Tiba ya maradhi ya kimaadili

Page 1

Tiba ya Maradhi ya Kimaadili ‫عالج األمراض األخالقية‬

Kimeandikwa na: Sheikh Abdur-Rasul Aal Unuz


‫ترجمة‬

‫عالج األمراض األخالقية‬

‫تأليف‬ ‫الشيخ عبد الرسول آل عنوز‬

‫من اللغة العربية الى اللغة السوا حلية‬


©Haki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: 978 - 9987 – 17 – 094 – 4 Kimeandikwa na: Sheikh Abdur-Rasul Aal Unuz Kimetarjumiwa na: Hemedi Lubumba Kimehaririwa na: Ustadh Abdalla Mohamed Kimepitiwa na: Mubarak A. Nkanatila Kimepangwa katika Kompyuta na: Al-Itrah Foundation Toleo la kwanza: Machi, 2015 Nakala: 1000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. - 19701, Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 / 2127555 Barua Pepe: alitrah@yahoo.com Tovuti: www.ibn-tv-com Katika mtandao: www.alitrah.info


Yaliyomo Neno la Mchapishaji.................................................................................. 1 Utangulizi................................................................................................... 2 Tiba ya Israfu na Ubadhirifu...................................................................... 9 Tiba ya kula Haramu, ikiwemo Rushwa.................................................. 11 Tiba ya kula Riba..................................................................................... 13 Tiba ya Kung’ang’ania kutenda Madhambi............................................. 16 Tiba ya Kupiga Punyeto........................................................................... 20 Tiba ya Kulipiza....................................................................................... 21 Tiba ya Ubahili......................................................................................... 22 Tiba ya Uzushi......................................................................................... 25 Tiba ya Dhulma na Uonevu..................................................................... 26 Tiba ya Kutokuwa na Mipango Mizuri.................................................... 28 Tiba ya Madhara ya Kimalezi na Kimafunzo.......................................... 30 Sifa za Mwalimu mwenye Mafanikio...................................................... 33 Wosia juu ya Malezi ya Watoto............................................................... 35 Tiba ya Starehe Zenye Uharibifu............................................................. 37 Utangulizi................................................................................................. 37 Tiba ya Maradhi ya Kuiga Umagharibi................................................... 39 Tiba ya Uzembe....................................................................................... 41 Tiba ya Uwoga......................................................................................... 41 Tiba ya Kukata Tamaa............................................................................. 43 Tiba ya Kupenda Cheo............................................................................. 45 Tiba ya Uchu wa Mali.............................................................................. 46 Tiba ya Husuda........................................................................................ 48 Tiba ya Hikdi........................................................................................... 51 Tiba ya Ulevi wa Pombe.......................................................................... 52 Tiba ya Kuingilia Yasiyokuhusu.............................................................. 56 Tiba ya Kukhini Amana........................................................................... 57 Tiba ya Kujionyesha (RIYA)................................................................... 59


Tiba ya Zinaa........................................................................................... 61 Tiba ya Dhihaka na Dharau..................................................................... 64 Tiba ya Kutembea kichwa wazi na bila Hijabu....................................... 65 Tiba ya Tabia Mbaya................................................................................ 67 Tiba ya kuwa na Dhana mbaya kwa Muumba na Kiumbe...................... 69 Tiba ya Ushoga na Usagaji...................................................................... 70 Tiba ya kuwa na Matumaini ya Kuishi muda Mrefu............................... 71 Tiba ya Majivuno..................................................................................... 73 Tiba ya kuwa na Haraka........................................................................... 76 Tiba ya Ushabiki na Kuficha Haki........................................................... 77 Tiba ya Kuvunja Ahadi............................................................................ 78 Tiba ya Ghadhabu.................................................................................... 80 Tiba ya Kusengenya................................................................................. 84 Tiba ya Ususuavu wa Moyo..................................................................... 86 Tiba ya Kutokujali Udugu........................................................................ 87 Tiba ya Tamaa.......................................................................................... 89 Tiba ya Kiburi.......................................................................................... 90 Tiba ya Uongo.......................................................................................... 92 Tiba ya Kukufuru Neema......................................................................... 94 Tiba ya Mabaya ya Ulimi......................................................................... 95 Tiba ya Mchezo wa Kamari..................................................................... 97 Tiba ya Njama na Hila............................................................................. 99 Tiba ya Kifo cha Moyo.......................................................................... 100 Tiba ya Unafiki....................................................................................... 102 Tiba ya Kuvunja Heshima ya Muumini................................................. 104 Tiba ya Kufuata Matamanio.................................................................. 106 Tiba ya Mabishano, Mijadala na Mizozo............................................... 108 Tiba ya Kanuniana................................................................................. 110 Tiba ya Wasiwasi................................................................................... 113 v


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

‫بسم اهلل الرحمن الرحيم‬ HIDAYA Kwa yule aliyetumwa kutimiza maadili mema! Kwa yule aliyewatoa watu toka kwenye giza mpaka kwenye nuru! Kwa ndugu zangu na jamaa zangu toka katika familia yangu! Kwa walezi na wenye dhamana na raia wao! Kwa kila mwenye nia ya kurekebisha mwenendo wake na kuitakasa nafsi yake! Kwa kila mwenye kujituma kurekebisha ada yake na mila yake na kuitibu! Kwa kila anayetaka kufikia utukufu wa juu katika maadili, kupata sharafu ya matendo mema, kububujikwa maadili mema na kufuzu kwa furaha na hongera! Natoa bidhaa hii duni nikitaraji kupata mapokezi. Mwandishi.

vi


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

‫بسم اهلل الرحمن الرحيم‬ NENO LA MCHAPISHAJI

K

itabu ulichonacho mikononi mwako asili yake ni cha lugha ya Kiarabu kwa jina la, ‘Ilaju ‘l-Amradhi ‘l-Akhlaqiyyah kilichoandikwa na Sheikh Abdur-Rasul Aal Unuz. Sisi tumekiita, Tiba ya Maradhi ya Kimaadili. Kitabu hiki kinazungumzia kuhusu watu kuishi kwa maadili mema na kuepukana na mambo yanayoporomosha maadili katika jamii kwa kuzingatia kwa ukamilifu mafundisho ya Kiislamu. Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana hususan wakati huu ambapo ulimwengu umejaa dhulma na uporomokaji mkubwa wa maadili. Taasisi yetu ya al-Itrah imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili. Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa na manufaa makubwa kwao. Tunamshukuru ndugu yetu al-Hajj Ustadh Hemedi Lubumba Selemani kwa kufanikisha tarjuma ya kitabu hiki katika lugha ya Kiswahili, pia na wale wote waliosaidia kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha chapisho la toleo hili kuchapishwa na kuwa mikononi mwa wasomaji. Allah awalipe wote malipo mema hapa duniani na kesho Akhera pia. Amin! Mchapishaji: Al-Itrah Foundation

1


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

‫بسم اهلل الرحمن الرحيم‬ UTANGULIZI Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu

K

ila sifa njema ni ya Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa viumbe wote. Swala na salamu ziwe juu ya Muhammadi na aali zake watukufu watoharifu. Mwenyezi Mungu amesema: “Ambao husikiliza maneno, wakafuata mazuri yake zaidi. Hao ndio aliowaongoza Mwenyezi Mungu, na hao ndio wenye akili.” (Sura Az-Zumar: 18). Na amesema: “Na ni juu ya Mwenyezi Mungu njia iliyo sawa. Na nyingine ni kombo. Lau angelitaka angeliwaongoza nyote.” (Sura An-Nahli: 9). Na amesema: “Kwa sababu ya rehma itokayo kwa Mwenyezi Mungu, umekuwa mpole kwao, lau ungelikuwa mkali mwenye moyo mgumu bila shaka wangelikukimbia. Basi wasamehe na uwaombee maghfira na ushauriane nao katika mambo. Utakapoazimia, basi mtegemee Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wamtegemeao.” (Sura Aal Imran: 159) Na amesema: “Enyi mlioamini! Mwitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapowaita kwenye lile litakalowapa uhai. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba mtakusanywa Kwake.” (Sura Anfal: 24).

2


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

Imam as-Sadiq (a.s.) amesema: “Ukitaka kuheshimiwa kuwa mpole. Na ukitaka kudharaulika kuwa mkali.”1 Na amesema tena (a.s.): “Hakika tabia mbaya huharibu amali kama siki iharibuvyo asali.”2 Na amesema tena (a.s.): “Mwenye tabia mbaya huiadhibu nafsi yake.”3 Na amesema tena (a.s.): “Hakika mtu mmoja alikwenda kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akamwambia: ‘Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Niusie.’ Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akasema: ‘Je utafuata wasia wangu iwapo nitakuusia?’ akamwambia hivyo mara tatu na katika kila mara mtu yule akisema ndio ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu. Ndipo Mtume wa Mwenyezi Mungu akasema: ‘Hakika mimi nakuusia kwamba utakapokusudia kufanya jambo kwanza tafakari matokeo yake, kama kuna faida litekeleze na kama lina hasara liache.”’4 Na imam Ali (a.s.) alimwambia mtu mmoja: “Hakika wewe umefanywa tabibu wa nafsi yako, umebainishiwa dawa, umetambulishwa alama ya ugonjwa na umejulishwa dawa yake, basi angalia ni jinsi gani unaipima nafsi yako.”5 Wabobezi wa somo la maadili wametaja dalili nyingi na ushuhuda mwingi kuhusu tiba ya maadili na namna ya kuyanyoosha, kiasi kwamba wameyafananisha na miili, wakasema: Kama ambavyo miili hupatwa na maradhi na mabadiliko, kama kukonda, kusawijika rangi na kupatwa na udhaifu, kadhalika maadili hupatwa na maradhi, na hudhihirika alama za mabadiliko na udhaifu wake katika sura ya mkondo wa kimaadili, mmomonyoko wa kisaikolojia na hasira kwa kadiri ya kiwango cha maradhi na mizizi yake na madaraja ya mabadiliko yatokeayo juu ya miili na katika maadili.   Al-Kafiy Juz. 1, Kitabu cha akili na ujahili, Hadithi ya 29. Al-Bihar Juz. 68, Uk. 393.   Al-Kafiy Juz. 2, Mlango wa tabia mbaya, Hadithi ya 1. 3   Wasailus-Shia Juz. 16, Uk. 28. 4   Al-Bihar Juz. 68, Uk. 339. Kanzul-Fawaid Uk. 194. 5   Tuhaful-Uquul Uk. 305. 1 2

3


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

Kama ambavyo miili yenye maradhi hutibiwa na hatimaye siha yake na uchangamfu wake kurudi, kadhalika maadili yaliyopatwa na maradhi hutibiwa na kurudia katika hali yake ya kawaida na ya sawa, katika hilo hutofautiana kulingana na mabadiliko na hulka za mhusu, kama ilivyo kwenye miili. Bila shaka tumeshaona na kushuhudia jinsi gani mgonjwa anavyotii ushauri wa matabibu, na wanavumilia taabu za matibabu na uchungu wa kujihami ili wapate kupona. Na tumeshuhudia na bado tunashuhudia watu wakifanya kazi kwa kufuata ushauri na maelekezo ya wagunduzi wa chombo fulani cha kimakenika ili wakilinde na uharibifu na wafaidike nacho vizuri iwezekanavyo. Na lau si kwamba inawezekana kutibu maadili na kuyanyoosha basi juhudi zote za Manabii katika kuwafunza watu tabia njema na kuwaelekeza upande wa kheri na wema zisingekuwa na faida, na mwanadamu angekuwa katika hilo kama mnyama, bali mwenye thamani duni na mwenye hali mbaya zaidi kushinda mnyama, ingetupiliwa mbali kuusiana haki na kuusiana subira, pia ingeachwa kuamrishana mema, kukatazana mabaya, mawaidha, nasaha, na adabu za kisharia, na wala mweka sharia (Mwenyezi Mungu) asingehimiza kuboresha maadili kwa kufanya mazoezi na kuyakuza hatua kwa hatua, bali ingekuwa ni vituo vya mazoezi ya wanyama. Mmoja wetu anaweza kujaribu kuyatibu baadhi ya maradhi yamtokeayo miongoni mwa maradhi ya kimaadili, lakini akashindwa kuyatibu ipasavyo, na hatimaye akayaacha maradhi yamtafune huku akiamini kwamba hayana tiba hasa baada ya kushindwa kwake. Sababu ya kushindwa kwake ni kutokujua kwake njia ya matibabu au kutokuwa na azma katika kupambana na nafsi yake, kwa sababu anaona kwamba kuitibu nafsi ni rahisi na ni jambo lililopo chini ya mikono yake, na pindi aonapo ni jambo gumu hulipa mgongo na kuamini kwamba ni jambo muhali. 4


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

Tumeandika yale anayoyahitaji mwenye kujitibu katika maradhi yote ambayo hushambulia maadili na hatimaye kumtoa mhusika katika ubinadamu. Ndiyo, huenda mwanadamu akapatwa na maradhi na akawa mkali mwenye kukunja uso na mwenye kwenda kinyume na hali yake njema ya kimaadili, kwa sababu mbali na akili pia ana kichocheo na kishawishi chenye nguvu, mfano hali ya kujipenda, ghadhabu ya kimwili na mengineyo, hivyo asipoyadhibiti na akayaacha yatawale akili yake humdhibiti na kumwendesha na hatimaye mwanadamu kuwa kama wababe wengine wa kihistoria na waovu wake, na mwenye hatari kubwa zaidi kushinda mbwa mwitu mkali. Sababu ya hali hiyo inawezekana ikawa ni moja ya mambo yafuatayo: 1.

2. 3. 4.

5.

6.

Ufakiri, wenyewe husababisha ukali, chuki, husuda na umimi kutokana na udhalili wa ufukara na machungu ya kutokuwa na kitu, au kwa sababu ya huzuni ya kuondokewa na neema na kukosa utajiri. Utajiri, mara nyingi humpelekea mwenye nao kuchoka, kuwa na kiburi, jeuri, mbabe na mwenye maringo. Mashaka, humbadili mwenye tabia njema na kumpotosha toka katika maadili mema na tabia njema. Unyonge, udhaifu, mabadiliko ya kiafya na kufikia ukongwe na uajuza, jambo ambalo hufanya mishipa yake ichoke na hatimaye kushindwa kufanya subira na kuwavumilia watu na maudhi yao. Ghadhabu, inaweza kumfanya awe na kiburi kwa watu na kuleta mabadiliko katika maadili kutokana na udhaifu wa nafsi au uduni wa hulka. Upweke na kutengwa, husababisha mtu kujihisi kushindwa na kudharaulika, jambo ambalo humfanya awe mwenye 5


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

kukunja uso mwenye kuhisi upweke na mwenye kuwadhania watu vibaya. Kwa kuwa tabia mbaya ni miongoni mwa sifa mbaya na sifa duni kushinda zote, haina budi kwa mwenye kupenda kuifunza tabia njema nafsi yake na kusafisha maadili yake na kuyapamba, afuate ushauri ufuatao: 1.

Achunguze fadhila za tabia njema, athari zake nzuri na hadithi zinazosifia na kuhimiza tabia hizo.

2.

Daima adhibiti viungo vyake na ang’oe visababishi vya tabia mbaya, achunguze sababu zinazopelekea maadili yake kupatwa na mabadiliko, atafute vichocheo, ikiwa ni maradhi ya kiroho au ya kimwili basi ayatibu.

3.

Akumbuke hasara za tabia mbaya na madhara yake makubwa, na kwamba husababisha kuchukiwa na Mwenyezi Mungu, kukimbiwa na watu na kukerwa naye.

4.

Akumbuke ile sura iliyotolewa na Aya tukufu na Hadithi tukufu ya madhambi ya kutisha na hasara zake za kimaada na kiroho hapa duniani na huko Akhera.

5.

Atazame fadhila za toba na athari njema wapatazo wenye kutubu, na pia ukarimu wa msamaha wafunikwao na Mwenyezi Mungu, malipo mema, umuhimu na upole wafanyiwao na Mwenyezi Mungu.

Kuitathmini nafsi dhidi ya kutenda madhambi na kufanya maovu, kwa kuikanya kwa ukali, kurejea na kujitahidi kujuta, kuacha kwa dhati na kutenda faradhi alizowajibisha Mwenyezi Mungu juu yake, kwani nafsi ikipuuzwa hujitenga na haki na hupotoka na kudumbukia kwenye mashaka na maangamio. Na kama ikifunzwa tabia njema 6


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

huangaza kwa maadili mema, hububujika tabia njema na hutukuka kwa furaha na hongera. Mwenyezi Mungu amesema: “Na kwa nafsi na kwa yule aliyeitengeneza. Kisha akaifahamisha uovu wake na wema wake. bila shaka amefaulu aliyeitakasa. Na bila shaka amepata hasara mwenye kuitweza.” (Sura As-Shamsu: 7 – 10). Na amesema: “Basi anayefanya wema sawa na chembe atauona. Na anayefanya uovu sawa na chembe atauona.” (Sura Zilzalah: 7 – 8). Na amesema: “Mwenye kutenda mema, mwanamume au mwanamke, naye akawa ni muumini, tutamhuisha maisha mema; na tutawapa ujira wao kwa mazuri zaidi waliyokuwa wakiyafanya.” (Sura Nahli: 97). Na amesema: “Mwenye kutenda wema basi ni kwa ajili ya nafsi yake, na mwenye kufanya uovu ni juu yake, kisha mtarudishwa kwa Mola wenu Mlezi.” (Sura al-Jathiya: 15). Na amesema: “Atawatengenezea matendo yenu na atawaghufiria dhambi zenu. Na mwenye kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hakika amefuzu kufuzu kukubwa.” (Sura Ahzab: 71). Na amesema: “Na wale ambao wanatenda mema Hakika Mwenyezi Mungu yuko pamoja na wenye kucha.” (Sura anNahli: 128). Pamoja na haya yote inakuwaje mwanadamu asimtii Muumba wake Mtukufu na Mwendeshaji wake Mwenye hikima Mjuzi wa siri zake katika manufaa yake na madhara yake. Na tunaloliamini sisi ni kwamba ni muhali juu ya mwanadamu kupata furaha, usalama, utulivu na raha aitakayo ila kwa kumtii 7


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

Mwenyezi Mungu Mtukufu na kutii sheria Yake na kutekeleza kanuni Zake, kwa kujilazimisha na uchamungu, ile hazina adhimu iliyokusanya aina zote za amani, matarajio ya kimaada na ya kiroho, ya kidini na ya kidunia. Kwa mazungumzo haya nilikuwa na bado naendelea kuizoesha na kuipa dawa nafsi yangu na wapendwa wangu miongoni mwa wanafunzi wa chuo cha Imam al-Hadi (a.s.) mpaka zikakusanyika kwangu karatasi nyingi ambazo waliniomba nizichape ili wafaidike nazo zaidi. Miongoni mwa walionisaidia na akaichosha nafsi yake, akatumia wakati wake pamoja nami katika kazi hii ni wapendwa wangu wawili walio watukufu mheshimiwa ndugu Sayyid Hasun al-Batata, na mheshimiwa ndugu Sheikh Ahmad al-Aliyyum, Mwenyezi Mungu awahifadhi, awalinde, nashukuru kujitolea kwao na abariki juhudi zao. Apokee toka kwetu sote kazi hii chache kwa mapokezi mazuri na atuwafikishe kuitekeleza na kufuata mwenendo wake wa sawa, na atushike mikono yetu sisi na nyinyi katika yale yenye kheri ya nyumba mbili, hakika yeye ni Msikivu Mwenye kujibu. Abdur-Rasul Aali Anuz 1423 A. H.

8


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

TIBA YA ISRAFU NA UBADHIRIFU

6

1.

Atafakari kwa kina Aya zinazopiga vita sifa hii mbaya. Mwenyezi Mungu anasema: “Enyi Wanadamu! Chukueni mapambo yenu katika kila msikiti, na kuleni na kunyweni wala msifanye ufujaji (israf), hakika Yeye hawapendi wafanyao ufujaji (israf).” (Sura al-Aaraf:31). Na amesema tena: “Bila ya shaka mnayeniitia, hastahiki wito duniani wala Akhera. Na hakika marejeo yetu ni kwa Mwenyezi Mungu. Na wanaopita kiasi basi hao ndio watu wa Motoni! (Sura al-Muumin / Ghafir:43). Na akasema: “Na mpe jamaa wa karibu haki yake na maskini na mwana njia, wala usifanye ubadhirifu. Hakika wabadhirifu wamekuwa ni ndugu wa mashetani, na shetani ni mwenye kumkufuru Mola Wake.” (Sura al-Israi: 26 – 27).

2.

Atafakari kwa kina riwaya zilizopokewa toka kwa Ahlul-Bait (a.s.) zinazopiga vita israfu na ubadhirifu.

3.

Akumbuke riwaya na Aya zenye kumsifu mwenye iktisadi na mwenye wastani katika maisha yake. Imam as-Sadiq (a.s.) amesema: “Nimemchukulia dhamana yule mwenye kufanya iktisadi kwamba kamwe hatafukarika.”7

Israfu ni kupindukia kipimo au ni kile kinachotolewa pasipo kumtii Mwenyezi Mungu, kiwe kingi au kichache, nayo ni kukiweka kitu pasipo mahala pake, nayo ni kile kivukacho kipimo cha ukarimu, nao ni kutokujua vipimo vya haki na hivyo kupindukia. Ubadhirifu ni kuiharibu mali, nao ni kutumia mali katika maasi, yaani kutoa mali yote kiasi kwamba asibakiwe na matumizi yake, nao ni kutokujua wastahiki wa haki na hatimaye kuitoa pasipo mahala pake. Ubadhirifu ni dhambi kubwa kushinda israfu, kwa sababu afanyaye israfu huwa amekosea kwa kuzidisha, ama mbadhirifu yeye huwa amekosea katika yote. Sifa zote mbili zimekemewa na sheria na zimesifiwa kwa sifa mbaya. 7   Al-Kabair Minad-Dhunubi Uk. 74. 6

9


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

4.

Atambue kwamba kitendo chake hiki kitampelekea kutengwa na watu wema, waumini na watu wa kheri, kwa sababu wao hawataki kujiweka karibu na rafiki wa shetani na ndugu yake.

5.

Atambue kwamba ubadhirifu utamletea marafiki wa uongo na marafiki waovu, ambao hawatamjua tena baada ya mali yake kwisha.

6.

Hakika ubadhirifu ni sababu ya kutenda mambo ya haramu, mfano kucheza kamari, kutumia mali katika kutenda maovu, na mengineyo mengi miongoni mwa madhambi.

7.

Ajue kuwa kwa kitendo chake hiki atapata hasara duniani na Akhera, kwa sababu hajaitumia mali sehemu yake ili afaidike nayo, na wala hajamnufaisha kwayo mja yeyote miongoni mwa waja wa Mwenyezi Mungu ili apate hadhi ya kupata radhi ya Mola Wake. Si kwamba tu anaweka kitu pasipo mahala pake bali pia ni kwamba anakiondoa mahala pake. Baadhi ya wenye hekima wamesema: “Kutoa kisichostahiki na kuzuia kinachostahiki, ni kosa lile lile moja.”8

Amirul-Muuminin (a.s.) amesema: “Mwenye kufanya israfu ana alama tatu: Hula kisichokuwa chake, huvaa kisichokuwa chake, na hununua kisichokuwa chake.”9 Imam al-Baqir amesema: “Ama yenye kuokoa ni: Kumhofu Mwenyezi Mungu katika siri na dhahiri, kufanya iktisadi katika utajiri na ufukara, na kusema uadilifu katika hali ya ridhaa na hasira.”10

Nurul-Haqiqah Uk. 230 – 231.   Al-Kabair Minad-Dhunubi Uk. 72, 75. 10   Al-Kabair Minad-Dhunubi Uk. 72, 75. 8 9

10


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

TIBA YA KULA HARAMU, IKIWEMO RUSHWA 1. 2.

3.

4.

5. 6.

Atafakari kwa kina athari zilizotajwa ambazo humpata yule anayekula kutokana na pato la halali.11 Achunguze athari za ajabu zinazoachwa na kitendo cha kula haramu. Muhimu kati ya hizo ni kwamba yeye amelaaniwa kwa ulimi wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), na kwamba kula haramu huzuia ibada isipokelewe, na husababisha ususuavu wa moyo, hupunguza riziki na kuiwekea vikwazo.”12 Ajue kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amemlaani mpokea mlungula na mtoa mlungula, amesema (s.a.w.w.): “Jiepusheni na rushwa, yenyewe ni ufukara halisi, na hatanusa harufu ya pepo yule mwenye kujihusisha na rushwa.”13 Ajue kwamba kula haramu huondoa baraka katika mali. Imam as-Sadiq (a.s.) amesema: “Atakayechuma mali kwa njia isiyo ya halali atatawaliwa na mjenzi, udongo na maji.”14 Ajue kwamba kitendo chake hiki kinazuia ibada kukubaliwa na dua kujibiwa. Atafakari kwa kina kauli za Ahlul-Bait (a.s.) zinazohimiza kutafuta halali, kati ya hizo ni kauli ya Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.): “Ibada ina sehemu sabini, sehemu bora kabisa kati ya hizo ni kutafuta halali.” Pia alisema: “Atakayekula halali Malaika atasimama juu ya kichwa chake amuombee maghufira mpaka atakapomaliza kula.”15

Ad-Dhunubu al-Kabirah Juz. 1, Uk. 409 – 412.   Ad-Dhunubu al-Kabirah Juz. 1, Uk. 409 – 412. 13   Ad-Dhunubu al-Kabirah Juz. 1, Uk. 406 – 409. 14   Ad-Dhunubu al-Kabirah Juz. 1, Uk. 406 – 409. 15  Ad-Dhunubu al-Kabirah Juz. 1, Uk. 411. 11

12

11


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

7.

Atosheke na kipato anachokimiliki hivi sasa, na hii ndio maana ya kupangilia kipato kulikosisitizwa na Maimamu wetu (a.s.) katika riwaya nyingi, mfano: “Kuwa na kipimo ni nusu ya kipato.” “Dini ni kupangilia katika kipato.” Lau wangezingatia hilo basi wasingepita njia hii ya kula rushwa, kwani wala rushwa wengi ni wale ambao pato lao la mwezi halikidhi mahitaji yao.

8.

Aimarishe kinga ya kidini, kwani yenyewe ndio pekee inayozuia kula haramu.

9.

