UADILIFU KATIKA UIslamu العدالة في اإلسالم
Kimeandikwa na: Ustadh Shahid Murtadha Mutahhari
Kimetarjumiwa na: Seif Bashir Rajab na Hemedi Lubumba Selemani
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 1
2/17/2017 1:24:27 PM
ترجمة
العدل في اإلسالم
تأليف األستاذ الشهيد مرتضى المطهري
من اللغة العربية الى اللغة السوا حلية
2/17/2017 1:24:27 PM
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 2
©Haki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: 978 - 9987 – 17 – 002 – 9 Kimeandikwa na: Ustadh Shahid Murtadha Mutahhari Kimetarjumiwa na: Seif Bashir Rajab na Hemedi Lubumba Selemani Kimehaririwa na: Hemedi Lubumba (Abu Batul) Kimesomwa-Prufu na: Ramadhani S. K. Shemahimbo Kimepitiwa na: Mbaraka A. Tila Kimepangwa katika Kompyuta na: Al-Itrah Foundation Toleo la kwanza: Juni, 2011 Nakala: 1000 Toleo la pili: Juni, 2017 Nakala: 2000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Al-Itrah Foundation S.L.P. - 19701, Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 / 2127555 Barua Pepe: alitrah@yahoo.com Tovuti: www.alitrah.info
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 3
2/17/2017 1:24:27 PM
YALIYOMO Dibaji.............................................................................1
Uadilifu Ulivyokuwa Kwa Ali ď ‚................................2
Uadilifu Katika Uislamu...............................................4
Upendeleo Wa Haki Na Usiokuwa Wa Haki.............66
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 4
2/17/2017 1:24:27 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
بسم هللا الرحمن الرحيم
DIBAJI
K
itabu hiki ni toleo la Kiswahili la taasisi ya Al Itrah Foundation. Chapisho lake limelenga kukidhi mahitaji ya kiroho ya zama hizi pamoja na Ubongo na fikra zinazokuwa za Muislam. Jitihada kubwa zimefanywa na Taasisi kuweka chapisho hili la Kiswahili katika msingi wa haki na wenye kukubalika katika Uislam. Unaombwa kwa Taadhima ukisome kitabu hiki katika malengo yaliyokusudiwa. Pia Unaombwa kuwasilisha kwetu maoni yako huru juu ya chapisho letu hili, jambo ambalo tutashukuru sana. Kutangaza ujumbe wa Uislam ni kazi ambayo inahitaji ushirikiano wetu sote. Taasisi inakuomba kuungana na kushirikiana kama ilivyoagizwa katika aya ya Qur’an: (Surat Saba’ 34:46). Na rehma za Allah ziwe juu yako.
Wako katika Uislam Al Itrah Foundation Barua Pepe: alitrah@yahoo.com SMS: +255 778 300 140 1
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 1
2/17/2017 1:24:27 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
بسم هللا الرحمن الرحيم Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.
UADILIFU ULIVYOKUWA KWA ALI B
M
wenyezi Mungu amesema:
َاب َو ْال ِمي َزانَ لِيَقُو َم َ ت َوأَ ْنز َْلنَا َم َعهُ ُم ْال ِكت ِ لَقَ ْد أَرْ َس ْلنَا ُر ُسلَنَا بِ ْالبَيِّنَا ْ اس ِ النَّاسُ بِ ْالقِس ِ َّْط ۖ َوأَ ْنز َْلنَا ْال َح ِدي َد فِي ِه بَأسٌ َش ِدي ٌد َو َمنَافِ ُع لِلن َزي ٌز ُ َولِيَ ْعلَ َم للاهَّ ُ َم ْن يَ ْن ِ ص ُرهُ َو ُر ُسلَهُ بِ ْال َغ ْي ِ ب ۚ إِ َّن للاهَّ َ قَ ِويٌّ ع “Kwa hakika tuliwapeleka Mitume wetu kwa dalili waziwazi, na tukateremsha Kitabu pamoja nao na mizani, ili watu wasimame kwa uadilifu. Na tumekiumba chuma chenye nguvu nyingi na manufaa kwa watu, na ili Mwenyezi Mungu amjue anayemsaidia Yeye na Mitume wake kwa siri. Kwa hakika Mwenyeezi Mungu ni mwenye kushinda.” (Qur’ani Sura Hadiid 57:25). 2
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 2
2/17/2017 1:24:27 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
Na akasema:
ْ ان َوإِيتَا ِء ِذي ْالقُرْ بَ ٰى َويَ ْنهَ ٰى ع َِن ِ إِ َّن للاهَّ َ يَأ ُم ُر بِ ْال َع ْد ِل َوالإْ ِ حْ َس َْالفَحْ َشا ِء َو ْال ُم ْن َك ِر َو ْالبَ ْغ ِي ۚ يَ ِعظُ ُك ْم لَ َعلَّ ُك ْم تَ َذ َّكرُون “Kwa hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha uadilifu na hisani, na kuwapa jamaa; na anakataza uchafu na uovu na uasi, anakuwaidhini ili mpate kukumbuka.” (Qur’ani Sura an-Nahli 16:90).
Aya hizi mbili zinapatikana katika Sura mbili tofauti ndani ya Qur’ani, ya kwanza ni ya ishirini na tano katika Sura al-Hadid, na ya pili ni ya tisini katika Sura an-Nahli, na zote mbili zinazungumzia maudhui moja, nayo ni Uadilifu, ijapokuwa pia kila Aya kati ya hizo mbili ina maudhui nyingine muhimu. Katika Aya ya kwanza tunakuta kwamba lengo kuu la dini za Mwenyezi Mungu ni kutilia mkazo vigezo vya Uadilifu. Na katika Aya ya pili Mwenyezi Mungu anaamrisha kutekeleza Uadilifu na hisani, kwa kuzingatia kwamba matendo haya ni miongoni mwa misingi ya Uislamu na roho ya Uislamu, ambayo inazuia maovu, machafu na kila aina ya dhuluma. Hakika maudhui ya Uadilifu na hisani, na hususan Uadilifu, ukiachia mbali kwamba imekaririwa mara
3
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 3
2/17/2017 1:24:27 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
kwa mara ndani ya Qur’ani, pia ina mlango mpana sana katika historia ya Uislamu na baina ya Waislamu, sawa iwe upande wa historia ya elimu zote za Kiislamu, au upande wa siasa na elimu zote za kijamii. Hivyo kwa kuwa Uadilifu ni nguzo moja miongoni mwa nguzo za Uislamu wa kweli, basi hatuna budi kuuzungumzia, na hasa kwa kuwa kwetu sisi wafuasi wa Ahlul-Bait G wenyewe ni msingi miongoni mwa misingi ya dini. Uadilifu ni miongoni mwa misingi ya dini: Misingi ya dini ni mitano, nayo ni: Tawhid, Uadilifu, Unabii, Uimamu na Siku ya Kiyama. Uimamu na Uadilifu kwa wafuasi wa Ahlul-Bait G ni miongoni mwa misingi ya kidini, na pia huhesabika kuwa ni miongoni mwa misingi ya madhehebu. Na hii inamaanisha kwamba kwa mtazamo wa dini ya Uislamu, hakika hayo mambo mawili (Uimamu na Uadilifu) ni miongoni mwa misingi ya Uislamu pia. Kufikia hapa inaeleweka waziwazi kwamba Uadilifu kwa mtazamo wa madhehebu na njia ya Ahlul-Bait G ni msingi wenye umuhimu mkubwa, na si suala la kimaadili tu. Hivyo hakika mimi nachukua nafasi hii ya mikesha hii mitukufu, kuzungumzia kwa kadri ya uwezo wangu, nguzo hii na historia yake inayofungamana na mustakabali wetu na hali tuliyonayo sasa. 4
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 4
2/17/2017 1:24:27 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
Pia ni kwamba hakika mikesha hii ya mwezi mtukufu wa Ramadhan inafungamana na Imam aliye mwadilifu katika kila kitu, aliye mfano halisi wa Uadilifu na usawa, aliyeishi maisha ya Uadilifu na uungwana, aliyekuwa mfano na chombo kamili kilichobeba upendo, huruma, mahaba na hisani kwa wanadamu wote, mtu huyu si mwingine bali ni Imam Ali B kiongozi wa wachamungu. Ambaye wasiokuwa yeye wamemtolea wasifu kwamba: “Aliuawa kishahidi mihrabuni kwa sababu ya ukamilifu wa Uadilifu wake.� Ali Bni muhanga wa Uadilifu: Kwa hakika Ali al-Murtadha B alikuwa sura halisi ya Uadilifu na mfano halisi wa huruma, upendo na hisani. Ndani ya mkesha kama huu dharuba kali lilitua juu ya kichwa cha muhanga wa Uadilifu. Dharuba lililotua kwa sababu ya ukakamavu wake usio na upindishaji katika haki na Uadilifu, na katika kutetea haki za binadamu. Dharuba ambalo lilimwachia maumivu makali, uchungu, mateso na mahangaiko aliyoyavumilia, na hatimaye likamwangusha akiwa anatekeleza faradhi yake. Dharuba ambalo lilimpa raha ya kuuacha ulimwengu huu huku likiuhuzunisha ulimwengu milele kwa kifo cha Imam mwadilifu ambaye lau serikali yake 5
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 5
2/17/2017 1:24:27 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
ingedumu kwa muda mrefu basi ungetimia mfano kamili wa jamii ya Kiislamu yenye mafanikio angavu. Hakika kauli ya kwamba amepumzika na kupata raha kwa kuyaacha maisha haya ya dunia, ni kauli iliyotoka ndani ya kinywa chake kupitia ulimi wake mwenyewe, kwani alipokuwa mahututi kitandani baada ya dharuba ile, alisema maneno haya: “Na sikuwa ila ni kama chombo kilichotia nanga na mtafutaji aliyepata.� Uadilifu uliopelekea Ali B kufa kishahidi: Hakika katika mkesha huu mtukufu wa leo nataraji kuuweka wazi Uadilifu wa Kiongozi wa wachamungu B na hisani yake. Nitajaribu kufafanua vipi Uadilifu wa Imam Ali B kuwa ndio uliomuuwa, na ni vipi ukakamavu wake katika njia hii uliwapelekea wale waliothubutu kumdhuru kupitia Uadilifu huo kueneza machafuko na maasi. Je! Uadilifu huu ulikuwa wa aina gani? Na je! Uadilifu huu ulikuwa wa kitabia tu kama ule tunaouhitaji kwa imam wa sala ya jamaa, au kwa Kadhi, au kwa shuhuda wa talaka, au katika ushahidi wa kisharia? Kwa hakika ni kwamba aina hizi za Uadilifu haziwezi kamwe kumsababishia mtu kifo, bali kinyume chake humpa mtu umaarufu, heshima na kupendwa na 6
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 6
2/17/2017 1:24:27 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
watu. Hakika Uadilifu uliomuuwa Imam Ali B ni ile falsafa yake ya kijamii na fikra zake maalum kuhusu Uadilifu wa kijamii wa Kiislamu, kwani alikuwa mathubuti katika kusisitiza rai hii ya kuwepo Uadilifu wa kijamii wa Kiislamu na falsafa ya kijamii ya Kiislamu. Yeye hakuwa tu mwadilifu basi, bali alikuwa pia mpigania Uadilifu, kwani kuna tofauti baina ya mwadilifu na mpigania Uadilifu, kama ambavyo kuna tofauti baina ya mtu huru na mpigania uhuru, kwani mtu huru humaanisha kwamba yeye binafsi ndiye aliye huru, ama mpigania uhuru, yeye hutetea uhuru wa jamii na huona kwamba uhuru ndio lengo kuu la jamii. Kadhalika ni kama hivyo kwa aalimu, huyu ni aalimu yeye binafsi, na mwingine ukiachia mbali kuwa ni aalimu pia hueneza elimu, maarifa na taalimu katika jamii. Na ni hivyo hivyo kuhusu Uadilifu, huyu ni mwadilifu, lakini mwingine ni mpigania Uadilifu, yaani kwake yeye Uadilifu ni hitajio la kijamii. Aya tukufu inasema: “Kuweni wenye kusimamia usawa.� Kusimamia usawa maana yake ni kueneza Uadilifu, na hii hutofautiana na kitendo cha yeye binafsi kukomea kuwa mwadilifu tu.
7
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 7
2/17/2017 1:24:27 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
Kipi kilicho bora, Uadilifu au ukarimu? Awali ya yote nawatajia ibara iliyotamkwa na ulimi wake B. Imepokewa kwamba mtu mmoja alimuuliza Imam Ali B kwamba: “Ni kipi kilicho bora, ukarimu au Uadilifu?” Imam B alimjibu kwa msemo huu: “Uadilifu huyaweka mambo sehemu yake, na ukarimu huyatoa toka katika mwelekeo wake.” Hivyo Uadilifu maana yake ni kumpa kila mwenye haki haki yake. Na ukarimu ni mwenye haki kuisamehe haki yake na kumpa haki hiyo yule asiyekuwa na haki. Hivyo ukarimu huyatoa mambo toka katika mwelekeo wake. Na akasema sehemu nyingine: “Uadilifu ni haki ya wote, na ukarimu ni upendeleo maalumu.” Hivyo Uadilifu ni msingi wa uendeshaji wa mambo ya jamii nzima, msingi ambao ndio chanzo cha kanuni zote za maisha ya kijamii. Ama ukarimu wenyewe ni hali mahsusi ya yule anayewapa kipaumbele wenzake kabla yake mwenyewe. Haiwezekani kuzingatia kwamba ukarimu na uungwana ni miongoni mwa misingi mama ya maisha ya jamii nzima, kiasi kwamba tuweke kanuni za ulazima kutokana na mambo hayo, bali ni kwamba lau ikitokea ukarimu, ihisani na uungwana kuwekwa chini ya mamlaka ya sheria na utekelezaji wa lazima,
8
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 8
2/17/2017 1:24:27 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
basi havitaitwa tena ukarimu, ihisani wala uungwana. Kwani hakika ukarimu na uungwana vinapata sifa hiyo pale vinapotendwa bila msukumo wa sheria ya ulazima, bali ni kwamba binadamu kwa hulka yake binafsi ya ukarimu, heshima na upendo kwa wenzake hufanya ukarimu na uungwana, bali pia huwa ni kwa sababu ya kupenda kuishi, hivyo Uadilifu ni bora kushinda ukarimu. Hili ndilo lililokuwa jibu la Imam Ali B katika kuufadhilisha Uadilifu juu ya ukarimu. Bila shaka mtu asiye na fikra za kijamii na mwenye kuyapima mambo haya kwa kipimo cha mtu binafsi, kwa hakika hawezi kamwe kutoa jibu kama hili, na wala hawezi kuona kwamba Uadilifu ni bora kushinda ukarimu. Lakini Imam Ali B katika maneno yake ya thamani, anautazama Uadilifu kwa mtazamo wa kijamii, na anaupima kwa kipimo cha kijamii. Hakika ni maneno ya mtu aliye na falsafa ya kijamii iliyo wazi. Ukarimu na Uadilifu katika mtazamo wa tabia ya mtu binafsi: Ingawa wanazuoni wa tabia wanasema kwamba ukarimu una daraja ya juu zaidi kushinda Uadilifu, lakini Imam Ali B amedhihirisha wazi wazi na kutoa dalili tosha kwamba Uadilifu ni bora kushinda ukarimu. 9
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 9
2/17/2017 1:24:28 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
Bila shaka fikra hizi mbili tofauti zinatokana na mitazamo miwili tofauti. Lau tukitazama maudhui hii kwa mtazamo wa tabia ya mtu binafsi, utaona kwamba ukarimu ni bora kushinda Uadilifu. Hiyo ni kwa sababu mtu mwadilifu huonekana amefikia kiwango hicho cha ukamilifu wa kibinadamu kwa kuwa tu havunji haki za wengine, hachukui mali za wengine, wala hawavunjii heshima watu. Ama mtu mkarimu na muungwana, ukiachia mbali kuwa yeye hana tamaa na mali ya wengine, pia yeye huwapa wengine mali yake kwa ukarimu wake, ukiachia mbali kuwa yeye hachukui nafasi za wengine, pia huwapa wengine nafasi yake kwa ukarimu wake, ukiachia mbali kuwa yeye hamjeruhi yeyote, pia huwazuru majeruhi na wagonjwa katika viwanja vya mapambano, hospitalini au majumbani, na hutoa dawa, hutibu majeraha yao na kuwauguza bila kutaka ujira. Na ukiachia mbali kuwa yeye hamwagi damu ya yeyote, pia yupo tayari kumwaga damu yake ili kuifidia jamii nzima kheri na mafanikio. Hivyo kwa mtazamo wa sifa za kimaadili za mtu binafsi, ukarimu ni bora kushinda Uadilifu. Uadilifu na ukarimu katika mtazamo wa kijamii: Lakini ni upi mtazamo wa kijamii? Ni vipi kwa upande wa maisha ya kijamii kwa jumla? Mtazamo ambao un10
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 10
2/17/2017 1:24:28 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
aitazama jamii kama mwili mmoja? Bila shaka tukilitizama jambo hili kwa upande huu tutakuta kwamba Uadilifu una hadhi ya juu kushinda ukarimu. Uadilifu katika jamii ni kama nguzo ya jengo, na ukarimu ni kama urembo wa rangi katika jengo hilo. Hivyo ni lazima kutilia maanani na nguvu nguzo kwanza kabla ya marembo. Ikiwa msingi wa jengo ni dhaifu kuna maana gani au haja gani ya kuremba jengo hilo kwa rangi na nakshi? Lakini msingi wa jengo ukiwa ni thabiti na imara basi twaweza kuishi ndani yake hata kabla ya rangi na marembo mengine. Wakati mwingine waweza kupoteza gharama katika kulipaka rangi jengo na kulitia marembo mengi ya nje, lakini msingi wa jengo hili ukabaki kuwa ni dhaifu, na hapo mvua kubwa ikinyesha mara moja hutosha kuliporomosha na kuwaangamiza wakazi wake. Kisha tujue kwamba ukarimu, hisani na uungwana ambao una manufaa na ubora mkubwa, huenda wakati mwingine usiwe na ubora wowote kwa mwenye kutekelezewa, hili nalo ni muhimu kulizingatia, kama ambavyo ni muhimu kuzingatia jinsi jamii itakavyofaidika, kwani iwapo hatutaleta uwiano wa kijamii na tukaacha mambo yaende bila uwiano, basi ubora huu wa kitabia unaweza kusababisha utasa katika uzalishaji wa jamii na hatimaye uharibifu wa kijamii. Kwa mfano sadaka nyingi zisizo na malengo, wakfu 11
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 11
2/17/2017 1:24:28 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
nyingi zisizo na malengo na nadhiri nyingi zisizo na malengo, vyaweza kuwa tufani yenye kughirikisha jamii, kwani yaweza kueneza uvivu baina ya wanajamii na hatimaye kujenga jamii isiyo na harakati. Na hali hiyo ndio mfano halisi wa Aya:
ٌّصر ِ يح فِيهَا ٍ َمثَ ُل َما يُ ْنفِقُونَ فِي ٰهَ ِذ ِه ْال َحيَا ِة ال ُّد ْنيَا َك َمثَ ِل ِر ْ َصاب َ ْت َحر ث قَوْ ٍم ظَلَ ُموا أَ ْنفُ َسهُ ْم فَأ َ ْهلَ َك ْتهُ ۚ َو َما ظَلَ َمهُ ُم للاهَّ ُ َو ٰلَ ِك ْن َ َأ ْ َأَ ْنفُ َسهُ ْم ي َظلِ ُمون “Mfano wa wanavyovitoa katika maisha haya ya dunia ni kama mfano wa upepo wenye baridi kali uliofikilia shamba la watu waliodhulumu nafsi zao, ukaliangamiza. Na Mwenyezi Mungu hakuwadhulumu, lakini wanajidhulumu wenyewe.” (Qur’ani Sura Aali Imran 3:117)
Kwa hakika jamii haiwezi kuongozwa kwa Ukarimu na hisani, hivyo msingi wa serikali ya kijamii ni Uadilifu, kwani hakika ukarimu na hisani visipotekelezwa kwa lengo maalumu bila shaka huyatoa mambo kwenye msitari wake. Imam as-Sajjad B anasema: “Watu wangapi wamepotoshwa kwa kauli nzuri! Ni watu wangapi wamedanganywa kwa sitara nzuri! Na ni watu wangapi wamevutwa kwa hisani!” Na hii ndio 12
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 12
2/17/2017 1:24:28 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
