Sauti ya uadilifu wa binadamu

Page 1

Sauti ya Uadilifu wa Binadamu (Sawtu ‘l-‘Adalati ‘l-Insaniyyah)

Kimeandikwa na: George Jordac

Kimetarjumiwa na: Ramadhani Kanju Shemahimbo

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 1

9/4/2017 3:47:44 PM


©Haki Ya Kunaikli Imehifadhiwa Na: Al-Itrah Foundation

ISBN: 978 - 9987– 427– 22 – 2

Kimeandikwa na: George Jordac

Kimetarjumiwa na: Ramadhani Kanju Shemahimbo

Kimesomwa Prufu na: Mbarak A. Tila

Kimepangwa katika Komputa na: Al-Itrah Foundation

Toleola kwanza: Novemba 2008 Nakala: 1000 Toleo la pili: Machi, 2018 Nakala: 1000

Kimetolewana kuchapishwa na: Al -Itrah Foundation S.L.P. 19701, Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255222110640 / 2127555 Barua Pepe: alitrah@yahoo.com Tovuti: www.alitrah.info Vitabu mtandaoni: www.alitrah.info/ebooks/

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 2

9/4/2017 3:47:44 PM


Yaliyomo Dibaji ..................................................................................................................... 1 Neno la Mchapishaji................................................................................................... 2 Utangulizi.................................................................................................................... 4 Rasi (Peninsula) Ya Arabia......................................................................................... 5 Kuja kwa Mtume (s.a.w.w.)........................................................................................ 8 Kutupia macho historia............................................................................................. 12 Mtume (s.a.w.w.) na Abu Talib Ž............................................................................. 22 Mtume (s.a.w.w.) na Ali (a.s.)................................................................................... 26 Ali (a.s.) ni ndugu yangu........................................................................................... 28 Sifa za Ali (a.s.)......................................................................................................... 36 Elimu na Hekima za Ali (a.s.)................................................................................... 54 Haki za Binadamu na Ali (a.s.)................................................................................. 61 Umasikini na matokeo yake...................................................................................... 66 Hali ya mambo kabla ya Ali (a.s.)............................................................................. 82 Mtawala ni mmoja kati ya watu................................................................................ 93 Uhuru na vyanzo vyake ........................................................................................ 103 Uhuru wa mtu binafsi.............................................................................................. 112 Uwajibikaji.............................................................................................................. 115 Kuwasaidia wenye haja........................................................................................... 125 Sio ama ushabiki wa kupindukia wala hali kutokukosea........................................ 142 Ta’asub - Ushabiki uliokithiri................................................................................ 146 Vita na Amani......................................................................................................... 149 Kupambana na Dhulma........................................................................................... 161

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 3

9/4/2017 3:47:44 PM


Utawala wa Ali(a.s.) ............................................................................................... 168 Mkataba wa Umoja wa Mataifa juu ya Haki za Binadamu.................................... 172 Ali (a.s.) na thamani ya maisha............................................................................... 190 Mazingira yaliyokuwepo baada ya Ali (a.s.).......................................................... 196 Koo (Familia) mbili za Quraishi............................................................................. 216 Mu’awiyah na warithi wake.................................................................................... 224 Husein (a.s.) na Yazid............................................................................................. 241 Yazid alikuwa ni nani?............................................................................................ 245 Wafuasi wa makundi hayo mawili.......................................................................... 255 Wauaji wa Uthman.................................................................................................. 282 Mfululizo wa Shutuma............................................................................................ 291 Nini kilimtokea Abu Dhar baada ya kuhamishwa kwake....................................... 308 Maelezo kuhusu kuuawa kwa Uthman................................................................... 312 Maelezo ya makosa................................................................................................. 322 Njama kubwa watu wanaohusika na mauaji ya Uthman........................................ 336 Uasi dhidi ya Ali (a.s.)............................................................................................ 349 Ewe Mola! Kuwa Shahidi...................................................................................... 371 Walaghai wawili...................................................................................................... 379 Maafa ................................................................................................................. 399 Je! Ilikuwa ni halali?.............................................................................................. 408 Utashi wa Ki-Mbinguni.......................................................................................... 415 Waache waomboleze............................................................................................... 420

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 4

9/4/2017 3:47:44 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

َّ‫بِس ِْم ه‬ ‫َّح ِيم‬ ِ ‫للاِ الرَّحْ ٰ َم ِن الر‬

DIBAJI

K

itabu hiki ni toleo la Kiswahili la taasisi ya Al-Itrah Foundation. Chapisho lake limelenga kukidhi mahitaji ya kiroho ya zama hizi pamoja na Ubongo na fikra ­zinazokuwa za Muislam. Jitihada kubwa zimefanywa na Taasisi kuweka chapisho hili la Kiswahili katika msingi wa haki na wenye kukubalika katika Uislam. Unaombwa kwa Taadhima ukisome kitabu hiki katika malengo yaliyokusudiwa. Pia Unaombwa kuwasilisha kwetu maoni yako huru juu ya chapisho letu hili, jambo ambalo tutashukuru sana. Kutangaza ujumbe wa Uislam ni kazi ambayo inahitaji ushirikiano wetu sote. Taasisi inakuomba kuungana na kushirikiana kama ilivyoagizwa katika aya ya Qur’an: (Surat Saba’ 34:46). Na rehma za Allah ziwe juu yako. Wako katika Uislam. Al Itrah Foundation Barua Pepe: alitrah@yahoo.com SMS: +255 778 300 140

1

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 1

9/4/2017 3:47:44 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

َّ‫بِس ِْم ه‬ ‫َّح ِيم‬ ِ ‫للاِ الرَّحْ ٰ َم ِن الر‬

Neno La Mchapishaji

K

itabu kilichoko mikononi mwako, ni tarjuma ya kitabu cha Kiingereza kwa jina la: “The voice of Human Justice” Kitabu hiki lugha yake ya asili ni ya Kiarabu kwa jina la “Sawtu ‘l-’Adalati ‘l-Insaniyyah” Sisi tumekiita: “Sauti ya uadilifu wa Binadamu.” Kitabu hiki, “Sauti ya uadilifu wa Binadamu.” ni matokea ya utafiti wa kielimu uliofanywa na Mwanachuoni Mkiristo, George Jordac juu ya maisha ya Imamu Ali (as).

Imamu Ali (as) hakuwa kiongozi wa Waislamu tu bali wa wanadamu wote, kama anavyodhihirisha mwandishi huyu ambaye si Mwislamu. Maisha na mwenendo wa Imamu Ali (as) umewavutia watu wote marafiki na maadui, hali ambayo imemfanya kuwa kiongozi wa umma. Kwa hiyo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakukosea pale aliposema: “Man kuntu maulahu fahadha Aliyun maulahu – Ambaye mimi kwake ni kiongozi basi na huyu Ali ni kiongozi wake.” Mwanachuoni mtafiti huyu na mtu asiye na upendeleo wala ushabiki kama alivyo, amefanikiwa katika kuyaelezea maisha ya Imamu kwa kiasi kikubwa kwamba wale watakaobahatika kukisoma kitabu hiki wakawa nao si wenye upendeleo au chuki, watalazimika kusema kwamba ni kitabu cha wasifu wa mtu mkubwa mashuhuri ambaye alikuwa wa pili kwa Mtume wa Uislamu. Hili tena ni jaribio letu kubwa la kutoa kitabu kikubwa kinachohusu historia ya mtu kubwa kama huyu ambaye alilelewa na Mtukufu Mtume mwenyewe (s.a.w.w.), na akasoma katika shule yake kuanzia utoto wake mpaka alipofariki mwalimu wake huyo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Na ili kututhibitishia kwamba yeye (Imamu Ali) amesoma na kupata ujuzi na elimu kubwa kutoka kwake, Mtukufu Mtume akasema: “Anna madinatu’l ilm wa Aliyun babuha – Mimi ni jiji la elimu na Ali ni lango lake” Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote, ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni mambo ambayo hayana nafasi tena katika akili za watu.

2

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 2

9/4/2017 3:47:44 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Kutokana na ukweli huo, Taasisi yetu ya ‘Al-Itrah Foundation’ imeona ikitoe kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili, kwa madhumuni yake yale yale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili. Tunamshukuru ndugu yetu, Al-Akh Ramadhani Kanju Shemahimbo kwa kukubali jukumu hili la kukifanyia tarjuma kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwa kitabu hiki. Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa ni mwanga kwa wasomaji wetu na kuzidisha upeo wao wa elimu ya dini na ya kijamii. Mchapishaji: Al-Itrah Foundation

3

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 3

9/4/2017 3:47:44 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

َّ‫بِس ِْم ه‬ ‫َّح ِيم‬ ِ ‫للاِ الرَّحْ ٰ َم ِن الر‬

Utangulizi

H

istoria ya watu mashuhuri ni chemchemi ya maarifa, imani na zinduko kwetu sisi – chemchemi ambayo kamwe haitakauka. Watu mashuhuri wa ulimwengu ni kama vilele vilivyoinuka juu sana vya milima ambavyo tunatamani kuvipanda kwa hamu na shauku kubwa. Wao ni minara ya taa ambayo inafukuza giza kutoka karibu yetu. Ni kutokana na mifano ambayo wameiweka wao kwamba mpaka sisi tumepata kujiamini. Wametufanya sisi tuwe na matumaini ya maisha, wakatufundisha malengo na madhumuni yake na wakatusaidia sisi kunufaika na vistawishi vyake. Kama nafsi hizi maarufu zisingekuwepo, basi tungeangukia kuwa mawindo ya ukata tamaa wakati tunapokabiliana na nguvu zisizoonekana na zinazofahamika na tungesalimu amri wenyewe kwenye kifo. Hata hivyo, watu waadilifu hadi sasa hawajajisalimisha wenyewe mbele ya kukata tamaa na wala hawatafanya hivyo katika siku za usoni, kwa sababu wao wamejaaliwa ushindi na mafanikio. Hili linathibitishwa na ukweli kwamba katika historia watu wengi wamekuwa na mafanikio na kushinda, na Ali ni mmoja wao. Watu watatu ambao walishinda kifo wako nasi wakati wote. Ingawa wakati na nafasi vinawatenganisha wao na sisi, sio wakati unaotukataza sisi kusikia maneno yao wala umbali kutuzuia sisi kuziona nyuso zao.

Ushahidi bora kabisa wa kile kilichosemwa hapo juu ni kitabu hiki tulichonacho sasa hivi. Ni wasifu wa mtu mashuhuri sana. Ingawa alizaliwa Arabuni lakini utu wake haukukusudiwa kwa Arabia peke yake tu. Ingawa chemchemi za upole wake na fadhila zake zilichipukia kutoka kwenye Uislamu, yeye hakuwekewa mipaka kwa Waislamu peke yao. Kama angekuwa kwa ajili ya Waislamu tu, Mkristo asingeshawishika bila kujijua kuchunguza matukio ya maisha yake na kusifu sana kama mshairi, maamuzi yake ya kuvutia sana, matendo yake ya ujasiri wa ajabu na matukio ya kuvutia ya maisha yake. Ubingwa wa Ali haukuishia kwenye uwanja wa vita tu. Yeye alikuwa vilevile halinganishiki katika masuala ya imani, uchamungu, usafi, fasaha, ukarimu, msaada kwa wale wasiojaliwa kuwa na kitu na waliokandamizwa na kuunga mkono ukweli. 4

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 4

9/4/2017 3:47:44 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Kiasi kwamba hata baada ya kupita miaka zaidi ya kumi na nne elfu mafanikio yake ya ajabu yamekuwa ni mwanga mkubwa kwetu sisi, na wenye msaada mkubwa sana kwa ajili ya kuyafanya maisha yetu kuwa ya hali ya juu sana. Mwandishi ameyaelezea matukio mbalimbali kwa ufupi na pia akataja kwa kirefu maoni na imani za Imam kuhusiana na masuala ya kidini, siasa, na kiuchumi. Zaidi ya hayo, ameyaeleza matukio ya maisha ya Ali kwa umahiri na kwa namna ambayo hayajawahi kuandikwa hapo kabla. Hakuna mwanahistoria au mwandishi, awe stadi au mahiri kiasi gani, anayeweza kuleta taswira ya Amirul-Mu’minin hata katika kurasa elfu moja, wala anayeweza kuyaelezea yale matukio ya kutisha yaliyotokea katika wakati wa uhai wake. Mambo ambayo mtu huyu wa kipekee na asiye na kifani aliyoyafikiria, na aliyoyashughulikia, hayajawahi hadi sasa kuonwa au kusikiwa na mtu yoyote. Ni mengi zaidi kuliko kiasi anachoweza kuandika mwanahistoria hata katika tasnifu ya kinaganaga sana. Hivyo, picha au taswira yoyote itakayoelezwa na mwandishi itakuwa kwa vyovyote vile bila kupingwa ni isiyokamilika. Hata hivyo, lengo la mtunzi katika kuandika kitabu kama hiki ni kukusanya maelezo ya matendo na maneno ya Amirul-Mu’minin kutoka kwenye vyanzo vyote vinavyowezekana na kutafakari juu ya hayo kwa makini kabisa na kisha kuyawasilisha katika namna ambayo itawezekana kupata japo kuona picha ya juu juu ya Imam kama alivyokuwa. Hiki ndio ambacho mtunzi huyu amefanya ndani ya kitabu hiki. Nina uhakika kwamba George Jordac, mwanachuoni mtafiti na mtu asiye na upendeleo wala ushabiki kama alivyo, amefanikiwa katika kuyaelezea maisha ya Imam kwa kiasi kikubwa na wale waliokisoma watalazimika kusema kwamba ni kitabu cha wasifu wa mtu ambaye alikuwa wa pili kwa Mtume wa Uislamu. Michael Na’iman. *Huu ni utangulizi wa toleo la kwanza la tafsiri ya Kiarabu iliyochapishwa mnamo mwaka 1956. Rasi (Peninsula) Ya Arabia Eneo la Arabia ni la ajabu sana na la kimuujiza, na litadumu na sifa hii hata katika siku za baadaye. Lina majangwa makubwa sana. Kama majangwa haya yasingekosa mvua, na yakawa ya kijani na yenye rutuba, ardhi hii ingeweza kuwalisha wenye njaa na kuwavisha wasio na nguo wa dunia nzima. Hata hivyo, kwa bahati mbaya, 5

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 5

9/4/2017 3:47:44 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Arabia siku zote imebakia kuwa jangwa. Ina maeneo makubwa yaliyo na matuta ya mchanga, vilima vidogo na vikavu na maeneo yenye mawe ambayo hayalimiki wala hayakaliki. Kama ukulima ungewezekana, jimbo au eneo hili lingekuwa na watu wakazi wengi sana, lakini hali ni kinyume chake. Ingawaje nchi hii imezungukwa na bahari katika pande zake tatu, mvua zake ni ndogo sana na kuna joto sana wakati wa kiangazi. Vile vile huwa inanyesha katika baadhi ya sehemu ambapo inafanya hali ya hewa kupoa kiasi. Hata hivyo, wakati pepo zenye joto kali zinapovuma, kunakuwa na joto sana kiasi kwamba miti na mimea hukauka na hata wanyama hufa kwa joto. Washairi wa Kiarabu hufananisha zile pepo za magharibi, ambazo huvuma kutoka upande wa mashariki na upepo mwanana wa Peponi. Hakuna mito ya kudumu ndani ya Arabia. Hata hivyo, pale mvua zinapofika na vijito kuanza kutiririka, watu wanaitumia nafasi hiyo na kuhifadhi maji kwa kujenga mabwawa. Maji haya yanatosha kwa muda tu. Ngamia ni mnyama wa asili wa Arabia ambaye ana nafasi ya kipekee, akilinganishwa na wanyama wanaopatikana katika maeneo mengine. Mwenyezi Mungu Mtukufu amempa miguu mirefu ili aweze kutembea masafa marefu kwa urahisi na asiweze kuchoka katika majangwa ya kuhuzunisha. Kwato zake pia ziko katika namna ambayo kwamba nyayo zake hazizami katika michanga. Pia anao ustahimilivu (stamina) wa kutosha kuweza kuvuka zile njia ngumu na zenye matatizo, na anaweza kuvumilia joto na kiu vile vile. Mungu amemjaalia kuwa na tumbo la kipekee ambalo linaweza kuhifadhi maji ya kutosheleza kwa siku nyingi, na wakati ambapo maji hayapatikani, mmiliki wake pia hutoa maji kwa namna fulani kutoka tumboni mwake kwa ajili ya matumizi yake binafsi. Waarabu wamempa mnyama huyo maelfu ya majina. Uotaji majani ni wa nadra sana katika nchi hii. Vichaka kadhaa vya miiba huwa vinaota, lakini navyo pia vinanyauka kwa sababu ya upungufu wa maji na joto kali. Makazi ya watu kwa kawaida ni mahema ambayo hayawezi kuwalinda ama kutokana na pepo zenye joto au kutokana na joto la jua. Kwa kweli hakuna tofauti ya kuishi kwenye mahema haya na kule kuishi chini ya anga tupu. Kutokana na sababu hizi, idadi ya watu wake ni ndogo sana na iliyotawanyika. Watu wa Arabia kwa kawaida hawaishi mahali pamoja kwa maisha ya kudumu bali huwa wanahama kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine. 6

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 6

9/4/2017 3:47:44 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Chakula kikuu cha Waarabu ni tende zilizokaushwa. Juu ya hizi inaongezeka nyama ya ngamia na wanyama wa kuwindwa. Kwa sababu ya kutumia kwao maisha yao kudumu ndani ya majangwa, mambo ya vita na umwagaji damu yamekuwa ni sehemu ya asili yao. Ni joto sana katika jangwa na mabonde ya Rasi ya Arabia, kiasi kwamba ardhi inalimbikiza joto la kutosha kuwawezesha watu kuoka wanyama wao kwenye mchanga. Majangwa kama hayo hayo, yaliyojaa mchanga, yenye idadi ndogo ya watu iliyotawanyika, na kufanana kwa hali ya mazingira, ni mambo ya kuchosha sana na yanafanya maisha kuwa yasiyopendeza. Hamu ya kupata kitu bora, na matumaini ambavyo ni vitu vya msingi wa maisha ya starehe havipatikani mahali popote katika jangwa hili. Katika mazingira magumu kama haya, na maisha yasiyobadilika, ilikuwa haiwezekani kwa Waarabu wahamaji kuweza kuzoeana na mabadiliko ya maisha, na njia na tabia mbalimbali za watu wengine wa dunia hii. Kuwepo kwa uadilifu na uchamungu ambako kunaufanya moyo wa mwanadamu kuikubali dini, hakuwezi kufikiriwa katika ardhi kame. Tabia kama hizo zinachipukia kwenye nchi iliyostawi na yenye rutuba, na sio kwenye maeneo ya mawe na makavu. Zinakua ndani ya watu waliopata neema za kila aina na sio katika nyoyo za wale ambao wamezikosa neema hizo. Miji midogo midogo michache na makazi ya nyakati zile haikuwa yenye maana sana, kwanza kwa sababu idadi yao ilikuwa ndogo sana, na pili hadhi yao haikuwa tofauti na mahema machache yaliyosimikwa kwenye jangwa tupu, ambalo lilikuwa lipatwe na mashambulizi ya upepo mbaya usiofaa. Kwa kweli, huko Taif na Madina hali nzuri ya kimaisha ilikuwa inapatikana. Na kuhusu Makkah, yenyewe ilikuwa ni hekalu la masanamu. Wakazi wake walikuwa ni wachuuzi ambao machoni mwao dinari moja ilikuwa na thamani kuliko maisha ya mwanadamu. Maisha ya umasikini na ufukara ndani ya jangwa linalochoma kama jahannam na kudhihiri kwa ukatishaji tamaa na mustakabali usio na matumaini – hii ndio iliyokuwa hali ya ile iliyokuwa ikiitwa Rasi ya Arabia. Kinachoshangaza ni hiki kwamba, ingawa kuna ardhi nyingi sana zinazopakana na Arabia, ambazo zina rutuba na zina vistawishaji vyote muhimu kwa maisha, kuna watu ambao walipuuza urahisi wote huu, na kupendelea kuishi maisha duni katika ardhi hizi kame. Wao, kwa hiyo, kamwe hawakufikiria kutoka nje ya jangwa hili. 7

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 7

9/4/2017 3:47:44 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Na cha kushangaza zaidi ni kwamba, watu wa pale waliiona ardhi yao ya nyumbani kama bora zaidi kuliko dunia yote iliyobakia. Hawakutaka imma kuiacha wala kuchagua sehemu nyingine kama ardhi ya nyumbani kwao. Huu ulikuwa ni muujiza wa Jangwa la Arabia, hata kabla ya mtume wa Uislamu hajateuliwa katika kazi hiyo ya kitume. Hata hivyo, kama tutalinganisha hivi vijito baridi na vitamu, ardhi yenye rutuba na ya kijani, mandhari mazuri, utajiri na neema zote nyingine zinazopatikana kwenye nchi mbalimbali, mbali na Arabia, na kile kilichotokea katika ardhi hiyo, neema zote hizo na fursa muhimu zinaonekana kutokuwa na thamani. Jangwa la Arabia, nchi ya miujiza mingi, ilitoa kitu ambacho ni bora juu ya neema zote nyinginezo. Kiumbe yule muungwana alikuwa ndio haiba, mtu mashuhuri ambaye alitawanyisha rehema zake juu ya wanadamu wote, ambaye alisafisha chemchemi zote za ukweli, kwa sababu yake ambaye thamani ya maisha ilikuja kujulikana, uadilifu na wokovu vikawa ni mambo makubwa, na ukweli ulinyanyuliwa hadhi, yaani, Muhammad. Kuzaliwa na binamu yake Muhammad, Ali, katika Arabia, ambako maisha yalikuwa na thamani ndogo kuliko dinari kulikuwa ni muujiza wa pili wa Jangwa hili. Kuja Kwa Mtume {S.A.W.W.} Pamoja na macho yanayomeremeta kama jua linalowaka, ukweli kwenye midomo ming’aavu kuliko mwanga wa jua, moyo msafi zaidi kuliko maua ya bustani za Yathrib na Ta’if, tabia na maadili mazuri zaidi kuliko usiku wa mbaramwezi wa siku za Hijazi, akili yenye wepesi kuliko upepo wenye nguvu, ulimi unaoduwaza, moyo wenye mwanga wa kiungu; dhamira na utambuzi imara kama upanga mkali na maneno ya ki-ungu katika huo ulimi – huyo alikuwa ni Muhammad mwana wa Abdullah, Mtume wa Arabia, mtume ambaye aliyabomoa masanamu ambayo yalikuwa yamewatenganisha ndugu na ndugu. Hakuyavunja masanamu ya miti na mawe tu, bali pia aliyavunja masanamu ya utajiri, tabia mbaya na mwelekeo wa kivikundi. Kitu pekee wale Maquraishi waoga walichokitaka ni kwamba pesa ziweze kuhamishwa kutoka kwenye mikono ya wale Waarabu wahamaji hamaji, kuja kwenye mifuko yao wenyewe. Thamani pekee waliyoiambatanisha kwenye maisha ilikuwa ni kwamba, ili waweze kupata faida, wapasike kusafiri kupita kwenye jangwa juu ya migongo ya

8

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 8

9/4/2017 3:47:44 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

ngamia, wakikabiliana na matatizo makubwa, na kisha warudi kwenye mji wao wa nyumbani Makkah – Makkah hiyo hiyo ambayo ilikuwa jiji la ibada ya masanamu, na ambako ni pesa tu ndio ilikuwa na thamani. Ghafla waliisikia sauti ambayo iliwavunja moyo. Matumaini yao yaliharibika kabisa. Dunia iliwapa kisogo ikisema: “Thamani ya mwanadamu sio sawa na hiyo mliyokadiria, na lengo la kuumbwa kwa Waarabu wahamaji sio sawa na hilo mnalofikiria ninyi kuwa.” Hii Ilikuwa Ni Sauti Ya Muhammad Banu Asad na Banu Tamim walikuwa wapumbavu na wajinga kiasi kwamba waliwazika mabinti zao wakiwa hai, bila ya sababu yoyote. Hapakuwa na haki juu ya wao kufanya hivyo, isipokuwa kwamba ilikuwa ni desturi ambayo ilidumu miongoni mwao. Walikuwa wako kinyume na utashi wa Ki-ungu. Waliuchukia uzuri wa maumbile asilia. Na halafu wakasikia sauti, ambayo ilikuwa yenye kuonyesha hisia za upendo wa kina na huruma juu ya watu ikisema: “Msiwazike mabinti zenu wakiwa hai. Mabinti hao ni viumbe wazuri wa Mwenyezi Mungu kama walivyo watoto wenu wa kiume. Hakuna mwanadamu mwenye haki ya kuwanyima wengine uhai wao. Ni Mwenyezi Mungu peke yake anayewaumba watu na kuwafanya wafe.” Hii Ilikuwa Ni Sauti Ya Muhammad Waarabu walikuwa wakipigana wakati wote. Walipigana na kumwaga damu kwa miaka mingi, kwa sababu ya mambo ya kipuuzi yasizo na maana hata kidogo. Waliwaua ndugu zao wenyewe na kisha wakafurahia na kujisifu wenyewe juu ya hilo. Kuyatoa mhanga maisha yao wenyewe kwa ajili ya ujinga wao binafsi lilikuwa ni jambo la kawaida tu kwao. Watoto walilia na kupiga makelele, na wakakua katika hali ambayo haikusaidia katika kujenga mapenzi na huruma kwa yoyote katika akili zao. Katika mazingira haya waliisikia sauti nyingine ambayo ilisema: “Mnafanya nini ninyi? Mnauana ingawaje ninyi nyote ni ndugu, kwa sababu wote mmeumbwa na Mwenyezi Mungu. Ugomvi ni jambo la kishetani. Amani na urafiki ni mambo yenye faida zaidi kwenu. Neema ambazo kwazo mnapigania haziwezi kupatikana ila kwa kupitia kwenye amani.” 9

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 9

9/4/2017 3:47:44 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Hii, Pia Ilikuwa Ni Sauti Ya Muhammad Waarabu walikuwa ni watu kiburi na wabinafsi sana. Waliwaona wale wasiokuwa Waarabu kama ni watu duni kwao wenyewe. Sio hivyo tu bali pia waliwaona wasiokuwa Waarabu kama sio binadamu kamwe. Muhammad hakuipenda kabisa tabia hii ya Waarabu. Akiongea na watu hawa kiburi, yeye alisema: “Hakuna Mwarabu ambaye ni bora kuliko asiye Mwarabu isipokuwa awe ni mchamungu sana. Ama mpende msipende, wanadamu wote ni ndugu kwa kila mmoja wao.” Walikuwepo waliokandamizwa, wasiokuwa na makazi na watu wasiojiweza, ambao nyuso zao zimepaushwa na upepo wenye joto. Jamii iliwatelekeza na kuyafanya maisha yao kuwa ya wasiwasi. Walikuwa dhalili mbele ya macho ya watu kuliko chembe chembe za mchanga, na maisha yao yaligeuka kuwa yasiyotamanika kabisa. Na hawa walikuwa ndio marafiki halisi wa Mtume wa Uislamu, kama vile masikini na waliotengwa na jamii walivyokuwa marafiki wa Nabii Isa (Yesu Kristo), na watu wengine mashuhuri wa dunia. Walikuwa ni watu hawa hasa ambao Mtume wa Uislamu aliwatafutia manufaa yao ili kuzuia kushamiri kwa udikteta, utumwa haramu, akamuokoa mwanadamu kutokana na hali ya kufungwa na wanadamu wenziwe, na akaanzisha hazina ya umma ili wote waweze kunufaika kutokana nayo, bila ya ubaguzi wa aina yoyote. Akazielekeza juhudi za watu katika ustawi wa kijamii. Alisisitiza juu ya Maquraishi, ambao walikuwa ndugu zake, katika kila hatua kwamba wanapaswa kubadilisha tabia zao, wafanye matendo mema, na kuweka mazingatio yao, kwa moyo wote, kuelekea kwa Mwenyezi Mungu, ambaye ameviunganisha viumbe vyote vilivyotawanyika kwenye kuwa kitu kizima kimoja. Hata hivyo, Maquraishi waliwachochea watu wasioelewa, na watoto wao halikadhalika, kumpiga mawe na kumdhihaki yeye Mtume. Wale wasiojiweza, walioonewa na watumwa wasiokuwa na makazi, ambao miongoni mwao mmoja ni Bilal, yule Muadhini wa Mtume, walizidiwa na furaha pale waliposikia haya: “Wanadamu wote wanalishwa na Mwenyezi Mungu. Yeye anampenda sana yule ambaye ni mwenye msaada sana kwa viumbe wake.” Hii Ilikuwa Ni Sauti Ya Muhammad Wale ambao walikuwa maadui zake, na wakampiga mawe na kumdhihaki, waliisikia sauti hii yenye uhai wa kusisimua: “Kama wewe (Muhammad) ungekuwa mkali 10

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 10

9/4/2017 3:47:44 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

na mwenye moyo mgumu, basi wangekukimbia wote kitambo kirefu kilichopita. Wasamehe na umuombe Mwenyezi Mungu awasamehe (dhambi zao) na ushauriane nao katika jambo maalum. Lakini mnapofikia uamuzi mtegemee Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu anawapenda wale wanaomtegemea Yeye.” Hii Ilikuwa Sauti Ya Muhammad Maneno safi na halisi yafuatayo yaliganda kwenye vichwa vya wale waliokuwa wakijitahidi katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa ajili ya maisha bora, na waliokuwa tayari kumsaidia yeye (Muhammad) katika mapambano yake dhidi ya ibada ya masanamu na utenda maovu, na waliohofia isije ikawa haki zao na mienendo yao mizuri ikapotea bure kwenye uwanja wa vita. “Kumbuka! Usiwe mdanganyifu. Usivunje ahadi ya amana. Usiue japo mtoto mdogo au mwanamke au mzee au mtawa katika nyumba ya watawa. Usichome mti wa mtende na wala usikate mti wowote wala kuangusha chini jengo.” Hii Ilikuwa Ni Sauti Ya Muhammad Waarabu waliisikia sauti hii ya ki-mbinguni kutoka kwa Muhammad nao wakaieneza katika pembe zote nne za ulimwengu. Waliwaenezea watawala wenye nguvu na wafalme na sauti hii, wakaanzisha udugu miongoni mwa wanadamu na wakawafunga wote katika imani moja, na wakatengeneza uhusiano kati ya mwanadamu na Mungu. Kivuli cha Muhammad kikaenea sana kiasi kwamba Dunia ya Zamani yote ikawa chini ya kivuli hicho na ardhi kutoka mashariki hadi magharibi ikaanza kutoa matunda ya wema, elimu, amani na urafiki. Mtume wa Uislamu akaunyoosha mkono wake na akapanda mbegu za urafiki na udugu duniani kote. Mkono huo bado ungali umenyooshwa na unashughulika katika kupandikiza mbegu hizo. Hivyo, hakuna sehemu ya dunia ambayo kwamba wafuasi wa Muhammad hawapatikani. Mmoja wao anaweza akawa yuko Pakistani na mwingine anaweza akawa yuko Hispania, lakini licha ya hilo, wote wanachukuliwa kuwa chini ya kiwango kimoja hicho hicho. Mtume alitoa heshima na taadhima kwa watu wa mashariki ambayo hata sasa bado inang’ara kama taji juu ya vichwa vyao. Sauti hii ya Mtume, ilikuwa ni mwito kwa ajili ya udugu wa kibinadamu. Ilizuia mikono ya watawala kuzifikia mali za raia wao, na kutoa haki sawa kwa wanadamu wote. 11

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 11

9/4/2017 3:47:44 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Katika dini yake hakuna ubaguzi kati ya mtu wa kawaida, mtawala na raia, na Mwarabu na asiyekuwa Mwarabu, kwa sababu binadamu wote ni waja wa Mwenyezi Mungu, na ni Yeye anayegawa riziki kwao wote. Sauti hii iliwakomboa wanawake kutokana na ukandamizaji wa wanaume, ikawaweka huru vibarua kutokana na dhulma ya mabwanyenye na ikawatoa watumwa kutoka kwenye udhalilishwaji wa utii kwa mabwana zao. Kinyume na Plato na wanafalsafa wengine, ambao waliwanyima wafanyakazi haki zao za kijamii kwa sababu ya shughuli zao za kihila, na wakaigawanya jamii kwenye tabaka nyingi, Mtume wa Uislamu yeye aliwafanya wanadamu wote washiriki kwenye shughuli za serikali. Yeye vilevile alikataza riba na unyonyaji wa mtu mmoja juu ya mwingine. Baada ya Mtume wa Uislamu, alikuwa ni Ali bin Abi Talib ambaye aliwalingania watu kwenye maadili mema. Kutupia Macho Historia Kama utatupa sikio kwenye historia ya ulimwengu, utasikia habari za tukio kubwa, ambalo mfano wake haujawahi kutokea hata baada ya kupita karne zaidi ya kumi. Kama utatafakari kwa makini kuhusu matukio mbalimbali katika dunia, utasisimuliwa na nafsi moja maarufu, ambayo kwa fikra zake kubwa kila kitu kinaonekana kuwa hakina maana. Dunia pamoja na maisha yake, na watoto, ndugu, mali na utawala havina umuhimu wowote mbele ya macho yake. Nafsi hii ni kuu, mashuhuri sana kuweza kuisimamisha kwenye msitari wa watu wa kawaida, na umaizi wake ni makini sana kiasi kwamba unafanana na fikra za mtu wa kawaida kwa jina tu. Kama utasikia kwa masikio na moyo wako, historia itakusimulia hadithi ya waliokufa kishahidi katika njia ya ukweli na haki, ambao kwa damu yao mipaka ya mbingu imefunikwa. Kama utaangalia mwisho wa upeo wa macho, utaona aina mbili za wekundu; moja ni ule wekundu wa kawaida, na huo mwingine ni ule wa damu ya mashahidi katika njia ya kweli na haki. Hebu iangalie historia ya Mashariki na uone ule uwezo mkubwa wa ufahamu na uelewa, ambao ni kiini cha kila duru ya fikra za hali ya juu, na chanzo cha kila hekima na mantiki. Kila utafiti wa kisasa na mawazo mapya kuhusu maisha ya ulimwengu huu na ule wa Akhera unahusiana naye. Maoni ambayo yanaweza kuja kukupambanukia 12

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 12

9/4/2017 3:47:44 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

kuhusiana na mfumo wa mwanadamu na sheria, kanuni za ustaarabu na desturi za maadili, zimechipukia kut ia mali, kwa maafisa wa serikali kufanya mambo yatendeke bure na kuwaweka watu wengi chini ya udhibiti kwa wazushi kukusanya wafuasi watiifu. Je, unamtambua yule mwenye hekima, mashuhuri sana ambaye miaka zaidi ya elfu moja iliyopita, alianzisha ukweli ambao ulishinda kabisa maefu ya itikadi za kidhana na maoni ya kupita kiasi na akasema: “Kama mtu anashinda na njaa ni kwa sababu ya ukweli kwamba fungu lake limechukuliwa na mtu mwingine.” Na akaongeza: “Sijawahi kuona neema iliyozidi ambayo haihusiani na haki iliyovunjwa.” Kuhusu kuhodhi, yeye alimwandikia mmoja wa magavana wake: “Wakataze watu kuhodhi, kwa sababu ni jambo linalowezesha hasara kwa umma, na linaloleta jina baya kwa watawala.” Mtu maarufu na aliyetaalimika, aliitambua siri halisi ya ubinadamu zaidi ya miaka elfu moja, na akahukumu kwamba wale watu ambao walikuwa hawana thamani machoni mwa wafalme na watawala, walijaaliwa na maadili na murua mzuri, na kila uonevu uliofanywa juu yao ulionekana kwa watawala kana kwamba ni halali, unaruhusika. Yule mchongaji sanamu wa Kitaliano, Raphael, alitengeneza sanamu la Bikira Maria katika umbile la mkulima wa kike wa Kitaliano, na akafanya zile sifa zote nzuri za kibinadamu zionekane ndani yake. Tolstoy, Voltaire na Goethe pia walipendekeza na kuthibitisha kwa mshughuliko wa akili zao na udhanifu wao, kitu kile kile kilichoonyeshwa na Raphael katika sanamu hilo. Hata hivyo, Ali aliifafanua dhana hii karne nyingi zilizopita. Alipambana dhidi ya makabaila, tabaka linalotawala, walanguzi na watu wenye ubinafsi, akapinga namna yao ya fikra mbovu na ya kipumbavu juu ya wanaokandamizwa na akasema: “Wallahi! Nitazitwaa haki za mtu anayedhulumiwa kutoka kwa dhalimu, na nitamlazimisha dhalimu huyo kwenye chemchemi ya ukweli kwa kuweka kipini ndani ya pua yake, ingawaje yeye hatalipendelea hilo.” Mambo aliyoyasema kuhusu watu wa wakati wake, yanaonyesha kwamba aliwaelewa vizuri sana. Walikuwapo kwa upande mmoja, makabaila wasiokuwa na thamani na wengine walioshikilia nafasi kubwa licha ya uzembe wao, na kwa upande mwingine na watu waliokuwa hawajiwezi na walioonewa, na ambao walikuwa ha-

13

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 13

9/4/2017 3:47:44 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

wana jinsi ila kutii. Yeye kwa hiyo, alisema kifupi: “Waliokandamizwa wenu wanaheshimika, na wenye nguvu wenu ni waovu na duni.”1 Kwa maneno haya ana maana kwamba, wale watu wa chini hawawezi kuonyesha maadili yao mema na vipaji vyao, kutokana na kutojiweza kwao na ukandamizwaji na tabaka la wenye uwezo, na watu wanaoshikilia nafasi kubwa wanaficha mapungufu yao kwa mavazi yao ya thamani kubwa. Aliwaambia watu kwamba ukweli na uadilifu ni mambo madhubuti na ya milele, ambayo yamekuwepo siku zote, na yataendelea kuwepo daima. Katika undani wa moyo wake, kila binadamu analiamini hili, ingawaje watu tofauti watalitafsiri kwa njia mbalimbali. Hata ummati za kale kabisa zilistawi chini ya ulinzi wa imani hii, ingawaje wanaweza kuwa hawakulijua hilo. Wamerithi maoni yao na imani zao kutoka kwa wahenga wao na wakazitwaa, kwa sababu kwa kufanya hivyo wameokolewa kutokana na usumbufu wa kuchunguza na kutafiti. Kuigiza kwa hiyo kumekuwa ni chanzo chao cha pili. Msingi wa imani zote na fikra ni huu kwamba, kunakuweko na ukweli kamili ambao unapaswa kuwa ndio mahali pa kuanzia pa mijadala na maoni yote. Ubora wa kichwa chake na moyo, vilimuwezesha Ali kuutambua ukweli huu na aliamini kwa moyo mmoja kwamba kitu chochote ambacho kimeegemezwa kwenye ukweli hakiwi chenye kuyumba. Alikuwa ni mfano kamilifu wa uimara na binafsi alijikuta mwenye kufanikiwa katika tukio la ushindi na la kushindwa halikadhalika. Katika medani ya vita na pia katika uwanja wa siasa, ilikuwa haidhuru sana kwake kushinda au kushindwa, kwa sababu alijua kwamba ukweli ulikuwa pamoja naye na ni yeye mwenyewe aliyekuwa kipimo cha kupambanua baina ya ukweli na uongo. Katika historia yote ya ulimwengu, ni vigumu kumpata mtu mwenye dhamira madhubuti kama hiyo, kwamba hawezi kuyumba katika mazingira yoyote, na moto wa maasi hauwezi kumfanya atetemeke. Hakuna kitu kingine kinachoweza kuitingisha imani ya mtu kuliko kule kwamba maadui zake wanamshutumu na makosa ma1

apa Amirul-Mu’minin alizungumzia yale matatizo yaliyofanywa wakati wa Ukhalifa wake, na ambayo H yalileta madhara yasiyorekebishika kwenye umma wa Kiislamu. Ingawa maneno haya hayachukui ile maana iliyokusudiwa na mwandishi, bado ni ukweli uliothubutu, na ni dhahiri kutoka kwenye kauli zake nyinginezo. Kwa kweli lengo kuu la kuteuliwa kwa Mitume kwenye ujumbe wao na njia ya mafanikio yao ilikuwa ni hivi kwamba, walitambulisha uhuru wa mtu mmoj mmoja na uhuru wa fikra kinyume na sera ya madhalimu kama Nimrud na Firauni ambao waliyadhibiti maisha na mali za watu na kuulemaza uwezo wao wa kufikiri. 14

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 14

9/4/2017 3:47:44 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

baya sana, na hata upotofu na uasi wa dini. Na hakuna kitu kinachoweza kumuweka mtu kwenye wasiwasi kuliko tishio la kifo, au mashambulizi kwenye imani ya mtu, ambayo ni mabaya kuliko kifo. Hata hivyo, Ali hakuyumba katika mazingira yoyote yale na hakuna kitu kilichoweza kumfanya akengeuke kwenye njia yake. Yeye hakuacha juhudi zake kwa ajili ya utekelezaji wa Uislamu, na hakutamani kabisa mali au cheo kama malipo kwa ajili ya juhudi zake. Malipo yake pekee yalikuwa ni mafanikio katika dini. Umepata kuona katika historia ya dunia; mtu mkarimu mwenye moyo mpole na wenye upendo, aliyezungukwa na watu waroho, wakaidi na waliojawa na kisasi, wenye mioyo migumu, wakali wa kunyonyana wenyewe kwa wenyewe, lakini alikuwa akiweza kuwalingania kwenye amani na ustawi, na bado waliweza kuungana na kupigana dhidi yake? Zipo hadithi nyingi ambazo watu wanazirudia kwa mazungumzo au kwa maandishi, na kila mtu anachagua mojawapo kulingana na asili yake kuwa kama ndio wito wake. Hata hivyo, umepata kumuona mtu mwingine yoyote ambaye anaweza kuwa mfano halisi wa utakaso na staha katika maana yake halisi? Miongoni mwa watu mashuhuri wa dunia Ali alikuwa wa mbele kabisa katika masuala ya upendo na uaminifu. Uaminifu ulikuwa ni tabia na asili yake, na moyo na nafsi yake vilikuwa vimejawa navyo. Yeye aliwapenda watu lakini hakuhusisha mapenzi na nafsi yake mwenyewe binafsi. Alitimiza ahadi zake. Uaminifu ulikuwa ndio kiini cha uhai wake. Kwa akili yake ya kawaida na ya kina aliona kwamba uhuru ni kitu cha kuheshimika sana. Ulimwengu wote inautamani na hauoni neema nyingine yoyote yenye kulingana nao.2 Ni watu huru tu walio na uwezo sahihi wa kufikiri na tabia njema, na mapenzi ya kweli na uaminifu halisi pia hauwezekani bila ya kuwa na uhuru. Yeye kwa hiyo, alisema: “Ndugu mbaya kabisa ni yule ambaye ni lazima uchunguze kanuni zake.� Kwa hiyo, mtu bora ni yule ambaye sio wa aina hii. Je, unamjua mtawala yoyote ambaye kamwe hakula akashiba kwa sababu watu wengi miongoni mwa raia zake hawakupata chakula cha kutosha kushibi2

wanadamu anapenda uhuru. Endapo kwa hiyo, mtu anawekwa katika jela na mahitaji yote ya maisha yakaM patikana kwake, bado vivyo hivyo atapendelea uhuru kuliko maisha ya jela. Mitume walipambana dhidi ya madhalimu na wakafanikiwa, kwa sababu wao walitangaza kwamba mtu amepewa haki ya kudhibiti shughuli zake na mali yake ambapo wale watawala wa kidhalimu waliwanyima watu haki hii na wakawaingiza kwenye aina zote za mateso na uonevu. 15

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 15

9/4/2017 3:47:44 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

sha matumbo yao, au hakuvaa nguo nzuri kwa sababu watu wengi wanavaa nguo chakavu, au hakulimbikiza mali kwa sababu walikuwepo watu wengi masikini na wenye shida? Ali alipendekeza kwa wanawe na marafiki kufuata (nyayo) mwenendo wake. Alikataa kutoa hata kiasi cha dinari moja kwa ndugu yake, kwa sababu hakuwa na haki nayo. Alichukulia hatua kali dhidi ya masahaba zake, wafuasi wa chini yake na watumishi wa dola, kama wangechukua angalau kipande cha mkate kama hongo au rushwa. Alimuonya mtu dhidi ya kuvunja masharti ya uaminifu kuhusiana na mali ya umma kwa maneno haya yafuatayo: “Ninamuapa Mwenyezi Mungu kwamba kama utavunja uaminifu kuhusiana na mali ya umma nitachukua hatua kali dhidi yako kiasi kwamba utakuwa masikini, uliyelemewa na kudhalilika.” Na alimwambia mtu mwingine kwa maneno haya fasaha: “Nimefanywa nielewe kwamba umefagia sakafu na kuing’aza kabisa, umejitwalia kila kilichokuwa chini ya miguu (mamlaka) yako na hukubakisha kitu. Unapaswa, kwa hiyo, utume hesabu yako kwangu.” Vilevile yeye alimuonya kwa maneno haya mtu ambaye alikuwa tajiri kwa kupokea mahongo: “Muogope Mwenyezi Mungu na urudishe hizo mali za watu kwa wenyewe. Kama hutafanya hivyo na Mungu akanipa uwezo wa kukushika wewe, basi nitatekeleza wajibu ambao ninadaiwa na Mwenyezi Mungu kuhusiana na wewe na nitakupiga na upanga ambao umempeleka Motoni kila yule ambaye umempiga.” Je, umewahi kusikia mtawala ambaye alikuwa akisaga nafaka kwa mikono yake mwenyewe na kujitengenezea mkate, ambao ungeweza kuvunjwa tu kwa kuukandamiza na goti? Yeye ambaye alirekebisha viatu vyake yeye mwenyewe? Ambaye hakujilimbikizia utajiri wowote wa kidunia, kwa sababu hakuwa na lengo lolote isipokuwa kuwasaidia wale walio matesoni na wanaoonewa, ili aweze kuwapatia haki zao kutoka kwa madhalimu na kuwafanya wawe wenye furaha? Yeye ambaye kamwe hakujali kuhusu chakula chake na kamwe hakufikiria juu ya usingizi mnono, kwa sababu baadhi ya watu katika nchi yake walikuwa wana njaa? Yeye ambaye alitamka kauli hii fasaha: “Je nishindane mwenyewe na hiki ambacho watu wananiita ‘Amirul-Mu’minin’ na nisishiriki kwenye magumu ya maisha pamoja nao?” Kama serikali na utawala havitekelezi lengo la kusimamisha ukweli na kuuondoa udanganyifu, basi hivyo ni vitu vibaya sana vya ulimwengu katika macho ya Ali. 16

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 16

9/4/2017 3:47:45 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Ni mtu yupi kati ya wale ambao ni maarufu kwa uadilifu wao, ambaye yuko katika namna ambayo kwamba, hata kama wakaazi wote wa dunia wakiungana pamoja dhidi yake ni lazima itasemwa kwamba yeye ni mkweli, na kwamba wapinzani wake wote ni waongo. Alikuwa ni Ali aliyekuwa na sifa hii, kwa sababu ukweli wake na uadilifu havikuwa vya kutafutwa bali vya kurithiwa, na kutokana na navyo hivyo watu wengine walipata masomo. Kanuni zake hazikuundwa kwa sababu ya dharura za serikali na sera zake, bali serikali na sera ziliwekwa kwa msingi wa sheria hizo. Yeye kwa makusudi kabisa hakutwaa njia ambayo ingeweza kumuongozea yeye kwenye utawala, lakini alitwaa njia ambayo ingemuwezesha yeye kujipatia nafasi yake kwenye nyoyo safi. Uadilifu ulikuwa ni sehemu ya nafsi yake, na ulikuwa umekolea kwenye moyo wake na uliunganisha na sifa nyingine pia pamoja nao wenyewe. Ilikuwa haiwezekani kwa yeye kukengeuka kutoka kwenye haki na kutoka kwenye madai ya asili yake. Haki ilikuwa ni sifa ya msingi ambayo ilikuwa imesokotwa katika mwili wake mzima, na ilitembea katika mishipa yake kama damu. Umewahi kuona mtu shujaa katika kurasa za historia, ambaye alipingwa na kundi la wapenda makuu, ambalo pia lilihusisha jamaa zake, na kisha vita vikatokea, na watu wale wakawa washindi na yeye akashindwa, na pamoja na hayo alitawala juu yao? Ilikuja kutokea hivyo kwa upande wa Ali na akatawala juu yao, kwa sababu walikuwa hawana sifa za kibinadamu na walikuwa wameasi katika nafasi ya wakandamizaji; wakitumia silaha za udanganyifu, hongo, hali ya tamaa na ulaghai, ambapo yeye alitoa mhanga manufaa yote, hata uhai wake katika njia ya ubora wa utu, uadilifu na ulinzi wa haki za wengine. Ilikuwa ni kwa sababu hii kwamba ule ushindi wa maadui zake ulikuwa kwa kweli ni kushindwa, na kushindwa kwake kukawa ni mafanikio makubwa juu ya sifa za kibinadamu. Je umewahi kukutana na mpiganaji mashuhuri katika kurasa za historia ambaye ameweza kuwapenda hata maadui zake, na kutaka kuwaona wao wakijaaliwa na tabia za kibinadamu. Ali alikuwa ndiye mtu kama huyo. Alikuwa mwenye huruma sana kwa maadui zake, kiasi kwamba alipendekeza kwa masahaba zake kwamba: “Msiwe wenye kuanza katika kupigana nao. Pale wanaposhindwa kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu msiwafukuzie au kuwaua wale wanaokimbia. Msiwaue wale wasiojiweza, wasiokuwa na msaada wowote na waliojeruhiwa na msiwabughudhi wanawake.� 17

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 17

9/4/2017 3:47:45 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Jeshi la maadui likiwa na wapiganaji kumi na moja elfu, ambao walipenda sana kumwaga damu yake, lilizuia njia yake ya kuyafikia maji ili aweze kufa kwa kiu. Hata hivyo, aliporudisha udhibiti juu ya maji hayo kwake, yeye aliwaambia: “Sisi tunakata kiu yetu kwa maji. Na ndege nao pia wananufaika kwayo. Ninyi pia mnapaswa kuja kuchukua maji ili kukidhi mahitaji yenu.” Imam Ali alikuwa mara kwa mara akisema: “Kama mtu atauawa wakati akipigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, thawabu zake sio zaidi ya zile za yule ambaye anaweza akalipiza kisasi; lakini akajizuia kufanya hivyo, kwa sababu mtu kama huyo ni mmoja wa Malaika wa Mwenyezi Mungu.” Pale mtu mwovu alipompiga upanga kichwani mwake, na kama matokeo ya hilo, alikuwa anaiaga dunia alipowaambia masahaba zake: “Endapo mtamsamehe mtu huyu, kitendo chenu hicho kitakuwa kinakaribia sana uchamungu na uadilifu.” Alikuwa mpiganaji mashuhuri, ambaye alikuwa amechanganya ushujaa wake na huruma. Aliwabainisha kwa mdomo tu maadui, ambao walikuwa wamejikusanya kumpinga yeye, ingawaje angeweza kuwadhibiti nguvu zao kwa upanga wake. Hata pale alipokwenda kuwaonya wao, yeye alikwenda mikono mitupu na bila deraya yoyote, ambapo wao walikuwa na silaha na mavazi kiasi kwamba hata nyuso zao zilionekana kwa taabu sana kupitia kwenye kofia zao za chuma (helmeti) na mavazi ya chuma. Halafu akawakumbusha kuhusu undugu wa zamani na urafiki, na akalia sana kwa sababu ya kutwaa kwao njia potovu. Hata hivyo, hata pale alipotambua kwamba ushauri wake huo haukuleta athari yoyote kwao na walikuwa wamedhamiria katika kumwaga damu yake, hakuanza mapigano yeye mwenyewe, bali aliyachelewesha mpaka pale wao wenyewe walipoyaanza. Katika wakati huo yeye aliuchomoa upanga wake kwa ajili ya wale wanaoonewa na akatuma shambulizi ambalo liliwatawanyisha kama chembechembe za mchanga ndani ya jangwa. Baada ya wale wakandamizaji wenye inda, ambao walionyesha uadui wazi wazi na uasi walipokuwa wameuawa na yeye mwenyewe akapata ushindi, bado alilia juu ya miili yao iliyokufa, licha ya ukweli kwamba walikuwa wamekutana na balaa hili kwa sababu ya ubinafsi wao na ulafi mbaya. Je, umewahi kusikia juu ya mfalme yoyote ambaye alikuwa amejiandaa vizuri kwa kila namna ya mamlaka na utajiri ambao ulikuwa haupatikani kwa wengine, lakini yeye akachagua mateso na machungu kwa ajili yake mwenyewe? Kwa kweli 18

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 18

9/4/2017 3:47:45 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Ali alifanya uchaguzi huo. Yeye alikuwa wa heshima ya kiungwana lakini alisema: “Hakuna hadhi iliyokuwa kubwa sana kuliko unyenyekevu na uvumilivu.” Ali alikiadhibu vikali kikundi ambacho kilimchukulia yeye kuwa na umungu. Aliwashauri kama ndugu watu wa kundi lililokuwa na mwelekeo wa upendeleo wa kuelekea kwake. Baadhi ya watu walimtukana. Wafuasi wake watiifu hawakulivumilia hili na wakawatukana wale watu katika kuwajibu. Hapo yeye akasema: “Mimi silipendi hili la kwamba ninyi ambao ni marafiki zangu muwe ni watu wanaotumia lugha chafu ya matusi.” Baadhi ya watu walikuwa wenye uhasama dhidi yake. Walimdhuru na kumkashifu na walisimama kumpinga. Licha ya haya yeye alikuwa mara kwa mara akisema: “Muadhibu ndugu yako kwa kumtendea wema, na utengeneze tabia yake kwa zawadi na heshima nyingi.” Ali vile vile alisema: “Ndugu yako hana uwezo na nguvu zaidi yako katika kuvunja mafungamano ya upendo na urafiki, alimuradi wewe unajaribu kuyaimarisha, na sio mwepesi kuliko wewe katika kufanya madhara kama wewe utakuwa na tabia njema kwake.” Baadhi ya watu walipendekeza kwake kuwatendea madhalimu kwa upole na huruma ili serikali yake iweze kuimarika. Yeye katika kuwajibu alisema: “Rafiki yako ni yule anayekuzuia kufanya maovu, na adui yako ni yule ambaye anakushawishi kufanya uovu.” Pia alisema: “Twaeni ukweli hata kama utakuwa na madhara kwenu, na jiepusheni na kusema uwongo ingawaje unaweza kupata manufaa kutokana nao.” Ali alifanya wema kwa mtu. Wakati mmoja mtu huyo huyo alikuja kupigana naye. Halafu Ali akasema kujiambia yeye mwenyewe: “Kama mtu hana shukurani juu ya wema wako, hii haina maana kwamba ukatishe wema wako.” Wakati mmoja neema za ulimwengu zilikuwa zinajadiliwa mbele yake. Ali akasema: “Katika neema za kidunia maadili mema ni neema tosha.” Wakati watu fulani walipomshauri kutumia njia zote zinazowezekana, yeye kama mfalme, ili kupata ushindi, Ali alisema: “Mtu ambaye moyo wake umelemewa na maovu, yeye sio mshindi, na yeye yule anayetawala kwa kutumia matendo maovu, kwa hakika ndiye mtu aliyeshindwa.” Ali alipuuza yale matendo maovu ya maadui zake, ambayo yeye peke yake ndiye aliyeyatambua, na akasema kwa kurudia rudia: “Tabia nzuri ya mtu muungwana ni kwamba aweze kuchukulia yale anayoyaona kuwa kama yasiyoonekana.”

19

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 19

9/4/2017 3:47:45 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Kama maadui zake au mapunguani miongoni mwa marafiki zake walisema jambo ambalo yeye hakulipenda, yeye alikuwa akisema: “Kama unasikia jambo kutoka kwa mtu, na kukawa kuna uwezekano wa lenyewe kuwa zuri basi usilitilie wasiwasi juu yake.” Je, unamjua kiongozi yeyote wa kidini ambaye ametoa maelekezo kwa watendaji wake katika maneno haya: “Watu, ama ni ndugu zako katika dini au wako sawa na wewe katika suala la uumbwaji. Kwa hiyo, uyapuuze mapungufu yao kwa namna ile ile ambayo wewe ungependa Mwenyezi Mungu ayapuuze ya kwako.” Je, unamfahamu mfalme yoyote aliyetelekeza falme yake na kwenda kusimamisha ukweli? Na je, umewahi kumuona mtu yeyote mwenye mali ambaye ameweza kujitosheleza mwenyewe kwa kipande cha mkate ili kuhimili maisha yake, na maisha machoni mwake yakawa na maana ya kutenda wema kwa wanadamu, na akawa ameweza kuuambia ‘ulimwengu’ usimhadae yeye bali uhadae mtu mwingine? Miongoni mwa kumbukumbu za Mashariki, umewahi kusoma kitabu kiitwacho Nahjul-Balaghah (Tafsiri ya Kiingereza ya kitabu hicho adhimu imechapishwa na Islamic Seminary) na ukaona jinsi sentesi zake zilivyo fasaha na za kuvutia? Kinashughulika na mambo mbalimbali, na pia kinatoa habari kuhusu hiyo dunia nyingine (Akhera). Kiko kama matukio ya dunia ambayo hayawezi kugeuzwa, na kama hata neno moja litaondolewa mahali pake, madhumuni yote mazima yatapitiwa na mabadiliko. Kitabu hiki kitabakia kuwa cha kuvutia ilimradi mwanadamu na akili yake, na hisia za moyoni vinadumu. Ufasaha wake unashinda kila fasaha nyingine yoyote. Una kila sifa zote za lugha ya Kiarabu, ambayo ilikuwapo kwa wakati ule na zilizoanzishwa baadae. Hivyo, imesemekana kwamba kiko chini kuliko maneno ya Mwenyezi Mungu, na juu zaidi kuliko kile ambacho kimesemwa na viumbe wa Mwenyezi Mungu. Hekima kubwa, elimu ya kiwango cha hali ya juu kabisa, ufasaha usio na kifani, ujasiri kamilifu na mapenzi yasiyo na kikomo na upole, vyote vilikusanyika kwa Ali. Kama mtu atamiliki hata moja ya sifa hizi, basi itatosha kuwashangaza wengine, na kama vingekusanyika ndani ya mtu mmoja, umashuhuri wake bila shaka ni dhahiri ungevuka mipaka. Wakati mwingine huwa inatokea kwamba mwanafalsafa huyu, mwandishi, mwanachuoni, msimamizi, mtawala na jemadari alijitenga na dunia, na hakuwa na shughuli yoyote na watu wengine. Yeye aidha alitaka kusisimua sifa za binadamu na 20

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 20

9/4/2017 3:47:45 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

kuamsha hisia za moiyoni, na akatamka haya maneno mazuri na halisi ambayo ni ushahidi wa upendo na hisia nzito, ili yafike kwenye masikio ya mioyo kwa upole na uangalifu: “Kukosa marafiki ni sawa na umasikini.” “Usionyeshe furaha katika mikasa ya wengine.” “Wasogeze watu karibu yako kwa njia ya upole na ukarimu.” “Msamehe mtu anayekuonea wewe.” “Usimkoseshe ukarimu wako yule anayekunyima ukarimu wake.” “Anzisha mahusiano mapya na yule mtu anayevunja uhusiano na wewe.” “Kuwa mwema kwa yule mtu ambaye ana uadui juu yako.” Alikuwa ni mtu mashuhuri ambaye aliwazidi wanafalsafa wote wa dunia katika kuwa na fikra kubwa, waadilifu wa dunia kwa wema, wanachuoni wa dunia katika masuala ya elimu kubwa, watafiti wa dunia katika suala la umaizi wa kina, wote wenye uhisani kuhusiana na upendo na huruma, watu wachamungu wote katika suala la kujihini, na wanamageuzi wote wa dunia katika suala ya maoni ya kimageuzi. Alishiriki taabu za wasiojiweza, na akasaidia waliokandamizwa katika huzuni zao. Aliwafundisha watu wasiokuwa na elimu, wa dunia ya sanaa juu ya fasihi, na akawapa wale watu majasiri mafunzo katika mbinu za kivita. Yeye alikuwa wakati wote yuko tayari kuyatoa muhanga maisha yake kwa ajili ya kuimarisha ukweli. Alifika juu ya hatua ya juu zaidi ya maadili ya mwanadamu na ukamilifu. Yeye alizionyesha sifa hizi sawa katika maneno yake na vitendo. Alikuwa maarufu sana kiasi kwamba utawala wa maadui zake juu yake ulikuwa hauna maana yoyote, na ushindi wao haukonyesha umuhimu wowote, kwa sababu katika wakati huo, kila kitu kilikuwa kimegeuka juu chini. Mkono wa kulia ulikuwa upande wa kushoto, na mkono wa kushoto ulikuwa upande wa kulia. Juu na chini, mwanga na giza, ardhi na mbingu, vilikuwa vyote vimepata sura tofauti. Haileti tofauti yoyote katika nafasi ya Ali kama historia imtambue au isimtambue yeye, na kama utukufu wake unaonekana mkubwa sana au mdogo zaidi. Licha ya haya, historia imeshuhudia kwamba yeye alikuwa ndiye hatua ya kina sana ya fikra ya mwanadamu. Aliyatoa mhanga maisha yake kwa ajili ya haki na ukweli. Yeye alikuwa ni baba wa mashahidi na mtetezi wa haki. Alikuwa ndiye mtu wa kipekee wa Mashariki, ambaye ataishi milele!

21

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 21

9/4/2017 3:47:45 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Mtume Na Abu Talib Kama tukiacha maelezo ya kina, na tukatupia macho sio kwenye hali za dhahiri bali kwenye ukweli, inaonekana kwamba hali na vituko vya maisha ya Ali mwana wa Abu Talib vilikuwa sawasawa na vile vya Mtume Muhammad, na mwelekeo wa wafuasi wake kwa Mu’awiyah na washirika wake ulikuwa sawa sawa na ule wa Mtume na Waislamu kwa Abu Sufyan, Abu Jahl na Quraishi wengineo. Tofauti kati yao ilikuwa ni hii kwamba Mtume alipata nguvu ya muhimu kuanzisha dola na kuwashinda wakuu wa Maquraishi ambapo mazingira na hali zilibadilika wakati wa siku za Ali, na yeye hakufanikiwa kuwashinda wapinzani wake. Ingawaje Ali hakuweza kutawala juu ya watu kama Bani Umayyah, hakunyimwa kutawala juu ya mioyo safi ya watu waadilifu. Na alikuwa amejaaliwa vizuri na sifa za mtu mkamilifu ambazo zilistahiki kutawala hiyo mioyo. Kabla hatujaanza mazungumzo yetu kuhusu Ali ni muhimu tuutupie mwanga kidogo ule uhusianao ambao ulimshirikisha yeye na Muhammad mwana wa Abdullah. Uhusiano huu ulikuwepo kwenye matukio hatari ya maisha yao, na vilevile katika sifa zao za kiroho ambazo zilikutana katika familia moja. Mtume alikuwa ndiye mtu mkamilifu zaidi, na mwana wa Abu Talib alifuatia nyayo zake, na alikuwa ndiye mtu mkamilifu zaidi kumfuatia yeye na aliwazidi wengine wote. Wakati Mtume alipokuwa amekoseshwa mapenzi ya wazazi wake, babu yake, Abdul-Muttalib, ambaye alikuwa babu yake Ali pia, alianza ulezi wake. Babu yake alikuwa amempenda sana. Wakati mwingi ilitokea kwamba alimkazia macho mjukuu wake na akawaambia wale waliokuwepo pamoja naye: “Mtoto huyu ni mtukufu sana.” Alimpa Muhammad heshima kubwa sana ingawaje alikuwa mtoto bado, na katika mikutano mikuu alimfanya akae katika sehemu kwenye kivuli cha Ka’bah ambapo hata ndugu zake hawakuwa na mategemeo ya kupakaa hapo. Wakati babu yake Mtume alipofariki, malezi yake yalianzwa na ammi yake, Abu Talib, baba yake Ali. Mtume aliendesha maisha ya starehe kabisa chini ya malezi ya ammi yake, na akanufaika sana kutokana na mapenzi na tabia bora na maadili, ambayo aliyarithi kutoka kwa Abdul-Muttalib. Maadili mema hayo, ambayo yalikuwa ni sifa ya familia ya Abul-Muttalib yalirithiwa ndani ya nafsi ya Muhammad na yalionekana dhahiri katika maneno na vitendo vyake.

22

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 22

9/4/2017 3:47:45 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Inaweza ikasemekana kwamba pale Mwenyezi Mungu alipomchagua mjumbe wake kutoka kwenye ukoo wa Bani Hashim,Yeye pia alimchagua ammi yake mkarimu kumpa mafundisho. Inaonekana kwamba Malaika mjumbe alikuwa amemuarifu Abu Talib kuhusu muujiza uliohusika kwa mpwa wake ambao kwamba wengine hawakuutambua. Wakati mmoja katika kipindi cha njaa na ukame, mtoto huyu aliombwa na ammi yake kumuomba Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kunyeshesha mvua, na mgongo wake ukiwa umeegemea kwenye ukuta wa Ka’bah tukufu. Mtoto huyu alikubaliana na matakwa ya ammi yake na akaonyesha kidole chake kuelekea angani. Kulikuwa hakuna mawingu huko angani kwa wakati huo. Hata hivyo, ghafla mawingu yalikusanyika kutoka pande zote, na ikanyesha mvua kubwa kiasi kwamba mashamba yalijaa maji na ardhi ikapata uhai mpya. Watu wakamuuliza Abu Talib, “Huyu mtoto ni nani?” Yeye akajibu: “Yeye huyu ni mpwa wangu Muhammad ambaye kuhusu yeye nilisema: Yeye ni yule mwenye uso mweupe. Kwa njia ya uso wake mwangavu maji yanatafutwa kutoka mawinguni. Yeye ni kimbilio la mayatima na mlinzi wa wajane.” Simulizi hii inaashiria upendano wenye hamasa na mapenzi wa ammi na mpwa wake. Abu Talib wakati wote aliyakidhi mahitaji ya mtoto huyu kwa uangalifu sana na alikuwa mpole sana kwake. Wakati mmoja ambapo Abu Talib alipokwenda Syria, alimchukua pamoja naye mpwa wake (Muhammad) pia ambaye alikuwa wakati huo na umri wa miaka takriban kumi na nne. Baada ya kuwa amekwishaivuka Madyan, lile Bonde la Oara nchi ya Samud, walifika karibu na mabustani ya Syria. Walifurahia mandhari tofauti na waliona humo siri za maumbile. Maoni ya Abu Talib kuhusu Muhammad yalithibitishwa na mtawa Bahira wakati alipomwambia yeye kwamba mpwa wake atakujakuwa mtu wa juu sana katika siku za baadaye. Kutokea hapo na kuendelea alichukua tahadhari kubwa sana ya mpwa wake kwa sababu alikuja kutambua kwamba kuna muujiza uliokuwa umeunganishwa na nafsi yake. Pale Abu Talib alipowasikia watu wa Makkah wakimwita Muhammad kwa cheo cha ‘al-Amin’ (aliye mwaminifu) alifurahi kupita kiasi, na machozi ya furaha yakaanza kudondoka kutoka machoni mwake.

23

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 23

9/4/2017 3:47:45 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Khadija, mkuu wa wanawake wa ki-Quraishi, yeye mwenyewe alipendekeza kuolewa na Muhammad ingawa alikuwa tayari amekwishakataa posa za matajiri waungwana wa ki-Quraishi. Msiri pekee na mshauri wa kweli wa Muhammad alikuwa ni Abu Talib. Kwa hiyo, yeye alimtaka ushauri katika suala hili. Abu Talib alikuwa anaitambua kabisa tabia na maadili ya Muhammad na alijua kwamba yeye hakuelekea kwenye jambo lolote isipokuwa la heri na wema. Aliunga mkono muungano huo kwa sababu kile mpwa wake alichokuwa amemuuliza kilikuwa haswa ni jambo lile lile ambalo yeye Abu Talib mwenyewe alikuwa akilitamani kutoka kwenye kiini cha moyo wake. Baada ya zile Ayah za Qur’ani Tukufu kuwa zimeshuka kwa Muhammad ndani ya Pango la Hira, mtu wa kwanza kuonyesha kumuamini yeye na kuswali pamoja naye alikuwa ni mke wake Khadija na binamu yake Ali. Pale Abu Talib alipokuja kujua kuhusu kukubali Uislamu kwa Ali, yeye alimwambia: “Mwanangu! Ni kitendo gani unachofanya? Ali akamjibu: “Baba yangu mpendwa! Nimeitwaa dini ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, nikathibitisha kile alichokileta na kumfuata katika kutekeleza swala.” Abu Talib akasema: “Mwanangu! Kuwa mtiifu kwake wakati wote, kwa sababu yeye kamwe hatokulingania kwenye jambo lolote isipokuwa wema na uadilifu.” Wakati Mtume wa Uislamu alipowaagiza Waislamu kuhamia Ethiopia, alimfanya Ja’far mwana wa Abu Talib kuwa kiongozi wa wahamaji hao, na katika watu wote hao, yeye alimpenda sana binamu yake zaidi. Abu Talib alikuwa ndiye mtu wa kwanza katika Uislamu aliyetunga beti za kumsifia Muhammad na akawahimiza watu kumuunga mkono Mtume. Wakati mmoja kikundi cha Maquraishi kilikuja kwa Abu Talib wakamtaka amtoe Muhammad kwao wao. Yeye aliwajibu: “Madhali sisi wote hatujakwisha, hatutamtoa kwenu ninyi, wala hatutazuilia msaada juu yake.” Katika maisha yake yote, Abu Talib hakusahau angalau kwa kitambo kidogo kwamba Muhammad alikuwa ni mtu mashuhuri na ndugu yake (yeye Abu Talib) Abdullah na baba yake Abdul-Muttalib wote pia walikuwa ni watu mashuhuri sana. Wakati wa kifo cha Abu Talib ulipokaribia, aliitisha idadi kubwa ya watu wa ukoo wake mwenyewe karibu ya kitanda chake, na akasema kuwaambia wao: “Ninakusihini ninyi kuwa na mwendo mwema kwa Muhammad kwa sababu yeye anajulikana kama ‘mwaminifu’ miongoni mwa Maquraishi, na ni maarufu miongoni mwa Waarabu kwa ajili ya ukweli wake, na sifa zote hizi zimeunganika katika nafsi 24

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 24

9/4/2017 3:47:45 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

yake. Ninaweza kudhania vizuri sana kwamba, wale mafukara na wahamahamaji wamekusanyika karibu naye na wameukubali ulinganio wake na kuthibitisha maneno yake. Vuguvugu lao limekuwa na nguvu. Wakuu na wazee wa Maquraishi wamefedheheshwa. Wale watu wanyonge wamekuwa wa kuheshimika. Wale waliokuwa wakimpinga sana sasa ndio watiifu sana kwake, na wale waliokuwa mbali sana naye wananufaika sana kwa kubakia kwao kwenye huduma yake.” “Enyi Maquraishi! Muungeni mkono na mheshimuni yeye. Naapa kwa jina la Allah kwamba yeyote atakayefuata hiyo njia yake ataokolewa, na yeyote atakayefanya mambo yake kutokana na ushauri wake atakuja kustawi. Kama ningeishi na kifo kikanipa nafasi ya kukawia, ningemlinda yeye kwenye mabalaa ya wakati kwa sababu ni mkweli na mwaminifu. Ukubalini mwito wake, shirikianeni nyote katika kumuunga mkono yeye na kupigana dhidi ya maadui zake, kwa sababu madhali dunia inaendelea kuwepo, yeye ndiye msingi wa heshima na utukufu juu yenu.” Abu Talib alitoa msaada kwa Mtume kwa miaka arobaini na mbili. Aliwapinga Maquraishi kwa ajili yake na akaliunga mkono tangazo lake la Utume mpaka alipovuta pumzi zake za mwisho. Baada ya kifo cha Abu Talib, Mtume alijihisi kwamba amemkosa msaidizi wake mkuu, ambaye alikuwa akimlinda dhidi ya madhara ya Maquraishi. Abu Talib alikuwa ndiye mkuu wa ukoo ambamo Mtume alikuwa amelelewa, na alikuwa ndiye msaidizi wake dhidi ya maadui zake. Yeye alimpenda Muhammad kwa shauku kubwa na aliyakinga madhara yote ya Maquraishi wakaidi dhidi yake. Mtume mwenyewe alisema: “Alimuradi ammi yangu Abu Talib alikuwa hai, watu hawakuweza kunifanyia mimi madhara yoyote.” Kama sote tunavyojua, Muhammad alikuwa mwenye subira sana na mtulivu, na licha ya ukweli kwamba maadui zake walikuwa wengi kwa idadi na marafiki zake kuwa wachache, aliamini kwa dhati kwamba atafanikiwa katika ujumbe wake. Swali hasa kwa hiyo linajitokeza, juu ya ni kwa nini alihuzunika katika kifo cha ammi yake. Kwa kweli sababu ilikuwa ni yale mapenzi yao mazito waliyopendana, kwa sababu mtu anampenda yule mtu ambaye ni mpole kwake na anayemsaidia yeye. Machozi yake yanayotiririka yalionyesha kwamba Mtume alikuwa akijihisi kwamba amepoteza kitu ambacho kilikuwa na thamani kubwa kwake, kama ile ya maisha yake mwenyewe.

25

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 25

9/4/2017 3:47:45 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Mtume Na Ali Moyo mzuri na halisi ulikuwemo ndani ya familia ya Abu Talib. Iliuangalia ulimwengu kwa jicho la kipekee kabisa, na iliona vitu vyote kama vilivyohusiana na kuungana kila kimoja na kingine. Moyo huu ulikuwa na nguvu sana kwa Mtume na Ali, na kukawa na uhusiano madhubuti sana kati yao, kwa sababu Ali alilelewa na kukuzwa na Mtume kutoka utotoni mwake mpaka akawa kijana. Ikiwa tutakubali kwamba inawezekana kuwa maadili mema kwa kawaida yanaweza kuwa imara katika moyo na nafsi; tunapaswa pia kusema kwamba, Ali alizaliwa na imani kamilifu katika utume wa Muhammad na msaada kwake, kwa sababu zile tabia na sifa za familia ya Abu Talib ambamo Mtume alilelewa, zilihamishiwa kwa binamu yake tangu kuzaliwa kwake.3 Haiba ya Ali iliendekea kukua pamoja na sifa za familia yake. Ilikuwa ni mahali hapa ambapo alikuwa akimsikia Muhammad akizungumza, na ulinganio kwenye Uislamu ulianzia hapo. Ali alikuwa bado ni mdogo sana wakati Mtume alipojiambatanisha naye na kumwita ndugu yake. Katika hotuba inayojulikana kama “Qasi’a” Ali anaelezea uangalifu uliotolewa kwake na Mtume na anasema: “Je unajua, kwamba kutokana na uhusiano wangu, na kwa sababu ya thamani na ustahili wangu, mahusiano yangu na Mtume yalikuwa ni yapi. Tangu mwanzoni mwa maisha yangu, yeye alinipenda mimi nami nilimpenda yeye. Alinichukua mapajani mwake wakati nilipokuwa mtoto mdogo, na tokea hapo wakati wote nilikuwa pamoja naye, yeye mara kwa mara alikuwa akinikumbatia kifuani mwake, alikuwa akinifanya nilale karibu naye; tulizoea kuwa karibu sana na kila mmoja wetu kiasi kwamba nililihisi joto la mwili wake na kupata kuvuta harufu nzuri ya pumzi zake. Wakati nilipokuwa mdogo, alinilisha kwa mikono yake, mara kwa mara akitafuna chembe chembe ngumu kwa ajili yangu. Hajanikuta kamwe nikiwa nimelala wala mnyonge na mwenye kutetereka.Tokea wakati wa utoto wake Mwenyezi Mungu alikuwa amemuweka Malaika Mtakatifu kuwa wakati wote pamoja naye, na Malaika huyu mkuu alikuwa akimwongoza kuelekea kwenye sifa za kupigiwa mfano na maadili ya murua wa hali ya juu, na mimi nilimfuata Mtume hatua kwa hatua kama 3

ali sahihi ni hii kwamba, Abu Talib na watu wa familia yake, au namna na tabia za wakati ule au mazingira H hayakuwa na mvuto juu ya Utume wa Muhammad au Uimamu wa Ali. Mambo haya yalihusika na mwongozo wa kimungu na sio Abu Talib wala watu wa familia yake walioshiriki katika siri za utume na uimamu. 26

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 26

9/4/2017 3:47:45 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

mtoto wa ngamia anavyomfuata mama yake. Kila siku alikuwa akiniwekea mbele yangu kiwango kipya cha ufanisi na alikuwa akiniagiza nikifuate hicho. Kila mwaka alikuwa akikaa kwenye pango la Milima ya Hira kwa muda fulani, na hakuna aliyekuwa akikaa pamoja naye bali ni mimi. Hakuna aliyeweza kwa hiyo, kumuona au kumsikia au kuwa karibu sana naye bali mimi tu. Katika siku hizo, Uislamu ulikuwa ni dini ya Mtume na mke wake Khadija, na mimi nilikuwa watatu wao (Mtume, Khadija na Ali). Hakuna mtu mwingine yeyote katika dunia hii aliyekuwa ameukubali Uislamu, na hata nilikuwa nikiuona mwanga wa mtukufu wa Wahyi na Utume na kuinusa harufu ya ki-ungu ya utume. Wakati Mtume alipopokea Wahyi wa mwanzo, Shetani alilalamika kwa sauti kubwa sana. Nilimuuliza Mtume: “Ni nani huyo anayelalamika, na kwa nini?” Yeye akajibu akasema: “Ni Shetani ambaye amekata tamaa ya kupata mvuto kamili juu ya akili za wanadamu. Katika kusikitika kwake analalamikia fursa aliyoipoteza. Kwa hakika, Ali, na wewe pia unakisikia kila kinachoteremshwa kwangu na pia unaona kila ninachooneshwa mimi. Kwa tofauti hii tu kwamba, wewe hukupewa utume, lakini utakujakuwa mrithi wangu, msaidizi na waziri, na siku zote utakuwa unatetea ukweli na haki.” Utotoni ndio umri ambao mtu ana uwezo kamili wa kupata sifa nzuri. Ali aliishi kiasi kikubwa cha maisha yake pamoja na Mtume peke yake. Aliigiza mwenendo wa Mtume na alidumu kuwa ametengana na jamii yake ambayo ilikuwa ikiendesha maisha ya taabu, iliyokuwa imefungwa kwa umadhubuti na nyororo za desturi za kurithi. Kwa miaka mingi Ali aliishi katika mazingira safi kando ya binamu yake na alikuwa amependwa sana naye. Hakuna hata mmoja wa masahaba na wafuasi wa Mtume aliyeweza kuendeleza uhusiano wa karibu naye kama huo. Ali alifungua macho yake katika njia ambayo ilikuwa imefunguliwa na binamu yake kwa ajili yake. Alijifunza jinsi ya kumwabudu Mwenyezi Mungu kutokana na swala za Muhammad. Alifaidi mapenzi, upole na undugu na Muhammad. Uhusiano wake na Muhammad ulikuwa sawa na ule wa Muhammad na Abu Talib. Wakati Ali alipopata hisia za mapenzi kwa mara ya kwanza kabisa akilini mwake alimpenda Muhammad. Alipozungumza kwa mara ya kwanza alizungumza na Muhammad. Katika tukio la kwanza hasa alilotakiwa kuonyesha ujanadume wake na ujasiri, alionyesha kuwa tayari kumsaidia Muhammad. Marafiki wa Muhammad walikuwa marafiki kwake, 27

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 27

9/4/2017 3:47:45 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

na maadui zake pia waliiheshimu haiba yake. Ali alikuwa mfuasi na mwanafunzi wa Mtume kiasi kwamba akawa ni nafsi na sehemu ya viungo vyake. Katika siku za mwanzoni za ujumbe wa kitume wa Mtume, baadhi ya watu wazima miongoni mwa Maquraishi ambao walichukia ibada ya masanamu walijiunga naye. Watumwa na watu wasiokuwa na uwezo walikuja karibu yake kwa matarajio ya haki na uhuru. Na baada ya alipokuwa amefanikiwa na kuwa mshindi, kundi la tatu pia lilijiunga naye, kwa sababu wale watu hawakuwa na njia nyingine iliyobakia. Walitaka kunufaika kutokana na ile hali mpya, na wengi wa Bani Umayyah walikuwemo kwenye kundi hili. Makundi haya tofauti yalijiunga na Uislamu katika nyakati tofauti na ingawa yalifanana, kundi moja na jingine, katika suala la utiifu kwa Mtume, viwango vya imani zao vilitofautiana. Hata hivyo, kwa vile Ali alikuwa amezaliwa na kulelewa katika mzunguko wa utume, imani yake ilikuwa ya asili na ya kimaumbile, na alijitokeza kutoka kwenye mwili wa mama yake pamoja na imani yake ndani ya moyo wake. Imani yake haikuhusiana chochote na umri au mabadiliko ya wakati. Aliswali na kushuhudia utume wa Muhammad katika umri ambao mtoto hawezi kuelezea mawazo yake. Na aliyafanya yote haya bila ya kupata amri au ushauri kutoka kwa mtu yeyote yule. Wengi wa watu waliosilimu katika siku za awali za utume wa Muhammad walikuwa wamewahi kuabudu masanamu katika siku zilizopita. Hata hivyo, wakati Ali aliposujudu kwa mara ya kwanza ilikuwa ni mbele ya Allah wa Muhammad. Hiki ndio kilikuwa kiwango cha sifa ya imani ya yule mtu ambaye alijaaliwa kukua kama muunga mkono na mtakia heri wa Mtume, kuwaongoza waumini baada ya Mtume, na kuwaokoa watu kutokana na mabalaa ya wakati. Ali Ni Ndugu Yangu Ili kuonyesha ni kwa kiwango gani undugu wa kiroho uliokuwepo baina ya Mtume na Ali, kwa kiasi gani Ali alirithi maadili ya Mtume, jinsi nafsi ya Ali ilivyopata rangi ya utume, kiasi gani alipendwa na Mtume na kwa kiasi gani alimheshimu na kumtukuza Mtume kwa moyo na ulimi, ni muhimu kwamba hadithi chache ziweze kunukuliwa. Ni baada ya hapo tu, ambapo tunaweza kuhitimisha kwamba, kulingana na kanuni adhimu ambazo zilikujakuwa chanzo cha kuimarisha dini ya Uislamu, Mtume alikuwa anaandalia njia kwa ajili ya ukhalifa wa Ali. Na alikuwa akifanya hivyo, kwa sababu aliweza kuuona uso wake mwenyewe katika kioo cha kiwiliwili cha Ali na zile tabia nzuri alizokuwa nazo yeye, alikuwa nazo Ali pia kama itakavyoelezwa 28

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 28

9/4/2017 3:47:45 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

baadaye. Tabrani amemnukuu Ibn Mas’ud akisema kwamba Mtume alisema: “Kuuangalia uso wa Ali ni ibada.” Na Sa’d Ibn Abi Waqqas ananukuu kutoka kwa Mtume akisema: “Yeyote atakayemuudhi Ali ameniudhi mimi.” Ya’qubi amesimulia katika sehemu za historia (Tarikh) yake kwamba, wakati Mtume alipokuwa akirejea Madina kutoka kwenye “Hijjatul-Wadaa” – Hijja ya Muago – mnamo mwezi 18, Dhul-Haj, alisimama mahali paitwapo Ghadir-Khum karibu na Juhfah, akatoa hotuba na kisha akaushika mkono wa Ali na akasema: “Yeyote yule ambaye mimi ni bwana kwake, Ali pia ni bwana kwake. Ewe Mwenyezi Mungu! Mpende anayempenda Ali na uwe adui kwa yule atakayemfanyia uadui Ali.” Fakhrud-Din ar-Razi amesimulia katika Tafsirul-Kabir kwamba baada ya hapo, Umar ibn al-Khattab alimsalimia Ali na akasema kumwambia yeye: “Ewe Ali! Umekuwa bwana wangu na vile vile bwana wa kila Muislamu mwanaume na mwanamke.” Hadithi hii imesimuliwa kutoka kwa masahaba kumi na sita wa Mtume na Ulamaa na wanahistoria kama Tirmidhi, Nasa’i, Ahmad ibn Hanbal, na vile vile imethibitishwa na washairi wengi, wa mbele sana miongoni mwao akiwa ni Hasan bin Thabit Ansari. Yeye anasema: “Katika siku ya Ghadir Mtume aliwaita watu pale Khum, na akaifanya sauti yake iyafikie masikio ya wote na akasema: Ni nani mkuu na bwana wenu? Watu hawakujifanya hawajui na wakasema: Mungu Wako ndiye Bwana wetu na wewe ni Mtume wetu nasi sio watovu wa utii kwako.” Halafu Mtume akamwambia Ali: ‘Nyanyuka; kwani kwa hakika nimekuchagua wewe kuwa Imam na kiongozi baada yangu.’ Hivyo, kwa yeyote yule ambaye mimi ni bwana kwake, huyu Ali pia ni bwana kwake. Mnapaswa kwa hiyo, muwe marafiki zake wa kweli na wafuasi wake.” Abu Tamam Tai ni mmoja wa washairi ambao wamelitaja tukio hili la siku ile. Mshairi mwingine, Kumait Asadi ametoa maelezo ya kina juu yake katika kitabu chake, al-Qasidah al-Ainiyya. Yeye anasema pamoja na mambo mengine: “Katika ardhi ya Ghadir-Khum Mtume alifanya tangazo kuhusu ukhalifa wake. Nilitamani kwamba uamuzi wa Mtume ungekubaliwa. Sijawahi kuona siku muhimu kama ile siku ya Ghadir na sijawahi haki kama hiyo ikikiukwa.” Abu Sa’id Khudri amenukuliwa katika Kitab Aal Ibn Khalwiyya kwamba amesema kwamba Mtume alimwambia Ali:

29

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 29

9/4/2017 3:47:45 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

“Mapenzi juu yake ni imani; na uadui kwako ni unafiki.” “Rafiki yako atakuwa ndiye mtu wa kwanza kuingia Peponi na adui yako atakuwa mtu wa kwanza ambaye atatupwa kwenye Moto wa Jahannam.” Wasimulizi wanaamini kwamba Mtume aliungalia uso wa Ali kila mara, na akasema: “Huyu ni ndugu yangu.” Abu Huraira amesimuliwa kuwa amesema kwamba Mtume aliwahutubia masahaba zake akisema: “Kama mnataka kuiona elimu ya Adam, ushupavu wa Nuh, tabia za Ibrahim, swala na maombi ya Musa, uchamungu wa Isa na uongozi wa Muhammad vikiwa vimekunywa vyote ndani ya mtu mmoja, mwangalieni yule mtu anayekujieni.” Wakati watu walipoamsha vichwa vyao walimuona kwamba alikuwa ni Ali.” Wakati mmoja mtu alilalamika kuhusu Ali mbele ya Mtume. Katika kumjibu, Mtume akasema: “Wewe unataka nini kutoka kwa Ali? Unataka nini kutoka kwa Ali? Unataka nini kutoka kwa Ali? Ali anatokana na mimi, na mimi natokana na Ali na baada yangu yeye ndiye bwana wa waumini wote.”4 Mtume alimtuma Ali kwenda Yemen. Baadhi ya masahaba zake walimuomba awape wale ngamia waliopokelewa kama sadaka, wawapande ili kwamba ngamia wao wenyewe waweze kupumzika. Ali hakuridhika na ombi lao. 4

tume alituma vikosi viwili maalum vya wapiganaji kwenda Yemen – kimoja chini ya uongozi wa Imam Ali M na kingine chini ya uongozi wa Khalid bin Walid na akasema kwamba kama vikosi vyote vitafika pale pamoja, uongozi utabakia na Ali. Khalid ambaye alikuwa amejawa kikamilifu na hisia za zama za ujahilia alikasirishwa sana kwa jambo hili. Baada ya kumalizika kwa kazi hiyo, kwa hiyo, aliwatuma watu kwa Mtume kulalamika dhidi ya Ali. ahaba Buraidah, mchukuaji wa barua hiyo anasema: “Niliiweka mbele ya Mtume barua ile niliyokuwa nimeiS leta na akaisomewa. Mtume alikasirika sana kiasi kwamba niliona dalili za hasira katika uso wake. Halafu nikasema: “Ewe Mtume wa Allah! Ninatafuta hifadhi kwako. Barua hiyo ilitumwa na Khalid na aliniamuru mimi kuileta kwako. Kwa vile alikuwa ni kamanda wangu, basi nilitii amri yake.” Mtume akasema: “Usizungumze vibaya kuhusu Ali. Yeye anatokana na mimi, na mimi natokana naye na yeye ndiye bwana wako na mtu mwenye mamlaka baada yangu mimi.” (Musnad - Ahmad Hanbal, Juz. 5, uk. 356; al-Khasais – Nasa’i, uk.24) dani ya moja ya vitabu vya Hadith, nyongeza kwenye hadithi iliyotajwa hapo juu inapatikana na ni kwamba, N pale Buraidah alipoona tabia na hasira kali ya Mtume aliingiwa na shaka katika akili yake kuhusu imani yake mwenyewe, na, kwa hiyo, akamwambia Mtume: “Natoa kiapo kwako cha haki za usuhuba ambao upo kati yetu kwamba unaweza kunyoosha mkono wako ili nichukue kiapo cha utii upya na dhambi yangu iweze kusamehewa.” (Majmaul-Zawaid, Juz. 9, uk. 128) Kwa msingi wa simulizi hii, Imam ndiye msimamizi, mtu mwenye mamlaka na mlezi wa Waislamu, baada ya Mtume. Yaani anakuwa na ulezi ule ule juu ya maisha na mali za watu, katika kiwango cha mrithi wa Mtume kama Mtume mwenyewe na kwa kweli, anatumia mamlaka yake kwa manufaa yao ya kidunia na kiroho kama dharura za mazingira zinavyohitajia. 30

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 30

9/4/2017 3:47:45 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Pale wote waliporudi Madina, wale watu ambao maombi yao yalikuwa yamekataliwa na Ali wakalalamika dhidi yake kwa Mtume. Sa’d ibn Malik Shahiid akawa kama msemaji wao. Yeye alisema kwamba Ali alikuwa mkali kwao na pia akalielezea hilo tukio husika.Wakati alipokuwa akizungumza, Mtume alipiga paja lake kwa mkono wake na akasema kwa sauti: “ Oh, Sa’d! Acha kulalamika dhidi ya Ali. Unapaswa kutambua kwamba yeye amejitolea katika njia ya Mwenyezi Mungu.” Inajitokeza kutoka kwenye hadithi iliyotajwa hapo juu, na vile vile kutoka kwenye nyingine nyingi ambazo hazikunukuliwa hapa kwamba Mtume alimchukulia Ali kama ndugu yake, na Ali pia, alikuwa amefurahi sana kwa udugu huo. Zaidi ya hayo, Mtume alikuwa akivuta mazingatio ya watu kwenye sifa na maadili ambayo yalikuwa yamejishajiisha katika nafsi ya Ali, ili waweze kujua kwamba yeye alikuwa ndiye mtu bora wa kuubeba ujumbe wa Uislamu baada yake. Baadhi ya mifano imetajwa katika hadithi sahihi, ambayo inaonyesha kwamba hali za asili pia zilisaidia katika kujenga ulinganifu baina ya Muhammad na Ali, na zikatengeneza matukio na mazingira kwa namna ambayo kwamba Ali alionyesha sifa zake ambazo hazikushirikiana mtu mwingine pamoja na yeye. Moja ya sifa hizo ilikuwa kwamba yeye alizaliwa ndani ya Ka’bah, ambayo ndio “Qibla” cha Waislamu, na kuzaliwa kwake kulitokea wakati wito wa Uislamu ulikuwa karibu kutolewa na Muhammad, na hakuufanya hadharani. Katika siku hizo, yeye alikuwa akikaa kwenye nyumba ya baba yake Ali, Abu Talib. Ali alipofungua macho yake alimuona Muhammad na Khadijah wakitekeleza swala. Yeye alikuwa ndiye mwanaume wa kwanza kuonyesha imani juu ya Muhammad ingawa alikuwa bado hajakuwa mtu mzima. Pale watu walipomlaumu kwa kujiunga na Uislamu bila ya ruksa ya baba yake, yeye aliwajibu mara moja: “Mwenyezi Mungu ameniumba mimi bila ya kutaka mapatano na Abu Talib. Basi kwa nini nilazimike kupata ruksa ya baba yangu kumuabudu Mwenyezi Mungu?” Kwa kiasi cha muda mrefu, dini ya Uislamu ilibakia katika mipaka ya nyumba ya Muhammad na kwa wakati huo walikuwepo Waislamu wanne katika dunia ambao ni Muhammad, mke wake Khadija, binamu yake Ali na mtumwa wake Zaid bin Harith. Katika siku ambayo Muhammad aliwaalika jamaa zake kwenye karamu, na akataka kuwahutubia na kuwasilisha huo ujumbe wa Uislamu kwao, ammi yake Abu 31

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 31

9/4/2017 3:47:45 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Lahabi alimkatisha na kuwachochea wale waliokuwepo dhidi yake. Matokeo yake watu wote hao wakasimama na kuondoka nyumbani kwa Muhammad. Mtume akaja akawakaribisha mara nyingine tena na akasema, baada ya kumaliza kula chakula: “Simfahamu mtu yeyote katika Arabia ambaye ameweza kuwaletea zawadi ambayo ni bora kuliko hiyo ambayo mimi nimeileta kwenu. Ni nani miongoni mwenu atakayenisaidia mimi?” Watu wote waliokuwa wamehudhuria hapo walikataa kuukubali wajibu huo na wakataka kuondoka humo nyumbani kama pale mwanzoni, lakini wakati huo huo Ali, ambaye alikuwa bado ni kijana mdogo na hajapata umri wa utu uzima alisimama na akasema: “Ewe Mtume wa Allah! Mimi nitakusaidia na nitapigana dhidi ya yeyote atakayekupinga wewe.” Jamaa wa ukoo wa Bani Hashim walicheka sana na halafu wakaondoka huku wakimdhihaki Abu Talib na Ali. Katika kila vita Ali alikuwa ndiye mshika bendera wa Mtume. Aliutoa ujasiri wake, damu, moyo, ulimi na maisha yake yenyewe kwa ajili ya binamu yake, Mtume, na kwa ajili ya mafanikio na ushindi wa Uislamu. Aliwaponda ponda maadui wa Muhammad na akaonyesha uhodari wake kama, na wakati hali ilipodai. Katika wakati wa vita vya Handak, pale masahaba wa Mtume walipokuwa na wasiwasi na kufadhaika kwa sababu ya hofu na woga juu ya maadui, Ali alisimama kama jiwe mbele ya wale wakuu wa Maquraishi na akaonyesha vitendo vya ujasiri kiasi kwamba Waislamu wakawa na matumaini ya ushindi wao, na Maquraishi na washirika wao ikawabidi washindwe. Katika vita vya Khaybar, Ali alifanya Jihadi ambayo ilikuwa inashangaza. Zile ngome za Khaybar, ingawa zilikuwa imara sana, zilitekwa mikononi mwake. Hii ilikuwa licha ya ukweli kwamba wapiganaji mashujaa sana na wenye uzoefu walikuwa wamekusanyika pale na masahaba wa Mtume walikuwa wanawaogopa. Kwa kifupi kule kuzingirwa kwa ngome hiyo na Waislamu kulichukua muda mrefu. Wapiganaji waliokuwa ndani yake walikuwa wakijilinda kwa ushupavu sana, kwa sababu walijua kwamba kama watashindwa na Muhammad nguvu zao katika Rasi ya Arabia zitakuwa zimefikia mwisho na shughuli zao na mamlaka vitaondoka. Mtume alimtuma Abu Bakr kwenda kuiteka ngome hiyo. Yeye alionyesha uwezo wake katika namna yake mwenyewe na akarudi bila kupata mafanikio. Katika siku iliyofuatia alimtuma Umar ibn Khattab, lakini pia yeye alirudi kama Abu Bakr bila ya kupata mafanikio yoyote yale, na hakuweza kuishinda ile ngome ya juu na wale

32

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 32

9/4/2017 3:47:45 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

wapiganaji wenye silaha. Mtume ndipo akamwita Ali na kumuagiza akaishinde na kuiteka ile ngome. Ali kwa furaha sana alitoka kwenda kutekeleza wajibu wake kwa ajili ya Uislamu. Wakati alipoikaribia ngome hiyo, na wale waliokuwa ndani walipokuja kutambua kwamba safari hii, Ali mwana wa Abu Talib, ambaye alikuwa hajapata kushindwa katika pambano lolote lile, amekuja kujiunga na vita hivyo, vikosi vyao vingi vilitoka nje ya ngome hiyo mara moja, na mmoja wa wapiganaji wao akashambulia kwa nguvu sana kiasi kwamba ngao ilidondoka kutoka mkononi mwa Ali. Yeye mara moja aliling’oa lile lango la ngome hiyo na akaendelea kupigana, akilitumia hilo kama ngao yake, hadi ngome hiyo ilipotekwa. Na ngome hiyo haikutekwa tu bali hadi idadi kadhaa ya wapiganaji ilipokuwa imeuawa, na wa kwanza miongoni mwao alikuwa ni Harith bin Abi Zainab. Katika hatua hii tunakutana na jambo moja la ajabu. Katika historia ya wahenga wetu tunawakuta mashujaa wengi ambao walikuwa wamepigana vita kwa ajili ya imani zao, lakini ndani ya roho za nyoyo zao walitaka amani na walitamani kwamba tatizo hilo lingesuluhishwa bila ya kukimbilia kwenye vita. Mbali na hao, pia tunawajua mashujaa wengi ambao waliokufa kishahidi ili kufanikisha malengo yao. Hata hivyo, vita kama hivyo na vifo vya mashahidi sanasana vilikuwa sio vya kufikiriwa au kupangwa. Ni matukio ya ghafla ambayo kwa kawaida yanatokea kutokana na kuzuka kwa tamaa na hamasa mbele ya watazamaji. Hata hivyo, suala la Ali mwana wa Abu Talib ni la kustusha sana kwa sababu ili kuilinda dini ya Muhammad na yake yeye mwenyewe, na kwa ajili ya undugu, na katika njia ya Mwenyezi Mungu, alijianika mwenyewe kwenye hatari mbaya kabisa. Ni tukio ambalo halina kifani katika historia na kwa wingi sana, linathibitisha ule umoja na ulinganifu wa watu hawa wawili mashuhuri mno. Pale usumbufu wa Maquraishi ulipofikia kiwango chake cha hali ya juu kabisa, na walipokuwa wanapanga kumuua Muhammad na kuuangamiza Uislamu, Mtume alikwenda kwenye nyumba ya Abu Bakr na kumwambia kwamba kwa vile Maquraishi walikuwa wanapanga njama ya kuuwa, yeye ameamua kuhama. Abu Bakr alionyesha nia yake ya kutaka kuandamana na Mtume, naye Mtume akamkubalia maombi yake. Wakati wote walipoamua kuhama, walikuwa na uhakika kwamba Maquraishi watawafuatilia. Kwa hiyo Muhammad alipendekeza kufuata njia ya mchepuko na 33

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 33

9/4/2017 3:47:45 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

kwamba waondoke majumbani kwao katika wakati ambao kwa kawaida hawawezi kutegemewa kufanya hivyo. Ndani ya usiku huo huo, ambao Muhammad aliamua kuhama, hao Maquraishi walikuwa wameamua kumuua na walikuwa wameweka kikundi cha wapiganaji wazoefu kuizunguka nyumba yake ili asije akaweza kutoroka kwenye kinga ya giza. Hata hivyo, Muhammad alimuomba binamu yake Ali kwa siri kabisa alale kwenye kitanda chake na kujifunika mwenyewe na lile shuka lake la kijani. Alimuomba abakie pale Makkah hadi atakapokuwa amezirudisha kwa watu zile amana walizokuwa wamezihifadhi kwake Muhammad. Kama kawaida Ali alitii yale maagizo ya Mtume kwa furaha kabisa. Kama ilivyoelezwa hapo juu, Maquraishi walikuwa wameizingira nyumba ya Mtume. Walichungulia kupitia kwenye matundu na wakamuona mtu amelala juu ya kitanda cha Mtume. Wakawa kwa hiyo wameridhika kwamba Mtume hakuwa ametoroka. Katika sehemu ya mwisho ya usiku huo pale maadui walipodhania kwamba Mtume alikuwa amelala kitandani kwake, yeye kwa kweli alikuwa yuko kwenye nyumba ya Abu Bakr, ambako kutokea hapo wote wawili walitoka kuelekea kwenye Pango la Thuur. Baada ya kupata ishara, Maquraishi hao walifika sehemu hii pia, lakini Mwenyezi Mungu akawaficha kutoka machoni mwa maadui hao. Mifano ya kujitolea muhanga nafsi iliyoonyeshwa na Ali ni ya nadra sana. Mtu anasitasita kati ya uhai na kifo na anatafakari endapo mtu anapaswa kutoa mhanga maadili ya hali ya juu, ambayo ndio msingi wa maisha yake mtu, kwa ajili ya starehe duni za maisha ya kidunia. Kama, katika tukio kama hilo, mtu anachagua kufa kishahidi, ni ushahidi wa ukweli kwamba katika macho yake maisha halisi ni maisha ya milele na sio maisha ya mpito ya kidunia. Kwa kweli, utii kama huo na muhanga wa nafsi ni nadra sana hapa duniani. Kama Socrates na wengine kama yeye walikikaribisha kifo kwa furaha, Ali mwana wa Abu Talib vile vile aliyaweka maisha yake mikononi mwa Mtume kwa hiari yake huru mwenyewe. Hata hivyo, kuingia kwenye medani ya vita na kukikaribisha kifo, au kunywa kikombe cha sumu ni rahisi sana vikilinganishwa na kitendo hicho cha kishujaa kilichotendwa na Ali. Hebu fikiria namna ilivyo vigumu kwa mtu kulala katika kitanda cha mtu ambaye maadui zake wamepania juu ya kumuua, na sio rahisi kutoroka kutoka mikononi mwao, hususan pale ambapo pengine watakuwa wanaangalia kutoka umbali 34

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 34

9/4/2017 3:47:45 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

wa hatua chache na kuonyesha ishara za mashambulizi ya kikatili, na yeye awe anaangalia nyendo zao na kuyasikia maneno yao na kuziona panga zao zenye uchu wa damu zikipunga kichwani mwake, na huenda aupitishe usiku wote katika hali kama hii. Katika hatua hii ya hatari, Ali alimuigiza Mtume na akaonyesha uwezo wa stahimili ambao alikuwa ameupata kutokana na kushirikiana kwake na binamu yake adhimu. Kulala kwake juu ya kitanda cha Mtume kulikuwa ni kipimo cha jihadi yake na juhudi kwa ajili ya uendelezaji wa dini aliyokuwa akiilingania. Jambo hili la hatari linaifichua asili ya Imam kwamba matendo yake hayakuwa yametiwa doa na unafiki, na yalifanana na kutoka nje kwa lulu kutoka kwenye koa. Linaonyesha vile vile akili yake kubwa na umaizi usio na kifani, kwa sababu haiwezekani kwa mtu mwingene yeyote kuelewa kikamilifu ukweli wa ulinganio wa Uislamu katika umri mdogo kama huo. Ukweli huu pia unaonyesha sifa bainifu nyingine nyingi za Ali. Unaonyesha kwamba hakuweka umuhimu wowote ule katika maisha ya kidunia. Alikuwa mwaminifu na mkweli sana. Hakujipendelea yeye mwenyewe kuliko watu wengine. Alikuwa vile vile yuko tayari kujitolea uhai wake kwa ajili ya wale wanaokandamizwa, ili waweze kuwa wameondokewa na udhalimu huo, na ule ujumbe wa ki-utume wa Mtume uweze kufanikiwa. Uaminifu, ushupavu na ujasiri wa uadilifu, na sifa nyingine zote njema, zilikuwa zimeunganika katika nafsi ya mtu huyu. Kujitolea muhanga kulikoonyeshwa na yeye katika hatua hii, kulikuwa ni utambulisho wa matendo ya kishujaa aliyoyafanya yeye katika siku za baadae. Palikuwepo na uhusiano madhubuti wa upendo na undugu baina ya Muhammad na Ali, na walisaidiana wao kwa wao kuhusiana na wito wa Uislalmu. Ushirikiano huu ulianza pale Muhammad alipomtambua Abu Talib, na Ali kumtambua Muhammad, yaani kuanzia pale watu hawa mashuhuri na adhimu walipokuwa wanaishi pamoja ndani ya nyumba ambayo iliwekwa juu ya misingi ya uchamungu na maadili. Ilikuwa ni moja ya sifa ya nyumba hiyo ya Abu Talib, ambayo ilikuwapo humo kwamba Ali na Abu Talib waliweza kuutambua utukufu wa Muhammad. Kama matokeo ya hili, Abu Talib aliweka mapenzi na upole wake juu ya Muhammad, na Ali akaonyesha utiifu na upendo kwake. Utambuzi huu huu hasa, ulimuandaa Ali kwa mihanga mikubwa. Mtume pia aliutambua ukweli huu vizuri kabisa. 35

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 35

9/4/2017 3:47:45 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Yeye alimpenda Ali kupita kiasi. Hakumpenda tu Ali yeye peke yake, bali pia alitafuta kuwafanya na wengine pia wampende, hivyo kwamba aweze kuchukua wajibu wa ukhalifa baada yake. Alitamani kwamba watu wangetambua kikamilifu sifa za Ali, ili baada ya kifo chake mwenyewe waweze kuona ndani ya Ali ile haiba ya Muhammad mwenyewe, kana kwamba Muhammad alikuwa bado yu hai. Hivyo, waweze kumchagua yeye kwa mapenzi na upole wa hiari zao, na sio kwa sababu alitokana na familia ya Bani Hashim, na kwamba alikuwa binamu wa Mtume. Hii ilikuwa hivyo kwa sababu Mtume mwenyewe alipinga ubaguzi wa namna hiyo na aliwakataza watu kabisa. Ilikuwa ni kwa sababu hii kwamba, kama vile ambavyo yeye alivyoepuka manufaa ya kilimwengu, yeye pia aliwaweka Bani Hashim mbali na kazi za kiserikali ambazo zingeweza kuwaletea manufaa ya kidunia.5 Sifa Za Ali Kati ya watu waliosimulia sifa za Imam Ali ibn Abi Talib, mwandishi wa kitabu Dhakhair al-Uqbah anaandika kwamba: “Kimo chake kilikuwa cha wastani na mfupi kidogo. Ngozi yake ilikuwa ya rangi ya ngano na ndevu zake zilikuwa nyeupe na ndefu. Macho yake yalikuwa makubwa na meusi. Alikuwa na uso mchangamfu na alikuwa na tabia tulivu. Shingo yake ilikuwa ndefu kama bilauri iliyotengenezwa kwa fedha. Mabega yake yalikuwa mapana. Viungo vya mikono yake vilikuwa kama vya simba anayenguruma, kwa sababu mikono yake na vifundo vyake vilikuwa vimeungana kabisa, na kuvipambanua hivyo ilikuwa ni kazi kubwa kabisa. Viganja vyake na vidole vilikuwa na nguvu sana, vinene vya wastani na vyenye nyama. Miundi yake ilikuwa na misuli minene na sehemu zake za chini zilikuwa nyembamba. Mikono yake vilevile ilikuwa minene kwa namna hiyo hiyo. Alitembea kwa utulivu kama Mtume. Hata hivyo, kama, na wakati alipokuwa akitoka kwenda kupigana, basi yeye alitembea haraka na kwa uchangamfu na bila kugeuza kichwa chake kuangalia kitu kingine chochote kile. Nguvu zake za kimwili zilikuwa zisizowazika. Alikuwa kwa kawaida akiwanyanyua wale wapiganaji ambao alibahatika kuwashika kwa mikono yake na kuwatupa chini bila ya taabu au juhudi yoyote, kana 5

tume alitangaza Zaka, ambayo iliunda sehemu kubwa ya rasilimali za hazina ya Umma kuwa ni haramu M kwa Bani Hashim, kwa kiasi kwamba hata hakuwatuma kwenda kukusanya zaka ili watu waweze kutambua kwamba ilikuwa haitumiwi na familia ya Mtume, na ilikusanywa tu ili kuwasaidia watu masikini na kukidhi haja za kawaida za Waislamu. 36

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 36

9/4/2017 3:47:45 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

kwamba walikuwa watoto wadogo. Na kama alishikilia mkono wa mpiganaji yoyote ndani ya kiganja chake, basi mpiganaji huyo asingeweza hata kupumua. Inafahamika kabisa kwamba yeye hakuwahi kupigana na mtu yeyote yule ambaye hakumshinda, hata ingawa angekuwa na nguvu sana na shujaa anayetambulika. Wakati mwingine alinyanyua lango kubwa ambalo idadi kadhaa ya watu wenye nguvu wasingeweza kulifunga au kulifungua, na akalitumia yeye kama ngao ya kujikingia mwenyewe. Katika baadhi ya nyakati yeye alitupa kwa mkono mmoja, jiwe ambalo lisingeweza hata kutingishwa na idadi kadhaa ya watu. Wakati mwingine yeye alinguruma katika medani ya vita kwa sauti kubwa sana ya kutisha, kiasi kwamba watu majasiri kabisa walipatwa na hofu ingawaje idadi yao ingeweza kuwa kubwa sana. Yeye alikuwa na uwezo mkubwa sana kiasi cha kuweza kuhimili matatizo, kiasi kwamba hakuogopa madhara yoyote kutokana na joto au baridi. Alikuwa akivaa mavazi ya kiangazi wakati majira ya baridi, na katika majira ya baridi alivaa mavazi ya kiangazi.” Wakati mmoja mtu alipeleka malalamiko juu ya Ali kwa Umar ambaye wakati huo alikuwa ndiye khalifa. Umar akawaita wote wawili na akasema: “Ewe Abul Hasan! Simama bega kwa bega na huyu mwingine.” Dalili za kuchukia zikaonekana kwenye uso wa Ali. Papo hapo Umar akamuuliza kama alikuwa hapendi kusimama pamoja na yule mtu mwingine. Ali akajibu. “Hapana. Sio hivyo. Hata hivyo, nimeona kwamba wewe hukudumisha usawa kati yangu na mpinzani wangu. Umeniita kwa jina langu la ubaba ‘Kuniyah’ na hivyo kunionyesha mimi heshima ambapo hukufanya vivyo hivyo kwake yeye.”6 Ni vigumu sana kuelezea kikamilifu desturi na tabia za wanadamu na hususan za watu mashuhuri kwa sababu sifa binafsi za watu zinahusiana zenyewe, na kila moja yao huathiri zile nyingine. Kila sifa inahusiana na sifa nyingine, na kila tabia ni chanzo cha tabia nyingine na matokeo ya tabia ya tatu, au mbili kati ya hizo ni athari ya nyingine, vivyo hivyo na kuendelea. Hivyo, ninapendekeza kuchunguza chache kati ya sifa za Ali kutoka kwenye pande tofauti, na kuzilinganisha na mtu huyo huyo ili kufikia kwenye baadhi ya maamuzi kwa njia ya uchambuzi huu wa kiakili. Kwa kuanza kabisa nitaziwasilisha kwa kifupi sifa mbalimbali za Ali kwa kuzihitimisha kutokana na shughuli zake za kawaida na matendo yanayofahamika vizuri 6

aarabu walikuwa hawakuona ni sahihi kuwaita watu wenye kuheshimika kwa majina yao halisi. Endapo, W kwa hiyo, walitaka kutoa heshima kwa mtu, basi walimwita kwa ‘Kuniyah’ yake. 37

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 37

9/4/2017 3:47:46 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

sana ili desturi, tabia na silika zake zinajulikana na maelezo yetu mafupi katika sura zinazofuata yaweze kukomea kwenye sifa na tabia hizo. Sasa tunaanza maelezo yetu kwa kuyarejea matendo yake ya ibada. Ali alijulikana sana kwa uchamungu wake na kujizuia. Alifanya mambo mengi kwa ajili yake mwenyewe, na vilevile kwa ajili ya watu wake mwenyewe na wengineo, kwa vile alikuwa mchamungu sana. Ninaamini kwamba uchamungu wa Ali haukuwa matokeo ya mazingira kama ule wa watu wachamungu wengine, ambao walijishughulisha wenyewe katika ibada kwa sababu ya udhaifu wa nyoyo zao, au kukwepa mabadiliko ya maisha na kukaa mbali na watu, au katika kuwaigiza wahenga wao, na athari za matukio ya maisha zinathibitisha hivyo, kwa sababu kama kanuni, watu wanatoa heshima kwenye mila na desturi za jadi zao.7 Ukweli ni kwamba, uchamungu wa Imam Ali ulisimama katika msingi imara na ulikuwa umeunganika na kile kiungo chenyewe, ambacho kipo katika sehemu zote za maumbile na kimefunga mbingu na dunia kwa pamoja. Ibada yake ilikuwa kwa kweli ni juhudi na kampeni endelevu dhidi ya madhara kwa ajili ya faida ya maisha ya mwanadamu na ustawi wake. Alipigana dhidi ya vipengele vyote vya uovu na ufisadi. Kwa upande mmoja alipigana dhidi ya unafiki na ubinafsi, na kwa upande mwingine dhidi ya woga, unyonge, uduni, kutojiweza na sifa nyingine mbaya ambazo zilikuwa zimewapata watu wakati wa zile siku mbaya. Kulingana na Ali kiini cha uchamungu ni mtu kujitoa muhanga maisha yake kwa ajili ya ukweli na haki. Yeye amesema: “Imani yako iwe kwa kiwango ambacho uwe unapendelea ukweli kuliko uwongo, hata ingawa ukweli huo unaweza kukusababishia hasara, na uwongo ukawa unaweza kukupatia manufaa.” Uchamungu wake ulikuwa wa aina ile ile kama aliyoifafanua yeye. Aliuawa kishahidi kwa sababu ya ukweli huu huu haswa, na kama ingewezekana kutoa jina au cheo cha “Shahidi” kwa watu ambao bado wako hai inaweza kusemekana kwamba hata pale alipokuwa hai, yeye alikuwa ni shahidi katika njia ya ukweli na uadilifu. Kama mtu atachunguza uchamungu wa Imam kwa makini itampambanukia kwamba hata katika siasa na serikali, alikuwa na utaratibu maalum katika suala la 7

wa mujibu wa Wakristo, ‘Ibada’ inajumlisha maisha ya kujitenga na ya ki-utawa. Hata hivyo, utawa hauruhuK siwi katika Uislamu. Ni kwa sababu hii kwamba Waislamu wachamungu hawakukwepa kufanya juhudi katika maisha wala kujitenga na wanadamu wengine. Kwa upande mwingine, nyakati zingine kwa ujasiri kabisa walihatarisha maisha yao yenyewe hasa, hata pale ambapo ingefaa wanyamaze kimya (na wanafanya hivyo hata nyakati hizi za sasa). 38

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 38

9/4/2017 3:47:46 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

ibada ambao aliufuata kwa uimara kabisa. Wakati aliposimama mbele za Mwenyezi Mungu alifanya maombi (Du’a) yake kwa mazingatio kamili, kama vile mshairi anavyozama katika uzuri wa maumbile. Kauli ifuatayo ya Ali ni yenye maelekezo sana kwa wale wanaomwabudu Mwenyezi Mungu na kuonyesha uchamungu: “Kundi moja linamuabudu Mungu ili kupewa upendeleo wa neema Zake. Hii ni ibada ya wachuuzi. Kundi jingine linamuabudu Mungu kwa sababu ya hofu juu Yake. Hii ni ibada ya watumwa. Kundi la tatu humuabudu Mungu kwa njia ya kutoa shukurani. Hii ni ibada ya mtu huru, muungwana.” Tofauti na watu wengi, ibada ya Imam haikuwa kwa sababu ya hofu, na pia haikuwa kama ya mchuuzi kwa matumaini ya kupata Pepo. Kwa upande mwingine pale watu mashuhuri wanaposimama mbele ya Mwenyezi Mungu wanajikuta wao wenyewe wakiwa wanyenyekevu na kulazimika kujiona wenyewe kama waja Wake waovu. Msingi wa ibada hii ni akili, ufahamu na ukamilifu wa kiroho. Mtu atakayetoa nafasi ile ile kwenye ibada kama aliyotoa Ali kwa hakika atayaona maisha katika namna ile ile kama alivyoyaona Ali. Mtu kama huyo hayatafuti maisha kwa manufaa ya dunia na starehe za mpito. Kwa upande mwingine anayatafuta ili kupata maadili mema zaidi na kupata aliyoyakusudia ambayo yanachukuana na tabia yake. Ilikuwa ni kwa sababu hii kwamba Ali alichagua uchamungu hapa duniani, na hakutafuta umaarufu na kuonyesha fahari. Yeye alikuwa mkweli katika suala la uchamungu kwa namna ile ile kama alivyokuwa mkweli katika suala la matendo yake, maneno na manuizi. Hakuwa na ari ya kuelekea kwenye starehe za dunia kwa namna ile ile kama asivyokuwa na raghba juu ya utawala, na mambo mengine ambayo yalikuwa yakipendwa sana na watu wengine. Aliishi na watu wa familia yake katika kibanda ambacho pia kilikuwa ndio makao ya serikali yake. Utawala wake haukuwa katika namna ya ufalme bali katika muundo wa Ukhalifa. Alikula mkate wa shairi uliotayarishwa kutokana na unga uliosagwa na mke wake. Kama mambo yalivyokuwa, serikali yake na watumishi wake walitumia starehe ambazo zilikuwa zimepata kuwepo kutoka Syria, Misri na Iraqi. Mara kwa mara hakumfanya mke wake apate taabu ya kusaga unga na aliifanya mwenyewe kazi hiyo. Ingawa yeye alikuwa ndiye Amirul-Mu’minin lakini alikula mkate ambao ulikuwa mkavu na mgumu kiasi kwamba uliweza kuvujwa kwa kuukandamiza na goti lake. Pale kulipokuwa na baridi sana wakati wa majira ya baridi,

39

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 39

9/4/2017 3:47:46 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

yeye hakuwa na mavazi kwa ajili ya msimu huo na alijitosheleza mwenyewe kwa mavazi ya majira ya kiangazi. Haruun ibn Antara anasimulia hivi kutoka kwa baba yake: “Nilifika mbele za Ali katika Nyumba ya utawala ya Khurnaq wakati wa majira ya baridi na nikaona kwamba yeye alikuwa amevaa shuka chakavu la zamani na alikuwa akitetemeka kwa baridi. Mimi nikamuuliza: “Oh, Amirul-Mu’minin! Mwenyezi Mungu ameweka fungu kwa ajili yako katika hazina ya umma, na licha ya hivyo bado unaishi katika hali hii?” Yeye alijibu akasema: “Namuapa Mwenyezi Mungu kwamba mimi sichukui chochote kutoka kwenye mali yenu ya umma na shuka hili ni lile lile nililokuja nalo kutoka Madina.” Yeye alitumia siku za maisha yake katika nyumba ndogo kwa kuridhika kabisa hadi alipokuja kuuawa kishahidi mikononi mwa Ibn Muljam. Ingawa yeye alikuwa Khalifa, lakini hapakuwa na hata mtu mmoja miongoni mwa Waislamu ambaye aliishi maisha rahisi na kuridhika nayo kama alivyoishi Ali. Kwa kweli huku kukosa tamaa kwa upande wake katika starehe za kidunia kulihusiana na ushujaa wake. Watu wengine wanadhani kwamba sifa mbili hizi ziko mbalimbali na kila mojawapo, lakini maoni haya sio sahihi. Kusema ukweli ushujaa wake ulikuwa ni pamoja na umuhimu wa nafsi yake na juhudi zake za kupata mafanikio makubwa na kuwasaidia masikini na mafukara na wenye shida bila ya kujali manufaa yake mwenyewe binafsi. Ukweli ni kwamba yeye hakuwa tayari kufurahia starehe za maisha wakati ambapo anaishi kwenye mji ambamo ndani yake wasiojiweza wengi na watu masikini walikuwa wakiishi humo pia. Umar ibn Abdul Aziz alikuwa ni Khalifa wa ukoo wa Bani Umayyah. Ukoo huu ulikuwa na uadui mkubwa kwa Ali, walimkashifu na kumtukana kutoka kwenye mimbari za misikiti. Mbali na yote haya, yeye alilazimika kutamka hivi kwa mtazamo wa tabia adhimu ya Ali: “Mtu safi na mchamungu sana hapa duniani alikuwa ni Ali mwana wa Abu Talib.” Inasemakana kwamba Ali hakuweka hata ingawa jiwe juu ya jiwe jingine au tofali juu ya tofali na hakuunganisha tete na tete jingine. Kwa maneno mengine yeye hakujijengea mwenyewe hata nyumba ya matete. Ingawaje lile Kasiri (Ikulu) Jeupe lilijengwa kwa ajili yake, yeye hakukaa humo kwa sababu hakupenda kuishi katika nyumba bora kuliko vile vibanda vilivyojengwa kwa miti vinavyokaliwa na watu masikini. Tabia ambayo Ali aliendesha nayo maisha inaakisiwa katika kauli yake 40

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 40

9/4/2017 3:47:46 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

mashuhuri sana ifuatayo: “Hivi nitosheke mwenyewe na hili kwamba watu wananiita Amirul-Mu’minin na nisishiriki katika mabadiliko ya maisha pamoja nao.?” Ibn Athiir amesimulia kwamba wakati Ali alipomuoa binti ya Mtume, Fatimah, kitanda chao kilikuwa na ngozi ya kondoo tu. Waliitumia ngozi hiyo kama godoro wakati wa usiku, na wakaweka majani wakati wa mchana kwa ajili ya kumlisha ngamia wao. Hawakuwa na mtumishi zaidi ya mmoja. Katika Ukhalifa wa Ali, mali kadhaa zilipokelewa kutoka Isfahani. Yeye aliigawanya sehemu saba. Ilikuwa pia na bofulo la mkate na yeye aliuvunja mkate huo pia katika vipande saba. Ujana-dume ulikuwa umejitokeza ndani ya Ali katika hali zote na ilikuwa ni pamoja na sifa zake zote muhimu. Kukubali mawazo ya wengine na kusamehe ni viambatani muhimu vya ujanadume na vilikuwa vimekolea sana kwenye desturi za Imam. Ilikuwa ni kwa sababu hii kwamba hakufikiria hata kumdhuru mtu yeyote ingawa angekuwa na uwezo wa kumdhuru, na hakumkandamiza mtu ambaye kuhusu yeye alijua kwamba alitaka kumuua yeye. Bani Umayyah walimtukana na kumkashifu lakini yeye hakulipiza kisasi kwa njia hiyo hiyo, kwa sababu watu wakarimu huwa hawawatukani watu wanaowatukana wao. Imam Ali aliwakataza wafuasi wake mwenyewe kuwatukana Bani Umayyah. Wakati wa vita vya Siffin yeye alijulishwa kwamba baadhi ya masahaba zake walikuwa wakiwatukana Bani Umayyah, juu ya hili yeye alisema: “Mimi sipendelei kwamba ninyi muwe wamojawapo wa wale wanaotumia lugha ya matusi. Hata hivyo, kama mtataja makosa yao na tabia zao, mtakuwa na uhalali wa kufanya hivyo na mtakuwa mnatamka kauli ya mwisho. Katika kuyajibu matusi yao mnapaswa mseme: “Ewe Mola! Ilinde damu yetu na ya kwao vile vile. Ziokoe roho zetu na zao kutokana na upotofu, na utuongoze sisi ili kwamba yule ambaye hajautambua ukweli aweze kuutambua, na yeye yule ambaye anajihusisha katika udhalimu na upotofu aweze kuacha.” Hana wa mfano wake katika historia kwenye suala la msamaha na kufumbia macho makosa, na kuna matukio yasiyo na idadi ambayo yanatoa mwanga kwenye sifa hizi za Imam. Inasemekana kuhusiana na hili kwamba katika tukio la vita alitoa pamoja na mambo mengine, maelekezo yafuatayo kwa wapiganaji wake: “Msimuue adui anayekimbia zake. Msizuie msaada kwa mtu ambaye hajiwezi na aliyejeruhiwa. Msimvue nguo mtu yoyote. Msichukue mali ya mtu yeyote kwa kutumia nguvu.”

41

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 41

9/4/2017 3:47:46 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Mwishoni mwa vita vya Ngamia yeye aliswali swala ya maiti kwa ajili ya wale maadui waliokuwa wameuawa, na akamuomba Mwenyezi Mungu kwa ajili ya msamaha wao. Pale alipopata udhibiti juu ya wale maadui wa jadi kama vile Abdullah ibn Zubayr, Marwan ibn Hakam, na Sa’d ibn al-Aas, yeye aliwasamehe, akawatendea kwa upole na akawakataza wafuasi wake kuwaadhibu, ingawa alikuwa katika nafasi nzuri ya kuwafanyia vitendo vikali, na wao pia hawakutegemea kwamba wataachiwa huru. Mfano mwingine wa kufumbia macho makosa ni huu kwamba, alipoweza kumshinda Amr bin al-Aas, aligeuzia uso wake pembeni na kumuachia aondoke, ingawaje kwa vyovyote alikuwa ni tishio dogo kuliko Mu’awiyah na alibakia na uadui wake hata baada ya huruma zake Ali. Pale alipouona upanga wa Ali (Dhulfiqar) juu ya kichwa chake, alitenda tendo fulani na akatarajia kwamba endapo atafanya hivyo, basi Ali atafumba macho yake na kumuacha.8 Kama Ali angemuua Amr ibn al-Aas wakati ule, udanganyifu ungeweza kuondoshwa, na jeshi la Mu’awiyah pia lingeweza kuangamizwa. Katika vita vya Siffin, Mu’awiyah na wafuasi wake waliamua kumshinda Ali kwa kuwaathiri yeye na masahaba zake kwa kiu. Kwa siku kadhaa, kwa hiyo, walizuia njia yake ya kwenda mto Furati na kutishia kwamba hawataruhusu jeshi lake kutumia maji hayo na watawafanya wafe kwa kiu. Hata hivyo, jeshi la Ali lilifanya shambulizi na kupata udhibiti wa ukingo wa mto huo. Lakini Ali alimtendea Mu’awiyah katika namna tofauti. Bila ya kujali ule ukweli kwamba angeweza kusimamisha mgao wa maji kwa jeshi hilo la Syria, kama hatua ya kulipiza kisasi, yeye aliwaruhusu kuyatumia maji kama vile ambavyo watu wake mwenyewe walivyokuwa wakiyatumia. Mara tu alipopata kuelewa kwamba watu wawili walikuwa wanamshutumu Aisha kwa kuanzisha vita hivyo vya Ngamia, na juu ya kupanga kwao kumuua yeye Ali. Aliagiza kwamba kila mmoja wao aweze kuchapwa viboko mia moja kwa njia ya adhabu kwao. Baada ya kupata ushindi katika vita vya Ngamia, yeye alimrudisha Aisha kwenda Madina kwa hadhi inayostahiki na heshima pia. Alimsindikiza kwa kitambo cha 8

I nasemekana kwamba wakati Amr ibn al-Aas alipokuja kupigana na Ali katika vita vya Siffin alikuwa na woga mwingi sana. Hakuweza kufikiria njia nyingine yoyote isipokuwa kwamba alale chini na kufunua sehemu zake za siri ili kwamba Ali aweze kufumba macho yake, na yeye mwenyewe aweze kuponyoka. Kwa hiyo, yeye alifanya hivyo na kwa hiyo akayaokoa maisha yake. 42

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 42

9/4/2017 3:47:46 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

maili chache na pia akawatuma baadhi ya watu pamoja naye, ili waweze kumtumikia humo njiani, na yeye afike Madina kwa starehe kabisa. Licha ya kuwa kwake jasiri, Ali aliepuka kuwa mkandamizaji. Wasimulizi wa Hadith na wanahistoria wanakubaliana kwamba yeye alichukia vita na hakuikimbilia, isipokuwa wakati kulipokuwa hakuna njia nyingine mbadala iliyokuwa imebakia. Yeye wakati wote alijaribu kwamba mambo yaweze kumalizwa na maadui bila ya kumwaga damu na mapigano. Alikuwa akimshauri mwanawe Hasan asije akamualika mtu yeyote kwenye mapigano. Wakati wote alikuwa mwaminifu juu ya kile alichokisema na alifuata sera ile aliyoipendekeza kwa mwanawe hadi alipolazimika kufanya vinginevyo. Kwa mfano pale Khawarij walipokuwa wanajiandaa wenyewe kwa vita, masahaba wa Ali walimshauri kwamba awashambulie kabla hawajawa tayari kuanzisha vita. Ali, hata hivyo alijibu: “Mimi sitaanza kupigana mpaka wao waanze vita hivyo wenyewe.” Imani yake na sifa za kibinadamu zilimlazimu yeye kuwazuia watu kutokana na kupotoka kwa njia ya ushauri. Siku moja alikuwa anatoa hotuba kwenye mkusanyiko wa watu, na Ma-Khawarij wengi ambao walimchukulia yeye kuwa ni kafiri pia walikuwepo na walikuwa wakimsikiliza. Mmoja wao aliyekuwa akistaajabia lugha yake tamu na fasaha akasema: “Mwenyezi Mungu amuue kafiri huyu! Ana hekima na akili kiasi gani hiki!” Wafuasi wa Ali wakataka kumuua mtu huyo. Yeye Ali, hata hivyo akawaambia: “Amefanya jambo la makosa kwa ulimi wake. Ninyi mnapaswa kwa hiyo, ama kulipiza kisasi kwa ulimi au kumsamehe.” Tumekwishataja hapo juu kwamba jeshi la Mu’awiyah lilizuia njia ya Ali kwenda mto Furati ili waweze kusalimu amri kwa sababu ya kiu, lakini pale Ali alipopata udhibiti wa ukingo wa mto huo, hakulizuia jeshi la Mu’awiyah kuyatumia maji hayo. Matukio mengi kama hilo yalitokea kiasi Mu’awiyah anavyokuwa amehusika, lakini haiwezekani kutoa maelezo yake hapa. Matukio yote haya yanaonyesha kwamba kama ilivyotakiwa na nafsi yake ya kimalaika, alikuwa mpole hata kwa maadui zake na alikuwa mwadilifu na mkarimu kwa wote. Mwanahistoria mmoja anasimulia hivi kuhusiana na vita vya Siffin: “Mtu anayeitwa Kariiz ibn Sab’ah Humeri alijitokeza kutoka kwenye jeshi la Mu’awiyah kuja kwenye uwanja wa vita na akasema akiwa amesimama katikati ya maadui: ‘Kuna mtu ambaye anaweza kutoka kuja kupigana na mimi?’ Mmoja wa wapiganaji wa Ali akatoka kupigana naye na akauawa. Yule mtu akauliza tena kuhusu mpinzani mwingine. 43

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 43

9/4/2017 3:47:46 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Mpiganaji mwingine akatoka lakini na yeye aliuawa, na bado mtu mwingine akakutana na kifo mikononi mwa Kariiz. Pale alipodai mpinzani mwingine kwa mara ya nne, hakuna aliyetoka kwenda kupigana naye. Watu waliokuwa safu ya mbele walirudi nyuma. Ali akahisi kwamba palikuwa na hatari ya jeshi lake kuvunjika moyo. Yeye, kwa hiyo, akatoka mwenyewe kwenda kupigana na Kariiz na akamuua. Kisha akaua mtu mwingine, na baada ya hapo mtu mwingine wa tatu pia alikutana na balaa hilo hilo. Baada ya kuwa amewaua wapiganaji watatu, Ali akasema kwa sauti kubwa maneno haya ambayo yalisikiwa na wote: “Kama msingeanza vita hivi, sisi tusingepigana na ninyi.” Baada ya kuyasema haya akarudi kwenye nafasi yake.” Inasimuliwa vile vile kuhusiana na vita vya Ngamia kwamba, wakati maadui walipojikusanya kwa ajili ya mashambulizi, Ali pia aliliweka jeshi lake tayari kwa vita, lakini akawaambia: “Msirushe mshale wala kufanya shambulizi kwa mkuki au upanga mpaka kwanza tutakapowaalika kwenye amani.” Yeye hakupenda kwamba vita vitokee na kuishia kwenye umwagaji damu na kupoteza maisha. Baada ya muda, mtu mmoja anayetokana na jeshi la upande wa upinzani alirusha mshale ambao ulimpiga sahaba wa Ali na ukamuua. Ali akasema: “Ewe Mola wangu! Shuhudia hili.” Halafu mshale mwingine ukaja na kuua mtu mwingine. Yeye akasema tena: “Ewe Mola! Shuhudia.” Halafu mshale ukampiga Abdullah ibn Badil na ndugu yake akamleta mbele ya Ali. Ali akasema tena: “Ewe Mola! Shuhudia.” Na kisha hapo vita vikaanza. Kuepukana na ukatili na udhalimu ilikuwa ni kanuni ya maadili ya Ali, na ilijenga sehemu ya tabia na silika yake. Kamwe yeye hakuwa akivunja mapatano, na hakuwa na uadui na marafiki zake wa awali, isipokuwa wao wenyewe ndio walivunja mapatano na kuonyesha uadui kulipiza na upole wake. Muundo bora wa urafiki na maana ya usahihi ni kwamba mpiganaji, wakati anaposimama katika uwanja wa vita anapaswa kuangalia marafiki zake wa zamani, ambao wanaweza kuwa wamekuja kupigana katika nafasi ya maadui, kwa jicho lile lile la kidugu, apaswe kuwaalika kwenye amani na kuwakumbusha mapenzi yao ya awali na urafiki, ili kwamba pengine waweze kujiepusha na kuvunja mkataba wa makubaliano na usaliti, au achukue zile silaha kutoka mikononi mwao na kutatua yale matatizo magumu kwa majadiliano na mazungumzo ya amani.

44

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 44

9/4/2017 3:47:46 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Kupigana na mtu aliyekuwa rafiki mwanzoni kusipashwe kuanza haraka, kwa sababu inawezekana kwamba akakumbushwa juu ya uhusiano wa awali, na anaweza akajizuia kutokana na kupigana na upinzani. Kama kushika ahadi na kuheshimu urafiki wa awali kusingetawala moyo wa Ali, asingeweza kuvitegemea hivyo kwa ajili ya kuwafukuzilia mbali maadui. Umadhubuti wa Imam katika kuchunga ahadi unadhihirika kwenye tabia ya heshima aliomfanyia Zubayr ibn Awam na Talha ibn Ubaidullah. Watu hawa wawili waliwatenganisha Imam na marafiki na wasaidizi wake, na wakawachukua upande wa maadui zake. Wao vile vile, walimpotosha Aisha na kumfanya atoke kama mpinzani wa Ali. Wale waliokuwepo hapo; kama walikuwa marafiki au maadui, wamesimulia kwamba pale Talha na Zubayr walipoamua kupigana dhidi ya Ali, wakavunja kiapo cha utii na kuonyesha dhamiri zao mbaya katika vita vya Ngamia, Ali aliwaendea akiwa mikono mitupu na bila ya kuvaa vazi lolote la chuma kujihami nalo au deraya, hapo akimaanisha kwamba alikuwa amekuja kwa makusudi ya amani. Halafu yeye akamwita Zubayr akisema: “Ewe Zubayr! Hebu njoo hapa kwangu.” Zubayr alitoka akiwa amejiandaa kikamilifu na silaha. Wakati Aisha aliposikia kuhusu hilo alipiga yowe: “Ni aibu gani hii kwamba patokee mapigano!” Yeye Aisha alisema hivyo kwa sababu alijua kwamba yeyote aliyekwenda kupigana dhidi ya Ali lazima atauawa, hata angekuwa jasiri na mwenye nguvu kiasi gani. Na inaweza kusemwa kwa uhakika kwamba, Zubayr asingeweza kujiokoa mwenyewe kama angepigana na Ali. Hata hivyo Ali alimkumbatia Zubayr. Aisha na waunga mkono wake walifadhaika sana kuona hivi. Ali akasema katika sauti ya upendo kabisa: “Ewe Zubayr! Kwa nini wewe umekuja kupigana dhidi yangu?” Zubayr akajibu akasema: “Kulipiza kisasi cha kifo cha Uthman.” Ali akasema: “Mwenyezi Mungu amuuwe yule mtu anayehusika juu ya kifo cha Uthman.” Halafu Ali akamkumbusha Zubayr juu ya usuhuba uliopita na undugu wao, na akalia kwa mara kadhaa wakati alipokuwa akizungumza. Hata hivyo, Zubayr alikuwa amedhamiria kupigana na akampinga Imam mpaka yeye akauawa. Ali ambaye aliweka umuhimu mkubwa kwenye kiungo cha urafiki, alihuzunika sana pale Zubayr alipokutana na kifo chake. Ali hakuzuia mapendekezo yake kwa Makhalifa waliomtangulia, na aliwasaidia wao katika maneno na vitendo vyao.9 Ingawaje mtu huyu muungwana alikuwa imara katika urafiki wake, hao marafiki zake hawakumpatia ile heshima inayostahiki kwenye urafiki wake, kwa sababu ha9 li aliwasaidia Makhalifa hao kwa sababu kila kitendo chake yeye kilikuwa ni kwa ajili ya manufaa ya Uislamu A na hakuyaacha maslahi ya dini kuvurugwa ili aweze yeye kupata haki yake binafsi. 45

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 45

9/4/2017 3:47:46 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

wakuwa wakitegemea kwamba angeweza kutenda kinyume na tabia yake asili na kuiachia huru mikono yao kupora haki za wengine. Imam Ali amesimuliwa kuwahi kusema kwamba: “Hata kama maeneo yote saba ya dunia na kila kilicho chini ya mbingu vingetolewa kupewa mimi ili nimuasi Mwenyezi Mungu na kunyang’anya kidhalimu ganda la shairi kutoka kwa mdudu chungu, mimi sitafanya hivyo. Mbele ya macho yangu mimi hii dunia yote ni duni kuliko jani ambalo linaweza likaminywa kwenye kinywa cha nzige.” Katika suala hili maneno na vitendo vya Ali vilipatana vyote. Hakuwa kama wengine ambao hujiingiza katika maneno ya kujivuna, ambayo vitendo vyao vinayaonyesha yasivyokuwa ya kweli. Yeye alichochewa kuyasema maneno haya na ile tabia yake ambayo iliunda msingi wa mwenendo wake. Ali alikuwa mpole zaidi kwa watu kuliko mtu mwingine yeyote yule, na alijiepusha na kumdhuru mtu yoyote. Alikuwa asiyetambua nafsi yake mwenyewe ili aweze kuwasaidia wengine, na alichukulia huku kujikana mwenyewe kama sehemu muhimu sana ya maisha yake. Uhai wake wote ulitolewa kwenye msaada wa wale wanaokandamizwa na wasio na uwezo kiasi kwamba aweze kuwapatia haki zao kutoka kwa madhalimu ambao walijiona wao wenyewe kuwa na haki ya kupora haki za wengine, kwa sababu ya ubora wa kizazi chao na ubaguzi wa rangi na kikabila. Ali aliwapinga Maquraishi na akapigana nao, kwa sababu waliutaka sana ukhalifa kwa ajili ya manufaa binafsi na ili kupata hadhi, utajiri na utawala. Aliukana ukhalifa na hata maisha ya kidunia, na akatelekeza kila kitu kwa sababu hakuweza kufanya kama watu wa kidunia, na hakuweza kukubali kuwaruhusu kuwanyonya wale wanyonge na wasiojiweza. Ali alikuwa na huruma sana kwa watu wa chini kiasi kwamba, wakati ndugu yake Aqiil alipomuomba ampatie kitu kutoka kwenye hazina ya umma, cha zaidi ya fungu lake halali, yeye alimkatalia ombi lake na kama matokeo ya hilo, Aqiil akaenda zake kwa Mu’awiyah. Ali alivumilia utengano na ndugu yake huyo, lakini hakukubali kumpa kitu chochote kutoka kwenye hazina ya umma wa Waislamu bila ya kustahiki. Ali alikuwa kama baba mwenye huruma kwa wanadamu wote. Alitoa maagizo kwa maafisa wake na magavana wake kuwatendea watu kwa upole. Alikuwa mkali kwa wale ambao waliwaonea na kuwakandamiza watu, na akawatahadharisha na kuwaonya juu ya matokeo mabaya. Maagizo yafuatayo ambayo 46

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 46

9/4/2017 3:47:46 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

aliyatoa yeye, yaliyafikia masikio ya magavana wake kwa mfululizo: “Rekebisheni manung’uniko ya watu na muwatimizie haja zao kwa sababa mnapata msingi wenu kutoka kwao. Msimnyime mtu yoyote kile anachohitaji, na msimzuie kutimiza lengo lake. Msiuze vazi la kiangazi au la majira ya baridi la mtu yoyote ili kujipatia mapato. Msichukue kutoka kwa mtu yoyote mnyama wa miguu mine ambaye anahitajiwa na yeye mwenyewe kwa shughuli zake, na msimchape mtu viboko kwa ajili ya angalau peni moja. Ali alikuwa ndiye mtu aliyeandika wasia bora kabisa kwa ajili ya Malik Ashtar Nakha’I, wakati alipomchagua kuwa gavana wa Misri na maeneo yanayopakana nayo. Yeye aliandika hivi: “Usiishi na watu kama wanyama wakali, na usiifanye riziki yao kuwa ni ngawira ya vita, kwa sababu watu wa Misri wanaangukia kwenye moja ya hali mbili: imma wao ni ndugu zako katika imani kwa mtazamo wa dini au ni sawa na wewe kwa sababu ya kuwa kwao binadamu kama wewe. Yapuuze mapungufu yao na usamehe makosa yao, kama vile unavyotegemea Mwenyezi Mungu atakusamehe makosa na dhambi zako. Usijutie kumsamehe kwako mtu na usisisitize juu ya kutoa adhabu.” Aliongezea: “Kataza na kuzuia kuhodhi mali.” Ali alikataza vikali sana kuhodhi mali, ambako kulikuwa ndio sababu kubwa ya Mu’awiyah na kundi lake kumpinga yeye, kwa sababu wao walitaka hiyo nchi, utajiri na ngawira za kivita ziwe ni kwa ajili yao ambapo, Ali alizitaka kwa ajili ya wanadamu wote. Ali alikuwa na huruma kwa wanadamu kiasi kwamba, kama tutakavyoeleza kwa kinaganaga baadaye, aliagizia muuaji wake, yule muovu Ibn Muljam ashughulikiwe kwa upole. Katika mapendekezo aliyoyatoa yeye kwa wanawe Hasan na Husein yeye alisema: “Kuweni maadui wa madhalimu na wasaidizi wa wale wanaodhulumiwa.” Vile vile alisema: “Kuwa adui wa dhalimu hata kama atakuwa ni ndugu yako wa karibu na msaidie yule mtu aliyekandamizwa hata kama atakuwa hana uhusiano wa kidugu na wewe na akaweza kuwa ni mgeni.” Yeye siku zote alijitahidi kuwaadhibu wakandamizaji na kuwaondolea watu ule uovu wao. Ili kufanikisha lengo hili, yeye alitumia moyo wake, ulimi, upanga na damu. Wakati wote alibakia kuwa msaidizi wa wanaokandamizwa na adui wa madhalimu. Hakusita kuifuata njia hii hadi mwisho wa maisha yake. Mtu asije akashangaa kwamba Ali alikuwa mtu muadilifu. Lingekuwa ni jambo la kushangaza kama angekuwa sio muadilifu. Mifano ya uadilifu wake ambayo imek47

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 47

9/4/2017 3:47:46 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

wishasimuliwa ni vipaji vya thamani sana katika historia na anapaswa kuionea fahari mifano hiyo. Ndugu yake Aqiil alimuomba yeye ampatie pensheni maalum kutoka kwenye hazina ya umma, lakini yeye alikataa kuridhia maombi yake akisema: “Hii sio mali yangu binafsi kwamba ninaweza kumpa yeyote nimtakaye. Wapo watu wengine vile vile wasiojiweza na watu wenye shida, ambao wanastahiki zaidi kuliko ulivyo wewe, na ni lazima niwazingatie hao.” Aqiil akasema: “Kama hutanipatia penshini kutoka kwenye mali hii basi mimi nitakwenda kwa Mu’awiyah.” Hata hivyo, Ali hakujali kile alichokisema yeye, na wala hakubadili uamuzi wake. Ndugu yake akaondoka zake na akajiunga na Mu’awiyah na alikuwa akitumia kusema: “Mu’awiyah ni mbora kwa ajili ya dunia yangu.” Ushughulikaji wa Mu’awiyah ulimridhisha kwa sababu hiyo hazina ya umma ilikuwa ni zana mikononi mwake, ambayo yeye aliimarishia ufalme wake, akafanikisha malengo yake na alitaka kufufua zile siasa zilizopita na umaarufu wa Bani Umayyah. Imam hakudai upendeleo wowote kulinganisha na raia wake na alionekana kwenye mabaraza kama mtu sawa na wao. Hii ilikuwa hivyo kwa sababu ule moyo wa uadilifu ulikuwa umepenya ndani ya kina cha nafsi yake. Wakati mmoja Ali aliona vazi lake la pete za chuma – deraya – kwenye miliki ya Mkristo. Alimpeleka kwenye mahakama ya kadhi aliyekuwa akiitwa Shurayh ili aweze kutoa uamuzi kuhusiana na umiliki wake. Pale wote walipofika mbele ya kadhi, Ali akasema: “Vazi hili la deraya ni langu. Sijaliuza wala kumzawadia mtu yeyote yule.” Kadhi akamuuliza yule mtu mwingine: “Una nini cha kusema kuhusu madai haya yaliyotolewa na Amirul-Mu’minin?” Yule Mkristo akasema: “Vazi hili la chuma ni langu. Pamoja na hayo hata hivyo, mimi simchukulii Amirul-Mu’minin kwamba ni mwongo.” Kisha kadhi Shurayh akamgeukia Ali na akasema: “Unaweza ukaleta shahidi anayeweza akathibitisha kwamba vazi hili la deraya ni lako?” Ali akatabasamu na kusema: “Shurayh yuko sahihi. Mimi siwezi nikatoa shahidi kama huyo.” Kadhi huyo akatoa hukmu kumpendelea yule Mkristo ambaye alichukua vazi hilo la chuma na akaondoka. Amirul-Mu’minin alibakia kumwangalia kwa nyuma. Baada ya kuwa amekwenda hatua chache, hata hivyo yeye akarudi na kusema: “Mimi ninashuhudia kwamba utaratibu huu unafanana na utaratibu wa manabii, kwa sababu mtu ambaye ni Kion48

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 48

9/4/2017 3:47:46 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

gozi wa Waumini ametokeza pamoja na mtu kama mimi mwenyewe katika mahakama ya kadhi ambaye pia yuko chini yake, na kadhi huyo ametoa hukumu dhidi yake kiongozi huyo.”10 Halafu yeye akaongezea: “Ewe Amirul-Mu’minin! Ninaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kwamba vazi hili la chuma ni lako na kwamba madai yangu ni ya uwongo.” Baadaye watu walikuja kumuona yule Mkristo akitumikia kwenye jeshi la Ali kama mpiganaji mwaminifu, na alipigana kwa shauku kubwa dhidi ya Khawarij, katika vita vya Nahrawan. Ibn Abi Rafi’i amesimulia hivi: “Mimi nilikuwa ndiye msimamizi wa hazina ya umma katika kipindi cha ukhalifa wa Ali na pia nilikuwa mwandishi wake. Mali iliyopokelewa kutoka Basra kwa ajili ya hazina ya umma ilikuwa pamoja na mkufu wa lulu. Binti yake Ali alituma ujumbe kwangu akisema: ‘Ninaelewa kwamba kuna mkufu wa lulu katika hazina ya umma ambayo inadhibitiwa na wewe. Nitumie huo mkufu kwa kuuazima ili niweze kuuvaa katika siku ya Idd-ul-Udh’ha. Baada ya hapo nitaurudisha.’ “Mimi niliutuma mkufu huo kwake kwa masharti kwamba yeye atakuja kuwajibika endapo utapotea au kuharibika, na kwamba yeye aurudishe ndani ya siku tatu. Yeye alikubali masharti haya.” “Kwa bahati macho ya Amirul-Mu’minin yaliangukia kwenye mkufu huo na akautambua. Akamuuliza binti yake kama ni wapi alikoupata mkufu huo. Binti yake akajibu: ‘Nimeuchukua kwa kuuazima kutoka kwa Ibn Abi Rafi’i, yule msimamizi wa hazina ya umma, ili niuvae kwenye sikukuu ya Idd-al-Udh’ha na nimeahidi kuurudisha kwake ndani ya siku tatu.’ “Amirul-Mu’minin aliniita na akasema: “Je, unaona kwamba ni halali kitendo cha kuvunja ahadi ya dhamana na Waislamu?” Mimi nikajibu: “Mwenyezi Mungu aepushilie mbali kwamba mimi niweze kufanya udanganyifu kwa Waislamu.” Papo hapo yeye akasema: “Basi kwa nini uliuazima mkufu kadha wa kadha kwa binti yangu bila ya kupata ruhusa yangu na bila ya makubaliano ya Waislamu?” “Nilijibu nikasema: Ewe Amirul-Mu’minin! Yeye ni binti yako. Yeye aliuazima ili kujipamba na alihakikisha kuurudisha kwa salama ili niweze kuurudisha maha10

atika zile nchi huru za dunia ya sasa mahakama na mahakimu wamefanywa wa kudumu na hakuna anaK yeweza kuwaondoa kwenye ofisi zao. Hili limefanywa ili waweze kufanya maamuzi bila ya hofu yoyote au upendeleo, na waweze kutoa hukumu dhidi ya watu maarufu au hata wajumbe wa serikali. 49

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 49

9/4/2017 3:47:46 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

li pake panapostahili.” Ali akasema: ‘Uchukue uurudishe leo hii na usije ukafanya hivyo tena baadaye, vinginevyo nitakuja kukuadhibu.’ “Pale binti yake Ali alipokuja kufahamu juu ya hilo, alimwambia baba yake: ‘Ewe baba! Mimi ni binti yako kipenzi. Ni nani mwingine anayestahili kuvaa mkufu huu?’ Ali akajibu: “Oh, binti ya Abu Talib! Usikengeuke kutoka kwenye njia iliyonyooka. Je, unaweza kuniambia ni wanawake wangapi wa Muhajir na Ansari wanaojipamba wenyewe na mkufu kama huo?” Hatimae niliuchukua ule mkufu kutoka kwa binti ya AmirulMu’minin na nikaurudisha mahali pake panapostahili.” Ali aliuchunga uadilifu hata katika mambo madogo na yasiyokuwa na muhimu. Kama ilikuwa ni lazima kwake yeye kugawana kitu na watu wengine, alitoa haki ya kuchagua kwa yule mwingine ili watu wasije wakafikiri kwamba kulikuwa kunafanyika ubaguzi katika suala la kugawana kati ya watu wenye mamlaka na wale watu wa chini yao. Siku moja alikwenda kwenye duka la muuza nguo aliyekuwa akiitwa Abu al-Nawar akifuatana na mtumwa wake na akanunua mashati mawili. Kisha akamwambia mtumwa wake achague moja kati ya mawili hayo. Yule mtumwa aliokota moja na Ali akabaki na lile jingine.11 Maagizo yote na barua ambazo alizituma kwa magavana wake na watumishi wengine zinazunguuka katika egemeo la uadilifu. Watu wa karibu wa Ali na wengineo pia waliungana katika kumpinga yeye. Ilikuwa ni kwa sababu ya ukweli kwamba yeye hakuwapa upendeleo katika mtazamo wa usawa na haki, na hakutoa tahafifu yoyote kwa ndugu zake. Yeye hakushawishiwa na mtu yeyote na aliyakubali yale mambo ya sawasawa tu kutoka kwa wengine. Wakati Uthman bin Affan alipokuja kuwa khalifa, alitoa uhuru kamili kwa ndugu zake, marafiki na washirika wake kulimbikiza mali, na aliwafuata wale waliompa ushauri potovu. Marwan alikuwa na ushawishi mkubwa sana juu yake. Hakunufaika kutokana na mapendekezo ya busara ambayo Abu Bakr aliyafanya kwa Umar. Abu Bakr alikuwa amesema: “Msiwe karibu na wale watu ambao wana shauku ya kujaza matumbo yao na kujipatia vyeo na utajiri. Msivutiwe na ule ukweli kwamba 11

atukio kama hayo yanaonyesha kwamba viongozi wa dini hii walikuwa wakijali sana haki za watu wa M chini yao. Wale wanaojionyesha katika kuwasaidia watu wasio na uwezo, na wakaishutumu dini kwamba ni kikwazo katika suala la watu wanyonge kupata haki zao, hawajafanya vyakutosha kwa wa chini yao kama alivyofanya Imam Ali. 50

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 50

9/4/2017 3:47:46 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

walikuwa wameshirikiana na Mtume na kumtumikia yeye. Ichambueni asili ya kila mtu na muone ni mtu wa namna gani.” Ali aliwachukia watu walafi kama hao. Hivyo wakati alipokuwa khalifa aliamua kushughulika nao kwa uadilifu. Yeye, kwa hiyo, aliwafukuza baadhi yao na alikomesha ulafi wa wengine juu ya vyeo, hadhi na utajiri. Kulikuwa na kikundi cha watu ambao walitaka kuzipa kanuni za Uislamu muundo mpya, na kuzifanya ni njia ya kujipatia vyeo na utajiri, na kuzifanya zile nchi za Kiislamu mali ya urithi ya ukoo wao. Ali alipigana dhidi yao na akawaambia kwa sauti kubwa: “Ninakijua kinachoweza kuwawekeni mbali na uasi na fitna, lakini kile kitu ambacho ni chanzo cha furaha kwenu ninyi ni njia ya maovu kwangu mimi.” Hatua ambayo kushughulika kwa Ali nao kama hao inajulikana vizuri. Pale wakandamizaji hao waliposhindwa walikimbilia kwenye ulaghai na ule moyo wa uadilifu ulifanikiwa katika nyoyo za Ali na wafuasi wake, ingawa ni dhahiri kwamba wao walikuwa ndio watesekaji. Wakati Ali alipopata shahada yake mikononi mwa Ibn Muljam, mwanamke wa kabila la Nakh’ii aliyekuwa akiitwa Ummul Haisham aliandika shairi la maombolezo kwa ajili yake. Ubeti wa shairi hilo unaonyesha yale maoni ya watu kuhusu mwenendo na uadilifu wake: “Alisimamisha kweli na hakukaribisha shaka yoyote kuhusu hilo. Alikuwa na tabia ya uadilifu mkubwa kwa jamaa zake na kwa wageni vile vile.” Uaminifu na uhodari ni sifa za watu mashuhuri, na zilikuwa zimemilikiwa na Ali kwa ubora wa kiwango cha hali ya juu kabisa. Uaminifu, ukweli, ujasiri na ukakamavu na sifa nyingine zote kama hizo zimeingiliana. Hivyo yeye hakuonyesha kitu chochote ambacho kilipingana na nia na dhamira yake halisi. Yeye hakufanya udanganyifu, ingawa alijua kwamba kwa kufanya hivyo angeweza kuziondosha balaa za maadui zake. Kile kilichosemwa hapo juu kuhusu ukweli na tabia ya Imam kinathibitisha kabisa uaminifu na uhodari wake. Moja ya kanuni zake na maadili ilijumuisha urahisi katika kila kitu. Alichukia urasimu vibaya sana na alitumia kusema: “Ndugu mbaya kabisa ni yule ambaye kwa ajili yake, mtu anapaswa kujiingiza kwenye matatizo.” Alikuwa pia akisema: “Endapo muumini atafanya urasimu kwa ndugu yake ina maana kwamba yeye amejitenga mwenyewe na yeye. Kama alisimulia wazo au kutoa ushauri au katoa zawadi fulani, basi kitendo chake hiki hakikuchafuliwa na ufahari. Desturi hii ilikuwa imetopea sana katika tabia yake kiasi kwamba watu walafi hawakuweza kumfanya afuate matakwa yao, na wala wale wenye kujipendekeza wa51

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 51

9/4/2017 3:47:46 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

sitegemee kuiteka akili na mazingatio yake. Watu hawa walikuwa wakisema kwamba Imam alikuwa na moyo mgumu, mwenye hasira na kiburi. Hata hivyo, Imam hakuwa na moyo mgumu wala mwenye hasira wala kiburi. Kinyume chake, kama ilivyotakiwa na tabia yake, alisema kila kile alichokuwa anapaswa kukisema bila ya urasimu au udanganyifu wowote ule. Idadi kubwa ya watu ambao walikuwa wamekusanyika karibu yake walitamani manufaa binafsi. Ali alitia shaka juu yao na hakuficha wasiwasi wake. Maelezo ya maoni yake kuhusu watu hao hayawezi kuitwa kiburi au ufidhuli. Ali alichukia ufidhuli na alikuwa huru kabisa kutokana na ubinafsi. Yeye aliwakataza wanawe, masahaba na watumishi wake kuonyesha kiburi na kufanya ubinafsi. Alipokuwa akiwapa ushauri alikuwa akisema: “Epukeni ubinafsi. Mnapaswa kutambua kwamba ubinafsi ni sifa mbaya na msiba mkubwa kwenye akili.” Alichukia urasimu. Yeye aliwazuia watu pia kwenda mbali sana wakati walipokuwa wakimsifia na akawaambia: “Mimi ni duni kuliko ninyi mnavyosema.” Wakati mwingine ilitokea kwamba alimchukulia mtu aliyehusika (na kumsifia kupindukia) kuwa kama adui yake. Katika tukio kama hilo yeye hakujizuia kuielezea hali ya akili ya mtu huyo ambayo yeye aliitambua na akamwambia: “Mimi ni bora zaidi ya vile unavyoamini kuhusu mimi ndani ya moyo wako.” Ali alichukia baadhi ya marafiki zake kumtukuza sana, kwa namna ile ile, kama alivyochukia kule kudhalilishwa kwake na maadui zake. Alisema: “Watu wa aina mbili wameangamizwa kwa sababu ya mwelekeo wao kwangu mimi. Wale marafiki ambao wametia chumvi katika sifa zangu, na maadui zangu wenye inda.” Yeye hakuonyesha majivuno wala kujidhalilisha mwenyewe bila ya sababu ya msingi. Alijiwakilisha mwenyewe kama vile alivyokuwa hasa. Alikuwa hana tabia ya kujifanya wala unafiki. Ni vigumu kumpata mtu mnyofu, muwazi kama yeye. Alinunua mfuko mzima wa tende na alikuwa amezibeba kuelekea nyumbani. Watu kadhaa waliliona hili na wakajitolea kumbebea mfuko huo. Yeye, hata hivyo, aliwaambia kwa ukweli kabisa kwamba mkuu wa familia alikuwa na wajibu wa kuubeba mfuko huo. Inasemekana kimakosa kwamba unyenyekevu wa bandia na upole vinatengeneza sifa njema. Kwa kweli ni udanganyifu na kujifanya kutupu ambako mtu anakoweza kuonyesha ili kujifanya dhalili kuliko vile mtu huyo alivyo hasa. Ali hakuwa mnyonge kwa maana hiyo na alikuwa pia hana majivuno. Alijidhihirisha kama vile alivyokuwa hasa bila ya unyonge wala majivuno, kwa sababu mambo mawili haya sio miongoni mwa sifa za watu wakakamavu. 52

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 52

9/4/2017 3:47:46 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Yule mwandishi wa “Abqari’atul-Imam” anasema: “Ali aliingia kwenye medani ya vita akiwa mikono mitupu kwenda kupigana na maadui ambapo wao walikuwa wamejifunika barabara kwa chuma cha pua na chuma cha kawaida. Inawezekana vipi kusemwa kwamba kitendo chake hiki kilikuwa kimeegemea kwenye unafiki?” Sifa nyingine ya Ali ilikuwa ni ule moyo wake wa kiungwana. Yeye hakuwa akiweka kinyongo moyoni mwake dhidi ya mtu yeyote yule, ingawaje anaweza kuwa ni adui yake wa jadi. Kama tulivyokwishaeleza, aliwaelekeza watoto wake na marafiki zake wasimuue muuaji wake (Ibn Muljam). Ingawaje Talha alikuwa amekuja kama adui ili kumuua, yeye aliililia maiti yake na akasoma shairi la dhati ya moyo kwa ajili yake. Ingawa Khawariji walikuwa ni maadui zake wabaya kabisa na walikwishapigana dhidi yake, na muuaji wake pia alikuwa ni mmojawao, na kwa hakika hawakumletea matatizo madogo ikilinganishwa wao na Mu’awiyah na Amr bin Aas, lakini aliwashauri marafiki na wafuasi wake wasipigane dhidi yao. Alitoa maelekezo haya kwa sababu alijua kwamba watu wale walikuwa mawindo ya kutokuelewa, na walikuwa wamepotoka. Walikuwa wanaoitafuta kweli lakini walikuwa wamekosea katika suala la uchambuzi wao, kinyume na Mu’awiyah na wafuasi wake, ambao walikuwa watafutaji wa batili na wakafanikiwa katika kuipata. Hakuna kinachoweza kuonekana katika wasifu wa Ali ambacho kinaweza kuonyesha kwamba alikuwa aliyejawa na kisasi. Katika mazingira yote yeye aliuonyesha ukweli, uaminifu, unyofu na ushika-upanga mahiri. Watu waungwana sio wenye kisasi, na pia huwa hawavumilii udhalimu na ukandamizaji. Wanachukizwa na mtu ambaye anawaonea watu wengine. Ingawaje Ali hakuwa akiweka kinyongo moyoni mwake dhidi ya mtu yeyote, ilimbidi yeye kukabiliana na kundi lenye chuki. Maneno yake yenye maana kabisa yanaonyesha ni jinsi gani alivyokuwa amehuzunika. Huzuni yake ilikuwa ya namna kwamba ilichipukia kutokana na huruma na upole. Alihuzunika kuona kwamba watu walijidhuru wenyewe. Sifa nyingine ambayo ilimtofautisha na wengine na ambayo ilikuwa kikamilisho cha sifa zake nyinginezo, ilikuwa ni imani kamilifu katika vitendo na itikadi zake, na kila alipofanya jambo lolote lile, aliamini katika usahihi wake na kuwa kwake kwenye njia iliyonyooka. Pale alipoamua kupigana na Amr ibn Abdulwuud, yule shujaa maarufu wa Arabia, yeye alitahadharishwa na Mtume pamoja na masahaba zake kuhusu matokeo yake. Yeye hata hivyo, aliamua kupigana kwa sababu licha ya kuwa jasiri, alikuwa vile vile na shauku ya kuusaidia Uislamu.

53

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 53

9/4/2017 3:47:46 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Tunarudia kusema kwamba, wakati maadui walipokuwa wamemzunguka Ali kutoka pande zote, yeye alijishughulisha na kuswali bila ya kuwa na mlinzi wa kumlinda yeye kutokana na mabalaa ya maadui hao, na matokeo yake Ibn Muljam akafanikiwa katika kumjeruhi kwa upanga wake wenye sumu. Jambo hili hasa, lenyewe ni ushahidi mkubwa wa kutosha wa ukweli kwamba alikuwa na uhakika wa usahihi wa kile alichokifanya, kwa sababu mtu muadilifu huwa hahofii kitu chochote. Maneno yote na vitendo vya Ali vinakuja kuthibitisha kwamba alikuwa na imani kamilifu na madhubuti katika matendo yake. Hii ilikuwa hivyo kwa sababu matendo yake yote yalianzia kwenye hekima na uwezo.12 Wakati watu walipogawanyika katika makundi mawili kwenye mwelekeo wao juu yake (yaani, marafiki na maadui), yeye hakuwa na woga juu ya hao maadui, na hakuweka silaha chini mbele yao, kwa sababu alikuwa na imani kamilifu katika ukweli wake mwenyewe, na uadilifu na usahihi wa matendo yake. Ilikuwa ni katika muktadha huu kwamba yeye alisema: “Hata kama nitaipiga pua ya muumini ili aweze kuwa adui yangu, yeye huyo hatakuwa adui yangu, na hata kama nitazimimina neema zote za dunia hii juu ya adui yangu ili aweze kuwa na urafiki juu yangu, huyo hatakuwa rafiki yangu.” Juu ya hili yeye pia alisema: “Mimi siogopi kupigana dhidi ya watu hawa peke yangu hata kama ulimwengu wote utajiunga na jeshi lao.” Pale alipokuja kugundua kwamba kikundi cha watu wa Madina kilikuwa kimejiunga na Mu’awiyah, yeye akamwandikia Sehl ibn Hanif, gavana wa Madina: “Ninatambua kwamba kikundi cha wakazi wa jiji lako kimejiunga kwa siri na Mu’awiyah. Hata hivyo, wewe usije ukawa na wasi wasi kwa sababu hii kwamba baadhi ya watu watakuacha na hawatakusaidia wewe. Ninaapa kwa jina la Allah kwamba watu hawa hawakuacha udhalimu na ukandamizaji na hawakushikilia usawa na uadilifu.” Elimu Na Hekima Za Ali Ali hakuwa na kifani kwa kiasi uwezo wa utambuzi unavyohusika. Usomi wa Kiislamu unazunguka juu ya kiini cha akili yake. Yeye alikuwa ndio chemchemi ya elimu. Hakuna tawi la ujuzi katika Arabia ambalo halikuasisiwa na yeye, au katika msingi ambao yeye hakuwa ndiye mhusika mkuu. Tutaandika kwa kina baadaye kuhusu umahiri wake mkubwa katika elimu za kijamii, kwa sababu somo hili linastahili kujadiliwa tofauti peke yake. Katika sura hii ninapendekeza kushughulika kifupi tu na elimu yake ya Shari’ah, falsafa ya uwanachuoni na fasihi ya Kiarabu, na vile vile 12

ababu yake ilikuwa kwamba Ali alikuwa ma’sum na alisema na kufanya kila kitu kwa mujibu wa msukumo S na mienendo ya Mtume wa Uislamu. Hivyo, yeye hakutilia shaka yoyote kuhusu maoni yake na matendo. 54

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 54

9/4/2017 3:47:46 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

upevu wa akili ya kihakimu. Nitachukua kifupi kwa sababu watu wengine wengi wameandika juu ya somo hili, na baadhi yao wamefanya utafiti wa kina. Mimi kwa hiyo, nitaelezea kwa ufupi yale mambo ambayo wameshughulika nayo kwa kina, na nitaelezea kwa kirefu yale mambo ambayo wao wameshughulika nayo kwa kifupi tu. Ninaanza na Qur’ani Tukufu na Hadith (Sunnah), na nitaandika kuhusu elimu zingine baadae ili kwamba iweze kujulikana ni kwa kiasi gani maneno haya yafuatayo, ya Mtukufu Mtume yalivyothubutu kuwa ya kweli kabisa kuhusu Ali: “Mimi ni jiji la elimu na huyu Ali ndio lango lake.” Ali alilelewa na binamu yake. Alikuwa mfuasi wake na alizitwaa tabia zake na mwenendo. Urithi wa Mtume ukawa umepandikizwa ndani ya moyo na ubongo wake. Alitafakari juu ya Qur’ani kwa akili na jicho la mwenye hekima, na akajifunza ukweli wake uliofichika. Mazingira yalimpatia wakati mzuri wa kutafakari juu ya Qur’ani. Alimuradi Abu Bakr, Umar na Uthman walijishughulisha na ukhalifa, yeye aliweka mazingatio yake yakiwa yameelekea kwenye Qur’ani Tukufu. Aliyamudu maneno yake na maana zake. Ulimi wake uliweza kusoma kwa ufasaha na moyo wake ulizama ndani yake. Ujuzi wake wa hadith za Mtume ulikuwa kiasi kwamba hakuna yeyote mwingine aliyeweza kushindana naye katika hilo. Na hakuna kitu cha kustaajabisha kuhusu hilo, kwa sababu alikuwa wakati wote akishirikiana na Mtume na alinufaika kutoka kwake zaidi kuliko sahaba au mujahid yoyote alivyokuwa. Kila chochote kile kilichosikiwa na wengine, yeye alikisikia pia,+ na kila alichokisikia yeye sio lazima kwamba kilisikiwa na wengine. Ni ukweli unaojulikana sana kwamba Ali hakusimulia hadithi kutoka kwa yeyote isipokuwa kutoka kwa Mtume tu. Hii ilikuwa hivyo kwa sababu alikuwa na uhakika kwamba hakuna hata neno moja la ndani ya hadithi za Mtume ambalo lilifichika masikioni mwake na moyoni mwake. Aliwahi kuulizwa: “Imekuwaje kwamba wewe umewazidi masahaba wote wengine katika suala la elimu na Hadith?” Yeye alijibu: “Imekuwa hivyo kwa sababu Mtume aliniambia kila kile ambacho nilikiuliza kutoka kwake, na kama nilikuwa sikuuliza kuhusu kitu chochote kile, Mtume mwenyewe alikifanya kijulikane kwangu.” Ali aliwapita wengine wote katika masuala ya Shariah (fiqh) na usomi wote wa Kiislamu kiasi kama vile alivyozitumia hizo kwa njia bora zaidi kuliko wengine. Wale ambao walikuwa wa wakati wake hawakuweza kupata faqihi mkubwa na kadhi 55

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 55

9/4/2017 3:47:46 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

mashuhuri kuliko yeye. Abu Bakr na Umar siku zote walimwendea yeye kwa ajili ya ufumbuzi wa mas’ala magumu. Hawa makhalifa wawili walinufaika sana kutokana na elimu na hekima zake. Masahaba wengine wa Mtume pia walimtaka ushauri juu ya ufumbuzi wa mas’ala yao magumu. Hakuna aliyeweza kutoa hoja bora zaidi kuliko yeye kuhusiana na masuala ya kisheria. Na kuhusiana na Shariah (fiqh), elimu ya Ali ilikuwa haikuishia kwenye maandiko na maagizo. Yeye alikuwa hodari zaidi kuliko wale wa wakati wake katika matawi mengine ya elimu pia, kwani elimu yao ilikuwa inalazimu kuwepo faqihi (kwa mfano hisabati). Abu Hanifa anaitwa ‘Imam Mkuu’ katika uwezo wa fiqh. Yeye alikuwa mwanafunzi wa Ali, kwa sababu yeye alijifunza elimu ya Shariah (fiqh) kutoka kwa Imam Ja’far as-Sadiq na nyororo ya walimu wake inapofuatiliwa kwa kwenda juu, iliishia kwa Ali. Kwa namna hiyo hiyo, Malik ibn Anas pia alikuwa mwanafunzi wa Ali kupitia walimu wachache hapo katikati. Malik alijifunza fiqh kutoka kwa Rabiya. Huyu alisoma kutoka kwa Akrama, ambaye alisoma kutoka kwa Abdullah, na Abdullah alisoma kutoka kwa Ali. Abdullah ibn Abbas ambaye alikuwa pia ni mwalimu wa wengine wote aliulizwa: “Ni uwiano gani wa elimu yako kwa ile ya binamu yako, yaani, Ali bin Abi Talib?” Yeye alijibu akasema: “Uwiano wenyewe ni kama ule uliopo kati ya tone na bahari.” Masahaba wamemnukuu Mtume kwa kauli moja akisema kwamba: “Hakimu bora miongoni mwenu ni Ali.” Ali aliwazidi watu wote wa wakati wake katika masuala ya sheria, kwa sababu yeye aliijua Qur’ani na amri na kanuni za kidini vizuri zaidi kuliko wengine wote, na katika Uislamu hukumu sahihi zinategemea katika mambo mawili haya. Alikuwa na kiasi cha elimu, hekima na uwezo wa kufikiri ambacho pale inapotokea mgogoro, yeye aliweza kutoa maamuzi yenye hekima kubwa kabisa. Dhamiri yake ilikuwa na nguvu sana kiasi kwamba alikuwa na uwezo wa uamuzi makini na adilifu kabisa, baada ya kuchunguza na kuvielewa vipengele mbali mbali vya jambo linalohusika. Umar ibn Khattab amesimuliwa kuwahi kusema: “Oh, Abul Hasan! Tatizo hilo nalisiwe na bahati (ya kujitokeza), ambalo kwa ufumbuzi juu yake wewe utakuwa hupatikani.”

