika maeneo ya makazi linaloitwa Bani Zariyq na Imam Ali Amirul–Muuminina (as) alikuwa ana nyumba anayoimiliki humo, basi akaifanya kuwa ni sadaka yenye kuendelea. Imam Ja’fari Swadiq (as) amesema Amirul-Muuminina (as) alitoa sadaka nyumba yake katika Bani Zariyq akaandika: Kwa Jina la Mwenyezi Mungu haya ni ambayo ametoa sadaka Ali bin Talib, naye akiwa hai na akili timamu, anatoa sadaka nyumba yake ambayo haiuzwi wala hatiolewi zawadi hadi airithi Mwenyezi Mungu ambaye ndiye mrithi wa mbingu na ardhi. Na waliishi humo mama zake wadogo kadiri walivyoishi na vizazi vyao.26 Na walipomalizika aliisha yeyote mwenye haja kati ya waislamu.

3. Chemchem ya Abi Nizar na Baghiybah Imam Ali (as) alikuwa na bustani mbili, moja inajulikana kwa chemchem ya Abin Nizar na ya pili inajulikana kwa Baghiybah na msimamizi wake ni mwanaume anayeitwa Abu Nizar. Anasema: Alinijia Ali bin Abi Talib (as) kisha akachukua koleo akawa anachimba maji yakachewa kutoka, akatoka na uso wake umejaa jasho akafuta jasho kwenye uso wake kisha akachukua koleo tena na akarejea katika chemchem akawa anachimba huku aunguruma, basi yakatoka kana kwamba ni shingo za ngamia, akatoka haraka akaandika: kwa jina la Mwenyezi Mungu, haya ni ambayo ametoa sadaka mja wa Mwenyezi Mungu Ali bin Abi Talib, ametoa sadaka bustani mbili zinazojulikana kwa Aynu Abiy Nizar na Al-Baghiybah kwa mafakiri wa Madina na wasafiri ili Mwenyezi Mungu aukinge uso wake na joto la Moto Siku ya Kiyama, haiuzwi wala haitolewi zawadi hadi airithi Mwenyezi Mungu naye ni mbora wa warithi, lakini kama atazihitaji Hasani na Husein basi wao ni miliki yao na wala si kwa yeyote asiyekuwa wao. – Muhamadi bin Hisham amesema Husein akawa ana deni Muawiya akampa dinari laki mbili kwa ajili ya chemchem ya Abiy Nizar akakataa (as) kuiuza akasema; Hakika baba yangu amezitoa sadaka ili Mwenyezi Mungu akinge uso wake 26 Wasailus-Shiah. Juz. 6, uk. 304

24


Sadaka yenye kuendelea kutokana na joto la Moto na sitoziuza kwa chochote.

4. Ardhi na bustani Imam Ali alikuwa na ardhi na bustani zilizokuwa zinamwingizia faida kubwa na mali nyingi, akazitoa katika njia ya Mwenyezi Mungu ili zibaki kuwa ni sadaka yenye kuendelea baada yake, na akausia juu ya hilo na katika yafuatayo nakutajia ndugu msomaji – tamko la wasia ili utafakari na utazame msukumo ambao ulimfanya Imam (as) kutoa ardhi hiyo na bustani hizi na kwamba lengo ni kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu na kupata mchumo, thawabu za ziada na daraja kubwa: “Haya ni ambayo ameusia na kuhukumu katika mali yake Amirul-Muuminina Ali bin Abi Talib kwa ajili ya kutaka radhi za Mwenyezi Mungu ili aniingize peponi na aniepushe na moto na kuuepusha moto na uso wangu siku ambayo nyuso zitakuwa nyeupe na nyuso zingine zitakuwa nyeusi, yale ambayo nilikuwa nayamiliki katika Yanbu’u kati ya mali inajulikana kuwa ni yangu na pembezoni mwake, basi ni sadaka pamoja na watumwa wake. Na yote yaliyokuwa miliki yangu, na vyote vilivyomo humo ni sadaka, na sadaka hii ni ya wajibu abadani, nikiwa hai au maiti itatumika katika kila matumizi ambayo yanatakiwa humo radhi za Mwenyezi Mungu na katika kizazi cha Bani Hashim na Bani Abdul-Mutwalib, wa karibu na wa mbali, na kwamba msimamizi wa hayo ni Hasan bin Ali. 27

5. Bustani nyingine Imepokewa kwamba mwanaume alikuwa na bustani humo kuna mitende na baadhi ya matawi ya mitende yake yamening’inia katika nyumba ya jirani yake fakiri mwenye watoto, na wakati mwingine baadhi ya tende zinaanguka katika nyumba yake na watoto wanaziokota na kuzila, mwenye bustani anakuja na kuchukua tende kwao na wakati mwingine anazitoa kwenye vinywa vya watoto. Fakiri akamlalamikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) kuhusu yule mwanaume tajiri kutokana na ubakhili wake 27 Mustadrakul Wasail, Juz. 14, uk. 52

