Uislamu wa shia

Page 1

Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:19 AM Page A

Uislamu wa Shia VYANZO, ITIKADI, MATENDO YA KIIBADA

Kimeandikwa na: Muhammad Ali Shomali

Kimetarjumiwa na: al-Haj Ramadhani S. K. Shemahimbo


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:19 AM Page B

B


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:19 AM Page C

Haki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: 978 - 9987 - 17 - 018 - 0 Kimeandikwa na:

Muhammad Ali Shomali Kimetarjumiwa na: Al-Hajj Ramadhani Salehe Kanju Shemahimbo Kimehaririwa na: Al-Hajj Hemedi Lubumba Kupangwa katika Kompyuta na: Hajat Pili Rajab Toleo la kwanza: Mei, 2012 - Nakala: 1000 Toleo la pili: Septemba, 2013 - Nakala: 7000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255  22  2110640 Simu/Nukushi: +255  22  2127555 Barua Pepe: alitrah@yahoo.com Tovuti: www.ibn-tv.com Katika mtandao: www.alitrah.info


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:19 AM Page D

YALIYOMO Utangulizi.........................................................................2

Mlango wa kwanza Vyanzo vya Ushi’ah..........................................................................7 Maana ya Ki-Istilahiya Neno Shi’ah................................................8 Ushi’ah ulianza lini?........................................................................11 Shi’ah wa Mwanzo..........................................................................19

Mlango wa Pili Vyanzo vya itikadi ya Shi’ah...........................................................24 Shi’ah wanakanusha kuwepo mabadiliko yoyote ndani Qur’ani....25 Kauli za wanachuoni wa Shi’ah kuhusu Qur’an.............................27

Mlango wa Tatu Mafunzo ya Dini........................................................................................67 Msingi wa wa Dini.....................................................................................70

Mlango wa Nne Matendo ya Ibada..........................................................................108

Mlango wa Tano Sifa za jumla za uislamu na Ushi’ah.............................................119

Mlango jwa Sita Mashia’h katika Ulimwengu...................................................................148


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:19 AM Page E

NENO LA MCHAPISHAJI Kitabu  kilichoko  mikononi  mwako  ni  tarjuma  ya  kitabu  cha  Kiingereza kiitwacho, Shi’i Islam kilichondikwa na Sheikh Muhammad Ali Shomali na kutarjumiwa na al-Haj Ramadhani S. K. Shemahimbo. Sisi tumekiita, Uislamu wa Shia. Ni ukweli usiopingika kwamba madhehebu ya Kiislamu ya Shia imekuwa ikijulikana  kwa  muda  mrefu  kama  ni  madhehebu  isiyoeleweka  vizuri miongoni  mwa  Waislamu  walio  wengi  ulimwenguni.  Hii  imetokana  na kukandamizwa kwa muda mrefu wafuasi wa madhehebu hii kulikofanywa na  dola  zinazojiita  za  Kiislamu.  Kwa  nini  wamefanya  hivyo?  Historia inayo majibu ya hilo. Waandishi  wanavyuoni  wengi  wa  sasa  wamejitahidi  na  wanaendelea  na jitihada  hiyo  kuuelemisha  Umma  kuhusu  Waislamu  hawa  wa  Shia;  na kitabu hiki ni miongoni mwa vitabu vingi vilivyoandikwa na wanavyuoni hawa juu ya usahihi wa madhehebu hii. Ni muhimu kukubaliana na kuziheshimu tofauti za kila mmoja na kutambua msimamo na mtazamo wa kila mmoja. Matatizo huja pale mtu anapolazimisha tabia, imani na mila zake zitawale wengine au kuzifisha itikadi na misimamo ya wengine. Ni  muhimu  kufikiria  kila  aina  ya  maoni  katika  kujaribu  kuamua  ukweli. Uislamu kimsingi uko dhidi ya kufuata kibubusa.  Wafuasi wa madhehebu nyingine kiumakini wanaweza kuchambua mada zilizomo  katika  kitabu  hiki  ili  kujenga  maoni  yao  wenyewe  kuhusu mtazamo mzuri wa mtu mwenyewe. Ni muhimu mtu kuelewa hoja za wale


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:19 AM Page F

ambao  hakubaliani  nao.  Inaweza  ikasemwa  kwamba  wale  ambao hawaelewi  kabisa  mtazamo  wa  maoni  tofauti,  hawaelewi  kwa  ukamilifu mtizamo wa kwao wenyewe. Tumekiona  kitabu  hiki  ni  chenye  manufaa  sana,  hususan  wakati  huu  wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote, ambapo uwongo, ngano za  kale  na  upotoshaji  wa  historia  ni  mambo  ambayo  hayana  nafasi  tena katika akili za watu. Kutokana  na  ukweli  huo,  Taasisi  yetu  ya  al-Itrah  Foundation  imeamua kukichapisha  kitabu  hiki  kwa  lugha  ya  Kiswahili  kwa  madhumuni  yake yaleyale  ya  kuwahudumia  Waislamu,  hususan  wazungumzaji  wa Kiswahili. Tunamshukuru  ndugu  yetu,  al-Haj  Ramadhani  S.  K.  Shemahimbo  kwa kukubali  jukumu  hili  la  kukitarjumi  kitabu  hiki.  Vilevile  tunawashukuru wale  wote  walioshiriki  kwa  njia  moja  au  nyingine  hadi  kufanikisha kuchapishwa kwake. Ni  matumaini  yetu  kwamba  kitabu  hiki  kitakuwa  ni  changamoto  kubwa kwa wasomaji wetu.  Mchapishaji: Al-Itrah Foundation


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:19 AM Page G

G


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:19 AM Page 1


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:19 AM Page 2

U i s l a m u wa S h i a

Utangulizi Kabla ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislam ndani ya Iran mnamo mwaka 1979, ni kidogo sana kilichokuwa kimeandikwa kuhusu Uislam wa Shi’ah katika Lugha za Kimagharibi.  Elimu kuhusu tawi hili la imani ya Kiislam ilikuwa imekomea takriban kwa wanachuoni wachache sana ambao walibobea zaidi katika uchunguzi wa mambo ya Kiislam au katika Lugha za Kimashariki,  hususan  Kiajemi.  Walikuwepo  pia  wanadiplomasia,  watalii na  wafanyabiashara  ambao  walikuwa  na  elimu  ya  mwanzoni  juu  ya mataifa na jumuiya za Shi’ah katika Mashariki ya Kati kupitia uzoefu wao binafsi na mahusiano. Hata hivyo, kuanzishwa kwa Serikali ya Kiislam huko Iran chini ya uongozi wa Ulamaa wa Kishi’ah, hasa Ayatullah Khomeini, kuliamsha shauku zaidi  katika  imani  ya  Kishi’ah.  Mapinduzi  ya  Kiislam  hayakuchukua wajibu  muhimu  tu  katika  uhuishaji  wa  utambuzi  wa  Kiislam  na  harakati kote  ulimwenguni  na  kuwa  na  athari  kubwa  juu  ya  uchumi  wa  dunia  na siasa, bali pia yalichochea tamaa miongoni mwa watu wa kawaida vilevile kama vile miongoni mwa wanasiasa na vyombo vya habari kutaka kufahamu  zaidi  kuhusu  Uislam  wa  Shi’ah.  Matukio  fulani  katika  miongo miwili  iliyopita,  kama  vile  mapambano  ya  Mashi’ah  wa  Iraqi  na  nchi nyingine  za  Kiarabu  katika  eneo  hilo,  kuongezeka  kwa  wahamiaji  wa Kishi’ah  huko  Magharibi  na  wajibu  wa  mbele  kabisa  wa  wapiganaji  wa Kishi’ah  wanaopigana  dhidi  ya  uvamizi  huko  Lebanoni  ya  Kusini  na kukomboa  maeneo  yaliyokaliwa  kimabavu,  kumeongezea  nguvu  katika tamaa hii. Kwa kawaida miradi mingi ya utafiti imeendeshwa na fasili nyingi zimetengenezwa juu ya vipengele tofauti vya Uislam wa Shi’ah. Ingawa vitabu vingi  vya  kutegemewa  na  vya  kiwanachuoni  vimeandikwa,  mwandishi hawezi kukanusha kuhusika kwa machapisho ya lugha ya Kiingereza katika  eneo  hili.  Baadhi  yake  yameandikwa  na  waandishi  ambao  hawana 2


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:19 AM Page 3

U i s l a m u wa S h i a maarifa  mengi  na  kamili  juu  ya  somo  lenyewe.  Baadhi  nyingine  yameandikwa kwa sababu ya kisirani na chuki kuhusu kile wanachokiona kama jambo lenye kutishia (hatari). Bado kuna mengine ambayo kimsingi ni ya halali,  lakini  kwa  bahati  mbaya  hayaratibiwi  kwa  mpangilio  ama yanaandikwa vibaya na hivyo hayafikii mahitaji na matarajio ya wasomaji  wa  Kiingereza.  Kwa  hiyo  kunabakia  haja  kubwa  na  kwa  kweli  inayoongezeka kwa ajili ya utafiti zaidi na uchapishaji juu ya mada hiyo. Kitabu  kilichopo  sasa  kinawakilisha  jaribio  dhaifu  la  kujaza  baadhi  ya mapengo  yaliyopo  katika  nyanja  ya  utafiti  wa  Kiislamu  kwa  jumla  na hususan utafiti kuhusu Shi’ah. Ingawa imeandikwa kirahisi na wazi kabisa, ni  matokeo  ya  takriban  miaka  ishirini  ya  uhusikanaji  katika  utafiti  wa Kiislam na falsafa ya Ulaya, na kutegemea kwa kiasi fulani juu ya mfululizo  wa  hotuba  mbili  kuhusu  Uislam  wa  Ushi’ah  zilizotolewa  kwenye hadhara za watu wanaoongea Kiingereza; idadi ya kwanza ya hotuba hamsini ilitolewa katika Jami’at al-Zahra’ (seminari ya Kiislamu inayoongoza ya wanafunzi wanawake) huko Qum mnamo mwaka 1995 na mwaka 1996, na idadi ya pili ya takriban hotuba thelathini iliyotolewa katika Taasisi ya Kiislam ya Manchester na Kituo cha Kijamii cha Shi’ah cha Manchester mnamo mwaka 1998 na mwaka 1999.  Mlango wa kwanza unaanza kwa kuelezea juu ya maana zote, ile ya neno kwa neno na ile ya kitaalam za neno Shi’ah na kurejea kwenye maelezo ya wanachuoni maarufu kuhusiana na hili. Unaendelea katika kutafiti vyanzo vya Shi’ah na maendeleo yake ya baadae katika miaka ya upatikanaji wa umbo la Uislamu. Mlango wa pili unachunguza vyanzo vya fikira za Shi’ah, yaani Qur’ani na Sunnah,  mantiki  na  ijmai,  yaani  maafikiano  ya  wengi.  Kujadili  hadhi  ya Qur’ani, mlango huu unazidi kuthibitisha kwamba Shi’ah kama Waislamu wengine,  wanaamini  juu  ya  mjalada  wa  Qur’ani  ambao  upo  leo  hii  na kwamba  wanachuoni  wa  Shi’ah,  tangu  enzi  za  awali  kabisa  hadi  leo  hii wamekanusha na wanaendelea kukanusha tuhuma zozote za mabadiliko ya 3


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:19 AM Page 4

U i s l a m u wa S h i a Qur’ani.  Vilevile  unaelezea  kwamba  ule  Msahafu  wa  Fatima,  ambao unatajwa katika baadhi ya Hadith za Shi’ah, hauna chochote cha kuhusiana na  Qur’ani,  na  kwamba  neno  ‘Mus’haf’  hapa,  kama  katika  sehemu nyingine  nyingi,  limetumika  katika  maana  yake  ya  asili  ambayo  ni ‘kitabu.’ Mlango huo kisha unajadili chanzo muhimu cha pili, Sunnah, ambayo inajumuisha  maneno,  vitendo  na  kukubali  kwa  kimya  kimya  kwa  Mtukufu Mtume Muhammad. Qur’ani yenyewe inawataka Waislamu kumchukulia Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.)  kama  kigezo  cha  mfano  kwao,  kumwendea yeye  kwa  kuhukumu  na  kuamua  migogoro  na  migongano  yao,  na inazungumzia Mtume kama anayesoma, kufundisha na kuielezea Qur’ani. Mlango huo pia unashughulika na umuhimu wa kukusanywa kwa Hadith za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), na unaelezea jinsi Shi’ah, tangu mwanzoni kabisa,  walivyodhamiria  kuziandika  na  kuzisimulia  wakati  ambapo Waislam  wasiokuwa  Shi’ah  walikuwa  bado  wako  chini  ya  amri  ya kutokuziandika wala kusimulia hadith, hali ambayo iliendelea kwa takriban karne nzima. Mlango huu pia unarejelea kwenye Nyumba ya Mtukufu Mtume  Ahlul-Bayt  na  wajibu  wa  wajumbe  wake  katika  kuiwakilisha Sunnah.  Unafuatia  mjadala  juu  ya  umuhimu  na  sababu  na  wajibu  wake katika kuelewa imani, maadili na sheria tendani au kwa maneno mengine, juu  ya  theolojia,  uadilifu  na  fiqhi.  Mwishowe  mwandishi  anahusika  na maafikiano ya kisheria (al-Ijma), na jinsi yanavyoshushwa kuwa kwenye Sunnah kwa mtazamo wa Shi’ah.  Mlango wa tatu unachunguza baadhi ya itikadi za kitheolojia za imani ya Shi’ah.  Baada  ya  maelezo  machache  ya  Uislam  na  kanuni  zake,  yaani Upweke  wa  Allah,  Utume  na  Ufufuo,  baadhi  ya  kanuni  nyingine  za muhimu za nyongeza zinachunguzwa pia. Upo uwezekano kwamba sehemu ya kanuni hizi huchangiwa na Waislam wengine, lakini Shi’ah ni wale wanaoamini juu ya zote hizi.

4


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:19 AM Page 5

U i s l a m u wa S h i a Mlango wa nne ni maelezo mafupi sana juu ya ibada za Shi’ah pamoja na marejeo mafupi kwenye shabaha na misimamo inayozilazimu. Ibada hizi kimsingi  zinachangiwa  na  Waislam  wote,  ingawa  kunaweza  kuwa  na tofauti kidogo na umahususi miongoni mwa madhehebu tofauti za Kiislam. Mlango  wa  tano  unachunguza  zile  sura  tatu  kuu  za  Uislam  wa  Shi’ah; mambo  ya  kiroho,  mantiki  na  kutafuta  haki.  Hizi  tatu  zinaonekana kuchomoza sana katika nadharia na historia ya Uislam wa Shi’ah. Katika kujadili hali ya kiroho, rejea zinafanywa kwenye umuhimu wa maadili na njia ya kiroho. Miongoni mwa udhihirisho wa kiroho wa Uislam wa Shi’ah ni  utajiri  wa  fasili  na  madu’a,  hususan  al-Sahifah as-Sajjadiah,  iliyotafsiriwa  kwa  Kiingereza  kama  “The Psalms of Islam” –  Zaburi  ya Uislam. Mlango wa sita na wa mwisho ni mjadala mfupi wa ulimwengu wa Shi’ah leo  hii.  Mlango  huu  umegawanywa  sehemu  mbili.  Sehemu  ya  kwanza inapitia  takwimu  za  hivi  karibuni  kuhusu  idadi  ya  sasa  ya  Waislam  na Shi’ah ya ulimwengu mzima. Vilevile kuna uanishaji wa ushirikishwaji wa kidini wa baadhi ya nchi ambazo zina historia ndefu ya uwepo wa Shi’ah. Ingawa hakuna takwimu zinazokubalika kilimwengu juu ya idadi ya sasa ya Shi’ah duniani, juhudi zimefanyika hapa kukusanya taarifa mpya zaidi na sahihi kabisa juu ya jambo hili. Sehemu ya pili ya mlango huu inamtambulisha  msomaji  kwenye  miji  mitakatifu  mikuu  kwa  Waislamu  wa Shi’ah na maeneo yao muhimu ya kutembelea na kuzuru. Kwa jumla, kitabu hiki cha sasa kinanuia kujibu yale maswali ambayo yeyote  mwenye  shauku  ya  kutaka  kujua  kuhusu  Uislam  wa  Shi’ah  anaweza akayauliza.  Kwa  hiyo  kinasimama  kama  chanzo  cha  utambulisho  juu  ya hali muhimu na za msingi za madhehebu hii. Na wakati huo huo, mwandishi anatarajia, kwa sababu ya mtindo na lugha ya kitabu hiki na habari na hoja zinazowasilishwa ndani yake, vilevile kuwasaidia wale ambao wana uzoefu  na  itikadi  hii  lakini  wanataka  kupata  taarifa  sahihi  nyingi  zaidi, zinazowasilishwa kimfumo na kiutaratibu kuhusu vyanzo, imani na ibada 5


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:19 AM Page 6

U i s l a m u wa S h i a zake na namna ya mipango ya wakati huu katika hali ya ubinadamu. Napaswa pia niseme kwamba kitabu cha sasa kinajumuisha wajibu mzito sana  kwenye  umoja  wa  Kiislam  na  kinaonyesha  matumaini  kwamba kinawasilisha  hatua  ya  staha  kuelekea  kwenye  udugu  wa  Kiislam.  Kwa kweli, moja ya njia bora kabisa ya kupata umoja huu na udugu ni kuzidisha kufahamiana kwetu na kushinda zile chuki za kihistoria ambazo zinazuia kuelewana  baina  ya  madhehebu  mbalimbali.  Kwa  mujibu  wa  methali  ya Kiarabu: “Watu ni maadui wa kile wasichokijua,” ni kweli kwamba kitalu cha  mbegu  ya  chuki  ni  kutokujua  kwa  mwingine,  ambapo  kitalu  cha mbegu ya upendo ni kujua kwa yule mwingine. Kwa sababu hii, na kwa faida ya wale ambao sio Shi’ah, rejea za kwenye imani za msingi za Shi’ah zimetolewa vilevile kwenye vyanzo vikuu vya ki-Sunni. Mwisho, ningependa kuchukua fursa hii kuwashukuru watu wote na taasisi zote  ambazo  zimenitia  moyo  na  kunisaidia  wakati  wa  kipindi  cha  kutoa hotuba hizi na maandalizi kwa ajili ya kitabu hiki, yaani Jami’at al-Zahraa (Qum), Manchester Islamic Centre, Shi’ah Welfare Centre (Manchester), Ayatullah  Muhsin Araaki,  Bw.  Muhsin  Ja’far,  Dr. Ali  Heshmati  na  Mrs. Badr  al-Saadaat  Omraanii.  Ningependa  pia  kumshukuru  Profesa  Hamid Algar, Dr. Reza Shah Kadhimii, Dr. Muhammad Legenhausen, Bw. Abbas Virjee na Mrs. Nadhmina Virjee kwa kuusoma muswada wa kitabu hiki na kutoa maoni yao yenye thamani kubwa. Ningependa kuishukuru hususan ile taasisi ya Islamic College for Advanced Studies iliyoko mjini London na hususan kwa Mkurugenzi wake mwenye maarifa mengi, Dr. Ja’far Elmi kwa  kufadhili  na  kuchapisha  kitabu  hiki,  ambacho  kitakuwa  na  manufaa zaidi kama kitabu cha kiada kwa masomo yao juu ya uchunguzi wa Shi’ah. Mwisho bali sio kwa umuhimu, natoa hisia zangu nzito za shukurani kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kwa neema Zake zote alizozijaalia juu yetu sisi hapo kabla na wakati huu wa sasa.  Muhammad A. Shomali Februari, 2003. 6


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:19 AM Page 7

U i s l a m u wa S h i a

MLANGO WA KWANZA Vyanzo Vya Ushi’ah Maana ya Neno Shi’ah: Lugha nyingi zina maneno ambayo yana aina mbili za maana: Ile ya asili au  ya  msingi  na  ile  ya  kitaalam  au  maana  ya  pili.  Kwa  mfano,  neno ‘Salaat’ kwa kiarabu kwa asili lilimaanisha tu kuomba, du’a. Hata hivyo, baadae  lilipata  maana  nyingine,  aina  maalum  ya  ibada  katika  Uislam ambayo inajulikana kama ‘Namaaz’ kwa lugha ya ki-Ajemi na kwa lugha nyingine nyingi. Kwa kweli kama mtu anavyoweza kuona katika suala hili, lazima pawe na viunganishi na mfanano baina ya aina mbili hizi za maana. Ndani ya kitabu chake, Mu’jam Maqaayis al-Lughah, Ahmad bin Faaris, mwanafalsafa mashuhuri wa karne ya tano ya Kiislam, anachunguza chimbuko  la  neno  Shi’ah,  yaani  Sha-ya-‘a.  Yeye  anaonyesha  maana  mbili: Msaada (huduma) au kusaidia, na kueneza. Angalau moja ya maana hizi lazima  ipatikane  katika  hali  za  kunyambulika  kwa  chimbuko  hili,  iwapo yatumike kwa maana zao za asili au katika maana za kiistilahi. Kwa mfano, Qur’ani (24:19) inatumia kitenzi nyambulishi cha chimbuko hili kumaanisha “kuenea.” Neno  Shi’ah  kiasili  linamaanisha  mfuasi  mmoja,  wawili  au  kikundi  cha wafuasi,  kwa  maana  ya  kwamba  wafuasi  wa  mtu  maalum  ni  wale wanaomhudumia  au  kumsaidia  yeye  katika  mambo  yake.  Ndani  ya Qur’ani  tukufu,  neno  hili  linatumika  mara  nyingi  kwa  maana  hii.  Kwa mfano katika 28:15 Mwenyezi Mungu anazungumzia juu ya mfuasi mmoja wa Nabii Musa kama ni mmoja wa Shi’ah wake. Mahali pengine, Ibrahim (a.s.) anatambulishwa kama Shi’ah wa Nuh (a.s.) [37:83].

7


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:19 AM Page 8

U i s l a m u wa S h i a

Maana ya ki-Istilahi ya Neno Shi’ah: Mwanzoni mwa historia ya Kiislamu, neno Shi’ah lilitumika katika maana yake ya asili au ya kawaida kwa ajili ya wafuasi wa watu mbalimbali. Kwa mfano, baadhi ya hadith zinazungumzia “Shi’ah wa Ali bin Abi Talib” na nyinginezo  juu  ya  “Shi’ah wa Mu’awiyah bin Abi Sufyan.”  Hata  hivyo, kama  tutakavyoona  baadae,  neno  hili  polepole  likapata  maana  ya  pili  au maana ya kiistilahi; yaani ya wafuasi wa Ali, wale ambao wanaamini katika suala la Uimamu (Uongozi ulioteuliwa kimbinguni). Katika makamusi mengi ya Kiarabu, hili neno Shi’ah limeelezewa katika maana zote, za neno kwa neno na ile ya kiistilahi, kwa namna ambayo ni rahisi kuona uhusiano wa baina ya maana mbili hizo, ya wafuasi kwa jumla na ya wafuasi wa Ali. Hali ni hivyo hivyo katika vyanzo vingi vya kitheolojia.  Kwa  mfano,  Abu  al-Hasan  al-Ash’ari  (kafariki  330  AH),  katika kitabu  chake  mashuhuri  Maqaalat al-Islamiyin wa Ikhtilaaf al-Musallin anaelezea juu ya maana ya kiistilahi na anasema: “Waliitwa Shi’ah tu kwa sababu  walimfuata  Ali  waliamini  kwamba  yeye  anazo  fadhaili  nyingi kuliko masahaba wengine wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)”1 Shahristanii  (kafariki  548A.H.)  katika  kitabu  chake,  al-Milal wa Nihal, chanzo  maarufu  kuhusiana  na  madhehebu  tofauti  ndani  ya  Uislamu, anaandika hivi: “Shi’ah ni wale waliomfuata Ali hasahasa na wakaamini juu ya Uimam na ukhalifa wake kwa mujibu wa mafundisho ya wazi na ushuhuda wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).”2 Haya ni maelezo sahihi kabisa, kwa  vile  Shi’ah  wenyewe  wanaamini  kwamba  sababu  ya  kumfuata  Ali (a.s.) ni kwamba iliamriwa na kutakiwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na 1 al-Asha’ri, Ali ibn Ismail Abu al-Hasan, Maqaalat al-Islamiyin wa Ikhtilaf alMusallin (Beirut:  Dar  Ihya’  al-Turath  al-‘Arabi),  uk.  5,  (uk.  65  katika  toleo  la Muhyi al-Din Abd al-Hamid). 2 Shahristani,  Muhammad  ibn  Abd  al-Kariim  (1414/1993),  al-Milal wa Nihal (Beirut, Dar al-Maarifah, chapa ya tatu) Jz. 1, uk. 169. 8


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:19 AM Page 9

U i s l a m u wa S h i a kwamba haukuwa ni uamuzi wao wenyewe wa kuchagua ni nani wamfuate.  Kinyume  chake,  wasio  Shi’ah,  baada  ya  kifo  cha  Mtukufu  Mtume (s.a.w.w.) wao walimfuata yule aliyechaguliwa katika ukumbi wa Saqifah na waliamini kwamba Mtukufu Mtume aliwaachia watu waamue wenyewe wamfuate nani. Hata hivyo, Abu Bakr ibn Abi Quhafah, Khalifa wa kwanza, ambaye yeye mwenyewe alichaguliwa kwa njia hiyo, aliamini kwamba yeye ni lazima ateue mrithi wake yeye mwenyewe. Khalifa wa pili, Umar bin al-Khattab badala yake yeye aliteuwa baraza la watu sita, ambao wao wachague  mmoja  kati  yao  kwa  mujibu  wa  utaratibu  tete  sana  aliokuwa ameuandaa  yeye  mwenyewe  Umar.  Inatia  fora  ajabu  kuona  kwamba ilikuwa ni Ali bin Abi Talib, Khalifa wa nne, ambaye ndiye alichaguliwa, (sio kuteuliwa) na kwa hakika aliyelazimishwa na takriban Waislam wote baada  ya  kuuliwa  kwa  khalifa  wa  tatu,  Uthman  bin  Affan,  ili  achukue nafasi hiyo ya Ukhalifa. Ndani  ya  kitabu  chake  cha  Firaq al-Shi’ah,  al-Hasan  bin  Musa  alNawbakhti, mwanachuoni mashuhuru wa Shi’ah (kafariki 313A.H.), yeye anaandika:  “Shi’ah  ni  kundi  la  Imam Ali  ibn Abi  Talib  (a.s.).  Walikuwa wakiitwa  kwa  jina  la  ‘Shi’ah  wa Ali’  wakati  wa  uhai  wa  Bwana  Mtume (s.a.w.w.) na baada ya kufariki kwake, na wanafahamika kama wafuasi wa Ali na wanaoamini Uimam wake.”3 Sheikh al-Mufid (kafariki, 423A.H.) mmoja wa wanachuoni wakubwa na mashuhuri wa Shi’ah wa mwanzoni kabisa,  anafafanua  Shi’ah  kama  ni  wale  wanaomfuata  Ali  (a.s.)    na wanaoamini urithi wake wa baada tu ya kufariki kwa Mtukufu Mtume.4

3 al-Nawbakhti, al-Hasan ibn Musa (1404/1984), Firaq al-Shi’ah, Beirut, Dar alidhwa, uk. 17 4 Tazama:  Awa’il al-Maqaalaat;  (Qum:  Kungereh-e-Shaykhe-e-Mufid,  1413) chake Sheikh Muhammad bin M. Nu’man, uk. 36 (katika toleo hili maudhui kuu inaanzia uk.33) 9


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:19 AM Page 10

U i s l a m u wa S h i a Akielezea kwa nini Shi’ah pia wanaitwa ‘Imaamiyah’ yeye anasema: “Hiki ni  cheo  kwa  ajili  ya  wale  wanaoamini  juu  ya  ulazima  na  umuhimu  wa Uimam na muendelezo wake katika zama zote, na kwamba kila Imam ni lazima ateuliwe kwa uwazi dhahiri na lazima awe ni Ma’sum na mkamilifu.”5 Hivyo inaweza kusemwa kwamba Shi’ah ni wale wenye imani zifuatazo kuhusu urithi ama uandamizi wa Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.): 1.    Urithi  (Uandamizi  –  Ushikamakamu)  wa  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.) unategemea juuya uteuzi wa kimungu. 2.   Kwa vile Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliteuliwa na Mwenyezi Mungu, mwandamizi  wake,  Imam,  vilevile  ni  lazima  ateuliwe  na  Mwenyezi Mungu Mwenyewe na kutambulishwa na Mtume. 3.   Yule mrithi wa mara moja wa Mtume Muhammad (s.a.w.w.) alikuwa ni Ali.  Wasiokuwa  Shi’ah  au  Waislam  wa  Sunni  wanaamini  kwamba  urithi  wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) sio cheo cha kimbinguni, na kwa sababu hiyo wale  waliomrithi  Mtume,  wale  Makhalifa,  haikuwa  lazima  wawe  na kiwango kikubwa cha elimu au mambo ya kiroho, kwa kweli hawakutakiwa kuwa wenye elimu zaidi na wachamungu sana wa umri wao. Kwa desturi  wamekuwepo  baadhi  ya  makhalifa  ambao  vitendo  vyao  wala havikuendana na mazingatio ya Kiislamu. Wala ule uhamishaji wa mamlaka miongoni mwa makhalifa haukuwa wakati wote ukikubalika kimaadili. Kile kilichoelezewa hapo juu ni yale matumizi ya kawaida sana ya neno Shi’ah kupitia mwote ndani ya historia ya Uislam. Katika baadhi ya vitabu vya zamani mtu anaweza akakutana na namna fulani tofauti ya matumizi 5 Awa’il al-Maqaalaat, uk. 38 10


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:19 AM Page 11

U i s l a m u wa S h i a ya neno hili. Kwa mfano, baadhi ya wanahistoria na waandishi wa kamusi za wasifu wa wasimulizi wa hadith wamelitumia neno hili Shi’ah hata kwa wale  Waislam  wa  Sunni  ambao  waliamini  kwamba Ali  (a.s.)  alikuwa  ni mbora katika elimu au Imani au huduma kwa Uislam kuliko yule Khalifa wa tatu au hata kwa Makhalifa wote watatu wa kwanza.

Ushi’ah ulianza lini? Hili  ni  swali  ambalo  kwa  kawaida  hujitokeza.  Swali  hili  linaweza kugawanywa katika maswali madogo mawili: 1.  Ni lini ilikuwa ni mara ya kwanza kwamba kikundi cha watu kilikuja kuamini  juu  ya  umuhimu  wa  kumfuata  Imam Ali  (a.s.)  kama  mrithi mwandamizi  wa  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.)  aliyeteuliwa  kimungu? Kwa maneno mengine, ni lini wazo la Uimam lilianza? 2.  Ni lini neno Shi’ah lilipopata maana yake ya kiistilahi? Kwa maneno mengine,  ni  lini  neno  Shi’ah  lilianza  kutumika  kwa  wafuasi  wa Ali (a.s.) na wanaoamini juu ya Uimam wake? Maswali haya ni muhimu sana, kwa sababu imesemekana kwamba imani ya Shi’ah haikuwa na msingi katika Uislamu katika kipindi cha upatikanaji wa sura yake wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), na kwamba wazo  hili  lilichipukia  tu  baadae  miongoni  mwa  watu  fulani  au  mataifa fulani kama vile Wa-Irani. Pamekuwepo na vitabu vingi vya kiwanachuoni juu  ya  tathmini  ya  nadharia  tete  hizi,  na  vingi  ya  hivyo  havichukuliwi maanani sana tena katika dunia ya kitaalamu. Katika kitabu hiki cha sasa, tutachunguza vyanzo vikuu vya Kiislamu ili kuona kwamba ni lini wazo la Uimam lilianza na ni lini neno Shi’ah lilitumika kwa wafuasi wa Ali (a.s.) kwa mara ya kwanza. Mara tutakapokuwa tumezifumbua hakika za kihistoria,  basi  hakutakuwa  na  haja  ya  kuchunguza  nadharia  mbadala  moja baada ya nyingine.

11


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:19 AM Page 12

U i s l a m u wa S h i a Kuna  hadith  nyingi  sana  zilizosimuliwa  na  wote  Shi’ah  na  wasio  Shi’ah kuhusiana  na  suala  la  Uimam,  ambazo  tutazichunguza  baadae tutakapokuwa tunajadili itikadi za Shi’ah. Katika kinachofuata, hata hivyo, tutachunguza  tu  zile  hadith  ambamo  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.) alizungumzia kundi la watu kama Shi’ah (wafuasi) wa Ali na kisha turejee kwenye hadith nyingine zaidi na vipengele vya historia ya Uislam, hadithi ambazo  zinaweza  kutoa  mwanga  zaidi  katika  somo  la  sasa  hivi.  Hadith zote zilizotajwa hapo chini zinasimuliwa kutoka kwenye vyanzo vinavyoheshimika vya Sunni. Hizo ni sampuli tu ya nini kinachoweza kupatikana katika vyanzo vilivyotajwa hapa na vinginevyo pia. 1.  Ibn  Asakir  (kafariki  571  A.H.)  amesimulia  kutoka  kwa  Jabir  bin Abdillah al-Ansari kwamba yeye alisema: “Wakati mmoja tulikuwa pamoja na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) pale Ali alipowasili, ambapo Mtukufu Mtume alisema: ‘Naapa kwa Yule ambaye maisha yangu yamo mikononi mwake kwamba hakika mtu huyu na Shi’ah wake watakuwa na furaha katika Siku ya Kiyama,’ na  kisha  ikashuka  aya  hii:  “Hakika wale walioamini na kutenda mema, hao ndio wabora wa viumbe.” (98:7). Baadae,  wakati wowote  masahaba  wa  Mtukufu  Mtume  Muhammad  (s.a.w.w.) walipomuona  Ali  akija,  walikuwa  wakisema;  ‘Mbora  wa  watu amekuja.’”6 2. Al-Suyuti (kafariki 911 A.H.) amesimulia kutoka kwa Ibn Abbas kwamba: “Wakati  ile  aya  ya  (98:7)  iliposhuka,  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.) alimwambia Ali (a.s.): ‘Hao ni wewe na Shi’ah wako na katika Siku ya  Kiyama  mtakuwa  radhi  na  wenye  kumridhisha  hasa  Mwenyezi Mungu.’”7 6 Ibn Asakir, Tarikh Ibn Asakir, Jz. 2, uk. 442, na Suyuuti, al-Durr al-Manthur, Jz. 8, uk. 589. 7 As-Suyuti, al-Durr al-Manthur, Jz. 8, uk. 589. 12


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:19 AM Page 13

U i s l a m u wa S h i a 3. Ibn Hajar (kafariki 974 A.H.) amesimulia kutoka kwa Ibn Abbas kwamba: “Wakati  ile  aya  ya  (98:7)  iliposhuka,  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.) alimwambia  Ali  (a.s.):  ‘Hao  ni  wewe  na  Shi’ah  wako.  Wewe  na Shi’ah  wako  mtatokeza  Siku  ya  Kiyama  wakati  mkiwa  mmeridhia na  wenye  kumridhisha  Mwenyezi  Mungu  sana,  na  maadui  zako watakuja  wakiwa  wamechukia  na  wamekamatwa  kwenye  shingo zao.’”8 4. Ibn al-Athiir (kafariki 774 A.H.) amesimulia kwamba, akimwambia Ali (a.s.), Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “O  Ali!  Wewe  na  Shi’ah  wako  mtakutana  na  Mwenyezi  Mungu mkiwa  mmeridhika  Naye  na  wenye  kumridhisha  sana  Yeye,  na maadui  zako  watakutana  Naye  wakiwa  wamechukia  na  watakuwa wameshikwa kwenye shingo zao.” Kisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akaonyesha  jinsi  hili  litakavyokuwa  kwa  kuweka  mkono  wake  juu ya shingo yake mwenyewe.’”9 Kuna  hadith  nyingine  ambamo  Mtukufu  Mtume  Muhammad  (s.a.w.w.) akiongea  na  Ali  (a.s.)  alikuwa  akitumia  msemo  “Shi’ah wetu.”  Hili linakubaliana  sana  na  kile  kilichoonyeshwa  hapo  juu,  kwamba  Shi’ah  ni wale  wanaomfuata  Ali  (a.s.)  kwa  mujibu  wa  mafundisho  ya  Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na sio kwa uamuzi wao binafsi. Kwa mfano, Ibn Asakiir amesimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: 8 Ibn Hajar, al-Sawa’iq al-Muhriqah, Sehemu ya 11, Mlango wa 1. Katika kitabu hicho hicho, Ibn Hajar amesimulia pia kutoka kwa Umm Salamah kwamba usiku mmoja, wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa nyumbani kwake, binti yake Fatima aliwasili pamoja na Ali akimfuatia. Halafu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akamwambia Ali (a.s.): “O Ali! Wewe na wafuasi wako ni wa Peponi. Wewe na Shi’ah wako ni wa Peponi.” 9 Ibn al-Athiir, al-Nihayah kitomeo cha ‘qa-ma-qa.’ 13


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:19 AM Page 14

U i s l a m u wa S h i a “Hakika kuna mto huko Peponi mtamu zaidi kuliko nekta (majimaji matamu  katika  maua),  laini  kuliko  siagi,  baridi  kuliko  barafu,  na  ambao unanukia  kuliko  miski.  Katika  kijito  hicho  kuna  udongo  wa  ufinyanzi (tiinah)  ambao  kutoka  humo  sisi  (watu  wa  nyumbani  kwangu  na  mimi mwenyewe)  tuliumbwa  kutokana  nao,  na  Shi’ah  wetu  wanaumbwa kutokana na ufinyanzi huo huo.”10 Bado kuna hadith zingine ambamo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa akizungumza na Ali (a.s.) alikuwa akitumia usemi wa “Shi’ah wa kizazi chako.” Hili linathibitisha kile tulichodokezea hapo juu, kwamba Shi’ah ni wale  wanaomfuata  Ali  (a.s.)  kwa  sababu  wanaamini  katika  asasi  ya Uimam. Kama tutakavyoona kwa upana zaidi baadae, Shi’ah wanaamini kwamba Ali (a.s.) alikuwa ndiye Imam wa kwanza, baaada yake Uimam uliendea katika kizazi cha Ali na Fatima, ambao waliteuliwa na Mwenyezi Mungu  na  kutambulishwa  na  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.).  Kwa  mfano Zamakhshari  (kafariki  538 A.H.)  katika  Rabi’ al-Abrar yeye  anasimulia kwamba Mtume (s.a.w.w.) alisema: “O Ali! itakapowadia Siku ya Kiyama, mimi  nitakuwa  nimeshikamana  na  Mwenyezi  Mungu,  nawe  utakuwa umeshikamana  na  mimi,  kizazi  chako  watakushikilia  wewe  na  wafuasi wao Shi’ah watawashikilia wao. Halafu utaona tutakapopelekwa.” Ilikuwa ifahamike kwamba, kwa mujibu wa Qur’ani, utume nao pia unarithiwa. Qur’ani inasema: “Na bila shaka tulimpeleka Nuhu na Ibrahim na katika kizazi chao Unabii na Kitabu …..” (57:26). Hii  ina  maana kwamba  wale  ambao  walistahiki  kuteuliwa  kwenye  nafasi  ya  Utume  na Mwenyezi  Mungu  walikuwa  wamejumuishwa  kwenye  kizazi  chao.  Na ndani ya Qur’ani (2:124) kuna maelezo ya jinsi ambavyo Ibrahim ambaye tayari alikuwa ni Nabii na Khaliilu-llah (rafiki wa Allah) alivyonyanyuliwa na Mwenyezi Mungu kuwa Imam juu ya watu. Kisha yeye Ibrahim akamuomba  Mwenyezi  Mungu  kuuweka  Uimam  kwenye  kizazi  chake  vile vile.  Mwenyezi  Mungu  alijibu  kwamba  Ahadi  Yake  (hapa  ikimaanisha 10 Ibn Asakir, Jz. 1, uk. 131, hadith ya 180. 14


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:19 AM Page 15

U i s l a m u wa S h i a Uimam)  haitawafikia  watu  madhalimu.  Kwa  njia  hii  Ibrahim  alitambua kwamba Uimam utarithiwa na kizazi chake kiadilifu na cha wachamungu. Kwa nyongeza ya hadithi zilizotajwa hapo juu na za mfano wao, na hadith juu ya Uimam ambazo zitatajwa baadae, bado kuna sababu nyingine kadhaa za kwa nini kujitokeza kwa kundi la watu kama lile la Shi’ah katika wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) lilikuwa ni jambo la kawaida na jambo la muhimu vile vile. Kwa mfano, pale mwanzoni mwa Uislam wakati  Mwenyezi  Mungu  alipomuamuru  Mtukufu  Mtume  kuanza  ulinganio  wake  wa  ummah  kwenye  Uislam  kwa  kuwaalika  jamaa  zake  wa karibu, Mtukufu Mtume aliwaalika jamaa zake kwenye chakula. Baada ya chakula hicho Mtume alitangaza ujumbe wake na akawaalika wageni wake hao kuukubali Uislam, na akasema kwamba yeyote atakayeamini Uislam miongoni mwao na akamsaidia yeye basi huyo atakuwa mrithi wake. Wote walikaa kimya. Mtu mmoja pekee aliyekubali mwaliko wa kumsaidia yeye alikuwa  ni  Ali,  aliyekuwa  kijana  wakati  ule.  Mtume  (s.a.w.w.) akamwambia akae chini kimya na akalirudia ombi lake kwa mara ya pili na ya tatu. Tena na tena alikuwa ni Ali tu aliyeonyesha utayari wake wa kumsaidia Mtume. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ndipo akaukubali mwitikio wa  Ali  kwenye  mapenzi  ya  Mwenyezi  Mungu  na  akatekeleza  amri  ya Mwenyezi  Mungu  ya  kumteua  yeye  kama  mrithi  wake.  Tukio  hili  limeandikwa kwenye vyanzo vingi tu.11 Katika kauli muhimu sana, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa uwazi kabisa amethibitisha kwamba Ali (a.s.) alikuwa mkweli na aliyeepukana na imani potovu na vitendo visivyo sahihi, iwe ni kwa tabia yake binafsi au katika maneno  yake  na  maamuzi  yake  na  kwa  kujitokeza  kabisa  aliwataka 11 Miongoni  mwa  vyanzo  visivyo  vya  Shi’ah,  mtu  anaweza  akarejea  kwenye Tarikh al-Umam wa al-Muluuk cha Tabari (kafa 310 A.H.) Jz. 3, uk. 62, 63; alKamiil fiy al-Tarikh cha Ibn Athiir (kafa 630 A.H.), Jz. 2, uk. 40, 41; na Musnad Ahmad bin Hanbal, Musnad al-Ashrah al-Mubashsharin bi al-Jannah, Sakhr mfululizo namba 841.  15


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:19 AM Page 16

U i s l a m u wa S h i a Waislam  kumfuata  yeye  Ali  (a.s.).  Umm  Salamah  amesimulia  kwamba Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.)  amesema:  “Ali  wakati  wote  yuko  na  haki  na Qur’ani, na ukweli siku zote uko pamoja na Ali, na mpaka Siku ya Kiyama hawatatengana.” Hadith hii maalum imesimuliwa na ibn Abbas, Abu Bakr, Aisha, Abu Sa’id al-Khudri, Abu  Layla na Abu Ayyub al-Ansari vilevile.12 Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) pia ananukuliwa akisema: “Mwenyezi Mungu ambariki Ali, Mwenyezi Mungu aifanye haki wakati wote kuwa pamoja na Ali.”13 Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.)  vilevile  amethibitisha  katika  nyakati  mbalimbali  tofauti  kwamba Ali  (a.s.)  ndiye  mtu  mwenye  elimu  zaidi  miongoni mwa watu wake katika masuala ya kufungamana na elimu na sayansi za Kiislam.  Kwa  mfano,  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.)  amesema:  “Hekima imegawanywa  sehemu  kumi,  tisa  zimetolewa  kwa  Ali  na  sehemu  moja imegawanywa kwa watu wote waliobakia.”14 Baadae Khalifa wa pili amesisitiza  tena  zile  hadith  za  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.)  kwa  kusema: “Mwenyezi  Mungu  asinihuzunishe  na  tatizo  gumu  wakati  Ali  akiwa hayupo.”15 Mtu anapaswa vilevile kuzingatia zile huduma za thamani na za muhimu na kujitoa muhanga kwa Ali (a.s.) ili kuweza kuelewa nafasi yake miongoni mwa Waislam. Kwa mfano, wakati makafiri wa Makka walipopanga kumuua Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Mwenyezi Mungu akamfahamisha juu  ya  njama  yao  hiyo,  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.)  alimuuliza  Ali  (a.s.) 12 Kwa mujibu wa kitabu Ghafari, uk. 10, hadith hii imesimuliwa kupitia njia 15 zisizo  za  ki-Shi’ah,  kama  vile  Mustadrak ya  al-Hakim  al-Nishaburi,  al-Sawa’iq cha Ibn Hajar, Kanz al-Ummal na Yanabiul-Mawaddah. 13 Tazama  kwa  mfano,  al-Tirmidhi,  Kitab al-Manaqib,  Sakh  mfululizo  namba 3647. 14 al-Bidayah wa al-Nihayah cha Ibn Kathir (kafa 774 A.H.), Jz. 7, uk. 369. 15 Tazama kwa mfano al-Isabah fi Tamiiz al-ahaabah cha Ibn Hajar, Jz. 2, uk. 509 na al-Bidayah wa al-Nihayah cha Ibn Kathir, Jz. 7, uk. 59. 16


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:19 AM Page 17

U i s l a m u wa S h i a iwapo alikuwa tayari kuhiari kulala katika nafasi yake ili kwamba wapagani hao wafikirie kwamba Mtume alikuwa bado yuko nyumbani kwake, na  kumruhusu  yeye  kuondoka  Makka  kwa  usalama. Ali  (a.s.)  alilikubali jukumu  hilo,  ambapo  aya  hii  ilishuka:  “Na miongoni mwa watu wapo wale wanaouza nafsi zao kwa kutaka radhi za Mwenyezi Mungu.” Kuhama  kwa  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.)  kutoka  Makka  kwenda  Madina kunaashiria mwanzo wa kalenda ya Kiislam. Ali alitumikia njia ya Uislam kwa kupigana vita vya Badr, Uhud, Khaybar, Khandaq na Hunayn, ambapo katika vita vyote hivyo alishika majukumu muhimu sana. Yote haya yameandikwa katika idadi kadhaa ya vitabu vya historia na makusanyo ya hadith yaliyofanywa na wanachuoni wasiokuwa wa Shi’ah. Tunahitimisha sehemu hii ya mjadala kwa kurejea kwenye hadith inayojulikana sana ya Ghadir. Akirejea kutoka kwenye Hijja yake ya mwisho ya Makka, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwataka maelfu ya Waislam waliofuatana naye kusimama hapo njiani. Alisimama kwenye jukwaa au mimbari iliyotengenezwa  kwa  ajili  yake  kutokana  na  matandiko  ya  vipando  na akasema:  “Yeyote  ambaye  amenichukulia  mimi  kama  Mtawala  (mawla) wake, basi Ali sasa hivi ni Mtawala wake.” Kisha watu waliokuwa pale, pamoja na wale makhalifa wa kwanza na wa pili wa baadae walitoa kiapo cha utii kwa Ali (a.s.) na wakampongeza. Hadithi hii imesimuliwa na zaidi ya vyanzo mia moja. Kwa ajili ya orodha ndefu ya vyanzo visivyo vya kiShi’ah vya hadith hii, angalia majuzuu kadha ya ‘Abaqaat al-Anwaar’ cha Mir  Hamid  Husayn  al-Hindi  (kafariki  1306  A.H.).  Wakiwa  wamekwishathibitisha  ukweli  wa  hadith,  baadhi  ya  waandishi  wa  Sunni wamelitafsiri  neno  ‘Mawla’ lililotumika  katika  hadith  hiyo  kumaanisha “urafiki.”  Iwapo  hili  linaweza  kukubalika  ama  hapana,  hakuna  shaka kwamba  hadithi  hii  na  tukio  hili  lilimpa  Ali  (a.s.)  cheo  cha  kipekee  na kikuu miongoni mwa masahaba wa Mtume (s.a.w.w.).   Hivyo inaelekea kwamba makundi tofauti ya hadithi na pamoja na ushahidi  wa  kihistoria  uliotajwa  hapo  juu  yasingeacha  shaka  yoyote  kwamba wakati  wa  uhai  wa  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.)  Waislam  wengi  walikuja 17


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 18

U i s l a m u wa S h i a kumpenda  sana Ali,  walitafuta  usuhuba  naye  na  walidhamiria  kumfuata yeye baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Watu hawa walikuwa mara kwa mara  na  kwa  uwazi  zaidi  wakiitwa  Shi’ah  wa  Ali,  kiasi  kwamba  neno Shi’ah  peke  yake  lilikuja  kuwa  sawa  na  wafuasi  wa Ali.  Muhimu  zaidi wazo la Uimam wa Ali kwa hakika lilianza wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume  Muhammad  (s.a.w.w.).  Kifo  cha  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.)  kwa kawaida  kililileta  suala  la  Uimam  kwenye  kitovu  cha  mambo  na kuwafanya wale ambao bado waliamini katika umuhimu wa kumfuata Ali (a.s.)  kuwa  tofauti  na  Waislam  wengine,  ambao  hapana  budi  walikuja kuamini  katika  uanzishwaji  wa  Ukhalifa  kama  wenye  kutoa  urithi  wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika kutawala jumuiya ya Kiislam na sio cheo cha  kimungu.  Akielezea  matukio  baada  ya  kifo  cha  Mtukufu  Mtume (s.a.w.w.),  al-Mas’ud  (kafariki  345  A.H.),  mwanahistoria  mashuhuri  wa Sunni  anaandika:  “Kwa  kweli  Imam Ali  na  wale  ambao  miongoni  mwa Shi’ah wake  ambao  walikuwa  pamoja  naye  walibakia  ndani  ya  nyumba yake wakati ambapo kiapo kwa Abu Bakr kilipofanywa.” Matukio ya baadae, kama vile vita vilivyotokea wakati wa Ukhalifa wa Ali (a.s.) na ule msiba wa Karbala ambamo Imam wa tatu wa Shi’ah na watu 72  wa  familia  yake  na  wafuasi  wake  waliuawa  yalisaidia  umaarufu  kwa Shi’ah  wa  Ali  kuvutia  uundaji  wa  utambulisho  wa  Shi’ah.  Kwa  mfano tunakuta katika moja ya vitabu vya awali kwamba Ali, wakati akimshutumu  Talha  na  Zubeir  alisema:  “Kwa  hakika  wafuasi  wa  Talha  na  Zubeir huko  Basra  wamewauwa  Shi’ah  wangu  na  mawakala  wangu.”  Abu Mikhnaf  (kafariki  158  A.H.)  anasimulia  kwamba  baada  ya  kifo  cha Mu’awi  yah,  Mashi’ah  walikusanyika  kwenye  nyumba  ya  Suleiman  bin Surad  na  yeye  akawaambia:  “Mu’awiyah  amefariki.  Husein  (a.s.) amekataa kutoa kiapo cha utii kwa Bani Umayyah na ameondoka kwenda Makka, na ninyi ni Shi’ah wake na Shi’ah wa baba yake.” Kuna kauli ya kuvutia iliyotolewa na Abu Haatam al-Sijistaanii (kafariki 322  A.H.)  ndani  ya  kitabu  chake  kiitwacho  al-Ziinah:  “Neno  Shi’ah lilikuwa  ni  jina  la  kwanza  ambalo  lilitokeza  katika  Uislam  kwa  ajili  ya 18


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 19

U i s l a m u wa S h i a madhehebu fulani na lilikuwa ni cheo cha masahaba wanne wa Mtukufu Mtume  (s.a.w.w.):  Abu  Dharr,  Ammaar,  Miqdad  na  Salman  al-Farsii. Wanne hawa pia walikuwa ndio wafuasi wa Ali waliojitokeza sana.” Yeye vilevile anaongezea: “Baadae, wakati wa vita vya Siffin neno hilo lilitumika kwa wafuasi wote wa Ali (a.s.).”