maana ya kauli ya Imam Ali B: “Uadilifu huyaweka mambo sehemu yake, na ukarimu huyatoa toka katika mwelekeo wake.” Watu wengi wasikiapo kwamba hakika Ali B ni mfano halisi na kamili wa ukarimu na upaji, basi huona kwamba ukarimu ni bora kushinda Uadilifu. Lakini hushangaa na kujiuliza: Ni vipi Imam Ali B aone Uadilifu ni bora kushinda ukarimu? Ni vipi mtu huyu ambaye ni kinara wa ukarimu, upaji na uungwana aseme kuhusu ukarimu: “Ukarimu huyatoa mambo toka katika mwelekeo wake.”? Kwa hakika ukweli ni kwamba maswali haya humfika yule mwenye kuyatazama mambo haya kwa mtazamo wa maadili ya mtu binafsi, na kwa mtazamo huu maswali haya ni sahihi. Lakini upande mwingine muhimu ni upande wa jamii juu ya kadhia hii, upande ambao mara nyingi hatuutazami na kuutilia manani, na sababu ya hilo ni kwamba mwanadamu ni juzi tu ndio kajua umuhimu wa maarifa ya jamii na kuweka sheria na kanuni zitakazoiendesha jamii. Ama huko kabla ni ulamaa wetu wachache tu ndio waliokuwa wakilitilia umuhimu hilo tena bila kulifanya kuwa ni elimu yenye kurithishwa. Hiyo ni kwa sababu mtazamo ulikuwa umejikita upande wa maadili ya mtu binafsi tu. Kwa hakika mimi mwenyewe sikumbuki kama nimewahi kusoma somo hili katika kitabu chochote, 13
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 13
2/17/2017 1:24:28 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
ijapokuwa somo hili (maarifa ya jamii) limo katika kitabu cha Nahjul-Balagha, kitabu ambacho kinapatikana kwa watu wote. Naamini kwamba sababu iliyosababisha hali hiyo ni kwamba hawakuwa na uwezo wa kuoanisha fikira hii na vigezo vya kimaadili, hivyo walishindwa kutoa mwelekeo unaokubalika. Lakini leo kwa fadhila ya maendeleo ya elimu za kijamii, tumefikiwa na vigezo vingine visivyokuwa vya kimaadili, na kwa mwangaza wa vigezo hivyo tumejua thamani ya maneno hayo ya Ali B, maneno yaliyokuwepo kabla ya maendeleo hayo ya kielimu, bali hata kabla ya zama za Sayyid Radhiyyu ambaye ndiye mkusanyaji wa kauli za Imam Ali B katika sura ya kitabu kwa jina la Nahjul-Balagha. Hata katika zama hizo Sayyid Radhiyyu yeye mwenyewe ambaye ndiye mkusanyaji wa maneno hayo, wala Avicena mwanafalsafa mkubwa ambaye aliishi ndani ya zama hizo, hawakuwa na uwezo wa kubainisha ukweli wa juu wa kijamii kama huo. Tofauti iliyopo baina ya ukarimu na hisani: Ukarimu na hisani ni maneno mawili yanayokaribiana kimaana, na ndani ya Qur`ani tukufu Uadilifu umekuja pembezoni mwa hisani: “Kwa hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha uadilifu na hisani.� Na aliyem14
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 14
2/17/2017 1:24:28 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
uuliza Imam Ali B kuhusu ukarimu na Uadilifu ni kana kwamba ameashiria Aya hii: “Kwa hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha uadilifu na hisani.� Hivyo akauliza ni ipi tofauti ya Uadilifu na hisani, na ni kipi kilicho bora, ni Uadilifu au hisani? Ni wazi kwamba hisani na ukarimu ni maana mbili zilizo karibiana sana ijapokuwa si kitu kimoja, kwa sababu hisani hujumuisha pia ukarimu, kwani hujumuisha upaji wa mali na matendo mengine mema. Kwa mfano, ukimshika mkono kipofu na kumvusha barabara, kitendo hiki si ukarimu bali ni hisani. Ukimwelimisha mjinga au kumwongoza aliyepotea, bila shaka umemtendea hisani, na wala huo si ukarimu. Uadilifu ni falsafa ya kijamii: Shabaha ya kunukuu swali lile na jibu lake ilikuwa ni kutazama ni upi mtazamo wa Imam Ali B kuhusu Uadilifu, je anautazama kwa jicho la maadili tu, au anatilia maanani sana upande wa kijamii? Hivyo kupitia maneno na vitendo vya Imam Ali B na hususan alivyovitenda wakati wa uongozi wake, inabainika wazi kwamba Uadilifu kwa mtazamo wa Imamu wa wachamungu B ni falsafa ya jamii ya Kiislamu, na una nafasi ya juu katika fikra zake kwa kuzingatia kwamba wenyewe ndio kanuni muhimu kushinda kanuni zote 15
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 15
2/17/2017 1:24:28 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
za Kiislamu. Siasa yake yote ilisimamia juu ya msingi huu, na kamwe hakuweza kwenda kinyume na msingi huu katika lengo lolote na kwa shinikizo lolote. Hii ndio iliyokuwa njia yake, na ndio njia pekee iliyomsababishia matatizo mengi, na wakati huo huo imekuwa ufunguo wa mwanahistoria na muhakiki katika kufungua milango ya matukio ya ukhalifa wa Imam Ali B, kwa sababu Imam B alikuwa shupavu sana katika jambo hili na hakuyumbishwa na lolote. Kwa hakika ukiutazama ukakamavu wa Imam B katika Uadilifu wake na ambao ndio Uadilifu wenyewe, na kwa mtazamo mwingine ndio haki za binadamu, inatosha kusema kuwa ndio falsafa iliyompelekea kuukubali ukhalifa baada ya Uthman, baada ya kuona kwamba uzani wa Uadilifu wa kijamii haupo tena, na watu wamegawanyika matabaka mawili, tabaka la walionacho na wasionacho. Imam B anasema kuhusu hili: “Lau si kufika kwa watu na kulazimu hoja ya kuwepo wasaidizi, na ahadi iliyochukuliwa na Mwenyezi Mungu kwa wanachuoni, kuwa wasiridhike kimya kimya na ulafi wa madhalimu na kusagwa haki ya mdhulumiwa, ningeitupa kamba ya ukhalifa kwenye bega lake, na ningemtendea wa mwisho kama wa kwanza.�
16
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 16
2/17/2017 1:24:28 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
Maneno haya yana maana kwamba baadhi ya wasaidizi wa Imam B na kundi la Answari, walimjia Imam B na kumtolea hoja, kisha ni kwamba Mwenyezi Mungu alishachukua ahadi kwa watu wenye busara na wenye dhamira hai, kwamba wanaposhuhudia dhuluma ikitendwa, madhalimu wakijinyakulia mali, utajiri na neema za Mwenyezi Mungu, wanakula mpaka wanaugua kwa kuvimbiwa, ilihali kundi lingine likinyang’anywa haki zao kiasi kwamba hawapati cha kuweza kumeza, basi wasinyamaze na kuweka mikono nyuma. Hivyo lau si kuhisi hali hiyo na wajibu alionao juu ya hali hiyo, angejitenga na wala asingechukua serikali, bali angeendelea kuwa kama alivyokuwa mwanzo. Huzuni na kutoa hoja: Hakukawia Imam B katika uongozi wake katika mpango wa kuangamiza udhalimu na kuzirejesha haki za watu, bali alifanya bidii sana na kuhakikisha kwamba haki zote zilizo nyakuliwa zimeregeshwa na kutumika katika njia ipasayo. Alikuwa anajua kwa kina jinsi mpango huo utakavyozusha hasira na chuki katika siasa, na kwa ajili hiyo aliupokea ukhalifa na hali ni mwenye huzuni nyingi, na akawaambia waliokuja kumtaka achukue serikali: “Niacheni 17
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 17
2/17/2017 1:24:28 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
mimi na mchagueni asiyekuwa mimi. Kwa hakika sisi tunalipokea jambo ambalo lina nyuso na rangi mbalimbali, nyoyo hazitalikubali wala akili hazitatulia kwalo. Na hakika giza limetanda angani na hoja zimekataliwa.” Kisha ili Imam B atoe hoja juu ya hawa waliyomjia na hali wakimsisitiza aukubali ukhalifa, alisema: “Na jueni kwamba hakika mimi ikiwa nitawakubalia, basi nitawapeleka nijuavyo mimi.” Yaani hakika ikiwa nitaridhia mtakalo basi nitafuata utaratibu niujuao mimi, sintapinda wala kumsikia mwingine yeyote. Ama mkiniacha nilivyo bila kunibebesha jukumu la serikali na ukhalifa, basi sintakuwa na mamlaka bali upeo wangu utakuwa ni kutoa ushauri kama ilivyokuwa hapo kabla. Mgao wa Uthman: Kisha anagusia mgao wa Uthman, nao ni zile ardhi za Waislamu wote ambazo Uthman aliwamilikisha baadhi ya Waislamu, anasema: ‘Naapa kwa Jina la Mwenyezi Mungu kwamba, hata ningezikuta zimetumika zikiwa mahari kwa kuolea wake, na vijakazi wamemilikiwa kwazo, ningezirudisha.’
18
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 18
2/17/2017 1:24:28 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
Aunganisha yaliyotangulia: Hakika kulizuka matatizo mengi wakati wa serikali yake, chanzo cha hayo ilikuwa ni kwamba yeye B aliunganisha yale yaliyotangulia, yaani hakuwa anasema: “Mwenyezi Mungu asamehe yale yaliyotangulia.” Bali alikuwa akisema: “Hakika lazima niyafikishe katika mikono ya sheria yale yaliyotangulia.” Kwani hakika yaliyopita ndio hutengeneza ya sasa na yajayo, hivyo huwezi kujenga jengo refu na imara juu ya msingi mbovu na uliopinda.” Ulimwengu mpana wa Uadilifu na ulimwengu finyu wa dhulma: “Kwa hakika katika Uadilifu kuna wasaa. Na ambaye umemuwia dhiki Uadilifu, udhalimu kwake utakuwa dhiki mno.” Uadilifu humgusa kila mmoja, huwaleta watu pamoja na kuwaridhisha. Hakika mazingira pekee yanayoweza kuwakusanya watu wote pamoja ni Uadilifu tu. Hivyo lau hulka ya mmoja wao itakengeuka na hatimaye kutotosheka na haki yake na mipaka yake, na akaona kwamba Uadilifu wambana na kumgandamiza, basi bila shaka ujeuri na dhuluma vitambana zaidi na kumgandamiza zaidi na kumuumiza zaidi. Hiyo ni kwa sababu mgandamizo umfikao mwanadamu una namna 19
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 19
2/17/2017 1:24:28 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
mbili: Namna moja ni ule usababishwao na mazingira na jamii inayomzunguka, kama vile kupigwa kwa mfupa, kujelidiwa kwa mjeledi au kutupwa gerezani. Ila ni kwamba kuna namna nyingine ya mgandamizo, nayo ni ile inayoipata roho ya mwanadamu kwa ndani, kama vile mgandamizo wa husuda, chuki, hasira, tamaa na uchu. Hivyo lau Uadilifu utaenezwa katika jamii, bila shaka watu watasalimika na migandamizo ya nje, kwani mtu hataweza tena kupora haki ya mwingine, na kwa hili mtu hataweza kusababisha mgandamizo juu ya roho za wengine na kuwadhikisha. Ama usipoenezwa Uadilifu, na uwanja wa jamii ukawa kituo cha nguvu, dhulma, ujeuri na unyang’anyi, basi wale waliopo chini ya sababu za mgandamizo wa kiroho, wa tamaa na uchu, tamaa yao itaongezeka na hatimaye sababu hizo za mgandamizo wa kiroho zitawagandamiza zaidi na kuwaongezea adhabu na maumivu. Hivyo yule ambaye mazingira ya Uadilifu ni mazito juu yake basi mgandamizo wa mazingira ya dhulma ni mzito zaidi juu yake. Ibnu Abi Hadid anasema kwamba: “Baada ya kuuawa Uthman watu walijumuika msikitini kushauriana kuhusu jambo la ukhalifa, na ilipoonekana
20
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 20
2/17/2017 1:24:28 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
kuwa hakuna mwingine atakayefuatwa na watu isipokuwa Ali B, huku wakati huo huo baadhi ya makhatibu wakiwahutubia watu kwa kuwatajia fadhila za Ali B katika Uislamu za hapo kabla, watu walisongamana kwenda kumpa kiapo cha utii Ali B.” Hakika maneno ya Ali B tuliyoyanukuu katika kurasa zilizotangulia, hakika aliyasema pindi watu waliposongamana kumpa kiapo cha utii, ili maneno hayo yawe hoja juu yao. Onyo muhimu: Ibnu Abi Hadid anasema kwamba: “Siku ya pili baada ya kuchaguliwa, alipanda mimbari msikitini na akagusia yale aliyoyasema siku iliyotangulia, akasema kuwa hataki ukhalifa uwe kama Ikulu na uraisi, akasema: “Hakika mimi nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu 2 akisema: ‘Hakika mwenye kushika hatamu ya mambo baada yangu, kitakuwa kirefu sana kisimamo chake juu ya Sirat na Malaika watakifungua kitabu cha matendo yake, hivyo ikiwa alifuata Uadilifu, basi bila shaka Mwenyezi Mungu atamuokoa kupitia Uadilifu huo, la sivyo ataingia motoni.” Kisha Imam B akawatazama watu waliokuwa wamemzunguka kuliani kwake na kushotoni kwake, kisha akasema: ‘Kwa hakika yule aliyepotezwa na dunia kwa mito na nga21
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 21
2/17/2017 1:24:28 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
mia...... bila shaka nitazichukua hizo kwao na kuzirudisha Hazina kuu ya Waislamu (Baytul-Mali), na wala sintowapa ila haki yao tu. Sitaki waje kusema kuwa hakika Ali amewasahau, na kwamba mwanzoni mwa jambo (ukhalifa) alisema kitu lakini sasa anatenda ambacho hakusema, na kwamba amekuja na kututenganisha na kila tunachokimiliki. Hakika mimi tangia sasa nawatangazieni njia yangu ya wazi.’ “Kisha akaendelea kuwafafanulia hilo. Na kwa sababu kulikuwa na watu waliokuwa wakijiona kuwa wana upendeleo maalumu kwa kuwa walikuwa sahaba wa Mtukufu Mtume na kuwa wao walitenda hili na lile katika njia ya Uislam, na wakahimili taabu na matatizo makubwa, aliwaambia: ‘Hakika mimi sikanushi ubora wa sahaba na mchango wao wa hapo kabla na huduma yao katika Uislamu, isipokuwa ni kwamba hakika mambo hayo malipo yake yapo kwa Mwenyezi Mungu na thawabu zake zipo Kwake. Lakini hayo hayahalalishi uwepo wa tofauti baina yao na wengine wala hayo si sababu ya upendeleo.”’ Mwanzo wa manung’uniko na kujitenga naye: (Ibnu Abi Hadid) anasema kwamba: “Na siku nyingine walikuja wale waliokuwa wakijua kwamba 22
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 22
2/17/2017 1:24:28 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
watadhibitiwa na serikali ya Ali B, wakajitenga pembeni na kuanza kushauriana wao kwa wao, kisha wakamtuma mwakilishi wao Walid bin Uqba bin Abu Mu’it, akasema: ‘Ewe Abal-Hasan, hakika unaelewa kwamba hakika sisi tuliyopo hapa hatukupendi kwa sababu ya yale tuliyotanguliza pamoja nawe katika vita vya Kiislamu, kwani wengi wetu ni kati ya wale waliouawa kwa mkono wako, lakini sisi tunafumbia macho hayo na tunakupa kiapo cha utii kwa masharti mawili: Usiunganishe yale yaliyotangulia, usitazame yale yaliyopita, na unaweza ukatenda utakalo baada ya hayo. Pili, utukabidhi wale waliomuuwa Uthman ili tulipize kisasi kwao. Usiporidhia lolote kati ya hayo mawili hatutakuwa na uwezo ila kujiunga na Muawiya huko Sham.”’ Ibnu Abi Hadid anasema kwamba: “Imam Ali B alimjibu: ‘Ama damu iliyomwagwa hapo mwanzo haikutokana na chuki binafsi, bali ilitokana na tofauti zilizojitokeza katika akida na imani. Tulikuwa tukipigana katika haki huku wao wakipigana katika upotovu, na hatimaye haki ikaishinda batili. Ikiwa malalamiko yenu ni juu ya hilo na mnataka fidia yao basi pelekeni ombi lenu kwa Mwenyezi Mungu kwa nini aliiangusha batili na kuiangamiza. Ama ombi lenu la kwamba nisamehe yaliyotangulia, hilo sintaweza, 23
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 23
2/17/2017 1:24:28 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
hakika hilo ni haki ya Mwenyezi Mungu aliyoiweka kwangu. Ama kuhusu wauwaji wa Uthmani, lau ningelikuwa najua lanihusu mimi, ningelipa kisasi mimi mwenyewe kwao.”’ Walid aliposikia jibu hili la kukinaisha, alirudi kwa jamaa zake na kuwajulisha hali, ndipo wakaondoka na hali wakiwa wameazimia kumkhalifu na kumfanyia uadui, na hatimaye wakatangaza hilo. Ombi la wafuasi: Ibnu Abi Hadid anasema kwamba: “Baadhi ya wafuasi wa Ali B walipopata habari kwamba kuna kundi la watu linapinga uongozi wa Imam B, na limeanza harakati za kuuangusha na kuwashawishi watu, walimwendea Imam B na kumueleza kwamba: Sababu kubwa ya manung’uniko na kutoridhika kwa watu hawa ni ule ung’ang’anizi wako katika kutimiza haki na usawa baina ya watu. Kadhia ya mauaji ya Uthman si chochote ila ni njia tu ya kuwachochea na kuwashawishi watu wenye upeo finyu.” Ibnu Abi Hadid anasema kwamba: “Baadhi wanasema kwamba Malik al-Ashtar alikuwa miongoni mwa watu hao, na kwamba ndiye aliyetoa maoni ya kumtaka atizame upya msimamo wake. Ali B aligundua 24
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 24
2/17/2017 1:24:28 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
kwamba fikra hii lazima itakuwa imeenea katika nyoyo za watu, na wao vilevile wanataka alegeze msimamo wake katika kuutimiza Uadilifu, hivyo aliondoka na kuelekea msikitini kwa lengo la kuwahutubia watu. Alikuwa kavaa joho lake huku kashika upanga wake. Alipanda mimbari na akaegemea upanga wake na akaanza hotuba yake kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu na kumsifu kwa neema zake zote zinazoonekana na zisizoonekana, kisha akasema: ‘Hakika mtu aliye mbora kushinda watu wote mbele ya Mwenyezi Mungu ni yule amchaye Mwenyezi Mungu kushinda watu wote, afuataye Sunna ya Mtume Wake 2 kushinda watu wote na ahuishaye Kitabu Chake kushinda watu wote.’ Na akasema: ‘Mtu yeyote hawi mbora kushinda mwingine ila kwa kipimo cha utiifu na uchamungu, na hakika Qur’ani ipo mbele yetu, na ni hii hapa Sunna ya Mtume wa Mwenyezi Mungu baina yetu, imejengwa juu ya Uadilifu na usawa, na hilo halikufichikana kwa yeyote, ila yule aliye na malengo yake binafsi na ubishi, na hilo ni jambo jingine. “Enyi watu ! Hakika sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekufanyeni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni (yule) aliye mchamungu zaidi katika nyinyi. (Sura Hujurat: 13)’ Na hakusoma Aya hii ila ni ili awaambie 25
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 25
2/17/2017 1:24:28 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
kuwa kwa mujibu wa Aya hii upendeleo wa aina yoyote ile umeondolewa.” Amri ya kurejesha mali: Ibn Abi Hadid anakariri kauli ya Imam B: “Wallahi hata ningezikuta zimetumika zikiwa mahari kwa kuolea wake, na vijakazi wamemilikiwa kwazo, ningezirudisha.” Na anasema (Ibn Abi Hadid): “Hakika alitekeleza alilowaahidi, akarejesha mali za umma toka kwao ila toka kwa yule ambaye hakuwepo au alikimbilia mbali ambapo mkono wa dola yake haukuweza kufika. Hakika kanuni ya kuunganisha yaliyopita au kanuni ya kurejesha mambo yanayohusiana na haki za umma, inatokana na msingi usemao: ‘Hakika haki ya kale haibatilishwi na chochote.’” Haki daima ni hai haiondolewi na mpito wa wakati. Barua ya Amru bin ‘Aas kwenda kwa Muawiya: Katika barua hii ya Amru bin ‘Aas kwenda kwa Muawiya, mlikuwa na: “Ikiwa hujatenda basi tenda kabla ya mwana wa Abu Talib hajakutenganisha na kila unachokimiliki kama uchunavyo maganda toka kwenye fimbo.”