56

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 56

9/4/2017 3:47:46 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Wakati alipokuwa akitoa hukumu yake, Ali alikuwa na mazingatio kwa mdai na kwa taifa na umma kwa jumla. Hii fikira yake ya ziada na mazingatio kwa upande wake vilikuwa vyenye kutegemeana. Alikuwa ndiye hakimu wa kwanza kuthibitisha haki za watu katika mtazamo wa kifalsafa, na akasema kwamba ni wajibu wa watawala kufanya mazingatio yanayostahili kwenye haki hizi. Aidha katika suala la mlalamikaji, ni lazima pia kuzingatia uadilifu katika suala la watu wote katika suala la usimamizi wa kawaida. Watu wako chini ya wajibu wa kufanya matendo fulani kwa ajili ya marekebisho ya jamii ambamo wao wanaishi. Kuna uhusiano wa pamoja kati ya binaadam, na sheria za taifa zimewaunganisha wote pamoja. Ni lazima kuziheshimu sheria hizi kwa ajili ya mabadiliko ya taifa, na sio kwa kujipatia mafanikio binafsi tu. Ali alisimamisha sheria na umoja wa kitaifa, na aliwachukulia watu binafsi wote kama mtu mmoja katika suala la haki na wajibu. Katika maagizo na hukumu zake, yeye aliitekeleza kikamilifu kanuni hii ambayo inafuatwa hasa hasa na wale watu wa nyakati hizi waliostaarabika. Usiku mmoja Ali alimsikia mtu anayeteseka akipiga kelele ya kutaka msaada. Alikimbilia kuelekea alikokuwa mtu huyo mara moja na akasema: “Muokoaji amekuja.” Aliona kwamba mtu mmoja alikuwa amemshika mwingine kwenye ukosi wake. Mtu huyo alipomuona Ali, akamuachia mpinzani wake. Kisha akasema kumwambia Ali: “Mimi niliuza kipande cha nguo kwa mtu huyu kwa thamani ya dirham tisa, na vile vile sikuvunja sharti lolote la majadiliano ya bei. Yeye alinipa sarafu duni; na pale nilipomuomba anipe sarafu nzuri badala yake, yeye alinitusi na kunipiga kibao.” Ali alimwambia yule mnunuzi achukue zile sarafu zake duni na kisha ampe muuzaji zilizo nzuri. Halafu akamuuliza yule mtu mwingine kama alikuwa na shahidi yeyote wa kuthibitisha kwamba yule mnunuzi alikuwa amempiga kibao. Alitoa ushahidi uliotakiwa. Papo hapo Ali akamwambia yule mnunuzi akae chini na kumwambia yule mtu mwingine kulipiza kisasi. Yeye hata hivyo, aliamua kumsamehe. Wakati Ali alipoona kwamba yule mdai ameitelekeza haki yake na amemsamehe yule mwenziwe, yeye hakumbana ili kulipiza kisasi. Yeye, hata hivyo aliweka jambo hili katika mazingatio kuhusiana na tukio hili kwamba ilikuwa ni lazima kuchunga haki za watu wa kawaida, na ilikuwa ni wajibu wake kumwadhimu yule mwonevu, ili kiungo cha uadilifu kiweze kubakia imara miongoni mwa watu, na haki za kitaifa zisije zikakiukwa. 57

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 57

9/4/2017 3:47:47 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Yeye vile vile alizingatia ule ukweli kwamba, katika kila jamii kuna watu wengi wenye nguvu na wakatili, ambao hupora mali na haki za wanyonge, na hao wanyonge hawawezi kuzirudisha au kuzidai hizo haki zao kwa sababu ya udhaifu au woga, ingawaje ingefaa tu kwamba haki zao zisiweze kuingiliwa. Yeye kwa hiyo, alijifikiria moyoni mwake: “Ni nani aliyepo hapa, mbali na mimi mwenyewe, ambaye angepaswa kuwasaidia na kuzidai haki zao, ili waweze kuishi maisha ya kijamii yenye amani, na waweze kuhakikishiwa kwamba hakuna tofauti kati ya watu mmoja mmoja kuhusiana na haki za kijamii, na kwamba haki zao ziko salama.?” Katika suala lililotajwa hapo juu, kwa hiyo, Ali alimwachia kuondoka, yule mtu ambaye alikuwa amepigwa, lakini akamkamata yule mshari mkononi mwake na akampiga mara tisa mbele ya yule mtu mwingine huku akisema: “Hii ndio haki ya mtawala.” Ali hakuridhika na muonekano wa jambo lolote kwa nje tu, na alikuwa akipenda sana kuzama kwa kina katika mambo. Alitafakari juu ya Qur’ani na dini kwa uhodari sana kwa namna ile ile ambayo wanafikra wengine wanavyotafakari juu ya mambo ya kidunia. Hapana shaka mtu mwenye uwezo wa ki-mbingu kama Ali huwa haridhiki binafsi na maagizo ya dhahiri ya dini, kule kutekeleza wajibu uliowekwa na taratibu za ibada. Zaidi hasa watu wanaiangalia dini kama ni amri zinazohusika kwenye amali na hukumu kwa namna ya upurukushani tu. Hata hivyo, Ali aliangalia katika maana na ukweli wao wa ndani kabisa pia. Aliyafanya mambo haya kama kiini cha tafakari na utafiti wake, na alithibitisha kwamba dini imesimama katika kanuni ambazo zimeunganishwa na kuhusiana na kila moja yao. Hili lilisababisha uanzishwaji wa elimu ya falsafa ya uwanachuoni na falsafa ya Kiislamu. Ali alikuwa ndiye Mwanachuoni wa falsafa wa kwanza (‘arif) na muasisi wa falsafa ya uwanachuoni. (kwa maelezo zaidi rejea: “On Ilmul Kalam wal Irfan. ISP 82). Wanachuoni wa falsafa wa kale walipata elimu ya kina kutoka kwenye chemchemi yake, kwa sababu walipata misingi na kanuni za uwanachuoni wa falsafa kutoka kwake. Wanachuoni wa baadaye pia wanamkiri kama kiongozi wao, kwa sababu wao pia walipata mwongozo kutoka kwake. Wasil ibn ‘Ata alikuwa kiongozi na mtu mashuhuri wa madhehebu ya Mu’tazila. Hii ilikuwa ndio madhehebu ya kwanza katika Uislamu ambayo iliingiza hekima 58

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 58

9/4/2017 3:47:47 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

katika dini na kutetea kwamba maagizo ya kidini lazima yakubaliane na kanuni za mantiki, na usahihi wa dini lazima uthibitishwe kwa njia ya hekima. Wasil mwana wa ‘Ata, alikuwa mwanafunzi wa Abu Hashim ibn Muhammad ibn Hanafiya, na baba yake, Muhammad, alikuwa mwanafunzi wa Ali. Jambo hilo hilo linaweza kusemwa kuhusu wale Asha’ira, kwa sababu wao walikuwa ni wanafunzi wa Mu’tazila, ambao walipata elimu kutoka kwa Wasil ibn ‘Ata, na yeye aliipata kupitia kwa watu wa katikati kutoka kwa Ali. Chanzo na msingi wa Usufi kimeegemea kwenye Nahjul-Balaghah. Kabla ya kuwa na utambuzi wa falsafa ya Kigiriki, Waislamu Masufi walikuwa wamezikubali semi za Ali kuwa ndio chanzo cha mawazo yao, kwa sababu hadi wakati huo, hizo falsafa za kigiriki na ya Kiajemi zilikuwa bado hazijahamishiwa kwenye lugha ya Kiarabu. Mwenyezi Mungu alijaalia kwamba kuhusu suala la elimu ya dini, Ali awe ndio nguzo na kiini cha usomi wa Kiarabu. Sio hata mtu mmoja katika wakati wake aliyeweza kushindana naye katika suala la fasihi ya Kiarabu. Pamoja na elimu yake kamilifu ya sintaksi (ya kupanga na kuhusisha vipashio na maneno kisarufi), ulimi fasaha na uwezo mkubwa wa kufikiri, yeye aliunda sheria na kanuni za lugha sahihi ya Kiarabu. Aliithibitisha kwa hekima ya kimantiki na hoja. Uhodari wake katika hekima ya kimantiki unaweza kutambulikana kutoka kwenye ukweli kwamba yeye aliweka msingi wa elimu za Kiarabu na akaandaa njia kwa ajili ya wengine kuziendeleza. Historia inaonyesha kwamba Ali alikuwa ndiye muasisi wa elimu ya sintaksi. Siku moja Abu’l Aswad, ambaye alikuwa mmoja wa wafuasi wake alikuja na akaona kwamba kichwa cha Ali kilikuwa kimeinamishwa chini na alikuwa akitafakari juu ya jambo fulani. Yeye akasema: “Ewe Amirul-Mu’minin! Unafikiria nini?” Ali akamjibu: “Katika jiji lenu (yaani, Kufah) nimesikia jambo ambalo lilielezewa na mzungumzaji kwa namna ya makosa. Mimi, kwa hiyo, nimeamua kuandika kitabu cha msingi juu ya kanuni za lugha ya Kiarabu. Kisha yeye akampa Abu’l Aswad karatasi ambayo juu yake ilikuwa imeandikwa kwamba maneno yako katika aina tatu; nomino, kitenzi na kihusishi. Tukio hilo vile vile limesimuliwa katika njia nyingine na imesemekana kwamba Abu’l Aswad alilalamika mbele ya Ali kwamba watu kwa kawaida walikuwa wana59

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 59

9/4/2017 3:47:47 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

zungumza lugha isiyo sahihi, kwa sababu tangu Waarabu walipochanganyika, baada ya ushindi wao, pamoja na wasiokuwa Waarabu, misemo isiyokuwa sahihi imejipenyeza kwenye maongezi yao. Imam alitafakari kidogo halafu akamwambia Abu’l Aswad aandike kile atakachokuwa anakitolea imla. Abu’l Aswad akatoa kalamu na karatasi, na halafu Ali akasema: “Lugha ya Kiarabu imeundwa na nomino, kitenzi na kihusishi. Nomino inaeleza kuhusu yale mambo ambayo yanabeba jina, kitenzi kinaelezea kuhusu msogeo na kitendo cha jambo hilo, na kihusishi kinawasilisha ambayo sio nomino wala kitenzi. Mambo yako ya namna tatu, yaani mambo ya dhahiri, mambo yaliyofichika na mambo ambayo sio ya dhahiri wala yaliyofichika.” (Baadhi ya wanachuoni wa sintaksi wanasema kwamba kwa ile namna ya tatu ya mambo, Ali alimaanisha ‘kiwakilishi kionyeshi’). Halafu Ali akamwambia Abu’l Aswad apanue na kukamilisha somo hilo kulingana na ‘nahau’ hiyo hiyo (yaani utaratibu au mwenendo). Kuanzia siku hiyo na kuendelea tawi hili la elimu likaanza kuitwa ‘Nahau’ – sintaksi. Moja ya sifa nyingine za Ali ilikuwa ni ile akili yake kali na kuelewa haraka. Mara kwa mara ilitokea kwamba, iwe ilikuwa ni kwenye mkusanyiko wa marafiki zake au wa maadui zake yeye alitamka maneno ya hekima ya papo kwa hapo bila kujiandaa, ambayo yalikujakuwa ni methali na zikapita kutoka ulimi mmoja hadi mwingine. Mafumbo magumu ya kihesabu ambayo yalikuwa yanatatanisha kwa wengine, yeye aliyafumbua mara moja bila kuchukua muda. Inasemakana kwamba mwanamke mmoja alikuja mbele ya Ali na akalalamika kwamba kaka yake alifariki na kuacha nyuma yake dinari mia sita, lakini kati ya pesa hizo, yeye alikuwa amepewa dinari moja tu. Ali akamjibu hivi: “Huenda warithi wa kaka yako ni pamoja na mjane mmoja, mabinti wawili, mama, ndugu wa kiume kumi na wawili na wewe mwenyewe.” Na hali ikatokea kuwa ni sawa na vile ilivyotajwa na Imam. Siku moja wakati Ali alipokuwa anatoa hotuba kutoka juu ya mimbari, mmoja wa wale waliokuwepo akasema: “Mtu mmoja amefariki na ameacha mjane wake, baba, mama na mabinti wawili.” Ali alijibu mara moja: “Lile fungu la moja ya nane la huyo mjane litabadilika na kuwa moja ya tisa.” Kwa vile Imam alitoa hukumu wakati akiwa juu ya mimbari tatizo hilo likaanza kuitwa “Wajibu wa Mimbari.”

60

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 60

9/4/2017 3:47:47 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Ali alikuwa ndiye mwanafalsafa wa Uislamu. Falsafa inakuja kuwepo kwa njia ya hekima na akili na uwezo wenye nguvu wa utambuzi na uamuzi. Mwanafalsafa ni yule, ambaye anaelezea idadi ya mambo muhimu katika simulizi fupi na anayejitahidi kuishi kulingana na maneno yake. Ali anachukua nafasi ya juu kabisa sio tu miongoni mwa wanafalsafa wa Kiislam, bali pia miongoni mwa watu wasio na kifani wa jamii ya mwanadamu. Ni vigumu sana kupata mtu kama Ali ambaye anaweza kuamua mambo ya kinadharia na kibusara kwa uwezo wa akili yake, na akayaeleza katika sentensi nzuri na fupi kwa namna ambayo wakati utaweza kuyahifadhi, na yaweze kuwa methali. Elimu za Kiislamu na usomi vilichukua hali ya ubinadamu katika muonekano wake kwa njia ya falsafa ya kimbingu na chemchemi zao zilikuwa ni wale watu wawili mashuhuri, kwa maana ya Muhammad na Ali. Imam Ali aliziangalia kwa hali ya kifalsafa zile siri za maumbile, maisha ya mwanadamu na jamii, na hadithi nyingi mno kuhusiana na Upweke wa Mwenyezi Mungu, mambo matakatifu, na metafizikia zinapatikana. Tayari tumekwishataja hapo juu kwamba yeye alikuwa ndiye muasisi wa falsafa ya uwanachuoni na theolojia. Yeye alikuwa ni mwalimu, ambaye ustadi na uhodari wake na uongozi, vimekubaliwa na kila mtu ambaye alikuja baada yake na maoni yake au kauli. Ndani ya Nahjul-Balaghah amefanya utungo wa lulu nyingi (semi) za hekima ambazo zimemfanya asimame katika safu ya kwanza ya wanafalsafa wa ulimwengu. Muhammad kwa kweli alitaja kuhusu Ali pale aliposema: “Wanachuoni miongoni mwa wafuasi wangu ni kama mitume wa Bani Israil.” Haki Za Binadamu Na Ali Mtihani Mgumu Wallahi! Ninaukiri ukweli mimi mwenyewe kabla ushahidi wowote haujatolewa dhidi yangu. Suala letu ni gumu sana. Maneno yetu yanaweza kueleweka tu kwa wale wenye nyoyo za uaminifu na akili za kuona mbali. – Imam Ali. Ali aliunda kanuni imara sana na aliwasilisha maoni madhubuti mno kwa ajili ya haki za wanadamu na ustawi wa jamii ya binadamu, kwamba mizizi yake inapenya ndani ya vina vya ardhi na matawi yake yanarefuka hadi mbinguni. Elimu zote za kijamii ambazo zipo kwa wakati huu, nyingi zake zinathibitisha maoni na kanuni hizi. Ingawa hizi elimu za kijamii za kisasa zinaweza kupewa majina mengi, na zinaweza kuwasilishwa katika miundo mingi, lengo lao ni moja, na ni moja tu kwam61

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 61

9/4/2017 3:47:47 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

ba, mwanadamu sharti alindwe kutokana na ukandamizaji na paundwe jamii ambayo italinda haki za binadamu katika njia bora – jamii ambamo hadhi ya mwanadamu lazima iheshimiwe, na uhuru wa maneno na vitendo uweze kuwa salama kwa kiwango ambacho asiumizwe mtu yoyote. Masharti na mazingira ya wakati yana athari kubwa katika uundaji wa elimu za kijamii. Ni masharti na mazingira haya haya ambayo yanawasilisha elimu za kijamii katika muundo mmoja kwa wakati mmoja, na katika muundo mwingine kwa wakati mwingine. Wakati tunapoichunguza historia na kukutana na matukio mbalimbali, tunakuja kujua kwamba kulikuwepo na mgongano kati ya makundi mawili tofauti ya wanadamu, na maoni na mawazo ya namna mbili tofauti. Kundi moja lilikuwa likipenda sana kuwa la kidhalimu na kupora haki za mtu wa chini na kumuondolea uhuru wake, ambapo hilo kunde jingine lilitamani uadilifu, demokrasia, uhifadhi wa haki za watu na uhuru wao. Wakati wa zamani, mavuguvugu yote yalianzishwa na waliokandamizwa, na wanamageuzi walitokana wakati wote kutoka miongoni mwao ili waweze kukomesha ukandamizaji na udhalimu, na kusimamisha serikali zilizoegama kwenye misingi ya usawa na uadilifu, ambao lazima ukubaliane na mantiki na masharti na mazingira ya jamii vile vile. Ali anayo nafasi ya juu kabisa katika historia ya haki za binadamu. Maoni yake yaliunganishwa na namna ya fikra za Kiislamu. Nukta muhimu ya maoni yake ilikuwa kwamba udhalimu lazima ufikie mwisho wake, na ubaguzi wa matabaka lazima uondoshwe kutoka miongoni mwa watu. Yeyote yule aliyekuwa amemtambua Ali; na akawa amezisikia kauli zake, na akaelewa imani yake na maoni yake kuhusu undugu wa kibinaadamu anajua kwamba yeye alikuwa ni upanga uliochomolewa juu ya shingo za watu waonevu. Nadhari yake yote ilikuwa imeelekezwa kwenye utekelezaji wa kanuni za usawa na uadilifu. Mawazo yake na mwenendo wa serikali yake na siasa zake vyote vilikuwa vimetolewa kwa ajili ya kufanikisha lengo hili. Kila mara dhalimu alipoingilia haki za watu au kuwafanyia udhalilishaji watu wanyonge au kupuuza ustawi wao, na akautupa uzito wa matatizo yake mwenyewe juu ya mabega yao dhaifu, basi Ali alipambana naye huyo vikali kabisa. Ulelewaji wa ki-akili wa Imam ulitokea sambamba na kufikiria kwake huku kwamba usawa na uadilifu lazima visimamiwe katika namna ambayo kulingana kui62

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 62

9/4/2017 3:47:47 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

marishwe, na tabaka moja lisiwe na ubora juu ya jingine, na kila mtu apaswe kupata kile anachostahili tu. Sauti yake ilidumu kuwa kubwa kwa mfululizo kwa ajili ya utekelezaji wa uadilifu, na rungu lake wakati wote lilishughulika ili kufikia mafanikio haya. Alimnyanyua mwanadamu na wakati wote alikuwa tayari kumlinda. Serikali yake ilikuwa mfano bora wa uongozi katika wakati ule. Ilikuwa ni serikali ambayo ilikuwa adilifu na yenye kulinda haki za binadamu, na ambayo ilifanikiwa katika malengo yake kwa njia zote zilizowezekana. Imam alitambua wazi wazi kabisa kwamba ile jamii ya wakati ule ilikuwa imesimama katika ulaghai, udanganyifu na shughuli zenye madhara, na urekebishaji wake ulikuwa ni muhimu kabisa. Pia alijua vizuri kabisa jinsi jamii hiyo inavyoweza kurekebishwa na ingechukua muda kiasi gani ili kufanya hivyo. Ingawa alifikiria juu ya ustawi wa watu katika hali zote, mambo ambayo aliyazingatia zaidi yalikuwa ni kubadilika kwao. Hakuna kilichoweza kumzuia kufanya juhudi juu ya hili. Alichokitaka zaidi kilikuwa ni kuimarisha ukweli na kuangamiza udanganyifu na hapakuwa na mwingine yeyote ambaye angekuwa na uwezo zaidi wa kupambanua ukweli na udanganyifu, haki na batili. Ali aliyatathimini mambo kwa usahihi kabisa na alijishughulisha mwenyewe katika kazi yake bila woga kabisa kulingana na ukadiriaji wake. Hakuwa na mashaka kwamwe kuhusu jambo lolote lililohusiana na ustawi wa umma. Wakati pale mtumishi yoyote au gavana alipowaonea raia, Ali hakukaa kimya wala hakufumbia macho matendo yao. Yeye hakuonyesha kamwe kulegea wakati alipogundua kwamba watu fulani wameunda kikundi dhidi ya serikali halali. Wakati mwingine mipango yake ya kufikia makusudio yake ilipingwa, sio tu kwa matakwa ya maadui zake, bali pia kwa wale marafiki zake vile vile, lakini yeye hakulijali hili. Yote haya yeye aliyafanya ili ile haki ya kila mtu kuendesha maisha ya amani iweze kuhakikishwa, na watu wasije wakawa wamegawanyika kwenye makundi mawili, ambayo mojawapo likawa na furaha sana na lile jingine likawa limehuzunishwa sana. Ali alikuwa ameelewa wazi kabisa kwamba itakuwa ni hatari sana kuwagawa watu kwenye tabaka mbili, na kulipendelea moja juu ya jingine. Hili litawadumaza wale watu wenye akili, kusababisha uovu ndani ya nafsi za watu, na kuanzisha ukandamizaji na udhalimu katika maamuzi na shughuli, na aina zote za fitna na upotovu zitajitokeza. Matokeo yatakuwa kwamba malengo ya maisha yatakufa na watu wa63

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 63

9/4/2017 3:47:47 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

takuwa bila rajua, na watakaribisha nia mbaya kwa kila mmoja wao. Hatimaye jamii itakuwa imeangamizwa. Alimuradi matabaka mawili haya yanakuwepo katika jamii, mgogoro kati yao hauepukiki na utahusisha na kupotea kwa maisha ya watu wengi. Katika wakati wa mwisho wa ukhalifa wa Uthman, wale watu mashuhuri wa dola, na hususan watu wa ukoo wa Bani Umayyah, ambao walikuwa jamaa na ndugu zake khalifa, walifanya ni desturi kuzipinga waziwazi sheria na kanuni za Kiislamu. Waliwadhalilisha watu, wakawafanya kama watumwa na wakawafanya wawe wenye woga sana na mtawala wao, kiasi kwamba hawakuweza kujasiri kusimama mbele yake na kutoa manung’uniko yao. Walicheza na maisha yao kwa namna ileile kama wanavyocheza na mali zao. Hawakujizuia kumwaga damu ya watu kwa ajili ya manufaa yao wenyewe na hakuna aliyethubutu kulipiza kisasi. Hawakuhofia kuchukua rushwa au kupora mali za wengine. Shughuli zao zilizoendelea, hali na mazingira vilionyesha nia zao zilikuwa nini. Ilikuwa dhahiri kwamba walikuwa waje kupakaza mikono yao kwa damu ya watu, kuganyaga haki zao na kuugeuza ukhalifa kuwa ufalme, na ile demokrasia ya Kiislamu kuwa udhalimu na udikteta wa mtu mmoja. Nafasi ya watu wa kundi hili, kati ya ile tabia adilifu hasa ya Ali, na ulafi wao binafsi wa mali, ilikuwa ni ile ya wacheza kamari. Kwa upande mmoja, Ali alidhamiria kutekeleza usawa na uadilifu kwa nguvu zake zote, na kwa upande mwingine watu hawa walikuwa na uchu sana wa kuwa na hatamu za serikali katika mikono yao wenyewe, na kumiliki utajiri na mali kwa kiasi kikubwa kiwezekanacho. Kati ya hali hizi mbili walikuwa kama wacheza kamari, wakitegemea kupata fursa ya kuleta mapinduzi na mwishowe kujitwalia manufaa yote wao wenyewe. Waliwazia uchu na tamaa mbaya kabisa vichwani mwao. Hakuna shaka kuhusu ukweli kwamba ule wajibu uliochukuliwa na Ali ulikuwa mgumu na wa kuhitaji jitihada kubwa sana. Sababu mbali mbali na mazingira yenye kutatanisha yalimfanya Ali kukabiliana na matatizo ambayo yasingeweza kudhibitika kirahisi. Dunia ya wakati ule ilikuwa shaghalabaghala, hali zilikuwa za kimapinduzi na matukio yalikuwa yanatisha, na majukumu ya Ali yalikuwa makubwa sana na mazito, ambayo ukhalifa na dini ya Uislamu vilitegemea juu yao. Kwa kuyatatua matatizo haya na kuyadhibiti magumu haya, Ali alifanya kazi ambayo ilifanya sifa zake zijulikane duniani. Dunia ilikuja kutambua alikuwa mwenye kujali kwa kiasi gani haki 64

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 64

9/4/2017 3:47:47 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

za umma, kiasi gani alijizatiti kuboresha maadili ya mtu binafsi na ya pamoja, na kwa subira na uvumilivu kiasi gani yeye alivyofanikisha malengo yake. Matatizo ya Ali yalikuwa sawa na yale matatizo aliyokabiliana nayo Mtume pale alipofanya ifahamike kwa Maquraishi kwamba yeye alikuwa ameteuliwa kwenye kazi ya utume, na wakawa wamegeuka kuwa dhidi yake. Kwa upande mmoja kulikuwa na ukweli, uadilifu, haki na usawa, na kwa upande mwingine kulikuwa na udanganyifu, ulanguzi na umimi. Mtume alitaka kuanzisha ukweli, uadilifu, haki na usawa ambapo Maquraishi walikuwa wamedhamiria kufanya udanganyifu, ulanguzi na majisifu. Ali vile vile alilazimika kukabiliana na hali ya matatizo kama hiyo hiyo. Hata hivyo ilionekana kuwa vigumu kwa mtazamo wa wengine. Kwa kadiri Ali alivyohusika, hata lile tatizo kubwa sana halikuweza kumfanya yeye akengeuke kwenye lengo lake. Kama mtu mwingine anakuwa anazo nguvu na uvumilivu ambao Mwenyezi Mungu amemjaalia Ali, kila tatizo litakuwa jepesi kwake vile vile. Kile ambacho kilikuwa hakivumiliki kwa Ali, kilikuwa ni kwamba apaswe kukaa katika kujitenga na asitekeleze usawa na haki – kwamba auponde ule moyo wa uhuru na asipandikize mbegu ya maadili. Mtume aliingiza sauti kwenye masikio ya Abu Sufyan, Abu Lahab, Umm Jamil, Hind – yule mlaini, na wachuuzi wa Kiquraishi, ambayo kwa sababu yake hiyo, ile misingi ya mipango yao ilibomoka, muundo wao ukavunjika na vitaji vyao vikaanguka chini. Hata hivyo, sauti hii hii hasa, ilikuwa ni bishara njema na ujumbe wa furaha kwa Waislamu na watu wale wasiojiweza. Alimwambia Abu Talib: “Ewe Ammi yangu mpendwa! Hata kama watu hawa wataweka lile jua kwenye mkono wangu wa kulia, na mwezi kwenye mkono wa kushoto ili niweze kutelekeza ule ulinganio kwenye Uislamu, mimi sitafanya hivyo hadi Mwenyezi Mungu atakapoifanya dini Yake ishinde au nitoe uhai wangu.” Siku moja wazee wa Kiquraishi walimwambia Muhammad: “Kama umeanzisha dini hii mpya ili kujilimbikizia utajiri, sisi tutaweka utajiri mwingi sana chini ya mamlaka yako, kiasi kwamba wewe utakuwa ndio mtu tajiri kabisa miongoni mwetu. Kama lengo lako ni kupata cheo kikubwa, sisi tuko tayari kukukubali wewe uwe ndio kiongozi – mtemi wetu. Na kama unataka kuwa mfalme sisi tuko tayari kukukubali kuwa mfalme wetu.” Yeye alisema katika kuwajibu: “Lengo langu katika kuwalingania watu kwenye Uislamu sio kupata utajiri au cheo, wala mimi sitamani kuwa mfalme wenu. 65

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 65

9/4/2017 3:47:47 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Ninautoa mwaliko huu kwa sababu Mwenyezi Mungu alinituma mimi kwenu katika nafasi ya mtume na amenifunulia Kitabu. Ameniagiza niwaonyeni juu ya adhabu Yake; na kukupeni bishara njema za Pepo. Mimi nimefikisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu kwenu. Kama mtaukubali basi mtaneemeka katika dunia hii na katika ile ya Akhera pia, na kama mtaukataa, mimi nitabaki kuwa mwenye subira hadi Mwenyezi Mungu atakapotoa hukumu Yake kuhusu ninyi na mimi mwenyewe.” Ali alifanya nini? Alikuwa na msimamo gani kuhusu mwana wa Abu Sufyan na Hind, yule mlaini, na juu ya wale wachuuzi, ambao walinunua na kuuza vyeo na kazi, na juu ya askari, ambao waliyatoa maisha yao muhanga kiupovu kwa faida ya wengine, na juu ya wale ambao waliiuza dini na imani zao mikononi mwa udanganyifu. Ali pia aliingiza sauti kwenye masikio yao ambayo iliporomosha misingi ya mipango yao, na akaifanya miundo yao na vitaji vyao kuanguka. Na sauti hii hii ikawa ni habari njema za furaha, na ujumbe wa maliwazo kwa wale watu waadilifu na wachamungu. Alisema: “Wenye nguvu wenu ni dhaifu na wadhaifu wenu ni wenye nguvu. Alimradi nyota zinazunguka kwenye mbingu mimi sitatoa uamuzi au hukumu inayopingana na uadilifu kamwe. Wallahi, nitafanya uadilifu kwa kiasi wakandamizaji na wale wanaoonewa wanavyohusika. Nitaweka kipini kwenye pua ya mkandamizaji na nitamvuta huyo kuelekea kwenye ukweli hata kama anaweza akauchukia sana. Ninaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kwamba ninaukubali ukweli kabla ushahidi wowote haujatolewa dhidi yangu. Mimi sijali kama ni ninayetembea kukielekea kifo au kifo ndio kinachokuja kuelekea niliko mimi.” Siku moja watu fulani walimwambia Ali: “Sisi ni watu wa jamiuiya hii tunaoheshimika.” Yeye akasema: “Mtu duni anaheshimika zaidi machoni mwangu mpaka nitakapoirudisha haki yake, na mtu anayeheshimika ni dhaifu mbele ya macho yangu hadi nitakapoirudisha haki ya mnyonge kutoka kwake.” Sasa tutachunguza jinsi Ali alivyoyaweka maneno yake haya kwenye vitendo na jinsi alivyoshughulika na watu. Umasikini Na Matokeo Yake Ali aliiangalia dunia kwa makini sana. Aliangalia kila kipengele chake bila ubaguzi wowote. Aliziweka haki za mtu mmoja mmoja na zile za watu wote kwa jumla akilini na hakupuuza kitu chochote. Aliwalingania watu kuuangalia uzuri wa dunia na maajabu ya maumbile, na wakati huo huo akawajulisha kila mmoja na jamii yote 66

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 66

9/4/2017 3:47:47 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

pia juu ya haki zao ili kwamba waweze kupata furaha ya hali ya juu na ustawi. Alizielezea haki za watu mmoja mmoja na za jamii ili kwamba watu binafsi wasaidiane kwa ushirikiano wa pande mbili na kujitahidi kwa ajili ya kudumu na kustawi kwa jamii, na waweze kunufaika kutokana nako katika nafasi zao binafsi. Mwanadamu ameumbwa kwa vitu vitatu; yaani, roho, kiwiliwili na viungo. Kiwiliwili ndio sehemu ya kimaada ya mwanadamu. Nacho pia kina haki yake ambayo ni lazima iheshimiwe. Ali ambaye juhudi zake zililenga juu ya utakaso wa nafsi na maadili mema, alijitahidi pia kuweka msingi wa jamii ya usawa na uadilifu, na kutekeleza sheria za haki kwa ajili ya maisha ya kimaada na ya kidunia ya mwanadamu. Lilikuwa pia ni lengo lake Ali kuwaongoza watu kwenye usafi wa moyo na upatikanaji wa tabia njema, na kulea na kuzoesha ufahamu wao katika namna ambayo kwamba wangeweza kutelekeza desturi mbaya kwa hiari zao wenyewe na wakajipamba wenyewe na sifa njema. Hata hivyo, haiwezekani kuendeleza desturi nzuri mpaka mtu awe na chakula cha kujilisha na mavazi ya kuvaa, na watu hawawezi kupata njia za maisha hadi uadilifu utakapoenea. Hivyo mpango wa ubadilishaji na usafishaji hauna budi uanze na upatikanaji wa mahitaji muhimu ya maisha kama vile chakula, nguo na kadhalika. Watu wanaweza kuvutiwa na utakasaji wa nafsi na maadili mema baada tu ya mahitaji haya kuwa yamekwisha kupatikana. Hili ndio lilikuwa lengo la mapenzi ya Ali, kabla na baada ya kuwa amekwisha shika ukhalifa. Ni vipi kibarua, ambaye anafanya kazi kwa bidii zote kutwa nzima, atakavyoweza kufaidi mandhari ya dunia na kutafakari juu ya ishara za utukufu wa Mwenyezi Mungu; wakati ambapo hapati malipo yake kamili, na ananyonywa na walanguzi na wakopesha-fedha? Atawezaje kuelekea kwenye sifa ya maadili mema wakati maisha yake yenyewe yamemchosha? Ni vipi watu wale wanyonge watakavyoweza kuelewa maana ya utakasaji wa nafsi, watu ambao wanalia wanapochapwa na watawala wao, na wanayaona maisha yao kama hayana thamani – ambao maisha yao yenyewe yamemilikiwa na watawala wao, ambao wanategemewa kuwatumikia na kuwasaidia, lakini badala yake wao katika hali halisi wanawanyonya? Wapo watu masikini wengi sana ambao hawamiliki hata senti moja. Hata hivyo, mksanyaji wa mapato anawanyang’anya mali yoyote ile wanayomiliki ili kujaza hazina za watawala wapenda anasa. Hawana hata kipande cha mkate cha kula na maisha 67

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 67

9/4/2017 3:47:47 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

yao na mali zao vyote pia havina usalama. Zaidi ya hayo, kama watatamka japo neno moja tu dhidi ya watawala wao, maisha yao yenyewe yanakuwa matatani. Ni vipi watu masikini wanyonge kama hao watatafakari juu ya siri na miujiza ya ulimwengu na kufanya juhudi ya kurekebisha na kusafisha mwenendo wao wa tabia? Wakati umasikini umemtenganisha mtu na kila jema, na umevuruga ule utulivu wa akili yake, na amekata tamaa juu ya kila kitu, na madhalimu wamemfunga mikono na miguu yake, na haiwezekani tena kwake kuurudisha uhuru wake, itawezekanaje kwake yeye kuwa mkweli, mwenye moyo safi na mchamungu, na asiwe mwenye wivu na kinyongo, na asikengeuke kutoka kwenye njia ya wema na uchamungu? Wakati njaa imewasha moto katika moyo wa mtu, ambao unakula kila tone la damu yake na kuiondoa imani yake, atayafurahiaje maisha, na kuamini katika uadilifu wa watu, na kuungana mkono na ndugu zake, na kuishi kwa upole na ndugu na jamaa zake? Mtu atawapendaje watu wengine ikiwa amefungwa kabisa na hali ya udhalili na utumwa, na ambapo hana tamaa yoyote iliyobaki katika maisha, na anayaona kama yasiyo na thamani kabisa? Mtu ambaye hana chochote cha kula hawezi kuwa na sifa za wema na uchaji, kwa sababu chakula ndio msaada wa kwanza kwa kila tabaka na ndio njia ya utulivu wa akili. Ni chakula kinachomuwezesha mtu kutafakari, na kinamfanya aweze kupata maadili mema, na kuonyesha tabia nzuri kwa wengine. Kuwa huru kutokana na umasikini ndio kitu kinachomnasua mtu kutokana na ufukara na huzuni, na kumnyanyua hadi kwenye ustawi wa hali ya juu. Umasikini unalegeza shauku za kibinadamu. Watu masikini wasiojiweza wanajiona wao kama ni wageni katika mji wao wenyewe. Wanahisi kana kwamba mji huo sio wao na ndugu zao kuwa kama sio ndugu zao hasa, na kwamba wao wenyewe ni kama wazururaji tu, wasio na faida yoyote humo. Kwa vile watu masikini na wenye dhiki hawajioni wenyewe kama wenye kustahili kuwa na matendo mema na sifa bora, wanaweza kuondokana na hali hii ya udhalili pale tu watakapokuwa salama kutokana na umasikini. Ni wakati huo tu ambapo wanaweza wakaamini kwamba na wao pia wanaweza wakawa raia wema na wakaweza kuzisafisha nyoyo zao kutokana na hisia za wivu na kinyongo. Walikuwepo wanafiki fulani ambao walikuwa wakisema kwamba njia pekee ya kudumisha kanuni na taratibu ilikuwa ni kwamba watu wapaswe kuwa wamegawanyika kwenye makundi mawili – wale ambao walikuwa wametosheka, na wale waliokuwa na njaa. 68

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 68

9/4/2017 3:47:47 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Kwa mujibu wa maoni yao wao; haikuwa ni lazima kwa wale waliotosheka kujilazimisha kwenye dharura za maisha – maisha yale yanayopendwa na watu wote – wala haikuwa lazima kwa wao kutamani mabadiliko yoyote katika hali zao wenyewe au zile za wengine. Wao walitaka kwamba hadhi ingedumishwa katika dunia. Kwa mujibu wa wanafiki hawa, wale wenye njaa vile vile walikuwa hawana haki ya kudai haki zao zilizoporwa, wala wasiililie ile riziki ambayo ilikuwa imenyakuliwa kutoka kwao na kuwekwa kwenye meza za chakula za mabepari. Kama mtu mwenye njaa alidai haki yake, na kulalamika dhidi ya kunyang’anywa tonge kutoka midomoni mwa wanawe, yeye aliwekwa katika fungu la kuitwa kafiri na mfanya fitna, ambaye amewavuruga watu wanaoendesha maisha ya amani. Wanafiki hawa walikimbilia kwenye mbinu mpya kila wakati kulinda njia zao za maisha ya starehe na anasa na kuwaweka watu masikini katika hali ya utumwa. Walitumia silaha mbalimbali hapo zamani za kale na zama za hivi karibuni, katika kuyafikia malengo yao. Silaha yao kubwa ilikuwa ni tafsiri potovu ya maagizo ya kidini. Sera hii haikuwa ya kipekee kwa Waislamu. Ilikuwa imetwaliwa pia na wanafiki wote waliokuwa wakidai kufuata dini ya Ubudha, ya Kiyahudi, Ukristo au Uislamu. Silaha rahisi kabisa, ambayo kwayo wanafiki waliitumia kwa manufaa yao, ilikuwa ni madai yao kwamba mitume wamewalingania watu kwenye kujihini, wakisisitiza juu ya kutelekeza starehe za kidunia na utajiri, wakapendelea umasikini na ufukara, na wakahimiza maisha ya kukinai na kutojishughulisha badala ya kufanya juhudi yoyote ile.13 13

wa vile mengi yamesemwa kuhusu ubora wa ukataaji wa dunia na kuhusu uchamungu inawezekana kwamba K baadhi ya watu wanaweza kudhani kwamba utafutaji wa mambo ya kidunia unakatazwa kabisa katika Uislamu. Kwa hiyo, ni muhimu kufafanua kwamba zipo ngazi tofauti za uchamungu, na kazi na wajibu wa mitume, mawalii na watumishi wengine wateule wa Mwenyezi Mungu pia ni tofauti na za watu wa kawaida. Kwa kiasi watu wa kawaida wanavyohusika, maana na mipaka ya uchamungu uliopendekezwa kwao vilevile umeainishwa vizuri wazi wazi. Imam Ali amesema: “Kiini cha uchamungu kimetajwa ndani ya Qur’ani Tukufu katika maelezo namna mbili. Mwenyezi Mungu amesema: “Usije ukahuzunika kwa yale ambayo yamekukosa, na wala usije ukafurahia katika yale ambayo Mwenyezi Mungu amekujaalia.” Kwa kuifuata Ayah hii mtu anapata uchamungu mkamilifu.” wenyezi Mungu anasema: “Enyi mlioamini! Msijiharamishie vitu ambavyo Mwenyezi Mungu amevifanya M kuwa halali juu yenu, na msipitukie mipaka. Mwenyezi Mungu hawapendi wale wenye kuvuka mipaka.” wenyezi Mungu vilevile anasema: “(Ewe Mtume!) Waulize kuhusu ni nani aliyeharamisha vitu vya maM pambo na vitu safi vya kula ambavyo Mwenyezi Mungu ameviumba kwa ajili ya waja Wake?” ya zilizonukuliwa hapo juu zinakuja kuonyesha kwamba kama ambavyo hairuhusiwi kuvifanyahalali vile A vitu ambavyo Mwenyezi Mungu amevitaja kuwa ni haramu, hairuhusiwi kuvifanya hara-mu – vile vitu safi na namna ya kujipamba kulikotajwa kuwa ni halali na Mwenyezi Mungu, na piahairuhusiwi kula kiapo cha kutokutumia vitu halali. Kiapo kama hicho hakitiliwa nguvu katika she-ria za kidini. 69

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 69

9/4/2017 3:47:47 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Wanafiki hao wanaeneza sana maoni yao hayo yaliyotajwa hapo juu; na wanatamani kwamba mtu wa kawaida ayakubali kuwa ni ya sahihi, ili kwamba wengine waweze kubaki kuwa wamenyimwa – wabakie kuwa masikini, na wao wenyewe waendelee kuwa matajiri na waweze kufaidi starehe za maisha. Ni muhimu kwamba, ili kuzuia propaganda zao za uwongo tunapaswa kubainisha ile hali halisi. Ni kwa kufanya hivyo tu kwamba tunaweza kuugundua msingi ambao juu yake sera za Ali na maagizo yake aliyoyatoa yalimokuwa yameegemea. Ni kweli kwamba dunia iliondolewa chini ya miguu ya Muhammad na kutandazwa chini ya miguu ya wengine. Starehe na mapambo yote ya kidunia yalikuwa yamezuiwa juu yake. Alikuwa mtu wa kujinyima hasa. Kamwe hakula akashiba, na chakula chochote kile alichokula hakikuwa kizuri mno. Aliiacha dunia katika namna kama alivyoieleza Abu Dhar: “Mtume hakuwahi kula aina mbili za chakula kwa siku moja. Pale alipokula tende, basi hakula mkate. Mara nyingi ilitokea kwamba chakula hakikupikwa ndani ya nyumba yake kwa miezi mingi mfululizo.” Ni kweli vile vile kwamba Ali alichukulia vipande viwili vya nguo kwamba vinatosha kwake mwenyewe, na pia aliridhika binafsi na vipande viwili vya mkate kwa siku. Nyumba yake vilevile ilifanana na nyumba za watu masikini. Mifano ya kujinyima na kuridhika kwake ni mingi mno na inayojulikana sana kwamba sio lazima kuitaja kwa kuihesabu hapa. Ni kweli pia kwamba wafuasi wake kama vile Abu Dhar aliridhika binafsi na mkate mkavu wa shayiri. Imam Ali anasema: “Uchamungu katika dunia una maana ya kupunguza matamanio ya mtu, kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema Zake na kujiepusha na mambo yaliyofanywa kuwa ni haramu na Mwenyezi Mungu.” (Jami’ul-Sa’adat) Ali anasema: “Uchamungu duniani hauna maana kwamba mali ziharibiwe au vitu halali vifanywe kuwa haramu. Kinyume chake una maana kwamba unapaswa usitegemee sana juu ya vitu vya kidunia ambavyo unavimiliki kulinganisha na vile ambavyo viko kwa Mwenyezi Mungu.” (Jami’ul-Sa’adat) Imam Ali vile vile anasema: “Kama mtu anapata kumiliki kila kitu duniani na lengo lake kwa kufanya hivyo ni kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu, huyo ni mchamungu, na kama anautelekeza ulimwengu wote lakini lengo lake katika kufanya hivyo sio kupata radhi za ki-mungu, huyo sio mchamungu.” Mtu mmoja alimuuliza Imam Ali: “Uchamungu ni nini?” Yeye akajibu: “Kuepuka mambo haramu ya dunia.” Kwa kifupi, uzuri au ubaya wa mambo ya kidunia unategemea nia ya mtu. Kama nia ni nzuri na vitu vya kidunia vinatafutwa ili kuwa kama njia ya furaha katika Akhera, kitendo chake hicho mtu kinakuwa kitukufu, vinginevyo kinastahili kulaaniwa. 70

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 70

9/4/2017 3:47:47 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Yeye na watu wa familia yake vile vile walikula mkate na walifurahia na kurid hika nao. Mambo yote haya ni ya kweli na sahihi kabisa. Hata hivyo, kuna kitu kingine pia ambacho nacho ni sahihi. Wote kwa pamoja walikuwa na wajibu juu ya elimu na mwongozo kwa watu; na waliishika kazi hiyo kubwa ya ‘mwelekezaji’ na ‘kiongozi.’ Kwa kutambua wajibu ulioambatana na kazi yao, walichukulia kiasi kidogo cha chakula na mahitaji mengineyo ya kutosheleza tu kwa ajili yao na walibaki wameridhika. Hata hivyo, kila mtu hawezi kuwa kama wao, na hawezi kustahimili zile dhiki ambazo zimevumiliwa na wao hao, wala ule mwanga ulionururisha mioyo yao na kuifanya michangamfu, hauwezi kuwaka katika kila moyo. Zaidi ya hayo, wao walijali sana kuhusu ustawi wa wafuasi wao kiasi kwamba hawakutilia maanani sana kwenye chakula chao, mavazi na starehe zao wenyewe.14 Wale ambao wamechunguza maisha ya viongozi hawa wa ulimwengu, lazima watakuwa wametambua kwanza kabisa kwamba wao walikuwa ndio viongozi mashuhuri wa mapinduzi, na malengo yao yalikuwa yamehusishwa na mapinduzi hayo. Chochote kile walichokifanya kilikuwa kwa ajili ya ustawi wa watu, na walikifanya kwa msaada wa watu hao. Ili kuyafanya mapinduzi hayo yafanikiwe, walitwaa mbinu ambazo zilikuwa zinafaa kwa nchi yao. Baadhi ya viongozi wa mapinduzi walikuwa ni wale ambao waliuawa, kwa mfano Ali mwana wa Abu Talib; na baadhi walikuwa ni wale ambao maadui hawakuweza kuwafanyia madhara yoyote, kwa mfano Mtukufu Mtume. Ilikuwa haiwezekani kwa viongozi hao wa mapinduzi kuishi maisha ya anasa na starehe, kwa sababu mazingira ya mapinduzi hayakuwaruhusu kufanya hivyo. Utulivu wa akili ni sharti kwa ajili ya maisha ya starehe, na utulivu wa akili kama huo viongozi hawa hawakufaidika nao. 14

I li kuyaweka maadili na fikira za watu masikini katika matumaini makubwa, wawakilishi wa serikali za Kiislamu wameelekezwa kuishi maisha ya kawaida. Wanapaswa kujiweka kwenye viwango vya wale masikini na kushirikiana nao kwa mapana na marefu, kwa kila hali, kama ilivyokuwa desturi ya Mtukufu Mtume. I mesimuliwa kuhusiana na mwenendo na desturi za Mtume kwamba yeye alisema: “Sitatelekeza mambo matano hadi kufariki kwangu; nayo ni, kula chakula pamoja na watumwa, kuketi chini juu ya ardhi, kukamua kondoo kwa mikono yangu mwenyewe, kuvaa nguo za sufi, na kuwasalimia watoto wadogo, ili iweze kuja kuwa ni desturi ya kawaida baada yangu mimi.” I mam Ali amesema: “Mwenyezi Mungu amenifanya mimi kuwa Imam wa watu na amelifanya ni jambo la wajibu juu yangu kupunguza starehe zangu binafsi na chakula, kwa kiasi kwamba hali yangu ya maisha iwe ni sawa na ile ya watu masikini, ili hao watu masikini waweze kufuata mfano wa mwenendo wangu wa maisha, na wale matajiri wasije wakawa waasi kwa sababu ya utajiri wao.” 71

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 71

9/4/2017 3:47:47 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Jambo la pili ni hili kwamba, shabaha ya kwanza ya maadui wa mapinduzi ni yule kiongozi wa mapinduzi. Mpaka pale tu mapinduzi hayo yatakapofanikiwa maisha yake yanabakia wakati wote katika hatari, na anabakia mwenye kufikwa na maonevu na mateso. Sasa je, itawezekana vipi kwa mtu ambaye maisha yake wakati wote yamo hatarini, kufaidi neema na starehe za kidunia? Hili litawezekana kwake tu kama mapinduzi yake yanafanikiwa au kama akiyatelekeza mapinduzi hayo. Hata hivyo, ni ukweli pia kwamba viongozi hao wa mapinduzi walikuwa huru kuendesha aina ya maisha waliyoitaka wao, na kuridhika na yale mahitaji ya maisha waliyoyaona kwamba yangetosheleza. Hakuna ambaye angepinga kuhusu uchaguzi wao au kutochagua jambo maalum kwa ajili yao wenyewe. Walikuwa wao wenyewe wamejitwalia maisha ya kujihini na kutosheka, lakini hawakuwalazimisha wengine kuyafuata. Mbali na mambo mengine yote, hivi Yesu Kristo hakushutumiwa na Warumi kwa kuwachochea watu kuasi dhidi ya Kaisari, na kuwazuia kutomlipa yeye kodi, na kwa matokeo yake ambapo yeye Kristo alishitakiwa na kuhukumiwa kifo? Kwa nini Kristo aliwazuia watu kulipa kodi kwa Kaisari? Je, haikuwa ni kwa sababu ya mkate ambao yeye Kaisari na wafuasi wake waliunyakua kutoka kwa watu masikini, wale wenye njaa na mayatima? Je, makasisi wa ki-Yahudi wa Jerusalem hawakumwambia mwakilishi wa Kaisari ili kuunga mkono mfumo wa serikali ya Kaisari, ambayo kulingana nayo masikini walinyonywa na mabepari wakawa matajiri, kwamba kama asingemsulubu Yesu Kristo, basi yeye hakuwa rafiki wa Kaisari? Alikuwa ni Muhammad, ndugu yake Kristo, ambaye alisimama dhidi ya jamii ya kidhalimu ya wakati ule, ambamo kulikuwemo na msuguano mkali baina ya waonevu na wanaoonewa. Qur’ani Tukufu inazungumza na watu kupitia kwake kwa maneno haya: “Tembeeni juu ya ardhi na mle na mnywe kile mlichoruzukiwa na Mwenyezi Mungu.” Hapa watu wameelekezwa kula na kunywa kwa sababu maisha yanategemea juu ya matendo haya. Maelekezo haya yametolewa kwa watu wote na sio kwa tabaka maalum. Kila mtu ana haki ya kufanya kazi na kujipatia njia ya mahitaji ya maisha. Katika tukio jingine imesemwa kwamba: “Mwanadamu anapaswa kukitazama chakula chake, Tumeteremsha mvua kutoka juu mbinguni, tukaipasua ardhi na 72

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 72

9/4/2017 3:47:47 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

tukapanda mbegu ndani yake na tukafanya mizabibu na miwa na mizeituni na tende vikue juu yake. Tulitengeneza bustani za kijani na matunda safi.” Kuna hadithi moja ya Mtume ambamo amesimuliwa kuwa amesema: “Kuna mambo matatu ambamo watu wana mafungu sawa – maji, mimea na moto.” Kila mtu analo fungu sawasawa katika maji ambayo Mwenyezi Mungu anayashusha kutoka juu, au anayoyafanya yatiririke juu ya ardhi. Hata hivyo, kama mtu atachimba mfereji ili kujipatia maji au anayahifadhi maji, watu wengine hawana haki ya kuyachukua maji hayo kutoka kwake, kwa sababu anayo haki ya awali juu yake. Vivyo hivyo, ile mimea ambayo inaota yenyewe ki-asili; hiyo hakuna mwenye haki ya kujitwalia mwenyewe binafsi kuwaondoa wengine. Vivyo hivyo, kama mtu anawasha moto hawezi kumnyima mtu mwingine moto huo, kwa sababu kama mtu anawasha taa yake kwa moto huo, wala moto huo hautapungua kitu. Katika zama za ujahilia ilikuwa ni desturi kwamba kiongozi au mtawala alijitwalia mwenyewe kipande chochote cha ardhi alichotaka kwa ajili ya kuchungia ngamia wake na wanyama wengineo. Wanyama waliokuwa wa watu wengine walikuwa hawaruhusiwi kuingia kwenye eneo hilo la malisho. Wanyama wake yeye hata hivyo, waliweza kuchungwa kwenye maeneo ya malisho ya kawaida ambayo yalitengwa kwa matumizi ya watu wengine wote. Hii ilikuwa ni mbinu mojawapo ya ukandamizaji ambayo ilichukuliwa katika zama hizo. Mtume aliipiga marufuku desturi hii ya kidhalimu pamoja na desturi nyingine nyingi. Mtume alilipa mishahara kamili kwa watumishi na pia aliwaelekeza wengine kufuata mfano wake ili kwamba pasiweze kubakia mtu masikini na fukara yoyote katika jamii. Wakati na kila pale pesa za hazina zilipopokelewa na yeye Mtume kutoka mahali popote aliligawa fungu la masahaba wake miongoni mwao mwanzoni kabisa na alimpa binti yake Fatimah fungu lake baadaye. Madhumuni yake ya kufanya hivyo yalikuwa kwamba mahitaji ya watu wa kawaida yaweze kutimizwa kwanza. Hatutaki tuandike kwa mapana na marefu juu ya suala la mwenendo wa Muhammad hapa katika jambo la utajiri na umasikini. Sisi tayari tumekwisha kutaja kwa kirefu katika sura iliyotangulia, jinsi gani Uislamu ulivyowatia moyo watu kufanya kazi yenye manufaa ili wasibakie watu masikini wasiweze kubakia katika jamii kiasi kwamba katika Uislamu kazi nzuri imependekezwa sana kuliko Swala na Saumu zilizopendekezwa. Mtume Muhammad ambaye alikuwa hapendi umasikini na utegemezi juu ya wengine amesimuliwa kuwa amesema: “Umasikini unaelekea kuwa ni sawa na ukafiri.” 73

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 73

9/4/2017 3:47:47 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Katika sura ifuatayo baadaye, tutakuja kuelezea jinsi Mtume wa Uislamu mwenye kuona mbali alivyozielewa siri nyingi na miujiza isiyo na idadi inayohusiana na jamii, na jinsi yeye alivyowatia watu moyo wa kufanya maisha yao yawe ya furaha. Abu Dhar al-Ghiffari alikuwa mtu wa kujinyima na kuridhika ambaye hakujali sana kuhusu starehe za kidunia. Ingawaje alichagua kuishi maisha yasiyo na ladha, alipigana vita vikali na vya dhati dhidi ya umasikini, na alijitolea mhanga maisha yake wakati akiwa anafanya kampeni juu ya kuunga mkono haki za watu. Kauli ifuatayo, ambayo aliitoa yeye ni yenye kuvutia sana: “Wakati umasikini unapoelekea kwenye mji, ukafiri unaomba kuandamana nao.” Bani Umayyah na watawala wa baadaye walifanya juhudi zao nzuri kabisa kwa ajili ya uendelezaji wa mamlaka yao na madaraka. Ili kufanikisha lengo lao hili waliwashawishi washirika na watumishi wao kusimulia hadithi za kughushi au za kuzusha wakizihusisha kwa Mtume ili ziweze kuwa zenye msaada kwa ajili ya kuwanyonya watu na kuwaweka katika hali ya utumwa.15 15

akati mwingine Bani Umayyah wenyewe walizitunga hadithi kama hizo na katika nyakati nyingine, kazi W hii ilifanywa kwa ajili yao na washirika wao au wanachuoni wa kulipwa. Hapa chini tunatoa mifano kadhaa ya hadithi za kuzusha kama hizo na michapo isiyo na mashiko ambayo Imam Bukhari ameisimulia kutoka kwa Abdullah ibn Umar kama ifuatavyo kutoka kwa wasimuliaji mbalimbali: Mtume amesema: “Baada yangu mtakabiliwa na utofautishaji usio halisi na vitendo visivyopendeza.” Masahaba wakamuuliza: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Wewe unaamrisha nini juu yetu (katika mazingira kama hayo).” Mtume akajibu kwamba: “Walipeni watawala hao haki zao na mtafute haki zenu wenyewe kutoka kwa Mwenyezi Mungu.” ( Sahih Bukhari, Juz. 8.) Bukhari vile vile amemnukuu Ibn Abbas kuwa amesema: Mtume amesema: “Kama mtu ataona jambo kutoka kwa mfalme wake ambalo analichukia, ni lazima afanye subira, kwa sababu yeyote ajitengaye na taifa hata kwa kiwango cha kitambo kidogo, atakufa kifo cha kijahilia.” (Sahih Bukhari. Juz. 8). ukhari amesimulia kwa vyanzo tofauti kutoka kwa Alqama bin Wail Hadhrami kwamba amesema: “Muslim B bin Zaid Ju’fi alimuuliza Mtume: ‘Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Ni yapi maagizo yako kama itatokea baadhi ya watu kuwa watawala wetu, ambao wanadai haki zao kutoka kwetu lakini wao hawatupi sisi haki zetu?’ Mtume akageuzia uso wake mbali na yeye. Muslim akalirudia swali lake hilo tena. Mtume akageuza uso wake mbali naye kwa mara nyingine tena. Muslim akauliza swali hilo hilo kwa mara ya tatu. Papo hapo Ash’ath bin Qais akamvuta na Mtume akajibu: “Ni lazima uvumilie kile wanachokisema. Wajibu wao unabakia kwao na wajibu wako unabakia juu yako.” (Sahih Bukhari, Juz. 2, uk. 119). ukhari amemnukuu Ajrafa kama amesema kwamba yeye amemsikia Mtume akisema: “Hivi punde tu mambo B yasiyofaa yatatokea. Kama mtu yoyote atataka kusababisha mgawanyiko katika umma mpigeni kwa upanga, kwa vyovyote itakavyokuwa.” (Sahih Bukhari, Juz. 2, uk. 211). Bukhari vile vile amemsimulia Abu Sa’id Khudhri kama amesema kwamba, Mtume amesema: “Pale ambapo kiapo cha utii juu ya makhalifa wawili kimetokea, muueni yule ambaye kiapo juu yake kimetolewa baadaye.” (Sahih Bukhari, Juz. 2, uk. 122). Zipo hadithi nyingi kuhusu suala hili na maana yake ya jumla ni hii kwamba Waislamu lazima wawewatiifu kwa serikali ya zama na wasilalamike juu ya mfalme hata awe dhalimu kiasi gani, kwasababu kwa kufanya hivyo watasababisha mgawanyiko na tofauti miongoni mwa Waislamu. iini cha hadithi zote hizi kinatolewa katika hadithi ifuatayo: “Machafuko yatatokea hivi karibuni.Wakati wa K machafuko hayo yule ambaye atakuwa amekaa na kutulia atakuwa kwenye nafasi nzurikuliko yule aliyesimama, na yule ambaye atakuwa amesimama atakuwa kwenye nafasi nzuri kulikoyule atakayekuwa anatembea, na yule atakayekuwa akitembea atakuwa kwenye nafasi nzuri kulikoyule atakayekuwa anakimbia. Na kama 74

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 74

9/4/2017 3:47:47 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Wafuasi wao kwa hiyo walitunga na kusimulia hadithi mpya nyingi ambamo watu walishauriwa kubakia kuwa na subira, kuvumilia kukandamizwa na watawala na kutekeleza amri zao bila kupinga. Swali la pili ni kwamba kama maneno haya ya Mtume ni halisi na ya kweli kwa mtazamo wa kihistoria, kwa nini masahaba hao waliyaendea kinyume chake wakati wa kifo chake, wakati palikuwa na mgogoro kuhusu ukhalifa, mfuatano wa uongozi na urithi? Zaidi ya hayo, kwa nini hadithi hizi hazikutolewa, na watu wakashauriwa kuwa na subira wakati kulipokuwa na mgogoro kuhusu wale waliokataa kutoa Zaka wanapotangazwa kama ni makafiri au la, na vile vile wakati khalifa Uthman aliposhambuliwa na watu wakataka kumuua? Aisha alikuwa ndiye mke kipenzi cha Mtume na alizikumbuka hadithi nyingi kwa kichwa. Talha na Zubair walikuwa pia ni masahaba wa karibu wa Mtume, na walikuwa wamebashiriwa habari njema kwamba wataingia Peponi. Kwa nini watu hawa hawakuzikumbuka hadithi hizi, na kwa nini wao waliasi dhidi ya Ali? Zaidi ya hayo, hadithi hizo zinapingana moja kwa moja na Ayah za Qur’ani Tukufu na hadithi sahihi, na hazina uhusiano na desturi nzuri ya Mtume na falsafa ya Kiislamu. Kwa mfano; Imesemwa katika Suratul-Baqarah: “Na piganeni katika njia ya Mwenyezi Mungu, na kumbukeni kwamba Yeye ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua.” Ndani ya Suratul-Maidah, Qur’ani inasema: “Adhabu ya wale wanaopigana dhidi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu na kuleta ufisadi katika ardhi ni kwamba wao wauawe au wanyongwe au mikono yao na miguu yao ikatwe.” katika wakati huo atapata mahali pa kujihifadhi basi aingiehumo.” (Musnad Imam Ahmad Hanbal, Juz. 2, uk. 282). adithi zilizosimuliwa hapo juu zinaonyesha kwamba kwa kuhofia mgawanyiko miongoni mwa wafuasi wake, H Mtume alisisitiza juu ya kubakia kwao kuwa waaminifu kwa watawala wao, hata kama watakuwa na hatia ya vitendo haramu. Hii itamaanisha kwamba Mtume alikuwa na shauku kwamba umoja wa Waislamu ni lazima udumishwe kwa gharama yoyote ile, hata kama dini aliyoileta yeye ikiharibiwa. Kwa hali hiyo, swali la kwanza linalojitokeza ni hili kwamba; kama Mtume alikuwa na shauku kiasi hicho juu ya umoja wa Waislamu kwamba aliupendelea hata kuliko dini ya Kiislamu, kwa nini alisababisha mgawanyiko miongoni mwa Waarabu washirikina kwa kuwalingania kwenye Uislamu? Waarabu hao walikuwa wameungana katika suala la ushirikina na uabudu masanamu, lakini yeye alisababisha ufa miongoni mwao kwa kuanzisha dini mpya. Aliyavunja masanamu yao na akazikanyaga imani zao ingawaje haya yalikuwa ni mambo waliyoyapenda mno 75

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 75

9/4/2017 3:47:48 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Ndani ya Suratul-Mujadilah inasemwa kwamba: “Hutawaona wale wanaomwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Kiyama wakifanya urafiki na maadui wa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake ingawaje wawe ni baba zao, watoto wao, ndugu au jamaa zao.” Katika Suratul-Mumtahinah inasema kwamba: “Enyi mlioamini! Msifanye urafiki juu wale ambao wamewajibikiwa na ghadhabu ya Mwenyezi Mungu.” Hizi ni baadhi ya Ayah za Qur’ani Tukufu ambazo zinapingana wazi wazi na hadithi za kughushi zilizotangulia kutajwa hapo juu. Sasa, hapa chini tunanukuu baadhi ya hadithi ambazo zinapingana nazo hizo. Imam Muslim anasimulia kutoka kwa Abdullah ibn Mas’ud kwa njia ya vyanzo mbali mbali kwamba Mtume amesema: “Miongoni mwa wafuasi wa mitume, ambao waliteuliwa kwa kazi ya utume, walikuwa ni viongozi na masahaba, ambao walifuata hadithi na maagizo ya mtume husika. Viongozi hawa na masahaba walirithiwa na watu ambao walisema jambo moja na wakafanya jambo jingine, na wakatenda vitendo ambavyo havikuruhusiwa. Yeyote anayepigana dhidi ya watu kama hao kwa mikono yake; ulimi au moyo, huyo ni muumini.” (Sahih Muslim, Juz.1.) Abu Sa’id al-Khudhri amesimuliwa kuwa amesema kwamba amemsikia Mtume akisema: “Yeyote atakayewaona watu wanaofanya vitendo visivyofaa ni lazima awazuie kwa mikono yake. Kama hawezi kuwazuia kwa mikono yake, anapaswa awazuie kwa ulimi wake. Na kama hawezi kuwazuia hata kwa njia hiyo, basi anapaswa kuwashutumu moyoni mwake. Na hiki ni kiwango cha chini cha imani dhaifu.” (Futuhat al-Dhahabiya). Kwa kifupi, yeyote ambaye ameyachunguza maisha ya mitume kwa makini anajua kwamba walichukia vitendo vya aibu na waliwaonya na Moto wa Jahannam wale wanafiki, ambao waliwavutia watu kwenye umasikini. Kama isingekuwa hivyo, mabepari wasingekuwa maadui wa mitume hawa, na watu wanyonge na wasio na uwezo wasingejikusanya karibu yao. Misemo ya watu wa hekima wa zama za kale wa Arabia, inaonyesha kwamba wao walijua vyema kuwa vitendo vya mtu katika uwezo wake binafsi, vina uhusiano wa karibu sana na mfumo wa jamii. Walikuwa wakitambua vema kwamba upatikanaji wa njia ya maisha ulikuwa na athari kubwa juu ya usafi wa silika, maadili na tabia za mtu. Ule uridhikaji unao76

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 76

9/4/2017 3:47:48 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

pendekezwa hauna maana kwamba mtu asifanye chochote na ajishughulishe na kujihini tu, ambako huleta umasikini, na kuharibu tabia njema na kuondoa imani. Na sio sahihi vile vile kusema kwamba mazingatio yote ya mtu lazima yaelekezwe kwenye mazoezi ya nafsi yake, na mwili wake upuuzwe, kwa sababu utii kwenye sheria hauwezekani ikiwa tumbo la mtu liko tupu. Ni watu mashuhuri tu wanaobakia kuwa na subira, kama vile Abu Dhar, hata kama wakiwa masikini, na kila mtu hawezi kuwa na uvumilivu na ustahimilivu ambao ulikuwa wa kipekee kwa Abu Dhar. Kwa mujibu wa Sa’adi wa Shiraz, maneno haya ya Mtume: “Umasikini ni jambo la fahari kwa mtu,” yanarejea kwa wale watu ambao walikuwa ni mabingwa wa nyanja ya utii kwa Mwenyezi Mungu na radhi tukufu, na sio kwenye umasikini wa wale watu ambao wanavaa (kujionyesha) vazi la watu wachaji, na kupata chakula wakati wote kwa gharama ya watu wengine. Na ile kauli: “Kuridhika ni hazina isiyo na ukomo” haikutamkwa kwa ajili ya watu walegevu ambao hawana wanachokifanya. Imetamkwa hasa kwa kuhusika na wale watu matajiri wenye tamaa, na watawala madhalimu, ambao hawatosheki na chochote na hawaridhiki hata kama neema zote za ulimwengu zikiwekwa mikononi mwao. Maisha yote ya Ali yalitumika katika kuyafanya maisha ya watu kuwa mazuri na kuwaondolea shida na umasikini. Kama tutakavyoelezea baadaye, huu ulikuwa ndio msingi hasa wa serikali yake. Ali mwenyewe alikuwa ndiye mwenye kujihini mkubwa, ambaye kwamba alikuwa huru kutokana na uchafu wote wa kidunia. Hata hivyo, hakutaka kabisa kwamba watu wengine pia wabakie kuridhika na umasikini. Kama isingekuwa hivyo asingeanzisha mapambano dhidi ya matajiri na wenye uwezo, na dhidi ya wale ambao walinyang’anya mali kinyume na haki, na akaigawanya miongoni mwa masikini na wenye shida. Tha’labi anasimulia kisa fulani katika maneno yafuatayo: “Siku moja wakati wa ujana wangu nilikwenda kwenye viwanja vya Rahba huko Kufa. Hapo nilimuona Ali akiwa amesimama juu ya marundo mawili ya dhahabu na fedha. Baadaye alianza kuugawanya utajiri ule, na akaugawa wote kabisa. Halafu akarudi nyumbani kwake katika hali ambayo hakuchukua kitu chochote kwa ajili yake binafsi. Ali huyo huyo ambaye alikuwa hakuchukua chochote kutoka kwenye mali hiyo anasema, akiwaambia watu: “Endeleeni kushughulikia manufaa yenu ya kidunia kwa namna ambayo kana kwamba mtaishi kwenye dunia hii kwa kudumu.” 77

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 77

9/4/2017 3:47:48 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Hakuna kitu kilichokuwa na muhimu mbele ya macho ya Ali kuliko kuuondoa umasikini wa watu. Kuhusiana na hili ametoa kauli ya wazi kabisa ambayo haiwezi kuelezewa katika njia nyingine yoyote. Yeye anasema: “Kama mnaendelea kutembea kwenye njia kuu za ukweli, vijinjia vitawakaribisheni na hakuna hata mmoja kati yenu atakayejiingiza kwenye ufukara.” Licha ya kuzishambulia njia na tabia zilizofuatwa na Waarabu wakati wa zama za jahilia, yeye vile vile alishutumu uridhikaji wao unaofanana na wa kidaruweshi. Yeye anasema: “Enyi Waarabu! Mliishi maisha sugu, mlikunywa maji yaliyochafuka na mkala chakula kilichooza kama watu mafukara.” Maneno ya Ali yanaonyesha kwamba sio kuwa hakupendelea chakula kizuri na kitamu, nguo nzuri na nyumba ya kifahari, kile ambacho hakukipenda yeye kilikuwa ni kwamba yeye mwenyewe aishi maisha ya starehe wakati ambapo watu wengine wanaweza wakawa hawana fursa kama hizo. Maneno yake ya dhahiri yanaonyesha kwamba yalikuwa ni mapenzi yake ya kweli kabisa kwamba kila mtu aweze kuwa na namna ya maisha ya kutosheleza katika udhibiti wake. Ali alikuwa ndiye kiongozi wa watu na ilikuwa ni wajibu wa kiongozi kuishi maisha magumu kama vile wafuasi wake wanavyoishi, mpaka umasikini ndani ya jamii uwe umetoweka kabisa. Pale itakapokuwa hakuna mtu masikini aliyebakia katika jamii, ule ufukara wa kiongozi pia utakuwa lazima ufikie mwisho wake. Namna yake ya maisha itakuwa inafanana na ile ya watu wengine, kwa sababu kuutia kasoro uongozi na utawala huo kutakuwa hakuna maana. Ali anasema: “Je, niridhike binafsi na hili la kwamba watu wananiita mimi Amirul-Mu’minin na kwamba nishiriki nao katika suala la mambo ya kuchukiza ya zama hizi?” Kwa ‘mambo ya kuchukiza’ yeye alikuwa na maana ya dhiki na umasikini. Ali hakumruhusu binti yake kujipamba kwa lulu kama mabinti wa watu wengine wengi hawakuwa katika hali ya kuweza kujipamba wenyewe kwa namna hiyo. Kama ilivyokwishatajwa katika kurasa zilizotangulia, yeye alimuamuru kwa mkazo kurudisha ule mkufu wa lulu kwenye hazina ya umma akisema: “Ewe binti ya mwana wa Abu Talib! Usikengeuke kutoka kwenye njia ya haki. Hivi wanawake wote wa Muhajirina na Ansari wanajipamba wenyewe katika siku ya Iddi kwa namna hii?” Yeye alisema “wanawake wote” na sio “wanawake wa waungwana.”

78

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 78

9/4/2017 3:47:48 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Wakati Ali alipopata ukhalifa, kitu cha kwanza kabisa ambacho yeye alikifanya kilikuwa kwamba alijitahidi kufuta umasikini wa watu. Na hili ndio ambalo Ali alipaswa kufanya, kwa sababu yeye alijua vizuri kabisa kwamba, ingawa mwanadamu alikuwa afikwe na matatizo mengi, umasikini ndio ulikuwa ni balaa kubwa sana kwake. Ni yeye ambaye aliyatamka maneno haya: “Mwenyezi Mungu hakumhusisha mwanadamu katika tatizo lolote ambalo lingeweza kuwa kubwa kuliko umasikini.” Kifungu hiki cha maneno, kwanza kabisa kinaonyesha kwamba yeye aliona ule uondoaji wa umasikini wa watu kuwa ni muhimu kabisa, na pili kwamba alikuwa amefanya uchambuzi sahihi uliokamilika kabisa wa hali na mazingira ya watu na matokeo yake. Baadhi ya watu wameusifia umasikini sana na wamewaalika watu kuelekea kwenye umasikini huo. Hata hivyo, kufikiria kwao sio sahihi. Ali alipambana dhidi ya umasikini katika namna ile ile ambayo Mtume na Abu Dhar Ghiffari, mwanamapinduzi mkuu kabisa na wa mbele kabisa miongoni mwa wafuasi wa Ali, na muathiriwa wa Bani Umayyah madhalimu, alipambana dhidi yake. Mtume; na vile vile hata Ali na Abu Dhar, wote walijua kwamba umasikini unaharibu kila aina ya sifa, kiasi kwamba inakuwa ndio chanzo cha ukafiri kwa upande wa waumini wachamungu. Ilikuwa ni kwa sababu hii kwamba Ali alipigana dhidi yake umasikini kila mara na kuwafedhehesha wale waliowaalika watu kuuelekea. Kwa mujibu wa imani ya Ali, umasikini unamfanya mtu mwenye busara kuwa kiziwi na bubu. Ni kwa kutokana na umasikini kwamba wakazi wa mji mmoja wanakuwa ni wageni na hata kuwa maadui wa kila mmoja wao. Hakuna shaka juu ya ukweli kwamba kifo ni msiba mkubwa sana, lakini umasikini ni mbaya kuliko kifo. Ali anasema: “Umasikini ndio kifo kikubwa mno.” Haya ndio maneno aliyoyasema Ali dhidi ya umasikini na ufukara, na pia dhidi ya wale waliouhubiri umasikini, ambayo yanashusha ndoto ya uongo wao na udanganyifu: “Kama umasikini utakuja mbele yangu katika umbile la mwanadamu, mimi nitauua kabisa.” Machoni kwa Ali, jamii ya mwanadamuni kama mwili ambao haukutengenezwa na chembe chembe za kinyume, wala mfumo wake kuwa kwenye msingi wa ubaguzi katika suala la haki na wajibu, kiasi kwamba watu wengine wanaweza kufanya watakavyo bila ya kuwepo mtu wa kuwazuia, na wengine wawe hawana uwezo bila ya kuwepo mtu yeyote wa kuwasaidia. 79

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 79

9/4/2017 3:47:48 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Katika jamii ambayo ilitakiwa na Ali, ilikuwa hairuhusiwi kwamba kundi moja la watu likue na kunenepa wakati jingine watu wake wakondeane na kuwa kama kiunzi cha mifupa au lile kundi moja lifanye kazi na jingine livune manufaa. Ingawaje Ali alikuwa ni mtu wa kiroho mkubwa mashuhuri, ambaye mazingatio yake wakati wote yalielekezwa kwa Mwenyezi Mungu, haikupita hata siku bila ambapo angeweza kutojali mambo ya watu, au akaweza kupuuza hata ingawa yale mambo yao yenye thamani ndogo kabisa, kwa sababu alimuona mwanadamu kuwa ndiye mfano bora wa viumbe walio bora kabisa. Aliutazama ulimwengu na wakazi wake katika namna ile ile hasa ambayo Mtume aliwaangalia. Qur’ani Tukufu inasema: “Tumeufanya usiku kuwa ni kifuniko na mchana kuwa wakutafutia riziki na maisha.” Aliufanya wahyi huu mtukufu kuwa msingi wa kuweka sawa katikati mazingatio yake juu ya jamii ya mwanadamu. Alizihuisha sheria za kijamii na akawa mwenye kushughulika na kuzisahihisha na kuziendeleza ili jamii yenye bahati na ustawi iweze kupata kuwepo. Alizitumia hotuba zake na mapendekezo katika wasaa wake sahihi na aliwajulisha watu juu ya wajibu na majukumu yao. Ali alikuwa na shauku sana ya kudumisha usawa na uadilifu. Lengo lake kuu lilikuwa kwamba uadilifu uweze kuimarishwa. Baada ya kuupata ukhalifa, baadhi ya watu walikuja kumpongeza na wakamkuta akishughulika sana na kurekebisha viatu vyake. Yeye aliwaambia: “Kama sitaweza kuimarisha haki na kuangamiza batili, viatu vyangu hivi vitakuwa na thamani sana kwangu kuliko utawala huo.” Wakati wote aliwataka wale watu wachamungu, ambao walikuwa na shauku ya Akhera, kuuhudumia umma ili upate neema za dunia ijayo. Yeye alisema: “Ni yule mtu tu, anayefanya kazi kwa ajili ya ustawi wa watu, ndio atakayefaulu katika Akhera. Na mambo mazuri sana yanayoweza kufanywa kuhusiana na ustawi wa umma ni haya: kuwalisha wenye njaa; kuwapatia maji wale wenye kiu; kuwapatia nguo wale wasiokuwa nazo; kuwajulisha watu juu ya haki na wajibu wao; na kulinda haki za wengine.” Siku moja Amirul-Mu’minin alikwenda kumtembelea mfuasi wake mmoja aliyekuwa akiitwa ‘Ala ibn Zaid Harasi. Alipoona jinsi nyumba yake ilivyokuwa na nafasi kubwa sana alimwambia: “Ukubwa huu wa nafasi ya nyumba yako una faida 80

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 80

9/4/2017 3:47:48 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

gani kwako katika dunia hii; wakati ambapo unahitaji zaidi nyumba yenye nafasi katika Akhera ambako utapaswa kuishi milele. Kwa kweli, kama unatamani pia nyumba yenye nafasi huko Akhera, basi unapaswa ukaribishe wageni katika nyumba hii, uwatendee wema juu yao jamaa na ndugu zako na ulipe haki za wengine katika muda muafaka. Kama utafanya hivyo basi utafuzu katika dunia ijayo.” Wakati akielezea umuhimu wa Saumu na Swala yeye alisema kumwambia Kumayl ibn Ziad: “Oh, Kumayl! Sio muhimu kwamba uzitekeleze Swala na kufunga Saumu na kutoa Zakat tu basi. Kilicho na muhimu zaidi ni kwamba unapaswa kuswali kwa moyo safi na halisi na kulingana na matakwa ya Mwenyezi Mungu.” Hata kabla ya Akhera, yeye alikuwa na shauku sana kuhusu maisha ya watu katika dunia hii kiasi kwamba, licha ya kuwa kwake Khalifa, yeye alikwenda kwenye maduka ya Kufa kama jambo la utaratibu wa kawaida wa kila siku, akisimama katika kila duka na kusema: “Enyi wachuuzi! Mcheni Mungu. Tafuteni kuwa karibu na wateja. Jipambeni wenyewe na uvumilivu. Msitoe viapo. Msiseme uwongo. Epukeni dhulma. Kuweni waadilifu kwa wale wanaokandamizwa na mfanye vipimo na mizani zenu sawasawa. Msiwapunje watu na kuwapa pungufu kuliko haki yao. Msieneze dhulma katika dunia.” Nauf Bukali amesimuliwa kwamba amewahi kusema: “Nilikwenda na nikamuona AmirulMu’minin katika msikiti wa Kufa. Nilimsalimia na yeye akazijibu salamu zangu. Mimi nikasema: “Ewe Amirul-Mu’minin! Naomba unipe ushauri kidogo.” Yeye akasema: “Kuwa mwema kwa watu na Mwenyezi Mungu atakufanyia wema.” Nilimuomba aseme kitu kingine zaidi. Yeye akasema: “Nauf! Kama unapenda kuja kuwa na mimi katika Siku ya Hukumu basi usiwasaidie madhalimu.” Kwa kifupi, nukta muhimu katika sera ya Ali ilikuwa ni huduma kwa wanadamu, kutimiza mahitaji yao na ufutiliaji mbali wa dhuluma. Wakati mmoja Mtume alimtazama yeye kisha akasema: “Oh, Ali! Mwenyezi Mungu amekupamba na pambo ambalo ndio pambo bora kabisa mbele ya macho Yake Mwenyewe. Amekutunuku na upendo kwa ajili ya wanyonge. Naliwe jambo lenye kukufarahisha wewe kwamba wao watapaswa kuwa ni wafuasi wako, na watakuwa na furaha na kuridhika kwa sababu ya wewe kuwa ndio Imam wao.”

81

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 81

9/4/2017 3:47:48 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Hali Ya Mambo Kabla Ya Ali Kabla hatujaelezea ni mawazo na imani gani alizokuwanazo Ali kuhusu undugu wa kibinadamu, na jinsi alivyoziheshimu haki za binadamu, inajitokeza kwamba ni lazima kwanza kutaja kile Mtume alichokifanya kwa ajili ya ustawi wa wanadamu, ni sheria na kanuni gani alizotoa, na ni kwa kiasi gani aliziheshimu haki za binadamu. Ni lazima kufanya hivyo, kwa sababu wajibu pekee wa Ali ulikuwa ni kuzitekeleza zile sheria zilizokuwa zimetangazwa na Mtume na kukamilisha yale aliyokuwa ameyataka Mtume. Alichokifanya Ali kilikuwa ni hitimisho la matendo ya Mtume, na kila hatua aliyoichukua yeye ilikuwa ikiungana na hatua zilizokuwa zimechukuliwa na Mtume. Mtume wa Uislamu aliweka mazingatio kwenye hali muhimu na za kijamii za watu. Uislamu umeweka sheria na kanuni kwa ajili ya jamii ya watu kwa namna ile ile ambamo uliziweka kwa ajili ya watu mmoja mmoja binafsi. Uislamu unaweka umuhimu mkubwa sana kwenye undugu wa kibinaadamu na jamii kwamba unachukulia kila huduma ya taifa kama ni ibada – hakika, kutumikia taifa kunapewa kipaumbele zaidi ya utekelezaji wa taratibu za kidini. Mtume amesema: “Kuamua tofauti na migogoro ni bora zaidi kuliko Swala na Saumu zilizopendekezwa.” Kadhia ifuatayo inaonyesha wazi ni kwa kiasi gani Mtume alivyokuwa anajali kuhusu ustawi wa umma na jamii: Ibn Abdullah anasema: “Sisi (masahaba) tulikuwa tumefuatana na Mtume katika safari moja. Baadhi yetu walikuwa wamefunga ambapo wengine hawakuwa wamefunga. Ilikuwa ni msimu wa kiangazi. Tulisimama mahali fulani. Hapakuwa na kivuli kilichopatikana kwa ajili yetu isipokuwa vipande vya nguo tulivyokuwa tumebeba. Walikuwepo wengi miongoni mwetu sisi ambao walikuwa wanakinga nyuso zao kutokana na mwanga wa jua kwa viganja vya mikono yao. Wale ambao kati yetu walikuwa hawakufunga walisimama na kisimika mahema na kuwapatia wanyama maji. Papo hapo Mtume wa Uislamu akasema: “Leo wale watu ambao hawakufunga wamejitwalia thawabu zote juu yao wenyewe.” Tukio hili linaonyesha kwamba, kufunga ambako ni kanuni muhimu ya kisheria ya ibada inakoma kuwa wajibu wakati wa safari kiasi kwamba mtu anaweza akaonyesha kuzembea katika masuala ya kiuchumi kwa sababu hiyo na anaweza akashindwa kuwatumikia viumbe wa Mwenyezi Mungu.

82

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 82

9/4/2017 3:47:48 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Mtume vilevile amesema: “Pale mmoja yeyote kati yenu atakapoona jambo la aibu likifanywa anapaswa kulizuia kwa mikono yake na kama hawezi kufanya hivyo basi anapaswa kulizuia kwa ulimi wake. Na kama hawezi pia kulizuia kwa ulimi wake basi alichukie na kulishutumu moyoni mwake. Na hii (njia ya tatu) ni hatua dhaifu sana ya imani.” ‘Kuamrisha kutenda wema na kukataza maovu’ ni amri ya wazi kabisa katika Uislamu kwa sababu kwa njia yake kila aina ya jema linaweza kufanywa kwa wengine, na namna zote za maovu zinaweza kufutiliwa mbali. Zipo hadithi nyingi zilizosimuliwa kutoka kwa Mtume ambazo zinaonyesha kwamba yeyote yule anayetoa utumishi wowote kwa umma ni mbora zaidi kuliko mtu mchamungu. Hii ni kuhusu watu wa kawaidi wanaotoa utumishi kwa umma. Ikiwa, hata hivyo, mtu anayetoa utumishi kama huo, pia ni mwanachuoni, yeye bila shaka atakuwa mbora kuliko mamilioni ya wachamungu mbele ya macho ya Mtume, kama vile tu mwezi ulivyo bora kwa mamilioni ya nyota. Mtume wa Uislamu amesema: “Mwanazoni kwa vyovyote vile ni bora kuliko mtu mchamungu kwa namna ile ile ambavyo mwezi ni bora kuliko zile nyota. Mtume ameitukuza hekima; kwa sababu ni hekima ndio ambayo inafanya juhudi ya kutafuta njia na namna kwa ajili ya ustawi wa watu. Mtu anaweza kufanya wema kwa watu tu kwa njia ya hekima. Mtume anasema: “Tafakari ya saa moja ni bora kuliko ibada ya mwaka mzima.” (katika baadhi ya hadithi inasemekana kwamba ni bora kuliko ibada ya miaka sabini). Uislamu umetoa mazingatio kamili kwenye ustawi wa jamii ya wanadamu na umoja wake na utangamano, na vile vile kwenye namna na njia zake za maisha, na umevuta mazingatio ya watu kwenye neema za ardhi na baraka za kazi. “Mwenyezi Mungu ameumba zawadi ya vitu vizuri vyote katika dunia kwa ajili yenu. Ardhi imeumbwa kwa ajili ya viumbe. Ni Mwenyezi Mungu aliyeitiisha ardhi juu yenu. Tembeeni juu ya njia zake na kuleni katika riziki iliyofanywa kupatikana kwenu na Mwenyezi Mungu.” Uislamu umefanya kuwa ni wajibu kwa mwanadamu kuwashukuru watu wengine. Mtu anaweza kumshukuru Mwenyezi Mungu pale tu ambapo anakuwa anawashukuru wengine, kwa sababu mtu ambaye hawatambui viumbe hawezi kumtambua Mwenyezi Mungu. ‘Yule mtu ambaye kwamba hakuwashukuru watu, basi hakumshukuru Mwenyezi Mungu.’

83

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 83

9/4/2017 3:47:48 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Mtume amezisifu sana shughuli zenye manufaa. Yeye hakuridhika binafsi yake na kuzisifu tu shughuli kama hizo, bali amechukulia pia kustahili kuibusu ile mikono ambayo imevimba kutokana kazi nyingi. Yeye anasema: “Huu ndio mkono ambao unapendwa na Mwenyezi Mungu na Mtume Wake.” Hadithi ifuatayo inaonyesha jinsi Mtume huyu mashuhuri alivyozichukulia zile kazi zenye manufaa na viwango vya ustawi wa jamii. Masahaba wa Mtume waliona mtu aliyejengeka vizuri na wakatamani kwamba angeweza kuwa amezitumia nguvu zake kwa njia ya Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu. Hapo Mtume akasema: “Kama mtu huyu amekuja kuwahudumia wazazi wake wanyonge na waliozeeka, hiyo ni kazi katika njia ya Mwenyezi Mungu. Kama ametoka kuja kuchuma kwa ajili ya watoto wake, hii pia ni kazi katika njia ya Mwenyezi Mungu. Kama ametoka kuja kuchuma kwa ajili ya mke wake ili kumlinda kutokana na mambo ya haramu, hii pia ni kazi katika njia ya Mwenyezi Mungu. Na kama ametoka kuja kuchuma kitu kwa ajili yake mwenyewe ili kwamba asiwe ni mwenye kuomba pia ni kazi katika njia ya Mwenyezi Mungu.” Vitabu vya hadithi vimejaa hadithi nyingi za Mtume ambazo zinaonyesha kwamba yeye alithamini sana kazi na kwamba aliwaheshimu sana wale waliofanya kazi kwa bidii sana. Yeye anasema: “Mwenyezi Mungu anampenda muumini ambaye anafanya kazi na kupata ujira wake. Hakuna chakula kilicho bora kuliko kile ambacho kilichopatikana kwa jasho lake mtu mwenyewe.” Hivyo, wakati kazi ni kitu cha thamani kiasi hicho; na hata inachukuliwa kuwa ni utukufu, ni muhimu juu yetu kufanya kazi kwa uvumilivu. Wakati mtu anapofanya kazi kwa bidii atanufaika yeye binafsi na wengine vile vile. Kuwepo kwake katika jamii kutaonekana ni kwenye heri na Mwenyezi Mungu pia atampenda. Mtume anasema: “Mwenyezi Mungu anapenda kwamba pale mmoja wenu anapofanya kazi basi aifanye vizuri na kwa uhakika.” Tumesema hapo juu kwamba Uislamu umeitiisha ardhi kwa mwanadamu. Anatembea juu yake na kuzitumia neema zake. Swali hata hivyo linajitokeza juu ya kwamba je, ni mwelekeo gani Uislamu umeutwaa katika suala la ugawaji wa neema hizi? Je, neema zote ni kwa ajili ya tabaka maalum na kuondoa wengine? Hivi ni kundi moja tu la watu lililokuwa na haki ya kunufaika kutokana nazo, na wengine wanabakia kunyimwa haki hiyo? Au zinapaswa kugawanywa kwa msingi wa juhudi na mahitaji? Je, neema hizi ni za kukusanywa na kuhifadhiwa na wafalme, madikteta, 84

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 84

9/4/2017 3:47:48 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

matajiri na waporaji, au zinapaswa zigawanywe kwa uadilifu miongoni mwa watu wote? Uislamu umeuangalia ubinadamu kwa jicho la uadilifu na mantiki na umeweka sheria juu ya hilo. Ama haukumnyima mtu yeyote fungu lake, wala kumpatia zaidi ya haki yake. Kila juhudi inakuwa na malipo na ni lazima kwa umma kuheshimu malipo haya. Jamii nzuri hairuhusu kwamba mfanya kazi kwa bidii akose chakula, na mtu asiyejishughulisha anufaike kutokana na mapato ya kazi ya huyu mchapakazi. Wala jamii nzuri haina maana kwamba mfanyakazi asipate malipo kwa ajili ya kazi yake na mtu mlegevu asiye na faida yoyote anyang’anye neema zote hizo, kama ilivyotokea katika jamii za nyakati zilizopita, na kama Bani Umayyah walivyojitahidi kufanya baada ya kuja kwa Uislamu, yaani kwamba waweze kuwatumikisha wengine wote na kutumia mali zao na kucheza na maisha yao kama walivyotaka. Tunaona kwamba Uislamu ulikataza israafu: matumizi mabaya ya fujo, na kujipamba kusikosahihi, hususan katika jamii ambamo idadi kubwa ya watu wake ni masikini. Sababu yake ni kwamba, kama kuna israafu na kujipamba kwa ajabu ajabu kwa upande mmoja, basi kutakuwa na umasikini na njaa katika upande mwingine, na pia kwa sababu hakuna mwenye haki ya kutwaa mapato ya juhudi za wengine; na maisha ya starehe katika jamii masikini yanawezekana tu pale baadhi ya watu wanapojilisha wenyewe kwa mapato ya juhudi za wengine. Mtume amezifanya zile nyumba za watu wabadhilifu kuwa ni makazi ya Shetani. Yeye anasema: “Nyumba za mashetani ni vitundu ambavyo vimejazwa na watu wenye mavazi ya hariri na yaliyotariziwa.” Qur’ani Tukufu inasema hivi: “Ilikuwepo miji mingi ambayo wakazi wake walizama katika starehe. Tuliwaangamiza wao na nyumba zao zikabomolewa. Hakuna walioachwa kukaa hapo isipokuwa wachache tu.” Mahali pengine Qur’ani inawaonya watu kwa namna ya ufasaha kabisa na inasema: “Tunapotaka kuuangamiza mji tunawaagiza wakazi wake wenye kupenda starehe kuwa wakware (yaani, tunawapatia namna ya maisha ya starehe na anasa) ili waweze kustahili kuangamizwa, na kisha tunauteketeza mji huo.”

85

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 85

9/4/2017 3:47:48 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Uislamu umekataza kuishi maisha ya starehe wakati mtu anapokuwa anaishi miongoni mwa masikini, kwa vile kunawavunja moyo, na umezuia njia zote zinazoongozea huko. Udhalimu na ukandamizaji kutoka kwa magavana na watumishi ulikuwa ni moja ya njia kama hizo. Mtume alikataza na kutangaza juu ya kuhodhi na kulimbikiza kinyume cha sheria, kupokea kazi kutoka kwa vibarua bila kuwalipa ujira wao, kuwa mmiliki wa ardhi bila kufanya lolote katika kuiendeleza, kupora mali za wengine, na matendo mengine kama hayo ya uonevu. Yeye alisema kuhusu kuhodhi mali: “Mtu anayehodhi mali ni mtenda dhambi.” Mtume wa Uislamu alionya kuhusu mateso makali kwa wale wanaopora ardhi na akasema: “Mwenyezi Mungu ataweka mnyororo wenye tabaka saba za ardhi kwenye shingo ya mtu anayepora ardhi za wengine.” Yeye vile vile alisema: “Mtu anayetwaa kwa mabavu mali za wengine atakutana na Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama katika hali ambayo kwamba Yeye atakuwa amemkasirikia huyo.” Uislamu umekataza aina zote za riba. Qur’ani Tukufu inasema kuhusu riba: “Enyi mlioamini! Msiendelee kula riba mchanganyiko.” Mahali pengine inasema: “Mwenyezi Mungu ameruhusu biashara na amekataza riba. Wanaokula riba wameonywa juu ya adhabu kali, kwa sababu ni aina ya kazi ya kulazimishwa na ni sawa na kuwafanya wengine kuwa watumwa.”16 Uadilifu una maana kwamba mtu apate ujira wake kulingana na kazi yake. Kama watu watakuwa hawatwai mali za wengine na hawahodhi bidhaa muhimu ili kuja kupata faida kubwa zaidi, utajiri hauwezi kuwekwa kwenye mikono michache. Kama mwanadamu na bidii yake ya kazi angepewa ule umuhimu unaostahili katika jamii, utumwa na utwana visingeweza kuwepo. Kama ilivyo kinyume kwenye jamii za kidhalimu ambamo thamani ya mtu inapimwa kwa kutilia maanani utajiri 16

una tofauti kubwa sana kati ya riba na biashara. Wafanyabiashara wanazitoa bidhaa kutoka kwenye sehemu K zinazohusika kwa thamani ndogo. Kila mtu hawezi kufanya shughuli hii. Wachuuzi wanazipeleka bidhaa hizo kwenye masoko yanayofaa kwa ajili ya kuziuza. Wakati mwingine wanapata faida na wakati mwingine wanapata hasara. Hilo sio suala la kuhusiana na riba. Mkopeshaji fedha hana juhudi yoyote anayofanya, haridhiki na faida kidogo na hapati hasara wakati wowote. Kwa hiyo tofauti kati ya shughuli mbili hizi ni ya dhahiri kabisa. 86

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 86

9/4/2017 3:47:48 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

wake, Uislamu una kigezo cha hali ya juu zaidi kwa ajili ya kutathmini thamani ya mtu. Kosa kubwa ambalo linaweza kufanyika katika jamii ni hili kwamba serikali na walanguzi watakapoungana kuwanyonya wanyonge na watu wasiojiweza. Qur’ani Tukufa inasema: “Msile mali za wengine kinyume na sheria wala kutoa rushwa kwa watawala ili muweze kutumia vibaya kila mtakachoweza kutoka kwenye mali za wengine, ingawaje mnalijua hilo.” Mtukufu Mtume amesema: “Hakuna chakula bora zaidi kuliko kile ambacho mtu amekipata kwa kazi ya mikono yake mwenyewe.” Katika Suratul-Zilzal ya Qur’ani Tukufu imesemwa kwamba: “Yeyote atakayefanya jambo la uovu dogo sawa na chembe atayaona matokeo yake.” Imesemekana kwamba: “Kila mtu atahukumiwa kulingana na vitendo vyake.” Ingawaje Uislamu umeukubali utajiri kama mali yake mtu, sheria za Kiislamu zimeundwa katika namna ambayo utajiri usije ukalimbikizwa katika mikono michache, na kwamba hao wachache wasije wakayafaidi manufaa yote wenyewe na kuwadhalilisha wengine, na kuwashurutisha katika kazi za kulazimishwa. Qur’ani Tukufu inasema: “…… ili kwamba utajiri usije ukawa ni kitu cha kuchezea kwenye mikono ya wale matajiri kati yenu.” Hivyo kwa mujibu wa Qur’ani na Hadith, utajiri unakwenda, mwanzoni kabisa, kwa umma, na watu wa umma huo wanaweza wakautumia kulingana na mahitaji yao na juhudi zao. Ni kwa sababu hii kwamba utwaaji wa mali ya watu wengine umeharamishwa katika Uislamu, na ulimbikizaji wa mali ya ziada vile vile umeharamishwa. Huu ndio ulikuwa msingi wa sera ya Mtume juu ya hazina ya umma na aliweka mifano juu ya hili kwa maneno na vitendo vyake, ambavyo ni lazima vifuatwe.17 17

ale ambao wameisoma Qur’ani wanatambua kwamba Uislamu ama hauwaungi mkono wale makabaila W waliolaaniwa wala mfumo wa ukomunisti ambao sio wa kawaida. Unakubali uanzishaji wa umiliki binafsi ili kila mtu aweze kufanya matumizi bora ya uwezo wake. Kwa vile ukatazaji wa kisheria tu hautoshelezi kwa ajili ya marekebisho ya kiuchumi, Uislamu vile vile umejitahidi kufanikisha lengo hili kwa njia ya mafunzo ya maadili. Hii ndio tofauti kubwa kati ya mifumo ya kiyakinifu na ule wa Kiislamu. Ukomunisti unayafunga maisha yetu yote kwa sheria, na matokeo yake tunashushwa na kuwa kama mashine. Hatimaye hatuwezi kutumia utashi wetu na dhamira zetu na hivyo kuchakaa na kutoweka kidogo kidogo. 87

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 87

9/4/2017 3:47:48 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Rafa’a bin Zaid alikuwa ni mmoja wa masahaba wapenzi wa Mtume. Katika moja ya vita yeye aliuawa kwa mshale. Watu wakaja kwa Mtume kutoa rambirambi za kifo cha Rafa’a na wakasema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Rafa’a alikuwa na bahati. Amekufa kifo cha kishahidi.” Kwa maneno haya, wao walitaka kumliwaza Mtume, lakini yeye hakuliwazika na akasema: “Kwa hakika sivyo. Kile kilemba ambacho alikichukua kutoka kwenye ngawira ya Khaybar bado ni muwako kama moto.” Licha ya ukweli kwamba Rafa’a aliuawa wakati akipigana jihadi, Mtume alimchukulia yeye kuwa ni mwenye dhambi kwa sababu alikuwa amechukua kitu kisicho na thamani kabisa toka kwenye mali ya umma, kwa uamuzi wake mwenyewe, ingawa alipaswa kusubiri hadi mali hiyo ilipogawanywa. Mwelekeo uliochukuliwa na Uislamu juu ya wanyang’anyi na walanguzi unaweza kuamuliwa kutokana na ukweli kwamba umeweka umuhimu wa hali ya juu kwenye maisha ya wanadamu. Mtu anayeishi tu ndio roho ya ulimwengu huu na Mwenyezi Mungu ameviumba vitu vyote kwa ajili yake. Katika mazingira haya ni vipi yeye atakavyonyimwa uhai na namna ya kuishi, na vipi itakavyowezekana kuwaruhusu baadhi ya watu kuwanyima watu wengine namna ya kuishi kwa sababu ya kuwa kwao ni wenye nguvu kuliko wao? Mbele ya macho ya Mtume wa Uislamu, utajiri unamaanisha kuhakikisha maisha ya raha kwa wanadamu wote. Kama vile tu ambavyo wanadamu wana haki sawa kuutumia mwanga wa jua na hewa, kwa namna hiyo hiyo wanayo haki sawa juu ya njia za maisha ambazo ni matokeo au matunda ya mwanga wa jua na hewa, na hakuna mwenye haki ya kuwanyima wengine manufaa haya. Mtume amesema: “Watu wote wanazo haki sawa juu ya mambo matatu; yaani, maji, mimea na moto.” Kwenye jamii yoyote ile mtu atakamokuwemo, haileti tofauti hata kidogo; kwani anayo haki ya kufaidi matunda ya kazi yake. Kila mtu katika udugu wa kibinadamu anawajibika kuwasaidia wengine, na wote kwa ujumla wao lazima wafanye juhudi za pamoja juu ya urekebishaji na uendelezaji wa mambo yao. Ni wajibu wa undugu wa kibinaadamu kutambua haki za mtu mmoja mmoja na kuwapa uhuru kamili wa kujipatia mahitaji yao ya maisha ili waweze kufanya kazi kulingana na uwezo wao na kufaidi matunda ya kazi zao. Ni lazima pia kwa wanajamii kusaidiana wao kwa wao na sio kufanya uhuru wao binafsi kuwa kikwazo katika njia yao. Na wala hairuhusiwi kwa undugu wa kibinaadamu kuwakandamiza watu binafsi, wala hairuhusiwi kwa watu binafsi kuudhuru huo undugu. 88

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 88

9/4/2017 3:47:48 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Ni lazima kwa hao watu binafsi kutilia maanani ustawi wa wengine kwa namna ile ile ambayo wanavyoujali ustawi wao wenyewe. Mtume amesema: “Kila mmoja wenu ni mchunga na kila mmoja wenu atakuja kuulizwa juu ya uchunga wake. Hakuna mwenye haki ya kuwadhuru wengine.” Mtume ameielezea hoja hii kwa mfano bora sana kama ilivyosimuliwa hapa chini: Baadhi ya watu walipanda mashua na kila mmoja wao akakalia nafasi yake. Wakati huo huo mmoja wao akanyanyuka kutoka kwenye kiti chake, akaokota shoka na akaanza kutoboa shimo katika ile nafasi ambayo alikuwa ameikalia yeye mwenyewe. Pale wenzake walipomuuliza kama alikuwa anataka kufanya nini, yeye alijibu kwamba kile kilikuwa ni kiti chake na alikuwa na uhuru wa kufanya hapo kile anachotaka. Papo hapo wengine wakamkamata mikono yake na hivyo wakamuokoa yeye na wao wenyewe vile vile kutokana na kuzama majini. Kama mtu huyo angeachwa tu mwenyewe, yeye na wale wengine pia wangezama kwenye maji. Ni wajibu wa kila mtu kuzuia maovu kwa namna yoyote yatakavyotendwa, na kufanya jitihada za kuhakikisha ustawi wa jamii unakuwepo. Mtume alisema: “Yeyote atakayeona jambo ovu likitendeka ni lazima alizuie.” Mtume wa Uislamu aliwaeleza wafuasi wake kila mara kwamba maadili mema yanatokana na mazoezi ya kivitendo na sio kwa mapendekezo ya maneno matupu na ushauri tu. Watu ni lazima waonyeshwe upole kwa vitendo na sio kwa maneno tu. Mtume hakujiweka mbali na watu, yeye alichanganyika nao kwa uhuru wa mapana, aliwasikiliza kwa utulivu yale waliyokuwa nayo ya kusema, na akawatumikia kama watu mashuhuri wanavyofanya. Abu Hurayra anasema: “Wakati mmoja niliandamana na Mtume kwenda kwenye mtaa wa maduka. Alinunua baadhi ya vitu kutoka kwa muuza duka na akamshauri kuchukua faida ya wastani katika mauzo ya bidhaa zake, na asiwe mwenye kuhodhi vitu, na sio kujipatia kitu chochote kwa njia zisizo halali, na sio kufikiri kwamba yeye anayo haki ya kuishi maisha ya starehe wakati wengine hawaishi hivyo.” Abu Hurayra akataka kuvibeba vile vitu vyote vilivyonunuliwa na Mtume, lakini yeye Mtume akamzuia kufanya hivyo, na akasema kwa tabasamu kubwa: “Viache hivi vitu. Mmiliki wao anayo haki ya kwanza ya kuvibeba vitu hivi.” Mtume wakati wote hakuwaamini wafalme na hakuwa akiwapa nafasi yoyote katika jamii, kwa sababu wao ni waovu na pia wanawadhulumu watu wengine. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:

89

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 89

9/4/2017 3:47:48 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

“Wakati wafalme wanapoingia kwenye mji wanauangamiza na kuwadhalilisha watu wake waungwana.” Moja ya matukio ambalo linaonyesha kwamba Mtume hakupenda fahari ni hili kwamba, ile siku ambayo mwanawe Ibrahim alifariki kulitokea kukamatwa kwa jua. Papo hapo watu wakasema kwamba na mbingu zilikuwa zinaomboleza kifo cha mwanawe Mtume. Wakati Mtume alipoyasikia maneno haya aliwahutubia watu kwa maneno haya yafuatayo: “Jua na mwezi ni ishara za Mwenyezi Mungu. Havikamatwi hivi kwa sababu ya kifo cha mtu yoyote.” Mafundisho ya Mtume yalikuwa ni pamoja na hili kwamba mtu anapaswa kuishi maisha yake katika namna nyepesi kiasi iwezekanavyo, na pasiwe na utatanishi au kanuni maalum ndani yake. Namna hii ya kuendesha maisha ndio msingi wa Uislamu. Kama matatizo ya Uislamu yakichunguzwa, inaonekana kwamba matatizo yote yameibuka kutoka kwenye chanzo kimoja ambacho ni cha kina sana na kinayagusa matatizo yote. Chanzo hicho ni kuuacha ule urahisi wa maisha, ambao haukutiwa dosari na hila, au udanganyifu, au kwa maneno mengine ‘uaminifu wa kimaisha.’ Wakati mmoja Mtume alimgonga bedui mmoja kwa fimbo yake bila kukusudia. Halafu yeye akasisitiza kwamba yule bedui naye ampige yeye kwa namna kama ile ile. Alipanda juu ya Mimbari na akasema: “Yeyote yule ambaye inawezekana nikawa nimempiga mgongoni mwake anapaswa kulipiza juu yangu na kama nimechukua mali ya mtu yeyote yule basi ajifidie mwenyewe kutoka kwenye mali yangu.” Mtume hakuwahi kumdhuru mtu yoyote yule kamwe. Hata hivyo, kile alichokisema kilikuwa ni uaminifu kwenye maisha ambao yeye aliudhihirisha kwa namna iliyo bora kabisa. Kama vile ambavyo maisha yake yalivyotakasika kutokana na unafiki na udhaifu, yalikuwa pia hayakutiwa dosari na majivuno. Alirekebisha viatu vyake yeye mwenyewe, na nguo zake, alikamua mwenyewe mbuzi wake, aliwasaidia watu wa familia yake katika shughuli za nyumbani, alibeba matofali pamoja na masahaba zake, na akafunga mawe kwenye tumbo lake kwa sababu ya njaa. Huu ulikuwa ni uaminifu kwenye maisha, ambao unathibitishwa na simulizi zote zilizosimuliwa hapo juu kuhusiana na Mtume. Na kuhusu watawala, wao wanapaswa 90

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 90

9/4/2017 3:47:48 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

kubeba majukumu au wajibu mwingi kiasi kwamba wanapaswa kuwa watumishi wa jamii na sio wafalme waonevu na waasi au wezi au wanyanganyi. Wasifu wa Mtume unaonyesha kwamba wakati mmoja, wakazi wa mahali fulani walilalamika kwamba gavana aliyewekwa hapo alikuwa akichukua zawadi na tunu kutoka kwa watu. Yeye akalichunguza jambo hilo, na ikaonekana kwamba malalamiko hayo yalikuwa ya kweli. Alikasirika sana juu ya hili, akamwita yule gavana na akamuuliza: “Kwa nini umechukua vitu ambavyo hukuwa na haki navyo?” Yule gavana akajibu: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Vile vilikuwa ni zawadi.” Mtume akasema: “Iwapo kama wewe ungekuwa umekaa nyumbani watu wangekuja kukupa wewe zawadi?” Kisha akamuamuru yule gavana kuiweka mali hiyo iliyohusika kwenye hazina ya Umma na pia akamuondoa kwenye kazi hiyo. Hivyo Mtume akawaelekeza watu wasiwe wanatoa hongo na rushwa, na pia akawaambia watumishi wasijihusishe katika vitendo vibaya kama hivyo. Kama vile mtu alivyoteuliwa kuwa mtawala wa watu, angepaswa kuwa kama baba kwao, na sio kama mnyang’anyi. Wakati Mtume alikasirika sana kwa gavana kupokea zawadi, inaweza kudhaniwa vizuri kabisa kwamba ni kiasi gani ambacho lazima atakuwa amekasirika pale utajiri ulipoporwa na haki za watu zilipoingiliwa visivyofaa. Katika Uislamu, mtawala anawekwa kwa uteuzi na chini ya mamlaka ya watu wenyewe,18 na atawatawala watu kulingana na matakwa yao wenyewe. 18

fumo huu wa serikali unakubaliwa na madhehebu zote za Kiislamu, pamoja na tofauti kwamba Shi’ah wanauM ona kwamba ni halali tu katika kipindi cha ghaibu ya Imamu-Zamaan (Imam wa wakati huu wa sasa). Vinginevyo Shi’ah wanatoa upendeleo kwa wale walioteuliwa au kuwekwa na Mtume na Maimamu. Lakini kwa mujibu wa Sunni, mara tu baada ya kifo cha Mtume, mfumo huu ukawa ndio mfumo wa sawasawa pekee wa serikali. Kwa mtazamo wa Shi’ah, tangu Ghaib Kuu ya Mahdi, Imam wa zama hizi mnamo mwaka wa 329 Hijiria, hakuna mtu maalum aliyechaguliwa kuwa mkuu na kiongozi wa Umma wa Kiislamu. Hii ndio sababu ya kwa nini katika taratibu na desturi zinazohusiana na uongozi katika kipindi hiki, ni zile sifa na tabia za kawaida zinazohitajika kiongozi kuwa nazo ndio zinazotajwa. Hii inaonyesha kwamba ni juu ya watu wenyewe kuchagua mtu kama kiongozi wao, akiwa na sifa na tabia zifuatazo: • Imani juu ya Mwenyezi Mungu, wahyi Wake na mafundisho ya Mtume Wake. • Uadilifu na uaminifu kwenye sheria za Kiislamu, na moyo wa dhati kuhusu utekelezaji wake. • Ujuzi na elimu ya kutosha, inayolingana na kufaa kwa nafasi yake hiyo mashuhuri. Uwezo wa kutosha kwa ajili ya kushika nafasi kama hiyo na kuwa safi kutokana na kila mapungufu yasiyoendana na uongozi wa Kiislamu. – Kiwango cha hali yake ya maisha kiwe sawa na kile cha watu wa kipato cha chini kabisa. • Kuhusiana na hili, kuna maneno ya kutosha kwenye hotuba za Ali (a.s.) na katika nyaraka alizozituma kwa maafisa wake. Katika idadi ya nyaraka hizo imesisitizwa kwamba afisa wa utawala anapaswa kuwa huru na tamaa ya fedha, ujinga wa kutojua mambo, uwezo mdogo, vitendo vya kijeuri, woga, rushwa, na uvunjaji wa amri za kisheria na desturi na asiwe na hatia ya umwagaji damu. (Kwa maelezo zaidi tazama: “Philosophy of Islam” ISP,1982) 91

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 91

9/4/2017 3:47:48 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Wakati wote anakuwa na shauku kuhusu ustawi wa watu wake. Uislamu umefanya ni lazima kwa watawala kushauriana na raia zao katika masuala muhimu, ambayo uvumbuzi wake wa sawa unakuwa mgumu. Kama Qur’ani Tukufu inavyosema: “Wanafanya mambo yao kwa kushauriana kwa pamoja.” Khalifa hakupewa haki ya kutwaa mali za watu bila ridhaa zao, wala hana uwezo wa kutengeneza sheria yoyote, kwa sababu sheria zote za lazima ni zile ambazo tayari zilikuwa zimekwishawekwa na Uislamu, na yeye amepewa haki tu ya kuyalinda maisha, mali na heshima ya raia. Hairuhusiwi kwa mtawala kutowajali watu wanaokandamizwa na kuonewa na asizilinde haki zao kutoka kwa wanaopituka mipaka na madhalimu. Haifai vile vile kwa mtawala kungojea mpaka yule mtu aliyeonewa amjie na malalamiko. Kinyume chake ni wajibu wake kwenda kumsaidia yule mtu ambaye amekandamizwa yeye mwenyewe binafsi, kwa sababu inawezekana kwamba yule aliyekandamizwa akawaasiwe na ujasiri wa kulalamika au anaweza asipate njia ya kumfikia huyo mtawala. Uislamu umemlaumu sana mtu aliyeonewa, ambaye anauvumilia kimya kimya uonevu na udhalilishwaji huo na umesema kwamba mtu kama huyo ni mkatili juu ya nafsi yake yeye mwenyewe. Uislamu umepongeza juhudi zake mtu, zile za kulinda maisha, mali na heshima yake. Mtume amesema kwamba: “Mtu ambaye anayatoa maisha yake kupinga maonevu na udhalimu ni shahidi.” Mtume vile vile amesema: “Kama watu watamuona dhalimu akitenda maonevu na wasimzuie kufanya hivyo, kuna uwezekano kwamba wote wanaweza wakastahili adhabu ya ki-ungu.” Uislamu umewachukulia wanadamu wote kama ndugu wa kila mmoja wao. Umefanya mapambano vile vile dhidi ya ushabiki wa kidini. Qur’ani tukufu inasema: “Hakuna kulazimishana katika suala la imani.” Umeweka upinzani wa hali ya juu kabisa dhidi ya upendeleo na ubaguzi wa kiukoo au kabila. Mtume amesema: “Mwanadamu ni ndugu wa mwanadamu, awe amelitaka hilo au hakutaka.” Qur’ani Tukufu inasema: “Tumeweka heshima juu ya wanadamu, tukawapatia njia za usafiri juu ya ardhi na majini, tukawapa vitu safi na halali vya kula na tukawapa ubora juu ya viumbe wengine wengi.” Kila wakati Mtume alipowahutubia watu, hotuba zake ziliwalenga wanadamu wote, wawe ni Waarabu au wasio Waarabu, na ama wawe weupe, wekundu au weusi. 92

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 92

9/4/2017 3:47:48 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Yeye aliwahutubia kama ndugu, wapole na wenye huruma wa kila mmoja wao, waliounganishwa pamoja kwa uhusiano wa kibinadamu na bila kujali utaifa wao na kadhalika. Kama ilikuwepo tofauti kati yao, ilikuwa ni katika msingi wa matendo mema na haikuwa kwa sababu ya rangi au utaifa. Mtume alisema: “Enyi watu! Mola wenu ni Mmoja. Vile vile mnaye jadi wa pamoja Adam. Hakuna Mwarabu ambaye ni bora juu ya asiyekuwa Mwarabu, na hakuna asiyekuwa Mwarabu ambaye ni bora kuliko Mwarabu, na vivyo hivyo hakuna mwenye rangi nyekundu aliyebora kuliko mtu mweupe na hakuna mwenye rangi nyeupe aliye bora kuliko mwekundu. Na kama mtu atakuwa na ubora juu ya wengine ni kwa sababu ya uchamungu wake. Wale ambao mpo hapa mnapaswa kuufikisha ujumbe huu kwa wale ambao hawapo hapa.” Mtawala Ni Mmoja Kati Ya Watu Kabla Ali hajaupata ukhalifa ilielekea kwamba ile serikali ya Bani Umayyah ingeweza kubadilishwa na kuingia kwenye ufalme – bali hasa ilikuwa tayari imekwisha kugeuzwa kuwa hivyo. Watawala na watu wengine waliokuwa kileleni mwa mambo walikuwa wenye mtazamo kwamba ukhalifa ulikuwa ni haki yao maalum, na ni wao tu waliokuwa na haki juu yake kwa sababu ya kutokana kwao na familia ya kiungwana. Ili kutilia nguvu mamlaka yao na kuanzisha serikali imara walivichukulia vitendo vyote visivyokuwa halali kama vile ubaguzi wa kikabila, uundaji wa vikundi, rushwa na kadhalika kuwa ni halali. Kulingana na wao, mtawala alikuwa ni bwana wa maisha, mali na heshima ya wale wanaotawaliwa na anaweza kuwanyonya kwa namna anavyotaka, bila ya wale wanaoonewa kuwa na haki ya kulalamika. Waliwaona watu wa chini kama wanyama wa miguu minne ambao wangeweza kuwabebesha mizigo mizito kabisa na kuwapiga kwa kiasi kama walivyopenda. Katika kipindi cha Uthman, magavana wa Bani Umayyah walipata fursa ya utawala wa kidikteta na waliutumia kwa kiasi cha kuridhisha nyoyo zao. Walijitahidi kuimarisha utawala wa ki-Bani Umayyah katika sehemu zote za nchi za Kiislamu. Waliwahonga masheikh na watu maarufu wa makabila ya Kiarabu kwa wingi sana ili kupata uungaji mkono wao. Walitoa uhuru kamili vile vile kwa watu waliokuwa katika nafasi ya kuweza kuwakandamiza watu wa chini katika namna yoyote waliyoitaka wao. 93

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 93

9/4/2017 3:47:48 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Vile vile waliyanunua majeshi ya kivita kwa kuwapa utajiri uliokithiri na kuwaahidi vyeo vya juu kabisa. Na kwa kweli watu hawakuweza kuwapinga wao kwa sababu kila aliyekuwa upande wao aliheshimiwa, na yeyote yule aliyewapinga alishutumiwa na kudhalilishwa. Kwa kifupi, serikali hiyo iliwekwa juu ya kanuni mpya kabisa. Haya yalifanywa na Bani Umayyah ambao nyoyo zao hazikuwa zimeukubali Uislamu kwa uaminifu haswa. Walisilimu kutokana na hofu na wakaendelea kubaki ndani ya mipaka yake kwa sababu ya hamu yao juu ya utajiri. Historia inaonyesha kwamba watu hawa walibakia, baada ya kusilimu, kama walivyokuwa wakati wa ujahilia. Wale masahaba mashuhuri wa Mtume ambao waliyasimamia mambo hapo kabla waliondolewa na kudhalilishwa.19 Walichukuliwa kama wasiokuwa na umuhimu sasa. Kama mambo yalivyokuwa, wale masahaba ambao walishirikiana na Bani Umayyah katika kuangamiza haki za Waislamu na kuimarisha serikali ya Bani Umayyah walitukuzwa. Watu hawa walizikabidhi funguo za hazina ya ummah na upanga au nyundo ya serikali kwa Bani 19

I likuwa ni jitihada ya dhati kabisa na tamaa ya moyoni hasa ya khalifa Uthman kwamba uleutawala wa kidikteta wa serikali ya Bani Umayyah uweze kusimama kwa uimara zaidi katika mijiyote ya Kiislamu na hakubakisha jitihada yoyote katika hili. Siku mbili au tatu baada ya Uthmankuwa khalifa, Abu Sufyan alikuja kumpongeza yeye. Kwa vile upendeleo wa Uthman kwa jamaazake ulikuwa unajulikana sana, Abu Sufyan alimwambia yale yaliyokuwa moyoni mwake akisema:“Chezeni na ukhalifa kama mpira na uwafanye Bani Umayyah kuwa ndio nguzo zake.” I ngawa Uthman alimshutumu kwa wakati ule, lakini kuanzia siku ile ile hasa aliyafanya maneno yaAbu Sufyan kuwa ndio wito wake na akakabidhi ugavana wa miji yote mikubwa kwa vijana wadogo wa ki-Bani Umayyah na wasiokuwa na ujuzi. Watu hawa hawakuwa amma na elimu wala tabianjema. Kwa kufanya uteuzi kama huo, Uthman alifungua milango ya fitna na machafuko, na akawaametoa njia ya kuiangamiza jamii ya Kiislamu na vile vile kifo chake yeye mwenyewe. llamah Abu Amr, yule mwandishi wa Isti’ab anasema kwamba wakati mmoja Shabil ibn Khalidaliwasili A wakati Uthman alikuwa amekaa pamoja na watu wengine wa Bani Umayyah tu. Shabilakasema: “Enyi Maquraishi! Ni nini kimekufikeni ninyi? Hakuna kijana ambaye mnayeweza kumtukuza aliyebakia pamoja nanyi? Hivi hakuna miongoni mwenu masikini ambaye mngetaka kumfanya awe tajiri? Hakuna miongoni mwenu mtu asiyejulikana ambaye mngeweza kumfanya ajulikane? Kwa nini mmemfanya Abu Musa Ash’ari kuwa gavana wa Iraqi, na mkampa lile jimbokuwa kama miliki yake huru ambamo anachuma kiasi kikubwa mno?” Papo hapo Uthman akaulizakama ni nani angeweza kuteuliwa kama gavana kuchukua nafasi ya Abu Musa Ash’ari. Walewaliokuwepo pale wakapendekeza jina la Abdullah ibn Asmir, binamu yake Uthman. Kwa hiyoyeye akamuuzulu Abu Musa na akamuweka Abdullah katika nafasi yake, ingawa alikuwa na umriwa miaka kumi na sita tu. Vijana hao wa Bani Umayyah hawakujali kile walichokifanya au kusemawatu. Uthman hakutilia maanani malalamiko yoyote dhidi ya vijana hawa wala hakuweka umuhimuwa makaripio kwa ajili hiyo. Mmoja wa vijana hawa alikuwa ni Sa’id ibn Aas, gavana wa Kufa.Alikuwa ni mtu mkaidi na mpenda starehe ambaye aliuambia mkusanyiko wa watu kutoka kwenyemimbari: “Hizi ardhi za Iraqi ni mabustani ya vijana wa kiQuraishi.” Hawa ndio vijana ambao kwamba Mtume alikuwa amekwishasema: “Wafuasi wangu watakujakuangamizwa mikononi mwa vijana wapumbavu wa ki-Quraishi.” (Sahih Bukhari, Kitab al-Fitan, sehemu ya 10, uk. 146 na Mustadrak, Juz. 4, uk. 470.) 94

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 94

9/4/2017 3:47:49 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Umayyah ili kuwafanya watu wawe watiifu kwao. Umma pia uligawanywa katika makundi mawili. Kundi moja lilikuwa na watu wachamungu ambao walikuwa ndio wale walioitakia mema jamii. Wao walitaka kiongozi muadilifu, ingawa asingeweka utajiri juu yao na asingewaachia kupora mali ya hazina ya ummah. Kundi la pili lilikuwa limekengeuka kutoka kwenye njia ya haki. Wao walitaka kuuza imani zao kwa Bani Umayyah kwa thamani iliyopangwa na wao. Kama Bani Umayyah walilipa kiwango hicho basi ilikuwa kheri, vinginevyo walidhamiria kufanya ajizi mpaka thamani waliyoitaka wao ilipolipwa. Wakati Amirul-Mu’minin Ali alipoupata ukhalifa hali ya mambo ilikuwa ya wasiwasi. Watu walikuwa wamegawanyika katika makundi mawili. Wale watu waliohusika na kundi mojawapo kati ya hayo walikuwa tayari kutoa maisha yao katika kuwaunga mkono Maimam wachamungu na waadilifu. Lile kundi jingine liliwaunga mkono Bani Umayyah na wakajitahidi kuiimarisha serikali na ufalme wao. Bani Umayyah walikuwa vile vile wakijitahidi kwa miaka mingi kusimamisha utawala wao katika hali ya kudumu. Wao walijua kwamba mpango wao ulikuwa umezongwa na matatizo, lakini walikuwa wamedhamiria kufanikiwa na waliamua kumfuta yeyote ambaye aliwawekea kikwazo, ingawaje angeweza kuwa mtu wa kidini mashuhuri na anayeheshimiwa sana. Ali hakuwa na mapenzi sana ya kuwa khalifa. Alimsaidia Abu Bakr na Umar pale, na kila walipokabiliwa na tatizo.20 20

i kweli kwamba Amirul-Mu’minin hakuwa na tamaa sana juu ya serikali ile ya kidunia. Kama aliupendaukhalN ifa ilikuwa ni kwa sababu kwamba Uislamu wa Mtume haukuweza kulinganiwa na kuenezwa na yeyoteisipokuwa yeye. Hii ilikuwa hivyo kwa sababu yeye alikuwa amelelewa kwenye mapaja ya Mtume na alikuwandio hazina ya hekima na elimu yake Mtume. Mtume alikuwa amemshibisha na elimu katika namna ile ileambamo ndege anamlisha kinda wake. Tokea siku ile hasa ya kuzaliwa kwake, hadi kifo cha Mtume, yeyealikuwa hakutenganishwa na Mtume. Muda wake wote ulitumika katika muambatano na Mtume. Hakunaaliyeijua Sunnah ya Mtume vizuri zaidi kuliko alivyokuwa yeye. eye alikuwa ni picha halisi haswa ya mwenendo na tabia za Mtume na mrithi wa mafanikio yake yote. Huu ni Y ukweli ambao ulikuwa umekubaliwa, siotu na marafiki zake bali pia hata na maadui zake, na hata wale waliokuwa wameichukua nafasi ya ukhalifa.Mwenyezi Mungu alitaka, na hata Mtume vile vile alipenda kwamba baada yake Ali apasike kuwa kilelenimwa hali ya mambo, kwa sababu ni yeye tu aliyekuwa na uwezo wa kutekeleza na kupanua dini ya Uislamukatika namna aliyoipenda Mwenyezi Mungu na Mtume Wake.Na kuhusu suala la kwamba ama alipinga au laa; kwa wengine kuutwaa ukhalifa, kurasa za Nahjul-Balaghahna vile vile historia inaonyesha kwamba alipinga dhidi ya hili katika nyakati zote na aliwasilisha hoja zake.Yeye alisema: “Mimi ninastahiki hicho kiapo cha utii zaidi kuliko ninyi mnavyostahili. Mimi sitatoa kiapo chautii kwenu bali ninyi mnapaswa kutoa kiapo hicho katika stahiki yangu. Mmeitwaa kazi hiyo kwa ubora juu yaAnsari kwa msingi wa ujamaa wenu kwa Mtume, na sasa mmedhamiria kuunyang’anya kutoka kwa watu waNyumba yake. Ninyi hamkutoa hoja hii mbele ya Ansari; kwamba mlikuwa na haki zaidi kwenye ukhalifa kwasababu Muhammad alikuwa ni mmoja wenu. Na waliikubali hoja hii, waliisalimisha kazi hii kwenu, nawakakuacheni ninyi kutwaa serikali. Sasa, mimi ninaitoa hoja hiyo hiyo mbele yenu ambayo mliitangulizadhidi ya Ansari. Sisi ndio warithi 95

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 95

9/4/2017 3:47:49 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Kila mara ule ukhalifa wa Kiislamu ulipokabiliwa na tatizo, Ali alilitatua. Yeye alionyesha huruma hata kwa Uthman, na kamwe hakulalamika dhidi ya utwaaji ukhalifa wa Uthman badala yake yeye mwenyewe. Kitu pekee ambacho kwamba alikuwa na shauku sana nacho kilikuwa ni usimamishwaji wa haki na uadilifu. Watu walimsihi sana kuukubali ukhalifa lakini yeye hakudhihirisha shauku juu yake. Historia inaonyesha; na kauli zake mwenyewe pia zinapatikana kuonyesha kwamba wakati, baada ya mauaji ya Uthman, watu walimjia kwa makundi na kumuomba ashike ukhalifa, yeye alisema: “Niachemi mimi na tafuteni mtu mwingine kwa kazi hiyo. Kama mtaniacha nilivyo, nitakuwa mwanajamii kama ninyi, na nitakuwa mwangalifu zaidi na mtiifu kuliko ninyi kwa huyo mtu mtakayemteua kama khalifa. Nitakuwa ni mwenye manufaa kwenu zaidi katika nafasi ya mshauri kuliko katika ile ya khalifa.” wa Muhammad katika wakati wa uhai wake na baada ya kifo chake vile vile.Endapo, kwa hiyo, mnamuamini Muhammad na Uislamu, ni lazima mfanye uadilifu kwetu, ambao kushindwakwake mtakuwa na hatia ya uonevu wa makusudi.”Utoaji msaada wa Ali kwa wale makhalifa watatu katika nyakati za matatizo ni ushahidi wa wazi wa uungwanana uadilifu wa hali ya juu. Ubora wa juu wa mtu ni kwamba pale panapokuwa na mgogoro baina ya maslahibinafsi na maslahi ya jamii, yeye apendelee ustawi wa jamii kuliko maslahi yake mwenyewe. Ubora mwinginemaarufu wa mwanadamu ni kwamba anapaswa kuwa mkweli na mwaminifu hata katika ushughulikaji wakena maadui zake. Kuwekea maanani maslahi binafsi katika masuala yote, na kuathiriwa na mapenzi na machukizo binafsinyakati zote ni sifa za mtu duni ambaye matendo yake yanatawaliwa na silika za kinyama badala ya maadiliya kibinadamu. Ni ukweli kwamba wengi wa wanadamu wakati wote wamejitahidi kusimamia maslahi binafsi, lakini kama vitendo vya idadi kubwa ya watu vitakubaliwa kuwa ndio kigezo, kila aina ya ufisadi itageukakuwa ndio ustaarabu na utamaduni, na kila sifa njema itakuwa uovu na udhaifu au upungufu.Hata hivyo, ni jambo la kusikitisha kwamba watu wamekuwa wakiangalia utaratibu wa matendo ya watumashuhuri kwa mujibu wa fikira zao wenyewe, na wamekuwa wakifanya maamuzi potovu.Ali ibn Abi Talib alikuwa ni kielelezo kamilifu cha mafundisho ya Kiislamu katika ulimwengu wa Kiislamu,na mfano bora wa sifa za kibinadamu na ukamilifu. Tabia zake zilikuwa zimejaa sifa zote zile zinazochukuliwa kuwa ni kiini cha ukamilifu wa kibinadamu, na mwelekeo maarufu kabisa wa silika yake ulikuwa ni kwamba yeye hakuruhusu kwamwe tofauti za kibinafsi, ubinafsi au uadui kuingilia kati masuala ya Kiislamu na yakijumla cha watu, wala hakuruhusu masilahi yake binafsi na hisia zake kupuuza unyofu na uadilifu. akazi wa ulimwengu ambao wamekuwa na mazoea; kwa sababu ya tabia zao wenyewe, na vile vile hao waitW wao viongozi wao, kuweka mbele mwelekeo wa maslahi binafsi katika kila kitu, wanapata uamuzi kutokakwenye tabia za Ali kwamba hakuwa na tofauti binafsi na mtu yoyote, na alionyesha upendo mkubwa na urafiki kwa wote katika akili yake. Hata hivyo, kama mtu atatafakari kidogo kwa utulivu wa mawazo, inakuja kujulikana kwamba kutoa mwongozo sahihi kwa wengine kwa ajili ya ustawi wa jamii, licha ya tofauti binafsi, ndiosifa kuu ya kibinadamu ambayo inaweza kuonekana wazi wazi katika tabia ya Ali. Kawaida hii ya AmirulMu’minin inaakisiwa kwa miundo mbalimbali katika matukio ya maisha yake ambayo kwayo zimejaa kurasaza historia. Watawala ambao walijitwalia ukhalifa wakipuuza sifa za Ali na haki yake kwenye cheo hicho, nawakadai kwamba wao ndio watu pekee ambao wangeweza kusimamia ustawi wa jamii, walimtaka ushauripale, na kila walipokuwa wamekabiliwa na tatizo na katika kila tukio kama hilo, yeye aliwapa ushauri borakabisa uliofaa kwenye mazingira ya wakati huo. 96

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 96

9/4/2017 3:47:49 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Katika siku ile alikuwa hakuridhiana na kuukubali ukhalifa kwani kwa kuzingatia kwake ya mbeleni zaidi, aliweza kuona hadi mwisho wa hali ya baadaye. Kama yeye alikuwa mdai ukhalifa hapo mapema kabla, haikuwa ni kwa sababu kwamba alitamani sana kuwa mtawala. Kinyume chake; alichokuwa amekitamani yeye ni kwamba Waislamu waweze kuyaendeleza, ndani yao wenyewe, yale maadili na ubora ambao Mtume alitaka kuyakazia ndani yao. Na kama alikataa kukubali kazi hiyo katika hatua ile (yaani baada ya kuuawa kwa Uthman) ilikuwa ni kwa sababu, kutokana na sera za watawala waliotangulia, desturi na tabia za Waislamu zilikuwa tayari zimeharibiwa na namna ya fikra zao ilikuwa imebadilika. Ule ufalme uliokuwa umeanzishwa kwa jina la dola ya Kiislamu ulikuwa umeumbwa katika mamlaka ya kidunia, na ulibeba zaidi dalili za udikteta wa Kaisari na Kisra. Lengo la Ali lilitofautiana na matakwa ya watu. Sio Ali aliyeweza kujishusha mbele ya matakwa ya watu, wala watu kuweza kukubali Ali afanikishe yale malengo aliyokuwa nayo mawazoni mwake. Yeye mwenyewe anaionyesha picha ya hali ya mambo ya kipindi kile kwa maneno haya yafuatayo: “Wakati sasa ni kinyume kabisa, na usiopendeza. Siku hizi mtu muadilifu anaonekana kuwa muovu, na ukaidi wa madhalimu unaongezeka. Hii ni kwa sababu anga limefunikwa na mawingu meusi na ishara za njia zimefutiliwa mbali. Watu wameingiwa na mashaka na kupenda anasa. Wanayo masikio lakini ni viziwi. Wanayo macho lakini ni vipofu. Hawako imara katika medani ya vita, wala sio wakutumainiwa katika mazingira magumu.� Ali alijua vizuri kabisa kwamba kama angeyakubali maombi ya watu na akauchukua wajibu wa kazi ya ukhalifa, wao wasingeweza kuvumilia ile namna ambamo yeye angeendesha utawala wake, na wasingezitii amri zake ila kama angekuwa mkali kwao. Hizi zilikuwa ndio hali ambazo Ali alikuwa akabiliane nazo baada kuuawa kwa Uthman. Wale watu mashuhuri na wale wa chini vile vile walikusanyika nje ya mlango wa nyumba yake tena na tena, na wakisisitiza juu ya yeye kukubali kupokea kiapo cha utii kutoka kwao. Hata hivyo, licha ya ukweli kwamba aliwazia kila la kheri moyoni mwake juu ya watu, bado alisita kukubali viapo vya utiifu kutoka kwao. Kulikuwepo, hata hivyo, na jambo moja ambalo lilimlazimisha yeye kufikiria juu ya kukubali maombi yao. Waislamu walikuwa wakisisitiza sana juu ya yeye kuikuba97

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 97

9/4/2017 3:47:49 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

li kazi hiyo, ambako kulimaanisha kwamba wajibu ulikuwa unawekwa mikononi mwao wa kuwaongoza wale ambao walikuwa na haja ya mabadiliko na mwongozo kutoka kwake. Zaidi ya hayo, kwa wakati ule usawa na uadilifu wa kijamii ulikuwa katika hatari. Watu waliokuwa kwenye madaraka walikuwa wakiziingilia haki za wanyonge kinyume cha uhalali; na maisha na mali, na heshima za watu wa chini hazikuwa na thamani yoyote. Ali hakuweza kuvumilia kwamba akae kimya ndani ya nyumba yake wakati raia masikini walikuwa wanaathiriwa na udhalimu. Mtu jasiri na imara kama Ali asingeweza kuwaachia Waislamu kuangukia mawindoni mwa ukatili wa mbwa mwitu wa Bani Umayyah na yeye abakie kuwa kimya tu. Kama asingetoka kuwaokoa Waislamu katika wakati ule mgumu angechukuliwa kuwa kama mwoga na sio yule yule jasiri na shujaa, kama anavyojulikana ndani ya historia. Yeye mwenyewe anasema: “Nilikuwa na wasiwasi na hofu isije wale watu wapumbavu na waovu wakaja kuwa watawala wa umma huu, na wakafanya mali ya Mwenyezi Mungu kuwa ni kitu chao cha kuchezea, na viumbe wa Mwenyezi Mungu kuwa ni watumwa wao na wakapigana na wale watu waadilifu na kuwafanya madhalimu kuwa ndio wasaidizi wao.” Kutokana na sababu hizi; alilichukulia kuwa ni jambo la wajibu juu yake kukubali kiapo cha utii ijapokuwa watu wengi sana waadilifu walijiona wao wenyewe kutokuwa na uwezo wa kuuhimili mzigo wa ukhalifa. Ali aliyachukia sana maisha ya kujitenga. Isipokuwa pale ilipokuwa inawezekana kuwatumikia watu kwa kubakia katika faragha, ilikuwa haikubaliki kwake kuutumia muda wake faraghani. Mtu anayetelekeza kuwatumikia viumbe wa Mwenyezi Mungu, pamoja na kuwa yeye yuko kwenye nafasi nzuri ya kufanya hivyo, anaiporomosha imani yake na dunia yake vile vile. Ali alikubali ukhalifa kwa dhamira thabiti na aliliona ni katika maslahi ya Waislamu kwamba anapaswa kuitwaa nafasi hiyo. Ili kuielewa namna ya utawala wa Ali na sera zake za kiuchumi na fedha, ni muhimu kujua ni jinsi gani Ali mwenyewe alivyoueleza ukhalifa na madaraka, ni nafasi gani ukhalifa ulikuwa nayo machoni mwake kutokana na mtazamo wa kidini, na manufaa gani uliyabeba mikononi mwake huo. Akiwa anawahutubia watu wakati wa kupokea kiapo cha utii kutoka kwao, Ali alisema akiwaambia: “Enyi watu! Mimi ni mmoja wenu. Ninazo haki zile zile ambazo mnazo ninyi. Majukumu yangu pia ni sawasawa na yenu. Hakuna kitu kinachoweza kubatilisha ukweli. (yaani mtawala au khalifa hawezi kubadilisha amri za Mwenyezi Mungu).”

98

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 98

9/4/2017 3:47:49 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Katika hotuba yake nyingine, yeye amesema: “Namuapa Mola Wangu kwamba kwanza kabisa mimi mwenyewe ninazitii zile amri za Mwenyezi Mungu ambazo ninawalinganieni ninyi kuzitii, na mimi binafsi ninajiepusha kwanza kutokana na yale mambo, ambayo kwayo ninakuagizeni kujiepusha nayo.” Kwa msingi huu, mtawala na khalifa sio wa kutiiwa katika nafasi yake binafsi. Ni lazima kumtii yeye kwa sababu anatekeleza usawa na uadilifu na kanuni za Shari’ah. Ukhalifa haumpi haki mtawala na khalifa ya kujitwalia mwenyewe kiasi chochote cha mali ya hazina ya umma kama anavyotaka, na kukitumia yeye mwenyewe au kukitoa kwa marafiki zake, washirika na jamaa zake. Kinyume chake, lengo la taasisi ya ukhalifa ni kwamba uadilifu lazima utekelezwe. Mtawala sharti atoe utendaji wa sawa kwa kila mtu, sharti azijali juhudi za mtu, ambaye analingania dini ya Mungu na kuutumikia umma, sharti akataze ulimbikizaji, na azuie uonevu na ukandamizaji, na sharti asikengeuke kutoka kwenye haki katika mazingira yoyote yale. Anapaswa asiache mpango wake ingawaje wale waovu na wakatili hawapendi mwenendo wa haki na wanaweza wakayaandama maisha yake. Ni wajibu wake pia kuwajulisha watu zile kanuni za uadilifu na kuzuia mkengeuko wao katika kanuni hizo. Ali aliandika kwa mmoja wa magavana wake kama ifuatavyo: “Kukamata kwako wadhifa huu hakukupi wewe haki ya kulimbikiza mali au kulipiza kisasi kutoka kwa mtu yoyote. Wajibu wako pekee ni kwamba ni sharti uangamize udanganyifu na uhuishe haki na ukweli.” Machoni kwa Ali ibn Abi Talib utawala na ukhalifa havikuwa na maana kwamba yule mtawala akalie juu ya kiti hicho cha heshima ili aimarishe mamlaka yake na kuifanya nafasi yake hiyo kama nyenzo ya kuwatia watu utumwani. Yeye anasema: “Ukarimu na urahimu ni chanzo kikuu kabisa cha mapenzi na upendo kuliko undugu wa nasaba na ujamaa. Hakuna umaarufu mkubwa kama unyeyekevu na hakuna manufaa kama elimu.” Ukhalifa hauna maana kwamba watu sharti watiishwe kwa ncha ya upanga, na kwa njia ya umwagaji damu na mabavu, au kwamba wao wamtii khalifa kwa sababu ya hofu au tamaa ya mali. Ali alikuwa ni mtu ambaye hakuwa akimwabudu Mwenyezi Mungu kwa sababu ya kutamani msamaha au kwa sababu aliogopa adhabu. Kinyume chake, yeye alimwabudu Mwenyezi Mungu kwa sababu Yeye alistahili kuabudiwa. Alipendelea kwamba watu wangemtii khalifa kwa sababu ya kustahili kwake kutiiwa na sio kwa sababu ya hofu au uroho wa mali.

99

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 99

9/4/2017 3:47:49 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Sasa kuhusiana na kupata ushauri kutoka kwa wengine, Amirul-Mu’minin amesema: “Mtu anayekabiliana na maoni mengi tofauti hutambua yale madoa ya makosa na mapungufu.” Mtu anayeyatambua makosa hufikia kwenye ukweli na vitendo sahihi. Yale maoni ya watu ni mambo muhimu sana ambayo yananufaisha nchi na watu vile vile, na shughuli zinaendeshwa katika namna ambayo kwamba hailazimu kuwa na aibu na masikitiko. Ali analithibitisha hili kwa maneno ya wazi kabisa na anasema: “Usahihi hauwezi kupatikana kwa kutelekeza mashauriano.” Haimpasi mtawala kuacha milango yake ikiwa imefungwa mbele za watu na kujaribu kufanikisha lengo fulani kwa kuwaacha watu gizani. Amirul-Mu’minin anatoa tahadhari kwenye nukta hii kwa kusema: “Jipatieni mwanga kutoka kwenye taa inayowaka.” Kwa mujibu wa Amirul-Mu’minin, haifai kwa khalifa kutafuta kuweka umbali kutokana nao, kuwa na kiburi na majivuno, au kuyapuuza mahitaji ya watu. Ukhalifa ni njia ya mtawala kushirikiana na watu, kuonyesha huruma kwao na kushughulika nao kwa unyenyekevu. Kama mtawala anabakia mbali na watu hakuna hata kimoja cha visingizio au hoja itakayoweza kukubaliwa. Kama watu wamekerwa na mtawala kwa sababu ya jambo lolote kama hilo wao watakuwa ni usumbuvu juu yake katika namna ile ile ambamo utawala wake utakuwa ni udhia kwao, kwa sababu watu watashughulika naye kama yeye anavyoshughulika nao. AmirulMu’minin anasema kuhusu jambo hili: “Nyoyo za raia ni hazina ya mtawala. Atapata kutoka humo kile anachokiweka, imma kiwe ni usawa na uadilifu au ukatili na udhalimu.” Machoni kwa Ali ukhalifa haukuwekwa juu ya msingi wa moyo wa ushabiki wa chama au upendeleo wa familia ambazo ni sifa mbaya sana. Aliuchukulia ukhalifa kujumuisha pamoja na sifa njema, vitendo vya kiuchamungu, kugawa uadilifu kwa watu na kujiepusha na udhalimu na fitna. Kwa hali yoyote; kwa mujibu wa Ali, utawala haukukusudiwa kwa wale watu ambao kuhusu wao alisema: “Ikiwa watu hawa watakuwa ndio watawala wenu watakuwa kama Kaisari na Kisra.” Wala hawakustahili kuwa watawala, wale watu wadanganyifu na waonevu. Kwa kuyaweka maanani mambo yote haya, Ali aliukubali ukhalifa kwa dhamira imara ya kusimamisha ukweli na kuangamiza udanganyifu na akishindwa hivyo basi kutoa muhanga maisha yake mwenyewe hasa. Ilikuwa ni kwa sababu hii kwamba 100

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 100

9/4/2017 3:47:49 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

yeye alisisitiza kuwa watu waangalie vitendo vya watawala wao na wasikubali mtawala ambaye hakuthibitika kuwa mtumishi wa umma. Yeye aliwashauri pia kuonyesha kutoridhika kwao katika vitendo vibaya vya mtawala au kuvikubali kwa upendeleo tu. Yeye alisema: “Hivi, hamjisikii kukerwa na kuchukizwa kama watu wapumbavu wanakuwa ndio watawala wenu na matokeo yake ninyi mnadhalilishwa na kuteswa na kuangamizwa?” Mbele ya macho yake yeye, kukerwa kwa ukatili na uonevu kulikuwa ni jambo lenye muhimu kama lilivyo la kukaribisha usawa na uadilifu. Yeye aliuheshimu uhuru binafsi wa watu mmoja mmoja na pia alitilia maanani haki za umma. Na kuhusu wale ambao hawakutoa kiapo cha utii kwake yeye alisema: “Haidhuru kama wao hawatachukua kiapo cha utii. Hata hivyo, wao wakae ndani ya nyumba zao na wasije wakaingilia katika mambo ya umma.” Sa’d ibn Abi Waqqas ambaye alikuwa mjumbe wa lile Baraza la Ushauri alikataa kutoa kiapo cha utii kwa Ali. Yeye Ali hakumlazimisha kuchukua kiapo cha utii na akamwacha huru. Sa’d alikuwa amesema: “Huna haja ya kuwa na wasiwasi na mimi. Sitasimama kuasi dhidi yako.” Vivyo hivyo, Abdullah ibn Umar hakutoa kiapo cha utii. Ali alimtaka atoe mdhamini, ambaye atatoa uhakikisho kwamba yeye hatasababisha vurugu ya aina yoyote, lakini yeye alikataa kufanya hivyo. Hapo Ali akamwambia: “Umekuwa huna adabu nzuri tangu utotoni mwako, na mimi ninakufahamu wewe tangu siku ya kwanza.” Halafu akawageukia watu na akasema: “Mwacheni na yeye vilevile. Ninahakikisha kwamba yeye hatasababisha vurugu yoyote ile.” Walikuwepo baadhi ya watu pia ambao walibakia wamejificha ndani nyumba zao na hawakupenda kuchukua kiapo cha utii. Ali alisema kuwahusu wao: “Mimi pia sina haja na wale watu ambao hawana haja na mimi.” Aliwaacha huru kwa masharti kwamba hawatakuja kusababisha vurugu ya aina yoyote na hawatawadhuru watu. Wengi wenye siasa kali walitaka kuwafungulia watu kama hao kuchukua kiapo cha utii lakini AmirulMu’minin hakukubaliana na hili. Katika suala la kiapo cha utii msimamo wake wa kawaida ulikuwa ni kile anachosema: “Nitakipokea kiapo cha utii kutoka kwa yule anayekichukua kwa hiari yake na nitampuuza yule anayekataa kukichukua.” 101

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 101

9/4/2017 3:47:49 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Hivyo uhuru wa mtu mmoja mmoja ulikuwa salama kabisa katika serikali ya Ali, haukuweza kuvunjwa isipokuwa pale walipokuwa na hatia ya kuwadhuru watu, kwa sababu katika hali hiyo haikuwezekana kwa Ali kuwaacha huru. Ilikuwa ni kwa sababu hii kwamba yeye hakuwaacha Talha, Zubayr na Mu’awiya vivi hivi tu, kama alivyokuwa amefanya katika suala la Sa’d ibn Waqqas na Abdullah ibn Umar. Hawa watu watatu walikuwa na ndoto ya kuutwaa ukhalifa na walikuwa wenye bidii sana ya kupora utajiri na mamlaka. Walitaka kuanzisha vurugu ili waweze kumuondoa Ali kutoka kwenye cheo chake na kujitwalia wenyewe mali ya umma ambayo ilikuwa ni ya Waislamu wote. Walikuwa wamejilimbikizia utajiri mwingi sana, na walikuwa wameandaa jeshi la kupigana na serikali ya Ali. Ilikuwa ni kwa sababu ya hali hii ya mambo kwamba Ali hakuwaacha wenyewe, na mambo yote haya yanathibitisha kwamba yale maoni aliyokuwa nayo yeye juu ya watu watatu hawa yalikuwa ni sahihi kabisa. Baadaye tutataja kwa kirefu ni machafuko gani yalizalika kutokana na njama za watu watatu hawa dhidi ya Ali. Kwa kifupi, utawala na ukhalifa ni haki ya watu na hairuhusiwi kumlazimisha mtu kuchukua kiapo cha utii. Lazima kama hiyo inawezekana kutekelezwa kwa maslahi ya umma bali sio kwa maslahi binafsi ya mtawala. Uhusiano mwema unaweza kudumu baina ya mtawala na raia pale tu watu watakapochagua mtawala wao wenyewe na kuchukua kiapo cha utii kwake kwa hiari zao. Kwa vile Ali alishirikiana na kuchanganyikana na watu kirahisi, ilikuwa, kwa hiyo, ni kawaida kwamba yeye aweze kutamani kuwa kila mmoja wa magavana na maafisa wengine pia washirikiane na watu kama mmoja wao. Alitoa nasaha kwa watumishi kwa msisitizo kabisa kuheshimu haki za watu. Ali alianzisha mwenendo bora kabisa wa ushirikiano wa watu na watawala. Mwenendo huu pia unakubaliana na ule mwenendo wa yale mataifa ya kisasa yaliyostaarabika. Aliwafanya raia kuwa wasimamizi wa vitendo vya watawala ili waweze kutenda kulingana na matakwa ya watu. Pale, na wakati Amirul-Mu’minin alipokabidhisha utawala wa jimbo, nchi au jiji kwa mtu, aliandika wasia na kumpa mtu huyo ili ausome mbele ya watu. Kama watu wa eneo hilo waliukubali wasia huo, basi ulifanya mkataba baina yao na mtawala huyo ambao hakuna mmojawao aliyeweza kuuvunja. Kama mkataba huo ungevunjwa na upande wowote ule ilikuwa ni lazima kwa Imam kuuadhibu upande uliohusika, na kumuondoa mtawala huyo kutoka kwenye cheo chake endapo ingetokea kwamba yeye ndiye mvunjaji. 102

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 102

9/4/2017 3:47:49 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Uhuru Na Vyanzo Vyake Mbinu iliyotwaliwa na Imam Ali katika suala la siasa, utawala na uongozaji wa Taifa ilikuwa katika msingi wa kanuni ya uhuru wa watu.21 Yeye alikuwa na imani yenye hamasa katika uhuru huu ambayo inaweza kuonekana katika vitendo vyake vyote. Ikiwa alisema jambo, au alitoa maagizo, au alikataza baadhi ya vitendo, ikiwa ilikuwa ni wakati wa amani au wa vita, au alifanya uteuzi wa gavana, na katika namna yoyote ile aliyowafanyia watu au watoto wake au alipomuabudu Mwenyezi Mungu – tabia yake iliegemea, katika nyakati zote hizi, juu ya uhuru huu. Swali hili, hata hivyo, linajitokeza la kwa nini wapaswe kuwa huru, kwa nini wafanye kazi kulingana na utashi na dhamira zao. Waliupata kutoka wapi uhuru huo na ni ipi mipaka yake? Kwa kulingann na Ali chanzo halisi cha uhuru huu ni ile jamii ya wanadamu ambayo lazima ipite kwenye njia ya hali ya kubarikiwa na kuneemeka. Uhuru ni matokeo ya uhusiano wa pande mbili, shauku na mwelekeo wa watu. Ulikuwa ni uhusiano wa karibu sana pamoja na mambo machache ambayo yanatumia ushawishi mkubwa sana juu yake. Akili na uzoefu vinathibitisha jambo hili na limetiliwa nguvu pia na Ali kwamba watu wa jamii moja wanahusiana na kila mmoja wao. Ushirikiano wao huu ni kwa sababu ya maslahi binafsi na kwa maslahi ya kitaifa vilevile.22 Ilikuwa ni sera ya Ali kurekebisha uhusiano huu na mafungamano haya, ili kwamba kila mtu aweze kuendesha maisha katika njia bora. Alitoa fursa kwa watu kuutumia uhuru wao kwa namna iliyokuwa bora zaidi kiasi iwezekanavyo na kuutekeleza kwa njia ya uhuru huu, ule wajibu ambao hauwezekani kuutekeleza bila ya uhuru huo. Kwanza kabisa Ali aliwafanya watu watambue kwamba kusimamisha uadilifu na kuangamiza batili ni wajibu wao wenyewe. Wanapaswa kushikilia uhuru wao, wasiwe watiifu kwenye amri za matabaka ya juu, na wasiisaliti jamii wala wasiwe wenye kujikatili wao wenyewe. Katika maisha yake yote na kabla ya kuufikia ukhalifa, na tunzi wa kitabu hiki amethibitisha katika Sura hii kwamba ule uhuru wa kisiasa uliopo katika mataifa yaM liyoendelea ya leo hii ni sawa na uhuru uliokuwepo katika kipindi cha Imam Ali. Hakuna dalili ya uhuru kama huo katika serikali zilizokuwepo mapema zaidi ya ukhalifa wa Ali. 22 Katika istilahi za wanafalsafa wa Magharibi, uhuru una maana ya jambo lile lile ambalo linamaanishwa na ile imani ya Waislamu ifuatayo: - “Hakuna anayeruhusiwa kumlazimisha mtu mwingine kufanya kazi maalum au kutwaa mali yake bila ya ruhusa yake mwenyewe.” Wanafalsafa hawa wanaamini kwamba chanzo cha kila uonevu ni kunyimwa wanadamu uhuru wao; na mauaji, uporaji na maovu mengine ndio matokeo yake. Wanasema kwamba uhuru na kujiamulia mambo yao ni rasilimali ya asili ya mwanadamu kwa namna ile ile ambayo joto ni sifa asili ya moto. 21

103

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 103

9/4/2017 3:47:49 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

vile vile baada ya hapo, aliwaelezea watu kwamba ni lazima watekeleze wajibu wao wa kusimamisha ukweli na kuangamiza udanganyifu. Ali alikuwa akijitahidi iwezekanavyo kuupatia ustawi wa watu njia za uwezo, na wakati huo huo alikuwa ni mkali sana wa kutoa adhabu kwa wahalifu, kiasi kwamba marafiki na maadui wote walikuwa na usawa machoni mwake katika suala hili, na hakuonyesha huruma kwa mtu yoyote yule. Ali alikuwa mwenye kujiamini kwamba uchamungu wake ulikuwa unajulikana kwa wote, na wao walikuwa wanatambua kwamba yeye alikuwa hana wa kulingana naye katika suala la uchamungu, na alichukukua kutoka duniani, kile tu ambacho kilitosheleza kwa maisha yake. Watu pia walijua kwamba lengo pekee la uhai wake lilikuwa kusimamisha uadilifu na kuwasaidia wenye kuhitaji na wale wanaoonewe, na kwamba aliyafanya mambo haya kama ni suala la wajibu na sio kuonyesha huruma kwa wengine. Hakupenda kula asali kwa sababu alihofia kwamba wangeweza wakawepo watu miongoni mwa raia zake ambao hata mkate wa shayiri ulikuwa hauwezi kupatikana. Alikuwa kamwe hajivishi nguo nzuri, kwa sababu angeweza kuwepo mtu wa jamii ambaye angeweza kuwa hana hata nguo chakavu ya kuvaa. Yeye hakupenda watu wamwite Amirul-Mu’minin na asiwe anashiriki katika matatizo yao. Ali alijiweka huru kutokana na uchafu ambao watawala wa wakati ule walijihusisha nao. Hakuitumia fursa ya nasaba yake tukufu. Hakutamani kamwe nchi, cheo kikubwa au utajiri. Hakuonyesha majivuno katika wakati wowote ule. Alijiweka mbali na mambo yote yasiyowiana na ya ovyovyo. Kamwe hakuwapendelea ndugu, jamaa na marafiki zake juu ya wengine. Hakuwa akiweka kinyongo dhidi ya maadui zake, wala hakulipiza kisasi juu ya mtu yoyote. Hakuwahi kufanya jambo lolote ambalo kwalo uzuri na usahihi wake hakuwa na uhakika nao. Hakuwahi kusema au kufikiria kitu chochote ambacho hakukipenda. Alikuwa hajali juu ya chochote ambacho alikula au kunywa, nguo gani aliyovaa, na nyumba ambamo aliishi. Alivitumia vitu hivi kwa kiasi kile tu ambacho kilikuwa muhimu sana kwake. Hakuchukua chochote kutoka kwenye hazina ya umma kwa kufanyia matumizi yake binafsi, ingawa angeweza kuchukua angalau kiasi kama kile magavana wa majimbo walichochukua.

104

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 104

9/4/2017 3:47:49 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Riwaya sahihi zinaonyesha kwamba aghalabu alilazimika kuuza upanga wake, deraya na vyombo vya nyumbani kwake ili kupata kujilisha yeye mwenyewe na watu wa nyumbani mwake. Hata hivyo, alitoa mishahara ya kutosheleza kwa magavana wake ili wasije wakalazimika kuchukua rushwa na hongo au kujipatia fedha kwa njia zisizo halali. Ali alijiweka huru kutokana na vifungo vyote kama vile ambavyo vingeweza kuingilia kati usimamiaji wake wa uadilifu baina ya marafiki na maadui. Yeye ameielezea hali yake mwenyewe katika maelezo haya mafupi yafuatayo: “Yeyote anayetelekeza matamanio huwa anabakia kuwa huru.” Uchamungu wake ulikuwa ni uchamungu wa watu waungwana. Haukutiwa dosari na ulafi wa aina yoyote ile. Alikuwa na imani kamilifu juu ya Mwenyezi Mungu na alishughulika kulingana na imani yake hiyo. Hapakuwa na kisingizio chochote cha unafiki katika matendo yake. Matendo yake mema hayakushawishiwa na hofu ya Jahannam au tamaa ya Pepo. Na kuhusu uhuru wa watu chini, hatua yake ya kwanza ni uhuru wa vitendo. Imam Ali amelipa lile kundi la wafanyakazi hadhi sawasawa kama ile iliyokuwanazo nyoyo za watu waadilifu huko Peponi; yaani, dunia hii inawapokea wafanyakazi kwa namna sawa na ile ambayo Pepo inavyobaki kuwa tayari kuwapokea watu waadilifu. Kuhusu hao watu waadilifu yeye anasema: “Nyoyo zao ziko Peponi na viwiliwili vyao vinahangaika kufanya kazi.” (yaani wao hawaambatanishi nyoyo zao na mambo ya kidunia). Aliinyanyua nafasi ya uhuru na aliichukulia kazi ya mtu huru kuwa mashuhuri sana. Alikuwa ameifanya ni kanuni yake kutomlazimisha mtu yoyote kufanya kazi yoyote maalum, kwa sababu kazi yoyote ambayo haikufanywa kwa hiari ni udanganyifu katika suala la uhuru, na katika kazi yenyewe vilevile. Yeye anasema: “Sio nia yangu kumlazimisha mtu yoyote kufanya kazi yoyote ile maalum.” Aliweka malipo kwa ajili ya kuwafanya watu kufanya kazi za maana na kuhifadhi uhuru, na kumnyima malipo mtu yoyote ambaye alilazimisha watu wengine kufanya kazi. Yeye anasema: “Mfereji ni mali ya yule aliyeuchimba kwa hiari yake mwenyewe na sio mali ya yule mtu aliyewalazimisha wengine kuuchimba” (au ya yule ambaye haufanyii kazi).

