Uimamu na Tamko la Kutawazwa اإلمامة والنص
Kimeandikwa na: Sayyid Abdul-Rahim al-Musawi
Kimetarjumiwa na: Hemedi Lubumba Selemani
Kimehaririwa na: Sheikh Haron Pingili
ترجمة
اإلمامة والنص
تأليف السيد عبد الرحيم الموسوي
من اللغة العربية الى اللغة السوا حلية
©Haki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION
ISBN: 978 - 9987 – 17 – 062 – 3
Kimeandikwa na: Sayyid Abdul-Rahim al-Musawi
Kimetarjumiwa na: Hemedi Lubumba Selemani
Kimehaririwa na: Sheikh Haron Pingili
Kimepangwa katika Kompyuta na: Al-Itrah Foundation
Toleo la kwanza: Agosti, 2014 Nakala: 1000
Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. - 19701, Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 / 2127555 Barua Pepe: alitrah@yahoo.com Tovuti: www.ibn-tv-com Katika mtandao: www.alitrah.info
Yaliyomo Neno la Mchapishaji........................................................................1 Neno la Jumuiya..............................................................................3 Uimamu na Tamko la Kutawazwa...................................................5 Nukta tenganishi kati ya kambi mbili wakati wa kuzungumzia Uimamu...............................................................9 Uhusiano kati ya Umaasumu na Tamko la Uimamu ........................................................................................ 11 Nadharia ya Tamko na Kanuni ya Shura.......................................14 Kwanza: Upande wa Kihistoria.....................................................15 Pili: Tamko la Nabii Juu ya Khalifa ni Dharura.............................18 Tatu: Hadhi ya Kisheria ya Maamuzi ya Shura, na Uhusiano wake na Uongozi uliothibiti kwa Tamko..................28 Uhusiano baina ya Baiya na Tamko la Kutawazwa.......................31 Mtukufu Mtume anafanya kazi ya kusisitiza nadharia ya Tamko.........................................................................34 Njia za Kidhana na Hali Halisi ya Kihistoria.................................40 Nadharia ya Tamko la Kutawazwa katika hadithi ya Imamu Ali na Ahlul-Bait...........................................................43 Kuwahusu Ahlul-Bait (a.s.) ...........................................................54
v
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
Yahusu Imam Ali (a.s.) kuwapa Baiya hawa watatu (Abu Bakr, Umar na Uthman) .......................................................58 Ushahidi wa Kihistoria Juu ya Usahihi wa Nadharia ya Tamko la Kutawazwa................................................61 Dalili za Kiriwaya zinazothibitisha Nadharia ya Tamko la Kutawazwa.....................................................................63 Ama yaliyopatikana kuhusu aina ya kwanza:................................64 Ama yaliyopatikana kuhusu aina ya pili: ......................................68 Mbabaiko wao katika kufasiri Hadithi hizi....................................69 Ama yaliyopatikana kuhusu aina ya tatu: .....................................76 Kuwaashiria Maimamu Kumi na Wawili, kupitia riwaya ya Kisunni..............................................................77 Muhtasari.......................................................................................78
vi
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
بسم اهلل الرحمن الرحيم NENO LA MCHAPISHAJI
K
itabu ulichonacho mikononi mwako asili yake ni cha lugha ya Kiarabu kwa jina la, al-Imamah wa ‘n-Nass kilichoandikwa na Sayyid Abdul-Rahaim al-Musawi. Sisi tumekiita, Uimamu na Tamko la Kutawazwa. Neno “Imam” linatokana na neno la Kiarabu imam. “Imam” maana yake ni kiongozi wa aina yoyote ile. Lakini katika istilahi za Kiislamu ni Kiongozi wa Umma wa Kiislamu, iwe ni taasisi au jumuiya ya Waislamu au mwenye kushika nafasi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) Katika muktadha huu Imam aliyekusudiwa hapa ni yule mwenye kushika nafasi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa amri ya Allah. Na katika hadithi mashuhuri ambayo hupatikana katika vitabu takriban vyote vya hadithi (riwaya), historia na tafsiri za Qur’ani, Mtume (s.a.w.w.) alisema kwamba watakuwepo baada yake Maimamu kumi na mbili. Bahati mbaya sana madhehebu za Kiislamu zimetofautiana juu ya suala hili la Uimamu na tafsiri zimekuwa nyingi kila mmoja akivutia upande wake na kupotosha maana halisi ya Uimamu kama ilivyoelezwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Hivyo, madhumuni makubwa ya kitabu hiki ni kuelezea maana halisi ya Uimamu kwa mujibu wa Qur’ani na hadithi za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni vitu ambavyo havina nafasi tena katika akili za watu. 1
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
Kwa hiyo, Taasisi yetu ya Al-Itrah imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu hususan wazungumzaji wa Kiswahili. Tunamshukuru ndugu yetu Al-Hajj Hemedi Lubumba Selemani kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kukitarjumi kitabu hiki kwa Kiswahili kutoka lugha ya asili ya Kiarabu. Aidha tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake. Allah awalipe wote malipo mema hapa duniani na kesho Akhera – Amin. Mchapishaji Al-Itrah Foundation
2
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
بسم اهلل الرحمن الرحيم NENO LA JUMUIYA
H
akika mirathi ya Ahlul-Bait ambayo imehifadhiwa na kambi yao na wafuasi wao dhidi ya upotovu inaonyesha ni kambi iliyokusanya aina mbalimbali za taaluma za Kiislamu. Kambi hii imeweza kulea nafsi mbalimbali zilizo tayari kunywa kutoka kwenye chemchemi hiyo, na kuupa umma wa Kiislamu wanavyuoni wakubwa wenye kufuata nyayo za ujumbe wa AhlulBait. Wanavyuoni waliokusanya vidodoso na maswali mbalimbali ya madhehebu na mitazamo tofauti ya kifikra kuanzia ndani ya desturi ya Kiislam hadi nje ya desturi hiyo, huku wao wakitoa majibu na utatuzi makini juu ya maswali hayo ndani ya karne zote. Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bait imefanya hima kutetea tukufu za ujumbe wa Uislamu na ukweli wake ambao umechafuliwa na makundi, madhehebu na wanaharakati mbalimbali wenye chuki na Uislamu. Jumuiya imefuata nyayo za Ahlul-Bait na za wafuasi wa kambi yao njema ambayo imefanya hima kujibu madai yenye kuendelea na daima ikijaribu kubaki ndani ya msitari wa mapambano kwa kiwango kinachohitajika ndani ya kila zama. Hakika uzoefu ambao umehifadhiwa ndani ya vitabu vya wanavyuoni wa kambi ya Ahlul-Bait katika dhamira hii ni wa aina ya pekee, kwa sababu una akiba ya kielimu inayotegemea akili na hoja, huku ukijiepusha na matamanio na upendeleo uliokatazwa. 3
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
Unazungumza na wasomi na wanafikra wenye fani maalumu, mazungumzo ambayo yanakubalika kiakili na yanapokewa na maumbile yaliyo salama. Jaribio hili la Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bait limekuja kuwapa watafuta ukweli hatua mpya ya uzoefu wa thamani katika ulingo wa mazungumzo na maswali na kujibu hoja za utata zilizotolewa zama zilizopita au zinazotolewa leo kwa njia ya Tovuti, na hasa kwa kupewa nguvu na baadhi ya duru zenye chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu. Ikijiepusha na uchochezi uliokatazwa, na ikiwa ni yenye kuhangaikia kuzishauri akili zenye kufikiria na nafsi zenye kutafuta haki, ili ziweze kufikia kwenye haki ambayo inatolewa na Kambi ya Ahlul-Bayt ulimwengu mzima, ndani ya zama ambazo akili inaerevuka na nafsi na roho zinaboreka kwa kasi ya pekee. Ni lazima tugusie kuwa mfululizo huu wa tafiti hizi umeandaliwa na Kamati maalumu toka jopo la wanavyuoni watukufu, hivyo tunatoa shukurani njema kwa hawa wote na kwa wasomi na wahakiki kwa kila mmoja miongoni mwao kupitia sehemu ya tafiti hizi na kutoa mchango wao wa thamani kuhusu tafiti hizi. Na sote tunategemea na kutaraji kuwa tutakuwa tumetoa kile tulichokiweza katika juhudi za kutekeleza baadhi ya wajibu tulionao mbele ya ujumbe wa Mtukufu Mola Wetu Mlezi ambaye alimtuma Mtume Wake na uongofu na dini ya haki ili aipe ushindi dhidi ya dini zote. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa shahidi. Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bait Kitengo cha utamaduni
4
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
بسم اهلل الرحمن الرحيم Bismillahi Rahman Rahiim
UIMAMU NA TAMKO LA KUTAWAZWA Mwenyezi Mungu amemuumba mwanadamu katika hali ya tabia, maumbile na uwezo unaomwezesha kutekeleza jukumu la ukhalifa wa Mwenyezi Mungu ardhini, na haiwezekani kwa kiumbe mwingine yoyote yule kusimamia jukumu hilo hata Malaika, kwani yeye mwenyewe aliamuriwa kumsujudia (binadamu). Na pambizoni mwa hayo, binadamu humiliki sehemu nyingine inayomzuia dhidi ya ufanisi wake, maendeleo yake na ukamilifu wake. Mwanadamu huyu kwa nguvu zake za juu upande mmoja, na kudidimia kwake upande mwingine, inaonyesha kuwa yeye ni kiumbe pekee ambaye anamiliki utashi na uhuru wa kuchagua kitendo imara na hatua munasibu kwa ajili ya kujenga maisha yake yenye raha. Na alipopewa mwanadamu huyu uwezo huo ambao umemtunuku harakati katika uwanja mpana na wigo wa mbali zaidi, kiasi kwamba harakati hizo zinavuka vitu vya kimaada, na pia kufichua kuwa uwepo wake una lengo maalumu lililowekwa na Mwenyezi Mungu, basi hakuumbwa bila lengo na hakuachwa bila majukumu, kama ilivyoeleza hilo Qur’ani Tukufu: “Je, mlidhani kwamba tumekuumbeni bure na kwamba nyinyi kwetu hamtarudiswa?” (Sura Muuminuna: 115) Na si mwanadamu pekee ndiye aliye na uhai katika ulimwengu huu chini ya lengo na mipango iliyohakikiwa, bali katika upande huu vinashirikiana naye viumbe vingine, mpaka maelezo ya Qur’ani 5
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
yakaweka wazi kuwa: “Na hatukuziumba mbingu na ardhi na vilivyomo kati yake kwa mchezo.” (Sura Dukhan: 38). Ikithibiti kuwa ulimwengu wote unakwenda kwa hekima na mpango, akiwemo mwanadamu, na vyote vinaelekea upande wa lengo hitajika, na kuwa kila kitu kina mwongozo wake, basi enyi walimwengu ni lipi lengo hasa ambalo kwa ajili yake mwanadamu kaumbwa? Qur’ani Tukufu inatenga lengo ambalo kwa ajili yake kaumbwa mwanadamu, Mwenyezi Mungu anasema: “Na sikuumba majini na watu ila wapate kuniabudu.” (Sura Dhariyat: 56). Hapa tunaona neno ‘Ila’, ambalo kwa mujibu wa lugha ya Kiarabu linamaanisha kuwa Mwenyezi Mungu hana lengo wala shabaha nyingine ya kumuumba mwanadamu ila ibada. Na herufi Lamu iliyopo kwenye kitenzi Liyaabuduni (Waniabudu) humaanisha sababu, hivyo mwanadamu kaumbwa kwa sababu ya ibada, na wala si jingine. Hivyo iwapo lengo la kuumbwa mwanadamu limefungika kwenye ibada na si jingine, basi ni ipi hiyo ibada yenyewe? Na ni upi uhalisia wake? Ikiwa shabaha na lengo kuu la kuumbwa mwanadamu ni kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu, na kumwabudu ambako kupitia huko mwanadamu hukamilika, basi ni kichocheo kipi na ni msukumo upi ulio na dhamana ya kumfikisha mwanadamu kwenye lengo lake na ukamilifu wake? Hakika mwanadamu kwa maumbile yake na tabia yake hutambua mahitaji yake ambayo kupitia hayo anaweza kuziba upungufu uliyopo kwake. Kama ambavyo hutambua haja yake ya kupata nyenzo zitakazomfikisha kwenye ukamilifu wake, na hapo hufanya juhudi kuzitafuta, lakini ni vipi atakavyofanikiwa kuufikia ukamilifu? 6
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
Kuanzia hapa tunakuta hekima ya Mola Mlezi imelazimika kuweka mikononi mwa mwanadamu huyu nyenzo hizo, na mifano halisi amabayo kupitia kwayo atapata maarifa, misingi na malezi ambayo yatamshika mkono hadi kwenye ukamilifu. Na ilipokuwa utambuzi wa mwanadamu pekee umeshindwa kumchukua mwanadamu huyu na kumwongoza njia ya sawa, hata kama atasaidiana na nduguye mwanadamu, kwa sababu la juu kabisa analolimiki mwanadamu ni msaada ulio ndani ya nyanja mbili za akili na hisia, na nyanja hizi mbili hazitoshelezi kutambua mambo yanayolazimu kupata ukamilifu. Hivyo kuanzia hapa ndipo uliponyooka mkono wa nguvu za ghaibu (Mwenyezi Mungu) ili kuielekeza haja hii ya mwanadamu, nayo ndio haja muhimu zaidi, hivyo mwanadamu wa kwanza akawa Nabii aliyetumwa na Mwenyezi Mungu, Mwenye kuongoza njia ya sawa. Na jukumu la Manabii mbele ya watu ni kubainisha maarifa, maadili na mambo yenye kufikisha kwenye ukamilifu na malezi sahihi juu ya hayo. Unabii hufanya kazi ya kufafanua maalumati ambayo mwanadamu anaweza kuyatambua ilihali akiwa anayahitajia, ila hafikii kiini chake kutokana na malezi mabaya. Au haya maalumati yanahitaji uzoefu wa muda mrefu ili mwanadamu ayagundue, mfano kanuni za kiungu ambazo jinsi zilivyo ni lazima zisambaratishe uhai wa mwanadamu. Au kanuni za kiungu ambazo lau kama mwanadamu atazichagua basi zitampelekea kupata wema wake na ukamilifu wake, lakini anajitenga nazo kutokana na msukumo wa mambo ya kimaada. Basi kuanzia hapa ndipo inajitokeza nafasi ya Nabii ili akumbushe na kuonya. Mwenyezi Mungu amesema: “Basi kumbusha hakika wewe ni mkumbushaji tu.” (Sura Ghashiya: 21). 7
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
Kama pia inavyodhihirika nafasi ya Nabii na dharura ya kuwepo kwake kama kigezo anayewakilisha katika amali njema, kwa sababu yeye ni mwanadamu mkamilifu katika mienendo yake, tabia zake, na mihanga yake, na hii ndio huitwa nafasi ya umaasumu. Mwenyezi Mungu amesema: “Na akiwatakasa na akiwafunza Kitabu na hekima” (Sura Jumua: 2). Ikiwa lengo la kuumbwa mwanadamu ni ibada ya Mwenyezi Mungu isiyo na mipaka, na mwanadamu kwa maumbile yake ameumbwa katika hali ya kufungamana na njia ambayo imedhamini kumfikisha kwenye ukamilifu, kwa sababu anaelekea kwenye ukamilifu na huba yake, kwa njia ya kimaumbile, na hapo kazi ya Nabii ni kuweka wazi miongozo ya njia na kubainisha maarifa ya kweli ambayo yatamfikisha kwenye ukamilifu, basi ni ipi sababu inayopelekea risala kuendelea kupitia Uimamu ambao Shi’ah wanaona ni sharti uwe na tamko na elimu ya kutunukiwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na pia umaasumu? Jibu la swali hili na maswali mengine linatupelekea kujiuliza: Ni upi Uimamu kwa mtazamo wa Mwenyezi Mungu? Na ni upi umuhimu wake? Na baada ya kuainika mahali pa mzozo tunaweza kujibu utata unaopatikana ndani ya vichwa kuhusu Uimamu na sharti zake. Kuanzia elimu, umaasumu na nyinginezo miongoni mwa sharti za lazima kwa Imamu (a.s.).
8
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
NUKTA TENGANISHI KATI YA KAMBI MBILI WAKATI WA KUZUNGUMZIA UIMAMU Uimamu na Ukhalifa kwa upande wa madhehebu ya Sunni umeelekea kwenye muhimili mmoja wenye kusisitiza kuwa Imam na Khalifa baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), ina maana ni kiongozi na mtawala wa kisiasa ambaye anaendesha na kusimamia shughuli za serikali ya Kiislamu baada ya kifo cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Na kwa msingi huu, kambi hii haioni sababu yoyote ya kiongozi huyu kuthibiti kwa tamko na uainisho kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na ubainifu wa Mtume (s.a.w.w.), bali jambo hilo limeachiwa umma, ambapo umsimike yeyote utakayemchagua na kumwona anafaa kusimamia jukumu hili. Kwa sababu nafasi ya Imamu na Khalifa kwa mtazamo wa kambi hii, haivuki zaidi ya uongozi wa kisiasa na utawala wa umma ndani ya mipaka hii. Hivyo kimantiki njia ya kumsimika Khalifa itakuwa ni ima kwa nadharia ya Shura au uamuzi wa wenye madaraka au kwa njia ya urithi. Imebaki tufahamu ni zipi sharti ambazo ni lazima awe nazo mtu huyu anayependekezwa kwa ajili ya ukhalifa wa kisiasa baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)? Hakika sharti ambazo ni lazima atimize Khalifa huyu mchaguliwa, tunaweza kuzipata kupitia mtazamo wenyewe, ambao unaona Uimamu na ukhalifa baada ya Mtume (s.a.w.w.) ni uongozi na utawala wa kisiasa tu. Hivyo inatosha kupatikana kwa mwanadamu huyu ule uadilifu wa kimatendo wa maana ya kawaida, pamoja na sharti la elimu ya kawaida, na wala si sharti kuwa na 9
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
umaasumu na elimu ya kutunukiwa, hivyo inatosha kuwa na uwezo utakaomnyanyua hadi mustawa wa kutekeleza majukumu yake katika serikali ya Kiislamu. Na matokeo ya rai ya kambi ya Kisunni kuhusu Uimamu na ukhalifa ni kuwa, wenyewe hauvuki zaidi ya kuwa uongozi wa kisiasa, na sheria ya kuupata inatimia kwa njia ya uchaguzi na Shura, au nguvu za kijeshi au urithi au wasia, kama ilivyo wazi jinsi ulivyotekelezwa utaratibu huu kivitendo na kiutata baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Na sharti lake ni uadilifu na elimu ya maana ya kawaida. Na kwa ajili hii baadhi wamekuwa wakihoji dharura ya kuwepo Imamu aliye ghaibu, au dharura ya kuwa maasumu, au dharura ya kuainishwa kwa tamko rasmi la Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Ama kambi ya Kishia, yenyewe katika kuusimika Uimamu na ukhalifa baada ya Mtume (s.a.w.w.), imeona kuwa ni mamlaka ya kiungu, kama yalivyo mamlaka ya Mtume, na ni yenye kuendelea mpaka mwisho wa dunia, hivyo wakaona ni sharti upatikane humo umaasumu hata kabla ya kubalehe, pamoja na elimu isiyokuwa ya kujifunza, na tamko rasmi ambalo huwakilisha hadhi ya kisheria kwa Imamu. Kwa ajili hii kambi ya Kisunni haioni kuwa sharti hizi zina maana yoyote, kwa sababu hazioani na mamlaka ambayo Khalifa ana dhamana ya kuyatekeleza, hivyo hapa sharti zina wigo mpana na mkubwa kuliko mamlaka ya uongozi wa kisiasa. Hili ndilo fundo na nukta tenganishi ambayo inatufasiria myumbo uliogubika katika kuuelewa Uimamu na kutilia shaka katika suala la umaasumu, au uhalali wa dharura ya kuwepo tamko la kutawazwa. Uwelewa huu umewasukuma baadhi kuhakiki misingi ya nadharia ya tamko la kutawazwa, ili matokeo yake yakomee 10
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
kwenye kutokuwepo ukweli wa kihistoria kuhusu nadharia hiyo katika maisha ya Maimamu. Hakika chochezi hizi kuhusu Uimamu, ukhalifa na nadharia ya tamko, na shaka ambazo zinaugubika, zimetokana na uwelewa wa Kisunni juu ya Uimamu. Lakini lililo sahihi ni kuwa, Uimamu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna unauvuka uwelewa huu, nao una upeo unaotofautiana kimsingi na uwelewa wa juu juu wa Uimamu wa kiungu baada ya unabii. Hivyo kambi ya Ahlul-Baiti inaitakidi kuwa Uimamu wa Maimamu kumi na wawili una nyanja zingine zinazolazimu kuwepo shuruti nzito na kali kuliko zile za uongozi wa kisiasa.1
UHUSIANO KATI YA UMAASUMU NA TAMKO LA UIMAMU Ikiwa nafasi ya Imam – yeye – ni marejeo ya kidini, na kuwa mamlaka yake kisheria yanavuka hadi kwenye nyanja mbalimbali katika akida, hukumu, maadili na uongozi, basi ni wajibu kumtii, kumfuata na kuchukua toka kwake, na kwa njia hii kauli za Imam maasumu, vitendo vyake na ridhaa zake vinakuwa ni hoja ya kisheria yenye kuondoa dhima na kuleta udhuru, kama ilivyo hoja ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Mamlaka haya nyeti kabisa ya kiungu yanalazimu mambo mengi, kati ya hayo ni awe maasumu kama umaasumu wa Mtume (s.a.w.w.) katika shakhsia yake, katika kupokea, kubalighisha na mwenendo. Na kutokana na haya inabainika kuwa umaasumu kwa maana hii si sharti kwa ajili ya uongozi wa kisiasa tu. 1
Rejea Bahthu Hawlal-Imamah cha Sayyid Kamalu Al-Haydariy. 11
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
Na mamlaka ya Uimamu yanawajibisha Imam awe Aalimu wa yale wanayoyahitaji watu katika mambo ya maisha yao na Akhera yao, na ni lazima awe mbora kuliko wote waliopo juu ya ardhi katika zama zake ili aweze kufanikiwa kutekeleza jukumu lake. Shi’ah wanasema kuwa Mtume (s.a.w.w.) hana nafasi ya kujitegemea katika kumwainisha Khalifa, bali yeye (s.a.w.w.) humsimika na kumtolea tamko la kumtawaza kwa amri ya Mwenyezi Mungu, kwa sababu lengo la Uimamu na shabaha yake ya kiungu vinafungamana na maudhui ya mwisho wa unabii na kuendelea kwa uongofu wa kiungu muda wote. Na hekima ya kuhitimisha unabii inafungamana na kitendo cha kumwainisha Imam maasumu, na Imam ndiye anayechukua dhamana ya kutimiza masilahi ya dharura ya umma wa Kiislamu baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Hivyo Uimamu hadhi yake ni itikadi na si kama hukumu za kifiqhi za kimatawi. Na nukta hii ndiyo ambayo inafanya sharti za Uimamu ziwe na ukubwa na upana wa namna hii, na kuwa zenyewe zinavuka wigo wa sharti za uongozi wa kisiasa. Ikiwa mamlaka ya Uimamu ni pana kuliko mamlaka makubwa ya uongozi wa kisiasa, na yamelazimu kuwepo sharti hizo, basi hili linapelekea iwe kuamiliana nayo na kuyasadiki ni msingi katika dini, kutokana na ukubwa wa risala yake. AsShahid At-Thaniy amesema katika Risala zake: “Msingi wa nne ni kusadiki Uimamu wa Maimamu kumi na wawili, na msingi huu umezingatiwa na kundi la haki la Imamiya katika kutimia imani, mpaka umekuwa ni miongoni mwa dharura za madhehebu yao, kinyume na wengine waliokhalifu, kwani hakika kwao wao msingi huu ni tawi.”2 2
l-Aqaidu Al-Islamiyyah Juz. 1, Uk. 282, nukuu kutoka kwenye Rasailus-Shahid AtA Thaniy Juz. 2 Uk. 145. 12
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
Hivyo tunakuta suala la kumchagua Imam na kumwainisha liko nje ya mipaka ya uwezo wa mwanadamu na vipaji vyao, na uchaguzi na pendekezo haviwezi kutambua umaasumu na anayeumiliki. Na pia uchaguzi hauwezi kumpata mtu ambaye anamiliki elimu ya kutunukiwa isiyo ya kujifunza, na mengineyo miongoni mwa vipawa na uwezo ambao wanaumiliki Maimamu (a.s.). Ama kuhusu uteuzi wa Imam kwa njia ya wanadamu kutokuwa shabihi ya unabii, ambao anauteua Mwenyezi Mungu na kugundulika kwa njia ya wahyi na tamko kuwa Yeye Mwenyezi Mungu ameuteua, bila shaka ni kuwa tofauti kati ya Nabii na Imam ni kwamba Yeye Mwenyezi Mungu humtambulisha Nabii kupitia muujiza na wahyi, na Imam kupitia muujiza na tamko la kutawazwa kutoka kwa Nabii. Sharifu Murtaza amesema ndani ya Risala zake katika mlango wa yale yaliyo wajibu kuyaitakidi katika unabii: “Mwenyezi Mungu ajuapo kuwa katika baadhi ya matendo tuna masilahi na manufaa, au humo mna yale yenye kuharibu katika dini, na akili haionyeshi hayo, huwajibika kumtuma Mtume ili atambulishe hayo. Na hakuna njia ya kumsadiki ila kwa muujiza. Na sifa ya muujiza ni uwe ni jambo lililo nje ya ada, na lenye kuoana na dai la Mtume na kuhusiana nalo, na liwe lisilowezekana juu ya viumbe katika jinsi yake, au sifa zake makhsusi, na liwe linatokana na tendo la Mwenyezi Mungu, au lenye kufuata nyayo za tendo lake Mwenyezi Mungu. Na iwapo litakaa mahali pa kusadiki basi ni lazima limtambulishe mwenye kusadikishwa, na la sivyo itakuwa vibaya (kiakili). “Na yale yaliyokuja kuhusu wenyewe katika mlango wa yale ambayo ni wajibu kuyaitakidi katika Uimamu na yanayohusiana nao, yamewajibisha umaasumu kwa Imam. Kwa sababu kama hatokuwa hivyo, haja ya kuwa na Imam itaendelea kuwepo, na hili litafika kwa maraisi na kukomea kwa Rais aliye maasumu. Na ni wajibu awe mbora kuliko raia wake na awe aalimu zaidi (yao), kutokana na 13
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
ubaya wa kiakili wa kumtanguliza asiye mbora mbele ya aliye mbora kuliko yeye, hivyo umaasumu ukiwajibika huwajibika kuwepo tamko kutoka kwa Mwenyezi Mungu juu yake, na kubatilika uteuzi wa Uimamu, kwa sababu viumbe hawana njia ya kumjua yule aliye na umaasumu.”3 Na kuanzia hapa ndipo tunakuta kuwa tamko la kutawazwa ni moja ya nguzo za Uimamu kwa mujibu wa mtazamo wa Shi’ah, ambao kwa nafasi yake unafichua ile siri ya kiroho na uwezo wa kiungu uliyowekwa kwa Imam. Na kisha tunakuta tamko linaweka wazi kwa kumteua Khalifa ambaye atachukua nafasi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu katika mamlaka yake ya kiungu na dharura ya kuendelea kwake (mamlaka).