26
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 26
2/17/2017 1:24:28 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
Uadilifu wake ndio uliomsababishia kuuawa: Maneno haya: “Aliuawa kishahidi mihrabuni kwa sababu ya ukamilifu wa Uadilifu wake,” yanamaanisha hili tulilolisema. Na kutokana na hilo inabainika wazi kwamba mambo mengine yote kama vile kuwakabidhi wauwaji wa Uthman na yale yaliyotokea katika vita vya Uislamu dhidi ya mushrikina, yalikuwa ni kisingizio tu, bali ukweli wa mambo ni kwamba chanzo hasa ni kule kutekeleza haki na kutimiza Uadilifu wa kijamii, na hasa kwamba Imam B hakukubali ulazima wa kufumbia macho yale yaliyopita, bali alikuwa akiona kwamba: ‘Hakika haki ya kale haibatilishwi na chochote.’ Ali B na ukhalifa: Kwa kumalizia nawatajia baadhi ya kazi zake alizokuwa akizitilia mkazo na kusisitiza yeye mwenyewe. Imam B hakuwahi kuiruhusu nafsi yake au kumruhusu mtu yeyote katika familia yake wala wafuasi wake kukitumia vibaya cheo chake cha ukhalifa, wala hakuridhia kutumia upendeleo sahihi ambao watu wenyewe kwa hiari yao walikuwa wakimpa, hivyo alikuwa aendapo sokoni kununua kitu, huenda kununua kwa yule asiyemtambua kuwa ni Khalifa na kiongozi wa waumini, ili 27
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 27
2/17/2017 1:24:28 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
kwamba asimpunguzie bei na hatimaye kumtofautisha na mwingine. Hadi hapa utaona kwamba hakuwa anataka kufaidika na cheo chake kama Khalifa wa Waislamu. Hakika kwa mtu ambaye anatekeleza wajibu wake na hapendi kutumia vibaya cheo chake, nafasi za kijamii si haki miongoni mwa haki zake, bali ni wajibu na dhamana aliyonayo. Hakika kuna tofauti baina ya haki na wajibu, kwani haki ni kufaidika na kunufaika. Ama wajibu ni dhamana na jukumu, hivyo tukiacha kutumia vibaya nafasi zetu za kijamii basi hatutaweza vyeo hivyo kuviita kuwa ni haki, bali ni wajibu juu yetu kuviita kuwa ni wajibu na dhamana. Hivyo tunapotaka kuchunguza baadhi ya vyeo juu ya kundi fulani au mtu fulani, ni wajibu juu yetu kusema: ‘Je wajibu huu unamfaa au la?’ Na si kusema: ‘Je hii ni haki yake au la?’ tukifanya hivyo sura nzima ya kadhia itabadilika. Kwa mfano tunapasa kusema: ‘Hakika uaskari ni wajibu si haki.’ Na kwa mtazamo huu tutasema: ‘Askari ana wajibu.’ Hivyo ili vyeo visitumiwe vibaya na kila mmoja atekeleze kazi yake ipasavyo ni lazima iwe wazi kwamba vyeo vyote ni wajibu na si haki. Pia ni kwamba hakika masharti ya wajibu si masharti ya haki. Hakika uongozi ambao Imam Ali B hakutaka
28
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 28
2/17/2017 1:24:28 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
kuutumia vibaya ulikuwa ni wajibu na si haki, kwa sababu wajibu ukiutumia katika njia isiyo sahihi, unaweza kujikuta unauita kimakosa kuwa ni ‘haki’. Kwa mfano, tunajua kwamba sala ni wajibu asilimia mia moja, lakini mtu akiitumia vibaya kwa kuifanya njia ya kujinufaishia kinyume na sheria, basi sala hiyo kwa mtazamo wa mtu huyo, au imamu huyo wa jamaa, inaweza kuonekana kuwa ni haki yake, tena haki kubwa,1 na si wajibu na dhamana, ilihali ukweli wa jambo ni wajibu na dhamana na wala si haki. Tukimtizama Ali B ambaye hataki kutumia cheo chake, kiasi kwamba ili kukwepa kutumia vibaya cheo chake anamtafuta mchuuzi asiyemtambua kuwa yeye ni Khalifa ili asipunguziwe bei kwa msukumo wa cheo chake, tutaona kuwa ukhalifa kwake yeye ulikuwa ni wajibu na si haki. Ni wajibu ambao hakuna wajibu mkubwa kushinda huo, bali ni mkubwa kushinda hata mazoezi ya nafsi yake. Katika siku za joto kali, alikuwa Ni kweli kisu kimegusa mfupa. Mtazamo huu ndio unaosababisha migogoro misikitini, na hatimaye watu kufika katika hali ya kugombania uimamu wa msikiti na hata kurogana na kufitiniana. Hayo yote ni kwa sababu mtu anaona nafasi aliyonayo msikitini ni haki yake ambayo haipasi mwingine kuiingilia. Wakati ukweli ni kwamba si haki bali ni dhamana na wajibu na utumishi aliokabidhiwa tu. Imefika wakati tubadilike na kuleta maendeleo ya kiroho na kijamii katika jumuiya zetu na hasa misikitini, tutekeleze wajibu na kuacha chuki, fitina na ung’ang’anizi kwa maslahi binafsi. – Mhariri.
1
29
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 29
2/17/2017 1:24:28 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
akitoka nje ya jengo la makao yake makuu na kuketi kivulini, akichelea kwamba huenda akatokea mwenye haja wakati wa joto hilo kali la jua na asimkute. Kwa hakika haya yote ni mazoezi ya nafsi na ndio wajibu mzito na mgumu kushinda wajibu zote. Imam alipompa ugavana wa Hijaz Qutham bin Abbas alimwambia katika barua yake: “Watengee vipindi viwili, mpe fatwa mwenye kuhitaji fatwa, mwelimishe mjinga, mkumbushe aalimu, na wala usiwe na balozi kwa watu ila ulimi wako, wala kizuizi ila uso wako.” Imam B anamwandikia pia Malik al-Ashtar kwamba: “Watengee wenye haja toka kwako fungu ambalo humo utawagawia utu wako na utaketi nao kikao cha pamoja, humo unyenyekee kwa ajili ya Mwenyezi Mungu aliyekuumba, na humo uwaweke mbali wanajeshi wako, wasaidizi wako, walinzi wako na askari wako ili mwenye kuzungumza nawe azungumze kwa uhuru bila ya kuogopa. Kwani hakika mimi nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu 2 akisema zaidi ya sehemu moja: ‘Kamwe umma hautatukuka mpaka pale haki ya mnyonge itakapochukuliwa toka kwa mwenye nguvu bila uoga wowote.’” Imam anaendelea kueleza kuhusu hali ya kiongozi
30
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 30
2/17/2017 1:24:28 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
kuwa mbali na watu: “Tahadhari sana usijifiche kwa muda mrefu mbali na raia wako, kwani ni ukweli usiokuwa na shaka kwamba viongozi kuwa mbali na raia wao ni alama ya dosari katika uongozi.”
31
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 31
2/17/2017 1:24:28 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
UADILIFU KATIKA UISLAMU
L
Sababu iliyowapelekea Waislamu kujitenga mbali na Uadilifu wa Kiislamu:
inapokuja swali: Kwa nini Uadilifu haujafuatwa, pamoja na kuwa Uislamu umetilia mkazo msingi huu miongoni mwa misingi ya dini, na kwa nini baada ya Mtume 2 kuondoka haukupita muda mrefu umma na jamii ya Kiislamu ikapatwa na hali mbaya mno ya dhuluma, ukosefu wa Uadilifu na ubaguzi? Wakati swali kama hilo linapoulizwa, akili huenda mbio kwa kutafakari, na jambo la kwanza itakalolikimbilia ni kwamba, haya yote yanawaangukia baadhi ya makhalifa waliozuia katiba hii ya Kiislamu isifanye kazi, na hiyo ni kwa sababu ufanyaji kazi wa katiba hii ulipasa kuanzia kwa makhalifa wa Waislamu na viongozi wao, lakini hawa walikuwa na nia mbaya na hawakuwa na sifa za kuwakilisha cheo hiki kikubwa, hivyo wakasimama kidete kuzuia Uadilifu usifanye kazi, na matokeo yake ni jamii ya Kiislamu kupatwa na aina mbalimbali za dhuluma na ubaguzi baina ya watu. Hakika jibu hili ni sahihi, hakika moja ya sababu ni kwamba wale wenye jukumu la kutekeleza Uadilifu
32
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 32
2/17/2017 1:24:28 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
hawakuutekeleza, bali walitenda dhidi yake. Historia ya watawala wa Kibani Umaiyyah na Kibani Abbas ni dalili tosha na bora juu ya hilo. Tafsiri mbaya ya Uadilifu: Lakini si kama hilo tu ndilo sababu, bali pia kuna sababu nyingine kubwa, na hata kama haikuwa na athari kubwa lakini kwa uchache ilikuwa na athari, na hili ndilo nataka kulizungumzia katika maudhui hii. Na sababu hii kubwa ni kwamba baadhi ya ulamaa wa Kiislamu walitoa tafsiri potofu ya Uadilifu katika Uislamu, na ijapokuwa baadhi ya ulamaa walisimama kidete dhidi ya tafsiri hiyo ya kimakosa lakini walishindwa. Hakika kanuni muhimu kama Uadilifu ni lazima itafsiriwe kwa maana nzuri inayostahili, na pili inatakikana iwekwe katika sura ya utekelezaji sahihi. Hiyo ni kwa sababu iwapo haitatafsiriwa kwa tafsiri sahihi, basi wale wanaotaka kuitekeleza kiusahihi hawataweza kutimiza hilo, kwa sababu utekelezaji wake unategemea tafsiri yake. Na ikiwa hawataki kuitekeleza ipasavyo basi tafsiri hiyo ya kimakosa itawasaidia katika azma yao. Hakika wafasiri wa kanuni yoyote ile wakiitafsiri kulingana na matakwa mabaya 33
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 33
2/17/2017 1:24:28 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
ya watekelezaji, bila shaka watakuwa wamewasaidia, wamewatumikia na kuwatia nguvu, hiyo ni bila kujali kwamba katika kutoa tafsiri hiyo ya kimakosa walikuwa wamekusudia kuisaliti jamii au la, muhimu ni kwamba wameifasiri kanuni kimakosa. Na hili ndilo lililotokea katika kuitafsiri kanuni ya Uadilifu. Hakika aghlabu ya wale waliokanusha Uadilifu kuwa katika misingi ya Uislamu, na huenda ni wote, hawakuwa na nia mbaya katika tafsiri yao hiyo, bali ni kwamba mtazamo usiokuwa wa kina na wa kimapokeo ndio uliowadumbukiza Waislamu katika hali hii, na hivyo hali hiyo ikausababishia Uislamu misiba miwili: Msiba wa kwanza: Nia mbaya katika utekelezaji, hiyo ni kwa sababu tangu mwanzo ukhalifa haukuwekwa katika kipimo sahihi, Waarabu walifadhilishwa kushinda wasiokuwa waarabu, makurayshi wakafanywa wabora kushinda makabila mengine, na mikono ya wengine ikaachwa huru juu ya haki na mali za umma huku mingine ikizuiliwa, mpaka alipochukua Ali B ukhalifa kwa lengo la kupiga vita upotokaji huu, jambo ambalo lilikomea kwa Ali B kufa kishahidi, kisha jambo la ukhalifa likaangukia mikononi mwa Muawiya na wale makhalifa waliokuja baada yake.
34
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 34
2/17/2017 1:24:29 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
Ama msiba wa Pili ni ule uliotufika kupitia mikono ya ulamaa wenye fikra ndogo isiyo ya kina, ambao waling’ang’ania fikra butu, na hivyo wakawa wanautafsiri Uadilifu kwa tafsiri potovu ambayo athari zake zimedumu ndani ya jamii hadi leo hii. Asili ya mjadala ni theolojia: Kanuni hii ya kijamii ina mzizi unaorejea kwenye elimu ya theolojia. Hakika elimu hii ya theolojia ilidhihiri katika nusu ya pili ya karne ya kwanza ya Hijriya, pale baadhi ya watu walipoanza kufanya uchunguzi na utafiti kuhusu misingi ya dini na yanayohusiana na tawhidi, sifa za Mwenyezi Mungu, taklifu na Kiyama, hivyo watu hawa wakapewa jina la Mutakalimuna (Wazungumzaji). Kuna kauli mbalimbali kuhusu sababu kuu iliyopelekea wao kuitwa kwa jina hili. Baadhi wamesema kwamba sababu inarejea kwenye kadhia muhimu iliyowashughulisha watu hawa muda mrefu, nayo ni kuchunguza kadhia ya kuumba au kutokuumbwa kwa Qur’ani tukufu ambayo ni maneno ya Mwenyezi Mungu. Wengine wanasema: Hakika hawa ndio walioipa fani yao hii jina hili al-Kalam (maneno), mkabala na 35
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 35
2/17/2017 1:24:29 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
fani ya mantiki ambayo ilikuwa ni punde tu imedhihiri. Hivyo walikuwa wanataka jina lililo sawa na mantiki katika maana, ambapo mantiki ni kutamka, hivyo wakachagua al-Kalam, neno ambalo humaanisha kauli. Baadhi wamesema kuwa ilipokithiri mizozo, mijadala na maneno, ndipo walipoitwa Mutakalimuna (Wazungumzaji). Vyovyote vile itakavyokuwa ni kwamba kuna kundi lilidhihiri chini ya jina hili. Uadilifu wa kiungu: Miongoni mwa maswala yaliyojadiliwa sana na wanatheolojia wa Kiislamu ni suala la Uadilifu wa kiungu. Je Mwenyezi Mungu ni mwadilifu au la? Swala hili lilikuwa na umuhimu mkubwa kiasi kwamba limezaa mambo mengi, na hatimaye mwisho likafikia kwenye kanuni ya Uadilifu wa kijamii, ambao hasa ndio maudhui yetu. Suala hili lililishinda hata suala la je Qur’ani imeumbwa au haikuumbwa, suala ambalo lilizua machafuko makubwa na umwagaji mwingi wa damu. Wasomi wanaojadili Uadilifu wa Mwenyezi Mungu wamegawanyika katika makundi mawili: Wanaokubali fikra ya Uadilifu wa Mwenyezi Mungu, na wasiokubali fikra hii. Kwa sura ya jumla ni kwamba Mashia ni wafuasi wa fikra ya Uadilifu wa Mwenyezi Mungu, na 36
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 36
2/17/2017 1:24:29 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
kwa ajili hii tangu kale wanajulikana kwa msimamo wao wa kwamba misingi ya dini ni mitano: Tawhidi, Uadilifu, Unabii, Uimamu na Marejeo. Yaani kwa upande wa maarifa ya Kiislamu wao ndio wanaoona kuwa Uislamu una misingi mitano. Katika maudhui hii ya Uadilifu wa kiungu, yanazungumziwa mambo mawili: La kwanza ni: Je! Uumbaji wa ulimwengu na vilivyomo kuanzia mbingu, ardhi, mimea, wanyama, dunia na Akhera yake vimeumbwa kwa kufuata vipimo vya Uadilifu? Na je hakuna kiumbe chochote kilichoguswa na dhuluma katika kuumbwa? Na je ulimwengu huu umesimama juu ya Uadilifu? “Je mbingu na ardhi zimesimama kupitia Uadilifu?� Au ukweli ni kwamba Mwenyezi Mungu Mwenye utashi usio na kizuizi, utashi Wake hauzuiliwi na chochote, hufanya atakalo na huhukumu atakavyo, na hivyo anachokiumba haiwezekani kifuate kanuni na kipimo, bali alifanyalo Mwenyezi Mungu ndio Uadilifu kwa kuwa Mwenyezi Mungu hutenda linalooana na Uadilifu. Kwa ajili hii, iwapo siku ya Kiyama Mwenyezi Mungu atampeleka huyu peponi na yule motoni, je itakuwa ni kwa mujibu wa vipimo na kanuni za Uadilifu au la? Hawa wanasema si hivyo, kwani
37
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 37
2/17/2017 1:24:29 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
hakuna kanuni yoyote inayoweza kutawala kitendo cha Mwenyezi Mungu, bali ni kwamba kila kanuni inafuata kitendo chake na amri zake, ikiwemo Uadilifu na dhuluma. Hivyo akimwingiza mtiifu peponi na aasi motoni huo ndio Uadilifu kwa kuwa Mwenyezi Mungu ndiye mtendaji. Hakika utashi Wake na kitendo Chake havifuati kipimo wala havifuati kanuni, kila kanuni na kila kipimo hufuata utashi Wake. Sehemu hii ya kwanza ilikuwa ikihusu asili ya Uadilifu katika uumbaji wa viumbe na muundo wa ulimwengu, je hayo yote yalitekelezwa kwa mujibu wa Uadilifu au la? Ama sehemu ya pili, yenyewe inahusiana na sheria na desturi za kidini, sheria za Mwenyezi Mungu zilizoletwa na Mtukufu Mtume 4 na zikapewa jina la ‘Sheria za Kiislamu’, je sheria hizi zina hali gani katika Uadilifu? Je utaratibu wa sheria unafuata vipimo vya Uadilifu au la? Katika kuwekwa sheria hizo je kulizingatiwa kigezo cha Uadilifu au la? Na je kila sheria inatokana na masilahi au uharibifu wa asili au la? Tunapozitazama sheria za Kiislamu tunapata kwamba baadhi ya mambo yameruhusiwa, bali mengine ni wajibu, na mambo mengine yameharamishwa na kuzuiliwa, mfano, uaminifu na ukweli ni katika mambo
38
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 38
2/17/2017 1:24:29 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
yaliyo ya wajibu, ambapo udanganyifu, usaliti na dhuluma ni miongoni mwa mambo yaliyokatazwa na kuharamishwa. Hakuna kigezo cha kusema kwamba yale tuliyoamrishwa kutenda ni mema, na yale tuliyokatazwa ni mabaya. Lakini swali ni kwamba je zuri ni zuri kwa asili na baya ni baya kwa asili na hivyo la kwanza likaamrishwa na la pili likakatazwa, au ni kwamba zuri halijawa zuri ila kwa sababu tu Uislamu umeamuru hilo, na baya halijawa baya ila kwa kuwa tu Uislamu umekataza hilo? Hivyo lau angeamuru kinyume, kwa mfano angeamuru uongo, usaliti na dhuluma basi vitu hivi vingekuwa vyema, na kama angekataza ukweli, uaminifu na Uadilifu vitu hivi vingekuwa vibaya? Sheria ya Uislamu inasema kuuza na kununua ni halali, na riba ni haramu, na hakuna shaka kwamba kuuza na kununua ni jambo jema na riba ni jambo baya. Lakini ni je uzuri wa kuuza na kununua ni wa asili wenye manufaa kwa watu, na kwa ajili ya manufaa hayo kumehalalishwa na Uislamu, na kwamba ubaya wa riba ni wa asili wenye kuwadhuru watu na jamii kwa jumla, na kwa ajili ya ubaya huo Uislamu umeharamisha riba na kusema: “Wale wanaokula riba hawatasimama ila kama anavyosimama yule ambaye shetani humpoozesha kwa kumshika�? Au ni kinyume na 39
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 39
2/17/2017 1:24:29 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
hivyo na kwamba kuuza na kununua ni jambo zuri kwa kuwa tu Uislamu umelihalalisha, na kwamba riba ni jambo baya kwa kuwa tu Uislamu umeliharamisha? Uzuri na ubaya wa kiakili: Kutokana na hayo kulijitokeza makundi mawili baina ya Waislamu, kundi moja likashikamana na upande wa uzuri na ubaya wa kiakili, likasema: Hakika amri za Mwenyezi Mungu zinategemea uzuri na ubaya, masilahi na uharibifu wa asili wa vitu. Na kundi lingine likakanusha uzuri na ubaya wa kiakili wa asili wa vitu, likasema: Hakika uzuri wa kitu au ubaya wake unatokana na sheria. Na katika kuzungumzia Uadilifu na dhuluma juu ya haki za watu na miliki zao, mambo ambayo ni miongoni mwa maudhui za kijamii, kulizuka mvutano, na kwa mujibu wa rai ya wanaokubali fikra ya Uadilifu wa Mwenyezi Mungu ni kwamba katika hali halisi kulikuwa kuna haki na mwenye haki, na kulikuwa kiasili kuna anayepasa kuichukua haki hiyo, kama ambavyo kiasili kulikuwa kuna yule asiyepasa kuchukua haki hiyo, kisha Uislamu ukaja na kuweka sheria katika namna ambayo kila mwenye haki ataifikia haki yake. Yaani Uislamu umeweka kanuni zake na sheria zake 40
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 40
2/17/2017 1:24:29 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
kulingana na haki na Uadilifu, hivyo Uadilifu maana yake ni kumpa kila mwenye haki haki yake. Hivyo haki na Uadilifu ni miongoni mwa mambo yenye uhalisia uliyopo ambao hata kama Uislamu usingeamrisha hilo uhalisia wake usingebadilika. Ama kwa mujibu wa kundi la pili ni kwamba haki, mwenye haki, dhuluma na Uadilifu, haya ni mambo yasiyokuwa na uhalisia wa asili, bali ni kwamba Mwenyezi Mungu ndiye awekaye kanuni. Hawa wanaamini kwamba kama ambavyo muundo wa ulimwengu ni kazi ya Mwenyezi Mungu na uzao wa utashi wa Mwenyezi Mungu usiokuwa na kizuizi, na wala haufuati kanuni wala mpangilio wa kanuni yoyote, ni hivyo hivyo sheria nayo haifuati kanuni yoyote miongoni mwa kanuni, hivyo kila kanuni inayowekwa na Uislamu ni haki, yaani ndipo inapokuwa haki, hivyo Uadilifu ni kile kipitishwacho na Mwenyezi Mungu. Uislamu ukitaka kupitisha kwamba anayetenda na kutaabika katika uzalishaji hana haki ya chochote katika alilolizalisha, na kwamba haki ni ya yule ambaye hakuhusika na chochote wala hakutaabika au hakuchoka, basi wakati huo inakuwa ni haki, yaani mwenye haki ni huyu ambaye hakutaabika kwa chochote na si yule aliyetaabika.