Shi’ah wa Mwanzoni: Kwa kawaida kabisa, Uislam wa Shi’ah ulianzia ndani ya Hijaaz miongoni mwa masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Tukirejea kwenye vitabu vya kihistoria na vya kiwasifu, tunaona kwamba orodha ya Shi’ah miongoni  mwa  masahaba  wa  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.)  inajumuisha  watu mashuhuri  wa  Bani  Hashim  (kizazi  cha  Hashim,  babu  mkubwa  wa Mtukufu Mtume Muhammad) wafuatao: Abdullah ibn al-Abbas, al-Fadhl bin  al-Abbas,  Ubaydullah  bin  al-Abbas,  Quthaam  bin  al-Abbas, Abd  alRahmaan  bin  al-Abbas,  Tamaam  bin  al-Abbas, Aqiil  ibn Abi  Talib, Abu Sufyan  bin  al-Haarith  bin  Abd  al-Muttalib,  Nawafil  bin  al-Haarith, Abdullah bin Ja’far bin Abi Talib, Awn bin Ja’far, Muhammad bin Ja’far, Rabi’at  bin  al-Haarith  bin Abd  al-Muttalib,  al-Tufayl  bin  al-Haarith,  alMughayrat bin Nawfil bin al-Haarith, Abdullah bin al-Haarith bin Nawfil, Abdullah  bin  Abi  Sufyan  bin  al-Haarith,  al-Abbas  bin  Rabi’at  bin  alHaarith, al-Abbas bin Utbat bin Abi Lahab, Abd al-Muttalib bin Rabi’at bin al-Haarith,  Ja’far  bin  Abi  Sufyaan  bin  al-Haarith.  Orodha  ya  Mashi’ah miongoni  mwa  wale  masahaba  wa  Mtume  (s.a.w.w.)  ambao  walikuwa hawatokani na Bani Hashim ni pamoja na: Salmaan, Miqdad, Abu Dharr, Ammaar binYasiir, Hudhayfat bin al-Yamaan, Khuzayma bin Thabit, Abu Ayyub al-Ansaari, Abu al-Haytham Maalik bin al-Tihaan, Ubayy bin Ka’b, Qays bin Sa’d, Ubadah, Adiy bin Hatam, Ubaadat bin al-Amir, Bilaal alHabashii,  Abu  Rafi’,  Hashim  bin  Utbah,  Uthman  bin  Hunayf,  Sahl  bin Hunayf,  Hakim  bin  Jiblat  al-Abdi,  Khaalid  bin  Sa’id  bin  al-Aas,  B.  alHusayb al-Aslamii, Hind bin Abi Haalat al-Tamimii, Ja’dat bin Hubayrah, Hujr bin Adiy al-Kindi, Amr bin al-Hamiq al-Khuza’i, Jaabir bin Abdillah al-Ansarii,  Muhammad  bin  Abi  Bakr  (mtoto  wa  Khalifa  wa  kwanza), 19


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 20

U i s l a m u wa S h i a Abaan bin Sa’id bin al-Asii, Zayd bin Sawhaan al-Zaydi.16 Kutokea Hijaz, Uislam wa Shi’ah ulienea kwanza huko Balaad al-Shaam (takriban Syria na Lebanon ya leo), hususan Jabal ‘Amil. Sababu ya hili ilikuwa kwamba Uthman bin Affan, Khalifa wa tatu, aliwafukuza sahaba wa  Mtume  (s.a.w.w.) Abu  Dharr  kwenda  Damascus  ambako  Mu’awiyah alikuwa anatawala. Abu Dharr hakukaa kimya, na aliizunguka Damascus na  kila  mahali  katika  eneo  hilo  akilalamika  dhidi  ya  ukengeukaji  ambao ulikuwa  umetokea  katika  ulimwengu  wa  Kiislam  na  kuwaita  kwenye mapenzi  na  uungaji  mkono  wa  Ali  (a.s.).  Sahaba  huyu  mkubwa  wa Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.)  alikwenda  Jabal ‘Amil iliyoko  kusini  mwa Lebanoni  ambako  alijenga  misikiti  miwili  na  akalingania  Uislamu  wa Shi’ah. Uislam wa Shi’ah uliimarika ndani ya Syria hususan katika wakati wa  utawala  wa  falme  ya  Hamdaan,  hasa  wakati  wa  utawala  wa  Sayf  alDawlah. Watu wa Ba’albak (Mji wa zamani ndani ya Lebanoni, karibu na mpaka wa Syria) walikuwa pia ni Shi’ah kuanzia mwanzoni mwa historia ya  Ushi’ah  katika  Bilaad  al-Shaam.  Leo  ni  moja  ya  vituo  muhimu  vya idadi ya Mashi’ah katika eneo hilo.

16 Angalia kwa mfano kwenye Buhuuth fi al-Milal wa an-Nihal cha J. Subhaani, Jz. 6, uk. 109 na 110. Sayyid Ali al-Madanii (kafa 1120 A.H.) katika kitabu chake al-Darajaat al-Rafi’at fi Tabaqat al-Shi’ah al-Imaamiyah anataja majina ya masahaba 69 wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambao walikuwa Shi’ah. Sayyid Abd alHusayn Sharafud-Diin (1377 A.H.) katika kitabu chake, al-Fujuul al-Muhimmah fi Ta’lif al-Ummah anataja  majina  ya  masahaba  zaidi  ya  mia  mbili  wa  Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.) ambao walikuwa Shi’ah, katika mpangilio wa alfabeti kuanzia Abu Rafi’ na kumalizia na Yazid bin Hawtharah al-Ansaari. Yusuf bin Abdullah (kafa 456 A.H.) ndani ya kitabu al-Isti’ab, Ibn Athiir ndani ya Usd ulGhaabah yake na Ibn Hajar (kafa 852 A.H.) ndani ya al-Isabah yake kuna majina ya wanachuoni wasio Shi’ah ambao wametaja baadhi ya watangulizi wa Shi’ah.   20


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 21

U i s l a m u wa S h i a Wakati wa Ukhalifa wa Ali (a.s.) na baada ya vita vya Jamal, mji wa Kufa huko  Iraq,  ambao  kiasili  ulianzishwa  kwa  ajili  ya  malengo  ya  kijeshi, uligeuka kuwa makao makuu ya dola ya Kiislamu na ya Shi’ah vilevile.17 Ushi’ah  uliendelea  na  kunawiri  ndani  ya  Kufa  na  kutokea  hapo  ulienea kwenye maeneo mengine ya dunia. Huko Yemen Ushi’ah unahusishwa na mazingira ambamo watu kule waliukubali  Uislam.  Kwa  mujibu  wa  vitabu  vya  historia,  Mtukufu  Mtume (s.a.w.w.) kwanza alimtuma Khalid bin al-Walid kwenda Yemen kuwalingania watu kwenye Uislamu. Yeye alikaa huko kwa muda wa miezi sita, lakini hakuwa na mafanikio. Halafu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akamtuma Ali (a.s.) akamtaka amrudishe Khalid. Al-Bura’, ambaye alikuwa mmoja katika  ujumbe  ulioongozwa  na  Ali  (a.s.),  anasema  kwamba  walipofika eneo la karibu sana na Yemen, Ali aliongoza swala ya Asubuhi na akamtaka  kila  mtu  asimame  kwenye  mstari  mmoja.  Kisha  akasogea  zaidi kuwaelekea  wenyeji  wa  pale.  Ali  (a.s.)  alianza  kwanza  kwa  kumtukuza Mwenyezi  Mungu,  na  halafu  akasoma  ule  ujumbe  wa  Mtukufu  Mtume (s.a.w.w.) kwao. Watu wote wa Hamdaan waliukubali Uislamu katika siku ile  ile  ya  kwanza  hasa  na  walifuatiwa  baadae  na  watu  wengine  wa Yemen.18 Kwa  hiyo,  Waislamu  wa Yemen  waliinukia  kuwa  na  mapenzi makubwa  kwa Ali  (a.s.),  hususan  baadae  wakati  waliposikia  sifa  za Ali kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na wakashuhudia ukatili wa maadui wa Ali (a.s.) kama vile Busr bin Arti’ah. Uislamu wa Shi’ah ndani ya Misri una historia kama hiyo, kwani kuanzia kuingia kwa Uislam katika nchi yao, Wamisri walijua juu ya Ushi’ah kupitia  mawasiliano  na  masahaba  wakubwa  wa  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.) ambao  walikuwa  wamehusika  katika  tukio  hilo,  kama  vile  Miqdad, Abu 17 Mnamo mwaka 661 makao hayo yalihamishiwa Damascus na Mu’awiyah bin Abi Sufyan. 18 Tazama al-Kamiil cha Ibn al-Athiir, Jz. 2, uk. 300. Tazama pia Kanz al-Ummal cha Muttaqii al-Hindi (kafa 975 A.H.), Jz. 6, uk. 158 na 392. 21


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 22

U i s l a m u wa S h i a Dharr, Abu Rafi’ na Abu Ayyub al-Ansarii. Katika kipindi cha Khalifa wa tatu, Ammar bin Yasir, Sahaba mkubwa wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Shi’ah  maarufu,  mwenyewe  binafsi  alitembelea  Misri.  Watu  wa  Misri walikuwa mashughuli sana katika matukio ambayo yalimlazimu Ali (a.s.) kuukubali  Ukhalifa  baada  ya  kuuliwa  kwa  Khalifa  wa  tatu.  Wakati  Ali alipomtuma  Qays  bin  Sa’d  kutawala  Misri,  alikaribishwa  vizuri  sana  na watu  wakatoa  kiapo  cha  utii  kwake.  Baadae,  Amr  bin  al-Aas  alimuua Muhammad bin Abu Bakr, ambaye alikuwa ameteuliwa na Ali (a.s.) kama gavana  wa  Misri  anayefuatia.  Chini  ya  Bani  Umayyah  na  Bani  Abbas hapakuwa  na  utawala  wa  Shi’ah  katika  nchi  hiyo,  lakini  watu  walikuwa wenye moyo mzuri kwenye njia ya Ushi’ah. Hili liliwezesha uanzishwaji wa  utawala  wa  Fatimia  ndani  ya  Misri  na  sehemu  kubwa  ya  Afrika  ya Kaskazini,  ambao  ulidumu  hadi  wakati  wa  Salaah  al-Din  al-Ayyubi ambaye aliurudisha umiliki wa Sunni katika eneo hilo.19 Katika Irani, Ushi’ah ulikuwa na hadithi tofauti. Wakati walipoanza kuingia kwenye Uislam kuanzia wakati wa Khalifa wa pili na kuendelea, wengi wa Wairani walikuwa Masunni. Kwa hakika, kwa sababu mahususi baadhi ya miji ilikuwa tangu mwanzoni ilikuwa ni ya Shi’ah yote mizima au sehemu yake, kama vile Qum, Rayy na Kaashaan. Watawala wa Buwayhid (walitawala miaka ya 320 – 447 A.H.), ambao walikuwa Shi’ah, walikuwa na  ushawishi  mkubwa  ndani  ya  majimbo  ya  Iran  na  pia  katika  makao makuu ya Khalifa huko Baghdad, na hata juu ya Khalifa mwenyewe. Hili liliwapa Mash’ah nguvu ya kutekeleza na kulingania imani yao waziwazi. Wakati  Mfalme  Muhammad  Khudaabandeh  alipoingia  Ushi’ah  katika karne ya saba ya Kiislamu, yeye alitoa fursa kubwa zaidi kwa Shi’ah wa 19 Ni  lazima  itambulike  kwamba  hao  Fatimia  walikuwa  ‘Isma’iliya’  na  sio ‘Ithnashari’  na  wakati  wa  utawala  wao  watu  wengi  walibakia  kuwa  Sunni. Ithnaashari  kwa  zaidi  ndio  kundi  kubwa  la  Uislam  wa  Shi’ah.  Hao  Ithnaasharia wanaamini  katika  Maimam  Kumi  na  Mbili.  Isma’iliya  ndio  kundi  la  pili  kwa ukubwa la Shi’ah. Wao wanaamini katika wale Maimam sita wa mwanzoni wa hao Kumi na Mbili. 22


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 23

U i s l a m u wa S h i a Irani. Idadi kadhaa ya harakati kama ile ya Sarbedaarid wa Khuraasaan pia ilijaribu  kuupa  umaarufu  Ushi’ah.  Hatimaye,  Mfalme  Isma’il  alianzisha utawala wa Safavid mnamo mwaka 905 A.H. na akaufanya Ushi’ah kuwa ndio madhehebu yenye umiliki ndani ya Irani. Kuanzia hapo, idadi kubwa ya wanachi wa Irani imekuwa wakati wote ni ya Shi’ah. Ukuaji  wa  Uislamu  wa  Shi’ah  katika  nchi  nyingine  yenye  Mashi’ah, ambayo  ni  Jamhuri  ya Azerbaijani,  ilifuata  njia  kama  hiyohiyo  ya  Irani, kwa  vile  ilikuwa  ni  sehemu  ya  Irani  mpaka  pale  ilipotekwa  na  Warusi mapema mnamo karne ya kumi na tisa (19).20 Uislamu uliingia Azerbaijani katika  karne  ya  kwanza  ya  Kiislam  (642  CE)  na  kuanzia  hapo  Uislam umekuwa ndio dini yenye umiliki pale. Waislam sasa wanafanya zaidi ya asilimia 95 ya idadi ya watu na waliobakia wengi wao wanafuata Kanisa la Orthodox  la  Russia  na  Kanisa  la  Kitume  la Armenia. Asilimia  Sabini  ya idadi yote ya watu ni Shi’ah. Mchakato ambamo kwamba Ushi’ah ulikuwa imani yenye umiliki ndani ya Azerbaijani unarudi nyuma hadi mwanzoni mwa karne ya 16 wakati wa utawala wa Mfalme Isma’il, mwanzilishi wa falme ya Safavid. Ingawa utekelezaji wa Uislamu wa Shi’ah ulizuiliwa chini ya utawala wa Urusi, baadhi ya watu wa Azerbaijani walibakia wakijishirikisha kwa bidii katika masuala ya kidini. Kuna misikiti mingi sana, kama vile ule Msikiti wa Taazeh Pir, Msikiti wa Jamaa na Msikiti wa Imam Husein. Zipo vilevile shule  za  Kiislam  na  seminari  kadhaa,  hususan  ndani  ya  Baku  na  Jalil Abaad.  Ni  kawaida  kwa  watu  kutembelea  makaburi  ya  watakatifu  wa Kiislamu,  kama  vile  makaburi  ya  dada  zake  Imam  ar-Ridhaa  (a.s.)  huko Naadaran, kaburi la Bibi Haybat karibu na Baku na kaburi linalohusishwa na Nabii Jerjis huko Biljan. Watu wa Azerbaijani walisherehekea kwa bidii sana  matukio  ya  Kiislam.  Kila  mwaka  wakati  wa  mwezi  wa  Muharram 20 Azerbaijani  ilibakia  chini  ya  utawala  wa  Russia  mpaka  wakati  wa  uhuru mnamo  1918.  Halafu  ikatekwa  na  Bolshevik  mnamo  April  1920.  Jamhuri  ya Azerbaijani ilikombolewa mnamo Agosti 30, 1991. 23


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 24

U i s l a m u wa S h i a (mwezi wa kwanza wa kalenda ya Kiislam), hususan katika siku ya mwezi kumi (siku ya Ashura) maandamano na hadhara za maombolezo hufanyika kote nchini.

MLANGO WA PILI Vyanzo vya Itikadi ya Shi’ah Kabla ya kuchunguza mafundisho na ibada za Shi’ah, ni muhimu kuainisha au kutambulisha vyanzo ambavyo juu yake Shi’ah wanategemea kwa ajili ya  kuuelewa  Uislamu  na  utaratibu  walioutwaa  katika  kuvitumia  vyanzo hivyo. Katika kinachofuatia, tutachunguza vile vyanzo vinne vya itikadi ya Shi’ah  kama  vinavyohusiana  na  elimu  ya  Shari’ah  (fiqh)  kiumahususia hasa; Qur’ani Tukufu, Sunnah, mantiki na maafikiano (Ijmah).

Qur’ani Tukufu: Qur’ani  bila  shaka  ndio  chanzo  cha  muhimu  kabisa  kwa  Waislam  wote, pamoja na Shi’ah. Qur’ani kwa hiyo inasimama kama chombo cha umoja miongoni mwa Waislam. Bila ya kujali tofauti zao za kimadhehebu na historia (usuli) ya kitamaduni, Waislam wote wanarejea kwenye Kitabu hicho hicho  kama  muongozo  wa  kimbinguni  wa  kutawala  maisha  yao.  Katika wakati  mwingine  wowote  wa  historia,  leo  kote  katika  ulimwengu  wa Kiislam kuna Qur’ani moja tu bila ya nyongeza yoyote wala mabadiliko. Mfano halisi wa msimamo wa Shi’ah juu ya Qur’ani unaweza kuonekana katika dondoo ifuatayo: “Sisi tunaamini kwamba Qur’ani ilizinduliwa kimungu, na kufunuliwa na Mwenyezi Mungu kwenye ulimi wa Mtume Wake Mtukufu, kuweka wazi kila  kitu,  ni  muujiza  wa  kudumu  milele.  Mwanadamu  hawezi  kuandika chochote  kama  hiyo  Qur’ani  kwa  sababu  ya  ufasaha  wake,  ubayana, ukweli  na  elimu  yake,  na  hakuna  mabadiliko  yanayoweza  kufanyika  juu yake. Hii Qur’ani tuliyonayo sasa ni kile hasa kilichotumwa kwa Mtume, 24


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 25

U i s l a m u wa S h i a na yeyote anayedai vinginevyo ni muovu, mpotoshaji mtupu au vinginevyo mtu  aliyeko  kwenye  makosa,  na  wote  hao  wamepotoka,  kwa  sababu  ni maneno ya Mwenyezi Mungu, na

“Hautakifikia upotovu mbele yake wala nyuma yake …..” (41:42) …..Tunaamini  vilevile  kwamba  ni  lazima  tuiheshimu  na  kuipa  hadhi Qur’ani tukufu, na hili ni kwa maneno na vitendo halikadhalika. Kwa hiyo, ni  lazima  isichafuliwe  kwa  makusudi,  hata  kwa  moja  ya  herufi  zake,  na lazima isiguswe na yeyote yule ambaye hana tohara. Inasemwa ndani ya Qur’ani  kwamba:  “Hakuna atakayeigusa isipokuwa wale waliotakaswa.” (56:79) (Muzaffar, uk. 26).

Shi’ah wanakanusha kuwepo mabadiliko yoyote ndani Qur’ani: Kama  ilivyoelezwa  hapo  juu,  Shi’ah  wanakanusha  kuwepo  mabadiliko yoyote yale ndani ya Qur’ani, na wanaamini kwamba Qur’ani iliyopo sasa hivi  ni  ile  ile  moja  kama  ilivyoteremshwa  kwa  Mtukufu  Mtume Muhammad (s.a.w.w.). Qur’ani imekamilika. Hata hivyo, baadhi ya watu ambao walikuwa hawana ufahamu juu ya Uislam wa Shi’ah na hawakuwa na  uhusiano  wa  karibu  na  jumuiya  za  Shi’ah  wamedai  kwamba  Shi’ah wanaamini  kwamba  Qur’ani  imebadilishwa  na  baadhi  ya  sehemu  zake zimefutwa. Msingi wa shutuma hizi unaweza ukawa sio chochote zaidi ya kuwepo  kwa  hadith    katika  makusanyo  ya  hadith  ya  Shi’ah  ambazo zimechukuliwa  kama  pendekezo  la  mabadiliko  katika  Qur’ani.  Sio  ile idadi  kubwa  ya  kushangaza  ya  wanachuoni  wa  kuheshimika  wa  Shi’ah wala waumini wa kawaida ambao kamwe wameweza kuwa na imani kama hiyo,  madai  haya  ni  ya  ajabu  sana  kiasi  kwamba  hayastahili  kutiliwa maanani,  na  wakati  yanapotolewa,  yanafanywa  kwa  malengo  ya  mabishano na uadui. 25


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 26

U i s l a m u wa S h i a Hakuna hata mtu mmoja ambaye ameona kamwe nakala ya Qur’ani tofauti na hii ya kawaida katika sehemu yoyote ile ya ulimwengu wa Kiislamu. Kuna  miswada  ya  Qur’ani  inayopatikana  leo  hii  ambayo  inarudi  nyuma hadi katika kipindi cha wakati wa Maimam wa Shi’ah na iko vile vile hasa sawa na hii ya sasa hivi. Kwa nyongeza ya nakala zilizohifadhiwa katika nyumba  za  makumbusho  za  Irani,  Pakistan,  Iraq  na  sehemu  nyingine  za ulimwengu,  nakala  za  thamani  kubwa  ya  kihistoria  iliyowekwa  ndani  ya Makumbusho ya Qur’ani katika mji wa Mashhad zinafaa hasa kufahamika.21 Qur’ani  Tukufu  kwa  uwazi  kabisa  inasema  kwamba  Mwenyezi  Mungu Mwenyewe  anailinda  Qur’ani  kutokana  na  mabadiliko  na  uharibifu  wa maandiko:

“Hakika sisi tumeiteremsha Qur’ani, na kwa hakika sisi ndio wenye kuilinda.” (al-Hijr; 15:9).22 Kuhusiana na aya hii, Allamah Tabatabai, mmoja wa wafasiri wakubwa wa 21 Muhammad  Baqir Ansaarii,  mtaalamu  katika  masuala  ya  sayansi  za  Qur’ani anaandika: “Binafsi nimeona baadhi ya nakala za Qur’ani Tukufu zilizoandikwa kwenye vipande vya ngozi ya mbawala zilizohifadhiwa. Kipindi cha kuandikwa kwa nakala hizi za Qur’ani kinarudi nyuma miaka zaidi ya elfu moja. Baadhi yao zimehusishwa  na  Imam  Ali  (a.s.),  Imam  as-Sajjad  (Imam  wa  nne),  Maimam wengine,  Ulamaa  wa  Shi’ah  na  wachamungu.  Kadhalika,  katika  majumba mengine ya makumbusho na maktaba kadhaa, kuna nakala za Qur’ani pia ambazo ni za kale sana, lakini mpaka hapa hakuna hata mmoja aliyeweza kudai kwamba walau hata neno moja la miswada hii ya Qur’ani inatofautiana na ile iliyopo sasa hivi kwa Shi’ah na kwa Sunni wa dunia nzima.  22 Imefahamika kwamba haya madai ya mabadiliko yameishia kwenye ufutwaji wa baadhi ya aya; vinginevyo sio Shi’ah wala Sunni ambao wamewahi kudaiwa kuongeza kitu kwenye Qur’ani. 26


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 27

U i s l a m u wa S h i a Qur’ani,  katika  kitabu  chake  maarufu,  al-Mizaan fi Tafsir al-Qur’an, anaeleza: “Qur’ani  ni  Ukumbusho  hai  na  wa  milele,  ambao  hautakufa  kamwe  na kuangukia kwenye kusahaulika. Umekingika kutokana nyongeza na upungufu.  Umekingika  na  kusalimika  dhidi  ya  mabadiliko  yoyote  yale  katika umbo  na  mtindo  ambao  unaweza  kuathiri  tabia  na  wajibu  wake,  yaani, kama ‘Ukumbusho wa Allah ambao unaelezea ukweli na elimu ya mbinguni.’ Kwa sababu hii, aya iliyotangulia kutajwa inaashiria kwamba hiki Kitabu  Kitukufu  siku  zote  kimekuwa  na  kitaendelea  kuwa  kimelindwa dhidi ya uharibifu na mabadiliko.” Katika  kinachofuatia  tutachunguza  baadhi  ya  kauli  za  wanachuoni  wa Shi’ah katika zama tofauti kuhusiana na jambo hili. Na kwa vile sababu ya kuwashutumu  Shi’ah  na  imani  ya  kwamba  Qur’ani  imebadilishwa imekuwa  ni  kuwepo  kwa  hadith  chache  ndani  ya  baadhi  ya  vitabu  vya Shi’ah ambazo zimechukuliwa kudokezea kuwepo kwa mabadiliko, tutarejea  pia  kwenye  mwelekeo  wa  utaratibu  wa  Shi’ah  katika  uchunguzi  wa hadith ili kuweza kuelewa mtazamo wa Shi’ah kwenye hadith kwa jumla na zile hadith zinazojadiliwa kwa umahususi zaidi. Inapaswa kufahamika kwamba  hadith  sawa  na  hizo  au  hata  zenye  nguvu  zaidi  ya  hizo  zinapatikana  katika  vyanzo  visivyo  vya  ki-  Shi’ah.  Hata  hivyo,  Shi’ah  hawajawahi  kamwe  kuwashutumu  ndugu  zao  Sunni  juu  ya  kuamini  katika mabadiliko  ya  Qur’ani,  kwa  vile  wakati  wa  kuhusisha  imani  fulani  na kundi  lolote  lile  mtu  anapaswa  kutaja  zile  kauli  zilizotolewa  na  vyanzo vyake  mwenyewe,  na  sio  kwenye  kauli  zilizotengeka  ambazo  wao wenyewe hawazikubali au kuzitafsiri kwa namna tofauti na kile ambacho watu wa nje wanaweza kukidai. Kauli za Wanachuoni wa Shi’ah Kuhusu Qur’ani: Njia  bora  ya  kuelewa  maoni  ya  Shi’ah  kuhusiana  na  Qur’ani  ni  kurejea kwenye kauli za wanachuoni wao wakubwa. Mifano inafuatia sasa:

27


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 28

U i s l a m u wa S h i a 1. Sheikh  al-Saduq  (kafariki  381),  anayefahamika  kama  ‘Shaykh alMuhadithiin’ (Bingwa wa hadith) katika kitabu chake, al-I’tiqaadaat alImaamiyah (Itikadi ya Shi’ah) anasema: “Imani yetu ni kwamba ile Qur’ani ambayo Allah aliiteremsha kwa Mtume Wake  Muhammad  (s.a.w.w.)  ni  (ileile)  moja  baina  ya  majalada  mawili (daffatayn).  Na  ndio  ile  ile  iliyoko  mikononi  mwa  watu,  na  sio  kubwa kuliko hiyo. Idadi ya Sura kama inavyokubalika kwa jumla ni mia moja na kumi na nne ….. Na yeyote atakayedai kwamba sisi tunasema kwamba ni kubwa kwa kiasi chake kuliko hiyo, huyo ni muongo.”23 2.   Sayyid al-Murtadha (kafariki 436/1044) anakeleza: “Elimu na uhakika kuhusu uthabiti wa hadithi ya Qur’ani Tukufu ni sawa na elimu na uhakika kuhusu kuwepo kwa nchi mbalimbali, miji, matukio maarufu ya kihistoria ….. Hii ni kwa sababu umakini na uangalifu uliotolewa juu ya Qur’ani, na ile hamasa kubwa juu ya kunakili na kulinda maandishi yake vilikuwa na nguvu zaidi kuliko uangalifu na mazingatio yaliyotolewa kwenye vitu vilivyotajwa hapo juu ….. Wakati wa uhai wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) Qur’ani ilikuwa ni utungo uliokusanywa kama  ulivyo  hivi  sasa.  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.)  alikuwa  pia  amekwishakabidhi kikundi cha masahaba zake jukumu la kuihifadhi kwa kichwa na kuilinda hiyo Qur’ani Tukufu. Wakati ule, ilikuwa ni jambo la desturi kwa  watu  kusoma  Qur’ani  mbele  ya  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.)  ili kuhakikisha usahihi wa maneno yake. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) vilevile aliwasikiliza  usomaji  wao.  Kundi  la  masahaba  kama  vile  Abdullah  ibn Ma’sud, Ubayy bin Ka’b na wengineo, waliisoma Qur’ani nzima mara kwa mara mbele ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).” Kwa  mazingatio  kidogo,  mtu  anakuja  kutambua  kwamba  mambo  yote haya  yanaelekeza  kwamba  Qur’ani  tukufu  ilikuwa  imekwisha  kuku23 Shi’ite Creed, Toleo la Kiingereza, uk. 77 28


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 29

U i s l a m u wa S h i a sanywa. Hakuna anayewatilia maanani wale wapinzani wa imani hii, wawe Imamiyah au  Hashwiyay,  kwani  maoni  yao  yametokana  na  kikundi  cha watu wa hadith ambao walisimulia hadith dhaifu juu ya jambo hili, wakifikiri  kwamba  wamesimulia  hadith  sahihi  na  thabiti.  Hata  hivyo,  hadith dhaifu kama hizi hazina uwezo wa kutia changamoto lolote jambo lililosimamia elimu ya uthabiti na uhakika.24 3. Muhammad  bin  al-Hasan  al-Tusi  (kafariki  460/1067),  anayefahamika kama Shaykh al-Ta‘ifah – bwana wa madhehebu ya Shi’ah anaeleza: “Kauli za kuhusu nyongeza na upungufu ndani ya maandishi ya Qur’ani hazifai  kuzingatiwa,  kuna  maafikiano  miongoni  mwa  Ulamaa  kuhusiana na ubatili wa jambo hili.” 4. Sheikh al-Tabarsi (kafariki 548/1153 au 538/1143?), katika kitabu chake maarufu cha tafsiri ya Qur’ani, Majma’ al-Bayaan, yeye anasema: “Kuna  maafikiano  na  kauli  ya  pamoja  miongoni  mwa Waislam  kwamba hakuna nyongeza iliyofanywa ndani ya Qur’ani tukufu. Lakini kuhusiana na mapungufu kutoka ndani ya maandishi ya Qur’ani, kikundi fulani cha Imamiyah na kikundi cha Hashwiyah (ambao ni Sunni) wamesema kwamba kuna mabadiliko na mapungufu ndani ya Qur’ani tukufu, lakini imani sahihi ya kweli inayokubaliwa na hao Imamiyah inasisitiza vinginevyo.” 5.  Sayyid  bin Tawuus  (kafariki  664/1265)  katika  kitabu  chake  kiitwacho Sa’d al-Su’ud yeye anasema:

24 Majibu juu ya maswali ya Tirablusiyaat. 29


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 30

U i s l a m u wa S h i a “Kwa  ukweli,  hawa  Imamiyah  wanaamini  juu  ya  kutokuwepo  kwa mabadiliko ndani ya Qur’ani Tukufu.”25 Hadithi za Shi’ah kuhusu Qur’ani: Hapa tunarejea tu kwenye mielekeo ya utaratibu (methodolojia) wa Shi’ah katika uchunguzi wa hadith ambazo zinahusiana na mada hii tuliyonayo na nyingine  zinazofanana  nayo.  Kwanza  kabisa  ni  lazima  iwekwe  wazi kwamba  hakuna  mkusanyo  wa  hadith  unaochukuliwa  na  Shi’ah  kama  ni sahihi  katika  ujumla  wake.  Kwa  ukubwa  na  umaarufu  kiasi  gani,  wenye thamani  na  usahihi  wa  jumla,  vyovyote  mkusanyiko  wa  hadith utakavyokuwa,  Wanachuoni  wa  Shi’ah  hawauchukulii  moja  kwa  moja kwamba yaliyomo humo ni sahihi. Kila hadith moja iliyotajwa katika mkusanyo  wowote  wa  hadith  ni  lazima  uchunguzwe  kipeke  yake.  Kuweza kutumia hadith kama rejea yake, mwanachuoni wa Shi’ah anahitaji kwanza kuangalia angalau mambo matatu muhimu: 1. Ile njia ambayo kwamba amekipata kile kitabu chenye hadith hiyo. Kwa mfano, kama hadith imetajwa ndani ya al-Kafi, ambacho kimeandikwa 25 Imedondolewa  ndani  ya  Ansaarii  (1997).  Kwa  kauli  nyingine  zaidi  rejea kwenye Al-Saafi cha Mulla Muhsin al-Kaashani (aliyefariki 1091/1680), Risaala fi Ithbaat ‘Adam al-Tahrif -  makala  juu  ya  kukosekana  mabadiliko  ndani  ya Qur’ani – ya Muhammad bin al-Hasan al-Hurrr al-Amilii (aliyefariki 1104/1692), Fawa’id al-Usuul cha  Muhammad  Mahdi  (aliyefariki  1212/1797)  anayejulika zaidi  kama  Bahrul-Uluum,  Kashf al-Ghitaa’‘An Mabhamaat al-Shari’at alGharra cha  Sheikh  Ja’far  (aliyefariki  1228/1813)  anayejulikana  kama  Kashf  alGhita,  Tanqib al-Maqaal cha  Sheikh  Muhammad  Hasan  al-Mamaqaani  (kafa 1323/1905),  Alaa al-Rahmaan cha  Muhammad  Jawad  al-Balaaghii  (aliyefariki 1352/1933), Ajwibat Masa’il Musa Jarullah cha Sayyid Abd al-Husayn Sharaf alDin (aliyefariki 1377/1957), Al-Mizaan cha Allamah Sayyid Muhammad Husayn Tabatabai (aliyefariki 1402), Al-Bayaan cha Ayatullah Sayyid Abu al-Qaasim alKhu’i (aliyefariki 1413), Ma’alim al-Madrasatayn cha Sayyid Murtadha ‘Askari na Tahdhib al-Usuul cha Ayatullah Khomeini (aliyefariki 1989). 30


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 31

U i s l a m u wa S h i a katika karne ya nne, mtafiti anapaswa kuhakikisha kwamba hiyo nakala ya  al-Kafi  aliyonayo  inafanana  na  ile  ya  nakala  ya  mwandishi mwenyewe.  Kwa  madhumuni  haya,  wanachuoni  wa  hadith  Shi’ah, kizazi baada ya kizazi, wamezikagua nakala zao za vitabu hivyo pamoja na mabingwa wao, hadith kwa hadith, na baada ya kukamilisha kazi hiyo  ndipo  wanaweza  kupata  ruhusa  kutoka  kwa  mabingwa  wao kusimulia kutoka kwa mwandishi wa kitabu cha awali na halisi. 2.  Baada  ya  kuhakikisha  kwamba  kile  kitabu  alichonacho  mikononi mwake  kinafanana  na  kile  cha  asili,  mwanachuoni  anahitaji  kuchunguza sanadi ya wasimuliaji ambayo kupitia hiyo ndimo amepokea riwaya hiyo kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) au Maimam (a.s.). Kwa lengo hili, mtafiti  anapaswa  kuhakikisha  kwamba  hakuna  kinachokosekana  katika nyororo ya wasimuliaji, kwamba watu wote wanaotokeza katika nyororo hiyo wametambulishwa kwa usahihi na mwishowe kwamba wote waliotajwa kama wasimuliaji ni waaminifu na wa kutegemewa. Kama mtu mmoja tu, tuseme, kati ya watu kumi akikosekana, ama hajulikani, au anajulikana kuwa ni muongo, basi nyororo yote inabatilika. 3. Pale majukumu hayo mawili ya mwanzo yanapokamilika, mwanachuoni wa hadith baada ya hapo ni lazima afanye uchunguzi namna mbalimbali wa jumla kuhusu yaliyomo ndani ya hadith  hiyo ili kumuwezesha kuitumia  hadith  hiyo  kama  rejea.  La  kwanza  ni  kukagua  kama  hadith  hiyo inakubaliana  na  Qur’ani  ama  laa.  Bila  ya  shaka  yoyote,  Shi’ah  wote wanaamini kwamba hadith yoyote inayopingana na Qur’ani au ambayo ni dhidi ya mafundisho ya Qur’ani ni lazima itupiliwe mbali na kukataliwa, hata kama wasimulizi wake wakitokea kuwa waaminifu. Kuna maelekezo ya  wazi  kutoka  kwa  Maimam  wa  Nyumba  ya  Mtume  kuhusiana  na  hili. Kwa mfano, Ibn Abii Ya’fuur anasema:   “Nilimuuliza Abu Abdillah Ja’far as-Sadiq kuhusu hadith mbalimbali zilizosimuliwa  na  wale  ambao  tunawaamini  na  vilevile  na  wale  ambao hatuwaamini.  Kulisikia  hili,  Imam  alijibu:  ‘Wakati  wowote  unapopokea riwaya  inayoungwa  mkono  na  aya  yoyote  kutoka  kwenye  Kitabu  cha 31


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 32

U i s l a m u wa S h i a Mwenyezi  Mungu  au  hadith  (iliyothubutu)  ya  Mtukufu  Mtume,  basi ikubali hiyo. Vinginevyo riwaya hiyo ni ya kuachwa kwa yule tu aliyekufikishia wewe.”26 Hakuna anayeweza kusema kwamba, kwa sababu fulani bin fulani alikuwa mwanachuoni mkubwa sana, chochote kinachotajwa kwenye kitabu chake ni sahihi. Kwa hiyo Shi’ah hawaamini juu ya kitabu cha hadith ambacho chote ni sahihi, kinyume chake na imani ya Sunni kuhusiana na makusanyo ya Bukhari na Muslim. Licha ya hadhi ya wanachuoni wote wa Shi’ah ya hali  ya  juu  isiyo  na  shaka,  vile  Vitabu  vinne  vya  hadith  (al-Kutub alArba’ah),  yaani;  al-Kaafi, Man laa Yahdhuruhuu al-Faqih, Tahdhib alAhkaam na al-Istibsaar, havichukuliwi  ama  na  wakusanyaji  wao  au wanachuoni wengine kama ni sahihi kwa ujumla wao (wa kuwa kitabu).27 Kwa Shi’ah Qur’ani ndio Kitabu sahih peke yake, ambacho kwacho kila chanzo  kingine  chochote  lazima  kikubaliane  nacho.  Hoja  hii  hii  hasa imetajwa  katika  utangulizi  wa  Usuul al-Kaafi cha  Sheikh  al-Kulayni mwenyewe. Ndugu  yangu,  Mwenyezi  Mungu  akuongoze  kwenye  njia  iliyonyooka. Unapaswa kujua kwamba sio kila mmoja anaweza kuutambua ukweli katika riwaya zinazotofautiana zinazohusishwa kwa Ulamaa (yaani Maimam), amani iwe juu yao, isipokuwa kupitia vipimo ambavyo vimetangazwa na Aalim – yaani Imam, amani juu yake: “Zipimeni riwaya (zinazohitilafiana) kwa Kitabu cha Mwenyezi Mungu, na ile inayokubaliana nayo ichukueni, na ile inayopingana nayo ikataeni.”  26 Usuul al-Kafi, toleo la kiingereza, Hadith ya 202. 27 Kwa  mfano,  Muhammad  Baqir  al-Majlisi,  mwanachuoni  mkubwa  wa  hadith ndani  ya  kitabu  chake,  Mir’at al-Uquul,  anazitathmini  hadith  zote  za  al-Kaafi moja baada ya nyingine na kutoa maoni yake binafsi kuhusu usahihi wao na yale yaliyomo kwenye hadith hizo. 32


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 33

U i s l a m u wa S h i a Kinyume chake, Waislam wa Sunni wanaamini kwamba kuna vitabu sita (as-Sahih al-Sittah)  ambavyo  vinaaminika  kwamba  ni  makusanyo  sahihi yote ya hadith.

Mas’hafu ya Fatima: Jambo jingine ambalo wakati mwingine linakuwa halieleweki ni suala la Mas’haf ya Fatima, binti ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Kwa mujibu wa baadhi ya riwaya za Shi’ah, kuna kitabu kilicho na jina hili, kilichohifadhiwa  na  Maimam  wa  Nyumba  ya  Mtume  (a.s.).  Katika  Kiarabu,  neno Mus’hafu linamaanisha ‘kitabu’ au ‘mkusanyiko wa kurasa,’ linalotokana na neno safhah lenye maana ya ‘ukurasa.’ Maneno yanayofanana na hilo ni suhuf (kama zile suhuf za Ibrahim na Musa zinazotajwa kwenye Qur’ani kwa kumaanisha vitabu walivyopokea) na sahifa, ‘gazeti’ katika Kiarabu cha kisasa. Hivyo neno Mus’haf  sio lazima limaanishe Qur’ani: neno hilo linaweza  kutumiwa  kote  kwenye  Qur’ani  na  kwenye  vitabu  vinginevyo. Baadhi ya watu wamedhani kwamba kwa vile Shi’ah wana riwaya zinazohusu  Mus’haf  wa  Fatima,  basi  wanaamini  katika  Qur’ani  nyingine. Kutokuelewa huku pengine kunasababishwa na kukosa elimu ya Kiarabu na hizo riwaya za Shi’ah. Huo  Msahafu  wa  Fatima  vilevile  sio  kitu  kinachojaribu  kupingana  na Qur’ani Tukufu. Ipo riwaya kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s.) inayosema kwamba huo Msahafu wa Fatima unajumuisha na taarifa kuhusu matukio yajayo  na  unayo  orodha  ya  majina  ya  wale  watu  watakaotawala  baadae, ikiwa ni pamoja na Bani Umayyah, Bani Abbas na kadhalika. Hakuna chochote  cha  Qur’ani  ndani  yake.  Wala  hamna  chochote  kinachohusiana  na sheria za kiutendaji za Uislamu.28 Kwa mujibu wa baadhi ya riwaya, wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipofariki, Fatima (a.s.) alikuwa amesikitika sana, hivyo Malaika Mkuu Jibril (a.s.)  alikuwa  akienda  kuzungumza  naye  kuhusu  matukio  ya  baadae  ili 28 Rejea Usuul al-Kaafi, hadith ya 636 na 637. 33


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 34

U i s l a m u wa S h i a kumliwaza.  Taarifa  alizomfikishia  zilikuwa  zikiwekwa  pamoja  katika namna ya kitabu na kikaja kujulikana kama Mus’haf wa Fatima. Wakitambua kwamba hakuna njia ya kuwashutumu Shi’ah kwa kuwa na Qur’ani nyingine, baadhi ya watu wanachukua mbinu ya kuwashambulia kwa  kusema  kwamba  Shi’ah  wanaamini  kwamba  Fatima  alikuwa  ni mjumbe wa Mwenyezi Mungu. Hata hivyo, kama tulivyoona hivi punde, huo  Msahafu  wa  Fatima  hauna  chochote  cha  kuhusiana  na  Utume.  Kwa mujibu wa Hadith kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s.) inayopatikana katika Usuul al-Kaafi, Fatima (s.a.) alifariki siku 75 baada ya kifo cha Mtukufu Mtume  (s.a.w.w.).  Alikuwa  mwenye  huzuni  sana  kutokana  na  kifo  cha baba yake, hivyo Jibril (a.s.) alikuwa akija na kuonyesha rambirambi zake kwa Fatima (a.s.) na kuongea kuhusu mahali pa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) huko Peponi ili kumfanya Fatima (a.s.) afarijike. Jibril vilevile alimuelezea Fatima (a.s.) kile kitakachomtokea yeye na kwa watoto wake (a.s.). Imam Ali  (a.s.)  aliyaandika  yote  hayo  katika  mkusanyo  ambao  baadae  ulikuja kujulikana  kama  Msahafu wa Fatima.  Halikuwa  suala  la  utume.  Shi’ah wote wanaamini kwamba Mtume Muhammad (s.a.w.w.) alikuwa ni Mtume wa mwisho, lakini hii haina maana kwamba Mwenyezi Mungu asingeweza kuwasilisha  jambo  lolote  kwa  mtu  yoyote  yule  baada  ya  kifo  chake Mtume. Kwa mujibu wa Qur’ani, ni wazi kabisa kwamba mwongozo au mawasiliano ya kiungu yanakuja katika miundo tofauti, baadhi yao ikiwa ni  ya  kipekee  kwa  Mitume  tu  na  mingine  sio  hivyo.  Kwa  mfano,  mama yake  Nabii  Musa  (a.s.)  aliongozwa  kwa  namna  ya  mawasiliano,  ingawa hakuna  madai  kwamba  alikuwa  ni  Nabii.  Kwa  kweli  Mwenyezi  Mungu anaweza kuongoza hata visivyokuwa wanadamu, kama vile nyuki:

“Na Mola wako akampa wahyi nyuki kwamba, tengeneza nyumba katika milima …..” (an-Nahl; 16:68). Aina hii ya mwongozo na mzinduo inaitwa Wahyi, lakini halikuwa ni suala 34


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 35

U i s l a m u wa S h i a la utume. Kwa hiyo neno Wahyi kwa kawaida linamaanisha ‘mwongozo,’ uwe ni wa kipekee kwa Mitume ama wa jumla zaidi. Uwezo  wa  Fatima  (a.s.)  kupata  taarifa  za  kimbinguni  kwa  hiyo  haina maana  kwamba  yeye  alikuwa  ni  Mtume.  Ilikuwa  ni  dalili  ya  utakaso  na uthibitisho wa mapenzi makubwa ambayo Mtume Muhammad (s.a.w.w.) alikuwa  amemuonyesha  yeye.  Inathibitisha  kwamba  chochote  Mtukufu Mtume  (s.a.w.w.)  alichokisema  kumhusu  Fatima  kilikuwa  sahihi,  kwani yeye alisema: “Fatima ni sehemu ya mwili wangu. Kinachomuudhi yeye kinaniudhi na mimi pia.”

Sunnah: Baada ya Qur’ani Tukufu, chanzo muhimu kabisa kwa ajili ya kuuelewa Uislam  na  hivyo  itikadi  ya  Shi’ah  ni  Sunnah  ya  Mtukufu  Mtume Muhammad (s.a.w.w.), ikiwa ni pamoja na maneno yake, vitendo vyake na idhini yake ya kimya kimya juu ya kile kilichotendeka mbele yake. Qur’ani yenyewe inatoa hadhi ya hali ya juu kabisa kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwani  anarejelewa  kama  ambaye  ndiye  mwenye  wajibu  wa  kuielezea Qur’ani (16:44), na kuifundisha Qur’ani na hikma (62:2). Mtume ni kigezo bora kwa waumini (33:21). Yeye kamwe hazungumzi kwa matamanio yake (53:3). Waislam wanatakiwa kushikamana na lolote atakalowapa na kujiepusha na kile anachowakataza. (59:7). Utambuzi wa aya hizo hapo juu na nyingine nyingi zinazohusiana na hadhi ya  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.),  pamoja  na  maafikiano  ya  kuwa  kwake mjumbe aliyechaguliwa moja kwa moja na Mwenyezi Mungu mwenyewe na  kuongea  Naye,  kuliwachochea  Shi’ah,  pamoja  na  Waislamu  wengine juu  ya  mapenzi  ya  kweli  na  utii  kwa  Mtukufu  Mtume  Muhammad (s.a.w.w.).

35


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 36

U i s l a m u wa S h i a

Ukusanyaji wa Hadith: Katika wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): Kuanzia mwanzo kabisa Waislamu walianza kuandika hadith za Mwisho wa  Mitume  na  kuzisimulia  kwa  wale  ambao  hawakuwepo  wakati matamshi yalipofanywa. Ukusanyaji wa hadith za Kitume unaojulikana na Sahifah, ulifanywa na watu kama Abdullah bin Amr bin al-Aas, Samarah bin Jundab, Sa’d bin Ubadah na Jabir bin Abdullah al-Ansari. Kwa mujibu wa  hadith  inayofahamika  sana,  Abdullah  bin  Amr  bin  al-Aas  alikuwa akiandika kila alichokisikia kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), lakini baadae  alikatazwa  kufanya  hivyo  na  Maquraishi.  Wao  walihoji  kwamba Mtume  alikuwa  ni  binadamu  anayeongea  wakati  akiwa  na  hasira  na anapokuwa  na  furaha  (kwa  maana  ya  kwamba  kauli  zake  zinaweza kuathiriwa  na  hisia    na  sio  za  kunuia  kikamilifu).  Kwa  hiyo  Abdullah akaacha kuandika hadith mpaka alipoongea na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuhusu lile lililotokea. Ndipo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliponyoosha kidole kuelekea mdomoni kwake na akasema: “Wewe andika! Naapa kwa Yule ambaye maisha yangu yako  mkononi  Mwake  kwamba  hakuna  chochote  kuliko  ukweli  ambao kamwe  umetoka  nje  yake.”29 Imam Ahmad  anasimulia  kutoka  kwa Abu Huraira  kwamba  Mtukufu  Mtume  Muhammad  (s.a.w.w.)  aliwaambia masahaba zake waandike hadith yake kuhusu mtu anayeitwa Abu Shaat.30 29 Sunan ya al-Daarimii, Kitab al-Muqaddamah, mfululizo wa Sakhr nsmba 484486  na  Sunan Abu Dawuud,  Kitab  al-Ilm,  mfululizo  wa  Sakhr  namba  3161. Vyanzo  vingine  vimethibitisha  kwamba  yeye  aliandika  hadith  kadhaa.  Angalia kwa mfano, Sahih Bukhari, Kitab al-Ilm, mfululizo wa Sakhr namba 110, Musnad Ahmad, Baaqii Musnad al-Mukhtirin, mfululizo wa Sakhr namba 8863 na Sunan Tirmidhii, Kitab al-Ilm, mfululizo wa Sakhr namba 8863.  30 Hadith hii imesimuliwa vilevile ndani ya Sahih Bukhari, Kitab al-Ilm, mfululizo  wa  Sakhr  namba  109,  Kitab  al-Luqatah,  namba  2254  na  Kitab  al-Duyaat, namba 6372. 36


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 37

U i s l a m u wa S h i a Kisha  Imam  Ahmad  anamnukuu  Abu  Abd  al-Rahmaan  kuwahi  kusema kwamba hakuna hadith yenye nguvu kuliko hii ambayo imewahi kusimuliwa  kuonyesha  umuhimu  wa  kuandika  hadith,  kwa  vile  kuna  amri  ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe. Tukio hili linaonyesha kwamba baadhi ya watu walikuwa hawana furaha na uandishi au uwekaji kumbukumbu za hadith kwa sababu walishindwa kutambua  sawasawa  ile  hadhi  ya  Mtume  Muhammad  (s.a.w.w.).  Hata hivyo,  Waislamu  hawakusikiliza  maoni  yao  na  wakaendelea  kuziandika hadith.31

Wakati wa Khalifa wa Kwanza: Mwanachuoni  mashuhuri  wa  Sunni,  Dhahabi,  ndani  ya  kitabu  chake Tadhkirat al-Huffadh (Ukumbusho wa kumbukumbu), anasimulia kwamba Abu Bakr aliwakusanya watu na akasema: “Enyi watu! Enyi masahaba wa Mtukufu Mtume! Mnasimulia jambo kutoka kwa Mtukufu Mtume ingawa hamna  makubaliano  miongoni  mwenu.  Ni  bora  kwa  hiyo  msisimulie hadith  za  Mtume  tena,  na  kama  mtu  akiwaulizeni  kuhusu  maoni  ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuhusu baadhi ya mambo, kifupi jibuni kwamba tunacho Kitabu cha Allah nacho kinatutosha kabisa. Kinatosha chochote kile  kilichoruhusiwa  ndani  ya  Qur’ani    ni  halali,  na  chochote  kilichokatazwa  ndani  ya  Qur’ani  ni  haramu.  Msiendelee  zaidi  ya  hapo. Msiseme chochote kuhusu mawazo ya Mtukufu Mtume na hadithi zake.”32 31 Kuna makundi tofauti ya hadith katika vitabu vikuu vya hadith vya Sunni zinazoashiria  umuhimu  wa  kusimulia  hadith  kwa  wale  ambao  hawajui.  Kwa  kweli, huu ni mfano wa wazi wa wajibu mkubwa sana wa jumla wa Kiislam wa kueneza elimu na kuwafundisha wale ambao hawajui. Ukataaji wa umuhimu wa kuandika na  kusimulia  hadith  kunaongozea  kwenye  kuukataa  ukweli  na  umuhimu  wa Sunnah na muongozo wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwanza kabisa. 32 Tadhkirat al-Huffadh cha Dhahabi, Jz. 1, uk. 2-3. 37


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 38

U i s l a m u wa S h i a

Wakati wa Khalifa wa Tatu Katika  wakati  huu  maamuzi  makali  zaidi  yalichukuliwa  dhidi  ya  wale ambao  walitaka  kusimulia  hadith  za  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.).  Kwa mfano,  katika  simulizi  ya  kusisimua,  mmoja  wa  masahaba  wa  Mtume, Qaradhah bin Ka’b anasema kwamba Khalifa wa pili alituma kikundi cha Ansari  kwenda  al-Kufa  na  akamtaka  yeye  afuatane  nao.33 Khalifa mwenyewe aliwasindikiza kwa umbali wa mpaka sehemu nje ya Madina panapoitwa Sira’ na akawauliza: “Je, mnajua kwa nini nimewasindikiza na kufuatana  na  ninyi  kwa  umbali  huu?”  Qaradhah  anasema  kwamba  wao walijibu:  “Kwa  sababu  ulitaka  kuonyesha  heshima  yako  kwa  Ansari.” Khalifa  wa  pili  akalithibitisha  hilo,  lakini  akaongezea  kwamba  analo jambo  zaidi  la  kusema.  Yeye  akasema:  “Mnakwenda  kwa  watu  ambao ndimi zao zinacheza na (usomaji wa) Qur’ani kama miti ya mitende inavyoyumba  na  upepo.  Mtakapofika  huko  watu  watasema:  ‘Masahaba  wa Muhammad  wamekuja.  Masahaba  wa  Muhammad  wamekuja.’ Watakuombeni  msimulie  hadith.  Jihadharini,  msiwakwaze  na  hadith  za Mtume  na  mimi  ni  mshirika  wenu.’”  Hivyo  Khalifa  wa  pili  aliwataka wasisimulie  hadith,  akasema  kwamba  atawaunga  mkono  katika  hili  na akathibitisha kwamba amejitwalia sera hiyo hiyo yeye mwenyewe. Kama alivyotabiri Khalifa wa pili, wakati ujumbe huo ulipofika Kufa, watu waliwaomba  kuwasimulia  hadith  za  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.),  kwa sababu wao, kama Waislamu wengine, walikuwa na mapenzi ya dhati kwa Mtukufu Mtume na walitaka kujua na kusikia chochote kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.). Walitaka kunufaika na mfano wa Mtukufu Mtume na maelezo yake  ya  Qur’ani.  Hata  hivyo,  Qaradhah  anasema:  “Mimi  sikusimulia hadith yoyote.”34 33 Ansari ni jina la Waislam walioishi katika mji wa Yathrib – baadae Madina – kabla  ya  Uislamu  na  wakamkaribisha  Mtume,  na  wale  waliohamia  baada  yake kutoka Makka wao waliitwa Muhajirina. 34 Sunan al-Darimii, Kitab al-Muqaddamah, mfululizo wa Sakhr namba 281 na 282, na Sunan Ibn Majah, Kitab al-Muqaddimah, mfululizo wa Sakhr namba 28. 38


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 39

U i s l a m u wa S h i a Al-Darimii anasimulia ndani ya Sunan yake kutoka kwa Sha’bii kwamba yeye  alifuatana  na  Abdullah  bin  Umar  (mtoto  wa  Khalifa  wa  pili)  kwa muda  wa  mwaka  mzima  na  hakusikia  hadith  yoyote  ya  Mtukufu  Mtume (s.a.w.w.)  kutoka  kwake.35 Al-Darimii  vilevile  anasimulia  kwamba  hili liliendelea kwa muda mrefu, yaani, kwa muda wa miaka miwili na nusu, na  kwamba  alisikia  hadith  moja  tu  kutoka  kwa  Abdullah.36 Anasimulia vilevile kutoka kwa Sa’d bin Yazid kwamba alikuwa pamoja na Sa’d bin Abi Waqqas katika safari yake kwenda Makka, katika kukaa kwake Makka na katika safari yake ya kurejea Madina, lakini hakusikia hadith yoyote ya Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.)  kutoka  kwake.  Bado  matukio  mengine  ya kusisimua  yalitokea  wakati  huo.  Kwa  mfano,  Dhahabi  anasimulia  katika Tadhkirat al-Huffaaz kwamba  masahaba  wakubwa  watatu  wa  Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) walifungwa jela kwa kosa la kusimulia hadith za Mtume. Mmoja  wao  alikuwa  ni  Ibn  Mas’ud,  mwandishi  wa  Mtukufu  Mtume (s.a.w.w.) mashuhuri anayefahamika sana na msomaji wa Qur’ani, ambaye alisilimu mapema sana na kuteswa sana na wapagani wa Quraishi.