Ajifunze toka kwenye familia zinazomzunguka ambazo zimepatwa na uharibifu na mfarakano, kwa sababu kwa kitendo chake hiki huwashirikisha wengine katika kula haramu, nao ni wale watoto wake na watu wa nyumba yake, na hali wao hawajui, na kwa hali hii hupatwa na athari mbaya bila kukusudia. Kati ya athari hizo ni: Kutowatendea haki wazazi wawili, kukata udugu, tabia mbaya, utovu wa nidhamu, kutokuwa na ghera, kutokuwa na staha, kutenda mambo ya haramu, ususuavu wa moyo na mengineyo kama ilivyokuja katika Hadithi: “Chumo la haramu hudhihirika katika kizazi.” Na kama ilivyonenwa: “Kheri humhusu mtu mmoja, na shari huwaenea wote.”16

16

Jamius-Sa’dat Juz. 2, Uk. 167. 12


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

TIBA YA KULA RIBA 1.

Atafakari kwa kina riwaya zinazokataza kula riba, na athari zinazotokana na kitendo hicho, ya chini kabisa ni Mwenyezi Mungu kulijaza tumbo lake moto wa Jahannam.17

2.

Ajue kwamba riba ni sababu ya tofauti ya kimatabaka, kwani mdai mali yake inaongezeka siku baada ya siku, huku mdaiwa ufakiri wake unakua na kumdhiki.

3.

Ajue kwamba kuharamishwa riba ni kukata moja ya njia za ukoloni na vita vya kimataifa, na ni kuipa kazi na juhudi heshima.18

4.

Akumbuke uharibifu mkubwa wa kiroho unaoachwa na kitendo hiki, nao ni: A. Kinamnyima athari za kheri na baraka za kiroho zitokanazo na kutafuta, kufanya kazi, na kujituma katika kupata mahitaji ya maisha. B. Kunamzuia kumtawakali Mwenyezi Mungu, kwa sababu ameitegemea riba iliyoharamishwa, na hajategemea chumo ambalo litabarikiwa na Mwenyezi Mungu. C. Kunamnyima malipo makubwa ambayo yameandaliwa kwa ajili ya mkopo mwema, kwani sadaka ni kwa mema kumi, lakini mkopo ni kwa mema kumi na nane. Na hili halipatikani katika riba,19 kwa sababu yenyewe ni haramu na malipo yake ni madhambi makubwa kisha ni moto.

Al-Kabair Minad-Dhunubi Uk. 28.   Ad-Dhunubu al-Kabirah Juz. 1, Uk. 183 19   Ad-Dhunubu al-Kabirah Juz. 1, Uk. 184 – 185. 17 18

13


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

5.

Ajue kwamba mali ya riba haina baraka. Mwenyezi Mungu amesema: “Mwenyezi Mungu huipunguza riba na huizidisha sadaka. Na Mwenyezi Mungu hampendi kila kafiri afanyaye dhambi.” (Sura al-Baqarah: 276).

6.

Ajue kwamba riba inaweza kuwa sababu ya jamii kuangamia. Hilo limesemwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

7.

Atafakari kwa kina ubaya wa kitendo na ukubwa wake katika Uislamu, kiasi kwamba kimezingatiwa kuwa ni kibaya kushinda kitendo cha kuzini na maharimu sabini ndani nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu.20

8.

Ajue kwamba katika kula riba kuna mambo yenye kuangamiza iwapo hatotubia kitendo hiki, na kumwomba Mwenyezi Mungu maghufira, kama ilivyokuja katika Aya mbili za Qur’ani Tukufu: 278 – 279 za Sura al-Baqarah. Jambo la kwanza ni kupigana vita na Mwenyezi Mungu. Pili ni kupigana vita na Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na tatu ni kuwa miongoni mwa watu wa motoni.

9.

Ajue kwamba kutaka kupata kupitia riba ni aina moja ya kupenda mali, na bila shaka Mwenyezi Mungu amekataza sifa hii ndani ya Kitabu chake, kama alivyoikataza Mtume wake kwa kusema: “Kupenda mali na cheo huotesha unafiki, kama maji yaoteshavyo nyasi.”21 Pia tambua kwamba mnafiki hanusi harufu ya Pepo milele. Na miongoni mwa athari za unafiki ni kwamba yeye humchukia Amirul-Muuminina Ali (a.s.) na watoto wake, na hatimaye huwa mwenye kumchukia Mwenyezi Mungu na Mtume Wake (s.a.w.w.), kama ilivyokuja ka-

20 21

Ad-Dhunubu al-Kabirah Juz. 1, Uk. 194.   Jamius-Sa’dat Juz. 2, Uk. 46.. 14


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

tika riwaya mutawatiri. Hivyo aichunguze nafsi yake kama ni muumini, je kweli yeye ni mwenye kumchukia Mola Wake?!! Basi ajiepushe kutenda hiki. Imam as-Sadiq (a.s.) amesema: “Dirhamu moja ya riba ni dhambi kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu kushinda kuzini na maharimu sabini ndani ya nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu.”22

22

Safinatul-Bihar Juz. 3, Uk. 296. 15


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

TIBA YA KUNG’ANG’ANIA KUTENDA MADHAMBI 1.

Achunguze kwa makini Hadithi zilizopokewa kuhusu jambo hili. Na akumbuke ubaya wa madhambi na ukali wa adhabu yake.23 Na pia yale yaliyopokewa katika kuwakemea watenda madhambi na waasi. Pia azingatie hekaya za Manabii na wanaibada wakubwa na amweke Mwenyezi Mungu mbele ya macho yake.

2.

Akumbuke zile Hadithi zilizopokewa kuhusu adhabu, zinazozungumzia adhabu za kijamii za madhambi, kama pombe, wizi na uuaji.24

3.

Asighafilike na kauli ya Mwenyezi Mungu: “Ole wetu! Kina nini kitabu hiki hakiachi dogo wala kubwa ila kinalihesabu?” (Sura al-Kahfi: 49). Na kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na ama yule aliyeogopa kusimama mbele ya Mola wake Mlezi, na akaikataza nafsi yake matamanio. Basi hakika pepo ndiyo makazi.” (Sura Naziat: 40 - 42).

4.

Akumbuke udhaifu wa nafsi yake na kushindwa kwake kuvumilia adhabu na mateso ya duniani, nayo ni adhabu yenye kuondoka, lakini pamoja na hivyo hawezi kuivumilia, itakuwaje kwa adhabu ya Akhera ambayo ni yenye kudumu isiyo na mwisho.

5.

Akumbuke uduni wa dunia na utukufu wa Akhera, hivyo aitoe muhanga ya kwanza kwa ajili ya kupata ya pili.25

Jamius-Sa’dat Juz. 3, Uk. 17. Majumuatuw-Waram Juz. 1, Uk. 6.   Al-Muhujatul-Baydhau Juz. 7, Uk. 96. 25   Jamius-Sa’dat Juz. 3 Uk. 87. 23 24

16


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

6.

Atubu dhambi.26

7.

Amdhukuru Mwenyezi Mungu bila shaka Yeye ndiye ponyo.27

8.

Adumishe udhu.28

9.

Akithirishe kwenda misikitini.29

10. Angojee Sala baada ya Sala.30 11. Azingatie hikaya na habari za waja wema waliotangulia, na yale matatizo yaliyowapata kwa sababu ya madhambi yao (wale ambao waliokuwa waovu kabla ya kubadilika kwao), hakika hilo lina athari sana na manufaa makubwa ndani ya nyoyo za viumbe.31 12. Ajue kwamba kuharakishiwa adhabu duniani kunatokana na dhambi, na kwamba kila tatizo analolipata mja ni kwa sababu ya makosa yake.32 13. Ajue kwamba uasi humletea kutelekezwa duniani na Akhera.33 14. Aombe maghufira na kujutia dhambi, na aazimie kutokurudia katika dhambi, aumie na alie na ahofu dhambi.34 15. Awe na tabia nzuri, kwani huondoa makosa. Ama tabia mbaya yenyewe hupelekea kutenda madhambi.35 16. Awasaidie wenye matatizo, hakika kufanya hivyo ni kafara ya madhambi.36   Majumuatuw-Waram Juz. 1, Uk. 6.   Majumuatuw-Waram Juz. 1, Uk. 8. 28   Majumuatuw-Waram Juz. 1, Uk. 5. 29   Majumuatuw-Waram Juz. 1, Uk. 5. 30   Majumuatuw-Waram Juz. 1, Uk. 5. 31   Al-Muhujatul-Baydhau Juz. 7, Uk. 94. 32   Al-Muhujatul-Baydhau Juz. 7, Uk. 95. 33   Miratur-Rashadi Uk. 23. 34   Al-Akhlaq Uk. 255. 35   Al-Akhlaq Uk. 255. 36   Al-Bihar Juz. 75, Uk. 21, Hadithi ya 21. 26 27

17


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

17. Akithirishe kusujudu, hakika kufanya hivyo kunafuta madhambi, kwa mujibu wa Hadithi ya Mtume (s.a.w.w.).37 18. Umra moja mpaka Umra nyingine ni kafara ya madhambi yaliyotokea baina ya Umra hizo mbili.38 19. Amsalie sana Mtume Muhammadi na aali Muhammadi, kwani kufanya hivyo ni kafara ya madhambi.39 20. Azingatie madhara ya dhambi, ambayo kati ya hayo ni kupatwa na mabalaa, kumwogopa mtawala, kupatwa na maradhi, kufungiwa riziki, kuteseka wakati wa kifo,40 kupatwa na adhabu ya Akhera41 na ususuavu wa moyo.42 21. Ajue kwamba katika madhambi mna kumchukiza Mwenyezi Mungu, kumuudhi Mtume (s.a.w.w.) na Maimamu (a.s.), kwa sababu vitendo vyote huonyeshwa kwao kila siku, hivyo wanapoona kitendo kizuri hufurahishwa nacho, na wanapoona kile kibaya huudhika nacho, hiyo ni kwa mujibu wa riwaya mbalimbali. Imam Ali (a.s.) amesema: “Lau hisabu isingekuwa na kitisho ila aibu ya kusimamishwa mbele ya Mwenyezi Mungu, na fedheha kufichuliwa mabaya yaliyojificha, basi ingestahiki kwa mtu kutokushuka toka kwenye vilele vya milima, wala kukimbilia kwenye majengo, kutokula, kutokunywa wala kulala ila kwa dharura ambayo imeungana na kifo (yaani kutenda lile ambalo ndio sababu   Al-Bihar Juz. 85, Uk. 162, Hadithi ya 6.   Al-Bihar Juz. 99, Uk. 50, Hadithi ya 46. 39   Al-Akhlaq Wal-Adab Uk. 255. 40   Al-Wasail Juz. 15 Uk. 304. 41   Jamius-Saadat Juz. 3, Uk. 92. 42   Na mengineyo yaliyotajwa ndani ya kitabu al-Bihari cha al-Majliisiy 37 38

18


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

ya kifo chake), mfano wa hayo hutenda yule ambaye anakiona Kiyama na vitisho vyake, na hali zake ngumu vikiwa ndani ya kila nafsi.”43 Mwenyezi Mungu amesema: “Na wajizuilie na machafu wale wasiopata cha kuolea, mpaka Mwenyezi Mungu awatajirishe katika fadhila zake. Na wale ambao wanataka kuandika katika wale ambao imewamiliki mikono yenu ya kuume, basi waandikieni kama mkiona wema kwao. Na wapeni katika mali ya Mwenyezi Mungu aliyowapa. Wala msiwalazimishe vijana wenu wa kike kufanya umalaya kwa ajili ya kutafuta pato la maisha, ikiwa wanataka kujichunga. Na atakaye walazimisha basi Mwenyezi Mungu baada ya kulazimishwa kwao huko ni Mwingi wa maghufira, Mwenye kurehemu.” (Sura Nuru: 33), kwa subira na Swaumu.

43

Al-Bihar Juz. 99, Uk. 50, Hadithi ya 46. 19


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

TIBA YA KUPIGA PUNYETO 1.

Ajue kwamba ni miongoni mwa madhambi ambayo yameahidiwa adhabu. Imam as-Sadiq (a.s.) amesema: “Watu wa aina tatu Mwenyezi Mungu hatowazungumzisha, wala hatawatazama na wala hatowaepusha na adhabu kali, bali wataipata: mwenye kung’oa mvi zake, mwenye kupiga punyeto na shoga.”44

2.

Ajue kwamba watu wakijua hutenda kitendo hicho watamwona mchafu na watajitenga naye. Imam as-Sadiq (a.s.) amesema: “….Nikimjua anayekitenda sintokula naye.”45

3.

Ajihifadhi kwa Swaumu na aitumie kuimarisha azma yake.

4.

Barobaro kapera atafute msaada kupitia kile kilicho halali, kama vile kujisomea na kufanya mazoezi kama kulenga shabaha, mashindano ya ngamia na njia nyingine za kisasa za mapumziko zilizo halali.

5.

Ni juu ya wazazi wa kiume na wa kike kuwafatilia watoto wao, khususan yule aliyefikia umri wa balehe, wawafuatilie kwa karibu sana, kiasi kwamba wajue kila dogo na kubwa walitendalo bila wao kujua.

6.

Kuna jukumu lingine la jamii, nalo ni kwamba watilie muhimu suala la ndoa, wapunguze kiwango cha mahari na mambo mengine yanayohusu ndoa. Na ni juu ya asasi za misaada kutimiza mahitaji ya lazima ya ndoa.

44 45

Wasailus-Shia Juz. 2, Uk. 131.   Wasailus-Shia Juz. 28, Uk. 364. 20


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

7.

Atafakari kwa kina kijana huyu maradhi ya kimwili na kisaikolojia yanayomsibu yule mwenye kutenda kitendo hiki, nayo ni mengi, nayo ni kulemaa kwa utupu, maradhi ya ngozi, kutokupata ladha ya kujamiiana na mke, utupu kutosimama barabara wakati wa kujamiina, na hiyo ni kutokana na mishipa kusinyaa na kuchoka, na mengineyo miongoni mwa mambo ya kisaikolojia ambayo humfanya mwanadamu kutokuwa na hamu ya kujamiiana na mkewe.

TIBA YA KULIPIZA 1.

Azingatie madhara yake hapa duniani na huko Akhera.

2.

Akumbuke faida za kuacha kufanya hivyo.

3.

Ajue kwamba kuhamishia ulipizaji huo kwa mlipizaji wa kweli ambaye ni Mwenyezi Mungu ndio vizuri na bora zaidi, na kwamba ulipizaji Wake ni wa ukali sana na nguvu sana.

4.

Azingatie faida za kusamehe na ubora wake, kitendo ambacho ni kinyume na ulipizaji.46 Malenga anasema: “Ukiwa unataka kuadhibu ili ujiridhishe, basi usijinyime malipo ya kusamehe.”47 Na kuna kauli ya Imam Ali (a.s.) kuhusu maana hii, nayo ni: “Ukimdhibiti adui yako basi fanya kumsamehe kuwa shukrani ya kumdhibiti kwako.”48

Jamius-Saadat Juz. 1, Uk. 301.   Jamius-Saadat Juz. 1, Uk. 259. 48   Al-Mustatraf Juz. 1, Uk. 257, Mlango wa 36. 46 47

21


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

TIBA YA UBAHILI 1.

Akithirishe kuzingatia habari zinazolaumu ubahili na kusifia ukarimu.49 Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Ubahili hukusanya mabaya ya moyo, nao ndio hatamu ambayo hutumika kuongozea kwenye kila lililo baya.”50 Hakika bahili yuko mbali na Mwenyezi Mungu na yuko karibu na moto. Mkarimu yuko karibu na Mwenyezi Mungu na yuko mbali na moto.

2.

Akithirishe kutafakari kuhusu hali za mabakhili, na jinsi Hadithi zilivyochukizwa nao,51 nazo ni nyingi sana kiasi kwamba hata baadhi ya waandishi wametenga milango makhususi kuhusu ubahili, kama ilivyo katika kitabu al-Mustafrif na vinginevyo.

3.

Ajikalifishe kutoa, wala asiutii ushawishi wa shetani ambaye anamwahidi ufukara.52

4.

Ama aliyezidiwa na maradhi ya ubahili, tiba yake ni aidanganye nafsi yake kwa kupata jina zuri na umaarufu wa ukarimu.53

5.

Ajiepushe na sababu zinazoleta maradhi haya mabaya, nazo ni54: A – Kuipenda dunia. B – Kujipa matumaini ya kuishi muda mrefu. C – Kuogopa ufukara. D – Kupenda.

Al-Muhujatul-Baydhau Juz. 6 Uk. 87.   Al-Mustatraf Juz. 1, Uk. 239, Mlango wa 34. 51   Jamius-Saadat Juz. 2, Uk. 120. 52   Jamius-Saadat Juz. 2, Uk. 120. 53   Jamius-Saadat, Juz. 2, Uk. 120. 54   Jamius-Saadat, Juz. 2, Uk. 120. 49 50

22


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

6.

Ajue kwamba ubahili ni sifa mbaya inayopelekea kukengeuka ahadi zote za kimaadili na za kibinadamu, na imuweka mwanadamu katika hatari ya kulalamikiwa, kudharauliwa na kushutumiwa na jamii, zaidi ya hapo ni kwamba mwisho hupelekea akili za bahili kugota na fikra zake kusimama.55 Mshairi amesema: “Ukiwa mkusanya mali zako mwenye kuzing’ang’ania, basi wewe ni mhazini Wake na mtunzaji Wake. Unazipeleka na hali ni mwenye kulalamikiwa kwa yule ambaye si mwenye kusifiwa. Anazila kwa moyo mtulivu na hali wewe ni mwenye kuzikwa.”56

7.

Ajue kwamba bahili hana raha wala faida na utajiri wake ila mahangaiko na maumivu.57 Mshairi amesema: “Amenipa kukusanya mali kisha nikaiweka hazina, umefika wakati wa kifo changu, je, nitaongezewa umri kwayo? Bahili anapoihifadhi mali bila shaka itamrithisha mashaka na kumwachia mzigo.”58

8.

Ajue kwamba hakika matajiri walio mabahili husababisha uharibifu wa kijamii, kwani hakika mgandamizo uliyomo ndani ya nafsi za walionyimwa ikiwemo mfundo wa kinafsi, machungu na taabu ambazo huisababishia uzito jamii ni miongoni mwa sababu za kuenea uharibifu na kuenea kwa maovu kwa aina zake mbalimbali.59

9.

Ajue kwamba sababu ya ujeuri na dhulma ni kupenda mali na utajiri kama ilivyokuwa kwa Qarun.60

Dirasatu Fil-Mashakil al-Akhlaqiyyah, Uk. 170.   Nurul-Haqiqah, Uk. 228. 57   Nurul-Haqiqah, Uk. 168. 58   Al-Mustatraf, Juz. 1, Uk. 239. 59   Dirasatu Fil-Mashakil al-Akhlaqiyyah, Uk. 169. 60   Al-Amthal, Juz. 12, Uk. 288. 55 56

23


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

10. Ajue kwamba anaweza kupata Akhera na maisha ya milele kupitia mali, hivyo asiukunje mkono wake shingoni mwake (asiwe bahili), wala asiukunjue moja kwa moja (asiwe mbadhirifu). Mwenyezi Mungu amesema: “Na utafute kwa aliyokupa Mwenyezi Mungu makazi ya akhera; wala usisahau fungu lako la dunia. Na fanya wema kama alivyokufanyia wema Mwenyezi Mungu, wala usitafute ufisadi katika ardhi; hakika Mwenyezi Mungu hapendi wafisadi.” (Sura al-Qasas: 77). 11. Ajue kwamba yeye huwa ni mhazini wa mwingine kwenye kipato chake kilichozidi juu ya maisha yake na mahitaji yake, na atahesabiwa juu ya hilo.61 12. Ajue kwamba sifa ya ghururi na ulevi zitokanazo na wingi wa mali, hazimruhusu mwanadamu kusikiliza nasaha za wengine na kumfuata atakayemtakia kheri.62 13. Mwanadamu ajue kwamba kama ambavyo yeye daima anataraji neema za Mwenyezi Mungu, hisani Yake, kheri Yake na huruma Yake, kadhalika wenzake wanataraji hayo kutoka kwake, hivyo awafanyie hisani.63 14. Azingatie yaliyomo ndani ya visa vya watu watukufu ambao wametoa mali na wala utoaji wao haujawapunguzia chochote bali umewazidishia heshima, utukufu, neema na hadhi. 15. Atizame utoaji wa maadui, na jinsi gani ambavyo wanapanga njama kupitia mali zao ili kuzinunua akili zetu na kila kilichopo kwetu. Na mkabala na hayo ni kwamba iwapo tutasimama na hali tumekunja mikono yetu basi watatekeleza njama zao kwa   Al-Amthal, Juz. 12, Uk. 290.   Al-Amthal Juz. 12, Uk. 302. 63   Al-Amthal Juz. 12 Uk. 291. 61 62

24


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

njia rahisi mno, na hatimaye tutasema wametoa ili muendelee. Amirul-Muuminin Ali (a.s.) amesema: “Bahili ananistaajabisha, anaukimbilia ufukara ambao aliukimbia, na anapitwa na utajiri ambao yeye aliutafuta. Hivyo anaishi duniani maisha ya mafukara, na Akhera atahesabiwa hesabu ya matajiri.”64

TIBA YA UZUSHI 1.

Ajue kwamba uzushi ni miongoni mwa madhambi makubwa bali kanuni ya ubora dhambi yake ni kubwa kushinda utesi, kwa sababu wenyewe umekusanya mambo mawili pamoja: Utesi na uwongo.65

2.

Azingatie yaliyomo kwenye riwaya ambazo hubainisha fedheha na matokeo mabaya ya uzushi siku ya Kiyama. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Atakayemzushia muumini wa kiume au wa kike au akamsemea asiyokuwa nayo, Mwenyezi Mungu atamsimamisha juu ya kilima cha moto Siku ya Kiyama mpaka afute aliyoyasema.”66

3.

Ajue kwamba tiba ya uzushi inapatikana tu katika imani na uimara wake wa kutafakari kwa kina athari mbaya za khiyana hapa duniani, na adhabu yake huko Akhera.

4.

Aliweke jambo la ndugu yake sehemu nzuri kushinda zote.

5.

Ajue kwamba ni haramu kuwa na dhana mbaya dhidi ya muumini. Muradi wa hilo ni kwamba moyo wake usiweke wala

Nahjul-Balagha, hikima ya 126.   Ad-Dhunubu al-Kabirah Juz. 2, Uk. 376. 66   Ad-Dhunubu al-Kabirah, Juz. 2, Uk. 376. 64 65

25


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

usimhukumu kwa ubaya bila kuwa na yakini. Ama mawazo na hali za kinafsi, hayo yamesamehewa. 6.

Jambo hilo lina adhabu ambazo zimewekwa na sharia juu ya kila anayewazushia waumini wasiyokuwa nayo. Qur’ani imewaita hao wenye kuzusha kuwa ni mafasiki.

7.

Imam as-Sadiq (a.s.) amebainisha kwamba: “Muumini anapomtuhumu nduguye, imani huyeyuka toka moyoni mwake kama chumvi iyeyukavyo ndani ya maji.”67

8.

Ajue kwamba mlango wa toba uko wazi kwake, hivyo aharakishe kutubu. Mwenyezi Mungu baada ya kutaja adhabu kali kwa mwenye kwenda kinyume na sharia, amefuatiliza kauli yake: “Isipokuwa wale waliotubia baada ya hayo na wakatengenea; kwani hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kughufiria, Mwenye kurehemu.” (Sura Nuru: 5).

TIBA YA DHULMA NA UONEVU 1.

Amuombe Mwenyezi Mungu kinga dhidi ya maradhi haya.68

2.

Ajue kwamba maradhi haya yasiyokubalika ni sawa na kumshirikisha Mwenyezi Mungu, na adhabu yake huanza hapa hapa duniani na baadaye ndio huko Akhera. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Hakika uovu wenye adhabu ya haraka ni dhulma.”69

Usulul-Kafiy, Juz. 2, Uk. 269.   Safinatul-Bihar Juz. 1, Uk. 338. 69   Jamius-Saadat Juz. 1, Uk. 364. 67 68

26


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

3.

Akate sababu zake ambazo ni: A – Ghururi. B – Kiburi. C – Ujinga. D – Uzembe. E – Uchache wa imani.

4.

Azingatie athari zake, nazo ni kwamba dhulma huondoa neema na huleta adhabu, husababisha kuangamizwa na husogeza karibu vifo na hupeleka motoni,70 kwa sababu ni kuwafanyia kiburi wenye haki.

5.

Azingatie sifa zilizopatikana katika kusifia kitendo cha kujisalimisha na kunyenyekea, na kwamba mwislamu wa kweli ni yule anayesalimisha mambo yake kwenye Uislamu na kwa viongozi wa Uislamu, na hivyo anafuata yale wanayomwamuru.71 Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Dhambi za aina tatu adhabu yake huharakishwa na wala haicheleweshwi mpaka Akhera: Kuwavunjia haki wazazi wawili, kuwadhulumu watu, na kutothamini hisani.”72 Mtume (s.a.w.w.) amesema tena: “Lau ikitokea mlima kuudhulumu mlima mwingine basi Mwenyezi Mungu atauangamiza ule uliodhulumu kati ya hiyo miwili.”73

Mizanul-Hikma Juz. 1, Uk. 441.   Bidayatul-Akhlaq, Uk. 88. 72   Al-Wasail, Juz. 16, Uk. 312. 73   Safinatul-Bihar, Juz. 7, Uk. 338. 70 71

27


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

TIBA YA KUTOKUWA NA MIPANGO MIZURI 1.

Ajue kwamba kupangilia mambo yake, muda wake na mambo yanayomzunguka, kunamuongezea juhudi na muda.

2.

Ajue kwamba nidhamu ndio muhimili wa ulimwengu ambao ni sanaa ya Muumba Mtukufu, sembuse sisi.74

3.

Hakika wale watu waliofanikiwa wamefanikishwa hilo kwa sababu walipangilia maisha yao kwa mpango makini, hivyo wao wanaendelea katika maisha kwa kufuata njia sahihi, na huu ndio muhimili wa mataifa yaliyoendelea. Wajapani hawajafika katika maendeleo hayo ila kwa sababu ya umakini katika kazi zao, mipango yao na wakati wao.75

4.

Hakika kutokuwa na mipango na kutoratibu muda kuna matokeo mabaya yasiyopendeza ambayo hupelekea kwenye hasara, au kufeli, au kupoteza na hasara nyingine mfano wa hizo.

5.

Ajue kwamba mipango na uratibu ni sehemu ya wosia wa Maimam (a.s.). Imepokewa kwamba Imam Amirul-Muuminin (a.s.) alisema saa za mwisho za uhai wake: “Nakuusieni nyinyi wawili – Hasan na Husain (a.s.) - na wanangu wote, jamaa zangu na kila atakayefikiwa na wosia wangu huu, kwanza kumcha Mwenyezi Mungu na kupangilia mambo yenu…” 76Mgawanyo wa nyakati katika ibada ni njia hai ya wosia wa Uislamu juu ya mgawanyo wa muda.77

Nahwu Hayati Afdhal Uk. 156 na 157.   Nahwu Hayati Afdhal, Uk. 156 na 157. 76   Nahjul-Balagha, barua ya 47, Uk. 421, chapa ya Subhis-Salih. 77   Nahwu Hayati Afdhal ,Uk. 157 na 158. 74 75

28


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

6.