41
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 41
2/17/2017 1:24:29 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
Athari ya kivitendo na kijamii ya uzuri na ubaya: Baadhi ya watu wanaweza kujiuliza: Suala la kujadili kadhia ya uzuri na ubaya lina faida gani kivitendo? Kwani makundi yote mawili yanaamini kwamba kanuni za Kiislamu zinazohusu jambo lolote zinafaa na kuafikiana pamoja na haki na Uadilifu. Na kwamba muhtasari wa kadhia ni kwamba kundi moja linaamini kuwa uzuri, ubaya, faida, madhara, haki na batili ni vitu vilikuwepo tangu kabla, kisha ndipo mweka sheria akaja na kuweka kanuni kulingana na mambo hayo. Na kundi lingine linaamini kuwa mambo haya yote (uzuri, ubaya, faida, madhara, haki na batili) hayakuwepo hapo kabla bali yameletwa na sheria za kidini. Hivyo baadhi wanasema uzuri, ubaya, haki, batili, Uadilifu na dhuluma ndio kigezo cha sheria za kidini. Na wengine wanasema kwamba dini ndio kigezo cha hayo. Na ni kwamba hakuna tofauti, sawa usahihi uwe ni kauli ya kwanza au ya pili, tija ni moja, na kwa ajili hii ndio maana ulamaa wa makundi yote mawili pindi wanapodadisi masuala ya kifiqhi na ya misingi ya sheria, hudadisi maudhui ya maslahi yaliyomo ndani ya sheria. Katika kujibu swali na hoja hiyo nasema: Jambo halikomei hapo tu, kwani jambo hilo lina athari muhimu ya kivitendo ambayo huiingiza akili
42
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 42
2/17/2017 1:24:29 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
na elimu katika mchakato wa kupata maamuzi ya Kiislamu. Hivyo lau tukichukua nadharia ya awali inayosema haki, Uadilifu, uzuri na ubaya ni mambo yaliyokuwepo tangu kabla, na kwamba mweka sheria za Kiislamu aliziweka kwa kuzingatia vigezo hivyo, basi tunapokutana na jambo ambalo liko wazi kiakili na kielimu kuwa ni haki na ni Uadilifu, au ni uzuri au ni ubaya, ni lazima tusimame na kuikubali akili iongozayo kwa kuwa imeweza kutofautisha faida na hasara, na hapo tutashikamana na kanuni ya wanaokubali fikra ya Uadilifu wa Mwenyezi Mungu, kanuni isemayo: “Kila kinachohukumiwa na akili (kuwa ni faida, au hasara, au uzuri au ubaya) huhukumiwa hivyo hivyo na sheria.” Au “Wajibu za kisheria huzunguka ndani ya wajibu za kiakili.” Tutaifuata akili hata kama kuna dalili ya kinukuu inayoikhalifu. Hiyo ni kwa sababu sisi tunaamini uwepo wa lengo na shabaha katika sheria za Uislamu, na kwamba Uislamu una lengo maalumu na kuwa hauwezi kwenda kinyume na lengo lake, hivyo tunakwenda pamoja na lengo hilo, na wala hatufuati sura na miundo ya kadhia. Hivyo tunapojua tu kuwa riba ni haramu na kwamba haijaharamishwa bila sababu, basi tunajua pia hata kama itabadilishwa katika sura na miundo mbalimbali bado uharamu wake utakuwepo hautaondoka. Riba ni riba tu, wizi ni wizi 43
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 43
2/17/2017 1:24:29 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
tu, dhuluma ni dhuluma tu na uporaji ni uporaji tu, hata kama vitakuwa vimewekwa ndani ya vazi la haki na Uadilifu. Ama kulingana na mtazamo wa pili, ni kwamba akili haiwezi kuwa kiongozi, kwani msingi unaoweka kanuni za Kiislamu kwa mujibu wa nadharia hiyo si mmoja kiasi kwamba uwe ni kanuni ya msingi. Kila kitu kina sura yake na muundo wake, na kila kitu kinabadilika sura na muundo. Ndio ni sahihi kwamba kwa mujibu wa nadharia hii twaweza kuzungumzia haki, Uadilifu, maslahi na kutanguliza maslahi mbele. Lakini ni maneno tu yasiyo na uhalisia katika uwelewa wa kweli, kwani ni sura na miundo ndio iliyopewa jina la haki na Uadilifu na si uhalisia wenyewe. Hivyo kwa mujibu wa nadharia ya awali haki na Uadilifu na maslahi ni vitu vyenye uhalisia vyenye kuonekana. Ama kwa mujibu wa nadharia ya pili ni dhana za kuwazika tu. Hakika moja ya sababu za kupotoka kwa watu wa zama za kabla ya kuja kwa Uislamu ni kule kutokuwa na akili ya kuweza kutambua kati ya mazuri na mabaya, kwao wao mabaya na mazuri yote walikuwa wakiyaweka ndani ya kapu moja kwa jina la dini, wanayaita kwa jina la kidini na kisharia. Na hili ndilo ambalo Qur’ani inawakosoa kwa kusema:
44
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 44
2/17/2017 1:24:29 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
ْاح َشةً قَالُوا َو َج ْدنَا َعلَ ْيهَا آبَا َءنَا َوللاهَّ ُ أَ َم َرنَا بِهَا ۗ قُل ِ ََوإِ َذا فَ َعلُوا ف ْإِ َّن للاهَّ َ اَل يَأْ ُم ُر بِ ْالفَحْ َشا ِء ۖ أَتَقُولُونَ َعلَى للاهَّ ِ َما اَل تَ ْعلَ ُمونَ قُل ۖ ْط ِ أَ َم َر َربِّي بِ ْالقِس “Na wanapofanya uchafu husema: Tumewakuta nayo baba zetu, na Mwenyezi Mungu ametuamrisha hayo. Sema: Hakika Mwenyezi Mungu haamrishi machafu: Je, mnasema juu ya Mwenyezi Mungu msiyoyajua? Sema: Mola Wangu ameamrisha uadilifu.” (Qur’ani Sura A’araf 7:28-29)
Kwa hakika iliwapasa watu hawa kuutambua ubaya kuwa ni ubaya kiasili, hivyo Mwenyezi Mungu hawezi kamwe kuamrisha ubaya. Hakika ile kuwepo ubaya tu yatosha kuonyesha kwamba hakika Mwenyezi Mungu hawezi kuamrisha jambo hilo. Uasharati hauwi utawa wala utawa hauwi uasharati, kwa sababu ni mambo mawili ambayo kila moja lina uhalisia wake, hivyo uasharati haugeuki na kuwa utawa wala utawa haugeuki na kuwa uasharati kwa kuamrisha na kukataza. Kisha ni kwamba hakika Mwenyezi Mungu haamrishi uasharati na kuuridhia, bali Mwenyezi Mungu anaamuru Uadilifu na usawa. Yaani haya ndio mnayopasa kuyajua nyinyi wenyewe na kuyamaizi na kuyafanya kipimo cha kujua ni yapi 45
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 45
2/17/2017 1:24:29 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
anayoyaamrisha Mwenyezi Mungu na kuyaruhusu, na ni yapi anayokataza na kutoyaruhusu. Dalili nne walizoziegemea: Kutokana na hayo ni kwamba kikundi kinachokubali fikra ya Uadilifu kinasema kwamba dalili za kisheria ni nne: Qur’ani, Sunna, Ijmai na akili. Ama kulingana na wanaopinga fikra ya Uadilifu hawaihesabu akili kuwa ni katika dalili za kisheria, na wala haiwezi kutambulika kama moja ya msingi ya Ijtihad, bali wao wanaona nukuu ndio zinazofaa kuongoza kila kitu. Dalili za aibu: Ni mshangao ulioje mtu kusikia kwamba ndani ya Uislam kulitokea kundi lililojidai na kujiona kuwa wao ndio wako kwenye njia ya haki, na ambao waliziona nafsi zao kwamba hakuna katika waja wa Mwenyezi Mungu anayemcha kushinda wao. Na kwamba wao ndio wenye ibada nyingi zinazokwenda sawia na mafundisho au Sunna ya Mtume 2 mia kwa mia bila kukosea. Lakini ili wao wathibitishe maneno yao hayo katika kuukana Uadilifu wa Mwenyezi Mungu, iwe katika upande wa kimaumbile au upande wa sheria, hutegemea dalili ambazo hazina uzito wowote. Lakini 46
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 46
2/17/2017 1:24:29 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
wao huzitoa hizi ili tu kuukana Uadilifu katika uumbaji wa Mwenyezi Mungu, jambo linalochekesha. Wao hutoa mathalani mfano wa maumivu anayoyahisi mtu anapokuwa mgonjwa na vilevile mfano wa kuumbwa shetani. Wanasema kwamba lau kama ulimwengu huu ungelikwenda katika hali ya Uadilifu basi asingeuawa Ali bin Abu Talib ili nafasi yake ichukuliwe na mtoto wa zinaa Ziadi na Hujaj bin Yusuf, na mengineyo miongoni mwa mambo ya uumbwaji. Ama kuhusu sheria na kanuni zake, wao ili wathibitishe kuwa hakuna kanuni yoyote ya Kiislamu inayofuata kigezo cha faida, hasara, uzuri na ubaya, wamesema: Hakika sheria za Kiislamu zimeundwa ili tu kuzuia tofauti na migawanyiko ya watu na jamii. Na kwa sababu hii ndiyo maana kukawepo migongano iliyoko sasa katika desturi za kidini. Mara nyingi utapata kwamba mweka sheria anatoa sheria moja bila kujali tofauti, na katika hali nyingine si hivyo, kwani katika kadhia mbili zinazofanana kikamilifu kwa mfanano unaopasa sheria moja, unakuta ameweka sheria mbili zenye kupingana. Wamesema: Kwa nini Uislamu umetofautisha baina ya mume na mke, ukamruhusu mwanamume kuoa wake hadi wanne,
47
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 47
2/17/2017 1:24:29 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
ambapo mwanamke hakuruhusiwa ila mume mmoja? Au kwa nini umesema mwizi akatwe mkono ambao ndio ala ya uhalifu wake, lakini haukuamuru ulimi wa mwenye kudanganya ukatwe kwa kuwa nao pia ndio ala ya uhalifu wake? Na pia katika zinaa na makosa mengine. Kwa hakika ni aibu kubwa mtu kusoma katika historia ya Kiislamu kwamba kulikuweko watu waliojidai na kujiona kwamba wao ndio walioifuata Qur’ani kikamilifu ilihali wao ndio wa kwanza kukana hekima, Uadilifu na nidhamu ya uumbaji, na hatimaye kuiondoa hekima katika kanuni za Uislamu. Ushindi wa wakanushaji wa Uadilifu: Msiba mkubwa kushinda hilo ni kwamba baada ya mijadala, mabishano mengi, umwagaji damu na machafuko makubwa, hawa wenye kukanusha Uadilifu walishinda na kufaulu kwa sababu ya mazingira ya kisiasa ya zama hizo. Ushindi huo ulitimia mikononi mwa Mutawakkil al-Abbasiy, ambaye aliiunga mkono fikra hiyo, ima ni kwa kuwa ilikuwa inaafikiana na matakwa yake na ima ni kwa kuwa hakuwa anaijua vilivyo. Masuudiy anasema ndani ya kitabu chake MuruujudDhahab: “Ulipofika ukhalifa kwa Mutawakkil alitoa amri ya kuachwa mijadala yote ya kidini, na kuachana na hali iliyokuwepo katika zama za al-Mu’tasim na al48
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 48
2/17/2017 1:24:29 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
Wathiq. Akaamuru watu wawafuate mashekh na wanahadithi na kudhihirisha Sunna na jamaa.” Kama pia alivyozuia falsafa iliyokuwa imeenea baina ya watu, kwa hoja kwamba ni kati ya mijadala ya kiakili isiyoruhusiwa. Mwanzo wa kutumika neno ‘Sunni’: Inatupasa hapa kusema kwamba neno Sunni ni lile ambalo lilitumika mkabala na neno ‘Shia’, hapo kabla halikuwa likitumika kwa maana hii, bali lilikuwa likitumika kuwaita wale waliokuwa wakikanusha msingi wa Uadilifu, na uwepo wa uzuri na ubaya wa asili katika vitu. Hivyo kwa kuwa ni Mashia na Muutazila tu ndio waliokuwa wanakubali fikra ya Uadilifu wa Mwenyezi Mungu, kisha Muutazila katika zama za al-Mutawakkil wakatoweka na wakashindwa kusimama kama madhehebu yenye kujitegemea, na hivyo katika imani hiyo ya Uadilifu wa Mwenyezi Mungu hawakubakia ila wanatheolojia wa kishia tu, ndipo watu wakawa wanawaita wasiokuwa mashia kwa jina la Ahlus-Sunna au al-Jamaa. Kadhalika inatupasa tujue kwamba si kila mwanachuo wa kisunni aliyetokea baadaye kuwa alijiunga na madhehebu ya al-Ash’ariy, hapana si hivyo, 49
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 49
2/17/2017 1:24:29 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
bali kuna ulamaa wengi baada ya hayo waliikubali fikra ya Uadilifu wa Mwenyezi Mungu. Mwanachuoni mkubwa kama Zamakhshary ni mfano, na alikuwa ni wa upande wa Muutazila, yeye aliikubali fikra ya Uadilifu wa Mwenyezi Mungu na pia pamoja naye wapo wanachuoni wengine wengi wa Kisunni. Mwelekeo wa Umma: Watu wengi wa kawaida walipendelea rai ya hawa wakanushaji wa fikra ya Uadilifu wa Mwenyezi Mungu, kwa sababu jamii ilikuwa imeundwa juu ya misingi ya kukubali kila kitu bila kuhoji au kujadili, na kwa kuwa watu hawa wote hawakuwa wenye kutafakari na kutumia akili zao, basi walijawa na khofu na kuliogopa sana jambo hili la kutafakari na kutumia akili zao, kwani waliona jambo hili kuwa ni hatari kubwa kwao. Kwa hivyo kulingana na sura hii ya mtazamo wa watu wa kawaida, ikiwa tutasema kwamba: “Sheria ya dini haifuati kanuni za akili.� basi itakuwa ni aina moja ya utukufu na neema muhimu sana katika dini. Na kwa ajili hii watu wote wa kawaida walifurahia sana kitendo cha Mutawakkil kuondoa uhuru wa kutafakari, na wakaona ni kuihami dini na Sunna ya Mtume 4, hivyo ijapokuwa Mutawakkil alikuwa mtu fasiki, muovu na mdhalimu bado watu wengi walimpenda na kumfua50
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 50
2/17/2017 1:24:29 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
ta, mpaka wakatunga kaswida katika kumshukuru na kusifia kitendo hiki kwa kudai eti ni kuinusuru dini ya Mwenyezi Mungu. Watu wakafanya hafla siku hiyo aliyotoa amri ya kukataza, ambapo kwa ukweli ilikuwa ni siku ya msiba mkubwa wa kivitendo na kifikra ulioufika Uislam, msiba uliozuia uhai wa fikra huru za Uislamu. Mshairi mmoja alitunga shairi lake katika kumsifu Mutawakkil akisema: “Leo Sunna ya Mtume 4 imetukuka baada ya kudhalilika, leo Sunna ya Mtume 4 ni yenye kung’ara na kuvutia, yametupwa masanamu ya upotovu na uongo juu ya ardhi. Kwa hakika leo wamedhihirika wazushi na wameenda zao motoni milele pasi na kurudi. Hakika Mwenyezi Mungu kupitia mkono wa Mutawakkil mwenye kufuata Sunna ya Mtukufu Mtume na mwenye kushikamana nayo, ameichukua haki ya Waislamu toka kwa watu wa uzushi. Na hakika Mutawakkil ndiye khalifa wa kweli wa Mola wangu, mwana wa ami yake Mtume wa Mwenyezi Mungu, mbora kushinda Banu Abbas wote, na yeye ndiye aliyeinusuru dini na kuiokoa dhidi ya mfarakano. Mwenyezi Mungu ampe maisha marefu, akidumishe kivuli chake juu yetu na amneemeshe kwa siha iliyo bora, nami kutokana na nusra yake kubwa juu ya dini, namtakia ajira ya pepo, na Mola amweke karibu na Manabii.” 51
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 51
2/17/2017 1:24:29 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
Huu ndio mukhtasari wa namna ilivyokuwa historia ya kiislam kuhusu jambo hili la mijadala juu ya Uadilifu wa Mwenyezi Mungu, na hivyo ndivyo walivyoshinda wakanushaji wa fikra ya Uadilifu wa Mwenyezi Mungu. Na kutokana na kuenea athari ya fikra za wakanushaji wa fikra ya Uadilifu wa Mwenyezi Mungu ndani ya mawazo ya wanaokubali fikra ya Uadilifu wa Mwenyezi Mungu, msingi wa Uadilifu wa kijamii katika Uislamu nao pia umepatwa na msiba na hatimaye yamepatikana matokeo mabaya. Vita baina ya kudumaa kiakili na kupevuka kifikra: Ni wazi kwamba hayo yote yaliyojiri baina ya wale wanaokubali fikra ya Uadilifu wa Mwenyezi Mungu na wale wanaokana fikra hiyo yalikuwa ni vita baina ya akili zilizo dumaa na fikra zilizopevuka. Na la kusikitisha ni kwamba ushindi katika vita hivi ulikwenda kwa akili zilizodumaa, na kwa matokeo haya Ulimwengu mkubwa wa Kiislamu ukapatwa na hasara kubwa sana, si hasara ya kimali bali ni ile ya kiroho. Kwani mwanadamu ana hisia inayompelekea kutii na kunyenyekea mbele ya mambo ya kidini, na hivyo katika hali kama hiyo hujikuta anatii na kunyenyekea mbele ya mambo yasiyokubalika na dini, na matokeo yake huwa ni kui52
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 52
2/17/2017 1:24:29 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
angamiza dini yenyewe. Mtukufu Mtume 4 amesema: “Kwa hakika wameupasua mgongo wangu watu wawili: mjinga mwenye kujigamba na msomi muovu.” Au alisema: “Kwa hakika wameuvunja mgongo wangu watu wawili: mjinga mwenye kujigamba na msomi muovu.” Na akasema katika hadithi nyingine: “Mwenyezi Mungu anazo hoja mbili: Hoja ya nje na hoja ya ndani, hoja ya ndani ni akili, na hoja ya nje ni Manabii.” Ali B ni muhanga wa akili: Kwa hakika kisa hiki cha kuuawa kwa Imam Ali B kwa mtazamo huu, yaani mtazamo wa kutenganisha baina ya akili na dini, kina mafunzo na mazingatio. Ali B alipokuwa msikitini akisali alipigwa dhoruba, na kwa dhoruba hiyo akafa kishahidi. Ndio ni sahihi kwamba “Aliuawa kishahidi mihrabuni kwa sababu ya ukamilifu wa Uadilifu wake.” Hapana shaka kwamba ukakamavu na kutolegea kwake katika kusisitiza Uadilifu ndio chanzo cha kuwa na maadui, na ndio chanzo cha kupigwa vita katika vita vya Jamal na Siffyn. Lakini ukweli ni kwamba ujinga na kudumaa kwa akili na mawazo kulidhihirika toka kwa watu ambao waliitwa kwa jina la Makhawariji, na hao wakampelekea Ali B kupata baraka ya muhanga.