Katika Wakati wa Khalifa wa Tatu: Uzuiaji wa hadith ulibakia na nguvu. La kufurahisha zaidi, khalifa wa tatu, Uthman bin Affan wakati mwingine alihoji juu ya umuhimu wa kuzizuia hadith za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa kurejea kwenye Sunna na mwenendo wa makhalifa wawili wa mwanzo. Kwa mfano, alikuwa mara kwa mara akisema kwamba hakuna mtu yoyote aliyeruhusiwa kusimulia hadith ambayo  haikuwahi  kusimuliwa  wakati  wa Abu  Bakr  au  Umar.  Kwa  vile tunajua kwamba hakuna aliyeruhusiwa kusimulia hadith wakati wa Khalifa wa kwanza na wa pili, basi hili lilitumika na wakati wake pia. 35 Sunan al-Darimii, Kitab al-Muqaddamah, mfululizo wa Sakhr 275 na Sunan Ibn Majah, Kitab al-Muqaddimah, mfululizo wa Sakhr namba 26. 36 Sunan al-Darimii, Kitab al-Muqaddamah, mfululizo wa Sakhr 274. Ni lazima ifahamike  kwamba  Abdallah  bin  Umar  hakuwa  akishikilia  kujizuia  kusimulia hadith,  kwani  kuna  hadith  zilizosimuliwa  kutoka  kwake.  Angalia  kwa  mfano Musnad Ahmad, mfululizo wa Sakhr namba 6225, 6302, 6304, na 6594.  39


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 40

U i s l a m u wa S h i a Kulikuwa  na  sababu  gani  ya  kujaribu  kuzuia  kuandikwa  na  kusimuliwa kwa hadith za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)? Maelezo yaliyokuwa yakitolewa  kwa  kawaida  yalikuwa  kwamba  kama  watu  wangeruhusiwa  kuzitaja hadith za Mtume kungeweza kuwaondoa kwenye kuzingatia Qur’ani.37

37 Inapasa  kufahamika  kwamba  hili  mwishowe  huongozea  kwenye  mawazo kwamba Qur’ani inatosha  na hakuna haja ya hadith. Licha ya ajabu hii, wazo hili limekuwa mara kwa mara likielezwa na baadhi ya watu. Kwa mfano Bukhari na wengineo wamesimulia kwamba Mtume Muhammad (s.a.w.w.) kabla ya kufariki kwake  aliwataka  watu  waliokuwa  karibu  yake  kumletea  karatasi  ili  kuandika jambo  ili  kwamba  wasije  wakapotea.  Wakati  ule,  Umar  bin  Khattab  alisema: “Mtume amezidiwa na maradhi (katika maandishi mengine, ‘mtu huyu anaweweseka’) na sisi tunacho Kitabu cha Allah ambacho kinatutosha.” Wale waliokuwa pale walianza kuzozana na hivyo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Ondokeni hapa!  msifanye  ugomvi  mbele  yangu.”  Bukhari  anaongeza  kwamba  Ibn Abbas alisema  kwamba  msiba  mkubwa  ulitokea  pale  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.) alipozuiwa  kuandika.  (angalia  kwa  mfano,  Sahih Bukhari,  Kitaab  al-Jihad, Mfululizo  wa  Sakhr  namba  2825,  Kitab  al-Jizyah,  mfululizo  wa  Sakhr  namba 2932, Kitab Maghaazii namba 4078 na 4079, Kitab al-Mardhaa namba 5237, na Kitab al-I’tisaam bi al-Kitaab wa al-Sunnah namba 6818; Sahih Muslim, Kitab alWasiiyah,  Int.  mfululizo  namba  3089-3091  na  Musnad Ahmad, Musnad Banii Haashim, mfululizo wa Sakhr namba 1834, 2835, 2945, na 3165). 40


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 41

U i s l a m u wa S h i a Kama wangeruhusiwa kuwa na vitu viwili sambamba, Qur’ani na Sunnah, wangeweza  kutoa  uzingatiaji  mdogo  kwenye  Qur’ani  na  wangeweza kuisahau, na hili badala yake lingeweza kuifanya Qur’ani ipatwe na upunguzwaji na ubadilishwaji.38 38 Sababu  nyingine  inayotolewa  na  wale  ambao  hawakusimulia  hadith  ama waliosimulia kiasi kidogo tu cha hadith ni kwamba walikuwa wakiogopa kusimulia hadith za uongo. Kwa mfano, Uthma bin Affan, (Musnad Ahmad, Musnad al‘Asharah al-Mubashsharin bi al-Jannah, Sakhr mfululizo namba 439). Zubayr bin Awwam (Sahih Bukhari, Kitaab al-Ilm, mfululizo wa Sakhr namba 104 na Musnad Ahmad,  Musnad al-Asharah al-Mubashsharin bi Jannah,  mfululizo  wa  Sakhr namba 1339 na 1353), na Anas bin Malik, (Bukhari, ibid namba 105 na Musnad Ahmad, Baaqi Musnad al-Mukthirin, mfululiza wa Sakhr namba 12303) wamesema kwamba wao hawakusimulia hadith kwa sababu walikuwa wamesikia kutoka kwa  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.):  “Yeyote  ambaye  kwa  makusudi,  atahusisha jambo lolote na mimi ambalo sikulisema ataingizwa Jahannam.” Inaelekea kwamba  riwaya  hizi,  pamoja  na  ushahidi  mwingine  zinaonyesha  kwamba  majaribio kiasi  cha  kutosha  yalifanyika  katika  kubuni  hadith  na  kuzihusisha  kwa  Mtume (s.a.w.w.). Hadith hizi za bandia zilienea hata miongoni mwa Waislam, na Mtume pamoja na masahaba zake watiifu waliingiwa na wasiwasi. Hata hivyo, hii haina maana kwamba mtu asije akasimulia zile hadith sahihi ambazo amezisikia kutoka kwa  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.)  au  amezipokea  kutoka  kwenye  vyanzo vinavyoaminika. Bali inaonyesha umuhimu wa kuwa muangalifu katika kusimulia hadith na katika kuzikubali hadith kutoka kwa wale wanaozisimulia.. Ndani ya Musnad yake, Imam Ahmad bin Hanbal anasimulia kwamba Imam Ali (a.s.) amesema:  “Ninapowasimulia  hadith  kutoka  kwa  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.)  ni  bora machoni  pangu  kuanguka  kutoka  mbinguni  hadi  juu  ya  ardhi  kuliko  kuhusisha kwa  Mtukufu  Mtume  jambo  ambalo  hakulisema.”  (Musnad al-Asharah alMubashsharin bi al-Jannah, mfululizo wa Sakhr namba 1072). Hii ndio sababu Nyumba ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na wafuasi wao hawakuacha kusimulia na kuandika  hadith  za  kweli  na  sahihi,  hata  hivyo  walikuwa  waangalifu  sana  na wenye  tahadhari  ya  hali  ya  juu  katika  kusimulia  kwao.  (Rejea  kwenye  mjadala kuhusu utaratibu wa Shi’ah katika uchunguzi wa hadith.) 41


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 42

U i s l a m u wa S h i a Hata hivyo, hakukuwa na sababu ya kuwa na wasiwasi kwa ajili ya uhifadhi wa Qur’ani kwa wakati ule, kwa sababu katika wakati wa uhai wa Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.)  walikuwepo  tayari  watu  wengi  waliokuwa wamehifadhi Qur’ani na idadi kubwa ya nakala zilizokwisha kuandikwa za Qur’ani  ilikuwa  imekwisha  kutengenezwa.  Tunajua  kwamba  Mtukufu Mtume  (s.a.w.w.)  mwenyewe  alitoa  maelekezo  kwa  Waislamu  kuhusu mpangilio wa aya na sura za Qur’ani. Tunajua vile vile kwamba Waarabu wakati ule walikuwa na kumbukumbu zenye nguvu sana, hivyo hapakuwa na sababu ya kuwa na wasiwasi kwamba Qur’ani inaweza kusahauliwa au kubadilishwa.  Ilikuwa  vilevile  hakuna  maana  ya  kudhani  kwamba Waislam  walikuwa  wazembe  sana  au  dhaifu  sana  kiasi  kwamba hawakuweza kuishughulikia Qur’ani na vilevile hadith za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)  kwa  wakati  huo  huo.  Ni  jambo  lisilowazika  kwamba  ummah kama  huo,  wenye  kuorodhesha  watu  mashuhuri  ambao  wengi  miongoni mwao walikuwa na vipaji vya kujaaliwa na Mwenyezi Mungu vya kuhifadhi,  kwamba  usingeweza  kushughulika  na  hazina  mbili  kwa  wakati mmoja. Kwa  hali  yoyote,  kwa  mujibu  wa  wasimulizi  wa  Shi’ah  na  baadae  wa Sunni (pamoja na makhalifa wa baadae, kuanzia Umar bin Abdul-Aziz na kuendelea),  wazo  hili  lilikuwa  halikubaliani  na  maelekezo  ya  wazi  ya Qur’ani  kufuata  mfano  wa  mwenendo  wa  Kiislamu  ambao  Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliuwasilisha katika Sunnah yake. Haiwezekani kudhania  kwamba  mwanzilishi  wa  shule  ya  fikra  aweze  kuwasilisha  mawazo yake lakini baada ya kifo chake au hata mapema kabla, watu waambiwe kuwa  wapuuze  kile  alichokisema  au  kukifanya  na  wasikisimulie  wala kukiandika. Je, watu wangetegemewa kwa suala kama hilo waweze kuelewa mafundisho ya shule hiyo, hasa kwa vile ilikuwa ni matokeo ya wahyi na watu walikuwa hawana njia ya haraka na ya moja kwa moja ya kufikia kwenye  chanzo  chake?  Ingewezekana  vipi  kuwataka  watu  waelewe Qur’ani  wakati  wakitelekeza  mafundisho  ya  yule  mtu  ambaye  Qur’ani hiyo ilishushwa kwake, na ambaye, kwa mujibu wa hiyo Qur’ani yenyewe yeye amepewa wajibu wa kufundisha na kuielezea Qur’ani? 42


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 43

U i s l a m u wa S h i a Katika kila tukio vile vile kuna maelekezo ya wazi yaliyosimuliwa na wote wanachuoni wa Shi’ah na Sunni, kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe juu ya umuhimu wa kutangaza hadith zake kwa wengine. Kwa mfano, katika mwaka wake wa mwisho wa maisha yake yaliyobarikiwa, na akiwa  anarejea  kutoka  Makka  katika  Hijja  yake  ya  mwisho  “HijjatulWidaa” katika kauli maarufu na ya kihistoria, Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Mwenyezi  Mungu  awape  furaha  wale  wanaosikiliza  hotuba  yangu, wakaielewa na kisha wakaitangaza kwa wale ambao hawakuisikia.” Kuna watu  wengi  wanaotangaza  elimu  hiyo  ingawa  wao  wenyewe  wanaweza wakawa  hawana  elimu,  na  kadhalika,  kuna  watu  wengi  wanaoweza kutangaza  elimu  kwa  wale  ambao  wanayo  elimu  kuliko  wao  wenyewe. Katika  riwaya  nyingi  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.)  amewaombea  wale ambao wanasikiliza hadith zake na kuzisimulia kwa wengine. Kwa mfano, Bukhari ndani ya Sahih yake anasimulia kwamba Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Yule aliyepo anapaswa kusimulia kwa yule ambaye hayupo, kwa sababu kunaweza kukawa na baadhi ya watu miongoni mwa wale ambao hawapo wanaoweza wakaelewa vizuri zaidi kuliko wale waliopo.”39 Naam, masahaba wengi wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na pia wasimulizi wakubwa wote wa hadith, kama vile Imam Ahmad bin Hanbal, Muslim na Bukhari ambao walikuja baadae na kukusanya hadith za Mtume (s.a.w.w.) na  hata  maneno  ya  masahaba  wake  na  wale  waliowafuatia  (al-Tabi’un), walihisi wajibu kwa ajili ya kuziandika hadith na kuziweka kwenye utumiaji wa wengine. Hii ilikuwa moja ya njia ambazo kwazo utamaduni wa Kiislam  ungeweza  kuenea  na  kuenea  zaidi.  Mafundisho  ya  Mtukufu 39 Kwa mfano, tazama Sahih Bukhari, kitab al-‘Ilm, mfululiza wa Sakhr namba 65,  Kitab  al-Hajj,  Sakhr  namba  1625,  Kitab  al-Maghazii,  Sakhr  namba  4054, Kitab al-Udhi, Sakhr namba 5124, Kitab al-Tawhiid, Sakhr namba 6893 na Kitab al-Fitan, namba 6551; Sahih Muslim, Kitab al-Qusaamah namba 3179; Sunan ibn Majah, Kitab al-Muqaddamah, namba 229; Musnad Ahmad; Musnad al-Basriyiin, namba 19594, 19512 na 19492 na Sunan al-Darimii, Kitab al-Manaasik, namba 1836.  43


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 44

U i s l a m u wa S h i a Mtume  (s.a.w.w.)  yalikuwa  yanahitajika,  sio  kwa  wale  tu  walikuwa  na fursa  ya  moja  kwa  moja  ya  kumfikia  yeye  (s.a.w.w.)  na  wakaweza  kujifunza  hadith  hizo  kutoka  kwake,  bali  pia  na  wale  wote  ambao  walikuja baada yao. Inastahili  kutajwa  hapa  kwamba  kutoka  mwanzo  kabisa  Shi’ah  walitoa umakini wa hali ya juu kwenye Sunnah ya Mtukufu Mtume na walikuwa wamedhamiria  kuandika  hadith  zake,  kama  sharti  kwa  ajili  ya  utendaji sahihi  na  ufikishaji  wa  ujumbe  wake,  ingawaje  baadhi  yao  walipoteza maisha yao katika kufanya hivyo na wengine walifungwa.

Sunnah na Nyumba ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): Tunageukia sasa kwenye wajibu wa Nyumba ya Mtume (s.a.w.w.) katika kuuwasilisha  Uislamu.  Hili  litahusisha  mada  mbili:  uhalali  wa  kuiona Nyumba ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kama chanzo cha kutegemewa katika kuuelewa Uislamu, na umuhimu wa kushikamana na mafundisho yao katika kuuelewa Uislam. Kuhusiana  na  mada  ile  ya  kwanza,  hakuna  kutokukubaliana  miongoni mwa  Waislam  kuhusu  uhalali  wa  kufuata  mafundisho  ya  Nyumba  ya Mtume  (s.a.w.w.)  katika  kuuelewa  Uislamu.  Hii  inajumuisha  pamoja  na Sunni, ambao wanawaona masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kama vyanzo vya kutegemewa kwa ajili ya kuuelewa Uislam.40 40 Waislam wa Sunni wanaamini kwamba yeyote aliyekutana na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hata kwa kipindi kimoja tu akiwa anamuamini anachukuliwa kama ni Sahaba wa Mtume na anaweza kutegemewa katika kupata elimu kuhusu Uislamu. Kwa sababu hiyo, watu wa Nyumba ya Mtukufu Mtume kama vile Imam Ali (a.s.) na Fatimah (s.a.) ambao wakati wote wamekuwa na Mtume na walikuwa na uhusiano wa karibu zaidi kwa Mtume (s.a.w.w.) bila shaka walikuwa ni vyanzo vya kuaminika. 44


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 45

U i s l a m u wa S h i a Uhalali wa kufuata mafundisho ya Nyumba ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) unakuwa wazi zaidi pale tunaporejea kwenye hadith kutoka kwa Mtukufu Mtume  (s.a.w.w.)  kuhusu  Nyumba  yake,  na  kuziangalia  riwaya  za wanachuoni wa Sunni kuhusu elimu ya Imam Ali (a.s.) na watu wengine wa  Nyumba  ya  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.).  Kwa  mfano,  Abu  Hanifah anasema:  “Kama  isingekuwa  kwa  ile  miaka  miwili,  kwa  hakika  mimi ningeangamia.”  Ile  “Miaka  miwili”  ilikuwa  ni  kile  kipindi  alichokitumia kusoma  kwa  Imam  Ja’far  as-Sadiq  (a.s.),  Imam  wa  sita,  na  kuhudhuria mihadhara  yake.41 Imam  Malik  anasema:  “Hakuna  macho  yaliyowahi kuona, hakuna masikio yaliyowahi kusikia na hakuna chochote kilichokuja  kwenye  moyo  wa  mwanadamu  yoyote,  bora  kuliko  Imam  Ja’far  asSadiq katika elimu yake, katika uchamungu wake, katika kujinyima kwake na katika utumwa wake kwa Mwenyezi Mungu.” Hivi ndivyo anavyosimulia  Ibn  Taymiyah  kutoka  kwa  Imam  Malik.42 Hakuna  utata  katika  kauli hizi,  ndio  sababu  wanachuoni  wa  Sunni  wameeleza  wazi  wazi  kwamba kila  Muislam  anaruhusiwa  kutenda  kwa  mujibu  wa  moja  ya  madhehebu hizi tano za kifiqhi: Ja’fariyah, Hanafia, Hanbali, Maliki, na Shafi’i. Sababu  ya  hili  iko  wazi:  hata  kama  Imam  Ja’far  as-Sadiq  ama  watu wengine  wa  Nyumba  ya  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.)  hawakuwa  na  elimu zaidi au njia bora ya kuifikia elimu ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuliko wengine,  mtu  anapaswa  kukubali  kwamba  lazima  iwe  alikuwa  angalau sawa  na  wengine,  hususan  kama  anasemekana  kuwahi  kuwafundisha. Watu ambao wameelimika au ambao wanaitafuta haki wanategemewa kwa hiyo  kuchunguza  vyanzo  vyote  vya  Kiislam  vilivyopo,  na  hivyo  kufikia uamuzi  kuhusu  njia  ambazo Waislamu  wanaweza  kuishi  maisha  ya  kimfano. Kwa hakika chanzo kimoja cha fahari ni mafundisho ya Nyumba ya 41 Katika ukaguzi kuhusu wale watu wanaosimulia kutoka kwa Imam Sadiq (a.s.), Sheikh  al-Mufid  (kafariki  mwaka  148  A.H.)  anathibitisha  kwamba  wale waliokuwa  ni  waaminifu    miongoni  mwao  kutoka  kwenye  madhehebu  tofauti wamefikia idadi ya watu 4,000 (al-Irshaad)  42 Al-Tawassul wa al-Wasilah, uk. 52, toleo la kwanza. 45


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 46

U i s l a m u wa S h i a Mtume  (s.a.w.w.).  Kihistoria  hata  hivyo,  kwa  sababu  moja  au  nyingine, pengine kwa sababu ya namna fulani ya shinikizo, sio wanachuoni wote waliowasilisha  kikamilifu  riwaya  za  Nyumba  ya  Mtukufu  Mtume (s.a.w.w.).  Hivyo  ni  dhahiri  kabisa  kwamba  yeyote  anayejaribu  kuelewa Uislam  na  Sunnah  ya  Mtume  (s.a.w.w.)  anaweza  akarejea  kwenye mafundisho ya Nyumba yake. Sasa  hebu  tuone  iwapo  kama  ni  lazima  kurejea  kwenye  Nyumba  ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ili kuuelewa Uislamu au kama ni suala la hiari tu. Katika kulijibu swali hili tutalenga kwenye hadith kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) zilizosimuliwa na wanahadith wakubwa wa Sunni na kukubaliwa na wanachuoni wote wa Sunni na Shi’ah. Kwanza ni lazima ifahamike hata  hivyo  kwamba  mafundisho  yote  ya  Nyumba  ya  Mtume  (s.a.w.w.) yalikuwa yameegemea kwenye Qur’ani Tukufu na Sunnah ya Mtume. Mtu yoyote asidhani kwamba, kwa mfano, Imam Ja’far as-Sadiq (a.s.) alisema jambo  lolote  kuhusiana  na  Uislamu  lililotegemea  kwenye  maoni  yake binafsi. Chochote kile ambacho yeye na Maimam wengine walichokisema kilikuwa hasahasa ni kile ambacho wao walikipokea kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Kuna hadith nyingi sana kuhusiana na hili. Kwa mfano, ndani ya al-Kaafi tunakuta kwamba Imam Sadiq (a.s.) alitangaza kwamba chochote alichokisema ni kile alichokipokea kupitia mababu zake kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Hii ni nukta muhimu sana: riwaya zote za Maimam (a.s.) zilipokelewa moja kwa moja kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).  Moja ya hadith inayoashiria huo umuhimu wa kuwafuata watu wa Nyumba ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ni ile hadith maarufu ya Thaqalayn. Hadith hii  ilitamkwa  na  Mtukufu  Mtume  katika  nyakati  na  sehemu  mbalimbali, kujumuisha  na  siku  ya  Arafah  katika  Hijja  yake  ya  mwisho  na  mnamo mwezi  18  ya  Dhil-Hijjah  mahali  panapoitwa  Ghadiir  Khumm.  Licha  ya tofauti ndogo ndogo katika maneno, maudhui ni yale yale katika matoleo yote  ya  hadith  hii.  Kwa  mfano,  katika  toleo  moja  Mtume  anasimuliwa kuwahi kusema: 46


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 47

U i s l a m u wa S h i a “Enyi watu! ninaacha miongoni mwenu vyenye thamani viwili: Kitabu cha Allah  na  watu  wa  Nyumbani  kwangu.  Mtakaposhikamana  navyo  hivyo hamtapotea kamwe.”  Au  katika  maelezo  mengine  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.)  anasimuliwa kuwahi kusema: “Ninaacha miongoni mwenu vitu viwili vyenye thamani, kama mkishikamana  navyo  hivyo,  hamtapotea  baada  yangu:  Kitabu  cha  Mwenyezi Mungu, ambacho ni kama kamba iliyonyooshwa kati ya mbingu na ardhi, na watu wa Nyumbani kwangu, Ahlul-Bayt. Vitu viwili hivi havitatengana mpaka  vinifikie  mimi  karibu  na  hodhi  Siku  ya  Kiyama.  Tahadharini  na kuweni waangalifu jinsi mtakavyovichukulia vitu hivi baada yangu.” Hili linaonyesha kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa na wasiwasi kuhusu namna ambavyo Waislam, au angalau baadhi yao, watakavyo itendea Qur’ani na Nyumba yake. Katika hadith nyingine yeye amesema: “Nawaachieni  makhalifa  wawili:  moja  ni  Kitabu  cha  Mwenyezi  Mungu, ambacho ni kama kamba iliyonyooka kati ya mbingu na ardhi, na pili ni watu wa nyumba yangu, Ahlul-Bayt. Hawatatengana mmoja kutokana na mwingine mpaka vije kwangu karibu na hodhi ya Kawthar.” Hadith hizo hapo juu zinaweza kupatikana katika vyanzo vikuu vya Sunni, kama vile Sahih Muslim Jz. 8, uk. 25, hadith ya 2408; Musnad Ahmad, Jz. 3,  uk.  388,  hadith  ya  10720;  Sunan Daarimii,  Jz.  2,  uk.  432;  na  Sahih Tirmidhii, Jz. 5, uk. 6432, hadith ya 3788. Zimesimuliwa vile vile ndani ya vitabu  kama  Usd al-Ghaabah ya  Ibn  al-Athiir,  Jz.  2,  uk.  13;    Sunan alKubraa cha Bayhaqii, Jz. 2, uk. 198; na Muttaqi al-Hindi katika Kanz alUmmal, Jz. 1, uk. 44. Maana  ya  hadith  iko  wazi  kabisa  kwamba  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.) ameacha  miongoni  mwa  Waislam  vizito  viwili:  Qur’ani  na  watu  wa 47


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 48

U i s l a m u wa S h i a Nyumbani  kwake,  na  kwamba  alimuradi  tu  watu  wakishikamana  navyo vyote, hawatapotea. Hii inaonyesha kwamba vitu viwili hivi lazima wakati wote  viwe  vyenye  kuona  na  kwamba  kamwe  visipingane.  Vinginevyo, Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.)  asingewapa  watu  maagizo  hayo  ya  kuvifuata vyote;  wataweza  kukanganyikiwa  kama  Nyumba  ya  Mtume  (s.a.w.w.) ingekuwa  iwaambie  waende  kuelekea  upande  mmoja  na  Kitabu  cha Mwenyezi Mungu kiwaambie waelekee upande mwingine tofauti. Ingawa hili  limedokezwa  mwanzoni  kabisa  mwa  hadith  hiyo,  Mtukufu  Mtume (s.a.w.w.)  mwenyewe  alilifanya  hilo  kuwa  wazi  kabisa  kwa  kuhitimisha hivi, “Havitatengana mpaka vinifikie mimi karibu na birika la Kawthar.” Hivyo hadith hii katika matoleo yake yote inaashiria kwamba: Tangu  wakati  wa  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.)  hadi  mwisho  wa  dunia, Kitabu  cha Allah  na  watu  wa  Nyumba  ya  Mtume  wakati  wote  vitakuwa pamoja.  Hakuna  anayeweza  kusema  kwamba  Kitabu  cha  Mwenyezi Mungu kinatutosha na kwamba hatuwahitaji watu wa nyumba ya Mtume, au kinyume chake kwani Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema wazi kabisa: “Ninaacha  vitu  viwili  vyenye  thamani  ambavyo  lazima  muvikamate  na kama mkifanya hivyo basi hamtapotoshwa.” Watu wa Nyumba ya Mtume (s.a.w.w.) kamwe hawafanyi makosa na wakati wote ni wakweli. Kama  vile  tu  kwa  Qur’ani,  Nyumba  ya  Mtume  (s.a.w.w.)  itafaidi  namna fulani  ya  muendelezo  hadi  Siku  ya  Kiyama  wakati  watakapojiunga  na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) karibu na hodhi ya Kawthar. Hivyo kizazi cha Mtume hakitatoweka, hata angalau kwa kipindi kifupi cha wakati. Hadith nyingine inajulikana kama hadith ya Safinah (Jahazi). Wanachuoni wa hadith wa Sunni na Shi’ah kadhalika wamesimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Tambueni  kwamba  mfano  wa  kizazi  changu  (ahlul-Bayt)  miongoni mwenu  ni  kama  safina  ya  Nuh  (a.s.).  Yeyote  aliyepanda  safina  ya  Nuh aliokolewa na yeyote aliyekataa kufanya hivyo alikufa maji.” 48


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 49

U i s l a m u wa S h i a Katika  hadith  nyingine,  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.)  anaongeza  kitu kingine. Baada ya kulinganisha kizazi chake na safina ya Nuh, yeye anakifananisha kizazi hicho na Lango la Hittah kwa ajili ya makabila ya Bani Israili, “ambao yeyote aliyeingia humo alisamehewa” (rejea Qur’ani 2:58). Hii ina maana basi kwamba yeyote anayeingia kwenye elimu  na ushauri wa  kizazi  chake,  na  akawa  ni  muungwana  na  mnyenyekevu  kwao,  yeye atasamehewa  na  Mwenyezi  Mungu  na  kuongozwa.  Ibn  Hajar, mwanachuoni  mkubwa  wa  Sunni  anazingatia  maoni  kwamba  sababu  ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuilinganisha familia yake na safina ya Nuh ni kwamba  yeyote  anayekipenda  na  kukiheshimu  kizazi  cha  Mtume  na akashikamana  na  muongozo  wa  watu  wa  nyumba  ya  Mtume  (s.a.w.w.) wenye elimu wataokolewa kutokana na giza la migongano na kutoelewana, wakati  ambapo  wale  wanaokataa  kuwa  pamoja  na  kizazi  cha  Mtume (s.a.w.w.)  watazama  katika  bahari  ya  kukosa  shukurani  juu  ya  neema  za kimungu na wataangamia. Kisha anaendelea kuelezea ni kwa nini Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwalinganisha kizazi chake na Bab al-Hittah. Ibn Hajar anasema  kwamba  kwa  mujibu  wa  Qur’ani,  yeyote  anayeingia  kwenye mlango huu, Bab al-Hittah (ambao unaweza ukawa ni ule mlango ama wa Jericho  au  Jerusalem  –  Bayt al-Maqdis –  kwa  unyenyekevu  na  pia  akamuomba Mwenyezi Mungu msamaha basi ataupata. Anamalizia kwamba kwa vile kuingia kupitia mlango huu kulipekea kupata maghfira kwa makabila  ya  Bani  Israili,  kufuatia  mafundisho  na  ushauri  wa  Kizazi  cha Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.)  kutapelekea  kupata  msamaha  kwa  ajili  ya Ummah wa Kiislamu.43 Katika  hadith  nyingine  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.)  alikilinganisha  kizazi chake kitukufu na nyota za angani ambazo zinawasaidia wasafiri kujua njia zao: “Nyota  zinawaokoa  watu  kutokana  na  kuzama  majini,  na  Kizazi  changu kinawaokoa  watu  kutokana  na  kutoelewana  na  migogoro.  Kama  kundi 43 Ibn Hajar, as-Sawa’iq al-Muhriqah, Mlango wa 11, uk. 91 49


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 50

U i s l a m u wa S h i a moja la Waarabu lisipokubaliana na kizazi changu watapatwa na kutoelewana  miongoni  mwao,  watapoteza  umoja  wao  na  kuwa  kundi  la Shetani.”44 Hadith  ya  Safinah  katika  matoleo  yake  mbalimbali  kwa  hiyo,  huwa  inasisitiza umuhimu ule ule wa Kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kama hiyo hadith ilivyoeleza hivi punde. Inaweza kupatikana katika vitabu mbalimbali vya Sunni kama vile Mustadrak al-Hakiim Nishabuurii, Jz. 3, uk. 149 na 151, Arba’in Hadith cha Nawbahaani na al-Sawa’iq al-Muhriqah cha Ibn Hajar. Kwa  mujibu  wa  hadith  hizi,  kufuata  mwongozo  wa  Kizazi  cha  Mtume (s.a.w.w.) ni kwa umuhimu wa hali ya juu sana; wale wanaokataa kufanya hivyo  watakuwa  hawawezi  kupata  mwelekeo  sahihi  na  watazama  katika bahari ya ujinga, migogoro na mifarakano. Kwa hiyo tunamalizia kwamba kuna sababu ya kutosha kukimbilia kuwafuata watu wa Nyumba ya Mtume (s.a.w.w.) katika kuelewa alichokimaanisha na kukieleza Mtukufu Mtume na kwamba kwa kweli ni muhimu sana kufanya hivyo. Angalizo: Hii  Hadith  ya  Thaqalayn  imetajwa  katika  vyanzo  vya  wote Sunni na Shi’ah na kwa hiyo inakubaliwa na Waislamu. Hata hivyo taarifa moja  ya  hadithi  hii,  Mtume  (s.a.w.w.)  ananukuliwa  akisema  “Sunnah yangu”  badala  ya  “watu  wa  nyumbani  kwangu.”  Ingawa  maelezo  haya yanaweza kupatikana tu katika baadhi ya vitabu vya Sunni, hakuna ugumu katika  kuelewa  hadith  hii  inamaanisha  nini,  kama  ukichukulia  maelezo haya kuwa ni sahihi. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika hadith nyingi zilizosimuliwa  na  Waislamu  wote  amesema:  “Ninawaachieni  vitu  viwili vyenye thamani, na hivyo ni Qur’ani Tukufu na watu wa nyumbani kwangu,”  ambapo  katika  riwaya  chache  zilizosimuliwa  na  kundi  moja  tu  la Waislamu anasimuliwa kuwa alisema: “Qur’ani tukufu na Sunnah yangu.” 44 Kwa  sababu  wakati  wanapogombana  kwa  kawaida  wanataka  kushindana  na wanasahau radhi ya Allah, na matokeo yake ni kwamba wanaishia katika kumfuata shetani. 50


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 51

U i s l a m u wa S h i a Bila  shaka  hitimisho  la  kuchukuliwa  hapa  ni  kwamba  kwa  vile  upande mmoja wa Ulinganisho ni ule ule, yaani Qur’ani tukufu, basi na ule upande mwingine pia ni lazima ufanane. Kwa hiyo, “Sunnah yangu” na “watu wa nyumbani kwangu” lazima vifanane, kwani vinginevyo mtu ataweza kusema kwamba Mtume alijipinga mwenyewe. Kurejea kwenye mafundisho na ushauri wa Kizazi cha Mtume (s.a.w.w.) kwa hiyo kunafanana na kurejea kwenye Sunnah ya Mtume. Njia pekee ya kuweza kupata kuifikia Sunnah ya Mtume (s.a.w.w.) na kuielewa kwa uhakika wake ni kurejea kwa wale ambao walikuwa na uhusiano wa karibu sana naye na waliojua vizuri zaidi kuliko  mtu  yoyote  mwingine  kile  alichosema  na  kukitenda  au  alichokithibitisha.

Ni nani wanaunda Nyumba ya Mtukufu Mtume (AhlulBayt)? Swali  jingine  linahusu  ile  maana  hasa  ya  “Nyumba  ya  Mtume.”  Katika hadith  nyingi  zinazotuagiza  kushikamana  na  Nyumba  ya  Mtume,  wao wanarejelewa kwa jina la Ahlul-Bayt au al-Itrah. Maneno haya yanatumika juu ya nini na ni watu gani wamezungukwa na nafasi hiyo ya Watu wa Nyumba ya Mtume? Je, inajumuisha yeyote na ndugu wote wa Mtukufu Mtume? Hoja tatu tofauti zitatolewa katika kujibu maswali haya, ingawa kila hoja inaweza kuonekana yenye kujithibitisha yenyewe. Kama mambo yalivyo hakuna shaka miongoni mwa Waislamu kwamba Fatima, binti ya Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.),  Imam  Ali,  na  watoto  wao  Imam  Hasan  na Imam Husein walitokana na Nyumba ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Swali pekee  ni  iwapo  ndugu  wengine  wa  Mtukufu  Mtume  wanaweza  kujumuishwa katika kundi hilo au hapana, na kama ni hivyo, je ni kwa kiasi gani. Baadhi ya Waislamu wa Sunni wanaamini kwamba ndugu wote wa Mtume wanapaswa kujumuishwa, ukiwaondoa, kama inavyotarajiwa, wale ambao hawakuukubali Uislamu, kama vile Abu Lahab, ami yake Mtume ambaye wakati huo huo alikuwa mmoja wa maadui zake wakubwa na kwa sababu  hiyo  alikuwa  amelaaniwa  ndani  ya  Qur’ani. Waislam  wa  Shi’ah, kinyume  chake,  wao  wanaamini  kwamba  Nyumba  ya  Mtukufu  Mtume 51


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 52

U i s l a m u wa S h i a (s.a.w.w.) ni wale watu ambao wana viwango vya imani na elimu ambavyo vinafanya iwezekane wao kutajwa pamoja na Qur’ani katika Thaqalayn na katika hadith nyinginezo. Zaidi ya hayo, wao wanaamini kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe amebainisha watu wa Nyumba yake.

Hoja ya Kwanza: Wakati wowote tunapokuwa na shaka kuhusu upeo wa jambo lolote lile, kama  vile  kanuni  au  dhana,  lakini  tukawa  tunajua  kwamba  ni  ukweli wenye kujuzu kwa ukomo fulani, ambao zaidi ya hapo unaingia kwenye mjadala, ni lazima tutumie tahadhari na tufuate tu lile la chini kabisa. Kwa mfano, tuseme kwamba mtu hana uhakika iwapo katika swala yake pale mwanzoni mwa rakaa mbili za awali anaweza kusoma Surat al-Fatihah tu au  kama  anaweza  kusoma  sura  zingine  za  Qur’ani  pia.  Akili  inaamua kwamba anapaswa kutahadhari  na lazima asome kile ambacho ana uhakika nacho –  ambacho ni Surat al-Fatihah. Sasa katika suala letu sisi kama mtu ana wasiwasi kuhusu upeo wa maneno Ahlul-Bayt au maneno kama hayo,  kibusara  anawajibika  kujifinya  kwenye  kadiri  iliyo  ndogo  ambayo kwamba yeye anao uhakika nayo. Sasa kama mtu ana shaka juu ya iwapo Mwenyezi Mungu anakubali kutajwa kwa watu zaidi ya Fatima na familia yake pamoja na Qur’ani, kama sehemu ya Nyumba ya Mtume (s.a.w.w.), akili  inamuelekeza  mtu  kuwa  na  tahadhari  na  kujikomeshea  mwenyewe kwa  wale  watu  ambao  haswa  wamejumuishwa  katika  upeo  wa  maneno haya.

Hoja ya Pili: Tumeona hapo mbeleni kwamba Kizazi cha Mtume (s.a.w.w.) kimepewa hadhi ya hali ya juu kabisa. Mtukufu Mtume amewataja wao kuwa baada ya Qur’ani: “Naacha miongoni mwenu vizito viwili, Qur’ani na watu wa Nyumbani  kwangu,  na  hivi  havitatengana.”  Hivyo  kizazi  cha  Mtukufu Mtume  (s.a.w.w)  wakati  wote  wapo  pamoja  na  Qur’ani  na  siku  zote watakuwa  hivyo;  hawatapingana  nayo.  Kwa  kuzingatia  kigezo  hiki 52


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 53

U i s l a m u wa S h i a kwenye vichwa vyetu, hebu natuchunguze ile historia ya awali kabisa ya Uislamu  ili  kuweze  kuwaona  wale  miongoni  mwa  ndugu  wa  Mtume ambao wanaendana sawa nayo. Watu  pekee  ambao  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.)  amewataja  kama  amana yake na kuwa kwa pamoja mshirika wa Qur’ani ni Ali, mke wake Fatima, na watoto wao, Hasan na Husein. Hakuna Muislam, awe Sunni au Shi’ah anayedai  kwamba  ndugu  wengine  wa  Mtume  walikuwa  na  elimu  kubwa ama uchamungu zaidi kuliko familia hii, au wameutumikia Uislam zaidi ya walivyofanya  familia  hii.  Zaidi  ya  hayo,  hakuna  anayeweza  kusema kwamba maneno “Nyumba ya Mtume” yanaweza kujumuisha ndugu wote wa  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.),  kwa  vile  baadhi  yao  kama  Abu  Lahab walikuwa  ni  makafiri  na  hata  wale  walioamini  Uislam  hawakuwa  wote katika  kiwango  kimoja. Wengi  wao  walikuwa  ni  watu  wa  kawaida  tu  na walisilimu  baadae  kabisa,  walichelewa.  Kwa  kweli,  watu  pekee  ambao kwamba nafasi hii kuandamana na Qur’ani daima (kwa maneno mengine “Ma’sumin”)  inadaiwa  kuwa  yao,  ni  Fatima  na  familia  yake.  Kadhalika kama  Muislam  ataulizwa  ni  nani  anayeweza  kuwa  Ma’sum,  asiyefanya makosa, yeye ama atataja kundi hili, kwa mujibu wa imani ya Shi’ah, au asitaje  mtu  yeyote  kabisa,  kwa  sababu  wale  wasiokuwa  Shi’ah  wao hawadai Uma’sum kwa kundi lolote lile la watu zaidi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).  Kuliweka  tofauti  kabisa,  yeye  hatamuweka  mbele  mtu  yeyote mwingine kama mwenye kuunda muambatano wa kudumu na Qur’ani.   Hapa hatuwasilishi hoja ya mzunguko inayosema kwamba watu hawa ni Ma’sum  kwa  sababu  Shi’ah  wanadai  kuwa  wao  wako  hivyo.  Suala  la Uma’sum litajadiliwa baadae katika haki yake lenyewe. Hoja yetu hapa ni kwamba,  kwa  mujibu  wa  hadith  za  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.),  kuna umuhimu  wa  lazima  wa  kuwepo  kikundi  cha  familia  yake  ambacho kitakuwa pamoja na haki wakati wote, na kwa vile nafasi hii imetangazwa kipekee  kwa  ajili  ya  watu  hawa,  ni  wazi  kwamba  Mtukufu  Mtume (s.a.w.w.) alikuwa nao akilini mwake wale ambao pekee walikuwa wamethibitishwa  kwa  ajili  ya  Uma’sum.  Kama  wale  wasiokuwa  Shi’ah 53


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 54

U i s l a m u wa S h i a wangekuwa wanadai kwamba watu fulani mbali na wale walioainishwa na Shi’ah  walikuwa  ni  Ma’sum,  mtu  atapaswa  kuamua  kati  ya  madai  haya mawili.  Hata  hivyo,  hili  sio  suala  lenyewe,  na  kama  ni  ya  kuleta  maana yoyote, msimamo wa Shi’ah kwa hiyo unaelekea kutoa ufumbuzi pekee.

