Swala ya maiti na kumlilia maiti

Page 1

Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:14 PM

Swala Ya Maiti na Kumlilia Maiti (Swalaatu 'l-Mayyit)

Kimeandikwa na: Sheikh Abdul Karim al-Bahbahani na Muhammad Jawad at-Tabasi

Kimetarjumiwa na: Sheikh Haroun Pingili na Hemedi Lubumba Selemani

Page A


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

B

7/15/2011

12:14 PM

Page B


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:14 PM

Haki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: 978 - 9987 - 512 - 25 - 6 Kimeandikwa na: Shaikh Abdul Karim al-Bahbahaniy na Muhammad Jawad at-Tabasi Kimetarjumiwa na: Shaikh Haroun Pingili na Ustadh Hemedi Lubumba Selemani

Kupangwa katika Kompyuta na: Hajat Pili Rajab Toleo la kwanza: Septemba, 2009 Nakala: 1000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Nukushi: +255 22 2127555 Barua Pepe: alitrah@raha.com Tovuti: www.alitrah.org Katika mtandao: www.alitrah.info

Page C


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:14 PM

Page D

Yaliyomo SWALA YA MAITI Neno la jumuiya ya kilimwengu ya Ahlul Bayt a.s…… ………………....7 Idadi ya takbira katika swala ya maiti…………………………………....11 Kwanza: Dalili za kauli ya takbira nne kutoka Sunnan-Nabawiyah. Pili: Mchango wa Khalifa wa pili katika kufanya ithibiti kauli ya takbira nne……………………………………………… ……………………....17 Tatu: Dalili za kauli ya takbira tano kutoka Sunnah Nabawiyah……......23 Nne: Mas’ala ya takbira ya maiti katika mwanga wa kuwa Ahlul Bayt (a.s.) ndio rejea…………………………………….……………………..........30 Utafiti halisi ……………………………………………………………..39 Faharasa……………………………………………………………….....40

KUMLILIA MAITI Dibaji..............................................................................................26

Sura ya Kwanza Dalili zinazoruhusu kumlilia maiti.................................................30

Sura ya Pili Utata uliyopo kuhusu kilio...............................................................40

Sura ya Tatu Fadhila za kuwalilia A’Ali Rasuli....................................................47

Sura ya kwanza Maeneo aliyoliliwa Mtume Aali zake mashahidi na watu wema...48


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:14 PM

Page E

NENO LA MCHAPISHAJI Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya vitabu viwili ambavyo tumevikusanya pamoja: Swala ya Maiti na Kumlilia Maiti. Cha kwanza kimeadikwa na Sheikh Abdul Karim al-Bahbahani na cha pili kimeandikwa na Muhammad Jawad at-Tabasi. Madhehebu zote za Kiislamu zinakubaliana kwamba ni wajibu kumfanyia maiti mambo manne: 1. Ghusl (josho la sheria), 2. Kafan (kumvisha sanda), 3. Swalatu ’l-mayyit (kumswalia maiti), na 4. Dafn (kumzika). Kuna hitilafu katika namna ya kumswalia maiti, hususan katika kutoa takbira. Wako wanaosema kwamba takbira ni nne, na wengine wanasema ni tano. Na katika suala la kumlilia maiti, wako wanaosema kuwa inafaa kulia (bila ya kutoa maneno) na wako wanaosema haifai. Wandishi wa kitabu hiki wamejaribu kuyafafanuwa masuala haya mawili kwa kutumia Qur’ani, Sunna na matukio ya kihistoria. Kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote. Kutokana na ukweli huu, Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili, ili kuongeza ujuzi wao katika masuala ya dini na ya kijamii. Tunamshukuru ndugu zetu, Sheikh Haroun Pingili kwa kukubali jukumu hili la kukitarjumi kitabu hiki sehemu ya Swala ya Maiti, na ndugu yetu E


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:14 PM

Page F

Lubumba Selemani Hemedi kwa kukitarjumi sehemu ya Kumlilia Maiti. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake. Mchapishaji: Al-Itrah Foundation S. L. P. 19701 Dar-es-Salaam, Tanzania.

F


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:14 PM

Page G

AHLUL-BAYT NDANI YA QUR’AN TUKUFU

AHLUL-BAYT KATIKA SUNNAH NABAWIY

Neno la Jumuia Kwa hakika urithi wa Ahlul Bayt (a.s.) uliohifadhiwa na madrasa yao na kulindwa na wafuasi wao usipotee waelezea kuihusu madrasa iliyokusanya matawi mbali mbali ya maarifa ya kiislamu. Madrasa hii imeweza kuzilea nafsi zilizojiandaa kuteka maji haya safi na kuupatia umma wa kiislam wanachuoni wakubwa wenye kufuata nyayo za kirisala za Ahlul Bayt a.s wakizichukua ta’athira zote na maswali ya madhehebu mbali mbali na mielekeo ya kifikra ndani ya hadhara ya kiislam na nje yake wakiipatia majibu thabiti na fumbuzi muda wa karne zote mfululizo. Jumuia ya kilimwengu ya Ahlul Bayt a.s imetilia kipaumbele – kuanzia majukumu yake iliyojibebesha mabegani mwake – kuihami miiko ya risala na hakika zake ambazo watu wa vikundi vikundi na wana madhehebu, na


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:14 PM

Page H

watu wa mielekeo tofauti inayokwenda kinyume na Uislam wamezitia ukungu. Ikifuata nyayo za Ahlulbayt a.s na wafuasi wa madrasa yao ya uongofu ambayo imetilia hima katika kujibu uchokozi unaoendelea, na imejaribu kubakia daima kwenye safu ya makabiliano na kwa kiwango kinachohitajika katika kila zama. Uzoefu unaohifadhiwa na vitabu vya wanachuoni wa madrasa ya Ahlulbayt (a.s.) katika kusudio hili ni wa aina ya pekee; kwa kuwa ni wenye akiba ya kielimu inayohukumiwa na akili na uthibitisho, na kujiepusha na uchu na upendeleo ulaumiwao, na unawasemesha wanachuoni na wanafikra walio mabingwa kwa usemesho unaolingana na akili na kupokelewa vyema na umbile lililo salama. Na limekuja jaribio la Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul Bayt (a.s.) ili kuwapatia wanafunzi - watafutao - ukweli daraja mpya ya uzoefu huu ulio tajiri katika mlango wa mazungumzo na swali na kuzipatia jibu shaka ambazo zilichochewa katika zama zilizopita au zinazochochewa hii leo, na hasa zinazoungwa mkono na baadhi ya duru zenye kinyongo dhidi ya uislamu na waislamu kupitia njia za mawasiliano km internet na zingine – Ikijiepusha mbali na chochezi zilaumiwazo na ikiwa na pupa ya kuzitimua akili zenye kufikiri na nafsi zinazo tafuta haki, ili zifunguke kuupokea ukweli unaotolewa na madrasa ya Ahlul Bayt ya kirisala kwa ajili ya ulimwengu wote. Katika zama ambazo humo akili zinachukua ukamilifu wake na nafsi na nyoyo zinawasiliana kwa haraka mno na kwa namna ya kipekee. Hapana budi tuishiriye kuwa mkusanyiko huu wa mjadala uliandaliwa katika kamati makhsusi ya kundi la watukufu. Na tunatoa shukrani kubwa sana kwa wote hao na kwa wenye utukufu na uhakiki kwa kufanya rejea kila mmoja miongoni mwao kiasi fulani cha tafiti hizi na kudhihirisha maoni yao ya thamani kuhusiana nazo.


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:14 PM

Page I

Sote tuna matumaini na kutarajia tuwe tumetoa tulichoweza miongoni mwa juhudi ya kutekeleza baadhi ya yaliyo wajibu juu yetu kuihusu risala ya Mola wetu Mtukufu. Risala ambayo amemtuma mjumbe Wake kwa mwongozo na dini ya haki ili aipe ushindi juu ya dini zote na Mungu ni shahidi tosha. Al’Majmaul’alamiy li Ahlil-bayt ( a.s. ) Al’muawiniyatu Athaqafiyatu

I


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:14 PM

Page 1


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:14 PM

Page 2

Swala Ya Maiti

IDADI YA TAKBIRA KATIKA SWALA YA MAITI Miongoni mwa mambo ambayo hitilafu zimejitokeza kati ya madhehebu za kiislamu, ni mas’ala ya takbira katika Swala ya maiti. Ama madhehebu ya Ahlul Bayt yameamua kuwa ni takbira tano, hali ikiwa madrasa ya makhalifa inayowakilishwa na madhehebu manne inasema kuwa ni takbiira nne.1 Na ili kuubainisha ukweli katika mas’ala hii mfululizo wa utafiti unahitajika katika pande kadhaa: Kwanza dalili za kauli isemayo takbira kuwa ni nne kutoka katika Sunnan Nnabawiy Kwa kweli mafaqihi wanne, na al-Thauriy, Auzaiy, Daudi na Abu Thauri wamesema hivyo: Wameelezea riwaya kutoka kwa Al-Hasan bin Ali na nduguye Muhammad bin Al-Hanafia, Umar, na Ibn Umar, Zaid, Jaabir, Abu Huraira, Al-Barau bin Aazib, Utbah bin Aamir na Atwau bin Abi Rabbahi .2 1 Al-Ummu 1: 270 na 283 na Al-Ummu (Mukhtaswarul’mazniy):38. na AlMajmu’u 5:231, na Umdatul-Qaari’iy 8: 116. Kifayatul’akhbar 1:103. Subulu salaam 2:558. Sharhu Fathul’qadiir1:460. Bidayatul’mujtahid 1:226. al’Hidayatu 1:92. Lubabu 1:133. al’Mughniy li Ibni Qudamatu 2:392-393. Bidayatul’mujtahid 1:240-241. na al’Haawiy al’Kabiir 3:52-53. 2 Al-Majmu’ 5:230. Al-Mabsutu lis Sarkhasiy 2:63. Al-Lubaabu 1:130. AlMughniy 2:387 na 389, Al-Sharhul’kabiir 2:350. Bulghatus Saaliku 1: 197. Bidayatul’mujtahid 1:234. al’Shar’hu al’Swaghiiru 1: 197. Subulus salaam 2:558 Ameisimulia Ibnu Abii Shaiba katika kitabu cha al-Janaizu mlango:Man kaana yukabbiru alal’janaizati sab’an wa tis’an3:30.4. 2


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:14 PM

Page 3

Swala Ya Maiti Wametolea dalili hizo kuwa Mtume (s.a.w.) aliwajulisha watu katika kifo cha An-Najaashiy na alisoma nao takbira nne.3 Katika Bidayatul’mujtahid amesema: “Imeelezwa riwaya kutoka kwa Abii Khithmah kutoka kwa baba yake amesema: “Nabii alikuwa anasoma takbira nne, tano, sita, saba na nane kwa ajili ya jeneza, mpaka alipokufa AnNajashiy, aliwasimamisha watu safu nyuma yake, na akasoma takbira nne, kisha alibaki thabiti (s.a.w.) kwenye takbira nne mpaka Mungu alipomfisha.4 Na katika hilo kuna hoja yenye ku’ngara kwa Jamhuri, yaani AhluSunnah.5 Na katika Fiqhil’kitabu wa Sunnah: Nguzo ya tatu: Ni takbiira: Nazo ni takbira nne kwa takbira ya ihram. Wala Swala ya jeneza haitokuwa sahihi bila ya hizo. Na hilo ndilo walilonalo wanataaluma wote. Nayo ndiyo kauli ya ma Hanafii, Shafi’iy, Malikiy kadhalika ma-Hanbali kwa kuwa wamekwenda mwendo huo kwa jumla. Ibnul’-Mundhir (r.a.) amesema: Imethibiti kuwa (s.a.w.) alisoma takbira nne. Na hivyo ndivyo alivyosema Umar bin al’Khatab. Na Ibn Umar, na Zaid bin Thaabit na al-Hasan bin Ali. Na al-Baraau bin Aazib. Pia Abu Huraira. Na Muhammad bin Al-Hanafia. Na Ataau, na Ath-Thauriy, na AlAuzaaiy, na Is’haaq 6

3 Sahihl’bukhariy 2: 92 na 112. Sahihu Muslim 2:656 Hadith ya 951. Sunanu Tirmidhiy. 3:342 Hadith ya 1022. Sunanu Abiy Daudi 3: 212 hadith ya 3204. Sunanu an-Nasaiy 4:72. al’Muwatau 1: 226 h 14. 4 Ameisimulia Ibnu Abii Shaiba katika kitabu cha al-Janaizu mlango:Man kaana yukabbiru alal’janaizati sab’an wa tis’an3:30.4. 5 Bidayatul’mujtahid1:322 chapa ya Daarul’maarifati. 6. Al-Badaai’u, 1:313. Na al-Majmu’u 5:230. Na Mughniy al-Muhtaaju 1:341. Na As’halul’madarik 1:354. Na Al-Anwaaru 1:173 3


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:14 PM

Page 4

Swala Ya Maiti Na huatolewa dalili juu ya hizo kwa jumla ya Nassu za khabar na athar: Muslim ametoa habari kutoka kwa Abu Huraira: Kuwa Mtume wa Mungu (s.a.w.) aliwajulisha watu kifo cha al-Najaashiy siku ambayo alifariki, alitoka nao na kuelekea nao kwenye mswala na alisoma takbira nne. 7 Na Muslim alitoa habari kutoka kwa Jaabir bin Abdillah kuwa Mtume wa Mungu (s.a.w.) aliswalia jeneza la Al-Najaashiy, alisoma takbira nne.8 Muslim ametoa habari kwa Sha’abiy: Kuwa Mtume wa Mungu (s.a.w.) aliswali juu ya kaburi baada ya mtu kuzikwa, alisoma takbira nne.9 Na Ad-Daaruqutniy ametoa habari toka kwa Ubayy bin Ka’ab: Kuwa Mjumbe wa Mungu (s.a.w.) alisema :

Kuwa malaika walimswalia Adam walimsomea takbiira nne na walisema: (Hii ndio Sunna yenu ee ninyi wana wa Adam).(1)10 Ad-Daaruqutniy ametoa habari toka kwa Anas alisema: Malaika walimsomea Adam takbira nne, na Abu Bakar alimsomea Nabii (s.a.w.) nne, na Umar alimsomea Abu Bakar nne. Na Suhaybu alimsomea Umar nne. Na Al-Hasan bin Ali alimsomea Ali (a.s) nne. Lau akisoma takbira tano au zaidi kwa kusahau, Swala yake haitobatilika; kwa kuwa hivyo si zaidi ya maneno ya mwanadamu aliyesahau. Wala haifanywi sijda ya sahau kama lau angesoma takbira au kusoma tasbiihi mahali pasipokuwa pake. Ama ikiwa imefanywa hivyo makusudi kuna kauli mbili: 7Sahihu Muslim 3: 8Sahih Muslim 3:55. 9Sahih Muslim 3:55. 10 Ad-Daaruqutniy 2:71. 4


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:14 PM

Page 5

Swala Ya Maiti Moja ni: Swala yake yabatilika; kwa sababu amezidisha rukni, hivyo atashabihiana na aliyezidisha rukuu au sijda. Hilo limesemwa na baadhi ya Mashafii. Na hilo liko dhahiri katika madhehebu ya Hanafii. 11 Ya pili: Swala yake haibatiliki. Nayo ni sahihi kwa madhehebu ya Shafi’iy. Nayo ni riwaya toka kwa Abi Yusuf. Kadhalika Mahanbali; kwa kuwa wao katika jumla ya kauli zao wanasema: Haijuzu zaidi ya takbira saba wala chini ya takbira nne, na bora ni nne haizidishwi zaidi ya hizo; Hadithi zimekuwa sahihi - kwenye suala hili kuwa takbira ni nne na tano, na hiyo ni miongoni mwa tofauti zinazoruhusiwa, na zote ni jaizi; Muslim ametoa toka kwa Abdur Rahman bin Abi Layla amesema: alisema: “Zaidu alikuwa anasoma takbira nne kwa jeneza zetu na kuwa yeye alisoma takbira tano kwa jeneza moja nilimuuliza akasema: Mtume wa Mungu (s.a.w.) alikuwa anaisoma.” 12 Al’Bayhaqiy ametoa habari toka kwa Abdillahi bin Muaqil: Kuwa Ali a.s alimswalia Sahlu bin Haniif, alimsomea takbira sita, kisha alitugeukia akasema: kuwa yeye ni miongoni mwa watu wa Badr.13 Al-Bayhaqiy ametoa toka kwa Musa bin Abdillahi bin Zayd: Kuwa Ali a.s alimswalia Abiy Qutada alimsomea takbira saba na alikuwa mwana Badr.14 Na kauli ya jumla katika hilo: Ni kuwa takbira tano ni jaizi kwa kusahau sio kwa kusudi. Na hiyo ni kauli ya Shaafi’iy na Hanbaliy na riwaya kutoka kwa Abiy Yusuf 15 11Al-Badaiu 1:312 . Na Al-Majmu’u 5:230. 12 Sahih Muslim 3:56. 13 Al-Bayhaqiy 4:36 14 Al-Bayhaqiy 4:36. 15 Al-Badaiu 1:312 na Mughniy Al-Muhtaaji 1:341. na Al-Mughniy 2 : 514. (2) Fiqhul’kitabi wa Sunnah 5 : 2798- 2800. 5


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:14 PM

Page 6

Swala Ya Maiti Na katika kitabu Al-Haawiy Al-Kabiir: Kuwa kauli ya takbira nne ndio iliyo sahihi mno na ni bora kwa mambo matatu: Kwanza: Riwaya nyingi katika maiti mbalimbali, hivyo basi Abu Huraira ameeleza kuwa yeye (s.a.w.) alimsomea al-Najaashiy takbira nne. Na Sahlu bin Haniif ameeleza kuwa yeye (s.a.w.) alisoma kwenye kaburi la Sukayna nne. Na Anas ameeleza kuwa yeye (s.a.w.) alimsomea takbira nne mwanawe Ibrahim, ni kitendo chake cha mwisho (s.a.w.) ikawa ni chenye kufutilia mbali kitendo chake cha hapo awali. Pili: Ameeleza Ibn Abbas na Ibn Abi Aufa: Kuwa takbira za mwisho alizosoma Mtume wa Mungu (s.a.w) kwa ajili ya jeneza ni nne. Jeneza la Suhaylu bin Baydhwai. Tatu: Tendo la maswahaba (r.a.) - wamefanya hivyo na kuafikiana kwao juu ya hilo. Ama kuhusu tendo la maswahaba, ni ile riwaya inayosema kuwa Abu Bakr (r.a.) alimsomea Mtume wa Mungu takbira nne. Na Ali alimsomea Abu Bakr takbira nne, na Suhaybu alimsomea Umar (r.a) nne. Na al-Hasanu alimsomea Ali (a.s) bin Abi Talib nne. 16 Ama kuhusu kuafikiana, ni ile riwaya isemayo kuwa Ibrahim an-Nakhaiy alisema: “Walihitilafiana swahaba wa Mtume wa Mungu (s.a.w.) baada ya kifo chake katika suala la takbiir ya Swala ya jeneza. Kaumu ilisema: “Husomwa takbiira nne.” Na kaumu ilisema: Tatu. Na kaumu ilisema: Tano. Hivo basi - Umar aliwakusanya maswahaba (r.a.) – na kushauriana nao; wakaafikiana zisomwe takbira nne. Kwa hiyo kufikia muwafaka kukaondoa hukumu tofauti zilizotangulia. Na Abul’ Abbas bin Sariij alikuwa anafanya hilo kuwa ni miongoini mwa hitilafu halali, na wala si baadhi zake ni bora kuliko zingine. Na hii ipo karibu na madhehebu ya Ibn Mas’ud. Na kufikia muwafaka tuliko kutaja kunabatilisha madhehebu hii.17 16 Al-Haawiy Al-Kabiir: 3 \ 54 kitabul-janaiz, babu takbiirati alal’janaizi. 17 Al-Haawiy Al-Kabiir – Ali bin Muhammad Al-Maarudiy Ash- Shaafi’iy 3:55 Kitabul’janaaizi. Babu At-Takbiir alal’janaizi. 6


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:14 PM

Page 7

Swala Ya Maiti

PILI: MCHANGO WA KHALIFA WA PILI KUTHIBITISHA KAULI YA TAKBIRA NNE. Ni kama hivi inabainika kuwa kuafikiana kwao juu ya takbira nne kunatokana na msimamo wa Umar bin Al-Khattab pindi alipowaona waislamu wanamsomea maiti takbira zenye idadi tofauti. Naye akawakusanya juu ya takbira nne na akawalazimisha nazo, hapo basi unakuwa si ulazima wa kisheria. Na kigezo alichokitegemea Umar ni mlandano na Swala iliyo ndefu mno – kama itakavyokuja – haiwi dalili ya lazima juu ya yeyote. Katika Fat’hul-Baariy kutoka kwa Ibn Al-Mundhir kuwa yeye amesema:

“Na ambalo twalichagua ni lile lililothibiti kutoka kwa Umar.” Kisha aliendelea kwa sanad sahihi mpaka kwa Said bin Al- Musayyib. Alisema: “Takbira zilikuwa nne na tano Umar aliwakusanya watu wasome nne.” Na Al-Bayhaqiy ameeleza kwa sanad nzuri mpaka kwa Abiy Waaili alisema: Zama za Mtume wa Mungu (s.a.w.) walikuwa wanasoma takbiira saba na sita na tano na nne, Umar aliwakusanya watu wasome takbira nne sawa na Swala iliyo ndefu mno…18 Na hilo ni kama ulionavyo ni tendo lisilo na dalili, na ni mwenendo unaofichua utashi wa Khalifa katika kuitolea hukumu sharia kwa msingi wa vigezo visivyo na tamko la kisharia. Na tendo lake hili limekuwa chanzo cha usemi wa hilo katika madhehebu nne. Na wanachuoni wa madhehebu hizi wamejaribu kulielekeza kulingana na muktadha za muundo wa 18. Fat-hul’bariy 3:157. 7


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:14 PM

Page 8

Swala Ya Maiti kifiq’hi, hivyo majaribio yao ni ya kuhalalisha. Na miongoni mwayo ni majaribio ya Al-Maarudiy Shafi’iy na dalili zake ambazo zimepita hivi punde. Dalili yake ya mwanzo: Ni isemayo kuwa riwaya za takbira nne ni nyingi mno kuliko riwaya za kauli zingine zilizo sahihi lau kupingana kati ya riwaya kungetafutiwa ufumbuzi. Na suala lake kufikia kanuni za ta’adulu wa tarjiihu. Na jambo ambalo sisi tupo ndani yake halipo hivyo. Mbele yetu kuna kauli yenye uwezekano wa hiyari na kauli nyingine ya kuangaliwa aina yake, kama itakavyokuja. Wala haifikii noba ya kutilia uzito upande wenye wingi wa riwaya. Kisha kanuni ya tarjiihu - kutilia uzito, hurekebisha hali ya kupingana kati ya riwaya ambazo suala lake hurejea kwa wapokezi, na wala ndani yake hakuna uwezekano wa kuwa sharia asili yake imo katika sura tofauti katika mas’ala moja. Kama ilivyo kwa kauli ya mkato katika mas’ala hii. Kwani kauli ya mkato kwa kauli moja kulingana na kauli za waislam wa pande zote mbili – yaani Suni na Shia - ni: Kuwa Nabii (s.a.w.) mwenyewe binafsi ameswali mara kwa takbira nne na mara nyingine kwa takbira tano. Hivyo basi tofauti hairejei kwa upande wa wapokezi hata tuipatie ufumbuzi kwa kutumia kanuni za tarjiihu, bali tofauti imethibiti toka asli ya uwekwaji wa sharia. Kwa minajili hiyo mas’ala tuliyonayo sio miongoni mwa mas’ala za tarjiihu aslan, hata ipatiwe ufumbuzi kwa njia ya kuangalia wingi na uchache - wa riwaya. Itakuwaje hivyo hali ikiwa Swahaba wamemuona Nabii (s.a.w.) mbele ya Umar bin Al-Khattab ameswali kwa takbira zaidi ya nne. Na Umar binafsi hakuuleta usemi huu. Ila tu amechagua hiyari mojawapo miongoni mwa hiyari zilizoelezwa kwake kwa kigezo kutokana na yeye binafsi ambacho hawajakitaja marawi kwake, nacho ni kushabihiana na swala iliyo ndefu mno. Hivyo tendo lake kuwa ni aina ya siasa ya kisheria ambayo – huenda – kwa hilo alitaka kuifanya tofauti iwe kidogo kati ya waislam. Kuwa kanuni ya tarjiihu katika fiqhi ya Imamiyya hailazimu kuzifanyia tarjiihu 8


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:14 PM

Page 9

Swala Ya Maiti riwaya nyingi juu ya riwaya chache, bali yalazimu kuzichukuwa nyingi ikiwa riwaya zinazo kabiliana nazo ni shaadhu - Si za kawaida na naadir, za nadra kama ambavyo kanuni ya tarjiihu katika fiqhi ya ki-Sunni huangalia aina ya wapokezi kabla ya kuzifanyia tarjiih zilizo nyingi juu ya chache. Kwa kuwa yamkini katika chache kukawa na wapokezi wenye uzito wa hadhi na daraja kuliko marawi ambao ni wengi, na mas’ala tuliyonayo yako hali hii kama inavyokuja katika tutakayo yanakili kutoka maneno ya Ibn Hazmi. Na muhtasari ni kuwa dalili ya kuifanyia tarjiihu nyingi kwa chache iko ukingoni mwa kuporomoka kwa sababu ya kutoingia mas’ala yetu kwenye mlango wa tarjiihu asilan. Na tuichukulie kuwa yaingia kimfano tu, kwa kweli kaanuni za tarjiihu hazipitishwi humo kulingana na usulul-fiqhi ya kisunni na Imamia. Ama dalili yake ya pili - Isemayo kuwa matendo ya maswahaba yamepita juu ya hilo ni dalili yenye kuporomoka mno kuliko iliyotangulia. Na riwaya aliyoifanya kutoka kwa idadi ya maswahaba kuwa wao walifanya takbira nne haijulishi kuwa wao walijilazimisha na hizo nne tu na hawakupata kufanya mahali pengine takbira tano, kwa hiyo dalili ni mahsusi mno kuliko dai. Itakuja kuwa idadi ya wengine miongoni mwa swahaba wamefanya swala kwa takbira tano. Miongoni mwao ni Imam Ali a.s., ni ambaye al-Maarudiy amemtaja kuwa ni miongoni mwa waliosoma takbira tano. Ni vipi basi tuseme kuwa tendo la maswahaba limefanyika hivyo – yaani wakisoma takbira nne?! Kisha tunasema kuwa Umar bin Al-Khattab aliwauliza Swahaba na kushauriana nao kuhusu mas’ala ya takbira na walimtajia kuwa ni nne na tano na yeye aliwakusanya kwenye takbira nne! Ni kuwa kauli ya pili haiendi sawa na ya kwanza, kwa kuwa Umar kutoa amri ya takbira nne yajulisha kuwa Swahaba hawakuwa wamejilazimisha nazo mpaka wakati ule, lau wangekuwa wenye kujilazimisha nazo, au lau kauli isemayo takbira ni nne ingekuwa mashuhuri iliyoenea, Khalifa hangekuwa na haja ya kuwakusanya na kuwauliza na kushauriana nao na kutoa amri ya takbira nne, kama ilivyo wazi, hivyo kitendo cha Umar kinajulisha 9