105

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 105

9/4/2017 3:47:49 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Inajitokeza kuwa ni muhimu kutaja jambo moja muhimu hapa. Hili neno uhuru kama lilivyotumika katika siku zile, halikuwa na maana kubwa sana kama iliyokuwa imewekwa na Ali. Wengine hawakumaanisha juu yake kile alichomaanisha Ali. Katika siku zile uhuru ulikuwa ni kinyume cha utumwa na mtu huru, muungwana alikuwa ni kinyume na mtumwa. Khalifa Umar alisema: “Uliwafanyaje watu kuwa ni watumwa wako wakati mama zao waliwazaa kama watu huru?” Pale tunapotafakari juu ya maneno haya na kutilia maanani ule wakati na hali ambamo yalitamkwa na Khalifa Umar tunaona wazi kwamba, kwa mtu huru yeye alikuwa na maana ya kinyume na mtumwa; yaani, mtu ambaye hawezi kununuliwa au kuuzwa. Hata hivyo, katika nyakati za sasa, maneno huru na uhuru hayana maana sawa na ile ile ambamo yalitumiwa na khalifa Umar. Hapa tunaleta ushahidi mwingine wa maoni yetu. Katika sentensi iliyonukuliwa hapo juu, khalifa Umar alikuwa ameonyesha kuchukia juu ya wale watu ambao walikuwa wamewashusha watu wa chini yao hadi kwenye hadhi ya utumwa. Aliwakemea wale watu wenye uwezo na akawaanbia kwamba wasiwachukulie wale wanyonge kama watumwa, kwa sababu mama zao waliwazaa kama watu huru. Khalifa Umar hakuwaambia wale watumwa kuwa wao walikuwa huru na wasiwatii wale waliodai kuwa ni mabwana wa watumwa wao. Kwa ufupi khalifa Umar katika maneno yake aliwaonya wale mabwana kutoa uhuru kwa wale wanaowatumikia na wale watu wanyonge. Kwa mujibu wa Imam Ali, maana ya uhuru ni tofauti kabisa kutokana na kile anachodhamiria khalifa Umar na inabeba maana iliyopanuka zaidi. Kwanza kabisa tunanakili hapa chini kauli yake ya wazi juu ya raia na baadaye tutakuja kunakili kauli nyingine, mapendekezo na maagizo yake, katika kutilia nguvu maoni yetu. Kinyume na kauli ya Umar, yeye anasema: “Usiwe mtumwa wa mtu yoyote yule wakati Mwenyezi Mungu amekuumba wewe ukiwa huru kabisa.” Khalifa Umar alikuwa amezungumza na wale mabwana wamiliki, na akawaambia wawape uhuru wale watu wa chini yao. Bali alikuwa hakuwaambia wale watumishi wenyewe waache kuwatii wamiliki wao. Ali hata hivyo, anazungumza na wale watu wa chini wenyewe, na anawaambia wajitegemee na wawe na hisia za uhuru. Anawashauri watambue haki yao ya uhuru ambayo ndiyo msingi wa maisha yao. Yeye pia anawakumbusha kwamba Mwenyezi Mungu aliwaumba wao kama viumbe huru na chochote kile wanachofanya au wasichokifanya lazima kitegemee juu ya haki yao hii ya asili. 106

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 106

9/4/2017 3:47:49 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Kwa kuyatamka maneno haya, Ali alipandikiza mbegu za mapinduzi katika nyoyo za wale watu wa chini, na akawaandaa kupambana dhidi ya jambo lolote litakaloingilia kati uhuru wao au kuwaingiza kwenye mkanganyiko. Wasomaji wanaweza wakafikiri kwamba hakuna tofauti kubwa sana kati ya maneno ya khalifa Umar na yale ya Ali, kwa sababu Umar alizungumza na kikundi maalum cha watu, yaani wale wamiliki – mabwana wasiwafanye watu kuwa watumwa, ambapo Ali amezungumza na watu wote na akawaambia kwamba wako huru. Ameufanya uhuru wao kutegemea juu ya dhamira zao wenyewe na sio juu ya makusudio ya mabwana zao ili kwamba waje kuwafanya watumwa kwa muda wautakao na kuwafanya huru pale tu, na wakati watakaoutaka wao (hao mabwana). Hata hivyo, kimsingi pana tofauti kubwa sana kati ya kauli hizi mbili. Maneno ya Ali yanaonyesha umaizi wa kina ambao alikuwa nao juu ya maana ya uhuru. Maneno yake yanaonyesha ule ukweli kwamba chanzo cha uhuru ni utu wa mtu mwenyewe. Amezaliwa akiwa huru na ni yeye mwenyewe anayepaswa kujichagulia njia yake ya matendo, na sio kwamba mtu mwingine yoyote amuonee huruma na kumuacha huru. Kauli hii ya Ali inaonyesha kwamba yeye aliuchukulia uhuru wa mwanadamu kuwa ni wa asili na wa kawaida na vitendo vyote vya mwanadamu ni matokeo ya uhuru huu wa asili na kawaida. Uhuru huu umesafika kutokana na athari zote za nje. Uhuru huu anaufaidi yeye ndani kwa ndani na sio kwa nje. Ni kama mwanga wa jua ambao hauwezi kutenganishwa nalo. Sio kama mwanga wa mwezi ambao huwa unashuka. Kwa hiyo kuna tofauti ya kweli na ya msingi baina ya yale maneno yaliyotamkwa na khalifa Umar na yale ya Ali. Kwenye namna moja wanahusika wale watu ambao uhuru wao unategemea juu ya matakwa ya wengine. Uhuru huu ni wa nje na hauchomozi kutoka kwenye chanzo chake chenyewe. Kwenye namna ile nyingine wanahusika wale watu ambao uhuru wao unategemea juu ya asili yao wenyewe. Huu ndio uhuru halisi na wa kweli. Watu huru kama hao wanatenda kulingana na akili na manufaa yao na hawafanyi kile wasichokitaka. Hata hivyo, wale ambao uhuru wao unategemea juu ya wengine hawako chini ya maoni na fikira zao wenyewe. Aina ya uhuru ambayo Imam Ali aliipenda ilikuwa ni ile ambayo imeegama juu ya uhusiano wa kibinadamu. Ni uhuru huu ambao kwa namna yake wanadamu wanaweza wakatembea bega kwa bega na kila mmoja wao katika njia ya ustawi. Ni uhuru huu ambao unaweza ukaleta kuwepo kwa ustaarabu mkubwa. 107

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 107

9/4/2017 3:47:49 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Kwa vile uhuru wa namna iliyotajwa hapo juu ulichukuliwa na Imam Ali kuwa ndio hasa uhuru halisi, maagizo yake yote yalitolewa kwa kuzingatia uhuru huu hasa, na vile vile alibainisha haki za binadamu kwa msingi huo. Tunaona kwa uwazi kabisa utekelezaji wa kanuni hii katika maagizo na kanuni zake zote. Aliwafanya wanadamu wote kuwa sawa katika suala la haki na wajibu na hakuweka mipaka yoyote kuhusu hili. Na kama aliweka mipaka yoyote kama hiyo, iliwekwa kwa kutilia maanani maslahi ya umma kwa jumla. Wakati tunapouchunguza mwendo wa Ali, tunaona wazi kwamba yeye hakuingilia uhuru huu katika sheria na amri, kanuni na taratibu zake, na alitilia maanani ustawi wa jamii katika vitendo vyake vyote. Aliwatendea kwa usawa marafiki na maadui zake. Tayari tumekwisha kutaja kwamba yeye hakumlazimisha mtu yeyote kufanya kazi yoyote kinyume na utashi wake mwenyewe, wala yeye hakuruhusu kazi za kulazimishwa. Vilevile tumesema kwamba yeye hakumlazimisha mtu yoyote kuchukua kiapo cha utii kwake. Wale ambao walikataa kuchukua kiapo cha utii kwake bila shaka walikuwa ni wahalifu, lakini yeye aliwaacha wenyewe tu kwa sababu alijua kwamba kule kutokuchukua kwao kiapo cha utii kusingeleta tofauti yoyote wala maslahi ya jamii yasingeathirika kwa sababu hiyo. Walijizuia kuchukua kiapo kwa muda mrefu sana, lakini kwa kufanya hivyo walijifanyia madhara wao wenyewe. Yeye hakuchukua hatua yoyote dhidi yao alimuradi hawakudhihirisha kuwa wenye mad-hara kwenye maslahi ya umma. Akizungumza na Mughirah bin Shu’ba yeye alisema: “Nakuruhusu kufanya lolote ulitakalo kukuhusu wewe mwenyewe.” Inaweza pia kutajwa kwamba wakati mmoja Habib ibn Muslim Fihr alimwendea na akasema: “Ungeng’atuka ili watu waweze kuchagua khalifa kupitia baraza la ushauri.” Hapo Ali akamjibu: “Wewe unahusika na nini kuhusu suala hili? Ungenyamaza kimya. Kwa nini unazungumza juu ya jambo ambalo kwalo wewe huhusiki hata kidogo.” Kisha Habib akasimama na akasema: “Wallahi utatukuta sisi kwenye sehemu ambayo wewe hutaipenda.” Tishio lililojificha katika maneno ya Habib liko dhahiri kabisa. Lakini, kwani Ali alifanya nini? Je, na yeye alimtishia kwa namna kama hiyo hiyo? Je, alimfunga jela ili asije akawa huru kumpinga yeye na asije akalichochea kabila lake kuasi dhidi yake? Ali aliyaona mambo haya. Kinyume chake yeye alimtupia jicho na akasema kama mtu ambaye anaamini kabisa uadilifu wake na anayeheshimu uhuru wa wengine: 108

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 108

9/4/2017 3:47:49 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

“Nenda ukakusanye wapiganaji wa chini kwa chini na wa farasi wengi kiasi unachotaka. Mwenyezi Mungu asiniweke hai mpaka siku ambayo utaweza kuona huruma juu yangu.” Ushahidi mwingine wa uhuru kamili ulioruhusiwa na Ali kwa watu ni kwamba watu wengi watokanao na Hijazi na Iraqi waliondoka zao na kwenda kujiunga na Mu’awiyah, lakini yeye hakuwazuia, wala hakuona kwamba ni jambo la muhimu kuwaweka chini ya uchunguzi. Walikuwa ni watu huru mbele ya macho yake na walikuwa huru kutwaa mwelekeo wowote ule walioutaka. Kama mtu alichagua njia ya haki ilikuwa vyema na vizuri, bali kama aliamua vinginevyo, ile njia ya Damascus ilikuwa wazi juu yake na Mu’awiyah pamoja na hazina zake, alikuwa akimngojea mtu kama huyo. Hivyo, pale Sahl bin Hanif Ansari, gavana wa Madina, alipomjulisha yeye kwamba baadhi ya watu wamekwenda upande wa Mu’awiyah, yeye alimwandikia katika kumjibu hivi: “Ninaelewa kwamba baadhi ya watu wanaotoka kwenye eneo lako wanajiunga kwa siri na Mu’awiyah. Huna haja ya kuwa na wasiwasi hata kidogo kuhusu ile idadi ya wale watu ambao wameondoka na msaada ambao tayari umekwishapotea. Inatosha kwa kukengeuka kwao na kule kuondokewa kwako na wasiwasi na huzuni kwamba, wanaikimbia kweli na mwongozo, na kuelekea kwenye ujahilia na upotovu. Wao ni watu wa kidunia ambao wanaelekea kwenye dunia na kuikimbilia. Wao walitambua, waliona, walisikia na kuijua haki. Wameelewa vizuri kabisa kwamba hapa wanachukuliwa kuwa sawa katika suala la haki na, kwa hiyo, wanakimbia kuelekea mahali ambako ubaguzi unafanyika. Kwa jina la Allah hawakukimbia kutoka kwenye udhalimu na hawakujiunga na haki, na sisi tunatumaini kwamba Mwenyezi Mungu atalifanyia wepesi kila gumu ambalo linahusika katika suala hili, na ataifanya ardhi ngumu ya mawe kuwa ya usawa kwa ajili yetu.” Ushahidi mwingine wa ukweli kwamba Ali aliamini katika uhuru kamili wa watu unatolewa na ushughulikaji wake na Khawariji. Kundi moja la Khawariji lilikuwa ni lile ambalo lilikuwa limeasi waziwazi na ilikuwa ni watu hawa ambao wengi wao waliuawa kwa upanga katika vita vya Nahrawan. Hata hivyo, walikuwepo wengine ambao walishikilia imani sawa na za Khawariji lakini walionelea kwamba inafaa kutoasi, na wao walichanganyika na watu wa Kufa. Imam Ali alifanya wema juu ya Khawariji wa hili kundi la namna ya pili na hakuwaruhusu wafuasi wake kupambana

109

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 109

9/4/2017 3:47:49 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

nao. Vile vile aliwapa Khawariji hawa pensheni kwa kiasi kama kile cha Waislamu na aliwapa uhuru wa kwenda popote pale walipotaka. Namna yake ya utendaji iliegemea kwenye uhuru mkamilifu, yaani, wanadamu wote wako huru na wanaweza kufanya kila wanalolitaka, na kumpenda au kumchukia wamtakaye. Hata hivyo, hakuna aliyeruhusiwa kuwadhuru watu au kusababisha uharibifu juu ya uso wa ardhi. Kama mtu yeyote angejiingiza kwenye vitendo vya uharibifu asingesamehewa na aliadhibiwa kwa ajili ya kosa alilolitenda. Wakati mmoja Khawarij mmoja aitwaye Khariir ibn Rashid alikuja kwa Imam Ali na akamwambia: “Kwa jina la Mwenyezi Mungu mimi sintakutii wewe na sitaswali pamoja na wewe.” Imam Ali hakumwingilia katika hilo na akamwacha huru kufanya lolote analolitaka. Baada ya muda fulani Khariir alikusanya idadi ya watu na wakaasi dhidi yake. Hata hapo; Ali hakuwazuia wale watu waliomuacha yeye na kujiunga na Khariir kufanya hivyo, ingawaje angeweza kuwazuia kujiunga na Khariir. Hata hivyo, pale watu hao walipochukua fursa hiyo iliyovuka mipaka ya uhuru huu na wakaanza kufanya unyang’anyi na mauaji alilituma jeshi lake na likawazima. Jambo la kushangaza sana ni kwamba hata katika nyakati mbaya sana za kipindi chake; Ali aliweka heshima inayostahili kwenye uhuru wa wanadamu na kamwe hakuuvunja. Alifanya hivi kwa sababu yeye aliuchukulia uhuru kuwa ni kitu muhimu sana kwa ajili ya ubinadamu. Hakupunguza kitu kutoka kwenye uhuru huu hata pale alipokuwa akipambana dhidi ya wale Nakithiin, Qasitiin na Mariqiin ambao walijitwalia maeneo makubwa ya ardhi kwa ajili yao wenyewe na walikuwa ndio maadui wa jadi wa Ali. Ilikuwa inaruhusiwa kwa mujibu wa kila sheria na kila dini kupigana dhidi ya watu kama hao, na kila mtu mwenye maamuzi ya busara angelichukulia pambano kama hilo kuwa ni la haki. Katika mazingira hayo ilikuwa ni muhimu kwa Ali kukusanya wafuasi wake na kwenda kupigana vita na adui. Hata hivyo, Ali hakumlazimisha mfuasi wake yoyote kushiriki katika vita, iwe alikuwa ndugu au jamaa yake au mtu mwingine yoyote. Ingawa alikuwa ndiye Khalifa na alikuwa na mamlaka, lakini hakuwalazimisha masahaba zake kutoa msaada wa kidunia au wa kiroho, kwa sababu kwa namna yoyote ile ambayo angeitumia kwenye kulazimisha ingekuwa imepingana na uhuru ambamo alikuwa ameamini juu yake.23 23

ata leo hii wale watu wa Magharibi hawautambui ule uhuru ulioruhusiwa na Imam Ali kama ilivyoelezewa na H mwandishi, ingawaje baadhi ya wataalamu wa kijamii kama vile Rousseu wamelizungumzia hilo katika vitabu vyao, na wamejitahidi kuwafanya watu kuliamini hilo. Baadhi ya watu wanaweza wakafikiri kwamba kanuni ya 110

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 110

9/4/2017 3:47:49 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Imam Ali alitimiza wajibu wake kwa kuwaonyesha waziwazi njia ya kweli na kuzishawishi akili na busara zao. Alitoa hoja kuhusiana na kuwa sawa kwake ili kwamba yeyote aliyeitaka angeweza kuitambua haki yake, na kumuunga mkono yeye, na yeyote ambaye hakuipenda angeweza kumpinga licha ya kuujua ukweli. Aliombea ustawi wa wale ambao waliitikia wito wake na kuwasifu. Na kuhusu wale ambao hawakuuitikia wito huo, yeye aliwaonya kuhusu kosa lao kwa kuwapa ushauri. Mtu yoyote, na mahali popote alipokuwepo, yeye alikuwa huru. Ali hakumlazimisha mtu yoyote na hakuchukulia ulazimishaji kuwa wenye kufaa. Hakupendelea kamwe kwamba mtu yoyote aungane naye bila tafakari inayofaa na imani na elimu. Yeye hakumlazimisha mtu yoyote kujiandikisha katika jeshi lake kwenda kupigana katika vita vya Ngamia, Siffin na Nahrawan kwani kama angependa, angeweza kujaza mawanda na milima kwa wapiganaji. Ali alijua vizuri kabisa uhuru ulikuwa ni kitu gani, na undani na unje wake ulikuwaje. Yeye aliuelezea kwa maneno yake na vitendo vyake na aliuchunga katika mwenendo wake kwa watu. Aliiweka kanuni ya uhuru maanani katika kuyaondoa maovu kutoka kwenye jamii, katika usimamizi wa sheria za kidini, katika uhamasishaji wa majeshi, katika kuwatawala watu, katika kufanya mapendekezo na kutoa ushauri, na, kwa kifupi, katika kila jambo. Kila siku ya maisha yake ilitoa ushahidi mpya wa ule ukweli kwamba haki ya mtu juu ya uhuru inastahili kuheshimiwa ilimuradi tu kwamba haisawiji ule uhuru wa umma kwa jumla na hii ndio maana halisi ya uhuru. adhabu ya Kiislamu inapingana na dai la mwandishi na pia kwamba Waislamu hawachukulii kuwa inaruhusika kwamba mtu aasi na kutoka kwenye Uislamu au atumie maneno machafu kuhusu Mwenyezi Mungu au mitume. Unywaji pombe uliadhibiwa wakati wa ukhalifa wa Ali na wakati wa makhalifa wengine pia, kununua na kuuza vileo kulichukuliwa kuwa ni kosa na waasi waliadhibiwa. Watu kama hao wanaweza, kwa hiyo, wakauliza kwamba huo uhuru unakuweko wapi. J ibu kwa kile ambacho mwandishi anataka kukithibitisha ni kwamba mambo yote haya (yaani adhabu juu ya uasi na makosa mengine) yako sahihi. Hata hivyo, uhuru unaostahili kutukuzwa na ambao uliungwa mkono na Ali sio ule uhuru aliofaidi mtu kwa kujitwalia mali yake na kuitumia kama anavyotaka na kutwaa shughuli anayoitaka. Kwa ufupi Ali aliamini katika uhuru wa kisiasa na kijamii. aislamu wote wanakubaliana kwamba kunywa pombe na uasi ni makosa. Sasa pale vitendo hivi vinapokuwa W ni maasi kwa mtazamo wa kijamii, ni vipi uhuru wa kuyatenda utakuwa wenye kukubaliwa? Hivyo kama Imam Ali angetoa uhuru kwa watu kuyatenda makosa haya, kitendo chake hicho kingekuwa kinapingana na amri za Mwenyezi Mungu na vilevile na uhuru wa watu. Kama khalifa Abu Bakr na Umar wasingepambana dhidi ya waasi wangekuwa wamepingana na idadi kubwa ya Waislamu. Hata sasa baadhi ya vyama katika nchi mbalimbali vinatangazwa kuwa sio vya kihalali, kwa sababu watu wengi wanachukulia maoni na imani za vyama hivi kuwa ni uhalifu. Vivyo hivyo, uasi ni uhalifu kulingana na Waislamu, kwa sababu kwa hakika unasababisha matatizo katika jamii. 111

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 111

9/4/2017 3:47:49 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Uhuru Wa Mtu Binafsi Utendaji wa Imam juu ya watu wengine na mwenendo wake juu yao ulitegemea juu ya uhuru wao. Dhamira ya mtu lazima ichukue maamuzi kulingana na azimio lake mwenyewe na pamoja na uhuru. Njia zenyewe zinakuwa na nguvu bila ya athari za nje. Vikwazo vya nje vinazizuia kwa kiasi fulani kutokana na kuwa na nguvu. Shughuli za pamoja zinakuwa sahihi tu pale zinapoendana na kanuni za dhamira huru na kanuni za asili24 ambazo zenyewe ziko huru. Mwanadamu yuko huru kimsingi. Nafsi iliyohuru inakuwa na hisia. Anafikiria kwa uwezo wake mwenyewe, anaongea kwa mamlaka na anatenda kwa dhamira yake. Kumuweka chini ya ulazima, kwa kweli kutafikia kwenye kuimaliza nafsi yake yenyewe. Hivyo itakuwa inaruhusiwa kudhibiti uhuru wa mtu pale tu inapokuwa inaruhusiwa kumuua.25 Kama unataka kupunguza mwanga wa jua na ukaweka pazia mbele yake kama matokeo ambamo kwamba haliwezi kuvifanya vile vitu vilivyoko nyuma yake kuwa na joto na mng’aro, wewe kwa hakika unauzima mwanga wake. Kama unaweza kuuzuia upepo usivume, kwa kweli wewe unaiteketeza hewa hiyo. Vivyo hivyo, kama unainyima mito mawimbi, yale maua ya majangwani, ndege wa angani na vitu vyote vilivyopo katika dunia hii kufanya shughuli zao za asili, ni sawasawa na kuwa umeviangamiza. Hivyo ndivyo ilivyo katika suala la mwanadamu na kumnyima uhuru ni sawa na kuwauwa wanadamu wote.26 wandishi anathibitisha katika sura hii kwamba uhuru wa mtu binafsi lazima, wanapokuwa huru, waangalie M na kujali juu ya maslahi ya taifa na lazima wafanye yale matendo kwa dhamira zao, kwa hiari zao na uchaguzi ambavyo vyote ni venye manufaa kwa ajili ya watu na waepukane na vitendo vyenye madhara, ili uhuru uwe umeishia kwenye uhuru wa mtu mwenyewe na usiishie kwenye kuwaweka wengine kwenye ulazima na ufungwa. 25 Kwa kauli hii mwandishi anataka kuthibitisha kwamba mtazamo wa wasoshalisti kwamba serikali ihodhi shughuli zote, na isimuache mtu yoyote kuwa huru kwa msingi kwamba, katika masuala mbalimbali watu wanasimamia maslahi yao binafsi na wasijali maslahi ya taifa sio sahihi. Wapinzani wa dhana hii wanasema kwamba hakuna maslahi yaliyoko juu kuliko uhuru, na baada ya kudhibiti uhuru wao, watu hawataweza kupatiwa neema ambayo inalingana na uhuru wao huo. Vilevile wanasema kwamba kila baraka na maendeleo ya viwanda na biashara yanaweza kupatikana katika namna nzuri kwa njia ya uhuru. Kama tunavyoweza kuona vizuri sana, fursa nyingi sana zinapatikana katika nchi huru na idadi ya wasomi na waliotaalimika wanaopatikana humo pia ni kubwa sana. Wafanyakazi katika nchi hizo wanaishi maisha ya starehe na kiwango cha uhalifu huko ni cha chini sana kiasi kwamba katika nyingi ya nchi hizo hakuna kesi ya uhalifu inayoorodheshwa kwa miaka mingi. 26 Watu wenye fitina na wapenda anasa pia wanasema kwamba uhuru ni kitu cha kuheshimika, na taifa lazima liwaache huru kujishughulisha katika shughuli zao za tama, na kuwakuza watoto na vijana katika hali isiyo ya kidini. Waambiwe kwamba uhuru wanaoudai wao ni uhalifu na endapo watapewa leseni hiyo, wengine ambao 24

112

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 112

9/4/2017 3:47:50 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Hii ilikuwa ndio dhana ya uhuru machoni mwa Imam Ali na hivi ndivyo yeye alivyofikia vina vyake. Aliuzungumzia uhuru kwa mdomo wake kama alivyouelewa na pia akashughulika kulingana nao. Kila kitendo chake kilikuwa sahihi kulingana na maoni na imani zake na vilevile kulingana na zile za wengine. Kanuni za asili na vile vile maslahi ya jamii yanaviunga mkono. Maneno na vitendo vya Ali ambavyo tumevichunguza barabara vinaonyesha jinsi alivyowaongoza watu kufanya kila kitu kwa dhamira zao na hiari ya nyoyo zao. Kwa hakika kulikuwa na kitu ambacho wakati wote alikitilia maanani, nacho kilikuwa ni uhuru wa mtu binafsi kwa namna ambayo kwamba uhuru wa wengine haukudhuriwa. Kundi la wanafalsafa wa zamani wa ki-Giriki na baadhi ya wanafalsafa wa Ulaya wa Enzi ya Kati walitilia maanani tu ule uhuru wa watu binafsi na hawakuweka umuhimu kwenye maslahi ya umma na uhuru wa kitaifa. Kulikuwepo pia na kundi jingine ambalo lilichukulia maslahi ya pamoja katika fikra zao na hawakupendelea uhuru na haki binafsi. Wao walichukulia shinikizo juu ya watu na kuwalazimisha katika kazi kwa nguvu kuwa ni jambo halali. Hata hivyo, Ali alichukulia uhuru wa watu binafsi na yale maslahi ya pamoja akilini mwake katika namna ambayo yote hakuna linaloweza kudhurika na akayafanya mambo yote haya kuendana, moja na jingine, ili kwamba mtu binafsi angeweza kushughulikia maslahi ya pamoja kwa hiari yake mwenyewe, na juhudi huru za watu binafsi ziweze kuwa kwa manufaa ya taifa. Yeye alitangaza kwamba watu binafsi walikuwa ni kwa ajili ya taifa na kwamba taifa lilikuwa ni kwa ajili ya watu binafsi. Tutaendelea na mjadala huu kusudi kwamba suala hili liweze kueleweka wazi kwa ukamilifu zaidi. Sasa tutaangalia jinsi alivyoratibu uhuru wa watu binafsi pamoja na manufaa ya umma. Ali alijua kwamba kwa vile watu binafsi walikuwa ni wanajumuiya wa taifa, wanapaswa kutumia uhuru wao kwa mambo ambayo hayawezi kudhuru maslahi ya taifa. Hapa uhuru hauna maana ya leseni au ruhusa ya jumla. Kinyume chake ni lazima uunganishwe na imani na hisia ya uwajibikaji, na mtu lazima achukulie kwamba ni jukumu lake kutilia maanani maslahi ya taifa pamoja na uhuru wake binafsi. Ali hakusema kama wanafalsafa wengine kwamba uhuru wa mwanadamu una mipaka, bali yeye alisema jambo la kina zaidi na hakuweka mipaka yoyote juu ya uhuru. Maneno yake ni ya thamani na ya hali ya juu sana kuliko yale ya wengine, na yanaonyesha kwamba yeye alikuwa ni mbora zaidi kuliko wale wengine katika kuelewa miujiza ya kiroho ya mwanadamu na kanuni na taratibu za kijamii. idadi yao ni kubwa kwa maelfu mara kuliko yao, watakuwa wamenyimwa uhuru wao. 113

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 113

9/4/2017 3:47:50 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Yeye aliikazia katika nyoyo za watu ile dhana ya uhuru, na akaongezea juu yake dhana ya kwamba kila mtu anao wajibu fulani ambao ni lazima autimize. Uthibitisho wa sera yake hii ni kwamba, mfereji katika kijiji ulikuwa umejaa udongo na ukawa hauna matumizi ya manufaa, na baadhi ya watu ambao walitaka kuuanzisha upya walimwendea gavana wa eneo hilo ili kuwalazimisha watu kuufanyia kazi, lakini Amirul-Mu’minin alilikataza hilo vikali kabisa na akasema: “Wanaweza kufanya kazi juu yake kwa utashi wa hiari zao na kupata mshahara kwa ajili hiyo. Na kuhusu mfereji huo utakuwa ni mali ya yule mtu ambaye anafanya kazi juu yake kwa hiari yake mwenyewe na kujiona mwenyewe mwenye kuhusika na matokeo yake.” Ali alitoa heshima kwa uhuru wa tabaka la wafanyakazi zaidi ya miaka elfu moja iliyopita, na Rousseau, yule mwandishi mashuhuri wa Kifaransa alikuwa amepata mawazo ya kutoa kauli kama hiyo takriban karne mbili zilizopita: “Heshima juu ya mwanadamu na mapenzi juu ya binadamu yanatushurutisha sisi tuseme kwamba tunapaswa kuwaona watu wa chini yetu kuwa ni binadamu na kama watu wenye akili hata kama watakuwa hawakufundishwa na ni wajinga.” Kanuni iliyowekwa na Imam inafanya kuwa ni lazima kwamba dhamira na mamlaka lazima viwekwe ndani ya mipaka yake, na mamlaka lazima yaunganishwe na imani juu ya majukumu. Hivyo, wajibu na majukumu havina madhara kwa mamlaka, bali pia vitayaunga mkono hayo mamlaka. Wajibu peke yake hautoshi kwa ajili ya utekelezaji wa vitendo vyema mpaka dhamira na uwezo pia viwajibike. Wajibu unawiana na uwezo. Jinsi uwezo na dhamira vinavyokuwa vikubwa zaidi ndivyo wajibu na majukumu yanapokuwa mazito zaidi. Wajibu unahusiana na uwezo kwa namna ile ile ambavyo unahusiana na akili na dhamiri. Mtu ambaye uwezo wake wa kufikiri umedumaa, na ambaye hawezi kutofautisha kati ya jema na ovu, na ambaye vipaji vyake vya kiakili vimevurugika hawezi kuchukuliwa kuwa na wajibu juu ya kitendo chochote. Vivyo hivyo, mtu ambaye amenyimwa uhuru wake na uwezo hawezi kulazimishwa kwenye wajibu wowote. Uhuru, uwezo na uchangamfu wa akili vinamfanya mtu kuweza kutofautisha baina ya jema na ovu na kutekeleza wajibu wake kama jambo la lazima. Ilikuwa ni kwa sababu hii kwamba Ali aliwaagiza magavana na watumishi wake wengine kuwatoa watu kwenye ufungwa wa aina yoyote na kuwaondolea minyororo mizito mikononi na miguuni mwao, ili waweze kufanya vitendo vyenye manufaa kwa taifa kwa hiari za nyoyo zao wenyewe, kwa sababu alimradi walikuwa hawako 114

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 114

9/4/2017 3:47:50 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

huru wangekuwa hawajiwezi, na watu wasiojiweza hawawi chini ya wajibu wowote. Hawajioni wao wenyewe kuwa wenye kuwajibika, na kwa hiyo, hawafanyi vitendo vyema, kwa sababu matendo mema yanaweza kufanywa tu kwa uhuru wa mawazo. Vitendo vya wale ambao hawana utashi sio vyao wenyewe. Hivyo ni vitendo vya serikali ambavyo vinatendwa kupitia kwao. Dhamira zao zinakuwa dhaifu na nguvu zao zinapotezwa katika nafasi zisizofaa. Baada ya Imam watu walifika kwenye ile hatua haswa tuliyoitaja. Ingawaje walikuwa huru wakati wa kipindi cha ukhalifa wake, na walisalimika kutokana na madhara na mateso ya watawala, yeye alikuwa ameweka kanuni ambayo kulingana nayo wao walitakiwa kukiri wajibu wao kwa utashi wao huru, na walikuwa watambue kwamba walikuwa wanadaiwa wajibu fulani kwa taifa, na kwamba taifa lilikuwa na haki kadhaa juu yao. Kama tulivyokwisha kuona tayari mara nyingi, na bado tutaona pia baadaye, maagizo na maelekezo yake yalikuwa kwenye msingi wa kanuni hii na aliamrisha na kuzuia na kuzawadia na kuadhibu watu kwa kuzingatia kanuni hii. Uwajibikaji Kama tulivyokwisha sema tayari, uhuru katika maana yake pana ulikuwa ndio msingi halisi wa serikali ya Ali. Machoni mwake yeye, uhuru huu ulikuwa na uhusiano sana na mahusiano ya pamoja wa watu kama yale ya akili na dhamira. Mwanadamu anayetaka kukaba hatua mbalimbali za kimaendeleo kwa njia ya ushirikiano wa pamoja na uhusiano wa kindugu hawezi kufikia mafanikio kwa ajili ya hili mpaka awe huru katika nafasi yake ya binafsi na ya pamoja. Na haiwezekani kwake yeye kuwa huru mpaka dhamira yake iwe huru kutokana na yale mapungufu ambayo yanashusha thamani ya mtu. Vivyo hivyo, mtu huyo hawezi pia kuwa huru, ambaye haki zake juu ya uhuru zinakubaliwa na jamii lakini zinakataliwa katika vitendo. Katika suala hili Ali alitoa utendaji sawa kwa watu binafsi na jamii, na vilevile kwa marafiki na maadui. Alifuata mwenendo huu wa utendaji kwa uimara sana. Hakuweza mwenyewe au kufanywa akengeuke kutoka kwenye lengo lake kwa vishawishi vyovyote au vitisho. Yeye alijua vizuri kabisa kwamba haki ilikuwa inachukiza kwa watu wengi. Ni kwa sababu hii kwamba yeye anasema: “Suala letu ni gumu sana.” Yeye alikuwa anatambua pia kwamba haki ilikuwa ni ngumu hasa kwa watawala. Yeye kwa hiyo anasema: “Haki ni nzito sana juu ya watawala na kila haki ni nzito.” 115

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 115

9/4/2017 3:47:50 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Hata hivyo, iwe haki ni nzito juu ya watawala na watu mashuhuri au nyepesi, ilikuwa sio muhimu sana kwa Ali, kwa sababu akili yake na dhamira vilimlazimisha yeye kutokengeuka kutoka kwenye haki hata kidogo, na hakuwa ameambatanisha umuhimu wowote ule kwenye mambo mengine mbali na akili na dhamiri. Fikra na dhamiri vilimlazimisha Ali asigeuze uso wake mbali na watu ambao walitafuta uadilifu na sio kuwaacha wanaotawaliwa chini ya watawala ili kwamba watu waweze kustahimilia ugumu wa mahitaji, na kuteseka kutokana na njaa ambayo ingeweza kukausha maonjo yao na kuwasha moto kwenye matumbo yao. Fikra na dhamiri hii vilimuelekeza Ali asiziache neema na baraka mikononi mwa wale ambao matumbo yao yalikuwa yamejaa, na ambao walikula bila ya kusikia njaa na walikunywa bila ya kiu, na walioendesha maisha ya anasa kwa gharama ya watu wa chini. Hofu ya Ali kwamba wale watu mashuhuri na maarufu wasingevumilia njia na utaratibu wa haki wa serikali yake, kama alivyoelezea hapo kabla viapo vya utii havijachukuliwa kwake ilithibitika kuwa kweli. Hivyo, baada ya kuchukua kiapo cha utii, wale waungwana na watu mashuhuri walidai kutoka kwake kwamba wao wangepewa mafungu makubwa kutoka kwenye hazina ya umma ikilinganishwa na watu wengine, lakini yeye Ali alijibu: “Mimi sitatoa kwa mtu yoyote kitu ambacho yeye hastahili kukipata.” Talha na Zubeir walimjia ili kufanya mapatano na wakasema: “Sisi tuko tayari kuchukua kiapo cha utii kwako kwa masharti kwamba sisi tutakuwa washirika wako katika kuiendesha serikali.” Hata hivyo, Ali akawajibu kwa kinyume chake bila ya kusita. Walipolisikia jibu hili waliondoka wakamwacha na wakaanza kukusanya jeshi la kupigana dhidi yake, kama itakavyoelezwa kwa kirefu baadaye. Ali alijua vizuri kabisa kwamba Talha na Zubeir walikuwa watu wenye ushawishi mkubwa, na kwamba walikuwa na idadi kubwa ya wafuasi huko Kufa na Basra. Hata hivyo, ulikuwa ni uadilifu ambao Ali aliupenda zaidi. Yeye alisema: “Ninyi mnanitaka mimi nifikie mafanikio kwa njia ya ukandamizaji. Wallahi hilo kamwe halitakuwa. Uamuzi usio wa haki ni ubadhilifu.” Chakula hakiletwi mbele ya mtu ambaye ameshiba. Utajiri, mdogo au mkubwa, haukuwa ni halali mbele ya macho ya Ali mpaka uwe ulipatikana kwa njia ya halali. Usiwe umepatikana kwa njia ya kuhodhi, au kwa kuwanyonya watu au kwa kuchukua fursa isiyostahili ya nafasi ya mtu kama mtawala.

116

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 116

9/4/2017 3:47:50 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Ali alisamehe makosa mengi sana ya wahalifu na alivipuuza vitendo vingi viovu vya wakandamizaji, lakini hakuvumilia kwamba wenye kuhodhi wawanyonye au kuwadhulumu watu. Kwa mujibu wake yeye ugandamizaji ulikuwa ni laana kwa sura yoyote ile utakaojitokeza nayo, lakini udhalimu mbaya sana ulikuwa ni ule ambao ulifanywa na wale wenye nguvu juu ya wanyonge, na mlimbikizaji juu ya umma, na ule wa mtawala juu ya waliotawaliwa. Hakuweza kupuuza udhalimu ambao ungeweza kusababisha ufisadi na uovu katika jamii. Isome na kuichunguza ‘Nahjul-Balaghah’ na utaona jinsi maneno yake yalivyo makali wakati anapozungumza kuhusu unyonyaji wa watu. Aliitaja nukta hii katika kila hotuba yake. Maelezo yake yanaonyesha kwamba alikuwa ameshawishika kabisa kabisa kwamba unyonyaji wa mali za wengine ni kosa la kijamii. Yeyote anayejikusanyia mali kwa njia za haramu ni mkandamizaji na ni lazima aadhibiwe kwa ajili ya kosa lake. Katika moja ya hotuba zake, Ali anasema kuhusu wenye kuhodhi: “Na ni lazima akumbuke ule utajiri aliojilimbikizia na hakujali kuhusu ameipata kutoka wapi (yaani, hakutofautisha kati ya vyanzo halali na haramu) na akakusanya utajiri kwa njia halali na haramu. Ni lazima ajihakikishie kwamba yeye ataadhibiwa kwa kulimbikiza mali kwa njia za haramu.” Hata hivyo, kuhusu ulimbikizaji wa mali ambao haukutiwa dosari na unyang’anyi, ukandamizaji na kuhodhi yeye anasema: “Yeyote anayekufa huku akichuma kwa njia za halali atakufa katika hali ambayo kwamba Mwenyezi Mungu atakuwa amemridhia.” Ilikuwa ni kwa sababu hii kwamba Ali aliamua kwamba yeye atayabomoa majengo yote ambayo yalikuwa yamasimamishwa juu ya misingi ya uporaji na ukandamizaji, kukomesha ile desturi ya utumiaji mali ya hazina ya umma juu ya ndugu zake mtu, na hataruhusu lile tabaka la wenye uwezo kuwanyonya watu wa kawaida. Katika moja ya hotuba zake alitamka hivi kwa maneno ya wazi kabisa: “Angalieni! Yeyote ambaye alipewa ardhi yenye kulipiwa kodi (Jagir) na Uthman kutoka kwenye mali ya Allah lazima airudishe kwenye hazina ya umma kwa sababu hakuna chochote kinachoweza kutangua haki ya zamani. Kama ninakuja kutambua kwamba wanawake waliolewa kwa kutumia pesa za hazina ya umma au kwamba pesa zimegawanywa kwenye miji mbalimbali, juhudi yangu kubwa kabisa itakuwa ni kuzirudisha pesa hizo mahali pake pa asili. Uadilifu unakaba uwanja mpana, na kama uadilifu ni mgumu juu ya mtu, basi udhalimu utakuwa ni mgumu zaidi juu yake.” 117

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 117

9/4/2017 3:47:50 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Inawezekana kwamba wameweza kuwepo wafalme na watawala ambao hawakuweza kutoa kitu chochote kwa mtu asiyestahili kutoka kwenye hazina ya umma na ambao hawakutumia pesa za umma kwa wingi sana juu ya marafiki na ndugu zao. Hata hivyo, hatukutani na mmojawapo kama Ali, ambaye aliwalazimisha wale ambao wamekuwa matajiri kwa njia haramu wakati wa vipindi vya serikali zilizotangulia, kutoa maelezo juu ya mapato yao na kurudisha kwenye hazina ya umma ile mali ambayo waliichuma kiharamu. Kitendo hiki cha kijasiri cha Ali kinashuhudilisha kwamba yeye alikuwa na ujuzi mwingi wa hali ya mambo na alikuwa na imani kamilifu katika uadilifu wa kijamii kiasi ambacho hakuwa nacho mtu mwingine yoyote tena. Ikiwa sheria kwamba yule mtu tu, anayefanya kazi kwa bidii na kutoa huduma kwa jamii ndiye anayepaswa kulipwa ndio sahihi, basi linakuja kuibuka swali la ni huduma gani kwa jamii aliyoitoa Harith ibn Hakam; kwamba alipaswa kupewa dirham mia tatu elfu na Uthman kutoka kwenye hazina ya umma katika ile siku ndoa yake (Harith) ilipofanyika? Hivi kumuoa binti ya Uthman kulikuwa ni huduma kwa umma?27 Ni huduma gani ambayo Talha na Zubeir waliyoitoa kwa Waislamu ambayo fidia ya malipo yake wao walipata viwango vikubwa sana vya dirham na dinar na Jagirs kubwa kubwa kutoka kwa Uthman ambazo kama zingegawanywa miongoni mwa mamia ya maelfu ya Waislamu wote wangeweza kuwa matajiri na wangeweza kupata zaidi ya kile ambacho wangeweza kutegemea na kukitamani? 28 27

thman alitoa dirham mia tatu elfu kwa Harith ibn Hakam (ndugu yake Marwan) ambaye alikuwa mkwe wake U wa pili na mume wa binti yake Ayesha (Kitab al-Ansab, Baladhuri, Juz. 5, uk. 58). Baladhuri anasema mahali pamoja kwamba: Ngamia waliopokelewa kama Zakat walifikishwa mbele ya Uthman na yeye akawatoa wote kumpa Harith mwana wa Hakam (Kitab al-Ansab, Juz. 5, uk. 28). llamah Ibn Qutaiba, Ibn Abd Rabih na Ibn Abil al-Hadid wamesimulia kwamba Mtukufu Mtume alikuwa A ameutoa ‘Mihzuul’, mtaa wa masoko na maduka wa Madina kwa Waislamu lakini Uthman akautoa kwa Harith kama ardhi yenye kulipiwa kodi (Ma’arif, uk. 84, Aqd al-Faraid, uk. 261, Sharhul-Nahjul-Balaghah, Juz. 1, uk. 27). Uthman alifanya upendeleo kwa Harith katika njia tatu: 1). Alitoa dirham mia tatu elfu kwa Harith ingawa kiasi hiki hakikuwa mali binafsi ya Uthman bali kilikuwa kinahusika na hazina ya umma ya Waislamu. 2). Alimpa Harith ngamia wote ambao walikuwa wamepokelewa kama Zakat.

3). Alitoa kwa Harith kwa njia ya ardhi yenye kulipiwa kodi ile mali yote iliyokuwa imetolewa na Mtume kwa Waislamu. 28 Kwa sababu ya upendeleo uliofanywa na Uthman kwa ndugu zake, marafiki na washirika wake, wao wakawa matajiri sana. Kama matokeo ya utaratibu alioutwaa yeye katika suala la ugawaji wa mali, ambao ulipingana na Kitabu na Sunnah, na vilevile ule uliotwaliwa na watangulizi wake, watu hawa walijipatia eneo la kulipiwa kodi kubwa, wakajenga makasiri ya kifahari na wakalimbikiza viwango vikubwa vya mali. Zubeir Ibn Awam 118

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 118

9/4/2017 3:47:50 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Ni haki gani za upendeleo walizokuwa nazo Talha na Zubeir kwamba wawe aliacha nyuma yake (baada ya kufariki) nyumba kumi na moja ndani ya Madina, mbili huko Basra, moja huko Kufa na moja huko Misri. Alikuwa na wake wanne. Wao walirithi moja ya nane ya mali yake na kila mmoja wao alipata milioni moja na mia mbili elfu. ivyo mali yote aliyoiacha ilifikia kiasi cha milioni 59 na elfu 800. (Sahih Bukhari, Juz. 5, uk. 21). Ndani ya H Sahih Bukhari ni idadi tu iliyotajwa; haikuainishwa kama imma ilikuwa ni dirham au dinari, lakini imeelezwa ndani ya Tarikh Ibn Kathiir kwamba zilikuwa ni dirham. llamah Ibn Sa’d anaandika kwamba Zubeir alikuwa na eneo la ardhi kubwa huko Misri na majumba huko A Alexandria, Kufa na Madina. Yeye alipokea pia mapato kutoka kwenye vitongoji vya Madina. (Tabaqaat Ibn Sa’d, Juz. 2, uk. 77, kilichochapwa huko Leiden). as’udi anasema: “Zubeir aliacha nyuma yake, katika kufariki kwake, farasi elfu moja, watumwa na watumwa M wa kike elfu moja na makasiri mengi na maeneo yenye kulipiwa kodi - Jagirs. (Muruujul-Dhahab, Juz. 1, uk. 34). Talha ibn Ubaidullah aliacha nyuma yake mabuhar (mifuko ya ngozi za ng’ombe) mia moja iliyojaa dhahabu. Allamah Ibn Abd Rabih amemnukuu Khashni kuwa amesema kwamba Talha aliacha mifuko ‘buhar’ mia tatu ya dhahabu na fedha. Sibt Ibn Jauzi anasema kwamba yeye aliacha nyuma yake dhahabu ambayo ingeweza kubebeshwa juu ya ngamia mia tatu. (Tabaqaat Ibn Sa’d, Juz. 3, uk. 158, Muruuj-al-Dhahab, Juz. 2, uk. 444, Aqd al-Faraid, Juz.2, uk. 275 n.k.) llamah Baladhuri amesimulia kwamba katika zama za ujahilia, Hakam ibn Aas alikuwa jirani yake Mtume A na baada ya kufika kwa Uislamu alikuwa ni mmoja wa maadui wabaya kabisa na watesaji wa Mtume. Wakati Makkah ilipotekwa mnamo mwaka wa nane wa Hijiria yeye alikuja Madina. Kuna wasiwasi kama yeye alisilimu. Alikuwa akimfuata Mtume na kufanya ishara za kumdhihaki mbele yake, alimwigiza na kukunja kunja uso, na wakati Mtume alipokuwa akiswali yeye pia alisimama nyuma yake na kufanya ishara kwa vidole vyake. Matokeo yalikuwa kwamba lile umbile aliloliweka kwenye uso wake wakati akimwigiza Mtume likawa ni la kudumu na halikubadilika mpaka alipofariki. Pia alikuja kuwa mwendawazimu. iku moja, wakati Mtume alipokuwa amekaa na kupumzika nyumbani kwa mmoja wa wake zake, Hakam alianS za kuchungulia. Mtume akamtambua yeye. Alitoka nje ya nyumba hiyo na akasema : “Ni nani atakayeniokoa kutokana na mtu huyu aliyelaaniwa, mwenye kutetemeka”? Halafu akaongezea kusema: “Huyu Hakam pamoja na kizazi chake hawawezi kuishi mahali ninapoishi mimi.” Kwa hiyo akamhamisha Hakam na familia yake kwenda upande wa Taif. Wakati Mtume alipofariki, Uthman alimfuata Abu Bakr na maombi kwamba Hakam aweze kuruhusiwa kurejea Madina. Abu Bakr hata hivyo alikataa kukubaliana na ombi hilo akisema kwamba yeye hawezi kutoa kimbilio la amani kwa mtu ambaye alikuwa amefukuziwa uhamishoni na Mtume. Pale Umar alipokuja kuwa khalifa baada ya Abu Bakr, Uthman alimwendea na maombi yale yale, lakini yeye pia alimpatia majibu yale yale aliyokuwa amepewa na Abu Bakr. ata hivyo, wakati Uthman mwenyewe alipokuwa khalifa alimwita Hakam na watu wa nyumbani kwake wote H na akawarudisha Madina. Aliwaambia Waislamu kwamba yeye aliwahi kupendekeza kwa Mtume ili amruhusu Hakam na watu wa familia yake kurejea Madina na kwamba Mtume alimuahidi kwamba angetoa ruhusa kama hiyo lakini alifariki dunia kabla hilo halijaweza kufanyika. Waislamu hawakuamini alichokisema Uthman na walichukia sana kule kuwa amekwisha kumruhusu Hakam na kizazi chake kurudi Madina. (Kitab al-Ansab, Juz. 5, uk. 27) thman hakumrudisha tu Hakam kuja Madina na kumfanya kuwa mshauri wake mkuu, bali pia alitoa kumpa U yeye ile mali yote iliyokuwa imekusanywa kama Zakat na Sadaka kutoka kabila la Bani Quza’a. akati Hakam alipoingia Madina alikuwa amejifunika matambara yaliyochakaa na watu waliweza kuona ni W hali mbaya kiasi gani aliyokuwa nayo. Alikuwa na mbuzi mmoja pamoja naye, ambaye alikuwa amempanda. Aliingia kwenye baraza la Uthman akiwa kwenye hali hii. Hata hivyo, pale alipokuwa anaondoka mahali hapo alikuwa amevaa joho la thamani sana la manyoya na huku amejifunika na shuka la gharama kubwa la hariri. (Tarikh Yaquubi, Juz. 2, uk. 41) 119

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 119

9/4/2017 3:47:50 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

wameweza kupata maefu ya watumwa na vijakazi? Hata kama inakubalika kwamba waliingia katika Uislamu katika hatua zake za mwanzoni kabisa na kwamba walikuwa ndio masahaba mashuhuri wa Mtume na kwamba walikuwa wametoa utumishi mkubwa sana kwa Uislamu, wao walifanya hivyo kwa ajili ya llamah Baladhuri anasema: “Miongoni mwa matendo mengi ya Uthman ambayo yaliwaudhi watu, moja A lilikuwa hili kwamba alimpa madaraka Hakam ibn Aas ya kukusanya Zakat kutoka kwa Bani Quza’a, ambayo ilifikia kiasi cha dirham mia tatu elfu, na pale Hakam alipozikusanya fedha hizi na kuzileta kwa Uthman, yeye alizitoa kiasi chote hicho kwake Hakam.” (Tarikh al-Ansab, Baladhuri, Juz. 5, uk. 28). llamah Yaquubi anasema kwamba Uthman alimuozesha binti yake kwa Abdullah ibn Khalid ibn Asiid na A akaamuru kwamba dirham mia sita elfu zitolewe kupewa yeye Abdullah. Alimwandikia Abdullah ibn Aamir kwamba kiasi hiki kiweze kilipwa kutoka kwenye ile hazina ya umma iliyoko huko Basra. (Tarikh Yaquubi, Juz. 2, uk. 145). llamah Ibn Abd Rabih Qartabi, Allamah Ibn Qutaibah na Allamah Ibn Abil-Hadiid wameandika kwamba UthA man alitoa dirha mia nne elfu kwa Abdullah (Aqd al-Farid, Juz. 2, uk. 261. Ma’arif, uk. 84. na Sharh NahjulBalaghah ya Ibn Abil-Hadiid, Juz. 1, uk. 66). oja ya tano (khums) ya ngawira ya kivita ambayo ilipokelewa kama matokeo ya vita vya ki-Afika ilifikia kiasi M cha sarafu za dhahabu mia tano. Uthaman alikitoa kiasi hiki chote kwa Marwan ibn Hakam, ambaye alikuwa ni binamu na mkwe wake, akiwa mume wa binti yake Umm Ayan. llamah Ibn Athiir anaandika hivi: “Khums (moja ya tano) ililetwa Madina, kutoka Afrika na Marwan akainunua A kwa thamani ya dinari mia tano elfu. thman alimsamehe kutokana na kufanya malipo ya kiasi hiki. Hiki kilikuwa ni moja kati ya vile vitendo vya U Uthman ambavyo vilishutumiwa na watu hapo baadaye. (Tarikh Yaquubi, Juz. 3, uk. 38). llamah Baladhuri na Ibn Sa’d wamesimulia kwamba Uthman aliitoa kwa Marwan ile “khums” ambayo iliA pokelewa kutoka kwenye vita vya Misri, na pia aligawa kiasi kikubwa cha fedha juu ya ndugu zake. Alivielezea vitendo hivi kwa kusema kwamba yeye ameonyesha huruma kwa jamaa zake. Watu hawakuvipenda vitendo hivi vya Uthman kabisa na walimshutumu. (Tabaqat ibn Sa’d, Juz. 3. uk. 24 – kilichochapishwa Leiden; na Kitab al-Ansab, Baladhuri, Juz. 5, uk. 25). thman alitoa dirham mia moja elfu kwa Sa’d ibn Aas. Ali, Talha, Zubeir, Sa’d ibn Waqas na Abdul-Rahman U ibn Awf walifanya mazungumzo naye kuhusiana na hili. Yeye, hata hivyo, aliwaambia kwamba Sa’d alikuwa ni ndugu na jamaa yake, na kwa kumpa kiasi hicho kilichotajwa, yeye alionyesha huruma kwa ndugu yake. (Kitab al-Ansab, Juz. 5, uk. 28). litoa kiasi kikubwa cha fedha kutoka kwenye hazina ya umma kumpa Walid ibn Uqba ibn Abi Muiit ambaye A alikuwa ni kaka yake kwa upande wa mama yake. llamah Baladhuri anasema: “Wakati Walid alipoteuliwa kama gavana wa Kufa, Abdullah Ibn Mas’ud alikuwa A ndiye msimamizi wa hazina ya umma. Walid aliazima kiasi kikubwa cha fedha kutoka kwenye hazina hiyo. Watawala walitumia kuazima kwa njia hii na kurudisha pale walipopata mishahara yao. Baada ya siku chache, Ibn Mas’ud alizidai fedha hizo zirudishwe. Walid akalalamika kwa Uthman dhidi ya madai haya ya Ibn Mas’ud. Hapo Uthman akamwandikia Ibn Mas’ud: “Wewe ni mtunza hazina tu. Usimshinikize Walid kurudisha fedha alizoziazima yeye. Haifai kupingana naye.” (Kitab al-Ansab, Juz. 5, uk. 1). iku ambayo Uthman alifanya dirham mia moja elfu zilipwe kwa Marwan kutoka kwenye hazina ya umma, S alifanya pia dirham mia mbili elfu zilipwe kwa Abu Sufyan. (Sharh Nahjul-Balaghah, cha Allamah Ibn AbilHadiid, Juz. 8, uk. 27). llamah Ibn Abil-Hadiid anasema kwamba Uthman aliitoa ngawira yote iliyopokelewa kutoka sehemu mbalimA bali za Afrika, ambako vita vilikuwa vimepiganwa, kwa kaka yake wa kunyonya, Abdullah bin Abi Sarha na kwa kuwaacha Waislamu wengine wote. (Sharh Nahjul-Balaghah, Juz. 1, uk. 27). 120

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 120

9/4/2017 3:47:50 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Mwenyezi Mungu na wangetegemea malipo yake kutoka kwa Mwenyezi Mungu huko Akhera. Mwenyezi Mungu huwa haziachii juhudi za waja wema kupotea tu vivi hivi. Huduma au utumishi wowote walioutoa kwa Uislamu, wao waliutoa kwa kuzitafuta radhi za Mwenyezi Mungu na ni Yeye ambaye hutoa malipo bora zaidi. Bali ni haki gani maalum waliyokuwa nayo juu ya hazina ya umma ambamo Waislamu wote walikuwa na haki sawa? Ni vitendo gani vya ustawi wa jamii vilivyotendwa na ndugu zake Uthman ambavyo kwa malipo juu yake aliiacha wazi milango ya hazina ya umma kwa ajili yao, akakabidhisha uendeshaji wa dola kwao, akawafanya mabwana wa maisha, mali na heshima za Waislamu na kuwaruhusu kutumia kila kitu kwa namna yoyote waliyoitaka wao? Mmoja wa ndugu zake hawa alikuwa ni Mu’awiyah, ambaye alikuwa anavuma kwa sifa mbaya ya kuchukua rushwa na mahongo. Na walikuwepo ndugu wengi wengine na marafiki zake, ikiwa ni pamoja na Hakam mwana wa Aas na Abdullah ibn Sa’d. Ni utumishi gani ambao Mu’awiyah alikuwa ameutoa kwa Uislamu, ambao kama malipo kwa ajili hiyo yeye alifanywa kuwa gavana wa Palestina na Hamas, mbali na Syria, na alikuwa pia amekabidhiwa ukamanda wa vikosi vya majeshi vine? Ni kutoka wapi ambako ndugu zake Uthman walipata utajiri mkubwa kama huo waliokuwa nao, na vipi walisimamisha makasiri ya kifahari katika miji na vijiji vyote? Wakati watu hawa hawakutoa utumishi wa umma wa aina yoyote ile, ni wapi walikopata mitaji ya kugharimia miradi hii? Kama mtu anakuwa na mali ya kupora kwa muda mrefu, yeye hawezi kuwa mmiliki wake wala utajiri huo hauwezi kuwa ni mali yake binafsi. Uwongo hauwi ukweli endapo kama utashadidi kwa muda mrefu. Ni kwa sababu hii kwamba Ali alikuwa ameamua irudishwe kwenye hazina ya umma, ile ardhi na mali yote ambayo ilikuwa imetolewa na Uthman kwa watu wasiostahiki kwa kuwanyima wale wanaostahili mali hizo, ingawaje utajiri huo ungeweza kuwa umetawanywa kwenye miji tofauti au kutolewa kwa wanawake kama mahari zao. Uadilifu ni njia ya ustawi na starehe kwa watu na hauwezi kuwekewa mipaka au kufungiwa. Jambo jingine ambalo linahitaji mazingatio ni hili kwamba, Ali alizichukulia zile ardhi ambazo zilikuwa zimefanywa kuwa mali binafsi na watu kwa sababu ya kuwa kwao ni ndugu au wapenzi wa Uthman, na vile vile yale manufaa yaliyopatikana ku121

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 121

9/4/2017 3:47:50 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

tokana nazo, kuwa ni mali ya unyang’anyi. Ali alijua vizuri kabisa ndugu wa Uthman walikuwa ni watu wa aina gani. Alikuwa anatambua kwamba baada ya kujitwalia ardhi hizo watalazimisha kazi za nguvu kutoka kwa watu wa chini na kujikusanyia mazao yake, na wangejipatia mali zaidi kwa kipato hicho. Hivyo mitaji yao ingeongezeka siku baada ya siku na pale ambapo wengine wangeendelea kuwa masikini zaidi, wao wenyewe wangezidi kuwa matajiri zaidi na zaidi. Halafu hawa wamiliki ardhi wakubwa wangenunua ardhi za wamilikaji wadogo na hatimae ni matabaka mawili tu yangebakia, yaani, mabepari na wale masikini ambao wangekuwa wategemee juu ya tabaka hili la mabepari na kuwatumikia. Katika maelezo yake kwa ajili ya Malik Ashtar, Ali anasema: “Tahadhari! Usije ukatoa ardhi kwa yeyote kati ya washirika na ndugu zako. Asije akategemea mtu kutoka kwako kwamba wewe utamruhusu kukalia ardhi ambayo ina madhara juu ya watu wa jirani yake katika suala la umwagiliaji au jambo lolote la kawaida, ili aweze kuutupa mzigo wote utokanao na hapo juu ya wengine.” Hofu ya Amirul-Mu’minin kuhusu hizi ardhi zenye kulipiwa kodi zilizotolewa kwa watu – Jagirs – ilithibitisha kuwa kweli. Watu wale walichukua kazi za kulazimisha kutoka kwa watu chini na wakawagandamiza kwenye kila aina ya udhalimu na uovu. Dr.Taha Husein anaandika katika juzuu ya kwanza ya kitabu chake kiitwacho ‘Al-Fitnatul-Kubra’: “Kwa upande mmoja walikuwepo wamiliki ardhi wakubwa na waungwana na kwa upande mwingine walikuwepo wale watu masikini ambao walikuwa ni watumwa wa hili tabaka la wamiliki ardhi na waungwana. Kutokana nao likazuka tabaka jipya katika Uislamu, yaani, wale waliokuwa wakuu wa taifa kwa mujibu wa mila na desturi za kikabila zilizokuwepo ndani ya Peninsula ya Arabia, na sasa limekuwa linatambulika zaidi na kuheshimiwa zaidi kwa sababu ya utajiri mwingi na idadi kubwa ya washiriki. Kulingana na Ali, wote wanayo haki ya kugawana ile faida ambayo inatokana na dhahabu na ardhi na ni yule mtu tu ambaye anafanya kazi kwa bidii zaidi na pia ni mhitaji zaidi, aliye na haki ya fungu kubwa. Yeyote anayeukataa ukweli huu anafanya usaliti kwa watu wake. Machoni kwa Ali usaliti ulio mkubwa zaidi ni ule usaliti unaofanyiwa umma. Ali anaona kwamba mtu anayefanya usaliti kwa umma kuwa yu duni na mwenye kusta122

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 122

9/4/2017 3:47:50 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

hili kudharauliwa. Kamwe yeye hakuwategemea watu kama hao na kamwe hakushirikiana nao. Ali alijitahidi kulinda haki za watu kwa kiwango cha hali ya juu kabisa. Wakati wowote yeye alipofanya maamuzi hakuna aliyeweza kumfanya akengeuke kwenye haki hiyo. Yeye hakujali kama watu wangemkimbia na kujiunga na adui yake. Yeye alikuwa ni mfano halisi wa haki, na kila alichokisema kilikuwa ni uadilifu kamili. Ali hakuonyesha upendeleo wa kiutendaji hata kwa wale masahaba wa Mtume watiifu, ambao walishiriki katika vita pamoja na yeye. Yeye anasema: “Tahadharini! Kuna watu miongoni mwenu ambao dunia imewafanya wastawi. Wamejitwalia ardhi na wamechimba mifereji. Wanawapanda farasi wenye nguvu na afya na wanayo idadi kuwa ya watumwa na vijakazi. Kama kesho nitawakataza kufanya mambo ambayo wamezama ndani yake, na nikawazuia kwenye haki za watu ambazo wao wanatambua kabisa, hawapaswi kulalamika kwamba Ali amewanyima uhuru wao. Kumbukeni! Imma wawe Muhajir au Ansari, yeyote kutoka miongoni mwao anayefikiri kwamba yeye ni bora juu ya wengine atakuwa amekosea. Ubora utaamuliwa juu yake mbele ya Mwenyezi Mungu katika Siku ya Kiyama. Ni Mwenyezi Mungu tu anayewalipa watu. Kumbukeni! Yeyote ambaye amemkubali Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, akaithibitisha jumuiya yetu, akajiunga na dini yetu na akaelekea kwenye qibla chetu, huyo anastahili yake kwenye haki na wajibu wa Uislamu. Ninyi wote ni waja wa Mwenyezi Mungu na utajiri huo ambao ni wa Mwenyezi Mungu utagawanywa miongoni mwenu sawa sawa. Hakuna mwenye ubora mbele ya mwingine. Watu waadilifu na wachamungu wao watapata malipo bora zaidi kutoka kwa Mwenyezi Mungu.” Utendeaji huu wa usawa uliotolewa na Ali kwa watu wa chini, uliwafanya wale watu waungwana na mashuhuri, miongoni mwa Quraishi kumwacha Ali na kujiunga na Mu’awiyah kama itakavyoelezwa kwa kina baadaye. Ilikuwa haiwezekani kwa Ali kuwapendelea wale waliokuwa na nafasi za juu kuliko wale ambao walikuwa wa hali ya chini wakilinganishwa nao, kwa sababu kwa kulingana na yeye, kigezo cha wema na ubora kilikuwa sio kile kilichokuweko katika siku zake. Yeye hakumpendelea Mquraishi kuliko asiyekuwa Quraishi au Mwarabu kwa asiyekuwa Mwarabu, kwa sababu yeye aliwachukulia watu wote kuwa ni ndugu wa kila mmoja wao. 123

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 123

9/4/2017 3:47:50 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Yeye hakuweza kuwabembeleza wale machifu na waungwana kama Mu’awiyah alivyofanya, wala hakuweza kuwavuta watu upande wake mwenyewe kwa njia ya mali ya Waislamu. Malik Ashtar alimwambia Amirul-Mu’minin: “Ewe Amirul-Mu’minin! Tulijiunga na watu wa Basra na Kufa na tukafanya jihadi dhidi ya watu wa Basra. Kwa wakati ule wote tulikuwa na wazo moja. Baada ya hapo tofauti zikazuka. Dhamiri zao zikawa dhaifu na idadi yao ikapungua. Wewe ni mwadilifu kwa wote na unafanya kulingana na kilichokuwa sawasawa. Hatimaye waliogopa kwa sababu ya uadilifu wako. Kwa upande mwingine waliziona sera na mbinu ambazo Mu’awiyah anazitwaa kuhusiana na wale matajiri na waungwana, kwa sababu kuna watu wachache sana duniani ambao hawana tamaa na manufaa ya dunia. Wako wengi wanaonunua upotofu kwa thamani ya ukweli na kuitwaa dunia. Endapo kwa hiyo, utagawa utajiri kwa ukarimu mno miongoni mwa watu na ukatoa zaidi kwa watu maarufu utaona jinsi shingo zao zitakavyokuwa zinaelekea kwako na jinsi wanavyoimba nyimbo za kukusifu na kuwa watakia wema wako. Mwenyezi Mungu akusahilishie mambo yako na atawanyishe na kuudhoofisha ushirikiano na ulaghai wa maadui zako. Yeye Mwenyezi Mungu kwa hakika anatambua juu ya matendo yao.” Ali akasema katika kumjibu: “Umesema kwamba mimi ninatenda kwa mujibu wa uadilifu. Sababu ya hilo ni kwamba Mwenyezi Mungu anasema: “Yeyote anayetenda matendo mema anayafanya hayo kwa faida yake na yeyote anayetenda matendo maovu atateseka kwa sababu ya matendo hayo. Mwenyezi Mungu hazidhulumu nafsi za waja Wake.” “Kama nitaikiuka kanuni hii, ninahofia kwamba nitateseka kwa sababu hiyo. Na kuhusu kusema kwako kwamba baadhi ya watu wametutelekeza kwa sababu haki haivumiliki kwao, Mwenyezi Mungu anajua vizuri zaidi kwamba wao hawakutuacha sisi kwa kuwa tumekuwa madhalimu juu yao. Na pia sio hivyo kwamba baada ya kutuacha sisi wametafuta kimbilio kwa mtu mwadilifu. Hakuna sababu ya kututelekeza kwao isipokuwa kwamba wametafuta dunia ya anasa na dunia hii sio ya kudumu. Hiyo Siku ya Hukumu wao watakuja kuulizwa kama walitafuta dunia au walishughulika kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Sasa kuhusu kutumia kwetu fedha ili kuwavutia watu hilo sio halali kwetu kumpa mtu yoyote kutoka kwenye mali ya umma zaidi ya kile anachopaswa kupata. (Na 124

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 124

9/4/2017 3:47:50 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

mimi sijali kama idadi ya wafuasi wangu ikipungua kwa sababu ya kuwa kwangu mwadilifu), Mwenyezi Mungu anasema hivyo, na anachokisema Yeye ndio sahihi: “Watu wengi ambao ni wachache kwa idadi wanawashinda wale ambao ni wenye nguvu kiidadi. Mwenyezi Mungu yuko pamoja na wenye subira.” “Mwenyezi Mungu alimteua Mtume kwenye kazi ya Utume wakati alipokuwa yuko peke yake kabisa. Alikuwa na wafuasi wachache na halafu idadi yao ikaongezeka. Aliweka heshima juu ya kundi lake baada ya wao kuwa wamedhalilishwa. Kama Mwenyezi Mungu akipenda kutoa malipo bora kwenye mambo yetu atayatatua matatizo haya na kuyafanya mambo yawe mepesi juu yetu.” Kiini cha sera zake na utaratibu wa serikali yake kimejumuishwa katika taarifa yake aliyoiandika na kumpa Malik Ashtar wakati akimteua kuwa gavana wa Misri. Yeye alisema ndani yake humo: “Jihadhari! Usijitwalie binafsi vile vitu ambavyo watu wote wana haki sawa.” Haki za umma ni zile ambazo zinatolewa kwa raia wote sawasawa na hizo ndizo haki ambazo Ali amezigusia katika maneno yake ya hapo juu. Kuwasaidia Wenye Haja Kuna zile haki za kawaida ambazo ziliheshimiwa na Ali mwenyewe na pia alizoweka ushawishi juu ya wengine kuziheshimu. Kulingana na yeye, wajibu halisi wa magavana wa majimbo na watumishi wengine ulikuwa kwamba wazilinde haki hizi na wasiruhusu zisiingiliwe kati. Kama Ali alimteua mtu yoyote kuwa mtawala au alimuondoa kwenye kazi yake, basi ilikuwa ni kwa sababu hii. Kwa mujibu wake yeye haki hizi zilibeba maana pana sana, na zilikuwa ni za aina nyingi. Madhumuni ya zote hizo yalikuwa, hata hivyo, ni kwamba mahitaji ya kila mtu lazima yatimizwe na asibakie mtu yoyote kuwa na njaa, kwa sababu kubaki na njaa ndio fedheha kubwa mno kwa ubinadamu. Hakuna ubaya katika kukiuka sheria ambazo haziwezi kuondoa ufukara wa watu. Kama ilivyo katika kanuni za imani ya Ali, ibada isimtenganishe mtu na jamii na dini ina maana ya tabia nzuri kwa watu, na imani halisi za kidini ni zile ambazo zinakuza na kuendeleza uadilifu, kwa namna ile ile ambayo sheria lazima iwe kiasi kwamba inatimiza mahitaji ya watu na kuhakikisha ufutaji wa ufukara na umasikini, ili kwamba mwanadamu asiweze kufedheheshwa mbele ya macho yake mwenyewe na akawa amevunjwa moyo. 125

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 125

9/4/2017 3:47:50 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Sio upendeleo bali ni haki ya mtawala na mtoa sheria na kutekeleza ilivyo sheria ambazo zinawaondolea watu shida na umasikini, na wanastahili kudai sheria kama hizo kutoka kwake. Ali alizilinda haki za watu kwa uangalifu sana kwamba takriban haiwezekani kukuta hotuba yoyote, mazungumzo au kauli yake yeye ambayo inaweza kuwa haikutaja haki hizi na inayowezakuwa haikuvuta mazingatio ya magavana na watumishi wengine kwayo. Kuyatimiza mahitaji ya watu bila shaka kulikuwa ndio wajibu mkubwa wa mtawala na mtoa sheria na ndio haki kubwa kabisa machoni kwa Ali. Alikuwa ni Ali ambaye aliziona dhambi kubwa za Kaisari na Kisra kuwa ni hizi hasa (ingawa orodha ya madhambi yao ilikuwa ndefu mno) kwamba waliwadhalilisha raia zao, hawakuziangalia haki zao, waliwanyima neema za ardhi na starehe za maisha na walijaribu kuwafanya masikini na wenye kustahili kudharauliwa. Yeye anasema: “Fikiria misukosuko na dhiki za watu wakati Kaisari na Kisra walipokuwa ndio watawala wao. Walikuwa wamewafukuza kwenye ardhi zenye rutuba na kwenye maji na sehemu zenye kustawi za Iraq na wakawahamishia kwenye eneo ambapo kulikuwa hakuna uoto na mimea na ambako hakukuwa na chochote zaidi ya pepo kali, na waliwafanya masikini na mafukara sana.” Wakati wowote gavana au mtumishi alipofanya kosa la kuvunja dhamana ya mali ya umma (hata kama kiasi kilichohusika kilikuwa kidogo au kikubwa namna gani) Ali alimtishia kwa adhabu kali. Yeye alikuwa akihuzunika sana wakati na pale alipokuja kujua kwamba gavana au mtumishi amepora mali au amekuwa na hatia ya kuhodhi, na alimkemea kwa hali ya ukali sana. Wakati mmoja aliandika kwa gavana mmoja hivi: “Ninaelewa kwamba umepora ardhi ambayo ni mali ya hazina ya umma na umejitwalia kilichokuwa chini ya miguu yako na umekula kilichokuwa kiko mikononi mwako. Unapaswa kwa hiyo, unitumie maelezo yako.” Hiki kifungu cha maneno “nitumie maelezo yako” katika barua ya AmirulMu’minin yanastahili mazingatio. Sentensi hii inabeba maana pana sana. Alikuwa hodari sana kusimamia uadilifu kiasi kwamba hakuweza kuvumilia kisingizio chochote au uzembe katika hili. Mbali na kuwa na imani thabiti, Ali alikuwa mchunguzi mpambanuzi na alikuwa akiitambua wazi miujiza ya jamii ya mwanadamu, na uhusiano wa pamoja wa watu. Alizijua ni haki gani zilizoingiliwa kati ndani yake na ni zipi ambazo zitakuja 126

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 126

9/4/2017 3:47:50 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

kuingiliwa juu yake. Alitambua wazi kwamba udhalimu na ukandamizaji ulikuwa ni hatari kwa jamii kwa ndani hata kwa nje, na wale waonevu na wenye kuonewa walikuwa wakitishiwa na hatari kubwa kubwa. Yeye alichukulia kutetea uadilifu na utekelezaji wake kuwa ni lazima kabisa ingawaje kutachukiwa na magavana na watumishi. Aliandika kwa kukereka sana: “Nitumie maelezo yako.” Alijulishwa kuhusu gavana mwingine kujitwalia mali ya umma. Alimwandikia mara moja kama ifuatavyo: “Muogope Mwenyezi Mungu na urudishe hiyo mali ya watu kwao wenyewe. Kama hutafanya hivyo na halafu Mwenyezi Mungu akanijaalia udhibiti juu yako nitajitoa mwenyewe kwenye wajibu katika suala hilo na nitakupiga kwa upanga wangu, na yeyote aliyewahi kuwa mawindo yake siku zote alikwenda moja kwa moja Jahannam. Wallahi, hata kama Hasan na Husein wangefanya kile ulichokifanya wewe nisingekuwa na huruma juu yao na wasingeweza kuwa na uwezo wa kunifanya mimi niridhie matilaba yao yoyote mpaka nitakapokuwa nimeirudisha ile haki (ya wengine) kutoka kwao na nikawa nimefutilia mbali yale matokeo yanayotokana na udhalimu.” Amirul-Mu’minin alimtuma mtu aliyeitwa Sa’d kwa Ziad ibn Abih kwenda kuleta pesa fulani ambazo zilikuwa zimelala kwake. Yeye Amirul-Mu’minin alikuwa amepata habari kwamba Ziad alikuwa akiendesha maisha ya anasa na kwamba alikuwa akilimbikiza mali mwenyewe, alikuwa hakuwapa chochote wajane, mayatima na mafukara. Wakati Sa’d alipomwendea Ziad na kudai pesa hizo, Ziad alifanya kiburi na akamkaripia. Sa’d alirudi na akamjulisha Amirul-Mu’minin Ali kuhusu nini kilichokuwa kimetokea huko. Papo hapo Ali aliandika barua kwa Ziad kwa mistari hii ya maneno: “Sa’d amenijulisha kwamba umemkaripia bila ya uhalali wowote na ukashughulika naye kwa majivuno na kiburi, licha ya ukweli kwamba Mtume amesema kuwa Ukuu ni wa Mwenyezi Mungu pekee na yeyote ambaye anakiburi anajipatia ghadhabu Yake. Sa’d vilevile amenijulisha kwamba wewe unakula chakula cha aina mbalimbali na kujitia manukato kila siku. Ni madhara gani yatakayoongezeka kwako endapo utafunga kwa siku chache kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kutoa sehemu ya mali yako kama sadaka katika njia ya Mwenyezi Mungu, na kula kwa mara nyingi kile chakula unachokula mara moja, au kumfanya mtu masikini kukila chakula hicho. “Wewe, ambaye unabiringika katika neema, huwaangalii majirani zako masikini, wanyonge na wajane wenye haja na mayatima. Je unapenda, mbali na yote haya, 127

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 127

9/4/2017 3:47:50 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

kwamba upate thawabu za watu waadilifu ambao wanatoa zakat? Sa’d ameniambia pia kwamba wewe unaongea kama mwadilifu lakini unatenda kama mtu mwovu? Kama kweli ukifanya hivyo, umekuwa mkatili juu ya nafsi yako mwenyewe na umeyapoteza bure matendo yako. Unapaswa kutubia mbele ya Mwenyezi Mungu na ubadili mwenendo wako na kurekebisha vitendo vyako. Utangulize mbele mali yoyote ya ziada uliyonayo kwa ajili ya siku ambayo utakuja kuihitaji mali hiyo, kama kweli wewe ni muumini wa kweli. Na utumie manukato kwa siku zinazopishana nayo isiwe zaidi sana. Mtume amesema: “Tumieni manukato kwa siku za kupishana na msiyatumie kwa wingi sana. Amani iwe juu yako.” Amirul-Mu’minin alituma maagizo mfululizo kwa magavana na kuwaonya vikali sana dhidi ya matumizi mabaya ya mali ya umma na kupokea rushwa. Aliziona shughuli kama hizo kuwa ndio uhusiano mbaya kabisa baina ya watawala na watawaliwa wao, na kizuizi kikubwa kati ya haki na mwenye kustahili haki. Alikuwa anatambua vizuri kabisa madhara ambayo tabia hizi mbaya zingeweza kuyafanya kwa watu. Wakati mmoja alipokea taarifa kwamba afisa mmoja wa jeshi alikuwa amepokea hongo. Alimshika mkono wake na akaupa mtingishiko mkali kiasi kwamba ulikuwa karibu ung’oke kutoka mwilini mwake. Halafu akamwambia: “Watu wa kabla yako waliangamizwa kwa sababu waliwanyima watu haki zao na wakawa, kwa hiyo, wamelazimika kuzipata haki zao kwa kutoa rushwa. Waliwalazimisha watu kufanya mambo yasiyo na maana ambapo matokeo yake yakawa uongo ukashamiri.” Wakati mmoja gavana alialikwa kwenye karamu. Gavana huyo akaukubali mwaliko huo na akashiriki katika tafrija hiyo. Wakati Amirul-Mu’minin alipokuja kugundua kuhusu hili, alimkemea yule gavana vikali sana akisema: “Kumkirimu gavana ni rushwa. Kwa nini rushwa hii ilitolewa? Kama ilitolewa ili kuthibitisha haki fulani, basi ni wajibu wa gavana kuwapatia wale watu wanaostahili haki zao bila ya kupokea rushwa, au rushwa hii ilitolewa ili kuhalalisha kitu fulani ambacho ni batili. Kama hivyo ndivyo, sio halali kwa gavana kufanya jambo lolote kama hilo hata kama dunia yote ingetolewa kwake kama rushwa.” Jambo la pili ni kwamba: kwa nini gavana huyo alishiriki katika karamu ambamo matajiri walialikwa lakini masikini wakapuuzwa na hivyo ukafanyika ubaguzi kati ya waja wa Mwenyezi Mungu? Ubaguzi huu uliwaudhi watu wengi na pia ulimhuzunisha Ali. Kwa kweli kama jamii imestawi na watu wakawa wana hali nzuri za kimai-

128

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 128

9/4/2017 3:47:50 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

sha hakuna ubaya katika kuwaalika baadhi ya watu tu kwenye tafrija na kuwaacha wengine. Hata hivyo, kama hali ziko katika namna kwamba kuna watu masikini na matajiri pia katika jamii, hivi karamu, uenezi wa mwaliko huo kwa gavana kushiriki katika karamu haulingani na kutoa rushwa kwake? Watu wengine wanaweza kufikiri kwamba ukali kama huo upande wa Ali kuhusiana na magavana na watumishi ulikuwa haufai, na wao hawakustahili kulaumiwa na kukaripiwa kwa namna hii. Hata hivyo, ikiwa watu kama hao watatambua huduma zilizotolewa na Ali kwa maafisa hao ambazo zilifanya kusiwe na lazima kabisa juu yao wao kupokea rushwa au kukimbilia matumizi mabaya ya fedha, watakubali kwamba ukali ulioonyeshwa na Ali kwa maafisa hao haukuwa bila haki. Jambo jingine pia linahitaji mazingatio hapa na ni kwamba, Ali hakuona inaruhusika kwamba maafisa hao waweze kuchukua fursa ya vyeo vyao kuhusiana na umma hata kwa kiwango cha karamu, kwa sababu fursa kama hiyo pia inalingana na wizi au rushwa. Na wakati ambapo Ali hakuwa amemruhusu mtumishi kukubali mwaliko wa kwenye karamu kwa njia ya rushwa, yeye angewezaje kuvumilia kwamba afisa huyo aweze kujitwalia mji wote yeye mwenyewe au achukue mali ya watu kutoka kwao kwa njia ya rushwa? Mtu anayeona mbali, ambaye ametupia jicho kwenye hali halisi anawajibika kukalikia na kuukomesha uovu upesi sana. Kizuizi juu ya watumishi kilianza katika siku za Ali na sio katika siku za Uthman. Ali alitoa mishahara minono sana kwa magavana ambayo ilitosheleza kwa mahitaji yao. Kusingekuwa kwa hiyo, na uhalali wowote wa kupokea kwao rushwa. Kama Ali alikuwa mkali kwa maafisa madhalimu, alikuwa pia ni mchangamfu kwa wale waadilifu. Alizitambua haki zao na aliwatia moyo kwa utii wao kwa Imam wao na kwa huduma zao kwa Waislamu. Barua ambayo aliiandika kwa Umar ibn Abi Salma, gavana wa Bahrain, ambapo alimuondoa kwenye kazi yake na kumtaka aje kwake ili afuatane naye kwenye mapambano ya Syria inastahili kuchunguzwa. Alimwandikia hivi: “Nimeyakabidhi madaraka ya ugavana wa Bahrain kwa Nu’man ibn Ajlan Zarqi na nimekuondoa wewe katika kazi hiyo.

129

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 129

9/4/2017 3:47:51 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Hata hivyo, mimi sikufanya hivyo kwa sababu umeonekana kutoimudu au kwa sababu umeshutumiwa kwa jambo lolote baya. Ukweli ni huu kwamba umeendesha utawala huo kwa uwezo na kwa uaminifu kabisa. Unapaswa kwa hiyo, kuja huku na kujiunga nami. Hakuna jambo lolote dhidi yako. Hali halisi ni hii kwamba mimi nimeamua kutoka dhidi ya waasi wa Syria na ninapenda kwamba wewe uweze kuwa pamoja nami kwa sababu wewe ni mmoja kati ya wale watu ambao wanaweza kunisaidia mimi katika kupigana na adui na kuisimamisha nguzo ya dini.” Wakati wote aliitwaa sera hii madhubuti kuhusiana na watumishi. Aliwapa moyo wale waadilifu na kuwa mkali kwa wale waliofanya vitendo viovu. Yeye kamwe hakuyumba wala hakukata maneno wala kukimbilia kwenye njama au udanganyifu. Lengo lake halisi lilikuwa ni ustawi wa Waislamu na usimamishaji wa uadilifu miongoni mwa wote, imma wawe ni watawala au wale wanaotawaliwa. Wale watumishi ambao hawakutumia vibaya fedha za umma, na ambao hawakupokea rushwa, walipokea mishahara yao kutoka kwenye hazina ya umma kulingana na mahitaji yao, na Amirul-Mu’minin aliwasifu na kuwatia moyo. Na kuhusu wale watumishi wasiokuwa waaminifu, hata hivyo, Ali aliwakaripia na kuwalaumu kwanza na halafu akawafukuza. Na kama makosa yao yalikuwa mabaya zaidi aliwahukumu pia kifungo. Mbali na magavana walikuwepo baadhi ya watu ambao walikuwa wamepora mali za wengine na walikuwa wamelimbikiza viwango vikubwa vya mali kwa njia za haramu. Amirul-Mu’minin aliwashurutisha kujieleza kinagaubaga na hakuwaonyesha huruma hata kidogo. Aliupinga kwa nguvu sana ulafi wao wa kulimbikiza mali na maisha yao ya kupenda raha na anasa, na alijitahidi kuwa ukuta kati yao na mali zao ambazo walikuwa na bidii ya kuziongeza. Alipinga kwa maneno na pia kwa vitendo uporaji wa mali ya wengine na alikataza kwa ukali kabisa kuhodhi. Katika wasia aliomuandikia Malik Ashtar aliandika kama ifuatavyo: “Liweke hili pia katika mazingatio kwamba wengi wa watu hawa wana tabia ya ubahili na uchoyo. Wanahodhi ili kupata faida na wanapunja vipimo na kutoza bei kubwa. Jambo hili ni hatari kwa watu na ni udhaifu wa watawala. Wewe unapaswa kwa hiyo, kuwazuia kutokana na kuhodhi kwao.” Kisha anasema: “Kama mtu ana hatia ya kuhodhi baada ya kuwa wewe umelikataza hilo ni lazima umuadhibu, lakini lazima uhakikishe kwamba hakuna kuzidisha au kuonea kunakofanyika katika utekelezaji wako.” 130

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 130

9/4/2017 3:47:51 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Na kuhusu kukaliwa na watu kwa maeneo yanayolipiwa kodi – Jagir – na ardhi nyingine, maoni yaliyoshikiliwa na Ali yalikuwa yanakubaliana na mantiki na pia chanzo cha maadili. Tumekwisha lijadili tayari suala hili katika kurasa zilizopita. Kuwatiisha watu wengine kwenye kazi za kulazimishwa na kuwanyonya mapato yao pia ni aina ya kuhodhi. Ali hakulivumilia hili pia, na amelitaja katika sehemu mbalimbali ndani ya Nahajul-Balaghah. Wakati akielezea hali ya watu wa wakati wake yeye anasema: “Kuna watu wengi ambao jitihada zao zimepotea na ambao juhudi zao zimekwenda bure. Ninyi watu mnaishi katika wakati ambapo wema unafifia na uovu unazidi kusogea karibu na karibu zaidi. Ulafi wa mali wa kishetani unawaua watu. Kila unapopatupia jicho lako utawaona watu masikini, ambao wanateseka kwa sababu ya ufukara, au watu matajiri ambao ni wakosefu wa shukurani kwa Mwenyezi Mungu, au watu mabahili ambao hawatoi haki za Mwenyezi Mugu na wana bidii ya kuongeza utajiri na mali zao. Ni nini kimewakuta wale watu wenu waadilifu na wachamungu? Wako wapi hawa watu waungwana na wakarimu, ambao walikuwa wachamungu katika kujipatia mali na wakweli katika vitendo na tabia zao?” Mambo kama yalivyokuwa, Amirul-Mu’minin alikuwa ameelewa wazi ukweli huu kwa njia ya kufikiri kwake kuliko sahihi, silika safi na uadilifu wa hali ya juu kwamba mfumo ambao hauwezi kuondoa umasikini wa watu hauna faida, na sheria ambayo haiwezi kufuta ubaguzi wa tabaka hauna maana na haufai, ni mbaya. Zile sheria zote za kijamii, ambazo zinazalisha jamii ambamo watu wanagawanyika katika matabaka, ni sheria za kuchezewa mikononi mwa wale wanaojiita wenyewe ni waungwana na wale maarufu na wananyonya haki na mali za watu wa chini kwa namna ya kuaibisha kabisa. Ali alichukua hatua zinazofaa ili kuondoa umasikini wa watu. Vitendo vyake vilikuwa katika msingi wa kanuni mbili: Kwanza kabisa kwamba mali yote ya hazina ya umma na ardhi na mashamba na njia zote za kuingizia utajiri zilikuwa ni za taifa na ni muhimu kwamba ziweze kugawanywa miongoni mwa raia wote kulingana na mahitaji yao na kustahili kwao. Kila mtu lazima afanye kazi na anufaike kutokana na rasilimali hizi kulingana na juhudi zake. Hakuna aliye na haki ya kujitwalia kila anachokitaka na kuibadili mali ya umma kuwa ni mali yake maalum. Na pia ni kwa faida ya mtu mmoja mmoja kwamba wanapaswa kushirikiana na jamii. 131

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 131

9/4/2017 3:47:51 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Wajionyeshe wenyewe kuwa wenye faida kwa ajili ya wengine na pia wanufaike kutokana na hao wengine. Manufaa watakayoyapata kutoka kwenye jamii yatakuwa mara elfu nyingi zaidi kuliko yale ambao watayatoa kwa jamii hiyo. Ali anasema: “Yeyote anayeuzuia mkono wake kutokana na kuwafanyia madhara watu wake ni dhahiri kwamba anazuia mkono mmoja tu lakini kwa hakika anayaweka maelfu ya mikono mbali na yeye mwenyewe binafsi.” Serikali inapaswa kutwaa sera hii adilifu kwa uaminifu wa sawasawa, kwa sababu watu ni kama mwili mmoja na ni muhimu kwa serikali kukishughulikia kila kiungo cha mwili huo kulingana na mahitaji yake. Isipuuze wala kutelekeza haki ya mtu yoyote, wala isiruhusu ubaguzi kati yao. Ni katika mazingira kama hayo kwamba itakuwa inawezekana kwa serikali kupata mapato na kujipatia haki zingine za hazina ya umma kutoka kwenye taifa na kuzitumia katika miradi ya ustawi wa jamii. Jambo la pili ambalo juu yake Ali aliweka msingi wa vitendo vyake lilikuwa ni uendelezaji wa ardhi, kwa sababu maisha ya wanadamu na ustawi wao unategemea ardhi. Alikuwa na mawazo kwamba magavana na watumishi wachukue upendeleo zaidi katika kuiendeleza ardhi kwa kulinganisha na juhudi zao ambazo wanazifanya kupata mapato ya serikali, kwa sababu kama ardhi haikuendelezwa hayo mapato yatapatikana kutoka wapi? Mtawala ambaye haendelezi ardhi, lakini anataka kupata mapato kutoka kwa watu ni mjinga na dhalimu. Angependa kwamba miji ingeharibiwa, watu waangamizwe na yeye mwenyewe apoteze hadhi na heshima yake. Ardhi haiendelezwi vivi hivi wala kwa njia za ujinga au madaraka ya watawala. Maendeleo ya ardhi pia hayana maana kwamba majumba makubwa yasimamishwe juu yake kuwapa makazi watu matajiri. Ardhi inaendelezwa kwa juhudi za wafanyakazi na wakaazi wa vijiji. Amirul-Mu’minin alikuwa ametoa maagizo makali kwamba kama watu watadhikishwa na wakawa hawana furaha na watawala wao, basi yasichukuliwe mapato kutoka kwao. Kanuni za upole na mapenzi kwa binadamu na maadili mema zinataka kwamba raia walipe mapato hayo kwa hiari na sio kwa vitisho. Ni wajibu wa magavana kuwafanya watu wastawi na kuwa na hali nzuri ya kimaisha kwanza kabisa, halafu ndipo wafikiri juu ya kukusanya mapato.

132

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 132

9/4/2017 3:47:51 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Amirul-Mu’minin aliwahutubia wakusanyaji wa mapato kwa maneno haya: “….. Msiziuze nguo za watu za wakati wa baridi au wa kiangazi au wanyama wanaowatumia wao ili kukusanya mapato. Msimpige viboko mtu yoyote au kumfanya asimame kwa miguu yake kwa sababu ya pesa, na msiuze vitu vyao vyovyote kwa ajili ya lengo hili, kwa sababu Mwenyezi Mungu ametuagiza sisi kuchukua kile ambacho ni cha ziada.” Yeye anasema pia kwamba: “Katika suala la mapato zingatieni maslahi ya wale wanaolipa mapato hayo, kwa sababu mambo ya wengine yanaweza kuwekwa sawa tu kwa njia ya kodi na walipa kodi wenyewe.” Maoni haya ya Amirul-Mu’minin kuhusu ardhi na maendeleo yake, na maamuzi yaliyochukuliwa na yeye kwamba ustawi wa serikali unategemea ustawi wa watu, ni sahihi kabisa kwamba hakuna kosa lolote lililopatikana kuyahusu hayo, hata baada ya kupita kwa karne nyingi hivyo. Nadharia zote za kiuchumi na kijamii za nyakati hizi za sasa pia zinathibitisha maoni haya. Ali aliweka kanuni ya jumla kwa ajili ya uendelezaji wa ardhi na kutoa utajiri kutoka kwenye rutuba yake, ambayo inakubaliwa na sayansi za kijamii za nyakazi zetu, kuwa ni za usahihi kabisa. Wakati wa zama za jahilia kulikuwa na desturi kwamba wale watu wenye nguvu waliwalazimisha watumwa, wafungwa na watu wa chini kuwaendelezea ardhi zao. Waliwapa wafanyakazi hawa mishahara midogo sana kwa utashi wao lakini wakajitwalia yale mazao ya ardhi hizo wao wenyewe bila ya kufanya kazi yoyote ile. Kulingana na sheria yao, mtu hakuwa na thamani yoyote ile na kazi yake ilikuwa haistahili malipo yoyote. Watawala hao waliwaona watu kama watumwa wao na waliwatiisha kwenye kazi za lazima. Dini yao hasa ilisimama kwenye msingi wa kuwafanya watu kuwa watumwa wao; au kwa maneno mengine, juu ya kuwauwa na kuwaangamiza wale watu wasiokuwa na uwezo na walio matesoni. Watu walikuwa wajinga, na watawala hao, kwa kuchukua fursa isiyostahili ya ujinga wao, waliwafanya kuwa watumwa wao. Wale makasisi wa kuabudu masanamu, ambao walikuwa ndio viongozi wa kidini wa nyakati zile pia walikuwa wameutangaza utumwa kuwa ni halali na walikuwa kwa hiyo, wameimarisha nguvu ya watawala hao. Makasisi hawa walikuwa wamewafanya watu kuwa wapumbavu katika namna ambayo walikuwa tayari kutoa makafara makubwa kwa ajili ya watawala wao, ili kuwawezesha kuongezea utajiri wao, na kuongeza ardhi mpya kwenye nchi zao. Yote haya yalifanyika imma kwa jina la nchi ya asili au kwa jina la mungu waliyekuwa wakimuabudu. 133

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 133

9/4/2017 3:47:51 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Mwanahistoria mashuhuri wa Kiingereza, H.G. Wells anasema: “Makasisi wa kuabudu masanamu waliwaambia watu kwamba zile ardhi za mashamba waliyokuwa wakiyalima hazikuwa mali yao. Zilikuwa ni mali ya miungu ambao masanamu yao wameyaning’iniza ndani ya mahekalu, na miungu hao walikuwa wamezitoa ardhi hizo kwa watawala. Sasa ilitegemea kwenye dhamira njema ya watawala hao kutoa ardhi hizo kwa wale watumishi wao waliowataka wenyewe.” Wakulima wadogo pia walianza kuwa na imani kwamba ile ardhi waliyokuwa wakilima haikuwa ni yao, bali ilikuwa ni mali ya mungu sanamu na kwamba ilikuwa ni wajibu wao kujitolea sehemu ya mazao ya mashamba hayo kwa wawakilishi wa mungu wao huyo. Au kwamba mungu alikuwa ameitoa ardhi hiyo kwa mtawala, na huyo alikuwa na haki ya kuweka humo kodi zozote alizotaka. Au kwamba mtawala ameitoa ardhi kwa mmiliki ambaye alikuwa ndiye bwana wao. Ikiwa nyakati fulani sanamu hilo, mtawala au mmiliki ardhi alihitaji utumishi wa mkulima mdogo ilikuwa ni wajibu kuacha kazi nyingine na kutekeleza maagizo ya bwana wake. Mkulima huyo wala hakufikiria kwamba alikuwa nayo haki yoyote juu ya ardhi aliyokuwa analima. Kwa ufupi mkulima hakuwa na amma uhuru wa hiari wala kufaidi haki yoyote ile. Historia ya Arabuni inatueleza kwamba wale watu waliochukua hatamu za serikali baada ya Ali waliihodhi ardhi, mazao yake, na hazina ya umma kwa ajili ya manufaa binafsi. Walikuwa wakitumia kusema: “Mali yote ni ya Mwenyezi Mungu na sisi ni wawakilishi wake na wasimamizi juu ya ardhi. Ni hiari yetu kuitoa mali hii kwa yeyote yule tumtakaye. Hakuna mwenye haki ya kutulaumu kuhusina na hili.29 29

kweli ni kwamba sera hii ilianza kutekelezwa katika wakati wa utawala wa Uthman. Wakati wa Mtume na U kipindi cha ukhalifa wa Abu Bakr na Umar, kila kitu kilikuwa mali ya Waislamu na walishughulikiwa kwa haki sawa. Hata hivyo, mwelekeo wa Uthman ulibadilika mno. Alikichukulia kila kitu kuwa mali ya Mwenyezi Mungu na akajiona yeye mwenyewe kuwa ndiye bwana wa Waislamu. Alitumia mali ya umma kama alivyotaka na akaitoa kwa yeyote yule aliyemtaka. AmirulMu’minin Ali ameelezea picha halisi ya kipindi hiki kwa maneno haya: “Hatimaye huyu wa tatu alichukua mamlaka ya ukhalifa kwa kiburi mno kana kwamba ulikuwa ni ardhi ya malisho binafsi na kwa matumbo yao manene yaliyovimba, yeye na watu wa ukoo wake (Bani Umayyah) wakaanza kupora mali ya dunia ya Waislamu katika namna ile ile ya ulafi usio na tahadhari unaofanana na ngamia wakati anapopapatikia nyasi za mavuno. Uthman aliwanyima wale wadai halali wa mali hiyo ambayo ilikuwa ni ya Waislamu wote, na akaitoa kwa ndugu zake na jamaa wa karibu na wale aliowapenda sana. Mara nyingi alitamka maneno ambayo yaliakisi zile imani za zama za jahilia ambazo kulingana nazo hizo, ardhi pamoja na mazao yake na hazina ya umma vyote vilikuwa mali ya mtawala, na yeye alikuwa na haki ya kuitoa kwa yeyote yule aliyemtaka. Kauli yake hii inapatikana katika vitabu vyote vya historia: “Hii ni mali ya Mwenyezi Mungu. Nitampa yeyote yule nimtakaye na sitaitoa kwa yeyote yule nisiyependa kumpa. Kama mtu yeyote atachukia mimi sijali.” Mu’awiyah na makhalifa wengine wa Bani Umayyah walikuwa ni ndugu zake Uthman. Chochote walichokifanya katika nyakati zao wenyewe kilikuwa kimefanywa kwa kumuiga Uthman. 134

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 134

9/4/2017 3:47:51 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Hata hivyo, Ali aliijua nafasi hiyo vizuri sana. Yeye alikuwa anaona mbali sana na alikuwa anatambua vema kabisa kwamba Mwenyezi Mungu hahitaji ardhi au mali, na kwamba ardhi ilikuwa ni mali ya wale wanaofanya kazi juu yake. Ali pia alijua kwamba kama wakulima wadogo ni masikini, ardhi itakuwa isiyotumika na itakuwa vigumu kupata mapato yoyote yale. Ardhi inaweza kuendelezwa tu na wale watu ambao ndio wamiliki wake na kupata faida kutoka kwenye mazao yake. Kama wakulima watalijua hilo kwa uhakika kwamba hawataweza kufaidi matunda ya kazi zao na yatazifikia hazina za watawala wabadhilifu, basi watafanya kazi kwa shingo upande na hawatafanya juhudi yoyote ya kuiendeleza ardhi. 30 Hatimaye wao wenyewe watakuwa katika huzuni na wengine pia watakuwa wamenyimwa matunda ya kazi zao. Endapo, hata hivyo, wao wanajua kwamba jinsi wanavyozalisha zaidi kwa kazi zao za bidii, ndio zaidi wao na watoto wao watakavyonufaika kutokana nazo, na watawala pia hawatagawanya mapato miongoni mwa marafiki na ndugu zao, bali watayatumia mapato hayo katika miradi ya ustawi wa jamii, basi watafanya kazi kwa moyo wote. Na kama matokeo ya hili, wao watakuwa na hali nzuri ya kimaisha na mapato ya ziada pia yatapatikana katika hazina ya serikali. Machoni mwa Amirul-Mu’minin, furaha na nia njema ya raia vilikuwa ndio chanzo pekee cha ustawi wa watu na vilevile hali nzuri ya watawala. Yeye hakuamini katika kushurutisha na alisema: “Chanzo bora cha uridhikaji na furaha ya moyoni kwa mtawala ni kwamba uadilifu uweze kuimarishwa, na mapenzi ya raia kwa ajili ya watawala wao yawe dhahiri. Hawaonyeshi upendo pindi ambapo kuna hisia mbaya katika nyoyo zao, na utii wao hauwezi kutegemewa juu yake madhali hawako tayari kumlinda mtawala wao, na hawaachi kufikiri kwamba utawala wake umekuwa wenye mzigo mzito na utakuja kufikia mwisho baada ya muda mrefu.” Ali aliuchukulia ukulima na taaluma nyingine zote kuwa za kuheshimika. Aliwakataza watu kukaa bure bila kazi na alionelea ni muhimu kwamba mfanyakazi alipwe mshahara kadiri iliyo sawa na kazi yake. Alifanya ukali zaidi katika masuala haya ili watu waweze kutambua kwamba yeye hatakuja kulipa kitu chochote ambacho hakikupatwa na mtu anayehusika kwa njia ya kazi yake. Kadhia ya kaka yake halisi, Aqiil ibn Abu Talib inaju likana sana. Yeye Aqiil alimwendea Ali ili amfanyie 30

ii inaonyesha kwamba kama wakulima wadogo wanaruhusiwa kuchangia mazao pamoja na wamiliki wa ardhi H watafanya kazi kwa bidii ili kupata faida zaidi kutoka kwenye ardhi. Hata hivyo, ikiwa nafasi yao itakuwa ni ile ya wapokea mishahara (kama katika usoshalisti) hawatajitahidi kuongeza mazao, wakijua kwamba watapata mshahara ule ule kwa kiwango chochote cha mazao kitakachokuwa. Zaidi ya hayo, serikali za kisoshalisti ni mzigo mzito kwa raia zake. Zinaingilia mambo yote ya raia na hao raia wenyewe pia, sio waaminifu sana kwa serikali zao, kwa sababu zenyewe hazina imani yoyote juu yao. 135

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 135

9/4/2017 3:47:51 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

malipo fulani bila kazi au huduma yoyote, lakini Ali alikataa kukubali maombi yake hayo. Machoni mwa Ali kulikuwa hakuna dhuluma kubwa kuliko kwamba mfanyakazi asilipwe ujira wake au kwamba anyimwe haki yake hata kwa kiasi kidogo kabisa. Kulingana na yeye ilikuwa haifai kabisa kwamba kazi iliyofanywa na watu wa tabaka la juu itukuzwe ambapo ile iliyofanywa na watu wa kawaida iangaliwe kwa dharau. Kwa maoni yake yeye, cha muhimu kilikuwa ni kazi na thamani yake halisi, iwe kama ilifanywa na mtu mkubwa ama mtu wa kawaida. Walikuwepo wafanyakazi wengi katika wakati wake ambao walifanya kazi kwa bidii lakini walikuwa hawakulipwa kwa kazi yao. Amirul-Mu’minin alilichukia hilo vibaya sana. Maneno yake haya ni mwanga bainishi katika njia ya kanuni za kijamii na kimaadili: “Tupia macho kwenye mafanikio ya kila mtu na usiyahusishe mafanikio ya mtu mmoja kwa mtu mwingine, na usimnyime yule mtu hasa malipo ambayo ana haki nayo kwa sababu ya kazi aliyoifanya. Kamwe usiifanye kazi ya kawaida kuwa kubwa sana kwa sababu ya cheo kikubwa cha mwenye kuifanya, na kamwe usiifanye kazi kubwa kuwa ya kawaida kwa sababu ya cheo cha chini cha mtu aliyeifanya.” Kuendeleza ardhi na malipo kamili ya ujira kwa kadiri iliyo sawa na kazi iliyofanywa zilikuwa ndio nguzo kubwa mbili ambazo juu yake alinuia kusimamisha ujenzi wa jamii nzuri na ya kiuchamungu. Watu kadhaa wanaotoka mahali fulani walikuja kwake na wakasema: “Kuna mfereji kwenye eneo letu ambao kwa sasa hivi umejaa mchanga. Kama utachimbwa tena utakuwa na manufaa sana kwetu.” Halafu walimuomba yeye kuandika barua kwa gavana wa eneo hilo kufanya iwe ni lazima kwa kila mtu kuuchimba mfereji huo. Amirul-Mu’minin aliidhinisha kuchimbwa kwa mfereji huo, lakini hakukubaliana na ombi lao kwamba watu walazimishwe kuuchimba. Aliandika hivi kwa Qarza ibn Kaa’b, gavana wa eneo hilo: “Watu fulani kutoka kwenye eneo lako walikuja kwangu na kuniambia kwamba kuna mfereji katika jimbo hilo ambao sasa umejaa mchanga. Kama watu hawa watauchimba tena mfereji huo utaongozea kwenye maendeleo ya jimbo hilo, nao watakuwa na uwezo wa kulipa kodi. Hii pia itapelekea kwenye ongezeko katika mapato ya Waislamu wanaokaa katika eneo hilo. “Watu hawa waliniomba kukuandikia barua ya kukutaka wewe kuwakusanya watu wa sehemu hiyo ili kuuchimba mfereji huo na kufanya ni wajibu juu yao kubeba gharama za kazi hiyo.” 136

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 136

9/4/2017 3:47:51 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

“Mimi sioni kwamba inafaa kumlazimisha mtu yoyote kufanya kazi ambayo yeye hataki kuifanya. Unapaswa, kwa hiyo, uwaite watu na kuwaajiri wale kati yao, ambao wako tayari kwa hiari yao kufanya kazi hiyo. Mfereji utakapokuwa tayari, ni wale watu wanaofanya kazi ya kuchimba tu, ndio watakaokuwa na haki ya kuutumia, na wale ambao hawatashiriki katika kazi hiyo hawatukuwa na haki juu ya maji yake. Kama watu hao wataendeleza eneo lao na hali yao ya kifedha ikainuka, ni bora zaidi kuliko kubakia kwao kuwa wanyonge.” Ali hakuona kwamba ni halali kumlazimisha mtu yoyote kwenye kazi kwa nguvu, ingawaje kikundi cha watu kilitaka kukimbilia kwenye mwenendo huu. Jambo lenye muhimu ni kwamba mtu lazima afanye kazi. Ali kwa hiyo, aliwaambia watu wale: “Mmeagizwa kufanya kazi (na sio kukaa bure tu). Na kuhusu mfereji huo ni wale watu tu, ambao watashiriki katika uchimbaji, ndio watakaokuwa na haki ya kunufaika kutokana nao. Wale ambao hawataki kuifanya kazi hii hawawezi kulazimishwa kuifanya. Kazi lazima ifanywe kwa hiari na sio kwa kushurutishwa.” Hii ndio kanuni ambayo Ali aliifuata kwa makini sana. Kwa kuunda kanuni hii kuhusu kazi na wafanyakazi karne nyingi zilizopita, Ali amewazidi wanafikra wa magharibi. Wanafikira wa magharibi wanaweka mbele kwa nguvu sana jambo hilohilo leo, ambalo lilisemwa na Ali takriban karne kumi na tatu zilizopita. Aliweka msingi kwa ajili ya uadilifu, na msingi bora zaidi ya huo hauwezi kudhaniwa.31 Na msingi huo ni kwamba mtu yoyote asilazimishwe kwenye kazi za nguvu, hata kwa faida gani kazi hiyo itakavyokuwa, kwa sababu kuchukua kazi kwa nguvu ni fedheha kwa ubinadamu. Kunapunguza thamani ya mtu na kunahalifu uhuru wake wa asili. Zaidi ya hayo, kazi inayofanywa chini ya ulazimishwaji inapoteza thamani yake, kwa sababu mtu ambaye analazimishwa kufanya kazi fulani hataifanya kwa moyo mmoja. Ali, hata hivyo, aliwatia watu moyo kwa njia nyingine kuifanya kazi kwa kusema kwamba, ni wale watakaoshiriki kwenye uchimbaji wa mfereji tu, ndio watakaokuwa na haki ya kunufaika kutokana nao.Yeye alisema: “Wamiliki wa mfereji huo ni wale watu ambao wanashiriki katika uchimbaji wake na sio wale wanaojizuia kutokana na kufanya hivyo.”32 anafalsafa wa magharibi wamegawanyika makundi mawili juu ya suala hili. Kundi moja linaona kwamba W kazi za lazima ni udhalimu na sio halali, ambapo kundi jingine linaziona kazi hizo kuwa za muhimu. Usoshalisti unashikilia haya maoni ya mwishoni. 32 Mwanzoni mwa barua yake aliyoandika kwa gavana huyo, Amirul-Mu’minin alimwambia kwamba awahamasishe watu kuchimba mfereji huo na kubeba gharama za kazi hiyo. Yule ambaye hataweza yeye mwenyewe 31

137

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 137

9/4/2017 3:47:51 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Kanuni iliyotamkwa wazi na Ali ndio nguzo ambayo juu yake imani kubwa na mawazo ya wanafikira wa magharibi yameegemea. Kwa hiyo ni lazima kwa kila mtu kufanya kazi. Hakuna aliye mkubwa au mdogo isipokuwa kwa kupitia kwenye kazi yake. Yeyote anayefanya kazi atalipwa kwa kazi hiyo. Wale makabaila na watu mashuhuri hawana haki ya kupora mapato ya wengine na kuingilia haki zao. Kama ilivyosemwa na Ali, kama Mwenyezi Mungu anampenda mtu yoyote, basi anampenda mfanyakazi mwaminifu. Kama mtu atajipatia utajiri kwa kazi ngumu, bila shaka inakuwa ni yake kwa sababu ameifanyia kazi. Hata hivyo, ni lazima pia aweke maanani maslahi ya taifa. Mali hiyo inayosemekana itachukuliwa kuwa ni mali yake binafsi alimuradi maslahi ya taifa hayahatarishwi. Kama maslahi ya taifa yanataka kwamba sehemu ya mali binafsi ya watu ichukuliwe na kutumika kwa ustawi wa umma, hili litafanyika. Mali hii imekusudiwa kwa manufaa ya watu binafsi na pia kwa ustawi wa jamii (ilikuwa ni kwa sababu hii kwamba fedha zilichukuliwa kutoka kwa wamiliki wa mfereji kwa ajili ya hazina ya umma) wakati umiliki unapokuwa umewekewa mipaka katika namna hii hakutakuwa na amma utajiri wa ziada kwa mtu yoyote wala kuwepo kwa mtu masikini katika jamii. Katika kila taifa, kuna watu fulani (kwa mfano mayatima wadogo) ambao hawana uwezo wa kufanya kazi. Je, Ali aliwapuuza watu kama hao kama inavyofanywa na nchi za magharibi, au aliwashughulikia kulingana na kanuni za uadilifu na uungwana? Hakuna shaka kuhusu ukweli kwamba taifa lina haki juu ya watu binafsi, na kwamba watu binafsi nao wana haki juu ya taifa. Taifa ni kama mwili ambao umeundwa kwa viungo tofauti. Ni muhimu kwa kila kiungo kusaidia viungo vingine. Kila mtu anayo haki ya kufaidi matunda ya kazi yake. Mwenyezi Mungu ameruzuku fungu la mahitaji muhimu ya maisha kwa kila mtu. Hakuna, kwa hiyo, ambaye anayo haki ya kujitwalia mahitaji ya maisha na kuwaacha wengine. Hata hivyo, ni jukumu la taifa kuwasaidia wale ambao hakufanya kazi, amuajiri mtu mwingine kufanya kazi hiyo kwa niaba yake. Kuwa ‘wamiliki wa mfereji’ kuna maana kwamba wale wanaoshiriki katika uchimbaji kwa nguvu zao au kifedha, wanayamiliki maji yake na pindi mahitaji yao hayajatimizwa, wengine hawawezi kuyatumia. Wanayo haki ya kuwazuia wengine kuyachukua maji hayo au kuwaruhusu kuyachukua kwa malipo. Hii ndio maana ya hadithi iliyonukuliwa hapo juu, yaani “Wamiliki wa mfereji ni wale watu ambao wanashiriki katika uchimbaji wake na sio wale wanaojizuia kutokana na kufanya hivyo.” 138

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 138

9/4/2017 3:47:51 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

wana uwezo wa kujipatia malipo, kwa mfano watoto wadogo na watu wazima, wazee.33 Ni lazima lifanye uadilifu kwa wale wasio na uwezo kwa namna ile ile ambamo linafanya uadilifu kwa wengine. Ni haki yao ya kipekee, na wala sio kitendo cha huruma, na serikali na wawakilishi wake wanao wajibu wa kuilipa haki hii. Ali anasema: “Katika watu wote wa jamii, watu hawa wanastahili kufanyiwa uadilifu zaidi. Hivyo ni lazima mlipe haki ya kila mmoja wao na mjipatie wenyewe kisingizio cha kutosimamishwa mbele ya Mwenyezi Mungu. Waangalieni mayatima na watu wazee ambao hawawezi amma kujipatia mahitaji yao ya maisha wala kusimama mbele ya watu wengine na kuomba.” Ali amewatangulia maelfu ya wanafikra na wanafalsafa wa magharibi katika jambo hili. Yeye aliutambua umuhimu wa kulipa haki za wale wasiokuwa na uwezo na akalifanya hilo kuwa ni wajibu wa serikali. Hakulifanya jambo hilo litegemee kwenye huruma na ukarimu wa watu matajiri ili kwamba wanafiki wadanganyifu wasiweze kupata nafasi yoyote ya kueneza fitna.34 Dhamiri ya Ali na akili yake vile vile vilikuwa na utambuzi mzuri juu ya ukweli kwamba binadamu wote wanayo haki ya kuishi. Haki hii ni mojawapo ya mahitaji muhimu ya maisha ya kijamii. Uhuru unakuwa hauna maana endapo riziki haipatikani na jamii nzuri haiwezi kupatikana bila ya riziki hiyo. Yeye aliitangaza rasmi sheria ya kwamba wanadamu wanazo haki sawa. Halafu kwa kuzingatia sheria hiyo hiyo yeye aliamua kwamba wale watu wenye haja walikuwa na haki ya kipaumbele juu hazina ya umma kulinganishwa na wale matajiri ingawaje wale watu matajiri wanaweza kuwa waliingia Uislam mapema atika sheria ya Kiislamu Zakat imefanywa kuwa ni lazima kwa sababu hii hasa. Abdullah ibn Sanan amenK ukuliwa katika al-Kafi kwamba alisema kuwa Imam Ja’far Sadiq amesema: “Mwenyezi Mungu ameweka fungu la watu masikini katika mali ya matajiri ambalo linaweza kuwatosheleza. Kama angeliona kuwa halitoshi Yeye angeweza kuamuru kwamba malipo zaidi yafanyike.” 34 Kutimiza mahitaji ya masikini na mafukara na watu wasiokuwa na uwezo sio wajibu wa serikali tu kama ilivyoelezwa na mwandishi. Katika sheria ya Kiislamu, serikali na vile vile watu binafsi wamefanywa kuwa na wajibu wa kuwasaidia wale wenye haja. Endapo ukusanyaji wa Zakat na ugawanyaji wake miongoni mwa masikini ungekuwa ni wajibu wa serikali tu, kungekuwa na nafasi kubwa sana ya uongozi mbaya, kwa sababu wale watu walioko karibu na serikali wangenufaika mbali na wale ambao walikuwa mbali kidogo na serikali, na hawakuwa na nafasi ya kuwafuata wakubwa wanaohusika. Ni kwa sababu hii kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu ameagiza watu binafsi kwamba walipe na kutoa Zakat kwa ndugu zao wa karibu, majirani, na watu masikini wa mji wao wenyewe kati ya wale masikini wanaoweza kuwatambua, na wakabidhi kwa serikali pale tu itakapokuwa hakuna kati ya ndugu zao, majirani, jamaa, na wakazi wa mji wao aliye na haki kwenye Zakat hiyo. 33

139

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 139

9/4/2017 3:47:51 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

z­ aidi. Ni kazi ndio ambayo inayompa mtu haki ya malipo na ni kazi pia ambayo kwa njia yake mtu anaweza akawa mmiliki wa ardhi na mali nyinginezo. Katika maagizo ambayo Amirul-Mu’minin aliyatuma kwa magavana na watumishi wengine kwa kila mara, yeye aliwaonya vikali sana wasiwanyanyase watu. Aliwaelekeza kutowashinikiza wakulima masikini kwa ajili ya malipo ya mapato bali kuwapatia msaada ili kwamba waweze kufanya kazi kwa bidii na kuzalisha zaidi kutoka kwenye ardhi. Kodi lazima zichukuliwe kutoka kwa watu matajiri ili mapato ya hazina ya umma yaweze kuongezeka na yaweze kutumika kuwasaidia wale wenye haja. Ni kwa umaarufu na utukufu kiasi gani ambavyo Ali anaonekana mbele ya macho yetu, pale tunapokuja kujua kwamba miaka kumi na nne elfu iliyopita yeye alitoa maagizo yenye mkazo kwa magavana wake katika maneno haya: “Msiyauza mavazi ya watu ya majira ya kivukwe au ya kiangazi, au nafaka zao, au wanyama wanaowatumia, ili muweze kukusanya mapato. Msimpige viboko mtu yeyote au kumfanya asimame kwa nyayo zake kwa ajili ya pesa. Msiuze vifaa vya nyumbani vya mtu yeyote ili kupata mapato – na tilieni maanani sana kwenye uendelezaji wa ardhi kuliko kwenye ukusanyaji wa mapato. Amirul-Mu’minin ameitaja sababu ya hali ya kuhuzunisha, ya watu masikini wa wakati wake katika maneno mafupi ya mkato, na ameelezea maana zake katika wasia nyingi na maagizo yake. Yeye anasema: “Kama mtu masikini akibaki na njaa ni kwa sababu mtu tajiri amezuia fungu lake.” Huu ni ukweli mkubwa sana ambao ni msingi wa mfumo wa kisasa wa haki. Ali alielewa ukweli huu miaka kumi na nne elfu iliyopita na akaunda kanuni za wazi na taratibu kama zile zilizofaa kwa wakati wake yeye. Mwandishi wa ki-Lebanoni ambaye ametokea kuwa rafiki yangu anasema kwamba wakati mmoja alikuwa akikaa kwenye mji mkubwa wa Ulaya na vuguvugu la kukomesha umasikini lilikuwa likiendelaea hapo. Siku moja alikutana na Waziri wa Elimu wa nchi ile na akamwambia wakati wa mazungumzo yao: “Sisi Waarabu tulitambua karne kumi na nne zilizopita huu ubaguzi wa tabaka na ubaya wake ambao ninyi mnajitahidi kuuondoa sasa hivi.” Yule Waziri akasema: “Vipi?” Yeye akajibu: Miaka kumi na nne elfu iliyopita, Ali ibn Abi Talib alisema: “Sijaona utajiri wa kupita kiasi kwa mtu yeyote yule isipokuwa kwamba niliona kwa wakati huo huo kulikuwa na haki ya mtu mwingine ikiwa inavunjwa.” 140

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 140

9/4/2017 3:47:51 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Yule Waziri akasema: “Sisi ni bora kuliko ninyi.” Yeye akauliza: “Vipi?” Yule Waziri wa Elimu akasema: “Kwa sababu ingawa Mwarabu alikuwa ameelewa ukweli huu miaka kumi na nne elfu iliyopita, mpaka sasa hamjajitahidi kuuondoa ufukara na bado mmo ndani yake ambapo sisi tayari tunajitahidi kuondoa umasikini. Hivyo ninyi mko miaka kumi na nne elfu nyuma yetu, yaani, kama tungekuwa tumesikia maneno haya ya Ali kwa wakati ule, tungekuwa tumechukua hatua muhimu juu ya hili mara moja.” Kabla hatujamalizia sura hii, itakuwa ni vema tukirudia kwa mukhtasari kile kilichoelezewa hapo, juu na kuwataka wasomaji kulinganisha maoni ya Ali katika masuala ya kijamii, na yale maoni ya wanafikira wa kisasa na kuyatafakari kwa busara. Tunaweza kutaja zile kanuni za kijamii na maoni ya Ali katika sentesi tisa. Kanuni na maoni haya yanakuwa pamoja na sababu za utajiri na umasikini na tofauti ya tabaka ya watu au kwa maneno mengine kanuni na taratibu bora kwa ajili ya kuondoa umasikini na shida, na kusimamisha usawa wa haki kati yao. Kuzuia kuhodhi mali Hakuna mtu masikini aliyebakia na njaa isipokuwa kwa sababu mtu tajiri amepora fungu lake masikini huyo. Sijaona utajiri wa kupita kiasi kwa mtu yoyote isipokuwa kwamba nimeona kuna haki ya mtu mwingine ikiwa inavunjwa. Ni lazima muwe na shauku ya kuendeleza ardhi kuliko kukusanya mapato. Sioni kwamba inafaa kuwa mtu alazimeshwe kufanya kazi ambayo haitaki. Nyoyo za watu wachamungu ziko Peponi na viwiliwili vyao viko vinashughulika katika kufanya kazi hapa duniani. Mfereji unakuwa ni mali ya yule ambaye anashiriki katika uchimbaji wake na sio kwa yule ambaye hakutoa msaada wa nguvu au wa kifedha katika kuuchimba. Zingatieni mafanikio ya mtu, na msihusishe mafanikio ya mtu mmoja kwa mtu mwingine. Tahadharini! Msijitwalie wenyewe vile vitu ambamo watu wote wana haki sawa. Kama maneno haya ya Ali yatachunguzwa kwa makini inakuja kufahamika kwamba haki za mtu katika jamii ya wanadamu zinaweza kulindwa na uhuru wake unaweza kuhakikishwa tu kwa ushughulikaji juu ya kanuni hizi.

141

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 141

9/4/2017 3:47:51 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Sio Ama Ushabiki Wa Kupindukia Wala Hali Kutokukosea Ali alitembea kwa uthabiti katika njia ya matendo aliyoiweka yeye kwa ajili yake mwenyewe. Wakati wote aliangalia juu. Aliweka haki za kiuchumi za mwanadamu na vile vile haki nyingine ambazo bila hizo haki za kiuchumi haziwezi kujitokeza. Yeye hakufanya upendeleo kwa imani yoyote maalum, rangi au taifa. Wanadamu wote ni sawa na wote wanayo haki ya kuishi na kushirikiana vistawishi vya maisha ingawaje wanaweza kuwa tofauti katika imani zao, rangi na taifa. Ali alikuwa mwenye busara na kuwafikiria wanadamu wote. Kwa mujibu wake yeye hapakuwa na tofauti kati ya wale wenye rangi nyeupe na wale wenye rangi nyeusi, Waarabu na wasiokuwa Waarabu, Waislamu na wasiokuwa Waislamu katika suala la haki za kiuchumi na vistawishi vya maisha. Ingawaje Ali alikuwa makamu wa Mtume, ngome ya Uislamu, na Jemadari wa waumini, yeye hakupenda kabisa kwamba wale wasiokuwa Waislamu walazimishwe kuukubali Uislamu. Kwa mujibu wake yeye, watu walikuwa huru kumuabudu Mwenyezi Mungu kama walivyotaka na kushikilia imani za chaguzi zao kwa masharti kwamba hawakuwadhuru watu wengine.35 Aliruhusu uhuru wa kuabudu kwa sababu wanadamu wote ni waja wa Mwenyezi Mungu na kwamba dini ni njia ya kiunganisho kati Yake na viumbe Wake. Kulingana na Ali mtu kule kuwa kwake ni binadamu kulitosha sana kwa ajili ya kuheshimiwa kwake, kufanyiwa urafiki na kufanyiwa upole na vile vile kwa haki zake kukingika kutokana na kuingiliwa kati na watu wengine. Katika wasia alioandika kwenda kwa Malik Ashtar, gavana wa Misri, yeye alisema: “Usiwe mnyama mkatili kwao ili kwamba uweze kuwameza.36 Kuna aina mbili za watu miongoni mwa raia hao, ambao baadhi yao ni ndugu zako katika dini na wengine ni viumbe wa Mwenyezi Mungu kama wewe, na unapaswa kuwa msamehevu mbele yao kama vile tu ambavyo unamtaka Mwenyezi Mungu awe Msamehevu juu yako. Unapaswa kutokuwa na hisia za kufurahia wakati unapotoa adhabu. Katika hali hiyo kila mtu anayo haki ile ile kama uliyonayo wewe, ingawaje baadhi au jumla nzima ya imani zake zinaweza kuwa kinyume na zako. islamu unaruhusu uhuru wa kuabudu kwa Wayahudi, Wakristo na Majusi. Hawa wanaitwa ‘Dhimmi’ amU bayo ina maana ya wasiokuwa Waislamu wanaoishi chini ya ulinzi wa serikali ya Kiislamu. 36 Wamisri ambao kuhusu wao Amirul-Mu’minin alitoa maelekezo haya kwa Malik Ashtar walikuwa ni Wakristo. 35

142

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 142

9/4/2017 3:47:51 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Lengo la dini kwa uhakika ni kwamba ikuwezeshe kuimarisha uhusiano wa kidugu pamoja na wengine. Wengine ni wanadamu hasa kama ulivyo wewe. Mfanano huu wa maumbile ni kiungo cha nguvu sana kati yako na wengine. Unapaswa kwa hiyo, uwe na tabia ya upole kwa wanadamu wote. Endapo ndugu yako atafanya kosa au dhambi unapaswa kupuuza kutekeleza kwake na umsamehe, na usione aibu kabisa katika kufanya hivyo. Safisheni nyoyo za wengine kutokana na uadui na kinyongo kwa kusafisha nyoyo zenu wenyewe kwanza kutokana na sifa hizi mbaya.” Ni wajibu kwa kila mwanadamu, awe kwenye dini gani awayo au imani yoyote, kwamba awe na huruma kwa binadamu wenziwe. Anapaswa apendelee wengine kile anachopendelea kwa ajili yake mwenyewe na asiwapendelee wao kile asichokipendelea yeye mwenyewe. Atarajie kutoka kwa watu kwa kiwango kile kile ambacho yeye anatimiza matarajio ya wengine. Mu’mini halisi ni yule anayejitahidi kufanya matendo mema. Tendo bora kabisa ni uadilifu kamilifu ambao ina maana kwamba awe ni mwadilifu kabisa na asibague kati ya watu tofauti. Yule anayefuata nyayo za Muhammad katika kuyaendesha maisha yake hana tofauti na yule anayefuata nyayo za Yesu (Isa) au watu wengine maarufu waliotimilika. Lengo la kuumbwa kwa mwanadamu ni hili kwamba ajipatie maadili na ubora na ajipatie sifa njema. Yuko huru kufanikisha lengo hili kwa namna yoyote aitakayo. Ali anasema: “Ni lazima juu yako kufuata vitendo vya Mtume, kwani dunia iliumbwa kutoka chini ya nyayo zake naye aliepushwa mbali na starehe na mapambo. Na kama ukipenda unaweza kumwangalia Yesu ambaye alizoea kuegemea kwenye jiwe, kuvaa nguo chakavu na kula chakula kisichokuwa na utamu na kisicho na ladha. Njaa ilikuwa ndio mkate wake, mwezi ulikuwa ndio taa yake, mashariki na magharibi ndio kivuli chake, na nyasi ndio zilikuwa matunda yake na manukato. Hakuwa na mke ambaye angeweza kumtamanisha yeye na hakuwa na watoto ambao kwa ajili yao angekuwa na wasiwasi. Hakuwa na mali ambayo ingeweza kumvutia wala hamu yoyote ya kupata kitu ambayo ingemfedhehesha. Nyayo zake zilikuwa ndio namna yake ya usafiri na mikono yake ilikuwa ndio watumishi wake.” Mahali pengine Imam Ali anasema: “Hawa ndio watu ambao waliifanya ardhi kuwa ndio zulia lao na udongo wake ndio kitanda. Walijiridhisha wenyewe na maji badala ya marashi na walifariki dunia kama Yesu alivyofanya.” 143

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 143

9/4/2017 3:47:51 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Ukweli ule ule aliokuwa nao kwenye mawazo yake pale aliposema: “Mitume ni ndugu wa kila mmoja wao. Mama zao ni tofauti lakini dini yao ni moja na hiyohiyo.” Ukweli huohuo ulikuwa mbele ya Ali pale aliposema kuhusu Muhammad: “Mtume alipitisha maisha yake katika namna ileile ambamo mitume waliotangulia walipitisha maisha yao.” Katika kauli hizi mbili imekubalika wazi kwamba maadili ndio kitu kinachowaunganisha watu mahali pamoja kama ubinadamu kimsingi ulivyo mahali pa kuunganishia. Kilichoelezewa hapo juu kinafanya iwe wazi kabisa kwamba kama vile mwanadamu alivyo na haki nyingine nyingi tu, anayo, kwa mujibu wa sheria zilizowekwa na Ali, haki hii pia kwamba anapaswa awe huru katika suala la imani zake na pasiwe na kizuizi au makatazo katika kushikilia kwake imani yoyote anayoitaka. Uhuru hauwezi kugawanyika. Haiwezekani kwamba mwanadamu awe huru katika baadhi ya mambo na awe mtumwa katika mengine. Muislamu ni ndugu wa Mkristo apende asipende, kwa sababu mtu ni ndugu wa mtu awe analikubali hilo au hapana. Kama katika macho ya Ali lengo kuu la kuumbwa kwa mwanadamu kama kiumbe huru lisingekuwa hili kwamba afanye jitihada za kujipatia maadili na kama kwa mujibu wake yeye, uhuru usingekuwa haki tukufu, yeye asingewasifia wafuasi wa Yesu katika namna hiyohiyo ambamo aliwasifia wafuasi wa Muhammad. Katika kurasa zilizopita tumeeleza kwamba Mkristo aliiba vazi la deraya la Ali na akadai kwamba alikuwa amelinunua. Tumeeleza pia jinsi Ali alivyofanya na Mkristo huyo kama mtu sawa na yeye mwenyewe, kwa usahihi zaidi, katika namna ambamo baba anakuwa na tabia kwa mwanawe. Tumeelezea pia jinsi Ali alivyotoa lalamiko lake kwenye mahakama ya hakimu Shurayh na nini yalikuwa matokeo yake na jinsi Mkristo yule alivyokuja kuwa mmoja wa wafuasi wake waaminifu na akamsaidia kwa bidii kabisa. Historia ya Arabuni inajivunia juu ya maneno ya Ali yafuatayo ambayo yanapamba kurasa zake: “Kama zulia linatandikwa kwa ajili yangu nami nikakaa juu yake, nitaziamua kesi za Wayahudi kwa mujibu wa kitabu chao ‘Taurati’, za Wakristo kulingana na kitabu chao ‘Injiil’ na zile za Waislamu kulingana na Qur’ani yao, kwa namna ambayo kwamba kila kimoja ya vitabu hivi kitasema: “Ali amesema kweli.” Ali alimshauri Ma’qal ibn Qais kama ifuatavyo:-“Ewe Ma’qal! Muogope Mwenyezi Mungu. Usiwe muovu kwa Waislamu na usiwaonee ma-Dhimmi. Usiwe na kiburi kwa sababu Mwenyezi Mungu hawapendi wale wenye kiburi.” 144

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 144

9/4/2017 3:47:51 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Inaonyesha kwamba kulingana na Ali ‘kumuogopa Mwenyezi Mungu’ kuna maana hii kwamba mtu asiwaonee wanadamu wenzie na asiwe, kwa namna yoyote ile, muovu juu yao. Zaidi ya hayo, anawaweka Waislamu na wasiokuwa Waislamu kwenye daraja sawa na hafanyi upendeleo kwa yeyote kati yao. Usawa huu wa Waislamu na wasiokuwa Waislamu unaweza kuonekana katika kila agizo la Ali. Itaonekana kwamba aliona ulinzi wa watu kutokana na dhulma na uonevu kuwa muhimu zaidi na lazima kuliko kupata maadili mengine ya Kiislamu. Yeye anasema: “Kama unafuata njia ya haki, na mafundisho ya Uislamu yakawa wazi kwako, sio Muislamu wala dhimmi atakayeonewa.” Aliwakaripia vikali sana Waislamu wakati Sufyan ibn Auf Asadi, kamanda wa jeshi la Mu’awiyah alipovamia mji wa Anbar na kufanya ukatili kwa raia wake lakini wao (Waislamu) hawakusimama kwenye haki, na hawakufanya lolote kuzuia uonevu huo. Wakati wa hotuba yake yeye alisema: “Nimepata habari kwamba, mtu wa kundi hili alikuwa akiingia kwenye nyumba za wanawake wa Kiislamu na za ma-Dhimmi na akaondoa furungu (bangili) kutoka kwenye miguu yao na bangili kutoka mikononi mwao, na pia mikufu na hereni ambazo walikuwa wamevaa na walikuwa hawana namna yoyote ya ulinzi isipokuwa walikuwa waseme tu: “Sisi tumetoka kwa Mwenyezi Mungu na wote tutarejea Kwake” na wakabakia wenye subira……. Sasa kama Muislamu anakufa kwa huzuni kwa sababu ya misiba hii hawezi kulaumiwa kwa hilo. Kwa maoni yangu mimi ingepaswa kuwa hivyo.” Ali aliwalaumu na kuwakaripia watu wale kwa sababu walishindwa kuwalinda kaka na dada zao waishio mjini humo – kama walikuwa Waislamu au Dhimmi – dhidi ya maonevu. Wakati alipomteua Muhammad ibn Abi Bakr kama gavana wa Misri alimwagiza hivi: “Ninakushauri wewe kuwa mwenye haki kwa ma-Dhimmi, kuwa mwadilifu kwa mtu aliyeonewa, kuwa mkali juu ya muonevu na kuwa mtaratibu kwa watu kwa kiasi inavyowezekana na kuwa mpole kwao. Ni muhimu pia kwamba katika suala la haki, wa mbali na wa karibu wawe sawa machoni mwako.” Maneno yafuatayo pia yalijitokeza katika maafikiano aliyofikia na Wakristo wa Najran: “Hawatafikwa na udhalimu na uonevu wala haitapunguzwa haki yao yoyote ile.” Yeye pia alipanga fidia ya damu ile ile kwa ajili ya Mkristo, ambayo ndio fidia ya damu kwa ajili ya Muislamu. Kwa mujibu wa Ali kila binadamu alikuwa na haki ya 145

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 145

9/4/2017 3:47:52 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

kuheshimiwa. Ilikuwa ni kwa sababu hii kwamba ingawa wafuasi wajinga na wasio na akili wa dini zote zilizopita walikuwa na ta’asub (ushabiki) kali sana na walichukia dini nyingine, Ali alipendwa sana kwa ajili ya uadilifu wake na wale Wakristo wenye elimu katika wakati wake mwenyewe na vilevile hata baadae. Wote walimsifu na kumtukuza yeye. Allamah Ibn Abil-Hadid anaandika hivi katika Nahjul-Balaghah: “Mimi niseme nini kuhusu mtu yule (Ali) ambaye Dhimmi walimpenda kwa shauku kubwa ingawaje hawakuukubali utume wa Muhammad.” Ali alikuwa ameweka msingi hasa wa ushughulikiaji wa wale wasiokuwa Waislamu juu ya kanuni hii: “Mali yao ni kama mali yetu na maisha yao ni kama maisha yetu.” Ukweli wote uliosimuliwa hapo juu unaonyesha wazi kwamba ushabiki wa kidini ulichukuliwa na Ali kama jambo lisilofaa na lenye kustahili kudharauliwa. Uhuru, ambao yeye katika huo aliamini, katika maana pana, na kuupima kwa kipimo kilichozidi ulikuwa unapingana kabisa na ta’asub – yaani – ushabiki uliokithiri. Pale tunapovuta taswira kichwani, ya utendaji uliofanywa na Ali kwa wale wasiokuwa Waislamu, na tukaulinganisha na utendaji wa mapadri wa kanisa katika Ulaya ya Zama za Kati, hususan wale wachungaji ambao walihusika na ule “uchunguzi,” na pale tunapoonyesha tofauti kwa kulinganisha upole na usamehevu ulioonyeshwa na Ali na ule ukali na ukatili wa viongozi wa kidini wa Ulaya, tunakuja kutambua jinsi Ali alivyokuwa ametukuka na jinsi gani watu wale walivyokuwa duni. Kwa kifupi pasiwepo na wasiwasi kuhusu hilo kwa sababu imani ya Ali ilichipukia kutoka kwenye mizizi ya ubinadamu, uhuru na mamlaka na ilikuwa ni kwa mujibu wa mtazamo wa imani ambao Ali aliushikilia kuhusu maisha. Imani ya Ali ilikuwa na msingi wake juu ya uhuru na aliuchukulia uhuru kuwa wa kuheshimika ambapo imani ya viongozi wa kidini wa Ulaya iliegemea juu ya tabia na uigizaji wa wahenga wao na uhuru ulikuwa hauhusiki na lolote katika hilo. Ta’asub - Ushabiki Uliokithiri Siku hizi tuko katika vita dhidi ya ta’asub ya kidini na tunaichukulia kama isiyofaa na yenye kustahili kudharauliwa, ingawa ushabiki wa kidini sio hatari sana kama aina zingine za ushabiki. Utakutana na watu wengi sana ambao hawana kabisa ushabiki, au ta’asub ya kidini lakini wanajihusiaha katika ushabiki wa rangi, asili, kabila, utaifa, itikadi za kisiasa na kadhalika.

146

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 146

9/4/2017 3:47:52 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Wema na usamehevu unawezekana katika suala la ta’asub ya kidini lakini hauwezekani katika suala la ushabiki wa aina zingine. Ushabiki kama huo umeegemea katika majisifu, ujinga na ulanguzi na wale walio na namna hii ya ushabiki wanasema kwamba maoni yao ni sahihi, na ni kile tu walichoamua ndio sawa, na mtazamo wao kuhusu mwanadamu na maisha haupingiki. Huwauoni mtazamo wa mtu mwingine yoyote kama una maana na uhalali kama wao. Tangu pale mwanadamu alipowasili katika dunia hii ushabiki wa kila aina umekuwa ni wa asili ndani yake, na hapajakuwa na wakati wowote ambamo hakuonyesha ushabiki. Kiongozi mkuu wa ulimwengu, Ali, hakupigana dhidi ya ushabiki wa kidini peke yake bali dhidi ya aina zote za ta’asub. Aliuona ushabiki wa kikabila kuwa sawa na uasi na fitna, na unaounguza ile sura ya kuvutia ya maisha. Kwa mujibu wa Ali mtu kujivunia mwenyewe juu ya jadi yake kulikuwa pia ni aina ya ta’asub. Anawahutubia wenye ta’asub wa wakati wake katika maneno haya: “Tazameni! Mmempinga Mwenyezi Mungu waziwazi, mmekuwa madhalimu hasa na mmesababisha vurugu juu ya uso wa dunia. Muogopeni na mcheni Mwenyezi Mungu katika suala la kujivuna wenyewe kwa sababu ya kuwa na kiburi cha zama za ujahilia, kwa sababu ni chanzo cha uhasama na kinyongo na kitovu cha minong’ono ya Shetani ambayo kwayo ameyashawishi mataifa yaliyopita. Angalieni! Ogopeni kuwafuata machifu na wakongwe wenu ambao wanajikweza wenyewe kwa sababu ya nafasi na fahari zao, na wanajivuna kwa sababu ya vizazi vyao (yaani, wale wanaowaona wengine ni wanyonge na wa kudharaulika, wanapinga kanuni za ki-Mungu na wanaukataa upole wa Mwenyezi Mungu ili waweze kuzuia neema Zake). Hawa ndio watu hasa ambao ndio misingi ya kina ya ta’asub na nguzo za nyumba ya fitna. Kwanza kabisa Ali aliifananisha familia na ushabiki wa kikabila na uasi na kuharibu sura ya maisha. Halafu aliufanya mtazamo kuwa wa kawaida kabisa na akatangaza kila ushabiki, kama wa kikabila, wa kisiasa au kidini kuwa wenye kufanana na uasi na fitina na akaazisha kanuni ya kawaida, ambayo usahihi wake utaimarishwa zaidi na zaidi jinsi muda unavyopita. Yeye anasema: “Mimi nimeangalia pande zote na sikuona hata mtu mmoja katika dunia hii ambaye anaunga mkono jambo bali lile ambalo kwamba anayo sababu 147

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 147

9/4/2017 3:47:52 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

mawazoni mwake juu ya hilo, ambayo inakuwa chanzo cha kosa la kijinga, au kwamba anayo hoja ambayo inagandamana kwenye akili ya mtu mpumbavu.” Unaweza ukayapitia yale yote yaliyosemwa kuhusu ta’asub na maelezo yaliyotolewa kuhusu hilo, lakini hutakuta chochote kilichosemwa na mtu yoyote ambacho kitaweza kuwa zaidi ya alichokisema Ali. Washabiki wanajiingiza kwenye ta’asub imma kwa sababu ya ujinga au upumbavu na yote hayo yanabeba uasi na fitina katika mapaja yao. Ali ameiweka picha ya ukweli huu katika kauli zake mbili zilizotolewa hapo juu. Kwa ufupi Ali aliuchukulia ushabiki wa kila aina kuwa usiofaa na wa kudharaulika. Kwa kweli kama upendeleo utatendeka, unapaswa kutendeka katika suala la wema, uadilifu na haki za jamii. Mtu anapaswa kuwa pamoja na wale wanaodhulumiwa ambao wananyimwa mapato na haki zao na waonevu, madhalimu. Mtu arudi pamoja na haki na dhamira. Mtu awe na upendeleo kwa ajili ya uhuru wa binadamu na heshima na kwa ajili ya kuwalinda wale wasio na uwezo kutoka kwa mashabiki wa kupindukia. AmirulMu’minin anasema: “Kama unapenda kuwa shabiki wa kupindukia na mwenye upendeleo, basi uunge mkono maadili ya hali ya juu, tabia njema na sifa zinazofaa, kwa mfano kulinda haki za jirani yako, kuenzi mikataba yako, kuwatii wenye haki, kuwapinga waasi, kuwa na tabia nzuri, kuepukana na dhuluma, kujiepusha na umwagaji damu, kufanya uadilifu na kutosababisha fitna na mabalaa juu ya ardhi.” Ni kiasi gani aliuchukia ushabiki uliokithiri kinaweza kutambulikana kutokana na mapendekezo ambayo aliyafanya kuhusu Khawarij, ingawa walikuwa maadui zake. Walipigana vita vikali dhidi yake, lakini yeye anasema: “Msije kupigana na Khawarij baada yangu, kwa sababu mtu anayetafuta kweli lakini akapotea sio kama yule anayetafuta upotovu na akaupata.” Amirul-Mu’minin aliwafanya watu kutambua kwamba kwa vile kulikuwa na uwezekano wa maoni na imani zao kuwa na makosa, ilikuwa ni muhimu kwamba wasilitie mkazo juu ya usahihi wa maoni na imani zao, wala wasizisukume juu ya wengine. Yeye aliwaambia wasijizuie kufanya mashauriano na wasisite katika kuukubali ukweli.

148

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 148

9/4/2017 3:47:52 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Vita Na Amani Kuna haki za pamoja nyingi zilizotumiwa na watu. Mojawapo ni kwamba wanapaswa kuimarisha mafungamano yao ya upendo na urafiki. Mshikamano huo lazima uwepo baina ya watu binafsi na vile vile kati ya makabila na mataifa, kwa sababu raia wa nchi zote ni ndugu wa kila mmoja wao kwa mwingine. Wote ni kazazi cha baba mmoja na asili yao ni moja. Wanayo njia moja ya pamoja na madhumuni na malengo yao pia hayatofautiani. Uhuru na utajiri, sheria zilizowekwa, na juhudi mpya vyote hivyo vimelengwa kwa ajili wa mwanadamu. Haya yote hata hivyo, hayana maana panapokuwepo vita na umwagaji damu ambavyo vinaweza kuwaangamiza wanadamu. Mambo yote haya ni kwa ajili ya mwanadamu. Ni nini faida ya haya yote (vistawishi na starehe) ikiwa maisha ya mwanadamu hayako salama? Kila kauli ambayo inawataka watu kuwatumikia wanadamu, lakini ikawa haiwalinganii kwenye amani ni mbaya na yenye kuchukiza. Maadili yote kuhusu mwanadamu na maisha yake hayana maana isipokuwa yawe yanaendeleza undugu wa kibinadamu. Yataonekana ni ya aibu kiasi gani maneno hayo, vitendo na maadili wakati mifereji inageuzwa kuwa mito ya damu, mabustani yanaharibiwa na makasiri yanageuka kuwa magofu! Maneno haya, vitendo na maadili yataonekana ni ya kipuuzi kiasi gani wakati mwanadamu anatupwa katika mdomo wa vita na uzuri wa maisha yake, matumaini yake na matakwa, na utu wake wenyewe hasa vinashushwa thamani na kuwa si chochote. Vita ni chanzo cha vifo na maangamizi, ambapo amani ndio njia pekee ya kuepuka maangamizi. Hili ndio lengo linaloongozea kwenye madhumuni na malengo mengine mengi. Ni katika wakati wa amani tu ambapo wanadamu wanaweza wakatumia vipaji vyao vyote na kufanikisha matakwa yao ya pamoja kwa juhudi za pamoja. Kanuni na taratibu za Ali zinatumika kwenye nyanja zote kwa namna ile ile ambamo matawi ambayo yanachomoza kutoka kwenye mzizi mmoja yanatawanyika pande zote. Yeye alikuwa ametambua kwamba amani ni ukuta mrefu unaomzunguka mwanadamu na maisha ambao huvilinda vyote kutokana na kila janga. Akiwahutubia watu yeye anasema: “Mwenyezi Mungu hakuwaumbeni ninyi bure bure hivi tu.� Na kuhusiana na maoni ya Ali kuhusu madhumuni ambayo kwayo Mwenyezi Mungu amemuumba mwanadamu, yeye anasema: “Mwenyezi Mungu amekuumbeni ninyi wa kuheshimika juu ya ardhi Yake, na salama miongoni mwa viumbe Wake. 149

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 149

9/4/2017 3:47:52 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Neema Zake zimetandaza mbawa za huruma juu ya vichwa vyenu na kufanya mito ya faraja kutiririka kwa ajili yenu.” Kwa mujibu wa Ali, upendo na urafiki ndio neema kubwa kwa mwanadamu. Yeye anasema: “Mwenyezi Mungu Mtukufu ameimarisha mshikamano wa upendo kati ya wanadamu. Ni upendo ambao chini ya kivuli chake watu wanatembea huku na huko, na ambao kwenye mapaja yake wao wanatafuta hifadhi. Upendo huu ni neema tunu, yenye thamani sana, kwa sababu ni ghali sana kuliko gharama yoyote itakayokadiriwa juu yake, na kubwa kuliko kila kitu kikubwa.” Ali anasema kwamba kila mtu ni lazima aimarishe urafiki na upendo na watu wengine ili amani iweze kuwepo, kwa sababu katika wakati wa amani hali ya mji huwa tulivu na watu wanakuwa hawahisi hofu ya aina yoyote ile. Mtu lazima aepuke mambo ya vita, kwa sababu vita ni uonevu na ni jambo la kuchukiza sana na lisilofaa kabisa kuwaonea viumbe wa Mwenyezi Mungu. Hata kama matokeo ya vita ni ushindi au kurudi nyuma bado ina madhara kwa hali zote hizo. Vita ni uharibifu na maangamizo kwa mshindi, na kwa mwenye kushindwa vile vile. Vita vinaharibu heshima ya mwanadamu. Mshindi anachukuliwa kuwa mpinzani wa akili na dhamira, ni adui wa upendo, anayeyafanya maisha ya mwanadamu kutokuwa na thamani, na yule aliyeshindwa anafedheheka, na maisha yake na mali pia vinaharibika. Ali anasema: “Hakuna jambo baya kama mapigano na umwagaji damu.” Ali alichukulia uporaji na unyang’anyi, ambavyo vilikuwa ndio mwanzo wa vita kati ya makabila katika zama za jahilia kuwa moja ya vitendo vibaya sana. Kulingana na Ali, uporaji na unyang’anyi, kuabudu masanamu, na kuwazika wasichana wakiwa hai, vilikuwa ni dhambi za aina moja na asili yao ilikuwa ni moja na ile ile. Asili hiyo ni kwamba mwanadamu hatambui thamani yake mwenyewe wala ile ya maisha, na hakuwezi kuwa na ujinga mkubwa zaidi kuliko huu. Yeye anasema: “Wao walikuwa wamefikia lindi kubwa la ujinga. Waliwazika wasichana wao wakiwa wako hai, waliabudu masanamu na waliibiana na kunyang’anyana wenyewe kwa wenyewe.” Alichukia sana mapigano kiasi kwamba aliyakataza hata katika mazingira magumu sana kwamba mtu mmoja ampe mwingine changamoto ya kupambana. Yeye anasema: “Kamwe usimuite mtu mwingine kuja kupigana nawe.” Wakati tunapoyachunguza maisha na tabia za Ali, inajitokeza wazi kabisa kwamba yeye alishutumu tabia nyingi za watu na aliyaona mambo mengi katika dunia hii kuwa ya kuchukiza mno. Kuhusu tabia za watu, kwanza kabisa alishutumu mwelekeo wa kwenye fitna na umwagaji wa damu. 150

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 150

9/4/2017 3:47:52 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Na kuhusu yale mambo yanayochukiza mno, hakukuwa na jambo lililoudhi sana mbele ya macho yake kuliko mambo ya vita. Maneno yake haya yanastahili kuzingatiwa akilini: “Dunia hii ni makazi ya vita, unyang’anyi na umwagaji damu.” Kupigana kuna madhara sana juu ya haki, kwani ndio chanzo cha hifadhi ya upotovu. Ni kwa njia ya haki ambapo mwanadamu anatukuzwa, jamii inaimarika na dunia inakuwa yenye kustawi. Upotovu ni mkusanyiko wa fedheha na aibu. Ni dhahiri kwa hiyo, kwamba hakuwezi kuwa na jambo baya zaidi kuliko vita. Ndio chanzo cha upumbavu wote, kwa sababu wasiwasi unakuwepo, vita na upotovu vinashamiri, na sauti ya haki inazimwa, ambapo amani ndio haki yenyewe, na yeyote anayekiuka haki anapotea. Huu ndio ulikuwa msingi wa maoni na imani uliokuwa umeshikiliwa na Ali kuhusu vita, na hili halishangazi pia, kwa sababu imani hii ilikuwa inachukuana na wazo la uhuru na matumaini ambayo alikuwanayo juu ya mwanadamu wa kawaida, na heshima aliyokuwanayo juu ya maisha, na vile vile kwa ajili ya wale waliokuwa hai. Ni kwa sababu hii kwamba nyakati zingine, ili kuweza kulimaliza tatizo na kuwalingania marafiki zake kwenye amani yeye alisema: “Kwa maadui zenu hasara hii inawatosha ya kwamba wamepotea.” Imam Ali alikuwa akimtaka mkosaji na mhalifu kuonyesha majuto yake kwa ajili ya kupitiwa kwake ili mapigano yasije yakatokea. Kuhusu watu waliodhulumiwa alikuwa akiwataka wakubali maombi ya msamaha ya yule mhalifu hata kama kosa lake litakuwa na ukubwa kiasi gani. Yeye alisema: “Yakubali maombi ya msamaha ya mtu anayekuomba radhi.” Vile vile yeye anasema: “Shindana na matamanio yako ya kidunia kwa kutumia akili. Kama ukifanya hivyo watu wataendelea kukupenda.” Yeye kwa hiyo, aliichukulia kuwa ni sifa bora kwa wafuasi wake kwamba wapende amani, wachukie vita na watafute usalama kwa ajili yao wenyewe na pia kwa wengine. Na kuhusu ni sifa gani wafuasi wake wanapaswa kuwa nazo, yeye anasema: “Wakati wafuasi wangu wanapokasirika huwa hawafanyi uonevu. Wao ni rehema na neema kwa majirani zao na chanzo cha usalama kwa marafiki zao.” Hata hivyo, chuki juu ya vita na mielekeo isiyo ya kawaida kwenye amani haikuwa na maana kwamba Ali angejisalimisha kwa adui yake. Chuki juu ya vita na mwelekeo kwenye amani havina maana kwamba mtu akwepe majukumu yake na kuwaacha wafanya madhara wawe huru kufanya wanavyotaka, kwa sababu vita 151

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 151

9/4/2017 3:47:52 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

yenyewe hasa sio jambo la kuchukiza, bali inakuwa mbaya kwa sababu ya vitisho vyake na maangamizi yanayofuatana nayo, na amani sio kitu kizuri tu chenyewe, bali inakuwa nzuri, kwa sababu inaleta usalama kwa watu, inatoa nafasi ya kuendeleza jamii, na inafungua njia ya maisha mbele ya wale ambao wanaishi. Kwa ufupi, ama iwe vita au amani, vyote hakuna chochote ambacho kwa asili ni kizuri au kibaya. Uzuri wao au ubaya wao unathibitika kutokana na kumbukumbu za watu wengine. Kama vita au amani vingekuwa na thamani halisi, zile juhudi za kimapinduzi zilizofanywa na wale watu wa dunia walioonewa, dhidi ya wafalme na watawala waonevu na wakoloni zingekuwa uovu na dhambi, na utii kwa madhalimu wale ungekuwa ni heri, lakini kwa hakika sio hivyo. Jambo halisi ambalo lina maana ni ustawi wa watu. Kama wanaishi katika faraja na mali zao na heshima viko salama, amani ni bora kwao. Endapo, hata hivyo, wanaishi maisha ya taabu na haki zao zinavunjwa, basi vita ndio heri kwao mpaka mazingira ya amani halisi yatakapotengenezwa, amani, ambayo imeegemea juu ya thamani ya mwanadamu na imeondokana na fedheha na kutojiweza, na unyenyekevu kwenye dhulma na uonevu. Hili ndio alilokuwa nalo Ali mawazoni. Alichokichukia ni vile vita vya Abu Lahabi na Abu Sufyan dhidi ya Muhammad na wala sio vile vita vya Muhammad dhidi ya Abu Lahabi na Abu Sufyan. Alivichukia vile vita ambavyo vilipiganwa na madhalimu dhidi ya waadilifu, na sio vita vilivyopiganwa na watu watiifu na wachamungu dhidi ya madhalimu na wanafiki. Ali aliwataka watu wasije wakawa kama Changez Khan, Halaku, Hitler au Mussolini, bali hakupenda pia wawe kama wale waliofanywa watumwa na Changez, Halaku, Hitler na Mussolini. Hakuna ubaya wowote kwa vita ambavyo vinapiganwa ili kurudisha haki ya mtu aliyeonewa kutoka kwa muonevu, au kulinda heshima ya watu. Kwa kweli hilo ni haja ya kijamii na jambo ambalo ubinadamu unalidai. Sharti la kigezo kwa vita kama hivyo ni kwamba kabla ya kuikimbilia, juhudi zote muhimu kwa ajili ya amani na suluhisho lazima zifanywe. Wakati wafuasi wa Ali walipokosa uvumilivu kwa sababu ya yeye kuwa amechelewesha ruhusa pale Siffin ya kufanya Jihadi yeye aliwaambia: “Na kuhusu kuuliza kwenu kama ucheleweshaji huu ni kutokana na ukweli kwamba mimi nina152

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 152

9/4/2017 3:47:52 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

chukia kifo na ninataka kukikwepa, ninaapa kwa jina la Allah kwamba mimi sijali kama ninatoka kukielekea kifo au kifo kinatoka kunielekea mimi. Na vivyo hivyo kuhusu kuuliza kwenu kwamba huenda nina mashaka kuhusu uhalali wa jihadi dhidi ya watu wa Syria, naapa kwa jina la Allah kwamba sikuvichelewesha vita hata kwa siku moja isipokuwa kwa mawazo kwamba watu fulani kutoka miongoni mwao huenda wanaweza wakaja kukutana nami na wakawa wameongoka kupitia kwangu na wanaweza pia wakaiona nuru yangu kwa macho yao yaliyotanzwa. Nalipenda hili zaidi kuliko kuwaua wakiwa katika hali ya ujinga, ingawa wao wenyewe watakuwa kwa hali yoyote ile wanahusika kwa makosa yao.” Sharti la pili kwa ajili ya vita ni kwamba lengo lake lisije likawa ni kwa ajili ya kupata ushindi tu. Zaidi ya hayo, ushindi huo usijekuwa wa kutaka kulipiza kisasi. Asiwatese maadui na asije akawaonea mateka na wale ambao wameteseka kwa sababu ya vita. Asije akawafukuzia wale wanaokimbia, na asiwadhuru wazee, wanawake na watoto. Kama yule anayeingia vitani anafikiri kwamba yeye yuko kwenye haki, na anadai kwamba anapigana kwa ajili ya uadilifu, na adui yake ni dhalimu, na ni lazima kulipiza kisasi juu yake, ajiridhishe mwenyewe kwa kuiweka haki mahali pake. Kama lengo hili linapatikana baada ya mapigano mafupi ni lazima azuie mkono wake kutokana na kuendeleza vita. Katika vita vyote vilivyopiganwa na Ali, kanuni ya msingi aliyoifuata yeye ilikuwa kwamba umwagaji damu usikimbiliwe isipokuwa itakapokuwa ni lazima kabisa na hapakuwa na njia nyingine mbali na vita. Wakati wote alijitahidi kuwashauri adui yake na kumfanya akubali kufuata busara. Alitumia kusema: “Wallahi kwa hakika nitafanya uadilifu kwa yule aliyeonewa na nitatoa ushauri kwa muonevu.” Wakati ushauri na juhudi kwa ajili ya amani na suluhu viliposhindwa yeye alikimbilia kwenye vitisho, kwa sababu lengo lake hasa lilikuwa kwamba kama ikiwezekana, hata tone moja la damu lisiweze kumwagwa. Wakati akiwatishia watu wa Nahrawan, yeye alisema: “Ninakuonyeni kwamba mtauawa na mtaanguka mchangani katika mzunguko wa mfereji na miteremko yake imara katika hali ambayo hamtakuwa na hoja ya maana au ushahidi wa wazi wa kutoa mbele ya Mwenyezi Mungu kama kisingizio. Hali ni hii kwamba mmekuwa hamna makazi na halafu hukumu ya ki-mungu ina mshiko madhubuti juu yenu. Nilikuwa tayari nimewakataza kutokana na kukubaliana na usuluhishaji huu lakini mlikataa kutii maagizo yangu kama wavunja sheria wapinzani, kiasi kwamba nililazimika kukubaliana na kile mlichokitaka. 153

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 153

9/4/2017 3:47:52 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Ninyi ni kundi ambalo vichwa vyenu havina uelewa wala akili. Ole wenu! Mimi sikukuhusisheni katika matatizo yoyote wala kukutakieni mabaya.” Sasa hebu tafadhali soma dua hii ya ajabu ya Ali na upate taswira ya uadilifu wake wa hali ya juu na huruma ambayo alikuwa nayo moyoni mwake juu ya maadui waliouawa. Wakati vikosi vya maadui pale Siffin hatimae vilipoamua kupigana, na juhudi zote juu ya amani na suluhu zikawa zimeshindwa, yeye alimuomba Mwenyezi Mungu katika maneno haya: “Ewe, Mungu Wangu, Mola wa dunia hii, ambayo umeifanya kuwa ni makazi ya wanadamu, na sehemu ya kuzurura ya wanyama watambaao, wale wa miguu minne na viumbe wengine wasio na idadi, wanaoweza kuonekana au wasioweza kuonekana. Ewe Mola wa milima yenye nguvu ambayo umeifanya kuwa kama misumari kwa ajili ya ardhi na njia ya mahitaji ya maisha kwa ajili ya viumbe vyako! Kama utatujaalia ushindi dhidi ya maadui utukinge kutokana na kufanya udhalimu na utuweke kwenye njia iliyonyooka ya haki, na kama utawafanya maadui zetu kuwa washindi basi tupe vifo vya kishahidi na utuokoe kutokana na vivutio vya maisha.” Bidii ya Amirul-Mu’minin kwa ajili ya amani na juhudi zake juu yake hata muda mchache kabla ya kuanza kwa vita, ni ukweli usiopingika, ambao unathibitishwa na marafiki zake na hata maadui zake pia. Katika uhai wake wote alionyesha mapenzi juu ya amani na chuki juu ya vita. Wakati wote alijaribu kwa uwezo wake wote kwamba vita viepukwe na suluhu iweze kuchukua nafasi. Wakati, katika vita vya Ngamia, Aisha, Talha na Zubeir walipokuwa tayari kupigana dhidi yake, aliwapanga wafuasi wake na akawaambia: “Msitupe mshale na msirushe mkuki au upanga ili iweze kuthibitishwa kwamba mmetekeleza wajibu wenu.” Hata hivyo, Ali hakuanza kupigana mpaka maadui wawe wametumbukiza mishale kwenye miili ya wafuasi wake watatu na akawa amemuomba Mwenyezi Mungu mara tatu kuwa shahidi kwenye kitendo chao hicho. Alifika mbele ya maadui zake mara nyingi bila silaha mkononi na bila ya vazi la deraya ingawa wao walikuwa wamejiandaa kikamilifu kwa silaha. Katika kujibu maneno yao makali na ukaidi, na sauti kali, yeye alizungumza kwa upole kabisa na akawapa ushauri katika namna ya kirafiki kabisa. Mbele yake wakiwa wamesimama maadui zake ambao walionekana kama usiku wa giza kwa vile walikuwa wamefunikwa na mavazi ya chuma na ngao, lakini vazi lake yeye lilikuwa ni heshima juu ya wanadamu; ngao yake ilikuwa ni imani yake 154

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 154

9/4/2017 3:47:52 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

juu ya kuwa yuko kwenye haki na katika mtindo wake wa utendaji ukiwa sahihi, na upanga wake ulikuwa ni ulinganifu wake na amri za busara na dhamira. Kwa kweli upole wake kwa wanyonge, kuunga mkono kwake haki na kutaka amani kwake vilikuwa ni bora kama maelfu ya ngao kwa ajili yake. Alikuwa ni yeye aliyesema: “Kama unajihisi kusalimika kutokana na kuchokozwa na mtu, jaribu kumfanya kuwa ndugu yako.” Imam Ali alikuwa ni mtu aliyechukia uadui na kinyongo kwa sababu mambo haya mawili yanazaa kutoelewana na yanaharibu maadili ya mtu na alama za taifa. Yeye alisema: “Jizuieni kutokana na uadui na migogoro, kwa sababu mambo haya mawili yanaufanya moyo kuwa na maradhi, na kutokupatana kunaanzia kwenye mambo haya.” Mara nyingi alifika mbele ya maadui zake mikono mitupu na bila vazi la deraya au ngao. Alifanya hivi ili kuwafanya wao watambue kwamba yeye alichukia vita na alikuwa na bidii ya kutatua matatizo katika njia ya kirafiki na kindugu. Yeye alisema: “Fanya wema kwa adui yako kwa sababu ushindi huu ni wenye kukubalika zaidi na ni mzuri.” Lengo jingine la kuwaendea wapinzani wake katika hali hii lilikuwa kwamba yeye alitaka kuweka wazi kwamba vita ni kitu kibaya, na manufaa ambayo kwayo mshindi anayapata kutokana nayo ni manufaa ambayo yanapatikana kutoka kwenye uovu na hayana thamani. Yeye anasema: “Uzuri wa jema ambalo linapatikana kupitia kwenye uovu ni lisiloleta manufaa, na utajiri ambao ni matokeo ya ufukara na dhiki hauna thamani.” Ali aliuondoa uovu huu (vita) kwa njia zote zinazowezekana na alijaribu kuboresha hali za watu bila ya umwagaji damu au migongano. Kiasi kwamba pale maadui walipokuwa wamedhamiria kupigana vita na wakawa hawana madhumuni mengine zaidi ya kumwaga damu yake na ya wafuasi wake waadilifu vilevile, yeye aliwashauri na alijitahidi kwa bidii zake zote kuzuia mapigano. Na pale juhudi hizi zilipokwama na kukawa hakuna njia nyingine iliyobakia isipokuwa kujiunga na vita tu, hakuanzisha yeye mapigano. Vita vilianzishwa na maadui na yeye alijibu tu mashambulizi yao. Na alipokamata upanga mkononi mwake alijitokeza mbele, na sasa hapo alikuwa ni Ali mwana wa Abu Talib. Kama kifo hakikutoka kumwendea, basi yeye mwenyewe alitoka kukiendea kifo hicho. Aliwaangamiza mashujaa na kuwafanya wapiganaji hodari kukimbia. Ali alipenda usawa na uadilifu, ambapo maadui zake walitamani sana udhalimu na uonevu. 155

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 155

9/4/2017 3:47:52 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Yeye alitamani sana wanadamu waweze kustawi, ambapo wao walitaka kusababisha fitna na balaa. Yeye alitaka watu wafurahie uhuru na faraja, ambapo wao walikuwa na bidii ya kuwafunga kama watumwa. Alitamani kwamba waja wa Mwenyezi Mungu wawe wenye nguvu na kuheshimika, ambapo wao walitaka kuwafanya watumwa na kuwafedhehesha. Mambo ambayo ni lazima yawepo kwenye jamii, na ambayo pia yanachukuliwa na sheria na akili kuwa muhimu yalikuwa hatarini. Sasa katika hali hizi, kubakia kuwa mtazamaji mkimya kulikuwa ni sawa na utepetevu, uzembe, kukosa uaminifu, na kuyalinda hayo kulimaanisha ujasiri na ushujaa. Kuhusu kupigana dhidi ya Mu’awiyah yeye anasema: “Nimelipima na kulichambua jambo hili kwa makini sana na nimeamua kwamba ni njia mbili tu zilizowazi mbele yangu, imma nipigane vita dhidi ya Mu’awiyah au nigeuke kuwa muasi, kafiri.” Hebu tazama tu alivyovuta picha ya vita vya Ngamia katika namna fupi na ya dhahiri na pia ameelezea msimamo wake: “Talha na Zubeir walikuwa ndio watu wa kwanza kuchukua kiapo cha utii kwangu. Baadaye wakakivunja kiapo hicho bila sababu ya haki, na wakamchukua Ummul-Mu’minin Aisha kwenda Basra. Nililazimika vile vile kuwachukua Muhajir na Ansari ili kuwafuatilia. Nilijaribu kwa uwezo wangu wote kwamba waweze kuchukua tena kiapo kile ambacho wamekivunja lakini wakakataa kufanya hivyo. Niliwashauri sana na nikashughulika nao kwa wema.” Wakati Ali alipokuwa bado yuko njiani na alikuwa bado hajakabiliana nao, alimtuma mwanawe Hasan na binamu yake Abdullah ibn Abbas, pamoja vilevile na Ammar ibn Yasir na Qais bin Sa’d bin Ubada kwenda kufanya mazungumzo nao (Talha na Zubeir) akitegemea kwamba wangeweza kuitikia mwito wake kwenye busara, na umwagaji wa damu kuweza kuepukwa. Wao hata hivyo, walibakia wasiokubali mapatano. Amirul-Mu’minin anasema hivi kuhusu hili: “Nilishika njia pamoja na Muhajir na Ansar na tukasimama karibu na Basra. Niliwalingania kwenye amani na suluhu, nikaacha kujali kuteleza kwao na nikawakumbusha juu ya kile kiapo cha utii walichokuwa wamechukua. Hata hivyo walizidi kukataa katakata na wakasisitiza juu ya kupigana. Nilitaka msaada kutoka kwa Mwenyezi Mungu na nililazimika kujitayarisha kwa ajili ya ulinzi dhidi mashambulizi yao. Matokeo yakawa kwamba wale waliokuwa wauawe wakauawa na wengine wakakimbia zao. Hapo sasa waliniomba juu ya amani ile ile ambayo niliitaka kabla ya mapigano hayajachukua nafasi. 156

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 156

9/4/2017 3:47:52 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Niliyakubali mapendekezo hayo juu ya amani na nikawaacha huru. Nilimteua Abdullah ibn Abbas kama gavana wao na nikamtuma Zafar bin Qais kwao kama mjumbe. “Sasa unaweza kuwaendea hawa watu wawili ili wakuambie wewe kila unachotaka kujua kutuhusu sisi na wao.” Ali alikuwa mshindi kwa sababu ya ushujaa wake wa ajabu na imani kamilifu na ya kina. Yeye alikuwa, hata hivyo, akisikitikia sana na ushindi wake kama vile walivyokuwa maadui zake juu ya kushindwa kwao. Machozi yalimtiririka kutoka machoni mwake na alihuzuniska sana. Kila baba anawapenda sana wanawe. Kama mtoto hajichungi sawasawa, baba yake atakuwa achukue hatua za usahihishaji na kumwadhibu ingawa kitendo kama hicho kinamsikitisha sana yeye. Vivyo hivyo, ndivyo ilivyokuwa kwa Ali. Aliwafanya Waislamu kama watoto wake. Mtume wa Uislamu alisema: “Mimi na Ali ndio mababa wa umma huu.” Ali aliwapenda sana watoto hawa. Alilazimika kuchukua hatua za usahihishaji dhidi yao kwa sababu ya udhalimu na makosa yao, lakini alihuzunika sana kuona mateso yao. Ali hakuchukia kitu chochote zaidi kuliko umwagaji damu. Alikuwa wakati wote ana wasiwasi, asaa magavana na watumishi wake wakajiingiza kwenye umwagaji damu usio halali. Yeye kwa hiyo, aliwaonya tena na tena wasije wakajihusisha na umwagaji damu. Alichukua tahadhari kwenye mtazamo wa kimaadili na pia wa kisiasa na kiutawala kwamba damu isije ikamwagwa bila sababu. Aliukataza katika nafasi zote, kwa sababu aliona kwamba, kama matokeo ya umwagaji damu kama huo, serikali inaweza ikaanguka na pia ulikuwa ukipingana na falsafa ya serikali. Hakumsamehe mtumishi yeyote kwa ajili ya kuteleza kuhusu hili. Katika barua aliyoiandika kwa gavana mmoja, yeye anasema: “Usije ukajaribu kuimarisha serikali yako kwa umwagaji damu bila sababu ya haki, hilo litaifanya serikali yako kuwa dhaifu zaidi bado, kwa usahihi zaidi itaondolewa mikononi mwako na itaishia kwenye mikono ya mtu mwingine. Kama utakuwa na hatia ya umwagaji damu wa makusudi, Mwenyezi Mungu hataichukulia dhambi yako hii kama ni yenye kusameheka, na mimi pia sitaichukulia hivyo.” Je, amewahi kuwepo mtawala mwingine yoyote hapa duniani, ambaye anaweza kuwa ametoa maelekezo yenye mkazo kwa magavana wake kumteua kamanda wa kijeshi mtu ambaye ni mnyenyekevu na mvumilivu, anayechukia umwagaji damu na mauaji, anayeweza kuamua mambo kwa majadiliano ya pamoja, ambaye hana hatia ya umwagaji damu usio na uhalali, ni mpole na mkarimu, sio mkatili katika 157

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 157

9/4/2017 3:47:52 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

kutaka kazi iwe imefanywa na watu wengine na ambaye hana mazoea ya ukali na vurugu? Katika wasia aliouandika kwa ajili ya Malik Ashtar wakati alipomteua kuwa gavana wa Misri, Ali anasema: “Mchague kuwa kamanda wa jeshi lako mtu ambaye unamuona kuwa mwaminifu zaidi na mbora kuliko wengine katika suala la unyenyekevu na uvumilivu. Yeye asiwe mwepesi wa kukasirika na akubali kuombwa msamaha. Awe mpole kwa wanyonge na awe mgumu kwa wenye nguvu. Asiwe na hasira kutokana na ukali na asiwe asiyejiweza kutokana na udhaifu.” Hivyo ni dhahiri kwamba Ali alikuwa mtu mpenda amani. Wakati wote alipendekeza amani. Alichukia sana vita na wakati wote alikuwa akivikataza. Kamwe yeye hakupiga hatua kuelekea kwenye vita isipokuwa vita vilipopiga hatua kumwelekea yeye, na hata kama alipiga hatua kuilekea vita, ilikuwa ni wakati alipokuwa amemaliza juhudi zote za kuizuia kwa njia za kirafiki, upendo, wema na upole. Kama alilazimika kupigana vita alijaribu kuona kwamba ni idadi ndogo ya watu wanaouawa. Na wakati alipopata ushindi juu ya adui alimsamehe. Alisikitika sawa hali kadhalika katika tukio la kushinda ama kushindwa. Wakati wowote adui yake alipoomba amani alikubali maombi yake kwa furaha kabisa na kwa moyo wote. Alikuwa akisema: “Katika wakati wa amani wapiganaji wanakuwa katika faraja, wasiwasi wa watu unakuwa mdogo zaidi na hali ya usalama inakuwa inapatikana katika miji.” Alituma maagizo mengi sana kwa magavana na watumishi ambamo alipendekeza kwao kwa msisitizo pamoja na mambo mengine, kwamba wanapaswa kufuata mfano wake na wasichomoe panga zao kwa sababu ya mambo ya kawaida kama ilivyokuwa imefanywa na watu wakati wa zama za ujahilia. Imam Ali anasema: “Msiweke mikono na panga zenu kwenye mshughuliko kama ulimi kwa sababu ya mambo yasiyo na maana.” “Sipendi kumuadhibu mtu vivi hivi tu kwa sababu ya kumtilia mashaka au kumtuhumu.” “Sitapigana na mtu yeyote mpaka kwanza nimlinganie kwenye amani na hivyo kutekeleza wajibu wangu katika suala hilo. Kama atajuta, mimi nitakubali kutubia kwake, lakini kama atakataa kufanya hivyo na akawa amedhamiria kupigana, basi mimi nitaomba msaada kwa Mwenyezi Mungu na nitapigana dhidi yake.” Tutaeleza kwa kirefu baadae jinsi Ali alivyowatendea maadui zake wakali. 158

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 158

9/4/2017 3:47:52 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Ni wajibu wa kila mtu kushikilia ahadi alizoziweka yeye. Kwa njia hii amani inadumishwa kati ya watu mmoja mmoja na katika jamii na nafasi za kutokea vita zinafutika. Mkataba ni lazima uheshimiwe, uwe umefikiwa baina ya wafuasi wa dini moja au wa dini tofauti, kati ya watu wa kabila moja au makabila tofauti na kati ya marafiki au maadui. Hii ilikuwa ndio kanuni ambayo ilifuatwa na Ali siku zote. Kama ilivyoelezwa hapo juu, utimizaji wa ahadi ni njia ya amani, na amani inahakikisha kudumu kwa hali ya usalama na ustawi, na ni huduma kubwa sana kwa umma. Inakuwa hivyo kwa sababu mikataba na sheria ni njia za ummoja na mshikamano wa umma. Utimizaji wa ahadi ni tabia ya mtu muungwana, na sababu ya mtulizano wa mawazo na akili, na upatikanaji wa maadili ya hali ya juu ambayo kwayo AmirulMu’minin alifanya juhudi katika maisha yake yote. Kuwa mwaminifu kwenye mikataba yake mtu, kunahakikisha urafiki na upendo katika hali zote na ni udhihirisho wa heshima kwa ajili ya wanadamu. Pande zote zinakuwa zimeridhika kama matokeo ya uaminifu huu, na pale wote wanaporidhika kila mmoja wao anaweza akaamua kwa utulivu wa akili kuhusu ni vipi atakavyoendesha mambo yake. Kinyume chake kama hawakuridhika, haitawezakana kwao kufanya kazi zao kwa urahisi. Katika kipindi cha ukhalifa wa Ali utimizaji wa ahadi ulikuwa ni kanuni ambayo ilikuwa ni muhumu kabisa kwa watu kuifuata. Kila mtu alitegemewa ama kutimiza ahadi yake au kutoa uhai wake hasa. Ali alichukia uvunjaji wa ahadi kwa kiasi kile kile kama alivyochukia umwagaji damu. Katika moja ya hotuba zake, yeye anasema: “Utimizaji wa ahadi na haki siku zote vimekwenda mkono kwa mkono na kwa kiasi ninavyotambua mimi, hakuna ngao bora za kumlinda mtu kuliko hizi. Yeyote anayeuelewa uhakika wa “Marejeo” yake basi hafanyi udanganyifu. Hata hivyo, wakati wetu uko kwa namna kwamba watu wengi wamedhania udanganyifu na uongo kuwa na maana ya akili na hekima, na watu wajinga wamezifanya njia na taratibu zao kuwa ni busara. Mwenyezi Mungu awaangamize hao! Ni nini kilichowatokea hawa? Wakati mtu ambaye ameona hali zote za maisha na anatambua mabadiliko ya wakati, anajitengenezea mpango kwa ajili yake mwenyewe lakini akakuta amri za kimungu katika njia yake, anauacha ule mpango wake, ingawaje anaweza akawa na uwezo wa kuutekeleza. Kwa upande mwingine yule ambaye njia yake haikwazwi na hisia za kidini anakuwa nayo fursa. Katika wasia ambao 159

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 159

9/4/2017 3:47:52 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

aliuandika kwa ajili ya Malik Ashtar wakati alipomteua kuwa gavana wa Misri yeye anasema: “Kama mnawekeana masharti fulani na maadui zako au mnafanya mkataba naye unapaswa ujiondolee mzigo wake kwa kuuheshimu. Ni lazima utekeleze kwa uaminifu yale majukumu unayoyachukua na ujitengenezee mwenyewe ngao kwa ajili ya ulinzi wa ahadi yako. Kwa hiyo, usije ukatelekeza kile unachakusudia kukifanya wala kuvunja mikataba unayofanya na usije ukamdanganya adui yako.” Zaidi ya hayo, hakuridhika tu binafsi na kutilia mkazo kwamba kusije kukafanyika udanganyifu juu ya adui; bali pia alikataza kabisa kufanya makubaliano yenye utata pamoja na adui ambayo inaweza kutafsiriwa kwa njia mbalimbali tofauti, na hii inaweza kutoa uhalali wa kuvunja makubaliano hayo. Pia alielekeza kwamba baada ya kukamilisha mkataba na ukahakikishwa, fursa ya makosa ya mdomo isije ikachukuliwa kuuvunja mkataba huo. Wakati wowote Ali alipopata wazo au alipotoa amri, yeye, kwanza kabisa, alichunguza na kuvichambua vipengele vyake kwa uangalifu na makini kabisa. Kwa vile aliamini sana katika kutimiza ahadi; hata vizuizi vigumu kabisa na matatizo havikuweza kumfanya yeye akengeuke kutoka kwenye kanuni yake hii. Moja ya wakati ambapo aliheshimu ahadi yake licha ya kuwa na hali ngumu sana ulikuwa ni ule wa Siffin. Wakati wa vita vya Siffin iliamuliwa kuurejesha mgogoro huo kwenye usuluhishi. Maafikiano yalifanyika baina ya Amirul-Mu’minin na Mu’awiyah, kwa makubaliano kwamba wasuluhishi hao wawili watakapotoa uamuzi wao vita visimame kwanza. Baada ya mapigano kusimamishwa na maafikiano hayo yakawa yamekamilishwa, wafuasi wa Amirul-Mu’minin wakatambua kwamba walikuwa wamedanganywa. Mtu mmoja aliyeitwa Muhammad ibn Harith hapo akamwendea Ali na akasema: “Ewe Amirul-Mu’minin! Je, hatuwezi kuyapuuza haya maafikiano na tukaanza vita tena? Nina wasiwasi kwamba makubaliano haya yatakuwa ni chanzo cha fedheha na twezo juu yetu.” Amirul-Mu’minin akajibu: “Tuyavunje maafikiano baada ya kuyafunga? Hili haliruhusiki.” Na alikuwa ni Ali vilevile aliyesema: “Simama imara kwenye wajibu ambao umeuchukua. Ninawajibika kwa maneno yangu na ninahakikisha usahihi wake.” Mambo yaliyosimuliwa hapo juu yanaeleza kwamba juhudi za Ali juu ya kudumisha amani zilikubaliana kabisa na matakwa ya watu kwa sababu ya matokeo yake mapana yenye athari nyingi.