25


Sadaka yenye kuendelea na lawama zake, Nabii akaja na akawambia: Niuzie bustani yako hii kwa bustani ya peponi. Tajiri akasema: Siuzi kilichopo kwa kijacho. Nabii (saww) akalia28 na akaelekea Msikitini – njiani akakutana na Imamu Ali (as) na akamwambia: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu kitu gani kinakuliza? Mwenyezi Mungu asiyalize macho yako. Akamweleza maneno ya yule mwanaume tajiri na jirani yake fakiri. Amirul- Muuminina akaelekea kwenye nyumba ya yule mwanaume na akamwambia: Niuzie nyumba yako. Akasema kwa bustani yako ya Al–Husnaa. Akampa mkono kuashiria kukubali. Kisha akamgeukia mwanaume fakiri na akamwambia nenda kwenye nyumba yako kwani Mwenyezi Mungu mlezi ameshaimiliki kwa niaba yako, kisha akaelekea kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) na hali Jibril keshateremka kwa Nabii akisema: Ewe Muhammad soma: “Walaili idha yakhsha… hadi mwisho wa sura.” Msomaji mtukufu tafakari Suratul-Laili ili uone jinsi gani inalandana na kadhia hii ya kihistoria. Imam Ali (as) alifanya biashara hii ya kiungu katika mwanzo wa usiku - kama ilivyokuja katika baadhi ya tasfiri - Mwenyezi Mungu akaapa kwa usiku. Kisha akasema (swt): “Hakika amali zenu ni mbali mbali” yaani kila mmoja wenu anafanya kwa ajili ya jambo fulani, baadhi yenu wanafanya amali kwa ajili ya dunia na baadhi yenu wanafanya amali kwa ajili ya akhera. Ama yule aliyetoa na akamcha Mwenyezi Mungu na anasadikisha wema basi tutamfanyia wapesi. Tafakari juu ya kauli yake (swt): “Na akasadikisha wema” Kusadikisha malipo ya 28 Hakika kulia kunatokana na furaha au huzuni, na hapa sio mahala pa furaha, hivyo ni lazima iwe ni kutokana na huzuni. Na huzuni hii ni ya nini? Jibu huenda ni kutokana na kumhurumia yule fakiri kwa yale anayopata kwa yule jirani yake muovu na tajiri au inatokana na kumsikitikia yule muovu aliyeinyima nafsi yake akhera isiyokwisha na kupupia kwake dunia isiyobaki. Na dhana hii inaungwa mkono na kauli yake (swt): Pengine unawasikitikia kwa kuwaonea huruma wasipoamini maneno haya: “Anasikitika sana kutokana na maasi ya waovu na kupetuka kwao.”

26


Sadaka yenye kuendelea Mwenyezi Mungu na utoaji wa kiungu ndio ambayo yanamsukuma mwanadamu katika kutoa mali yake katika njia ya Mwenyezi Mungu (swt). Ama wale dhaifu wa imani na wasiosadikisha, wao wanaipendelea dunia yenye kupita kwa akhera inayokuja baadae kama aliposema (swt): “Hakika hawa wanapenda yapitayo na kuacha nyuma yao siku nzito.” Na kauli yake (swt): “Wema” yaani malipo mema yenye kuongezwa maradufu ambayo Mwenyezi Mungu ameyaandaa kwa wanaotoa sadaka. Na imekwishatangulia kwamba bibi Fatma Zahraa (as) alikuwa na bustani inayoitwa Al-Husna katika jumla ya bustani saba – akaifanya kuwa ni sadaka yenye kuendelea kwa Bani Hashim na Bani Abdul-Mutwalib.

6. Sadaka zingine Imepokewa kutoka kwa Imam Ja’fari Swadiq (as) kwamba alimtaja Ali bin Abi Talib akasema: Alikuwa ni mja wa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ameshawajibisha pepo kwake, alikusudia katika mali yake, basi akaifanya ni sadaka abadani, ili itumike kwa ajili ya mafakiri baada yake na akasema: Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi nimeyafanya haya ili uepushe moto na uso wangu na ili uso wangu uepushwe na moto.29 Na amesema Imam Muhammad Al-Baqir (as): Vipi watu wanajinyima kufanya kheri? Wakati Ali naye ni mja wa Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu ameshamuwajibishia pepo - alitoa mali sadaka ili zitumike kwa mafakiri baada yake. Akasema: Eee Mwenyezi Mungu hakika nimeyafanya haya ili uepushe uso wangu na moto na ili moto uepushwe na uso wangu. Na katika Tarekh Al-Baladhary: Pato la mazao ya Ali (as) lilikuwa ni dinari Arobaini elfu, akaifanya kuwa ni sadaka. Na kuna hadithi nyingi zinazozungumzia sehemu mbalimbali za sadaka za Imamu Ali, AmirulMuuminina (as), tunataja baadhi yake katika yafuatayo: 29 Mustadrakul-Wasail, Juz. 14, uk. 46

27


Sadaka yenye kuendelea

1. Sadaka ya usiku Imepokewa kutoka kwa Imamu Hasan Al-Mujtaba alipomuosha baba yake Ali (as), waliokuwepo hapo walitazama sehemu za kusujudia kuanzia magoti mawili, sehemu ya juu ya nyayo zake wakakuta ni kama magoti ya ngamia na wakatazama mabega yake wakakuta ni kama sehemu za kusujudia. Wakamwambia Imam Hasan (as): Ewe mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu haya tunayajua ni kutokana na kudumu katika swala na sijida ndefu, lakini nini hii tunayoiona katika mabega yake? Akasema Imam (as): Ama kama angekuwa hai nisingewaambia, ilikuwa haimpitii siku isipokuwa anamshibisha fakiri au zaidi kadri iwezekanayo, unapokuja usiku anaangalia kilichobakia miongoni mwa chakula cha familia yake na anakiweka katika viroba na panapotulia na watu kulala anavibeba na kuzunguka na kuwapelekea wale watu wasioomba kwa kuona aibu anagawa baina yao bila ya wao kumjua yeye ni nani? Na wala hajui yeyote katika familia yake isipokuwa mimi, mimi nilishaona hilo kutoka kwake, hali ya kuwa anataraji kwa hilo fadhila za kutoa sadaka kwa mkono wake kwa siri, na alikuwa anasema hakika kutoa sadaka kwa siri kunazima hasira za Mola mlezi kama maji yanavyozima moto.30 2. Na imepokewa kwamba Imam Ali (as) siku moja alitoka akiwa na diriham tano, fakiri akamwapia kuwa hana kitu, basi akampa zote, alipoondoka akakutana na bedui amepanda ngamia akamwambia nunua ngamia huyu. Akasema (as): Sina fedha za kumnunua. Akamwambia mnunue kwa mali kauli. Akamnunua kwa dirham mia moja, kisha mtu akamjia akamnunua kwa dirham mia moja na hamsini taslim. Akalipa diriham mia moja kwa muuzaji na akarejea nyumbani na dirihamu hamsini. Fatma (as) akamuuliza juu ya hilo. Akasema nimefanya biashara na Mwenyezi Mungu nimempa moja na akanipa mahala pake kumi.31 30 Mustadrakul-Wasail, kitabu Zakat Babus-Swadaqah