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:14 PM

Page 10

Swala Ya Maiti kuwa sera ya maswahaba haikuwa imejifunga kwenye takbira nne. Na la ajabu zaidi ya yote hayo ni ile dalili yake ya tatu ambayo amedai kuwa imefikiwa Ijmau - yaani makubaliano juu ya takbira nne. Kwa kuwa kitendo cha Khalifa wa pili kilikuwa ni kitendo cha kiserikali hakina mafungamano na asili ya kisharia, kwa kuwa Ijmau haiwi kwa amri ya kiutawala bali huwa kwa kuafikiana maswahaba juu ya amali maalumu ya kisharia. Na tendo hili la Khalifa laonesha kutokuwa na Ijmau katika mlango wa takbira za Swala ya mayit. Ibn Hazmi ameishambulia vikali dalili hii, ameandika akisema: “Abu Muhammad amesema: Wametoa hoja waliozuia zaidi ya takbira nne kwa habari tuliyoieleza kwa njia ya Wakiiu kutoka kwa Sufiani Ath-Thauriy kutoka kwa Aamir bin Shaqiiqu kutoka kwa Abi Waailu amesema: Umar Bin al’Khattab aliwakusanya watu na kuwataka ushauri kuhusu takbiira za jeneza, wakasema: Nabii (s.a w.) alisoma takbira saba, tano, na nne. Umar aliwakusanya juu ya takbira nne kama ilivyo Swala ndefu mno.” Na pia tumeieleza riwaya kwa njia ya Abdul-Razzaaq kupitia Sufyani AthThauriy kutoka kwa Umar bin Shaqiiq kutoka kwa Abu Waaili alisema. “Walisema: Hii ni ijmau, wala haifai kinyume chake.” Abu Muhammad amesema: “Na huu ni ufisadi wa mwisho kabisa, amelifanyia ta’awili hilo kuwa habari hizi sio sahihi, kwa sababu zinatoka kwa Aamir bin Shaqiiqu hajulikani ulimwenguni yeye ni nani!! Mungu apishe mbali! Umar atake ushauri katika kuzusha faradhi kinyume na alivyofanya Mtume wa Mungu (s.a.w.) au kwa ajili ya kuzuia baadhi ya aliyofanya (s.a.w.). hali alivyotawafu yaruhusiwa, na baada yake aharamishe. Hamdhanii hivi Umar ila ni mjinga wa nafasi ya Umar katika dini na Uislam ni mwenye kuwakebehi Salafi (radhwia llahu an’hum).” Kisha Abu Muhammad (Ibn Hazmi ) amesema: “Yakataliwa Ijmai yeyote inayomtoa Ali bin Abi Talib, Abdullahi bin Mas’ud, na Anas bin Malik, Ibn Abbas na Swahaba wa Sham (r.a.) kisha taabiuna wa Sham, na Ibn Syirin, 10


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:14 PM

Page 11

Swala Ya Maiti Jaabir bin Zayd na wengine kwa sanad iliyo katika ukomo wa usahihi. Na yu adai Ijmai kinyume na hao kwa sanadi dhaifu basi ni nani mjinga zaidi kuliko huyu ambaye hii ndio njia yake?” Ni nani mwenye bidhaa iliyo na hasara zaidi kuliko ya ambaye akilini mwake mnaingia kuwa kuna ijmai ameitambua Abu Hanifa, Malik na Shaafi’iy, na elimu yake imefichikana mbali na Ali, Ibn Mas’ud, Zayd Bin Arqam, Anas bin Maliki, Ibn Abbas kiasi kuwa wamekuwa kinyume na Ijmai. Ama - usomaji wa takbira wa Umar, Ali, Ibn Al-Mukaffaf, Ibn Abi Aufa, Zayd bin Thaabit, Zayd Bin Arqam na Anas, takbira nne hilo ni sahihi, lakini hao hawajakanusha takbira tano - na imesihi kuwa Nabii (s.a.w.) alisoma takbira ne na tano. 19

TATU: DALILI ZA KAULI YA TAKBIRA TANO NI KATIKA SUNNA YA NABII Havitofautiani vyanzo vya Hadithi ya Nabii kwa Ahlus-Sunnah na vyanzo vya Hadithi kwa Imamia katika kubainisha na kuleta habari zinazoonesha kauli kuwa swala ya maiti huwa kwa takbira tano. Muslim na al-Nasaaiy na Abu Daudi na al-Tirmidhiy wameandika kuwa Zaydu bin Arqam aliswalia jeneza na alisoma takbira tano na akasema: Alisoma hivyo Mjumbe wa Mungu (s.a.w.).20 Na katika Majmauz-Zawaidu kutoka kwa Kabiir bin Abdillahi kutoka kwa babu yake kutoka kwa baba yake alisema: Nabii (s.a.w.) alimswalia An19 Al-Mahalaa 5:124- 127. 20 Muslim ameieleza riwaya hii Namba 957 katika al’Janaaizu, babu Aswalatu alal’qabri. Na Abu Daudi Namba 3197. katika al’Janaizu. Babu al’Takbiiru alal’janazati. Na al’Tirmidhiyu Namba 10 23 katika al’Janaizi. Babu Ma ja’a fi al’takbiir alal’janazati. Na al’Nasaiy 4: 72 katika al’Janaizi, babu adadu takbiir alal’janazati. Jaamiul’usul 6:216. Sunanu Daru qutniy 2: 73 hadith na. 8. 11


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:14 PM

Page 12

Swala Ya Maiti Najaashiy kwa tano. Nilisema: Ibn Maaja ameeleza aliacha kumtaja AnNajaashiy, Tabaraniy ameeleza katika Al-Kabiir na al’Ausatu. 21 Na katika Fathul’Baariy kutoka kwa Ibn Al-Mundhir kutoka kwa Ibn Mas’ud: Kuwa yeye aliswalia jeneza la mtu mmoja miongoni mwa Bani Asad akasoma takbira tano. 22 Na katika Al-Mahaliy: Kuwa Zayd bin Arqam alisoma takbira tano baada ya Umar. Na kuwa Alqamatu alikuja kutoka Sham mpaka Kuufa alimwambia Ibn Mas’ud kuwa: Ndugu zako huko Sham wanasoma takbira tano kwa jeneza zao lau mungetuwekea wakati tuwafuateni kwa hizo? Abdullah aliinamisha kichwa muda, kisha alisema; angalieni jeneza zenu, zisomeeni takbira jinsi walivyosoma Maimamu wenu si wakati wala si idadi. Pia ameeleza kuwa Ibn Mas’ud alisoma takbira tano, kadhalika Imam Ali a.s. 23 Imam Ahmad ametoa katika Hadithi za Zayd bin Arqam kutoka kwa Abdullah kuwa yeye alisema: “Niliswalia jeneza nyuma ya Zayd bin Arqam alisoma takbira tano, Abu Isa Abdur Rahman Ibn Abi Layla alimwendea alimshika mkono wake na akasema: Umesahau? Alisema: “Hapana, lakini mimi niliswali nyuma ya Abil’Qaasim mpenzi wangu (s.a.w.w.) alisoma takbira tano sitoziacha abadan. 24 Na Zayd bin Arqam alimswalia Sa’ad bin Jubayr maarufu Saad bin Habtata, na huyu Habtata ni mama yake. Na yeye ni miongoni mwa Swahaba alisoma takbira tano ya jeneza lake, kulingana na alivyoeleza Ibn Hajar katika tarjuma ya Saad katika Isaba yake. Na Ibn Qutayba ameeleza katika Ahwali Abi Yusufu katika Maarifu yake, na Saad huyu alikuwa babu wa Abu Yusufu Al-Qaadhiy. 21 Majmauz-Zawaidi 3: 38 22 Fathul’Baariy 3:157. 23 Al- Muhala 5: 126 – 127. 24 Rejea uk.370 Jalada. la nne ya Musnad. 12


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:14 PM

Page 13

Swala Ya Maiti Na ametoa Imam Ahmad miongoni mwa Hadithi za Hudhaifa kwa njia ya Yahya bin Abdillahi al’Jaabiri, Amesema: “Nimeswali nyuma ya Isa huria wa Hudhaifa huko Madaini na alisoma takbira tano, kisha alitugeukia na akasema: Sikukosea wala sikusahau lakini nimesoma takbira kama alivyosoma bwana wangu na walii wa neema yangu Hudhaifa bin AlYamani aliswalia jeneza na alisoma takbira tano, kisha alitugeukia na alisema: Sikusahau wala sikukosea lakini nimesoma takbira kama alivyosoma Mtume wa Mungu (s.a.w.). 25 Na Ali a.s alimsomea Sahlu bin Haniifu takbira tano.26 Swahiba wa Muaadhi walikuwa wanazisomea jeneza takbira tano.27 Na Ibn Maajah ameufanyia anuwani mlango ndani ya Sunanu yake: Mlango wa yaliyokuja kuwahusu waliosoma takbiira tano. 28 Na amenakili katika Fathul’bariy kutoka kitabu Al-Mabsutu fil’fiqhil’Hanafiy kutoka kwa Abu Yusuf kuwa yeye alikuwa anasoma takbira tano. 29 Na katika Bidayatul-Mujtahid: Kuwa Ibnu Abi Layla na Jaabir Bin Zaid walikuwa wanafutu isomwe takbiira tano. Na imenakiliwa kutoka kwa Muhammad bin Aliy bin Imran al’Tamimiy al’Malikiy kuwa yeye alisema katika kitabu chake kwa jina la Fawaidu Muslimi (Kuwa Zayd alisoma takbira tano na kuwa Mtume wa Mungu (s.a.w) alikuwa hivyo hivyo anazisoma, lakini ameacha madhehebu hii kwa kuwa imekuwa ni utambulisho wa kauli ya Rafdhu).30 25 Musnad Ahmad 5: 406, Dhahabiy pia ameeleza katika Tarjuma ya Yahya bin Abdillahi Al-Jaabiri katika Mizanul’itidali. Muswanifu Ibn Abi Shayba 3:303. Sunanu al-Daaru-Qutniy 2:93 Hadith ya 9. Na Majmauz-Zawaidi 3:34. 26 Al- Mughniy 2:387, Al-Sharhul’Kabiir 2:349 nukuu kutoka kwa Saeed ndani ya Sunan yake. 27 Muswanifu Ibn Abi Shayba 3: 303. Sunanul’Bayhaqiy: 37. 28 Sunan Ibn Maajah: hadithi ya 1505. 29 Fat-hul’baariy 3:158 30 Jawahirul’kalam 12:31. 13


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:14 PM

Page 14

Swala Ya Maiti Na katika pambizo (haashia), ya Sindiy kuihusu Sunanu Nasaiy katika maelezo yake kuyahusu maneno ya Ibn Abi Layla kuwa Zaidu aliswalia jeneza kwa takbiira tano, Sindiy alisema: “Walisema takbiira za jeneza zilikuwa zinatofautiana hapo awali, kisha hitilafu iliondolewa na suala hili liliafikiwa juu ya takbira nne ila ni kwamba baadhi ya swahaba hawakujua hilo hivyo wakawa wanafanya kulingana na suala lilivyokuwa hapo awali, na Mungu swt ni mjuzi mno.31 Na kwa kukusanya maoni pamoja na asli natija ni kuwa asli ya mwanzoni takbiira za jeneza ni tano. Au sihaba kuwa kauli ya takbira tano ilikuwa ndio yenye kuenea na kusambaa kwa wingi, kiasi kwamba baadhi ya swahaba walibakia kwenye tano pamoja na kupita itifaqi ya kuwa zisomwe takbira nne. Haya ndiyo yaliyomo katika vitabu vya walio wengi miongoni mwa madhehebu nne yaani masunni na wengine. Ama Imaamia kauli ya takbira tano kwao ni kama dharura ya kimadhehebu kulingana na ibara ya Sheikh mtunzi wa kitabu al-JawahirulKalaam.32 Na maneno ya wanachuoni wao hapo zamani na hivi sasa yanatilia nguvu hilo, kama Sayyid al’Murtadhwa katika al’Intiswar,33 na Sheikh al’Mufiidu katika al’Muqniah,34 na Sheikh al-Tuusiy katika al-Khilaafu,35 Na al-Allama al’Hilliy katika Tadhkiratul’fuqahaau36 na wanafanya sanad ya madhhebu yao katika hilo kwa Mjumbe wa Mungu37 zaidi ya riwaya 31Sunanu Nasaiy kwa haashia ya Sindiy 2:375. 32 Jawahirul’kalaam12:31. 33 Al- Intiswar:175 34 Al’Muqniah:227. 35 Al’Khilaaf 1:729 36 Tadhkiratul’fuqahau 2:68. 37 Tazama: Man la yahdhuruhu’fuqahau 1:163. 14


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:14 PM

Page 15

Swala Ya Maiti walizonazo kuhusiana na hilo kutoka kwa ma Imamu wa Ahlul Bayt a.s. Na miongoni mwa maneno ya wanachuoni wa kileo katika uwanja huu ni kauli ya Sayyid al-Hakiim (r.a) ndani ya al-Mustamsik: ‘Kwa kweli takbira tano ni suala la ijmai, kama ilivyo katika al-Intiswaar, na al’Ghuniyah, al-’Tadhkirah, Adh-Dhikraa, na Jaamiul-Maqaaswid, al-Rawdhu na alMadaariku, na vingine, bali huenda ikawa miongoni mwa dharura ya kimadhehebu. Na hilo latolewa ushahidi na Sahihu Ibn Sinaan kutoka kwa Abii Abdillahi (a.s): (??????? ??? ????? ??? ???????) – (Takbiira za swala ya mayit ni takbiira tano) Na Sahih ya Abi Wilada: Nilimuuliza Abu Abdillahi a.s kuhusu takbira ya mayit akasema (a.s.): (???? – ni tano) na mfano wa hizo mbili kuna zingine ambazo ni nyingi mno bali huenda ni mutawatir, ndani ya baadhi zina maelezo ya sababu:- nayo ni kuwa: imechukuliwa kutoka kila swala moja katika swala tano takbira moja. Au ni kuwa imechukuliwa kutoka kila nguzo moja kutoka nguzo tano ambazo juu yake uislamu umejengwa takbira moja.38 Na amesema Sayyed al’Khuiy (r.a.): “Hapana mushkili kuwa swala ya mayit kwetu sisi huswaliwa kwa takbira tano, na hilo limejulishwa na kundi la riwaya zikiwemo sahihi na nyingine. Kama riwaya sahihi ya Abdillahi bin Sinaan kutoka kwa Abi Abdillahi (a.s): Takbira za swala ya mayit ni tano. Na riwaya zingine. Na katika baadhi ya zingine:

Kuwa Nabii (s.a.w.) alikuwa akiswali kwa takbiira nne pengine, na kwa tano mara nyingine. Imekuja sherehe ya hilo katika baadhi ya habari nyingine kwa madhumuni ya kuwa kila takbiira ni ishara ya asili na ni itikadi miongoni mwa itika38 Mustamsiku al’Urwatul’wuthqaa: 4 \ 234. 15


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:14 PM

Page 16

Swala Ya Maiti di za kiislamu kama vile Swaumu, Swala, Zaka Hija na Wilayah. Kwa minajili hiyo ndio maana alikuwa akiwaswalia kwa takbira nne wanaafiki wakanushao wilayah na kwa takbira tano kwa waumini. Haya yote kwa muujibu wa riwaya zetu. Ama kuhusu riwaya za Masunni zimehitilafiana katika jambo hili. Katika baadhi ya hizo ni kuwa Nabii (s.a.w.) alikuwa akiswali kwa takbira sita au saba. Na katika baadhi ya zingine ni kuwa Umar aliwakusanya swahaba zake na rai yake ikakita kwenye uamuzi wa kuwa maiti aswaliwe kwa takbira nne. Vyovyote iwavyo: Kuwa – Swala ya maiti ni kwa takbira tano ni jambo lisilo na ishkali kwetu, na endapo itapunguwa humo takbiira moja itakuwa batili kwa kuwa murakkabu hukosa kuendelea kuwa kwa kukosekana baadhi ya sehemu zake, wala haiwezi kujumuishwa na Hadith (?? ????) kwa kuwa hiyo ni mahsusi kwa swala yenye rukuu sijda na tohara. Ama zikizidi ikiwa kwa kusahau haiwi sababu ya kubatilika, kwa kuwa ni ziada baada ya kumalizika kwa amali, na ziada baada ya amali haisababishi ubatilifu. Ama ikiwa ziada kwa makusudi, ilivyo sahihi pia ni kuwa haisababishi ubatilifu, kwa sababu ni ziada baada ya a’amali kwa kuishia swala baada ya takbiira ya tano, ila ikiwa atairejesha kwenye sharia katika asili ya a’amali kuwa awe amejengea tokea mwanzo kuwa yenyewe ni takbira sita kwa hiyo awe yuaiswali kwa jengo hili kisheria, vinginevyo lau akijengea kuwa atasoma takbira ya ziada baada ya ile ya tano, hiyo haisababishi ubatilifu wake.39 Na kutokana na hayo yote inamuwia wazi mtafiti mwenye insaafu kuwa: Kauli ya takbira tano kwa swala ya maiti kama si kauli yakinifu kwa wadhifa wa kisharia, si haba kuwa yenyewe ni kauli inayozungukwa na dalili nyingi na zenye nguvu, na ina ishara peke yake kuwa ni yenye kuafikiana na ihtiyati - hadhari, kwa namna ambayo yule ambaye asomaye takbira 39 At-Tanqiihu fii sharhil –’uruwatil’wuthqa: 9 \ 69-70. 16


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:14 PM

Page 17

Swala Ya Maiti tano anakata shauri kuafikiana kwake na sharia kwa mujibu wa madhehebu zote, hali ikiwa yule asiyezisoma takbira tano hapati ukataji shauri huu, na amali yake inabaki imezungukwa na uwezekano wa kubatilika.

Nne: Mas’ala ya takbira ya Swala ya maiti katika mwanga wa kuwa Ahlul’bayt (a.s) ndio rejea. Na mas’ala ambayo tuikusudiayo inawakilisha ushahidi wa kimatendo miongoni mwa mamia ya shuhuda zinazoonesha kuwa waislamu baada ya kitabu na Sunna Nabawiy wanahitajia rejea ya kifikra iliyo hai iwezayo kutawalia jukumu la kutoa tafsir ya Kitabu na Sunna Nabawiy tafsiri iliyo na dhamana kutoka upande wa kisharia itakayokihifadhi Kitabu na Sunna Nabawiy mbali na ingizo za nafsi na uwezekano wa kupotoshwa ambao unaweza kujitokeza kwa anuwani ya Ijtihadi au vinginevyo. Na katika ambayo sisi tuliyonayo kuna Siira ya Nabii mahali maalumu. Riwaya zimeafikiana kutoka pande mbili Shia na Sunni kuwa Nabii (s.a.w.) ameswalia jeneza mara kwa takbira nne na mara nyingine kwa takbira tano na nyingine kwa takbira zaidi ya tano. Na mfano wa hali kama hii yumkini ukafasiriwa kuwa ni suala la hiyari kwa mwenye dhima kuchagua idadi ya takbira. Na yawezekana pia ukatafsiriwa kuwa ni suala linaloendana na aina ya maiti husika, ni kuwa Nabii (s.a.w.) alisoma takbira nne kwa ajili ya jeneza za watu fulani wenye sifa maalumu na alisoma takbira tano kwa watu wengine fulani wenye sifa nyingine na kama hivyo. Na ni wazi kuwa kuichagua tafsiri mojawapo kati ya tafsir hizi mbili ni kuipa uzito moja ya tafsiri unaohitajia sababu, na haiyumkiniki iwe bure bure tu bila ya dalili, wala kwa kusukuma tu bila ya msingi.

17


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:14 PM

Page 18

Swala Ya Maiti Na ilimbidi khalifa wa pili asimame kwenye nukta hii asiharakie kuchagua umbo la unne wa swala ya maiti na kwa namna ya papo kwa papo. Na hayo yote yanatoa ushahidi wa kuwa madrasa ya Ahlul Bayt ndiyo ya kweli na uhakika na uwiano kimantiki pindi iliponadi dharura ya kuisajili fiq’hi kulingana na marjaiy ya kifiqhi yenye dhamana na kuhifadhika yenye kustahiki stahiki ya kufaa katika kusudi la kufichua makusudi ya wahyi na haki yake ya asili. Na ilipothibitisha kwa dalili ya makumi kadhaa ya Aya za Qur’ani na Riwaya Nabawiy kuwa kumtakasa Muumba mtukufu na sharia zake takatifu mbali na mchezo inalazimu kutosihi kuitelekeza sheria kwa kuiacha bila ya Rejea ya kidini iwezayo kuilinda isipotoshwe baada ya Nabii (s.a.w.). Na izingatiwe kuwa baadhi ya Swahaba wa Nabii (s.a.w.) kuwa na fadhailu hakumaanishi kuwa wanastahiki marjaiy itakiwayo baada ya Rasuul (s.a.w.). Na kuwa Kitabu Kitukufu pamwe na Sunna vinajulisha kwa dalili ya kata shauri yenye nguvu, kuwa maimamu wa Ahlul-bayt (s.a.w.) ndiwo rejea itakiwayo baada ya Rasuul (s.a.w.), ili kuihami sharia na kuilinda risala, mbali na mchezo wa wafanyao mchezo kama historia ilivyolithibitisha hilo. Hapo basi, katika kukabiliana na fumbo za Kitabu na Suna ambazo zinakubali zaidi ya tafsiri moja, hapana budi tuichukuwe tafsiri ambayo inayoishiriwa na rejea kwa Ahlul Bayt (a.s.) kwa kuizingatia kuwa ni tafsiri ambayo Kitabu na Sunna vimetuamuru tuzichukue kutoka rejea hizi, na kutupilia mbali tafsiri zingine zisizo hizo kwa kuzizingatia kuwa zimetoka vyanzo visivyoelekezwa na Kitabu wala Sunna kuzichukua, kwani hizo ni tafsiri zilizoachwa kwa mujibu wa Sheria. Na sisi tupo katika mas’ala yenye hali hii, kwamba tunaikuta fiqhi isiyo ya Imamiyah katika kuitendea kazi kwake Siiran-Nabawiy katika uwanja wa Swala ya maiti wamejengea kuzichukua riwaya zisemazo takbira nne na imezidondosha riwaya zingine bila ya kuzitilia manani, kwa kihalalishi kisichoweza kuzingatiwa, nacho ni kushabihiana na Swala ndefu zaidi. 18


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:14 PM

Page 19

Swala Ya Maiti Na umbali unaoweza kufikiwa wa kuulinda mwenendo huu ni kuthibiti kuwepo na tofauti katika idadi ya takbira ambazo Nabii (s.a.w.) alizisoma katika hali tofauti katika kuwaswalia kwake maiti inaweka wazi kuwa sharia inataka kuwaacha mukalafiina wakiwa na hiyari katika hilo wala haiwawekei mpaka maalum. Hivyo Khalifa wa waislamu alitaka wachaguwe mojawapo miongoni mwa takbira hizi zilizoruhusiwa, na imekuja katika baadhi ya riwaya kuwa Umar bin Al-Khattab aliwahutubia maswahaba aliowakusanya na aliwaambia: Ee ninyi maswahaba wa Muhammad mutofautianapo watatofautiana watu baada yenu, na watu wapo karibu mno na zama za Jaahilia, hivyo basi kuweni pamoja kwenye kitu, nao watakuwa pamoja watakaokuwa baada yenu. Hapo rai za swahaba wa Muhammad (s.a.w.) kuwa waangaliye jeneza la mwisho takbira Nabii alizosoma kabla hajafishwa wazichukue hizo na waachane na zingine. Wakaangalia wakakuta jeneza la mwisho Mtume wa Mungu alizisoma takbiira nne.40 Na msimamo wa Khalifa na maswahaba wengine waliomuitika unaweka wazi kuwa wao walifahamu kutokana na tofauti za takbira za Nabii (s.a.w.) kuwa sheria imeacha hilo kuwa hiyari kwa mukalafina. Hivyo basi wakaafikiana juu ya takbira nne, ili kuuzima mzozo ambao ungeweza kupanuka zaidi hapo baadaye, wakiwa wameghafilika kuwa tendo lao hili…ni kiburi juu ya sheria. Ikiwa sheria imewaacha mukalafiina na hiyari yao kuhusu suala la takbira, kwa hiyo kujinga’ng’aniza kwenye hiyari moja na kuzifungilia mbali hiyari zingine ni kitendo kinachokwenda kinyume na sheria na kusudi zake, upeo wa kuwa wao wako sahihi kutenda ni kuzitendea kazi nne na 40 Al-Haawiy al’kabiir cha Ali bin Muhammad al’Maarudiy 3: 53. Katika pambizo ya mwenye kuhakiki kitabu, nukuu kutoka kitabu: al’Aatharu cha Muhammad bin al’Hasan al’Shiibaniy akinukuu kutoka kwa Ustadh wake Abu Hanifa naye kutoka kwa ustadhi wake Hammad bin Abi Sulayman kutoka kwa Ibrahim anNakha’iy. 19


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:14 PM

Page 20

Swala Ya Maiti bila ya kuzifunga hiyari zingine. Hilo litakuwa na natija iliyo kinyume na ilivyo fiqhi ya madhehebu nne na itaafikiana na ilivyo fiq’hi ya Ibn Hazimi. Na endapo sheria itakuwa haikuwahiyarisha mukalafiina katika takbira hizi, na kwamba yenyewe ina lengo lingine kama itakavyo kuwa wazi hivi punde, na kuwa sharia imewafunga mara kwenye takbira nne na nyingine kwenye tano, kwa hiyo kitendo cha Khalifa kilichoafikiwa na maswahaba wengine kinakuwa hakina msingi wowote wa kisheria. Na hii yamaanisha kuwa usemi wa takbira nne ni batili kwa yamkini zote. Hivyo haki inabaki kwenye uwigo wa waliyonayo Ahlul Bayt (a.s.) kwamba kutofautiana kwa takbira za Nabii (s.a.w.) za Swala ya jeneza hakujulishi kuwa mukalafu wana hiari juu ya hizo, bali kwajulisha kuwa Nabii (s.a.w.) aliswali katika hali tofauti, na ulikuwa utekelezaji wake katika hali moja unatofautiana na wa hali nyingine. Zakujia dondoo za ubainifu kutoka kwa Maimam (a.s.) katika kuyaweka wazi mas’ala ya takbira na tafsiri ya tendo la Nabii (s.a.w.). Katika al’Istibswar ya Sheikh Tusi twasoma mlango kwa anuwani: ??? ????????? ??? ??? ????) ??? Mlango wa idadi ya takbira za swala ya maiti). Katika mlango huu ameleta riwaya kumi na moja tunazinakili kwa tamko lake: 1. Al-Husein bin Said kutoka kwa Fadhwalatu kutoka kwa Abdillah bin Sinan kutoka kwa Abu Abdillah (a.s.) alisema: ??????? ??? ????? ??? ??????? Takbira za Swala ya maiti ni takbira tano. 2. Said Bin Abdillahi kutoka kwa Ibrahim bin Mahziyaar kutoka kwa Hammad Bin Shuaib kutoka kwa Abu Abdillah (a.s.) alisema: ??????? ??? ????? ??? ??????? = Takbira ya Swala ya maiti ni tak20


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:14 PM

Page 21

Swala Ya Maiti biira tano. 3. Ali bin al-Husayn kutoka kwa Muhammad Bin Ahmad Bin As-Swalat kutoka kwa Al’Hasan Bin Ali kutoka kwa Ibn Bakir kutoka kwa Qudaamata Bin Zaidata, alisema: “Nilimsikia Abu Jaafar (a.s.) akisema: Mjumbe wa Mungu (s.a.w.) alimswalia mwanawe Ibrahim alisoma takbiira tano). 4. Abdullah Bin Swalat kutoka kwa Al-Hasan Bin Mahbub kutoka kwa Abu Wilada alisema:

Nilimuuliza Abu Abdillah (a.s) kuhusu takbiira ya Swala ya mayit, akasema: Ni tano. 5. Al-Husein Bin Said kutoka kwa Fadhwalata kutoka kwa Kulaybu alAsadiy alisema (mbele yake) Tano:

Nilimuuliza Abu Abdillah (a.s.) kuhusu takbiira ya mayit, alisema: Ni tano. 6. Ama riwaya iliyoelezwa na Ahmad bin Muhammad bin Isa kutoka kwa Muhammad bin Khalid al’Barqiy kutoka kwa Ahmad bin An-Nadhwar AlKhuzazi kutoka kwa Amr Bin Shimr kutoka kwa Jaabir alisema:

Nilimuuliza Abu Jaafar (a.s.) kuhusu takbiira za jeneza; je, kuna kitu kwa wakati? Alisema: Hapana. Mtume wa Mungu (s.a.w.) alisoma takbira kumi na moja, tisa, saba, tano, sita na nne. 21