NADHARIA YA TAMKO NA KANUNI YA SHURA Ikiwa mtazamo wa Uislamu kuhusu ukhalifa baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) unalazimu nadharia ya tamko, ambayo inaona ukhalifa baada ya Mtume unavuka zaidi ya uongozi wa kisiasa, basi ni upi msimamo wa Uislamu dhidi ya kanuni ya Shura, ambayo baadhi wameshikamana nayo kama nadharia ya utawala mkabala na nadharia ya tamko? Na ni upi uhusiano wa Shura na maamuzi yake dhidi ya Uimamu uliyothibiti kwa tamko la Mtume (s.a.w.w.)? Tutafuatilia suala hili kwa upande wa kihistoria kwanza, kisha pili tutagusia dharura ya kuwepo tamko juu ya Khalifa toka kwa Mtume. Na tatu, baada ya hapo tutazungumzia hadhi ya kisheria ya maamuzi ya Shura na uhusiano wake na utawala ambao umethibiti 3
l-Aqaidu Al-Islamiyyah Juz. 1, Uk. 281, nukuu kutoka kwenye Rasailus-Shahid AtA Thaniy Juz. 3, Uk. 18. 14
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
kwa tamko, ili tukomee kwenye hitimisho kuwa Shura haikuwa nadharia ya utawala wa Kiislamu, bali yenyewe ni kanuni tu yenye hadhi ya kimaelekezo inayosaidia kutoa maamuzi ya Kiislamu katika sekta za maisha na nyinginezo. Wakati huohuo maamuzi hayo hayawi na ulazima wa kushiriki Imam maasumu. Na hakika Shura iliyoundwa ndani ya tamaduni ya Kiislamu isiyokuwa ya Kiimamiya, si chochote ila ni nadharia tu yenye kuhalalisha tukio, na kujaribu kuongeza sura ya sheria juu yake (juu ya tukio hilo). Na inawezekana kusema kuwa, yenyewe ni nadharia ya kuhalalisha tukio na si nadharia ya kuweka sheria.
KWANZA: UPANDE WA KIHISTORIA Lililothibiti ni kuwa Uislamu haukuuacha umma kwa kuutelekeza bila nadharia ya uongozi, kutokana na kuamini kuwa jambo la kidini na kidunia halitimii ila kwa kuwepo kiongozi wa umma, mwenye kuongoza katika yale yenye wema wake (umma) katika maisha yake na akhera yake. Na kutokana na msingi huu wamesema: Hakika Uislamu uliuachia umma uteue wenyewe mfumo wa kiuongozi, na unaoona kuwa unafaa zaidi kuhifadhi serikali yake na kulinda sheria, na hapo haitohesabika kuwa ni utelekezaji. Na kwa hali hii ukachomoza mtazamo ndani ya historia ya Kiislamu wenye kuegemeza suala la uongozi kwa ukamilifu kwenye tukio la kihistoria lililoukumba umma zama za masahaba. Na suala hili kubwa katika nidhamu ya dini ni vipi tutalipatia ufumbuzi hali ya kuwa sheria kupitia vyanzo vyake vikuu: Qur’ani na Sunnah, vimeghafilika nalo, na hatimaye jambo hilo kuuachia umma? Kuanzia hapa tunamuuliza je, kuna kanuni thabiti ambayo umma unaitegemea katika kumwainisha Khalifa? Na ni upi wigo wa kisheria wa kanuni hii? 15
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
Jibu - Wamesema: Kuna njia tatu za kumwainisha Khalifa: Njia ya Kwanza: Uteuzi wa watu wenye hadhi maalumu, yaani utaratibu wa Shura. Lakini utaratibu huu haukuchukua sura moja kwa sahaba, hivyo wameugawa kufuatana na tofauti hiyo, wakasema Shura ina sura mbili: (A) Utaratibu wa Shura mwanzo kama ulivyotokea kwenye Baiya ya Abu Bakr na Ali bin Abi Talib. (B) Utaratibu wa Shura wenye idadi maalumu inayoainishwa na Khalifa anayeondoka, kama alivyofanya Umar. Njia ya Pili: Urithi. Nayo ni Khalifa kabla ya kifo chake atoe tamko la mtu atakayechukua nafasi yake, na urithi huu una sura tatu: (A) Khalifa amrithishe mmoja, kama alivyofanya Abu Bakr kwa kumrithisha Umar ukhalifa. (B) Alirithishe kundi ambalo mmoja wao ndiye atakayekuwa Khalifa, kama alivyofanya Umar, pale alipouacha ukhalifa mikononi mwa kundi la watu sita, kati yao wamchague Khalifa atakayefuata. (C) Auache mikononi mwa watu wawili au zaidi, lakini aratibu ukhalifa kati yao kwa kusema: Khalifa baada yangu ni fulani, atakapofariki basi Khalifa baada yake atakuwa ni fulani. Katika utaratibu huu ukhalifa utahama baada yake kwa kufuata utaratibu aliouweka. Kama Sulayman bin Abdul Malik alivyomkabidhi Umar bin Abdul Aziz baada yake, kisha ukaenda kwa Yazid bin Abdul Malik, na hivyo hivyo aliuratibu Harun kati ya wanawe watatu wa kiume. Njia ya Tatu: Nguvu za kijeshi na ushindi wa silaha: Imamu Ahmad amesema: “Uimamu ni kwa aliyeshinda.”4 Dhahiri ni kuwa nadharia hii kwa njia zake ni nadharia ya kuhalalisha na si nadharia ya kuweka sheria. Yenyewe ni nadharia ya kuhalalisha tukio na kuliongezea baraka ya kisheria, na sababu ya pekee iliyopelekea 4
Al-Ahkam As-Sultaniyah, Uk. 20-23. 16
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
kuwepo uhalalisho huu ni kuwaepusha masahaba na tuhuma ya kuunda jambo hili la hatari, bila dalili yoyote ya kisheria, na kuficha tija iliyotokana na kitendo hicho. Kwa ajili hiyo ndani ya nadharia hii (ya Uislamu kuuachia umma uteue wenyewe mfumo wa kiuongozi) kumezuka hali ya kutumia nguvu na ulazimishaji usiyofichika, na kati ya hali hiyo ni:
5
a.
Yoyote kati ya njia hizi tatu, haitegemei dalili yoyote ya kisheria, na wala hawaitambui hata wanafiqhi wa zama za sahaba kabla haijadhihiri (njia hiyo) kupitia tukio.
b.
Hakika kanuni ya Shura iliyotajwa katika njia ya kwanza iliyochukuliwa toka kwenye Baiya ya Abu Bakr, haikutimia kwenye Baiya hiyo, na hakuna yeyote anayeweza kudai utimilifu huo baada ya Umar kuisifia kuwa ni ya vurugu tupu, isiyo na ushauri wowote. Isipokuwa baadaye walikuja (miongoni mwa masunni) wakakiongezea kitendo hicho rangi ya Shura ili kutokana nacho waweke ndani ya vazi lake jipya sura ya kwanza ya kisheria katika kumchagua Khalifa, na baadhi wakakiongezea rangi ya Ijmai.5
c.
Khofu ya kutokea machafuko ilikuwa udhuru uliyoteuliwa katika kuhalalisha Baiya ya kwanza ya Khalifa wa kwanza pindi ilipotimu bila ya ushauri wowote, na wala haikungojewa wahudhurie wengi miongoni mwa sahaba wakubwa kati ya Muhajirina na Ansari, miongoni mwa wale wanaofaa kuwa vinara wa watu wenye hadhi maalumu. Hivyo udhuru uliopelekea kuharakisha ni khofu dhidi ya tofauti na vurugu, jambo hili ni dhahiri kwenye maelezo ya hotuba ya Umar.
Minhajus-Sunnah cha Ibnu Taymiyya Juz. 3, Uk. 215-218. 17
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
Lakini la ajabu ni kuwa vurugu imerudi na kuwa njia ya kisheria kati ya njia za kumwainisha Khalifa katika njia ya tatu, kwani wanaona nguvu na ushindi wa silaha ni njia ya kuupata ukhalifa, na daima mwenye kushinda ndiye Khalifa wa kisheria ambaye ni wajibu kumtii. Na bado njia hiyo iko wazi mbele ya kila mwenye kutamani. Na je kuna vurugu kuliko hiyo?
PILI: TAMKO LA NABII JUU YA KHALIFA NI DHARURA Al-Farau amesema ndani ya kitabu Al-Ahkam As-Sultaniya: “Hakuna mzozo kuwa ndani ya tamko imethibiti haki ya Khalifa anayechukua nafasi yake, na hakuna shaka kuwa tamko hili linafanya kazi, kwa sababu Imamu ndiye mwenye haki zaidi na hilo, hivyo uteuzi wake ndani ya hilo ni wenye kufanya kazi, na katika hilo hautegemei ridhaa ya watu wenye hadhi maalumu.”6 Hiyo imekuwa haki ya khalifa kuchelea yasitokee machafuko na umma kutikisika.7 Na kwa ajili hiyo ndio maana baadhi ya masahaba walikuwa wakimrejelea Umar wakimuomba atoe tamko la kuonyesha ni nani atakayechukua nafasi yake.8 Ibnu Hazmi ameunga mkono maneno haya, akasema: “Tumekuta kuwa usimikaji wa Uimamu unasihi kwa njia mbalimbali: Ya kwanza, ambayo ni sahihi zaidi na bora zaidi ni Imamu anayetarajia kufariki amrithishe mwanadamu atakayemchagua kuwa Imamu baada ya kifo chake. Sawa afanye hivyo wakati wa siha yake au wa kifo l-Ahkam As-Sultaniyah cha Al-Farau Uk. 10; Al-Ahkam As-Sultaniyah cha Al-Baghawi A Uk. 25-26. 7 Al-Fiswalu Juz. 4, Uk. 169. Tarikhul-Umam Al-Islamiyyah cha Al-Khadhariyyu Juz. 1, Uk. 196. 8 Al-Kamil Fit-Tarikh Juz. 3, Uk. 65. 6
18
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
chake, kama alivyofanya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa Abu Bakr, na kama alivyofanya Abu Bakr kwa Umar, na kama alivyofanya Sulayman Ibnu Abdul Malik kwa Umar bin Abdul Aziz.” Akasema: “Na njia hii ndio tuliyoichagua na hatupendelei nyingine, kutokana na muungano wa Uimamu uliyomo ndani ya njia hii, na kule kupangika kwa uongozi wa Uislamu na Waislamu, na kule kuondoa ikhtilafu na vurugu inayokhofiwa, ambayo inatarajiwa kupatikana katika njia nyinginezo, ikiwa ni pamoja na kubakia umma bila mwelekeo, kugawanyika uongozi na kuzuka wenye tamaa.”9 Isipokuwa ni kuwa tu tamko linalodaiwa juu ya Abu Bakr halijathibiti, bali hakuna yeyote aliyedai uwepo wake, bali umma umekongamana juu ya kutokuwepo kwake, hivyo atakayetaka kuthibitisha tamko mfano wa hili kwa Abu Bakr pekee, ni juu yake kulikataa tukio la Saqifa kimukhtasari na kiundani. Na ni juu yake apinge yote yale yaliyothibiti kunakiliwa ndani ya Sahih Sita, kuanzia maneno ya Abu Bakr, Umar, Ali, Abbas na Zubair kuhusu ukhalifa. Na baada ya hapo ni juu yake abomoe misingi yote ambayo juu yake imesimama nadharia ya Masunni kuhusu Uimamu. Kwanza nadharia hii haijajengeka ila juu ya msingi mmoja, nao ni Baiya ya Abu Bakr, kwa njia ile ambayo ilitimia ndani ya Saqifa na baada yake, kutokana na tukio hilo, kwanza ilizalika nadharia ya Shura kati ya watu wenye hadhi maalumu. Na ni juu yake akanushe Ijmai iliyothibiti kwao: “Ijmai ya kuwa hakuna tamko limpalo haki (ya ukhalifa) Abu Bakr.”10 Kuanzia hapa ndipo Al-Ghazali alipofuatilizia maneno yenye kuafiki Ijmai hii, humo ameitia dosari ile hoja aliyojengea Ibnu Hazmi kauli yake. Al-Ghazali amesema huku akijiuliza: “Je, mumesema kuwa kutoa tamko ni wajibu kutoka kwa Mtume na Khalifa, ili kwalo 9
Al-Fiswalu Juz. 4, Uk. 169. Sharhul-Maqaswid Juz. 5, Uk. 255.
10
19
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
akate kamba ya ikhtilafu?” Kisha akajibu akisema: “Tumesema kuwa lau kama ingekuwa ni wajibu basi Mtume angetoa tamko juu yake, na yeye hajatoa tamko, na pia Umar hajatoa tamko.”11 Ibnu Hazm anapoendelea kuonyesha nadharia yake unamwona anazidi kuivunjilia mbali kwa ukamilifu nadharia ya Shura na ule uteuzi wa watu wenye hadhi maalumu, na analiegemeza suala la uteuzi wa Khalifa kwenye tamko, kwa sababu yeye amekinaika na dharura ya kuwepo tamko la kutawazwa, lakini yeye anataka tamko lenye kuoana na tukio lililotokea (lile la Baiya ya Abu Bakr), hata kama halina nguvu ya dalili. Hakika tamko ndani ya nadharia hii halijajificha abadani asilani, na Shura hapa si hatamu isiyo na kitanzi, hivyo watu wenye hadhi maalumu hawana haki ya kumchagua wamtakaye bila sharti lolote, kwa sababu kuna mipaka ambayo ni lazima Shura iiheshimu, na mipaka hii imewekwa na tamko lililothibiti. Wamesema: Hakika kati ya sharti za Uimamu ni nasaba ya Kikuraishi. Haupatikani Uimamu kwa mwingine…… Na wakathibitisha hilo kwa tamko lililothibiti, kwani bila shaka imethibiti kutoka kwa Nabii (s.a.w.w.) kuwa alisema: “Maimamu ni kutoka kwa Kuraishi.” Na akasema (s.a.w.w.): “Watangulizeni Makuraishi na wala msiwatangulie.” Na tamko hili halina mkabala wenye kufanana nalo, na wala kauli yenye kukhalifiana nalo.12 Na wameona ni sharti Mkuraishi huyu awe ni wa asili, atokanaye na kizazi cha Nadhiri bin Kinana, ili tamko litimie ilivyo.13 Imamu Ahmad amesema: “Asiyekuwa Mkuraishi hawi Khalifa.”14 Na Al-Iqtiswad Fil-Iitiqad, Uk. 151. Al-Ahkam As-Sultaniyah cha Al-Mawaridiy Uk. 6. 13 Al-Ahkam As-Sultaniyah cha Al-Farau Uk. 20. Al-Fiswalu Juz. 4, Uk. 89. MaathirulInafah Juz. 1, Uk. 37. Muqaddimat Ibnul-Khaldun, sehemu ya 26 Uk. 242 – 245. 14 Al-Ahkam As-Sultaniyah cha Al-Farau Uk. 20. 11
12
20
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
wametoa dalili kuthibitisha ueneaji wa tamko hili, kwa kile kitendo cha Ansari kuwakabidhi na kuwaachia ukhalifa Muhajirina walio Makuraishi, pindi walipowatolea hoja kupitia tamko hili huko Saqifa.15 Ibnu Khaldun amesema: “Jamuhuri wamebakia kwenye kauli ya kuwa wenyewe – Ukuraishi - ni sharti, na ukhalifa unasihi kwa Mkuraishi hata kama ni mtu asiyeweza kusimamia mambo ya Waislamu.”16 Hivyo ndivyo lilivyothibiti tamko la kisheria na kuthibiti ueneaji wake, na Ijmai ikathibiti juu yake. Na lenye kuweka wazi zaidi jambo hili ni pale msingi wa tamko ulipoushinda msingi wa Shura, pale Khalifa wa pili alipoona dharura ya kuwepo tamko juu ya yule atakayechukua nafasi yake, hapo tamko likashika hatamu ya mfumo wa kisiasa, japokuwa wenyewe unatokomeza mbali kanuni ya Shura kwa ukamilifu. Zaidi ya hapo ni kuwa tamko la Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Maimamu ni kutoka kwa Makuraishi.” Linaushinda msingi wa Shura mbele ya upanga, hivyo atakayeushinda umma na akanyang’anya ukhalifa kwa upanga, na akawa ni Mkuraishi basi ukhalifa wake unasihi, kwa sababu hatokuwa nje ya tamko lililotangulia. Na hivyo hivyo halijali sharti za wajibu ambazo ni wajibu awe nazo Khalifa, ikiwemo ijtihada (katika dini), uadilifu na uchamungu. Hivyo ikiwa Khalifa ni Mkuraishi basi ukhalifa wake unasihi hata kama ni dhalimu, bali hata kama hawezi lolote katika majukumu ya ukhalifa. Hivyo basi Shura inapasa isitoke nje ya wigo wa tamko hili, hivyo haimteui ila yule aliye Mkuraishi wa asili kinasaba. Muhtasari wa suala hili ni kuwa: Limethibiti kwetu tamko la 15 16
Muqaddimat Ibnul-Khaldun, sehemu ya 4, Uk. 89. Al-Ahkam As-Sultaniyah cha Al-Farau Uk. 243. 21
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
wazi, sahihi na lenye nguvu katika nadharia hii, nalo ni Hadithi tukufu: “Maimamu ni kutokana na Kuraishi.”. Bukhari, Muslim na waandishi wa Sunnan na Sira, wameiandika kwa lafudhi tofauti, na kiini chake ni hicho. Lakini tamko hili linahitaji kufanywa mahususi, na hilo ni kutokana na baadhi ya mambo, ikiwemo: 1.
Hakika tamko lililotangulia: “Maimamu ni kutokana na Kuraishi,” lenyewe pekee haliuhakikishii umma shabaha ilengwayo na ambayo ndani yake kuna ulinzi wa dini na jamii, kiasi kwamba masahaba wao wenyewe walitambua ukweli huu tangu kuisha kwa ukhalifa wema.
Ndani ya Sahih Bukhar mna habari kuwa: “Ulipokuwepo mzozo kati ya Marwan bin Al-Hakam akiwa Sham, na Abdullah bin Zubair akiwa Makka, jamaa walimwendea Abu Barzata Al- Aslamiy wakamwambia: ‘Ewe Abu Barzata! Hivi huoni walimodumbukia watu?’ Akasema: ‘Hakika mimi nataraji mbele ya Mwenyezi Mungu, hakika mimi nimekuwa nayachukia makabila ya Makuraishi. Hakika yule aliyopo Sham, Wallahi hapiganii lolote ila dunia. Na hakika yule aliyopo Makka, wallahi hapiganii lolote ila dunia.”’17 2.
17 18
Na huko kuna matamko mengine sahihi yanaufinya wigo wa tamko lililotangulia, ikiwemo maelezo ambayo Mtume (s.a.w.w.) alihadharisha kujighuri kwa nasaba ya Kikuraishi, na kuonya kuwa hilo litapelekea kuangamia kwa umma na kufarakana jambo lao. Ndani ya Sahih Bukhari imeandikwa kuwa yeye (s.a.w.w.) alisema: “Kuhiliki kwa umma wangu kumo mikononi mwa vijana watokanao na Makuraishi.”18 Hivyo basi vipi itawezekana kuziweka pamoja hadithi hizi
Sahih Bukhar. Fitna, mlango wa 20, Hadithi ya 6695. Sahih Bukhari. Fitna, mlango wa 3, Hadithi ya 6649. Fat’hul-Bariy Bisharhis-Sahih Bukhar 13: 7 – 8. 22
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
mbili; “Maimamu ni kutoka kwa Kuraishi,” na ile “Kuhiliki kwa umma wangu kumo mikononi mwa vijana watokanao na Makuraishi.?” Ni lazima hilo litimie kwa njia ya kuzifanyia umakhususi zile habari zilizopatikana kuhusu haki ya Makuraishi. Na kuna aina mbili za umakhsusi: A.