Ajiepushe na mahusiano ya kijamii yanayopelekea kupoteza wakati, juhudi na uwezo uliopo, na ukomee kwenye majukumu ya dharura tu.78

7.

Augawe wakati wake kama walivyousia Maimamu (a.s.), Imam Kadhim (a.s.) amesema: “Jitahidini kwamba zama zenu ziwe na saa nne: Saa kwa ajili ya kumwabudu Mwenyezi Mungu. Saa kwa ajili ya kutafuta maisha. Saa kwa ajili ya kujumuika na familia, waaminifu ambao wanawaonyesheni dosari zenu na wanatoa kwenu la moyoni mwao kwa ikhlasi. Na saa kwa ajili ya faragha yenu na starehe isiyo ya haramu, kwani saa hii ndio itakayowawezesha kutimiza majukumu ya saa tatu zilizotangulia.”79

8.

Ajue kwamba moja ya sababu za ufukara na kuzorota kwa uchumi wa mtu mmoja mmoja na jamii kwa jumla ni kutokuwepo kwa mipango na mahesabu makini katika harakati mbalimbali. Imam Amirul-Muuminin (a.s.) amesema: “Kutokuwa na mipango katika maisha kunaleta ufukara.”80

9.

Ajue kwamba ubadhirifu hautomwachia chochote, na kwamba upole katika kupangilia maisha ni bora kushinda kuwa na mali nyingi.81

10. Ajue kwamba upole, mikakati na mipango mizuri, mambo haya yana baraka na kheri. Kutokuwa mpole ni kujinyima kheri. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Hakika katika upole mna kheri na baraka, atakayenyimwa upole kany  Mir’atur-Rashad Uk. 109.   Tuhaful-Uquul Uk. 302. Nahwu Hayati Afdhal, Uk. 162. 80   Al-Wasail, Juz. 1, Uk. 42. Nahwu Hayati Afdhal, Uk. 162 81   Al-Wasail, Juz. 15, Uk. 270, hadithi ya 5. 78 79

29


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

imwa kheri.”82 Amirul-Muuminin (a.s.) amesema: “Mikakati mibaya ni sababu ya uharibifu.” Akasema tena (s.a.w.w.): “Mikakati mibaya ni ufunguo wa ufukara.”83

TIBA YA MADHARA YA KIMALEZI NA KIMAFUNZO 1.

Ajifunze kwa undani utamaduni wa Kiislamu, thamani yake na maendeleo yake. Na aonyeshe athari zilizoachwa na utamaduni huu katika tamaduni nyingine za kibinaadamu.

2.

Aisome jamii ya sasa ya Kiislamu ili aweze kujua nyenzo za mabadiliko yenye kuendelea na ili atambue maeneo yenye nguvu na yenye udhaifu. Na ajue kila nukta kati ya nukta zake ili aweze kuchangia na kusaidia kutengeneza jamii ya Kiislamu yenye mwamko, imara na yenye umoja, ambayo inalenga kusimamia uadilifu, kuboresha mustawa wa maisha, na kuleta amani ya mtu mmoja mmoja na jamii kwa jumla.

3.

Kuonyesha mshikamano wa kijografia na kitamaduni baina ya miji ya Kiislamu, na kwamba ipo katika umoja wa kweli uliokamilika ambao kila sehemu inaathirika na yale yanayoipata sehemu nyingine.

4.

Kusoma kwa mfumo wa kulinganisha ili kunadhimu malezi na mafunzo katika miji yote ya Kiislamu.

82 83

Al-Wasail, Juz. 15, Uk. 271, hadithi ya 10.   Ghurarul-Hikam, Juz. 1, Uk. 393, Hadithi ya 22 – 23. 30


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

5.

Kuwawezesha wanafunzi wa Kiislamu na walimu wao kutembelea miji mingine ya Kiislamu na kuwa na mahusiano na vyuo vingine vya elimu na malezi.

6.

Kuamsha hisia za Uislamu ndani ya nyoyo za wanafunzi, kuwapa roho ya kujivunia Uislamu wao, ili hali hiyo iweze kujiakisi ndani ya mwonekano wa mwenendo wao wa mtu mmoja mmoja na jamii kwa jumla.

7.

Kusoma historia ya Uislamu na jografia yake kwa undani ili aweze kujua mafanikio ya Waislamu wa zama zilizopita, na maslahi yao katika zama tulizo nazo.

8.

Kutoa mabingwa wenye kubobea katika nyanja za maendeleo ya kibinadamu na Uislamu.

9.

Kuwafahamisha chipukizi wajibu wao mbele ya Uislamu, na waweze kuutumikia katika sekta ya kijamii na kisiasa.

10. Kuwalinda raia dhidi ya vita vya kifikra viletwavyo na maadui wa Uislamu ambayo hulenga kuharibu roho ya Kiislamu. 11. kuwafumbua macho Waislamu juu ya hatari ambazo zinawakabili toka kwa wagandamizaji na Uzayuni. 12. Kuwahamasisha Waislamu kutenda kwa faida ili kuzikomboa ardhi zao zinazokaliwa kwa mabavu na kundi la kizayuni. 13. Kuwalea katika mwenendo wa Kiislamu uliyojengwa juu ya msingi wa kusaidiana, mshikamano wa pamoja na kuhisi majukumu na kutanguliza maslahi ya umma kabla ya mtu binafsi. 31


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

14. Silabasi ya masomo ijumuishe majukumu ya mwanafunzi mbele ya wazazi wake na ukoo wake. 15. Kwa kuwa sisi ni Waislamu lazima tukumbushe mas’ala ya kifiqhi anayoyahitaji mwanafunzi katika maisha yake, hususan katika miaka ya taklifu. 16. Kuanzisha maktaba makhususi zenye vitabu vya kidini ambavyo vitakuza mustawa wa kifikra kwa mwanadamu Mwislamu. 17. Kuingiza teknolojia mpya katika hatua zote za masomo. 18. Kuyatenga mbali na mfumo wa mafunzo baadhi ya makundi yaliyoathirika na fikra hatari za kiharibifu. 19. Kufaidika na wahubiri wa Kiislamu katika kuhadhibisha (kulea) mwenendo wa mwanafunzi, na hili liwe kwa namna ya kuendelea kila siku au kila wiki. 20. Kuweka vikao vya kila wiki au kila nusu mwezi ili kujadiliana mambo yanayowahusu wanafunzi. 21. Kuweka Silabasi kuu inayohusu maendeleo ya elimu ili kugundua vipaji vya wanafunzi na kuviendeleza. Na hiyo iwe kwa msaada wa wanafunzi wao wenyewe.

32


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

SIFA ZA MWALIMU MWENYE ­MAFANIKIO 1.

Afikie angalau kiwango cha kati katika maarifa na elimu, ­jambo ambalo litamsaidia kujua hulka ya kibinadamu na mwenendo wake, pia sababu na vichocheo vilivyojificha ­nyuma ya mwenendo huu.

2.

Awe na uzoefu na baadhi ya fani zitakazomsaidia dhidi ya jaribio la baadhi ya watu la kutaka kumtenga na baadhi ya harakati.

3.

Awe na uzoefu na baadhi ya makundi ya kujitolea ambayo yatamsaidia kuamiliana na wanafunzi wake kwa mafanikio.

4.

Awe mtu makini mwenye uwezo wa kuchukua maamuzi na kuzingatia mazingira na hali mbalimbali.

5.

Ajitathmini mwenyewe kupitia kazi alizowapa wanafunzi, na aendelee na zile kazi ambazo zimetoa matunda mazuri katika sekta ya mabadiliko.

6.

Kila siku awafuatilie wanafunzi wake, na airekebishe hali ya yule inayohitaji kurekebishwa.

7.

Atekeleze kivitendo imani yake aliyonayo ili aweze kuwa kigezo kwa wengine.

8.

Awahimize wanafunzi kutafuta elimu na taaluma za kisasa, ili tuweze kuwakabili maadui kwa elimu na maarifa.

33


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

9.

Awe na mawasiliano kamili na viongozi wa mambo, na aweze kuwafafanulia mahitaji mapya moja baada ya moja.

10. Aonyeshe vipaji vya asili walivyonavyo watoto au wanafunzi. 11. Ajitahadhari na upotofu na vita vya kielimu vilivyomo ndani ya selabasi za masomo zilizopo sasa, huku akichukua tahadhari dhidi ya mambo mapya yaliyomo humo.

34


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

WOSIA JUU YA MALEZI YA WATOTO

B

aba, familia, shule na jamii wanaweza kuchangia sana katika kutengeneza utu ulionyooka wa watoto wao. Watoto wana vipaji vikubwa ambavyo hudhihiri kwao tangu utotoni mwao, hivyo vipaji hivyo vinaweza kutunzwa kupitia: 1.

Kupandikiza kwa moto moyo wa kujiamini, kumpa zawadi yule aliyeshinda, na kutomdharau yule aliyefeli, au kumuhisisha uzembe na kutoweza. Bali ni lazima kuongea naye kwa kuijadili hali kwa pamoja ili ahisi umuhimu wa utu wake, na wakati huohuo agundue makosa yake, kama ambavyo ni lazima aendelee majukumu yake kadiri ya uwezo wake mpaka siku moja zionekane kwake sifa za kiuongozi za kimafanikio.

2.

Kutokumkalifisha mtoto baadhi ya kazi asizozipenda au zilizo juu ya uwezo wake, ili asikabiliane na kushindwa kwa kujirudiarudia, na hatimaye akakosa moyo wa kujiamini.

3.

Kukuza ari ya juu kwa mtoto kwa kuziheshimu na kuzipenda shakhsia zilizotangulia na zilizopo, na kubainisha siri ya uadhama na maeneo yenye nguvu kwa shakhsia hizi za kijamii. Na pia kubainisha njia ya kufikia viwango hivi vya juu ili kutimiza malengo makuu ambayo ni mwanadamu kupata radhi za Mwenyezi Mungu.

4.

Kumfuatilia mtoto ili kuchukua tahadhari asije kutumbukia ndani ya ujeuri na kiburi kutokana na mafanikio yake au kujihisi yuko juu. Pia kumfunza na kumwelimisha sifa za maadili mema na ambazo ni wajibu awe nazo.

35


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

5.

Kubainisha hali iliyonayo jamii yetu kwa sasa, na jinsi ya kuweza kuibadili na kuiendeleza na kuifanya kinara mbele ya jamii nyingine katika ulimwengu huu kwa kazi na utendaji. Na hilo litatimia kwa: a.

Kuzalisha fikra za lazima za kiimani.

b.

Kubainisha nafasi ya maendeleo yaliyoletwa na umma wetu katika historia ya mwanadamu.

c.

Kumfunza kukabiliana na changamoto zinazoikabili jamii ya Kiislamu na kukuza kwake roho ya mapambano na kuendeleza nguvu zake katika mapambano, iwapo ataandaliwa vizuri kwa ajili ya mapambano hayo.

d.

Kubainisha sababu za msingi zilizopelekea umma wa Kiislamu kubaki nyuma, na jinsi unavyoweza kuvuka vikwazo vyake. Pia kuondoa hali ya kukata tamaa ya kwamba hauwezi kuvivuka vikwazo hivyo.

e.

Kubainisha maeneo mengi yenye nguvu na uwezo wa kuleta mabadiliko iliyonayo umma wetu wa Kiislamu.

f.

Kubainisha hali yaliyonayo mataifa mengine yanayodai kwamba yameendelea, hiyo ni kwa kubainisha hali za udororaji wa maadili yao ya kijamii, na aina nyingi za udororaji mwingi walio nao.

g.

Kusisitiza mchango wa vyombo vya habari katika kujenga utu wa muumini wa kweli, vyombo kama vile runinga, video, majarida, magazeti vipeperushi vyenye picha na machapisho mbalimbali, tovuti na njia za mawasiliano.

36


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

TIBA YA STAREHE ZENYE UHARIBIFU Utangulizi

L

inalosikitisha sana ni kwamba tunaishi katika nchi za Kiislamu lakini tunataka kuwafuata wamagharibi katika kila kitu, na hasa katika yale yanayohusu starehe binafsi, ilihali kwa mujibu wa mafunzo ya Uislamu sisi tunamiliki njia ya halali ya kustarehesha nafsi, na bila shaka Uislamu umetatua jambo hili na kulitilia sana umuhimu. Mwenyezi Mungu amesema: “Na utafute kwa aliyokupa Mwenyezi Mungu makazi ya akhera; wala usisahau fungu lako la dunia. Na fanya wema kama alivyokufanyia wema Mwenyezi Mungu, wala usitafute ufisadi katika ardhi; hakika Mwenyezi Mungu hapendi wafisadi.” (Sura al-Qasas: 77). Imam Kadhim (a.s.) amesema: “Ziwekeeni nafsi zenu fungu toka katika dunia kwa kuzipa kile cha halali inachokitamani, ikiwa tu hakiondoi heshima wala hakina ubadhirifu. Na tumieni hayo kujisaidia katika mambo ya kidunia.” 84Akasema tena (a.s.): “Si miongoni mwa wafuasi wetu yule aliyeacha dunia yake kwa ajili ya dini yake.” Hivyo ni wajibu kuacha kustarehe kwa kutumia yale aliyoharamisha Mwenyezi Mungu miongoni mwa michezo inayopigiwa sana upatu na ukoloni wa kimagharibi, kwa sababu ina athari na madhara hatari sana na yasiyoonekana moja kwa moja, ambayo humpata mtendaji wake hata kama hajui uharamu wake. Miongoni mwa michezo hiyo ni drafti, puul, kamari na michezo mingine ya rehani na dau. 84

Nahwu Hayati Afdhal, Uk. 92. 37


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

Kuna njia alizotufundisha kiongozi wa Uislamu, hapa tunataja baadhi yake tu, nazo ni: 1.

Kujisomea: Hakika kujisomea ni miongoni mwa njia za kustarehe zenye athari kubwa katika kuiongoza fikra na roho. Imam Ali (a.s.) amesema: “Pumzisheni nafsi zenu kwa hikima nzuri kwani hakika zenyewe huchoka kama ichokavyo miili.”85

2.

Safari: Ni moja ya njia za kuipumzisha nafsi na kuistarehesha, zinazosaidia mwili na roho kupata usalama. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Safirini mpate siha.”86

3.

Mazoezi: Ni moja ya njia salama za kustarehesha nafsi na yenye kusaidia uchangamfu na kuleta usalama na siha kwa mhusika. Yanasaidia kuiletea roho furaha, kwani mwanadamu hapati furaha ila kwa roho yake na mwili wake kupata furaha.87

4.

Shabaha: Kujifunza shabaha ukiachilia mbali kwamba kunastarehesha mwili pia humpa mwanadamu Mwislamu maandalizi ya kupambana na adui na kuitetea heshima ya Qur’ani na ubinadamu kwa jumla.88

5.

Kupanda ngamia: Kuna umuhimu mkubwa katika Uislamu kutokana na faida kama ile inayopatikana katika nukta ya nne. Nabii wa Uislamu alikuwa hata yeye mwenyewe akipanda ngamia.89

Al-Kafiy, Juz. 1, Uk. 48.   Mustadrakul-Wasail, Juz. 8, Uk. 7, Hadithi ya 2. 87   Nahwu Hayati Afdhal, Uk. 98. 88   Nahwu Hayati Afdhal, Uk. 96. 89   Nahwu Hayati Afdhal, Uk. 100 na 101. 85 86

38


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

6.

Kuogelea: Kunaleta nguvu na faida nyingi na hukomaza viungo na roho ya mwanadamu, kiasi kwamba hufichua vipaji vilivyojificha kwake na hatimaye huleta furaha. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Wafunzeni wanenu kuogelea na shabaha.”90

TIBA YA MARADHI YA KUIGA ­UMAGHARIBI 91

1.

Tuwajengee vijana wetu roho ya kujitegemea, kisha tutafakari kwa kina na tuunde mageuzi ya kimaadili, kielimu na kimawazo, mageuzi ambayo yatafuta hali yote ya kujisalimisha kwa wageni, na ambayo yatajumuisha matumizi ya uwezo na mwendelezo wa vipaji na uwezo kwa watu.92

2.

Ni lazima kupandikiza historia ya Uislamu halisi ndani ya akili za umma na kuandaa nyenzo za kufanyia uhakiki na uchunguzi wa kielimu kwa vijana, na kuvitangaza viwanda na teknolojia za ndani.93

Nahwu Hayati Afdhal, Uk. 100 na 101.   Nchi za Magharibi ni zile zilizopo Magharibi mwa nchi za Kiislamu. Hakika wamagharibi ni watu wenye mila zao, desturi zao na njia zao makhususi, kama ambavyo nasi tuna mila na desturi zetu, na hivyo hivyo ni kwamba kila dini na imani ina mila yake makhususi, hivyo ni wajibu kwa kila mwenye akili na ufahamu kuchukua toka kwa mwenzake kile tu chenye kumnufaisha na kumfurahisha, kisichomdhuru wala kumpeleka katika upotofu na maangamio. Tambua kwamba mila zinazotufikia toka Magharibi si zile mila sahihi zinazoendesha jamii hizo, bali ni zile zinazotekelezwa na wapuuzi wao, wale duni na wapotofu miongoni mwao, na ambazo hazipendwi na wamagharibi wengi, na ambazo zinatangazwa na ukoloni na ukafiri ili kuharibu jamii yetu, kutokana na husuda yao juu ya jamii yetu baada ya jamii yao kuporomoka na kuharibika kimaadili. Hivyo ni wajibu kuzipiga vita na kuzitetea mila zetu, desturi zetu, tamaduni zetu na dini yetu na matukufu yetu. 92   Nahwu Hayati Afdhal, Uk. 62 na 63. 93   Nahwu Hayati Afdhal, Uk. 62 na 63. 90 91

39


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

3.

Muigaji ajue kwamba hana msingi na muhimili wa kiimani wenye kumhisisha uwepo wake, utu wake na asili yake, na hivyo yeye anategemea fahari za mababa, desturi zao na mila zao. Au katika zama zetu hizi anategemea tamaduni potofu ili ajitengenezee utu wa uwongo na asili dhaifu.94

4.

Ni wajibu juu yetu kufanya mapinduzi ya kielimu na kimalezi ambayo yatazipa harakati zile nguvu walizonazo watu, na yataendeleza vipaji vyao vya ndani.95

5.

Hakuna kizuizi katika kuzichambua mila za mababa na zile zililizoingizwa na umagharibi, hivyo zile zinazooana na akili na mantiki zihifadhiwe, na zile za udanganyifu na upotofu zitupiliwe mbali.96 Imam as-Sadiq (a.s.) amesema: “Mwenyezi Mungu alimfunulia mmoja wa Manabii wake kwamba: Waambie waumini: Msivae mavazi ya maadui zangu, wala msile vyakula vya maadui zangu, na wala msiwe na mwenendo wa maadui zangu, mkaja kuwa maadui zangu kama wao walivyo maadui zangu.”97

Tafsirul-Amthal, Juz. 1, Uk. 481.   Nahwu Hayati Afdhal, Uk. 62. 96   Tafsirul-Amthal, Juz. 1, Uk. 481. 97   Nahwu Hayati Afdhal, Uk. 62. 94 95

40


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

TIBA YA UZEMBE 1.

Ni lazima aondoe sababu zake nazo ni, ujinga, tabia mbaya, kiburi, majivuno na ghadhabu.98

2.

Akumbuke madhara yake ya kidunia na Akhera, na kwamba haulingani na mtu mwenye akili ambaye anataka kuishi katika jamii yake maisha mazuri yenye kuachiana maslahi.99

3.

Ni juu yake kutafakari kwa kina kutokuwa na haraka katika kila kitendo anachotaka kutenda.100

4.

Ajue kwamba sifa hii mbaya haikubaliwi na Uislamu wala jamii yoyote ya kidini, nayo ni sifa iliyo nje ya sifa za Kiislamu.

TIBA YA UWOGA 1.

Ajue kwamba uwoga ni mapungufu ya nafsi na ni sababu ya kuiangamiza katika baadhi ya hali.101

2.

Aamshe vichocheo vya ghadhabu vilivyomo ndani ya nafsi hata kama ni dhaifu, kwani vikichochewa na vikaongozeka kwa mfululizo huzidi na kupata nguvu kama moto dhaifu unavyoongezeka.102

Tahdhibul-Akhlaqi, Uk. 164.   Tahdhibul-Akhlaqi, Uk. 46. 100   Tahdhibul-Akhlaqi, Uk. 46. 101   Jamius-Saadat, Juz. 1, Uk. 207. 102   Jamius-Saadat, Juz. 1, Uk. 207. 98 99

41


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

3.

Aifunze nafsi yake kupambana kwa kupitia yule ambaye vitimbi vyake havitamdhuru, hiyo ni ili aamshe nguvu za ghadhabu zake.103

4.

Ajue kwamba uvivu hupelekea kukosa. Amefaulu kwa kupata matamu yule tu aliye jasiri.

5.

Ajue kwamba ujasiri hauharakishi kifo wala kukichelewesha.

6.

Ajue kwamba yeye si mkamilifu kiume, hivyo ni wajibu juu yake kutenda yaliyo kinyume na hali hiyo, na shujaa ni shujaa hata kama ni kwa kuua nyoka.

7.

Aishi pamoja na wenye nguvu, majasiri na mashujaa, kwani mtu huchukua toka kwa yule anayechanganyikana naye.

8.

Azingatie zile nukuu zinazomsifu shujaa na kumlaumu mwoga, na ajue kwamba ni shujaa ndiye huitetea dini yake, heshima yake na nchi yake, na hili linatosha kuwa sababu ya kumsukuma mtu awe shujaa. Imam as-Sadiq (a.s.) amesema: “Baba yangu alisema: ‘Hana amani mtu mwenye ubahili, husuda na woga. Na wala hawi muumni yule aliye mwoga, mwenye tamaa na bahili.”’104 Ahlul-Bait (a.s.) wamesema: “Shujaa ni shujaa tu hata kama ni kwa kuuwa nyoka.”

Jamius-Saadat, Juz. 1, Uk. 207.   Safinatul-Bihar, Juz. 1, Uk. 548.

103 104

42


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

TIBA YA KUKATA TAMAA 1.

Ajikumbushe riwaya za Ahlul-Bait (a.s.) zinazosifia subira na kutokukata tamaa, na ajue kwamba Mwenyezi Mungu yu pamoja na wenye kusubiri, na mwenye kufanya subira hushinda.105

2.

Aimarishe kichocheo cha dini na adhoofishe kichocheo cha matamanio kwa kufanya juhudi na mazoezi ya nafsi hatua kwa hatua.

3.

Akumbuke madhara na ubaya wa kukata tamaa, na kwamba hakuna matokeo mazuri. Na kama ilivyosemwa: “Ziache siku zifanye zitakavyo, tuliza nafsi pindi makadara yapitapo. Usikate tamaa kutokana na tukio la usiku, kwani matukio ya dunia hayatadumu.”

4.

Ajue kwamba hakika thawabu za kufanya subira juu ya msiba ni nyingi kushinda za yale yaliyopita, na kwamba kwa sababu ya kufanya subira atapata rehema kupitia msiba.106

5.

Ajue kwamba kwa kila hali machungu huondoka kadiri muda na saa zipitavyo na umri uishavyo. Na kwamba saa iliyopita furaha yake haitabaki wala machungu yake hayataendelea, na ifuatayo hajui ni ipi hali yake, na hakika yenyewe ndio saa uliyomo.107

6.

Achunguze hali za wale waliojaribiwa na Mwenyezi Mungu kwa misiba Yake mikubwa lakini wakafanya subira,108 hususani misiba ya Ahlul-Bait (a.s.).109

Majmuatuw-Waram, Juz. 2, Uk. 40. al-Wasail, Juz. 15, Uk. 236.   Al-Akhlaq, Uk. 231. al-Wasail, Juz. 15, Uk. 237. 107   Mir’atur-Rashad, Uk. 43. 108   Mir’atur-Rashad, Uk. 43. 109   Mir’atur-Rashad, Uk. 43. 105 106

43


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

7.

Ajue kwamba lililompata ni kutoka kwa Mwenye hikima Mwenye huruma, na kwamba yeye hamchagulii mja wake ila lile lenye maslahi kwake naye hana haja nalo, na kwamba yeye ni Muweza wa kila kitu.110

8.

Ajue kwamba kulalamika na kukata tamaa hakuna faida yoyote ila ni kumfurahisha adui na kumhuzunisha rafiki.

9.

Aifariji nafsi yake kwa kulia na hususani wakati wa matatizo, na huo ndio mwenendo wa Manabii (a.s.) kama alivyokuwa akifanya Ya’aqubu (a.s.).111

10. Ajue kwamba miongoni mwa tabia njema kama vile utawa, uchamungu, kujidhibiti, ushujaa na uvumilivu, hizi zote zinategemea subira, na hiyo inatosha kuwa fadhila kubwa.112 11. Ajue kwamba ukubwa wa majaribu yatokanayo na maudhi huonyesha ukaribu wako kwa Mwenyezi Mungu. Imam as-Sadiq (a.s.) amesema: “Nafasi ya subira kwenye imani ni sawa na kichwa kwenye mwili, kichwa kikiondoka na mwili nao huondoka. Kadhalika subira ikiondoka imani nayo huondoka.”113

Mir’atur-Rashad, Uk. 43, 49, 52.   Mir’atur-Rashad, Uk. 43, 49, 52. 112   Mir’atur-Rashad, Uk. 43, 49, 52. 113   Al-Wafiy, Juz. 3, Uk. 65. 110 111

44


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

TIBA YA KUPENDA CHEO 1.

Ajue kwamba sababu iliyomfanya apende cheo mwisho wake ni kifo.114

2.

Atafakari maafa ambayo wamejaribiwa kwayo vinara wa vyeo duniani, na kutokana na wingi wa maafa bado ulamaa wakubwa na wachamungu wanaikimbia tabia hiyo kama mtu amkimbiavyo nyoka mweusi.115

3.

Ajue kwamba tiba yenye nguvu katika kung’oa tabia ya kupenda cheo ni kujitenga na watu, na kuhamia maeneo duni.116

4.

Ili kutibu maradhi haya aombe msaada kupitia habari za Ahlul-Bait (a.s.) zilizopatikana katika kuipiga vita sifa hii.117 Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Kupenda cheo na mali huotesha unafiki moyoni kama maji yaoteshavyo mbogamboga.”118

5.

Ajue ni lipi lililo ukamilifu wa kweli, kwani kujua hilo kutadunisha cheo machoni mwake.119

6.