53
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 53
2/17/2017 1:24:29 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
Makhawariji: Katika vita vya Siffin kulizuka kadhia ya suluhu, na kutokana na kadhia hiyo baadhi ya wafuasi wa Ali B wakamuasi na kutoka nje ya utii wake, na hao ndio walioitwa Makhawariji. Upanga uliopasua kichwa cha Ali B ulikuwa mikononi mwa mmoja wao, na hawa ni kundi linalonasibika na Uislamu, nao kwa mujibu wa itikadi yetu ni makafiri, lakini wao walikuwa wakijiona kuwa ni Waislamu, bali zaidi ya hapo walikuwa wakiona kwamba hakuna mwislamu zaidi yao, na kwamba wengine wote waliobaki wameritadi. Hakika ni kwamba hakuna mtu aliyesema kuwa Makhawariji hawaamini Uislamu, bali wote tunakiri kwamba wao walipindukia katika kushikamana na dini hadi kiwango cha kuvuka mipaka. Hakika alama waliyonayo ni kwamba wao wako mbali na tafakari na akili. Imam Ali B mwenyewe alikuwa akiwakumbusha kwa kuzingatia kuwa wao ni waumini wa Uislamu lakini wajinga wasiotafakari. Walikuwa wakifanya ibada na kusimama usiku kwa ibada na wakisoma Qur’ani tukufu, lakini walikuwa wajinga, wachache wa tafakari na akili, bali walikuwa katika dini wakikhalifu akili na tafakari. Katika kuithibitisha hoja yake kwao, Imam Ali B aliwaambia: “Kwa hakika niliwakatazeni jambo hili
54
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 54
2/17/2017 1:24:30 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
la suluhu, nanyi mkaenda kinyume kwa kukataa na kuyapuuza maneno yangu, mkayaona maneno yangu kwa kipimo cha matakwa yenu. Ambapo kwa hakika nyinyi ni watu bado hamyaelewi yajayo na ni wajinga wa ukweli wenyewe wa mambo.” Akawaambia kwamba nyinyi wenyewe ndio mlioitisha suluhu hii, na leo ni nyinyi wenyewe tena mnaopinga suluhu hii. Mnasema kwamba mliyoyafanya yalikuwa ni kosa, na leo mmetubu kwa Mwenyezi Mungu na kunitaka nami nitubu ili tuelewane. Kwa hakika toka mwanzoni niliwatahadharisheni kutoikubali suluhu hii, lakini mkakataa, mkatoa panga zenu huku mkisema kwamba: “Hakika sisi tunapigana katika njia ya Qur`ani, na hawa wametafuta suluhu kupitia Qur`ani.” mpaka nikalazimika bila kupenda na bila hiyari kuingia kwenye makubaliano. Itakuwaje leo tena mseme kwamba lilikuwa kosa na mwaniomba niyatupilie mbali makubaliano. Vipi nitauvunja huu mkataba ilihali Qur’ani imesema: “Tekelezeni makubaliano” (Qur’an 5:1), na Mtukufu Mtume 2 hakuwahi kuvunja mkataba wowote aliouweka baina yake na mushrikina, kwa kuwa hakuruhusu udhuru wowote na shinikizo lolote liupeleke mkataba kinyume na makubaliano, hiyo ni kwa upande wowote ule wa mkataba, hata kama ni mkataba dhidi ya mushrikina na 55
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 55
2/17/2017 1:24:30 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
waabudu masanamu. Sasa inakuwaje nyinyi mwanitaka nivunje mkataba? Imam Ali B alikuwa kila mara akiwakumbusha mambo haya katika matukio mbali mbali, hasa akitumia ibara yenye kutonesha majeraha yao: “Ambapo kwa hakika nyinyi ni watu bado hamyaelewi yajayo na ni wajinga wa ukweli wenyewe wa mambo.” Ninyi ni wapungufu wa akili na mtazamo, wajinga msiojua mustakbali wa mambo. Na huu ndio udhaifu wenu, mara mnaunga mkono suluhu kwa kasi na nguvu, na mara tena mnajipinga wenyewe kwa kasi na nguvu zote. Hakika huo ulikuwa ni ukafiri na uritadi. Kwa hakika historia ya Makhawarij ni yenye kustaajabisha na wakati huo huo ni yenye mafunzo kwa mwenye kuzingatia. Kwa hali hii inatuonesha wazi maafa yanayopatikana pindi imani inapochanganyika na ujinga na ushupavu wa kipumbavu. Ibnu Abbas anasema kwamba; aliona maajabu kwa Makhawariji pale alipotumwa na Imam Ali B kuzungumza nao, anasema: “Niliona nyuso zilizokuwa sugu kwa wingi wa kusujudu, na mikono iliyokauka kama kwato za ngamia, na walikuwa wenye kuvalia kanzu za hali ya chini sana, na wasiofanya shughuli yoyote ila kukaa msikitini.” 56
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 56
2/17/2017 1:24:30 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
Wanahistoria wanasema kwamba: Makhawariji walikuwa wenye kufanya bidii sana katika kujiepusha na dhambi kama vile uwongo, hivyo hawakuwa wanalificha dhehebu lao hata mbele ya mtu mfano wa Ziyad, mtu aliyekuwa katili kushinda makatili wote. Walikuwa kinyume na watu wenye kuasi, baadhi yao walikuwa wafanya ibada usiku na wenye kufunga mchana, lakini wao kwa upande mwingine itikadi zao zilikuwa za kitoto. Hivyo katika kadhia ya ukhalifa wao hawakuwa wakiona dharura ya kuwepo khalifa, na kwamba kwao wao watu wangetosheka na Qur’ani tu! Ibnu Abil Hadid anasema kwamba: “Walipoona kuwa hawawezi bila kuwa na kiongozi na Rais, wakaachana na itikadi hii, wakampa kiapo cha utii Abdullah bin Wahab ar-Rasiy ambaye alikuwa ni miongoni mwao. Walikuwa wafinyu wa fikra katika mambo mengi ya itikadi zao kama ilivyo hali ya wapungufu wa akili. Wengi wao walikuwa wakiona kwamba makundi mengine ya Kiislamu yote ni makafiri, hivyo hawakuwa wakiamiliana nao, walikuwa hawali vichinjwa vyao wala hawaoi kwao wala kuwaoza mabinti zao. Walikuwa wakiona kwamba amali ni sehemu ya imani, na huu ndio ufinyu wa fikra zao na imani zao, na kwa ajili hii 57
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 57
2/17/2017 1:24:30 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
walikuwa wakimkufurisha yule atendaye moja ya madhambi makubwa. Walikuwa wakisema: Sisi tu ndio tuliookoka, lakini wengine wote ni makafiri na mafikio yao ni motoni.” “Makhawarij walikuwa wakijisifu kwamba wao tu ndio huamrisha mema na kukataza maovu. Baada ya kukata tamaa ya kumvutia Imam Ali B upande wao, waliitisha mkutano wao wa kwanza ndani ya moja ya nyumba huko katika mji wa Kufa, ambapo mmoja wao alisimama na kuwahutubia wengine akisema: ‘Kwa hakika naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kwamba haiwezekani kamwe kwa watu wanaomwamini Mwenyezi Mungu na wanaofuata sheria ya Qurani, kutanguliza dunia hii kabla ya kitendo cha kuamrisha mema, kukataza maovu na kusema ukweli, hata kama atasalimika au kudhurika. Kwa hakika mwenye kudhurika au kusalimika hapa duniani (kwa ajili ya kuamrisha mema na kukataza maovu), hakika malipo yake siku ya Kiyama ni kupata radhi za Mwenyezi Mungu na kubakia peponi milele. Hivyo ndugu zanguni tokeni toka ndani ya mji huu ambao watu wake ni madhalimu na nendeni kwenye vilele vya milima au katika baadhi ya miji na huku ni wenye kukataa bidaa hii potofu.’”
58
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 58
2/17/2017 1:24:30 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
Masharti ya kutekeleza wajibu wa kuamrisha mema: Kuamrisha mema kuna masharti yake, nayo yametajwa na wanazuoni wa Kishi’a na wa Kisunni, nao hawaruhusu kuwavunjia watu haki kwa jina la kuamrisha mema na kukataza maovu, na hasa kama ukiukaji huo wa sheria utakuwa kwa njia ya kutumia nguvu, kipigo, silaha na umwagaji damu, hiyo ni kwa sababu utumiaji wa njia hizo una masharti yake mengi, kati ya masharti hayo ni sharti mbili ambazo ni miongoni mwa sharti za kuamrisha mema na kukataza maovu, sharti ambazo ni lazima zitimie katika hali zote za kuamrisha mema na kukataza maovu, na kwa bahati mbaya sana Makhawariji hawakuzitimiza, bali walikuwa wakiikanusha sharti moja. Sharti hizo mbili ni: Ujuzi katika dini na ujuzi katika matendo. Ujuzi katika dini maana yake ni kuwa na maarifa sahihi na ya kutosha kuhusu mambo ya dini, kuwa na uwezo wa kumaizi baina ya halali na haramu na jambo la wajibu na lisilo la wajibu. Na hili ndilo ambalo Makhawariji hawakuwa nalo, na kwa ajili hiyo walijiegemeza kwenye Aya: “Hapana hukumu ila ya Mwenyezi Mungu, anaelezea yaliyo kweli, naye ni Mbora wa kuhukumu.” (Sura al-An’am: 57). Na wakafanya “Hakuna hukumu ila ya Mwenyezi Mungu” kuwa ndio 59
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 59
2/17/2017 1:24:30 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
wito wao, ijapokuwa Aya hii haina uhusiano wowote na maudhui hii. Ama sharti la pili la kuwa na ujuzi katika matendo, ni kwamba kuna sharti moja katika kuamrisha mema na kukataza maovu linajulikana kwa jina la ‘Mafanikio tarajiwa.’ Na sharti lingine lajulikana kwa jina la ‘Kutosababisha madhara’. Yaani amri ya kuamrisha mema na kukataza maovu inahitajika ili kueneza mema na kuondoa uovu, na kutokana na hilo ni wajibu kuamrisha mema na kukataza maovu pale panapokuwa na matarajio ya kupatikana mafanikio na athari hii. Hivyo tutakapokuwa na yakini kwamba athari nzuri na mafanikio yanayohitajika hayatapatikana basi kuamrisha mema na kukataza maovu hakuwi wajibu. Na pia ni kwamba tutakapokuwa na yakini kuwa mafanikio yatapatikana ni sharti pia utekelezaji wa amri hiyo ya kuamrisha mema na kukataza maovu usilete hasara kubwa. Masharti haya mawili yanawajibisha mtu awe na ujuzi wa kina katika matendo, hivyo iwapo mtu hana ujuzi wa kina katika matendo atakayo kutenda hatakuwa na uwezo wa kutambua ni faida ipi ataipata katika kitendo chake au ni hasara ipi italetwa na kitendo chake, na kwa ajili hii tunakuta kuwa kitendo cha mjinga kuamrisha mema na kukataza maovu kinaweza kusababisha hasara kubwa kama ilivyokuja katika 60
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 60
2/17/2017 1:24:30 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
Hadithi kwamba huleta hasara kubwa kushinda faida anayoikusudia. Sharti kama hili halijawekwa kwenye faradhi nyingine, si sharti katika faradhi hizo kwamba ili uzitekeleze ni lazima uwe na matarajio ya mafanikio na faida, ijapokuwa kila faradhi ina faida na hasara kama tulivyosema huko nyuma. Hivyo kutambua faida na hasara za faradhi hizo si wajibu uliowekwa juu ya shingo za watu. Katika Sala si wajibu kwamba ili uitekeleze ni sharti utaraji uwepo wa faida katika sala hiyo, na ni hali hiyo hiyo katika Saumu, Hija, Zaka na Jihadi, faradhi hizo hazina sharti hilo na wala wajibu wake hauondoki kwa kukosekana sharti hilo. Hali hiyo ni kinyume na wajibu wa kuamrisha mema, wenyewe umewekewa sharti la kutaraji athari nzuri na faida, uchunguze je kutekeleza kwangu kutawanufaisha Waislamu na Uislam kwa jumla au la? Hivyo katika kutekeleza wajibu huu ni lazima mtu atumie mantiki, akili na ujuzi katika matendo na awe na matarajio ya kufanikiwa na kupata faida. Na hii ndio maana ya kusema kwamba kuamrisha mema na kukataza maovu si faradhi isiyo na tafakari.
61
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 61
2/17/2017 1:24:30 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
Rai ya Makhawariji kuhusu kuamrisha mema: Makundi yote ya Kiislamu yamekubaliana kuhusu sharti la kuwa na ujuzi katika kuamrisha mema na kukataza maovu isipokuwa Makhawariji. Wao kwa sababu ya kudumaa kwao kiakili, ufinyu wa mawazo yao na kudumaa kwao kifikra, walikuwa wakisema kwamba, hakika kuamrisha mema na kukataza maovu ni ibada isiyohitaji tafakari, na haina sharti lolote lile linalohusu ulazima wa ‘Mafanikio tarajiwa’ wala ‘Kutosababisha madhara.’ Wakasema: Wala mtu haipasi kutafakari mambo hayo bali ni faradhi ambayo ni wajibu kuitekeleza bila sharti lolote. Basi kwa ajili ya uwelewa wao huu walianzisha uasi ijapokuwa walikuwa wakitambua kuwa uasi wao hauna faida yoyote, na kwamba wao wanamwaga damu zao bila faida yoyote bali ni kuleta hasara tu, wakawa wakiwateka watu na kuwapasua matumbo yao. Hivyo si tu hawakuwa na ujuzi katika matendo yao bali pia walikana sharti hilo kuwepo katika kuamrisha mema na kukataza maovu, na kuanzia hapa ndipo ukapatikana msiba mkubwa juu ya ulimwengu wa Kiislamu. Msiba ulioletwa na Makhawariji katika Uislamu: Hivi ni msiba upi mkubwa na wa kuhuzunisha kushinda kitendo cha Abdurahman bin Muljim muasi wa kimad62
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 62
2/17/2017 1:24:30 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
hehebu kumpiga dhoruba Ali bin Abu Talib B, hakika kama alivyosema Ali B mwenyewe ni kwamba baina yao wawili hakukuwa na chuki yoyote binafsi wala tofauti yoyote binafsi, bali ni kwamba kabla ya hapo Ali B alikuwa alishamtendea wema mwingi, isipokuwa ni kwamba mtu huyu mjinga mwenye ujasiri wa kijinga aliamini na kuyaafiki madhehebu yake katika itikadi ya kwamba hakika Ali B ni kafiri, na kwamba yeye B ni mmoja wa watu watatu waliosababisha machafuko baina ya Waislamu, hivyo alikutana na watu wawili huko Makka na wakakubaliana kumuuwa Ali B, Muawiya na Amru bin al-Aas ndani ya usiku mmoja, na wakaafikiana kwamba uwe ni usiku wa kuamkia mwezi kumi na tisa Ramadhan au mwezi kumi na saba Ramadhan. Kwa nini walichagua usiku huo? Ibnu Abil Hadid anasema: “Hebu shangazwa na ujasiri huu wa kipumbavu pale unapokuwa pacha wa ujinga, hakika wao walichagua usiku huo kwa kuwa ni usiku mtukufu na uliobarikiwa, ni usiku wa ibada, walitaka kutekeleza ndani ya usiku huo uliyobarikiwa jinai hiyo waliyokuwa wakiamini kuwa ni ibada.” Waliifanya: ‘Hakuna hukumu ila ya Mwenyezi Mungu’ kuwa ndio wito wao, lakini Imam B kwa kujua 63
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 63
2/17/2017 1:24:30 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
kwake ubaya wa fungu lao na kwamba wao ni masikini waliochoka katika njia ya upotovu, hakuwa akiwafanyia ukali ijapokuwa waliendelea kumuhangaisha, mpaka akasema B: “Msiwaue Makhawariji baada yangu, kwani hawawi sawa yule aliyeitafuta haki akaikosa na yule aliyeitafuta batili akaipata.” Maana yake ni kwamba watu hawa wanatofautiana na wafuasi wa Muawiya, kwa sababu Makhawarij wanaitaka haki na dini, lakini kwa sababu ya ujinga wao na kutoipata kwao haki, walitumbukia katika makosa. Ama Muawiya na Amru bin al-Aas na wafuasi wao, toka mwanzoni malengo yao yalikuwa ni kutafuta dunia na wao bila shaka waliipata na wakaifuata. Imam Ali B pamoja na kuwa Makhawarij walimkufurisha waziwazi ila ni kwamba yeye hakuwanyima haki yao kutoka Baitul-Mali, kwa sababu aliwachukulia kama wajinga wasiojua walitendalo. Walikuwa wanakuja msikitini na kujibanza pembeni, kisha walikuwa kila Imam B anapohutubu wao huanza kuikata hotuba yake kwa maneno yao, walikuwa wakisema kwa sauti ya juu: “Hakuna hukumu ila ya Mwenyezi Mungu” au wakati mwingine wakisema: “Hukumu ni ya Mwenyezi Mungu wala sio yako ewe Ali.”
64
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 64
2/17/2017 1:24:30 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
Siku moja Imam B alikuwa anawasalisha watu msikitini sala ya jamaa, na humo alikuwemo khawariji mmoja, basi alipoanza Imam kusoma Alhamdu, huyu bwana naye bila kusita alianza kuisoma Aya hii: “Na kwa hakika yamefunuliwa kwako na kwa wale waliokuwa kabla yako: kama ukishirikisha, bila shaka vitendo vyako vitaharibika na lazima utakuwa miongoni mwa wenye hasara.” (Qur’ani 39:65). Yaani wewe Ali umekufuru na kumshirikisha Mwenyezi Mungu. Kwa sababu ya kuipa heshima Qur`ani inaposomwa, Imam B alinyamaza na kumsikiliza hadi alipoimaliza Aya hiyo, kisha Imam B akaanza kisomo chake mara ya pili, lakini mtu huyu aliirudia Aya hiyo mara ya pili. Kwa ajili ya kuiheshimu Qur`ani inaposomwa, Imam B alinyamaza na kumsikiliza hadi alipoimaliza Aya hiyo, kisha Imam B akaanza kisomo chake mara ya tatu, lakini mtu huyu aliirudia Aya hiyo mara ya tatu. Kwa ajili ya kuiheshimu Qur`ani inaposomwa, Imam B alinyamaza mara ya tatu na kumsikiliza hadi alipoimaliza Aya hiyo. Ndipo Imam B akasoma Aya hii: “Basi subiri, bila shaka ahadi ya Mwenyeezi Mungu ni haki, wala wasikuhafifishe wale wasiokuwa na yakini.” (Quran 30:60), mtu huyu alipoisikia Aya hii alibaki kimya hadi Sala ilipomalizika. 65
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 65
2/17/2017 1:24:30 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
Watu hawa walieneza vitisho na woga mkubwa baina ya watu. Na ibara “Hakuna hukumu ila ya Mwenyezi Mungu” ilikuwa ikileta khofu ndani ya nafsi, ndipo alikwenda Abdurahman bin Muljim katika mji wa Kufa, na akakutana na Makhawariji wenzake wawili, na katika usiku waliokubaliana walielekea katika msikiti wa Kufa, na katika sekunde ile ambayo upanga ulimpata Ali B ilisikika sauti kali inayoshabihiana na radi ndani ya usiku wa giza, sauti hiyo ilikuwa ni ya Ibnu Muljim ikisema: “Hakuna hukumu ila ya Mwenyezi Mungu.”