Hoja ya Tatu: Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.)  mwenyewe  ameeleza  wazi  ni  nini  kinachomaanishwa  na  Ahlul-Bayt wake    au  al-Itrah.  Hili  linaakisiwa  katika hadith zifuatazo zinazopatikana kwenye vyanzo vikuu ya Sunni: 1. Muslim anasimulia kutoka kwa Aisha: “Mtukufu  Mtume  alitoka  nje  akiwa  amevaa  shuka  jeusi  la  manyoya, wakati Hasan mtoto wa Ali alipomjia, basi Mtume alimruhusu Hasan kuingia ndani pamoja naye akiwa amemfunika kwenye shuka lake. Kisha akaja Husein na yeye pia akaingia ndani. Halafu akafuata Fatima. Yeye aliingia ndani vile vile. Kisha Ali naye akaja. Yeye pia aliingia chini ya shuka, kiasi kwamba shuka lilimfunika Mtume, Ali, Fatima, Hasan na Husein. Ndipo Mtume  akasoma:  “Hakika si mengineyo Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume, na kuwatakasa kabisa kabisa.” (33:33).45 2. Muslim anasimulia kutoka kwa Sa’d ibn Abi Waqqas kwamba yeye aliulizwa  na  Mu’awiyah  ni  kwa  nini  alikataa  kumtukana Ali  kwa  maneno. Sa’d  alijibu:  “Nakumbuka  hadith  tatu  za  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.) kuhusu Ali ambazo zilinisababisha mimi kutokusema lolote baya kuhusu yeye. Kama ningekuwa na japo moja ya sifa hizi ingekuwa ni bora kwangu  kuliko  ngamia  wekundu.46 La  kwanza  ilikuwa  ni  kwamba,  wakati 45 Sahih Muslim, Jz. 4, uk. 1883, hadith ya 2424. Kitab Fadha’il al-Sahabah, Bab Fadha’il Ahlul-Bayt, mfululizo wa Sakhr namba 4450. 46 Ngamia wekundu walichukuliwa kuwa na thamani sana katika siku zile. 54


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 55

U i s l a m u wa S h i a Mtume alipokuwa anataka kwenda kwenye vita vya Tabuk, alimuacha Ali hapo Madina. Ali alihuzunika sana kwamba hakuwa na bahati ya kutosha ya  kujiunga  na  jeshi  na  kupigana  kwa  ajili  ya  Allah.  Alikwenda  kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema: “Unaniacha mimi pamoja na watoto na wanawake?” Mtukufu Mtume alimjibu: “Huridhiki wewe kuwa kwangu ni kama Haruun alivyokuwa kwa Musa isipokuwa kwamba hakutakuwa na mtume baada yangu?” La pili ni kile nilichosikia kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika siku ya kutekwa kwa Khaybar: “Hakika nitampa bendera (ya Uislam) mtu ambaye anampenda Mwenyezi Mungu na Mtume Wake  na  yeye  anapendwa  na  Mwenyezi  Mungu  na  Mtume  Wake.” Tulitarajia kupewa hiyo, lakini Mtukufu Mtume akasema: “Niitieni Ali.” Ali alitokeza mbele, ingawa alikuwa anasumbuliwa na maumivu ya macho yake.  Mtukufu  Mtume  akampa  bendera  na  mikononi  mwake  Mwenyezi Mungu  akajaalia  ushindi.  La  tatu  ni  kwamba  wakati  aya  ya  Mubaahilah ilipoteremshwa, Mtukufu Mtume alimwita Ali, Fatima, Hasan na Husein na akasema: “Mola Wangu! Hawa ndio watu wa Nyumbani kwangu.’”47 3. Muslim anasimulia kwamba watu fulani walimuomba Zayd bin Arqam awasimulie  alichokisikia  kutoka  kwa  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.).  Yeye akasema: “Nimekuwa mtu mzima sasa na ilikuwa ni muda mrefu uliopita. Pia  nimesahau  baadhi  ya  yale  niliyojua  kutoka  kwa  Mtukufu  Mtume (s.a.w.w.).  Hivyo  chochote  nitakachokuambieni  kikubalini,  na  chochote ambacho  sitawaambia  ninyi  msinilazimishe  niwaambie.”  Kisha  akasema kwamba  wakati  mmoja  Mtukufu  Mtume  alisimama  na  kuongea  nasi mahali  kati  ya  Makka  na  Madina  panapoitwa  Ghadir  Khumm.  Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alianza kwa kumtukuza Mwenyezi Mungu na kuhutubia. Kisha  Mtukufu  Mtume  akasema:  “Enyi  watu!  Jueni  kwamba  mimi  ni mwanadamu na karibuni mjumbe kutoka kwa Mwenyezi Mungu (malaika wa kifo) atanijia na mimi nitamjibu. Hakika mimi ninawaachieni miongoni mwenu vitu viwili vya thamani. Cha kwanza ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu ambamo ndani yake mna mwongozo na nuru, hivyo shikamaneni 47 Sahih Muslim, Jz. 4, uk. 1871, namba 2408 Kitab Fadha’il al-Sabahah, Sakhir namba 4420. 55


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 56

U i s l a m u wa S h i a na Kitabu cha Mwenyezi Mungu.” Baada ya kuwatia moyo na kuwasisitiza  watu  kufanya  hivyo,  Mtukufu  Mtume  kisha  akasema:  “Na  cha  pili  ni kizazi  changu,  watu  wa  nyumbani  kwangu.”  Aliongeza  mara  tatu: “Nakukumbusheni  Mwenyezi  Mungu  kuhusu  (jinsi  mtakavyowatendea) kizazi changu.” Halafu Husein bin Subrah akasema: “Oh, Ziyad! Ni nani hao watu wa Nyumba ya Mtume? Je wake zake wamejumuishwa?” Ziyad alijibu  kwamba  wake  za  Mtukufu  Mtume  ni  ndugu  zake,  lakini  Kizazi chake  ni  wale  ambao  hawawezi  kupokea  sadaka,  na  wake  zake  hawana nafasi kama hiyo. Kisha mtu huyo akauliza: “Kwa hiyo hao ni akina nani?” Ziyad  akajibu:  “Familia  ya  Ali  (binamu  yake  Mtume),  familia  ya  Aqil (ndugu yake Ali), familia ya Ja’far (ndugu mwingine wa Ali) na familia ya Abbas (ammi yake Mtukufu Mtume na Ali).48 4.  Chini  ya  kichwa  cha  habari  hicho  hicho  Muslim  anasimulia  maelezo mengine ya hadith hiyo, ambayo mwanzo wake ni kama mwanzo wa ile iliyotajwa hapo juu, lakini ambayo mwisho wake ni tofauti. Kwa mujibu wa maelezo haya katika majibu ya swali la iwapo wake za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) walijumuishwa katika watu wa Nyumba yake, Ziyad bin Arqam anasema:  “Hapana,  naapa  Wallahi,  mke  anaishi  na  mume  kwa  kipindi fulana cha wakati na kisha anaweza akaachika akapewa talaka na kurudi kwa baba yake na familia yake. Kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ni wale  tu  ambao  wanatoka  kwenye  chanzo  na  asili  ileile  kama  Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na wale ambao hawaruhusiwi kupokea sadaka hata baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kufariki.”49 Hivyo, maneno “Nyumba ya Mtukufu Mtume” (Ahlul-Bayt) hayahusishi ndugu wote wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Wake za Mtume hawahesabiwi kutokana na Nyumba ya Mtume katika maana hii maalum, ingawa ni watu  wa  kwenye  familia  hii  na  wanaoheshimiwa  sana.  Kwa  mujibu  wa hadith,  maneno  Ahlul-Bayt  au  al-Itrah  yana  maana  maalum  na  yenye maana yenye mipaka. 48 Sahih Muslim, Jz. 2, uk. 1873, Kitab Fadha’il Sahabah, Sakhr namba 4425. 49 Sahih Muslim, Jz. 2, uk. 1874. 56


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 57

U i s l a m u wa S h i a Kwa  kutegemea  hadithi,  wanachuoni  wa  Shi’ah  wanaamini  kwa  kila dhuria  wa  Hashim,  babu  mkubwa  wa  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.)  kwa maana fulani ni kizazi cha nyumba yake  na anaitwa ‘Sayyid.’ Kuna kanuni fulani  kwenye  sharia  ya  Kiislam  (fiqh)  zinazofungamana  nao,  kama  vile kuzuiwa  kupokea  sadaka.  Lakini  tena  kwa  mujibu  wa  Hadith  na  hoja  za hapo juu, maneno Ahlul-Bayt katika maana yake ya ki-Qur’ani na katika maana  iliyotumika  katika  hadith  za  Mtume  kama  zile  za  Thaqalayn, Safinah  na  kishamia  (shuka)  ina  mipaka  zaidi,  kwani  inatumika  tu  kwa Fatima, Ali, Hasan na Husein na kisha Maimam wengine wa Nyumba ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) 5. Imam Ahmad bin Hanbali anasimulia kutoka kwa Umar bin Maymuun kwamba yeye alisema: “Tulikuwa tumekaa karibu na Ibn Abbas, binamu yake  Mtukufu  Mtume  na  mwanachuoni  mkubwa.  Kikundi  cha  watu  tisa kilimjia na kumuomba waondoke naye ama wale watu waliokuwepo pale wawapishe. Ibn Abbas akaondoka pale pamoja nao. Baada ya muda kiasi, Ibn Abbas alirudi akiwa amechukia sana kutokana na maneno mabaya aliyoyasikia kutoka kwao kuhusu Ali (a.s.).” Msimuliaji anaongeza kwa kusema kwamba, kisha Ibn Abbas akaanza kuelezea nafasi ya Ali (a.s.) mbele ya  macho  ya  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.)  na  baadhi  ya  sifa  zake. Alitaja muhanga  wa Ali  wa    Khaybar  na  kutangazwa  kwa  ufunuo  wa  Surat alTawbah kwa washirikina kulikofanywa na Ali (a.s.).50 Halafu akataja tukio jingine  ambamo  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.)  alizungumza  na  mabinamu zake na akauliza: “Ni nani miongoni mwenu ambaye yuko tayari kuniamini na kunifuata katika ulimwengu huu na ule wa Akhera?” Imam Ahmad bin  Hambali  anasema  kwamba  mabinamu  wote  wa  Mtukufu  Mtume walikataa kutoa majibu ya kukubali. Kulikuwa na jibu moja tu la kukubali na hilo lilitoka kwa Imam Ali (a.s.). Swali hili na jibu lake vilirudiwa kwa mara  nyingine  katika  kikao  hicho  hicho.  Mwishowe  Mtukufu  Mtume akasema:  “Wewe  ni  walii  wangu  (mshika  makamu)  katika  dunia  hii  na akhera.”  Ibn Abbas  vilevile  alieleza  kwamba Ali  alikuwa  ndiye  mtu  wa 50 Kuhusu  simulizi  ya  ushindi  wa  Khaybar  tazama  pia  Sahih Muslim,  Kitab Fadhail al-Sahabah, Sakhir namba 4422, 4423 na 4424. 57


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 58

U i s l a m u wa S h i a kwanza kusilimu. Tukio jingine ambalo Ibn Abbas alilieleza na ambalo ni lenye kufaa sana kwenye mjadala wetu hapa ni kwamba Mtukufu Mtume alichukua shuka lake, akamfunika nalo Fatima, Ali, Hasan na Husein na akasoma aya hii:

“Hakika si mengineyo Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume, na kuwatakasa kabisa kabisa.” (33:33).51 6.  Al-Tirmidhi  anasimulia  kwamba  Umar  bin  Abi  Salaamah,  ambaye alikuwa ni mtoto wa kambo wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisimulia kutoka kwa mama yake, Umm Salamah kwamba Mtukufu Mtume aliwaita Ali, Fatima,  Hasan  na  Husein  kuingia  chini  ya  shuka  lake,  na  kwamba  kisha akasema:  “Ewe  Mungu!  Hawa  ndio  watu  wa  Nyumbani  kwangu,  AhlulBayt wangu. Waondolee uchafu wote na uwatakase kwa utakaso uliotakata  hasahasa!”  Ndipo  Mwenyezi  Mungu  akateremsha  aya  ya  33:33  kwa Mtume Wake.  Umm  Salamah  anasema:  “Mimi  nilikuwepo  pale  na  nikamuuliza Mtukufu Mtume: Je, mimi ni mmojawapo wa watu wa Nyumbani 51 Musnad  Ahmad  bin  Hanbal,  Musnad  ya  Bani  Hashim  namba  2903.  Katika sehemu ya hadith iliyobakia, Ibn Abbas alielezea matukio mengine ambamo Ali alitoa utumishi kwa Uislam, kama vile katika kadhia ya Laytat al-Mabit, wakati alipolala kwenye nyumba ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ili kuwafanya wapagani wadhanie kwamba Mtukufu Mtume alikuwa bado yuko nyumbani kwake akiwa amelala, ambapo kwa kweli alikuwa anahama kwenda Madina. Vilevile anaelezea kwamba  wakati  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.)  alipokuwa  anataka  kwenda  Tabuuk, alimuacha  Imam  Ali  (a.s.)  kuchukua  nafasi  yake  hapo  Madina.  Ibn  Abbas  pia anaeleza kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alifunga milango yote binafsi iliyoelekea Msikitini isipokuwa mlango wa Imam Ali (a.s.), hivyo ni yeye peke yake aliyekuwa  na  uwezo  wa  kuingia  msikitini  moja  kwa  moja  kutoka  nyumbani kwake. 58


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 59

U i s l a m u wa S h i a kwako?”  Mtume  (s.a..w.w.)  akajibu:  “Wewe  unayo  sehemu  yako,  wewe uko katika wema.”52 Hivyo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alithibitisha ubora wake, lakini sio kama mmoja wa Ahlul-Bayt. 7. Imam Ahmad bin Hanbal anasimulia kutoka kwa Anas bin Malik kwamba wakati ile aya ya Utakaso (33:33) iliposhuka, kwa muda wa miezi sita mfululizo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akipita nyumbani kwa Ali na Fatima kila asubuhi akiwa njiani kuelekea msikitini kwa ajili ya swala ya al-Fajr na akiita kwa sauti: “Swala, enyi Watu wa Nyumba!”53 Zipo  pia  hadith  zinazobainisha  ile  maana  ya  neno  al-Qurbaa  (watu  wa karibu zaidi), ambalo linatokea mara kadhaa ndani ya Qur’ani, kama pale Mtume  anapoagizwa  asiombe  malipo  yoyote  kwa  kazi  ya  kufundisha kwake bali tu kwamba watu wapaswe kuwapenda Qurbaa wake (42:23).54 Zamakhshari,  mwanachuoni  mkubwa  wa  Sunni  na  mfasiri  wa  Qur’ani anasema kwamba wakati aya hii iliposhuka, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliulizwa kwamba ni akina nani waliolengwa na aya hii. Mtume (s.a.w.w.) alijibu: “Hao ni Ali, Fatima na watoto wao wawili wa kiume.”55

52 Sunan at-Tirmidhi, mfululizo wa ndani namba 3719. Hadith kama hiyo inaweza kupatikana  katika  kitabu  hicho  hicho,  hadith  namba3129.  Tazama  pia  Musnad Ahmad, Baqii Musnad al-Ansaar, mfululizo wa Sakhr namba 25300. 53 Musnad Ahmad bin Hanbal,  Sakhir  namba  13231.  Tazama  pia  Sunan alTirmidhi, Sakhir namba 3130. 54 Angalia Sura ya tatu, al-Imraan - Mapenzi kwa Mtukufu Mtume. 55 Al-Kashshaf ya Zamakhshari, Jz. 3, uk. 467.

59


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 60

U i s l a m u wa S h i a

Akili: Shi’ah  wanaamini  kwamba  akili  ni  chanzo  cha  kuaminika  cha  elimu  na kwamba  kipo  katika  upatanifu  na  ufunuo.  Kwa  mujibu  wa  baadhi  ya hadith, Mwenyezi Mungu uthibitisho (hujjah) namna mbili ambazo kwazo wanadamu  wanaweza  kuelewa  matakwa Yake:  ile  ya  ndani  kabisa,  akili (al-aql),  na  ya  nje,  Mitume.  Wakati  mwingine  akili  inaitwa  “Nabii  wa ndani”  na Mitume wanaitwa “akili ya nje.” Kuna kanuni madhubuti miongoni  mwa  mafaqihi  wa  Shi’ah  kwamba  uamuzi  wowote  unaofanywa  na akili  ni  sawa  na  uliofanywa  na  dini  (shar’)  na  kinyume  chake. Vile  vile imekubalika  kwa  kauli  moja  kwamba  moja  ya  shuruti  za  wajibu  wa kimaadili  au  kisheria  ni  kuwa    na  akili  timamu.  Kama  mtu  ana  wazimu hachukuliwi kuwa mwenye wajibu juu ya vitendo vyake. Kinachotegemewa kwa watu katika dini vilevile kinatofautiana kulingana na uwezo wao wa kiakili na busara. Wale wenye kiwango cha juu cha akili au  elimu  wanategemewa  kuwa  na  ujuzi  zaidi,  wachamungu  na  watiifu kuliko wale wenye elimu ndogo au wajinga. Kwa mfano, kwa mujibu wa hadith ya ki-mungu (hadith al-quds), Mwenyezi Mungu (swt) anawazawadia na kuwaadhibu watu kulingana na akili zao. Kwa  mujibu  wa  Qur’ani,  Mwenyezi  Mungu  anawataka  wanadamu  wote kutumia uwezo wao wa kibusara na kutafakari juu ya dalili na mawasiliano Yake  katika  ulimwengu.  Mara  nyingi  sana  wasioamini  wanalaumiwa  na kushutumiwa  kwa  sababu  ya  kushindwa  kwao  kufikiri  au  kutenda  kwa mujibu wa matakwa ya busara. Kwa mfano, wanalaumiwa kwa sababu ya uigaji  wao  wa  kibubusa  wa  wahenga  wao,  na  kuna  aya  nyingi  zenye maswali fasaha yanayowataka watu kufikiri, kama vile: “Je, hamfikiri?” au “Je, hamtafakari?”  Kwa jumla, akili inachangia kwenye elimu za kidini katika maeneo makuu matatu: La kwanza ni kuuelewa uhalisia wa ulimwengu, kama vile kuwepo  kwa  Mungu,  ukweli  wa  dini  na  mambo  ya  kweli  yaliyothibitishwa 60


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 61

U i s l a m u wa S h i a kisayansi. La pili ni uwasilishaji wa kanuni za kimaadili na kisheria kama vile  ubaya  wa  ukandamizaji  na  haki  ya  kisheria.  La  tatu  ni  uwekaji  wa viwango na michakato ya kimantiki ya hoja na maamuzi. Wajibat zote tatu za akili zinatambuliwa na hata kutiwa moyo katika Uislamu. Ni  akili  ambayo  huwa  inachukua  hatua  ya  awali  kuelekea  kwenye  dini, kuichunguza na kutafiti juu ya ukweli wake. Ni akili ambayo ndio inayotusukuma  sisi  kuchukua  jambo  kwa  umakini  na  inatuambia  kwamba maslahi yetu yatadhurika iwapo madai ya dini ni ya kweli lakini bado sisi tunashindwa kuyagundua na kuuamini Uislamu. Mara  tunapokuwa  tumeanza  tafiti  zetu  na  uchunguzi,  ni  akili  tena  inayotuelekeza sisi jinsi ya kufikiri na kuhoji. Ni akili vilevile tena inayotuambia kwamba tuwe wema, wachamungu, watafuta ukweli na kufungamana na  haki  wakati  na  baada  ya  mchakato  mzima  wa  ugunduzi  wa  kiakili. Hatuwezi kusema kwamba mtu lazima amuamini Mungu au Uislamu kwa sababu Mwenyezi Mungu anasema hivyo au kwa sababu Qur’ani inataka hivyo.  Wala  hatuwezi  kusema  kwamba  mtu  auchunguze  ukweli  wa  dini kwa sababu dini yenyewe inatuambia tufanye hivyo. Ni akili inayotusisitiza  sisi  kuchunguza  kuhusu  dini  na  hapo  kuweza  kugundua  ukweli  wa Qur’ani na Mtume (s.a.w.w.). Akili kwa hiyo ina jukumu muhimu sana juu ya  imani  ya  kidini.  Kila  mmoja  lazima  afanye  uchunguzi  wake  binafsi kuhusiana na dini  na kugundua ukweli mwenyewe kabisa, na hakuna mtu anayeweza kutegemea juu ya wengine. Bila shaka, mara ukweli wa Mtume aliyetajwa  au  kitabu  ukithibitishwa,  ukweli  mwingi  zaidi  unaweza  ukagundulika kutoka kwa Mtume huyo au kitabu hicho. Kuhusu sheria za kiutendaji na maadili mema, kanuni zinazofaa zinatambuliwa  na  akili.  Maelezo  bila  shaka  yanatolewa  na  vyanzo  vya  kidini, ingawa  mchakato  wa  kuyaelewa  maandiko  na  maana  na  matumizi  ya hukmu  za  kidini  nako  tena  kunatawaliwa  na  akili.  Kwa  mfano,  kama Mwenyezi  Mungu  anasema  ni  lazima  utekeleze  ibada  ya  Hijja  (kwenda kuhiji Makka), maana ya kiakili ni kwamba ni lazima tufanye maandalizi yote muhimu, kama vile kununua tiketi na kupata viza (visa). Kama kuna 61


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 62

U i s l a m u wa S h i a mgongano kati ya wajibat mbili kama vile kuokoa maisha ya mtu asiye na hatia na kutekeleza swala zetu, je hapo tufanye lipi? Katika suala kama hili, hata kama hakuna maagizo ya wazi au maalum ya kidini, bado tunaelewa kwamba ni lazima tutende kulingana na uamuzi wa hakika na wa wazi wa akili zetu, ambao ni kuokoa maisha ya mtu. Kinyume cha hayo, jukumu la ufunuo au maandiko katika sayansi za kidini linaweza kuhitimishwa kama ifuatavyo: Kuthibitisha mambo ya kweli ambayo tayari akili inayajua; Kuwasilisha mambo mapya ambayo akili haiyajui, kama vile maelezo ya kina juu ya ufufuo (siku ya mwisho) na maelezo ya kina juu ya mifumo ya maadili na ya kisheria. Kuthibitisha  ruhusa  inayostahili  ya  fidia  kupitia  mifumo  iliyoamuliwa kidini, ya malipo na adhabu. Ni lazima ielezwe hapa kwamba baada ya kuhakikisha ukweli wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Qur’ani, tunakuja kutambua mambo mengi ambayo tulikuwa  hatuna  uwezo  wa  kuyatambua  sisi  wenyewe,  kwa  sababu  ya ukosefu  wetu  wa  kuyafikia  maeneo  fulani  ya  ukweli  au  ushahidi  fulani. Mtu  kwa  hiyo  ni  lazima  atofautishe  kati  ya  kile  kilichopo  nje  ya  uwezo wake halisi wa kimantiki na migongano na viwango vya kimantiki. Suala la  kwanza  linahusu  mambo  ambayo  yanawezekana  kabisa,  kwani linafanana  na  uzoefu  wetu  katika  maisha  yetu  ya  kila  siku  na  tunajua vilevile kwamba uwezo wetu wa kuelewa unaweza hatimaye ukaongezeka taratibu. Suala la pili linahusu mambo ambayo hayawezekani. Kwa kifupi, hakuna jambo lisilo la kiakili katika Uislam. Bila shaka mtu anapaswa kutofautisha  kati  ya  hukumu  za  hakika  na  za  kimaamuzi  ya  kimatiki  kwa upande mmoja, na maoni ya kukisia au ya kibinafsi kwa upande mwingine. Kama katika suala fulani inaelekea kwamba uamuzi wa kiakili unagongana na sheria ya kidini, mtu lazima achunguze kosa liko wapi; ama ulikuwa sio 62


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 63

U i s l a m u wa S h i a uamuzi  wa  kweli  au  sahihi  kiakili  au  ilikuwa  sio  sheria  ya  kidini. Mwenyezi Mungu huwa hawapotoshi watu wake kamwe kwa kuwaambia wafanye  jambo  moja  kupitia  Mitume,  na  jambo  kinyume  na  hilo  kupitia akili  zao  walizopewa  na  Mungu.  Mara  kwa  mara  kumekuwa  na  uamuzi uliotokana na akili na ukachukuliwa kama unaopingana na msimamo wa kidini,  ambao  baada  ya  uchunguzi  wa  karibu  umethibitisha  kwa  kweli kuwa ni kinyume na kauli yenye maamuzi ya kimantiki. (Sheikh) M.R. Muzaffar katika maelezo yake juu ya akili anasema yafuatayo: “Tunaamini  kwa  Mwenyezi  Mungu  ametujaalia  zawadi  ya  akili  (aql)  na kwamba Yeye ametuamuru tutafakari juu ya Viumbe Vyake, kuangalia kwa makini dalili za Uwezo na Utukufu Wake kote ulimwengu mzima na pia ndani yetu sisi wenyewe. Imeelezwa ndani ya Qur’ani:

“Tutawaonyesha dalili zetu katika nchi za mbali mpaka iwabainikie kwamba hayo ni kweli.” (41:53). Mwenyezi  Mungu  ameonyesha  kutokuridhishwa  Kwake  na  wale  ambao wanafuata kibubusa njia za wale waliokuwa kabla yao.

“Wanasema: Bali tutafuata yale tuliyowakuta nayo baba zetu.’ Je, hata kama baba zao walikuwa hawafahamu chochote wala hawakuongoka?” (2:170). Na Yeye ameonyesha kuchukia Kwake kwa ajili ya wale ambao hawafuati 63


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 64

U i s l a m u wa S h i a chochote bali mawazo yao wenyewe binafsi ya juu juu:

“Hawafuati ila dhana na hawakuwa ila wenye kuzua tu.” (6:116). Naam,  akili  zetu  zinatulazimisha  kutafakari  juu  ya  Maumbile  ili  kuweza kumjua  Muumba  wa  ulimwengu,  kama  vile  tu  inavyokuwa  ni  lazima kwetu  kuchunguza  madai  ya  mtu  kwenye  utume  na  kuangalia  ukweli  ya miujiza  yake.  Sio  sahihi  kukubali  mawazo  ya  mtu  bila  kuyahakiki,  hata kama mtu huyo anayo zawadi ya elimu kubwa au anashikilia cheo kikubwa cha heshima sana.

Makubaliano (Ijma’): Kwa desturi, moja ya vyanzo vya kuuelewa Uislam inafikiriwa kwamba ni makubaliano  (Ijma’).  Kwa  mujibu  wa  utaratibu  wa  fikra  wa  Shi’ah, makubaliano ya watu wote au kundi la watu, kama vile wanachuoni, hayatoshi  kwa  yenyewe  kutumika  kama  uthibitisho  (Hujjah),  kwani  mtu mmoja  tu  anaweza  akafanya  kosa  moja,  mawili,  matatu,  maelfu  au  hata wote wanaweza kufanya hivyo. Hata hivyo wakati wowote panapokuwepo na  mgongano  miongoni  mwa  Waislam  au  wanachuoni  wa  Kiislam  kiasi kwamba  unaivua  Sunnah,  unaweza  kutumika  kama  uthibitisho,  kama chombo  cha  kugundulia  mapenzi  ya  Mwenyezi  Mungu.  Kwa  mfano, wakati  tunapoona  kwamba  Waislam  wote  katika  wakati  wa  Mtukufu Mtume  (s.a.w.w.)  waliswali  katika  namna  fulani  tunatambua  kwamba Mtume  alikuwa  amewaelekeza  kufanya  hivyo;  vinginevyo  kusingekuwa na  kipengele  kinachowajibika  kwa  ajili  ya  umoja  wao  wa  kivitendo. Haiwezekani kudhania kwamba wote walitenda kibubusa na bila maelekezo,  au  kwamba  wote  walikuwa  katika  makosa    na  Mtukufu  Mtume (s.a.w.w.) alishindwa kuwasahihisha. Hivyo  kwa  Shi’ah  makubaliano  (Ijma)  yenyewe  sio  uthibitisho  tosha;  ni 64


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 65

U i s l a m u wa S h i a yenye kuaminika tu pale yanapoongozea kwenye kuigundua Sunnah. Kwa mtazamo huo, kama Waislamu leo hii watakubaliana juu ya jambo fulani, mwanachuoni  ambaye  ana  shaka  juu  ya  jambo  hilo  hawezi  kiruhusa kuwazuia  bali  kuitikia  maoni  ya  wengi  na  kuyathibitisha.  Kumekuwa  na mambo mengi katika historia ambamo wanadamu walishikilia imani fulani ambayo baadae ilikuja kuwa kosa, kwa mfano kwamba dunia ni bapa. Ni Qur’ani tu na Sunnah pekee ambavyo ni sahihi bila mjadala na ambavyo vimesalimika kutokana na kasoro na makosa. Mtazamo huu unatoa namna ya  uzito  kwenye  itikadi  ya  Shi’ah,  kiasi  kwamba  kila  kizazi  cha wanachuoni – kwa kweli, kila mwanachuoni mmoja – ana uwezo na kwa hakika anatakiwa kurejea moja kwa moja kwenye Qur’ani na Sunnah na kufanya ijtihadiya asili, yaani, uchunguzi na hukumu huru (ijitihadi kamwe haikufungwa au kusimamishwa katika ulimwengu wa Shi’ah). Wao Shi’ah wanaamini  kwamba  maoni  ya  kwamba  hakuna  faqihi,  hata  awe  na  cheo kiasi  gani,  aliyekingika  na  maswali  ya  kiwanachuoni  au  changamoto  ya kibusara.  Bila  shaka,  kama  ilivyo  katika  nidhamu  yoyote  nyingine,  kila mwanachuoni wa kidini anahitaji kupitia vitabu vya watangulizi wake na kuvichunguza kwa makini.    Baadhi ya Waislam wa Sunni wanaamini kwamba wakati wowote katika zama zozote Waislam wote au wanachuoni wa Kiislam wakikubaliana kwa kauli moja juu ya jambo, lazima wawe wako sahihi. Inawezekana kwamba mtu au kikundi cha Waislamu wakaweza kufanya kosa, lakini haiwezekani kwamba  wote  wafanye  hivyo.  Wanaegemeza  wazo  hili  juu  ya  hadith wanayosimulia  kutoka  kwa  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.):  “Ummah  wangu kamwe hautakubaliana kwenye kosa.” Shi’ah  wanaamini  kwamba  hata  kama  usahihi  wa  hadith  hii  ukisadikika, una athari ndogo ya kiutendaji au uwezo wa kumaliza mijadala au kuondosha  shaka,  kwa  sababu  wanachuoni  wa  Kiislamu  ni  mara  chache  sana kukubaliana juu ya masuala yenye utata kwa ajili ya utatuzi ambao kwamba  hakuna  ushahidi  unaoweza  kupatikana  kutoka  kwenye  Qur’ani  ama Sunnah. Zaidi ya hayo, wao Shi’ah wanaamini kwamba wakati wote kuna 65


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 66

U i s l a m u wa S h i a Imam  Ma’asum  miongoni  mwa  Waislam;  kwa  vile  yeye  huwa  hakosei, Ummah  wa  Kiislam  ukichukuliwa  kama  mmoja  kamwe  hautakubaliana juu  ya  kosa  fulani  lolote.  Tatizo  bila  shaka  ni  kuhakikisha  kwamba Waislamu  wote,  pamoja  na  huyo  Imam  Ma’asum  wamekuwa  na  maoni mamoja juu ya suala linalohusika.

66


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 67

U i s l a m u wa S h i a

MLANGO WA TATU Mafunzo ya Dini Licha  ya  tofauti  zao  zote,  Waislam  wote  katika  historia  wamekuwa wakichangia katika makubaliano makubwa sio tu katika nyingi ya kanuni za  Kiislam  pekee,  bali  pia  katika  mengi  ya  matendo  yake.  Qur’ani  na shakhsiya tukufu ya Mtume kwa upande mmoja, na mapenzi ya dhati na utiifu  wa  Waislam  wote,  vyote  viwili  hivyo  kwa  upande  wa  pili  vimewaunganisha Waislam na vikawajenga na kuwa ummah halisi ambao una utambulisho  wake,  urithi,  shabaha,  malengo  na  mustakabali  wake. Uhasama  wa  maadui  wa  Uislam,  ambao  wakati  wote  wamekuwa  wakijaribu kuung’oa Uislam kwa jumla, na changamoto za zama vilevile vimesaidia kuamsha na kuimarisha ile hisia ya umoja na udugu miongoni mwa Waislam. Wito wa  Qur’ani na Kiutume juu ya umoja na undugu umekuwa ukirudiwa  siku  zote  na  watu  mashuhuri  wanaoongoza  wa  madhehebu tofauti za Kiislam: Kuhusiana na itikadi, Waislam wote wanaamini juu ya Mwenyezi Mungu na  Upweke  Wake,  katika  Mitume  kwa  jumla  na  hususan  ujumbe  wa Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.), ambao ni kuwasilisha ujumbe wa mwisho  wa  Mwenyezi  Mungu  juu  ya  wanadamu,  pamoja  na  ufufuo  na utendewaji wa haki na usawa juu ya kila mtu katika Siku ya Kiyama. Hizi ndio  itikadi  za  msingi  kabisa  za  Uislamu,  ambazo  zinakubaliwa  na Waislamu wote. Mawazo ya mtu wa nje juu ya kiwango cha makubaliano baina  ya  Waislam  wa  Shi’ah  na  Sunni  yanaelezewa  katika  dondoo  ifuatayo: Tangu  kutokea  Mapinduzi  ya  Iran  kila  mtu  anajua  kwamba  Shi’ah  ni Waislam, ambao kama Waislam wengine wa Sunni, wanaheshimu imani ya msingi ya Upweke wa Mwenyezi Mungu, maandiko yale yale matakatifu (Qur’ani), Mtume yuleyule Muhammad (s.a.w.w.), imani ileile ya ufufuo ukifuatiwa  na  Hukumu  ya  mwisho  na  wajibu  za  msingi  zilezile,  Swala, 67


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 68

U i s l a m u wa S h i a Saumu,  Hijja,  Zaka  na  Jihadi.  Nukta  hizi  za  kawaida  ni  muhimu  zaidi kuliko hizo tofauti: hakuna katazo la kinadharia kwa Shi’ah kuswali swala zake  pamoja  na  Sunni  na  kinyume  chake,  ingawa  matatizo  mengi yamekuwepo huko nyuma na kimazoea yamekuwa bado yapo.56 Katika  kinachofuatia,  kwanza  tutatoa  maelezo  mafupi  ya  kanuni  za Kiislam  na  kisha  kuchunguza  vipengele  vya  ibada  vilivyoorodheshwa hapo juu kwa kirefu zaidi. Mwishowe zile imani za tofauti za kipekee za Shi’ah zitafafanuliwa.

Maelezo Mafupi ya Uislam: Katika majibu ya maombi kutoka kwa al-Ma’mun, Khalifa wa Bani Abbas wa  wakati  wake,  ambayo  alimuandikia  maelezo  mafupi  ya  misingi  ya Uislam.  Imam  Ali  bin  Musa  ar-Ridha  (a.s.)  (aliyefariki  203  A.H.) alithibitisha yafuatayo: “Kwa  kweli,  misingi  ya  Uislam  ni:  kushuhudia  kwamba  hakuna mungu  isipokuwa  Allah,  aliye  mmoja  tu  na  Mungu  wa  kipekee kabisa  ambaye  hapenyeki,  aliyejitosheleza,  Mwenye  kusikia, kuona,  Mwenye  kudura,  wa  milele,  Hai,  wa  Daima,  Mjuzi  kiasi kwamba Yeye hashindwi, Mkwasi kiasi kwamba kamwe hahitaji, Mwadilifu kiasi kwamba hadhulumu au kuonea na kwa kweli Yeye ndiye Muumba wa kila kitu. Hakuna kinachofanana na Yeye. Hana mpinzani, hana mwenzi na wa kulingana Naye na kwa hakika Yeye ndio lengo la ibada, swala, matumaini na hofu. “Na ni kushuhudia kwamba kwa hakika Muhammad ni Mja Wake, Mtume  Wake,  muaminiwa  Wake,  mbora  miongoni  mwa  watu Wake,  bwana  wa  Mitume  na  Manabii,  Muhuri  (mwisho)  wa Mitume  na  kiumbe  bora  kabisa.  Hakuna  Mtume  baada  yake  na hakuna mabadiliko katika dini yake na hakuna mabadiliko katika 56 Kitabu cha Richard, Shi’ite Islam, uk. 5, pamoja na ufupisho 68


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 69

U i s l a m u wa S h i a sheria (Shari’ah) yake na kwa kweli kila alichokileta Muhammad ibn  Abdillah  (s.a.w.w.)  ni  ukweli  wa  dhahiri  (na  ni  kuwakubali yeye na Mitume na Manabii wote, na mawasii wote wa kabla yake) na  kukikubali  Kitabu  chake  chenye  ukweli,  kitukufu  ambacho  ni cha  namna  ambayo  “batili  haikifikii  kutokea  mbele  au  nyuma; wahyi  kutoka  kwa  yule  ambaye  ni  Mwenye  hekima,  Mwenye utukufu,” na kwa kweli Qur’ani aula kwa vitabu vyote na ni kweli kuanzia mwanzo hadi mwisho. Tunaamini juu ya aya zake muhkam (zenye  kujihukumu),  na  mutashaabih (zenye  utata),  Amm na khaass, ahadi na vitisho, batilishi na zilizobatilishwa, simulizi na taarifa zake. Hakuna kiumbe anayeweza kuleta kitu mfano wake.   “Na  kushuhudia  kwamba  kiongozi  baada  yake  na  shahidi  juu  ya mu’min na mtetezi wa mambo ya Waislam na mzungumzaji kwa niaba  ya  Qur’ani  na  mwenye  elimu  ya  sheria  zake,  ndugu  yake, mrithi wake, mtekelezaji wa wosia wake, mlinzi wake na ambaye alikuwa kwake kama Haruun alivyokuwa kwa Musa ni Ali ibn Abi Talib,  kamanda  wa  waumini  na  kiongozi  wa  wachamungu,  wasii bora na mrithi wa elimu ya Mitume na Manabii, na baada yake ni Hasan na Husein wale “mabwana wawili wa vijana wa Peponi” na kisha Ali bin Husein, fahari ya wale wenye kuabudu, kisha Ja’far bin  Muhammad  as-Sadiq  (mkweli),  mrithi  kwenye  elimu  ya mawasii, kisha Musa bin Ja’far al-Kadhim, kisha Ali bin Musa arRidhaa, kisha Muhammad bin Ali, kisha Ali bin Muhammad, kisha Hasan bin Ali, kisha al-Hujjah, yule anayeibukia, anayesubiriwa. “Nashuhudia  juu  ya  urithi  na  Uimam  wao  na  kwamba  dunia haitakosa kamwe kuwepo kwa shahidi wa kiungu (Hujjah) juu ya watu wake katika zama yoyote, na kwamba wao ndio wasimamizi imara  na  Maimam  wa  uongofu  na  mashahidi  juu  ya  watu  wa ulimwengu hadi mwisho wa dunia. Wao ndio wafasiri wa Qur’ani na wazungumzaji kwa niaba ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na yeyote  atakayefariki  bila  kuwajua  hao  atakuwa  amekufa  kifo  cha 69


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 70

U i s l a m u wa S h i a kijahilia. Imani yao inakusanya uchamungu, elimu, ukweli, swala, uaminifu, jitihada, kurudisha amana (walizopewa kwa ajili ya kuhifadhi) kwa wenyewe, wawe hao ni wema au wabaya, kusujudu kwa muda  mrefu,  kufunga  wakati  wa  mchana,  kuabudu  wakati  wa usiku, kujiepusha na yaliyokatazwa, kungojea faraja kwa subira na uvumilivu, maliwazo mazuri na uungwana wa usuhuba. Kisha Imam akaendelea kufafanua sheria za kiutendaji za Kiislam.

MISINGI YA DINI Upweke wa Allah: Dini ya Kiislam imejengwa na matamko ya ukweli (shahada) namna mbili: kwamba  hakuna  mungu  (yaani  anayepasa  kuabudiwa)  ila  Mwenyezi Mungu  (Allah)  na  kwamba  Muhammad  ni  mtume  Wake.  (LAA ILAHA ILALLAH MUHAMMADUR-RASULULLAH). Waislam wanaamini kwamba Mwenyezi Mungu ni Mmoja. Yeye hana mshirika wala watoto, Yeye ni wa Mwanzo na Mwisho. Yeye ni Mwenye kudura, Mjuzi wa yote, Mwenye kuenea kila mahali. Yuko karibu na mwanadamu zaidi kuliko mshipa wake wa shingo, lakini hawezi kuonwa na macho au kuzingirwa na akili. Katika du’a, Imam Ali (a.s.) anasema: “Ewe  Mungu,  hakika  mimi  nakuomba  kwa  Jina  Lako,  kwa jina la Allah, Mwingi wa rehema, Mwenye huruma, Mwenye utukufu  na  fahari,  Hai  na  Mwenye  kujitosheleza,  wa  Milele, hapana mungu kuliko Wewe.”

Utume: Mwenyezi Mungu amemuumba mwanadamu kwa hekima kabisa na kwa lengo (51:56). Amempa mwanadamu akili na hiari ya kujitafutia njia yake mwenyewe  kuelekea  kwenye  ukamilifu  wake  na  furaha.  Vilevile 70


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 71

U i s l a m u wa S h i a ameiongezea  akili  ya  mwanadamu  wahyi  wa  mbinguni.  Kupitia  busara Zake  na  haki,  Yeye  hakuwaacha  watu  wowote  au  pembe  ya  dunia  bila muongozo; Ametuma Mitume kwa nyumati zote kwenda kuwaelekeza na kuwaongoza. (10:47 na 16:36). Mtume wa kwanza alikuwa ni Nabii Adam (a.s.) na wa mwisho alikuwa ni Muhammad (s.a.w.w.), aliye Muhuri wa Mitume (33:40). Qur’ani inawataja kwa majina Mitume 25 na inaelezea kwamba walikuwepo wengi zaidi, (40:78). Kupitia dalili zilizoko kwenye hadith, Waislam wanaamini kwamba walikuwepo Mitume 124,000. Miongoni mwa wale waliotajwa ndani ya Qur’ani  ni  Adam,  Nuh,  Ibrahim,  Isma’il,  Is’haaq,  Lut,  Yaquub,  Yusuf, Ayuub, Musa, Haruun, Hizqiil, Daudi, Suleiman, Yunus, Zakariah, Yahya (Yohana  mbatizaji),  Isa,  na  Muhammad  (amani  iwe  juu  yao  wote). Miongoni  mwao,  Nuh,  Ibrahim,  Musa,  Isa  na  Muhammad  walikuwa  na ujumbe  wa  fani  zote  na  walileta  kanuni  maalum  za  sheria.  Wao  hawa wanaitwa “Uluu al-‘Adham” – ‘wenye dhamira kubwa.’  Mbali  na  Qur’ani  yenyewe,  hiyo  Qur’ani  inazungumzia  juu  ya  vitabu vinne vilivyoshuka: Kitabu cha Ibrahim (87:19), Zaburi ya Daudi (4:163 na  17:55),  Taurati  ya  Musa  (2:87,  3:3-4,  6:91  na  154);  na  Injiil  ya  Isa (5:46). Waislam lazima waamini katika vitabu vyote hivi vilivyoshushwa (2:4 na 285)  na  waamini  Mitume  wote  (4:152).  Kama  tutakavyoona  baadae, Shi’ah  wao  wanaamini  pia  kwamba  Mitume  wote  walikuwa  ni  Ma’sum, waliohifadhiwa kutokana na makosa, kipindi cha kabla ya ujumbe wao na wakati wa ujumbe wenyewe.

Ufufuo: Dunia itakuja kufikia mwisho wake mnamo Siku ya Ufufuo – ya Kiyama au Hukumu. Watu wote watafufuliwa na kufikishwa mbele ya Mwenyezi Mungu ambaye ataamua juu ya hatima ya kila mmoja wao kulingana na 71


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 72

U i s l a m u wa S h i a imani zao na matendo yao katika ulimwengu huu. Kutakuwa na malipo ya thawabu  kwa  wale  wema  na  adhabu  kwa  wale  waovu..  (22:1-2,  6-10; 3:185;  6:62;  98:6-8;  99:6-8;  101:4-11).  Mwenyezi  Mungu  atawatendea watu kwa haki lakini jambo litakalotawala katika utekelezaji wa Haki Yake litakuwa ni Rehma Yake. (6:12).

Angalizo: Ingawa Waislamu wote wanaamini misingi ya Uislam iliyotajwa hapo juu, kuna tofauti ndogo katika jinsi ya uelezaji fasaha wa imani zao na ibada zao. Waislam wa Shi’ah wanazielezea imani hizo hapo juu kama misingi au mizizi ya dini (Usuul al-Din) na vitendo vya ibada kufuata kama desturi au matawi ya dini (Furu’ al-Din). Sababu ya uelezaji kama huo ni kwamba itikadi hizo ndio vipengele vya msingi zaidi vya dini na vigezo kwa ajili ya kuonekana kama Mwislam. Hata hivyo, vitendo vya ibada vya lazima ni dalili za kuwa mwaminifu, kwa vile imani halisi hujionyesha yenyewe katika  vitendo.  Waislam  wa  Sunni  wakati  wote  wanawasilisha  tamko  la Uislam (kalimah) – lenye kujumuisha kushuhudia kwamba hakuna mungu ila Allah swt. na kwamba Muhammad ni Mtume Wake – pamoja na vitendo  vinne  vya  ibada,  yaani  swala  za  kila  siku,  saumu,  kuhijji  Makka  na zakat kama ndio Nguzo Tano za Imani. Wanachukulia vitendo vingine vya ibada  kama  vile  kuamrisha  mema  na  kukataza  maovu,  na  jihadi  kama matendo ya wajibu, lakini hawayaingizi katika Nguzo za Imani.

Itikadi za Shi’ah: Baada ya kuwa tumewasilisha mtazamo wa imani za jumla za Kiislamu, sasa tunapanuka kwenye baadhi ya itikadi za Uislam wa Shi’ah kwa maelezo ya kina zaidi. Baadhi ya itikadi hizi bila shaka zinachangiwa na baadhi ya Waislam wasiokuwa Shi’ah vile vile, angalau katika kanuni ama maelezo. Sababu ya kuchagua itikadi hizi hapa ni umuhimu wake kwenye fikra na imani za Shi’ah, yeyote anayeamini juu ya zote hizo anaweza kutambulika kama Shi’ah.

72


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 73

U i s l a m u wa S h i a

Mapenzi juu ya Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.): Kama  Waislam  wengine,  Shi’ah  wana  mapenzi  makubwa  kwa  Mtume Muhammad  (s.a.w.w.).  Wao  wanaona  ndani  yake  kigezo  kamilifu  kwa matumaini yote juu ya Mwenyezi Mungu, elimu ya kina ya Allah, uaminifu  kamili  kwa  Mwenyezi  Mungu,  utiifu  wa  kweli  kwenye  matakwa  ya mbinguni,  tabia  bora  kabisa,  na  chanzo  cha  upole  na  huruma  kwa wanadamu  wote.  Haikuwa  ni  bahati  mbaya  kwamba  alichaguliwa  na Mwenyezi Mungu kuwasilisha Ujumbe Wake wa mwisho na wa muhimu sana kwa wanadamu. Kama ilivyopendekezwa kabla, uwezo wa kupokea wahyi mtukufu unahitaji umiliki wa uhodari wa hali ya juu, na uwezo wa kupokea wahyi ulio  kamilifu zaidi kuliko mahitaji yote, uhodari wa hali ya juu kuliko wote. Sifa na tabia binafsi za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) zilichangia sana katika maendeleo  ya  Uislam.  Alijulikana  kama  mtu  mwaminifu,  mkweli  na mchamungu  tangu  utotoni  mwake.  Katika  wakati  wa  utume  wake  aliishi kwa kanuni na maadili yake. Katika nyakati za ushwari na vilevile za matatizo, wakati wa usalama na pia wa hofu, wa amani na pia wa vita, wakati wa  ushindi  na  vilevile  wa  kushindwa,  alikuwa  wakati  wote  akionyesha unyenyekevu,  haki  na  kujiamini.  Alikuwa  mnyenyekevu  kiasi  kwamba hakujikweza  binafsi,  hakujiona  bora  kamwe  kuliko  wengine  na  kwamba hakuishi maisha ya anasa. Wakati alipokuwa peke yake na asiye na uwezo na vilevile wakati alipoitawala rasi ya Arabia na Waislam wakiwa wanamfuata yeye kwa moyo mmoja na wakichukua kila tone la maji yake aliyochukulia udhuu, bado yeye aliendelea na hali hiyohiyo. Aliishi maisha ya kawaida  sana  na  wakati  wote  pamoja  na  watu,  hususan  masikini.  Yeye hakuwa  na  Kasri  wala  baraza  au  walinzi.  Wakati  alipokuwa  akikaa  na masahaba  zake  hakuna  mtu  aliyeweza  kumtofautisha  na  wengine  kwa sehemu aliyokuwa ameketi ama kwa nguo alizokuwa amevaa. Yalikuwa ni maneno yake na hali yake ya kiroho ambavyo vilimtofautisha na wengine. 73


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 74

U i s l a m u wa S h i a Alikuwa mwadilifu sana kiasi kwamba kamwe hakuwa akipuuza haki za mtu  yeyote,  hata  zile  za  maadui  zake.  Alionyesha  kwa  mifano  katika maisha yake ile amri ya Qur’ani,

“Enyi mlioamini! Kuweni wasimamizi madhubuti kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, mtoao ushahidi kwa uadilifu. Wala kuchukiana na watu kusiwapelekeeni kutofanya uadilifu. Fanyeni uadilifu, huko ndiko kunakokurubisha kwenye takua…..” (5:8). Kabla ya kwenda vitani, alikuwa akitoa maelekezo kwa wapiganaji wake kwamba wasiwadhuru wanawake, watoto, wazee na wale waliojisalimisha wenyewe,  wasiharibu  mashamba  na  mabustani,  wasiwafuatilie  wale waliotoraka kwenye uwanja wa vita, na aliwaamuru kwamba wakati wote wawe  wapole  kwa  mateka  wao.  Punde  tu  kabla  ya  kifo  chake,  yeye  alitangaza  hapo  msikitini:  “Yeyote  yule  anayejihisi  ananidai  au  ambaye sikumtendea  haki  zake,  tafadhali  ajitokeze  mbele  na  adai  haki  yake.” Waislam walilia kwa vile walikumbushwa juu ya zile huduma zote ambazo Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.)  amewafanyia  na  taabu  zote  zilizomkuta  ili  tu kuwaongoza  wao.  Wao  walijua  kwamba  Mtume  hajatoa  kipaumbele kwenye mahitaji yake yeye mwenyewe na kamwe hakupendelea mapunziko yake na wasaa kuliko yale ya wengine. Wao kwa hiyo walitoa kauli za shukurani  nzito  na  heshima.  Lakini  mtu  mmoja  alisimama  na  akasema: “Mimi ninakudai kitu. Kabla ya vita mojawapo ulikuwa unawapanga wapiganaji wako na fimbo yako ikanigonga. Sasa nataka kulipiza kisasi.” Bila kusita Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimwambia mmoja wa sahaba zake wa karibu aende nyumbani kwake na akalete fimbo ile ile  na akamtaka yule mtu  alipize  kisasi  chake  kwa  kumpiga  yeye.  Lakini  yule  mtu  akasema: “Fimbo yako iligonga ngozi ya tumbo langu.” Kwa hiyo Mtume (s.a.w.w.) akanyanyua shati lake ili mtu huyo apate kupiga ngozi. Badala ya kufanya 74


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 75

U i s l a m u wa S h i a hivyo, yule mtu ghafla akambusu mwili wake. Matilaba yote ya mtu huyo ya  kudai  haki  ya  kulipiza  kisasi  inawezekana  ikawa  ilikuwa  ni  kumbusu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa sababu ya heshima na mapenzi. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa anajiamini kabisa kwamba hakuwahi kamwe kujiwa na shaka kuhusu kazi ya ujumbe wake. Uadui wa washirikina ulijidhihirisha wenyewe katika yale mateso, mashambulizi na mauaji juu ya Waislam, unyang’anyi wa mali zao na kueneza uvumi wakipakazia wendawazimu au uchawi kwa Mtukufu Mtumu; lakini hakuna lolote kati ya  haya  lililomsimamisha  yeye.  Imam  Ali  yule  mpiganaji  jasiri  wa Uislamu  na  mshindi  mtekaji  wa  Khaybar,  yeye  anasema  kwamba  kila wakati vita vilipopamba moto na kuwa vikali, Waislam wangekimbilia kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kujihifadhi.57 Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.)  alibarikiwa  na  kupendwa  sana  kiasi  kwamba Mwenyezi  Mungu  (swt.)  alituma  rehema  Zake  juu  yake  popote  pale alipokuwa yeye (s.a.w.w.). Kwa mujibu wa hadith, Mitume wengine walijulishwa juu ya nafasi yake tukufu ya juu kwa Mwenyezi Mungu na katika mara kadhaa wao walimuomba Mwenyezi Mungu ayakubalie maombi yao kwa sababu yake yeye. Kuna hadith nyingi zinazozungumzia hili, kote katika  vyanzo  vya  Shi’ah  na  wasiokuwa  wao.  Kwa  mfano,  al-Hakim  alNishaabuuri na wengineo wanasimulia kutoka kwa Umar kwamba Adam (a.s.)  alimwambia  Mwenyezi  Mungu:  “Ewe  Mola  Wangu,  nakuomba unisamehe  mimi  kwa  haki  ya  Muhammad.”  Mwenyezi  Mungu akamwambia:  “Ewe Adam,  ulijuaje  kuhusu  Muhammad  wakati  ambapo Mimi bado sijamuumba yeye?” Adam akajibu: “Ewe Mola Wangu, [mimi ninamjua] kwa sababu wakati uliponiumba  mimi  kwa  mkono  Wako  na  ukapuliza  roho  Yako  ndani yangu, nilinyanyua kichwa changu na niliona imeandikwa kwenye nguzo za Arshi,  “Hapana mungu isipokuwa Allah. Muhammad ni 57 Nahjul-Balaghah 75


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 76

U i s l a m u wa S h i a Mtume wa Allah.” Hapo mimi nilijua kwamba huyo ambaye jina lake  Umeliweka  karibu  na  la  Kwako  lazima  awe  ni  mtu  aliye mpendwa Wako sana.’”   Ndipo  Mwenyezi  Mungu  akasema:  “Uko  sahihi.  Hakika  yeye  ndiye ambaye ni kipenzi sana Kwangu Mimi. Niombe Mimi kwa haki yake, na nitakusamehe. Isingekuwa kwa ajili ya Muhammad, Mimi nisingekuumba wewe.”58 Kumuomba Mtume kwa ajili ya Msaada: Waislam katika wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) walimuomba sana yeye msaada. Kwa mfano, Ahmad bin Hanbal, al-Tirmidhii na Ibn Maajah  wamesimulia  kwamaba  mtu  mmoja  kipofu  alikwenda  kwa Mtukufu  Mtume  na  kumuomba  amuombee  kwa  Mwenyezi  Mungu  ili aweze  kumponya.  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.)  akasema:  “Kama  ukitaka mimi  nitaomba,  lakini  kama  uko  tayari  kuwa  na  subira  hilo  litakuwa  ni bora  kwako.”  Yule  mtu  akarudia  ombi  lake.  Mtume  (s.a.w.w.) akamwambia  achukue  udhuu  wa  sawasawa  na  kusema:  “Ewe  Mola! Hakika  ninakuomba  Wewe  na  ninamuita  Mtume  Wako  Muhammad, Mtume  wa  rehema.  Ewe  Muhammad!  Kwa  hakika  ninamuita  Mungu wangu kupitia kwako katika maombi yangu ili kwamba yaweze kukubaliwa. Mola Wangu! Mfanye Muhammad kuwa muombezi wangu.”59 Ni dhahiri kabisa kumuomba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa ajili ya msaada kunaendelea baada ya kifo chake. Kwa mujibu wa Uislamu, kifo hakiashirii  kuangamia.  Kifo  ni  lango  kwenye  maisha  makubwa  na  ya  akili 58 Mustadrakul-Hakiim, Kitabu cha Tarikh mwishoni mwa Kitab cha al-Ba’th, Jz. 2, uk. 615. 59 Musnad Ahmad, Musnad al-Shaamiyin,  Sakhr  mfululiza  namba  16604  na 16605;  Sunan al-Tirmidhii,  Kitaab  al-Da’awaat,3502  na  Sunan Ibn Maajah, Kitaab Iqaamah al-Salah wa al-Sunnah fiyha, mfululiza wa Sakhr namba 1375. 76


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 77

U i s l a m u wa S h i a zaidi. Qur’ani kwa wazi kabisa inazungumzia maisha baada ya kifo kwa watu wote, na wale wema watapata maisha mazuri ya kupendeza mpaka watakapofufuliwa mnamo Siku ya Hukumu na kuingia kwenye ukweli wa milele. Qur’ani inatuelekeza sisi tusizungumze juu ya mashahidi kama ni wafu (2:154) au hata kuwafikiria wao kama wamekufa (3:169). Wanadamu wote wako hai baada ya kifo, lakini wale walio mashahidi ‘wako hai karibu na Mwenyezi Mungu na wanaruzukiwa kutoka kwa Mola Wao.’ (3:169). Kwa kuzingatia hilo, Waislam wote wa Shi’ah na Sunni wanaamini kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) yuko hai haswa na kwamba upokeaji wake wa miito yetu na uwezo wake aliopewa na Mwenyezi Mungu kutusaidia sisi  havipungui  kwa  kufariki  kwa  mwili  wake.  Al-Daarimii  anasimulia kwamba  watu  wa  Madina  walikuwa  na  njaa  ya  kufa,  hivyo  walikwenda kwa  Aisha  mke  wa  Mtume  (s.a.w.w.)  kulalamika  juu  ya  hali  yao.  Yeye Aisha alisema: “Liangalieni  (na  kulitembelea)  kaburi  la  Mtume  (s.a.w.w.). Toboeni  kijishimo  juu  ya  kaburi  kuelekea  juu  angani,  kiasi kwamba kuwe hakuna kizuizi baina ya kaburi na hilo anga.” Daarimii anaongeza kwamba watu hao wa Madina walifanya kama alivyowaelekeza yeye na kisha ikanyesha mvua kiasi kwamba nyasi ziliota na ngamia wao wakanenepa.60 Cha kushangaza, Bukhari anasimulia kwamba Khalifa Umar kwa mara kadhaa alimuomba Mwenyezi Mungu kwa ajili ya mvua  kwa  ajili  ya  haki  ya  Abbas  ambaye  alikuwa  ammi  yake  Mtume (s.a.w.w.),  kama  vile  tu  ambavyo  aliwahi  kumuomba  Mwenyezi  Mungu mvua kwa haki ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe.61 Mapenzi kwa Nyumba ya Mtume (Ahlul-Bayt): 60 Sunan al-Daarimii, Kitaab al-Muqaddamah, mfululizo wa Sakhr namba 92. 61 Sahih al-Bukhari,  Kitaab  al-Jumu’ah,  mfululizo  namba  954  na  Kitaab  alManaaqib, mfululizo wa Sakhr namba3434. 77


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 78

U i s l a m u wa S h i a Ingawa  Waislam  walikuwa  na  deni  kubwa  sana  kwa  Mtukufu  Mtume (s.a.w.w.)  na  walikuwa  tayari  kufanya  lolote  kwa  ajili  yake,  Mtukufu Mtume hakuwataka chochote kama malipo. Aliyafanya yote aliyoyafanya kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.