Atafute mahitaji ya maisha yake kwa juhudi za mkono wake, na aondoe tamaa ya waliyonayo watu kwa ukinaifu, kwani atakayekinai hatohitaji ya watu, na asipohitaji moyo wake hautashughulishwa na waliyonayo watu. Na wala cheo haki-

Al-Muhujatul-Baydhau, Juz. 6, Uk. 129. Jamius-Saadat Juz. 2, Uk. 363.   Al-Akhlaq Uk. 193. Jamius-Saadat Juz. 2, Uk. 364. 116   Al-Akhlaq, Uk. 193. Jamius-Saadat, Juz. 2 Uk. 364. 117   Jamius-Saadat, Juz. 2, Uk. 365. 118   Jamius-Saadat, Juz. 2, Uk. 349. 119   Al-Muhujatul-Baydhau, Juz. 6, Uk. 129. 114 115

45


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

takuwa na thamani yoyote moyoni mwake, na hatoacha kupenda cheo ila kwa ukinaifu na kuacha tamaa.120 7.

Ajue kwamba hata kama atapata cheo lakini ipo siku kitakwisha, na kwa kuwa ni jambo la kutoweka basi halina kheri. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Kati ya mbwa mwitu waliotumwa kwenye kundi la kondoo hakuna mwenye madhara zaidi kushinda tabia ya kupenda cheo na mali iliyo na madhara katika dini ya Mwislamu.”121

TIBA YA UCHU WA MALI 1.

Akumbuke sifa za ukinaifu, heshima yake, utukufu wa nafsi na ubora wa uhuru.122

2.

Akumbuke sifa mbaya ya uchu, uduni, udhalili na kutii. 123

3.

Ajue kwamba asiyetanguliza heshima ya nafsi juu ya tumbo ni mchache wa akili na punguwani.124

4.

Akumbuke maafa ya kidunia na adhabu za Akhera vitokanavyo na kujilimbikizia mali.125

5.

Akithirishe kutafakari hali waliopitia viumbe watukufu na wenye hishima kati yao miongoni mwa Manabii (a.s.), na ni jinsi gani walivyovumilia kichache.126

Al-Muhujatul-Baydhau Juz. 6, Uk. 131.   Jamius-Saadat, Juz. 2, Uk. 349. 122   Jamius-Saadat, Juz. 2, Uk. 103 – 104. 123   Jamius-Saadat, Juz. 2, Uk. 103 – 104. 124   Jamius-Saadat, Juz. 2, Uk. 103 – 104. 125   Jamius-Saadat, Juz. 2, Uk. 103 – 104. 126   Jamius-Saadat, Juz. 2, Uk. 103 – 104. 120 121

46


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

6.

Ajue kwamba kuipupia dunia ni miongoni mwa sifa na hali za wanyama na ambazo humtoa kwenye ubinadamu.127

7.

Inampasa asimtizame yule aliye juu yake bali amtizame yule aliye chini yake katika neema na mali.128

8.

Asihangaike sana kwa ajili ya mustakabali. Linaloweza kumsaidia juu ya hilo ni kuwa na matumaini mafupi katika dunia.129

9.

Awe na uwiano katika maisha.130

10. Ajifunze dini.131 11. Ajue kwamba mwenye uchu hashibi hata akipewa neema za ulimwengu wote, kama ambavyo moto haushibi kuni vyovyote utakavyouchochea kuni, na bado husema je kuna nyongeza?132 12. Ajue kwamba uchu kwa wanajamii hubadili maisha yao ya kijamii na huyafanya eneo la vita, mizozo na ugomvi, badala ya kuwa eneo la uadilifu, amani, msimamo na utulivu.133 Hakika uchu huondoa heshima ya nafsi na kuleta hali ya kukwama ndani ya mambo yasiyofahamika uhalali wake, kama wenye busara walivyosema: “Uchu huharibu dini na murua.”134 13. Atibu sababu za uchu kama vile kuwa na matumaini marefu, kuwa na umri mrefu na kuhofia kukosa riziki baadaye.   Jamius-Saadat, Juz. 2, Uk. 103 – 104.   Jamius-Saadat, Juz. 2, Uk. 103 – 106. 129   Al-Muhujatul-Baydhau, Juz. 6, Uk. 56. 130   Majmuatuw-Waram, Juz. 1, Uk. 167. 131   Majmuatuw-Waram, Juz. 1, Uk. 167. 132   Dirasatu Fil-Mashakilil-Akhlaqiyah, Uk. 178. 133   Dirasatu Fil-Mashakilil-Akhlaqiyah, Uk. 178. 134   Nurul-Haqiqah, Uk. 157. 127 128

47


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

14. Ajue kwamba anayoyafanyia uchu yanamzuia kumkumbuka Mwenyezi Mungu, kutafuta elimu na kutekeleza haki. Mwenyezi Mungu amewasifu wale ambao hawajaipa kipaumbele mali na wingi wake, akasema: “Watu ambao biashara wala kuuza hakuwashughulishi na kumdhukuru Mwenyezi Mungu, na kuisimamisha Swala na kutoa Zaka. Wanaihofu siku ambayo nyoyo na macho yatageuka.” (Sura Nuru: 37). Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Mfano wa mtu mwenye uchu hapa duniani ni sawa na nondo wa hariri kila azidishavyo kujitanda ute wake ndivyo umzuiavyo kutoka mpaka anakufa.”135 Katika maana hii malenga amesema: “Mwenye uchu humaliza muda wake kwa kukusanya mali, huku matukio na siku vikiwa havimuachi, kama vile nondo wa hariri ayajengayo humuuwa, na huku asiyekuwa yeye akifaidika na yale aliyoyajenga.”136

TIBA YA HUSUDA 1.

Ang’oe vyanzo vya husuda, navyo ni vingi, kati ya hivyo ni uovu wa nafsi, uadui, kupenda cheo, ushindani, kujipenda, kujivuna dhidi ya wengine na malezi mabovu.137

2.

Ajikalifishe kutenda yale yanayopingana na husuda katika kauli na vitendo. Ikiwa husuda humlazimisha kufanya kiburi basi yeye ajilazimishe kuwa mnyenyekevu. Na kama itamlazimisha kuteta na kukosoa basi aulazimishe ulimi wake kusifu.138

Jamius-Saadat, Juz. 2, Uk. 100. Akhlaqu Ahlul-Bayti, Uk. 67.   Akhlaqu Ahlul-Bayti, Uk. 67. 137   Al-Muhujatul-Baydhau, Juz. 5, Uk. 347. 138   Jamius-Saadat, Juz. 2, Uk. 206. al-Haqaiqu Uk. 84 – 85. 135 136

48


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

3.

Hasidi ajue kwamba husuda humdhuru yeye mwenyewe katika dini na dunia, na wala haimdhuru mhusudiwa.139 Malenga anasema: “Vuta subira juu ya husuda ya hasidi kwani hakika subira yako yamuuwa. Moto hujiteketeza wenyewe pale ukosapo ukuni wa kuuteketeza.” Malenga mwingine akasema: “Mwenyezi Mungu atakapo kueneza fadhila huzimwa, kwani huvamiwa na ulimi wa hasidi. Lau si moto kuwaka katika yale yaliyouzunguka, harufu nzuri isingejulikana kujulikana kwa udi.

4.

Hasidi ajue kwamba anaizuilia nafsi yake msaada na vigezo vitakavyomsaidia kupata msaada.140

5.

Ajue kwamba husuda itakapoenea baina ya wanajamii magomvi mengi yataenea katika jamii yao.141

6.

Hasidi ajue kwamba neema ambazo zinamfanya awahusudu watu chanzo chake ni Mwenyezi Mungu, hivyo amuombe yeye.142

7.

Ni wajibu juu ya baba kwamba asibague baina ya watoto katika zawadi na muamala, la sivyo atapandikiza mbegu za husuda baina yao.143

8.

Ajue kwamba husuda inadhuru afya yake ya kimwili kama ilivyokuja habari kutoka kwa Amirul-Muuminina (a.s.).144

9.

Ni juu ya mwanadamu kubadili nia yake kutoka kwenye husuda kwenda kwenye wivu, kwa maana ya kwamba: Atamani kupata neema bila kutamani imtoke mwenye nayo.145

Al-Akhlaq,Uk. 151. al-Haqaiqu Uk. 84.   Dirasatu Fil-Mashakilil-Akhlaqiyah, Uk. 95 na 96. 141   Dirasatu Fil-Mashakilil-Akhlaqiyah, Uk. 95 na 96. 142   Dirasatu Fil-Mashakilil-Akhlaqiyah, Uk. 98 na 99. 143   Dirasatu Fil-Mashakilil-Akhlaqiyah, Uk. 98 na 99. 144  Ghurarul-Hikam, Juz. 1, Uk. 48, Hadithi ya 102. Uk. 88, Hadithi ya 179. 145   Ad-Dhunubu al-Kabirah, Juz. 2 Uk. 330. 139 140

49


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

10. Ni juu ya mwanadamu aifuatilie nafsi yake na aichunguze je ameshakuwa ndani ya kundi la mahasidi? Ili kujua hilo, azingatie mambo yafuatayo: a.

Hasidi hufurahia shari.

b.

Hasidi hudhihirisha mapenzi yake kwa kauli zake na si kwa vitendo vyake.

c.

Hasidi huona kwamba mwenzake kuondokewa na neema ni pigo juu yake na au ni neema kwake.146

d.

Mwenye maudhi huchukiwa, na hasidi ni mwenye maudhi, hivyo yeye ni mwenye kuchukiwa.

e.

Husuda husaidia kuchochea fitina, kuharibu uhusiano na kuwaudhi viumbe.

11. Ajue kwamba husuda inachukiwa kiakili, achia mbali inavyopigwa vita na Aya na riwaya, kwa sababu ni kuyakasirikia makadara ya Mwenyezi Mungu katika kutofautisha viwango vya neema baina ya waja wake. 12. Hakika husuda si dhulma ambayo ni wajibu kujitenga nayo bali yenyewe ni maasi ya hasidi kwa Mola Wake. Hivyo iwapo ataacha husuda atakuwa amemridhisha Mola Wake na kufaulu kupata ladha za dunia na Akhera. Na hili linahitaji mtu awe jasiri kama ilivyosemwa: “Yule aliye jasiri ndiye hufaulu kupata ladha.” Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Husuda huteketeza mema kama moto unavyoteketeza kuni.”147 Imam as-Sadiq (a.s.) amesema: “Hasidi hujidhuru mwenyewe kabla hajamdhuru mhusudiwa, kama Ibilisi alivyojisababishia   Ghurarul-Hikam Juz. 1, Uk. 114, Hadithi ya 2127.   Al-Kafiy Juz. 8, Uk. 45. al-Bihar, Juz. 70, Uk. 255.

146 147

50


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

laana, na kumsababishia Adam uteule.”148 Imam as-Sadiq (a.s.) amesema tena: “Husuda huteketeza imani kama moto unavyoteketeza kuni.”149

TIBA YA HIKDI 1.

Atafakari athari za hikdi yenye kufedhehesha, kama vile ambavyo yenyewe ni chanzo cha ghadhabu, ugumu wa maisha, fitina na mengineyo.

2.

Aamiliane na mhusudiwa muamala wa wapendwa wake, asuhubiane naye kwa furaha, upole na kwa kumtekelezea mahitaji yake, na ajitahidi kufanya hivyo mara kwa mara.

3.

Akumbuke faida za nasaha ambayo ni dhidi ya hikdi. Nasaha inamaanisha: Kukusudia kheri na kuchukia shari.

4.

Ajue kwamba uadui huu utamsababishia maumivu baadaye, na kwamba hikdi yake haimdhuru chochote yule mwenye hikdi naye. Na mwenye akili huwa hadumu ndani ya hali yenye kumdhuru mwenyewe na kumnufaisha mwingine.

5.

Ajue kwamba uso wa furaha huondoa chuki na usongo.

6.

Ang’oe shari na hikdi moyoni mwake ili aweze kuing’oa moyoni mwa sahiba wake.

7.

Hakika shida huondoa hikdi.

Biharul-An’war, Juz. 73, Uk. 255, Hadithi ya 23.   Al-Kafiy, Juz. 2, Uk. 306.

148 149

51


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

8.

Ajiepushe kulaumulaumu, kwani husababisha chuki, na ajitahidi kumvumilia ndugu yake alivyo.

9.

Ajue kwamba hii si sifa ya waumini. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Muumini hana usongo.” Imam alAskari (a.s) amesema: “Kati ya watu wote wenye usongo ndio wenye raha kidogo.” Imam Ali (a.s.) amesema: “Ng’oa shari toka kwenye kifua cha mwenzako kwa kuing’oa toka kwenye kifua chako.”

TIBA YA ULEVI WA POMBE 1.

Azingatie madhara ya pombe yaliyotajwa ndani ya Qur’ani na riwaya za Ahlul-Bait (a.s.). Mwenyezi Mungu anasema: “Enyi mlioamini! Hakika pombe na kamari na mizimu na mburuga ni uchafu katika kazi ya Shetani. Basi jiepusheni nayo, ili mpate kufaulu. Hakika Shetani anataka kuwaingizia uadui na bughudha baina yenu kwa pombe na kamari na kuwazuia kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kuswali, basi je, mtakoma.” “(Sura al-Maidah: 90 – 91). Imam as-Sadiq (a.s.) alipoulizwa: Kwa nini Mwenyezi Mungu ameharamisha pombe na hali hakuna chenye ladha tamu kushinda yenyewe? Alisema: “Aliharamisha kwa sababu yenyewe ni mama wa maovu na kichwa cha kila shari. Mnywaji wake hufikiwa na wakati ambao akili zake humtoka, hamjui Mola Wake wala haachi maasi yoyote ila huyatenda, wala heshima yoyote ila huivunja. Mlevi hatamu yake imo mikononi mwa shetani, akimwamuru asujudie masanamu huyasujudia, na huelekea kule amwongozako.”150

Wasailus-Shia, Juz. 17, Uk. 253.

150

52


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

2.

Ayajue madhara ya pombe ambayo ni: a.

Madhara ya kifikra na kisaikolojia: Elimu ya sasa imethibitisha kwamba asilimia ya ongezeko la maradhi ya kisaikolojia inalingana na asilimia ya ongezeko la kuenea kwa ulevi wa pombe.

b. Pombe huathiri mfumo wa kizazi: Hakika nguvu ya pombe huathiri mpaka kizazi cha saba, na kwamba mbegu za kiume zinapotua katika kizazi hutembea kwa sura isiyo ya kawaida, kwa kasi na kwa nguvu, hiyo yote ni kutokana na pombe. c.

Madhara ya kimwili: Kwa uthibitisho wa elimu ya sasa ni kwamba pombe huathiri viungo vyote vya mwili, na hususani huleta kifua kikuu.151

d. Pombe ni chanzo cha uhalifu: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Hakika mmoja wa wafalme wa Bani Israil alimshika mtu mmoja na akampa hiyari ya kunywa pombe, kuuwa, kula nyama ya nguruwe au amuuwe. Mtu yule alichagua pombe, na alipokunywa alitenda yote aliyomtaka.”152 e.

Madhara ya kiuchumi na kimali ni jambo lisilopingika: Hakika ulevi wa pombe huiachia pigo kubwa hali ya uchumi wa raia. Mwishoni mwa karne iliyopita raia wa Marekani walitumia dola 181,900,000,000, kwa matumizi ya pombe.

Nahwu Hayat Afdhal, Uk. 144.   Al-Ghadir, Juz. 2, Uk. 257.

151 152

53


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

f.

Na pia kuna madhara ya kimaadili ambayo humpata mlevi: Hupatwa na tabia mbaya ambazo humpelekea kwenye uzinzi, uhalifu, uuwaji, ufichuaji wa siri, kuvunja heshima na kutokujali kanuni na heshima zote za kibinadamu ambazo ndio msingi wa furaha ya maisha, hasa heshima utawa juu ya wake, nafsi na kauli.

g.

Usisahau athari za kemikali juu ya akili ambayo ni matokeo ya athari zake dhidi ya ubongo, na kwa matokeo hayo huifanya akili ishindwe kufanya kazi.153

3.

Ajue kwamba Uislamu una njia yake ya pekee katika kumwepusha mnywaji kimawazo na kivitendo ili kwamba wanywaji wajione ni watu duni wapweke ili waache vitendo vyao hivyo, kama ambavyo ni onyo pia kwa wengine.

4.

Ajikumbushe hatima yake huko Akhera. Imam as-Sadiq (a.s.) amesema: “Na ni haki juu ya Mwenyezi Mungu kumnywesha udongo mchafu nao ni usaha wa watu wa motoni na uchafu utokao kwa wazinzi.”154

5.

Aimarishe azma yake na aimarishe misingi ya imani ndani ya nafsi, na hii ndio njia ya kwanza.

6.

Ajiepushe kujichanganya na wale waliosibiwa na maradhi haya hatari, badala yake ajichanganye na watu wenye mwenendo mwema.

7.

Ajikumbushe hali yake awapo ndani ya ulevi, kuanzia vitendo vibaya atendavyo mpaka kauli chafu atoazo, hususani akirekodiwa kwa vyombo vya kisasa au asimuliwe na mtu amwaminiye.

153  154

Ad-Dhunubul-Kabira, Juz. 1, Uk. 235. Wasailus-Shia, Juz. 17, Uk. 299. 54


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

8.

Badala ya ulevi atumie mambo ya halali yenye manufaa, na iwe kwa hatua baada ya hatua mpaka aweze kujinasua na unywaji wa pombe bila kizuizi chochote.

9.

Azingatie maradhi ya kudumu yatokanayo na ulevi, nayo ni mengi sana: a.

Mlevi anastahili adhabu ambayo imeainishwa na sheria tukufu ya Uislamu ambayo ni viboko themanini.

b.

Mtu huyu anastahili kutengwa na jamii yote hususan katika suala la ndoa. Imam as-Sadiq (a.s.) amesema: “Atakayemuoza bintiye kwa mlevi bila shaka amekikata kizazi chake.”155

c.

Hakika mlevi hata akitetewa haukubaliki utetezi wake, hasadikishwi aongeapo, hakabidhiwi amana wala akiugua hatembelewi.

10. Ajue kwamba ulevi huleta uadui na chuki baina ya watu. Mwenyezi Mungu swt. amesema: “Hakika Shetani anataka kuwaingizia uadui na bughudha baina yenu kwa pombe na kamari na kuwazuia kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kuswali, basi je, mtakoma.” (Sura al-Masidah: 91).

Wasailus-Shia, Juz. 1, Uk. 253.

155

55


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

TIBA YA KUINGILIA YASIYOKUHUSU 1.

Akumbuke madhara yake na manufaa ya kukaa kimya kama ilivyo ndani ya riwaya za Ahlul-Bait (a.s.).156

2.

Ajue kwamba yeye ataulizwa dhidi ya kila neno azungumzalo.

3.

Ajitenge na watu kadiri awezavyo.

4.

Ailazimishe nafsi yake kukaa kimya dhidi ya baadhi ya yale yasiyomhusu ili auzoeshe ulimi wake kuacha kuongea yasiyomhusu.

5.

Atafakari kwa kina na kufikiri kabla ya neno lolote atakalo kuzungumza, kama lina faida ya kidini au ya kidunia, la sivyo aliache.157

6.

Autumie muda wake kwa kufanya kazi na kutafuta maisha yake, hilo lina manufaa zaidi kwake, kwa sababu kujiingiza katika yasiyokuhusu ni kazi ya mtu asiye na kazi.

7.

Atakaye tiba ya moja kwa moja basi ajiepushe na sababu zake, nazo ni: a.

Kutaka kujua asiyo na haja nayo: Na bila shaka tumeshaeleza tiba yake mahala pake.

b.

Kushirikiana na jamaa na kutokata mazungumzo yao: Tiba yake ni abadili mazungumzo yao na kuyapeleka kwenye

  Jamius-Saadat, Juz. 2, Uk. 186 na 189.   Jamius-Saadat, Juz. 2, Uk. 186 na 189.

156 157

56


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

yale yenye manufaa, kama vile awaulize swali gumu ili watofautiane katika jibu. Hilo litawafanya waache mazungumzo waliyokuwa nayo. c.

Kuutumia wakati wa faragha: Tiba yake ni kujisomea kwa manufaa na kwa mazoezi na mambo mengine ya manufaa.

Imepokewa kwamba siku ya Uhudi alikufa kishahidi kijana mmoja toka katika masahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), likakutwa jiwe lililofungwa juu ya tumbo lake kutokana na njaa. Mama yake akafuta udongo toka kwenye uso wake na akasema: “Hongera kwa kupata Pepo ewe mwanangu.” Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akasema: “Kitu gani chakujulisha hivyo, huenda alikuwa akizungumzia yasiyomhusu na akizuia yasiyomdhuru.”158

TIBA YA KUKHINI AMANA 1.

Akumbuke riwaya za Ahlul-Bait (a.s.) zinazokemea khiyana, na kwa uchache ni zile zisemazo kwamba mfanya khiyana atafia nje ya mila ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).159

2.

Ajue kwamba Mwenyezi Mungu amewasifu waaminifu. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Maadui wa Mwenyezi Mungu wameongopa, hakuna kitu kilichokuwepo zama za ujahiliya ila kiko chini ya nyayo zangu, ila amana, haki yenyewe hutekelezwa kwa mwema na muovu.”160

Jamius-Saadat, Juz. 2, Uk. 185.   Ad-Dhunubul-Kabira, Juz. 1, Uk. 355 na 368. 160   Ad-Dhunubul-Kabira, Juz. 1, Uk. 235. 158 159

57


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

3.

Ajue kwamba mahusiano ya kijamii yanategemea roho njema, ukweli, uaminifu na kuaminiana wao kwa wao. Mambo haya ndio siri ya furaha ya mwanadamu, kuharibika kwa baadhi ya mambo haya ndio kuharibika kwa nidhamu yote. Na bila shaka iwapo khiyana itaenea ndani ya jamii basi hakuna litakalotengemaa.

4.

Hakika mwenye sifa hii hutengwa na wengine, na muamala wao kwake huwa sawa na wanavyoamiliana na mwizi, mnyang’anyi na jambazi, na hatima yake ni kutengwa mbali na jamii.

5.

Ajue kwamba khiyana huleta ufukara.161

6.

Ajue kwamba kipimo cha kumjua mtu ni ukweli na kutekeleza amana, na wala si wingi wa Sala na sijda ndefu, kama ilivyo ndani ya maelezo ya Ahlul-Bait (a.s.).162

7.

Ajue kwamba uaminifu humfanya mtu awe mkweli.163

8.

Kuna watu hawana uaminifu nao ni: Mlevi, asiye muumini na mfanya khiyana.164

9.

Hakika khiyana ni moja ya sababu za mwanadamu kushuka hadhi na kudorora katika sekta ya maisha, kama ambavyo pia ni nyenzo hatari ya kudhoofisha hali ya kuaminiana baina ya watu.165 Imam as-Sadiq (a.s.) amesema: “Msitazame urefu wa sijda ya mtu wala rukuu yake, kwani hilo ni mazoea yake, na iwapo ataacha atajihisi vibaya. Lakini tazameni ukweli wa mazungumzo yake na utekelezaji wa amana.”166

Ad-Dhunubul-Kabira, Juz. 1, Uk. 456.   Al-Akhlaq Wal-Adab, Uk. 135. 163   Ghurarul-Hikam, Juz. 1, Uk. 79, Hadithi ya 1617. Al-Akhlaq Wal-Adab, Uk. 236. 164   Al-Akhlaq Wal-Adab, Uk. 136. 165   Akhlaqu Ahlul-Bayti, (a.s.) Uk. 97. 166   Akhlaqu Ahlul-Bayti, (a.s.) Uk. 135. 161 162

58


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

TIBA YA KUJIONYESHA (RIYA) 1.

Akate sababu za kujionyesha, nazo ni kule kupenda sifa na kukimbia kulaumiwa, na kutamani yaliyomo mikononi mwa watu.167

2.

Akumbuke madhara ya kujionyesha na jinsi anavyopitwa na fursa ya kuurekebisha moyo wake na anavyonyimwa taufiki hapa duniani, nafasi mbele ya Mwenyezi Mungu huko Akhera, na adhabu, ghadhabu na hizaya vitakavyompata huko Akhera.168

3.

Hakika mwenye kujionyesha hapa duniani ni asiyetulia, mwenye kuzongwa na mawazo kwa sababu ya nyoyo za watu, kwani kuwaridhisha ni jambo lisilodirikiwa.169

4.

Ajue kwamba ikiwa kujionyesha kwake ni kwa sababu ya kutamani vilivyomo mikononi mwa watu inampasa ajue kwamba Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kuzitiisha nyoyo katika kunyima au kutoa.170

5.

Tiba yake ya kivitendo ni aizoeshe nafsi yake kuficha ibada na kufunga milango dhidi yake.171

6.

Ajue kwamba atendaye kwa ajili ya Mwenyezi Mungu tu bila kumshirikisha na chochote atamfanya awe mwenye kupendwa na watu.172

Jamius-Saadat Juz. 2 Uk. 396.   Al-Muhjatul-Baydhau Juz. 6 Uk. 172. Jamius-Saadat Juz. 2 Uk. 396 – 397. 169   Al-Muhjatul-Baydhau Juz. 6 Uk. 172. Jamius-Saadat Juz. 2 Uk. 396 – 397. 170   Al-Muhjatul-Baydhau Juz. 6 Uk. 172. 171   Jamius-Saadat Juz. 2 Uk. 399. 172   Al-Arbaun Haditha Uk. 50. 167 168

59


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

7.

Atake msaada kwa Mwenyezi Mungu na aipige vita nafsi yake, kwani juhudi ni kutoka kwa mja na uongofu ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu amesema: “Na wale wanaofanya juhudi kwa ajili yetu, hakika tutawaongoza kwenye njia zetu. Na hakika Mwenyezi Mungu yuko pamoja na wema.” (Sura Ankabut: 69).173

8.

Ajue kwamba ridhaa ya watu ni malengo yasiyofikiwa, hivyo asiichoshe nafsi yake wala kupoteza juhudi zake, bali amkusudie yule asiyepoteza amali ya mtendaji, naye ni Mwenyezi Mungu.

9.