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:14 PM

Page 22

Swala Ya Maiti Yaliyomo kwenye habari hizi miongoni mwa kuzidi kwa takbiira na kuwa zaidi ya tano zimeachiwa kwa ijmai, na inawezekana (a.s.) alikuwa anaelezea kitendo cha Mtume (s.a.w.) kwa maelezo hayo. Kuwa yeye alikuwa anasoma takbira ya jeneza moja au mbili na huletwa jeneza lingine kwa hiyo yeye huanza alipoishia takbira tano, hivyo hizo zikiongezwa juu ya takbira alizokwisha soma huwa zaidi ya takbira tano. Na yajuzu hivyo kulingana na tulivyobainisha katika kitabu chetu kikubwa. Ama mulimo na maelezo ya takbira nne yachukuliwa katika hali ya taqiyya. Kwa kuwa ni madhehebu ya wote walio khilafu na Imamiyah, au inakuwa ni kuelezea kitendo cha Nabii (s.a.w.) kuwahusu munafiqina au wanaotuhumiwa kuwa waislam kwa kuwa yeye (s.a.w.) alivyokuwa anafanya yajulisha hivyo. 7. Aliyoyaeleza Al-Husein Bin Said kutoka kwa Muhammad Bin Abi Umayr kutoka kwa Hammad Bin Uthman na Hisham Bin Salim kutoka kwa Abu Abdillah (a.s.) alisema:

Mtume wa Mungu (s.a.w.) alikuwa anawasomea watu takbira tano na wengine nne na endapo atamsomea mtu takbira nne mtu huyo hutuhumiwa. 8. Ali Bin Husein kutoka kwa Abdullah bin Jaafar kutoka kwa Ibrahim Bin Mahzayar kutoka kwa nduguye Ali, kutoka kwa Ismail Bin Hammam kutoka kwa Abul-Hasan (a.s.) Alisema: Abu Abdilllah (a.s.) amesema: Mtume wa Mungu aliswalia jeneza akasoma takbira tano, na aliswalia jingine akasoma takbira nne. Ama lile alilolisomea takbira tano alimhimidi Mungu na kumtukuza katika takbira ya kwanza, na katika ya pili alimuombea Nabii (s.a.w.). Na katika ya tatu aliwaombea waumini 22


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:14 PM

Page 23

Swala Ya Maiti wanaume na waumini wanawake, na katika ya nne alimuombea maiti, na aliondoka baada ya takbira ya tano. Amma lile alilolisomea takbira nne alimhimidi Mungu na kumsifu katika takbira ya kwanza, na alijiombea binafsi na Ahlu bayt wake katika ya pili, na aliwaombea waumini wanaume na waumini wanawake katika ya tatu, na aliondoka katika ya nne, na wala hakumuombea kwa sababu alikuwa munaafiqi. 9. Ali Bin Husein kutoka kwa Ahmad Bin Idrisa kutoka kwa Muhammad Bin Salim kutoka kwa Ahmad Bin Nadhwar kutoka kwa Amru Bin Shimri, alisema: Nilimwambia Jaafar Bin Muhammad (a.s): “Nimejitoa fidia kwako, kwa kweli sisi huongea huko Iraq kuwa Ali (a.s.) alimswalia Sahlu Bin Haniif alisoma takbiira sita kisha aliwageukia waliokuwa wanasawali nyuma yake, na alisema: ‘Kwa kweli yeye alikuwa mtu wa Badri.’ Alisema: Hapo Jaafar alisema: ‘Kwa kweli haikuwa hivyo, lakini yeye alimswalia kwa tano kisha alimnyanyua na kwenda naye punde kisha alimteremsha na alimsomea takbira tano na alifanya hivyo mara tano mpaka ikafikia takbira ishirini na tano.’” Riwaya ya Ali bin Husein kutoka kwa Muhammad bin Yahya kutoka kwa Muhammad bin Ahmad Al-Kuufiy laqabu yake ni Hamdani kutoka kwa Muhammad bin Abdullah kutoka kwa Muhammad bin Abi Hamza kutoka kwa Muhammad bin Yazid kutoka kwa Abu Baswiir, alisema: “Nilikuwa nimeketi kwa Abu Abdillah (a.s.) mtu mmoja aliingia akamuuliza kuhusu takbira za jeneza. Alisema: “Ni takbira tano.” Halafu aliingia mwingine akamuuliza kuhusu Swala ya jeneza. Alimwambia: “Ni swala nne.”41 Yule wa kwanza alisema nimejitoa muhanga kwako, nilikuuliza ulisema ni tano, 41 Na yamkini iwe alikusudia kwa kauli yake: Nne kueleza yasemwayo kati ya takbira miongoni mwa dua, kwa sababu takbira ya tano haina dua baada yake, bali huondoka mbali na jeneza mswaliaji badala ya dua

23


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:14 PM

Page 24

Swala Ya Maiti na huyu amekuuliza, ukasema ni nne! Alisema: “Wewe uliniuliza kuhusu takbira na huyu aliniuliza kuhusu Swala.” Halafu alisema: “Kwa kweli ni takbira tano ambazo kati yake kuna du’a (swala) nne.” Halafu alikunjua mkono wake na akasema: Nazo ni takbiira tano kati yake du’a nne. 42

DONDOO YA MJADALA Kuwa Swala ya maiti kulingana na madhehebu ya Ahlul Bayt (a.s.) huwa kwa takbira tano. Na Swala ya Nabii pengine – na kwa baadhi ya maiti alikuwa akisoma takbira nne, kwa ajili ya mambo mahsusi yakizingatiwa kuwahusu baadhi ya maiti waliokuwa wakiswaliwa. Kuwa kauli ya takbira nne tu haina baraka za Sunnan-Nabawiy, bali hiyo yatokana na tendo la Khalifa wa pili alipojiwa na wazo hilo.

42Al-Istibswar 1: 474 - 476. 24


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:14 PM

Kumlilia Maiti

Kumlilia Maiti Kwa Mujibu wa Sunna na Sira

Kimeandikwa na: “Muhammad Jawad at-Tabasi�

Kimetarjumiwa na: Ustadh Hemedi Lubumba Selemani

25

Page 25


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:14 PM

Page 26

Kumlilia Maiti

DIBAJI Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu Kila sifa njema ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu. Amani na salamu zimwendee bwana wetu Muhammad na kizazi chake kitoharifu. Kulia ni miongoni mwa maudhui ambazo zimeingia katika duru lenye kutiliwa umuhimu na wasomi, waandishi, malenga, wanafasihi na ‌‌.. Hawa wote kila mmoja huhusika na sehemu yake kwa mujibu wa upande wake maalumu unaomuhusu. Kwa mfano, wanasaikolojia huizungumzia kupitia faida zake na athari zake juu ya nafsi ya mtu, kama vile kumpunguzia huzuni na yanayotokana na huzuni hiyo. Wengine huizungumzia upande wa kielimu, kama vile ala zake, namna kinavyotokea, athari yake juu ya siha ya jicho na afya kwa ujumla. Kama ambavyo wengine huizungumzia kishairi na kinathari, na mara nyingi hali hiyo huwa katika kumwomboleza aliyetutoka, au kuelezea hisia za kweli za kukutana au kutengana na vipenzi. Na unaotuhusu sisi ni ule upande unaosimama juu ya msingi wa swali lifuatalo: Je, kumlilia maiti ni jambo linaloruhusiwa kisheria? Au ni kukata tamaa kulikokatazwa na ni kumdhania vibaya Mwenyezi Mungu, Yeye na yale aliyokadiria na kupitisha? Inaonekana kuwa swali hili limetokana na utata unaoletwa na baadhi ya waislamu, nao ni kuharamisha kumlilia maiti. Utata huu umezushwa katikati ya jamii yetu ya kiislamu, jambo ambalo limefanya akili za baad26


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:14 PM

Page 27

Kumlilia Maiti hi kushikamana nao, kana kwamba kulia ni jambo jipya linalopingana na akili salama na maumbile ya kibinadamu. Kana kwamba ni suala ambalo halijagusiwa na maelezo ya kidini na wala Mtume, watu wa nyumba yake, sahaba na tabiina hawakuwahi kulia. Na wala vyanzo vyetu vya riwaya na historia havijajaa suala hilo, na hivyo lenyewe ni bidaa iliyoingia katika maisha ya waislamu, ambayo inawajibika kusimama dhidi yake na kuing’oa mizizi yake na kuwapiga vita wale wenye kushikamana nayo! Msimamo huu umeacha athari mbaya katika mahusiano ya waislamu, kati ya wale wanaopinga kumlilia maiti, nao ni wachache, na wale wanaoruhusu kumlilia maiti na hasa Mtume na watu wa nyumba yake, nao ndio wengi. Suala ambalo limetoa nafasi kwa wenye kuunyemelea Uislamu na waislamu kuzamisha ndoo yao iliyojaa uchafu na chuki na hatimaye kupanua duru la mfarakano. Ukweli wa mambo ni kinyume kabisa na vile wanavyodhani wale wenye kuleta utata wa kuharamisha kumlilia maiti, kwa sababu wao wamesahau maumbile aliyoyaweka Mwenyezi Mungu ndani ya kiumbe huyu hai, ambaye laiti matarajio yake yatatimia basi bila shaka huhisi raha na furaha. Na pale yanapozimika au akapatwa na hali ya kuondokewa na mke au mtoto walionyakuliwa na uwezo wa Mola, basi huhuzunika, na wakati mwingine hujimaliza na hatimaye kukomea kwenye jambo lichukizalo. Lakini vilevile kuna wakati hujizuia na kuvumilia mbele ya hali hiyo na mbele ya kila kikwazo vyovyote kiwavyo. Na msimamo huu umeishangaza sheria ya kiislamu na imeuhimiza na kuuwekea thawabu kubwa, thawabu za wenye kuwa na subira. Msimamo wake huu haudhuriki wala subira yake na thawabu zake havipatwi na dosari kwa kule tu kutokwa na machozi, kwa sababu kilio ambacho hukimbilia mwenye msiba kina hali ya kujitoa kwenye msiba na kina hali ya kupunguza uchungu na uzito ulioifika nafsi yake mliaji, na pia kina hali ya kujitoa kwenye matatizo ya dunia na huzuni za nafsi, vitu ambavyo humpata mwanadamu, na huenda vikadhibiti mwenendo wa 27


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:14 PM

Page 28

Kumlilia Maiti maisha yake. Kama ambavyo katika kilio hicho kuna utulivu wa nafsi ndani ya ulimwengu wetu huu uliorundikana matukio yenye kutisha na kuumiza. Humo mwanadamu anahitaji kiliwazo kama vile kilio ambacho ndani yake anapata wasila bora wa kuirudisha nafsi kwenye utulivu ili iendeleze jihadi yake na kazi yake. Kisha hakika kumlilia maiti laiti ingekuwa ni aibu na jambo baya basi kitendo hicho kisingekuwa miongoni mwa sifa za watukufu. Huyu hapa Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amlilia mwanawe Ibrahim. Na alikuwa amuonapo shangazi yake Swafiyyah binti AbdulMuttalib akimlilia kaka yake Hamza naye hulia, na azamapo ndani ya kilio naye huzama. Kama ambavyo amuonapo Fatimah akilia naye hulia. Na alipomuona Hamza akiwa ameuwawa kishahidi alilia. Hivyo kumlilia maiti si suala lililokatazwa kisheria, na wala kamwe halikinzani na subira, na pia haliendi kinyume na imani iwapo tu kilio hicho ni pamoja na kuridhia pitisho la Mwenyezi Mungu na kadirio lake. Itakuwaje likinzane na imani ilihali haya hapa maelezo mengi yaliyothibiti kwenye makundi yote ya kiislamu, kama utakavyoona hapo baadaye, yanahimiza kuwa Mtume (s.a.w.w.), watu wa nyumba yake, sahaba zake na waislamu wote kwa ujumla waliwalilia mawalii wao na vipenzi vyao? Hakika kilio ambacho Mtume (s.a.w.w.) alikielezea akasema kuwa ni huruma, na kuwa “jicho linatoka machozi na moyo unahuzunika lakini hatusemi lile linalomghadhibisha Mola Mlezi‌.â€? ni aina ya kilio kisichokuwa na shaka, na sheria ya kiislamu inakiruhusu na inakihimiza. Kama tunavyolipata hilo kupitia dalili yakinifu tulizonazo, na pia sira yakinifu na hoja ya kivitendo. Mambo yoye haya yanapelekea uhalali wa kumlilia maiti, bali ni Sunna iwapo ni kumlilia Mtume (s.a.w.w.), hilo la kwanza. Na kumlilia maiti ikiwa amekusanya sifa bora au amejitoa muhanga yeye 28


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:14 PM

Page 29

Kumlilia Maiti mwenyewe, familia yake na mali zake katika njia ya Mwenyezi Mungu ili wengine wafuate, hili la pili. Ama kilio cha kukata tamaa, kulalamika na kutamka maneno yanayoonyesha kuchukizwa na kutoridhia pitisho na kadirio la Mwenyezi Mungu, huku kikibeba hali ya kudhihirisha upinzani dhidi ya hekima ya Mwenyezi Mungu, kilio cha namna hii kimekatazwa na wala hakuna yeyote apingaye. Mwisho tunaleta maelezo mengi kutoka kwenye Sunna na Sira, ambayo tumeyapangilia katika namna munasibu ndani ya sura zifuatazo, ili kumrahisishia mpenzi msomaji. Tumeonyesha humo ruhusa ya kulia na kisha tumebatilisha utata wa wapingaji. Muhammad Jawwad At-Tabasiyyu 18, Jamadul-Uwla 1416 (A.H.).

29


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:14 PM

Page 30

Kumlilia Maiti

SURA YA KWANZA DALILI ZINAZORUHUSU KUMLILIA MAITI 1. Kitendo cha Mtume (s.a.w.w.) na sera yake: Miongoni mwa dalili dhahiri juu ya ruhusa ya kisheria ya kumlilia maiti ni kile kitendo cha Mtume (s.a.w.w.), hakika yeye alimlilia waladi wake na binti yake, na pia alimlilia Zayd, Ja’far, Ibnu Ruwwah, Ibnu Madh’un, Sa’ad bin Rabi’i na wengineo wengi. Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akilia mpaka machozi yake yanatiririka juu ya mashavu yake, na alipokuwa akiulizwa juu ya hilo husema: “Hakika yenyewe ni huruma anayoiweka ndani ya nyoyo za waja Wake.” An-Nasai amepokea kwa njia yake kutoka kwa Usama bin Zayd amesema: “Kuna binti alimtumia Mtume ujumbe kuwa: “Mwanangu wa kiume amefariki, njooni.” Basi (s.a.w.w.) akamtumia ujumbe akimpa salamu na kumwambia: “Hakika ni cha Mwenyezi Mungu anachokichukua na anachotoa, na kila kitu kwa Mwenyezi Mungu kina muda maalumu, hivyo kuwa na subira na uvumilie.” Binti akatuma ujumbe akimuhimiza aende, ndipo akasimama akiwa pamoja na Sa’ad bin U’bada, Ma’adh bin Jabal, Ubayya bin Ka’ab, Zayd bin Thabit na wengineo. Basi Mtume akamwinua kijana huku nafsi yake ikitoa kwikwi ya kilio, na hatimaye machozi yakambubujika. Sa’d akasema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu kitu gani hiki?” Akajibu: “Ni huruma anayoiweka ndani ya nyoyo za waja Wake. Hakika Mwenyezi Mungu huwafanyia huruma wale walio na huruma miongoni mwa waja wake.”1 1 Sunan An-Nasaiy 4: 22. Al-Muswannaf cha Ibnu Abu Shaybah 3: 266. AlMuhimmah 93. 30


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:14 PM

Page 31

Kumlilia Maiti Mtume (s.a.w.w.) alimwambia Abdullah bin Awf alipomuuliza: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, kwani hukukataza kulia?” Akamjibu: “Bila shaka nilikataza kuomboleza kwa sauti mbili za kijinga za kiovu: Sauti wakati wa kughani kwa upuuzi, mchezo na zumari za shetani. Na sauti wakati wa msiba kwa kujikwaruza uso na kuchana mifuko ya nguo….. lakini (uliaji wangu) huu ni huruma….”2 2. Mtume (s.a.w.w.) ahimiza kumlilia maiti: Miongoni mwa dalili dhahiri juu ya ruhusa ya kisheria ya kumlilia maiti ni kile kitendo cha Mtume (s.a.w.w.) kuhimiza kumlilia maiti, hilo ni pale alipoingia Madina baada ya vita vya Uhud akawaona wanawake wakiwalilia maiti wao, ndipo naye akalia na kusema: “Ama Hamza hana wa kumlilia.” Ibara hii iko wazi kabisa kuwa yeye (s.a.w.w.) aliwahimiza wanawake wamlilie Hamza. Na pia aliwahimiza watu kumlilia Ja’far bin Abu Talib aliposema: “Mtu mfano wa Ja’far wamlilie wenye kulia.” Kwani laiti ingekuwa kumlilia maiti ni jambo lisiloruhusiwa kisheria basi Mtume asingehimiza jambo hilo. Na ifuatayo ni baadhi tu ya mifano juu ya suala hilo: a. Ahmad amepokea ndani ya Musnad yake, amesema kuwa: “Mtume alirejea toka Uhud ndipo wanawake wa kianswari wakawa wanawalilia waume zao waliouliwa, Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akasema: “Lakini Hamza hana wa kumlilia.” Amesema: “Kisha akalala, na alipoamka akawakuta wanawake hao wakimlilia Hamza. Hivyo wao leo wanapolia huwa wanamwomboleza Hamza...”3 b. Ibnu Abdul Barri amesema katika wasifu wa Hamza akimnukuu AlWaqidiy: “Baada ya kauli ya Mtume wa Mwenyezi Mungu “Lakini 2 Al-Muswannaf 3: 266. 3 Musnad Ahmad, Juz. 2, uk. 40. 4 Al-Isti’ab kwenye maelezo ya Al-Iswabah 1: 275, na pia kwenye Al-FusululMuhimmah: 92. 31


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:14 PM

Page 32

Kumlilia Maiti Hamza hana wa kumlilia.” Hakuna mwanamke yeyote wa kianswari aliyemlilia maiti mpaka leo hii ila kwanza alianza kumlilia Hamza.”4 c. Ndani ya Shifaul-Gharam: “Wanawake wa Bani Ash’hali waliposikia hivyo walikwenda wakimlilia ami ya Mtume wa Mwenyezi Mungu huku sisi tukiwa kwenye mlango wa msikiti. Alipowasikia aliwatokea na kusema: “Rejeeni, Mwenyezi Mungu awarehemu, bila shaka mmeshiriki kwa nafsi zenu.”5 d. Alipotaka kutoka nyumbani kwa Ja’far baada ya kumpa mkono wa tanzia Asmaa binti Umays, alisema (s.a.w.w.): “Mtu mfano wa Ja’far wamlilie wenye kulia.”6 3. Mtume (s.a.w.w.) aruhusu kumlilia maiti: Mtume (s.a.w.w.) aliruhusu kumlilia maiti, kama alivyopokea Ibnu Mas’ud, Thabit bin Zayd na Qar’dhatu bin Ka’ab, wamesema: “Alituruhusu kulia.” Amesema: “Niliingia kwa baba yangu Mas’ud wakiwa na Qar’dhatu wakasema: “Hakika yeye alituruhusu kulia wakati wa msiba.”7 Mtume (s.a.w.w.) akawaambia wanawake waliokuwa wakimlilia maiti pindi mmoja wa sahaba zake alipowakataza: “Waache walie, na jiepusheni na mlio wa shetani. Vyovyote vile vitokavyo jichoni na moyoni ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu na ni kutokana na huruma. Na vyovyote vile vitokavyo mkononi na ulimini ni kutokana na shetani.”8 Ibnu Shibah amepokea kwa njia yake kutoka kwa Ibnu Abbas amesema: “Alipofariki Ruqayyah binti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) 5 Shifaul-Gharam 2: 347. 6 Ansabul-Ashraf: 43. 7 Al-Muswannaf 3: 268. 8 Kanzul-Ummal 15: 621. 32


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:14 PM

Page 33

Kumlilia Maiti Mtume wa Mwenyezi Mungu alisema: “Jiunge na aliyetutangulia aliye bora Uthman bin Madh’un.” Amesema: “Wanawake wakalia, ndipo Umar akaanza kuwapiga kwa mjeledi wake. Mtume (s.a.w.w.) akamnyang’anya kwa mkono wake na kusema: “Ewe Umar waache.” Na akasema: “Waache walie, na jiepusheni na mlio wa shetani. Vyovyote vile vitokavyo jichoni na moyoni ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu na ni kutokana na huruma. Na vyovyote vile vitokavyo mkononi na ulimini ni kutoka kwa shetani”.”9 Al-Hakim amepokea kwa njia yake kutoka kwa Abu Hurayra amesema: “Mtume alitoka kwa ajili ya jeneza akiwa pamoja na Umar bin Al-Khattab, ndipo akasikia wanawake wakilia, Umar akawakataza. Mtume wa Mwenyezi Mungu akasema: “Ewe Umar waache, hakika jicho hutokwa na machozi, nafsi hupatwa na msiba na ahadi iko karibu”. Hadithi hii ni sahihi kwa sharti za mashekhe wawili.10 4. Mtume (s.a.w.w.) hakukataza kumlilia maiti: Miongoni mwa dalili dhahiri juu ya ruhusa ya kisheria ya kumlilia maiti ni kuwa Mtume (s.a.w.w.) hakukataza kumlilia maiti pindi alipomsikia Jabir na binti ya Umar wakimlilia Abu Jabir. Hivyo kitendo cha Mtukufu Mtume kusikia na kutomkataza Jabir ni dalili ya wazi kuwa kama ingekuwa kumlilia maiti ni jambo lililokatazwa na sheria ya kiislamu basi Mtume (s.a.w.w.) angelimkataza palepale. Na kwa kuwa hakumkataza basi tunajua kuwa ni jambo linaloruhusiwa kisheria. An-Nasai amepokea kwa njia yake kutoka kwa Jabir amesema: “Siku ya Uhud aliletwa baba yangu akiwa amefanyiwa vitendo vya kinyama, akawekwa mbele ya Mtume wa Mwenyezi Mungu huku kafunikwa nguo, basi nikataka kumfunua, ndipo jamaa zangu wakanikataza. Mtume akaa9 Tarikhul-Madinatul-Munawwarah Juz. 1, Uk. 103. 10 Bukhari na Muslim- Mtarjumi - Mustadrakul-Hakim 1: 381. Sunan An-Nasai 4:190. Kanzul-Ummal 15: 620. Musnad Ahmad 2: 333. Al-Muhla 5: 160. 33


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:14 PM

Page 34

Kumlilia Maiti muru anyanyuliwe akanyanyuliwa, aliponyanyuliwa ghafla akasikia sauti ya mliaji wa kike, akasema: “Ni nani huyo?” akaambiwa: “Huyu ni binti ya Umar au dada ya Umar.” Akasema: “Usilie, au kwa nini unalia ilihali malaika walikuwa bado wamemfunika kwa mbawa zao mpaka aliponyanyuliwa.”11 Pia imepokewa kutoka kwake kutoka kwa Jabir kuwa baba yake aliuwawa siku ya Uhud. Amesema: “Nikawa namfunua uso wake huku nikilia na watu wakinikataza, ilihali Mtume wa Mwenyezi Mungu hanikatazi. Na shangazi yangu akawa anamlilia, Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akasema: “Msimlilie malaika walikuwa bado wamemfunika na mbawa zao mpaka mlipomnyanyua.”12 Inaweza kusemwa kuwa: Hivi kukataza huku hakutoshi kuwa dalili ya kutokuruhusiwa kisheria kumlilia maiti? Tunasema: Kwanza, hakutoshi kwa sababu kwenye matukio haya mawili ni watu au jamaa wa Jabir ndio waliokuwa wakikataza kulia na si Mtume (s.a.w.w.), na inajulikana fika kuwa katazo la asiyekuwa Mtume halina athari yoyote katika sheria tukufu. Pili: Bila shaka katika riwaya ya pili imetamkwa wazi kuwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakuwa anamkataza kulia. Tatu: Hakika kauli hii “Usilie” kwa mfumo huu, ndani ya sheria haichukuliwi kuwa ni katazo la kuharamisha, kwa sababu lengo la Mtukufu Mtume aliposema: “Msimlilie malaika walikuwa bado wamemfunika na mbawa zao ...” ni kuwapunguzia wafiwa uchungu wa msiba, na kubainisha utukufu wa shahidi. Wala hakuwa analenga kukataza kulia. 11 Sunan An-Nasai 4: 13. Al-Maghaziy 1: 266. 12 Sunan An-Nasai 4: 13. Al-Maghaziy 1: 266. Shifaul-Gharam 2: 348 japo ni kwa tofauti kidogo. 34


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:14 PM

Page 35

Kumlilia Maiti 5. Kizazi toharifu chamlilia maiti: Miongoni mwa dalili juu ya ruhusa ya kisheria ya kumlilia maiti ni kile kitendo cha kizazi cha Mtume kitoharifu kumlilia maiti. Hapo baadaye utaona maeneo waliyomlilia Mtume, aali zake, mashahidi na watu wema. Wao walikuwa wakimlilia sana Husein muda wote wa maisha yao, bali walikuwa wakiwahimiza wengine kufanya hivyo. Pia walikuwa wakimlilia yule aliyewatoka miongoni mwa jamaa zao na wafuasi wao, hususan mashahidi miongoni mwao, kama Husein bin Ali alivyowalilia wanae wawili mashahidi, na watu wengine wa nyumba yake na sahaba zake. Na kama walivyowalilia baba zao baada ya kufariki kwao na pindi wanapoyazuru makaburi yao. Kama bibi Fatimah Az-Zahra alivyomlilia baba yake Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) baada ya kifo chake. Na kama alivyolia Imam Ali (a.s.) kuwalilia Muhammad bin Abu Bakr, Ammar, Hashim Al-Mirqal na wengineo, kama yalivyo hayo ndani ya riwaya. 6. Sahaba wamlilia maiti: Miongoni mwa dalili dhahiri juu ya ruhusa ya kisheria ya kumlilia maiti na kuwa si jambo la bidaa, ni kitendo cha sahaba kuwalilia wenzi wao zama za Mtukufu Mtume na baada yake pale tu mmoja wao anapowatoka. Hivyo ima tukadhibishe maelezo yote yaliyomo ndani ya vyanzo vya hadithi na historia, yanayohusu kitendo cha sahaba kuwalilia wenzi wao. Na ima tuwafokee kwa kitendo chao hicho kwa kuwa ni jambo lisiloruhusiwa kisheria. Au tukubali kuwa inaruhusiwa kisheria kumlilia maiti. Imam Ali (a.s.) alimlilia Ammar bin Yasir na sahaba nao wakamlilia Imam Ali. Aisha binti Abu Bakr akalia pindi alipopata habari za kuuwawa kwa Ali (a.s.). Sahaba wakamlilia Husein bin Ali, mfano wa hao ni Abu Hurayra, Said bin Al-‘Aas na Ibnu Abbas. Kama ambavyo Zayd bin Arqam, Ibnu Abbas, Anas bin Malik na wengineo walimlilia Husein (a.s.). 35


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 36

Kumlilia Maiti Ifuatayo ni mifano ya hilo. Ibnu Mas’ud amlilia Umar bin Al-Khattab: Al-Andalusiy amesema: “Alipozikwa Umar bin Al-Khattab alikuja Abdullah bin Mas’ud ikiwa Swala imempita. Akasimama juu ya kaburi lake huku akilia na akitupa joho lake, kisha akasema…..”13 a. Umar amlilia An-Nu’uman bin Muqrin: Ibnu Abu Shaybah amepokea kutoka kwa Abu Usamah, amesema: “Ametusimulia Sha’abah kutoka kwa Ali ibnu Zayd, kutoka kwa Abu Uthman, amesema: “Nilimletea Umar habari za kifo cha An-Nu’uman bin Muqrin, basi akaweka mikono yake juu ya kichwa chake na kuanza kulia”.”14 b. Abdullah bin Rawwah amlilia na kumwomboleza Hamza: Ibnu Hisham amesema: “Abdullah bin Rawwah alisema huku akimlilia Hamza bin Abdul Muttalib: “Jicho langu limelia na ni haki yake lilie, na wala kilio na kelele havitosaidia. Juu ya simba wa Mungu, kesho watasama: Hamza wenu ameuwawa. Waislamu wote wamepatwa na msiba huko, na bila shaka Mtume amepatwa na msiba.” Akaendelea mpaka mwisho wa beti zake”.15 13 Al-Aqdu Al-Faridah Juz. 3, uk. 195. 14 Al-Muswannaf 3: 175. 15 As-Siratu An-Nabawiyyah 3: 171. 36