28


Sadaka yenye kuendelea Ewe msomaji mtukufu hakika malipo ya amali njema hayahusiani tu na akhera bali na katika dunia pia. Naiunga mkono maana hii, ni hadithi nyingi zilizopokelewa katika nyanja hii. Na kisa hiki kinatupa somo hili tukufu kwamba kufanya biashara na Mwenyezi Mungu ina faida duniani na akhera na wala hakuna ihtimali ya kupata hasara na madhara abadani, wakati ambapo biashara ya kidunia kuna ihtmali ya kupata faida na hasara, ni matajiri wangapi wamepoteza mali zao kwa sababu ya hasara ya kibiashara, hivyo wakawa ni mafakiri wasio na chochote. Ama kufanya biashara na Mwenyezi Mungu, dirham moja ni sawa na dirham kumi, na wakati mwingine ni sawa na dirham mia saba na inaweza kuwa ni nyingi zaidi ya hayo kama aliyosema (swt):

“Mfano wa wale wanaotoa mali zao katika njia ya Mwenyezi Mungu ni kama mfano wa punje inayotoa mashuke saba na kila shuke linatoa punje mia saba na Mwenyezi Mungu anamzidishia anayemtaka na Mwenyezi Mungu ni Mkwasi, Mjuzi.” (Sura al-Baqara: 261). Na imepokewa kutoka kwa Imam Al-Baqir (as) katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Ama yule aliyetoa, akamcha mungu na akasadikisha wema.” Akasema hakika Mwenyezi Mungu anatoa kumi kwa moja hadi elfu mia moja na zaidi ya hayo. “Basi tutamfanyia wepesi katika mema.” Akasema hatotaka chochote cha kheri isipokuwa Mwenyezi Mungu atamfanyia wepesi.

31 Mustadrakul-Wasail, kitabu Zakat Babus-Swadaqah

29


Sadaka yenye kuendelea

Al – Imamul-Hassan na sadaka yenye kuendelea Hakika maisha ya Imamu Hasan Al-Mujtab (as) yamejaa visa vya kheri na sadaka katika njia ya Mwenyezi Mungu hadi amekuwa mashuhuri kwa jina “Mkarimu wa Alhul Bait. ” Na katika muhtasari huu tunatosheka kwa haya yafuatayo:1. Hakika yeye (as) ametoa mali yake yote mara mbili na maana ya hiyo ni kwamba alitoa sadaka yote aliyokuwa anamiliki; mali, nyumba, ardhi, watumwa, vijakazi na mengineyo katika njia ya Mwenyezi Mungu. Na amali hii imetoa - mara mbili katika maisha yake - naye anastahiki kuwa ni kati ya aina kubwa kabisa za sadaka. Hakika mara nyingi mwanadamu anatoa sadaka sehemu tu ya mali yake katika njia ya Mwenyezi Mungu isipokuwa Imam huyu mtukufu alitoa mali yake yote mara mbili. 2. Hakika yeye (as) alimgawia Mwenyezi Mungu mali yake mara tatu yaani alitoa sadaka nusu ya mali aliyokuwa anaimiliki katika njia ya Mwenyezi Mungu na hii ni amali tukufu pia. Pongezi kwa wale wema ambao wanapambana dhidi ya nafsi na mashetani, na kumfanya Imamu huyu kuwa mfano na kigezo chema kwao katika maisha na hivyo wanapata faida kubwa akhera katika makazi ya kweli mbele ya Mfalme Muweza.

Imamul-Husein (as) na sadaka yenye kuendelea Imepokuwa kwamba Imamu Husein (as) alinunua sehemu ambayo humo kuna kaburi lake – kutoka kwa watu wa Nainawaa na Ghadhariyah kwa dirham elfu sitini na akaitoa sadaka kwao na akatoa sharti kwamba waonyeshe kaburi lake na wawakaribishe wenye kulizuru kwa muda wa siku tatu.32 Imepokewa kwamba Husein bin Ali (as) alirithi ardhi na vitu vingine akav30


Sadaka yenye kuendelea itoa sadaka kabla hajavipokea.33 Nakutoka kwa Imam Al-Baqir (as) amesema Husein bin Ali (as) alitoa nyumba sadaka.34 Na kuna hadithi zingine zinazotusimulia sehemu ya sadaka za Imamu Husein (as), ni sawa sawa ziwe sadaka zenye kuendelea au nyinginezo, kati ya hizo ni hadithi hii. Bedui alikuja kwa Imamu Husein (as) naye amedhamini fidia kamili na ameshindwa kuilipa, akamwambia Imamu: Ewe mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu nimeshadhamini fidia kamili na nimeshindwa kuilipa, nikajisemea katika nafsi yangu: Namuomba mbora wa watu na sijaona mbora na mkarimu kuliko Ahlul-Bait wa Mtume wa Mwenyezi Mungu. Imamu Husein akamwambia. Ewe ndugu wa waraabu nakuuliza mambo matatu ukiyajibu yote nakupa yote. Bedui akasema: Ewe mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu aliye mfano wako anamuuliza aliye mfano wangu! Wewe ni kati ya wenye Elimu na utukufu? Husein akasema (as) ndio, nimemsikia babu yangu Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) anasema wema ni kwa kadri ya maarifa. Bedui akasema: Uliza unayotaka kama nitaweza nitajibu vinginevyo nitajifunza kutoka kwako, na hakuna uwezo ila kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Imam akamwambia amali gani ni bora zaidi? Bedui akasema: Kumwamini Mwenyezi Mungu Husein akamwambia: Ni kipi kitakachomwokoa mtu dhidi ya maangamio? Bedui akasema: Kumtumainia Mwenyezi Mungu Husein akamwambia: Ni lipi pambo la wanaume? 32 Mustadrakul-Wasail, Juz. 14, uk. 61 33 Mustadrakul-Wasail, Juz. 14, uk. 50 34 Mustadrakul-Wasail, Juz. 14, uk. 48

31


Sadaka yenye kuendelea Bedui akasema: Elimu pamoja na upole Hapa Imamu kwa swali hili akafungua matawi mawili, kamwambia: Kama akikosa hilo? Bedui akasema: Basi ni mali pamoja na heshima Husein akamwambia: Kama akikosa hilo Bedui akasema: Ufakiri uliyo na subira Husein akamwambia: Kama akikosa hayo Bedui akasema: Basi radi iteremke kutoka mbinguni na kumwagamiza, kwani anastahili hayo. Husein (as) akacheka na akampa kifuko humo kuna dinari elfu moja, na akampa pete yake yenye kito cha thamani, chenye thamani ya dirham laki mbili na akasema; Ewe bedui dhahabu mpe mdeni wako na pete itumie katika matumizi yako. Bedui akachukua na akasema: Mwenyezi Mungu anajua mahali pakuweka ujumbe wake.35