160

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 160

9/4/2017 3:47:52 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Wanadamu wote wanatamani sana uadilifu, usawa na uhuru, na juhudi za Ali juu ya amani zilikuwa ni udhihirishaji wa matakwa yao. Kwa kweli ilikuwa ni tamaa ya moyoni ya Ali mwenyewe ambayo pia aliidhihirisha katika amri na maagizo yake. Katika suala la juhudi zake za kuhakikisha kwamba mwanadamu ampende mwanadamu mwenzie; Ali yuko kwenye daraja moja na mitume waliotangulia, watu wema wa wanadamu. Kufanana kukubwa kulikoje kwa juhudi za Ali juu ya amani na ile sauti ya upole ya Muhammad ambaye aliwahi kusema: “Enyi waja wa Mwenyezi Mungu! Kuweni ndugu wa kila mmoja wenu.” Ni kiasi gani vile vile juhudi zake zilivyofanana na maneno ya Mtume ambaye, wakati alipoulizwa kuhusu ni tendo gani jema zaidi, yeye alijibu: “Kitendo chema kabisa ni kwamba mtu ajitahidi kwa ajili ya ustawi wa dunia.” Kupambana Na Dhulma Katika mambo yote ya kawaida, Ali aliendesha maisha yenye msimamo thabiti na wenye kulingana. Maadili yake ya hali ya juu, na busara zake zisizo za kawaida, vitendo vyake kuhusiana na usimamiaji wa dola, uongozi wa jeshi na tabia na sifa nyingine binafsi vyote vilikuwa sawa na vinavyohusiana. Alichukia riba, kuhodhi na dhulma vibaya sana. Alikuwa adui mkali wa watu matajiri na wenye uwezo ambao waliwaonea wengine, wajinga hawa walijiona wao kuwa ni bora kuliko wengine, na walishikilia maoni yao ya kikaidi yaliyotokana na ujinga. Alikuwa na bidii sana ya kuwasaidia wanyonge na masikini, kwa sababu wao pia walikuwa ni binadamu na sio halali kabisa kuwafanya wao kuwa duni na wasio na muhimu. Alitamani uhuru wa viumbe wa Mwenyezi Mungu kutoka ndani ya kiini cha moyo wake, kwa sababu Mwenyezi Mungu amewaumba huru na haistahili kabisa kwamba wao wafikwe na fedheha na udhalilishaji. Kufedheheka na kudhalilika kwao ni kufedheheka na kudhalilika kwa ubinadamu, na yeyote anayefedhehesha ubinadamu anastahili kuchukuliwa kama adui. Inaweza kutambuliwa na kila mtu kutokana na kile kilichoelezwa hapo juu kwamba ni msaidizi na mhurumiaji mkubwa kiasi gani wa wasiojiweza na walioonewa Ali alivyokuwa, jinsi alivyopambana dhidi ya maadui wa maadili na wema, na hasira

161

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 161

9/4/2017 3:47:52 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

kiasi gani alizoonyesha dhidi ya wale ambao walikwenda kinyume na kanuni za akili na dhamira. Hata hivyo, kile tulichokiandika sisi juu ya jambo hili hakionyeshi kuwa chenye kutosheleza. Inaonekana kuwa muhimu kutenga sura nzima tofauti, na yenye maelezo ya kina juu ya suala linaoonyesha jinsi Ali alivyojishughulisha na wadhalimu, na ni yapi yalikuwa maoni yake kuhusu udhalimu na uonevu. Kuna aina nyingi za udhalimu. Kwa mfano kunyang’anya mali ya mtu ni udhalimu wa aina mojawapo, na kudhuru heshima na sifa yake ni udhalimu wa aina nyingine. Wakati mwingine dhulma iko wazi ambapo wakati mwingine ina utata. Tutazijadili aina zote hizi za udhalimu moja baada ya nyingine. Sio rahisi kukuta hotuba au kauli yoyote ya Amirul-Mu’minin ambamo atakuwa hakutaja na kuishutumu dhulma kwa ukali sana. Maisha yake yote yalitumika katika kupigana vita dhidi ya dhulma na uonevu na dhidi ya madhalimu na waonevu. Alipigana vita hivi kwa mikono yake mwenyewe, ulimi na amri na maagizo, na vile vile kwa upanga wake. Vita dhidi ya dhulma na uonevu vinapiganwa tangu pale mwanadamu alivyowasili katika ulimwengu huu. Hata hivyo, vita hivi vimekuwa vikipiganwa katika njia tofauti na hali tofauti. Wale waliojitolea kupambana dhidi ya waonevu na madhalimu wa wakati wao walikuwa ni mamia ya maelfu kwa idadi. Hawa mashujaa wakubwa walikuwa ni chanzo cha fahari kwa ubinadamu ambapo wale waonevu walizijaza madoa kurasa za historia kwa matendo yao maovu. Wale mashujaa walikuja kwa mfuatano, mmoja baada ya mwingine na kila mmoja wao alirithi vita hivi vitakatifu kutoka kwa mwingine. Walikuwepo pia baadhi ya watu mashuhuri miongoni mwa wanadamu, ambao maisha yao yote yalitumika katika kupigana vita dhidi ya dhulma na ukandamizaji. Wasifu za akina Ibrahim, Musa na Yesu (Isa) zimekuwa na vita dhidi ya ukandamizaji, riba na dhulma. Mapambano ya Muhammad dhidi ya washirikina yalikuwa pia katika uendelezaji wa, na ukamilishaji wa vita vilivyoanzishwa na Isa. Alianzisha vuguvugu kubwa la kimapinduzi la kung’oa dhulma na uonevu, na hakupumzika hadi pale waliokandamizwa walipokombolewa na maisha yao yakageuka kuelekea kwenye ubora.

162

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 162

9/4/2017 3:47:53 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Ukatili huwa unakuwa ni tabia ya pili ya baadhi ya watu. Wanafanya maovu kwa urahisi kabisa kwa namna ile ile ambayo wanafanya vitendo vingine vya kawaida kama vile kula, kunywa, kutembea na kupumua. Kwenye kundi la namna hii wamo watu kama Nero, Changez Khan, maafisa wa Ulaya wa kundi la “Uchunguzi” la wakati wa Zama za Kati, na aina nyingine nyingi na watawala kama Hajjaj bin Yusuf, Ziad bin Abith, Ubaidullah bin Ziad, Muslim bin Aqba na kadhalika. Na vivyo hivyo historia inatuambia kuhusu watu wengine wengi wasio na idadi ambao kwao upinzani juu ya dhulma ulikuwa ni wa asili na umekuwa ni tabia yao ya pili. Sababu ya wakandamizaji wa zamani kutokuwa na aibu juu ya maovu waliyoyatenda ilikuwa kwamba wao walikuwa hawakukerwa na vitendo vyao vya ukatili. Hawakukandamiza au kuwaonea wengine kwa nia yoyote au lengo maalum. Wao walifanya hivyo kwa kuwa ilikwishakuwa ni tabia yao. Wakati mmoja Hajjaj alikuwa anakula chakula chake pamoja na baadhi ya marafiki zake. Mbele yake alikuwa amesimama mtu mzee asiyekuwa na hatia ambaye alikuwa anatetemeka kwa hofu. Hajjaj alinyanyua kichwa chake na akamwangalia yule mzee. Halafu akamwamuru mmoja wa watumishi wake kumkata kichwa chake. Amri hiyo ilitekelezwa mara moja na yule mzee akakatwa kichwa chake. Hajjaj akaendelea kula kana kwamba hakuna chochote kilichotokea pale. Akamwambia mtumwa wake kwa sauti kubwa: “Lete maji ya baridi.” Nero aliuchoma moto mji wa Roma. Wakati mji wa Roma ulipokuwa ukiungua Nero alikuwa akijishughulisha na kujifurahisha kwake. Umadhubuti na uimara wa wale ambao walipambana kwa msimamo kabisa dhidi ya dhulma na ukandamizaji unaweza vile vile kuelezewa katika namna hiyo hiyo. Kama vile tu hao watu waliotajwa hapo juu walivyofanya dhulma kwa sababu ilikuwa ni asili katika tabia zao, kwa namna hiyo hiyo hawa watenda wema wa ubinadamu walipigana dhidi ya dhulma na kuwasaidia wale watu waliokandamizwa, kwa sababu walilazimishwa na tabia zao kufanya hivyo. Socrates alikinywa kikombe cha sumu kana kwamba kilikuwa cha dawa kwa sababu kukinywa kwake kulikuwa ni kuonyesha umadhubuti na uimara dhidi ya udanganyifu. Voltaire37 alipigana vita dhidi ya mabwanyenye na waungwana wa Ul37

oltaire, mwandishi maarufu wa Kifaransa na mtu mashuhuri wa wakati wake alizaliwa mjini Paris mnaV mo mwaka 1694 A.D. na akafariki mwana 1778 A.D. Aliishi sehemu kubwa ya maisha yake huko England, 163

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 163

9/4/2017 3:47:53 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

aya. Alilazimika kupigana vita hivi kwa tabia yake kama vile mtu mwenye njaa anavyolazimika kula chakula, au mtu mwenye kiu anavyolazimishwa na hamu yake ya ndani kabisa ya kupata maji ya kukata kiu yake. Wafuasi wa Imam Husein pia walijitoa muhanga maisha yao katika kumuunga mkono kwenye ujumbe wake, ingawaje walikuwa wanaweza kuliona jeshi kubwa la Bani Umayyah likiwa limejipanga dhidi yao. Watu hawa walikuwa ni waqfu wa wanadamu na nafsi maarufu na karimu miongoni mwa wanadamu, ambao mkuu na kiongozi wao alikuwa Ali ibn Abi Talib. Yeye alikuwa amekuja ulimwenguni kusimamisha haki na kuvunja batili. Alisimama na lengo lake na pia akaukubali ukhalifa kwa lengo hili hasa mawazoni mwake. Hata hivyo, ulimwengu, pamoja na upana wake wote, haukuweza kukubali zile sheria na kanuni za Ali. Madhalimu na wale makatili walikuwa wengi kwa idadi na walikuwa na nguvu nyingi. Ile kazi ambayo Ali alitaka kuitimiza ilikuwa ngumu na ya hatari vilevile. Ali aliwaambia watu kwamba wasiwe ama madhalimu wala wenye kudhulumiwa. Alipenda kwamba mtu yeyote asidhulumu wengine na mtu yeyote asiivumilie dhuluma. Hata hivyo, watu wa wakati huo hawakuwa tayari kukubali maoni ya Ali na hawakuweza kuunga mkono makusudio yake. Kiasi kwamba hata wale waliodhulumiwa hawakuwa upande mmoja naye, kwa sababu walikuwa wamehofishwa sana na wale madhalimu na walikuwa wanaogopa uhasama na kinyongo chao. Walikuwa wapumbavu kiasi kwamba walipokea hongo kutoka kwa maadui zake Ali na wakajitoa katika kumuunga mkono yeye. Hatimaye wachamungu wachache na watu majasiri walibakia pamoja naye, na hawakumtelekeza kwa gharama yoyote ile. Hata hivyo, je, ilikuwa ni sawa kwamba Ali aonyeshe udhaifu na unyonge katika hatua hii ambapo majeshi ya uovu yameunda vuguvugu dhidi yake? Je, inawezekana kwa mtu jasiri kuvunjika moyo na kutupilia mbali jitihada kwa sababu anakabiliwa na majanga na matatizo pamoja na watu kama wala nyama karibu yake, hususan wakati ambapo kila mtu anaogopa kifo pia? Hivi Ali angeweza kuwa amevunjika moyo na kuwa goigoi wakati maadui walikuwa wanazidi kuwa waasi zaidi na zaidi, wakati watu waliokuwa kwenye mamlaka Russia na Swetzerland. Aliwashutumu vikali sana watawala na viongozi wa kidini wa wakati wake. Alikuwa ni yeye aliyesafisha njia kwa ajili ya yale Mapinduzi Makubwa ya Ufaransa ya mwaka 1789 A.D. Yeye ndiye mwandishi wa vitabu vingi vyenye maana na thamani. 164

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 164

9/4/2017 3:47:53 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

walikuwa wamepoteza akili zote za busara, walikuwa wanauza dini kwa ajili ya dunia, walikuwa wakikimbilia kipumbavu kabisa kwenye utajiri na vyeo, wamesababisha machafuko kwenye miji, walikuwa wakishadidi kwenye dhuluma, walikuwa wamejaa kiburi na majivuno, wakifanya uzushi na mambo yasiyo na maana mbele ya mambo ya sawa, wakitukuza makosa na kufaya uovu, na bado wakitegemea malipo mazuri na mema, walikuwa wameangamiza uadilifu na utenda haki, na wameanzisha uasi, na machafuko, na udhalimu wao na ukatili vikiwa havina mipaka. Hivi yeye angeweza kuwa mnyonge na mchovu, mlegevu wakati hali ya wafuasi wake ilikuwa hivi: “Yeyote aliyewaita kwa ajili ya msaada hakufanikiwa kamwe. Yeyote aliyekutana nao hakupata utulivu wa akili. Yeyote aliyeingia kwenye uwanja wa mapambano akiwa amefuatana nao alishindwa. Walikuwa viziwi licha ya kuwa na masikio, na walikuwa mabubu ingawa walikuwa nao uwezo wa kuzungumza. Wao hawakuonyesha uimara kwenye uwanja wa vita kama watu wenye maadili na wenye raghba, wala mtu asingeweza kutegemea juu ya huruma na msaada wao wakati wa mkasa.” Kwa kweli katika hali na mazingira kama hayo mtu angeweza kuwa mnyonge na dhaifu na lazima akae chini kilegevu – lakini kwa kutegemea sharti kwamba mtu huyo asiwe ni Ali ibn Abi Talib. Mapenzi mazito ambayo Ali alikuwa nayo moyoni mwake kwa ajili ya kila mwanadamu, yalimlazimisha yeye kuonyesha huruma ya kiasi cha chini kabisa kwa mtu ambaye alifanya madhara kwa watu, japokuwa kama yeye (Ali) alikuwa ayatoe maisha yake katika kampeni hiyo. Mtu anayeona kwamba ni upendo na upole, na dalili ya uungwana kubakia kimya mbele ya madhalimu, imma ni mwongo au hafahamu maumbile ya mwanadamu, kwa sababu nafasi hiyo iko kinyume chake. Upendo wa kweli na huruma kwa ajili ya mwanadamu una maana kwamba wale madhalimu lazima washughulikiwe vikali, ili kwamba waweze kuwaacha watu huru kutokana na vifungo. Katika mazingira Fulani, huruma na upole vinamlazimisha mtu kukimbilia kwenye ukali wa hali ya juu. Mtu anapenda uzuri kwa kiasi kile kile anavyochukia ubaya. Anachukia dhulma na uonevu kwa kiasi kama anavyopenda haki. Anaogopa sana baridi ya kukosa uhai kama anavyopenda joto la uhai. Mtu hawezi kushusha upanga kwenye shingo za waasi na madhalimu isipokuwa kama anayaona maisha kuwa ni rehma. Kwa kifupi mtu ambaye hachukii hawezi kupenda vile vile. 165

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 165

9/4/2017 3:47:53 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Uthibitisho mzuri wa ukweli kwamba Ali alikuwa ni mkali sana juu ya madhalimu, kama vile alivyokuwa mpole kwa wengine na alivyokuwa tayari kuwa mkali kabisa kuondoa udhalimu, unatolewa na kadhia ya Saudah binti ya Ammarah Hamdaniyah. Saudah anasema: “Nilimwona Amirul-Mu’minin ili kulalamika dhidi ya wakala aliyemuweka yeye ili kukusanya zakat. Wakati niliposimama mbele yake yeye alisema kwa upole mwingi sana: “Je, unataka jambo lolote lifanyike?” Mimi nikamlalamikia dhidi ya yule wakala. Baada ya kusikia yale niliyoyasimulia yeye alianza kulia na akasema akimuomba Mwenyezi Mungu: “Ewe Mola! Mimi sikuwaagiza mawakala hawa kuwaonea watu, wala kuwataka waitelekeze haki yako.” Halafu akatoa kipande cha karatasi kutoka mfukoni mwake na akaandika juu yake kama ifuatavyo: “Pima na kuweka viwango sawasawa na usitoe kilicho pungufu kwa watu wala usieneze ufisadi katika ardhi. Unapoipokea barua hii viweke vile vitu vilivyoko chini ya mamlaka yako katika hifadhi ili mtu mwingine aweze kuja na kupokea vivyo hivyo kutoka kwako.” Inaweza kuonekana vizuri kabisa kutoka kwenye tukio hili, kwamba ni jinsi gani Ali alivyokuwa na huruma kwa mwanamke huyu aliyedhulumiwa, kwa sababu alianza kulia katika kuisikia simulizi yake. Na ni dhahiri vile vile jinsi huruma hii ilivyobadilishwa kuwa ukali kwa ajili ya wale mawakala. Hii inakubaliana na ile kanuni ya upole wa hali ya juu kwa ajili ya waliodhulumiwa na ghadhabu kali sana kwa yule dhalimu. Ali kamwe hakuacha kufanya mapambano dhidi ya ukaidi na dhulma. Wakati wowote alipoona mtu anaonewa na mwingine, hakuonyesha unyonge katika kumuondolea uonevu huo. Na vipi angeweza kuonyesha udhaifu au kusita wakati upole na huruma vimemuandaa yeye na ujanadume na uimara usio wa kawaida, na vimemfanya yeye kuwa mwenye kupenda sana kupambana dhidi ya upotovu na kusimamisha haki. Ilikuwa ni imani yake thabiti kwamba: “Kuwepo kwa Imam ambaye kupitia kwake haki ya mtu mnyonge inaweza kurudishwa kutoka kwa yule mtu mwenye nguvu, na ile ya mtu aliyedhulumiwa kutoka kwa huyo dhalimu, ni lazima ili wale watu waadilifu waweze kuishi kwa furaha na kujihisi salama kutokana na fitna na wafanya maovu.”

166

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 166

9/4/2017 3:47:53 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

“Mwenyezi Mungu ametoa ulinzi kwa watu kutokana na kudhulumiwa.” Na wakati Mwenyezi Mungu ametoa ulinzi basi pasiwepo na fursa kwa ajili ya dhulma lakini “Mwenyezi Mungu anawapa mtihani watawala kwa njia ya dhulma.” Hivyo, kama watawala ni waonevu utawala wao utafika mwisho kwa sababu: “Hata kama yule dhalimu atapata nafasi ya kupumua, bado hawezi kukwepa kutiwa mikononi na Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu Mwenyewe anatayarisha uvamizi kwa ajili yake na kuvamia Kwake kutakuwa kukali sana. Siku ya Kiyama itakuwa nzito sana kwa dhalimu kuliko ile ambayo alimdhulumu mwingine. Yule mtu aliyedhulumiwa atakuwa hakupata mateso sana kama yule dhalimu atakavyoteseka hiyo Siku ya Hukumu.” Yafuatayo yanaunda sehemu ya maagizo ya Ali ambayo ni lazima wakati wote yatimizwe: “Ninakuagizeni kuwa wakali kwa waonevu. Mkamateni mkono yule dhalimu mpumbavu na mumzuie kufanya udhalimu.” Bila shaka zile huruma na upendo ambavyo Ali alikuwa navyo akilini mwake vilithibitisha uimara wake katika vita kati ya haki na uovu. Wakati wowote alipotafakari kuhusu haki na uovu yeye alisema: “Ewe Mola! Jitihada zetu pekee ni kwamba amani na utulivu viweze kupatikana katika miji Yako, ili waja Wako waweze kubaki salama.” Na wakati alipoanzisha mapambano alikuwa akisema: “Ninaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kwamba nitairudisha haki ya mtu aliyedhulumiwa kutoka kwa dhalimu. Nitaweka kipini kwenye pua ya muonevu na kumvutia kwenye chemchem ya haki kwa kiasi chochote anachoweza kulichukia hilo.” Au alisema: “Ni muhimu kwamba muonevu anajizuia kutokana na kutenda udhalimu, anahusiana na watu kwa usawa na haenezi ufisadi katika ardhi.” Kama mapigano yaligeuka kuwa makali na Ali akagundua kutofautiana kati ya idadi ya wafuasi wake na maadui, na akailinganisha hali yake mwenyewe na ile ya wapinzani wake yeye alisema: “Mimi sikuonyesha unyonge au ugoigoi. Nitaendelea kupigana dhidi ya uovu hadi nitakapochomoa haki kutoka ndani yake.” Ali alikiona kifo kikimtazama machoni mwake lakini sio mikono yake iliyochoka katika kupigana, wala yeye hakuendekeza hata chembe ndogo ya hofu ndani ya moyo wake. Asingeweza kuwa na woga hata kama idadi yote ya watu wa Arabuni ingeungana na kumzingira yeye. Yeye alitegemea kikamilifu juu ya uadilifu na usawa wake mwenyewe, na aliamini kwa dhati kwamba chochote kile alichokuwa anakifanya kilikuwa ni kwa mujibu wa kanuni za usawa na uadilifu. Alikuwa wakati wote akisema: 167

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 167

9/4/2017 3:47:53 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

“Mtu mnyonge ana nguvu machoni mwangu mpaka pale nitakapofanya alipwe haki yake, na mtu mwenye nguvu ni dhaifu sana mbele ya macho yangu hadi nitakapoipokea haki hiyo kutoka kwake.” Vile vile alisema: “Ninaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kwamba siogopi kama kifo kinaniangukia juu yangu au kama mimi ninaangukia kwenye kifo.” Wakati alipopigana dhidi ya kikundi cha watu madhalimu na akawashinda lakini wakaendelea kuonyesha upinzani, yeye alisema: “Kuna kiasi cha uhai bado kimebakia ndani ya madhalimu. Kama Mungu akipenda basi tutawang’oa. Endapo, hata hivyo, baadhi yao wakikimbilia kwenye miji mbalimbali jambo hilo litakuwa kinyume chake.” Kwa mujibu wa Ali, wale watu waliosoma ndio viongozi wa umma na kwa sababu hii hasa, idadi ya majukumu imekabidhiwa juu yao. Wajibu wao mkubwa ni kwamba wao ni lazima wampinge mtu muonevu na wamsaidie yule mtu ambaye ameonewa. Yeye anasema: “Mwenyezi Mungu ameifanya kuwa ni sheria juu ya ulamaa kwamba wao wasibakie kama watazamaji wakimya wa uonevu wa dhalimu na huzuni na unyonge wa mtu anayeonewa.” Ili waonevu waweze kuondolewa kutoka kwenye jamii, na kwamba asiwepo pia mtu yoyote ambaye anaweza kusaidia katika uendelezaji wa uonevu au awezaye kuuvumilia kwa hiari yake kabisa, Ali amezigawanya dhambi za watu katika makundi tofauti. Kuna dhambi fulani ambazo zinaweza kusamehewa lakini udhalimu na uonevu haviwezi kusamehewa kwa hali yoyote ile. Yeye anasema: “Na dhambi ambayo haitasamehewa ni kwamba mtu mmoja amuonee mwingine.” Yeye alikuwa na maoni kwamba: “Kumuonea mtu mnyonge ndio aina mbaya sana ya udhalimu.” Hivyo alijitahidi kwa njia na hali zote kuuondoa udhalimu; na hii ilibakia kuwa ndio sera yake ya msingi katika suala la kushughulika na watu. Alipigana dhidi ya waonevu kwa ulimi wake na vilevile kwa upanga wake na alidumu kuwa imara katika juhudi zake. Aliendelea kupigana dhidi ya udhalimu na madhalimu wenyewe hadi alipokutana na kifo chake cha kishahidi. Kama mabadiliko ya wakati yasingezuia mpango wake; na mazingira yasingekuwa mabaya upande wake, angeweza kuleta mabadiliko katika baadhi ya mambo. Utawala wa Ali Baada ya kuja kujua kwamba mwenendo wa Amirul-Mu’minin kwa jamii ya mwanadamu ulikuwa wa haki kabisa; na alitwaa sera iliyokuwa sahihi kabisa, ya kuanzisha 168

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 168

9/4/2017 3:47:53 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

mahusiano ya pamoja ya wanadamu katika misingi ya usawa na uadilifu, inaonekana kuwa ni muhimu hapa kunakili ule wasia ambao aliuandika kwa ajili ya Malik Ashtar wakati akimteua yeye kama gavana wa Misri. Wasia wake huu una maelezo ya kina zaidi kuliko nyingine zote, na ni wa muhimu sana kutokana na mtazamo wa utukufu na ubora wake. Wakati tulipokuwa tunaandika kuhusu tabia ya Amirul-Mu’minin tumetumia nyingi ya barua zake, maagizo na wasia, kwa sababu takriban katika zote hizo ametaja haki za mtu binafsi na za jamii halikadhalika. Hata hivyo, ule wasia aliouandika yeye kwa ajili ya Malik Ashtar ni mpana sana na umekusanya maoni yake na imani zake zote juu ya suala la utawala wa umma. Unasomeka kama ifuatavyo: “Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu. Ifahamike kwako, ewe Malik, kwamba ninakupeleka kama Gavana kwenye nchi ambayo katika siku zilizopita ilipitiwa na vyote, utawala wa haki na wa kidhalimu. Watu watavichunguza kwa makini vitendo vyako kwa jicho linalodadisi, sawa na vile ulivyokuwa ukivichunguza vitendo vya wale waliokuwa mbele yako, na watazungumza juu yako sawa na vile ulivyokuwa ukizungumza juu yao. Ukweli ni kwamba umma utakuwa unazungumza vema juu ya wale tu ambao wanafanya wema. Ni wao wanaotoa ushahidi wa vitendo vyako. Hivyo hazina kubwa sana unayoweza kupata kutamani, inapaswa iwe ni hazina ya matendo mema. Yaweke matamanio yako chini ya udhibiti na jikataze mwenyewe yale ambayo umekwishaonywa dhidi yake. Kwa kujizuia huko peke yake, wewe utakuwa na uwezo wa kupambanua kati ya jema na baya. Endeleza katika moyo wako hisia za upendo kwa ajili ya watu wako, na ifanye iwe ni chanzo cha huruma na neema kwao. Usishughulike nao kama mshenzi, na usijitwalie mwenyewe kile ambacho ni mali yao. Kumbuka kwamba raia wa nchi ni wa makundi mawili. Wao imma ni ndugu zako katika dini au ni ndugu zako kama wanadamu. Wao ni wenye kupatwa na udhaifu na wanaoweza kufanya makosa. Baadhi yao kwa hakika wanafanya makosa, lakini wewe uwasamehe kama vile ambavyo ungependa Mwenyezi Mungu akusamehe wewe. Zingatia kwamba wewe umewekwa juu yao, kama mimi nilivyowekwa juu yako. Na halafu kuna Mungu ambaye yuko hata juu ya yule aliyekupa wewe cheo cha Gavana ili kwamba uweze kuwaangalia wale walioko chini yako na uwe mwenye kutosheleza kwa ajili yao. Kumbuka! Utakuja kuhukumiwa kwa kile utakachofanya kwao. Usijiweke mwenyewe dhidi ya Mwenyezi Mungu, kwani imma wewe huna nguvu ya kujikinga mwenyewe dhidi ya kukasirika Kwake, wala huwezi kujiweka

169

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 169

9/4/2017 3:47:53 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

nje ya mpaka wa huruma na msamaha Wake. Usisikitike juu ya kitendo chochote cha msamaha, wala kufurahia juu ya adhabu ambayo unaitoa kwa mtu yeyote yule. Usijipandishe hasira wewe mwenyewe, kwani hakuna jema litakalopatikana kutoka kwenye hasira hizo. Usije ukasema, “Mimi ndio kabaila na dikteta wenu, na kwamba kwa hiyo lazima mnyenyekee kwenye amri zangu,” kwani hilo litaupotosha moyo wako, kudhoofisha imani yako katika dini na kusababisha machafuko katika dola hiyo. Ikiwa utasisimuliwa na mamlaka, au kuiachia akili yako kuingiliwa na hisia yoyote ya majivuno na makuu, basi angalia yale mamlaka na utukufu wa utawala wa ki-mungu juu ya ulimwengu ambao huna udhibiti wowote kabisa juu yake. Huo utairudisha hisia ya uwiano kwenye akili yako ya ajabu na kukupa wewe hisia ya utulivu na uchangamfu. Jihadhari! Kamwe usije ukajiweka mwenyewe dhidi ya utukufu na ukuu wa Mwenyezi Mungu na usiige kamwe Kudra Zake, kwani Mwenyezi Mungu amemshusha kila muasi juu Wake na kila dhalimu wa mwanadamu. Acha akili yako, kupitia kwenye vitendo vyako, iziheshimu haki za Mwenyezi Mungu na haki za wanadamu, na vivyo hivyo, washawishi marafiki na ndugu zako kufanya hivyo hivyo. Kwani vinginevyo, utakuwa unajifanyia dhuluma wewe mwenyewe na binadamu. Hivyo, wote, mwanadamu na Mungu watakuwa maadui zako. Hakuna utetezi popote pale kwa ajili ya mtu anayejifanya mwenyewe kuwa adui wa Mwenyezi Mungu. Atachukuliwa kama mtu aliyeko vitani na Mwenyezi Mungu mpaka atakapotubia na aombe msamaha. Hakuna kinachomkosesha mwanadamu baraka wala kinachoamsha ghadhabu za ki-Mungu dhidi yake kwa urahisi zaidi kuliko udhalimu. Hivyo ni kwamba Mwenyezi Mungu anaisikiliza sauti ya mwenye kudhulumiwa na kumkinza nguvu yule muonevu.” Mtu Wa Hali Ya Chini Dumisha haki katika uongozi na uilazimishe juu yako wewe mwenyewe, na utake ushauri wa watu, kwani, kutoridhika kwa umma kunafisha kuridhika kwa wale matajiri wachache na kutoridhika kwa wachache kunapotea kwenyewe katika kuridhika kwa wengi. Kumbuka! Wale matajiri wachache hawatajikusanya karibu nawe wakati wa matatizo. Wao watajaribu kukwepa haki. Watakuomba wewe zaidi ya kile wanachostahili na hawataonyesha shukurani kwa fadhila watakazotendewa wao. Watahisi mihangaiko wakati wa majaribu na hawataomba samahani kwa yale mapungufu yao.

170

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 170

9/4/2017 3:47:53 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Ni mtu wa chini ambaye anapigana na maadui. Hivyo uishi kwa mawasilano ya karibu na watu na uwe mzingativu wa ustawi wao. Kaa mbali na yule ambaye anafichua udhaifu wa wengine. Hata hivyo, umma hauko huru kuondoka na madhaifu. Ni wajibu wa mtawala kuwakinga hao. Usibainishe yale ambayo yamefichika, bali wewe ujaribu kuyaondo yale madhaifu ambayo yamebainishwa. Mwenyezi Mungu analiona kila ambalo limefichikana kwako, na Yeye peke yake tu ndiye atakayeshughulika nayo. Yafunike makosa ya watu kwa kiasi cha uwezo wako ili Mwenyezi Mungu aweze kufunika makosa yako ambayo unataka kuyaficha mbele ya macho ya watu. Lifungue kila fundo la chuki juu ya watu na uikatilie mbali kila kamba ya uhasama baina yao. Jilinde mwenyewe kutokana na kila lile tendo ambalo linawezakuwa sio sahihi sana kwako. Usifanye haraka katika kutafuta uthibitisho wa maneno ya umbea, kwani yule msengenyaji ni mtu mdanganyifu anayejitokeza katika sura ya urafiki. Washauri Kamwe usije ukachukua ushauri wa mtu bakhili, kwani yeye ataharibu ukarimu wako na kukutishia juu ya umasikini. Usitafute ushauri kutoka kwa mtu mwoga vilevile, kwani yeye atadhoofisha umahiri wako. Usichukue ushauri kutoka kwa mtu mchoyo, kwani yeye atadukiza uchoyo ndani yako na utageuka kuwa dhalimu. Ubakhili, woga na choyo vinamnyang’anya mtu imani yake juu ya Mwenyezi Mungu. Mshauri mbaya zaidi ni yule ambaye amekwishawahi kuwa mshauri kwa watawala madhalimu na akashiriki maovu yao. Hivyo usiwaruhusu kamwe watu ambao wamewahi kuwa marafiki wa waonevu au walioshiriki katika maovu yao kuwa ni washauri wako wewe. Unaweza kupata watu bora kuliko hawa, watu waliojaaliwa na akili na uona mbali, lakini hawakuchafuliwa na makosa, watu ambao wajawahi kamwe kumsaidia muonevu katika uonevu wake wala mhalifu katika uhalifu wake. Watu kama hao hawatakuwa mzigo kwako kamwe. Kwa upande mwingine, watakuwa ni chanzo cha msaada na nguvu kwako wakati wote. Watakuwa marafiki kwako, na wageni kwa maadui zako. Chagua watu kama hao tu kwa ajili ya usuhuba sirini au mbele za watu vile vile. Hata miongoni mwa hawa, uonyesha upendeleo zaidi juu wale ambao wana mazingatio ya kimazoea juu ya kweli, kwa kiasi chochote kile wakati mwingine ukweli wao utakavyoweza kuthibitika kuwa mtihani juu yako, na ambao hawakuungi mkono katika kuonyesha tabia ambazo Mwenyezi Mungu huwa hapendi marafiki Zake kuwa nazo. 171

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 171

9/4/2017 3:47:53 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Kuwa karibu na wale waadilifu na wachamungu, na liweke wazi kwao kwamba hawapaswi kamwe kukudanganya wewe na kamwe wasikusifie kwa ajili ya jema lolote lile ambalo unawezakuwa hukulifanya, kwani uvumilivu wa udanganyifu na sifa zisizofaa zinaamsha kiburi ndani ya mtu na kumfanya awe jeuri. Usiwafanye wale watu wema na waovu kuwa sawa. Hilo litawavunja moyo wale wema na kuwapa nguvu wale waovu katika kazi zao mbaya. Mfidie kila mtu kutokana na haki yake. Kumbuka kwamba kuaminiana kwa pamoja, na mapenzi kati ya mtawala na anayetawaliwa kunaadilishwa tu kupitia kwenye ukarimu, haki na huduma. Hivyo endeleza mapenzi miongoni mwa watu, kwani mapenzi yao pekee yatakuokoa kutokana na matatizo. Ukarimu wako kwao utalipizwa kwa imani zao juu yako, na ukatili wako kwa kutoridhika kwao. Usije ukazipuuza zile desturi bora zilizowekwa na wahenga wetu; ambazo zimeendeleza upatanifu na maendeleo miongoni mwa watu, na usije ukaanzisha jambo lolote ambalo linaweza kupunguza ufanisi wa desturi hizo. Watu ambao walianzisha desturi hizo tukufu walikuwa wamepata malipo yao; lakini uwajibikaji utakuwa juu yako kama zitaachwa. Jaribu wakati wote kujifunza kitu kutokana na uzoefu wa watu wenye elimu na busara, na mara kwa mara shauriana nao katika masuala ya dola, ili uweze kudumisha amani na upendo ambao watangulizi wako walikuwa wamevisimamisha juu ya ardhi. Matabaka Mbalimbali Ya Watu Kumbuka kwamba watu wako na matabaka mbalimbali. Maendeleo ya mojawapo yanategemea maendeleo ya kila moja yao, na hakuna linaloweza kuwa lisilotegemea lile jingine. Tunalo jeshi lililoundwa na wapiganaji wa Mwenyezi Mungu. Tunao watumishi wetu wa umma pamoja na taasisi zao, idara yetu ya mahakama, wakusanyaji mapato wetu na maafisa wa uhusiano wa jamii. Umma wote wenyewe unajumuisha Waislamu na Dhimmi – (wasiokuwa Waislamu), na miongoni mwao wamo wachuuzi na mafundi stadi, wasioajiriwa na masikini. Mwenyezi Mungu ameweka kwa ajili yao haki zao mbalimbali, majukumu na wajibu. Yote yamefafanuliwa na kuhifadhiwa ndani ya Qur’ani na Hadith za Mtukufu Mtume.

172

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 172

9/4/2017 3:47:53 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Jeshi, kwa rehema za Mwenyezi Mungu, ni kama ngome kwa watu na linaleta heshima kwa dola. Linatetea hadhi ya dini na kudumisha amani ya nchi. Bila ya hilo, dola haiwezi kusimama. Nalo hilo haliwezi kusimama bila msaada wa dola. Wapiganaji wetu wamethibitisha kuwa na nguvu mbele ya maadui kwa sababu ya fadhila za Mwenyezi Mungu zimewafanya wao wapigane kwa ajili Yake, lakini wanayo mahitaji yao ya kidunia ya kutimiza na kwa hiyo wanahitaji kutegemea juu ya mapato yanayotolewa kwa ajili yao kutoka kwenye hazina ya umma. I le idadi ya wanajeshi na ile ya kiraia wanaolipa mapato hayo wanahitaji ushirikiano wa wengine – wanasheria, watumishi wa umma na taasisi zao. Hakimu anasimamia sheria za madai na za jinai, watumishi wa umma wanakusanya mapato na kushughulikia utumishi wa serikali kwa msaada wa taasisi zao. Na halafu kuna wale wafanyabiashara na wachuuzi ambao wanachangia kwenye mapato ya umma. Ni wao wanaoyaendesha masoko na wako kwenye nafasi nzuri kuliko wengine katika kutekeleza wajibu wa kijamii. Halafu kuna lile tabaka la watu masikini na wenye shida ambao kuwagharimia kwao ni wajibu juu ya matabaka mengine. Mwenyezi Mungu ametoa fursa inayofaa kwa huduma kwa mmoja na wote; halafu kuna zile haki za haya matabaka yote juu ya utawala ambayo mtawala anapaswa kuzitimiza kwa jicho la wema juu ya idadi nzima ya watu – jukumu ambalo hawezi kulitimiza kikamilifu mpaka awe na shauku binafsi katika utekelezaji wake na kutafuta msaada kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Kwa hakika ni wajibu juu yake kujitwisha mwenyewe wajibu huu juu yake yeye mwenyewe na kustahimili kwa uvumilivu ule usumbufu na matatizo yanayoambatana na jukumu lake. Jeshi Kuwa mzingativu hasa wa ustawi wa wale walioko ndani ya jeshi, ambao kwa maoni yako, wana imani madhubuti kwa Mola Wao na Mtume na ni waaminifu kwa kiongozi wao, na ambao katika wakati wa matamanio wanaweza kujizuia wao wenyewe na kusikiliza kwa utulivu juu ya malalamiko ya kuyapinga, na ambao wanaweza kuwaauni wale wanyonge na kuwaangamiza wale wenye nguvu na uwezo, ambao uchochezi mkali hautawaingiza kwenye hasira kali na ambao hawatasita katika hatua yoyote ile. Watunze kwa upole ambao kwamba ungetunza nao watoto wako, na usiongee mbele yao kuhusu wema wowote ambao ungewezakuwa umewafanyia wao wala 173

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 173

9/4/2017 3:47:53 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

usipuuze dalili yoyote ya upendo ambayo watakuonyesha kama malipo, tabia kama hiyo inavutia uwajibikaji, utiifu na mapenzi. Shughulikia kila shida yao ndogo na sio kubaki umeridhika na ule msaada wa jumla ambao utawezakuwa umewapatia, kwani wakati mwingine mazingatio kwa muda muafaka kwenye shida zao ndogo yanawaletea ahueni kubwa. Kwa kweli watu hawa hawatakusahau wewe katika wakati wako mwenyewe wa shida. Huna budi kujichagulia kama Amiri Jeshi Mkuu mtu ambaye anajituma mwenyewe kama wajibu, ile kazi ya kutoa msaada kwa watu wake na ambaye anaweza akawazidi kwa upole wale maafisa wengine wote, atapasika kushughulikia mahitaji ya watu hao walioko chini yake na kuzitazama familia zao wakati wanapokuwa mbali na majumbani kwao; kiasi kwamba jeshi lote zima liweze kujihisi limeungana katika furaha zao na huzuni zao. Umoja huu wa lengo utawapa nguvu za ziada dhidi ya maadui. Endelea kudumisha mwelekeo wa kihuruma kwao ili kwamba wao waweze kujihisi kamwe kuambatana nawe. Ukweli ni kwamba ile furaha halisi ya watawala na starehe yao kubwa mno imo katika kuimarisha uadilifu katika dola na kuendeleza uhusiano wa upendo na watu. Unyofu wa hisia zao unaonekana katika mapenzi na heshima wanayoonyesha kwako, ambayo juu yake pekee ndimo unamotegemea usalama wa watawala hao. Ushauri wako kwa jeshi utakuwa hauna faida, isipokuwa na mpaka utakapoonyesha upendo kwa wote, watu na maafisa, ili wasije wakaiona serikali kama mzigo wa uonevu au wakachangia katika uangukaji wake. Endelea kuridhisha mahitaji yao na uwasifie tena na tena kwa ajili ya ule utumishi walioutoa. Mwelekeo kama huo, Mungu akipenda, utawatia moyo wale majasiri kwenye vitendo vya kijasiri zaidi na kutoa woga kwenye matendo ya kijasiri. Jaribu kuingia kwenye hisia za wengine na usije ukalazimisha kosa la mtu mmoja juu ya mwingine, na usiwe na kinyongo katika kutoa heshima inayostahili. Hakikisha kwamba, huonyeshi upendeleo kwa mtu ambaye hakufanikisha lolote bali kutegemea tu juu ya nafasi ya familia yake, na usizuie malipo halali kwa mtu ambaye amefanya matendo makubwa kwa sababu tu anashikilia nafasi ndogo sana ya chini maishani mwake.

174

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 174

9/4/2017 3:47:53 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Mwongozo Halisi. Rejea kwa Mwenyezi Mungu na Mtume kwa ajili ya mwongozo wakati wowote unapohisi kutokuwa na uhakika katika vitendo vyako. Kuna amri ya Mwenyezi Mungu iliyotolewa kwa wale watu ambao Yeye anataka kuwaongoza sawasawa: “Enyi mlioamini! Mtiini Mwenyezi Mungu na mtiini Mtume na wale wenye mamlaka miongoni mwenu. Na lolote mtakalohitilafiana kwalo lirejesheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake.” Kurejea kwa Mwenyezi Mungu kwa ukweli ni kukiangalia Kitabu cha Mungu; na kurejea kwa Mtume ni kufuata zile Sunna na Hadith zinazokubalika kwa ujumla wa wote. Kadhi Mkuu Mteue kama Kadhi Mkuu kutoka miongoni mwa watu, yule mtu ambaye kwa mbali sana ndiye mbora miongoni mwao – mtu ambaye hakujawa na hofu juu ya matatizo ya nyumbani, mtu ambaye hawezi kutishiwa, mtu ambaye hafanyi makosa ya mara kwa mara, mtu ambaye hageuki kutoka kwenye njia iliyonyooka mara anapoigundua, mtu ambaye sio mbinafsi au mlafi wa mali, mtu ambaye hataamua kabla ya ukweli kamili, mtu ambaye atapima kwa uangalifu mashaka yanayoambatana na kutamka hukumu ya wazi baada ya kuchukulia kila kitu kwenye mazingatio kamili, mtu ambaye hatahangaishwa na hoja za mawakili na ambaye atachunguza kwa utulivu kila ufichuliwaji mpya wa jambo na ambaye atakuwa mwadilifu kabisa katika uamuzi wake, mtu ambaye udanganyifu hauwezi kumpotosha, mtu ambaye hashangilii sana juu ya cheo chake. Lakini watu kama hao ni wachache sana. Mara utakapokuwa umeteua yule mtu wa sawa kwa ajili ya kazi hiyo, mlipe yeye vizuri vya kutosha hasa, ili kumfanya aishi kwa faraja na kupatana na cheo chake, kiasi cha kutosha kumweka nje ya vishawishi. Mpatie nafasi katika baraza lako iliyo ya juu sana kiasi kwamba hakuna anayeweza kuota kuitamani na ya juu sana kiasi kwamba sio usengenyaji wala ulaji njama unaoweza kumgusa yeye. Kadhi Msaidizi Jihadhari! Uangalifu wa hali ya juu kabisa ni lazima utumike katika uchaguzi wake, kwani ni nafasi hii ya juu ambayo wapenda makuu hatari wanagombea kuipata na kuitumia katika manufaa yao ya kichoyo. Baada ya uteuzi wa Kadhi Mkuu wako, toa 175

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 175

9/4/2017 3:47:53 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

mazingatio makini kwenye uteuzi wa maafisa wengine. Wathibitishe katika kazi zao baada ya majaribio yaliyothibitika. Kamwe usiwateue watu kwa ajili ya nafasi za wajibu imma kwa kutokana na heshima yoyote kwa ajili ya uhusiano binafsi au kwa ushawishi wowote, kwani hilo linaweza kuongozea kwenye dhulma au uonevu. Katika hawa, wateue kwa ajili ya nafasi za juu watu wenye uzoefu, watu imara katika dini na watokanao na familia nzuri. Watu kama hao hawataangukia kuwa mawindo rahisi kwenye vishawishi, na watatekeleza kazi zao kwa kutazamia juu ya kuwatakia mema wengine. Uwaongezee mishahara yao ili kuwapatia maisha ya kuridhisha. Maisha ya kuridhisha ni msaada kwenye utakasaji wa nafsi. Hawatajihisi shauku ya kushika kodi mapato ya watu wa chini yao kwa ajili ya gharama zao wenyewe. Basi watakuwa hawana kisingizio cha kwenda kinyume na maagizo yako au kufuja fedha za umma. Fanya doria juu yao bila ya wao wenyewe kujua. Labda wanaweza kukuza uaminifu wa kweli na kujali kihalisi juu ya ustawi wa umma. Lakini wakati wowote mmoja wao yeyote atakaposhutumiwa kwa kukosa uaminifu, na hatia ikathibitishwa na taarifa ya idara yako ya usalama, basi ione hiyo kuwa inatosha kumtia hatiani. Fanya adhabu yake iwe ya kutandikwa na lifanye hili lishughulikiwe hadharani kwenye sehemu ya kushushia hadhi iliyoteuliwa. Usimamizi Wa Mapato Uangalifu mkubwa lazima ufanyike katika usimamizi wa mapato, ili kuhakikisha ustawi wa wale wanaolipa mapato hayo kwa dola, kwani juu ya ustawi wao ndiko ustawi wa wengine unakotegemea, hususan umma wenyewe. Hakika, dola inakuwa hai juu ya mapato yake. Lazima uchukulie utunzaji sahihi wa ardhi katika ukulima kama wenye umuhimu mkubwa kuliko ukusanyaji wa mapato, kwani mapato hayawezi kupatikana isipokuwa kwa kuifanya ardhi iwe yenye kuzalisha. Yeyote anayedai mapato bila ya kusaidia yule mkulima na akaangamiza dola, utawala wa mtu kama huyo hauwezi kudumu kwa muda mrefu. Kama wakulima wataomba punguzo katika ushuru wao wa ardhi kwa sababu ya kupatwa na magonjwa ya mlipuko au ukame au kuzidiwa na mvua au kukosa rutuba kwa ardhi yenyewe au mafuriko yaliyoharibu mazao yao, basi punguza ushuru huo kiasi inavyostahili, ili hali zao zipate kuongezeka.

176

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 176

9/4/2017 3:47:53 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Usijali kupotea au kupungua kwa mapato kwa sababu hiyo, kwani hayo yatakuja kurudi kwako siku moja maradufu katika wakati wa ustawi mkubwa wa ardhi na kukuwezesha wewe kuendeleza hali ya miji yako na kunyanyua hadhi ya dola yako. Utakuwa ndio mlengwa wa sifa za kilimwengu. Watu wataamini katika busara zako za uadilifu. Ile imani watakayoweka juu yako matokeo yake itathibitisha nguvu yako, kwani watakutwa wako tayari kushiriki matatizo yako. Unaweza ukatuliza juu ya ardhi idadi yoyote ya watu, lakini watapatwa na kutoridhika kama ardhi hiyo haitaendelezwa. Chanzo cha kuangamia kwa wakulima ni watawala ambao wamedhamiria kwa msisimko mkubwa katika kulimbikiza utajiri kwa gharama yoyote ile, kwa kuhofia kwamba utawala wao unaweza usidumu kwa muda mrefu. Hao ndio watu ambao hawajifunzi kutokana na mifano au vitangulizi. Taasisi Ya Maandishi Tupia macho taasisi yako na waandishi wako na uteue mbora miongoni mwao kwa ajili ya mawasiliano yako ya siri; miongoni mwa kama hao, mwenye tabia ya hali ya juu na anayestahili imani yako kamilifu – watu ambao hawatumii nafasi zao za upendeleo kwenda kinyume na wewe, na ambao hawatakuwa wazembe wa wajibu wa kazi zao, na ambao katika kuandaa miswada ya makubaliano hawatanywea kwenye vishawishi na kudhuru maslahi yako au kushindwa kukupatia msaada unaofaa na kukuokoa kutokana na matatizo, na ambao, katika kutekeleza kazi zao, watatambua wajibu wao mkubwa, kwani yule ambaye hatambui wajibu wake mwenyewe ni vigumu sana kuweza kutathmini wajibu wa watu wengine. Usije ukateua watu kwa ajili ya kazi kama hizo kwa uzito wa maoni yako ya awali tu ya upendo au imani nzuri kama jambo la uhakika, kujifanya kwa wengi sana ambao kwa kweli hawana uaminifu wala kizazi bora, kunaweza kuidanganya hata idara za upelelezi za watawala. Uteuzi unapaswa ufanyike baada ya majaribio yanayostahili – majaribio ambayo sharti yawe ndio kipimo cha uadilifu. Kufanya uteuzi wa moja kwa moja kutoka kwa watu na wenye sifa ya kuwa waaminifu kwa ajili ya uteuzi kama huo kunakubalika, kote, kwa Mwenyezi Mungu na kwa mtawala. Kwa kila idara ya utawala fanya awepo kiongozi mkuu, ambaye hakuna kazi yenye usumbufu inayoweza kusababisha hofu na hakuna shinikizo la kazi linaloweza kumchukiza. Na kumbuka kwamba kila kuteleza kwa waandishi, ambako unaweza ukakupuuza, kutaandikwa dhidi yako katika kitabu chako cha matendo. 177

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 177

9/4/2017 3:47:53 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Biashara Na Viwanda Unashauriwa kuwatendea vyema wafanyabiashara na mafundi stadi na kuwaelekeza wengine kufanya vivyo hivyo. Baadhi yao wanaishi mijini na wengine wanahama kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine pamoja na bidhaa zao na zana na wanapata maisha yao kwa kazi za mikono. Wao ndio chanzo hasa cha faida kwa dola na watoaji wa bidhaa zitumikazo. Wakati watu wote hawaelekei kubeba machovu hayo, wale ambao wanashughulika na kazi hizi wanachukua uzito wa kukusanya bidhaa kutoka mbali na karibu, kutoka kwenye nchi kavu na kutoka ng’ambo ya bahari, na kutoka milimani na misituni na bila shaka wanazalisha manufaa. Ni tabaka hili la watu wenye kupenda amani, ambalo kutoka kwao hakuna ghasia inayohitajia kuhofiwa. Wanapenda amani na utulivu. Kwa hakika hawawezi kusababisha kutoelewana, walinde kama wanafanya biashara katika sehemu yako ama katika miji mingine. Lakini zingatia akilini kwamba wengi sana kati yao ni wenye tamaa sana na wamefungwa katika biashara mbaya. Wanahodhi nafaka na kujaribu kuiuza kwa bei ya juu na hili lina madhara sana kwa umma. Ni aibu katika jina la mtawala kutolipinga ovu hili. Wazuie kuhodhi; kwani Mtume wa Mwenyezi Mungu alilikataza hilo. Hakikisha kwamba biashara inaendeshwa kwa urahisi wa hali ya juu kabisa, kwamba mizani zimewekwa sawa na kwamba bei zimepangwa kiasi kwamba sio muuzaji wala mnunuzi anapata hasara. Na kama, licha ya maonyo yako, mtu yoyote atakwenda kinyume na amri zako na akatenda kosa la kuhodhi, basi toa adhabu juu yake iliyo kali sana. Masikini Jihadhari! Muogope sana Mwenyezi Mungu wakati hasa unaposhughulika na matatizo ya masikini ambao hawana wa kuwalea, ambao ni wakiwa, mafukara, wasiojiweza na wamekanganyikiwa vibaya katika akili zao – waathirika wa mabadiliko ya wakati. Miongoni mwao wamo baadhi ambao hawahoji bahati yao katika maisha na ambao, licha ya taabu zao, bado hawazunguki huku na huko wakatafuta sadaka. Tafadhali sana, zilinde haki zao kwani juu yako wewe ndimo ulimo wajibu wa kulinda maslahi yao.

178

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 178

9/4/2017 3:47:53 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Tenga fungu kutoka kwenye hazina ya umma kwa ajili ya kuwanyanyua, popote pale watakapokuwa, imma karibu pa kufikiwa na mkono wako au mbali nawe. Haki za wawili hao lazima ziwe sawa machoni mwako. Usiruhusu mshughuliko wowote ukawaponyoka wao kutoka kwenye akili yako kwani hakuna kisingizio kwa namna yoyote ile kwa ajili ya upuuzaji wa haki zao kitakachokubalika kwa Mwenyezi Mungu. Usiyafanye maslahi yao kama yasiyo na umuhimu wowote kuliko yako wewe mwenyewe na kamwe usiwaweke nje ya utambuzi wa fikira zako muhimu, na uwaangalie wale watu ambao wanawaangalia hao kwa dharau na ambao wanakuficha kuhusu hali zao hao. Teua kutoka miongoni mwa maafisa wako watu ambao ni wanyoofu na wachamungu na ambao wanaweza wakakuweka mwenye kufahamu vizuri juu ya hali za masikini. Fanya maandalizi kwa ajili ya watu masikini hawa ambayo hayatakulazimisha kutoa visingizio mbele ya Mwenyezi Mungu hiyo Siku ya Hukumu, kwani ni sehemu hii ya watu ambayo zaidi ya yoyote ile, inastahili utendewaji wa kikarimu. Tafuta thawabu zako kwa Mwenyezi Mungu kwa kutoa kwa kila mmoja wao kinachostahili kwake na ujiamuru wewe mwenyewe kama ni wajibu wa dhati, ile kazi ya kutimiza haja zao watu wazee miongoni mwao, kwa vile hawana njia huru za kuendesha maisha yao na wanaona karaha kutafuta sadaka. Ni utekelezaji wa wajibu huu ambao kwa kawaida unathibitika kuwa wenye mtihani kwa watawala, lakini ni wenye kukubalika sana kwa jamii ambazo zimejaaliwa na umaizi. Ni jamii kama hizo tu au mataifa ambayo kwa kweli yanatimiza kwa utulivu wa moyo maagano yao na Mwenyezi Mungu ya kutekeleza wajibu wao kwa masikini. Mikutano Ya Wazi Kutana na wale walioonewa, na watu wa chini kila baada ya kipindi fulani katika mkutano wa wazi na mwenye kutambua mahudhurio ya ki-mungu hapo, fanya mazungumzo ya faragha pamoja nao na usimruhusu yoyote yule kutoka kwa walinzi wako au watumishi wa serikali, au mtu kutoka idara ya polisi au idara ya usalama kuwa karibu yako wakati huo, ili wale wawakilishi wa masikini waweze kuelezea manung’uniko yao bila ya hofu yoyote na bila kuyabakisha. Kwani nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu akisema kwamba hakuna taifa au jamii ambamo wale wenye uwezo hawatimizi wajibu wao kwa wanyonge am179

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 179

9/4/2017 3:47:53 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

balo litakuja kupata nafasi ya juu. Beba kwa uvumilivu lugha yoyote chafu ambayo wanaweza wakaitumia, na usikasirike endapo hawataweza kulielezea suala lao kwa kufahamika vizuri zaidi. Hata hivyo, Mwenyezi Mungu atakufungulia mlango Wake wa neema na thawabu. Chochote unachoweza kuwapa, kitoe bila ya kinyongo na chochote ambacho huwezi kukimudu kukitoa, lifanye hilo wazi kwao kwa kukubali kujishusha kwa hali ya juu. Kuna mambo maalum ambayo yanahitaji kushughulikiwa kwa haraka sana. Mojawapo ni mawasiliano kuhusiana na kurekebisha manung’uniko ambayo watumishi wako wazembe wameshindwa kuyashughulikia. Hakikisha kwamba malalamiko au maombi yaliyoletwa kwa ajili ya kuyafikiria kwako yanafikishwa mbele yako bila kucheleweshwa kwa kiasi chochote kile ambacho maafisa wako wanaweza kuyaingilia. Tupilia mbali kazi za siku hiyo hasa, kwani siku inayofuatia italazimisha kazi zake yenyewe. Kuungana Na Mwenyezi Mungu Usisahau kutenga muda wako bora kabisa kwa ajili ya kuungana na Mwenyezi Mungu, ingawaje kila muda wako wote ni kwa ajili Yake tu, madhali unatumika kwa uaminifu katika kuwatumikia watu wako. Wajibu ambao unadaiwa moja kwa moja na Mwenyezi Mungu unapaswa kuingizwa kwenye shughuli zako zote. Kwa hiyo jitolee baadhi ya muda wako kila mchana na usiku kwa ajili ya swala ili uweze kuwa katika muungano na Mwenyezi Mungu. Fanya swala yako iwe kamilifu iliyoondokana na dosari kwa kiasi iwezekanavyo, licha ya adha ya kimwili inayoweza kuhusika nayo. Na wakati unapoongoza swala ya jamaa, usiwakere watu kwa swala ndefu isiyo na lazima, wala usiiharibu kwa ufupi usioidhinishwa. Wakati, pale nilipopokea maagizo ya kuelekea Yemen, nilimuuliza Mtume wa Mwenyezi Mungu, ni vipi nilipaswa kuongoza swala za jamaa huko, yeye alisema: “Tekeleza swala yako kiasi hata yule mnyonge kabisa miongoni mwenu ataweza kuswali na uweke mfano wa busara unaoweza kufikirika kwa waumini.” Kujitenga Hakufai Kuhusu kuyafuata yale yote niliyoyasema, zingatia jambo moja akilini mwako. Kamwe usijitenge na watu kwa kiasi chochote cha muda, kwani kufanya hivyo ni kujiweka wewe mwenyewe katika kutoyajua mambo yao. 180

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 180

9/4/2017 3:47:53 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Inakuza na kuendeleza kwa mtawala, mtazamo mbaya na kunamfanya yeye ashindwe kutofautisha kati ya ni kipi cha muhimu na kipi kisichokuwa cha muhimu, kati ya kweli na uongo na kati ya haki na batili. Mtawala hata hivyo yeye ni binadamu, na hawezi kujenga hoja sahihi juu ya kitu ambacho kipo mbali na macho yake. Hakuna dalili ya kipekee iliyoambatanishwa kwenye haki ambayo inaweza kumfanya mtu atofautishe kati ya namna nyingi za haki na uovu. Ukweli ni kwamba wewe lazima uwe kimojawapo ya vitu viwili hivyo. Imma uwe mwadilifu au dhalimu. Kama basi hutajitenga na watu, bali utawasikiliza na kutimiza mahitaji yao. Lakini kama wewe ni dhalimu, watu wao wenyewe watakaa mbali nawe. Kuna ubora gani uliopo kwa wewe kujitenga? Kwa matukio yote, kujitenga hakufai, hususan pale inapokuwa ni wajibu wako kushughulikia mahitaji ya watu. Malalamiko ya uonevu wa maafisa wako au madai kwa ajili ya haki yasidhihiri kuwa ya kero kwako. Upendeleo Wa Kindugu Fanya hili liwe wazi juu yako kwamba wale ambao wako karibu sana au waliokuzunguka watapenda kuzitumia nafasi zao kutamani sana kile ambacho ni mali ya wengine na kufanya vitendo vya uonevu. Zizuie hali kama hizo ndani yao. Fanya iwe ni kanuni ya tabia yako kamwe kutotoa hata kipande kidogo cha ardhi kwa yeyote kati ya jamaa zako. Hilo litawazuia kutokana na kusababisha madhara kwenye maslahi ya wengine na kukuokoa wewe kutokana na kukaribisha kutoridhika kwa wote, Mwenyezi Mungu na watu. Fanya uadilifu sawasawa bila kujali ukweli kwamba mmoja ni ndugu yako au laa. Ikiwa mmojawapo wa ndugu zako au rafiki zako wanavunja sheria, toa ile adhabu iliyoamriwa na sheria, kwa kiasi chochote kile itakavyokuwa chungu au itakavyouma kwako wewe mwenyewe binafsi, kwani itakuwa ni bora kabisa kwa dola. Kama katika wakati wowote ule watu wakawa na mashaka kwamba wewe umekuwa si mwadilifu kwao katika hali yoyote ile, wafichulie na uwaondolee wasiwasi wao huo. Kwa namna hii, akili yako itapatanishwa kwenye hisia za uadilifu na watu wataanza kukupenda. Hili litatimiza vilevile matakwa yako kwamba uweze kupata imani yao.

181

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 181

9/4/2017 3:47:54 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Amani Na Maafikiano Zingatia akilini kwamba hulitupilii mbali pendekezo la amani ambalo adui yako mwenyewe anaweza akalitoa. Likubali, kwani hilo litamfurahisha Mwenyezi Mungu. Amani ni chanzo cha faraja kwa adui. Inapunguza wasi wasi wako na kuendeleza utulivu katika dola. Lakini angalia! Ujihadhari wakati amani hiyo inapotiliwa saini, aina fulani ya maadui hupendekeza masharti ya amani kiasi tu cha kukuliwaza kwenye hisia za usalama; ili kuja kukushambulia tena wakati utakapokuwa umejisahau na ukawa huko katika hali ya ulinzi. Hivyo unapaswa kutumia uangalifu wa hali ya juu kwa upande wako na usiweke imani iliyovuka mipaka katika kushuhudia kwao. Bali, kama chini ya mkataba huo wa amani umekubali wajibu wowote, tekeleza wajibu huo kwa hadhari sana. Hiyo ni amana; na lazima itetewe kwa uaminifu kabisa, na wakati wowote utakapokuwa umeahidi kitu chochote, kidumishe kwa nguvu zote ambazo unazo, kwani tofauti yoyote ya maoni inaweza kuwepo katika masuala mengine, hakuna kitu bora sana kama utimizaji wa ahadi. Hili linatambulika hata miongoni mwa wasiokuwa Waislamu, kwani wao wanayajua matokeo ya kutisha yanayofuatia baada ya uvunjaji wa mikataba. Hivyo kamwe usifanye visingizio katika kutekeleza wajibu wako na usivunje kamwe ahadi yako, wala kumdanganya adui yako, kwani uvunjaji wa ahadi ni kitendo dhidi ya Mwenyezi Mungu na hakuna isipokuwa wale waovu wa kweli, anayetenda kinyume na Mwenyezi Mungu. Kwa hakika ahadi za ki-Mungu ni neema zilizoenea kwa wanadamu wote. Ahadi ya Mwenyezi Mungu ni hifadhi inayotafutwa, hata na wale wenye uwezo na nguvu kabisa juu ya ardhi, kwani hakuna hatari ya kudanganywa. Hivyo, usiweke ahadi yoyote ile ambayo wewe huwezi kuitimiza, wala kumshambulia adui yako bila shauri la mwisho kwa sababu hakuna isipokuwa kiumbe bazazi na mjinga atakayethubutu kumtaka shari Mwenyezi Mungu ambaye, katika huruma Yake isiyo na ukomo, amefanya mikataba na makubaliano kama zana za utakatifu wa hali ya juu kwa ajili ya viumbe Vyake; kwa kweli, amani inatoa hifadhi chini ya kivuli kichangamfu ambacho kwacho wote wanatafuta kimbilio, na katika ujirani ambao wote wanasikilizia juu ya mpita njia. Mkataba kwa hiyo, unapaswa uwe hauna ulaghai, undumakuwili, na udanganyifu. Usihitimishe kamwe mkataba ambao unakaribisha tafsiri, bali wakati unapokuwa umehitimishwa, usitumie misemo isiyo dhahiri, kama ipo yoyote; wala usikatae kukubali mkataba wowote ambao uliofikiwa kwa kuzingatia amri za

182

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 182

9/4/2017 3:47:54 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

kisheria za ki-Mungu, hata katika hali ya matatizo mabaya na magumu kabisa. Kwa vile kuna malipo ya thawabu katika maisha ya Akhera, ni bora kukabiliana na matatizo kuliko kuvunja mkataba huo ukiwa na hisia za kiwewe cha kuwajibika Siku ya Kiyama. Kuwa mwangalifu! Jizuie kutokana na kumwaga damu bila ya sababu ya maana, kwa vile kunakaribisha ghadhabu za Mwenyezi Mungu, kunamuanika mtu wazi kwenye adhabu Yake kali mno, kunamnyima mtu rehema Zake na kunafupisha maisha ya mtu. Hiyo Siku ya Kiyama ni kosa hili ambalo kwalo mtu atapaswa kujibu kwanza. Hivyo, jihadhari! Usipende kujenga nguvu ya dola yako kwa damu, kwani, ni damu hii ambayo hatimaye inadhoofisha mamlaka na inahujumu madaraka na kuutingisha msingi wake haswa; h7alafu mamlaka yanahamia kwenye mikono mingine. Mauaji ni kosa ambalo linaadhibiwa kwa kifo. Kama kwa maelezo yoyote yale, adhabu ya kutandikwa viboko inatolewa na dola kwa kosa lolote lile dogo, ikasababisha kifo cha mwenye hatia, usiifanye heshima ya dola izuie ndugu wa marehemu kudai fidia ya damu. Maelekezo Ya Mwisho Epukana na kujiabudu mwenyewe, usijiingize katika kujisifu mwenyewe wala usiwashawishi wengine kukutukuza sana, kwa sababu katika mitego yote ya kutangua matendo mema ya wachamungu, Shetani anategemea sana juu ya majisifu na udanganyifu. Imma usizidishe kiwango wala usijiingize katika majivuno kuhusu fadhila ambazo umezitoa juu ya watu. Kitendo cha kuvunja ahadi kinamuudhi Mwenyezi Mungu na mwanadamu halikadhalika. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema ndani ya Qur’ani Tukufu: “Mwenyezi Mungu anachukia sana kama hutekelezi yale uliyoyasema (katika ahadi).� Usiwe na haraka ya kufanya jambo kabla ya wakati wake, wala kuliacha pale wakati wake hasa unapowadia. Usishikilie katika kufanya jambo ambalo sio sahihi, wala kuonyesha kuzembea katika kurekebisha jambo lisilo sahihi. Tekeleza kila jambo katika wakati wake unaofaa na wacha kila jambo lichukue mahali pake panapostahili. Wakati watu wote kwa jumla wanapokubaliana juu ya jambo, usije ukaweka maoni yako mwenyewe juu yao na usije ukazembea kutekeleza

183

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 183

9/4/2017 3:47:54 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

wajibu ambao uko mikononi mwako kama matokeo yake. Kwani macho ya watu yatakuwa juu yako na utawajibika kwa lolote lile unalowafanyia. Kutowajibika japo kwa kiasi kidogo tu kutaleta adhabu yake kwenyewe. Dhibiti hasira zako na chunga mikono na ulimi wako. Njia bora kabisa ya kuzuia ghadhabu zako ni kuahirisha adhabu hadi utakapotulia na kurudia kwenye hali yako. Huwezi kulifanikisha hilo mpaka uwe unakumbuka kwamba hatimaye utarejea kwa Muumba wako. Ni sharti kwamba unachunguza kwa makini ile miongozo ambayo imewatia msukumo watawala wema na waadilifu ambao wamekutangulia wewe. Fikiria kwa karibu sana kwenye mifano ya Mtume wetu, hadithi na sunnah zake, na amri za Qur’ani na chochote unachowezakuwa umepata kutokana na njia yangu mwenyewe ya kushughulika na mambo. Jitahidi kwa kiasi cha uwezo wako wote kutekeleza maelekezo ambayo nimeyatoa hapa na ambayo umekubali kwa dhati kuyafuata. Kwa njia ya maagizo haya, ninaagiza juu yako kwamba usishindwe kwenye vishawishi vya moyo wako mwenyewe, wala usirudi nyuma katika kutekeleza majukumu yaliyokabidhiwa kwako. Ninaomba hifadhi kwa Mwenyezi Mungu na uwanja Wake wa neema usio na mipaka, na ninakulingania wewe kuomba pamoja nami kwamba aweze kutupatia sisi sote ile neema ya kujisalimisha kwa hiari kabisa utashi wetu kwenye utashi Wake, na kutuwezesha kutenda vyema sisi wenyewe mbele Yake na viumbe Vyake, ili kwamba wanadamu wazihifadhi kwa upendo mkubwa kumbukumbu zetu na kazi yetu ipate kudumu. Ninanuomba Mwenyezi Mungu rehema Zake na ninaomba kwamba Yeye aweze kukuruzuku wewe na mimi neema Zake na heshima ya (kufa) shahidi katika njia Yake. Kwa hakika, sisi tutarejea Kwake. Rehema na amani ziwe juu ya Mtume wa Mwenyezi Mungu na kizazi chake kilichobarikiwa. Mkataba Wa Umoja Wa Mataifa Juu Ya Haki Za Binadamu Kanuni zilizowekwa na Ali juu ya haki za binadamu zinaonekana kuwa bora na zenye ufanisi zaidi kulinganisha na tamko lililotolewa na Umoja wa Mataifa juu ya suala hilo. Wasomaji tayari wamezielewa vizuri zaidi zile haki za binadamu kama zilivyotamkwa wazi na Ali. Hata hivyo, inaonekana kuwa ni muhimu kuzirudia kwa

184

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 184

9/4/2017 3:47:54 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

muhtasari katika sura hii na kuvichunguza vipengele vyake mbali mbali tukitilia maanani mambo au viini vyao muhimu. Tumejitahidi kuyaelewa kikamilifu maoni ya Ali na mawazo yake kuhusu haki maalum na za kawaida kutokana na wasia zake mbali mbali, barua na maagizo aliyoyatuma kwa magavana na watumishi wake wengineo, ambazo tumeshughulika nazo katika sura tofauti na tumejitahidi kiasi cha uwezo wetu kuzielezea kwa uwazi kiasi iwezekanavyo. Hivyo itakuwa ni rahisi sana kwa msomaji kuzifahamu sheria na kanuni zilizowekwa na Ali kuhusiana na haki za binadamu kwa kurejea kwenye sura zinazohusika. Ili kuweza kuwasilisha maoni na imani za Ali kwa namna ya kutokeza zaidi na kugundua kwa njia bora na ya wazi zaidi, ni kwa nguvu za ki-mbinguni kiasi gani maelekezo haya yalitolewa na yeye, tunapendekeza kutaja hapa baada ya maudhui muhimu za mkataba wa Umoja wa Mataifa na tamko la haki za binadamu ambayo yameidhinishwa na wawakilishi wa mataifa yote. Kama kuna tofauti yoyote kati ya kanuni zalizowekwa na Ali na huo mkataba wa Umoja wa Mataifa basi itawezekana kwa msomaji kuitambua na pia kugundua sababu ya kwa nini imekuwa hivyo. Tunaweza kusema kwa kifupi kwamba kutokana na mtazamo wa madhumuni yake hakuna tofauti kati ya kanuni zilizowekwa na Ali kuhusu haki za binadamu na ule mkataba wa Umoja wa Mataifa. Kama itaonekana tofauti ndogo yoyote, ni dhahiri kwamba ni kutokana na mabadiliko ambayo yametokea katika Istilahi katika kupita kwa wakati, na sio ya msingi au katika kanuni. Hakuna sura katika mkataba wa Umoja wa Mataifa ambayo haiendi sawia na kanuni zilizowekwa na Ali. Kwa kweli mambo mazuri na yenye manufaa zaidi yanapatikana katika maelekezo yaliyotolewa na Ali. Kwa maoni yangu, tofauti kati ya makundi haya mawili ya kanuni ni kutokana na sababu nne zifuatazo: Kwanza kabisa huu mkataba wa Umoja wa Mataifa ulirasimiwa na maelfu ya wataalamu wanaotokana na takribani nchi zote za dunia; wakati ambapo zile kanuni za Alawia zilitangazwa na mtu mmoja tu, yaani Ali mwana wa Abu Talib. Pili, Ali alikuja ulimwenguni humu zaidi ya miaka elfu moja na mia nne iliyopita.

185

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 185

9/4/2017 3:47:54 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Tatu, wale ambao walirasimu ule mkataba wa Umoja wa Mataifa, au kwa kweli waliokusanya taarifa zilizohitajika kwa ajili yake, walijiingiza kwenye mazungumzo yaliyopita kiasi na kujisifu na kutamba kwamba dunia ilikuwa ina deni kwao kwa ajili ya sababu hiyo. Kinyume chake, Ali alionyesha unyenyekevu mbele ya Mwenyezi Mungu na alikuwa hana majivuno mbele za watu. Yeye hakutafuta ukubwa au ubora. Wakati wote alimuomba Mwenyezi Mungu na aliwataka watu kwamba matendo yake ya utoaji mamlaka na uondoaji kwenye hayo mamlaka yaweza kusamehewa na kutotiliwa maanani. Sababu ya nne juu ya tofauti hizo; na ambayo ni ya muhimu zaidi kuliko hizo tatu zilizotajwa hapo juu ni kwamba, mataifa mengi, kati ya yale yaliyoshiriki katika ule Mkataba wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa na kuuidhinisha, yalikiuka tangazo hili na yakaanzisha migongano ya kivita kulibatilisha na kulivuruga, lakini popote pale ambapo Ali aliweka mguu wake, na popote pale alipotamka chochote, au alipouchomoa upanga wake, alifanya hivyo kuuteketeza uonevu na udhalimu na alielekeza kusonga mbele kwenye njia ya haki na uadilifu. Kiasi kwamba aliipata shahada yake katika kutetea haki za binadamu ingawa kwenye kipindi cha uhai wake alikuwa amekwisha kuuawa kishahidi mara elfu nyingi. Sasa tunatoa hapa chini, maudhui ya ile sura kubwa ya ule mkataba wa Umoja wa Mataifa ambao unashughulika na haki za binaadamu. Umekusanywa na mwandishi wa kifaransa aitwaye Barbabech na kutafsiriwa kwa Kiarabu na Muhammad Manduur na kuchapishwa na Umoja wa Nchi za Kiarabu, (UAR). Wanadamu wote ni sawa katika suala la heshima na haki. Wameumbwa na uwezo wa kutafakari na ufasaha wa kutofautisha kati ya wema na uovu. Hivyo wote wanapaswa kutendeana kama ndugu. Kila binadamu anapaswa kufaidi haki zake zote, na fadhila zilizotolewa na mkataba huu. Usifanyike ubaguzi wowote ule kati yao kwa sababu ya tofauti katika kabila, rangi, lugha, dini, maoni ya kisiasa, nchi, kanuni za kijamii, utajiri, umasikini, nasaba na familia. Haki zilizotajwa katika Mkataba huu pia zinapatikana kwa raia wa nchi zile na pia kwa raia wa nchi ambazo serikali zao ziko nchi ya serikali za nchi nyingine. Hivyo raia wa maeneo hayo wako sawa na wakazi wa nchi zilizo huru.

186

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 186

9/4/2017 3:47:54 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Kila mtu anayo haki ya kumiliki njia ya maisha na kuendesha maisha yake kwa usalama na amani. Utumwa hauruhusiwi juu ya mwanadamu. Utumwa na kushughulika na watumwa vimekatazwa kwa hali yoyote ile. Hairuhusiwi kudhuru au kuonea wanadamu. Sio sheria kuwalazimisha bila sababu. Jambo lolote ambalo ni sawa na kitendo cha kukashifu tabia au sifa ya mtu limekatazwa. Kila mtu anayo haki kwamba nafasi yake ya kisheria ni lazima ikubalike katika nchi yoyote ile atakamokuwa. Wanadamu wote wako sawa mbele ya sheria. Kila mtu anayo haki ya kutafuta msaada wa kisheria. Hakuna tofauti kati ya wanadamu. Kila mmoja anayo haki ya kupinga ubaguzi ambao unaingilia yaliyomo katika mkataba huu. Kila mtu anayo haki ya kutoa malalamiko mbele ya mahakama ya kawaida ambayo imeanzishwa kutoa maamuzi kuhusu haki na ukiukwaji wa sheria zilizopo. Hakuna anayeweza kukamatwa, kufungwa na kufukuzwa kutoka kwenye mji wake. Hairuhusiwi kwamba mtu yoyote aingilie maisha binafsi au ya familia au mawasiliano ya mtu mwingine bila ya kuwa na haki ya kufanya hivyo. Hakuna anayeruhusiwa kushambulia heshima au sifa ya mtu mwingine, na kila mtu anayo haki ya kuziendea mamlaka za utekelezaji wa sheria katika tukio la kudhulumiwa au kuingiliwa.38 Kila mtu anayo haki ya kutembea kwa uhuru katika nchi yake na kufanya makazi popote anapotaka. Zaidi ya hayo, kila mtu amepewa haki ya kuhama toka kwenye mji wowote na pia kurudi kwenye mji huo pale atakapopenda. Kila mtu anayo haki ya kutafuta hifadhi katika nchi nyingine wakati anapoathiriwa na udhalimu na uonevu. Kila mtu ana haki za kumiliki katika nafsi yake binafsi au kama mwenzi na hakuna anayeweza kunyimwa umiliki wa mali yake iliyoko chini ya udhibiti wake. Kila mtu amepewa haki ya kutafakari kwa uhuru kabisa na serikali hazina haki ya kuingilia imani na matendo ya kidini ya watu. 38

Sehemu kubwa ya yaliyomo katika mkataba huu haiendani na malengo ya usoshalisti, kwa sababu katika nchi za kisoshalisti uhuru kamili wa mtu binafsi unachukuliwa kuwa ni wenye kupingana na maslahi ya Taifa. 187

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 187

9/4/2017 3:47:54 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Kila mtu amepewa haki ya kuwa na mawazo au maoni huru na kuyaeleza, na kwa kumuingiza lawamani, hakuna mtu anayeweza kumdhuru kwa sababu ya maoni yake.39 Kila mtu anayo haki ya kuingilia kati katika shughuli za Idara ya mambo ya kijamii ya nchi ima moja kwa moja au kupitia kwa mwakilishi aliyeteuliwa kwa uhuru kabisa. Kila mtu anayo haki ya kushiriki katika shughuli za kijamii katika hali ya usawa, na kujiamulia kwa watu ndio chanzo na msingi wa mamlaka ya serikali. Kila mtu anayo haki ya kunufaika kutokana na wajibu wa kawaida wa wanajamii ambao wanawajibikiana kwawo. Haki za kiuchumi, kijamii na kielimu, ambazo ni za lazima kwa mtu kulingana na hali yake zinahakikishwa juu yake na taifa zima pamoja na ushirikiano wa serikali ambazo zina wajibu wa kulipia haki hizi. Kila mtu anayo haki ya kuchagua ujuzi anaoutaka na kudai mazingira yanayotosheleza kwa ajili ya kazi hiyo ambayo yanaendana na haki. Anayo haki vile vile ya kusaidiwa kuondokana na kukosa ajira. Watu wote wanayo haki, bila ya kuacha hata mmoja, kudai malipo yanayofaa kwa kazi wanazozifanya. Kila mfanyakazi anayo haki ya kudai malipo ambayo yanatosha kwa ajili ya riziki yake yeye na ya familia yake na ambayo ataweza kwayo kujenga maisha yake kulingana na hadhi ya kibinadamu. Ikiwa katika wakati wowote ule, yale malipo ya kawaida hayatoshelezi kumkimu anapaswa afidiwe. Kwa njia yoyote ya pamoja.40 Ni haki ya kila mtu kwamba yeye na familia yake waishi maisha yao kwa njia ya ustawi na usalama, hususan katika suala la chakula, mavazi, mahali pa kulala, afya na mambo ya kijamii. Zaidi ya hayo, yeye anapaswa kusaidiwa katika hali ya kukosa ajira, udhaifu, uzee ukongwe, na ujane, na katika mazingira yote yale yanayoweza kufanya asipate kipato. Kila mtu anayo haki ya kupata elimu. Elimu inapaswa iwe ya bure na elimu ya msingi iwe ni ya lazima. Lengo la elimu liwe ni uleaji wa utu wa mtu na heshima kwa ajili ya haki na uhuru wa kisiasa. Ni muhimu vile vile kwamba elimu iweze kuwa ni njia ya kuimarisha maelewano ya pamoja, kusameheana na urafiki baina ya mataifa na iweze kuusaidia Umoja wa Mataifa katika kazi yake maalum ya kudumisha amani. aoni ambayo yanaingilia sheria na utaratibu au yanayosababisha vurugu au ni yenye madhara kwa uhuru na M msimamo wa Taifa ni makosa kwa mujibu wa Sheria, na sheria za kila nchi zinazingatia makosa kama hayo. 40 Uhuru wa kutenda, migomo na malalamiko ya wafanyakazi na mambo mengine kama hayo hayaruhusiwi kwa kufuatana na itikadi ya kisoshalisti, kwa sababu kila chochote kile kinachohusiana na vitendo na uchumi kinadhibitiwa na ile serikali ya kidikteta na upinzani kwa serikali unachukuliwa kama ni uasi dhidi yake. 39

188

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 188

9/4/2017 3:47:54 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Watu mmoja mmoja wanawajibu kwa jamii wajibu ambao ni lazima wao wautimize, kwa sababu haiba ya mtu binafsi inajengwa chini ya himaya ya jamii. Watu binafsi hawawezi kuzuiwa kudai haki zao na kufaidi uhuru isipokuwa katika suala ambalo sheria zimewekwa kulinda na kuheshimu haki na uhuru wa wengine, au kanuni zimetolewa na jamii kwa ajili ya ulinzi wa maadili mema, uendeshaji wa serikali na ustawi wa jamii. Haki na uhuru huo vinapaswa visiingilie kwa hali yoyote yale malengo na madhumuni ya Umoja wa Mataifa. Vifungu na lugha ya mkataba huu visije vikatafsiriwa katika namna ambayo kwamba serikali yoyote, chama au mtu binafsi anaweza kuwa na haki ya kujibu na kubatilisha kiutendaji uhuru uliotolewa katika mkataba huu. Hizi ndio dondoo muhumu sana ambazo zimeandikwa katika mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusiana na haki za binadamu na uhuru wake. Hizi ndio haki zilezile ambazo zinavunjwa mara kwa mara na serikali zile zilizosaini mkataba huo. Nadhani kwamba wasomaji lazima watakuwa wametambua utoshelevu wa maelekezo haya kwa msaada wa kanuni zilizotamkwa na Imam Ali, na watakuwa pia wametambua kufanana kwao, mbali na tofauti ya istilahi ambayo imebadilika pamoja na upitaji wa wakati, na mawazo ambayo yamejitokeza kwa sababu ya maendeleo, ambayo yametendeka katika zama hizi za sasa. Hata hivyo, ule upendo na upole, ambao unaonekana katika kanuni zilizoundwa na Imam Ali, unakosekana katika mkataba wa Umoja wa Mataifa. Katika sura ifuatayo tutataja yale maadili ya hali ya juu na sifa za Ali na jinsi alivyozingatia uhusiano wa kimaisha ambao upo kati ya viumbe hai na jinsi alivyouheshimu kwa maneno na vitendo vyake. Katika sura nyingine tutaangalia kwa kina zile hali za ulimwengu wa Kiarabu katika vipindi vya Bani Umayyah, Bani Abbas na watawala wengineo, na tutaelezea jinsi walivyozivunja kanuni hizi, ili kwamba, kwa uchunguzi linganishi wa mwenendo wa Ali na wa kwao, thamani ya kanuni alizozitamka yeye ziweze kujulikana kwa namna bora. Wakati tukizitoa kwa kirefu kanuni zilizotolewa na Imam Ali katika sura zilizopita, tayari tumekwishaonyesha kustahili na thamani yao, na katika hizi sura mbili tunahitimisha mjadala wetu kuhusu Ali na haki za binadamu, ili kwamba tuweze kugeuza mazingatio yetu kwenye mambo mengine.

189

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 189

9/4/2017 3:47:54 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Ali Na Thamani Ya Maisha Tumekwishajua kwamba Ali alihuzunika sana kwa sababu ya hali ya ufukara ya wale walioonewa. Aliwasaidia wao kupata haki zao na akawafanya watambue kile walichopaswa kutarajia. Yeye pia alishiriki matatizo na masikini na wale walionyimwa, ili thamani ya uadilifu iweze kujulikana na kiwango chake kiweze kunyanyuliwa. Tumejifunza mbinu zake za kuondoa uonevu, na zile kanuni ambazo alizifuata katika nafasi ya mtawala, na imekuja kujulikana kwamba kanuni na sheria zake zina nafasi ya juu sana miongoni mwa kanuni zilizotamkwa na watu mahodari sana na wenye busara, wa Mashariki na Magharibi pia. Tumekwishataja mchango wake kwenye lugha, falsafa, na elimu na tumeeleza kwamba yeye alikuwa ndio msingi na chanzo cha matawi haya ya elimu. Tumegusia kwenye uwezo usio na kifani ambao alikuwa nao wa kuamsha mwelekeo na uadilifu wa kawaida kwa ajili ya watu, na ufasaha wa ajabu ambao kwao alielezea sifa na matakwa yao. Uwezo wake wa asili na sifa zake binafsi viliingiliana; na kwa msaada wa hizo, yeye alipandikiza mti mpya katika kila fursa na akaupatia majani na maua kukamilisha ujuzi wa mwanadamu. Aliweka msingi mpya kupitia ujuzi wake wa kusoma na kuandika na kazi nyingine ambazo kwazo lugha ya Kiarabu, elimu ya sheria (fiqh), na elimu za kijamii zimesimamia humo, na ukweli ni kwamba zile nadharia zilizoelezewa na wengine ni machipukizi ya elimu ile ile ambayo yeye alituachia sisi. Kitabu hiki kikubwa sana kuhusu utambuzi wa mtu; hakiwezi kikakusanywa isipokuwa mpaka mwandishi aelezee asili ya wanadamu, azigundue athari za mabadiliko ya nyakati katika asili yao, aiongoze akili yake na mwelekeo wa asili kuelekea kwenye ustawi wao, na halafu achukue uamuzi kulingana na asili yao ya mmoja mmoja na ya jumla yao na msukumo wa wakati. Imam Ali aliitwaa mbinu hii katika semi na maagizo yake, ambayo hayana kifani baada ya hadith na maagizo ya Mtume. Katika baadhi ya maagizo yake amezungumzia mantiki ya kinadharia. Katika mengine amezungumzia mantiki ya utendaji. Na katika mengi yao amezungumzia yote. Maagizo yanayohusu mantiki ya nadharia yana maana ya ni jinsi gani jambo litakavyotafutwa, na yale yanayohusu mantiki ya vitendo yana maana ya ni nini kifanyike ili kupata neema. 190

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 190

9/4/2017 3:47:54 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Kuhusu ile aina ya kwanza ya maagizo inaweza ikasemwa kwamba Ali aligundua ile asili halisi ya mambo. Kwa akili pambanuzi aliyachunguza mema na maovu ya wakati ule, akafikia uamuzi sahihi baada ya kufanya majaribio muhimu, na akayafanya maamuzi hayo kujulikana kwa watu.41 Maagizo yake yalikuwa ya busara sana na ya uhakika hasa kiasi kwamba inaweza ikasemekana kwamba yamepatikana kwa njia ya mahesabu ya kijometria. Yameelezewa katika namna nzuri ambayo kiasi kwamba kutokana na mtazamo wa maana, na vilevile tafsiri zake, yanaunda msingi wa fasihi ya Kiarabu. Fikra na maoni yote ya Imam yaliyokusanywa ndani ya Nahjul-Balaghah ni ya kiwango hiki. Katika maagizo ambayo Amirul-Mu’minin amezungumzia mantiki ya kijometria, amewaacha watu katika mas’ala ya akili na maoni ili waweze kuuona msimamo wa ukweli na watende kutokana na kuelewa na kutambua kwao. Maagizo kama hayo hayapo katika namna ya amri, makatazo au matakwa. Kinyume chake, ni kauli za kifalsafa ambazo ndani yake asili na tabia za marafiki na maadui, za waadilifu na waovu, wenye busara na wapumbavu, wakarimu na mabakhili, waonevu na wenye kuonewa na kadhalika zimeelezwa kikamilifu. Kuhusu yale maagizo yake yanayohusiana na mantiki ya vitendo, au zote; mantiki ya vitendo na ya nadharia, inaweza kuelezwa kama ifuatavyo: Wale ambao wanafikiri kwamba zile sheria, kanuni, taratibu na mfumo wa serikali zinatosheleza juu ya uendeshaji wa mambo ya umma, hao wamekosea, kwa sababu mtu anapaswa kuchukua wajibu wa ulinzi na utekelezaji wa kanuni na sheria hizi baada ya maelezo yanayotosheleza ya haki za binadamu. Kama ilivyo muhimu kwamba mtu anayezitunga sheria hizi lazima awe na busara, mwenye uzoefu na mwadilifu, ni muhimu pia kwamba yule anayezitekeleza awe na sifa hizi na anapaswa ayapate yale matokeo yanayotakikana. Hili ni hivyo kwa sababu uendeshaji au usimamiaji wa mambo ya umma unategemea sana juu ya hizo sifa nzuri au mbaya za wale wanaoeneza sheria hizo na pia unahusiana na zile busara na mazingatio ya watu ambao juu yao sheria hizo zimetungwa. Licha ya yote haya ni lazima ikubalike kwamba sheria na kanuni mbalimbli mpya ambazo zimeundwa, nyingi zao zinatofautiana sana. Kwa sababu tofauti zilizopo kati ya nchi; haiwezekani kuzitekeleza sheria hizi bila ya kutumia nguvu na udhibiti, na zile mamlaka za kusimamia utekelezaji wa sheria zinaruhusiwa kuepuka kuzitekeleza 41

Kwa mujibu wa imani ya Shia kila chochote kile alichokisema Imam kilikuwa juu ya msingi wa msukumo na nguvu ya kimbingu, yaani, msukumo wa Uimamu na sio rahisi kuipata elimu yote aliyokuwa nayo yeye kwa njia ya akili na uzoefu. 191

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 191

9/4/2017 3:47:54 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

kwa kiasi fulani. Kanuni na sheria za serikali za zamani zilikuwa takriban ni zenye kuchukuana na tabia na maadili ya wale waliozitekeleza. Hii ilikuwa ni kwa sababu ambazo ziko nje ya uwanja wa mjadala wetu wa sasa.42 Hebu tuchukulie kwamba; inawezekana kwa wanadamu kutunga sheria za maana, na kuwalazimisha watu kwenda kwa mujibu wa sheria hizo. Hata hivyo, kama majukumu hayatekelezwi kwa mujibu wa maamrisho ya ufahamu na imani, basi yanakuwa hayana thamani zaidi. Tunaamini kwamba kila tendo ambalo halitendwi na mwanadamu kwa uthibitisho wa mantiki ya busara, matakwa binafsi, na dhamira imara na bila kulazimishwa, haliwezi kufanywa kama ni tendo la kibinadamu. Kitendo maarufu na cha thamani sana cha mwanadamu ni kile ambacho amekitenda kwa kuchochewa na ufahamu wake mtu. Kanuni na sheria zinazoundwa na serikali hazitoshelezi hata kidogo kuendeleza mahusiano ya wanadamu, mpaka ile hekima ya kinadharia na kivitendo imfanye mwanadamu kuwa ameridhika nazo hizo. Katika hali hiyo; dhamiri na matendo mema ya watu vitapatana vyote pamoja, na kuwafanya watu mmoja mmoja na vikundi kufikia makusudio yao kwa njia ustaarabu, kwa sababu watu kama hao hawahitaji kitu chochote isipokuwa matendo mema. Kila chochote tulichokisema kuhusu watu mmoja mmoja na vikundi kinajulikana sana kwa wasomi na wanafalsafa na kwa ulamaa waliopita na wanachuoni wa utafiti, na tunaamini kwamba dhamira na imani viliwalazimisha kutumikia. Tunapoichunguza kwa makini historia ya wale ambao walitumikia wanadamu na ustaarabu, tunakuja kujua kwamba ingawa hekima pekee ndio iliyokuwa dira yao ya kuelewa kila jambo, bado haikuwa peke yake katika historia ya maisha yao. Nguvu ya ujuzi wa kinadharia imedorora na kukauka. Yenyewe peke yake tu haiwezi kufanya lolote. Ni lazima iwe na vifuasi na visaidizi vya aina mbalimbali, pamoja na sifa zao na idadi yao. Nguvu hii inakuonyesha 42

wandishi amethibitisha hapa kwamba ni wajibu wa watu kuiona sheria kama ni neema juu yao. Wanapaswa M wawe na imani juu yake na wajichukulie wao wenyewe kama wenye kuwajibika kuitii, badala ya serikali kuwa na wajibu wote kabisa wa kuitekeleza na watu kuitii kwa hofu ya kuadhibiwa. anachuoni wa Kiislamu wameielezea hoja hii ndani ya vitabu vyao kwa kirefu; na Waislamu wote wanajua W kwamba, sheria zilizotungwa na binadamu hazitoshelezi kuhakikisha furaha katika dunia hii na wokovu katika Akhera. uhusu sheria ya ki-mbinguni ni lazima kwamba Mtume aitekeleze kupitia wahyi na watu waitii kama kanuni K ya ibada. 192

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 192

9/4/2017 3:47:54 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

njia tu, bali sio ile kasi, na haikulazimishi wewe kutembea juu ya njia hiyo. Jambo linalokufikisha wewe kwenye hatua ya utendaji ni shauku na mwelekeo. Marconi (mwanasayansi wa Kitaliani aliyevumbua simu ya upepo) aliipenda hiyo, kwa sababu ya shauku na mwelekeo wake, kutofurahia burudani za dunia na kubakia kwenye kujitenga kutumikia wanadamu na ustaarabu, kwani vinginevyo ni kwa nini alijichagulia mwenyewe kujitenga, kama hekima na shauku ya kivitendo haikumsukuma kutumikia wanadamu? Jambo hilo hilo linaweza kusemwa kuhusu baadhi ya watu wengine maarufu. Hivyo wale watumishi wa wanadamu wenye mawazo ya kiungwana walifanya matendo mema kwa shauku kubwa na bidii. Kwa vile watu waovu na wasio na bahati walikosa busara halisi ya kweli na nia njema, hawakuweza kufanya utumishi wowote kwa wanadamu, licha ya hekima zao za kinadharia. Kwenye kundi hili wamo Adolf Hitler, Hajjaj bin Yusuf, Changez Khan, Alexander wa Macedonia na wanasayansi mashuhuri wengi wa zama zetu hizi ambao walitumia majaribio yao kuhusiana na watu. Wote hao walikuwa na nguvu ya akili kama watumishi wa wanadamu lakini licha ya hivyo, utendaji wao haukuwa chochote ila umwagaji damu, kukosa heshima juu ya maisha ya mwanadamu, uharibifu wa mafanikio ya ustaarabu wa mwanadamu, na vifo na uangamizaji wa wanaume na wanawake wasio na hatia wasio na idadi. Hii ilikuwa ni kwa sababu kwamba hekima zao za kinadharia na fikira hazikuwa zimeunganishwa na hekima ya vitendo na hisia njema. Kama mambo mawili haya (yaani, hekima ya vitendo na hisia njema) hayapo, hekima ya kinadharia haina maana yoyote na kwa kweli ni yenye madhara. Sina maana ya kusema kwamba ule uwezo tofauti walionao wanadamu, yaani; hekima ya kinadharia na ya kivitendo na mwelekeo vinatofautiana. Kwa hakika nguvu hizi zinasaidiana na kuathiriana kila moja na nyingine. Ninachomaanisha kusema hapa ni kwamba; zile busara za nadharia zinavijumuisha vitu vyenyewe, zinaunganisha visababisho na athari pamoja, na kutoa mipaka iliyo thabiti na kanuni ambazo hazibadiliki kwa sababu ya mabadiliko yanayotokea katika maadili na mataifa, lakini busara za kivitendo na hisia ziko tofauti kutokana na tofauti zilizopo kwa watu. Busara ya kinadharia inakuwepo ndani ya kila mtu na inalijumuisha jambo kwa usahihi kabisa. Ni muhimu kwamba iwe na mwelekeo, na hekima ya kivitendo inapaswa kuifanya iendelee kwenye njia ya wema na mafanikio. 193

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 193

9/4/2017 3:47:54 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Likishindwa hili, mtu anayehusika atatumia hekima yake katika kufanya uvumbuzi ambao utakuja kuwa chanzo cha uangamizaji wa wanadamu na pia cha bahati yake mbaya. Hili ni kweli kwa mtoa sheria kama kwa wale ambao kwamba sheria hiyo imetungwa kwa ajili yao. Dhamiri na mwelekeo wao utakuwa uwe wenye kuhitaji kutii sheria zilizoko juu ya msingi wa usawa na haki na kukiri kwao kielimu tu kwa wema wao hakutoshi. Nyoyo zao lazima ziondokane na uchafu ili kuhakikisha ukamilifu wa mafanikio ya kibinadamu, ili kwamba waweze kufanya jitihada kwa shauku kwa ajili ya ustawi wa umma. Zaidi ya hayo, ni muhimu kwamba wawe na maadili mema, kwa sababu tabia nzuri ya mwanadamu inalinda sheria na taratibu kutokana na watenda maovu na watenda dhambi kama ngome. Ilikuwa ni kwa sababu hii kwamba Imam Ali aliamsha mielekeo mema katika nyoyo za watu na akatoa hotuba zenye kuendeleza maadili mema. Katika hotuba zake, wasia na mazungumzo, yeye siku zote alizungumzia dhamiri za watu, kwa sababu alijua kwamba kwa ajili ya usimamiaji wa mambo ya watu na mahusiano yao mazuri, ilikuwa ni lazima kwamba wapaswe kuwa na maadili mema. Utakaso wa nafsi unamhakikishia mwanadamu ukamilifu na pia unasaidia uadilifu, na unalinda mipaka yake. Zaidi ya hayo, kunaongozea kuelekea kwenye mawazo na matakwa ya watu ambayo hukamilisha ustawi na furaha. Ali alikuwa na uwezo usio wa kawaida wa kushauri na kuwasafisha watu, na maneno yake yalimvutia sana kila mtu. Alizijua tabia zao na njia ya mienendo yao. Alizilinganisha sifa zao njema na mbaya na akajumuisha uhalisi wao katika kauli zake. Alizielezea aina zao tofauti. Yeye aliwaagiza watu kufanya mambo fulani na akawakataza kutenda mambo maovu. Alikuwa na maoni mazuri sana kuhusu dhamiri ya watu kuwa na uwezo wa kutofautisha kati ya wema na uovu. Maoni haya mazuri ya Ali kuhusu dhamiri ya wanadamu yalifanana na maoni kama yale yaliyoshikiliwa na wahisani wakubwa wa ubinadamu (kama Isa – Yesu) na Muhammad ambao waliongoa akili na nyoyo zenye upole na upendo, na ambao mapenzi yao juu ya watu hayakuwa na mipaka. Kila mwanga ulikuwa na umuhimu mbele ya kile ambacho kimechochewa ndani ya nyoyo zao. Ali alikuwa ameweka msingi wa maagizo yake kwenye maoni haya haya mazuri na kuzungumzia kwake dhamiri ya mwanadamu katika ushauri na hotuba zake, pia ni kwa sababu ya maoni mazuri aliyoshikilia kuhusu maumbile ya mwanadamu. 194

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 194

9/4/2017 3:47:54 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Kwa vile Ali alikuwa na maoni mazuri kuhusu watu, licha ya matatizo yote aliyoyapata mikononi mwao, yeye wakati wote alijitahidi kukazia maadili mema ndani ya nyoyo zao. Yeye alijua kwamba wema na uovu vyote vinakuwemo ndani ya maumbile ya mwanadamu. Hata hivyo, inambidi mtu mwenye uvumilivu kuelekeza moyo wake kwenye wema na kuulea. Aliwaelimisha watu kupitia mifano na vilevile kwa tabia njema, kwa sababu mbinu hii ya elimu ni yenye athari nzuri sana. Imam Ali aliwasisitizia watu kila wakati kuwa na maoni mazuri kuhusu dhamiri za watu. Yeye alisema: “Kama mtu atashikilia maoni mazuri juu yako, jaribu kulithibitisha wazo lake kuwa ni la kweli.” Amesema vilevile kwamba: “Endapo mtu atafanya jambo fulani usichukulie wazo baya juu ya jambo hilo madhali inawezekana kupata hatima nzuri kutokana nalo hilo.” Kama alishutumu vitendo fulani vya watu wadanganyifu na wauovu, ilikuwa ni kwa sababu yeye aliona kwamba kuwarekebisha kwao kunawezekana kwa njia ya makaripio na ushauri, ingawaje ingeweza kulazimu kiasi kikubwa cha juhudi na muda. Mtu muadilifu huwalipa wale ambao wanafanya matendo mema, lakini huwaadhibu wale wafanya maovu kwa sababu anategemea kwamba kwa kufanya njia hii itawezekana kuwarekebisha. Kama Imam Ali asingelitarajia hili asingestahimili yale matatizo yasiyovumilika ambayo yalisababishwa na watu waovu. Ali alisema kuhusu dunia na watu wapenda dunia: “Watu wapenda dunia hungurumiana kama mbwa na wanayama wakali. Wenye nguvu wao huwameza wanyonge na wakubwa huwadhalilisha wadogo.” Aliyasema haya kwa sababu alipata mateso sana kwa sababu ya uporaji na utovu wa utii na udhalimu wa watu, na alikuwa amechukizwa sana kwa sababu ya usumbuvu waliousababisha wao. Kwa kuyasema mambo haya alipambana dhidi ya madhalimu, wakatili na waonevu kwa namna ile ile ambayo daktari anapambana na wadudu kwa ajili ya ustawi na afya ya mgonjwa. Yeye alipendelea kifo kuliko uhai na alitumaini juu ya wokovu wa watu. Ali aliuheshimu uhai, kwa sababu ni neema kubwa ya Mwenyezi Mungu. Aliwachukulia viumbe hai kama wa kuheshimiwa ili kwamba mfano wa dalili za maumbile ubakie salama katika uhai wao.

195

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 195

9/4/2017 3:47:54 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Alikuwa na maoni mazuri sana kuhusu dhamiri na usafi wa asili ya mwanadamu, na alikuwa mwenye matumaini sana juu ya mafanikio ya mwanadamu. Yeye alitamani kwamba watu wangeweza kuwa huru kama yeye alivyopaswa kuwa. Kwa kukosekana kwa maoni haya mazuri na matumaini, asingeweza kuwa na tabia nzuri kwa watu kama hiyo na asingesema: “Kama ukisikia jambo kutoka kwa mtu usichukulie maoni mabaya kulihusu hilo madhali inawezekana kupata hatima njema kutokana nalo hilo.” Kama hivyo ndivyo; asingeweza pia kuzungumzia dhamiri za watu kwa upole kama mitume, na asingewaongoza kwa moyo mzito kuelekea kwenye wema kwa hotuba zake na kuwaasa kwake. Alitamani kuyalinda maadili ya watu kwa hotuba na maagizo yake, na kulea shauku ya kibinadamu ndani yao ili kwamba waweze kufanya matendo mema kwa msaada wa hekima na akili zao wenyewe. Katika kila kazi, Imam Ali aliteua wapelelezi fulani kutoka miongoni mwa watu wenyewe, ili kuwachunguza na kutangaza kwamba viungo vya miili yao vilikuwa vinajitayarisha kwa uvamizi juu yao. Kwa vile alikuwa na imani juu ya makadirio yao wenyewe, yeye alisema: “Enyi watu! Kumbukeni kwamba nafsi zenu zinajiandaa kwa uvamizi juu yenu, na viungo vyenu ni wapelelezi juu yenu, ambao wanatunza hesabu ya matendo yenu na hata ya kupumua kwenu.” Kutokana na imani yake katika dhamiri ya mwanadamu na heshima yake juu ya uhai, yeye aliwaambia watu wa wakati wake kwamba maisha ya mwanadamu hayawezi kuwekwa kifungoni, na hayawezi kuwekwa kwenye kitanda kidogo cha utotoni kwa muda mrefu. Yasiwekwe kifungoni yasije yakawa machafu na hatimae yakaangamizwa. Katika sura nyingine tutakuja kwa kunukuu baadhi ya semi za kipekee za Ali ambazo zitadumu kuwa hai alimuradi watu waadilifu bado wanaishi duniani. Semi hizo zitadumu milele. Tumezichagua semi hizi kutoka kwenye Nahajul-Balaghah, na zinahusiana na upatikanaji wa maadili mema na tabia njema na kwenye utakaso wa mwanadamu. Mazingira Yaliyokuwepo Baada Ya Ali Haya majanga na maovu ya kijamii na kimaadili yalianza kujitokeza katika ulimwengu wa Kiarabu, na yakapata nguvu huko Mashariki kutokea ile siku ambayo ule mkono wa uovu wa Ibn Muljam uliponyooshwa kuelekea kwenye kigezo cha haki na mfano wa maadili, yaani, Ali mwana wa Abu Talib. 196

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 196

9/4/2017 3:47:54 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Unajitokeza umuhimu wa kutaja kwa ufupi ile hali ya taifa la Kiarabu baada ya kuuawa kishahidi kwa Imam Ali; na kuelezea ni sura gani ambayo mambo yalichukua katika vipindi vya Bani Umayyah na Bani Abbasi, shughuli za watawala hawa, ambao walipotoka kutoka kwenye kanuni zilizowekwa na Ali, zilikuwa ni zipi, na jinsi mtu wa kawaida alivyokuja kuwa duni na akahamishwa kama mirathi kutoka kundi moja kwenda jingine. Ukhalifa wa Imam Ali ulikuwa ni kipindi cha mpito kati ya kipindi cha Uthman na kile cha Mu’awiyah na warithi wake. Katika kipindi hiki cha mpito, haki na uadilifu vilipata nafasi ya juu sana. Hata hivyo, katika kipindi kilichotangulia hiki, haki za watu zilivunjwa na kukiukwa sana. Wale watu waliokuwa wa tabaka la juu hawakuyatii mamlaka ya serikali hiyo. Matokeo yake yalikuwa kwamba dhulma na uonevu vilienea. Wakuu wa umma, watumishi na magavana walikuwa wamegeuka kuwa chanzo cha mateso juu ya watu na walikuwa wakitafuna mali zao. Washauri na washirika wa Uthman walikuwa madhalimu wakamilifu. Itakuwa ni bora kuelezea hapa ile hali ya watawala na raia zao katika vipindi vya Bani Umayyah na Bani Abbas; ili thamani ya watawala hao, na zile kanuni alizoziweka Ali viweze kueleweka wazi wazi, na wasomaji waweze kutambua ni jinsi gani hekima na fikara za Ali zilivyokuwa adhimu mno. Upanga wake ulikomesha ubinafsi upesi sana mwanzoni mwake na mkono wake muadilifu uliteketeza upotovu. Mara tu Ali alipokuwa amekwishauawa kishahidi mikononi mwa mlaaniwa Ibn Muljam, Mu’awiyah ibn Abu Sufyan akaanza kupanga mipango dhidi ya wapinzani wa ukhalifa wake. Alimuadhibu vikali sana kila mtu ambaye alikataa kumkubali kama khalifa wa Mwenyezi Mungu. Alikuwa bado hajamaliza kazi yake hii wakati alipoanza kusawazisha njia kwa ajili ya urithi wa mwanae, yule Yazid mwenye kuvuma kwa ubaya, kuwa kama khalifa. Alizitwaa njia zote zilizowezekana ambazo zingeweza kuwa na manufaa kwenye ufalme wa mwanawe. Alitoa heshima kwa baadhi ya watu na akawanyima wengine vyeo na madaraka. Kati ya mipango mingi ambayo Mu’awiyah aliibuni kwa ajili ya kuchukua kiapo cha utii kutoka kwa watu kwa ajili ya Yazid, hapa tunataja mmoja ambao utakuja kuonyesha ule msingi ambamo ukhalifa wa Yazid na warithi waliomfuatia ulisimamia. Mu’awiyah aliandaa mkusanyiko ili watu wa kutoka maeneo mbalimbali waweze kuchukua kiapo cha utii kwa mwanawe, wote kwa pamoja katika wakati wa uhai 197

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 197

9/4/2017 3:47:54 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

wake yeye mwenyewe. Pale watu hao walipokusanyika tayari, Mu’awiyah na Yazid pia walikuwepo. Wakati huo mnafiki anayejipendekeza, aliyeitwa Yazid ibn Muqanna alisimama na akasema, huku akimuashiria Mu’awiyah: “Huyu ndiye Amirul-Mu’minin” halafu akamnyooshea kidole Yazid na akasema: “Kama Mu’awiyah atafariki, basi atakuwa ni yeye huyu.” Kisha akauashiria upanga wake na akasema: “Kama mtu yeyote hatakubaliana na hili, basi adhabu yake itakuwa ni huu.” Mu’awiyah akasema: “Kaa chini, wewe ndio bingwa wa wasemaji.” Watu wa Hijazi hawakukubali kutoa kiapo cha utii kwa Yazid. Hawakuweza kushawishiwa ama kwa utajiri wala hawakuogopa nguvu za kijeshi. Tabia ya Mu’awiyah kwa watu hao inashangaza. Wakati mmoja aliwatishia akisema: “Ninaapa kwa jina la Allah kwamba kama mtu yeyote atatamka hata neno moja hapa dhidi yangu, atakatwa kichwa chake kabla hajatamka neno la pili. Ninyi kwa hiyo, myachunge maisha yenu na msikitafute kifo.” Aliweka waangalizi wawili kwa kila mtu mmoja atokanaye na Hijaz na akawaambia hao maafisa wa polisi: “Yeyote kutoka miongoni mwa watu hawa atakapofunua midomo yake kukanusha ama kukiri, kichwa chake kikatwe.” Ilikuwa ni kwa namna hii kwamba Yazid ibn Mu’awiyah alifikia kwenye ukhalifa. Abdullah ibn Hanzala alisema: “Tulihofia kwamba kama tusingempinga Yazid, basi yangetudondokea mawe kutoka mbinguni na sote sisi tungeangamia kwa sababu ya ghadhabu ya ki-mbingu. Ilikuwa ni kwa sababu hii kwamba sisi tulimpinga Yazid.” Alikuwa ni Yazid huyo huyo ambaye alimuua Imam Husein katika namna ya kuhuzunisha sana, aliizingira Ka’aba na akaipiga mawe kwa msaada wa chombo cha kurushia mawe kwenye vita, akaihalalisha damu na mali ya watu wa Madina kwa ajili ya wapiganaji wake, na akaishi maisha ya kupenda anasa na starehe. Alikuwa akicheza na majibwa na manyani hadi alipokufa, na alirithiwa na watu wengine wa ukoo wa Bani Umayyah. Walizigawanya mali za hazina ya umma miongoni mwa ndugu zao na washirika wao. Ile nafasi ya haki ambayo iliundwa na Ali iliharibiwa na wao, na kikundi cha kidhalimu kikashika hatamu za serikali. Kundi moja la watu hawa likawa tajiri sana na jingine likarudishwa kwenye umasikini uliokithiri. Wakati maelfu walikuwa wanashinda na njaa, khalifa wa Bani Umayyah alitoa dinari kumi na mbili elfu kumpa mwimbaji aliyeitwa Ma’abad, kwa sababu alimfurahisha khalifa kwa muziki wake. 198

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 198

9/4/2017 3:47:54 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Wale waungwana walimiliki watumwa wasio na idadi pamoja na watumwa wa kike. Sabini elfu kati yao waliachwa huru na Suleiman ibn Abdul Malik peke yake. Upendeleo na ubaguzi kwa sababu ya ukabila, ukoo au kundi ulikuwa ni wa kawaida kabisa wakati wa utawala wa Bani Umayyah ingawa Uislam ulikuwa umevunja ubaguzi kama huo na Imam Ali alikuwa hakuuruhusu kabisa. Katika zama zile upambanuzi ulifanyika baina ya watu wa Yemen na Bani Qais. Waarabu walidai ubora juu ya wasiokuwa Waarabu na vivyo hivyo Maquraishi walidai ubora juu ya wengine. Mabaraza yao yalijaa watu wanaopenda starehe ambao walipata mafungu makubwa kutoka kwenye hazina ya umma bila ya kufanya kazi yoyote ya umma. Historia inaelezea kwamba Walid bin Abdul Malik alikataza mishahara ya wapokea mishahara hiyo zaidi ya elfu ishirini. Hizi zilikuwa ndio njia na tabia za Bani Umayyah wote isipokuwa Umar ibn Abdul Aziz. Walipata madaraka juu ya maeneo mbalimbali kwa njia ya ukandamizaji, na wakafanya kazi ya Mu’awiyah na Yazid. Abdul Malik bin Marwan alikuwa akitoa amri kulingana na matakwa yake mwenyewe na hakuweka umuhimu wowote kwenye maisha ya watu na mali zao. Aliamuru visima na mito ya Bahrain vijazwe michanga ili wakazi wa maeneo hayo waweze kuwa mafukara, na kuitii serikali. Aliteua mtu mkatili na mwenye kiu ya damu kama vile Hajjaj ibn Yusuf kuwa gavana wa Iraqi. Amin Rayhan anasema hivi kuhusu Bani Umayyah: “Watawala wa Bani Umayyah walikuwa wameigeuza haki ambayo ingekuwa ni muhimu kufuatwa na mfalme. Hili lilikuwa ni kundi la watu ovyo na wasiokuwa na uwezo. Kama mmoja wao alikuwa mpumbavu, mwingine alikuwa mwenye kustahili kudharauliwa. Kama mmoja alikuwa mnyonge na asiyekuwa na heshima, mwingine alikuwa mlevi na muonevu. Angalau mtu hawezi kupuuza ule mwenendo wao wa kuchukiza na wa kiovu ambao ulimtukana Ali na wanawe kutoka kwenye mimbari zao.” Miongoni mwa Bani Umayyah alikuwepo khalifa muadilifu mmoja tu na yeye alikuwa ni Umar ibn Abdul Aziz. Yeye alianza utawala wake kwa kuondoa udhalimu. Alitaka kufanya ile mali iliyoporwa kutoka hazina ya umma kurudishwa huko na kutwaa sera ya maana kwa ajili ya ukhalifa wake. Hata hivyo, baadhi ya watu walikuwa hawakufurahishwa na mwelekeo wake huu na wakamuua. Bani Umayyah walifikia kwenye ukhalifa kwa udanganyifu, na wakaubadilisha kuwa ufalme kwa kushurutisha, na wakaanzisha ufalme ambamo hamkuwa na dalili ya usawa na haki. Hatimaye jumba la serikali yao likaja likayumba na kuanguka juu 199

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 199

9/4/2017 3:47:54 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

ya vichwa vyao wenyewe. Baada yao wakaja Bani Abbasi na wale watu waadilifu wakawasifu Bani Umayyah kama wakilinganishwa nao hawa. Amin Rayhani anasema: “Bani Abbasi walipata udhibiti juu ya nchi kwa njia ya kumwaga damu. Kulikuwa na vituko vya kutisha vya mauaji ya halaiki na umwagaji damu huko Syria, Palestina na Iraqi na baada ya hayo wakuu wengine pia walifuata mfano wa Abu’l-Abbas Saffah katika mauaji na umwagaji wa damu. Mtu mmoja aliyeitwa Amiitar aliwakaribisha watu kwake huko Syria. Watu wa Yemen walimtii lakini Bani Qais waliasi dhidi yake. Amiitar alituma shambulizi la usiku juu yao na akachoma mali na nyumba zao. Mtu mwingine aliyeitwa Ibn Bahiis alipigana dhidi ya Amiitar, akapata udhibiti juu ya Damascus na akawaadhibu wakazi wa mji ule. Katika wakati wa Bani Abbasi maasi na ghasia yalikuwa yameenea sana na moyo wa ushabiki ulikuwa unazidi kupata nguvu. Na hawakuwa ni wale waasi wakatili wenye kiu ya damu tu waliokuwa wakiteseka, bali wale raia masikini waliokuwa wakilipa kodi na ambao walikuwa wakati wote wako tayari kushiriki katika Jihadi, pia na wao walihusika katika matatizo hayo.” Baada ya hapo, akirejea kwenye zile himaya kubwa na ndogo za siku za mwisho za Bani Abbas, Amin Rayhani anasema: “Watu walioishi katika zama zile za giza walikuwa na bahati mbaya sana. Kila mtawala alichuana na mwingine katika umwagaji wa damu na vita na alikuwa akijivunia maovu yake. Aliwaambia wapiganaji wake: ‘Ninakufanyieni kuwa ni halali kwenu kufanya lolote mtakalo kwenye mji huu kwa muda wa siku tatu.’ Kwa maneno haya, wao waliruhusu uporwaji wa mji na umwagaji wa damu ya wakazi wake. Mutanabhi anasema: ‘Wale wanawake ambao walifanya urafiki nao walikuwa wafanywe watumwa, watoto wao walikuwa wauawe, utajiri walioulimbikiza wao ulikuwa utekwe nyara na mazao yao kuchomwa moto.’ Aibu juu ya wakati ule, na aibu juu ya watu wa wakati ule. Mwenyezi Mungu awarehemu wale watu waliokuwa hawana uwezo na wale watawala na wapiganaji wale walaanike! Je, mwanadamu ambaye ni kiumbe bora cha Mwenyezi Mungu anageuzwa wakati mmoja kuwa mnyama mkali? Je, nduli hawa wanastahili kwamba kurasa hamsini za historia ziweze kutengwa kwa ajili yao? La hasha; vitendo vyao vijumuishwe kwenye msitari mmoja tu; walikuja kuwa maadui katili wa kila mmoja 200

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 200

9/4/2017 3:47:54 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

wao, walipigana, wakauwa, wakapora na kuchoma na walikuwa na hatia ya maovu au kwa maneno mengine, wao waliyachukulia maisha, mali na heshima za wengine kuwa ni halali juu yao wenyewe. Haya ndio maelezo ya Amin Rayhani kuhusu kile kipindi cha Bani Abbasi na ule uporaji na umwagaji damu wa zile himaya ndogo katika wakati wa siku za mwisho za ukhalifa wao; yaani, wakati makhalifa walikuwa jina tu, na mamlaka halisi yalikuwa yamewatoka mikononi mwao. Sasa tutazungumza kwa ufupi kuhusu kile kipindi cha Bani Abbasi. Imekwisha kuelezwa mapema, kwamba Bani Umayyah wakipinga ule mfumo wa serikali ambao AmirulMu’minin alitaka kuuanzisha, na kutelekeza ile sera adilifu aliyokuwa ameitwaa yeye, wao waliifanya serikali kuwa ni mali ya ukoo wao. Hawakumruhusu mtu yeyote kushiriki katika mamlaka yao. Walifuata sera za kifashisti kana kwamba serikali hiyo na mapato yake yalikuwa ni mali iliyohusikana na wao tu na hakuna mwingine tena ambaye alikuwa na angalau fungu dogo tu ndani yake. Wakati Bani Abbas walipofikia kuyadhibiti mambo baada ya Bani Umayyah, wao pia waliegemezea utawala wao kwenye malengo hayo hayo. Wao pia walishikilia ule mtazamo kwamba mfalme alikuwa ni mwakilishi (khalifa) wa Mwenyezi Mungu juu ya ardhi na kwamba ilikuwa ni haki yake ya asili kutawala. Hakuna mwengine aliyekuwa na haki ya kuleta mabadiliko yoyote katika mpango huu. Ilikuwa ni kwa sababu ya mtazamo huu hasa, kwamba Mansur, khalifa wa pili wa Bani Abbasi, alisema wakati akizungumza mbele ya mkusanyiko wa hadhara kwamba: “Enyi watu! Mimi ndiye mfalme wa dunia niliyeteuliwa na Mwenyezi Mungu. Ninatawala juu yenu kwa baraka na msaada Wake. Mimi ndiye mlinzi wa mali ya Mwenyezi Mungu. Ninaitumia hazina ya umma kwa ridhaa Yake. Chochote ninachompa mtu kimetolewa kwa idhini Yake, kwa sababu Yeye amenifanya mimi kuwa kufuli la hazina Yake. Kama Yeye anataka kukupeni ninyi kitu chochote, basi atalifungua kufuli hilo na kama Yeye hataki kukupeni kitu chochote, Yeye ataliacha kufuli hilo likiwa limefungwa.” Sera hizo hizo ndio zilifuatwa na makhalifa wengine wa Bani Abbasi. Kila mmoja wao alikuwa mwakilishi wa Mwenyezi Mungu juu ya ardhi! Hii inakuja kuonyesha wazi wazi kwamba ukatili ulikuwa ndio msingi wa serikali ya Bani Abbasi na wana wa kifalme na watawala wadogo wa chini yao. Kwa mtazamo wao, utawala ulikuwa ni kipaji cha ki-mbinguni. Mwenyezi Mungu alitoa 201

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 201

9/4/2017 3:47:55 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

kipaji hiki kwa wale ambao aliwataka Yeye na wakati aliporidhia ustawi wa watu, Yeye aliwapatia mtawala mpole, mwenye hekima na mkarimu. Matokeo ya njia hii ya fikra na lengo na imani hii yalikuwa kwamba, watu walibaki kuwa watiifu kwa watawala wa Bani Abbasi na walistahimilia kwa uvumilivu kila lililowakuta, wao wakilichukulia kwamba linatoka kwa Mwenyezi Mungu. Baghdad, makao makuu ya Bani Abbasi, ulikuwa ukifurika kwa utajiri, lakini utajiri wote huu ulilengwa kwa khalifa tu, na ndugu na washirika wake. Wengine, hata kwa uhalali kiasi gani walioweza kuwa nao na utumishi wowote wanaoweza kuwa wameutoa kwa umma, hawakuwa na fungu katika utajiri huo, na waliandikiwa ufukara na unyonge isipokuwa mpaka wamemsifia khalifa na kujidhalilisha mbele yake. Kama matokeo ya hili, matabaka mawili ya watu yakaja kujitokeza. Kulikuwa na tofauti kubwa sana kati ya matabaka haya mawili. Watu wa tabaka moja walijizogomeza kwenye utajiri wakati wale wa tabaka jingine, juu ya kuwa na uhodari na ufanisi kiasi gani, wao walibakia kuwa mafukara na masikini, na waliendesha maisha ya taabu sana. Kodi na mapato ya serikali yalitumiwa na khalifa, jamaa zake na washauri wake katika kuendesha maisha ya starehe. Walitumia mamilioni juu ya washirika wao, wenye kujipendekeza na kuwasifu, watumwa wa kike na matowashi. Kutokana na mtazamo wa mali, khalifa, watoto wa kifalme, waungwana na watumishi wa serikali walikuwa kwenye tabaka la hali ya juu kabisa. Wachuuzi walifuatia. Ingawa maisha na mali zao pia yalikuwa kwenye hatari ya kudumu kwa sababu ya watu wa vyeo vya juu, lakini kuhusu utajiri wao walikuwa na nafasi baada ya wale waungwana. Mambo pekee ambayo yaliangukia kwenye fungu la watu wa kawaida na wa chini yalikuwa hata hivyo ni ufakiri, kukosa uwezo, njaa na vifo. Huko Baghdad majumba ya fahari ya matajiri na mabanda mabovu ya masikini yalisimama yakitazamana upande huu na upande ule. Inaweza ikasemwa kwamba yaliwakilisha mandhari ya pepo na jahannam. Mshairi wa wakati ule anasema hivi kuhusu Baghdad: “Baghdad hii inafaa tu kwa watu matajiri kuishi ndani yake, na sio kwa masikini na mafukara. Endapo mtu tajiri kama Korah atatokea kuja Baghdad, yeye pia atajawa na huzuni na mfadhaiko.

202

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 202

9/4/2017 3:47:55 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Baghdad ndio ile pepo hasa ambayo tuliyoahidiwa sisi, lakini imekuja kabla haijakomaa kwenye mikono ya wale ambao wanacho cha kutosha kula na kuvaa. Ndani ya Baghdad wamo ma-hurulain na watumishi vijana, na mna kila kitu unachoweza kukitaka. Kitu ambacho hakipatikani hapa ni binadamu.” Tajiri mpenda starehe mmoja anasema: “Je, umewahi kuona mji kama Baghdad katika dunia yote nzima? Hii Baghdad ndio pepo juu ya dunia. Ndani ya Baghdad chemchemi ya furaha ni halisi na mti wa starehe umestawi kijani. Mahali kwingine hata hivyo, maisha sio safi wala sio ya furaha. “Mtu anafaidi maisha marefu ndani ya Baghdad. Chakula na maji yake ni vitamu na vizuri. Hapana shaka kuhusu ukweli kwamba chakula na maji ya nchi nyingine ni bora kuliko yale ya nchi zingine.” Haipingiki kwamba Baghdad ilikuwa ni pepo juu ya ardhi katika kipindi cha Bani Abbasi au kwa jambo hilo, katika vipindi vyote. Na vile vile sio uongo kwamba chemchem ya furaha katika mji huo ilikuwa safi na mti wa starehe ulikuwa kijani. Vile vile hakuna mad-hara juu ya maisha ya watu wa mji ule kuwa marefu. Hakuna chochote katika mambo haya ambacho ni cha uwongo, mwanadamu siku zote anatafuta kuishi maisha katika pepo, ambamo mna aina zote za starehe – matunda na maua na kila kitu kizuri. Lakini vitu vyote hivi vinaweza kuwa vizuri tu kama havikupatikana kwa njia ya kuwanyonya watu masikini na wasiojiweza, au kwa kuvikwapua kutoka kwa mayatima na wajane. Hali hizi za starehe zilipatikana kutoka wapi, wakati kulikuwa na maelfu ya watu mafukara ambao hawakula wakashiba angalau mara moja katika maisha yao ndani ya mji huo? Yule mshairi mashuhuri, Abul-Atahiya anamzungumzia khalifa wa wakati wake, hivyo akionyesha hisia za watu: “Kuna yeyote anayeweza kunifikishia ushauri wangu wa mara kwa mara kwa khalifa? Ninaona kwamba gharama ya maisha ya watu iko juu sana na vipato vyao viko chini mno. Mahitaji yao hayana idadi na wanashambuliwa asubuhi na jioni na mabalaa na matatizo chungu nzima. Mayatima na wajane wamekaa mikono mitupu ndani ya majumba yao. Wanaume na wanawake pia wananyoosha mikono yao kuelekea kwako ili uweze kuwapendelea na chochote. 203

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 203

9/4/2017 3:47:55 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Wote wanalalamika juu ya matatizo ya maisha, na wananyanyua vilio katika sauti za chini. Wanatarajia huruma zako ili kwamba waweze kuyaondoa matatizo yao na waione hali ya furaha. Akina mama, pamoja na watoto mikononi mwao wanapitisha usiku katika njaa na wanafunga wakati wa mchana. Ni nani aliyepo, ambaye anapaswa kuyajaza matumbo yao matupu na kuvisha miili yao iliyoko uchi? Mimi ninakujulisha kuhusu mambo ya kweli kwa niaba ya raia zako.” Mtu mmoja alikwenda kumuona khalifa Wathiq Billah. Analeta taswira ya fahari na ukuu na utukufu wa kasri lake kwa maneno haya (ikumbukwe kwamba hii ni kuhusu utukufu wa kasiri moja tu): “Mtumishi mmoja alinikabidhi kwa mwingine na yule wa pili akanikabidhi kwa watatu. Baada ya kupita kwa namna hii mikononi mwa watumishi wengi nilifika kwenye jengo, ambalo uwanja wake na kuta vilikuwa vimefunikwa na hariri iliyotariziwa na kupakwa rangi. Kisha nikawasili kwenye baraza ya kifalme. Ardhi yake na kuta pia zilikuwa zimefunikwa na hariri iliyotariziwa. Katikati ya ukumbi, Wathiq alikuwa amekaa juu ya kiti chake cha kifalme. Kiti hicho kilikuwa kimepambwa kwa lulu. Mtumwa wake wa kike, Farida, alikuwa amekaa na gitaa mkononi mwake. Wathiq na vile vile yule mtumwa wa kike walikuwa wamevaa nguo za hariri za gharama kubwa.” Maisha haya ya anasa na starehe ya kibepari yalikuwa ni ugonjwa wa kuigana ambao wote pamoja na khalifa, ndugu zake na washauri na vile vile baadhi ya wafanya biashara walikuwa wanaugua. Na kuhusu vitendo vingine vya aibu ambavyo vilikuwa vikifanyika ndani ya jumba la kifalme hilo ni bora tusivitaje hapa. Ununuzi na uuzaji wa watumwa na watumwa wa kike kwa pesa ambao haukuwa umeruhusiwa na imma Mtume au Imam Ali, 43 ulikuwa unaendelea sana kiasi kwamba katika kila mji kulikuwa kuna mtaa wa biashara uliotengwa maalum kwa ajili ya biashara hii tu. Ndani ya Baghdad, ambao ulikuwa ndio makao makuu ya Bani Abbasi, barabara ya Daral-Raqiq ni sehemu inayojulikana sana ambayo ilitumika kwa madhumuni haya. Wachuuzi katika biashara ya watumwa walikuwa na watumwa na watumwa wa kike wa kila kabila na rangi. Watumwa weusi waliletwa kutoka kusini kuja kwenye miji ya Bani Abbasi na kuuzwa kwa dirham mia mbili (kiasi cha rupia hamsini mpaka 43

islamu unaruhusu utumwa wa makafiri tu ambao wanastahili kupigana nao vita, au mateka ambao wanaU tekwa kama matokeo ya Jihadi. Katika kipindi cha makhalifa na baada ya hapo, hata hivyo, hali ilikuja kuwa kwamba wakati wowote wale majambazi walipomuona mtu yoyote ambaye hana ulinzi katika mji wowote wa Kiislamu walimkamata na kumuuza. 204

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 204

9/4/2017 3:47:55 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

hamsini na tano) kwa kichwa kimoja. Watumwa wenye rangi nyeupe na wasichana watumwa waliletwa kutoka Samarkand ambayo ilikuwa ni soko kubwa kwa ajili ya watumwa wa aina hii. Walikuwepo watumwa wa kike wa aina nyingi. Baadhi yao walitokana na Kandhar na Sind. Walikuwa wembamba na walikuwa na macho meusi na nywele ndefu. Baadhi yao walikuwa ni wale ambao walikuwa wamefundishwa huko Madina. Walikuwa ni wenye kutia ashiki na wachezaji muziki hodari. Wale waliokulia Makkah walikuwa hawana kifani katika madaha yao na sura zao zinazoduwaza. Baadhi ya watumwa wa kike vile vile walikuja kutoka nchi za magharibi. Yule mlanguzi Abu Uthman ambaye alikuwa na taarifa kamili kuhusu sifa za watumwa na watumwa wa kike wa wakati ule anasema: “Mtumwa wa kike azaliwe huko Barbary na aondoke nchini mwake katika umri wa miaka tisa. Aishi miaka mitatu huko Madina na miaka mitatu huko Makkah. Katika umri wa miaka kumi na sita aende Iraqi akajifunze tabia za kiungwana huko. Anapaswa auzwe pale anapofikia umri wa miaka ishirini na tano. Mtumwa wa kike kama huyo atajumuisha ndani yake mwenyewe ule uchangamfu wake wa asili, utamanishaji wa Madina, madaha ya Makkah na adabu na tabia za Iraqi.� Kwa bahati mbaya Abu Uthman ameshindwa kutaja kuhusu ni bei kiasi gani mtumwa wa kike kama huyu angeweza kuchukua. Mbali na watumwa wa kike wanaotokana na Barbary walikuwepo pia Wahabeshi kutoka Ethiopia, Waturuki, Wacyprasi, Warumi na Waarmenia, ambao sifa zao hazihitaji kutajwa hapa. Watumwa wa kike wanaotokana na kila nchi walikuwa na sifa na tabia maalum za kipeke yao ambazo zimeelezwa kwa kirefu na wataalamu wa wakati ule. Licha ya kuzungumza juu ya watu masikini katika kipindi cha Bani Abbasi, hata wale watu matajiri hawakuhisi kwamba maisha na mali zao vilikuwa salama. Maisha ya watu yalikuwa mikononi mwa mfalme na walikuwa wanahofia kwamba wanaweza wakapoteza mali zao au maisha yao wakati wowote. Hivyo, kama kwa upande mmoja ule ukarimu wa khalifa na waungwana wake ulikuwa hauna mipaka, hapakuwa na mipaka ya unyonywaji wa watu kutoka kwao pia. Kama katika wakati mmoja khalifa alitoa maefu ya dinari kumpa mtu kwa kutamka kwake maneno au beti nzuri, na katika wakati mwingine yeye aliamuru kwamba kichwa cha mtu kikatwe mara moja na mali yake itaifishwe.

205

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 205

9/4/2017 3:47:55 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Attabi ametengeneza picha halisi kabisa ya hali iliyokuwepo wakati wa uhai wake. Aliulizwa ni kwa nini hakujaribu kutafuta cheo kwenye baraza la kifalme wakati ambapo alikuwa ni msomi na mwandishi maarufu. Yeye alijibu hivi: “Ninaona kwamba kwa wakati mmoja khalifa anampa mtu maelfu ya dinari bila uhalali na bila kustahili kuzipata, na wakati mwingine anaamuru kwamba mtu asiye na hatia atupwe chini kutoka kwenye paa la kasiri lake. Kama nitajiunga na baraza la kifalme hilo sitajua ni lipi kati ya majaaliwa mawili haya litakalonikuta.” Wakati mmoja khalifa Mehdi alimwita Mufazzal Zabi kwenye baraza yake. Pale mtumishi wa khalifa alipomwendea, yeye alihofia kwamba inawezekana ikawa mtu amemzungumza vibaya mbele ya khalifa. Yeye, kwa hiyo, alivaa sanda chini ya nguo zake na akafika kwenye baraza la kifalme akiwa amejiandaa kabisa kwa kifo chake. Alimsalimia khalifa, naye akamwitikia salamu zake. Kisha akasimama kimya kabisa. Baada ya muda kiasi alitambua kwamba khalifa alikuwa hana nia ya kumuua, na, kwa hiyo, akaja akatulia, Mehdi akamuuliza: “Ni Mwarabu gani aliyetunga beti bora kabisa juu ya mada ya fahari na kusifia?” Khalifa pia alimuuliza maswali mengineyo na Mufazzal akatoa majibu yaliyostahili. Mehdi alifurahishwa na majibu yake na akamuuliza kuhusu mambo yake binafsi. Mufazzal akamwambia kuwa alikuwa anadaiwa, na papo hapo khalifa akaamuru kwamba apewe dirham thelathini elfu. Ma’mun alimuua waziri wake Fazal bin Sehl na kisha akaitoa nafasi ya uwaziri huo kwa Ahmad ibn Abi Khalid, lakini yeye akakataa kuikubali nafasi hiyo. Katika kuulizwa ni kwa nini ameikataa nafasi hiyo, Ahmad alijibu: “Uzoefu wangu ni kwamba yeyote yule ambaye ameishika kazi hii hatimaye amepoteza maisha yake.” Matokeo ya utajiri ni kwamba sherehe zilikuwa hazina mipaka na zilienea kama ugonjwa wa kuambukiza. Katika kila nyumba kulikuwa na watumwa wa kike wasiokuwa na idadi ambao walikuwa mabingwa katika kuimba, kucheza na kutamanisha kiashiki.44 Wakati wale matajiri walipochoka na namna moja ya starehe walibuni nyingine. Nyakati zingine walipozidiwa na furaha kwa kusikia wimbo mzuri; na wakawa hawajui jinsi ya kuonyesha furaha yao, walizuzuliwa na furaha na wakajipiga na kujijeruhi vichwa vyao wenyewe kwa kitu chochote walichoweza kukikamata mikononi mwao. Abul-Faraj Isfahani katika kitabu chake ‘Aghani’ na wanahistoria wengi wamesimulia matukio mengi ya namna hiyo. Sababu ya kuzuzuka kwao ilikuwa kwamba wa44

islamu hauruhusu kumfanya mtumwa Muislamu au Dhimmi (asiyekuwa Muislam) au kafiri asiyeamini U kabisa, ambaye mkataba pamoja naye umekamilishwa. Ilitokea vile vile, hata hivyo, kwamba katika kipindi hiki wengi wa watumwa na watumwa wa kike walitokana na makundi haya. 206

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 206

9/4/2017 3:47:55 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

likuwa hawajui jinsi ya kuonyesha kicheko na furaha yao; kwa hiyo, walivumbua mbinu mpya kila siku. Katika upande mwingine walikuwepo watu masikini, wengi wasiokuwa na idadi, ambao kwa kuishi katika dhiki na ufukara kabisa, walikuwa wamechoshwa na maisha yao. Kundi moja lilikuwa likiendesha maisha ya starehe kubwa kupita kiasi, ambapo watu wa kundi jingine walikuwa wamechoshwa na ule uhai wao wenyewe hasa. Waliyadharau maisha yao na vile vile jamii yao na utamaduni wao. Walikuwa hawana matumaini ya kubadilika kwa hali ya jamii yao kuwa bora. Abul-Atahiya anazielezea hisia za watu hao kwa maneno haya: “Ule mkate mkavu ambao unaula ukiwa umekaa kwenye pembe na ile nyumba finyu ambamo unapitisha siku zako; au pembe ya Msikiti ambamo unaweza kuishi kwa kujitenga, ni bora kuliko zile nyakati ambazo zinatumika chini ya kivuli cha majengo ya fahari. Huu ni ushauri kutoka kwa mtu anayeijua ile hali halisi vizuri kabisa. Atafurahi yule mwenye kuusikia ushauri wangu. Ninaapa kwa maisha yangu kwamba kipande hiki cha ushauri kinatosha juu yake. Tegea masikio yako kwenye ushauri huu wa mtakia wema wako ambaye anaitwa Abul-Atahiya.” Hali zote za kujiua kwa kujitumbukiza mwenyewe kwenye furaha na vicheko au kwa kuitelekeza dunia kunapingana na maumbile na asili ya mwanadamu. Mwenyezi Mungu hakumuumba mwanadamu imma kwa ajili ya muundo huu au ule wa maisha, hata hivyo, katika kipindi cha Bani Abbasi maovu ya namna zote mbili hizi yalikuwa ni ya kawaida. Kilichoelezwa hapo juu ni utupiaji macho wa mara moja wa hali za watu katika kipindi cha siku za mwanzoni za utawala wa Bani Abbasi. Baadae maisha yao yakaja yakawa ya taabu kiasi kwamba haiwezekani kufikiria udhalilikaji wao. Wale matajiri wakawa matajiri zaidi, na masikini wakazidi kuwa masikini maradufu. Matajiri walikuwa ni wachache kwa idadi lakini mafukara walikuwa hawahesabiki. Hata hivyo, maisha na mali za yeyote kati yao hazikuwa na salama. Ni watu wachache tu, yaani mtawala na ndugu zake na washirika wake ndio waliokuwa salama na kuridhika. Hakuna katika hao matajiri wengine aliyekuwa na utulivu wa akili. Walikuwa na woga wakati wote kwamba khalifa anaweza akawakasirikia wakati wowote na hili linaweza kuishia kwenye kukamatwa kwa mali zao na kupoteza maisha yao. Aina hii ya ukatili ilianza katika wakati wa Mutawakkil – yule mtu aliyejenga jahannam sambamba na pepo.

207

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 207

9/4/2017 3:47:55 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Matajiri waligeuka kuwa hawana haya kabisa. Walikunywa pombe na wakapoteza fahamu zao kabisa. Walipanga kufanya karamu ya vyakula na vinywaji kwenye makasiri yao na wakawa na starehe za fujo na ghasia. Wakati mwingine walichana nguo zao na kugaragara kwenye mchanga. Walipoteza fahamu zote za mwenendo mwema na wakajiingiza kwenye vitendo vyote vya kiovu. Wakiwa wamelewa, baadhi yao walidhani kwamba wameifanya ardhi itetemeke kwa kupiga miguu yao juu yake. Hadithi nyingi kama hizo zimesimuliwa na Abu Hayyan Tauhidi katika kitabu chake kiitwacho ‘Al-Mata’a wa al-Mawanisah.’ Idadi ya wasichana watumwa katika nyakati hizo ilikuwa haitabiriki. Mutawakkil, ambaye aliwatukana watu wenye busara na wenye ghera kwa kiasi kikubwa iwezekanavyo, alijaribu kwa uwezo wake wote kuizamisha kwenye maji kaburi ya Imam Husein na akawaruhusu wale majambazi ndani ya baraza lake kumdhihaki na kumtukana Imam Ali, na alikuwa na watumwa wa kike kwa maelfu ndani ya kasiri lake kubwa. Baadhi ya makhalifa wa Bani Abbasi walikuwa na idadi ya watumwa wa kike kiasi cha takriban elfu kumi. Mbali na watumwa wa kike walikuwepo na matowashi wasiokuwa na idadi katika makasiri yao. Watu matajiri na wale watokanao na tabaka la kikabaila waliweka matowashi katika nyumba zao kwa ajili ya ulinzi wa wanawake zao. Katika kipindi cha siku za Amin idadi ya matowashi hao iliongezeka sana. Khalifa Muqtadir alikuwa na matowashi wengi kiasi cha elfu kumi na moja. Tabaka la kati pia lilikuwa na watumwa wengi ambao walikuwa wachafu. Wamiliki walichukua huduma chafu zisizo na haya kutoka kwa watumwa wao. Sababu ya msingi ya maovu yote haya ilikuwa kwamba lile tabaka la watu waungwana na matajiri walipuuza zile kanuni zilizowekwa na Mtume na Imam Ali. Hawakuwaona binadamu kuwa ni wenye kulingana sawa. Matajiri na wale watu waliokuwa kwenye daraja za juu walijiona kuwa wao ni bora kuliko watu wengine wa kawaida na waliishi maisha ya anasa kwa kuwanyonya masikini. Tungependa kuzungumzia kwa mara nyingine tena kuhusu tabia na maadili ya watu katika kipindi cha Bani Abbasi ili kutoa picha juu ya maisha ya anasa na starehe nyingi waliyoishi waungwana na matajiri, na ule ufukara na kutojiweza ambako wale masikini walipatwa nako. Ukweli ni kwamba katika jamii ambayo watu wake kwa kawaida ni mafukara, humo mambo mawili ambayo ni utajiri na umasikini yanaelekea kutokea. Tunaweza kuligundua jambo hili katika kuzingatia kile alichosema Imam Ali: “Sijaona utajiri 208

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 208

9/4/2017 3:47:55 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

uliokithiri kwa mtu yoyote isipokuwa kwa pamoja hapo nimeona na haki ikiwa inavunjwa.” Majumba makubwa ya kifahari yalijengwa na juu yao viwango vikubwa vya pesa vilitumika. Mutawakkil alifanya majumba mengi yajengwe, ambayo uzuri na fahari yake vilikuwa katu havielezeki. Katika moja ya majumba haya lilijengwa bwawa la kuogelea kwa ajili ya wanawake na watumwa wa kike. Wakati yule mshairi maarufu, Behtri, alipoliona jumba hilo, alivutiwa sana na ufahari wake kiasi kwamba alidhani lilikuwa limejengwa na mashetani na majinni. Akilielezea jumba hilo, yeye anasema: “Inaonekana kana kwamba wale majini watiifu kwa nabii Suleiman ndio wamejenga jumba hili na wakafanya bidii katika kila kitu. “Kama Bilquis, malikia wa Sheba angekuwa apite katika jumba hili angedhani kwamba ni kasiri la Suleiman kwa sababu ya kule kufanana mno kati ya mawili hayo. “Unapoliangalia bwawa hili wakati wa usiku, na kuona kuakisiwa kwa nyota ndani yake, utafikiria kwamba bwawa hilo ndio mbingu na nyota zimepigiliwa ndani yake. Samaki hawawezi kuufikia ukingo wa bwawa hilo, kwa sababu kuna umbali mkubwa sana kati ya mwanzo na mwisho wake.” Yaqut Hamawi anaandika katika kitabu chake, ‘Maj’maul-Bayan’ hivi: “Hakuna hata mmoja kati ya makhalifa wengine aliyejenga majumba ya kufahari ya namna hiyo katika mji wa Samarrah kama aliyoyajenga Mutawakkil. Mbali na majumba mengine, kulikuwa na idadi ya majumba yaliyojulikana kama Qasr al-Arus, ambalo liligharimu dirham milioni thelathini, Qasr al-Ja’far, Qasr al-Gharib, Qasr al-Shaidan, Qasr al-Burj na Qasr al-Bustan Aitakhiyah ambayo kila moja liligharimu dirham kumi milioni, Qasr al-Maliih na Qasr al-Subh ambayo yaligharimu dirham milioni tano kila moja.” Baada ya kutoa orodha ndefu ya maqasir, Yaqut Hamawi anasema kwamba jumla ya dirham mia tatu milioni zililtumika kwa ajili ya maqasiri hayo. Akilisifia Qasr al-Ja’fari la Mutawakkil, yule mshairi Ali ibn Jehm anasema: “Zimo kazi bora za sanaa katika Qasr hili zisizowahi kuonekana kwa wafalme wa Roma na Irani katika muda wao mrefu wa utawala. Kuna viwanja vikubwa ndani yake kiasi kwamba macho lazima yasafiri mbali ili kuona sanaa adhimu na tunu zake za kipekee. Na kuna makuba marefu kiasi kwamba inaweza ikasekana kwamba yanaongea na nyota angani.

209

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 209

9/4/2017 3:47:55 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Ibn Mu’tiz alifanya lijengwe kasiri ambalo kwamba paa lake lilijengwa kwa matofali ya dhahabu, na miti ilipandwa kulizunguka. Behtri analisifia jengo hilo kwa maneno haya: “Paa lake lilijengwa kwa dhahabu na lilikuwa na nuru na ung’aavu. Mwanga wake ulienea kila mahali. Upepo mwanana ulizagaa ndani yake, na miti isiyokuwa na matunda na ile yenye matunda, siku zote iliburudisha. Ilikuwa kama wanamwali wa kuvutia wanaotoka nje kutembea – baadhi yao wakiwa na mapambo na wengine wakiwa hawanayo.” Moja ya makasiri hayo, lililojengwa na khalifa Mu’tazid lilikuwa linaitwa Qasr al-Surayya. Lilikuwa na nafasi kubwa sana na lilikuwa limepambwa vizuri sana, kiasi kwamba huyo ibn Mu’tiz ambaye alilijenga kasiri hili yeye mwenyewe aliliona kuwa ni kama ufundi stadi wa majini. Mwanahistoria Khatib Baghdadi ameleta taswira pana ya kasiri hili wakati akielezea ule mkutano wa balozi wa Roma na khalifa. Yeye anasema: “Muqtadir alikuwa ana matowashi elfu kumi na moja, watumwa wa Sicilia, wa kiroma na wa kihabeshi. Huu ulikuwa ni upande mmoja wa kasiri hilo. Vilikuwepo pia vitu vingine visivyokuwa na idadi ambavyo vilichangia kwenye uzuri wake na usanifu wake. Muqtadir alikuwa ameagiza kwamba balozi huyo atembezwe kwenye kasiri lote na aonyeshwe na maghala ambamo ndani yake mmehifadhiwa vitu vyenye thamani kwa utaratibu wa kupendeza sana. Lulu za bei ya ghali sana zilikuwa zimewekwa katika masanduku ambayo yalikuwa yamevunikwa kwa nguo za hariri zilizopakwa rangi nyeusi. Balozi huyo alifikishwa kwenye ukumbi ambamo ulisimama mti uliotengenezwa kwa fedha halisi ambayo ilikuwa na uzito wa dirham mia tano elfu. Walikuwemo pia ndege wengi waliotengenezwa kwa madini ya fedha ambao walikuwa wamewekwa kwenye matawi ya mti huo na pale, na wakati upepo ulipovuma walianza kutoa milio. Balozi huyo alipumbaa kwa mshangao kuyaona yote haya. Mapazia yaliyoning’inizwa kwenye kuta za kasiri hili yalikuwa na idadi ya elfu thelathini na nane. Mapazia yote haya yalitengenezwa kwa hariri na nguo zilizotariziwa. Yalipakwa rangi kwa namna nyingi na yalikuwa na picha za wanyama na mashua. Mapazia hayo makubwa yalikuwa ni mfano bora wa usanii wa watu wa Armenia na Venetia. Mengine yao yalikuwa wazi na mengine yalikuwa yamepakwa rangi. 210

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 210

9/4/2017 3:47:55 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Baada ya hapo, balozi huyo alifikishwa kwenye zizi. Baraza ya jengo hili ilijengwa kwenye nguzo za marumaru. Katika nusu ya upande wa kulia wa zizi hilo walikuwepo farasi mia tano walioandaliwa kikamifu kwa hatamu, matandiko na vitambaa vya hariri vya kuvunika matandiko. Kwa kila farasi alikuwepo mtumishi aliyevalishwa sare ya gharama kubwa. Halafu balozi huyo akapelekwa kwenye jengo ambamo wanyama wa porini wanaofungwa wamewekwa humo. Walikuwa wakija kwa wale wageni wanaowatembelea na kuwanusa, na vilevile kula vitu kutoka mikononi mwao. Kisha balozi huyo akafikishwa kwenye jengo jingine ambamo aliwaona tembo wanne waliofunikwa kwa maguo ya hariri. Watumishi wengi walikuwa wamewekwa hapo kuwaangalia tembo hao. Pale balozi huyo alipowaona tembo hao alishikwa na hofu. Baada ya hapo balozi huyo alipelekwa kwenye jengo ambamo wanyama wakali mia moja walikuwa wamewekwa humo. Hamsini kati yao walikuwa wamewekwa kwenye sehemu moja ya jengo hilo na hamsini wengine kwenye sehemu nyingineyo. Kisha akapelekwa kwenye sehemu iitwayo ‘Josaq.’ Sehemu hii ilikuwa imezungukwa na mabustani na katikati yake kulikuwa na bwawa lililojengwa kwa mseto wa bati na risasi. Mfereji ambao pia ulijengwa kwa mseto wa bati na risasi ulijengwa kwa kulizunguka bwawa hilo. Bwawa hili, ambalo lilikuwa na urefu wa dhiraa thelathini na upana wa dhiraa ishirini lilikuwa zuri mno kuliko lililojengwa kwa shaba. Lilikuwa na mashua nne ambamo mlikuwa mmewekwa viti vya dhahabu ndani yake vya kukalia. Ilikuwemo miti mia nne ndani ya bustani hiyo iliyowekwa kulizunguka bwawa hilo, na kila mmoja wa miti hiyo ulikuwa na urefu wa kwenda juu wa dhiraa tano. Kila mti ulikuwa umefunikwa kuanzia juu hadi chini kwa rangi ya mpingo, ambamo pete za shaba nyeusi zimepachikwa ndani yake. Kwenye ukingo wa kulia wa bwawa hilo kulikuwa na masanamu kumi na tano ya askari wa farasi waliovaa hariri ambao walishikilia mikuki kwenye mikono yao, kana kwamba wanataka kumshambulia adui. Masanamu kumi na tano zaidi yalikuwa nayo pia yamesimamishwa kwenye ule ukingo wa kushoto. Baada ya balozi huyo kuwa ametembezwa kwenye makasiri ya kifahari yapatayo ishirini na tatu, alifikishwa kwenye uwanja wa jumba unaoitwa “Tas’iini.” Katika uwanja huu watumwa vijana walikuwa wamesimama, na wote walikuwa na silaha 211

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 211

9/4/2017 3:47:55 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

kikamilifu. Halafu akafikishwa mbele ya khalifa Muqtadir kwenye Qasr al-Taj ambalo lilikuwa kwenye ukingo wa mto Tigris. Alikuwa amevaa taji linaloitwa Tawiila na alikuwa amevaa nguo za hariri na zilizotariziwa, kutoka kichwani hadi miguuni. Kiti chake cha kifalme kilikuwa kimetengenezwa kwa mpingo, na zulia lake lilikuwa limetengenezwa kwa hariri iliyotiwa rangi na tarizi. Nyuzi tisa za lulu ya thamani kubwa zilikuwa zimening’inizwa kwenye upande wa kulia wa kiti hicho, na nyingine nyingi kwenye upande wa kushoto.” (Sakhi al-Islam, Juz. 1, uk. 100 -102). Makhalifa wa Bani Abbasi waliendelea kutumia kiasi kikubwa cha fedha kwa namna hii. Kila khalifa aliyefikia kwenye kiti hicho alijaribu kumzidi yule aliyemtangulia katika suala la ubadhilifu hadi zamu ya Muhtada ikafikia. Yeye alikuwa mtu mchamungu, lakini haku jaaliwa kuishi muda mrefu, kwani aliuawa na ndugu zake mwenyewe. Mawaziri pia hawakubakia nyuma katika suala la ubadhilifu. Waziri wa Mutawakkil, Fateh bin Khaqan alijenga majumba marefu kiasi kwamba minara yake ilionekana kama inagusa mbingu. Yule mshairi, Behtri anasema: “Minara hiyo ambayo ni mirefu kama mbingu inaonekana kama manyoya ya njiwa weupe wanaoruka angani.” Waziri Ibn Maqla alikuwa amekusanya wanyama wa porini na ndege wengi sana ndani ya jumba lake kiasi kwamba haiwezekani kwa hazina ya kiserikali kubeba gharama zake. Waziri Ibn Furat alimiliki maeneo makubwa ya ardhi na alikuwa na utajiri mkubwa. Alikula chakula chake kwa vijiko vya vuwele angavu. Alitumia kijiko kimoja kama hicho kwa tonge moja na hakukitumia tena. Zaidi ya vijiko thelathini viliwekwa kwenye meza yake ya chakula. Waziri Muhlabi alikuwa mpenda maua. Mtu mmoja ambaye alikuwa amemuona yeye anasema: “Waridi nyekundu zenye thamani ya dinari elfu moja zilinunuliwa kwa ajili ya Muhlabi katika siku tatu. Maua hayo hayo yalitawanywa kwenye ukumbi wake na katika bwawa lenye nafasi kubwa la kasiri lake. Chemchem za ajabu zilijengwa kwenye bwawa hilo. Maua hayo yalitupwa kwenye bwawa hilo, na chemchem hizo zikayasambaza katika ukumbi wa Muhlabi ambako yalidondokea kwenye vichwa vya wale waliokuwemo humo. Pale mkutano ulipokwisha, maua hayo yalitekwa nyara na watu hao.” Nguo nene ya hariri, inayoitwa Thiyab al-Na’al ilikuwa ikinunuliwa kwa ajili ya viatu vya mama yake khalifa Muqtadir. Nguo hiyo hiyo ilitumiwa kwa ajili ya sehemu ya juu na soli ya viatu hivyo, na ziliunganishwa kwa njia ya maski iliyoy212

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 212

9/4/2017 3:47:55 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

eyushwa, na ambari. Mama malikia huyo hakuvivaa viatu hivyo kwa zaidi ya siku kumi. Baada ya hapo watumishi walivichukua, wakabandua ile maski na ambari na wakazitumia. Mawaziri na watumishi wa ngazi za juu vile vile walijitahidi wasirudi nyuma ya khalifa katika suala la ufahari na utajiri. Ali bin Ahmad Razi, gavana wa Jundishapur, Sus, na Muzaria aliacha nyuma yake, baada ya kufa kwake, dhahabu, shaba, lulu, mawe ya thamani na vitu vingine ambavyo vilikuwa ghali kiasi kwamba kama vingegawanywa miongoni mwa watu masikini wote wangekuwa matajiri. Zaidi ya hayo, aliacha matowashi wengi sana na watumwa weupe na weusi ambao kama wangetumwa kwenye nchi katika nafasi ya jeshi wangeiteka nchi hiyo. Wingi wa utajiri uliomilikiwa na magavana wengine unaweza kukisiwa kutokana na hicho ambacho kimeelezwa hapo juu kuhusu utajiri wa Ali bin Ahmad Razi. Wafanya biashara matajiri pia waliishi maisha ya starehe. Maisha ya watu masikini yalitegemea juu ya mapenzi ya khalifa, wasimamizi wakuu wake na mawaziri. Walikuwa salama na bila hofu alimuradi wale watu waliokuwa kwenye uongozi wa mambo hawakukerwa nao. Ni kutoka wapi matajiri hawa walikopata utajiri wote huo? Ni jibu gani linaloweza kutolewa kwa swali hili isipokuwa kwamba walilimbikiza mali zote hizi kwa kuwanyonya watu wa chini, ambao walishushwa kufikia umasikini na kutojiweza? Mfumo wa kikatili kabisa ulitwaliwa katika kupata kodi za serikali na kukusanya utajiri. Khalifa na mawaziri wake na mawakala waliuza mapato yote ya ardhi kwa mtu mmoja. Mtu huyo alilipa milioni chache za dirham au dinari kwenye hazina ya serikali na kisha akapata pesa nyingi sana kutoka kwa watu kutokana na kodi kiasi kama alivyotaka mwenyewe. Huu ulikuwa kama ule mfumo ulioanzishwa na masultani wa Kituruki katika nchi za Kiislamu ambazo walizitawala wao. Idara ya Sheria, pia, ilikuwa shaghalabaghala. Wenye vyeo wa dola wakati wote waliingilia ufanyaji kazi wa mahakama na hakuna hakimu aliyethubutu kutoa hukumu kinyume na matakwa ya watawala hao. Rushwa ilikuwa imeenea sana. Ufukara wa watu ulikuwa ukiongezeka na matatizo na mateso yalikuwa yakizidi. Kwa kiasi kwamba kama mtu alikufa alistahili pongezi badala ya rambirambi.

213

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 213

9/4/2017 3:47:55 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Ibn Lunak wa Basrah anasema: “Tunashuhudia mabadiliko ya ajabu sana. Kama ingekuwa tuyaone kwenye ndoto yale tunayoyaona tukiwa macho, basi tungeamka katika hali ya huzuni kubwa.” Anamuomba Mwenyezi Mungu aweze kuwapa watu ule uvumilivu wa nabii Ayubu. Yeye mwenyewe analia kwa ajili yao kama Ayubu, na anasema: “Watu wanateseka sana kiasi kwamba kama mmoja wao atafariki anastahili kupongezwa.” Yeye anaongezea kusema: “Wallahi tumekamatwa katika makucha ya nyakati ngumu na onevu na tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu atujaalie na ustahamilivu wa Ayubu. Dunia imekosa uzuri wake. Hivyo lieni kama Yaakub.” Watu wenye hekima, wasomi na wale mashuhuri; ambao kuhusu wao, Ali alikuwa ametoa mapendekezo kwa wanawe Hasan na Husein (kwa ajili ya kuwaongoza watu) kwamba wawe wanashirikina nao, wasikilize maneno yao kwa makini na kutambua hadhi zao. Yeye pia aliwaelekeza magavana kuwataka ushauri na kuwaheshimu kwa vile wao ni mwanga miongoni mwa Waislamu na watadumu hivyo hadi ulimwengu utakapokwisha. Walikuwa katika hali ya kufanikiwa sana katika wakati wa Bani Abbasi, isipokuwa kwa wale ambao walikuwa wamejiuza wenyewe kwa watawala hao. Abu Hayyan ambaye alikuwa mwanachuoni mashuhuri na mtunzi wa vitabu vingi vya thamani anasema ndani ya kitabu chake kiitwacho Al-Amta’ wal-Mawanisah: “Nimelazimika kuuza dini yangu na huruma na kukimbilia kwenye unafiki na kufanya matendo ya aibu, ambayo hakuna mtu muungwana ambaye angependa kuyaandika.” Alifikia kiasi cha kuchoshwa sana na dunia katika siku za mwisho za uhai wake, na alisikitishwa sana na serikali ya wakati ule kiasi kwamba alivichoma vitabu vyake vyote. Abu Ali Qali alikuwa pia amelazimika kuuza vitabu vyake ambavyo vilikuwa ndio mtaji wake wa thamani kabisa. Yeye anasema: “Kwa miaka ishirini vitabu hivi ni chanzo cha kitulizo juu yangu na nilihuzunika sana wakati iliponibidi kuviuza. Nilikuwa sijafikiria kuviuza ingawaje ningeweza kuwa nimelazimika kubakia jela kwa mfululizo kwa sababu ya kuwa kwangu na madeni. Hata hivyo, kutokana na ufukara; na pamoja na mawazo ya kuwalisha wanangu wadogo, nililazimika kuviuza vitabu hivi.” Khatib Tabrizi alikuwa na nakala ya kitabu cha Azhar kiitwacho ‘Tahzib-alLughat’ ambacho kilikuwa katika juzuu nyingi. Alipenda kusikia maudhui zake ku214

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 214

9/4/2017 3:47:55 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

toka kwa mtaalamu na kuzichunguza. Watu walimshauri kumuona Abul-‘Ala Muarri. Alikiweka kitabu hicho kwenye gunia na akaenda Muarratul-Nu’man kwa kutembea kwa miguu akiwa amebeba gunia hilo mgongoni mwake kwa vile alikuwa hana pesa ya kutosha chombo cha uchukuzi. Wakati wa safari hiyo alitokwa sana na jasho kiasi kwamba juzuu zote za kitabu hicho ziliharibika. Akilalamika dhidi ya shida yeye anasema: “Wengine wanaweza wakachoka kusafiri lakini mimi nimechoka kusimama. Huko Iraqi ilinibidi kuishi miongoni mwa watu ambao ni duni na ni vizazi vya watu duni.” Akilalamika dhidi ya maamuzi yasiyoridhisha ya wakati na maonevu yake kwa watu wenye mawazo ya kiungwana, Ibn Lunak wa Basrah anasema: “Ewe wakati! Umewafanya watu waungwana kuvaa vazi la fedheha na ufukara. Sikuchukulii wewe kuwa ‘wakati.’ Wewe ni fadhaisho. Ni vipi mtu yeyote atategemea jambo lolote jema kutoka kwako hali ya kuwa wewe unachukulia uwezo na ukamilifu kuwa ni aibu. Ni uhalisi gani wa hali yako kama tunavyoiona? Je, ni wazimu, ukosa haya au ufidhuli?” Wakati wa kipindi chote cha utawala wa Bani Abbasi,45 watu walikuwa wamegawanyika kwenye makundi mawili. Moja kati yao lilikuwa ni lile la watu matajiri na jingine la watu masikini. Makundi yote yaliteseka kutokana na maovu mengi ya kimaadili kulingana na mazingira yao husika. Ushukaji wa maadili ulikuwepo kwa kiasi kile kile katika siku za mwisho za utawala wao kama mwanzoni. Bali ulikuwa katika kiwango cha hali ya juu mno. Matajiri waliendesha maisha ya starehe na anasa na wakajitumbukiza kwenye ufisadi usio na mipaka. Na kuhusu wale masikini, uhasama, husuda, upotofu na udanganyifu vilitapakaa miongoni mwao. Kutokana na ufukara watu walikimbilia sana kwenye kujinyima raha na kwenye usufii. Haukuwa hata hivyo, ule usufii ambao unaanzia kwenye maadili mema na kwenye kuichukulia dunia kama ni ya mpito. Ulikuwa ni usufii ambao ni matokeo ya kutojiweza, kushindwa na kukata tamaa. Kutokana na ufukara tabia nyingine mbaya nyingi kama kupenda uchawi, kiinimacho (mazingaombwe) na ushirikina vilianza ndani mwa watu. Hii ilikuwa ni 45

ila shaka, makhalifa wengi wa Bani Abbasi waliendesha maisha ya anasa na starehe, na walikuwa na sifa B mbaya, kwa sababu ya kuwaonea raia zao. Hata hivyo, walikuwepo wachache miongoni mwao ambao walikuwa waadilifu. Baadhi yao waliendeleza fasihi na viwanda, na walifanya kazi kwa ustawi wa jamii kwa namna nyingi. Walijenga sehemu nyingi za kuangalilia mambo ya angani (jua, mwezi na nyota) ambazo namna yake ilikuwa haijulikani kwa Warumi na Wagiriki. Walianzisha vile vile mahosipitali makubwa na kufundisha madaktari na wanachuoni. Mambo yote haya, yamenakiliwa katika kurasa za historia. 215

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 215

9/4/2017 3:47:55 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

kwa sababu mtu anaposhindwa kujipatia maisha yake kwa njia ya halali anakimbilia kwenye njia mbaya. Serikali zile ambazo zilianzishwa baada ya kuanguka kwa ufalme wa Bani Abbasi zilikuwa na tofauti nyingi za kitabaka na uvunjaji wao wa maadili ulikuwa mbaya zaidi. Kuanzia wakati ule mkono wa yule dhalimu (Ibn Muljam) uliponyooshwa kumwelekea Imam Ali ibn Abi Talib; na yule tegemeo na mlinzi wa haki za binadamu akauawa, mabalaa haya yakawa ndio majaaliwa ya Waarabu, na yakawafika mfululizo katika miundo mipya. Kwa ufupi watu wa Mashariki walipatwa na mateso na matatizo haya kwa hali ya kudumu daima. Koo (Familia) Mbili Za Quraishi Mtume alikwisha kusema kwa usahihi kabisa: “Wafuasi wangu watakutana na maangamizi mikononi mwa vijana wa Quraishi.” Vijana hawa waliotajwa na Mtume; ambao walikuwa waje kusababisha matatizo na kula njama, walizaliwa mahali ambapo palikuwa kama chimbuko kwa ajili ya watu wasio na haya kama Yazid bin Mu’awiyah. Mtume aliweza kuona kwamba kundi hili lilikuwa linapigana vita kwa wakati mmoja ili kulinda utawala na mamlaka yao ya jadi na, ukiwa unajisalimisha na kujionyesha kama Waislamu katika wakati mwingine, ili kupata utawala na mamlaka. Wakati alipotazama sehemu mbalimbali na akawaona watu hawa, yeye alisema kwa huzuni sana na wasi wasi: “Wafuasi wangu watakutana na maangamizi mikononi mwa vijana wa Quraishi.” Wasomaji wanaombwa kuweka mbele ya macho yao ile historia ya Quraishi, ambayo nitaisimulia, ili ipate kuwezekana kuwabainisha kila mmoja wao. Uadui baina ya Bani Umayyah na Bani Hashim ulikuwa mkongwe, ni wa tangu zamani sana. Walipingana na kila mmoja wao, kabla ya mapambano kwa ajili ya utawala na mamlaka hayajazuka baina yao, na hata kabla Uislamu haujapata nguvu kubwa. Uadui na kila mmoja wao ulisimama juu ya sababu nyingi. Kwa kweli sababu kubwa zote, za ndani na nje kwa ajili ya upinzani zilikuwa zimeungana. Miongoni mwao ziliingia moyo wa umoja wa kikabila, hisia za kujifanya bora, kinyongo kikongwe, kupenda kisasi cha mauaji ya ndugu, mawazo ya kisiasa, hisia za binafsi,

216

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 216

9/4/2017 3:47:55 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

tofauti katika njia za maisha na namna ya fikra na kadhalika. Bani Umayyah na Bani Hashim walikuwa ndio wakuu wa Makkah na walishikilia nafasi za juu hata wakati wa zama za jahilia. Hata hivyo, ukuu wa Bani Hashim ulikuwa wa kiroho,46ambapo ule ulioshikiliwa na Bani Umayyah ulikuwa wa kisiasa na walikuwa pia ni wachuuzi na walimiliki utajiri mkubwa. Wanahistoria wote wa Kiislamu na Mustashirki wa Ulaya wanakubaliana kwamba kabla ya kuja kwa Uislamu, Bani Hashim walikuwa hawakuzoea hila na udanganyifu kama wale makasisi wa uabudu masanamu. Wao hawakuwadanganya wale watu wenye akili za kawaida kwa kisingizio cha uongozi wao wa kidini na kiroho. Wao hawakuwanyonya wengine wala kutanguliza maslahi yao binafsi. Walikuwa na imani juu ya Mola wa Ka’aba na waliamini kwa unyofu katika kile ambacho kimehalalishwa au kuharamishwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kwa mujibu wa kanuni yao, kuwasaidia wanaokandamizwa, kuwahurumia wasiojiweza, kutokomeza udhalimu, na kutimiza mahitaji ya mafukarai kwao ilikuwa ni wajibu wa lazima. Walikuwa na moyo safi katika imani yao. Hawakumdanganya mtu yeyote na hawakuuona unafiki kama wenye kuruhusiwa. Kwa mfano, ilikuwa inawezekana kwamba Abdul Muttalib, babu yake Mtume na Ali angemchinja mmojawapo wa wanawe katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa sababu alikuwa na imani thabiti juu ya Mola wake na alikuwa ameweka nadhiri kwamba endapo wanawe kumi wangeishi, yeye angemchinja mmoja wao kwa ajili ya Mwenyezi Mungu katika kizingiti cha Ka’aba. Hakuridhika kuhusu kutimia kwa nadhiri yake mpaka alipokuwa amethibisha kwa kuzingatia imani yake kwamba kumuua mwanawe kusingekuwa ni njia ya kumridhisha Mwenyezi Mungu. 46

Shamsul-Ulama Shibli Nu’mani anaandika hivi katika juzuu ya kumi na mbili ya kitabu chake kiitwacho Siirat al-Nabi: “Alikuwa ameweka nadhiri kwamba kama atawaona wanawe wa kiume kumi wote wakiwa wamekua watu wazima atamchinja mmoja wao katika njia ya Mwenyezi Mungu. Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu akamjaalia matakwa yake haya. Halafu ndipo akawaleta wanawe wote ndani ya Ka’aba na akamuomba muongoza ibada kupiga kura. Ilitokea kwamba kura ilimuangukia Abdullah. Ndipo yeye akaenda pamoja na Abdullah kwenye sehemu ya kutolea kafara. ada zake Abdullah ambao walikuwepo pale wakaanza kulia na kupendekeza kwamba ngamia kumi waweze D kuchinjwa badala ya Abdullah. bdul Muttalib akamuomba mfanya ibada huyo kupiga kura na kuona kama kura itamuangukia Abdullah A au juu ya ngamia hao. Kwa bahati kura ikamuangukia Abdullah. Abdul Muttalib akaongeza idadi ya ngamia hadi ishirini lakini kura ikamuangukia Abdullah. Aliendelea kuongeza idadi ya ngamia na kura ikawadondokea ngamia pale tu idadi yao ilipofikia mia moja. Abdul Muttalib ndipo akawachinja wale ngamia mia moja na maisha ya Abdullah yakaokolewa. Wanahistoria wanasema kwamba Abdul Muttalib hakuridhika hata pale kura ilipowaangukia wale ngamia, yeye alisema: “Ninaapa kwa jina la Allah kwamba sitakubaliana na (kuchinjwa kwa ngamia mia moja badala ya Abdullah) isipokuwa labda kura zipigwe mara tatu, na kila mara ziangukie juu ya ngamia hao.” Hili lilifanyika na Abdul Muttalib aliridhika tu pale kura zilipowaangukia wale ngamia mara tatu zote. 217

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 217

9/4/2017 3:47:55 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Imani yake ilikuwa madhubuti sana na alikuwa ni mwenye bidii sana ya kuwasaidia masikini na wenye haja, kiasi kwamba alifikia mkataba na baadhi ya familia za Quraishi kufanikisha lengo hili. (Bani Umayyah hawakuwa washiriki katika kuweka saini mkataba huu). Moja ya masharti maalum ya mkataba huu lilikuwa kwamba wao watakuwa upande mmoja na mtu mwenye kudhulumiwa na kumfanya dhalimu kurudisha haki yake hiyo, kusaidiana katika masuala ya kifedha na kuwazuia watu wenye nguvu kutokana na kuwaudhi wanyonge. Tukio ambalo lilisababisha kufikiwa kwa mkataba huu lilikuwa kama ifuatavyo:Quraishi mmoja alinunua vitu fulani kutoka kwa mtu anayetokea sehemu nyingine, na akaahidi kulipa kiasi cha bei hiyo baada ya muda uliopangwa. Hata hivyo, hakufanya malipo katika ile tarehe iliyostahili. Alikuwa akijiamini kwamba kutokana na hadhi ya familia yake, na nguzo ya ndugu zake, hakuna atakayemlazimisha yeye kufanya malipo hayo. Zaidi ya hayo, yule mtu ambaye kutoka kwake alinunua vitu hivyo alikuwa si mtu wa Makkah na alitokana na familia ya kawaida tu, na hakuwa anaungwa mkono na mtu yeyote. Hata hivyo, Bani Hashim wakaamua kumsaidia. Walifanya mkataba wa pamoja ambamo waliamua kuipata ile gharama ya vile vitu vilivyonunuliwa na Quraishi huyo na kutekeleza haki. Hata hivyo, kwa vile mkataba huu haukuendana na tabia ya Bani Umayyah, wao waliupinga kwa nguvu zote. Ule uongozi wa kidini na wa kiroho uliorithiwa na Bani Hashim kutoka kwa wahenga wao; kizazi baada ya kizazi, uliendana na tabia zao. Walikuwa wamerithi moyo mzuri na uungwana kutoka kwa wahenga wao. Kila kizazi chao kilionyesha yale maadili kiliyoyarithi, na Bani Hashim waliendelea kudumisha hadhi na ubora hadi Mwenyezi Mungu alipomteua Muhammad kwenye kazi ya Utume na pia akamuumba Ali mwana wa Abu Talib kama wawakilishi wa uadilifu na ukamilifu wa ukoo wa Bani Hashim. Hebu iangalie historia ya Bani Hashim baada ya kufa kwa Mtume (yaani kizazi cha Abu Talib), na utaona kwamba, kama historia hiyo inajumlisha miaka mia moja au miaka mia mbili au miaka mia tano, wamekuwa siku zote ni kielelezo cha sifa tukufu na maadili. Ule ujanadume, ujasiri uchamungu na ukweli ambao walikuwa nao mababu zao; unaweza pia kuonekana kwa watoto na wajukuu zao. Historia iliendelea kukunjua majani yake, lakini yeyote aliyekuja kutoka miongoni mwao alikuwa ni kielelezo cha mababu zake.