UPENDELEO WA HAKI NA USIOKUWA WA HAKI Upendeleo wa haki na usiokuwa wa haki: Katika sehemu hii ningependa kuelezea maana kamili ya Uadilifu na usawa ili tumaizi baina ya upendeleo usiokuwa wa haki na ule wenye Uadilifu. Je waweza kusema kuwa kila upendeleo na tofauti za kijamii baina ya watu ni kwenda kinyume na Uadilifu? Na je Uadilifu unalazimu kutokuwepo aina zote za tofauti baina ya watu? Au Uadilifu unalazimu kwamba kusiwepo kundi linalofaidika na mazingira kinyume na haki, na wala
66
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 66
2/17/2017 1:24:30 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
kusiwepo upendeleo usiokuwa wa haki? Ikiwa jibu ni hili swali la mwisho, basi hujitokeza swali jingine, nalo ni: Ni kipi kipimo cha kutambua upendeleo wa haki na ule usiokuwa wa haki? Au cha kutambua tofauti ya haki na ile isiyo ya haki? Yaani ni msingi upi unaotegemewa kuthibitisha kuwa tofauti hizi ni za haki na zile si za haki? Maana ya Uadilifu kwa mujibu wa Imam Ali B: Hapo mbeleni tumetaja jibu la Imam B wakati alipoulizwa kwamba kati ya Uadilifu na ukarimu ni kipi kilicho bora kuliko kingine? Imam B alijibu kwamba Uadilifu ni bora, na akalitia nguvu jibu lake kwa dalili mbili alizozitoa. Kwanza ni kwamba Uadilifu hukiweka kila kitu katika nafasi yake, ambapo ukarimu hukitoa kitu katika mwelekeo wake. Hakusema Uadilifu ni bora kwa sababu tu unawaweka watu katika msitari mmoja bali alisema kwamba Uadilifu ni bora kwa kuwa unakiweka kila kitu katika nafasi yake. Na kutokana na maneno haya ya Imam Ali B, Maulawi akasema katika shairi lake kwamba: “Uadilifu huweka kila neema katika nafasi yake, si ili maji yamwagiliwe katika kila pembe. Dhulma huweka kitu pale pasipokuwa pake, nayo si chochote bali ni chanzo cha balaa. Uadilifu ni kum67
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 67
2/17/2017 1:24:30 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
wagilia maji kwenye miti, na dhulma ni kumwagilia maji kwenye miba.� Jibu hili la Imam B kuhusu Uadilifu na ukarimu linatokana na kwamba Uadilifu haulazimu kuzipuuza tofauti zilizopo baina ya watu, bali linatokana na kwamba Uadilifu unalazimu kuzikubali tofauti zilizopo baina ya watu katika haki zao. Na hapa ndipo panapojitokeza swali: Ni kipi kipimo cha kutambua upendeleo wa haki na ule usiokuwa wa haki? Au cha kutambua tofauti ya haki na ile isiyo ya haki Jamii ni mwili hai: Swali hili tutalijibu baada ya maelezo mafupi yafuatayo: Kwa hakika hakuna mfano bora tunaoweza kuufananisha na jamii ila huu mfano wa mwili wa binadamu. Kama vile mwili wa binadamu unavyojengwa kutokana na viungo mbalimbali vya mwili na kwamba kila kiungo kina kazi yake katika mwili, basi vile vile jamii pia inajengwa kutokana na watu mbalimbali ambao kila mmoja hufanya shughuli na kazi yake inayohitajika katika jamii husika. Bila shaka viungo vya mwili vina vituo na nafasi tofauti, baadhi hutoa amri na vingine hutekeleza amri hiyo, hakika baadhi vina nafasi ya juu kushinda vingine, halikadhalika ndivyo ilivyo jamii. 68
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 68
2/17/2017 1:24:30 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
Yaani kila jamii vyovyote iwavyo ni lazima ifuate mgawanyo wa majukumu na kazi, baadhi wanaamuru na wengine wanatekeleza, baadhi wana vyeo vya juu na wengine wana nafasi za chini, huyu anaratibu na kuchora, yule anazalisha na kutimiza, huyu ni afisa wa juu na yule ni mfanyakazi wa chini. Hili ni jambo lisiloepukika, mpangilio wa kila jamii lazima uwe katika namna hiyo. Mwili wa binadamu unaweza kuwa salama na wakati mwingine unaweza kupatwa na maradhi, halikadhalika jamii inaweza kuwa salama na wakati mwingine inaweza kupatwa na maradhi. Mwili huzaliwa, hukua, hudhoofika na hatimaye hufariki, halikadhalika ndivyo ilivyo jamii. Mwili ukiwa salama, viungo vyake huimarika, hukua na kufanikiwa, halikadhalika ndivyo ilivyo hali ya jamii pindi inapokuwa salama na hai, kwani roho ya jamii huimarika. Mtukufu Mtume 4 alitoa tashbihi ifuatayo katika kuipa nguvu jamii akisema: “Mfano wa waumini wanavyopendana na kuhurumiana baina yao, ni mfano wa mwili mmoja, kiungo kimoja kinaposhtakia maradhi, basi viungo vyote mwilini hupata harara na hata kukosa usingizi.� Kwa hakika tukisema kwamba tuendelee kutoa mifano ya ushabihiano unaopatikana baina ya mwili
69
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 69
2/17/2017 1:24:30 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
wa binadamu na mwili wa jamii, kwa kweli hatuwezi kuimaliza mifano hiyo kwa kuwa ni mingi mno. Inatupasa tuelewe kwamba, tunapofananisha mwili wa binadamu na wa jamii, haina maana kwamba miili hii miwili inafanana katika kila kitu. Laa hasha, bali inatofautiana katika baadhi ya mambo, hivyo tutaweka wazi tofauti hizo hivi punde, ili ziweze kutusaidia kufahamu maana kamili ya Uadilifu. Tofauti zilizopo baina ya jamii na mwili hai: Moja ya tofauti inayopatikana ni kwamba tunapotazama viungo vya mwili wa binadamu tunapata kwamba kila kiungo katika mwili huu kipo katika sehemu maalum na hufanya kazi yake maalum. Ambapo viungo hivi haviwezi kamwe kubadilika na kwenda sehemu nyingine katika mwili au kufanya kazi nyingine isiyokuwa yake, lakini si hivyo kwa wanajamii. Kwa mfano jicho, sikio, mkono, mguu na vinginevyo, ni viungo vya mwili ambavyo viko thabiti katika nafasi zao, vikiwa tayari kabisa kutekeleza shughuli maalumu zilizopangiwa na Muumba, hivyo basi hakuna kitakachoweza kusimama katika nafasi ya kiungo kingine ili kutekeleza shughuli ya kiungo kingine, jicho haliwezi kusikia wala sikio haliwezi kuona, mguu hauwezi kupumua wala figo haliwezi kutembea. Na hivyo ndivyo vilivyo viungo vingine. 70
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 70
2/17/2017 1:24:30 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
Ama viungo vya jamii, ambavyo ni watu wake, kila mmoja ana uhuru wa kutosha. Kwa hivyo anaweza kufanya shughuli yoyote katika hiyo jamii, wala roho iliyoko katika jamii hii haina uwezo wa kuamrisha watu wake kubakia katika nafasi moja bila kwenda nafasi nyingine. Kwa kuwa kila mmoja ameruzukiwa akili na Muumba, kwa hivyo katika kutumia akili zao wanaweza kujitahidi na kufanya mengi katika jamii. Viungo vya mwili wa binadamu vinakuwa thabiti katika sehemu moja na kutenda majukumu yake bila kuchagua kwa sababu viko chini ya mamlaka na amri ya roho ambayo ndiyo inayotoa amri yake mwilini, hiyo ni kwasababu havina akili ya kubainisha na kuchagua linalofaa kutekelezwa, ambapo viungo hivi vinaoana na maneno matukufu ya Mwenyezi Mungu: “Kamwe hawamuasi Mola wao katika yale aliyowaamrisha.” Lakini wanajamii hawako hivyo, ndio ni kweli jamii ina uhai na roho lakini roho yake haina mamlaka hayo na nguvu hiyo juu ya viungo vyake ambavyo ni wanajamii. Maana ya usemi: Mwanadamu ni mwanajamii kimaumbile: Wanafalsafa walisema tangu hapo zamani kwamba “Mwanadamu ni mwanajamii kimaumbile.” Yaani mwanadamu ameumbwa katika maumbile ya kijamii. 71
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 71
2/17/2017 1:24:30 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
Baadaye walikuja wasomi wengi kuelezea na kufafanua nini maana ya “Mwanadamu ni mwanajamii kimaumbile.” Ikiwa makusudio ni hii tofauti iliyopo kati yake na mimea au wanyama, yaani uwezo na vipaji vya ukamilifu ambavyo hawezi kuvitimiza ila kwa mwangaza wa maisha ya kijamii, na kwamba mahitaji ya maisha ya kibinadamu hayawezi kutimia bila uwepo wa maisha ya kijamii, basi kauli hiyo ni sahihi. Ama ikiwa makusudio ni kwamba maisha ya kijamii ni jambo lililo nje ya hiari na uchaguzi, kama ilivyo kwa baadhi ya wanyama, kama vile mdudu chungu au nyuki ambao utaona wanaishi maisha yao kijamii katika sura ya kiala bila hiari, na kwamba kila mmoja anaishi maisha yaliyoandaliwa na jamii yake na kutekeleza jukumu lake, na hivyo mdudu huyo katika jamii hiyo anaishi chini ya shinikizo la lazima, basi ikiwa usemi “Mwanadamu ni mwanajamii kimaumbile” una maana hii, si sahihi, na maisha ya kijamii ya binadamu hayako hivyo. Ama ikiwa maana yake ni kwamba binadamu anahitajia kukaa kijamii kwa kuwa kuna mahitaji ambayo hayapatikani ila kwa kushirikiana na wengine, na kwamba ndio yamsukumayo mwanadamu kuishi kijamii, basi usemi huo ni sahihi, na hali hii haimfanyi binadamu kukosa uhuru na hiari ya uchaguzi, hivyo twaweza kusema kwamba maisha ya mwanadamu ni ya kijamii chini ya mkataba wa hiari binafsi, yaani 72
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 72
2/17/2017 1:24:31 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
mwanadamu anaweza kuchagua maisha ya kijamii kwa mwongozo wa akili na utashi binafsi. Mwanafalsafa mkubwa wa Kifaransa anayeitwa Jean-Jacque Rousseu aliandika katika karne iliyopita kitabu kinachoitwa Social Contract (Mkataba wa Kijamii) ambacho ndani yake ameashiria kuwa maisha ya mwanadamu katika jamii ni ya mkataba. Mkataba huo unaafikiwa kwa maelewano na wala si wa kulazimishana. Ijapokuwa nadharia ya Rousseu inayokana mwanadamu kuwa mwanajamii haikubaliki, lakini ni kwamba kauli yake ya kuwa hiari binafsi ina mchango katika hilo si kauli muhimu kwetu, nasi hatungependa kujadili mambo ya kifalsafa katika maudhui haya. Kusudio letu kubwa ni kwamba wakati tunapopata mfanano mkubwa baina ya jamii na mwili, ni wakati huo huo tunapata tofauti iliyopo, nayo ni kwamba viungo vya mwili viko sehemu thabiti na maalumu katika mwili bila kubadilika, na shughuli zao katika mwili pia hazibadiliki, kila kiungo kinafanya kazi moja bila kuingilia kazi ya kiungo kingine. Hii ndiyo tofauti yake na jamii, kwani watu katika jamii wana haki ya kufanya shughuli yoyote wanayoitaka na bila kulazimishwa.
73
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 73
2/17/2017 1:24:31 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
Ukweli wa mambo ni kwamba hakuna mtu yeyote ambaye ameandikiwa katika kipaji chake kwamba ni lazima afanye kazi fulani bila kufanya nyingine, si kwamba mtu fulani ni lazima awe mwalimu au mfanyabiashara, na mwingine awe daktari, au ni lazima huyu awe mhandisi na yule awe mkulima, au huyu awe dereva na yule fundi umeme, au huyu mwanahabari na yule mfamasia, na kwamba daima asijihusishe na jukumu lingine, bali ni kwamba kila mmoja ana uhuru wa kufanya kile alicho na ujuzi nacho na utashi nacho. Kwa ufupi ni kwamba viungo vya mwili vimepangwa kila kimoja katika nafasi yake ya kimaumbile na vikawekewa mpaka na daraja maalumu kikazi na kimajukumu, ama habari nzuri kwa jamii ni kuwa mambo haya walikabidhiwa wanadamu wajigawanyie wenyewe na kila mtu mwenyewe achague kile ambacho amejihusisha nacho kwa mapenzi yake na kwa uhuru wake bila kulazimishwa. Hapo swali linajitokeza, vipi na kwa njia gani tutagawanya shughuli au vyeo baina ya watu? kama vile kuchagua ama kutofautisha na kugawanya nafasi za kazi za vyeo, na ni katika msingi gani na ni njia ipi ambayo yapasa kuifuata? Lazima kupatikane njia moja ya kutatua haya maswali ili kusiwe na kukirihishana ama kulazimishana, na watu wote wawe huru. Uwanja 74
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 74
2/17/2017 1:24:31 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
huu wa kuchagua unafaa kuwa wazi ili kila mmoja awe huru kuchagua nafasi yake kulingana na ujuzi wake, kipaji chake na utashi wake. Mapambano au mashindano ya kuendelea kuishi: Baadhi ya watu wamefananisha maisha na uwanja wa vita, wakasema kwamba maisha ni mapambano ya kuendelea kuishi, kwa ibara iliyo nzuri twaweza kusema kuwa maisha ni mashindano ya kuendelea kuishi. Kwa mtazamo wa baadhi ya watu ni kwamba kanuni ya kwanza katika maisha ya binadamu ni ugomvi na uadui, ama kusaidiana, amani na kuweka suluhisho baina ya watu ni mambo ambayo huwa lazima kwa mwanadamu. Kwa sasa hatuna muda wa kulijadili hili, isipokuwa ni kwamba tungependa kusema kuwa maisha si hivyo, bali uhakika ni kwamba kiasili maisha hayana vita wala ugomvi, lakini kushindana ni jambo lisiloachana na maisha. Bali la wajibu kwanza ni kupatikana uhuru baina ya watu wote, na pili ni kuwepo nidhamu ya kijamii. Hebu tuchukulie michezo inayoandaliwa na jamii kama vile mieleka, riadha au kuinua vitu vizito, michezo hii huwa ina zawadi na medali, kufuzu na kupendeza, na mwenye kufuzu katika michezo hii ni yule anayecheza vyema kushinda mwengine. Kwa hakika hakuna mtu 75
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 75
2/17/2017 1:24:31 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
ambaye amezaliwa na kuandikiwa kuwa yeye peke yake awe ndiye mwenye kufuzu na kuwa si haki kwa mwingine kufuzu, bali ni kwamba haki ya kushiriki na kufuzu iko wazi kwa kila mtu, hivyo watu wote wana uhuru wa kushiriki na kushindana, na yeyote mwenye kutaka kufaulu na kufuzu ni lazima afanye juhudi nyingi na mazoezi mengi ili kupata alama za juu. Ni mfano wa wanafunzi wanaohudhuria darasa kwa muda wa mwaka mmoja kwa juhudi nyingi kisha katika mwisho wa mwaka wakapokea mtihani kutoka kwa mwalimu wao, utapata kwamba kuna wale watakaofaulu na watakaoanguka mtihani huu. Hao waliofaulu ni kwa sababu ya bidii na juhudi zao ama walioanguka ni kwa sababu hawakufanya mazoezi ya kutosha kuwawezesha kufaulu. Na hivyo kila mwanafunzi hupata alama na zawadi kulingana na juhudi zake na maandalizi yake binafsi. Jamii inatofautiana na mwili wa binadamu kwa baadhi ya mambo, mfano kazi wanazofanya wanajamii hawazifanyi nje ya hiari yao na utashi wao, hiyo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu alimuumba mwanadamu na kumpa uhuru wote katika kuchagua na hakumuwekea mpaka wowote au kumchagulia nafasi atakayosimama, na vile vile hakumchagulia kazi moja mahsusi ambayo hafai kuiacha na kuchagua nyingine, bali Mwenyezi 76
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 76
2/17/2017 1:24:31 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
Mungu alimwekea nafasi pana katika kazi yake na uchaguzi wake kwa uhuru kamili. Hivyo tukiyachukuwa mambo haya yote tunapata kwamba jamii inakuwa sawa na uwanja au sehemu ya mashindano kwa kuwa ndipo mahali wanapoonyesha watu ulinganifu, ujuzi, uwezo wao na vipaji vyao, ili kupata haki zao kulingana na vipaji vyao na maandalizi yao. Na wala sisemi kuwa watu wako sawa katika vipaji na uwezo katika kutenda kazi mbalimbali, kwani bila shaka watu wametofautiana katika sifa, na kwa ajili hii ndio maana waona mtu fulani aelemea sana kufanya kazi fulani kuliko nyingine, na mwingine kinyume na hiyo, lakini ni kwamba si kuwa tangu siku ya kwanza ya kuumbwa kwake kaumbwa ili kufanya kazi fulani na kwamba haruhusiwi kuhama toka kazi moja kwenda nyingine kama ilivyo hali ya viungo. Hivyo jamii inafaa kuweka nidhamu na mazingira bora ili kila mmoja awe na haki ya kushiriki katika mashindano ya maisha, na jamii iwe katika mpangilio bora utakaotoa fursa kwa wanajamii wote kuonesha vipaji vyao, majaliwa yao na uwezo waliopewa na Mwenyezi Mungu. Mambo yasiyoingia katika mashindano: Katika michezo kuna mambo mawili: Kwanza ni mchezo wenyewe unaofanyiwa mashindano, na pili ni 77
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 77
2/17/2017 1:24:31 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
zawadi na heshima wanayoipata hao waliofuzu. Mambo haya mawili pia yapo katika uwanja wa mashindano ya kijamii ambayo ni utendaji wa kazi inayofanyiwa mashindano, na pili ni zawadi na malipo anayopata mshindi. Lakini swali ni hili, je! Ni kazi gani inafaa kushindaniwa? Na ni zawadi gani anayofaa kupewa huyu mshindi? Tukizingatia vilivyo katika maelezo yafuatayo bila shaka tutaweza kuyajibu maswali hayo. Bila shaka matendo au kazi inayofaa kushindaniwa katika jamii ni kazi yoyote ambayo italeta faida na manufaa katika jamii, kwa mfano mashindano katika elimu, kumcha Mwenyezi Mungu, ukweli, msimamo katika dini, kutumia akili katika kutafakari, kufanya bidii na juhudi nyingi katika kazi na uzalishaji, na vile vile kutumikia jamii. Ama zawadi anazotunukiwa katika kuyatenda haya, bila shaka ni hizo haki na upendeleo ambao watu katika jamii hutunukiwa kwa sababu ya mazuri ambayo wameyafanya na kulingana na viwango vya kazi na juhudi zao na kile wanachostahiki kupata. Kwa hakika haki hizi wanazotunukiwa kila mmoja katika jamii hazitofautiani kamwe na hizo zawadi za waliofuzu katika michezo au anazozipata mwanafunzi baada ya mtihani wake. Ni lazima kuelewa maudhui ya mashindano na pia kanuni ambayo wanaoshiriki 78
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 78
2/17/2017 1:24:31 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
wanafaa kuijua ili waweze kufaulu katika mtihani kwa daraja ya juu, ni masomo yapi yatakayokuwa na mtihani na ni alama zipi zitakazopelekea kupata zawadi. Katika maswala ya dini, mashindano ambayo yapo ni katika matendo mema, hivyo tukishaelewa mambo haya yote, tunaweza kujua vizuri yupi tutakayempa zawadi na daraja ya juu, na yupi tumpe chache. Kwa hakika niliyoyataja hapo awali ni kwamba haki na wajibu katika Uislamu vinaenda sawiya na wala havifarakani. Hivyo uwanja wa mashindano ni uwanja wa wajibu na majukumu, na haki ndio zawadi na alama zinazoafikiana na mashindano katika wajibu na majukumu, nazo hutolewa zawadi kwa watu. Kwa hakika kama tungaliweza kujua chanzo cha haki na majukumu, na kuweza kutambua vizuri kuwa tusemapo maisha ni mashindano, humaanisha kushindana katika kutekeleza wajibu na majukumu, na kwamba mtu hatapata ila yale aliyoyafanya, na tukaelewa kwamba faida na mavuno ya mashindano ni kule kuburudika na haki za kijamii, lau tungejua hayo yote tungekuwa tumeujua msingi mkubwa wa haki za kijamii katika Uislamu, na kwamba msingi huu utatuongoza kama taa ing’arayo katika masuala yote, na utatuokoa na dhulma nyingi.