Ajiepushe na watu na mikusanyiko yao, bali ajitenge yeye pamoja na nafsi yake angalau kwa wakati maalumu ili aizoeshe nafsi yake ikhlasi na kutokujionyesha.174

10. Akumbuke Aya na riwaya zinazopiga vita sifa hiyo, na kwamba kitendo hicho ni sawa na kumshirikisha Mwenyezi Mungu.175 11. Akumbuke Aya na riwaya zinazosifia ikhlasi na kwamba amali haikubaliki ila pamoja na ikhlasi kwa Mwenyezi Mungu.176 12. Ang’oe vyanzo na sababu za kujionyesha, navyo ni kupenda sifa, tamaa na kufunika na kuficha uhalisia wake ambao haujulikani ni upi. Huenda kuna kitu anakikimbia au anataka kutenda kitu, hivyo anajionyesha ili wengine wasiwe na shaka naye.177 Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Hakika jambo ninalohofu sana juu yenu ni shirki ndogo.” Wakasema: Ni   Al-Akhlaq Uk. 164.  Bidayatul-Akhlaq Uk. 221. 175   Mizanul-Hikma Juz. 4 Uk. 28. 176   Mizanul-Hikma Juz. 3 Uk. 57. 177   Akhlaqu Ahlul-Bayti, (a.s.) Uk. 134. 173 174

60


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

ipi hiyo shirki ndogo? Akasema: “Kujionyesha. Siku ya Kiyama Mwenyezi Mungu atawaambia wenye kujionyesha pindi atakapowalipa waja kulingana na amali zao: ‘Nendeni kwa wale ambao mlikuwa mkijionyesha kwao duniani, muone je mtapata malipo toka kwao”’178

TIBA YA ZINAA 1.

Ajue kwamba zinaa ni miongoni mwa maradhi hatari ya kijamii, kwa sababu husababisha fitina kuchemka, mirathi kubatilika, undugu kukatika na haki za wazazi juu ya watoto kupotea, pia kupotea haki za watoto juu ya wazazi. Mwenyezi Mungu amesema: “Wala msiikurubie zinaa. Hakika hiyo ni uchafu na njia mbaya.” (Sura Israi: 32).179

2.

Akumbuke kwamba Mwenyezi Mungu humwondolea mzinzi imani.180

3.

Hakika zinaa hupelekea kifo cha ghafla na huleta ufukara.181

4.

Ajue kwamba zinaa haitimizi malengo ambayo yameelekezwa na dini za kimbinguni nyuma ya ndoa, ambapo malengo yake ya msingi ni kuendeleza kizazi cha mwanadamu, ili kwamba atekeleze jukumu lake alilowekewa na Mwenyezi Mungu katika maisha haya, kwani kupoza ya kimwili ni lengo la pili kwa mtazamo wa Uislamu.

Jamius-Saadat, Juz. 2 Uk. 375.   Al-Amthal, Juz. 11, Uk. 18 – 19. 180   Mjmuatu Warram, Juz. 1, Uk. 39. 181   Al-Kabair Minadhunub, Uk. 29. 178 179

61


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

5.

Hakika zinaa hupelekea kuporomoka kwa hali ya uchumi kutokana na maradhi ya zinaa yanayompata mhusika, na kutokana na maelfu ya watoto wa haramu inayowaleta, pia ni kutokana na mali anazozitumia mzinifu ili afanikiwe kumgharamia na kumpata mzinifu mwenza.182

6.

Azingatie athari zitokanazo na zinaa, sawa iwe ni hapa duniani au ni huko Akhera: a. Huondoa haiba. b. Huharakisha kifo. c. Hukata riziki.183 d. Husababisha kifo cha ghafla.184 e. Malipo mabaya Siku ya Kiyama. f. Husababisha kupatwa na hasira za Mwenyezi Mungu. g. Kuishi milele motoni.

7.

Ni wajibu juu ya akina baba kuheshimu hali ya kijinsia ambayo huwatokea vijana mwanzoni mwa balehe yao, na hivyo ni wajibu juu yao kuizuia hali hiyo kwa kuwaozesha mapema watoto wao.

8.

Ni wajibu juu ya asasi za Kiislamu vikiwemo vituo vya sayansi za kidini (Hawza) na wenye madaraka, kuchukua hatua za kivitendo ili kukidhi mahitaji ya wajibu wa ndoa na kusaidia ipasavyo kwa kadiri ya uwezo. Na eneo hili ndio eneo muhimu la kutumia mapato ya kisharia (Zaka – Khumsi, nk.).

Ad-Dhunubul-Kabira, Juz. 1, Uk. 197.   Al-Kabair Minadhunub, Uk. 29 na 30. 184   Al-Kabair Minadhunub, Uk. 29 na 30. 182 183

62


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

9.

Kijana atumie Swaumu na Itikafu kupambana na matamanio ya kijinsia, mpaka ayavunje yake au afanikiwe kuyapeleka mawazo yake kwenye maarifa ya juu.185

10. Na hapa kuna mambo ambayo yamewajibishwa na Uislamu, na laiti kama Waislamu watayafuata basi watajiepusha na maangamizi mengi ya zinaa: a.

Wanawake washikamane na hijabu ya Kiislamu. Yenyewe ndio kizuizi kikubwa cha zinaa.

b.

Pande zote mbili ziangushe macho chini, kwani hakika mtazamo ni mshale miongoni mwa mishale ya Ibilisi.

c.

Ni haramu faragha ya jinsia mbili ambazo ni ajinabi.

d.

Adhabu zinazozuia zinaa, kama vile kumpopoa mawe mzinifu na kumjeledi.186 Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Atakayezini na mwanamke wa Kiislamu au wa kimajusi, huru au mtumwa, kisha asitubu na akawa amekufa akiwa katika hali hiyo, Mwenyezi Mungu atamfungulia ndani ya kaburi lake milango mia tatu, ndani ya kila mlango watatoka nyoka na nge wa moto, ataendelea kuungua mpaka siku ya Kiyama. Atakapofufuliwa toka kaburini watu watakerwa na riha ya uvundo wake, kwa riha hiyo yatajulikana aliyokuwa akiyatenda huko duniani, mpaka itakapoamuriwa apelekwe motoni. Eh! Hakika Mwenyezi Mungu ameharamisha haramu na ameiwekea adhabu na hakuna yeyote mwenye ghera kushinda Mwenyezi Mungu, na kutokana na ghera Yake ameharamisha uchafu.”187

Ad-Dhunubul-Kabira, Juz. 1, Uk. 201. Ad-Dhunubul-Kabira, Juz. 1, Uk. 205. 187  Man Layahdhuruhu al-Faqih Juz. Uk. 6, Hadithi ya 1. 185

186

63


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

TIBA YA DHIHAKA NA DHARAU 1.

Ajue kwamba dharau hupelekea nafsi yake kudhalilika Siku ya Kiyama mbele ya Malaika, Manabii na mbele ya watu wote.188

2.

Akumbuke jinsi dharau ilivyolaumiwa katika Aya na riwaya za Ahlul-Bait (a.s.).189

3.

Mwanadamu kwanza atazame dosari zake na ajishughulishe kuziondoa.190

4.

Ajue kwamba sifa hii ni sifa ya wanafiki, hivyo ni wajibu juu yake kujiepusha nayo. Mwenyezi Mungu amesema: “Na wanapokutana na walioamini husema: Tumeamini; na wanapokuwa peke yao kwa mashetani wao, husema: Hakika sisi tu pamoja nanyi. Tunawacheza shere (wao) tu.” (Sura al-Baqarah: 14).

5.

Mwenye dharau atambue kuwa yu mbali na watu, hapendwi na jamii wala hakuna yeyote ampendaye, hivyo ni wajibu juu yake kuacha tabia hiyo, atapendwa na watu na atapata heshima yao.191

6.

Ang’oe sababu zake, na iliyo muhimu kati ya hizo ni kiungo cha kijamii ambacho ndio asili ya sifa hii.

7.

Huenda unayemdharau ni bora mbele ya Mwenyezi Mungu kukushinda wewe, na huenda ni walii miongoni mwa mawalii Wake, nawe unamchupia mipaka walii miongoni mwa walii Wake.

Mizanul-Hikma, Juz. 4, Uk. 415. Jamius-Saadat Juz. 2, Uk. 289.   Jamius-Saadat, Juz. 2, Uk. 288. 190   Dirasatu Fiil-Mashakil al-Akhlaqiya Uk. 79. 191   Mizanul-Hikma, Juz.4, Uk. 415. 188 189

64


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

8.

Huenda sababu inayokufanya ujione bora ni batili lakini wewe waiona kuwa ni sahihi, kama vile kumdharau kwa sababu ya lakabu, au sehemu aliyozaliwa, au lugha, na vipimo vyote hivi havina ubora wowote.

9.

Hakika hii ni sifa ya majahili ambao hawana dalili sahihi waitegemeayo, hivyo wanalazimika kutumia njia ya dharau. Mwenyezi Mungu amesema: “Enyi ambao mmeamini! Kaumu isidharau kaumu nyingine, huenda wakawa bora kuliko wao; wala wanawake kwa wanawake wengine, huenda wakawa bora kuliko wao. Wala msitiane kasoro, wala msiitane majina ya kejeli. Na wasiotubu, hao ndio madhalimu.” (Sura Hujrat: 11). Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Hakika wenye kuwadharau watu atakuwa mmoja wao anafunguliwa mlango wa Pepo kisha anaambiwa: ‘Njoo! Njoo!’ naye anakuja na matatizo yake na ghamu yake. Anapofika anafungiwa mlango, kisha anafunguliwa tena mlango….. ataendelea kuwa hivyo mpaka itafikia kwamba mtu anafunguliwa mlango na kuambiwa: ‘Njoo!’ lakini haendi.”192

TIBA YA KUTEMBEA KICHWA WAZI NA BILA HIJABU 1.

Mwanamke ajue kwamba kutembea uchi na mfano wake kunawashawishi wanaume na kuamsha hisia zao pamoja na kuua mishipa yao ya fahamu, na baadhi ya nyakati huwa chanzo cha maradhi ya saikolojia. Na hali hiyo inaweza kumfanya ambake mwanamke pindi hisia za kijinsia zinapochemka.193

Mizanul-Hikma, Juz. 4, Uk. 415. Jamius-Saadat, Juz. 2, Uk. 288.   Tafsirul-Amthal, Juz. 11, Uk. 81.

192 193

65


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

2.

Mwanamke ajue kwamba idadi ya talaka na idadi ya ndoa zilizovunjika imeongezeka kwa sura ya kutisha katika ulimwengu huu, na sababu yake ni kutembea uchi, kwa sababu watu aghlabu ni wafuasi wa matamanio, na hivyo ndivyo mapenzi ya mwanaume yanavyohama toka kwa mwanamke huyu kwenda kwa mwanamke mwingine, kila siku na kila saa.

3.

Ajue kwamba kuenea kwa uchafu na kuongezeka kwa watoto wa haramu ni miongoni mwa matokeo mabaya kabisa ya kupuuza hijabu, na wala hakuna haja ya kunukuu asilimia katika suala hili, kwani ushahidi wake uko dhahiri katika jamii ya kimagharibi, na uko wazi kwa kiwango kisichohitaji maelezo.

4.

Ajue kwamba kutembea uchi kunampelekea mwanamke kutaka kutafuta urembo, kujidhihirisha kwa fedheha na kudidimia kimaadili, na hivyo utu wa mwanamke huporomoka katika jamii ambayo imejikita katika mvuto wa kijinsia, na mporomoko huu humwondolea mwanamke thamani yake yote ya kibinadamu.

5.

Mwanamke ajue kwamba mwenendo wake nyuma ya kutembea kwake uchi utampelekea kuwaacha watoto, kutowatunza na kutowahurumia, jambo ambalo hupelekea utu wao kushuka, na haya yote huiweka jamii kwenye hatari.

6.

Mwanamke asisikie wala kusikiliza yasemwayo na vyombo vya habari vya kimagharibi vya kimarekani iliyo duni, pamoja na hoja wazitoazo juu ya hijabu, na azipuuze hoja hizo, kama ile ya kwamba hijabu humtenga mwanamke na jamii na kumzuia kutekeleza harakati zake za kijamii, na kwamba hijabu hutenganisha baina ya wanawake na wanaume na hatimaye kuwazidishia wanaume uchu wa wanawake badala ya kuwapoza, kwa sababu mtu huwa na uchu na kile alichozuiwa. Hivyo ni 66


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

lazima mwanamke apuuze madai haya kwa sababu ni madai yasiyo na maana wala msingi, bali kinyume ndio sahihi. 7.

Mwanamke ajue kwamba Uislamu kwa kanuni hizi na kwa kuhifadhi hijabu ya mwanamke kwa namna hii, unampa heshima na utukufu mwanamke, na wala hautaki awe mdoli baina ya wanaume ambao wanamfanya kivutio cha biashara zao.

8.

Azingatie kusoma Aya na riwaya zinazokemea sifa hiyo.

9.

Ajue kwamba mtembea uchi yupo katika ghadhabu ya Mwenyezi Mungu na mbali na rehema zake, ila kama atajuta na kutubia.

10. Ajue kwamba yeye kwa kitendo chake hiki anampiga vita Mwenyezi Mungu, Mtume Wake na Maasumu (a.s.), na anauumiza moyo wa Imam wa zama hizi (a.t.f).

TIBA YA TABIA MBAYA 1.

Akumbuke ubaya wa tabia mbaya na madhara yake mabaya, na kwamba husababisha ghadhabu za Mwenyezi Mungu, kuchukiwa na watu na kutengwa nao.194 Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Tabia mbaya ni hatamu ya adhabu ya Mwenyezi Mungu, ncha moja ipo katika pua ya mwenye nayo na ncha nyingine imo mikononi mwa shetani, na shetani humkokotea kwenye shari, na shari humpeleka motoni.”195 Imesemwa kwamba Mwenyezi Mungu hakubali toba ya mtu

Jamius-Saadat, Juz. 1, Uk. 307. Akhlaqu Ahlul-Bayti (a.s.) Uk. 22.   Sharhu Nahjul-Balagha, Juz. 6, Uk. 338. Nahjus-Saadah, Juz. 7, Uk. 243.

194

195

67


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

mwenye tabia mbaya, kwa sababu yeye hatoki kwenye dhambi ila huingia kwenye dhambi nyingine kwa sababu ya tabia yake mbaya. Malenga amesema: “Aitakapo tabia, tabia zake humvutia kwenye hulka ya asili ya kale.” 2.

Atazame uzuri wa tabia njema, na kwamba ni miongoni mwa maadili ya Manabii (a.s.), na huonyesha ukamilifu wa mwanadamu na fadhila zake.196

3.

Atafakari kwa kina na kuzama katika kila harakati na katika kila neno alisemalo ili apunguze matendo mabaya ayatendayo.197

4.

Achukie maadili yote mabaya na aazimiye kuyakhalifu, arudie hali hiyo mpaka yamwondoke.198

5.

Asiishi na kufanya urafiki na mtu asiye msafi, kwani mwanadamu huiga hali za kiroho toka kwa wale wanaomzunguka katika maisha.199

6.

Azingatie athari nzuri za kidunia za tabia njema, kama vile kupewa umri mrefu, kuimarisha majumba na kuongezewa riziki.200 Imam as-Sadiq (a.s.) amesema: “Wema na tabia njema huimarisha majumba na huzidisha umri.”201

Nahjus-Saadah, Juz. 1, Uk. 307.   Nahjus-Saadat, Juz. 1, Uk. 307. 198   Al-Arbaun Haditha Uk. 40. 199   Dirasatu Fiil-Mashakil al-Akhlaqiya Uk. 17 na 22 – 23. 200   Dirasatu Fiil-Mashakil al-Akhlaqiya, Uk. 17 na 22 – 23. 201   Dirasatu Fiil-Mashakil al-Akhlaqiya, Uk. 22 . Jamius-Saadat, Juz. 1, Uk. 309. 196 197

68


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

TIBA YA KUWA NA DHANA MBAYA KWA MUUMBA NA KIUMBE 1.

Inapasa kila muumini asikate tamaa na rehema za Mwenyezi Mungu, wala asidhani kwamba hatomrehemu bali atamwadhibu, wala hatomwepusha na adhabu.

2.

Ajue kwamba balaa na misiba aipatayo duniani si shari kwake wala si adhabu, bali Mwenyezi Mungu ni Mrehemevu kushinda kila mwenye kurehemu, na ni Mwenye huruma kushinda wazazi wake, bali mabalaa yampatayo duniani ni kheri na wema kwake.

3.

Avitafsiri namna sahihi vitendo vya watu na kauli zao, na wala asivitafsiri kwa namna mbaya, bali akubali udhuru wao.

4.

Aizowezeshe nafsi yake kuwa katika hali iliyotangulia mpaka iwe ni tabia ya kudumu, kwa sababu hupelekea kukana ubaya toka kwa watu, kama ilivyokuja katika riwaya.202

5.

Ajue kwamba madhara ya kuwadhani vibaya viumbe humrudia mwenyewe, na kwamba yeye ni mtu mbaya.203 Imam Ali (a.s.) alisema: “Dhana mbaya huharibu mambo na huleta ubaya, na mtu mbaya kushinda watu wote ni yule asiye mwamini yeyote kwa sababu ya dhana yake mbaya.”204

6.

Ajue kwamba kumdhania vibaya Mwenyezi Mungu ni miongoni mwa madhambi makubwa, hivyo ni wajibu juu yake kujie-

Mizanul-Hikma, Juz. 5, Uk. 627.   Mizanul-Hikma, Juz. 5, Uk. 627. 204   Mizanul-Hikma, Juz. 5, Uk. 627. 202 203

69


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

pusha nayo.205 Imam Ali (a.s.) amesema: “Jambo la ndugu yako liweke katika tafsiri nzuri mpaka ufikie hoja itakayokushinda. Wala usilidhanie vibaya neno lolote litokalo kwa ndugu yako ilihali una nafasi ya kulitafsiri vizuri.”206 Na amesema tena (a.s.): “Dhana nzuri ni raha ya moyo na usalama wa dini.”207

TIBA YA USHOGA NA USAGAJI 1.

Akumbuke madhara yake, na ya chini kabisa ni kupotea, na maradhi ya kimwili ambayo husababisha kifo cha haraka, la sivyo ni kuuwawa, kukonda, kukoma kwa ukoo na kutokuwa na kizazi.

2.

Avunje ya kijinsia kwa njaa na kwa Swaumu.208

3.

Azibe njia inayopelekea kufanya vitendo hivyo, kama kutazama, kuongea, kukaa faraghani na kutazama filamu za ngono. Na sababu yenye nguvu sana na yenye kuchochea sana vitendo hivyo ni kutazama na kupenda faragha.209

4.

Atumie njia za halali ambazo zitazuia haya, kwa ndoa ya kudumu au ya muda mfupi.

5.

Azingatie maelezo yaliyopatikana toka kwa Ahlul-Bait (a.s.) yanayomsifia yule mwenye kujiepusha na kwa sababu ya kumwogopa Mwenyezi Mungu, na sifa ya chini kabisa ni kwamba moto utakuwa haramu juu yake, na Mwenyezi Mungu atamsalimisha na fadhaa kubwa.210

Mizanul-Hikma, Juz. 5, Uk. 631.   Safinatul-Bihar, Juz. 5, Uk. 391. 207   Mizanul-Hikma, Juz. 5, Uk. 1784, Darul-Hadith. 208   Jamius-Saadat, Juz. 2, Uk. 11. 209   Jamius-Saadat, Juz. 2, Uk. 12. 210   Al-Wsail, Juz. 15, Uk. 209, Hadithi ya 1. 205 206

70


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

6.

Ajue kwamba sifa hii ni miongoni mwa sifa za kinyama, mwanadamu hajaumbwa kwa sifa hiyo, bali ameumbwa ili afikie katika ukamilifu wa kiroho wa hali ya juu kabisa.

7.

Azingatie na arejee kwenye Aya nyingi na riwaya mutawatiri zinazokemea vitendo hivi na zinazoonyesha adhabu yake, na hatimaye azingatie maelezo yake. Hakika atakayetubu Mwenyezi Mungu atapokea toba yake. Tambua kwamba Ulamaa wa Kiislamu wamekitengea mlango makhususi katika vitabu vya fiqhi na vya Hadithi kila kitendo kiendacho kinyume na maumbile. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Mtupo wa macho ni mshale wa sumu miongoni mwa mishale ya Ibilisi, atakayeuacha kwa sababu ya kumwogopa Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu atampa imani ambayo atapata utamu wake ndani ya moyo wake.”211 Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema tena: “Enyi kundi la vijana! Ni juu yenu kuoa, asiye na uwezo afunge, kwani hakika kufunga ni kinga kwake.”

TIBA YA KUWA NA MATUMAINI YA KUISHI MUDA MREFU 1.

Kwa kuwa chanzo cha matumaini ya kuishi muda mrefu ni ujinga na kuipenda dunia, basi inampasa auondoe ujinga kwa fikra safi dhidi ya ukungu wa upofu. Na aondoe hali ya kuipenda dunia kwa kujinyima, kwani hata kama ataitumainia dunia vyovyote iwavyo bado matumaini hayo yatatoweka.212

Jamius-Saadat, Juz. 2, Uk. 12 - 13.   Jamius-Saadat, Juz. 3, Uk. 34.

211

212

71


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

2.

Asikilize nasaha toka kwa watu wasafi.213

3.

Azingatie riwaya zinazokemea sifa hii, nazo zinatosha kuwa mnasihi214 na msifiaji wa kuwa na matumaini ya kuishi muda mfupi, riwaya ambazo zinasisitiza kukumbuka kifo, kwa sababu kitendo hicho huulainisha moyo na hupelekea kujielekeza kwenye matendo mema na mazuri.

4.

Atazame kuvunjika kwa viungo vyake na udhoofu wake na kwamba hatima yake ni kufunikwa na udongo.215

5.

Ajue kwamba kuwa na matumaini ya kuishi muda mrefu husahaulisha Akhera, na hali hiyo ina hasara kubwa na ni mlango wa kutenda kila la haramu na kufuata kila tamanio.216 AmirulMuuminin Ali (a.s.) amesema: “Enyi watu! Hakika ninahofia sana juu yenu mambo mawili: Kufuata matamanio na kuwa na matumaini ya kuishi muda mrefu. Kufuata matamanio kunazuia kuifuata haki. Na kuwa na matumaini ya kuishi muda mrefu kunasahaulisha Akhera.”217 Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Hakuna mtu aliyerefusha matumaini ya kuishi ila aliharibu amali.”218 Mmoja wa wenye hikima alisema: “Jiepusheni na kuwa na matumaini ya kuishi muda mrefu, kwani hakika atakayelevywa na matumaini yake atadhalilishwa na amali yake.”219

Jamius-Saadat Juz. 2, Uk. 34. Jamius-Saadat, Juz. 2, Uk. 34. 215   Majmuat Warram, Juz. 1, Uk. 278. 216   Al-Wasail, Juz. 15, Uk. 280, Hadithi ya 7. 217   Al-Wasail, Juz. 17, Uk. 280, Hadithi ya 8. 218   Jamius-Saadat, Juz. 3, Uk. 35. 219   Al-Mustatraf, Juz. 1, Uk. 104. 213

214

72


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

TIBA YA MAJIVUNO 1.

Akumbuke kwamba maradhi haya yana maafa, nayo ni: a.

Kiburi, ujeuri na ubinafsi. Atakayejivuna dhidi ya watu na kuwafanyia jeuri, ajue hilo litasababisha kuchukiwa na watu na kupuuzwa.

b.

Kunampofusha mwenye nayo dhidi ya mapungufu yake na mabaya yake, na hatimaye anashindwa kujituma na kufanya bidii ya kujirekebisha, kwa kudhani kwamba ameshajitosheleza na amefaulu kwa kupata kitakachomwokoa, na huko ni kuangamia kwa wazi kusiko na shaka hata kidogo.

c.

Kunapelekea kujiona ana matendo mengi ya utiifu kwa Mwenyezi Mungu, na hivyo kusahau dhambi na makosa, na hatimaye kuyapuuza na kutokumbuka chochote kati ya hayo. Na hata kama atayakumbuka atayadharau, jambo ambalo litamzuia kufanya toba, na hatimaye madhambi yake yatazidi kukua kushinda jabali kubwa na hatimaye yatamhilikisha.220 Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Hakika sababu za kuhiliki mtu miongoni mwenu ni: Kujivuna, kuona matendo yake ni mengi na kuona dhambi zake ni chache.”221 Imam as-Sadiq (a.s.) amesema: “Atakayeingiwa na majivuno ameangamia.”222

Jamius-Saadat, Juz. 1, Uk. 325. Akhlaq Ahlul-Bayt Uk. 141. Al-Haqaiq Uk. 97 – 98.   Adabun-Nafsi, Juz. 1, Uk. 203. 222   Akhlaq Ahlul-Bayt, Uk. 139. 220 221

73


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

2.

Ajitahidi kutoathiriwa na vyanzo vya majivuno, navyo ni elimu, maarifa, utiifu, ibada, na mengineyo miongoni mwa ukamilifu wa kinafsi, kama vile uchamungu na ushujaa.”223

3.

Azingatie athari nzuri zitokanazo na unyenyekevu, na ya chini kabisa ni kuingia Peponi.

4.

Aondoe nafsini mwake sababu za siri ambazo Imam Ali na Imam as-Sadiq (a.s.) wametutanabahisha nazo, nazo ni:

5.

a.

Ujinga. Imam as-Sadiq (a.s.) amesema: “Hakuna ujinga wenye kudhuru kushinda majivuno.”224

b.

Mwanadamu kuridhika na nafsi yake. Imam Ali (a.s.) amesema: “Kuridhika na nafsi yako ni kuharibu akili yako.”225

c.

Upumbavu. Imam Ali (a.s.) amesema: “Majivuno ni kilele cha upumbavu.”226

Atazame madhara ya maradhi haya na sababu zake, nayo ni mengi: a. b. c. d. e.

Upweke. Kuangukia kwenye makosa. Kudhihirisha mapungufu. Kubomoa kila jema alilolijenga mwanadamu. Hupelekea kuchukiwa.

Al-Muhujatul-Baydhau, Juz. 6, Uk. 286.   Biharul-An’war, Juz. 69, Uk. 400, Hadithi ya 93. 225   Ghurarul-Hikam, Juz. 1, Uk. 382, Hadithi ya 29. 226   Ghurarul-Hikam Juz. 1 Uk. 22, Hadithi ya 469. 223 224

74


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

f.

Husababisha kuhiliki.

g.

Huharibu akili na kusababisha upumbavu.

h.

Ni kizuizi kizuiacho kujiongezea, na huondoa neema.227

6.

Ajue kwamba kila alipatalo mwanadamu linatokana na fadhila za Mwenyezi Mungu, naye ndiye aliyeumba kila kitu na kukikadiria riziki yake.

7.

Ni lazima mwanadamu aijue nafsi yake. Imam Ali (a.s.) amesema: “Ziba njia ya majivuno kwa kuijua nafsi yako.”228

8.

Atafakari kwa kina na azingatie yaliyomo ndani ya Aya na riwaya zenye kukemea sifa hii, na zile zenye kuusifu unyenyekevu. Ajishushe na wala asijikweze.

9.