Imamu Zainul - Abidiyn (as) na Sadaka Yenye Kuendelea Imamu Zainul-Abidiyn (as) alikuwa anatoka usiku wa giza anabeba mizigo juu ya mgongo wake anakwenda mlango hadi mlango kisha anagonga na kumpa anayetoka na alikuwa anafunika uso wake anapompa fakiri - ili asimtambue.36 Kutoka kwa Muhammad bin Is’haq amesema watu wa mji wa Madina walikuwa wanaishi na wala hawajui chakula chao kinatoka wapi, alipofariki Ali bin Husein wakakosa waliyokuwa wanapelekewa usiku. Na alikuwa analisha nyumba mia moja za watu Madina na kila nyumba ilikuwa na jamaa wengi. Alikuwa unapoingia usiku na watu kulala, anato35 Biharul Anwar, Juz. 44, Uk. 196 36 Biharul Anwar, Juz. 46, uk. 89

32


Sadaka yenye kuendelea ka katika nyumba yake na anakusanya chakula kilichobakia kwa Ahali zake na kukiweka kwenye mifuko na kuvibeba mgongoni mwake na kwenda katika nyumba za mafakiri, naye anafunika uso na kuvigawa baina yao, na walio wengi walikuwa wanasimama kwenye milango ya nyumba wakimsubiri wanapomuona wanapeana habari na wanasema amekuja mbeba mifuko. Imepokewa kutoka kwa Imamul–Baqir (as) kwamba yeye anasema nilipokuwa namuosha baba yangu Ali bin Husein nilikuwa pamoja na waliomuona kati ya Ahali Bait zake, wakatazama sehemu za kusujudia - magoti mawili, migongo ya miguu miwili, matumbo ya viganja vyake na paji la uso wake wakakuta zimekuwa ngumu kutokana na athari za uchamungu hadi zimekuwa kama vile magoti ya ngamia, kisha wakatazama mabega yake wakakuta yamekuwa magumu wakamwambia Imamu: Ama alama hizi tumeshazijua. Je, hii ni nini iliyopo katika mabega yake? Akasema ilikuwa inapopita theluthi ya usiku anaamka na watu wote katika nyumba wameshalala anatawadha anasawali rakaa mbili nyepesi kisha anatoa kilichobakia katika chakula cha familia yake anakiweka katika mifuko kisha anakibeba mgongoni na anatoka hali akitaraji thawabu kwa siri bila yeyote kujua, na kuziendea nyumba ambazo humo kuna masikini na mafakiri, kisha anawagawia hali ya kuwa wao hawamtambui ila wao wameshajua hayo kutoka kwake, wakawa wanamsubiri na anapowasili wanasema huyu ndio mwenye kubeba mifuko na wanamfungulia milango yao, anawagawia yaliyomo katika mifuko na anaondoka nayo ikiwa tupu baada ya kutoa yaliyomo humo hali ya kuwa anatarajia fadhila za sadaka ya siri kwa hilo na fadhila ya mkono wake, kisha anarejea anasimama katika mihrabu anaswali usiku uliobakia, na hii alama mnayoiona katika mabega yake ni athari ya mifuko hiyo.

33


Sadaka yenye kuendelea

Al- Imam Swadiq (as) na Sadaka Yenye Kuendelea Kutoka kwa Hisham bin Salim amesema: “Abu Abdillah Swadiq (as) alikuwa linapoingia giza na ikapita nusu yake anachukua mfuko humo kukiwa kuna mikate, nyama na dirhamu, anabeba mgongoni mwake kisha anaenda nazo kwa wenye haja kati ya watu wa Madina na kuzigawa kwao, hali ya kuwa wao hawamtambui. Abu Abdillah Swadiq (as) alipofariki waliyakosa hayo, wakajua kwamba ni Abu Abdillahi ndiye aliyekuwa akiwapelekea. Na amepokea Al-Ma’aliy bin Khunaysi amesema: Abu Abdillah Swadiq (as) alitoka usiku na mvua ya rasharasha inanyesha, naye anakusudia kwenda kwa jamaa wa Bani Sa’idah, basi nikamfuata akawa ameangusha kitu, akasema: Bismillah, Ewe Mwenyezi Mungu kirudishe kwangu. Nikamwendea na kumsalimia. Akasema: Ma’aliy? Nikasema ndio, nijaaliwe kuwa fidia kwako. Akasema tafuta kwa mkono wako chochote utakachokikuta nipatie. Basi nikakuta mikate mingi imesambaa nikawa nampatia kipande kimoja, viwili naye akawa ana mfuko uliojaa mikate. Nikamwambaia niwe fidia kwako, nibebeshe. Akasema mimi nafaa zaidi kuliko wewe, lakini nifuate. Basi tukafika kwa jamaa tukawakuta wakiwa wamelala, ndipo akawa anaweka mkate mmoja, miwili hadi akamwendea wa mwisho wao. Tulipoondoka nikamwambia: Je, hawa wanajua jambo hili? Akasema (as) hapana. Hakika Mwenyezi Mungu hajaumba kitu isipokuwa kina mwangalizi wake anayekihifadhi, isipokuwa sadaka, kwani Mola Mlezi anaihifadhi Yeye Mwenyewe. 37

Miongoni mwa athari za sadaka duniani na akhera Zimepokewa hadithi nyingi kutoka kwa Nabii (saww) na Ahali zake watoharifu (as) kuhusiana na sadaka na athari zake nzuri duniani na yale aliyoyaandaa Mwenyezi Mungu kwa wenye kutoa sadaka huko akhera miongo37 Biharul-Anwar, Juz. 48

34


Sadaka yenye kuendelea ni mwa thawabu nzuri na neema zisizoisha. Na katika yafutayo tunataja baadhi ya hadithi hizo:-

Zinazima ghadhabu ya Mola Mlezi Anasema Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww): Hakika sadaka inazima ghadhabu ya Mola Mlezi.38