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 37

Kumlilia Maiti Hasan bin Thabit amlilia na kumwomboleza Khubaybu bin ‘Adiy: Ndani ya As-Siratu An-Nabawiyyah: “Hasan bin Thabit alimlilia Khubayb huku akisema: “Lina nini jicho lako mbona halilowi kwa machozi yake, ili wingu litue kifuani kama lulu itembeayo. Ikimlilia kijana Khubaybu, vijana wametambua fika kuwa, hakuna kufeli wala kuruka pindi umkutapo.” Akaendelea mpaka mwisho wa beti zake.”16 Na pia Hasan akasema ikamwomboleza na kumlilia Khubaybu: “Ewe jicho langu fanya ukarimu kwa machozi toka kwako yenye kumwagika, mlilie Khubaybu pamoja na vijana……” Akaendelea mpaka mwisho wa beti zake.17 c. Hasan bin Thabit awalilia na kuwaomboleza wahanga wa kisima cha Ma’una: Ibnu Hisham amesema: “Hasan bin Thabit akawalilia wahanga wa kisima cha ma’una, na hasa akimlenga Al-Mundhir bin Amru akasema: ‘Kwa ajili ya wahanga wa ma’una bubujika, machozi ya jicho kwa wingi bila uchache. Kwa ajili ya ngamia wa Mtume wamepata kifo chao, na kadirio limewakuta.” 16 As-Siratu An-Nabawiyyah 3: 187. 17 As-Siratu An-Nabawiyyah 3: 187. 37


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 38

Kumlilia Maiti Akaendelea mpaka mwisho wa beti zake.”’18 Swafiyyah amlilia kaka yake Hamza: Swafiyyah shangazi wa Mtume alimlilia sana kaka yake Hamza bin Abdul Muttalib mpaka Mtume wa Mwenyezi Mungu naye akawa analia aliapo na kuhuzunika ahuzunikapo.19 Ibnu Is’haqa amesema: “Swafiyyah binti Abdul Muttalib alimlilia kaka yake Hamza bin Abdul Muttalib akasema: ‘Nimewaulizia watu wa Uhud nikihofia mabinti wa baba, yule asiye fasaha na aliye fasaha. ‘Yule aliye fasaha akasema: Hakika Hamza ameshakufa. Waziri wa Mtume wa Mwenyezi Mungu tena waziri aliye bora. ‘Mungu wa haki mwenye arshi kuu amemwita, wito wa kwenda peponi aishi humo kwa furaha. ‘Hilo ndilo tulilokuwa tukitumainishwa na tukilitaraji, Hamza siku ya mkusanyo kuwa na mafikio mazuri. ‘Wallahi sikusahau kila asubuhi ichomozapo, kwa kilio na huzuni, nyumbani na safarini.” Akaendelea mpaka mwisho wa beti zake”’.20 d. Kanuni ya ubora yaruhusu kisheria kumlilia maiti: Miongoni mwa dalili juu ya ruhusa ya kisheria ya kumlilia maiti ni ile 18 As-Siratu An-Nabawiyyah 3: 198. Ar-Rawdhu Al-Anfu 6: 182. 19 Al-Fusulul-Muhimmah: 92. Al-Mughaziy 1: 290. 20 As-Siratu An-Nabawiyyah 3: 176. 38


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 39

Kumlilia Maiti kanuni ya ubora. Nayo ni kuwa pindi sheria iliporuhusu kuwalilia wale walio hai kwa sababu yoyote ile, kama vile kwa kutengana nao, au kuwa mbali nao kwa muda mfupi, basi ni bora na vizuri zaidi iwe kuwalilia maiti ni halali kwa sababu ileile ya kutengana nao. Ikiwa kilio cha bwana wetu Ya’aqub kumlilia mwanawe Yusuf kilikuwa kwa sababu ya kutengana naye, huku akijua fika kuwa Yusuf bado yu hai, lakini alimlilia mpaka macho yake yakapofuka kutokana na huzuni, na akasema: “Hakika mimi namshitakia Mwenyezi Mungu sikitiko langu na huzuni yangu,” Mwenyezi Mungu hakupinga kitendo hiki bali alikisimulia kwa Mtume wake na kwa umma wa Mtume wake ndani ya Qur’an Tukufu akasema: “Naye akajitenga nao, na akasema: Ah! Masikini Yusuf! Na macho yake yakawa meupe kwa huzuni aliyokuwa akiizuia. Wakasema: “Wallahi! Huachi kumkumbuka Yusuf mpaka uwe mgonjwa au uwe miongoni mwa walio hiliki.” Akasema: “Hakika mimi namshitakia Mwenyezi Mungu sikitiko langu na huzuni yangu. Na ninajua kwa Mwenyezi Mungu msiyoyajua nyinyi.” (Sura Yusuf: 86.) Basi ni kwa nini tuzuie kulia pindi tuwapotezapo wapendwa wetu miongoni mwa wake, watoto na wengineo. Ilihali yeye alilia kwa kutengana, na bado kipimo hicho hapa pia kipo?!!! Hilo tunalolisema linaungwa mkono na yale aliyosema Umar pindi aliposimama juu ya mwili wa Mtume (s.a.w.w.) huku akilia na kusema: “Baba yangu na mama yangu ni fidia kwako, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ulikuwa na kisiki ambacho ulihutubia watu ukiwa juu yake, walipoongezeka ulikifanya mimbari, mlio wa kisiki unawafikia kwa kutengana na wewe…..bila shaka umma wako ndio unaowajibika zaidi kukulilia pindi ulipotengana nao…”21 21 Swidqul-Khabar: 238. 39


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 40

Kumlilia Maiti Pia linaungwa mkono na yale aliyopokea Ibnu Asakir kwa njia yake kutoka kwa Muhammad bin Ya’aqub bin Siwar, kutoka kwa Ja’far bin Muhammad, amesema: “Ali bin Husein bin Ali bin Abu Talib aliulizwa kuhusu kupindukia kwake katika kulia. Akasema: “Msinilaumu, kwani hakika Ya’aqub alimpoteza mtoto kati ya wanawe akalia mpaka macho yake yakapofuka huku akiwa hajui fika kama ameshafariki. Ilihali mimi niliwaona kwa macho yangu watu kumi na nne kati ya watu wa nyumba yangu wakichinjwa ndani ya siku moja. Hivi mnadhani huzuni yangu kwao kamwe itaondoka moyoni mwangu.”22

SURA YA PILI UTATA ULIYOPO KUHUSU KILIO Kuna utata ulioletwa kuhusu kumlilia maiti. Miongoni mwa utata huo ni: e. Hakika maiti huadhibiwa kwa kitendo cha jamaa zake kumlilia: Imepokewa kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) kuwa alisema: “Hakika maiti huadhibiwa kwa kule kuliliwa na aliye hai.” Riwaya hii inatuongoza kwamba kumlilia maiti ni jambo lililokatazwa na ni haramu kwa mujibu wa sheria ya Uislamu. Tunajibu kuwa: Kwanza: Hadithi hii na mfano wake hata kama imenukuliwa ndani ya sahihi sita na vitabu vinginevyo, lakini ni habari inayopingwa na Hadithi 22 Tarikhu Damashqi: 56. 40


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 41

Kumlilia Maiti mfano wake. Hebu na tujaalie kuwa Hadithi hii ni sahihi imetoka kwa Mtume, basi alipokuwa kwenye maiti ya yahudi na akasikia wakimlilia alisema: “Ninyi mnamlilia na yeye bila shaka anaadhibiwa.” Hadithi hii Muslim ameipokea ndani ya Sahih yake kwa njia yake kutoka kwa Aisha kama ifuatavyo: Kutoka kwa Hisham bin ‘Ur’wa, kutoka kwa baba yake, amesema: “Ilitajwa mbele ya Aisha kauli ya Ibnu Umar kuwa maiti huadhibiwa kwa kule kuliliwa na jamaa zake. Akasema: ‘Mwenyezi Mungu amrehemu baba Abdu Rahman, amesikia kitu lakini hajakihifadhi. Hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu alipita kwenye jeneza la yahudi huku wao wakimlilia ndipo akasema: “Ninyi mnamlilia na bila shaka yeye anaadhibiwa.’’23 Hakuna shaka kuwa kauli hii ya Mtume (s.a.w.w.) ni kuwazindua kuwa yahudi huyu ni mwenye hasara na ni miongoni mwa watu wa motoni, na anaadhibiwa kaburini mwake kwa sababu ya matendo yake na kupinga kwake unabii wa hitimisho la manabii. Kuna uhusiano gani kati ya hili na lile la muumini kuadhibiwa kwa sababu ya kuliliwa na jamaa zake? Na katika riwaya nyingine pia kutoka kwa Aisha, aliposikia kauli ya Ibnu Umar “Maiti huadhibiwa kwa kule kuliliwa na jamaa zake.” Akasema: “Ni hivyo?!!! Bali Mtume wa Mwenyezi Mungu alisema: Huadhibiwa kwa makosa yake au dhambi yake….”24 Aisha ashangazwa na kauli ya Ibnu Umar: Aisha alishangazwa na kauli ya Ibnu Umar pindi aliposikia usemi wa Ibnu Umar, akaikanusha na kumshutumu kuwa amesahau na kushindwa kuhifadhi, akasema: “Amesikia kitu lakini hajakihifadhi.” 23 Sahih Muslim Juz. 3, uk. 44. 24 Sahih Muslim 3: 44. 41


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 42

Kumlilia Maiti Vyovyote vile iwavyo ni kuwa usemi wa Ibnu Umar umepingwa na Aisha mama wa waumini. Na pia akamshutumu Umar bin Al-Khattab, na akaapa kwa Mwenyezi Mungu kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) hakusema hilo, pindi aliposikia usemi huo toka kwa Ibnu Abbas. Amesema: “Suhaybu aliingia huku akilia na kusema: “Ee kaka yangu, ee rafiki yangu.” Umar akasema: “Ewe Suhaybu unanililia ilihali Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema: “Hakika maiti huadhibiwa kwa kule kuliliwa na jamaa zake?” Ibnu Abbas amesema: “Umar alipofariki na Aisha akatajiwa hilo, alisema: “Mwenyezi Mungu amrehemu Umar, hapana, wallahi Mtume wa Mwenyezi Mungu hakusimulia kuwa muumini huadhibiwa kwa kule kuliliwa na mtu. Lakini alisema: “Hakika Mwenyezi Mungu humzidishia kafiri adhabu kwa kule kuliliwa na jamaa zake.”25 Hivyo, kwanza si vibaya kukubali kuwa maiti kafiri huadhibiwa kaburini kwa kule kuliliwa na aliye hai. Ama muumini, kwa nini tuseme hivyo juu yake, ilihali Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitamka waziwazi kuwa Mwenyezi Mungu humzidishia kafiri adhabu kwa kule kuliliwa na jamaa zake? Pili: Hadithi hizi hata tukisema kuwa zinatoka kwa Mtume lakini hazioani na dhahiri ya aya za Qur’an ambazo miongoni mwazo ni: “Na mbebaji hatabeba mzigo wa mwingine..” (Sura Fatir:18). Ni jambo la kushangaza kuona Mwenyezi Mungu ndani ya Kitabu chake akisema: “Na mbebaji habebi mzigo wa mwingine..,” kisha maiti anaadhibiwa kwa kule tu kuliliwa na familia yake au jamaa wengine. Kwa ajili hiyo ndio sababu tunamwona Aisha akikanusha dai hilo, na akawa ametumia Aya hii kutoa ushahidi wa kumjibu yule asemaye: “Hakika maiti huadhibiwa kwa kule kuliliwa na jamaa zake.” Akasema: “Qur’an yawatosha “Na mbebaji hatabeba mzigo wa mwingine..”26 25 Sahih Muslim 3: 44. 26 Sahih Muslim 3: 43. 42


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 43

Kumlilia Maiti Tatu: Riwaya hizi ni zenye kupingana na kutenzana, hivyo iwapo tutajaalia kuwa njia za upokezi wa riwaya zote hizi ni sahihi, basi kwa mujibu wa kanuni inapasa kuzitupilia mbali, na hatimaye kurejea kwenye msingi wa asili,27 nao ni halali na si haramu kumlilia maiti. Nne: Huenda ila iliyopelekea Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kukataza kuwalilia maiti ni yale maombolezo batili, kukata tamaa na kufadhaika kunakovuka mipaka. Pia matendo mengine yaliyokatazwa kama vile kuujeruhi uso kwa ajili ya maiti. Tunajibu kuwa: Hata dhana hii pia nayo haikubaliki, kwa sababu Aya imetamka wazi kuwa maiti habebi mzigo wa mwingine, hivyo itawezekana vipi maiti abebe mzigo wa waombolezaji na wasemaji wa maneno batili, na kwa nini asibebe mzigo wake mwenyewe? Tano: Hebu tujaalie kuwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikataza kumlilia maiti kwa sauti ya juu, dhana ambayo Mashafi’i na Mahambali wameipinga wakasema: “Ni halali,”28 basi ni kwa nini hairuhusiwi kumlilia maiti kwa sauti ya chini na kwa machozi yenye kutiririka kwa kumkosa. Sita: Riwaya zote hizi zinakinzana na kitendo cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alichokifanya sehemu nyingi. Alimlilia mwanae wa kiume, binti yake na mkewe mpendwa. Pia akamlilia Fatimah binti Asad, An-Najashi 27 Msingi huu wa asili ambao ni maarufu kwa wanataaluma wa fani ya Usululfiqhi unasema: “Kila kitu ni halali hadi pale itakapothibiti kisheria kuharamishwa kwake kisheria”, hivyo kwa kuwa dai hili la uharamu wa kumlilia maiti halina dalili ya kisheria inayothibitisha hali hiyo, basi uhalali wa kumlilia maiti unaendelea kuwepo kwani wenyewe ndio asili kwa mujibu wa msingi husika. Kwa ufafanuzi zaidi rejea vitabu vya fani husika.– Mtarjumi28 Al-Fiqhi ala Madhahibil-Arba’ah 1: 533 43


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 44

Kumlilia Maiti na wengineo miongoni mwa sahaba wema kama utakavyoona hapo baadaye. Hivyo itakuwa ni ajabu sana kwa Mtume (s.a.w.w.) akataze kwa ulimi wake kisha jicho lake lilie na moyo wake uhuzunike. Tunachokigundua kutokana na kauli ya Ibnu Abbas ni kuwa, maiti haadhibiwi kwa kule kuliliwa na aliye hai,29 Hadithi hii ni miongoni mwa Hadithi zilizogeuzwa. Tunamshangaa yule aliyeharamisha kumlilia maiti iwapo ni kwa sauti ya juu. Pia yule aliyeitafsiri kauli “Maiti huadhibiwa kwa kule kuliliwa na aliye hai.” kuwa ni kulia kwa kuomboleza, akasema: “Inatafsiriwa kuwa ni kulia kwa kuomboleza, hiyo ni ili kuoanisha kati ya riwaya” huku akitegemea kauli ya An-Nawawi aliposema: “Hadithi hii inatafsiriwa kuwa ni maiti kuusia kuliliwa kwa kuomboleza.”30 Hebu tuwaulize hawa wanakusudia nini wanaposema kuomboleza? Ikiwa makusudio yao ni maneno yamchukizayo Allah yatokayo kwa aliyepatwa na msiba, basi hilo ni haramu na wala hakuna mjadala katika hilo. Ama ikiwa makusudio ya kuomboleza ni kulia kwa sauti ya juu tu hata kama mtu hatamki maneno yamchukizayo Allah, basi hakuna dalili yoyote inayothibitisha uharamu wa aina hii ya kilio. Ikiwa kulia kwa sauti ni jambo lililoharamishwa basi ni kwa nini Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimlilia Hamza kwa sauti ya juu mpaka akazidiwa na kilio?31 Na kwa nini wakazi wa Madina na sahaba kwa ujumla walipiga mayowe kama mayowe ya mahujaji kwa kutokwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu 29 Kanzul-Ummal 15: 728. 30 Tazama maelezo ya Sahih Muslim 3: 41. Al-Fiqhi a’la Madhahibil-Arba’ah 1: 533. Fatawal-Imam An-Nawawiy: 58. 31 Dhakhairul-U’qba: 180. 44


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 45

Kumlilia Maiti siku aliyofariki?32 Kwa nini jiji la Madina lilienea siahi siku aliyofariki Hasan bin Ali (a.s.)?33 Na kwa nini wanawake wa kibani Hashimu waliweka maombolezo mwezi mzima wakimlilia Hasan (a.s.)?34 Na kwa nini Husein alimlilia mdogo wake Abbas kilio kikubwa? Na kwa nini Aisha alimlilia na kumfanyia maombolezo baba yake?35 Matokeo ni kuwa kulia kwa sauti na kwa kuomboleza iwapo hakuambatani na maneno yamchukizayo Allah ni jambo lisilo na mushkeli na linaruhusiwa kisheria. Hakika Umar bin Al-Khattab alikataza kulia: Wakati mwingine kutoruhusiwa kumlilia maiti hutegemea kauli isemayo kuwa, Umar ibnu Al-Khattab alikataza kufanya hivyo, hivyo lau lisingekuwa ni jambo lililokatazwa basi Umar asingelikataza. Tunajibu kuwa: Kwanza ukatazaji huu haujathibiti, hilo ni hata kama umepokewa na waandishi wa sahih sita na wengineo, na kwa sababu hiyo ndio maana Abdullah bin Akramah alikuwa akistaajabishwa na kitendo cha kumnasibisha Umar na ukatazaji wa kumlilia maiti. Na alikuwa akisema: “Nastaajabishwa na kauli ya watu kuwa: “Umar bin Al-Khattab alikataza kuomboleza!!” Wakati bila shaka alimlilia Khalid bin Walid huko Makka, na wanawake saba wa Bani Mughira wakamlilia huko Madina huku wakichana nguo na wakijipiga nyuso. Na walilisha chakula ndani ya siku hizo mpaka zikapita bila Umar kuwakataza”.36 32 Kanzul-Ummal 7: 265. 33 Tarikhu Damashqi (Imam Hasan): 222. 34 Al-Mustadrak Alas-Sahihayn 3: 173. 35 Tarikhut-Tabariy 2: 349. 36 Kanzul-Ummal 15: 731. 45


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 46

Kumlilia Maiti Pili: Itakuwaje katazo hilo liwe limetoka kwa Umar ilihali bila shaka alimlilia An-Nuuman bin Muqrin37 na Zayd bin Al-Khattab?38 Tatu: Itakuwaje katazo hilo liwe limetoka kwa Umar ilihali bila shaka aliamuru kumlilia Khalid bin Walid? Ibnu Abu Shaybah na Ibnu Rabah AlAndalusiy wamepokea kuwa, na hapa tunanukuu tamko la wa pili: “Alipofariki Khalid bin Walid zama za Umar bin Al-Khattab wanawake walijizuia kumlilia, basi zilipomfikia habari hizo Umar alisema: “Si vibaya kwa wanawake wa bani Mughira kujing’arisha kwa machozi yao juu ya baba Salman ilimradi tu isiwe kwa kuinua sauti wala kuiremba.”39 Nne: Lau ikithibiti kuwa Umar alikataza kumlilia maiti, basi hilo linatenguliwa na kauli ya Aisha alipopinga na kukanusha, akisema Mtukufu Mtume hakusema wala kusimulia hilo.40 Ibnu Hazmi amesema: “Bila shaka tumepokea kutoka kwa Ibnu Abbas kuwa alimkanusha yule aliyekanusha kumlilia maiti akasema: “Mwenyezi Mungu ndiye achekeshaye na alizaye.”41

37 Al-Muswannaf 3: 244. 38 Al-Iqdu Al-Farid 3: 191. 39 Al-Iqdu Al-Farid 3: 193. Al-Muswannaf 3: 175. Kanzul-Ummal 15: 730. 40 Sahih Muslim 3: 43. 41 Al-Muhla 5: 148. 46


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 47

Kumlilia Maiti

SURA YA TATU FADHILA ZA KUWALILIA A’ALI RASULI Zimepatikana riwaya nyingi zikibainisha fadhila za kuwalilia aali Rasuli na kizazi kitoharifu, ikiwa ni nyongeza ya zile zinazozungumzia fadhila za kumlilia Husein bin Ali (a.s.). Na kuwa mwenye kulia na kuomboleza msiba wao ameandaliwa pepo, na siku ya Kiyama atasalimika na ghadhabu ya Mwenyezi Mungu, moto na mengineyo. Al-Qunduz Al-Hanafiy amepokea kutoka kwa Al-Baqir (a.s.) kuwa amesema: “Baba yangu Ali bin Husein (a.s.) alikuwa akisema: “Muumini yeyote ambaye kwa ajili ya kuuawa kwa Husein na waliokuwa naye, macho yake yatatoa machozi mpaka yakachururuzika juu ya mashavu yake, basi Mwenyezi Mungu atamwandalia kinywaji cha maziwa peponi. Na muumini yeyote ambaye kwa ajili ya adha tuliyoipata toka kwa maadui zetu, macho yake yatatoa machozi mpaka yakachururuzika juu ya mashavu yake, basi Mwenyezi Mungu atamwandalia maandalizi bora. Na muumini yeyote ambaye amepatwa na adha kwa ajili yetu, macho yake yakatoa machozi mpaka yakachururuzika juu ya mashavu yake kutokana na uchungu wa adha iliyompata kwa ajili yetu, basi Mwenyezi Mungu atamwondolea adha na kumsalimisha na ghadhabu ya moto siku ya Kiyama”.42 Pia amepokea kutoka kwa As-Sadiq (a.s.) kuwa amesema: “Atakayetutaja au tukatajwa mbele yake kisha machozi yakamtoka mfano wa bawa la mbu, basi Mwenyezi Mungu atamsamehe madhambi yake hata kama yatakuwa mfano wa mgando wa bahari.”43 42 Yanabiul-Mawaddah: 429. 43 Yanabiul-Mawaddah: 429. 47


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 48

Kumlilia Maiti Kutokana na riwaya zote hizi na kile kitendo cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kukililia kizazi kitoharifu, Ali, Husein na wanawe wengine, na kutokana na kitendo cha kuhimiza kwake kumlilia Hamza na Ja’far, hususan aliposema: “Juu ya mtu mfano wa Ja’far wamlilie wenye kulia”, tunapata kuwa kuwalilia ali Rasuli ni jambo bora na ni sunna. Na ni juu ya kila mwislamu kudhihirisha mapenzi juu ya makaburi yao au wanapotajwa, kwa kuwalilia na kusikitika kwa yale yaliyowapata, kwani wao si chini ya Hamza na Ja’far katika ubora.

SURA YA NNE MAENEO ALIYOLILIWA MTUME, AALI ZAKE, MASHAHIDI NA WATU WEMA Mtume (s.a.w.w.) alia: Bila shaka Mtukufu Mtume aliwalilia wanawe, aali zake na kizazi chake kitukufu zama za uhai wao na baada ya kifo chao. Bali alimlilia pia mkewe mpendwa mwaminifu Khadija binti Khuwaylid alipotajwa mbele yake. Na hivyo hivyo ndivyo alivyomlilia mama yake na mama wa Ali bin Abu Talib (a.s.), ami zake na wengineo. Ama kilio alichokuwa akiwalilia aali zake zama za uhai wao ni kwa ajili ya dhulma watakayofanyiwa baada yake, adha na uvunjiwaji wa heshima utakaowapata. Kama yatakavyokufikia hayo yote katika sura hii. 1. Mtukufu Mtume awalilia aali zake baada yake: Al-Hafidh Abu Bakr ibnu Abu Shaybah ameandika kutoka kwa Muawiya bin Hisham, kutoka kwa Ali bin Salih, kutoka kwa Yazid bin Abu Ziyad, kutoka kwa Ibrahim, kutoka kwa Alqamah, kutoka kwa Abdullah bin 48


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 49

Kumlilia Maiti Mas’ud amesema: “Tulipokuwa kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) ghafla lilijitokeza kundi la Bani Hashim, basi alipowatazama macho yake yalilengalenga machozi na rangi yake ikabadilika.” Amesema: “Nikamwambia: Bado tunaona usoni mwako kitu ukichukiacho.” Akasema (s.a.w.w.): “Hakika sisi Ahlul-Baiti Mwenyezi Mungu ametuchagulia akhera kuliko dunia, na hakika watu wa nyumba yangu watakumbwa na mtihani, watatawanywa na kufukuzwa….”44 Na pia ameipokea Al-Hakim An-Nisabur na Ad-Dhahabiy, isipokuwa wao wawili wameongeza: “Na miongoni mwao ni Hasan na Husein.”45 2. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amlilia Ali bin Abu Talib (a.s.): Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mara nyingi alilizwa na yale yatakayomsibu Ali (a.s.) baada yake, na kuna kipindi alilia kwa sauti ya juu kabisa. Al-Khawarizmiy amepokea kwa njia yake kutoka kwa Abdu Rahman bin Abu Layla, amesema: “Baba yangu aliniambia: “Mtume alikabidhi bendera kwa Ali bin Abu Talib siku ya Khaybar, Mwenyezi Mungu akashinda mikononi mwake. Akamsimamisha siku ya bonde la Khum, akawatambulisha watu kuwa yeye (a.s.) ni mtawala wa kila aliye muumini, wa kiume na wa kike, na akamwambia: “Wewe watokana na mimi, nami natokana na wewe.” Akamwambia tena: “Utapigania tafsiri kama nilivyopigania ufunuo”. Akamwambia: “Wewe kwangu mimi una nafasi ya Harun kwa Musa.” Akamwambia tena: “……” kisha (s.a.w.w.) akalia. Akaulizwa: “Ni kipi kikulizacho ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?” akasema: “Jibril amenipa habari kuwa wao watamdhulumu na kumzuilia haki yake, watamuuwa na kukiuwa kizazi chake na watawadhulumu baada yake.” 46 Al-Khawarazamiy amepokea tena kwa njia yake kutoka kwa Abu Uthman An-Nahdiy, kutoka kwa Ali bin Abu Talib (a.s.) amesema: “Nilikuwa 44 Al-Muswannaf 7: 697. Al-Fusul Al-Muhimmah: 155. 45 Al-Mustadrak Alas-Sahihayn 4: 464. 46 Manaqib Al-Khawarazimiy: 24. 49


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 50

Kumlilia Maiti nikitembea na Mtume kwenye baadhi ya njia za Madina, ghafla tukafika kwenye bustani, nikamwambia: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Uzuri ulioje wa bustani hii!!” akasema: “Ni nzuri mno, nawe peponi unayo nzuri kuliko hiyo.” Kisha tukaja kwenye bustani nyingine, nikasema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Uzuri ulioje wa bustani hii!!” akasema: “Nawe peponi unayo nzuri kuliko hiyo.” Mpaka tukazifikia bustani saba, kwenye kila bustani nikisema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Uzuri ulioje wa bustani hii!!” anasema: “Nawe peponi unayo nzuri kuliko hiyo.” basi njia ilipobaki faragha alinikumbatia na kuanza kulia, nikasema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu kipi kikulizacho?” akasema: “Chuki binafsi zilizomo ndani ya vifua vya watu, hawatozidhihirisha kwako ila baada yangu.” Nikasema: “Nitakuwa salama katika dini yangu?” akasema: “Utakuwa salama katika dini yako.”47 3. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amlilia Husein (a.s.): Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimlilia Husein (a.s.) huko Madina, mara nyingi na sehemu mbalimbali, hususan baada ya kuwa tu Imam Husein (a.s.) kazaliwa. Waandishi wa vitabu vya sunna na wengineo wamepokea hilo ndani ya vitabu vyao, kama vile At-Tabaraniy, Al-Haythamiy, AlKhawarazamiy, An-Nisaburiy, Ahmad, Abu Nua’im, Ibnu Asakir, Ibnu Hajar, Abdur-Razaq, Abu Ali na wengineo. Nasi hapa tutataja baadhi tu ya sehemu hizo. Al-Muhibbu At-Tabariy amepokea kwa njia yake kutoka kwa Asmaa binti Umaysi kuwa amesema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu alimfanyia akiki Hasan siku ya saba, kwa kumchinjia kondoo wawili…….Baada ya mwaka akazaliwa Husein, Mtume (s.a.w.w.) akaja akamfanyia kama awali”. Asmaa anasema: “Akamweka mapajani mwake kisha (s.a.w.w.) akalia. Nikasema: “Baba yangu na mama yangu ni fidia kwako, ni kipi kikuliza47 Manaqib Al-Khawarazimiy: 26. Tadhkiratul-Khuwas: 45. 50