79
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 79
2/17/2017 1:24:31 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
Je, ni Uadilifu au usawa? Katika kulijibu swali ambalo liliulizwa hapo awali kwamba, ni nini maana ya Uadilifu? Ni upendeleo upi na tofauti ipi huukabili Uadilifu? Je kila tofauti iliyopo baina ya wanajamii huwa ni kinyume na Uadilifu, na kwamba Uadilifu unalazimu usawa katika kila kitu? Au ni kwamba Uadilifu haulazimu usawa katika kila kitu, bali katika baadhi ya mazingira hukubali dharura ya uwepo wa tofauti na upendeleo, na kwamba la msingi tu ni upendeleo huu na tofauti hii isiwe bila msingi wa haki? Ikiwa jibu ni hili la mwisho basi ni kipi hicho kipimo na kigezo cha haki na kutokuwepo haki? Tuliweza kuelezea hapo awali kwamba Uadilifu haumaanishi kwamba ni lazima watu wote wawe katika mustawa mmoja au kuwa katika daraja moja. Ukweli ni kwamba vyeo na daraja zinazokuwepo katika jamii ni kama mwili wa binadamu, na pindi kunapokuwa na hivyo vyeo lazima kuwepo na mipaka na kanuni ili kubainisha hivyo vyeo, na njia pekee ya kutimiza lengo hilo ni kumpa uhuru kila mmoja na kuweka wazi uwanja wa mashindano. Na pindi watakapoingia katika mashindano hayo, bila shaka ndipo kitajulikana kiwango cha kila mmoja, na ndipo bila shaka itabainika nafasi ya kila mmoja na maandalizi yake binafsi, na ndipo
80
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 80
2/17/2017 1:24:31 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
itaonekana kwamba bidii na juhudi za watu hazilingani, kwa hivyo lazima kutokana na haya idhihirike tofauti zao na kubainika vyeo vyao, atajulikana mzito na mwepesi, wa kwanza na wa mwisho, wa chini na wa juu. Hivyo tofauti hizi ni sehemu ya Uadilifu na ni lazima zipatikane katika jamii sambamba na vipaji vya wanajamii na kulingana na ujuzi na uwezo wa kila mmoja. Uadilifu unalazimu kwamba mwanafunzi apate alama anayostahiki kutokana na mtihani ambao umewashirikisha wanafunzi wote. Si Uadilifu kuwapa wanafunzi wote walioshiriki mtihani alama sawa bila kujali usahihi wa majibu yao, eti kwamba tusipowapa alama sawa tutakuwa tumefanya ubaguzi na upendeleo ambao ni dhulma. Hakika ukweli ni kinyume na hivyo kabisa, kwani kuwapa alama sawa inamaanisha kwamba ni kutokumpa kila mwenye haki ile haki yake anayostahiki, na hii ndio dhulma. Ni Uadilifu kwamba ubingwa katika mashindano uzingatie ustadi na uwezo, na hicho ndicho kipimo cha ubingwa huo, na si Uadilifu kwamba uwape alama sawa yule aliyeonyesha ustadi na ambaye hakufanya hivyo. Hakika aina hii ya usawa ni dhulma halisi, na hakika kutambua tofauti hizi zilizopo baina ya watu kulingana
81
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 81
2/17/2017 1:24:31 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
na kazi zao na uwezo wao wa kudhihirisha vipaji vyao ndio Uadilifu halisi. Hakika usawa ambao ni Uadilifu ni ule ambao mazingira ya haki yamelingana sawa, lakini si pale ambapo hayakulingana. Yaani katika mashindano ya kielimu au kimichezo kipimo cha ubingwa kiwe ni ule uwezo, ustadi na vipaji vyao, kwani katika washiriki huenda akawepo ambaye ni mweupe au mweusi, mtoto wa tajiri na mtoto wa masikini, na pia huenda akawepo ambaye ni mwanachama wa chama fulani au kundi fulani, na huenda akawepo ambaye si mwenye sifa hizo, na huenda mshiriki akawa ni rafiki wa mwalimu au ana ujamaa naye, na mwingine akawa hana uhusiano wowote na wasimamizi wa mashindano hayo, hivyo sifa hizo hazipasi kuwa kipimo na kigezo cha ufaulu na ubingwa kwa sababu hazina uhusiano wowote na ustadi, uwezo na kipaji. Hivyo tusipotizama kiwango cha uwezo, ustadi na vipaji na tukawa tumewapa washiriki wote alama sawa, bila shaka tutakuwa tumefanya dhulma, na hata tukisema kwamba tofauti zipo, lakini ikiwa kigezo ni sifa za namna hiyo bado tutakuwa tumefanya dhulma. Kwa hakika hii ndio tofauti baina ya kule kutofautisha kwa misingi ya haki na kule kusikokuwa kwa misingi ya haki, na hii ndio maana ya kauli inayohusu Uadilifu kuwa: �Uadilifu ni kumpa kila 82
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 82
2/17/2017 1:24:31 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
mwenye haki, haki yake,” na huu ndio uthibitisho wa maneno ya Imam Ali B aliposema kwamba: “Uadilifu huyaweka mambo sehemu yake.” Imam hakusema kwamba Uadilifu ni kuweka kila kitu katika sifa moja na kwa mustawa mmoja. Uadilifu ni kuweka mazingira bora, masharti na mipaka maalum inayofaa katika mashindano hayo ya kijamii, ili kila mwanajamii afaidike na haki za kijamii. Lakini maana ya usawa na kutazama kwa jicho la usawa, ni kuhakikisha isiingie athari ya kibinafsi katika kuamiliana na watu, na iwe ni bila kuangalia matabaka yao. Mtukufu Mtume 2 amesema : “Watu ni jamii moja kama meno ya kitana.” Na akasema: “Hakika ninyi nyote Mola wenu ni Mmoja, na baba yenu ni mmoja, nyote mmetokana na Adam na Adam ametokana na mchanga.” Kisha akaongeza: “Hana ubora wowote wa mwarabu juu ya asiyekuwa mwarabu ila kwa uchamungu.” Qur’ani pia inaondolea mbali tofauti inayojengeka kwa msingi wa rangi na jinsia au nasaba ikasema:
يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّا َخلَ ْقنَا ُك ْم ِم ْن َذ َك ٍر َوأُ ْنثَ ٰى َو َج َع ْلنَا ُك ْم ُشعُوبًا ۚ َوقَبَائِ َل لِتَ َعا َرفُوا ۚ إِ َّن أَ ْك َر َم ُك ْم ِع ْن َد للاهَّ ِ أَ ْتقَا ُك ْم “Enyi watu! Hakika Sisi tumewaumba kuto-
83
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 83
2/17/2017 1:24:31 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
kana na mwanamume na mwanamke. Na tumewafanya mataifa na makabila ili mjuane. Hakika mtukufu zaidi yenu mbele ya Mwenyezi Mungu ni aliye na takua zaidi yenu. ” (Qur’ani Sura al-Hujuraat 49:13).
Kisha Qur’ani tukufu inaendelea kueleza kwamba hawawezi kuwa sawa yule aliyesoma na jahili, au fisadi na asiyekuwa fisadi, Mwenyezi Mungu akasema:
ت َك ْال ُم ْف ِس ِدينَ فِي ِ أَ ْم نَجْ َع ُل الَّ ِذينَ آ َمنُوا َو َع ِملُوا الصَّالِ َحا َّار ِ ض أَ ْم نَجْ َع ُل ْال ُمتَّقِينَ َك ْالفُج ِ ْالأْ َر “Je, Tuwafanye walioamini na wakatenda mema kama wafisadi katika ardhi? Au tuwafanye wenye takua kama waovu ?” (Qur’ani Sura Swad 38:28).
Akasema tena:
ك ۚ نَحْ ُن قَ َس ْمنَا بَ ْينَهُ ْم َم ِعي َشتَهُ ْم فِي ْال َحيَا ِة َ ِّأَهُ ْم يَ ْق ِس ُمونَ َرحْ َمتَ َرب ضهُ ْم بَ ْعضًا ُ ت لِيَتَّ ِخ َذ بَ ْع َ ْضهُ ْم فَو ٍ ْض َد َر َجا َ ال ُّد ْنيَا ۚ َو َرفَ ْعنَا بَ ْع ٍ ق بَع ۗ س ُْخ ِريًّا “Kwani wao ndio wanaogawa rehema ya Mola Wako? Sisi tumewagawanyia baina
84
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 84
2/17/2017 1:24:31 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
yao maisha yao katika uhai wa duniani, na tukawainua baadhi yao juu ya wengine kwa daraja nyingi ; kwa hivyo baadhi yao wanawafanya wengine wawatumikie.” (Qur’ani Sura az-Zukhruf 43:32).
Tofauti za watu kivipaji: Hakika miongoni mwa maajabu ya uumbaji ni uwepo wa tofauti za kimaumbile baina ya watu, huku aliye juu katika hili huenda akawa chini katika lile, hivyo matokeo ni kwamba kila mmoja anamuhitajia mwenzake. Jamii zilizoendelea ulimwenguni zinafanya juhudi ili kuwepo Uadilifu na usawa baina ya wananchi wao, lakini hata hizo jamii zilizofuzu hazijafikia kusema kwamba kuwepo usawa kati ya watu walio na vipaji na wasio na vipaji, mwerevu na mjinga, mwaminifu na mkora, mchangamfu na zoba, mwenye nguvu na dhaifu. Usawa wa kweli : Usawa ulio wa hakika ni kutoa fursa sawa kwa wote na kuufungua uwanja wazi kwa kila mmoja kwa usawa ili aweze kushiriki kulingana na kadri ya uwezo wake na utashi wake, na hivyo akiwepo yeyote na wa tabaka lolote mwenye uwezo wa kushiriki na kufikia mafanikio basi
85
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 85
2/17/2017 1:24:31 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
ashiriki, na kama akishindwa basi ajilaumu mwenyewe. Jamii inafaa kuweka mikakati ya kupata elimu kwa kila mmoja kwa hali ambayo kila mmoja atapata nafasi ya kuingia shule na vile vile kuendelea kupata elimu ya juu zaidi katika vyuo vikuu, na isiwe kwamba tunawapendelea wengine bila haki. Kwa hali yoyote ile, ni lazima mipango hii ipangwe kwa njia ya usawa kwa kila mmoja kuweza kupata elimu ya ngazi zote, kiasi kwamba hata mtoto wa masikini na mkulima wa kijiji cha mbali ambaye ana uwezo na kipaji cha kumwezesha kuingia katika uwanja wa maisha kwa kupata masomo hadi kiwango cha juu katika nyanja fulani ya elimu, au ana uwezo na kipaji cha kufikia kiwango cha waziri, basi awe na nafasi na fursa na mazingira sawa ya kufanya hivyo. Ama tofauti ambayo haina sura ya haki, ni ile ya kutokuwepo mipango ya usawa kwa watu wote katika jamii ambayo inaweka njia za maendeleo na miundombinu yake katika hali na fursa ya kuwafikia tu baadhi ya watu huku ikiwaepuka wengine. Au tofauti hiyo inawafanya watu wengine kubaki katika hali duni hata kama wana ustadi, uwezo na vipaji vya kuweza kuwafikisha ngazi za juu, huku tofauti hiyo ikiwafikisha wale wasio na ustadi, uwezo na vipaji katika ngazi ya juu ijapokuwa hawana ujuzi wa uongozi, na huku ikiwapa mamlaka kwa njia isiyokuwa ya haki. 86
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 86
2/17/2017 1:24:31 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
Jamii haifai kukaa bila kujua thamani ya elimu, ujuzi na taaluma, la sivyo kutazuka ndani yake machafuko. Ukweli ni kwamba jamii inayoendeshwa kwa Uadilifu ni ile ambayo inaweka usawa na kutoa fursa sawa kwa watu wote na kuwatendea watu kama vile wanavyowatendea wenye kushiriki katika mashindano ya michezo. Jamii inalazimika kuhusisha watu wote hata kama ni watoto wa masikini na walala hoi, ina wajibu wa kuweka na kutoa fursa sawa kwa wote ili waweze kuendelea na masomo yao na kufikia kiwango cha kuwa mawaziri, makatibu wakuu na watendaji wa kuu katika hali ya kushindania fursa, kwani hakika jamii inayotoa fursa sawa kwa wote hufuata kauli ya Mtukufu Mtume 4 inayosema : “Watu ni jamii moja kama meno ya kitana.” Na katika kutofautisha baina ya walio na ujuzi na wasiokuwa nao ni kulingana na Aya inayosema: “Je, waweza kuwa sawa wale wanaojua na wale wasiojua?” (Qur’an 39 :9). Na pia ni kulingana na Aya: “Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni aliye mchamungu zaidi katika nyinyi.” (Sura Hujurat: 13). Hii ndiyo jamii inayotakikana. Je, hali hii haikuwepo mwanzoni mwa Uislamu? Je si katika maneno ya Mwenyezi Mungu: “Na tunataka kuwafanyia hisani wale waliodhoofishwa 87
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 87
2/17/2017 1:24:31 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
katika ardhi na kuwafanya viongozi na kuwafanya warithi.” (Qur’ani; 28:5). Na je hawajadhihiri katika Uislamu wasomi wachamungu ambao walikuwa watumwa au watoto wa watumwa, mfano wa Abdallah bin Mas’ud ambaye alifikia kiwango cha utukufu? Je, hawakushushwa chini mabwana wakubwa wenye nguvu, mfano wa Abu Jahl, Abu Lahab na Walid bin Mughira? Je hujaona vijana katika tabaka ya chini waliofikia daraja za juu za uongozi kwa sababu ya nguvu zao, uchamungu wao na ustadi wao? Huku mabwana wakubwa mafisadi wakishushwa na kuondolewa ? Jamii ya Kiislamu isiyo na matabaka : Pamoja na kuwa Uislamu ni dini ya kijamii, inayotambua heshima ya jamii, uhai wake na kifo chake, mafanikio yake na hasara yake, faida yake na uharibifu wake huku ukitanguliza maslahi ya jamii kabla ya maslahi ya mtu binafsi, huku ukifutilia mbali tofauti za kimatabaka, lakini pamoja na hayo yote haufumbii macho haki binafsi za mtu binafsi na tofauti zao zilizo katika msingi wa haki, kwani haumtazami mtu kuwa si chochote mbele ya jamii, ambapo ni kinyume na baadhi ya wanaharakati. Uislamu hausemi kuwa mtu hana umuhimu na kuwa muhimu ni jamii, na kwamba haki ni ya jamii na si ya mtu binafsi, na kuwa mmiliki ni jamii na si 88
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 88
2/17/2017 1:24:31 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
mtu binafsi, na kuwa asili ni jamii na si mtu binafsi. Hakika bila shaka Uislamu unatambua haki binafsi ya mtu binafsi, umiliki binafsi na uhuru binafsi, na wala hauoni kuwa ni Uadilifu jamii kuimeza haki binafsi ya mtu, bali unaona Uadilifu ni kutoa fursa sawa na kamili katika mazingira ya ushindani, na kuwapa wanajamii haki na upendeleo makhususi kutokana na alama za kila mmoja katika kutimiza wajibu na majukumu yake. Hapana shaka kwamba Uislamu umehimiza kuwepo Uadilifu katika jamii, ili kuenea kote na kutumika katika mashindano yatakayojiri katika jamii na kuwezesha jamii kumpa kila mmoja haki yake na upendeleo binafsi utakaotokana na msingi wa utendaji, uchamungu, elimu, juhudi na haki. Kwa hakika jamii bora ya Kiislamu isiyo ya kimatabaka ni ile isiyo na ubaguzi, ni ile isiyopima ubora kwa wasifu usio na haki, na wala si ile inayopuuza viwango vya ustadi, uwezo na vipaji binafsi. Juwaybir na Zulfa: Mtu mmoja kutoka Yamamah aliyeitwa Juwaybir aliyekuwa mweusi, mwenye sura mbaya na masikini asiyemiliki lolote alihamia katika mji wa Madina. Juwaybir aliusoma Uislamu hadi kuuelewa na aliuku89
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 89
2/17/2017 1:24:31 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
bali Uislamu bila kusita. Kwa sababu ya kukosa makazi, bwana huyu alikuwa akilala msikitini na baada ya muda usiokuwa mrefu walikusanyika kikundi cha mafukara Waislamu mfano wake, Mtume 2 alipoona wamekuwa wengi alitoa amri walale wote msikitini. Mafukara hawa Waislamu walizidi kuongezeka katika idadi, ndipo ikashuka amri kutoka kwa Mwenyezi Mungu kuwa msikiti uachwe katika hali ya tohara na usiwe mahala pa kulala. Vile vile ikashuka amri kuwa wale ambao milango ya nyumba zao ni njia ya kuingia msikitini ifungwe ila mlango wa Imam Ali na Fatima Zahra J Baada ya amri ya Mwenyezi Mungu kutekelezwa kama alivyoamrisha, Mtume 2 naye aliamrisha masahaba wake kujenga ukumbi wa kulala kwenye mji wa Madina ili kuwahifadhi wale mafukara. Masahaba hao mafukara waliishi hapo na wakawa maarufu kwa jila wa watu wa Swafah, na Juwaybir alikuwa mmoja wao. Mtume 2 pamoja na masahaba wake wote walikuwa wenye kuwahurumia sana huku wakiwakidhia haja zao za kimaisha. Siku mmoja Mtume 2 aliwatembelea watu wa Swafah na alipojitokeza Juwaybir, alimwambia: �Ewe Juwaybir, ni uzuri ulioje ikiwa utaoa ili kama ukiwa na haja yako (mkeo) awe ni mwenye kukusaidia katika 90
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 90
2/17/2017 1:24:32 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
dunia na akhera yako?” Alijibu akisema: ”Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu nani katika wanawake atampenda mtu kama mimi? Mtu ambaye hana cheo, ukoo, mali wala uzuri? Mwanamke yupi atakaye mpenda mwanamume mfano wangu?” Mtume 2 aliposikia maneno haya alijibu akisema: ”Hakika kupitia Uislamu, Mwenyezi Mungu alimfanya duni yule aliyekuwa mtukufu wakati wa ujahiliya, akamtukuza aliyekuwa duni na akampa nguvu yule aliyekuwa amedhalilishwa wakati wa ujahiliya; watu wote wakiwemo weupe na weusi, Qureishi, mwarabu na asiyekuwa mwarabu, wote wanatokana na Adam B, na Adam Baliumbwa na Mwenyezi Mungu kutokana na udongo. Kwa hivyo basi hawi mbora wenu kwa mwingine ila kwa uchamungu.” Kisha akamwambia kwamba hakuna mtu yeyote katika Waislamu Muhajirina au Ansari, ambao wako hai mpaka leo, ambaye atakuwa mbora kushinda wewe ila kwa uchamungu. Kisha Mtume 2 alimwamrisha Juwaybir kwenda nyumbani kwa Ziyad bin Lubaid ili amwambie kwamba Mtume2 amenituma kwako kumposa binti yako Zulfa. Na Juwaybir alifanya kama alivyoamrishwa na Mtume 2. Ziyad alikuwa mwenye kuheshimika sana katika mji wa Madina. Juwaybir aliingia kwa Ziyad, na akamkuta akiwa na watu wa familia yake. Aliomba 91
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 91
2/17/2017 1:24:32 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
idhini ya kuketi na akaruhusiwa, aliketi chini kisha alimgeukia Ziyad akamwambia: ”Nimekuletea ujumbe kutoka kwa Mtume 2 je unautaka kwa siri au kwa dhahiri?” Ziyad akasema: ”Kwa hakika ujumbe huu kutoka kwa Mtume 2 ni fakhari kubwa.” Na ndipo alipoamrishwa kuzungumza wazi wazi mbele ya kila mmoja, naye akasema: ”Hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 amenituma akinishauri nimuoe binti yako Zulfa, je wasemaje? Sema ili nimrudishie Mtume 2 jibu lako.” Ziyad alishangaa na kustaajabu, kisha akamuuliza: ”Je ni Mtume 4 ndiye aliyekutuma na jambo hili?” Juwaybir akajibu: ”Naam ni Mtume wa Mwenyezi Mungu ndiye aliyenituma na jambo hili, wala mimi simzulii uwongo Mtume wa Mwenyezi Mungu.” Ziyad alisema sio katika ada zetu kuwaozesha binti zetu kwa mtu asiye Ansari, sasa wewe nenda na nitamuona Mtume 4 mimi mwenyewe. Juwaybir alitoka akiwa amekumbwa na fikra nyingi na hapo hapo aliyakumbuka maneno ya Mtume 2 kwamba Uislamu uliyaondolea mbali majivuno, au kujiona mbora kwa sababu ya nasaba au familia. Upande mwingine aliyafikiria maneno ya huyu bwana Ziyad kwamba wao hawaozeshi ila katika tabaka lao. Kisha alijisemea moyoni mwake hakika yale anayoyasema huyu mtu yanaenda kinyume na mafundisho ya 92
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 92
2/17/2017 1:24:32 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
Qur’ani. Kisha bwana Juwaybir aliapa kwa jina tukufu la Mwenyezi Mungu akisema: ”Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kwamba Qur’ani haikushuka na maneno ya huyu bwana, wala utume haukudhihiri kwa Muhammad 2 na maneno hayo. ” Wakati habari hizi zikizungumzwa, huyu msichana anayezungumziwa alikuwepo miongoni mwao, na aliyasikia yote yaliyozungumzwa, lakini ili kuhakikisha, alimuuliza baba yake kuhusu jambo hili. Baba yake alimwelezea kisa hadi mwisho, basi hapo mara moja Zulfa alisema: ”Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kwamba Juwaybir ni mkweli.” Akamwambia baba yake: ”Tafadhali usifanye hivyo, usimrudishe Juwaybir kwa Mtume 4 na hali amehuzunika moyoni, tuma mtu amrudishe Juwaybir kwako. ” Basi maneno hayo yalimsumbua baba yake kisha alituma Juwaybir arudishwe hapo nyumbani, na kisha Ziyad alisimama yeye mwenyewe kwenda kwa Mtume 2 na akamwambia Mtume 2 : “Baba na mama yangu wawe fidia kwako ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, alinijia Juwaybir na ujumbe kutoka kwako, na nikamwambia kuwa sio kawaida yetu kuwaozesha binti zetu kwa asiyekuwa katika kabila letu. ” Mtume 2 bila kusita alimwambia: ”Ewe Ziyad, Juwaybir ni muumini, ambapo muumini mume 93
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 93
2/17/2017 1:24:32 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