Zinaongeza mali Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww): “Hakika sadaka haiongezei mali isipokuwa wingi, toeni sadaka Mwenyezi Mungu atawahurumia.” Mtu alimwambia: Nifundishe kazi nitakayoifanya itaongeza mali yangu. Akasema (saww): Ukitaka mali yako iongezwe basi zidisha kutoa sadaka. Na imepokewa kwamba Imam Swadiq (as) alimwambia mwanae Muhammad: Ewe Mwangu kiasi gani kilichobakia pamoja nawe katika matumizi hayo? Akasema Dinari arobaini. Akasema: Toka kazitoe sadaka. Akasema hazijabaki isipokuwa hizo tu. Akasema zitoe sadaka kwani Mwenyezi Mungu ataziongezea. Je, hujajua kwamba kila kitu kina ufunguo wake na ufunguo wa riziki ni sadaka, hivyo zitoe sadaka. Akafanya hivyo. Hakukaa Abu Abdillah Swadiq (as) isipokuwa siku kumi tu, akapata badala yake dinari elfu nne. Akasema (as) Ewe mwanangu tumempa Mwenyezi Mungu dinari arobaini na Mwenyezi Mungu akatupa dinari elfu nne. Na kutoka kwake (as) amesema: Teremsheni riziki kwa sadaka, mwenye kuwa na yakini ya kuongezewa anakuwa na ukarimu wa kutoa. Anasema Imamu Ali, Amirul–Muuminina (as): Mnapopatwa na ufakiri basi fanyeni biashara na Mwenyezi Mungu kwa kutoa sadaka. 38 Hadithi hii na zitakazo kuja zipo katika Mustadrakul–Wasail ‘Kitabuz Zakat abuwab swadaqah’

35


Sadaka yenye kuendelea

Huleta baraka Baraka maana yake ni kuongezeka, na kuongezeka kwa kila kitu ni kulingana na umbo lake, na sadaka ni kati ya mambo ambayo huleta baraka katika mali, na inamsaidia mwanadamu kulipa deni zake vile vile. Amesema Imam Swadiq (as): Hakika sadaka hulipa deni na kuleta baraka. Na amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww): Kamwe haijapungua mali kwa kutoa sadaka, basi toeni na wala msiogope.39 Hakika kutotoa sadaka maana yake ni woga mbele ya nafsi na shaitani, kama ambavyo kutoa sadaka maana yake ni ushujaa na changamoto. Na hadith ifuatayo inaunga mkono maana hii: Amesema Imam Ali (as): Siku moja nilitoa sadaka dinari moja, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) akasema: ”Ewe Ali! Hujui kwamba sadaka ya muumini haitoki mkononi hadi akombolewe na vitimbi sabini vya shetani wote wanaomwamrisha kutofanya hivyo.” Ikiwa mashetani wanashawishi katika moyo wa mwanadamu na kuuzuia mkono wake usitoe sadaka, basi hakika kutoa sadaka ni ushujaa na ushindi dhidi yao, kama ambavyo kutotoa sadaka ni woga na kujisalimisha kwao, na kwa sababu hii amesema Imam Ali Amirul-Muuminina (as): ”Shujaa kuliko watu wote ni yule aliyeshinda matamanio ya nafsi yake.”

Ni ponyo kwa mgonjwa Amesema Mtukufu Mtume (saww): Watibuni wagonjwa wenu kwa sadaka. Pia amesema ukitaka Mwenyezi Mungu ampe afya mgonjwa wako basi toa sadaka kwa wingi. Na akasema wala msidharau dua ya masikini kwa 39 Biharul-Anwar, Juz. 97, uk. 131

36


Sadaka yenye kuendelea wagonjwa wenu, kwani dua zao hukubaliwa kwenu na wala haikubali kwa ajili ya nasfi zao. Amesema Imam Ali (as): Sadaka ni dawa yenye kufaulu.

Inafuta Qadhwaa na Qadari Qadhwaa na Qadar iko aina mbili: Iliyotegemezwa Iliyohukumiwa Ya kwanza ndio ambayo kuna uwezakano wa kuizuia na kuiondoa, na uondoaji huu haupatikani isipokuwa kwa kufanya kheri na kutoa sadaka, kinapotokea kwa mwanadamu kinachofuta, hufutwa na kuondoka, vinginevyo inateremka. Ya pili ni ambayo haiwezekani kuizuia na kuiondoa kwa sababu imeshahukumiwa akidi. Sadaka ina athari kubwa sana katika kubadilisha Qadhaa na Qadar iliyotegemezwa, na kuepusha balaa kwa mwanadamu. Imepokewa kwa Nabii (saww) siku moja alipitia kwa Myahudi anakata kuni jangwani akawaambia masahaba wake; “Hakika huyu Myahudi leo atang’atwa na nyoka na kufa. Ulipofika mwisho wa mchana Myahudi alirejea na kuni kichwani mwake kama kawaida yake. Watu wakamwambia: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu hatujaona useme yasiyotokea. Mtume (saww) akasema na ni kipi hicho? Wakasema: Hakika umetoa habari leo kwamba huyu Myahudi atang’atwa na nyoka na kufa lakini amesharejea! Akasema (saww) niitieni. Akaja kwake akasema: Ewe Myahudi weka kuni na zifungue, akazifungua akaona nyoka. Akasema: Ewe Myahudi umefanya wema gani leo? Akasema: sijafanya kitu isipokuwa nilitoka na keki mbili nikila moja kisha 37


Sadaka yenye kuendelea akaniomba masikini, nikampa ile nyingine. Akasema (saww): Hiyo keki ndio imekuokoa kutokana na nyoka. Basi akasilimu mbele yake. 40

Huongeza umri Amesema Imamu Baqir (as): Wema na sadaka huondoa umaskini na huongeza umri na vinamkinga mwenye kuvifanya na balaa sabini.

Huondoa balaa Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww): “Sadaka inazuia balaa hata kama imeshaanza kuteremka.� Na amesema (saww): Hakika mwombaji alisimama katika hema na humo kuna mwanamke na mbele yake kuna mtoto mchanga kwenye susu, alikuwa anakula na haikubakia isipokuwa tonge moja tu, basi akampa, baada ya muda mbwa mwitu akampora mtoto kwenye susu yake, akamfuata kidogo basi akamtupa bila ya kumdhuru, na akasikia sauti inasema tonge kwa tonge.