Umakhsusi wa kuvua: Kunapatikana baadhi ya matamko ya wazi yanayolivua kundi fulani la Kikuraishi na kulitenga mbali na wigo wa kuheshimiwa. Ibnu Hajar AlHaythamiy amesema kuhusu Hadithi iliyopokewa kwa njia hasani, kuwa Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Kabila ovu kati ya makabila ya waarabu ni kizazi cha Umaiyyah, kizazi cha Hanifa na kizazi cha Thaqifu.” Akasema: “Na katika hadithi sahihi Al-Hakim amesema: Kwa mujibu wa sharti za Masheikh wawili - yaani Bukhari na Muslim - kutoka kwa Abu Barzata, alisema: “Waliokuwa wanachukiwa mno na Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) kati ya makabila au watu, ni kizazi cha Umaiyyah.”19
Zaidi ya hapo ni kuwa zile hadithi zilizopatikana khususan zikimshutumu Al-Hakam baba yake Marwan ni nyingi na mashuhuri. Sasa je, inasihi Uimamu kuuegemeza kwenye kabila ovu kati ya makabila ya Kiarabu, na ambalo ni watu wachukiwao mno na Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.)?! Hivyo ikiwa hawa ndio viongozi waliotokea, basi ni juu yetu tushuhudilie kuwa tukio hili limekwenda kinyume na tamko, badala ya kwenda mbio kufanya juhudi za kulihalalisha na kulitetea kupitia kivuli cha tamko. 19
Tatwhirul-Janan Walisan Uk. 30. 23
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
B.
Umakhsusi wa kukubali: Hadithi ambayo imewamaizi Makuraishi kwa kuwateua juu ya makabila mengine, ambayo haikuja kwa ajili ya wigo mpana wa Makuraishi, bali imehusu kundi maalumu miongoni mwa kabila hilo. Akasema Mtume (s.a.w.w.): «Hakika Mwenyezi Mungu alimteua Kinana toka kizazi cha Ismaili, na akamteua Kuraishi toka kizazi cha Kinana, na akamteua Hashim toka kizazi cha Kuraishi, na akaniteua mimi toka kizazi cha Hashim.»20 Na hii ni kukitanguliza kizazi cha Hashim mbele ya Makuraishi wengine.
Ibnu Taymiyya ameiandika hadithi hii sahihi na akaongeza akisema: “Na ndani ya Sunani mna habari kuwa Abbas alishitakia kwake (s.a.w.w.) kuwa baadhi ya Makuraishi wanawadharau! Mtume (s.a.w.w.) akasema: ‘Naapa kwa Yule Ambaye nafsi yangu imo mikononi Mwake, hawaingii peponi mpaka wawapendeni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kwa ajili ya ukaribu wangu.’. Na iwapo ndio viumbe bora basi hapana shaka amali zao ndio amali zilizo bora…..Aliye mbora zaidi kati yao ndiye mbora kuliko kila mbora toka makabila mengine ya Kikuraishi na Kiarabu, bali kuliko wana wa Israili na wengineo.”21 Hapa si sehemu ya ubora tu, bali ni kuwa Makuraishi imani yao haisihi maadamu hawajawapenda kizazi cha Hashimu mahaba ya aina mbili: Kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kwa ajili ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Je, inasihi Makuraishi wote wawe sawa katika haki ya kutangulia na Uimamu, na hali kati yao wamo kizazi cha Hashimu ambao tamko limewanyanyua mpaka hadhi ya juu kabisa, na kati 20 21
Sahih Muslim. Kitabu cha fadhila, Hadithi ya 1. Raasul-Husain cha Ibnu Taymiyya Uk. 200 – 201. Kimechapishwa kikiwa pamoja na kitabu Istish’hadul-Husain cha Tabari. 24
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
yao wamo kizazi cha Umaiyyah ambao tamko limewashusha mpaka kiwango cha chini kabisa? Ikiwa tukio limetufikisha katika hali hii basi ni juu yetu tushuhudilie kuwa ni tukio lililokwenda kinyume na tamko, na wala si tufanye juhudi kulihalalisha na kulisafisha. Na mukhtasari wa yaliyotangulia unaonyesha kwa uwazi kabisa kuwa, sisi hapo hatukufanikiwa kuhakiki nadharia iliyoshikana kuhusu maudhui ya Uimamu, na sababu halisi ya kutofanikiwa huku ni kule kufuata tukio kama lilivyo na kujibidiisha ili kulihalalisha, na kulifanya kuwa chanzo kikuu katika kutoa wasifu wa mfumo wa siasa. Hakika mkinzano wa kulichukulia tukio kama lilivyo, uliopo katika duru zake mbalimbali, wote umedhihiri ndani ya nadharia hii, jambo ambalo limeikosesha hadhi yake ya kuwa nadharia ya Kiislamu katika utatuzi wa moja ya kadhia kubwa za Kiislamu. Hivyo kauli inayodai kuwepo tamko la kisheria haikufuatwa kiasi cha kufikia kwenye kiini cha tamko, wala hazikuheshimiwa shuruti zake na mipaka yake. Ama kauli ya kuwepo Shura, yenyewe imekula mweleka mbele ya tamko la Khalifa aliyetangulia na pia mbele ya kanuni za Shura, nguvu za kijeshi na ushindi wa silaha. Ama utaratibu wa watu wenye hadhi maalumu, wenyewe ndio fumbo gumu lisilojulikana, kwani kuna kipindi hao watu wenye hadhi maalumu, anakuwa ni mtu mmoja amejisimika mwenyewe na hatimaye wawili wakamfuata, kama ilivyo kwenye ndoa. Au akafuatwa na wane, au wanakuwa sita wanaoainishwa na Khalifa aliyetangulia, na si umma. Bali jambo hili lilipiga hatua sana hadi imefikia mwanafalsafa makini kama Ibnu Khaldun amewafanya ndugu, jamaa, wanafamilia na karaba wa Khalifa, bila kujali kiwango cha elimu yao, juhudi zao na uchamungu wao, kuwa nao ni watu wenye hadhi maalumu, ambao walimshinikiza Khalifa 25
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
Maamun ahamishie ukhalifa kwa Ali ar-Ridha, awe Khalifa baada yake.22 Na ukweli ambao tunataraji usimguse mtu ni kuwa, hili lilidhihiri hapo kabla katika nusu ya pili ya ukhalifa wa Uthman, pale ambapo walichomoza viongozi wa ushauri na sera toka katika karaba zake maalumu, ambao hawakuwa na fadhila yoyote wala juhudi yoyote katika dini, japokuwa walikuwapo wengi wasiokuwa wao waliokuwa na sifa hizo zama hizo. Na hawa watu wenye hadhi maalumu walikuwa ni Abdullah bin Amir, Abdullah bin Saad bin Abu Sarhi,23 Said bin Al-Aas, Muawiya bin Abu Sufyan na Marwan bin Al-Hakam. Tabari amenukuu kwa njia mbili kuwa: “Uthman aliwaita Muawiya, Abdullah bin Saad bin Abu Sarhi, Said bin Al-Aas, Amru bin Al-Aas na Abdullah bin Amir, akawakusanya ili awatake ushauri kuhusu jambo lake, akawaambia: ‘Hakika kila mtu ana mawaziri na washauri, nanyi ndio mawaziri wangu na washauri wangu na waaminifu wangu. Tayari watu wameshafanya yale mliyoyaona na wameniomba niwaondoe magavana wangu kazini, na niyarejeshe yote toka kwenye yale wanayoyachukia mpaka kwenye yale wayapendayo, hivyo fanyeni bidii kutoa rai zenu na kunionyesha.’ “Walimpa ushauri, alitenda kwa mujibu wa mjumuiko wa ushauri wao kama alivyoona, hivyo akawarudisha kwenye kazi zao na akawaamuru kuwabana waliokuwa kabla yao, na akawaamuru kuwapeleka watu mipakani kwa hoja ya kulinda mipaka, na akaazimia kuwanyima vipawa vyao ili wamtii na wamuhitajie.”24 Nadharia hizi Nadhariyatul-Imamah cha Dr. Ahmad Mahmud Subhiy Uk. 26. Na huyu ndiye aliyeritadi kurudi kwenye ushirikina zama za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ndipo Mtume akahalalisha damu yake na akaamuru auwawe hata kama atakutwa chini ya sitara za Kaaba. Rejea wasifu wake kwenye kitabu Al-Istiaab, Usudul-Ghaba na Al-Iswaba. 24 Tarikhut-Tabar, matukio ya mwaka 34 A.H. Juz. 4, Uk. 333-335. 22 23
26
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
zenye kupingana ni muhali zote kukusanyika katika nadharia moja, na hatimaye iwe nadharia yenye kuungana yenye sura iliyo wazi na yenye uwelewa uliyo sawa. Haya yote na zile shaka zinazojitokeza kuhusu ufaaji wa nadharia hii, vyote vinaipa nguvu rai nyingine ambayo inategemea tamko la kisheria katika kuainisha Khalifa wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Matokeo kama haya pia ameyatoa kwa ufupi Dr. Ahmad Mahmud Subhiy akiwa anadurusu nadharia ya Uimamu pale aliposema: “Ama upande wa kimawazo Ahlus-Sunna hawajatoa nadharia yenye kuungana kwenye siasa, yenye kuainisha maana ya Baiya, Shura na watu wenye hadhi maalumu, ukiachia mbali maneno yenye kutenganisha kati ya nadharia na utekelezaji, au kati ya lile lililo la sheria na kati ya yale yenye kuendelea kwenye tukio. “Hakika nadharia za Ahlus-Sunna zilidhihiri katika siasa zama za baadae baada ya dola ya Kiislamu kuimarika kwa nguvu. Kama ambavyo nyingi zilikuja kwa ajili ya upinzani dhidi ya Shia, na baadhi yao wakaomba watoe hukumu za kisheria kwa kufuata mfumo wa uongozi wa Makhalifa watatu wa mwanzo. Na hakika…….kati ya utoaji wa sheria wa wanafiqhi na kati ya hali halisi ya Makhalifa, ukiachia mbali uduni wa rai nyingi kati ya hizi, na kutoweza kwake kutoa kanuni ya kisheria, ndio kulikoimakinisha rai pinzani – kauli ya kuwepo tamko - yenye kuwakilishwa na kundi la Shia.”25
25
z-Zaydiyya Uk. 35-37. Pia tazama As-Siyasatu Al-Muaswiratu Lil-Shiatil-ImamiyatilA Ithna Ashariyya Uk. 25, cha Muhammad Abdul-Karim Attum. 27
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
TATU: HADHI YA KISHERIA YA MAAMUZI YA SHURA, NA UHUSIANO WAKE NA UONGOZI ULIOTHIBITI KWA TAMKO Hakika miongoni mwa vielelezo vya kisheria ambavyo nadharia ya Shura inavitegemea ni Aya Tukufu: “Na ushauriane nao katika mambo.” (Sura Aali Imran: 159)26 Aya hii inamlazimisha Imam Mtawala awajibike kufanya Shura, hiyo ni kwa mujibu wa rai ya yule aliyesema: “Hakika Aya katika kumsemesha Mtume (s.a.w.w.) imetamka wazi amri ya kufanya Shura, na amri huonyesha wajibu, na Aya kwa maana hii haina lingine zaidi ya kumtaka achukue ushauri kutoka kwa Waislamu: “Na ushauriane nao” (Sura Aali Imran: 159) na kwa kuwa haiwezekani kuchukua ushauri toka kwa Waislamu wote, basi ni lazima kufuata njia iwezekanayo katika ushauri huu, nayo ni kuchukua ushauri kutoka kwa wale werevu na wataalamu.”27 Na kwa maana hii je kinachohitajika hapa ni Shura yenyewe au yenyewe ni njia tu ambayo kupitia yenyewe yanatimia malengo mengine? Bila shaka Shura yenyewe kama Shura, haihitajiki hapa, na wala yenyewe si shabaha ilengwayo, bali Shura hapa ni njia tu ya kutimizia malengo mengine, na lengo muhimu zaidi kati ya malengo haya ni kujua mitizamo ya nadharia za wengine, mawazo yao, changamoto zao na fikra zao. Mawazo haya na fikra hizi vinapopatikana kutoka kwenye vyanzo tofauti na hatimaye kujikusanya eneo moja, huwa na 26
27
r-Raaziy amesema: “Wanachuoni wengi wanasema alifu na lamu zilizopo A kwenye tamko: al-Amri رمألاni alifu na lamu za ahadi siyo za istighraq, na kilichoahidiwa katika Aya hii ni vita na kumkabili adui, hivyo inakuwa kauli yake (swt): “Na ushauriane nao katika mambo.” ni mahususi kwa vita tu.” Tazama Tafsirul-Kaashif Uk.189. – Mhariri. Tafsirul-Mafatihil-Ghaib cha Fakhru Razi Juz. 2, Uk. 83. 28
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
thamani kubwa katika kuendesha siasa ya uongozi, idara, uchumi, amani na vita, na mengineyo ndani ya nchi, na upande huu hutimia kutoka kwa wasiokuwa maasumu, miongoni mwa wenye madaraka. Mpaka hapa yamekuwa wazi malengo ya kuwekwa kwa sheria ya Shura, lakini bado limebakia swali kuhusu hadhi ya kisheria iliyonayo Shura, na je matokeo yatokanayo na Shura ya Ijmai au ya wengi, ni maamuzi ambayo ni lazima kutekelezwa na Mtawala? Au la? Wanachuoni wa Kisunni katika kujibu swali hili wako katika makundi mawili: La kwanza: Kundi hili linaona kuwa matokeo ya Shura ni maamuzi ya lazima kwa Mtawala na serikali kwa ujumla. Miongoni mwao ni Sheikh Muhammad Abduh, amesema katika tafsiri yake: ‘Wenye madaraka’ (Sura Nisai: 59) maana yake wenye madaraka ya umma katika serikali yake, nayo ni amri iliyoashiriwa katika kauli yake: “Na mwendo wao ni kushauriana wao kwa wao.” (Sura Shura: 38) na haiwezekani kupatikana Shura kati ya wanaumma wote, hivyo inalazimika Shura iwe kati ya kundi linalowakilisha umma….na hawa si wengine bali ni watu wenye hadhi maalumu, ambao tumeshawataja mara kwa mara.” Akaongeza: “Na ni juu ya watawala kuendesha na kutekeleza yale yanayoamuliwa na wenye madaraka – yaani wajumbe wa Shura-.”28 La pili: Kundi hili linaona kuwa hadhi ya Shura ni mawazo tu, na haina hadhi ya kisheria katika kumlazimisha mtawala kutekeleza maamuzi yake. Miongoni mwa hawa ni Al-Qurtubiy, pale anaposema katika tafsiri yake: “Na Shura imejengeka juu ya rai tofauti, na mwenye kutaka ushauri huchunguza tofauti hiyo na kuitazama ni 28
Tafsirul-Manar Juz. 5 Uk. 187 – 188. 29
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
ipi iliyo karibu mno na Kitabu na Sunna kama inamwezekania, basi iwapo Mwenyezi Mungu atamwongoza kwenye yale Ayatakayo, huazimia na kuyatekeleza huku akimtawakali Yeye.”29 Ama wanachuoni wa Kiimamiyya, wenyewe wanaelekea kwenye rai ya pili katika kutafsiri Aya ya Shura. Amesema Sheikh Muhammad Jawwad Al-Balaghiy: “Na ushauriane nao katika mambo” (Sura Aali Imran: 159): Chunguza lililo jema kwao na vutia nyoyo zao kwa ushauri, si kwa kuwa wao watamfidisha kwa kumwongoza sawa na kwa elimu ya lile lililo jema. Vipi liwezekane hilo na hali Mwenyezi Mungu ndiye anayemwongoza sawa: “Wala hasemi kwa hawaa ya nafsi. Hayakuwa haya ila ni Wahyi uliofunuliwa.” (Sura Najmi: 3 – 4). Hivyo ukiazimia yale aliyokuamuru Mwenyezi Mungu kupitia nuru ya unabii na kukuongoza sawa humo: “basi mtegemee Mwenyezi Mungu.” (Sura Ali Imran: 159)”30 Hivyo Shura kwa mtazamo wa Kambi ya Ahlul-Baiti kwa mukhtasari ni kuwa, rai ya Waislamu haimlazimishi Mtume wa Mwenyezi Mungu, kwani Mwenyezi Mungu amesema: “Na unapoazimia basi mtegemee Mwenyezi Mungu.” (Sura Ali Imran: 159) hivyo utendaji wa jambo unategemea azma ya Mtume (s.a.w.w.) na si maoni ya waumini. Kisha ushauri wake ulikuwa pale anapotaka kujua rai za Waislamu katika namna ya kutekeleza hukmu za Kiislamu, na si kutoa hukmu za kisheria kwa njia ya ushauri. Zaidi ya yote hayo ni kuwa Mwenyezi Mungu amesema: “Haiwi kwa mwanaume aliyeamini wala kwa mwanamke aliyeamini, Mwenyezi Mungu s-Shura Fidhili Nidhamul-Hukmi Al-Islamuy cha Abdur-Rahman Abdul-Khaliq Uk. 113 A – 114. 30 Alaur-Rahman Uk. 364. Na ulamaa wengine wa Kishia wako karibu na hali kama vile Al-Faydhu Kashani katika tafsiri As-Swafiy Juz. 1, Uk. 31. Na Sayyid Shibri katika tafsiri yake Uk. 165. 29
30
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
na Mtume wake wanapokata shauri, wawe na khiari katika shauri lao. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hakika amepotea upotovu ulio wazi. (Sura Ahzab: 36). Hivyo haja ya ushauri inakomea kwenye lile ambalo Mwenyezi Mungu na Mtume Wake hawajalitolea maamuzi. Ama lile ambalo Mwenyezi Mungu na Mtume Wake tayari wameshalitolea maamuzi, kutaka ushauri katika hilo inakuwa ni kumwasi Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, na ni upotovu wa wazi. Hivyo Shura ina hadhi ya utoaji mawazo unaosaidia maamuzi ya Kiislamu katika kila sekta ya maisha, nayo haimlazimu Imam Maasumu, kwa sababu yenyewe haileti sheria mpya mkabala na kauli ya maasumu, kitendo chake na ridhaa yake, na yenyewe hukomea kwenye mambo ambayo Mwenyezi Mungu na Mtume Wake hawajayatolea maamuzi. Ama upande wa kihistoria kama tulivyotaja ni kuwa Shura haikuwa mfumo wa kisiasa wa kisheria wa kiutawala, kwa sababu yenyewe imekuja ili kuhalalisha jambo lililotokea, na zimefanywa juhudi za makusudi ili kuifanya kuwa chanzo kikuu cha wasifu wa mfumo wa kisiasa uliokuwa ukitawala zama hizo. Na ni kuwa ukhalifa hautimu ila kwa tamko kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) kwa ajili ya Khalifa anayekuja baada yake.
UHUSIANO BAINA YA BAIYA NA TAMKO LA KUTAWAZWA Baiya ni kumtii mwanadamu ili aendeleze mwelekeo wake katika kulingania njia ya Mwenyezi Mungu, na jihadi katika njia Yake, au shughuli za kiutawala na siasa. Uislamu kwa tabia yake hautaki maisha ya Waislamu yaendelee nje ya utashi wao, mwamko wao na maamuzi yao. Na hapa ndipo 31
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
umuhimu wa utii unachomoza katika kutekeleza majukumu ya daawa, tablighi, majukumu ya dola na majukumu ya jihadi. Na utii kwa Imamu Maasumu unaongezeka katika vigawanyo vyake vitatu kupitia Baiya. Na wala hii haimaanishi kuwa utii kwa Imamu Maasumu unaporomoka pale Baiya inapokosekana, kwani ikiwa Baiya kwa mujibu wa mtazamo huu inasisitiza na kukazia uhusiano wa Uimamu na utii kwake, baada ya kuwa Uimamu umethibiti, je inawezekana kwetu kusema: Hakika Baiya ni sharti la kusihi utii kwa Imamu? Au kuwa yenyewe ni sharti la wajibu wa kumtii na kuthibiti Uimamu kwake? Na kuwa bila Baiya hakuna Uimamu? Kama ambavyo pia hakuna usahihi wa kumtii? Tunasema: Hakika Baiya ni msisitizo na mkazo wa kufuata uongozi na utawala wa Imamu, na wala si kuanzisha uongozi au sharti la kusihi kwa utii, kwani utii na Uimamu havitegemei Baiya kwa yule ambaye tayari uongozi umeshathibiti kwake kwa tamko la kutawazwa. Na kwa ajili hii tunamkuta Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kutokana na uwelewa huu, amefanya kazi ya kuchukua Baiya ndani ya maisha yake, kama lilivyo wazi hilo katika Baiya ya Aqabatul-Uwla, Aqabatut-Taniya na ile ya Ghadiri. Sura hizi tatu za Baiya zilitimia kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) japokuwa uongozi ulikuwa umethibiti kwake kabla ya kutokea Baiya hizi. Na kitendo cha Waislamu kumpa Baiya au kutokumpa katika kuukubali wito wake au jihadi na uongozi, hakijabadili haki ya Mtume (s.a.w.w.) aliyonayo juu ya umma ya kutiiwa katika amri ya daawa, jihadi na uongozi. Na pia uongozi ulikuwa tayari umeshathibiti kwa Ali (a.s.) pale kwenye bonde la Khum. Uongozi huu haukuthibiti kwa Baiya ya 32
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
Waislamu kwake siku hiyo, hata kama Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) aliwaamuru kufanya hivyo, kwani Baiya hii kwa upande wa sheria hadhi yake si zaidi ya kusisitiza uongozi huu na utii kwake. Na suala la kuwa Uimamu hupatikana kwa urithi limepitishwa na Ahlus-Sunna pia, wamesema: “Iwapo Khalifa atamrithisha ukhalifa mtu mwingine baada yake, basi bila shaka Baiya inathibiti, na bila shaka ridhaa ya umma haizingatiwi, na dalili juu ya hilo ni kuwa Baiya ya Sidiq (Abu Bakr) kwa Umar haikutegemea ridhaa ya masahaba wengine.”31 Hii ndio kauli yao, japokuwa sisi kwa hakika kabisa hatupati Baiya kati ya Abu Bakr na Umar, bali kilichopo ni urithishaji tu, na si jingine. Basi urithishaji wa Mtume (s.a.w.w.) ndio aula kufuatwa bila kuwapo halalisho la kuukhalifu, wenyewe ulipatikana na kupitia wenyewe ulithibiti ukhalifa kwa Ali (a.s.) moja kwa moja baada ya Mtume (s.a.w.w.), hiyo ni sawa umma uwe ulimpa Baiya ili umtii au haukumpa. Baiya huanzisha fungamano la utii na kukabidhi funguo za serikali na idara, hili lenyewe halikamiliki ila kwa Baiya. Kisha na Abbas alitaka kufanya hivyo kwa Ali (a.s.), lakini alikataa (a.s.) ila iwe ni jahara, mbele ya watu wote ndani ya msikiti wa Mtume (s.a.w.w.), kisha ilipomjia Baiya, na watu nao wakampa Baiya kwa lengo lile lile, ikawa ni Baiya kwa ajili ya serikali. Na hivyo ndivyo hali ilivyokuwa kwa Imam Hasan na Husein (a.s.). Na pale Baiya ilipozuiliwa dhidi ya Maimamu ambao Mwenyezi Mungu na Mtume Wake (s.a.w.w.) waliwateua ndipo walipowazuia wao kuendesha serikali na idara kuu, lakini bila ya kuwanyang’anya wao haki ya Uimamu ambayo imethibiti kwao. 31
Maathirul-Anafah Juz. 1, Uk. 52. Al-Ahkam As-Sultaniyah cha Al-Mawaridiy Uk. 10. Al-Ahkam As-Sultaniyah cha Al-Farau Uk. 25 - 26. 33
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
Hali yao hiyo ni sawa na hali ya Manabii wengi ambao nyumati zao ziliwaasi na zikawazuia dhidi ya kuendesha majukumu yao halisi katika kuwaongoza na kuelekeza, lakini bila ya kuwanyang’anya cheo chao hicho ambacho Mwenyezi Mungu aliwapa.32 Hivyo hadhi ya Baiya mbele ya Imam Maasumu si zaidi ya mkazo na msisitizo kwa yule ambaye uongozi umethibiti kwake kwa tamko, kama ambavyo Baiya haianzishi uongozi mkabala na uongozi mwingine wa mtu aliyethibitishwa kwa tamko, kama vile Mtume au Imamu, na tamko linalothibiti kwa Imamu linawajibisha utii kwake na kuthibitisha uharamu wa kukhalifu kutoa Baiya kwake.