ni sitara kwa muumini mke. Na mumini mke ni sitara kwa muumini mume.� Ziyad aliporudi nyumbani, alimwambia binti yake yote yaliyotokea baina yake na Mtume. 2 Binti yake alisema kwamba, kwa sababu ni Mtume 2 ndiye aliyemtuma, basi mimi sina budi kukubali. Hapo hapo Ziyad alimchukua Juwaybir akaja naye mbele ya familia yake na kumuoza binti yake kwa Juwaybir katika sunna ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. Na kwa kuwa Juwaybir hakuwa na nyumba, Ziyad aliwapa nyumba iliyokuwa tayari ikiwa na kila kitu kilichohitajika. Vilevile Ziyad aliwavisha bwana na biharusi kwa mavazi mazuri, na baada ya kuwaandaa vilivyo aliwasindikiza hadi kwenye nyumba waliyotayarishiwa. Juwaybir alipoingia katika nyumba ile waliyotayarishiwa, alimshukuru Mwenyezi Mungu sana kwa neema ya Uislamu kwa kuwa Uislamu ndio uliomtukuza hadi kiwango kile. Kutokana na neema hii aliyoipata, alijipa siku tatu mfululizo akimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kukesha kwa ibada, kufunga na ibada zingine mbali mbali. Shaka kubwa ilimwingia biharusi, na kuanza kudhania kwamba labda Juwaybir hakuwa na haja naye. Habari hizi zilimfikia Mtume, 2 naye alimwita Juwaybir ili kujua kuhusu hali hii; alipomuuliza alisema kwamba, “Nilipoingia katika nyumba niliyoandaliwa, kwa namna 94
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 94
2/17/2017 1:24:32 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
ilivyo kuwa na kila kitu ndani yake na mke mrembo, kwa hakika sikuwa na budi ila kumrudishia Mwenyezi Mungu shukrani kwa kunitukuza baada ya umaskini. Kwa sababu hii niliazimia kufunga mchana kisha usiku nakesha kwa kumshukuru. ” Mtukufu Mtume 4 alichukulia uzito suala la kuondoa desturi mbaya: Mtukufu Mtume 2 alikuwa akilichukulia uzito mkubwa suala la kuondoa tofauti na ubaguzi ambao ulitokana na desturi na mila zilizoota mizizi ndani ya jamii, tofauti ambazo hazikutokana na ushindani wa kimatendo na utekelezaji wa maadili mema na vitendo vya kheri, wala hazikutokana na kauli ya Mwenyezi Mungu: “Basi shindaneni kutenda mema.” Bali zilitokana na mila na desturi, hivyo alifanya kila awezalo kuhakikisha anatokomeza mila hizo ili kuziondoa ndani ya jamii. Ili afanikiwe katika hilo, Mtume 2 alikuwa katika vikao akihimiza kuketi kwa namna ya duara, na kumweleza yeyote aliyefika hapo kuketi popote pale palipo na nafasi, na si washindanie kuketi sehemu fulani maalumu. Mtume 2 alitaka watu wote waelewe kwamba hakuna kuchagua kwamba watu fulani waketi sehemu fulani na wengine sehemu tofauti, bali watu wote walikuwa sawa. Mtume 4 alikuwa hapendi kui95
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 95
2/17/2017 1:24:32 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
nukiwa pindi anapoingia katika kikao chochote kile, na kama akimuona mtu yeyote akimuinukia, basi alikuwa akimwamrisha aketi chini. Vilevile hakupendezwa alipokuwa amempanda farasi wake, kuwe kuna mtu anayefuatana naye huku akitembea kwa miguu, hivyo ima atampandisha katika farasi wake, au atamuomba atangulie au yeye Mtume atangulie na huyo mwenda kwa miguu aje baadaye, au Mtume 2 ateremke na atembee kwa miguu pamoja. Na pia alikuwa akiketi juu ya ardhi na akikamua maziwa kwa mkono wake mwenyewe. Maisha ya Mtukufu Mtume 2
kijamii:
Mtume 2 alikuwa mnyenyekevu sana, kwa kiasi ambacho hakuwahi kughafilika hata kidogo na kujihisi kuwa yeye si mja wa Mwenyezi Mungu. Alikuwa akijiona kwamba yeye ni dhaifu na mnyonge sana mbele ya Mwenyezi Mungu: “Hamiliki kwa ajili ya nafsi yake manufaa yoyote wala madhara yoyote, uhai wala ufufuo.” (Qur’ani 25:3) Mtume 2 alikuwa akiamiliana na watu wote kwa hali ya unyenyekevu, upole na huruma, huku akionesha kiwango cha juu kabisa cha unyenyekevu mbele ya Mwenyezi Mungu. Siku moja mwanamke mmoja alimwambia Mtume 2 kwamba: “Kila ulichonacho ni wema mtupu, lakini wewe una 96
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 96
2/17/2017 1:24:32 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
dosari moja tu, nayo ni kwamba hujithamini, unakaa juu ya ardhi na kujiweka kama mtumwa.” Mtume 2 akamjibu: “Ni nani kati ya waja wa Mwenyezi Mungu aliye mtumwa kunishinda mimi?” Kwa hakika tabia na mwenendo wa Mtume wa Mwenyezi Mungu 2 uliojaa unyenyekevu vinaonesha kwamba alizingatia sana na kuhimiza kwamba jamii ijae tabia hizi za kijamii. Kwa sababu alijua kwamba tabia za kimila, kidesturi, kiheshima, kivyeo, kimajina na kinafasi, zilizokuwa zimeenea, ijapokuwa zinaonekana ni jambo dogo, lakini zina hatari kubwa katika jamii iwapo zitaachwa zichukue nafasi, na hatimaye zitajenga ukuta wa ubaguzi baina ya watu, na mwishowe ni kuathiri nyoyo zao. Mambo kama hayo ndio huleta matatizo na vikwazo vya kijamii, kwani mwanzo huanza kama kitu duni lakini baadaye huleta madhara makubwa yasiyoepukika, kwani hakika kuitana majina fulani, kukwezana na kudharauliana ndio mbegu na chanzo cha ubaguzi baina ya wanajamii. Tulikuwa na mwalimu wetu aliyekuwa mchamungu na mwenye kujinyima, yeye alikuwa akiamini kwamba hakika moja ya mafanikio makubwa yaliyopatikana mwishoni mwa karne hii ni kung’oa mtindo wa kuitana majina mabaya na kukwezana. Siku moja Mtukufu Mtume 2 na masahaba wake walikuwa safarini. 97
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 97
2/17/2017 1:24:32 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
Ulipofika wakati wa adhuhuri walishuka sehemu moja na kusali, kisha waliamua kumchinja mbuzi ili awe chakula chao. Masahaba walianza kugawana kazi ya kufanya ili kurahisisha shughuli za upishi. Mmoja alichagua kuchinja, mwingine kuchuna ngozi, wa tatu akasema yeye atapika. Mtukufu Mtume 2 naye akasema: “Mimi nitaleta kuni.” Masahaba wake waliposikia hivyo walisema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, wewe pumzika sisi tutafanya kila kitu.” Mtukufu Mtume 2 alisema: “Kwa hakika Mwenyezi Mungu anamchukia mja anayejiona yeye ni mbora kushinda wenzake.” Kwa hakika kuna mambo mengi mfano wa kisa hiki ambayo yamefanywa na Mtukufu Mtume 2 na Maimamu watukufu G, na yote yanaeleza kuwa walikuwa wakifanya kila waliwezalo kuhakikisha wanaondoa mambo haya madogo madogo ambayo huishia kuleta ubaguzi katika haki na majukumu. Muhtasari wa maneno: Muhtasari wa maneno haya ni kwamba maana ya Uadilifu na usawa ni kuuondoa huu ubaguzi wa rangi, nasaba, mali, vyeo na mengineyo mengi ambayo yanasababishwa na desturi mbaya za kidhulma. Ama zile tofauti ambazo hutokana na ustadi, vipaji, kazi, ujuzi, 98
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 98
2/17/2017 1:24:32 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
juhudi na kujituma katika uwanja wa mashindano ya utu na haki, ni lazima ziheshimiwe na zitumike vyema baina ya watu katika jamii. Pia kama ambavyo uwanja wa mashidano ni lazima uwe sawa kwa wanamashindano wote, kadhalika ni lazima fursa na mazingira ya kushindania haki za kijamii yawe sawa kwa wanajamii wote, na yatoe nafasi kwa kila mwanajamii kushiriki mashindano haya ya kijamii, hivyo ni lazima mazingira yaandaliwe kwa ajili ya kila mmoja kwa usawa. Lakini ni kama tunavyojua kuwa mashindanoni huwa kuna kadhia ambayo huwa haiwahusu waandaaji wa mashindano bali humuhusu mshindani mwenyewe, nayo ni ile bidii, harakati na kujituma kwake, na hili ndilo ambalo huwezesha mshindani kushinda au kushindwa, hili ndilo jukumu la kila mwanajamii mshiriki, ambaye kwa kadiri ya juhudi zake ndivyo atakavyopata alama zake ambazo ndio haki yake ambayo ni lazima iheshimiwe na jamii. MWISHO
99
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 99
2/17/2017 1:24:32 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
Orodha Ya Vitabu Vilivyo Chapishwa Na Al-Itrah Foundation 1.
i) Qur’ani Tukufu – Pamoja na Tarjuma ya Kiswahili ii) Qur’an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Thelathini 2. Uharamisho wa Riba 3. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza 4. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili 5. Hekaya za Bahlul 6. Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) 7. Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (a.s.) 8. Hijab vazi Bora 9. Ukweli wa Shia Ithnaashari 10. Madhambi Makuu 11. Mbingu imenikirimu 12. Abdallah Ibn Saba 13. Khadijatul Kubra 14. Utumwa 15. Umakini katika Swala 16. Misingi ya Maarifa 17. Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia 18. Bilal wa Afrika 19. Abudhar 20. Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu
100
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 100
2/17/2017 1:24:32 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
21. Salman Farsi 22. Ammar Yasir 23. Qur’an na Hadithi 24. Elimu ya Nafsi 25. Yajue Madhehebu ya Shia 26. Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur’an Tukufu 27. Al-Wahda 28. Ponyo kutoka katika Qur’an 29. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii 30. Mashukio ya Akhera 31. Al Amali 32. Dua kwa Mujibu wa Ahlulbayt (a.s) 33. Udhuu kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna 34. Haki za wanawake katika Uislamu 35. Mwenyezi Mungu na sifa zake 36. Kumswalia Mtume (s) 37. Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) 38. Adhana 39. Upendo katika Ukristo na Uislamu 40. Qur’ani na Kuhifadhiwa Kwake 41. Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu 42. Kupaka juu ya khofu 43. Kukusanya Sala Mbili 44. Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara 101
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 101
2/17/2017 1:24:32 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
45. Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya 46. Kusujudu juu ya udongo 47. Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s) 48. Tarawehe 49. Malumbano baina ya Sunni na Shia 50. Kupunguza Swala safarini 51. Kufungua safarini 52. Umaasumu wa Manabii 53. Qur’an Yatoa Changamoto 54. as-Salaatu Khayrun Mina -’n Nawm 55. Uadilifu wa Masahaba 56. Dua e Kumayl 57. Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu 58. Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake 59. Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata 60. Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mtume Muhammad (s) 61. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza 62. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili 63. Kuzuru Makaburi 64. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza 65. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili 66. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu 67. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne 68. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano 69. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita 102
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 102
2/17/2017 1:24:32 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
70. Tujifunze Misingi Ya Dini 71. Sala ni Nguzo ya Dini 72. Mikesha Ya Peshawar 73. Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu 74. Ubora wa Imam ‘Ali na Ushia ndio njia iliyonyooka 75. Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake 76. Liqaa-u-llaah 77. Muhammad (s) Mtume wa Allah 78. Amani na Jihadi Katika Uislamu 79. Uislamu Ulienea Vipi? 80. Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) 81. Dhana ya Ndoa ya Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) 82. Urejeo (al-Raj’ah) 83. Mazingira 84. Utokezo (al - Badau) 85. Hukumu ya kujenga juu ya makaburi 86. Swala ya maiti na kumlilia maiti 87. Uislamu na Uwingi wa Dini 88. Mtoto mwema 89. Adabu za Sokoni Na Njiani 90. Johari za hekima kwa vijana 91. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza 92. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili 93. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu 94. Tawasali (AT- TAWASSUL) 103
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 103
2/17/2017 1:24:32 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
95. 96. 97. 98. 99. 100. 101. 102. 103. 104. 105. 106. 107. 108. 109. 110. 111. 112. 113. 114. 115. 116. 117. 118. 119.
Imam Mahdi katika Usunni na Ushia Hukumu za Mgonjwa Sadaka yenye kuendelea Msahafu wa Imam Ali Maimamu wa Ahlul Bait – Ujumbe na Jihadi Idi Al-Ghadir Kusoma sura zenye Sijda ya wajibu Hukumu zinazomuhusu mkuu wa kazi na Mfanyakazi Huduma ya Afya katika Uislamu Sunna za Nabii Muhammad (saww) Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza) Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili) Shahiid Mfiadini Mwanamke Na Sharia Ujumbe -Sehemu ya Kwanza Ujumbe - Sehemu ya Pili Ujumbe - Sehemu ya Tatu Ujumbe - Sehemu ya Nne Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu Hadithi ya Thaqalain Ndoa ya Mutaa Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza Ukweli uliopotea sehemu ya Pili Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu Ukweli uliopotea sehemu ya Nne
104
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 104
2/17/2017 1:24:32 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
120. Ukweli uliopotea sehemu ya Tano 121. Mkutano wa Maulamaa wa Baghdad 122. Safari ya kuifuata Nuru 123. Fatima al-Zahra 124. Myahudi wa Kimataifa 125. Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi 126. Visa vya kweli sehemu ya Kwanza 127. Visa vya kweli sehemu ya Pili 128. Elimu ya Ghaibu ya Maimamu 129. Mwanadamu na Mustakabali wake 130. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Kwanza) 131. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Pili) 132. Khairul l’Bariyyah 133. Uislamu na mafunzo ya kimalezi 134. Vijana ni Hazina ya Uislamu 135. Adhana ni Ndoto au ni Wahyi? 136. Tabaruku 137. Saada Kamili – Kitabu cha Kiada cha Maadili 138. Vikao vya furaha 139. Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje? 140. Visa vya wachamungu 141. Falsafa ya Dini 142. Kuhuzunika na Kuomboleza 143. Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah 105
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 105
2/17/2017 1:24:32 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
144. Mjadala wa Kiitikadi 145. Kuonekana kwa Allah 146. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza) 147. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili) 148. Ndugu na Jirani 149. Ushia ndani ya Usunni 150. Maswali na Majibu 151. Mafunzo ya hukmu za ibada 152. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 1 153. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 2 154. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 3 155. Abu Huraira 156. Vipengee kadhaa katika Swala ya Jamaa na Msikiti. 157. Mazingatio kutoka katika Qur’an - Sehemu ya Kwanza 158. Mazingatio kutoka kaitka Qur’an - Sehemu ya Pili 159. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya kwanza 160. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya Pili 161. Shia na Qur’ani – Majibu na Maelezo 162. Falsafa ya Mageuzi ya Imam Husein (a.s) 163. Amali za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani 164. Elimu ya Tiba za Kiislamu - Matibabu ya Maimamu 165. Uislamu Safi 166. Majlisi za Imam Husein Majumbani 167. Je, Kufunga Mikono 168. Uislam wa Shia 106
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 106
2/17/2017 1:24:33 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
169. Amali za Makka 170. Amali za Madina 171. Asili ya Madhehebu katika Uislamu 172. Sira ya Imam Ali kuhusu Waasi 173. Ukweli uliofichika katika neno la Allah 174. Uislamu na Mifumo ya Uchumi 175. Umoja wa Kiislamu na Furaha 176. Mas’ala ya Kifiqhi 177. Jifunze kusoma Qur’ani 178. as-Sahifatul Kamilah as-Sajjadiyyah 179. Hayya ‘Alaa Khayri’l-’Amal Katika Adhana 180. Ukweli kuhusu Funga ya Siku ya Ashura 181. Dua za Miezi Mitatu Mitukufu (Rajabu, Shaabani na Ramadhani) 182. Uadilifu katika Uislamu 183. Mahdi katika Sunna 184. Maswali Ya Uchunguzi Kuhusu Uislam 185. Kazi na Bidii ni njia ya maendeleo 186. Abu Talib – Jabali Imara la Imani 187. Ujenzi na Utakaso wa Nafsi 188. Vijana na Matarajio ya Baadaye 189. Historia maana na lengo la Usalafi 190. Ushia – Hoja na Majibu 191. Mateso ya Dhuria wa Mtume (saww) 192. Maombolezo – Msiba wa Bwana wa Mashahidi (a.s.) 193. Shahidi kwa Ajili ya Ubinadamu 107
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 107
2/17/2017 1:24:33 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
194. Takwa 195. Upotoshaji Dhahiri katika (Turathi) Hazina ya Kiislamu 196. Amirul Muuminina (as) na Makhalifa 197. Tawheed Na Shirki 198. Kuvunja hoja iliyotumika kutetea Uimamu wa AbuBakr 199. Adabu za vikao na mazungumzo 200. Hija ya Kuaga 201. Uwazi baina ya Maslahi na Vikwazo 202. Fadhila za watukufu watano katika Sahih Sita 203. Mdahalo baina ya Mwanachuoni waKisunni na Kishia (Al- Muraja’aat) 204. Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (as) 205. Imam Husain ni Mfumo wa Marekebisho na Mageuzi 206. Mtazamo kuhusu msuguano wa Kimadhehebu 207. Nchi na Uraia – Haki na wajibu kwa Taifa 208. Mtazamo wa Ibn Taymiyyah juu ya Imam Ali (as) 209. Uongozi wa Kidini – Maelekezo na Utekelezaji wa Kijamii 210. Maadili ya Ashura 211. Mshumaa – Shahidi na Kifo cha Kishahidi 212. Mizani ya Hekima – Hadithi za Ahlul Bait (as) – Sehemu ya Kwanza 213. Imam Ali na Mambo ya Umma 214. Imam Ali na Mfumo wa Usawa 215. Uimamu na Tamko la Kutawazwa 216. Mfumo wa Wilaya 217. Vipi Tutaishinda Hofu? 108
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 108
2/17/2017 1:24:33 PM
UADILIFU KATIKA UIslamu
218. Kumswalia Mtume ni Ufunguo wa Utatuzi wa Matatizo 219. Maeneo ya Umma na Mali Zake 220. Nahju ‘L-Balagha– Majmua ya Khutba, Amri, Barua, Risala, Mawaidha na Semi za Amirul-Muuminin Ali bin Abu Talib (a.s.) 221. Mukhtar – Shujaa aliyelipiza kisasi dhidi ya wauaji wa Imam Husein (as) hapo Karbala 222. Mazingatio Katika Swala 223. Imam Hasan na Mfumo wa Kujenga Jamii 224. Vyakula Na Vinywaji 225. Kuelewa Rehema ya Mwenyezi Mungu 226. Imam Mahdi na Bishara ya Matumaini 227. Mtazamo Mpya - Wanawake katika Uislamu 228. Shia Na Sahaba - Majibu na Maelezo 229. Majanga Na Jukumu la Jamii 230. Shia Na Hadith - Majibu na Maelezo 231. Upotofu Ndani ya Kitabu cha Mitaala kwa Shule za Sekondari 232. Ugaidi Wa Kifikra Katika Medani Ya Kidini 233. Yafaayo kijamii 234. Uswalihina Dhahiri Na Batini Yake 235. Mkakati wa Kupambana na Ufakiri 236. Mwanamke Katika Harakati Za Mageuzi 237. Jihadi 238. Hija Katika Maneno Na Ujumbe Wa Imam Khomeini (R.A) 239. Tiba Ya Maradhi Ya Kimaadili 109
02-17_-4-75 x 7_Uadilifu Katika Uislamu_17 Feb_2017 .indd 109
2/17/2017 1:24:33 PM