“Sema: Sikuombeni malipo juu ya hayo…..” (38:86). Hata  hivyo  Mwenyezi  Mungu  Mwenyewe  alimtaka  kuwaambia  watu kwamba wanapaswa kuwapenda watu wa Nyumbani kwake:

“Sema: Kwa haya siombi malipo yoyote kwenu isipokuwa mapenzi kwa ndugu zangu (kizazi changu) wa karibu…..” (42:23). Hili haliupingi ule ukweli kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakuomba kitu  chochote  kwa  ajili  yake  binafsi,  kwa  sababu  wafaidika  na  mapenzi haya ni watu wenyewe. Qur’ani inasema tena hapa:

“Sema: Ujira niliowaomba ni wenu nyinyi. Sina ujira ila kwa Mwenyezi Mungu…..” (34:47) Kwa  namna  hii,  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.)  aliekeza  hisia  za  kawaida  za shukurani za watu kuelekea kwenye jambo ambalo litawaongoza. Bali ni kama  mzazi  ambaye  anafanya  kila  kitu  kwa  ajili  ya  mwanae,  kama  vile kumpatia chakula, huduma za afya, nguo na fedha, na kisha akamuandikisha  kwenye  shule  na  kumwambia:  “Sihitaji  kitu  chochote  kama  malipo kutoka kwako. Ninakutaka tu ujifunze kutoka kwa mwalimu wako na ufuate ushauri wake.” 78


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 79

U i s l a m u wa S h i a Kwa hiyo ni wazi kabisa kwa nini Shi’ah wanaipenda Nyumba ya Nabii Muhammad  (s.a.w.w.).  Mapenzi  haya  yalianzishwa  na  Mtukufu  Mtume (s.a.w.w.)  na  kwa  kweli  na  Mwenyezi  Mungu  Mwenyewe  kama  “Njia kuelekea  kwa  Mola”  (25:57),  na  Shi’ah  kwa  sababu  hiyo  wameyageuza mapenzi haya kuwa ndio njia ya maisha. Inapaswa izingatiwe kwamba Mitume waliopita pia hawakuomba malipo, mifano ikiwa ni Nuh (26:145 na 11:29 na 10:72), Hud (26:127 na 11:5), Saleh (26:145), Lut(26:164) na Shu’aib (26:180). Mbali kabisa na ukweli kwamba  Mtukufu  Mtume  Muhammad  (s.a.w.w.)  alikuwa  na  kazi  ngumu zaidi ya Mitume wote, tofauti moja ya dhahiri katika suala lake  ni kwamba  yeye  ndiye  pekee  kwenye  kumbukumbu  kuwahi  kuambiwa  na Mwenyezi  Mungu  awaombe  watu  wake  kuwapenda  Ahlul-Bayt  wake kama  njia  kuelekea  kwa  Mola  Wao.  Sababu  ya  hili  iko  wazi.  Mtukufu Mtume Muhammad alikuwa ndiye Muhuri wa Mitume na hakuna mtume angekuja baada yake. Ili kubakia kwenye njia iliyonyooka, wafuasi wake baada ya pale walihitaji watu ambao wangeweza kuhifadhi na kuwasilisha mafundisho  yake  halisi,  hususan  kwa  vile  yalihusiana  na  maelezo  ya Qur’ani  tukufu.  Kama  ilivyoonekana  mapema,  hoja  hii  imewekwa  wazi kabisa katika hadith ya Thaqalayn na Safinah, hadith ambazo zinakubaliwa na Waislam wote. Waislam  wanawapenda  watu  wa  Nyumba  ya  Mtume  sio  tu  kwa  sababu walikuwa ni ndugu zake au Masahaba lakini pia kwa sababu wao walikuwa mfano  wa  athari  na  manufaa  yote  yaliyolinganiwa  na  Mtukufu  Mtume. Hakuna shaka yoyote miongoni mwa Waislam kwamba Ahlul-Bayt (a.s.) wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ni mkusanyiko wa mfano bora wa sifa na maadili wa ummah wa Kiislam. Wakati Mtume Muhammad alipokuwa na majadiliano  na  Wakristo  wa  Najran,  Mwenyezi  Mungu  alimteremshia yafuatayo:

79


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 80

U i s l a m u wa S h i a

“Na watakao kuhoji baada kukufikia elimu hii, waambie: Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wanawake zetu na wana wanawake wenu, na nafsi zetu na nafsi zenu, kisha tuombe kwa unyenyekevu tutake laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie waongo.” (3:61). Vyanzo vyote vya Kiislam vinasimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwachukua  pamoja  naye  Hasan  na  Husein  wakiwasilisha  watoto  wa Waislam (abna’ana – watoto wetu), na Fatima akiwakilisha wanawake wa Kiislam (nisa’ana – wanawake zetu). Alimchukua na Ali pia pamoja naye, bali ni kama sehemu ya uwepo wake pale (anfusanaa – na sisi wenyewe). Zipo pia hadith sahihi zinazothibitisha cheo cha hawa watu wanne. Kwa mfano,  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.)  amesema:  “Fatima  ni  pande  la  mwili wangu. Kinachomkasirisha yeye kinanikasirisha mimi.” Vile vile alisema: “Fatima  yuko  mbele  kabisa  miongoni  mwa  mabibi  wa  Peponi.”  Juu  ya Hasan  na  Husein,  Mtume  alisema:  “Hasan  na  Husein  ni  mabwana  wa vijana wa Peponi” na Husein anatokana na mimi na mimi ninatokana na Husein.”  Ni  ukweli  uliothubutu  pia  kwamba  wakati  Mtukufu  Mtume alipokuwa  akitaka  kusimamisha  ahadi  ya  undugu  (ahd  al-ukhuwwah) miongoni mwa Muhajirina na Ansari hapo Madina, yeye alimchagua Ali kama  mwenza  wake  na  ndugu  yake  yeye  mwenyewe,  ingawa  wote walikuwa  ni  Muhajirina.  Zaidi  ya  hayo,  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.)  aliwaambia Ali, Fatima, Hasan na Husein: “Mimi niko vitani na wale ambao wapo vitani na ninyi, na katika amani na wale ambao mnayo amani nao.” Mapenzi juu ya Nyumba ya Mtume Muhammad kwa hiyo yanashikiliwa kiulimwengu  wote  na  Waislam  wa  madhehebu  zote,  na  wakati  wote 80


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 81

U i s l a m u wa S h i a imekuwa  ikichukuliwa  kama  ni  matokeo  ya  imani  na  mapenzi  juu  ya Mtukufu  Mtume  mwenyewe.  Shi’ah  kwa  umakhususi  wamejaribu kutimiza masharti yote ya mapenzi haya, ambayo yameanzishwa ndani ya Qur’ani kama “malipo” kadiri iliyo sawa na kazi ya Mtume (s.a.w.w.) na kama ni “njia kuelekea kwa Mola.” Masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): Kama  Waislam  wengine,  Shi’ah  wanayo  heshima  kubwa  sana  kwa Masahaba  wa  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.),  yaani,  wale  ambao  waliingia katika Uislam kwa uaminifu kabisa na wakaiunga mkono kazi ya Mtume (s.a.w.w.)  kwa  maisha  yao  na  mali  bila  ya  kutarajia  malipo  yoyote  wala cheo, na ambao walibakia kuwa watiifu kwa Mtume katika mazingira yote, hususan baada ya kifo chake, mpaka mwisho wa uhai wao. Qur’ani inasema:

“….. wale waliomwamini yeye na kumtukuza na kumsaidia na wakaifuata nuru iliyoteremshwa pamoja naye, hao ndio wenye kufaulu.” (7:157)

“Na wale walioamini na wakatenda mema na wakaamini yaliyoteremshwa juu ya Muhammad, nayo ni haki itokayo kwa Mola wao, atawafutia makosa yao na atastawisha hali zao.” (47:2).

81


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 82

U i s l a m u wa S h i a

“Muhammad Mtume wa Mwenyezi Mungu na walio pamoja naye, wana nguvu mbele ya makafiri, na wanahurumiana wao kwa wao….. Mwenyezi Mungu amewaahidi walioamini na wakatenda mema katika wao maghufira na ujira mkubwa.” (48:29). Shi’ah wanawapenda wale masahaba wa Mtume walioonyesha sifa zilizotajwa hapo juu katika maisha yao, ingawa hakuna amri makhsusi ndani ya Qur’ani ya kuwapenda hao. Wala mapenzi juu yao sio kama “malipo” kwa ajili  ya  kazi  ya  Mtume  au  kama  “njia  kuelekea  kwa  Mola  wa  mtu.” Utendaji juu ya haki na matendo mema unahitajia utendaji kwa wale wote walioendesha  maisha  yao  katika  uaminifu  kwa  Mwenyezi  Mungu    na wakawa wamefanya matendo mema, haswa wale watangulizi waliowatangulia  wengine katika kuukubali Uislam na kuusaidia katika wakati wake mgumu. Qur’ani inasema:

“Wale walioamini na wakahama na wakapigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, kwa mali zao na nafsi zao, wana cheo kikubwa mbele ya Mwenyezi Mungu, na hao ndio wenye kufuzu.” (9:20). Masahaba  wachamungu  wa  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.)  hawakuwa  tu  na 82


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 83

U i s l a m u wa S h i a kazi ya kuulinda Uislam dhidi ya vitisho vya washirikina, bali pia iliwabidi kuwa na tahadhari kamili kuhusiana na wanafiki ambao walijipenyeza kwenye jamii ya Waislam na walikuwa wakiendelea kupanga njama mfululizo pamoja na maadui zake wa nje. Qur’ani inasema:

“Na miongoni mwa mabedui walio pambizoni mwenu wamo wanafiki na katika wenyeji wa Madina wako waliobobea katika unafiki. Huwajui, sisi tunawajua. Tutawaadhibu mara mbili, kisha watarudishwa kwenye adhabu kubwa.” (9:101). Kuukinga Uislamu dhidi ya wanafiki kulikuwa ndio kazi ngumu sana kwa Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.)  na  wafuasi  wake,  kwa  vile  wanafiki  hao walikuwa wamejipenyeza kwenye jumuiya na wakajifanya kuwa waaminifu  kwa  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.)  bila  ya  kutambulika  wazi.  Tunasoma tena ndani ya Qur’ani:

“Na wanaapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba wao ni katika nyinyi, na wala wao si katika nyinyi. Lakini wao ni watu wanaogopa.” (9:56). Wanafiki hao walikuwa na mipango ya kumuua Mtume na kuanzisha vita vya wenyewe kwa wenyewe ndani ya Madina.62 Waliongea kwa ulaghai 62 Tazama  kwa  mfano  aya  ya  9:48  na  63:8.  Kwa  maelezo  zaidi  rejea  kwenye vitabu vya historia vya maisha ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) 83


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 84

U i s l a m u wa S h i a sana juu ya mambo ya Waislamu na juu ya mapenzi yao kwa Waislam kiasi kwamba  ilionekana  wanapaswa  kuhesabiwa  kuwa  miongoni  mwa Masahaba watiifu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.):

“Na unapowaona miili yao inakupendeza, na kama wakisema, unasikiliza usemi wao, wao ni kama boriti zilizotengenezwa, wanadhani kila kishindo ni juu yao, wao ni maadui jihadhari nao, Mwenyezi Mungu awaangamize, ni vipi wanageuzwa?” (63:4). Walifika mbali zaidi hata kufikia kujenga msikiti ulioitwa kama Masjid alDhiraar,  na  wakamualika  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.)  kwenda  kuswali hapo.  Mwenyezi  Mungu  akazifichua  nia  zao  kwa  Mtukufu  Mtume (s.a.w.w.) na akamwambia asiende kuswali humo. Kwa kweli huu ulikuwa ndio  msikiti  wa  kwanza  kubomolewa,  sio  na  maadui  wa  Uislam  bali  na Mtukufu Mtume mwenyewe. Qur’ani inasema:

“Na wale waliotengeza msikiti kwa ajili ya kudhuru na ukafiri na kuwafarikisha Waumini na mahali pa kuvizia kwa yule aliyempiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume hapo kabla. Na bila shaka wataapa kwamba hatukukusudia ila wema; na Mwenyezi Mungu anashuhudia kuwa wao ni waongo.” (9:107). 84


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 85

U i s l a m u wa S h i a Kwa  nyongeza  ya  matatizo  yaliyowakuta  wakati  wa  uhai  wa  Mtukufu Mtume  (s.a.w.w.),  wafuasi  wake  watiifu  walikuwa  wastahimili  matatizo makubwa zaidi baada ya kifo chake. Iliwabidi kuulinda Uislam kutokana na vitisho kutoka kwa maadui wa nje kama vile Byzantini na vile vilivyoonyeshwa na maadui wa ndani. Hawa wa ndani walijumisha pamoja na wanafiki  ambao  walikuwa  hawakumuamini  kamwe  Mtukufu  Mtume (s.a.w.w.)  na  ujumbe  wake,  na  wengine  ambao  waliamini  lakini hawakubakia  katika  njia  iliyonyooka  ya  haki.  Hili  ni  jambo  ambalo Qur’ani ilikuwa imekwisha kulionya juu yake:

“Hakuwa Muhammad ila ni Mtume; wamekwisha pita Mitume kabla yake. Je, akifa au akiuliwa mtarudi nyuma kwa visigino vyenu?.....” (3:144). Vita vingi na migogoro ilitokea wakati baada ya kifo cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)  ambamo  angalau  kundi  moja  lazima  liwe  lilikuwa  kwenye makosa  na  kutenda  kinyume  na  maslahi  ya  Uislam  na  maadili  ambayo Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.)  aliyalingania.  Bukhari,  Muslim,  Ibn  Majah, Ahmad  bin  Hanbal  na  wengine  wote  wamesimulia  kwamba  Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema:

85


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 86

U i s l a m u wa S h i a “Nitakuwepo  pale  kwenye  Bwawa  la  Kauthar  kabla  yenu,  na nitapigania  baadhi  ya  watu  lakini  itanibidi  nishindwe.  Nitakuwa nikisema:  ‘Mola  Wangu,  hao  ni  masahaba  wangu,  masahaba wangu’ na itasemwa: ‘Hujui waliyozusha nyuma yako.’”63 Bukhari  vilevile  anasimulia  kwamba  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.)  alisema akiwa na masahaba zake: “Nitakuwa  kwenye  Birika  nikiwasubiri  wale  ambao  watanijia kutoka  miongoni  mwenu.  Wallahi,  baadhi  ya  watu  watazuiwa kunifikia mimi, na mimi nitasema: ‘Mola Wangu, hao ni wafuasi wangu na watu wa Ummah wangu.’ Na Mwenyezi Mungu atasema:  “Wewe  hujui  waliyoyafanya  baada  yako;  walikuwa  wakati wote wakigeuka nyuma kwa visigino vyao.’”64 Licha ya matatizo yote hayo, shukurani ni kwa Mwenyezi Mungu na uongozi wa Mtukufu Mtume, Waislam waaminifu hawakupata utata wowote katika kuitambua njia ya haki iliyonyooka tangu kufariki kwake. Mtukufu Mtume  (s.a.w.w.)  aliwaelekeza  kushikamana  na  Qur’ani  na  Ahlul-Bayt wake,  “Vizito  viwili  ambavyo  havitatengana  mpaka  vikutane  vyote kwenye  bwawa  na  Kawthar”  pamoja  na  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.). Tutamalizia mjadala huu kwa du’a kutoka kwa Imam ‘Ali bin Husein.’ “Ewe  Mungu,  mrehemu  Muhammad,  Aliyeaminishwa  na  Wewe 63 Angalia Sahih Bukhari, Kitab al-Riqaaq, Sakhr mfululizo namba 6096, 6097 na 6104, Kitab al-Fitan 6527 na 6528; Sahih Muslim, Kitaab al-Fadha’il, Sakhr mfululizo  namba  4250  na  4259;  Sunan  al-Nisaa’i,  Kitaab  al-Iftitaah,  Sakhr  namba 894; Sunan Ibn Majah, Kitaab al-Manaasik, Sakhr namba 3048; Musnad Ahmad, Musnad al-Mukthiriin min al-Sahabah, namba 2212, 3547, 3621,  3657 na kad-

halika.

64 Sahih Bukhari, Kitaab al-Riqaaq, namba 6090 na 6527; Sahih Muslim, Kitaab

al-Fadha’il, namba4250 na Musnad Ahmad, Musnad al-Mukthirin min al-Sahaba, namba 3457, 3621, 3672, 3837, 3966 na kadhalika. 86


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 87

U i s l a m u wa S h i a juu ya Wahyi Wako, aliyetofautishwa Nawe miongoni mwa viumbe Wako, mtiifu Kwako miongoni mwa waja Wako, Imam wa rehma, kiongozi wa wema, ufunguo wa neema, aliyeitengeneza nafsi yake kwa  ajili  ya  mambo  Yako,  aliyehatarisha  mwili  wake  kwenye mambo mabaya kwa ajili Yako, alionyesha uhasama wa wazi kwa ndugu wa karibu kwa kuitwa na Wewe. Alipigana dhidi ya familia yake  kwa  ajili  ya  radhi  Zako  nzuri,  alivunja  mafungamano  ya tumbo kwa kutia uhai kwenye dini Yako,  aliwapeleka mbali wale wa karibu kwa ajili ya kukukanusha kwao,  akawaleta karibu wale wa mbali kwa sababu ya muitikio wao Kwako, alionyesha urafiki kwa watu wa mbali sana kwa ajili Yako, alidhihirisha uhasama kwa wale  wa  karibu  sana  kwa  ajili  Yako,  aliifanya  nafsi  yake  kuwa vumilivu  katika  kuwasilisha  ujumbe  Wako,    aliichosha  katika kuikusanya  imani  Yako,  aliishughulisha  katika  kuwashauri  wale waliostahili miito Yako,  alihamia kwenye nchi ya ugenini na sehemu  ya  umbali  kutoka  nyumbani  kwa  shogi,  njia  ya  miguu  yake, ardhi ya mazazi yake, makazi ya ndani kabisa ya nafsi yake, akidhamiria  kunyanyua  dini Yako  na  akitafuta  msaada  dhidi  ya  wale wasiokuamini Wewe.65 Waislamu wote wanajua kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwadilifu (‘adil), na  kwamba  Yeye  kamwe  hafanyi  dhulma  kwa  waja  Wake  na  kamwe hamuonei yeyote. Ukweli huu umeelezewa wazi ndani ya Qur’ani:

“Na bila shaka Mwenyezi Mungu sio dhalim kwa waja Wake.” (3:182; 8:51; na 22:10).

65 Psalms of Islam, Du’a ya Pili uk. 21 na 22. 87


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 88

U i s l a m u wa S h i a “Na Mola Wako sio dhalimu (japo kidogo) kwa waja Wake.” (41:46). “….. wala Mimi siwadhuluma waja.” (50:29)

“Hakika Mwenyezi Mungu hadhulumu (hata) uzani wa chembe…..” (4:40)

“Hakika Mwenyezi Mungu hawadhulumu watu chochote, lakini watu wanajudhulumu wenyewe.” (10:44) Katika 95:8, Qur’ani inasema: “Je, Mwenyezi Mungu si Hakimu kuliko mahakimu (wote)?” Na tena katika 21:47 inasema, “Na tutaweka mizani ya uadilifu Siku ya Kiyama, na nafsi yoyote haitadhulumiwa hata kidogo, na kama kukiwa na uzito wa chembe ya khardali tutaileta, nasi tunatosha kuwa wenye kuhesabu.”66 Kwa nyongeza ya umuhimu uliotolewa kwenye uadilifu wa ki-ungu ndani ya Qur’ani na Hadith, yumkini ipo sababu ya kihistoria kwa ajili ya msisitizo uliowekwa kwenye itikadi hii na Shi’ah. Ash’ari, kikundi kimoja cha wanachuoni wa Sunni wamethibitisha kwamba hakuna kipingamizi katika kigezo cha kutofautisha haki ya kimaadili na matendo potofu. Wema ndio anaofanya  au  kuamuru  Mwenyezi  Mungu,  hivyo  chochote  anachoamuru Mwenyezi Mungu ni wema na haki kwa udhahiri. Wao wanaamini kwamba  kama  Mwenyezi  Mungu  angetuamuru  kusema  uongo,  basi  kusema uongo  kungekuwa  ni  wema,  na  kama  Mungu  angewaingiza  watu wachamungu  motoni,  huo  ungekuwa  ni  uadilifu.  Wanaamini  kwa  kweli 66 Kuna  aya  nyingine  nyingi  ndani  ya  Qur’ani  zinazothibitisha  uadilifu  wa  kimungu. 88


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 89

U i s l a m u wa S h i a kwamba  Mwenyezi  Mungu  kamwe  hafanyi  mambo  kama  hayo,  sio  kwa sababu  yenyewe  ni  makosa,  bali  kwa  sababu  Yeye  Mwenye  amesema kwamba  matendo  hayo  ni  mabaya,  ni  maovu.  Ash’ari  pia  wanaamini kwamba  wanadamu  hawana  hiari  huru  na  kwamba  ni  Mwenyezi  Mungu ambaye anayatengeneza matendo yao bila ya wao kuwa na wajibu wowote isipokuwa kule “kupatikana” kwa matendo hayo; wanadamu ni vyombo tu kwa ajili ya matendo ya ki-mungu. Shi’ah na baadhi ya wanatheolojia wengine wa Sunni kama vile Mu’tazila, wao wanaamini kwamba wema na ubaya au haki na batili ni malengo na kwamba kuna vigezo vya kibusara kwa ajili ya maamuzi ya kiadilifu. Kwa maneno mengine, wao wanaamini juu ya wema wa asili na uovu wa asili. Kuna tofauti halisi na lengo kati ya uadilifu na uonevu, na sio jambo lisilo na mantiki kwamba Mwenyezi Mungu ametuagiza sisi tuwe waadilifu na tusimdhulumu  yoyote  yule,  hata  akiwa  ni  adui  yetu.  Hawa  Mu’tazila wanaamini zaidi kwamba wanadamu wako huru na wenye kuwajibika juu ya matendo yao kwa njia ya tafwiid, yaani Mwenyezi Mungu ametoa kwa wanadamu mamlaka Yake juu ya vitendo vyao vya hiari ili kwamba wawe na  udhibiti  kamili  juu  ya  hivyo  vitendo.  Shi’ah,  kinyume  chake,  wakati wanapokanusha ushurutishwaji (jabr) kwamba ni kinyume na uadilifu wa ki-mbingu na kuthibitisha kwamba wanadamu wako huru, pia wanaamini kwamba  uhuru  wa  binadamu  una  mipaka,  kwani  Mwenyezi  Mungu anashikilia mamlaka juu ya vitendo vyao. Mafundisho haya yanaelezewa katika maelezo mashuhuri ya Imam Ja’far as-Sadiq (a.s.): “Hakuna kulazimisha (jabr), wala uwakilishi kamili wa mamlaka (tafwiid); ukweli upo katikati ya mawili haya.”  Kwa sababu ya umuhimu wa hali ya juu kabisa wa suala hili kwa mfumo wowote wa maana, Shi’ah wakati wote wameweka mkazo juu ya uadilifu wa kimbinguni na mara kwa mara wameujumuisha, pamoja na Upweke wa Allah, Utume na Uimamu na Ufufuo miongoni mwa nguzo tano (Usuul alMadhhab)  za  madhehebu  yao.  Kwa  kutofautisha,    Upweke  wa  Allah, 89


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 90

U i s l a m u wa S h i a Utume na Ufufuo vinahesabika kama nguzo tatu za dini (Usuul al-Diin), kwani hizi zinachangiwa na Waislam wote. Msisitizo huu juu ya uadilifu wa kimbinguni umeathiri sio tu ule mwelekeo wa  kinadharia  wa  Ushi’ah,  kwani  Shi’ah  wanachukulia  uadilifu  kama kipengele cha msingi sana cha Uislamu kiasi kwamba kila mara wamedai juu ya utekelezwaji wake katika jamii. Harakati za Shi’ah katika historia yote  mara  kwa  mara  zimejulikana  kwa  wito  kwa  ajili  ya  uadilifu. Tutalijadili jambo hili zaidi wakati tutakapoziangalia zile tabia bainifu za Uislam wa Shi’ah.

Uimamu: Shi’ah wanaamini katika taasisi ya Uimam kama muendelezo wa Utume. Katika  Kiarabu  neno  ‘Imam’  lina  maana  ya  kawaida  ya  ‘kiongozi’  bila kujali  tabia  na  sifa  zake  binafsi  na  ukomo  wa  uongozi  wake,  ambao unaweza kuanzia kwenye jamaa ya msikiti mpaka kwenye ummah mzima. Katika matumizi ya Shi’ah hata hivyo, neno hilo linapata maana maalum kama ni yule mtu aliyewekwa kwenye madaraka ya mambo yote ya kisiasa  na  kidini  ya  ummah  wa  Kiislamu.  Kwa  usahihi  zaidi,  Imam  ni  mtu aliyechaguliwa na Mwenyezi Mungu na kuteuliwa na kwanza na Mtume na  kisha  na  kila  Imam  mrithi  kupitia  uteuzi  wa  wazi  (nass),  kuuongoza ummah  wa  Kiislamu,  kutafsiri  na  kulinda  dini  na  sheria  (Shari’ah)  kwa pamoja na kuongoza ummah katika mambo yake yote. Imam ni muwakilishi  wa  Mwenyezi  Mungu  juu  ya  ardhi  (Khalifatul-llah)  na  mrithi  wa Mtume, wote kwa pamoja. Ni lazima awe hana dhambi na awe na elimu aliyojaaliwa na Mwenyezi Mungu ya dhahiri na ya siri ya Qur’ani. Madhehebu ya Shi'ah yenye idadi kubwa ya waislam wa Shi'ah Ithan'ashari wanaamini  kwamba  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.)  alirithiwa  na  Maimam Kumi na Mbili nao ni hawa wafuatao: 1. Imam Ali ibn Abi Talib                             amefariki mwaka wa 40/659 2. Imam Hasan bin Ali                                 amefariki mwaka wa 50/669 90


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 91

U i s l a m u wa S h i a 3. Imam Husein bin Ali                                amefariki mwaka wa 61/680 4. Imam Ali b. Husein - as-Sajjad                 amefariki mwaka wa 95/712  5. Imam Muhammad b. Ali - al-Baqir         amefariki mwaka wa 114/732 6. Imam Ja’far b. Muhammad – as-Sadiq    amefariki mwaka wa 148/765 7. Imam Musa b. Ja’far – al-Kadhim          amefariki mwaka wa 183/799 8. Imam Ali b. Musa – ar-Ridhaa               amefariki mwaka wa 203/817 9. Imam Muhammad b. Ali – al-Jawaad     amefariki mwaka wa 220/835 10. Imam Ali b. Muhammad – al-Haadi     amefariki mwaka wa 254/868 11. Imam Hasan b. Ali – al-‘Askarii          amefariki mwaka wa 260/872 12. Imam Muhammad b. Hasan – al-Mahdi Huyu amezaliwa mwaka wa 256/868 Wakati wa kifo cha baba yake mnamo mwaka 260 AH. al-Mahdi, Imam wa Kumi  na  Mbili  aliingia  mafichoni  (ghaybat),  akijitokeza  tu  kwa  Shi’ah wachache wanaoongoza. Tutazichunguza imani kuhusiana na yeye baadae. Maoni ya Sunni: Waislamu  wa  Sunni  wanalitumia  neno  hili  ‘Imam’  katika  muktadha maalum  kuwa  kama  ni  sawa  na  neno  ‘Khalifa’,  neno  la  Kiarabu  kwa maana  ya  ‘Mrithi.’  Neno  Khalifa  lilitumika  kama  cheo  kwa  yeyote aliyechukua  madaraka  na  kutawala  dola  ya  Kiislamu  baada  ya  kifo  cha Mtukufu  Mtume  Muhammad  (s.a.w.w.).  Khalifa  anaweza  kuchaguliwa, kuteuliwa  na  mtangulizi  wake  au  kuchaguliwa  na  kamati,  na  anaweza vilevile kutwaa madaraka kwa nguvu za kijeshi. Khalifa hana haja ya kuwa hana dhambi, wala hahitaji kuwa mbora kwa wengine katika sifa kama vile imani au elimu. Itakuwa  ni  sawasawa  kurejea  hapa  kwenye  idadi  ya  hadith  ambamo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anataja kwamba kutakuwa na viongozi kumi na mbili  baada  yake.  Kwa  mfano,  Bukhari  anasimulia  kwamba  Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Kutakuwa na viongozi kumi na mbili baada yangu.”67 Kisha msimuliaji anasema kwamba Mtume alisema kitu amba67 Neno la Kiarabu katika maelezo ya asili pale kwa ajili ya ‘kiongozi’ ni Amiir. 91


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 92

U i s l a m u wa S h i a cho yeye hakuweza kukisikia. Alimuuliza baba yake, ambaye pia alikuwepo hapo wakati huo, kumwambia kile ambacho Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikisema.  Baba  yake  alimwambia  kwamba  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.) alisema:  “Viongozi  wote  hawa  kumi  na  mbili  watatokana  na  kabila  la Quraishi.68, 69 Muslim  vilevile  anaisimulia  hadith  hii,  akisema  kwamba mpokeaji wa hadiht hii alikwenda na baba yake mahali ambapo Mtukufu Mtume  (s.a.w.w.)  alipokuwa,  na  Mtume  akasema:  “Dini  hii  haitakwisha mpaka iwe kumekuwa na warithi kumi na mbili.”70 Kisha mpokeaji anasema:  “Mtume  (s.a.w.w.)  alisema  maneno  ambayo  sikuyaelewa  na  nikamuuliza baba yangu. Yeye akaniambia kwamba Mtume alikuwa amesema: “Wote wanatokana na Quraishi.’”71 Katika  riwaya  nyingine,  Muslim  anasimulia  kwamba  Mtukufu  Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Mambo ya watu yataendeshwa sawasawa madhali tu watu kumi na mbili watawaongoza.”72 Bado katika riwaya nyingine yeye amesema:  “Dini  hii  itatukuzwa  alimuradi  wanakuwepo  warithi kumi na mbili.”73 Inavutia  kwamba  baadhi  ya  simulizi  za  hadith  hii  zinaonyesha kuwepo  kwa  hawa  kumi  na  mbili  kutaishia  pamoja  na  kule  kuisha  kwa 68 Sahih Bukhari, Kitab  al-Ahkam,  Sakhr  ya  6682.  Tazama  pia  Sunan atTirmidhii, Kitab al-Fitan, Sakhr ya 2149 na Musnad Ahmad, Musnad al-Basriiyiin, Sakhr ya 19920. 69 Quraishi ni kabila ambamo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Ahlul-Bayt yake na baadhi ya familia hapo Makka walitokana nalo. Kuna hadith mbalimbali tofauti ambazo zinasisitiza jambo la kwamba wale viongozi wote baada ya Mtume wanatokana na Quraishi. Kwa mfano, kuna mlango mzima ndani ya Sahih Muslim juu ya mada hii (Kitab al-Imaarah, Mlango wa kwanza).  70 Neno la Kiarabu katika maelezo ya asili hapa kwa ajili ya ‘Mrithi’ ni ‘Khalifah.’ 71 Sahih Muslim, Kitaab al-Imaarah, Sakhr ya 3393. 72 Sahih Muslim, Kitaab al-Imaarah, Sakhr ya 3394. 73 Sahih Muslim,  Kitaab  al-Imaarah,  Sakhr  ya  3395,  3396  na  3397,  Sunan Abu Dawuud,  Kitab  al-Mahdi,  Sakhr  ya  3732,  Musnad Ahmad, Musnad Basriyiin, Sakhr ya 19936, 20019 na 20032. 92


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 93

U i s l a m u wa S h i a ulimwengu na kwa Uislam. Kwa mfano, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Dini hii (Uislam) itadumu alimuradi wanakuwepo warithi kumi na mbili kutokana  na  Quraishi.”74 Maana  yake  inaelekea  kuwa  kwamba warithi  kumi  na  mbili  watakuja  baada  ya  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.)  na jumla ya muda wao wa kuishi utarefuka mpaka mwisho wa wakati. Kundi hili la hadith linaibua idadi ya maswali. Hawa watu kumi na mbili ni akina nani? Warithi wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ni akina nani? Ni vipi muda wa uhai wa hawa watu kumi na mbili utakavyorefuka mpaka mwisho wa wakati? Ni akina nani ambao ndio chanzo cha utukuzwaji wa Uislamu? Na  hao  warithi  kumi  na  mbili  ni  nani  ambao  wanatokana  na  Quraishi? Shi’ah wanaamini kwamba majibu ya maswali yote haya ni kuwatambulisha  hao  watu  kumi  na  mbili  wanaotajwa  katika  riwaya  hizo  kama  ndio Maimam  Kumi  na  Mbili.  Baadhi  ya  wanachuoni  wasiokuwa  Shi’ah wamekwenda mbali sana na kutunga orodha tofauti ya watu kumi na mbili waliotajwa. Baadhi yao walitaka kujumuisha Makhalifa wote kuanzia na Abu  Bakr,  lakini  walipofika  kwa  Yazid  bin  Mu’awiyah,  walilazimika kumuondoa  yeye,  kwani  alikuwa  ndiye  yeye  aliyemuua  mjukuu  wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na wengi wa jamaa zake na Masahaba wa

74 Sunan Abu Dawuud, Kitab al-Mahdi, Sakhr ya 3731, Musnad Ahmad, Musnad Basriyiin, Sakhr ya 19873 na 19901. Zipo hadith nyingi pia ambazo zinasisitiza hili jambo la kwamba madhali wanabakia watu wawili duniani, atakuwepo mmoja kutoka Quraishi atakayewaongoza. Tazama kwa mfano, Sahih Bukhari, Kitab alAhkam,  Sakhr  ya  3240  na  6607,  Sahih  Muslim,  Kitab  Imaarah,  Sakhr  ya  3392, Musnad Ahmad, Musnad al-Mukthiriin min al-Sahaba, Sakhir ya 4600, 5419 na 5847.

93


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 94

U i s l a m u wa S h i a Mtume  mnamo  mwaka  wa 61AH  na  akaishambulia  Madina  mwaka 62AH.75 Tatizo jingine wanalokutana nalo ni kwamba wakati wanapofikia mteuliwa wa kumi na mbili katika orodha yao, wanaona kwamba hakuna tofauti  kubwa  kati  yake  na  mrithi  mwenye  uwezekano  wa  kumi  na  tatu, akiwa na sifa sawa na za watangulizi wake. Juhudi za namna hii hazikuzaa matokeo yoyote ya kuridhisha.

Hali ya kutokosea (Uma’sum): Waislamu kwa kufanana wote wanaamini kwamba Mitume wote walikuwa wamehifadhiwa na makosa na dhambi (Ma’sumin) katika mambo yanayohusiana  na  ujumbe  wao.76 Kumekuwa  hata  hivyo  na  tofauti  za  maoni miongoni mwa madhehebu mbalimbali za Kiislam juu ya urefu na muda wa  huyo  ma’sum  anayehitajika.  Shi’ah  wanaamini  kwamba  Mitume kamwe hawakutenda dhambi kubwa ama ndogo, kabla au baada ya kuanza  utume  wao,  kwa  kusudia  ama  vinginevyo,  endapo  ni  katika  masuala yanayohusiana na ujumbe wao au maisha yao binafsi. Waislamu wa Sunni kwa  jumla  wanaamini  kwamba  Mitume  walikuwa  ma’sumin  kwenye 75 Kwa  mujibu  wa  Sunan at-Tirmidhii,  Sakhr  ya  2152,  na  Musnad Ahmad, Musnad al-Ansaar, Sakhr ya 20910, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Katika Ummah  wangu  kutakuwa  na  Ukhalifa  kwa  niaka  30  na  kisha  kutakuwa  na ufalme.” Tirmidhi anaongezea kwamba kisha mpokeaji, ambaye alikuwa anaitwa ‘Safinah’ akasema kwamba Ukhalifa wa Abu Bakr, Umar, Uthman na Ali ulidumu kwa miaka 30. Sa’id, ambaye ameipokea hadith hii kutoka kwa Safinah anasema kwamba  alimwambia  Safinah  kwamba  Bani  Umayyah  walidhania  kwamba  na wao  ni  makhalifa.  Lakini  Safinah  alijibu  kwamba  wao  walikuwa  ni  waongo  na

wafalme wa aina mbaya sana.

76 Neno ‘Ma’sum’ limetokana na mzizi ‘a-sa-ma. Mzizi huu kwa maana ya neno kwa neno ni kuweka, kulinda au kuokoa kitu, hivyo ma’sum kwa neno kwa neno lina  maana  ya  mtu  ambaye  ameokolewa  au  kulindwa.  Kiufundi  ma’sum  ni  yule mtu  ambaye  ana  sifa  ya  (‘ismah)  ambayo  inamzuia  yeye  kutokana  na  kutenda madhambi na kuangukia kwenye makosa.

94


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 95

U i s l a m u wa S h i a masuala  yanayopasika  moja  kwa  moja  na  ujumbe  wao.  Ash’aria,  kwa mfano, wanaufunga uma’sum kwenye dhambi zilizokusudiwa ziwe ndogo au  kubwa  ili  kwamba  Mitume  wangeweza  kuwa  wametenda  baadhi  ya dhambi bila kukusudia. Mu’tazila wanaamini kwamba Mitume walikuwa ma’sum kuhusiana na madhambi makubwa, kwa kusudia au kwa kutokusudia, lakini kwamba wangeweza kutenda madhambi madogo. al-Baghdadi katika kitabu chake, Al-Farq bayn al-Firaq anaelezea itikadi ya Waislamu wa Sunni kama ifuatavyo: “Wao wanaamini katika uma’asum wa Mitume kuhusiana na dhambi. Wametafsiri kile ambacho kimesimuliwa kuhusu kuteleza kwao kama kulikotokea kabla ya utume wao.”77 Allamah al-Hilli katika Al-Baab al-Hadii ‘Ashar yake anaielezea itikadi ya Shi’ah kama ifuatavyo: “Kwa kweli, Mitume ni ma’sumin kutoka mwanzo wa maisha yao hadi mwisho, kwa sababu mioyo ya watu haielekei kuwatii wale ambao wao wamewashuhudia hapo kabla wakitenda aina mbalimbali za dhambi ndogo na kubwa na vitendo vya kuchukiza au visivyofaa.” 78 Waislam wamebishana juu ya umaasum wa Mitume kwa njia nyingi. Aya ifuatayo mara nyingi imetolewa kama ushahidi:

“Na Mola wake alipomjaribu Ibrahim kwa matamko, naye akayatimiza. Alimwambia: Hakika mimi nimekufanya Imam wa watu. Akasema: Na katika Kizazi changu (pia) Akasema: Ahadi yangu haiwafikii madhalimu.” (2:124). Ingawa mwanzo wa aya unahusu nafasi ya Uimamu, kifungu cha kumal77 Al-Baghdadi, Al-Farq bayn al-Firaq, uk. 343. 78 Al-Hilli, Bab al-Haadi ‘Ashar, uk. 63. 95


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 96

U i s l a m u wa S h i a izia kinashauri kanuni ya kawaida: kuweza kufaulu kwa ajili ya nafasi yoyote iliyotolewa kimungu, mtu lazima awe na kiwango kisicho cha kawaida cha  uchamungu  na  utakaso  wa  nafsi.  Kwa  mujibu  wa  Qur’ani,  uvunjaji wowote wa sheria za kidini unachukuliwa kama ni kitendo cha kidhalimu (dhulm). Wale ambao walitenda dhambi, hususan ya shirk (kumshirikisha Mungu  na  chochote),  dhambi  iliyo  mbaya  kuliko  zote,  hawezi  kwa  hiyo kuwa  ameteuliwa  na  Mwenyezi  Mungu  kuwa  mtume.Wale  ambao hawaamini juu ya umuhimu na ulazima wa umaasum kabla ya mwanzo wa utume wanadhani kwamba haina madhara iwapo nabii mtarajiwa atatenda dhambi  moja  au  nyingine,  kwa  masharti  kwamba  hali  kama  hiyo  halafu huja kukoma. Kuna  hoja  za  kitheolojia  vile  vile  kwa  ajili  ya  umaasum,  kama  ile  inayopatikana katika maneno ya M.R. Mudhaffar:  “Sababu ya umaasum wa Mitume ni kwamba kama atatenda dhambi au kosa, au akawa msahaulifu au jambo lolote linalofanana na hilo,  tunapaswa  kuchagua  kati  ya  njia  mbili:  ama  tuitii  dhambi yake  na  makosa,  ambapo  kwa  mtazamo  wa  Uislamu,  tutakuwa tunafanya  makosa,  au  tuwe  hatulazimiki  kukubali  madhambi  na makosa yake, ambavyo pia sio sahihi, kwa sababu hili ni kinyume na  wazo  la  utume  ambamo  utii  ni  lazima,  aidha,  kama  kila  kitu atakachosema au kufanya kina uwezekano wa kuwa ama sawa au kosa,  basi  haiwezekani  kwetu  sisi  kumfuata  yeye.  Matokeo  ni kwamba faida ya ujumbe wake imepotea; inakuwa haina umuhimu, na nabii huyo anakuwa kama watu wa kawaida ambao matendo na maneno  yao  hayana  ubora  ule  tunaoutafuta,  kwa  matokeo  ni kwamba  kutakuwa  hakuna  utii  na  vitendo  vyake  vitakuwa  haviaminiki.79 Inapasa kuzingatiwa kwamba hoja juu ya umaasum wa Mitume zinatofau79 Mudhaffar, Kitabu ‘The Faith of Shi’ah Islam,’ uk. 21  96


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 97

U i s l a m u wa S h i a tiana katika mawanda yao na kuhusika kwao, baadhi wakihusisha umaasum wao kwenye maisha yao yote na wengine wakilenga kwenye maisha yao  baada  ya  kuanza  kwa  utume  wao.  Katika  kinachofuata,  tutajaribu kuteua na kujadili vipengele tofauti vya umaasum. 1. Umaasum  baada  ya  kuanza  kwa  utume  katika  kulingania  na  kufikisha ujumbe  wa  mbinguni.  Hili  ni  jambo  ambalo  Waislam  wote wanakubaliana juu yake, kwani kama mtume anafanya makosa au anapuuza wajibu wake katika kulingania ujumbe wa mbinguni, ile faida ya kufikisha ujumbe huo itakuwa imepotea na zaidi ya hapo, watu watapotoshwa kwa kumfuata yeye.80 2. Umaasum  baada  ya  kuanza  kwa  utume  katika  maisha  binafsi,  kwa mfano katika kushughulika na familia, marafiki, majirani na kadhalika. Baadhi  ya  Waislam  wanachukulia  aina  hii  ya  umaasum  kama  usio  na muhimu kuhusiana na dhambi ndogo ndogo ama zile zilizotendwa bila ya  kukusudia.  Shi’ah  na  baadhi  ya  wengine  wanaamini  hata  hivyo kwamba, kadiri hii ya umaasum pia ni muhimu, kwa sababu Mitume sio tu  wahadhiri  na  walinganiaji  tu;  wameteuliwa  na  Mwenyezi  Mungu kupamba njia ya ukamilifu na uchamungu katika simulizi zao na ujumla  wa  tabia  zao.  Watu  wanahitaji  aidha,  mifano  ya  kivitendo  kwa nyongeza  ya  masomo  ya  nadharia.  Nabii  ambaye  katika  maisha  yake hakuyapamba  yale  maadili  aliyokuwa  akiyalingania  atakuwa hakukamilisha ujumbe wake. Atakuwa pia amedhoofisha ujumbe wake, kwa sababu utambuzi wowote wa mapungufu katika maisha yake binafsi  kutawafanya  watu  kufikiri  kwamba  yeye  mwenyewe  hakuwa  ameshawishika kikamilifu na ujumbe wake mwenyewe. Ni  vipi  kuhusu  dhambi  na  makosa  ambayo  hayakukusudiwa  ambayo kwamba  kwa  kawaida  mtu  hachukuliwi  kuhusika  nayo?  Inaelekea  wazi kwamba hata katika suala hili mengi ya matatizo sawa na hayo yanaweza 80 Angalia kwa mfano ‘Aqa’id al-Ja’fariyah, namba 13 cha Sheikh al-Tusi (385460),. 97


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 98

U i s l a m u wa S h i a kuibuka.  Kwanza,  watu  wakati  wote  hawataweza  kutofautisha  miongoni mwa yale matendo yaliyokusudiwa na yale yasiyokusudiwa. Kwa mfano, kama  wanaona  kwamba  nabii  anavunja  sheria,  anapuuza  haki  za  mtu  au hafanyi  kitendo  cha  kidini,  haitakuwa  rahisi  wakati  wote  kwao  kuamua iwapo anazingatia vitendo vyake au hapana. Watu ambao wanatafuta visingizio vya kuhalalisha makosa yao wenyewe watakuwa hasa mafidhuli wa kushikilia  kwenye  matukio  kama  hayo.  Aidha,  hata  kama  tukifikiria kwamba  watu  walikuwa  na  uwezo  kwa  desturi  wa  kutofautisha  kati  ya dhambi zilizokusudiwa na zile zisizokusudiwa, ni jambo la kutegemewa tu kwamba mara tu walipomuona nabii wao kuwa mwenye kukosea na akawa na  makosa  na  mapungufu  yake  mwenyewe,  wao  watapoteza  imani  juu yake  kuhusiana  na  huko  kulingania  ujumbe  wake.  Kama  nabii  alisahau miadi  au  alisahau  kutekeleza  Swala  yake,  watu  watakuwaje  na  uhakika kwamba  hakufanya  makosa    au  hakusahau  jambo  katika  kuwasilisha ujumbe uliofunuliwa? Watu watakuwaje tayari kukabidhi maisha na nafsi zao kwa mtu kama huyo? Lazima  ikubalike  kwa  kweli  kwamba  waumini  wa  kawaida  ambao  ndio wanachukua idadi kubwa ya wale wanaozungumziwa na huo ujumbe wa kinabii wasingeweza kupata zile tofauti nzuri ambazo baadhi ya wanatheolojia  wanazipendekeza.  Naam,  wengi  wa  wanatheolojia  hawa  hawa wasingeweza kupata tofauti hizohizo katika uzoefu wao wenyewe, kama vile ile tofauti kati ukweli wa kile kilichosemwa na uadilifu au nia ya msemaji.  Watu  wengi,  hata  kama  wao  wenyewe  ni  Waislam,  wasingemtilia maanani mhubiri mahiri na msomi ambaye anafahamika kutenda vitendo visivyo  vya  kiadilifu  katika  maisha  yake  binafsi.  Kinachofuatia  basi  ni kwamba  wasioamini  ambao  wameishi  maisha  ya  kujiendekeza  yasiyodhibitiwa  na  imani  yoyote  juu  ya  Mungu  hawatakuwa  na  mwelekeo  wa kumfuata mtu mwenye tabia ya kutia wasiwasi anayewalingania kubadili maisha yao kabisa, kujiingiza wenyewe kwenye maadili mapya na kuwa tayari kujitoa muhanga. Kama hali ilivyo, kumekuwa na watu wachamungu wengi katika ulimwen98


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 99

U i s l a m u wa S h i a gu  wa  Kiislamu,  hususan  miongoni  mwa  wanachuoni,  ambao  wameishi maisha ya usafi wa kupigiwa mfano. Tofauti kati ya watu hao na Manabii ni kwamba umaasum wa Mitume ni wa juu ya kila kitu, na kwamba tofauti  na  Manabii,  wao  hawakulindwa  kutokana  na  uwezekano  wa  kutenda dhambi. 3. Umaasum kabla ya utume. Kwa kuzingatia yaliyopita hapo juu, inaweza kueleweka kwamba ni kwa nini Shi’ah wanaamini kwamba Mitume ni lazima  wawe  maasum  kabla  ya  utume  wao  vile  vile.  Ingawa  Mitume walikuwa  ni  binadamu  ambao  waliishi  pamoja  na  watu  wengine  na wakashirikiana mambo yao ya kibinadamu, wao walikuwa wakati wote ni watu  waliojipambanua  wanaoheshimiwa  na  watu  na  kupendwa  hata  na maadui  zao.  Kwa  mfano,  Mtume  wa  Uislam  alijulikana  kama  al-Amin (mwaminifu) katika jamii ya kipagani ya Makka, na alikuwa ni mfano bora wa maadili tangu utotoni mwake hadi kufariki kwake. Kwa kweli, maisha adilifu ya nabii yoyote kabla ya kuanza kwa utume wake na kabla ya watu kuja  kumuamini  ni  katika  hali  ya  umuhimu  sana,  kwani  wakati  wenye changamoto sana unakuja wakati nabii anapotaka kuwashawishi watu juu ya  neno  lake;  kama  anaweza  kuaminika  katika  masuala  mengine  yote, anaweza  kustahili  kabisa  kuwataka  imani  zao  kuhisiana  na  Mwenyezi Mungu na dini. Sababu nyingine kwa ajili ya imani juu ya umaasum, inayotumika katika vipindi vyote, kile cha kabla na cha baada ya utume na kile kinachofuatia ni kwamba uteuzi wa Mwenyezi Mungu sio wa holela. Kuzungumzishwa na Mwenyezi Mungu, kupata wahyi na mawasiliano ya moja kwa moja ya papo hapo kutoka kusikoonekana (ghaib), kunadai au kunahitaji kwa kadiri isiyo ya  kawaida hali ambayo inaweza kubebwa tu na mtu mwenye uwezo wa kiroho wa hali ya juu. Qur’ani inasema: “Hakika tutakufunulia maneno mazito.” (73:5). Hakuna anayeweza kufikia nafasi hiyo ya masharti kama ametiwa madoa na imani potofu au dhambi, kwani madhambi yana madhara  kwenye  nafsi  na  kwenye  utakaso  wa  moyo,  hata  kama  yakitendwa bila kukusudia. Mtu anayetenda dhambi kwa bahati mbaya bila kukusudia 99


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 100

U i s l a m u wa S h i a anaweza akasamehewa, kama kwa mfano mtu anayekunywa pombe bila ya kutambua kuwa ni pombe, lakini kosa hilo hata hivyo lina athari ya kawaida juu ya nafsi. Shi’ah kwa hiyo wanauchukulia utume kwa heshima ya hali ya juu sana. Wao wanaamini kwamba Mitume walikuwa wachamungu na wasafi katika maisha yao yote na kwamba walikuwa na kinga ya kutotenda madhambi na vitendo vingine viharibifu kwenye roho zao au kwenye uaminifu wa watu juu yao. Katika hali halisi ya umaasum, Nasir al-Din al-Tuusi, mwanachuoni mkubwa  wa  Shi’ah  ambaye  aliweza  kulinganisha  theolojia  (kalam)  na  falsafa anasema:  “Umaasum  ni  pale  mtumishi  (wa  Mungu)  anapokuwa  na uwezo wa kutenda madhambi, lakini akawa hapendi kufanya hivyo kabisa hata kidogo. Na huku kukosa mapenzi (kwa ajili ya  dhambi)  au  kuwepo  kwa  kitu  ambacho  kinamzuia    yeye kutokana  na  hilo  ni  rehema  za  Mwenyezi  Mungu  juu  yake. Hivyo  yeye  hamuasi  Mwenyezi  Mungu,  sio  kwa  sababu kwamba yeye hawezi kufanya hivyo, bali ni kwa sababu yeye hapendi kufanya hivyo, au kwa sababu kuna kitu kinachofanya kinyume  na  utashi  wake.  Hivyo  ukiangalia  uwezo  wake  (na hiari yake) inawezekana kwake yeye kufanya madhambi, lakini  ukiangalia  ukosefu  wake  wa  nia  au  kuwepo  kwa kipingamizi kinachokwenda kinyume, hilo linawezekana.”81 Al-Iji,  mwanatheolojia  mashuhuri  anayefahamika  sana  wa  ki-Ash’aria anaelezea umaasum kama ifuatavyo: “Kwetu  sisi  (Ash’aria)  umaasum  ni  kwamba  Mwenyezi Mungu  haumbi  ndani  yao  (Manabii)  dhambi  yoyote.  Kwa wanafalsafa,  ni  silika  (al-malakah)  ambayo  ndio  inayomzuia 81 al-Tuusi, Talkhis al-Muhassal, uk. 525. 100


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 101

U i s l a m u wa S h i a mtu  kutokana  na  kutenda  madhambi  na  inasababishwa  na kujua ubaya wa madhambi na ustahilifu wa kumtii Mwenyezi Mungu na inaimarishwa na ukaririwaji wa wahyi wa amri za Mwenyezi Mungu.”82 Wanatheolojia  na  wanafalsafa  wa  Shi’ah  wanaamini  kwamba  kwa  vile Manabii ni binadamu na lazima wawe ni mifano kwa wanadamu, kimsingi  inawezekana  kwa  wao  kufanya  madhambi.  Mitume  sio  kama  malaika ambao hawawezi kutenda madhambi. Hata hivyo, Mitume hao ni wasafi sana  katika  nafsi  zao,  waliozama  katika  kuelewa,  wenye  umaizi  katika tabia  zao  na  wazingativu  kwa  Mwenyezi  Mungu  kiasi  kwamba  ama hawatamani kufanya vitendo vya kiovu wala haiwajii kwao kufanya vitendo  vibaya  kama  hivyo.  Kwa  kweli,  wengi  wetu  ni  wasiotenda  makosa kuhusu  vitendo  fulani,  kama  vile  kula  matope,  kuwapiga  wazazi  wetu, kutembea  uchi  hadharani  ama  kujirusha  wenyewe  kutoka  maghorofani. Ingawa  tunao  uwezo  wa  kufanya  vitendo  vyote  hivyo  hapo  juu,  tunayo aina  ya  kinga  kuhusiana  na  hayo,  kiasi  kwamba  haiwezi  hata  kujitokeza akilini kwetu kufanya mambo ya ajabu kama hayo. Hili linasababishwa na kujiheshimu  kwetu  wenyewe  na  kujali  kwetu,  kwa  upande  mmoja,  na kuelewa kwetu kwa uwazi kwa madhara na ubaya wa vitendo hivyo kwa upande mwingine. Mitume  walikuwa  nayo  kinga  hii  kuhusiana  na  aina  zote  za  dhambi. Walikuwa  pia  hawakutosheka  na  ondoleo  hili  kutokana  na  dhambi  za kawaida.  Kwao  wao,  kushindwa  kumkumbuka  Mwenyezi  Mungu  kwa kitambo  kidogo  tu,  hata  wakati  wa  kutekeleza  majukumu  ya  kijamii kulikuwa  hakukubaliki.  Walivichukulia  vitendo  vingi  vilivyoonekana kama ni vya uchamungu na ibada kwa watu wa kawaida kama visivyotosheleza na walimuomba Mwenyezi Mungu msamaha wakati walipoyatenda  hayo.  Ni  lazima  ifahamike  kwa  hiyo  kwamba  kile  Mitume  walichokichukulia wenyewe kama dhambi juu yao na ambacho kwacho waliomba msamaha hakikuwa ni dhambi kwa maana ya kawaida.  82 al-Ilj, al-Mawaaqif, uk. 262. 101


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 102

U i s l a m u wa S h i a Wakitegemea wenyewe juu ya hoja hizo zilizotajwa hapo juu na mafunzo ya wazi ya watu wa Nyumba ya Mtume, Shi’ah hawakubali riwaya ama simulizi yoyote inayoashiria utendwaji wa madhambi au kitendo chochote na Mitume ambako kunaweza kuwafanya watu kuwadharau au kujiweka mbali nao. Wanachuoni wa Shi’ah wamezichunguza aya zote za Qur’ani ambazo wakati mwingine zinachukuliwa kuashiria vinginevyo na wameonyesha  kwamba  tafsiri  halisi  na  ya  kweli  ya  aya  hizo  hazipingani  na mawazo hayo hapo juu.83 Shi’ah wanayo tathmini ya hali ya juu sana kwa ajili ya Mtukufu Mtume Muhammad  (s.a.w.w.)  na  wanaona  katika  kila  kipengele  cha  tabia  yake kigezo bora na kamili kabisa. “Bila shaka mnao mfano mwema kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu…..” (33:21) Wao wanaamini pia kwamba Maimam (a.s.) lazima wawe na sifa hiyo hiyo ya umaasum. Sababu ya hili ni kwamba Uimam pia ni nafasi inayotolewa kutoka mbinguni ambayo inahitaji kiwango cha hali ya juu sana cha utakaso na cha kiroho. Hakuna anayeweza kuifikia nafasi hii bila ya kuwa huru kabisa  kutokana  na  madhambi  na  vitendo  vichafu.  Kama  ilivyoelezwa hapo juu, hata mambo mengi ambayo yanaruhusiwa kwa ajili ya watu wa kawaida lazima yaepukwe na watu kama hawa, kama vile kuongea sana, au  kula  au  kulala  kupita  kiasi  cha  lazima.  Na  kwa  vile  watu  ni  lazima wawaamini  moja  kwa  moja,  wao  lazima  waepukane  na  kutenda  makosa vilevile. Kwa  nyongeza  ya  aya  2:124,  ambayo  tuliijadili  hapo  juu,  kuhusiana  na watu wa Nyumba ya Mtukufu Mtume (Ahlul-B ayt) Qur’ani inasema:

83 Kwa nyongeza juu ya tafsiri za Qur’ani, vitabu huru vimeandikwa juu ya maudhui hii, kama vile Tanzih al-Anbiyaa cha Sayyid al-Murtadhaa. 102


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 103

U i s l a m u wa S h i a

“ Hakika si mengineyo Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume, na kuwatakasa kabisa kabisa.” (33:33) Qur’ani inatamka wazi kwamba Ahlul-Bayt wa Mtume wamelindwa na pia kutakaswa kutokana na aina zote za uchafu ikiwa ni pamoja na dhambi na tabia mbaya. Wao wako huru, wameepukana kutokana kila kisichopendwa na wanadamu. Kuepukana  na kitendo cha kutenda madhambi ndio ambacho  kwa  hakika  kimelengwa  na  aya  hiyo  hapo  juu;  vinginevyo kusingekuwa na tofauti kati yao na waumini wengine ambao wanajilinda wao wenyewe, kama Qur’ani inavyosema:

“Hakika wale wanaomcha Mwenyezi Mungu, zinapowagusa pepesi za shetani mara hukumbuka, tahamaki wamekwishaona njia.” (7:201) Aya  hii  inaonyesha  kwamba  wale  wachamungu  sio  tu  kwamba  wao hawakusudii kufanya makosa bali pia wao hawadanganywi na Shetani.