Ajue chanzo chake ni kutokana na nini, na ameumbwa kwa kitu gani.229 Imam Ali (a.s.) amesema: “Nashangaa mwanadamu eti anajivuna, wakati mwanzo wake ni mbegu chafu na mwisho wake ni mzoga wa kunuka, naye baina ya hali hizo mbili huwa amebeba kinyesi.”230

Ghurarul-Hikam, Juz. 1, Uk. 43, Hadithi ya 899.   Al-Bihar, Juz. 78, Uk. 164, Hadithi ya 1. 229   Ghurarul-Hikam, Juz. 2, Uk. 272, Hadithi ya 214. 230   Ghurarul-Hikam Juz. 2, Uk. 272, Hadithi ya 214. 227 228

75


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

TIBA YA KUWA NA HARAKA 1.

Akumbuke madhara yake na hatima yake mbaya, na jinsi inavyosababisha uduni na kudharauliwa na watu, husababisha majuto na hasara, maangamio na kuteleza.231 Kama ilivyosemwa: “Polepole ni usalama na harakaharaka ni majuto.” Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Haraka yatokana na shetani na polepole yatokana na Mwenyezi Mungu.”232

2.

Aweke utukufu wa utulivu mbele ya macho yake, ambao ni dhidi ya haraka, na kwamba wenyewe ni sifa ya Manabii (a.s.) na watu wema, nao humpa heshima mwenye nao baina ya wenzake.233

3.

Aazimie kutokutenda chochote ila baada ya kutafakari kwa kina na kuvuta subira, na wala asiache kuwa mtulivu na mpole, nje na ndani, katika vitendo vyake vyote na harakati zake zote.234 Imam as-Sadiq (a.s.) amesema: “Usalama watokana na utulivu, na majuto yatokana na haraka. Atakayeanza amali kabla ya wakati wake ataifikia kabla ya wakati wake.”235

Safinatul-Bihar, Juz. 1, Uk. 489. Mizanul-Hikma Juz. 6, Uk. 72.   Jamius-Saadat, Juz. 1, Uk. 274. 233   Bidayatul-Akhlaq, Uk. 63. 234   Jamius-Saadat, Juz. 1, Uk. 279. 235   Safinatul-Bihar, Juz. 1, Uk. 489. 231 232

76


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

TIBA YA USHABIKI NA KUFICHA HAKI 1.

Ajue kwamba hizo ni sifa mbili zinazopelekea kupatwa na ghadhabu ya Mwenyezi Mungu, na zinaweza kumpeleka kwenye ukafiri, Mwenyezi Mungu apishie mbali hilo. Mwenyezi Mungu anasema: “Wala msichanganye haki na batili, na mkaficha haki na hali mnajua.” (Sura al-Baqarah: 43).

2.

Akumbuke faida za vinyume vya sifa hizo, navyo ni sifa ya uungwana na msimamo katika haki.

3.

Aikalifishe nafsi yake kudhihirisha lile lililo haki na kuifanyia kazi hata kama ni kwa taabu kubwa, mpaka hali hiyo iwe ada kwake.236

4.

Atafakari kwa kina athari za ushabiki wenye fedheha ambazo kati ya hizo ni kuharibika kwa matendo, na kwamba wenyewe ni ufunguo wa kila shari, na kwamba huchukiza moyo, kwa sababu akili yake haimiliki yasiyokuwa hayo.237

5.

Ushabiki wake auelekeze kwenye tabia njema, matendo mema na mambo mazuri.238

6.

Ajue kwamba ushabiki ni tabia mbaya ambayo itamfanya Mwenyezi Mungu amfufue siku ya Kiyama pamoja na mabedui wa kijahiliya.239

Safinatul-Bihar, Juz. 1, Uk. 367 – 368.   Al-Wasail, Juz. 15, Uk. 358, Mlango wa 53. 238   Nahjul-Balagha, Hotuba al-Qaswi’ah, namba 192. 239   Usulul-Kafiy, Juz. 2, Mlango wa ushabiki, Uk. 232. 236 237

77


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

7.

Ajue kwamba kuwapinga watu au raia bila haki yoyote kutamfanya awe mbali na watu, hivyo ni juu yake kusema haki vyovyote iwavyo hata kama ni dhidi ya nafsi yake.

Imam as-Sadiq (a.s.) amesema: “Atakayefanya ushabiki bila shaka amevua mkufu wa imani toka shingoni mwake.”240 Imam Zainul-Abidin (a.s.) amesema: “Hakika ushabiki ambao mwenye nao hupata dhambi ni: Mtu aone shari ya watu wake kuwa ni kheri kushinda kheri za watu wengine. Si ushabiki mtu kuwapenda watu wake, lakini ushabiki ni mtu kuwasaidia jamaa zake kufanya dhuluma.”241

TIBA YA KUVUNJA AHADI 1.

Ajue kwamba kuvunja ahadi kwa ukweli ni kujitoa kwenye miko ya heshima na murua, na kwamba kuvunja mikataba pasi na makubaliano ya pande mbili ni aina mojawapo ya kutokuwa na murua.242

2.

Ajue kwamba kutekeleza ahadi ni moja ya sababu za kuishi vizuri na jamii, nako ni moja ya nguzo ya furaha ya kijamii,

Usulul-Kafiy Juz. 2, Mlango wa ushabiki, Uk. 232.   Akhlaq Ahlul-Bayt, Uk. 106. 242   Ahadi ni kila alichoahidi Mwenyezi Mungu, na makubaliano yaliyopo baina ya waja. Kauli yako kumwambia mtu: “Nakuahidi kwamba nitakupa kitu fulani au nitafanya kitu fulani, hiyo ni ahadi. Na kitendo cha kutokutekeleza hayo au kuakhirisha mpaka mtu yule akate tamaa na hatimaye kuingiwa na huzuni na machungu ambayo hayajui ila Mwenyezi Mungu, kitendo hicho ni kuvunja ahadi au kukhalifu ahadi. Nayo ni aina mbaya sana ya uwongo na iliyo hatari sana, kwa sababu kwa kitendo hicho ni kuwadhihaki watu na kuwadanganya, na kadhalika ni kumdanganya Mwenyezi Mungu, na hiyo ni sifa mbaya sana na ni miongoni mwa viangamizi vikubwa na ni moja ya mitego ya shetani. Dirasatu Fil-Mashakil al-Akhlaqiyyah Uk. 148. 240 241

78


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

na kuna athari kubwa katika shughuli zote za maisha ya watu, maendeleo na mafanikio yote yanajengwa juu ya msingi huu.243 3.

Ajue kwamba kuvunja ahadi hurithisha unafiki, na kunamfanya mtu afe kafiri na afufuliwe katika kundi la wanafiki.244

4.

Na ili mzazi asipandikize sifa hii mbaya ndani ya nafsi ya mwanae, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ameusia bali amemkataza baba kumwahidi mwanae kisha kutomtekelezea ahadi. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Mtu asimwahidi mwanae kisha asimtekelezee.”245 Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Sifa tatu atakayekuwa nazo ni mnafiki hata kama atakuwa ana swali na kufunga na kudai kwamba yeye ni Mwislamu: Anapoaminiwa hukhini, anapozungumza huongopa, na anapoahidi hatekelezi.”246 Mshairi amesema: “Lau maafa yakikusanywa basi yaliyo mabaya zaidi ni ubahili. Na yaliyo mabaya zaidi kushinda ubahili ni ahadi na kuakhirisha (kutekeleza). Ahadi ya uongo haina kheri, na kauli isiyo na kitendo haina kheri.”247 Mwingine akasema: “Hakika umeahidi nawe ni mwenye kuahidi uliye mkarimu sana. Ahadi isiyo timia haina kheri. Mwenyezi Mungu amenineemesha kwa ukarimu wake yale uliyoniahidi, basi kuakhirisha huondoa furaha ya kuneemeshwa.”248

Dirasatu Fil-Mashakil al-Akhlaqiyyah Uk. 148.   Ad-Dhunubu al-Kabirah Juz. 1, Uk. 34. 245   Dirasatu Fil-Mashakil al-Akhlaqiyyah Uk. 152. 246   Ad-Dhunubu al-Kabirah Juz. 1, Uk. 347. 247   Al-Mustatraf Juz. 1, Uk. 272. 248   Al-Mustatraf Juz. 1, Uk. 272. 243 244

79


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

TIBA YA GHADHABU 1.

Aondoe sababu zinazoamsha ghadhabu, nazo ni kujivuna, fahari, kiburi, hadaa, ubishi, dhihaka, kuaibisha, ugomvi, uchu wa sifa na mali, ambayo ni mambo ya kupita.

2.

Akumbuke madhara ya ghadhabu na hatima yake mbaya, na jinsi sharia ilivyokemea sifa hiyo.

3.

Akumbuke sifa na thawabu zilizomo ndani ya riwaya zinazoonyesha ubora wa kuondoa ghadhabu impandapo.249

4.

Akumbuke faida ya upole na kuzuia hasira, na ajipe mazoezi ya kuwa hivyo angalau kwa kujilazimisha.

5.

Atangulize fikra na akili katika kila kitendo au kauli imtokayo, na ailinde nafsi yake isipandwe na ghadhabu.

6.

Ajikinge kusuhubiana na watu wa ghadhabu, na ajichagulie kuketi na watu wapole na wenye kuzuia ghadhabu.

7.

Ajue kwamba yatokeayo hutokea kwa makadara na majaaliwa ya Mwenyezi Mungu, na kwamba mambo yote yako mikononi mwake na katika uwezo wake.250

8.

Ajue kwamba ghadhabu ni maradhi ya moyo na ni upungufu wa akili, hutokana na udhaifu wa nafsi yake na mapungufu yake na si kutokana na ushujaa wake na nguvu yake, na hiyo huonyesha udhaifu wa imani yake.251

Jamius-Saadat, Juz. 1, Uk. 291. al-Muhujatul-Baydhau, Juz. 5, Uk. 305.   Jamius-Saadat, Juz. 1, Uk. 291. 251   Mir’atur-Rashad, Uk. 75. 249 250

80


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

9.

Ajue kwamba anayemfanyia ghadhabu anaweza kupatwa na nguvu na hatimaye akakabiliana naye kinyume na mategemeo yake, na hatimaye akamuudhi kupitia nafsi yake mwenyewe, familia yake, mali yake au mke wake.252

10. Ajue kwamba Mwenyezi Mungu anapenda tusighadhibike, na mpenzi wa kweli huchagua lile alipendalo mpendwa wake, hivyo ikiwa kweli ampenda Mwenyezi Mungu basi azime ghadhabu zake kwa kumpenda Mwenyezi Mungu Mtukufu. 11. Atafakari kwa kina ubaya wa sura yake na vitendo vyake pindi aghadhibikapo.253 12. Ajikinge kwa Mwenyezi Mungu dhidi ya shetani mlaaniwa pindi ghadhabu ichemkapo, kwa sababu yenyewe ni kitendo cha shetani. Imam al-Baqir (a.s.) amesema: “Hakika ghadhabu hii ni kaa la moto toka kwa shetani ambalo huwashwa ndani ya moyo wa mwanadamu….”254 13. Kama amesimama aketi, na kama ameketi alale.255 14. Achukue wudhu au aoge kwa maji baridi.256 15. Aondoke sehemu ambayo ghadhabu imempanda akiwa hapo.257 16. Tiba yake ya kivitendo ni aiondoe nafsi yake kwenye ghadhabu pale tu ianzapo.258   al-Muhujatul-Baydhau, Juz. 5, Uk. 306.   al-Muhujatul-Baydhau, Juz. 5, Uk. 306. 254   Jamius-Saadat, Juz. 1, Uk. 295 na 288. 255   al-Muhujatul-Baydhau, Juz. 5, Uk. 307. Mir’atur-Rashad Uk. 76. 256   Al-Akhlaq, Uk. 146. 257   Al-Arbaun Haditha, Uk. 136. 258   Al-Arbaun Haditha, Uk. 136.s 252 253

81


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

17. Ikiwa ghadhabu yake imesababishwa na ndugu yake wa damu basi tiba yake ni huyo ndugu ampanguse kwa mwili wake, ghadhabu yake itatulia.259 18. Atazame athari mbaya za kiafya zitokanazo na ghadhabu kama vile kulemaa kwa mishipa na matatizo ya figo, na kutokwa na damu, na inaweza kupelekea kifo cha ghafla. Amirul-Muuminin (a.s.) amesema: “Atakayeiachilia ghadhabu yake atafikwa haraka na kifo chake.”260 19. Ni lazima aiimarishe akili yake, kwani hakika akili imara inaweza kwa kufuatilia kuidhibiti ghadhabu.261 20. Asahau au ajisahaulishe tukio lililopelekea kughadhibika.262 21. Anywe maji, hakika kitendo hicho hutuliza ghadhabu, kama ilivyokuja katika riwaya ya Abu Hasan (a.s.).263 22. Ale zabibu, hakika yenyewe hutuliza ghadhabu.264 23. Aombe dua hii: “Ewe Mwenyezi Mungu! Niondolee hasira za moyo wangu na nikinge na viletavyo machafuko. Nakuomba Pepo yako na ninajikinga kwako na shirki. Ewe Mwenyezi Mungu, niimarishe katika uongofu na sawa, na nifanye niwe mwenye kuridhia si mwenye kupotea wala kupoteza.”265 24. Asisahau athari za kuzuia ghadhabu Siku ya Kiyama, atakayeizuia ghadhabu yake dhidi ya watu Mwenyezi Mungu atailinda nafsi yake Siku ya Kiyama, atasitiri aibu zake na atampa Pepo.266   Usulul-Kafiy Juz. 2, Uk. 229, Hadithi ya 2.   Dirasatu Fil-Mashakil al-Akhlaqiyyah Uk. 139. 261   Nahwu Hayatul-Afdhal, Uk. 108 na 113. 262   Nahwu Hayatul-Afdhal, Uk. 108 na 113. 263   Al-Mahasin cha al-Barqiy, Juz. 2, Uk. 398, Hadithi ya 16. 264   Al-Ikhtisas, Uk. 124. 265   Makarimul-Akhlaq, Juz. 2, Uk. 154, Hadithi ya 2377. 266   Thawabul-Aamal cha as-Saduq, Uk. 161, Hadithi ya 1. 259 260

82


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

25. Ajue kwamba wasaidizi wengi huwa upande wa aliye mpole, ambapo huwa kinyume na yule aliye na ghadhabu. AmirulMuuminina (a.s.) amesema: “Mbadala wa chini kabisa aupatao mpole kutokana na upole wake ni kwamba watu huwa wasaidizi wake juu ya mjinga.”267 26. Ajue kwamba ghadhabu humpeleka kwenye udhalili wa kumwomba msamaha yule aliyemghadhibikia.268 27. Aitumie ghadhabu yake sehemu ipasayo, kama vile aghadhibike kwa ajili ya dini yake au uzalendo au awaghadhibikie maadui wa dini.269 Imam Ali (a.s.) amesema: 28. “Ghadhabu humwangamiza aliyenayo, na humfichulia aibu zake.”270 29. Amkumbuke Mwenyezi Mungu Mtukuka na aiache ghadhabu hiyo kwa kumwogopa na kwa kuwa Yeye ni mwenye uwezo juu yake, Naye ndiye Jabari Mwenye kuadhibu, hilo limfanye awe mpole na mtiifu. Imam as-Sadiq (a.s.) amesema: “Mwenyezi Mungu alimfunulia wahyi mmoja wa Manabii wake kwamba: Ewe mwanadamu! Nikumbuke wakati wa ghadhabu yako nitakukumbuka wakati wa ghadhabu Yangu, sintakuangamiza pamoja na nitakaowaangamiza. Na ridhia kwa ajili Yangu na hali ni mwenye kutetea, kwani hakika utetezi Wangu kwako ni bora kushinda utetezi wako juu ya nafsi yako.”271

Al-Wasail, Juz. 15, Uk. 268, Hadithi ya 13.   Al-Akhlaq Wal-Adab, Uk. 143. 269   Safinatul-Bihar, Juz. 7, Uk. 308. 270   Ghurarul-Hikam Juz. 1, Uk. 85, Hadithi ya 1738. 271   Nurul-Haqiqa, Uk. 215. Akhlaq Ahlul-Bayt, Uk. 48. Jamius-Saadat, Juz. 1, Uk. 291. 267 268

83


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

TIBA YA KUSENGENYA 1.

Akumbuke madhara yake ya huko Akhera na adhabu ambayo Mwenyezi Mungu amemwandalia msengenyaji.272

2.

Akumbuke madhara yake ya kidunia, nayo ni mengi, kati ya hayo ni:

3.

Usengenyaji unaweza kumfikia yule aliyetetwa na hatimaye ukawa chanzo cha uadui au kuongezeka kwa uadui.273

4.

Watu kutokumheshimu tena mtesi na kuondoa kwake hali ya kumwamini kwao.274

5.

Hakika utesi ukiwa ni hulka iliyoota mizizi huacha athari ndani ya nafsi, kati ya athari hizo ni nongwa na uadui dhidi ya mwenye kutetwa, ambao huongezeka kidogo kidogo.275

6.

Aziweke mbele ya macho yake zile faida za vitendo vilivyo kinyume na kuteta, ambavyo ni ukweli, kulinda heshima za watu, kupendwa na watu na kuaminiwa na watu.

7.

Ang’oe sababu zake ambazo ni: Ghadhabu, chuki, husuda, dharau na dhihaka, fakhari, kumuonea huruma mtetwa.276

8.

Achunge ulimi wake na maneno yake, na alitafakari kila neno atakalo kulitamka, kama lina utesi anyamaze asilitamke na aikalifishe nafsi yake kubakia katika hali hiyo.

Adh-dhunubul-Kabira, Juz. 2, Uk. 280.   Jamius-Saadat, Juz. 2, Uk. 303. 274   Al-Arbaun Haditha, Uk. 191. 275   Al-Arbaun Haditha, Uk. 191. 276   al-Muhujatul-Baydhau, Juz. 5, Uk. 265. 272 273

84


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

9.

Ajue kwamba amejiweka katika hatari ya kukasirikiwa na Mwenyezi Mungu na ameporomosha mema yake ya hapo kabla, na amestahili kuingia motoni, na hilo linatosha kuwa kizuizi cha kumzuia kufanya utesi.277

10. Ajue kwamba mema yake yamehamia kwa amtetaye, na mabaya ya mtetwa yamehamia kwake yeye mtesi.278 11. Ajue kwamba kuacha utesi kunapelekea mahusiano ya kijamii kuwa safi na kuimarika na hatimaye kuishi kwa amani.279 12. Ajue kwamba kuwateta watu na kutaja aibu zao ni moja ya mgandamizo wa kiroho na udhaifu wa shakhsiya ya mtu.280 13. Aache kuchanganyika na watu kadiri awezavyo, kwani aghlabu katika mkusanyiko wa watu ndiko kwenye utesi na ndiko utakakosikiliza utesi huo.281 14. Akiona jambo la aibu kwa mtu ambalo linaweza kumfanya mtu huyo atetwe, ni wajibu juu yake amfuate kwa upole na heshima kisha amnasihi na kumwomba aondoe aibu hiyo, au amwondolee yeye mwenyewe ikiwa anaweza, na hii ni miongoni mwa amali bora kwa Mwenyezi Mungu, kwa sababu ni kumsitiri ndugu yake na kumwepushia lile ambalo linavunja heshima yake na kupunguza hadhi yake, hivyo atakuwa ni mtu mwenye kupendwa na mtu huyo bali na watu wote, na si amtete akaja kuihilikisha nafsi yake na hatimaye heshima yake kuporomoka mbele ya watu wote.   Al-Akhlaq, Uk. 38.   Ad-Hunubul-Kabira, Juz. 2, Uk. 281. 279   Dirasatu Fil-Mashakil al-Akhlaqiyyah Uk. 78 na 80. 280   Dirasatu Fil-Mashakil al-Akhlaqiyyah Uk. 78 na 80. 281   Mir’atur-Rashad, Uk. 110. 277 278

85


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Siku niliyopelekwa Mir’aji nilipita sehemu na nikakuta kundi la watu wakizikwaruza nyuso zao kwa kucha zao. Nikasema: Ewe Jibril, hawa ni akina nani? Akasema: Hawa ni wale ambao huwasengenya (teta) watu na kuwavunjia heshima zao.”282 Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Atakayetetea heshima ya nduguye na hali akiwa hayupo, ni haki juu ya Mwenyezi Mungu kulinda heshima yake Siku ya Kiyama. Na ni haki juu ya Mwenyezi Mungu amwepushe na moto.”283

TIBA YA USUSUAVU WA MOYO 1.

Aache vitendo na mambo yapelekeayo ususuavu wa moyo mgumu, aache kila ambacho ni matokeo ya ususuavu wa moyo, kama vile kuwaudhi wenzake na kutowasaidia wenye matatizo.

2.

Adumu na atende mambo ambayo yatampelekea kuwa na huruma, na atende hayo walau kwa kujilazimisha.284

3.

Alie au kujiliza, kwa sababu ni sababu ya moyo kulainika.

4.

Ahudhurie maeneo ambayo hupelekea nyoyo kulainika, kama vile vikao vya maadili, hospitali na makaburini.

5.

Adumu katika kula adasi, hakika zenyewe huleta huruma kama ilivyokuja katika riwaya.285 Miongoni mwa munajati wa Mwenyezi Mungu kwa Musa (a.s.) ni: “Ewe Musa! Usiyarefushe

Al-Akhlaq Wal-Adab, Uk. 61   Jamius-Saadat, Juz. 2, Uk. 298. 284   Jamius-Saadat, Juz. 1, Uk. 370. 285   Al-Mahasin, Juz. 2, Uk. 306 – 307, Mlango wa 84. 282 283

86


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

matumaini yako katika dunia hatimaye moyo wako ukasusuwaa, na msusuavu wa moyo yuko mbali nami.”286

TIBA YA KUTOKUJALI UDUGU 1.

2.

Azingatie madhara yake yatokanayo na kitendo cha kutokujali udugu, nayo ni mengi: a.

Kuteremkiwa na ghadhabu ya Mwenyezi Mungu.

b.

Asipowajali ndugu mali zake atakuwa ameziweka mikononi mwa waovu.

c.

Ni miongoni mwa madhambi yaharakishayo kifo.

d.

Hakika Mwenyezi Mungu huwa hamtazami asiyejali udugu.

e.

Hakika kunaondoa rehema ya Mwenyezi Mungu.

f.

Ajue kwamba kutokujali udugu kunasogeza karibu muda wa kifo.287

g.

Asiyejali udugu adhabu yake huanza hapa hapa duniani kabla ya Akhera

Azingatie faida zitokanazo na kujali udugu, nazo ni: a.

Umri kurefushwa.

b.

Riziki kupanuka.

Safinatul-Bihar, Juz. 7, Uk. 308.   Biharul-An’war Juz. 16, Uk. 28. Ad-Hunubul-Kabira Juz. 1, Uk. 172. Al-Akhlaq Wal-Adab, Uk. 114-115.

286 287

87


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

c.

Kupata radhi ya Mola.288

d.

Kuwa na tabia njema.

e.

Kuwa na mkono wa ukarimu.

f.

Kuwa na nafsi njema.289

g.

Huamirisha majumba.290

3.

Ajue kwamba jamii huongezeka nguvu na utukufu kadiri uongezekavyo mshikamano, hali ya kusaidiana, na kuungana mkono katika makundi madogo madogo ambayo huonekana katika familia. Ukweli huu unaashiriwa na Hadithi tukufu: “Kujali udugu kunaamirisha majumba.”291

4.

Ang’oe sababu zake nazo ni: Hikdi, husuda, ujinga, kiburi na kutokujali. Hadithi Qudsi inasema: “Mimi ni Mwingi wa huruma, na hii ni huruma, kutokana nayo nimenyambua jina miongoni mwa majina yangu, atakayemfanyia (huruma) nduguye nami nitamfanyia, na atakayeikata (huruma) nami nitamkatia.”292 Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Jiepusheni na Haliqah. Hakika yeye huua wanaume.” Wakasema: Haliqah ni nini? Akasema: “Kutokujali udugu.”293

Mustadrakul-Wasail, Juz. 15, Uk. 234, Mlango wa 11.   Ad-Hunubul-Kabira, Juz. 1, Uk. 158. 290   Tafsirul-Amthal, Juz. Uk. 144. 291   Tafsirul-Amthal, Juz. Uk. 144. 292   Ad-Hunubul-Kabira Juz. 1, Uk. 169. 293   Jamius-Saadat, Juz. 2, Uk. 257 – 258. 288 289

88


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

TIBA YA TAMAA 1.

Ni lazima mja ajue kwamba ukinaifu ni utukufu wa duniani na Akhera, na ni raha ya mwili, kwa sababu usipokuwa mkinaifu unaweza kujikuta watenda yale yaondoayo heshima yako mbele ya waja duniani, na ambayo yatakuangushia ndani ya adhabu huko Akhera, na kwenye taabu na matatizo.294

2.

Awe na bajeti katika mambo yote ili akusanye mahitaji yake na asihitajie yaliyomo mikononi mwa watu.

3.

Hakika mja akiwa mkata, mchache wa mali, ni lazima atosheke na alichofanikiwa na aridhike na alichokadiriwa, na wala asimfichulie yeyote siri yake na wala asidhihirishe ufukara wake, kwani hakika watu ni watwana wa dunia hivyo wakijua siri ya ufukara wake huenda wakamdharau, wakamshusha thamani na wakamdhalilisha.295

4.

Hakika riziki ni mgao na kadirio, ameugawa Mwenye hekima kulingana na hekima Yake na masilahi ayaonayo, hivyo haiongezeki kwa kujidhalilisha wala haipungui kwa kujiheshimu. Imam Ja’far as-Sadiq (a.s.) amesema: “Mara nyingi Amirul-Muuminin (a.s.) alikuwa akisema: ‘Tambueni kwa yakini kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu hajamjalia mja uwezo wa kulitangulia fungu alilotajiwa ndani ya utajo wenye hikima (Qur’ani) – hata kama ataongeza juhudi kiasi gani, awe na ujanja kiasi gani na akithirishe mbinu kiasi gani.”296

Mir’atur-Rashad, Uk. 61.   Mir’atur-Rashad, Uk. 63. 296   Al-Kafiy, Juz. 5, Uk. 81, Mlango wa wastani katika utafutaji, Hadithi ya 9. 294 295

89


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

5.

Ajue kwamba kupeleka malalamiko yake kwa viumbe ni kumshitaki Mgawaji wa riziki, na hilo litampelekea kupatwa na ghadhabu Yake hapa duniani kwa bei kupanda, na huko Akhera kwa kuingizwa motoni.297 Hadithi Qudusi inasema: “Naapa kwa nguvu Zangu na utukufu Wangu, nitakata matumaini ya kila mwenye matumaini ambaye humtumainia asiyekuwa mimi, na hakika nitamvisha vazi la udhalili mbele ya watu, na nitamtenga mbali na faraja yangu na fadhila yangu.”298

TIBA YA KIBURI 6.