MTUKUFU MTUME ANAFANYA KAZI YA KUSISITIZA NADHARIA YA TAMKO Lau tukichunguza kwa undani upande wa historia, na tukachunguza hatua za Mtume (s.a.w.w.) katika kuulea umma na kuuelimisha kuhusu suala muhimu sana la kiungu, nalo ni ukhalifa, tutamkuta ameusisitizia nadharia ya tamko la kutawazwa na si Shura, na wala haipatikani harakati yoyote inayomtaja Mtume (s.a.w.w.) kuwa katika kuuelimisha umma na kuulea ana nadharia nyingine isiyo hii, kuanzia kuteremka kauli yake tukufu: “Na uwaonye jamaa zako wa karibu.” (Sura Shuaraa: 214) na mpaka kuteremka kwa kauli yake: “Ewe Mtume! Fikisha uliyoteremshiwa kutoka kwa Mola Wako, na kama hukufanya, basi hukufikisha ujumbe wake. Na Mwenyezi Mungu anakulinda na watu” (Sura Maida: 67). Imekuja kutoka kwa Ibnu Abbas (r.a) toka kwa Imam Ali (a.s.) kuwa alisema: “Ilipoteremka Aya hii: “Na uwaonye jamaa zako 32
Tarikhul-Islam At-Thaqafiy Was-Siyasiy, cha Swaib Abdul-Hamiid Uk. 259 – 260. 34
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
wa karibu.” (Sura Shuaraa: 214) kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) aliniita akaniambia: ‘Ewe Ali! Hakika Mwenyezi Mungu ameniamuru niwaonye jamaa wa karibu, nikaishiwa nguvu kwa hilo, na nikajua pindi mimi nitakapowadhihirishia jambo hili nitaona kwao yale nisiyoyapenda, ndipo nikakaa kimya mpaka Jibril aliponijia, akaniambia: ‘Ewe Muhammad! Kama hufanyi unayoamrishwa atakuadhibu Mola Wako.’ Hivyo tutengenezee pishi la chakula na uweke juu yake mguu wa mbuzi na tujazie birauli la maziwa, kisha nikusanyie wana wa Abdul-Muttalib ili niwazungumzie na kuwafikishia yale niliyoamrishwa.’ “Nikafanya aliyoniamuru kisha nikamwitia, na kipindi hicho wakiwa ni wanaume arobaini na kidogo au pungufu, wakiwamo ami zake Abu Talib, Hamza, Abbas na Abu Lahabi.” Akaendelea kusimulia mpaka akasema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu akaongea akasema: ‘Enyi wana wa Abdul-Muttalib! Wallahi hakika mimi simjui shababi katika waarabu ambaye amewaletea jamaa zake jambo bora kuliko nililowaletea, na hakika mimi nimewaletea kheri ya dunia na Akhera. Na Mwenyezi Mungu ameniamuru niwalinganie kwalo, basi ni yupi kati yenu atanisaidia juu ya jambo hili, awe ndugu yangu, wasii wangu na khalifa wangu kwenu?’” Imamu Ali (a.s.) anasema: “Watu wote wakakaa kimya, nikasema na hali mimi ndio mdogo wao kiumri: Mimi ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, nitakuwa waziri wako juu ya hilo. Akaishika shingo yangu kisha akasema: ‘Hakika huyu ni ndugu yangu, wasii wangu, na khalifa wangu kwenu, hivyo msikilizeni na mumtii.” 35
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
Ali (a.s.) amesema: “Watu wakanyanyuka huku wakicheka na kudhihaki wakimwambia Abu Talibi: ‘Amekuamuru umsikilize mwanao na umtii.”’33 Hivyo ndivyo Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alivyoanza kuuandaa umma kwa kuanzia jamaa zake wa karibu, na akiuelekeza upande wa ukhalifa wa Ali (a.s.) baada yake, akitoa tamko rasmi la undugu, usia, ukhalifa na wajibu wa kumfuata. Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akimulika mwanga juu ya maana za Aya za Qur’an ambazo zilikuwa zikiteremka kuzungumzia haki yake (a.s.), khususan zile Aya ambazo zina uhusiano moja kwa moja na nafasi ya ukhalifa na Uimamu. Zamakhshariy ametaja ndani ya tafsiri yake katika kutafsiri kauli yake (s.w.t.): “Hakika kiongozi wenu khasa ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na Walioamini ambao husimamisha Swala na hutoa Zaka na hali ya kuwa wamerukuu.” (Sura Maida: 55) “Hakika Aya hii iliteremka ikimuhusu Ali pindi ombaomba alipomwomba na hali yeye (a.s.) akiwa amerukuu ndani ya Swala yake, ndipo akamvulia pete yake.”34 Na ili kuondoa utata na kutupilia mbali taawili yoyote ile ya muradi wa neno ‘Kiongozi’, na ili kumwainisha katika sehemu kama hizi, Mtume (s.a.w.w.) alitamka bayana kwenye minasaba zaidi ya mmoja: “Hakika Ali hutokana na mimi, na mimi hutokana na yeye, na yeye ni Kiongozi wa kila muumini baada yangu.”35 arikhut-Tabar Juz. 3, Uk. 218 – 219. Tazama rejea za Hadithi hii katika MawsuatutT Tarikh Al-Islamiyy Juz. 1, Uk. 407 – 427. Na kitabu Manazala Minal-Qur’an Fii Aliy, cha Abu Naiim- Kimekusanywa na Sheikh Al-Mahmahudiy Uk. 155. Tafsirul-Khazin Juz. 3 Uk. 371. 34 Al-Kashaf cha Zamakhshari Juz. 1, Uk. 649. 35 Sunanut-Tirmidhiy Juz. 5, Uk. 591, mlango wa fadhila za Imam Ali. At-Taju Al-Jamiu Lil-Usuul Juz. 3 Uk. 335. 33
36
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
Na ili kutilia mkazo uongozi wa Imamu Ali (a.s.) na nafasi yake muhimu katika kubainisha mafunzo ya risala ya Kiislam, na kutimiza malengo yake kupitia utendaji wa uongozi kwa kutekeleza hukmu zake na kuilinda dhidi ya kila linaloweza kuipotoa na kuibadili baada ya Mtume (s.a.w.w.), akasema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.): “Ali anatokana na mimi, na mimi natokana na Ali, na wala hatekelezi kwa niaba yangu ila mimi mwenyewe au Ali.”36 Mtume (s.a.w.w.) akajenga uwelewa huu kwa kitendo mchana peupe, tena jahara katika kadhia ya kubalighisha Surat Baraa. Imamu Ahmad bin Hanbal ameandika riwaya hii ndani ya Musnad yake, toka kwa Abu Bakr pale aliposema: “Hakika Mtume (s.a.w.w.) alimtuma na Baraa akawasomee wakazi wa Makka, akatembea siku tatu, kisha (s.a.w.w.) akamwambia Ali: ‘Mfuate umrudishe Abu Bakr kwangu na ukaibalighishe wewe.’ Abu Bakr alipofika kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: ‘Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Je kuna lolote limetokea kuhusu mimi?’ Akasema (s.a.w.w.): ‘Hakuna lolote lililotokea kuhusu wewe ila kheri, lakini nimeamrishwa asiibalighishe ila mimi au mtu atokanaye na mimi.”’37 Na ndani ya Al-Kashaf: “Imepokewa kuwa Abu Bakr alipokuwa njiani kwenda kuibalighisha Sura Baraa, Jibril aliteremka na kusema: ‘Ewe Muhammad! Habalighishi ujumbe wako ila mtu atokanaye na wewe, hivyo mtume Ali…..”38 Na mwisho Qur’ani Tukufu ilihitimisha maudhui hii ya kimaisha na iliyo muhimu, nayo ni ile kazi ya maandalizi ya kifikra na kimalezi ya namna ya kuamiliana na maudhui ya ukhalifa na uongozi baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), kupitia sehemu ya mwisho S unanut-Tirmidhiy Juz. 5, Uk. 594, mlango wa fadhila za Imam Ali. At-Taju Al-Jamiu Lil-Usuul Juz. 3, Uk. 335. 37 Musnad Ahmad bin Hanbal Juz. 1 Uk. 3. Sunanut-Tirmidhiy Juz. 5, Uk. 594. Al-Kashaf cha Zamakhshariy Juz. 2, Uk. 243. 38 Al-Kashaf cha Zamakhshariy Juz. 2, Uk. 243. 36
37
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
kuteremka katika Aya ya tablighi, kisha katika Aya ya ukamilifu wa dini, baada ya kadhia mashuhuri ya bonde la Khum, kiasi kwamba mtoa udhuru hajabakiwa na udhuru wowote. Na kadhia ya kwenye bonde la Khum japokuwa wapokezi wameipokea kwa tofauti kidogo, lakini yenyewe ni kama lifuatavyo: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) aliporejea kutoka Hijja ya mwisho, wahyi ulimteremkia kwa kusisitiza: “Ewe Mtume! Fikisha uliyoteremshiwa kutoka kwa Mola Wako, na kama hukufanya, basi hukufikisha ujumbe Wake. Na Mwenyezi Mungu anakulinda na watu” (Sura Maida: 67),39 akaushusha msafara eneo la bonde la Khum, na akawakusanya watu katikati ya mchana, huku joto likiwa kali, na kisha Mtume akawahutubia akisema: “Kama kwamba nimeitwa na nimejibu, na bila shaka mimi nawaachieni vizito viwili: Kimojawapo ni kikubwa kuliko kingine, Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu.” Na kwa mujibu wa riwaya ya Muslim40 ni: “Na Ahlul-Baiti wangu.” “Angalieni ni jinsi gani mtakavyoishi navyo nyuma yangu, kwani hakika hivyo viwili kamwe havitoachana mpaka vinifikie kwenye hodhi….” Kisha akasema (s.a.w.w.): “Hakika Mwenyezi Mungu ni Mtawala wangu na mimi ni Mtawala wa kila muumini.” Kisha akaushika mkono wa Ali (a.s.) na kusema: “Yule ambaye mimi ni Mtawala wake basi huyu Ali ni Mtawala wake.41 Ewe Mwenyezi Mungu! Mpende ampendaye, mfanyie uadui amfanyiaye uadui, Al-Wahid amesema katika kitabu Asbabun-Nuzuul Uk. 135: Iliteremka Ghadir Khum. Sahih Muslim Juz. 4 Uk. 1874. 41 Sunan Tirmidhiy Juz. 5, Uk. 591. At-Taju Al-Jamiu Lil-Usuul Juz. 3, Uk. 333, ameiandika toka kwa Zaid bin Arqam kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) 39 40
38
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
mtelekeze amtelekezaye na msaidie amsaidiaye,42 na izungushe haki iwe pamoja naye atakapozunguka….”43 Tukio hili kubwa punde tu lilifuatiwa na uteremkaji wa ufunuo mara nyingine kwa kauli Yake (s.w.t.): “Leo nimekukamilishieni dini yenu, na kukutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni Uislamu uwe dini yenu.” (Sura Maida: 3). Na ndani ya maelezo yaliyopokewa imepatikana kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) baada ya kuteremka Aya hii ndani ya siku hiyo iliyoshuhudiwa, nayo ni siku ya kumi na nane ya mfungo tatu,44 ambayo ni siku ya Ghadir, alisema: “Allahu Akbar. Kila sifa njema ni ya Mwenyezi Mungu kwa kuikamilisha dini, kuitimiza neema, na Mola Mlezi kuridhia ujumbe wangu na utawala wa Ali baada yangu.”45 Na katika riwaya ya Ahmad: “Umar bin Khattab akakutana naye – Yaani akakutana na Ali (a.s.) - baada ya hapo, akamwambia: ‘Hongera ewe mwana wa Abu Talib, umekuwa Mtawala wa kila muumini wa kiume na wa kike….”46 Katika maisha ya Mtume (s.a.w.w.) hatukuti juhudi nyingine Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amelenga kuthibitisha suala la ukhalifa wa baada yake zisizokuwa nadharia ya tamko la usnad Imam Ahmad bin Hanbal Juz. 4, Uk. 281 na 368. Sunan Ibnu Majah, utangulizi M 1, mlango wa 11. Tafsiri Ibnu Kathir Juz. 1, Uk. 22. Bidayatu Wan-Nihaya cha Ibn Kathir, ameiandika kwa njia kadhaa Juz. 7, Uk. 360 – 361. 43 At-Taju Al-Jamiu Lil-Usuul Juz. 3, Uk. 337, amepokea ikiwa pekee: “Mwenyezi Mungu amrehemu Ali. Ewe Mola izungushe haki pamoja naye atakapozunguka….” 44 Al-Itqan cha Suyutiy Juz. 1, Uk. 75. Asbabun-Nuzuul cha Al-Wahid Juz. Uk. 135. 45 Manaqibu Amiril-Muuminiina cha Hafidh Muhammad bin Sulayman Al-Kufiy Al-Qadhi Juz. 1, Uk. 119. 46 Musnad Imam Ahmad bin Hanbal Juz. 4, Uk. 281. Walimtolea ushahidi Ali watu kadhaa, wakamtolea ushahidi watu thelathini kuwa wao waliisikia Hadithi hii kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.). Na Al-Bidayatu Wan-Nihaya cha Ibnu Kathir Juz. 7, Uk. 360. 42
39
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
kutawazwa, ambayo katika shabaha yake ya kisheria inamaanisha jambo kubwa zaidi kuliko uongozi na utawala wa kisiasa, nalo ni uongozi wa kiungu wenye dhamana ya kutimiza yale ambayo risala ya Mtume (s.a.w.w.) inayahitaji, kiasi kwamba Qur’ani imemweleza Mtume (s.a.w.w.) ikiwa hatobalighisha hilo – ambalo ni kubalighisha ukhalifa na utawala wa baada yake - atakuwa hajabalighisha risala nzima ya Mola Wake Mlezi, ambayo ndani ya kipindi cha zaidi ya miongo miwili ya umri wake uliobarikiwa, alikuwa akijitolea juhudi katika kuibalighisha.
NJIA ZA KIDHANA NA HALI HALISI YA KIHISTORIA As-Shahid As-Sadri amehoji suala hili kwa mujibu wa hali yake halisi ya kihistoria kupitia dhana mbalimbali ambazo zinaweza kuugubika ubongo. Kati ya hizo ni: Dhana ya kuwa Mtume (s.a.w.w.) alipita njia ya kupuuuzia – yaani Mtume asilani hakujishughulisha na kitendo cha kuwabalighishia Waislamu na kuwalea kuhusu suala la utawala na uongozi wa baada yake. – Dhana hii ni batili kwa kuwa inapingana na cheo cha unabii chenye kukidhibiti kila kinachofungamana na risala. Na pia inapingana na maelezo ambayo yameeleza jinsi Mtume (s.a.w.w.) alivyoutilia umuhimu umma baada yake, ndani ya uhai wake na muda mfupi kabla ya kifo chake, na katika sekunde za mwisho za uhai wake uliobarikiwa.47 47
ejea kisa cha siku ya kuwaonya jamaa wa karibu, na msimamo wa Mtume katika vita R vya Tabuk, Sura Baraa, Hija ya kuaga na msiba wa siku ya Alhamisi pale Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipotaka kuandika wasia muda mfupi kabla ya kifo chake. Rejea katika Sahih Bukhar na Sahih nyingine na Masaanid. 40
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
Kama alivyohoji As-Shahidi As-Sadri njia ya pili – nayo ni dhana ya Shura - kwa kusema: “Hakika mazingira ya ujumla yaliyothibiti kwa Mtume (s.a.w.w.) na kizazi cha Muhajirina na Ansari, yanakataa dhana ya kuwa Mtume (s.a.w.w.) alifuata njia hii, kwani lau kama Mtume (s.a.w.w.) alikuwa ameliacha jambo hili mikononi mwa kizazi cha Muhajirina na Ansari bila kulihusisha na Ahlul-Baiti wake tu, basi kati ya mambo ya mwanzo kabisa ambayo hali hii inayahitaji ni Mtume (s.a.w.w.) kufanya kazi ya kuuamsha umma juu ya utaratibu wa Shura, ufafanuzi wake na kuiandaa jamii ya Kiislamu ili iukubali utaratibu huu. “Na lau kama Mtume (s.a.w.w.) angefanya kazi ya kuuamsha basi kwa kawaida hali hiyo ingejiakisi ndani ya Hadithi zilizopokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) na ndani ya bongo za Muhajirina na Ansari, hali sisi ndani ya Hadithi zilizopokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) hatukuti sura yoyote ile ya Kisheria yenye kulenga utaratibu wa Shura. Ama bongo za Muhajirina na Ansari hatukuti humo alama au sura zenye kufichua mwamko wa kabila hii, na hakika kizazi hiki kiligawanyika kwa kufuata sera mbili: Ya kwanza: Sera ambayo inaongozwa na Ahlul-Baiti iliyokuwa inaamini wasia. Na nyingine ni ile iliyowakilishwa na ukumbi wa Saqifa, na ikasimika ukhalifa ambao ulichukua madaraka kivitendo baada ya kifo cha Mtume (s.a.w.w.). “Kila takwimu na ushahidi katika sira ya waumini wa sera hii inaonyesha kwa sura isiyokubali shaka kuwa Abu Bakr hakuwa anaamini Shura, kwani pale maradhi yalipomzidia Abu Bakr alimpa ukhalifa Umar bila ya kumshaurisha yeyote yule, na akamtawalisha juu ya umma bila ushauri wa Waislamu au watu wenye hadhi maalumu. Na Umar naye akafuata njia ileile, pale alipowateua watu sita wamteue mmoja kati yao, na alikuwa akisema: ‘Lau kama Salim angelikuwa hai, nisingeliweka kwenye 41
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
Shura.’ Na hili ni tamko la bayana kutoka kwake kuwa haamini kanuni ya Shura.48 “Na lau kama Mtume (s.a.w.w.) angeamua kukipa kizazi cha Muhajirina na Ansari usimamizi wa daawa baada yake, basi ingewajibika kwake akiandae kizazi hiki maandalizi ya kirisala na ya kifikra iliyo pana, itakayokifanya kiwe na uwezo wa kukabiliana na matatizo ya kifikra ambayo daawa inakumbana nayo katika hali ya kufunguka kwake mbele ya watu mbalimbali na ardhi mpya. Lakini sisi hatupati athari yoyote ya maandalizi hayo, na maarufu ni kuwa masahaba walikuwa wakijizuia kumuanza Mtume kwa swali, bali pia walijizuia kuandika athari za Mtume (s.a.w.w.) na Sunnah zake, japokuwa ndio chanzo cha pili kati ya vyanzo vya Uislamu katika uwanja wa Sheria, na japokuwa uandishi ndio njia pekee ya kuzihifadhi. “Matukio ya baada ya kifo cha Mtume (s.a.w.w.) yamethibitisha kuwa kizazi cha Muhajirina na Ansari hakikuwa kinamiliki mafunzo yoyote yenye kuweza kutatua matatizo mengi makubwa, mpaka hata Khalifa na gavana wake hawakuwa na sura yoyote iliyowekwa kisheria kuhusu lile eneo kubwa la ardhi ambalo lilifikiwa na mapinduzi ya Kiislamu. Hawakujua je linagaiwa kwa wapiganaji au linawekwa wakfu kwa Waislamu wote, bali walitofautiana hata katika idadi ya Takbira ndani ya Sala ya maiti, baadhi yao wakawa wanasema: ‘Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akitoa takbira mara tano.’ Na mwingine akisema: ‘Nilimsikia akitoa takbira mara nne.’. Hivyo ndivyo ilivyobainika kuwa Mtume hakupita njia ya pili pia, na kuwa kuuachia umma uongozi na usimamizi ilikuwa ni mapema mno na kabla ya wakati wake kimazingira. Hivyo 48
Tarikh Tabari Juz. 3, Uk. 292. 42
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
haikubali ila njia ya tatu, nayo ni kuwa Mtume (s.a.w.w.) kwa amri ya Mwenyezi Mungu alimwandaa Ali (a.s.) na akamwainisha kuwa msimamizi wa risala na umma, kwa kumzingatia kuwa ndiye mteule wa usimamizi huu kimazingira, kwa kule kubobea kwake katika harakati za risala, kuijua kwa ukamilifu, na uwezo wake wa kusimamia harakati zake baada ya Mtume (s.a.w.w.), kama matukio ya kihistoria yalivyothibitisha hilo ndani ya kipindi cha miongo mitatu ya umri wake baada ya Mtume (s.a.w.w.), huku wanahistoria wakikiri hilo. “Maelezo yaliyokithiri kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) kuhusu Ahlul-Baiti na Ali, si chochote ila ni kueleza kule kupita kwake (s.a.w.w.) njia ya tatu ambayo hata kabla ya hayo (maelezo) mazingira ya vitu yalikuwa tayari yameshaiweka na kuitambulisha.”49
NADHARIA YA TAMKO LA KUTAWAZWA KATIKA HADITHI YA IMAMU ALI NA AHLUL-BAIT Ni wazi sana unaposoma ile historia utakuta kuwa Ali (a.s.) ndiye mara nyingi aliyedhihirisha maelezo na ishara zinazoonyesha kuteuliwa kwake kushika Ukhalifa wa Mtume (s.a.w.w.), au kutajwa kwa jina. Na kazi ya kutaka kujua usahihi wa kunasibishwa maneno haya kwake imeshamalizwa na wahakiki pale walipojiepusha na matamanio, na wakaridhika nayo zaidi ya ulamaa khamsini miongoni mwa wafafanuzi wa maneno yake, wakayaletea utetezi wa heshima kupitia hoja zinazopelekea utulivu.50 49 50
Nash’atut-Tashayyuu Washia Uk. 63 – 64. Sharhu Nahjul-Balaghah cha Subhiyu Swalih Uk. 12 – 18. Sharhu Nahjul-Balaghah cha Muhammad Abul-Fadhli Ibrahi Juz. 1, Uk. 8. Sharhu Nahjul-Balaghah cha Ibnu AbulHadid Juz. 10, Uk. 127 – 129. Murujud-Dhahab Juz. 2, Uk. 431, chapa ya Darul-Maarifa. 43
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
Ali (a.s.) ndiye aliyerudisha ndani ya bongo zile Hadithi za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) zinazoonyesha haki yake ya ukhalifa bila pingamizi. Hadithi hizo zilikuwa zimegandamizwa kwa kufunikwa na jiwe zito zama za makhalifa, pale walipozuia Hadithi zisisimuliwe ila zile zinazohusu faradhi, wakikusudia kuchukua hukmu na vipengele vya ibada. 1.