103


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 104

U i s l a m u wa S h i a Itikadi juu ya al-Mahdi: Imani juu ya mwokozi atakayekuja mwishoni mwa wakati inachangiwa na dini nyingi. Katika Uislamu, Bwana mkubwa huyu anajulikana kama alMahdi (Muongozaji); yeye atatokeza pamoja na rehema tukufu na ataujaza ulimwengu na haki baada ya kuwa umejazwa dhulma na ukandamizaji.84 Akitoa mukhtasari wa imani za Waislam wote juu ya al-Mahdi (a.s.), Ibn Khaliduun (kafariki 808/1406), anaandika hivi: “Ijulikane kwamba ni tukio lililosimuliwa na Waislam wote katika kila zama, kwamba mwisho wa wakati, mtu mmoja kutoka kwenye familia  ya  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.)  bila  kukosa  atatokeza  na atauimarisha Uislamu na kueneza haki; Waislam watamfuata huyo na atapata umiliki juu ya dola ya Kiislam. Yeye ataitwa al-Mahdi.85 84 Kumekuwepo na vitabu vingi sana vilivyoandikwa na wanachuoni wa Sunni na Shi’ah  juu  ya  al-Mahdi.  Kuna  takriban  wanachuoni  mashuhuri  35  wa  Sunni kwenye  kumbukumbu  ambao  wameandika  vitabu  46  juu  ya  maudhui  hii  pekee. Haya  hapa  ni  majina  ya  baadhi  ya  vitabu  hivyo:  Kitaab al-Mahdi cha  Abuu Dawuud; Alaamaat al-Mahdi cha Jalalud-Din as-Suyuuti; Al-Qawl al-Mukhtasaar fi ‘Alaamaat al-Mahdi al-Muntadhar cha Ibn Hajar; Al-Bayaan fi Akhbaar Sahib al-Zamaan cha Abdillah bin Muhammad Yusuf al-Kanji al-Shafi’i; ‘Iqd al-Durar fi Akhbar al-Imam al-Muntadhar cha  Sheikh  Jamaal  al-Din Yusuf  al-Dimashqi; Mahii Al-i Rasuul cha  ‘Ali  bin  Sultaan  Muhammad  al-Harawi  al-Hanafi; Manaaqib al-Mahdi cha  al-Hafidh  Abuu  Nu’aym  all-Isbahaanii;  Al-Burhaan fi Alaamaat Mahdi Akhir al-Zamaan cha al-Muttaqi al-Hindi; Arba’in Hadith fi alMahdi cha  ‘Abd  al-Alaa  al-Hamadaani;  na  Akhbaar al-Mahdi cha  Hafidh Abu Nu’aym. (Tazama Shi’ah Encyclopedia). 85 Ibn Khalidun, An Introduction to History, uk.257-258. Ni lazima ikumbukwe kwamba  Ibn  Khalidun  mwenyewe  hakuwa  na  moyo  na  wazo  hilo  la  al-Mahdi, lakini bado katika maelezo yake sahihi juu ya wazo hilo yeye anakubali wazi wazi kwamba Waislam wote wanaliamini hilo. 104


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 105

U i s l a m u wa S h i a Wazo  la  mwokozi  atakayeanzisha  kipindi  cha  uadilifu  mwishoni  mwa wakati  limeashiriwa  ndani  ya  aya  nyingi  za  Qur’ani  na  Hadith.  Kwa mfano, tunasoma ndani ya Qur’ani tukufu yafuatayo:

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale ambao wameamini na wakatenda mema kuwa hakika atawafanya makhalifa katika ardhi, kama alivyowafanya waliokuwa kabla yao. Na kwa yakini atawaimarishia dini yao aliyowapendelea na hakika atawabadilishia amani baada ya hofu yao. Wawe wananiabudu, hawanishirikishi …….” (24:55)

“Na hakika tulikwishaandika katika Zaburi baada ya ukumbusho kuwa Ardhi watairithi waja wangu walio wema.” (21:105)

“Na tunataka kuwafadhili waliodhoofishwa katika ardhi na kuwafanya wawe ni viongozi na kuwafanya ni warithi.” (28:5) Ifuatayo  ni  mifano  michache  ya  Hadith  kuhusiana  na  al-Mahdi  zilizosimuliwa na vyanzo vya wote Sunni na Shi’ah: 105


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 106

U i s l a m u wa S h i a 1. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Hata  kama  muda  wote  wa  kuwepo  kwa  dunia  utakuwa  umekwisha,  na  kukawa  kumebakia  siku  moja  tu  (kabla  ya  Siku  ya Kiyama),  Mwenyezi  Mungu  atairefusha  siku  hiyo  kwa  urefu  wa muda ambao utaupa wakati ufalme wa mtu kutoka kwenye familia yangu ambaye ataitwa kwa jina langu.” 86 2. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema vilevile:  “Mahdi ni katika sisi, mtu kutoka kwenye Nyumba yangu (AhlulBayt).  Mwenyezi  Mungu  ataandaa  kwa  ajili  yake  (mambo  yake) katika usiku mmoja.”87 3.  Na tena amesema: “Mahdi  atakuwa  anatokana  na Ahlul-Bayt  wangu,  wa  kizazi  cha Fatima.”88 4. Imesimuliwa pia kutoka kwa Jabir ibn Abdillah al-Ansari kwamba yeye alisema alimsikia Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.) akisema: 86 Sunan at-Tirmidhii,  Kitab  al-Fitan,  Sakhr  ya  2156  na  2157;  na  Sunan Abu Dawuud, Kitab al-Mahdi, Sakhr ya 3733 na 3734. Kwa mujibu wa Abu Dawuud, Hadith  hiyo  inaishia  na:  “Ataijaza  dunia  na  uadilifu  kama  itakavyokuwa  imejaa dhulma  na  ukandamizaji.”  Tazama  pia  Musnad Ahmad, Musnad al-Asharah alMubashshariin bi al-Jannah, Sakhr ya 734, na Sunan Ibn Majah, Kitab al-Jihad, Sakhr ya 2769. 87 Sunan Ibn Majah, Kitab al-Fitan, Sakhr ya 4075, na Musnad Ahmad, Musnad al-Asharah al-Mubashshariin bi al-Jannah, Sakhr ya 610  88 Sunan Abu Dawuud,  Kitab  al-Mahdi,  Sakhr  ya  3735. Tazama  pia  Sunan Ibn Majah, Kitab al-Fitan, Sakhr ya 4076 106


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 107

U i s l a m u wa S h i a “Kikundi  cha  ummah  wangu  kitapigana  kwa  ajili  ya  haki  mpaka karibu na Siku ya Hukumu, wakati Isa mwana wa Mariam atakaposhuka, na kiongozi wao atamwambia aongoze Swala, lakini Isa atakataa  akisema:  ‘Hapana,  hakika  miongoni  mwenu  Mwenyezi Mungu amefanya viongozi kwa ajili ya wengine ili kuupa heshima ummah huu.’”89 Ni jambo la wazi kabisa kwamba al-Mahdi ni tofauti kabisa na Isa mwana wa  Maryam,  ingawa  wote  watakuja  kutokeza  kwa  wakati  mmoja  uleule. Hebu tuzingatie kwamba ndani ya Qur’ani na vyanzo vingine vya Kiislam, neno al-Masih likiwa na maana ya ‘aliyesafishwa, aliyetakaswa,’ ni cheo kwa ajili ya Isa (a.s.). Cheo hiki kinabeba kufanana na neno la Kiingereza la  ‘messiar,’  linalotumiwa  na  Wakristo  kwa  Isa  (Yesu).  Hata  hivyo,  hili neno ‘messiar’ linaweza pia kutumika kuelekea kumhusu yule mfalme na mwokozi  wa Wayahudi,  au  kisitiari  kiongozi  aliyetabiriwa  au  kutarajiwa wa kundi fulani au daawa. Messiah kwa hiyo limetumika katika maandishi fulani  ya  lugha  ya  Kiingereza  kuhusu  vilevile  yule  Mahdi  wa  imani  ya Kiislam,  lakini  hili  lisichukuliwe  kumaanisha  kwamba  al-Mahdi  ni  alMasih  neno  lililohifadhiwa  katika  matumizi  ya  Kiislam  kwa  ajili  ya  Isa (Yesu). Al-Mahdi atakuwa na ujumbe wa ulimwengu mzima, kutoka kwenye nchi za  Kiarabu.  Jina  lake  litakuwa  ni  sawa  na  lile  la  Mtukufu  Mtume Muhammad na atatokana na kizazi cha Fatima binti Muhammad (s.a.w.w.). Shi’ah  wanaamini  kwamba  yeye  ni  mwana  wa  Imam  Hasan  al-‘Askari. Yeye alizaliwa mnamo mwaka 255AH. Aliingia mafichoni (Ghaib) katika mwaka wa 260AH. Yeye yungali hai bado na amehifadhiwa na Mwenyezi Mungu  katika  ghaibu  mpaka  hali  itakapokuwa  tayari  kwa  ajili  ya  kujitokeza  kwake.  Hayo  hayo  yanaaminiwa  na  baadhi  ya  wanachuoni  wa Sunni,  lakini  wengine  miongoni  mwao  wanaamini  kwamba  yeye  bado 89 Sahih Muslim, Kitab al-Imaan, Sakhr ya 225, na Musnad Ahmad, Baqii Musnad al-Mukthiriin, Sakhr ya 14193 na 14595 107


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 108

U i s l a m u wa S h i a hajazaliwa. Sayyid Muhsin al-Amin katika kitabu chake, A‘yaan al-Shi’ah ametaja  mifano  kumi  na  tatu  ya  hao  wanachuoni  wa  Sunni  ambao wanathibitisha  kwamba  al-Mahdi  ni  mtoto  wa  Imam  Hasan  na  kwamba tayari amekwisha kuzaliwa, ikiwa ni pamoja na Muhammad bin Yusuf alKanji  al-Shafi’i  katika  kitabu  chake,  al-Bayaan fi Akhbaar Sahib alZamaan na Kifayat al-Talib fi Manaqib Ali bin Abi Talib; Nur al-Diin Ali bin  Muhammad  al-Maliki  katika  al-Fusuul al-Muhimmah fi Ma‘rifat alA’immah na  Ibn  al-Jawzi  katika  kitabu  chake  mashuhuri,  Tadhkirat alKhawaiss.  Kwa kuhitimisha, tunaweza kutaja ile fatwa iliyotolewa Makka na Muslim World League (Rabitat al-‘Alam al-Islam) mnamo tarehe 11 ya mwezi wa Oktoba,  1976/Shawwaal  23,  mwaka  1396.  Inaeleza  kwamba  zaidi  ya masahaba  ishirini  wamesimulia  riwaya  kuhusiana  na  al-Mahdi  na  inatoa orodha  ya  wanachuoni  wa  Hadith  ambao  wamesimulia  riwaya  hizi,  na vilevile  wale  wanachuoni  ambao  wameandika  vitabu  juu  ya  al-Mahdi. Maandishi yake yanasomeka katika sehemu yake ifuatavyo: “Mahafidh  na  wanachuoni  wa  Hadith  wamethibitisha  kwamba  kuna Hadith sahih na zenye kukubalika (hasan) miongoni mwa riwaya zilizosimuliwa kuhusiana na al-Mahdi. Nyingi ya riwaya hizi zimesimuliwa  kupitia  vyanzo  mbalimbali  (mutawaatir).  Hakuna  shaka  kwamba hadhi ya hadith hizo ni Sahih na mutawaatir, kwamba imani juu ya alMahdi ni wajibu, na kwamba ni moja ya itikadi za Ahlus-Sunnah wa al-Jamaa’ah. Ni wale wasio na elimu ya Sunnah tu na wazushi katika itikadi hiyo ndio wanaoikataa.” 90

90 Angalia kwa mfano Utangulizi wa kwenye al-Bayaan cha al-Kanji al-Shafi’i, Beirut, 1399/1979, uk. 76-79. 108


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 109

U i s l a m u wa S h i a

MLANGO WA NNE MATENDO YA IBADA Matendo makuu ya wajibu ya ibada yanayokubaliwa na Waislamu wote wa Sunni na Shi’ah ni kama yafuatayo: 1. Swala za kila siku: Kila  Mwislamu  kuanzia  wakati  anapopata  balehe  lazima  atekeleze  ibada ya swala tano za kila siku. Kuweza kuanza swala mtu ni lazima achukue udhuu kwa utaratibu ulioagizwa. Kisha mtu anasimama kuelekea Makka na  kufanya  nia  ya  kutekeleza  swala  maalum  ya  wakati  huo  ili  kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu swt. Nia hii lazima ibakie akilini katika muda wote wa swala hiyo. Kama mtu pale mwanzoni ama baadae akisahau kile anachokifanya, au akaswali kwa ajili ya kujionyesha au kwa sababu yoyote ile ya kibinafsi swala yake inakuwa batili. Swala yenyewe hasa inaanza  pale  mtu  anapotamka:  Allahu Akbar (Mwenyezi  Mungu  ni  Mkubwa). Kwa  tamko  hili  yeye  anaingia  kwenye  hali  rasmi  ya  swala  na  kubakia humo hadi atakapomaliza swala yake. Kila swala ina rakaa mbili hadi nne.91 Kila rakaa inajumuisha: a) Kusoma Sura ya kifunguzi cha Qur’ani (al-Fat-ha) ikifuatiwa na Sura nyingine kama vile ile ya Tawhii au Qadr.92 b) Kurukuu na kumtukuza na kumsifu Mwenyezi Mungu katika hali hiyo 91 Swala  ya  asubuhi  (al-Fajr)  ambayo  inaswaliwa  baina  ya  mapambazuko  na kuchomoza kwa jua, ina rakaa mbili, swala ya adhuhuri (Dhuhr) na ile ya mchana (‘Asr) zina rakaa nne, ile swala ya jioni (Maghrib) ina rakaa tatu na ile ya usiku (‘Isha’i) ina rakaa nne. 92 Katika swala ya rakaa tatu na ya rakaa nne, ile rakaa ya tatu na ya nne zina kisomo cha Sura ya kifunguzi cha Qur’ani au kisomo cha dhikiri maalum inayoitwa ‘at-Tasbihat al-Arba’ah’ kisha  kurukuu    na  kusujudu.  Katika  swala  hizi uthibitishaji  wa  upweke  wa  Mwenyezi  Mungu  na  utume  wa  Mtukufu  Mtume Muhammad na kumswalia yeye na kizazi chake vinafanywa kote katika rakaa ya pili na rakaa ya mwisho baada ya salam. 109


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 110

U i s l a m u wa S h i a ya rukuu (kuinama na mikono magotini). c) Kufanya  sajida  mbili    na  kisha  kumsifu  na  kumtukuza  Mwenyezi Mungu. Swala zinamalizika kwa kushahadia kwamba Mwenyezi Mungu ni Mmoja na  hana  washirika  na  kwamba  Muhammad  ni  mjumbe  Wake  na  Mtume Wake pamoja na swala ya mtume na kizazi chake (tashahudi) na kumtakia rehema na amani Mtukufu Mtume, watu wema wote na wale wote ambao wanashughulika katika swala (taslim). Swala za kila siku ndio muundo muhimu sana wa ibada ukumbusho juu ya Mwenyezi Mungu. Qur’ani inasema:

“…..hakika Swala inakataza machafu na maovu. Na hakika dhikri (utajo) ya Mwenyezi Mungu ni kubwa kabisa. Na Mwenyezi Mungu anayajua mnayoyafanya. (29:45). 2. Saumu: Tendo  la  pili  la  ibada  ni  kufunga  (saumu)  katika  mwezi  wa  Ramadhani, mwezi  wa  tisa  wa  kalenda  ya  Kiislam.  Katika  mwezi  huu  kila  Mwislam mtu  mzima  lazima  ajizuie  na  kula,  kunywa  na  vitendo  vya  kujamiiana kuanzia alfajiri hadi machweo ya jua.93 Kama vitendo vingine vya ibada, kufunga  saumu  lazima  kufanyike  kwa  nia  safi  na  halisi,  yaani  ni  lazima ifanyike hasa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu tu na kujikurubisha Kwake. Sambamba  na  kuwa  karibu  na  Mwenyezi  Mungu  na  kupata  radhi  Zake, 93 Makundi kadhaa ya watu huwa yanasamehewa, kama vile wagonjwa au wale walioko safarini. 110


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 111

U i s l a m u wa S h i a kuna faida nyingine nyingi zinazopatikana kutokana na saumu, kama vile kuimarisha dhamira ya mtu, kukumbusha watu juu ya neema za Mwenyezi Mungu  kama  vile  chakula  ambacho  wanakifaidi  kila  siku  na  ambacho wanaweza  kujichukulia  uhakika,  kukumbuka  njaa  na  kiu  ya  Siku  ya Kiyama, kuwasaidia matajiri kuelewa kile kinachowapata watu masikini ili kuzindua  hisia  zao  za  ukarimu  na  huruma,  kudhoofisha  hamu  na  matamanio ya mtu na kujenga uelewa wa kibusara na utambuzi wa kiroho. Kwa maelezo mafupi Qur’an inasema:

“Enyi mlioamini! Mmeandikiwa kufunga kama walivyoandikiwa waliokuwa kabla yenu, ili mpate kumcha Mungu.” (2:183). 3. Kwenda Hijja Makka: Kila Mwislam aliyekwisha kubalehe, na ana uwezo wa kifedha na kiafya ni  lazima  kwa  mara  moja  katika  uhai  wake  atekeleze  ibada  ya  kwenda Hijja  Makka  katika  mwezi  wa  Dhul-Hajj,  mwezi  wa  kumi  na  moja  wa kalenda ya Kiislam. Ndani ya Makka ndio ulipo msikiti muhimu kwa ajili ya  Waislam  ulimwenguni  kote,  Masjid  al-Haraam,  ambao  unazunguka utakatifu wa Ka’aba. Waislam wote wanaelekea kwenye Ka’aba wakati wa swala  zao.  Hiyo  Ka’aba  ni  jengo  la  mchemraba  lililojengwa  na  Nabii Ibrahim  na  mwanawe,  Nabii  Isma’il,  juu  ya  msingi  wa  kile  ambacho mwanzoni kilijengwa na Nabii Adam (a.s.). Kwa kweli, kwa kiasi kikubwa  Hijja  ya  kwenda  Makka  ni  ujenzi  upya  wa  ishara  ya  mfano  wa  kile ambacho Nabii Ibrahim (a.s.) yule mwanatawhidi wa kwanza alichopitia katika  sehemu  hii  hii  takriban  miaka  elfu  nne  iliyopita.  Wakati  Ibrahim (a.s.)  alipowasili  mjini  Makka  baada  ya  safari  ndefu,  aliagizwa  na Mwenyezi Mungu afanye maandalizi kwa ajili ya watu kufanya Hijja hapo Makka. Qur’ani inasimulia zile amri alizozipokea: 111


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 112

U i s l a m u wa S h i a

“……. na uitwaharishe nyumba yangu kwa ajili ya wanaozunguka na wakaazi na wanaorukui na wanaosujudi. Na watangazie watu Hijja; watakujia kwa miguu na juu ya kila mnyama aliyekonda kutoka kila njia ya mbali. Ili washuhudie manufaa yao na walitaje jina la Mwenyezi Mungu katika siku maalum juu ya wanyamahowa aliowaruzuku.” (22:26-28).

Hakika nyumba ya kwanza waliyowekewa watu ni ile iliyoko Makka yenye kubarikiwa na mwongozo kwa viumbe. Humo mna ishara zilizo wazi: Mahali aliposimama Ibrahim. Na mwenye kuingia humo huwa katika amani; Na ni haki ya Mwenyezi Mungu juu ya watu kuhiji nyumba hiyo kwa mwenye kuweza njia ya kuiendea. Na atakayekufuru, basi Mwenyezi Mungu si muhitaji wa viumbe. (3:96-97). Kuhiji Makka kumejaa hali ya uzoefu usiosahaulika, zinazojitokeza sana kati ya hizo pengine ni kutokuwa mbinafsi, udugu, usawa na urahisi. Kila mwaka  mamilioni  ya  Waislam  kutoka  mabara  mbalimbali  wanaziacha 112


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 113

U i s l a m u wa S h i a nyumba  zao,  familia  zao,  shughuli  zao  na  kila  wanachokipenda  sana  na kutoka  kwenda  kwenye  safari  yao  kuelekea  Makka,  mji  uliopo  ndani  ya jangwa.  Kila  mtu  anatakiwa  kuwepo  hapo,  katika  mahali  pamoja  kwa wakati  mmoja,  wote  wakiwa  wamevaa  nguo  namna  moja  na  wakifanya ibada moja hiyo hiyo. Matajiri na masikini, mfalme na mtu wa kawaida, wasomi  na  maamuma,  wote  wanasimama  bega  kwa  bega  na  waliovalia vipande viwili vya nguo nyeupe isiyoshonwa. Yote haya ni jambo ambalo kila mmoja lazima alipitie angalau mara moja katika uhai wake, na kisha ajaribu  kutekeleza  katika  maisha  yake  ya  kila  siku  zile  kanuni  zilizodokezwa katika uzoefu huu (alioupata hijja). 4. Utoaji Sadaka: Kutoa sadaka kumependekezwa sana katika Qur’ani na Sunnah na malipo kwa ajili ya vitendo vya sadaka ni makubwa sana. Ingawa kila kitu ikiwa ni  pamoja  na  mali  za  kifedha  za  mtu  ni  vya  Mwenyezi  Mungu,  Qur’ani inawasilisha utoaji sadaka kama kutoa mkopo kwa Mwenyezi Mungu:

“Ni nani atakayemkopesha Mwenyezi Mungu mkopo mwema, ili amrudishie maradufu, na apate ujira mzuri.” (57:11). Kwa nyongeza juu ya sadaka za hiari, kuna aina fulani za sadaka ambazo ni za wajibu. Kwa mfano, aina moja ya utoaji sadaka ni Zaka, kodi ya mali ya asilimia ndogo tu (kwa kawaida ni asilimia 2.5). Kulipa Zaka sio kutoa zawadi kwa masikini bali ni haki waliyonayo, ambayo ni lazima itimizwe.

“Na katika mali zao ipo haki ya mwenye kuomba na anayejizuia.” (51:19) Imam Ali (a.s.) amesema: 113


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 114

U i s l a m u wa S h i a “Mwenyezi  Mungu  amepanga  riziki  ya  mafukara  katika  mali  ya matajiri. Matokeo yake, wakati wowote mafukara watakapokuwa na  njaa,  ni  kwa  sababu  baadhi  ya  watu  matajiri  wamekataa  na fungu lao.” Na  wale  ambao  umiliki  wao  wa  ngano,  shayiri,  tende,  zabibu,  dhahabu, fedha, ngamia, ng’ombe na kondoo unapita kiwango fulani cha wingi lazima walipe Zaka katika msingi wa kila mwaka kuwapa wale wasiobahatika kuwa nacho miongoni mwa ndugu zao, yatima, wenye kuhitaji, wasafiri na wengineo. Zaka  inaweza kutumika kwa kutoa chakula, makazi, elimu, uangalizi wa afya, makazi ya yatima na huduma nyingine za jamii. Inafaa  kuzingatiwa  kwamba  katika  aya  nyingi,  kutoa  Zaka  kumetajwa baada ya mtu kutekeleza swala yake kama ishara ya dini na imani juu ya Mwenyezi  Mungu.  Kutoa  Zaka    ni  kitendo  cha  ibada,  hivyo  ni  lazima kufanyike  kwa  ajili  ya  Mwenyezi  Mungu  tu.  Kwa  hiyo,  sio  tu  kwamba inawasaidia  wenye  haja  na  kuchangia  kwenye  uimarishaji  wa  haki  za kijamii na maendeleo, bali pia inatakasa kutokana na ubahili na choyo katika nyoyo za wale wanaoitoa. Qur’ani inasema:

“Chukua sadaka katika mali zao uwasafishe na uwatakase kwayo. Na uwaombee rehema……” (9:103) Khumsi: Waislam  wa  Shi’ah  vilevile  wanaamini  katika  kodi  nyingine  ya  wajibu inayoitwa ‘Khums’ ambayo ina maana ya moja ya tano. Ni kodi ya asilimia  ishirini  katika  faida  ya  ziada  ambayo  mtu  anaitengeneza  kwa  mwaka. Mwishoni mwa mwaka wa fedha, mtu analipa asilimia ishirini ya mapato

114


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 115

U i s l a m u wa S h i a yake yote, baada ya matumizi yake ya nyumbani na gharama za biashara.94 Wajibu wa kulipa khums umetajwa ndani ya Qur’ani:

“Na jueni kwamba chochote mlichopata ghanima, basi khumsi yake ni ya Mwenyezi Mungu na Mtume na jamaa na mayatima na masikini na msafiri. Ikiwa nyinyi mmemwamini Mwenyezi Mungu na tuliyoteremsha kwa mja wetu…..” (8:41) Waislamu wa Sunni kwa kawaida wanaamini kwamba aya hiyo inahusiana na kile Waislam wanachokipata kwenye vita tu, yaani ngawira za kivita. Kwa mujibu wa fiqhi ya Shi’ah, nusu ya khums hiyo inamhusu Imam wa Kumi  na  Mbili,  mtu  wa  mwisho  aliyebakia  wa  Nyumba  ya  Mtume (s.a.w.w.) na mrithi wake, na nusu hiyo nyingine inawahusu wale wenye haja miongoni mwa kizazi cha Mtume wanaoitwa Masayyid – (Masharifu kwa  Sunni).  Khums  lazima  itumike  chini  ya  usimamizi  wa  kiongozi  wa kidini wa Shi’ah (Marja‘al-Taqliid), yaani yule faqihi ambaye mtu anamfuata  kuhusiana  na  masuala  ya  matendo  ya  ibada.  Hii  ni  kuhakikisha kwamba inatumika katika njia ambayo inamridhisha Imam al-Mahdi (a.s.). Ile sehemu inayomhusu Imam mwenyewe kwa kawaida inatumika katika seminari za Kiislam na miradi mingine ya kielimu kama vile kuchapisha vitabu vyenye manufaa na kujenga misikiti  na shule.

94  Kuna  masuala  mengine  yaliyotajwa  katika  fiqhi  ya  Shi’ah  ambamo  kulipa khums unakuwa ni wajibu wa lazima. Maoni yaliyotajwa hapo juu ndio ya kawaida kabisa. 115


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 116

U i s l a m u wa S h i a 5. Jitihada kwa ajili ya Mwenyezi Mungu: Kila  Mwislam  anapaswa  kufanya  jitihada  sana  kupambana  kwa  ajili  ya Mwenyezi  Mungu  katika  njia  mbalimbali  ili  kuleta  maendeleo  kwenye maisha ya mwanadamu kwa jumla na hususan kwa maisha binafsi. Qur’ani inasema:

“……Yeye ndiye aliyewaumba kutokana na ardhi na akaifanya iwe koloni lenu…..” (11:61) Kutojiingiza kwenye misiba ya wanadamu au kuwa mvivu katika maisha yake  mtu  binafsi  kunashutumiwa  sana.  Kinyume  chake,  mtu  anayefanya kazi kwa bidii na kupata fedha ya kutumia juu ya familia yake na kuboresha  hali  zao  za  maisha  anachukuliwa  kama  shujaa  katika  kujitahidi  kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, ni Mujtahid. Mfano wa wazi sana na muhimu wa mapambano haya (Jihad) ni kupigana ili kulinda haki na maadili kama ukombozi, uhuru, uadilifu, heshima na msimamo wa ummah wa Kiislam. Qur’ani inasema:

“Wameruhusiwa (kupigana) wale wanaopigwa vita kwa sababu wamedhulumiwa. Na kwa hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kuwasaidia. Wale ambao wametolewa majumbani mwao pasipo haki, ila tu kwa kuwa wanasema Mola wetu ni Mwenyezi Mungu……” (22:39-40). 116


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 117

U i s l a m u wa S h i a

“Na mna nini hampigani katika njia ya Mwenyezi Mungu na ya wale wanaoonewa katika wanaume na wanawake na watoto ambao husema: Ewe Mola wetu! Tutoe katika mji huu ambao watu wake ni madhalimu, na tujaalie mlinzi kutoka kwako.” (4:75) Jihadi vilevile inajumuisha mambo binafsi mengi ambamo familia ya mtu, mali yake, au heshima yake vinaweza kuwa hatarini, kuporwa au kuharibiwa. Kwa mujibu wa Hadith nyingi, mtu anayeuliwa wakati akitetea familia  yake  au  ardhi  anahesabika  kuwa  sawa  na  askari  ambaye  ameuawa kishahidi kwenye uwanja wa vita. Jihadi ni lazima iendelee hadi pale haki itakapopatikana. Qur’ani inasema: Na piganeni nao mpaka kusiwe na fitina, …..” (2:193). Katika kipimo kikubwa, bila shaka vita vimekuwa vikipiganwa mfululizo kuanzia mwanzo wa kuumbwa mwanadamu, vita kati ya wema na uovu, haki na batili, kati ya kundi la Mwenyezi Mungu na la kundi la Shetani. Vita hivi vitaendelea  hadi  mwisho  wa  wakati  pale  ambapo  dunia  itakuwa  imejazwa  na haki na usawa, chini ya himaya ya al-Mahdi (a.s.). Iwapo ipiganwe kwa kalamu, ulimi, silaha au njia nyingine yoyote, jihadi ni kitendo cha ibada, na ni lazima ifanywe kwa nia safi, yaani, kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kwa ajili ya kupatikana kwa haki. Hairuhusiwi kupigana au kupambana kwa ajili ya malengo ya kidunia, kwa ajili ya heshima binafsi au ya kabila lolote lile, mbari au taifa, kwa ajili ya kukalia ardhi ya wengine ili kuwa tajiri zaidi au na uwezo zaidi. Kwa kweli, jihadi kwanza kabisa inaanza ndani ya nafsi ya huyo mujahidi. Ili kuhakikisha kwamba mtu anaweza kushinda vita vya nje dhidi ya maovu, mtu ni sharti kwanza 117


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 118

U i s l a m u wa S h i a apigane na matamanio yake mabaya na hawaa zake, na ni lazima kwanza aukomboe moyo wake mwenyewe kutokana na kuwa makazi ya shetani ili kupata hadhi na heshima ambayo Mwenyezi Mungu (swt.) ameitunuku juu ya wanadamu. Qur’ani inasema:

“Ewe nafsi yenye kutulia, rejea kwa Mola Wako hali ya kuridhia (na) mwenye kuridhiwa. Basi ingia katika waja wangu wema. Na ingia kwenye Pepo Yangu.” (89:27-30). Kwa mujibu wa hadith inayojulikana sana, wakati mmoja Mtukufu Mtume Muhammad  (s.a.w.w.)  aliwaambia  kundi  moja  la  masahaba  zake  ambao walikuwa  wameshinda  vitani:  “Vizuri  sana.  Karibuni  enyi  watu  ambao wamekamilisha jihadi ndogo (al-jihaad al-asghar) na ambao juu yao jihadi  kubwa  (al-Jihad al-akbar)  inabakia  kuwa  wajibu.”  Wakiwa  wameduwaa, masahaba hao, ambao walikuwa wamewashinda maadui na ambao walikuwa  wamejiandaa  kutoa  muhanga  maisha  yao  katika  kuutetea Uislamu,  wakauliza:  “Ni  ipi  hiyo  jihadi  kubwa?”  Mtukufu  Mtume Muhammad (s.a.w.w.) alijibu: “Hiyo jihadi kubwa ni kupambana dhidi ya nafsi  zenu  wenyewe.”  Hivyo  kuzuia  tamaa,  kuikata  nafsi  yake  mtu kutokana na kufanya maovu na kutakasa tumbo lake mtu ndio jihadi kubwa sana na ngumu.  Kwa kumalizia hebu turejee kwenye baadhi ya sifa za wale ambao wanajitahidi  kwa  ajili  ya  Mwenyezi  Mungu  kama  ilivyoelezwa  na  Mwenyezi Mungu Mwenyewe:

118


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 119

U i s l a m u wa S h i a

“Wale walioamini na wakahama na wakapigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, kwa mali zao na nafsi zao, wana cheo kikukbwa mbele ya Mwenyezi Mungu, na hao ndio wenye kufuzu. Mola wao anawabashiria rehema kutoka kwake na radhi na pepo ambazo watapata humo neema zitakazodumu. Watadumu humo milele. Hakika kwa Mwenyezi Mungu kuna malipo makubwa.” (9:20-22). 6. Kuamrisha mema na kukata maovu: Kuamrisha mema (al-amr bi al-ma‘ruuf) na kukataza maovu (al-nahy ‘an al-munkar) ni matendo mawili ya ibada ambayo kila Mwislam aliyebalehe anapaswa  kuyatenda  wakati  wowote  yanapohitajika.  Hakuna  Mwislam anayeweza  kutojali  yanayotokea  katika  ulimwengu  unaomzunguka. Sehemu  ya  wajibu  wa  kijamii  wa  kila  Mwislam  mmoja  ni  kuchunga maadili ya kibinadamu na ya kidini, na wakati wowote moja kati ya hayo kwa  makusudi  likapuuzwa  au  kuvunjwa  ni  lazima  awashauri  na kuwaelekeza  wale  wanaohusika  kwenye  kutekeleza  mema  na  kuacha maovu na matendo ya dhambi. (3:103, 110, 114; 7:199; 9:71, 112; 22:41).

MLANGO WA TANO SIFA ZA JUMLA ZA UISLAMU NA USHI’AH Njia sahihi ya kuuangalia Uislam ni kuutazama kama mfumo. Uislam sio idadi ya imani na matendo ya hapa na pale, wala idadi ya taratibu usio na kiini  cha  uunganishaji.  Bali  ni  mfumo  kamili  ulioshushwa  na  Mwenyezi Mungu kutoa mwelekeo wa vipengele vyote vya maisha ya mwanadamu, 119


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 120

U i s l a m u wa S h i a katika zama zote na katika hali tofauti. Uislam ni mfumo kwa vile una vitu vyote vya asili vinavyohitajika kukidhi mahitaji yote ya mwanadamu katika  kuenea  na  kukamilika  kwake.  Uislam  umeanzisha  maadili  na  njia  za kinadharia  na  kivitendo  zinazohitajika  kuyafikia.  Uwezo  wa  Uislam  wa kushughulika na upana mkubwa wa changamoto na matatizo katika zama zote tofauti na kuleta maendeleo thabiti chini ya mazingira kadhaa ya kiutamaduni, kijamii, kiuchumi na ya kivitendo bila ya kupoteza utambulisho na msimamo wake ni ishara ya kufaa kusiko kifani kwa mfumo wa fikra wa  Uislamu.  Waislamu  ndio  wa  kwanza  kukubali  kwamba  sababu  ya mafanikio haya na nguvu hizi imo ndani ya Uislamu wenyewe na sio ndani yao Waislam au watawala wao. Katika kinachofuata, nitarejea kwenye sifa kuu tatu za Uislam kutoka kwenye mtazamo wa Shi’ah, au kwa kulieleza tofauti, sifa kuu tatu za Uislam wa Shi’ah: kiroho, kimantiki na kutafuta haki.  Bila  shaka,  kuna  nyingine  ambazo  kimantiki  zinapaswa  kuchunguzwa, kama vile uwezo wa mtu, msukumo wa sanaa, sayansi na namna nyingine za ustaarabu, na namna ya ufahamu. Kiroho: Uislam unawahimiza wafuasi wake kwenda zaidi ya mambo ya kimaada ya maisha ya kila siku na kutafuta ile asili hasa ya ya uhai wa mwanadamu na uhusiano wake na dunia isiyoonekana na dunia ya kiroho. Katika kipande cha ushairi kinachohusishwa na Imam Ali (a.s.) mkazo umewekwa juu ya umuhimu  wa  dunia  ya  kiroho  ambayo  binadamu  wanaificha  ndani  yao wenyewe: “Tiba unayo wewe, lakini huoni,  na maradhi ni kutoka kwako wewe, lakini hutambui. Wewe ni kitabu cha waziwazi ambacho  herufi zake hudhihirisha yaliyofichika. Unadhani wewe ni bonge dogo fulani Wakati ambapo ndani yako wewe mnakaa ile dunia muhimu sana?”95 95 Insaan-e Kaamil cha Mutahhari, uk. 203. 120


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 121

U i s l a m u wa S h i a Katika Uislamu, imani juu ya ufufuo na dunia nyingine ni ukweli uliopo daima  uliounganishwa  na  mtazamo  wa  mtu  kwenye  maisha  haya,  sio jambo  lisilo  na  maana  na  lililowekwa  kwenye  mustakabali  ujao  siku  za usoni za mbali kabisa. Ikiligusia hili, Qur’ani inasema:

“Wanajua dhahiri ya maisha ya dunia na wameghafilika na Akhera.” (30:7) Qur’ani inawaalika wanadamu kuchunguza ulimwengu wa kiroho ulioko ndani yao wenyewe kama mlango wa kwenye mambo ya dunia ya kiroho:

“Na hivi karibuni tutawaonyesha alama zetu kwenye peo za macho na ndani ya nafsi zao wenyewe, mpaka iwe wazi kwao kwamba ni kweli.” (41:35)

Na katika ardhi zipo Ishara kwa wenye yakini Na katika nafsi zenu, Je, hamwoni?” (51:20-21). Katika  hadith  maarufu,  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.)  anaunda  kama  ifuatavyo ule uhusiano kati ya elimu ya mtu juu ya nafsi yake na elimu ya mtu juu ya Mwenyezi Mungu: “Yeyote anayejijua yeye mwenyewe (nafsi yake) anamjua Mola Wake.” Uchunguzi wa uhusiano huu, yaani, uhusiano kati ya elimu ya mtu juu ya Mwenyezi  Mungu  na  elimu  juu  ya  nafsi  yake  inarejewa  moja  kwa  moja ndani ya Qur’ani:

121


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 122

U i s l a m u wa S h i a

“Wala msiwe kama wale waliomsahau Mwenyezi Mungu, kwa hiyo akawasahaulisha nafsi zao, hao ndio wavunjao sharia.” (59:19). Kwa hiyo, elimu juu ya nafsi takatifu na ya juu kwa mujibu wa dini yoyote,  yaani  Mwenyezi  Mungu,  imeunganishwa  na  elimu  yake  mtu  binafsi juu  ya  uhalisia  wake  mwenyewe,  ambayo  kwa  hali  yoyote  ile  haiwezi kutambuliwa kwa hali ya kimaumbile ya binadamu, yaani mwili.96 Inapaswa pia kufahamika kwamba elimu ya nafsi ya mtu pekee haitoshi. Baada ya kujua uhalisia wa nafsi, mtu anapaswa kuishughulikia kwa kuielimisha, kuifundisha na kuitakasa. Mchakato wa kulea na kukuza mambo ya kiroho unaweza kuhitimishwa kama ifuatavyo: 1.  Uangalifu  kwa  nafsi  ya  mtu  (kinyume  na  kuipuuza  na  mzamo  katika maisha ya uyakinifu);   2.  Mtu  kuijua  nafsi  yake,  pamoja  na  uhalisia  wake,  akili  timamu, uwezekano na kila chenye kuinufaisha au kuidhuru; 3. Mtu kuitunza nafsi yake.97 Mchakato wa kuitunza nafsi yake mtu inahusisha yafuatayo: a) Kupata imani na dini inayofaa; b) Kujizuia na matendo maovu na kufanya vitendo vya uchamungu; 96 Majlis, Biharul-Anwaar, Jz. 2, uk. 32, namba 22 na Jz. 95, uk. 456, namba 1. 97 Qur’ani inasema: “Enyi mlioamini! Jiangalieni nafsi zenu. Hawawadhuru waliopotea ikiwa mmeongoka. (5:105). Imam Ali (a.s.) anasema: Wakati wowote elimu ya mtu inapoongezeka, mazingatio yake juu ya nafsi yake pia huongezeka na anafanya juhudi zote kuizoesha na kuitakasa. (Mustadrakul-Wasa’il cha Nuuri, Jz. 11, uk. 323, namba 16)

122


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 123

U i s l a m u wa S h i a c) Kuwa na sifa nzuri na kuondoa zile mbaya; d)  Kuendeleza  safari  ya  kiroho  hadi  mtu  anakuwa  mtumwa  wa  kweli anayekutana na Mola Wake.98 Kutegemea katika mafundisho ya Qur’ani na Hadith za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)  na Ahlul-Bayt  wake  (a.s.)  Uislam  una  urithi  mkubwa  sana  wa mambo  ya  kiroho  uliojengwa  karibu  na  mambo  hayo  hapo  juu.  Yeyote anayetaka  kujizoeza  mambo  ya  kiroho  ya  Kiislam  ni  lazima  pia  ajue kwamba  ni  mfumo  uliofunzwa  na  wenye  uzoefu  wa  muda  mrefu, unaopenyeza  vipengele  vyote  vya  maisha.  Katika  Uislam  kila  kitu kimepangwa ili kuhudumia mambo ya kiroho ya mwanadamu na kurahisisha  ukaribu  wake  kwa  Mwenyezi  Mungu,  kutoka  kwenye  vitendo  vya kidini kama vile kuswali na kufunga hadi kwenye mfumo wa kijamii kama vile uchumi wa Kiislam, siasa na sheria za kimahakama. Idadi ya mfano ya riwaya na du’a za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Ahlul-Bayt kuhusiana na matunda ya safari ya kiroho na mchakato wa kupata ukaribu na kukutana na Mwenyezi Mungu sasa utawasilishwa.99 Msaada Kamili wa Mwenyezi Mungu: Katika  Hadith  maarufu,  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.)  anasimulia  kwamba 98 “Kukutana  na  Mwenyezi  Mungu”  (liqa’-ul-lah)  ni  maneno  ya  ndani  kabisa katika  usufi  wa  Kiislamu.  Msemo  huo  una  mizizi  yake  ndani  ya  Qur’ani.  Kwa mfano, Qur’ani inasema: “…..Mwenye kutarajia kukutana na Mola wake, basi na atende matendo mema, wala asimshirikishe yeyote katika ibada ya Mola wake. (18:110). Bila shaka, ni dhahiri kwamba kukutana huko sio kwa kimwili. 99 Kwa  nyongeza  ya  kinachofuata  katika  maelezo  haya,  kumkaribia  Mwenyezi Mungu kuna matokeo mengine kwa kiwango cha mtu binafsi na kwa jamii kwa jumla,  kama  vile  amani,  kujiamini,  furaha,  uhakika  na  neema  za  kimaada.  Hizo zilizotajwa  katika  maelezo  ni  zilizoteuliwa  tu  kwa  sababu  ya  umuhimu  wao  na ukatikati  (centrality) wao.  Kwa  ajili  ya  mjadala  juu  ya  baadhi  ya  matokeo  ya ukaribu na Mwenyezi Mungu, tazama Shomali, 1996, uk. 148-158. 123


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 124

U i s l a m u wa S h i a alimuuliza  Mwenyezi  Mungu  kuhusu  hali  ya  waumini,  na  majibu  ya Mwenyezi Mungu yalijumuisha  yafuatayo: “Hakuna  mmoja  kati  ya  waja  Wangu  anayeweza  kuomba ukaribu na Mimi kwa kile ambacho ni chenye kupendeza sana Kwangu  kuliko  vitu  ambavyo  nimevifanya  kuwa  ni  wajibu kwake.  Kisha,  kwa  kufanya  vitendo  vilivyopendekezwa (nawaafil),  yeye  anaendelea  kupata  ukaribu  na  Mimi,  kiasi kwamba  Mimi  ninampenda.  Wakati  ninapompenda  yeye, nitakuwa  ni  sikio  ambalo  kwalo  yeye  anasikia  nalo,  macho ambayo anaona kwayo, na mkono ambao anapigia nao. Kama akiniita, Mimi nitamjibu wito wake, na kama akifanya maombi, Mimi nitamkidhia.”100 Elimu Kamili: Kuna Hadith nyingi zinazoashiria kwamba moja ya matokeo ya kuwa mtu amepata  ukaribu  wa  kiroho  na  Mwenyezi  Mungu  ni  kujaaliwa  kuwa  na elimu  nyingi  juu  ya  uhalisia  wa  ulimwengu,  ikiwa  ni  pamoja  na  miujiza mingi  ambayo  haiwezi  kujulikana  kwa  njia  za  kawaida  za  kujifunza  na kufundisha.  Tena  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.)  anamnukuu  Mwenyezi Mungu akisema kuhusiana na mja ambaye amepata ukaribu na Yeye: “Nitampenda  wakati  yeye  akinipenda  Mimi  na  nitamfanya apendwe na viumbe Wangu, na nitamfungulia macho yake ya ndani  kwenye  utukufu  Wangu  na  heshima,  na  sitamfichia (elimu  ya)  teule  ya  maumbile  Yangu.  Hivyo  katika  giza  la usiku  na  mwanga  wa  mchana,  Mimi  nitamwambia  siri  ili kwamba  maongezi  yake  na  viumbe  na  maswahiba  zake yatakatika. Nitamfanya ayasikie maneno Yangu na maneno ya malaika  Zangu  na  nitamdhihirishia  siri  nilizozificha  kwa 100 Usuul al-Kafi, Jz. 2, uk. 352 na 353. 124


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 125

U i s l a m u wa S h i a viumbe Wangu.”101 Kujitenga kwa ajili ya kumuabudu Allah: Kutengwa kabisa na kila kitu mbali na Mwenyezi Mungu kuna maana ya kuwa  huru  kutokana  na  kutegemea  juu  ya  kitu  chochote  badala  ya Mwenyezi Mungu, na kukiona kila kitu kama ishara Yake na udhihirisho wa uwezo na huruma. Waja wa kweli wa Mwenyezi Mungu wanaishi ndani ya jamii huku wakibakia wazingatiaji jumla jumla wa Mwenyezi Mungu, na wanamkumbuka Yeye mfululizo. Qur’ani inakisifia kikundi cha watu: “Watu ambao biashara wala kuuza hakuwashughulishi na kumdhukuru Mwenyezi Mungu, na kuisimamisha Swala na kutoa Zaka….. (24:37). Imam Ali na watu wengine wa Nyumba ya Mtukufu Mtume walimuomba Mwenyezi Mungu wakisema: “Mola Wangu! Nifanye niwe nimejitenga na kila kitu mbali na Wewe, na uongoe umaizi wa nyoyo zetu kwa nuru ya kukuangalia  Wewe,  mpaka  uoni  wa  nyoyo  zetu  upenye  mapazia  ya mwanga na ufikie Chanzo na Utukufu na kuziweka nafsi zetu kuwa zimening’inia kwenye fahari ya utakatifu Wako.”102 Lango la kwenye Uwanja wa Nuru: Hadith hizo hapo juu na nyingine nyingi zinarejelea kwenye ukweli kwamba moja ya matokeo ya maendeleo katika njia ya kiroho ni kuondosha giza na  kuingia  kwenye  uwanja  wa  nuru.  Jambo  hili  limeelezewa  wazi  na Qur’ani.103 101 Biharul-Anwaar, Jz. 77, uk. 28 na 29. 102 al-Munaajaat al-Sha’baniyah ndani ya Mafaatiih al-Jinaan. 103 Tazama  kwa  mfano  aya  ya  2:257  na  5:16.  Uwanja  wa  nuru  ni  maudhui muhimu sana katika falsafa ya Kiislam na usufii.  125


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 126

U i s l a m u wa S h i a Mapenzi Makubwa juu ya Mwenyezi Mungu: Sufi’i  sio  yule  anayempenda  Mwenyezi  Mungu  tu,  bali  ni  yule  anayempenda  Mwenyezi  Mungu  peke  yake,  kwa  sababu  kupenda  kwake  ama kuchukia  jambo  lolote  ni  kwa  ajili  ya  Mwenyezi  Mungu  pekee.  Yeye anaridhia na kupenda kile tu ambacho Mwenyezi Mungu, Mpendwa wake anakiridhia  na  kukipenda.  Hana  utashi  au  matamanio  mbali  na  yale  ya Mwenyezi Mungu. Mapenzi ya sufi’i juu ya Mwenyezi Mungu yanapenya kwenye mapenzi yake juu ya kitu kingine chochote kile.104 Imam Ja’far as-Sadiq (a.s.) anasema: “Moyo safi ni ule unaokutana na Mola Wake wakati ambapo upo huru kutokana na mtu mwingine yeyote yule.” Hakuna chochote mbali na kumfikia Mwenyezi Mungu kinachoweza kumridhisha msafiri wa kiroho. Qur’ani inasema:

“Ehe! Kwa kumdhukuru Mwenyezi Mungu nyoyo zinatua.” (13:28) Imam Ali bin Husein, Zaynul-Abidiin (a.s.) anasema: “Hakuna  kitakachopoza  kiu  yangu,  bali  kukufikia  Wewe; kitakachotuliza shauku yangu bali kukutana na Wewe, kitakachopunguza  uchu  wangu  bali  kuuangalia  uso  Wako;  kitakachonituliza  katika  sehemu  yangu  ya  makazi  bila  ya  ukaribu Nawe.”105 104 Kwa maelezo ya kina juu ya mapenzi, tazama Love in Christianity and Islam (2002) cha M. Heydarpoor 105 The Psalms of Islam (zaburi ya Kiislam), uk. 251 na 252. 126


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 127

U i s l a m u wa S h i a Kumshuhudia Mwenyezi Mungu katika kila kitu: Sufi’i ndiye anayemshuhudia Mwenyezi Mungu katika kila jambo. Imam Husein (a.s.) anasema: “Ewe Mola Wangu! Kupitia namna mbalimbali za dalili Zako (katika  ulimwengu  wa  uhai)  na  mabadiliko  katika  hali  na tabia, nilitambua kwamba lengo ni kufanya Wewe ufahamike kwangu  katika  kila  jambo,  ili  kwamba  nisiweze  kukupuuza katika jambo lolote.”106 Imam Ali (a.s.) anasema: “Mimi  sikuangalia  kitu  chochote  ila  nilimuona  Mwenyezi Mungu ndani yake, pamoja nacho na baada yake.”107 Ni dhahiri kwamba uoni huu unaozungumziwa, juu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu umetukuka bila kikomo zaidi ya kadiri ya jicho la kimwili. Shi’ah kwa kauli moja wanaamini kwamba Mwenyezi Mungu hawezi kuonekana kwa jicho la kawaida, ama katika dunia hii au katika ile ijayo ya Akhera. Mjadala uliopita unaonyesha kwamba usufi’i (hali ya kiroho) wa Kiislam umemlenga Mwenyezi Mungu kikamilifu kabisa. Thamani ya mtu, maudhui ya safari hii na bora ya viumbe wa Mwenyezi Mungu, unafafanuliwa na nafasi ambayo anaishikilia katika njia kuelekea kwa Mwenyezi Mungu, kwa kiwango ambacho anacho ama mbali na Yeye au karibu na Naye. Du’a: Moja ya udhihirisho wa usufi’i katika Uislam wa Shi’ah ni du’a, kitendo kilichosisitizwa  sana  ndani  ya  Qur’ani  na  Hadith  za  Mtukufu  Mtume (s.a.w.w.) na Ahlul-Bayt wake (a.s.). Kwa mfano Qur’ani inasema: 106 Du’a ya ‘Arafah katika Mafaatiih al-Jinaan. 107 Sadr al-Din al-Shiraazii, al-Asfaar, Jz. 1, uk. 117, Jz. 4, uk. 479 na Jz. 5, uk. 27. 127


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 128

U i s l a m u wa S h i a

“Sema, Mola wangu asingewajali lau si kupewa kwenu mwito (wa swala)……” (25:77).