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 51

Kumlilia Maiti cho?” Akasema: “Mwanangu huyu ewe Asmaa! Kwani hakika yeye atauliwa na kundi asi toka katika umma wangu, Mwenyezi Mungu hatowapa shufaa yangu. Ewe Asmaa! Usimpe habari hizi Fatimah, kwani hakika yeye ni punde tu katoka kujifungua.”48 Ummul-Fadhli binti Abbas amepokea kuwa yeye aliingia kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu akasema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Usiku nimeota ndoto ichukizayo,” akasema: “Ni ipi hiyo?” Nikasema: “Nimeona kipande cha mwili wako kimekatwa na kuwekwa kwenye mapaja yangu.” Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akasema: “Umeona kheri, Fatimah atajifungua mwana wa kiume na atampakatisha mapajani mwako.” Ndipo Fatimah akajifungua Husein. Amesema: “Basi nikampakata kama alivyosema Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w), nikaingia naye kwake na kumweka mapajani mwake, kisha nikageuka kidogo, ghafla nikakuta macho ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) yakitoa machozi. Nikasema: “Baba yangu na mama yangu ni fidia kwako, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu ni kipi kikulizacho?” Akasema: “Jibril amenijia na kunipa habari kuwa umma wangu utamuuwa mwanangu huyu. Ameniletea sehemu ya udongo wake huku ukiwa mwekundu”’49 Na ameipokea Al-Hakim ndani ya kitabu chake Al-Mustadrak, na amesema: “Hadithi hii ni sahihi kwa mujibu wa sharti za mashekhe wawili50 japo hawajaiandika.”51 At-Tabaraniy amepokea kwa njia yake kutoka kwa Urwah kutoka kwa Aisha, amesema: “Husein bin Ali (a.s.) aliingia kwa Mtume wa Mwenyezi 48 Dhakhairul-Uqba: 119. Mustadarakul-Hakim 3: 176. Tarikhul-Khamis 1: 418. Yanabiul-Mawaddah: 220. Wasilatul-Maal: 183. 49 Al-Fusulul-Muhimmah: 154. Maqtalul-Husayn 1: 163. 50 Bukhari na Muslim - Mtarjumi. 51 Al-Mustadrak Alas-Sahihayn 3: 176. 51


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 52

Kumlilia Maiti Mungu (s.a.w.w.) ilihali (s.a.w.w.) akishushiwa wahyi, akapanda mgongoni kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu huku (s.a.w.w.) akiwa ameinama, na akacheza juu ya mgongo wake. Jibril akamwambia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.): “Ewe Muhammad! Je unampenda?” akasema: “Ewe Jibril! Kwa nini nisimpende mwanangu.” Akasema: “Hakika umma wako utamuuwa baada yako.” Hapo Jibril akanyoosha mkono wake na kumpa udongo mweupe na akamwambia: “Mwanao atauwawa katika udongo huu ewe Muhammad, na jina lake ni Tufi.” Jibril alipoondoka toka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alitoka akiwa na udongo mkononi mwake huku akilia, akasema: “Ewe Aisha! Hakika Jibril amenipa habari kuwa Husein mwanangu atauawa kwenye ardhi ya Tufi, na kuwa umma wangu utazua fitina baada yangu.” Kisha akawatokea sahaba zake akiwemo Ali, Abu Bakr, Umar, Hudhayfa, Ammar na Abu Dhar, akiwa analia. Wakamwambia: “Ni kipi kikulizacho ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?” Akasema: “Jibril amenipa habari kuwa mwanangu Husein atauwawa baada yangu huko katika ardhi ya Tufi. Na ameniletea udongo huu, na Jibril amenipa habari kuwa na hapo ndipo lilipo kaburi lake.”52 At-Tabaraniy amepokea tena kwa njia yake kutoka kwa Ummu Salamah kuwa amesema: “Siku moja Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alikuwa amekaa nyumbani kwangu, akasema: “Asiingie yeyote kwangu.” Basi nikangojea na ghafla akaingia Husein (a.s.), ndipo nikasikia sauti ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akilia. Nilipochungulia nikamwona Husein akiwa mapajani mwake huku Mtume akimfuta paji lake ilihali yeye (s.a.w.w.) akilia. Nikasema: “Wallahi sikujua alipoingia.” Akasema: “Jibril alikuwa pamoja nasi nyumbani akasema: “Unampenda?” Nikasema: “Ndio”, akasema: “Hakika umma wako utamuuwa huyu huko 52 Al-Mu’ujam Al-Kabir 3: 107. Al-Amaaliy: 165. Majmauz-Zawaid 9: 187. Maqtalul-Husayn 1: 159. Kanzul-Ummal 13: 111. As-Sawaiqul-Muhriqah: 190. Rawdhul-Azhar: 104. Al-Kawakibud-Duriyyah 1: 56. Yanabiul-Mawaddah: 318. Al-Fathul-Kabir 1: 55. Japo kuna tofauti kidogo. 52


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 53

Kumlilia Maiti katika ardhi inayoitwa Karbala.” Jibril akachukua udongo wake na kumwonyesha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Alipozingirwa Husein pindi alipouawa, alisema: “Ardhi hii yaitwaje?” Wakamjibu: “Karbala”. Akasema: “Amesema kweli Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, ni ardhi ya matatizo na balaa ‘Karbala’.53 Wapokezi waaminifu wamepokea mengi kutoka kwa Ummu Salamah kuhusu Mtume kumlilia mwanae Husein, wamepokea kwa njia nyingine huku kukiwa na tofauti kwenye matamshi.54 4. Mtukufu Mtume awalilia mashahidi wa Fukhu: Ndani ya kitabu Maqatilut-Twalibin amepokea kwa njia yake kutoka kwa Muhammad bin Is’haqa, kutoka kwa Abu Ja’far Muhammad bin Ali (a.s.), amesema: “Mtume (s.a.w.w.) alipita Fukhu akateremka na kusali rakaa ya kwanza, aliposali ya pili alilia huku akiwa ndani ya sala. Watu walipomwona Mtukufu Mtume akilia nao walilia, alipoondoka akawauliza: “Kitu gani kilichowaliza?” Wakajibu: “Tulipokuona unalia nasi tukalia ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu.” Akasema: “Jibril alinishukia niliposali rakaa ya kwanza na kuniambia: “Ewe Muhammad! Hakika mtu kutoka katika kizazi chako atauwawa sehemu hii, na malipo ya shahidi atakayekufa pamoja naye ni sawa na malipo ya mashahidi wawili.”55 53 Rejea Al-Mu’ujam Al-Kabir 3: 106 na 108 na 109. Al-Mustadrak AlasSahihayn 4: 398. Tarikhur-Riqqah: 75. Nadhmuduraris-Samtwayn: 215. AlGhanihi Litwalibi Twariqil-Haqi 2:56. Maqtalul-Husayn 1: 158. An-Nihayah 2: 212. Lisanul-Arab 11: 349. Maswabihus-Sunnah: 207. Kifayatut-Twalib: 286. Dhakhairul-Uqba: 148. Tarikhul-Islam 2:350. Siratu A’alamun-Nubalai 3:213. AlBidayatu Wan-Nihayah 8: 200. As-Sawaiqul-Muhriqah: 191. Tarikhul-Khulafai: 10. Al-Khasaisul-Kubra 2: 126. Yanabiul-Mawaddah: 320. At-Taju Al-Jamiu 3: 318. Dhakhairul-Mawarith 4: 300. Tarikhul-Khamis 2: 300. Al-Kamil 3: 303. 54 Al-Mu’ujam Al-Kabir 3: 107. Majmauz-Zawaid 9: 189. Kanzul-Ummal 6: 223. 55 Maqatilut-Twalibin: 436 53


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 54

Kumlilia Maiti 5. Mtukufu Mtume amlilia mwanae Ibrahim: Kutoka kwa Jabir bin Abdullah amesema: “Mtume (s.a.w.w.) aliushika mkono wa Abdur-Rahman bin Awf akaenda naye kwenye mitende. Akamkuta mwanae akiwa mapajani mwa mama yake huku akiwa kajisalimisha kwenye mauti, Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akamchukua na kumweka mapajani mwake, kisha akasema: “Ewe Ibrahim! Hakika sisi hatukunufaishi chochote kutoka kwa Mwenyezi Mungu.” Kisha macho yake yakabubujika machozi, akasema: “Ewe Ibrahim, lau isingekuwa kifo ni haki, ahadi ni kweli na wa mwisho wetu atakutana na wa mwanzo wetu, bila shaka tungehuzunika juu yako huzuni kali zaidi ya hii. Na bila shaka sisi ni wenye huzuni kwa ajili yako ewe Ibrahim. Jicho linalia, moyo wahuzunika na wala hatusemi yamchukizayo Mola Mlezi.”’56 Ibnu Abdu Rabbah amesema: “Wamesema: “Alipotawafu Ibrahim bin Muhammad (s.a.w.w.) alimlilia sana, akaulizwa kunako hilo, akasema: “Macho yatoa machozi, moyo wahuzunika na wala hatusemi yamchukizayo Mola Mlezi.”57 6. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amlilia binti yake Ummu Kulthum: Al-Muhibbu At-Tabariy amepokea habari zinazohusu kifo cha bibi Ummu Kulthum binti wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w), kutoka kwa Anas kuwa amesema: “Tulimshuhudia binti ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) huku Mtume wa Mwenyezi Mungu akiwa amekaa juu ya kaburi, ghafla tukaona macho yake yakitoa machozi….”58

56 Dhakhairul-Uqba: 155. Al-Bukhari 2: 179. Siratu Ibnu Is’haqa: 270. 57 Al-Aqdu Al-Farid 3: 190. 58 Dhakhairul-Uqba: 166. Al-Muhli 5: 145.

54


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 55

Kumlilia Maiti 7. Mtume (s.a.w.w.) amlilia babu yake Abdul Muttalib: Ibnu Al-Jawziy amenukuu kutoka kwenye At-Tabaqat kutoka kwa kundi la ulamaa akiwemo Ibnu Abbas, Mujahid, Atwau Az-Zahri na wengineo kuwa: “Abdul Muttalib alifariki mwaka wa pili huku Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akiwa na umri wa miaka minane, na tayari Abdul Muttalib alikuwa keshafikia umri wa miaka mia moja na ishirini, na akawa amezikwa huko Hujuni. Ummu Ayman amesema: ‘Mimi nilimwona Mtume wa Mwenyezi Mungu akitembea chini ya kitanda chake huku akilia.”59 8. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amlilia Abu Talib: Ibnu Sa’ad ameandika ndani ya kitabu chake At-Twabaqat, kutoka kwa Ubaydullah bin Abu Rafiu, kutoka kwa Ali kuwa amesema: “Nilimpa Mtume wa Mwenyezi Mungu habari za kufariki kwa Abu Talib, basi akalia kisha akasema: ‘Nenda kamwoshe, mvishe sanda na mzike. Mwenyezi Mungu amghofirie na amrehemu.”’60 Ibnu Al-Jawziy ameitaja kutoka kwa Al-Waqidy sehemu hiyo aliyoipokea Ibnu Sa’ad, amesema: “Akalia kilio kikubwa, kisha akasema: “Nenda umwoshe, umvishe sanda na umzike. Mwenyezi Mungu amghufirie na amrehemu.” Abbas akasema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, wewe unatarajia chochote kwa ajili yake?” Akasema: “Ndiyo wallahi, hakika mimi nataraji chochote kwa ajili yake”. Mtume wa Mwenyezi Mungu akaanza kumwombea maghfira muda wa siku nyingi huku akiwa hatoki nyumbani mwake.”61

59 Tadhkiratul-Khawas: 7. 60 At-Tabaqat Al-Kubra 1: 105. 61 Tadhkiratul-Khawas: 8. 55


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 56

Kumlilia Maiti Al-Ya’aqubiy amesema “Mtume wa Mwenyezi Mungu alipoambiwa kuwa Abu Talib amefariki, lilimuuma hilo moyoni mwake na huzuni ikamzidia, kisha akaingia akampangusa sehemu ya kulia ya paji lake mara nne, na ya kushoto mara tatu, kisha akasema: “Ewe ami umenilea nikiwa mdogo, ukanilinda nikiwa yatima na ukanisaidia nikiwa mkubwa, namwomba Mwenyezi Mungu akulipe kheri kwa ajili yangu.” Akatembea pembezoni mwa kitanda chake, akawa anamfunua na kusema: “Rehema zikufikie na ulipwe kheri”. Na akasema: “Katika siku hizi umma huu umekusanyikiwa na misiba mikubwa miwili, sijui ni upi kati ya hiyo ni wenye kuniumiza sana.” Akimaanisha msiba wa Khadija na msiba wa Abu Talib.”62 9. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amlilia Ja’far bin Abu Talib: Imepokewa kutoka kwa Anas kuwa: “Hakika Mtukufu Mtume aliomboleza kifo cha Ja’far na Zayd huku macho yake yakibubujika machozi, hata kabla ya kuja kwa habari zao.” Imepokewa kutoka kwa Asmaa binti Umaysi, amesema: “Alipofariki Ja’far na swahiba zake, Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) aliingia kwangu nikiwa nimeshakausha ngozi arubaini, nimeshakanda unga na nimeshawaogesha, kuwasafisha na kuwapaka mafuta wanangu. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akasema: “Niletee wana wa Ja’far.” Basi nikamletea na hapo macho yake yakabubujika machozi. Nikasema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Baba yangu na mama yangu ni fidia kwako, kitu gani chakuliza? Je zimekufikia habari zozote kuhusu Ja’far na maswahiba zake?” Akasema: “Ndiyo, ameuwawa leo yeye na maswahiba zake.” Asmaa anasema: “Tukanyanyuka na wanawake wakakusanyika, Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akatoka kwenda kwa wakeze, akasema: “Msighafilike mkaacha kuitengenezea chakula familia ya Ja’far, kwani hakika wao wameshughulishwa na msiba wa mtu wao.”63 62 Tarikhul-Ya’aqubiy 2: 35. 63 Tarikhul-Ya’aqubiy 2: 35. 56


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 57

Kumlilia Maiti Al-Baladhuri amepokea kuwa: “Mtume wa Mwenyezi Mungu pindi ulipomfikia msiba wa Ja’far, aliingia kwa Asmaa binti Umaysi na kumuhani. Akaingia Fatimah huku akilia na kusema: “Ewe ami yangu!” Mtume wa Mwenyezi Mungu akasema: ‘Mtu mfano wa Ja’far wamlilie wenye kulia.”64 Al-Ya’aqubiy ameongeza kuwa: “Mtume wa Mwenyezi Mungu akatoka huku akiburuza joho lake akiwa hawezi kuzuwia kilio chake huku akisema: ‘Mtu mfano wa Ja’far wamlilie wenye kulia.”65 10. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amlilia Hamza: Imepokewa kutoka kwa Jabir bin Abdullah, amesema: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipomtazama Hamza akiwa ameuawa alilia, alipoona unyama aliofanyiwa aliishiwa pumzi kwa kilio.”66 Pia imepokewa kutoka kwa Abdullah bin Mas’ud, amesema: “Kamwe hatukumwona Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akilia sana kama alivyomlilia Hamza bin Abdul Muttalib alipouawa. Kisha (s.a.w.w.) alisimama kwenye jeneza lake akalia kwa sauti mpaka akazidiwa kwa kilio huku akisema: “Ewe Hamza, ewe ami wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, simba wa Mwenyezi Mungu na simba wa Mtume wake. Ewe Hamza, ewe mtenda kheri. Ewe Hamza, ewe mwondoa matatizo. Ewe Hamza, ewe mwenye kujitoa muhanga kwa ajili ya uso wa Mtume wa Mwenyezi Mungu.” Amesema: “Akarefusha kilio, kisha akamwita mtu mmoja mmoja mpaka wakamsalia sala sabini huku Hamza akiwa katika hali yake.”67

64 Ansabul-Ashrafu: 43. 65 Tarikhul-Ya’aqubiy 2: 66. 66 Dhakhairul-Uqba: 180. As-Siratul-Halbiyah 2: 242. 67 Dhakhairul-Uqba: 180. As-Siratul-Halbiyah 2: 242.. 57


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 58

Kumlilia Maiti Ndani ya kitabu Shifaul-Gharam imeandikwa: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliporejea Madina alisikia kilio na mayowe juu ya wahanga, basi macho yake yakatoka machozi na kulia, kisha akasema: “Lakini Hamza hana wa kumlilia,” ndipo wanawake wa Bani Al-Ash’hal waliposikia hivyo wakaja na kuanza kumlilia ami ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) huku sisi tukiwa kwenye mlango wa msikiti. Alipowasikia alitoka na kusema: ‘Rejeeni, Mwenyezi Mungu akurehemuni, bila shaka mmeshashiriki kwa nafsi zenu.”’68 At-Tabari amenukuu kutoka kwa Al-Waqidiy kuwa: “Tangu Mtume wa Mwenyezi Mungu aliposema: “Hamza hana wa kumlilia”, hakuna mwanamke wa kiansari baada ya kauli ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mpaka leo aliyemlilia maiti yeyote ila kwanza alianza kumlilia Hamza, kisha humlilia maiti wake.”69 11. Mtukufu Mtume amlilia Fatimah binti Asad: Imepokewa kuwa (s.a.w.w.) alimsalia, akaingia kaburini mwake na akalia, akasema: “Allah akulipe kheri, hakika ulikuwa mama bora.” Alimwita mama kwa kuwa yeye alikuwa mlezi wake (s.a.w.w.).70 Ibnu As-Sabagh Al-Malikiy amesema kwenye sura aliyoitenga kwa ajili ya Fatimah binti Asad: “Alisilimu na kuhama pamoja na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), naye alikuwa miongoni mwa watu wa awali kuamini, na alikuwa na nafasi ya mama kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Alipofariki, Mtukufu Mtume alimvisha sanda kwa kanzu yake, akamwamuru Usama bin Zayd, Abu Ayyub Al-Answariy, Umar bin Al-Khattab na kijana mweusi wakachimba kaburi lake, walipofikia mwanandani Mtukufu Mtume aliuchimba yeye mwenyewe kwa mkono wake na akatoa udongo wake 68 Shifaul-Ghuram 2: 347. As-Siratun-Nabawiyyah 3: 105. Ar-Rawdhu Al-Anfu 6: 24. 69 Dhakhairul-Uqba: 183. 70 Dhakhairul-Uqba: 56. 58


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 59

Kumlilia Maiti mwenyewe. Alipomaliza alilala humo na kusema: “Allah ndiye anayeuhisha na kufisha, Naye yu hai hafi. Ewe Mola mghufirie mama yangu Fatimah binti Asad, mlakinishe hoja yake na mpanulie eneo lake atakaloingia. Kwa utukufu wa Nabii Wako Muhammmad na manabii waliokuwa kabla yangu, kwani hakika Wewe ni mbora wa kurehemu.” Akaambiwa: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Tumekuona umemfanyia kitu ambacho kabla yake hujamfanyia yeyote.” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: ‘Nimemvisha kanzu yangu ili avishwe nguo za peponi na nimelala ndani ya kaburi lake ili apunguziwe mbinyo wa kaburi, kwani hakika yeye alikuwa kiumbe anitendeaye wema kuliko viumbe wengine wa Mwenyezi Mungu baada ya Abu Talib, Mwenyezi Mungu awe radhi nao na amrehemu.”71 Ndani ya kitabu Tarikhul-Ya’qubiy imeandikwa kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) aliambiwa: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, kihoro chako juu ya Fatimah kimezidi mno.” Akasema: “Hakika yeye alikuwa mama yangu, alikuwa akiwaacha na njaa wanawe lakini ananishibisha mimi, anawaacha bila kuwapaka mafuta lakini ananipaka, kwa kweli alikuwa ni mama yangu.”72 12. Mtume (s.a.w.w.) amlilia mama yake kwenye kaburi lake: Al-Hakim ndani ya kitabu chake Al-Mustadarak amepokea kwa njia yake kutoka kwa Sulayman bin Baridah, kutoka kwa baba yake amesema: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alizuru kaburi la mama yake akiwa na waonekanaji elfu moja, na siku hiyo hakuna aliyeonekana akilia kuliko yeye.” Hadithi hii ni sahihi kwa mujibu wa sharti za upokezi wa mashekhe wawili73 lakini hawajaziandika. 71 Al-Fusulul-Muhimmah: 13. Manaqib Ibnu Al-Mughaziliy: 77. 72 Tarikhul-Ya’aqubiy 2: 14. 73 Bukhari na Muslim - Mtarjumi. 59


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 60

Kumlilia Maiti Na imepokewa toka kwa Abu Hurayra amesema: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alizuru kaburi la mama yake, akalia na kuwaliza waliomzunguka.”74 Ibnu Abu Shaybah amepokea kutoka kwa Sulayman bin Baridah, kutoka kwa baba yake amesema: “Pindi Mtume wa Mwenyezi Mungu alipoukomboa mji wa Makka alikuja eneo la kaburi kisha akakaa akiwa amelielekea, akawa kama mwenye kutoa hotuba, na watu wakamzunguka, ghafla akasimama akiwa analia. Umar bin Al-Khattab akamkabili, naye alikuwa ndiye mtu jasiri kwake, akasema: “Baba yangu na mama yangu ni fidia kwako, ewe Mtume wa Mwenyezi Mugu ni kipi kikulizacho? Akasema: “Hili kaburi la mama yangu, nimemwomba Allah nilizuru akanipa idhini, lakini nimemkumbuka ndipo nafsi yangu ilipotoa machozi nikalia”. Amesema: ‘Siku hiyo hakuonekana yeyote alikuwa akilia sana kuliko yeye (s.a.w.w.).”75 13. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amlilia Khadija binti Khuwaylid: Ali amesema: “Baada ya kupita mwezi aliingia kwangu ndugu yangu Aqil akasema: “Wallahi ewe ndugu yangu, katu sikufurahishwa na kitu kama nilivyofurahishwa na kitendo cha kumuoa kwako Fatimah Az-Zahrau binti ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.). Ewe ndugu yangu! Vipi mbona humwombi Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amlete kwako, macho yetu yatulie kwa muungano wenu”. Nikasema: “Wallahi ewe ndugu yangu, hakika mimi napenda iwe hivyo, lakini hakuna kinachonizuia nisimwombe Mtume wa Mwenyezi Mungu hilo ila ni kule kumwonea haya.” Akasema: “Nakuapia, simama twende pamoja nami,” basi tukasimama na kuelekea kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, ndipo njiani tukakutana na Ummu 74 Al-Mustadarak Alas-Sasihayan 1: 375. Tarikhul-Madinatil-Munawwarah 1: 118. 75 Al-Muswannaf cha Ibnu Abu Shaybah 3: 224. Tarikhul-MadinatilMunawwarah 1: 118. 60


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 61

Kumlilia Maiti Ayman, suria wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, tukamwelezea hilo, akasema: ‘Ewe baba Hasan76, usifanye hivyo tuachie sisi tulizungumze hili, kwani bila shaka maneno ya wanawake katika hili ni bora na yenye kuvutia kwenye nyoyo za wanaume.” Amesema: “Kisha akarejea akaingia kwa Ummu Salamah binti Abu Umaiyyah bin Al-Mughira mke wa Mtume (s.a.w.w.), akawa amemjulisha hilo na kuwajulisha wakeze Mtume (s.a.w.w.) wote. Basi wakeze Mtume wakajikusanya kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na muda huo alikuwa nyumbani kwa Aisha, wakamzunguka na kumwambia: ‘Baba zetu na mama zetu ni fidia kwako, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Bila shaka tumekusanyika hapa kwa ajili ya jambo ambalo lau Khadija angekuwa hai basi lingetuliza macho yake.” Ummu Salamah amesema: “Tulipomtaja tu Khadija Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akalia kisha akasema: ‘Khadija, na yuko wapi mfano wa Khadija! Alinisadikisha pindi watu waliponikadhibisha, akaniunga mkono juu ya dini ya Mwenyezi Mungu na akanisaidia kwa mali yake. Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu aliniamuru nimbashirie Khadija kuwa ana nyumba peponi ya kito cha zamaradi, humo hamna kelele wala machovu.”’ Ummu Salamah amesema: “Tukasema: ‘Baba zetu na mama zetu ni fidia kwako, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Hakika hakuna jambo ulilolitaja kuhusu Khadija ila ndivyo lilivyokuwa, isipokuwa yeye ametangulia kwa Mola wake Mlezi na Mwenyezi Mungu akampa hongera kwa hayo, na ametukusanya sisi na yeye katika madaraja ya pepo yake, rehema zake na radhi yake. Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Huyu ndugu yako katika dini na mwana wa ami yako katika nasaba Ali bin Abu Talib anatamani kuingia kwa Fatimah……”’77 76 Ni suna mtu kupewa jina la heshima angali mtoto, ndio maana jina hili lilitumika kwa Imam Ali hata kabla ya kumzaa Hasan –Mtarjumi. 77 Manaqibul-Khawarazimiy: 253. 61


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 62

Kumlilia Maiti 14. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amlilia Uthman bin Madh’un: Al-Hakim amepokea kwa njia yake kutoka kwa Al-Qasim bin Muhammad, kutoka kwa Aisha, amesema: “Hakika Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimbusu Uthman bin Madh’un akiwa maiti huku (s.a.w.w.) akilia”. Amesema: “Huku macho yake yakibubujika.”78 Pia ameipokea Al-Bayhaqiy kwa njia yake kutoka kwa Aisha: “Aliingia kwa Uthman bin Madh’un akiwa maiti, akamfunua uso wake kisha akamwangukia na kumbusu, akalia mpaka nikaona machozi yakitembea juu ya mashavu yake”.79 15. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amlilia Zayd na Ibnu Rawwah: Ibnu Sa’ad amesema ndani ya kitabu At-Tabaqat kutoka kwa Ibnu Umar, ametusimulia Sulayman bin Harb, ametusimulia Hammad bin Zayd kutoka kwa Hamid, kutoka kwa Hilal, kutoka kwa Anas bin Malik kuwa “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimlilia Ja’far na Zayd na Ibnu Rawwah hata kabla ya kuja habari zao, aliwalilia huku macho yake yakibubujika.”80 16. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amlilia Sa’ad bin Rabiu: Al-Waqidy amesema: “Na Jabir bin Abdullah amesema: “Alipouwawa Sa’ad huko Uhud, Mtume wa Mwenyezi Mungu alirejea Madina kisha akaenda Humraul-Asad…na mke wa Sa’ad alikuwa mwanamke mwenye subira, alitengeneza chakula mkate na nyama, kisha akamwita Mtume wa Mwenyezi Mungu, kipindi hicho (mke wa Sa’ad) alikuwa huko AlAsuwaf, basi asubuhi tukaenda kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu 78 Al-Mustadarak Alas-Sasihayan 1: 361. 79 Sunanul-Bayhaqiy 3: 407. 80 Tadhkiratul-Khuwwas: 172 kutoka kwa Ibnu Sa’ad. Al-Mu’ujam Al-Kabir 2: 105. 62


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 63

Kumlilia Maiti (s.a.w.w.), tukiwa bado tumekaa kwake tukihadithia tukio la Uhudi na kuwakumbuka waislamu waliouwawa na tukimtaja Sa’ad bin Rabiu, ghafla Mtume wa Mwenyezi Mungu akasema: “Simameni twende.” Basi tukasimama pamoja naye na tulikuwa watu ishirini, tukaenda mpaka AlAsuwaf, basi Mtume wa Mwenyezi Mungu akaingia nasi tukaingia pamojanaye, ndipo tukamkuta (mke wa Sa’ad) tayari ameshamwagilia kati ya mitende miwili na ameondoa makuti makavu.” Jabir bin Abdullah anasema: “Wallahi haukutulia mto wala busati tukawa tumekaa huku Mtume wa Mwenyezi Mungu akitusimulia kuhusu Sa’ad bin Rabiu na akimwombea rehema na akisema: “Siku hiyo niliyaona meno ya silaha yakimwelekea mpaka akauwawa.” Basi wanawake waliposikia hivyo wakalia, na macho ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) yakatoa machoza, na wala hakuwakataza kulia hata kidogo…”81 Imam Ali bin Abu Talib(a.s) alia: 1. Kiongozi wa waumini amlilia Az-Zahra (a.s.): Ibnu As-Swabbagh amesema: “Ja’far bin Muhammad (a.s.) amepokea, amesema: “Fatimah alipofariki, Ali (a.s.) alikuwa akizuru kaburi lake kila siku.” Amesema: “Siku moja akaja akajitupa juu ya kaburi akalia na kuanza kusoma shairi: Nina nini nimepita kwenye makaburi, nikalitolea salamu kaburi la hababi lakini hajanirudishia jawabu. Ewe kaburi mbona humjibu akuitaye, baada yangu umejitenga na mapenzi ya mahababi 81 Al-Mughaziy 1: 329.