218

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 218

9/4/2017 3:47:55 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Kama ukoo huu usingekuwa wa kiuchamungu na kisharifu kwa asili; usingeweza kuwa kielelezo cha uchamungu na usafi kwa sababu katika nyakati zile majisifu, ubinafsi, majivuno na tamaa ya makuu vilikuwa vimeenea, kiasi kwamba wote walikuwa wameshuka kimaadili, na maovu haya yalikuwa ni ya kawaida kabisa miongoni mwao. Ni rahisi kuanguka kwenye lindi kuu ukilinganisha na kupanda au kubaki imara kwenye nafasi yake mtu. Hata hivyo, licha ya ukweli kwamba hali ya hewa ya mambo ilikuwa mbaya na ufisadi ulikuwa kila mahali, Bani Hashim hawakuathiriwa na mambo haya, na sifa zao tukufu na maadili yalibaki kamili na salama. Hata hivyo, Bani Umayyah walikuwa kinyume kabisa na hali hii. Katika zama za ujahilia wao walikuwa ni wachuuzi na wanasiasa; na ni dhahiri kwamba yeyote yule anayeshughulika na uchuuzi na siasa anakuwa ana mali na mamlaka, na anajitahidi kuendelea kumiliki vitu hivi na kuvifanya vibakie kwenye ukoo wake. Hakuna mtu yoyote mwenye akili anayeweza kuukataa ukweli kwamba wakati mtu anapojishughulisha na biashara; na jamaa zake wa karibu nao wakawa pia ni wafanya biashara, anaweza kufanya lolote lile ambalo litatumikia maslahi yake. Anaweza angalau akawaghilibu wateja wake, akahodhi mali, akajiingiza kwenye udanganyifu, na akafanya ajizi kwenye utendaji wa shughuli zake. Bani Umayyah walijichagulia wenyewe mambo haya kwa vile yanaendana na desturi na tabia zao. Ilikuwa ni kama vile tu ambavyo Bani Hashim walivyojichagulia utakaso wa tabia, uaminifu na usafi juu yao, kwani viliendana na tabia na silika zao. Bani Umayyah walikuwa wamezoea matendo haya ya kuchukiza kwa sababu yalikuwa yamejiingiza kwenye mienendo yao kwa muda mrefu na yamekuwa ndio tabia yao. Wao hawakuwasaidia wale wanaokandamizwa kwa sababu hili halikuwapatia faida yoyote, na kwa kweli lilihitaji gharama kubwa. Wao hawakujiunga na ule mkataba uliosemwa (ambao unahukumu madhalimu) kwa sababu hili lingemaanisha kujihusisha wenyewe kwenye matatizo. Umayyah, huyo mhenga wa Bani Umayyah alikuwa sio mtu mwenye mawazo ya kiungwana na msafi kama Hashim; hivyo hakuweza kujizuia kuacha kuwakera wanawake waungwana. Wakati ulipotokea mgogoro kati ya Abdul Muttalib, babu yake Ali na Harith mtoto wa Umayyah, babu yake Mu’awiyah, walilipeleka suala hilo kwa Nafiil bin Adi. Nafiil aliamua jambo hilo kwa faida ya Abdul Muttalib na akamsifia. Akizungumza na Harith alisoma pia ushairi ambao ndani yake alileta picha kamili ya Umayyah na Hashim. Shairi hilo ni kama ifuatavyo: 219

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 219

9/4/2017 3:47:55 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

“Baba yako alikuwa mzinzi na baba yake alikuwa safi. Yeye (Abdul Muttalib) alililazimisha jeshi la Abraha kuondoka Makkah.” Katika ushairi huu Nafiil alirejea kwenye kadhia ya Abraha, ambaye alipanda juu ya tembo na akifuatana na jeshi kubwa, alikuja kutaka kuivunja Ka’aba. Yeye pia aliyashutumu maovu ya Umayyah, baba yake Harb na mhenga wa Bani Umayyah, ambaye alijipatia jina na heshima mbaya katika suala la wanawake. Wakati mmoja, kutokana na mwenendo wake muovu, aliponyoka kifo. Aliihalifu staha ya mwanamke atokanaye na kabila la Zohra. Watu wa kabila hilo wakamshambulia kwa panga zao, lakini majeraha aliyoyapata hayakuwa na athari mbaya sana. Hadithi nyingi za kushangaza zimesimuliwa kuhusu ashiki yake. Wakati Muhammad, yule mtoto maarufu wa familia ya Bani Hashim alipoteuliwa kwenye wadhifa wa utume alikutana na upinzani kutoka kwa watu wengi. Hata hivyo, wa mbele kabisa miongoni mwa maadui zake alikuwa Abu Sufyan, ambaye kwa wakati ule alikuwa ndiye mkuu wa ukoo wa Bani Umayyah. Yeye aliwachochea washirikina wote dhidi yake. Yeye alikuwa ndio mtu muhimu katika njama zote na uhamasishaji wa majeshi dhidi ya Mtume. Alikuwa ni yeye ambaye alivumbua njia nyingi za mateso kwa ajili ya Mtume na masahaba na wafuasi wake. Kama upinzani wa Abu Sufyan kwa Mtume ungekuwa ni kwa sababu za imani za kidini; na kama angefanya yale yote ambayo angeweza kufanya ili kutetea kanuni na imani zake za zamani, pangeweza kuwa na uhalali kidogo kwa ajili hilo, kwa sababu wakati mtu anaamini kikweli kweli juu ya jambo, imma liwe sahihi au la makosa, anayo haki katika kuitetea imani yake. Hata hivyo, suala halikuwa hivyo kwa Abu Sufyan. Kamwe hakujiona yeye mwenyewe kuwa na uhalali wa kumpinga Mtume wala hakuwahi kutoa madai kama hayo kwa ulimi wake. Upinzani wake kwa Mtume haukuwa kwa sababu ya mawazo yoyote ya kidini. Alichokuwa anakitaka hasa ni kwamba ile nguvu na mamlaka ya Bani Umayyah juu ya wengine isije ikaathiriwa – nguvu na mamlaka yale yale ambayo yalikaa juu ya msingi wa kufanya ukiritimba kwenye biashara, ulanguzi, maslahi binafsi na kuwatumikisha wanyonge. Aliamua kumpinga Mtume wakati alipoona kwamba nguvu na mamlaka ya ukoo wake ambayo tayari yalikuwa yamekwisha dhoofishwa na kuyumba yalikuwa yaangamizwe na Mtume. Kwa sababu ya tabia yake ya ulanguzi, ambayo itakuwa sahihi kuiita ni desturi ya Bani Umayyah, Abu Sufyan hakuuamini Uislamu kwa unyofu hata baada ya kusilimu. 220

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 220

9/4/2017 3:47:55 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Yeye wakati wote aliupima katika mizani ya utajiri na mamlaka, na akadhani kwamba Uislamu si chochote isipokuwa kwamba mamlaka yamehamishwa kutoka kwa Bani Umayyah kwenda kwa Bani Hashim. Hakuweza kuufurahia ule mwenendo wa Mtume na masahaba zake na makafara waliyoyafanya wao, na hakuwahi kamwe kufikiri juu ya thamani ya mwanadamu ambayo kwa ajili ya kuinyanyua kwake ndiyo Mtume amekuja duniani. Pale wakati wa kutekwa kwa Makkah alipoona jeshi kubwa lenye watiifu wa Mtume, yeye alimwambia Abbas, ammi yake Mtume: “Ewe Abul Fazal! Mpwa wako amepata ufalme mkubwa sana.” Aliyatamka maneno haya kwa sababu hakuweza hata kufikiria yale malengo adhimu na mafunzo ya kiroho ambayo kwayo ndio Mtume ameyajia. Yalikuwa ni malengo hayo adhimu na mafunzo ya kiroho ambayo Bani Hashim walikuwa wameyaelewa vizuri sana na katika kuyalingania hayo, wao waliyatoa hata maisha yao muhanga. Baada ya ushindi wa Makkah familia ya Abu Sufyan iliukubali Uislamu lakini kilikuwa ni kidonge kichungu sana kwao kukimeza. Machoni kwa Abu Sufyan na mke wake Hind, Uislamu ulikuwa na maana ya kuumbuka kwao binafsi. Kwa muda mrefu baada ya kuukubali Uislamu; Abu Sufyan aliendelea kuiona athari ya dini hii kama kushindwa kwake yeye binafsi. Hakuyachukulia mafanikio ya Uislamu kuwa ni matokeo ya kuwa kwake ni dini ya kweli. Alidhani kwamba ilikuwa ni kwa sababu ya udhaifu wa watu wake mwenyewe. Siku moja alimtazama Mtume ndani ya msikiti kama mtu aliyekanganyikiwa na akajisemea mwenyewe moyoni: “Lo, laiti ningeweza kujua ni kwa sababu gani Muhammad amepata ushindi dhidi yangu mimi.” Mtume aliutambua utazamaji wa Abu Sufyan. Alimgusa bega lake kwa kitanga cha mkono wake na akasema: “Oh, Abu Sufyan! Ilikuwa ni kwa sababu ya Mwenyezi Mungu kwamba nimepata ushindi dhidi yako.” Mtume alijaribu kumliwaza Abu Sufyan kabla, na vilevile hata baada ya kutekwa kwa Makkah. Kabla ya kuiteka Makkah alimuoa binti yake Umm Habibah, na baada ya kutekwa kwa Makkah aliitangaza nyumba yake kuwa sehemu ya kimbilio, ama hifadhi, kwa kusema kwamba yeyote atakayeingia nyumba yake hatabughudhiwa. Mtume aliliweka jina lake juu kabisa katika orodha ya wale ‘Muallifatul-Qulub’, (wale watu waliopewa fungu kubwa la ngawira ya kivita kulinganishwa na Waislamu wengine, ili wapate kuliwazika, na ile chuki waliyokuwa nayo nyoyoni mwao kwa ajili ya Uislamu iweze kutoweka) na akampa tahafifu nyingi. 221

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 221

9/4/2017 3:47:55 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Licha ya yote haya, Waislamu hawakumtegemea na kumuamini yeye. Walikuwa waangalifu katika kushughulika naye na walijizuia kushirikiana naye. Abu Sufyan alikuwa na wasiwasi juu ya hili na akatamani kwamba Waislamu wangekuwa na sehemu ya upole nyoyoni mwao kwa ajili yake na familia yake. Kwa hiyo alimuomba Mtume kumteua Mu’awiyah kama mwandishi wake. Wakati Mtume alipofariki na tofauti zikazuka kuhusu ukhalifa kati ya Muhajiriina na Ansari, na baadaye kati ya Muhajir wenyewe kwa wenyewe, Abu Sufyan aliiona ni fursa nzuri ya kutumia tofauti hizi na kujitwalia ukuu wa Quraishi yeye mwenyewe. Alifikiri kwamba baada ya mafanikio haya haitakuwa vigumu kwake yeye kuwa mkuu wa umma wote wa Kiislamu. Yeye kwa hiyo, alimwendea Abbas na Ali akiwachochea wao kumpinga khalifa kwa kuwahakikishia kuwaunga mkono wao. Yeye alisema: “Ewe Ali! Ewe Abbas! Ni vipi ukhalifa umechukuliwa na ukoo (yaani ukoo wa Abu Bakr) ambao ni duni sana na pia mdogo kwa idadi ya watu wake? Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba kama nikitaka ninaweza kujaza mitaa ya Madina kwa askari wa farasi na wa miguu.” Abu Sufyan alikuwa hakutambua kwamba anazungumza na yule Ali ambaye hatasita kuitoa dunia yote ili kutekeleza amri moja halali, na ambaye alikuwa sio mwenye kutotambua ule ukweli kwamba yeye (Abu Sufyan) kuchukia kwake hakukuwa kwa sababu ya Bani Hashim kunyimwa ukhalifa, kwa sababu kama ungebakia kwa Bani Hashim yeye angekasirika zaidi ya hapo, na angeweza kuufanya ukoo wake, kabila lake, na dunia yote kuwa dhidi yao Bani Hashim. Ali alimshutumu Abu Sufyan na kumwambia: “Ewe Abu Sufyan! Waumini ni wale ambao wanatakiana kheri wao kwa wao; na kuhusu wanafiki wao ni walaghai na wadanganyifu, ingawa nyumba zao zimekutanishwa na miili yao imeunganishwa.” Abu Sufyan alitokana na tabaka la kikabaila – tabaka ambalo linajiona lenyewe kuwa ni bora kuliko wengine, na kuwaona watu wa kawaida kama watumwa wao. Aliuangalia Uislamu kutoka kwenye msimamo huu. Kwa mujibu wake yeye, ule mwaliko wa Mtume kwenye Uislamu ulikuwa ni njia tu ya kufikia kwenye mamlaka na madaraka. Kwa mujibu wake yeye, hapakuwa na tofauti kati ya kanuni na misingi ya Uislamu na masanamu, na kwamba vyote vilikuwa ni chanzo cha faida. Alizichukulia kanuni za Uislamu kama chanzo cha mapato kwa ajili ya waanzilishi wa dini ile, kwa namna ile ile ambayo masanamu yalikuwa ni chanzo cha 222

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 222

9/4/2017 3:47:56 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

mapato kwa ajili ya makuhani wa waabudu masanamu. Hakuweza kufikiria kwa njia nyingine isipokuwa kwamba watu walikuwa wawatii wazee na wakuu wao – imma wawe wale makuhani wa Ka’aba au wale watu mashuhuri wa Uislamu. Kwa mujibu wa Abu Sufyan, tofauti pekee iliyopo kati ya Uislamu na uabudu masanamu ni kwamba Uislamu ulikuwa una faida zaidi na kwamba ndani yake kulikuwepo na uwezekano mkubwa wa watu wa tabaka la chini kunyenyekea kwa lile tabaka la waungwana na makabaila. Endapo hata hivyo, hao watu wa tabaka la chini hawakuwa wanyenyekevu kwa hao makabaila katika Uislamu, mfumo huu, kwa mujibu wake yeye, ulikuwa hauna thamani na ulistahili kubadilishwa na mmoja ambao wenye maana na faida zaidi. Pale baada ya Abu Bakr na Umar ukhalifa ulipotwaliwa na Uthman ambaye alikuwa ni Bani Umayyah, Abu Sufyan alidhania kwamba yale madaraka na mamlaka yaliyokuwa hapo awali mikononi mwa Bani Umayyah yamerudi tena kwao. Kile kinyongo na chuki ya muda mrefu aliyokuwa nayo moyoni mwake juu ya Hamzah ilimfanya aende kwenye kaburi lake. Alilipiga mateke kaburi la Hamzah kwa mguu wake na akasema: “Oh, Hamzah! Nyanyuka na uone kwamba ule utawala ambao tulikuwa tukiupigania pamoja umerudi kwa mara nyingine kwenye ukoo wetu.” Ule uchungu na uadui ambao maneno haya yamebeba unajionyesha dhahiri. Hivi ndivyo alivyozionyesha hisia za moyoni mwake. Kwa kiasi ukhalifa ulivyokuwa kwa Abu Bakr na Umar, Bani Umayyah hawakuweza kuonyesha kile walichokuwa wamekificha nyoyoni mwao, na ule mpango ambao kulingana nao huo walikuwa wamejipendekeza katika kusilimu, ndio kusema kwamba, mara tu walipoipata fursa wangeweza kuibadili hiyo serikali ya Kiislamu kuwa ufalme. Waliipata fursa hii wakati Uthman alipoufikia ukhalifa. Hakuna anayeweza kuamini kwamba Bani Umayyah walikuwa wanatambua ile dhana halisi ya ukhalifa. Kwa mujibu wa maoni yao wao; hapakuwa na tofauti kati ukhalifa na ufalme, na hawakuweza kupata taswira vichwani mwao; ya zile nukta nzuri za ukhalifa wa Kiislamu. Imani yao katika Uislamu ilikuwa ya juu juu kabisa, na walikuwa wameukubali kwa kusitasita, kwa shingo upande tu. Moyo wao wa ushabiki wa zama za ujahilia uliwachochea kuzitwaa tena zile njia na desturi za zama hizo. Hawakuweza kusahau kwamba Mtume hakutokana na ukoo wao bali alikuwa mtu wa Bani Hashim, na wao wakati wote walikuwa ni maadui wa ukoo huo. Wao kwa hiyo, walikuwa wakiitafuta fursa ya kuunyakua utawala.

223

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 223

9/4/2017 3:47:56 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Ukhalifa wa Uthman ulifungua njia kwa ajili ya kutimiza matakwa yao. Mara tu alipokuwa khalifa, Bani Umayyah wote walikusanyika karibu yake na kumtenga na umma wote. Kwa hiyo hakuna aliyeweza kumuona na kumfahamisha matatizo yake. Serikali ya Kiislamu sasa ikawa ni serikali ya Bani Umayyah. Ni Bani Umayyah peke yao walioweza kunufaika nayo. Walikuwa ni Bani Umayyah na marafiki zao tu walioweza kugombea kuwa magavana na kushika zile nafasi muhimu. Marwan bin Hakam alikuwa mkuu wao. Yeye alikuwa ndiye mtu wa kwanza ambaye aliwachochea Waislamu dhidi ya Waislamu, na kuwashawishi watu kuasi dhidi ya khalifa. Alikuwa ndiye mtu wa kwanza ambaye alitamka kwamba ufalme ulikuwa ni bora kuliko ukhalifa, na kwamba ni Bani Umayyah tu waliokuwa na haki ya kuwa wafalme. Alimlazimisha Uthman kuwafukuza wale magavana ambao walikuwa wamezishikilia nafasi hizo tangu zama za Abu Bakr na Umar na kuwabadilisha na Bani Umayyah. Utajiri na mamlaka vikawa ni mali pekee ya Bani Umayyah. Hakuna mwingine tena aliyeweza kutumainia kunufaika kutokana nayo au kushika mali na madaraka. Tutakuja kutaja katika sura inayofuata jinsi Marwan alivyokuwa mkatili na mwenye tabia mbaya, mienendo mibaya aliyofanya wakati alipokuwa kwenye madaraka, na ni watu wangapi wasiokuwa na hatia ambao aliwaua kwa kuridhisha matakwa yake. Alikuwa ni Marwan bin Hakam huyo huyo ambaye alikuwa amependekeza kwa gavana wa Madina kumuua Imam Husein; na alimkemea yeye kwa kule kutokukubaliana na matakwa yake wakati aliposhindwa kuchukua hatua hiyo mbaya sana. Marwan alitamani sana madaraka, utawala na starehe, kama vile wahenga wa jadi yake walivyovitamani hivyo wakati wa ujahilia, na alikuwa amejizatiti kwamba hata kama hatakuwa na mamlaka yeye mwenyewe binafsi, yaweze kubakia na Bani Umayyah mwingine yoyote, lakini yasitoke nje ya ukoo wao. Mbinu ambazo alizitumia kupata mamlaka na utawala zinaonyesha kwamba yeye hakuwa na hata sifa moja ambayo ingeweza kujenga mapenzi japo kidogo kwa ajili yake katika mioyo ya watu. Mu’awiyah Na Warithi Wake Mu’awiyah ibn Abu Sufyan alikuwa ni kielelezo halisi cha sifa na tabia za Bani Umayyah. Tunapozichunguza tabia za Mu’awiyah kwa makini tunakuja kujua 224

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 224

9/4/2017 3:47:56 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

kwamba hakuwa na angalau hata chembe ya maadili ya kibinadamu ya Kiislamu; na hakuwa na sifa yoyote ile ya wale Waislamu wa zile zama nadhifu na safi. Kama tukiuchukulia Uislamu kama upinzani dhidi ya njia na desturi za Waarabu wa zama za jahilia (kwa mfano kushughulika na maslahi binafsi mawazoni na kuwafanya watu wa chini kama wanyama na chanzo cha mapato kwa ajili ya waungwana na makabaila) inaweza kusemekana kwa uhakika, kama tutakavyoeleza baadae, kwamba Mu’awiyah alikuwa hana lolote la kuhusiana na Uislamu. Na badala yake kama Uislamu ni jina la dini ambayo maagizo yake yanatumika kwa kila mtu, ni dhahiri kabisa kwamba hakuwa pia na uhusiano wowote na Uislamu wa namna hii. Hili lilikiriwa na Mu’awiyah mwenyewe. Alikuwa akitumia kuvaa nguo za hariri na kula chakula chake katika vyombo vya dhahabu na fedha. Abu Darda, sahaba wa Mtume alipinga jambo hili na akasema: “Nimemsikia Mtume akisema kwamba Moto wa Jahannam utakuja kumiminwa kwenye tumbo la mtu ambaye anakula milo yake kwenye vyombo vya dhahabu na fedha.” Mu’awiyah hata hivyo alijibu bila ya kujali kwamba: “Mimi silioni hilo kama ni lenye kuchukiza.” Tunapoona kwamba Waislamu wa mwanzoni walikuwa makini sana katika masuala ya dini, walitoa heshima zinazostahili kwa kila kile kilichoagizwa au kukatazwa na Mtume, na walitoa muhanga hata maisha yao kwa ajili ya dini yao, na kisha tutupie macho hili jibu la kifidhuli ambalo Mu’awiyah alimjibu Abu Darda katika kumuasi dhahiri Mtume, tunaridhika kwamba Mu’awiyah kamwe hakuwa amejiunga na lile kundi la wale Waislamu ambao waliamini kikamilifu katika mafunzo ya maadili na kiroho ya Kiislamu. Tabia ya Mu’awiyah baada ya kuukubali Uislamu ilikuwa inafanana na ile ya baba yake Abu Sufyan wakati wa jahilia, yaani, ile ya kabaila ambaye aliwatumikisha watu kazi kwa nguvu na kuwafanya kama watumwa. Alikuja kuwa Muislamu kwa shingo upande na alibakia kuwa Muislamu kwa shingo upande vivyo hivyo. Ni nani anayeweza kutambua vizuri zaidi akili ya Mu’awiyah na ustahili wa imani yake katika Uislamu kuliko watu wa wakati wake ambao wamemuona kwa macho yao wenyewe. Je, hao watu wa wakati wake hawakumshutumu yeye kwa mambo ambayo tutayaelezea baadae? Hivi Ali hakumjua zaidi kuliko mtu mwingine yeyote na je, hakueleza picha yake halisi pale aliposema katika barua yake: “Wewe unawaigiza mababu zako katika kutoa madai ya uwongo, kuwadanganya watu, kudai kuwa na nafasi kubwa kuliko ile uliyonayo na kunyakua vitu ambavyo vimeharamishwa?”

225

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 225

9/4/2017 3:47:56 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Je, alikuwepo hata mtu mmoja miongoni mwa Waislamu wa siku za Mtume au za makhalifa wa halisi ambaye alikuwa mlaghai au mwongo na akawa anaitwa Muislamu? Je, alikuwapo Muislamu katika kipindi kile halisi cha Waislamu ambaye kuhusu yeye Ali alisema: “Wale watu wote wa familia yako walioukubali Uislamu wameukubali kwa shingo upande.” Kuhusu baadhi ya sifa za Mu’awiyah kama vile uvumilivu, ulaini na ukarimu, inaweza kusemwa kwamba zote zilikuwa ni njia ya kufanikisha malengo yake maovu. Alikuwa ametambua kutokana na akili yake kwamba ili kufanikisha malengo yake na kuupata ufalme, mambo haya yatakuwa na maana sana kwake. Nafikiri Mu’awiyah alikuwa ameelewa vizuri sana kwamba watu hawakupenda zile sifa na tabia za mababu zake na zile za Bani Umayyah za wakati wake mwenyewe, na yale madaraka na mamlaka, ambayo wakati mmoja wahenga wake waliyashika, yamekoma kuwa na thamani tena. Alijitahidi kuwaghilibu watu kwa kujifanya kuonyesha uvumilivu na ukarimu ili kwamba watu wasiweze kujua ukweli wa mambo na wapate kupendezwa na uvumilivu na ukarimu wake, kwa sababu kama ukarimu wa kutosha na uungwana wa kuzaliwa vingechukuliwa kama kigezo cha utawala, Bani Umayyah wasingeweza kabisa kushindana na Bani Hashim. Je, alionyesha uvumilivu ili kupata kuungwa mkono na watu, na kwa hiyo, kupata madaraka na kile ambacho kingeweza kuwa mpango unaofaa kuweza kuwapata watu na kuficha maovu ya ukoo wake kuliko kuwapa zawadi? Wafuasi wa Mu’awiyah walimsifu sana kwa uvumilivu na ukarimu wake, lakini kwa kweli sera yake ni ile iliyotumiwa na mwonevu kwa yule aliyeonewa; ilikuwa ni sera ya ukatili, uonevu, ukandamizaji na utekaji nyara ambao aliacha wasia kwa ajili ya watawala wa Bani Umayyah waliomfuatia yeye. Ni aina gani ya uvumilivu na ukarimu wa Mu’awiyah inayosifiwa na wafuasi wake, wakati yeye alimtuma Busr bin Artat kwa maelekezo ya kuwateka watu huku akimwambia: “Nenda huku ukipora, na upitie Madina, na uwafanye watu wakimbie. Teka humo njiani mwako unamopita kila makazi ambayo watu wake ni wafuasi wa Ali.” Ni aina gani ya uungwana na ustahimilivu huo, wakati alimtuma Abu Sufyan mwana wa Ghamadi kwenda Iraqi katika msafara wa uporaji na akampa maagizo yafuatayo: “Tembea ukingoni mwa mtu Furati na ufike Hait. Kama ukiyakuta hapo majeshi ya Ali yashambulie, vinginevyo songa mbele na ufike Anbar 226

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 226

9/4/2017 3:47:56 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

na uwapore wakazi wake. Kama hutakutana na upinzani wowote hapo pia, basi endelea mpaka ufike Cresiphon (Madaen). Unapaswa kujua kwamba kushambulia Madaen na Anbar ni bora kama kushambulia Kufa yenyewe. Ewe Sufyan! Mashambulizi haya yatawaogofya watu wa Iraqi, na wale miongoni mwao ambao ni wafuasi wetu watafurahi. Wakaribishe watu upande wetu na uwapige kwa upanga wale watu ambao hawatakubaliana na wewe. Teka kila kijiji unachokipita, na unyakue kila mali utakayoweza kwa mikono yako, na kupora mali ni sawa na kuuwa, hakika inahuzunisha sana. (Maelezo ndani ya Nahjul-Balaghah ya ibn al-Hadiid, uk. 144). Zuhhak bin Qais Fihr alitumwa na Mu’awiyah kwenda kushambulia baadhi ya miji ambayo ilikuwa chini ya udhibiti wa Imam Ali na alipewa maelekezo haya: “Shika njia na ufike Kufa. Shambulia humo njiani wale Waarabu wote ambao ni wafuasi wa Ali na uziteke silaha zao kama wakiwa nazo.” Zuhhak aliyatekeleza maagizo ya Mu’awiyah kwa namna ileile ambayo Busr bin Artat na Sufyan bin Ghamadi walivyozitekeleza. Aliuwa kwa halaiki na kuwapora watu na kuwatendea ukatili wa hali ya juu kabisa. Mu’awiyah alifanya maonyesho ya ajabu ya uvumilivu na upole wake wakati alipoelezea maoni yake kuhusu mamilioni ya Waarabu. Alisema kuwahusu wao kwamba: “Ninaona kwamba wasiokuwa Waarabu watatuzidi kwa idadi, na kama hali hii ya mambo itaendelea, nina wasiwasi kwamba siku haiko mbali sana ambayo watakuja kufutilia mbali majina ya mababu zetu. Ninajihisi kama kuwaachia nusu yao tu kuishi, ili mitaa ya masoko na njia kuu zibakie kuwa kamili.” Kama Akhnaf bin Qais asingemshawishi kutokutekeleza mpango wake juu ya hili, Mu’awiyah angewauwa maelfu ya watu wasio na hatia ambao kosa lao pekee lilikukwa kwamba wao walikuwa sio Waarabu. Mu’awiyah alikuwa mpole tu wakati alipokuwa akabiliane na mtu mwenye nguvu, aliyemuogopa kwamba angeweza kudhibiti mamlaka yake na kuangusha serikali yake. Alivumilia chochote mtu kama huyo alichokisema, akamlaghai na kukubali chochote alichopendekeza. Wakati wowote alipokuwa amekaa miongoni mwa marafiki na washirika wake, na mtu maarufu akamshutumu, yeye mara moja alionyesha usikivu na uvumilivu, isije ikawa mtu huyo mwingine akamshambulia. Yeye pia aliwataka waandishi wake kuandika yale maneno ya karipio akisema: “Hicho ni kipande cha hekima.” Hata hivyo, kama mtu huyo mwingine hakuwa na nguvu na ushawishi, Mu’awiyah hakuo227

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 227

9/4/2017 3:47:56 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

nyesha unyenyekevu wowote. Na hata kama mtu huyo hakusema maneno yoyote ya ukali, alitamani kumuua kwa njia ya kikatili kabisa. Mu’awiyah alikuwa mnyenyekevu, mpole na mvumilivu wakati alipokuwa anatarajia kunufaika kutokana na huyo mtu mwingine. Alikubalilana na chochote mtu huyo mwingine alichokisema, hata kama angeweza kuwa muonevu na dhalimu, madhali tu alimsaidia kufanya utawala wake kuwa imara. Kwa mtu kama huyo angeweza kuitoa Misri na wakazi wake kama alivyofanya katika suala la Amr bin al-Aas. Kwa upande mmoja, upole wa Mu’awiyah ulikuwa mkubwa sana kwamba aliitoa Misri na raia zake kwa Amr bin al-Aas; na kwa upande mwingine ulikuwa mfinyu sana, kiasi kwamba aliichukua haki ya Misri na wa-Misri ya kuishi na kuvifanya zawadi kwa mtu mmoja. Kama huu ndio unaoitwa upole na uvumilivu, Nero, Genghiz (Changez), Rawan na Halagri (Halaku) nao pia walikuwa wapole na wavumilivu sana. Wakati mtu anapoichunguza kwa makini sera ya Mu’awiyah, anashangazwa kukuta ni njia gani alizotumia kuwapata watu. Undumila kuwili uliofanywa na yeye katika ujuzi wa uongozi ulikuwa ni udanganyifu wa asili mia kwa mia. Mauwaji, uporaji na ugaidi ndivyo vilivyounda sera yake ya msingi; na kutoa ahadi za kuvutia na kufanya vitisho kulikuwa pia ni sehemu ya sera hiyo. Ilijumuisha pia uuaji wa watu wema na wasio na hatia, akiwatukuza majambazi na wahuni, propaganda za uongo na kutafuta msaada wa watu makatili na wasio na adabu. Mu’awiyah alikiri mara kadhaa kwamba siasa zake zilikuwa hazina usawa na haki, na yeye hakutoa msaada kwa wakati wowote ule kwenye ukweli. Tukio lililosimuliwa hapo chini linatoa mwanga juu ya siasa zake na linaelezea maoni yake kuhusu usawa na uadilifu. Mutrat bin Mughira bin Shu’ba anasema: “Nilifuatana na baba yangu Mughira kwenda kumuona Mu’awiyah. Baba yangu alimtembelea kila siku na alimsifu sana wakati wa kurudi kwake. Wakati aliporudi usiku mmoja, alikuwa na huzuni sana na hakula hata chakula cha jioni. Katika kumuuliza kwangu kuhusu sababu ya huzuni yake; yeye alisema: ‘Mwanangu! Usiku huu nimekuja baada ya kukutana na mtu muovu kabisa.’ Katika kuwa nimemuuliza mtu huyo alikuwa ni nani, yeye alisema: “Nilimwambia Mu’awiyah faraghani: umefanikiwa kupata matakwa yako yote. Sasa itakuwa ni katika ukamili wa mambo endapo utawatendea watu kwa upole. Umekuwa mzee sasa. Unapaswa uwatendee kwa wema Bani Hashim ambao ni ndugu na jamaa zako. Hakuna sababu ya wewe kuwa na hofu juu yao sasa! Mu’awiyah alijibu: Kamwe! Kamwe! Yule mtu atokanaye na

228

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 228

9/4/2017 3:47:56 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

ukoo wa Taym (Abu Bakr) alikuwa khalifa. Wakati alipokufa hakuzungumzwa tena. Sasa anaitwa tu na watu wote kwa jina ‘Abu Bakr’. Baada yake Umar akawa khalifa na akatawala kwa muda wa miaka kumi. Kwa kifo chake, yeye pia alikoma kuzungumziwa habari zake na watu sasa wanamwita ‘Umar.’ Halafu ndugu yetu Uthman akawa khalifa. Alitokana na ukoo wetu mtukufu kabisa. Yeye alitawala kwa uadilifu lakini wakati alipokufa, yeye pia akakoma kuzungumzwa habari zake. Hata hivyo, jina la yule mtoto wa Bani Hashim (yaani, Muhammad) linatangazwa mara tano wakati wa mchana na usiku (kila mtu anasema: Nashuhudia kwamba Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu). Sasa ni nini tena cha kufanywa na jina lake isipokuwa kwamba nilibomoe kabisa.” (Muruuj al-Dhahab, Juz. 2, uk. 241). Mu’awiyah alilelewa katika mazingira ya watu ambao waliukataa Utume. Alitokana na ukoo ambao uliichukia dini. Kutoka utotoni mwake kabisa; yeye alikuwa amemuona baba yake akiandaa kupigana dhidi ya Waislamu, akiongoza jeshi kubwa dhidi yao, na kupanga kuwaua masahaba wa Mtume na vilevile Mtume mwenyewe, ili kuulinda uchifu wake, mamlaka na mapato ya kimali. Alikuwa ameona kwamba baba yake alitaka kubakia akiwa chifu ingawaje hili lingeweza kuishia kwenye kuangamiza ule moyo wa uadilifu ulioanzishwa na Mtume na kifo cha Mtume na masahaba zake, ni msiba wa Arabia yote. Katika mambo yote haya, Mu’awiyah alikuwa amerithi ule moyo wa babu wa jadi yake, Umayyah ibn Abd al-Shams. Kama vile mwenendo wa Abu Sufyan ulivyokuwa na athari kubwa katika tabia ya Mu’awiyah, ambaye alikuwa ni picha halisi ya baba yake katika suala la ubinafsi na uchu wa madaraka, katika namna hiyo hiyo mama yake Hind, yule mlaini, alifanya mgandamizo wa nguvu sana kwenye moyo wake Mu’awiyah. Wote wawili (baba na mama) waliathiri sana desturi na tabia zake. Katika historia yote ya Arabuni haiwezekani kabisa kupata mwanamke mwingine anayeweza kuwa sawa na Hind katika umimi, ubinafsi, fujo, ushenzi na uovu. Alikuwa na moyo mgumu kiasi kwamba mtu mwenye kiu sana ya damu hawezi kuwa sawa na yeye. Washirikina wa Quraishi walikuwa wamejiandaa tayari kikamilifu kupigana dhidi ya Mtume hapo Badr, na vita vikali vilipiganwa. Washirikina wengi sana waliuawa. Wanawake wa Makkah waliomboleza vifo vya ndugu zao kwa muda wa mwezi mmoja. Halafu walikuja kwa Hind, mama yake Mu’awiyah na wakamuuliza; “Kwa nini wewe huombolezi kama sisi?” Yeye akasema kwa sauti iliyojaa kisasi na chuki 229

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 229

9/4/2017 3:47:56 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

ya muda mrefu ambayo haiwezi kupatikana kwa mwanamke mwingine: “Kwa nini mimi nilie? Hivi nilie ili habari zifike kwa Muhammad na marafiki zake, na wao wapate kufurahi, na wanawake wa Ansari waweze na wao kufurahi pia? Kwa jina la Mungu mimi sitalia mpaka niwe nimelipiza kisasi kwa Muhammad na masahaba zake, na sitazipaka mafuta nywele zangu mpaka vita vimepiganwa dhidi yao.” Baada ya hapo yeye aliendelea kuwachochoea washirikina dhidi ya Waislamu na hatimaye vita vya Uhud vikatokea. Maneno yaliyonukuliwa hapo juu yanaonyesha jinsi alivyokuwa mkatili na mwenye moyo mgumu. Yeye hakuamini katika kujiondolea majonzi kwa kulia na kuomboleza. Wanawake wana mioyo laini kwa asili, lakini yeye alikuwa wa mwelekeo tofauti. Aliyatazama mambo kwa jicho la mwanaume. Yeye aliamini kwamba uchifu na utawala vilikuwa na maana ya kuvumilia matatizo ya hali ya vita ili kuweka kiwango cha ubora na hadhi ya mtu ya juu kabisa. Wakati washirikina wa Makkah walipoelekea Madina wakifanya maandalizi kamili kupigana vita vya Uhud; Hind pia aliandaa kikosi cha wanawake, na akawasili kwenye uwanja wa vita akifuatana nao ili kuwachochea wanaume kupigana kijasiri, ili kwamba yeye aweze kukidhi haja yake ya kisasi kwa kuangalia damu inayotiririka na maiti za wale waliouawa. Mwanaume mmoja alipinga wanawake kwenda kwenye eneo la vita. Hata hivyo, Hind alikemea katika kujibu: “Kwa hakika sisi tutakwenda kuangalia mapigano kwa macho yetu wenyewe.” Hind alishikilia uamuzi wake na akaenda kwenye uwanja wa vita pamoja na wanawake hao. Alifanya kila aliloweza ili kukidhi haja yake ya kulipa kisasi. Wakati mapigano makali yalipoanza yeye pamoja na wanawake hao wengine walikwenda kwenye kila safu ya jeshi la washirikina. Walipuliza matarumbeta na waliimba mashairi yafuatayo: “Enyi kizazi cha Abd al-Dar! Fanyeni haraka, kuna wale watu kwenye migongo yenu (yaani wanawake) ambao ni lazima muwalinde; chomoeni panga zenu.” “Kama mkisonga mbele kwenye uwanja wa mapambano tutawakumbatieni na tutawawekea mito laini chini ya vichwa vyenu. Lakini kama mtakimbia kutoka kwenye uwanja wa vita tutawatelekezeni, kwani katika hali hiyo sisi hatuwezi kuwapenda ninyi.” Hind alikuwa ametoa ahadi nyingi za zawadi kwa yule mtumwa wa ki-Habeshi aliyeitwa Wahshi, kama angewaua baadhi ya Waislamu, hususan ammi yake Mtume, 230

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 230

9/4/2017 3:47:56 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Hamza, ambaye alikuwa na kinyongo sana naye. Katika vita hivi washirikina walifanikiwa na Waislamu walipata hasara kubwa. Hind alifurahi sana. Mmoja kati ya wale waliouawa pale Uhud alikuwa ni Hamza ambaye aliuawa na Wahshi. Wakati alipouawa, Abu Sufyan alipiga ukulele: “Leo tumelipiza kisasi cha vita vya Badr. Tutakutana tena mwaka ujao.” Mke wake Hind hata hivyo, hakuwa ameridhika kwamba mtu shujaa kama Hamza alikuwa ameuawa. Alizisogelea zile maiti za wale mashahidi akiwa pamoja na wale wanawake wengine wa ki-Quraishi. Walikata mikono, nyayo za miguu, pua na masikio ya wale waliouawa; na kutokana navyo hivyo wakatengeneza mikufu na hivyo kuonyesha unyama, ambao hata dhalimu mkatili kabisa asingeweza kuufikiria. Halafu akalichana tumbo la Hamza, kama mtu muuza nyama, na akalitoa ini lake. Alitaka kulitafuna na kulimeza lakini hakuweza kufanya hivyo. Kitendo chake hiki kilikuwa cha kuchukiza mno kiasi kwamba hata mume wake, Abu Sufyan alionyesha kukarahishwa nacho. Alimwambia Muislam mmoja: “Maiti za watu wenu ambao waliuawa zilikatwa viungo. Wallahi mimi sikufurahi wala kuchukia juu ya hili. Mimi sikuagiza jambo hili lifanywe wala sikulikataza.” Kutokana na kitendo hiki Hind ndipo akaanza kuitwa mlaini. Wakati Abu Sufyan alipoukubali Uislamu kwa kusitasita, wakati wa ushindi wa Makkah mke wake Hind aliwaambia Maquraishi kwa sauti kubwa kwa maneno haya: “Enyi Maquraishi! Muuweni mtu huyu muovu na mchafu asiye na thamani yoyote. Sijawahi kuona jeshi la ulinzi baya kama watu ninyi. Kwa nini hamkulinda mji wenu na maisha yenu?” Hind hakuvutiwa kabisa na kule kutendewa kwa upole alikofanya Mtume kwa mumewe na watoto wake. Alikuwa ni Abu Sufyan huyu huyu, na Hind huyu huyu waliomlea Mu’awiyah. Zaidi ya hayo, alikuwa nazo tabia bainishi zile maalum za wahenga wake kwa kuzaliwa (yaani, kupenda madaraka na mamlaka, matumizi ya njia zote, mbaya na nzuri katika kufanikisha lengo lake, ambayo inaitwa ‘diplomasia’ katika tekinolojia ya kisasa, rushwa, uigaji, uonevu n.k.). Kwa kifupi alikuwa ni kielelezo kikamilifu cha mababu zake. Alilelewa na, akajifunza mawazo ya watu ambao kwamba kuwahusu wao AmirulMu’minin Ali alisema: “Wao ni watu waovu na wadanganyifu wanaoendesha maisha ya kifisadi dhidi ya wengine. Kama wataruhusiwa kutawala watu, basi watawakandamiza, kujiona wao wenyewe ni bora kuliko wengine, kuonyesha mamlaka, kujiingiza katika vurugu na kusababisha matatizo juu ya ardhi.”

231

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 231

9/4/2017 3:47:56 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Bani Umayyah waliendeleza juhudi zao za uovu ili kuboresha maslahi ya ukoo wao kama katika zama za jahilia; hata wakati wa uhai wa khalifa Umar, lakini waliyafanya yote hayo kwa siri na ustadi mkubwa chini ya kivuli cha udanganyifu. Hata hivyo, pale Uthman, ambaye alitokana na ukoo wao alipoutwaa ukhalifa njama zao zikawa dhahiri. Kuanzia wakati huo na kuendelea walijitahidi kwa uwezo wao wote kuhakikisha kwamba serikali hiyo iwe ni serikali ya ukoo wao na kwamba ije kurithiwa na watoto na wajukuu zao. Hawakuzingatia heshima imma juu ya ukhalifa wala juu ya Uislamu. Walinyakua utajiri mwingi kiasi ilivyowezekana. Pia waliandikisha jeshi kubwa. Waliifanya hazina ya umma, ambayo ilikuwa mali ya Waislamu wote kuwa ni mali yao binafsi. Waliwahonga wale watu mashuhuri kwa fedha za umma na kupata kuungwa mkono nao. Walikuwa wakiingojea fursa ya kupata utawala kwa ajili yao na vizazi vyao. Walikuwa wakisubiri kuanzisha ufalme kwa ajili ya ukoo kwa namna na maana ile ambayo mhenga wao Abu Sufyan alivyokuwa ameutafsiri ‘Utume’ wakati aliposema kumwambia ammi yake Mtume, Abbas kwamba: “Mpwa wako ameanzisha ufalme mkubwa.” Aliuchukulia utume wa Mtukufu Mtume kama ufalme, ambapo yeye (Mtume) wala hajafikiria kamwe juu ya kuanzisha taasisi kama hiyo. Kuuawa kwa Uthman nako kulitoa fursa nyingine kwa Bani Umayyah. Tutakuja kuonyesha kwenye kurasa zifuatazo kwamba Mu’awiyah mwenyewe alikuwa na ushiriki katika mauaji ya Uthman. Kuanzia wakati huo na kuendelea, hila, udanganyifu na njama za Mu’awiyah zilijulikana kwa wote, na kuanzia wakati huo na kuendelea, ushindani ukaanza kati ya asili mbili ambazo zilikuwa zinatofautiana. Kwa upande mmoja kulikuwa na maadili, umadhubuti na usafi wa tabia, na kwa upande mwingine kulikuwa na uchu wa madaraka, ubinafsi, ufashisti, udhalimu na maovu mengineyo. Ali aliwakilisha ile seti ya kwanza ya sifa, na Mu’awiyah na ndugu na jamaa zake waliwakilisha ile ya pili. Miito au kauli mbiu za Ali zilikuwa: Mimi sitamdanganya mtu yeyote yule wala kufanya kitendo cha kufedhesha au kisichostahili. Wapendelee wengine jambo lile lile unalojipendelea wewe mwenyewe. Usiwatakie wengine yale ambayo huyatakii nafsi yako mwenyewe. Usiwaonee wengine kama vile ambavyo wewe usivyopenda kuonewa na wengine. 232

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 232

9/4/2017 3:47:56 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Kwa kulinganisha na vitendo vya dhulma vya ndugu yako, wewe unapaswa uwe hodari vya kutosha katika kufanya wema juu yake.” Kwa upande mwingine Mu’awiyah alikuwa wakati wote akisema: “Jeshi la Mwenyezi Mungu limo ndani ya asali.” Kwa neno ‘asali’ yeye alikuwa na maana ya ile asali ya sumu ambayo yeye aliitumia kuwamaliza maadui zake, ili njia iwe imesafishwa kwa ajili ya kufikia kwake kwenye utawala. Mu’awiyah aliwachukulia wale watu wote wema na wachamungu kuwa ni maadui zake ambao wamesimama katika njia yake ya kufanikisha malengo yake maovu. Wakati, na pale Mu’awiyah alipohofia kwamba mtu anaweza kuwa kipingamizi katika ufanikishaji wa matakwa yake basi alimmaliza, hata kama mtu huyo angekuwa mwadilifu na mchamungu. Kiasi kwamba hakuweza kuwaacha marafiki zake wafujaji ambao walikuwa wafuasi wake. Yeye alimuua Imam Hasan kwa asali hiyo hiyo. Aliwanunua marafiki na kuwahonga watu maarufu kwa pesa za hazina ya umma, ambazo zilipaswa kutumika kwa madhumuni ya ustawi wa jamii. Wakati alipokwenda Makkah kuwalazimisha watu kutoa kiapo cha utii kwa Yazid; aliweka jeshi lenye nguvu upande mmoja, na marundo ya dhahabu na fedha kwa ule upande mwingine, na akasema kuwaambia watu wa Makkah: “Ninamtaka Yazid awe khalifa wa jina tu. Mamlaka ya kuwateua au kuwauzulu watumishi au kugharimia matumizi yatabakia kwenu ninyi.” Hata hivyo, pale watu walipokuwa hawako tayari kumkubali Yazid kama khalifa wao, yeye Mu’wiyah aliwaambia kwa namna ya kuwatishia: “Nimekujulisheni juu ya matokeo ambayo kwayo mimi sitachukua dhamana yoyote. Mimi nitawahutubia. Kama mtu yoyote atasimama kunipinga mimi shingo yake itakatwa kabla hajatamka neno. Kwa hiyo chungeni maisha yenu.” Wakati Mu’awiyah aliposhutumiwa kwa tapanya pesa za hazina ya umma – pesa zile zile ambazo Ali alikuwa akizitumia kwa malengo ya ustawi wa jamii – yeye Mu’awiyah akawa akitamka maneno haya ya Bani Umayyah: “Dunia ni mali ya Mwenyezi Mungu na mimi ndiye mwakilishi wake. Chochote kile nitakachokichukua ni cha kwangu na vilevile ninayo haki ya kuchukua kile ambacho sikichukui.” Wakati alipoambiwa aruhusu uhuru wa mawazo na imani kwa watu alikuwa akijibu: “Madhali mtu hasimami kati yangu na utawala wangu basi sina matatizo naye.”

233

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 233

9/4/2017 3:47:56 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Katika kitabu chake kiitwacho ‘Uislamu na udikteta wa kisiasa’ Profesa Muhammad Ghazal wakati akitoa maoni juu ya sera za kidikteta za Mu’awiyah anasema: “Ni uovu mkubwa sana kuwa mbinafsi na mkaidi. Kama mtu anapata utawala ni lazima ashike kazi hiyo na watu wanapaswa kumuunga mkono tu hadi wakati ambapo kwamba anatimiza mahitaji ya watu na akawa anafanya kazi kulingana na matakwa yao………..” Mahali pengine anaandika hivi: “Ukaidi na ufashisti wa wafalme unachukiwa na Mwenyezi Mungu na mitume Wake na hata na watu vile vile. Ni ukweli usiopingika kwamba katika zama zote namna ya kufikiri kwa wafalme imebakia ile ile. Wafalme hawa hawaachi ubinafsi wao hata kama wafuasi wao na watakia kheri wao watawapenda kupita kiasi..” Mu’awiyah alinyakua utawala kwa njia ya sera zake za hila. Aliubadilisha ukhalifa kuwa ufalme na akauacha kama urithi kwa ajili ya kizazi chake. Kutokana na hili, Mu’wiyah alikuwa kielelezo kikamilifu cha ile tabia ya umimi, ubinafsi wa Bani Umayyah – Bani Umayyah hao hao ambao walikuwa wakali wakati wa zama za ujahilia, na walibakia hivyo hata baada ya kuukubali Uislamu. Baada ya Ali kukutana na kifo chake cha kishahidi mikononi mwa Ibn Muljam, Mu’awiyah alianza kupanga kumuua mtu yeyote ambaye hakuwa tayari kumkubali yeye kama khalifa wa Mwenyezi Mungu. Alisema waziwazi: “Tutawaacha watu kuwaingilia pale tu tutakapokuwa tumewafanya watumwa.” Yeye pia anasema: “Hatuna cha kufanya na mtu isipokuwa atakaposimama baina yetu na utawala wetu.” Aliwaambia watu kwa masharti ya wazi: “Madaraka ni mali yangu mimi na baada yangu yatakuwa ni mali ya Bani Umayyah. Watu wako huru madhali hawawi kikwazo baina ya Bani Umayyah na utawala wao.” Akaanza kuwakamata watu na kuwaadhibu kwa kuwatilia wasiwasi tu, ingawa hili halijawahi kutokea katika vipindi vya makhalifa waliotangulia. Alianza kuuwa bila huruma wale masahaba wa Mtume, masahaba wa masahaba na waumini wengine, ambao waliwakilisha maoni ya umma na kuifuata njia iliyonyooka. Mara tu alipopata udhibiti juu ya dola alianza kuandikisha utajiri na mali za watu kama urithi kwa ajili ya mwanawe muovu. Alitumia maefu ya njia kupata kiapo cha utii kwa ajili ya Yazid kwa nguvu. Tunasimulia hapa chini tukio ambalo litaonyesha ni juu ya msingi gani serikali ya Yazid na makhalifa wengine wa Bani Umayyah zilivyoundwa. 234

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 234

9/4/2017 3:47:56 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Mu’awiyah aliamua kumuondoa Mughira ibn Shu’ba kwenye ugavana wa Kufa na kumteua Sa’ad ibn Aas kuchukua mahali pake. Pale Mughira alipokuja kulijua hilo alikwenda kumwona Mu’awiyah na akamshauri kwamba angemteua Yazid kuwa khalifa baada yake. Mu’awiyah alifurahi sana kusikia ushauri huu na akamwambia Mughira: “Ninakuruhusu uendelee kuwa gavana wa Kufa. Wewe unapaswa urudi Kufa ukalitoe pendekezo hili mbele ya watu ambao unawaona wanaaminika.” Mughira alirudi Kufa na akaliweka pendekezo hili mbele ya watu kama hao. Wao wakaafiki; Mughira akawachagua watu kumi kati yao na akawatuma kwa Mu’awiyah katika namna ya wawakilishi. Pia akawapa wao dirham thelathini kila mtu na akamteua mwanawe Musa kama kiongozi wao. Watu hawa walikutana na Mu’awiyah na wakalisifu sana lile pendekezo linalohusu urithi wa Yazid. Mu’awiyah akamuuliza Musa: “Baba yako amewalipa kiasi gani watu hawa ili kununua dini yao?” Musa akamwambia kwamba Mughira alikuwa amelipa dirham thelathini kwa ajili ya madhumuni hayo. Mu’awiyah akasema: “Haya ni mapatano mazuri.” Kisha Mu’awiyah akalipeleka pendekezo hili kwa magavana wote na akawaagiza watume wajumbe kwake kutoka kila mji na wilaya. Ujumbe mwingi ulikuja na kubadilishana maoni juu ya suala hili. Halafu Yazid mwana wa Muqanna akasimama na kusema huku akimnyooshea kidole Mu’awiyah: “Huyo ndiye Amirul-Mu’minin.” Kisha akimnyooshea kidole Yazid, yeye akasema: “Wakati atakapofariki Mu’awiyah, huyo Yazid atakuwa ndiye Amirul-Mu’minin.” Kisha akauashiria upanga wake mwenyewe na akasema: “Huu ni kwa ajili yake yule ambaye hakubaliani nasi.” Mu’awiyah akasema: “Njoo. Hebu kaa chini. Wewe ni mkuu wa wenye ufasaha wa kuzungumza.” Ulazimishaji na nguvu ambavyo Mu’awiyah alivitumia kupata kiapo cha utii kwa ajili ya Yazid kutoka kwa watu wa Hijazi ni vya ajabu na vilevile vinashangaza. Ili kuweza kupata kuafiki kwao aliwaendea akiwa na jeshi, vilevile na mifuko mingi ya dirham na dinari pia. Hata hivyo, walipokuwa hawakutishiwa na jeshi hilo na walipokuwa hawakuhakikishiwa na utajiri, Mu’awiyah akasema: “Nimefanya wajibu wangu. Hadi sasa utaratibu umekuwa kwamba wakati wowote nilipohutubia, na mmojawapo kati yenu akasimama na kunikanusha, mimi nilivumilia na kumsamehe. Hata hivyo, sasa hivi nitahutubia na ninamuapa Mwenyezi Mungu kwamba; kama yeyote kati yenu atatamka maneno dhidi ya nitakachokisema, upanga utakifikia kichwa chake kabla hajatamka kauli ya pili. Kwa hiyo, mjihadhari na maisha yenu.” Kisha akamuagiza afisa wake wa polisi kuweka askari wawili kila upande wa kila mmoja wa waliohudhuria pale na kuagiza 235

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 235

9/4/2017 3:47:56 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

kwamba kama mtu yeyote atazungumza lolote katika kumuunga mkono au dhidi ya atakachokisema yeye Mu’awiyah, basi akatwe kichwa chake. Mu’awiyah na watu wengine wa ukoo wa Bani Umayyah walitekeleza yale mamlaka ya kifashisti ya zama ujahilia. Walikuwa madikteta ambao walimiliki kila kitu, na Waislamu walikuwa ni sawa na watumwa wao, ambao walitegemewa wasilete upinzani wowote. Waliwakata vichwa wale wote waliokataa kuchukua kiapo cha utii kwa Yazid. Kuhusu wale ambao walichukua kiapo hicho cha utii mikono yao ilipigwa michoro, kwani ilikuwa ni alama maalum ya yule mtu aliyehusika, ya kuonyesha kwamba yeye ni mtumwa. Warithi waliomfuata Mu’awiyah walikuwa wamepinda zaidi na kupotoka. Baadhi yao walimzidi yeye katika masuala ya maovu na upotofu, bali hawakuwa na hata kidogo zile sifa za dhahiri ambazo alikuwa nazo yeye. Watu kwa hiyo wakateseka zaidi wakati wao hao. Walilazimika kuweka utajiri wao na vilevile shingo zao mikononi mwa watawala. Mawakala wao na waajiriwa walikuwa makatili na madhalimu. Waliwakandamiza watu popote pale walipopewa madaraka. Waliwadhalilisha wasiokuwa Waarabu ambao waliukubali Uislamu. Pia waliwaonea madhimmi, ambao kwao wao wema na upole ulikuwa umehimizwa na Uislamu. Hawakuwaacha hata Waarabu na wakawauwa wale waliokataa kuwalisha kwa minofu na damu zao. Waliwateuwa kama watawala wale watu ambao walitoza kodi kubwa juu ya watu, na wakaikamata kodi hiyo hiyo kwa kiburi na katika namna ya aibu sana. Hiyo ndio sababu ya kwa nini Sa’d ibn Aas ambaye aliteuliwa na Uthman kama gavana wa Iraqi alikuwa akisema: “Iraqi ni bustani ya Maquraishi, tutachukua kutoka humo kile tunachokitaka na kuacha kile tusichokitaka.” Na wakati dhimmi (asiyekuwa Muislamu) alipotaka kujua kutoka kwa Amr bin Aas ni kiasi gani cha kodi walichotakiwa kulipa yeye alijibu: “Wewe ni hazina yetu.” (yaani, tutachukua kutoka kwako chochote tunachokitaka). Makhalifa wa Bani Umayyah walikuwa ni mahodari sana wa kujitwalia hazina ya umma wao wenyewe na kuwafanya marafiki na washirika wao kuwa matajiri kiasi walivyoweza. Wale maafisa walioteuliwa katika nchi za Kiislamu walinyakua chochote kile walichoweza na pia walijitwalia viwango vikubwa vya pesa kutoka kwa watu kama uthibitisho wa uaminifu wao kwa watawala. Kwa mfano, Khalid ibn Abdullah Qasra, ambaye alikuwa ni mmoja wa magavana wa Hisham ibn Abdul Malik, alikuwa akichukua dirham milioni moja kutoka kwenye 236

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 236

9/4/2017 3:47:56 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

hazina ya umma kila mwaka. Alichukua mamilioni ya dirham vilevile mbali na kiasi hiki. Lile jengo la uadilifu lililosimamishwa na Uislamu na Imam Ali liliangushwa na Bani Umayyah. Matabaka mawili, yaani, lile la matajiri na lile la masikini yakaibuka miongoni mwa watu. Hatimaye baadhi yao walikuwa wakibiringika katika utajiri; ambapo wengine hawakuweza hata kuishi kulingana na kipato chao. Mmoja wa makhalifa wa Bani Umayyah alitoa dinari kumi na mbili elfu kwa muimbaji aliyeitwa Ma’bad, kwa sababu alipenda maonyesho yake, ambapo walikuwepo watu wasiokuwa na idadi ambao walitamani kuishi kama watu huru. Kabla Suleiman bin Abdul Malik hajawa khalifa idadi ya watumwa ilikuwa imefikia mamia ya maelfu. Hii ilithibitisha ule ukweli kwamba watumwa elfu sabini pamoja na watumwa wa kike waliachiwa huru na yeye. Katika wakati wa kipindi cha Bani Umayyah moyo wa ushabiki ulikujakuwa mkali kwa kiasi ambacho hakikuruhusiwa kabisa na Uislamu, Mtume na Ali. Mkazi wa Yemen hakuweza kufaidi haki ambazo zilifaidiwa na mtu wa kabila la Qais, na mtu asiyekuwa Mwaarabu hakuwa na upendeleo aliokuwanao Mwarabu. Ilikuwa ni wakati wa kipindi cha Bani Umayyah ambapo idadi ya washauri wapenda starehe ilipokuwa imeongezeka kwa upesi sana. Wao hawakufanya kazi yoyote lakini walipata ujira mkubwa sana kutoka kwenye hazina ya umma, kama ilivyokuwa ni kawaida hata sasa hivi katika baadhi ya nchi za Kiarabu. Historia inatuambia kwamba Walid bin Abdul Malik alisimamisha ulipaji wa mishahara iliyokuwa ikitolewa kwa watu wengi kiasi cha elfu ishirini hivi. Watawala wa Bani Umayyah vile vile walifanya maovu mabaya sana ili kulinda miliki yao juu ya miji mbalimbali. Abdul Malik alikuwa ni dhalimu haswa ambaye alitawala kwa namna ya kuabisha sana. Alifanya visima na chemchem za Bahrain vijazwa michanga ili watu wawe hawana msaada na wawe masikini na hatimaye kuwa watiifu kwa watawala (Tazama vitabu vya Ibn Rayhani vyenye jina la ‘Muluk al-Arab’ Juz. 2, uk. 206 na al-Nukabat, uk. 64). Aliikabidhi serikali ya Iraqi na Hijazi kwa yule mtu wa hizaya na mwenye kiu ya damu anayejulikana kama Hajjaj bin Yusuf. Itatosheleza kutaja mfano mmoja (ule wa Yazid bin Abdul Malik) ili kuonyesha ni thamani gani watawala wa Bani Umayyah waliiambatanisha na watu wa kawaida, na jinsi walivyounajisi ukhalifa na walivyowaangalia watu kwa dharau. Siku moja 237

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 237

9/4/2017 3:47:56 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

alikunywa pombe nyingi sana na akalewa kupindukia. Mtumwa wa kike aliye kipenzi chake kabisa, Hubaba, alikuwa amekaa kando yake. Alimwambia, “Wacha nipoteze fikira.” Yeye Hubaba akauliza, “Na Waislamu utawakabidhi kwa nani?” “Kwako wewe” ndio lilikuwa jibu lake. Akiandika kuhusu Bani Umayyah, Amin Rayhani anasema: “Utekelezaji wa uadilifu kwa raia ndio msingi wa serikali. Wale waliokikalia kiti cha utawala hata hivyo, walifikiri vinginevyo. Kama mlivyokuja kujua walikuwepo miongoni mwa watawala wa Bani Umayyah watu wasiofaa, walevi na madhalimu.” (al-Nakabat, uk.70). Isisahaulike pia kwamba watawala wa Bani Umayyah walianzisha utaratibu wa aibu wa kumtukana Ali na kizazi chake. Hata hivyo, aliyekuwa muungwana zaidi miongoni mwao alikuwa ni Umar ibn Abdul Aziz ambaye alitoa heshima kwa watawala wa Mashariki na wanadamu halikadhalika. Mara tu alipokipanda kiti cha utawala aliwaondolea watu ukandamizwaji, akazirudisha haki zao, akawateua watumishi waadilifu na wenye huruma. Alianzisha usawa wa kweli baina ya Waarabu na wale wasiokuwa Waarabu, na baina ya Waislamu na wasiokuwa Waislamu. Kama ishara ya heshima juu ya hadhi ya mwanadamu yeye alisimamisha utekaji nyara zaidi. Alipiga marufuku kodi zote isipokuwa zile ambazo zililipwa na watu kwa hiari. Vile vile alisimamisha kule kumtukana Ali ambako kulikuwa kumeendelea kwa muda mrefu. Alirudisha kutoka kwa waungwana na makabaila zile mali na utajiri, ambao ulikuwa umenyakuliwa na wao kinyume cha sheria, na akawashauri kufanya kazi kwa ajili ya kukimu maisha yao. Utawala wa mtu huyu mashuhuri haukuendelea kwa muda mrefu na akawa muathirika wa njama na hila za Bani Umayyah wenyewe, na akapoteza maisha yake. Wao walimuua kama vile walivyokuwa wamemuua Mu’awiyah bin Yazid hapo mapema – kosa lake pekee likiwa kwamba alitaja matendo yao maovu, akaonyesha kutofurahia kwake juu ya uvunjaji wao wa haki za watu, akakiri kwamba baba yake na babu yake walikuwa makosani, na akapendelea maisha ya kujitenga faraghani kuliko utawala. Inashangaza sana kwamba baadhi ya waandishi wa kisasa ni mashughuli (wanaoshuhulika) sana katika kuhalalisha matendo ya watawala wa kidhalimu na kiovu wa Bani Umayyah na mawakala wao. Wao wanasema mambo ambayo wao wenyewe lazima wawe hawawezi kuridhika nayo.

238

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 238

9/4/2017 3:47:56 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Wanafanya hivyo tu kwa ajili ya kuwaunga mkono wahenga wao, na kwa hiyo, wanatoa utetezi wa ajabu na usio na maana kwa niaba yao. Hivi wale watu wa wakati uleule wa Bani Umayyah; ambao walikuwa mashahidi wa kuona kwa macho yao, wa utawala wao hawakuwa wakweli zaidi? Ni nini watakachokisema waandishi hawa wa kisasa baada ya kusoma riwaya hii ifuatayo? Siku moja Ubaydah bin Hilal Yashkari alikutana na Abu Harabah Tamimi, Ubaydah akamwambia Abu Harabah: “Nataka kukuuliza maswali kadhaa. Je, utanipa majibu sahihi?” Abu Harabah akajibu kwa kukubali. Hapo mazungumzo yafuatayo yakatokea baina yao: Ubaydah: Unasemaje kuhusu makhalifa wako wa Bani Umayyah? Abu Harabah: Walikuwa wakimwaga damu bila ya uhalali wowote. Ubaydah: Waliutumiaje utajiri? Abu Harabah: Waliupata pasi na uhalali na waliutumia bila uhalali pia. Ubaydah: Waliwatendea vipi mayatima? Abu Harabah: Wao walinyakua mali ya yatima, wakawanyima haki zao na wakazifedhehesha staha za mama zao. Ubaydah: Ole wako, ewe Abu Harabah! Hivi watu kama hao wanafaa kufuatwa na kutiiwa? Abu Harabah: Nimekueleza kuhusu kile ulichoulizia. Sasa usinilaumu mimi. Haya maneno ya Abu Harabah “sasa usinilamu mimi” yanakuja kueleza kwa kawaida kwamba wakati wa utawala wa Bani Umayyah na mawakala wao haikuwezekana kwa mtu yoyote kupanga maoni yake mwenyewe na kuyaeleza. Ni vipi hawa watetezi wa Bani Umayyah wa wakati huu watakavyoyaeleza yale maoni ya watu wa Madina ambayo waliyaeleza mbele ya yule Khawarij Abu Hamzah? Baada ya kuwafukuza Bani Umayyah kutoka Madina, Abu Hamzah aliulizia kutoka kwa wakazi wa mji huo juu ya ni matatizo gani waliyokuwa wakiyavumilia mikononi mwa makhalifa wa Syria na mawakala wao. Walisema kwa maneno ya wazi kwamba walikuwa wakiwaua kwa kuwatilia shaka tu, na wakiyaona kuwa ni mambo ya halali, yale ambayo yalitangazwa na Uislamu kuwa ni ya haramu, na ambayo pia ni ya haramu machoni mwa busara, dhamiri, na heshima ya mwanadamu. Katika hotuba iliyotolewa na Abu Hamzah katika tukio hili, yeye alisema maneno haya pia: 239

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 239

9/4/2017 3:47:56 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

“Hamuoni yaliyotokea kwenye ukhalifa wa ki-mungu na kwa Uimamu wa Waislamu? Kiasi kwamba Bani Marwan walikuwa wakicheza navyo kama mpira. Walikula kilafi mali ya Mwenyezi Mungu na wakacheza na dini Yake. Waliwafanya waja wa Mwenyezi Mungu kuwa ni watumwa. Kila mtu mzima wao aliwafanya vijana wao kuwa warithi kwa ajili ya malengo haya. Walinyakua utawala na wakaung’ang’nia kama miungu wa kujitengenezea wenyewe. Miliki yao ilikuwa ni miliki ya madikteta, madhalimu. Walifanya maamuzi kulingana na haja na vigeugeu vyao. Kama walipata kukasirishwa basi waliwaua watu. Waliwaweka watu kizuizini kwa kuwatilia wasiwasi tu, na walisimamisha adhabu kwa kupata ushauri. Waliwafanya watu wadanganyifu kuwa ndio wadhamini na wakawapuuza wale ambao walikuwa ni waaminifu. Walikusanya mapato kutoka kwa watu hata kama haikustahili kutoka kwao na wakayatumia kwa madhumuni yasiyokuwa ya halali.” Ni vipi watetezi hawa wa Bani Umayyah watakavyolielezea shairi la Bakhtari ambamo ameonyesha mawazo ya watu wa zama zile na kuonyesha picha halisi ndani yake: “Tunalichukulia kundi lile la Bani Umayyah kuwa ni makafiri ambao walijitwalia ukhalifa kwa njia ya hila na udanganyifu. Vitendo viovu, utawala dhalimu, na mipango mibaya ya Bani Umayyah; ambayo kwa hakika ilijulikana kwa watu wa mwanzoni, ilikuja kujulikana kwa wale waliofuata baadae, na waandishi wasiokuwa Waarabu wameutaja ukatili na maovu yao kwa namna ileile ambayo imeelezwa na waandishi wa Kiarabu. Ni ukweli ambao unakubaliwa hata na waandishi wa Misri na wengineo ambao wanawaunga mkono kwa bidii sana Bani Umayyah. Wao wanasema: “Wengi wa wanahistoria wa mashariki na magharibi wanawashambulilia kwa nguvu sana na kutowaamini Bani Umayyah, ni ule mwelekeo wa Polios Wilharzan ndio wa wastani kwa kiasi fulani.” Itaonekana kwamba mwelekeo wa mustashirki mmoja ambaye hakubaliani na wengine pia sio wa ‘wastani’ bali tunaweza kuuita ni wa ‘wastani kwa kiasi fulani.’ Kauli hii ya mwandishi wa ki-Misri ni kukubali kwa dhahiri ule ukweli kwamba huyu mustashirki pekee hakuweza kupata ushahidi wa kutosha katika msingi ambao kwamba angeweza kuwaunga mkono Bani Umayyah kwa uwazi zaidi na mtazamo wake juu yao kuweza kuwa wa wastani kuliko kuwa wa wastani kiasi fulani. Hata hivyo, tungependa kumwambia huyu mwandishi wa ki-Misri kwamba yupo pia mustashirki mwingine, ambaye amewaunga mkono Bani Umayyah kwa ukamilifu kabisa. 240

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 240

9/4/2017 3:47:56 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Yeye ni yule mwanahistoria wa Kifaransa, La Mius, ambaye ametoa uungaji mkono kamili kwa ukoo ule kwa sababu ya matilaba maalum. Tutaelezea juu ya maandishi ya mwanahistoria huyu baadaye. Ukiwaacha mustashirki hawa wawili wengi wao wametoa picha ya mwana wa Abu Sufyan na kizazi cha Marwan, ambayo haitapendwa na waunga mkono wao. Miongoni mwa mustashirki hawa, aliye maarufu zaidi ni Kazanofa ambaye anasema: “Tabia ya Bani Umayyah iliundwa na mambo mawili: Kwanza kabisa tamaa ya utajiri kwa kiasi cha ulafi; na pili tamaa ya ushindi ili kupora, na kwa ajili ya ufalme kufaidi starehe za dunia.” Aidha, wawe ni wanahistoria wa Kiarabu ama mustashirki; hakuna hata mmoja wao aliyetoa picha halisi ya Bani Umayyah kiasi kama iliyotolewa na khalifa wa Bani Umayyah, Walid bin Yazid katika mashairi yaliyotafsiriwa hapo chini: “Usiwataje watu wa Ukoo wa Sa’di. Sisi ni bora juu yao katika suala la idadi na vilevile la utajiri. Sisi tunashika madaraka juu ya watu na kuwadhalilisha kwa kila namna na kuwatesa kwa njia mbalimbali. Tunawadhalilisha na kuwafikisha karibu ya kuangamia na kuharibikiwa, na hapo pia wanakutana na udhalili na kuangamia tu.” Hata kama wafuasi wa Bani Umayyah watayakataa yote yale yaliyosemwa na wanahistoria wa zamani na wa sasa na mustashirki kuhusu tabia za Bani Umayyah, je, wanaweza kukataa yaliyosemwa na Walid bin Yazid? Husein Na Yazid Matukio yote haya ambayo Husein alikuwa ayapitie; yanathibitisha kwamba kwa mtazamo wa uadilifu, yeye alikuwa ameshika nafasi ya juu ya utukufu, na matukio yote ambayo kwamba Yazid aliyapitia ni ushahidi wa ukweli kwamba alikuwa katika hali ya chini kabisa ya fedheha. Ule msiba wa Karbala ni ushahidi tosha kwa ajili hiyo. Tukio hili linashuhudilia sana ufisadi wake mgumu. Yazid alikuwa ni mlevi wa kupindukia. Yeye alikuwa akivaa nguo za hariri. Alikuwa akipiga kijingoma. Husein mwana wa Ali na Yazid mwana wa Mu’awiyah walikuwa ndio watu waliokuja duniani kama vielelezo kamilifu vya sifa za koo mbili hizo, yaani, Bani Hashim na Bani Umayyah. Husein alikuwa ni Bani Hashim mkamilifu wa wakati wake, kama Yazid alivyokuwa Abd al-Shams. Kama zile sifa makhsusi za mtu zinaweza kuwa ndio picha halisi ya mazingira ambayo amelelewa, hakuna shaka kuhusu ule ukweli kwamba Husein na Yazid walikuwa ni mifano halisi ya familia zao. Husein aliwakilisha Bani Hashim na Yazid ali241

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 241

9/4/2017 3:47:56 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

wakilisha Bani Umayyah. Tofauti pekee ilikuwa kwamba Husein alikuwa kielelezo bora cha maadili na ubora wa Bani Hashim; ambapo Yazid alikuwa hana angalau hata zile sifa nzuri ambazo walikuwa nazo Bani Umayyah. Husein alikuwa ni mtoto wa binti yake Mtume, Fatimah na Ali ibn Abi Talib. Wakati alipozaliwa, Mtukufu Mtume alimchukua kwenye mapaja yake na kumtamkia ‘Adhana’ masikioni mwake ili kuingiza nafsi yake mwenyewe ndani ya nafsi ya mjukuu wake, kumfanya kuwa ni sehemu muhimu ya utu wake, na kugandamiza juu yake kwamba yeye amezaliwa kutekeleza kazi maalum, na kwamba lengo la maisha limekadiriwa kwa ajili yake. Katika siku ya saba ya kuzaliwa kwake Mtume alisema kwa furaha kubwa: “Nimempa mwanangu huyu jina la Husein.” Mtoto huyo alikuwa siku baada ya siku katika hali ambayo kwamba alikuwa na nafsi ya babu yake ndani yake, mapigo ya moyo ya baba yake, na chapa ya kina ya utume ndani ya akili yake. Sifa zote na ubora wake pia viliendelea kuwa dhahiri zaidi. Upitishaji wa sifa za mababu kwa watoto wao ni kanuni ya maumbile ambayo kuhusu hiyo hapawezi kuwa na shaka ya aina yoyote. Kama vile tu watoto wanavyorithi rangi, muonekano wa sura, sifa za kimwili na kadhalika kutoka kwa wahenga wao, wanarithi pia na maadili ya kawaida. Husein alibakia chini ya usimamizi wa babu yake hadi umri wa miaka saba. Baada ya kufariki kwa Mtume, masahaba zake waliendelea kumuiga katika suala la mapenzi kwa Husein. Sababu maalum ya kuonyesha kwao mapenzi juu yake ilikuwa ni kwamba maumbile yake yalifanana sana na yake ya Mtume. Hili linaonyeshwa na kauli za wale watu ambao walimuona Mtume na Husein vile vile. Majina mashuhuri ya mababu zao na mafanikio yao yana mengi ya kuhusika na maendeleo ya watoto wao, na kuyafanya maangavu mambo yao ya maisha ya baadae. Wakati mtoto anaposikia kuhusu mafanikio ya wahenga wake katika umri wake wa mwanzoni kabisa, picha yao inajichora katika bongo lake, na hatimae anazitwaa sifa na tabia za wahenga wake hao. Mtoto kwa kawaida anarithi tabia za mababu zake, lakini kuishi kwake pamoja nao katika sehemu ileile kunatupa athari kubwa juu yao. Mbali na Mtume, Husein pia alimuona baba yake anayestahiki kuheshimiwa. Aliuona uvumilivu wake, uthabiti, uadilifu, huruma, msaada juu ya walioonewa na hasira juu ya waonevu, na vile vile utendaji mwema na upole ulioonyeshwa kwa maadui.

242

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 242

9/4/2017 3:47:56 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Alifuatana na baba yake katika vita vya Ngamia, Siffin na Nahrwan, na akaona ujasiri wake wa kushangaza, na akajifunza kutoka kwake namna za kupigana kwa ajili ya wema, na pia akajua kutoka kwake jinsi ya kuyatoa muhanga maisha yake mtu kulinda wale walioonewa na wasiojiweza kutokana na udhalimu. Mtukufu mama yake Husein alikuwa bibi mpole sana na mwenye huruma. Kwa sababu ya upole huu hasa, alikuwa wakati wote akihuzunika kuona shida ambazo baba yake, Mtume na masahaba zake walizokuwa wakipatishwa na Maquraishi. Alisikitika sana katika siku ya vita vya Uhud wakati Waislamu wengi walipouawa mikononi mwa washirikina wa ki-Quraishi na miili yao kukatwa vipande vipande. Yalikuwa ni mandhari ya kusononesha sana kwake yeye kumuona baba yake akimlilia ammi yake Hamzah. Inasemekana kwamba baada ya kifo cha Mtume, Anas bin Malik alikwenda siku moja kumtembelea bibi Fatimah na kumuomba aidhibiti huzuni yake kwa faida ya afya yake mwenyewe. Yeye alitoa jibu hili tu: “Ewe Anas! Wewe ulivumilia vipi wakati wa kuuweka mwili wa Mtume kwenye kaburi?” Kisha akalia machozi, na Anas naye akaanza kulia. Alirudi na moyo ambao umevunjwa vunjwa na huzuni ya Fatimah. Husein alikuwa akimuona dada yake mdogo, Zainab, mwenye huzuni na akajihisi kumsikitikia sana. Husein alimwangalia mama na dada yake na akafikiria yale mateso na shida ambazo wakati ulikuwa umeyahifadhi kwa ajili yake mwenyewe, dada yake na kizazi chao. Alihisi kwamba karibuni tu, yeye na dada yake watakuja kutoa machozi juu ya kifo cha mama yao na halafu kuomboleza kifo cha kishahidi cha baba yao, na kizazi chao kitakuwa kikabiliane na shida kubwa. Siku chache baadaye, Husein alimsikia mama yake akitoa mapendekezo yafuatayo kwa dada yake Zainab: “Usiwaache Hasan na Husein. Wafanyie matunzo kamili. Baada yangu utekeleze zile kazi za mama yao.” Mama yake alivuta pumzi zake za mwisho na kufariki baada ya miezi mitatu ya kifo cha baba yake. Husein alikuwa amesimama kando yake na kumuaga mama yake. Wakati mwingine alimwangalia dada yake ambaye alikuwa amebumbuazwa na huzuni. Halafu akamwangalia baba yake ambaye alikuwa analia kwa uchungu sana juu ya kufariki kwa bibi Fatimah. Husein aliishi ujana wake katika hali kama hiyo ya masikitiko na huzuni. Wakati alipopata makamu aliwaona watu wakishindana, na kuzuia njia ya baba yake mtukufu katika kila hatua. Tabia za Mama wa waumini, Aisha na wafuasi wake zilimfanya 243

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 243

9/4/2017 3:47:57 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

asikitike zaidi. Aliuona pia usaliti uliokuwa ukifanywa na Mu’awiyah, Amr bin Aas, na vibaraka wao kwa baba yake. Hili liliongeza huzuni yake zaidi na akahisi kwamba isipokuwa pale maovu yatakapozimwa kwa ule ujasiri na nguvu ambayo kwayo baba yake alijitahidi kuizuia, maisha yatakuwa hayana maana yoyote. Siku ya huzuni kabisa ilikuwa ni ile ambayo mkono wa mhalifu na mtenda dhambi alipojeruhi paji la uso la baba yake adhimu wakati alipokuwa anaswali katika msikiti wa Kufa. Imam Ali hakuweza kunusurika kwa jeraha hili na akafariki baada ya siku mbili. Hivyo kile kikwazo katika njia ya wakandamizaji na madhalimu kwa ajili ya kuanzisha mamlaka yao kikawa kimeondolewa. Baada ya muda kiasi, kaka yake Hasan akakutana na kifo chake cha kishahidi kutokana na kulishwa sumu. Na huzuni yake na mshangao havikuwa na mpaka wakati alipoona kwamba Bani Umayyah na wafuasi wao walikuwa wanarusha mishale kwenye jeneza la mazishi ya ndugu yake. Pia alikuja kutambua kwamba Mu’awiyah alikuwa ameagiza kwamba baba yake Husein na kaka yake wawe wanatukanwa kutoka kwenye mimbari za misikitini. Kwa kweli yeye alimsikia Mu’awiyah mwenyewe akifanya hivyo. Kwa ufupi sababu mpya juu ya huzuni yake ziliendelea kujitokeza. Hizi ndizo sababu haswa ambazo zilifikia kilele chake katika masaibu ya Karbala – ile sehemu ambayo ule uovu mbaya kabisa ulitendeka kwa ushirikiano wa wapiganaji wakatili wa Yazid na maafisa wake waovu. Walifanya ukatili juu ya Husein na kikundi kidogo cha wafuasi wake na watu wa familia yake, ukatili ambao mtu anagwaya kuufikiria. Hivi ndivyo alivyolelewa Husein katika mtazamo wa urithi na mazoezi; na hizi zilikuwa ndio sababu za huzuni zake ambazo alikuwa azipitie kutoka wakati ule hasa wa kuzaliwa kwake. Kama alivyokuwa ameona yale mateso ya babu, baba na mama yake, huzuni na masikitiko vilikuwa vimetopea katika tabia yake. Ilikuwa ni kwa sababu ya sifa zilizorithiwa na kutwaliwa na Husein ambazo kwamba alikuwa wakati wote akisema: Uvumilivu ni ngazi, uaminifu ni ujanadume, kiburi ni upumbavu na unyonge na kushirikiana na waovu ni jambo ambalo linamfanya mtu kuwa na shaka na kuyumba. Jaribu kukipata kile kitu ambacho unastahiki. Ni fedheha na unyonge kuishi na madhalimu. Haki ni heshima na batili ni kutojiweza.

244

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 244

9/4/2017 3:47:57 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Yazid Alikuwa Ni Nani? Yazid alikuwa ni mtu ambaye alikuwa amerithi zile sifa na tabia zote mbaya za familia ya Bani Umayyah. Silika yake, imani zake, namna ya kufikiri na mwenendo wa kuangalia mambo mbalimbali vilikuwa ni sawa sawa kabisa kama vile vya Bani Umayyah kwa jumla. Licha ya maovu aliyoyarithi kutoka kwa wahenga wake, alikuwa pia na mwelekeo wa fitna na sifa za kishetani vile vile. Hakuwa na zile sifa dhahiri za baba yake ambazo zinachukuliwa kuwa ndio sifa zake (Mu’awiyah) njema ingawaje zilikuwa ni zana zake tu za kuimarishia utawala wake. Kwa kweli inaweza kusemwa kwamba wakati ambapo sifa zote mbaya za ukoo wake zilikuwa zimejumuika kwake yeye, hakuwa na tabia yoyote nzuri hata kidogo. Hapakuwa na msherehekaji mwingine miongoni mwa Bani Umayyah kama Yazid, na ilikuwa ni kwa sababu ya kuwa kwake mpenda starehe sana kwamba alipoteza maisha yake. Inasemekana kwamba siku moja, akiwa amepanda juu ya farasi, alikuwa akijaribu kumshinda mbio nyani. Katika mashindano haya, hata hivyo, alianguku kutoka juu ya farasi na akafa. Watu wa wakati wake wametoa picha yake sahihi na fupi kabisa kwa maneno haya: “Yeye alikuwa mlevi. Alikuwa akivaa nguo za hariri na alikuwa akipiga kijingoma.” Ikiwa Husein amethibitisha kuwa mfano wa wema na maadili mema, Yazid alithibitisha kuwa kielelezo kibaya kabisa cha maovu ya jadi yake. Kama Husein alikuwa mwenye huruma kwa wengine kama vile watu wakarimu kwa kawaida wanavyokuwa, Yazid hakuwa na mawazo ya kibinadamu na alikuwa hana aibu kabisa. Yazid alilelewa katika familia ambayo iliuchukulia Uislamu kama vuguvugu la kisiasa. Kwa mujibu wa Bani Umayyah, utume wa Mtukufu Mtume ulikuwa ni kisingizio tu cha kujipatia madaraka na mamlaka, na Uislamu ulikuwa na maana ya kuhamisha madaraka kutoka mikononi mwa Bani Umayyah na kwenda mikononi mwa Bani Hashim. Yazid aliwaona watu wa nchi yake kuwa kama ni jeshi tu ambalo kazi yake ilikuwa ni kudumu kuwa watiifu kwa mtawala. Machoni mwake lengo la kuwepo wale watu wa nchi yake ni kwamba wao wapasike kulipa mapato ya ardhi na kodi na kuongeza utajiri wa hazina ambayo ilikuwa itumike kwa mujibu wa apendavyo mtawala. Kwa vile Yazid alizaliwa na kulelewa katika familia kama hiyo, ilikuwa ni lazima kwamba yeye naye vile vile atwae njia zile ambazo zilitwaliwa na mababu zake, na watu wengine wa familia yake katika zama za jahilia na baada ya kuja kwa Uislamu. 245

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 245

9/4/2017 3:47:57 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Zaidi ya hayo, yeye alikuwa amelelewa katika nyumba ya baba ambaye alitumia viwango vikubwa vya pesa za hazina ya umma kama alivyotaka, kwa raha zake. Pale utajiri na ujahilia vinapochanganyika, matokeo yake hayawezi kuwa chochote kingine isipokuwa ufisadi na ubadhilifu. Ilikuwa ni kwa sababu hii kwamba, kama vile anavyokuwa kila mtu mjinga ambaye anamiliki utajiri, Yazid alikuwa mlevi na mwenye kupenda maisha ya starehe na alicheza na mbwa. Mara tu alipopanda kwenye kiti cha utawala alianza kutumia fedha kwa wingi mno kuendesha maisha ya ubadhilifu na utamanifu wa anasa. Aligawa viwango vikubwa vya fedha kwa washirika wake, watumwa, na watumwa wa kike, waimbaji na kadhalika. Alikuwa na idadi kubwa ya mbwa ambao walilala kando yake; na walivalishwa mapambo ya dhahabu na fedha na nguo za hariri, ambapo watu masikini, ambao kodi inakusanywa kutoka kwao kwa kulazimishwa, walishinda na njaa na kuteseka kwa shida. Alitawala kwa muda wa miaka mitatu na nusu tu, lakini katika kipindi kifupi hiki alijikusanyia fedheha, upumbavu na ufidhuli wote, ambavyo vilikuwa ni matokeo ya siasa za Bani Umayyah. Mbali na usherehekaji uliotajwa hapo juu na ubadhilifu ambao Yazid amerithi kutoka kwa wahenga wake, vile vile alifanya jinai nyingine nyingi mbaya kabisa. Katika mwaka wa kwanza wa utawala wake alimuua Imam Husein na wafuasi wake, na akawafanya watu wa familia yake kuwa wafungwa. Katika mwaka wa pili aliivamia na kuipora Madina bila ya kujali hata kidogo juu ya utakatifu wake. Aliwaruhusu askari wake kufanya kila lolote walilotaka na watu wa mji huo kwa kipindi cha muda wa siku tatu. Matokeo yake watu elfu kumi na moja ikiwa ni pamoja na masahaba mia saba wa Mtume kutoka miongoni mwa Muhajir na Ansari waliuawa na staha ya wasichana bikira takriban elfu moja zilihalifiwa. Ilikuwa ni silika ya kawaida ya Imam Husein kwamba analazimika kupambana dhidi ya udhalimu na ukandamizaji kwa kufuata mfano uliowekwa na babu na baba yake. Alikuwa mara zote akisema: “Ni aibu na fedheha kuishi pamoja na dhalimu.� Kinyume chake Yazid siku zote aliweka heshima juu ya watu makatili na waovu na akawapa zawadi kubwa kubwa kwa kutenda maovu mabaya. Na vile vile aliwataka na wengine wawaheshimu na kuwastahi watu kama hao. Kwa mfano, siku moja wakati alipokuwa anajishughulisha na kula na kunywa pamoja na marafiki zake, na Ubaidullah ibn Zaid, yule mhusika mkuu wa masaib ya Karbala alikuwa amekaa kulia kwake alimwambia yule muandaa divai kama ifuatavyo:

246

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 246

9/4/2017 3:47:57 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

“Nipatie mvinyo ambao kwamba utaifanya roho yangu itulie. Halafu toa mvinyo huo huo kwa ibn Zaid ambaye ni msiri na mdhamini wangu, na chanzo cha kupata kwangu ngawira za vita na kushinda mapambano.” (Kadhia hii ilitokea siku chache tu baada ya kuuawa kishahidi kwa Imam Husein). Kule kuheshimiwa ibn Zaid na Yazid kunafanana na kuheshimiwa kwa dhalimu na mhalifu mkubwa, Hajjaj. Kwa kifupi ikiwa katika wakati wa Mu’awiyah ‘jeshi tukufu’ lilikuwa ni pamoja na asali yenye sumu, basi ‘jeshi tukufu’ wakati wa Yazid lilikuwa ni sumu bila mchanganyiko wa asali. Wakati wa utawala wa Yazid ule moyo wa ushabiki wa kiBani Umayyah wa zama za jahilia ulifufuliwa kikamilifu. Hakuna katika matukio ya historia linaloweza kutoa mtu wa kupuuzika kuliko Yazid – yule yule Yazid ambaye alikuwa ndiye mtunzi wa msiba wa Karbala. Na vivyo hivyo, hakuna kati ya matukio ya kihistoria linaloweza kutoa mtu ambaye anapaswa kuwa na sifa ya utukufu ya hali ya juu kama Husein – Husein yule yule ambaye alikuwa ndiye shahidi wa Karbala. Kurasa zinazohusiana na Yazid ni nyeusi kabisa ambapo zile zinazohusiana na Husein zimejaa hadhi na heshima. Kwa upande mmoja kulikuwa na uchuuzi na uchifu wa Umayyah na watumwa wake na wauaji; na kwa upande mwingine kulikuwa na zile tabia na sifa bora za hali ya juu na ujasiri wa familia ya Abu Talib na watu wake huru na wenye ghera, na mashahidi katika njia ya haki na uadilifu. Mantiki na akili havina mafanikio sana ya kuthibitisha ukweli wa jambo kama yalivyo matukio yanayohusiana nalo. Kwa vile matukio yanakuwa na hoja zenye kuondoa shaka ndani yao yenyewe, basi hakuna shaka kuhusu ukweli kwamba yale matukio yote ambayo Husein alikuwa ayapitie yanathibitisha kwamba kutokana na mtazamo wa sifa za kimaadili, yeye alishika cheo cha hali ya juu kabisa, yale matukio yote ambayo Yazid aliyapitia ni ushahidi wa ukweli kwamba yeye alikuwa katika tabaka la chini kabisa la ushukaji wa hadhi. Masaibu ya Karbala ni ushahidi wa kutosha wa jambo hili. Tukio hili linatoa ushahidi wa kutosha kwa hilo, na litakuwa siku zote likielekeza kwenye tabia tukufu kabisa ya Husein, na ufisadi wa muovu wa waovu, Yazid. Kabla ya msiba wa Karbala, kulikuwa kumetokea kadhia nyingine ambamo alikuweko kwa upande mmoja Husein, yule mfano wa uaminifu na huruma ya kibinadamu, na kwa upande mwingine alikuweko Yazid ambaye alikuwa mfano wa ubadhilifu na ufisadi. 247

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 247

9/4/2017 3:47:57 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Kadhia hii, mbali na kubainisha zile sifa husika za Husein na Yazid, pia inakumbusha mkataba uliofanywa na Bani Hashim, ambao ulikuwa ukiitwa ‘Hilf al-Fuzul.’ Mkataba huu ulifanywa na wao kwa ushirikiano wa baadhi ya makabila ya Kiarabu. Moja ya dondoo zake ilikusudia kusema kwamba watia saini mkataba huu watawasaidia wanaokandamizwa, na kuzirudisha haki zao kutoka kwa wale wakandamizaji, na watawazuia wale watu wenye nguvu kutokana na kufanya uonevu kwa wanyonge na wasiojiweza. Wahenga wa Yazid walikuwa wameupinga mkataba huu na wale wa Husein waliuunga mkono kwa moyo wote. Kwa kweli, mmoja wa wahusuka wa kadhia hii ni Husein na mwingine ni Yazid. Huyu Yazid mwana wa Mu’awiyah alikuja kujua uzuri wa Urainab binti Ishaq ambaye alikuwa mke wa yule Quraishi Abdullah bin Salam. Urainab alikuwa ndio mwanamke mzuri sana aliyekamilika hasa wa wakati wake, na alimiliki utajiri mkubwa sana. Yazid alimpenda bila kumwona wala kukutana naye. Alipoteza subira zote na akalieleza jambo hili kwa mtumwa kipenzi wa Mu’awiyah aliyeitwa Rafiq. Yule mtumwa alimjulisha Mu’awiyah kuhusu mapenzi haya na akamwambia kwamba mwanae anapenda sana kumuoa Urainab. Mu’awiyah alimwita Yazid na kutaka kujua kutoka kwake kuhusu jambo hili. Yazid alikubali kwamba kila alichokiambiwa Mu’awiyah kilikuwa ni sahihi. Mu’awiya akasema: “Tulia na uwe mvumilivu mwenye subira. Kutafanywa kitu juu ya hili.” Yazid akasema: “Ni bure tu kuniliwaza mimi sasa hivi kwa sababu jambo lenyewe tayari limekwisha. Tayari amekwisha kuolewa.” Mu’awiyah akasema: “Mwanangu mpendwa! Itunze siri hiyo moyoni mwako, kwa sababu kama itatobolewa haitakusaidia lolote. Mwenyezi Mungu hukamilisha kila kile alichokiamulia na ambacho kimekwishatokea hakiwezi kusaidia tena.” Mu’awiyah alianza kufikiri namna ya kulitatua tatizo hili na kutimiza matakwa ya Yazid ya kumuoa Urainab. Abdullah ibn Salam, mumewe Urainab alikuwa kwa wakati huo ni gavana wa Iraqi. Mu’awiyah alimwandikia barua akisema: “Nina shughuli ya haraka na muhimu na wewe. Tafadhali njoo unione mapema iwezekanavyo. Jambo lenyewe ni lenye manufaa kwako.” Katika kuipokea barua ya Mu’awiyah, Abdullah aliondoka kwenda Syria mara moja na akaonana na Mu’awiyah. Alipokelewa kwa heshima kubwa na taadhima. Wakati huo Abu Darda na Abu Huraira, masahaba wawili wa Mtume walikuwa pia wanapatikana hapo Damascus. Mu’awiyah aliwaita hawa na akawaambia: “Binti yangu aitwaye fulani sasa amekua 248

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 248

9/4/2017 3:47:57 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

na nina shauku ya kumuozesha kwa mume. Ninadhani kwamba Abdullah ibn Salam ni mtu mzuri na ningependa binti huyu aolewe naye.” Wote wawili wakamsifia Mu’awiyah kwa akili na uchamungu wake na wakasema kwamba yale yote aliyokuwa ameyafikiri yalikuwa yanafaa kabisa. Mu’wiyah akawaambia: “Wote nyie mkamuone Abdullah na mkamueleze yeye jambo hili na muyajue maoni yake kuhusu hili. Ingawa nimemruhusu binti yangu kuolewa na mume amtakaye, lakini ninayo hakika kwamba atampenda Abdullah bin Salam na hatokataa kuolewa naye.” Abu Darda na Abu Huraira wote wakaenda kukutana na Abdullah. Wakati huo huo Mu’awiyah alikwenda kwenye kasiri lake na akamwambia binti yake: “Ewe binti yangu mpendwa! Hebu nisikilize haya mimi nitakayokwambia. Wakati watakapokujia Abu Darda na Abu Huraira na kukwambia kwamba mimi ninataka kukuozesha kwa Abdullah bin Salam, wewe useme hivi: “Kwa kweli Abdullah ni mtu mzuri na ni ndugu wa karibu na mwenye hadhi sawa na sisi. Hata hivyo, yeye tayari amekwisha kumuoa Urainab binti ya Ishaq na mimi ninahofia kwamba kama nitaolewa naye ninaweza vile vile nikawa na wivu juu yake kama walivyo wanawake wengine. Ikiwa, katika hali hiyo nitasema neno lisilofaa kuhusu Abdullah, nina wasiwasi kwamba nitazikaribisha ghadhabu za Mwenyezi Mungu kwa kufanya hivyo. Hata hivyo, ikiwa Abdullah atamtaliki Urainab mimi ninakubaliana na kuolewa naye.” Wakati Abu Dard na Abu Huraira walipouwasilisha ule ujumbe wa Mu’awiyah kwake Abdullah bin Salam, yeye alifurahi kupita kiasi na akawaambia waende wakamjulishe Mu’awiyah kwamba pendekezo hilo limekubaliwa na yeye. Walipomjulisha Mu’awiyah juu ya maendeleo haya, yeye aliwaambia: “Kama nilivyokwisha kuwaambia, mimi ninaitaka ndoa hii. Hata hivyo, mimi nimekwishamruhusu binti yangu kuolewa na mtu wa chaguo lake. Kwa hiyo, ninyi mngekwenda kwake na kumuuliza iwapo yeye yupo tayari kuolewa na Abdullah bin Salam.” Walipomwendea msichana huyo, yeye aliwapa majibu yale yale ambayo alikuwa ameyafundishwa na Mu’awiyah kuyatoa. Halafu wao wakayafikisha majibu yake haya kwa Abdullah. Pale Abdullah bin Salam alipokuja kufahamu kwamba isingewezekana kumuoa binti ya Mu’awiyah isipokuwa kwamba mpaka amuache mke wake, yeye alitenzwa nguvu na hamu kubwa ya kumpata, na akamtaliki mke wake Urainab. Aliwaambia Abu Darda na Abu Huraira: “Kuweni mashahidi katika jambo hili la kwamba mimi 249

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 249

9/4/2017 3:47:57 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

nimemtaliki Urainab. Mnapaswa mwende mkamwarifu Mu’awiyah kuhusu hili na papo hapo muwasilishe pendekezo langu (la posa ya binti yake) kwake.” Walipofika kwa Mu’awiyah na kumweleza yale yaliyotokea, yeye akasema: “Loh! Abdullah amefanya nini? Kwa nini amemtaliki mke wake? Asingekuwa na haraka kiasi hicho. Angeweza kusubiri kwa siku chache mimi ningeweza kupanga ndoa yake na binti yangu bila ya kuruhusu mambo kutokea kama hali ilivyotokea. Basi, vyovyote iwavyo, mnapaswa sasa mwende na mumuulize binti yangu iwapo anakubaliana na ndoa hii.” Abu Darda na Abu Huraira walimwendea binti yake Mu’awiyah kwa mara nyingine tena na wakamwambia kwamba Abdullah amekwisha mtaliki na kumwacha mke wake. Walieleza pia kwamba Abdullah alikuwa mtu mwenye akili nzuri sana na hodari na wakamuuliza iwapo yeye alikuwa tayari kuolewa naye. Binti yake Mu’awiyah akajibu: “Abdullah bila shaka anayo nafasi ya juu sana miongoni mwa Quraishi. Hata hivyo, kama mnavyotambua kwamba ndoa sio jambo la thamani ndogo kiasi kwamba mtu anaweza kukubali tu bila ya kutafakari kwa makini juu ya jambo hilo. Huo ni mkataba wa maisha yake yote mtu. Kwa hiyo, waungwana ninyi mnaweza kwenda sasa. Mimi nitafikiri juu ya suala hili na kuwapeni majibu baadaye.” Wote wawili wakamtakia kila la kheri na wakaondoka. Halafu wakaenda kwa Abdullah bin Salam na kumfahamisha kuhusu kile alichokisema binti huyo. Abdullah akasema: “Sawa sawa. Ngoja sisi tusubiri. Kama halitakamilishwa leo, basi litakamilishwa kesho.” Lilikuwa ni gumzo la mjini kwamba Abdullah bin Salam amemwacha mke wake na ametoa posa kwa binti yake Mu’awiyah. Kwa vile wote walikuwa wanaulewa ujanja wa Mu’awiyah na tabia mbovu za Yazid, walimshutumu na kumlaumu Abdullah kwa kumta liki mke wake bila kwanza kupata ridhaa ya binti yake Mu’awiyah. Baada ya siku chache Abdullah aliwatuma Abu Darda na Abu Huraira tena kwa binti yake Mu’aiyah. Wao wakamshauri atoe jibu la mwisho ambapo hapo yeye akasema: “Nina hakika kwamba Mwenyezi Mungu ameniamulia vema, kwani Yeye huwa hamtupi yule anayemtegemea. Mimi nimetafakari sana juu ya suala hili na nimefikia uamuzi kwamba kuolewa kwangu na Abdullah hakutakuwa kwenye ma250

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 250

9/4/2017 3:47:57 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

fanikio. Vile vile mimi nimeshauriana na wanitakiao mema wangu katika jambo hili. Baadhi yao wameikubalia ndoa hiyo lakini wengine wameipinga.” Wakati Abdullah alipokuja kutambua kuhusu yale majibu ambayo yalikuwa yametolewa na binti yake Mu’awiyah, yeye alipata uhakika kwamba alikuwa amelaghaiwa. Hili lilimsikitisha sana kupita kiasi. Habari zilipoenea zikawa ndio gumzo la mjini. Watu wakamlaumu Mu’awiyah kwa kule kumghilibu Abdullah na kumfanya amwache mke wake ili aweze baadaye kuolewa na Yazid. Mu’awiyah alipata mafanikio katika hatua ya mwanzo ya mpango wake wa kutimiza matakwa ya mwanawe lakini hatimae utashi wa kimungu uliupinga utaratibu huo usifanyike. Mpango wake ulishindwa kutokana na kuingiliwa na Husein ambaye alikuwa amekulia katika mtindo wa maisha wa baba yake maarufu. Kuwasaidia wanaokandamizwa na kuonewa kulikuwa ni tabia yake. Wakati kipindi cha kusubiri – Edda – kilipokwisha Mu’awiyah alimtuma Abu Darda kwake Urainab kuwasilisha posa kwa niaba ya Yazid. Abu Darda aliondoka Damascus na akafika Kufa. Ilitokea kwamba Husein bin Ali pia alikuwa yuko Kufa wakati huo. Abu Darda akaona inafaa kwanza akatoe heshima zake kwa mtoto wa Mtume. Kwa hiyo alijifikisha mwenyewe mbele za Imam kwanza. Imam Husein akamuuliza sababu za kutembelea kwake Kufa. Abu Darda akamfahamisha kwamba yeye alikuwa ametumwa na Mu’awiyah kuja kumposa Urainab bint Ishaq kwa niaba ya mwanawe Yazid. Kisha akamsimulia Imam kwa kirefu matukio yote yaliyokuwa yamekwishapita. Imam Husein akasema: “Hata mimi pia nilifikiri kwamba Urainab ataolewa na mtu mwingine na nilinuia kupeleka posa yangu baada ya ‘edda’ yake itakapokuwa imekwisha. Sasa kwa sababu wewe umekishawasili hapa, itakuwa ni bora kama utawasilisha posa yangu kwake. Yeye anaweza akamchagua yeyote amtakaye. Hata hivyo, mimi niko tayari kumlipa mahari sawa na ile aliyoahidiwa na Yazid.” Abu Darda akaahidi kuifikisha posa ya Imam kwa Urainab. Kisha akamuaga Imam Husein na akaondoka na kwenda nyumbani kwake Urainab. Akamwambia: “Bibi! Imejaaliwa kwamba Abdullah bin Salam aweze kukutaliki na kukuacha wewe. Hutakuwa mwenye kupoteza kwa sababu hiyo. Yazid bin Mu’awiyah na Husein ibn Ali wote wanapenda kukuoa wewe. Wote wamewasilisha posa zao kwako kupitia kwangu. Unaweza ukamchagua yeyote unayemtaka.” Urainab akanyamaza kimya kwa kitambo kiasi na halafu akasema: “Kama mtu mwingine angeleta posa hizi mbili kwangu, mimi ningekuita wewe kwa ajili ya 251

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 251

9/4/2017 3:47:57 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

ushauri, na ningetekeleza kwa kulingana na pendekezo lako. Sasa kwa vile wewe mwenyewe ndiye uliyeleta posa hizi, ninakuachia wewe uamuzi wa mwisho.” Abu Darda akajibu: “Ilikuwa ni wajibu wangu kuwasilisha posa hizi kwako, lakini wewe mwenyewe ndiwe hakimu bora katika suala hili.” Urainab akasema: “Hapana; hilo haliko hivyo. Mimi ni mpwa wako na siwezi nikaamua katika suala hili bila kutaka ushauri wako.” Pale Abu Darda alipoona kwamba amedhamiria juu ya kupata maoni yake, yeye akasema: “Mimi ninahisi kwamba huyu mtoto wa Mtume ni chaguo bora zaidi.” Urainab akasema: “Mimi ninakubaliana na wewe. Na vile vile ninampenda.” Imam Husein ndipo akamuoa Urainab na akamlipa kile kiwango kilichoamuliwa cha mahari. Mu’awiyah alipokuja kufahamu juu ya kile kilichotokea alipata kukasirika sana na akamtukana Abu Darda. Halafu akajisemea mwenyewe: “Abu Darda hakuwa na makosa. Lilikuwa ni kosa langu mwenyewe. Kama mtu anakabidhi kazi ngumu kama hiyo kwa mtu juha ni lazima ashindwe.” Wakati wa kuondoka kwenda Damascus, Abdullah bin Salam alikuwa amekabidhi kiasi kikubwa cha fedha kwa Urainab. Baadae pale alipomtaliki, na binti yake Mu’awiyah naye pia akakataa kuolewa naye, ilikuja kujulikana kwa watu kwamba Abdullah alikuwa ameghilibiwa na Mu’awiyah na akafanywa amuache mke wake. Hili lilikuwa ni jambo la fedheha kwa Mu’awiyah na yeye akamchukulia Abdullah kuhusika na lawama za hilo. Kwa hiyo, yeye akamfukuza kazi na akasimamisha malipo yake ya mshahara. Abdullah akawa hana pesa kabisa. Kwa hiyo, yeye akarudi Iraqi kwa matumaini kwamba anaweza akazirudisha kutoka wa Urainab zile pesa ambazo alikuwa amemuachia. Hata hivyo, yeye alipatwa na wasiwasi kwamba Urainab anaweza akakataa kumrudishia pesa hizo kutokana na tabia yake mbaya na kwa kule kumtaliki kwake bila ya sababu ya haki. Baada ya kurejea kwake Iraqi, alikutana na Imam Husein na akasema: “Kama ambavyo ni lazima utakuwa unatambua, nilikuwa nimeghilibiwa na kufanywa nimtaliki Urainab. Wakati nilipokuwa ninaondoka kwenda Damascus mimi nilimuachia pesa kama amana.” Kisha akamsifia sana Urainab na akasema: “Nitashukuru sana endapo utazungumza naye na kumuomba anirudishie pesa hizo. Inawezekana kwamba kwa kuwa na kiasi hicho cha pesa mkononi ninaweza nikaokoka kutokana na ufukara.” 252

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 252

9/4/2017 3:47:57 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Imam Husein alikwenda kwa Urainab na akasema: “Abdullah bin Salam amenijia. Akakusifia sana wewe kwa uaminifu wako ambao umenifurahisha sana mimi. Pia aliniambia kwamba alikukabidhi kiasi cha pesa wakati alipokuwa anaondoka kwenda Damascus. Ingefaa tu kama utamrudishia pesa hizo kwa sababu nadhani kile alichokieleza ni sahihi.” Urainab akajibu: “Ni kweli kwamba aliniachia mifuko fulani, lakini sijui ndani yake mna kitu gani. Bado ingalipo imefungwa, kama ilivyokuwa. Nitaileta kwako nawe unaweza ukairudisha hiyo kwake.” Imam Husein akamsifia sana Urainab katika kuyasikia haya na akasema: “Je, haitakuwa bora kama nikimwita yeye hapa ili wewe uweze kumrudishia mifuko hiyo wewe mwenyewe?” Kisha akakutana na Abdullah bin Salam na akamwambia: “Nimefikisha ujumbe wako kwa Urainab. Anakiri kumwachia kwako mifuko kadhaa; bado iko imefungwa kama ilivyokuwa. Itakuwa bora kama utakuja kwa Urainab na kuichukua mifuko hiyo kutoka kwake.” Abdullah alijihisi aibu sana na akasema: “Ningekuomba ufanye mipango ya kurudishwa fedha hizo kwangu.” (yaani: ninaona aibu kukabiliana na Urainab). Imam Husein akamjibu: “Hapana. Hilo haliwezi kuwa. Unapaswa kuzichukua fedha hizo kutoka kwake kwa namna ileile ambayo ulizitoa kwake.” Kwa hiyo alimchukua Abdullah mpaka nyumbani kwake na kisha akamwambia Urainab: “Abdullah mwana wa Salam amekuja na anataka vile vitu ambavyo alikukabidhi. Virudishe hivyo kwake katika hali ileile ambayo ulivichukua kutoka kwake.” Urainab akaileta ile mifuko, na akiiweka nje ya pazia akamwambia: “Kile ulichonikabidhi mimi hiki hapa.” Abdullah alimshukuru Urainab na akamsifu sana kwa uaminifu wake. Halafu Imam Husein akaondoka mahali hapo na kuwaacha wenyewe. Abdullah akavunja kifungo cha mfuko, akachukua kiasi cha dinari kutoka humo na akaziwakilisha kwa Urainab akimuomba azikubali na kuzipokea kutoka kwake. Papo hapo machozi yakaanza kutoka machoni mwao na wakaanza kulia kwa sauti kubwa. Imam Husein alizisikia sauti hizo za vilio vyao. Ndipo akarudi tena pale chumbani na akasema kwa upole sana: “Hebu nisikilizeni. Ninamuomba Mwenyezi Mungu ashuhudie kwamba nimemtaliki Urainab sasa hivi tu. Ninamuomba Mwenyezi Mungu ashuhudie kwamba sikumuoa yeye kwa sababu ya uzuri wake au utajiri. Nilichokitamani mimi kilikuwa kwamba iwezekane kuwa halali juu yake kuolewa tena na mume wake wa kwanza.” 253

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 253

9/4/2017 3:47:57 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Hivyo Urainab akawa mke wa Abdullah bin Salam kwa mara nyingine tena na njama za Mu’awiyah zikashindwa. Baada ya kumuoa tena Urainab, Abdullah alimwambia: “Unapaswa kurudisha kile kiasi cha mahari ambacho Imam alikupatia.” Urainab akazileta zile fedha na akampa Abdullah azitoe kwa Imam. Hata hivyo, Imam Husein alikataa kuzipokea fedha hizo na akasema: “Thawabu nitakazopata kesho Akhera kwa ajili ya amali njema hii ni bora kabisa kuliko utajiri wa kidunia.” Yule Bani Hashim, Ali ibn Abi Talib alisema: “Namuapa Mwenyezi Mungu kwamba mimi sikulimbikiza hazina kutoka kwenye dunia yenu kama wengine; na sikukusanya utajiri na mali. Sikutumia vazi lolote isipokuwa joho hili lililochakaa. Kama ningependa ningeweza kula asali na ngano na pia ningeweza kuvaa nguo za hariri. Hata hivyo, haiwezekani kwamba tamaa zinizidi nguvu mimi na ulafi uweze kunifanya nile chakula kitamu. Inawekana kwamba anaweza akawepo mtu ndani ya Hijazi na Yamama ambaye anaweza kuwa hatarajii kupata hata tonge la chakula na akawa hajala na kujaza tumbo lake katika maisha yake yote. Hivi nijitosheleze mwenyewe kwa chakula na nilale usingizi mnono wakati wanaweza kuwepo katika mzunguko wangu, watu wengi ambao wanateseka kwa njaa? Hivi mimi niwe Amirul-Mu’minin kwa jina tu na nisishiriki matatizo na huzuni za watu?” Alimwandikia gavana wa Ahwaz hivi: “Namuapa Mwenyezi Mungu kuwa kama nitakuja kutambua kwamba umetumia vibaya kitu chochote; kikubwa au kidogo ambacho ni mali ya Waislamu nitakupa adhabu kali kiasi ambacho itakufanya uwe masikini, uliyelemewa na kufedheheka.” Kinyume chake Mu’awiyah bin Abu Sufyan alikuwa akitumia kusema: “Ardhi ni mali ya Mwenyezi Mungu, na mimi ni khalifa Wake. Ninaweza kuchukua chochote ninachotaka kutoka kwenye mali ya Mwenyezi Mungu na pia ninayo haki juu ya kile nitakachoacha.” Mu’awiyah, Yazid, Marwan bin Hakam na watawala wengine wa Bani Umayyah walitumia fedha juu ya wafuasi wao na marafiki ili kuimarisha serikali yao na kudumisha mamlaka yao. Walikata vichwa vya watu. Walikuwa na jeshi la asali iliyochanganywa na sumu na pia la sumu bila asali. Makundi yote, yaani Ali na kizazi chake na vile vile Mu’awiyah, Yazid na Bani Umayyah wengine walikuwa na wafuasi wao husika.

254

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 254

9/4/2017 3:47:57 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Wafuasi Wa Makundi Hayo Mawili Sifa kuu au tabia bora kabisa ya wafuasi wa ukoo wa Abu Talib ilikuwa ni ukarimu wao. Lengo la maisha yao lilikuwa kwamba wakati wote wawasaidie wanaokandamizwa, kuendeleza imani za kweli na kutoa muhanga maisha yao katika njia ya haki. Idadi yao bila shaka ilikuwa ni ndogo sana. Hili, hata hivyo, halikuleta mapungufu, kwa sababu watu wakarimu na wenye fikra tukufu wakati wote wanakuwa wachache kwa idadi, lakini zile athari nzito wanazoacha nyuma yao hazifutiki kabisa, na yale matokeo ya juhudi zao siku zote yana athari nyingi. Udogo wa idadi yao ni ushahidi tosha wa umashuhuri wa lengo lao, na ukubwa wa nia zao. Wakati mwingine hutokea kwamba mtu mmoja anatekeleza tendo gumu ambalo haliwezi kutekelezwa na maelfu yakichanganywa pamoja. Wafuasi wa kizazi cha Abu Talib vile vile walikuwa madhubuti katika imani zao, na imara katika kuziendeleza, ingawa idadi yao ilikuwa ndogo. Hawa hawa marafiki hasa wa Imam Ali waliahidiwa na Mu’awiyah utajiri na vyeo vikubwa ili kwamba waweze kumtukana Imam Ali na kizazi chake, lakini wao wakakataa kufanya hivyo. Kisha yeye akawatishia kwa mateso. Wao hata hivyo, walipendelea kuvumilia matatizo yote kuliko kumtukana Imam Ali. Siku moja Mu’awiyah alikuwa amekaa na washirika wake na Ahnaf bin Qais pia alikuwepo. Wakati huo huo mtu mmoja wa Syria akafika na akaanza kutoa hotuba. Mwishoni mwa hotuba yake akamtukana Ali. Papo hapo Ahnaf akamwambia Mu’awiyah: “Bwana! Kama mtu huyu atakuja kutambua kwamba wewe unafurahia iwapo mitume wakitukanwa, yeye atawatukana vile vile. Muogope Mwenyezi Mungu na usijihangaishe na Ali zaidi ya hapo. Yeye tangu hapo amekwishakutana na Mola Wake. Sasa hivi yuko peke yake ndani ya kaburi lake na ni matendo yake tu yaliyoko pamoja naye. Namuapa Mwenyezi Mungu kwamba upanga wake ulikuwa umetakata kabisa na mavazi yake pia yalikuwa masafi na nadhifu. Msiba wake ni mkubwa.” Kisha mazungumzo yafuatayo yakatokea baina yake na Mu’awiyah: Mu’awiyah: O Ahnaf! Umetupa mavumbi machoni mwangu na umesema kila ulilolitaka. Wallahi utapanda kwenye mimbari na kumtukana Ali. Kama hutamtukana kwa hiari yako, basi utalazimishwa kufanya hivyo.

255

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 255

9/4/2017 3:47:57 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Ahnaf: Itakuwa bora kwako wewe kuniacha mimi nisifanye hivyo. Hata hivyo, wewe hata ukinilamisha mimi sitatamka maneno kama hayo hata moja. Mu’awiyah: Simama na upande kwenye mimbari. Ahnaf: Nitakapopanda kwenye mimbari nitafanya mambo kwa uadilifu. Mu’awiyah: Iwapo utafanya uadilifu ni nini utakachosema? Ahnaf: Baada ya kuipanda mimbari nitamtukuza Mwenyezi Mungu Mtukufu; halafu nitasema hivi: “Enyi watu! Mu’awiyah ameniamrisha nimtukane Ali. Bila shaka Ali na Mu’awiyah walipigana. Kila mmoja wao alidai kwamba yeye na kundi lake walikuwa wamekosewa. Hivyo, nitakapokuwa namuomba Mwenyezi Mungu nyote mseme ‘Amin.’ Halafu nitasema: ‘Ewe Allah mlaani yule ambaye, kati ya wawili hawa ni muasi na uwafanye malaika Wako na mitume na viumbe wengine wote wamlaani yeye. Ewe Allah! Shusha laana zako juu ya kundi la uasi. Enyi watu! Semeni ‘Amin.’” Oh Mu’awiyah, mimi sitasema kingine zaidi au pungufu kuliko haya hata kama itabidi nipoteze maisha yangu. Mu’awiyah: Kwa hali hiyo ninakusamehe (kupanda kwenye mimbari na kulaani). (Iqdal-Faraid, Juz. 2, uk. 144 na Mustatraf, Juz. 1, uk. 54). Nyakati zingine ilitokea kwamba Mu’awiyah, ili kuonyesha chuki yake dhidi ya Ali, yeye aliwatesa wafuasi wake. Watu wale hawakuweza kulivumilia hili (la kulaaniwa Ali) na wakamtukana Mu’awiyah na kizazi chake. Wao walifanya hivyo licha ya ukweli kwamba kwa wakati huo Ali alikuwa kaburini kwake, na hapakuwa na manufaa yoyote yaliyoweza kutegemewa kutoka kwake, na yule katili na dikteta Mu’awiyah alikuwa ndio mtawala wa zama hizo. Historia imesimulia matukio mengi ambayo yanaonyesha kwamba watu waliichukia vibaya sana tabia ya Mu’awiyah. Yeye alimnyonga Hujr ibn Adi, sahaba maarufu wa Mtume na marafiki zake kwa sababu tu kwamba walikataa kumlaani Ali na kizazi chake kutoka juu ya mimbari. Tutatoa maelezo ya kina kuhusu kadhia hii baadaye. Wafuasi wa Ali, kwa ghera kabisa waliendelea kutafuta maadili ya hali ya juu na sifa nzuri ambazo zilikuwa zimepandikizwa na yeye katika nyoyo zao mpaka zikazaa matunda. Wote hawa, imma wanaume au wanawake, wakubwa kwa wadogo, walikuwa wanafanana. Katika kipindi cha utawala wake, wakati fulani Mu’awiyah alikwenda Makkah kuhiji. Aliulizia kuhusu mwanamke aliyekuwa anaitwa Darmiyah Hajuniyah ambaye alitokana na kabila la Kinanah na akafahamishwa kwamba alikuwa bado yungali hai. 256

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 256

9/4/2017 3:47:57 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Darmiyah alikuwa ni mwanamke mwenye rangi nyeusi aliyeumbwa vizuri. Mu’awiyah akamwita na katika kuwasili kwake mazungumzo yafuatayo yakatokea baina yao: Mu’awiyah: Ewe binti ya Ham!47 Wewe umekujaje hapa? Darmiyah: Iwapo unaniita mimi ‘binti ya Ham’ kwa mzaha naweza kukwambia kwamba mimi sio kizazi cha Ham. Mimi ninatokana na kabila la Kinanah. Mu’awiyah: Uko sahihi kwa hilo, hata hivyo, unafahamu kwa nini nimekuita? Darmiyah: Mwenyezi Mungu pekee ndiye ayajuaye mambo yaliyofichika. Mu’awiyah: Nimekuita ili uweze kuniambia ni kwa nini ulimpenda sana Ali na ukawa mwenye uhasama juu yangu. Darmiyah: Ningekuomba unisamehe katika kulijibu swali hili. Mu’awiyah: Hapana; hilo haliwezekani. Ni lazima unipe majibu. Darmiyah: Kama unasisitiza juu ya kupata jibu basi sikiliza nitakayosema. Nilimpenda Ali kwa sababu alikuwa ni mtawala muadilifu na alimpatia kila mtu kilichokuwa haki yake. Na nilikuwa dhidi yako kwa sababu ulishindana na mtu ambaye alikuwa ndiye mwenye kustahiki zaidi kuliko wewe kuwa mtawala, na ulitamani kitu ambacho ulikuwa hustahili. Nilimtii Ali kwa sababu Mtume alikuwa amemteua yeye kama Amirul-Mu’minin na mtawala wetu. Yeye aliwapenda masikini na wenye dhiki na aliwaheshimu wale waumini wa kweli. Na nilikudharau wewe kwa sababu ulimwaga damu ya Waislamu bila sababu ya haki, ulitoa hukumu za kionevu na kuamua mambo kiholela. Mu’awiyah: Hivi ni kwa sababu hiyo ndio maana tumbo lako limevimba, kifua chako kimechomoza, na matako yako yakawa manene hivyo. Dirmiyah: Namuapa Mwenyezi Mungu kwamba mambo haya yanasemwa kimethali kuhusu mama yako na sio kuhusu mimi. Mu’awiyah: Ngoja kidogo. Nimesema jambo zuri tu. Wakati tumbo la mwanamke linapokuwa kubwa huwa anazaa mtoto mwenye afya nzuri. Pale kifua chake kikiwa kikubwa anaweza kumnyonyesha vizuri mwanawe. Na wakati matako yake yanapokuwa manene anaonekana mzuri anapokuwa amekaa. Sasa, hebu niambie, je uliwahi kumuona Ali? 47

abii Nuh alikuwa na watoto wa kiume watatu walioitwa Ham, Sam na Japhet. Lile taifa lenye rangi nyeusi N ni kizazi cha Ham. Mu’awiyah alimwita ‘binti ya Ham’ kwa namna ya mzaha kwa sababu ya rangi yake nyeusi. 257

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 257

9/4/2017 3:47:57 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Darmiyah: Ndio, Wallahi nimemuona. Mu’awiyah: Ulimuonaje wewe? Darmiyah: Ninauapa Mwenyezi Mungu kwamba nilimuona katika hali ambayo kwamba mamlaka hayakufanya awe na kiburi kama wewe na cheo cha ukhalifa pia hakikumfanya awe na majivuno kama wewe. Mu’wiyah: Je, uliwahi kumsikia akizungumza? Darmiyah: Ndio, Wallahi nilimsikia, kwa maneno yake alikuwa akiondosha shaka na giza la mioyo na kuitia nuru katika namna ile ile ambamo mpako wa dhahabu unavyong’arisha chombo. Mu’awiyah: Hiyo ni kweli. Sasa niambie ni nini ninachoweza kukufanyia wewe? Darmiyah akamuelezea kuhusu mahitaji yake. Papo hapo Mu’awiyah akamuuliza: Endapo nitakutimizia mahitaji yako utanifanya mimi kuwa sawa na Ali?” Darmiyah akajibu vikali: “Wewe huna cha kulingana naye kabisa.” Mu’awiyah akayatimiza mahitaji yake na akasema: Wallahi kama Ali angukuwa yuko hai asingekupatia utajiri kiasi hiki.” Darmiyah akajibu: “Sawa kabisa, umesema kweli. Yeye hakutoa kamwe hata pene moja kutoka kwenye mali ya Waislamu kumpa mtu yeyote yule isipokuwa awe na haki nayo.” (Balaghat an-Nisa, uk. 72 na Iqd-alFarid, Juz. 1, uk.216). Wakati mmoja Adi bin Hatim alikuja kumuona Mu’awiyah wakati wa kipindi cha utawala wake. Mu’awiyah akamuuliza kwa kejeli: “Ni nini kilichompata ‘Tarafat’? 48 Adi akajibu: “Waliuawa wakati wakimsaidia Ali.” Mu’awiyah akasema: “Ali hakuwa mwadilifu kwako. Watoto wako wewe waliuawa lakini wanawe walibakia hai.” Adi akajibu: “Hata mimi pia sikuwa muadilifu. Ali tayari amekwisha kuuawa lakini mimi bado niko hai.” Mu’awiyah aliumbuliwa moyoni kwa kuyaona mapenzi haya na utii wa Adi juu ya Ali. Alisema kwa namna ya kutishia: “Tone moja la damu ya Uthman bado limebakia. Linaweza kuoshwa tu kwa damu ya mmoja wa waungwana wa Yemen (yaani Adi).” Adi hakuvijali vitisho vya Mu’awiyah na akasema: “Naapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba zile nyoyo ambazo tulibakia kuwa maadui zako bado zingaliko kwenye vifua vyetu, na zile panga ambazo kwazo tulipigania dhidi yako bado ziko mabegani mwetu. Kama utatusogelea kwa hila hata kwa kiasi cha kidole tutasonga kukuelekea kwa kiasi cha kudumu. Ni rahisi kwetu kwamba vichwa vyetu vikatwe na vifua vy48

Tareef, Tarif na Turfa, watoto wa kiume wa Adi. 258

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 258

9/4/2017 3:47:57 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

etu vikanyagwe juu yake ukilinganisha na kusikia kwetu japo neno dhidi ya Ali. Toa upanga kwa muuaji (ili aweze kukata kichwa changu).” Mu’awiyah ndipo akageukia kwenye utoaji sifa bandia kama ilivyokuwa kawaida yake. Akiwahutubia wale waliokuwepo pale akasema: “Haya ni maneno ya hekima. Yaandikeni.” (Muruujul-Dhahab, Juz. 2, uk. 309). Mu’wiyah wakati mmoja alikwenda Makkah kwa ajili ya kufanya Hijja. Wakati alipofika Madina na akakutana na Sa’d bin Abi Waqqas, alimuomba waongozane naye. Sa’d akakubali. Baada ya kutekeleza kanuni za Hijja wote wakaenda hadi Daral-Nadwa na wakaongea hapo kwa muda mrefu. Kwa vile Sa’d alikuja kuhiji kwa pendekezo la Mu’awiyah, yeye Mu’awiyah alidhani kwamba Sa’d alikuwa anamuunga mkono. Ili kuweza kutambua ni kwa kiasi gani Sa’d alikuwa akimuunga mkono mwelekeo wake juu ya Ali, alianza kumlaani na kumtukana Ali na akamuuliza Sa’d kwa kumbembelaza: “‘Kwa nini humlaani na kumtukana Ali?” Sa’d akakasirika na akasema: “Wewe umenifanya mimi nikae kwenye zulia lako halafu ukaanza kumtukana Ali. Naapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba kama ningekuwa na japo sifa moja kati ya sifa nyingi alizokuwa nazo Ali ingekuwa na thamani sana kwangu kuliko kitu kingine chochote duniani. Naapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba sitakuja kukutembelea muda wote nikiwa hai.” Kisha akaondoka mahali hapo akiwa katika hali ya hasira.’” (MuruujulDhahab, Juz. 2, uk. 317). Amr bin Humq pia alikuwa ni mmoja wa wafuasi madhubuti wa familia ya Abu Talib. Ziad bin Abih alimuua kwa kosa tu la kuwa alikuwa anampenda Ali. Baada ya kumuua akamkata kichwa chake na akakipeleka kwa Mu’awiyah. Katika historia ya Uislamu kilikuwa ndio kichwa cha kwanza kutumwa kwa mtu yeyote kama zawadi. Mfuasi mwingine mwaminifu wa Ali alikuwa ni Maitham Tammar. Alikuwa ni sahaba wa karibu sana wa Ali na alikuwa akiitambua ile hadhi na cheo cha juu cha Imam. Alikuwa ameshirikiana na Ali kwa muda mrefu sana. Imesemekana kwamba kwa kawaida Ali alilitembelea duka lake mara nyingi na hata kama alitoka kwa shughuli maalum, yeye Ali aliziuza tende kwa niaba yake. Pale Amirul-Mu’minin Ali na Husein walipouawa na Ibn Ziad akawa hana chochote cha kuogopa tena hapo Kufa, alimtishia Maitham akisema kwamba kama ataendelea kumpenda Ali na kumsifia kwa usawa na uadilifu wake, yeye atamuua. Alijaribu kumrairai kwa kusema kwamba kama atakuwa ataunga mkono utawala wa 259

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 259

9/4/2017 3:47:57 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Bani Umayyah jina lake litapendekezwa kwa mfalme kwa ajili ya yeye kuzawadiwa kiasi kikubwa cha fedha na zawadi nyinginezo. Hili lilitokea katika wakati ambapo Ibn Ziad alipomsikia Maitham akitoa hotuba na akavutiwa sana na ufasaha wake na uhodari wake wa utoaji hoja. Amr bin Haris, mnafiki mwenye kujipendekeza wa baraza la Ibn Ziad akamuuliza iwapo alikuwa anamtambua mtu huyo alikuwa ni nani; na juu ya kuonyesha kutokujua kwake kuhusu yeye, (Amr) akasema: “Huyu ni yule muongo Maitham, mfuasi wa yule muongo Ali mwana wa Abu Talib.” Ibn Ziad akawa mwangalifu na akamwambia Maitham: “Je, unasikia ni nini anachosema Amr?” Maitham akajibu: “Yeye anasema uongo. Imam wangu Ali alikuwa mtu mkweli na khalifa wa kweli na mimi pia ni mkweli.” Ibn Ziad akakasirika na akasema: “Jitenganishe mwenyewe na Ali na mtukane na kuonyesha mapenzi kwa Uthman na umsifie, ama sivyo nitakata mikono na miguu yako na kukunyonga.” Maitham alivijibu vitisho hivi kwa kusimulia hadharani sifa za Ali na akaanza kulia akikumbuka uadilifu wake na upole wake, na halafu akamkaripia na kumshutumu Ibn Ziad na Bani Umayyah kwa uasi na upinzani wao. Ibn Ziad akakasirika sana na akamwambia Maitham: “Namuapa Mwenyezi Mungu kwamba nitaikata mikono na miguu yako lakini nitaubakisha ulimi wako ili niweze kuthibitisha kwamba wewe ni muongo na huyo Imam wako alikuwa ni muongo pia.” Mikono na miguu ya Maitham ilikatwa na akapelekwa kwenye kiunzi cha mti wa kunyongea. Hata katika hali hiyo, alisema kwa sauti kubwa: “Enyi watu! Yeyote anayetaka kusikia Hadith ya Mtume kuhusu Ali naaje kwangu.” Watu wakakusanyika karibu yake na yeye akaanza kusimulia zile tabia tukufu na sifa za Ali. Wakati huohuo Amr bin Haris alipita upande ule na akauliza kwa nini watu wamekusanyika pale. Baada ya kuwa amejulishwa kwamba walikuwa wanasikiliza mienendo ya Ali ikisimuliwa na Maitham, alikimbilia kwenda kumjulisha Ibn Ziad kuhusu jambo hilo na akasema: “Tafadhali tuma mtu haraka kwenda kuukata ulimi wa Maitham, kwani ninahofia kwamba endapo ataendelea kusimulia sifa za Ali watu wa Kufa watageuka dhidi yako na kuasi.” Ibn Ziad akatuma mtu kwenda kuukata ulimi wa Maitham. Aliwasili mahali hapo na akamwambia Maitham atoe ulimi wake ili upate kukatwa kulingana na maagizo ya gavana. Maitham akasema: “Kwani yule mtoto wa kahaba hakusema kwamba atatuthibitisha mimi na Imam wangu kwamba tuwaongo? Sasa unaweza kuukata ulimi wangu.” Yule chakari akaukata ulimi wake na damu ikatiririka kutoka kwenye ulimi 260

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 260

9/4/2017 3:47:57 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

huo kwa wingi sana kiasi kwamba Maitham akafariki. Ibn Ziad ndipo akausulubu mwili wake uliokwishakufa (maiti). Mfuasi mwingine wa Imam Ali na shahidi katika njia ya Mwenyezi Mungu alikuwa ni Rashid bin Hujari ambaye alikuwa sahaba wake wa karibu sana. Kisa chake kinafanana na kile cha Maitham. Ibn Ziad alimwambia kwamba maisha yake yatasitiriwa iwapo atajitenga na kuondokana na Ali. Yeye alikataa katakata kufanya hivyo. Ibn Ziad alimuuliza ni vipi ambavyo angetaka kufa. Baada ya hapo, mikono na miguu yake ikakatwa. Umaarufu na uaminifu wa marafiki zake Ali unaweza kuchambuliwa kutoka kwenye ukweli kwamba walimpenda kwa moyo wote na wakamchukulia kwa taadhima kubwa bila ya shinikizo wala kulazimishwa. Hawakutafuta zawadi yoyote au sifa kwa kufanya hivyo. Matakwa yao pekee yalikuwa kwamba waweze kuishi na kufa wakiwa wanaunga mkono haki. Mapenzi yao juu ya Ali yalikuwa ni sawa na yale ya Muhajir na Ansar wa mwanzo juu ya Mtukufu Mtume. Ammar bin Yasir, mfuasi wa Ali mwenye ghera, katika kuliona jeshi kubwa la Mu’awiyah katika vita vya Siffin alizitaja kwa dhati kabisa hisia za mioyoni za Shia wa Ali katika maneno haya: “Namuapa Mwenyezi Mungu kwamba hata kama watapigana kwa mikono yao na kuturudisha nyuma juu ya sehemu ya mbali, bado tutabakia tumeondoa shaka na kusadikisha kwamba sisi tunafuata haki na wao wanafuata upotovu.” Masahaba na wafuasi wa Imam Husein walikuwa vilevile kama wale wa baba yake, Ali. Mbele yao walikuwa na lengo bora kama lile lile ambalo wafuasi wa Ali walikuwa nalo katika mawazo yao. Katika usiku wa Ashura wakati fursa mbadala pekee iliyokuwa imebaki mbele ya Husein ilikuwa ni kupigana na kukutana na kifo cha kishahidi, na ambapo yalikuwa yamebaki masaa machache tu kwa hilo kutokea, Husein alilihutubia lile kundi dogo la wafuasi wake na akawaambia: “Watu hawa wanakitaka kichwa changu tu. Kwa hiyo sio lazima kwa ninyi kupoteza maisha yenu. Mnaweza mkaondoka katika giza hili la usiku ili mtu yeyote asiweze kuwaona.” Inawezekana kwamba aliwashauri kuondoka wakati wa usiku ili wasije wakaona aibu ya kumuacha peke yake katika mwanga mpana wa mchana, au kwamba wasiweze kuonekana na wakakamatwa. Huu ulikuwa ni udhihirisho wa tabia adhimu ya Imam Husein. Hata hivyo, masahaba zake wakasema kwa sauti moja: “Tutayatoa maisha yetu na kufa mbele ya miguu yako.”

261

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 261

9/4/2017 3:47:57 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Muslim bin Awsajah Asadi akasema: “Yaani sisi tukutelekeze wewe? Kwa nini tusifanye kuomba radhi kwetu kukaeleweka wazi mbele ya Mwenyezi Mungu kesho kwa kutimiza wajibu wetu juu yako? Naapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba sitakuacha hadi nitakapovunja mkuki wangu kwenye vifua vya maadui. Madhali upanga uko mkononi mwangu na ninazo nguvu, mimi nitaendelea kuwashambulia. Kama nitakuwa sina silaha yoyote nitawapiga kwa mawe na nitaendelea kupigana mpaka nitakapoyatoa maisha yangu mbele ya macho yako hasa.” Muslim alithibitisha aliyokuwa ameyasema. Aliyatoa maisha yake kijasiri mbele ya Imam. Wakati Muslim alipokuwa amejeruhiwa vibaya sana, na akaanguka chini kutoka kwenye farasi wake, Habib ibn Muzahir alikuja karibu yake na kusema: “Kama ningekuwa sijui kwamba hivi karibuni tu nitakufuata ningekuambia ufanye wasia.” Papo hapo Muslim akajibu, na hayo yalikuwa ndio maneno yake ya mwisho: “Wasia wangu pekee nitakaoweza kutoa ni kwamba uyatoe maisha yako muhanga kwa ajili ya Imam huyu.” Wakati Hur bin Yazid al-Riyahi alipoviona vitendo vya kiovu na upurukushani wa Yazid na wafuasi wake, na akaiona ile tabia njema ya hali ya juu ya Imam Husein na ile imani na umadhubuti wa masahaba zake, dhamira yake ilimsuta na kuamka na yeye akayatupilia mbali manufaa ya kidunia na vyeo. Hur huyu alikuwa ni mmoja wa makamanda wa jeshi la Bani Umayyah ambaye alikuwa ameahidiwa zawadi na malipo makubwa kwa kupigana dhidi ya Imam Husein na kumuua yeye na wafuasi wake. Ubaidullah bin Ziad, gavana wa Kufa alikuwa ameikabidhi kazi hii hasa kwake Hur. Hata hivyo, alipoikaribia kambi ya Imam Husein alionyesha mkanganyiko na wasiwasi mkubwa kiasi kwamba wenzie wakawa na mashaka (juu ya uaminifu wake kwa utawala wa Bani Umayyah). Hatimae alimtoa shoti farasi wake, akafika mbele ya Imam Husein na akasema: “Ewe mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu! Mimi ninaona aibu sana kwa yale niliyoyafanya na ninamuomba Mwenyezi Mungu anisamehe. Mimi nitapigana kwa ajili yako hadi nitakapoyatoa maisha yangu mbele ya miguu yako.” (Haya yalitokea kabla mapigano hayajaanza). Hur aliipata shahada yake mbele ya Imam Husein. Wafuasi na masahaba wote wa Imam Husein walikuwa wa ubora huu huu wa tabia na akili. Idadi yao ilikuwa ni ndogo sana lakini walikabiliana na maadui ambao walikuwa maelfu na maelfu kwa idadi. Walizidiwa na kiu na walikuwa katika hatari kubwa ya maisha yao, lakini jambo pekee walilokuwa wakilipenda lilikuwa ni kifo cha kishahidi. Watu hawa majasiri

262

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 262

9/4/2017 3:47:57 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

waliyatoa maisha yao mbele ya miguu ya Imam Husein. Kila mmoja wao alitamani kupata shahada. Walikichukulia kifo hiki kuwa heshima kubwa sana juu yao. Husein mwana wa Ali bin Abi Talib aliuawa kishahidi, na serikali ya Yazid na washirika wake ikawa ni ukweli uliosimama. Sasa kulikuwa hakuna matumaini tena kwamba ukhalifa utaweza kurudi kwenye familia ya Abu Talib. Wafuasi wao wakawa na uhakika kwamba zile neema za ardhi (dunia) hazitagawanywa tena miongoni mwa watu kupitia wao (Bani Hashim). Hata hivyo, familia ya Abu Talib na wasaidizi na wafuasi wao, imma hawakukaa kimya wala moyo wao haukudhibitiwa. Kwa kweli ulizidi kuamshwa kuliko hapo kabla, na ukawa na nguvu zaidi. Kwa mfano, wakati habari za kuuawa kwa Imam Husein na masahaba zake zilipofika Kufa, ibn Ziad aliwakusanya watu kwa ajili ya swala ya jamaa. Katika hotuba baada ya kwisha kwa swala hiyo, yeye alisema: “Sifa na shukrani zimwendee Mwenyezi Mungu ambaye amedhihirisha ukweli na kuwapa ushindi watu wakweli. Amemsaidia AmirulMu’minin! Yazid na watu wake na kumuua muongo mwana wa baba muongo – Husein bin Ali na washirika wake.” Alikuwa bado hajamaliza kauli yake wakati mzee mmoja aliyekuwa akiitwa Abdullah ibn Afif Azadi, ambaye alikuwa sahaba wa Ali na alikuwa amepigana kishujaa pamoja naye katika vita vya Ngamia na Siffin, aliposimama na akasema kwa sauti kubwa: “Ewe mwana wa Marjana! Unawauwa kizazi cha mitume halafu unadiriki kusimama kwenye mimbari, ambayo ni sehemu iliyokusudiwa kwa ajili ya ukweli! Wewe ni muongo na baba yako alikuwa ni muongo, na yeye pia ni muongo, huyo aliyetunuku utawala juu yako na baba yako.” Ingawa kama matokeo ya hili yule mzee alinyongwa kesho yake katika kiwanja cha Kufa, tukio hili linathibitisha kwamba ukatili na udhalimu wa Bani Umayyah haukuzima moyo wa wafuasi wa Ali. Bali utashi na dhamira zao zilipata kasi zaidi kabisa. Yule mshairi anayefahamika sana; Farazadaq, alisoma wazi wazi na tena mbele hasa ya Bani Umayyah wenyewe, ile Qasidah (ya hotuba ya wasifu) ambayo alikuwa ameitunga kwa ajili ya kumsifu Imam Zainul-Abidin. Wakati huo utawala wa Bani Umayyah ulikuwa kileleni kabisa na hakuna aliyeweza kuthubutu kutamka hata neno moja tu dhidi yao. Hata hivyo, Farazadaq hakujali kuhusu maisha yake. Yeye hakumsifu Imam huyo ili kupata zawadi au kupenda upendeleo wowote ule. Ulikuwa ni udhihirisho tu wa mapenzi na ile shauku motomoto kwa ajili ya utii kwake Imam vilivyomchochea kutunga hotuba hiyo ya wasifu. Kisa chenyewe kiko kama ifuatavyo: 263

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 263

9/4/2017 3:47:58 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Khalifa wa Bani Umayyah, Hisham bin Abdul-Malik alikwenda Makkah kutekeleza Hijja wakati alipokuwa ni mtoto wa mfalme. Baada ya kuizunguka Ka’aba alipenda kulibusu lile Jiwe Jeusi lakini hakuweza kulifikia. Kwa kiasi fulani ilikuwa ni kwa sababu ya ile chuki ambayo watu walikuwa nayo katika nyoyo zao juu ya Bani Umayyah kwamba hawakuweka njia kwa ajili ya Hisham, na kiasi ilikuwa kwa sababu idadi ya mahujaji ilikuwa ni kubwa sana kiasi kwamba hakuweza kufika hapo. Hisham kwa hiyo hakuwa na jinsi nyingine bali kurudi na kukaa kwenye kiti. Wakati huohuo, Imam Sajjad ibn Husein alikuja na akaelekea kwenye lile Jiwe Jeusi. Watu mara moja wakarudi nyuma na wakawacha njia kwa ajili yake, naye akalibusu lile Jiwe Jeusi bila ya kipingamizi chochote. Wale waliokuwa wamekuja na Hisham kutoka Syria wakamuuliza kuwa yule mtu mheshimika alikuwa ni nani. Yeye alikuwa ni nani ambaye kwa ajili yake mahujaji wote walirudi nyuma? Hisham alimjua kwamba ni nani, lakini kwa kuhofia kwamba wale watu wa Syria watavutiwa na Imam yeye akasema: “Mimi sijui mtu yule ni nani.” Farazdaq hakuweza kuvumilia utovu wa adabu huu juu ya Imam kutoka kwa Hisham. Kwa hiyo yeye akasimama na akasema: “Mimi ninamfahamu.” Kisha akachukua sehemu iliyonyanyuka kidogo na akasoma kwa ghera kubwa na ujasiri ile qasidah yote ambayo daima itabaki kuwa ukumbusho wa kudumu katika historia ya maandishi ya Arabia. Mstari wake wa kwanza unasema: “Ni yule mtu mashuhuri ambaye nyayo zake zinajulikana Makkah, kwenye Ka’abah, kwenye Haram na mazingira yake.” Hisham alikasirika sana kusikia qasidah hii na akamfunga jela Farazdaq. Wakati akiwa jela Farazdaq aliandika tashtiti dhidi ya Hisham na Bani Umayyah bila ya kujali ukatili wote watakaoweza kuufanya juu yake. Ndani ya tashtiti hiyo alisema hivi kuhusu Hisham: “Anakigeuza kichwa ambacho sio kichwa cha chifu. Ana makengeza na mapungufu yake yapo dhahiri.” Tumetaja mifano michache tu ambayo itaonyesha mwanga juu ya tabia na mwenendo wa wafuasi wa familia ya Abu Talib. Wao kwa hali yoyote wanaonyesha wazi kwamba walikuwa imara katika mapenzi yao na taadhima kwa ajili ya familia ile adhimu na walikuwa tayari kujitoa maisha yao kwa ajili ya Ali. Hata hivyo, kuhusu wafuasi wa Bani Umayyah waliweza kugawanyika katika makundi mawili. Kundi la kwanza lilikuwa la wale ambao dhamira zao zilikuwa zimenunuliwa na Bani Umayyah kupitia rushwa na mahongo. 264

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 264

9/4/2017 3:47:58 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Na lile kundi la pili lilikuwa na wale ambao walizaliwa ni wahalifu. Watu waovu kwa asili yao ni wenye madhara kwa wale waungwana na wakarimu. Kwa vile wanakuwa hawana tabia na sifa nzuri, wanakuwa na kinyongo dhidi ya wale ambao ni wema, na wanafanya urafiki na kuwaunga mkono wale ambao ni waovu na wenye hasira kama wao wenyewe. Wale watu waliokuja kuwa wafuasi wa Bani Umayyah kwa njia ya kuhongwa walikuwa ni wale wasaidizi na wanaomuunga mkono Abu Sufyan. Dhana ya hongo ni tofauti kuhusiana na kila mtu mmoja mmoja. Kila mtu alihongwa kwa kulingana na cheo na nafasi yake. Abu Sufyan aliwahonga baadhi ya watu kwa njia ya utajiri na wengine kwa kuwaahidi uhuru. Kwa mfano, alimuahidi Wahshi, mtumwa wa Kihabeshi (yule muuaji wa Hamzah) kwamba ataachiwa huru iwapo atauwa yeyote kati ya Muhammad, Ali na Hamzah. Baadhi ya watu walipewa vyeo vikubwa kama hongo. Walikuwapo wengi ambao walikuwa upande mmoja na Bani Umayyah na wakapigana dhidhi ya Mtume na masahaba zake kwa matumaini ya kwamba zile nafasi na vyeo walivyokuwa navyo wakati wa zama za jahilia vitabakia kamilifu. Mmoja wa wafuasi wa Mu’awiyah alikuwa ni Amr bin Aas ambaye alikuwa ndiye msaidizi mkuu. Tutazungumza kuhusu yeye kwa kirefu baadae. Wale askari wa Syria ambao Mu’awiyah aliwapeleka Siffin kupigana dhidi ya Ali pia walikuwa wanatokana na kundi hili. Lengo lao lilikuwa ni kumtumikia yule mtu aliyewalipa mishahara yao na kufanya ahadi za kuvutia za utajiri na vyeo kama itatokea wakashinda. Katika kundi hili vile vile walikuwamo pia jeshi la Yazid. Watu hawa walikuwa wamehongwa mahongo mazito na Yazid na washauri wake, ambao walikuwa wamewaahidi usalama wa maisha yao kama watawaunga mkono. Wengi wa askari hawa walikuwa wamekuja kupigana dhidi ya familia ya Ali kwa sababu walihofia kwamba kama watakataa kufanya hivyo watakuja kupatwa na manyanyaso na mateso. Ni dhahiri kabisa kwamba sio kila mtu ana moyo wa kujitoa muhanga. Historia inasimulia kwamba wakati akiondoka Makkah kuelekea Kufa, Imam Husein alikutana na yule mshairi Farazdaq na akamuuliza kuhusu mwelekeo wa watu wa Kufa. Farazdaq akajibu: “Nyoyo za watu wale ziko pamoja na wewe lakini watachomoa panga zao dhidi yako kesho.” 265

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 265

9/4/2017 3:47:58 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Husein alifanya uchunguzi kama huo huo kutoka kwa Majm’a ibn Ubaid Aamari. Majm’a akajibu: “Wale watu maarufu na wenye mvuto wamehongwa kwa mahongo mazito. Ni maadui zako wakali. Na kuhusu wengine, hao ni wafuasi wako mioyoni lakini panga zao zitachomolewa dhidi yako kesho.” Na kuhusu lile kundi jingine la wafuasi wa Bani Umayyah, yaani wale watu waliochagua kuwa upande wao kutokana na uovu wao wa asili, idadi yao ilikuwa ni kubwa sana. Waovu na wahalifu hawa wangekuwa maadui wa kizazi cha Abu Talib kwa sababu ya kuwaridhisha wakubwa wao tu wangeweza kusamehewa kwa kiasi fulani, na ingeweza kusemwa kwamba hawa ni watu waliokuwa na mawazo ya dunia tu ambao walipigana dhidi ya kizazi cha Abu Talib kwa ajili ya manufaa ya kidunia tu. Uhasama wao na familia hii haukuwa, hata hivyo, kwa sababu ya utajiri au vyeo walivyotaka kuvipata. Uhasama wao ulikuwa wa msingi na wa asili kama vile tu giza linavyopingana na mwanga, upotovu unapingana na uongofu na batili inapingana na haki, na uonevu na udhalimu unapingana na uadilifu na usawa. Walikuwa na mioyo migumu sana na wakatili kuliko wanyama wakali. Walikuwa ni maadui wabaya sana wa kila mtu mwema kwa sababu ya uovu wao wa asili. Ni watu waovu kama hao tu wanaoweza kukata viungo vya maiti, kuchinja watoto na kuwanyanyasa wanawake wasio na uwezo. Mmoja wa madhalimu hawa alikuwa ni Busr ibn Artat ambaye amepewa jina la chakari na wanahistoria. Wakati mtu anapoichunguza tabia yake, ile tabia ya lile kundi la pili la wafuasi wa Bani Umayyah inaweza kutambulika vizuri sana. Yeye alikuwa ndio msaidizi mkuu wa Mu’awiyah katika suala la udhalimu na uonevu. Alifanya maovu ambayo mtu anagwaya hata kuyafikiria. Aliuwa watu wazee ambao hata migongo yao ilikuwa imepinda. Aliwavuta watoto kutoka mapajani mwa mama zao na kuwachinja. Na yote haya aliyafanya yeye kutia nguvu utawala wa Mu’awiyah. Wakati Mu’awiyah alipompeleka Yemen pamoja na jeshi kwenda kuteka nyara na kupora, alionyesha udhalimu na ukatili kiasi ambacho hakilinganishiki katika historia yote. Kabla ya kuondoka kwake Mu’awiyah alimwita na akasema: “Chukua njia ya Hijazi na ufike Yemen kupitia Makkah na Madina. Kama utapita mahali ambapo wakazi wake ni wafuasi wa Ali, watishie kiasi ambacho wanaweza wakashawishika kwamba maisha yao hayatabakishwa.

266

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 266

9/4/2017 3:47:58 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Halafu walazimishe kuchukua kiapo cha utii kwangu. Wauwe wale watakaokataa kufanya hivyo. Wauwe wafuasi wa Ali popote pale utakapowakuta.” Baada ya kuwa amepata maagizo haya Busr aliondoka na akafika Madina. Gavana wa Madina alikuwa ni Abu Ayyub Ansari, mwenyeji wa kwanza kabisa wa Mtukufu Mtume katika mji huo. Alipoona kuwa ni vigumu kumpinga Busr, yeye akaondoka Madina. Busr aliingia mjini hapo na akatoa hotuba. Alitupa matusi juu ya watu na akasema: “Nyuso zenu naziwe nyeusi!” Kisha akazungumza na Ansari wenyewe hasa na akasema: “Enyi Mayahudi na kizazi cha watumwa! Nitawateseni kwa namna ambayo kwamba wale waumini watapata fahamu zao tena.” Halafu akazichoma moto nyumba nyingi sana. Baada ya hapo akafika Makkah. Qasham bin Abbas, gavana wa Makkah akakimbia zake. Hapo napo Busr aliwatukana watu na kuwatishia. Kalbi anasema kwamba akiwa njiani kutoka Madina kwenda Makkah, Busr aliuwa na kupora idadi kubwa ya watu. Pale watu wa Makkah walipokuja kulitambua hilo waliukimbia mji. Watoto wawili wa kiume wa Ubaidullah bin Abbas pia waliukimbia mji. Busr akawakamata na kuwauwa. Baadhi ya wanawake wa kabila la Kinana vile vile waliutoka mji. Mmoja wao alisema: “Ninaweza kuelewa kule kuuawa kwa wanaume, lakini sijui ni kosa gani watoto walilolifanya. Watoto hawakuuawa kamwe hata katika zama za jahilia au baada ya kuja kwa Uislamu.” Kisha alipokwishapita Taif, Busr alifika Najran ambapo alimuua Abdullah bin Abdul Madan na mwanawe Malik. Huyu Abdullah alitokana na familia ya wakwe zake Ubaidullah bin Abbas. Halafu akawakusanya pamoja watu wa Najran na akawahutubia hivi: “Enyi Wakristo! Enyi ndugu wa masokwe! Kama nitajulishwa juu ya kitendo chenu chochote ambacho kwamba mimi nitakuwa sikipendi nitawatendea kwa namna ambayo kwamba taifa lenu litakuwa limetoweka kabisa, mashamba yenu yataangamizwa na nyumba zenu zitageuka kuwa mahame.” Baada ya hapo alifika San’a na akauwa idadi kubwa ya watu katika mji huo. Ujumbe wa Ma’arib ulimngojea yeye lakini akawauwa wajumbe wote. Wakati wa kuondoka hapo San’a aliwauwa tena maelfu ya watu wakaazi wa mji huo. Alikuja kurudi tena hapo San’a na akawauwa wazee kadhaa watokanao na nchi ya Uajemi. (Sharh Nahjul-Balaghah, cha Ibn Abil-Hadid, Juz. 1, uk. 271.)

267

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 267

9/4/2017 3:47:58 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Wanahistoria wanasema kwamba huyu Busr aliwauwa watu takriban elfu thelethini. Hawa hawajumuishi wale aliowachoma wakiwa hai. (Sharh Nahjul-Balaghah, cha Ibn al-Hadid, Juz. 1, uk. 30). Washairi wametunga mashairi mengi kuhusu maovu yaliyotendwa na huyu mhalifu mwenye moyo mgumu. Yazid bin Muzr’a anasema: “Mahali popote anapokwenda Busr, yeye hupapora na kupachoma moto. Historia nzima ya maisha yake imejaa maovu kama hayo.” Mhalifu mwingine anayehusiana na kundi hili alikuwa ni Ziad bin Abih ambaye aliwauwa kwa halaiki na kuwapora watu wa Iraqi katika hali ya kutisha sana. Katika mfano wa kwanza kabisa Mu’awiyah alimkubali kuwa kama ndugu yake na akampa jina la Ziad bin Abu Sufyan ili kupata kuungwa mkono. Halafu akamteua kuwa gavana wa Basra. Alipofika Basra alitoa hotuba inayofahamika sana iitwayo ‘khutbah al-Batra.’ Halafu akajishughulisha katika uimarishaji wa utawala wa Bani Umayyah. Aliwauwa baadhi ya watu na akawaadhibu wengine kwa kuwashuku tu na kuwatilia wasiwasi. Hakukuwa na kitu rahisi kwa wafuasi na mawakala wa Bani Umayyah kuliko kukata mikono na miguu ya wapinzani wao, kuwanyonga au kuwafunga jela, kupora mali zao, kuwachoma wakiwa bado wako hai, na kuwadhalilisha wakati wa uhai wao na pia baada ya kufa kwao. Wakati wa utawala wa Ziad watu walipata mateso na matatizo yasiyosemeka. Hakuna aliyemzidi kwa ukatili na udhalimu kutoka miongoni mwa manaibu na mawakala wa Bani Umayyah isipokuwa Hajjaj ambaye alikuwa ni mhalifu mkubwa zaidi hasa kuliko yeye. Akizungumzia juu ya sera zake mwenyewe na utaratibu wa kushughulikia mambo Zaid alisema hivi katika Khutbah-al-Batra iliyotajwa hapo juu: “Naapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba nitamuweka kizuizini aliye bwana badala ya mtumwa wake, mtu aliyepo badala ya aliyekimbia, mtiifu badala ya mkorofi, na yule mwenye afya njema badala ya mgonjwa mpaka mmoja wenu atamwambia mwingine: ‘Oh! Sa’d! toroka kwani Sa’id ameuawa.’ Mimi sitakula wala kunywa kitu chochote mpaka nimekushikisheni adabu na kuuangamiza mji wa Basra na kuchoma na kubomoa nyumba zake. Jihadharini! Asitoke hata mmoja wenu nje ya nyumba yake wakati wa usiku. Yeyote atakayefanya hivyo atakatwa kichwa chake. Naapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba wengi wenu mtauawa mikononi mwangu. Kila mmoja ajichunge kwamba mimi siimwagi damu yake.” Baada ya Basra akaja akawa gavana wa Kufa. Katika ile siku ya kwanza hasa, akiwa amekaa langoni mwa Msikiti alifanya mikono ya watu themanini ikatwe. Alifuata sera ya ukandamizaji na ugaidi ili kumfurahisha Mu’awiyah. Madaini anaandika hivi: 268

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 268

9/4/2017 3:47:58 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

“Aliendelea kuwasaka Shia wa Ali, na kwa kuwa yeye alikuwa ni mmojawapo wakati wa kipindi cha Ali, basi ilikuwa ni rahisi kwake kuwagundua. Aliwagundua kila mahali. Aliwabughudhi na kuwatishia, akawakata mikono na miguu yao, akawafanya kuwa vipovu, akawaning’iniza kwenye miti ya mitende na akawafukuza kutoka Iraqi. Matokeo yalikuwa kwamba hapakuwa na Shia maarufu aliyebakia pale. Hivi punde tutasimulia kisa cha Ziad na Hujr Adi, ambaye alikuwa mmoja wa wafuasi wa Ali.” Kwenye kundi hili hasa la wahalifu walikuwemo Ubaidullah bin Ziad, yule muasisi wa msiba wa Karbala na muuaji wa Amr bin Hamq, Maitham Tammar, yule mzee Abdullah bin Afif Azdi na maelfu ya watu wengine wasio na hatia. Lilikuwa ni jambo la kawaida kabisa kwake yeye kunyonga, kuua na kuwakata viungo wengine kiholela. Muslim bin Aqil alisema kumhusu yeye: “Kwa sababu tu ya hasira, uhasama na kushuku, yeye anauwa wale ambao kuuawa kwao kumekatazwa na Mwenyezi Mungu. Na hili haliathiri kufurahi na kustarehe kwake. Anajihisi kana kwamba hakufanya kitu. Aina mbaya ya ukatili na roho mbaya ilijionyesha yenyewe katika ile siku ambamo alimuua Imam Husein. Hata baada ya kufa shahidi kwa Imam upujufu, ufisadi na uduni wa ibn Ziad haukuwa na mipaka.” Shimr ibn Zil Jaushan pia alikuwa balaa katika uovu na ufidhuli wake kama bwana wake Ibn Ziad. Alikuwa na sifa bainifu ya kuwa na kinyongo na uhasama dhidi ya watu waungwana na wakarimu wote. Aliwafanya watoto wadogo wengi wa Husein wakafa kwa kiu, ingawaje mto Furati ulikuwa unatiririka mbele yao tu. Aliwaamuru askari wake kuukanyaga mwili wa Imam Husein kwa kwato za farasi wao ambapo matokeo yake mgongo na mbavu zake nyingi zilivunjika vipande vipande. Nguo yake ambayo ilikuwa imechanika kwa sababu ya mapigo ya mishale na panga, ilikuwa tayari imekwishaporwa. Kama wale watoto wadogo wa Imam Husein wangetoka nje ya mahema yao, wale askari wa Syria wangewakata vipande vipande pia. Mhalifu mwingine kama huyo alikuwa ni Hasin ibn Numayr. Imam Husein alikuwa amenyimwa maji kuanzia ile siku ya saba ya Muharam. Katika siku ya kumi ya Muharram aliufikia ukingo wa Furati baada ya kupambana na maadui na akachota maji kwenye kiganja chake cha mkono ili anywe na kukata kiu yake. Mtu huyu duni wa kudharaulika ghafla akarusha mshale ambao ulipiga kwenye mdomo wa Imam na matokeo yake mdomo wake na viganja vikajaa damu. Alipoyaona haya mtu huyu muovu akacheka bila haya na akaondoka.