Aliwakusanya watu zama za ukhalifa wake akawahutubia ile hotuba yake iliyonukuliwa kwa wingi, humo akiwaapiza sahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu: Ni nani aliyemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu huko Ghadir Khum akihutubia na kusema: ‘’Yule ambaye mimi ni Mtawala wake basi Ali ni Mtawala wake.’’. Pale aliposimama na kushuhudilia.51
2.
Na Ali ndiye aliyerudisha usambazaji wa Hadithi nyingine imteuwayo juu ya Abu Bakr na Umar pekee, pale Mtume (s.a.w.w.) alipotoa habari kuwa kati ya masahaba zake yumo atakayepigania tafsiri ya Qur’ani kama yeye (s.a.w.w.) alivyopigania uteremkaji wake, ndipo Abu Bakr akatamani yeye ndiye awe mtu huyo, lakini Mtume (s.a.w.w.) hakusadiki tamanio lake, bali alimwambia: “Hapana.” Umar naye akatamani hilo kwa ajili ya nafsi yake, lakini hakuwa na bahati nzuri kuliko Abu Bakr, kisha ndipo Mtume (s.a.w.w.) akakata matamanio yote pale alipowapa habari kuwa ni Ali (a.s.) na si mwingine.52
Hadithi hizi na nyinginezo japokuwa zimepokewa kutoka kwa mwingine, ila ni kuwa kupokewa kwake kutoka kwake (a.s.) kumejitofautisha kwa kuwa kwake hotuba mbele ya jamuhuri ya usnad Imam Ahmad bin Hanbal Juz. 1, Uk. 84, 88 na 181. Al-Bidayatu Wan-Nihaya M Juz. 5, Uk. 229 na 232 na Juz. 7, Uk. 383 na 385 karibu njia ishirini. 52 Sunan Tirmidhiy Juz. 5, Uk. 33715. Sunan Al-Kubra cha Nasai Juz. 5, Hasdithi ya 8416. 51
44
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
watu, na si Hadithi ya mtu mmoja au kundi la watu, na hii ni fasaha zaidi katika kusisitiza haki yake ambayo alikuwa na yakini nayo, na akaamini kwa yakini kuwa wengi kati ya masahaba walikuwa wanaijua na wanaitambua. 3.
Imetajwa kutoka kwake zaidi ya mara moja siku ya Shura au baada yake, lakini wametofautiana katika ufafanuzi wake na njia yake ya upokezi, japokuwa Hadithi hiyo imethibiti kwao kwa ujumla. Na kwa uchache kati ya waliyoyataja katika kuwaapiza kwake huko, ni ile habari aliyoiandika Ibnu Abdu-Bari: “Ali aliwaambia wajumbe wa Shura: ‘Nawaapisha Mwenyezi Mungu, je kati yenu yupo yoyote asiyekuwa mimi, Mtume wa Mwenyezi Mungu aliweka undugu kati yake na yeye, pale alipoweka undugu kati ya Waislamu?’”
Baada ya hapo Ibnu Abdul-Bari akasema: “Tumepokea kwa njia mbalimbali kutoka kwa Ali (a.s.) kuwa yeye alikuwa akisema: ‘Mimi ni mja wa Mwenyezi Mungu na ndugu wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, halisemi hilo asiyekuwa mimi ila ni mwongo.”’53 Na wameipokea ndani ya Kanzul-Ummal Hadithi ndefu kutoka kwa Abu Tufayli, kuwa yeye alimsikia Ali siku ya Shura akisema:…..Hadi mwisho wa Hadithi.54 Aliyoyaandika Ibnu Abdul-Bari ni sehemu tu ya Hadithi. Lakini njia ya upokezi ya Kanzul-Ummal ina watu wasiojulikana55, na umepita mjadala kuihusu, ikasemwa: Al-Istiab Juz. 3, Uk. 35. Kanzul-Ummahl Juz. 5, Uk. 724, Hadithi ya 14243. 55 Zaffir kutoka kwa Al-Harith bin Muhammad, kutoka kwa Abu Tufayli. 53 54
45
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
“Ameipokea Zaffir kutoka kwa mtu, hivyo hajulikani, na Zaffir hajafuatiliwa.” Na baadhi yao wakaikanusha kwa ajili ya matamshi yake. Hadithi hii haipuuzwi kwa ukanushaji huu, kwa sababu wenyewe umejengwa juu ya misingi ya uwelewa usiyo na asili yoyote, wenye kusawiri Baiya ya Abu Bakr kuwa ilikuwa ni Ijmai au mfano wa Ijmai, na yule aliyekhalifu taswira hii ndiye mwenye kuikanusha, na hii ni upungufu wa kimawazo, kama ilivyo thabiti. Ama njia ya upokezi ni kuwa Zaffir amefuatiliwa kama ilivyo kwenye njia ya upokezi ambayo ameiandika Abdul-Bari ndani ya kitabu Al-Istiabu.56 Na Ibnu Hajar Al-Askalaniy amesema: “Hakika Zaffir hajatuhumiwa kwa uongo, na yeye anapofuatiliwa juu ya Hadithi huwa hasana.”57 Mwanzoni mwa Hadithi hii amesema Abu Tufayli: “Siku ya Shura nilikuwa mlangoni, ndipo zikapaa sauti kati yao, nikamsikia Ali akisema: ‘Watu walimpa Abu Bakr Baiya na hali mimi Wallahi nilikuwa aula kwa jambo hilo kuliko yeye, na mwenye haki kwalo kuliko yeye. Nikamsikiliza na kumtii, nikikhofia watu wasirejee kuwa makafiri, baadhi yao wakizikata shingo za wengine kwa upanga. Kisha watu wakamfuatiza Umar na hali mimi Wallahi nilikuwa aula kwa jambo hilo kuliko yeye, na mwenye haki kwalo kuliko yeye. Nikamsikiliza na kumtii, nikikhofia watu wasirejee kuwa makafiri, baadhi yao wakizikata shingo za wengine kwa upanga. Kisha nyinyi mnataka kumpa Baiya Uthman, basi nitasikia na kutii!’” bdul-Warith: Ametusimulia Qasim: Ametusimulia Ahmad bin Zuhair: Ametusimulia A Amru bin Hammad Al-Qattad: Ametusimulia Is’haqa bin Ibrahim Al-Azdiy, kutoka kwa Maaruf Ibnu Kharbudh kutoka kwa Ziyad bin Al-Mundhir, kutoka kwa Said bin Muhammad A-Azdiy kutoka kwa Abu Tufayl. 57 Kanzul-Ummahl Juz. 5, Uk. 726 – 727. 56
46
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
Kisha akataja suala la Shura na akaanza kuwahesabia fadhila zake na sifa zake za pekee alizonazo juu yao, ambazo kwazo ametofautiana nao, na mwanzo wake ulikuwa kile kipande alichokipokea Ibnu Abdul-Bari katika undugu.58 Na maneno haya yana ushahidi kama itakavyokuja katika ibara zifuatazo. 4.
Ali (a.s.) alijadidi ukumbusho wa yale yanayodhihirisha haki yake juu ya Abu Bakr pekee, pale alipowakumbusha watu kuchukua kwake Sura Baraa toka mikononi mwa Abu Bakr. Anasi amepokea kwa njia sahihi kutoka kwa Ali kuwa: “Hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) alituma Baraa kwa wakazi wa Makka ikiwa na Abu Bakr, kisha nyuma akamtumia Ali, na kumwambia: ‘Chukua maandiko na nenda nayo kwa wakazi wa Makka.’. Anasema (a.s.): Nikamkuta na nikachukua maandiko toka kwake, Abu Bakr akaondoka huku akiwa amehuzunika, akasema: ‘Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Je kimeteremka chochote kunihusu?’ Akasema (s.a.w.w.): ‘Hapana, hakika mimi nimeamrishwa niibalighishe mimi mwenyewe au mtu toka katika Ahlul-Baiti wangu.’”59
Na kila moja kati ya Hadithi hizi ni jibu kwa yule anayesema hakika Ali hajasema chochote kinachoonyesha haki yake ya ukhalifa, ni haya, na bado hatujaingia ndani ya uwanja wa Nahjul-Balaghah. 5.
Miongoni mwa kauli zake mashuhuri ni ile kauli yake pale zilipomfikia habari za Saqifa, na kuwa watu wamempa Baiya Abu Bakr: “Makuraishi wamesema nini?” Wakasema:
azama habari ya uapizaji huu katika kitabu Swawaiqul-Muhriqa, mlango wa 11 Aya T ya 9. Al-Manaqib cha Al-Khawarazmiy Uk. 213, kutoka kwa Abu Dhari, na humo mna habari kuwa ilikuwa ni baada ya Shura pindi walipoazimia kumpa Baiya Uthman. 59 Sunan An-Nasai Juz. 5, Uk. 128, Hadithi ya 8461. 58
47
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
“Wametoa hoja kuwa wao ni mti wa Mtume.” Akasema (a.s.): “Wametoa hoja kupitia mti na hali wametelekeza matunda.”60 6.
Na miongoni mwa hoja zake mashuhuri juu ya matokeo ya Saqifa ni kauli yake kumwambia Abu Bakr: “Ikiwa ni kwa Shura umemiliki mambo yao, basi ni vipi hili (limetimu) na hali watoa ushauri hawakuwepo. Na ikiwa ni kwa ukaribu umemtolea hoja mpinzani wao, basi asiyekuwa wewe ndiye aula kwa Mtume na wa karibu mno (kwake kuliko wewe.)”61
7.
Na miongoni mwa maneno yake ni hotuba ya Shaqshaqiya ambayo daima imepata hadhi kwa uaminifu wa ziada,62 na yenyewe ni miongoni mwa maneno yake mashuhuri, yaliyo na uwazi, uthibitisho na ufafanuzi mwingi: “Amma Wallahi fulani ameuvaa (ukhalifa) hali akiwa anajua kuwa nafasi yangu kuhusiana nao ni sawa na mahala pa muhimili
Nahjul-Balaghah Uk. 97, Khutba ya 67. Nahjul-Balaghah Uk. 502, sehemu ya hekima: 190. 62 Ibnu Abil-Hadid amenukuu kauli kutoka kwa baadhi ya mashekhe zake: “Wallahi niliikuta Khutba hii katika vitabu vilivyoandikwa miaka mia mbili kabla ya kuumbwa Radhwii.” Kisha akasema: Na hakika mimi mwenyewe nimeikuta sehemu kubwa ya Khutba hii katika utunzi wa mashekhe zetu, Abul-Qasim Al-Balkhiy Imam wa watu wa Baghdad wa Muutazila, aliyezaliwa mwaka 279 A.H. na akafariki mwaka 317 A.H.Kumbuka kuwa Sharif Radhwi amezaliwa mwaka 360 A.H.- Tazama Sharhu NahjulBalaghah Juz. 1 Uk. 69. Sibtu Ibnu Al-Jawzi ameinukuu kutoka kwenye rejea ambazo si zile alizozitegemea Sharif Radhwi, akasema: Khutba nyingine na inatambulika kwa jina la Shaqshaqiyya, baadhi ya sehemu yake ameitaja mwandishi wa Nahjul-Balaghah, na ameacha sehemu nyingine, nami bila shaka nimeileta kwa ukamilifu. Ametusimulia hiyo Shaikh wetu Abul-Qasim An-Nafiis Al-Anbariy kwa njia yake kutoka kwa Ibnu Abbas……- Tazama Tadhkiratul-Khuwwas Uk. 124. Ar-Rawandi aliyefariki mwaka 573 A.H. katika ufafanuzi wake ameileta katika njia inayofika kwa Hafidh Ibnu Mardawayhi, kutoka kwa Tabaraniy, kwa njia yake mpaka kwa Ibnu Abbas.- Tazama Minhajil-Baraah Juz. 1 Uk. 131 – 132. Ili upate kuzifikia rejea zake, rejea vyanzo vya Nahjul-Balaghah na njia zake Juz. 1 Uk. 309 – 318. 60 61
48
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
wa jiwe la kusagia, maji ya mafuriko huniporomokea wala ndege hawezi kunirukia. Nilijikinga nao kwa nguo na nikajiweka kando nao. Nikajifikiria, je? Nishambulie na mkono butu, au nivumilie giza la upofu………Nikaona kuivumilia hali hii ni busara, basi nikasubiri hali jichoni mwangu mna utongotongo, na kooni kuna kitu kilichokwama. Naiona mirathi yangu imepokonywa, wa kwanza akapita katika njia yake, akampasia fulani baada yake….. “Ajabu ilioje! Alikuwa anaomba wamuuzulu wakati wa uhai wake,63 punde si punde akaagiza uende kwa mwingine baada ya kifo chake! Kwa hakika wameshirikiana viwele vyake viwili wao kwa wao tu…….Nilivumilia kwa muda mrefu wote huo, ingawaje ulikuwa mtihani mgumu. Na alipofikia muda wake akauweka chini ya uchunguzi wa kundi la watu, akadai akinidhania mimi ni mmoja kati yao. Eee Mungu! Nahusika nini mimi na Shura! Lini ameingiwa na shaka na mimi wa kwanza wao kiasi niwe naambatanishwa na mfano wa hawa!....”64 Hivyo hata Abu Bakr mwenyewe alikuwa anatambua fika kuwa nafasi ya Ali (a.s.) kwenye ukhalifa ni nafasi ya muhimili wa jiwe la kusagia. Na hili linaweza kuonekana gharibu mno kwa yule aliyezowea taswira ya kuuheshimu mfuatano wa ukhalifa, taswira ile iliyotengenezwa na historia kwa kufuata mfumo ambao tumeusoma kwenye vifungu vilivyotangulia. Na kuanzia hapa ndipo walimkanusha kama walivyokanusha maneno yake mengine kuhusu ukhalifa, na kabla yake wamekanusha baadhi ya Hadithi za Mtume (s.a.w.w.) zinazobomoa heshima na mfuatano huo. Lakini ukweli ni ukweli tu, kwani lau wewe utaitafutia taswira hiyo ya kiheshima ushahidi wenye kuisadikisha toka ndani ya 63 64
Anaashiria kauli ya Abu Bakr: Niuzulini niuzuluni. Nahjul-Balaghah, Khutba ya 3. 49
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
hali halisi, bila shaka utarudi bila kitu. Lakini historia haijazoea kumsikiliza Ali (a.s.), kwani historia ambayo imethibitisha kwa namna ambayo haiachi nafasi ya utafiti, kuwa Ali hakumpa Abu Bakr Baiya ila baada ya miezi kadhaa, ni hiyo hiyo iliziba masikio yake bila kusikiliza hoja yoyote ile ya Ali (a.s.) ndani ya kipindi hiki. Mpingano ambao haujamsimamisha yeyote kati ya wasomaji wa historia, na vipi utawasimamisha wao kwenye aibu zake wenyewe, na hali ni wenyewe pekee uliyosikiliza taswira zao na elimu yao? 8.
Miongoni mwa maneno yake ni yale ya baada ya Shura, wakiwa tayari wameshaazimia kumpa Baiya Uthman: “Kwa kweli mnajua kuwa mimi ni mwenye haki nao (ukhalifa) zaidi kuliko mwingine yeyote asiyekuwa mimi. Na Wallahi nitamwachia (Uthman) maadamu mambo ya Waislamu yatakuwa katika amani kwa kumwachia, na dhulma haitokuwa isipokuwa kwangu tu. Nikitaraji ujira wa hilo na fadhila zake, na kujiweka mbali na mnachoshindania na kujiweka kando na kuyafikia mapambo yake ambayo mnagombania.”65
Ibnu Abdul-Hadid amekuta kuwa hilo ndio neno la mwisho alilolisema Ali (a.s.) siku hiyo kati ya maneno aliyonukuu hapa, baada ya kuondokewa na kila aina ya shaka kuhusu usahihi wake, akasema: “Sisi hapa tunataja katika maudhui hii yale yaliyokithiri katika riwaya za maapizo yake kwa wajumbe wa Shura, watu wameyapokea hayo na wakakithiri. Na lililo sahihi kwetu ni kuwa jambo halikuwa kama lilivyopokewa toka ndani ya idadi hiyo ndefu, lakini aliwaambia baada ya wao kumpa Uthman Baiya, na hali yeye (a.s.) akijizuia kutoa Baiya: ‘Hakika sisi tuna haki, ikiwa tutapewa tutaichukua, na tukinyimwa tutasubiri, hata kama mwendo utakuwa mrefu.’ Kati ya maneno waliyoyataja waandishi wa Sira. 65
Nahjul-Balaghah, Uk. 102, Khutba ya 74. 50
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
“Kisha akawaambia: ‘Nawaapieni Mwenyezi Mungu, je miongoni mwenu yumo yeyote asiyekuwa mimi, Mtume wa Mwenyezi Mungu ameweka undugu kati yake na yeye?’ Wakasema: ‘Hapana.’ “Akasema: Kati yenu yupo yeyote yule asiyekuwa mimi, Mtume wa Mwenyezi Mungu amemwambia: ‘Wewe kwangu mimi una nafasi ya Harun kwa Musa, ila ni kuwa hakuna Nabii baada yangu?’ Wakasema: ‘Hapana.’ “Akasema: Kati yenu yupo yeyote yule asiyekuwa mimi, aliyeaminiwa juu ya Sura Baraa, na Mtume wa Mwenyezi Mungu akasema: ‘Hakika hafikishi kwa niaba yangu ila mimi mwenyewe au mtu atokanaye na mimi’? Wakasema: ‘Hapana.’ “Akasema: Hivi hamjui kuwa masahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu walimkimbia kwenye mapambano makali ya vita, eneo zaidi ya moja, na katu sikukimbia? Wakasema: ‘Ndio (twajua).’ “Akasema: Hivi hamjui kuwa mimi ndiye mtu wa kwanza kuukubali Uislamu? Wakasema: ‘Ndio (twajua).’ “Akasema: Kati yenu ni yupi aliye karibu mno na Mtume wa Mwenyezi Mungu kinasaba? Wakasema: ‘Wewe.’ “Ndipo Abdur-Rahman bin Auf alipokata maneno yake na kusema: ‘Ewe Ali! Watu wamekataa ila juu ya Uthman, hivyo usiiwekee nafsi yako njia.’ Kisha Abdur-Rahman akamwelekea Abu Talha Al-Ansariy66 na kumwambia: ‘Ewe Abu Talha! Ni jambo lipi alilokuamuru Umar?’ Akasema: ‘Nimuuwe atakayeivunja fimbo ya jamaa.’. Abdur-Rahman akamwambia Ali: ‘Hivyo toa Baiya, na la sivyo utakuwa mwenye kufuata njia isiyokuwa ya waumini na tutatekeleza kwako lile tuliloamrishwa.’ 66
tu ambaye siku hiyo ya Shura Umar alimpa uongozi wa kuongoza kundi la watu khamsini M wakiwa na mapanga, ili wamuuwe yule atakayelikhalifu kundi alilomo Abdur-Rahman. 51
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
“Ali (a.s.) akasema neno lake hili: ‘Kwa kweli mnajua kuwa mimi ni mwenye haki nao (ukhalifa) zaidi kuliko mwingine yeyote asiyekuwa mimi. Na Wallahi nitamwachia (Uthman) maadamu mambo ya Waislamu yatakuwa katika amani kwa kumwachia, na dhulma haitokuwa isipokuwa kwangu tu….’”.67 Hivyo maneno haya habari yake ni ya wapokezi wengi, nayo si miongoni mwa habari ngeni au zisizokubalika. 9.
Msemaji alisema: Hakika wewe ni mwenye pupa na jambo hili, ewe mwana wa Abu Talib. “Nikasema: Bali Wallahi nyinyi ndio wenye pupa zaidi na wa mbali mno, na mimi ni makhsusi mno (na jambo hili) na wa karibu mno (na jambo hili). Bila shaka nimetafuta haki yangu, na nyinyi mnazuia kati yangu na yenyewe, na mnanizuia nisiipate! Nilipomgonga kwa hoja mbele ya kundi la waliohudhuria alitahayari kama amepigwa na butwaa, hajui anijibu nini kwayo.”68
Msemaji hapa ima ni Saad bin Abu Waqqas siku ya Shura, kwa mujibu wa kauli ya Masunni. Au ni Abu Ubayda, baada ya siku ya Shura, kwa mujibu wa kauli ya Shia. Na awe ni yoyote yule, muhimu ni kuwa maneno haya ni mashuhuri, wameyapokea watu wote, kama asemavyo Msunni Ibnu Abdul-Hadid Al-Muutazaliy.69 10. “Ewe Mola Wangu! Hakika mimi nakuomba uwe adui juu ya makuraishi na wasaidizi wao, bila shaka wao wamekata kizazi changu na kuufanya mdogo ukubwa wa daraja yangu, na wakaungana kuninyang’anya jambo ambalo ni la Sharhu Nahjul-Balaghah cha Ibnu Abul-Hadid Juz. 6, Uk. 167 – 168. Nahjul-Balaghah, Uk. 246, Khutba ya 172. 69 Sharhu Nahjul-Balaghah cha Ibnu Abul-Hadid Juz. 9, Uk. 305. 67 68
52
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
kwangu. Kisha wakasema: Fahamuni, hakika katika haki ima uichukue, na katika haki ima uiache.”70 11. “Ama baad, hakika Mwenyezi Mungu alipomfisha Nabii Wake, tulisema: Sisi ni ahli zake, warithi wake, kizazi chake, na vipenzi vyake kinyume na watu wengine. Hatatupora uongozi wake yeyote yule, wala hatamani haki yetu yeyote mwenye kutamani. Ghafla ikaibuka kwa ajili yetu kaumu yetu na kutupora uongozi wa Nabii wetu, hapo uongozi ukawa kwa wengine…….” Huu ni utangulizi wa hotuba yake huko Madina, mwanzoni tu mwa utawala wake, na wala utawala wake ulikuwa hauna zaidi ya mwezi.71 12. “Ama kutawala, bila shaka ilikuwa ni kujimilikisha makamu haya juu yetu, kulikopupiwa na nafsi za watu, na kudharauliwa na nafsi za wengine. Hukmu ni ya Mwenyezi Mungu na marudio ni kwake Siku ya Kiyama.” Aliyasema haya ikiwa ni jibu la aliyemuuliza: “Vipi jamaa zenu wamekuondoeni kwenye nafasi hii na hali nyinyi ndio wenye haki zaidi?” Kisha anaunganisha jibu lake (a.s.) kwa yale anayoyanukuu (katika shairi): “Acha ngawira, ilinadiwa pembeni. Lakini mazungumzo si mazungumzo ya ngamia. Na yataje maajabu ya jambo kwa mwana wa Abu Sufiyan, bila shaka dahari imenichekesha baada ya kumliza…..”72
Nahjul-Balaghah, Uk. 246, Khutba ya 172. Sharhu Nahjul-Balaghah cha Ibnu Abul-Hadid Juz. 1, Uk. 307. 72 Nahjul-Balaghah, Uk. 231, Khutba ya 162. 70 71
53
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
KUWAHUSU AHLUL-BAIT (A.S.) Kama ulivyodhihiri huko uwazi na msisitizo wa kuonyesha haki yake makhsusi (a.s.), pia hapa unadhihiri ukiwahusu Ahlul-Baiti (a.s.), kupitia maneno yake (a.s.): 1.