63


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 64

Kumlilia Maiti Ndipo sauti ikamjibu ilihali mwenyewe haonekani, ikasema: ‘Hababi akasema: Vipi niwajibu ilihali mimi ni rahani wa jabali na udongo. Udongo umekula mema yangu nami nikawasahau, na umenitenga na familia yangu na ukoo wangu. Salamu iwafikie toka kwangu, imekatika toka kwangu na kwenu chachu ya mahusiano.”’82 Sibtu Ibnu Al-Jawzi amesema: “Ali alipomzika Zahra (a.s.): alisoma shairi akisema: ‘Kila mkusanyiko wa mahalili wawili una mtengano, na kila usio na mtengano ni mchache. Na hakika kumkosa kwangu Fatimah baada ya Ahmad ni dalili ya kuwa halili hadumu.” Pia akasema: “Ewe mauti ambaye hutoniacha, nibebe kwani bila shaka umemmaliza kila halili. Nakuona uko macho na wale niwapendao, kana kwamba wewe unaelekea upande wao kwa dalili”. Kisha alikuja kwenye kaburi la Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na kusema: ‘Salamu iwe juu yako ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Na juu ya binti yako aliyeteremka pembezoni mwako, aliyeharakisha kukutana nawe. Subira yangu kuhusu yeye imepungua, na uvumilivu wangu umedhoofika kwa kutengana naye. Hakika kuomboleza kwangu mshituko mkubwa wa kutengana nawe na athari ya msiba wako kunatosheleza. 82 Al-Fusulul-Muhimmah: 130. Kashful-Asrari 1: 626. 64


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 65

Kumlilia Maiti Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu na kwake Yeye tutarejea. Hakika nimerejesha amana na nimechukua rahani. Ama huzuni yangu juu yenu ni ya kudumu, na usiku wangu ni mkesha, mpaka Mwenyezi Mungu anichagulie nyumba yako ambayo wewe filihali unaishi humo, na anihamishe toka nyumba ya uchafu na madhambi. Binti yako atakupa habari za yale tuliyokutana nayo baada yako, muhoji kwa maswali, na mdadisi mambo na hali mbalimbili, haya yote ni kwa kipindi kifupi na wala si kwa muda mrefu. Salamu iwe juu yenu toka kwangu, salamu ya kuaga, isiyo na raha wala mchoko, ikiwa naondoka basi si kwa kuchoka, na kama naendelea kubaki basi si kwa dhana mbaya dhidi ya yale ambayo Mwenyezi Mungu amewaahidi wenye subira na kuwaandalia waovu.”83 2. Imam Ali (a.s.) amlilia Husein (a.s.): Ali (a.s.) alikuwa akilia akumbukapo kifo cha Husein (a.s.) na watu wa nyumba yake watukufu. Na (a.s.) alikuwa akimlilia mwanawe pindi aonapo machozi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) yakiteremka juu ya mashavu yake kwa kumlilia Husein (a.s.). Ibnu Asakir amepokea kutoka kwa Abdullah bin Najiyyu, kutoka kwa baba yake kuwa aliondoka na Ali pindi alipokuwa akienda kwenye vita vya Siffin, na walipofika usawa wa Naynawa, Ali alinadi “Fanya subira ewe Abu Abdullah, Fanya subira ewe Abu Abdullah pembezoni mwa mto furati.” Nikasema: “Kuna nini?” Akasema: “Siku moja niliingia kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) nikamkuta macho yake yakibubujika machozi, nikamwambia, ewe Mtume kuna yeyoye kakukasirisha, mbona macho yako yanabubujika? Akasema: “Bali punde tu Jibril kaondoka toka kwangu, amenisimulia kuwa Husein atauawa pembezoni mwa mto furati.” Ali anasema: ‘Akaniambia: “Je, unatamani nikunusishe harufu ya udongo wake?” Nikasema: “Ndiyo”, basi akanyoosha mkono wake akachukua gao 83 Tadhkiratul-Khuwwas: 320. Al-Fusulul-Muhimmah: 130 65


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 66

Kumlilia Maiti la udongo na kunipa, basi sikuweza kuyazuia macho yangu yasibubujike machozi.”84 Al-Qunduziy amepokea, kutoka kwa Ibnu Sa’ad kutoka kwa Sha’abiy, amesema: “Ali alipita Karbala kwenye safari yake ya kuelekea Siffin, basi akalia mpaka ardhi ikalowana kwa machozi yake, akasema: “Niliingia kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu nikamkuta analia, nikamuuliza: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu baba yangu na mama yangu ni fidia kwako, kipi kukulizacho?” Akasema: ‘Punde tu Jibril alikuwa pamoja nami, na amenipa habari kuwa mwanangu Husein atauwawa pembezoni mwa mto furati eneo liitwalo Karbala. Kisha Jibril akachukua gao la udongo wake na kuninusisha, hivyo nimeshindwa kuyazuia macho yangu yasibubujike machozi.”’85 3. Imam Ali (a.s.) amlilia Ammar bin Yasir (r.a): Ibnu Qutaybah amesema: “Alipouawa Ammar watu walivurugana mpaka wabeba bendera wakaviacha vituo vyao na kuwashambulia wakazi wa Sham, na hilo lilitokea mwishoni mwa mchana….Adiyyu bin Hatim akasema: “Wallahi ewe kiongozi wa waumini, tukio hili halijatuachia sisi wala wao muhimili wowote, pigana mpaka Mwenyezi Mungu akupe ushindi, kwani hakika bado kati yetu tupo.” Ali akasema: “Ewe Adiyyu ameuawa Ammar bin Yasir?” akasema: “Ndiyo”. Basi Ali akalia na kusema: ‘Mwenyezi Mungu akurehemu Ammar, anawajibika kupata maisha yenye riziki tukufu….”’86 84 Tarikhud-Damashqi (Al-Imam Husein): 238. Manaqib Ibnu Al-Mughazaliy: 397, hadithi ya 451. Tahdhibut-Tahdhib 2: 300. Istish’hadul- Imama Husein: 125, humo mna Yahya badala ya Naiyyu. As-Sawaiqul-Muhriqah:191. AlMu’ujam Al-Kabir 3: 105. Musnad Ahmad 1: 58. 85 Yanabiul-Mawaddah: 384. 86 Al-Imamah Was-Siyasah 1: 110. 66


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 67

Kumlilia Maiti 4. Imam Ali (a.s.) amlilia Hashim bin Ut’bah (r.a): Amesema ndani ya kitabu At-Tadhkirah: “Siku hiyo pia aliuawa Hashim bin Ut’bah bin Abu Waqqas, basi Ali akawalilia wote wawili na kuwasalia, akamweka Ammar mbele yake na Hashim bin Ut’bah upande wa kibla (yaani mbele ya Ammar), na wala hakuwaosha.”87 5. Imam Ali (a.s.) amlilia Muhammad bin Abu Bakr (r.a): Ali akaambiwa: “Kihoro chako juu ya Muhammad bin Abu Bakri kimezidi” akasema: “Mwenyezi Mungu amrehemu Muhammad, hakika alikuwa kijana barobaro, na nilitaka kumpa ugavana wa Misri Hashim bin Ut’bah, na hata kama ningempa utawala yeye (Hashim bin Ut’bah) bado wasingeacha uwanja wazi bila kumshambulia Muhammad. Kwangu alikuwa ni mwana wa kulea, na alikuwa ni kaka kwa upande wa wana wa ndugu yangu Ja’far, nami nilikuwa nikimuhesabu kuwa ni mwana wangu wa kuzaa.”88 Sibt Ibnu Al-Jawzi amesema: “Ali (a.s.) akapata habari za kuuwawa kwa Muhammad, basi akamlilia na kusikitika na akamlaani muuwaji wake”.89 6. Imam Ali (a.s.) amuhuzunikia Malik Al-Ashtar (r.a): Ibnu Abil Hadid amesema: “Ibrahim amesema: ‘Ametusimulia Muhammad bin Abdullah, kutoka kwa Ibnu Abu Sayfu Al-Madainiy, kutoka kwa kundi la mashaibu wa kinakha’i, wamesema: ‘Tuliingia kwa kiongozi wa waumini pindi zilipomfikia habari za kuuawa kwa Al-Ashtar, tukamkuta akihuzunika na kusikitika, kisha akasema: “Kheri ya Malik ni ya Mwenyezi Mungu! Ni nani Malik! Lau angekuwa ni mlima basi ni 87 Tadhkiratul-Khuwwas: 94. 88 Ansabul-Ashraf: 404. Tarikhut-Tabari 6: 62. 89 Tadhkiratul-Khuwwas: 107. 67


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 68

Kumlilia Maiti mlima mkubwa, na lau angekuwa ni jiwe basi ni jabali. Wallahi kwa hakika kifo chako kitauangusha ulimwengu na bila shaka kitaufurahisha ulimwengu. Mtu mfano wa Malik, wamliliye wenye kulia. Na je anatarajiwa kupatikana kama Malik!!? Na je yupo kama Malik!?” Alqamah bin Qays An-Nakha’i amesema: ‘Ali aliendelea kuhuzunika na kusikitika mpaka tukadhani kuwa yeye hasa ndiye mfiwa na si sisi, na hali hiyo ilionekana usoni mwake muda wa siku nyingi.”90 Fatimah Az-Zahra (a.s.) alia: 1. Bibi Fatimah (a.s.) amlilia baba yake (s.a.w.w.): Az-Zahra alimlilia sana baba yake kipindi chote cha uhai wake, na alihuzunika sana kwa kumpoteza Mtume wa Mwenyezi Mungu, alikuwa akimlilia usiku na mchana mpaka alipoungana naye. Ibnu Al-Jawziy amesema: “Kisha yeye (a.s.) alijitenga na kaumu na akaendelea kumwomboleza Mtume wa Mwenyezi Mungu na kumlilia mpaka alipoungana naye.”91 Imepokewa kutoka kwa Hammad bin Salmah kutoka kwa Thabit, kutoka kwa Anas bin Malik amesema: “Tulipomaliza kumzika Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) Fatimah alinikabili na kusema: “Ewe Anas! Vipi nafsi zenu zimeridhia kumwagia udongo juu ya uso wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.)!!?” Kisha akalia na kunadi: ‘Ewe baba yangu mpendwa, ambaye Mola Mlezi amemwita na ameitikia wito. Ewe baba yangu mpendwa, ambaye Mola wake Mlezi amemsogeza. Ewe baba yangu mpendwa, ambaye Mola wake Mlezi amemwita. Ewe baba yangu mpendwa, ambaye tunampa Jibril habari za kifo chake. Ewe baba yangu mpend90 Sharhu Nahajul-Balaghah, 6: 77. 91 Tadhkiratul-Khuwwas: 318.

68


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 69

Kumlilia Maiti wa, ambaye pepo ya Firdawsi ndio mafikio yake….”’92 Imepokewa kutoka kwa Ali (a.s.) amesema: “Hakika Fatimah binti ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alikuja kwenye kaburi la baba yake baada ya kifo chake, akasimama juu yake na kulia. Kisha akachukua gao la udongo wa kaburi na kuuweka juu ya macho yake na uso wake na akasoma shairi akisema: ‘Atakayenusa udongo wa Ahmad, hatonusa manukato ya ghawaliya muda wote. Nimemwagiwa masaibu ambayo lau mchana ungemwagiwa basi ungegeuka na kuwa usiku.” 93 Hammad anasema: “Thabit alikuwa asimuliyapo hadithi hii hulia mpaka mbavu zake zinatetemeka.”94 2. Bibi Fatimah (a.s.) amlilia mama yake (r.a): Al-Ya’aqubiy amesema: “Alipofariki Khadija, Fatimah alimkumbatia Mtume wa Mwenyezi Mungu huku akilia na akisema: “Mama yangu yuko wapi, mama yangu yuko wapi?” Ndipo Jibril akateremka na kusema: “Mwambie Fatimah: ‘Hakika Mwenyezi Mungu amemjengea mama yako nyumba peponi ya kito cha zabarijadi, humo hamna machovu wala kelele.”95

92 Al-Aqdu Al-Farid 3: 194. Mustanad Fatimahh cha As-Suyutiy: 30. KanzulUmmal 7: 261. 93 Al-Fusulul-Muhimmah: 130. Al-Wafau Biahwalil-Mustafa 2: 560. 94 Hayatus-Sahabah 2: 374. 95 Tarikhul-Ya’aqubiy 2: 35. 69


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 70

Kumlilia Maiti 3. Bibi Fatimah (a.s.) amlilia dada yake Ruqayya: Ibnu Shibbah amepokea kwa njia yake kutoka kwa Ibnu Abbas (r.a.) kuwa amesema: “Alipofariki Ruqayyah binti ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Ungana na kheri iliyotutangulia. Uthman bin Madh’un amesema: ‘Basi Fatimah (r.a) akalia akiwa juu ya mdomo wa kaburi, Mtukufu Mtume (s.a.w..w) akaanza kumfuta machozi machoni kwa upande wa nguo yake.’”96 4. Bibi Fatimah (a.s.) awalilia mashahidi wa Uhud: Al-Makkiy amesema: “Ja’far bin Muhammad As-Sadiq (a.s.) amepokea kutoka kwa baba yake kutoka kwa babu yake kuwa: ‘Fatimah binti ya Mtume wa Mwenyezi Mungu alikuwa akienda mara kwa mara kwenye makaburi ya mashahidi wa Uhud, kati ya siku mbili na tatu, anasali huko, anaomba dua na kulia mpaka (r.a.) alipofariki.”’97 5. Bibi Fatimah (a.s.) amlilia ami yake Ja’far (a.s.): Al-Baladhuriy amesema: “Na Mtume wa Mwenyezi Mungu akaingia kwa Asmaa binti Umays pindi zilipomfikia habari za kifo cha Ja’far, akampa pole. Fatimah (a.s.) naye akaingia huku akilia na akisema: “Ewe ami yangu!” Mtume wa Mwenyezi Mungu akasema: “Mtu mfano wa Ja’far wamlilie wenye kulia.” Kisha akenda kwa wakeze, akawaambia: “Wapikieni aali wa Ja’far chakula, kwani hakika wameshughulishwa na nafsi zao.” Akamkumbatia Abdullah bin Ja’far na kumfuta kichwa chake huku macho yake yakitoka machozi, akasema: ‘Ewe Mola mpe Ja’far mbadala wa kizazi chake, aliye mwema kuliko yule uliyempa yeyote miongoni waja wako walio wema.”’98 96 Tarikhul-Madinatil-Munawwarah 1: 103. Umdatul-Akhbar: 152. 97 Shifaul-Gharam 2: 350. 98 Ansabul-Ashraf: 43. Dhakhairul-Uqba: 218. 70


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 71

Kumlilia Maiti Imam Hasan Al-Mujtaba (a.s.) alia: 1. Imam Hasan (a.s.) na wakazi wa Kufa wamlilia Ali (a.s.): Ibnu As-Sabbagh Al-Malikiy amesema: “Kundi la waandishi wa sira na wengineo wamepokea kuwa: “Hasan bin Ali (a.s.) alitoa hotuba asubuhi ya siku aliyofariki kiongozi wa waumini Ali (a.s.). Akamuhimidi Mwenyezi Mungu na kumtukuza, akamsalia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kisha akasema: “Bila shaka ndani ya usiku huu amefariki mtu ambaye hawajamtangulia wa awali na wala wa mwisho hawajamfikia. Bila shaka alikuwa akipigana bega kwa bega pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), akimpeleka na bendera yake na hapo Jibril humlinda kuliani na Mikail kushotoni, basi harejei mpaka Mwenyezi Mungu apate ushindi mikononi mwake. Bila shaka amefariki ndani ya usiku ambao Isa bin Mariam alipaishwa humo, na humo alifariki Yoshua bin Nun. Na hakuacha njano wala nyeupe (dhahabu na fedha) ila dirhamu mia saba zilizobaki katika mgao wake, na kwazo alitaka kununua mtumishi kwa ajili ya wakeze.” Kisha kilio kikamshika akalia, na watu wakalia pamoja naye, kisha (a.s.) akasema: ‘Mimi ni mwana wa mbashiri mwonyaji. Mimi ni mwana wa taa iangazayo. Mimi ni mwana wa mlinganiaji kwa Mwenyezi Mungu kwa idhini Yake. Mimi ni mwana wa wale ambao Mwenyezi Mungu amewaondolea uchafu na kuwatakasa kabisa…”’99 Imam Husein (a.s.) alia: 1. Imam Husein (a.s.) amlilia mwanawe Ali Akbar: Amesema: “Kisha akachomoza Ali Akbar bin Husein, naye akiwa mwana wa miaka kumi na saba….. Aliendelea kupambana mpaka akawauwa watu 99 Al-Fusulul-Muhimmah cha Ibnu As-Sabaghu Al-Malikiy: 142. Sharhu NahjulBalaghah 4: 11. 71


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 72

Kumlilia Maiti themanini miongoni mwao, kisha mtu mmoja toka kaumu ile akampiga juu ya kichwa chake kitukufu, akaanguka ardhini. Kisha akakaa sawa huku akisema: “Ewe baba yangu mpendwa! Huyu hapa babu yangu Muhammad Al-Mustafa na Ali Al-Murtaza, na huyu hapa bibi yangu Fatimah Az-Zahra na Khadija Al-Kubra.” Ndipo Imam akawashambulia na kuwatawanya maadui, akakiweka kichwa chake mapajani mwake na kuanza kumfuta damu usoni mwake huku akisema: “Mwenyezi Mungu ailani kaumu iliyokuuwa ewe mwanangu, wamekuwa na ujasiri wa namna gani hawa juu ya Mwenyezi Mungu, na katika kuvunja heshima ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.)”. Macho yake yakabubujika machozi, na wanawake nao wakapiga mayowe ya kilio, ndipo Imam akawanyamazisha, akawaambia: ‘Nyamazeni, kwani hakika kilio kiko mbele yenu….”’100 2. Imam Husein (a.s.) amlilia ndugu yake Abbas bin Ali: Al-Qunduziy Al-Hanafiy amesema: “Kisha Abbas bin Ali alipigana sana akauwa watu wengi miongoni mwao huku akisema: “Sihofishwi na kifo pindi kifo kitakaponikuta, mpaka nizikwe kwenye mashujaa waliokwenda kwa haja maalumu. “Nitaikinga nafsi tohara kupitia nafsi yangu, hakika mimi ni mwenye subira mwenye kushukuru kwa yale ninayokutananayo. “Siogopi kitisho kinapotisha, bali nakata kichwa na kumdhoofisha aliye mwingi wa mauwaji”. 100 Aliwaambia hivyo kwa lengo la kuendelea kuwataarifu kuwa, msiba wa leo ni mkubwa sana hautokomea kwa Ali Akbar tu, bali bado huko mbele hata Abbas na mimi mwenyewe tutauwawa, na haitokomea hapo bali nyinyi wenyewe mtateswa sana. Na hivyo ndivyo ilivyokuwa. – Mtarjuma. Yanabiul-Mawaddah: 415. 72


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 73

Kumlilia Maiti Basi Al-Abrad bin Shayban akamshambulia mkono wa kulia ukadondoka na upanga, akauokota kwa mkono wake wa kushoto akawashambulia maadui zake huku akisema: “Wallahi lau mkinikata mkono wa kushoto basi bila kusita nitapigana kuihami dini yangu. Na Imam msadikishaji wa yakini, mjukuu wa Mtume mtoharifu mwaminifu.” Basi akaua watu wengi miongoni mwao, ndipo Abdullah bin Yazid akampiga mkono wake wa kushoto….Kisha aliwashambulia kaumu ile huku mikono yake miwili ikiwa imekatwa, na hatimaye alichoka kutokana na wingi wa majeraha, ndipo wote kwa ujumla wakamshambulia na hatimaye mtu mmoja kati yao akampiga kichwani kwa nguzo ya chuma na hapo azma yake ikaondoka, akadondoka ardhini huku akisema: “Ewe Abu Abdullah, ewe Husein, amani iwe juu yako toka kwangu.” Imam akasema: Ewe Abbas!! Ewe damu ya moyo wangu!!” Akawashambulia maadui na kuwatoa kwake, akateremka na kumbeba juu ya farasi wake, akamwingiza ndani ya hema lake na akalia sana akasema: ‘Mwenyezi Mungu akulipe malipo bora zaidi kwa ajili yangu, bila shaka umepigana jihadi ya kweli…”’.101 3. Imam Husein (a.s.) amlilia Muslim bin Aqil: Ahmad bin A’atham Al-Kufiy amesema: “Na Husein akaenda mpaka akateremka Shuquq, ghafla akamwona malenga Farazdaq bin Ghalib mbele yake, akamsalimu kisha akamsogelea na kubusu mikono yake. Imam Husein akasema: “Umetokea wapi ewe Abu Faras?” Akasema: “Nimetoka Kufa ewe mwana wa Mtume wa Mwenyezi Mungu.” Akasema: “Umewaachaje watu wa Kufa?” Akasema: “Nimewaacha watu wakiwa pamoja nawe huku panga zao zikiwa pamoja na bani Umaiyyah, na Mwenyezi Mungu hufanya atakavyo kwa viumbe wake.” Akasema (a.s.): “Umesema kweli na umefanya wema, hakika amri ni ya Mwenyezi Mungu, hufanya atakavyo, na Mola wetu Mlezi kila siku yupo 101 Yanabiul-Mawaddah: 409. 73


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 74

Kumlilia Maiti katika jambo. Pitisho lake likiteremka na jambo tunalolipenda basi kila sifa njema ni ya Mwenyezi Mungu juu ya neema zake, Naye ndiye aombwaye msaada ili kutekeleza shukurani. Na kama pitisho lake litazuia matarajio basi hatochupa mipaka yule ambaye haki ndio nia yake.” Farazdaq akasema: “Ewe mwana wa binti ya Mtume wa Mwenyezi Mungu! Vipi unawategemea wakazi wa Kufa ilihali wao tayari wameshamuua mwana wa ami yako Muslim bin Aqil, na wafuasi wake?” Msimuliaji anasema: “Basi Husein akashikwa na huzuni kwa kulia, kisha akasema: ‘Mwenyezi Mungu amrehemu Muslim, ameshakuwa kwa Mwenyezi Mungu kwenye riziki yake nzuri, pepo yake na radhi Zake. Bila shaka ameshatimiza wajibu wake na umebaki wajibu wetu….”’102 Pia amesema: “Husein bin Ali akafikiwa na habari kuwa Muslim bin Aqil ameuawa, Mwenyezi Mungu amrehemu, na hiyo ni baada ya kufikiwa na mtu kati ya wakazi wa Kufa, Husein akamwambia: “Umetokea wapi?” Akasema: “Nimetokea Kufa, na sikutoka humo mpaka nilipomwona Muslim bin Aqil na Haniy bin Ur’wah Al-Madh’hajiy, Mwenyezi Mungu awarehemu wameuwawa, wamesulubiwa, wameburuzwa ndani ya soko la wachinja nyama na vichwa vyao vimepelekwa kwa Yazid bin Muawiyyah.” Msimuliaji anasema: “Basi Husein akashikwa na huzuni kwa kulia, kisha akasema: ‘Hakika sisi sote ni wa Mwenyezi Mungu, na bila shaka sisi sote kwake Yeye tutarejea.”103 4. Imam Husein (a.s.) amlilia mwanawe mchanga: Hisham bin Muhammad amesema: “Husein alipowaona wameng’ang’ania kumuuwa, alichukua msahafu na kuufunua akauweka juu ya kichwa chake akanadi: “Kati yangu na nyinyi kuna kitabu cha Mwenyezi Mungu na babu 102 Al-Futuhu 5: 124. 103 Al-Futuhu 5: 110. 74


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 75

Kumlilia Maiti yangu Mtume wa Mwenyezi Mungu. Enyi kaumu, kwa kigezo kipi mnahalalisha damu yangu, je mimi si mwana wa binti ya Mtume wenu? Je haijawafikia kauli ya babu yangu kuhusu mimi na kaka yangu: “Hawa wawili ni mabwana wa vijana wa peponi?” Kama hamnisadikishi basi muulizeni Jabir, Zaydi bin Arqam na Abu Said Al-Khudriy. Hivi Ja’far mwenye mbawa si ami yangu?.....” Basi Husein alipogeuka akamwona mwanaye akilia kwa kiu, akamchukua mikononi mwake na kusema: “Enyi kaumu, kama hamwezi kunihurumia mimi basi mhurumieni mtoto huyu.” Ndipo mtu mmoja miongoni mwao akamfuma kwa mshale na kumchinja. Husein akaanza kulia huku akisema: “Ewe Mola wangu! Hukumu kati yetu na kaumu hii, wametuita ili watusaidie hatimaye wametuuwa.” Ndipo sauti ikaita kutoka angani: ‘Mwache ewe Husein, hakika yeye ana nyonyo peponi.”’104 Al-Qunduziy amesema: “Ummu Kulthum akasema: “Ewe kaka yangu, mwanao Abdullah hajaonja maji tangu muda wa siku tatu, nenda ukamtafutie angalau kinywaji kidogo toka kwa kaumu ili umnyweshe.” Ndipo akamchukua na kwenda naye kwa kaumu, akasema: “Enyi kaumu, mmewauwa sahaba zangu, wana wa ami yangu, ndugu zangu na mwanangu na amebakia huyu tu, yeye ni mtoto wa miezi sita, analalamika kiu naomba mumnyweshe maji angalau kidogo.” Basi alipokuwa akiendelea kuwahutubia ghafla ukamjia mshale na kutua kwenye koo la mtoto na kumuuwa. Na inasemekana kuwa mshale ulirushwa na Aqabah bin Bashir Al-Azdiy Mwenyezi Mungu amlaani. Husein (r.a.) akasema huku akilia sana: ‘Ewe Mola wangu! Wewe ni shahidi juu ya watu hawa walaanifu, hakika wao wamekusudia kutokubakisha kizazi cha Mtume Wako (s.a.w.w.).….”’105

104 Tadhkiratul-Khuwwas: 252. 105 Yanabiul-Mawaddah: 415. 75


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 76

Kumlilia Maiti 5. Imam Husein (a.s.) amlilia Qays bin Musahar: Husein akaandika barua kuwapelekea wakazi wa Kufa akiwa njiani kuelekea Kufa, akampa Qays bin Musahar As-Saydawiy, na akamwamuru aende Kufa. Ibnu Al-A’atham amesema: “Qays akaenda Kufa huku Ubaydullah bin Ziyad akiwa tayari ameshaweka majasusi na taa njiani, kiasi kwamba yeyote hawezi kuvuka ila ni lazima atakaguliwa. Qays bin Musahar alipokaribia Kufa alikutana na adui wa Mwenyezi Mungu aitwaye Al-Haswain bin Namir As-Sukuniy, basi Qays alipomwona akiwa amejificha, haraka sana alitoa barua akaichanachana mpaka mwisho. AlHuswain akawaamuru jamaa zake wakamchukua Qays na wakachukua barua iliyochanwa wakamleta kwa Ubaydullah bin Ziyad. Ubaydullah bin Ziyad akamuuliza: “Wewe ni nani?” akasema: “Mimi ni mfuasi wa kiongozi wa waumini Husein bin Ali (r.a.).” Akasema: “Kwa nini umechana barua uliyokuwanayo?” Akasema: “Sikutaka ujue yaliyomo.” Akasema: “Barua hii imetoka kwa nani na inaelekea kwa nani?” Akasema: “Ilikuwa inatoka kwa Husein inaelekea kwa baadhi ya jamaa wa Kufa, siwajui majina yao.” Ndipo Ibnu Ziyad akakasirika sana na kusema: “Wallahi sintokuacha, la sivyo unijulishe hawa jamaa walioandikiwa barua hii, au upande mimbarini na umtukane Husein, baba yake na kaka yake, uokoke toka mikononi mwangu, au nikukatekate.” Qays akasema: “Ama kuhusu jamaa hawa mimi siwafahamu. Ama kuhusu kumlaani Husein, baba yake na kaka yake mimi nitafanya hivyo.” Msimuliaji anasema: “Akaamrishwa na kuingizwa msikiti mkuu, kisha akapanda mimbari na akakusanyiwa watu ili wakusanyike na kusikiliza laana. Basi Qays alipojua kuwa watu wameshakusanyika alisimama wima, akamuhimidi Mwenyezi Mungu na kumtukuza, kisha akamsalia Muhammad na aali zake, na akakithirisha kumtakia rehema Ali na wanawe. Kisha akamlaani Ubaydullah bin Ziyad na kumlaani baba yake na akawalaani wafuasi wa bani Umaiyyah hadi wa mwisho wao, kisha akawaomba watu wamnusuru Husein bin Ali. Ndipo Ubaydullah bin Ziyad 76