269

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 269

9/4/2017 3:47:58 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Mkosefu mwingine kama huyu alikuwa ni Amr Sa’d. Alimtii bwana wake muovu Ubaidullah bin Ziad na akafanya juhudi zake zote kutekeleza amri zake, ingawa angeweza kuchagua kutoshiriki katika msiba wa Karbala (kwa sababu Ubaidullah hakumlazimisha kushika ukamanda wa majeshi ya Bani Umayyah bali alimueleza kwamba alikuwa tayari kukabidhi vikosi hivyo kwa kamanda mwingine). Baada kuuawa kishahidi kwa Imam Husein na wafuasi wake, Amr Sa’d aliwafanya wanawake wa familia ya Mtume kuwa mateka na akawafanya wapite karibu na zile maiti za mashahidi ambazo vichwa vyao vilikuwa vimekatwa. Amr bin Sa’d alikuwa ndiye mtu wa kwanza kurusha mshale kwenye vikosi vya Imam Husein na kuanzisha mapambano. Halafu akawaambia wale askari wake: “Kuweni mashahidi kwenye jambo hili la kwamba mshale wa kwanza nimeurusha mimi.” Mfuasi mwingine wa Bani Umayyah alikuwa ni Muslim bin Uqbah ambaye alitenda maovu yakuogopesha na kuchukiza sana. Yazid alimpeleka Hijazi katika nafasi ya kamanda wa jeshi. Alionyesha ushenzi wa kupita kiasi pale. Huko Madina aliwauwa watu wengi sana kiasi kwamba damu ilianza kutiririka katika mitaa ya mji huo. Alilifanya ni halali kwa wapiganaji wake kufanya tendo lolote haramu humo Madina kwa muda wa siku tatu. Kwa matokeo ya hili, wanaume kwa wanawake waliuawa bila kuchagua kwa busara, na mali zao zikaporwa. Staha ya wanawake ilihalifiwa. Watoto walitolewa kwenye mapaja ya mama zao na kutupwa kwenye kuta kiasi kwamba mifupa yao ikavunjika na wakafa. Nyumba ziliteketezwa kabisa. Vizazi vya Muhajir na Ansar wa Mtume havikubakishwa. Katika siku tatu hizi Muhajirina na Ansari elfu moja na mia saba waliuawa, mbali na wanaume na wanawake wengineo. Hapa tunaitoa baadhi ya mistari ya barua ambayo Muslim bin Uqbah alimwandikia Yazid baada ya tukio hili. Katika barua hii amejiingiza katika kujisifia mwenyewe kwa kutokana na mafanikio yake, na kwa kushangaza vya kutosha, yeye ameyahusisha makosa na maovu yake yote kwenye utashi na uamuzi wa Mwenyezi Mungu. Yeye anasema: “Ninapaswa kumjulisha Amirul-Muminin – Mwenyezi Mungu amhifadhi – kwamba niliondoka Damascus. Maandalizi tuliyoyafanya kabla ya kuondoka kwetu wewe uliyaona. Marwan bin Hakam vile vile alirudi kutoka Damascus na akafuatana nami. Alithubutu kuwa mwenye kufaa sana kwa ajili ya kupambana na maadui zetu. Mwenyezi Mungu naaweke hadhi juu ya Amirul-Mu’mini. Marwan alishughulika vizuri sana na alikuwa mkali sana juu ya maadui kiasi kwamba ninatumaini kwamba utumishi wake hautaachwa bila kuzawadiwa na Imam wa Waislamu na khalifa wa Mungu. 270

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 270

9/4/2017 3:47:58 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

“Mwenyezi Mungu naaweke wafuasi wa Amiri wa waumini wenye afya njema na nguvu! Hakuna hata mmoja aliyesumbuliwa na hakuna katika maadui aliyewakabili wakati wa mchana. Mimi sikuswali katika Msikiti wa Madina mpaka maelfu ya watu walipokuwa wameuawa na mali zao kuporwa kwa urahisi. Kila mtu aliyefika mbele yetu alipigwa upanga. Yeyote aliyejaribu kutoroka alifuatiliwa. Yule aliyekuwa akifa kutokana na majeraha alimaliziwa kabisa. Kama Amiri wa waumini alivyoagiza tuliipora Madina kwa muda wa siku tatu. Namshukuru Mwenyezi Mungu aliyeniponya mimi na wasiwasi wangu wakati nilipowauwa wale wapinzani na wanafiki wakongwe. Ukaidi wao ulivuka mipaka yote na walikuwa waasi wakongwe.” Mhalifu mkubwa kabisa miongoni mwa wafuasi wa Bani Umayyah alikuwa ni Hajjaj bin Yusuf Saqafi. Kulingana na maagizo ya khalifa wa Bani Umayyah, Abdul Malik bin Marwan, Hajjaj alitoka kwenda Hijazi kupigana dhidi ya Abdullah bin Zubeir. Aliizingira Makkah ambako Abdullah alikuwa amekimbilia. Alitupa mawe na moto juu ya Makkah kwa kutumia mitambo ya kurushia mawe ya kivita na matokeo yake sehemu ya Ka’abah ikaungua moto. Alipopata ushindi, alikata vichwa vingi vya wapinzani wa Bani Umayyah na akavipeleka kwa Abdul Malik huko Damascus. Alimkata kichwa Abdullah kisha akampeleka kwenye kiunzi cha mti wa kunyongea. Sio hilo tu bali aliuacha mwili wa marehemu kubakia kwenye kiunzi hicho kwa muda wa siku nyingi. Asma, binti yake Abu Bakr, ambaye alikuwa ndiye mama yake Abdullah alikuwa ni mzee sana wakati huo na kifo cha mwanawe kilimhuzunisha sana. Nuru yake ya macho pia ilikuwa imedhoofika. Alikuja kwenye ile sehemu ambapo mwili wa Abdullah ulikuwa umening’inia na akasema: “Muda haujafika bado ambapo mpandaji huyu angepaswa kushuka chini?” Hili likamuudhi Hajjaj vibaya sana na akamtukana na kumkemea mwanamke huyu mzee masikini. Ikiwa kama zawadi kwa ajili ya mafanikio yake, Abdul Malik akamteua Hajjaj kuwa gavana wa Hijazi. Hapo ndipo akauwa watu wasio na idadi na akatoa adhabu za kikatili kwa wengineo. Hajjaj alijisifu mwenyewe kwa maneno haya: “Mimi ni mkatili sana, mwenye kisasi kupita kiasi, na mwenye kijicho cha hali ya juu sana.” Haiwezekani kukadiria ni kiasi gani mtu huyu aliwachukia wanadamu. Baada ya muda fulani Abdul Malik akamteua kuwa gavana wa Iraqi kwa ajili ya kuzima machafuko katika eneo hilo na kurudisha sheria na amani. Hajjaj aliwasi-

271

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 271

9/4/2017 3:47:58 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

li Kufa akifuatana na askari kumi na mbili tu. Hata hivyo, yeye alimtanguliza mtu mmoja ili kwamba watu waweze kutambua juu ya kukaribia kufika kwake. Kila mtu alianza kumsubiri pale msikitini. Ulikuwa ni mwezi wa Ramadhan. Wakati watu walikuwa wanaonyesha kutoridhika na chuki zao katika kuteuliwa kwake kama gavana, yeye akawasili kwenye eneo hilo. Alikuwa amevaa kilemba cha hariri nyekundu kichwani mwake ambacho kwacho sehemu kubwa ya uso wake ilikuwa imefunikwa, na alikuwa ameshika upanga na upinde mkononi mwake. Alitembea hatua kwa hatua kwa ukimya kabisa. Mkusanyiko ule wa watu ulikuwa kimya pia. Mwishowe alipanda kwenye minmbari na akaagiza watu wote waitwe. Watu wa Kufa wakaingia ndani ya msikitini huo. Hajjaj aliendelea kubaki kimya juu ya mimbari kwa kitambo kirefu kiasi. Watu wakachoka kusubiri na wakaanza kumtukana kwa sauti za chini chini. Baadhi yao hata wakafikia kuokota michanga na wakaanza kumtupia. Mara ghafla hata hivyo, akaanza kuongea na ile michanga ikadondoka kutoka mikononi mwa watu kutokana na hofu. Akiondoa kilemba chake kutoka kichwani mwake, Hajjaj akasema: “Mimi ni mtoto wa mtu jasiri na wa kutisha sana, ambaye alijitumbukiza mwenyewe kwenye hatari akiwa amefumba macho. Nitakapoondoa kilemba kutoka usoni mwangu mtanitambua kwamba mimi ni nani. Wallahi ninaziona nyuso zilizonyanyuliwa, na shingo zenye ukaidi, na vichwa ambavyo wakati wake wa kukatwa umefika, na mimi ndiye nitakayevikata. Ninaona damu tu baina ya vichwa na ndevu. Angalieni! Amiri wa waumini (Abul Malik bin Marwan) alitandaza pongono yake na akaichunguza miti yake. Halafu akagundua kwamba mimi ndio mti mgumu na amenituma kwenu. “Enyi watu wa Iraqi! Naapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba ninyi ni chanzo cha uasi na udanganyifu; ninyi ni watu wa tabia mbaya sana. Mimi nitawachanja kama kuni zinavyochanjwa na nitawapigeni wapigwavyo ngamia wageni. Ninyi ni kama watu wa kijiji ambacho wakaazi wake walikuwa wanaishi maisha ya starehe na walikuwa na vya kutosha kula na kunywa, na walipoonyesha utovu wa shukurani kuhusiana na neema za Mwenyezi Mungu, Yeye akawatia kwenye hofu na njaa. Enyi watu wa Iraqi! Enyi watumwa wa fimbo na watoto wa wasichana watumwa! Mimi ni Hajjaj bin Yusuf. Naapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba wakati ninapoapia kufanya jambo huwa ninalifanya. Sasa makundi haya yapo mbele yangu. 272

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 272

9/4/2017 3:47:58 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Ni lazima mfuate njia iliyonyooka kwani ninaapa kwa Yeye ambaye anadhibiti maisha yangu kwamba nitakufanyeni ninyi kiasi kwamba kila mmoja wenu atabaki akishughulika na mwili wake mwenyewe (yaani: nitawapeni kipigo ambacho itawachukueni muda wa kutosha kupona kutokana na athari zake). Ni lazima kwa hiyo mkubali haki na mtelekeze batili kabla sijawafanyieni kitendo ambacho wanawake zenu watabaki kuwa wajane na watoto wenu kuwa mayatima. Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba kama nyote ninyi hamtatoka kwenda kujiunga na jeshi la Mohlab ndani ya siku tatu, nitawauwa wale watakaoonekana hapa na nitataifisha mali zao na kuvunja nyumba zao.” Hivi havikuwa vitisho vitupu. Aliwafanyia watu wa Kufa ukatili mkubwa zaidi kuliko yale aliyowatishia nayo. Hajjaj alikuwa ni mwenza kamili katika maovu yote mabaya yaliyofanywa na Bani Umayyah kama ilivyoelezwa kwa kirefu hapo juu. Aliwauwa watu wasio na hatia bila idadi. Yeye mwenyewe alikuwa kila mara akisema: “Kitu ambacho nilikufurahia sana ni umwagaji wa damu, na kufanya mambo ambayo hakuna mtu mwingine yoyote awezaye kupata ujasiri wa kuyafanya, na ambayo hayajawahi kufanywa na mtu yoyote kabla. (Muruuj-al-Dhahab, cha ibn Mas’udi, Juz. 3, uk. 67). Mara tu jina lake linapotajwa, mtu papo hapo hukumbushwa juu ya ukatili na udhalimu. Inaonekana kwamba Hajjaj na dhulma ni viambata vya kila kimojawapo. Wanahistoria wanasema: Baada ya Ubaidullah bin Ziad – yule muuaji wa Imam Husein, alifuatia Hajjaj bin Yusuf. Yeye aliwauwa wafuasi wa Ali mmoja baada ya mwingine kwa kuwatilia shaka na madai yasiyo na msingi. Alipenda zaidi kama mtu angeitwa kafiri au mshirikina mbele yake kuliko kuitwa mfuasi wa Ali. Kwa kweli kwa maoni yake makafiri na wenye kuabudia mungu zaidi ya mmoja walistahili kudekezwa na hata zawadi na tuzo, lakini wafuasi wa Ali walifaa kuuawa tu. Hajjaj alianza utawala wake katika namna hii ya ukandamizaji na hakukinai kwamwe na maovu ya kutisha ambayo aliyaendekeza. Hapo Kufa aliandikisha watu kisheria kwenye jeshi kwa muda wa siku tatu na akawatuma kila mmoja wao kwenye eneo la utendaji. Hapakuwa na hata mmoja ambaye hakwenda kwenye uwanja vita. Kwa kiasi kwamba hata watoto ambao walikuwa bado hawajafikia utu uzima waliandikishwa na kupelekwa kwenda kupigana. Wakati huo huo Umayr bin Zabi Hanzali akamjia na akasema: “Mwanangu ni mdogo na mwenye nguvu sana.” Hajjaj akasema: “Mtoto huyu atathibitika kuwa bora kuliko baba yake.” 273

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 273

9/4/2017 3:47:58 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Halafu akamuuliza: “Wewe ni nani?” Umayr akajibu: “Mimi ni Umayr bin Zabi Hanzali.” Hajjaj akasema: “Wewe siye mtu yule yule aliyepigana dhidi ya Uthman bin Affan?” Umayr akasema: “Ndio, mimi ndiye mtu huyo.” Hajjaj akasema: “Ewe adui wa Mwenyezi Mungu! Kwa nini ulifanya hivyo?” Umayr akajibu: “Nilifanya hivyo kwa sababu Uthman alimfunga baba yangu ambaye alikuwa ni mzee sana na dhaifu. Yeye hakumuachia mpaka baba akafa ndani ya jela.” Hajjaj akasema: “Je, wewe hukutunga shairi hili: ‘Nilitamani kumuua lakini sikumuua. Oh! Ningefanya hivyo, ili wake wa Uthman waweze kuomboleza kifo chake.’” Halafu akaongezea: “Nafikiri miji miwili hii, Basra na Kufa itanufaika kama wewe utauawa. Udhuru wako uko wazi kabisa na udhaifu wako uko dhahiri. Hata hivyo, ninahofia kwamba kama wewe utaachwa na wengine pia watapata ujasiri wa kutotii amri zangu.” Baadae yeye alikatwa kichwa chake kwa mujibu wa maagizo ya Hajjaj, mali zake zikaporwa na nyumba yake ikabomolewa kabisa. Hajjaj alimteua Abdur-Rahman bin Ubayd Tamimi, ambaye alikuwa mtu katili sana kuwa kaimu wake huko Kufa. Wakati aliporidhika na hali zilizokuwa zikiendelea hao Kufa, yeye akaelekea Basra. Huko Basra kulikuwa na upinzani mkubwa dhidi ya ufalme wa Bani Umayyah na mji ulikuwa katika hali ya ghasia. Hapo akatoa hotuba na akawatukana sana watu wa Basra. Vile vile aliwatishia kwa namna ileile alivyowatishia watu wa Kufa. Aliwaambia kwamba ikiwa hawatajiunga na jeshi la Mohlabi ndani ya siku tatu basi wataadhibiwa vikali sana. Aliposhuka kwenye mimbari ikatokea kwamba mtu mmoja mzee aliyeitwa Sharik bin Amr Yashkari ambaye alikuwa na jicho moja tu na aliyekuwa anaugua henia alimjia na akasema: “Mwenyezi Mungu ampe baraka Amir! Mimi ni mgonjwa wa henia. Busr bin Marwan, ndugu yake khalifa na gavana wa zamani wa Basra, alikuwa vilevile amenisamehe katika shughuli za kijeshi.” Hajjaj akasema: “Nafikiri unayosema ni kweli.” Hata hivyo, mara tu, baada ya kuyasema haya, yeye akaamuru kichwa chake kikatwe. Matokeo yake yakawa kila kijana na mzee wa Basra akajiunga na jeshi la Mohlab. Siku moja Hajjaj huyu huyu alikuwa anakula chakula chake, na baadhi ya washirika wake walikuwepo hapo kwenye meza yake ya chakula. Kwa wakati huo huo mapolisi wakamleta mtu mmoja na wakasema kwamba huyo alikuwa mtovu wa utii. Huyo mtu alikuwa anatetemeka kwa hofu na woga. Akamwambia Hajjaj: “Tafadhali sana usiniuwe. Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba sijakopa pesa kamwe kutoka kwa mtu yeyote wala sijawahi kujiunga na

274

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 274

9/4/2017 3:47:58 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

jeshi lolote. Mimi ni mfumaji na nilikamatwa na kuletwa hapa wakati nikiwa kwenye kitanda changu cha mfumi.” Hajjaj akaagiza mtu huyo akatwe kichwa chake mara moja. Wakati mtu yule masikini alipouona upanga akasujudu na kichwa chake kikakatwa wakati akiwa ndani ya mkao huo wa sajidah. Hajjaj aliendelea kula kana kwamba hakuna lolote lililotokea. Hata hivyo, washirika wake waliacha kula. Walishangazwa kuona ukatili huu. Hajjaj akakasirika na akasema: “Ni nini kimewafikeni? Kwa nini rangi ya nyuso zenu imebadilika na kwa nini matonge ya chakula yamedondoka kutoka mikononi mwenu? Je, ni kwa sababu mtu mmoja tu ameuawa? Mtu asiyetii hutoa mfano kwa wengine wasitii. Mtawala anayo haki ya kumuua au kumwacha.” Kulingana na Hajjaj wale watu wa Kufa na Basra wanaweza kushikishwa akili zao tu wanapofanyiwa udhalimu na ukatili wa namna hii. Tulichokitaja hapo ni maelezo mafupi tu ya maovu yaliyofanywa na Hajjaj huyu, vinginevyo kitabu kikubwa kabisa kinahitajika kwa kunakili vitendo vyake vya kikatili na mauaji ambayo ameyafanya kwa njia mbalimbali. Ibn Juruud aliasi dhidi ya ukatili na uonevu wa Hajjaj lakini uasi huo haukufanikiwa na Hajjaj akawa ndiye mshindi. Alikata vichwa vya idadi kubwa ya waasi hao na akavituma kwa Mohlab akimtaka avionyesha kwa mapana sana ili wale ambao wanaweza wakawa wanafikiria juu ya uasi waweze kutafakari juu ya matokeo ya kitendo kama hicho. Kisha akaandikisha kisheria mamia kwa maelfu ya watu wa Kufa na Basra ili kupigana dhidi ya maadui wa Bani Umayyah. Kwa kufanya hivyo alitaka kuchukua kisasi kwa wafuasi wa Ali, na kwa wakati huo huo aliwatumia askari hao kutumikia maslahi yake mwenyewe binafsi. Na kwa matokeo ya hili hapakuwa na hata kijana mmoja aliyebaki katika miji miwili hiyo ambaye hakulazimishwa kukutana na kifo. Waliuawa imma mikononi mwa Hajjaj au kwa panga za maadui zake. Watu wa Iraqi walifanya maasi dhidi ya Hajjaj kila mara lakini maasi haya yalikuwa dhaifu na waasi hao walizidiwa nguvu haraka sana na Hajjaj na wakawa ndio shabaha ya hasira zake. Wengi wao waliuawa, nyumba zao zikachomwa moto, na mali zao zikataifishwa. Mamia ya watu yaliuawa kila siku. Wale wanaume na wanawake waliokuwa wamefungwa katika majela ya Iraqi walipatwa na mateso makubwa mno na wakasubiria zamu zao za kuuawa. Iwapo Hajjaj au askari wake hawakuwa na muda wa kuwamaliza basi walikufa kwa njaa. Watu waliishi siku zao kwa dhiki kubwa. Hali zao zilikuja kuwa mbaya zaidi wakati Hajjaj alipokuwa mshindi kwenye vita vya Zawiah na Dayr Jamajam.

275

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 275

9/4/2017 3:47:58 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Kama matokeo ya vita vya Zawiah, ambavyo Hajjaj alikuwa mshindi na Muhammad bin Ash’ath alikuwa ameshindwa, yeye aliwateka Wairaqi elfu kumi na moja. Kwanza kabisa aliahidi kwamba maisha yao yataachwa, lakini waliposalimisha silaha zao, yeye akawakata vichwa wote. Kwa matokeo ya vita vya Dayr Jamajam, Wairaqi walishindwa kabisa. Mbali na kuwepo kwa upungufu wa chakula, ugonjwa wa tauni pia ulilipuka. Wale waasi wote walikamatwa na Hajjaj na hakumbakisha hata mmoja wao. Hata baada ya maangamizi yote haya yaliyoenea sehemu kubwa, vurumai na uporaji, Kufa na Basra hazikupata amani. Hajjaj aliendelea kuwanyanyasa na idadi ya wale waliouawa ikaongezeka siku baada ya siku. Kabla ya kuwaua aliwatukana vibaya sana bila mpango na kuwadhalilsha na kuyakebehi maoni na imani zao. Kama vile kuwachinja kwake watu kulivyokuwa hakuna mipaka, kuwatukana na kuwadhalilisha kwake kulikuwa pia kwenye upeo wake wa juu kabisa, kiasi kwamba hata watu walipokuwa wakikutana misikitini na masokoni hawakuzungumza juu ya lolote isipokuwa kwamba yule fulani wa fulani ameuawa siku iliyopita, yule nani na nani watapelekwa kwenye kiunzi cha kunyongea siku ile, na jinsi mtu fulani alivyotendewa maonevu kabla ya kuuawa kwake. Ile kauli maarufu ya Hajjaj: “Askari! Mkate kichwa chake” ilikuwa ni gumzo la kawaida la mjini huko Iraqi. Alikuwa na mfundo dhidi ya Shia wa Ali kiasi kwamba yeye aliwauwa wale watu waliokuwa na majina ya yeyote kati ya familia ya Abu Talib (kwa mfano; Ali, Husein). Watu wengi walikuja na wakatoa nyudhuru kwa ajili ya majina yao. Inasemekana kwamba mtu mmoja alikuja mbele yake na akasema: “Ewe Amir! Wazazi wangu wamenifanyia dhuluma sana. Walinipa jina la Ali ingawa mimi ni masikini na nisiyejiweza na ninahitaji msaada wako.” Kwa ufupi ukatili wa Hujjaj ulikuja ukawa wakutumika sana, na wafuasi wa Ali walikuwa ndio shabaha yake maalum. Wakati wale waliouawa kwa kulingana na maagizo yake walipohesabiwa, ilijulikana kwamba walifikia idadi ya mia moja na ishirini elfu (120,000). Wakati wa kifo chake yeye, wanaume hamsini elfu na wanawake hamsini elfu walikuwa kifungoni kwenye jela. Hata hivyo, khalifa wa Bani Umayyah – Abdul Malik bin Marwan alitoa ushauri huu kwa wanawe wa kiume: “Mheshimuni Hajjaj, kwa sababu yeye ndiye aliyezikanyaga mimbari, akaiteketeza miji na akawakomesha maadui kwa ajili yenu.” Ushauri huu ulitekelezwa kikamilifu. Baada ya kifo cha Abdul Malik, mwanawe

276

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 276

9/4/2017 3:47:58 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Walid alimuacha Hajjaj aendelee kuwa gavana wa Kufa, Basra na majimbo ya mashariki. Kabla ya kumalizia sura hii inaelekea kuwa ni muhimu kutaja tukio la huzuni kubwa sana. Tukio hili linaonyesha wazi kabisa tabia na sifa bainifu za Bani Umayyah na kizazi cha Abu Talib na wafuasi wao husika. Kama kwa upande mmoja linaonyesha umashuhuri na hadhi ya wafuasi wa Ali, linadhihirisha kwa upande mwingine uduni na uovu wa Bani Umayyah. Kwa kifupi kadhia yenyewe ni hii: Hujr bin Adi Kandi alikuwa mfuasi mwaminifu wa Ali. Wakati Imam Hasan alipolazimika kufanya amani na Mu’awiyah, Hujr pia pamoja na wengine alichukua kiapo cha utii. Lakini hili halikumfanya atupilie mbali mapenzi yake juu ya Ali na kuonyesha chuki juu yake. Bali alitamani kufuata katika nyayo za Ali. Alitaka tabia yake iwe kielelezo halisi cha tabia za Ali. Hujr alikuwa mtu mwaminifu na mnyofu sana. Alipenda amani na kuchukia kupigana na migongano. Aliunga mkono haki za kijamii kwa moyo mmoja. Yeye hakuchukulia mamlaka kama ni kitu kingine mbali na chanzo cha utumishi kwa umma. Katika masuala yote haya mawazo yake yalikuwa sawa na yale ya Ali. Iwapo mtawala aliwasaidia watu, yeye alimuunga mkono, lakini vinginevyo yeye alikuwa ni adui wa jadi. Hivyo ilikuwa ni jambo la kawaida kwamba asiweze kuwapenda Bani Umayyah wakimtukana Ali kutoka juu ya mimbari na aweze kuonyesha kuudhika kwake waziwazi dhidi ya mwenendo huu ingawaje angeweza kupata matatizo mikononi mwa mtawala wa wakati huo. Historia inasema kwamba Mughirah bin Shu’ba, gavana wa Kufa alimtukana Ali kutoka juu ya mimbari. Hujr bin Adi alisimama na kusema kwa sauti kubwa: “Ni nini hivi mazungumzo yote haya ya kibadhilifu. Tulipe ujira wetu ambao umeuzuia. Pesa hizo sio kwa ajili yako, na magavana waliotangulia hawakuzitamani kamwe. Unamtukana AmirulMu’minin na kuwatukuza na kuwasifu wahalifu.” Watu wengine wengi walimuunga mkono Hujr na hatimae Mughirah ikambidi ateremke kwenye mimbari bila ya kumalizia hotuba yake. Hujr aliendelea kuwashutumu Bani Umayyah na hakukaa kimya pale na wakati alipoona sheria za kidini zikiingiliwa na kuvunjwa. Katika wakati huo huo Mughirah akafariki na akarithiwa na Ziad bin Sumayyah. Wakati mmoja Ziad na Hujr walikuwa marafiki, lakini urafiki wao ulikuja kufikia mwisho kwa sababu ya tukio fulani. Ilitokea hivi kwamba Muislamu mmoja Mwarabu alimuua Dhimmi mmoja asiyeamini.

277

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 277

9/4/2017 3:47:58 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Suala hilo likaletwa mbele ya Ziad ambaye aliamua kwamba Muislamu huyo hana haja ya kuadhibiwa kutokana na kosa hilo bali alipe fedha ya fidia ya damu. Warithi wa Dhimmi huyo wakakataa kupokea fidia ya damu. Msimamo wao ulikuwa kwamba: Katika Uislam watu wote ni familia ya Mwenyezi Mungu. Kila binadamu ni ndugu wa binadamu mwingine atake asitake. Hakuna Mwarabu ambaye ni bora kuliko asiye Mwarabu. Ni uchamungu tu na kutenda mema ambako kunaweza kumfanya mtu kuwa bora juu ya wengine. Hujr aliamini katika uadilifu ambao Imam Ali aliufanya kuwa ndio wito wake, na kwa ajili yake huo ndio ameutoa uhai wake. Yeye kwa hiyo, aliyachukia maamuzi ya Ziad. Hakuweza kukaa kimya. Alisisitiza kwamba katika suala la kisasi Waislam na wasiokuwa Waislam wote walikuwa sawa. Waislam wengine wengi walimuunga mkono Hujr. Ziad na watu wake wakahofia kwamba machafuko yanaweza yakatokea. Ziad kwa hiyo, akaagiza kwa shingo upande kwamba yule mhalifu aweze kuadhibiwa. Baada ya hapo akaandika barua kwa Mu’awiyah akilalamika kuhusu mwenendo wa Hujr na marafiki zake. Mu’awiyah akamshauri Ziad kufuatilia nyendo na shughuli za Hujr na marafiki zake ili pengine anaweza akagundua jambo lililofanywa na wao ambalo linaweza kuwa kama ushahidi dhidi yao. Kuanzia wakati huo na kuendelea, tofauti kati ya makundi mawili hayo ikazidi kukua. Ziad alituma baadhi ya wakazi wa Kufa kwa Hujr ili wakamshauri kwamba ajiepusha na shughuli zake. Walirudi baada ya kukutana na Hujr na wakasema kwamba yeye alikuwa ameshika kani katika mawazo yake. Baada ya hapo Ziad akamwita Hujr lakini akakataa kuja. Hatimaye Ziad akatuma ujumbe wa afisa wa polisi kwenda kumkamata Hujr. Mapigano yakatokea hata hivyo, kati ya Hujr na huyo polisi, na Hujr akaingia mitini (mafichoni). Ziad alikasirika sana. Alimwita Muhammad bin Ash’ath bin Qais ambaye alikuwa mfuasi wa Hujr na mtu maarufu wa kabila la Kandi na akamtishia kwamba kama hatamuonyesha Hujr alipo atamuweka kifungoni jela, na miguu na mikono yake itakatwa na atanyongwa. Hujr hakupenda mtu mwingine ateseka kwa sababu yake. Kwa hiyo yeye mwenyewe akajitokeza mbele ya Ziad, lakini kabla ya kufanya hivyo alipata dhamana kutoka kwake kwanza kwamba hatamkera bali badala yake atampeleka kwa Mu’awiyah ambako huko atalisuluhisha suala hili naye mwenyewe. 278

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 278

9/4/2017 3:47:58 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Hata hivyo, mara tu Hujr alipokuja alikamatwa na kutupwa kizuizini. Baada ya hapo msako ulifanyika kuwasaka wafuasi wake. Baada ya umwagaji damu kiasi, baadhi yao wakakamatwa nao wakatupwa kizuizini pia. Halafu Ziad akawaita watu wa Kufa na kuwataka watoe ushahidi dhidi ya watu hawa na akawatishia. Baadhi yao hata hivyo wakashuhudia kwamba Hujr na marafiki zake walimpenda Ali na sio mtu mwingine badala yake, na walimshutumu Uthman na kumtukana Mu’awiyah. Ziad hakuridhika na kile walichokisema kwa sababu alikuwa akitaka ushahidi wenye uwezo wa kuamua. Wakati huo huo Abu Burdah bin Abu Musa Ash’ari akaandaa hati ya ushahidi dhidi ya Hujr hivi: “Huu ndio ushahidi ambao Abu Burdah mwana wa Abu Musa Ash’ari ameutoa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Yeye anathibitisha kwamba Hujr na marafiki zake walikoma kuwa watiifu na wameondoka kwenye kundi. Wamekoma kuwa na uhusiano na ukhalifa wa Mu’awiyah na wameamua kuanza kupigana kwa mara nyingine tena.Pale Abu Burdah alipomaliza kuandika hati hiyo, Ziad aliwataka watu wa Kufa kuweka saini zao juu yake. Takriban watu sabini waliweka sahihi zao kwenye hati hiyo. Ziad kwa udanganyifu tu akaandika juu yake majina ya baadhi ya watu ambao imma hawakuwepo kwa wakati huo wala walikuwa hawakuweka sahihi zao. Mmoja wao hawa alikuwa ni yule Kadhi Shurayh. Mara moja yeye huyu akatuma ujumbe kwa Mu’awiyah kujiondoa binafsi na hati hii ya ushahidi na akasema kwa maneno ya wazi kabisa: “Ninashuhudia kwamba Hujr ni mtu mchamungu na ni mmoja wa watu mashuhuri wa zama hizi.” Hujr na marafiki zake baadae wakapelekwa kwa Mu’awiyah. Barua ya Ziad na ile hati ya ushahidi pia vilimfikia Mu’awiyah. Yeye akazisoma nyaraka zote mbili mbele ya watu. Papo hapo baadhi ya watu wakamshauri kuwafunga wale wahusika. Wengine walishauri kwamba wangeweza kuwekwa kwenye miji mbalimbali ya Syria na wasiweze kuruhusiwa kurudi tena Iraqi. Mu’awiyah akawasilana na Ziad kuhusu suala hilo. Yeye akajibu: “Kama unataka kuiweka Iraqi mikononi mwako basi usije ukawaruhusu hao kurudi hapa. Baada ya muda wa siku chache Mu’awiyah akamtuma mtu kwa Hujr na marafiki zake na kupendekeza kwamba kama wao wataacha kujihusisha na Ali na wakamtukana na kumtukuza Uthman, maisha yao yatabakishwa, bali wale watakaokataa kufanya hivyo watauawa. Hujr na marafiki zake wakalikataa pendekezo hilo na hatimaye wakauawa. Kisa hiki cha kuhuzunisha pia kimesimuliwa kwenye vitabu vyote vya historia. Kinao279

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 279

9/4/2017 3:47:58 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

nyesha ubora wa hali ya juu wa tabia, umadhubuti wa watu hawa majasiri, kwani waliweza kuyaona makaburi yao kwa macho yao wenyewe na panga zikining’inia juu ya vichwa vyao na bado hawakuweza kuyatelekeza mahaba yao juu ya Ali japo kwa kitambo kidogo. Kile ambacho Mu’awiyah na watu wake walichokuwa wamekifanya katika suala lao kilikuwa ni kwamba walichimba kaburi mbele ya kila mmoja wao ili kwamba yoyote yule atakayekataa kuonyesha karaha dhidi ya Ali aweze kukatwa kichwa na kutupwa ndani ya kaburi. Baadhi ya wanahistoria wameeleza kuhusiana na watu hawa kwamba wawili kati ya marafiki wa Hujr waliogopa pale walipoona panga na makaburi hayo na wakawaomba walinzi wa Mu’awiyah wawapeleke kwa khalifa, wakisema kwamba wao hawana tofauti zozote na Mu’awiyah kuhusu Ali na Uthman. Wao kwa hiyo, wakachukuliwa na kupelekwa kwa Mu’awiyah. Mmoja wao akaonyesha chuki juu ya Ali waziwazi, lakini yule mwingine akamtukuza Ali na sahaba zake, na akamtukana Mu’awiyah na wafuasi wake na akasema maneno makali sana kuhusu Uthuman, ambayo Mu’awiyah hakuweza kuyavumilia. Aliamuru mtu huyo kurudishwa kwa Ziad kwa maelekezo kwamba auawe katika namna ambayo hajawahi kuuawa mtu mwingine katika ulimwengu wa Kiislam hadi kufikia wakati ule. Ziad akamzika mtu huyo akiwa hai. Inasemekana kwamba wakati Hujr alipokuwa anakwenda kuuawa alisema maneno haya tu: “Kuna Mwenyezi Mungu kati yetu na Waislam hawa. Watu wa Iraqi wametoa ushahidi dhidi yetu na watu wa Syria wakatuua.” Hakuna shaka kuhusu ukweli kwamba ule mfano wa utawala wa kidhalimu na kidikteta ulioanzishwa na ufalme wa Bani Umayyah; na maovu ambayo wameyatenda wao yalikuwa hayalinganishiki, na maisha ya Ali na kizazi chake yalikuwa kwa upande mwingine ndio kielelezo bora cha usafi wa akili na vitendo, na wa demokrasia. Wao hawakuwanyonya watu kama walivyofanya Bani Umayyah bali waliyachukulia mazao ya ardhi kuwa ni haki ya watu wa kawaida badala ya kuwa ya matajiri na wale watu maarufu. Hulka ya wafuasi na wasaidizi wa Bani Umayyah ilikuwa na tofauti kubwa kabisa na ile ya kizazi na wafuasi wa Ali. Wale watu mashuhuri wenye mawazo ya dunia waniinamia kuelekea kwa Bani Umayyah kwa ajili ya manufaa ya kidunia, na watu wa chini pia wakawa wafuasi wao kwa idadi kubwa. Hili lilitokea kwa sababu kwa wakati ule watu walikuwa ha280

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 280

9/4/2017 3:47:58 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

wakukadiria thamani ya maadili na hawakuelewa ni nini kingeweza kuwa na manufaa kwao baadae, na nini kingeweza kuwa na madhara kwao. Kwa hiyo wao walifikiria juu ya manufaa ya karibu na hawakutambua ni aina gani ya watu waliokuwa wanawaunga mkono. Na pale walipolitambua hilo wakati ulikuwa tayari umekwishapita na walikuwa wamechelewa mno. Kwa upande mwingine watu ambao hulka yao, maadili na mienendo na tabia zinafanana na zile za Ali na kizazi chake walielemea upande wao, na wamebakia imara katika njia ya haki. Walipatishwa usumbuvu na mateso makali na Bani Umayyah na wafuasi wao lakini hawakuyumba wala kusita kamwe. Wakifuata mfano wa Imam wao, Amirul-Mu’minin Ali, walijitolea mhanga maisha yao bali hawakuvumilia kule kuzimwa kwa haki za kijamii. Kama vile tu wafuasi na marafiki wa Ali na kizazi chake walivyokuwa waadilifu na wakapata sifa za hali ya juu za ukarimu, huruma na uchamungu, kwa namna hiyo hiyo wafuasi wa Bani Umayyah walikuwa waathiriwa wa maovu kama vile ubinafsi, ukaidi, uonevu na unyonyaji. Itakuwa ni bora kama tutataja kwa mara nyingine tena yale mawazo yaliyoelezwa na baadhi ya waandishi wa Kiarabu bila ya kutoa maoni juu yao kwa sababu kile tulichokisema katika sura hii kinakanusha kabisa mazungumzo yao yasiyofaa. Kati ya waandishi hawa wa Kiarabu tunaweza tukamchukua Muhammad Kurd Ali na kile alichokieleza yeye kuhusu umaarufu na umashuhuri wa Bani Umayyah kinaweza kufanywa kama kielelezo cha sifa zilizomwagwa juu yao na wengine. Kumsifia Mu’awiyah na maafisa wake wa jeshi wenye kiu ya damu, ambao wamefanya maovu yasiyokuwa na idadi kama ilivyoelezwa katika kurasa zilizopita, Muhammad Kurd Ali anasema ndani ya kitabu chake kiitwacho ‘Al-Islam wa al-Hazarat al-Arabiyah’: “Kitendo muhimu kabisa ambacho Mu’awiyah alikichukua kilikuwa kwamba yeye aliongeza mishahara ya jeshi, na kutokana na bahati yake njema pia alipata msaada wa baadhi ya watu hodari sana kama Ziad bin Abih, Mughirah bin Shu’bah, Zuhhak bin Qais, Muslim bin Uqbah, Busr bin Artat na kadhalika.” Kuwapongeza watu hawa wenye uchu wa damu Kurd alisema kwamba wao walikuwa hodari sana na watu mashuhuri wa nchi, ingawa ilikuwa ni muhimu kwake kuelezea kwamba hauhusiani chochote na watu madhalimu na waonevu kama hawa, na watu wote waliostaarabika, iwe Waarabu au wasiokuwa Waarabu, wanawachukia watu wakatili kama hao. 281

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 281

9/4/2017 3:47:58 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Inashangaza sana kwamba Muhammad Kurd Ali hahisi hata chembe ya wasiwasi wakati akiandika mambo kama haya, wala hafanyi uadilifu na wale wanaoishi katika karne ya ishirini kwa kupotosha mambo ya kihistoria. Anashindwa kukumbuka vile vile kwamba hapo mwanzoni alikuwa ameandika kwenye kitabu chake: “Katika siku za Mu’awiyah mtu mchamungu aliuliza: ‘Je, umewaacha watu katika hali gani?’ Yeye akajibu: ‘Nimewaacha katika hali mbili – wanaoonewa ambao hawapati haki na wakandamizaji ambao hawachoshwi na udhalimu.’” Wauaji Wa Uthman Maelezo mafupi ambayo tumeyatoa ya mwenendo na tabia za Bani Umayyah na kizazi cha Ali na wafuasi wao husika yanaonyesha wazi kwamba kupenda mamlaka na utawala, na ubinafsi na uchoyo vilikuwa vimechukua mizizi ya kina katika nyoyo za Bani Umayyah, na wafuasi wao ambao walikuwa na tabia na desturi sawa na za mabwana zao walikuwa pia wenye tamaa kama wao. Kama tulivyoeleza mapema, Bani Umayyah na wafuasi wao walimpinga Mtume wa Uislamu, kwa sababu wao walikuwa na fikra za wakuu wa Maquraishi ambao hawakuweza kuvumilia kwamba Uislamu uwazuie kutokana na matendo yao maovu na kuharibu sheria zao za kijamii ambazo bila shaka zilikuwa na manufaa kwa wafanya biashara na watu matajiri, lakini zilikuwa ni hati ya kifo kwa masikini na wasiojiweza. Tokea ile siku ambapo Mtume alitangaza kuteuliwa kwake kwenye kazi ya utume hadi siku ya kutekwa Makkah (Fatihu-Makkah), wakuu na watu maarufu miongoni mwa Quraishi waliukubali Uislamu, lakini matumaini na malengo ya kila mmoja wao yalikuwa tofauti. Matukio yanaonyesha kwamba watu hawa wanaweza kugawanywa katika makundi matatu kama ilivyoelezwa hapa chini: Kwanza kabisa walikuwepo watu ambao waliuchukulia Uislamu kuwa ni dini ya kweli na wakasilimu kwa hiari ya dhati kabisa. Idadi yao miongoni mwa wakuu wa Maquraishi ilikuwa ndio ndogo kabisa. Pili kulikuwa na wale ambao walikuwa wanatazama ni lipi kati ya makundi mawili – Waislamu na Quraishi litakalofanikiwa. Wao walitaka kujiunga na kundi lenye kufanikiwa. Kwenye kundi hili alikuwamo Amr Aas. Tutaelezea baadae yale mazingira ambamo yeye aliukubali Uislamu.

282

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 282

9/4/2017 3:47:58 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Tatu kulikuwa na watu ambao waliukubali Uislamu kwa kusitasita. Wao walikuwa wamepoteza hadhi na nafasi zao za heshima; na walikuwa wamejiunga na safu za Waislamu kwa nia ya kuubadilisha Uislamu kwa ujinga mara tu fursa itakapojitokeza. Katika kundi hili la wakuu na wazee wa Quraishi alikuwamo Mu’awiyah, baba yake Abu Sufyan bin Harb na wale wakuu wa kikabila waliokuja kuwa makafiri mara tu baada ya kifo cha Mtume. Wakuu na wazee wa Quraishi ambao walikuwa wa kundi lile la kwanza walibakia madhubuti katika imani zao lakini Uislamu wao ulikuwa, bila ya kutambua, umechanganyika na hisia za wao kutokana na familia za juu. Na kuhusu wale watu walio wa makundi yale mengine mawili egemeo la siasa zao lilikuwa ni ule mwelekeo wa kiuchumi tu, na ile hima yake ya kijamii. Wakuu wa Quraishi waliokuwa wa makundi haya waliungana kwa manufaa yao binafsi. Kama maslahi yao yalikuwa mamoja walisaidiana wao kwa wao; bali kama yalikuwa yameachana, basi walifanya kila mtu tofauti kivyake. Uwajibikaji juu ya udhalimu na madhara unakabidhiwa juu ya wakuu wanaotokana na makundi yote matatu, ingawaje wakuu wa makundi haya mawili ya mwisho walikuwa na sehemu kubwa katika hilo. Hawakupenda kukosa fursa yoyote ya kupata utajiri na pesa na hawakujali juu ya ni majukumu mangapi yaliyokuwa katika siku zile mabegani mwa Waislamu kuhusiana na uendelezaji wa Uislamu. Dalili za kupenda utajiri na faida zilikuwa zimeanza kujitokeza tangu mwanzoni mwa kipindi cha ukhalifa wa Abu Bakr. Ushahidi wa hili ni lile tukio la Khalid bin Walid na maneno makali waliotupiana Abu Bakr na Umar kuhusiana na hilo. Kisa chenyewe kwa kifupi ni kwamba, Khalid alimuua Malik bin Nuwaira kikatili na kwa uonevu ili kupata ngawira, na akaihalifu staha ya mke wake ambaye alikuwa mrembo sana. Wakati habari hizi zilipomfikia Abu Bakr, yeye alishangazwa sana na pia akapata huzuni na akatamka kauli hii maarufu sana: “Ngawira za vita zimewafanya Waarabu kuwa walafi mno na Khalid amevunja amri zangu.” Wakati Khalid alipokuja kuonana na Abu Bakr alikuwa na mishale mitatu kwenye kilemba chake. Pale Umar alipomuona alisema: “Ewe adui wa Mwenyezi Mungu! Matendo yako yote haya ni ya kinafiki. Wallahi kama nitapata udhibiti juu yako nitakupiga mawe hadi ufe.” Kisha akaivuta ile mishale kutoka kwenye kilemba cha Khalid na akaivunja. Khalid hakuweza kupata ujasiri wa kusema lolote kwani alikuwa akielewa kwamba Umar alikuwa anashughulika kwa mujibu wa maelekezo ya Abu Bakr. 283

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 283

9/4/2017 3:47:58 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Baadae Khalid alimuona Abu Bakr na akatoa visingizio vingi mbele yake. Abu Bakr akamuamini na akakubali visingizio vyake. Wakati Umar alipokuja kujua kuhusu hili, alimchochea Abu Bakr dhidi ya Khalid na akashauri kwamba Khalid lazima aadhibiwe kwa kumuua Malik. Abu Bakr akasema: “Ewe Umar! Bora ungenyamaza. Khalid sio mtu wa kwanza ambaye amefanya makosa katika suala la kutafsiri (sheria).” Wakati wa kipindi cha Umar wale watu maarufu wa kabila la Quraishi vile vile walitamani manufaa ya kidunia, na kuna mifano isiyo na idadi inayothibitisha ukweli huu. Ushahidi bora ni zile beti ambazo mshairi alizitunga na kuzituma kwa Umar. Katika beti hizo ilisemekana kwamba katika baadhi ya miji na majimbo; wale watu maarufu na wenye hadhi walitumia vibaya mali ya umma, na wakachukua tahadhari kwamba yeye (Umar) asiweze kuja kugundua kuhusu hilo. Ikaongezewa kwamba watu walikuwa wakipata dhiki sana kutokana na unyonyaji huu. Mshairi huyo anasema: “Wanapotafuta, na sisi tunatafuta. Wanapofanya jihadi na sisi pia tunafanya jihadi. Sasa ni wapi walikoupata utajiri huu, wakati sisi tuko mikono mitupu? “Wakati mchuuzi wa Kihindi anapoleta miski, inaonekana ikitiririka kwenye vichwa vya hawa wenye hadhi. Chukua mali ya Mwenyezi Mungu kutoka kwa yeyote unayeweza. Watu hawa watakuwa wameridhika hata kama utawafanya wabakie na nusu ya mali zao.” Umar aliagiza baadhi ya watu hawa wasiondoke kwenye sehemu zao au makazi yao na akawauzulu wengine kutoka kwenye nafasi zao. Pia aliwafanya baadhi yao kutoa maelezo ya mapato yao na kuukamata utajiri wao. Uthman alitoa uhuru kamili kwa wale wenye hadhi, na ule udhibiti ambao ulikuwa umewekwa na Umar juu ya ulafi wao uliondolewa. Wenye hadhi hawa wakawa washindi chini ya uongozi wa Bani Umayyah, ambao ulitokeza kwa wakati mmoja na kutoweka wakati mwingine. Matokeo yalikuwa kwamba watu hawakuwa na budi kupatwa na matatizo makubwa, na wale wenye hadhi wakajiingiza katika vitendo viovu sana kiasi ambacho hakijawahi kuonekana katika wakati wa Mtume au katika ule wa Abu Bakr na Umar. Haitakuwa nje ya maudhui kutaja hapa kile alichokuwa amekisema Ali kuhusu Uthman na Bani Umayyah kabla Uthman hajawa khalifa. Alikuwa amemwambia ami yake Abbas: “Nina uhakika Maquraishi watakuja kumfanya Uthman ashike ukhalifa, na Uthman ataanzisha uzushi. 284

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 284

9/4/2017 3:47:59 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Kama ataishi nitakukumbusha juu ya maneno yangu haya na kama atauawa au akafariki tu, Bani Umayyah watauweka utawala uzunguuke juu yao wenyewe tu.” Ni kweli kiasi gani ubashiri huu wa Imam Ali ulivyothibiti katika suala la Uthman! Wakati Uthman alipokalia ukhalifa ilimbidi kukabiliana na matatizo ambayo yalikuwa yanatatanisha sana. Bani Umayyah badala ya kumsaidia yeye kuyatatua, wao waliyafanya kuwa magumu zaidi. Zaidi ya hayo, wao walichukua fursa kubwa sana ya upole wa Uthman kiasi walivyoweza, na wakaweka misingi ya sera zao juu ya ubaguzi wa kikabila, ushawishi binafsi na mamlaka na upuuzaji wa ustawi wa jamii. Wakitumia uwezo wote wa mamlaka ya kiserikali; walizuia nafasi na vyeo vyote wao wenyewe, na wakaubadilisha ule mfumo wa serikali ya Kiislamu kuwa mfumo wa kibepari halisi, na ukhalifa kuwa ufalme. Rasilimali zote za nchi zikawa ni za ukiritimba wa marafiki na watumwa wao. Mara tu baada ya kuutwaa ukhalifa, Uthman alianza kuwafanya watu kuwa watumwa wa Bani Umayyah. Aliwafanya Bani Umayyah kuwa watawala wa miji yote na majimbo ya Kiislamu, na akawapa maeneo makubwa ya ardhi. Aliifanya mali ya Waislamu kuwa ni kitu cha kuchezea cha matajiri, na akalisaidia kwa uwazi kabisa lile tabaka la kibepari ambalo lilikuwa limevunjwa na Uislamu hapo mwanzoni. Matokeo yalikuwa kwamba wale watu wenye hadhi na uwezo wakawa matajiri zaidi, na watu wa chini wakawa watumwa wao. Tunasimulia hapa chini mifano michache ambayo itaonyesha ni nafasi gani waliyokuwa nayo Bani Umayyah wakati wa kipindi cha Uthman na jinsi dola ilivyokuwa kitu cha kuchezea ndani ya mikono yao. Uthman alitoa moja ya tano ya ngawira iliyopokelewa kutoka kwenye ushindi wa nchi za Kiafrika kwa binamu yake, Marwan bin Hakam. Uzushi huu mpya ulikasirikiwa sana na watu! Abdur-Rahman bin Hanbal; akiwakilisha mawazo ya umma anasema: “Naapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba Yeye Mwenyezi Mungu hakuacha kitu chochote hivi hivi bure tu, bali wewe Oh, Uthman umesababisha fitna juu yetu. Huu ni mtihani juu yako, au huenda ni mtihani kwetu sisi.” Fadak, ambayo kwa kweli ilikuwa imerithiwa na Fatmah, ilitolewa na Uthman kwa Marwan. Uthman vile vile alimpa dirham mia moja elfu kutoka kwenye hazina ya umma. Bani Umayyah mmoja – Abdullah bin Khalid bin Usayd alimuomba msaada na yeye akampa dirham mia moja elfu, ingawa kulikuwa hakuna uhalali wowote kwa ajili ya ubadhilifu huo. Alikuwa mpole hususan hasa kwa Hakam bin Aas ambaye 285

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 285

9/4/2017 3:47:59 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

alikuwa adui wa jadi wa Uislamu, na Mtume alikuwa amemfukuza kutoka Madina. Uthman alimpa huyu dirham mia moja elfu. Kulikuwa na soko linaloitwa Mehzool hapo Madina ambalo lilitolewa na Mtume kwa Waislamu. Uthman alilitoa kwa Harth bin Hakam. Kulikuwa na malisho karibu ya Madina, ambayo yalikuwa yametangazwa na Mtume kama ardhi ya wote kwa ajili ya kuchungia wanyama ambao ni mali ya Waislam wote. Uthman aliyanyakua malisho hayo kutoka kwa Waislam na akayahifadhi kwa ajili ya Bani Umayyah pekee. Kutokea hapo na kuendelea, ni wale ngamia mali ya Bani Umayyah tu walioweza kuchungwa hapo. Kiwango chote cha kodi zilizopokelewa kutoka kwenye jimbo la Afrika; yaani, kutoka Misri hadi Tangiers, yeye alikitolea kwa Abdullah Bani Sarah. Siku ambayo alitoa dirham mia moja elfu kwa Marwan bin Hakam, alitoa vile vile dirham mia mbili elfu kwa Abu Sufyan bin Harb. Juu ya hili, Zaid bin Arqam, yule mtunza hazina, alikuja kwa Uthman na, akiwa anatokwa na machozi machoni mwake, akamtupia funguo za Hazina ya Umma mbele yake. Uthman akasema: “Kwa nini unalia? Mimi nimeonyesha heshima kwa watu hawa kutokana na udugu wetu.” Zaid akasema: “Hata kama ungetoa dirham mia moja tu kwa Marwan zingekuwa ni nyingi sana, lakini umempa dirham mia moja elfu!” Uthman akasema: “Wacha funguo hizo zibakie hapa. Itawezekana kwangu mimi kupata watunza hazina wengi.” Kiasi kikubwa cha mali kilipokelewa kutoka Iraqi. Kiasi chote hicho kiligawanywa na Uthman miongoni mwa Bani Umayyah. Alipomuozesha binti yake Aisha kwa Harth bin Hakam, alimpa huyo Harth dirham mia moja elfu mbali na kile ambacho alikuwa amekwishampatia. Yeye pia alimpa Harth idadi kubwa ya ngamia ambao walipokelewa kutoka kwenye nchi mbalimbali za Kiislam. Vile vile alimpa kazi ya kukusanya Zaka kutoka kwenye kabila la Qaza’ah na akampa kiasi chote alichokikusanya huko. Kiasi hicho kilikuwa ni dirham milioni tatu. (Sharh Nahjul-Balaghah, Juz. 1, uk.98). Wakati mmoja masahaba maarufu ambao walikuwa wameongozwa na Ali walikutana na Uthman na wakawa na mazungumzo naye kuhusu Harth. Uthman alisema: “Yeye ni ndugu yangu wa karibu.” Masahaba wakasema: “Kwani Abu Bakr na Umar hawakuwa na ndugu wa karibu? Kwa nini wao hawakuweka upendeleo juu yao?” Uthman akajibu: “Abu Bakr na Umar walitafuta malipo kwa Mwenyezi Mungu kwa kuwanyima ndugu zao, ambapo mimi natafuta malipo 286

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 286

9/4/2017 3:47:59 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

kwa Mwenyezi Mungu kwa kuwafanyia upendeleo juu yao.” Hao masahaba wakasema: “Tunapendelea mwenendo wao kuliko wako.” Uthman alifanya mambo mengi kama kuwahimiza wale watu waliokuwa madarakani kulimbikiza mali kwa njia haramu. Aliwaacha watu wenye uwezo huru kufanya chochote walichotaka; bali alifanya mambo kuwa mepesi kwao ili waweze kuja kuwa washiriki katika maovu ya Bani Umayyah na wasiweze kupata wasaa wa kushutumu shughuli zao. Talha bin Abdullah alisimamisha jumba la fahari huko Kufa; ambalo lilikuja kujulikana kwa Waarabu baada ya karne tatu kwa jina la Dar al-Talhatain. Na kuhusu mapato yake, Mas’ud amesema ndani ya Murujul-Dhahab kwamba kutoka Iraqi peke yake alipokea kila siku nafaka zenye thamani ya sarafu elfu moja za dhahabu, bali ilikuwa ni zaidi ya hizo. Kiasi sawa na hicho kilipokelewa kutoka Kanas. Mapato kutoka Sirat na vitongoji vyake yalikuwa makubwa zaidi. Hapo Madina alisimamisha jumba la kifahari ambalo lilifanana na lile la Uthman. Abdur-Rahma bin Auf alijenga makasiri na majengo mengi makubwa na yenye nafasi. Alikuwa na mazizi mengi na ndani ya kila zizi walitunzwa farasi mia moja. Alimiliki pia ngamia elfu moja na mbuzi elfu kumi. Mbali na utajiri wote huu, bado alikuwa na sarafu milioni tatu za dhahabu. Zaid bin Thabit aliacha nyuma yake dhahabu nyingi sana ambayo ilibidi ivunjwe kwa shoka katika vipande vipande ili kugawanywa kwa warithi wake. Mbali na haya, aliacha nyuma yake kiasi kikubwa cha mali nyinginezo. Laila bin Umayyah aliacha nyuma yake nusu milioni ya sarafu za dhahabu. Mas’ud anaandika kuhusu Zubeir bin Awam kwamba katika wakati wa Uthman yeye alimiliki watumwa elfu moja na watumwa wa kike elfu moja pia. Alijenga majumba ya fahari katika sehemu mbalimbali kama Basra, Kufa na Alexandria na alimiliki sarafu za dhahabu hamsini elfu taslim na farasi elfu moja. Baada ya kuandika yote haya, Mas’ud anasema: “Inahitaji majuzuu kuhadithia jinsi utajiri wa wale matajiri ulivyoongezeka wakati wa kipindi cha Uthman. Hii haikuwa ndio hali ya wakati wa Umar. Utajiri wa mtu ambaye Uthman na Bani Umayyah wengine walifurahishwa naye ulikuwa hauna mipaka. Watu wa chini waliteseka kwa njaa ambapo ndugu na marafiki wa Uthman walibingirika katika utajiri. Walikusanya mali nyingi kiasi ambacho watu walikuwa hawajawahi kukiona au kusikia juu yake. Yeye mwenyewe alikuwa tajiri sana. Wakati wa kuuawa kwake, mtunza hazina wake alikuwa na sarafu za dha287

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 287

9/4/2017 3:47:59 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

habu mia moja na hamsini elfu na maelfu ya dirham. Alikuwa na mali yenye thamani ya takriban dirham mia moja elfu katika bonde la Qura’ na Hunayn. Alikuwa pia na ngamia na farasi wasiokuwa na idadi (tazama kitabu kiitwacho ‘Uthman’ kilichoandikwa na Sadiq Arjun, kilichochapishwa Misri). Vito na mapambo ya wafalme wa Kiirani, ambayo yalipatikana kama ngawira za kivita wakati wa kipindi cha Umar yaliwekwa katika Hazina ya Umma. Wakati wa kipindi cha Uthman, hata hivyo, yalionekana yakimeremeta kwenye miili ya mabinti zake Uthuman. Watu walijionea kwa macho yao wenyewe haki zao zikikanyagwa. Watu waliokuwa madarakani waliwadhihaki raia masikini ambao hawakuweza kusema lolote katika kuwajibu. Mas’ud anasema kuhusu Uthman ndani ya Murujul-Dhahab: “Uthman alikuwa mfujaji sana. Magavana wake na watu wengine pia walifuata mfano wake. Uthman alijenga hapo Madina, kasiri moja ambalo milango yake ilikuwa ya mbao za mvule. Alipata vile vile mali nyingi, mabustani na chemchem nyingi ndani ya Madina. “Uthman alitoa ruhusa ya wazi kwa Bani Umayyah kuteua au kuuzulu watumishi. Walijilimbikizia mali na wakaanzisha maeneo ya ushawishi na mamlaka kwa ajili ya kuendeleza utawala wao. Chanzo cha maovu yote haya alikuwa ni Marwan bin Hakam ambaye aliteuliwa na Uthman kama waziri wake. Uthman alifuata ushauri wake katika masuala yote. “Vivyo hivyo, Uthman aliwagawa watu kiuchumi katika matabaka mawili. Tabaka moja lilikuwa la maafisa na ndugu zake Uthman, ambao walibingirika katika utajiri na wakafanya aina zote za maovu, na tabaka jingine lilikuwa ni watu wa kawaida ambao walikuwa wamenyimwa na ambao walikuwa hawajiwezi. “Hapo kabla utaratibu ulikuwa kwamba mapato ambayo yalikusanywa kutoka mji fulani au jimbo yalitumika kwanza kabisa kwa kuwasaidia wale wenye shida wanaotokana na maeneo yale husika na kile kiasi cha ziada kilitumwa makao makuu, ili kwamba khalifa aweze kukitumia juu ya wenye haja hapo. Uthman aliagiza kwamba kiasi chote kitumwe makao makuu. Wale wenye kujipendekeza walichukua fursa kubwa ya mabadiliko haya ya sera katika kujinufaisha sana.” Dr. Taha Husein anasema kwamba: “Tatizo la kwanza kabisa ambalo lilijitokeza kwa kutokana na utaratibu huu lilikuwa kwamba ubepari ulienea ndani ya Iraqi na majimbo mengine kwa kiasi kikub288

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 288

9/4/2017 3:47:59 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

wa mno. Utaratibu huu uliwanufaisha wale ambao walikuwa ni mabepari wakubwa walioweza kununua mali za wale waliokuwa wa tabaka la waliojaaliwa kwa kiasi kidogo. Hivyo Talha na Marwan bin Hakam wakanunua mali nyingi. Kutokea hapo na kuendelea, ukaanza utaratibu wa kununua na kuuza, rehani, kukodisha na kadhalika, sio katika Hijazi na Iraqi tu, bali pia katika nchi nyingine za Kiarabu na maeneo yaliyotekwa, na maeneo ya mashamba makubwa yakaja kuwepo. Katika mazingira haya watu wote wakajishughulisha katika kutengeneza pesa, matokeo yake yakiwa ni kuzuka kwa tabaka la watawala matajiri. Liliheshimika sana kuliko lile tabaka ambalo lilikuwa na mashamba ya nasaba. “Tatizo la pili ambalo lilijitokeza lilikuwa kwamba wale watu walionunua mali katika miji ya Kiarabu kwa jumla; na hususan Hijazi, walijitahidi kupata faida ya juu kabisa kutoka kwenye ardhi zao. Walinunua idadi kubwa ya watumwa. Mara tu, Hijaz ikawa kama pepo. Hivyo tabaka la wamiliki ardhi likazuka na kuwepo katika miji kama Madina na Ta’if. Wao wenyewe hawakufanya kazi, na walitumia muda wao katika kustarehe, na kazi zote zilifanywa na watumwa wao. Mambo yote ya mabwana hawa yalisimamiwa na watumishi wao. Mabwana hawa walikuwa kwa kweli ndio watumwa; na hao watumwa walikuwa ndio mabwana halisi hasa. Kwa upande mwingine walikuwako wale mabedui ambao walikuwa wamenyimwa vistawishi vyote vya maisha. Hawakumiliki ardhi yoyote hapo Hijaz ambayo wangeweza kuuza ili kununua ardhi huko Iraqi, na vile vile hawakuwa na ardhi yoyote huko Iraqi ambayo wangeweza kuiuza na kununua nyingine huko Hijaz. “Vitendo hivi vilivyotumiwa na Uthman kwa maamuzi yake mwenyewe, au kwa mapendekezo ya washauri wake, vilizaa matokeo mabaya sana ya kisiasa na kijamii. “Matokeo ya kisiasa yalikuwa kwamba ni watu wachache tu waliogeuka kuwa wamiliki wa utajiri mkubwa. Kila bepari aliwavuta watu upande wake mwenyewe kwa njia ya utajiri wake, akaanzisha kikundi cha wafuasi wake na akaanza kufikiria kuwa mtawala. Watu kama hao walijitahidi kuitumia vizuri fursa ya kusambaratika kwa watu. “Kutoka kwenye mtazamo wa kijamii, watu waligawanyika kwenye matabaka mbali mbali. Kwenye tabaka moja walikuwamo watu ambao walikuwa matajiri na walikuwa na ushawishi na mamlaka, na kwenye tabaka jingine walikuwamo watu masikini na wasiojiweza. Watu wanaotokana na tabaka la kwanza walikuwa na maeneo makubwa ya mashamba na watumwa na watumishi, ambao waliwafanyia kazi katika ardhi zao na kutoa huduma nyinginezo. Katikati ya matabaka haya mawili lilikuwepo tabaka la kati. Wale ambao walikuwa wa tabaka hili waliishi katika miji 289

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 289

9/4/2017 3:47:59 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

ya mbali. Waliwashambulia maadui na kuilinda mipaka. Maisha ya watu na mali zao yalikuwa salama kwa sababu ya tabaka hili. “Wale watu matajiri waliwafanya watu wa tabaka hili kuwa ni kama zana zao. Walianzisha faraka baina yao na wakawagawanya kwenye makundi mbalimbali. Historia ya Waislamu inaonyesha kwamba mfarakano ulitokea kwanza miongoni mwa watu wakwasi. Kwanza kabisa mabepari walipingana wenyewe kwa wenyewe, na baadae tofauti zilizuka kati ya watu wa lile tabaka la kati na matajiri. Kuhusu lile tabaka la tatu, wale waliokuwemo humo waliwatumikia matajiri na wakafanya kazi kwenye ardhi zao. Ni dhahiri hawakutwaa ushawishi wowote katika jamii na hawakushiriki katika mifarakano hiyo ya wengine. Tofauti zao zilikuja kujitokeza katika hatua za baadae kabisa. (Al-Fitnatul-Kubra, Juz. 1, ‘Uthman’ uk. 105 - 109). Hadi wakati huo Waarabu walikuwa hawakuzoea tofauti za matabaka na hakuna aliyewahi kuonekana akifaidi nafasi ya kipekee au kupokea zawadi maalum bila ya uhalali unaostahili. Ilikuwa pia bado haijatokea hadi wakati huo kwamba ustawi wa kijamii wa watu fulani uwe umepewa kipaumbele juu ya ustawi wa watu wote. Mwenendo wa Mtume, uadilifu na ukarimu wake vilikuwa vimeingia sana kwenye akili zao. Walikuwa wamezoea sana ile serikali ambayo ilikuwa serikali ya watu na sio ya watu wachache tu, serikali ya uadilifu na sio ya udhalimu – serikali ambayo ilishiriki matatizo ya watu na sio ile ambayo ilisababisha vurugu na ghasia. Wakati Uthman alipomrithi Umar kama khalifa na akatwaa hizo sera zilizotajwa hapo juu, watu walisumbuliwa sana. Walilalamika dhidi ya sera hizi kwa Uthman mara kwa mara, na pia wakaonyesha kuchukizwa dhidi ya magavana wa Bani Umayyah na maafisa waliofuata sera hizi. Wakati mwingine ilitokea kwamba Uthman alijisikia aibu kwa sababu ya vitendo viovu vya watawala wa Bani Umayyah, akayasikiliza malalamiko kwa subira na akaahidi kuwaondoa wale watumishi waonevu. Mara tu baadae, hata hivyo, watumishi hao walimshawishi Uthman na wakaendelea kushikilia nafasi zao za kazi, wakajiingiza kwenye vitendo viovu zaidi na wakachukua kisasi cha kikatili sana juu ya wapinzani wao. Mara kwa mara Waarabu walimwendea Uthman katika namna ya ujumbe na wakalalamika dhidi ya watumishi wa Bani Umayyah. Uthman aliwaahidi kwamba manung’uniko yao yatarekebishwa. Hata hivyo, waliporudi kwenye miji yao ya nyumbani, magavana na watumishi wanaohusika waliwaua viongozi wao. Wale ambao 290

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 290

9/4/2017 3:47:59 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

walinusurika na adhabu walikwenda Madina tena na wakalalamika kwa wale masahaba mashuhuri wa Mtume. Masahaba hao walimwendea Uthman na wakaunga mkono ile njia ya walalamikaji. Uthman alitoa amri kumuuzulu yule mtawala dhalimu na kuteua mwingine mpya badala yake. Hata hivyo, kabla huyo mpya hajakwenda kwenye sehemu yake ya kazi, mjumbe alitumwa kwa yule mtawala aliyeuzuliwa, akiwa na barua yenye maelekezo kwamba yule mteuliwa mpya na vile vile wale watu waliomwendea khalifa kwa namna ya ujumbe wauawe mara tu watakapowasili. Hatimae yule mtawala wa zamani alibakia katika kituo chake na akatekeleza maagizo ya khalifa kwa uangalifu sana na akawa mkali zaidi katika udhalimu wake. Hizi ndio zilikuwa sera ambazo alizitwaa Uthman kwa ushauri wa watu wenye ushawishi, ili kujihakikishia ustawi wao na kulinda maslahi yao. Watu wa chini walipatwa na maonevu makubwa katika kipindi hicho. Wakati mwingine walibakia kimya na nyakati zingine walipinga na kushutumu utawala huo wazi wazi. Baadhi ya washairi wametoa taswira halisi kabisa ya mabepari wa wakati ule. Walikuwepo watu waungwana pia katika jamii hiyo; ambao walikuwa na akili zilizoongoka na ndimi zinazozungumza, na walipata heshima kubwa miongoni mwa Waislamu. Walikuwa pia wametishika sana kama watu wengine kutokana na hali zilizokuwepo. Hata hivyo, walipinga vikali sana utawala wa kitajiri wa Bani Umayyah na sera alizozitwaa Uthman na washirika wake. Upinzani wao ulikuwa, hata hivyo, umeegama kwenye kanuni na bila nia mbaya yoyote ile. Sababu zao zilikuwa za maana sana na zisizo na chuki binafsi. Baadae tutaona jinsi watu hawa wenye nia safi, waaminifu na wachamungu wakosoaji wema walivyotendewa ukatili. Mfululizo Wa Shutuma Kama tulivyoeleza hapo juu, Bani Umayyah na wafuasi wao, na matajiri, na wenye ushawishi wa wakati ule, walikuwa wanahusika na mapungufu katika sera za uongozi, siasa na uchumi za Uthman ambazo zilisababisha maovu makubwa, vurugu na ghasia. Uthman mwenyewe alikuwa anahusika na hali hii ya mambo kwa kiwango kikubwa kwa sababu aliwategemea Bani Umayyah na akawapendelea, akaagizia chochote walichokitaka na akakataza kile walichokuwa hawakitaki. Kwa kweli walikuwa ndio watawala halisi hasa na Uthman alikuwa ni mtumishi wao mtiifu. 291

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 291

9/4/2017 3:47:59 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Imam Ali alionyesha picha halisi kabisa ya khalifa kwa kusema: “Yeye ni kama mtu anayepaliwa na maji ya kunywa.” (kwa sababu dawa ya kupaliwa ni maji ya kunywa, lakini kama anapaliwa kutokana na kunywa maji hapawezi kuwa na dawa kwa ajili yake tena). Imam anaendelea kusema: “Mtu ambaye wapenzi wake na wasiri ni madhalimu, yeye ni sawa na mtu aliyepaliwa na maji.” Kama vile tu Uthman alivyokuwa ametoa uhuru kamili kwa Bani Umayyah kujipatia utajiri na mamlaka, na akawaruhusu watu wenye hadhi kujikusanyia na kuhodhi mali kwa kuwanyonya watu wa chini, alikuwa pia amewaruhusu washauri wake kuzima uhuru wa wale masahaba mashuhuri wa Mtume iwapo wangezua vipingamizi vyovyote vile, na akawataka wafanye uadilifu kwa umma. Ilitokea mara kwa mara kwamba kuweka vikwazo juu ya wale wakweli na waumini wapenda uadilifu hakukuonekana kutosha; bali Uthman aliwapa adhabu kali ama kwa uamuzi wake yeye mwenyewe, au kwa ushauri wa Marwan. Aliwachukulia waumini hao kuwa maadui zake kana kwamba walitaka kumnyang’anya uzuri wa Marwan na ndugu yake Harth. Uthman katika mambo yote imma madogo au makubwa, alifuata ushauri wa Bani Umayyah ambao walikuwa ndio washauri wake wakuu, na hatimae aliyapoteza maisha yake kwa sababu yao. Waliyachukua madaraka yote mikononi mwao wenyewe, imma kwa kupenda au kutopenda kwake Uthman na wakamfanya asijiweze. Kwa kweli wao walikitaka kifo chake, na wakaasi dhidi yake kwa siri, ili Bani Umayyah mwingine aweze kuwa khalifa. Wafuasi wao wote waliwasaidia katika suala hili na wakati Uthman alipozingirwa na maadui zake, wao Bani Umayyah wakakimbia, wakimuacha katika shida kama vile wafuasi wake wengine walivyoponyoka. Uthman aliwaweka mbali naye wale wamtakiao mema wote; ambao kwa msaada wao hali ingeboreka, na akawafanya Bani Umayyah kuwa ndio wasiri na washauri wake. Walimshauri kuwaepuka wale watu wote ambao walifikiriwa kuwa ni maadui zake ingawa kwa kweli hawakuwa maadui zake. Yule mtu mwenye fitna na tabia mbaya, Marwan, alikuwa ndiye mshauri wake mkuu, lakini hakumfikiria Ali kwamba anafaa kuaminiwa, ingawa endapo mawazo yake yangepewa uzito angeweza kumpa Uthman ushauri wa kuaminika na wa uangalifu, na angeweza kumzuia na upendeleo na kuonyesha fadhila maalum kwa marafiki zake. Angeiweka serikali kwenye njia imara na yenye faida, na kipaumbele kingetolewa kwenye ustawi wa watu wa chini, ambao walikuwa wamelindwa kutokana na uonevu na udhalilmu. 292

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 292

9/4/2017 3:47:59 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Marwan alikuwa na ushawishi kwa Uthman kiasi kwamba kamwe hajishughulishi tena, akaenda kwa Uthman na akamwambia kwamba Ali na masahaba wengine maarufu walikuwa wanapanga njama dhidi yake. Alikuwa wakati wote akimwambia kwamba: “Watu hawa wanauchochea umma dhidi yako. Njia pekee ya kudumisha sheria na amani na kuuokoa ukhalifa ni kwamba uwauwe Ali na masahaba maarufu wengine wote wa Mtume ili kwamba mambo ya Dola yaweze kupangwa kulingana na ushauri wa Bani Umayyah. Wao ndio ndugu zako na watakia heri wako halisi ambao watapenda utawala wako uendelee. Wakati uasi wa jumla ulipotokea dhidi ya Uthman katika miji yote, yeye aliitisha mkutano kufikiria njia na namna ya kurudisha sheria na amani. Ni Bani Umayyah tu na wafuasi wao ndio walioalikwa kuhudhuria mkutano huu. Ilikuwa ni Bani Umayyah hawa hawa ambao dhidi yao wale masahaba wa Mtume na umma kwa jumla walikuwa na malalamiko, na ilikuwa ni kwa sababu yao kwamba watu wakaasi. Hata hivyo, badala ya kuwaita masahaba wa Mtume na kufanya mashauriano nao ili kutengeneza hali vizuri; Uthman aliwaita wale ambao walikuwa ndio kiini cha matatizo yote, na ambao kwa sababu yao hao, watu wamekuwa maadui wa Uthman. Wale wote walioshiriki katika mkutano huo walitoa mawazo yao, na wakapendekeza njia na namna ya kuishughulikia hali hiyo. Inaweza kuonekana kwamba baadhi yao walitaka vurugu ziendelee kwa sababu manufaa yao yangetumikiwa vizuri kwa njia hii. Wengine walitaka tatizo lizidi kulipuka kwa sababu hizo hizo. Bado wengine walitaka kurekebishwa kwa hali hiyo alimuradi kwamba ushawishi na mamlaka yao havikudhurika. Wale wote waliohudhuria mkutano huo walikuwa na uadui na Ali. Walikuwa wanahofia kwamba uadilifu wake, ukweli na uchamungu vingeweza kuvuruga mchezo wao na kukomesha shughuli zao za kidhalimu, na sera yake ya usawa na haki inaweza kuifanya serikali yao ya kibepari ianguke chini. Wajumbe mashughuli, hai sana wa mkutano huo walikuwa Mu’awiyah, Marwan na Amr bin Aas. Inaweza kwa hiyo ikadhaniwa vema kwamba matokeo ya mashauriano hayo yangekuwa nini. Ali hakujali kama Uthman hakumtaka ushauri yeye katika mazingira yale magumu. Alikuwa na shauku kwamba hali ya Waislamu iweze kuboreshwa na uadilifu na usawa vipate kusimamishwa, ingawa Uthman na wafuasi wake wanaweza wakawa maadui zake. Aliendelea kumshauri Uthman mpaka wasaa wa mwisho kurekebisha 293

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 293

9/4/2017 3:47:59 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

malalamiko ya watu na kuwafidia kwa uonevu walioteseka nao ili ukhalifa usije ukahatarishwa. Wakati mmoja watu walipokuja kuwa na hasira na wakataka kumshambulia Uthman, yeye aliwatuliza na pia akamshauri Uthman kwa maneno haya:49 “Watu wananingojea huko nje na wamenituma kwako kuja kumaliza tofauti zilizopo kati yako na wao. Naapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba siwezi kuelewa nini cha kukuambia wewe wakati mimi sijui kitu chochote ambacho wewe hukijui, na sina kukufikishia habari zozote ambazo bado hazijakufikia. Ninajua kile unachokijua. Sikijui kitu chochote ambacho ninaweza 49

Ili kufanya ukali wa ushauri upendeze Imam Ali alizungumza mwanzoni katika namna ambayo kwamba badala ya kukasirika, Uthman aweze kuhisi kazi na majukumu yake. Ali alitaka kuvuta mazungatio yake kuelekea kwenye wajibu wake, na kwa lengo hilo mawazoni mwake alitaja usahaba wake (Uthman) wa Mtume na pia umuhimu wake na ukaribu kwa Mtume kwa sababu ya undugu. Vinginevyo huu kwa dhahiri kabisa haukuwa wasaa wa kumsifu yeye; na maneno haya yasije yakachukuliwa kuwa kama hotuba ya wasifu, na kupuuza ile sehemu ya mwisho ya kauli ya Ali. Yale maneno ya ufunguzi yanalenga kuonyesha kwamba chochote kile alichokifanya Uthman, alikifanya kwa makusudi, kwa kudhamiria. Haikuwa kwamba alifanya makosa yasiyokusudiwa, ambayo yanaweza kutotiliwa maanani. Kama ni maadili kwamba hata baada ya kubakia katika usahaba wa Mtume na akazijua sheria na kanuni zote za Uislam mtu anaweza kufanya mambo katika namna ambayo dunia yote ya Kiislamu ianze kupiga kelele na kulia kwa sababu ya uonevu wake, basi maneno haya yanaweza kuchukuliwa kuwa kama sifa. Kama sio tabia njema, basi kule kutajwa kwake hakuwezi kuitwa ni sifa. Kwa kweli maneno ambayo yametumika kama sifa ni uthibitisho wa uzito wa maovu yake. Ovu lililotendwa kwa makusudi ni zito zaidi kuliko lile lililotendwa kwa kughafilika. Inasemekana kwamba Uthman anayo haki ya hadhi kubwa kwa nafasi yake ya kuwa mkwe wa Mtume kwa vile Mtume alimuozesha mabinti zake wawili waitwao Ruqqayah na Umm Kulthum, mmoja baada ya mwingine. Kabla ya kuichukulia miungano hii ya kindoa kama chanzo cha heshima, hata hivyo, asili ya ukwe huu lazima kwanza iangaliwe. Historia inatuambia kwamba Uthman hakupata kutangulia katika jambo hili. Ruqqayah na Umm Kulthum mwanzoni waliolewa na Utba na Atiiba, watoto wa kiume wa Abu Lahab. Licha ya hilo, hawa watu wawili hawakuchukuliwa kuwa na haki ya hadhi yoyote au heshima hata kabla ya kuchomoza kwa Uislamu. Katika mazingira hayo, ni vipi uhusiano huu uchukuliwe kama chanzo cha hadhi kwa Uthman bila ya kutilia maanani sifa zake binafsi? aidi ya hayo, sio ukweli uliothibitika kwamba mabibi hawa wawili walikuwa mabinti halisi wa Mtume. Wapo Z baadi ya ambao hawawakubali kuwa mabinti halisi wa Mtume bali wanasema kwamba walikuwa ni mabinti wa dada yake Khadijah iliyeitwa Hala au mabinti zake kutokana na mume wake wa awali. Alkuti (Aliyefariki 352 A.H.) anasema: “Muda mfupi baada ya Bibi Khadijah kuolewa na Mtume, dada yake Hala alifariki na akaacha nyuma yake mabinti wawili waliokuwa wakiitwa Ruqqayah na Umm Kulthum. Walilelewa na Khadijah na Mtume. I likuwa ni desturi kabla ya Uislamu kwamba iwapo yatima atalelewa na mtu basi aliitwa ni binti au kijana wa huyo mlezi.” (Kitab al-Istighatha, uk. 69). “Kabla ya kuolewa na Mtume Bibi Khadijah alikuwa ameolewa na Abi Hala bin Malik na akapata mtoto mmoja wa kiume aliyeitwa Hind na binti aliyeitwa Zainab kutoka kwa mume huyo. Mapema zaidi kabla ya hapo aliolewa na Atiq bin Aa’iz na alikuwa amepata kijana mmoja na binti mmoja kutoka kwake.” (Siirah ibn Hisham, Juz. 4, uk. 293). ii inaonyesha kwamba Khadijah alikuwa na mabinti wawili kabla hajaolewa na Mtume. Kama ilivyotajwa H hapo juu, kwa mujibu wa desturi zilizokuwepo wakati huo, walikuwa waitwe ni mabinti wa Mtume, na mume wao aitwe mkwewe. Hata hivyo, nafasi yake kama mkwe wake itakuwa ni kipimo kilicho sawa na mabinti hao. Hivyo, kabla ya kuzichukulia ndoa hizi kuwa chanzo cha hadhi, ile hali na nafasi halisi ya hao mabinti (uhalisia wa kuzaliwa kwao) lazima utiliwe maanani. 294

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 294

9/4/2017 3:47:59 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

kukwambia wala sijasikia lolote kwa siri ambacho ninaweza kukujulisha. Uliona kama nilivyoona na ulisikia kama nilivyosikia. Ulikuwa pamoja na Mtume kama tulivyokuwa sisi. Wajibu wa kutenda inavyotakiwa haukutua zaidi kwa watoto wa Abi Quhafa na Khattab kuliko unavyotua mikononi mwako. Kwa kweli wewe uko karibu zaidi na Mtume kwa sababu ya undugu kuliko walivyokuwa wao, na kwa namna fulani wewe ni mkwe wake Mtume, ambapo wao hawakuwa. Ni lazima umuogope Mwenyezi Mungu. Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba sikupi wewe ushauri huu kwa sababu ati huwezi kuona kitu chochote na sikuambii yote haya kwa sababu eti huyajui. Na hakuna suala la kutokujua kwako kwa sababu njia ya sheria za kidini iko dhahiri na wazi. Lichukulie moyoni mwako kwamba kati ya waja Wake Mwenyezi Mungu anampenda sana mtawala mwadilifu, ambaye ni mtu aliyeongoka yeye mwenyewe na anawaongoa wengine pia, anayeimarisha desturi zinazoeleweka na kuteketeza uzushi usiojulikana. Na mtu wa kudharaulika kabisa mbele ya Mwenyezi Mungu ni yule mtawala dhalimu ambaye anabakia mpotovu, na wengine pia wanapotoka kwa sababu yake. Mimi nimemsikia Mtume akisema kwamba katika Siku ya Kiyama muonevu ataletwa katika hali ambayo hakutakuwepo na mtu wa kumsaidia au kumuombea shifaa na yeye atatupwa katika moto wa Jahannam papo hapo.” (Nahjul-Balaghah) Uthman hakushangaa pale alipoyasikia yale maneno ya busara ya Ali. Yeye alisema tu: “Mimi sijafanya makosa yoyote. Nimekuwa mpole tu na mkarimu kwa ndugu na jamaa zangu.” Haki ilichanganywa na batili na wema ukachanganywa na uovu. Matendo maovu ya Bani Umayyah yaliendelea kuongezeka. Uthman aliwapa uhuru wa kufanya mambo na yeye mwenyewe akawa hana msaada mbele yao. Ali amevuta taswira fupi na sahihi kabisa juu ya ukhalifa wa Uthman katika maneno haya: “Aliwasaidia ndugu zake kwa namna ya kipumbavu kabisa.” Kuhusu ndugu zake wa Bani Umayyah yeye anasema: “Pamoja naye wakasimama Bani Umayyah, kizazi cha baba yake, na wakaanza kutafuna mali ya Mwenyezi Mungu kama vile ngamia anavyokula majani ya msimu wa kuchipua.” Kwa hiyo Bani Umayyah na wafuasi wao wakampeleka Uthman katika njia ambayo ilikuwa ni njia ya maangamizo na uharibifu. Ilikuwa ni kwa sababu ya upendeleo wake kwa ndugu ambapo alipoteza maisha yake. Mke wake Na’ila pia alijua ni kwenye mwelekeo gani Bani Umayyah walikuwa wakimpeleka. Yeye alifahamu pia kwamba Ali alikuwa ndiye mtu mwaminifu na mkweli na mtakia mema halisi 295

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 295

9/4/2017 3:47:59 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

wa Uthman. Yeye kwa hiyo, alisisitiza kwa kukazia kabisa kwamba yeye Uthman amtake ushauri Ali. Hata hivyo, wale washauri waovu na fitna ambao wakati wote walikuwa wakivinjari karibu na Uthman waliyapinga mapendekezo ya Na’ila na wakasema kwamba yeye alikuwa ni mwanamke asiye na busara na asiyategee masikio yale mambo aliyoyapendekeza. Wakati mmoja Marwan alimwambia Uthman: “Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba ni bora kubaki kwenye dhambi zako na kuomba msamaha kwa Mwenyezi Mungu kuliko eti utubie kwa hofu.” Ina maana kwamba Marwan alikiri kwamba sera ya Uthman ilikuwa mbaya na taratibu zake zilikuwa ni taratibu za wafanya makosa, lakini kwa mujibu wake yeye Marwan, ilikuwa ni bora kung’ang’ania kwenye makosa yake mtu na utenda maovu wake, kuliko kuona haya na kuyatubia maovu hayo. Hakuna ushauri ulioweza kuingia kwenye masikio ya Uthman isipokuwa ule ambao ulitamkwa na Marwan. Uthman alikubali mara moja kile alichokisema Marwan lakini hakusikiliza yaliyosemwa na watu wengine. Marwan alizungumza na watu katika jina la khalifa na kile alichokisema kilikuwa hakina chochote isipokuwa makaripio, vitisho na ukaidi, na yalikuwa yanatosha kuzusha ghasia dhidi ya Uthman. Wakati mmoja alisema, akiwahutubia wale waasi waliokuwa wameizingira nyumba ya Uthman: “Ni nini kimewatokeeni enyi watu? Kwa nini mmekusanyika hapa? Mnataka kutunyang’anya serikali?” Maneno haya ya Marwan yanatosha kuonyesha namna ya kufikiri kwa Bani Umayyah, kwa mujibu wao wale watu wote walioonewa ambao walikuwa wamekuja kufanya malalamiko yao yarekebishwe wamekuja tu kufanya uporaji na unyang’anyi. Madai kwa ajili ya kurudisha haki zilizoporwa, na kurudisha serikali adilifu, na kuzuia uonevu na kuchukua hatua dhidi ya wale waliokiuka haki za watu, na mambo mengine kama hayo ambayo kuhusiana nayo hayo ndio watu wamekuja kutoa malalamiko yao, yalikuwa ni mambo ambayo, kulingana na maoni ya Marwan hayakustahili kuangaliwa na kuzingatiwa. Kwa mujibu wake yeye ukhalifa, madaraka na utawala vilikuwa ni njia ya kuonyeshea nguvu na mamlaka na havikuhusiana chochote na ulinzi wa haki za watu au uhifadhi wa imani na sheria za kidini. Kwa maoni yake yeye huo ulikuwa ni ufalme wa Bani Umayyah ambao walikuwa wakingojea kwa muda mrefu sana kuukamata, na hivyo kusimamisha upya nguvu na mamlaka yao ambayo yalikuwa yamevurugwa 296

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 296

9/4/2017 3:47:59 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

na Uislamu. Na mambo yakiwa ni hivyo, basi hakuweza kuelewa ni kwa nini watu waweze kujaribu kuwanyang’anya Bani Umayyah serikali yao ya kurithi. Wale watu wote ambao hawakuzipenda zile sera za kiuchumi na kiuongozi za Bani Umayyah; na wakawakosoa kwa moyo safi kabisa, wakawa ni walengwa wa ghadhabu za Uthman kwa mapendekezo ya Marwan na washirika na washauri wake wengine. Mmoja wa wale watu waliopinga sera na taratibu hizi alikuwa ni Abdullah bin Mas’ud, sahaba maarufu wa Mtume. Ili kuelezea ni kiasi gani watu walihuzunishwa kutokana na udhalimu ambao sahaba huyu maarufu wa Mtume alifanyiwa, inaonekana ni muhimu kutoa maelezo mafupi ya historia ya maisha yake. Abdullah bin Mas’ud alikuwa ni mmoja wa wale watu ambao waliukubali Uislamu mapema mwanzoni kabisa kabla ya wote. Inasemekana yeye ni mtu wa sita katika orodha. Yeye alipata heshima ya kuhama mara mbili, kwanza kabisa kwenda Ethiopia na halafu Madina. Wakati wote alikuwa pamoja na Mtume. Alikuwa mmoja wa wale watu ambao Mtume aliwapenda na kuwaheshimu sana kwa sababu ya ukweli, uaminifu na uchamungu wao. Waislamu wa zama za mwanzoni walimchukulia Ibn Mas’ud kuwa mmoja wa wanachuoni wakubwa sana. Ilikuwa ni kwa sababu ya elimu yake ya kina ambapo Umar alimpeleka Kufa kwenda kuwaongoza na kuwaelimisha watu wa mji huo, ingawa yeye mwenyewe aliuhitaji ushauri wake hapo Madina. Wakati akimtuma yeye huko Kufa, Umar alituma barua kwa wakazi wa Kufa. Yeye aliandika hivi: “Ninamtuma Abdullah bin Mas’ud kuja kuwaelimisheni ninyi. Kwa kumtuma yeye huko Kufa mimi nimewapeni upendeleo kuliko juu yangu mwenyewe. Hamna budi ninyi kuchukua elimu kutoka kwake.” Watu wengi wa Kufa walinufaika kutokana na Abdullah bin Mas’ud. Idadi ya wanafunzi wake iliongezeka siku hadi siku na wakawa wanachuoni maarufu. Yule Tabi’i (mfuasi wa masahaba wa Mtume) maarufu, Sa’id bin Jaybar alikuwa kila mara akisema: “Wanafunzi wa Abdullah bin Mas’ud walikuwa ndio taa za mji huu (yaani Kufa).” Waislamu wote wamemkubali Abdullah bin Mas’ud kuwa mwanachuoni mwenye elimu kubwa. Kiasi kwamba katika wakati wa kipindi cha Umar, alikuwa ni yeye ambaye watu wa Kufa walimrejelea katika kufutu mas’ala yao ya kidini na ni hukumu zake tu zilizokubaliwa na wao.

297

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 297

9/4/2017 3:47:59 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Katika suala la ufafanuzi na tafsiri pia alikuwa mmojawapo wa mabingwa wa juu kabisa, na hadhi yake takriban ilikuwa karibu sawa na ile ya Abdullah ibn Abbas. Alikuwa na wanafunzi wengi ambao walijipatia sifa kubwa katika tawi hili la elimu, kama vile Qatada na Masruuq ibn Ajda‘. Kwa kifupi Abdullah ibn Mas’ud alikuwa ndiye mtu wa wakati wake aliyeheshimika sana. Yeye alitukuzwa katika miji yote ya Kiislamu zaidi sana kuliko masahaba wengine wa Mtume. Uthman alishughulika vipi na sahaba huyu mashuhuri? Abdullah ibn Mas’ud alikuwa mmoja wa wale masahaba maarufu ambao kwa uwazi kabisa walionyesha kutoridhia na bila woga wakazishutumu sera na taratibu za utendaji za Bani Umayyah. Katika kila siku ya Ijumaa hapo Kufa alikuwa akisema: “Maneno sahihi kabisa ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu, na muongozo bora ni ule uliotolewa na Mtukufu Mtume Muhammad, na mambo mabaya kabisa ni uzushi ‘Bidaa’. Kila uzushi ni upotovu na kila uotovu unamuongozea mtu kwenye moto wa Jahannam.” Maneno hayo hapo juu ya ibn Mas’ud yalikuwa na shutuma za wazi juu ya Uthman na hatua alizokuwa amezichukua kwa faida ya Bani Umayyah pekee na watu matajiri, na wenye uwezo kupuuza ustawi wa watu wa chini. Yeye alisema maneno mengi ya kumshutumu Uthman, kwa mfano alisema: “Machoni kwa Mwenyezi Mungu Uthman hana thamani hata kiasi cha ile ya unyoya wa inzi.” Walid bin Uqba, gavana wa Kufa, aliyachukia sana maneno ya Ibn Mas’ud kuhusu Uthman. Walid huyu alikiwa ni ndugu ya Uthman kutokana na upande wa mama yake, na alikuwa ni mlevi wa kutupwa na mtu fisadi kabisa. Uthman alikuwa amemteua kama gavana wa Kufa licha ya kukereka kwa watu wa mji ule. Walid aliandika barua kwa Uthman kumjulisha kwamba ibn Mas’ud alikuwa akimshutumu na kumtukana yeye (Uthman). Uthman alimuomba amrudisha Abdullah kwake yeye. Imesimuliwa kwamba wakati Abdullah alipoondoka Kufa kuelekea Madina watu wengi sana walikuja kuagana naye. Kila mmoja wao alimuomba yeye asiondoke Kufa na wakamhakikishia kwamba hawataweza kumuacha apatwe na madhara yoyote yale. Yeye, hata hivyo, akajibu: “Kuna jambo ambalo ni lazima litokee hivi karibuni haraka sana.”

298

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 298

9/4/2017 3:47:59 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Abdullah ibn Mas’ud aliwasili Madina siku ya Ijumaa usiku. Pale Uthman alipotambua kuhusu kuwasili kwake, aliwafanya watu wakusanyike ndani ya Msikiti na akawaambia: “Hebu angalieni mnyama duni anakujieni mbele yenu, ambaye anakanyaga juu ya chakula chake, anatapika na kunya.” Abdullah ibn Mas’ud akasema: “Mimi siko kama hivyo. Kwa kweli, mimi ni sahaba wa Mtume. Nilikuwa naye katika vita vya Badr na pia nilishiriki katika Bai’at al-Ridhwan (kile kiapo cha utii ambacho kilichukuliwa chini ya mti kule Hudaybiyyah). Aisha akasema kwa sauti kubwa kutoka nyumbani kwake: “Uthman! Unayasema maneno hayo kumhusu sahaba wa Mtume!” Wengine pia hawakuyapenda maneno hayo na wakaonyesha kuchukizwa kwao. Kama ilivyoagizwa na Uthman, maafisa na watumwa wake walimtoa Ibn Mas’ud nje ya msikiti huo katika namna ya kikatili sana. Walimburuza mpaka kwenye lango la msikiti na hapo wakamtupa chini ardhini. Halafu wakampiga bila ya huruma kabisa kiasi kwamba wakamvunja mifupa yake na kutoka hapo akabebwa kupelekwa nyumbani kwake kama mwili wa mtu aliyekufa. Uthman hakutosheka na kule kupigwa na kutukanwa ambako alifanyiwa sahaba huyu mashuhuri wa Mtume. Alizuilia na ujira aliokuwa akiupata siku zote kutoka kwenye Hazina ya Umma na kumzuia vyanzo vyake vyote vya kujipatia maisha. Pia aliwaamuru watu wasiende kumtembelea na kumjulia hali juu ya afya yake. Hatimae Ibn Mas’ud akafariki dunia na Ammar Yasir akamswalia swala ya maiti na akamzika kwa siri. Wakati Uthman alipojulishwa kuhusu hili, yeye alikasirika sana. Mtu mwingine mstahiki aliyekuja kuwa shabaha ya ghadhabu ya Uthman alikuwa ni Ammar Yasir. Yeye alikuwa ni mmoja wa wale watu mashuhuri wa Uislam ambao wanajulikana sana kwa mema yao, maadili yao ya hali ya juu na uchamungu. Heshima na thamani yake ilijulikana vema kwa Mtume na yeye alijua ni tabia njema kubwa kiasi gani alizokuwa nazo. Hii ndio sababu ya kwa nini Mtume alimtukuza kwa utukufu unaong’ara ambao aliustahiki vya kutosha. Kwa mfano, alisema kumhusu yeye: “Wakati migawanyiko itakapotokea baina ya watu, mwana wa Sumayyah (yaani, Ammar) atakuwa kwenye upande wa haki.” Tofauti nyingi zilizuka miongoni mwa Waislamu wakati wa siku za mwanzoni za Uislamu na Ammar wakati wote alirudi upande mmoja na Ali. Ilikuwa ni kutokana na sifa na maadili haya kwamba Waislamu walimpenda yeye na Bani Umayyah na wafuasi wao walikuwa ni maadui zake wa jadi. 299

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 299

9/4/2017 3:47:59 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Kitendo cha kwanza cha Uthman ambacho Ammar hakupendezewa nacho kilikuwa kwamba yeye aliufanya utajiri ni chombo cha kuchezea mikononi mwa watu wenye uwezo. Kama ilivyoelezewa na Ammar mwenyewe, alikuwa akikutana na Uthman mara kwa mara na akamshauri kusimamia uadilifu, kuepukana na upendeleo wa kikabila na kujizuia na kuwafanya Bani Umayyah kuwa makabaila juu ya watu. Matokeo yake Uthman akamkasirikia na aliwakasirikia wale watu wengine wote waadilifu. Imesimuliwa kwamba kulikuwa na kikasha ndani ya Hazina ya Umma ambacho kilikuwa na mapambo na vito vya thamani. Uthman aliviondoa vito hivi kutoka kwenye hazina na akavitoa kwa mmoja wa wake zake kuvivaa. Watu walilipinga hili na wakamshutumu vibaya sana, kushutumiwa ambako kulimfanya aghadhibike. Akiongea katika mkusanyiko wa hadhara yeye alisema: “Nitachukua chochote nikitakacho kutoka kwenye ngawira za vita, na sitajali kama mtu atalichukia hilo.” Kuhusu hilo Ali akasema: “Kwa tukio lile wewe utazuiwa kufanya hivyo na ukuta utanyanyuliwa kati yako na hazina ya umma.” Ammar akasema: “Namuomba Mwenyezi Mungu ashuhudie kwamba mimi ni mtu wa kwanza kuchukia haya matumizi mabaya.” Kwa sababu ya hayo Uthman akasema: “Ewe Ammar! Vipi unathubutu kuzungumza dhidi yangu? Mkamateni.” Mara ghafla akasimama Marwan na akasema kumwambia Uthman: “Ewe AmirulMu’minin! Mtumwa huyu (Ammar) amewachochea watu dhidi yako. Endapo utamuua huyu na wengine watajifunza kutokana na yeye.” Uthman akawa tayari mara hiyo hiyo kutenda kwa ushauri wa Marwan. Alinyanyua fimbo yake na akampiga nayo Ammar bila huruma. Watumwa wake na watu wengine wa Bani Umayyah pia wakamsaidia. Uthman pia alimpiga mateke kwa namna ya kumfedhehesha kabisa na alimpiga mateke mengi tumboni mwake chini ya kitovu kiasi kwamba akamsababishia kupatwa na henia. Baada ya hapo akatupwa barabarani wakati ikiwa mvua inanyesha na ngurumo za radi, na akawa karibu kama amekufa. Sahaba mwingine maarufu wa Mtume ambaye alipatishwa mateso ya kutisha na Uthman na watu wengine wa ukoo wa Umayyah alikuwa ni yule mwana mageuzi mkubwa Abu Dhar Ghiffari. Alikuwa ni Abu Dhar huyo huyo ambaye ni mashuhuri sana kwa sababu ya ubinadamu wake na mapenzi juu ya uadilifu. Alikuwa msaidizi na mfuasi mtiifu wa Ali.

300

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 300

9/4/2017 3:47:59 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Ili kuelezea ile nafasi halisi ya wapinzani wa sera za Uthman na mwenendo wa Bani Umayyah; tunatoa maelezo mafupi hapa chini ya historia ya maisha ya Abu Dhar, ambaye alikuwa mmoja wa watu mashuhuri wa wakati wake. Wakati wa zama za jahilia Abu Dhar alikuwa ni mtu fukara, lakini licha ya hayo yeye alikuwa mkuu wa kabila lake. Pale aliposikia habari kuhusu Mtume, yeye alikuja Makkah katika hali ambamo alikuwa amevaa joho chakavu lililotatukiana. Katika kuwasili Makkah, alianza kuzurura huku na huko mitaani. Mwishowe alipochoka alilala chini karibu na Ka’abah, akiliweka joho lake chini ya kichwa chake. Wakati huohuo Ali akabahatika kupita karibu yake na akamuonea huruma sana, kwa sababu ilionekana kwamba alikuwa ni mgeni aliyekumbwa na umasikini, ambaye alikuwa hafahamiani na mtu yoyote ndani ya mji huo. Walitambulishana wenyewe, na Ali akamchukua Abu Dhar kwenda naye nyumbani kwake. Baadae alimpeleka kwa Mtume. Katika kukutana na Mtume, Abu Dhar mara tu akaukumbatia Uislamu. Yeye alikuwa ni mtu wa tano kuikubali dini hii. Abu Dhar alikuwa mwaminifu sana na jasiri kiasi kwamba baada ya kuukumbatia Uislamu alisimama karibu na Ka’abah ambapo idadi kubwa ya Maquraishi – maadui wa jadi wa Uislam – walikuwa wamekusanyika. Hapo akayadhihaki masanamu na akawaalika wale waliokuwepo pale kwenye Uislamu. Hadi kufikia wakati huo hapo, kulikuwa hakuna aliyewahi kuweza kuonyesha ushujaa kama huo. Maquraishi wakamvamia na wakampiga sana kiasi kwamba karibu afariki. Abu Dhar alikuwa ndiye sahaba kipenzi sana na mpendwa wa Mtume kwa sababu ya umaizi, busara, hekima, ghera ya mageuzi yake, na mapenzi juu ya masikini. Watu vile vile walimtegemea na walimheshimu sana. Masahaba wote walimchukulia katika heshima kubwa. Ali alisema kuhusu yeye: “Abu Dhar anayo elimu kubwa kiasi kwamba hakuna aliyeweza kulingana naye.” Wakati Uthman alipoupata ukhalifa, mshangao wa Abu Dhar ulikuwa hauna kifani wala mpaka. Hakuweza kuelewa ni kwa nini Uthman amefanywa kuwa khalifa mbele ya watu wenye elimu na uchamungu kama Ali. Hata hivyo, hakunyanyua mdomo wake dhidi ya kuteuliwa kwake kwa sababu Ali hakutaka machafuko yoyote yaweze kutokea kwa ajili yake. Mara tu, baadae, hata hivyo, Abu Dhar aliona kwamba, ambapo watu wa chini wanaendesha maisha ya taabu sana, Bani Umayyah walikuwa wakilimbikiza utajiri na kuishi katika anasa. 301

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 301

9/4/2017 3:47:59 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Alihisi kwamba Uthman anamwaga utajiri juu ya ndugu zake kwa kuwanyima watu wa kawaida haki zao, na hili lilimchafua sana akili yake. Aliishutuma wazi wazi sera hii ambayo ilikuwa imewagawanya watu katika makundi mawili – matajiri na mafukara. Abu Dhar mara kwa mara aliwahutubia watu kwa maneno haya: “Mambo kama haya yanatokea kama yasivyowahi kuonekana au kusikika hapo kabla. Naapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba vitendo kama hivi havikubaliwi kamwe, imma na Qur’ani – Kitabu cha Mwenyezi Mungu, wala kuungwa mkono na Sunnah ya Mtume. Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kwamba ninaona haki ikikandamizwa na batili inatiwa moyo. Mambo ambayo ni ya haki na kweli yanakanushwa, na watu wasio wachamungu wanapendelewa. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: “Waambie wale wanaolimbikiza dhahabu na fedha na ambao hawatumii utajiri wao katika njia ya Mwenyezi Mungu kwamba mapaji ya nyuso zao, mbavu na migongo yao itapigwa chapa kwa moto.” Akaongeza kusema: “Mmejitwalia mapazia ya hariri na viti na mmekuwa na mazoea ya kulala katika hariri ya azrabi ambapo Mtume alikuwa akilala juu ya mkeka. Mnakula chakula cha aina mbalimbali ambapo Mtume hakula japo mkate wa shayiri akashiba.” Abu Dhar alilitaka kundi lililokuwa madarakani kufanya uadilifu kwa watu masikini ambao walikuwa wamenyimwa haki zao. Aliwahimiza watu kupata haki zao kwa juhudi ya kutumia nguvu, na kukomesha umasikini ambao ni chanzo cha fedheha na ni adui wa wema. Yeye alizoea kutamka maneno yafuatayo mara kwa mara: “Ninashangaa kwa nini mtu ambaye hana chochote cha kula ndani ya nyumba yake hachomoi upanga na kuwashambulia watu.” “Wakati umasikini unapoelekea kwenye mji udanganyifu huuomba ufuatane nao.” Alikirihishwa sana vile vile na ubinafsi na ulanguzi wa Bani Umayyah kiasi kwamba aliondoka Hijazi na akaenda zake Syria, kusudi kwamba asiweze kuona ubadhilifu wa Uthman na Marwan kwa macho yake mwenyewe. Hata hivyo, katika kuwasili huko aligundua kwamba shughuli za Mu’awiyah zilikuwa za kupingika zaidi kuliko zile za Uthman na Marwan. (Ukweli ni kwamba Abu Dhar hakwenda Syria kwa hiari yake mwenyewe.

302

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 302

9/4/2017 3:47:59 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Alihamishwa huko na Uthman). Hapo alisema kwamba ubadhilifu wa Mu’awiyah ulikuwa umezidi sana ule wa Uthman na Marwan. Aliona kwamba Mu’awiyah amekuwa ndio mmiliki wa Hazina ya Umma na vile vile wa maisha na mali za watu. Aliona kwamba alifuja mali ya Hazina ya Umma, alinyakua mapato ya Waislamu na alimuua yeyote aliyemtaka kumuua. Yote haya yalimfanya akasirike sana. Wakati Mu’awiyah alipolijenga lile Kasiri la Kijani, Abu Dhar alimtumia ujumbe akisema: “Kama umelijenga kasiri hili kwa kutumia mali ya Mwenyezi Mungu basi umekuwa na hatia ya udanganyifu, na kama umetumia pesa kutoka kwenye mfuko wako mwenyewe basi umekuwa mbadhilifu vibaya sana.” Bani Umayyah hawakuweza kumvumilia mtu mkweli kama huyo, mpenda uhuru na asiyeogopa kusema kweli, wala hawakuweza kumruhusu kuchanganyika na watu. Marwan alimchochea Uthman kila mara baada ya muda kumuua yeye Abu Dhar. Uthman akamuomba Mu’awiyah kuchukua hatua za ugandamizaji dhidi ya Abu Dhar. Mu’awiyah alimtoa Abu Dhar nje ya baraza lake na akaamuru kwamba mtu yeyote asishirikiane naye. Ilikuwa ni kwa amri ya Uthman ambapo Mu’awiyah alimwambia huyu sahaba maarufu wa Mtume: “Ewe adui wa Mwenyezi Mungu! Wewe unawachochea watu kuwa dhidi yangu na kufanya unavyotaka. Kama ningeua sahaba yeyote wa Mtume bila ya kupata ruksa kwanza ya khalifa anayetawala, mtu huyo angekuwa ni wewe.” Abu Dhar akajibu: “Mimi sio adui wa Mwenyezi Mungu au wa Mtume Wake. Bali ni wewe na baba yako ambao mmekuwa maadui wa Mwenyezi Mungu. Nyote mliukumbatia Uislamu kwa nje tu na ukafiri bado umejificha ndani ya nyoyo zenu.” Abu Dhar hakuweka umuhimu wowote kwenye vitisho vya Mu’awiyah, na akaendelea kuirekebisha jamii ya Syria kwa raghba na shauku kubwa sana kiasi kwamba Mu’awiyah akawa anachanganyikiwa. Watu matajiri wa Syria walihofia sana shughuli zake za kimageuzi kama walivyokuwa watu wa Madina. Walihofia kwamba watu wa kawaida wangeweza kuwashambulia. Wao, kwa hiyo, waliliona ni jambo la muhimu kwamba Abu Dhar atolewe nje ya Syria mapema sana iwezekanavyo, na pia azuiwe kutoa hotuba ili asiweze kufichua matendo yao maovu. Wakati huohuo mtu mmoja aliyeitwa Jundab bin Fihri akaja kwa Mu’awiyah na kusema kama mshauri mwaminifu na kwa sauti nyonge: “Abu Dhar atasababisha matatizo juu yako ndani ya Syria. Kama unaitaka Syria basi unapaswa kuishughulikia mara moja.”

303

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 303

9/4/2017 3:47:59 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Mu’awiyah akafikiria juu ya kumuua Abu Dhar lakini akaogopa kwamba watu wanaweza wakaasi. Kama ilivyosemwa na Hasan Basri: “Mu’awiyah hakujizuia kumuua sahaba maarufu kama Abu Dhar kwa sababu alihofia kukasirika kwa Uthman. Yeye hakumuua Abu Dhar kwa sababu alikuwa anaogopa kukasirika kwa umma. Yeye kwa hiyo, alimwandikia Uthman na kumtaka ushauri wake. Uthman akajibu: “Mlete Abu Dhar kwangu akiwa amepanda juu ya mnyama mkali pamoja na mtu ambaye atampa matatizo mengi kiasi iwezekanavyo humo njiani.” Mu’awiyah alifanya kama alivyoshauriwa na Uthman. Alimfanya Abu Dhar apande ngamia mwenye matandiko ambamo hamkuwa na kinga. Kwa muda aliowasili Madina, vipande vya nyama vilikuwa vimekatika kutoka kwenye mapaja yake; na kutokana na urefu wa safari hiyo, alikuwa amevunjika mgongo. Kutoka Damascus hadi Madina alikuwa amefuatana na maaskari wakali na makatili ambao hawakujali imma ile hali ya hewa ya joto au uchovu wake. Alikuwa amechoka sana na alikuwa amedhoofu na mnyonge wakati alipofika mbele ya Uthman. Mara tu alipomuona Abu Dhar, Uthman akalalamika dhidi ya mishughuliko yake. Abu Dhar akajibu: “Nilikutakia heri lakini umenidanganya. Nilimtakia heri rafiki yako vivyo hivyo, lakini naye pia akanidanganya.” Uthman akasema: “Wewe ni muongo. Unataka kusababisha matatizo. Umeigeuza nchi yote ya Syria dhidi yetu sisi.” Abu Dhar akasema kwa kujiamini kabisa na kwa utulivu: “Unapaswa kufuata nyayo za Abu Bakr na Umar. Endapo utafanya hivyo hakuna atakayesema lolote dhidi yako.” Uthman akasema: “Naakufie mama yako! Unahusika nini katika jambo hili?” Abu Dhar akajibu: “Kwa kiasi nihusikavyo mimi, nilikuwa sina njia nyingine isipokuwa kuwaamuru watu kutenda mema na kuepukana na maovu.” Mabishano kati ya Abu Dhar na Uthman yalizidi kuwa makali zaidi. Abu Dhar alimshutumu Uthman kwamba kuwa mtumwa wa matakwa yake ni kukosa kumtii Mwenyezi Mungu, na mkatili kwa viumbe Vyake. Uthman akawa amekasirika sana na akapiga ukelele: “Enyi watu! Hebu niambieni jinsi ya kushughulika na huyu mzee muongo. Je, nimvumilie au nimuue au nimpeleke uhamishoni kutoka kwenye nchi za Kiislamu? Amesababisha mgawanyiko miongoni mwa Waislamu.”

304

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 304

9/4/2017 3:47:59 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Wakati huo Ali pia alikuwepo. Alihuzunika sana kuona vitendo vilivyofanywa na Uthman kwa mwanamageuzi mkubwa na sahaba maarufu kama Abu Dhar. Alimgeukia Uthman na akasema: “Nimemsikia Mtukufu Mtume akisema kwamba baina ya ardhi na mbingu hakuna aliye mkweli zaidi kuliko Abu Dhar.” Uthman aliendelea kumchachafya Abu Dhar. Aliwaamuru watu wasishirikiane naye. Halafu akafikiria kusuluhishwa na Abu Dhar. Yeye kwa hiyo, akampelekea sarafu za dhahabu mia mbili ili kukidhi haja zake. Abu Dhar akamuuliza yule mtu ambaye alikuwa ameleta pesa hizo kwake: “Je, Uthman ametoa kiasi kama hiki kwa kila Muislamu?” Yule mtu akajibu kwa kinyume chake. Abu Dhar akazirudiaha pesa hizo kwa Uthman na akasema: “Mimi ni mmoja katika jamii ya Waislamu na kwa hiyo ninapaswa kupata tu kiasi kama kile cha wengine wanachopata.” Wakati anazikataa na kuzirudisha sarafu hizo za dhahabu, nyumbani mwake mlikuwa hamna kitu chochote cha kula isipokuwa kipande kilichochacha cha mkate wa shayiri! Kwanza kabisa Uthman alimkabidhi Abu Dhar kwa wanyongaji. Baada ya kufikiria upya, hata hivyo, aliamua kumhamishia Rabazah. Lilikuwa ni eneo kame ambako sio mtu wala mnyama wala mimea iliyoweza kuwa hai hapo. Wakati wa kuondoka kwa Abu Dhar ulipokaribia, Uthman aliwakataza watu, ili kuweza kumhuzunisha, kumfedhehesha na kumdhalilisha yeye, wasiende kumsindikiza. Hakuna aliyepata ujasiri wa kumsindikiza kwa hiyo, isipokuwa watu watano tu. Watu watano hawa walikuwa ni Ali, ndugu yake Aqil, Hasan, Husein na Ammar Yasir tu. Jukumu la kusimamia uondokaji wa Abu Dhar lilikuwa mikononi mwa Marwan ambaye alikuwa ndio chanzo cha maovu yote. Alikuwa ni yeye ambaye alilazimisha amri ya Uthman kwamba mtu yoyote asije akazungumza na Abu Dhar na watu wa familia yake au kuwashuhudia wakati wakiondoka. Alikuwa shupavu kiasi cha kumzuia Ali na masahaba zake kumsikindikiza Abu Dhar. Ali alimshutumu, akamgonga na fimbo yake na akakemea: “Ondoka hapa! Mwenyezi Mungu naakutupe wewe kwenye Moto wa Jahannam.” Kisha akamuaga Abu Dhar kwa maneno haya: “Oh, Abu Dhar! Umewakasirikia watu hawa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo utegemee malipo yako pia kutoka kwa Mwenyezi Mungu tu. Wamekuogopa kwa sababu kutokana na matendo yako wao wanaweza kuipoteza dunia (yaani maslahi ya kidunia) na wewe ulikuwa ukiwaogopa wao kwa sababu ulitaka kulinda imani yako. 305

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 305

9/4/2017 3:48:00 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Kwa hiyo waachie lile jambo ambalo kwalo walikuogopa nalo wewe na ukae mbali nao, wewe pamoja na imani yako. Angalia ni kiasi gani wanavyoihitaji ile imani ambayo wewe hukuwaruhusu kuidhibiti, na angalia wewe uko huru kiasi gani na dunia ambayo wamekunyima! Utakuja kujua kesho (Siku ya Kiyama) ni nani amekuwa mshindi na ni nani aliyeonyesha kijicho. Hata kama mtu amezuiliwa kutokana na dunia na vile vile kutokana na mbingu lakini anamuogopa Mwenyezi Mungu, Yeye kwa hakika hufungua njia kwa ajili yake mtu huyo. Utadumu siku zote katika mapenzi na haki na utaepukana na batili. Kama na wewe pia ungeitarajia dunia basi wao wangekupenda na kama ungekopa kutoka katika dunia hii wangekupatia kimbilio la hifadhi.� (Nahajul-Balaghah) Kisha Ali akamuomba Aqil na Ammar kumuaga ndugu yao na pia akawaambia Hasan na Husein wamwambie ami yao kwa heri. Uthman alipokuja kufahamu juu ya tukio hili alimkasirikia sana Ali. Mtu anaweza akauliza kuwa ilitokea vipi kwamba Ali alimuona Abu Dhar akipewa mate-so na maonevu lakini hakuchukua hatua zozote kumuokoa kutokana na udhalimu wa khalifa wa wakati huo? Abu Dhar alikuwa ni sahaba mashuhuri wa Mtume na muungaji mkono mkuu wa Ali na alikuwa akimpinga khalifa sio kwa sababu ya maslahi yoyote binafsi bali kwa kuhakikisha ustawi wa watu. Basi kwa nini Ali alibakia kimya? Kama angetaka angeweza kumzuia Uthman kutokana na kumhamisha Abu Dhar na angeweza kutumia uwezo wake wote kuwafanya watu wasimame kuwapinga Bani Umayyah. Na hakuna shaka yoyote kuhusu ule ukweli kwamba Waislamu wangeweza kumuunga mkono Ali kwa moyo mmoja. Sasa ni ipi ilikuwa sababu ya ukimywa huu wa Ali? Kama vile tu ambavyo swali hili linavyojitokeza kwenye akili ya kila mtu, ilitokea hata kwenye akili yangu pia. Nilifikiri kwamba, ambapo mwelekeo mmoja wa Ali kubakia kimya katika kadhia hii iko wazi na dhahiri kabisa na nyingine ni yenye kutatiza sana na haieleweki kwa kila mtu. Mwelekeo wenye utatanishi ni kwamba wakati wa Ali sio huu uliokuwepo sasa. Yeye aliishi miaka zaidi ya 1300 iliyopita. Hali na mazingira yaliyokuwepo wakati huo hayawezi kuchanganuliwa sawa sawa katika karne hii ya ishirini wala hatuwezi kuelewa vipengele vyake vyote. Kuchunguza sababu halisi bado hakujawezekana licha ya udadisi wa kina uliofanywa na watafiti wengi. Ali alijua na kuelewa nyeti nyingi za wakati wake mwenyewe ambazo hazikuonekana kwa wengine, na mbinu yake ya utendaji ilitegemea juu ya dharura za wakati huo ambazo zilijulikana kwake tu. 306

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 306

9/4/2017 3:48:00 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Hata hivyo, mwelekeo wa ukimya wake ambao uko dhahiri kabisa ni kwamba moyo wa kutoa muhanga ulikuwako katika tabia ya Ali na alikuwa yuko tayari kupata matatizo yoyote kwa ajili ya ustawi wa watu. Alikuwa akizingatia sana usalama wa Uislamu kwamba hakupenda kitu kingine chochote isipokuwa hicho tu. Jinsi tunavyochunguza kwa kina zaidi tabia na mwenendo wa Ali na kuangalia vipengele vyote vya maisha yake, ndio jinsi tunavyoridhishwa zaidi na ukweli huu. Hakuweza kuvumilia kwamba maendeleo na ulinganiaji wa Uislamu upungue nguvu japo kidogo. Alizijua vizuri fikra za Bani Umayyah kabla na baada ya kumbatio lao kwenye Uislamu, lakini alihofia kwamba kama Waislamu wangejipanga dhidi yao mitafaruku ingetokea miongoni mwa wafuasi wa Uislamu nayo ingekuwa na madhara juu ya dini hii. Ali alifahamu kwamba Bani Umayyah walitaka kuwauwa wale waumini wa kweli wote ambao walifanya mhimili halisi kwa ajili ya Uislamu, ili waweze kujinasua wenyewe kutoka kwenye makatazo yaliyowekwa na sheria za Kiislamu, na asiwepo yoyote wa kubakia kupinga shughuli zao. Je, sio ukweli kwamba Marwan bin Hakam alimchochea Uthman kumuua Ali na masahaba wengine mashuhuri wa Mtume kama Abu Dhar na Ammar? Lengo lake katika kutoa ushauri huu ni kwamba, kwa kuwaondoa watu hawa kutoka kwenye mandhari, Bani Umayyah wangeweza kuwa huru kufanya kile wanachokitaka, kwa sababu iwapo hawa masahaba wa Mtume wachamungu na wasio na hofu wakiwa wapo, Bani Umayyah wasingeweza kusababisha madhara na kutenda kama mtawala mwenye mamlaka yote. Kama matakwa ya Marwan yangetimizwa, haiwezi kutathminiwa ni matatizo kiasi gani ambayo Bani Umayyah wangeyasababisha. Ilikuwa kwa hiyo, ni kilele cha uona mbali wa Ali na ustahimilivu kwamba alionyesha tu wingi wa uchungu katika suala la udhalimu aliofanyiwa Abu Dhar kama alivyokuwa siku zote akionyesha kuhusiana na dhulma ambayo yeye mwenyewe alifanyiwa. Alifanya hivi ili kwamba Waislamu wasije wakawa ni maadui wa kila mmoja wao wenyewe kwa wenyewe. Haya yalitokea mapema vile vile katika tukio la Saqifah. Umar alikuja nyumbani kwa Ali na akamburuza kwa kumshikia upanga ili kuchukua kiapo cha utii kwa Abu Bakr. Waislamu walikusanyika karibu na Ali wakati huo. 307

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 307

9/4/2017 3:48:00 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Wengine wao walishangaa ambapo wengine walikuwa wamegubikwa na ghadhabu. Wote walikuwa wakitarajia ishara kutoka kwake ili waweze kupigana kwa ajili ya ulinzi wake. Bila shaka, Ali ambaye alikuwa ndio nguzo ya Uislamu, ngome ya uadilifu, na Imam wa watu wote, lakini nini alichokifanya juu yake mwenyewe? Wakati watu walipomuona Umar akimpeleka Ali mbele ya khalifa kwa ncha ya upanga, wao walishangaa sana. Hata hivyo pale walipomuangalia usoni mwake hawakuona dalili yoyote ya hasira juu yake. Yeye hakuwachochea watu wala hakunyanyua sauti yake, wala hakuwaruhusu kuchomoa panga zao. Watu walizidi kushangaa zaidi pale muda mchache baadae walipomuona Ali akiwa amesimama mbele yao (yaani, Abu Bakr na Umar n.k.) kwa utulivu kabisa na akihoji suala lake kwa wazo la kuwaridhisha wao kuhusu haki yake. Hakuna aliyethubutu kufungua mdomo wake katika kumjibu. Alikuwa akithibitisha haki yake kwa hoja nzito lakini akavumilia uporwaji wa haki yake kwa maslahi ya watu. Ali aliridhika katika kuthibitisha haki yake kupitia malalamiko na hoja, na pia alikuwa ameridhika katika kuonyesha subira, utulivu, uvumilivu na usamehevu. Yeye alijijua mwenyewe vizuri sana. Wafuasi wa Ali walishangazwa sana na msimamo alioutwaa. Lakini kulikuwa na jambo moja ambalo Ali alilijua bali wengine hawakulifahamu. Na hilo lilikuwa ndio jambo ambalo Ali alilikusudia na ambalo lilikuwa ni chanzo cha amani ya akili yake. Hili linahusiana kwenye ukweli kwamba yeye alikuwa amefanya kazi na Mtume ya kuweka msingi wa Uislamu. Alichangia sawasawa katika jukumu la ulinganiaji wa Uislamu. Ni vipi angeweza kuvumilia kwamba dini hii ikumbwe na maangamizi? Hiyo ilikuwa ndio sababu kwa nini alizitoa muhanga haki zake mwenyewe, na akafanya katika suala la Abu Dhar kwa namna ileile aliyokuwa amefanya katika suala lake mwenyewe. Nini Kilimtokea Abu Dhar Baada Ya Kuhamishwa Kwake Sahaba huyu maarufu wa Mtume na mzee mkongwe alifariki kwa njaa. Yeye na watu wa familia yake waliishi katika hali ngumu sana na walilazimika kukubwa na taabu zisizo na kifani. Watoto wao pia walikufa kutokana na kukosa chakula. Imesimuliwa kwamba baada ya vifo vya watoto wao; Abu Dhar na mke wake wakawa dhaifu sana kwa sababu ya njaa. Siku moja Abu Dhar alimwambia mkewe: “Hebu twende tukapande kwenye kilima kile.

308

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 308

9/4/2017 3:48:00 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Inawezekana kwamba tunaweza tukapata matunda pori huko.” Walipanda kwenye kilima hicho. Upepo mkali ulikuwa unavuma na hawakuweza kupata kitu chochote cha kula. Abu Dhar akaanza kuzimia. Ingawaje upepo wenye baridi kali sana ulikuwa unavuma; lakini Abu Dhar alikuwa anatokwa na jasho, na alilifuta jasho lake tena na tena. Wakati mke wake alipomtazama alitambua kwamba atafariki punde. Akaanza kulia. Abu Dhar akamuuliza kwa nini analia. Akajibu: “Kwa nini nisilie? Unapumua pumzi zako za mwisho kwenye ardhi hii kame, na sina hata kipande cha nguo kinachoweza kutumika kama sanda kwa ajili yako na mimi pia.” Maneno yake yalimhuzunisha Abu Dhar sana sana. Yeye akamwambia mkewe: “Nenda ukasimame kando ya njia. Inawezekana ukakutana na muumini anayeweza kuwa anapita njia hiyo.” Mkewe akajibu: “Ni nani atakayepita njia hii sasa? Msafara wa mahujaji umekwishapita tayari na barabara iko pweke.” Abu Dhar akayakumbuka maneno ambayo Mtume alikuwa ameyatamka kuhusu yeye. Akamwambia mkewe: “Nenda ukatazame vizuri. Endapo utaona mtu akija basi utaondolewa wasiwasi wako. Na kama hutaona mtu yoyote basi uufunike mwili wangu uliokufa na uuweke kando ya barabara. Wakati na pale utakapobahatika kukuktana na mpanda-mnyama wa kwanza, basi mwambie hivi: “Abu Dhar, yule sahaba wa Mtume amefariki. Sasa nisaidie kumuosha na kumvisha sanda.” Mkewe Abu Dhar alikipanda kile kilima mara kwa mara lakini hakuweza kumuona binadamu yoyote. Baada ya muda kiasi, hata hivyo, aliwaona wapandaji kwa mbali na akawapungia kwa kutingisha nguo yake. Walikuja mpaka pale alipokuwa na wakasema: “Ewe mja wa kike wa Mwenyezi Mungu! Kuna jambo gain hapa?” Yeye akajibu: “Huyu hapa ni Muislamu ambaye anafariki; tafadhali andaeni kumuosha, kumvika sanda na kumzika. Mwenyezi Mungu atawalipeni kwa hili.” Wakamuuliza: “Ni nani mtu huyu?” Yeye akajibu: “Jina lake ni Abu Dhar Ghiffari.” Wale watu hawakuweza kuamini kwamba sahaba mashuhuri wa Mtume kama huyo anaweza akafa kwenye jangwa. Wao, kwa hiyo, wakamuuliza yule mama: “Ni Abu Dhar yupi huyu? Ni yule sahaba wa Mtume?” Yeye akajibu: “Ndio.” Wao wakasema: “Wazazi wetu nawawe fidia yake! Mwenyezi Mungu ametupa sisi heshima kubwa.” Kisha wakakimbilia pale mahali ambapo Abu Dhar alikuwa amelala. Abu Dhar alikuwa anayasikia maumivu ya kifo. Aliwakodolea macho kwenye nyuso zao kwa kitambo kiasi akijaribu kuzikumbuka nyuso zao, halafu akasema: “Wallahi mimi sijasema uongo. Kwa jina la 309

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 309

9/4/2017 3:48:00 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Mwenyezi Mungu kama ningekuwa na nguo ya kutosha kwa sanda yangu na ya mke wangu kwa kweli ningevikwa sanda kwa nguo hiyo. Ninakuombeni kwa jina la Mwenyezi Mungu kwamba kama mmoja wenu yoyote amewahi kuwa mtawala au muajiriwa wa serikali au mtumishi au chifu kwa wakati wowote ule asije akanivika sanda.” Wale waliokuwepo pale walikanganyikiwa kusikia maneno haya kwa sababu takriban wote hawa walikuwa wamewahi kuzishika nafasi hizo katika wakati mmoja au mwingine. Mara ghafla kijana mmoja kutoka miongoni mwa Ansari alijitokeza mbele na kusema: “Ewe ami yangu! Nitakuvisha sanda kwa joho hili ambalo nimelinunua kwa pesa ambayo niliipata kwa kufanya kazi ngumu. Nitakuvika sanda kwa nguo hii ambayo nyuzi zake zilifumwa na mama yangu ili niweze kuitumia kama Ihram (vazi la hujaji).” Akamwambia kijana huyo: “Nivishe sanda kwa vipande hivi vya nguo, kwani ni visafi kabisa.” Sasa akafurahi na kuridhika. Kisha akawatupia macho kwa mara nyingine tena na akafariki kwa amani kabisa. Kisha yale mawingu meusi na mazito yakalivunika anga. Upepo wenye nguvu na mkali ukaanza kuvuma na mchanga wa jangwa ukaruka juu na kulitia giza lile angahewa. Inaweza ikasemekana kwamba lile jangwa la Rabazah liligeuka kuwa bahari inayonguruma. Yule kijana wa ki-Ansari akasimama kando ya kaburi la Abu Dhar na akaomba kwa maneno haya (wanahistoria wameyahusisha kwa Malik Ashtar): “Ewe Allah! Abu Dhar huyu ni mmoja wa masahaba wa Mtume Wako. Alikuabudu Wewe miongoni mwa wenye kuabudu. Alipigana Jihadi dhidi ya waabudu masanamu. Hakubadili hata Sunnah moja ya Mtume wala hakugeuza sheria yoyote. Aliona mambo mabaya na ya aibu yakitendeka, na akaonyesha kuyachukia kwake hayo kwa moyo na kwa ulimi wake. Na matokeo yake watu wakamuonea na kumfedhehesha, na wakamtoa nje ya nyumba yake. Walimnyima haki zake na kumdhalilisha, na hatimae akafariki katika mazingira yasiyokuwa na msaada. Mwenyezi Mungu aivunje miguu ya wale watu waliomnyima (vistawishi vya maisha) na kumhamisha kutoka kwenye mji mtukufu wa Madina ambako yeye alikuwa amehamia.” Wale wote waliokuwa pale wakaitikia “Amin!” kwa uaminifu sana. Abarikiwe sana Abu Dhar ambaye alisimama na akajitahidi kusimamisha haki hadi alipofariki. Alikuwa na imani katika utukufu wa mwanadamu na haki zake. Alikuwa ni mtu 310

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 310

9/4/2017 3:48:00 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

mkarimu na mpole. Hakuwa akiogopa kifo kamwe, wala sio kama hakuvutiwa na dunia kamwe. Matukio haya ya huzuni ya Abu Dhar na mke wake na watoto yalikoroga damu za watu na kila mmoja wao aliihurumia ile familia iliyodhulumiwa. Wakati ambapo vitendo vingine vingi vya Uthman viliwainua watu dhidi yake, hili tukio moja liliongezea chuki zao zaidi dhidi yake na Bani Umayyah. Ilichukuliwa kwamba ni sera ya kiovu kwamba yeyote aliyepinga ubinafsi na upendeleo wa kifamilia lazima atendewe kikatili kama ilivyofanywa kwenye suala la Abdullah bin Mas’ud, Ammar Yasir, na Abu Dhar. Walidhalilishwa na kupigwa; na pensheni zao, malipo yao ya ujira wao yakasimamishwa. Kinyume chake, hao Bani Umayyah walimiminiwa manufaa yote, utajiri na vyeo. Uthman aliweka heshima nyingi juu yao na akawapa utajiri mkubwa, ingawa ilikuwa ni lazima kwake kwamba alipaswa kuwaondoa kwenye nafasi muhimu kutokana na matendo yao maovu. Kitendo kingine cha Uthman ambacho kiliamsha hasira za watu kilikuwa ni uonevu wake juu ya watu ambao walikwenda kwake kulalamika dhidi ya Walid bin Uqba. Maelezo juu ya kadhia hii ni kama haya yafuatayo: Uthma alimuuzulu Sa’d bin Abi Waqqas kutoka kwenye ugavana wa Kufa na akambadilisha mahali pake na Walid bin Uqba, ambaye alikuwa ni kaka yake Uthman kutokana na upande wa mama yake. Watu wa Kufa walisikitishwa sana kutokana na uteuzi huu. Inasemekana kwamba pale Walid alipowasili hapo Kufa na akapita karibu na nyumba ya Umar ibn Zararah Nakh‘i, huyu Umar alisimama na kusema: “Ewe Bani Asad! Uthman ametutendea sisi vibaya sana. Je, ilikuwa ni kwa upande wake tu kutuondolea kutoka miongoni mwetu Sa‘d bin Waqqas, ambaye alikuwa mpole na mwenye tabia njema, na kuteua katika nafasi yake, ndugu yake Walid ambaye ni mpumbavu, mwendawazimu na fisadi mkongwe.” Baada ya uteuzi wa Walid, ilizoeleka kusemwa na watu wa Kufa kwamba Uthman amewadhalilisha wafuasi wa Mtume Muhammad na amejaribu kumheshimu ndugu yake. Malalamiko mengi yalitolewa kwa Uthman dhidi ya Walid; lakini yeye hakumuondoa kwenye ugavana huo, ingawa wengi wa walalamikaji walikuwa ni masahaba wa Mtume. Tabia ya Uthman kuhusu Walid ilikuwa ni sawasawa kama ilivyokuwa kuhusu ndugu zake. Kama vile tu ambavyo hakukubali mapendekezo yoyote, au kukaribisha malalamiko yoyote dhidi ya ndugu zake wa karibu, pia hakutilia maanani malalamiko dhidi ya Walid vile vile. 311

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 311

9/4/2017 3:48:00 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Allamah Bin Abd Rabbih anamnukuu Sa‘id bin Musayyab katika kitabu chake kiitwacho ‘Iqdu al-Farid akisema kwamba masahaba wa Mtume hawakuupenda ukhalifa wa Uthman kabisa, kwa sababu wengi wa maafisa aliowateua yeye walitokana na Bani Umayyah, na walifanya mambo ambayo yalichukiwa na masahaba hao. Malalamiko yalitolewa dhidi ya maafisa hawa kwa Uthman lakini yeye hakuwaondoa maafisa hao. Mshairi Hati’ah anasema kuhusu Walid: “Hati’ah atatoa ushahidi Siku ya Kiyama, kwamba Walid hana hatia. Wakati swala ilipokwisha, yeye aliwauliza watu kwa sauti kubwa: ‘Kama mkisema, ninaweza kuiongeza.’ Alitaka kufanya nyongeza juu ya jambo zuri. Kama watu wangekubali, angeiongoza swala ya asubuhi ambayo ingezidi rakaa kumi. Lakini O Abu Wahab, watu walikataa kukubali. Kama wangekubali mapendekezo yako, ungechanganya Shaf na witr. Wewe ulisonga mbele, lakini watu walikizuia kigwe chako. Kama wangekiachia, ungetembea zaidi na zaidi.” Idadi kadhaa ya watu walikuja kutoka Kufa na wakalalamika kwa Uthman dhidi ya Walid. Uthman hata hivyo aliwakemea na kuwatishia badala ya kutilia maanani malalamiko yao, na akawapiga viboko wale waliotoa ushahidi dhidi ya vitendo vyake viovu, ingawa kosa lao pekee lilikuwa kwamba waliyafikisha yale matendo maovu ya Walid kwenye ufahamu wa Uthman. Adhabu kali sana iliyotolewa na Bani Umayyah kwa wapinzani wao au kwa wale waliowaona kuwa katika kundi la wapinzani wao (kwa sababu walitaka umma uweze kuwa na haki katika ukhalifa, na usiwe ni mali ya Bani Umayyah), ilionekana kwenye ushughulikaji na Muhammad bin Abi Bakr na wale Wamisri ambao walikuwa wakielekea Misri. Kwa vile kadhia hii ina muungano wa karibu na mauaji ya Uthman, tutakuja kuielezea kwa kirefu katika sura inayofuatia. Maelezo Kuhusu Kuuawa Kwa Uthman Miaka kumi na moja na miezi mingi ikapita. Mfundo wa watu dhidi ya sera za Uthman uliendelea kuongezeka siku hadi siku. Raia wa nchi zote za Kiislamu walimpinga Uthman kuzidi kiasi, zaidi sana kiasi kwamba kulikuwa na wasiwasi kila mahali. Kitu ambacho kiliwaogopesha sana Waislamu kilikuwa kwamba; katika kipindi cha utawala wa Uthman, zile namna na matendo yaliyokuwapo wakati wa Mtume na Abu 312

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 312

9/4/2017 3:48:00 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Bakr na Umar ambayo waliyapenda sana yalivurugwa, shaghalabaghala na hakuna chochote cha kipindi kilichopita kilichobakia salama na kamilifu tena. Walikuwa wamezoea kuona kwamba khalifa analinda haki zao na kuendeleza maslahi yao. Wakati ambapo magavana na maafisa walipomuonea mtu au walipokuwa na tabia mbaya, khalifa aliwafukuza kazi mara moja na akayarekebisha manung’uniko ya watu. Hata hivyo, mara tu Uthman alipokuwa khalifa alizipuuza kanuni na taratibu zilizoegama juu ya uadilifu, na akaanzisha serikali yake juu ya sera ya upendeleo wa ndugu, ambao watu hawajawahi kuuona kamwe kabla ya hapo, na ambao hawakuweza kuuvumilia. Jambo ambalo liliwakera sana watu ni kwamba; ndugu zake Uthman walizipora haki zao na wakawa matajiri zaidi siku hadi siku, na wale watu wa kawaida walinyimwa hata mahitaji muhimu ya maisha. Vile vile walichukia sana utendewaji uliofanywa na khalifa kwa tume za wawakilishi wao ambazo zilimwendea kutoa malalamiko yao dhidi ya magavana na maafisa wengineo. Watu vile vile walikasirika sana kutokana na fedheha na udhalilishaji ambao kwamba masahaba maarufu wa Mtume kama Abu Dhar, Ammar, na ibn Mas’ud uliwapata. Hawakupenda pia sera yake ya kuwaondoa magavana na maafisa wa kutegemewa na maarufu kwa kuwaweka badala yao watu waliokuwa madhalimu na waonevu. Waislamu wachamungu hawakupenda pia kwamba hao watawala wawakandamize Madhimmi, kwa sababu, hata hivyo, wao pia walikuwa ni binadamu. Hawakupendezewa kwamba jamii itiwe sumu ya ubaguzi na ubinafsi, na vile watu wasio na uwezo waweze kupewa kipaumbele juu ya wale waaminifu na wenye uwezo. Katika siku za mwisho za ukhalifa wa Uthman watu walikosa uvumilivu kiasi kwamba waliasi dhidi yake. Hili lilikuwa jambo la kawaida kabisa kwa sababu mbegu za uasi zilikuwemo kwenye sera zake mwenyewe. Inasemekana kwamba siku moja Uthman alibahatika kupita karibu na nyumba ya mtu mmoja aliyeitwa Jabala bin Amr Sa’id. Huyu Jabala alikuwa amekaa miongoni mwa watu wa kabila lake na alikuwa ameshika mnyororo mkononi mwake. Uthman akawasalimia na wale waliokuwepo pale wakazijibu salamu zake, isipokuwa Jabala. Akawaambia wale watu wa kabila lake: “Kwa nini mmejibu salamu za mtu ambaye amefanya mambo haya na haya na yale.” Kisha akamwambia Uthman: “Naapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba isipokuwa pale utakapowaondoa wale vipenzi wako 313

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 313

9/4/2017 3:48:00 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

waovu kama Marwan, Ibn Aamir na Abi bin Sarah, vinginevyo nitauweka mnyororo huu shingoni mwako.” Allamah Ibn Abil-Hadid anasema kwamba watu walikuja kuwa majasiri kiasi kwamba siku moja wakati Uthman alipokuwa anawahutubia watu akiwa ameweka mkono wake kwenye ile fimbo ambayo alikuwa akiishika Mtume na Abu Bakr na Umar walipokuwa wakitoa hotuba, mtu mmoja aliyeitwa Jehjah Ghifari aliinyakuwa ile fimbo kutoka mkononi mwake, akaikandamiza kwenye goti lake na akaivunja. Hapo mwanzoni watu hawakuweza kupata ujasiri wa kutosha kumkosea adabu Uthman. Hata hivyo, pale matendo maovu ya Marwan na wengineo yalipozidi kuongezeka sana, na Uthman, badala ya kuwazuia kutokana na vitendo vyao viovu alionyesha kuwaendekeza, vurugu na uasi pia ukawa umeenea. Mpaka hapo, ni watu mmoja mmoja binafsi tu waliompinga na kumshutumu Uthman, na ni mtu mmoja au wawili tu walioonyesha utovu wa adabu mbele ya Uthman. Hata hivyo, jinsi muda ulivyozidi kusonga mbele, umma wote wa Waislamu wakawa ni maadui zake. Watu wa Madina waliandika barua kwa Waislamu wa miji mingine kwa maneno haya: “Kama mnapenda kufanya Jihadi basi mnapaswa mje hapa, kwa sababu dini ya Muhammad inachafuliwa na khalifa wenu. Njooni mumuondoe kwenye ukhalifa.” Wakazi wa miji yote wakageuka dhidi ya Uthman. Kufikia mwaka wa 35 A.H. matukio yalitokea kiasi kwamba wakazi wa miji mbali mbali waliandikiana barua wao kwa wao wenyewe wakipendekeza kwamba lazima kufanyike kitu ili kuwaondoa Bani Umayyah na Uthman, na magavana wote na maafisa lazima waondolewe kutoka kwenye nafasi zao. Taarifa kuhusu shughuli hizi zilimfikia Uthman pia. Yeye aliandika barua kwa wakazi wa miji mbalimbali na akajaribu kuwapatanisha. Halafu akawaita magavana wake na maafisa wa ngazi za juu na akafanya mashauriano nao. Baadhi yao walipendekeza kwa Uthman kwamba yeye angetawala kwa uadilifu na kutwaa sera za Abu Bakr na Umar. Wengine waliyauma maneno yao na hawakutoa ushauri wowote wa dhahiri. Mmoja wa wale watokanao na kundi hili la mwisho ni Mu’awiyah bin Abu Sufyan. Bado walikuwepo wengine ambao hawakufaa kutoa mapendekezo yoyote kwa sababu wakati wote mapendekezo yao yaliegama kwenye ubinafsi. Mtu mmoja wa aina hiyo alikuwa ni Sa’id bin Aas ambaye alisema kwamba hali ya mambo iliyokuwepo wakati huo ilikuwa ni ya mpito tu na dawa pekee juu yao ilikuwa ni uchomoaji wa panga. 314

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 314

9/4/2017 3:48:00 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Mkutano uliisha bila ya kupata makubaliano yoyote ya pamoja ya kuweza kutatua nayo hali hiyo. Sababu ya hili ni kwamba magavana na maafisa wote waliipenda sera ya Uthman ambayo kwa kupitia sera hiyo wao waliweza kuingilia juu ya haki za watu na kujitengenezea pesa nyingi kiasi walivyoweza. Wao kwa hiyo hawakutoa ushauri wowote wa kiaminifu. Walikuwepo baadhi miongoni mwao hata hivyo, ambao walidhani kwamba maslahi yao yatatimia vizuri kama wataweza kumuondoa Uthman na walikuwa, kwa hiyo, wakijitahidi kwa siri, na wengine wao hata kwa wazi kulifanikisha lengo hilo. Sababu juu ya mwelekeo huu wa watu wanaohusika zitaelezewa baadae. Na jambo muhimu sana kuhusu mkutano huo lilikuwa kwamba Marwan alikuwa anawaangalia kwa karibu sana wale washiriki wote. Hivyo, hata kama baadhi yao wangekuwa wametoa mapendekezo mazuri sana, yangekuwa hayana maana yoyote kwa sababu kauli ya mwisho juu ya suala hili ilikuwa iwe ile ya Marwan. Uthman wakati wote alitekeleza ushauri wake. Hatimae uasi ukalipuka. Waislamu wa nchi na majimbo yote walikuwa wamegeuka dhidi ya uongozi, sera na ukhalifa wa Uthman, ambavyo kwa kweli, kwa namna isiyo dhahiri, vilikuwa mikononi mwa Marwan na washirika wake. Katika wakati huo huo baadhi ya watu kutoka Misri walimwendea Uthman kumlalamikia dhidi ya Ibn Abi Sarah, gavana wa huko Misri. Uthman aliwasikiliza kwa makini, akamkemea Ibn Abi Sarah kwa matendo yake maovu na akawaahidi watu hao kwamba manung’uniko yao yatafanyiwa kazi na kurekebishwa. Kisha akaandika barua kwa Ibn Abi Sarah akimtaka arekebishe mwenendo wake na kumtishia kwamba kama hatatii maagizo yake basi ataadhibiwa. Marwan hakuyapenda maendeleo haya. Wakati walalamikaji walipotoka nje ya kasiri la khalifa, yeye pia alitoka na akawakaripia. Halafu akasisitiza kwamba khalifa azipuuze hizo ahadi alizozitoa kwa watu wale na asiyatilie maanani malalamiko yao. Wamisri wale walirudi pamoja na barua hiyo na wakaikabidhi kwa Ibn Abi Sarah. Alikerwa sana baada ya kuisoma barua hiyo na akakataa kutii yale maagizo ya khalifa. Alikasirika sana kiasi kwamba alimuua mmoja wa wale wajumbe. Kiburi hiki cha Ibn Abi Sarah kilitokana na ukweli kwamba yeye alikuwa ni ndugu wa kunyonya wa Uthman na ilikuwa ni kutokana na uhusiano huu kwamba yeye alimteua kuwa gavana wa Misri. Watu wa Misri walichukia sana kitendo walichotendewa na Ibn Abi Sarah. Waliamua kutuma ujumbe mwingine kwenda Madina uliokuwa na watu elfu moja. 315

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 315

9/4/2017 3:48:00 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Walifikia katika msikiti wa Mtume na wakatangaza kwamba wao hawatawaingilia wale watakaobaki ndani ya nyumba zao na ambao hawakuchukua silaha dhidi yao. Baada ya hapo baadhi ya watu wao maarufu walikutana na masahaba wa Mtume. Waliwaelezea ukatili uliofanywa na Ibn Abi Sarah, pamoja na mauaji ya mtu asiye na hatia ambaye kosa lake pekee lilikuwa kwamba yeye alikuwa mmoja katika ule ujumbe ambao ulimngojea Uthman hapo mapema kabla. Baadhi ya masahaba walikwenda kumuona Uthman na wakajadiliana naye juu ya hali ya mambo iliyokuwepo huko Misri. Baada ya hapo, watu wengi sana wakiongozwa na Ali walikutana na Uthman kuhusu suala hili. Waliongea naye kwa njia ya busara na mantiki kabisa na wakasema: “Hawa watu wanachotaka tu ni kwamba umuondoe Ibn Abi Sarah kutoka kwenye ugavana na uteue mtu mwingine badala yake. Hapo mapema walilalamika pia kuhusu kuuawa kwa mtu asiye na hatia. Unapaswa kumuuzulu Ibn Abi Sarah kutoka kwenye kazi hiyo na pia utoe uamuzi kuhusu malalamiko yao. Kama Ibn Abi Sarah atathibiktika kuwa na hatia basi umuadhibu na hivyo kutoa haki kwa watu hawa.” Uthman akaapia mbele ya watu hao, na akawahakikishia kwamba atajitahidi kufanya kila aliwezalo kwa ajili ya faida ya watu. Pia akawaomba wapendekeze jina la mtu anayeweza kuteuliwa kama gavana wa Misri badala ya Ibn Abi Sarah. Wale watu wa Misri baada ya kushauriana ipasavyo wakapendekeza jina la Muhammad bin Abi Bakr. Uthman akamteua kama gavana wa Misri na akampeleka pamoja ni kikundi chenye Muhajirina na Ansar kwenda kuchunguza yale maovu ya Ibn Abi Sarah. Siku tatu baada ya kuondoka kwao Madina, Muhammad bin Abi Bakr na masahaba zake waliona mtumwa wa kihabeshi ambaye alikuwa anampeleka ngamia wake mbio mbio kuelekea Misri. Watu hawa wakapatwa na mshangao. Wao kwa hiyo, wakamsimamisha na kumuuliza ni kwa nini alikuwa anakwenda mbio namna hiyo na lipi lilikuwa lengo la safari yake. Baada ya kuulizwa sana maswali yeye akasema: “Mimi ni mtumwa wa Amir wa waumini Uthman, na nimetumwa kwenda kumuona gavana wa Misri.” Wale watu wakamwambia: “Gavana wa Misri huyu hapa pamoja nasi.” Yule mtumwa akajibu: “Sina maana ya huyu.” Wakati Muhammad bin Abu Bakr alipojulishwa kuhusu jambo hili yeye alimwita yule mtumwa na akamuuliza kama yeye 316

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 316

9/4/2017 3:48:00 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

alikuwa ni nani. Yeye akasema: “Mimi ni mtumwa wa Amir wa waumini.” Kisha kwa kujipinga yeye mwenyewe akasema: “Hapana, hapana. Mimi ni mtumwa wa Marwan.” Kwa hiyo akaendelea kuzungumza maneno yanayopingana. Halafu Muhammad akamuuliza: “Wewe unakwenda wapi?” Akajibu akasema: “Ninakwenda Misri kumuona gavana.” “Kwa ajili gani?” akamuuliza Muhammad. Yule mtumwa akajibu: “Ninakumfikishia ujumbe kwake.” Katika Muhammad kumuuliza mtumwa yule iwapo amebeba barua yeye akajibu kwa kinyume chake. Papo hapo Muhammad akaagiza mwili wake kupekuliwa. Baada ya upekuzi wa uangalifu sana barua ilipatikana kwake ambayo ilikuwa imeandikwa na Uthman kwenda kwa Abdullah Ibn Abi Sarah. Muhammad akaifungua barua hiyo mbele ya Muhajir na Ansari waliokuwa wakiongozana naye. Ilisomeka kama ifuatavyo: “Wakati Muhammad mwana wa Abu Bakr na watu wengine fulani na fulani watakapowasili huko Misri, unapaswa uwaue wote kwa mfano mmoja au mwingine. Ichukulie barua atakayokuletea Muhammad kama iliyofutwa na uendelee kuishika nafasi yako mpaka maagizo ya baadaye. Mfunge mtu yeyote atakayekufuata na malalamiko na kisha usubiri maagizo kutoka kwangu.” Wakati barua hiyo iliposomwa kwa sauti wale wote waliokuwepo pale walipigwa na butwaa na kimya kizito kikatanda hapo. Hakuna hata mmoja aliyeweza kudhania kwamba khalifa anaweza akafanya mpango wa kiovu namna hiyo, wa kutoa uhai wa raia zake ikiwa ni pamoja na Muhajir na Ansari. Muhammad bin Abu Bakr akaifunga bahasha ile tena na akaigandisha kwa idhini ya Muhajir na Ansar. Kundi hilo likaamua kurejea Madina na kuonyesha barua hiyo kwa masahaba wa Mtume. Wakati barua hiyo iliposomwa hapo Madina mbele ya masahaba, akiwemo Ali, wote hao walihuzunika sana. Njama hii dhidi ya Waislamu na Uislam; ambayo ilikuwa haijawahi kutokea, iliwafanya wao wakasirike sana. Ghadhabu ya watu ambao tayari walikuwa wamekwisha kuchukizwa kutokana na vitendo vilivyotendwa kwa Abu Dhar na Ammar Yasir na kadhalika ilikuwa haina mipaka kabisa. Ujumbe ukiongozwa na Ali ambao ulikuwa na akina Sa’d bin Abi Waqas na Ammar Yasir uliundwa na wakaenda kuonana na Uthman. Waliichukua na ile barua, pia na yule mtumwa na ngamia ambaye alikuwa amempanda. Mazungumzo yafuatayo yalitokea kati ya Ali na Uthman: Ali: Huyu ni mtumwa wako? 317

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 317

9/4/2017 3:48:00 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Uthman: Ndiyo Ali: Na ngamia huyu pia ni wako? Uthman: Ndio Ali: Je, mhuri uliogandishwa kwenye barua hii ni wako? Uthman: Ndio. Ali: Kwa hiyo ina maana barua hii ni wewe uliyeituma? Uthman: Hapana. Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kwamba mimi sikuiandika barua hii mwenyewe wala sikuagiza mtu mwingine yoyote kuiandika, wala sikumtuma mtumwa huyu kwenda Misri. Masahaba walipata kuelewa kwamba Uthman alikuwa anaeleza ukweli. Katika kudadisi zaidi waligundua kwamba barua ile ilikuwa katika mwandiko wa Marwan. Wao kwa hiyo, walimuomba Uthman amwite Marwan mbele yao ili kwamba wao waweze kuulizia juu ya jambo hilo, na wamuulize ni kwa nini ameandika barua hiyo. Uthman akakataa kumwita Marwan. Ingawa Marwan alikuwa wakati huo yuko naye hapo makao makuu; hakuwa na ujasiri wa kutokeza mbele ya watu wale kuja kukiri kosa lake, na kwa hiyo kuthibitisha kutokuwa na hatia kwa Uthman. Masahaba kwa hiyo wakarudi kwenye nyumba zao kwa hofu kuu na mshangao. Waliamini kwamba Uthman asingeweza kuapia kiuongo uongo, bali baadhi yao walisema kwamba watamchukulia kuwa hana hatia pale tu atakapokuwa amemkabidhi Marwan kwao ili waweze kumuuliza na kulichunguza jambo hilo, na kuupata ukweli hasa wa mambo kuhusu barua ile. Walisema pia kwamba endapo barua hiyo itakuwa imeandikwa na Uthman basi wao watamuuzulu madarakani, lakini kama itakuwa imeandikwa na Marwan kwa amri yake watatafakari juu ya jambo hilo na kuamua juu ya ni vipi Marwan atakavyoshughulikiwa. Hata hivyo Uthman hakukubali kumtoa Marwan. Waasi sasa wakaanza kusisitiza zaidi na kwa nguvu zote kwamba Marwan lazima akabidhiwe kwao, ili kwamba wao waweze kumuuliza na kuchunguza shughuli zake. Uthman, hata hivyo akakataa katakata kukubaliana na madai haya. Baada ya hapo matukio mengi ambayo yameandikwa katika vitabu vya historia yalijitokeza. Imam Ali alijaribu kwa uwezo wake wote kuleta maafikiano kati ya waasi na Uthman ili umwagaji damu uweze kuepukwa.