“Ewe Mungu! Ndio ardhi haikosi mwenye kusimamisha hoja ya Mwenyezi Mungu, ima ni dhahiri shahiri, na ima ni mwenye khofu aliyehifadhiwa, ili hoja za Mwenyezi Mungu na ubainifu wake visibatilike.”73
Ibnu Abil-Hadid Al-Muutazaliy anaona kuwa maelezo haya yakaribia kuwa ni kuyatamka bayana madhehebu ya Imamiya.74 2.
“Aali Muhammadi hawalinganishwi na yeyote katika umma huu, wala hawawi nao sawa kabisa ambao neema zao zimepitia kwao….. Wao ndio msingi wa dini na nguzo ya yakini…… Haki ya uongozi ni makhususi kwao, na kwao kuna wasia na urithi….”75
Baada ya kutaja haki ya uwalii, hii ndio sehemu moja miongoni mwa sehemu anazotaja wasia kwa kuutamka bayana.76 Kisha ndio sehemu yenye tamko bayana zaidi lenye kunasibisha wasia kwake na kwa Ahlul-Baiti. Pamoja na haya lakini ndio sehemu ambayo Dr. Muhammad Ammarat ameipuuzia, hali akiwa anaorodhesha msamiati ‘Wasia’ toka kwenye maneno ya Ali (a.s.), au tuseme alighafilika nayo ili aseme: “Hakika sisi hatupati neno hili katika hotuba za Ali, wala ndani ya maneno yake na barua zake, ambavyo vimekusanywa na Nahjul-Balaghah.” Nahjul-Balaghah, Uk. 497, Hekima ya 147. Sharhu Nahjul-Balaghah cha Ibnu Abul-Hadid Juz. 18 Uk. 351, Khutba ya 143. 75 Nahjul-Balaghah, Uk. 47, Khutba ya 2. 76 Nahjul-Balaghah, Khutba ya 88 na ya 183. 73 74
54
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
Haya yote ni ili ayape nguvu maneno yake aliyoyaweka mwanzoni pindi aliponasibisha neno ‘Wasia’ lililopo kwenye Hadithi ya Mtume (s.a.w.w.): “Hakika wewe ni ndugu yangu na wasii wangu.” kuwa ni uzushi wa Mashia, ambao waliliweka badala ya neno ‘Waziri wangu.’77 Japokuwa riwaya za Kisunni zinazozungumzia Hadithi hii hazilitambui ila neno ‘Wasii wangu’.78 3.
“Hakika Maimamu kutoka kwa Kuraishi walipandwa ndani ya tumbo hili kutoka kwa Hashim, halifai kwa wasiokuwa wao, na wala uwalii haufai kutoka kwa wengine wasiokuwa wao.”79
Hapo kabla tulipata kundi la maelezo sahihi ambayo yalikiteua kizazi cha Hashim kutoka kwa Kuraishi na kuwatanguliza juu yao. Na pia tulipata kundi la matukio na hali ambayo iliwatanguliza kizazi cha Hashim juu yao, hivyo makuraishi hawatoi hoja yoyote ile ila kizazi cha Hashim kitakuwa ndio aula kwayo. 4.
“Mnakwenda wapi! Basi mnageuzwa wapi! Na hali alama zipo na Aya ziko wazi na minara imesimamishwa! Mnapotezewa wapi! Na vipi mnakuwa vipofu! Na hali kati yenu kuna kizazi cha Mtume wenu (s.a.w.w.). Nao ndio hatamu za haki, na ni alama ya dini na ndimi za ukweli. Hivyo wawekeni daraja nzuri mno sawa na Qur’ani, na muwaendee mwendo wa ngamia walio na kiu kali. Enyi watu! Chukueni kutoka kwa Hitimisho la Manabii: ‘Hakika hufa afaye katika sisi na wala si mfu, na huoza aliyeoza katika sisi wala si mwenye kuoza.’….”80 Ni masikitiko juu ya watu
l-Khilafatu Wan-Nash’atul-Madhahib Al-Islamiyyah cha Dr. Muhammad Ammarat Uk. A 33 na 157 – 158. 78 Maalimut-Tanziil cha Baghawi Juz. 4, Uk. 278. Al-Kamil Fii Tarikh cha Ibnu Al-Athiir Juz. 2, Uk. 64. 79 Nahjul-Balaghah, uhakiki wa Dr. Subhi Swalih Uk. 201, Khutba 144. 80 Nahjul-Balaghah, uhakiki wa Dr. Subhi Swalih Uk. 119, Khutba 87. 77
55
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
hawa waliokiacha kizazi cha Mtume wao (s.a.w.w.) japo kuna dalili za kuwafuata. 5.
“Hakika sisi ni asili ya mifupa ya migongo ya watu wa Safina, na kama alivyookoka katika ile yule aliyeokoka, ataokoka katika hii yule atakayeokoka. Ole wako! Ni rehani kwa atakayejitenga nao. Hakika mimi kwenu ni sawa na pango kwa vijana wa pangoni, na hakika mimi kwenu ni sawa na mlango wa Hitta, atakayeingia kupitia huo ataokoka, na atakayejiepusha nao ataangamia. Hoja toka mwezi wa Dhulhija katika Hijja ya kuaga: ‘Hakika mimi nimeacha migongoni mwenu kile ambacho mkishikamana nacho hamtapotea baada yangu abadani: Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu Ahlul-Baiti wangu.”’81
6.
“Waangalieni Ahlul-Baiti wa Mtume wenu, na jiambatanisheni na mwendo wao, na fuateni nyayo zao, hawatokutoeni nje ya mwongozo, na hawatokutumbukizeni kwenye maangamizi, wakikaa kaeni, wakiinuka inukeni, msiwatanguliye mtapotea. Wala msibaki nyuma yao mtaangamia.”82
7.
“Je sikukifanyia kazi kwenu kizito kikubwa na ninaacha kwenu kizito kidogo?!......”83 izito kikubwa ni Qur’ani Tukufu, na kizito kidogo ni K Imam Ali, Fatima, Hasan na Husain (a.s.).
8.
“Mahdi ni kutoka kwetu Ahlul-Bait, Mwenyezi Mungu atamdhihirisha katika usiku mmoja.” Ahmad na Suyuti wameiandika wakiitoa kwa Ali (a.s.).84
Tarikhul-Yaaqubiy Juz. 2, Uk. 211 – 212. Nahjul-Balaghah, Uk. 143, Khutba ya 97. 83 Nahjul-Balaghah, Uk. 119, Khutba ya 87. 84 Musnad Ahmad, Juz. 1, Uk. 84. Al-Jamius-Swaghir Juz. 2, Uk. 672, Hadithi ya 9243. 81 82
56
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
“Mahdi ni kutoka kwetu, kutoka kizazi cha Fatima.” Suyuti ameiandika akiitoa kwa Ali (a.s.).85 Hivyo ndivyo yalivyogawika maneno ya Ali (a.s.) kati ya Hadithi ya Mtume kwa herufi yake au madhumuni yake, na kati ya sifa au kutoa kalenda ya tukio zito la kihistoria, na katika yote haya hakuna lililokwenda nje na hali halisi ya kihistoria, si katika kubwa wala dogo. Na muhtasari wa msimamo wa Ali (a.s.) na yakini yake juu ya haki yake katika ukhalifa, ni kuwa alikuwa ni mwenye yakini na nafasi yake ya pekee mbele ya Mtume (s.a.w.w.), na uhai wake wa kujitolea kwa ikhlasi katika Uislamu. Hakika katika zama za Mtume alikuwa akisema (a.s.): “Basi je, akifa au akiuliwa mtarudi nyuma kwa visigino vyenu?” (Sura Aali Imran: 144). Wallahi hatugeuki nyuma kwa visigino vyetu baada ya Mwenyezi Mungu kutuongoza. Wallahi akifa au kuuawa bila shaka kwa hakika nitapigania lile alilopigania mpaka nifikwe na mauti. Wallahi bila shaka mimi ni ndugu yake, walii wake, mwana wa ami yake na mrithi wa elimu yake, basi ni nani mwenye haki zaidi kuliko mimi?”86 Na yeye (a.s.) ndiye aliyesema: “Alipoondoka (s.a.w.w.) Waislamu waligombania jambo baada yake, Wallahi sikuwa nafikiri wala kunijia fikra kuwa waarabu watalitoa jambo hili baada yake (s.a.w.w.) toka kwa Ahlul-Bait wake, wala wao kuwa watalizuia mbali nami baada yake. Nilishtushwa na kundi la watu likimiminika kwa fulani kumpa Baiya….”87 Musnad Fatima cha Suyuti Uk. 224, Hadithi ya 94. Al-Mustadrak Juz. 3, Uk. 126. Majmauz-Zawaid Juz. 9, Uk. 134, amesema: Wapokezi wake ni sahihi, baadhi wameijadili kwa kufuata madhehebu, haina dosari katika njia yake ya upokezi. 87 Nahjul-Balaghah Uk. 451, Barua ya 62, barua yake kwa watu wa Misri. 85 86
57
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
Hivyo ndivyo: “Alitaka haki watu waitafute, na sio yeye awatangulie kuitafuta.”88
YAHUSU IMAM ALI (A.S.) KUWAPA BAIYA HAWA WATATU (ABU BAKR, UMAR NA UTHMAN) Wamehoji juu ya Baiya ya Imam Ali (a.s.) kwa hawa watatu: Abu Bakr, Umar na Uthman. Wakadai kuwa Baiya hiyo haikufanyika kwa sababu ya maslahi, au Taqiyya au kulazimishwa, hivyo yote hayo yanapelekea kutia dosari haki ya Bwana wetu Imam Ali (a.s.). Hakika suala la kulazimishwa kutoa Baiya na kutoharakia kufanya hivyo yeye mwenyewe, ni jambo lililonukuliwa na wanahistoria na wanasira. Bukhari ameandika: “Hakika Ali alijizuia kufanya Baiya muda wa miezi sita mpaka alipofariki Fatima Zahra (a.s.).”89 Na katika Khutba ya Imam Ali (a.s.) yamekuja yale yanayobainisha kwa uwazi sababu zilizopelekea yeye kutoa Baiya, na anafichua siri yake, hivyo haibaki nafasi kwa mwenye kufasiri kutoa tafsiri yake, yeye anasema: “Wallahi lau kama si kukhofu mfarakano, na ukafiri kurudi na dini kuangamia, tungeghairi hilo, hivyo tukavuta subira juu ya baadhi ya machungu.”90 Na pia anasema katika Nahjul-Balaghah: “Niliangalia na kuona sina msaidizi isipokuwa watu wa nyumba yangu, hivyo nilijiepusha kuwatumbukiza kwenye mauti, nilifumba macho yakiwa na chembe ya vumbi, na nilikunywa hali ya kwamba kooni kuna mfupa atumatuz-Zahrai Wal-Fatimiyuuna cha Abbas Mahmud Al-Aqqad, mjaladi wa pili toka F kwenye Al-Majmuatul-Kamilah Uk. 326. 89 Sahih Bukhari Juz. 5, Uk. 288. Tarikh Tabari Juz. 2, Uk. 234. 90 Nahjus-Saada Juz. 1, Uk. 248, cha Shaikh Al-Mahmudiy. 88
58
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
uliokwama, na nilivuta subira katika kuvuta pumzi, na kwa uchungu mno kuliko ladha ya shubiri.”91 Je unaweza kuletwa ubainifu uliyo bayana mno kuliko huu? Basi ni lipi eneo la dosari baada ya malalamiko haya? Na hali yeye ndiye mjuzi mno wa hali na matarajio. Ndio, lau asingewatolea hoja, na akawa ametoka kwenda Saqifa kwa juhudi kabisa, huku akiwa ameuacha mwili wa Mtume kipenzi (s.a.w.w.), na hatimaye haraka sana akaweka mkono wake juu ya mikono yao (akatoa Baiya), kweli hapo dosari ingekuwa na nafasi kwenye hoja kama hii. Hivyo ikithibiti kupitia sira ya Ali bin Abu Talib kuwa aliishambulia nadharia ya Shura, na akatamka bayana kuwa haina misingi ya Sheria, na akatamka bayana kulazimishwa kwake kutoa Baiya kwa hawa makhalifa watatu, basi utoaji wake wa Baiya hauna dalili yoyote juu ya uhalali wa kisheria wa ukhalifa wao, kama ilivyo thabiti katika maelezo yake ya bayana. Kisha yeye (a.s.) amebainisha kuwa ndiye aula na ukhalifa huo kuliko mwingine. Je tunaweza kusema kuwa uhalali wa kisheria wa ukhalifa wake utokanao na ile hali ya Ali (a.s.) kuwa aula na ukhalifa, ni aula ya ubora na si aula ya kuwa makhsusi (na ukhalifa)? Rai hii inakanushwa na maelezo na maneno ya Ali, pale aliposema: “Watu walimpa Baiya Abu Bakr na hali mimi ndiye mtu aula kwao kuliko kwenye kanzu yangu hii.” Ambalo laonyesha kuwa maana yake ni aula ya umakhsusi na si aula ya ubora, ni kuwa hakuna maana nyingine yoyote ya yeye kuambatanisha baina ya uaula wake na jambo husika (Baiya) na uaula wake na kanzu yake, kwa sababu yeye ndiye mmiliki wake (wa kanzu). Na yeye (a.s.) anasema hakika uaula wake na watu ni wenye nguvu na mkazo kuliko uaula wake na kanzu yake. 91
Nahjul-Balaghah, Uk. 68, Khutba ya 26. Uhakiki wa Dr. Subhi Swalih. 59
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
Na kadhalika kauli yake: “……Nikajifikiria, je? Nishambulie na mkono butu, au nivumilie giza la upofu, mtu mzima humo huzeeka, na mdogo humo huwa kijana, muumini anataabika humo mpaka akutane na Mola Wake Mlezi. Nikaona kuivumilia hali hii ni busara, basi nikasubiri hali jichoni mwangu mna utongotongo, na kooni kuna kitu kilichokwama. Naiona mirathi yangu imepokonywa……”92 Maana yake ni: Nikawa naiakhirisha nafsi yangu baina ya kuufikia kwa nguvu isiyotosha, kama ilivyo kwenye kauli yake: “Niliangalia na kuona sina msaidizi isipokuwa watu wa nyumba yangu, hivyo nilijiepusha kuwatumbukiza kwenye mauti…..”93 hivyo lau angepata nguvu za kutosha angewapiga vita wanasaqifa, nalo hilo ni maarufu toka kwenye kauli yake: “Lau ningewapata arobaini wenye azma thabiti basi ningewashambulia jamaa.”94 Msimamo huu kutoka kwa Ali hauoani na fikra ya aula ya ubora, bali waoana na fikra ya aula ya umakhsusi. Kadhalika kauli yake: “Au nivumilie giza la upofu….”, hakika maana yake ni kuwa hakika lililopatikana haikuwa ni kupora uongozi wa kidunia tu, bali hiyo ilikuwa ni mwanzo wa mapinduzi ya kifikra na upotovu unaojumuisha umma mzima. Na hilo ndilo alilolitilia mkazo baada ya mauaji ya Uthman, pale walipomjia wakimwomba wampe Baiya, akasema: “Niacheni na mtafuteni mtu mwingine…… Kwa kweli msitari wa upeo wa macho umefunikwa na mawingu, na njia iliyonyooka haijulikani tena”95 Na kauli yake (a.s.): “Na hakika mimi nahofia juu yenu msiwe katika kipindi (kingine), na hali bila shaka mambo yameshapita, iharul-Anwar Juz. 28, Uk. 313, amenukuu kutoka kwenye Nahjul-Balaghah cha Ibnu B Abil-Hadid Juz. 10, Uk. 151. 93 Nahjul-Balaghah, Khutba ya 21. 94 Sharhu Nahjul-Balaghah cha Ibnu Abil-Hadid Juz. 2, Uk. 47. 95 Nahjul-Balaghah, Uk. 136, Khutba ya 92. Uhakiki wa Dr. Subhi Swalih. 92
60
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
humo mmepinda mpindo ambao ndani yake mlikuwa si wenye kusifika vizuri kwangu.”96
USHAHIDI WA KIHISTORIA JUU YA USAHIHI WA NADHARIA YA TAMKO LA KUTAWAZWA Kuna ushahidi mwingi mno katika maisha ya Mtume (s.a.w.w.) na Ali (a.s.) ukithibitisha kuwa Mtume alikuwa akimwandaa Ali (a.s.) maandalizi maalumu ya ujumbe maalumu. Bila shaka Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akimuanza kwa kipawa cha kifikra pindi maswali yake (a.s.) yanaposita. Na anakaa naye faragha saa nyingi usiku na mchana, akimfumbua macho yake kuhusu uelewa wa utume na matatizo ya njia hiyo, mpaka mwisho wa maisha yake (s.a.w.w.). Nasaiy amepokea97 kwa njia yake kutoka kwa Abu Is’haqa, amesema: “Nilimuuliza Qutham bin Abbas, vipi Ali alimrithi Mtume wa Mwenyezi Mungu?” Akasema: “Kwa kuwa yeye alikuwa wa kwanza wetu kukutana naye, na mwenye kuambatana naye sana kuliko sisi.” Na pia alipokea kutoka kwa Ali (a.s.) kuwa alisema: “Nilikuwa niombapo hupewa, na nikaapo kimya huanzwa.”98 Abu Naiim amepokea ndani ya kitabu Hilyatul-Awliyai, kutoka kwa Ibnu Abbas kuwa alisema: “Tulikuwa tukizungumza kuwa Mtume (s.a.w.w.) alimkabidhi Ali mirathi sabini, ambazo hakumkabidhi mwingine yeyote.”99 ahjul-Balaghah Juz. 2, Uk. 256, Khutba ya 178. Uhakiki wa Dr. Subhi Swalih. Shubhatu N Warudud Juz. 3, Uk. 47. 97 Al-Khaswais Uk. 91, uhakiki wa Al-Juwayniy, chapa ya Darul-Kutubi Al-Ilmiyyah. AlMustadrak cha Hakim Juz. 3, Uk. 136. 98 Al-Khaswais Uk. 98. Al-Mustadrak cha Hakim Juz. 3, Uk. 135. 99 Hilyatul-Awliyai Juz. 1, Uk. 68. 96
61
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
Na Nasaiy amepokea kutoka kwa Ali kuwa alisema: “Nilikuwa na hadhi kwa Mtume ambayo hakuwa nayo yeyote kati ya viumbe. Nilikuwa namjia kila usiku na kusema: ‘Assalaam Alayka ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu.’ Iwapo akijikohoza huondoka kurudi kwa ahli wangu, na laa sivyo huingia.”100 Na pia imepokewa kutoka kwake (a.s.) kuwa alisema: “Nilikuwa na nafasi mbili za kuingia kwa Mtume: Nafasi ya kuingia usiku, na nafasi ya kuingia mchana.”101 Na maandalizi haya maalumu ya Ali kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) yalijiakisi pindi alipokuwa ndio kimbilio na marejeo pekee ya kutatua tatizo lolote lile ambalo linashindikana kutatuliwa na uongozi uliokuwa ukitawala wakati huo. Na wala hatujui katika historia ya uzoefu wa Kiislamu zama za Imam Ali (a.s.), tukio lolote lile ambalo Ali (a.s.) alirejea kwa mwingine ili kutaka kujua hukumu ya Kiislamu juu ya tukio hilo husika, au kutaka kujua njia ya utatuzi wake. Bali sisi tunajua katika historia makumi ya matukio ambayo makhalifa hawa watatu (Abu Bakr, Umar na Uthaman) walirejea kwa Ali (a.s.) kuomba utatuzi, japokuwa waliendelea kung’ang’ania maudhui hii. Ama ushahidi wa Mtume kutangaza mipango yake kumuhusu Ali na Ahlul-Baiti wake, yenyewe ni mingi mno na ni katika minasaba mbalimbali, kama vile katika Hadithi ya kuwaonya jamaa wa karibu, Hadithi ya vizito viwili, Hadithi ya hadhi, Hadithi ya Ghadiri na makumi ya Hadithi za Mtume (s.a.w.w.).102
l-Khaswais Uk. 97, uhakiki wa Al-Juwayniy, chapa ya Darul-Kutubi Al-Ilmiyyah. A Al-Khaswais Uk. 96, uhakiki wa Al-Juwayniy, chapa ya Darul-Kutubi Al-Ilmiyyah. 102 Rejea Sahih Tirmidhiy Juz. 5, Uk. 297. Sunan Ibnu Majah Juz. 1, Uk. 44, Hadithi ya 119. Hilyatul-Awliyai Juz. 1, Uk. 63. Al-Kashaf cha Zamakhshariy Juz. 1, Uk. 649. Tarikh Damashqiy Juz. 2, Uk. 476, Hadithi ya 996 na 997. Shawahidut-Tanziil Juz. 1, Uk. 161, Hadithi ya 216 mpaka ya 239. Majmauz-Zawaid Juz. 9, Uk. 111. Swawaiqul-Muhriqah Uk. 101 na 135 na 137. Musnad Ahmad Juz. 3, Uk. 7 na 26. 100 101
62
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
DALILI ZA KIRIWAYA ZINAZOTHIBITISHA
NADHARIA YA TAMKO LA KUTAWAZWA Baada ya kuthibitisha kihistoria kuwa nadharia ya tamko la kutawazwa ndio njia pekee ya kiungu ya kisheria ambayo Mtume (s.a.w.w.) aliithibitisha ndani ya maisha yake, na kuwa Imam Ali bin Abu Talib amekataa matamshi yote na badala zote zilizoingizwa ndani ya Uislamu zisizokuwa tamko la kutawazwa, na akasimama kivitendo kutetea nadharia ya tamko la kutawazwa, basi imebaki tuulize kuhusu dalili za nukuu ambazo zathibitisha kuwa Mtume (s.a.w.w.) aliusia ukhalifa kwa Ali baada yake, kama ambavyo yeye Imam (a.s.) alivyousia ukhalifa kwa kizazi chake maasumu baada yake. Hakika Shia Imamiya wanaamini Uimamu wa Ali bin Abu Talib (a.s.), wanawe wawili Hasan na Husain (a.s.), na wa Maimamu tisa kutoka kizazi cha Husain (a.s.). Na Uimamu wa hawa umepatikana kwa tamko kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), na kwa tamko kutoka kwa kila Imam juu ya Uimamu wa Imam wa baada yake. Maelezo ya Mtume yanayohusu hilo yamegawanyika katika aina tatu: Aina ya Kwanza: Yameweka marejeo ndani ya mipaka ya Ahlul-Baiti (a.s.) tu, bila kutaja majina yao, mfano Hadithi ya vizito viwili na Hadithi ya Safina, nazo ni mutawatiri kwa njia ya wote Sunni na Shia. Aina ya Pili: Ni yanayoweka kikomo cha idadi ya makhalifa na Maimamu kuwa ni kumi na wawili. Na kuwa wao ni kutokana na Kuraishi, au wao ni kutokana na Hashim. Na ni wazi kuwa idadi hii inaoana na Maimamu wa Ahlul-Baiti, na hakuna mushkeli wowote katika hilo, kinyume na unapotaka kuioanisha na wengine wasiokuwa wao. 63
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
Aina ya Tatu: Tamko litajalo majina ya Maimamu kumi na wawili, kupitia njia za Sunni na Shia.