“Na waja Wangu watakapokuuliza habari Yangu, Mimi niko karibu. Naitikia maombi ya mwombaji anaponiomba.” (2:186)

“Na Mola wenu amesema: Niombeni nitawaitikia…..” (40:60) Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.)  amesema:  “Du’a  ni  silaha  ya  mu’mini  na  ni nguzo ya dini.” Maimam wa Ahlul-Bayt wa Mtukufu Mtume (a.s.) wamesema: “Bora ya ibada ni du’a.’ ‘Du’a ndio kiini cha ibada,’ ‘Hakika du’a ni tiba kwa aina zote za maradhi.’” Riwaya nyingi za Ahlul-Bayt wa Mtukufu Mtume (a.s.) zinaelezea vipengele mbalimbali vya du’a, kama vile maana yake na lengo, maelekezo juu ya  jinsi  gani  na  lini  ufanye  du’a,  na  vipingamizi  kwenye  kujibiwa  du’a. Kwa  nyongeza,  kuna  matini  nyingi  fupi  na  ndefu  zilizosimuliwa  kutoka kwa  Maimam  wa Ahlul-Bayt  (a.s.)  zilizomo  kwenye  vyanzo  vya  Shi’ah. Mijaladi  kadhaa  imeandikwa  kwa  matokeo  ya  hilo  na  wanachuoni  wa Shi’ah kwa njia ya maelezo juu ya matini hizo. Mkusanyiko wa du’a unaojulikana vizuri katika Uislam kwa jumla ni alSahifatus-Sajjadiah kilichoandikwa  na  Imam  Ali  bin  Husein,  Zaynul128


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 129

U i s l a m u wa S h i a Abidiin  (a.s.).108 Kitabu  hiki  ni  kazi  mahiri  ya  mambo  ya  kiroho  ya Kiislam ambayo inajumuisha mambo ya kitheolojia, kifalsafa na kisaikolojia  vile  vile.109 Kile  kilichoongezea  katika  umuhimu  wa  kitabu  hiki  ni kwamba du’a zote hizo zinahusika na moja ya nyakati muhimu katika historia ya Uislam, yaani, kipindi cha baada ya kifo cha kishahidi cha Imam Husein (a.s.), yule mjukuu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na wafuasi wake pamoja na watu wake 72. Imam Ali ibn al-Husein (mtoto wa Imam Husein ajulikanaye  kama  Zaynul-Abidiin  –  pambo  la  wenye  kuabudu)  alikuwa mgonjwa sana wakati wa tukio la Karbala mwaka 61AH. na alichukuliwa mateka pamoja na dada yake Zaynab, mjukuu wa kike wa Mtukufu Mtume na  wanawake  wengine  na  watoto  wa  familia  yake.  Kuanzia  kuachiwa kwake baadae hadi mwisho wa uhai wake, au kwa usahihi zaidi, mpaka  Katika kumtukuza Mwenyezi Mungu  Rehma na amani juu ya Muhammad na Ahlul-Bayt wake Rehma na amini kwa Wabebaji wa Arshi     Rehma na amani kwa Wathibitishaji wa Arshi Du’a yake kwa ajili yake na marafiki zake maalum Du’a yake wakati wa asubuhi na jioni Du’a yake kwa ajili ya kazi zenye wasiwasi Du’a yake kwa ajili ya kutafuta hifadhi Du’a yake kwa ajili ya shauku Du’a yake kwa ajili ya kutafuta kimbilio kwa Mwenyezi Mungu Du’a yake kwa ajili ya matokeo mazuri Du’a yake kwa ajili ya kukiri Du’a yake katika kutafuta mahitaji Du’a yake katika matendo maovu Du’a yake wakati akiwa mgonjwa Du’a yake kwa ajili ya kuomba kutolewa katika dhambi Du’a yake dhidi ya Shetani 108 Kitabu  hiki  kimetafsiriwa  kwa  Kiingereza  zaidi  ya  mara  moja. Tafsiri  iliyo nzuri zaidi ni ile ya William Chittick kwa jina la The Psalms of Islam. 109 Al-Sahifah as-Sajjadiah kimetengenezwa na Du’a 54 kama zifuatazo: 129


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 130

U i s l a m u wa S h i a Du’a yake wakati wa hatari Du’a yake kwa ajili ya kuomba mvua wakati wa ukame Du’a yake kwa ajili ya tabia tukufu za kimaadili Du’a yake wakati alipohuzunishwa na jambo Du’a yake wakati wa dhiki Du’a yake kwa ajili ya afya njema Du’a yake kwa ajili ya wazazi wake Du’a yake kwa ajili ya watoto wake Du’a yake kwa ajili ya majirani na marafiki Du’a yake kwa ajili ya watu wa mipakani Du’a yake katika kukimbia Du’a yake wakati mahitaji yake yalipopungua Du’a yake kwa ajili ya msaada katika kulipa madeni Du’a yake kwa ajili ya kutubia Du’a yake katika swala ya usiku Du’a yake kwa ajili ya kuomba lililo bora Du’a yake wakati anapokuwa matesoni Du’a yake katika kuridhika na amri za Mwenyezi Mungu Du’a yake wakati anaposikia mlio wa radi Du’a yake kwa ajili ya kutoa shukurani Du’a yake kwa ajili ya kuomba msamaha Du’a yake kwa ajili ya kutafuta maghfira Du’a yake wakati kifo kilipotajwa Du’a yake kwa ajili ya kuomba kinga na ulinzi Du’a yake katika kumaliza usomaji wa Qur’ani Du’a yake wakati alipouangalia mwezi mwandamo mpya Du’a yake kwa ajili ya ujio wa mwezi mtukufu wa Ramadhani Du’a yake kwa ajili ya kuuaga mwezi wa Ramadhani Du’a yake kwa ajili ya siku ya Iddi na siku ya Ijumaa Du’a yake kwa ajili ya Siku ya Arafah Du’a yake kwa ajili ya siku ya kutoa kafara na siku ya Ijumaa Du’a yake kwa ajili ya kuzuia hila za maadui Du’a yake wakati wa hofu 130


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 131

U i s l a m u wa S h i a Du’a yake katika kukiri makosa na udhalili Du’a yake katika kusihi Du’a yake katika kujishusha yeye mwenyewe Du’a yake kwa ajili ya kuondokewa na usumbufu

Kuuliwa  kwake  kishahidi,  Imam  Zaynul-Abidiin  na  wafuasi  wake  waliwekwa kwenye kifungo na uchunguzi. Chini ya mazingira haya, kutunga matini  za  du’a  kulitumika  kama  njia  inayofaa  kwa  ajili  ya  kuwasilisha mafundisho sahihi ya Kiislam na mambo ya kiroho (Usufi’i). Mtu anaweza akaona tena ni jinsi gani usufi’i katika Uislam ulivyofungamana na wajibu wa  kijamii;  Mwislam  wa  kweli  katika  nyakati  zake  za  faragha  kabisa  za swala hawezi kupuuza kile kinachotokea katika mazingira yanayomzunguka au kutokujali wajibu wake wa kijamii. Mantiki: Moja ya mambo muhimu katika masomo ya kidini na katika falsafa ya dini ni  kufafanua  wajibu  wa  mantiki  na  uhusiano  wake  na  wahyi.  Kama tulivyokwisha  kuona,  Uislam  unachukulia  mantiki  kama  moja  ya  neema kubwa sana iliyotolewa na Mwenyezi Mungu kwa binadamu. Ni kwa njia ya mantiki kwamba tunajielewa sisi wenyewe na dunia iliyotuzunguka sisi. Ni  kwa  njia  ya  mantiki  kwamba  tunatambua  umuhimu  wa  kuchunguza asili yetu na Yule aliyetuumba. Lau tusingekuwa na mantiki, tusingekuwa tunawajibika kwa ajili ya vitendo au imani zetu. Katika Uislam wa Shi’ah hususan, msisitizo mkubwa umekuwa wakati wote ukiwekwa juu ya mantiki na elimu ya mantiki. Msisitizo huu unatokana na Qur’ani na hadith za Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.)  na  Maimam  wa  Ahlul-Bayt  yake.  Qur’ani inasema katika aya mbalimbali:

“Hakika katika hayo kuna ishara kwa watu wanaotia akilini (mambo).” (13:4; 16:12; 30:24 131


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 132

U i s l a m u wa S h i a Qur’ani vilevile inawalaumu zaidi ya mara moja wale ambao hawafikiri au kutumia  mantiki.  Riwaya  ifuatayo,  iliyochaguliwa  kutoka  kwenye  idadi kubwa  ya  hadith  zinazopatikana  juu  ya  jambo  hili,  inaonyesha  nafasi  ya mantiki katika itikadi ya Shi’ah. Imam Ja’far as-Sadiq (a.s.) anasema: “Yeyote  mwenye  akili  anayo  imani  na  kila  mwenye  imani ataingia Peponi.”110 Kwa  kuwa  na  mantiki  mtu  anakuja  kuelewa  ukweli,  kuamini  Uislam  na kufuata  mafundisho  ya  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.),  na  hatimaye  mtu atakuwa na uwezo wa kuingia Peponi. Katika riwaya yenye umaizi mkubwa akizungumza na mmoja wa wafuasi wake, Hishaam bin Hakam, Imam Musa Kadhiim (a.s.) amesema:  “Kwa  mantiki  Mwenyezi  Mungu  anakamilisha  hoja  Yake. Mwenyezi  Mungu  amewaandaa  Manabii  Wake  pamoja  na uwezo  wa  kuelezea  maoni  yao  katika  namna  ambayo  watu wote  wataweza  kuelewa.  Mwenyezi  Mungu  amewaonyesha watu umola Wake kupitia mantiki.’ Halafu Imam akasoma aya hii ya Qur’ani tukufu: “Mungu wenu ni Mungu Mmoja, hakuna  mungu  isipokuwa  Mwenyezi  Mungu  ambaye  Mpole  na Mwenye rehema ….. Hakika katika kuumba mbingu na ardhi na katika kupishana kwa mchana na usiku, na katika merikebu zinazosafiri  baharini,  na  katika  mvua  inayoshuka  kutoka mawinguni kuleta uhai juu ya ardhi, na aina zote za wanyama ambao  Mwenyezi  Mungu  amewaeneza  juu  ya  ardhi,  na  pia katika mwenendo wa upepo na mawingu ambavyo Mwenyezi Mungu  ameviweka  baina  ya  ardhi  na  mbingu  –  katika  vyote hivi kuna ishara kwa wale wenye kufikiri.” Kisha Imam (a.s.) akasema:  ‘Mwenyezi  Mungu  amezifanya  ishara  hizi  kuwa hoja  ya  kuwaonyesha  watu  kwamba  wao  wanaye  Muumba Ambaye  anapanga  kila  kitu  kwa  ajili  yao  na  Ambaye anakielekeza  kila  kitu,  kwa  sababu  kisha  Mwenyezi  Mungu 110 Usul al-Kafii, Jz. 1, uk. 11 132


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 133

U i s l a m u wa S h i a anasema: “Hakika kuna ishara katika mambo haya kwa wale wanaotumia mantiki.’”111 Rejea  nyingine  nyingi  kwenye  Qur’ani  zimefanyika  katika  riwaya  hii, ambazo zinaonyesha kwamba Mwenyezi Mungu katika ujumbe Wake wa mwisho anachukulia mantiki kama njia pekee ambayo kwayo wanadamu wanakuwa wanawajibika na kuja kuelewa ukweli. Maswali yote Siku ya Kiyama ni yenye kuwiana na uwezo wa kimantiki wa watu. Wale ambao wamepewa elimu kubwa zaidi wao wataulizwa kwa kina zaidi kuliko watu wa kawaida. Moja ya kazi za msingi za mantiki ni kutuelekeza kwenye ukweli wa dini. Shi’ah wanaamini kwamba matumizi ya mantiki ndio njia pekee ambayo mtu  anaweza  kuja  kuelewa  kwamba  Mwenyezi  Mungu  yupo,  kwamba Yeye  amewatuma  watu  maalum  kama  Mitume Wake  na  kwamba  ufufuo utakuja kutokea. Kwa hakika ni wajibu wa kila Mwislam kuchunguza na kuhoji  itikadi  zake  mpaka  apate  uhakika,  na  awe  na  uwezo  wa  kutetea itikadi zake kwa hoja za kimantiki. Waislam hawaruhusiwi kusema kwamba  wanamuamini  Mwenyezi  Mungu  bila  ya  sababu  yoyote  maalum  ama kujiita  Waislam  kwa  sababu  tu  wazazi  wao  ni  Waislam  au  kwa  sababu wamezaliwa kwenye jamii ya Kiislam. Imani ni jambo la kifikira na sio la kuigiza. Kila mmoja anashauriwa kupata imani yake kwa hoja madhubuti. Kwa njia hii, mtu anaweza kujiamini katika imani yake, na hakuna kinachoweza kumsababishia shaka ndani yake.  Jambo jingine linaloibuka kuhusiana na kazi ya mantiki ni katika kuelewa maadili  mema  na  mabaya,  au  lipi  la  sawa  na  lipi  la  makosa.112 Hii imekuwa ni mada muhimu inayohusika kwa ajili ya riwaya za kidini, hususan Ukristo na Uislam. Kwa mujibu wa “Nadharia ya Amri za Mwenyezi 111 Usul al-Kafii, Jz. 1, uk. 13 112 Ifahamike kwamba mantiki hapa inajumuisha kile ambacho kwa kawaida linajulikana  kama  dhamira  njema.  Kwa  maelezo  ya  kina  zaidi,  tazama  mjadala  wa wanafalsafa wa Kiislam kuhusu mantiki ya kivitendo au hekima ya kiutendaji. 133


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 134

U i s l a m u wa S h i a Mungu”  ‘wema’  au  ‘sawa  kimaadili’  ina  maana  ya  “yaliyoamrishwa  na Mwenyezi  Mungu”  na  ‘mbaya’  au  ‘ovu  kimaadili’  ina  maana “lililokatazwa  na  Mwenyezi  Mungu.”113 Kwa  upande  mwingine,  baadhi ya wanatheolojia vilevile wamehojiana kwa ajili ya mtazamo wa kimantiki kwenye maadili. Wao wanaamini kwamba kuna vigezo huru vya wema na  uovu  ambavyo  vinaweza  kueleweka  kwa  mantiki  zetu.  Kwa  maneno mengine, muumini wa kidini huwa hana njia ya kipekee ya kwenye ukweli wa  kimaadili.  Mwenyezi  Mungu  amewafanya  watu  wote  wenye  kuweza kufikiri.  Kwa  wote,  muumini  na  asiye  muumini,  kufanya  uamuzi  wa maana  wa  kimaadili  ni  suala  la  kusikiliza  mantiki  na  kuifuata. Amri  za Mwenyezi  Mungu  sio  zisizo  na  msingi  na  tunaweza  kutumia  mbinu  za kimantiki  ili  kugundua  kanuni  za  maadili.  Miongoni  mwa  wanatheolojia wa Kiislam, Ash’ari walishikilia maoni hayo mwanzoni, na Mu’tazilah na Shi’ah wameshikilia haya ya baadae.114 Kwa  mujibu  wa  Ash’ariah,  maadili  yote  yanaamuliwa  kwa  mapenzi  ya Mwenyezi Mungu, na dhana za maadili kama vile ‘wema’ na ‘haki’ hazina maana zaidi ya ‘kile apendacho Mwenyezi Mungu’ au ‘kile kilichoamriwa na  Mwenyezi  Mungu.’  Haya  maneno  ‘wema’  na  ‘haki’  hayana  maana yenye  lengo.  Kwa  mujibu  wa  Shi’ah  na  Mu’tazilah  hata  hivyo,  maadili kama vile uadilifu na wema yana uhai halisi, ulio huru kutokana na hiari 113 Kuhusu hili, George Hourani anasema: “Sio [maoni ya Ash’ariah, au kile anachokiita ‘udhahinia wa ki-mungu mmoja,’ (theistic subjectivism), au kile ambacho wengine  wamekiita  ‘uhiari  wa  kimaadili’  (ethical  voluntarism)]  ya  kipekee  kwa Uislam, kwa vile inatokea katika Uyahudi wa zama za kati na mara kwa mara katika fikra za Magharibi; lakini huenda kwa kweli ilikuwa maarufu na kuenea sana katika  Uislam  kuliko  kwenye  ustaarabu  mwingine  wowote  ule”  ‘Reason na Tradition in Islamic Ethics,’ uk. 57. 114 Mbali na baadhi ya tofauti kati ya Shi’ah na Mu’tazilah, wote wanaitwa Ahl al-‘adl – ‘watu wa uadilifu’, kwani wote wanaamini katika maadili mema huru na uwepo wa vigezo vya kimantiki kwa ajili ya kuamua lipi ni jema na lipi ni baya, na  wanautetea  kwa  nguvu  sana  uadilifu  wa  Mwenyezi  Mungu,  kwa  kutegemea itikadi ya katika viwango vya wema na ubaya vilivyo huru na kiadilifu. 134


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 135

U i s l a m u wa S h i a ya mtu yoyote, hata ya Mwenyezi Mungu, kwa vile maadili yana malengo. Kutegemea jambo hilo hapo juu, ubishani mwingine umeibuka kuhusiana na  swali  la  endapo  wema  au  uovu  unaeleweka  kimantiki  (al-husn wa’lqubh al-‘aqliyaan)  au  kupitia  wahyi  –  ufunuo.  Shi’ah  na  Mu’tazilah wanaamini  kwamba  wema  na  uovu  una  shabaha  na  kwa  hiyo  unaweza kujulikana kwa kutumia akili. Allamah al-Hilli, mwanachuoni mkubwa wa Shi’ah  katika  maelezo  yake  juu  ya  kitabu  Al-Yaquut cha  al-Nawbakhtii anaandika: “Kanuni ambamo matatizo yanayohusiana na haki yanategemea ni kwamba  Mwenyezi  Mungu  ni  Mwenye  Hekima; Yeye  kamwe  hafanyi  vitendo viovu, wala Yeye hashindwi kutekeleza kitendo chochote cha wajibu. Pale kanuni hii inapothibitishwa, maswali kuhusu uadilifu, kama vile uzuri wa wajibu (taklif), umuhimu wa huruma (lutf) na mengine kama hayo yanaundwa juu yake. Na kwa vile kanuni hii inategemea juu ya elimu ya wema na uovu na mantika zao, mwandishi, yaani Nawbakhti alianza mjadala pamoja na haya.”115 Mahali pengine anaandika hivi: “Maimam na wafuasi wao, na Mu’tazilah, wanaamini kwamba wema na uovu wa baadhi ya vitendo yanafahamiwa na akili kwa dhahiri, kama vile elimu  yetu  ya  wema  au  manufaa  ya  kusema  kweli  au  uovu  wa  uongo wenye  madhara,  ambao  hakuna  mtu  mwenye  akili  anayeutilia  shaka,  na uhakika  wake  kuhusu  hili  hauna  upungufu  kuliko  uhakika  wake  kuhusu mahitaji  ya  nafsi  isiyo  na  hakika  (katika  uhai  wake)  juu  ya  chanzo  au kuhusu usawa wa vitu viwili ambavyo vyote viko sawa na kitu cha tatu. Wao wanaamini kwamba kuna baadhi ya vitendo ambavyo uzuri au uovu wake  unaweza  kufahamika  kwa  kutafakari,  kama  vile  ubora  wa  kusema ukweli wenye madhara na uovu wa uongo wenye manufaa, na mwishowe kwamba kuna baadhi ya vitendo ambamo akili inashindwa kutoa uamuzi, 115 Al-Hilli, uk. 104. 135


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 136

U i s l a m u wa S h i a na  wema  wake  au  uovu  wake  ni  wa  kutangazwa  na  sheria  ya  kidini (Shar’iah) kama vile jinsi ya kutekeleza vitendo vya ibada.”116 Kwa  upande  mwingine, Ash’ariah  wanakanusha  ile  mantiki  ya  wema  na uovu  kwa  pamoja.  Shahristaani  katika  kitabu  chake,  Al- Milal wa alNihaal anayaelezea maoni yao kama ifuatavyo: “Masuala  yote  ya  wajibu  lazima  yasomeke  kutoka  kwenye wahyi. Akili  haifanyi  jambo  lolote  kuwa  wajibu  na  haifanyi jambo lolote kustahili kuchukuliwa kama jema au baya. Hivyo kumjua Mwenyezi Mungu kunawezekana kiakili na kunakuwa wajibu  kwa  maandiko  (sam‘).  Mwenyezi  Mungu, Aliye  Juu kabisa,  anasema:    “…..Wala sisi hatuadhibu mpaka tupeleke Mtume.” (17:15). Hali  kadhalika  shukurani  kwa ajili  ya  rehema  iliyotolewa,  kumlipa  mtiifu  na  kumuadhibu muovu kunakuwa wajibu kwa wahyi na sio kwa mantiki.”117 Kinyume  chake,  Shi’ah  na  Mu’tazilah  wamehoji  kwamba  sisi  tumepewa uwezo wa kuelewa ni nini ndio wema na nini ni uovu. Hata wale ambao hawaamini  dini  yoyote  wanaelewa  angalau  maadili  mema  ya  msingi  na kwa hiyo wanawajibika kimaadili. Kama wema na uovu vingeamuliwa na dini tu na sio kupatikana kwa mantiki, makafiri wasingeyatambua hayo leo hii  au  kabla  ya  kuufahamu  wahyi.  Lakini  tunajua  kwamba  kuna  maadili mengi na kanuni za kimaadili zinazochangiwa na waaminio mungu mmoja na  wakanushaji  wao.  Abd  al-Jabbaar,  mwanatheolojia  mashuhuri  wa Mu’tazilah  anasema:  “Mtu  yoyote  mwenye  akili  timamu  anajua  wajibu wake hata kama hajui kama kuna Muamrishaji na Mkatazaji.”118 Shi’ah na Mu’tazilah wamehoji vilevile kwamba kama tusingekuwa uhuru kama  huo  wa  kuelewa,  tusingeweza  kuamua  juu  ya  unyofu  wa  madai 116 Al-Hilli, uk. 82. 117 Al-Shahristaanii, Jz. 1, uk. 115. 118 Abd al-Jabbaar, Al-Mughnii fi al-Tawhiid wa al-‘Adl, Jz. 1, uk. 45 136


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 137

U i s l a m u wa S h i a yaliyofanywa  na  Manabii,  kwa  sababu  mtu  angeweza  kufikiria  kwamba inawezekana kwa Mwenyezi Mungu kutoa nguvu ya miujiza kwa Manabii wa uongo. Ni akili zetu zinazotuambia sisi kwamba kuwapotosha watu ni makosa na kwamba Mwenyezi Mungu, Mwenye Hekima, Mwenye rehema, ambaye anathibitishwa na akili kule kuwepo Kwake, anafahamika kwa kutokufanya kosa lolote kamwe. Itakuwa ni maagizo (sekula) kuwaambia wale ambao kwamba hawajapata bado ukweli wa dini  kwamba Mwenyezi Mungu kamwe hapotoshi, kwa sababu Yeye Mwenyewe au Qur’ani imelitangaza hili kuwa ndio hali halisi. Qur’ani yenyewe kwa kweli inadokeza katika kauli nyingi kwamba elimu ya kile ambacho ni wajibu, wema na uovu ni yenye kufikiwa na kila mtu. Hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha uadilifu na hisani na kuwapa jamaa na anakataza uchafu na uovu na dhulma…..” (16:90). Wema na uovu huu lazima uwe umetambulika kama hivyo kabla ya wahyi. Upekee wa  manufaa  ya  kimaadili  unathibitishwa  mwote  katika  Qur’ani.  Kwa mfano,  ile  amri  ya  Mwenyezi  Mungu    iliyokaririwa  mara  kwa  mara  ya kufanya  kilicho  sawa  ingekuwa  haina  nguvu  na  mzinduko,  kama  yote vilivyomaanisha  vilikuwa  ni  “Kufanya  kile  Mungu  alichowaamrisha kufanya.” Ingekuwa ni vigumu zaidi kuleta maana kwa kauli za kwamba Mwenyezi Mungu wakati wote ni mwadilifu kwa waja wake kwa kukisia kwamba “haki” maana yake ni “kilichoamrishwa na Mwenyezi Mungu.” Hakuna chochote kati ya haya, kwa kweli, ambacho kinamaanisha kwamba  binadamu  hawahitajii  muongozo  wa  kidini.  Hoja  ni  hasa  kwamba  ili kunufaika kikamilifu kutokana na mwongozo wa kidini, wanadamu wamejaaliwa  na  akili,  na  ni  wakati  ule  tu  wanapokuwa  na  fikira  na  mantiki kwamba  wanaweza  wakauelewa  wahyi.  Ukweli  wa  dini    na  kanuni  za kimaadili  vinaeleweka  kwa  akili,  lakini  kuna  mengi  zaidi  ya  kujifunza kutoka  kwenye  wahyi.  Kulingana  na  wanafikra  wa  Shi’ah,  dini  inaweza kutupatia maelezo kamili zaidi na mapana juu ya maadili, na zaidi ya hayo kutuhamasisha sisi kutekeleza mahitaji ya maadili.

137


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 138

U i s l a m u wa S h i a Juu ya nafasi za sayansi za kisomi miongoni mwa Shi’ah, Yann Richard anaandika:   “Leo hii hata hivyo, moja ya upekee wa ajabu wa Uislam wa Shi’ah  ni  kule  kutambua  kwamba  metafizikia  (falsafa  ya kuchunguza chanzo cha uhai na maarifa) na hotuba za kifalsafa  vina  nafasi  fulani  katika  elimu  ya  kidini.  Kituo  cha Masomo  ya  Kitheolojia  huko  Qum  kwa  hakika  ndio  sehemu pekee  ya  masomo  ya  Kiislam  ulimwenguni  ambapo  mtu anathubutu  kutoa  maoni  juu  ya  maandiko  ya  kifalsafa  ya Aristotle  au Avicenna,  na  ambako  ile  desturi  ya  kifalsafa  ya baada  ya  Plato  imebakia  kuwa  hai.  Ayatollah  Khomeini alikuwa anajulikana hapo Qum tangu miaka ya 1950 kwa ajili ya uelekeo wake wa falsafa.”119 Katika  mfululizo  na  maendeleo  ya  desturi  hiyo  ya  falsafa,  S.M.H. Tabataba’i (1892-1981), mwenyewe akiwa bingwa maarufu sana wa zama hizi juu ya falsafa ya Kiislam anaandika hivi: “Kwa  namna  ileile  ambayo  kuanzia  mwanzo  Ush’ah ulichukua jukumu lenye nguvu sana katika uundaji wa mawazo ya kifalsafa ya Kiislam, lilikuwa vile vile ni jambo kuu katika maendeleo ya ziada na ulinganiaji wa falsafa na sayansi za Kiislam ….. Kwa namna hiyohiyo, katika sayansi nyingine za kisomi, walijitokeza watu maarufu wengi kama vile Nasiir AlDin  Tuusii  (ambaye  alikuwa  na  mwanafalsafa  na  pia mwanahisabati)  na  Birjandi,  ambaye  pia  alikuwa  ni mwanahisabati mashuhuri. Sayansi  zote,  hususan  metafizikia  au  theosofia  (falsafah-i ilaahii au  hikmat-i ilaahii)  zilileta  maendeleo  makubwa, shukurani  kwa  juhudi  zisizo  na  kuchoka  za  wanachuoni  wa 119 Richard, uk. 61 138


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 139

U i s l a m u wa S h i a Shi’ah. Ukweli huu unaweza kuonekana kama mtu atalinganisha  kazi  za  Nasiir  al-Din Tuusii,  Shams  al-Din Turkah,  Mir Daamaad  na  Sadr  al-Din  Shiraazii  pamoja  na  maandiko  ya wale waliokuja kabla yao.120 Utafutaji wa Uadilifu: Moja ya itikadi kuu za Shi’ah ni uadilifu. Mwenyezi Mungu ni mwadilifu na kamwe hafanyi dhulma au kinyume na kigezo cha uadilifu. Uadilifu wa Mungu unajulikana kwa akili na unathibitishwa na wahyi. Qur’ani tukufu inasema:

“Hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha uadilifu, hisani na kuwapa jamaa …….” (16:90) Ni wajibu wa kila mtu kutekeleza uadilifu pote katika maisha yake binafsi na  yale  ya  kijamii.  Mwislam  ni  mtu  ambaye  ni  mwadilifu  kwake  yeye mwenyewe,121 kwa  mkewe  na  watoto122 na  kwa  kila  mtu  mwingineo, ikiwa ni pamoja na maadui.123 Kwa mujibu wa fiqhi ya Shi’ah, kuna nafasi 120 Tabataba’i, Shi’it Islam, Jz. 2, ‘Outstanding Intellectual Figures of Shi’ism’ (Wasomi Mashuhuri wa Ushi’ah.) 121 Katika falsafa ya maisha ya Kiislam, yeyote anayemuasi Mwenyezi Mungu amejidhulumu  mwenyewe.  Qur’ani  inasema:  “….. na anayeruka mipaka ya Mwenyezi Mungu, basi hakika amejidhulumu nafsi yake, …..” (65:1). 122 Kwa  mujibu  wa  Hadith,  ambayo  ziko  nyingi  kama  hiyo:  “Hakuna  kinachomkasirisha Mwenyezi Mungu zaidi kuliko dhuluma juu ya wanawake na watoto.” 123 Waislam wanatakiwa kushughulika kwa uadilifu na wema hata kwa maadui zao.  Qur’ani  inasema:  “Wala kuchukiana na watu kusiwapelekee kutofanya uadilifu. Fanyeni uadilifu ndiko kunakokurubisha kwenye takua……” (5:8). 139


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 140

U i s l a m u wa S h i a nyingi  za  kidini  au  siasa  na  kijamii  ambazo  zinahitaji  mwenye  kushika nafasi  hizo  kuwa  mwadilifu.  Kwa  mfano,  wale  wanaoongoza  swala  za jamaa ama swala za Ijumaa, mashahidi, mahakimu, viongozi wa kidini na watawala, wote hawa ni lazima wawe waadilifu. Katika Uislam, serikali inachukuliwa kama njia isiyobadilishika ya kusimamisha na kulinda uadilifu wa jamii. Jamii adilifu inaweza kuendelezwa tu  kwa  mgawanyo  mzuri  wa  madaraka  na  mali.  Zifuatazo  ni  baadhi  ya Hadith kuhusiana na jambo hili kutoka kwa Bwana Mtume (s.a.w.w.) na Ahlul-Bayt wake (a.s.): 1.  Katika mwaka wa kutekwa Makka, mwanamke mmoja kutoka kwenye familia tajiri na maarufu alifanya wizi. Bwana Mtume (s.a.w.w.) akaamua  kumuadhibu  yeye.  Watu  wa  familia  yake  na  baadhi  ya  watu wengine walikwenda kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kumuombea msamaha.  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.)  hakuyakubalia  maombi  yao  na akawakusanya  watu  pamoja,  akisema  kwamba  ummah  zilizotangulia ziliangamia kwa sababu walifanya ubaguzi dhidi ya masikini na watu wa hali ya chini.  2.  Akielezea ni kwa nini aliukubali Ukhalifa baada ya kifo cha Khalifa wa tatu, Imam Ali (a.s.) anasema: “Tazameni!  kwa  Yule  anayepasua  nafaka  (ili  kuota)  na aliyeumba  viumbe,  kama  watu  wasingenijia  mimi  na waungaji  mkono  wasingeishadidia  hoja  hiyo,  na  kama kusingekuwa  na  ahadi  ya  Mwenyezi  Mungu  na  wasomi inayosema  kuwa  wasije  wakaridhia  ulafi  wa  madhalimu na  njaa  ya  wanaokandamizwa,  ningeitupa  kamba  ya Ukhalifa kwenye mabega yake yenyewe, na ningamfanyia yule  wa  mwisho  vilevile  nilivyomfanyia  wa  kwanza. Halafu  mngeona  kwamba,  kwa  maoni  yangu,  hii  dunia

140


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 141

U i s l a m u wa S h i a yenu sio bora kuliko kupiga chafya kwa mbuzi.”124 3.  Akifafanua mipango yake na sera zake za kurekebisha mgawanyo wa rasilimali uliopita wa kidhalimu, Imam Ali (a.s.) alisema kwamba yeye atazirudisha mali zote zilizoporwa  kwenye  hazina  ya  ummah  na  kwa  wale  wenyewe halisi: “Wallahi, hata kama nitagundua kwamba kwa pesa kama hizo  zimetumika  kuolea  wanawake,  au  wanawake watumwa wamenunuliwa kwazo, mimi nitazirudisha kwa sababu  kuna  eneo  kubwa  katika  ugawaji  wa  haki,  na anayeona hili kuwa ni gumu la kutenda haki ataona vigumu zaidi kushughulika na udhalimu.125 4.  Wakati  mmoja  Imam Ali  (a.s.)  aliona  mkufu  kwenye  shingo  ya  binti yake. Alimuuliza  ni  wapi  alikoupata. Yeye  akajibu  kwamba  alikuwa ameuazima kutoka kwenye hazina ya ummah. Imam alimwita mtunza hazina na akamuuliza ni kwa nini amempa mkufu huo. Yeye akajibu kwamba ni mkopo uliosajiliwa. Imam alimruhusu kuondoka na akasema  kwamba  laiti  ingekuwa  ni  vinginevyo,  yeye  kwa  hakika  angemuadhibu binti yake huyo. Kwa mujibu wa Uislamu, watawala lazima wawe waadilifu katika maisha yao  binafsi  na  vilevile  katika  maisha  ya  kijamii.  Ni  lazima  watimize majukumu  yao  binafsi  na  pia  yale  ya  kijamii,  ikiwa  ni  pamoja  na kuheshimu haki za raia wao. Lazima watende haki katika mambo yao na yale  ya  utawala  kadhalika.  Na  kwa  nyongeza  ni  lazima  wasimamishe uadilifu wa kijamii na kuhakikisha kwamba sio mawakala wao wala raia wa kawaida wanavunja viwango vya haki. Imam Ali (a.s.) alisema: 124 Nahjul-Balaghah, Hotuba ya 3. 125 Nahjul-Balaghah, Hotubu ya 15. 141


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 142

U i s l a m u wa S h i a “Kama  ningependa  hivyo,  ningeweza  kwa  urahisi  kabisa kupata njia na namna ya kujipatia mwenyewe asali halisi na safi kabisa, aina bora ya ngano na nguo za hariri nzuri kabisa  ambazo  zingeweza  kufumwa.  Lakini  tamaa  ya kibadhilifu haiwezi kunipata mimi na ulafi hauwezi kunishawishi  mimi  kujipatia  mahitaji  bora,  wakati  ndani  ya Hijazi  na  Yemen  wanaweza  wakawepo  watu  ambao hawana  hata  matumaini  ya  kupata  walau  kipande  cha mkate  na  ambao  hawajawahi  kushiba  kamwe.  Siwezi kujiridhisha na kujikinaisha mwenyewe wakati kuna watu wanaonizunguka  ambao  njaa  na  kiu  vinawahangaisha  na kuwaumiza.  Hivi  mnanitaka  mimi  niwe  kama  yule  mtu ambaye mtu fulani amesema vya kufaa sana, ‘Je, maradhi haya hayakutoshi wewe kiasi kwamba unaendelea kulala na tumbo lililojaa, na kwenye mzunguko wako kuna vinywa  vyenye  njaa  ambavyo  vinaweza  kula  kwa  kufakamia hata ngozi ya mbuzi iliyokaushwa?’”126 Imam Ali (a.s.) amesema vilevile kwamba: “Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu amefanya ni wajibu kwa viongozi wakweli kwamba wajiweke wao wenyewe katika viwango vya hali ya wanyonge ili masikini wasije wakalia juu ya ufukara wao.127 Moja ya sura za mfumo mzuri wa kisiasa katika Uislam ni kwamba watu waweze kupinga dhidi ya uvunjaji wowote wa sheria ya Kiislam au kukiukwa  kwa  haki  za  binadamu.  Katika  barua  yake  kwa  gavana  mpya  wa Misri, Malik al-Ashtar, Imam Ali (a.s.) anaandika: 126 Nahjul-Balaghah, Barua ya 45 127 Nahjul-Balaghah, Hotubu ya 208 142


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 143

U i s l a m u wa S h i a “Nje  ya  muda  wako  wa  kazi,  tenga  muda  kwa  ajili  ya  wale wasioridhika na kwa ajili ya wale wanaotaka kukuona wakiwa na manung’uniko yao. Katika muda huu usiwe unafanya kazi nyingine  yoyote  bali  kuwasikiliza  na  kuzingatia  malalamiko na manung’niko yao. Kwa madhumuni haya ni lazima uandae hadhara ya wazi kwa ajili yao, ambamo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu,  ni  lazima  ushughulike  nao  kwa  upole,  uungwana  na heshima. Usiruhusu jeshi lako na polisi kuwepo kwenye hadhara  hiyo  katika  nyakati  kama  hizo  ili  wale  walio  na malalamiko  dhidi  ya  utawala  wako  waweze  kuongea  kwa uhuru, uwazi na bila ya hofu yoyote.  Yote  haya  ni  jambo  muhimu  kwa  utawala  wako  kwa  sababu nimekuwa  wakati  mwingi  nikimsikia  Mtukufu  Mtume (s.a.w.w.) akisema: ‘Ummah au serikali ambamo haki zinakandamizwa,  mafukara  na  wanaokandamizwa  hawaangaliwi  na ambamo wenye nguvu na uwezo hawalazimishwi kuwapa haki zao haiwezi kupata wokovu.’”128 Waislam lazima wasiwe wenye kupuuza vitendo viovu na tabia za kidhalimu  za  wengine,  ni  lazima  waangalifu  zaidi  hasa  kwenye  uhalifu  unaotendwa na dola, kwani viongozi wahalifu ndio waovu zaidi ya waovu.129 Wakati  watawala  wanapodharau  sheria  za  Kiislam  au  uadilifu,  ni  lazima washauriwe kuacha, kushindwa kufanya hivyo, Waislam lazima wapinge na kusimama dhidi yao. Qur’ani inasema: 128 Nahjul-Balaghah, Barua ya 53. Barua hii inachukuliwa kama “moja ya kumbukumbu iliyopo, nje ya maandiko ya Qur’ani na Hadith za Bwana Mtume (s.a.w.w.) juu ya muundo wa utawala, kwa nadharia na vitendo.” Tazama – Expectation of New Millennium: Shi’ism in History cha Nasir, uk.73, na W.C. Chittick katika “A Shi’it Anthology,” 1981, uk. 66.

129 cf. Nahjul-Balaghah, Barua ya 26 143


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 144

U i s l a m u wa S h i a

“Mmekuwa ni umma bora mliotolewa kwa watu, mnaamrisha mema na kukataza maovu na mnamwamini Mwenyezi Mungu……” (3:110)

“Hapendi Mwenyezi Mungu maneno ya kutangaza uovu ila kwa mwenye kudhulumiwa; na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kusikia, Mjuzi.” (4:148) Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.) amesema: “Jihadi bora ni kutamka maneno  ya  haki  mbele  ya  kiongozi  dhalimu.”130 Yeye  amesema  vilevile kwamba:  “Kwa  kweli  ni  lazima  uamrishe  mema  na  kukataza  maovu, vinginevyo  watu  waovu  watawatawaleni  kiasi  kwamba  hata  kama  watu wema miongoni mwenu wataomba, du’a zao hazitajibiwa.” 131 Maimam wa Ahlul-Bayt (a.s.) wakati wote walipinga uonevu wa watawala madhalimu. Ushahidi wa kutosha wa utayari wao wa kupitia mihanga ya aina  zote  ni  ule  ukweli  mwepesi  kwamba  wao  wote  wamepatwa  na  vifo vyao kupitia kuuliwa (isipokuwa bila shaka huyo Imam wa Kumi na Mbili ambaye yuko Ghaibu). Wengi wa wafuasi wao pia walifungwa au kuuawa. Historia  ya  Shi’ah  imejaa  mapambano  na  harakati  za  kimapinduzi  wakilingania utekelezaji wa sheria ya Kiislam na haki. Kadhia ya kuvutia sana na yenye kuzindua zaidi katika historia yote ya Shi’ah ilikuwa ni ule msiba wa Karbalaa. Akielezea lengo lake katika kukataa kutoa kiapo cha utii kwa Yazid (yule Khalifa mporaji wa madaraka) na kusimama dhidi yake, Imam Husein (a.s.) alisema: 130 Usuul al-Kaafi, Jz. 5, uk. 60 131 Usuul al-Kaafi, Jz. 5, uk. 56 144


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 145

U i s l a m u wa S h i a “Ninakiona  kifo  kama  wokovu,  na  maisha  pamoja  na  madhalimu kama balaa.”132 Katika kitabu chake, Taariikh al-Umam wa al-Muluuk, Tabari anasimulia kutoka kwa Imam al-Husein (a.s.): “Enyi  watu,  yeyote  atakayemshuhudia  mtawala  dhalimu akiruhusu  matendo  maovu  yaliyokatazwa  na  Mwenyezi Mungu,  akivunja  maagano  ya  Mungu,  akienda  kinyume  na Sunnah  ya  Bwana  Mtume  (s.a.w.w.)  akiwatendea  watu  kwa uovu  na  uadui  –  yeyote  atakayeshuhudia  yote  haya  na  kisha asiyapinge kwa maneno au vitendo kwa hakika atatendewa na Mwenyezi Mungu hiyo hiyo kama huyo mkandamizaji.” (Jz. 3, uk. 307). Matukio ya tanzia ya Karbala na matokeo yake yanaonyesha kwamba jamii ya  Kiislamu  ilikuwa  imepotoka  vibaya  sana  kutoka  kwenye  njia  ya Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.). Njia pekee ya kunusuru Uislam na Sunnah  ya  Bwana  Mtume  na  kuwaamsha  watu  ilikuwa  ni  kuwashitusha kwa njia ya msiba mkubwa na wenye kuchochea mawazo, ambalo lilikuwa ni ule muhanga mkubwa uliofanywa na mjukuu pekee wa Bwana Mtume (s.a.w.w.) aliyekuwa hai. Makumi ya ndugu na wafuasi wake waliuliwa, na Imam Ali ibn Husein (a.s.) na wanawake na watoto wa familia ya Mtukufu Mtume  (s.a.w.w.)  walichukuliwa  kama  mateka.  Akiwa  njiani  kuelekea Karbala,  Imam  Husein  (a.s.)  alimuona  Mtukufu  Mtume  katika  ndoto akimwambia  yeye  kwamba  Mwenyezi  Mungu  swt.  amependa  kumuona yeye akiuliwa kishahidi na wanawake kuchukuliwa kama mateka. Watu wengi walitingishwa kutoka usingizini mwao kwa msiba huu. Maasi kadhaa na harakati za kipinzani zilitokea ambazo zilifikia kilele chake katika  kuuangusha  utawala  wa  Bani  Umayyah.  Watawala  wa  Bani  Abbasi 132 al-Hasan ibn Shu’bah al-Harraanii, Tuhfatul al-Uquul, uk. 245 145


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 146

U i s l a m u wa S h i a ambao  walichukua  zamu  baada  yao  walitegemeza  madai  yao  kwenye madaraka  juu  ya  sehemu  moja  katika  wito  wa  kulipizia  kisasi  watu  wa Nyumba  ya  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.)  ambao  walikuwa  waathirika  wa ukandamizaji wa Bani Umayyah. Wao pia walikengeuka katika haki, hatua kwa hatua, wakihusika na vifo vya Maimam kadhaa wa Ahlul-Bayt (a.s.) na  watu  wengi  ambao  hawakuwa  na  hatia  yoyote.  Shi’ah  waliendeleza upinzani wao juu ya udhalimu kwa njia yoyote ile waliyoweza. Imam Husein (a.s.) alithibitisha kwamba kifo cha kishahidi ni lengo takatifu na pia chombo chenye uwezo kwa ajili ya kulinda kanuni na maadilli ya Kiislamu na kuushinda udhalimu, ukandamizaji na maasi ya kidini. Hii ndio  sababu  kwamba  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.)  alisema:  “Huseini  anatokana na mimi, na mimi ninatokana na Husein.”133 Imam  Husein  (a.s.)  ni  dhahiri  kabisa  alitokana  na  Mtukufu  Mtume  kwa maana ya kwamba alikuwa ni mjukuu wake. Hakuna hoja ya kibaiolojia hata hivyo inayoweza kutolewa kueleza ni kwa nini Bwana Mtume alijiona kwamba  yeye  mwenyewe  kama  aliyetokana  na  Imam  Husein.  Inaelekea kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa anarejelea kwenye ule ukweli kwamba kubakia hai kwa Uislamu na ujumbe wake wa kiutume kungehitajia  haya  mageuzi  ya  kishujaa  ya  Husein.  Kama  Imam  Husein asingekuwepo  na  mapambano  yake  yasingetokea,  Uislam  halisi  na  wa kweli usingeendelea: “Kama dini ya Muhammad haiwezi kuendelea isipokuwa kwa kuuliwa kwangu, basi enyi panga njoni mnichukue mimi.” – Imam Husein (a.s.). Dhana  ile  ya  kuwepo  kwa  mkombozi  anayejulikana  kama  al-Mahdi vilevile inahusiana na dhamira ya uadilifu wa Kiislam katika Uislam, husu133 At-Tirmidhi katika kitabu al-Manaqib, Sakhr ya 3708, Sunan ibn Majah, alMuqaddimah, Sakhr ya 141 na Musnad Ahmad, Musnad al-Shaamiyin, Sakhr ya 16903. 146


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 147

U i s l a m u wa S h i a san katika Uislam wa Shi’ah. Jukumu la mbele kabisa la Imam al-Mahdi na  wafuasi  wake,  dondoo  ya  kwanza  ya  ajenda  yao  itakuwa  ni  “kuujaza ulimwengu na haki,” kifungu cha maneno kinachojitokeza kwenye hadith nyingi. Kwa mfano, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema:  “Sisi  (mimi  na  familia  yangu)  ni  watu  wa  Nyumba  (AhlulBayt),  ambao  kwamba  Mwenyezi  Mungu  ametuchagulia maisha  ya  akhera  juu  ya  maisha  ya  dunia  hii;  na  watu  wa Nyumba  yangu  watapatwa  na  mateso  makubwa.  Wao  watafukuzwa  kwa  nguvu  kutoka  kwenye  majumba  yao  baada  ya kufariki  kwangu;  halafu  watakuja  watu  kutokea  Mashariki wakiwa wamebeba bendera nyeusi, na wataomba wema fulani wafanyiwe,  lakini  watanyimwa  huduma;  kwa  sababu  hiyo, wao watasimamisha vita na kutokea kuwa washindi, na watapewa  kile  ambacho  walikitaka  mwanzoni,  lakini  watakataa kukipokea na watakikabidhi kwa mtu kutoka kwenye familia yangu  ambaye  atakuja  kutokeza  ili  kuijaza  Dunia  na  haki kama itakavyokuwa imejaa udhalimu na ukandamizaji. Hivyo yeyote atakayekuwa hai wakati huo atapaswa aende kuungana nao,  hata  kama  itawabidi  watambuke  kwenye  barafu,  kwani miongoni  mwao  atakuwemo  Khalifa  wa  Mwenyezi  Mungu (Khalifat ul-laah) al-Mahdi.”