318

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 318

9/4/2017 3:48:00 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Alionana tena na Uthman na akamshauri kwamba aweze kutoka mbele ya kadamnasi na kutoa hotuba ambayo ingeweza kusikiwa na wote, na katika hotuba hiyo apaswe kuthibitisha zile ahadi alizozitoa kwa watu ili kwamba waweze kuridhika. Pia alimwambia Uthman: “Naapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba nchi zote za Kiislamu zimegeuka dhidi yako. Ninahofia kwamba watu wa Kufa na Basra pia wanaweza wakaja Madina kama walivyokuja watu wa Misri, na unaweza ukalazimika kuniomba mimi niwatulize.” Uthman akatoka nje ya nyumba yake na akatoa hotuba mbele ya mkusanyiko huo. Alionyesha huzuni yake kubwa kwa kuteleza kwake kulikopita na akaahidi kwamba mambo kama hayo hayatatokea tena katika siku za baadae. Aliwaahidi pia kwamba madai yao yatatekelezwa na Marwan na washirika wake watawekwa pembeni. Hotuba ya Uthman ilikuwa na athari njema. Wakati alipokuwa anazungumza, machozi yalitiririka kutoka machoni mwake. Wengine pia wakaanza kulia na ndevu zao zikaloa kwa machozi. Pale aliposhuka kutoka kwenye minmbari ya msikitini na akaenda nyumbani, aliwaona Marwan, Sa’id bin Aas, na watu wengine wa familia ya Umayyah wakiwa wanamngojea. Hawakuwepo wakati Uthman alipokuwa anaongea, lakini walikuwa wametambua juu ya kile alichokuwa amekisema. Wakati Uthman alipoketi chini Marwan akamuuliza: “Oh, mkuu wangu! Niseme maneno kidogo au ninyamaze kimya?” Uthman akasema: “Sema hicho unachotaka kusema.” Marwan ndipo akasema kwa namna ya kulaumu: “Wewe umewatia moyo tu watu hawa na hukufanya jingine lolote.” Uthman akajibu kwa kujuta kiasi fulani: “Nimesema nilichokisema. Siwezi nikayarudisha maneno yangu nyuma (kuyameza).” Marwan akasema: “Watu wamekusanyika mbele ya lango la nyumba yako kama mlima, na hii ni kwa sababu umewatia moyo. Endapo mmoja wao atalalamika juu ya uonevu, mwingine atadai kuuzuliwa kwa gavana. Umekuwa mkatili sana wa ukhalifa wako. Ingekuwa ni bora kwako kama ungebaki na subira na kimya.” Uthman akasema: “Naona aibu ya kwenda kinyume na maneno yangu. Unaweza, hata hivyo, ukaenda kuongea nao.” Kwa kupata ruhusa hii, Marwan akaja pale kwenye lango la nyumba na akasema kuwaambia wale watu waliokuwa wamekusanyika pale: “Kundi lote hili ni la nini? Inaelekea kwamba mmekuja kuipora nyumba hii. Nyuso zenu nazifanywe kuwa nyeusi! Hivi mmekuja kwetu kutupokonya serikali? Wallahi kama mnakusudia kutufanyia madhara, sisi tutawashughulikieni katika namna ambayo kamwe hamtaweza 319

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 319

9/4/2017 3:48:00 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

kuisahau. Rudini majumbani kwenu. Sisi hatuwezi kuvumilia kuingiliwa mamlaka yetu na mtu yeyote yule.” Watu waliondoka wakiwa wamekata tamaa, huku wakiwatukana na kuwatishia hao watawala. Mtu mmoja alimjulisha Ali kuhusu maendeleo haya mapya. Kwa vile Uthman amepuuza mapendekezo yake na akatenda kulingana na ushauri wa Marwan, Ali angeweza sana kujizuia kwenda kwa Uthman tena na kumpa ushauri wowote ule. Hata hivyo, huruma juu ya khalifa huyu mzee, mapenzi ya moyoni ya kutaka suluhu miongoni mwa Waislamu, na kiasi kidogo cha matumaini kwamba Uthman anaweza akafuata njia ya busara ndio yalimlazimisha yeye kumshauri Uthman kwa mara nyingine tena. Wakati usiku ulipoingia, na Uthman alipokuja kumuona Ali kwa mashauriano kwa mapendekezo ya mke wake Na’ila, Ali akamwambia: “Baada ya kutoa hotuba katika minmbari ya Mtume ulikwenda nyumbani kwako na halafu Marwan akatoka na kuwatukana watu. Baada ya hapo ni kipi cha kufanya kilichobakia na mimi nitakusadia nini?” Uthman alijilaani sana mwenyewe kwa kule kupotoka kwake. Ndipo Ali akamwambia: “Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kwamba mimi nimejitahidi sana, zaidi kuliko mtu mwingine yeyote kuwaweka watu mbali na wewe. Hata hivyo, kila ninapopendekeza jambo kwako, ambalo ninategemea kwamba litakufurahisha wewe, Marwan anaingilia kati. Na kwa bahati mbaya unakubali kile anachokisema yeye na kupuuza kile ambacho mimi ninapendekeza.” Ali alikuwa sahihi kabisa katika kuyasema haya kwa sababu hata safari hii pia Marwan alikuwa ameliharibu jambo hilo. Wale waasi walianza kusisitiza juu ya madai yao kwa mara nyingine tena. Walitaka kutimizwa kwa zile ahadi zote walizoahidiana nao. Na pia walidai kwamba Marwan, ambaye alikuwa ndiye sababu ya kiini cha fitna zote, akabidhiwe kwao ili waweze kulipiza kisasi juu yake. Hata hivyo, mwelekeo wa Uthman ukawa mgumu na akakataa kwa ukali kabisa kumkabidhi Marwan kwao. Waasi nao pia wakawa wakaidi. Vurugu na uasi ukawa mkali na waasi hao wakaizingira nyumba ya Uthman. Kwa kweli waasi hao hawakutaka kumdhuru Uthman. Walichokitaka tu ni kwamba apaswe kutubia kwa upotovu wake na aachie mamlaka. Hili linathibitishwa na ukweli kwamba mtu mmoja aliyeitwa Nayyar bin Ayaz ambaye alikuwa mmoja wa masahaba wa Mtume alichukua nafasi yake katika safu ya mwanzoni ya waasi hao na akamwambia Uthman kwa sauti kubwa: “Unapaswa tu kuondoka madarakani na ninakuhakikishia kwamba utabaki bila kudhurika.” Wakati 320

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 320

9/4/2017 3:48:00 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

alipokuwa akiyasema haya, Kathir bin Salat Kandi, ambaye alikuwa mfuasi wa Uthman, na alikuwemo ndani ya nyumba wakati ule, alimpiga mshale na kumuua Nayyar bin Ayaz. Waasi hao walipiga makelele: “Mkabidhini muuaji wa ibn Ayaz kwetu.” Uthman akajibu: “Nitakabidhi kwenu vipi mtu ambaye ananilinda mimi?” Wale waasi (kwa Uthman) wakalishambulia lango la nyumba ambalo mara tu likafungwa haraka sana. Ndipo wakalichoma moto na watupa mishale wao wakamimina mishale kwenye kasiri la khalifa. Hatimaye Muhammad bin Abu Bakr na wafuasi wake wawili waliingia kwenye nyumba hiyo kutokea upande wa nyumba ya Muhammad ibn Abi Khurram Ansari. Walipofika karibu yake, walimkuta mkewe Na’ila akiwa pamoja naye. Wale wafuasi wawili wa Muhammad ibn Abu Bakr wakamshambulia kwa silaha zao kali na wakamuua.50 Kisha wakatoroka kupitia njia ile ile waliyokuwa wameingilia kwenye nyumba hiyo. Na’ila alipiga makelele: “Watu wamemuua Amiri wa waumini!” Uthman alikutana na kifo chake kwa namna hii. Watu ambao walihusika na kifo chake walikuwa wa namna mbili. Kwenye kundi moja walikuweko wale ambao walipata hasira sana kwa ajili ya haki. Walimtaka Uthman kutubia kwa ajili ya upotovu wake na pale alipokataa kufanya hivyo, wao waliizingira nyumba yake na kumuua. Miongoni mwao waliingia watu wa Hijaz, Misri na Iraqi na miji yote ya Kiislamu. Kwenye kundi la pili walikuwemo wale ambao walipagawa kutaka ngawira za kivita. Pamoja nao alikuwepo kiongozi ambaye alitiiwa, na watu hawa walimuacha Uthman kwenye shida. Tumekwisha kuandika tayari kuhusu watu wanaohusika na kundi la kwanza. Na kuhusu hili kundi la pili tutazungumza kuhusu wao katika sura inayoitwa: “Njama Kuu” kwa sababu watu hawa wanahusika kwa karibu sana na vitendo alivyotendewa Ali na udanganyifu na hila ambazo zilimpata. 50

I ngawa inasemekana kwamba Ali alijaribu kumuokoa Uthman na akawatuma wanawe wawili, Hasan na Husein kwenda kulinda lango la nyumba yake, lakini hali halisi ni kwamba Ali hakuwepo Madina wakati Uthman alipouawa na yale madai yanayofanywa juu ya hili sio sahihi. Akikanusha Hadith nyingine kama hii, Allamah Haithami anasema: “Ni dhahiri kabisa kwamba riwaya hii sio sahihi. Ali alikuwa hayupo Madina, imma wakati wa kuzingirwa nyumba ya Uthman au wakati pale alipouliwa. (Majma-ul-Zawaid, Juz. 7, uk. 63). thman mwenyewe alikuwa amemtaka Ali kwenda kwenye shamba lake huko Yanb’a ili watu wasi je waU kampendekeza jina lake kwa ajili ya ukhalifa. Maombi kama hayo yalikuwa tayari yamekwisha kufanyika mari nyingi kama alivyotaja Ali kwenye Nahjul-Balaghah hivi: “Uthman ananifanya mimi kama ngamia ambaye amabeba maji kwenda na kurudi. Wakati mwingine ananiambia mimi niende Yanb’a. Ninapokwenda huko yeye huniita nirudi kuja kutatua baadhi ya matatizo. Na ninapokuwa nimemuondolea uzito wake huo, yeye tena hunitaka nirudi tena Yanb’a.” 321

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 321

9/4/2017 3:48:00 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Maelezo Ya Makosa Kuna baadhi ya waandishi humu duniani ambao huwa hawajali juu ya imma mambo ya kweli ya kihistoria au juu ya hali ya mazingira ya maisha. Wao wanataja sababu za ajabu juu ya maasi ambayo wale watu walioonewa wameyafanya dhidi ya Uthman na wanasisitiza kwamba matukio ya wakati ule yalikuwa ni matokeo ya utashi na matakwa ya mtu maalum ambaye alitembelea nchi zote za Kiislam na akawachochea watu kuasi dhidi ya Uthman na serikali yake. Maelezo yanayotolewa na waandishi hawa bila shaka yatakufanya ucheke, kwa sababu lengo lao pekee ni kwamba wale watu ambao kwa kweli walihusika na mauaji ya Uthman wasiweze kulaumiwa au kukosolewa, vinginevyo watu wataanza kutilia shaka imani za waandishi hawa. Waandishi hawa ni kama wale watu wanaojaribu kugeuza mwelekeo wa maji yanayodondoka kutoka juu. Wanawachukulia wasomaji wao kuwa mapunguani na wajinga. Mmoja wa waandishi hawa ni Sa’id al-Afghani, yule mwandishi wa kitabu “Ayesha wa al-Siyasah.” Amejaribu kwa uwezo wake wote kuwafanya wasomaji wake waamini kwamba yale matukio yaliyotokea kwenye nchi ya Kiislamu na kusababisha kwenye kuuawa kwa Uthman na baada ya hapo, yalikuwa ni kwa kutokana na shughuli za mtu mmoja aliyeitwa Abdullah bin Saba.51 51

atika kitabu kiitwacho “Abdullah bin Saba” (ndani ya juzuu tatu) kilichoandikwa hivi karibuni na mwanaK chuoni Aalimu aitwaye Allamah Murtadha al-Askari (ambacho kwa bahati nzuri kimetafsiriwa katika lugha za Ki-Urdu, Kiingereza, Kiajemi na Kiswahili vile vile) uadilifu umetendeka juu ya maudhui hiyo kwa namna yenye ustadi wa kuridhisha kabisa na pazia limeondolewa kutoka kwenye sura yenye utata ya mtu huyu wa kubuniwa, ambaye amekuwa ndio shujaa halisi wa zile simulizi za kubuni zilizoandikwa dhidi ya Shi’a katika kitambo cha karne kumi na tatu zilizopita. atika kitabu hicho, Allamah al-Askari, kama mtafiti halisi ametwaa njia sahihi kwa ajili ya kuonyesha sura K halisi ya mtu huyu wa kubuniwa tu. Alianza uchunguzi wake kwa kuzipitia nyaraka mashuhuri kama vile Kamil ya Ibn Athir, Tarikh ya ibn Khaldun, Tarikh Tabari, Tarikh Ibn Kathir, Ibn Asakir na Dhahabi na amejitahidi kukitafuta chanzo cha simulizi (ngano) hii. Baada ya utafiti kamili na uchunguzi, yeye amegundua kwamba sasa ni zaidi ya miaka elfu moja kwamba wanahistoria wameendelea kunukuu ngano ya Abdullah bin Saba na shughuli zake kutoka kwa mtu anayeitwa Saif bin Umar. Wengi wao kama Tabari amenukuu moja kwa moja kutoka kwa Saif, na waandishi wengine wa hivi karibuni, waliopita na wa sasa wameinukuu ngano hii kutoka kwake Tabari na wanahitoria wengine waliotajwa hapo juu. Baada ya hapo alielekeza utafiti wake kwenye utambulisho wa Saif bin Umar; kwa sababu mazungumzo yote kuhusu Abdullah bin Saba yanaanzia kwake yeye. Kwa matokeo ya utafiti huu, amemtambulisha Saif bin Umar kwetu sisi katika maelezo yafuatayo kwa kuzingatia ushahidi ulioandikwa wazi. eye alikuwa ni mtu aliyefariki baada ya mwaka wa 170 A.H., na akakabidhi vitabu viwili vilivyoitwa “alY Futuh wal-Raddah” na “al-Jamal-wa-Masiru Ayesha wa Ali.” chunguzi wa taarifa kamili juu Saif ndani ya vitabu, na vile vya wasifu na wa nini kilichokuwa kimeandikwa U kumhusu yeye na wanachuoni kutoka karne ya tatu hadi ya kumi Hijiria, unaonyesha kwamba alikuwa ni mdanganyifu, mwandishi wa hekaya za kubuni na mtengeneza hadithi za bandia ambaye wakati mwingine alikuwa 322

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 322

9/4/2017 3:48:00 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Madai haya na shutuma hizi humuongozea mtu kwenye kuhitimisha kwamba serikali ya Uthman na waziri wake Marwan ilikuwa bora sana, na Bani Umayyah na magavana wao na maafisa wengineo walikuwa viongozi mashuhuri wa undugu wa kibinadamu na haki za kijamii katika Arabia, lakini kwa bahati mbaya, mtu mmoja aliyeitwa Abdullah ibn Sab’a aliufanya uwezo wao wote na matendo yao mazuri kuja kubatilika. Alifanya ziara kwenye wilaya na majimbo yote, na akawachochea watu kuasi dhidi ya magavana na maafisa ambao walikuwa wachamungu sana, na wanamageuzi wakubwa vilevile. Bila ya mtu huyu (Abdullah ibn Sab’a) watu wangeweza kuishi maisha ya furaha na amani kwa msaada wa ukarimu wa Marwan, uadilifu wa Walid na uvumilivu wa Mu’awiyah. Madai kama hayo yanakuwa ni sawa na kupotosha ukweli wa mambo, dhulma kwa watu na jaribio lisilo sahihi la kuunga mkono maoni fulani. Yanakuwa sawa pia na kuwapoteza watu kuhusiana na ukweli wa msingi ambao historia imeegama juu yake, kwa sababu lengo la jaribio kama hilo lisiloleta manufaa yoyote ni kwamba wajibu wa matukio ya wakati, kwa usahihi zaidi wa nyakati nyingi, uwekwe juu ya mabega ya mtu mmoja ambaye alizurura kutoka eneo hadi eneo na watu wa maeneo yote hayo wakaasi dhidi ya serikali kutokana na propaganda zake potovu na sio kutokana na sababu nyingine yoyote ile. Na kuhusu sera za serikali, na hali zake za kusikitikia za mfumo wa kiuchumi na kijamii, na ukaidi wa wale walioshirikiana na serikali, matumizi mabaya ya fedha za akiitwa kama “Saif bin Umar Zindiq” (mkanamungu au mwenye kuabudu miungu mingi) vilevile. chunguzi wa vitabu vyake viwili pia unathibitisha ule ukweli kwamba alikuwa na sifa hizo kweli, kwa sababu U nyingi ya simulizi zake hazioani na nyaraka za kihistoria na zina mandhari kamili ya habari za kubuniwa. shahidi wote wa maandishi uliokusanywa kwa sababu hii unaonyesha kwamba Saif bin Umar aliunda idadi U ya watu wa kubuni na pia haiwezekani kwamba aliagizwa kufanya hivyo. Mmoja wa watu hawa wa bandia ni huyu Abdullah ibn Sab’a hasa. Kwa mwenendo huu tunaona kwa masikitiko makubwa sana kwamba mtu huyu (Abdullah ibn Sab’a) ambaye alikuwa, kwa zaidi ya miaka elfu moja, ametumika kama kisingizio kwa propaganda dhidi ya Shi’a na ametambulishwa kama Myahudi na mwanzilishi wa Uislamu wa Ki-Shi’a, hakuwa kwa hakika ameishi kihalisia, na alikuwa ni kiumbe cha ubunifu wa akili ya mdanganyifu na mtu mwenye fikra za kinjozi aliyeitwa Saif bin Umar at-Tamimi! unazialika dhamiri njema na ongofu za Waislamu wenye hekima kwa ajili ya kutoa uamuzi na tunauliza: Hivi T inastahiki kweli kwamba dini ambayo mzizi wake umenyweshwa na vyanzo halisi kabisa vya mfano wa kuvutia, yaani Familia ya Bwana Mtume inaweza kupatwa na uzushi kama huu na maneno machafu yaweze kupita dhidi yao kwa idhini ya hekaya za uongo bila utafiti wowote au uchunguzi? Je, huu ndio uadilifu ambao Qur’ani Tukufu inatutaka sisi tuufuate? Na je, hii ndio maana ya amri tuliyopewa kuhusiana na ukubalikaji wa kauli? “Ennyi mlioamini! Kama fasiki akikujieni na khabari yoyote, basi ichunguzeni, msije mkawadhuru watu kwa ujahili na mkawa wenye kujuta juu ya yale mliyoyatenda.” (al-Hujaraat; 49: 6) aelezo zaidi juu maudhui hii yanaweza kuwa ni kurejea kwenye kazi bora ya kitafiti ya Allamah Murtadha M al-Askari, “Abdullah ibn Sab’a.” (Kimetafsiriwa na kupatikana kwa lugha ya Kiswahili pia) 323

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 323

9/4/2017 3:48:00 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

umma na utumiaji wa mbinu za kidikteta uliofanywa na Bani Umayyah, na utendewaji maovu wa watu wanaoheshimika kama Abu Dhar na Ammar Yasir, mwandishi hayawekei umuhimu wowote na hafikiri kwamba mambo haya ndio yalikuwa chanzo cha uasi wa jumla wa watu. Kulingana na yeye ghasia zote dhidi ya Uthman zilikuwa ni kwa sababu ya vitendo vya Abdullah ibn Sab’a ambaye aliwazuia Waislamu kutokana na kuwatii viongozi wa kidini wa Kiislamu na akasababisha fujo na mifarakano. Ni akili ya hatari kiasi gani kwamba matukio muhimu ambayo yalikuwa ya mfululizo na yenye kuhusiana, moja na jingine, na yalikuwa na uelekeo mkubwa juu ya jamii na mfumo wa kiuchumi na kijamii wa wakati ule yaweze kuelezewa kwa kusema kwamba sababu ya msingi ya mambo yote haya ilikuwa ni njama ya mtu mmoja, ambaye kwa mujibu wa Sa’id Afghan, alizurura toka mji hadi mji na akapandikiza mbegu za mfarakano na fitna ndani ya jamii safi. Na kwa jamii safi ni dhahiri ana maana ya ile jamii ambayo ilikuwa ikiongozwa na Marwan ibn Hakam. Inastahili kuangaliwa kwamba Sa’id Afghani anaweka umuhimu mkubwa sana juu ya Abdullah ibn Sab’a au Ibn al-Sawda katika kitabu chake kilichotajwa hapo, juu na anamnyanyua daraja Mu’awiyah bila kujijua na kumshusha hadhi Abu Dhar, ingawa Mu’awiyah alikuwa ni Mu’awiyah na Abu Dhar alikuwa ni Abu Dhar. Afghani anaandika hivi: “Abdullah ibn Sab’a alizizungukia nchi zote za Kiislamu na akatembelea kila mahali. Alianza shughuli zake za kiovu ndani ya Hijazi na halafu akaenda Syria. Wakati huo Syria ilikuwa ikitawaliwa na mtu mwenye uzoefu na anayeona mbali anayeitwa Mu’awiyah ibn Abu Sufyan, ambaye aliihisi hatari mara moja na akamfukuza kutoka hapo. Hata hivyo, fitna zake ziliacha kiasi cha athari juu yake. Ibn Sab’a akaichambua hali hiyo na akapandikiza mbegu za fitna. Alimshawishi sahaba maarufu mmoja wa Mtume kuasi dhidi ya Mu’awiyah. Abu Dhar alikuwa ni mtu ambaye maneno yake yaliaminiwa na watu wa Syria. Mu’awiyah, ambaye alikuwa ni mtu mvumilivu na mwanadiplomasia vilevile, alivurugikiwa sana. Yeye kwa hiyo, akamuomba Uthman kumuondoa mtu huyo kutoka Syria, yule sahaba mashuhuri alikuwa ni Abu Dhar ambaye habari zake zinafahamika sana.” (Ayesha wa al-Siyasah). 324

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 324

9/4/2017 3:48:00 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Kile ambacho mwandishi huyu anachoelekea kumaanisha kukielezea kinaweza kikafupishwa hivi: Wakati wa ukhalifa wa Uthman, watu wa majimbo mbalimbali walikuwa wakiishi maisha ya furaha na neema sana. Jimbo la Syria, lenyewe hasa, wakati huo lilikuwa likitawaliwa na mtu mwangalifu sana na mwenye uzoefu aitwaye Mu’awiyah. Na kuhusu yule mwanamageuzi mashuhuri, Abu Dhar, alikuwa mtu duni na angeweza kubakia hivyo kama Abdullah ibn Sab’a asingeonana naye na kumuamsha. Na pale alipomwamsha, alifanya hivyo kumfanya asababishe fitna, kwa sababu, kwa mujibu wa mwandishi, yeye (Abdullah ibn Sab’a) alikuwa ndiye chanzo cha matatizo yote na lengo lake la kuzizungukia nchi za Kiislamu lilikuwa ni kuzusha fitna. Matokeo yalikuwa kwamba Abu Dhar alifanya kile Abdullah ibn Sab’a alichokitaka, yaani, alianzisha fitna, akawapotosha watu na akawafanya waasi dhidi ya viongozi. Kulingana na mwandishi huyu tuliyemtaja, vitendo vya Abu Dhar vilikuwa vya hatari kwa Waarabu, Uislamu na historia, kwa sababu aliwachochea masikini dhidi ya matajiri. Kwa sababu hii hasa Mu’awiyah alichoka naye na akaonyesha huruma kwa wale Waislamu waliosilimu karibuni na pia huruma kwa historia kwa kumfukuza Abu Dhar kutoka Syria. Kama ilivyo wazi, madhumuni ya Sa’id Afghani yananikumbusha moja ya mantiki za wale watawala ambao wanawatangaza wapenda haki wote kuwa ni waasi wa waenezaji wa fitna. Hivi sio jambo la kuchekesha kwamba; wakati ambapo wanahistoria wa zamani waweze kutambua sababu za ghasia hizo, wale wanahistoria wa kisasa wasiwe na uwezo wa kuzijua, ingawaje vyanzo vya habari vya hao wa zamani ni vikubwa mno. Mwandishi wa kitabu “Ayesha wa al-Siyasah” analihusisha lile vuguvugu la kimapinduzi dhidi ya Uthman na shughuli za Abdullah ibn Sab’a, ambapo Tabari na wanahistoria wengine wa kipindi cha mwanzoni kabisa na wale wa baadae yake wanaelezea matukio hayo kwa usahihi na wanatoa sababu zao ambazo zinaridhisha kabisa. Wakati akiorodhesha sababu na harakati au vuguvugu hilo Tabari anasema: “Wale watu ambao hawakupata fursa ya kutangulia katika kuukubali Uislamu, wala hawakuwa na cheo chochote katika Uislamu, hawakuweza kuwa sawa na wale ambao walijiunga na Uislamu katika hatua zake za mwanzoni kabisa na wakapata hadhi kubwa na umuhimu. 325

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 325

9/4/2017 3:48:00 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Hawa Waislamu wa mwanzoni kabisa waligundua kasoro katika upewaji wa mazawadi makubwa na waliuchukulia kama ni dhulma, kwa vile mafungu yao ya mgao wakati wote yalikuwa ni madogo sana. Wakati Waislamu wapya au Waarabu mabedui au watumwa walioachwa huru walipokutana nao (hao Waislamu wa mwanzoni) wao walivutiwa sana na yale waliyoyasema. Matokeo yakawa kwamba ile idadi ya wapinzani wa Uthman iliendelea kuongezeka. Kwa kiasi kwamba wale waliokuwa wakimpinga Uthman wakawa wengi sana kwa idadi kuliko wale waliokuwa wakimfurahia. Matokeo yakawa kwamba ghasia zikawepo. Inashangaza kwamba waandishi wengine wa siku hizi pia wamefanya kosa hilohilo. Miongoni mwa wengine alikuwa ni Ahmad Amin, mwandishi wa kitabu “Fajr al-Islam.” Yeye anafikiri kwamba Abu Dhar alikuwa bwege aliyelaghaiwa na Abudullah ibn Sab’a kwenye kuamini mawazo ya ukomunist (Mazdakite) ili kwamba aweze kuthibitika kuwa mwenye kufaa kwa ajili ya kuharibu hali ya hewa ya miji mbalimbali. Na jambo la kushangaza zaidi ni ule ukweli kwamba ili kuthibitisha kwamba Abu Dhar aliathiriwa na mawazo ya Mazdakite, yeye ametaja maneno yake (Abu Dhar) ambayo yamenukuliwa na Tabari. Abu Dhar anasimuliwa kuwahi kusema wakati akiwahutubia watu wa Damascus kwamba: “Enyi watu matajiri! Kuweni na huruma juu ya masikini. Wale wanaohodhi dhahabu na fedha wabashirie adhabu ifedheheshayo.” (Fajr al-Islam, uk. 110). Ahmad Amin anaweza hasa akaulizwa iwapo kufanywa huruma na matajirI juu ya watu masikini ni nadharia ya Mazdakite tu na kwamba sio agizo halisi la Kiislamu, na iwapo kauli ya Abu Dhar: “Enyi watu matajiri! Kuweni na huruma juu ya masikini” haihusiani kwa karibu kabisa na Aya ya Qur’ani: “Wale wanaohodhi dhahabu na fedha na wakawa hawatumii katika njia ya Mwenyezi Mungu, wabashirie adhabu iumizayo.” Katika mahali pengine ndani ya ‘Farj al-Islam’ Ahmad Amin akimfanya Abdullah ibn Sab’a kuwa ndio sababu ya msingi wa fitna anasema: “Mtu huyu alimshawishi Abu Dhar kuhubiri ukomunist, na alikuwa ndiye kiongozi wa maasi ya wale wapiganaji waasi ambao walitoka sehemu mbalimbali kuja kumshambulia Uthman. Alikuwa ni yeye aliyejitahidi kupotosha imani ya Waislamu. Aliitembelea Hijazi, Basra, Kufa, Syria na Misri kwa mapana sana. Hivyo inawezekana kwamba ameweza 326

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 326

9/4/2017 3:48:01 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

kuwazoesha mawazo ya Mazdakite kutoka kwa wa-Mazdakite wa Iraqi au Yemen na Abu Dhar pia anaweza akawa ameyapenda mawazo haya na kuyatwaa.” Ni bahati mbaya sana kwamba mwandishi wa ‘Farj al-Islam’ hatafakari juu ya ni jambo gani jipya lilitokea katika imani ya Kiislamu ya Abu Dhar. Je, Uislamu wenyewe hautangazi kwamba masikini wanafaidi haki fulani juu ya matajiri; na kwamba Waislamu wote ni sawa na je, Qur’ani haisemi kwamba vipaji vya nyuso, mbavu na migongo ya wale wanaohodhi dhahabu na fedha itabanikwa kwenye moto wa Jahannam kwa dhahabu na fedha hiyo hiyo? Basi ni mawazo gani hayo Mazdakite ambayo Abu Dhar alianza kuyaamini? Ukweli ni kwamba Abu Dhar alikuwa anapigana dhidi ya wale watu ambao Uislamu wenyewe umepigana nao na kuwaahidi Moto wa Jahannam. Swali hili pia linajitokeza la iwapo Abu Dhar, ambaye alikuwa sahaba mashuhuri wa Mtume, wa mbele sana miongoni mwa Shi’a wa Ali, na mtu wa tano kusilimu, yeye mwenyewe alikuwa hajui kwamba Waislamu wote walikuwa na haki ya kugawana utajiri wa taifa, na sio kwamba watu wachache tu waihodhi mali hiyo. Na je, hakuweza kutambua kwamba katika ukhalifa wa Uthman mali ya umma ilikuwa imekamatwa na watu wachache na watu wengine walikuwa wanafanyiwa dhulma na uonevu na kwa vile mambo haya yanapingana na mafundisho ya Uislamu, ilikuwa ni wajibu wa Waislamu kuasi dhidi ya Uthman? Na halafu swali ni kwamba: Hivi Abu Dhar alikuwa punguani (simpleton) kiasi hicho kwamba ilimbidi amtegemee Abdullah ibn Sab’a amuelezee yeye kwamba Uthman alikuwa anatumia upendeleo wa kindugu na kufuata njia za Kaisari na Kisra? Hivi Abu Dhar pamoja na watu wote walikuja kujua pale tu Abdullah ibn Sab’a alipowaambia kwamba watawala wamepotoka na watu walikuwa wamenyimwa haki zao na matokeo yake ndipo Abu Dhar na wengineo wakaonyesha kuchukia kwao? Waandishi hawa wamemuelewa Abdullah ibn Sab’a na kanuni za imani za kiMasdakite lakini hawakumuelewa Abu Dhar na Uislamu! Wameliona lile vuguvugu la kimaasi la Abdullah ibn Sab’a na kuchochea kwake watu kuasi dhidi ya khalifa kuwa la kuogopesha sana. Lakini hawakuyaona yale matendo ya Uthman kuwa ya kuogopesha, ambayo yaliwaudhi Waislamu – matendo ambayo yanayaudhi mataifa yote katika zama zote, yaani, upendeleo wa ndugu, ufadhili na kufuata sera ya ubaguzi. Watafiti wanakhitlafiana kuhusu sababu ambazo zimepelekea kuuawa kwa Uthman. Tukio maarufu sana kuhusu ambalo kuna tofauti ya maoni kati yao ni ile barua 327

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 327

9/4/2017 3:48:01 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

iliyoandikwa kutoka Madina kwenda kwa Ibn Abi Sarah, gavana wa Misri, ambaye alielekezwa kumuua yule gavana mteule – Muhammad ibn Abu Bakr katika kuwasili kwake hapo Misri. Tukio hili limetajwa kwa kirefu hapo kabla. Na kuhusu wale ambao hawalichukulii kwamba ni tukio la kweli, inajitokeza kuwa muhimu kutaja maoni ya mmoja wao, kwa jina Dr. Taha Husein, kwa sababu amepata hadhi kubwa kama mwanachuoni mtafiti wa historia ya Uislamu na dunia ya Kiarabu. Yeye anasema hivi katika juzuu ya kwanza (inayoitwa Uthman) ya kitabu chake, “Al-Fitnatul-Kubra”: “Maelezo ya barua hiyo yanasimuliwa hapa. Wasimulizi wa hadith wanasema kwamba wakati watu wa Misri walipokuwa wakirejea, baada ya kuwa wameridhishwa na ahadi za Uthman, waliweza kumkamata humo njiani mtumwa ambaye alikuwa amebeba barua kwenda kwa Ibn Abi Sarah. Nadhani hadithi hii imebuniwa. Ushahidi mkubwa kabisa juu ya hili ni kwamba masahaba wa Mtume walibishana na wale Wamisri juu ya hoja hii na wakawauliza: “Wakati ninyi na watu wa Kufa na vilevile wale wa Basra mlikuwa mkienda kwenye njia zenu husika, ni vipi watu wa Kufa na Basra wakaja wakajua kwamba ninyi mmegundua barua kama hiyo? Kwa hili Wamisri hao hawakutoa jibu lolote na wakasema: “Lolote mtakalofikiri, sisi hatumhitaji mtu huyu (Uthman). Kwa hakika sisi tutamuondoa kwenye cheo hicho na kuteua khalifa mpya kuchukua mahali pake.” “Haiwezi kuaminika kwamba Uthman angeweza kuwadanganya Waislamu kwa kumuuzulu gavana wa Misri kwa kumbadilisha na mwingine; na halafu aandike barua ya siri kwa gavana aliyekuweko kuwaua Waislamu hao katika kuwasili kwao.” “Vile vile haiwezi kuaminika kwamba Marwan angeweza kuthubutu kuandika barua akielekea kumaanisha kwamba inatoka kwa Uthman na akagandisha muhuri wake juu yake na kisha aitume kupitia kwa mtumwa wake akiwa amepanda juu ya ngamia.” “Suala lenyewe kwa hiyo ni rahisi sana. Uthman anaweza kuwa ameahidi kupokea madai ya waasi wa Kufa, Basra na Misri na wakamuamini. Baadae wakaja wakajua kwamba hakuwa ametimiza ahadi zake. Wao, kwa hiyo, wakakasirika na wakarudi kwa hasira kubwa kuja kulimaliza suala hilo na wasirudi majumbani kwao mpaka watakapokuwa wamemuondoa Uthman kwenye cheo chake au kumuua na wawe wamekwishafanya mipango mingine juu ya ukhalifa. Wakati walipowasili Madina walikuta kwamba masahaba wa Mtume walikuwa tayari kupigana nao. Wao hata hivyo wakajizuia kupigana na masahaba na wakarudi 328

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 328

9/4/2017 3:48:01 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

kutoka Madina kwa udanganyifu. Pale walipokuja kupata kuwa na uhakika kwamba masahaba wameweka silaha zao pembeni na kwamba walikuwa wakipumzika kwenye nyumba zao, wao (waasi) walirudi na wakachukua udhibiti wa Madina bila ya umwagaji damu.” (Al-Fitnatul-Kubra, Juz. 1, ‘Uthman’). Ni wakati ambapo kwamba yale matukio ya kihistoria ambayo kwamba waandishi wanatofautiana yanastahili kutiliwa shaka, hususan yale matukio ambayo yanahudumia maslahi ya kimadhehebu au yanaunga mkono imani moja yoyote ile. Shaka hii haiwezi kuondolewa isipokuwa kwamba historia itoe uthibitisho wenye kuamua au inafanyiwa uchambuzi na kutafsiriwa katika njia ambayo yenyewe inakuwa kama uthibitisho wa kutosheleza. Tukio la barua linalojadiliwa bila shaka ni ambalo kwamba ni lazima Dr. Taha Husein atilie shaka usahihi wake; na sababu za kulifanya kwake lenye mashaka zinaweza kukubalika, alimuradi tu kwamba mambo fulani ambayo yanazuia njia ya kukubalika kwa sababu hizo kama zenye kutosheleza zinakuwa hazipo. Dr. Taha Husein anasema kwamba pale masahaba wa Mtume walipowauliza watu wa Kufa na Basra kuwa ni vipi walivyokuja kujua kwamba watu wa Misri walikuwa wamepata barua kama hiyo ambapo kila kundi lilikuwa likienda njia yake lenyewe, hawakuweza kutoa jibu. Hili, hata hivyo, sio jambo ambalo linaweza kumfanya mtu akatae hilo tukio la barua moja kwa moja. Kulingana na simulizi na vilevile ule mfuatano wa matukio, ni ukweli uliothubutu kwamba Uthman alikuwa amemteua Muhammad ibn Abu Bakr kama gavana wa Misri, na alikuwa pia ametuma kundi la Muhajir na Ansari pamoja naye. Muhammad pamoja na masahaba zake walikuwa na imani kamilifu juu ya barua hiyo ambayo Uthman alikuwa amewapa, na wao kwa hiyo, wakaondoka Madina kuelekea Misri. Hata hivyo, kabla ya kufika waendako wakarudi Madina. Sasa swali linakuja la kwa nini watu wale walirudi wakiwa wamekasirika sana? Na kwa nini walingojea fursa ya kuingia mjini hapo bila ya umwagaji damu? Sio historia wala wale wanaokataa kuwepo kwa barua yoyote ya namna hiyo wanaotaja sababu yoyote ya kurejea kwa Muhammad na masahaba zake hadi Madina. Ni sababu moja tu inayotajwa na hiyo ni ile barua iliyoko kwenye mjadala. Zaidi ya hayo, wale Muhajir na Ansari ambao walitumwa pamoja na Muhammad kwenda Misri kuchunguza vitendo vya Ibn Abi Sarah, na kuifanya hali ya huko kuwa yenye kufaa kwa ajili ya serikali ya Muhammad, walikuwa wote ni watiifu kwa Uth329

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 329

9/4/2017 3:48:01 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

man na baadhi yao, kama sio wote, walitumikia nafasi ya waunga mkono wa Uthman na washirika wake. Ni vipi mtu anaweza akadhania kwamba watu hawa, ambao walikuwa ndio watakia mema wa Uthman, wanaweza wakaghushi barua iliyotiwa saini na yeye Uthman? Na kama itasemekana kwamba barua hiyo haikughushiwa na Muhajir na Ansari hao bali ilisainiwa na mtu mwingine, basi swali linajitokeza la ni vipi watu hawa waliikubali barua hiyo kwamba ilikuwa imeandikwa na Uthman. Na kama itasemekana kwamba hakuna barua kama hiyo iliyowahi kupatikana, basi ni lazima pia ikubalike kwamba Muhammad Ibn Abu Bakr na masahaba zake hawakurudi Madina kutokana na barua yoyote ile, na kwamba hekaya za barua hiyo zilibuniwa na maadui wa Uthman baada ya kuuliwa kwake. Katika hali hiyo, swali linajitokeza la kwa nini Dr. Taha Husein na wanahistoria wengine na wasimuliaji wanakubali kuwepo kwa barua kama hiyo; na kusema kwamba masahaba wa Mtume walibishana na waasi hao kwa sababu ya barua hii, na wakauliza kuwa ni vipi watu wa Kufa na Basra walivyokuja kujua kuhusu watu hao wa Misri kuikuta barua, wakati kila kundi lilikuwa likienda na njia yake tofauti? Mazingira ya kuwepo kwa barua hiyo hayawezi kukanushwa. Swali, kwa hiyo, linabakia la ni nani aliyeandika barua hiyo na akapanga mpango wa kumuua Muhammad ibn Abu Bakr, wale Muhajir na Ansari waliofuatana naye, na wapinzani wa Ibn Abi Sarah? Kama ilivyoelezwa hapo juu, Dr. Taha Husein haamini kwamba Uthman angeweza kuandika barua kama hiyo na kuwadanganya Waislamu. Maoni haya ya Dr. Taha Husein ni ya kweli. Uthman asingeweza kufanya udanganyifu kama huo. Hata hivyo, ni ukweli kwamba Uthman alikuwa wa tabia ya upole sana. Upole huu hasa mara kwa mara ulimfanya atii matakwa ya Bani Umayyah; na ulaghai na hila za Bani Umayyah vinajulikana vizuri sana. Tunajifunza kutoka kwenye historia ya maisha ya Uthman kwamba katika wakati fulani yeye alitoa maagizo, na baadae akayafuta, akaonyesha kusikitika kwa kutoa maagizo hayo, na akaanza kulia. Vitendo vilivyotendwa na Uthman kwa Abu Dhar ni mfano wa wazi wa namna ambayo Bani Umayyah walimshawishi kufanya mambo yanayopingana na haki na dhamira nzuri na kisha akalazimika kuonyesha masikitiko. Alimgandamiza Abu Dhar kwenye fedheha kubwa na mateso, na halafu akafanya kila aliloweza kumsuluhisha. Mara tu baadae, hata hivyo, alikuja kumkasirikia Abu Dhar tena na akamhamisha, na matokeo yake yakawa kwamba yeye na watu wa familia yake wakafariki kwa njaa. 330

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 330

9/4/2017 3:48:01 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Tukio jingine kama hilo lilikuwa ni ile fedheha ambayo Uthman alimfanyia sahaba mashuhuri wa Mtume aitwaye Abdullah ibn Mas’ud. Kwa kutekeleza maagizo yake, mtu mmoja akamnyanyua Abdullah na akamtupa chini mchangani na matokeo yake mifupa yake ikavunjika. Akasimamisha pia malipo ya ujira wake. Mara tu baadae, hata hivyo, alijisikia aibu na akaomba msamaha kwa Abdullah. Wasifu wa Uthman pia unaonyesha kwamba alimtaka Ali kuondoka Madina na kisha akamtumia wajumbe kumuomba arudi. Hili lilitokea kwa mara nyingi. Kiasi kwamba ilimlazimu Ali aseme: “Uthman anataka kunifanya mimi kama ngamia ambaye anabeba maji ili kwamba niweze kuendelea kuja na kuondoka. Alinitaka mimi niondoke Madina na kisha akaniita nirudi. Na sasa ananitaka niondoke tena hapa niende zangu.” Uthman anatoa kibali cha jumla kwa Abdullah ibn Abi Sarah cha kuwatendea watu wa Misri kiasi anavyotaka. Ibn Abi Sarah anawafanyia watu wa Misri uonevu mkali. Wamisri hao wanakuja Madina na kulalamika kwa Uthman. Uthman anawahutubia. Anawatukuza wao, anaonyesha masikitiko, na anatubia kwa ajili ya matendo yaliyopita. Kwa kiasi kikubwa kwamba anaanza kulia na anaahidi kwamba atambadilisha Ibn Abi Sarah kwa gavana wa chaguo lao. Halafu anarudi kwenye kasiri lake ambako anakutana na Marwan. Huyu Marwan anamfanya ayatafune maneno yake na hatimizi ahadi yoyote aliyoitoa kwa watu wa Misri! Kwa Uthman lile suala la Abu Dhar na Abdullah ibn Mas’ud halikuwa rahisi kama lile la Muhammad Ibn Abu Bakr au la watu wa Misri. Maonyo yaliyotolewa na wote hao kwa ndugu zake yalikuwa yanauma sana kuliko mashambulizi ya watu wa Misri ya wakati mmoja katika mji mkuu wa Madina na wakati mmoja juu ya gavana wa Misri. Wakati alipoweza kuwa na tabia mbaya kwa Abu Dhar na Abdullah ibn Mas’ud kwa kukubaliana na matakwa ya ndugu zake mwenyewe, Muhammad na wale watu wa Misri walikuwa ni dhahiri hawana umuhimu mbele ya macho yake. Zaidi ya hayo, ni ukweli uliothibitika kwamba Muhammad bin Abu Bakr alikuwa ni mpinzani wa siasa za Uthman ambapo Ibn Abi Sarah alikuwa ni mmoja wa wasiri wake na alipenda sana sera zake na taratibu za serikali yake. Kwa kuzingatia mambo haya inawezekana kwamba Uthman aliujutia uteuzi wa Muhammad bin Abu Bakr badala ya Ibn Abi Sarah, na vile vile zile ahadi alizoziwekeana na watu wa Misri, na anaweza kuwa aliamua kwenda kinyume na maneno yake kwa shinikizo la Marwan na Bani Umayyah wengine.

331

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 331

9/4/2017 3:48:01 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Kwa kulitaja lile tukio la barua hatuna maana ya kuwaunga mkono wale wanaodai kwamba barua hiyo iliandikwa na Uthman mwenyewe. Tunachomaanisha kukisema ni kwamba Uthman alikuwa na tabia ya upole kiasi kwamba Marwan na kile kizazi cha Hakam; ambao wote walikuwa katika uongozi wa Uthman, wangeweza kumshawishi yeye na kuweza kumdanganya kwa urahisi sana ili kufanikisha malengo yao. Kwa hiyo kama haiwezi kukubaliwa kwamba Uthman angeweza kuwadanganya Waislamu, basi inaweza kabisa hasa kukubalika kwamba Marwan angeweza kuzidisha shinikizo juu ya Uthman kufanya mambo yafanyike kulingana na matakwa yake. Sasa tunamgeukia Dr. Taha Husein kwa mara nyingine tena. Yeye anafikiri kwamba, kwa sababu mbili ambazo tumezitaja kabla, hadithi ya barua ni ya kubuni na haina msingi. Kisha anatoa sababu nyingine katika kuunga mkono madai yake ambayo kwa maoni yetu sisi, hayo ni dhaifu sana. Yeye anasema: “Sio jambo la busara na la kukubalika kwamba Marwan angeweza kujasiri kuandika barua kana kwamba imeandikwa na Uthman, akagandisha muhuri wake Uthman juu yake, na akaituma kupitia kwa mtumwa wake Uthman.” Tunasema katika kujibu kwamba haishangazi kwamba Marwan angeweza kuchukua hatua hiyo. Kinachotushangaza sisi ni kwamba Dr. Taha Husein anakichukulia kitendo cha Marwan kuwa nje ya mantiki. Analishikilia wazo hilo licha ya ukweli kwamba alikuwa ni Marwan huyo huyo ambaye alijiona yeye mwenyewe kuwa ni bwana na watu kuwa ni watumishi na watumwa wake, ambao angeweza kuwaruhusu kuishi au kuwaua kwa hiari yake mwenyewe. Sasa tungependa kuzungumzia juu ya maoni ya Dr. Taha Husein kwamba hadithi hizi haziko wazi. Ziko hadithi ambazo zinaeleza kwamba barua hiyo iliandikwa na Marwan na kwamba mpango wote mzima ulikuwa ni matokeo ya sera na mbinu zake za uongozi, kwa sababu yeye alikuwa ndiye mtawala halisi wa nchi za Kiislamu. Kuhusiana na hili, kuna umuhimu wa kuweka baadhi ya nukta katika mazingatio: Kwanza kabisa riwaya zote zinaungana kusema kwamba ule ujumbe ulioongozwa na Ali ulimsubiri Uthman. Uliwahusisha pamoja na Ammar, Talha, Zubeir na Sa’d ibn Waqas. Ali aliishika barua hiyo inayosemekana mkononi mwake. Alimchukua

332

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 332

9/4/2017 3:48:01 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

pia yule mtumwa na ngamia wake. Alifanya mazungumzo na Uthman kuhusu barua hiyo na halafu wale masahaba wakaja kujua kwamba barua hiyo ilikuwa imeandikwa na Marwan. Kisha wao walimtaka Uthman kumwita Marwan mbele yao ili waweze kumhoji. Uthman hakukubaliana nalo hili na masahaba hao wakaondoka zao wakiwa wamekasirika sana. Tumekwisha kuinukuu tayari riwaya hii kwa kirefu katika kurasa zilizotangulia. Pili, maoni ya Marwan kuhusu ukhalifa wa Uthman ni lazima pia yazingatiwe. Kuhusiana na hili, swali linajitokeza la iwapo mbele ya macho yake Uthman alikuwa ni khalifa kama Abu Bakr na Umar, au Bani Umayyah mmoja ambaye kupitia kwake Bani Umayyah wote walikuwa wapate tena madaraka na mamlaka ambayo yalikuwa yameharibiwa na Uislamu. Marwan alikuwa ni kielelezo kamili cha msimamo wa liwezekanalo kuwa, au ubahatishaji - (opportunism) wa Bani Umayyah. Kulingana na yeye, ukhalifa ulikuwa hauhusiani chochote na suala la kwamba Uthman alikuwa Quraishi, Muhajir, sahaba wa Mtume na mwenye kuamini juu ya utume wake. Bali yeye alimchukulia tu Uthman kuwa ni mmoja wa familia ya Umayyah. Kwa mujibu wa Marwan ukhalifa haukuwa kitu ambacho kilimaanisha serikali ya haki iliyoegemezwa kwenye kanuni ya ustawi wa jamii; na ambayo ilitegemewa kufuata Sunnah ya Mtume, na mwenendo wa wale makhalifa waliotangulia. Huo ulikuwa ni ufalme ambao uliponyoka kutoka kwenye mikono ya Abu Bakr na Umar, kwa sababu hawakuwachagua watoto wao kama warithi wao. Ilikuwa, hata hivyo, ni wajibu juu ya Uthman, ambaye alikuwa ni Bani Umayyah, asije kurudia kosa hili kiasi kwamba watu wataweza kudhania kwamba ukhalifa ni wa Bani Umayyah tu. Ilikuwa ni muhimu kwa Uthman kwa hiyo, awe na tabia juu ya watu kwa namna ile ile ambayo mfalme mwangalifu anayofanya kwa raia zake. Kama Uthman hakuwa na uwezo wa kutawala kwa namna hiyo, basi alikuwepo Marwan kumwongoza yeye. Maneno yaliyotamkwa na Marwan wakati akiwahutubia wale waasi, ambayo tuliyanakili hapo kabla, yanafafanua hali halisi ya fikra zake. Alikuwa amesema: “Kwa nini ninyi watu mmekusanyika hapa? Je, mnataka kutunyang’anya ufalme wetu?” Katika siku zile ukhalifa kwa kweli ulikuwa ni ufalme wa Marwan. Raia walikuwa hawana haki ya kunyanyua sauti zao na kudai mahitaji yao na uhuru wao kutoka kwa mfalme. Marwan alikuwa ndie mfalme atokanaye na ukoo wa Bani Umayyah na watu walikuwa ni watumwa wake.

333

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 333

9/4/2017 3:48:01 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Anawezaje mtu, ambaye alimuona khalifa na ukhalifa katika namna ambayo imeelezwa hapo juu na akatoa amri kulingana na fikra hiyo, atarajiwe kuvumilia kwamba watu waweze kuleta madai yao mbele ya serikali ya ndugu yake Uthman (ambayo ilikuwa kama ni serikali ya Marwan mwenyewe) na mfalme ayakubalie matakwa yao na kumuuzulu gavana ambaye alikuwa ni mtu muhimu kwenye utawala wa Bani Umayyah na kumteua mahala pake, Muhammad bin Abu Bakr ambaye alikuwa ni mpinzani wa serikali ya Uthman na mfuasi madhubuti wa Ali? Hatuwezi vile vile kupuuza ule ukweli kwamba ilikuwa ni wale waasi na masahaba wa Mtume ambao walikuwa wamekasirishwa na Uthman na wakawa wamependekeza jina la Muhammad bin Abu Bakr kuwa gavana wa Misri, na Marwan alikuwa hakutakiwa ushauri juu ya suala hili. Kama mambo yalivyokuwa, Marwan hakuweza kuvumilia kwamba mamlaka yake yakiukwe katika namna kama hii. Wakati maoni ya Marwan kuhusu ukhalifa yanajulikana, inakuwa ni dhahiri kwamba asingeweza kupuuza ule ukuu ambao ulikuwa umerudi kwa mara nyingine tena kwenye familia ya Bani Umayyah. Na wakati inapotambulikana kwamba badala ya kumchukulia Uthman kama khalifa wa Waislamu, Marwan alimfanya yeye kuwa ni mtu mmojawapo wa familia ya Bani Umayyah na mwakilishi wa serikali ya Bani Umayyah, basi isiwe ni vigumu kuelewa kwamba yeye angeweza kuwa mwenye kujiamini mno kuhusiana na Uthman. Hata hivyo, kama alikuwa mwenye kujiamini, alikuwa hivyo kutoka kwenye mtazamo wetu. Kwa kadiri Marwan mwenyewe alivyohusika, alikuwa akishughulika hivyo tu kwa ajili ya ulinzi wa haki zake. Kusema kwake Dr. Taha Husein kwamba Marwan asingeweza kuthubutu kuandika barua kwa jina la Uthman na kugandisha mhuri wake juu yake, hakuleti mantiki. Historia inatuambia sisi juu ya mifano mingi ambamo alionyesha kujiamini mno na ukakamavu. Kwa mfano, alimshauri Uthman kuwaua wale masahaba wa Mtume ambao walishutumu serikali yake (yaani, Ali, Ammar, Abu Dhar na kadhalika). Alipendekeza kwa Uthman kwamba asije akatoa nafasi kwa Abdullah ibn Mas’ud kuigeuza Syria dhidi yake kwani alikuwa tayari amewafanya watu wa Kufa kuwa maadui zake. Uthman bila ya kusita aliukubali ushauri wake. Alijaribu kuwazuia Ali, wanawe, Aqil na Abbas kumuaga Abu Dhar, na hakuacha kufanya hivyo mpaka pale Ali alipompiga mnyama wake wa kipando na alikuwa karibu ampige na yeye pia. 334

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 334

9/4/2017 3:48:01 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Alikuwa akijiamini sana katika matukio nyeti. Aliwatukana na kuwatoa nje ya mji wawakilishi wa vikundi vya ujumbe mbalimbali ambao walikuja kutoka sehemu nyinginezo. Uthman alisikia na kuona yale aliyoyafanya lakini hakusema lolote. Alishauri waziwazi kwa Uthman kumuua Ammar. Katika masuala mengine mengi Marwan alikuwa akijiamini kupita kiasi. Aliongea kifidhuli na Na’ila, mkewe Uthman, mbele ya mume wake, lakini Uthman alinyamaza kimya. Tukio hili lilikuwa kama ifuatavyo: Na’ila alikuwa ni mwanamke mwenye busara. Alizichukia sera za Marwan vibaya sana na mara kwa mara alimshauri mume wake kutenda mambo kwa ushauri wa Ali. Wakati Uthman alipotoa hotuba mbele ya wawakilishi wa Misri, Basra na Kufa, aliwaahidi kuridhia kwenye madai yao na halafu akarudi nyumbani kwake, ambako Marwan akamwambia: “Ewe Amiri wa waumini! Je, nisema kitu ama ninyamaze kimya.” Papo hapo mkewe Uthman akamwambia: “Ni bora unyamaze kimya. Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kwamba ninyi watu mtamuua Uthman na kuwafanya watoto wake kuwa mayatima. Haifai kwamba Uthman arudi nyuma na azikiuke ahadi alizozitoa.” Marwan akamwambia: “Wewe unahusika nini na mambo haya. Wallahi, baba yako, ambaye sasa amefariki, hakujua jinsi ya kuchukua udhu sawa sawa.” Ni dhahiri kwamba iwapo Marwan ameweza kuzungumza kwa namna ya kifidhuli kama hiyo kwa mke wa khalifa; mbele ya khalifa mwenyewe, mtu hawezi kushangaa juu ya kuwa kwake ameandika barua yenye jina la khalifa bila ya kujua kwake khalifa. Katika kipindi cha ukhalifa wa Uthman pia watu walijua jinsi Marwan alivyokosa adabu mbele yake, na jinsi gani alivyokuwa anajiamini katika kushughulika na khalifa. Watu hawakuficha kule kujiamini kwake bali walimkemea na pia wakamuonya Uthman dhidi yake. Hata hapo, Uthman hakupuuza ushauri uliofanywa na Marwan. Akiwakilisha maoni ya watu, Imam Ali alisema kumwambia Uthman: “Utamfurahia Marwan naye atakuwa ameridhika na wewe tu pale anapokunyang’anya imani yako na akili; na akakupeleka popote anapotaka, kama ngamia wa kufugwa na aliye mnyonge.” Kujiamini mno kwa Marwan vile vile kuliwatia moyo wengine kukosa adabu mbele ya Uthman. Tumekwishasimulia tayari katika kurasa zilizopita kile kisa cha Jalabah ibn Umrah Sa’idi. Ilikuwa ni kujiamini mno kwa Marwan ambako kulimtia moyo Jalabah kumwambia Uthman: “Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kwamba 335

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 335

9/4/2017 3:48:01 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

nitaiweka nyororo hii kwenye shingo yako isipokuwa tu kama utawaondoa ndugu zako waovu kutoka karibu yako.” Dr. Taha Husein anaweza akaulizwa vizuri sana iwapo kujiamini huku kwa Jalabah kunapingana zaidi na akili au kule kwa Marwan ambaye aliandika barua kana kwamba ilikuwa imeandikwa na Uthman, wakati yeye alikuwa ni mkwe kipenzi wa Uthman na alikuwa na ushawishi mkubwa juu yake! Njama Kubwa Watu Wanaohusika Na Mauaji Ya Uthman Tumeelezea kikamilifu katika kurasa zilizopita kwamba watu walikuza chuki ndani ya nyoyo zao dhidi ya sera za Uthman; hapo Madina, na vile vile katika nchi nyingine za Kiislamu. Mwanzoni kabisa watu walikosa kuridhika nyoyoni, lakini baadae wakaanza kulalamika na baada ya hapo walalamikaji wakaanza kuunda hali ya kukosa utii ambayo iliishia katika kuzingirwa kwa nyumba ya Uthman na kuuliwa kwake. Tumetaja pia kwamba wale ambao walishutumu sera za Uthman na wakampa ushauri mzuri na wenye manufaa walikuwa sio wale watu wa kawaida bali ni masahaba maarufu wa Mtume. Hata hivyo, badala ya Uthman kuachilia mbali sera zake potovu na upendeleo wa kindugu, yeye na jamaa zake waliwafanyia bughudha masahaba hao na mateso na adhabu kali kali. Kama masahaba hawa walizishutumu sera na mbinu za Uthman, ilikuwa sio kwa sababu ya matamanio yao juu ya manufaa yoyote binafsi, bali ni kutokana na mapenzi yao juu ya uadilifu na imani. Wao walikuwa ndio chaguo la kikundi cha watu. Waliujua wajibu wao kikamilifu kabisa, ambao ulifanana na ule wa mitume. Kama Ali aliishutumu sera ya Uthman ya kutoa maeneo makubwa ya ardhi kwa ndugu zake bila uhalali wowote, haikuwa ni kwa sababu yeye mwenyewe alitaka eneo lolote. Na kama alizikataa sera zake za kiuchumi haikuwa ni kwa sababu yeye binafsi alielekea kuwa na matakwa ya kupata utajiri. Kila mmoja anajua kwamba yeye hakuthamini mali kamwe. Kama alilalamikia upendeleo wa kindugu wa Uthman na fikra zake za ki-Bani Umayyah sio kwamba yeye alitaka ustawi na ubora wa familia yake mwenyewe. Haiwezekani hata kujaribu kudhania kwamba Ali angeweza kushawishiwa na motisha kama hizo. Ali alikuwa ni nguzo ya Uislamu, binamu na mkwe wa Mtume na baba wa wajukuu zake vipenzi. Alikuwa ni yeye aliyetamka maneno haya: “Heshima na thamani ya mtu inaamuliwa kutokana na vitendo vyake. Mtu ambaye vitendo vyake ni bora atapata heshima na hadhi kubwa zaidi.” Kauli yake hii ilivunja ndoto za heshima na hadhi ya familia na ya kikabila ambayo mtu huwa anairithi. 336

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 336

9/4/2017 3:48:01 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Ule upinzani kwa, na chuki dhidi ya sera za Uthman kutoka kwa Ammar na Abu Dhar ulikuwa kwenye misingi ya sababu hizi hizi ambamo upinzani wa Ali uliegemea. Hivyo, upinzani wao haukuwa na maana kwamba utakuwa umelazimika kufikia kileleni katika kifo cha Uthman. Walichokitaka wao kilikuwa kwamba atupilie mbali fikira za ki-Umayyah na upendeleo wa kindugu, na badala yake, usawa na uadilifu vipate kuwepo. Hakuna hata mmoja wao aliyependa yeye auliwe. Dola ya Kiislamu wakati wa siku za Uthman ilikuwa imechukua maeneo makubwa na ilikuwa ni kawaida kwamba katika Dola kubwa kama hiyo upinzani wa namna nyingine lazima pia ujitokeze. Upinzani huu ulikuwa ni kutoka kwa wale watu ambao walitamani madaraka na mamlaka na manufaa zaidi, na walitaka kupanua eneo lao la ushawishi. Walimpinga Uthman kwa matumaini kwamba endapo ataondolewa kutoka kwenye cheo chake na akarithiwa na mtu mwingine mwenye kufaa zaidi kwao, hadhi zao na umaarufu vitaweza kuongezeka. Upinzani wa aina hii unatokea katika kila eneo na katika kila zama. Washirika wa kila mtawala hubadili mwelekeo wao mara kwa mara ili kufanikisha malengo yao binafsi. Wapinzani wa aina hii katika kipindi cha Uthman walikuwa hawafanani wote. Wapenzi wake wale ambao walikuwa wakilimbikiza mali kama matokeo ya zawadi alizowapa yeye walikuwa wanampinga, na ni vivyo hivyo pia walivyokuwa wale ambao walinyimwa neema kama hizo. Na suala lilikuwa hivyo hivyo kwa upande wa ndugu zake, maafisa na wafuasi wake ambao alikuwa amewaruhusu, sio tu kuwadhibiti watu, bali na yeye mwenyewe vile vile. Watu hawa walikuwa ndio wauaji wake halisi hasa. Tumekwisha kuelezea tayari katika kurasa zilizotangulia jinsi Uthman alivyotoa njia za kifo chake mwenyewe na jinsi Marwan na wapenzi wake walivyougeuza ulimwengu wa Kiislamu dhidi yake kwa vitendo vyao vya ubaya. Ukweli halisi ulifahamika kwa wale watu ambao walikuwa na uhusiano wa karibu sana na Uthman. Mmoja wao alikuwa ni Muhammad bin Muslimah. Alipokuwa karibu ya kufariki, mtu mmoja alisema: “Uthman ameuawa.” Hapo yeye (Muhammad) akasema: “Uthman mwenyewe amehusika na kifo chake.” Mkewe Uthman akamwambia Marwan na vipenzi wengine wa mume wake: “Naapa kwamba mtamuua Uthman na kuwafanya wanawe kuwa mayatima.” Na akiongea na Uthman alisema: “Kama utafuata ushauri wa Marwan atakuua.”

337

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 337

9/4/2017 3:48:01 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Na kuhusu wale magavana wa ki-Bani Umayyah maafisa, na wafuasi ambao Uthman alikuwa amewaruhusu kuwatumikisha na kukwatiisha watu, na baadhi yao ambao walinufaika na neema zake na wengine ambao walikuwa hawaridhiki naye, tutawajadili mmoja mmoja hivi punde, kwa sababu idadi kubwa ya watu hawa walibuni njama kubwa dhidi ya Ali – njama ambayo ilikuwa haijawahi kutokea huko Mashariki. Njama hiyo iliendeshwa na wale watu hasa ambao waliwachochea watu dhidi ya Uthman na hivyo wakaipakaza mikono yao na damu yake. Njama hiyo ilikuwa kwamba wao walimshutumu Ali kwa mauaji ya Uthman. Walilichukua lile shati la Uthman lililokuwa limetapakaa damu na wakasema kwamba wanataka kulipiza kisasi kwa kifo cha Uthman. Mu’awiyah ambaye sio kweli kwamba alitaka kulipiza kisasi kwa kifo cha Uthman, bali kwa hali hali si alikuwa anapenda hasa kuimarisha utawala wake yeye mwenyewe na ule wa kizazi chake vile vile. Juhudi zake zilikuwa zimeelekezwa kwenye uimarishaji wa utawala wake huko Syria kwanza kabisa. Halafu alitaka kupanua ufalme wake kwa kunyakua nchi nyingine na hatimae kuwa mtawala mwenye mamlaka yote, dikteta wa nchi zote za Kiislamu. Hakumtilia maanani Uthman imma katika uhai wake au hata baada ya kifo chake. Chote alichokitaka yeye ni kwamba Uthman aweze kumfanya yeye kuwa mwenye nguvu sana siku hadi siku ili kwamba hatimae ataweza kufanikisha lengo lake la mwisho. Hivyo alitaka kwamba ampe uhuru wa kiwango cha juu kabisa wa kutenda na aweze kuwa ngao kwa ajili yake, ili aweze kufanikisha malengo yake. Hata pale wakati Uthman alipokuwa ameuliwa, Mu’awiyah hakujali kabisa juu ya kifo chake. Alitaka tu kuitumia fursa ya kudai kuwa ndiye mrithi wa khalifa, na kumuondoa yule Khalifa mpya. Je, alifanya nini na wale wauaji wa Uthman wakati yeye mwenyewe alipokuja kuwa mtawala pekee wa nchi za Kiislam? Angekuwa kweli amehuzunika kutokana na mauaji ya Uthman basi angewatafuta na kuwaua kila mmoja wa wauaji wake. Hata hivyo, alikisahau kabisa kifo cha Uthman na kumlipizia kisasi, ingawa ilikuwa ni juu ya kisingizio hiki hasa kwamba aliasi dhidi ya Khalifa mpya na hivyo kusababisha umwagaji wa damu ya mamia ya maelfu ya Waislamu. Zaidi ya hayo, angeweza kutuma jeshi kubwa kutoka Syria kwenda kumlinda Uthman wakati nyumba yake ilipozingirwa na waasi. Yeye alikuwa ni gavana wa kudumu wa Syria na Uthman alikuwa amempa uhuru mkubwa. 338

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 338

9/4/2017 3:48:01 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Aliweza kufanya kila alilolitaka na hakuna mtu ambaye angeweza kumwita kujieleza. Hivyo angeweza kutuma jeshi kubwa la Syria kwenda Madina, kabla na hata baada ya nyumba ya Uthman haijazingirwa. Kwa kweli angeweza pia kumshauri Uthman asiwe mkaidi kwenye maoni ya umma. Hata hivyo, yeye hakufanya lolote kati ya mambo haya, kwa sababu alikuwa na shauku ya kunyakua ukhalifa baada ya Uthman na hakuweza kufikiria kuhusu jambo jingine lolote. Kutoka siku ile hasa ambayo Uthman aliitisha kikao na wasiri wao, ambacho kilihudhuriwa pia na Mu’awiyah, na ambacho kiliisha bila ya kufanyika maamuzi yoyote, Mu’awiyah aliamua mwishoni kuukamata ukhalifa, kwa sababu alipata uhakika kabisa kwamba Uthman atakuja kuuliwa. Kwa vile Syria ilikuwa mikononi mwake, na raia wa maeneo hayo walikuwa watiifu kwake, alitambua kwamba endapo Uthman atauliwa, basi atapata silaha bora kabisa (yaani kisasi cha mauaji ya Uthman) ya kufanikishia lengo lake. Alijua pia kwamba miongoni mwa magavana wa Uthman hakuna aliyekuwa na nguvu na uwezo wa kukusanya jeshi kwa kuwatishia wazee na wakuu wa makabila kama yeye mwenyewe alivyokuwa. Hivyo, katika siku hiyo hiyo, yeye aliamua kuwa khalifa siku moja na harakati hai kuelekea kwenye kufanikisha lengo lake. Yeye mwenyewe aliwahi kusema wakati mmoja: “Hakuna ambaye ana nguvu na uwezo wa kutawala kama mimi. Umar aliniteua mimi kuwa gavana na aliridhika na mwenendo wangu.” Mu’awiyah alikuwa na uhakika wa kuuawa kwa Uthman na pia alimiliki mamlaka ya kutosha huko Syria ya kuweza kuukamata ukhalifa. Allamah Ya’qubi anaandika kwamba wakati wale waasi walipokaza mzingiro wa nyumba yake, Uthman aliandika barua kwa Mu’awiyah kumuomba aje kumsaidia. Mu’awiyah aliondoka Damascus pamoja na jeshi kubwa, lakini wakati alipoufikia mpaka wa Syria akaliacha lile jeshi hapo, akisema kwamba kwanza kabisa atakutana na Amiri wa waumini mwenyewe kuitathmini hali halisi. Halafu akawasili Madina na akakutana na Uthman. Yeye Uthman akamuuliza kwamba jeshi lake liko wapi. Mu’awiyah akamjibu: “Nimeliacha jeshi nyuma kwa sababu, kwanza kabisa nilitaka kufanya mashauriano na wewe. Sasa nitarudi na tutakutana tena nikiwa pamoja na jeshi langu.” Juu ya hili Uthman akasema: “Oh, Mu’awiyah! Hiyo sio kweli. Ukweli ni kwamba wewe unataka mimi niuawe ili uweze kuwa katika nafasi ya kudai kwamba unayo haki ya kulipiza kisasi cha damu yangu. Nenda upesi na ukawalete watu hapa kuja kunisaidia.”

339

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 339

9/4/2017 3:48:01 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Ulipokuwa umepita muda mrefu sana baada ya Uthman kuuliwa, Mu’awiyah alikwenda Madina na akaitembelea nyumba ya Uthman. Binti ya Uthman aitwaye Ayesha hapo akamkumbuka baba yake na akaanza kulia. Mu’awiyah alimliwaza na akaanza kulia. Akasema: “Ewe mpwa wangu mpendwa! Watu wamekuwa watiifu kwangu na nimewapatia amani. Nimeonyesha uvumilivu ambao chini yake hasira zilikuwa zimefichika na wao wakaonyesha utiifu ambao una uadui na chuki ya muda mrefu chini yake. Kila mwanaume anao upanga mkononi mwake na pia anajua jinsi wafuasi wake walivyo. Kama tukiwadanganya na wao watatudanganya na haiwezi ikasemwa kwamba ni nani atakayeshinda. Unapaswa kuridhika kwamba kwa sasa hivi unaitwa binti ya Amiri wa waumini Uthman na mpwa wake Amiri wa waumini Mu’awiyah. Kama nitasimama kulipiza kisasi kwa niaba yako na hatimae nikainyang’anywa serikali, wewe utakuja kuwa mwanamke wa kawaida tu.” Hivyo, wakati Mu’awiyah alipokuja kuwa Amiri wa waumini na matokeo yake binti yake Uthman akawa mpwa wa Amiri wa waumini, yeye Mu’awiyah akakoma kufikiri au kuzungumza kuhusu Uthman, ingawa kwa kipindi ukhalifa ulipokuwa umebaki mikononi mwa Ali, kifo cha Uthman kilikuwa ndio mada inayokera sana kwake. Sasa serikali alikuwa nayo Mu’awiyah na alikuwa amepata fursa ya kutimiza matakwa ya baba yake Abu Sufyan, ambayo aliyaeleza wakati Uthman alipokuwa ameutwaa ukhalifa. Abu Sufyan alikuwa amesema: “Enyi watoto wa Umayyah! Chezeni na serikali kama watoto wanavyocheza na mpira. Naapa kwamba nilikuwa siku zote nikiitamani serikali hii kwa ajili yenu. Sasa itashuka chini hadi kwa watoto wenu kama urithi.” Ni dhahiri, baada ya Mu’awiyah ukhalifa ukawa uende kwa Yazid na halafu kwa watoto wengine wa Bani Umayyah. Katika barua zilizoandikwa na Ali kwenda kwa Mu’awiyyah alieleza wazi kwamba wakati Uthman alipotafuta msaada kutoka kwa Mu’awiyyah, yeye hakuridhia kwenye maombi yake. Hakuja yeye mwenyewe wala hakutuma jeshi lolote kuja kumlinda Uthman. Katika barua kwa Mu’awiyah, yeye anasema: “Halafu umelitaja lile suala kuhusu mimi na Uthman. Unayo haki ya kupata jibu juu ya hili, kwa sababu una uhusiano wa kindugu naye. Haya basi niambie (kwa usahihi kabisa) juu ya ni nani kati ya sisi wawili aliyekuwa na uadui zaidi hasa kwake, na ni nani aliyetoa njia za kifo chake? Ni nani ambaye alitoa msaada ambao ulikataliwa na Uthman, au ni nani ambaye kutoka kwake Uthman aliomba msaada na ni nani 340

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 340

9/4/2017 3:48:01 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

alishindwa kumsaidia na akatoa njia za kifo chake hadi kifo kikamchukua katika namna ile ambayo iliamuliwa juu yake.” Katika barua nyingine anaandika hivi: “Wewe ulimsaidia Uthman pale ambapo kumsaidia kwako kulitumikia maslahi yako binafsi na ulijizuia kutokana na kumsaidia wakati yeye Uthman alielekea kunufaika.” (Kinachomaanishwa na maneno ya Ali hapo juu ni kwamba Mu’awiyah alisimama katika kumsaidia Uthman baada ya kifo chake, kwa sababu aliwakusanya watu katika maslahi yake mwenyewe kwa kunyanyua ule wito wa kisasi cha mauaji ya Uthman, lakini wakati Uthman alipokuwa bado yuko hai na msaada wake Mu’awiyah ungeweza kuwa wa manufaa kwake, yeye aliuzuia. Uthman akabakia amezingirwa, na Mu’awiyah hakuruhusu jeshi lake kwenda Madina kumlinda). Chochote kile kilichosemwa hapo juu kuhusu Bani Umayyah na watu wao mashuhuri kama Mu’awiyah na Marwan kuhusiana na kifo cha Uthman, kinaweza pia kusemwa kuhusu watu wengine waliotajwa hapo juu. Kwa kweli mambo kama hayo hayo yanaweza kusemwa kuhusu maadui wa Ali na wale ambao walikula njama dhidi yake. Watu hawa walikuwa wanahusika na kifo cha Uthman na wala sio Ali. Inawezekana kwamba kunaweza kukawa na watu ambao hawakuipakaza mikono yao na damu ya Uthman lakini ni ukweli usiopingika kwamba wao walifurahia wakati alipokutana na kifo chake. Amr bin Aas, ambaye alikuwemo kwa kiasi kikubwa katika kubuni njama dhidi ya Ali na kumkashifu, alimchochea kila mtu aliyekutana naye kuasi dhidi ya Uthman na akawahimiza watu kumuua, kwa sababu alikuwa amemfukuza yeye kutoka kwenye ugavana wa Misri. Yeye mwenyewe alikuwa akisema: “Bila ya kuzungumza juu ya wale watu wenye hadhi kubwa na machifu, niliwachochea hata wachungaji mifugo kuasi dhidi ya Uthman.” Wakati machafuko yalipoanza mjini Madina yeye alikimbilia zake Palestina ambako alikuwa amejenga jumba kubwa. Siku moja alipokuwa amekaa ndani ya jumba lake hilo pamoja na wanawe wawili walioitwa Muhammad na Abdullah; mpanda kipando alionekana akija kutoka upande wa Madina. Watu walifanya uchunguzi kutoka kwake kuhusu Uthman naye akawaambia kwamba alikuwa amekwisha kuuawa. Hapo Amr bin Aas akasema: “Mimi ni Abdullah. Wakati ninapokata jeraha ninahakikisha kwamba damu inatoka kwenye jeraha hilo.” (Alikuwa na maana ya kusema kwamba aliwachochea watu kuasi dhidi ya Uthman na matokeo yake yeye (Uthman) amepoteza uhai wake.)

341

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 341

9/4/2017 3:48:01 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Talha bin Ubaidullah, ambaye mwanzoni alichukua kiapo cha utii kwa Ali, na halafu akapigana dhidi ya Ali kwa kisingizio cha kulipiza kisasi cha Uthman alikuwa mtu mwingine wa namna hiyo. Alichukua nafasi tendi katika kuwachochea watu kuasi dhidi ya Uthman. Imesimuliwa kwamba Uthman alitafuta msaada kutoka kwa Ali dhidi ya Talha mara nyingi, na Ali wakati wote aliyakubali maombi yake. Katika wakati mmoja kama huo Ali alikwenda kwa Talha na akaona kwamba idadi kubwa ya waasi walikuwa wamekusanyika karibu naye. Alihisi kwamba Talha alikuwa na sehemu kubwa katika kuzingirwa kwa Uthman, na yeye (Talha) alikuwa akifikira juu ya kumliza kabisa. Ali alimkaripia na akasema: “Ewe Talha! Ni nini hiki ulichomtendea Uthman?” Vile vile alijitahidi kumzuia Talha kutokana na shughuli zake lakini yeye alikataa kutenda kwa ushauri wa Ali. Kisha Ali akaenda kwenye hazina ya Umma na akatamani kwamba ingefunguliwa. Hati hivyo, funguo hazikupatikana. Mlango wa hazina ukawa wakati huo ukavunjwa chini ya maelekezo yake na akagawanya pesa zote alizozikuta humo ndani yake, miongoni mwa wale watu ambao Talha alikuwa amewakusanya kwa ajili ya kumuua Uthman. Wakati Uthman alipokuja kufahamu juu ya hilo alifurahi sana na akatambua (ingawa katika hatua za mwisho kabisa) kwamba hakuna mwingine tena ambaye alikuwa na huruma na uaminifu, na uwezo wa kutatua matatizo ya Waislamu kama Ali. Kisha Talha akaja kwa Uthman na kuomba msamaha kwake na akasema: “Ninatubia mbele ya Mwenyezi Mungu. Nilikuwa nimeamua kutenda kitendo lakini Mwenyezi Mungu ameingilia kati.” Uthman akasema: “Wewe hukuja kama mtubiaji, bali kama mtu ambaye amekuwa hajiwezi tena. Mwenyezi Mungu akuadhibu!” (Tarikh al-Kamil, Juz. 3, uk. 7; Tarikh Tabari, Juz. 6, uk. 154; Tarikh Ibn Khalidun, Juz. 2, uk. 297). Tabari anasimulia kwamba mara tu wale waasi walipoizingira ile nyumba ya Uthman, Talha akaanza kujitayarisha kuwa khalifa. Alikuwa na uhakika kwamba baada ya Uthman watu watamchagua yeye kama khalifa anayefuatia. Kitendo cha kwanza alichokichukua yeye kilikuwa kwamba alichukua udhibiti juu ya Hazina ya Umma, akazipata funguo, na akawateua walinzi wake kuilinda. Pale mzingiro wa nyumba yake uliposhamiri na kuwa mkali zaidi Uthman akasema: “Ewe Mwenyezi Mungu! Nisaidie dhidi ya Talha. Amewashawishi watu kuasi dhidi yangu. Naapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba ninatumaini hatapanda kwenye cheo cha ukhalifa na atapoteza maisha yake vile vile.” Maneno haya yaliyotamkwa na Uthman 342

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 342

9/4/2017 3:48:01 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

yanaonyesha kwamba Talha alitaka kummaliza yeye na kuwa khalifa yeye mwenyewe. Uthman alikuwa amempa Talha uhuru wa kutumia mali ya Hazina ya Umma kwa namna yoyote aliyotaka, lakini alikuwa ni mtu ambaye hakuweza kutosheka na chochote chini ya ukhalifa. Uthman alikuwa kila mara akiyatamka maneno haya katika siku za mwisho za kuzingirwa kwa nyumba yake: “Msiba umpate Talha! Mimi nilimpa dhahabu nyingi na sasa ana kiu na damu yangu.” Wale ambao wamenakili matukio yanayohusiana na kuzingirwa kwa nyumba ya Uthman wamesema kwamba, katika ile siku ambayo Uthman aliuawa ,Talha alikuwa amefunika uso wake na alikuwa akirusha mishale kwa siri kumwelekea Uthman. Imesimuliwa pia kwamba wakati wazingiraji walipokuwa wameshindwa kupata njia ya kuingilia nyumbani kwa Uthman, Talha alipanga uingiaji wao kutoka kwenye nyumba iliyokuwa inapakana nayo ambayo ilikuwa ni mali ya Ansari mmoja na halafu wakamuua Uthman. Tabari amesimulia kupitia kwa Hakim bin Jabir kwamba wakati nyumba ya Uthman ilipokuwa imezingirwa, Ali alimwambia Talha: “Ninakuomba sana juu ya tafadhali kumuokoa Uthman kutokana na watu.” Talha akajibu: “Wallahi hilo haliwezekani isipokuwa mpaka Bani Umayyah watakapolipa deni lote.” (Tarikh Tabari, Juz. 5, uk. 139). Baada ya mauaji ya Uthman, Ali alikuwa akisema mara kwa mara kwamba: “Mwenyezi Mungu amlaani Abu Shabal (Talha)! Uthman alimpa vingi mno na yeye (kwa kumlipa) akamfanyia namna hii.” Kauli ya Ali kuhusu Talha inaonyesha kwamba yeye alikuwa ndiye mtu aliyewachochea watu zaidi kuasi dhidi ya Uthman na yeye alikuwa na bidii sana kuliko mtu mwingine yoyote kuona kwamba Uthman anauliwa. Yeye anasema: “Wallahi Talha alifanya haraka sana kutoa madai ya kulipiza kisasi cha mauaji ya Uthman ili isije ikawa kisasi hicho kikageukia kulipizwa kwake yeye, kwa sababu yeye pia alihusika katika jambo hilo. Hakuna aliyekuwa na kiu zaidi ya damu ya Uthman kuliko yeye. Kwa kujifanya kudai kulipiza kisasi alijaribu kuwapotosha watu ili ule ukweli uweze kubaki umefichika na watu waweze kujiingiza kwenye mashaka.” Na kuhusu Zubeir bin Awam imesimuliwa kwamba yeye hakufanya lolote kuwageuza wale waasi kuondoka kutoka kwa Uthman, bali inasemekana kwamba wema wake ulikuwa pamoja na waasi. Sera alizozichukua yeye kuhusiana na Uthman zi343

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 343

9/4/2017 3:48:01 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

naonyesha kuwa hata yeye pia alitaka kwamba angemalizwa kabisa mapema iwezekanavyo, na alikuwa na matumaini kabisa ya kuja kuwa khalifa anayefuatia. Yeye alimwambia Ali wazi wazi kwamba aliutaka ukhalifa yeye mwenyewe. Wakati Ali alipomuuliza kitambo kidogo kabla ya kuanza kwa vita vya Ngamia kuhusu ni vipi yeye alikuwa amefika pale, yeye alijibu: “Wewe ndio umekuwa sababu ya kuwasili kwangu hapa. Mimi sikuoni wewe kama unafaa kuwa khalifa, wala kumuona mtu mwingine yoyote yule kuwa mwenye kustahili zaidi kwenye cheo hiki kuliko mimi mwenyewe.” Kila mwanafunzi wa historia anajua jinsi Aisha alivyowashawishi watu kwa bidii sana kuasi dhidi ya Uthman. Aisha alimshutumu yeye vikali sana na akawashawishi watu kumuuwa. Alikuwa ana hasira sana naye tangu siku ile alipopunguza ujira wake na alikuwa siku zote akitafuta fursa ya kumdhuru yeye. Siku moja alimsikia Uthman akitoa hotuba kutoka kwenye mimbari ya Mtume. Mara moja akatoa shati la Mtume na akilionyesha kwa watu alisema kwa sauti kubwa: “Enyi Waislamu! Shati hili la Mtume bado halijachakaa na Uthman tayari ameipotosha Sunnah yake.” Ibn Abil-Hadid anasema kwa idhini ya wanachuoni wa wakati wake kwamba Aisha alimchochea kila mtu aliyekutana naye kuasi dhidi ya Uthman. Yeye anaendelea kusema: “Aisha alitoa kipande cha nguo ya Mtume na akakitundika kwenye ukuta kwenye nyumba yake. Kila aliyekuja kumtembelea, yeye alimwambia: “Vazi hili la Mtume bado halijachakaa lakini Uthman ameichafua na kuiharibu Sunnah yake.” Baladhuri anasema: “Wakati mmoja Ibn Abbas alibahatika kukutana na Aisha. Mwaka ule Uthman alikuwa amemteua yeye kama Amir wa Hijja. Aisha akamwambia wazi wazi: “Oh, Ibn Abbas! Mwenyezi Mungu amekupa wewe akili, hekima na uwezo wenye nguvu wa kuongea. Wafanye watu wamgeuke huyu muasi (Uthman).” Baladhuri ameyanukuu maneno ya Aisha ambayo yanaonyesha kwamba yeye alimchukia Uthman zaidi kuliko mtu mwingine yoyote anavyoweza kuchukia mwanadamu mwingine. Alimwambia Marwan: “Ewe Marwan! Natamani kwamba Uthman angekuwa ndani ya mfuko wangu mmojawapo ili kwamba ningeweza kuuokota mfuko huo mimi mwenyewe na kuuzamisha kwenye bahari.” Alikuwa akisema mara nyingi kwamba: “Muueni Na’athal. Na’athal amegeuka kuwa kafiri.” Aisha alikitamani sana kifo cha Uthman kiasi kwamba alianza kuwataka watu 344

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 344

9/4/2017 3:48:01 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

wazi wazi kabisa wamuue. Ilikuwa ni kwa sababu ya hili kwamba alikuwa na uhakika kwamba baada ya Uthman kufariki, Talha, na sio Ali, atakuwa ndiye khalifa. Hili linathibitishwa na ukweli kwamba pale habari za kuuliwa kwa Uthman zilipowasilishwa kwake huko Makkah, yeye mara moja akasema: “Laana juu ya Na’athal! Vizuri kabisa enyi watu mlio na vidole! Vizuri sana Abu Shabal! Wewe ni mtu mashuhuri kiasi gani, ewe binamu yangu! Inaonekana kana kwamba ninaweza kuona kwa macho yangu mwenyewe vidole vyake na watu wakichukua kiapo cha utii kwake.” Yule mtu mwenye vidole maana yake ni Talha. Vidole vyake vilikatwa katika vita vya Uhud, na kuanzia siku ile na kuendekea akawa anaitwa yule mtu mwenye vidole. Wakati mtoto wa Talha, aitwaye Muhammad alipoulizwa kuhusu maelezo ya kina juu ya kuuliwa kwa Uthman, yeye alimshutumu baba yake na Aisha vile vile kwa kuhusika katika mauaji hayo. Mwandishi wa Al-Badr wa al-Tarikh anasema: “Maadui wakubwa kabisa wa Uthman walikuwa ni Talha, Zubeir na Aisha.” Walikuwepo watu mashuhuri wengi ambao walichochea maasi dhidi ya Uthman na kwa hiyo walishiriki katika mauaji yake. Kwa mfano pale Abdul-Rahman bin Auf ambaye utajiri wake ulikuwa umeongezeka mara nyingi sana wakati wa utawala wa Uthman alipoingiwa na maradhi, na watu wakaenda kuulizia kuhusu afya yake, yeye aliwaambia: “Mshughulikieni Uthman kabla hajapata nguvu.” Miongoni mwa maadui wa Uislamu ambao walichochea watu kuasi dhidi ya Uthman waliingia watu wengi ambao baadae walipigana dhidi ya Ali na wakadai kisasi juu yake kwa mauaji ya Uthman. Mwandishi wa ‘Halif Makhzum’ anaandika ndani ya kitabu chake: “Wale katika Maquraishi ambao walikuwa maadui wa jadi walikuja kuwa waunga mkono wake baada ya kufa kwake, na inawezekana nafasi ya Aisha katika msiba huu ni mfano wa wazi wa kule kuwa mwenye kujipinga vibaya sana ukilinganishwa na ule wa Maquraishi walafi. Yeye Aisha aliwachochea watu wazi wazi kumuua Uthman kwa sababu alitegemea kwamba serikali baada ya hapo itarudi kwenye familia ya Tayim (Familia ya Aisha), na binamu yake Talha ataweza kuwa ndiye khalifa. “Uthman aliuawa na Talha, Zubeir na Sa’d bin Abi Waqas. Aliuawa na Mu’awiyah na kundi lake kupitia utajiri wao na njama nyingi. Walimuacha kwenye shida. Aliuawa na Marwan na kizazi chake na marafiki wa Bani Mu‘iz, kutokana na ubinafsi wao, na kushindwa kuonyesha umuhimu wowote kwenye mambo ya Uthman. 345

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 345

9/4/2017 3:48:01 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

“Hata hivyo, wakati Uthman alipouliwa, na Waislamu wakamchagua Ali kwa kauli moja kama khalifa wao mpya, watu wote hawa ghafla wakabadili mwelekeo wao. Uthman yule yule aliyeitwa dhalimu na kafiri katika uhai wake, wakaanza wao kumwita mtu aliyeonewa na shahidi baada ya kifo chake.” Haitakuwa nje ya mahali pake kutaja hapa yale maneno ambayo yalitamkwa na Sa‘id bin Aas na Mughirah bin Shu’ba wakati walipokutana na Aisha na jeshi lake hapo Khaybar pale alipokuwa ametokea Makkah kwenda Basra kupigana dhidi ya jeshi la Ali. Walichokisema kinaonyesha dhahiri kwamba Talha na Zubeir walihusika kikamilifu juu ya kuuliwa kwa Uthman. Katika tukio hilo Sa‘id alikutana na Aisha na mazungumzo yafuatayo yalitokea kati yao: Sa‘id: Ewe Mama wa waumini! Unakwenda wapi? Aisha: Ninakwenda Basra. Sa‘id: Kwa ajili gani? Aisha: Kwenda kulipiza kisasi kwa wauaji wa Uthman. Sa‘id: Mbona wauaji wa Uthman tayari wako pamoja nawe. Kwa nini huwaui? Kisha Sa‘id akaongea na Marwan na wakazungumza kama ifuatavyo: Sa‘id: Unakwenda wapi? Marwan: Ninakwenda Basra. Sa‘id: Ni nini utakachokifanya huko? Marwan: Nitachukua kisasi juu ya wauaji wa Uthman. Sa‘id: Wauaji wa Uthman tayari wako pamoja nawe. Ameuawa na Talha na Zubeir. Waliutamani ukhalifa wao wenyewe. Hata hivyo, wakati waliposhindwa (yaani pale watu walipochukua kiapo cha utii kwa Ali) wao wakasema: “Sisi tutasafisha damu kwa damu na kulipa fidia ya dhambi zetu kwa kutubia.” Kisha Mughirah akawahutubia watu hivi: “Kama mmekuja kuandamana na Mama wa waumini itakuwa bora kama mtarudi pamoja naye. Na kama hasira zenu ni kutokana na kuuawa kwa Uthman, mnapaswa kujua kwamba hawa hawa wakuu wenu hasa ndio wamemuua Uthman. Na kama mnamchukia Ali kwa sababu fulani

346

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 346

9/4/2017 3:48:01 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

basi nifahamisheni sababu yenyewe ni ipi. Ninakuombeni juu ya tafadhali msije mkasababisha vurugu mbili katika mwaka mmoja.� (Al-Imamah wa al-Siyasah, Juz. 1, uk.58). Huu ulikuwa ndio utaratibu na mwenendo wa wale watu ambao walichochea uasi dhidi ya Uthman na wakasababisha kifo chake. Na wakati Uthman alipouliwa walileta shati lake na wakasimama kudai kisasi juu ya Ali. Na kuhusu Ali tumekwishaelezea msimamo wake katika mfululizo wa matukio yaliyoelezewa hapo mapema. Kama tulivyoelezea hapo juu, Uthman alikuwa ana wasiwasi kuhusu Ali. Marwan alimshauri Uthman kila wakati kumuua Ali na masahaba wengine mara tu fursa itakapopatikana. Lengo lake lilikuwa kwamba hawa watu waadilifu ambao wanaangalia na kushutumu shughuli za kiovu za Bani Umayyah wangeondoka kwenye mandhari ya mambo ili kwamba wao (Bani Umayyah) waweze kufanya kila walilolitaka na kusiwe na yoyote wakuwatoa makosa. Hata hivyo, Ali alikuwa na msimamo na tabia ya kiungwana ya kutoweza kulea chuki binafsi akilini mwake kwa ajili ya mtu yoyote. Ali alikuwa mbali kabisa na fikra ndogo ndogo kama hizo, kwamba angelea chuki dhidi ya Uthman kutokana na kutomtaka ushauri yeye, na kwamba angeweza kufurahi kama Uthman angempendelea. Umbali na Uthman na ukaribu naye vilikuwa havina maana kwake. Mambo ambayo kwamba Ali alikuwa na shauku nayo yalikuwa ni Uislamu na ustawi wa umma. Wakati wote aliepuka kuridhika, isipokuwa kama ilikuwa ni muhimu kukukimbilia ili kuondosha udhalimu na kusimamisha usawa na haki. Hivyo wakati wowote ilipokuwa inawezekana kwa Ali kutoa ushauri wa manufaa kwa Uthman; yeye hakuuzuia ushauri wake wa kuaminika, ingawaje ungeweza kuwa usiopendeza kwa wapenzi wa Uthman. Wala yeye hakuonyesha uzembe katika kumsaidia Uthman, kuwageuza maadui zake mbali na yeye na kumuokoa kutokana na hatari ya kifo. Watu walimwendea Ali mara nyingi na maombi kwamba aweze kuutwaa ukhalifa yeye mwenyewe lakini aliyakataa maombi yao kwa ukali sana na akawafukuza mbele yake, na akamuokoa Uthman kutokana na wapenzi na washirika wake mwenyewe ambao wenyewe walikuwa ndio kiini cha matatizo yote. Tumekwisha elezea tayari katika kurasa zilizopita jinsi Ali alivyomsaidia Uthman wakati nyumba yake ilipozingirwa na waasi, ingawa kitendo cha Ali lazima kitakuwa kimewachukiza washauri na washirika wa Uthman. 347

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 347

9/4/2017 3:48:02 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Ilikuwa ni matakwa motomoto ya Ali kwamba ile ghuba ya tofauti kati ya waasi na Uthman isije ikapanuka zaidi na kusiwe na tukio sumbufu, ambalo linaweza kuwadhuru Waislam ambalo liweze kutokea. Yeye aliamini kabisa kwamba umwagaji damu ulikuwa sio dawa pekee ya kuboresha hali. Wanaweza wakafanikisha lengo lao bila ya kukimbilia kwenye umwagaji wa damu. Sio rahisi kuweza kufikiria ni jinsi gani Ali alivyokuwa mwadilifu na mwenye moyo wa kiungwana. Wakati nyumba yake ilipokuwa imezingirwa na wale waasi, yeye Uthman wakati mwingine alimuomba Ali kuondoka Madina, na baada ya kuondoka kwake alijisikia aibu na akatuma mjumbe kwenda kumwita arudi. Ali alikubaliana na maelekezo yake kila wakati na kamwe hakumuuliza kwa nini alimtaka aondoke Madina na kwa nini baadae alimtaka arejee. Ulikuwa ni ubora wa kiroho wa Ali kwamba alikuwa wakati wote ni mpole kwa wengine. Uthman alimtaka Ali kuondoka toka Madina ili kwamba aweze kuwa hayupo mbele ya wafuasi wake, na wao wasiweze kulisikia jina lake. Alimwita arudi ili kuja kuwashauri wale waasi na kumuokoa yeye kutokana nao. Hili lilitokea mara nyingi. Wakati mmoja pale Ibn Abbas alipotumwa kuwasilisha ujumbe wa khalifa kwa Ali ili aondoke Madina, Ali alisema: “Ewe Ibn Abbas! Uthman anataka kunifanya mimi kama ngamia ambaye anabeba maji kwenda na kurudi. Yeye kwanza alinitaka niondoke Madina, na kisha akaniomba nirejee. Na sasa ametuma ujumbe kwamba niondoke kutoka hapa. Wallahi, mimi nimemlinda sana yeye kiasi kwamba ninaogopa kwamba ninaweza kuchukuliwa kama mtenda dhambi.” Muhammad ibn Hanafiyyah anamsimulia kuwahi yeye kusema kwamba: “Kama Uthman akiniamuru mimi niondoke zangu, basi mimi nitaitii amri yake.” Yeye aliyasema haya kwa ajili tu ya kuuhami Uislamu na kuondoa sababu za fitna. Maneno yafuatayo yanayoonekana kwenye barua aliyoiandika yeye Imam Ali kwenda kwa Mu’awiyah, yanaashiria kikamilifu kutokuwa na hatia kwake kuhusu mauaji ya Uthman. “Unataka kuchukua kisasi juu yangu kwa jambo ambalo sio mikono yangu wala ulimi wangu vimehusika humo. Mimi nilimpa mapendekezo na nikamuonyesha njia iliyonyooka. Kama hilo ndio kosa langu basi hutokea mara kwa mara kwamba mtu analaumiwa bila haki kwa makosa ambayo yeye hakuyatenda.” Ali alimsaidia Uthman wakati wa uhai wake na alikuwa na huruma sana kwake hata baada ya kufariki kwake. Hata hivyo, wakati Uthman alipouliwa, baadhi ya watu wakamlaumu Ali bila haki kwa kushiriki katika mauaji yake. 348

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 348

9/4/2017 3:48:02 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Muhammad ibn Sirin ameeleza kwa usahihi kabisa pale anaposema: “Mimi sina habari kama mtu yoyote alimshutumu Ali juu ya kuwa ameshiriki katika mauaji ya Uthman hadi pale kiapo cha utii kilipochukuliwa kwake. Lawama kama hiyo ilielekezwa dhidi yake wakati kiapo kilipokuwa kimekwisha kuchukuliwa.” Uasi Dhidi Ya Ali Ukimya ulikuwa umetanda hapo Madina kwa muda wa siku nyingi baada ya kuuawa kwa Uthman. Wakazi wa Madina, Muhajirin na Ansari, na vile vile wale watu ambao walikuwa wamewasili pale kutoka sehemu nyinginezo walikuwa katika kutafuta khalifa mpya. Wamisri hususan walisisitiza kwamba Ali awe ndiye khalifa lakini yeye alikataa kukubali kazi hii. Katika mapambano haya ya msisitizo na ukataaji, yeye aliwahutubia watu na akasema pamoja na mambo mengine: “Niacheni mimi na mumtafute mtu mwingine kwa ajili ya ukhalifa huu. Endapo mtaniacha mimi mwenyewe, nafasi yangu itakuwa kama yenu. Kama hivyo ndivyo, itawezekana kwamba mimi niweze kuwa mwangalifu na mtiifu kwa mtawala ambaye mtamchagua kuliko mlivyo ninyi. Ni bora (kutokana na mtazamo wenu wa maslahi ya kilimwengu) kwamba niwe mshauri kuliko kuwa mtawala.” Aliendelea kugoma kuukubali ukhalifa hadi watu wote wa Madina walipokusanyika mlangoni kwake, na wakasisitiza kwamba yeye anapaswa akikubali cheo hicho. Umati ulikuwa mkubwa sana kiasi kwamba alihofia kwamba baadhi yao wanaweza wakakanyagwa na wengine. Wote kwa jumla walikuwa wanasema kwa sauti moja: “Hatuwezi kumpata mwingine mwenye kustahiki zaidi kwa cheo hiki kuliko wewe, na sisi hatuchagui khalifa mwingine. Tafadhali kubali kupokea kiapo chetu cha utii. Baada ya hapo hakutakuwa na tofauti ya vikundi miongoni mwetu.” Malik Ashtar Nakhai aliukamata mkono wa Ali kwenye mkono wake mwenyewe na akachukua kiapo cha utii na wengine wote pia wakafuatia. Kila mmoja wao alikuwa akisema: “Hakuna isipokuwa Ali anayefaa kwa ukhalifa.” Kila mmoja alikuwa akilikariri jina la Ali na wote walijawa na furaha. Walikuwa wamefurahi kwa sababu walijua kwamba walikuwa wamechukua kiapo cha utii kwa mtu ambaye alikuwa anayajua mahitaji yao; na alizitambua haki zao, na alikuwa mwaminifu, mwenye elimu na hekima, na yeye alikuwa kama baba kwao.

349

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 349

9/4/2017 3:48:02 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Walikuwa na furaha kwamba Ali alikuwa ameukubali ukhalifa. Kwa vile walikuwa wamepata matatizo makubwa kwa muda mrefu katika wakati wa utawala wa giza wa Bani Umayyah, walikuwa wameweka mategemeo makubwa sana juu yake. Amirul-Mu’minin mwenyewe analeta taswira ya kile kiapo cha utii kilichochukuliwa kwake na watu katika maneno haya: “Watu walikuwa na furaha sana pale kiapo cha utii kilipochukuliwa kwangu kiasi kwamba watoto walianza kushereheka, wazee walijitokeza mbele kwa miguu yao inayotetemeka kuja kuchukua kiapo cha utii, wale ambao walikuwa hawajisikii vizuri pia waliweza vivyo hivyo, na hata wasichana wadogo walitoka kwenye kutawa kwao.” Wakati Ali alipopanda kwenye mimbari katika ile Ijumaa ya kwanza; wale ambao hawakuweza kuchukua kiapo cha utii hapo mapema walifanya hivyo siku hiyo. Katika siku hiyo Talha alikuwa wa kwanza kuchukua kiapo cha utii na alifuatiwa na Zubeir. Walikuwa ni Talha na Zubeir wale wale ambao baadae walisema: “Wakati tulipochukua kiapo cha utii kwa Ali hali zilikuwa kiasi kwamba upanga ulikuwa unaning’inia kwenye shingo zetu.” Inaweza ikaulizwa vile vile ni nini kile Talha na Zubeir walichokimaanisha kwa kuyasema haya. Inaweza ikasemekana kuhusiana na hili kwamba haya hayakuwa maoni ya Talha na Zubeir tu, bali wengi wa Maquraishi walikuwa na maoni kama hayo kuhusu ukhalifa wa Ali. Hawakuupenda ukhalifa wa Ali kutokana na wivu, au kwa sababu wao walihofia kwamba Ali asingeweza kuwaruhusu wao yale madaraka na mamlaka ambayo kwayo walikuwa wameyazoea, na hatavumilia kule kutengeneza kwao mapato ya haramu. Wao walijua kwamba yeye hakulichukulia kama ni jambo linaloruhusika kuwa mpole visivyostahili kwa wale watu wasiofaa au kutoa pesa kwa watu wasiostahili. Asingeweza kupoteza mali ya Hazina ya Umma ambayo ilikuwa imelengwa kwa ajili ya wenye haja na masikini. Sasa fikiria ule ukweli kwamba watu wote wenye hadhi na vyeo miongoni mwao walikuwa wakitamani kupanda kwenye ukhalifa. Ali ameeleza katika kauli ya mkato wa wazi kabisa kile kinyongo ambacho Talha na Zubeir na Maquraishi wengine walichokilea dhidi yake katika nyoyo zao. Yeye anasema: “Mimi nina uhusiano gani na Maquraishi? Siku za nyuma nililazimika kupigana nao kutokana na ukafiri wao, na sasa itanibidi nipigane dhidi yao kwa sababu ya kuwa kwao waasi. Kwao wao mimi ni yule yule leo kama nilivyokuwa jana.” 350

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 350

9/4/2017 3:48:02 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Idadi kubwa ya Maquraishi walimchukia Ali, na wengi wao waliasi na kupanga njama dhidi yake. Wa mbele kabisa kati ya maadui zake miongoni mwa Maquraishi walikuwa ni Talha na Zubeir. Watu hawa, hata hivyo, hawakuweza kuepuka kuchukua kiapo cha utii kwa Ali kwa sababu wakazi wa Arabia yote na nchi zote zisizo za Kiarabu ambazo zilitekwa, na hususan watu wa Misri, hawakuwa tayari kumkubali mtu mwingine yeyote kama khalifa. Alikuwa ni Ali peke yake tu aliyekuwa na sifa ambazo wale wapinzani wa Uthman walitaka kuziona ndani ya mtawala wao. Talha na Zubeir walikuwa ni wapinzani wakubwa wawili wa Ali katika suala la ukhalifa. Walikuwa na bidii sana ya kupanda kwenye cheo hicho. Hata hivyo, hakuna hata tabia moja ambazo wapinzani wa Uthman walitaka kuziona kwa khalifa wao zilizopatikana kwao. Wote wawili, ni kama vile Uthman tu, na yale mambo ambayo yaliwafanya watu waasi dhidi yake yote yalipatikana kwao. Walikuwa wakitaka sana madaraka na mamlaka. Katika kurasa zilizotangulia tayari tumekwisha kumnukuu Uthman akisema kuhusu Talha kwamba: “Talha naalaaniwe! Nimempa dhahabu nyingi sana na bado anataka kuchukua maisha yangu.” Watu walikuwa wakiyatambua vema mambo haya kwa wagombea wa ukhalifa, na walikuwa hawana wasi wasi kuhusu kutofaa kwao kwenye cheo hicho. Hiyo ndio sababu ya kwa nini wote walielemea kwa Ali na wakakivunja Talha na Zubeir pia kuchukua kiapo cha utii kwake Ali. (Tumekwisha jadili kwa kirefu chini ya kichwa cha makala ‘Hadhrat Amir al-Mu’minin’ sehemu ya III), iwapo Talha na Zubeir walichukua kiapo cha utii kwa Ali kwa hiari au bila hiari, na pia tumenukuu ile fatwa ya yule mwanachuoni wa Misri Dr. Taha Husein kwamba wote hao walichukua kiapo cha utii kwa hiari kwa matumaini kwamba Ali angewafanya kuwa wenzi wake katika mambo ya ukhalifa, lakini yeye alipokataa kutimiza matakwa yao hayo wao wakakivunja kiapo na kujiunga na Aisha, wakisema kwamba kiapo hicho kilipokelewa kutoka kwao chini ya vitisho. Na kuhusu kuchukua kwao kiapo cha utii kwa Ali na halafu wakakivunja na kuasi dhidi yake, Ali anasema: “Wawili hawa waliingia kwenye utii kwa nyuso za watenda dhambi, na wakatoka nje yake kwa sura za makafiri.” (Ina maana kwamba wakati ambapo watu wengine walichukua kiapo cha utii kwa Ali ili kwamba mambo yaweze kuwekwa sawa; lakini wawili hawa hawakuchukua kiapo hicho kwa lengo hilo akilini mwao, na wakati walipokivunja kiapo hicho ulikuwa ni ukosefu wa uaminifu tu 351

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 351

9/4/2017 3:48:02 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

na udanganyifu kwenye kanuni ya Ali ambayo msingi wake ulikuwa juu ya ukweli na haki). Tokea siku ile ile ya kwanza Ali aliposhika madaraka au ukhalifa alitingwa na shughuli ya kufanya mageuzi. Aliwaondoa wale magavana na maafisa waonevu na madhalimu kutoka kwenye kazi zao, na akaanza kuchunguza kuhusiana na utajiri uliochukuliwa na watu mbali mbali bila uhalali kutoka kwenye Hazina ya Umma. Katika kuchukua hatua hizi hakujali juu ya uadui wa wale ambao wanampinga yeye na mageuzi ambayo alikusudia kuyaanzisha. Katika kipindi cha ukhalifa wake, Imam Ali ilimbidi akabiliane na hali ngumu. Watu mashuhuri wote walikuwa wameungana dhidi yake. Vivyo hivyo ndivyo ilivyokuwa suala la wapenda makuu ambao idadi yao ilikuwa kubwa sana. Ali aliamua kupigana katika pande zote. Aliamua kusimamisha uadilifu na kubomoa udhalimu. Vile vile aliamua kusimamisha serikali iliyoegemea kwenye uchumi halisi, maadili ya kijamii na unyofu. Na alipigana kwenye pande zote hizi mbili kwa ujasiri na uimara ambao ulikuwa haulinganishiki na usio wa kawaida. Alifanya maamuzi imara kwamba ataondoa giza lote na kwamba elimu yake kama mionzi ya jua itaangaza pembe zote za dunia. Mara tu watu walipomchagua Ali kama kiongozi wao kuirekebisha jamii, Bani Umayyah na marafiki zao hapo Madina na kwenye miji mingine walikusanya utajiri wao na silaha na kuingia mafichoni (kichinichini). Baadae, mara tu walipoipata fursa, wakaenda Makkah ambako wangeweza kujiingiza kwenye shughuli za kichochezi dhidi ya serikali ya Ali, na kuwashawishi watu kuasi dhidi yake, na endapo kama wasingepata mafanikio pale wangeweza kwenda Syria na kujiunga na Mu’awiyah. Kama watu hawa wangefikiria juu ya ustawi wa umma na wasingeutamani ukhalifa, ilikuwa sio lazima kabisa kwao kufanya upangaji wote huu. Hata hivyo, walijiingiza kwenye shughuli kama hizo kwa matumaini kwamba wangeweza kuupata tena huo ukhalifa; na endapo wangefanikiwa kumwondoa Ali kutoka kwenye njia yao, cheo hiki kisingeponyoka tena kamwe kutoka mikononi mwao. Zaidi ya hayo, walikuwa wamelimbikiza utajiri wa ajabu wakati wa siku za utawala wa Uthman na hili pia liliwachochea kwenda kusikofikika juu ya khalifa wa haki kwa sababu wangeweza kuutumia utajiri huu katika kujiimarisha wenyewe kwa ajili ya ufanikishaji wa lengo hilo. 352

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 352

9/4/2017 3:48:02 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Ali hakuwa kama hautambui mpango wa Bani Umayyah. Alijua ni kwa lengo gani wao walikuwa wamekimbia pamoja na utajiri wao na silaha. Yeye, kwa hiyo, aliweka masharti katika kuondoka kwao Madina ili wasije wakawa ni hatari kwa hiyo serikali mpya. Wakati wa mazingira haya magumu, baadhi ya masahaba wa Mtume, ikiwa ni pamoja na Talha na Zubeir, walikuja kumuona Amirul-Mu’minin na wakasema: “Sisi tulichukua kiapo cha utii kusudi sheria za adhabu ziweze kutekelezwa. Kwa hiyo unapaswa kuwaadhibu wale watu ambao walifanya uasi dhidi ya Uthman.” Ali aliwajibu hivi: “Enyi ndugu zangu wapendwa! Kama mnavyotambua mimi sio kama silizingatii jambo hili. Hata hivyo, swali ni iwapo kama ninazo nguvu za kutosha kufanikisha lengo hili. Kwa sasa hivi hao waasi wana uwezo mkubwa sana. Ni wao wanaotumiliki (kwa sasa hivi) na sio sisi tunaowamiliki wao. Zaidi ya hayo, watumwa wenu na Waarabu wa jangwani pia wameungana nao, na wako katika hali ya kuweza kuwafanyieni nyie madhara ya kila namna. Katika mazingira hayo kuna uwezekano wowote ule wa kuweza kufanikisha hilo mnalolitaka?” Wote hao wakajibu kwa kinyume chake; hapana. Ndipo Ali akaendelea: “Naapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba sidhani kama mnao. Wakati suala hili litakapojadiliwa, watu watakuwa na maoni tofauti kuhusu hilo. Baadhi yao watakuwa na maoni kama mliyokuwa nayo ninyi, ambapo wengine watakuwa na maoni yanayopingana na yenu. Na bado kutakuwa na wengine ambao watakuwa hawana upande. Kwa hiyo mnapaswa kusubiri hadi hali itakapotulia, watu wakapata utulivu wa akili na halafu inakuwa rahisi kupata haki. Kwa kiasi ambacho mimi ninahusika, mnapaswa kubaki mkiwa mmeridhika na kusubiri maagizo yangu. Ni hapo tu ndipo ambapo sasa mtaweza kunijia mimi.” Watu hawa walikuja kumuona Ali wakiwa na mashaka akilini mwao kuhusu serikali yake na mwelekeo wake kwa watu. Yeye hata hivyo, aliwapa majibu ambayo yaliwabadili mashaka yao kuwa uhakika. Walikuwa wameweka sharti kwa ajili ya kushika kwake ukhalifa kwamba ni lazima awaadhibu wale watu ambao juu yao, sio yeye wala wao ambao walikuwa na udhibiti wowote juu ya watu hao. Watumwa wao wenyewe na Waarabu wa jangwani walikuwa miongoni mwa wapinzani na wauaji wa Uthman. Yeye aliwapa majibu ya kuridhisha kiasi kwamba iliwabidi kukubali kwamba alikuwa na ujuzi bora wa hali za mambo kuliko waliokuwa nao wao, alikuwa anafanya juhudi kubwa kuboresha mambo, na aliuelewa unyeti wa hali hiyo vizuri 353

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 353

9/4/2017 3:48:02 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

zaidi kuliko wao. Kwa bahati mbaya, hata hivyo, watu hawa walikuwa hawautambui ukweli ambao Amirul-Mu’minin aliufahamu kwa uwazi kabisa na wakati ambapo ilikuwa ni muhimu kubaki kuwa mvumilivu, walimtaka yeye achukue hatua za haraka haraka. Watu hawa walikuwa na mawazo potovu kwamba Waislamu wote waliyaona mauaji ya Uthman kwa namna moja, na walichukulia kwamba damu yake lazima ilipiziwe kisasi. Hata hivyo, kwa vile Ali alikuwa na ujuzi bora zaidi wa hali hiyo kuliko waliokuwa nao wao, aliondoa kutoelewa kwao kwa kusema kwamba iwapo suala la kuwaadhibu wauaji wa Uthman lingechukuliwa katika hatua ile, maoni ya watu juu ya suala hilo yatagawanyika. Watu wale walikuwa wamekuja kwa Ali pamoja na shauku zao, matamanio yao, na malengo binafsi. Hata hivyo, Ali alikabiliana nao kwa hoja na mantiki. Badala ya kumwita yeye ‘Amirul-Mu’minin’ (kiongozi wa waumini) wao walisema: “Ewe Ali!” Ukali na ufidhuli wa maneno haya uko dhahiri kabisa ambapo lile neno ndugu lililotumiwa na Ali kwa ajili yao lilibeba hisia za mapenzi na upendo. Walikuja kuhusu madai ya kisasi kwa ajili ya mauaji ya Uthman, ingawaje wengi wao walikuwa wao wenyewe wanahusika kwa mauaji yake. Hata hivyo, katika kuyajibu madai yao; Ali alionyesha msamaha usio na kifani, ambao ulikuwa ni wa asili katika tabia yake. Ali alianza kuwaweka Maquraishi chini ya uchunguzi mkali isije ikawa wakaweza kusababisha vurugu. Kama mambo yalivyokuwa, kitendo hiki kwa upande wake kilikuwa sahihi kabisa na kiliegemea kwenye uona mbali na uangalifu. Ali alianza kuwaondoa magavana wa Uthman kwenye kazi zao, mmoja baada ya mwingine. Hakukuwa na suala la kumbakisha yeyote kati yao na kuwafukuza wengine kwa sababu walikuwa wote wanafanana katika suala la udhalimu, uonevu na utovu wa heshima kwenye sheria za Kiislamu. Ilikuwa ni kwa sababu ya uonevu na upotofu ambapo vurugu zikatokea katika sehemu mbali mbali za nchi za Kiislamu; na kama matokeo, ikambidi Uthman kupoteza maisha yake. Ali hakukubali kuwaachia watu hawa kuendelea katika kazi zao hata kwa kipindi kifupi tu cha wakati kwa sababu haki na batili haviwezi kwenda pamoja; na uonevu, udhalimu na upotofu haviwezi kuondolewa ila mpaka kiini cha maovu haya kiwe kimeondolewa.

354

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 354

9/4/2017 3:48:02 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Ibn Abbas na wengine wengi walipendekeza kwa Ali kuwaacha magavana hao kushika nafasi zao hadi serikali yake itakaposimama imara lakini yeye hakukubali kukimbilia kwenye hila za kisiasa au kuimarisha serikali yake kwa kuwafurahisha wapenda makuu. Yeye, kinyume chake, alitegemea juu ya wajibu wake, akili na upanga, na akabakia imara katika dhamiri yake ya kuyaondoa maovu yote. Syria ilikuwa ndio wasiwasi wake mkubwa. Tumekwishataja tayari katika kurasa zilizotangulia, yale mawazo ambayo Ali alikuwa nayo juu ya Mu’awiyah. Aliamua kumuondoa Mu’awiyah kutoka kwenye ugavana wa Syria, na yeye Mu’awiyah alikaidi kwamba hatachukua kiapo cha utii kwake. Siku moja Ziad bin Hanzala alikutana na Ali kutaka kujua ni uamuzi gani ameuchukua kuhusu Mu’awiyah ili aweze kuwajulisha watu juu ya hilo. Imam Ali akamwambia Ziad: “Oh, Ziad! Jiandae.” Ziad akauliza: “Ewe Amirul-Mu’minin! Nijiandae kwa ajili ya kitu gani?” Ali akamjibu: “Kukusanya majeshi ili kuishambulia Syria.” Ziad akasema: “Ewe Amirul-Mu’minin! Itakuwa bora kuwa mpole na mvumilivu.” Hapo ndipo Ali akasoma Aya ambayo ina maana: “Utakuwa huru kutokana na udhalimu pale tu ambapo akili yenye uelewa wa haraka, upanga mkali, na pua yenye hisia za heshima vikichanganyika pamoja.” Ali alianza kufanya maandalizi kwa ajili ya kutoka dhidi ya Syria na kumwadhibu Mu’awiyah. Katika kuiona shauku yake, watu nao pia wakawa mashughuli na wakawa tayari kumuunga mkono. Hata hivyo, walikuwepo pia watu ambao walikuwa wamedhamiria kumpinga Ali na katika kundi hilo walikuwemo Talha na Zubeir. Wao walikuja kukutana naye na wakasema: “Ewe Amirul-Mu’minin! Tunakuomba uturuhusu kwenda Makkah kufanya Umra. Kama utakuwa bado upo hapa mpaka tutakapokuwa tumekwisha kutekeleza taratibu za ibada ya Umra, basi tutarudi kuja kuungana nawe. Na endapo kama utaandamana nasi basi tutakufuata.” Ali aliwaangalia nyusoni mwao kwa kitambo kidogo na halafu akasema: “Lengo lenu halisi sio kufanya Umra, bali kufanya usaliti dhidi yangu. Hata hivyo, mnaweza kwenda popote mnapotaka kwenda.” Talha na Zubeir ndipo wakaondoka kwenda Makkah. Bani Umayyah, Talha na Zubeir waliungana kula njama dhidi ya Ali. Walifanya kila aina ya udanganyifu na ulaghai na wakatumia pesa nyingi sana kwa ukarimu mwingi ili kuwageuza watu dhidi yake. Wale magavana ambao walikuwa wameteuliwa na Uthman, na wakawa wameondolewa na Ali, waliwasaidia watu hawa kwa kila namna. Walikuwa tayari wamekwisha hamisha utajiri na silaha zao kwenda Makkah

355

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 355

9/4/2017 3:48:02 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

ambayo sasa ilikuwa ndio makao yao makuu. Aisha, binti yake Abu Bakr na mke wa Mtume alikuwa akijihangaisha sana kufanya maandalizi kwa ajili ya vita na Ali kutoka siku ile alipopokea taarifa kuhusu kuchaguliwa kwake kama khalifa. Jinsi gani alizipata taarifa hizi na alizichukuliaje inaweza kukadiriwa vizuri kutoka kwenye kadhia iliyosimuliwa hapo chini. Allamah Tabari anasema kwamba wakati akirejea kutoka Makkah, Aisha alifika sehemu inayoitwa ‘Sarf.’ Alikutana na mtu aliyeitwa Abd ibn Umm Kilab ambaye alikuwa ni ndugu yake kwa upande wa mama yake. Akamuuliza kuhusu hali zilivyokuwa zikiendelea huko Madina. Mazungumzo yafuatayo yakatokea baina yao: Abd ibn Umm Kilab: Watu wamemuua Uthman kisha wakasubiri kwa siku nane. Aisha: Walifanya nini halafu? Abd ibn Umm Kilab: Idadi yote ya watu wa Madina walipata njia kutokana na makubaliano ya pamoja. Wote wamekubali Ali kuwa khalifa. Aisha: Kama unayoyasema ni kweli, natamani kwamba mbingu zingeangukia juu ya ardhi. Nirudisheni. Nirudisheni. Aisha alikuwa anatoka Makkah kwenda Madina baada ya kutekeleza ibada ya Hijja. Hata hivyo, pale aliposikia kuhusu kule kuwa kwake Ali ndio khalifa, ghafla alirejea Makkah akisema: “Uthman ameuawa bila haki, kadhulumiwa! Wallahi nitalipiza kisasi juu ya kifo chake!” Abd ibn Umm Kilab: Haya yote ni ya nini tena? Namuapa Mwenyezi Mungu kwamba wewe ulikuwa ndio mtu wa kwanza kabisa katika kumshutumu Uthman. Ulikuwa wakati wote ukisema: “Muueni Nath’al. Yeye amegeuka kuwa kafiri.” Aisha: Watu wamemuua baada ya kuwa amekwishatubia. Ndio, niliyasema maneno haya, lakini ninachokisema sasa hivi ni bora kuliko yale niliyoyasema hapo kabla. Abd ibn Umm Kilab: Ewe Ummul-Mu’minin, hicho ni kisingizio kisichofaa kabisa. Hapa Tabari amenukuu baadhi ya beti za Abd ibn Umm Kilab, ambaye ametupia lawama za kuhusika kote na mauaji ya Uthman juu ya Aisha. Yeye anasema: “Ilikuwa ni wewe uliyeyaanzisha. Mabadiliko yaliletwa na wewe, na matatizo yote yalianzia upande wako. Ulituagiza tumuue Uthman. Ulisema kwamba yeye alikuwa amegeuka kuwa kafiri. Tumekutii wewe na tukamuua yeye. Tu356

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 356

9/4/2017 3:48:02 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

nashikilia maoni kwamba muuaji wa Uthman ni yule mtu ambaye ameagiza kwamba auawe. Sio mbingu zilizotuangukia, wala jua na mwezi havikupatwa.” (Tarikh Tabari, Juz. 5, uk. 140). Aisha alirejea Makkah na alikuwa amezamia kwenye mawazo yake mwenyewe binafsi. Wakati alipofika Makkah, Talha akakutana naye. Akamwelezea jinsi Ali alivyokuja kuwa khalifa na kile ambacho watu walimfanyia (yeye Talha). Alisema: “Watu walichukua kiapo cha utii kwa Ali na halafu wakaja kwangu na wakanishinikiza kwa nguvu sana kiasi kwamba na mimi pia ikanibidi kuchukua kiapo hicho.” Aisha akasema: “Ali atatumiaje madaraka juu yetu sisi? Madhali serikali yake ipo Madina, mimi sitarejea tena kwenye mji ule.” Kuanzia wakati ule na kuendelea mbele, yeye alianza harakati za fitna dhidi ya Ali. Akaanza kuwachochea watu kulipiza kisasi cha mauaji ya Uthman na kumuua Ali. Katika kuangalia kwa makini mwelekeo uliochukuliwa na Aisha kwa hali ya mambo jinsi ilivyo, mtu anaweza kutambua vizuri kabisa ule mfundo wa kisasi aliokuwa anaulea moyoni mwake dhidi ya Ali. Ili kuuelewa huu mwelekeo wake ni muhimu kujua ile sababu ya uhasama wake dhidi ya Ali. Chuki na uadui wa Aisha dhidi ya Ali ulikuwa ni wa zamani sana, na kwa mujibu wa wanahistoria wengi, haya yalianza siku ile hasa ambayo Aisha aliingia kwenye nyumba ya Mtume kama mke wake. Sababu moja kubwa sana ya uadui dhidi ya Ali ni kwamba yeye Ali alikuwa ni mume wa Fatimah. Fatimah alikuwa ni binti ya Khadija, na Khadija alikuwa ndiye Bibi aliyekuwa akiheshimiwa sana na Mtume wakati wa uhai wake na vile vile baada ya kufariki kwake kwa ajili ya uaminifu wake, ukarimu na maadili na tabia bora kabisa. Licha ya juhudi zake bora kabisa, Aisha hakuweza kumfanya Mtume amsahau Khadija. Kuhusiana na hili; dondoo ifuatayo kutoka kwenye gazeti la ‘Al-Azhar’, ambalo ni chombo cha Chuo Kikuu cha Azhar inastahili kuangaliwa: “Mbali na sifa nyingine ambazo Aisha alikuwa nazo, alikuwa ni jasiri sana na alikuwa akipenda sana kupata daraja la juu sana la umaarufu. Yeye hakuridhika na ile nafasi ya juu sana ambayo alikuwa nayo katika moyo wa Mtume ukilinganisha na wake zake wengine, bali alitamani kupata nafasi katika moyo wake sawa na ile ya Bibi Khadija. Yule mkweli wa mwanzo, ambaye alimpenda sana. Mtukufu Mtume hakuchoka kamwe kuongea kuhusu yeye Bi. Khadija na kumsifu sana. Ilikuwa ni kutokana na yeye huyo kwamba Mtume pia alionyesha wema na huruma kwa wanawake, ambao walikuwa marafiki zake Bi. Khadija. Pamo357

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 357

9/4/2017 3:48:02 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

ja na sifa zake zote na utimilifu, Aisha alifanya jitihada tupu kumfanya Mtume aamini kwamba Mwenyezi Mungu amempatia mke bora kuliko Bibi Khadija. Alipaswa kukubali ubora wa Khadija na alipaswa kutambua kwamba ilikuwa ni kazi bure kushindana na Mtume kwa sababu ya yule mke wake ambaye alikuwa ndiye maarufu kabisa miongoni mwa wanawake waungwana na mashuhuri wote, alikuwa ndiye mwaminifu kabisa, na alikuwa wa kwanza kuufuata Uislamu. Wivu huu wa Aisha haukufanya madhara yoyote kwa Khadija. Kinyume chake ulifanya umaarufu wake kujulikana duniani kote na ukampatia heshima ya kudumu.” (The Al-Azhar Magazine, May, 1956). Aisha mwenyewe anasema: “Sikujihisi kamwe kuwa na wivu kwa mke mwingine yoyote wa Mtume kama niliokuwa nao kwa Khadija, ingawaje sikuwahi kumuona. Mtume alizungumza juu yake kila mara. Na nyakati nyingine alichinja kondoo na kupeleka vipande vya nyama kwa marafiki zake Khalija kama zawadi. Nilimwambia mara nyingi sana (kutokana na namna ambavyo alizungumza kuhusu Khadija) kwamba ilionekana kana kwamba hakuna mwingine tena katika dunia isipokuwa Khadija. Yeye, hata hivyo, alikuwa akijibu kwamba yeye Khadija alikuwa na sifa kama hizo na pia alimzalia watoto.” Hivyo Aisha anakiri kwamba Mtume alimpendelea zaidi Khadija kuliko wake zake wengine wote, na hili lilimfanya yeye Aisha amuonee wivu Khadija. Na bila shaka kabisa kwa vile mapenzi haya ya kupita kiasi juu ya Khadija ndio yaliyokuwa chanzo cha wivu wa Aisha dhidi yake, alijihisi wivu vile vile juu ya Fatimah na pia akamchukia mume wake Ali na wanawe Hasan na Husein. Sababu nyingine ya Aisha kuwa na kinyongo dhidi ya Ali ilikuwa ni yale mapendekezo yaliyotolewa na Ali kwa Mtukufu Mtume wakati wa tukio lililoitwa Ifk (shutuma za uongo). Katika kadhia hiyo yeye alikuwa amesema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Hakuna upungufu wa wanawake kwa ajili yako. Unaweza ukaoa wanawake wengine wengi mbali na Aisha.” Zaidi ya hayo, ni ukweli pia kwamba Aisha alikuwa akijiamini kwamba baada ya Uthman kuwa ameuawa, ukhalifa ungerudi kwenye familia yake mwenyewe (yaani, Bani Tayim) na Talha angekuwa ndio khalifa. Tumekwisha kutaja hapo kabla, ni jinsi gani alivyokuwa amejisikia furaha pale aliposikia habari za kuuawa kwa Uthman, akitarajia kwamba Talha lazima atakuwa amechaguliwa kama khalifa mahali pake Uthman. Mara tu alipowasili Makkah Aisha akaanza kuandikisha jeshi la kupigana dhidi ya Ali na serikali yake. Uhasama wake wa dhahiri na Ali uliimarisha mikono ya Bani 358

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 358

9/4/2017 3:48:02 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Umayyah na ile ya Talha na Zubeir na wafuasi wao halikadhalika. Wote walikuwa wameungana katika jambo la kuanzisha vita dhidi ya Ali. Kwa hali ya mambo yalivyokuwa, watu wa familia ya Ummayah walikuwa wamekwenda kujificha kichini chini ndani ya Hijaz na kadhalika. Baada ya Ali kuwa tayari amekwishakuwa ndio khalifa, wao wakajitokeza. Walijaribu kupata mafanikio ya hali ya juu kabisa kutoka kwenye uasi wa Maquraishi dhidi ya Ali. Waliungana na Aisha, Talha na Zubeir na wakaweka mikononi mwao ule utajiri wao ambao walikuwa wameunyakua katika wakati wa Uthman; ili kwamba waweze kuutumia katika kufanya maandalizi kwa ya ajili ya vita, na serikali ya Ali iweze kuzuiwa kuendelea. Waliondoka kwenye zile sehemu ambazo walikuwa wamejificha na wakaenda Makkah kumsaidia Aisha. Msimamo waliouchukua wao ulikuwa kwamba Uthman alikuwa ameuawa bila haki na kwa vile Aisha, Talha na Zubeir wameamka kulipiza kisasi mauaji yake, ilikuwa ni muhimu sana kuwasaidia. Mu’awiyah aliiona hali hiyo kuwa yenye kufaa sana kwake. Hata hivyo, shauku zake zilitofautiana na zile za Talha na Zubeir kwa sababu kila mmoja wao alikuwa akigombea kuwa khalifa. Mu’awiyah alitaka kwamba Talha na Zubeir wapigane na Ali, kwa sababu matokeo ya pambano hilo kundi moja lilikuwa na hakika ya kushindwa na lile jingine lililopata ushindi litakuwa dhaifu na itakuwa rahisi kwake yeye (Mu’awiyah) kulishinda nguvu na kulitiisha. Ilikuwa ni kwa sababu ya haiba yake binafsi na kwa sababu ya kule kuwa mke wa Mtume ambako Aisha aliweza kukusanya jeshi kubwa sana hapo Makkah. Hata hivyo, wakati jeshi hilo lilipokuwa tayari, tofauti zikazuka kati ya Talha, Zubeir na kadhalika, kuhusu ni wapi waelekee na ni hatua inayofuatia iwe nini. Kama harakati na mambo ya wale watu ambao walikuwa kama viongozi wa mkusanyiko huu yanachunguzwa kwa karibu na kwa kina; na juhudi ikafanywa ya kutafuta matilaba au sababu za kukusanya jeshi kubwa kama hilo, hali halisi itakuwa wazi na dhahiri. Halafu itajulikana kwamba hawakukusanyika ili kulipiza kisasi cha mauaji ya Uthman, kama walivyodai wao, wala kwa kurekebisha hali iliyokuwepo, ambayo kulingana na maoni yao, Ali hakuweza kufanya hivyo, wala kwa jambo jingine lolote ambalo wameongea kuhusu hilo katika hotuba zao za kuchochea watu kuasi dhidi ya Ali. Kama mambo yalivyokuwa, wao walikuwa na nia na malengo tofauti, kila mmoja na yake. 359

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 359

9/4/2017 3:48:02 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Kama mmoja wao alikuwa dhidi ya Ali, kwa sababu, kutokana na yeye hawezi akaupata ukhalifa, mwingine alijiunga na mkusanyiko huu kutokana na kinyongo cha tangu zamani dhidi ya khalifa huyo mpya, na bado mwingine alitaka kurudisha heshima na mamlaka ya familia yake ambayo hayakuwa rahisi mbele ya kuwepo Ali katika nafasi ya khalifa. Aisha alikuwa na mawazo kwamba jeshi hilo litembee kuelekea Madina ili yale makao makuu yaweze kutekwa kabla Ali hajakuwa katika hali ya kuweza kuyalinda, na ukhalifa wake ufikishwe mwisho wake. Baadhi ya wengine walipendekeza kwamba wangepaswa kwenda Syria ambayo ilikuwa ni sehemu ya salama. Bani Umayyah, hata hivyo, waliyapinga mapendekezo haya. Wao walikuwa na maoni kwamba usalama wa eneo ambalo wao tayari walikuwa wamekwishajiimarisha vizuri lisije kuwekwa katika hatari. Walijua vizuri kabisa kwamba Mu’awiyah alikuwa ameitawala Syria kwa muda mrefu na watu walikuwa watiifu kwake. Wao hawakutaka, kwa hiyo, kwamba Syria iwe ndio uwanja wa vita. Zaidi ya hayo, Bani Umayyah waliichukulia Syria kuwa ndio kimbilio lao la mwisho endapo watashindwa na Ali, na kwa hiyo, hawakuliona ni katika maslahi yao kusababisha matatizo kwa ajili ya Mu’awiyah ambaye alikuwa akijishughulisha kwa bidii kuanzisha ufalme huko, na halafu kupafanya ni medani ya vita. Talha na Zubeir waliyakataa mawazo ya kwenda ama Madina au Syria na wakapendekeza kwamba waelekee Basra, kwa sababu walikuwa na idadi kubwa ya wafuasi huko Kufa na Basra. Kwa kushauri kwamba waelekee Basra, Talha na Zubeir walikuwa na mpango mzito vichwani mwao. Walijua kama endapo watafanikiwa dhidi ya Ali kwa msaada wa watu wa Kufa na Basra mmoja wao atachaguliwa kuwa khalifa, kwa sababu ukhalifa kwa hali yoyote utakwenda kwa mtu ambaye wafuasi wake walikuwa ni wengi zaidi kwa idadi. Bani Umayyah pia waliunga mkono pendekezo hili. Wote kwa hiyo wakamwendea Aisha na wakamwambia: “Ewe Ummul-Mu’minin! Ni bora uachane na lile wazo la kwenda Madina, kwa sababu watu tulionao hawataweza kupigana dhidi ya waasi kwa mafanikio zaidi. Kwa hiyo, ungefuatana nasi kwenda Basra. Inawezekana kwamba watu wa sehemu hiyo wanaweza kutokubaliana nasi na wakaweka mbele kisingizio cha kwamba tayari kiapo cha utii kwa Ali kimekwishatimizwa. Kama hali itakuwa ni hivyo, basi utawaandaa kuchukua kisasi cha mauaji ya Uthman kwa namna ile ile ambayo umewaandaa watu wa Makkah kwa ajili ya lengo hili.” 360

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 360

9/4/2017 3:48:02 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Bani Umayyah walitumia kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya upatikanaji wa vifaa vya kivita. Mpiga mbiu alitoa tangazo lifuatalo katika mitaa ya Makkah: “Ummul-Mu’minin Aisha, Talha na Zubeir wanaelekea Basra. Yeyote yule anayeusikitikia Uislamu, anayeutakia heshima yake, na anataka kupigana dhidi ya maadui na kulipiza kisasi cha mauaji ya Uthman, anapaswa kuandamana nao. Kama mtu hana mnyama wa kipando na mahitaji mengine ya vifaa, anapaswa akavipate kutoka kwao.” Pale Aisha alipokuwa amekwisha kulikusanya jeshi, na alikuwa tayari kuondoka kuelekea Basra, Umm Salma, mke mwingine wa Mtume, alikutana naye na akapingana naye. Yeye alisema: “Mpaka hivi karibuni ulikuwa ukiwachochea watu kuasi dhidi ya Uthman, na ulimuongelea vibaya. Hukumuita kwa jina jingine lolote mbali na lile la Na’thal.” Halafu alisisitiza juu ya Aisha kwamba abakie nyumbani na asiongoze jeshi dhidi ya Ali. Hata hivyo, alipotambua kwamba Aisha alikuwa amedhamiria katika kuanzisha vita dhidi ya Ali, yeye akamtuma mwanawe, Umar bin Abi Salamah kwa Ali pamoja na barua ambayo ilisomeka kama ifuatavyo: “Oh, Amirul-Mu’minin! Kama isingekuwa ni sawa na kutomtii Mwenyezi Mungu; na kama nisingekuwa na uhakika vile vile kwamba usingependa kuandamana kwangu nawe, mimi ningeandamana nawe katika vita hivi. Ninamtuma mwanangu Umar. Namuapa Mwenyezi Mungu kwamba yeye ni kipenzi sana kwangu kuliko maisha yangu mwenyewe. Yeye atabakia na wewe na atashiriki katika kila vita akiwa upande wako.” Aisha aliwaalika wake zake wengine Mtume kuandamana naye kwenda Basra. Wote isipokuwa Hafsa binti ya Umar walikataa kukubaliana na ombi lake hilo. Hafsa alijiweka tayari kuungana naye kupigana dhidi ya Ali. Hata hivyo, kaka yake, Abdullah ibn Umar alimzuia kufanya hivyo akisema: “Lazima ubakie ndani kama wake wengine wa Mtume.” Hafsa kwa hiyo, akatuma ujumbe kwa Aisha kumsamehe yeye kwa sababu kaka yake alikuwa hakubaliani na pendekezo hilo. Jeshi lote liliondoka kuelekea Basra chini ya kamandi ya Aisha. Wakati walipofika Khaybar, Aisha, Talha, Zubeir na Marwan walikutana na Sa’id bin Aas na Mughirah bin Shu’ba. Tumekwishaelezea mazungumzo yao katika kurasa zilizotangulia. Kisha kulingana na mpango mzima wa Bani Umayyah, Sa’id bin Aas alijitahidi kuwagawanya watu hawa na kuwafanya wapigane wenyewe kwa wenyewe ili kwamba kwa kufanya hivyo wao waweze kupoteza nguvu zao na serikali iweze kure361

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 361

9/4/2017 3:48:02 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

jea kwa Bani Umayyah. Yeye kwa hiyo, akazungumza faraghani na Talha na Zubeir kama ifuatavyo: Sa’id: Hebu niambieni kwa dhati, ni nani mtakayemchagua kuwa khalifa kama mkifanikiwa? Talha na Zubeir: Yeyote kati ya sisi wawili atakayechaguliwa na watu. Sa’id: Hapana. Mnapaswa muitoe kazi hii kwa mmoja wa watoto wa Uthman, kwa sababu ni kifo chake ndio ambacho mnachowazia kukilipizia kisasi. Talha na Zubeir: Ha haa haa! Yaani tumnyanyue kijana mdogo kwenye cheo hiki mbele ya kuwepo watu maarufu chungu nzima? Sa’id: Kama mambo ni hivyo, basi ni lazima nijitahidi kwamba ukhalifa hautoki mikononi mwa kizazi cha Abd Manaf. Marwan pia akajaribu tena na tena, kama Sa’id bin Aas kuwagawanya watu hawa. Alifanya hivyo kwa hila ambayo ilikuwa ndio mfano bora kabisa wa udanganyifu na ulaghai. Imam Ali pia alikuja kujua kwamba jeshi kubwa sana lilikuwa limeondoka Makkah kuelekea Basra kwa kisingizio cha kulipiza kisasi kwa wauaji wa Uthman. Alivurugikiwa sana kutokana na tofauti na mifarakano hii kati ya Waislamu. Pia ilimkera sana kwamba kutokana na tofauti na faraka hizi haitawezekana kuendelea na kukamilisha ule mpango wa marekebisho aliouanzisha yeye, kwa sababu kwa kufuata mfano wa waasi hawa na wengine pia watapata moyo wa kuasi na magavana mbali mbali waliokuwa wameteuliwa na Uthman wanaweza pia kufuata nyayo za Mu’awiyah na wakakataa kuyatambua mamlaka ya serikali kuu. Mara tu alipozipata taarifa hizi, aliwakusanya watu wa Madina, na akawahutubia kwa maneno haya: “Mwenyezi Mungu ameahidi msamaha kwa ajili ya udhalimu wa umma huu na mafanikio na wokovu kwa wale ambao ni watiifu na imara. Ni yule mtu tu, ambaye hawezi kuvumilia haki ndiye anayekimbilia kwenye batili. Mnapaswa kujua kwamba Talha, Zubeir na mama wa waumini Aisha wameungana dhidi ya serikali yangu na ukhalifa wangu na wamewaalika watu kuelekea kwenye mapinduzi. Alimuradi sioni hatari yoyote kutoka kwao juu yenu ninyi na kwangu mwenyewe, basi nitabakia mwenye subira na madhali wanaizuia mikono yao, mimi pia nitaizuia yangu. Na ninaridhia binafsi na taarifa kuhusu wao ambazo nimekwisha zipata hadi kufikia sasa hivi.” 362

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 362

9/4/2017 3:48:02 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Imam Ali alichukulia kuwa ni muhimu kuzuia maendeleo ya vurugu hizo na kuwasimamisha watu wa Makkah njiani kabla hawajaweza kufika Madina, kwa sababu hii ilikuwa ndio njia nzuri ya kuepuka machafuko na umwagaji damu. Yeye kwa hiyo, alimteua Sahl bin Hanif kama mwakilishi wake hapo Madina na akatoka kuelekea Makkah pamoja na jeshi ambalo alikuwa amelikusanya hapo kabla kwa ajili ya kushambulia Syria. Humo njiani watu wengi wanaotokana na mji wa Kufa na Basra pia walijiunga naye. Wakati Ali alipofika Rabazah pamoja na jeshi lake alikuja kutambua kwamba Talha na Zubeir walikuwa wamekwishaondoka Makkah na tayari walikwishapita hapo Rabazah wakiwa njiani kuelekea Basra. Alikaa hapo Rabazah kwa siku chache na akafanya maandalizi ya muhimu. Katika wakati huo huo alifanya jitihada zote zinazowezekana ili kwamba hali ambazo zilikuwa zimeharibika kwa sababu ya harakati za Talha, Zubeir na Aisha ziweze kukarabatika. Hivyo, yeye alituma barua kwa Aisha akisema: “Umekhalifu utii kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake kwa kutoka kwako nje ya nyumba yako. Unagombea kitu ambacho huhusiki nacho japo chembe. Na vile vile unadai kwamba unataka kuwarekebisha watu. Tafadhali, je unaweza kunieleza kuhusu – wanawake wanahusika vipi na kuongoza majeshi? Wewe pia unadai kwamba unataka kulipiza kisasi juu ya mauaji ya Uthman. Haya, sasa Uthman alikuwa ni Bani Umayyah ambapo wewe ni mwanamke wa kabila la Taym Bani Murrah. Ninaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kwamba kosa la wale waliokushawishi wewe katika kutwaa njia hii ya utendaji na wakakufanya wewe umuasi Mwenyezi Mungu na Mtume Wake ni kubwa na baya sana kuliko lile la wauaji wa Uthman. Hukuja kukasirika wewe mwenyewe bali ulifanywa ukasirike. Wewe hukutaharuki mwenyewe bali watu wengine wamehusika katika kukutia taharuki. Aisha! Muogope Mwenyezi Mungu na urejee nyumbani kwako ukabakie ndani. Kila la kheri juu yako.” Ali alitaka kumfanya Aisha kama mwenye kusameheka katika suala la kuasi kwake na kuongoza jeshi. Hiyo ndio sababu alisema: “Hukuja kukasirika wewe mwenyewe bali umefanywa ukasirike, na hukutaharuki mwenyewe bali watu wengine walihusika katika kukutia taharuki.” Kujali juu ya huruma kwa wanawake na heshima juu ya Aisha ambavyo maneno haya yamebeba ndani yake ni kwa dhahiri. Kwa kusema kwamba alikuwa muasi kwa amri ya wengine, yeye alimwekea pia njia ya kujitenga yeye mwenyewe kutoka kwenye maasi na vurugu.

363

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 363

9/4/2017 3:48:02 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Aliwashikilia makosani wale watu ambao walikuwa wamemchochea yeye Aisha kutotii na kumfanya yeye aondoke nyumbani kwake. Alikitangaza kitendo chao kuwa ni kikubwa na dhambi mbaya zaidi kuliko ile ya wauaji wa Uthman. Mwishoni kabisa alimshauri kumuogopa Mwenyezi Mungu na kurejea nyumbani kwake, kwa sababu ni kwa hali hiyo tu kwamba amani ingeweza kurejeshwa ndani ya nchi na watu pia wangeyapenda mabadiliko ya maendeleo kama hayo. Aisha hata hivyo hakutilia maanani hata kidogo ushauri huo wa Ali. Alishikilia uamuzi aliokuwa tayari amekwishauchukua. Katika majibu kwa barua ya Ali – Amirul-Mu’minin, yeye aliandika mstari mmoja tu ambao, japo mfupi kabisa, lakini unaonyesha kikamilifu uadui wake binafsi na kinyongo ambacho alikilea dhidi ya Ali ndani ya moyo wake. Yeye aliandika hivi: “Ewe mwana wa Abu Talib! Hakuna nafasi sasa iliyobaki kwa ajili ya suluhu. Sisi kamwe hatutanyenyekea kwako. Unaweza kufanya unavyotaka. Na amani iwe juu yako.” Talha na Zubeir halikadhalika walimtumia majibu kama hayo hayo. Wakati jeshi la Aisha lilipofika karibu na Basra, viongozi walifanya mashauriano kuhusu kama waingie mjini au wasiingie. Walijua vyema kabisa kwamba idadi ya wafuasi wa Ali hapo Basra haikuwa ndogo hata kidogo. Hivyo wao waliona kwamba ingefaa kufanya mashauriano ya pamoja na kuwasiliana na watu wa Basra ili kujua ni kwa kiasi gani walikuwa waaminifu kwa Ali. Hatimae iliamuliwa kwamba kabla ya kuingia hapo mjini wale watu wazima na maarufu lazima washawishiwe kuasi dhidi ya Ali na juhudi lazima zifanywe ili kuweza kuziteka nyoyo zao. Talha na Zubeir kwa hiyo, wakaandika barua kwa Kadhi Ka’b ibn Suur wakisema: “Wewe ni mtu mashuhuri wa Basra na mkuu wa watu wenye asili ya Yemen na ulichaguliwa kama kadhi na khalifa Umar. Ulimkasirikia Uthman kutokana na dhulma aliyokuwa amekufanyia. Sasa unapaswa uwakasirikie wale waliomuua Uthman.” Ka’b ibn Suur aliwaandikia barua ya majibu: “Kama Uthman aliuawa kwa kuwa kwake dhalimu, kwa nini mnakuwa na shauku ya kulipiza kisasi juu ya kifo chake, na yeye anastahili vipi kwamba kifo chake lazime kilipiziwe kisasi? Na kama ameuawa bila uhalali wowote, wapo wengine wanastahili zaidi kuliko ninyi katika kuchukua kisasi juu ya wauaji wake. Na kama suala la Uthman lilikuwa gumu kwa wale waliokuwepo wakati wa kuuawa kwake, basi ni gumu zaidi kwa wale ambao hawakuwepo wakati huo.” Wawili hawa; Talha na Zubeir waliandika barua kwa Manzar bin Jaruud pia ambayo ilisomeka kama ifuatavyo: “Baba yako alikuwa ndio mkuu wa kabila lako katika

364

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 364

9/4/2017 3:48:02 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

zama za ujahilia na pia kiongozi katika Uislamu. Cheo chako kwa kulinganishwa na baba yako ni kile kile ambacho farasi anayechukua nafasi ya pili katika mashindano ya farasi anachopata kwa kulinganishwa na farasi aliyeshika nafasi ya kwanza. Uthman aliuawa na watu ambao ni duni kuliko wewe, na wale watu ambao wamekuja kukasirika kutokana na kuuliwa kwa Uthman ni bora kuliko wewe. Na amani iwe juu yako.” Manzar bin Jaruud alisema hivi katika kuwajibu: “Nitashirikiana na watu waadilifu tu kama ninaweza kubakia bora kuliko wafanya maovu. Haki ya Uthman ilikuwa muhimu na ya lazima jana kwa kiasi kama ilivyo leo. Alikuwa miongoni mwenu lakini mlimuacha bila kumpatia ulinzi na hamkumsaidia. Ni lini mmefanya magunduzi haya mapya na ni vipi wazo hili jipya lilivyojitokeza kwenu?” Aisha aliandika barua kwa Zaid bin Sauhan katika mistari hii: “Kutoka kwa Aisha, binti ya Abu Bakr, Mama wa waumini na mke kipenzi cha Mtume, kwa mwanawe Zaid bin Sauhan. “Kimbilia kuja kunisaidia mara tu upatapo barua yangu hii, na kama hutakuja, basi wazuie watu kutokana na kumuunga mkono Ali.” Zaid bin Sauhan aliandika hivi katika majibu yake: “Mimi bila shaka ni mwanao mwaminifu, alimradi tu ukiacha kujihusisha mwenyewe na suala hili na ukarejea nyumbani kwako. Vinginevyo mimi nitakuwa wa mbele zaidi miongoni mwa wapinzani wako.” Katika Iqdal-Farid, Jamhra Rasail al-Arabi na Sharh Nahjul-Balaghah ya ibn Abi al-Hadid majibu ya Zaid bin Sauhan yamenukuliwa katika maneno haya: “Amani iwe juu yako. Mwenyezi Mungu Mtukufu amekupa wewe amri moja na ametupa sisi nyingine. Wewe umeamriwa usitoke nje ya nyumba yako na sisi tumeamriwa kupigana ili kwamba uovu uweze kuzimwa. Wewe, hata hivyo, umetelekeza kile ulichoamriwa kukifanya na unatuzuia sisi kufanya kile tulichoamriwa kufanya. Matakwa yako hayatatimizwa na barua zako hazitajibiwa. Na amani iwe juu yako.” Bani Umayyah hawakuandika barua kwa wafuasi wao kwa uwazi kama Aisha, Talha na Zubeir. Wao waliendesha mawasiliano ya siri na wale ambao, kama walivyotegemea, watakuwa tayari kumpinga Ali na kuwasaidia katika kuiporomosha ndoto yake ya ukhalifa. Mawasiliano haya ya kisiri siri yanaelezea kikamilifu hali yao ya kisaikolojia.

365

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 365

9/4/2017 3:48:02 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Kama watu hawa walisimama kulipiza kisasi cha kifo cha Uthman, basi haikuwa na umuhimu wa kufanya mawasiliano na wafuasi wao mmoja mmoja kwa siri, na endapo walikuwa wameasi dhidi ya Ali kwa ajili tu ya kumsaidia Aisha, Talha na Zubeir, vile vile haikuwa na muhimu kuyachukulia mambo yao wenyewe tofauti na wengine. Ukweli ni kwamba juhudi zao zote zilielekezwa kwenye kutengeneza mazingira yanayofaa kwa ajili yao wenyewe na waliwasiliana na wale watu tu ambao kuhusu msaada wao walikuwa hawana mashaka akilini mwao. Hiyo ndio sababu mawasiliano yao kwa kawaida yalikuwa ya siri. Wakati makamanda wa jeshi la Aisha walipokuwa wakifanya mawasiliano na watu wa Basra, mwana wa Abu Sufyan, akiwa ametulia huko Damascus, alikuwa akiangalia hali za wale wote ambao walikuwa wameasi dhidi ya Ali na vile vile za wale ambao walikuwa wamekataa kupigana dhidi ya Ali. Alifanya makadirio tofauti kuhusiana na makundi yote mawili na pia alijua matokeo ya mwisho ambayo wote walikuwa wamejaaliwa kuyafikia. Yalikuwa ni matamanio yake ya kweli kabisa kwamba Talha na Zubeir waweze kuidhoofisha serikali ya Ali kwa kupigana dhidi yake. Ilikuwa ni baada ya hapo tu kwamba anaweza akaibadilisha serikali ya Kiislamu kuwa ufalme wa Bani Umayyah kwa sababu alikuwa anajua kwamba kuhusu Bani Umayyah wengine, hakuna aliyekuwa na nguvu na mwenye ushawishi kama yeye mwenyewe alivyokuwa. Mu’awiyah alianza kuwachochea kwa siri kila mtu kuasi dhidi ya Ali, hususan wale ambao walikuwa bado hawana upinzani kwake. Alikuwa akitambua wazi kwamba mara tu Aisha, Talha, Zubeir na viongozi wa maasi wengine wa jeshi lao watakapofanikiwa katika kupata ushindi, wataanza kupigana wenyewe kwa wenyewe. Kushindana kote huku na ukusanyaji wa vikosi dhidi ya Ali ulikuwa tu ni kwa ajili ya ukhalifa. Baada ya kushindwa kwake, Talha na Zubeir walikuwa na uhakika wa kugombana wenyewe ili kuwa khalifa, na kisha Mu’awiyah, ambaye nguvu zake zitakuwa zimesalimika katika kipindi chote hicho, ataweza vizuri sana kuingilia kati na kuunyakua ukhalifa. Mu’awiyah aliandika barua kwa Sa’d ibn Abi Waqas akisema: “Ilikuwa ni lazima kwa wale wajumbe wa lile baraza la ushauri kumsaidia Uthman kwa sababu walikuwa ni wao waliomchagua kama khalifa. Talha na Zubeir walimsaidia (kwa kudai kisasi juu ya mauaji yake). Wote walikuwa ni wajumbe wa baraza hilo kama wewe, na umuhimu unaoufaidi katika Uislamu pia wao hao wanaufaidi. Ummul-Mu’minin 366

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 366

9/4/2017 3:48:02 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Aisha pia ameamua kumsaidia Uthman. Hivyo usikichukie kitu ambacho wao wamekipenda na usikikatae kile ambacho wao wamekikubali.” Inaweza ikaonekana vizuri sana ni uhodari kiasi gani juhudi ilivyofanywa ya kumshawishi Sa’d bin Abi Waqas (ambaye alikuwa mmoja wa wagombea wa ukhalifa walioteuliwa na Umar) kuasi dhidi ya Ali bila ya kulionyesha lengo halisi. Hata hivyo, Sa’d bin Abi Waqas aliuhisi ulaghai huo na hakuingia katika mtego. Aidha, yeye pia alikuwa ni mmoja wa Maquraishi na alikuwa anatambua vema hila ambayo wakati wote Bani Umayyah waliitumia katika kufanikisha malengo yao. Yeye kwa hiyo, akamtumia Mu’awiyah majibu butu ambayo lazima awe hakuyategemea. Yeye (Sa’d) alimtukuza Ali juu ya tabia zake na ujuzi wake na akatamka kwamba hakuna mwingine yoyote anayeweza kulingana naye. Vile vile alimwambia Mu’awiyah kwamba nia ambayo kwayo yeye alikuwa anachochea watu nayo kuasi dhidi ya Ali, alikuwa anaitambua na kwamba ilikuwa wazi kwamba alikuwa anataka kuufikia ukhalifa. Yeye, hata hivyo, aliongezea kwamba juhudi zake zote kuhusu hili zilikuwa hazina maana kwa sababu ilikuwa haikubaliki kwa mtu kama yeye (Mu’awiyah) kushika cheo hicho. Aliandika: “Umar aliwachagua kwenye baraza la ushauri wale watu tu ambao walikuwa na ustahiki wa kuwa khalifa. Hakuna yeyote kati yetu sisi aliyekuwa na haki ya mbele kwenye cheo hicho kwa kulinganisha na wengine isipokuwa kwamba tungemchagua mmoja wetu kama khalifa. Kama mambo yalivyo, Ali alikuwa na sifa zote ambazo tulikuwa tunazo sisi, lakini pia alikuwa na sifa maalum ambazo hakuna kati yetu aliyekuwa nazo. Na kuhusu Talha na Zubeir, ingekuwa ni bora kwa wao kubakia nyumbani. Na kuhusu mama wa waumini, Mwenyezi Mungu amsamehe.” Majibu haya yaliyotumwa na Sa’d kwa Mu’awiyah yanaonyesha wazi kwamba ni maoni gani aliyokuwa nayo Sa’d kuhusu wale ambao walikuwa wamesimama kupigana dhidi ya Ali na kusababisha vurugu katika nchi. Zile barua, ambazo zilifanyiwa mabadilishano kati ya watu wa ngamia na raia wa Basra na pia kati ya raia wa miji mingine, ambao baadhi yao walikuwa wafuasi wa watu wa ngamia na wengine hawakuwa, zinafanya iwe dhahiri kwamba watu walikuwa wanatambua wazi juu ya sababu za vurugu hizo. Zilionyesha pia ile haiba ya Ali. Inakuja kujulikana pia kwamba wale watu waadilifu walimpenda sana Ali na waliyachukulia maneno yake na vitendo vyake kuwa vya kweli na sahihi.

367

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 367

9/4/2017 3:48:02 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Jambo jingine muhimu pia linakuja kujulikana na hilo ni kuwa wafuasi wa Ali walijaribu kwa uwezo wao wote kuwazuia watu wa ngamia kutokana na kusababisha ghasia na vurugu na kutenda kwa busara na akili. Hii inaonyesha kwamba walifikiri na waliongea katika msimamo ule ule aliokuwa nao Ali. Ali alikuwa ameweka athari juu yao kwa maneno na vitendo vyake kwamba kuanzisha vurugu na ghasia ni kitendo cha kishetani na amani na utulivu ndio jambo bora. Hivyo, mwelekeo aliouchukua yeye kabla na vile vile baada ya kuanza kazi ya ukhalifa akitilia maanani hali ya mahitaji ya wakati huo ulichukuliwa na watu hao kuwa ni wa sahihi kabisa. Mtu anaweza hasa akauliza: Ni kitu gani hasa hawa watu wa ngamia walichokuwa wanakitaka Ali akifanye, wakati serikali yake iliyoundwa hivi punde ilikuwa bado haijasimama kikamilifu? Ni hatua gani ya Ali waliyoweza kuchukia wakati walipokuwa wameonyesha uadui mkubwa sana kwake na kuanza kuchochea watu kuasi dhidi yake mara tu baada waliposikia taarifa za kuchaguliwa kwake kama khalifa? Kwa nini walimkasirikia wakati walikuwa hawawezi kukabiliana na hoja zake za busara? Na ni vipi wanaweza kumchukulia kama mwenye kuhusika juu ya mauaji ya Uthman wakati wao wenyewe ndio waliokuwa wauaji wake? Maswali haya yaliulizwa na wafuasi wa Ali kila mara katika mawasiliano na watu wa ngamia. Zaidi ya hayo, wawakilishi wa raia wa Basra ambao walikuja kuwaona pia waliwauliza maswali haya tena na tena. Wakati jeshi la Aisha lilipokuwa bado halijafika kwenye maeneo ya karibu na Basra, na wale watu waliokuwa wamebeba zile barua zilizoandikwa naye Aisha na Talha na Zubeir kwa watu wa Basra walikuwa bado wako njiani, Uthman bin Hunaif alimtuma Abul-Aswad Dueli na Imran bin Hasin kwa Aisha kwenda kujua kutoka kwake juu ya ni kwa nini ameasi dhidi ya Ali na kumshauri kuacha kulifuatilia lengo hilo ambalo kwalo ametoka nje ya nyumba yake. Halafu tena akatuma ujumbe kwa Talha na Zubeir pia kwa makusudi hayo hayo lakini wakarudia kile walichokuwa wakikisema na wakajaribu kuingia Basra kwa nguvu. Kama mambo yalivyokuwa, Uthman bin Hunaif hakuweza kuvumilia uingiaji wao kwenye mji huo. Aliwakusanya watu, akawapatia silaha na wakatoka hadi kwenye kambi iitwayo Marbad ambako jeshi la Aisha lilikuwa limepiga kambi. Wakati majeshi hayo mawili yaliposimama ana kwa ana, uso kwa uso, moja na jingine, Talha alijitokeza mbele na akatoa hotuba. Akiwa amesimama kati yao, alimtukuza Mwenyezi Mungu na kisha akazungumza kuhusu Uthman. Alizihesabu sifa 368

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 368

9/4/2017 3:48:03 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

zake, akaelezea jinsi alivyouawa bila ya haki na akawataka watu hao kuchukua kisasi cha kifo chake baada ya amani itakupokuwa imerejeshwa. Halafu Zubeir akasimama na akatoa hotuba kama hiyo. Baada ya wote kuwa wamekwisha zungumza, wafuasi wake wakasema kutoka upande wake wa kulia: “Kila ulichokisema ni kweli.” Kama hali ilivyokuwa, wale watu waliokuwa na Uthman bin Hunaif wakasema kutokea upande wa kushoto: “Yote uliyoyasema ni ya uongo. Ulichukua kiapo cha utii kwa Ali na halafu ukakivunja na ukaunda umoja dhidi yake.” Hili lilisababisha vurumai na kila mtu akaanza kupiga makelele. Halafu Aisha akasimama ili kuongea. Yeye akasema: “Watu walimshutumu Uthman na wakawatoa makosa maafisa wake. Walikuwa wakija Madina na kutuona sisi kwa ushauri. Pale tulipotafakari juu ya malalamiko ya watu dhidi ya Uthman tulimuona yeye kuwa hana hatia, mchamungu, mkweli, na wale, ambao walisababisha vurugu, kuwa ni wakosaji na waongo. Walikuwa na jambo jingine mioyoni mwao. Wakati idadi yao ilipoongezeka, wakaingia nyumbani kwa Uthman bila ya uhalali wowote, kwani alikuwa hana makosa, na wakamwaga damu ambayo ilikuwa sio halali kuimwaga. Walipora mali kwa dhuluma na wakainajisi ardhi ambayo walipaswa kuiheshimu.” Wale watu wa Basra wakakasirika na wakaitafsiri hotuba yake kwa kufanya makelele. Yeye hata hivyo, akaguta kwa sauti: “Enyi watu! Hebu nyamazeni kimya.” Papo hapo watu wakawa kimya. Akiendeleza hotuba yake alisema: “Kama mambo yalivyokuwa, Amir wa waumini, Uthman alifanya uzushi lakini aliendelea kusafisha upotovu wake kwa kufanya toba hadi alipochinjwa bila haki kama ngamia. Mnaweza kuona kwamba Maquraishi walirusha mishale kwenye shabaha na wakajeruhi nyuso zao wenyewe. Hawakupata faida yoyote kwa kumuua Uthman na hawakufuata vile vile ile sera ya wastani. Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kwamba watalazimika kukabiliana na matatizo makali mno – matatizo ambayo yatawaamsha wale waliolala na kuwafanya wale waliokaa wasimame wima. Na watamilikiwa na watu ambao hawatawahurumia hata kidogo na watakaowaweka kwenye mateso makali kabisa. Tazameni! Uthman ameuawa bila ya haki. Watafuteni wauawaji wake na wakati mtakapokuwa mmewakamata mikononi mwenu basi wauweni. Halafu lile baraza la mashauriano lichukue uamuzi kuhusu uchaguzi wa khalifa. Wajumbe wa baraza wawe ni wale wale waliokuwa wameteuliwa na khalifa Umar, isipokuwa yule mtu ambaye anaweza kuwa ameshiriki katika mauaji ya Uthman. Mmechukua kiapo cha utii kwa Ali ibn Abi Talib chini ya ulazimishwaji wa nguvu na kwa kuchochewa hisia bila ya kuushauri umma.” 369

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 369

9/4/2017 3:48:03 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Hivyo Aisha akaanza kuwachochea watu wamuue Ali. Alisema kwamba kile kiapo cha utii kilichochukuliwa kwa Ali kilichukuliwa kwa kulazimisha kwa nguvu na uchocheaji wa hisia bila ya kupata ushauri wa umma. Aliongezea kwamba Ali alistahili kuuawa kwa vile alishiriki katika mauaji ya Uthman na kwa ajili hiyo ilikuwa ni muhimu kuchagua khalifa mpya kupitia ile kamati iliyokuwa imeundwa na Umar ambayo kwamba Ali asiweze kuwa mjumbe tena. Wasikilizaji hao walikanganyikiwa kusikia hotuba hiyo ya Aisha. Wengi wao akiwemo Ahnaf bin Qais na Jariyah bin Qadamah Sa’id walimuuliza maswali makali sana. Pale alipomaliza hotuba yake Jariyah akamwambia: “Ewe mama wa waumini! Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kwamba kifo cha Uthman hakina umuhimu kiasi hicho kwamba kikilinganishwa na hali mbaya kwamba mtu kama wewe binafsi aweze kutoka nje ya nyumba yake kuja kupigana dhidi ya Waislamu. Umeichana stara ambayo Mola Wako amekupatia, na umeuvunja ule utakatifu ambao Yeye ameuamuru. Unapaswa kutafakari tu kwamba yeyote anayeamua kupigana dhidi yako atanuia vile vile kukuua. Endapo, kwa hiyo, umeandamana na jeshi hili kwa hiari ni bora ungerejea Madina, na kama wamekuleta kwa nguvu basi unapaswa kutafuta msaada dhidi yao kutoka kwenye umma. Hapo ndipo na mimi nitakuwa na wewe.” Talha na Zubeir pia waliulizwa maswali mengi sana na watu mbalimbali, ambao hawakuweza kuwajibu. Mjadala mrefu ukatokea lakini bila ya matokeo yoyote isipokuwa Aisha, Talha na Zubeir wakawa wamekasirika sana na wakazidisha dhamiri ya kupigana. Aisha mwenyewe alikuwa ndio Kamanda Mkuu wa jeshi lake na aliliamrisha akiwa amepanda juu ya ngamia. Ilikuwa ni kwa sababu hii kwamba vile vita vilivyopiganwa kule Basra vikaja vikajulikana kwa jina la Vita vya Ngamia. Aliwateua makamada wadogo na akaandika barua kwa jina lake mwenyewe kwa wale watu ambao walitegemewa kumsaidia yeye. Tumekwisha itoa barua moja tayari hapo juu iliyoandikwa kwa Zaid ibn Sauhan. Barua nyingi za Aisha zilikuwa za aina hii: “Kutoka kwa Ummul-Mu’minin Aisha binti ya Abu Bakr, kwa wanawe, fulani na fulani: Mara tu uipokeapo barua hii unapaswa kuamka na kuja kunisaidia, na unapaswa angalau kuwazuia watu kutokana na kumuunga mkono Ali.” Watu wengi waliitikia mwito wake na pia walikuwepo wengi waliokataa kumfuata.

370

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 370

9/4/2017 3:48:03 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Ewe Mola! Kuwa Shahidi Jeshi la Aisha lililazimisha njia yake ya kuingia kwenye mji wa Basra wakati wa usiku wenye baridi kali. Waliwaua raia wengi ndani ya msikiti. Kisha wakaingia kwenye nyumba ya Uthman bin Hanif wakamfanyia ubaya na kumdhalilisha. Talha na Zubeir walichukia sana vile vitendo ambavyo alitendewa Uthman bin Hanif na askari hao kwa sababu yeye pia alikuwa ni sahaba mashuhuri wa Mtume. (Tumekwisha andika kwa kirefu kwenye kichwa ha habari: “Hadhrat AmirulMu’minin” Sehemu ya tatu kwamba vile vitendo vibaya kwa Uthman bin Hanif huko Basra vilifanywa kwa maagizo ya Talha na Zubeir). Wao wakaenda kwa Aisha kuelezea huzuni zao juu ya tukio hilo. Katika kuwajibu, Aisha akaagiza kwamba Uthman bin Hanif anaweza kuuawa. Amri hiyo ilikuwa karibu kutekelezwa wakati mwanamke mmoja alipopiga kelele: “Ewe Mama wa waumini! Tafadhali juu ya tafadhali, kuwa na huruma juu ya mwana wa Hanif. Hebu chukulia tu kule kuwa kwake ni sahaba wa Mtume.” Aisha akafikiria kwa muda kiasi juu ya jambo hilo, na halafu akasema: “Basi ni sawa. Msimuue huyo bali mfanyeni kuwa ni mateka.” (Tarikh Tabari; n.k.) Afisa mmoja wa jeshi la Aisha hata hivyo akasema: “Mpigeni sana Uthman halafu mumng’oe nywele za ndevu zake.” Askari hao wakampiga sana na kumvuta na kung’oa nywele za kichwa, ndevu, nyusi na kope za macho halafu wakamchukua mateka. Talha na Zubeir wakaanza kuzunguka kwenye majeshi yote na kutoa khotuba zao za kuwataka watu wachukue kisasi cha Uthman kwa Ali. Wakati Zubeir alipokuwa anatoa mojawapo ya hotuba zake kama hizo, mtu mmoja wa kabila la Abd al-Qais alisimama na kumwambia: “Tafadhali nyamaza kwa muda kidogo kwa sababu mimi ninataka kusema kitu fulani.” Halafu akazungumza na Muhajirina ambao waliunda sehemu ya watu wa vita vya ngamia kwa maneno haya: “Enyi Muhajirina! Ninyi ndio watu mlioukubali Uislamu mapema kuliko wengine walivyokuwa, kwa hiyo heshima ni juu yenu kuhusiana na hili. Baada ya kifo cha Mtume mkamchagua mtu kuwa Khalifa bila ya kutushauri sisi. Baada ya kifo chake huyo mkachagua mtu kuwa Khalifa bila ya kututaka ushauri na bado tukamkubali. Baada ya Khalifa wa pili suala la kuchagua mrithi wake liliamuliwa na kamati ya watu sita na mkachukua kiapo cha utii kwa Uthman bila ya kututaka ushauri. 371

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 371

9/4/2017 3:48:03 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Kisha mkawa hamkuridhika naye na mkamuuwa bila ya kututaka ushauri. Sasa mmechukua kiapo cha utii kwa Ali bila ya kutushauri sisi. Sisi hatukukataa kumkubali yeyote kati yao kuwa kiongozi wa Umma na tumethibitisha uchaguzi wenu. Sasa mtuambie ni kwa nini mmejiandaa kupigana dhidi ya Ali. Je, ametumia vibaya ngawira ya vita na akakunyimeni ninyi? Je, amefanya jambo lolote la haramu kinyume cha sharia? Je, amefanya kosa lolote ambalo limemuondolea sifa zinazofaa kwa Ukhalifa? Na halafu maswali haya: Kwa nini mna bidii sana kwamba na sisi pia tujiunge nanyi kupigana dhidi ya Ali?” Alimalizia hotuba yake kwa maneno haya: “Ikiwa hakuna jambo lolote kama hilo ambalo limetokea, kwa nini mmesababisha kero yote hii?” Hakuna aliyeweza kutoa jibu lolote juu ya hotuba yake. Wote walipigwa na butwaa. Hata hivyo, nguvu ya ukatili huwa haifuati mantiki yoyote. Wafuasi wa Talha na Zubeir walimshambulia mtu huyo lakini ndugu zake wakaja kumsaidia. Mapigano makali yakatokea hapo na hatimae yule mzungumzaji akauawa pamoja na watu sabini wa kabila lake. Wale watu wa vita vya Ngamia wakapata udhibiti juu ya sehemu zote muhimu na wakakikamata kiasi chote cha mapato na Hazina ya Umma vile vile. Zubeir na mwanawe Abdullah wakaigawanya mali yote hiyo ya Hazina ya Umma miongoni mwa wafuasi wao. Hakim bin Jabalah ambaye alikuwa mtiifu na mwaminifu sana kwa AmirulMu’minin alivurugikiwa sana kutokana na mishughuliko ya watu hawa. Aliwakusanya wengi wa wafuasi wake na wakawashambulia wale watu wa Ngamia. Alisema kuhusu Talha na Zubeir: “Walichukua kiapo cha utii kwa Ali kwa hiari zao na wakaahidi kumtii yeye. Sasa wamekuja kupigana dhidi yake kama wapinzani wake na wanataka kulipiza kisasi cha mauaji ya Uthman. Wao wemezusha tofauti kati ya watu ingawa wote sisi ni wa mji mmoja na tulikuwa majirani wa kila mmoja wetu. Ewe Mungu! wala sio nia ya yoyote yule kati yao ya kulipiza kisasi juu ya mauaji ya Uthman.” Hakim aliuawa, na vile vile mwanawe na ndugu yake pia waliuawa. Baada ya hapo, Talha na Zubeir wakawatwanga watu wa Basra kwa panga zao na kuwaua. Watu wa vita vya Ngamia sasa wakawa na udhibiti kamili juu ya Basra na wakawa watawala wa kidikteta wa mji huo. Watu wa Basra wakachukua kiapo cha utii kwa Talha na Zubeir – baadhi yao kwa hiari zao na wengine kwa vitisho.

372

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 372

9/4/2017 3:48:03 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Baada ya kuwa wameidhibiti Basra, hao watu wa vita vya Ngamia wakawa na furaha kupindukia. Zubeir akasema: “Kama ningekuwa na wapanda farasi elfu moja ningetoka kwenda kupambana na Ali na nina uhakika kwamba ningeweza kuwa nimemuua kabla yeye hajawasili hapa.” Aisha alituma habari njema za mafanikio yake kwa Hafsa ambaye alikuwa yuko Madina. Yeye aliandika hivi: “Ninapaswa kukujulisha kwamba Ali amepiga kambi mahali paitwapo Zi Qar. Anaogopa sana kwa sababu amepokea habari kuhusu jeshi letu kubwa na zana zake. Kwa sasa hivi hali yake ni sawa na ya ngamia ambaye miguu yake inaweza kukatwa endapo atasogea japo hatua moja mbele na ambaye anaweza kuchinjwa endapo atarudi nyuma.” Talha na Zubeir sasa wakageukia kwenye propaganda mbaya na chafu dhidi ya Ali. Propaganda hasa ina maana kwamba taarifa zinasambazwa kulingana na mtu yule anayezieneza jinsi anavyotaka mwenyewe. Ukweli unaonyeshwa kuwa kama uongo na kinyume chake, na wanatia chumvi juu ya hali halisi. Kama ilivyosimuliwa na Ibn Abil-Hadid kutoka kwa Madaini na Waqidi, wao (Talha na Zubeir) walianza kuwahutubia watu hivi: “Enyi watu wa Basra! Kama Ali atashinda basi atawauweni mmoja baada ya mmoja, na kuivunja heshima yenu na hadhi zenu. Atawaua watoto wenu na kuwafanya wanawake wenu kuwa watumwa. Kwa hiyo ni lazima mlinde heshima na hadhi zenu na mpigane dhidi yake kama mtu ambaye tayari amejitolea kupoteza maisha yake kwa ajili ya heshima ya familia yake.” Licha ya uhasama huu wa wazi na mashambulizi yaliyoandaliwa, AmirulMu’munin hakuchukua hatua za haraka dhidi yao, bali aliwasubiri wao waanze. Alitarajia kwamba wao wangeweza hata hivyo kuachana na uasi na kuepusha umwagaji wa damu, kwa sababu kile kisingizio ambacho kwamba wao walitaka kupigania dhidi yake kilikuwa ni dhaifu kabisa. Alitegemea kwamba wangeweza kutambua kwamba ile njia waliyokuwa wanaifuata ingeunyima huo ukhalifa hadhi yake; na umma ambao ulikuwa umeweka mategemeao makubwa juu ya kupatikana uadilifu, uchamungu na umadhubuti wa Ali utakuwa umevunjwa moyo. Kutoka Rabazah Ali alituma barua kwa watu wa Kufa na akawataka wajiunge naye dhidi ya watu wa Ngamia. Abu Musa Ash’ari, aliyekuwa gavana wa Kufa, alijizuia kumsaidia Ali na pia akawakataza wengine kutoa msaada kwake. Amirul-Mu’minin akamuuzulu kwenye kazi yake mara moja. 373

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 373

9/4/2017 3:48:03 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Baada ya watu wa vita vya Ngamia kuwa wameikalia Basra, watu wa kabila la Abd al-Qais waliondoka mjini hapo na kujikusanya mahali kati ya Zi-Qar na Basra. Walikuwa wanamngojea Ali ili waweze kujiunga na jeshi lake. Wakazi elfu tisa wa Kufa pia walijiunga naye. Imam Ali akatoa hotuba ndefu mbele yao. Yeye alisema pamoja na mambo mengine kwamba: “Nimewaita kuja kunisaidia dhidi ya watu wa Basra. Lengo langu pekee ni suluhu. Kama watu wa Basra wataacha hizo harakati zao, basi lengo langu litakuwa limetimia. “Hata hivyo, kama watashikilia ukaidi wao, tutashughulika nao kwa upole na tutajizuia kupigana mpaka wao watakapofanya maonevu na wakaamua kupigana. Sisi hatutaacha kufanya kila liwezekanalo ili kupatikana suluhu na tutapendelea amani kuliko vurugu katika hali zote.” Kutokana na yaliyoelezwa hapo juu inakuwa dhahiri juu ya ni tofauti kubwa kiasi gani iliyokuwepo kati makundi hayo mawili. Kwa upande mmoja walikuwepo wale watu wa Ngamia ambao walimshutumu Ali kwa jambo ambalo walipaswa kujilaumu wao wenyewe. Ali alikuwa hana hatia kabisa juu ya shutuma zozote kama hizo. Watu hawa walimlaumu kwa makosa bila ya haki yoyote, wakavunja kiapo chao cha utii kwake na wakaasi dhidi yake. Waliamua kupigana dhidi yake na vile vile wakawachochea wengine pia kufanya hivyo, ingawa watu hao walikuwa wamechukua kiapo cha utii kwake. Waliushambulia mmoja wa miji yake iliyokuwa chini ya udhibiti wake, wakamfedhehesha gavana wake na kumpiga, wakamfanyia unyama kisha wakawaua raia na wakagawana mali ya Hazina ya Umma miongoni mwao, ingawaje ilikuwa ya Waislamu wote. Walifikiria pia juu ya kumshambulia Ali kwa askari wa farasi elfu moja na kumuua yeye. Kwa upande mwingine alikuwepo Amirul-Mu’minin, yule Imam halisi ambaye watu wote walikuwa wamechukua kiapo cha utii kwake. Kama hali ilivyo, yeye hakuwa tayari kupokea na kukubali kiapo chao cha utii bali wao walikisisitizia, na wakasema kwamba hawakuweza kuona mtu mwingine anayefaa kuwa kiongozi wao bora; na kama atakubali kuishika nafasi hiyo ya khalifa, tofauti zao zingefikia mwisho. Watu hawa ndipo wakawataka na wengine pia wachukue kiapo cha utii kwake. Ali aliukubali utii wa wale watu waliochukua kiapo na akawaachia wale ambao hawakuchukua kiapo. Hakumlazimisha kamwe mtu yoyote yule kuchukua kiapo cha utii kwake. Siku chache baadae, hata hivyo aliona kwamba baadhi ya watu walikuwa wanawachochea wengine kuasi dhidi yake na walikuwa wanajaribu kuanzi-

374

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 374

9/4/2017 3:48:03 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

sha fitina na vurugu. Walikuwa wanawashambulia watunza hazina wake, magavana na wafuasi wake na walikuwa wanapanga kumuondoa yeye kwenye Ukhalifa na kisha kumuua. Alizipata habari kuhusu harakati zao hizi lakini hakuwa na kinyongo chochote dhidi yao akilini mwake. Aliwahutubia wafuasi wake katika maneno yanayoonyesha ni kiasi gani alivyokuwa na heshima ya hali ya juu kabisa juu ya ubinadamu, yeye alisema. “Enyi watu wa Kufa! Nimewaiteni ninyi kuja kunisaidia dhidi ya ndugu zetu wa Basra……” Hakujiridhisha mwenyewe kwa kuonyesha namna hii ya upole bali pia alituma ujumbe kwa Aisha, Talha na Zabeir akiwataka wajiepusha na maasi na uonevu na akawataka wamsaidie kuelekea kwenye umoja na nia njema. Hapa tunanukuu tukio ambalo litaonyesha ni maoni gani aliyokuwa nayo kuhusu wapinzani wake, na ni wajibu gani aliuhisi baada ya kuchaguliwa kwake kama khalifa, kuhusu usawa na haki, na kwa nini watu walielekea upande wake. Wakati Amirul-Mu’minin alipofika karibu na Basra, watu wa mji huo walimtumia mtu aliyeitwa Kulaib Jarmi kuja kuona sababu za tofauti kati yake na watu wa vita vya ngamia, ili kwamba ile hali ambayo mpaka wakati huo ilikuwa ni ya mashaka na wasiwasi akilini mwao iweze kuwa yenye kueleweka wazi. Ali alimwelezea hali nzima. Alimwambia jinsi watu wale walivyokuwa wamechukua kiapo cha utii kwake lakini baadae wakakivunja ili waweze kuunyakua huo ukhalifa wao wenyewe. Kulaib aliridhika kwamba msimamo wa Ali ulikuwa wa haki, akaukiri hivyo mbele ya Amirul-Mu’minin. Baada ya hapo Ali akamtaka achukue kiapo cha utii kwake, Yeye, hata hivyo, katika kumjibu alisema kwamba yeye alikuwa amekuja kuwawakilisha watu wa Basra na hawezi kuchukua hatua yoyote kama hiyo hadi atakapokuwa amerudi huko mjini na awe amewasilisha taarifa kwa wale waliomtuma. Amirul-Mu’minin ndipo akasema kumwambia yeye: “Tuchukulie kwamba wale watu wamekutuma wewe kwenda kutafuta sehemu yenye uoto na maji na ukawa umewajulisha kwamba vitu hivi vilikuwa vinapatikana mahali fulani, lakini wakakataa kwenda mahali hapa na badala yake wao wakaenda kwenye sehemu kame, ni upi ungekuwa mwelekeo wako wa maamuzi? Je, ungekwenda kwenye ile sehemu ambayo kijito na uoto wa mimea vinapatikana, au ungewafuata watu hao kule kwenye sehemu yenye ukame?”