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 77

Kumlilia Maiti akapewa habari hiyo, akampandisha juu ya kasri kisha akamtupa chini kwa kudondokea kichwa chake, akawa amefariki, Mwenyezi Mungu amrehemu. Habari hizo zikamfikia Husein akahuzunika kwa kulia, kisha akasema: ‘Ewe Mola wangu tujaalie sisi na wafuasi wetu mafikio ya heshima Kwako, na tukusanye sisi na wao kwenye makazi ya kudumu ya rehema Zako, hakika Wewe juu ya kila kitu ni muweza.”106 6. Imam Husein (a.s.) amlilia Hurr bin Yazid Ar-Riyyah: Al-Qunduziy amesema: “Kisha akachomoza Hurr…akasema: “Enyi wakazi wa Kufa! Huyu Husein mmemwita wenyewe na mkadai kuwa nyinyi mtamsaidia na mtazitoa nafsi zenu kwake, sasa mmemvamia na kumzingira kila pande, mmeizuia familia yake isinywe maji ambayo mbwa na nguruwe wanayanywa. Ni jambo baya sana mlilofanya, namwomba Mwenyezi Mungu asiwanyweshe siku ya kiu kubwa ikiwa hamtaacha yale mliyonayo.” Kisha akawashambulia akawauwa watu hamsini miongoni mwao, kisha (r.a.) akawa ameuwawa, kichwa chake kikakatwa na kutupwa upande wa Imam. Akamweka juu ya mapaja yake ilihali akilia na akifuta damu usoni mwake na akisema: ‘Wallahi mama yako hakukosea alipokupa jina la Hurr, kwani bila shaka wewe ni mtu huru duniani na ni mwema huko Akhera.”’107 Imam As-Sajjad Ali bin Husein (a.s.) alia: 1. Imam As-Sajjad (a.s.) amlilia baba yake Husein (a.s.): Na miongoni mwa watu waliomlilia Husein (a.s.) mpaka walipokutana na Mola wao Mlezi ni Imam Zaynul-Abidina (a.s.), alimlilia mzazi wake aliyekufa kishahidi Husein bin Ali takribani muda wa miaka arubaini, kiasi kwamba hakupelekewa chakula wala kinywaji ila alilia na kumkumbuka 106 Al-Futuhu 5: 145. 107 Yanabiul-Mawaddah: 414. 77


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 78

Kumlilia Maiti Husein, kifo chake na yale yaliyowapata aali wa Mtume wa Mwenyezi Mungu huko Karbala. Mpaka watu wakawa na hofu juu yake kutokana na wingi wa kilio chake, wakamwambia: “Hivi haujafika wakati huzuni yako ikakoma….?” Ibnu Asakir amepokea kwa njia yake kutoka kwa Muhammad bin Ya’aqub bin Sawar, kutoka kwa Ja’far bin Muhammad, amesema: “Alipoulizwa Ali bin Husein bin Ali bin Abu Talib kuhusu wingi wa kilio chake, alisema: ‘Msinilaumu, kwani hakika Ya’aqub alimpoteza mtoto wake akalia mpaka macho yake yakapofuka ilihali hakuwa na yakini kuwa amekufa. Mimi nimewaona watu kumi na nne toka katika watu wa nyumba yangu wakichinjwa, tena ndani ya siku moja, hivi mnadhani huzuni yangu kwao kamwe itaondoka ndani ya moyo wangu.”’108 2. Imam As-Sajjad na wakazi wa Madina wamlilia Husein: Bashir bin Jadhlam amesema: “Tulipofika karibu na Madina Imam ZaynulAbidina (r.a.) aliniamuru niwape habari wakazi wa Madina, hivyo nikaingia Madina na kuwaambia: “Enyi waislamu hakika Ali bin Husein ameshafika kwenu akiwa pamoja na shangazi zake na dada zake.” Basi hakuna mtawa aliyebaki ila alitoka ndani ya utawa wake huku akijikwangua uso na kujipiga mashavu na wakitamka maneno ya huzuni na msiba.” “Msimuliaji anasema: “Sijawahi kumwona mwanaume au mwanamke akilia sana kama walivyolia siku hiyo. Ndipo Imam akatoka kwenye hema huku mkononi akiwa na leso akijifuta machozi yake, akakaa juu ya kiti akamuhimidi Mwenyezi Mungu na kumtukuza, kisha akasema:

108 Tarikhud-Damashqi (Wasifu wa Imam Zaynul-Abidina): 56. Hilyatul-Awliyai 3: 138. 78


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 79

Kumlilia Maiti “Enyi watu! Hakika Mwenyezi Mungu ana sifa za kuhimidiwa na kushukuriwa, bila shaka ametutahini kwa misiba mikubwa na msiba wetu ni pengo kubwa katika Uislamu na ni msiba kwa viumbe. Baba yangu Husein ameuwawa yeye, kizazi chake na wahami wake, wakeze na kizazi chake wamechukuliwa mateka. Kichwa chake kimezungushwa mijini juu ya mikuki. “Huu ni msiba unaoishinda misiba yote, ardhi saba zimelia kwa kuuwawa kwake na mbingu saba kwa kutoweka kwake. Bahari zimemlilia kwa mawimbi yake, ardhi kwa pande zake, miti kwa matawi yake, ndege kwa viota vyao na nyoka ndani ya giza la bahari na wanyama huko bara na jangwani, na pia malaika wakuruba, mbingu na ardhi pia. “Enyi watu, ni moyo upi haugongi kwa kuuwawa kwake na wala hauhuzuniki kwa ajili yake. Enyi watu, tumekuwa watu wa kutawanywa, kufukuzwa na wenye kutengwa na miji yetu, bila kosa lolote tulilotenda wala baya tulilofanya wala doa lolote tulilotia ndani ya Uisilamu, wala chafu lolote tulilofanya. Wallahi lau Mtukufu Mtume angewausia kutuuwa basi wasingetufanyia yale waliyozidisha katika kutuuwa, kwa hakika sisi sote ni wa Mwenyezi Mungu na hakika sisi sote kwake tutarejea”. Kisha akasimama na kwenda Madina ili aingie mji huo, basi alipoingia kwanza alimzuru babu yake Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na ndipo akaingia nyumbani kwake.’”109

109 Yanabiul-Mawaddah: 425. 79


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 80

Kumlilia Maiti Imam Al-Baqir Muhammad bin Ali (a.s.) alia: 1. Imam Al-Baqir (a.s.) amlilia baba yake As-Sajjad (a.s.): Ibnu Asakir amepokea kwa njia yake kutoka kwa Abu Musa Al-Muaddibu, amesema: “Qays bin An-Nu’man amesema: “Siku moja nilitoka nikaelekea makaburi ya Madina na ghafla nikamkuta mtoto amekaa kwenye kaburi huku akilia sana, na uso wake ukitoa mionzi ya nuru, basi nikamwelekea na kumwambia: “Ewe mtoto, ni kitu gani ulichokiwekea huzuni mpaka kikakutenga faragha sehemu za maiti na kuanza kuwalilia waliotoweka….?!!” Anasema: “Akainua kichwa chake na kuinamisha na akakaa muda fulani bila kutoa jibu, kisha akainua kichwa chake na kusema: “Hakika utoto ni utoto wa akili, hakuna udogo wala ukubwa wenye kumdharau mwenye akili kati yetu.” Kisha akaniambia: “Ewe, hakika ondoa pumba kwenye akili salama na utumbo kwenye joto, umeamini ukaribu wa kifo kwa matarajio yenye kurefuka. Hakika kilichonitenga faragha kwenye maeneo ya waliotoweka ni kukumbuka kauli ya Mwenyezi Mungu: ‘Mara watatoka makaburini wakikimbilia kwa Mola wao Mlezi.” Nikasema: “Kwa haki ya baba yangu na mama yangu, wewe ni nani? Kwani kwa hakika mimi nasikia maneno mazuri.” Akasema: “Hakika miongoni mwa uovu wa watu wenye balaa ni kutowafahamu vizuri watoto wa manabii!! Mimi ni Muhammad bin Ali bin Husein bin Ali, na hili ni kaburi la baba yangu, ni liwazo lipi lilewezalo kuliko kuwa karibu naye, na ni upweke upi zaidi ya alio nao.” Kisha akaanza kusoma shairi akisema: “Hayakupunguka machozi yangu wakati wa tukio ila nilikufanya sababu ya kulia.

80


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 81

Kumlilia Maiti Hakika mimi nachukua sehemu kubwa ya unyevunyevu, na kumpaka nimwonaye kuwa asikitika kwa ajili ya asiyekuwa wewe. Nikukumbukapo machozi yangu hunyong’onyea kwa ajili yako, na hatimaye hunitoka na kunimwagika.” Qays anasema: ‘Nikaondoka na tangu siku hiyo sikuacha kuzuru makaburi.”110 Waislamu walia: 1. Waislamu walia kwa kuondokewa na Mtume (s.a.w.w.): Ibnu A’atham Al-Kufiy pindi anapozungumzia ukumbi wa Saqifa bani Sa’idah amesema: “Hakika waislamu walikusanyika wakalia kwa kuondokewa na Mtume wa Mwenyezi Mungu. Abu Bakri akawaambia: “Mkidumu katika hali hii ndivyo ipasavyo….”111 Swahaba walia: 1. Swahaba wamlilia kiongozi wa waumini: Alimlilia kiongozi wa waumini Ali bin Abu Talib rafiki hadi adui, na wakamlilia wakazi wa Kufa na Madina, bali sahaba walimlilia pindi zilipowafikia habari za kufa kishahidi wasii wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na khalifa wake, kama anavyotusimulia Allamah Sibt Ibnu Al-Jawziy akisema: “Al-Waqidiy amesema: ‘Zilipowafikia sahaba habari zake walimlilia.”112

110 Tarikhud-Damashqi (Wasifu wa Imam Zaynul-Abidina): 146. 111 Al-Futuhu 1: 2. 112 Tadhkiratul-Khuwwas: 182. 81


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 82

Kumlilia Maiti Wakazi wa Madina walia: 2. Wakazi wa Madina wamlilia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): Abu Dhuaybu Al-Hadhliy amesema: “Nilifika Madina huku watu wake wakipiga mayowe kwa kilio kama mayowe ya mahujaji wanaohirimia. Nikasema: “Ni nini?” Wakasema: ‘Amefariki Mtume wa Mwenyezi Mungu.”113 3. Wakazi wa Madina wamlilia Hasan (a.s.) siku saba: Ibnu Asakir amepokea kwa njia yake kutoka kwa Ibn Abu Najih kutoka kwa baba yake, amesema: “Walimlilia Hasan bin Ali siku saba, huko Makka na Madina, wanawake, watoto na wanaume.”114 4. Wakazi wa Madina wamlilia Hasan hadi wafunga masoko: Ziada ya kumlilia kwao Hasan bin Ali (a.s.) muda wa siku saba vilevile walifunga masoko yao. Kama alivyopokea Ibnu Sa’ad kwa njia yake kutoka kwa Abu Ja’far, amesema: “Watu walikaa wakimlilia Hasan bin Ali siku saba huku masoko yakiwa hayafanyi kazi.”115 Na pia kutoka kwa Ibn Asakir kwa njia yake, kutoka kwa Ubaydullah bin Mirdas, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Hasan bin Muhammad bin AlHanafiyyah, kwenye Hadithi aliyosema: “Hasan alipofariki Madina ilijaa mayowe, hakukutwa yeyote ila alikuwa analia.”116 113 Kanzul-Ummal 7: 265. Hayatus-Sahabah 2: 371. 114 Tarikhud-Damashqi (Wasifu wa Imam Hasan): 235. 115 At-Tabaqat 8: 168. Al-Mustadrak Alas-Sahihayn 3: 173. 116 Tarikhud-Damashqi (Wasifu wa Imam Hasan): 222. Siyaru A’alamunNubalai 3: 275. 82


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 83

Kumlilia Maiti Wanawake wa Bani Hashim walia: 1. Wanawake wa Bani Hashim wamlilia Hasan bin Ali: Al-Hakim amepokea kwa njia yake kutoka kwa Ummu Bakri binti ya AlMusawir kuwa amesema: “Alipofariki Hasan bin Ali wanawake wa Bani Hashim walimlilia mwezi mzima.”117 Ibn Athir ameongeza kuwa: “Na wakavaa nguo nyeusi ya msiba mwaka mzima.”118 Wakazi wa Sham walia: 1. Sham wamlilia na kumwomboleza Husein bin Ali (a.s.): Mateka wa aali Muhammad walipoingizwa kwa Yazid bin Muawiyah huko Sham, Yazid alimwamuru mhutubu apande mimbari, akasema: “Panda mimbari uwape watu habari za mabaya ya Husein na Ali na waliyoyafanya.” Amesema: “Mhutubu akapanda mimbari, akamhimidi Mwenyezi Mungu na kumtukuza, kisha akazidisha kumshusha hadhi Ali na Husein na akifululiza kumsifu Muawiyah na Yazid…. Basi Ali bin Husein akapiga yowe: “Ole wako ewe mhutubu! Umenunua radhi za kiumbe kwa kumchukiza muumba!....” Kisha Ali bin Husein akasema: “Ewe Yazid! Je unanipa idhini nikwee nguzo hizi na kuzungumza maneno yenye ridhaa ya Mwenyezi Mungu na ridhaa ya watu hawa walioketi, yenye thawabu na ujira mwema?” Yazid akakataa. Watu wakasema: “Ewe kiongozi wa waumini, mpe idhini apande mimbari huenda tukasikia kitu kutoka kwake.” Akasema: “Hakika yeye 117 Al-Mustadrak Alas-Sahihayn 3: 173. Tarikhud-Damashqi (Wasifu wa Imam Hasan): 209. 118 Usudul-Ghabah 2: 15. 83


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 84

Kumlilia Maiti iwapo atapanda basi ataendelea mpaka anifedheheshe au kuwafedhehesha kizazi cha Abu Sufiyan…” Anasema: “Waliendelea kumwomba mpaka akapanda mimbari, akamhimidi Mwenyezi Mungu na kumtukuza, kisha akatoa hotuba ambayo ndani yake aliyaliza macho na kuzitetemesha nyoyo, kisha akasema: “Enyi watu! Aliyenitambua ameshanitambua, na asiyenitambua basi nitampa habari za nasaba yangu na ukoo wangu. Enyi watu! Mimi ni mwana wa Makka na Mina, Zamazam na Swafa. Mimi ni mwana wa mbora wa waliohiji, kutufu, kutembea kati ya Swafa na Mar’wa na kuitikia wito….. Mimi ni mwana wa aliyewaswalisha malaika wa mbinguni, mimi ni mwana wa Fatimah Az-Zahra, mimi ni mwana wa mbora wa wanawake wa ulimwengu.” Anasema: “Aliendelea kukariri maneno hayo mpaka watu wakapiga mayowe kwa kilio, Yazid akaingiwa na hofu isije ikatokea tafrani, ndipo akamwamuru mwadhini akisema: “Tukatie maneno haya.” Anasema: “Aliposikia mwadhini amesema Allahu Akbar, kijana akasema: “Hakuna kitu kitukufu zaidi kuliko Mwenyezi Mungu…” Mwadhini aliposema: “Nakiri kwa moyo kuwa Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu” Ali bin Husein alimgeukia Yazid toka juu ya mimbari na kumwambia: “Huyu Muhammad ni babu yangu au ni babu yako? Ukidai kuwa ni babu yako utakuwa umesema uwongo na kukufuru, na ukidai kuwa ni babu yangu basi ni kwa nini umeuwa kizazi chake.” Mwadhini alipomaliza kuadhini na kukimu, Yazid alitangulia na kuwaswalisha watu Swala ya adhuhuri, baada ya kumaliza Swala yake akatoa amri akachukuliwa Ali bin Husein, dada zake na shangazi zake (r.a.) wakatengewa nyumba na kuwekwa huko, wakakaa huko siku kadhaa wakimlilia na kumwomboleza Husein (a.s.).119

119 Al-Futuhu 5: 247. 84


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 85

Kumlilia Maiti Ibn Abbas alia: 1. Ibn Abbas amlilia Imam Hasan bin Ali (a.s.): Ibnu Qutaybah Ad-Daynuriy amesema: “Ulipoingia mwaka wa hamsini na moja Hasan bin Ali aliugua ugonjwa wake uliomuua, basi gavana wa Madina akaandika barua kwa Muawiya kumpa habari za maradhi ya Hasan. Muawiya akamwandikia barua akisema: “Ukiweza kuwa isipite siku yoyote inayonipita ila ziwe zimeshanifikia ndani ya siku hiyo habari zake, basi fanya hivyo.” Basi aliendelea kumwandikia habari za hali yake mpaka alipofariki, akamwandikia kumpa habari hiyo. Alipofikiwa na habari alidhihirisha furaha mpaka akasujudu na waliokuwa naye nao wakasujudu, habari hizo zikamfikia Abdullah bin Abbas, kipindi hicho alikuwa Sham, ndipo akaingia kwa Muawiya, na alipoketi Muawiya akasema: “Ewe Ibn Abbas, Hasan bin Ali amehiliki.” Ibn Abbas akasema: “Ndio amehiliki, hakika sisi sote ni wa Mwenyezi Mungu na hakika sisi sote Kwake tutarejea” akakariri usemi huo. Kisha akasema: “Zimenifikia habari za furaha na nderemo ulizodhihirisha kwa ajili ya kifo chake, wallahi mwili wake hauzibi shimo lako wala upungufu wa muda wa kifo chake hauongezi umri wako. Bila shaka yeye amekufa naye ni mbora kuliko wewe, na kama tumepatwa na msiba wake, tayari tulishawahi kupatwa na msiba wa aliye mbora kuliko yeye, babu yake Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), Mwenyezi Mungu akaziba msiba wake na baada yake akachukua vizuri mno nafasi yake juu yetu.” Kisha Ibnu Abbas akapatwa na kwikwi ya kilio akalia, na wakalia waliokuwepo kwenye hadhara na Muawiya naye akalia, sikuona siku aliyolia sana kama siku hiyo. Muawiya akasema: “Zimenifikia habari kuwa ameacha watoto wadogo.” Ibn Abbas akasema: “Sisi sote tulikuwa wadogo kisha tukakua.” Muawiya akasema: “Amefikisha umri gani?” Ibn Abbas akasema: “Jambo la Hasan 85


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 86

Kumlilia Maiti ni tukufu mno kuliko mtu kutojua mazazi yake.” Anasema: “Muawiya akanyamaa kidogo kisha akasema: “Ewe Ibn Abbas! Umekuwa Sayyid wa kaumu yako baada yake.” Ibn Abbas akasema: ‘Maadamu Mwenyezi Mungu bado amembakiza Abu Abdullah Husein siwezi…”’120 2. Ibn Abbas amlilia Imam Husein (a.s.): Sibt Ibnul-Jawziy amesema: “Alipouawa Husein, Ibn Abbas aliendelea kumlilia mpaka akapofuka.”121 Abu Bakr alia: 1. Abu Bakr amlilia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.): Abdullah bin Hasan Basha amesema: “Imesihi kuwa alipofariki Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alikuja Abu Bakr (r.a.) baada ya kufikiwa na habari, akaingia kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akamfunua uso wake, kisha akamwangukia na kumbusu, kisha akalia na kusema: ‘Baba yangu na mama yangu ni fidia kwako, unapendeza katika hali ya uhai hadi ya mauti, tutaje ewe Muhammad kwa Mola wako Mlezi na tuwe katika kumbukumbu yako.” Katika riwaya ya Ahmad: “Akabusu paji lake kisha akasema: “Ewe Mtume!” kisha akambusu mara tatu na kusema: “Ewe Mteule!” kisha akambusu mara tatu na kusema: ‘Ewe Kipenzi!”122 An-Nasai amepokea ndani ya kitabu chake As-Sunan kutoka kwa Abu Salmah kuwa: “Aisha alimpa habari kuwa, Abu Bakr alifika akiwa juu ya farasi toka maskanini kwake huko Sunhi, akateremka na kuingia msikitini, 120 Al-Imamah Was-Siyasah 1: 150. Al-Aqdu Al-Farid 5: 110. 121 Tadhkiratul-Khuwwas: 152. 122 Sidqul-Khabar Fikhawarijil-Qarni At-Thani Ashar: 328. Al-Muswannaf cha Ibnu Abu Shaybah 8: 565. 86


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 87

Kumlilia Maiti hakumsemesha mtu mpaka akaingia kwa Aisha huku Mtume wa Mwenyezi Mungu akiwa amefunikwa kisaa cha Yemen, akamfunua uso wake kisha akamwangukia na kumbusu, akalia na kusema: ‘Baba yangu na mama yangu ni fidia kwako, wallahi kamwe Mwenyezi Mungu hatokusanya mauti mbili juu yako, ama mauti aliyokuandikia Mwenyezi Mungu tayari yameshakufika.”123 Umar bin Al-Khattab alia: 1. Umar bin Al-Khattab amlilia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.): Amesema ndani ya Swidqul-Khabar kuwa: “Na Umar (r.a.) alipothibitisha mauti ya (s.a.w.w) kupitia kauli ya Abu Bakr, alisema huku akiwa analia: “Baba yangu na mama yangu ni fidia kwako, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Ulikuwa na kisiki ambacho ulihutubia watu ukiwa juu yake, walipoongezeka ulikifanya mimbari, mlio wa kisiki unawafikia kwa kutengana na wewe, mpaka ulipoweka mkono wako juu yake ndipo kikatulia, hivyo bila shaka umma wako ndio unaowajibika zaidi kukulilia pindi ulipotengana nao…”124 Bilal Al-Habashi alia: 1. Bilal Al-Habashi alia kwenye kaburi la Mtume (s.a.w.w.): Al-Jazriy amesema: “Kisha Bilal alimwona Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) usingizini akimwambia: “Ewe Bilal mbona umenitenga sana? Hivi haujafika wakati ukaja kutuzuru?” Ndipo akazinduka akiwa mwenye huzuni, akapanda rikabu kuelekea Madina, akaja kwenye kaburi la Mtukufu 123 Sunanun-Nasai 4: 11. Sunanul-Bayhaqiy 3: 406. Al-Muhli 5: 146. KanzulUmmal 7: 226. 124 Sidqul-Khabar Fikhawarijil-Qarni At-Thani Ashar: 238 87


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 88

Kumlilia Maiti Mtume (s.a.w.w.) na akaanza kulia hapo na kugaragara juu yake. Ndipo wakaja Hasan na Husein wakaanza kumbusu na kumkumbatia, wakamwambia: “Tunatamani uadhini kabla kidogo ya alfajri.” Hivyo akapanda juu ya paa la msikiti, basi alipotamka: “Allah Akbar, Allah Akbar” Madina ilitikisika. Na alipotamka: As-Sh’hadu an’lailaha illa llah “Nakiri kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila Allah” mtikisiko wake ukaongezeka. Na aliposema: “Nakiri kuwa Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu,” wanawake walitoka ndani ya utawa wao, basi hakuna siku iliyoonekana ikiwa na watu wenye kulia sana, wanaume kwa wanawake, kama siku hiyo.”125 Abu Hurayra alia: 1. Abu Hurayra amlilia Imam Hasan (a.s.): Ibnu Asakir amepokea kwa njia yake kutoka kwa Musawir, mtumwa wa Bani Sa’ad, amesema: “Nilimwona Abu Hurayra siku aliyofariki Hasan bin Ali akiwa amesimama kwenye mlango wa msikiti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu huku akilia na kunadi kwa sauti yake ya juu: ‘Enyi watu! Leo amefariki habibi wa Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w.w. hivyo lieni.”126 Said bin Al-‘Aas alia: 1. Said bin Al-‘Aas amlilia Imam Hasan (a.s.): Al-Hakim amesema: “Ibn Amru amesema: ‘Amenisimulia Muslimah kutoka kwa Muharibu kuwa amesema: ‘Hasan bin Ali alifariki mwaka wa hamsini na tano siku tano zilizopita tangu kuingia kwa mfunguo tano, huku 125 Usudul-Ghabah 1: 208. Sidqul-Khabar: 240. 126 Tarikhud-Damashqi (Wasifu wa Imam Hasan): 229. Siyaru A’alamunNubalai 3: 277. 88


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 89

Kumlilia Maiti akiwa na umri wa miaka arubaini na sita. Sa’id bin Al-‘Aas ndiye aliyemsalia na alikuwa akimlilia. Maradhi yake yalichukua siku arubaini.”127 Muawiya alia: 1. Muawiya na hadhira yake wamlilia Ali (a.s.): As-Sibtu Ibnul-Jawziy amepokea kutoka kwa babu yake, amesema: “Amenipa habari babu yangu Al-Faraju, Mwenyezi Mungu amrehemu, amesema: “Ametupa habari Abu Bakr bin Habib As-Sufiy, amesema: “Ametupa habari Abu Sa’id bin Abu Sadiq, ametupa habari Abdullah bin Bal-Wiyh As-Shiraziy. Ametusimulia Abdullah bin Fahd Ibnu Ibrahim AsSabahiy. Ametusimulia Zakariya bin Dinar, kutoka kwa Al-Abbas bin Bakkar, kutoka kwa Abdul-Wahid bin Amru na Al-Asadiy, kutoka kwa Muhammad bin As-Saibu Al-Kalbiy, kutoka kwa Abu Salih, amesema: “Aliingia Dharar bin Dhamrah kwa Muawiya, akamwambia: “Ewe Dharar nipe wasifu wa Ali.” Akasema: “Huniachi?” akasema: “Sikuachi”. Akasema hivyo mara tatu, na ndipo Dharar akasema: “Basi ikiwa haina budi ni kuwa: Wallahi alikuwa katika kilele cha juu kabisa, mwingi wa nguvu, akiongea fasaha, akihukumu kwa uadilifu, elimu yabubujika toka kwake na hekima ikitamka toka kwake huku akitishwa na dunia na mapambo yake na kuliwazwa na usiku na giza lake. “Wallahi alikuwa mwingi wa machozi, mwingi wa fikara, akigeuza kitanga chake na kuisemesha nafsi yake, akipendezwa na kuukuu miongoni mwa mavazi na kigumu miongoni mwa vyakula. Wallahi alikuwa kama mmoja wetu, atujibu tumuulizapo, atuanza tumjiapo, atujia tumwitapo. “Wallahi sisi pamoja na ukuruba wake kwetu na kujongea kwake kwetu tulikuwa hatumsemeshi kwa ajili ya haiba yake, wala hatumwanzi kwa ajili ya heshima yake. Akitabasamu basi ni kama lulu iliyonadhimiwa. 127 Al-Mustadrak Alas-Sahihayn 3: 173. 89