Ama athari za sadaka katika akhera nakutajia baadhi yake Huongezeka mbele ya Mwenyezi Mungu Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) amesema: Eee Mwenye kutoa sadaka basi kwa kila uzani wa dirhamu una mfano wa mlima Uhud miongoni mwa neema za peponi. Na anasema (saww): Mwenye kutoa dirhamu moja katika njia ya Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu humwandikia mema mia saba. 40 Mustadrakul-Wasail

38


Sadaka yenye kuendelea

Hutakasa maovu Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww): Unapofanya kosa basi toa sadaka.� Na anasema tena (saww): Sadaka hufuta makosa kama maji yanavyozima moto.

Huzuia Moto Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) amesema: Toeni sadaka, kwayo mtazuia nyuso zenu na Moto. Na amesema (saww): Naapa kwa aliyenituma kwa haki kuwa Nabii, hakika kati ya waja wa Mwenyezi Mungu watasimama sehemu ambapo zinatoka ndimi za moto kubwa kuliko milima yote ya duniani na hapatokuwa na kizuizi baina yake na ndimi hizo, atakapokuwa awetayari katika hali hiyo ghafla itaruka hewani mikate, vipande vya fedha alizompa ndugu yake muumini katika kumkirimu kwake, na kuteremka karibu yake na kuwa kama mfano wa mlima mkubwa kabisa wenye kumzunguka na kumzui na moto, hivyo halitompata joto lake wala moshi wake hadi atafika peponi.

Zitakuwa Kivuli Siku ya Kiyama Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) amesema: Muumini atakuwa katika kivuli cha sadaka yake Siku ya Kiyama. Na amesema (saww): �Ardhi ya Kiyama yote ni moto isipokuwa kivuli cha muumini, kwani sadaka yake itampa kivuli.

Katika adabu za sadaka Kuna adabu za kutoa sadaka nazo zimetajwa katika Aya za Qur’ani na hadithi tukufu, tunaashiria baadhi yake katika yafutayo:-

1. Kuiona kuwa ni ndogo Yaani usiione sadaka yako kuwa ni kubwa na nyingi bali izingatie kuwa ni ndogo na ni chache. Imam Ali Amirul-Muuminina (as) amesema katika 39


Sadaka yenye kuendelea khutuba ya Al-Mutaqiyna: “Hawatosheki na amali zao chache wala kingi hawakioni kuwa ni kingi.

2. Kuifanya kwa siri Hakika kutoa sadaka kwa siri ni bora zaidi kuliko sadaka ya wazi. Amesema (swt):

“Kama mtadhihirisha sadaka zenu basi ni vizuri na kama mtaitoa kwa siri na kuwapa mafakiri basi ni bora zaidi kwenu na inawafutia maovu yenu, na Mwenyezi Mungu ni mjuzi wa mnayoyafanya.” (Sura al–Baqarah: 271).

3.Kufanya haraka kuitoa Hakika kufanya haraka kutoa sadaka na kufanya kheri ni jambo linalotakiwa na ni mustahabu kisheria. Anasema (swt):

“Fanyeni haraka kuyaendea maghfira ya Mola wenu na pepo ambayo upana wake ni sawa na upana wa mbingu na ardhi, imeandaliwa kwa ajili ya wachamungu ambao wanatoa katika hali ya neema na wakati wa dhiki.” (Sura Al Imran: 133). Amesema Imam Ali, Amirul-Muuminina (as) katika wasia wake kwa 40


Sadaka yenye kuendelea mtoto wake Imamu al-Hasan (as): Kama utampata kati ya watu mafakiri mwenye kubeba mzigo wako hadi Siku ya kiyama na kukupatia kesho ambapo unaihitajia, basi mtumie na umbebeshe na muongezee zaidi ukiweza, kwani huenda utamtafuta na wala usimkute tena.41 Na adabu hizi tatu zinakusanywa na hadithi hii tukufu: Anasema Imam Swadiq (as): Nimeona kwamba mambo mema hayatengenei ila kwa mambo matatu: kuiona kuwa ni dogo, kuifanya kwa siri na kuharakisha, kwani unapoiona kuwa ni ndogo utaiheshimu kwa yule unayemfanyia, na unapoifanya kwa siri utaikamilisha, na unapoifanya haraka utamburudisha, na ikiwa haikuwa hivyo basi utaiharibu. Ewe msomaji mtukufu, zimepokewa hadidhi nyingi zinazokataza kuahirisha jambo la kheri na kumhadharisha mwanadamu kuchelewesha, nayo ni kusema nitafanya kadhaa, nitatoa sadaka katika njia ya Mwenyezi Mungu n.k. Mtume wa Mwenyezi Mungu anasema (saww): Ewe Abu Dhar, jihadhari na kuchelewesha matarajio yako kwani wewe ni wa siku uliyomo na wala sio wa siku ijayo. Na Imam Baqir (as) amesema: Jihadhari na kuahirisha kwani hiyo ni bahari humo wanaghariki wenye kuangamia.42 Na Imamu Swadiq (as) amesema: Unapokusudia jambo la kheri basi usilicheleweshe. Hakika maisha ni fursa na fursa inamalizika na wala haibaki, na majuto ni kwa yale uliyoyapoteza. Imam Ali, Amirul-Muuminina (as) amesema: Iwahi fursa kabla haijakuwahi. 41 Nahjul-Balaghah. 42 Biharul Anwar, Juz. 77

41


Sadaka yenye kuendelea Imamu Hasan Al- Mujtaba (as); Amesema Fursa ni yenye kupita haraka na hurejea pole pole mno. 43 Na amesema (swt): Hamtapata wema hadi mtoe mnayoyapenda.

4. Kubusu mkono Ni suna mwanadamu kubusu mkono wake baada ya kutoa sadaka kwani imepokewa kwamba Mwenyezi Mungu huichukua kabla haijafika katika mkono wa muombaji. Na amesema (saww): “Na anachukua sadaka.” (Sura Al Imran. 92). Hapana shaka kwamba Mwenyezi Mungu ametakasika kutokana na kiwiliwili na viungo, hivyo Aya hii na mfano wake – ni majazi ya kumkubalia haraka, wingi wa malipo na thawabu.

5. Dua Ni suna kwa mwenye kutoa sadaka kumuomba yule anayempa sadaka amuombee dua, kwani imepokewa kwamba dua ya fakiri inajibiwa kwa muombaji.