375

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 375

9/4/2017 3:48:03 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Kulaib akajibu: “Kwa hakika ningekwenda kwenye ile sehemu ambako kulikuwa na maji na kijani kibichi.” Baada ya hapo Ali akasema: “Basi nyoosha mkono wako uchukue kiapo cha utii kwangu.” Yule mtu ndipo akasema: “Wallahi! Baada ya kuninyamazisha kwa hoja zako za kuvutia hakuna sababu ya kupinga kwangu. Sasa nyoosha mkono wako nami ninatoa kiapo changu cha utii kwako,” Wakati watu wa vita vya ngamia walipojipanga wenyewe dhidi ya Ali, AmirulMu’minin aliliambia jeshi lake: “Enyi watu! Jizuieni nafsi zenu na msiwashambulie watu hawa, wala kusema lolote kwa ndimi zenu. Wao ni ndugu zenu katika Imani. Vumilieni maonevu kwa subira, na msianze kupigana, kwa sababu yoyote yule anayegombana leo atalazimika kuja kujieleza na kuwajibika katika Siku ya Hukumu.” Ali aliendelea kufanya juhudi kwa ajili ya amani kwa njia hii. Wakati wa kuondoka kwenda Basra pamoja na watu ishirini elfu, nia yake halisi ilikuwa ni kuwashauri hao watu wa ngamia kujizuia kutokana na vurugu na uasi na kuwalingania kwenye amani na umoja.” Aliipenda amani kiasi kwamba hata pale wakati majeshi hayo mawili yalipokuwa yamejipanga moja dhidi ya jingine na kukawa hakuna matumaini ya suluhu, alifanya juhudi ya dhati katika dakika za mwisho ili kuepusha umwagaji wa damu. Alipowaona Talha na Zubeir alijitokeza mbele yao bila silaha yoyote kabisa, kuashiria kwamba yeye alitaka amani na sio vita, na akamwita kwa sauti: “Ewe Zubeir! Tafadhali hebu njoo kwangu.” Zubeir akajitokeza mbele akiwa na silaha kikamilifu kabisa. Wakati Aisha alipoona hivi alipiga makelele kwa hofu kuu “Hakuna kupigana!” kwa sababu alikuwa anatambua kwamba kupigana na Ali kulimaanisha kifo cha uhakika kwa Zubeir. Yeye aliamini kwamba, adui yoyote wa Ali, awe na nguvu na ujasiri kiasi gani, kwa vyovyote ni lazima atakutana na mwisho wake, kifo. Kama mambo yalivyokuwa, pale Aisha na wafuasi wake walipoona kwamba Ali na Zubeir walikuwa wanakumbatiana, wao walishikwa na butwaa na kukanganyikiwa. Ali alimshikilia Zubeir kufuani mwake kwa muda mrefu na akaanza kuzungumza naye kwa namna ya upole na upendo sana. Alisema: “Huzuni ikupate wewe! Kwa nini umeasi dhidi yangu wewe?” Zubeir akajibu: “Tunataka kulipiza kifo cha Uthman.” Ali akasema: “Mwenyezi Mungu amuue yule mmoja kati yetu ambaye mikono yake imepakazwa na damu ya Uthman.” 376

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 376

9/4/2017 3:48:03 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Nafasi iliyochukuliwa na Talha na Zubeir katika mauaji ya Uthman ilikuwa ni inayojulikana vizuri kwao wenyewe kama ilivyokuwa inajulikana kwa Ali na wengine kama Ibn Abbas ambaye alikuwa ametoa mapendekezo haya kwake wakati alipoingia kwenye kazi ya ukhalifa. “Mteue mwana wa Talha kuwa gavana wa Basra na yule wa Zubeir kama gavana wa Kufa, na mruhusu Mu’awiyah kuendelea kama gavana wa Syria, mpaka hali zirudie kwenye kawaida na watu wajione wako salama pasi hofu, na wale wauaji wa Uthman na wale ambao wanataka kulipiza kisasi wakiwa wametulia.” Ali alikuwa na mambo yote haya katika mawazo yake na maneno yafuatayo ya Talha na Zubeir yalikuwa pia yanagonga kichwani mwake: “Tunachukua kiapo cha utii kwako kwa masharti kwamba tutaruhusiwa nasi kushiriki katika mambo ya ukhalifa huo.” Kwa vile harakati kama hizi zote zilikuwa ni njia tu ya kuupata ukhalifa, hakuna kati yao aliyekuwa mawazoni mwake na kile kisasi cha mauaji ya Uthman. Kabla majeshi hayo mawili hayajakuja kukabiliana uso kwa uso, Ali aliviamuru vikosi vyake kujipanga. Halafu akawapa maelekezo: “Tazameni hapa! Msirushe mshale na msishambulie kwa mkuki au upanga kuanza vita, ili msije mkalaumiwa (kwa kuanzisha vita hivyo). Kitambo kidogo baadae, hao watu wa ngamia wakaua askari wa jeshi la Ali kwa mishale yao. Ali akasema kwa sauti kubwa: “Ewe Mola! Kuwa shahidi.” Kisha mtu mwingine akauawa na Amirul-Mu’minin akasema tena: “Ewe Mola! Kuwa shahidi.” Kisha Abdullah bin Badil akauawa na ndugu yake akauleta ule mwili wa marehemu mbele ya Ali. Hapo yeye akasema tena: “Ewe Mola! Kuwa shahidi,” na akaliamuru jeshi lake kushambulia. Halafu mapigano makali yakazuka. Kwa upanga mkononi, Ali aliwashambulia waasi hao. Upanga wake uliwaka kama mwale wa moto. Aliwarudisha nyuma Maquraishi na akavisambaratisha vikosi vya kulia na vya kushoto vikaparaganyika. Lile jeshi la miguu ambalo lilikuwa likiongozwa na Zubeir likakimbia zake. Zubeir akawa amezingirwa na wapiganaji wa jeshi la Ali, lakini hakuna aliyemshambulia na wakamruhusu kukimbia. Ammar Yasir alianzisha shambulio kali. Wakati Zubeir alipohisi kwamba Ammar atampiga dhoruba kwa upanga wake akasema: “Ewe Abul-Yaqzan (kuniya ya Ammar) unataka kuniuwa mimi?” “Hapana, hata kidogo!” Ammar alisema na akasogea pembeni. Kitendo cha Ammar kwa Zubeir ni kama kile kilichofanywa na Ali katika vita vya Siffin kwa Amr bin Aas. Maelezo yake yatatolewa baadae. Kama mambo yal377

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 377

9/4/2017 3:48:03 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

ivyokuwa, Ammar na jamaa zake walikuwa wamepewa mafunzo na mwalimu wao Ali – Amirul-Mu’minin halisi, ya kuheshimu maisha ya binadamu, kwa kiasi kiwezekanacho, hata katika medani ya vita. Zubeir aliondoka kwenye uwanja wa mapambano na akaenda kwenye bonde lililoitwa al-Saba‘. Imesemekana kutoka kwa baadhi ya wasimuliaji kwamba kuanzia pale Ali alipomkumbatia na kumkumbusha yeye juu ya mapenzi yaliyopita zamani na upendo, dhamira yake ilikuwa imehuishwa na alikuwa hana mwelekeo wa kupigana. Hata hivyo, Aisha na mwanae Abdullah walimkemea, kwa sababu hiyo na alilazimika kubakia kwenye uwanja wa vita. Baada ya Ammar kuyasamehe maisha yake, yeye aliamua kuondoka zake. Aisha alijitahidi sana kudumisha hamasa ya jeshi lake ambalo lilikuwa na watu elfu thelathini. Aliwaita watu wa makabila mbali mbali kwa majina na akawataka kupigana kishujaa ili kulipiza mauaji ya Uthman. Matokeo yake yakawa kwamba mapigano yakawa makali zaidi. Baadhi ya askari walitupilia mbali silaha zao na wakashambuliana kwa mikono yao. Bendera ya Aisha ilikuwa imepachikwa nyuma ya ngamia wake, na wafuasi wake walikuwa wanailinda kwa ghera kubwa. Wakati mmoja wao alipouawa, mwingine alichukua zamu yake. Hapakuwa na dalili ya upande wowote kushinda vita hivyo. Wafuasi wa Aisha pia walikuwa wakipigana kwa ujasiri mkubwa kabisa. Miito kwa ajili ya Aisha na dhidi ya Ali, na kinyume chake iliweza kusikika kutoka pande zote. Mapigano yalikuwa makali kiasi kwamba inakuwa vigumu kuyapatia mfano wake katika historia. Watu wengi sana waliuawa katika vita hivyo kiasi kwamba uwanja wote wa vita ulikuwa umesheheni miili ya watu waliokufa. Hali hii ya mambo ilimtia wasiwasi Ali kwa kiasi kikubwa. Yeye kwa hiyo, alifikiria juu ya mpango ambao, pale utakapotekelezwa unaweza ukahakikisha usalama wa wale ambao walikuwa bado wako hai. Aliwaamuru askari wake kukata miguu ya ngamia wa Aisha. Watu majasiri kadhaa walikimbilia mbele mara moja na kupiga panga zao kwenye miguu ya ngamia huyo. Ngamia huyo akayumba na akaanguka chini. Baada ya hapo, wale wote waliokuwa wakimlinda wakakimbia na jeshi lote likafuatilia kukimbia. Talha na Zubeir pia waliuawa. Na kuhusu kifo cha Zubeir, simulizi zinahitilafiana. Mojawapo ni kwamba mtu mmoja aliyekuwa anaitwa Amr bin Jazmuuz alimfukuzia mpaka kwenye bonde la al-Saba na akamuua huko kwa mkuki wake. Talha aliuawa na Marwan kwa mshale, ingawa alikuwa akipigana bega kwa bega pamoja naye kwa kipindi chote kilichochukuliwa na vita hivyo. Imesimuliwa kwamba wakati 378

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 378

9/4/2017 3:48:03 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

alipokuwa akirusha mshale huo, Marwan alikuwa akisema: “Baada ya kupita muda huu ninaweza nisipate tena fursa ya kulipiza kisasi cha mauaji ya Uthman.” Wale ambao wanatambua akili na vitendo vilivyopita vya Marwan wanaweza kuelewa vizuri sana kwamba kitendo hiki cha Marwan hakikuwa ni jambo geni kwake yeye. Alitenda kulingana na sera za kawaida za Bani Umayyah, yaani, kumuondoa katika njia yao mtu yoyote ambaye aligombea kuwa khalifa, ili kwamba asije akawepo yoyote aliyebakia kushindana na Bani Umayyah katika hili. Na kuhusu Marwan mwenyewe alichukuliwa mateka na akaletwa mbele ya AmirulMu’minin. Alitarajia kusamehewa, na matarajio yake yalitimizwa. Ali alimsamehe. Matokeo ya vita hivi yalikuwa yanatisha sana. Elfu kumi na saba ya wafuasi wa Aisha, na watu elfu moja na sabini waliokuwa wa jeshi la Ali waliuawa. Watu wote hawa masikini waliangukia kuwa waathirika wa ulafi wa wapinzani wa Ali. Wakati baadhi ya wafuasi wa Ali walipofikiria kumuua Aisha (kwa vile alikuwa anahusika na matatizo yote haya), Ali akawasimamisha mara moja na akatoa tangazo lifuatalo: “Mtu yoyote ambaye amejeruhiwa asije akauawa na asiwepo anayekimbia akawa anafuatiliwa. Yeyote atakayeweka chini silaha zake, au akabakia ndani ya nyumba yake atakuwa salama.” Historia yote ya kivita duniani kote inakuja kuonyesha kwamba Ali alikuwa ni mtu mwenye uungwana sana, mwenye tabia njema na msamehevu mno, na kitendo alichowafanyia wapinzani wake kilikuwa cha kiungwana kupita kiasi. Baada ya vita kuwa vimekwisha Ali aliuangalia ule uwanja wa vita na machozi yakatiririka kutoka machoni mwake pale alipoona mateso ya binadamu na umwagikaji wa damu ambao haukuweza kuepukika licha ya juhudi zake bora kabisa. Kisha ndipo akamuomba Mwenyezi Mungu kwa maneno haya: “Ewe Mola! Tusamehe sisi na uwasamehe pia watu hawa ambao walikuwa ni ndugu zetu, ingawa walikuwa waonevu kwetu sisi.” Halafu akafanya swala za mazishi kwa ajili ya maiti wa pande zote. Na kuhusu Aisha, yeye alimrudisha kwenye nyumba yake huko Madina katika namna ya heshima kabisa. Walaghai Wawili Ile njama iliyopangwa, ambayo ilikuwa inaandaliwa dhidi ya Amirul-Mu’minin haikufikia mwisho hata baada ya udanganyifu wa wapinzani wake katika Vita vya Nga-

379

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 379

9/4/2017 3:48:03 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

mia, kwa sababu ile tamaa ya wapinzani wake na chanzo cha uhasama wao dhidi yake vilikuwa bado vipo pale pale. Kama kundi moja la wale waliokula njama dhidi yake lilikuwa liko Hijazi, jingine lilikuwa liko Syria na makundi yote haya yalikuwa na wafuasi wengi wa Aisha, Talha na Zubeir. Viongozi wa maasi wa watu hawa walikuwa ni wale magavana na maafisa wengine ambao walikuwa wamelimbikiza utajiri mkubwa visivyo halali, kinyume cha she-ria, katika kipindi cha Uthman na walikuwa hawakutegemea uingiliwaji wowote kutoka kwa Ali. Waunga mkono wa Ali ndani ya Hijazi walikuwa wote ni waumini mafukara au masahaba wa Mtume waliokuwa wachamungu. Cheo chake huko Hijazi kilikuwa sawa na kile cha binamu yake, Mtume, na kama kulikuwa na tofauti yoyote, ilikuwa ni kutokana na wakati na mazingira. Kufanana huko kunathibitishwa na ukweli kwamba maadui wake yeye takriban walikuwa ni Maquraishi, ambao walikuwa maadui wa Mtume hapo kabla. Ali anasema: “Waache Maquraishi wajiingize wenyewe kwenye upotofu na usijali kuhusu mifaraka ambayo wanaianzisha au ubinafsi wanaouonyesha. Wameungana kupigana dhidi yangu kama vile ambavyo walikuwa wameungana kupigana dhidi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu.” Huko Syria, Mu’awiyah alikuwa akishughulika katika shughuli zake za uovu dhidi ya Ali – khalifa wa haki. Alikuwa akitumia viwango vikubwa vya pesa na kutoa ahadi za kuvutia sana ili kupata uungwaji mkono na watu. Alikuwa pia na jeshi kubwa ambalo alikuwa ndiye kiongozi mkuu binafsi. Jeshi hili linaweza kuelezewa kifupi hivi: “Walikuwa mamluki wapumbavu. Walikuwa wakilipwa na Mu’awiyah ambaye alichukua tahadhari kwamba kwa kiasi iwezekanavyo wabakie bila kuwa na uwezo wa kufikiri.” Tunataja hapa chini tukio ambalo linaelezea tabia ya ushupavu wa Mu’awiyah, na pia linaloonyesha kwamba yeye alikuwa amesadiki kwamba adui yake Ali alikuwa kwenye haki, na haikuwa vigumu kwake kupata mafanikio dhidi yake kwa sababu yeye alikuwa akabiliane na Ali akiwa yeye (Mu’awiyah) ana askari ambao walikuwa hawana uwezo wa kutofautisha kati ya dhulma na haki au kwa maneno mengine, kati ya Mu’awiyah na Ali. Baada ya jeshi la Ali kurejea kutoka Siffin, mtu mmoja wa Kufa alikuja Damascus akiwa amepanda juu ya ngamia wake. Mmoja wa watu wa Syria alidai kwamba ngamia-jike yule alikuwa ni mali yake na alikuwa ameporwa kutoka kwake na mtu 380

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 380

9/4/2017 3:48:03 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

huyo wa Kufa wakati wa vita vya Siffin. Jambo hilo lilifikishwa mbele ya Mu’awiyah na yule Msyria akaleta mashahidi hamsini kuthibitisha kwamba ngamia-jike huyo alikuwa ni wake. Mu’awiyah kwa hiyo akaiamua kesi hiyo kwa kumpendelea yeye. Yule mtu wa Kufa akamwambia Mu’awiyah: “Mwenyezi Mungu akusamehe! Huyu ni ngamiadume na sio ngamiajike.” Mu’awiyah akasema kwamba kwa vile uamuzi umekwisha kutolewa haiwezekani kuubadilisha tena. Pale baraza hilo lilipokuwa limetawanyika, na palikuwa hapana hata mtu mmoja pale, alimwita yule mtu wa Kufa kwa siri na akamuuliza juu ya thamani ya ngamia wake yule. Alipotaja bei yake, Mu’awiyah alimpa mara mbili ya kiasi hicho na kitu kingine zaidi na akasema: “Utakapofika Kufa umwambie Ali kwamba nitaleta watu mia moja elfu kupigana dhidi yake, ambao hawajui kutofautisha kati ya ngamia-dume na ngamia-jike.” Jahiz pia ameyathibitisha maneno haya ya Mu’awiyah na ameelezea ni kwa nini wale watu wa Syria walikuwa ni watiifu sana kwake. Yeye anasema: “Sababu ya watu wa Syria kuwa watiifu ilikuwa kwamba wao walikuwa wapumbavu na wajinga. Ilikuwa ni katika tabia zao kuwafuata wengine kibubusa na kushikilia mawazo pale yanapotolewa na wao. Kama mtu angetetwa mbele yao mwenyewe akiwa hayupo, wao hawakujali kuhakikisha kama ilikuwa ni kweli au uongo. Kama ilivyotajwa hapo juu, njama na hila za maadui wa Ali hazikuishia kwenye Vita vya Ngamia tu bali vilikuwa ni kiungo cha mlolongo wa njama kubwa zaidi dhidi yake. Baada ya kulishinda jeshi la Aisha, Talha na Zubeir, alianza kufanya maandalizi ya kumpigisha magoti Mu’awiyah. Lengo lake pekee lilikuwa ni kuwaongoza watu kuelekea kwenye maadili ya hali ya juu na matendo mema, kuwazuia wao kutokana na kufanya maonevu na kuanzaisha serikali ambayo ingepaswa kuona kwamba ulinzi wa haki zao kuwa ndio wajibu wake wa mbele kabisa. Utaratibu wa Ali ulikuwa tofauti na wale ambao wanawapendeza wenye uwezo, kuwasamehe waasi na kutaka msaada wao, na kuwaendea watu maarufu wawasaidie katika kuusimamisha imara utawala wao. Tayari tumekwisha kueleza hapo mapema kwamba Ali hakutafuta kupata fidia yoyote kutoka kwa watu kwa utumishi aliowafanyia isipokuwa kwamba wamtii tu. Mara kwa mara alikuwa akitamka maneno haya: “Kama elimu, busara na uadilifu vingeweza kupimwa, mimi ningevipima kwa ajili yenu bure. Hata hivyo, ambacho ni muhimu kwa ajili ya hilo ni kwamba niweze kupata mtu mwenye uwezo na akili ya kisomi.” 381

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 381

9/4/2017 3:48:03 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Mu’awiyah hakuwa chombo kama kasha ambamo elimu, busara na uadilifu vinaweza kuwekwa ndani yake. Uadilifu na haki za umma havikuwa salama mikononi mwake, na kama vingeachwa kwake hapakuwa na dhamana ambayo angeweza kuvipitishia hadi kwa watu. Hii ndio sababu ya kwa nini Ali hakumruhusu kuendelea kama gavana wa Syria. Endapo Ali angekuwa sio mwangalifu katika kutekeleza haki, ilikuwa inawezekana kwamba yeye angeweza kufanya kujisingizia na Mu’awiyah. Mu’awiyah hakuchukua kiapo cha utii kwa Ali na hakuzitii amri zake. Hii inaonyesha kwamba alikuwa akipanga kuanzisha ufalme wake yeye mwenyewe. Upinzani wa Aisha, Talha na Zubeir kwa Ali na matokeo yake ya Vita vya Ngamia vilimpatia fursa ya kujiimarisha mwenyewe. Baada ya Vita vya Ngamia vilipokuwa vimekwisha, Ali aliandika barua zilizokwenda kwa Mu’awiyah zikimvutia yeye kujiepusha na uhasama na kumtaka achukue kiapo cha utii kwake kama walivyofanya wengine. Mu’awiyah alimjibu kama ifuatavyo: “Naapa kwa maisha yangu mwenyewe kwamba mimi sijali yoyote yule aliyechukua kiapo cha utii kwako. Ungeweza kuwa kama Abu Bakr na Umar kama ungekuwa huna hatia ya mauaji ya Uthman. Kama mambo yalivyo, wewe uliwachochea Muhajirin kuasi dhidhi yake Uthman na ukawazuia Ansari kumsaidia yeye. Watu wajinga wakakutii na wanyonge wakawa wenye nguvu kwa sababu yako wewe. Watu wa Syria hawatajizuia kupigana dhidi yako isipokuwa pale utakapowakabidhi kwao wale watu ambao walimuua Uthman. Baada ya hapo suala la ukhalifa litaamuliwa kupitia baraza la ushauri. Watu wa Hijazi walikuwa ndio watawala wa watu alimuradi waliunga mkono haki. Wao sasa wameitelekeza haki na hatimaye watu wa Syria sasa wanastahili kutawala. Hoja iliyotolewa na wewe dhidi ya Talha na Zubeir haina uzito wowote katika suala la watu wa Syria. Wao walichukua kiapo cha utii kwako lakini sisi hatukufanya hivyo. Na kuhusu ubora na umaarufu wako katika Uislamu na uhusiano wako wa damu na Mtume ni jambo ambalo siwezi nikalikataa. Na amani iwe juu yako.” Barua iliyotolewa maelezo yake hapo juu inafanya nia ya Mu’awiyah kuwa dhahiri kabisa. Alitaka kukwepa kuchukua kiapo cha utii kwa Ali kwa kisingizio kimoja au kingine. Alijua kwamba asingeweza kumdanganya Ali kwa maneno yake. Alikuwa pia anatambua kwamba Ali hakuhusika na lolote juu ya mauaji ya Uthman. Yeye kwa hiyo, akasema kwamba hata kama wale ambao walikuwa wametoa kiapo cha 382

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 382

9/4/2017 3:48:03 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

utii kwa Abu Bakr na Umar wawe wamechukua pia kiapo cha utii kama hicho kwake yeye na alistahiki kuwa khalifa, ilikuwa ni lazima kwake kuwakabidhi kwa watu wa Syria wale wauaji wa Uthman ambao walikuwa wamepewa hifadhi na yeye. Hata hivyo, hata kama kukosa hatia kwa Ali kuhusu mauaji ya Uthman kulithibitika, Mu’awiyah hakuwa tayari kumkiri kama khalifa wa haki kisheria lakini alitaka suala hilo lipelekwe kwenye baraza la ushauri. Zaidi ya hayo, hakuwa tayari kuwaachia watu wa Hijazi na Iraqi kuchagua khalifa, kwa sababu, kwa mujibu wake yeye, haki hii imehamishiwa kwa watu wa Syria kwa sababu wao walikuwa ndio watawala halali. Ni dhahiri kwamba kama masharti yote haya yangetimizwa, hakuna mwingine zaidi ya Mu’awiyah ambaye angeweza kuwa khalifa. Ali alionyesha subira na uvumilivu usiokuwa wa kawaida. Hata hivyo, subira hii haikuwa ni kutokana na kukosa maamuzi au kuzembea upande wake yeye. Hali ilikuwa kwamba kwa wakati ule Waarabu walikuwa wamegawanyika katika makundi mawili na mojawapo lilikuwa likielekea kushindwa licha ya tofauti zilizokuwa kati yao. Kwa upande mmoja walikuwepo wale wanyonge na wasiokuwa na uwezo ambao walitaka maisha ya amani na usalama kwa ajili yao wenyewe na vile vile kwa ndugu zao. Walikuwepo pia wale masahaba wachamungu wa Mtukufu Mtume ambao walitamani nchi ambayo uadilifu utapatikana. Na kwa upande ule mwingine walikuweko wale waliotaka kuwanyonya wale wanyonge na kulimbikiza mali kwa njia zozote zitakazowezekana. Lile kundi la kwanza liliongozwa na Ali ibn Abi Talib, wale ambao walipenda haki walikuwa ndio wafuasi wake na watakia heri wake. Mkuu wa kundi la pili alikuwa Mu’awiyah bin Abu Sufyan, na wale wote ambao walikuwa wamezoea kuonea wengine ndio waliokuwa wafuasi wake. Malipo ya lile kundi la kwanza yalikuwa ni dhamiri yao ya wazi na zawadi ya lile kundi la pili ilikuwa ni hazina ya Mu’awiyah. Kulikuwepo na watu wapenda haki wengi ambao walimuacha Mu’awiyah na wakajiunga na Ali, na vivyo hivyo, walikuwepo wapenda dunia wengi ambao walimwacha Ali na wakahamia kwa Mu’awiyah. Hapa tutataja hali kadhaa ambamo watu baadhi waliondoka kwa Ali na wakaenda kwa Mu’awiyah. Itadhihirisha wazi kama walikuwa ni watu wa aina gani na kwa nini walikuwa upande mmoja na Mu’awiyah.

383

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 383

9/4/2017 3:48:03 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Mtu mmoja aliyeitwa Yazid bin Hujiyah Tamimi aliteuliwa na Ali kuwa gavana wa Ray na sehemu zinazoungana nayo. Alilimbikiza kiasi kikubwa cha mali na akaitumia vibaya. Wakati Ali alipokuja kujua kuhusu habari hizo alimrudisha na akamfunga. Akamteua mtu aliyeitwa Sa’d kuwa mlinzi. Wakati Sa’d alipokwenda kulala, Yazid akatoroka kutoka mle gerezani. Alimpanda mnyama wake wa kipando na akafika Damascus ambako alijiunga na Mu’awiyah. Alitunga beti zifuatazo kuhusiana na kutoroka kwake: “Nilipanda kipando changu na kumdanganya Sa’d na nikaja zangu Damascus. Nilichagua mtu bora.” “Pale Sa’d alipokwenda kulala nikatoroka. Sa’d si chochote zaidi ya mtumwa mpotovu na aliyekanganyikiwa.” Yazid huyu alimdhihaki Ali katika beti zake ambazo alizituma Iraqi na akafanya ijulikane kwa Ali kwamba yeye (Yazid) alikuwa adui yake Ali. Mu’awiyah alimpa kiasi kikubwa cha pesa, kwa hiyo akamtukuza sana yeye na watu wa Syria, na akasema kwamba Syria ilikuwa ni nchi takatifu na watu wa Syria walikuwa waumini wa kweli. Yeye alisema: “Niliwapenda watu wa Syria kuliko watu wengineo na nililia sana kwa ajili ya Uthman.” “Syria ni nchi takatifu na wakazi wake ni waumini wa kweli na wafuasi hasa wa Qur’ani.” Mtu mwingine aliyeitwa Za‘qa‘ bin Sa’d aliteuliwa na Amirul-Mu’minin kama mtawala wa Kaskar. Alikusanya kiwango kikubwa cha mali kwa njia zote zilizowezekana na akaitumia mali hiyo kwa anasa na ufujaji. Kiasi kwamba alimuoa mwanamke na akampa dirham mia moja elfu kama mahari yake. Alipokuja kujua kwamba Ali ametambua matendo yake mabaya aliondoka kwenda Syria akichukua pamoja naye kiasi kikubwa cha fedha alichoweza kubeba. Ali alimuadhibu mtu aliyeitwa Najashi kwa ajili ya kunywa pombe. Yeye alikuwa mmoja wa wafuasi wa Ali, kwa hiyo, alifikiri anastahili kuwa mbora zaidi kwa kulinganishwa na wengine. Yeye hakupenda kwamba Ali – Amirul-Mu’minin amuadhibu kama alivyowaadhibu wengine. Pale Mu’awiyah alipomuahidi kumpatia hifadhi, yeye kwa hiyo akakimbilia Syria. Baada ya kuwasili hapo, alitunga shairi hili akimdhihaki Ali:

384

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 384

9/4/2017 3:48:03 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

“Ni nani atakayenifikishia ujumbe wangu huu kwa Ali, kwamba sasa niko salama na sihisi hatari yoyote ile.” Wakati Najashi alipoadhibiwa, watu wengi wa asili ya Yemen walikasirika sana, kwa vile yeye pia alikuwa mmoja wao. Kwa hiyo na wao walimtelekeza Ali na wakaenda kujiunga na Mu’awiyah. Kama vile tu watu wenye mawazo ya dunia walivyokuwa wengi kwa idadi kuliko wengine, idadi ya wale waliomtelekeza Ali na kujiunga na Mu’awiyah pia ilikuwa kubwa. Kila mtu hana uwezo wa kuivumilia haki au kusema au kufanya kitu kilicho sahihi. Kwa hiyo kila mtu asingeweza kumpenda Ali ambaye alikuwa mkali katika suala la kweli na haki na hakuweza kukengeuka kutoka kwenye haki na uadilifu hata kwa ndugu zake wa karibu kabisa. Kwa mazingira haya kwa nini yule gavana asingemuacha na kujiunga na Mu’awiyah ambaye Imam Ali alimwandikia kama ifuatavvyo: “Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kwamba kama nitakuja kutambua kwamba umetumia vibaya mali ya Waislamu, hata kwa kiasi kidogo kabisa, nitakupa adhabu ambayo itakufanya uwe masikini, uliyelemewa na uliyefedheheka.” Vivyo hivyo, kwa nini gavana huyo asimtelekeze yeye wakati amemuandikia katika maneno haya: “Najua kwamba umeifanya Hazina ya Umma kuwa tupu kabisa na umenyakua kila ulichoweza kukikamata kwa mikono yako. Umetumia vibaya kila kilichoingia mikononi mwako. Tafadhali, unaweza kunitumia yale mahesabu ambayo umeyaandaa?” Ingewezekana vipi watu duni wafikie kwenye vilele vya uchamungu na ukweli, na vipi mtawala kama huyo aweze kuupenda ujumbe ufuatao wa Amirul-Mu’minin? “Endapo taarifa nilizopokea kuhusu wewe ni sahihi, ngamia wako na kamba za viatu vyako ni bora kuliko wewe.” Vipi mabepari wenye uwezo na washirika wao madhalimu wangeweza kuvumilia kwamba Ali awe ndiye khalifa – Ali huyo huyo ambaye alitaka kutumia utajiri kwa ajili ya ustawi wa watu wa chini, na alikuwa wakati wote katika vita na waonevu na washirika wao? Wangewezaje kumpenda khalifa ambaye alisema: “Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kwamba ni heri kwangu mimi kulala juu ya miiba na kufungwa minyororo kuliko kwamba niweze kumuonea na kumdhulumu mtu yoyote au kunyang’anya japo kitu cha kawaida kabisa.”

385

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 385

9/4/2017 3:48:03 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Kwa nini watu hawa wasiweze kuasi dhidi yake ambaye alisema wazi: “Ni wajibu wangu kusimamisha vita dhidi ya udhalimu na wadhalimu, na dhidi ya wale ambao wananyakua kinyume cha haki mali ya wengine, na nitakuja kuwajibika juu ya hilo Siku ya Kiyama.” Kama Ali asingeuchukulia wajibu huu kuwa muhimu, yeye angeweza kuyaacha mambo kama yalivyokuwa. Angewaacha watu kwenye majaliwa yao wenyewe. Wengine wangeweza kuwa ndio madhalimu na wengine wenye kudhulumiwa. Yeye anasema: “Kama Mwenyezi Mungu Mtukufu angekuwa hakuchukua ahadi kutoka kwa watawala kwamba hawatakaa kimya kama itatokea kwa dhalimu kuvimbiwa kwa chakula wakati wanaodhulumiwa wanabaki na njaa, ningeweza kuzitupa hatamu za ukhalifa mabegani mwake (yaani angeyaachia mambo kuendelea kuchukua mzunguko ambao yamekwishauchukua tayari) na angeuridhisha ule wa mwisho wake kama ule wa kwanza. Ndipo sasa mngeikuta dunia yenu kuwa isiyokuwa na thamani machoni mwangu kama mchemuo wa mbuzi.” Vipi watu wadanganyifu wangeweza kumuacha mtu kama huyo kuchukua usimamizi wa mambo yao; wakati Ali alikuwa ameshikilia maoni yafuatayo kuhusu wao na watu wa wakati wake: “Mtu ambaye anajua jinsi atakavyotoa hesabu yake hawezi kuwa mdanganyifu. Tunaishi katika wakati ambamo watu wanafanya udanganyifu na ulaghai wakiuchukulia kuwa ni busara, na watu wajinga wanaichukulia kwamba ni sera nzuri.” Hii ndio sababu idadi kubwa ya watu wenye uwezo ambao walimpinga Ali walikuwa ni wale watu ambao walikuwa wamelimbikiza viwango vikubwa vya mali kwa njia za hara-mu, na walitaka Mu’awiyah awafanye kuwa matajiri zaidi kwa gharama ya mtu wa chini na kupitia Hazina ya Umma. Na kuhusu watu wengine, mbali na hawa mabepari ambao walikuwa kinyume na Ali, walikuwa wale watu wapumbavu ambao walikuwa hawajui ni kipi kilikuwa kizuri kwao na kipi kilikuwa na madhara juu yao. Kama tulivyokwisha kueleza hapo juu, Waarabu wa wakati ule walikuwa wamegawanyika katika vikundi vingi. Kila kikundi kilikuwa kitiifu kwa mkuu wao. Waliwatii wakubwa zao kibubusa bila kujielewa na hawakuwauliza wao juu ya ni kwa nini walikuwa na furaha au kutokuwa na furaha na mtu fulani. Ali amewarejea watu wa wakati wake wa namna hii, kila mara. Katika maelezo yake kuwahusu wao, kuna huzuni na kero la baba mwenye huruma kuhusiana na watoto wake ambao hawamtii yeye na wanatoa kwa kusudia au bila kukusudia, njia za maangamizo yao wenyewe.

386

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 386

9/4/2017 3:48:03 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Anasema kuhusu wao: “Ninalalamika kwa Mwenyezi Mungu dhidi ya wale watu ambao wanatumia maisha yao katika ujinga.” Akizungumza na watu hao yeye anasema: “Maadui zenu sio wasahaulifu juu yenu ambapo ninyi mmesahau kila kitu kutokana na kutojali kwenu.” Akielezea jinsi watu kama hao wanavyojisikia wakati wanapoitwa kuja kupigana dhidi ya waasi yeye anasema: “Wengine wao wanakuja kwa shingo upande, wengine wanatoa visingizio vya uongo na bado wengine wanazuia msaada wao kwa makusudi.” Yeye anaongeza: “Muulizaji kutoka miongoni mwao anajaribu kuleta utatanishi, na yule anayetoa majibu anayatoa bila kutafakari juu yake. Kwa kawaida zile hisia za furaha na kukosa furaha zinamfanya mtu aliyekuwa na maoni sahihi kupotoka kutoka kwenye njia iliyonyooka. Na kuhusu yule mtu kutoka miongoni mwao ambaye akili yake imekomaa inawezekana kwamba kuangalia mara moja kunaweza kumuathiri yeye, na neno moja linaweza kuleta mapinduzi katika akili yake. Katika sentensi yake ya mwisho, Amirul-Mu’minin ameelezea hali ya akili ya watu mashuhuri wenye heshima wa wakati wake kwa namna ya kufahamika kirahisi. Anasema: “Katika wakati huu kama kuna watu wenye busara hapo hisia zao ni tiifu kwenye choyo na ulafi wao, na maoni yao yanategemea juu ya furaha na kuchukizwa kwao. Kama wana ridhaa na mtu fulani wanatoa maamuzi kwa faida upande wake bila uhalali wowote; kama wanachuki na mtu yoyote wanatoa maamuzi potovu upande wake kwa kutokana tu na kuchukia kwao. Na kuhusu wale wenye akili zilizokomaa, kutazama mara moja tu yale mambo wanayoyapenda kunatosha kuwafanya wakengeuke kwenye ile njia ambayo tayari wanaifuata, na neno moja tu la mtu mwenye mvuto na uwezo au mtoa hongo linatosha kuwafanya waunge mkono udhalimu na kumsaidia muonevu.” Wakati, baada ya kushindwa kwa watu wa Ngamia, kile kituo cha njama dhidi ya Ali kilihamia Damascus, Mu’awiyah bin Abi Sufyan, kiongozi wa Bani Umayyah alizidisha maandalizi yake ya kupigana dhidi ya Ali na kuiangusha serikali yake. Katika kuipokea barua ya kwanza ya Ali ambayo ndani yake alimtaka achukue kiapo cha utii kwake kama walivyofanya wengine, yeye aliwaita kuja Damascus kwa ajili ya mashauriano, wale watu wote, ambao kutoka kwao aliweza kutegemea msaada wao. Mashuhuri sana miongoni mwao alikuwa Amr Aas. Baada ya kupokea barua ya Ali; Mu’awiyah mara moja akamwandikia barua Amr: “Lazima utakuwa umekuja kuyajua majaaliwa yaliyowakuta Talha, Zubeir na Aisha. Marwan baada ya kuondoka Basra, amekuja kujiunga nami. Sasa Jarir bin

387

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 387

9/4/2017 3:48:03 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Abdullah ameniletea barua kutoka kwa Ali. Mimi sitaki kumtumia majibu bila ya kushauriana na wewe. Unapaswa kwa hiyo ufike hapa mapema iwezekanavyo.” Baada ya kuipokea barua ya Mu’awiyah, Amr aliwaita watoto wake Abdullah na Muhammad kutaka ushauri wao kuhusu majibu ambayo yangeweza kutumwa kwake. Abdullah akasema: “Mimi nafikiri kwamba wakati Mtume alipofariki alikuwa ameridhika na wewe, na Abu Bakr na Umar pia waliridhika na wewe wakati walipofariki. Iwapo utapotosha imani yako sasa kwa kuwa upande mmoja na Mu’awiyah, wewe na yeye wote mtakwenda motoni Siku ya Kiyama.” Halafu Amr akamuuliza mwanae wa pili Muhammad ili naye atoe maoni yake katika suala hili. Yeye alijibu: “Unapaswa kwenda kwa haraka sana na ukajiunge na Mu’awiyah. Ni bora kuwasili mapema na kuwa mkuu kuliko kuja kuwa mfuasi wa kambi.” Asubuhi yake Amr alimwita mtumwa wake aliyekuwa akiitwa Durdan na akamwambia aweke matandiko juu ya mnyama wake wa kipando. Kisha akamwambia ayaondoe. Alifanya awekwe na kuondolewa matandiko mara tatu. Dardan akamuuliza: “Bwana mkubwa! Kwani kuna jambo gani? Ninatumaini hutajali kama nitakuambia yaliyoko moyoni mwako.” Amr akasema: “Sema hayo unayotaka kuyasema.” Hapo Dardan akasema: “Kwa sasa hivi dunia hii na ile ya kesho akhera zimeleta wasiwasi mkubwa akilini mwako. Unatafakari kwamba ile ya kesho akhera iko pamoja na Ali lakini sio dunia hii, na dunia hii iko kwa Mu’awiyah na sio dunia ya kesho akhera. Unayumba kati ya hizi mbili. Ushauri wangu mimi ni kwamba unapaswa ubakie nyumbani. Kama waumini watafanikiwa, utaongea nao na endapo wale wenye mawazo ya dunia wakiwa washindi, wao kwa hakika watahitaji msaada wako.” Hata hivyo, zile ahadi alizota Mu’awiyah kwa Amr Aas hazikuwa ndogo kwamba angeweza kuzipuuza na angekaa nyumbani akifuata ushauri wa mwanawe Abdullah au mtumwa wake Dardan. Aliamua kumpinga Ali na kujiunga na Bani Umayyah na Mu’awiyah. Kwa vile Amr alikuwa mashughuli katika kupanga njama dhidi ya Ali kwa kiasi kisichopungua kuliko kile cha Mu’awiyah; ni muhimu kutoa kwa kifupi picha ya maisha yake, ili kwamba tuweze kujua sababu ya kwa nini alimuacha Ali na akajiunga na kundi la Mu’awiyah na ni thamani gani aliyokuwa nayo kwa kundi lake.

388

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 388

9/4/2017 3:48:03 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Kabla hajakubali Uislamu, Amr Aas alikuwa akijulikana sana kwa kuuza na kulangua kwake. Huu ni ukweli ambao hauwezi kukataliwa. Ameelezea yeye mwenyewe kwa uwazi kabisa sifa bainifu yake hii katika maneno haya: “Baada ya kurejea kutoka kwenye Vita vya Handaki nilikusanya pamoja baadhi ya watu kutoka miongoni mwa Maquraishi ambao kwa kawaida waliyakubali maoni na walinisikiliza kwa makini. Niliwaambia: “Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kwamba ninaweza kubashiri kwamba Muhammad atashinda. Katika mazingira haya tunapaswa kuhama kwenda Ethiopia kudumu na kufanya makazi huko. Ni bora kuishi chini ya Negus kuliko kujitiisha kwa Muhammad. Kama Muhammad atawashinda watu wetu tutabakia mbali na nje ya uwezo wake na endapo watu wetu watamshinda yeye tutadumu kufaidi zaidi. Walikubaliana na mimi na wakasema: “Kila ulichokisema ni sahihi kabisa. Kisha nikawaomba kupata zawadi kwa ajili ya Negus…………..” Dr. Hasan Ibrahim Hasan wa Misri ambaye ni mshabiki sana wa Amr na amepata shahada ya udaktari kutoka Chuo Kikuu cha London juu ya msingi wa tasnifu yake yenye kicha cha maneno “Amr mwana wa Aas” anaandika hivi wakati akitoa maelezo juu ya aina ya Uislamu wake. “Wakati tunapoyaangalia mambo ya Maquraishi ni kwamba hapo mwanzoni kila mmoja wao alikuwa amedhamiria katika kuuangamiza Uislamu. Kila ushindi wa Mtume na kila kushindwa kwa Maquraishi badala ya kuwavunja moyo, wao walizidi kuwa na ghadhabu. Hata hivyo, baada ya kushindwa mfululizo na wakuu wao na watu mashuhuri wakawa wameuawa, wale vijana wakajihisi wasi wasi na wakaanza kufikiri kuhusu mwelekeo wao wa utendaji wa baadae. Waliweza kuona giza katika upande mmoja na mwanga wa matumaini katika upande mwingine. Walijua kwamba hata kama wangejiunga upande mmoja na ile nguvu ya Uislamu iliyokuwa inaendelea kuongezeka katika hatua ile hawatapata mafanikio yoyote. Hata hivyo, walihofia vile vile kwamba kwa kufanya hivyo wataweza kupoteza ile heshima na hadhi ambayo walikuwa nayo miongoni mwa watu wao na pia wanaweza wakapoteza uhuru wao wa tangu awali. Baadhi yao waliyapuuza mashaka haya yote na walipofika Madina wakachukua kiapo cha utii kwa Mtume. Wengine ambao hawakuweza kuchukua uamuzi wowote ule waliacha kupinga Uislamu na ilipokuja kuwa dhahiri kabisa kwao kwamba kwa hali yoyote ile Mu389

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 389

9/4/2017 3:48:03 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

hammad alikuwa atapata ushindi juu ya Maquraishi wao pia waliamua kunufaika na fursa hiyo kabla hawajachelewa sana na wakaukubali Uislamu. Hili lilitokea kabla ya kutekwa kwa Makkah. Wa mbele kabisa miongoni mwa makundi hayo mawili husika alikuwa ni Khalid bin Walid na Amr Aas. Huyu Amr alikuwa ameondoka Bara Arabu kwenda Ethiopia kuchunguza hali za huko. Kama mambo yalivyokuwa, pale alipogundua kwamba kulikuwa na uhusiano mzuri sana kati ya Mtume na Negus, na huko Arabuni Uislamu ulikuwa utafikia kilele cha mafanikio na kuanguka kwa Makkah kulikuwa ni suala la masiku tu, aliamua kujiunga na wale ambao tayari walikuwa wameukubali Uislamu na kufanya kwa hiari kile ambacho atalazimika kufanya kwa vyovyote itakavyokuwa baadae.” (Amr Aas cha Dr. Hasan Ibrahim Hasan cha Ki-Misri, pia tarjuma ya ki-Urdu iliyochapishwa na Idara Maktaba Jadid, Lahore, uk.4344) Msimamo wa liwezekanalo (opportunism) uliendelea kuwa hai katika moyo wa Amr Aas katika maisha yake yote. Kwa hali hii alikuwa kama wale wakuu wa makabila na watu wengine mashuhuri ambao dhidi yao Abu Bakr, Umar na Ali walilazimika kupigana nao vita. Tumeelezea katika kurasa zilizopita kwamba wakati Amr Aas alipokuwa gavana wa Misri, alikusanya kiasi kikubwa cha mali. Umar alimuamuru kukabidhi nusu ya mali hiyo kwenye Hazina ya Umma. Alijaribu kukwepa malipo hayo kwa visingizio tofauti lakini Umar hakuridhika. Alimuandikia Amr Aas akisema: “Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kwamba mimi sitadanganywa kwa maneno yako ya ulaghai. Ninyi watu mmelimbikiza mali na hamuogopi chochote…… Sikiliza! Unakusanya fedheha na unaacha nyuma yako moto kama urithi. Ninamtuma Muhammad bin Muslima kwako. Unapaswa ukabidhi nusu ya mali yako kwake.” Wakati Muhammad ibn Muslima alipokutana na Amr akiwa na barua hiyo; alifanya viandaliwe vyakula vya gharama sana kwa ajili yake, lakini Muhammad alikataa kuvila. Amr akamuuliza: “Je, unaona ni haramu kula chakula nyumbani kwangu?” Muhammad akamjibu: “Kama ungeweka mbele yangu kile chakula ambacho kwa kawaida ndicho kinachoandaliwa kwa wageni mimi nisingekataa kukila hicho. Kama hali ilivyo, chakula ambacho umekiandaa kwa ajili yangu ni kitangulizi cha upotovu (yaani si chochote zaidi ya rushwa). Kwa hiyo sasa ukiondoe chakula hiki hapa na unikabidhi nusu ya mali yako.” 390

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 390

9/4/2017 3:48:04 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Kwa hiyo, Amr Aas akakabidhi kwake nusu ya kila kitu alichokuwa nacho. Jozi ya viatu ilibakia kwake ambayo Muhammad alichukua kiatu kimoja pia, na kuacha kile kiatu kingine kibakie kwake. Amr Aas hakuweza kulivumilia hili. Yeye kwa hiyo, akamwambia Muslima: “Balaa iwe juu ya wakati ule nilipoteuliwa na Umar kama gavana. Wallahi ninaitambua hali ya baba yake Umar wakati alipokuwa akibeba mzigo wa kuni juu ya kichwa chake na Umar pia alibeba mwingine. Wote wawili walikuwa hawana nguo za kutosha kuvunika miili yao. Kila mmoja wao alivaa nguo ya ngozi ya simba ambayo haikufika hata kwenye magoti yao. Na ninaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kwamba baba yangu, Aas alikuwa akiishi maisha ya starehe kabisa, kiasi kwamba alikuwa haridhiki hata kwa koti la hariri lenye vifungo vya dhahabu juu yake.” Kadhia hii inaonyesha jinsi Amr alivyokuwa hodari wa kunufaika na kila fursa ya kujipatia mali. Inaonyesha pia zile fikira ngumu kufahamika za watu mashuhuri. Amr hakuweza kuona kasoro yoyote kwa Umar na baba yake isipokuwa kwamba walikuwa masikini na hawakuwa na nguo za kutosha kuvaa na walifanya kazi kwa mikono yao na kubeba mizigo ya kuni juu ya vichwa vyao na hakuweza kutaja sifa yoyote ya baba yake isipokuwa kwamba alikuwa akivaa nguo za hariri. Itakuwa ni makosa kudhania kwamba kile alichokisema Amr kuhusu Umar kilisababishwa na mtingishiko wa ghafla na hasira. La hasha. Hali haikuwa hivyo. Ukweli ni kwamba alikuwa wakati wote akifikiria kwamba kwa kuwa Umar na baba yake walikuwa masikini na baba yake mwenyewe, Aas alikuwa tajiri, basi baba yake alikuwa bora kuliko Khattab, na yeye mwenyewe alikuwa bora kuliko Umar. Mtazamo wa Amr ulikuwa kwamba wanadamu wote hawalingani. Kwa mujibu wake yeye watu wengine walikuwa duni na wengine walikuwa waungwana, na kigezo cha uungwana kilikuwa ni nasaba ya mtu tu na si kinginecho chochote. Yeyote ambaye alitokana na familia ya kiungwana na ya kitajiri alikuwa ni muungwana na mtu ambaye alizaliwa duni alikuwa mwenye kustahili kudharauliwa. Yule muungwana alikuwa na haki ambazo hazikubaliki kwa wengine na ilikuwa ni wajibu wa watu kuwatii. Wanahistoria wote wanakubaliana kwamba kuhusiana na uongozi na serikali ya Misri, maoni ya Amr yalikuwa kwamba ilikuwa ni muhimu kwa yoyote ambaye alitaka uboreshaji na maendeleo asisikilize malalamiko yaliyokuwa yakifanywa dhidi ya uungwana na watu watokanao na matabaka ya chini.” (Al-Islam wa al-Hazarat al-Arabiyyah).

391

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 391

9/4/2017 3:48:04 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Kwa namna hii Amr Aas alikuwa ameshikwa na uroho wa tabia ya kujifurahisha na ya anasa. Aliamini kwamba kuwanyonya watu wa chini ni haki ya kuzaliwa nayo ya wale wanaotokana na familia za kiungwana. Wakati mwingine akili yake iliyumba kuhusu kama aiweke dhamiri yake hai au aiuwe kwa ajili ya maslahi ya kidunia, lakini mara baadae aliamua kwa faida ya anasa na mali. Kama ilivyoelezwa hapo juu, jambo hilo hilo ndio lilitokea wakati Mu’awiyah alipomwita. Alitafakari kwa muda kiasi kama aungane na Ali au na Mu’awiyah, lakini hatimae aliamua kuelekea Syria. Wanahistoria na wasimulizi wa Hadith wanazihusisha beti fulani kwa Amr Aas. Alizitunga wakati alipokuwa anakwenda kwa Mu’awiyah. Katika beti hizi yeye ameelezea wazi maoni yake kuhusu Ali na Mu’awiyah. Mbele ya macho yake, Ali alikuwa ni mtu mashuhuri sana na Mu’awiyah hakuwa na mlingano wowote naye. Inaweza ikasemwa kwamba yeye alikuwa na mioyo miwili ndani ya kifua chake. Mmojawapo ulimzuia kwenda kwa Mu’awiyah ambapo huo mwingine ulimtuma aende akamuone Mu’awiyah. Anamalizia shairi lake kwa beti zifuatazo: “Niliutwaa ulimwengu kwa makusudi kutokana na ulafi, ingawa hapakuwa na sababu ya msingi ya kuitwaa dunia” “Naelewa vizuri sana hasara zihusikazo na kuitwaa dunia, lakini ni kweli pia kwamba nina tamaa mbalimbali za kidunia.” “Kitu hasa ni kwamba akili yangu inatamani maisha ya hadhi na heshima. Nani atakubali kuishi maisha ya fedheha.” Kwa mujibu wa Amr Aas maisha ya heshima na hadhi yalijifungia kwenye mapato ya haraka ya kidunia na ahadi za Bani Umayyah. Kama vile wakati wa Umar kigezo cha hadhi machoni mwake kilikuwa kiasi kwamba baba yake alikuwa akivaa nguo za hariri, kiwango cha fedheha, kulingana na yeye, katika wakati wa Ali kilikuwa ni kumsaidia yule ambaye hakufanya uuzaji yeye mwenyewe wala hakuwaruhusu wengine kufanya hivyo. Kiwango hiki cha fedheha kilikuwa ni sawa na ule uvaaji wa kimasikini wa Umar na baba yake. Wakati Amr Aas alipowasili kwenye baraza la Mu’awiyah, yeye Mu’awiyah alimwambia: “Ewe Abu Abdillah! Nakulingania kufanya jihadi dhidi ya yule mtu (yaani Ali ibn Abi Talib) ambaye amemkaidi Allah na amesababisha mfarakano miongoni mwa Waislamu na akautawanyisha umma.” 392

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 392

9/4/2017 3:48:04 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Amr Aas akasema: “Wewe utanipa nini mimi endapo kama nitajiunga na wewe kupigana dhidi ya Ali nikijua kama unavyojua wewe kwamba jambo lenyewe ni la hatari sana?” Mu’awiyah akasema: “Nitakupa chochote utakachoomba.” Amr akasema: “Ninataka ugavana wa Misri.” Baada ya hapo mazungumzo marefu ya hila yakatokea kati yao. Kila mmoja wao alijaribu kumdanganya mwenzie. Kila mmoja alikuwa na faida binafsi ndani ya mawazo yake. Mazungumzo yao ya kilaghai hata hivyo yaliishia na kuwekeana masharti kila mmoja wao. Amr Aas alimkubali Mu’awiyah kama khalifa na akachukua kiapo cha utii kwake na kwa malipo yake Mu’awiyah akampa mamlaka kamili juu ya Misri na wakaazi wake na akamuahidi kutoingiliwa kutoka upande wake. Ali ametengeneza taswira ya uwekeanaji masharti huu katika maneno yafuatayo: “Hakuchukua kiapo cha utii kwa Mu’awiyah mpaka alipokubali kumlipa bei ya thamani ya kiapo chake. Ijaaliwe mikono ya yule mtu aliyeapa kiapo hiki isiwe na ushindi na isipate mafanikio! Na mnunuzi wa kiapo hiki ahuzunike na kufedheheka! (Wakati sasa umefika ambao kwamba) uwe tayari kwa vita na uandae zana za muhimu.” Ali anaendelea kusema zaidi juu ya uwekeanaji masharti huu: “Nimefanywa nielewe kwamba Amr Aas hakuchukua kiapo cha utii kwa Mu’awiyah bure hivi hivi tu. Alimfanya akubali kabla kabisa kwamba atakuja kulipa thamani yake – kwamba atapaswa kuja kumpa zawadi kwa ajili ya kuitupilia mbali imani ya dini.” Amr Aas hakuridhika binafsi na majadiliano ya thamani yaliyopita. Matilaba yake ilikuwa ni jambo jingine kabisa. Alimshauri Mu’awiyah kuandaa vuguvugu la propaganda dhidi ya Ali ili iweze kuja kuwa na manufaa kuhusiana na vita ambavyo vinaweza kuja kupiganwa baadae. Alimwambia hivi pamoja na mambo mengine: “Watume watu wanaoaminika kwenda kwenye miji tofauti kwenda kutangaza kwamba ni Ali aliyemuua Uthman.” Amr Aas aliyafanya yote haya licha ya ukweli kwamba yeye alijua vizuri kabisa kwamba Ali hakuhusika kabisa na kifo cha Uthman, na kwa kweli lile kundi ambamo yeye yumo lilikuwa na sehemu kubwa sana katika suala hilo, kama tulivyokwisha kuelezea katika sura zilizopita.

393

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 393

9/4/2017 3:48:04 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Pale wakati wa vita vya Siffin Mu’awiyah alipomtaka Amr Aas kuvipanga vikosi yeye hakutekeleza matakwa yake hadi alipokuwa amepata ahadi kutoka kwake kwa mara nyingine tena kwamba wakati Ali atakapokuwa ameuawa na serikali yake (Mu’awiyah) ikawa imeanzishwa yeye atampa ugavana wa Misri. Uthibitisho mwingine wa ukweli kwamba Amr Aas alikuwa hodari sana katika kujadiliana na kulinda maslahi yake ni kwamba, wakati yeye na Abu Musa Ash’ari walipoketi pamoja kuhusiana na ile kadhia maarufu sana ya tukio la Suluhu na wale waliokuwa wakiziwakilisha pande zote mbili wakapendekeza majina ya watu tofauti kwa ajili ya ukhalifa, Abu Musa alitaja jina la Abdullah ibn Umar al-Khattab. Wengine pia walimuunga mkono wakisema kwamba Abdullah alikuwa ndiye anayestahili zaidi kwa ajili ya ukhalifa. Abu Musa akasema kwa kurudia tena na tena: “Ningependa kuhuisha jina la Umar al-Khattab kama ningeweza.” Hapo Amr Aas akamwambia Abu Musa: “Kama unataka kumfanya Abdullah bin Umar kuwa ndiye khalifa kwa ajili ya ushika dini wake, kwa nini humchagui mwanangu Abdullah kwa nafasi hiyo? Wewe unazitambua vema sifa zake na uwezo wake.” Hivi ndivyo jinsi Amr Aas alivyokuwa akijadiliana. Yeye alikuwa amekuja kama msuluhishi aliyeteuliwa na Mu’awiyah lakini mara alipohisi kwamba kulikuwepo na uwezekano wa mwanawe kuwa khalifa alijaribu kuitumia fursa hiyo na akalipendekeza jina lake kwa ajili ya cheo hicho. Wakati ule alikuwa pia amesahau kwamba katika vita vya Siffin yeye alikuwa jemadari mkuu wa vikosi vya Mu’awiyah na kama itatokea kupata ushindi alikuwa amemuahidi ugavana wa Misri, na akapuuza ule ukweli kwamba alikuwa ni msuluhishi kutoka upande wa Mu’awiyah na usuluhishi pia ulikuwa unafanyika kutokana na hila na ulaghai wake. Ukweli ni kwamba wote, Mu’awiyah na Amr walikuwa wanajua kwamba walikuwa wakimfanyia dhulma Ali. Ndani ya nyoyo zao walikuwa wanatambua kwamba Ali alikuwa bora kuliko wao. Wote walikuwa wakijitahidi kila mtu kufanikisha malengo yao wenyewe binafsi. Ni dhahiri walikuwa marafiki na watakia heri wa kila mmoja wao lakini katika hali halisi walikuwa na uhasama; na uadui wao ulidhihirika kutoka kwenye rangi ya nyuso zao, na kutoka kwenye maneno yao waliyoyatamka. Baada ya Vita vya Siffin kuwa vimemalizika Mu’awiyah aliwauliza washauri wake siku moja: “Ni kitu gani cha kushangaza sana?” Kila mmoja wao alitoa maoni yake juu ya jambo hilo. Pale ilipofika zamu ya Amr, yeye akasema: “Jambo la kushangaza sana ni, kwamba upotovu

394

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 394

9/4/2017 3:48:04 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

uweze kupata ushindi juu ya haki.” Kwa kusema haya, alidokeza kuhusu Mu’awiyah na Ali. Mu’awiyah akasema katika kumjibu mara moja: “Hapana. Jambo la kushangaza zaidi hasa ni kwamba mtu anaweza, bila ya kumuogopa mtu mwingine; na akijua kwamba hawezi kumfanyia madhara yoyote, kumpa yeye kitu ambacho hastahili kukipata.” Hapa alimaanisha kwamba yeye alikuwa ametoa ugavana wa Misri kwa Amr Aas ingawaje yeye Amr asingeweza kumletea madhara yoyote na pia hakustahili kuwa gavana. Maoni yaliyoshikiliwa na Amr Aas kuhusu Ali na Mu’awiyah yalikuja kudhihirika kutokana na kukiri alikofanya yeye kwa maneno haya: “Mimi nimedanganyika. Lilikuwa ni kosa kubwa sana kumwacha Ali na kumsaidia Mu’awiyah.” Kukubali huku na kukiri kwa Amr kunaonyesha ushushaji hadhi wa hali ya juu wa washirika na wafuasi wa Mu’awiyah. Walikuwa wakijidanganya wenyewe kwa makusudi kabisa. Wakati Ali alipokuwa amekwisha kupata shahada yake na muda mfupi tu baadaye Mu’awiyah akawa mtawala pekee wa nchi za Kiislamu; alianza kutumia mbinu za kigugumizi na kusita katika kumteua Amr Aas kama gavana wa Misri. Amr alidai kwamba Mu’awiyah lazima atimize ahadi yake. Kama mambo yalivyokuwa, baada ya Mu’awiyah kutotekeleza ombi lake, aliandika shairi refu na akalituma kwake. Baadhi ya beti zake ni kama zifuatazo: “Oh, Mu’awiyah! Usisahau thamani ambayo uliniahidi. Usikengeuke kutoka kwenye njia ya haki.” “Ewe mwana wa Hind! Nilikusaidia dhidi ya kiongozi mashuhuri na maarufu sana (yaani Ali ibn Abi Talib) kutokana na ujinga wangu” “Ni ulinganisho gani ulionao pamoja na Ali? Ni vipi upanga ukalinganishwe na shoka, Kilimia (mkusanyiko wa nyota ndogo ndogo) na tabaka la mwisho la dunia, au Ali na Mu’awiyah?” Baada ya kulipokea shairi hili, Mu’awiyah mara moja akamteua Amr Aas kuwa gavana wa Misri. Ni kiasi gani Mu’awiyah na Amr Aas, ambao maslahi yao binafsi, na masuala ya maafikiano yalivyowaleta pamoja, walivyochukiana pia kunadhirishwa na tukio lifuatalo:

395

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 395

9/4/2017 3:48:04 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Wakati Mu’awiyah alipomuweka Amr Aas kuimarisha ule mpango wa Usuluhishi na kutumia fursa ya upumbavu wa Abu Musa Ash’ari, yeye (Mu’awiyah) alisema jambo ambalo lilimuudhi Amr. Yeye kwa hiyo akasoma ubeti wenye dhihaka kuhusu Mu’awiyah ambao ni maarufu sana. Papo hapo Mu’awiyah akamtuma mmoja wa washauri wake aliyekuwa akiitwa Abdur-Rahman bin Umm Hakam kujibu ubeti huo na kuandika tashtiti juu yake. Abdur-Rahman akamdhihaki Amr katika idadi kadhaa ya beti ambamo alimtishia na kumlaani na pia akamlaumu kwa kukimbia kutoka kwenye uwanja wa mapambano wa Siffin wakati akiwa anakabiliana na Ali. Abdur-Rahman alisema: “Unapaswa kuacha uasi na ukaidi kwa sababu muasi ni mtu aliyelaaniwa. Wewe hukukimbia katika siku ya Siffin ukiwa unakabiliana na Ali? Ulikuwa hodari sana wa kuokoa maisha yako na ulihofia ungeweza kukabiliana na kifo, ingawaje kila mtu atakuja kufa siku moja.” Ni dhahiri kabisa watu wote hawa walikuwa na fikira za ajabu. Kwa upande mmoja walikuwa wameungana kudai kisasi juu ya mauaji ya Uthman na kumtangaza Ali kuwa ni dhalimu na kuchukua kisasi toka kwake, na kwa upande mwingine walitishiana, kukashifiana na kulaumiana wenyewe kwa wenyewe. Kulikuwa na kikundi miongoni mwa Waislamu ambacho kiliamua mengi ya masuala kulingana na maamuru ya akili na dhamiri njema. Wamewachukulia wote, Mu’awiyah na Amr Aas kuwa wadanganyifu, kwa sababu walipigana dhidi ya Ali ambaye alikuwa ndiye khalifa wa haki. Mu’tazilah walishikilia maoni haya. Mu’tazilah walikuwa majasiri kulinganishwa na madhehebu nyingine za Kiislamu katika suala la uchambuzi na uhakiki wa vitendo vya watu. Kama ilivyoelezwa na mwandishi wa al-Munyah wal-Amal, wengi wa Mu’tazilah wamejitenga na Mu’awiyah na Amr Aas na wamewatangaza kuwa ni wezi na wanyang’anyi, ambao wamepora Mali ya Umma. (Tazama Fajr al-Islam, uk. 240). Mu’awiyah alikuwa hasa kama alivyoelezwa na Ali. Yeye anasema: “Yeye ni mtu mwenye domo kubwa na tumbo lililovimba. Alikula kila alichoweza kukipata na alikuwa anatafuta kile ambacho hakuweza kukipata.” Na kuhusu Amr Aas yeye anasema: “Yeye alikuwa anasema uongo na alikuwa akizivunja ahadi. Kama alitaka kuazima kitu kutoka kwa mtu mwingine, yeye alim396

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 396

9/4/2017 3:48:04 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

kera kwa ajili hiyo, na kama mtu mwingine alimuomba yeye kitu, alionyesha hali ya choyo. Na kama alifanya makubaliano yoyote au ahadi basi yeye aliivunja.” Sifa zote hizi zilikuwa ni za kawaida kwa Mu’awiyah na Amr Aas, na hii ndio sababu ya kwa nini walishirikiana pamoja. Wakati mtu mwenye mdomo mkubwa akawa pia na tumbo kubwa kwa kawaida hula kila anachokiona, na anaendelea kutafuta kingine zaidi. Huwa hajali kama kitu hicho anachotumia ni cha halali au cha haramu; wala hana habari na hisia ya usawa na haki, ukatili na uonevu, zuri na baya na uadilifu na wema na ubaya. Na mtu anapokuwa ni muongo huwa anavunja ahadi anazoziweka yeye mwenyewe. Anapotaka kuazima kitu kutoka kwa mtu mwingine anambana kwa nguvu zote lakini anaonyesha uchoyo wakati yeye mwenyewe anapoombwa kitu. Huyavunja makubaliano na ahadi alizotoa. Anayafanya mambo yote haya kwa manufaa yake binafsi. Kile alichokisema Ali kuwahusu wote wawili kina maana kwamba vitendo vyao vilitegemea juu ya matilaba zao za ubinafsi. Katika mazingira hayo hakuna kitu kinachoweza kuwazuia kushirikiana pamoja katika udanganyifu na uasi, hususan wakati kama wote wawili wanategemea kunufaika kutokana nao, ingawa ndani ya nyoyo zao wanachukiana. Ali analirejea jambo hili pale anaposema: “Nimeisoma barua ya watu wawili hawa watenda maovu (Mu’awiyah na Amr Aas) ambao wameungana katika kukaidi amri za Mwenyezi Mungu.” Maadui wa Ali walipanga njama dhidi yake kwa ustadi mkubwa. Walaji njama hao walikuwa wengi, na nia na malengo yao yalikuwa pia ni tofauti kati ya mmoja na mwingine. Walikuwa, kama mambo yalivyokuwa, wameungana katika nukta, moja nayo ni kwamba Ali asije akawa mtawala wao. Mu’awiyah alikuwa na sehemu kubwa katika kupanga na kuimarisha hizo njama. Yeye alikuwa ndio kiongozi wa waasi na wengine wote walikuwa ni waunga mkono na wafuasi wake. Kwa kweli ilikuwa ni yeye ambaye alisababisha Vita vya Ngamia pia. Kama asingegawa zana kwa askari waasi, bila ya yeye mwenyewe kuja kwenye mstari wa mbele, vita hivi visingetokea. Madai haya pia yanathibitishwa na ukweli kwamba mara tu baada kupokea taarifa kuhusu Ali kuuchukua ukhalifa yeye alituma barua kwa Zubeir kupitia kwa mtu anayetokana na kabila la ‘Amis. Barua hiyo ilisomeka kama ifuatavyo:

397

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 397

9/4/2017 3:48:04 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

“Kutoka kwa Mu’awiyah bin Abi Sufyan kwa Amirul-Mu’minin Abdullaha ibn Zubeir. Baada ya salamu, napenda kukujulisha kwamba nimepokea viapo vya utii kwako kutoka kwa watu wa Syria na mara moja wao wamekukubali wewe kama khalifa wao. Sasa ni muhimu kwako wewe kujitahidi kwamba na watu wa Basra na Kufa pia waungane na wewe, kwa sababu kama raia wa miji hii miwili wakijitiisha kwako, mambo yatakuwa ni rahisi sana kwako. Baada yako wewe, nimepokea kiapo kwa ajili ya Talha bin Ubaydullah. Sasa wewe udai kulipiza kisasi cha mauaji ya Uthman kutoka kwa Ali na uwavute watu upande wako. Ninyi nyote mnapaswa kufanya juhudi za hali ya juu katika suala hili na kwa haraka vile vile. Mwenyezi Mungu akupe mafanikio na awaangamize maadui zako.” Wakati Zubeir alipoipokea barua hiyo inayosemekana, yeye alifurahi sana na akaionyesha kwa Talha pia. Wote wawili walidanganywa na uonyeshaji wa uaminifu wa Mu’awiyah. Wakavunja kiapo chao na Ali haraka sana, wakishughulika juu ya ushauri wa Mu’wiyah, na wakaamua kupigana dhidi yake. Matokeo yake Vita vya Ngamia vikaibuka. Matakwa ya Mu’awiyah yakatimia kwani alitaka kwamba khalifa wa wakati huo, Ali na wale wanaogombea ukhalifa, Talha na Zubeir waweze kupigana ili nguvu zao ziweze kudhoofika. Wakati Vita vya Ngamia vilipokwisha, Mu’awiyah alitumia viwango vikubwa vya pesa kuwahonga wale ambao kuhusu wao alihisi kwamba wanaweza wakamsaidia au angalau hawatamuunga mkono Ali. Na kama alijua kwamba mtu hatamsaidia yeye wala hatakaa kama mtazamaji mkimya wakati yeye (Mu’awiyah) atakapoasi, yeye alitwaa mbinu mpya kuwadanganya na kuwapotosha. Amr alikuwa mshauri mkuu na msaidizi wa Mu’awiyah katika njama zote. Ali hakujaribu kumbembeleza au kumpendeza Amr Aas na kuweza kumpata hata pale alipojua kwamba anashirikiana kisaliti na Mu’awiyah. Alibakia kuwa mwadilifu na mkweli kama alivyokuwa siku zote daima na hata ule muungano wa Amr Aas na Mu’awiyah haukuathiri umadhubuti wake. Yeye kwa hiyo alimwandikia barua Amr Aas kama ifuatavyo: “Umeifanya imani yako ya dini ifuate dunia ya mtu ambaye upotovu wake sio jambo lililofichika, unajulikana kwa wote. Anabadili hata mtu mwenye akili ya kiungwana ambaye atakaa naye karibu, na kumfanya mjinga mtu mwenye busara na uvumilivu. Umemfuata yeye na ukayatamani sana makombo yake kama vile tu mbwa anavyomfuata simba akiziangalia kucha zake kilafi na akitarajia kupata mabaki ya mawindo yake.

398

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 398

9/4/2017 3:48:04 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Kwa kufanya hivyo umeiangamiza dunia yako ya sasa na ile ya akhera vile vile, ingawaje ungefanikisha lengo lako hata kama ungebakia kwenye haki. Sasa endapo Mwenyezi Mungu atanijaalia ushindi juu yako na mwana wa Abu Sufyan nitawaadhibuni wote vinavyofaa hasa kwa matendo yenu maovu na hata kama sitaweza kupata udhibiti juu yenu na mkaendelea kuishi baada yangu, bado hatima yenu itakuwa mbaya kupita kiasi. Maafa Mara tu baadae Mu’awiyah aliondoka kwenda Iraqi pamoja na watu mia moja na ishirini elfu na wakapiga kambi karibu na ukingo wa mto Furati katika bonde la Siffin karibu na Raqqa. Waliendelea mbele na wakatwaa eneo kubwa la ardhi ya wazi na sawa (tambarare). Siffin ni bonde karibu na Furati. Katika siku zile kulikuwa na chemchemi nyingi za maji katika bonde hilo na vilevile idadi kubwa ya miti kati yake na mto Furati. Ali pia aliondoka Kufa pamoja na jeshi lake na wakafika Siffin baada ya kupita Mada’ini na Raqqa. Nia yake ilikuwa ni kumzuia Mu’awiyah kutokana na vita kwa njia ya ushauri na upole na kuishia kupigana tu iwapo kama ataonyesha ukaidi. Wakati alipofika Siffin aliona kwamba jeshi kubwa ambalo lilikuwa limepiga kambi katika ukingo wa mto huo lililkuwa limezuia njia ya jeshi lake mwenyewe ya kuweza kuyafikia maji. Ali akatuma ujumbe kwa Mu’awiyah akisema: “Sisi hatukuja hapa kupigana kwa ajili ya maji. Kama tungewasili hapa mapema kuliko ninyi tusingewazuini kuchukua maji.” Amr Aas alimshauri Mu’awiyah asiifunge njia ya jeshi la Ali kwenye maji. Alisema: “Ujasiri na ushujaa wa Ali unajulika sana duniani na amefuatana na jeshi kubwa la askari hodari. Haiwezekani kwamba wao watakubali hali hii ya sasa na wakae na kiu.” Mu’awiyah akajibu: “Wallahi haya ndio mafanikio yangu ya kwanza. Mwenyezi Mungu asinitosheleze kwenye haudh ya Kauthar kama watu hawa wanakunywa maji ya mto huu. Hata hivyo, kama wao watakuwa washindi, basi suala hili litakuwa tofauti.” Wafuasi wa Mu’awiyah walikuwa wamehamasika sana kiasi kwamba walimwambia Ali usoni mwake: “Wewe hutapata hata tone la maji hapa mpaka unakufa.” Kimkakati hali ya Ali ilikuwa dhaifu sana. Yeye kwa hiyo alimtuma Malik Ashtar kwenda kutwaa udhibiti wa ukingo wa mto huo. Aliwatawanyisha watu wa Mu’awiyah kwa ujasiri wake usio na kifani. Sasa ukingo ule ukawa chini ya udhibiti 399

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 399

9/4/2017 3:48:04 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

wa vikosi vya Ali. Kwa mujibu wa Allamah Ibn Qutaibah, Amr Aas alijisikia furaha kwa kushindwa huku kwa Mu’awiyah na akamwambia: “Ewe Mu’awiyah! Hebu niambie kitu kimoja: Tuseme na wao wakizuia maji kwa ajili ya jeshi lako kama vile ulivyokuwa umeyazuia wewe kwa ajili yao, utaweza kupigana dhidi yao ili kupata udhibiti wa huo ukingo wa mto huo? Kama mambo yalivyo, kuna uhakika kabisa kwamba Ali hataliruhusu jambo kama hilo ambalo wewe uliliona ni lenye kukubalika.” Baadhi ya sahaba wa Ali walitaka kumrudishia Mu’awiyah na jeshi lake adhabu ile ile na kuwazuia mgao wa maji, lakini yule mtu adhimu akawakatalia pendekezo lao na akaruhusu matumizi huru ya maji hayo kwa maadui zake. Masahaba zake walisisitiza sana wakisema: “Ewe Amirul-Mu’minin! Zuia huduma ya maji juu yao kama wao walivyokufanyia wewe. Usiwaruhusu kunywa hata tone la maji. Waache wafe kwa kiu. Kutakuwa hakuna haja ya kupigana. Unaweza hata ukawakamata kwa mikono yako mwenyewe.”Ali alijibu: “Mimi siwezi kufanya walivyofanya wao. Waachieni waweze kuyafikia maji.” Kama wafuasi wa Mu’awiyah wangekuwa ni watu wa tabia ya kiungwana wangeweza kuielewa tofauti kati ya Ali na Mu’awiyah na wangeweza kutambua kwamba ni yupi aliyekuwa kwenye njia ya haki na ni nani aliyekuwa amepotoka. Wangeweza kujua kwamba kumsaidia dhidi ya Ali kulikuwa ni kama kumsaidia mwizi au mnyang’anyi, au mtu ambaye alikuwa anapigana na Mtume. Imani yoyote ile aliyokuwanayo Amr Aas, alikuwa tayari amekwishaiuza kwa Mu’awiyah kwa ajili ya ugavana wa Misri. Vinginevyo kungekuwa hakuna uhalali wa kumsaidi kwake Mu’awiyah wakati alikuwa anajua kwamba alikuwa hawezi kulinganishwa na Ali. Katika Vita vya Siffin watu wa Syria walimkashifu na kumlaani Ali. Mu’awiyah alifurahishwa sana kusikia yote haya. Yumkini kabisa yeye mwenyewe binafsi aliwachochea na kuwaamuru kufanya hivyo kwa namna ile ile ambayo alikuwa amewaamuru katika kipindi cha utawala wake mwenyewe kwamba Ali atukanwe kutoka kwenye mimbari za misikiti. Kitendo hiki kiovu ni alama isiyofutika ya fedheha katika hatima yake, na kwa sababu hii ataangaliwa kwa dharau na wengine daima. Watu wa Iraqi walipowasikia watu wa Syria wakitumia lugha chafu kama hiyo, na wao pia walitamani kujibu kwa namna hiyo hiyo. Lakini wakati Ali alipokuja kujua kuhusu hilo alilichukulia kama hizaya juu ya uungwana na jina zuri la jeshi lake. Yeye kwa hiyo, alitoa hotuba mbele ya watu wake, ambayo ilifanya nyongeza 400

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 400

9/4/2017 3:48:04 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

nzuri sana kwenye kanuni za hali ya juu za serikali yake. Aliwaambia wawe na tabia ya heshima kwa kila mtu – imma alikuwa rafiki au alikuwa ni adui. Alisema: “Mimi sipendelei kwamba ninyi muanze kuwatusi hao. Kama mtaonyesha matendo yao maovu na mkataja mambo ya kweli kuhusu wao hilo litakuwa ni jambo linalokubalika na mtakuwa mmefanya wajibu wenu. Badala ya kutumia lugha chafu mnapaswa mseme: Ewe Mola! Zilinde imani zetu na imani zao pia. Ifanye suluhu yetu ipate kuwezekana na uwaondoe kwenye ujinga na wawe wenye busara ili waweze kutofautisha kati ya haki na batili na watelekeze upotovu na uasi.” Kama ilivyokuwa kawaida kwa Ali, alifanya juhudi zake bora kabisa kuepuka umwagaji damu na kuleta suluhu, lakini hakufanikiwa katika kazi hii. Aliuacha wazi mlango wa mapenzi na ukarimu kwa muda kiasi lakini watu wa Syria walikuwa wapumbavu kiasi kwamba hawakuweza kukuza uwezo wa kutofautisha kati ya wema na uovu. Masahaba wa Ali walishangaa kuona kwamba alikuwa anachelewesha uanzishaji wa vita hivyo, na alikuwa hawapi ruhusa ya kupigana. Kwao wao yeye akasema: “Na kuhusu kuuliza kwenu kwamba huenda ninachelewesha kuanza kwa vita kwa sababu ninaogopa kifo na ninataka kukiepuka, Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kwamba mimi sijali hata kidogo kama ninaelekea kwenye kifo au kifo ndio kinachonielekea mimi. Na vivyo hivyo kuhusu kusema kwenu kwamba nina mashaka kuhusu uhalali wa jihadi dhidi ya watu wa Syria, namuapa Mwenyezi Mungu kwamba sikuichelewesha vita japo kwa siku moja isipokuwa kwa sababu kwamba nilidhani baadhi ya watu hawa wangeweza kujiunga nami na wakawa wameongoka kupitia kwangu mimi na kuiona nuru yangu kwa macho yao yaliyofanywa kutoona vizuri. Ninalipendelea hili kuliko kuwaua wakati wakiwa katika hali ya ujinga, ingawa kwa nia na madhumuni yote wao wenyewe watawajibika kwa dhambi zao.” Pale Ali alipokuwa na uhakika kwamba watu wa Syria hawatakuja hata kidogo kwenye njia ya haki, na kupigana kukawa hakuepukiki, alichukua nafasi na kusimama kati ya majeshi hayo mawili na akasema: “Ewe Mola Wangu! Kama ningejua kwamba utakuwa radhi kama ningeweka ncha ya upanga juu ya tumbo langu na nikajipinda juu yake, na kuukandamiza kwa nguvu sana ili uweze kupenya kwenye mwili wangu na kutokea mgongoni kwangu, Wewe unatambua kabisa kwamba ningefanya hivyo. Ewe Mola! Mimi ninajua tu kile ulichonifundisha. Leo siwezi kufikiri juu ya kitu chochote bora kuliko kufanya jihadi dhidi ya watu hawa waovu. Kama tendo jingine lolote lingekuwa ni lenye kuridhisha zaidi Kwako, kwa hakika nisingejiepusha kulifanya.” 401

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 401

9/4/2017 3:48:04 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Kisha akasema: “Ewe Mola wa ulimwengu ambao umeufanya kuwa ni makazi kwa ajili ya wanadamu na sehemu ya kutembea tembea ya wanyama wenye kutambaa na wanyama wengine na viumbe wengine wasio na idadi wanaoonekana na wale wasioonekana! Ewe Mola wa milima thabiti ambayo umeifanya kama misumari kwa ajili ya ardhi, na kama njia ya uhai kwa ajili ya viumbe! Kama utatufanya kutawala juu ya maadui zetu basi tulinde na udhalimu na tuweke imara kwenye njia ya haki, na kama unawafanya maadui zetu kuwa washindi, tutunuku na shahada na utulinde na vishawishi vya maisha.” Muda kidogo kabla ya vita kuanza Amr Aas alitunga beti kadhaa na akazituma kwa Ali. Mojawapo ilisomeka kama ifuatavyo: “Oh! Abul-Hasan! Usikae bila kukerwa kuhusu sisi. Tunapolichukua jambo mkononi tunalifanya kuwa imara kikamilifu.” Mmoja wa masahaba wa Ali alitoa majibu ya ubeti huu katika maeno yafuatayo “Jihadhari na Abul-Hasan ambaye ni simba wa mwitu wa ujasiri na baba simba wengi. Yeye wakati wote ni mwangalifu na mwenye hadhari sana. Atakuponda ponda kama vile tu kitu kinavyopondwa na mchi kwenye kinu. Ewe mtu mjinga! Umekuwa mpumbavu kiasi gani kwamba unauma mikono yako na kusaga meno yako!” Wengi wa watu wa kabila la Rubiyya na Mazar walikuwa wafuasi wa Ali. Wakihutubiana mmoja na mwingine kati yao waliambiana: “Ole wako! Wewe huitamani pepo?” Walipoyasemezana haya, waliwashambulia watu wa Syria na kuzitawanyisha safu zao. Waliwaua maadui wengi sana kiasi kwamba upungufu mkubwa katika jeshi la Syria ukawa unaonekana wazi. Jeshi lote zima liligeuka shaghalabaghala. Mahraz bin Saur aliyetokana na kabila la Rabiyya akasoma ubeti huu wa kishujaa: “Ninawaua watu wa Syria kwa upanga wangu, lakini simuoni Mu’awiyah mwenye kengeza na tumbo kubwa. Moto wa Jahannam umemteketeza yeye. Huko mbwa wabwekao ndio majirani zake. Yeye ni muovu sana na aliyepotoka.” Watu wa kabila la Rabiyya na Mazar waliridhika kabisa kwamba wao walikuwa wanaunga mkono haki. Mmoja wa washairi wao alisema: “Watu wa kabila la Rabiyya walikimbia kwa haraka sana, kwenda kuiunga mkono haki. Haki ndio njia yao kuu.”

402

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 402

9/4/2017 3:48:04 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Mapigano makali sana yaliibuka na watu wengi sana waliuawa. Ali aliwashambulia kama kifo cha ghafla; na kila mtu aliyeshambuliwa naye alipelekwa Jahannam. Alikuwa sio yeye anayeutumia upanga wake, bali Majaaliwa ndio yaliyokuwa yanautumia upanga huo. Wakati alipokuwa anashambulia kiongozi anayeasi, huyo alikiona kifo juu ya kichwa chake na akakimbia kwa hofu na woga. Walikuwa wamejawa na hofu kweli kweli. Watu wa Syria walipoteza askari wengi sana kutokana na ujasiri na imani thabiti ya watu wa Iraqi. Vita hivyo vilidumu kwa miezi mitatu na siku ishirini; ambazo ndani yake mapambano tisini yalichukua nafasi ya kujitokeza. Hata hivyo, mapigano makali sana yalifanyika kwa majuma mawili. Mapigano haya hasa yanajulikana kama tukio la Harir. Katika vita hivi watu mia moja na ishirini watokanao na pande zote mbili waliuawa. Wale waliokuwa wakipigana kutoka pande zote mbili walikuwa ni ndugu, marafiki, jamaa wa kila mmoja wao na waliwaua vipenzi na watu wa karibu sana kwa mikono yao wenyewe. Watu wa kabila la Azd walisema kwa hali ya mambo yalivyokuwa: “Tunaikata mikono yetu kwa mikono yetu wenyewe. Hawa watu tunaowaua ni viganja na mikono yetu.” Wakati wa vita hivyo, askari wa Ali walilifikia hema la Mu’awiyah mara nne na walikuwa karibu wamteke yeye. Pale Mu’awiyah alipoona kwamba kushindwa kwake kulikuwa kunaelekea kutokea upesi, alipatwa na hofu sana. Yeye kwa hiyo aliamua kukimbia na akaamuru farasi aletewe kwa ajili yake. Kule kwenye upande mwingine Ali aliendelea kuwakata kata watu wa Syria vipande vipande. Kama mambo yalivyokuwa, Mu’awiyah aliwaamuru askari wake kuendelea kupigana, akitumaini kwamba Shetani kwa ajili yake na kwa ajili ya Amr Aas ataweza kuwapatia njia ya kwenye usalama. Mapigano makali yakaanza tena na yakaendelea kwa siku tatu. Wanahistoria wanasema kwamba upoteaji wa uhai wa watu katika siku hizi tatu ulikuwa hauna kifani katika vita vyovyote ndani ya historia ya Uislamu. Ibn Qutaiba anasema kwamba wakati wa usiku wa manane Ali alifanya tangazo litolewe ndani ya jeshi lake kwa ajili ya kuondoka. Pale sauti za ngamia zilipofika masikioni kwa Mu’awiyah, alimwita Amr Aas na kutaka kujua kutoka kwake kwamba kulikuwa kuna nini.

403

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 403

9/4/2017 3:48:04 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Amr akajibu: “Nadhani Ali anajiandaa kuondoka kwenye uwanja wa vita.” Kama hali ilivyokuwa, wakati jua lilipochomoza walimuona Ali amekwishafika karibu sana na wao. Ndipo Mu’awiyah akamwambia Amr: “Wewe uliniambia kwamba Ali alikuwa anapanga kukimbia lakini sasa mambo yamekuwa ni kinyume chake kabisa.” Amr akacheka na kusema: “Hii ilikuwa pia ni sehemu ya mkakati wa kivita wa Ali.” Mu’awiyah hapo akawa na uhakika kabisa kwamba kifo chake kimefika karibu mno. Wakati huo huo hata hivyo, watu wa Syria walipiga makelele: “Kuna Kitabu cha Mwenyezi Mungu kati yenu na sisi.” Wapiganaji wa Syria walikuwa wamevunjwa moyo na walikuwa hawana uwezo wa kupigana uliokuwa umebakia. Walifunga nakala za Qur’ani kwenye mikuki, wakapanda kwenye kilima na wakaanza kupiga makelele: “Ewe Abul-Hasan! Usikikate Kitabu cha Mwenyezi Mungu. Wewe unayo haki ya kutenda kwa mujibu wake na kutii hukumu zake.” Hila hii ilikuwa imepangwa na Amr Aas. Masahaba wa Ali walimchukia mtu yule vibaya sana kwa sababu alikuwa ameuza imani yake kwa ajili ya manufaa ya kidunia na akampendelea Mu’awiyah kuliko Ali. Ali alijua vizuri sana kwamba hila hii imefanywa na watu wa Syria ili kuokoa maisha yao, kwa sababu vinginevyo walikuwa hawahusiki chochote na Qur’ani hiyo. Yeye kwa hiyo, akalikataa pendekezo hili la usuluhishi lakini tofauti zikajitokeza kati ya wafuasi wake juu ya suala hilo. Baadhi yao walikuwa na maoni kwamba kwa vile vita vilikuwa vikipiganwa kwa ajili ya kuhakikisha utii kwenye Kitabu cha Mwenyezi Mungu na watu hao wa Syria walikuwa wanakiweka mbele Kitabu hicho hicho ili kuamua suala linalojadiliwa, pendekezo lao linaweza kukubaliwa na mapigano yakasimamishwa mara moja. Wengine hata hivyo walikuwa wametambua kwamba juhudi ilikuwa imefanyika ili kuwadanganya ambapo walikuwa wanaelekea kushinda. Wao kwa hiyo, wakasisitiza kwamba mapigano yaendelezwe. Hakuna kati ya makundi mawili hayo lililokuwa tayari kutelekeza msimamo wake. Ali alipata matatizo zaidi mikononi mwa marafiki zake kuliko mikononi mwa maadui zake. Kama Jibran Khalil anavyosema kuwa alikuwa kama mtume aliyetumwa kwa umma mbali na ule wake na katika kipindi mbali na kile anachohusika nacho, kwa sababu hata wale masahaba zake wa karibu sana hawakuweza kumwelewa sawasawa. Walikuwepo wakati wote watu makatili wenye hasira kali katika jeshi lake ambao walivunja ahadi walizokuwa wameziweka wao wenyewe na kusababisha vurugu. Wale ambao walikuwa watiifu kwake na wale ambao walikuwa wamejiunga naye shingo upande walifanana katika suala hili. 404

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 404

9/4/2017 3:48:04 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Mmoja kama hao alikuwa Ash’ath bin Qais. Alikuwa ni mlafi sana na mdanganyifu moyoni mwake. Alimsaliti Ali mara nyingi tu, lakini usaliti alioufanya yeye hapo Siffin ulikuwa mbaya zaidi. Wakati askari wa Mu’wiyah waliponyanyua Qur’ani kwenye mikuki na kusema kwamba kuna Kitabu cha Mwenyezi Mungu kati yao, na kipaswe kuamua suala linalojadiliwa, bwana huyu (yaani Ash’ath) alimwendea Ali na akasema: “Inaonekana kwamba watu hawa wako tayari kuafikiana na watu wa Syria na kuikubali Qur’ani kama msuluhishi. Kama unaafiki, ninaweza kwenda kumuona Mu’awiyah ili kujua nia yake ni nini.” Kwa wakati huu yale mabishano kati ya yale makundi mawili ya watu wa Iraqi (yaani, wale ambao walitaka kuendeleza mapigano na wale waliotaka yasimamishwe) yakawa makali zaidi. Ash’ath akaja kwa Ali tena na kusisitiza kwamba lile pendekezo la usuluhishi kwa kutumia Qur’ani likubaliwe. Ali na masahaba zake hawakuwa tayari kulikubali pendekezo hilo, lakini pole pole idadi ya wanaomuunga mkono Ash’ath ikaongezeka na wengine wao wakawa jeuri kiasi cha kumtishia Ali wakisema: “Oh, Ali! Lazima ukubali uamuzi wa Qur’ani ambao unalinganiwa, kushindwa kwako sisi tutakuua kwa panga zile zile ambazo kwazo tulimuulia Uthman, au tutakutoa na kukukabidhi kwa Mu’awiyah. Mu’awiyah ametutaka tutende kwa mujibu wa Kitabu cha Mwenyezi Mungu na sisi tumekubali kufanya hivyo. Wallahi na wewe pia unapaswa kukubali, vinginevyo tutakushughulikia kwa namna ile ambayo tumeitaja tayari.” Sasa nafasi ya Ali ikawa ngumu sana. Kulikuweko na njia mbili mbele yake – imma kutenda kwa namna ambayo mgawanyiko utaweza kutokea kati ya wafuasi wake au aafikiane na kile waasi walichokisema. Hali iligeuka kuwa ya hatari kabisa wakati wale waasi wakiongozwa Ash’ath bin Qais walipomtaka Ali amrudishe Malik Ashtar, kamanda wa jeshi lake kutoka kwenye uwanja wa vita na wakamtishia kwamba wangemuondosha madarakani na kumuua kama atashindwa kufanya hivyo. Ali akamwita Malik Ashtar arejee kutoka kwenye uwanja wa vita kwa shingo upande na akalikubali lile pendekezo la usuluhishi chini ya vitisho. Mu’awiyah na wale Wasyria walimteua Amr Aas kama msuluhishi kutoka upande wao. Ash’ath akamwambia Ali: “Sisi tunamteua Abu Musa Ash’ari kama msuluhishi kutoka upande wako.” 405

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 405

9/4/2017 3:48:04 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Amr Aas alikuwa jangili mkamilifu kabisa ambapo Abu Musa alikuwa zumbukuku tu – kiasi mtu mpumbavu hivi. Ali aliwajua wote vizuri sana. Yeye, kwa hiyo akasema: “Mimi simtaki Abu Musa Ash’ari. Huyu alinitelekeza katika wakati mgumu na akawazuia watu kunisaidia. Kisha akakimbia zake kwenda kuokoa maisha yake na ilikuwa ni mimi niliyempatia hifadhi. Hata hivyo, ninamteua Ibn Abbas kuwa ndiye msuluhishi.” Ash’ath na wafuasi wake wakajibu: “Tunataka msuluhishi awe ni mtu asiye na upande na awe hana mwelekeo imma kwako wewe au kuelekea kwa Mu’awiyah.” Maneno haya yanaonyesha jinsi watu hawa walivyokuwa wadanganyifu kwa Ali. Walikuwa ama ni mawakala wa Mu’awiyah au walitaka tu kumsaidia yeye. Amirul-Mu’minin alikuwa hakukubali kabisa kumteua Abu Musa kama msuluhishi. Yeye, kwa hiyo akasema: “Haya. Kama Ibn Abbas hakubaliki kwenu, mnaweza kumteuwa Malik Ashtar.” Kama mambo yalivyokuwa, waasi hao hawakukubali hata pendekezo hili. Ash’ath alikuwa na wivu sana juu ya Malik Ashtar. Malik Ashtar alikuwa ni mfano bora wa haki na uaminifu. Yeye alikuwa ni mtu anayeona mbali na dhamiri madhubuti. Alikuwa ni mpiganaji mashuhuri. Ash’ath kama ilivyokuwa, yeye alikuwa hana hata sifa moja kati ya hizi. Ilikuwa ni kutokana na sifa zake za kipekee kwamba Ali alikuwa anamheshimu sana Ashtar. Alikuwa hana staha kama hiyo kwa mtu mwingine yoyote ikiwa ni pamoja na Ash’ath mwenyewe. Ash’ath akasema kwa ghadhabu kali: “Alikuwa ni Ashtar aliyewasha moto huu. Ni yeye ambaye chini ya amri zake sisi tumebanwa.” Ali na marafiki zake hawakuweza kushinda dhidi ya waasi hao, ambao idadi yao ilikuwa imeongezeka sana. Inawezekana moja ya sababu ya ukaidi wa wale watu ilikuwa kwamba vita hivyo vilichukua muda mrefu sana. Walikuwa wamekwishachoka na hawakuwa katika hali ya kupenda kupigana tena. Ilikuwa ni kwa sababu hii kwamba walitwaa mwelekeo huu kwa Ali na wakamuunga mkono Ash’ath. Wakati Ali alipoona msimamo wao usiobadilika na pia akakadiria kwamba idadi ya wafuasi wake ilikuwa imepungua akasema: “Hivi ni kweli mmedhamiria katika kumteua Abu Musa kuwa ndiye msuluhishi?” Wao wakajibu kwa kuthibitisha hilo. Hapo ndipo akasema: “Wakati sina kauli juu ya suala hili basi mnaweza kufanya chochote mnachotaka.” Katika jeshi la Ali, wale ambao walikuwa hawakukubaliana na usuluhishi na wakataka kuendeleza mapigano walikuwa wameudhika sana kwamba binadamu 406

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 406

9/4/2017 3:48:04 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

yoyote anaweza kuteuliwa kama msuluhishi katika suala la Kitabu cha Mwenyezi Mungu. Na kwa nini yeye ateuliwe wakati suala lenyewe lilikuwa liko wazi kabisa? Kulikuwa hakuna shaka kuhusu ukweli kwamba Ali alikuwa na haki na Mu’awiyah na wafuasi wake walikuwa kwenye batili. Huu ndio msingi ambao kwamba vita hivyo vilipiganwa dhidi ya Mu’awiyah. Katika vita vile idadi kubwa ya wafuasi wa Ali walikuwa wameuawa. Wote hao waliamini kwamba walikuwa wanaiunga mkono haki kwa kupigana kutokea upande wa Ali. Hivyo ilikuwa ni makosa kwa Ali kuendekeza shaka yoyote yeye mwenyewe kuhusu kuwa kwenye haki na kukubaliana na usuluhishi. Mmoja wa wapiganaji akatunga wito wa: “Hakuna hakimu isipokuwa Allah.” (Baadae maneno hayo yakawa ndio wito wa msingi wa Khawariji na imani zao zote zilikuwa ndani ya wito huo). Wito huu ulipenya ndani ya jeshi lote zima kwa muda mfupi sana uliowezekana. Kila mmoja alikuwa anapiga kelele: “Hakuna hakimu isipokuwa Allah.” Wale ambao walipinga usuluhishi waliyafanya ndio kanuni ya msingi ya dini yao mpya. Watu hawa walianza kumpinga Ali wazi wazi na wakadai kwamba lazima akubali kosa lake, kwa usahihi zaidi, ukafiri wake, kwa sababu ya kukubali kwake suluhu, ingawaje uamuzi uko kwa Mwenyezi Mungu. Walidai pia kwamba atupilie mbali yale makubaliano aliyoyafanya na Mu’awiyah. Wakaongeza kwamba wao wataweza kumuunga mkono na kupigana dhidi ya Mu’awiyah tu endapo angeridhia madai yao na kushindwa kufanya hivyo, wao watapigana dhidi yake. Amirul-Mu’minin hakuridhia kwenye madai yao. Makubaliano yalikuwa tayari yamekwisha kamilishwa na Mu’awiyah na makundi yote yalikuwa yamekubali kuzingatia kauli ya wasuluhishi na yeye alikuwa sio mtu wa kuweza kuvunja kauli yake. Hakuweza pia kukubali ukafiri wake, kwa sababu alikuwa ndiye Muislamu mwaminifu kwa wakati wote na alikuwa hajavunja sheria yoyote ya kidini au kumkosea mtu yoyote. Kama angekuwa kama Mu’awiyah na Amr Aas ambao kamwe hawakujali juu ya makubaliano yoyote waliyoyafanya wao, yeye pia angeweza kuafikiana na ushauri wa Khawarij, kutumia msaada uliopendekezwa na wao na hatimae kupata ushindi juu ya Mu’awiyah. Ilikuwa ni katika mazingira haya kwamba Ali alisema kwa uchungu sana, akizingatia kutokuwa na msaada kwake na ukaidi na uasi wa Khawarijii: “Enyi watu ambao 407

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 407

9/4/2017 3:48:04 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

juu yenu hila ya udanganyifu ilichezwa na ambao mlipatwa na ulaghai! Ninyi, ambao mlidanganywa licha ya kuwa mnautambua ulaghai na hila za mdanganyifu huyo. Ninyi, ambao mlibaki na msimamo usiobadilika, mliofuata hisia zenu, mkapotea njia na mkaanza kutangatanga hapa na pale. Haki ilikuwa dhahiri kabisa, lakini mligeukia mbali nayo. Njia ilikuwa wazi nyeupe lakini mkaiacha na mkaenda kwenye njia potovu. Ninaapa kwa Yeye ambaye aliipasua mbegu na aliyeumba nafsi kwamba ninyi mlikuwa mmepata elimu kutoka kwenye asili yake, mkakusanya wema kutoka kwenye sehemu yake halisi, mkatwaa ile njia ya wazi na mkapita kwenye njia kuu ya haki, njia zile zingewakaribisheni na dalili za haki zingekuwa dhahiri kwenu. Halafu hakuna hata mmoja ambaye angekuwa mwathirika wa ufukara na hakuna kati ya Waislamu au wasiokuwa Waislamu ambaye angedhulumiwa.” Matokeo ya suluhu ile yanajulikana vema. Khawariji waliasi dhidi ya AmirulMu’minin. Kama ilivyokuwa haja yake, Ali alijaribu kwa juhudi zake zote kwamba watu wale waweze kuacha uasi, na kupigana kusiweze kutokea. Khawariji walidai kwamba Abu Musa na Amr Aas walikuwa wamepinga amri za Mwenyezi Mungu kwa kujifanya wasuluhishaji, na ndugu zao (yaani, watu wa jeshi la Ali) wamekuwa makafiri kwa kule kukubaliana na usulihishi, kwa sababu walikuwa wameafikiana na uamuzi wa wanadamu katika suala la dini. Khawariji wakasema: “Sasa tunawaacha, na Mwenyezi Mungu apewe shukurani sana kwamba kwa kulinganishwa na wengine, sisi tuko kwenye njia iliyonyooka, njia ya haki.” Je! Ilikuwa Ni Halali? Katika kuendeleza yale yaliyoelezwa na kabla ya kutoa maelezo juu ya Khawariji, inaonekana kuwa na muhimu kutaja matukio mawili makhsusi ambayo yalitokea katika Vita vya Siffin. Tunahisi kwamba matukio haya mawili ni ushahidi mkubwa sana wa ule ukweli kwamba Ali alifikia lengo lake kwa mafanikio sana, kwa sababu mafanikio halisi yana maana ya kuziteka nyoyo za watu na wala sio kusimika bendera katika ngome ya adui. Tunapendekeza kuyataja matukio haya kwa kina hasa, kwa sababu wengi wa wapenzi wa Ali wanafikiri kwamba katika matukio haya mawili hakufanya ya kufaa sana na alimfanyia Mu’awiyah na jeshi lake katika namna ambayo hawakustahili. Watu hawa wanasema kwamba kama asingefanya alivyofanya katika matukio haya mawili angeweza kufanikiwa bila ya mapigano hasa na hata kama ingekuwa ni lazima kupigana vita hivyo visingeweza kuwa vikali sana na virefu kiasi hicho. 408

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 408

9/4/2017 3:48:04 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Tukio la kwanza lilikuwa lile ambalo tumekwishalieleza katika kurasa zilizotangulia yaani ni kusema, wakati Ali alipopata udhibiti juu ya ukingo wa mto Furati aliwaruhusu maadui zake kutumia maji ya mto huo kama lilivyotumia jeshi lake mwenyewe, ingawaje hapo mapema, wakati ukingo huo wa mto ulipokuwa unadhibitiwa na watu wa Syria, wao walikuwa wamekataa kumruhusu Ali na sahaba zake kuyafikia maji, na walisema: “Hatutakupa maji hata tone mpaka ufe kwa kiu.” Lakini Ali akawatawanyisha, na baada ya kupata udhibiti juu ya mto huo, akauacha ukingo wake wazi kwa maadui. Mu’awiyah alikuwa ameuchukulia udhibiti wa ukingo wa mto huo kama mafanikio yake ya kwanza; na alikuwa ameahidi kwamba hatawaruhusu watu wa Iraqi kuchukua hata tone la maji, isipokuwa labda wapate udhibiti wa ukingo wa mto huo kwa kutumia nguvu. Kama mambo yalivyotokea, baada ya Ali kuwafukuza Wasyria hao na akaukalia ukingo wa mto huo aliwaambia: “Mnaweza ninyi kunywa maji kama vile tu tunavyokuwa tunayanywa sisi.” Tukio la pili linahusiana na Amr Aas ambaye muda fulani alikuwa chini ya huruma za Ali wakati wa mapambano, lakini yeye hakumuua. Kwa kifupi kadhia yenyewe ni kama ifuatavyo: Wakati Ali alipoona vita vikali vikiendelea na watu wengi wakiwa wanauawa, yeye alipanda kwenye kipando na akasema: “Ewe Mu’awiyah!” Naye Mu’awiyah akaitika: “Naam.” Hapo ndipo Ali akasema: “Kwa nini watu wote hawa wauane wenyewe bila umuhimu kwa sababu yetu sisi? Waachie watu hawa na uje kwenye uwanja wa mapambano wewe mwenyewe ili sisi wawili tuweze kuamua suala hili kwa kupigana sisi. Yeyote atakayeshinda ataweza kuwa ndiye khalifa.” Amr Aas akamwambia Mu’awiyah: “Hiyo ni sawa kabisa! Ali amesema jambo la haki kabisa.” Mu’awiyah akacheka na kusema: “Oh, Amr! Na wewe pia umekuwa mwathirika wa tamaa.” Alikuwa na maana ya kusema kwamba kama yeye atakwenda kupigana na Ali kwa vyovyote vile atauawa, na kifo chake kingesafisha njia kwa ajili ya Amr kuwa khalifa. Amr akasema: “Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kwamba unaweza tu kuiokoa hadhi na heshima yako iwapo kama utapigana na Ali.” Mu’awiyah akajibu: “Wallahi wewe unafanya utani. Mimi nitapigana na Ali nikiwa pamoja na jeshi langu.” Kwa maneno haya alikuwa na maana kwamba ilikuwa haiwezekani kuanza kupigana na Ali katika pambano la watu wawili wawili. Wanahistoria wanasema kwamba Amr Aas alisema kwa kumkebehi Mu’awiyah: “Hii ni aibu kwamba unaonyesha woga katika kukabiliana na Ali uso kwa uso na ku409

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 409

9/4/2017 3:48:04 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

jeruhi hisia za watakia-heri wako. Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kwamba hata kama itanibidi kufa mara elfu moja nisingeacha kupigana dhidi ya Ali. Amr alitoka kuja kupigana na Ali. Ndani ya muda kama wa mpepeso wa jicho Ali alimshambulia kwa mkuki wake na adui akaanguka chini. Kisha upanga wa AmirulMu’minin ukawaka kwenye kichwa cha Amr kama radi na Ali alikuwa karibu amuue, lakini yeye Amr akajiweka uchi. Ndipo Ali akageuza uso wake na akaondoka mahali hapo kwa sababu staha yake ya kurithi na uungwana wake havikumruhusu yeye kuangalia sehemu za siri za mtu yoyote yule. Wale wanaompenda Ali, na wanataka kwamba angekuwa amefaulu, wanasema kwamba katika matukio mawili yote haya yeye hakufanya yanayostahili. Wao wanayo maoni kwamba pale alipokuwa amepata udhibiti wa ule ukingo wa mto alikuwa na haki ya kuwanyima watu wa Syria maji yale kwa sababu mbili: Kwanza kabisa inaruhusiwa katika vita kutumia mbinu ambayo itamfanya adui asalimu amri au inayomdhoofisha kwa kiasi kikubwa hadi anakuwa katika hali ya kutoweza kupigana kwa nguvu tena. Kwa mambo haya kuwa dhahiri, Mu’awiyah alikuwa amepata udhibiti juu ya ukingo wa mto na akauita kuwa ni mafanikio yake ya kwanza. Pili, Ali alipata udhibiti juu ya ukingo wa mto huo baada ya kupigana, na sasa ulifikia kuwa sawa na ngawira ya kivita. Kwa mujibu wa sheria za kivita au kijeshi, kwa hiyo, angeweza kuwa na haki ya kukataza matumizi yake kwa Mu’awiyah na jeshi lake. Hali kadhalika, wanasema kwamba Ali alifanya kinyume wakati alipomruhusu Amr Aas kukimbia na kuyahifadhi maisha yake. Amr alikuwa ndiye kamanda mkuu wa vikosi vya Mu’awiyah, mla njama mwerevu wa kisiasa na adui wa jadi wa Ali. Aliwachochea watu kuasi dhidi ya Ali na akakusanya jeshi kubwa kupigana dhidi yake. Kama angemuua papohapo wakati upanga wake - Dhul-Fiqar ulipokuwa umekifikia kichwa chake angekuwa na sababu ya kufanya hivyo kwa sababu namna tatu. Kwanza kabisa, kulingana na sheria za kijeshi, kumuua Amr kungekuwa na maana ya kumuua mmoja wa makatili hatari kabisa wa Syria. Baada ya kifo chake majeshi ya adui yangekuwa yamevunjwa moyo na yangeweza kukimbia. Mu’awiyah angekuwa amepoteza msaidizi mkuu wake na Ali angekuwa amemuua mtu mdanganyifu kupita kiasi, mwenye hila na adui mwenye ushawishi na mvuto. Pili Amr Aas alitokana na jeshi ambalo halikuwa na kiapo cha utii kwa Ali na alikuwa na uadui kwake na kwa marafiki zake. 410

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 410

9/4/2017 3:48:04 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Tatu alikuwa ni Amr Aas aliyekuja kupigana dhidi ya Ali na alimtia changamoto yeye. Kama angekuwa jasiri kama Ali, na angepata fursa ya kumuua yeye, kwa hakika asingemuacha. Hali ikiwa kama hivyo, endapo Ali angemuua Amr hakuna mtu yeyote ambaye angeweza kumlaumu yeye. Kwa kuzingatia ukweli wa kwamba Ali alikuwa ndiye kamanda wa jeshi na katika matukio haya mawili mafanikio yalikuwa miguuni kwake, ilikuwa ni muhimu kwake kutoipoteza fursa hiyo, kwa sababu ni sheria ya vita. Sifa halisi ya kamanda wa kijeshi ni kwamba huwa haipotezi hata fursa ndogo kabisa ya kushinda vita. Kutokana na mtazamo halisi wa kijeshi, upinzani uliotolewa na wakosoaji hawa ni sahihi. Lakini swali ni kwamba: Je, hivi Ali alikuwa ni Kamanda wa jeshi tu basi? Kile ambacho tumekisema kuhusu Ali mpaka hapa kinaonyesha wazi kwamba kulikuwa hakuna undumilakuwili au ukinzani katika utu wake. Basi ni vipi ingewezekana kwamba kwa upande mmoja aweze kuwa na sifa za kiwango cha hali ya juu na kuyatazama mambo kwa kukubali kusikiliza mawazo ya wengine japo asikubaliane nayo, na kwa upande mwingine aweze kuwa na akili finyu na ubinafsi kiasi kwamba aweze kutelekeza maadili na kanuni zote ili kupata ushindi tu? Ukweli ni kwamba yeye hakutaka ushindi tu katika vita kama makamanda wengine bali pia yeye alilinda kanuni za kibusara na kibinadamu na alikuwa na heshima kubwa sana juu ya thamani ya mwanadamu. Sifa za Ali na kanuni za maadili zilikuwa viambatani vya nafsi yake na kamwe hakuziacha japo kwa kitambo kidogo. Tabia yake ilikuwa ni ile ile katika Vita vya Siffin kama katika Vita vya Ngamia. Maadui zake walikuwa wameziba njia yake ya kwendea kwenye ukingo wa mto, na walisema kwamba wasingemruhusu yeye kuchukua japo tone moja la maji hadi atakapokufa. Lakini aliwashauri watu kwa maneno haya: “Kama ndugu yako amechukizwa nawe, jaribu kumridhisha kwa njia ya wema, na epuka madhara yake kwa kuwa mpole kwake.” “Mshinde adui yako kwa njia ya wema na upole. Ushindi kama huo ni wenye kupendeza sana.” “Kuna faida gani ya yale mazuri ambayo yanapatikana kwa kupitia kwenye maovu.”

411

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 411

9/4/2017 3:48:05 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

“Cheo cha mtu ambaye anafanya jihadi na akauawa kishahidi katika njia ya Mwenyezi Mungu, sio cha juu sana kuliko cha yule ambaye haruhusu adui yake kudhurika baada ya kumshinda. Mtu kama huyo yuko karibu sana na malaika.” Ni Ali yule yule ambaye alikuwa amesema kuhusu muuaji wake baada ya Vita vya Siffin: “Endapo mtamsamehe basi kitendo chenu kitakuwa karibu kabisa na wema.” Bila shaka mtu mashuhuri huwa hafungwi na mipaka ambayo wapenzi wa Ali wanataka kushauri kwa ajili yake. Sifa za Ali zilikuwa sio sawa na zile za kamanda wa jeshi ambaye anataka kupata ushindi kwa gharama yoyote ile. Wakati wa vita maadili ya hali ya juu na wema wa kibinadamu, kwa kawaida huwa vinapuuzwa na hakuna umuhimu ambao unawekwa kwenye maisha ya mwanadamu. Dhamiri na akili za watu maarufu na waungwana, hata hivyo, zinaheshimu mambo haya. Kwa hakika Ali alikuwa mtu muungwana sana kuweza kuwanyima hata maadui zake maji, ingawa kwa kufanya hivyo angeweza kuwafanya washuke kwa magoti yao. Alikuwa ameunda kanuni kwa ajili ya hadhi na heshima ya uhai wa mwanadamu ambazo zilikuwa bora sana kuliko kanuni na sheria zilizopo sasa. Staha na uungwana wake havikuweza kumruhusu yeye kumuua Amr Aas wakati alipokuwa amemdhibiti ingawa ingeweza kuwa sahihi kabisa kumuua yeye kwa mujibu wa kanuni za kivita. Kwa kutwaa kwenye matukio haya mawili ile tabia ya kipekee ya, Ali aliongeza sura ya dhahabu katika historia ya mwanadamu. Uungwana ni jambo moja na ujasiri ni jingine. Uungwana unajumuisha dhana ya ujasiri pamoja na moyo mkunjufu na mapenzi juu ya wanadamu. Mtu ambaye ndani yake sifa hizi zote zimekusanyika anakuwa si wa kawaida, ni wa kipekee kama akilinganishwa na wengine, na mwenye kuheshimika mbele ya wote wenye busara na elimu. Kama ujasiri una maana ya kushambulia adui na kupata ushindi dhidi yake, uungwana na ujanadume una maana ya yote haya na vile vile kumcha Mungu, uvumilivu, upendo, upole na muhanga. Huyo anayeitwa jasiri huwa haamini juu ya mipaka yoyote au masharti katika suala la ushindi na anataka kumzidi nguvu adui kwa njia zote zinazowezekana. Mtu janadume na muungwana, kama mambo yalivyo, hufuata sheria na kanuni fulani katika suala hili. Huwa hafurahii ushindi isipokuwa uwe unaendana na uadilifu na heshima ya binadamu. Anapendelea kufa yeye mwenyewe kuliko kuvunja haki na heshima za kibinadamu. Na kama sifa hizi zilikuwa zimekusanyika kwa mtu yoyote kamwe, basi alikuwa ni Ali ibn Abi Talib. 412

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 412

9/4/2017 3:48:05 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Je, ingewezekana kwa Ali kuwanyima wanadamu, hata kama wangekuwa ni maadui zake, maji yale ambayo yalikuwa yakitumiwa hata na wanyama na ndege? Angeweza kustahimili kumuua mtu ambaye alitaka kuishi kama wengine wote? Hivi Ali angeweza kumuua mtu ambaye alitaka kuishi pamoja na wengine, kuliangalia jua na mwezi kama wanadamu wengine, kula mkate, na kunywa maji? Hawa wapenzi wa Ali hawatambui kwamba matukio haya mawili ambayo yalitokea hapo Siffin yanafanana na mengine mengi ambayo kutokana nayo wakosoaji wake wanapinga sera yake ya jumla ya serikali? Wakosoaji hawa wanasema kwamba yeye alifanya idadi ya makosa ya kisiasa. Kwanza kabisa alimuuzulu Mu’awiyah kwenye ugavana wa Syria mara tu baada ya kuwa khalifa; ingawa ilikuwa ni muhimu kwake yeye kuchelewesha kitendo hiki, hadi pale serikali yake itakaposimama imara. Pili, aliwachokoza Talha na Zubeir. Kama angedumisha uhusiano mzuri nao Vita vya Ngamia visingetokea na nguvu zake zisingepungua. Tatu, alikuwa mkali sana kwa magavana wake na maafisa wengine na hakuwaruhusu kulimbikiza mali kwa njia zisizokuwa za halali, ingawaje angeweza kuwa mpole kwao ili waweze kumuunga mkono. Vitendo hivi hasa vya Ali ambavyo vinashutumiwa na wakosoaji wake vilikuwa, kwa maoni yetu sisi, ndio matendo yake bora na yalikuwa ni matokeo ya hisia zake za upendo na dhamira njema. Tunadhani kwamba wakosoaji wake wanatoa vipingamizi hivi kwa sababu wao wanavihukumu vitendo vyake kwa mujibu wa viwango vya wakati ambapo uaminifu na uadilifu vimekoma kuwepo. Vitendo vyake vinaweza kupingika kwa kuzingatia viwango vya maadili vya nyakati za Bani Umayyah na Bani Abbas lakini kwa hakika havipingiki wakati tunapoweka wakati wake yeye mwenyewe katika mazingatio. Katika masuala ya mipango na siasa Ali alikuwa mwangalifu na mwenye hekima kuliko hata wale Waarabu wanasiasa maarufu. Alikuwa na umaizi wa kina katika masuala ya kisiasa na kijeshi na alizijua hisia za ndani kabisa za watu vizuri zaidi kuliko mtu mnafiki kama Mu’awiyah. Kama hali ilivyokuwa, yeye alichukia uchochezi wa kisiasa na msimamo wa liwezekanalo naliwe (ubahatishaji). Alidharau kila kitu ambacho kilimfanya mwanadamu kuweza kufedheheka. Yeye hakutamani mafanikio yoyote ambayo yalipatikana kwa ulaghai na udanganyifu. Yeye wakati wote alipenda uadilifu. 413

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 413

9/4/2017 3:48:05 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Hata pale Mu’awiyah alipokuwa akivuma vibaya kwa uchochezi na udanganyifu na ikawa inasemekana kwamba Ali hakuwa mjanja kama yeye alisema: “Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kwamba Mu’awiyah sio mwerevu sana zaidi yangu lakini yeye ni mdanganyifu na muovu. Kama nisingedharau udanganyifu, mimi ningekuwa ndiye mjanja zaidi hasa miongoni mwa Waarabu.” Tumeyaelezea kwa ufupi yale matukio mawili ya Vita vya Siffin ili kuonyesha kwamba sio tu wakosoaji wa Ali bali pia hata wapenzi wake hawakuweza kuielewa haiba ya Ali vizuri. Wengine wanashutumu uongozi wake na wengine wanasema kwamba yeye hakuitumia vizuri ile fursa ya ushindi katika Vita vya Siffin. Kwa kweli wote hao wameshindwa kumuelewa Ali kikamilifu kwa sababu machoni kwake asili ya maana ya siasa na kanuni za kivita ilikuwa ni moja, au kwa maneno mengine ilikuwa ni nafsi ya Ali, ambayo dalili zake tofauti zilikuwa katika upatanifu kamili kati ya moja na nyingine, na ni pete tofauti za mnyororo mmoja. Kwa mujibu wake yeye kigezo cha wema na uovu, kufuata sheria na uhalifu kilikuwa ni dhamiri njema na tabia za upole. Rafiki yangu mmoja, ambaye ni mwandishi mwenye elimu nyingi na mwenye ghera sana juu ya historia ya Uislamu safari moja aliniambia: “Wewe huwezi kunishawishi kwamba Ali alikuwa na ujuzi sana katika siasa, na uwezo wa kutosha kuongoza mambo ya watu kama unavyodai wewe.” Mimi nikamjibu: “Chukulia kwamba Ibn Muljam asingepanga kumuua Ali, na hata kama alipanga, lakini akawa hakufanikiwa katika kukamilisha lengo lake kutokana na kuwepo kwa marafiki zake Ali karibu naye, na akabakia kuwa hai. Na uchukulie kwamba alipigana na Mu’awiyah kama alivyokuwa tayari amekwishanuia na akawa amepata ushindi dhidi yake, kama ilivyokuwa ikielekea kutokea. Au chukulia kwamba ule mpango wa suluhu wa Mu’awiyah ulishindwa na jeshi la Ali halikuwa limegawanyika katika makundi mawili na aliiendeleza vita na akamkamata Mu’awiyah na Amr Aas. Kwa maneno mengine matokeo ya vita hivi yangekuwa ni sawa na yale ya vita vya Ngamia, na Ali akawa amemshinda Mu’awiyah kama alivyokuwa amemshinda Talha na Zubeir. Katika hali zote hizi mengi yangetegemea juu ya mazingira ya bahati. Hapo basi wewe ungesema nini kuhusu uongozi wa mikakati ya vita ya Ali? Basi usingesema 414

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 414

9/4/2017 3:48:05 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

kama sisi kwamba licha ya ufasaha wa usemaji wake, busara, uungwana na maadili ya hali ya juu, Ali alikuwa mwanasiasa mjanja zaidi kuliko Mu’awiyah; na mwenye uwezo zaidi wa kutatua matatizo kuliko Amr Aas. Hivyo kama alikuwa hakupata ushindi dhidi ya Mu’awiyah kwa nini isemekane kwamba alikuwa hana ujuzi wa siasa na mbinu za vita. Kwa nini isisemekane kwamba bahati zilikuwa ndio sababu halisi ya huku kubaki bila kufanikiwa. Na kile tulichokisema kuhusu siasa za Ali kuhusiana na matukio ya Siffin ni chenye kutumika sawa sawa na kule kuuzuliwa kwa Mu’awiyah na magavana wengine. Kama ambavyo kushindwa kwake hapo Siffin kulikuwa ni kutokana na mazingira, katika njia hiyo hiyo, yeye hakufanikiwa katika suala la kuuzuliwa kwa Mu’awiyah na wengineo. Bahati za wakati ule, siasa za Uthman na mazingira yaliyobadilika, ndivyo vilitoa silaha kama hizo za udanganyifu na udhalimu kwa magavana hao, kama isivyoweza kutumiwa na Ali kutokana na uungwana wake, ukunjufu wa moyo, busara, umashuhuri na hadhi yake.” Watu wote ikiwa ni pamoja na wakosoaji hao na wanahistoria wamekuwa na mazoea kuyaangalia matukio mbalimbali na kuyatolea hukumu kulingana na mawazo ya wengi, na kukadiria uwezo wa watu mashuhuri kwa kuzingatia mafanikio na kushindwa kwao. Hawatilii maanani zile njia zilizotumiwa na wao wala hawazingatii yale maadili ya hali ya juu na sifa duni za makundi pinzani. Imetokea mara kwa mara kwamba wanasiasa mashuhuri na watu wenye uwezo kabisa wakashindwa kwa sababu ya bahati na matukio ya ghafla, na watu wa kawaida wakafanikiwa kwa sababu hizo hizo. Imma wale wanasiasa maarufu hawakuweza kuyazuia matukio hayo yasitokee, wala hao watu wa kawaida kuyasababisha yatokee kwa njia ya nguvu zao wenyewe na utashi. Kwa kifupi, wapenzi wa Ali wanataka kwamba Ali pia angetwaa diplomasia na sera ya ulaghai na udanganyifu na hatimae angeweza kuwa mshindi. Ali hakuwa tayari, kama mambo yalivyokuwa, kukengeuka kutoka kwenye haki na uadilifu. Watu hawa wanatamani kwamba Ali angekuwa Mu’awiyah bin Abu Sufyan, wakati yeye alikuwa ni Ali mwana wa Abu Talib – mfano halisi wa sifa za Mtume wa Uislamu. Utashi Wa Ki-Mbinguni Sasa tunayageukia yale matukio ambayo tuliyasimamisha hapo mapema. Lile kundi la watu ambalo lilikuwa limemchukiza Ali (yaani, Khawariji) liliondoka Kufa na 415

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 415

9/4/2017 3:48:05 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

likaweka makazi katika kijiji cha karibuni kilichoitwa Harura. Kwa sababu hii na wao pia wanaitwa ‘Haruriyah.’ Na kwa vile wito wao ulikuwa “La Hakam illallah” – Hakuna hakimu ila Allah, wao wanaitwa ‘Muhakkamah’ vile vile. Hata hivyo, jina lao linalojulikana zaidi ni Khawariji. Ali alishika njia kuwaelekea wao pamoja na jeshi lake. Yeye hata hivyo, alitamani sana kwamba kusiwe na umwagaji damu utakaotokea, na kwamba wangeweza kufanywa wakatoa upya kiapo chao cha utii kwake, na kutelekeza imani yao potovu kwa njia ya majadiliano. Yeye, kwa hiyo, aliwatumia ujumbe akisema: “Nitumieni kutoka miongoni mwenu, yule ambaye mnamuona kuwa ndiye mwenye akili sana na busara, ili aweze kuhojiana nami. Kama anao uwezo wa kunishawishi mimi, basi nitafanya kama mnavyonitaka nifanye. Vinginevyo mnapaswa mtoe upya kiapo chenu cha utii kwangu.” Khawariji walimtuma kiongozi wao Abdullah bin al-Kawa kama mwakilishi wao. Majadiliano marefu yalitokea baina yake na Amirul-Mu’minin. Ali aliltoa majibu ya kuridhisha na ya kuvutia kwa maswali yote aliyoyauliza yeye. Alirudi kwa marafiki zake, akawajulisha kuhusu mambo yaliyojitokeza kwenye mjadala wao, na akawaambia kwamba Ali alikuwa amemridhisha kikamilifu ,naye alikuwa kwenye haki. Khawariji hao, kama mambo yalivyojitokeza, walibakia kuwa wakaidi na wala hawakuukubali ushauri wa kiongozi wao. Walisema kwamba kama walivyokuwa wamekwisha kumtangaza Ali kuwa ni kafiri ilikuwa haiwezekani kwao kutoa tena kiapo cha utii kwake. Wao walimlaumu Abdullah bin al-Kawa kwa kutokuwa na uwezo katika kuhojiana na kuthibitisha imani yake na wakamtaka kutofanya majadiliano zaidi na Ali wala kuyatoboa kwa yoyote yule, yale ambayo alikuwa amekwishajadiliana naye. Hivyo wakaendelea kuwa waasi na mahasimu juu yake, na wakamchukulia yeye pamoja na wafusi wake wote kama makafiri na wakanamungu. Ali alisikitika sana kuona kwamba marafiki zake na wafuasi wake wa zamani wamekuwa ni maadui zake na hawakuwa tayari kusikiliza busara. Wao walikuwa watu wa mawazo ya kidunia, na walikuwa watumwa wa matamanio yao ya kimwili. Alitambua kwamba ulikuwa ni upanga tu ambao ungeweza kuamua mambo kati yao na yeye. Hili limekuja kuwa ni muhimu kwa sababu watu wale walikuwa wamechukua sheria mikononi mwao wenyewe. Waliwaua wale ambao juu yao waliweza kuwakamata, na wakawapora na kuwanyang’anya raia watulivu wenye amani.

416

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 416

9/4/2017 3:48:05 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Hata hivyo Amirul-Mu’minin hakuacha kuendelea kuwashauri watu hao kuja kwenye njia ya haki. Yeye pia aliwashawishi askari wake wasijekuwa wa mwanzo katika kuanzisha vita. Kama mambo yalivyokuwa, Khawariji ghafla wakatoa mwito wao: “Hakuna Hakimu isipokuwa Allah” na wakamshambulia Ali kwa nguvu zote. Hapo Amirul-Mu’minin na askari wake nao wakachomoa panga zao na yale mapambano ya kuogofya ya Vita vya Nahrawan yakaanza. Wakati kupigana kulipofikia mwisho, takriban Khawariji wote walikuwa wameuawa. Ni watu mia nne tu waliosalimika, ambao hata hivyo walikuwa wamepata majeraha mabaya. Wangekuwa sio nusu maiti kutokana na majeraha yao, inawezekana kwamba wao pia wangeweza kufa huku wakipigana, au wangeweza hata kupata ushindi. Ali aliamuru watu hawa kufanyiwa upole na akawakabidhi kwenye familia zao na makabila yao, ili kwamba waweze kuwafanyia mipango juu ya matibabu yao yanayofaa. Baada ya kuwa amekwisha shughulika na hao Khawariji, Ali alitamani kuelekea Syria kwenda kumuadhibu Mu’awiyah. Hata hivyo, wakati huu pia Ash’ath bin Qais alimvurugia mipango yake kwa mbinu zake za harakati za udanganyifu. Alifanya idadi kubwa ya askari kulitelekeza jeshi lake na kujificha kwenye miji ya karibu. Alitoa hoja kwamba askari hao walikuwa wamechoka kupigana kwa muda mrefu na kwamba walihitaji mapumziko. Aliongezea kwamba atakuja kuliunganisha jeshi hilo baada ya kuwa wamepata mapumziko na kuwa na nguvu mpya. Amirul-Mu’minin akarejea Kufa kwenda kufanya maandalizi kwa ajili ya kuishambulia Syria. Jeshi lake Mu’awiyah mwenyewe lilikuwa aminifu kwake na Khawariji nao pia walimsaidia bila kujijua kwa kupigana dhidi ya Ali. Na kuhusu Ash’ath bin Qais, wanahistoria wanasema kwamba ndani ya moyo wake alikuwa ni mfuasi na mwenye kumhurumia Mu’awiyah. Baadhi ya wanahistoria wameeleza wazi kwamba yeye alikwenda Damascus, akakutana na Mu’awiyah, akapata utajiri mkubwa kutoka kwake na akaanza kusubiri maendeleo ya baadae. Katika hatua hii bahati ilimpiga Ali mshale ambao yule mtu mashuhuri aliathirika kwawo, na hapo maadui zake wakafanikisha lengo lao. Hata hivyo, mafanikio haya ya maadui zake hayakuwa ni matokeo ya ulaghai wao, ujanja, busara, nguvu au uangalifu wao. Ulikuwa ni bahati tu na ajali ya ghafla ambayo ilisafisha njia kwa ajili ya mafanikio yao. 417

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 417

9/4/2017 3:48:05 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Baadhi ya Khawariji wang’ang’nizi walikutana mahali na wakaanza kuongea juu ya marafiki zao na ndugu na jamaa zao ambao walikuwa wameuawa katika Vita vya Nahrawan. Walieleza mawazo yao kwamba wajibu kwa ajili ya umwagikaji damu huo ulikuwa juu ya mabega ya watu watatu, ambao walikuwa, kwa mujibu wa imani zao, ni viongozi wa wale waliokuwa wamepotoka kutoka kwenye njia ya haki, yaani, Ali, Mu’awiyah na Amr Aas. Mmoja wa Khawarijii hao aliyeitwa Bark bin Abdullah alijitolea kumuua Mu’awiyah, mwingine aliyeitwa Amr bin Bakr aliahidi kumuua Amr Aas; na wa tatu aliyeitwa Abdul-Rahman ibn Muljam alichukua jukumu la kumuua Ali. Khawariji hao watatu waliotajwa hapo juu waliamua kuwaua Ali, Mu’awiyah na Amr Aas katika usiku mmoja, na iwe huohuo mmoja tu. Watu hawa watatu walikuwa washikiliaji, wang’ang’nizi wa mambo, wenye kisasi na wenye kujusuru na walikuwa tayari kikamilisha lengo lao kwa gharama yoyote ile. Kama mambo yalivyokuwa, katika suala la Abdul-Rahman ibn Muljam, lilitokea jambo la ajabu ambalo lilitia chonjo azma yake na kuifanya iwe imara sana kiasi kwamba hata kama wale Khawariji wengine wawili walikuwa wamesita katika kuwaua Mu’awiyah na Amr Aas, hapakuwa na uwezekano wa kuyumba kwake yeye katika kumuua Ali. Ilitokea hivyo kwamba alikuja kutoka Makkah hadi Kufa na akakaa hapo na rafiki yake mmoja. Hapo alikutana ghafla na mwanamke aliyekuwa akiitwa Qattam binti al-Akhzar ambaye alikuwa mrembo asiyekuwa na kifani wa wakati wake, na ambaye baba yake na kaka yake walikuwa wameuawa katika Vita vya Nahrawan. Abdul-Rahman akatokea kumpenda mwanamke huyu na akamchumbia mara moja. Binti huyu alimuuliza yeye kama ni mahari gani atakayompatia yeye. Abdul-Rahman akamwambia kwamba atampatia kitu chochote atakachotaka. Papo hapo binti akasema: “Mimi nataka unipe dirham elfu tatu, mtumwa mmoja na kijakazi mmoja na pia kumuua Ali ibn Abi Talib.” Yeye akajibu: “Ni rahisi kutoa dirham elfu tatu, mtumwa na kijakazi lakini ni vipi nitaweza kumuua Ali?” Binti huyo akajibu: “Muue kwa ujanja fulani. Kama ukimuua utajihisi kuridhika na pia utafurahia kuwa pamoja nami kwa muda mrefu.” Kabla hajakutana na Qattam na kuongea naye; Abdul-Rahman ibn Muljam alikuwa kwa kiasi fulani ametingishika katika maamuzi yake ya kumuua Ali, kwa sababu licha ya ukatili wake, haikuwa ni kazi rahisi kwake yeye kumuua Imam kwa sababu ya kosa ambalo kwamba yeye hakuhusika nalo.

418

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 418

9/4/2017 3:48:05 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Hali kadhalika haikuwa rahisi kwake yeye kuchukua hatua ya kutisha, ambayo matokeo yake yalielekea kuwa ya hatari kabisa. Hata hivyo bahati iliruhusu kwamba Abdul-Rahman ibn Muljam aweze kuthibitishwa katika uamuzi wake na kuwa tayari kutenda uhalifu uliokuwa mbaya kabisa. Bahati ilichukua mshale mwingine tena kutoka kwenye zaka lake na ukauweka kwenye mkono wa Ibn Muljam ili kuulenga kwenye kifua cha Imam. Bahati ilimchukua Abdul-Rahman kumpeleka kwenye nyumba ya rafiki yake na pia ikamleta Qattam mahali hapo. Halafu yakatokea mazungumzo ya ajabu kuhusu mahari, ambayo kuyahusu hayo mshairi mmoja anasema: “Imma sijaona katika Arabia wala mahali pengine popote, mtu yoyote yule hatari sana ambaye ameweza kutoa; kwa mwanamke yoyote mahari inayolingana na ile ya Qattam. Dirham elfu tatu, mtumwa mmoja, kijakazi mmoja, na kuuawa kwa Ali kwa upanga mkali. “Kwa kiasi chochote kile mahari itakavyokuwa kubwa, Haiwezi kuwa kubwa kuliko Ali, Na kila mauaji ni rahisi zaidi, yakilinganishwa na yale ya Ali, Ambayo yalifanywa na ibn Muljam.” Mazungumzo ya Qattam na ibn Muljam yaliisha kwa kauli hii ya ibn Muljam: “Basi sawa. Itakuwa kama unavyotaka. Ninaahidi kumuua Ali.” Wale Khawariji watatu waliokuwa wamepanga njama dhidi ya maisha ya Ali, Mu’awiyah na Amr Aas katika usiku ulioteuliwa, wote walikwenda kwenye vituo vyao. Na halafu jambo moja la ajabu, na inawezekana kwamba lilikuwa ni la kipekee likatokea, ambalo kwalo hakuna anayeweza kushikiliwa kuwajibika. Yule mtu aliyekwenda kumuua Amr Aas hakufanikiwa kukamilisha lengo lake. Huenda bahati iliruhusu kwamba asimshinde Amr Aas. Ilitokea kwamba katika usiku huo Amr alikuwa mgonjwa kidogo na ugonjwa huu uliyaokoa maisha yake. Hakutoka nje ya nyumba yake imma kwenda kuswali au kufanya kazi nyingine yoyote ile. Alimuomba afisa wa polisi wa mji huo aliyeitwa Kharija ibn Huzafa kuongoza swala ya Asubuhi badala yake. Pale yule afisa wa Polisi alipotoka nje ya nyumba yake, Amr bin Bark alifikiria ni Amr Aas na akamuua. Wakati Amr bin Bark alipokamatwa na kupelekwa kwa Amr Aas, yeye Amr Aas akamwambia: “Wewe ulitaka kuniuwa mimi lakini Allah amependa kwamba Kharija auawe.” Kisha akaamuru Amr bin Bark auliwe kwa kukatwa kichwa chake.

419

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 419

9/4/2017 3:48:05 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Wakati Mu’awiyah alipokuja Msikitini na Bakr bin Abdullah alipomuona yeye alilenga upanga wake kwenye kichwa chake, lakini upanga huo kwa kweli ulikwenda kupiga kwenye matako yake na shambulio hilo likawa halikufanikiwa. Matako ya Mu’awiyah yalikuwa kama ngao yake na maisha yake yakaokoka. Waache Waomboleze Mtu mgeni amekaa kwenye pembe ya dunia, mbali kabisa na watu, katika hali ya kusikia uchungu mkali kabisa. Amekaa peke yake na upweke wake umemlemea sana. Yeye ni mgeni ingawa anaishi miongoni mwa watu wake, lakini ni mwenye huzuni sana kwa sababu yao. Wakati haukumtambua yeye, ingawa ameutumia. Dunia haikumtambua yeye, ingawa hadithi zake tamu na za busara ziliendelea kuvuma ndani yake nayo iliona kwa macho yake yenyewe zile hofu zake kubwa. Mgeni huyu alikuwa akitumia kila kitu alichomiliki juu ya wengine lakini hakutafuta kupata chochote kutoka kwao. Alipatwa na maonevu makubwa, lakini hakufikiri kamwe juu ya kulipiza kisasi. Aliwasamehe maadui zake baada ya kupata ushindi juu yao. Alikuwa hajafanya dhuluma yoyote kamwe kwa maadui zake na kamwe hakufanya tendo lolote lisilo la kisheria kwa ajili ya marafiki zake. Yeye alikuwa ni msaidizi wa wanyonge, ndugu wa masikini, baba wa mayatima na rafiki mpole wa wale ambao walikuwa wamechoshwa na maisha yao. Wakati wote walimfuata kwa ajili ya ufumbuzi wa matatizo yao na walitarajia huruma kutoka kwake katika matatizo yote. Alikuwa mjuzi, na alikuwa mvumilivu kupita kiasi. Hata hivyo, moyo wake ulikuwa umejaa huzuni. Utukufu na fahari yake vilikuwa vikitoa mwangwi katika milima yote na majangwa. Alikata vichwa vya wababe wake lakini yeye mwenyewe alijawa na upendo na upole. Wakati wa mchana alisimamia haki na kutekeleza sheria za kimungu na katika giza la usiku alilia kwa uchungu sana kwa ajili ya masikini na wasiojiweza. Yeye alikuwa ni mgeni ambaye sauti yake yenye kunguruma iliwafanya madhalimu kutetemeka kila wakati na pale mtu yoyote aliyeonewa alipomwendea na malalamiko. Kila wakati mtu alipomlalamikia yeye upanga wake uliwaka kama radi na kuliteketeza giza la wadanganyifu. Wakati wowote mtu aliyenyimwa alipomwita yeye, upendo na huruma vilianza kumiminika kutoka moyoni mwake ambavyo huzima ile kiu na kila kitu kikavu na kuathiriwa na njaa.

420

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 420

9/4/2017 3:48:05 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Alikuwa ni mgeni katika uso wa ardhi ambaye kila neno lake lilikuwa la kweli na sahihi. Alivaa mavazi duni na alitembea kwa unyenyekevu na kila wakati watu walipokwenda chini yeye alinyanyua uso wake juu. Alikuwa ni mgeni na mtu mzuri ambaye aliteseka kwa aina zote za matatizo kiasi kwamba watu waweze kudumu wenye furaha. Je, alikuwa ni nani mgeni huyu wa kipekee na jasiri ambaye alijua kila kitu na akatupa macho yake pande zote? Alikuwa ni nani huyu ambaye alitafuta ustawi wa watu katika dunia hii na vile vile katika ile ya akhera, ingawa walikuwa siku zote wakimhuzunisha na kumdhuru? Alikuwa ni nani huyu, mtu wa kipekee na wa ki-malaika ambaye maadui zake walizikataa sifa zake kutokana na wivu na ulafi wao, na ambaye marafiki zake walimtelekeza kutokana na woga? Alipambana peke yake dhidi ya udhalimu na maangamizi. Tabia yake kwa watu ilikuwa wakati wote iko kwenye msingi wa haki na uaminifu. Alikuwa kamwe hana tamaa ya ushindi na hakuvunjwa moyo na kushindwa. Alikuwa ni mfano bora wa haki na kamwe hakujali juu ya kitu kingine mbali na haki, iwapo baadhi ya watu walizikataa sifa zake na baadhi ya wengine walimuogopa yeye. Mtu huyu anaweza akawa ni nani isipokuwa Ali, yule Amirul-Mu’minin aliyeudhiwa na kudhikishwa, ambaye kwa damu yake mtu mwovu na mchafu alikuwa aipakaze mikono yake ili iweze kuwa kama mahari kwa ajili ya mwanamke mchafu na muovu? Ulikuwa ni usiku wa giza nene kabisa na wa kutisha. Mawingu yalikuwa yametanda angani. Wakati mwingine radi iliwaka na kueneza mwanga wake pande zote. Tai walikuwa wamekaa kwenye viota vyao na vichwa vyao vimetazama chini, kwa sababu katika siku inayofuatia manyoya yao yatakuja kupukutika chini na walikuwa waje kuomboleza kwa ajili ya mkuu wa ulimwengu. Imam alikuwa hakulala na macho yalikuwa hayana usingizi, kwa sababu watu walikuwa wanagumia kwa sauti ya huzuni kutokana na uonevu: baadhi ya watu walijiingiza kwenye anasa na walikuwa tayari kuasi. Watu wenye uwezo walikuwa madhalimu kabisa kwa watu wanyonge. Maadui zake kwa maafikiano ya siri ya wao kwa wao walikuwa wanasababisha vurugu na kupanga kufanya maasi. Miongoni mwao walikuwemo watenda maovu ambao walihubiri upendo juu ya kila mmoja. Baadhi ya wafuasi wake walikuwa pia wametelekeza haki na wamejizuia kutokana na kusaidiana. Yote haya yalikuwa yakimuuma sana Ali. Usiku ule aliyatathmini maisha yake yote yaliyopita. 421

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 421

9/4/2017 3:48:05 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Alikumbuka kwamba kutoka ujana wake hasa; upanga wake uliwafanya Maquraishi kutetemeka, na alifanya kila aliloweza katika kuueneza Uislamu. Watu wake walizichukulia shughuli zake kuwa za kitoto, lakini yeye alibakia imara na alitoa kila msaada uliowezekana kwa Mtume ili kuifanya kazi yake ifanikiwe. Aliukumbuka vile vile ule usiku wa kuhama wakati alipolala kwenye kitanda cha Mtume chini ya kivuli cha panga za Maquraishi kwa matumaini kwamba Abu Sufyan na washirikina wengine watakuwa wamekosea na hawatakuwa na uwezo wa kufanya madhara yoyote yale kwa Mtume. Vile vile yeye alikumbuka vile vita ambavyo alimlinda Mtume na Uislamu dhidi ya maadui. Aliweza kupata taswira ya makafiri walipokuwa wakitawanyika kama nzige ambao wanatimuliwa na tufani ya mchanga. Alipata taswira ya Mtume akimkumbatia kwa mapenzi motomoto na akisema: “Huyu ni ndugu yangu.” Aliukumbuka ule wakati ambapo Mtume alikuja nyumbani kwake siku moja wakati yeye akiwa amelala. Fatimah alitaka kumuamsha lakini Mtume akasema: “Muache alale, kwa sababu baada yangu mimi atakuja kunyimwa usingizi kwa muda mrefu.” Na hapo Fatimah akalia sana. Alikumbuka ule wakati ambapo Mtume alisema: “Oh, Ali! Mwenyezi Mungu amekupamba wewe kwa tabia bora kabisa. Amekujaalia wewe na mapenzi juu ya masikini na wasio na uwezo. Wao watafurahia kukufanya wewe kuwa Imam wao nawe utafurahi kuwaona wao kama wafuasi wako.” Pia alikumbuka ule wakati ambapo Mtume alimtazama kwa mara ya mwisho usoni mwake na kisha akavuta pumzi zake za mwisho. Yeye vile vile alikumbuka ile huzuni ya Fatimah ambayo ilimfanya afariki siku arobaini baada ya kifo cha baba yake. Alizikumbuka pia zile nyuso za masahaba wa Mtume ambao walizoea kusema: “Wakati wa uhai wa Mtume tuliweza kuwatambua wanafiki kwa sababu ya uadui wao na Ali.” Mtume aliwahi kusema, sio mara moja, bali mara nyingi tu: “Ewe Ali! Ni yule ambaye ni mnafiki tu, ndiye atakayekuwa na uadui juu yako.” Kufikia wakati huu alikumbuka marafiki zake ambao walifanya jihadi pamoja naye wakati wa uhai wa Mtume. Walikuwa wameungana, walisaidiana wenyewe kwa wenyewe, na walidumisha mafungamano ya undugu. Lakini baadae, katika wakati wake yeye mwenyewe, baadhi yao waliungana naye ambapo baadhi yao wengine walimpinga. 422

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 422

9/4/2017 3:48:05 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Wengine waliokuwa wakitamani kuwa watawala au kupata manufaa ya kidunia walikuwa wamefariki na wengine walikuwa bado wako hai. Wale masahaba wenye mioyo mikunjufu ambao walikuwa wamedhamiria kuendeleza haki na uadilifu (Mwenyezi Mungu awarehemu!) walikuwa wageni katika dunia hii. Waliyatoa maisha yao katika njia ya haki na uaminifu na uonevu wa maadui uliwazika katika vina vya ardhi. Mmoja wao alikuwa ni Abu Dhar Ghiffari – sahaba maarufu wa Mtume ambaye hakuweza kuvumilia kwamba maisha ya mwanadamu yadhalilishwe, na kwa hiyo alisimama kupinga udhalimu na uonevu. Alikuwa ni mtu mashuhuri ambaye alikuwa hakuwa na rafiki aliyebakia kutokana na ukweli wake isipokuwa Ali na ambaye alikutana na mwisho wa kuhuzunisha. Ali alikumbuka ule wakati ambapo Abu Dhar alipokuwa mbele ya Mtume akiwa amevaa joho lililochakaa na akajiweka mwenyewe chini ya mamlaka ya Mtume kwa ajili ya utumishi wowote utakaokuwa. Kuanzia wakati ule na kuendelea alibakia kuwa mfuasi madhubuti wa haki, kiasi kwamba katika kipindi cha Uthman yeye alianzisha kampeni dhidi ya Bani Umayyah katika kuwaunga mkono na kuwasaidia wale walioonewa na waliokuwa hawana uwezo. Kwa matokeo ya hili, yeye alihamishwa na Marwan na Uthman kwenda kwenye sehemu kame isiyo na watu iliyokuwa ikiitwa Rabazah, ambako watoto wake walifariki mbele ya macho yake. Mke wake mwenyewe alikuwa anawaona wakifariki na alikuwa akiomba kwamba yeye aweze kufa kabla ya Abu Dhar ili asije akaishi baada yake, kwani vinginevyo itakuwa ni kifo chake mara mbili. Abu Dhar alikufa kwa njaa, ambapo Bani Umayyah walikuwa na mali yote ya dunia chini ya mamlaka yao. Alimkumbuka pia ndugu yake mchamungu na mwaminifu, Ammar Yasir ambaye aliuawa wakati wa usiku kama huo siku chache kabla na kikundi kilichoasi na cha kidhalimu katika Vita vya Siffin. Ndiyo! Walikuwa wapi wale ndugu zake Ali ambao walikuwa ni wafuasi wa njia ya haki – wale ambao imma hawakujiingiza kwenye mazungumzo ya porojo, wala hawakumsengenya mtu wala hawakufanya ulaghai au udanganyifu na hila? Wale watu waadilifu wote walikuwa wameitoka dunia hii mmoja baada ya mwingine na Ali aliachwa kupigana vita vikali vya kutisha dhidi ya watu madhalimu na waovu. Kama Mwenyezi Mungu angemjaalia ushindi Ali dhidi ya waasi wale angeweza kumaliza maasi hayo na kushughulika na waasi hao katika njia inayofaa.

423

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 423

9/4/2017 3:48:05 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Vilikuwa ni vita ambavyo haki ilikuwa peke yake katika upande mmoja ingawa hapo nyuma ilikuwa na waunga mkono wengi. Vilikuwa ni vita ambamo yeye na watu ambao watoto wao walikuwa wamepotoshwa, ambao vijana walikuwa wauaji na ambao wazee hawakuwa na mazoea ya kuwaamuru wengine kutenda wema na kukataza maovu. Walimhofia yule mtu tu ambaye ulimi wake ungeweza kuwaletea madhara na walimheshimu tu yule ambaye walitegemea kupata chochote kutoka kwake. Kama yeye angewaacha waende njia zao wasingemuacha, na endapo angewafuata wangemshambulia kwa ghafla. Walikuwa ni masahaba katika upotovu na walikashifiana wenyewe kwa wenyewe pale walipotengana. Vita ambavyo Ali alilazimishwa kupigana dhidi ya utashi wake vilikuwa kama wimbi la bahari ambalo halijali kama mtu atazama na kufa maji au hapana, au kama mwali wa moto ambao unachoma chochote na kukifanya kuwa majivu. Vilikuwa ni vita kati ya Ali, ambaye alipenda wengine wafaidi neema za dunia, na kati ya wale watu ambao walitaka kuwatoa watu wanaowamiliki kutoka kwenye zile ardhi zenye rutuba na kuwatupa kwenye majangwa makame na pepo zinazonyausha. Oh! Ni maisha gani haya aliyoishi Ali! Maisha yake yalitumika imma katika kupigana jihadi au kuteseka na matatizo. Oh! Ni watu waungwana na waadilifu kiasi gani waliokuwepo katika dunia! Walikufa mmoja baada ya mwingine na wakamuacha Ali peke yake. Baada ya kuondoka kwao, dunia ilijazwa na udhalimu na uonevu. Huyu mgeni wa kipekee alipata taswira ya siku inayofuatia, ambayo giza lake lingedumu kwa muda mrefu kuliko usiku wa zile siku za masikini, na usiku ambao ungekuwa na baridi sana kuliko dhamiri za wale ambao si waaminifu kwenye ahadi zao. Utakanyaga kwa nguvu kabisa juu ya wale wenye bahati mbaya tu. Ile siku inayofuatia ambayo wale watu watakaokuwa watawala kwa njia za udanganyifu hawataweka umuhimu wowote kwa raia zao. Ni wale waongo, wasengenyaji, na waeneza vurugu tu ndio watakaopata fadhila za watawala hao. Hiyo itakuwa ndio siku ambayo watu madhalimu na wakatili wakayofanywa kuwa ndio wakuu na wale watu ambao ni duni tu na wasio na haya watakaoishi maisha ya amani. Ali alikuwa akivuta taswira ya hali ya mambo katika siku hiyo inayofuatia kwa moyo na akili yake. Itakuja kuwa ni siku ya kusikitisha sana. Baada ya usiku huo hakuna hata mtu mmoja katika wale waliokuwa kwenye nafasi atakayependelea haki kuliko batili, kama batili ilikuwa ndio yenye faida zaidi kwake. Baada ya usiku huo 424

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 424

9/4/2017 3:48:05 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

hakutakuwa na mtawala atakayekuwa kama baba kwa watu na aweze kupenda haki licha ya matatizo yote ambayo anaweza akayapata kuacha starehe zote zikianzia kutoka kwenye batili. Baada ya usiku huo hakutakuwa na moyo na akili kama hiyo itakayowatendea watu kwa uadilifu na kufuata haki hata kama milima itatetemeka na ardhi kupasuka. Kwa bahati mbaya! Ifuatayo ni siku ambapo mtu jahilia, mjinga alikuwa atende ule uhalifu mbaya kabisa hadi mfalme mwenye majigambo, dhalimu atakuja kutawala, na yule mtu muungwana adhimu alikuwa anakuja kukutana na kifo chake na maangamizi wakati akipigana na uonevu wa madhalimu. Amirul-Mu’minin aliweka mkono wake kichwani mwake na akabaki analia kwa muda mrefu. Alitazama kuelekea angani na akaona katika usiku ule wa giza vipande pande vya mawingu na nyota ambazo zilikuwa zikiakisi mwanga katika makasiri ya mabepari na vibanda vya masikini halikadhalika, na yalikuwa yanaficha udhalimu na madhara ya watu waovu na huzuni na mateso ya wale waadilifu vile vile. Aliiangalia dunia na akijisemea mwenyewe kwayo alisema: “Ewe dunia! Danganya mwingine bali sio mimi.” Muda uliendelea kupita na usiku ulizidi kuwa wa giza nene zaidi. Ali alijihisi yuko peke yake katika dunia. Ni sehemu ya upweke, ya kutisha na ngeni kiasi gani dunia hii ilivyokuwa! Alikwenda kulala kwa muda mfupi pamoja na kumbukumbu zote zikiwa mpya katika akili yake. Wakati akiwa amelala alipata ndoto ambamo alimuona Mtume na akamwambia: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Nimeteseka kiasi kikubwa sana mikononi mwa wafuasi wako na nimelazimika kukabiliana na upinzani mkali kutoka kwao.” Mtume akasema: “Waombee laana juu yao.” Ali akasema: “Ewe Mola! Nipatie masahaba bora kuliko watu hawa, na uweke juu yao, mahali pangu, mtawala mbaya kabisa.” Ilipokuwa ni alfajiri, hewa nyepesi ilikuwa inavuma na anga lilikuwa linatoa machozi (manyunyu mepesi). Ali ibn Abi Talib aliekea msikitini taratibu kwani nyayo zake zilikuwa zikiongea na ardhi na kuiambia hadithi ya zile nyakati za majonzi mazito. Ndege pia walihuzunika. Alikuwa bado hajaufikia uwanja wa msikiti wakati bata walipokimbia kumwelekea yeye na wakaanza kulia. Sawia pamoja nao ule upepo baridi wa asubuhi pia ukaanza kunguruma.

425

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 425

9/4/2017 3:48:05 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Wale ambao walikuja kuswali walijitokeza mbele na wakajaribu kuwafukuza wale bata. Hata hivyo, hawakuondoka wala kuacha kulia. Vivyo hivyo, ule upepo uliendelea kutoa sauti ya mchakarisho. Iliweza kutokea kwamba wale bata na ule upepo walikuwa tayari wamekuja kujua kwamba Amirul-Mu’minin alikuwa anaelekea kwenye balaa lake la mwisho. Amirul-Mu’minin alivisikiliza vile vilio vya wale mabata kwa makini kabisa na kisha akiwageukia wale watu akasema: “Msiwafukuze, kwani wanaomboleza.” Kwa maneno haya Amirul-Mu’minin alibashiri lile balaa lililokuwa linakaribia kutokea ambalo lilikuwa limfike yeye. Kwa nini mabata hawa wasiwe wameomboleza? Kwa nini wale watu walikuwa wakijitahidi kuwazuia wasilie? Na kwa nini Amirul-Mu’minin asiwe amewatazama kwa mapenzi na upendo? Alikuwa tayari amekwishaona asubuhi nyingi kwa maelfu lakini asubuhi hii ilikuwa imebeba siri katika kifua chake, ambayo asubuhi nyingine hazikuibeba. Siku ile alikuwa anahisi kitu ambacho alikuwa hajakihisi kamwe hapo kabla. Hivi mtu huyu mashuhuri hakuwa na haki ya kusikia maombolezo yake katika namna ya vilio vya bata hao na mvumo wa pepo hizo? Je, hakuwa na haki ya kuaga na kusema kwa heri kwa jua na kivuli ambavyo vinaelekea kutoviona tena? Hivi hakuwa na haki ya kutazama kwa mara ya mwisho katika zile sehemu alizokuwa akiishi maisha ya kimasikini na kuwafanya wengine matajiri? Sehemu hizi zimeona mandhari nyingi za ushujaa wake na ujasiri, udhihirikaji wa haiba yake inayoshangaza, na mateso magumu mengi na majonzi ambayo ilimbidi ayavumilie. Zimeona pia mikesha mirefu kabisa ambayo aliipitisha huku akilia katika kumnyenyekea Mwenyezi Mungu. Kama wakazi wa dunia hii wangeshikilia kwenye haki na uadilifu asingelisikitika sana katika kuziacha siku na usiku zake. Kilichomuuma sana kilikuwa ni kwamba dunia ilikuwa imejazwa mno na watu waovu na wadanganyifu. Dunia ilikuwa inaugulia kwa shinikizo la watu hao na wakaazi wake wameangukia kuwa mawindo ya ukataji tamaa. Wale watu walionyimwa huko Iraqi, Hijazi na Suria walikuwa wanaishi maisha ya taabu sana. Wanafiki walikuwa wanatengeneza faida kubwa mno. Kwa hakika dunia ilikuwa haijapoteza chochote iwapo ingemruhusu Ali kuchukua hatua moja au mbili kuleta mabadiliko katika mambo ya dola iliyokuwepo wakati huo. 426

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 426

9/4/2017 3:48:05 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Kwa bahati mbaya dunia haitaki kwamba mabadiliko yapatikane katika hali zilizokuwepo. Yule mtu mashuhuri mwenye roho ya ki-mbinguni alihisi kwamba nyayo zake zilikuwa zinamfanya aende kwenye safari ndefu. Alisimama kwenye lango la msikiti kwa muda mfupi alipokuwa anawaangalia wale bata wanaoomboleza. Halafu akawageukia wale watu waliokuwa wamesimama mbali kidogo kutoka pale alipokuwa yeye na akasema maneno haya mara kadhaa: “Msiwafukuze hao, kwani wanaomboleza.” Ali aliwasili msikitini na akasujudu mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Abdur-Rahman ibn Muljam naye pia akaingia msikitini humo akiwa amebeba pamoja naye upanga wenye bapa lililopakwa sumu. Alimpiga dhoruba kali kichwani mwa Imam kiasi kwamba, kama alivyosema yeye Ibn Muljam mwenyewe, kama ingepigwa kwenye vichwa vya wakazi wote wa mji huo, hakuna ambaye angepona. Mhalifu huyu mwenye nia mbaya apatwe na kisasi cha mbinguni na laana ya Mwenyezi Mungu na viumbe Wake wote imshukie yeye! Na aweze kupata mateso yaliyo makali kabisa ndani ya Jahannam. Upepo mkali ulianza kuvuma na kila kitu kikapinduka chini juu. Mawimbi ya vumbi yalitimuka kutoka pande zote na yakasababisha vurumai kubwa. Ile siku angavu ikageuka kuwa giza nene kama usiku usio na mwezi. Yalikuwa ni mandhari ya kutisha. Ndege walitoa vilio na miti ikatetemeka. Wafuasi na wapenzi wa Ali walishitushwa na wakaangua vilio na machozi. Wapenda haki na uadilifu wataendelea kulia juu ya msiba huu hadi Siku ya Kiyama. Kila kitu katika dunia hii kilikuja kikavunjika moyo na kusikitika isipokuwa ule uso wa Ali ambao ulikuwa mchangamfu kabisa. Yeye hakuonyesha nia yoyote ya kutaka kulipiza kisasi wala hakuonyesha hasira yoyote. Watu walikusanyika langoni mwa nyumba yake wakiwa na nyuso zilizohuzunika sana na walikuwa wanamuomba Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kupona kwake kwa haraka. Walimshambulia Abdur-Rahman ibn Muljam na wakamkamata. Pale alipoletwa mbele ya Amirul-Mu’minin akasema: “Mpeni chakula kizuri na kitanda laini.” Kama mambo yalivyotokea, ule uchangamfu wa uso wake ulikuwa ukihuzunisha sana kuliko mabalaa yote ya ulimwengu huu. Kwa wakati huo uso wake ulifanana na ule wa Socrates pale watu wajinga na wapumbavu walipomfanya anywe kikombe cha sumu. Ulifanana na uso wa Isa Masihi (Yesu) pale Wayahudi walipomtesa.

427

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 427

9/4/2017 3:48:05 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Ulifanana na uso wa Mtume wa Uislamu, Muhammad, wakati wale watu wajinga wa Ta’if walipomrushia mvua ya mawe mengi na walikuwa hawajui kwamba walikuwa wanampiga mawe mwanadamu mashuhuri aliyewahi kuzaliwa kamwe. Madaktari bora wa Kufa waliitwa kwa ajili ya kumtibu Imam Ali. Athir ibn Amir bin Hani ambaye alikuwa ndiye stadi na bingwa zaidi miongoni mwao alilichunguza kwa makini kabisa lile jeraha kwenye paji la uso wa Ali na akasema kwa masikitiko makubwa sana na kukata tamaa: “Eewe Amirul-Mu’minin! Bora ungetengeneza wasia wako kwa lolote unalolitaka kuusia, kwa sababu pigo lililopigwa na AbdurRahman ibn Muljam limepenya mpaka kwenye ubongo wako.” Imam hakukasirishwa na maelezo ya daktari yule wala kutamka neno lolote la kulalamika. Alijiweka mwenyewe chini ya mamlaka na utashi wa Mwenyezi Mungu. Ali aliwata wanawe, Hasan na Husein na akatoa mapendekezo kadhaa kwao. Alisisitiza pia juu yao kwamba wasije wakasababisha usumbufu wowote wala kukimbilia kwenye umwagaji damu kwa sababu ya kuuliwa kwake. Na kuhusu huyo muuaji yeye alisema: “Kama mtamsamehe yeye, basi itakuwa ni karibu na uchamungu.” Baadhi ya mapendekezo yaliyofanywa na Ali juu ya wanawe Hasan na Husein yalikuwa kama yafuatayo: Naweka juu yenu kiapo kwa jina la Mwenyezi Mungu kwamba mtakuwa wenye kuwajali na kuwaheshimu majirani zenu. Nakulisheni kiapo kwa jina la Allah kwamba mtawashughulikia wenye dhiki na masikini na kuwafanya washirikiane nanyi katika riziki na kipato chenu. Na kama ilivyoamriwa na Mwenyezi Mungu mtaongea kwa ulaini na kila mtu na kusema maneno mazuri kila mtakapokuwa mnazungumza na hamtaacha kuwaamuru wengine kutenda mema na kuwakataza katika kutenda maovu. Ni wajibu wenu kuwa na uhusiano mzuri na wa upole miongoni mwenu wenyewe. Muwe na tabia ya kienyeji na mfanye mambo kwa urahisi. Msije mkavunja uhusiano kati yenu na wala msije mkaishi tofauti kwa kutengana. Baada ya muda mfupi aliwageukia watu na akasema: “Hadi kufikia jana nilikuwa mtawala wenu, leo mimi ni njia yenu ya kuchukulia somo kutoka kwangu, na kesho nitawaacheni. Mwenyezi Mungu atusamehe sisi sote!” Ali alipata jeraha kwenye kichwa chake siku ya Ijumaa asubuhi. Baada ya hapo aliishi siku mbili kwa maumivu makubwa kabisa, lakini hakulalamikia maumivu hayo au usumbufu. Aliendelea kutafuta msaada wa Mwenyezi Mungu na kupende428

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 428

9/4/2017 3:48:05 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

keza kwa watu kufanya wema kwa wale wenye dhiki na haja na wasiojiweza. Alifariki wakati wa usiku wa mwezi 21 Ramadhan, 40 Hijiria. Yule mtu mashuhuri na wa kipekee, ambaye aliteseka mikononi mwa maadui zake na vile vile mwa marafiki zake, akafariki. Alikuwa ni yule mtu muungwana ambaye alikuwa Shahidi maisha yake yote na alikuwa baba wa mashahidi wakati wa kifo chake. Yule shahidi wa njia ya uimara, uadilifu na huruma alikuwa amefariki. Shahidi wa utakaso na uungwana, ambaye kamwe hakuonyesha kuzembea japo kidogo katika masuala ya haki na uaminifu, aliondoka duniani. Yule mtu mashuhuri alifariki. Ilikuwa ni bahati mbaya sana kwamba alikuwa hakupata fursa ya kuanzisha serikali ambayo ingeweza kuwa kama mfano kwa ajili ya serikali za baadae, na watu wa kawaida wangeweza kuwa wameishi maisha ya amani pamoja na baraka za jina lake, na kuwaweka wafanya madhara kwenye fedheha na aibu. Aliitoka dunia na akaiacha nyuma yake familia ambayo kila mwanakaya alikutana na kifo cha kishahidi katika njia ya haki. Alimuacha nyuma yake binti yake Zainab, aliyekuwa amekumbwa na huzuni kuvumilia matatizo na watu wa dunia hii wakawa na tabia mbele yake, ya ukatili na unyama ambao haujawahi kutokea kamwe. Alimuacha Hasan na Husein kwenye mateso ya maadui zake wa jadi kama yule mwana wa Abu Sufyan na wengineo. Kipindi cha kwanza cha njama dhidi ya Ali na watoto wake kilikuwa kimefika mwisho. Kilifuatiwa na vipindi vingine vingi ambavyo vilikuwa vimejaa matatizo ya kutisha zaidi na mazito mno kwa ajili yao. Matokeo ya baada ya kupata shahada kwa Amirul-Mu’minin makasiri marefu yaliwaka kama mazigazi katika majangwa yenye ukame. Chemchemi za maji zilikauka. Mashamba yakawa ardhi isiyotumika. Ile serikali ya wenye kuasi na walaghai ikapata kuimarika. Wale watu, ambao walichukulia udanganyifu na ulaghai kuwa unaruhusiwa kwa mtawala, wakawa wamehuika mara tu baada ya kifo cha kishahidi cha Ali. Ni za kisirani kiasi gani zile serikali ambazo misingi yake imesimama juu ya kuuliwa kwa wale ambao wana haki ya kuheshimiwa! Ni masikitiko kiasi gani wale wapenzi wa Ali watakayokuwa wameyahisi kutokana na msiba ambao uliwafika wao kama matokeo ya mauaji yake ya kutia majonzi. 429

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 429

9/4/2017 3:48:05 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Wamehuzunika kiasi gani wale watu waadilifu watakakokwa nako kwa muda mrefu kwa sababu ya tukio hili la kutisha. Ni msiba mkubwa kiasi gani, kwani ilikuwa ni kutokana nao huo kwamba Bara Arabu yote ilibakia kuwa ni uwanja wa vurugu na upotovu kwa karne nyingi. Ni ukubwa kiasi gani ilivyokuwa huzuni hiyo ambayo iliendelea kuongezeka na ikaota mizizi imara kwa kupita kwa wakati na hatimae ikavunja nguvu ya watawala madhalimu na wafuasi wao. Ilikuwa na faida gani serikali ile ambayo ilianzishwa juu ya machozi ambayo waliokandamizwa na wasio na uwezo walikuwa wakiyamwaga katika kuomboleza mauaji ya Ali mwana wa Abu Talib? Ali alikuwa na mazoea ya kuwaliwaza watu. Alikuwa mpole kwa wenye haja na wasiojiweza kama baba kwao. Utajiri wote wa dunia na hazina zake zote hazikuweza kulingana na kamba ya kiatu chake. Wale makhalifa wakandamizaji wote na mali na utajiri wao ni upuuzi tu mbele ya maneno ya Nahjul-Balaghah na maoni ambayo ameyaelezea ndani yake. Hayana thamani kabisa hata mbele ya tone moja la chozi lake. Yule mtu mashuhuri na muungwana mkarimu alifariki na wale ambao walijiona wao wenyewe kuwa ni mashuhuri bila uthibitisho wowote walibakia nyuma. Mtu mmoja alikufa na aliheshimika, na umma ukabakia hai na ukathibitika kuwa duni na wa kudharaulika Imam aliwaacha maadui zake wakawa hai duniani, lakini maisha yao yalikuwa sawa na kama maangamizo tu.

430

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 430

9/4/2017 3:48:06 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu

Orodha Ya Vitabu Vilivyo Chapishwa Na Al-Itrah Foundation: 1. i) Qur’ani Tukufu – Pamoja na Tarjuma ya Kiswahili ii) Qur’an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Thelathini 2. Uharamisho wa Riba 3. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza 4. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili 5. Hekaya za Bahlul 6. Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) 7. Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (a.s.) 8. Hijab vazi Bora 9. Ukweli wa Shia Ithnaashari 10. Madhambi Makuu 11. Mbingu imenikirimu 12. Abdallah Ibn Saba 13. Khadijatul Kubra 14. Utumwa 15. Umakini katika Swala 16. Misingi ya Maarifa 17. Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia 18. Bilal wa Afrika 19. Abudhar 20. Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu 21. Salman Farsi 22. Ammar Yasir 23. Qur’an na Hadithi 24. Elimu ya Nafsi 25. Yajue Madhehebu ya Shia 26. Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur’an Tukufu 27. Al-Wahda 28. Ponyo kutoka katika Qur’an 29. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii 30. Mashukio ya Akhera 31. Al Amali

431

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 431

9/4/2017 3:48:06 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu 32. Dua kwa Mujibu wa Ahlulbayt (a.s) 33. Udhuu kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna 34. Haki za wanawake katika Uislamu 35. Mwenyezi Mungu na sifa zake 36. Kumswalia Mtume (s) 37. Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) 38. Adhana 39. Upendo katika Ukristo na Uislamu 40. Qur’ani na Kuhifadhiwa Kwake 41. Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu 42. Kupaka juu ya khofu 43. Kukusanya Sala Mbili 44. Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara 45. Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya 46. Kusujudu juu ya udongo 47. Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s) 48. Tarawehe 49. Malumbano baina ya Sunni na Shia 50. Kupunguza Swala safarini 51. Kufungua safarini 52. Umaasumu wa Manabii 53. Qur’an Yatoa Changamoto 54. as-Salaatu Khayrun Mina -’n Nawm 55. Uadilifu wa Masahaba 56. Dua e Kumayl 57. Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu 58. Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake 59. Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata 60. Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mtume Muhammad (s) 61. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza 62. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili 63. Kuzuru Makaburi 64. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza 65. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili 66. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu 67. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne

432

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 432

9/4/2017 3:48:06 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu 68. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano 69. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita 70. Tujifunze Misingi Ya Dini 71. Sala ni Nguzo ya Dini 72. Mikesha Ya Peshawar 73. Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu 74. Ubora wa Imam ‘Ali na Ushia ndio njia iliyonyooka 75. Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake 76. Liqaa-u-llaah 77. Muhammad (s) Mtume wa Allah 78. Amani na Jihadi Katika Uislamu 79. Uislamu Ulienea Vipi? 80. Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) 81. Dhana ya Ndoa ya Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) 82. Urejeo (al-Raj’ah) 83. Mazingira 84. Utokezo (al - Badau) 85. Hukumu ya kujenga juu ya makaburi 86. Swala ya maiti na kumlilia maiti 87. Uislamu na Uwingi wa Dini 88. Mtoto mwema 89. Adabu za Sokoni Na Njiani 90. Johari za hekima kwa vijana 91. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza 92. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili 93. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu 94. Tawasali (AT- TAWASSUL) 95. Imam Mahdi katika Usunni na Ushia 96. Hukumu za Mgonjwa 97. Sadaka yenye kuendelea 98. Msahafu wa Imam Ali 99. Maimamu wa Ahlul Bait – Ujumbe na Jihadi 100. Idi Al-Ghadir 101. Kusoma sura zenye Sijda ya wajibu 102. Hukumu zinazomuhusu mkuu wa kazi na Mfanyakazi 103. Huduma ya Afya katika Uislamu 433

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 433

9/4/2017 3:48:06 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu 104. Sunna za Nabii Muhammad (saww) 105. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza) 106. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili) 107. Shahiid Mfiadini 108. Mwanamke Na Sharia 109. Ujumbe -Sehemu ya Kwanza 110. Ujumbe - Sehemu ya Pili 111. Ujumbe - Sehemu ya Tatu 112. Ujumbe - Sehemu ya Nne 113. Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu 114. Hadithi ya Thaqalain 115. Ndoa ya Mutaa 116. Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza 117. Ukweli uliopotea sehemu ya Pili 118. Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu 119. Ukweli uliopotea sehemu ya Nne 120. Ukweli uliopotea sehemu ya Tano 121. Mkutano wa Maulamaa wa Baghdad 122. Safari ya kuifuata Nuru 123. Fatima al-Zahra 124. Myahudi wa Kimataifa 125. Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi 126. Visa vya kweli sehemu ya Kwanza 127. Visa vya kweli sehemu ya Pili 128. Elimu ya Ghaibu ya Maimamu 129. Mwanadamu na Mustakabali wake 130. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Kwanza) 131. mam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Pili) 132. Khairul l’Bariyyah 133. Uislamu na mafunzo ya kimalezi 134. Vijana ni Hazina ya Uislamu 135. Adhana ni Ndoto au ni Wahyi? 136. Tabaruku 137. Saada Kamili – Kitabu cha Kiada cha Maadili 138. Vikao vya furaha 434

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 434

9/4/2017 3:48:06 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu 139. Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje? 140. Visa vya wachamungu 141. Falsafa ya Dini 142. Kuhuzunika na Kuomboleza 143. Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah 144. Mjadala wa Kiitikadi 145. Kuonekana kwa Allah 146. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza) 147. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili) 148. Ndugu na Jirani 149. Ushia ndani ya Usunni 150. Maswali na Majibu 151. Mafunzo ya hukmu za ibada 152. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 1 153. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 2 154. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 3 155. Abu Huraira 156. Vipengee kadhaa katika Swala ya Jamaa na Msikiti. 157. Mazingatio kutoka katika Qur’an - Sehemu ya Kwanza 158. Mazingatio kutoka kaitka Qur’an - Sehemu ya Pili 159. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya kwanza 160. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya Pili 161. Shia na Qur’ani – Majibu na Maelezo 162. Falsafa ya Mageuzi ya Imam Husein (a.s) 163. Amali za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani 164. Elimu ya Tiba za Kiislamu - Matibabu ya Maimamu 165. Uislamu Safi 166. Majlisi za Imam Husein Majumbani 167. Je, Kufunga Mikono 168. Uislam wa Shia 169. Amali za Makka 170. Amali za Madina 171. Asili ya Madhehebu katika Uislamu 172. Sira ya Imam Ali kuhusu Waasi 173. Ukweli uliofichika katika neno la Allah 174. Uislamu na Mifumo ya Uchumi 435

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 435

9/4/2017 3:48:06 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu 175. Umoja wa Kiislamu na Furaha 176. Mas’ala ya Kifiqhi 177. Jifunze kusoma Qur’ani 178. as-Sahifatul Kamilah as-Sajjadiyyah 179. Hayya ‘Alaa Khayri’l-’Amal Katika Adhana 180. Ukweli kuhusu Funga ya Siku ya Ashura 181. Dua za Miezi Mitatu Mitukufu (Rajabu, Shaabani na Ramadhani) 182. Uadilifu katika Uislamu 183. Mahdi katika Sunna 184. Maswali Ya Uchunguzi Kuhusu Uislam 185. Kazi na Bidii ni njia ya maendeleo 186. Abu Talib – Jabali Imara la Imani 187. Ujenzi na Utakaso wa Nafsi 188. Vijana na Matarajio ya Baadaye 189. Historia maana na lengo la Usalafi 190. Ushia – Hoja na Majibu 191. Mateso ya Dhuria wa Mtume (saww) 192. Maombolezo – Msiba wa Bwana wa Mashahidi (a.s.) 193. Shahidi kwa Ajili ya Ubinadamu 194. Takwa 195. Upotoshaji Dhahiri katika (Turathi) Hazina ya Kiislamu 196. Amirul Muuminina (as) na Makhalifa 197. Tawheed Na Shirki 198. Kuvunja hoja iliyotumika kutetea Uimamu wa AbuBakr 199. Adabu za vikao na mazungumzo 200. Hija ya Kuaga 201. Uwazi baina ya Maslahi na Vikwazo 202. Fadhila za watukufu watano katika Sahih Sita 203. Mdahalo baina ya Mwanachuoni waKisunni na Kishia (Al- Muraja’aat) 204. Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (as) 205. Imam Husain ni Mfumo wa Marekebisho na Mageuzi 206. Mtazamo kuhusu msuguano wa Kimadhehebu 207. Nchi na Uraia – Haki na wajibu kwa Taifa 208. Mtazamo wa Ibn Taymiyyah juu ya Imam Ali (as) 209. Uongozi wa Kidini – Maelekezo na Utekelezaji wa Kijamii

436

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 436

9/4/2017 3:48:06 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu 210. Maadili ya Ashura 211. Mshumaa – Shahidi na Kifo cha Kishahidi 212. Mizani ya Hekima – Hadithi za Ahlul Bait (as) – Sehemu ya Kwanza 213. Imam Ali na Mambo ya Umma 214. Imam Ali na Mfumo wa Usawa 215. Uimamu na Tamko la Kutawazwa 216. Mfumo wa Wilaya 217. Vipi Tutaishinda Hofu? 218. Kumswalia Mtume ni Ufunguo wa Utatuzi wa Matatizo 219. Maeneo ya Umma na Mali Zake 220. Nahju ‘L-Balagha– Majmua ya Khutba, Amri, Barua, R­isala, Mawaidha na Semi za AmirulMuuminin Ali bin Abu Talib (a.s.) 221. Mukhtar – Shujaa aliyelipiza kisasi dhidi ya wauaji wa Imam Husein (as) hapo Karbala 222. Mazingatio Katika Swala 223. Imam Hasan na Mfumo wa Kujenga Jamii 224. Vyakula Na Vinywaji 225. Kuelewa Rehema ya Mwenyezi Mungu 226. Imam Mahdi na Bishara ya Matumaini 227. Mtazamo Mpya - Wanawake katika Uislamu 228. Shia Na Sahaba - Majibu na Maelezo 229. Majanga Na Jukumu la Jamii 230. Shia Na Hadith - Majibu na Maelezo 231. Upotofu Ndani ya Kitabu cha Mitaala kwa Shule za Sekondari 232. Ugaidi Wa Kifikra Katika Medani Ya Kidini 233. Yafaayo kijamii 234. Uswalihina Dhahiri Na Batini Yake 235. Mkakati wa Kupambana na Ufakiri 236. Mwanamke Katika Harakati Za Mageuzi 237. Jihadi 238. Hija Katika Maneno Na Ujumbe Wa Imam Khomeini (R.A) 239. Tiba Ya Maradhi Ya Kimaadili 240. Yusuf Mkweli 241. Taqiyya Kwa Mujibu Wa Sheria Ya KIISLAMU 242. Imam Mahdi (A.S) Imam Wa Zama Hizi Na Kiongozi Wa Dunia

437

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 437

9/4/2017 3:48:06 PM


Sauti ya Uadilifu wa Binadamu 243. Talaka Tatu 244. Safari Ya Kuelekea Kwa Mwenyezi Mungu 245. Hotuba Za Kiislamu Juu Ya Haki Za Binadamu 246. Mashairi Ya Kijamii 247. Ngano Ya Kwamba Qur’ani Imebadilishwa 248. Wito Kwa Waumini: “Enyi Mlioamini” 249. Imam Husain (a.s) ni Utu na Kadhia 250. Imam Husain ni Kielelezo cha Kujitoa Muhanga na Fidia 251. Imam Mahdi ni Tumaini la Mataifa 252. Kuchagua Mchumba 253. Mazungumzo ya Umoja – Ukosoaji na Usahihishaji 254. Utamaduni wa Mwamko wa Kijamii 255. Hekima za kina za Swala 256. Kanuni za Sharia za Kiislamu 257. Utamaduni kufuatana na Qur’ani na Utekelezaji wa Kivitendo (Sehemu ya Kwanza) 258. Kauli sahihi zaidi katika kufafanua Hadithi

KOPI ZIFUATAZO ZIMETAFSIRIWA KWA LUGHA KINYARWANDA 1.

Amateka Na Aba’ Khalifa

2.

Nyuma yaho naje kuyoboka

3.

Amavu n;amavuko by;ubushiya

4.

Shiya na Hadithi

5.

Kor’ani Nziranenge

6.

Kwigisha Mu Buryo Bw’incamake Uka Salat Ikotwa

7.

Iduwa ya Kumayili

ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION KWA LUGHA YA KIFARANSA 1.

Livre Islamique

438

06_17_B5 SIZE-SAUTI YA UADILIFU_4_Sep_2017.indd 438

9/4/2017 3:48:06 PM


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.