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 90

Kumlilia Maiti Anawaheshimu wanadini na kuwapenda masikini, hamtamani mwenye nguvu katika batili yake wala dhaifu hakati tamaa kutokana na uadilifu wake. “Nakiri kwa Mwenyezi Mungu hakika nilimwona usiku katika baadhi ya misimamo yake, huku usiku ukiwa umeshajifunika giza lake na zimeshachomoza nyota zake, amesimama wima mihrabuni kwake huku kazishika ndevu zake akijigeuza mgeuzo wa mtu salimini na huku akilia kilio cha mwenye huzuni. Nami ni kama namsikia akisema: “Ewe dunia, mghuri asiyekuwa mimi, kwangu mimi umejionyesha ama una shauku na mimi?! Kamwe haiwezekani, kamwe haiwezekani, nimeshakutaliki talaka tatu sipasi tena kukurejea. Umri wako mfupi, maisha yako dufu na hatari yako kubwa. Naumia kutokana na uchache wa masurufu, umbali wa safari na kitisho cha njia.” Amesema: “Machozi ya Muawiya yakabubujika juu ya ndevu zake, hakuweza kuyazuia huku akiyafuta kwa leso yake, na huku watu wakiwa wameshikwa na kilio. Kisha Muawiya akasema: “Mwenyezi Mungu amrehemu Abu Hasan, wallahi hivyo ndivyo alivyokuwa, vipi huzuni yako juu yake ewe Dharar?” Akasema: ‘Huzuni ya mama ambaye mtoto wake kachinjwa juu ya mapaja yake, kilio chake hakitulii wala huzuni yake haikomi.”128 Muhammad bin Al-Hanafiyyah alia: 1. Muhammad bin Al-Hanafiyyah amlilia kaka yake Hasan bin Ali (a.s.): Alipozikwa Hasan bin Ali alisimama mdogo wake Muhammad bin AlHanafiyya juu ya kaburi lake huku akilia, akasema: “Mwenyezi Mungu akurehemu ewe Abu Muhammad, ikiwa uhai wako umetia nguvu basi kifo chako kimeidhoofisha, hakika roho njema ni roho iliyojenga mwili wako, na bila shaka mwili bora ni mwili uliokumbatiwa na sanda yako. Itakuwaje 128 Tadhkiratul-Khuwwas: 118. Al-Fusulul-Muhimmah cha Ibnu As-Sabaghu AlMalikiy: 111. Hayatus-Sahabah 1: 130. 90


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 91

Kumlilia Maiti isiwe hivyo ilihali wewe ni kizazi cha uongofu, mwambata wa wachamungu, na wa tano kati ya watu wa kishamiya, umelelewa kwenye mapaja ya uislamu na umenyonya chuchu za imani. Nawe una heshima adhimu kuliko wengine na malengo ya hali ya juu mno, kupitia kwako Mwenyezi Mungu amesuluhisha makundi mawili makubwa na kuondoa mgawanyiko wa dini. Basi amani iwe juu yako, hakika unapendeza ukiwa hai hadi ukiwa katika mauti.” Kisha akasoma shairi akisema: ‘Nikipake mafuta kichwa changu ama mema yangu yapendeza, ilihali shavu lako limo udongoni nawe umenyakuliwa. Nitakulilia muda wote watakaolia njiwapori wa Aykati, na muda wote ambao tawi litakuwa kijani katika miti ya Riyadh. Mgeni na pande za Hijazi zimemzunguka, fahamu kila aliyekuwa chini ya udongo ni mgeni”’.129 Anas bin Malik alia: 1. Anas bin Malik amlilia Husein (a.s.): Al-Qunduziy amesema: “Kilipobebwa kichwa kitukufu kwa Ibnu Ziyad alikiweka ndani ya bakuli akaanza kukichokora kwa kijiti huku akisema: “Sijawahi kumwona mfano wa huyu.” Anas alikuwa pale akaanza kulia na kusema: “Alikuwa akishabihiana sana na Mtume wa Mwenyezi Mungu kati yao.” Ameipokea At-Tirmidhiy na Bukhari.”130

129 Tadhkiratul-Khuwwas: 213. Tarikhud-Damashqi (Wasifu wa Imam Hasan): 234. Al-Aqdu Al-Farid 2: 8 na 3: 197. 130 Yanabiul-Mawaddah: 389, amenukuu kutoka kwenye Sunan Tirmidhiy 5: 659, japo kuna tofauti kidogo. 91


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 92

Kumlilia Maiti Na imepokewa kutoka kwa As-Shajariy kwa njia yake kutoka kwa Anas, amesema: “Jicho halikuwahi kuona machozi kama siku ambayo kichwa cha Husein bin Ali kililetwa ndani ya bakuli, kikawekwa mikononi mwa Ubaydullah bin Ziyad, Mwenyezi Mungu awalaani wote wawili (baba na mtoto), akawa akikigusa kwa fimbo yake huku akisema: ‘Ikiwa kweli ni maridadi, ikiwa kweli ni jamili.”’131 Zayd bin Arqam alia: 1. Zayd bin Arqam amlilia Husein (a.s.) kwenye baraza la Ibnu Ziyad: Ibnu Abu Ad-Dun’ya amepokea kuwa yeye alikuwa kwa Ibnu Ziyad, ndipo Ibnu Arqam akamwambia: “Ondoa fimbo yako, naapa wallahi ni mara nyingi nimemwona Mtume wa Mwenyezi Mungu akibusu kati ya midomo hii miwili.” Kisha Zayd akawa analia, Ibnu Ziyad akamwambia: “Namwomba Mwenyezi Mungu ayalize macho yako, lau usingekuwa ni kikongwe uliyekwisha ningeipiga shingo yako.” Zayd akasimama huku akisema: “Enyi watu! Baada ya leo ninyi ni watumwa, mmemuuwa mwana wa Fatimah na kumpa utawala mwana wa Marjanah, wallahi kwa hakika atawauwa wabora wenu na bila shaka atawafanya watumwa wale waovu wenu, yuko mbali na heshima yule atakayeridhia udhalili na aibu…..”132

131 Kitabul-Amaliy: 164. 132 Tadhkiratul-Khuwwas: 257. Usudul-Ghabah 2:21. Siyarul-A’alamuinNubalai 3: 315. Yanabiul-Mawaddah: 324. Tarikhud-Damashqi (Wasifu wa Imam Hasan): 381. Al-Kamil fit-Tarikh 3: 434. Al-Istish’hadul-Imam Husayan cha Ibnu Athir: 106. 92


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 93

Kumlilia Maiti Hasani Al-Basriy alia: 1. Hasan Al-Basriy amlilia Husein (a.s.): Az-Zahriy amesema: “Hasan Al-Basriy alipofikiwa na habari za kuuawa kwa Husein alilia mpaka nywele za eneo la kati ya jicho na sikio zikang’oka, kisha akasema: “Umma duni mno ni ule uliomuua mwana wa binti ya Mtume wake, wallahi kichwa cha Husein kitarudi kwenye kiwiliwili chake, kisha babu yake na baba yake watalipiza kisasi kwa mwana wa Marjanah.”133 Ar-Rabi’u bin Khaytham alia: 1. Ar-Rabi’u bin Khaytham amlilia Husein (a.s.): Az-Zahriy amesema: “Ar-Rabi’u bin Khaytham alipopata habari za kuuawa kwa Husein alilia na kusema: “Hakika wameliuwa kundi ambalo lau Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) angewaona basi bila shaka angewapenda kwa mkono wake na kuwakalisha juu ya mapaja yake.” 134 Ibnu Al-Habariyyah alia: 1. Malenga Ibnu Al-Habariyyah amlilia Husein bin Ali (a.s.): As-Sibtu Ibnul-Jawziy amenukuu kuwa malenga Ibnu Al-Habariyyah alipita Karbala, akawa anamlilia Husein na jamaa zake (r.a), akaomboleza kwa shairi akisema: “Je Husein babu yako ametumwa kwa uongofu, naapa haki itakuwa inauliza kuhusu yeye. Lau ungekuwa shuhuda Karbala, 133 Al-Istish’hadul-Imam Husayan cha Ibnu Athir: 268. Yanabiul-Mawaddah: 331. 134 Al-Istish’hadul-Imam Husayan cha Ibnu Athir: 268. Yanabiul-Mawaddah: 331.

93


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 94

Kumlilia Maiti basi ungelitoa juhudi za mbadhirifu katika kujifariji.” Kisha akalala sehemu yake, ndipo akamwona Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akimwambia: “Mwenyezi Mungu akulipe kheri, jibashirie mema, kwani hakika Mwenyezi Mungu ameshakuandika pamoja na wale waliojitolea muhanga mikononi mwa mwanangu Husein.”135 Sulayman bin Qittah alia: 1. Sulayman bin Qittah alizwa na masaibu ya Husein: Al-Qunduziy amesema: “Sulayman bin Qittah alisimama kwenye miili ya Husein na aali zake (r.a.) na akawa analia huku akisema: ‘Nimepita kwenye nyumba za aali Muhammad, sijaona mfano wake siku zilipofikwa. Hakika muuliwa wa Tufi toka aali Hashim, amedhalilisha shingo za maqurayshi, nazo zikadhalilika. Hivi huoni ardhi imeugua kwa sababu ya kumkosa Husein, na kisha nchi imetetemeka. Hakika nimeiona mbingu ikimlilia kwa kumkosa, na nyota zake zikimwomboleza na kutoa sauti. Kwetu sisi walikuwa ni mvua lakini wakarudi wakiwa msiba, bila shaka msiba huo umekuwa mkubwa na adhimu.”’136

135 Tadhkiratul-Khuwwas: 272. Yanabiul-Mawaddah: 332. 136 Yanabiul-Mawaddah: 428. 94


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 95

Kumlilia Maiti Az-Zahriy alia: 1. Az-Zahriy amlilia Imam As-Sajjad (a.s.): Abu Na’im Al-Ispahaniy amesema: “Az-Zahriy alikuwa amtajapo Ali bin Husein hulia na kusema: ‘Pambo la wafanya ibada.”137 Ummu Salamah alia: 1. Ummu Salamah amlilia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.): Al-Waqidiy ameandika kutoka kwa Ummu Salamah (r.a.), amesema: “Tulipokuwa tumejikusanya tukilia huku tukiwa hatujalala, na Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akiwa ndani kwetu, nasi tukiwa tunajiliwaza kwa kumtazama juu ya kitanda, ghafla tulisikia sauti ya kengele za kondoo kabla kidogo ya alfajiri.” Ummu Salama anasema: ‘Tukapiga mayowe na wakapiga mayowe watu wa msikitini, ndipo Madina ikatetemeka kwa mayowe ya pamoja, na Bilal akaadhini kwa ajili ya sala ya alfajiri, hivyo alipomtaja Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alilia na kuinua sauti kwa kilio, nasi akatuzidishia huzuni. Watu wakatatua kitendo cha watu kuingia kwenye kaburi lake, hivyo wakafunga ili kuwazuia, ni msiba mkubwa kiasi gani huu!! Hatukupatwa na msiba mwingine wowote ila ulikuwa mdogo pindi tunapoukumbuka msiba wake (s.a.w.w.) kwetu.”138 2. Ummu Salamah amlilia Husein (a.s.): Ibnu Asakir amepokea kwa njia yake kutoka kwa Shahru bin Hawshab, amesema: “Sisi tulikuwa kwa Ummu Salamah mke wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), tukasikia mwanamke akipiga mayowe, basi kugeuka hivi 137 Hilyatul-Awliyai 3: 138. 138 Hayatus-Sahabah 2: 371. 95


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 96

Kumlilia Maiti nikamwona Ummu Salamah, akasema: “Husein ameuwawa.” Akasema tena: “Kweli wameyafanya? Basi Mwenyezi Mungu azijaze nyumba zao moto.” Na hapo akaanguka akiwa amezimia, na ndipo tukasimama.”139 As-Sibtu Ibnu Al-Jawziy amepokea kutoka kwa Ibnu Sa’ad kutoka kwa Ummu Salamah: “Tulipopata habari za kuuwawa kwa Husein (a.s.) alisema: “Mpaka wameyafanya, Mwenyezi Mungu azijaze nyumba zao na makaburi yao moto.” Kisha akalia mpaka akazimia.”140 Aisha alia: 1. Aisha na wakazi wa Maidina wamlilia Ali (a.s.): Imepokewa kutoka kwa Ibnu Rabih Al-Andlusiy, kutoka kwa Abul Qasim Ja’far kuwa, Muhammad bin Al-Hasaniy amesema: “Ametupa habari Muhammad bin Zakariyya Al-Ghallabiy, amesema: “Ametusimulia Muhammad bin Najiu An-Nawbakhatiy, amesema: “Ametusimulia Yahya kuwa Sulayman amesema: “Baba yangu amenisimulia naye alikuwa kati ya watu waliowakuta sahaba, amesema: “Niliingia mji wa Kufa na ghafla nikamkuta mtu mmoja akiwasimulia watu, nikasema huyu ni nani? Wakasema: “Bakru bin At-Tarmah” basi nikamsikia akisema: “Nilimsikia Zayd bin Husein akisema: “Alipouwawa kiongozi wa waumini Ali bin Abu Talib habari za kifo chake zililetwa Madina na Kulthum bin Amru, muda huo alioleta msiba huo ulikuwa unafanana na muda ambao Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu alifariki, hiyo ni kutokana na waliaji na wapigaji mayowe, wanaume kwa wanawake, mpaka sauti ya vilio vya watu ilipotulia ndipo sahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu 139 Tarikhud-Damashqi (Wasifu wa Imam Hasein): 390. Istish’hadul- Husayan: 128. 140 Tadhkiratul-Khuwwas: 267. Tahdhibut-Tahdhib 2: 306. Yanabiul-Mawaddah: 398. 96


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 97

Kumlilia Maiti (s.a.w.w.) wakasema, njooni twende kwa Aisha mke wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ili tukaone huzuni yake juu ya mwana wa ami ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.). Basi wakasimama watu wote wakaja mpaka nyumbani kwa Aisha (r.a.), wakamwomba idhini na ndipo walipokuta tayari habari zilikuwa zimeshamfikia, naye alikuwa katika kina cha huzuni na wimbi la masikitiko, huku akiwa hachoshwi na kilio na mayowe tangu aliposikia habari zake. Watu walipoiona hali hiyo toka kwake waliondoka, ilipowadia kesho yake inasemekana kuwa: Hakika yeye aliamkia kwenye kaburi la Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), basi hakuna yeyote aliyebaki msikitini miongoni mwa muhajirina isipokuwa alimwelekea kumsalimia, ilihali yeye akiwa hasalimu wala hajibu salamu na wala hawezi kutamka neno kutokana na wingi wa machozi na mzamo wa huzuni huku akikwamwa na machozi yake na yakitapakaa kwenye nguo zake ilihali watu wakiwa nyuma yake. Mpaka akafika chumbani akashika viunzi vya mlango kisha akasema: ‘Amani iwe juu yako ewe Mtume wa uongofu. Amani iwe juu yako ewe Abul Qasim. Amani iwe juu yako ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Na juu ya sahiba wako wawili. Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, mimi ni mwenye kukuletea habari za kifo cha mwenye hadhi kubwa miongoni mwa vipenzi vyako, na ni mwenye kukutajia yule mwenye heshima kubwa kwako miongoni mwa hababi zako. Wallahi ameuwawa hababi wako AlMujtaba na mteule wako Al-Murtadha, wallahi ameuwawa yule ambaye mke wake ndiye mbora wa wanawake, wallahi ameuwawa yule aliyeamini na kutekeleza, hakika mimi ni mwenye kuomboleza niliyehemewa na ni mwenye kumlilia, na lau udongo ungeondolewa juu yako basi ungesema: “Hakika ameuwawa mwenye heshima kubwa kwako kuliko wao, na mwenye hadhi ya juu mbele yako kuliko wao.”141 141 Al-Aqdu Al-Farid 3: 144. 97


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 98

Kumlilia Maiti Zaynab binti Ali alia: 1. Bibi Zaynab binti Ali amlilia Husein (a.s.): Ibnu Kathir amesema: “Ama aali zake na wakeze waliobaki Umar bin Sa’ad aliwawekea mtu atakayewalinda na kuwasimamia, kisha akawapandisha kwenye vipando juu ya viti vyenye kuumiza, basi walipopita eneo la vita na wakamwona Husein na sahaba zake wakiwa wametelekezwa hapo, wanawake walimlilia na wakapiga mayowe na Zaynab akamwomboleza kaka yake Husein na ndugu zake, akasema huku akilia: “Ewe Muhammad! Ewe Muhammad! Mwenyezi Mungu na malaika wa mbinguni wakuswalie. Huyu hapa Husein uwanjani akiwa ametapakaa damu na amekatwakatwa viungo, ewe Muhammad mabinti zako wamechukuliwa mateka na kizazi chako kimeuawa huku wakipigwa na upepo wa Mashariki.” Msimuliaji anasema: ‘Wallahi akamliza kila mmoja, adui mpaka rafiki.” Marrah bin Qays anasema: “Wanawake walipopita kwenye miili ya wahanga walipiga mayowe na kujipiga mashavu…”142 Ummu Kulthum alia: 1. Bibi Ummu Kulthum amlilia Husein (a.s.): Bibi Ummu Kulthum alipoelekea Madina alianza kulia na kuomboleza akisema: “Mji wa babu yetu usikubali, kwa masikitiko na huzuni tumekuja. Tulitoka kwako tukiwa ndugu wote, sasa tumerejea tukiwa hatuna wanaume wala vijana. Mpe habari Mtume wa Mwenyezi Mungu kuhusu sisi, kuwa tumepat142 Istish’hadul- Husayan cha Ibnu Kathir: 111. 98


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 99

Kumlilia Maiti wa na msiba wa kaka yetu. Na hakika wanaume wetu wako Tufi wamelala, bila vichwa na wamewachinja wanetu. Kizazi chako ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu kimeshinda hapo Tufi kikiwa kimeporwa. Hakika wamemchinja Husein na wala hawajachunga heshima yako kwetu ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu. Natamani macho yako yawaone mateka, wakiwa juu ya migongo ya ngamia wamebebwa. Mtume wa Mwenyezi Mungu baada ya hifadhi, macho ya watu yamekuwa yakitutazama. Ulikuwa ukitukinga mpaka macho yako yakavuka, leo maadui wamezuka kwetu. Fatimah lau ungewatazama wametawanywa katika nchi.

mabinti

zako

mateka

wakiwa

Fatimah lau ungewatazama wenye kutahayari, na lau ungemtazama Zaynul-Abidina. Fatimah lau ungetuona tukikesha, na kutokana na mkesha tumekuwa vipofu. Fatimah hukukumbwa kutoka kwa maadui zako na yale tuliyokumbana nayo. Lau uhai wako ungedumu, basi ungeendelea kutuomboleza mpaka 99


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 100

Kumlilia Maiti siku ya Kiyama. Panda huko Baqii usimame na kunadi: Yuko wapi hababi wa kipenzi cha Mola Mlezi wa ulimwengu. Na sema: Ewe ami, ewe Hasan uliyetakasika, familia ya mdogo wako wameshinda wakiwa wamepuuzwa. Ewe ami yangu, hakika mdogo wako ameshinda akiwa mbali nawe, akiwa rehani kwenye joto kali. Bila kichwa, ndege na wanyama pori wamwomboleza waziwazi porini. Lau ewe bwana wangu ungeona jinsi walivyowatembeza harimu, hawakupata msaidizi. Juu ya migongo ya ngamia bila tandiko, na ungeshuhudia familia ikiwa haina sitara. Wakati wa kutoka tulikuwa tumekusanya kila kitu, na sasa tumerejea tukiwa tumepata hasara wenye kuporwa. Tulikuwa kwenye amani ya Mwenyezi Mungu waziwazi, sasa tumerejea kundi dogo lenye khofu. Na bwana wetu Husein akituliwaza, tumerejea huku Husein akiwa rehani. Hivyo sisi ni wenye kupuuzwa bila mlezi, na sisi ni wenye kupiga mayowe juu ya ndugu yetu. Na sisi ni wenye kutembea juu ya migongo, tunatembezwa juu ya 100


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 101

Kumlilia Maiti ngamia wenye kutuchukia.” Mpaka mwisho wa beti zake.143

Zaynab binti Aqil alia: 1. Zaynab binti Aqil amlilia Husein (a.s.) na mashahidi wa Karbala: Al-Qunduziy amepokea kutoka kwa Al-Waqidiy kuwa: “Kilipofika kichwa kitukufu cha Husein Madina, hakuna yeyote aliyebaki humo, walitoka huku wakipiga mayowe kwa kilio, na Zaynab binti Aqil bin Abu Talib akatoka akiwa amejifunua uso wake na kutawanya nywele zake huku akipiga mayowe: “Ewe Husein! Ewe ndugu yangu! Ewe ahli wangu! Ewe Muhammad! Ewe Ali! Ewe Husein!” Kisha akasema: ‘Mtasema nini pindi Mtume atakapowaambia: Mmefanya nini ilihali ninyi ni umma wa mwisho. Kwa watu wa nyumba yangu na wanangu, hivi hamna ahadi ambayo mnapasa kuitekeleza kwa dhima. Kizazi changu na wana wa ami yangu wamepuuzwa, miongoni mwao wamo mateka na wengine wameuwawa wakiwa wametapakazwa damu. Hivi haya ndio malipo yangu nilipowanasihi, kunifanyia ubaya kwa kizazi changu baada ya kuondoka kwangu.”’144

143 Yanabiul-Mawaddah: 425. 144 Yanabiul-Mawaddah: 398. 101


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 102

Kumlilia Maiti Al-Kunjiy As-Shafiiy ameongeza kuwa: “Zaynab Sughra binti Aqil bin Abu Talib alitoka kwa watu huko Baqii akiwalilia wale jamaa zake waliouwawa huko Tufi huku akisema: ……”145 Ummul Banina alia: 1. Ummul Banina awalilia mashahidi wa Karbala: Ummul Banina ambaye ni mama wa ndugu wanne146 waliouwawa alikuwa akitoka kwenda Baqii na kuwaomboleza wanawe kwa maombolezo ya huzuni mno, anawakusanya watu sehemu hiyo na wanakaa kumsikiliza. Marwan alikuwa ni miongoni mwa watu waliokuwa wakija kwa ajili hiyo, alikuwa akiendelea kusikiliza maombolezo yake mpaka analia. Hilo limesemwa na Ali bin Muhammad bin Hamza kutoka kwa An-Nawfaliy, kutoka kwa Hammad bin Issa Al-Jahniy, kutoka kwa Muawiya bin Ammar, kutoka kwa Ja’far bin Muhammad (a.s.).147 Fakhitah binti Qardhah alia: 1. Fakhitah binti Qardhah amlilia Hasan (a.s.): Muhammad bin Jarir At-Tabariy amesimulia kutoka kwa Muhammad bin Hamid Ar-Raziy, kutoka kwa Ali bin Mujahid, kutoka kwa Muhammad bin Is’haqa, kutoka kwa Al-Fadhlu bin Abbas bin Rabi’ah, amesema: “Abdullah bin Abbas alimtembelea Muawiyah, wallahi muda huo nilikuwa msikitini pale Muawiya alipotoa takbira kwa watu wa Iraq, nao wakazi wa Iraq wakatoa takbira, kisha waliokuwa msikitini wakatoa takbira kama ya watu wa Iraq, ndipo akatoka Fakhitah binti Qardhah bin Amru bin Nawfal 145 Kifayatut-Talib: 441. 146 Nao ni: Abbas, Abdullah, Uthman na Ja’far. Ambao ni wana wa Ali bin Abu Talib. 147 Maqatilut-Talibiyin: 56. 102


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 103

Kumlilia Maiti Ibnu Abdu Manafi kutoka kwenye mlango wake mdogo, kisha akasema: “Mwenyezi Mungu akupe furaha ewe kiongozi wa waumini, ni kitu gani hasa kilichokufikia hadi kikakufurahisha?” Akasema: “Kifo cha Hasan bin Ali.” Akasema: “Hakika sisi sote ni wa Mwenyezi Mungu na hakika sisi sote kwake Yeye tutarejea,” kisha akalia na kusema: “Amekufa Sayyid wa waislamu na mwana wa binti ya Mtume wa Mwenyezi Mungu.” Muawiya akasema: ‘Ni vizuri wallahi ulivyofanya, kwani hakika yeye alikuwa hivyo, anastahiki umlilie.”148 Na mwisho wa dua zetu ni kumshukuru Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa ulimwengu.

148 - Murujud-Dhahbi 2: 339. 103


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 104

Kumlilia Maiti

ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL - ITRAH FOUNDATION: 1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9. 10. 11. 12. 13. 14. 15. 16. 17. 18. 19. 20. 21. 22. 23. 24. 25. 26. 27.

Qur'an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Ishirini Uharamisho wa Riba Uharamisho wa uwongo - Juzuu ya kwanza Uharamisho wa uwongo - Juzuu ya pili Hekaya za Bahlul Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.) Hijab vazi Bora Ukweli wa Shia Ithnaashari Madhambi Makuu Mbingu imenikirimu Abdallah Ibn Saba Khadijatul Kubra Utumwa Umakini katika Swala Misingi ya Maarifa Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia Bilal wa Afrika Abudharr Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu Salman Farsi Ammar Yasir Qur'an na Hadithi Elimu ya Nafsi Yajue Madhehebu ya Shia Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur'an Tukufu Al-Wahda 104


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 105

Kumlilia Maiti 28. 29. 30. 31. 32. 33. 34. 35. 36. 37. 38. 39 40. 41. 42. 43. 44. 45. 46. 47. 48. 49. 50. 51. 52. 53. 54. 55. 56. 57. 58. 59.

Ponyo kutoka katika Qur'an. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii Mashukio ya Akhera Al Amali Dua Indal Ahlul Bayt Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna. Haki za wanawake katika Uislamu Mwenyezi Mungu na sifa zake Amateka Na Aba'Khalifa - Kinyarwanda Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) Adhana. Upendo katika Ukristo na Uislamu Nyuma yaho naje kuyoboka - Kinyarwanda Amavu n’amavuko by’ubushiya - Kinyarwanda Kupaka juu ya khofu Kukusanya swala mbili Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Kusujudu juu ya udongo Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s) Tarawehe Malumbano baina ya Sunni na Shia Kupunguza Swala safarini Kufungua safarini Umaasumu wa Manabii Qur’ani inatoa changamoto as-Salaatu Khayrun Mina'n-Nawm Uadilifu wa Masahaba Dua e Kumayl Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata 105


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 106

Kumlilia Maiti 60. 61. 62. 63. 64. 65. 66. 67. 68. 69. 70. 71. 72. 73. 74.

Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mitume Muhammad (s) Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili Kuzuru Makaburi Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu Tujifunze Misingi Ya Dini Sala ni Nguzo ya Dini Mikesha Ya Peshawar Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu Ubora wa Imam 'Ali Juu ya Maswahaba Na Ushia ndio njia iliy onyooka Shia asema haya, Sunni asema haya, Wewe wasemaje? Liqaa-u-llaah Muhammad (s) Mtume wa Allah

75.

Amani na Jihadi Katika Uislamu

76.

Uislamu Ulienea Vipi?

77.

Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s)

78.

Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s)

79.

Amali za Ramadhani

82.

Ujumbe Sehemu ya Kwanza

83.

Ujumbe sehemu ya Pili

84.

Ujumbe sehemu ya Tatu

85.

Amali za Ramadhan

86.

Uhalisi wa Ushia

87.

Fatmatuz-Zahra 106


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:15 PM

Page 107

Kumlilia Maiti

BACK COVER Madhehebu zote za Kiislamu zinakubaliana kwamba ni wajibu kumfanyia maiti mambo manne: 1. Ghusl (josho la sheria), 2. Kafan (kumvisha sanda), 3. Swalatu ’l-mayyit (kumswalia maiti), na 4. Dafn (kumzika). Kuna hitilafu katika namna ya kumswalia maiti, hususan katika kutoa takbira. Wako wanaosema kwamba takbira ni nne, na wengine wanasema ni tano. Na katika suala la kumlilia maiti, wako wanaosema kuwa inafaa kulia (bila ya kutoa maneno) na wako wanaosema haifai. Wandishi wa kitabu hiki wamejaribu kuyafafanuwa masuala haya mawili kwa kutumia Qur’ani, Sunna na matukio ya kihistoria. Kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote. Kutokana na ukweli huu, Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili, ili kuongeza ujuzi wao katika masuala ya dini na ya kijamii.

Kimetolewa na kuchapishwa na: Al-Itrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Nukushi: +255 22 2127555 Barua Pepe: alitrah@raha.com Tovuti: www.alitrah.org Katika mtandao: www.alitrah.info

107


Swala ya maiti final Lubumba Final-D.Kanju.qxd

7/15/2011

Swala Ya Maiti

108

12:15 PM

Page 108


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.