Azingatie Aya na riwaya zikemeazo sifa hiyo, zatosha kabisa kwa atafutaye na kuitaka haki.

7.

Azingatie sifa za unyenyekevu, na kwamba wenyewe ndio tabia iliyo karibu mno na ubinadamu kushinda kiburi.

8.

Ajue kwamba anayemfanyia kiburi anaweza kuwa na hulka za siri ambazo zitamwokoa, ambapo ni kinyume na mwenye kiburi.299

9.

Ajue kwamba kiburi hakimfai ila Mwenyezi Mungu peke Yake, hivyo asimnyang’anye Mwenyezi Mungu joho Lake.

10. Ajue kwamba yeye atakapofanya kiburi atakuwa mwenye kuchukiwa na Mwenyezi Mungu na atastahili adhabu Siku ya Kiyama.   Mir’atur-Rashad, Uk. 64..   Al-Wasail, Juz. 15, Uk. 214, Hadithi ya 1. 299   Jamius-Saadat, Juz. 1, Uk. 301. 297 298

90


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

11. Ajue kwamba atakapofanya kiburi atakuwa mwenye kuchukiwa na watu, ambapo ni kinyume na unyenyekevu, kwani wenyewe humwongezea mwenye nao heshima na upendo. 12. Mwanadamu daima ajitahidi kuizoesha nafsi yake na aifanye iwe yenye kuchukia kiburi na yenye kupenda unyenyekevu. 13. Ang’oe sababu za kiburi, aisemeshe nafsi yake kwamba uzuri, nguvu, utajiri na nasaba, haya yote ni mambo ya kupita, hayanufaishi si duniani wala si Akhera. Na hakika chanzo kikuu cha kiburi ni ujinga. 14. Akubali haki. Ahlul-Bait (a.s.) wamesema: “Kubalini haki, hakika kukubali haki humtenga mtu mbali na kiburi.”300 15. Aombe istighfari. 16. Atende kinyume na aamrishwavyo na nafsi yake, awatangulize jamaa zake wakati wa kutembea, aitikie wito wa fakiri, avae nguo za kawaida, na ale pamoja na watu wa kawaida.301 17. Akithirishe ibada, hakika yenyewe itavunja muhimili wa mwenye kiburi.302 Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: Kiburi ni vazi Langu na uadhama ni joho Langu, atakayeninyang’anya moja kati ya hayo mawili nitamtupia ndani ya moto.”303

Biharul-An’war, Juz. 69, Uk. 399, Hadithi ya 91.   Jamius-Saadat, Juz. 1, Uk. 206. 302   Nahjul-Balagha, Hikma ya 252. 303   At-Targhib Wat-Tarhib, Juz. 3, Uk. 563, Hadithi ya 41. 300 301

91


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

TIBA YA UONGO 1.

Ajue kwamba hushusha utu wake na heshima yake kwa watu.

2.

Humwondolea hali ya kuaminiwa, na hasa katika kauli zake na habari zake.

3.

Ailakinishe nafsi yake kwamba wenyewe ni ufunguo wa maovu na husababisha kudhalilika.

4.

Akumbuke matokeo yake ya kutisha ya kidunia na kiakhera, na adhabu waliyoandaliwa waongo.

5.

Ajiepushe na rafiki muovu, na awe anaketi na watu wema na wakweli.

6.

Ajiepushe na njia zenye kuandaa mazingira ya uongo, kama vile‌‌ na kuongeza chumvi. Ajizoweze kukaa kimya kadiri awezavyo.

7.

Atafakari kwa kina faida za ukweli.

8.

Aonyeshe madhara ya kimaada na ya kiafya toka kwa mwongo.

9.

Azingatie kila atakalo kulitamka.

10. Adumu katika kukuza hali yake ya kiroho na kinafsi, kupata murua, kutafuta utu wa juu na kupanda hadi kwenye ukamilifu wa kiroho. 11. Aimarishe imani, kwani hakika uongo hutokana na uchache wa imani. 92


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

12. Ang’oe sababu zake, nazo ni: Kutokujua hatima ya mambo, kusuhubiana na watu wenye tabia mbaya, na kuwa katika jamii mbovu.304 13. Ajue kwamba uongo una madhara ya hatari sana, kati ya hayo ni: a.

Ajue kwamba huleta sifa mbaya, huondoa heshima na kupelekea kutokuaminiwa.

b.

Huondoa hali ya watu kuaminiana, na hueneza hali ya kukimbiana na kutengana.

c.

Hupelekea watu kupoteza wakati na juhudi ya thamani ili kumaizi baina ya ukweli na uongo.

d.

Huacha athari mbaya za kiroho kwa kila mtu.305

14. Uongo una madhara makubwa ambayo mtu anaweza kughafilika nayo, nayo ni kwamba muongo hunasibishiwa maneno ambayo hajayasema bali ameyasema mwingine. Ni uzuri ulioje wa yale yaliyomo ndani ya shairi: “Balaa hili lamtosha muongo, ambalo ni baadhi ya yale yasimuliwayo juu yake. Uongo usikiwapo toka kwa mwingine, hunasibishwa kwake.”306 Imam alBaqir (a.s.) amesema: “Hakika Mwenyezi Mungu ameiwekea shari makufuli, na amefanya funguo za makufuli hayo ni ulevi, na uongo ni shari mbaya kushinda ulevi.”307 Imam al-Askariy (a.s.) amesema: “Maovu yote yaliwekwa ndani ya nyumba, na uongo ukafanywa ufunguo wake.”308   Jamius-Saadat Juz. 2, Uk. 332. al-Akhlaq Wal-Adab Uk. 68. Dirasatu Fil-Mashakil alAkhlaqiyyah Uk. 59. 305   Akhlaq Ahlul-Bayt, Uk. 28 – 29. 306   Al-Mustatraf, Juz. 1, Uk. 341. 307 Al-Kafiy, Juz. 2 Uk. 254, Hadithi ya 3. 308   Jamius-Saadat, Juz. 2, Uk. 323. 304

93


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

TIBA YA KUKUFURU NEEMA

M

wenyezi Mungu amesema: “Siku ambayo kila nafsi itakujajitetea. Na kila nafsi italipwa sawa na yale iliyoyafanya, nao hawatadhulumiwa.” (Sura Nahli: 111) 1.

Ajue kwamba kukufuru neema huwajibisha adhabu na huiondoa neema. Na kwamba kushukuru neema huwajibisha kuongezeka kwake. Mwenyezi Mungu amesema: “Na alipotangaza Mola wenu: Mkishukuru nitawazidishia na mkikufuru basi adhabu yangu ni kali.” (Sura Ibrahim: 7).

2.

Hakika sababu iliyopelekea baadhi ya umati zilizotangulia kuadhibiwa ni kukufuru neema, kama ilivyokuwa kwa watu wa Sabai.

3.

Hakika kukufuru neema ni miongoni mwa aina za ukafiri. Mwenyezi Mungu amesema: “Basi nikumbukeni nitawakumbuka, na nishukuruni wala msinikufuru.” (Sura al-Baqarah: 152).309

4.

Ni miongoni mwa madhambi ambayo adhabu yake huharakishwa na wala haingojei mpaka Akhera. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Madhambi ya aina tatu adhabu yake huharakishwa wala haingojei mpaka Akhera: Kuvunja haki za wazazi, kuwafanyia watu ujeuri na kukufuru hisani.”310

5.

Hakika kukufuru neema ya wazi kunampelekea kukufuru neema kubwa, na ya mwanzo ni kukufuru utawala wa aali Muham-

Ad-Dhunubul-Kabira, Juz. 2, Uk. 351.   Al-Wasail, Juz. 16, Uk. 312.

309 310

94


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

madi (s.a.w.w.), kukufuru uwepo wa ulamaa na hasa wa kiroho, na kadhalika kukufuru kiunganishi kilichowekwa na Mwenyezi Mungu baina yake na neema zake, na ndipo ikasemwa: “Asiyemshukuru kiumbe hatamshukuru muumba.” Abu Faras alHamdaniy amesema kuhusu shukurani: “Hakuna neema yoyote isiyoshukuriwa niliyomfanyia hisani asiye na shukurani, itanizuia kupata nyingine. Nitatenda wema muda wote wa uhai wangu, kwani hakika nisipofidia shukurani nitafidia malipo.”311 Imam ar-Ridha (a.s.) amesema: “Dhambi yenye adhabu ya haraka kushinda zote ni kukufuru neema.”312

TIBA YA MABAYA YA ULIMI Imam Ali (a.s.) amesema: “Jiepushe kubwabwaja, kwani mwenye maneno mengi madhambi yake huwa mengi.”313 1.

Akumbuke maelezo yaliyomo ndani ya riwaya za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na watu wa nyumba yake (a.s.). Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Hakuna kitakachowatupia watu motoni ila mazao ya ndimi zao.” Pakasemwa: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, uokovu ni nini? Akasema: “Udhibiti ulimi wako.”314

2.

Hakika ulimi na maneno yana pande mbili: Mmoja hupeleka Peponi, na mwingine hupeleka motoni, hivyo ajihadhari na moto na aelekee Peponi.

3.

Mwanadamu asizungumzie yasiyomhusu. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Miongoni mwa akili za mtu ni uchache wa maneno katika lile lisilomhusu.”315

Al-Mustatraf, Juz. 1, Uk. 323.   Akhlaq Ahlul-Bayt Uk. 166. 313   Ghurarul-Hikam, Juz. 1, Uk. 159, Hadithi ya 7. 314   Al-Bihar, Juz. 71, Uk. 290, Hadithi ya 57 315   al-Akhlaq Wal-Adab, Uk. 34. 311

312

95


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

4.

Maneno yasiyohitajika hudhihirisha aibu.316

5.

Hakika uchache wa maneno ni utimilifu wa akili. Imam Ali (a.s.) amesema: “Akili ikitimu maneno hupungua.”317

6.

Mwanadamu asizungumze kila ajualo. Imam Ali (a.s.) amesema: “Miongoni mwa akili ya mtu ni asizungumze yote aliyo na elimu nayo.”318

7.

Katika baadhi ya hali kukaa kimya ni bora kushinda kuongea.319 Luqman mwenye hikma (a.s.) alisema: “Ikiwa maneno ni madini ya fedha basi ukimya ni madini ya dhahabu.”320

8.

Ni lazima asifike kwa mema ya ulimi, nayo ni: a.

Ukweli.

b.

Kusoma Qur’ani, dhikri na sala.

c.

Kuamkia na kutoa salamu.

d.

Kupatanisha baina ya watu, nasaha, na kuwawaidhi wengine.

e.

Hotuba.

f.

Kuamrisha mema na kukataza maovu. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Mwenyezi Mungu humrehemu mja ambaye amesema kheri akafaidika, au amekaa kimya bila kusema baya akasalimika.”321

Ghurarul-Hikam, Juz. 1, Uk. 166, Hadithi ya 89.   Al-Bihar, Juz. 71, Uk. 290, Hadithi ya 62. 318   al-Akhlaq Wal-Adab, Uk. 35. 319   al-Akhlaq Wal-Adab, Uk. 35. 320   Al-Haqaiq, Uk. 70. 321   Akhlaq Ahlul-Bayt, Uk. 243. 316 317

96


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

TIBA YA MCHEZO WA KAMARI Tiba na kinga yake ni: 1.

Kutilia mkazo maadili mema katika jamii, na kuinua kiwango chake cha imani na akida, hiyo ndio njia ya kwanza na iliyo bora zaidi.322

2.

Kuteketeza sababu zipelekeazo kamari kuenea na klabu zilizoandaliwa kwa michezo hiyo, huku mkazo ukitiliwa katika kuzifunga.

3.

Tuzuie hali ya kubweteka, starehe za haramu na vikao vya mambo ya kipuuzi, mambo ambayo hutengeneza sababu ya kuenea kwa utovu wa maadili na kuelemea kwenye kamari. Bali tuwaite watu katika kufikiria mambo yajengayo na harakati za msingi.323

4.

Ajue kwamba kamari huleta uadui, kwani mcheza kamari ima apate faida na ima hasara, hivyo faida yake huwafanya wenzake wamuone kama mwizi na aliyechukua mali zao bure. Na apatapo hasara huifidia hasara yake kwa chuki dhidi ya mwenzake na kuwaona kama wezi wake na waliochukua mali zake bure, ni mara chache sana hutokea kwamba kikao cha kamari kinakwisha bila mzozo na ugomvi. Aya tukufu ni dalili bora juu ya hilo: “Hakika Shetani anataka kuwaingizia uadui na bughudha baina yenu kwa pombe na kamari na kuwazuia kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kuswali, basi je, mtakoma?” (Sura al-Maida: 91).324

Akhlaq Ahlul-Bayt, Uk. 243.   Nahwu Hayatu Afdhal, Uk. 213. 324   Ad-Dhunubul-Kabira, Juz. 1, Uk. 259. 322 323

97


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

5.

Ajue kwamba mchezo wa kamari huleta uharibifu na machafuko, hiyo ni kwa sababu mcheza kamari anapopata faida fikra zake huelekea katika uharibifu, upuuzi, makasino na vituo vya uchafu na uovu.325

6.

Mpata faida ajue kwamba kutokana na faida ya haramu aipatayo mahusiano yake na kamari huimarika na hatimaye hufa ari ya kufanya harakati, kazi na zile juhudi za kutafuta riziki ya halali, na hatimaye mtu huwa mbwetekaji, mvivu mfuata.326

7.

Ajue kwamba hakika mchezo wa kamari hupelekea kujimaliza, hiyo ni kwa sababu atakapoliwa mali zake zote katika vikao mbalimbali anaweza kufikia katika hali ya kumuuwa mwenzake au kujiuwa mwenyewe baada ya kushindwa kurejesha mali zake. Na haya ni mambo tunayoyashuhudia wazi.327

8.

Ajue kwamba mchezo wa kamari humzuia kumkumbuka Mwenyezi Mungu, na humfanya awe mbali na kumtii Mwenyezi Mungu. Mcheza kamari anaweza kumaliza saa nyingi akiwa katika kamari, naye kwa kitendo chake hiki anakuwa anapoteza wajibat nyingi za kidini, na hususan Sala ambayo ndio nguzo ya dini.328 Mwenyezi Mungu amesema: “Hakika Shetani anataka kuwaingizia uadui na bughudha baina yenu kwa pombe na kamari na kuwazuia kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kuswali, basi je, mtakoma?” (Sura al-Maida: 91).

9.

Aelekee kwenye starehe za halali ambazo zimetajwa chini ya kichwa cha habari: “Tiba ya starehe zenye uharibifu.”

Ad-Dhunubul-Kabira, Juz. 1, Uk. 260 – 261.   Ad-Dhunubul-Kabira, Juz. 1, Uk. 260 – 261. 327   Ad-Dhunubul-Kabira, Juz. 1, Uk. 260 – 261. 328   Ad-Dhunubul-Kabira, Juz. 1, Uk. 260 – 261. 325 326

98


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

TIBA YA NJAMA NA HILA 1.

Azingatie ubaya wa hatima yake na ubaya wa mwisho wake, na kwa uchache ni kwamba humpeleka mtu motoni.329

2.

Akumbuke kwamba madhara ya kila njama na hila hurejea kwa mhusika mwenyewe hapa duniani.330

3.

Akumbuke faida za lile lililo kinyume na njama, nalo ni nasaha.331

4.

Atafakari kwa kina kila kitendo kitokacho kwake, ili kisiwe na njama au hila.332

5.

Afikirie yale yatakayoinufaisha nafsi yake na waumini, na ashiriki katika kila kazi itakayowaletea manufaa.

6.

Atumie njama zake na hila zake katika kukabiliana na maadui, na ateketeze mipango yao kwa mipango bora kushinda yao.

7.

Aimarishe kinga ya kidini ya uchamungu na kumwogopa Mwenyezi Mungu Mtukufu.

8.

Ajue kwamba hakika sifa hii ni miongoni mwa sifa zilizokemewa ambazo hawawi nazo wenye imani, hivyo ni juu yake kuiacha. Amirul-Muuminin (a.s.) amesema: “Lau si kumsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akisema: ‘Hakika njama na uongo hupeleka motoni,’ ningetaka ningekuwa bingwa wa njama kushinda waarabu wote.”333

Jamius-Saadat, Juz. 1, Uk. 203.   Jamius-Saadat, Juz. 1, Uk. 203. 331   Jamius-Saadat, Juz. 1, Uk. 203. 332   Jamius-Saadat, Juz. 1, Uk. 203. 333   Thawabul-Aamal cha as-Saduq Uk. 320, Hadithi ya 3. 329 330

99


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

TIBA YA KIFO CHA MOYO 1.

Lazima ajue mambo ambayo hupelekea moyo kufa, nayo ni: a.

Ukavu wa macho.334

b.

Kung’ang’ania kutenda madhambi.335

c.

Kuipenda dunia.336

d.

Kujifungamanisha na dunia na mapambo yake

e.

Kuacha kusoma Qur’ani na kumdhukuru Mwenyezi Mungu.

f.

Maneno mengi yasiyomridhisha Mwenyezi Mungu.

g.

Kusikiliza upuuzi na miziki.

h.

Kufanya urafiki na madhalimu, waharibifu na wenye tabia mbaya.

ix. Kukithirisha kucheka na kuwadhihaki wengine.337 2.

Ama mambo yanayotibu sababu zilizotangulia ni: a.

Kusikiliza Qur’ani, kuisoma, kutadabari Aya zake na kusoma vitabu vya dini.

Al-Bihar Juz. 80, Uk. 52, Hadithi ya 11.   Al-Bihar, Juz. 80, Uk. 52, Hadithi ya 11. 336   Al-Kafiy, Juz. 2, Uk. 309, Hadithi ya 1. 337   Akhlaq Ahlul-Bayt, Uk. 174. 334 335

100


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

b.

Kukithirisha dua, tawasuli na Sala kwa kumnyenyekea Mwenyezi Mungu.

c.

Kusikiliza mawaidha.

d.

Kujifunza adabu za Kiislamu na kuzitekeleza katika nyanja zote za maisha.

e.

Kufanya urafiki na watu wenye tabia njema na ulamaa.

f.

Kuhudhuria vikao vya mawaidha na ushauri, na kushiriki katika Sala za jamaa misikitini.

g.

Kukidhi mahitaji ya watu, kuwalisha chakula masikini na kupitisha mkono juu ya vichwa vya mayatima.

h.

Kukithirisha kukumbuka kifo, kukumbuka misiba ya dunia, na kukumbuka habari za wale waliotangulia.338

3.

Apunguze kuongea na wanawake.339

4.

Asiwe mwingi wa kuchekacheka.340

5.

Asiketi na watu duni kidini.341

6.

Ajiepushe na matamanio.342

7.

Atafakari uumbaji wa Mwenyezi Mungu.343

Akhlaq Ahlul-Bayt, Uk. 174.   Mizanul-Hikma, Juz. 8, Uk. 237 na 244. 340   Mizanul-Hikma, Juz. 8, Uk. 237 na 244. 341   Mizanul-Hikma, Juz. 8, Uk. 237 na 244. 342   Al-Musdar, Juz. 8, Uk. 228. 343   Mizanul-Hikma, Juz. 8, Uk. 245. 338 339

101


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

8.

Ajikumbushe elimu kwa kufanya mahojiano.344 Abu Abdillah (a.s.) amesema: “Baba yangu alikuwa akisema: Hakuna kitu kinachoharibu moyo kushinda makosa, hakika moyo hutumbukia katika makosa, huendelea kuwa humo mpaka makosa yanaushinda, na hatimaye moyo hugeuka chini juu na juu chini.”345

TIBA YA UNAFIKI 1.

Atazame uharibifu ambao huletwa nao, kwani hakika mwanadamu atakapotambulika kwa sifa hii miongoni mwa watu hudharaulika na kufedheheka kwa watu wote wa karibu hadi wa mbali, na heshima yake hutoweka mbele ya marafiki zake.346

2.

Mwanadamu afuatilie harakati zake na matendo yake kwa uangalifu sana na atumie sehemu ya wakati wake kuchunguza vitendo vyake na hatimaye atende yale yanayokhalifu ya nafsi yake na matamanio yake. Na ajitahidi kuvifanya vitendo vyake na kauli zake ziwe na sura moja nje na ndani, ajiepushe kujionyesha na kufanya udanganyifu katika maisha yake ya kivitendo.347

3.

Ajue kwamba mnafiki daima ni mwenye mashaka na mahangaiko, akizoea unafiki hawezi tena kuamiliana kwa moyo mkunjufu na safi na mtu yeyote kati ya watu anaoishi nao. Na hakika juhudi zake za kutaka kuficha ukweli haziwezi kumwacha awe katika amani dhidi ya mashaka na mahangaiko.

Mizanul-Hikma, Juz. 8, Uk. 245.   Safinatul-Bihar, Juz. 7, Uk. 340. 346   Al-Arbaun Haditha, Uk. 156. 347   Al-Arbaun Haditha, Uk. 156. 344 345

102


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

4.

Kila wakati ajaribu kuoanisha alama za unafiki na nafsi yake ili aweze kujiepusha nazo, na zilizo wazi kati ya hizo ni zile zilizotajwa na Ahlul-Bait (a.s.): “Mnafiki ana alama tatu: Moyo wake hupingana na ulimi wake, moyo wake hupingana na vitendo vyake, na siri yake hupingana na dhahiri yake.”348

5.

Amdhukuru sana Mwenyezi Mungu, kufanya hivyo kutamwepusha na mambo mawili: Kutamwepusha na moto na kutamwepusha na unafiki.349

6.

Ajue kwamba unafiki ni aina moja ya maradhi, kwani mwanadamu mwenye afya njema ana uso mmoja tu, ama mnafiki ana nyuso mbili. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Sifa tatu atakayekuwa nazo ni mnafiki hata kama atafunga na kusali na akadai kuwa ni mwislamu: Ambaye akiaminiwa hukhini amana, akiongea huongopa, na akiahidi hatekelezi. Mwenyezi Mungu amesema ndani ya Kitabu chake: “Ambao wanasimamisha Swala. Na wanatoa katika yale tuliyowaruzuku.” (Sura al-Anfal: 3). Na amesema tena: “Na mtaje katika Kitabu, Ismail. Hakika yeye alikuwa mkweli wa ahadi na alikuwa Mtume, Nabii.” (Sura Maryam: 54).”350

Dirasatu Fil-Mashakil al-Akhlaqiyyah Uk. 7.   Usulul-Kafiy, Juz. 2, Uk. 362, Hadithi ya 3. 350   Al-Wasail, Juz. 15, Uk. 340, Hadithi ya 4. 348 349

103


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

TIBA YA KUVUNJA HESHIMA YA MUUMINI

K

uvunja heshima ya muumini huwa kwa dharau, matusi, kumtia dosari, kumdhalilisha, kumdunisha, kumfokea na kumuudhi. Imam al-Baqir (a.s.) amesema: “Hakuna mwanadamu atakayelitia dosari jicho la muumini ila ni lazima atakufa kifo kibaya, na ni haki kwamba asirejee kwenye kheri.”351 Tiba yake ni: 1.

Aliweke jambo hili mbele ya macho yake, nalo ni kwamba Mwenyezi Mungu amelitilia umuhimu wa kipekee suala la muumini na heshima yake, mpaka imefikia kuwa heshima yake ni jambo tukufu kushinda heshima nyingine, na kuvunja heshima yake ni miongoni mwa madhambi makubwa na ni sawa na kumwaga damu yake.352

2.

Hakika Mwenyezi Mungu amewajibisha juu ya nafsi yake kumsaidia muumini. Mwenyezi Mungu amesema: “Na hakika tulikwishawatuma mitume kwa kaumu zao na wakawajia na hoja zilizo waziwazi. Tukawaadhibu wale waliofanya makosa na ilikuwa ni haki juu yetu kuwanusuru waumini.” (Sura Rum: 47).

3.

Yule mwenye kuwadharau wengine ajue kwamba hao wengine wanaweza kuwa wabora kushinda yeye, na wanaweza kuwa ni miongoni mwa mawalii wa Mwenyezi Mungu, na kwa kitendo chake hicho atakuwa amemdhalilisha walii wa Mwenyezi Mungu.353

Ad-Dhunubul-Kabira, Juz. 2, Uk. 302.   Ad-Dhunubul-Kabira, Juz. 2, Uk. 297. 353   Ad-Dhunubul-Kabira, Juz. 2, Uk. 300. 351 352

104


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

4.

Hakika mwenye kumtusi muumini ni sawa na aliyeangamia, na haya ni maelezo ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.).354

5.

Hakika mwenye kuwatusi watu atakufa kifo kibaya sana. Imam al-Baqir (a.s.) amesema: “Hakuna mwanadamu atakayelitia dosari jicho la muumini ila ni lazima atakufa kifo kibaya, na ni haki kwamba asirejee kwenye kheri.”355

6.

Ajue kwamba Mwenyezi Mungu ameharamisha Pepo kwa mtu mwenye ulimi mchafu.356

7.

Hakika kutukana ni haramu ikiwa ni sababu ya yeye kutukanwa au ya muumini mwingine kutukanwa. Kadhalika haijuzu kutukana matukufu ya kidini ya dini nyingine, kwa sababu kutukana huko kutapelekea kutukanwa itikadi za mwislamu aliyetukana.357

8.

Hakika anayepokea riwaya juu ya muumni kwa lengo la kumtia dosari, kubomoa heshima yake na kumtoa thamani machoni mwa watu, Mwenyezi Mungu atamtoa toka kwenye utawala wake na kumwingiza kwenye utawala wa shetani, lakini shetani hatamkubali. Hiyo ni kama ilivyokuja kwenye riwaya ya Imam as-Sadiq (a.s.).358

Ad-Dhunubul-Kabira, Juz. 2, Uk. 301.   Adh-Dhunubul-Kabira, Juz. 2, Uk. 302. 356   Al-Kafiy, Juz. 2, Uk. 243. 357   Ad-Dhunubul-Kabira, Juz. 2, Uk. 305. Akhlaq Ahlul-Bayt, Uk. 33. 358   Ad-Dhunubul-Kabira, Juz. 2, Uk. 307. 354 355

105


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

TIBA YA KUFUATA MATAMANIO 1.

Azingatie zile riwaya zilizopokewa zikikemea sifa hii mbaya.359

2.

Ajue kwamba kufuata matamanio ni chimbuko la ukafiri na ni kutokuwa na imani.

3.

Ajue kwamba kufuata matamanio kunazuia uadilifu na uungwana.

4.

Ajue kwamba yenyewe ni sifa inayopelekea kughafilika na huzuia taufiki ya Mwenyezi Mungu.

5.