6. Kipaumbele ni kwa jamaa wa karibu Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) amesema hakuna kutoa sadaka hali ya kuwa jamaa wa karibu anahitaji. Hivyo kipaumbele katika kutoa sadaka ni wajibu iwe kwa jamaa na ndugu wa karibu kisha watu wema kati ya waumini. Bila shaka wazazi wawili wao ndio wa mwanzo, bali ni juu ya mwanadamu kuwatanguliza wao katika matumizi na kufanya haraka kuwafanyia wema kwani radhi ya Mwenyezi Mungu (swt) ni kutokana na 43 Kitabul Ghaarat, Juz. 2 uk: 635

42


Sadaka yenye kuendelea radhi ya wazazi wawili.

7. Kujiepusha na Majigambo na Adha Amesema (swt):

“Ambao wanatoa mali zao katika njia ya Mwenyezi Mungu kisha hawafuatizii waliyoyatoa kwa majigambo wala adha wana malipo kwa Mola wao na hakuna hofu juu yao na wala hawatohuzunika.” (Sura al-Baqarah: 262) Na amesema (swt):

“Enyi mlioamini msibatilishe sadaka zenu kwa masimbulizi na adha.” (Sura al-Baqarah: 264) Baadhi ya wafasiri wamesema: Al-manna (masimbulizi)– hapa ni kuiona nafsi yake kuwa ni njema, ni wajibu wa mwenye kutoa kuzingatia kwamba yeye anamuwakilisha Mwenyezi Mungu, na kwamba majigambo ni ya Mwenyezi Mungu juu yake, na kwamba yeye ni mwenye upungufu katika kutoa. Na adha maana yake ni kuaibisha, kukunja uso na kumdharau muombaji, yote haya ni katika adha ambayo hubatilisha malipo.

43


Sadaka yenye kuendelea

Maelezo Raghaba yangu ilikuwa ni kutaja kutoka katika maisha ya kila Imamu kati ya Maimamu watoharifu (as) mifano ya sadaka yeye kuendelea na mema yenye kubakia isipokuwa mazingira magumu yalinizuia kufikia raghaba hii. Namuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu anipe tawfiki ya hilo katika chapa ya pili ya kitabu hiki Inshallah. Na baada ya yote hayo hakika mimi sidai kuyajua na kuyaeleza yote bali ni tone tu, katika bahari kubwa. Namuomba Mwenyezi Mungu ayakubali haya kwa upole Wake na ukarimu Wake. Na rehema na amani zimwendee Bwana wetu Muhammad (saww) na kizazi chake chema kitoharifu. Mwisho wa ulingano wetu; shukrani zote anastahiki Mola Mlezi wa walimwengu.

44


Sadaka yenye kuendelea

ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION 1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9. 10. 11. 12. 13. 14. 15. 16. 17. 18. 19. 20. 21. 22. 23. 24. 25.

Qur'an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Thelathini Uharamisho wa Riba Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili Hekaya za Bahlul Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.) Hijab vazi Bora Ukweli wa Shia Ithnaashari Madhambi Makuu Mbingu imenikirimu Abdallah Ibn Saba Khadijatul Kubra Utumwa Umakini katika Swala Misingi ya Maarifa Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia Bilal wa Afrika Abudharr Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu Salman Farsi Ammar Yasir Qur'an na Hadithi Elimu ya Nafsi Yajue Madhehebu ya Shia 45


Sadaka yenye kuendelea 26. 27. 28. 29. 30. 31. 32. 33. 34. 35. 36. 37. 38. 39 40. 41. 42. 43. 44. 45. 46. 47. 48. 49. 50. 51. 52. 53. 54.

Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur'an Tukufu Al-Wahda Ponyo kutoka katika Qur'an. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii Mashukio ya Akhera Al Amali Dua Indal Ahlul Bayt Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna. Haki za wanawake katika Uislamu Mwenyeezi Mungu na sifa zake Kumswalia Mtume (s) Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) Adhana. Upendo katika Ukristo na Uislamu Tiba ya Maradhi ya Kimaadili Maana ya laana na kutukana katika Qur'ani Tukufu Kupaka juu ya khofu Kukusanya swala mbili Bismillah ni sehemu ya Qur'ani na husomwa kwa Jahara Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Kusujudu juu ya udongo Kusherehekea Maulidi Ya Mtume (s) Tarawehe Malumbano baina ya Sunni na Shia Kupunguza Swala safarini Kufungua safarini Umaasumu wa Manabii Qur'an inatoa changamoto as-Salaatu Khayrun Mina -'n Nawm 46


Sadaka yenye kuendelea 55. 56. 57. 58. 59. 60. 61. 62. 63. 64. 65. 66. 67. 68. 69. 70. 71. 72. 73. 74. 75. 76. 77. 78. 79. 80. 81. 82.

Uadilifu wa Masahaba Dua e Kumayl Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mtume Muhammad (s) Nahju'l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza Nahju'l-Balaghah - Juzuu ya Pili Kuzuru Makaburi Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita Tujifunze Misingi Ya Dini Sala ni Nguzo ya Dini Mikesha Ya Peshawar Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu Ubora wa Imam 'Ali Juu ya Maswahaba Na Ushia ndio njia iliyonyooka Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake Liqaa-u-llaah Muhammad (s) Mtume wa Allah Amani na Jihadi Katika Uislamu Uislamu Ulienea Vipi? Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) Urejeo (al-Raja'a ) 47


Sadaka yenye kuendelea 83. 84. 85. 86. 87. 88. 89. 90. 91. 92. 93. 94. 95. 96. 97. 98. 99. 100. 101. 102 103. 104. 105. 106. 107. 108. 109. 110. 111.