Ama yaliyopatikana kuhusu aina ya kwanza: Tirmidhiy amepokea kutoka kwa Jabir kuwa alisema: “Nilimwona Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) katika Hijja yake siku ya Arafa akiwa juu ya ngamia wake akitoa khutba, nikamsikia akisema: ‘Enyi watu! Hakika mimi naacha kati yenu yale ambayo lau mkiyachukua kamwe hamtapotea: Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu Ahlul-Baiti wangu.”’ Tirmidhiy anasema: “Na katika mlango huu kuna iliyopokewa kutoka kwa Abu Saiid, Zaid bin Arqam na Hudhaifa Ibnu Asiid.”103 Na ndani ya Sahih Muslim, Musnad Ahmad, Sunan ya AdDaramiy na ya Al-Bayhaqiy na wengine wasiokuwa hao wawili, na tamko ni la wa kwanza, imepokewa kutoka kwa Zaid bin Arqam, amesema: “Hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu alisimama kuhutubia eneo liitwalo Khum, lililopo kati ya Makka na Madina…. kisha akasema: ‘Fahamuni, Enyi watu! Hakika mimi ni mwanadamu nakaribia kujiwa na mjumbe na nitajibu, na bila shaka mimi ni mwenye kuacha kati yenu vizito viwili: Cha kwanza ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu, humo mna uongofu na nuru, basi kichukueni Kitabu cha Mwenyezi Mungu na mshikamane nacho……na AhlulBaiti wangu.”’104 Na katika Sunan ya Tirmidhiy na Musnad ya Ahmad, na tamko ni la wa kwanza: “Hakika mimi ni mwenye kuacha kati yenu ambavyo mkishikamana navyo hamtapotea baada yangu, kimoja t-Tirmidhiy Juz. 5, Uk. 621, mlango wa fadhila za watu wa nyumba ya Mtume. Pia rejea A Kanzul-Ummahl Juz. 1, Uk. 48. 104 Sahih Muslim, mlango wa fadhila za Ali bin Abu Talib. Musnad Ahmad Juz. 4, Uk. 366. Sunan Daramiy Juz. 2, Uk. 431. Sunanul-Bayhaqiy Juz. 2, Uk. 148 na Juz. 7, Uk. 30 japo kwa tofauti kidogo. Mushkilul-Athar cha Twahawi Juz. 4, Uk. 368. 103
64
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
ni kikubwa kuliko kingine: Kitabu cha Mwenyezi Mungu, kamba iliyonyooka toka mbinguni hadi aridhini, na kizazi changu watu wa nyumba yangu, na havitafarikiana mpaka vinikute kwenye Hodhi, basi angalieni ni jinsi gani mtakavyobaki navyo.”105 Na miongoni mwa maelezo ambayo yamepatikana katika aina hii ni Hadithi ya Safina. Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema: “Fahamuni, hakika Ahlul-Baiti wangu kwenu nyinyi ni mfano wa Safina ya Nuh kwa kaumu yake, atakayeipanda ataokoka na atakayejitenga nayo atazama.”106 Kundi miongoni mwa ulamaa wanaona kuwa Ahlul-Baiti ni watano watukufu waliyo wema: Sayyiduna Rasuli wa Mwenyezi Mungu, Imam Ali, Sayyidatu Fatima Zahrau, Hasan na Husain (a.s.). Rai hii imesemwa na wengi miongoni mwa masahaba, ameisema Abu Said Al-Khudri, Anas bin Malik, Wathalit bin As-Asqau, mama wa waumini Ummu Salamah, Aisha, Ibnu Abi Salama, Saad bin Abu Waqqas na wengineo. Na pia imesemwa na jamaa miongoni mwa wafasiri na wanahadithi, miongoni mwao ni Al-Fakhru Razi katika tafsiri AlKabiir, Zamakhshariy katika Al-Kashaf, Al-Qurtubiy katika AlJamiu Liahkamil-Qur’an, As-Shawkaniy katika Fat’hul-Qadiir, Tabariy katika Jamiul-Bayan An-Taawiil Ayil-Qur’an, Suyuti katika Durul-Manthur, Ibnu Hajar Al-Asqalaniy katika Al-Iswaba, AlHakim katika Al-Mustadrak, Dhahabiy katika Talkhis, na Imam Ahmad bin Hanbal katika Musnad. Huenda rai hii ndiyo iliyo karibu mno na usahihi, bali ndio ipewayo kipaumbele, na hilo ni kutokana na kauli zifuatazo: irmidhiy Juz. 5, Uk. 622. Usudul-Ghaba Juz. 2, Uk. 12 katika wasifu wa Imam Husain. T Durul-Manthur katika tafsiri ya Aya ya Mawadda ya Sura Shura. 106 Al-Hakim katika Al-Mustadrak Juz. 3, Uk. 151. 105
65
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
Muslim amepokea ndani ya Sahih yake kwa njia yake kutoka kwa Amir bin Saad bin Abu Waqqas, kutoka kwa baba yake, amesema: “Muawiya bin Abu Sufiyan alimwamuru Saad, akasema: ‘Kitu gani kilichokuzuia usimtukane Abu Turabi (Ali)?’ Akasema: ‘Ama nikumbukapo mambo matatu aliyoyasema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) kumwambia yeye (a.s.) sintomtukana, kuwa nalo moja kati ya hayo ni jambo nilipendalo mno kuliko ngamia mwekundu. Baada ya kumwacha katika moja ya vita vyake, Ali alimwambia: ‘Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Umeniacha pamoja na wanawake na watoto wadogo?’ Nikamsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu akimwambia: ‘Hivi huridhii kwangu mimi (wewe) kuwa na cheo cha Haruna kwa Musa, ila ni kuwa hakuna unabii baada yangu.’ “Na nilimsikia (s.a.w.w.) siku ya Khaibar akisema: ‘Bila shaka nitamkabidhi bendera mtu ambaye Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanampenda, naye anawapenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake.’ Hapo tukatamani hadhi hiyo, akasema (s.a.w.w.): ‘Niitieni Ali.’ Akaletwa, naye alikuwa anaumwa macho, ndipo akatemea mate machoni mwake, na akamkabidhi bendera na Mwenyezi Mungu akaleta ushindi mikononi mwake. Na ilipoteremka Aya hii: “Basi waambie: Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu” (Sura Imran: 61) Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alimwita Ali, Fatima, Hasan na Husain, akasema: ‘Ewe Mola! Hawa ndio ahli wangu.”’107 Na Tirmidhiy ameipokea ndani ya Sahih yake kwa njia yake kutoka kwa Amr bin Saad bin Abu Waqqas, amesema: “Mwenyezi Mungu alipoteremsha Aya hii: “Basi waambie: Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu” (Sura Imran: 61) Mtume wa 107
Sahih Muslim Juz. 15, Uk. 175 – 176. 66
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alimwita Ali, Fatima, Hasan na Husain, akasema: ‘Ewe Mola! Hawa ndio ahli wangu.”’108 Na ameipokea Al-Hakim ndani ya Al-Mustadrak,109 na Bayhaqiy ndani ya As-Sunan.110 Mwandishi wa Al-Kashaf anasema: “Hakuna dalili yenye nguvu kuliko hii juu ya ubora wa watu wa kishamia, nao ni Ali, Fatima, Hasan na Husain. Kwa sababu ilipoteremka Aya ya Maapizano, Mtume (s.a.w.w.) aliwaita akamkumbatia Husain kifuani, akamshika Hasan mkono, Fatima akatembea nyuma yake na Ali nyuma yake (ya Fatima), basi ikajulikana kuwa wao ndio muradi wa Aya. Na kuwa watoto wa Fatima na kizazi chao huitwa watoto wake (s.a.w.w.), na wanajinasibu kwake kwa nasaba sahihi, yenye kunufaisha duniani na Akhera.”111 Imamu Ahmad amepokea katika Al-Fadhail kwa sanadi yake kutoka kwa Shadad Abu Ammar, amesema: “Niliingia kwa Wathilu bin Al-Asqau, alikuwa na watu, wakamtaja Ali na kuanza kumtukana, nami nikamtukana pamoja nao. Waliponyanyuka akaniambia: ‘Nikupe habari ya yale niliyoyaona kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu?’ Nikasema: Ndio. Akasema: ‘Nilimwendea Fatima kumuuliza kuhusu Ali, akasema: ‘Ameelekea kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu.’ Basi nikaketi nikimngojea hadi alipokuja Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akiwa pamoja na Ali, Hasan na Husain, huku kamshika kila mmoja mkono, akaingia, akamsogeza karibu Ali na Fatima, na akawakalisha mbele yake, na akawakalisha Hasan na Husain kila mmoja juu ya paja lake, kisha akawafunika kwa nguo yake, kisha akasoma Aya hii: “Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu watu wa nyumba (ya Mtume), na kukutakaseni kabisa.” (Sura Ahzab: 33), kisha akasema: ‘Ewe Sunanut-Tirmidhiy Juz. 2, Uk. 166. Al-Mustafrak cha Hakim Juz. 3, Uk. 150. 110 Sunan cha Al-Bayhaqiy Juz. 7, Uk. 63. 111 Tafsirul-Kashaf cha Zamakhshari Juz. 1, Uk. 147 – 148. 108 109
67
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
Mungu hawa ndio Ahlul-Baiti wangu, na Ahlul-Baiti wangu ndiyo wenye haki mno.”’112 Imam Tabariy ameipokea ndani ya Tafsiri,113 Tirmidhiy ndani ya Sahih yake,114 Suyuti ndani ya Durul-Manthur,115 Al-Haythamiy ndani ya Majmauz-Zawaid,116 Al-Hakim ndani ya Al-Mustadrak 117 na Ahmad ndani ya Al-Musnad.118
Ama yaliyopatikana kuhusu aina ya pili: Ama ambayo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ametaja humo idadi ya Maimamu kuwa ni kumi na wawili, ni kuwa Mtukufu Mtume alitoa habari kuwa idadi ya Maimamu ambao watafuata baada yake ni kumi na wawili na hao ndio makhalifa wa baada yake, kama walivyopokea waandishi wa vitabu vya Sahih Sita na Masaanid vifuatavyo: Amepokea Muslim kutoka kwa Jabir bin Samra kuwa alimsikia Mtume (s.a.w.w.) akisema: “Dini itaendelea kusimama mpaka Kiyama kisimame, au wawe juu yenu makhalifa kumi na wawili, wote ni kutokana na Kuraishi.”119 Na katika riwaya ya Sufyan bin Uyayna amesema: “Mtume (s.a.w.w.) aliongea neno sikulisikia vizuri, nikamuuliza baba yangu: ‘Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema nini?’ Akasema: ‘Wote ni kutoka kwa Kuraishi.”’120 Al-Imam Ahmad bin Hanbal, Kitabul-Fadhail As-Swahaba Juz. 2, Uk. 557-578. Tafsirut-Tabar Juz. 22, Uk. 5 – 6. 114 Sahih Tirmidhi Juz. 5, Uk. 351 – 663. 115 Tafsirud-Durul-Manthur Juz. 5, Uk. 198. 116 Majmauz-Zawaid Juz. 9, Uk. 166. 117 Al-Mustadrak cha Al-Hakim Juz. 3, Uk. 147. 118 Musnad Imam Ahmad Juz. 4, Uk. 107. 119 Sahih Muslim Juz. 6, Uk. 4. 120 Fat’hul-Bariy Juz. 13, Uk. 181, Kitabul-Ahkam, mlango wa ukhalifa. MustadrakusSwahihayn Juz. 3, Uk. 617. 112 113
68
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
Na katika riwaya nyingine alisema: “Wote ni kutoka kizazi cha Hashim.”121 Ahmad na Al-Hakim wamepokea kutoka kwa Masruq, na tamko ni la wa kwanza, amesema: “Tulikuwa tumekaa usiku kwa Abdullah (Ibnu Masuud) akitusomea Qur’ani, mtu mmoja akamuuliza, akasema: ‘Ewe babaye Abdur-Rahman! Je mlimuuliza Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) umma huu utamiliki makhalifa wangapi?’Abdullah akasema: ‘Hajaniuliza yeyote kabla yako kuhusu hilo tangu nimefika toka Iraq.’ Kisha akasema: ‘Ndiyo, tulimuuliza Mtume wa Mwenyezi Mungu akasema: ‘Kumi na wawili kama idadi ya viongozi wa wana wa Israil.”’122
MBABAIKO WAO KATIKA KUFASIRI HADITHI HIZI Wanachuoni wa kambi ya Kisunni wamejaribu kuleta makusudio ya ibara ‘kumi na wawili’ iliyopo kwenye riwaya hizi zilizotangulia, na hatimaye kauli zao zikagongana. Ibnu Al-Arabi amesema anapofafanua kitabu Sunanit-Tirmidhiy: “Tukahesabu maamiri kumi na wawili baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), tukawakuta ni Abu Bakr, Umar, Uthman, Ali, Hasan, Muawiya, Yazid, Muawiya bin Yazid, Mar’wan bin AlHakam, Abdul-Malik bin Mar’wan, Al-Walid, Sulayman, Umar bin Abdul-Aziz, Yazid bin Abdul-Malik, Mar’wan bin Muhammad bin Mar’wa, na As-Saffah….” 121 122
Yanabiul-Mawadda: 3 mlango wa 77. Musnad Imam Ahmad Juz. 1, Uk. 398 na 406. Fat’hul-Bariy Juz. 16, Uk. 339. MajmauzZawaid Juz. 5, Uk. 190. Swawaiqul-Muhriqa Uk. 12. Tarikhul-Khulafai cha Suyuti Uk. 10. Al-Jamiu As-Swaghiir cha Suyuti Juz. 1, Uk. 75. Kanzul-Ummahl Juz. 13, Uk. 27. Faydhul-Qadiir Fisharhil-Jamius-Swaghiir cha Nawawi Juz. 2, Uk. 458. Tarikh Ibnu Kathir Juz. 6, Uk. 248. 69
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
Kisha baada ya hao akahesabu makhalifa ishirini na saba kuanzia zama za Bani Abbas mpaka zama zake, kisha akasema: “Tukihesabu kumi na wawili kati yao, idadi kwa sura hii itakomea kwa Sulayman. Na tukihesabu kwa kimaana basi itamaanisha watano kati yao, makhalifa wanne na Umar bin Abdul-Azizi, na sijajua maana ya Hadithi hii.”123 Kadhi Iyyadh amesema katika jibu lake kwa yule aliyesema: Hakika walitawala wengi kuliko idadi hii: “Hoja hii ni batili, kwa sababu (s.a.w.w.) hajasema: ‘Hawatawali ila kumi na wawili.’ Na bila shaka idadi hii wametawala, na hilo halizuii kuwa zaidi ya hao.”124 Suyuti amenukuu jibu, amesema: “Muradi ni kupatikana makhalifa kumi na wawili ndani ya muda wote wa Uislamu mpaka Kiyama, ambao wanatenda kwa haki hata kama hawatafuatana.”125 Na katika kitabu Fat’hul-Bariy amesema: “Na wamepita kati yao makhalifa wanne, na ni lazima idadi itimie kabla ya kusimama Kiyama.”126 Ibnu Al-Jawziy amesema: “Na kutokana na haya, muradi wa ‘Kisha yatakuwepo machafuko.’ Ni vurugu yenye kuruhusu kutokea Kiyama, ikiwemo kutokea kwa Dajjal na ya baada yake.”127 Suyuti amesema: “Kati ya kumi na wawili wameshapatikana makhalifa wanne, na Hasan, Muawiya, Ibnu Zubair na Umar bin Abdul-Aziz, hawa ni nane. Na inawezekana kumuunganisha kwao Al-Mahd Al-Abbasiy, kwa sababu katika Bani Abbas yeye ni kama Sharhul-Arabiy Alas-Sunan At-Tirmidhiy Juz. 9, Uk. 68 – 69. Sharhun-Nawawi Ala Muslim Juz. 12, Uk. 201 – 202. Fat’hul-Bariy Juz. 16, Uk. 339 na ameikariri katika Uk. 341. 125 Tarikhul-Khulafai cha Suyuti Uk. 12. 126 Tarikhul-Khulafai cha Suyuti Uk. 12. 127 Tarikhul-Khulafai cha Suyuti Uk. 12. 123 124
70
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
Umar bin Abdul-Aziz katika Bani Umaiyyah. Na pia Tahir AlAbbasiy kutokana na uadilifu aliyopewa, hapo wanabakia wawili wenye kungojewa, mmojawapo kati ya hao wawili ni Mahdi, kwa sababu yeye ni kutokana na Ahlul-Baiti.”128 Na imesemekana: Muradi ni wawe kumi na wawili muda ule wa nguvu ya ukhalifa, nguvu ya Uislamu na kunyooka kwa mambo yake, awepo ambaye Uislamu utapata nguvu katika zama zake na wakongamane Waislamu juu yake.129 Bayhaqiy amesema: “Idadi hii imepatikana wakati wa Al-Walid bin Yazid bin Abdul-Malik, kwa sifa iliyotajwa. Kisha yakatokea machafuko na vurugu kubwa, kisha ukadhihiri ufalme wa Bani Abbas, na hakika kwa mujibu wa habari wanazidi idadi iliyotajwa, iwapo itaachwa sifa iliyotajwa humo au kuhesabiwa kati yao wale waliokuwepo baada ya machafuko yaliyotajwa.”130 Na wamesema: “Na ambalo wamekongamana juu yake ni: Makhalifa watatu, kisha Ali mpaka pale lilipotokea suala la mahakimu wawili katika vita vya Suffin, hivyo siku hiyo Muawiya akaipata alama ya ukhalifa. Kisha wakakongamana juu ya Muawiya wakati wa suluhu ya Hasan, kisha wakakongamana juu ya mwanae Yazid, na hapo Husain hakungojea jambo (ukhalifa) bali aliuwawa kabla yake. Kisha alipofariki Yazid walitofautiana mpaka walipokongamana juu ya Abdul-Malik bin Mar’wan baada ya kuuawa Ibnu Zubair. Kisha wakakongamana juu ya wanae wanne: Al-Walid, kisha Sulayman, kisha Yazid, kisha Hisham, na kati ya Sulayman na Yazid alikaa Umar bin Abdul-Aziz. Na wa kumi na mbili ni Al-Walid bin Yazid arikhul-Khulafai cha Suyuti Uk. 12. Swawaiqul-Muhriqah Uk. 19. Kwa mujibu huu T wafuasi wa kambi ya Kisunni wana Maimamu wawili wenye kungojewa kati ya hao wawili mmojawapo ni Mahdi. 129 Ameashiria hilo Suyuti katika Tarikhul-Khulafai Uk. 10. Na Nawawi katika Sharhu Muslim Juz. 12, Uk. 201 130 Amenukuu Ibnu Kathiir katika Tarikh yake Juz. 6, Uk. 249 kutoka kwa Bayhaqiy. 128
71
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
bin Abdul-Malik, watu walikongamana juu yake baada ya Hisham, na alitawala miaka mine.”131 Kwa mujibu wa haya ni kuwa ukhalifa wa hawa kumi na wawili ulikuwa sahihi kwa kule Waislamu kukongamana juu yao, na Mtume (s.a.w.w.) alikuwa ameshawabashiria Waislamu ukhalifa wao baada yake katika kuwapelekea watu Uislamu. Ibnu Hajar amesema kuhusu rai hii kuwa: “Ndio ipewayo kipaumbele kati ya rai.” Ibnu Kathir amesema: “Hakika njia ambayo ameipita Bayhaqiy na wakamwafiki baadhi ya jamaa, kuwa muradi wa makhalifa kumi na wawili waliotajwa katika hadithi hii ni hao waliofuatana mpaka zama za Al-Walid bin Yazid bin Abdul-Malik, fasiki ambaye tumeshatanguliza mazungumzo kumhusu kwa lawama na adhabu, ni njia yahitaji uchunguzi. “Na ufafanuzi wa hilo ni kuwa makhalifa mpaka zama za huyu Al-Walid bin Yazid, kwa kadirio lolote ni zaidi ya kumi na wawili, na dalili juu ya hilo ni kuwa makhalifa wane: Abu Bakr, Umar, Uthman na Ali ukhalifa wao umethibiti…..Kisha baada yao ni Hasan bin Ali kama ilivyotokea, kwa sababu Ali alimuusia na wakazi wa Iraki wakampa Baiya….mpaka alipofanya suluhu na Muawiya……. “Kisha ni mwanae Yazid bin Muawiya, kisha mwanae Muawiya Ibnu Yazid, kisha Mar’wan bin Al-Hakam, kisha mwanae AbdulMalik bin Mar’wan, kisha mwanae Al-Walid bin Abdul-Malik, kisha Sulayman Ibnu Abdul-Malik, kisha Umar bin Abdul-Aziz, kisha Yazid bin Abdul-Malik, kisha Hisham bin Abdul-Malik, hawa ni kumi na watano. Kisha Al-Walid bin Yazid bin Abdul-Malik, na iwapo tutauzingatia utawala wa Ibnu Zubair kabla ya Abdul-Malik, watakuwa kumi na sita. 131
Tarikhul-Khulafai Uk. 11. Swawaiqul-Muhriqah Uk. 19. Fat’hul-Bariy Juz. 16, Uk. 341. 72
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
“Kwa kadirio lolote lile, ni kuwa wao ni kumi na wawili kabla ya Umar bin Abdul-Azizi, na kwa makadirio haya anaingia Yazid bin Muawiya ndani ya kumi na wawili, na anatoka miongoni mwao Umar bin Abdul-Azizi, ambaye Maimamu wameungana katika kumshukuru, kumsifu kwa mazuri na kumjumuisha katika idadi ya makhalifa wema. Na watu wote wamekongamana juu ya uadilifu wake, na kuwa siku za utawala wake zilikuwa kati ya siku adilifu mno, hata marafidhi wanalikubali hilo. “Iwapo akisema: Mimi simzingatii ila yule ambaye umma umekongamana juu yake, kauli hii itamlazimu asimjumuishe Ali bin Abu Talib wala mwanae (Hasan), kwa sababu watu hawakukongamana juu yao, hiyo ni kwa kuwa wakazi wa Sham kwa ukamilifu wao hawakuwapa hawa wawili Baiya. “Na (Bayhaqiy) ametaja kuwa: Hakika baadhi yao wamemuhesabu Muawiya na mwanae Yazid na mwana wa mwanae Muawiya bin Yazid, na wala hawajaweka mpaka kwa siku za Mar’wan wala za Ibnu Zubair, kwa sababu umma haujakongamana juu ya yeyote kati ya hao wawili. Tunasema: Kwa mujibu wa haya amewajumuisha makhalifa watatu katika njia yake hii, kisha Muawiya, kisha Yazid, kisha Abdul-Malik, kisha Al-Walid bin Sulayman, kisha Umar bin Abdul-Aziz, kisha Yazid, kisha Hisham, hawa ni kumi. Kisha baada yao ni Al-Walid Ibnu Yazid bin Abdul-Malik fasiki mkubwa, na kwa kauli hiyo inamlazimu kumtoa Ali na mwanae Hasan, nalo hilo ni kinyume kabisa na yale waliyoyasema Maimamu wa Usunni bali hata Mashia.”132 Ibnu Al-Jawziy katika kufichua mushkeli uliyopo, amenukuu jibu kwa mitazamo miwili: Wa kwanza: “Kuwa (s.a.w.w.) katika Hadithi yake aliashiria yale yatakayokuwa baada yake na baada ya masahaba zake, na 132
Tarikh Ibnu Kathir Juz. 6, Uk. 249 – 250. 73
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
kuwa utawala wa masahaba zake unafungamana na utawala wake, hivyo akatoa habari kuhusu tawala zitakazotokea baada yao, kwa hilo ni kama aliashiria idadi ya makhalifa wa Bani Umaiyyah, na ni kama kauli yake: ‘Dini itaendelea’ ni maana yake ni utawala mpaka watawale makhalifa kumi na wawili.” Kisha anahamia kwenye sifa nyingine nzito zaidi kuliko ya kwanza: “Na wa kwanza katika Bani Umaiyyah ni Yazid bin Muawiya na wa mwisho wao ni Mar’wan punda, na idadi yao ni kumi na watatu, na wala hahesabiwi Uthman na Muawiya wala Ibnu Zubair kwa kuwa kwao sahaba, hivyo tukimtoa kati yao Mar’wan bin Al-Hakam kutokana na tofauti iliyopo kuhusu uswahaba wake, au kwa kuwa alikuwa ni mwenye kushindwa baada ya watu kukongamana juu ya Abdullah bin Zubair, idadi inasihi. Na ulipotoka ukhalifa mikononi mwa Bani Umaiyyah kulitokea machafuko makubwa na vita vingi mpaka ilipotulia dola ya Bani Abbas, ndipo hali ikabadilika bayana kinyume na ilivyokuwa kabla.” Ibnu Hajar amejibu utoaji dalili huu, ndani ya kitabu Fat’hulBari.133 Wa pili: Ibnu Al-Jawziy amenukuu toka kwenye juzuu ambalo alilikusanya Abul Husain bin Al-Munadiy kuhusu Al-Mahdi, na kuwa alisema: “Inawezekana hili likawa ni baada ya Mahdi ambaye atatokea mwisho wa zama. Nimekuta ndani ya kitabu Danieli: ‘Atakapofariki Mahdi watamiliki baada yake wanaume watano kutoka kizazi cha Sibtul-Akbar 134 (Mjukuu mkubwa), kisha watano kutoka kizazi cha Sibtul-Asghar (Mjukuu mdogo), kisha wa mwisho at’hul-Bari Juz. 13, Uk. 183, kutoka kwa Ibnu Al-Jawziy katika kitabu chake F Kashful-Mushkil. 134 Kwa jinsi tujuavyo Sibtul-Akbar ni Imam Hasan bin Ali (a.s.), na Sibtul-Asghar ni Imam Husain bin Ali (a.s.), ambao Mtume (s.a.w.w.) aliwaita kuwa hao wawili ni Sibti wake.- Mtarjumu. 133