147


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 148

U i s l a m u wa S h i a

MLANGO WA SITA MASHI’AH KATIKA ULIMWENGU Idadi yao: Kwa mujibu wa UNFPA (Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Idadi ya Watu) na  vyanzo  vingine,  idadi  ya  watu  duniani  ilizidi  billioni  sita  mwaka 1999.134 Takriban  asilimia  ishirini  ya  jumla  hiyo  (ambayo  ni  karibu  billioni  2.2)  wanafuata  Uislamu.  Mchanganuo  wa  idadi  ya  Waislamu  ya ulimwengu mzima mnamo katikati ya 1998 inakisiwa kama ifuatavyo:135 Afrika:                       Asia:                          Ulaya:                         Amerika ya Kusini:      Amerika ya Kaskazini:    Oceania:

315,000,000 812,000,000 31,401,000 1,624,000 4,349,000 248,000

Waislam  wanaishi  kote  duniani.  Jumla  ya  idadi  ya  nchi  zenye  wakazi Waislam ni 208.136 Wengi wa Waislam wanaishi mashariki mwa mipaka ya  Irani,  hususan  ndani  ya  Pakistani,  India,  Baghladeshi,  Malaysia  na Indonesia. Na Indonesia ndio nchi yenye Waislam wengi sana. 134 Idadi ya watu duniani mnamo Januari mosi 2002 inakadiriwa kwamba ilikuwa ni  watu  6,196,141,294.  (Tazama:  U.S.  Census  Bureau  Official  website  at www.census.gov.) 135 Britannica, 2002, toleo la Deluxe. Kwa mujibu wa chanzo hiki, idadi ya jumla ya Waislamu ya dunia nzima katika miaka ya 1998 ilikuwa ni 1,164,622,000, ambayo ni asilimia 19.6 ya idadi ya watu duniani. 136 Britannica, 2002. Taarifa ya Deluxe. 148


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 149

U i s l a m u wa S h i a Uislam ndio dini inayokua kwa haraka sana na ni ya pili kwa ukubwa duniani. Kiwango cha ukuaji wake kinazidi kile cha ukuaji wa idadi ya watu duniani  na  asilimia  ya  yote  kwa  hiyo  inaongezeka.  Samuel  Huntington, mwandishi  wa  kitabu  chenye  kusababisha  mabishano  cha  The Clash of Civilizations – Mgongano wa Ustaarabu – anaandika hivi: “Asilimia ya Wakristo duniani ilifikia kilele cha takriban asilimia 30 katika miaka ya 1980, ikashuka chini, na sasa inaanguka,  na  huenda  ikakadiriwa  kuwa  takriban  asilimia  25  ya idadi  ya  watu  ifikapo  2025.  Kama  matokeo  ya  ukuaji  wa kiwango cha juu wa idadi ya watu, kadiri ya Waislamu duniani itaendelea kukua kwa dhahiri kabisa, kufikia asilimia 20 ya idadi  ya  watu  duniani  wakati  wa  kupindukia  kwa  karne,  na kuizidi  idadi  ya  Wakristo  miaka  kadhaa  baadaye,  na  huenda ikafikia takriban asilimia 30 ya idadi ya watu duniani ifikapo mwaka 2025.”137 Shi’ah  wako  takriban  asilimia  10  ya Waislamu,  au  120,000,000.138 Kwa mfano, Britannica 2002 inasomeka hivi: Kwa karne kadhaa harakati za Shi’ah zimekuwa zikiwavutia Waislam wote wa Sunni, na wafuasi wake wanafikia idadi ya takriban 60 hadi 80 millioni mwishoni mwa karne ya 20, au moja ya kumi ya Waislam wote. Ushi’ah 137 Kitabu  –  The Clash of Civilization and the Remaking of World Order (Touchstone Books 1998), uk.65 na 66. 138 Wengi  ni  Waislam  wa  Sunni  wakijumuisha  Hanafia  (walioko  zaidi  Misri, Lebanoni,  Syria,  Jordan,  Iraq,  Uturuki,  Balkania, Asia  ya  Kati,  China),  Malikii (walioenea  Morocco,  Sudan  na Afrika  ya  Magharibi),  Shafi’ii  (ndani  ya  Syria, Yemen,  Omani,  Falme  za  Kiarabu  –  Emirates,  Bahrain,  Kuwaiti,  Afrika  ya Mashariki,  Malaysia  na  Indonesia,  na  ipo  pamoja  na  madhehebu  zingine  huko Jordan na Misri) na Hambali. Kwa mujibu wa taasisi ya MEDEA, chini ya kichwa  cha  habari  “SUNNISM”  madhehebu  ya  Hanbali  ndio  madhehebu  rasmi  ya Saudi Arabia na Qatar. 149


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 150

U i s l a m u wa S h i a (Kiarabu: Shi’ah au Uislam wa Shi’i) ndio imani ya wengi ndani ya Iran, Iraq, na pengine Yemen (San’a’) na ina wafuasi ndani ya Syria, Lebanoni, Afrika ya Mashariki, India na Pakistani. Kwa mujibu wa baadhi ya vyanzo, tarakimu yenyewe ni asilimia 11.139 Hii itawapa  idadi  ya  Shi’ah  wa  ulimwengu  sasa  hivi  kama  takriban  watu 132,000,000.140 Uainishaji wa idadi katika baadhi ya nchi za Asia ambako

139 Yann Richard (1991 tafsiri ya Kiingereza 1995), uk. 2 akitumia zaidi tarakimu zilizotolewa na Md. R. Djalili, Religion et revolution, Paris, Economica, 1981, uk. 23ff, na M. Momen, An Introduction to Shi’i Islam, New Haven na London, Yale University Press, 1985, uk.264ff. Hivyo tarakimu za Richard hazihusiani na lolote zaidi ya miaka ya 1980. Uainishaji wake ni kama ifuatavyo: Iraq asilimia 55, au watu 18,000,000; Bahrain: asilimia 70, au karibu watu 170,000; Kuwait: asilimia 24 ya wananchi wa Kuwait, au watu 137,000; Qatar asilimia 20 ya idadi ya watu, au 50,000; Umoja wa Falme za Kiarabu: asilimia 6, au watu60,000; Saudi Arabia: asilimia 7 ya raia wote wa Saudia, au watu440,000; Lebanon, moja ya tatu ya watu wote, au watu 1,000,000; India: asilimia 15 hadi 20 ya idadi ya Waislam, ambayo ni  jumla  ya  watu  80  millioni,  au  asilimia  12  ya  jumla  ya  idadi  yote  ya  watu (Imamia na Ismailia) Pakistan: 12,000,000; Afghanistan: asilimia 15, au takriban million 2.5; Azerbaijan: jamii kubwa ya Shi’ah, million 4.5; Uturuki: 1,500,000 mbali  na  Alawiyah;  Syria:  50,000  mbali  na  Alawiyah  (kiangalizo:  Shi’ah  na Alawiyah kwa pamoja wanafikia jumla ya 4,900,000). 140 Kwa  bahati  mbaya,  hakuna  takwimu  sahihi  zinazoakisi  idadi  hasa  ya Waislamu kwa jumla na hususan Shi’ah. Kilichopendekezwa hapo juu kimetegemea  kwenye  wingi  wa  vyanzo  vinavyopatikana  juu  ya  mada  hii.  Hata  hivyo, imependekezwa  kwamba  Shi’ah  wanafanya  asilimia  23  ya  Waislamu.  Tazama S.M.Qazwini, uk. 4, iliyochukuliwa kutoka kwenye The Bulletin of Affiliation: AlMadhhab – Schools of Thought, Jz. 17, namba 4 (Desemba 1998), uk. 5. 150


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 151

U i s l a m u wa S h i a Shi’ah wanaunda idadi kubwa ya watu au idadi ndogo imara ni kama ifuatavyo:141 Afghanistan

Idadi  ya  watu  (1998):  24,792,000;  uhusiano  wa  kidini (1990): Waislam wa Sunni asilimia 84; Waislam wa Shi’ah asilimia 15; wengineo asilimia 1.142

Azerbaijan

Idadi  ya  watu  (1998):7,650,000;  uhusiano  wa  kidini (1991): Waislam wa Shi’ah asilimia 70; Waislam wa Sunni asilimia 30.

Bahrain

Idadi ya watu (1998): 633,000; uhusiano wa kidini (1991): Waislam  asilimia  81.8  ambayo  Shi’ah  asilimia  61.3; Waislam  wa  Sunni  asilimia  20.5;  Wakristo  asilimia  8.5; wengineo asilimia 9.7.143

141 Tarakimu zilizotajwa katika maelezo hayo ni kwa mujibu wa Britannica 2002, Taarifa  ya  Deluxe.  Tarakimu  zinahusiana  na  mwaka  1998.  Kwa  hiyo,  idadi  ya watu lazima itakuwa imeongezeka ndani ya miaka michache iliyopita. Hata hivyo asilimia hizo zinawezekana kuwa zimebakia ni zilezile. Inapaza kuzingatiwa kwamba orodha hiyo hapo juu haikusudiwi kuwa jumuishi, ni uteuzi ulioegemea juu ya taarifa zilizokusanywa kutoka kwenye chanzo hicho katika  kila  nchi.  Kwa  mfano,  Qatar  inakosekana,  ambapo  kwa  mujibu  wa MEDEA, asilimia 10 ya idadi ya watu huko ni Shi’ah. 142 Kitabu cha mambo ya kidunia cha CIA (CIA World Factbook) kinakisia idadi ya watu ya Afghanistan mnamo Julai 2001kama ifuatavyo: 26,813,057/Waislam wa  Sunni,  asilimia  84;  Waislam  wa  Shi’ah  asilimia  15,  wengineo  asilimia  1. Nitakirejea chanzo hicho hapo chini kama CWF. 143 Kwa  mujibu  wa  CWF,  Shi’ah  wa  Bahrain  wana  asilimia  70  ya  idadi  ya Waislamu  wote.  Kwa  mujibu  wa  MEDEA  (European  Institute  for  Reseach  on Mediterranean  and  Euro-Arab  Cooperation)  asilimia  85  ya  watu  ni  Waislam ambao kati yao theluthi moja ni Sunni na theluthi mbili ni Shi’ah (idadi kubwa ni Waarabu lakini kuna Wairani 70,000).

151


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 152

U i s l a m u wa S h i a Misri

Idadi  ya  watu  (1998):  63,261,000;  uhusiano  wa  kidini (1990): Waislam wa Sunni asilimia C. 90; Wakristo asilimia C. 10.144

India

Idadi  ya  watu  (1998):  984,004,000;  uhusiano  wa  kidini (1995):  Hindu  asilimia  81.3;  Waislam  asilimia  12.0, ambayo  Waislam  wa  Sunni  asilimia  9.0;  Waislam  wa Shi’ah  asilimia  3.0;  Wakristo  asilimia  2.3,  ambayo Protestanti  asilimia  1.1,  Romani  Katoliki  asilimia  1.0; Sighasigha asilimia 1.9; Budha asilimia 0.8; Jain asilimia 0.4; Zoroasta asilimia 0.01; wengineo asimila 1.3.

Iran

Idadi  ya  watu  (1998):  61,531,000;  uhusiano  wa  kidini (1995):  Waislamu  asilimia  99.0,  ambayo  Waislam  wa Shi’ah  asilimia  93.4;  Waislam  wa  Sunni  asilimia  5.6; Wakristo  asilimia  0.3;  Zoroasta  asilimia  0.05;  Wayahudi asilimia 0.05.145

Iraq

Idadi  ya  watu  (1998):  21,722,000;  uhusiano  wa  kidini (1994):  Waislam  wa  Shi’ah  asilimia  62.5;  Waislam  wa Sunni asilimia 34.5; Wakristo (hasa itikadi ya Chaldea na itikadi  ya  Syria  ya  Katoliki  na  Nestoria)  asilimia  2.7; wengineo (hasa Syncretia ya Yazidii) asilimia 0.3.146

Kuwait

Idadi  ya  watu  (1998):  1,866,000;  uhusiano  wa  kidini

144 Kulingana na CWF, Waislam (wengi wakiwa Sunni) wanafanya asilimia 94 ya idadi yote ya watu wa Misri. 145 Kwa mujibu wa CWF, Shi’ah wanafanya asilimia 89 ya idadi ya watu ya taifa. 146 Kwa mujibu CWF, Shi’ah wana idadi ya asilimia 60-65 na Sunni asilimia 3237 ya jumla ya idadi ya watu. Kulingana na MEDEA, Waislam wanaunda asilimia 97 ya idadi ya watu wa Iraq, ambayo Shi’ah ni asilimia 65 na Sunni asilimia 32.

152


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 153

U i s l a m u wa S h i a (1995):  Waislam  asilimia  85,  ambao  Waislam  wa  Sunni asilimia  45;  Waislam  wa  Shi’ah  asilimia  30;  Waislam wengineo asilimia 10; wengineo (hasa Wakristo na Hindu) asilimia 15.0.147 Lebanon

Idadi  ya  watu  (1998):  3,506,000;  uhusiano  wa  kidini (1995): Waislam asilimia 55.3 ambao Waislam wa Shi’ah asilimia 34.0; Waislam wa Sunni asilimia 21.3; Wakristo asilimia 37.6, ambayo Katoliki asilimia 25.1 (wa Maroni asilimia 19.0, Wakatoliki wa Kigiriki au Melchia asilimia 4.6),  Orthodox  asilimia  11.7  (Orthodox  wa  Kigiriki  asilimia  6.0,  Apostoliki  wa  Armenia  asilimia  5.2), Waprotestanti asilimia 0.5; wa-Druze asilimia 7.1.148

Oman

Idadi  ya  watu  (1998):  2,364,000;  uhusiano  wa  kidini (1993):  Waislam  asilimia  87.7  ambayo  Waislam  wa Ibaadiyah asilimia C.75 (Idadi ndogo kuu ni  Waislam wa Sunni  na  Shi’ah);  Hindu  asilimia  7.4;  Wakristo  asilimia 3.9; Budha asilimia 0.5; wengine asilimia 0.5.149

Pakistan

Idadi  ya  watu  (1998):  141,900,000;  uhusiano  wa  kidini (1993):  Waislam  asilimia  95.0,  ambao  (wengi  wao

147 Kulingana  na  CWF  na  MEDEA, Waislam  wa  Sunni  wa  Kuwaiti  wanafikia asilimia 45 na Shi’ah asilimia 40. 148 Kwa mujibu wa CWF, Waislam wanafanya asilimia 70 (ukichanganya Shi’ah, Sunni, Druze, Ismailia, Alawia au Nusayri). Kulingana na MEDEA, Waislam ni asilimia  70  (makundi  matano  ya  Kiislam  yanayotambulika  kisheria  –  Shi’ah, Sunni,  Druze,  Ismailia, Alawia  au  Nusayri)  na Wakristo  ni  asilimia  30  (vikundi kumi  na  moja  vya  ki-Kristo  vinavyotambulika  kisheria  –  vinne  ni  Wakristo  wa Orthodox, sita Katoliki, kimoja Protestanti). Wayahudi wana asilimia ndogo sana. 149 Kwa  mujibu  wa  CWF,  Waislam  wa  Ibaadi  ni  asilimia  75  na  waliobakia  ni Sunni, Shi’ah na Hindu. Kulingana na MEDEA, Waislam ni asilimia 75  ambao

robo tatu yao ni madhehebu ya Ibaadi. 153


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 154

U i s l a m u wa S h i a Waislam wa Sunni na Waislam wa Shi’ah wakiwa takriban asilimia 20 ya idadi yote ya watu); Wakristo ni asilimia 2.0; Hindu asilimia 1.8; wengineo (ikiwa ni pamoja na Ahamadiyah) asilimia 1.2.150 Saudi Arabia Idadi  ya  watu  (1998):  20,786,000;  uhusiano  wa  kidini (1992):  Waislam  wa  Sunni  asilimia  93.3;  Waislam  wa Shi’ah asilimia 3.3.151 Syria

Idadi  ya  watu  (1998):  15,335,000;  uhusiano  wa  kidini (1992): Waislam asilimia 86.0, ambao Waislam wa Sunni asilimia  74.0;  Waislam  wa  ‘Alawiyyah  asilimia  12.0; Wakristo asilimia 8.9; Druze asilimia 3.0; wengineo asilimia 1.0.152

Uturuki

Idadi  ya  watu  (1998):  64,567,000;  uhusiano  wa  kidini (1994): Waislam  wa  Sunni  asilimia  c.  80.0; Waislam  wa Shi’ah  asilimia  c.  19.8,  ambayo  Alawiyyah  wasio  wa Orthodox c. 14.0; Wakristo asilimia c. 0.2.153

150 Kulingana  na  CWF,  Waislam  ni  asilimia  97  (Sunni  77%  na  Shi’ah  20%). Wakristo, Hindu na wengineo wanafanya asilimia 3.0. 151 CWF hawataji asilimia ya Waislamu wa Shi’ah ndani ya Saudi Arabia, ingawa idadi ni kubwa kuliko katika baadhi ya nchi kwenye jedwali. Inasema tu kwamba Waislam ni asilimia 100. Kwa mujibu wa MEDEA, Shi’ah ni asilimia 2.5 ya jumla ya idadi yote na Sunni ni asilimia 97. 152 Kulingana na CWF, Waislam wa Sunni ni asilimia 74. Alawiyyah, Druze na madhehebu nyingine za Kiislam wanafanya asilimia 16.0 na Wakristo (madhehebu  mbalimbali)  asilimia  10.0.  Kuna  jamii  ndogondogo  za  Wayahudi  ndani  ya Damascus, al-Qamishli na Aleppo. Kwa mujibu wa MEDEA, Waislam wa Sunni ni  asilimia  75.0, Alawiyyah  asilimia  11, Wakristo  (itikadi  zote)  asilimia  10.0  na Druze asilimia 3.0. 153 CWF  wanataja  kifupi  tu  kwamba  asilimia  99.8  ni Waislam  (wengi  wakiwa Sunni)  na  wengine  (Wakristo  na  Wayahudi)  ni  asilimia  0.2.  Cha  kushangaza, MEDEA  hawazungumzii  hasa  hasa  kuhusu  idadi  ya  Shi’ah  ndani  ya  Uturuki, wakisema tu, “Dini: Waislam asilimia 99 Sunni, wengine asilimia 1.0 (Wakristo na Wayahudi).” (http://www.medea.be/en/index059.htm). 154


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 155

U i s l a m u wa S h i a UAE

Idadi  ya  watu  (1998):  2,744,000;  uhusiano  wa  kidini (1995): Waislam asilimia 96.0, ambao Waislam wa Sunni asilimia 80.0; Waislam wa Shi’ah asilimia 16.0; wengineo (hasa Wakristo na Hindu) asilimia 4.0.

Yemen

Idadi ya watu (2000): 18,260,000;154 uhusiano wa kidini (1995): Waislam asilimia 99.9, ambao Waislam wa Sunni asilimia  c.  60.0;  Waislam  wa  Shi’ah  asilimia  40.0; Waislam wengineo asilimia 0.1.155

Idadi  ya  Shi’ah  katika  baadhi  ya  nchi  inatiliwa  shaka.  Inaweza  ikawa kubwa  zaidi  kuliko  tarakimu  rasmi  zinavyoonyesha,  kwa  sababu  ama  ya kukosa takwimu sahihi au mazingatio ya kisiasa. Thomas S. Szayna (2000) anaandika katika uchunguzi wake wa kidemografia (taaluma ya takwimu za kima cha uzazi na vifo) ya Saudi Arabia mnamo 1997-1998 ifuatavyo:  Idadi  yao  (Shi’ah)  ina  wasiwasi  sana,  ingawa  wanafikia  takriban  watu 200,000 hadi 400,000.156 Wanaharakati wa Shi’ah wanadai kwamba nusu millioni  ya  Shi’ah  wanaficha  hali  yao  na  kujifanya  wao  ni  Sunni  kwa sababu ya mateso na vikwazo chungu nzima vinavyohusishwa na Ushi’ah. Katika eneo lao kubwa la makazi (Jimbo la Mashariki), Shi’ah wanawakilisha takriban asilimia 33 ya idadi ya watu wote. Alikuli hali, wanaharakati wa  Shi’ah  wanafikia  watu  milioni  moja,  au  hata  zaidi  ya  asilimia  25  ya 154 Hii  ni  kwa  mujibu  wa  SESRTCIC  iliyoshirikishwa  na  shirika  la  Kiislam  la OIC. 155 CWF wanasema tu: ‘Waislam ikiwa ni pamoja na Shafi’i (Sunni) na Zaydiyah (Shi’ah), idadi ndogo ya Wayahudi, Wakristo na Hindu.’ Kulingana na MEDEA, Waislam wa Sunni ni asilimia 55, Zaydiyyah asilimia 44 na Wakristo asilimia 1. 156 Kitabu ‘Saudi Arabia Handbook,’ cha Taasisi ya Federal Reseach Division, Maktaba ya Congress, Washington, Makala ya Intaneti.

155


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 156

U i s l a m u wa S h i a idadi  yote  ya  watu,157 ingawa  idadi  inayokubalika  zaidi  inaelekea  kuwa takriban asilimia 15.158 Hesabu hii ya mwishoni ingeweza kuunga mkono madai  ya  wanaharakati  wa  Shi’ah  ya  kuwepo  idadi  kubwa  ya  ‘Shi’ah wanaojificha.’159

Miji Mitukufu: Makka Mji  mtukufu  kabisa  katika  Uislamu,  Makka,  upo  katika  Milima ya Sirat upande wa Magharibi wa Saudi Arabia. Milima hiyo ya Sirat inajumuisha mlima  Hira’,  ambao  una  lile  pango  ambamo  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.) alikuwa  akijitenga  humo  kwa  ajili  ya  tafakari  na  ibada  kabla  ya  kuanza kwa ujumbe wake na ambako pia alianza kupokea Wahyi. Kusini mwa mji huo  upo  Mlima  Thawr (futi  2,490/mita  760),  ambao  ndimo  lilimo  lile pango  ambamo  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.)  alijificha  mbali  na  makafiri wakati wa kuhama kwake kwenda Madina. Ndani ya mji wa Makka imo ile Ka’bah, lile jengo la umbo la mchemraba lililojengwa na Nabii Ibrahim (a.s.)  na  mwanawe  Nabii  Isma’il  (a.s.)  juu  ya  misingi  ambayo  awali  ilijengwa na Nabii Adam. Waislam wote wanaelekea kwenye Ka’abah hiyo katika swala zao. 157 Kitabu ‘Mideast Mirror,’ Agosti 27, 1996, uk. 15 158 Katika ukurasa 276 mwandishi anarejea kwenye makadirio ya CIA ya idadi nzima ya watu wa kama millioni 20.1 (Julai,1997). Tarakimu hii inajumuisha millioni  5.2  ya  raia  wa  kigeni  ndani  ya  Saudi Arabia.  Mwandishi  vilevile  anarejea kwenye tarakimu za sensa ya hivi karibuni (septemba,1992) iliyotoa jumla ya watu millioni 16.9 (ambao millioni 4.6 walikuwa ni raia wa kigeni). 159 Kitabu cha Kiingereza kiitwacho “Identifying Potential Ethnic Conflict:

Application of a Prosess Model,” uk. 277 na 278. 156


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 157

U i s l a m u wa S h i a

Madina Mji wa pili kwa utukufu katika Uislam ni Madina, zamani ukiitwa Yathrib, upo upande wa Magharibi wa Saudi Arabia na ni kiasi cha maili 278 (kilomita  447)  kutoka  Makka  kwa  njia  ya  barabara  (maili  215/km.  345 Kaskazini ya Makka kwa urukaji wa kunguru). Tofauti na Makka, mji wa Madina umo katika chemchemi (sehemu yenye miti na chemchemi) yenye rutuba. Kabla ya Uislam, mji huo ulikuwa ukikaliwa na hasa na makabila mawili, Aus  na  Khazraji,  na  vilevile Wayahudi,  ambao  baadhi  yao  walitarajia kutokeza hapo kwa Mtume wa Mwisho. Mnamo mwaka 622 Miladia, Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.) alihama kutoka Makka kwenda Madina. Uhamiaji huu unachukuliwa kama mwanzo wa kalenda ya Kiislam katika mfumo wa mwezi na jua pia.160 Mara  mji  wa  Madina  ukawa  ndio  makao  makuu  ya  Dola  ya  Kiislam, iliyoanzishwa  na  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.)  na  uliendelea  kuwa  hivyo baada ya kutekwa Makka mnamo mwaka 630.  Madina ina maeneo mengi muhimu ya Kiislam, ikiwa ni pamoja na misikiti kadhaa iliyojengwa wakati wa Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.) na  makaburi  ya  Waislam  mashuhuri.  Mahali  muhumu  kabisa  ndani  ya Madina, ya pili tu kwa utukufu baada ya Makka, ni ule Msikiti wa Mtume – Masjidun-Nabi. Ndani ya Msikiti huo mna sehemu za maana sana kihistoria kama vile ile Minbar ya Mtukufu Mtume na ile Mihraab – sehemu ya kuswalia  ya  Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.).  Nyumba  ndogo  ya  Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ilikuwa karibu na ule msikiti wa asili na iliingizwa ndani baada ya msikiti kupanuliwa. Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipofariki, alizikwa ndani ya nyumba yake, na hili limeongezea kwenye umuhimu wa kidini na kiroho wa msikiti huo hasahasa na kwa mji wa Madina kwa 160 Wakati  wa  kuandikwa  kitabu  hiki  (2003Miladia),  ni  mwaka  wa  ki-mwezi 1422 na wa ki-jua 1380. 157


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 158

U i s l a m u wa S h i a jumla. Kila mwaka mamillioni ya Waislamu, Shi’ah na Sunni na madhehebu mengineyo kutoka kote duniani wanautembelea (ziarat) msikiti huo na kaburi ya Mtume Muhammad (s.a.w.w.). Vitu  vingine  vya  kimungu  vya  kutembelewa  na  Waislam  ni  pamoja  na Msikiti  wa  Quba ambamo  Mtukufu  Mtume  aliswali  swala  zake  mara  tu baada  ya  kuwasili  Madina;  Msikiti  wa  Qiblatayn, ambamo  Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akiswali wakati mwelekeo wa Qibla ulipobadilishwa  na  Mwenyezi  Mungu  kutoka  Jerusalem  kuelekea  Makka  na  makaburi  ya  Hamzah,  ami  yake  Mtume  na  mashahidi  wengine  wa  vita  vya Uhud. Eneo  la  makaburi  la  Jannat al-Baqii hususan  linafaa  kutajwa  miongoni mwa  maeneo  mengine  muhimu  ndani  ya  Madina.  Wengi  wa  watu  wa familia ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na masahaba zake, na vile vile wale waliowafuatia hao wamezikwa hapo. Jannat al-Baqii ni muhimu hasa kwa Waislam  wa  Shi’ah  kwa  vile  limo  kaburi  la  Imam  Hasan,  mjukuu  wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na mtoto wa Bibi Fatima na Imam Ali (a.s.), na ni Imam wa pili wa Shi’ah; Imam Ali ibn al-Husein kilembwe cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), mjukuu wa Bibi Fatima na Imam Ali, ambaye ni Imam wa nne wa Shi’ah; Imam Muhammad ibn Ali, Imam wa tano na mtoto wa Imam wa nne; na Imam Ja’far bin Muhammad as-Sadiq, Imam wa sita na mtoto  wa  Imam  wa  tano.  Inawezekana  kwamba  Fatima  binti  Rasuli Muhammad  pia  alizikwa  Jannat  al-Baqii,  ingawa  inawezekana  kuwa amezikwa ndani ya Msikiti wa Mtume – Masjidun-Nabii. Sababu ya utata huu  usio  na  kifani  ni  kwamba  kwa  mujibu  wa  wasia  wake,  yeye  alitaka mazishi yake kuwa ya siri na mahali pa kuzikwa kwake kubakia pasipojulikana kwa wale ambao walimuudhi wakati wa uhai wake.

Jerusalem Mmoja wa miji mitukufu sana kwa Waislam wote ni Jerusalem (Bayt alMuqaddas au  al-Quds).  Miongoni  mwa  maeneo  muhimu  ndani  ya 158


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 159

U i s l a m u wa S h i a Jerusalem ni al-Masjid al-Aqsaa (Msikiti wa Mbali). Kabla ya al-Ka’bah haijasimamishwa  kama  kitovu  cha  kuelekea  kwa  ajili  ya  swala  ya Mwislam,  al-Quds  ilikuwa  ndio  mahali  ambako  Waislam  walitakiwa kuelekea.  Msikiti  huu  pia  ndio  mahali  ambapo  kutoka  hapo  Mtukufu Mtume  (s.a.w.w.)  alipaa  kwenda  mbinguni  kwenye  usiku  wa  Mi’raj. Qur’ani inasema:

“Ametakasika aliyempeleka usiku mja wake kutoka Msikiti Mtakatifu mpaka msikiti wa mbali ambao tumevibariki vilivyo kandoni mwake, ili tumuonyeshe baadhi ya ishara zetu. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.” (Bani Israil; 17:1)

Najaf Mji wa Najaf upo juu ya mgongo wa milima (Jina la Najaf maana yake ni mgongo wa milima) ndani ya nchi ya Iraq, maili chache Magharibi mwa Mto  Furat  na  karibu  na  mji  wa  Kufa.  Mji  huo  ulianzishwa  na  Khalifa Harun al-Rashid mnamo mwaka 791Miladia, karibu na kaburi la Imam Ali (a.s.), binamu na mkwe wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Khalifa wa nne na Imam  wa  kwanza  wa  Waislam  wa  Shi’ah.  Mji  huo  kwa  muda  mrefu umekuwa kituo cha ziarat na masomo kwa Shi’ah.

Karbala Mji wa Karbala umejengwa katika Iraq ya kati, maili 55 (km.88) kutoka Baghdad,  kwenye  mpaka  kati  ya  jangwa  na  jimbo  la  kilimo.  Karbala  ni moja ya mahali patukufu sana kwa Waislam wa Shi’ah, kwani hapo ndipo mahali Imam Husein (a.s.) na watu wa familia yake na wafuasi wake wal159


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 160

U i s l a m u wa S h i a izikwa baada ya vifo vyao vya kishahidi katika vita vya Karbala mnamo mwaka 680 Miladia. Kaburi lake na lile la ndugu yake, Abu al-Fadhl Abbas na  vilevile  makaburi  ya  mashahidi  wengine  yote  yapo  Karbala.  Mji  wa zamani ulio na makaburi hayo umezungushiwa ukuta, na Karbala ya sasa imeendelea kukua kuelekea kusini mwake.

Kadhimayn Kadhimayn ni sehemu ya mji wa Baghdad, mji mkuu wa Iraq. Kwa asili kabisa mji huo ulikuwa ni eneo la makaburi la Maquraishi, kabila ambalo ametoka Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Ahlul-Bayt wake (a.s.) wanatokana nalo. Baada ya kuuliwa kwao, Imam wa saba na wa tisa wa Waislam wa Shi’ah, Musa bin Ja’far al-Kadhiim na Muhammad bin Ali al-Jawaad walizikwa  pale.  Mahali  hapo  palitembelewa  mara  kwa  mara  na  Shi’ah  na wengine  ambao  walikuwa  na  mapenzi  na  kizazi  cha  Mtukufu  Mtume (s.a.w.w.)  na  polepole  mji  wa  Kazimayn  (kwa  Kiarabu  sura  mbili  za Kadhiim) ukaundwa. Mnamo mwaka 336 AH. Mu’izz al-Dawlah aliyajenga  upya  makaburi  hayo  pacha.  Alijenga  pia  wigo  kuzunguka  makaburi hayo uliokuwa na mlolongo wa vyumba kwa ajili ya kuweka wanafunzi wa dini. Kulikuwepo pia na chumba cha mihadhara upande wa mashariki wa makaburu kilichoitwa Madrass (mahali pa kujifunzia).

Samarra’ Mji wa Samarra’ upo katika ukingo wa Mashariki mwa Mto Tigris, maili 70  (km.  97)  Kaskazini  mwa  Baghdad.  Mji  huo  ni  mahali  pa  makazi  ya kipindi kabla ya historia kuanzia muongo wa tano BC. Ulianzishwa kati ya karne ya tatu na ya saba AD. Mnamo mwaka 836, Khalifa wa Bani Abbas, al-Mu’tasim aliufanya mji wa Samarra’ kuwa makao yake makuu mapya. Mji huo uliendelea kukua mpaka pale Khalifa wa Bani Abbas al-Mu’tamid alipoyahamisha makao makuu hayo na kuyarudisha Baghdad. Wakati huu, mji  huo  ulipanuka  kwa  maili  20  (km.  32)  kandoni  mwa  Mto  huo. Imependekezwa  (Ernst  Grube,  1996)  kwamba  jina  hilo  linarudi  nyuma hadi kipindi cha nyakati kabla ya Uislam na limechapwa kwenye sarafu za 160


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 161

U i s l a m u wa S h i a Makhalifa  wa  Samarra’  (836-892)  kama  sura  ya  ufupisho  ya  Surr man ra’aa ikiwa  na  maana  ‘amefurahishwa  mwenye  kuiona.’161 –  Samarra inatukuzwa sana na Waislam wa Shi’ah kwa sababu Imam wao wa kumi na wa kumi na moja, Imam Ali ibn Muhammad al-Haadi na Imam Hasan bin Ali al-‘Askarii walifungiwa hapo na Khalifa wa wakati huo katika kambi ya  kijeshi.  Hatimaye  waliuawa  kishahidi  na  wakazikwa  hapo.  Kabla  ya kuingia  ghaibu  kwake,  Imam  wa  kumi  na  mbili  naye  aliishi  hapo  (255260).

Mashhad Mji wa Mashhad (kwa Kiarabu Mashhad ina maana ni sehemu ya shahada au kushuhudia) upo katika jimbo lenye rutuba lililoko Kaskazini mashariki ya Iran. Mashhad iliendelea kukua karibu na eneo alilozikwa Imam Ali ibn Musa ar-Ridhaa, Imam wa nane wa Shi’ah, ambaye aliuawa kishahidi hapo mnamo mwaka 818 Miladia. Vyote, kaburi na mji viliendelea kwanza  chini  ya  tawala  ya  Timurid  katika  karne  ya  15,  ukiupita  au  kuuzidi umaarufu mji wa karibu yake wa Tuus, na ulipanuliwa sana na watawala wa Safavid kuanzia karne ya 16 na kuendelea. Nadhir Shah (aliyetawala kuanzia  mwaka  1736-1747)  aliuchagua  Mashhad  kuwa  makao  yake makuu. Kila mwaka mamillioni ya Waislam huwa wanalitembelea kaburi la  Imam  ar-Ridhaa.  Mashhad  vilevile  ni  mahali  pa  baadhi  ya  seminari maarufu  za  Shi’ah,  ambamo  kutoka  humo  wanachuoni  wengi  mashuhuri huwa wanahitimu.

161 A. Northedge anasema: “Mji huo wa Khalifa awali uliitwa Surr man Ra’aa (yule mwenye kuiona hufurahia). Kwa mujibu wa Yaquut jina hili la awali baadae lilifupishwa  katika  matumizi  ya  kawaida  na  kuwa  Samarraa’  la  sasa.  Yumkini kuelekea  zaidi  hata  hivyo  kwamba  Samarra’  ni  tafsiri  ya  toponym ya  kabla  ya Uislam, na kwamba Surr Man Ra’aa, namna ya jina la utamkaji wa mdomo katika Kiarabu ambalo linabatilisha desturi ya zamani ya Wa-Akkadia na wa-Sumeria, ni mchezo wa maneno uliobuniwa katika baraza ya Khalifa.” (Encyclopaedia of Islam, CD-ROM Edition v.1.0, 1999). 161


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 162

U i s l a m u wa S h i a

Qum Mji  wa  Qum  upo  Mashariki  ya  kati  ya  Iran  kwenye  kingo  zote  za  mto wenye  jina  hilohilo,  takriban  maili  92  (km.  147)  Kusini  mwa  Tehran. Tangu karne ya kwanza ya Uislam, Qum wakati wote imekuwa moja ya vituo  mashuhuri  vyenye  kuunga  mkono  madhehebu  ya  Nyumba  ya Mtukufu  Mtume  (s.a.w.w.)  na  elimu  kwa  ajili  ya  Waislamu  wa  Shi’ah. Zama  za  Hajjaaj  bin Yusuf  al-Thaqafii,  kundi  la  Shi’ah  kutoka  ukoo  wa Ash’arii  lilihama  kutoka  Kufa  kwenda  Qum  na  kufanya  maskani  hapo. Abdullah  bin  Sa’d  al-Ash’ari  alikuwa  ndiye  kiongozi  wao  wa  kiroho  na mwalimu wao, na baadae watoto wake walianza kuhubiri Uislam na kulingania  mafundisho  ya  Mtukufu  Mtume  na  kizazi  chake Ahlul-Bayt  (a.s.). Baadae Ibrahim bin Hashim, sahaba wa Imam wa nane na mwanafunzi wa muhadith mashuhuri na mwanachuoni mkuu Yunus bin Abd al-Rahmaan aliweka makazi hapo Qum na akachangia sana kwenye ukuzaji wa elimu na sayansi za Kiislam, hususan elimu ya Hadith. Mnamo mwaka 816 Miladia, Fatima al-Ma’suumah, dada yake Imam wa nane alipatwa na maradhi wakati alipokuwa akisafiri kutoka Madina kwenda  kumtembelea  kaka  yake  huko  Marv.  Aliwaambia  wafuasi  wake wampeleke Qum. Yeye alifariki hapo Qum. Eneo la kuzikwa kwake hapo Qum  limekuwa  likitembelewa  na  Waislam  wa  Shi’ah,  kizazi  baada  ya kizazi. Mnamo karne ya 17 jumba lenye Kuba ya dhahabu na minara mirefu lilijengwa juu ya kaburi hilo. Idadi kadhaa ya watawala na wanachuoni wengi na watu watakatifu wamezikwa ndani ya mji wa Qum.   Mnamo mwaka 1340 AH, Ayatullah Abd al-Karim al-Haa’irii, mkurugenzi wa taasisi ya ufundishaji katika mji wa Kaskazini magharibi wa Arak, alikwenda kufanya Ziyarat kwenye mji wa Qum. Akitii shinikizo kutoka kwa wanachuoni na watu wa mji huo, yeye aliamua kufanya makazi hapo na kuzihuisha upya taasisi zao za mafunzo. Baada ya ujio wa Mapinduzi ya Kiislam ya Iran mwaka 1979, yaliyoongozwa na Ayatullah Khomeini na wanafunzi wake na wanachuoni wenziwe, Qum ikageuka kuwa kituo cha 162


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 163

U i s l a m u wa S h i a kiroho  cha  dola  hiyo,  na  mazingatio  zaidi  yalifanywa  kwenye  taasisi  za kisomi  za  Qum.  Mji  wa  Qum  sasa  ni  kituo  mashuhuri  cha  masomo  ya Kiislam ulimwenguni. Zaidi ya vyuo mia mbili vya kielimu au utafiti na taasisi zinafanya kazi hapo, na makumi ya maelfu ya wanachuoni na wanafunzi kutoka sehemu tofauti mbalimbali za dunia wanashughulika katika kujifunza ilmu mbalimbali za Kiislam. Msikiti muhimu wa Jamkaraan upo katika viunga vya mji wa Qum. Kwa mujibu  wa  wanahadith  (muhadithiin)  na  wanahistoria  wa  Shi’ah,  msikiti huu ulijengwa katika mwezi wa Ramadhan mwaka 393 AH na Hasan bin Muthleh  Jamkaraan  kwa  kuitii  amri  aliyoipokea  kutoka  kwa  Imam  wa Kumi  na  Mbili.  Kila  Jumanne  na Alhamisi  usiku,  makumi  ya  maelfu  ya wafanya ziyarat kutoka miji tofauti wanatembelea msikiti huu kufanya sala na du’a zao.

163


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 164

U i s l a m u wa S h i a

ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION 1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9. 10. 11. 12. 13. 14. 15. 16. 17. 18. 19. 20. 21. 22. 23. 24. 25. 26.

Qur'an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka  Thelathini Uharamisho wa Riba Uharamisho wa uwongo  Juzuu ya Kwanza  Uharamisho wa uwongo  Juzuu ya Pili Hekaya za Bahlul Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.) Hijab vazi Bora Ukweli wa Shia Ithnaashari Madhambi Makuu Mbingu imenikirimu Abdallah Ibn Saba Khadijatul Kubra Utumwa Umakini katika Swala Misingi ya Maarifa Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia Bilal wa Afrika Abudharr Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu Salman Farsi Ammar Yasir Qur'an na Hadithi Elimu ya Nafsi Yajue Madhehebu ya Shia Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur'an Tukufu 164


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 165

U i s l a m u wa S h i a 27. 28. 29. 30. 31. 32. 33. 34. 35. 36. 37. 38. 39 40. 41. 42. 43. 44. 45. 46. 47. 48. 49. 50. 51. 52. 53. 54.  55. 56.  57.

Al-Wahda Ponyo kutoka katika Qur'an.  Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii Mashukio ya Akhera Al Amali Dua Indal Ahlul Bayt Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna. Haki za wanawake katika Uislamu Mwenyeezi  Mungu na sifa zake Amateka Na Aba'Khalifa Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) Adhana Upendo katika Ukristo na Uislamu Nyuma yaho naje kuyoboka Amavu n’amavuko by’ubushiya Kupaka juu ya khofu  Kukusanya swala mbili Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Kusujudu juu ya udongo Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s) Tarawehe Malumbano baina ya Sunni na Shia Kupunguza Swala safarini Kufungua safarini Umaasumu wa Manabii Qur’an inatoa changamoto as-Salaatu Khayrun Mina -'n Nawm Uadilifu wa Masahaba  Dua e Kumayl Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu 165


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 166

U i s l a m u wa S h i a 58. 59. 60.

Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mitume         Muhammad (s) 61. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza 62. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili 63.  Kuzuru Makaburi 64. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza 65. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili 66. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu 67. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne 68. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano 69. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita 70. Tujifunze Misingi Ya Dini 71. Sala ni Nguzo ya Dini 72. Mikesha Ya Peshawar 73. Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu 74. Ubora wa Imam 'Ali Juu ya Maswahaba Na Ushia ndio njia  iliyonyooka 75. Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake 76. Liqaa-u-llaah 77. Muhammad (s) Mtume wa Allah 78. Amani na Jihadi Katika Uislamu  79. Uislamu Ulienea Vipi? 80. Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s)  81. Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s)  82.  Urejeo (al-Raja’a ) 83. Mazingira 84.       Utokezo (al - Badau)  85. Uadilifu katika Uislamu 86. Shahidi kwa Ajili ya Ubinadamu 166


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 167

U i s l a m u wa S h i a 87. 88. 89. 90. 91. 92. 93. 94. 95.

Uislamu Safi Mtoto mwema Adabu za Sokoni Johari za hekima kwa vijana Maalimul Madrasatain Sehemu ya  Kwanza Maalimul Madrasatain Sehemu ya  Pili Maalimul Madrasatain Sehemu ya  Tatu Tawasali Imam Mahdi katika Usunni na Ushia

96.

Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu

97.

Hukumu ya kujenga juu ya makaburi

98.

Swala ya maiti na kumlilia maiti

99.

Shiya na Hadithi (kinyarwanda)

100.

Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu

101.

Hadithi ya Thaqalain

102

Fatima al-Zahra

103.

Tabaruku

104.

Sunan an-Nabii

105.

Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza)

106.

Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili)

107.

Mahdi katika sunna

108.

Kusalia Nabii (s.a.w)

109.

Ujumbe -Sehemu ya Kwanza

110.

Ujumbe - Sehemu ya Pili

111.

Ujumbe - Sehemu ya Tatu

112.

Ujumbe - Sehemu ya Nne

113.

Kuhuzunika na Kuomboleza - Azadari 167


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 168

U i s l a m u wa S h i a 114.

Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah

115.

Kuonekana kwa Allah

116.

Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza

117.

Ukweli uliopotea sehemu ya Pili

118.

Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu

119.

Ukweli uliopotea sehmu ya Nne

120.

Ukweli uliopotea sehmu ya Tano

121.

Johari zenye hekima kwa vijana

122.

Safari ya kuifuata Nuru

123.

Ushia ndani ya Usunni

124.

Myahudi wa Kimataifa

125.

Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi

126.

Visa vya kweli sehemu ya Kwanza

127.

Maswali na Majibu

128.

Muhadhara wa Maulamaa

129.

Mwanadamu na Mustakabali wake

130.

Imam Ali binamu ya Mtume Sehemu ya Kwanza

131.

Imam Ali binamu ya Mtume Sehemu ya Pili

132.

Khairul Bariyyah

133.

Uislamu na mafunzo ya kimalezi

134.

Vijana ni Hazina ya Uislamu.

135.

Yafaayo  kijamii

136.

Abu Huraira

137.

Taqiyya

138.

Vikao vya furaha

139.

Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje? 168


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 169

U i s l a m u wa S h i a 140.

Uislamu na Mazingatio Sehemu ya  Kwanza

141.

Uislamu na Mazingatio Sehemu ya  Pili

142.

Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt  (Sehemu ya Kwanza)

143.

Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt  (Sehemu ya Pili)

144.

Mafunzo ya hukmu za ibada

145.

Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No  1

146.    Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No  2 147.      Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No  3 148.

Falsafa   ya Dini

149.

Elimu ya Tiba za Kiislam Matibabu ya Maimamu

150.

Ukweli uliofichika katika neno la Allah

151.

Sira ya Imam Ali kuhusu Waasi

152.

Uislamu na mfumo wa Jamii ya dini nyingi

153

Amali za Makka

154.

Amali za Madina

155.

Uislam wa Shia

156.

Majlis ya Imam Husein

157.

Mazingatio kutoka katika Qur’an - Sehemu ya Kwanza

158.

Mazingatio kutoka kaitka Qur’an - Sehemu ya Pili

159.

Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya kwanza

160.

Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya Pili

161.

Hukumu zinazomuhusu mkuu wa kazi na Mfanyakazi

162.

Falsafa ya mageuzi ya Imam Husein (a.s)

163.

Huduma ya Afya katika Uislamu

164.

Mas'ala ya Kifiqhi 169


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 170

U i s l a m u wa S h i a 165.

Asili ya Madhehebu katika Uislamu

166.

Uislamu na Mifumo ya Uchumi

167.

Umoja wa Kiislamu na Furaha

168.

Vipengee kadhaa katika Swala ya Jamaa na Msikiti

169.

Jifunze kusoma Qur'ani

170.

As-Sahifatul Kamilah as-Sajjadiyyah

171.

Hayya 'Alaa Khayri'l-'Amal Katika Adhana

172.

Ukweli kuhusu Funga ya Siku ya Ashura

173.

Dua za Miezi Mitatu Mitukufu (Rajabu, Shaabani na Ramadhani)

174.

Mtazamo wa Ibn Taymiyyah kwa Imam Ali (a.s.)

175.

Kazi na Bidii ni njia ya maendeleo

176.

Abu Talib - Jabali Imara la Imani

177.

Ujenzi na Utakaso wa Nafsi

178.

Vijana na Matarajio ya Baadaye

179.

Usalafi - Historia yake, maana yake na lengo lake

180.

Ushia - Hoja na Majibu

181.

Mateso ya Dhuria wa Mtume (saww)

182.

Maombolezo - Msiba wa Bwana wa Mashahidi (a.s.)

183.

Uongozi wa kidini - Maelekezo na utekelezaji wa Kijamii

184.

Takwa

185.

Amirul Muuminina ('as) na Makhalifa

186.

Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)

187.

Kuelewa Rehma ya Mwenyezi Mungu

188.

Mtazamo kuhusu msuguano wa kimadhehebu

189.

Upotoshaji Dhahiri katika Turathi (Hazina) ya Kiislamu

190.

Nchi na Uraia - Haki na wajibu kwa Taifa 170


Uislamu wa Shia Check Lubumba:Uislamu wa Shia Check Lubumba.qxd 7/16/2013 9:20 AM Page 171

U i s l a m u wa S h i a 191.     Qur’ani Tukufu - Pamoja na Tarjuma ya Kiswahili

BACK COVER Ni ukweli usiopingika kwamba madhehebu ya Kiislamu ya Shia imekuwa ikijulikana  kwa  muda  mrefu  kama  ni  madhehebu  isiyoeleweka  vizuri miongoni  mwa  Waislamu  walio  wengi  ulimwenguni.  Hii  imetokana  na kukandamizwa kwa muda mrefu wafuasi wa madhehebu hii kulikofanywa na  dola  zinazojiita  za  Kiislamu.  Kwa  nini  wamefanya  hivyo?  Historia inayo majibu ya hilo. Waandishi  wanavyuoni  wengi  wa  sasa  wamejitahidi  na  wanaendelea  na jitihada  hiyo  kuuelemisha  Umma  kuhusu  Waislamu  hawa  wa  Shia;  na kitabu hiki ni miongoni mwa vitabu vingi vilivyoandikwa na wanavyuoni hawa juu ya usahihi wa madhehebu hii. Ni muhimu kukubaliana na kuziheshimu tofauti za kila mmoja na kutambua msimamo na mtazamo wa kila mmoja. Matatizo huja pale mtu anapolazimisha tabia, imani na mila zake zitawale wengine au kuzifisha itikadi na misimamo ya wengine. Ni  muhimu  kufikiria  kila  aina  ya  maoni  katika  kujaribu  kuamua  ukweli. Uislamu kimsingi uko dhidi ya kufuata kibubusa.  Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255   22   2110640 / 2127555 Barua Pepe: alitrah@yahoo.com Tovuti: www.ibn-tv.com Katika mtandao: www.alitrah.info

171


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.