Mazingira Utokezo (al - Badau) Hukumu ya kujenga juu ya makaburi Swala ya maiti na kumlilia maiti Uislamu na Uwingi wa Dini Mtoto mwema Adabu za Sokoni Johari za hekima kwa vijana Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu Tawasali Imam Mahdi katika Usunni na Ushia Hukumu za Mgonjwa Sadaka yenye kuendelea Msahafu wa Imam Ali Ngano ya kwamba Qur'ani imebadilishwa Idil Ghadiri Kusoma sura zenye Sijda ya wajibu Hukumu zinazomuhusu mkuu wa kazi na Mfanyakazi Huduma ya Afya katika Uislamu Sunan an-Nabii Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza) Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili) Shahiid Mfiadini Kumswalia Nabii (s.a.w) Ujumbe - Sehemu ya Kwanza Ujumbe - Sehemu ya Pili Ujumbe - Sehemu ya Tatu 48


Sadaka yenye kuendelea 112. 113. 114. 115. 116. 117. 118. 119. 120. 121. 122. 123. 124. 125. 126. 127. 128. 129. 130. 131. 132. 133. 134. 135. 136. 137. 138.

Ujumbe - Sehemu ya Nne Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu Hadithi ya Thaqalain Maarifa ya Kiislamu Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza Ukweli uliopotea sehemu ya Pili Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu Ukweli uliopotea sehemu ya Nne Ukweli uliopotea sehemu ya Tano Safari ya kuifuata Nuru Fatima al-Zahra Myahudi wa Kimataifa Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi Visa vya kweli sehemu ya Kwanza Visa vya kweli sehemu ya Pili Muhadhara wa Maulamaa Mwanadamu na Mustakabali wake Imam Ali ('a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Kwanza) Imam Ali ('a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Pili) Khairul Bariyyah Uislamu na mafunzo ya kimalezi Vijana ni Hazina ya Uislamu. Yafaayo kijamii Tabaruku Taqiyya Vikao vya furaha Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje? 49


Sadaka yenye kuendelea 139. 140. 141. 142. 143. 144. 145. 146. 147. 148. 149. 150. 151. 152 153. 154. 155. 156. 157. 158. 159. 160. 161. 162. 163. 164. 165. 166. 167.

Visa vya wachamungu Falsafa ya Dini Kuhuzunika na Kuomboleza - Azadari Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah Mtazamo Mpya - Wanawake katika Uislamu Kuonekana kwa Allah Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza) Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili) Ndugu na Jirani Ushia ndani ya Usunni Maswali na Majibu Mafunzo ya hukmu za ibada Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 1 Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 2 Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 3 Abu Huraira Vipengee kadhaa katika Swala ya Jamaa na Msikiti. Mazingatio kutoka katika Qur'an - Sehemu ya Kwanza Mazingatio kutoka kaitka Qur'an - Sehemu ya Pili Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya kwanza Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya Pili Qur'ani Tukufu - Pamoja na Tarjuma ya Kiswahili Falsafa ya Mageuzi ya Imam Husein (a.s) Amali za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani Elimu ya Tiba za Kiislamu - Matibabu ya Maimamu Uislamu Safi Majlisi za Imam Husein Majumbani Mshumaa Uislam wa Shia 50


Sadaka yenye kuendelea 168. 169. 170. 171. 172. 173. 174. 175. 176. 177. 178. 179. 180. 181. 182. 183. 184. 185. 186. 187. 188. 189. 190. 191. 192. 193. 194. 195. 196.

Amali za Makka Amali za Madina Asili ya Madhehebu katika Uislamu Sira ya Imam Ali kuhusu Waasi Ukweli uliofichika katika neno la Allah Uislamu na Mifumo ya Uchumi Umoja wa Kiislamu na Furaha Mas'ala ya Kifiqhi Jifunze kusoma Qur'ani As-Sahifatul Kamilah as-Sajjadiyyah Hayya 'Alaa Khayri'l-'Amal Katika Adhana Ukweli kuhusu Funga ya Siku ya Ashura Dua za Miezi Mitatu Mitukufu (Rajabu, Shaabani na Ramadhani) Uadilifu katika Uislamu Mahdi katika Sunna Jihadi ya Imam Hussein ('as) Kazi na Bidii ni njia ya maendeleo Abu Talib - Jabali Imara la Imani Ujenzi na Utakaso wa Nafsi Vijana na Matarajio ya Baadaye Usalafi - Historia yake, maana yake na lengo lake Ushia - Hoja na Majibu Mateso ya Dhuria wa Mtume (saww) Maombolezo - Msiba wa Bwana wa Mashahidi (a.s.) Shahidi kwa Ajili ya Ubinadamu Takwa Amirul Muuminina ('as) na Makhalifa Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.) Kuelewa Rehma ya Mwenyezi Mungu 51


Sadaka yenye kuendelea 197. 198. 199. 200. 201.

Mtazamo kuhusu msuguano wa kimadhehebu Upotoshaji Dhahiri katika Turathi (Hazina) ya Kiislamu Nchi na Uraia - Haki na wajibu kwa Taifa Mtazamo wa Ibn Taymiyyah kwa Imam Ali (a.s.) Uongozi wa kidini - Maelekezo na utekelezaji wa Kijamii

KOPI NNE ZIFUATAZO ZIMETAFSIRIWA KWA LUGHA KINYARWANDA 1. 2. 3. 4.

Amateka Na Aba'Khalifa Nyuma yaho naje kuyoboka Amavu n'amavuko by'ubushiya Shiya na Hadithi

52


Sadaka yenye kuendelea

BACK COVER Vitendo anavyovifanya mwanadamu - ni sawa viwe vyema au viovu – vinagawanyika katika sehemu mbili:Kwanza : Vitendo vya muda maalumu na wakati maalumu Pili: Vitendo ambavyo vinabaki kwa muda mrefu vinavyovuka mipaka ya wakati Mfano: Unaweza kumlisha fakiri chakula na kuondoa njaa yake kwa masaa kadhaa kisha anarejea katika hali ya njaa tena. Na unaweza kumshtumu mwislam – Mungu apishe mbali hayo – na kujeruhi hisia zake kisha unamtaka radhi na kumuomba msamaha, kitendo cha awali ni chema kilichotokea kwako na una malipo kwa Mwenyezi Mungu na una daraja nyingi Kwake. Na cha pili ni kiovu kilichotokea kwako na utahisabiwa kwacho Siku ya Kiyama isipokuwa akikusamehe ndugu yako mwislamu, na ukamuomba Mola wako maghfira na akakusamehe. Hii ndio sehemu ya kwanza. Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 / 2127555 Barua Pepe: alitrah@yahoo.com Tovuti: www.ibn-tv.com Katika mtandao: www.alitrah.info

53


Sadaka yenye kuendelea

54


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.