Ajue kwamba mpangilio wa mbingu na ardhi ukifuata matamanio ya watu basi hakika uharibifu utaenea ulimwengu wote. Mwenyezi Mungu amesema: “Na lau haki ingelifuata yao basi zingeliharibika mbingu na ardhi na waliomo ndani yake. Bali tumewaletea utajo wao na wanajitenga mbali na utajo wao.” (Sura al-Muuminun: 71).

6.

Ajue kwamba mtu kwa kufuata matamanio saa moja anaweza akameza uchungu mpaka mwishoni mwa umri wake, na hili liko wazi kwani mlevi na mtumiaji wa madawa ya kulevya hupatwa na hayo kwa sababu ya kufuata matamanio saa moja tu.360

7.

Azingatie athari za sifa hii mbaya zilizotajwa na riwaya za Ahlul-Bait (a.s.), nazo ni: a.

Humfanya awe muovu.

Al-Kafiy, Juz. 2, Uk. 252, Hadithi ya 1 – 4.   Dirasatu Fil-Mashakil al-Akhlaqiyyah, Uk. 266.

359 360

106


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

b.

Matamanio humwondolea akili.

c.

Huwa hana akili yule mwenyekufuata matamanio.361

8.

Azingatie riwaya zinazomsifia yule mwenye kuacha matamanio zake, kwani Aya na riwaya zimemwahidi Pepo. Mwenyezi Mungu amesema: “Na ama yule aliyeogopa kusimama mbele ya Mola wake Mlezi, na akaikataza nafsi yake matamanio. Basi hakika Pepo ndiyo makazi.” (Sura Naziat: 40 - 42).

9.

Ajue kwamba neema za duniani vyovyote ziwavyo bado hufikwa na uchafu na matatizo mbalimbali, kamwe hakuna neema ya kimada isiyo na madhara au hatari.362 Imam as-Sadiq (a.s.) amesema: “Jihadharini na matamanio yenu kama mnavyojihadhari na maadui zenu, hakuna kitu kilicho adui mkubwa kwa watu kushinda kitendo cha kufuata matamanio yao na mavuno ya ndimi zao.”363

Nahjul-Balagha, Hotuba ya 86. Ghurarul-Hikam: 265 na 1053 na 10541.   Al-Amthal, Juz. 11, Uk. 272. 363   Safinatul-Bihar, Juz. 8, Uk. 729. 361 362

107


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

TIBA YA MABISHANO, MIJADALA NA MIZOZO 1.

Ajue kwamba mjadala, ubishi na ugomvi ni sifa za shetani. Mwenyezi Mungu amesema: “Wala msile wale wasiosomewa jina la Mwenyezi Mungu kwani huo ni ufasiki. Na hakika mashetani wanawafunza marafiki zao kubishana nanyi. Na kama mkiwatii, hakika mtakuwa washirikina.” (Sura alAn’am: 121).

2.

Ajue kwamba sifa hizo huuguza moyo na huleta unafiki.364

3.

Hakika mjadala na ubishi hudhihirisha na kufichua aibu za mtu na dosari zake na hudhihirisha undani wake mbaya.

4.

Ajue kwamba huondoa heshima ya mtu adhama yake, na humtoa kwenye sura halisi aliyowekewa na Mwenyezi Mungu, na hususan awapo hija. Mwenyezi Mungu amesema: “Hijja ni miezi maalum. Na anayejilazimisha kufanya Hijja katika miezi hiyo, basi hakuna kuingiliana na wanawake wala kutoka katika mipaka wala mabishano katika hijja. Na kheri yoyote mnayoifanya Mwenyezi Mungu anaijua. Na chukueni masurufu, na hakika masurufu bora ni ucha Mungu; na nicheni Mimi, enyi wenye akili.” (Sura al-Baqara: 197).

5.

Ajue kwamba husababisha kuchukiana, uadui, wapenzi kutengana, na hatimaye hukomea katika lile lisilo na mwisho mwema.365

Al-Arbaun Haditha, Uk. 343.   Jamius-Saadat, Juz. 2, Uk. 286. Al-Arbaun Haditha, Uk. 343.

364 365

108


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

6.

Akumbuke Aya na riwaya zinazokemea sifa hizi. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Atakayejadili bila elimu katika mzozo, ataendelea kuwa katika ghadhabu ya Mwenyezi Mungu mpaka atakapoacha.”366

7.

Adumu katika sifa hii iliyo kinyume na mambo haya, awe na maneno mazuri na aikalifishe nafsi yake kusema maneno mazuri mpaka kusema maneno mazuri iwe ni hulka yake, basi sifa zilizo kinyume na hiyo zitaondoka mara moja.367

8.

Azingatie Aya na riwaya zinazosifu ukimya, maneno mazuri na uchangamfu.368 Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Hakunijia Jibril ila ni lazima aliniwaidhi, mpaka akasema: ‘Jiepushe kubishana na watu, kwani kitendo hicho hufichua aibu na huondoa heshima.”369 Imam as-Sadiq (a.s.) amesema: “Jibril alimwambia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): Jiepushe kubishana na watu.”370 Na Imam as-Sadiq (a.s.) akasema tena: “Usimbishie mwerevu wala mpumbavu, hakika mwerevu atakushinda na mpumbavu atakuudhi.”371

Jamius-Saadat, Juz. 2, Uk. 285.   Jamius-Saadat, Juz. 2, Uk. 285. 368   Jamius-Saadat, Juz. 2, Uk. 285 369   Jamius-Saadat, Juz. 2, Uk. 285. 370   Al-Arbaun Haditha, Uk. 343. 371   Jamius-Saadat, Juz. 2, Uk. 285 366 367

109


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

TIBA YA KUNUNIANA 1.

Azingatie riwaya ambazo zinakemea kununiana, na zinazoonyesha athari za ajabu zitokanazo na sifa hii mbaya, na kwa uchache ni kwamba Maimam (a.s.) hujitenga na mtu huyo.

2.

Mwenye mawasiliano na ndugu yake hupata thawabu nzuri hata kama ni ndugu dhalimu, na malipo ya chini kabisa ni kuingia peponi.

3.

Ajitahadhari na matokeo mabaya yatokanayo na kitendo cha kununiana na ugomvi, nayo ni:

5.

a.

Kuenea kwa tofauti, kukata mawasiliano, matusi, uongo na mengineyo.

b.

Ugomvi huonyesha upumbavu wa mtu na wala haumzidishii haki yake.372

c.

Ugomvi huushughulisha moyo, huleta unafiki na husababisha chuki.373

d.

Hakika ugomvi huleta shaka, huporomosha amali na humwangamiza mhusika na huenda ukamfanya mtu akazungumza jambo ambalo hatasamehewa.374

Kununiana kunaweza kusababisha kupoteza malipo mema, hiyo ni kwa sababu mawasiliano hupelekea kujua hali za watu, na hatimaye kuwasaidia, kukidhi mahitaji yao, ambapo ni kinyume na hali ya kukatiana mawasiliano.

Ghurarul-Hikam, Juz. 1, Uk. 77, Hadithi ya 1587.   Al-Kafiy, Juz. 1, Uk. 228, Hadithi ya 8. 374   Al-Kafiy, Juz. 1, Uk. 73, Hadithi ya 4. 372 373

110


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

6. Ni lazima wenye madaraka na heshima ya kijamii kuingilia kati baina ya walionuniana na wenye ugomvi ili kwamba wazibe mwanya huu uliyo wazi na waondoe vizuizi vilivyojikita baina yao. Mwenyezi Mungu anasema: “Hakika Waumini ni ndugu, basi patanisheni baina ya ndugu zenu, na mcheni Mwenyezi Mungu ili mrehemiwe.” (Sura al-Hujurat: 10). Imam as-Sadiq (a.s.) alikuwa apitapo kwa jamaa wanaozozana hawavuki mpaka awaambie mara tatu: “Mcheni Mwenyezi Mungu, kwa uchaji huo ataondoa sauti yake (yaani sauti ya shetani).”375 7.

Miongoni mwa haki za ndugu yako zilizoko kwako ni umsamehe kosa lake na usahau ubaya wake. Ukimnunia utakuwa umekhini amana ya udugu na utakuwa haujatekeleza haki iliyo wajibu juu yako, katika hali kama hii utaombaje wengine wakutekelezee haki yako. Imam Ali (a.s.) amesema: “Jihadhari kwamba usighafilike kutimiza haki ya ndugu yako kwa kutegemea wajibu wa haki yako iliyo juu yake, kwani hakika ndugu yako ana haki kwako mfano wa ile uliyonayo kwake.”376

8.

Inaweza ukatokea ugomvi baina yako na rafiki yako, lakini usiufanye udumu siku tatu. Imam as-Sadiq (a.s.) amesema: “Baba alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: ‘Waislamu wawili wakinuniana na wakakaa siku tatu bila kusuluhishana, wakifa watakuwa wamekufa wakiwa nje ya Uislamu, na hakutakuwa na utawala (wa Ahlul-Bait) baina yao. Yeyote atakayetangulia kumsemesha nduguye atakuwa wa mwanzo kuingia peponi bila hisabu.”377

Tanbihul-Khawatir, Juz. 2, Uk. 125.   Ghurarul-Hikam, Juz. 1, Uk. 163, Hadithi ya 56. 377   Safinatul-Bihar, Juz. 8, Uk. 629. 375 376

111


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

9.

Ajue kwamba kuendelea kumnunia nduguye ni matokeo ya kumtii shetani na nafsi yake iamrishayo mabaya, hivyo ni wajibu juu yake kuipiga vita nafsi yake, kujilinda mbali na shetani na kukhalifu amri yake. Mwenyezi Mungu amesema: “Hakika Shetani anataka kuwaingizia uadui na bughudha baina yenu kwa pombe na kamari na kuwazuia kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kuswali, basi je, mtakoma?” (Sura alMaida: 91).

10. Kila mmoja miongoni mwetu apende kuzishikamanisha safu za waumini na kuleta umoja wa kijamii, na kuuepusha na mpasuko ambao husababishwa na kununiana huku, kwani kila mmoja kati yetu ni sehemu ya jamii, sehemu hii ikiharibika na sehemu zilizobaki nazo zitaharibika. Mwenyezi Mungu amesema: “Na saidianeni katika wema na takua wala msisaidiane katika dhambi na uadui. Na mcheni Mwenyezi Mungu; hakika Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu.” (Sura al-Maida: 2). 11. Ni juu yake kuvumilia maudhi ya ndugu zake, kwani hatampata mtu aliye maasumu asiye na makosa aridhini, kwani lau tukihesabu makosa ya kila mmoja wetu na tukataka kuyaletea athari basi hatutabakia na rafiki. Imam Ali (a.s.) amesema: “Pambo la urafiki ni uvumilivu.”378 12. Ukitazama makosa yako ambayo umeyafumbia macho na ulivyowakosea ndugu zako, utakuta si chini ya walivyokukosea. 13. Hakika moja ya sifa za watu wenye tabia njema na hata wenye akili, ni kujipendekeza kwa ndugu, kujiweka karibu nao na kutowanunia. Mwenyezi Mungu amesema: “Kwa sababu ya rehma itokayo kwa Mwenyezi Mungu, umekuwa mpo  Ghurarul-Hikam, Juz. 1, Uk. 385, Hadithi ya 17.

378

112


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

le kwao, lau ungelikuwa mkali mwenye moyo mgumu bila shaka wangelikukimbia. Basi wasamehe na uwaombee maghfira na ushauriane nao katika mambo. Utakapoazimia, basi mtegemee Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wamtegemeao.” (Sura Aal Imran: 159). Imam Ali (a.s.) amesema: “Kilele cha akili ni kujipendekeza kwa watu.”379 Na amesema tena (a.s.): “Miongoni mwa tabia njema ni kuvumilia makosa ya ndugu.”380

TIBA YA WASIWASI 1.

Ikiwa kinachosababisha wasiwasi ni shari na maasi, basi tiba yake ni atafakari kwa kina matokeo ya maasi na ubaya wa mwisho wake duniani na Akhera.381

2.

Azibe moyoni mwake mlango mkubwa wa shetani, nao ni: ghadhabu, na….kwani akikuta mmojawapo uko wazi ataingia na kuingiza wasiwasi unaohusiana na mlango husika. Kama atauziba basi hatakuwa na njia ila kwa njia ya kupita nje na kuvuka.382 Mwenyezi Mungu amesema: “Anayeifanyia upofu dhikri ya Mwingi wa rehema tutamwekea Shetani kuwa ndiye rafiki yake.” (Sura Zukhruf: 36).

3.

Auamirishe moyo kwa sifa zilizo dhidi ya sifa hiyo miongoni mwa tabia njema, sifa safi, uchamungu na kudumu katika ­kumwabudu Mola Wake Mtukufu.383

Ghurarul-Hikam, Juz. 1, Uk. 371, Hadithi ya 25.   Ghurarul-Hikam, Juz. 1, Uk. 249, Hadithi ya 30. 381   Jamius-Saadat, Juz. 1, Uk. 150. 382   Jamius-Saadat, Juz. 1, Uk. 153. 383   Jamius-Saadat, Juz. 1, Uk. 153. 379 380

113


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

4.

Baada ya kujiepusha na sifa hiyo mbaya akithirishe kuitaja kwa moyo na ulimi kauli ya Mwenyezi Mungu: “Hakika wale wenye takuwa zinapowagusa pepesi za shetani huzinduka.” (Sura Al-A’raf: 201).

5.

Wenye maradhi ya wasiwasi katika mambo ya kifiqhi wafuate fatwa za mafaqihi, na wala wasijali wasiwasi unaowatokea, nao kwa hilo wameepukana na dhima, waendelee na hilo kwa siku nyingi baadaye hali hiyo ya wasiwasi itaondoka ndani ya nafsi zao.

6.

Ajikinge kwa Mwenyezi Mungu dhidi ya shetani mlaaniwa, na ateme mate kushotoni kwake mara tatu.384

7.

Aseme wakati wa wasiwasi: “Nimemwamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake hali ni mwenye ikhlasi na dini.”385

8.

Ale komamanga.386

9.

Awataje Ahlul-Bait (a.s.) na kuwasalia.387

10. Atibu sababu zake, nazo ni: a.

Maradhi ya moyo.

b.

Nafsi ovu ya kiuadui.

c.

Hikdi.

d.

Kukithiri kwa dhambi.388

Safinatul-Bihar, Juz. 8, Uk. 471 na 477.   Safinatul-Bihar, Juz. 8, Uk. 471 na 477. 386   Safinatul-Bihar, Juz. 8, Uk. 471 na 477. 387   Safinatul-Bihar, Juz. 8, Uk. 479. 388   Bidayatul-Akhlaq, Uk. 44. 384 385

114


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

11. Aupinge wasiwasi kivitendo, akishakia idadi ya rakaa ni juu yake kuendelea na asijali wasiwasi wake na hata kama ataamini ubatilifu wa Sala yake. 12. Aoge kwa majani ya mkunazi.389 13. Apige mshwaki.390 14. Afunge saumu ya siku tatu kila mwezi, na saumu ya mwezi wa Shabani.391 15. Apake hina ndevu na nywele.392 Abu Abdillah (a.s.) amesema: “Mtu mmoja alikwenda kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu na kumwambia: ‘Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Nakushtakia wasiwasi ulionipata katika sala yangu kiasi kwamba sijui nilivyosali, ni zaidi au pungufu.’ Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akasema: “Ukiingia ndani ya sala libonyeze paja lako la kulia kwa kidole chako cha kulia chenye kusabihi, kisha sema: ‘Kwa jina la Mwenyezi Mungu ninatawakali kwa Mwenyezi Mungu. Najikinga kwa Mwenyezi Mungu Msikivu Mjuzi dhidi ya shetani mlaanifu.’ Hakika Wewe utamuuwa na kumfukuza.”393 Na mwisho wa dua zetu ni kumshukuru Mwenyezi Mungu swt. Mwingi wa huruma Mwenye kurehemu.

Safinatul-Bihar, Juz. 8, Uk. 478.   Safinatul-Bihar, Juz. 8, Uk. 478. 391   Al-Bihar, Juz. 97, Uk. 72. Mizanul-Hikma, Juz. 1, Uk. 452. 392   Safinatul-Bihar, Juz. 2, Uk. 603. 393   Furuul-Kafiy, Juz. 3, Uk. 358, Hadithi ya 4. 389 390

115


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION 1.

i) Qur’ani Tukufu – Pamoja na Tarjuma ya Kiswahili ii) Qur’an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Thelathini 2. Uharamisho wa Riba 3. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza 4. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili 5. Hekaya za Bahlul 6. Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) 7. Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.) 8. Hijab vazi Bora 9. Ukweli wa Shia Ithnaashari 10. Madhambi Makuu 11. Mbingu imenikirimu 12. Abdallah Ibn Saba 13. Khadijatul Kubra 14. Utumwa 15. Umakini katika Swala 16. Misingi ya Maarifa 17. Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia 18. Bilal wa Afrika 19. Abudhar 20. Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu 21. Salman Farsi 22. Ammar Yasir 23. Qur’an na Hadithi 24. Elimu ya Nafsi 25. Yajue Madhehebu ya Shia 26. Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur’an Tukufu 27. Al-Wahda 28. Ponyo kutoka katika Qur’an 29. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii 30. Mashukio ya Akhera 116


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

31. Al Amali 32. Dua kwa Mujibu wa Ahlulbayt (a.s) 33. Udhuu kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna 34. Haki za wanawake katika Uislamu 35. Mwenyezi Mungu na sifa zake 36. Kumswalia Mtume (s) 37. Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) 38. Adhana 39. Upendo katika Ukristo na Uislamu 40. Qur’ani na Kuhifadhiwa Kwake 41. Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu 42. Kupaka juu ya khofu 43. Kukusanya Sala Mbili 44. Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara 45. Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya 46. Kusujudu juu ya udongo 47. Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s) 48. Tarawehe 49. Malumbano baina ya Sunni na Shia 50. Kupunguza Swala safarini 51. Kufungua safarini 52. Umaasumu wa Manabii 53. Qur’an Yatoa Changamoto 54. as-Salaatu Khayrun Mina -’n Nawm 55. Uadilifu wa Masahaba 56. Dua e Kumayl 57. Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu 58. Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake 59. Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata 60. Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mtume Muhammad (s) 61. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza 62. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili 63. Kuzuru Makaburi 117


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

64. 65. 66. 67. 68. 69. 70. 71. 72. 73. 74. 75. 76. 77. 78. 79. 80. 81. 82. 83. 84. 85. 86. 87. 88. 89. 90. 91. 92. 93. 94. 95. 96.

Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita Tujifunze Misingi Ya Dini Sala ni Nguzo ya Dini Mikesha Ya Peshawar Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu Ubora wa Imam ‘Ali na Ushia ndio njia iliyonyooka Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake Liqaa-u-llaah Muhammad (s) Mtume wa Allah Amani na Jihadi Katika Uislamu Uislamu Ulienea Vipi? Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) Dhana ya Ndoa ya Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) Urejeo (al-Raj’ah) Mazingira Utokezo (al - Badau) Hukumu ya kujenga juu ya makaburi Swala ya maiti na kumlilia maiti Uislamu na Uwingi wa Dini Mtoto mwema Adabu za Sokoni Na Njiani Johari za hekima kwa vijana Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu Tawasali (AT- TAWASSUL) Imam Mahdi katika Usunni na Ushia Hukumu za Mgonjwa 118


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

97. Sadaka yenye kuendelea 98. Msahafu wa Imam Ali 99. Maimamu wa Ahlul Bait – Ujumbe na Jihadi 100. Idi Al-Ghadir 101. Kusoma sura zenye Sijda ya wajibu 102. Hukumu zinazomuhusu mkuu wa kazi na Mfanyakazi 103. Huduma ya Afya katika Uislamu 104. Sunna za Nabii Muhammad (saww) 105. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza) 106. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili) 107. Shahiid Mfiadini 108. Mwanamke Na Sharia 109. Ujumbe -Sehemu ya Kwanza 110. Ujumbe - Sehemu ya Pili 111. Ujumbe - Sehemu ya Tatu 112. Ujumbe - Sehemu ya Nne 113. Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu 114. Hadithi ya Thaqalain 115. Ndoa ya Mutaa 116. Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza 117. Ukweli uliopotea sehemu ya Pili 118. Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu 119. Ukweli uliopotea sehemu ya Nne 120. Ukweli uliopotea sehemu ya Tano 121. Mkutano wa Maulamaa wa Baghdad 122. Safari ya kuifuata Nuru 123. Fatima al-Zahra 124. Myahudi wa Kimataifa 125. Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi 126. Visa vya kweli sehemu ya Kwanza 127. Visa vya kweli sehemu ya Pili 128. Elimu ya Ghaibu ya Maimamu 129. Mwanadamu na Mustakabali wake 119


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

130. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Kwanza) 131. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Pili) 132. Khairul l’Bariyyah 133. Uislamu na mafunzo ya kimalezi 134. Vijana ni Hazina ya Uislamu 135. Adhana ni Ndoto au ni Wahyi? 136. Tabaruku 137. Saada Kamili – Kitabu cha Kiada cha Maadili 138. Vikao vya furaha 139. Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje? 140. Visa vya wachamungu 141. Falsafa ya Dini 142. Kuhuzunika na Kuomboleza 143. Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah 144. Mjadala wa Kiitikadi 145. Kuonekana kwa Allah 146. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza) 147. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili) 148. Ndugu na Jirani 149. Ushia ndani ya Usunni 150. Maswali na Majibu 151. Mafunzo ya hukmu za ibada 152. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 1 153. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 2 154. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 3 155. Abu Huraira 156. Vipengee kadhaa katika Swala ya Jamaa na Msikiti. 157. Mazingatio kutoka katika Qur’an - Sehemu ya Kwanza 158. Mazingatio kutoka kaitka Qur’an - Sehemu ya Pili 159. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya kwanza 160. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya Pili 161. Shia na Qur’ani – Majibu na Maelezo 162. Falsafa ya Mageuzi ya Imam Husein (a.s) 120


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

163. Amali za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani 164. Elimu ya Tiba za Kiislamu - Matibabu ya Maimamu 165. Uislamu Safi 166. Majlisi za Imam Husein Majumbani 167. Je, Kufunga Mikono 168. Uislam wa Shia 169. Amali za Makka 170. Amali za Madina 171. Asili ya Madhehebu katika Uislamu 172. Sira ya Imam Ali kuhusu Waasi 173. Ukweli uliofichika katika neno la Allah 174. Uislamu na Mifumo ya Uchumi 175. Umoja wa Kiislamu na Furaha 176. Mas’ala ya Kifiqhi 177. Jifunze kusoma Qur’ani 178. as-Sahifatul Kamilah as-Sajjadiyyah 179. Hayya ‘Alaa Khayri’l-’Amal Katika Adhana 180. Ukweli kuhusu Funga ya Siku ya Ashura 181. Dua za Miezi Mitatu Mitukufu (Rajabu, Shaabani na Ramadhani) 182. Uadilifu katika Uislamu 183. Mahdi katika Sunna 184. Maswali Ya Uchunguzi Kuhusu Uislam 185. Kazi na Bidii ni njia ya maendeleo 186. Abu Talib – Jabali Imara la Imani 187. Ujenzi na Utakaso wa Nafsi 188. Vijana na Matarajio ya Baadaye 189. Historia maana na lengo la Usalafi 190. Ushia – Hoja na Majibu 191. Mateso ya Dhuria wa Mtume (saww) 192. Maombolezo – Msiba wa Bwana wa Mashahidi (a.s.) 193. Shahidi kwa Ajili ya Ubinadamu 194. Takwa 195. Upotoshaji Dhahiri katika (Turathi) Hazina ya Kiislamu 121


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

196. Amirul Muuminina (‘as) na Makhalifa 197. Tawheed Na Shirki 198. Kuvunja hoja iliyotumika kutetea Uimamu wa AbuBakr 199. Adabu za vikao na mazungumzo 200. Hija ya Kuaga 201. Uwazi baina ya Maslahi na Vikwazo 202. Fadhila za watukufu watano katika Sahih Sita 203. Mdahalo baina ya Mwanachuoni wa Kisunni na Kishia (Al- Muraja’aat) 204. Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (as) 205. Imam Husain ni Mfumo wa Marekebisho na Mageuzi 206. Mtazamo kuhusu msuguano wa Kimadhehebu 207. Nchi na Uraia – Haki na wajibu kwa Taifa 208. Mtazamo wa Ibn Taymiyyah juu ya Imam Ali (as) 209. Uongozi wa Kidini – Maelekezo na Utekelezaji wa Kijamii 210. Maadili ya Ashura 211. Mshumaa – Shahidi na Kifo cha Kishahidi 212. Mizani ya Hekima – Hadithi za Ahlul Bait (as) – Sehemu ya Kwanza 213. Imam Ali na Mambo ya Umma 214. Imam Ali na Mfumo wa Usawa 215. Uimamu na Tamko la Kutawazwa 216. Mfumo wa Wilaya 217. Vipi Tutaishinda Hofu? 218. Kumswalia Mtume ni Ufunguo wa Utatuzi wa Matatizo 219. Maeneo ya Umma na Mali Zake 220. Nahju ‘L-Balagha – Majmua ya Khutba, Amri, Barua, Risala, Mawaidha na Semi za Amirul-Muuminin Ali bin Abu Talib (a.s.) 221. Mukhtar – Shujaa aliyelipiza kisasi dhidi ya wauaji wa Imam Husein (as) hapo Karbala 222. Mazingatio Katika Swala 223. Imam Hasan na Mfumo wa Kujenga Jamii 224. Vyakula Na Vinywaji 225. Kuelewa Rehema ya Mwenyezi Mungu 226. Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

122


Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

227. Yafaayo kijamii 228. Shia Na Hadith - Majibu na Maelezo 229. Mkakati wa Kupambanana Ufakiri 230. Mtazamo Mpya - Wanawake katika Uislamu 231. Taqiyya Kwa Mujibu Wa Sheria Ya Kiislamu 232. Imam Mahdi Na Bishara Ya Matumaini 233. Jihadi 234. Majanga Na Jukumu La Jamii 235. Muhadhara wa Maulamaa 236. Mashairi ya Kijamii 237. Ngano ya kwamba Qur’ani imebadilishwa 238. Mwanamke Katika Harakati za Mageuzi 239. Shia Na Sahaba - Majibu na Maelezo 240. Yusuf Mkweli 241. Hotuba Za Kiislamu Juu ya Haki Za Binadamu 242. Ugaidi wa Kifikra katika Medani ya Kidini

KOPI NNE ZIFUATAZO ZIMETAFSIRIWA KWA LUGHA KINYARWANDA 1. 2. 3. 4.

Amateka Ya Muhammadi (s.a.w.w) Na Aba’ Khalifa Nyuma yaho naje kuyoboka Amavu n’amavuko by’ubushiya Shiya na Hadithi

ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION KWA LUGHA YA KIFARANSA 1.

Livre Islamique

123


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.