74
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
wao atausia ukhalifa kwa mtu kutoka kizazi cha Sibtul-Akbar (Mjukuu mkubwa), kisha baada yake atamiliki mwanae, na kwa huyo watatimia wafalme kumi na wawili, kila mmoja kati ya hao ni Imam Mahdi.’” Akasema: “Na katika riwaya nyingine…..kisha jambo baada yake litatawaliwa na wanaume kumi na wawili: Sita kutoka kizazi cha Hasan na watano kutoka kizazi cha Husain, na wa mwisho ni kutoka kwa wasiokuwa wao, kisha atafariki na hatimaye zama kuharibika.” Ibnu Hajar amezungumzia Hadithi hii ya mwisho katika kitabu chake as-Sawaiq, akasema: “Hakika riwaya hii ni mbovu mno, haitegemewi.”135 Na kaumu wakasema: “Dhana kubwa ni kuwa yeye (s.a.w.w.) alitoa habari za maajabu yatakayotokea baada yake, ikiwa ni pamoja na vurugu, mpaka ifikie katika wakati mmoja watu kufarakiana juu ya maamiri kumi na wawili, na lau angekusudia jingine lisilo hili, angesema: Watakuwa maamiri kumi na wawili wanafanya kadha wa kadha. Lakini aliwatenga na habari, hivyo tukafahamu kuwa alikusudia kuwa wao watakuwa katika zama moja….”136 Wakasema: “Na hilo lilitokea mwaka wa mia tano, hakika huko Hispania peke yake kulikuwa na watu sita, wote wakiwa na alama ya ukhalifa, pamoja na hao ni mtawala wa Misri na wa Kibani Abbas huko Baghdad, na wale waliokuwa wakidai ukhalifa pande za ardhi, miongoni mwa Alawiya na Makhawariji.”137 Fat’hul-Bari Juz. 13, Uk. 184. Swawaiqul-Muhriqa cha Ibnu Hajar Uk. 19. Fat’hul-Bari Juz. 16, Uk. 338. 137 Sharhu An-Nawawi Juz. 12, Uk. 202. Fat’hul-Bariy Juz. 16, Uk. 339, na tamko ni la wa mwisho. 135 136
75
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
Ibnu Hajar amesema: “Nayo ni maneno ya ambaye hajafuatilia kitu chochote kati ya njia za Hadithi isipokuwa riwaya ambayo imetokea ndani ya Bukhari, ndivyo ilivyo kwa muhtasari….”138 Hakika uwepo wao katika zama moja hulea mfarakano halisi, hivyo haisihi uwe ndio muradi.139 Ndio hivyo, hawajaafikiana katika rai moja katika kutafsiri riwaya zilizotangulia, kisha wao hakika wamepuuzia kuleta riwaya ambazo humo Mtume (s.a.w.w.) ametaja majina ya Maimamu kumi na wawili, kwa sababu zenyewe zilikuwa zinakhalifu siasa ya watawala wa madhehebu ya Kisunni muda wote wa karne. Wanahadithi wa kambi ya Kiahlul-Bait wameziandika katika vitabu vyao kwa njia itokayo kwa masahaba wema, kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.).140
Ama yaliyopatikana kuhusu aina ya tatu: Kutoka kwa Abu Abdullah as-Sadiq (a.s.) amesema: “Hakika Jibril alimteremkia Muhammad (s.a.w.w.), akamwambia: ‘Ewe Muhammad! Hakika Mwenyezi Mungu anakubashiria mzawa atakayezaliwa na Fatima ambaye umma wako utamuuwa baada yako. ‘ Akasema (s.a.w.w.): ‘Ewe Jibril! Amani iwe juu ya Mola Wangu, sina haja na mzawa kutoka kwa Fatima ambaye umma wangu utamuuwa baada yangu.’ Akapaa kisha akateremka, akamwambia tena kama vile. Akasema (s.a.w.w.): ‘Ewe Jibril! Amani iwe juu ya Mola Wangu, sina haja na mzawa kutoka kwa Fatima ambaye umma wangu utamuuwa baada yangu.’ Jibril akapaa mbinguni kisha akateremka, akamwambia: ‘Ewe Muhammad! Hakika Mola Wako Mlezi anakutolea salamu, na anakubashiria kuwa hakika Yeye ni Mwenye kuuweka Uimamu, uwalii na wasia kwenye kizazi chake.’ Fat’hul-Bariy Juz. 13, Uk. 182. Fat’hul-Bariy Juz. 13, Uk. 183. 140 Maalimul-Madrasatayn Juz. 1 Uk. 541 – 546. 138 139
76
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
“Akasema (s.a.w.w.): ‘Hakika nimeridhia.’ Kisha akatuma ujumbe kwa Fatima: ‘Hakika Mwenyezi Mungu amenibashiria mzawa atakayezaliwa na wewe, umma wangu utamuuwa baada yangu.’ Fatuma akamtumia ujumbe: ‘Sina haja na mzawa ambaye umma wako utamuuwa baada yako.’ Ndipo (s.a.w.w.) akamtumia ujumbe: ‘Hakika Mwenyezi Mungu ameweka Uimamu, uwalii na wasia katika kizazi chake.’ Akamtumia ujumbe: ‘Hakika mimi nimeridhia katika: ‘Mama yake amechukua mimba yake kwa taabu na akamzaa kwa taabu, na kumbeba na kumwachisha ziwa ni miezi thelathini, hata anapofikia baleghe yake na akawa mwenye umri wa miaka arobaini, akasema: Ee Mola Wangu Mlezi! Niwezeshe nishukuru neema zako ulizonineemesha mimi na wazazi wangu, na ili nifanye vitendo vizuri unavyovipenda na unitengenezee watoto wangu…’ (Sura Ahqaf: 15).’ Lau si kuwa Yeye amesema: ‘Nitengenezee watoto wangu kwa ajili yangu.’ Basi watoto wake wote wangekuwa ni Maimamu.”141 Na Shia wanaamini kuwa kila Imam alitoa tamko la kumtawaza Imam anayefuata baada yake.142
KUWAASHIRIA MAIMAMU KUMI NA WAWILI, KUPITIA RIWAYA YA KISUNNI Al-Juwayniy143 amepokea kutoka kwa Abdullah bin Abbas kuwa amesema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: ‘Mimi Usulul-Kafiy Juz. 1, Uk. 465. Usulul-Kafiy Juz. 1, Uk. 286. Kitabu Hoja, mlango wa tamko la Mwenyezi Mungu juu ya Maimamu. Ithbatul-Hudat cha Muhammad bin Hasan Al-Huri Al-Amiliy. 143 Dhahabi amesema katika Tadhkratul-Huffadh Juz. 5, Uk. 150, anapotoa wasifu wa mashekhe zake: Imam mwanahadithi Mkamilifu wa kipekee, fahari ya Uislamu Swadrud-Din Ibrahim bin Muhammad bin Humwayhi Al-Jawniy Shafii Shaikh wa Kisufi, na alikuwa ni mchunguzi mno wa Hadithi. 141 142
77
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
ni bwana wa Manabii na Ali bin Abu Talib ni bwana wa Mawasii, na hakika Mawasii baada yangu ni kumi na wawili, wa kwanza wao ni Ali bin Abu Talib na wa mwisho wao ni Mahdi.”’144 Ibnu Abbas amesema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: ‘Hakika Makhalifa wangu na Mawasii wangu na Hoja wa Mwenyezi Mungu juu ya viumbe baada yangu ni kumi na wawili, wa kwanza wao ni ndugu yangu na wa mwisho wao ni mwanangu.’ Ikasemwa: ‘Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Ndugu yako ni nani?’ Akasema: ‘Ni Ali bin Abu Talib.’ Ikasemwa: ‘Mwanao ni nani?’ Akasema: ‘Mahdi ambaye ataijaza uadilifu na usawa kama ilivyojazwa ujeuri na dhulma. Naapa kwa Ambaye alinituma kwa haki kuwa mbashiri na mwonyaji, lau dunia haitobakiwa ila na siku moja, Mwenyezi Mungu atairefusha siku hiyo mpaka adhihiri humo mwanangu Mahdi, hapo atateremka Ruhullah Isa mwana wa Maryam na kuswali nyuma yake, na ardhi itang’aa kwa nuru ya Mola Wake Mlezi, na utawala wake (Mahdi) utafika Mashariki na Magharibi.”’145 Al-Juwayniy amepokea tena kwa njia yake, amesema: “Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akisema: ‘Mimi, Ali, Hasan, Husain na tisa kutoka kizazi cha Husain ni watoharishwa maasumu.”146
MUHTASARI Mwanadamu hakuumbwa bila shabaha bali kwa hakika ameumbwa kwa ajili ya ibada na uongofu. Unabii umechukua dhamana ya kuonya na kubalighi, na ama Uimamu wenyewe hakika umechukua Faraidus-Samtwayn Juz. 2, Uk. 312. Faraidus-Samtwayn Juz. 2, Uk. 312. 146 Faraidus-Samtwayn Juz. 2, Uk. 312. 144 145
78
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
dhamana ya kumwongoza mwanadamu upande wa kutimiza uongofu na kuushika mkono wa mwanadamu ili atekeleze (uongofu huo) kivitendo. Haiwezekani kuutambua unabii ila kwa ufunuo na miujiza, wala Uimamu hautambuliwi ila kwa tamko ambalo nalo kwa mchango wake humfichua maasumu. Na Baiya kwa Imam mwenye madaraka si uthibitisho wa wajibu wa kumtii kama Imam ambaye umethibiti juu yake uwalii kwa tamko, kama ambavyo pia (Baiya) haithibitishi Uimamu wake na ukhalifa wake. Ama Shura yenyewe si mbadala wa tamko, kama ambavyo haimwajabishi Imam Maasumu kutekeleza maamuzi yake (yaani maamuzi ya Shura). Mtume wa Mwenyezi Mungu alifanya amali zama za uhai wake ili kuimarisha nadharia ya tamko, kiasi kwamba historia haijathibitisha kuwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ana amali inayotajwa isiyokuwa na tamko. Ama Imam Ali (a.s.) yeye amali yake na harakati zake na misimamo yake vilikuwa pamoja na nadharia ya tamko, kiasi kwamba tunamkuta amekanusha badala nyingine zenye kuipinga nadharia ya tamko. Na mwisho tunakuta dalili za kiriwaya kwenye makundi yote mawili (Shia na Sunni) zinathibitisha kuwa ukhalifa na Uimamu wa Maimamu kumi na wawili ni kwa tamko la Mtume wa Mwenyezi Mungu, wa kwanza wao ni Ali bin Abu Talib (a.s.) na wa mwisho wao ni Imam Mahdi (a.s.). Na kwa haya nadharia ya tamko inakuwa ndio njia pekee ya kisheria ambayo inatimiza ibada na uongofu. Na mwisho wa dua zetu ni kumshukuru Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu.
79
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION 1. Qur’an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Thelathini 2.
Uharamisho wa Riba
3.
Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza
4.
Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili
5.
Hekaya za Bahlul
6.
Muhanga wa Imamu Husein (A.S.)
7.
Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.)
8.
Hijab vazi Bora
9.
Ukweli wa Shia Ithnaashari
10.
Madhambi Makuu
11.
Mbingu imenikirimu
12.
Abdallah Ibn Saba
13.
Khadijatul Kubra
14.
Utumwa
15.
Umakini katika Swala
16.
Misingi ya Maarifa
17.
Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia 80
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
18.
Bilal wa Afrika
19.
Abudharr
20.
Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu
21.
Salman Farsi
22.
Ammar Yasir
23.
Qur’an na Hadithi
24.
Elimu ya Nafsi
25.
Yajue Madhehebu ya Shia
26.
Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur’an Tukufu
27.
Al-Wahda
28.
Ponyo kutoka katika Qur’an
29.
Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii
30.
Mashukio ya Akhera
31.
Al Amali
32.
Dua Indal Ahlul Bayt
33.
Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna.
34.
Haki za wanawake katika Uislamu
35.
Mwenyezi Mungu na sifa zake
36.
Kumswalia Mtume (s)
37.
Nafasi za Ahlul Bayt (a.s)
38.
Adhana
39
Upendo katika Ukristo na Uislamu 81
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
40.
Tiba ya Maradhi ya Kimaadili
41.
Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu
42.
Kupaka juu ya khofu
43.
Kukusanya swala mbili
44.
Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara
45.
Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya
46.
Kusujudu juu ya udongo
47.
Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s)
48.
Tarawehe
49.
Malumbano baina ya Sunni na Shia
50.
Kupunguza Swala safarini
51.
Kufungua safarini
52.
Umaasumu wa Manabii
53.
Qur’an inatoa changamoto
54.
as-Salaatu Khayrun Mina -’n Nawm
55.
Uadilifu wa Masahaba
56.
Dua e Kumayl
57.
Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu
58.
Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake
59.
Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata
60. Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mtume Muhammad (s)
82
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
61.
Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza
62.
Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili
63.
Kuzuru Makaburi
64.
Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza
65.
Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili
66.
Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu
67.
Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne
68.
Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano
69.
Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita
70.
Tujifunze Misingi Ya Dini
71.
Sala ni Nguzo ya Dini
72.
Mikesha Ya Peshawar
73.
Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu
74. Ubora wa Imam ‘Ali Juu ya Maswahaba Na Ushia ndio njia iliyonyooka 75.
Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake
76.
Liqaa-u-llaah
77.
Muhammad (s) Mtume wa Allah
78.
Amani na Jihadi Katika Uislamu
79.
Uislamu Ulienea Vipi?
80.
Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s)
81.
Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s)
83
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
82.
Urejeo (al-Raja’a )
83.
Mazingira
84.
Utokezo (al - Badau)
85.
Hukumu ya kujenga juu ya makaburi
86.
Swala ya maiti na kumlilia maiti
87.
Uislamu na Uwingi wa Dini
88.
Mtoto mwema
89.
Adabu za Sokoni
90.
Johari za hekima kwa vijana
91.
Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza
92.
Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili
93.
Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu
94.
Tawasali
95.
Imam Mahdi katika Usunni na Ushia
96.
Hukumu za Mgonjwa
97.
Sadaka yenye kuendelea
98.
Msahafu wa Imam Ali
99.
Ngano ya kwamba Qur’ani imebadilishwa
100. Idil Ghadiri 101. Kusoma sura zenye Sijda ya wajibu 102 Hukumu zinazomuhusu mkuu wa kazi na Mfanyakazi 103. Huduma ya Afya katika Uislamu 84
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
104. Sunan an-Nabii 105. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza) 106. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili) 107. Shahiid Mfiadini 108. Kumsalia Nabii (s.a.w) 109. Ujumbe -Sehemu ya Kwanza 110. Ujumbe - Sehemu ya Pili 111. Ujumbe - Sehemu ya Tatu 112. Ujumbe - Sehemu ya Nne 113. Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu 114. Hadithi ya Thaqalain 115. Ndoa ya Mutaa 116. Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza 117. Ukweli uliopotea sehemu ya Pili 118. Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu 119. Ukweli uliopotea sehemu ya Nne 120. Ukweli uliopotea sehemu ya Tano 121. Mkutano wa Maulamaa wa Baghdad 122. Safari ya kuifuata Nuru 123. Fatima al-Zahra 124. Myahudi wa Kimataifa 125. Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi 85
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
126. Visa vya kweli sehemu ya Kwanza 127. Visa vya kweli sehemu ya Pili 128. Elimu ya Ghaibu ya Maimamu 129. Mwanadamu na Mustakabali wake 130. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Kwanza) 131. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Pili) 132. Khairul Bariyyah 133. Uislamu na mafunzo ya kimalezi 134. Vijana ni Hazina ya Uislamu 135. Yafaayo kijamii 136. Tabaruku 137. Taqiyya 138. Vikao vya furaha 139. Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje? 140. Visa vya wachamungu 141. Falsafa ya Dini 142. Azadari-Kuhuzunika na Kuomboleza 143. Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah 144. Mtazamo Mpya - Wanawake katika Uislamu 145. Kuonekana kwa Allah 146. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza) 86
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
147. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili) 148. Ndugu na Jirani 149. Ushia ndani ya Usunni 150. Maswali na Majibu 151. Mafunzo ya hukmu za ibada 152. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 1 153 Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 2 154. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 3 155. Abu Huraira 156. Vipengee kadhaa katika Swala ya Jamaa na Msikiti. 157. Mazingatio kutoka katika Qur’an - Sehemu ya Kwanza 158. Mazingatio kutoka kaitka Qur’an - Sehemu ya Pili 159. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya kwanza 160. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya Pili 161. Qur’ani Tukufu – Pamoja na Tarjuma ya Kiswahili 162. Falsafa ya Mageuzi ya Imam Husein (a.s) 163. Amali za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani 164. Elimu ya Tiba za Kiislamu - Matibabu ya Maimamu 165. Uislamu Safi 166. Majlisi za Imam Husein Majumbani 167. Je, Kufunga Mikono 168. Uislam wa Shia 87
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
169. Amali za Makka 170. Amali za Madina 171. Asili ya Madhehebu katika Uislamu 172. Sira ya Imam Ali kuhusu Waasi 173. Ukweli uliofichika katika neno la Allah 174. Uislamu na Mifumo ya Uchumi 175. Umoja wa Kiislamu na Furaha 176. Mas’ala ya Kifiqhi 177. Jifunze kusoma Qur’ani 178. As-Sahifatul Kamilah as-Sajjadiyyah 179. Hayya ‘Alaa Khayri’l-’Amal Katika Adhana 180. Ukweli kuhusu Funga ya Siku ya Ashura 181. Dua za Miezi Mitatu Mitukufu (Rajabu, Shaabani na Ramadhani) 182. Uadilifu katika Uislamu 183. Mahdi katika Sunna 184. Maswali Ya Uchunguzi Kuhusu Uislam 185. Kazi na Bidii ni njia ya maendeleo 186. Abu Talib – Jabali Imara la Imani 187. Ujenzi na Utakaso wa Nafsi 188. Vijana na Matarajio ya Baadaye 189. Usalafi – Historia yake, maana yake na lengo lake
88
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
190. Ushia – Hoja na Majibu 191. Mateso ya Dhuria wa Mtume (saww) 192. Maombolezo – Msiba wa Bwana wa Mashahidi (a.s.) 193. Shahidi kwa Ajili ya Ubinadamu 194. Takwa 195. Upotoshaji dhahiri katika Turathi (Hazina) ya Kiislamu 196. Amirul Muuminina (‘as) na Makhalifa 197. Uongozi na Utawala katika Mwenendo wa Imam ‘Ali (‘a) 198. Kuvunja hoja iliyotumika kutetea Uimamu wa AbuBakr 199. Adabu za vikao na mazungumzo 200. Hija ya Kuaga 201. Uwazi baina ya Maslahi na Vikwazo 202. Fadhila za watukufu watano katika Sahih Sita 203. Mdahalo baina ya Mwanachuoni wa Kisunni na Mwanachuoni wa Kishia (Al-Muraja’aat) 204. Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (as) 205. Mjadala wa Kiitikadi 206. Mtazamo kuhusu msuguano wa Kimadhehebu 207. Nchi na Uraia – Haki na wajibu kwa Taifa 208. Mtazamo wa Ibn Taymiyyah juu ya Imam Ali (as) 209. Uongozi wa Kidini – Maelekezo na Utekelezaji wa Kijamii 210. Maadili ya Ashura
89
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
211. Mshumaa – Shahidi na Kifo cha Kishahidi 212. Mizani ya Hekima – Hadithi za Ahlul Bait (as) – Sehemu ya Kwanza 213. Imam Ali na Mambo ya Umma 214. Imam Ali na Mfumo wa Usawa 215. Mwanamke na Sharia 216. Mfumo wa Wilaya 217. Vipi Tutaishinda Hofu? 218. Kumswalia Mtume ni Ufunguo wa Utatuzi wa Matatizo 219. Mahali na Mali za Umma 220. Nahjul-Balagha – Majmua ya Khutba, Amri, Barua, Risala, Mawaidha na Semi za Amirul-Muuminin Ali bin Abu Talib (a.s.) 221. Mukhtar – Shujaa aliyelipiza kisasi dhidi ya wauaji wa Imam Husein (as) hapo Karbala 222. Uimamu na Tamko la Kutawazwa 223. Imam Husain ni Mfumo wa Marekebisho na Mageuzi 224. Saada Kamili – Kitabu cha Kiada cha Maadili 225. Maeneo ya Umma na Mali Zake
90
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
KOPI NNE ZIFUATAZO ZIMETAFSIRIWA KWA LUGHA KINYARWANDA 1.
Amateka Na Aba’Khalifa
2.
Nyuma yaho naje kuyoboka
3.
Amavu n’amavuko by’ubushiya
4.
Shiya na Hadithi
91
Uimamu na Tamko la Kutawazwa
ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION KWA LUGHA YA KIFARANSA 1.
Livre Islamique
92